54
Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 1 OSW 233 MOFOLOJIA YA KISWAHILI (NUKUU) MUHADHARA WA KWANZA 1: MOFOLOJIA Fasili ya Mofolojia Mofolojia ni taaluma ya isimu inayoshughuliki muundo wa maneno. Ni taaluma inayoshughulikia vipashio vya lugha na mpangilio wake katika uundaji wa maneno. Mofolojia : ni utanzu mmojawapo katika tanzu za isimu Tanzu hizo za isimu ni: 1. Mofolojia 2. Fonolojia 3. Sintaksia 4. Semantiki na 5. Pragmatiki Uhusiano wa Mofolojia na matawi mengine ya isimu Mofolojia na fonolojia Vipashio vya kifonolojia (fonimu) ndivyo vitumikavyo kuunda vipashio vya kimofolojia (mofimu). Mfano soda limeundwa kwa fonimu /s/, /o/, /d/, /a/ na bibi limeundwa kwa fonimu /b/, /i/, /b/, /i/ Kanuni za kifonolojia huweza kutumika kuelezea maumbo ya kimofolojia ambayo yanaathiriana. Mfano: mofimu ya umoja katika ngeli ya kwanza inajitokeza kama m- ikifuatiwa na konsonanti ila hujitokeza kama mw- ikifuatiwa na irabu (m + ti = mti, mu + eupe = mweupe). Mofolojia na sintaksia Vipashio vya kimofolojia (mofimu/neno) huunda daraja ya sintaksia. Mfano: sentensi walitusafirisha imeundwa na mofimu wa-li-tu-safiri-sh-a Mabadiliko ya umbo la mofimu/neno huathiri muundo wa sentensi nzima (mf. umoja na wingi). (i) Mtoto mefu mweusi anakuja (ii) Watoto warefu weusi wanakuja

Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507 Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

  • Upload
    others

  • View
    626

  • Download
    58

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 1

OSW 233 MOFOLOJIA YA KISWAHILI (NUKUU)

MUHADHARA WA KWANZA 1: MOFOLOJIA

Fasili ya Mofolojia

Mofolojia ni taaluma ya isimu inayoshughuliki muundo wa maneno. Ni taaluma

inayoshughulikia vipashio vya lugha na mpangilio wake katika uundaji wa

maneno. Mofolojia : ni utanzu mmojawapo katika tanzu za isimu Tanzu hizo za isimu ni:

1. Mofolojia

2. Fonolojia

3. Sintaksia

4. Semantiki na

5. Pragmatiki Uhusiano wa Mofolojia na matawi mengine ya isimu

Mofolojia na fonolojia

Vipashio vya kifonolojia (fonimu) ndivyo vitumikavyo kuunda vipashio vya

kimofolojia (mofimu). Mfano soda limeundwa kwa fonimu /s/, /o/, /d/, /a/

na bibi limeundwa kwa fonimu /b/, /i/, /b/, /i/

Kanuni za kifonolojia huweza kutumika kuelezea maumbo ya kimofolojia

ambayo yanaathiriana. Mfano: mofimu ya umoja katika ngeli ya kwanza

inajitokeza kama m- ikifuatiwa na konsonanti ila hujitokeza kama mw-

ikifuatiwa na irabu (m + ti = mti, mu + eupe = mweupe).

Mofolojia na sintaksia

Vipashio vya kimofolojia (mofimu/neno) huunda daraja ya sintaksia. Mfano:

sentensi walitusafirisha imeundwa na mofimu wa-li-tu-safiri-sh-a

Mabadiliko ya umbo la mofimu/neno huathiri muundo wa sentensi nzima

(mf. umoja na wingi).

(i) Mtoto mefu mweusi anakuja

(ii) Watoto warefu weusi wanakuja

Page 2: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 2

Mofolojia na semantiki

Semantiki ni taaluma ya maana. Mofimu ni kipashio cha lugha chenye

maana mfano; neno kisu lina mofimu mbili ambazo ni ki- umoja na – su ya

mzizi. Ukizigawanya zaidi mofimu hizi utapata k-i-s-u; ambazo ni

sauti/herufi zisizo na maana na si mofimu. Hivyo mofimu si umbo ni maana

– ikiwa ni ya kisarufi au ya kileksika.

Mofolojia hujishughulisha na uundaji wa maneno katika lugha husika;

msingi wa neno ni maana. Hivyo mpangilio wa mofimu usioleta maana

katika lugha husika hauwezi kutambuliwa kama neno. Mfano. palingunywi

ni mfuatano wa fonimu uliozingatia taratibu za lugha ya Kiswahili lakini si

neno la Kiswahili kwa sababu halina maana katika lugha hiyo.

Mambo ya kuzingatia katika taaluma ya mofolojia

Uundaji wa maneno

Hapa tunaangalia vijenzi vya neno husika. Kwa mfano neno limeundwa na

mofimu huru pekee kama papai, mofimu huru na mofimu tegemezi kama

mpapai (m + papai) au mofimu tegemezi tupu kama mtu (m + tu).

Katika uundaji wa maneno tunaangalia vilevile njia mbalimbali za uundaji

wa maneno katika lugha ya Kiswahili kama vile kutohoa, uambatishaji,

urudufu, uhulutishaji, uambishaji, n.k.

NJIA ZA UUNDAJI WA MANENO /ISTILAHI/ MSAMIATI

Uundaji wa maneno ni mchakato unaowezesha lugha kujiongezea msamiati ili

kukidhi haja ya mawasiliano na kuendana na mabadiliko yanayotokea kila siku. Maneno ya lugha ya Kiswahili hayaundwi kiholela bali hufuata taratibu na

kanuni zinazokubalika kitaalamu.

Njia zitumikazo kuunda maneno ni kama zifuatazo:

Unyambuaji

Njia hii inatumia mzizi mmoja wa neno na kuzalisha maneno mapya kwa

kupachika viambishi nyambuaji.

Page 3: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 3

Mfano soma

Somo

Kisomo

Msomi

Msomaji lima

Mkulima

Kilimo

Mlimaji

Uambatishaji/mwambatano

Hii ni njia ya kuunda maneno mapya kwa kuambatanisha maneno mawili.

Mfano

Mwana+chama - Mwanachama

Askari+kanzu – Askarikanzu

Bwana+shamba - Bwanashamba

Urudufishaji / Uradidi

Hii ni mbinu ya kurudiarudia neno au sehemu ya neno na kuunda neno jipya

ambalo huwa na maana tofauti na maneno yanayorudiwarudiwa.

Mfano

(a) Pole : polepole

(b) Sawa : sawasawa

(c) Haraka : harakaharaka

Page 4: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 4

Akronimu/ufupishaji

Ufupishaji ni njia mojawapo ya kuunda maneno mapya, ufupishaji huweza

kufanyika kwa namna mbili ambazo ni.

Kufupisha kwa kuchukua herufi za mwanzo Mfano

CWT (Chama cha Walimu Tanzania) VVU (Virusi Vya Ukimwi)

Kufupisha kwa kuchukua silabi za mwanzo za maneno yanayofupishwa

Mfano

BAKITA (Baraza la Kiswahili la Taifa)

TUKI (Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili)

TATAKI (Taasisi ya Taaluma za Kiswahili)

Uhulutishaji

Ni njia ya kuunda maneno mapya kwa kuchukua vijisehemu vya neno pasipo

kufuata kanuni yoyote.

Mfano:

Mnyama mfu – nyamafu

Chakula cha jioni – chajio

Hati za kukataza – hataza

Mtu asiye kwao - msikwao

Utohoaji

Ni uchukuaji wa maneno toka lugha moja na kuyatumia kwenye lugha nyingine

baada ya kuyarekebisha kimatamshi na kimaandishi ili yaendane na sarufi ya

lugha inayotohoa.

Page 5: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 5

Mfano

Neno Lugha asilia Kiswahili

Shirt Kiingereza Shati

Schule Kijerumani Shule

Bakura Kiarabu Bakora

Benjera Kireno Bendera

Matching guys Kiingereza Machinga

Kuchukua

Hii ni mbinu ya kuongenza maneno kwa kuyachukua toka lugha yake ya asili

na kuyatumia kama yalivyo katika lugha inayotohoa. Uchukuaji hufanyika kwa

lugha zinazoendana kisarufi kama Kiswahili na lugha za kibantu.

Mfano Kitivo — kisambaa /kipare Ikulu - kinyamwezi Kigoda - kizaramo

Kubadili mpangilio wa fonimu Mfano

Lima – mila – imla - mali

Kufananisha umbo /sauti /tabia Mfano

Kufananisha umbo

Kifaru-(mnyama faru)

Mkono wa tembo-(mkonga wa tembo)

Kidole tumbo-(umbo la kidole)

Kufananisha Tabia

Page 6: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 6

Ubeberu-(beberu la mbuzi) Ukupe-(mdudu kupe)

Kufananisha Sauti Pikipiki (mlio wa pikipiki) Mtutu (mlio wa bunduki) Nyau (mlio wa paka) Kuku - kokoriko (mlio wa kuku) Njia ya udondoshaji Mfano

mkwe wake - mkwewe

mwana wake - mwanawe

ndugu yake – nduguye

Kuzingatia matumizi ya kitu Mfano

Banio - (kubana)

Chanio - (kuchana)

Fyekeo - (kufyeka)

Kutarjumi/kutafsiri

Mfano;

Fluid – (ugiligili) Acquired immunal deficiency syndrome - Upungufu wa kinga mwilini

Human immunal virus – virusi vya ukimwi Anti-rentro-virus - dawa za kufubaza makali ya ukimwi

Makundi na mahusiano ya maneno

Taaluma ya mofolojia inaangalia pia makundi ya aina za maneno kama vile

nomino, kitenzi, kivumishi, kielezi, n.k. na wakati huohuo huchunguza

uhusiano uliopo baina ya makundi hayo ya maneno. Kwa mfano kuna uhusiano

wa moja kwa moja baina ya nomino na kivumishi au baina ya kitenzi na kielezi

wakati ambapo hakuna uhusiano huo baina ya kitenzi na kivumishi au baina ya

nomino na kielezi. Aidha, hakuna uhusiano wowote wa kisarufi baina ya

vihisishi na maneno mengine yaliyomo katika tungo.

Page 7: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 7

Kanuni za uundaji wa maneno

Uundaji wa maneno hufuata kanuni mbalimbali za kimofolojia na za

kimofofonolojia. Miongoni mwa kanuni zinazotawala katika kuunda maneno ni

kama vile uyeyushaji, ukaakaishaji, odondoshaji, uingizaji, tangamano la irabu,

mvutano wa irabu, n.k.

Hivyo mwanaisimu yeyote anayejishughulisha na uwanja huu wa mofolojia lazima

ayajue na kuyazingatia kwa kina mambo haya.

MUHADHARA WA 2 : MOFU NA MOFIMU

MOFU

Fasili ya mofu

Mofu ni kipashio cha kimofolojia kiwakilishacho mofimu.kutokana na maana

hii twaweza kusema mofu ni kiwakilishi na mofimu ndiyo iwakilishwayo na

mofu.

Mofu ni umbo linalositiri mofimu. Hivyo mofu ni umbo tu linalodhihirika

kimatamshi kama fonimu/sauti na kimaandishi kama herufi.

Aina za mofu

Mara nyingi mofu huainishwa kwa kutumia vigezo vikuu viwili. Kigezo cha

kwanza ni kwa mujibu wa maana iwakilishwayo na mofu na kigezo cha pili ni

kwa mujibu wa muundo/mofolojia ya mofu yenyewe. Kwa kutumia kigezo cha

maana iwakilishwayo na mofu tunapata mofu huru, mofu funge na mofu tata.

Mofu huru

Ni yale maumbo yanayobeba maana zinazojitosheleza/kamili. Katika

Kiswahili mizizi ya maneno mengi huwa ni mofu huru kwa mfano nomino

(baba, kalamu, Magomeni, n.k.), vivumishi (safi, imara, bora, dhaifu, n.k.),

viwakilishi (sisi, wewe, wao, n.k.), vielezi (leo, haraka, taratibu, n.k.)

viunganishi (na, halafu, lakini).

Mofu Funge/tegemezi

Ni maumbo ambayo husitiri maana zisizojitosheleza. Mofu funge huhitaji

kufungamana na mofu nyengine ili kuzalisha umbo lenye maana kamili.

Kwa mfano; maumbo a, li, tu, lish, na a ni maumbo ambayo hatuwezi kujua

maana zake hadi pale maumbo hayo yatakapounganishwa na kuwa umbo

Page 8: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 8

moja alitulisha. Hapa sasa tunaweza kufafanua maana zilizofichwa ndani ya

maumbo haya ambazo ni:-

Mofu Maana (mofimu)

a- Nafsi (ya tatu)

Idadi (umoja)

Neli (ya kwanza A-WA)

-li- Mtenda

Wakati (uliopita)

-tu- Nafsi (ya kwanza)

Idadi (wingi)

-l- Mzizi

-ish- Usababishi/utendeshi

-a Dhamira arifu

Mofu tata

Ni mofu ambazo hubeba maana zaidi ya moja. Mfano neno ‘atanipikia’ lina

mofu sita (a-ta-ni-pik-i-a), mofu i- (ya pili kutoka kulia) inawakilisha

mofimu/inabeba maana ya utendea ambayo ndiyo chanzo cha utata; kwani

yaweza kueleweka kama:

Kupika kwa niaba yangu

Kupika kwa ajili yangu

Kigezo cha mofolojia ya mofu tunapata mofu kapa na mofu changamano.

Mofu kapa

Ni mofu zisizodhihirika kimatamshi wala kimaandishi ila athari zake zipo na

zinaeleweka kwa wamilisi wa lugha husika. Mofu hizi huwakilishwa kwa

alama Ɵ.

Mfano;

Umoja wingi

u-funguo Ɵfunguo

Ɵjani ma-jani

Ɵsimu Ɵsimu

Page 9: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 9

Mofu changamano

Mofu changamano ni mofu ambazo huundwa kwa kuweka pamoja angalau

mofu huru mbili au mofu funge na mofu huru na kuunda neno lenye kuleta

maana kamili, kwa mfano:

Mofu huru + Mofu huru

- {fundi} + {chuma} = fundichuma.

- {gari} + {moshi} = garimoshi.

Mofu funge + Mofu huru

-{mw} + {ana} + nchi = mwananchi.

{ki} + {ona} + mbali = kionambali.

MOFIMU

Mofimu ni kipashio dhahania cha lugha ambacho husitiriwa na mofu. Hivyo

tunapozungumzia mofimu tunaangalia zaidi maana ambayo ni dhahania na

siyo umbo. Kwa mantiki hii kigezo kikubwa cha kubainisha/kutambua

mofimu ni maana.

Aina za mofimu

Mofimu huru

Ni mofimu inayojitosheleza kimaana bila ya kuongezwa kiambishi cha aina

yoyote. Ina uwezo wa kusimama pekee kama neno. Mfano; Maryam, paka,

simu, papai, n.k.

Mofimu tegemezi

Ni aina ya mofimu ambazo hazijitoshelezi kimaana. Mofimu hizi hukamilika

kimaana zinapoongezwa mofimu nyengine. Haziwezi kusimama pekee kama

neno. Mfano; ki-tabu, m-tu, mu-ana-funz-i, n.k.

Matatizo ya utengaji/ubainishaji wa mofimu

Tatizo la kwanza ni kukosekana kwa umbo dhahiri la mofimu

Mfano: θ+chungwa : ma+chungwa

θ+bega : ma+bega θ+jiwe : ma+we

θ+shati : ma+shati

Page 10: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 10

Katika mifano hiyo mofimu za umoja ni //θ// na za wingi ni //ma//

Tatizo la pili ni kukosekana maneno asilia yanayozalisha maneno unde.

Mfano:

Fupi – fupika –fupisha Refu - refuka –refusha

*Kau – kauka – kausha

Mifano hiyo ina maneno asilia na maneno unde. Maneno (fupi na refu) ni maneno

asilia ya maneno unde fupisha na refusha. Lakini (kau) sio neno asili la neno

(kauka na kausha) kwa sababu neno hilo (kau) halikubaliki kwa maneno ya namna

hiyo.

Tatizo la tatu ni ugumu wa kutenganisha mofimu katika maneno mwambatano.

Mfano:

Mwanajeshi

Mu-ana-jeshi

Mw-ana-jeshi

Mw-an-a-jeshi

Mw-anajeshi

Maneno mwambatano yanaundwa kwa mzizi zaidi ya mmoja hivyo huwa ni

vigumu kubaini mofimu ni zipi na mizizi ni ipi.

KANUNI ZA KUTENGANISHA MOFIMU

Kanuni ya kwanza; zingatia maumbo yenye maana sawa. Maumbo hayo

huweza kufanana au kuhitilafiana kiumbo lakini hutokea katika mazingira

yaleyale.

Mfano

a) atakupiga

b) atampiga

ata-ku-pig-a

a-ta-m-pig-a

Page 11: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 11

c) alikupiga -li-ku-pig-a

d) utanipiga -ta-ni-pig-a

e) utatupiga -ta-tu-pig-a

f) mlijipiga -li-ji-pig-a

Mofimu

1. mofimu nafsi --------- (a)-3-umoja

--------- (u)-2-umoja

---------- (m)-2-wingi

---------- (tu)-1-wingi

2. mofimu njeo ------------- (ta)-ijayo

------------- (li)-iliyopita

-------------- (na)-iliyopo

3. yambwa ---------------- (ku)-wewe

--------- (m)-yeye

---------- (ni)-mimi

----------- (ji)-binafsi

Kanuni ya pili; Hapa kinachozingatiwa ni maumbo yenye maana moja

lakini yasiyo na umbo sawa la kimofolojia.

Mfano; a) mtumwa b) mvulana

c) mjakazi

d) mwenzi

e) mwanadamu

watumwa wavulana wajakazi wenzi

wanadamu

Page 12: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 12

mofimu mofimu za idadi

//umoja//---------m/-k -------- mw/-i

//wingi//--------- wa/-k ---------- w/-I

Kanuni ya tatu; Kanuni hii inadai kuwa alomofu moja au zaidi zimo katika

mtawanyo mkamilishano ambapo moja ikitokea basi ya pili haitokei. Yambwa na

yambiwa haziwezi kutokea katika mazingira yale yale.

Mfano

Baba alinimpigia mimi simu

Sisi tuliwamuona nyinyi

Yeye alimwakuta wao

(m) na (mu)

(wa) na (w)

Zimo katika mtawanyo mkamilishano au mgawanyo wa kiutowano

Kanuni ya nne; Umbo moja na zaidi huweza kuwa katika mpishano huru kama

maumbo hayo yana maana moja na yametokea katika mazingira yaleyale. Mfano ngombe badala ya ng’ombe

khabari badala ya habari

lafiki badala ya Rafiki

ntoto badala ya mtoto

Kanuni ya tano; inadai kuwa maumbo yenye maana tofauti ni mofimu

na maumbo tofauti yenye maana sawa ni alomofu.

Page 13: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 13

MUHADHARA WA 3 : ALOMOFU

Fasili ya alomofu

Alomofu ni maumbo mbalimbali yanayowakilisha dhana moja ya kisarufi.

Alomofu ni maumbo mbalimbali ya mofimu moja.

Alomofu hufafanuliwa kama maumbo zaidi ya moja (mbalimbali) ya mofimu

moja.

Mazingira ya utokeaji wa alomofu

Alomofu hazitokei kibahati nasibu tu. Mara nyingi utokeaji wa alomofu fulani

unategemea kupatikana kwa mazingira mahususi. Mazingira hayo yanaweza

kuelezeka kifonolojia, kileksika na kisarufi.

Mazingira ya kifonolojia

Kuna baadhi ya alomofu utokeaji wake hutegemea kuwepo au kutokuwepo kwa

sauti/fonimu fulani. Kwa mfano; mofimu iwakilishayo umoja katika ngeli ya KI-

VI hujitokeza kwa umbo la ki- ikifuatiwa na konsonanti lakini mofimu hiyo hiyo

huwakilishwa na umbo la ch- ikifuatwa na irabu.

Mfano:

Ki +tabu = kitabu, ki+buyu = kibuyu, ki+sima = kisima

Ki+umba = chumba, ki+ama =chama, ki+etu = chetu, ki+ekundu = chekundu

Mazingira ya kileksika (kikamusi/kimaana)

Alomofu pia hujitokeza kutokana na mazingira ya kileksika. Tofauti na mazingira

ya kifonolojia ambayo aghalabu hutabirika mazingira ya kileksika hayatabiriki na

hutegemea zaidi neno husika.

Mfano:

Mtume ---------mitume

Waziri---------mawaziri

Kiongozi ----viongozi

Malaika --------malaika

Page 14: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 14

Mganga --------waganga

Kwa kuzingatia mazingira ya kileksika ya mifano hapo juu tunaweza kusema kuwa

mofu ya umoja //m// inaweza kujitokeza kama //m//, /θ/ na /ki/ wakati mofu ya

wingi //wa// inajitokeza kama //mi//, //ma//, //vi// na // θ //.

Mazingira ya kisarufi

Wakati mwengine alomofu hutokea kwa sababu za kisarufi. Mfano mzuri

unapatikana katika mofimu za njeo. Mabadiliko ya wakati unaohusishwa na tendo

husababisha kupatikana kwa maumbo mbalimbali yawakilishayo njeo. Angalia

mifano ifuatayo:

A B

Anaandika - haandiki

Aliandika - hakuandika

Ataandika - hataandika

Ameandika - hajaandika

Kutokana na mifano hii maumbo yanayowakilisha njeo katika kifungu A ni //na//,

/li//, //ta// na //me// yanayoashiria wakati uliopo, wakati uliopita (muda mrefu) na

wakati uliopita (muda mfupi) hali yakinishi na katika kifungu B ni //i//, //ku//, //ta//

na //ja// yanayowakilisha nyakati hizohizo katika ukanushi.

Aina za alomofu

Alomofu za njeo : ----- -na-, -li-, -me-, -ta-, -ku-, -ja- (anasoma, alisoma,

amesoma, atasoma, hakusoma, hajasoma).

Alomofu za nafsi : ni, tu, u, m, a, wa (ninasoma, tunasoma, unasoma,

mnasoma, anasoma, wanasoma).

Alomofu za wingi : mi-, vi, wa-, ma-, n.k. (miti, vijiko, watoto, majembe)

Alomofu za umoja : ki-, m-, u-, li-, n.k. (kibanda, mkeka, ukuta, limeoza)

Alomofu za usababishi/utendeshi : ish, esh, z, fy, vy, sh (katisha, somesha,

liza, ogofya, levya, safisha)

Alomofu za ukanushi : si, ha, (hu-) (siandiki, haandiki, h(a)uandiki)

Page 15: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 15

Alomofu za urejeshi : ye, cho, po, vyo, ko, n.k. (aliyeondoka, kilichozama,

nilipokosa, ulivyokurupuka, walikokimbilia)

Alomofu za masharti : ki, nge, ngeli, ngali, ngeli, kama, endapo (akija,

angekuja, angalikuja, kama atakuja, endapo atakuja)

MUHADHARA WA 4 : KIAMBISHI

Fasili ya kiambishi

Kiambishi ni mofu iongezwayo kwenye mzizi wa neno na kuwakilisha maana ya

kisarufi.

Aina za viambishi

Aghalabu viambishi huainishwa kwa kutegemea mahali ambapo viambishi hivyo

huwekwa katika neno. Hivyo kwa ujumla tunapata aina kuu tatu za viambishi

ambazo ni; viambishi awali, viambishi ndani/kati na viambishi tamati.

Viambishi awali

Ni viambishi ambavyo huwekwa kabla ya mzizi wa neno. Mfano; neno

tunakuja……tu-na-ku ni viambishi awali vilivyowekwa kabla ya mzizi wa

neno –j- . mifano mingine ni hatulimi, wanasoma, n.k.

Viambishi ndani/kati

Hivi ni viambishi ambavyo huwekwa katikati ya mzizi wa neno. Hakuna

mfano wa neno la Kiswahili lenye kiambishi ndani kwa sababu lugha ya

Kiswahili haina muundo huo. Mifano tunaweza kuipata katika lugha

nyingine kama vile lugha ya Kibari kutoka Sudani ya kusini. Katika lugha

hii mofimu ya idadi huoneshwa kwa kutumia viambishi ndani. Mfano;

Popon ------------------------ shimo (umoja)

Popojin ---------------------- mashimo (wingi) –ji ni kiambishi ndani cha

wingi.

Bun ----------------------------- kitabu (umoja)

Bukan ------------------------ vitabu (wingi) –ka- ni kiambishi ndani cha

wingi.

Viambishi tamati

Ni aina ya viambishi ambavyo huwekwa baada ya mzizi wa neno.

Mfano

Page 16: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 16

Chumbani ------------------ chumba (mzizi) + -ni (kiambishi tamati)

Somo ------------------------som (mzizi) + -o (kiambishi tamati)

Pikisha --------------------- pik (mzizi) + ish + -a (viambishi tamati)

Kutokana na maelezo na mifano ya hapo juu tunaona kuwa lugha ya

Kiswahili ina aina mbili tu za viambishi; viambishi awali na viambishi

tamati. Jambo la kuzingatia ni kwamba viambishi vya aina zote huweza

kujitokeza katika neno moja la Kiswahili. Kwa mfano hatujawapigisheni-

maumbo yaliyokolezwa wino kabla ya mzizi –pig- ni viambishi awali na

yale yaliyo baada ya mzizi ni viambishi tamati. Vilevile tunaona kuwa

viambishi ni maumbo tegemezi yanayofanya kazi ya kuleta maana

yanapounganishwa na mzizi tu. Na pia tumegusia kuwa viambishi

huwakilisha maana za kisarufi tu.

Mpangilio wa viambishi

Katika lugha ya Kiswahili viambishi ni vingi. Na kama ilivyogusiwa hapo

juu kuwa vinaweza kujitokeza kwa pamoja katika neno moja ili kutoa maana

fulani ya kisarufi. Hivyo basi ni lazima kuwe na utaratibu maalumu wa

kuvipanga viambishi katika mzizi wa neno ili neno litoe maana na taarifa

iliyokusudiwa. Katika sehemu hii tutaonesha mpangilio wa viambishi katika

maneno ya lugha ya Kiswahili. Tutaangalia zaidi kitenzi na nomino.

Mpangilio wa viambishi awali katika kitenzi

Kwa kawaida kitenzi huanza na kiambishi nafsi, mfano a-cheka

Kiambishi nafsi hufuatiwa na kiambishi cha wakati mfano alicheka

Kiambishi cha wakati hufuatiwa na kiambishi rejeshi mfano

aliyecheka

Kiambishi rejeshi hufuatiwa na kiambishi yambwa/yambiwa mfano

aliyemcheka.

Mpangilio wa viambishi tamati katika kitenzi

Kama ilivyoelezwa awali kuwa viambishi tamati ni vile vinavyokaa baada

ya mzizi wa neno. Aghalabu viambishi tamati huwa ni vya mnyambuliko na

hutokea kimoja tu katika neno.

Mfano;

Wanapigwa – utendwa.

Wanapigana – kutendana

Page 17: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 17

Wanapigika – kutendeka

Wanapigisha – kutendesha

Wanapigiana – kutendeana, n.k.

Hata hivyo, iwapo kitenzi kitakuwa na viambishi tamati zaidi basi mzizi huo

huwa ni mzizi wa mnyambuliko na aghalabu unakuwa umeundwa kwa kiini

cha neno na mofimu ya kutendana (mf. pigan). Ikiwa mzizi una kiambishi

cha kutendana //an//, baadaye huja kiambishi cha kutendesha //sh,ish,esh//

n.k. na kisha hufuata kiambishi cha utendeka //ik, ek// au kiambishi cha

utendwa //w// (hutegemea na taarifa inayotolewa) na kumalizia na kiambishi

–a kinachokamilisha maana. Chunguza utaratibu huu katika maneno

yafuatayo:

Tuliowapiganisha

Tumepiganishika

Tumepiganishwa

Mifano iliyotolewa hapo juu ni ya vitenzi yakinifu tu. Hata hivyo, ni vyema

ieleweke kuwa utaratibu huu hufanya kazi hata katika hali ya ukanushi

isipokuwa kiambishi cha ukanushi si, ha (hu) hutokea mwanzoni kabisa

kabla ya kile cha nafsi.

Mfano.

Utapika ---------------- h(a)utapika (wakati ujao)

Tumepigana ---------- hatujapigana (wakati uliopita – muda mfupi)

Walitufurahisha --------- hawakutufurahisha (wakati uliopita)

Hata hivy, hali huwa tofauti kidogo kwa upande wa wakati uliopo kwani

kiambishi cha wakati na hudondoshwa na umbo la kitenzi humalisika kwa

irabu i badala ya a kama ilivyozoeleka. Kuna wataalamu wanaodai kuwa hii

irabu ya mwisho i ndicho kiambishi cha wakati uliopo katika ukanushi.

Mfano:

Tunasoma – hatusomi (*hatunasoma)

Ninapika – sipiki (*sinapika)

Mpangilio wa viambishi katika nomino

Aghalabu nomino huweza kuandamana na viambishi vya aina tatu tu. Viambishi

hivyo ni bya idadi (umoja na wingi), ukubwa na udogo. Mfano;

Mtoto (m ya umoja) kitoto (ki ya udogo) jitoto (ji ya ukubwa) kijitoto (ki ya

umoja na udogo na ji ya udogo).

Watoto – vitoto- mitoto – mijitoto – vijitoto

Page 18: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 18

Wakati mwingine hutokea nomino ikabeba viambishi vya aina mbili kwa pamoja.

Katika hali hiyo kiambishi cha idadi hutangulia na ndipo kikaja kiambishi cha

ukubwa/udogo kama ilivyo katika mifano hapo juu.

Viambishi nominishi: ni vile ambavyo vinapoambikwa katika neno lisilokuwa

nomino hulifanya neno hilo kuwa nomino.

Mfano

Ji > mchoraji, mtangazaji, uimbaji, muuaji, upimaji, n.k.

Zi> Upekuzi, uchaguzi, ufafanuzi

i > Ushindi, uchunguzi, ubishi, msomi

O > Somo, upendo, mkopo

fu > udanganyifu, usahaulifu, uchangamfu, usumbufu

kama ilivyoelezwa katika mifano hapo juu, utokeaji wa viambishi hivi aghalabu

huambatana na utokeaji wa viambishi awali vya nomino vinavyodokeza idadi,

udogo au ukubwa wa nomino (m/wa, ki/vi, u, ma, n.k.)

viambishi elezi: ni vile ambavyo vinapoambikwa katika neno lisilokuwa kielezi

hulifanya neno hilo kuwa kielezi.

Mfano

ni > sokoni, barabarani, darasani, n.k

ki > kijeuri, kiume, kikatili

vi > vizuri, vibaya

MUHADHARA WA 5 : MZIZI

Fasili ya mzizi

Mzizi ni neno au sehemu ya neno ambayo hubeba taarifa ya msingi na

haibadilikibadiliki.

Sifa bainifu za mzizi

Mzizi hubeba taarifa ya kileksika

Mzizi haubadilikibadiliki

Mzizi ni mofu muhimu kuliko mofu zote katika neno

Mzizi hauwezi kuachwa wakati wote neno linapotumika

Page 19: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 19

Aina za mzizi

Mzizi huru: ni mzizi usiopokea kiambishi cha aina yoyote. Mfano; mama,

sawa, chungwa, n.k.

Mzizi funge: ni mzizi unaoandamana na viambishi ili kukamilisha maana

mfano; kisu, mti, n.k. –su na –ti ni mfano wa mizizi ya maneno ambayo

maana zake hupatikana baada ya kufungamanishwa na viambishi.

Mzizi asilia: ni mzizi unaotokana na kiini cha neno. Mfano wa mzizi asilia

ni andik- katika neno andika, kat- katika neno kata, n.k.

Mzizi wa mnyambuliko: ni mzizi unaotokana na mzizi asilia pamoja na

viambishi. Kwa mfano andikish- ni mzizi wa mnyambuliko unaoweza

kuzalisha maneno kama andikisha, andikishwa, andikishana, andikishia, n.k.

na pigan- ni mzizi wa mnyambuliko unaoweza kuzalisha maneno kama vile

pigana, oigania, piganiwa, piganisha, n.k

Miundo ya mzizi

Neno zima: mf. sungura, mbuzi, kopo, bibi

Konsonanti pekee: mf. –p- katika nipe, -f- katika kifo

Irabu pekee: mf. –u- katika usiniue, o- katika wameoana

Silabi moja: mf. –ki katika kiti, to- katika toa, li-katika lia

Silabi moja au zaidi pamoja na sehemu tu ya silabi nyingine : mf. som-

katika soma, kat-katika kata, andik-katika andika, tafut-katika tafuta.

Silabi zaidi ya moja : mf. kimbi- katika kimbia, fafanu-katika ufafanuzi.

MUHADHARA WA 6 : NENO

Fasili ya neno

Neno ni kipashio cha kiisimu kinachoundwa na mofimu moja au zaidi na kutoa

maana fulani katika lugha husika. Maana hiyo yaweza kuwa ya kisarufi au ya

kileksika.

Aina za maneno

Maneno hugawanywa katika aina zake kwa vigezo viwili ambavyo ni: kigezo cha

muundo na kigezo cha kazi.

Page 20: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 20

Aina za maneno kimuundo

Neno sahili : ni neno linaloundwa kwa mzizi huru mmoja (mf. mama, wewe,

maji, hewa, n.k)

Neno ambatani : ni neno linaloundwa kwa mizizi miwili. Yawezekana ikawa

ni mzizi funge na mzizi huru au mizizi huru miwili (mf. mwanaanga,

mwanahewa, bwanashamba)

Neno changamano : ni neno linaloundwa kwa mzizi funge pamoja na

viambishi mbalimbali (mf. mapigo, mwendeshaji, n.k.)

Aina za maneno kikazi/kiuamilifu

Kwa kutumia kigezo cha kazi/uamilifu tunapata aina zifuatazo za maneno:-

Nomino (N)

Kiwakilishi (w)

Kivumishi (V)

Kitenzi (T)

Kielezi (E)

Kihusishi (H)

Kiunganishi (U)

Kihisishi/Kiingizi (I)

TAARIFA ZINAZOPATIKANA KATIKA NENO

Taarifa ya kifonolojia

Ni kujua fonimu zilizotumika kuunda neno hilo. Mf. neno /paka/ limeundwa

na fonimu /p/, /a/ na /k/

Taarifa ya kimofolojia

Ni kujua mofimu zinazounda neno hilo. Mf. neno /paka/ limeundwa kwa

mofimu moja huru na neno /mtu/ limeundwa na mofimu tegemezi mbili m-

na -tu

Taarifa ya kisintaksia

Ni kujua aina ya neno kulingana na uamilifu wake katika tungo. Mf;

(a) Kitu chema hakidumu (b) chema hakidumu

Page 21: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 21

Neno chema katika (a) ni kivumishi na neno chema katika (b) ni

kiwakilishi. Tunajua aina ya neno kwa kuangalia kazi na nafasi yake katika

tungo.

Taarifa ya kisemantiki

Ni kujua maana ya neno. Ili mkusanyiko wa silabi ukubalike kuwa ni neno

lazima uwe na maana katika lugha husika; hivyo mkusanyiko usioleta maana

si neno. Mf; paletihoju ni mkusanyiko wa silabi usioleta maana katika lugha

ya Kiswahili na hivyo hili si neno la Kiswahili.

Neno na leksimu

Imeelezwa katika fasili ya neno kwamba neno lazima liwe na maana ya

kisarufi au ya kileksika/kikamusi. Neno lenye maana kileksika huweza

kusimama peke yake kama kidahizo katika kamusi. Hivyo basi tunaweza

kusema leksimu ni kipashio cha kidhahania ambacho ni cha msingi katika

msamiati wa lugha na hubeba dhana ya kwanza ya neno. Ni maneno yenye

maana za kileksika ambayo huwa vidahizo katika kamusi.

Mfano;

Doa ji/ma – 1. Alama au tone ambalo lina rangi tofauti na mwili wa kitu

2. Aibu, dosari, ila, kasoro.

Maneno yenye maana za kisarufi ambayo hayawezi kutumika kama kidahizo

katika kamusi yanabaki kuwa maneno tu lakini si leksimu.

NENO NA MOFIMU

Neno ni mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa au kuandikwa na kuleta maana

fulani katika lugha. Mkusanyiko huo wa silabi unaweza kuwa ishara ya

maana ya kileksa au maana kisarufi.

Mofimu kwa upande mwingine ni kipashio cha kiisimu chenye maana ya

kileksika au kisarufi. Maneno huweza kuwa na mofimu moja au zaidi lakini

si lazima wakati wote iwe neno.

LEKSIMU NA MOFIMU

Leksimu ni kipashio kidogo cha msamiati kinachoweza kusimama peke yake

katika kamusi kama kidahizo. Mofimu inaweza kusimama peke yake hasa

ikiwa mofimu huru.

MUHADHARA WA 7: NENO (Aina za Maneno – Nomino)

Nomino: ni maneno ambayo hutaja majina ya watu, vitu, mahali, vyeo,

dhana na hata tendo.

Aina za nomino

Nomino za pekee

Page 22: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 22

Nomino za kawaida

Nomino za dhahania

Nomino za jumla

Dhima ya nomino

Kiima cha sentensi: Juma analima

Yambwa : Juma amenunua kitabu

Yambiwa : Juma amemnunulia Ali kitabu

Kijalizo : Juma ndiye kiongozi wetu

MUHADHARA WA 8 : NGELI ZA NOMINO (Mkabala wa Kimofolojia)

Fasili ya ngeli

Ni uwekaji wa nomino katika makundi mbalimbali kulingana na vigezo maalumu.

Vigezo hivyo vyaweza kuwa vya kimofolojia, kisintaksia n.k. kutokana na vigezo

hivyo ndipo tunapopata migawanyo tofauti ya ngeli; kama mgawanyo wa ngeli

kimapokeo na mgawanyo wa ngeli kimamboleo/kisasa.

Mgawanyo wa ngeli za nomino kimapokeo

Huu ni uainishaji wa ngeli kwa kutumia kigezo cha mofolojia ya nomino.

Tunapotumia kigezo hiki kugawa nomino za Kiswahili katika ngeli tunazingatia

zaidi viambishi awali vya idadi – umoja na wingi ambavyo ni vya kawaida katika

nomino hizo – si viambishi vyenye kuonesha dhana ya ukubwa na udogo. Kwa

kigezo hiki tunapata makundi yafuatayo ya ngeli:-

a) Ngeli ya M(U) – WA (Mtu-watu, mtoto-watoto)

b) Ngeli ya M-Mi (mti-miti, mkono-mikono)

c) Ngeli ya JI-MA (jicho-macho, jiwe-mawe)

d) Ngeli ya KI-VI (kinu-vinu, kiwete-viwete)

e) Ngeli ya U-N (ulimi-ndimi, ufa-nyufa)

f) Ngeli ya U-MA (uamuzi-maamuzi, upishi-mapishi)

g) Ngeli ya U-Ɵ (upawa- Ɵpawa, ukucha- Ɵkucha)

h) Ngeli ya Ɵ-MA (Ɵchungwa-machungwa, Ɵjani-majani)

i) Ngeli ya Ɵ- Ɵ (Ɵnyumba- Ɵnyumba, Ɵnguo- Ɵnguo)

UBORA WA KIGEZO CHA KIMOFOLOJIA

Page 23: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 23

a) Uwezekano wa kuzigawa nomino nyingi za Kiswahili ni mkubwa kwa kuwa

nyingi zimegawanyika katika maumbo hayo ya umoja na wingi.

b) Ni kigezo muhimu kwani kinajikita zaidi katika nomino na kivumishi chake

peke yake hakigusi aina nyingine ya neno tofauti na kigezo cha kisintaksia

ambacho hugusa hadi kitenzi.

c) Huwasaidia wanasarufi linganishi kuonesha uhusiano wa lugha za kikoa

kimoja.

d) Kilisaidia kuondokana na uainishaji ngeli kwa kutegemea tofauti za

kibayolojia.

e) Kinasaidia kutambua mofolojia ya nomino kama ni huru au changamano.

UDHAIFU WA KIGEZO CHA KIMOFOLOJIA

a) Kuna viambishi katika ngeli tofauti vinavyofanana. Mfano Kiambishi M-

kinajitokeza katika ngeli ya 1 na 3 na MA- inajitokeza katika ngeli ya 8 na

13.

b) Kuna nomino nyingine ambazo hazijidhihirishi katika umoja na wingi.

Mfano ngeli ya 8 na 9.

c) Nomino zenye hadhi tofauti kuwekwa kwenye ngeli moja mf. (kiwete,kinu),

(sikio,tawi).

d) Kuna matumizi ya vigezo viwili kwa pamoja, kigezo cha maumbo ya idadi

na kigezo cha sifa za nomino.

e) Idadi ya ngeli ni kubwa na hivyo humfanya msomaji kupata tabu ya

kuzikariri.

f) Wanamapokeo wamegawanyika pasipo sababu za msingi, kuna wenye ngeli

18, 16 na 9.

MUHADHARA WA 9 : MGAWANYO WA NGELI ZA NOMINO KIMAMBOLEO

Huu ni uainishaji wa ngeli kwa kutumia kigezo cha sintaksia ya nomino. Uainishaji

huu huzingatia uhusiano wa nomino na maneno mengine katika tungo kwa

kuangalia viambishi vya upatanishi wa kisarufi vinavyojitokeza mwanzoni mwa

maneno yanayoandamana na nomino katika tungo. Viambishi hivyo huathiriwa na

umbo la nomino inayozungumzwa katika tungo husika. Kwa kutumia kigezo hiki

tunapata makundi yafuatayo ya ngeli:-

Page 24: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 24

a) Ngeli ya YU-A/WA: mtoto yuasoma/mtoto anasoma-watoto wanasoma

b) Ngeli ya U-I: mkoba umechanika-mikoba imechanika

c) Ngali ya LI-YA: debe linauzwa-madebe yanauzwa

d) Ngeli ya KI-VI: kiatu kimetupwa-viatu vimetupwa

e) Ngeli ya I-ZI: ndizi imeiva-ndizi zimeiva

f) Ngeli ya U: ushawishi umemponza-ufisadi umekithiri

g) Ngeli ya U-YA: ugonjwa umetukatisha tamaa-magonjwa yametukatisha

tamaa

h) Ngeli ya U-ZI: ungo umeharibika-nyungo zimeharibika

i) Ngeli ya YA: maji yanamwagika, mafuta yamekwisha

j) Ngeli ya I: chai imenywewa

k) Ngeli ya KU: kulima kunakondesha, kula kwake kutamdhuru

l) Ngeli ya PA-MU-KU: kiwanjani petu panafaa, nyumba munagiza, kule

kunatisha

UBORA WA MTAZAMO WA KISASA

Kigezo cha kisintaksia kinachotumiwa katika mtazamo wa kisasa kugawa ngeli

kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi kina ubora wake kama ifuatavyo:

Kimepunguza makundi mengi ya ngeli za nomino

Ni rahisi kuzikariri kwani ni chache.

Kila nomino huweza kuingia katika ngeli yake kwa kuzingatia upatanisho

wa kisarufi.

Nomino hupangwa katika ngeli zake kulingana na sifa na hadhi yake.

Husaidia kubaini umoja na wingi wa nomino zisizo na maumbo dhahiri ya

idadi.

Page 25: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 25

Kigezo hiki kimepunguza kujirudiarudia kwa ngeli.

Husaidia kubainisha uhusiano wa nomino na maneno mengine katika tungo.

Husaidia kuonesha urejeshi wa vitenzi na nomino zake.

UDHAIFU WA MTAZAMO WA KISASA

Bado kuna ngeli za nomino zinazojirudia mf. Ngeli ya 2,6 na 7 umoja

zinatumia u.

Ngeli ya kwanza umoja ina viambishi viwili (Yu/A)

Bado kuna nomino zenye kuleta mgogoro katika ngeli mf. Makala, Jambazi,

marashi.

Pamoja na umoja na wingi kutawala, kigezo cha sifa ya nomino hujitokeza

ili kuepuka kuchanganya majina yenye sifa na hadhi tofauti mf. Kinyonga

hukubali zaidi ngeli ya (KI-VI) lakini huwekwa katika ngeli ya kwanza kwa

sifa ya kiumbe hai.

Kigezo hiki hakijaweza kuonesha mofolojia ya nomino.

MUHADHARA WA 10: VIWAKILISHI

Fasili ya viwakilishi

Viwakilishi ni maneno yanayosimama badala ya nomino au kikundi nomino.

Muundo wa viwakilishi

Kwa ujumla viwakilishi hujitokeza katika miundo miwili. Kiwakilishi huweza

kuwa huru au kiambata. Kiwakilishi huru ni kile kinachosimama pekee kikiwa

neno kamili kama vile mimi, yeye, nani, nini, n.k. kwa upande wa kiwakilishi

kiambata ni kiwakilishi ambacho huambatanishwa mwanzoni mwa kitenzi.

Aina za viwakilishi

1. Viwaklishi vya sifa : kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza

2. Viwakilishi vya idadi: wawil wameokolewa, mmoja hajulikani alipo.

Page 26: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 26

3. Viwakilishi vioneshi: yule habebeki, huyu nampenda

4. Viwakilishi viulizi: ipi unaitaka? Lipi limekuudhi?

5. Viwakilishi vimilikishi: wangu ni mweusi, wao amezidi mno

6. Viwakilishi nafsi: mimi sijali, nyinyi mnacheza

Nafasi ya kiwakilishi: kiwakilishi hutokea badala ya nomino/huchukua nafasi ya

nomino pale ambapo nomino haipo.

MUHADHARA WA 11 : VIVUMISHI

Fasili ya kivumishi

Vivumishi ni maneno ambayo huandamana na nomino ili kuongeza sifa au taarifa

muhimu kwa nomino (huifanya nomino ivume).

Muundo wa vivumishi

Kwa kutumia kigezo cha kimuundo kuna aina mbili za vivumishi ambazo ni:

Vivumishi vinavyoambishwa mf; dogo, refu, chungu, zuri, n.k

Vivumishi vinaweza kuambishwa kulingana na upatanishi wa kisarufi wa

nomino inayovumishwa. Hivyo tunaweza kupata tungo kama ki+dogo,

wa+refu, m+chungu, vi+zuri, n.k

Vivumishi visivyoambishwa-aghalabu vivumishi vya aina hii hutokana na

maneno yenye asili ya lugha ya Kiarabu mf; Jamali,dhaifu,n.k

Aina za vivumishi

Vivumishi vya sifa: hivi ni aina ya vivumishi vinavyotoa sifa ya nomino.

Mfano kitambaa kizuri, mti mrefu, mwanafunzi mvivu, mtandio mweupe.

Jambo la kuzingatia hapa si lazima ile sifa iwe njema hata sifa mbaya pia ni

kivumishi.

Page 27: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 27

Vivumishi vya idadi: hivi ni vivumishi vinavyoonesha idadi ya vitu

mbalimbali. Mfano watoto wawili, nyumba moja.

Vivumishi vya idadi vinaweza kujitokeza katika aina tatu ndogondogo.

- Vivumihi vya aina hii hutoa taarifa kuhusu idadi ya nomino ambazo kiwango

chake kimetajwa.

- Vivumishi vya idadi vinavyoweza kuvumisha nomino kwa kutaja idadi ya

nomino hizo kiujumla jumla bila kudhihirisha idadi halisi.

- Vivumishi vya idadi ambavyo huonesha nafasi iliyochukuliwa na nomino

fulani katika orodha.

Vivumishi vya kuonesha:vivumishi vya aina hii huonesha mahali au upande

kitu kilipo. Vivumishi vya aina hii hujengwa na mzizi {h} kwa vitu

vilivyopo karibu na mzizi {le} kwa vitu vilivyo mbali. mfano kijana huyu,

kuku wale

Vivumishi vya pekee: vivumishi hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila

kimojwapo huwa na maana maalumu. Pia kila kimojawapo huchukua

upatanisho wake wa kisarufi kulingana na ngeli ya nomino ambayo

kinaivumisha. Mizizi ya vivumishi hivi ni ote, o-ote, enye, enyewe, ingine,

ingineo. Mfano chakula chochote, wakati wowote

Vivumishi viulizi: hivi ni vivumishi ambavyo hufafanua nomino kwa

kuuliza habari zake. Mfano nguo ipi? Msichana yupi?watu wangapi?

Vivumishi vya jina kwa jina: ni vivumishi ambavyo jina huvumisha jina

lililotangulia katika mfuatano. mfano mwalimu Majaliwa, Mzee kipofu

Vivumishi vimilikishi: ni vivumishi vinavyoonesha kuwa kitu fulani kina

milikiwa na mtu au kitu kingine mfano: mali yangu, paka wako, nchi yetu

MODULI 4: VITENZI, VIELIZI NA VIUNGANISHI

VITENZI (T)

Page 28: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 28

Vitenzi ni maneno yanayosimamia kitendo. Kila kitenzi huwa na shina la

kitenzi (sehemu ndogo zaidi ya kitenzi ambayo ndiyo huwakilisha tendo hilo).

Shina la kitenzi huambatanishwa na viambishi ili kutoa maana iliyokusudiwa

kama vile mtendaji, mtendewa, wakati kitendo kinafanyika na pia kauli ya

kitenzi hicho.

Aina za Vitenzi

Vitenzi Halisi

Vitenzi Visaidizi + Vitenzi Vikuu

Vitenzi Vishirikishi

Vitenzi Sambamba

Vitenzi Halisi

Hivi ni vitenzi vinavyorejelea kitendo moja kwa moja. Vitenzi halisi

vinapoambatanishwa na vitenzi vidogo katika sentensi, huitwa vitenzi vikuu.

k.m: soma, kula, sikiza

Waziri Mwasimba aliwasili jana kutoka ng'ambo.

Kawia atapikia wageni.

Funga mlango wa dirisha.

Vitenzi Visaidizi

Vitenzi visaidizi hutangulia vitenzi halisi (vitenzi vikuu) katika sentensi ili

kuleta maana inayokusudiwa kulingana na wakati au hali.

k.m: -kuwa, -ngali,

Jua lilikuwa limewaka sana.

Bi Safina angali analala

Vitenzi Vishirikishi

Page 29: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 29

Vitenzi vishirikishi hutumika kuelezea hali iliyopo au mazingira. Kuna aina

mbili za vitenzi vishirikishi:

a) Vitenzi Vishirikishi Vipungufu - havichukua viambishi vyovyote.

k.m: ni, si, yu

Kaka yako ni mjanja sana.

Huyo si mtoto wangu!

Paka wake yu hapa.

b) Vitenzi Vishirikishi Vikamilifu - huchukua viambishi vya nafsi au ngeli.

Vitenzi hivi vinaweza kusimama peke yake au vinaweza kufuatiliwa na vitenzi

vikuu.

k.m: ndiye, ndio, ndipo

Sanita ndiye mkurugenzi wa kampuni

Huku ndiko kulikoibiwa

Muundo wa Vitenzi

Kwa kuzingatia muundo wa vitenzi, tunaweza kuweka vitenzi katika aina

zifuatazo:

1. Vitenzi vya Silabi Moja

2. Vitenzi vya Kigeni

3. Vitenzi vya Kibantu

Vitenzi vya Silabi Moja

Hivi ni vitenzi vyenye silabi moja pekee. Ili kuleta maana kamili, vitenzi hivi

huambatanishwa na kiungo KU- katika kauli ya kutenda. Kama vitenzi vingine,

vitenzi vya silabi moja vinaweza kunyambuliwa.

k.m: soma, kula, sikiza

1. -cha - kucha - jua linapochomoza asubuhi k.m kumekucha

Page 30: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 30

2. -fa - kufa - kuacha kupumua, kupoteza uhai k.m amekufa

3. -ja- kuja - fika mahali hapa k.m nimekuja

4. -la- kula - kutia chakula mdomoni k.m anakula

5. -nya- kunya - kutoa mabaki ya chakula toka tumboni k.m mtoto amekunya

6. -nywa- kunywa - kutia kinywaji kama vile maji au maziwa mdomoni k.m

ninakunywa uji

7. -pa- kupa - kumkabithi/kumpatia mtu kitu k.m amenipa pesa

8. -pwa- kupwa - kujaa hadi pomoni - k.m kisima kimekupwa maji

9. -twa- kutwa - jua linapozama magharibi na usiku kuingia k.m kumekutwa

10. -wa- kuwa - kutokea katika hali au mahali fulani k.m alikuwa

Vitenzi vya Kigeni

Hivi ni vitenzi vyenye asili kutoka kwa lugha nyingine badala ya Kibantu.

Baadhi ya lugha hizo ni Kiarabu, Kizungu, Kireno, Kihispania n.k. Vitenzi hivi

havifuatilii muundo wa kawaida wa vitenzi vya Kiswahili ambavyo huishia kwa

sauti -a. Badala yake, vitenzi hivi huishia kwa sauti nyingine kama vile -e, i, -o,

na u

k.m: haribu, tubu, shukuru, salimu, thamini, amini, samehe, baleghe

Vitenzi vya Kibantu

Hivi ni vitenzi vyenye asili ya Kibantu na ambavyo huishia kwa sauti -a.

Kitengo hiki hujumuisha asilimia kubwa zaidi ya vitenzi vya Kiswahili

k.m: simama, shika, tembea, beba, soma, lia

VIELEZI (E)

Vielezi ni maneno yanayotoa habari zaidi kuhusu kitendo kilivyofanyika. Pia

vielezi hutoa habari zaidi kuhusu hali, vivumishi au vielezi vingine.

Aina za Vielezi

Page 31: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 31

Vielezi vya Mahali

Vielezi vya mahali hutoa habari kuhusu mahali ambapo kitendo kilifanyika.

Aghalabu vielezi hivi huundwa kwa kutumia jina la mahali au kwa kuongeza

kiungo -NI mwishoni mwa neno linaloashiria mahali.

k.m: nyumbani, kazini, shuleni

Mtoto huyo hajatulia nyumbani tangu alipotoka Mombasa.

Msipitie sokoni mkienda kanisani.

Vielezi vya Wakati

Huelezea zaidi kuhusu wakati kitendo kipofanyika

k.m: jioni, jana, asubuhi, saa saba, mwaka juzi

Mzee Kasorogani amesema kwamba ataoga mwaka ujao

Musa alilazimishwa kuchimba mtaro saa sita usiku

Kisaka na Musa watakutana kesho

Vielezi vya Idadi

Vielezi vya idadi hutulezea kitendo kilifanyika mara ngapi

a) Idadi Kamili

Vielezi vya Idadi Kamili hutaja idadi kamili ya mara ngapi kitendo kilifanyika.

k.m: mara mbili, siku mbili kwa juma, mara kumi

Gibi alimzaba kofi mara tatu na kisha akakimbia.

Daktari alimwagiza mama huyo achukue dawa mara tatu kwa siku na arudi

hospitalini siku mbili kwa mwezi

b) Idadi Isiyodhihirika

Vielezi vya Idadi Isiyodhirika huelezea kiasi ambacho kitendo kilifanyika bila

kutaja kiasi kamili

Page 32: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 32

k.m: chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani

Mwizi wa kuku alipigwa mara kadhaa kabla ya kuokolewa na polisi.

Yeye hunipigia simu mara kwa mara

VIelezi Vya Namna

Huelezea jinsi au namna kitendo kinavyofanyika. Kitendo kinaweza kufanyika

kwa namna mbalimbali. Hivyo basi kuna aina mbalimbali za vielezi vya namna:

a) Vielezi vya Namna Halisi

Hutufahamisha jinsi kitendo kinavyofanyika kwa kutumia maneno halisi (bila

kuambatanishwa na maneno mengine au viambishi vingine).

k.m: vizuri, ovyo, haraka

Kioo cha bibi harusi kilianguka na kuharibika vibaya

Mama alipika chakula upesi

Amepigwa kalamu kwa kufanya kazi kiholela

b) Vielezi vya Namna Hali

Hutufahamisha hali ambayo kitendo kilifanyika. Vielezi hivi hujihusisha na

tabia ya kitu/mtendaji wa kitendo

k.m: kwa furaha, kwa makini,

Bibi harusi aliingia kanisani kwa madaha

Mtoto alilia kwa maumivu mengi

c) Vielezi vya Namna Kitumizi/Ala

Hutoa habari kuhusu kifaa, ala au mbinu iliyotumiwa kufanya kitendo fulani

k.m: kwa kisu, kwa jembe, kwa meno, kwa moto, kwa maji

Mkulima aliangusha mti mkubwa kwa shoka

Page 33: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 33

Mzee huyo alimpiga mke wake kwa bakora kabla ya kuchoma nguo zake

kwa makaa

d) Vielezi Vikariri

Husisitiza kitendo kinavyofanyika kwa kutaja kielezi kinachorejelewa mara

mbili mfululizo.

k.m: haraka haraka, ovyo ovyo, juu juu

Polisi walipoingia, wezi walitawanyika haraka haraka.

Wanafunzi wengi hufanya kazi yao ovyo ovyo

e) Vielezi vya Ki-Mfanano

Vielezi mfanano hutumia KI-mfanano kuelezea kitendo kinavyofanyika kwa

kulinganisha.

k.m: kitoto, kiungwana,

Babake huongea kiungwana.

Harida hutembea kijeshi

f) Vielezi Viigizi

Vielezi hivi huigiza sauti au mlio wa kitu, kitendo kitendo kilipofanyika kwa

kutumia tanakali za sauti

k.m: tuli, chubwi, tifu, chururu

Mwanafunzi alitulia tuli mwalimu alipomzaba kofi pa!

Kaswimu aliangusha simu changaraweni tifu na kujitumbukiza majini

chubwi

g) Vielezi vya Vielezi

Vielezi hivi hutumika kuelezea kielezi kingine. Hivyo basi, hutanguliwa na

kielezi badala ya kitendo

k.m: sana, kabisa, hasa, mno

Page 34: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 34

Mamake Kajino alitembea polepole sana.

Chungu kilivunjika vibaya kabisa

h) Vielezi vya Vivumishi

Hutoa habari zaidi kuhusu kivumishi

k.m: sana, kabisa, hasa, mno

Yeye ni mrefu sana

Mtoto wake ana tabia nzuri mno

VIUNGANISHI (U)

Viunganishi ni maneno yanayoutumika kuunganisha, kulinganisha au kuonesha

uhusiano wa dhana mbili au zaidi.

Aina za Viunganishi

Zifuatazo ni aina mbalimbali za viunganishi kulingana na matumizi yake

Kuonesha Umilikaji

A-Unganifu Kiatu cha Mzee Sakarani

kimepasuka.

KWA (umilikaji wa

mahali)

Mbinguni kwa kuna makao mengi.

Kujumuisha

na Baba, mama na watoto huunda familia kamili.

pamoja na Mwizi aliiba runinga pamoja na redio

fauka ya, licha Fauka ya mapigo yote, Kafa alikatakatwa kwa

Page 35: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 35

ya kisu.

zaidi ya, juu

ya

Unataka nini tena zaidi ya mema yote

niliyokutendea?

pia, vilevile Alimpiga mkewe na bintiye vilevile

mbali na Mbali na hayo nitakujengea nyumba ya

kifahari.

aidha Keti akitoka shuleni atapika. Aidha atampelekea

nyanya sukuma wiki.

wala

(kukanusha)

Kutofautisha

lakini, ila Ongea nayeilausimwambie mipango yetu.

bila Tasha aliondoka bila kusema lolote.

bali Sitawaacha kama mayatima bali nitawatumia

msaidizi.

kinyume na,

tofauti na

Jana kulinyesha kinyume na utabiri wa hali ya

hewa.

ingawa,

ingawaje

Nitamtembelea ingawa sijui nitamwambia

nini.

Page 36: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 36

japo, ijapokuwa Nakuomba upokee nilichokileta japo ni

kidogo sana.

ilhali Fungo zimepotea ilhali zilikuwa zimewekwa

vizuri.

minghairi ya Waliendelea kutenda dhambi minghairi

ya kuhubiriwa kanisani.

dhidi ya Vita dhidi ya gonjwa hilo vingali vinaendelea.

Kuonesha Sababu

ili Hanna aliumizwa ili asikumbuke aliyoyaona.

kwa, kwa

vile

Emili alinyamaza kwa vile kugombana na

rafikize.

kwa maana,

kwa kuwa

Aria alipigwa na butwaa kwa maana mpenzi

wake aligeuka kuwa mwalimu wake.

kwani Melisa alijificha kwani hakutaka kuonekana na

Spensa.

kwa

minanjili ya

Chali alitembea mwendo huo wote kwa minanjili

ya kuongea na Katosha.

maadam Wanawake katika familia hiyo hawali

maini maadam mama mkongwe alilaani maini

katika familia hiyo.

Page 37: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 37

madhali Madhali sote tuko hapa, tunaweza kuanzisha

mkutano mapema

Kuonesha Matokeo

basi,

hivyo basi

Umekula ng'ombe mzima, hivyo basi huna budi

kumalizia mkia.

kwa hivyo Alipatikana na makosa ya kumnajisi bintiye, kwa

hivyo akahukumiwa miaka kumi gerezani.

ndiposa Mama Kelele alipenda kuongea

sana, ndiposa wakamkata midomo.

Kulinganisha

kama, sawa

na

Kunywa pombe ni kama kujichimbia kaburi

mwenyewe.

kulingana na Mwalimu Makunza hafanyi kazi kulingana

na maadili ya shuleni.

kuliko, zaidi

ya

Talia ni mfupi kuliko Nuru

vile Mganga Daimoni hutibu vile alivyofunzwa na

Mganga Kuzimu.

Kuonesha Kitu kimoja kama sehemu ya kingine

kati ya Vitatu kati ya vitabu hivi vimepigwa marufuku.

Page 38: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 38

miongoni

mwa

Miongoni mwa walioachiliwa, ni Ngiri na

Mende.

baadhi ya Baadhi ya wasichana kutoka Vikwazoni

hawaheshimu miili yao.

mojawapo Mojawapo ya maembe uliyochuma yameoza.

Kuonesha Kitu kufanyika baada ya kingine

kisha Soma mfano huu kisha usome sentensi ifuatayo.

halafu Alichukua kisu halafu akatokomea gizani.

Kuonesha Kitu kufanyika badala ya kingine

badala ya Mapepo yalimchukua Shakawa badala ya bintiye

kwa niaba ya Mama Roga alitoa hotuba kwa niaba ya mumewe.

Kuonesha Uwezekano

labda, pengine Sina pesa leo, labda uje kesho.

ama, au Ama Anita au Katosha anaweza kuja.

huenda Huenda kesho ikifika, Mungu atende miujiza.

Kuonesha Masharti

Page 39: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 39

bora, muradi Sitakuuliza bora tu usichelewe.

ikiwa, iwapo Ikiwa huna jambo muhimu la kusema, nyamaza.

VIHISISHI, VIHUSISHI NA NJIA ZA KUUNDA MANENO

Vihisishi: ni sauti, neno au kikundi cha maneno kinachotamkwa na

mwanadamu kuashiria hisia tofauti kama vie furaha, huzuni, mshituko, n.k.

mfano wa vihisishi ni kama Mungu wangu!, mama wee! Mtume simama!

Kwa kawaida vihisishi ni maneno ambayo huwa hayana uhusiano wa kisarufi

na aina nyingine za maneno katika tungo. Hivyo vihisishi hujitegemea na

kujitosheleza.

Kimuundo vihisishi haviambishwi na wala havina kanuni maalumu ya

mfuatano.

Vilevile kwa vihisishi vyenye muundo wa kikundi hauwezi kubadilisha neno

moja kwa lingine hata kama yana hadhi sawa.

Kwa mfano hatuwezi kusema

*miungu yangu! (badala ya Mungu wangu!)

*baba wee! (badala ya mama wee!)

Aina za vihisishi/viingizi

Viingizi vinaweza kugawanywa kwa kutumia vigezo vya kisemantiki.

Mkabala huu unatumika kugawa viingizi kulingana na maana zinazowakilishwa

na viingizi vyenyewe.

Maana hizo ni hisia zinazobebwa na viingizi hivyo. Kutokana na hisia hizo

tunaweza kuvigawanya katika makundi ya maana zinazohusiana kwa karibu.

Kwa mtazamo huo, viingizi vinaweza kugawanywa katika makundi matatu

makuu ambayo ni:

Page 40: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 40

(a) Viingizi vinavyoonesha mhemko au hisia kali:

Viingizi hivi ni vile vinavyowakilisha hisia tofauti anazokuwa nazo

mzungumzaji ambazo zinaweza kuwa nzuri au mbaya. Kundi hili la kwanza

linaweza kugawanywa katika sehemu ndogo nne kutokana na hisia

mbalimbali alizonazo mzungumzaji zinazowakilishwa na aina hii ya

viingizi ni kama ifuatavyo:

(i) Viingizi vya furaha – hivi ni vile vinavyoonesha hali ya furaha

aliyonayo mzungumzaji, kwa mfano, oyaa!, oyee!, huree!, n.k.

(ii) Viingizi vya huzuni – hivi ni vile vinavyoonesha hali ya masikitiko

au huzuni iliyompata mzungumzaji, kwa mfano, pole!, maskini!

Jamani!, n.k.

(iii) Viingizi vya mshangao – hivi ni vile vinavyoonesha hali ya

mshangao uliompata mzungumzaji, kama vile. Eti!, salale!, ajabu!,

kumbe!, n.k.

(iv) Viingizi vya mshituko – hivi ni vile vinavyoonesha hali ya

mshituko uliompata mzungumzaji, kwa mfano loo!, amaa!, aisee!,

n.k

(b) Viingizi vya maamrisho au msisitizo wa jambo au tukio:

Viingizi vya namna hii huonesha amri anayotoa mzungumzaji, kama vile

haraka!, hima!, njoo!, nenda!, n.k.

(c) Viingizi vya maadili : hivi ni vile vinavyoonesha hisia zinazohusiana na

maadili mbalimbali, yawe mema au mabaya. Aina hii ya viingizi inaweza

kugawanywa katika makundi yafuatayo:

(i) Viingizi vya mwitiko – hivi ni vile ambavyo vinaonesha hisia za

mwitiko anaokuwa nao mzungumzaji akiwa ameitwa au

anapokabiliana na jambo katika mazungumzo, kwa mfano abee!,

bee!, rabeka!, naam!, n.k.

(ii) Viingizi vya ombi – hivi ni vile ambavyo vinaonesha hisia za ombi

kwa mfano, aha!, enhe!, simile!, astaghafirullah!, hodi!, n.k.

Page 41: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 41

(iii) Viingizi vya bezo – hivi ni vile ambavyo vinaonesha hisia za bezo

na dharau ya mzungumzaji, kwa mfano aka!, zii!, sasa!, n.k.

(iv) Viingizi vya kutakia heri – hivi ni vile vinavyowasilisha hisia za

mzungumzaji za kutakia heri na kupongezana, kama vile: inshaallah!,

ahsante!, hongera!, n.k.

(v) Viingizi vya kukiri jambo – hivi ni vile vinavyowasilisha hisia za

kukiri, kwa mfano; laity! Haya! Taib!, n.k.

(vi) Viingizi vya kiapo – hivi ni vile ambavyo vinaonesha hisia za kuapa

ili kuonesha mzungumzaji wa jambo fulani atalitenda au kukana

kutenda jambo, kwa mfano; wallah!

(vii) Viingizi vya salamu – hivi ni vile vinavyotumika kutoa salamu za

mzungumzaji kwa mtu mwingine wanapokutana watu wawili au

zaidi, kwa mfano; shikamoo! Marhaba! Hujambo!, n.k.

Kwa kawaida viingizi havina uhusiano wa kimuundo na maneno mengine katika

sentensi.

Huweza kuondolewa katika sentensi bila ya kuathiri muundo wa sentensi husika.

Hata hivyo, viingizi huipa sentensi dhamira/hali fulani.

VIHUSISHI

Ni maneno yanayojitokeza baada ya nomino na kufanya kazi ya kuhusisha dhana

tofauti. Umbo kuu/muhimu la kihusishi ni a-unganifu. Imeitwa a-unganifu

kutokana na namna maumbile yake ya utendaji kazi yalivyo – kwamba ni lazima

iunganishwe na mofu zinazowakilisha aina ya ngeli inayohusika mfano;

- Mtoto wa mama – wa-inahusisha mtoto na mama (ngei ya A-WA)

- Kiti cha mbao – cha – inahusisha kiti na mbao (ngeli ya KI-VI)

- Jiko la umeme – la – inahusisha jiko na umeme (ngeli ya (LI-YA)

Vilevile, kuna umbo na na kwa ambayo pia hutumika kama vihusishi ingawa yapo

pia katika kundi la viunganishi mfano;

- Ameondoka na mkoba wako

Page 42: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 42

- Ameangukiwa na jiwe

- Amejikata kwa kisu

- Tutasafiri kwa ndege, n.k.

Katika kujifunza aina za maneno ni muhimu kuelewa kuwa umbo la neno halitoshi

kutambulisha aina ya neno. Unaweza ukagundua kuwa neno moja linajitokeza

katika makundi tofauti; kwa mfano neno vizuri linaweza kuwa kiwakilishi,

kivumishi au kielezi pia, neno kulala linaweza kuwa nomino au kitenzi.

Halikadhalika neno Juma linaweza kuwa nomino au kivumishi. Hivyo ambo la

msingi ni kuangalia kazi na nafasi ambayo neno hilo huchukua katika tungo.

UUNDAJI WA MANENO (NJIA ZA UUNDAJI WA MANENO)

Uundaji wa maneno ni mchakato unaowezesha lugha kujiongezea msamiati ili

kukidhi haja ya mawasiliano na kuendana na mabadiliko yanayotokea kila siku.

Maneno ya lugha ya Kiswahili hayaundwi kiholela bali hufuata taratibu na kanuni

zinazokubalika kitaalamu.

Njia zitumikazo kuunda maneno ni kama zifuatazo:

Unyambuaji

Njia hii inatumia mzizi mmoja wa neno na kuzalisha maneno mapya kwa

kupachika viambishi nyambuaji

Mfano

Soma

Somo

Kisomo

Msomi

Msomaji

Page 43: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 43

Lima

Mkulima

Kilimo

Mlimaji

Uambatishaji/mwambatano

Hii ni njia ya kuunda maneno mapya kwa kuambatanisha maneno mawili.

Mfano

Mwana+chama - Mwanachama

Askari+kanzu - Askarikanzu

Bwana+shamba – Bwanashamba

Urudufishaji / Uradidi

Hii ni mbinu ya kurudiarudia neno au sehemu ya neno na kuunda neno jipya

ambalo huwa na maana tofauti na maneno yanayorudiwarudiwa.

Mfano

(d) Pole : polepole

(e) Sawa : sawasawa

(f) Haraka : harakaharaka

Page 44: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 44

Akronimu/ufupishaji

Ufupishaji ni njia mojawapo ya kuundia maneno mapya,ufupishaji huweza

kufanyika kwa namna mbili ambazo ni.

Kufupisha kwa kuchukua herufi za mwanzo Mfano

CWT (Chama cha Walimu Tanzania) VVU (Virusi Vya Ukimwi)

Kufupisha kwa kuchukua silabi za mwanzo za maneno yanayo fupishwa

Mfano

BAKITA (Baraza la Kiswahili la Taifa)

TUKI (Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili)

TATAKI (Taasisi ya Taaluma za Kiswahili)

Uhulutishaji

Ni njia ya kuunda maneno mapya kwa kuchukua vijisehemu vya neno pasipo

kufuata kanuni yoyote.

Mfano

Mnyama mfu – nyamafu

chakula cha jioni – chajio

hati za kukataza – hataza

Mtu asiye kwao - msikwao

Utohoaji

Page 45: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 45

Ni uchukuaji wa maneno toka lugha moja na kuyatumia kwenye lugha nyingine

baada ya kuyarekebisha kimatamshi na kimaandishi ili yaendane na sarufi ya lugha

inayotohoa.

Mfano

Neno Lugha asilia Kiswahili

Shirt Kiingereza Shati

Schule Kijerumani Shule

Bakura Kiarabu Bakora

Benjera Kireno Bendera

Matching Kiingereza machinga

guys

Kuchukua

Page 46: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 46

Hii ni mbinu ya kuongenza maneno kwa kuyachukua toka lugha yake na

kuyatumia kama yalivyo. Uchukuaji hufanyika kwa lugha zinazoendana kisarufi

kama Kiswahili na lugha za kibantu.

Mfano

Kitivo — kisambaa /kipare

Ikulu - kinyamwezi

Kigoda - kizaramo

Kubadili mpangilio wa fonimu

Mfano

Lima – mila – imla - mali

Kufananisha umbo /sauti /tabia

Mfano

Kufananisha umbo

- kifaru-(mnyama faru)

- mkono wa tembo-(mkonga wa tembo)

- kidole tumbo-(umbo la kidole)

Kufananisha Tabia

Ubeberu-(beberu la mbuzi)

Ukupe-(mdudu kupe)

Kufananisha Sauti

Pikipiki (mlio wa pikipiki)

Mtutu (mlio wa bunduki)

Page 47: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 47

Nyau (mlio wa paka)

Kuku - kokoriko (mlio wa kuku)

Njia ya udondoshaji

Mfano

mkwe wake - mkwewe

mwana wake - mwanawe

ndugu yake – nduguye

Kuzingatia matumizi ya kitu

Mfano

Banio - (kubana)

Chanio - (kuchana)

Fyekeo - (kufyeka)

Kutarjumi/kutafsiri

Mfano;

Fluid – (ugiligili)

Acquired immunal deficiency syndrome (Upungufu wa kinga mwilini)

Human immunal virus – (virusi vya ukimwi)

Anti-rentro-virus - (dawa za kufubaza makali ya ukimwi)

DHANA YA MOFOFONOLOJIA NA MOFOSINTAKSIA

Maana ya Mofofonolojia

Page 48: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 48

Ni taaluma inayoshughulikia uchanganuzi na uainishaji wa vipengele vya

kifonolojia vinavyoathiri maumbo ya mofimu katika mfuatano wake.

Mofofonolojia huzalisha kanuni ambazo zinaelezea mazingira ya utokeaji wa

mofu na alomofu zake.

Kanuni hizi huelezea maathiriano ya kifonolojia yanayoathiri mofolojia ya

maneno na jinsi badiliko la kimofofonolojia la neno linavyoelezeka kikanuni.

Kanuni hizi husaidia kujua jinsi maneno yanavyobadilika toka muundo ndani

wa neno hadi muundo nje wa neno.

Kanuni za kimofofonolojia hutawaliwa na sifa zifuatazo

1. Kanuni za kifonolojia hazina vighairi mfano; hakuna vighairi katika kanuni ya

kifonolojia isemayo mkazo katika Kiswahili huwekwa silabi ya pili kutoka

mwishoni mwa neno.

2. Kanuni za kimofofonolojia huwa na vighairi vingi; Kanuni hii huhusu lugha

mahususi na hutumika katika baadhi ya mofimu tu kwa mfano katika mofu ya

utendea.

mfano

piga>

pigia

Page 49: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 49

panga> pangia

funga> fungia

tenga> tengea

choma> chomea

//utendea//----->i/-mz+[a,i,u]

------->e/-mz+[e,o]

AINA ZA KANUNI ZA KIMOFOFONOLOJIA

1. Kanuni ya usilimisho

Kanuni hii inahusu maathiriano ya mofimu zinazofuatana. Maathiriano hayo

huzifanya mofimu zifanane zaidi kuliko zikiwa pekee.

Mfano(1)

a) n+goma----->{ngoma}

b) n+dizi------>{ndizi}

c) n+buzi----->{mbuzi}

Page 50: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 50

d) n+bingu----->{mbingu}

n------>m/-k

Huu ni usilimisho wa nazali inayofuatwa na konsonanti

a) n+refu----->{ndefu}

b) n+limi---->{ndimi}

r------>d/n-

l------->d/n-

Huo ni usilimisho wa konsonanti inayotanguliwa na nazali(N)

2. Ukaakaishaji

Haya ni maathiriano ambayo sauti isiyo ya kaakaa gumu hulazimishwa kuwa

sauti ya kaakaa gumu.

Mfano

a) ki+ama------->chama

b) ki+ombo------->chombo

c) ki+uma-------->chuma

d) ki+eo------>cheo

Page 51: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 51

3. Udondoshaji

Mofimu hudondoshwa kutokana na mfuatano wa mofimu unaoleta maathiriano

Mfano

a) wanasoma –hawasomi

b) anasoma-hasomi

c) nilikunywa-sikunywa //njeo// -------> θ/-ukanushi

4. Tangamano la irabu

Ni utaratibu wa irabu moja kukubali kuandamana na irabu nyingine katika

mazingira maalumu. Kwa kawaida irabu iliyo katika mzizi huathiri utokeaji wa

irabu ya mnyambuliko. Hivyo ikiwa irabu ya mzizi ni a,i au u irabu ya

mnyambuliko huwa i na ikiwa irabu ya mzizi ni e au o basi irabu ya

mnyambuliko huwa e.

Mfano

Panga ----- pangia

Funga …. Fungia

Piga ……pigia

Choma …..chomea

Sema …… semea

Page 52: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 52

5. Mvutano wa irabu

Ni hali inayojitokeza wakati irabu ya juu na irabu ya chini zinapofuatana katika

neno. Irabu hizo huvutana na kusababisha kutokea kwa irabu isiyo ya juu wala

chini. Mfano,

ma+ino = meno

wa+ingi = wengi

ma+ingine = mengine

6. Uyeyushaji

Ni kitendo cha kubadili irabu kuwa nusu –irabu au kiyeyusho. Hali hii hutokea

wakati irabu mbili zinapokutana mfano; irabu – u hubadilika na kuwa

kiyeyusho /w/ inapokaribiana na a au i (mu+alimu=mwalimu, mu+imbaji =

mwimbaji) na irabu -i- hubadilika na kuwa kiyeyusho /y/ inapokaribiana na

irabu a, o au u (vi+ama= vyama, vi+ombo = vyombo, vi+uma = vyuma)

7. Vighairi

Ni mofimu au maneno yanayokiuka kanuni za kawaida za lugha husika. Mfano;

Kiatu………… viatu

Kisu……………visu

Choo ………….vyoo

Chama ………..vyama

Page 53: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 53

Nomino choo, vyoo, chama, vyama ni vighairi kwa sababu yanaingia ngeli ya

KI-VI lakini hayabebi viambishi husika mwanzoni.

D11/9/2018HANA YA MOFOSINTAKSIA

Ni taaluma inayoshughulikia uchanganuzi na uainishaji wa vipengele vya

kisintaksia vinavyoathiri maumbo ya mofimu katika mfuatano wake.

Vipengele vya kisintaksia vinavyoathiri mofolojia ni:

(a) Umoja na wingi: maneno mengi ya Kiswahili huwa na maumbo tofauti

yanapokuwa katika hali ya umoja na yanapokuwa katika hali ya wingi.

Mfano

Umoja Wingi

Kidole vidole

Ungo nyungo

Jicho macho

Kwa kuangalia mifano ya hapo juu tunaona kuwa wingi wa kitu kinachotajwa ni

kilekile, mabadiliko ya maumbo hutokea kuingana na idadi ya kitajwa. Maneno

mengi tu ya Kiswahili huwa na tabia hii lakini sio yote. Hii ina maana kwamba

baadhi ya maneno hubaki kama yalivyo (hayabadiliki) ikiwa yapo katika umoja au

katika wingi. Mfano wa maneno hayo ni sabuni, njia, nguo, nyumba, zawadi, n.k.

(b) Njeo: katika Kiswahili kuna viambishi mbalimbali vinavyotumiwa

kuwakilisha njeo. Hivyo basi, kadiri mzungumzaji anavyofikiria dhana

Page 54: Mofolojia ya Kiswahili - mwalimuwakiswahili.co.tz · Mofolojia ya Kiswahili 2018 Maeda, T.S 0717104507  Uk 2 Mofolojia na semantiki Semantiki ni taaluma ya maana

Mofolojia ya Kiswahili 2018

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 54

ya wakati fulani katika mazungumzo yake ndipo umbo la neno

linapobadilika kulingana na wakati huo. Mfano;

analima,atalima,amelima,alilima (na – wakati uliopo, ta – wakati ujao,

me – wakati uliopita timilifu, li – wakati uliopita)

(c) Ukanushi : dhana ingine ya kisintaksia inayosababisha umbo la neno

kubadilika ni ukanushi. Angalia mifano ifuatayo:

A B

Uyakinishi Ukanushi

Anapika ……………. hapiki

Amepika …………… hajapika

Alipika …………….. hakupika

Atapika …………….. hatapika

Mifano hiyo inaonesha kwamba kutokana na kuwepo kwa mofimu ha ya ukanushi

katika maneno ya jozi B maumbo yanayowakilisha wakati yamebadilika. Umbo na

la wakati uliopo halionekani katika nafasi yake badala yake kuna umbo i mwishoni

mwa kitenzi, wakati uliopita (muda mfupi) unawakilishwa na ja badala ya me na

wakati uliopita unawakilishwa na ku badala ya li. Umbo linalowakilisha wakati

ujao pekee ndilo lisiloathiriwa na mabadiliko haya.

(d)