KENYATTA UNIVERSITY
INSTITUTE OF OPEN LEARNING
AKS 400SOCIOLINGUISTICS
NA
PAMELA M. Y. NGUGI NA LEONARD M. CHACHA
IDARA YA KISWAHILI NA LUGHA ZA KIAFRIKA
© KUIOL 2004
YALIYOMOLengo la Kozi ....................................................................(i)
SOMO LA KWANZA ............................................................1ISIMUJAMII ...................................................................11.0 Utangulizi ...............................................................11.1 Madhumuni .............................................................11.2 Isimu-jamii ni nini? ..................................................11.3 Mikabala ya Isimujamiii ........................................31.4 Historia fupi ya Isimujamii........................................ 41.5 Lugha na Jamii ........................................................101.6 Isimujamii na Taaluma nyingine ................................121.7 Mitazamo ya lugha ...................................................14
SOMO LA PILI ...................................................................18NADHARIA ZA KIJAMII .................................................182.0 Utangulizi ................................................................182.1 Madhumuni .............................................................182.2 Nadharia a Kiisimu................................................... 182.2.1 Uamilifu .................................................................182.2.2 Umaksi---------------------------------------------------------- 21
SOMO LA TATU .................................................................26DHANA ZA KIMSINGI KATIKA ISIMUJAMII .................263.0 Utangulizi ................................................................263.1 Madhumuni .............................................................263.2 Lugha .....................................................................263.2.1 Matumizi ya Lugha .................................................283.2.1 Mitazamo Elezi na Elekezi ya Lugha--------------------- 293.3 Lahaja------------------------------------------------ ---------- 323.3.1 Maana ya Lahajai ....................................................323.3.2 Kuzuka kwa Lahaja ----------------------------------------- 333.3.3 Nadharia ya Mawimbi---------------------------------------- 343.3.4 Istilahi Zinazotumika katika Lahaja----------------------- 353.5 Aina za Lugha------------------------------------------------- 363.6 Lugha au Lahaja--------------------------------------------- 383.7 Mtindo Pekee......................................................... 403.8 Mtindo--------------------------------------------------------- 403.9 Sajili------------------------------------------------------------ 463.10 Jumuia Lugha------------------------------------------------- 51SOMO LA NNE ...................................................................57LUGHA ZA MAWASILIANO PANA ...................................574.0 Utangulizi ................................................................57
2
4.1 Madhumuni .............................................................574.2 Lingua franka ..........................................................574.3 Pijini na Kirioli ..........................................................584.4 Nadharia za Asili ya Pijini ..........................................63
SOMO LA TANO .................................................................67UWILI LUGHA ...............................................................675.0 Utangulizi ................................................................675.1 Madhumuni .............................................................675.2 Uwili lugha ..............................................................675.3 Sababu za kuwepo na uwili lugha .............................685.4 Uchaguzi wa lugha katika jamii zenye uwili-lugha ......695.5 Mambo muhimu ya kuzingatiwa katika uwili-lugha .....705.6 Lugha Rasmi na Lugha ya Taifa ...............................735.7 Diglosia na Triglosia ...............................................745.8 Triglosia ................................................................825.9 Kubadili msimbo ....................................................825.10 Utowekaji wa lugha ...............................................84
SOMO LA SITA .................................................................91UPANGAJI LUGHA .........................................................916.0 Utangulizi ...............................................................916.1 Madhumuni ............................................................916.2 Upangaji lugha .......................................................916.3 Mawanda ya Upangaji lugha ....................................946.4 Mchakato wa upangaji lugha ....................................976.5 Lugha ya Taifa na Lugha Rasmi ................................1026.6 Sera ya lugha nchini Kenya .......................................102
SOMO LA SABA ...................................................................112ISIMU JAMII NA ELIMU ..................................................1127.0 Utangulizi .................................................................1127.1 Madhumuni ...............................................................1127.2 Ufunzaji, ujifunzaji na usomaji ....................................1127.3 Lugha katika Elimu .....................................................114
SOMO LA NANE ...................................................................124LUGHA NA JINSIA ............................................................1248.0 Utangulizi ..................................................................1248.1 Madhumuni ...............................................................1248.2 Jinsia na Isimu Jamii------------------------------------------ 1248.3 Lugha ya Wanawake na Wanaume ..............................125
3
Muhtasari wa Kozi Lengo la kozi hii ni kudadisi na kueleza uhusiano uliopo kati ya lugha na jamii.Somo hili linalenga kuchunguza hali mbalimbali za kijamii na jinsi zinavyoathirimatumizi ya lugha katika miktadha mbalimbali. Aidha, kozi hii itawawezeshawanafunzi kudhibiti mbinu na ujuzi wa mawasiliano miongoni mwao na watuwengine kwa kuzingatia kaida za lugha husika.
4
SOMO LA KWANZAISIMUJAMII
1.0 UtanguliziKatika somo hili tutatoa maana ya isimujamii pamoja na kueleza historia yake.Tutaeleza mikabala mbalimbali ya isimujamii. Vile vile tutaeleza uhusiano uliopokati ya lugha na jamii. Aidha, tutaonyesha uhusiano wa isimujamii na taalumanyingine. Na mwisho tutajadili mitazamo mbalimbali kuhusiana na swala lalugha.
1.1 Madhumuni
Baada ya kulipitia somo hili, tunatarajia kwamba utaweza:i. Kutoa maana kamili ya isimujamii pamoja na kueleza historia yake.ii. Kueleza kikamilifu mikabala ya isimujamii.iii. Kuonyesha uhusiano uliopo kati ya lugha na jamii.iv. Kueleza uhusiano wa isimujamii na taaluma nyingine.
1.2 Isimujamii ni nini?Wataalamu wametoa fasiri mbalimbali za neno isimujamii . Labov (1992:183)anaeleza kuwa, isimujamii ni mtazamo wa kiutafiti wa isimu unaolengamatumizi ya lugha katika jumuia lugha . Pride (1972:287) anasema kuwaisimujamii ni uchunguzi wa lugha kama sehemu ya utamaduni na jamii . Lyons(1981) anaiainisha isimujamii kama tawi moja muhimu la isimumakro(microlinguistics), matawi mengine yakiwa isimunafsia, isimuethnolojia, n.k.Hudson (1980:1) anaieleza isimujamii kuwa ni, uchunguzi wa jinsi lughainavyohusiana na jamii .
Kwa hivyo tunaweza kusema kuwa isimujamii ni taaluma inayochunguza lughakama inavyotumiwa na jamii katika fani na mazingira mbalimbali ya kila siku.
5
Mkazo katika isimujamii umewekwa kwa watumiaji wa lugha wenyewe. Basiisimujamii ni taaluma ambayo inapanua mawanda ya kimuktadha ya isimu kupitayale mazungumzo.KUMBUKA
Isimu jamii imejumuisha maneno mawili: Isimu na jamii.Isimu ni sayansi ya lugha.Jamii ni mkusanyiko wa vitu vinavyofana.
1.2.1 Isimu jamii inahusu nini?Wardhaugh (1986} anasema kuwa isimujamii inahusika na uchunguzi wa kuwekawazi uhusiano uliopo kati ya lugha na jamii ikiwa na lengo la kuelewa muundowa lugha na jinsi lugha inavyofanya kazi katika mawasiliano. Katika isimujamiitunaichunguza jamii ili kufahamu mengi zaidi kuhusu lugha.
Labov (1980) aneleza kuwa eneo jingine la utafiti ambalo limeongezwa katikaisimujamii ni sosholojia ya lugha.Hii hushughulika na maswala mengi yakijamii na jinsi yanavyoingiliana na lugha na lahaja. Haya ni pamoja na matatizoyanayohusishwa na kudhoofika na hata kufa kwa lugha na kumezwa kwa lughazenye watu wachache, maendeleo ya uwili-lugha, usanifishaji wa lugha, naupangaji wa lugha hasa katika mataifa yanayoendelea.
Eneo lingine ambalo linajumuishwa katika isimujamii na linahusika na lughakatika matumizi yake ni ethnografia ya mawsiliano. Ethnografia ni maelezoya kisayansi kuhusu mbari, mila, utamaduni wa binadamu. Mambo yanayohusikahapa ni kueleza na kuchanganua ruwaza za matumizi ya lugha na lahaja katikautamaduni fulani: matukio yanayozusha mazungumzo, uhusiano kati yamzungumzaji, hadhira, mada, njia ya kuwasilisha na muktadha. Pia katikaisimujamii kuna sajili au rejista ambayo hurejelea matumizi tofauti tofauti yalugha.
6
Pamoja na hayo kuna kuchanganya lugha tofauti hivi kwamba tunapata kubadilimsimbo (code switching) na kukopa, na jinsi lugha tofauti zinavyoingilianahata kusababisha pijini na krioli.
Hudson (1984:4-5) anasema kuwa, isimujamii hushughulikia wazungumzajibinafsi kama wanachama wa makundi ya kijamii na huuliza maswali kama vile,kwa nini kuna tofauti nyingi kati ya makundi haya, na tofauti hizo ni zipi .
1.3 Historia Fupi ya IsimujamiiKatika miaka 50 hivi iliyopita, utambuzi wa umuhimu wa uhusiano kati ya lughana jamii umepelekea kukua kwa taaluma mpya inayoitwa isimujamii. Ingawakulikuwa na haja ya kuichanganua lugha kulingana na miktadha yake yamatumizi katikati mwa karne iliyopita, jina la isimujamii halikutumika hadimwaka wa 1952 katika kazi ya Haver C. Currie, aliyekuwa Mshairi naMwanafalsafa(Tazama Mesthrie (2001). Miaka kumi baadaye istilahisociolinguistika ilitumika Urusi, na katika mwaka wa 1964 utafiti wa isimujamiiukasambaa Marekani.
Isimujamii kama taaluma imekua na kupata maendeleo makubwa katika miakaya mwishoni mwa sitini (1960 s) na mwanzoni mwa sabini (1970 s). Hata hivyouchunguzi ulioihusisha lugha na jamii umekuwepo tangu zamani hasa wataalamuwalipochunguza lahaja na uhusiano kati ya maana ya maneno na utamaduni.
Kongamano la kwanza la isimujamii lilifanyika katika Chuo cha University ofCalifornia- Los Angeles mwaka wa 1964. Huu ndio mwaka ambao isimujamiiimejitokeza kikamilifu kama taaluma. Tangu hapo utafiti mwingi umefanywa nawaandishi mashuhuri wa taaluma hii miongoni mwao wakiwa, Grimshaw, Hymes,Fishman, Gumperz, Labov, na Lieberson. Taaluma hii imejulikana pia kamasosholojia ya lugha.
7
1.4 Mikabala ya Isimu JamiiKama tulivyosema hapo mwanzoni, wanaisimujamii hawafasiri isimujamii kwanamna moja. Zipo sababu nyingi za kutofanya hivyo, lakini tutatoa tatu tu:(a) Sababu ya kwanza inatokana na fasiri ya lugha. Wapo wanaisimu
wachache kama vile Labov 1972, Trudgill 1974, Halliday and Martin 1981n.k ambao bado wanaichambua lugha ya jamii kwa kufuata misingi yakiisimu.
(b) Wataalamu waliofafanua isimujamii, walilielewa neno jamii kwa namnatofauti. Baadhi walishikilia maana pana ya kuhusisha watu wote waishiokatika taifa moja (lenye makabila na mataifa mbalimbali pamoja).Wengine wamechukua maana finyu ya kuhusisha wale watu waishiokatika sehemu moja walio na lugha moja na kuchangia utamaduni mmoja.
(c) Pia kumekuwepo na misisitizo mbalimbali katika ufafanuzi wa isimujamii.Wapo wanaisimu wanaoelezea lugha ya jamii kwa kufuata mwelekeo wakisaikolojia, kisosiolojia, kianthropolojia, kihistoria, kiethnolojia, nk.
Kwa sababu hii kumetokea mikabala mitatu ya isimujamii:(a) Mkabala wa kimaikro(b) Mkabala wa kimakro(c) Mkabala kati
1.4.1 Mkabala wa KimaikroMkabala wa kimaikro unajumuisha mitazamo yote ambayo inafafanua isimujamiikwa kufuata mbinu na nadharia za kiisimu. Mkabala huu hutazama isimujamiikama mwendelezo wa taaluma ya isimu.
Je, ni nini mawanda ya isimujamii kwa mujibu wa mkabala huu? Si rahisikusema kwa mkato kuwa mawanda ya isimujamii yanaanza hapa na kuishia pale.
8
Tunachoweza kusema ni kuwa wakati uchambuzi wa kiisimu unatilia mkazomaana itokanayo na kuchunguza uhusiano wa maneno kiwima na kiusilisila(syntagmatic uhusiano wa kiulalo wa vipashio vya tungo) katika sentensi,uchambuzi wa kupata maana kiisimujamii unaongezea juu yake sifa za kijamii.Kwa mfano:(i) Amekwenda ntoni kuchota maji(ii) Mtoto ayupo apaKatika mifano hii, mtaalamu wa isimu atakuwa na haya ya kusema.1. Atagundua kwamba mwandishi ametumia maneno ntoni , ayupo , apa
badala ya mtoni , hayupo na hapa . Katika ufafanuzi wake atasema kuwahayo si maneno sanifu ya Kiswahili ni maneno yatokanayo na lughambalimbali. Ataeleza ni kina nani wanazungumza lugha ya Kiswahili hivyo.
2. Licha ya kasoro za matumizi ya maneno hayo, sentensi zote mbili zinatoamaana zilizokusudiwa. Katika sentensi ya kwanza tunafahamu kuwa mtajwahakwenda mahali pengine isipokuwa mtoni kwa madhumuni ya kuchota maji.Sentensi ya pili ina maana kuwa mtu ambaye hayupo ni mtoto wala si mtu warika jingine. Tunazipata maana kwa kuzingatia uhusiano wa maneno kamayalivyotumika katika sentensi.Mwanaisimu jamii atazichambuaje sentensi hizo hapo juu?Kwanza, atakubaliana na uchambuzi uliofanywa hapo juu pamoja na maanazake.Pili, atataka kujua watu gani (wa sehemu gani [kabila], umri gani, kisomogani, kipato kipi, wake au waume) wanaotamka ntoni , ayupo na apabadala ya mtoni, hayupo na hapa.Tatu, atataka kujua sababu zinazowafanya watamke hivyo.Nne, atataka pia kujua ni wakati gani na katika mazingira gani mtu hutamkahivyo. Inawezekana wanatamka hivyo wanapoongea na watu wa makabilayao lakini wanayatamka vizuri wanapoongea na watu wa makabila tofauti.
Uchambuzi wa Kiisimujamii unatuonyesha mambo kadha wa kadha ya
9
kimsingi: Baadhi ya maneno (ntoni, ayupo na apa) yaliyotumika katika sentensi zetu
yanahusishwa na aina mbalimbali za watu katika jamii.Hii ina maanakuwa lugha si tu kuelewa maana ya maneno bali pia hutumika kuielewajamii ilivyo.
Pili, hatuwezi kudai kuwa mtu anayetumia maneno ya vilugha katikamazungumzo yake hajui kutamka maneno ya Kiswahili sanifu. Mtuanaweza kutumia vilugha kwa sababu zake mbalimbali ikiwemo ile yakutaka kuonyesha mshikamano wake na watu wa kabila lake au watuwatokao sehemu moja kihistoria na kijiografia.
Miongoni mwa wafuasi wa mkabala huu ni pamoja na Labov (1972) na Trudgill(1974). Labov (1972) amejitokeza kuwa mwanaisimu mashuhuri katika miaka yasabini (1970) kutokana na utafiti wake ulioonyesha uwezekano wa kuoanishaalama za kiisimu (linguisitic forms) na zile za kijamii na kufanikiwa kupata habarizaidi juu ya jamii hiyo.
Labov aliufanya utafiti mjini New York ulioonyesha kuwa watu wa tabaka la chinihutamka sauti (r) inayosikika katika kuyatamka maneno yenye fonimu /r/ kulikowatu wa matabaka mengine. Labov anatumia nadharia na mbinu zile zile zaisimu kuelezea isimu jamii. Pia anachunguza ni mazingira yapi na sababu zipi(kiisimu/kijamii) zinazoleta ubainifu miongoni mwa watumiaji wa lugha.
1.4.2 Mkabala wa KimakroHuu ni mkabala unaoangalia isimujamii kinyume na mkabala wa kimaikro. Nimkabala wa kimakro kwa sababu unahusisha watu wengi kijiografia. Mkabalahuu unaeleza na kufafanua lugha kwa kutumia mwingiliano wa mbinu na dhanambalimbali kutoka taaluma nyingine za kijamii. Mkabala huu huangalia mamboyote yanayohusu utumiaji wa lugha kwa ujumla katika jamii. Kujua lugha
10
zilizopo katika jamii na uhusiano wake na lugha nyingine ni moja tu ya mamboya kimsingi ya mkabala huu.
Kwa mfano, mwanaisimu jamii wa mkabala huu, hupenda kujua sababu zamsingi zinazofanya lugha moja iteuliwe kuwa lugha ya taifa, lugha rasmi, aulugha ya kufundishia katika elimu. Sababu kama hizo aghalabu huwa hazinabudi zitokane na misingi ya pamoja ya kiisimu na kijamii. Pia, hata zile lughaambazo hazikuteuliwa kuchukua dhima fulani kitaifa, bado kwa mujibu wamkabala huu lugha hizo ni muhimu kukuzwa na jamii zinazohusika ilikuziimarisha. Nani anazungumza lugha ipi, wapi, kwa nini, na kwa madhumunigani, ni miongoni mwa maswala muhimu yanayoshughulikiwa na mkabala huu.
Mwanaisimujamii haangalii maana ya tamko peke yake bali huangalia maana kwakuzingatia taratibu na kanuni za mawasiliano zinazotumika katika jamiiinayohusika. Hii ina maana kwamba, uchambuzi wa kupata maana katika lughahaufanywi nje ya taratibu za kijamii na mazingira ya tamko lenyewe. Nenomazingira hapa lina maana ya kuhusisha mahali tamko liliposemwa, kujuahabari za mzungumzaji na msikilizaji pamoja na uhusiano wao na kujua taratibuna kanuni zinazotawala mawasiliano ya lugha inayohusika.Mkabala huu hauchambuisentensi zisizotumiwa katika mazungumzo yamajibizano. Ni katika msingi huu ndipo sentensi:
(i) Amekwenda ntoni kuchota maji.(ii) Mtoto ayupo apa.
haziwezi kutupatia uchambuzi unaoridhisha kwa mujibu wa mkabala huu.Tunahitaji kuchambua sentensi au matamko yatokanayo na mazungumzo namajibizano kama mfano wetu hapa chini unavyoonyesha:
(iii) Baba Mkwe: Mwanangu, umefika salama?(iv) Mkwe: Ndiyo baba, tumefika salama.(v) Mkwe: Haya baba, mfike salama.
11
(vi) Baba Mkwe: Asante Mwanangu.
Katika kuchambua maana za sentensi hizi uhusiano wa mzungumzaji namsikilizaji ni muhimu sana kuzingatiwa. Uchambuzi unatuonyesha kuwa katikasentensi (iv) mkwe ametumia kiambishi cha wingi tu badala ya umoja. Vile vilekatika sentensi (v). Je, tunaweza kusema kuwa huyu mkwe hajui matumizisahihi ya viambishi nafsi?
Hapa, maswala kama ya utamaduni, kaida na kanuni za mawasiliano katika jamiin.k. yanafaa kuzingatiwa katika uchambuzi. Kwa mujibu wa kanuni zamawasiliano ya jamii hiyo, mtu aliye mdogo katika umri hutakiwa kutumiakiambishi cha nafsi ya kwanza wingi badala ya umoja anapozungumza na mtuwa umri mkubwa kama dalili ya kuonyesha heshima. Tumefikia maana hii baadaya kuzingatia taratibu na kaida zinazotumiwa katika mawasiliano ya lughainayohusika.
Fishman(1972) amesema kuwa ni muhimu kwa wataalamu wa lugha kutumiambinu za pamoja (kiisimu na kijamii) katika kufikia uteuzi wa lugha ili zichukuedhima mbalimbali katika jamii.
Zoezi
Je, unaweza kuonyesha tofauti kati ya isimu kimaikro na isimu kimakro kwakutumia mifano kutoka kwa jamii yako?
1.4.3 Mkabala KatiKimsingi, mkabala huu unazingatia yale mambo ya kimsingi tu kutokana namikabala yote miwili. Kudai kuwa lugha ielezwe na kufafanuliwa kwa kufuatakanuni za kiisimu peke yake, ni dai la kiwango cha juu. Lakini mkabala wa
12
kimaikro bado una mambo yake ya kimsingi ambayo yanaweza kuchukuliwa nakutumiwa katika kueleza lugha kiisimujamii. Kwa mfano, baadhi ya kanuni zafonolojia na mofolojia zinaweza kutumiwa sambamba na sifa nyingine za kijamiiili kueleza kaida zinazofuatwa na watumiaji wa lugha katika mazingirambalimbali.
Mwanaisimujamii anao uhuru wa kushughulikia uchambuzi wa lugha kwaviwango na idadi ya watu (watumiaji wa lugha) apendao mwenyewe kulinganana lengo la kazi yake.
Ervin Tripp (1971) ni miongoni mwa wanaisimujamii wachache wanaofuatamkabala wa kati. Anasisitiza umuhimu wa kuchunguza kanuni za kijamiizinazotawala mazungumzo mbalimbali ya kila siku. Anadai kuwa mazungumzoyanayofanywa na watu hayafanywi kiholela bali hufuata kanuni za mawasilianokatika jamii zinazohusika. Kwa mujibu wa mtazamo huu, isimujamii inapaswakushughulikia uchunguzi wa kanuni na kawaida za kijamii zinazotawalamawasiliano kwa jumla.
Tumeona kuwa isimujamii ni taaluma pana na inayovuka mipaka ya isimu nakuhusisha taaluma nyingine za kijamii. Si rahisi kuweza kueleza mipaka kati yaisimu na isimujamii. Hii ni kwa sababu taaluma hizi zinaingiliana sana.
Mwanaisimujamii hashughuliki na utoaji wa maamuzi yahusiyo lugha kwa niabaya jamii. Kazi ya mwanaisimujamii ni kueleza na kufafanua lugha kwa misingi yaisimujamii. Utoaji wa maamuzi yahusuyo lugha yameachiwa watumiaji wa lughawenyewe.
Swali
Ukizingatia kila mkabala, onyesha jinsi lugha inavyotumiwa katika jamii yako.
13
1.5 Lugha na JamiiIsimujamii ni dhana ambayo imetokana na isimu na inaingtia lugha kamainavyotumiwa katika jamii. Lugha si kifaa tu cha kuwasilisha habari bali ninamna muhimu ya kuanzisha na kudumisha uhusiano miongoni mwa watu.
Kila tunapozungumza, wasikilizaji wetu hupata habari fulani kuhusu sehemutunazotoka na sisi ni watu wa aina gani. Hata mielekeo yetu na mawazo yetuvinaweza kutumiwa na wengine kutuelewa zaidi. Mambo mawili haya ni muhimusana kutokana na mtazamo wa kijamii.
(a) Dhima ya lugha ya kuanzisha mahusiano ya kijamii.(b) Dhima ya lugha ya kuwasilisha habari fulani kuhusu mzungumzaji.
Kiisimu, lugha sanifu haichukuliwi kuwa bora kuliko lahaja au lugha nyinginezo.Lugha zote zina mifumo tata yenye kanuni za kipekee. Kule kusema kuwa lughamoja ni bora kuliko nyingine ni jambo la kijamii, si la kiisimu. Ikiwa watu nimaskini au wa ngazi ya chini, basi hata lugha zao zitadharauliwa. Kwa hivyomielekeo yetu kuhusu vilugha hivi huonyesha muundo wa kijamii wa watu.
Katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha na jamii, wataalamu wengiwamezungumzia nadharia tete ya Sapir-Whorf (Edward Sapir na Benjamin LeeWhorf). Nadharia hii inaeleza kuwa lugha asilia ya mtu hutawala jinsianavyouelewa ulimwengu. Hii ina maana kwamba tofauti za kiisimu huwezakuzusha utambuzi unaotofautiana. Ina maana kwamba hatuwezi kuwaza bilalugha. Basi ikiwa mtu anaweza kudhibiti lugha wanayojifunza watu, atakuwa nauwezo wa kudhibiti mawazo yao.
Kulingana na Sapir-Whorf (1956), binadamu huelewa mazingira kupitia kwalugha wanayoitumia. Wanatoa mfano wa Waeskimo ambao wana maneno
14
mengi yanayoelezea hali mbalimbali za theluji, huku Kiingereza kikiwa na nenomoja tu snow. Pia katika jamii ya Hopi, lugha yao inataja vitu kama mawinguna mawe kama vitu vilivyo hai. Hali hii inawafanya waufikirie ulimwengu kwanjia tofauti na watu wengine.
Eneo analoishi mtu hujitokeza katika lugha yake hasa katika muundo wamsamiati. Kwa mfano, mfumo wa aila katika jamii hujitokeza katika msamiati waaila kama vile mtoto, binti, babu, nyanya, shangazi, n.k.
Pia maadili ya jamii yanaweza kuwa na athari katika lugha ya jamii hiyo. Hayahutokea kupitia kwa miiko. Miiko huhusika na tabia ambazo zimekatazwa katikajamii fulani. Katika lugha, miiko inahusishwa na vitu au maneno yasiyotumika aukutajwa. Maneno ambayo ni mwiko katika lugha fulani hutuonyesha (kwa kiasifulani) mfumo wa maadili na imani za jamii hiyo.
Kwa hivyo mwiko ni swala la kiisimu kama lilivyo la kijamii. Miiko husababishamaneno fulani kupotea kutoka kwenye lugha na mengine kuzuka.
Kwa hivyo, isimujamii ni sehemu ya isimu inayoiangalia lugha kama sehemu yakijamii na utamaduni wa watu. Inachunguza nyanja za lugha na jamii, na inauhusiano wa karibu na taaluma nyingine kama anthropolojia, sosholojia,saikolojia na hata jiografia.
1.6 Isimujamii na Taaluma NyingineSi watafiti wa isimu na isimujamii pekee wanaohusika na uchunguzi wa lughakatika jamii. Wataalamu kutoka kwa taaluma nyingine kama vilewanaanthropolojia, wanasaikolojia, n.k huhusika pia.
15
1.61 Isimujamii na SaikolojiaTaaluma hizi mbili hushughulikia swala la mielekeo (attitudes) kuhusu aina fulaniza lugha. Ingawa wanaisimujamii wanachunguza kwa kina swala la mielekeokuhusu lugha, hili ni jambo la kisaikolojia kwa kuwa lipo katika akili ya mtu.Uchunguzi huu ni muhimu katika kueleza mabadiliko ya kiisimu yanayojitokezakatika lugha. Mara nyingi sababu hii hutumiwa kueleza kwa nini lahajainabadilika, lini na jinsi inavyobadilika. Kwa mfano, nchini Kenya vijanawanatamka neno best kama beshte ili kuafikiana na mielekeo ya vijana kuhusumatamshi ya maneno fulani hasa mijini.
Wanasaikolojia hutueleza jinsi mtoto anavyojifunza lugha kupitia kwa uwezomaalum anaozaliwa nao (innate capacity), lakini pia lazima tufahamu jinsi tofautiza kimazungumzo (mf kijinsia) zinavyokuzwa katika mchakato wa kuingilianakijamii.
1.6.2 Isimujamii na AnthropolojiaAnthropolojia ni taaluma inayohusika na elimu ya binadamu, hususan elimuinayohusu habari za asili na maendeleo yake ya awali. Inachukuliwa kuwa jinsibinadamu huyu alivyokua katika kikundi, alikuwa anazungumza lugha fulani.
Wanaanthropolojia kadha wamefanya utafiti ambao una misingi ya kiisimujamii,kwa mfano, kwa kuchunguza mfumo wa aila wa jamii. Tunajua kuwa mfumo waaila hujitokeza katika msamiati. Kwa mfano, utaona kuwa jamii nyingi za Kiafrikazina msamiati mpana unaoelezea uhusiano wa kiaila kuliko lugha za Wazungu.Jambo hili linatueleza mengi kuhusu jamii hizo. Kwa mfano, lugha ya Kiingerezahuzungumzia aina moja tu ya shangazi (aunt) lakini katika lugha nyingi zaKiafrika kuna maneno ya uhusiano huu kwa upande wa baba na wa mama.Zoezi
Taja majina ya kiaila katika jamii yako na ulinganishe na ya Kiingereza.
16
1.6.3 Isimujamii na ElimuWanaelimu wanatakiwa kutoa maamuzi kuhusu maswala yanayohusu lughakama vile ufundishaji wa lugha sanifu. Wanaisimujamii wamekuwa wakijaribukushawishi wanaelimu wabadili mielekeo yao kuhusu lugha fulanizinazozungumzwa na watoto fulani shuleni kama vile lugha zao za kwanza.Wapangaji lugha huhitajika kuwa na ufahamu fulani wa kiisimu ili waweze kutoauamuzi unaofaa kuhusu aina ya lugha inayotakiwa kukuzwa na kuhimizwa katikamiktadha fulani, daraja na shule nk.
1.6.4Isimujamii na UtamaduniWanaanthropolojia hushughulikia utamaduni ili kuweza kueleza tabia za watu zakiisimu; wanaisimujamii huoanisha lugha na utamaduni kwa kuzingatia sarufi.Uhusiano kati ya taaluma hizi mbili unatokana na ile haja ya kuyaelewa makundimbalimbali ya watu. Hivi ni kusema kwamba ni vigumu kwa wanaanthropolojiakuchunguza jamii za kale bila kuzingatia lugha za watu hao; na pia ni vigumukuchunguza lugha bila kuzingatia uamilifu wa mazungumzo fulani katika jamii.
Kwa kuzingatia lugha, maana ya ujumbe fulani ni kile kitu ambachokimewasilishwa kila wakati mwanajamii anapoongea. Na tukizingatia tabia zakijamii, maana ni kile kitu ambacho kimewasilishwa wakati mwanajamii fulaniametenda (kitu fulani) kitendo cha kitamaduni. Kwa hivyo lugha na utamadunini tabia za binadamu. Mtazamo wa kipragmatiki hutupa zaidi ya ile maana yamaneno.Unaangalia pia vikwazo vya kijamii anavyokabiliana navyo mtumiajilugha, na athari nyinginezo za kijamii katika matumizi ya lugha. Lazima piatuzingatie muktadha wa maongezi ili tuielewe kauli fulani.
17
1.6.5 Isimu na Sosholojia (Elimujamii)Wanaisimujamii hutalii miundo ya kijamii na namna miundo hiyo inavyoathirilugha. Kuna nguvu fulani za kijamii ambazo husababisha wanajamii kutakakuongea au kutamka maneno kwa njia fulani.Mkondo unaochukuliwa nakibadala (variant) fulani cha kiisimu katika jamii si jambo linalojitokeza kiholelatu, bali ni kitu kinachotokana na tathmini za kijamii. Uchaguzi wa kipashio fulanicha kiisimu unatokana na jinsi jamii inavyochukulia kipashio hicho.Lughahutueleza mengi kuhusu mtu katika jamii.
Kumbuka
Kwa sababu isimu-jamii ni taaluma inayohusika na jamii moja kwa moja,Ina uwezo wa kuhusiana na taaluma nyingi sana.
1.7 Mitazamo ya LughaWanazuoni mbalimbali wakiwemo Greenberg (1957), Hymes (1974), Dik (1978)nk wanaiangalia lugha kwa mitazamo miwili: mtazamo wa kiisimu na ule wakiisimujamii.
Katika mtazamo wa kwanza (wa kiisimu), lugha inaelezwa kuwa ni mfumo wasauti nasibu zinazotumiwa na watu wa jamii fulani wenye utamaduni unaofananaili kuwasiliana. Mtazamo huu unachukulia lugha kuwa kitu halisi ambachokinaweza kuainishwa katika vipande sauti vidogo vidogo ambavyo kwa pamojahuunda mfumo wa lugha wa mawasiliano.
Chomsky (1957) aliunga mkono mtazamo huu. Katika kuifafanua lugha,alitofautisha hali ya umilisi na utendaji. Umilisi ni kile ambacho mzungumzajianafahamu kuhusu lugha yake. Uwezo huu humwezesha kuelewa na kutoasentensi nyingi jinsi anavyotaka kuwasiliana. Huku ni kufahamu kanuni
18
zinazoitawala lugha husika na uwezo huu umo akilini mwake. Utendaji ni jinsimzungumzaji anavyoitumia lugha.
Kutokana na maelezo haya ni kama Chomsky anatueleza kwamba tusiichunguzelugha katika matumizi yake, au hata jinsi tunavyojifunza lugha, bila kwanzakufahamu lugha ni nini. Anaona kuwa kazi ya mwanaisimu ni kuandika aukutunga sarufi na kukuza uelewa wetu wa lugha.
Kuna wataalamu ambao wamepinga msimamo huu. Kwa mfano, Labov anaionasarufi kama mali ya kikundi/jamii au jumuia lugha na wala si mali ya kisaikolojiaya mtu binafsi. Hudson (1980:19) anaona kuwa mtazamo wa lugha usiohusishajamii una upungufu. Nadharia fika ya lugha lazima itaje matumizi ya lughahiyo. Anasema kuwa unweza kuitenga lugha na jinsi ya kwa nini inatumiwa.Kwa hivyo lugha ni sehemu ya jamii.
Umilisi wa kimawasiliano hauhusu tu kufahamu mfumo wa lugha, bali pia ni niniunachosema na kwa nani, na namna utakavyokisema katika muktadha fulani.Unashughulikia ujuzi wa kijamii na kitamaduni ambao hudhaniwa kuwawazungumzaji wanao unaowawezesha kufasiri mifumo ya kiisimu. Fonolojia,sintaksia na msamiati ni sehemu tu ya vipashio vinavyotumiwa katikamawasiliano. Pamoja na hivyo lazima kuwepo semantiki, muktadha na kwajumla mtazamo wa kijamii wa lugha.
Hivyo basi ufafanuzi wa Chomsky wa lugha una upungufu kwani unaichukulialugha kama kitu kinachojitosheleza. Unaiondoa lugha kutoka kwenye jamii.Hapa ndipo isimujamii inapoingilia ili ilete kipengele cha jamii katika lugha.
Mtazamo wa pili wa lugha ni wa kiisimujamii. Mtazamo huu unaangalia lughakama sehemu ya utamaduni wa jamii ulio na ruwaza ambazo hurithishwa nawatu wenyewe kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Mtazamo huu unaichukulia
19
lugha kama mali ya jamii. Wanaisimujamii wanakubaliana na fasiri hii ya pili yalugha.
Zoezi
Isimu jamii ni nini? Taja mikabala mitatu ya isimujamii na uonyeshe kwa kutoa mifano jinsi
inavyoingiliana na kutofautiana. Eleza uhusiano uliopo kati ya lugha na jamii. Isimujamii ni taaluma inayoingiliana na taaluma nyingi katika jamii.
Fafanua kauli hii.
Muhtasari
Katika somo hili, tumeeleza maana ya isimu jamii na mambo hayayamezingatiwa; Tumeonyesha mikabala mitatu ya isimujamii. Tumeonyesha uhusiano uliopo kati ya lugha na jamii. Tumeonyesha jinsi isimujamii inavyoingiliana na taaluma nyingine. Tumeeleza mitazamo miwili ya lugha kwa kuzingatia maoni ya wataalamu
mbalimbali.
20
Marejeleo TeuleChomsky, N.(1957),Syntactic structures.The Hague. MoutonDik, S.C.(1978) Functional Grammar . North-Holland Linguistics Series. North-Holland Publishing Company. New York.Fishman, J.A. (1967) Sociolinguistics and the Language Problems of DevelopingCountries katika Fishman, J.A. et.al. (eds.) Language Problems of Developing
Nations. John Wiley and Sons. Inc. London.(1972) Domains and the Relationship between Micro and MacroSociolinguistics katika Gumperz, John & Dell Hymes (eds.) Directions in Sociolinguistic:The Ethnography of communication.Basil Blackwell.oxfordGreenberg, J.H. (1957) Essays in Linguistics , Chicago: Phoenix Books.Hudson, R. (1980) Sociolinguistics : Cambrdige, University Press, Cambridge.Hymes, D. (1974) Foundations in Sociolinguistics : University of PennyslavaniaPress, Philadelpia.Labov (1980) (Mhr.) Locating Language in Time and Space . Academic Press.New York.Mesthrie, R. et.al. (2000) Introducing Sociolinguistics . Edinburgh UniversityPress, Edinburgh.Msanjila, Y.P. (1995) Mawanda ya Isimu Jamii katika Mbogo, E. na McOnyango,O. (wahariri) Baragumu Juzuu la 2 Nam. 1 & 2 Uk. 65-71, Chuo Kikuu Maseno.Pride, J. G. & Holmers J. (eds.) (1972) Sociolinguistics Harmondsworth:Penguin.Wardhaugh, R. (1992) An Introduction to Sociolinguistics . Blackwell.Whorf, B.L. (1956), Language, Thought and Reality : Selected Writings, J.B.Carroll (ed). Cambridge, MA:MIT press
21
SOMO LA PILI
NADHARIA ZA KIJAMII
2.0 UtanguliziSehemu hii inashughulika na kueleza nadharia za kijamii ambazo hutumika katikakuelewa uhusiano mbalimbali katika jamii. Nadharia hizi zinasaidia kuelewa waziswala la lugha na jamii.
2.1 MadhumuniMnamo mwisho wa somo hili utaweza kutimiza yafuatayo:1. Kueleza nadharia za kijamii.2. Kuonyesha jinsi nadharia hizo zinavyoingiliana na swala
la lugha.
2.2 Nadharia za KiisimuIli kuzingatia sehemu ya kijamii iliyo katika taaluma ya isimujamii, ni muhimukuelewa mitazamo mbalimbali inayotumiwa kuchunguza jamii za wanadamu.Katika sosholojia kunazo nadharia tatu kuu zinazoielezea jamii. Kuelewa lughakatika jamii kunahitaji pia kuzielewa nadharia hizi za kijamii. Katika
mada hiitutazijadili nadharia mbili za mwnzo kati ya hizi tatu. Nadharia hizo tatu ni:(a) Uamilifu (functionalism)(b) Umaksi (marxism)(c) Muingiliano (interaction)
2.2.1 UamilifuHii ni nadharia iliyoibuka kati ya miaka ya arobaini na sitini (1940 s and 1960 s).Inaeleza kuwa jamii inaweza kuchukuliwa kama mfumo ulio na sehemu zenyeuamilifu. Ili kuelewa sehemu yo yote ya jamii (kama familia au shule), lazimasehemu hiyo ichunguzwe kwa kuangalia uhusiano wake na jamii nzima. Kamavile mwanabiolojia anavyochunguza mchango wa moyo katika kuendeleza
22
maisha ya binadamu ndivyo sehemu ya jamii inavyochunguzwa kulingana namchango wake katika kuendeleza mfumo wa kijamii.
Mfumo wa kijamii unayo mahitaji fulani ambayo yanahitaji kutekelezwa ili jamiiidumu. Mahitaji haya ni pamoja na chakula, mavazi na malazi. Uamilifu wasehemu yo yote ya jamii ni ule mchango wake katika kuendeleza na kuimarishajamii hiyo kwa jumla. Hii ina maana kwamba kuna kiwango fulani chamuingiliano kati ya sehemu zote ambazo huunda jamii.
Wanauamilifu wanadai kuwa utaratibu na uimarikaji ambavyo huwa ni vitumuhimu vya kuendeleza jamii hutokana na kuwepo kwa amali (za pamoja) sawa,yaani makubaliano kuhusu mambo fulani katika jamii. Kutokana na mtazamohuu wanajamii hushughulikia mifumo midogo ya kijamii na amali sawazinazowaunganisha wanajamii.
Dhana zinazosisitizwa katika nadharia hii ya elimujamii na ambazo ni muhimukwa mwanaisimu jamii ni pamoja na: utamaduni, ujamiishaji (socialisation),kaida, amali, hadhi na majukumu/dhama.
(i) UTAMADUNIUtmduni hurejelea jinsi jamii inavyoishi; yaani mkusanyiko wa mawazo na tabia
wanazojifunza na kupokeza kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Katika hali hiiutamaduni ni mpangilio wa jinsi watu wanavyoishi. Utamaduni unafafanuamambo yanayokubalika na mfumo wa tabia katika jamii fulani.
(ii) UJAMIISHAJIDhana hii inarejelea njia ambazo kwazo watu hujifunza utamaduni wa jamii zao.Ujamiishaji wa kimsingi au awali hutokea utotoni, aghalabu katika familia.Mahirimu au marika (peer group) ni kukundi muhimu cha kuendeleza ujamiishaji.Marika humsaidia kumkuza mtu kijamii na kiisimu.
23
(iii) KAIDA NA AMALI(a) KAIDAKaida ni mwongozo maalumu wa jinsi ya kutenda mambo na kaida hueleza tabiazinazokubalika na zile zinazofaa katika miktadha maalumu. Mifano ya kaida hiziinaonekana katika mavazi ya shuleni, ya vijana,ya nyumbani, au ya dhifambalimbali. Katika hali ya ujamiishaji, kaida hufunzwa kwa kutuza (kumpa mtotoperemende, maneno ya kusifia) au kuadhibu. Baadhi ya kaida hufanywa kuwasheria za kutumikia umma wote. Kwa mfano, kukataza kuoga hadharani auwanawake kuhitajika kufunika nyuso zao hadharani.
AMALIAmali hutoa miongozo ya kijumla ya mambo ambayo yanachukuliwa kuwamazuri na yenye thamani.Kwa mfano, katika jamii nyingi za kisasa, watuhuthamini maisha ya binadamu sana. Baadhi ya amali zinazopendekezwa niumoja,uaminifu, upendo, n.k..
Wanauamilifu wanaamini kuwa ikiwa kaida hazitakubaliwa na kushirikishwamiongoni mwa wanajamii, jamii haziwezi kushirikiana na kufanya kazi pamoja.Hivyo basi jamii inahitaji kaida na amali za pamoja. Jambo hili limekuwa msingiwa tafiti nyingi za isimujamii.
(iv)HADHI NA MAJUKUMUHadhi hurejelea cheo cha mtu katika jamii (si lazima iwe kazi). Hadhi kama hizihuenda zimerithiwa, yaani mtu anapozaliwa anajipata ana hadhi fulani kwamfano malkia au mfalme. Anapoendelea kukua anajipata kuwa yeye ni mke aumume . Hadhi pia huenda ikapatikana kutokana na juhudi za kibinafsi za mtu,kwa mfano, kujiendeleza kitaaluma na kuwa mwalimu, daktari, mwanamichezo,n.k.
24
Kila hadhi katika jamii huwa na idadi fulani ya kaida ambazo zinaeleza namnamtu aliye katika hadhi hiyo anatakiwa kuendesha maisha yake. Kikundi hiki chakaida huitwa dhima au majukumu. Majukumu ya kijamii ndiyo huongozatabia. Kufikia mwisho mwa siku, mtu huwa ametekeleza majukumu mbalimbali:mwalimu (kazini), mama au mke (nyumbani), mteja (benki), manju (kilabu chastarehe), n.k. Kila jukumu huhitaji tabia fulani zizingatiwe, zikiwa ni pamoja natabia za kiisimu. Kila jukumu la kijamii humfanya mtu achague elementi fulani zakiisimu. Huku akitekeleza majukumu yake atatumia lugha kwa njia tofautitofauti.
Zoezi
Je, kwa maoni yako, unafikiri nadharia ya uamilif inajitokeza vipi katika jamiizetu na lugha tunazozitumia?
2.2.2 UMAKSIUmaksi unahusiana na nadharia kadhaa. Tunapoongea kuhusu uhakiki wa ki-maksi, huwa tunairejelea mikabala mbalimbali ambayo misingi yake ni mawazoyanayohusishwa na Karl Marx na Friedrich Engels.
Nadharia hii imepitia mabadiliko makubwa tangu kuweko kwa wataalamu hawa.Umaksi unahusu nyanja mbalimbali kama uchumi, historia, jamii na mapinduzi.Umaksi una sifa ya kijumla inayojitokeza katika mwelekeo wake wa kuligusia kilaeneo, na kuwa na la kusema kuhusu takriban kila kitu ikiwemo lugha.
Mawazo ya Karl Marx kuhusu historia na miundo ya kijamii yana nafasi kubwakatika nadharia hii. Umaksi ni falsafa yakinifu hasa kwa kuwa pana msisitizomkubwa kwenye msingi wa hali za kiyakinifu za maisha kama mazingira ya kuishikuliko mawazo katika maisha ya binadamu. Umaksi hauegemezi mfumo wake wa
25
kifalsafa kwenye dhana dhahania kama urembo, ukweli au ndoto baliunayaegemeza kwenye uhalisi unaoonekana.
Hebu basi tuchunguze mawazo ya kimsingi ya nadharia hii:(1) Historia ya maisha ya binadamu inaweza kuelezeka katika misingi yakinifu
ya kiuchumi. Misingi hii itachunguza njia za uzalishaji mali pamoja namiundo ya kiuchumi inayoathiri sio uzalishaji mali hiyo tu bali nausambazaji wake. Swala hili la uzalishaji mali na usambazaji wa mali hiyolinaunda kile ambacho hujulikana kama msingi au muundo msingi (base =infrastructure). Kwenye msingi huo ndiko kunakoegemezwa muundo wajuu au kikorombwezo (superstructure). Muundo wa juu ndio unaohusishamaadili, itikadi, dini, utamaduni ,n.k.
Sifa za muundo juu zinaathiriwa kwa kiasi kikubwa na muundo msingi.Hata hivyo mabadiliko yanayotokea katika muundo wa juu kama mageuzikatika muundo wa kiutawala huweza kuathiri muundo msingi.
(2) Daima historia ya binadamu itadhihirisha au kuakisi harakatizinazoendelea katika matabaka ya kiuchumi-jamii. Karl Maksi aliwahikusema kuwa historia ya maisha ya binadamu ni ya harakati za kitabaka.Je, harakati hizi zinasababishwa na nini? Tunajua kuwa kitu cha msingikatika maisha ya binadamu ni kula na kunywa, kupata malazi na mavazina mambo mengine.
Tendo la kwanza la kihistoria kwa hiyo, ni kutafuta njia ya kuyakidhimahitaji haya ya kimsingi. Ili kufanikiwa katika lengo hilo, binadamuhulazimika kujiunga pamoja au kuunda umoja ili kuimarisha ubora nawepesi wa kuizalisha mali ya kukidhi mahitaji hayo. Muungano huo huwana ugawaji wa majukumu au kazi ambayo ndiyo msingi wa kuundwa kwamatabaka katika jamii. Hatua ya juu ya mwendeleo huu ni ukuzaji wamfumo wa ubepari. Katika mfumo huu, mali inamilikiwa na idadi ndogo
26
ya watu. Watu hao wanaipata mali yao kutokana na unyonyaji wa ummana hasa wafanya kazi.
Kumbuka
Zingatia maoni haya katika muktadha wa lugha. Kwa mfano lugha-wenyeji na lugha za kigeni zilizopo hapa nchini.
Kadiri mfumo wa ubepari unavyoendelea ndivyo ubora wa uzalishaji majiunavyoongezeka na tofauti kati ya matabaka kuimarika kwa kuwa kuna watuwanaofaidika kwa njia zisizo za haki. Kufaidika huko kwa njia zisizo za haki,pamoja na mbegu za kujiangamiza zilizomo kwenye mfumo wa ubeparivinachangia kuuangusho mfumo wenyewe. Marx anaamini kuwa hayayanatokana na mfanyiko wa kiasilia wa kihistoria. Mfanyiko huo ni wa kipembuzi(dialectics). Kwa mujibu wa mawazo haya, historia huendelea kutokana namfululizosafu wa mkinzano wa mawazo. Matokeo ya mkinzano huo ni kuzukakwa hatua nyingine mpya ya kihistoria. Huu ndio msingi wa kile kinachoitwaupembuzi wa kiyakinifu (dialectical materialism).
(3) Matamanio na matakwa yaliyopo katika jamii na hasa tabaka lenye nguvuyanaakisiwa katika itikadi iliyopo katika jamii, jinsi na miundo ya mawazoambayo aghalabu huwa imeshika kwa nguvu na huwapo kila mahala kiasi chakuwa huenda wanajamii wasiitambue kwa haraka.(4) Njia ya kusaidia na labda hata kuharakisha kuangamizwa kwa mfumo wakibepari ni kudadisi, kukosoa, kushutumu, kulaumu na kufichua batili iliyopokatika itikadi ya kibwanyenye inayooimarisha ubepari.
Dhana za kimsingi zimeibuka katika nadharia hii: ukengeushi; ubidhaaishaji naitikadi.
27
(i) Ukengeushi (alienation): Ugawaji wa kazi unaishia kusababisha utenganofulani kati ya wanaohusika au binadamu. Hii ni hatua ya kimsingi yaukengeushi . Mfumo wa kibepari unapoendelea kuboreka unasababisha haliambapo uhusiano uliopo kati ya mfanya-kazi na tokeo la nguvu zake ni wa kitukigeni (alien object). Watu wanaishia kukengeushwa na jamii yao kutokana namfumo wa kiainisho (specialization) unaosisitizwa na kukuzwa na ubepari.
(ii) Ubidhaaishaji: Maksi anaitumia dhana ya bidhaa kukieleza au kukirejeleakitu kinachozalishwa sio kwa nia ya kutumiwa bali kubadilishwa katika mfumo wakibepari wa soko. Bidhaa hizo hazitathaminiwi kutokana na kazi yake bali nikutokana na bei zinazoweza kuvuta. Yaani msingi wa kuzitathmini sio thamanikimatumizi bali ni thamani kimabadilishano. Katika msingi huu, bidhaa zinaishiakuhusisha nguvu au kanuni fulani fiche ambazo huwavuta watu na kuwafanyawawe na mvuto mkubwa wa kukimiliki kitu fulani ambacho kinawasisimua. Huundio msingi wa kuabudu bidhaa (fetishism of commodities).
Hii ni sifa kuu katika mfumo wa kibepari na ni msingi wa uchumi wa kibidhaaambapo watu husukumwa na kani za kununua na kumiliki vitu ambavyo labdahawavihitaji au wanavikinai haraka na kutamani vingine. Sifa hii ya ubidhaaishajiinaishia kuwahusu binadamu ambao hawathaminiwi kama binadamu ila kutokanana uwezo wao wa kuzalisha mali.
(iii) Itikadi: Ni dhana telezi, lakini kimsingi ni uwasilishi wa pamoja wa mawazo,fikira na tajriba hasa ikiwa vitalinganuliwa na uhalisia wa kiyakinifuvinakoegemezwa. Dhanahii inaweza kufafanuliwa katika muktadha wa lughapale ambapo watu wanaamini kuwa kuzungumza lugha ya mama ni dalili yaushamba au kinyume chake kwamba kuzungumza lugha ya Kiingereza ni dalili
ya kuwa mtu wa tabaka la juu.
28
Zoezi
Kwa kuzingatia hali ya lugha nchini Kenya, ni kwa njia gani nadharia yaUmaksi inaeleza hali hii (zingatia mvutano kati ya lugha ya Kiingerezana lugha nyinginezo za Kiafrika).
Swali
Huku ukitumia nadharia moja ya Elimujamii, onyesha namna lughainavyoingiliana na jamii
2.4 HITIMISHOKatika somo hili tumejadili nadharia mbili za kijamii ambazo zitatusaidiakuelewa jamii. Nadharia hizi zitachangia katika kuelewa swala la lugha katikajamii.
Marejeleo Teule
Eagleton, T. (1983) Literary Theory: An Introduction . Oxford: Blackwell.Mesthrie, R. et al (2001) Introducing Sociolinguistics , Edinberg,EdinbergUniverstity Press.Wamitila, K.W. (2002) Uhakiki wa fasihi: Misingi na Vipengele vyake . Nairobi.
Phoenix Publishers Ltd.
29
SOMO LA TATULUGHA NA JAMIIDHANA ZA KIMSINGI KATIKA ISIMU-JAMII
3.0 UtanguliziKatika somo hili, tutashughulikia dhana za kimsingi katika isimujamii. Dhana hizini pamoja na lugha, lahaja, mtindo-pekee, sajili au mtindo na jumuiya lugha.Tutazingatia dhana hizi kwa kuonyesha maana yazo pamoja na kuonyesha jinsizinavyohusiana na uwanda mzima wa isimujamii.
3.1 Madhumuni
Baada ya kulipitia somo hili, tunatarajia kwamba utaweza:1. Kueleza maana ya lugha na matumizi yake.2. Kueleza maana ya lahaja na jinsi lahaja zinavyoibuka.3. Kueleza maana ya mtindo-pekee.4. Kueleza maana ya mtindo na sajili pamoja na kueleza sajili mbalimbali.5. Kueleza ni nini maana ya jumuiya lugha.
3.2 LughaLugha ni chombo kilichoundwa na wanadamu kwa ajili ya matumizi yao; kwahivyo kama wanadamu wasingekuwapo, hapana shaka kusingekuwapo na lughapia. Kutokana na huu uhusiano kati ya lugha na binadamu, ni dhahiri kuwa tabiana mabadiliko ya wanadamu yataiathiri lugha vilevile (Mdee, 1986). Wanaisimu,katika kuichunguza lugha, wanaichukua kama kitu na kuanza kuifafanua,wakiangalia miundo ya vipengele mbalimbali vinavyoijenga na kuikamilisha najinsi inavyoathiriwa na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni nakisaikolojia ya wazungumzaji.
30
Swali
Je, lugha ni nini?
Kujibu swali hili ni rahisi kwa sababu wanaisimu mbalimbali wamejaribu kutoamawazo yao juu ya swali hili. Hebu tuangalie wanachokisema wanaisimu.
Kwa mujibu wa Otto Josepersen, Encyclopedia Britannica, lugha ni njia yoyote yamawasiliano kati ya viumbe vyenye uhai. Kwa maana hii lugha ina maana kubwasana. Tunaona kwamba fasili hii inaeleza kimantiki kuwa kila kiumbe chenyeuhai kina lugha. Kwa hivyo, tunapata lugha kwa wanadamu, wanyama, waduduna mimea.
Kwa maana yake maalum lugha ni njia yoyote wanayoitumia wanadamu katikakuwasiliana. Maana hii ni sawa kidogo na hiyo ya mwanzo lakini mkazoumetiliwa kwa wanadamu tu. Maana hii inalingana na Trudgil (1974) katikaSociolinguistics anayesema kuwa lugha ni mfumo wa sauti nasibu zinazotumiwakwa mawasiliano miongoni mwa watu wa jamii fulani yenye utamaduni wake.
Kwa maana ya kiisimu, lugha ni utaratibu wa sauti za kusemwa, za nasibu, zajamii yenye utamaduni fulani ambazo huzitumia kwa kuwasiliana. Hapa,basi,tunaona kwamba maana hii inabagua kabisa maana zake tulizotaja mwanzoni.Kwa kutumia maana hii,hebu tuchambue kila kipengele:
Lugha:(a) ni sauti ya kusemwa. Mtu hutoa sauti fulani ambayo ina maana.
Tunatumia midomo, taya, ulimi, meno, koo, nyuzi, ufizi na kadhalika.(b) ni sauti za nasibu.Sauti hizi zimetokea tu kwa bahati katika ile lugha
isemwayo. Hakuna kitu kilichofanyika kupatana juu ya maneno. Kwa
31
mfano, maneno haya haya ya lugha mbalimbali huwakilisha neno kitiendeve (kimaragoli), chair (Kiingereza) na kadhalika.
(c) ni sauti zenye utaratibu kamili. Sauti za lugha yoyote huwa zimepangwakwa kufuata utaratibu fulani unaokubaliwa na jumuia hiyo ya watu.Utaratibu huo huitwa sarufi. Kwa mfano, hatusemi Maria tunda ana balijumuia imepatana kusema Maria ana tunda .
(d) ni sauti ya watu wa utamaduni fulani. Utamaduni ni mila na desturi zamaisha ya watu zilizojengwa tangu awali. Lugha inatawaliwa na manenoya utamaduni wa watu hao. Kwa mfano, wazungu wana maneno mengiya sayansi wakati Waafrika hawana maneno ya kuelezea, k.m. motokaa,santuri na kadhalika ni vitu ambavyo havikuwapo katika utamaduni wao.
(e) ni sauti za kueleza wazo. Yaani ni sauti zinazowawezesha watu kupashanaau kujulishana habari.
3.2.1 Matumizi ya LughaKwa jumla matumizi ya lugha yoyote hutegemea:(a) Mahali, kwa mfano nazi kwa watu wa pwani.(b) Wakati, kwa mfano, maneno ya kisiasa ya miaka hii kama vile, uwazi, haki
za binadamu na kahdalika.(c) Umri, kwa mfano, maneno ya sheng ambayo hutumiwa zaidi na vijana.(d) Hali ya kike au ya kiume, Kwa mfano, Aka kwa mwanamke, Ebo kwa
wanaume, Bee kwa wanawake na Naam kwa wanaume.(e) Kisomo, kwa mfano, ziara badala ya safari, stashahada badala ya cheti
na kadhalika.(f) Pia matumizi na mabadiliko ya lugha yanaweza kutegemea jadi, ada, kazi
au daraja ya mtu.
32
Swali
Jadili kauli kwamba Lugha na jamii hukamilishana na kuathirian a
3.2.2. MITAZAMO ELEZI NA ELEKEZI YA LUGHA(i) Mtazamo elezi wa lugha ni ule ambao unafafanua vipengele vya lughajinsi vilivyo. Ni mtazamo unaochunguza na kuweka wazi jinsi makundi tofauti yawatu yanavyoitumia lugha katika miktadha mbalimbali.Uchunguzi kama huuhaupendelei lugha ya kikundi kimoja kuwa ni bora kuliko ile ya vikundi vingine.Kwa mfano, mtu anaweza kuelezea lugha inayotumiwa darasani, ya wafanyakaziwa viwanda, ya wachuuzi mjini Nairobi, n.k, bila ubaguzi wo wote.
(ii) Mtazamo elekezi wa lugha huhusika na kanuni au adabu katika lugha.Huu ni mtazamo ambao unajaribu kuweka sheria za matumizi sahihi ya lugha iliwatumiaji wa lugha walazimike kuzifuata sheria hizo.
Mtazamo elekezi hujitokeza vizuri zaidi katika sarufi mapokeo, ambapo dhima yamwalimu wa lugha inaonekana ni kuhakikisha kuwa lugha safi au nzuriinahifadhiwa na kutumiwa. Hapa kanuni zinatolewa kuhusu vipashio mbalimbalivya matumizi ya lugha kwa mfano:
Sarufi: Sentensi huanza kwa herufi kubwa.Msamiati: Msamiati unaofaa umetumika.Maana: Kwamba mtu amemaanisha kile alichonuia.Matamshi: Mtu ametamka sauti ipasavyo.
Wanaoshikilia mtazamo huu wamejitetea kwa hoja zifuatazo:1. Kuna matumizi ya lugha yaliyo bora na yenye mantiki kuliko mengine.2. Wanarejelea mifumo iliyothibitika kuwa mizuri (classical form). Wakati
mwingine wanasarufi hutilia mkazo uamuzi wao kwa kurejelea lugha
33
zilizodhaniwa kuwa bora hapo zamani. Lugha kama Kilatini, Sanskrit,Tamil na Kiarabu zilichukuliwa kuwa vielelezo vya kuigwa. Mara nyingiKiingereza kililazimishwa kufuata mfumo wa Kilatini ili kionekane pia kuwasahihi.
3. Hupendelea mifumo ya zamani ya lugha hiyo.Wanaoshikilia mtazomo elekezi katika lugha huwa hawataki kuiona lughayao ikipitia mabadiliko yo yote. Hawataki visawe viongezeke, au maana,au mabadiliko ya kimuundo, yajitokeza katika lugha.
4. Wanakataza matumizi ya maneno ya kigeni.Huwa hawataki kukopa maneno ya kigeni na kuyatumia katika lugha zao.Kwa mfano, huko Ufaransa kuna taasisi inayoitwa The French Academy(Chuo cha Ufaransa) ambayo ina kazi ya kukitakasa Kifaransa kwakuondoa maneno yote ya lugha nyingine, hasa Kiingereza,yanayojipenyeza kwenye lugha hiyo.
Wanaopinga mtazamo elekezi wa lugha wanasisitiza kwamba lugha zote ni sawa,hakuna lugha au lahaja iliyo bora kuliko nyingine. Wanaisimu wanasema kuwamisingi ya lugha elekezi imejikita katika matumizi ya lugha au kiisimu ya watuwa tabaka la juu katika jamii, na si katika dhana ya usawa. Wamesemayafuatayo katika kuupinga mtazamo huo:
1. Mtazamo wa kimantiki wa lugha kama vile ilivyo katika hisabati unamatatizo. Kama utafiti wa sarufi uliofanywa na Chomsky (1965)ulivyoonyesha, kutatokea utata mwingi kwani sheria za lugha ni chungunzima.
2. Wanasema kuwa kila lugha ina upekee wa aina fulani. Kwa hivyo, hakunahaja ya kulazimisha lugha fulani kufuata mfumo wa lugha kielelezo auiliyochukuliwa kuwa bora hapo zamani.
3. Kuhusu matumizi ya mifumo ya zamani ya lugha, wanaisimu wanasemakuwa daima lugha, hubadilika kwa njia mbalimbali. Sheria mpya
34
zinapoibuka zinaingiliana na zile za zamani. Hili haliathiri ubora wa lughahiyo.
4. Wanaisimu elezi wanasema kuwa lugha zote hukopa maneno. Ukopaji wamaneno ni sehemu muhimu ya ukuaji wa lugha. Mara nyingi mabadilikoyanayotokea katika lugha huakisi mabadiliko yanayotokea katika jamiikama vile vitu vipya, mitindo mipya, nk.
3.2.3 MJADALA ZAIDIKwa muda mrefu wanaisimu wamepuuza mtazamo elekezi katika kuifafanualugha. Hata hivyo, inafikiriwa kwamba ikiwa kusudi ni kuzungumzia matumiziyote ya lugha na mielekeo kuhusu lugha basi, wanaisimu jamii sharti watambuemtazamo elekezi.Matumizi mabaya na mazuri ya lugha yapo katika jamii.Kama vile usafi ulivyo muhimu kwa afya bora, ndivyo lugha sahihi inavyohitajikakatika matumizi ya kila siku ya lugha.
Pili, hata wale ambao wanaupinga mtazamo elekezi huwa wanatumia lughasahihi katika maandishi na matamshi yao. Wakati mwingine wahakiki hukosoawanaisimujamii kwa kuhimiza au kukubali lahaja zote huku wao wanatumialahaja au lugha sanifu. Hata darasani watawaadhibu wanafunzi wao kwakutotumia lugha sanifu. Kwa hivyo, hatuwezi kuepuka kuwepo kwa kanuni zalugha.
Inaonekana basi kwamba mtazamo wa kati unahitajika; ule unaozingatia pandezote mbili. Katika matumizi yasiyo rasmi tunaweza kuitumia lugha tunavyotakalakini katika miktadha rasmi, kama ufundishaji wa lugha darasani, tutumie lughasanifu.
Hata wanaisimujamii hualikwa kama wataaalamu kushiriki katika upangaji walugha. Katika hali kama hizo, wao huulizwa kufanya uchaguzi kuhusu vibadalafulani vya lugha vinavyofaa, maneno na misemo.Hivyo basi wanaisimujamii
35
hawawezi kupuuza wazo kwamba ubora wa lugha ni sehemu ya mazingira yalugha katika jamii nyingi.
ZoeziHuku ukitumia mtazamo elekezi, toa mifano kumi ya makosa yanayofanywana watu katika lugha kisha urekebishe makosa hayo.
3.3 LAHAJAImethibitika kuwa lugha haitulii, huenda ikibadilika kila wakati. Hata katikalugha ya kundi moja, tofauti nyingi hudhihirika. Crystal (1995:3) amezungumziavibadala vifuatavyo vya lugha.
Vibadala kijamii/kitabakaVibadala vya muda
Vibadala kibinafsi Vibadala kimaeneo
Jinsi lugha inavyotofautiana kimfumo ni jambo linalowashughulishawanaisimujamii. Lugha pia inaweza kubadilika kulingana na muktadha, wakatina mzungumzaji au mhusika. Katika somo la isimujamii msisitizo huwa ni kwakikundi cha jamii na wala sio kwa mtu binafsi. Taaluma ya lughainayoshughulikia lahaja kwa ujumla huitwa elimulahaja (Dialectology).
3.3.1 MAANA YA LAHAJA
36
Lahaja ni mojawapo ya migao ya lugha ambayo hutokana na mabadiliko yalugha. Chambers & Trudgill (1980:3) wanaeleza kuwa katika matumizi ya kilasiku, ambayo yana upotoshi fulani, lahaja ni lugha ya kiwango cha chini ambayohaijakua vizuri, isiyo fahari, na inayohusishwa na makabwela. Katika matumizikama haya, inachukuliwa kwamba lahaja huzungumzwa katika sehemu za duniazilizojitenga na ni aina ya uzungumzi ulio na mushkili na usiofuata kanuni zalugha sanifu. Lakini tunajua kwamba mawazo haya hayana msingi wo wote.Katika lugha tunaamini kwamba hakuna lugha au lahaja iliyo bora kulikonyingine duniani lugha au lahja zote ni sawa.
Tunaweza kusema kuwa lahaja ni aina ya uzungumzaji unaotumiwa na kikundicha watu aghalabu katika eneo maalum, na hutofautiana na uzungumzaji wavikundi vingine vya lugha hiyo moja katika matamshi, msamiati na kwa nadrasana sarufi.
Inaonekana kuwa lahaja ni kama matagaa ya lugha moja. Mkusanyiko wa lahajahuunda lugha. Aina hizi za uzungumzaji hazitatizi mawasiliano kati ya vikundimbalimbali vya jamii vinavyozungumza lugha moja. Inaonekana kuwa kila mtuhuzungumza lahaja.
Lahaja sanifu huwa na hadhi ya juu kuliko zile lahaja zingine kwani huwaimeendelezwa kimsamiati na kimuundo.
3.3.2 KUZUK KWA LAHAJAKuzuka kwa lahaja mbalimbali duniani ni dhihirisho kuwa daima lughainabadilika. Wakati mwingine haya mabadiliko hukithiri kiasi kwamba hakunauelewano. Inapotokea hivyo, basi zile lahaja hujitosheleza zenyewe na kuwalugha kamili. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Kilatini ambapo lahaja kadhaa
37
zilibadilika na kuwa lugha za Kifaransa, Kihispania, Kiitaliano, Kireno, naKiromenia (Wardhaugh 1987).Kuna mambo matatu muhimu katika uzukaji wa lahaja. Mambo hayo ni:(a) vizuizi(b) umbali(c) muda
(i) Vizuizi (Barriers)Lahaja huzuka kutokana na vizuizi vinavyoibuka kati ya makundi ya watuwanaozungumza lugha moja. Vizuizi hivi vinaweza kuwa vya kijiografia kamavile bahari, mito, milima, misitu mikubwa, n.k. Vizuizi vinaweza pia kuwa vyakisiasa kama vile mipaka, uongozi, n.k. Vinaweza pia kuwa vya kijamii kama vilerangi ya mtu, kabila, tabaka, dini, n.k; au vinaweza kuwa vya kiuchumi.
(ii) Umbali (Distance) na Muda (Time)Watu wanaozungumza lugha moja wakihamia maeneo tofauti na kutengwa nawenzao kwa umbali fulani, baada ya muda lugha yao itaanza kuwa tofautihasa ikiwa hakuna uhusiano mkubwa wa kimawasiliano kati ya makundi hayo.
Pia tunajua kwamba lugha hupokezwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine, nabaada ya muda mabadiliko ya kimatamshi na kisarufi yanayoletwa na kizazikipya hukita. Mabadiliko haya yakikosa kusambaa katika eneo lote basi tofautizinajitokeza na tofauti hizi ndizo zinazoitwa lahaja.
3.3.3 NADHARIA YA MAWIMBI (WAVE THEORY)Nadharia ya mawimbi inaweza kutumiwa kuonyesha jinsi lahaja huibuka.Mwasisi wa nadharia hii ni Johanness Schmidt (1872). Inasemekana kuwamabadiliko ya kiisimu husambaa nje kuanzia kwenye kitovu fulani vile ambavyomawimbi yanafanya unapotupa jiwe kwenye kidimbwi. Mawimbi haya
38
yanatofautiana kwa ukubwa na yatakuwa na vitovu tofauti. Jinsi mawimbiyanavyosafiri kwenda mbali yanazidi kufifia.
Mawimbi haya ya mabadiliko husafiri kupitia kwa maeneo ya kijiografia au yakijamii au yote mawili. Yanaweza kuzuiwa au kupunguziwa kasi na vizuizi kamatabaka, jinsia, umri, kijiografia, n.k. Mabadiliko haya huwasilishwa na watubinafsi, na wakati fulani badiliko litakuwa limefikia watu fulani na kutowafikiawengine.
3.3.4 ISTILAHI ZINAZOTUMIKA KATIKA LAHAJA(i) Kizingasifa (Isogloss)Katika utafiti wa lahaja tunaweza kuchora ramani kuonyesha mahali ambapomatamshi, msamiati au muundo fulani hutumiwa. Kuna njia mbili za kuonyeshamambo haya:(a) Kwa kutumia ishara(b) Kwa kuunganisha sehemu hizo kwa laini inayoitwa kizingasifa.
Kizingasifa ni mpaka unaochorwa kulizungushia eneo ambalo lina sifa maalum zamatamshi, sarufi au msamiati katika ramani ya kiisimu.Kizingasifa hutumika ili kutenganisha sehemu zilizo na sifa fulani na zile ambazohazina sifa hizo. Tazama mchoro huu.
Kizingasifa
39
Kiidakho KimaragoliMukhwasi
KhMukwasi
k
Ruwaza ya vizingasifa huelezwa kwa kuzingatia vizuizi vya kijiografia ambavyovinatenganisha jamii mbili au zaidi zilizopakana. Vizuizi hivi ni kama mto wenyekina kirefu, msururu wa milima, n.k. Vizuizi vinaweza kuwa ni vya kijamii aukisiasa. Watu wa eneo fulani wanaweza kuwa na mfumo tofauti wa kisiasa nakijamii na hivyo wakawa na utamaduni tofauti na maeneo waliyopakana nayo.
(ii) Eneo la Fahari (Centre of Prestige)Vizingasifa vingine huwa na ruwaza inayoonyesha kusambaa kwa kipashio chakiisimu kutoka kwa eneo la fahari au kitovu, ambalo aghalabu huwa mji. Hapa,vizingasifa hivi hufanana na viwimbi vinavyotokana na jiwe lililotupwa majini.Ndivyo tulivyopata nadharia ya mawimbi. Wanaoshikilia nadharia hii huaminikwamba mabadiliko ya kiisimu husambaa kama mawimbi.
(iii) Sehemu masalio (Relic Areas)Wakati mwingine ruwaza hujitokeza ikionyesha sehemu ndogo ndogo ambazozimeachana lakini zenye sehemu zinazofanana kiisimu. Sehemu hizi hazina eneola fahari kama miji. Hizi ni zile sehemu ambazo hazijafikiwa na miundo mipya.Mara nyingi sehemu hizi huwa katika maeneo yaliyojitenga kama milima,mabonde au mipaka ya lugha fulani.(iii) Sehemu za Mpito (Transitional Areas)Hii ni sehemu ambayo mawimbi ya eneo la fahari moja hukutana na mawimbi yaeneo la fahari jingine. Katika hali kama hii eneo hilo halina sifa maalumutambulishi bali linashiriki sifa za maeneo mawili ya fahari yaliyo jirani. Kwamfano, Luanda, iliyo kati ya mkoa wa Nyanza na Magharibi.
3.5 AINA ZA LAHAJAKuna aina mbili za lahaja:3.5.1. Lahaja za KijiografiaHizi ni lahaja zinazozungumzwa katika maeneo fulani, nazo hutokea watu walugha moja wakihamia maeneo tofauti halafu wakatengwa kimawasiliano kwa
40
umbali, milima, bahari, mipaka, n.k (Fromkin & Rodman 1974:254). Mifano yalahaja za kijiografia ni zile za Kiswahili: Kiunguja, Kimvita, Kiamu, Kimrima,Kimgao, Kitumbatu, n.k.
Watu wanaofanyiwa utafiti ili kuthibitisha kuwepo kwa lahaja hizi ni wazee waliona umri mkubwa ambao wameishi mahali hapo kwa muda mrefu, wana kisomokidogo au hawana, na ambao hawajapata athari ya lugha au lahaja nyingine.
ZoeziTaja lugha nyinginezo mbili unazozifahamu na uonyeshe lahaja zake.
3.5.2. Lahaja za Kijamii/KitabakaHizi ni lahaja zinazotumiwa na makundi ya watu kulingana na hadhi yao, tabaka,elimu, kazi wanayofanya, pato, umri, uana, na vipengele vingine vya kijamii.Watu wanaokuwa katika lahaja moja ya kijamii si lazima wawe wanaishi katikaeneo moja.
William Labov, mwanaisimu wa Kimarekani, aliona kuwa lugha inao mfumo wavibadala ambao unaweza kuelezwa kuzingatia tofauti za kimatabaka katika jamiifulani.
Utafiti uliofanywa na watafiti wengi wakiwemo Labov na John Fischerunaonyesha kuwa watu hutumia vipashio fulani vya kiisimu si kwa sababu nirahisi kuvitamka bali kwa sababu ya jinsi wanavyohisi kuhusu hadhi yao na walewanaowazungumzia. Kwa mfano kusema:
Maalim badala ya mwalimu
Nchini Kenya, kumekuwepo na lahaja za kijamii kama Kisetla na Kihindi.
41
Zoezi
Je, kuna lahaja zingine zipi za kimatabaka nchini Kenya?
3.6 LUGHA AU LAHAJA?Vipengele vifuatavyo hutuwezesha kuamua kama tofauti za kiisimu zinazotokeazinaashiria tofauti za lahaja au za lugha.Unajuaje kuwa jinsi mbili zakuzungumza ni lahaja za lugha moja au ni lugha mbili tofauti?
3.6.1. Kusikilizana (Mutual Intelligibility)Ingawa lahaja hutofautiana, watu wanapozungumza huelewana. Ikiwa
wazungumzaji wawili walio na tofauti fulani katika lugha zao wataelewanawanapozungumza, basi itachukuliwa kwamba wanatumia lahaja tofauti za lughamoja. Lakini ikiwa hawataelewana basi wanazungumza lugha tofauti. Hatahivyo, kuna viwango mbalimbali vya kuelewana kati ya lahaja mbalimbali.Wazungumzaji wa Kinyala na Kibukusu kwa mfano ,wataelewana kwa sababuhizi ni lahaja za lugha moja, lakini wazungumzaji wa Kiingereza na Kikambahawataelewana.Watu wengi husema kuwa kipengele muhimu cha kuamua kamani lugha au lahaja ni hiki.
3.6.2. Mwendeleo lahaja (dialect continuum)Dhana hii hurejelea mfuatano wa jinsi lugha zinavyopakana kijiografia, yaani AB C D E F G ... Katika mkururo huo, huwa kuna kusikilizana katikalahaja zilizopakana, lakini zile zilizotengana kwa mbali huwa hakuna masikilizano.Kwa mfano, kuna uwezekanao kuwa wazungumzaji wa A na G hawataelewana.Hapa ndipo tatizo linazuka. Je, bado tunaweza kusema kuwa A na G ni lahaja zalugha moja?
3.6.3. Lugha sanifu
42
Kuwepo kwa lugha sanifu au maandishi yanayotumiwa na kundi la watuhutusaidia kujua kama zinazohusika ni lahaja au lugha. Ikiwa makundi mawili auzaidi yanayotofautiana katika maongezi hukubaliana kuwa yana mfumo mmojaulio sanifu au yanatumia aina moja ya maandishi, basi inachukuliwa kuwayanazungumza lahaja tofauti na wala si lugha tofauti.
Kwa mfano, nchini Uchina wazungumzaji katika sehemu mbalimbali za nchihutumia Mandarin, Cantonese, Wu, Hakka au Fukien. Wazungumzaji wavibadala hivi hawaelewani lakini kwa sababu wanatumia mfumo mmoja wakuandika (wa Kichina) na kusoma basi inachukuliwa kuwa hizo ni lahajambalimbali za Kichina.
3.6.4. Vipashio visivyo vya KiisimuSifa fulani zisizo za kiisimu hutumiwa pia kuamua kama kinachohusika ni lahajaau lugha. Sifa hizi ni kama utamaduni mmoja, utii wa kisiasa au dhamiri zawazungumzaji (conscious of the speakers).
Kwa mfano, wazungumzaji wa Cantonese (China kusini ) na Mandarin ( ChinaKaskazini) hawaelewani wanapozungumza lakini inachukuliwa kuwa wanatumialahaja tofauti za Kichina kwa sababu wote wanaishi Uchina (siasa) na wanashirikiutamaduni mmoja wa Kichina. Pia wanatumia mfumo mmoja wa maandishi.
Aidha, wazungumzajiwa Swedish, Danish na Norwegian wanasikilizanawanapozungumza lakini kwa sababu wanaishi katika nchi tofauti na wanatamaduni tofauti inachukuliwa kwamba wanazungumza lugha tofauti.
Hata pale ambapo sifa za kisiasa hazijitokezi sana, utamaduni pekee hupelekeawazungumzaji kufikiriwa kuwa wanazungumza lugha tofauti, kwa mfano, Wazuluna Waxhosa huelewana wanapozungumza, lakini wanahisi kwamba wao nitofauti na hata wana lugha tofauti kwa sababu wana tamaduni tofauti. Mfano
43
mwingine ni wa Wasuba na Waluo ambao wanaona kuwa wanazungumza lughatofauti.
Swali
1. Je, lugha yako ina lahaja ngapi? Andika maneno yanayotofautishalahaja moja na nyingi.
2. Kwa kurejelea nchiya Kenya ,onyesha zile lahaja ambazo zinaonekanakuwaLugha tofauti ilhali wazungmaji wanaelewana.
3.7 MTINDO-PEKEEWazungumzaji wote wa lugha fulani huelewana wanapozungumza, lakini hakunawatu wawili wanaozungumzakwa namna moja. Tofauti zinazotokeahusababishwa na umri, uana, afya ya mtu, ukubwa, hulka, hali ya kimawazo,tajriba na ubinafsi wa mtu. Tofauti hizi hujitokeza katika msamiati, matamshi nakwa kiasi kidogo katika sarufi. Sifa ya namna ya uzungumzi unaohusishwa namtu binafsi huitwa mtindo pekee .
Mtindo pekee ni matamshi ya kipekee ya msemaji au mzungumzaji yanayotokanana athari za mazingira. Hii ina maana kwamba kuna mfumo fulani wa kiisimuunaohusishwa na kila mzungumzaji. Jambo hili linadhihirika wazi pale ambapotunamtambua mtu kupitia kwa matamshi au sauti yake bila kumwona. Kilamzunguzaji wa lugha ana mtindo wa kipekee wa lugha. Mtindo pekee wa mtuhuweza kubadilika katika vipindi mbalimbali vya maisha yake.Zoezi
Pambanua tofauti za kiisimu zinazojitokeza miongoni mwa marafiki zako.
44
3.8 MTINDODhana ya mtindo ni tatanishi kwa sababu kuna misimamo na mitazamo chungunzima inayotokana nayo. Kwa mfano, dhana ya lafudhi inayomaanisha ubinafsikatika matumizi ya lugha, inayomtambulisha mtu kama mtu,
yaelekeakupendekeza kuwa labda kuna mitindo mingi ya matumizi ya lugha kama kulivyona watumizi wengi wa lugha husika. Kwa hivyo yaonekana kwamba kila mtuulimwenguni ana mtindo wake.
3.8.1 Maana ya mtindo.Ili kutoa maana ya dhana ya mtindo hebu tuangalie yale wanayosema Crystal naDavy (1969) katika Investigating English Style .Wamefafanua mtindo kwakutumia mitazamo ifuatayo.(i) Mtindo kama tabia za mtu katika matumizi ya lugha.(ii) Mtindo kama tabia za kimakundi katika matumizi ya lugha.(iii) Mtindo kama tabia za kitathmini yaani kiupimaji.(iv) Mtindo kulingana na lugha ya fasihi.Hebu basi tutoe maelezo ya kila moja.
(i) Mtindo kama tabia ya mtu.Kwa mujibu wa mtazamo huu, uchambuzi humulika na kuangalia tabia za kiisimuzinazoambatana na lugha ya mtu katika uyakinifu wake. Neno tabia katikamuktadha huu linatumiwa kumaanisha kanuni za kiisimu zinazotambulisha lughaya mtu anayehusika.
Mtindo hutumiwa hapa kurejelea namna mtu anavyotumia lugha. Jambo ambalolina upekee fulani wa kiisimu. Huu upekee ndio unaotambulisha na kumsawiriyeye kama yeye.
Mtazamo huu ndio unaowaruhusu wachambuzi kuzungumza kuhusu mtindo wawaandishi au wasemaji mbalimbali (tazama Kitsao 1975). Kwa mfano, unaweza
45
kuzungumza kuhusu mtindo wa uandishi wa Shaaban Robert, Ebrahim Husseinau Said Ahmed Mohamed.
Buffun katika hotuba aliyoitoa mnamo Agosti 27, 1753, alisema kuwa mtindo nimtu mwenyewe , na huu umekuwa msingi wa mtazamo huu. Maoni hayayanajadili kuwa kila mwandishi au msemaji ana lugha yake ambayo hudhihirikakatika kazi zake zote na ambayo humtofautisha na waandishi au wasemajiwengine. Hivi ni kusema kwamba hulka ya mwandishi inatarajiwa kuonekana aukudhihirika kutokana na matumizi yake ya lugha.
Uchunguzi unaonyesha kuwa katika kujifunza lugha, kwa kawaida, watu hukuzana kupalilia tabia fulani za kipekee katika matumizi yao ya lugha. Matokeo nitabia za kibinafsi ambazo hubainika kwenye mawasiliano yake. Hivyo basi,mtindo unakuwa matokeo ya moja kwa moja ya jinsi mtu anavyojielezakulingana na tajriba yake katika kujifunza lugha.
Zoezi
Pambanua tabia za kiisimu ambazo zinaibuka katika usemi wa rafikiyako. Taja elementi tano za kiisimu kwa kila moja ambazo humtofautishana mtu mwingine.
Kwa vile imetambuliwa kwamba kuna mitindo mingi kama kulivyo na waandishina wasemaji, uchambuzi wa mtindo hauna budi kumshughulikia kila mtunzikivyake. Kwa mfano, tunaweza kusema kuwa mwandishi Shabaan Robertanajulikana kwa matumizi ya sentensi ndefu hata zinazofikia maneno thelathini.Aidha anatumia uhuishi na jazanda katika kazi zake.
46
(ii) Mtindo kama tabia za kimakundi.Katika upana wake dhana ya mtindo inaweza kurejelea tabia za kundi la watukatika matumizi yao ya lugha. Mtazamo huu ndio mhimili wa misingi ya sajilikatika matumizi ya lugha. Kwa hivyo, mtindo wa matumizi ya lughaunapokubalika kimakundi unakuwa utaratibu unaofaa kuzingatiwa katika sajiliinayohusika.
Kwa mfano, kuna kanuni za kuanzisha na kuhitimisha ngano katika jamii zaKiafrika:Msimulizi: PaukwaHadhira: PakawaMsimulizi: Kaondokea chanjagaa
Kajenga nyumba kakaaMwanangu mwana SitiKijino kama ChikichiCha Kujenga kikuta navilango vya kupitia.
Au:Msimulizi: Hadithi! Hadithi!Hadhira: Hadithi njooMsimulizi: Hapo zamani za kale paliondokea ...
Pia kuna mtindo wa kuandika mashairi ya kimapokeo. Mwandishi anazingatiaidadi ya mizani katika mshororo, vina, idadi ya mishororo katika ubeti nautoshelezi. Katika uandishi wa tenzi mwandishi huanza kwa ombi na kadhalika.
47
Zoezi
Eleza mtindo unaodhihirika katika bara rasmi na fomu za serikali.
(iii) Mtindo Kiutathmini.Madhumuni ya kuwasiliana huwekewa vikwazo au mipaka na mtazamo huuhupima na kutoa masharti kuhusu namna ya kuwasilisha wasilisho fulani.Mtazamo huu unaongozwa na maoni kwamba kila mtindo unao maneno yafaayona mahali pafaapo kwenye muundo wa sentensi. La muhimu hapa ni kwamba,ujumbe utolewe kwa njia ifaayo kabisa kisarufi na kimaana: Hebu tueleze kwakutoa mifano ya sentensi hizi:
1 (a) Kwa sababu ya kuchelea kuwa huenda ng ombe wake akapotea tena,mchungaji alimkamata na kumfunga miguu ya mbele na ya nyuma kwakamba.
1 (b) Kwa sababu ya kuchelea kuwa huenda ng ombe wake akapotea tena,mchungaji alimkamata na kumfunga kwa kamba miguu yake ya mbele naya nyuma.
Katika sentensi hizi mbili tunaona kuwa mpangilio wa maneno ni tofauti.
Zoezi
Eleza tofauti za kimaana zinazotokea katika mifano ya sentensi hapo juu
48
Wakati mwingine, tatizo huwa kubwa zaidi kiasi cha kuhitaji sio tu manenokupangwa upya bali pia kurekebishwa au kubadilishwa kwa viwakifishi.
Wataalamu wamefafanua mtazamo huu kwa kutilia mkazo kwamba mtindo mzurihutokana na kuchagua taashira zifaazo kwa wasilisho linalonuiwa kuwasilishwa.
Kwa ufupi, uchambuzi wa mtindo kulingana na mtazamo unaohusika hapa nikukadiria namna mwasilishi alivyofaulu katika wasilisho lake, kulingana na uteuzikimsamiati na kisarufi.
(iv) Mtindo kulingan na lugha ya Fasihi.Kwa mujibu wa mtazamo huu mtindo ni utunzi wa fasihi ya hali ya juu kabisa.Hata hivyo tunaona kuwa maelezo haya yanatatiza kimaana kwa sababuhayazingatii kikamilifu mahusiko ya dhana ya mtindo yenyewe. Vile vile, maonihaya yanalifinya swala hili la mtindo. Inaonekana kuwa maoni haya yanalengaumbuji au ubunifu wa kurejelea mbinu za kujieleza kama vile matumizi yatamathali za usemi. Lakini mtindo, tunajua ni zaidi ya mbinu hizi. Mtindo sio tujinsi waandishi wanavyoandika lakini pia ni njia mbalimbali zinazotumiwa na watukuongea au kuandika katika hali za kawaida za kila siku. Kwa hivyo, mtindo nijumla ya namna lugha inavyotumiwa na wanajamii.
Swali
Onyesha tofauti zilizopo kati ya:1. Mtindo kama tabia za mtu na mtindo kama tabia za kimakundi.
49
3.9 SAJILIKulingana na Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha (1990) sajili, ambayo piainajulikana kama rejista ni lugha inayotumika katika muktadha maalumu. Sajilihuelekea katika kupambanua lugha ifaayo katika miktadha fulani. Sajilihutofautiana kutegemea mambo kama vile, miundo ya lugha, msamiati, uundajiwa sentensi, kupanda na kushuka kwa sauti na unyambuaji.
Sajili ni sehemu ya umilisi wa mawasiliano ambao kila mzungumzaji huwa nao.Umilisi huu humwezesha kubadili matumizi ya lugha, kuteua vipengele fulani vyamatamshi, msamiati na kadhalika katika miktadha mbalimbali.
Akishughulikia swala la sajili, Halliday (1964) alisema kuwa sajili hutofautianakutokana na :(a) Mada inayozungumzwa.(b) Uhusiano kati ya watu wanaowasiliana. Kwa mfano, nani anashiriki
katika mazungumzo? Ni mtu na mkubwa wake, au ni mtoto na mzazi auni rafiki tu?
(c) Njia ya mawasiliano ambayo inatumiwa ikiwa ni andishi au zungumzi auishara?
3.9.1 CHANZO CHA SAJILI.Inawezekana kwamba matumizi ya sajili mbalimbali yameibuka kutokana namikatale ya kijamii. Watu wana miiko mbalimbali inayohusu matumizi ya lugha,kwa mfano, ukitumia lugha inayoambatana na mazingira kama vile inayoonyeshafuraha mazikoni basi huenda ukaathiriwa. Kwa hivyo, lugha imegawika katikasajili mbalimbali kutokana na imani za watu na pia kukidhi mahitaji ya muktadha.Mfano mwingine ni kwamba baadhi ya jamii huamini kwamba lazima nganozihadithiwe mahali maalumu, wakati maalum na sharti ziambatane na matumizimaalumu ya lugha.
50
Pili, tunaweza kutuhumu kuwa sajili inatokana na kugawika kwa jamii katikamakundi ya kazi mbalimbali ili kujikimu. Kila kundi likiwa na msamiatiunaoelezea hali, mazingira na zana zake za kazi.
Msamiati huu, na upekee wa uzungumzaji ulizua sajili mbalimbali. Tunawezakuhusisha jambo hili na ukuaji wa binadamu kimaendeleo. Jinsi binadamualivyoendelea ndivyo kazi mbalimbali zilivyojitokeza na hivyo kukawa na lughamaalum ya kuelezea hali hizo. Kwa mfano, maendeleo upande wa sayansi nateknolojia yamezua sajili ya kisayansi na kiteknolojia.
3.9.2 MIFANO YA SAJILI NA SIFA ZAKE ZA KIISIMU1. Matangazo ya biashara:
Sifa zake1. Lugha ya mvuto.2. Lugha ya kimajazi.3. Lugha shawishi au msukumo (kutaka mtu awe mteja wao).4. Misemo maalumu inayonasa.5. Wingi wa porojo.6. Kuchanganya lugha.7. Uradidi wa sauti au maneno.
2. Matangazo ya mpira1. Lugha changamfu 7. Matumizi ya kidato cha juu2. Lugha ya kutia chumvi. 8. Maswali ya balagha.3. Lugha batebate. 9. Mbinu rejeshi.4. Lugha hugeuka kuwa kelele. 10. Msisitizo.5. Kuchanganya lugha. 11. Kutokamilika kwa sentensi.6. Uundaji wa msamiati.
51
(Kwa ufafanuzi zaidi wa aina a sajili,rejelea mtaala wa AKS 101)Zoezi
Taja sifa za sajili zifuatazo:i. Sajili ya kidini.ii. Sajili ya sheria-(andishi).
3.9.4MASHARTI YA MATUMIZICrystal na Davy (1969) pamoja na Kitsao (1988) wameshughulikia masharti yamatumizi ya lugha. Haya ni mambo yanayomwongoza mzungumzaji aumwandishi ili kuteua sajili inayofaa katika mawasiliano yake. Crystal na Davy(ibid) wameyaita mawanda ya matumizi kimuktadha na wamejadili vipengelevinane.1. Ubinafsi2. Lahaja.3. Wakati.4. Kazi.5. Hadhi.6. Namna ya kuwasilisha.7. Upekee.8. Aina ya mazungumzo
Kitsao (1988) kwa upande wake amejadili masharti kama:1. Mazingira.2. Uhusiano.3. Cheo.4. Hali.5. Madhumuni.6. Kichwa cha mazungumzo.
52
7. Lugha azijuazo mtu.8. Tabaka na malezi.9. Umri.
Hebu tutoe maelezo kwa masharti anayotoa Kitsao(ibid)
(i) MazingiraKulingana na lugha katika mazingira, itaonekana, kwa mfano, kuwa matanganikutakuwa na matumizi ya lugha ya huzuni, kupeana mkono wa pole nakuliwazana. Pia mtu akiwa ofisini analazimika kutumia lugha rasmi lakiniakiingia mitaani miongoni mwa watani atazungumza lugha isiyo rasmi.
(ii) UhusianoUhusiano wa watu katika jamii husababisha lugha kutumiwa kwa mtindo fulaniufaao. Kati ya mzazi na mwanawe kuna miiko inayowataka wawasiliane kwa njiaya heshima. Mathalani, si kawaida mzazi na mwanawe kutaniana au mwanakumwita babake kwa jina lake katika jamii za Kiafrika. Lakini watani wa mtuhuwa na uhuru mkubwa katika matumizi ya lugha miongoni mwao.
(iii) CheoCheo ni muhimu katika matumizi ya lugha kwani kuna lugha anayostahili kutumiaProfesa, kuna lugha ya wazee, lugha ya vijana na kadhalika. Ndiposa tunawezakusikia lawama kuwa ijapokuwa fulani ana cheo hazungumzi kulingana na cheochake.
(iv) HaliNi kweli kwamba lugha ya mtu hubadilika au kuathirika kulingana na hali ya mtuhuyo. Mtu anapokuwa mgonjwa hutumia lugha ya kuvuta huruma. Lugha yamlevi huwa legevu na ovyo. Mtu anapokasirishwa hutumia lugha kali na yakutisha.
53
(v)MadhumuniLugha inaweza kutumiwa kulingana na madhumuni au msimamo wa mtu katikajambo fulani. Inawezekana kuwa madhumuni ni kuvutia au kuteka watu kiakiliambapo mwongezi atatumia lugha nyenyekevu na ya ushawishi mkubwa. Lughayaweza kutumiwa kwa lengo la kuchukiza, kuchekesha, kuamrisha kupigavijembe na kadhalika.
(vi) Kichwa cha MazungumzoSajili mbalimbali zitafaa kwa vichwa tofauti vya mijadala. Kwa mfano, ikiwa watuwanazungumza juu ya mambo ya kisheria itabidi warejelee sajili ya kisheria kwakutumia istilahi zifaazo kama hakimu, mshtakiwa, wakili na kadhalika. Katikamazungumzo kama haya haitakuwa muhali kuingiza sajili ya matangazo yampira. Maoni yetu ni kwamba vichwa mbalimbali vya mada ndio msingi wa sajili.
(vii)Lugha azijuazo MtuSharti hili ndilo msingi wa kubadili msimbo. Mtu asiyejua Kiingereza hataingizalugha hiyo kwenye matumizi yake ya lugha. Lakini yule anayefahamu lughanyingine anaweza kuzitumia lugha hizo zote kwa pamoja.
(viii) Tabaka na MaleziTabaka na malezi tofautitofauti hukuza viwango mbalimbali vya ujuzi wa lugha.Jinsi mtu anavyowezeshakutalii na kumudu lugha kikamilifu ndivyoatakavyoweza kuitumia kwa ukwasi na ufasaha zaidi. Mtu mwenye malezimazuri huchuja lugha yake lakini mwenye malezi mabaya hutumia lugha yenyematusi.
(iX) UmriInaonekana kuwa lugha miongoni mwa jamii hukua na kukomaa kulingana najinsi mtu anavyokua kutoka utotoni hadi uzeeni. Kwa hivyo, mtoto anapotumia
54
lugha isiyokuwa na ustaarabu kama Naenda kukojoa , kijana wa makamoatatumia lugha yenye heshima kidogo kwa kusema Naenda haja ndogo ilhalimzee atatumia lugha fiche kama vile Naenda kutema mate .
Bila shaka kunayo masharti mengi sana yanayosimamia matumizi ya lugha lakinihayo machache yanatosha.
Zoezi
Eleza kwa kutoa mifano, jinsi kila moja ya masharti hayoyanavyoweza kuathiri lugha anayotumia mtu.
3.10 JUMUIA LUGHAKimsingi, wana-elimujamii huchunguza jamii kwa kuzingatia kategoria kama vilematabaka, ukoo, usehemu na uchumi.
Dhana ya Jumuia ni neno linalorejelea ile hali ya kundi la watu kufahamu jambofulani kwa pamoja, au wana umiliki sawa wa tabia zinazofanana. Wanaisimuhuhusisha dhana hii ya Jumuia na swala la lugha, ndipo tunapata dhana yaJumuiya lugha.
Kulingana na TUKI (1990) jumuia lugha ni kundi la watu wanaokaa katika eneomoja na kutumia namna moja ya lugha.
Kimsingi dhana hii inasisitiza kwamba tabia au matendo ya lugha yanaweza kuwakitu ambacho kinaunganisha kundi fulani la watu. Hata hivyo, kumekuwepo nautata mwingi juu ya maana halisi ya dhana hii. Jambo hili linadhihirika wazikutokana na jinsi wataalamu mbalimbali walivyoifasiri.
55
Yule (1996) anasema kuwa jumuia lugha ni kikundi cha watu ambao wana kaida,sheria na matarajio ya pamoja kuhusiana na matumizi ya lugha.
Lyons (1970) anasema kuwa, jumuia lugha ni jumuia ya watu wanaotumia lughamoja (au lahaja moja).
Kutokana na maelezo haya, jumuia lugha zinaweza kuingiliana (kwa mfano, palekuna watu ambao wanaongea lugha zaidi ya moja) na watu hawa hawahitajikuwa na umoja wowote wa kijamii au kitamaduni. Ukweli ni kwamba ni rahisikutenga jumuia lugha kwa njia hii, kwa sababu tunaweza kuzitenganisha lughana lahaja.
Hocket (1968), Bloomfield (1933) na Gumperz (1962) wanakubaliana kuwa kilalugha huifasiri jumuia lugha na kwamba jumuia lugha ni kundi la watuwanowasiliana ama moja kwa moja au kwa njia nyingine kupitia kwa lugha moja.
Katika fasiri hii, tunaona kuwa kigezo cha muingiliano wa mara kwa marakinajitokeza. Hii inaweza kuchukuliwa kuwa, ikiwa jamii mbili zinazozungumzalugha moja lakini hazina utagusano basi zitachukuliwa kuwa jumuia lugha tofauti.Fasiri hii imeondoa msisitizo wa lugha ya pamoja na kuzingatia mawasiliano.
Nao Hymes (1972) na Halliday (1978) wanasema kuwa, tunapozungumziajumuia lugha ni muhimu kuzingatia sheria za pamoja za uzungumzaji na ufasiriwa matendo ya uzungumzaji. Katika fasiri hii, tunaona kuwa msisitizo unawekwakwa jumuia lugha kama ni kikundi cha watu ambao wanahisi kuwa wao nijumuia.
Naye Labov (1972) anatilia mkazo mielekeo ya watu kwa lugha na thamani zaokuhusu miundo ya lugha na matumizi.
56
Fasiri hizi zote ni sahihi kwa sababu zinaeleza jumuia lugha ni nini. Kutokana nafasiri hizi basi tunapata sifa zifuatazo za jumuia lugha:1) Ni kundi la watu.2) Watu wanaowasiliana kwa lugha moja.3) Wanaweza kuwa wanaishi eneo moja au maeneo tofauti.4) Kuna mtagusano au kuingiliana kwa watu hawa mara kwa mara.5) Ni watu walio na mielekeo sawa kuhusu lugha.6) Ni watu walio na utamaduni sawa.
SwaliJe, unaweza kusema kuwa Kenya ni Jumuia-lugha moja? Toa sababuza kukubali au kupinga taarifa hii.
HITIMISHO
Maswala kadha wa kadha ya lugha yameshughulikiwa katika somo hili.Tulianza kwa kueleza maana ya lugha pamoja na matumizi yake. Kishatuliona kuwa lugha huweza kujitenga katika makundi mbalimbali ambayoyanajulikana kama lahaja.Tuliona jinsi lahaja inavyozuka, na tukarejeleanadharia ya mawimbi kutilia msingi hoja hii. Vile vile tuliona jinsi mtuanavyoweza kutambua lahaja na lugha. Swala la mtindo pekee kamaishara ya tabia za kiisimu za mtu fulani limejadiliwa. Isitoshe, swala lamtindo na sajili vimeshughulikiwa kwa kuchunguza jinsi lugha inavyotumiwana vikwazo vinavyosimamia matumizi ya lugha. Na mwisho, dhana yajumuiya-lugha imeelezwa.
57
Marejeleo Teule1. Chacha, L.M. na wengine (2003) AKS 100: Introduction to the Study of
Language: Kiswahili Module . Nairobi. Institute of Open Learning,Kenyatta University.
2. Chambers, J.k. & Trudgill P. (1980) Dialectology . Cambridge. CambridgeUniversity Press.
3. Crystal, D. and Davy, D. (1969) Investigating English Style . New York:Longman.
4. Fromkin, V. & Rodman, R. (1988) An Introduction to Language , New YorkHarvourt Brace. Jovanivich College Publishers.5. Halliday, M.A.K. et.al. (1964) The Linguistic Science and Language Teaching .
London. Longman.6. Kitsao, J. (1975) A Stylistic Approach Adopted for the Study of Kiswahili
Prose Texts . M.A. Thesis: Nairobi University. (haijachapishwa).7. Lyons, J.L. (ed.) (1970) New Horizons in Linguistics . Penguin Book.8. Mdee, J.S. (1986) Kiswahili: Muundo na Matumizi Yake . Nairobi,
Intercontinental Publishers Ltd.9. Musau, P.M. (1990) Swahili Part Three: Kiswahili in the Twentieth Century .
Nairobi: University of Nairobi.10. Onyango, J.O. (2002) AKS 102: Historical Development of Kiswahili: Kiswahili
Module. Nairobi. Institute of Open Learning, Kenyatta University.11. Ryanga, S. na Mukobwa, M. (2003) AKS 101: Language Skills in Kiswahili1 :
Kiswahili Module : Nairobi Institute of Open Learning, KenyattaUniversity.
12. TUKI (1990) Kamusi Sanifu ya Lugha na Isimu . Dar es Salaam, Universityof Dar es Salaam.
13. Wardhaugh, R. (1987) Languages in Competition , Oxford, Basil BlackwellCo.
58
SOMO LA NNE
LUGHA ZA MAWASILIANO PANA
4.0 UTANGULIZIKatika somo hili, tutashughulikia lugha za mawasiliano pana.Hizi ni lughaambazo zinavuka mipaka ya jamii moja. Tutajadili hizo pamoja na dhana zalingua franka, Pijini na Kirioli.
4.1 Madhumuni
Baada ya kulipitia somo hili, tunatarajia kwamba utaweza:1. Kueleza maana ya lingua franka.2. Kueleza maana ya Pijini na Kirioli na kuonyesha kuibuka kwa lugha hizi.
4. 2 Lingua FrankaLingua franka ni lugha inayotumiwa kama chombo cha mawasiliano kati ya watuambao hawana lugha moja asilia wanayofahamu wote. Hii ni lugha inayotumiwana watu wote katika eneo kubwa hata kama wana lugha zao nyingine. Kwamfano, Kiingereza ni lingua franka ya ulimwengu wote. Wakati fulani Kifaransakilikuwa lingua franka ya itifaki (diplomacy) na kilatini kilikuwa pia lingua frankaya dini ya Ukristo.
Baadhi ya lugha zinazotumiwa kwa maana hii, kwa mfano, Kiingereza naKifaransa si za kiasili bali huwa zimefahamika kupitia kwa elimu ya shuleni auelimu rasmi. Hata hivyo, lingua franka nyingine barani huwa za kiasilia nahupata jukumu hilo kutokana na kabila linalohusika kuwa na nguvu za kisiasakama vile Luganda; au kwa kuwa wafanyibiashara mashuhuri kama vile Kiswahili.
59
Kihausa ni lingua franka ya Afrika Magharibi kwa sababu ya nafasi yake katikabiashara.Kiyunani kilikuwa lingua franka hapo zamani hasa kwa sababu ya vita vyaAlexander the Great .
Kilatini vile vile kilikuwa lingua franka katika nchi za magharibi kwa sababu yaupanuzi wa utawala wa Roma.
Lugha ya Kiswahili inaweza kudai kuwa lingua franka ya sehemu za AfrikaMashariki na kati. Jambo hili ni wazi hasa tukizingatia lugha mbalimbali ambazozinatumika katika sehemu hii. Kando na hayo, Kiswahili bado kimebakia imarahata katika hali ya ushindani kutoka kwa lugha mbili zilizo na nguvu yaaniKiingereza na Kifaransa. Kiswahili kimeweza kuendelea sana hata katikamazingira hatari, hasa kuanzia kipindi cha kwanza cha karne ya 18 na karneiliyopita. Ni lugha ambayo inatumiwa sana katika sehemu nyingi za AfrikaMashariki na Kati.
Baadhi ya lingua franka nyingine katika bara la Afrika ni Bambara na Wolof,ambazo zote zinapatikana Afrika Magharibi, (Chimera 2000).
Swali
Kiswahili sio lugha ya Afrika Mashariki tu, bali ni lugha ya Kimataifa.Fafanua kauli hii.
4.3 PIJINI NA KIRIOLIUtafiti katika lugha za kipijini na kikirioli unakisiwa ulianza mnamo mwishoni mwakarne ya 19 na mwansaisimu-jamii, Hugo Schuchardt, Swale
(1997).
60
Yasemekana kuwa alichapisha mfululizo wa vitabu vilivyojulikanakamaKroelische Studien katika miaka ya 1880.Hata hivyo, somo hili lilipuuzwa. Lakini baada ya kupuuzwa, utafiti katikanyanja ya pijini na kirioli ulianz hasa mwanzo mwanzoni mwa karne ya 20.Kufikia mwaka 1945 ndipo wanaisimu walipojitosa tena katika utafiti wake. Tafitichache zilifanywa katika kipindi cha vita vikuu vya kwanza na vya pili. Baadhi yawanaisimu wa mwanzo kutafitia pijini na kirioli ni pamoja na Jacobs (1932), Boas(1933), Reinecke na Tokimasa (1934), Hall (1948, 1953) na Turner (1949).
4.3.1 SIFA BAINIFU ZA PIJINIWanaisimu-jamii wengi wameafikiana kuwa, lugha za kipijini na krioli ziliibukakatika miktadha ya kibiashara na katika zama za biashara ya utumwa. Lugha hiziziliibuka ili kuwawezesha watu walioongea lugha tofauti tofauti kuwasiliana kwadhamira fulani fulani. Kama asemavyo David Decamp (1975:15),
Pijini ni lugha ya mawasiliano na ambayo kwa hali za kawaida,si lugha asilia ya watumizi wake.
Pijini nayo, huwa krioli pale inapopata waongeaji wazaliwa, yaani pijiniinapokuwa ni lugha ya kwanza ya mtu. Muhlhauster (1986:1) anasema yakwamba, dhana ya pijini huenda ilitokana na hali au miktadha ifuatayo:(i) Kutokana na matamshi ya jamii ya Wachina ya neno la Kiingereza
business .(ii) Kutokana na neno la Kiyahudi pidjom .(iii) Kutokana na neno Pidian la Wahindi wekundu wa Amerika Kusini; na(iv) Kutokana na matamshi ya jamii ya watu wa Bahari za Kusini ya neno
beach .
Tunaporejelea asili na miktadha mbalimbali hapo juu, inatubainikia wazi kuwalugha za kipijini ziliibuka miongoni mwa jamii za watu walioongea lugha
61
tofautitofauti kwa minajili ya kufaulisha mawasiliano baina yao (Tazama Chachana wengine katika AKS 100: Introduction to the Study of Language).
Mwanaisimu-jamii Loreto Todd (1990) anapambanua na kutofautisha pijini-finyuna pijini-pana.
(i) Pijini-finyuPijini-finyu huibuka katika muktadha wa dharura sana kati ya jamii za watuwanaoongea lugha tofauti. Pijini zinazoibuka katika miktadha ya aina hii, huwana sifa bainifu zifuatazo:(a) Huwa na miundo sahili hasa ya kisintaksia na aghalabu, huhusisha kauli
za kuamrisha na huambatisha ishara za kimwili kama za mikono, machona viungo vingine vya mwili. Kwa mfano, pijini za Afrika Magharibizilizoibuka kipindi cha vita vikuu kati ya askari jeshi Waingereza nawenyeji wa eneo hilo.
(b) Idadi kubwa ya msamiati hutokana na lugha ya tabaka la juu au tawala,na kutiwa kwenye mfumo wa matamshi ya lugha ya wenyeji. Toddanadai kuwa Kisetla kilichotumika nchini Kenya kati ya masetla wazunguna Waafrika ni mfano mwafaka.Hili ni jambo ambalo wanaisimuwanaweza kulitafitia ili kulithibitisha.
(c) Aghalabu pijini finyu huhusisha lugha mbili tu na uhusiano kati yazounapokatishwa basi pijini ile hufa. Miktadha yake aghalabu huwa ni yadharura za kimawasiliano kama vile katika shughuli za biashara, shughuliza kijeshi na hii leo, katika shughuli za sekta ya utalii.
(ii) Pijini – PanaSifa za pijini-pana ni kamai zifuatazo:(a) Huibuka kutokana na kudumishwa kwa mazingira ya pijini finyu.
62
(b) Maneno ya pijini finyu yanapopanuka huwa ni lugha ambayo badohaijakuwa thabiti kimuundo, kimsamiati na kadhalika bali ni matumizi yakeyanayopanuka.(c) Inapoimarika na kupata waongeaji wazaliwa, basi huwa ni kirioli na
hatimaye inaweza ikawa lingua franka (lugha sambazi) ya eneo fulani lakijiografia.
4.3.2 Dhana ya KirioliBickerton (1971) anasema kuwa, lugha za kikirioli zinaweza kuibuka kutokana namiktadha au mazingira yafuatayo:(a) Pijini zilizopata wazungumzaji wazaliwa.(b) Katika jamii ambamo asilimia ishirini (20%) ya waongeaji ni wenyeji na
asilimia themanini (80%) ni ya matumizi ya lugha zingine za kigeni.(c) Krioli huwa na miundo iliyoimarika ya kisarufi msamiati mpana na
kadhalika na hazitumii ishara (kwa wingi) wala uigizaji ili kufafanua maanakama ilivyo pijini.
Sifa hizi zinazifanya krioli kuwa na hadhi ya lugha kama lugha zingine asilia(zisizoibuka katika mazingira tuliyotaja) na hutumika rasmi katika elimu,biashara, kuandika fasihi na hata huweza kuwa lingua franka. Mfano wa nchizinazotumia kirioli ni Sierra Leone, Liberia, Gambia, Hawii, na Mauritius.
Wanaisimu-jamii wengi wanasema kuwa dhana za kipijini na kikrioli ni mfanobora wa jinsi binadamu wote, wanavyoweza kuutumia uwezo wao jumuishikatika mazingira tofautitofauti.
Majedwali haya yanaeleza kwa muhtasari jinsi kirioli inavyoibuka.
63
1. Lugha za wazazi (Pijini)
Uwezo jumuishi
Lugha ya watoto (Kirioli)
2.Pijini ya mama Pijini ya babaLugha finyu Lugha finyu
Mazingira
Kirioli (lugha ya watoto)
3. Pijini finyu 4 Pijini finyu
Kirioli Pijini Thabiti(krioli ya Hawaii)
Kirioli(Krioli ya Kiingereza ya
Torress Straits)
5 Pijini finyu
Pijini Thabiti
Pijini Pana Thabiti
64
Kirioli (Tok Pisini ya Papua New Guinea)
Kutokana na majedwali haya, inatudhihirikia kwamba, ili lugha yoyote ya pili(kama Pijini) iwe lugha asili (ya mama) au kirioli, itabidi ifanyiwe marekebishofulani fulani na watumizi wake.Marekebisho yenyewe yatahusu kuondoaupungufu wowote uliomo katika viwango vyote vya kiisimufonolojia,mofolojia, sintaksia na msamiati. Hapo ndipo lugha hiyo (kirioli) itakapowezakuwa chombo kiaminifu na kinachosadifu mawasiliano ya jamii husika katikangazi mbalimbali.
4.4 NADHARIA ZA ASILI YA PIJININadharia kadhaa zimependekezwa kuelezea asili ya pijini:1. Nadharia mahsusi za lugha.
(a) Nadharia ya lugha ya kibaharia (nautical jargon)(b) Nadharia ya lugha ya kitoto (baby talk)
2. Nadharia za kijumla.(c) Nadharia ya uundaji upya leksimu (relexification)(d) Nadharia jumlishi (universalist)
3. Nadharia zinazozingatia tofauti.(e) Nadharia zenye kiini kimoja (common-core)(f) Nadharia zenye safu msingi (substratum)
Hebu tuzifafanue nadharia hizi.4.4.1 Lugha ya Kitoto.Hii ni nadharia inayoshikilia kwamba pijini zilizuka kutokana na kuiga nakurahisisha lugha aliyoisikia mtu. Hii ina maana kwamba, mtu anajifunza lughalakini hajifunzi lugha hiyo vyema. Kuna hata wataalamu, kama Hesseling (1933),wanaodai kuwa pijini zilizuka kutokana na ujifunzaji makosa wa lugha uliofanywana watumwa.
65
Bloomfield (1933) anaeleza kuwa pijini ilizuka pale ambapo watu walijaribukuiga jinsi wenzao wasioifahamu lugha vizuri wanvyozungumza. Kwa mfano,mwajiri (Bwana) anapozungumza na mtwana anairahisisha ile lugha yake nakuiga lugha mbovu ya mtwana yule ili waelewane. Vivyo hivyo, mtu mzimaanapozungumza na mtoto ambaye bado hajaimudu lugha vizuri anairahisishalugha yake ili ilingane na ile ya mtoto. Basi mtwana anaposikia jinsi mwajiriwake anavyozungumza anakosa kielelezo cha kuiga na anaiga lugha mbovu.
Nadharia hii basi inazo harakati mbili. Moja huanzishwa na wazungumzaji walugha yenye hadhi ya juu ambao hurahisisha lugha yao. Ya pili, huanzishwa nawazungumzaji wa lugha ya hadhi ya chini ambao hurahisisha lugha wanayoisikiapale wanapojaribu kujifunza lugha hiyo. Katika hali ya kwanza, kikundi cha hadhiya chini kinaiga kinachosikia kutoka kwa kundi lenye hadhi ya juu. Katika hali yapili, kundi lenye hadhi ya chini ndilo huongoza katika kufanya makosa, na lile lahadhi ya juu linaimarisha tu makosa hayo.
4.4.2. Lugha ya Kibaharia (Nautical jrgon theory)Kwa mujibu wa nadharia hii meli zilizoabiri bahari zilikuwa na mabahariawaliozungumza lugha na lahaja tofauti. Kwa hivyo ilibidi kuwepo na lugha mojailiyoeleweka na mabaharia wote. Lugha hii iliyotumiwa na mabahariaikafahamika na Waafrika, Wazungu na Wahindi waliofanya kazi ya ubaharia.Yamkini msamiati wa kibaharia ulikuwa kiini cha lugha hii, na lugha hii ilipanuliwakwa nyongeza kutoka kwa lugha za asili za mabaharia. Hii ndiyo sababu pijini nakrioli katika maeneo fulani ulimwenguni zitafanana, lakini zitofautiane na zile zamaeneo mengine.
Nadharia hii inapata msukumo kutokana na utafiti wa Todd (1990:33)anayesema kuwa kuanzia karne ya 17 mabaharia walikuwa na lugha yaomahsusi. Pia kuna msamiati wa kibaharia katika pijini nyingi duniani. KatikaCameroon pidgin tunapata maneno kama:
66
Hib < heave sukumaKapsal < capsize pindukaManawa < man of war mtu wa vita
Reinecke (1937) alifanya utafiti na akakuta kwamba mabaharia waliozungumzalugha tofauti katika meli moja waliunda msamiati mpya wanaoufahamu wote wamaneno 300 katika kipindi cha miezi michache.
Ingawa tunakiri kwamba mabaharia walisambaza msamiati wa kibaharia katikapijini mbalimbali ulimwenguni, nadharia hii haielezi kwa nini pijini zenye misingiya Kiingereza, Kifaransa, Kireno, na Kihispaniola zinafanana.
4.4.3.Asili moja (Monogenesis Theory)Usuli wa nadharia hii ya asili moja ni kwamba pijini zote zinahusiana kinasaba nazimetoka kwa proto-pijini au pijini-mame moja. Kwa hivyo, kule kufanana kwapijini kunaelezwa kuwa kunatokana na jadi moja (common ancestor) hapozamani.
Inafikiriwa kwamba hii proto-pijini inayozungumziwa katika nadharia hii ni pijiniya Kireno ambayo labda ilikuwa ni mabaki ya lugha ya Sabir. Sabir ilikuwa linguafranka ya zamani iliyotumiwa na wapiganaji wa Kikristo (crusaders) na pia kamalugha ya kibiashara ya eneo la Mediterranean.
Nadharia hii inafafanua kwamba tofauti zinazopatikana katika pijini mbalimbali nimatokeo ya kubadilisha msamiati kunakoendelea.Kulingana na nadharia hii,kipijini cha Kireno ndicho kilikuwa msingi wa pijini nyingine ambazo ziliundwabaadaye, lakini pijini hizi zilibadilisha msamiati wa pijini msingi na kutumiamsamiati kutoka kwa lugha nyingine huku zikihifadhi msingi wa kisarufiunaofanana.
67
Njia hii ya kubadilisha msamiati wa lugha fulani huku ukihifadhi muundo wakisintaksia inajulikana kama uundaji upya wa leksimu (relexification).
Kwa hivyo nadharia hii inadai kuwa pijini na kirioli za Ulaya ni vibadala vya pijiniya Kireno ya Karne ya 15 vilivyoundiwa msamiati mpya. Pijini hii mwanzoilitumiwa katika upwa wa Afrika na baadaye ikafika India na nchi nyinginezo zaMashariki ya Mbali (Far East). Kwa njia hii, pijini zote za Ulaya zinahusianakupitia kwa mchakato wa kudumisha sarufi na kubadili msamiati.
4.4.4 Maendeleo Sambamba (Independent Parallel).Msingi wa nadharia hii ni kwamba pijini na krioli zilizuka kila moja kivyake na
zikaendelea kukua sambamba kwa sababu zilitumia malighafi ya kiisimuiliyofanana na zilikulia katika mazingira yaliyofanana.
Kwanza, lugha kuu za wazungu hazikuwa tofauti kimuundo. Vile vile lughanyingi za waafrika (watumwa) zilitokana na kikundi kimoja cha familia ya lughaambazo wanaisimu huzibainisha kama Lugha za Afrika Magharibi.
Hall (1961) alieleza kuwa ingawa lugha hizi zilizuka kila moja kivyake kulikuwepona maeneo machache ya mwingiliano kama inavyoonyeshwa hapa chini.
English Melanesian(French n.k) (Chinese,
African n.k.)
4.4.5 Lugha ya hadhi ya chini (Substratum theory)Mahlhausler (1986:119) anatoa wazo kwamba pijini huunganisha msamiati walugha yenye hadhi ya juu (superstratum) na sarufi ya lugha ya hadhi ya chini(substratum). Hii ina maana kwamba pijini ni lugha ya mseto.
68
Naye Romaine (1988:102) anadai kuwa sura mbalimbali za kifonolojia, kisintaksiana kileksia, zinazopatikana katika pijini zimetokana na lugha za Kiafrika.Wanazuoni wengi wanasema kuwa pijini na kirioli zina msingi wa Kiafrika.Goodman (1964) ametoa hoja kwamba ni baada tu ya kukubali kuwa kirioli zotezenye msingi wa Kifaransa zina asili yake Afrika Magharibi ndipo tutaelewa kwanini zinafanana.
Pijini na kirioli huzungumzwa hasa katika nchi za ulimwengu wa tatu.Zinahusishwasana na maswala ya kisiasa na kijamii. Kuna takriban pijini nakirioli mia moja duniani. Pijini nyingi zina misingi yake katika lugha za Ulaya,hususan Kihispania, Kireno, Kifaransa, Kiingereza na Kidachi. Kikundi kinginekinachofuata kwa ukubwa kina misingi yake katika lugha za Kiafrika.
Zoezi
Kwa kuzingatia nadharia hizi, unafikiria Sheng ni pijini au kirioli. Toa sababuzako.
4.6 HITIMISHO
Katika somo hili, tumeanza kwa kujadili swala la lingua franka natumeonyesha majukumu yake katika jamii. Vilevile tumeeleza nakuonyesha jinsi zinavyotumika kama lingua franka. Pili, tumefafanuadhana za pijini na kirioli na vilevile kuonyesha nadharia mbalimbaliambazo zimetolewa na wanaisimu kuhusiana na swala la kuzukakwa lugha hizi..
69
Marejeleo Teule Bickerton, D. (1971) Inherent Variability and Variable Rules. Foundations of
Language 7 .Bloomfield,L. (1933) Language . New York. Holt. Rinehart and Winston.Chimera, R. (2000) Kiswahili: Past, present and Future Horizons . Nairobi.
Nairobi University Press.Guthrie, M. (1967) The Classification of the Bantu Languages . London Dawsons
of Pall.Mbaabu,I. (1978) Kiswahili Lugha ya Taifa . Nairobi: Kenya Literature Bureau.Onyango, J.O. (2002) AKS 102: Historical Development of Kiswahili:Kiswahili
Module. Nairobi: Institute of Open Learning, Kenyatta University.Polome, E.C. (1967) Swahili Language Handbook . Washington D.C. Centre for
Applied Linguistics.Swaleh A. (1997) Lugha ya Kiswahili (ni) pijini au krioli? Makala
yaliyowasilishwa katika Idara ya Kiswahili. Chuo Kikuu cha Nairobi.Todd, L. (1990) Pidgins and Creoles . Routledge.London.
70
SOMO LA TANOUWILI LUGHA
5.0 UtanguliziKatika somo hili tunanuia kuelezea maana ya uwili-lugha na ulumbi. Pamoja nahayo, tutaonyesha athari ambazo hutokana na lugha mbili au zaidi kuwa pamoja.Vile vile tutajadili swala la lugha rasmi, lugha ya taifa , diglosia na triglosia. Namwisho tutaangalia swala la utowekaji wa lugha katika jamii.
5.1 Madhumuni
Baada ya kulipitia somo hili, tunatarajia kwamba utaweza:1. Kueleza maana ya uwili-lugha na kuonyesha athari zake.2. Kueleza maana ya lugha rasmi na lugha ya taifa.3. Kueleza kwa fasili dhana za diglosia na triglosia.4.Kuonyesha sababu za utowekaji wa lugha na jinsi ya kuzilinda lugha hizi.
5.2 UWILI-LUGHAMtagusano wa wanajamii huzua hali ya uwili lugha katika jamii mbalimbali. Kwamujibu wa Bloomfiled (1933) uwili-lugha ni umilisi wa lugha mbili kama ulealionao mzawa wa lugha moja katika lugha yake.
Haugen (1956) naye anaona kuwa uwili-lugha ni kitu ambacho huanza wakatimzungumzaji wa lugha moja anapoweza kutoa kauli kamili na zenye maanakatika lugha nyingine.
Katika hali ya wingi lugha tunaweza kuzungumzia kuhusu mtu mmoja auwanajamii wote au wengi kuwa wana wingi-lugha.
71
Mtaalamu Grosjean (1982:vii) anakadiria kuwa karibu nusu ya idadi ya watuulimwenguni huzungumza zaidi ya lugha moja. Naye Romaine (1989:6) anadaikuwa hata zile nchi ambazo zinafikiriwa kuwa na lugha moja tu kama vileUfaransa, Ujerumani na Uingereza zina wazungumzaji ambao ni wana uwililugha. Kwa mfano, utapata kuwa maeneo ya kimipaka, kwa mfano, Ufaransa,kuna lugha hizi:-Breton, Flemishi, Occitan, na kadhalika. Mara nyingi watuwanaopakana hujipata wakizungumza lugha ya jirani zao.ZingatiaKatika somo hili tutatumia istilahi ya uwili- lugha kurejelea pia wingilugha
5.3 Sababu za kuwepo na Uwili lugha .Kunazo sababu nyingi ambazo zinawafanya watu kuzungumza zaidi ya lughamoja. Sababu hizi ni pamoja na:
1. Ndoa mseto Hali ya ndoa mseto ni jambo la kawaida katika ulimwengu wa sasa. Hali hiiinapotokea mke au mume hulazimika kujifunza lugha ya pili.
2. Elimu Aghalabu watu wanapoenda shuleni wanafunzwa lugha ya pili. Kwa mfano,mtoto anapokuwa mdogo hujikuta katika mazingira ambayo wazazi wakewanatumia lugha wenyeji. Anapotimia umri wa miaka sita, mtoto huyu hujiungana shule. Shuleni, hufunzwa Kiingereza na Kiswahili. Ripoti ya hivi karibuniinaonyesha kuwa zaidi ya wanafunzi elfu mia nne wako katika nchi mbalimbalikwa masomo ya juu. Wale walio katika nchi zinazotumia lugha nyinginezo kamavile Kijerumani au Kifaransa hulazimika kujifunza lugha hizi hata kabla yakujiunga na vyuo hivyo.
72
3. Dini Dini anayofuata mtu inaweza kuwa katika lugha fulani, kwa mfano, ikiwa dini niya Kiislamu, utapata kwamba Waislamu wengi wanafahamu Kiarabu kwa sababuhii ndiyo lugha ambayo hutumiwa sana katika mahubiri hasa kukariri korani.
Swali
Je, waweza kufikiria sababu zingine zinazomfanya mtu kutaka kujua zaidiya lugha moja?
5.4 Uchaguzi wa lugha katika jamii zenye uwili-lugha- Dhana yahimaya
Tunapoangalia Afrika kwa mfano, tunaona kuwa mtu yeyote anayesafiri kwasababu za kiuchumi au kuhamia sehemu fulani kwa sababu mbalimbali huwamwana uwili lugha. Hata kama kuna wazungumzaji wa lugha moja tu, wengiwa watu ni wana uwili-lugha, (Myers- Scotton 1993).
Tafiti nyingi ambazo zimefanywa katika jamii zenye uwili-lugha zimejihusisha natabia ya uchaguzi wa lugha wanaofanya wazungumzaji. Istilahi hii ya tabia yauchaguzi ni muhimu. Katika hali nyingi, wazungumzaji wanaweza kutumialugha zao wanapozungumza na wenzao. Ukweli ni kwamba, lugha fulanihuhusishwa na miktadha fulani. Kwa mfano, mandhari, mada na wahusikakatika mazungumzo hayo, Mesthrie (2000).
Mtaalamu Fishman (1967) katika kulishughulikia swala hili, alijihusisha nakuonyesha ruwaza ya matumizi ya lugha. Aliibuka na dhana ya himaya(domains) kama namna ya kuonyesha ruwaza hizi. Alidai kuwa katika jamiiyenye uwili-lugha, lugha mbalimbali huhusishwa na himaya tofauti za matumizi.
73
Mifano ya himaya hizi ni pamoja na familia, elimu, kazi au ajira, urafiki, utawalawa kiserikali, n.k.
Hivyo basi katika himaya hizi, mtu atachagua mojawapo ya lugha anazozifahamuili kuzitumia. Kwa mfano, Myers Scotton (1992) amegundua kuwa katika bara laAfrika, ruwaza ambayo inajitokeza kwa wingi ni lugha ya kwanza yamzungumzaji, pamoja na lingua franka ya wenyeji, kwa mfano, Kiswahili, kishalugha ya kigeni kama vile Kiingereza au Kifaransa.
Ruwaza ya matumizi ya lugha katika sehemu nyingi za Afrika zinategemea hali yakijamii ya mtu na aina ya muingiliano ambayo mtu hujihusisha nayo (Mesthrie2002).
Zoezi
Kwa kuzingatia dhana ya himaya, onyesha namna marafiki zakowanavyotumia lugha wanazozifahamu.
5.5 Mambo muhimu ya kuzingatiwa katika uwili-lugha
Mtaalam Makey (1962) anapendekeza mambo manne ambapo fasiri yo yote yauwili lugha inahitaji kuzingatia: kiwango, dhana, ubadilishaji na athari (auuingiliaji).
(a) KiwangoTumeona kuwa mwana uwili-lugha ni mtu ambaye anazungumza lugha mbili kwaustadi.Kwa mfano, Bloomfied anadai kuwa mwana uwili-lugha anahitaji kuwa naustadi, katika lugha ya pili kama alionao katika lugha yake ya kwanza.
74
Tunapowasikia watu wakiongea, tunatanbua kuwa watu hawa hutofautianakatika jinsi wanavyodhibiti lugha yao ya kwanza, na hali hii inawakumba walewanaojifunza lugha ya pili. Ni lini tunaweza kuamua kuwa sasa mtuanazungumza lugha ya pili kama anavyozungumza lugha yake ya kwanza ?.
Hivyo basi swali tunalohitaji kujiuliza ni je, kwa kiasi gani mzungumzajianafahamu lugha hizo mbili au tatu?
Mtazamo tofauti na huu ni ule ambao unachukuliwa na wanaisimu ambaohawatazami uwili-lugha kwa kuzingatia kiwango bali kwa kuzingatia dhima yalugha hiyo.
2. DhimaWana uwili-lugha huchagua lugha kulingana na kile watakachofanya na lughahiyo. Kwa mfano, uhusiano wao na watu wanaoongea nao na kilewanachozungumzia. Ruwaza ya uwili-lugha hubadilika kila mara kulingana nakazi itakayotendwa na lugha iliyochaguliwa kutumika.
Tuchukue mfano wa Mkenya ambaye ameishi Ujerumani kwa miaka mingi. Mtuhuyo anakifahamu Kijerumani, Kiingereza na Kiswahili. Sasa anaporudinyumbani na kwenda benki anafikiria kutumia Kiswahili. Lakini anatambua kuwahawezi kujieleza vilivyo kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu hajawai kuwa namajadiliano ya aina hii kwa Kiswahili. Itambidi achague lugha nyingine ambayoni Kiingereza ili kuwasiliana na meneja.
Hii inamaanisha kuwa kuna hali nyingi ambazo wana uwili-lugha wanawezakujieleza vizuri kwa lugha moja kuliko katika lugha nyingine.
3. Uingiliaji
75
Kuna tajriba fulani katika maisha ambazo humfanya mtu aweze kujieleza vizurikwa lugha moja kuliko nyingine. Hii haimaanishi kuwa hawaielewi lugha hiyo,La. Tatizo ni kwamba wao hujikuta kuwa hawalipati neno mwafaka ambalowanaweza kulitumia wanapozungumzia mada fulani. Weinreich (1953) anadaikuwa uingiliaji ni ile hali ambayo ukiukaji wa kaida katika lugha hutokea katikamazungumzo ya wana uwili-lugha kutokana na wao kujua zaidi ya lugha moja.Uingiliaji unaweza kutokea katika viwango vyote. Kwa mfano, unaweza kuwakatika kiwango cha fonetiki ambapo matamshi ya mtu yanakuwa kama yaleyanayopatikana katika lugha nyingine. Katika kiwango cha semantiki, mtuhuweza kushindwa kuchagua neno linalofaa. Ni rahisi kuona kuwa hata katikakiwango cha kisantaksia uingiliaji huu hutokea hasa katika mpangilio wa manenokatika sentensi.
4. UbadilishajiKatika hali hii tunaangalia kiasi ambacho mzungumzaji hubadili mazungumzokutoka kwa lugha moja hadi nyingine.
Zoezi
Ukirejelea Chacha L.M. na wengine (2002) AKS100: Introduction to the Study of Language , onyesha athari mbali mbali za kiisimu zinazojitokezakatika jamii yenye wingi lugha.
Kumbuka
Uwili lugha ni hali ambapo mtu anaweza kuzungumza lugha mbili. Wingi-lughani hali ya mtu kuzungumza zaidi ya lugha moja.
76
Swali1. Uwili lugha ni nini?2. Fafanua dhana ya himaya katika swala la uwili lugha3. Ni mambo gani tunahitaji kurejelea ili kujua viwango vya ufahamu vya
mzungumzaji fulani katika hali ya uwili lugha.
5.6 LUGHA RASMI NA LUGHA YA TAIFA
5.6.1 Lugha Rasmi
Hii ni lugha ambayo imeteuliwa katika nchi fulani ili itumiwe katika mawasilianoyote rasmi katika nchi hiyo. Lugha hii huchaguliwa ili kutumiwa katika shughuliza serikali, kwa mfano, afisini, kuzungumza na wageni, katika taasisi mbalimbalina ndiyo hutumiwa kwenye vyeti na shahada.
Nchi nyingi zilizotawaliwa zinatumia lugha za waliokuwa watawala wao kamalugha zao rasmi. Wakati mwingine baada ya nchi kupata uhuru, huamuakutumia lugha ya humo nchini kama lugha rasmi. Kwa mfano, Kenya na Ugandahutumia lugha ya Kiingereza kama lugha rasmi ilhali nchi ya Tanzania hutumiaKiswahili kama lugha rasmi. Tunasubiri kuona jinsi lugha ya Kiswahli naKiingereza zitatumika iwapo katiba mpya itakubali kuwa Kiswahili kiwe pia lugharasmi nchini.5.6.2 Lugha ya TaifaHii ni lugha ambayo kisiasa, kijamii na kiutamaduni inawakilisha watu fulani.Viongozi wa nchi huchagua lugha ya taifa hasa wanapogundua kuwa lugha nikipengele muhimu katika utamaduni wa taifa (Chimera 2002). Hivyo basi lugha
77
ya taifa huwa ni lugha inayotambulisha na kutumiwa na taifa fulani. Lugha hiihuweza vile vile kuwaunganisha wananchi wa matabaka mbalimbali. Tukitazamakwa mfano, viongozi wanaoshika hatamu, tunaona kuwa wanaweza kuchukuliwatu kama viongozi wa taifa zima bali sio wa makabila mbalimbali iwapo watatumialugha moja ya taifa.
Lugha ya taifa inaweza kulinganishwa na bendera ya taifa ya nchi.Vivyo hivyolugha huitambulisha taifa. Lugha ya taifa huwa na kusudi la kuibusha uzalendomiongoni mwa watu, (Chimerah 2002).
Katika baadhi, ya nchi utapata kuwa lugha rasmi ndiyo pia lugha ya taifa ingawasio lazima mambo yawe hivyo. Kwa mfano, katika nchi ya Tanzania, Kiswahili nilugha rasmi na pia lugha ya taifa.
Kumbuka
Si lazima kila nchi iwe na lugha ya taifa ingawa ni lazima kila nchi iwena lugha rasmi.
Swali
Huku ukitoa mifano eleza maana ya lugha Rasmi na lugha ya Taifa.
5.7 DIGLOSIA NA TRIGLOSIADiglosia ni hali ya kuwepo kwa lahaja mbili za lugha moja, kila moja ikikidhimahitaji tofauti ya kijamii.
Kuna wataalamu wawili wa isimujamii walioifafanua dhana hii ya diglosia lakinikwa misisitizo mbalimbali. Hawa ni Ferguson (1959) na Fishman (1967).
78
5.7.1 MAELEZO YA DIGLOSIA KAMA YANAVYOTOLEWA NA FERGUSONFerguson alitambua kwamba wazungumzaji hutumia vibadala tofauti vya lughakatika miktadha tofauti.Alieleza kuwa kulikuwa na hali maalum ambapovibadala viwili vya lugha vinakuwepo ubavu kwa ubavu katika jamii fulani, kilamoja ya vibadala hivyo ikiwa na dhima mahsusi. Hali hii ndiyo aliyoiita diglosia.
Ferguson aliona kuwa hali hii ni tofauti na pale ambapo lugha sanifu na lahajanyingine ya lugha hiyo zilitumika, au pale ambapo lugha mbili tofauti zilitumiwakatika jumuia lugha, kila moja ikiwa na dhima yake.
Ferguson aliifafanua dhana ya diglosia kupitia kwa vigezo tisa:dhima (function)fahari(prestige)urithi wa fasihi (literary heritage)upataji au ujifunzaji lugha (acquisition)usanifishaji (standardization)uthabiti/utangamano (stability)sarufi (grammar)leksimu (lexicon) msamiatifonolojia (phonology)
(i)DHIMADhima ndicho kigezo muhimu sana katika diglosia. Ferguson asema kuwa huwakuna vibadala viwili vya lugha hiyo moja, ambapo moja huwa ni lahaja ya Juu (J)na nyingine ni lahaja ya Chini (CH). Katika Kiarabu, J ni lugha kielelezo ya kale(Classical Arabic) ambayo ndiyo iliyotumiwa katika Korani, na CH hutumiwakatika miktadha isiyo rasmi na ya kujiburudisha. Hapa kuna mifano:
79
Hali/Miktadha na uteuzi wa (J) au (CH) katika diglosia
Hali J CH-Mahubiri kanisani au msikitini + _-Maagizo kwa watumishi, wahudumuhotelini, wafanyakazi, makarani _ +-Barua (ya kirafiki) - +-Hotuba bungeni + _-Mhadhara katika Chuo Kikuu + _-Mazungumzo kati ya marafiki x-Matangazo ya habari x _Lugha ya magazeti x _
(ii) FAHARIMielekeo ya wazungumzaji katika jamii zenye diglosia ni kwamba J ni bora,yenye madaha, sanifu, na yenye mantiki zaidi. Inaaminiwa kwamba CH ni duni.
(iii) URITHI WA FASIHIKuna fasihi au maandishi mengi katika J ambayo yanafurahiwa na kuvutiwa najumuia lugha hiyo. Aghalabu utamaduni wa fasihi ya J huwa hauna msingi wakekatika jamii ya kisasa. Misingi yake ipo katika wakati uliopita au jumuia lughanyingine (Kifaransa, Kijerumani nk).
(iv) UPATAJI AU UJIFUNZAJI LUGHAKatika diglosia, ujifunzaji wa lugha huwa tofauti kati ya kibadala J na CH. CHitatumiwa kuzungumza na watoto, na pia kati ya watoto wenyewe; hivi kwambawatu watafahamu CH bila juhudi za kimakusudi.
80
J huwa ni lugha ya ziada au ya pili ambayo watu hujifunza baada ya kuifahamuCH. J hufahamika kupitia mafunzo ya shuleni. Hii ina maana kwamba walewanaojifunza J kamwe hawawezi kupata ufasaha kama ule wanaofikia katika CH.Hii ni kwa sababu CH hutumiwa mara kwa mara katika mawasiliano ya kila sikuilhali J hujifunzwa kwa kukariri (memorise) sheria za kisarufi.
(v) USANIFISHAJIJ ndiyo husanifishwa kwa kuwekewa mpangilio kamili. Makamusi, vitabu vyasarufi, miongozo ya matamshi bora, na kwa ujumla vitabu vya matumizi sahihi yaJ huandikwa. Alfabeti na sheria za maendelezo katika J huwekwa.
Huwa hakuna uchunguzi wa kiusomi wa lahaja CH. Hata kuandika katika CHhuwa vigumu kwa sababu hakuna sheria za hijai zilizoimarika, na pia hakunaanayetaka kuandika katika CH.
(vi) UTHABITIDiglosia huwa ni hali iliyo thabiti na inaweza kudumu karne kadhaa. Ili lugha iwena zaidi ya lahaja au kibadala kimoja, sharti pawepo na diglosia katika lughahiyo. Mvutano kati ya J na CH katika diglosia hupungua kwa kiasi pale ambapokunatokezea mfumo wa lugha wa kati, unaochukua baadhi ya sifa za J na Ch. Nikawaida kwa CH kukopa maneno kutoka kwa J; lakini matumizi ya msamiati waCH katika J si jambo la kawaida.
(Viii) SARUFIIngawa J na CH ni maumbo ya lugha hiyo moja, huwa kuna tofauti nyingi kati yasarufi ya J na CH. Sarufi ya CH huwa sahili kuliko sarufi ya J.
(ix) MSAMIATIMsamiati wa J na CH hutumiwa katika lugha zote mbili. Istilahi na msamiati wakiusomi hupatikana tu katika J. Katika CH kuna msamiati unaorejelea vyombo
81
vya nyumbani kama vifaa vya shambani, vyombo vya kupikia/jikoni nk ambavyohavina vingine vinavyolingana navyo katika J.
Sifa ya kuvutia sana katika diglosia ni kuwepo kwa visawe (msamiati pacha)ambapo CH na J kila moja zinachangia neno kwa dhana hiyo moja. Kwa mfano:
children - rasmikids - simo
baba - rasmibuda - simo
Katika jamii zilizo na diglosia, mfumo wa J ndio unaowekwa katika maandishi nawa CH ndio unaotarajiwa kuwa katika mazungumzo ya kila siku.
Swali
Toa mifano ya sifa hizi tulizozitaja za diglosia kulingana na haliya lugha nchini Kenya.
Ferguson alichukulia Diglosia kuwa ni hali thabiti ya lugha ambayo, pamoja nalahaja za kimsingi za lugha hiyo, huwa na kibadala kilicho tofauti, cha hali ya juu,na chenye mpangilio kamili.Kibadala hiki huwa na kusanyiko kubwa la fasihiandishi lililotoka kwa jumuia lugha nyingine au kipindi cha awali cha lugha hiyo.Huwa inafunzwa shuleni na kutumiwa katika maandishi mengi na mazungumzorasmi.Lakini hakitumiwi na kitengo cho chote cha jamii hiyo kwa shughuli za kilasiku.
82
HATIMA YA DIGLOSIAFerguson (1972:248) anaeleza kuwa diglosia huweza kuwa na hatima tatutofauti:(a) itabakia thabiti kwa muda mrefu.(b) katika hali fulani, shinikizo fulani zinaweza kusababisha kumalizika kwake.
Kwa mfano; ongezeko la watu waliosoma, kutanda kwa mawasilianokatika nchi.
Watu wengi wanapoifahamu J na kutumia lugha ya kimaandishi kwa wingi,matokeo yake yanakuwa ni kupungua kwa tofauti za kiisimu kati ya J na CH. Piakukua kwa utaifa kunakoambatana na tamaa ya kuwa na lugha ya taifa kamaishara inayowaunganisha watu huchangia kumalizika kwa diglosia.(c) J itakua na kuwa lugha au lahaja sanifu.
J inaweza kuwa sanifu ikiwa:(i) tayari J ni lugha sanifu katika jumuia nyingine.(ii) ikiwa jamii hiyo yenye diglosia itaungana na jamii hiyo nyingine.
5.7.2 DIGLOSIA KWA MUJIBU WA FISHMANFishman (1967) anaamini kwamba tunahitaji kutofautisha kwa makini dhana zadiglosia na uwili lugha. Anasema kuwa uwili lugha ni swala linaloshughulikiwa nawanasaikolojia na wanaisimunafsia; inarejelea uwezo wa mtu binafsi kutumiazaidi ya vibadala au launi moja ya lugha (language variety launi za lughanamna tofauti za matumizi ya lugha kutegemea mazingira, wakati, muktadha,nk, k.v. lahaja, rejesta, nk). Diglosia hushughulikiwa na wanaelimujamii nawanaisimujamii kulingana na dhima zake.
Fishman alibadilisha mapendekezo ya Ferguson kwa namna mbili:1. Fishman hasisitizi sana umuhimu wa hali zilizo na vibadala viwili tu vya
lugha. Anaruhusu kuwepo kwa misimbo mingi tofauti inayowezakugawika katika makundi mawili: Juu na Chini.
83
2. Huku Ferguson (1972) akiona kuwa diglosia inachukua mstari wa kati wakiisimu (anasisitiza kwamba diglosia huwa na tofauti nyingi kuliko ilivyokati ya mitindo, na chache kuliko ilivyo baina ya lugha tofauti), Fishmananalegeza mipaka hiyo. Anaona kuwa diglosia haipo tu katika jamuiazenye ulumbi ambazo kirasmi zinatambua lugha mbalimbali, na pia sikatika jumuia zinazotumia lugha wenyeji (vernacular) na lugha vielelezo(classical varieties), lakini pia katika jamii zinazotumia lahaja tofauti, sajili,au vibadala vya lugha vyenye dhima tofauti.
Fishman anatumia istilahi diglosia kurejelea kiwango cho chote cha tofauti zakiisimu kuanzia kwenye tofauti ndogo za kimtindo katika lugha moja hadi kwenyematumizi ya lugha mbili tofauti.Jambo muhimu ni kwamba tofauti hizo zakiisimu ziwe zimetambuliwa na kupewa dhima tofauti katika jamii.
Uwili lugha humaanisha kuwa udhibiti wa J na CH unapatikana katika jamii yote.Diglosia hurejelea mgawanyo wa dhima kati ya J na CH.
UHUSIANO KATI YA UWILI LUGHA NA DIGLOSIA
Diglosia________________________________________
+ -
1. Diglosia na 2. Uwili lugha bilauwili lugha diglosia.
Uwili lugha 3. Diglosia bila 4. Hakuna uwili lughauwili lugha wala ulumbi.
1. Diglosia na uwili lugha
84
Katika jumuia lugha kama hiyo karibu kila mtu atafahamu J na CH. Kwa mfano,kule Paraguay, Guarani ni CH na Kihispania ni J. Kihispania ni lugha ya Kihindi-Kizungu na Guarani ni lugha ya wenyeji wa Marekani.
2. Diglosia bila uwili lugha Ili kuwa na hali kama hii, kunahitajika makundi mawili tofauti katika kitengokimoja cha kisiasa, kidini na kiuchumi. Kundi moja linakuwa la watawala nalinazungumza J pekee. Kundi la pili, ambalo ndilo kubwa, halina uwezo katikajamii na huzungumza tu CH. Kwa mfano, barani Afrika, wakoloni walizungumzaKiingereza huku wenyeji wakizungumza lugha zao.
Jumuia za kidiglosia zisizo na uwili lugha si jumuia lugha kwa sababu makundihayo mawili hayaingiliani kwa mawasiliano isipokuwa kwa kiasi kidogo sanakupitia kwa wakalimani au kwa kutumia pijini.
3. Uwili lugha bila diglosia Fishman anasema kuwa hali hii inarejelea jumuia ambazo zina wazungumzajiwengi wenye uwili lugha, lakini hawatengi lugha hizo kwa miktadha au dhimamaalum. Lugha yo yote kati ya hizo inaweza kutumiwa kwa dhima yo yote.Jumuia kama hizo huwa chache.
Uwili lugha bila diglosia hutokana na kuvuja kwa diglosia. Diglosia inayovujainarejelea hali ambazo, kibadala kimoja cha lugha kinavuja na kuchukua dhimazilizokuwa zimetengewa kibadala kingine. Matokeo ya uwili lugha bila diglosia niama kuzuka kwa kibadala kipya ambacho ni mchanganyiko wa J na CH, au mojakuchukua mahali pa nyingine. Kwa mfano, huko Ubelgiji katika eneokunakozungumzwaKijerumani, kuna mabadiliko ambapo watu wengiwanazungumza Kifaransa (J) ingawa mwanzoni walizungumza Kijerumani (CH).
85
4. Hakuna Uwili lugha wala diglosia
Hali hii inahitaji kundi ndogo lililojitenga linalozingatia usawa. Lazima pawepo nalugha moja tu na hakuna tofauti za majukumu zitakazopelekea kuwepo hatatofauti za kimtindo katika maongezi.
5.8 TRIGLOSIARuwaza ya matumizi ya lugha nchini Tanzania ni ile iitwayo triglosia Mekacha(1993). Hii ni hali ambapo watu wengi wanatumia lugha tatu tofauti kutegemeamuktadha. Kiingereza kinatumiwa katika shughuli za Kimataifa, kisayansi nakiteknolojia. Kiswahili kinatumiwa katika shughuli za kiserikali, mahakamani, nakatika utawala.Hii ndiyo lugha inayozungumzwa na watu wote. Tatu, kunalugha wenyeji. Hizi hutumiwa ili kuendeleza mahitaji ya makundi madogomadogo.Zoezi
Onyesha jinsi diglosia inavyodhihirika katika matumizi yako ya lughakatika miktadha mbalimbali
Swali
Diglosia inahusiana na uwili-lugha . Jadili kauli hii.
5.9 KUBADILI MSIMBOTunaweza kueleza kuwa kubadili msimbo ni kutumia lugha mbili au zaidi kwenyematini moja wakati wa mawasiliano. Hata hivyo fasiri hii ni pana mno. Kachru(1977:107) anaeleza kubadili msimbo kuwa ni kuchagua kutumia msimbo fulaniau ule mwingine kutegemea hali ilivyo. Yeye anatofautisha
dhana hii nakuchanganya msimbo (code mixing), anayoeleza kuwa ni kuhamisha vipashiovikubwa vya lugha kutoka kwa msimbo mmoja hadi mwingine. Katika kozi hiihatujaribu kutofautisha kati ya kubadili msimbo na kuchanganya msimbo.
86
Haugen (1956) anasema kuwa kubadili msimbo ni hali ambapo mwana uwililugha anaingiza neno ambalo halijatoholewa katika lugha yake kutoka kwanyingine.
Myers-Scotton (1998) anaeleza kuwa kubadili msimbo ni matumizi ya lugha mbiliau zaidi katika mazungumzo, bila kutohoa kifonolojia lugha moja ili iingiliane nanyingine.
Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha (1991) inaaeleza kuwa kubadili msimbo nikutumia aina mbili tofauti za misimbo kwenye matini moja wakati wamawasiliano.
Katika hali ya kawaida wazungumzaji wa lugha hutumia sarufi na msamiati walugha moja wanapozungumza. Dhana ya kubadili msimbo ni dhanainayochunguzwa na wanaisimu jamii na wanaisimu nafsia. Kuna uhusiano wamoja kwa moja kati ya uteuzi wa lugha na muktadha wa kijamii. Katikaisimujamii wachunguzi wanaangalia ni kwa nini mtu anabadilisha msimbo; mtuhuyo yuko katika hali gani? Katika kiwango cha isimunafsia kunachunguzwa uleuwezo unaomfanya mtu kubadili msimbo.
Baadhi ya watu wanachukulia kubadili msimbo kama ishara ya kuoza kwa uleuwezo wa kiisimu. Wanaona kwamba kubadili msimbo ni matokeo ya kutojualugha moja vilivyo. Kiisimu, hatuwezi kusema hivyo, kwa sababu kule kubadilimsimbo ni sifa muhimu katika usemi wo wote unaohusu uwili lugha.Kwa mfano1.Nilitaka kwenda kaw ofisi ya Foreign Affairs.
Kubadili msimbo ni mbinu ya kimazungumzo inayotumiwa (a) kuipa nguvu amri(b) kuchochea hisia (c) kuifanya kauli iwe na ukali (d) kusisitiza.
87
Uchunguzi wa kubadili msimbo uliofanywa ulionyesha kuwa: Kubadili msimbo katika jamii zenye uwili lugha kuna maana. Kunatekeleza
jukumu fulani katika mazungumzo. Uteuzi wa lugha wa mzungumzaji huhusu kujaribu kujitambulisha na wenzake
kijamii.Zoezi
Andika sentensi kumi zinazoonyesha namna watu wanavyobadili msimbo nazingine kumi zinazoonyesha kuchanganya msimbo.
Swali
Wazungumzaji hubadili misimbo na kuchanganya misimbo kwa sababufulani bali siyo ishara ya kutomilisi kikamilifu mojawapo ya lughazinazohusika.Tathmini kauli hii.
5.10 UTOWEKAJI WA LUGHASifa muhimu inayopatikana katika jamii zilizo na uwili lugha ni mabadiliko. Ninadra kupata hali ambapo lugha hizo mbili zinadumu zikiwa katika hali yakulingana. Ikiwa lugha ya hadhi ya chini inaweza kuendelea kuwepo licha yashinikizo na athari kutoka kwa lugha zenye nguvu, basi tunaiita hali hiyoudumishaji lugha (language maintenance). Kinyume na hali hiyo utakuta lughaduni zinasalimu amri na wazungumzaji wake wanamezwa na utamaduni wenyenguvu. Hali hii huitwa ugeuzaji lugha (language shift). Ugeuzaji lugha ni dhanainayotumiwa kurejelea hali ambapo lugha moja inachukua nafasi ya nyinginekama chombo muhimu cha mawasiliano na ujamiishaji katika jumuia.
Mambo mengine yanayoweza kutokea lugha zinapoingiliana ni kama ukopaji wamsamiati kati ya lugha hizo.Pia kunaweza kutokea lugha ya kati ambayo
88
aghalabu huwa pijini au krioli. Mwisho kunaweza kutokea kifo cha lugha(language death).
5.10.1 KUFA KWA LUGHALugha inaweza kufa polepole. Hii ina maana kwamba lugha moja itachukuanafasi ya nyingine polepole.
Lugha inaweza kufa ghafla. Inapofanyika hivi huwa hakuna kipindi cha uwililugha hapo katikati. Mzungumzaji wa mwisho wa lugha hiyo huwa anajua lughamoja tu. Kwa mfano, Tasmanian.
Pia wazungumzaji wanaweza kuamua kutotumia lugha yao kwa sababuwanaogopa kudhuriwa kisiasa. Katika hali hii lugha inakufa ikiwa nawazungumzaji fasaha. Vile vile wazazi wanaweza kukataa kuwafundisha watotowao lugha hiyo. Kwa mfano, mauaji ya maelfu ya Wahindi huko El Salvadormwaka 1932 yaliwafanya walionusurika kutoongea lugha za Cacaopera na Lencaili wasitambuliwe kuwa Wahindi. Hali kama ile ilyowakumba Wahutu kuleRwanda ni mfano wa njia ambazo zinaweza kuua lugha.
Kloss katika Mesthrie (2000) anazungumzia aina tatu za vifo vya lugha.(a) Lugha itakufa ikiwa wazungumzaji wake wote wamekufa.(b) Lugha hufa kwa sababu ya ugeuzaji lugha.(c) Lugha hufa baada ya juhudi nyingi za kuidunisha. Lugha huteremshwa
hadhi kuwa lahaja wakati jumuia lugha itaacha kuitumia katika maandishina watumie nyingine.
5.10.2 LUGHA HAI AU ILIYOKUFA?Ili tuseme kwamba lugha fulani i hai, lazima pawepo na wazungumzaji asilia walugha hiyo walio hai na wanaoitumia. Katika sehemu nyingi za ulimwengu, si
89
rahisi kuthibitisha kwamba kuna wazungumzaji asilia wa lugha hizo walio hai nawanaozitumia.
Ingawa lugha kama Kilatini, Kiyunani cha kale, na Sanskrit huitwa lughazilizokufa, hali hii si ya kawaida katika isimujamii. Lugha hizi zilibadilika kutokakizazi kimoja hadi kingine, zikawa lahaja na baadaye lugha sanifu.Siku hiziKilatini kipo kama Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiitaliano na Kiromenia. Lughaza Ulaya zilizokufa kabisa ni Gothic, Pictish na Etruscan.
Kiebrania (Hebrew) kilikufa kwa muda lakini kikafufuliwa mwishoni mwa karne ya19 na mwanzoni mwa karne ya 20.
5.10.3 HALI ILIVYOInakisiwa kwamba kuna lugha 6,000 zinazozungumzwa ulimwenguni leo.Thuluthi ya lugha hizi zimo katika hatari ya kufa (Mesthrie 2000). Pia thuluthimoja ya lugha zote ulimwenguni huzungumzwa na watu wasiozidi 1,000.Nilugha kama 600 tu hivi ambazo hazijatishwa na kifo.
Unajuaje kuwa lugha karibu ife? Ukiona wazazi hawawafunzi watoto wao lughayao asilia, na watoto hawataki kuifahamu, basi unajua kuwa lugha hiyo inaelekeakufa.
Katika ripoti ya hivi punde ya Umoja wa Mataifa (UN), 16 kati ya lugha za Kenyaziko katika hatari ya kuangamia. Tayari zingine zimeshakufa Suba, El Molo,Oropom, Lonioti, Yaaku, Sogoo, Kore, Segeju, Omotik na Kinare. Lugha zinginekama Dahalo (pwani), Bongom na Terik, lugha inayofanana na Kiluhya nainayopatikana katikati ya Wamaragoli na Wakalenjin i karibu kufa, (Opala, 2002,Ladefoged (1992) (Tazama ramani inayoonyesha lugha ambazo zinaelekea kufanchini Kenya na Tanzania).
90
Nchini Ethiopia, Ongota ina wazungumzaji 19, na Gafat haina .
5.10.4 KWA NINI HATUTAKI LUGHA IFE?Wanaisimu husema kwamba kila lugha ina upekee wa aina fulani. Lugha hubebautamaduni wa watu, inapokufa na utamaduni huo unapotea.
Pia wamesema kuwa lugha ni hifadhi ya mawazo ya muda mrefu na tajriba zawatu.Humo tunapata methali, misemo, jazanda; na haya yote ni elimu iliyokuzwakwa kipindi kirefu.
Katika miaka ya 1930, Edward Sapir na mwanafunzi wake Benjamin Lee Whorfwalidai kuwa lugha huelekeza fikra zetu. Lugha ndiyo huamua jinsitunavyofikiria. Kwa hivyo tukipoteza lugha tutapoteza namna ya kuiangaliadunia. Kila jamii ina tabia zake za kiakili, na kila jamii ina namna ya kuiangaliadunia.
5.10.5 MAMBO YANAYOSABABISHA KUFA KWA LUGHALugha hufa kutokana na mabadiliko ya kitamaduni na kugeuza lugha kwa sababuya kumezwa na utamaduni na lugha yenye nguvu zaidi. Inasemekana kwambakati ya 1490 1900, nusu ya lugha zote ulimwenguni zilikufa baada ya wazungukuanzisha makoloni katika sehemu nyingi duniani ambako lugha zaozilizungumzwa. Utandaradhi umeleta ubeberu lugha (language imperialism)unaofifisha lugha ndogo.
Maswala ya kiuchumi pia huchangia kufa kwa lugha. Vijana hutoka vijijini nakwenda mijini kutafuta ajira. Huko hawazungumzi lugha zao asilia. Watoto waohawatafahamu lugha hizo asilia. Baada ya kizazi kimoja, kina babu wanapofariki,
91
lugha inakufa. Biashara, kama ile ya utumwa, husababisha kufa kwa lugha asiliana kutokea kwa pijini.
Magonjwa yanaweza kuua watu wote wanaozungumza lugha moja na kufanyalugha hiyo ipotee. Kwa mfano, mwaka 1962, Trumai, iliyozungumzwa katika kijijikimoja kandoni mwa Mto Culuene kule Venezuela, ilipunguziwa wazungumzajihadi 10 kutokana na ugonjwa wa homa kali (influenza).
Sera ya lugha katika nchi inaweza kuathiri baadhi ya lugha. Kule Marekani ,Kijerumani kilikuwa lugha iliyosambaa zaidi kikifuatwa na Kiingereza, wakati wauhuru. Hivi sasa Kiingereza kimechukua nafasi ya kwanza na Kijerumanikinafahamika kama simo.
Mwelekeo hasi katika sera za serikali na jamii kunakotumika lugha hiyohusababisha kufa kwake. (Tazama, Ngugi, P. na Osore,M . 2003).
5.10.5 NAMNA YA KUZUIA LUGHA ZA KIAFRIKA ZISIFE1. Wakati huu wa demokrasia, lugha ichukuliwe kama haki ya kidemokrasia.2. Sera ya lugha ilenge lugha zote nchini.3. Mafunzo katika lugha wenyeji yahimizwe.4. Kifungu cha 9 cha Haki za Kiisimu Duniani kinasema Jumuia lugha zote
zina haki ya kusanifishwa, kuhifadhi, kukuza na kuendeleza lugha zao bilakuingiliwa.
Zeozi
Pendekeza njia zingine zinazoweza kuzuia kufa kwa lugha
92
Swali
Swala la utandarithi limesabisha utowekaji wa lugha nyingi ulimwenguni. Jadili kauli hii.
Hitimisho
Katika somo hili, swala la uwili-lugha na ulumbi limejadiliwa. Tumeonyeshaathari za kiisimu zinazotokana na wanajamii kuongea zaidi ya lugha moja.Tumelijadili pia swala la Diglosia na Triglosia. Mwisho tumeona utowekaji walugha, sababu za kutoweka kwa lugha na jinsi ya kuzuia lugha zisife.
Marejeleo TeuleBloomfied, L. (1933) Language . New York. Holt Rinehart and Winston.Chimera, R. (1999) Kiswahili through The Ages: The Question of Lexicon
Makala Yaliyowasilishwa katika Idara ya Kiswahili, 8 Agosti, Chuo Kikuucha Egerton, Njoro.
Denison, N. (1977) Language death or Language Suicide . International Journalof the Sociology of Language.
Fasold, R.W. (1997) Motivations and Attitudes influencing Vernacular Literacy:four African Assessments katika Vernacular Literacy : A Re-Evaluation.Oxford. Clarendon Press.
Fergerson, C. (1959) Diglossia. Word 15 .Haney, D. (1995) Linguistic Crisis looms as native tongues die in Daily Nation
93
28, 1995.Haugen, E.. (1956) Bilingualism in the Americas . TUSCOLOOSG. University of
Alabama Press.Kachru, B.B. (1977) Code Switching as a Communicative Strategy in India
Saville-Troike, Murie (wah) Linguistics and Anthropol ogy. Washington.
Georgetown University.Ladefoged, P. (1992) Another View of Endangered Language Language 68 .Mbaabu, I. (1995) Linguistic and Cultural Dependency in Africa in Baragumu ,
Vol. 2 No. 1.Mekacha, R.D.K. (1993) The Sociolinguistic Impact of Kiswahili on Ethnic
Community on Languages in Tanzania. A Case Study of Ekinata.Bayreuth African Studies.
Mesthrie, R. et. al. (2000) Introduction to Sociolinguistics . Edinburg UniversityPress, Edinburgh.
Myers-Scotton, C. (1992) Language in East Africa: Linguistic patterns andPolitical ideologies , in J.A. Fishman(ed) Advances in the Study of Societal Multilingualism.Moton.The Hague .
Ngugi, P. na Osore M. (2003) Linguistic Genocide of the African Languages:Protecting and Empowering . Makala iliyowasilishwa katika Kongamanola LASU Dar es Salaam Tanzania, Agosti 21 24.
Weinreich , U. (1974) Languages in Contact . The Hague. Mouton.
94
SOMO LA SITA
UPANGAJI LUGHA
6.0 UtanguliziKatika somo hili tutazungumzia swala la upangaji lugha kwa kuonyesha jinsililivyoshughulikiwa na wataalamu mbalimbali. Pia tutashughulikia mawandambalimbali ya upangaji lugha, na kuangalia majukumu mbalimbali ya lughakatika uwanda mpana wa upangaji lugha pamoja na mchakato wa upangajilugha. Vile vile tutazingatia swala la lugha Taifa na lugha Rasmi. Pamoja nahayo, tutachunguza sera ya lugha nchini Kenya.
6.1 Madhumuni
Baada ya kulipitia somo hili tunatarajia kwamba utaweza:(i) Kueleza maana ya upangaji lugha.(ii) Kueleza mawanda ya upangaji lugha na majukumu yanayopewa lugha.(iii) Kueleza mchakato wa upangaji lugha, lugha ya Taifa na lugha Rasmi.(iv) Kueleza sera ya lugha nchini.
6.2 UPANGAJI LUGHAKupanga ni tendo la kibinadamu linalotokana na haja ya kupata suluhisho kwashida fulani. Tendo hili linaweza kuwa (limepangwa na) la kimakusudi au liwelimetokea tu bila mpango kamili. Linaweza kutekelezwa na watu binafsi aulinaweza kuwa rasmi. Mpango wa kijamii ni tendo lililo na mawandayaliyofafanuliwa vyema katika jamii. Ikiwa upangaji umefanywa vema utahusuhatua kama ukusanyaji wa habari ili ukweli ufahamike, kuwa na njia badalia zakutekeleza jambo hilo, kufanya maamuzi, na utekelezaji wake katika njiamahsusi.
95
Utaratibu uliotajwa hapo juu unatumika pia katika Upangaji Lugha (UL). ULhuhitajika pale ambapo kuna matatizo ya lugha. Ikiwa watu wanahisi kwambahali fulani ya kiisimu haifai, basi kuna nafasi ya UL kutekelezwa hapo. Istilahi yaupangaji lugha ilianzishwa na mwanaisimu wa Kimarekani aliyeitwa EinarHaugen katika miaka ya mwisho ya 1950, na inarejelea juhudi zote zakimakusudi zenye lengo la kubadilisha tabia za kiisimu za jumuialugha. Inajumlisha mambo yote kuanzia kupendekezwa kwa nenojipya hadi kupendekezwa kwa lugha mpya.
Wakati mwingine istilahi ya sera ya lugha imetumiwa kama kisawe chaupangaji lugha. Hata hivyo, sera ya lugha hurejelea malengo ya kijumla yakiisimu, kisiasa na kijamii ambayo ndiyo msingi wa mchakato wa upangaji lugha.
Upangaji lugha ni tukio ambalo limesambaa na limetekelezwa kwa mudamrefu.Hata hivyo ni katika miaka ya sitini (1960 s), ambapo nchi nyingi za Afrikana Asia zilizokuwa zimejinyakulia uhuru zilikumbana na swala la uchaguzi nautekelezaji wa lugha ya taifa.Hapa ndipo swala la sera na upangaji wa lughalimejitokeza kama eneo la uchunguzi katika isimujamii.
6.2.1. UPANGAJI LUGHA NI NINI?Hapa kuna maelezo ya istilahi hii kutoka kwa wataalamu mbalimbali.
Rubin (1972), katika Can Language be Planned?, anaeleza kuwa hii ni mbinu yakuchunguza mabadiliko na matumizi ya lugha ili kuweza kufanya ubashiri kuhusujinsi ya kutekeleza mabadiliko hayo. Upangaji wa lugha unamaanishamaendeleo, utekelezaji na utathmini wa mbinu maalumu za kutatua matatizomahsusi ya lugha.
96
Haugen (1972), anasema , upangaji lugha ni shughuli ya kutayarisha othografia,sarufi, na makamusi ili kuwaongoza wazungumzaji na waandishi katika jamiiyenye lugha nyingi. Kwa kweli haya ni matokeo ya UL.Kwa hivyo UL niutathmini wa mabadiliko ya lugha.
Das Gupta (1971) alieleza kuwa UL huchukulia lugha kama amali na nyenzo yakijamii inayoweza kufanyiwa mabadiliko na inayohitaji hatua zilizopangwa kupitiakwa juhudi za pamoja za mamlaka za kisiasa, kielimu, kiuchumi na kiisimu.
Moshe Nahir (1977) anapendekeza kwamba upangaji lugha uangaliwe kama uliona majukumu matano bainifu ambayo yamejikita katika shughuli ambazowapanga lugha hujihusisha nayo. Majukumu hayo ni:(a) Uchujaji au utakasaji au usahihishaji lugha (Language purification)
Kuelekeza matumizi sahihi na kuhifadhi usafi wa lugha.(b) Ufufuaji Lugha
Huu ni ufufuaji wa lugha ya kale katika hadhi yake ya zamani au ufufuajiwa lugha iliyokufa, kwa mfano, ufufuaji wa Kiebrania.
(c) Ugeuzaji au Urekebishaji Lugha (Language Reform)Kuwezesha matumizi ya lugha kupitia kwa usahihishaji au urahisishaji wamsamiati na tahajia.(d) Usanifishaji wa Lugha (Standardization)
Kuhakikisha kwamba lugha moja au lahaja moja katika eneo au taifafulani imekubaliwa kama lugha kuu ya eneo au taifa hilo katika matumiziya jumla. Kwa mfano:Tanzania - KiswahiliEthiopia - Kiamharic
(e) Uingizaji usasa katika msamiati (Lexicomodernization)Kuziba pengo kati ya msamiati wa lugha na istilahi mpya zinazotokana nateknolojia ya kisasa.
97
Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha (1991) inasema kuwa upangaji lugha nijitihada za kuweka sera mbalimbali za lugha ambazo husaidia kutatua tatizo lamawasiliano katika jamii, kwa kuchunguza lugha na lahaja zilizopo ili kuteuazinazofaa kutumika.
Upangaji lugha ni sehemu ya sera ya lugha. Hii inamaanisha kwamba serikalifulani huchukua sera fulani kuhusiana na lugha zinazozungumzwa katika jamiifulani na ikatekeleza sera hiyo kwa njia ya upangaji lugha. Hali yo yote yaupangaji lugha itafanywa kwa kuzingatia sera ya lugha, na jambo hililitadhihirisha wazi sera za kijumla za serikali.
Zoezi
Kwa kuzingatia mtazamo wa Nihir, onyesha jinsi ambavyo lugha ya Kiswahiliimeshughulikiwa.
6.3 MAWANDA YA UPANGAJI LUGHAKloss (1969) alibainisha aina mbili za kimsingi za upangaji lugha:(a) Upangaji lugha kiukongoo (corpus planning)(b) Upangaji lugha kihadhi (status planning)
(a) Upangaji lugha kiukongooKongoo ni kusanyikoo la data za semi zilizoandikwa au kunukuliwa ambazohutumiwa kama kianzio cha ufafanuzi wa kiisimu.
Upangaji lugha kiukongoo unahusika na muundo wa ndani wa lugha. Mamboyanayozingatiwa hapa ni pamoja na kuunda othografia kwa lugha ambazo badohazijaandikwa, kuanzisha mabadiliko katika tahajia, kubuni maneno mapya nakuchapisha vitabu vya sarufi. Jambo la kimsingi katika upangaji lugha kiukongoo
98
(na pia upangaji lugha) ni usanifishaji wa lugha. Huu hueleweka kuwa niuanzishaji na uendelezaji wa kaida za kiisimu zilizo sare.
(b) Upangaji lugha kihadhiUpangaji huu hurejelea utoaji wa dhima mpya kwa lugha (kama vile kuitumialugha hiyo kufunzia shuleni au kama lugha rasmi). Jambo hili huathiri dhima yalugha katika jamii. Kwa mfano, uamuzi wa kutumia Kiebrania kama lugha yamafunzo katika shule za Wayahudi huko Palestine kuanzia mwishoni mwa karneya 19, ni mfano wa upangaji lugha kihadhi. Kabla ya hapo, Kiebrania hakikuwakinatumiwa katika mawasiliano ya kila siku ila katika maombi na maandishi yakidini na kiusomi.Uanzishaji wa shule zinazotumia Kiebrania ulijenga hali yakufufua Kiebrania kama lugha ya mawasiliano ya kila siku. Hadhi ya Kiswahilinchini Kenya pia imeinuliwa katika ngazi mbalimbali.
Wapangaji lugha hutofautisha majukumu mengi ambayo lugha huwezakutekeleza katika jamii. Haya ni:1. Lugha rasmi - hutumiwa katika miktadha ya kitaifa na inaunganisha watu
kisiasa na kitamaduni. Aghalabu hadhi hii huwa imetangazwa kwenyekatiba.
2. Lugha rasmi ya mkoa au jimbo matumizi ya lugha kama lugha rasmi yaeneo au jimbo fulani. Kazi ya lugha hii hutengewa mkoa si nchi nzima.Kwa mfano, katika mkoa wa Canada unaoitwa Quebec, Kifaransa ndiyolugha rasmi tangu mwaka 1974, ilhali Kiingereza na Kifaransa hutumikakama lugha rasmi katika mikoa mingine yote.
3. Mawasiliano mapanamatumizi ya lugha kama chombo cha mawasilianokinachovuka mipaka ya lugha mbalimbali katika nchi moja. Hii ni kamalingua franka. Kwa mfano, Kiswahili nchini Kenya na Tanzania, Kihindi naKiingereza nchini India.
99
4. Lugha ya kimataifa - matumizi ya lugha kama chombo kikuu chamawasiliano katika uwanja wa kimataifa; kama vile katika itifaki, utalii nabiashara. Kwa mfano, lugha ya Kiingereza ina dhima hiyo leo.
5. Lugha ya kikundi - matumizi ya lugha kama chombo cha mawasiliano kwawatu wa kundi moja au kabila moja.
6. Elimu - matumizi ya lugha kama chombo cha kufunzia shuleni.7. Dini - kuitumia lugha fulani katika matambiko ya dini fulani. Kwa mfano:Kiislamu - Kiarabu
Judaism - Kiebrania8. Vyombo vya habari- lugha inayotumiwa kwenye televisheni, redio na
magazeti.9. Kazini - matumizi ya lugha kama chombo cha mawasiliano kazini.10. Fasihi - lugha ya kiusomi.
Hata ingawa wapangaji lugha hutenga upangaji lugha kikongoo na upangajilugha kihadhi, ni muhimu kuelewa kuwa zote mbili zinahusiana sana. Kutolewakwa dhima mpya kwa lugha fulani huhitaji mabadiliko katika mfumo wa kiisimuwa lugha hiyo.
Hivi majuzi aina nyingine mbili za upangaji lugha zimejitokeza, nazo ni:
(a) Upangaji lugha kifahari (prestige planning)Upangaji lugha kifahari hulenga katika kutoa mielekeo chanya ya kisaikolojiaambayo ni muhimu ikiwa kutakuwepo na ufanisi wa muda mrefu katika upangajilugha. (Fahari kuu ambayo Kiebrania kilikuwa nayo kama lugha ya kidiniilisababisha kutokuwepo na haja ya kuwa na upangaji kifahari). Upangajikifahari huwa muhimu pale ambapo lugha ambayo imeteuliwa ilikuwa ya hadhiya chini (kama ilivyo katika diglosia). Ili watu wakubali hadhi ya lugha hiyoiliyotwazwa, kuna haja ya kuboresha na kuendeleza ufahari wa lugha hiyo.Hivyo basi, upangaji kifahari aghalabu hutangulia upangaji kihadhi.
100
(b) Upangaji lugha Kiurithi (acquisition planning)Hizi ni juhudi za kusambaza na kuendeleza ujifunzaji wa lugha. Hapa tunaonataasisi za kitamaduni zinazosambaza na kuendeleza lugha mbalimbali. Kwamfano, British Council na Taasisi ya Goethe ziliundwa na kufadhiliwa na serikalizao ili kusaidia ujifunzaji wa Kiingereza na Kijerumani kama lugha ya pili katikanchi nyingine. Pamoja na taasisi kuna zingine kama vile French Cultural Centre,Japanese Cultural Centre n.k. Taasisi hizi hutoa mafunzo ya mara kwa mara kwawalimu wanaofundisha lugha hizi.Swali
Kwa kurejelea lugha mbalimbali za Kenya, onyesha jinsi ambavyomawanda ya Upangaji lugha yameshughulikiwa.
6.4 MCHAKATO WA UPANGAJI LUGHAHaugen (1966, 1972, 1987) alisema kuwa mchakato wa upangaji lugha unazohatua nne ambazo zinaweza (ingawa si lazima) kufuatana. Hatua hizo ni:
1. Uteuzi (selection)2. Ukuzaji msimbo (codification)3. Utekelezaji (implementation)4. Upanuzi (elaboration)
(i) UteuziUpangaji lugha huanza kukiwepo na uwezekano wa kuchagua moja kati yavibadala vingi vya kiisimu.Uteuzi huu utatokea baada ya watu kutambuakwamba kuna shida fulani ya kiisimu.Basi lahaja au lugha moja kati ya zilezinazotumika huchaguliwa kuwa msingi wa usanifishaji. Uteuzi ni ule uchaguziwa lugha au lahaja ili ipewe dhima fulani katika jamii, kwa mfano, iwe rasmi, yakufunzia, ya dini, n.k. Hii ina maana kwamba lugha au lahaja ya fahari zaidi
101
ndiyo inayochaguliwa. Uchaguzi unazingatia umuhimu wa lahaja hiyo kijamii,kisiasa, kibiashara, kielimu nk. Kwa mfano, katika lugha ya Kiswahili:
Kiunguja - kibiasharaKiamu - kiusomiKimvita - kiusomi na kijamii
Kiunguja kilichaguliwa. Pia katika mwaka 1974 (Julai 4), Kenyatta alipotangazaKiswahili kiwe lugha ya taifa, hii inamaanisha kwamba Kiswahili kilichaguliwakutoka kwa lugha nyingi zinazozungumzwa humu nchini..
Uteuzi huu unaweza kutanguliwa na mijadala mikali kati ya watu hadi palewanapokubaliana, au unaweza ukaamuliwa na viongozi siku moja tu kama vileAtaturk alivyobadilisha hijai ya Kituruki kutoka kwa ile ya Kiarabu hadi kwa ile yaKiroma. Uteuzi hutekelezwa na jamii, kupitia kwa viongozi wake. Wanaohusikakatika uteuzi huu si tu taasisi za serikali bali pia watu binafsi, vikundi kamamakanisa, vyama vya kisiasa, mikoa na nchi yote.
Lahaja au lugha fulani inapochaguliwa inapendelea watu wanaoizungumza kwaniinawapa fahari na hawapotezi muda kujifunza. Uteuzi mbaya unawezakusababisha mgawanyiko katika nchi.
Wakati mwingine wapangaji lugha huunganisha lahaja mbalimbali. Kwa mfano,usanifishaji wa Basque, lugha inayozungumzwa kusini magharibi mwa Ufaransana kaskazini magharibi mwa Uhispania. Basque sanifu iliundwa miaka ya 1960kwa kuweka pamoja lahaja zake zote nne.
(ii) Ukuzaji MsimboSehemu hii hutekelezwa na wanaisimu au wataalamu wa lugha. Lahajailiyoteuliwa huwekewa kanuni au taratibu za matumizi. Huku ni kukuza mfumowa lugha hiyo k.v. fonolojia (othografia na matamshi), sarufi, msamiati namaana.
102
Ukuzaji msimbo ni uundaji wa kiwangogezi (norm or standard) cha kiisimu kwamsimbo fulani wa kiisimu. Shughuli hii hufanywa kupitia kwa hatua tatu:
(a) Kukuza mfumo wa maandishi (graphisation)(b) usarufishaji (grammatication)(c) uleksikishaji (lexicalisation)Kukuza mfumo wa maandishi Ikiwa lugha inayohusika ilikuwa ya kimazungumzo tu basi inatayarishiwa mfumowa maandishi. Wakati mwingine kinachofanyika ni kwamba wataalamuwanakopa mfumo wa kimaandishi wa lugha nyingine. Wataalamu wanaamuamfumo wa maandishi utakaoifaa lugha hiyo. Ni ule wenye msingi wa sauti(vokali na konsonanti), silabi au maneno? Kwa mfano lugha ya Kiswahili kwanzailiandikwa kwa herufi za kiarabu kabla ya kutumia zile za Kirumi.
Usarufishaji Hii ni sehemu nyingine ya mchakato wa upangaji lugha. Inahusu kuunda kanuniza kisarufi. Wanaamua maumbo na miundo ambayo itakuwa sanifu. Hali hiihupunguza vibadala au tofauti katika matumizi ya kisarufi.Vitabu vya sarufihutayarishwa.
Uleksikishaji Hurejelea uchaguzi na utayarishaji wa msamiati unaofaa. Kimsingi, hatua hiiinahusu kuamua maneno fulani yatumiwe katika mitindo ipi. Mara nyingiuleksikishaji hushughulikia uondoaji wa maneno yenye asili ya kigeni kutoka kwalugha. Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati Kihindi kilisanifishwa huko India, ambapomaneno mengi ya mkopo kutoka Uajemi, Uingereza na nchi nyinginezoyaliondolewa na maneno ya Sanskrit yakatumiwa. Makamusi ya lugha hiyohutayarishwa.
103
Matokeo ya ukuzaji mfumo huwa othografia mpya, sarufi na makamusi ambayoni elekezi.
Kuhusu lugha ya Kiswahili, ukuzaji mfumo ulitekelezwa na kamati ya Lugha(Kiswahili) ya Afrika Mashariki kwa niaba ya serikali za Afrika Mashariki.
(iii)Utekelezaji.Utekelezaji unahusisha shughuli za waandishi, taasisi, na serikali katika kuitumiana kuisambaza lugha ambayo imeteuliwa na kukuziwa msimbo. Hili linafanyikakwa kutoa au kuchapisha vitabu, majarida, magazeti, na makala katika lughahiyo iliyokuziwa msimbo. Wenye mamlaka huhakikisha kwamba lugha hiiinatumiwa pia kwenye vyombo vya habari kama kwenye redio, televisheni namagazeti.
Huku wanaisimu wakihusika sana na sehemu ya ukuzaji msimbo, sehemu hii yautekelezaji hushughulikiwa na dola.
Inabidi kuwepo na mbinu za kibiashara za kusambaza lugha hii. Waandishiwanaochapisha vitabu kwa lahaja hii sanifu wanatuzwa, wafanyakazi serikaliniwanaoifahamu lahaja hii sanifu wanapandishwa vyeo kazini, na lugha au lahajahii inatangazwa sana. Wakati mwingine kunawekwa sheria ambazo zinahimizamatumizi yake.
Lugha hii inahitaji kupata ukubalifu katika jamii. Ikiwa itakubalika itawaunganishawatu wanaozungumza lugha tofauti.
Kuhusu Kiswahili, Kamati ya Lugha (Kiswahili) ya Afrika Mashariki iliandaamashindano ya kuandika insha na vitabu katika Kiswahili sanifu na washindiwalituzwa. Pia kumekuwepo na tume mbalimbali za elimu ambazozimependekeza sera mbalimbali za lugha.Mfano ni tume ya Mackey(1981)
104
iliyopendekeza kuanzishwa kwa mfumo wa 8-4-4. Katika mfumo huu wa elimu,Kiwahili ni somo la lazima katika shule za msingi na sekondari na linatahiniwa.
(iv)UpanuziHii inarejelea ukuzaji wa istilahi na mitindo ili lugha iliyokuziwa msimbo itimizemahitaji ya kisasa ya mawasiliano katika ulimwengu unaoendelea kasi kisayansina kiteknolojia. Huku ni kuendelea tu na utekelezaji wa kiwangogezi ili kutimizadhima za lugha katika ulimwengu wa kisasa. Sehemu muhimu ya upanuzi lughani hiyo ya kuunda na kusambaza istilahi mpya, na kuhakikisha kuwa kuna mbinumbalimbali za kuundia msamiati. Hali kama hii inatokea katika lugha ya Kihausakule Afrika Magharibi chenye takriban wazungumzaji milioni 50.Kihausakinatumia mbinu tatu za kuufanya msamiati wake kuwa wa kisasa:(a) Ukopaji (kutoka kwa Kiarabu na Kiingereza)(b) Kupanua maana ya istilahi(c) Kubuni maneno mapya
Upanuzi wa lugha huendelea kila wakati. Hii ni kwa sababu lugha inahitajikujengwa upya kila siku kwani kuna dhana na vyombo vipya vinavyojitokeza kilasiku. Kuna haja ya kuwa na taasisi za kushughulikia upanuzi wa msamiati.Kuanzishwa kwa taasisi ya Kiswahili katika chuo kikuu cha Kenyatta mwaka wa2003 ni hatua nzuri katika kuliendeleza jambo hili.
Kwa mujibu wa Haugen (1987), ukuzaji msimbo na upanuzi ni sehemu yaupangaji lugha kiukongoo, ilhali uteuzi na utekelezaji ni sehemu ya upangajilugha kihadhi (pia kifahari na kiurithi). Kielelezo hiki cha upangaji lugha chaHaugen ni cha kiduara kwani upangaji lugha kihadhi unaweza kutokana naupangaji lugha kiukongoo. Upangaji kiukongoo ukifaulu au ufeli, utaathiriupangaji lugha kihadhi.
105
Zoezi
Kwa kurejelea mapendekezo ya Haugen (1972) ya mchakato wa upangajilugha, fafanua hatua nne za kufuata katika kupanga lugha.
6.5 Lugha ya Taifa na lugha Rasmi(Rejelea somo la 5.5 kuhusu mada hizi mbili).
6.6 SERA YA LUGHA NCHINI KENYA
Katika AKS 102: Historical Development of Kiswahili , Onyango (2002)amefafanua swala la sera ya lugha nchini Kenya hasa baada ya Uhuru. (Rejeleakazi hiyo)
Baada ya Uhuru, sera ya lugha nchini Kenya iliongozwa na mapendekezo yatume zilizoteuliwa kuchunguza maswala yanayohusu Kiswahili. Pia sera hiyoilitokana na maagizo ya watu mashuhuri. Onyango ameshughulikia matumizi yaKiswahili katika elimu, shughuli za serikali na vyombo vya habari.
6.6.1 ELIMUTume mbalimbali ziliundwa ili kutoa mapendekezo kuhusu matumizi ya lughashuleni na vyuoni. Tume hizo ni kama zifuatazo:
(a) Tume ya Ominde (1964)The Kenya Education Commission Report
Tume hii ilitoa mapendekezo yafuatayo:(i) Lugha ya kufundishia shuleni iendelee kuwa Kiingereza.(ii) Kiswahili kiwe somo la kufundishwa shuleni bila kutahiniwa.(iii) Idara ya Kiswahili ianzishwe katika Chuo Kikuu cha Nairobi.
106
(iv) Mafunzo ya Kiswahili kwa walimu wa shule za msingi yaendeshwe wakatiwa likizo.(Ominde 1964, Chimera 2000).
Mambo yafuatayo yalitekelezwa:(i) Kozi za kuwapandisha walimu vyeo zilianzishwa katika Chuo Kikuu Kishiriki
cha Kenyatta kuanzia mwaka wa 1978.(ii) Idara ya Isimu na lugha za Kiafrika ilianzishwa katika Chuo Kikuu cha
Nairobi mwaka wa 1969 ambapo Kiswahili kilianza kufundishwa.
(b) Tume ya Wamalwa (1972)“The Training Review Committee”
Tume hii ilitoa mapendekezo yafuatayo:(i) Lugha za Kimataifa kama vile Kifaransa na Kijerumani zifundishwe.(ii) Kozi za Kiswahili zianzishwe katika Taasisi ya utwala ya Kenya (Kenya
Institute of Administration) na Taasisi ya kutoa mafunzo kwa watumishiwa serikali (Government Training Institute). Hii ni kwa sababu kulikuwana watumishi wengi wa umma, wakiwemo wakuu wa wilaya ambaohawakuweza kuwasiliana kwa lugha ya taifa.
Mambo yafuatayo yalitekelezwa:(i) Kozi za lugha za kigeni zilianzishwa katika Chuo Kikuu cha Nairobi na ChuoKikuu cha Kenyatta.(ii) Vyuo vingi vya kutoa shahada za diploma nchini vilianza kufundisha lughaza kigeni.
(c) Tume ya Gachathi (1976)The National Committee on EducationObjectives and Policies”
107
Tume hii ilitoa mapendekezo yafuatayo: (i) Kiswahili kiwe somo la lazima na la kutahiniwa katika shule za msingi, za
upili na vyuo vikuu.(ii) Kiingereza kifundishwe kama somo kuanzia darasa la kwanza kisha kiwe
lugha ya kufundishia kuanzia darasa la nne.(iii) Lugha za kienyeji zitumiwe kufundishia kuanzia darasa la kwanza hadi la
tatu.(iv) Walimu wengi wa Kiswahili wapewe mafunzo.
(v) Elimu ya ngumbaro iendeshwe kwa lugha za kienyeji.Yaliyotekelezwa:
Pendekezo la (i) na la (iv) yalianza kutekelezwa tu baada ya Tume ya Mackaykuanzisha mfumo wa elimu wa 8-4-4. Pendekezo la (iii), na la (iv),hayakutekelezwa kikamilifu kwa sababu haikuwezekana kuchapisha vitabu katikalugha zote za kienyeji ambazo ni zaidi ya 40, wala watu wa kuviandika vitabuhivyo hawakuwepo. Pia haikuwezekana kutoa mafunzo kwa walimu wakufundisha lugha hizo zote.
(d) Tume ya Mackay (1981)Report of the Presidential Working Party on the Establishment of the
Second University in KenyaTume hii ilipendekeza yafuatayo:
(i) Mfumo wa elimu wa 7-4-2-3 ubadilishwe na kuwa 8-4-4.(ii) Chuo Kikuu cha pili kianzishwe na Kiswahili kifunzwe chuoni humo
kama somo la lazima. Hii ni kwa sababu kulikuwa na wanafunzi wengiwaliofuzu kutoka chuoni lakini hawakuweza kujieleza kwa ufasahakatika lugha ya taifa.
108
Mambo yafuatayo yalitekelezwa: (i) Mfumo wa elimu wa 8-4-4 ulianzishwa mwaka wa 1982 ambapo Kiswahilikilianza kuwa somo la lazima na la kutahiniwa katika mtihani wa darasa la nane(K.C.P.E 1985) na kidato cha nne (K.C.S.E 1989).(ii) Chuo Kikuu cha Moi kilianzishwa pamoja na Idara ya Kiswahili mwaka
1987.(iii) Wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu vya kitaifa walianza
kufunzwa vipengele vya Kiswahili kama sehemu ya kozi ya lazima yamawasiliano.
Hii ndiyo tume pekee yake ambayo inaonyesha kuwa na ajenda bora kuhusulugha ya Kiswahili kama lugha katika elimu. Kutokana na Tume hii tumeonaufanifu katika utekelezaji wa mapendekezo yake.Kule kukifanya Kiswahilikutahiniwa katika darasa la nane na vile vile kukifanya kuwa somo la lazimakatika shule za Sekondari imetoa mwelekeo mpya kwa wakenya, hasa vijanaambao ni washiriki maalumu katika lugha hii, Chimerah (2000).
(e) Tume ya Kamunge (1988)Report of the Presidential Working Party on Education and ManpowerTraining for the next decade and beyond
Uchunguzi uliofanywa na tume hiyo ulionyesha kwamba usajilishaji wa wanafunziwa gumbaro ulianza kupungua baada ya kufikia kilele mwaka wa 1978. Hii nikwa sababu vitabu mwafaka vya kusomwa katika baadhi ya lugha za kienyejihavikuwepo. Kwa hivyo ilipendekezwa kwamba vitabu hivyo viandikwe katikalugha mbalimbali.Lakini kama Mbaabu (1991b) anavyosema, ingefaa zaidikama vitabu hivyo vingeandikwa kwa Kiswahili ambayo ni lugha ya taifa.
109
(f) Tume ya Koech (1999)Yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyopendekezwa :
(i) Mfumo wa elimu wa 8-4-4 ubadilishwe na kuitwa TIQET (TotallyIntegrated Quality Education and Training) ambapo mtihani wa C.P.E.utafanywa katika darasa la saba na mtihani wa G.C.S.E. utafanywa katikakidato cha nne.
(ii) Lugha ya Kiswahili, Kiingereza na hesabu yawe masomo ya lazima katikashule za msingi na za upili.
(iii) Lugha ya Kiswahili na somo la fasihi yafundishwe kama masomo mawilitofauti. Kadhalika lugha ya Kiingereza na fasihi ya Kiingereza yafundishwekama masomo mawili tofauti.
(iv) Wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu waruhusiwe kujifunza kwalugha zao za kwanza (lugha ya mama) kwa sababu wengi wao hawawezikuwasiliana kwa Kiingereza. Lakini wale wanaosomea mjini watumieKiswahili.
(v) Masomo ya kitendaji (practical subjects) yafundishwe katika shule zamsingi lakini yasitahiniwe kwa sababu yanapoteza wakati na tenayanawavunja moyo wanafunzi, wazazi na walimu.
(vi) Katika mtihani wa C.P.E., masomo matano pekee yatahiniwe badala yamasomo saba yanayotahiniwa katika K.C.P.E.(vii) Katika mtihani wa G.C.S.E., kiwango cha chini cha masomo
yatakayotahiniwa ni masomo saba lakini alama zitolewe katika masomosita ambayo mwanafunzi atafanya vyema zaidi.
(viii) Mtihani wa kidato cha nne (G.C.S.E) ufanywe mara mbili kwa mwakaambapo wanafunzi wanaofeli mara ya kwanza wanaweza kuruhusiwakuufanya tena mara ya pili.
Baadhi ya mapendekezo hayo tayari yameanza kutekelezwa. Hata hivyo,msimamo wa serikali ni kwamba utekelezaji kamili wa ripoti ya Koech utagharimu
110
pesa nyingi sana, hivyo basi, baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa yatafanyiwamarekebisho kabla ya kutekelezwa.
Swali
Kati ya Tume hizi zote, ni ipi ambayo unaona imechangia sana ukuaji walugha ya Kiswahili? Toa maelezo.
6.6.2. SHUGHULI ZA SERIKALIMatumizi ya Kiswahili kama lugha ya taifa katika shughuli za serikali kwa ujumlayanajitokeza kwa njia zifuatazo:(i) Mawasiliano ya kila siku baina ya wananchi, wanasiasa na maafisa wa
serikali. Kwa mujibu wa King ei (2001:02) moja katika ya sifa za usemiwa kisiasa nchini Kenya ni kubadili na kuchanganya msimbo, na hali hiihutatiza maendeleo ya Kiswahili.
(ii) Bungeni: Ni wabunge wachache sana ambao hutumia Kiswahili katikamijadala,hasai wale wanaotoka Pwani na labda wale wasiokimuduKiingereza vizuri.Kiingereza ndicho hutumiwa kuendesha shughuli zaBungeni.
(iii) Magereza: Kiswahili hutumiwa katika kuendesha shughuli za magerezaingawa stakabadhi nyingi huandikwa kwa Kiingereza.
(iv) Katiba: Hivi sasa katiba ya Kenya yapatikana tu kwa lugha ya Kiingereza.Katiba Rasmi mpya ambayo inajadiliwa sasa imetafsiriwa kutokana namapendekezo ya watu wengi kwamba katiba itafsiriwe ili wananchi wengiwaisome na kuzielewa sheria za nchi hii vilivyo. Pamoja na kuzijua hakizao ili kutimiza lengo hilo la kuwaelimisha wananchi kikatiba, msomi waKiswahili, Prof. Kimani Njogu, amekuwa akichapisha mfululizo wa makalayanayoitwa Zijue Haki zako , katika gazeti la Taifa Leo.Katiba mpyaimependekeza Kiswahili kuwa lugha rsmi pamoja na Kiingereza.
111
(v) Sherehe za Kitaifa : Sherehe muhimu za kitaifa na hotuba zinazosomwakatika sherehe hizo huwa kwa Kiingereza lakini Kiswahili hupewa nafasikatika mazungumzo ya ziada.
(vi) Mikutano: Mikutano ya hadhara ya wanasiasa huendeshwa kwa Kiswahilikatika sehemu nyingi nchini isipokuwa mikutano ya sehemu fulani zavijijini.
(vii) Vituo vya Polisi na kambi za wanajeshi pia hutumia Kiswahili.(viii) Viapo vya watumishi wa serikali huendeshwa kwa Kiswahili. Watumishi
hao ni pamoja na Rais, mawaziri na wasaidizi wao na pia mahakimu.(ix) Baadhi ya vyeti kama vile vitambulisho, vyeti vya kuzaliwa na vya kifo,hati
za kusafiri, fomu mbalimbal za serikali huandikwa kwa Kiingereza naKiswahili pia.
Kwa jumla bado kuna mengi ambayo yanatarajiwa kufanywa kuhusu lugha yaKiswahili. Serikali ya Kenya haijabuni sera dhahiri ya kuendeleza Kiswahili kamalugha ya taifa. Mara nyingi lugha rasmi ya Kiingereza na hata lugha za kikabilahutumiwa katika miktadha ambamo lugha ya taifa (Kiswahili) ingepaswakutumiwa na jambo hili linatatiza maendeleo ya Kiswahili.
6.6.3 VYOMBO VYA HABARIVyombo vya habari vinajumlisha redio, runinga, magazeti, majarida, filamu natarakilishi, yaani kompyuta . Idhaa zinazotangaza kwa Kiswahili nchini Kenya nipamoja na Kenya Broadcasting Corporation (K.B.C), Nation F.M., Radio Citizen,Baraka F.M., Pwani F.M., Iqra F.M., Kameme F.M., Rehema F.M., East F.M.,Redio Sayari ,Eldoret, Radio Waumini, Kenya Television Network (K.T.N.), HopeF.M na Family T.V.
Kwa mfano, katika redio ya KBC vipindi vinavyoendeleza Kiswahili ni pamoja naLugha Yetu Ongea Lugha Sanifu ya Kiswahili , Ukwasi wa Lugha ChemshaBongo na Ushikwapo Shikamana. Katika runinga ya K.B.C. kuna vipindi kama
112
Sanaa ya Kiswahili , Vituko na Burudani la Taarabu . Katika redio ya NationF.M., kuna kipindi cha Kamusi ya Changamka na katika runinga ya Nation,kuna Lulu ya Nation . Vipindi vya kanisa vinavyoonyeshwa kwenye televisheniau kupitia redio vimechangia pakubwa ustawi wa Kiswahili.
Kulingana na Musau (2001:39) tatizo kubwa ni kwamba nchini Kenya hakunasera dhahiri katika vyombo vya habari inayoendeleza Kiswahili na kuhifadhiutamaduni wa kitaifa. Inaonekana kwamba vituo vingi vya redio na runingahutangaza kwa Kiingereza na kuonyesha vipindi vya Kigeni.
Zoezi
Tathmini matumizi ya lugha katika vyombo vya habari nchini Kenya.Zingatia sarufi na matumizi ya sheng; pamoja na mielekeo ya watu.
Kwa upande mwingine uchapishaji wa magazeti ya Kiswahili nchini Kenya nijambo la kusikitisha sana. Hivi sasa kuna magazeti mawili tu, gazeti la Taifa Leo
ambalo huchapishwa kila siku na toleo la Jumapili, na pia gazeti la Jamhuri
ambalo hutulewa mara chache. Taifa Leo ndio gazeti kongwe zaidi la Kiswahilihapa nchini. Gazeti la Jamhuri ni jipya na halijakita mizizi kikamilifu. Ni gazetiambalo lina mwelekeo unaofaa wa kukuza Kiswahili na linashughulikia madangumu zinazohusu lugha na maisha ya Kijamii. Gazeti hili lina uwezo wa kuletasura mpya katika ramani ya vyombo vya habari nchini Kenya. Kinyume na haliilivyo nchini Tanzania, nchini Kenya magazeti mengi na majarida huchapishwakwa Kiingereza na lugha za kikabila kama vile Kikuyu na Dholuo.
Kuna pia vijarida (newsletters) vya Kiswahili ambavyo huchapishwa namakampuni ya kibinafsi na mashirika ya kidini lakini havisambazwi sehemunyingi. Kwa ujumla magazeti ya Kiswahili yanayochapishwa nchini Kenyayamechangia ukuzaji wa lugha ya Kiswahili kwa njia nyingi ikiwa ni pamoja na
113
kuandika habari, makala, mashairi, mafumbo ya kujaza maneno, methali,vitendawili, tahakiki za vitabu vipya, hadithi, matangazo, majaribio ya mitihani yaKiswahili, maoni na hata kuchora vibonzo. Onyango (2000:8) ameeleza kwautondoti mchango wa magazeti katika ukuzaji wa Kiswahili; amesisitiza kwambamagazeti yanapotumiwa vilivyo, yanaweza kustawisha lugha hii na wakati huohuo kuwafahamisha, kuwaelimisha na kuwaburudisha kikamilifu wananchi.
Zoezi
Tathmini ubora wa magazeti ya Kiswahili yanayopatikana humu nchini
Swali
Huwezi kutenganisha lugha na siasa.Jadili kauli hii kwa kurejelea haliya lugha nchini Kenya.
HitimishoKatika somo hili, tumezungumzia swala la upangaji lugha na hatua zote ambazohurejelewa katika upangaji lugha. Tumeangalia sera ya lugha nchini na jinsiambavyo tume mbalimbali zimechangia katika kuendeleza Kiswahili.Tumeona piajinsi shughuli za serikali zinavyochangia, na mwisho tumeangalia mchango wavyombo vya habari.
Marejeleo TeuleChimera, R. (2000) Kiswahili: Past, Present and Future Horizons . Nairobi.
Nairobi University Press.
114
Haugen, E. (1956) Bilingualism in the Americas . University of Alabama Press.Tuscaloosa.
_______ (1983) The Implementation of Corpus Planning: Theory and Practice .Katika Progress in Language , eds. J. Cobarrubias and J.A. Fishman.Mouton. Berlin.
King ei, G. (2001) Matatizo ya matumizi ya lugha katika vyombo vya habari:Mifano kutoka Kenya, katika Swahili Forum VII German. University ofKoln Uk. 45-56.
Mbaabu, I. (1996) Language Policy in East Africa , Educational Research andPublication; Nairobi.
Mesthrie R. et.al. (2000) Introduction to Sociolinguistics . Edinburgh. EdinburgUniversity Press.
Mukhwana, A. (1995) Kiswahili Sanifu: Je, kipo katika Baragumu , Juzuu 2 Nam1 & 2, Maseno, Chuo Kikuu cha Maseno.
Musau, P. (2001) Freeing the Airwaves or Cultural Enslavement: The case ofmedia in Kenya katika Kiswahili: A tool for Development Themultidisplinary Approach Eldoret: Moi University Press.
Onyango, J.O. (2000) Magazeti ndio uti wa mgongo katika ustawishaji waKiswahili katika Gazeti la Jamhuri, Desemba 17-30, 2000 uk. 8.
____________ (2002) AKS 102: Historical Development of Kiswahili :Nairobi. Institute of Open Learning. Kenyatta University.
Rubin, J.R. na Jernudd, B. (1972) Can Language Be Planned ? University Press.Hawaii. Honolulu.
115
SOMO LA SABAISIMUJAMII NA ELIMU
7.0 UTANGULIZIIsimujamii-Elimu ni kitengo cha Isimu-jamii ambacho hujihusisha na uhusianouliopo baina ya lugha na elimu. Tafiti nyiingi zilizofanywa zimezingatia mazingiraya darasani. Hata hivyo, bado kuna maswali mengi kuhusu lugha katika elimu-iso rasmi kama vile elimu ya gumbaro na hata elimu-huria.
Katika somo hili tutatoa maana ya elimu na ujifunzaji. Kisha tutaonyesha jinsilugha katika fasiri yake pana ni muhimu katika ufunzaji na tajriba za ujifunzajiambazo hutokea shuleni. Tutaangalia lugha katika elimu pamoja na sera yalugha katika elimu na mwisho tutaangalia lugha ya darasani.
7.1 Madhumuni
Kufikia mwisho wa somo hili, tunatarajia kuwa utaweza: Kueleza maana ya elimu, ujifunzaji na ufunzaji. Sera ya lugha katika elimu nchini. Matumizi ya lugha darasani.
7.2 UFUNZAJI, UJIFUNZAJI NA USOMAJIKatika kila jamii huwa kuna arifa ambazo kila mwanajamii anahitaji kupata.Vile vile anahitaji kupata maarifa fulani ili aweze kutekeleza majukumu yakekama mwanajamii.
Elimu hapa inarejelea ile hali ya kufunza na kujifunza (teaching and learning)ambapo wanajamii huweza kupata arifa hizi pamoja na maarifa, Mesthrie (2000).Aghalabu ufunzaji husimamiwa na watu waliopewa mamlaka katika jamii na wao
116
hufanya hivyo kwa niaba ya jamii kwa minajili ya watoto wao. Harakati hiihujulikana kama ujamiishaji wa mtoto (child sociolization).
Hata hivyo ufunzaji pia huibuka miongoni mwa vizazi (generations),kwa mfano , mtu anapojifunza jinsi teknolojia mpya kama vile tarakilishiinvyofanya kazi. Hapa hivi tunaona kuwa watu wazima pia huwa wanafunzi.
Katika jamii za Kijadi, dhana ya elimu inajumuisha kule kuwatayarisha vijana kwakuwatia jandoni au sherehe nyingine ambazo zinaonyesha mpito kutoka hali yautoto hadi utu uzima.
Elimu pia inahusisha uchunguzi na uigaji wa wasanii na watu wenginewaliomakinika katika kazi za kisanii. Mambo yote yanayohusiana na utambaji wahadithi au malumbano ya hadharani ni sehemu ya ufunzaji na ujifunzaji.
Katika jamii za kisasa, utoaji wa arifa na maarifa hutokea kote katika jamii. Hatahivyo jukumu rasmi kuhusu elimu linapewa taasisi maalumu hasa shule nahuwa haiachiwi watu binafsi. Mambo wanayosoma watu katika mazingira yashule huenda yakawa tofauti sana na yale wanayojifunza nyumbani au mahalipopote pale katika jamii. Tofauti kati ya matumizi ya lugha ya nyumbani na yashule ndio huzua matatizo katika elimu. Hivyo basi lugha na elimu ni mada iliyona shauku kubwa katika tafiti za kiisimu-jamii.
Zoezi
Mfumo wa jadi wa elimu ulikuwa tofauti kwa njia gani na mfumowa sasa?
117
7.3 LUGHA KATIKA ELIMUMifumo ya elimu kote ulimwenguni imetambua umuhimu na nafasi ya lughakatika harakati ya kujifunza na kufunza. Lopez (2000) anachukulia harakati zakujifunza na kufunza kuwa ni ubadilishanaji mawazo na mawasiliano katika uasiliwake. Anaona kuwa, mawasiliano kwa upande mmoja ni sharti muhimu iliujifunzaji na ufunzaji uweze kutekelezwa. Kwa upande mwingine, anaonamawasiliano kama njia na namna walimu na wanafunzi wanavyowasiliana katikashughuli zao za darasani. Na hii ndio sababu kuwa kote ulimwenguni mfumo waelimu unasisitiza mawasiliano na lugha na huzichukulia kama vitengo muhimuvya mtalaa shuleni. Sio tu katika lugha na mawasiliano ndio tunaona uhusianowa karibu, bali pia kati ya lugha na fikra (Crystal 1994; Lopez 2000).
Ingawa swala la lugha ni muhimu na ni jambo la uhalisia katika harakati yaujifunzaji na ufunzaji katika jamii zote, kuna matatizo ambayo huibuka katikajamii zenye wingi lugha (Tazama Sura ya 4 kwa maelezo kuhusu uwili-lugha),ambapo wanafunzi hujiunga na mfumo wa shule wakiwa wanafahamu lugha zanyumbani (au lugha ya mama) ambazo mara nyingi huwa tofauti na lugha zaelimu. Katika hali hii, wanafunzi hawapati tu lugha zao za nyumbani ili kuzitumiakatika kupata maana ya ulimwengu unaowazingira bali pia umilisi katika lughazao za kwanza huwa kitangulizi cha kuweza kujifunza lugha nyingine. Hizi lughanyingine ambazo mtoto anakumbana nazo huwa ni lugha za mawasiliano panakatika jamii (Tazama Somo la 4 kuhusu lingua franka).
Watoto katika jamii kama hizi wanazo haki na wanatarajiwa kujifunza lugha hiziili waweze kuwa waamilifu katika serikali yao na ulimwengu mzima kwa jumla.Matumizi ya lugha ya mama kama lugha ya ufundishaji inachukuliwa kuwa ndiohumsaidia mtoto kukuza dhana ambazo humsaidia kupata ujuzi kwa urahisikatika lugha ya pili au hata ya tatu; na vivyo hivyo kumpa mtoto tajriba kuhusuutamaduni wa jamii zao (Muthwii, 2002; Sifuna, 1980; Parry, 2000; Milon, 1992).Isitoshe, lugha ya ufunzaji ni njia ambayo wanafunzi wachanga huweza kueleza
118
tajriba zao katika harakati za kusoma. Hivyo basi, swala la lugha katika elimu niswala muhimu katika harakati ya ujifunzaji na ufunzaji.Ni kwa sababu yaumuhimu huu wa lugha ndio tunapata kuwa sera za lugha katika jamii zenyewingi lugha zinahitaji kuwa wazi ili kuonyesha uhusiano unaohitaji kuwepo katiya lugha zinazotumika katika jamii na zile za elimu.
Umuhimu wa nafasi ya lugha katika elimu unaweza kupanuliwa zaidi. Tunawezakudai kuwa katika kumfundisha mtu binafsi, njia ya mafunzo (medium ofinstruction) ni njia ambayo mwanafunzi kama huyu anaweza kupata na kuelewaarifa ambazo zitamsaidia aweze kupata maarifa maishani mwake na kuyatumiamaarifa hayo na vilevile kuweza kuelewa harakati ya jinsi anavyokua, ikiwemokuelewa ukomavu wa kiuana. Utumiaji wa maarifa aliyoyapata hujumlishamielekeo kuhusu kazi na uwezo wa kufanya kazi hiyo.Maarifa ya maisha nipamoja na kuelezwa kuhusu mielekeo, amali na uwajibikaji katika jamii.
Zoezi
Je, wewe ulifahamu lugha ngapi kabla ya kujiunga na shule ya msingi?Ni matatizo gani uliyokumbana nayo shuleni katika kujifunza lugha mpya?
7.3.1 SERA YA LUGHA NA MATUMIZI NCHINI KENYASera ya lugha nchini Kenya imefasiriwa na kufanywa upya mara nyingi katikamiongo iliyopita (Tazama Somo la Sita). Hata hivyo mabadiliko hayayameathiriwa na nadharia zinazobishana, mielekeo tofauti, mitazamo tofauti yakisiasa na shauku, na kutokuwa na uamuzi.Mambo haya yote yameathiripakubwa harakati ya ufunzaji na ujifunzaji. Hata ingawa sera ya hivi karibuniimefaidika na tajriba za awali bado zinatoa changamoto kwa washikadau katikaelimu,( Muthwii,2002).
119
(Katika Somo la 6, tumeangalia sera ya lugha kulingana na mapendekezombalimbali ya Tume zilizoundwa. Ipitie sehemu hiyo tena).
Katika sehemu iifuatayo tutaangalia sera ya lugha kwa kuzingatia elimu nchiniKenya.
7.3.2 HALI ILIVYOKUWA NCHINI KENYAKabla ya ripoti kuhusu Elimu ya Waafrika nchini Kenya mwaka wa 1949,wanafunzi wa shule za msingi walifunzwa kupitia lugha zao za mama katikamiaka mitatu ya mwanzo ya shule, (Colony and Protectorate of Kenya 1949).Hata hivyo, ripoti hii ilipendekeza kwamba lugha ya Kiswahili ifanywe kuwa lughaya kufunzia katika viwango vya chini vya elimu. Ripoti ya mwaka wa 1951,kuhusu sera ya Elimu na utekelezi Afrika Mashariki na kati, kwa upandemwingine, ilipendekeza kuwa lugha ya Kiswhaili iondolewe kabisa katikamadarasa ya awali ya shule za msingi.
Ripoti iliyofuata hii katika mwaka wa 1953 ilipendekeza kwamba katika miakaminne ya mwanzo, lugha wenyeji iwe lugha ya kufunzia (The Nuffield Foundationand the colonial Office 1953). Mapendekezo ya ripoti hii kuhusu lugha yakufunzia yalitekelezwa mara moja na serikali ya kikoloni. Hivyo basi katika miakaya hamsini, wanafunzi wote wa shule za msingi nchini walifunzwa kupitia lughazao mbalimbali katika miaka minne ya mwanzo ilhali Kiingereza kilifunzwa kamasomo kwa miaka miwili au mitatu na baadaye ikawa lugha ya kufunzia katikadarasa la 5 8 (Sifuna, 1980).
Kufikia katikati ya miaka ya hamsini, kulikuwa na kutoridhika miongoni mwawatu kuhusu matokeo ya mitihani ya kitaifa miongoni mwa watoto wa Kiafrika naKieshia (Kihindi) hasa katika uandishi ikilinganishwa na watoto wa Kizungu,(Sifuna,1980). Walidai kuwa matokeo haya mabaya yalitokana na matumizi yalugha ya mama kama lugha ya kufunzia kwa muda mrefu katika masomo ya
120
msingi. Hivyo basi wizara ya elimu ilianzisha kituo maalumu katika idara yaukaguzi wa shule mwaka wa 1957. Kituo hiki maalumu kilikuwa na jukumu lakutayarisha vifaa vya ufunzaji na kuwatayarisha walimu kwa jaribio la kuanzakutumia Kiingereza kama lugha ya kufunzia kuanzia darasa la kwanza. Jaribiohilo ambalo lilianzishwa katika shule za watoto wa Kieshia, lilipanuka kwa kasikupitia mvuto wake kama lugha ya kufunzia na kwamba kulikuwa na vifaa vyakufunzia. Basi, kile kilichoanza kama jaribio la lugha ya Kiingereza kama lughaya kufunzia, ndio ulikuwa mwanzo wa mapinduzi katika elimu katika shule zoteza msingi nchini Kenya. Mapinduzi haya yalijulikana kama New PrimaryApproach (NPA), (Mbaabu 1996: sura ya 6). Kulingana na Sifuna (1980) katikamwaka wa 1961, kulikuwa na shule moja tu iliyotumia vifaa vya kufunzia lakinikufikia mwaka wa 1965, takribani madarasa 2,871 yalikuwa yanatumia vifaa hivi.Mfumo wa NPA ulisisitiza mtazamo wa kumweka mtoto kuwa katikati au kitovucha masomo kupitia lugha ya Kiingereza kama lugha ya kufunzia katika mtaalamzima wa shule ya msingi. Lugha ya Kiswahili ilifunzwa kama somo la lazima,(Muthwii, 2002).
Mabadiliko hayo ya ghafla katika elimu, falsafa na mbinu yaliandamana namatatizo chungu nzima kulingana na Hutasoit na Prator (1965) kwa mfano, idadiya wanafunzi ilizidi walimu na vifaa vilivyokuwepo ili kutekeleza kazi hii nzuri.Tulikuwa na walimu wengi ambao hawakuwa wamepata mafunzo ya ualimu nawalimu hawa walipewa majukumu ya kufunza NPA baada ya kupatia kozi fupi.Vile vile ukaguzi wa shule haukutekelezwa vilivyo na majengo ya shule na vifaavya kufunzia havikutosha. Matokeo yalikuwa, hapakuwa na usare wowote katikaviwango vya mpango wa NPA . Sehemu ambazo zilifaidika na mpango huuzilikuwa ni sehemu za mjini. Matatizo haya, pamoja na maoni kwamba lughamama ndio lugha ambayo mwanafunzi anaweza kusoma na kuandika nayo vizurikatika darasa la kwanza, yalizua mabadiliko mengine katika mjadala wa lugha yakufunzia.
121
Katika kuendelea kuunga mkono lugha mzazi, Anderson (1970 :70) alisemaTajriba ya muda mrefu imeonyesha kuwa lugha wenyeji kama lugha ya
kufunzia, kielimu ni bora kwa sababu ili pawe na ufunzaji wa maana, lazimapawe na asilimia fulani ya mtagusano kati ya maisha ya mtoto nyumbani, nalazima ufundishaji uhusishe dhana zilizojengwa na mtoto katika tajriba zake zaawali kabla hajajiunga na shule.Kufikia miaka 1976, lugha mzazi ilichukuliwakuwa ndiyo lugha bora kutumiwa katika shule nyingi za msingi. Katika shuleambazo hapakuwa na lugha ya mama moja, kwa mfano sehemu za mjini, lughaya Kiswahili ilitumika( Mbaabu 1996). Kufikia sasa, sera ya lugha imependekezakuwa katika shule za msingi, lugha ya mama itumike kama lugha ya kufunzia(hadi darasa la tatu). Kiingereza na Kiswahili zinafunzwa kama masomo yalazima, lakini Kiingereza kinatumika kama lugha ya kufunzia masomo mengine,Mbaabu (ibid).
Zoezi
Ni matatizo gani yanayokumba wizara ya elimu kuhusu kuwa na lughaza mama kama lugha za kufunzia nchini? Ni vipi tunaweza kuyasuluhisha?
Kwa kuzingatia nafasi ya lugha katika uwanda wa kujifunza na kufunza kamatulivyoeleza, inaweza kuchukuliwa kuwa sera za lugha ambazo zimechukuliwakwa sababu mbalimbali zinazua mtanziko kwa wazazi, wanafunzi na walimukatika nchi hii yenye wingi-lugha. Kwa mfano, wazungumzaji wengi ni wanauwiliuwili au wana-wingi lugha, hivyo basi wao huchagua Kiingereza kama lugha yakufunzia katika shule za msingi. Kwa sababu Kiingereza ni lugha ya elimu ya juu,wale ambao huchagua Kiingereza kama lugha ya kufunzia kuanzia darasa lakwanza huwa hatua moja mbele ya wale wanaotumia lugha ya mama auKiswahili. Na hii ndio hali ambayo husababisha kutokuwa na usawa kielimu. Vilevile hali hii inakanusha sera inayohimiza lugha ya mama kama lugha ya kufunziana ukweli uliopo kuwa mtoto anapoendelea kukua katika mfumo wa elimu, lugha
122
ya Kiingereza hutawala lugha nyingine. Lugha ya mama hupewa nafasi ya chinisana baada ya masomo ya shule ya msingi na inaondolewa kabisa katika mitihaniya Kitaifa katika elimu ya msingi. Hata hivyo, watoto wenyewe hawaoni lughazao zikipewa majukumu katika sekta nyingine yoyote isipokuwa nyumbani. Kwasababu hiyo, jukumu la kukamilishana ambalo linahitajika kuwepo baina ya lughaya elimu na ile ambayo inatumika katika mazingira mapana ya uchumi-jamii yamtoto hayapo. Hata katika hali zile ambazo tunaona majaribio yakifanyika ilikutekeleza sera ya lugha, walimu katika jamii nyingi hawawezi kutekeleza serahiyo kwa sababu ya matatizo ya kutokuwa na vifaa vya kutosha na pia wengiwao hawazifahamu barabara lugha zao za kwanza.
Zoezi
Umeombwa kutoa mhadhara kuhusu umuhimu wa lugha ya Kiswahili katikaMaisha ya mwanafunzi, kwa wanafunzi ambao hawafanyi vizuri katikasomo hili. Je, ni mambo gani utakayowaelezea?
7.3.4 LUGHA YA DARASANITafiti nyingi zimefanywa katika nchi za magharibi na hata humu nchini katikakuangalia uhusiano uliopo kati ya lugha na elimu, (Meshrie ,2000).
Watfiti hawa wamekubaliana kuwa ufunzaji na ujifunzaji unaoendeshwa darasaniunategemea matumizi ya lugha kwa kiwango kikubwa. Tafiti hizi zimegunduakuwa hata ingawa walimu watatumia vifaa-saidizi vya ufunzaji kama vile picha ilikuwasilisha arifa mpya, mazungumzo ya mwalimu ni njia ya msingi katikaufunzaji darasani (taz Muthwii, 2002).Kwa upande mwingine, mwanafunzianatarajiwa asikilize, ajibu maswali na aulize maswali. Muhimu pia ni lugha-andishi ambayo inapatikana darasani.Lugha hii andishi inahusu kuandikaubaoni, kusoma vitabu maktabani na vifaa vingine.
123
Kutokana na umuhimu wake katika swala la ufunzaji na ufundishaji, lugha yadarasani inadhibitiwa na mwalimu. Walimu ndio huwa waongezi darasani nalugha ya mwalimu ndio huwa sajili ya msingi wa matumizi. Wanafunzihawachukui nafasi kubwa katika mazungumzo ya darasani.
Bali na kuwa wazungumzaji wakuu katika maongezi ya darasani, walimu piahuwa wasimamizi wa mazungumzo hata kama wao hawazungumzi. Wao ndiohuamua mada zitakazoshughulikiwa darasani na hutawala haki ya kila mtoto yakuongea kuhusu mada hizo.Pia wanasimamia muda au wakati ambao kilamwanafunzi atatumia katika mjadala.
Mwalimu pia huwaongoza wanafunzi katika mbinu za uandishi. Huwaonyeshatofauti kati ya uandishi na mazungumzo ya ana kwa ana.
Tofauti kati ya lugha ya darasani na lugha ya nyumbani pamoja na tamaduni zawatu, ni baadhi ya mambo ambayo yanaonekana kusababisha matatizo ya lughaanayokumbana nayo mwanafunzi. Kwa mfano, Mesthrie (2000) ananukuu utafitiuliofanywa na Susan Phillips (1972 na 1983) kuhusu tofauti baina ya mamboyanayotawala mazungumzo na ukimya unaopatikana katika mazingira yakinyumbani nchini India na yale yanayopatikana katika shule za umma. Katikajamii hizi watoto hufunzwa katika maisha yao ya awali kuwa mazungumzo nimambo yaliyotengewa watu wazima; watoto wapo kusikiliza tu mazungumzo yawatu wazima, na wanatakiwa wajifunze tu kile wanachosikia. Inachukuliwakuwa watoto hawa wakiwa watu wazima, watakuwa wamepata arifa za kutoshakuzungumzia au kuwaambia watoto wao na hata vizazi vijavyo.
Katika mandhari ya darasani, maana za kijamii ambazo zinahusishwa na ukimyazinatafsiriwa tofauti na walimu na watawala wengine. Katika mazingira yashuleni, ukimya wa mwanafunzi unaashiria mwanafunzi kutomaliza kazi ya ziada
124
ya nyumbani, kutokuwa mzingativu darasani hasa kwa mijadala ya darasani aukukataa kushiriki darasani.
Hivyo basi, tofauti za utamaduni kati ya mazingira ya nyumbani na shule huzuamatatizo ya mawasiliano katika elimu.
Swali
1. Sera ya lugha ni kipengele muhimu katika elimu. Tathmini ukweli wakauli hii ukirejelea hali ya lugha nchini Kenya kwa ujumla.
2. Lugha na utamaduni huingiliana sana. Fafanua kauli hii kwa kurejelea seraya lugha ktika elimu.
7.4 HITIMISHO
Katika somo hili, tumeshughulikia swala na lugha na elimu. Tumeangaliadhana ya elimu, ufunzaji na ujifunzaji na usomaji. Tumeangalia sera yalugha kuhusu elimu nchini, na mwisho tumeangalia swala la lugha ya darasanina lugha ya nyumbani na jinsi utamaduni ambao amekulia mtoto unaathirimatumizi ya lugha darasani.
125
Marejeleo TeuleColony and protectorate of Kenya (1949): African Education in Kenya. Report of
the Committee appointed to inquire into the Scope, Content, Methodsand Administrtion of the African Education (Beecher Report) Nairobi:Government Printer.
Crystal, D. (1994) The University of Cambridge Language Encyclopaedia .Madrid. Taurus.
Hutasoit, M. and Prator C. (1965) A Study of the New Primary Approach in the
Schools of Kenya . Ministry of Education & Ford Foundation.Lopez, L.E. (2000) Cognition, Culture, Language and Learning: An introduction
to Education Planners in Multilingual and Multicultural Contexts KatikaDistance Learning Course in the language of Instruction in Basic Education (Nov. 27, 28, 29, December 2000).
Mbaabu, I. (1996) Language Policy in East Africa , Nairobi Educational Researchand Publication.
Mesthrie, R. et.al. (2000) Introducing Sociolinguistics , Edinburg, EdinburgUniversity Press.
Milon, J.P. (1992) Discourse in the Primary English syllabus of Botswana katikaUdo Bude (ed.) Culture and Environment in Primary Education . Thedemands of the Curriculum and the Practice in Schools in Sub-Saharan Africa. Bon. Education Science and Documentation Centre. GermanFoundation for International Development.
Muthwii, M. (Mha.) (2002) Language, Policy and Practices in Education in Kenya
and Uganda . Nairobi, Phoenix Publishers.Mwaura, P. (2003) Children learn Better in Mother Tongue Katika Daily Nation ,June
19, 2003.Parry, K. (Mha.) (2002) Language and Literacy in Uganda : Towards a Sustainable
Reading Culture . Kampala. Fountain Publishers.
126
Sifuna, D.N. (1980) Short essays in Education in Kenya . Nairobi KenyaLiterature
Bureau.
SOMO LA NANELUGHA NA JINSIA
127
8.0 UTANGULIZIMatumizi ya baadhi ya maneno katika jamii huwekewa vizuizi mbalimbali. Hiihaimanishi kwamba maneno hayo ni mabaya au mazuri. Lakini inamaanisha tukuwa hali hii inaakisi mitazamo ya jamii au mtu binafsi kuhusu maneno hayo.
Katika somo hili tutazungumzia swala la lugha na jinsia. Tunataka kuonyeshajinsi matumizi ya maneno huakisi mielekeo ya jamii kuhusu kikundi fulani chawanajamii. Kwa mfano, ni kwa nini wanawake watarajiwa kuongea kwa namnafulani wala si nyingine.
8.1 Madhumuni
Tunatarajia kuwa kufikia mwisho utaweza:Kuonyesha jinsi lugha inavyoakisi mielekeo ya jinsia katika jamii.
8.2 Jinsia na isimu jamiiHoja kwamba wanawake na wanaume hutumia lugha tofauti lina misingi yakekatika isimu-mila (folk linguistics). Dhana hii hurejelea seti fulani za imanikuhusu lugha.
Utafiti kuhusu lugha ya wanaume na wanawake umeanza katika miaka ya 1920,1930 na 1940. Hata hivyo tafiti kuhusu jinsia na lugha kama eneo pana la utafitizimeanza mwanzo wa miaka 1970. Hivyo basi lugha na jinsia ni mada ambayoina shauku kubwa sana na ni muhimu kwa sababu ya ule mchango wake wakusaidia kuelewa lugha na jinsi inavyofanya kazi na hasa katika uwanda waisimu-jamii.
Kama mada ya utafiti, swala la lugha na jinsia limepata mchango kutoka maeneombalimbali kama vile anthropolojia, uchanganuzi lugha, elimu, nadharia zaKifasihi, Saikolojia ya jamii na elimu-jamii.
128
8.2 LUGHA YA WANAWAKE NA WANAUMECoates (1986) anadai kuwa lugha haina jinsia lakini inaweza kutumiwakuonyesha uana katika jamii. Jinsia ni neno linalotumiwa kuelezea mambo yoteyanayohusiana na hali ya kuwa mke au mume.
Sifa inayobainika kati ya lugha na jinsia ni mielekeo ya watu kuhusu manenofulani katika lugha husika. Mielekeo kama dhana ni mitazamo ya watu kuhusumaisha. Mitazamo hii inaweza kuwa inayofaa au isiyofaa kutegemea na jamiihusika. Mielekeo ya Kijinsia inachukuliwa kama mitazamo ya jamii kuhusu hali yaKijinsia na mambo yote au majukumu wanayotekeleza kulingana na tofauti zaokijinsia.
Lugha kama chombo cha jamii kinafungamanishwa na miundo ya kijamii. Hivyobasi tofauti za matumizi ya lugha zinatokana na mielekeo hii. Katika muktadhawa kijamii, wanawake na wanaume wanatofautiana na hivyo basi jamii huwapamajukumu tofauti na kwa sababu hii, jamii inatarajia tabia tofauti kutoka kwawanajamii kulingana na jinsia yao. Hivyo basi, lugha inayotumika inaakisi tofautiza kifikra, kitabia na mahusiano yao. Kwa kutegemea mielekeo hii makundi yakijinsia yanaweza kusawiriwa kwa njia tofauti, na matumizi ya lugha nimojawapo.
Miiko ni jambo linaloathiri matumizi ya lugha kijinsia. Miiko ni lile jambo au kituambacho mtu haruhusiwi kutenda kwa sababu ya imani fulani. Kwa kawaidamiiko huwa haina maelezo ya kimantiki. Hata hivyo kila jamii huwa na miikotofauti kulingana na utamaduni na imani za wanajamii. Baadhi ya miiko hiihuathiri matumizi ya lugha katika jamii kijinsia. Kwa mfano, katika jamii yakikhoxa ya Afrika kusini ni mwiko mwanamke kutaja jina la babamkwe ambapohuenda akapata sauti [z] ambayo ni mwiko kuitamka. Neno kama amanzi (maji)litaeupukwa na wataibuka na neno amandabi ili wasitamke sauti {z}. Hivyo basi
129
tunaona kuwa wanawake hawa wana uwezo wa kuzitamka sauti hizi lakinihawaruhusiwi na mila kuzitamka.
Katika utafiti alioufanya Rochefort mwaka wa 1965 (Taz. Mesthrie 2000)miongoni mwa Wahindi wa Carib, aligundua kuwa wanaume walikuwa namatumizi tofauti ya lugha na wanawake, na hakuna aliyetaka kuongea lugha yajinsia nyingine katika kuchelea kuchekelewa au kudharauliwa.
Tofauti za kiisimu katika lugha mbalimbali zinaonyesha ithibati kuwa kunamiundo maalum ya kijinsia. Na katika miundo hii tofauti za kisarufi zinajitokezabaina ya wazungumzaji wa kike na wa kiume. Ushahidi wa awali kuhusu dai hilila kiisimu unadhihirika katika utafiti alioufanya Mary Haas (1944) katika jamii yaWakoasati ya Wamerika Asili (Native Americans). Kwa mfano, alipata tofautikatika miundo ya vitenzi.
Miundo ya wazungumaji wakike Miundo ya Kiume Maana Lakaw în laka î*s usikiinuelakawwil lakawwis ninaiinua
láwwili niliinualakawwilit
Tofauti za kimuundo zilizorekodiwa na Haas zilijitokeza sana katika wazungumzajiwazee, na zilionyesha kupungua miongoni mwa vijana.Wahakiki walioshughulikia tofauti za miundo hii waliona tofauti hizi kuwa niishara ya mazoea ya kijamii na imani zao. Na lugha ilifanya kazi kama kioo chajamii, kikimulika tofauti za kijamii, (Mesthrie 2000). Mesthrie (ibid) anamnukuuFurlery (1944) anayedai kuwa tofauti kati ya miundo ya wanawake na wanaumeinamaanisha wazungumzaji walitambua kuwa wanawake na wanaume wamokatika kategoria mbili tofauti.
130
Lugha ambayo imezua mijadala kuhusu miundo wanayotumia wanawake nawanaume ni lugha ya kijapani. Inasemekana kuwa tofauti za kijinsia zinajitokezawazi katika fonolojia, mofolojia na leksia ya lugha hii (Tazama mifano wanayotoaMesthrie (2000) katika jedwali lifuatalo).
Pronomino katika lugha ya Kijapani Nafsi ya (1) Usemi wa wanaume Usemi wa wanawakeRasmi watakusi watakusi
Watasi atakusiSio rasmi boku watasi
AtasiSio ruhusiwa ore Ø
Nafsi ya 2 Rasmi anata anataSio rasmi kimi anata
anta* anta*sio huhusiwa ome Ø
kisama alama hizi zinadhihirisha tofauti za kilahaja kijamii.
Katika jedwali hili, tofauti mbili zinajitokeza hapa.Kwanza ni toauti katikakiwango cha urasmi. Kiwango cha urasmi cha watasi ni cha kirasmi kwawanaume lakini sio rasmi kwa wanawake. Lakini ile ya anata ni rasmi kwawanaume na huenda ikawa rasmi au isiwe-rasmi kwa wanawake. Hii ina maanakwamba wanawake watarajiwa kutumia miundo mingi iliyo rasmi. Piatunatambua kuwa pronomino ambazo hazikubaliki kama vile ore, omae nakisama zinajitokeza katika miundo ya wanaume lakini sio miongoni mwa usemiwa wanawake. Hakuna neno lisilokubalika ambalo linatumika katika uneni wawanawake.
131
Matumizi haya ya miundo tofauti ni ishara ya mielekeo tofauti. Kukwepa kutumiamaneno yasiyokubalika ni ishara ya adabu nzuri. Hivyo basi tofauti zakikategoria katika mkusanyiko huu wa pronomino unadhihirisha ishara yaheshima na adabu miongoni mwa wanawake. Jambo hili linafanya uneni wawanawake uonekane kuwa wenye adabu zaidi (Ide 1989/1990 katika Mesthrie2000).
Reynolds (1980/90) ametambua kuwa, matumizi ya boku mimi (mwanamume)miongoni mwa wasichana wa sekondari yamekuwa kitu cha kawaida mjini Tokyo.Kwa sababu wasichana wanajua kuwa lugha ya boku haikubaliki katikamazingira nje ya shule, wao hutumia lugha-watasi (wanawake)wanapozungumza na wanajamii wengine. Inaweza kuchukuliwa kwamba,wasichana hawa wa shule ni wana uwili-lugha ambao wanatumia misimbo miwilitofauti a boku na ya watasi . Na wao huchagua msimbo kulingana namazingira.
Picha inayodhihirika katika miundo hii pia inaonyesha wanawake wakiwa wapole,wenye heshima, taratibu na wangwana wasioteta na wana uwezo wa kuhisimaono ya wengine (Okomoto, 1995).
Finalyson (1995) anajadili matokeo ya utafiti alioufanya Afrika Kusini katika jamiiya Wakhoxa. Alichunguza matumizi ya hnolipha (au isihnolipho saba jazi, lughaya kiheshima ya wanawake). Aligundua kuwa wanawake katika jamii hii hukwepakutamka silabi ambazo zinajitokeza kwenye majina ya wakwe zao hasa babamkwe, mama-mkwe na ndugu za babamkwe na wake zao na dada zakebabamkwe.
Hivyo basi wanawake wameibuka na harakati fulani za kiisimu ambazo waohutumia ili kukwepa kutamka silabi hizo. Wanaweza kudondoa konsonanti,
132
wabadilishe konsonanti moja na nyingine, wabadilishe neno moja na lingineambalo linakaribiana kisemantiki au waunde upya sentensi au ikiwa wamesoma,watatumia maneno ya Kiingereza au Kiafrikaans. Kwa mfano, ikiwa mwanamkeatapata baba mkwe ambaye jina lake ni Bheki au Bhengu atahitaji kukwepa silabibhe katika maneno kama vile i-bhekile (mkebe). Anaweza kuchagua kutokamojawapo wa miundo hii:
l-ekile (undondoaji wa konsonanti)l-wekile (kubadilisha konsonanti)I konkxa (sinonimu)lsikhelelo (uundaji upya-kitu ambacho kinatumiwa kuchotea)
Mazoea na matumizi ya hlonipha yanaendelezwa na familia pana ambayomsichana ameolewa. Hlonipha pia inahusishwa na miundo mingineinayoonyesha heshima kwa watu wazima hasa wanaume. Kando na matumizi yalugha, mwanamke anahitaji pia kujitenga na asitembelee sehemu ambazowanaume wanazoea kutembelea. Hali hii ya kuepukana iwe ya kiisimu au la niishara ya heshima na pia inahakikisha kuwa mtu mgeni na ambaye anachukuliwakuwa wa hadhi ya chini katika boma hilo hatawafanya watu kufikiria juu yake.
Hata hivyo hlonipha haitumiki sana katika sehemu za mjini kwa sababu hakunauhusiano wa moja kwa moja na wakwe wa msichana.
Hlonipha inaonyesha wazi tofauti kati ya wanawake na wanaume, naimehusishwa na kutokuwa na uwezo wa wanawake hasa katika jamii jadi.Hlonipha inadhihirisha hadhi ya chini ya kijamii ya wanawake na kama kitendocha kila siku inaendeleza tofauti ya kijinsia katika jamii.
Zoezi
133
Je, lugha yako inadhihirisha tofauti zozote za matumizi kati ya wanawake nawanaume? Onyesha tofauti hizo.
Mara nyingi katika maneno ambayo ni horomo, maneno yasiyodhihirisha wazijinsia huweza kufanya jamii kupendelea jinsia moja. Kwa mfano, watuwanaposikia sentensi kama hii, Binamu wangu ni profesa, au daktari auChansla watachukulia kuwa huyu ni mwanamume. Wazo hili halitokani na lughahii tu bali linatokana na sababu za kihistoria, kwamba wanawake hawakuwawakishikilia nyadhifa kama hizi (Fromkin na Rodman, 1988). Vivyo hivyo, mtuakisikia mwenzake akisema kuwa binamu wake ni nesi, mwalimu wa shule yamsingi au mhazili, mtu kuchukulia kwamba binamu huyu ni mwanamke.
Kutokana na hali hii tuliyoeleza hapo juu, maneno horomo hufanywa kuwamaneno ambatani ambapo ule muundo wake wa kimsingi unaweza kutumika najinsia yoyote. Kwa hivyo tunapata maneno ya Kiingereza kama vile malenurse,lady doctor, madam President. Haya hutumika kwa lengo la kudhihirisha wazimaana ya maneno hayo.
Tafiti zinazohakiki lugha inayotumika na wanaume katika kurejelea wanawake naambayo yana maana ya kushusha heshima au yanadokeza kujamiana,zinaonyesha kuwa matumizi ya maneno kama haya yalianza zamani. Wakatifulani, maneno hayakuwa ya kukashifu lakini hupata sifa za kikashifa baadayeFromkin na Rodman (1986) wanatoa mifano ya maneno haya katika Kiingereza.Wanasema kuwa baada ya muda maneno haya yamekuja kupata maana tofauti
hussy, laundress, a needleman, a spinister maneno haya baadaye yalitumikakama tasfida ya hawara.
Maneno yanayorejelea wanawake na hasa yale ambayo yanatumika kama matusini mengi. Maneno haya ni kama vile malaya, ambapo inachukuliwa kuwa
134
mwanamke tu ndiye malaya. Mifano mingine inajitokeza wazi katika lugha yaKiingereza bitch, piece of ass na kadhalika.
Jambo lingine linalodhihirika hasa katika lugha ya Kiingereza ni kwamba majinaya kiume huwa hayana utambulisho lakini ya wanawake yanaundwa kwakuongezea mofimu nyingine za kiutambulisho. Kwa mfano:
Prince PrincessAuthor authoressCount CountessPoet Poetess
Nomino zisizo na utambulisho zinazorejelea wanaume hutumika kurejelea dhanaza kijumla. Kwa mfano, maneno kama brotherhood na mankind hujumlishawanawake pia lakini sisterhood haijumlishi wanaume.
Maneno mengine ya kijozi ya kijinsia huwa na maana tofauti ingawa neno ni lilelile. Kwa mfano, governor ni mtu anayetawala nchi, lakini governess nimwanamke anayetunza watoto. Neno mistress halina maana sawa na masterkatika Kiingereza. Mara nyingi tunazungumzia kuhusu unwed mothers wala siunwed fathers au career women wala si career men. Kwa nini? Kwa sababukihistoria mwanamume asiyeoa hatiliwi waa au stigma yoyote na pia wanaumewanatakiwa wawe wafanyikazi. Hata hivyo, hivi karibuni tumeanza kusikiamaneno kama vile househusband, hali ambayo inaakisi mabadiliko katikamienendo ya jamii hasa uchumi ambapo mwanamke ndiye mfanyikazi na mumehana kazi.
Vilevile tunaona kuwa ni jambo la dharau mwanamke kuitwa spinister, kwamaana ya mwanamke asiyeolewa lakini jamii inaruhusu mwanamume kuitwabachelor. Hakuna chochote cha matusi katika neno spinister ila kwamba maanakimatilaba inatokana na mielekeo ya wanajamii kuhusu wanawake ambao
135
hawajaolewa. Wanawake kama hawa wanachukuliwa kama vimada, dai ambalosi kweli. Hivyo basi sio lugha ambayo imejaa dhanagande bali ni jamiiinapotaasisha mielekeo hii, basi lugha inaanza kudhihirisha upendeleo.
Mabadiliko mengi yamejitokeza ambayo yanaakisi utetezi wa haki na usawa wawanawake. Wanajamii nao wametambua kuwa lugha huakisi mielekeo ya jamiina kuendeleza dhanagande na upendeleo. Hivyo basi kuna maneno ambayoyameanza kutumika badala ya yale ya upendeleo. Wanafanya hivi kwakuchukulia kwamba hata wanawake wanaweza kutekeleza majukumuyaliyotengewa wanaume katika jamii. Haya ni mabadiliko ambayo yanatokanana mabadiliko ya kiuchumi katika jamii. Kwa mfano neno people linachukuamahali pa mankind, personnel badala ya manpower, nurturing badala yamothering, to operate badala ya to man, chair badala ya chairman. Manenomengine ni kama vile, postworker, fire fighter na public safety officer yanatumikabadala ya mailman, fireman, na policeman.
Swali
Lugha huakisi tofauti za kijinsia katika jamii . Fafanua kauli hii.
136
8.3 Hitimisho
Katika somo hili tumeonyesha jinsi lugha inavyoakisi tofauti za kijinsi.Tumetoa mifano katika jamii ambazo hali hii inadhihirika wazi.Mwisho tumeonyesha jinsi watetezi wa haki za wanawake wamejaribukuondoa au kubadilisha maneno yanayodhihirisha jinsia na kupendekezayale ambayo hayataonyesha tofauti hizi.
Marejeleo Teule
Coates, D. (1986) Women,Men and Language , Longman
Fromkin V. na Rodmn R.(1988) An Introduction to Language . New York,HarcourtBrace Jovanich College Publishers.
Mesthrie R. et. al. (2000) Introducing Sociolinguistics. Edinburg. EdinbergUniversity Press.
137
Marejeleo ya Jumla
Bickerton, D. (1971) Inherent Variability and Variable Rules , katika Foundations of Language 7. Bloomfield, L. (1933) Language . New York. Holt. Rinehart and Winston.Chacha, L.M. et l (2003) AKS 100: Introdution to the Study of Language :Kiswahili Module. Nairobi. Institute of Open Learning. Kenyatta University.Chambers, J.K. & Trudgil, P. (1980) Dialectology . Cambridge. CambridgeUniversity Press.Chimera, R. (1999) Kiswahili through the Ages: The Question of Lexicon .Makala Yaliyowasilishwa katika Idara ya Kiswahili, Agosti 8, Njoro. EgertonUniversity.(2000) Kiswahili: Past, Present and Future Horizons . Nairobi, NairobiUniversity Press.Coates, D. (1986) Women, men and language . Longman.Crystal, D. and Davy, D. (1969) Investigating English Style . New YorkLongman.Crystal, D. (1994) The Unviersity of Cambridge Language Encyclopaedia . MadridTaurus.Dik, S.C. (1978) Functional Grammar . New York. North-Holland LingusticSeries. North Holland Publishing Company.Denison, N. (1977) Language death or Language Suicide? International Journalof the Sociology of Language .Fasold, R.W. (199&) Motivations and Attitudes. Influencing Vernacular Literacy:Four African Assessments Katika Vernacular Literacy : A Re-Evaluation. Oxford.Clarendon Press.Ferguson, C. (1959) Diglossia . Word, 15.
Fishman, J.A. (1967) Sociolinguistics and the Language problems of Devleoping
138
Countries katika Fishman J.A. et.al. (Wah.) Language Problems of Developing
Nations. London. John wiley and Sons Inc.(1972) Domains and the Relationshipbetween micro- and macro- Sociolinguistics . In John and Dell Hymes (eds).Greenberg, S.H. (1957 Essays in Linguistics , Chicago Phoenix Books.Gumperz, J.J. (1962) Social Network and Language Shift katika J.J. Gumperz(Mhr.) Discourse Strategies . Cambridge. Cambridge University Press.Guthrie, M. (1967) The Classification of the Bantu Languages . London.Dawsons of Pall.Halliday, M.A.K. et.al. (1964) The Linguistic Science and Language Teaching .London.Longman.(1978) Language as Social Semiotic : The Social Interpretation ofLanguage and Meaning. London. Edward Arnold.Haney D. (1995) Linguistic Crisis looms as Native Tongues Die Katika Daily Nation, 28.Haugen E. (1956) Bilingualism in the Americas . Tuscoloosa. University ofAlabama Press.(1983) The Implementation of Corpus Planning: Theory andPractice Katika Progress in Language (Wah.) J. Cobarrubias and J.A. Fishman.Berlin. Mouton.Hocket, C. (1958) A Course in Modern Linguistics . Macmillan.Hudson, R. (1980) Sociolinguistics . Cambridge. Cambridge University Press.Hutasoit, M. and Prator, C. (1965) A Study of the New Primary Approach in the
Schools of Kenya . Ministry of Education & ford Foundation.Hymes, D. (1974) Foundations in Sociolinguistics . Philadelpia. University ofPennyslavania.Kachru, B.B. (1977) Code-Switching as a Communicative Strategy in Indiakatika Saville-Troike, Murie (Wah.) Linguistics and Anthropology . Washington.Georgetown University.King ei, G. (2001) Matatizo ya Matumizi ya Lugha katika Vyombo vya Habari.Mifano kutoka Kenya katika Swahili Forum VII , German. University of Koln 45-56.
139
Kitso, J. (1975) A stylistic Approach Adopted for the Study of Kiswahili ProseTexts M.A Thesis. University Of Nairobi (Haijachapishwa)Labov, N. (1980) (Mhr.) Locating Language in Time and Space . New York.Academic Press. (1972)Sociolinguistic Patterns . University of pennyslavaniaPress.Lopez, L.E. (2000) Cognition, Culture, Language and Learning: An Introductionto Education Planners in Multilingual and Multicultural Contexts Katika Distance
Learning Course in the Language of Instruction in Basic Education .Mackey, W.F. (1962) The Description of Bilingualism Canadian Journal ofLinguistics.Mbaabu, I. (1996) Language Policy in East Africa , Nairobi. Educational Researchand Publication.(1978) Kiswahili Lugha ya Taifa , Nairobi. Kenya LiteratureBureau.Mdee, J.S. (1986) Kiswahili: Muundo na Matumizi Yake . Nairobi.Intercontinental Publishers Ltd.Mesthrie, R. et. al. (2001) Introducing Sociolinguistics , Edinberg. EdinbergUniversity Press.Milon, J.P. (1992) Discourse in the Primary English Syllabus of Botswana katikaUdo Bude (Wah.) Culture and Environment in the Curriculum and the Practice in Schools in Sub-Saharan Africa . German Foundation for InternationalDevelopment.Msanjila, Y.P. (1995) Mawanda ya Isimu Jamii katika Mbogo, E. na McOnyango, O. (Wah.) Baragumu . Juzuu la 2 Nam. 1 & 2. Maseno. Chuo KikuuMaseno.
Mukhwana, A. (1995) Kiswahili Sanifu: Je, Kipo katika Baragumu , Juzuu, 2Nam. 1 & 2, Maseno, Chuo Kikuu cha Maseno.Musau, P.M. (2001) Freeing the Airwaves or Cultural Enslavement: The Case ofMedia in Kenya katika Kiswahili: A tool for Devleopment: The Multidisplinary Approach. Eldoret. Moi University Press.
140
Muthwii, M. (Mh.) (2002) Language Policy and Practices in Education in Kenya
and Uganda . Nairobi. Phoenix Publishers.Myers-Scotton, C. (1992) Code-Switching as a Mechanism of Deep Borrowing ,Language Shift and Language Death . Brenzinger Mathias (Mhr.)Mwaura, P. (2003) Children Learn Better in Mother Tongue in Daily Nation ,June 19.Ngugi, P. na Osore, M. (2003) Linguistic Genocide of the African Languages:Protecting and Empowering Makala iliyowasilishwa katika Kongamano la LASUDar-es-Salaam Tanzania.Onyango, J.O. (2002) Magazeti ndio Uti wa Mgongo katika Ustawishaji waKiswahili katika Jamhuri, Desemba 17-30.(2002) AKS 102: Historical Devleopment of Kiswahili . Nairobi. Institute of Open
Learning. Kenyatta University.Parry, K. (Mha.) (2002) Language and Literacy in Uganda: Towards a Sustainable
Reading Culture . Kampala Fountain Publishers.Pride, J.B. & Holmes, H. (Wah.) (1972) Sociolinguistics . Harmondsworth.Penguin.Rubin, J.R. na Jernudd, B. (1972) Can Language Be Planned ? Honolulu.University Press. Hawaii.Ryanga, S. na Mukobwa, M. (2003) AKS 101:Language Skills in Kiswahili 1 :Kiswahili Module, Nairobi. Institute of Open Learning, Kenyatta University.Swaleh, A. (1997) Lugha ya Kiswahili (ni) Pijini au Krioli? Makala Yaliwasilishwakatika Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nairobi.
Sifuna, D.N. (1980) Short Essays in Education in Kenya . Nairobi. KenyaLiterature Bureau.Trugdill, P. (1974) Sociolinguistics: An Introduction . Penguin.(1986) Dialects in Contact. Basil . Blackwell. Oxford.TUKI (1990) Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha . Dar es Salaam, University ofDar es Salaam.
141
Todd, L. (1990) Pidgins and Creoles . Routledge.Wardhaugh, R. (1992) An Introduction to Sociolinguistics . Blackwell.(1994) Investigating Language . Central Problems in Linguistics.Oxford Blackwell.Weinreich, U. (1974) Languages in Contact . Mouton: The Hague.Whitely, W. (1969) Swahili. The Rise of a National Language . New Feter Lare.Methuen and Co. Ltd.
142