UZOEFU WA UMOJA KATIKA KANISA LA AWALI
Somo la 5 kwa ajili ya Novemba 3, 2018
“Wakawa wakidumu katikafundisho la mitume, na katikaushirika, na katika kuumega
mkate, na katika kusali”(Matendo 2:42)
FUNGU KIONGOZI
Kanisa la awali ni kielelezo kikuucha umoja.
Je; Waliufikiaje huo umoja? Tunaweza kuwa na umoja kamahuo kanisani leo?
Maandalizi
Kazi ya Roho Mtakatifu
Kuwa na muda pamoja
Kuwa wakarimu
Kuwafikiria wengine
Angewakumbushayale Yesu aliyokuwaamewafundisha(Yohana 14:26)
Yeye afunuaye kwelimpya(Yohana 16:13)
Angewasaidiakushuhudiaulimwengu wote(Matendo 1:8)
“Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmojakatika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamumama yake Yesu, na ndugu zake.” (Matendo 1:14)
Kabla ya kupaa Mbinguni, Yesu aliahidi angekuja Msaidizi. Angefanya kazi maaluma ndani ya wafuasi wa Yesu :
Walijiandaa kwa siku 10 ili kupokea kipawa cha Roho:
Waliomba
Walirejea uzoefu wao na Yesu
Walitubu na kuungama dhambi zao
Waliomba kwa ajili ya Roho Mtakatifu
Waliweka tofauti zao kando
Kwa kadri walivyokuwa karibu na Yesu, ndivyo walivyokuwa wamoja.
KAZI YA ROHO MTAKATIFU
Sikukuu ya majuma au Pentekoste (Siku ya50) ilikuwa ni sherehe maradufu.
Upande mmoja, walisherekea sheriailiyotolewa pale mlima Sina. Sasa mwanzowa Israeli uliambatana na mwanzo waKanisa. Sheria na Injili vikakutana.
Upande mwingine, hii ilikuwa ni sikukuu yakutoa shukurani. Walishukuru kwa vipawavilivyopita na vijavyo kutoka kwa Mungu. Walitoa malimbuko ya mazao yao.
Roho Mtakatifu alikusanya matunda (roho3,000) kwa kuwapa wanafunzi karama yakunena kwa lugha za watu waliokusanyikaYerusalemu.
Utofauti wa lugha ulileta ugawanyiko kuleBabeli. Kizuizi hicho kilivunjwa katika siku yaPentekoste, hivyo wote wakawa na umojakatika Kristo.
“Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katikakuumega mkate, na katika kusali.”(Matendo 2:42)
Watu wengi waliguswa kutubu waliposikiahabari za ufufuo na kupaa kwake. Dhambi zaozilisamehewa kwa jina la Yesu.
Waliamua kutenga muda wakuwa na Mwokoziwao tangu siku ile:
• Muda wa kusoma Biblia• Muda wa kuzungumza wao kwa
wao na kujifunza habari za Yesu• Muda wa kula pamoja• Muda wa kuomba pamoja
Kujitoa kwao kulileta umoja kwa Kanisa. Ulikuwa ni ushuhuda wenye nguvu kwa wale waliokuwa wakiwatazama (Matendo 2:43)
“Wala hapakuwa na mtu mmoja miongonimwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu
wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile
vilivyouzwa.” (Matendo 4:34)
Ukarimu ulikuwa matokeo ya umoja wao nanamna walivyopendana.
Kila walichokimiliki walikishiriki na wengine kwakadri ya mahitaji yao.
Barnaba alikuwamafano waukarimu huu usiona ubunafsi(Matendo 4:36-37)
Kinyume chake, Anania na Safira waliacha choyo ikajaza mioyoyao wakamdaganya Roho Mtakatifu (Matendo 5:1-11)
Uchoyo ni dhambi hatari inayodidimiza umoja. Hukaa moyonina haionekani kwa nje.
Kanisa la awali lilihimiza tabia hii kamauthibitisho wa umoja miongoni mwawashiriki.
Paulo alihimiza makanisa ya wamataifakulisaidia kanisa lenye kuhitaji hukoYerusalemu, “mkitajirishwa katika vituvyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kaziyetu.” (2 Wakorintho 9:11)
“maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizokwa ajili ya watakatifu huko Yerusalemu walio maskini.” (Warumi 15:26)
Suluhisho la uchoyo ilikuwa kuachakujifikiria mwenyewe na kuanzakuwafikiria wengine. Ni lazima tumruhusu Roho Mtakatifu afanye hii kazimioyoni mwetu.
UMOJA KATIKA KANISA LA AWALIJe; Ni kitu kipi kilihimiza umoja katika kanisa la awali?
MaombiIbadaUshirikakujifunza BibliaKuhubiri injiliUpendo na kujali
1
2
3
4
5
6
Umoja wao ukazaa ukarimu nakusaidiana, katika kanisamahalia na miongoni mwamakanisa katika maeneotofauti ya kijiografia.
“Baada ya kushuka kwa Roho
Mtakatifu wanafunzi walisonga mbel
kumtangaza Mwokozi aliyefufuka.
Walifurahia katika utamu wa
ushirika na watakatifu. Walikuwa
wapole, wenye kuwafikiria wengine,
wenye kujikana nafsi, walio tayari
kujitoa kafara kwa ajili ya kweli.
Katika mahusiano yao ya kila siku
walidhihirisha upendo ambao Kristo
aliwaamuru kuudhihirisha. Kwa
maneno na matendo yasio na ubinafsi
walifanya bidi kuangaza upendo ulio
mioyoni mwao.”E.G.W. (Testimonies for the Church, vol. 8, cp. 38, p. 241)
“Ushuhuda wao katika uanzishwaji wa kanisa
la Kikiristo unatolewa kwetu sio tu kama
sehemu muhimu ya historia takatifu lakini pia
kama somo. Wote wanaolitaja jina la Kristo
wangoje, wakeshe, na kuomba kwa moyo
mmoja. Tofauti zote ziwekwe kando, na umoja
na upendo wa mmoja kwa mwingine vitawale
yote. Kisha maombi yetu yataenda kwa pamoja
juu kwa Baba yetu wa Mbinguni yakiwa na
nguvu na Imani thabiti. Kisha tukiungoja kwa
subira na tumaini utimilifu wa ahadi.”
E.G.W. (The Story of Redemption, cp. 32, p. 246)