View
30
Download
4
Category
Preview:
Citation preview
1
Kiongozi cha Mwezeshaji
Mafunzo Endelevu kwa Afisa Elimu Kata
Januari 2018
2
YALIYOMO
UTANGULIZI .................................................................................................................................. 3
SEHEMU YA KWANZA ................................................................................................................ 4
MAJUKUMU YA MWEZESHAJI .................................................................................................. 4
1.1 Kazi yako kubwa kama mwezeshaji ni .............................................................................. 4
1.2 Namna ya kuwezesha kipindi ................................................................................................. 4
1.3 Jinsi gani unaweza kuhamasisha majadiliano kati ya washiriki ............................................. 4
1.4 Jinsi ya kuwachukulia washiriki wenye tabia tofauti ............................................................. 4
1.6 Jinsi mafunzo haya yatakavyoendeshwa ................................................................................ 5
SEHEMU YA PILI .......................................................................................................................... 7
UWEZESHAJI WA MAFUNZO ENDELEVU .............................................................................. 7
SEHEMU YA TATU ..................................................................................................................... 11
VIAMBATISHO ............................................................................................................................ 57
MPANGILIO WA MADA ZA MAFUNZO .................................................................................. 57
3
UTANGULIZI
Mwezeshaji au mkufunzi yeyote mwenye mafanikio ni yule anayetumia muda mwingi
kubuni mbinu mbalimbali za kuendesha mafunzo au kufundisha watu ili washiriki watumie
muda mchache sana kuelewa na kupokea maarifa tarajiwa. Mwezeshaji mwenye mafanikio
ni yule anayetambua kuwa washiriki/wanafunzi wake wanajua mambo mengi, na baadhi yao
wanauelewa mpana wa mada wanazofundishwa. Hivyo, kazi ya mwezeshaji ni kuwezesha
washiriki kushirkishana na kupeana maarifa wao wenyewe ili kila mmoja anufaike na ujuzi,
maarifa na uzoefu wa mwingine.
Kosa kubwa kwa Mwezesaji yeyote ni kuwa na mtazamo kwamba washiriki wa mafunzo
HAWAJUI na wewe ndiye unayejua YOTE. Ni udhaifu mkubwa sana kwa mwezeshaji
kujifanya yeye ndo kila kitu na washiriki wamekuja kupokea kutoka kwake. Mtazamo huu
husababisha Mwezeshaji kushindwa kufikia malengo na washiriki kushindwa kutoa
ushirikiano kwa mwezeshaji. Kazi ya Mwezeshji siyo kufundisha wala kuelekeza. Ni
kuweka mazingira ya washiriki kujifunza wao wenyewe na kushirikisha uzoefu na maarifa
waliyonayo.
Mwongozo huu wa mwezesahji wa mafunzo endelevu ya kitaalaamu kwa Maafisa Elimu
kata ni moja ya dhana muhimu itakayomsaidia mwezeshaji kufuata mpangilio mzuri wa
kuwezesha masomo yanayohusu mafunzo endelevu. Pamoja na vitabu vingine mwongozo
huu umependekeza mbinu kadhaa za kutumia kuendesha mafunzo. Mbinu hizo siyo lazima
zitumiwe zote. Mwezeshaji anaruhusiwa kubuni mbinu nyingine nyingi zitakazowashirikisha
wana-semina wote kwa lengo la kufikia malengo ya mafunzo.
Tunawasihi wawezeshaji wote watumie kitabu hiki kama kiongozi chao kwenye kubuni
mbinu nyingi zaidi za kuwezesha ili mafunzo yalete manufaa tarajiwa.
4
SEHEMU YA KWANZA
MAJUKUMU YA MWEZESHAJI
1.0 Kueleweka kwa mada/somo ni kiini cha mafanikio ya Mwezeshaji
Mwezeshaji una jukumu kubwa la kuhakiksha malengo ya mafunzo yanafikiwa, na washiriki
wa mafunzo wanaelewa na kufuatilia somo kwa ukamilifu. Ubunifu binafsi wa mwezeshaji
na matumizi ya mbinu mchanganyiko wakati wa kuwezesha mafunzo vitakusaidia kufikia
malengo tarajiwa.
1.1 Kazi yako kubwa kama mwezeshaji ni:
Kutambulisha mada ya mafunzo na malengo yake
Kuhakikisha majadiliano hayatoki kwenye lengo lililokusudiwa na pia kufanya
majadiliano hayo yalete matokeo tarajiwa.
Kuwasaidia washiriki washirikishane uzoefu na kuangalia mbinu tofauti za kutatua
changamoto
Kuuliza maswali ya udadisi ili kuamsha fikra na kumfanya kila mmoja awe na
ushiriki na umuhimu ulio sawa.
Kusisitiza mambo muhimu na kufafanua eneo linalohitaji ufafanuzi au maoni ya
ziada
1.2 Namna ya kuwezesha kipindi
Mwazoni kabisa mwa kipindi, jitambulishe kwa lugha nyepesi, eleza kazi yako katika
kipindi,
Weka wazi malengo na matarajio ya kipindi kabla ya kuanza kipindi
Hamasisha washiriki kwa kuanza kipindi na mchezo mwepesi au bungua bongo
Hakikisha umeelewa mada vizuri kabla ya kuanza kuwezesha ili uwe na ujasiri wa
kutoa ufafanuzi au kujibu maswali.
Kama swali limeulizwa na huna uhakika wa jibu lake, tumia mbinu mbadala kujibu
mfano “hebu kila mmoja amgeukie mwenzake wa kushoto na wajadili”
Kazi yako sio kutoa mhadhara au kujibu maswali bali ni kuhimiza washiriki watoe
maoni yao na kushiriki kwenye kipindi
Katika kufunga kipindi waulize washiriki waeleze ni nini walichojifunza kwa kifupi
Malizia kipindi kwa kusisitiza jambo moja au mawili muhimu
Hakikisha kuwa unatunza muda
1.3 Jinsi gani unaweza kuhamasisha majadiliano kati ya washiriki
Anzisha hoja zenye utata ili kufanya washiriki wajadili kwa mapana
Wape washiriki mifano halisi na waache wajadili
Uliza maswali ya udadisi na ya kufuatilia mfano: halafu ikawaje? Unafikiri kwanini
aliamua hivyo? Kuna uhusiano gani kati ya matukio hayo mawili? Una uthibitisho
gani katika habari hii?
1.4 Jinsi ya kuwachukulia washiriki wenye tabia tofauti
Wazungungumzaji sana: Wakumbushe washiriki kuwa kila mmoja ana nafasi sawa
ya kuchangia mjadala. Gawa majukumu kwa zamu ili kila mmoja ashiriki.
Washiriki wasiozungumza sana: Wachague mara kwa mara kujibu au kuuliza
maswali au kufafanua jambo wale ambao hawazungumzi sana ili kuwahamasisha
washiriki kama wengine
5
Wanaotoka nje ya mada: Waruhusu watoke nje ya mada mara chache, washukuru
kwa mchango wao na kisha hakikisha unawarudisha kwenye mada husika mara moja.
Wakatisha tamaa wenzao: Wakumbushe sheria na kanuni za kipindi kila mara ili
wawahesimu na kuwathamini wengine
1.5 Mambo yanayoonesha kuwa kipindi kimefanikiwa
Washiriki wako huru kuuliza maswali na kutoa maoni yao.
Kila mshiriki anamheshimu na kumsikiliza mwenzake
Washiriki wanakuja wakiwa wamejiandaa kujifunza na kufundisha
Washiriki wanabaki kwenye mada hata kama kuna wengine wametoka nje ya mada
1.6 Jinsi mafunzo haya yatakavyoendeshwa
Mwongozo huu umegawanyika katika sehemu kuu tano. sehemu ya kwanza ni ya
lazima kwa kila Afisa Elimu Kata kujifunza mara mafunzo yanapoanza.
Sehemu ya kwanza: Mafunzo Elekezi ( Induction/Orientation)
Sehemu ya Pili: Uongozi na Usimamizi katika Elimu
Sehemu ya Tatu: Uelekezi na Ushauri Elimishi ( Coaching and mentoring)
Sehemu ya Nne: Uwezo wa kujiongoza mwenyewe na Mwenendo bora kiutendaji na
mahusiano na wengine (Uongozi binafsi)
Sehemu ya Tano : TEHAMA
1.7 Hatua na taratibu za kufuata kutekelea mafunzo Endelevu kwa Maafisa Elimu
Kata
Mwezeshaji eleza kwa mapana hatua na taratibu kadhaa muhimu zinazopaswa kufuatwa
ili kutekeleza mafunzo endelevu:
Hatua ya kwanza
Idara ya elimu ya wilaya pamoja na ofisi ya uthibiti ubora ya wilaya watatoa mafunzo
kwa Afisa elimu kata wote katika wilaya juu ya mpango huu.
Mada za sehemu ya kwanza katika mwongozo huu ni ya LAZIMA zifundishwe kwa
Maafisa Elimu kata wote
Mafunzo elekezi yatatolewa kwa muda wa saa moja, na inapendekezwa saa moja
kabla ya kuanza mkutano wa elimu wa mwezi wa wilaya itumike kutoa mafunzo
haya. Mfano kama mkutano unaanza saa nne asubuhi, basi mafunzo yafanyike
kuanzia saa tatu hadi saa nne asubuhi .
Nukuu za mafunzo zinaweza kutumiwa lakini haimfungi mwezeshaji kuongeza
nukuu nyingine
Mafunzo mengine (TEHAMA) AEK anatakiwa kutafuta wanapota mafunzo ya
vitendo.
Hatua ya pili
Baada mafunzo elekezi, kila Afisa Elimu Kata atatakiwa kujaza fomu ya maombi ya
kujiunga kulingana na hitaji lake. (fomu imeambatishwa)
Maombi yatapelekwa ofisi ya elimu kuanzia mwezi wa Januari hadi Februari
mwishoni, na Julai hadi Agusti mwishoni
Ofisi ya elimu itapitia maombi yatakayopelekwa na kuyapitisha au kuyakataa au
kupendekeza vinginevyo kwa kusema sababu za kufanya hivyo
6
Ofisi ya uthibiti ubora wa shule wa wilaya itamjulisha AEK kama amechaguliwa
kuanza masomo
AEK anatakiwa kujibu barua ya kukubali au kukataa mafunzo hayo muda wa siku 14
tangu amepokea barua ya kutakiwa kujiunga na mafunzo endelevu
Hatua ya tatu
Ofisi ya Uthibiti Ubora wa shule watakusanya maombi yote na kutengeneza ratiba ya
mafunzo kulingana na maombi waliyopokea
Mafunzo yataanza mwezi wa tatu kila mwaka hadi itakapobadilishwa kutokana na
mahitaji
Ofisi ya uthibiti ubora wa shule wilaya pamoja na ofisi ya Elimu Wilaya wafafuatilia
maendeleo ya AEK anayehudhuria mafunzo kwa kuangalia mendeleo na mabadiliko
ya utendaji kazi wake.
Taarifa ya maendeleo ya mafunzo itajumuishwa katika ripoti ya utendaji wa ofisi ya
uthibiti ubora na ofisi ys elimu za kila robo mwaka.
Wawezeshaji wa mafunzo haya ni:
Ofisi ya Elimu Wilaya
Ofisi ya uthibiti ubora wa shule wa wilaya
Ofisi ya mipango ya wilaya
Ofisi ya TSC wilaya/mkoa
Wengine wanaruhusiwa kulingana na mahitaji
Usimamizi
Mthibiti mkuu wa ubora shule wa Wilaya ndiyo atakuwa msimamizi mkuu wa
mafunzo haya akisaidiwa na afisa toka ofisi ya Elimu Wilaya.
Uthibitisho wa kuhitimu
Baada ya mafunzo Ofisi ya Elimu na Uthibiti ubora itatengeneza cheti ambacho
kitatolewa kwa washiriki waliohitimu kwa nadharia na vitendo.
7
SEHEMU YA PILI
UWEZESHAJI WA MAFUNZO ENDELEVU
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
KIPINDI CHA KWANZA:
Mada: Kuuelewa kwa kina Mwongozo wa Mafunzo kwa Afisa Elimu Kata Muda dk:
60 Mada hii ni LAZIMA kufundishwa kwa kila mafunzo mapya yanapoanza hata kama
washiriki walishapata mafunzo mengine ili kuwa na uelewa wa pamoja.
Vifaa
Mwongozo wa Mafunzo Endelevu kwa AEK
Malengo ya somo: elezea lengo la somo
Kazi ya 1: Kuelewa maana ya mafunzo endelevu dakika 5
Elezea
Tumia njia mbalimba kuhakikisha washiriki wanapata fursa ya kutafakari maana ya mafunzo
Endelevu kulingana na wanavyojua. Baada ya kupata tafsiri kadhaa unganisha tafakari zao
na hii hapa chini.
Ni mchakato endelevu wa kujifunza ili kuongeza Maarifa, Ujuzi, Uzoefu na Umahiri
unaofanyika kwa njia rasmi au isiyo rasmi kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utendaji
kazi wa kila siku.
Kazi ya 2:
i. Wape muda wa dk 30 kila mmoja apitie muongozo
ii. Baada ya dk 30 wagawe katika makumdi 3 na kila kundi liandike maeneo ambayo
yanahitaji ufafanuzi zaidi (dakika 10)
iii. Fafanua kulingana na maswali ya washiriki (dk 10)
Hitimisho la Kipindi
Hitimisha kipindi kwa kuwaalika washiriki katika kipindi kijacho, wape taarifa endapo kuna
vifaa vya kuchukua katika kipindi kijacho. Kabla ya kipindi kuisha, hakikisha kila mshiriki
amepata mwongozo.
KIPINDI CHA PILI: FAIDA ZA MAFUNZO ENDELEVU DAKIKA: 60
Mada hii ni LAZIMA kufundishwa kwa kila mafunzo mapya yanapoanza hata kama washiriki
walishapata mafunzo mengine. Hii itawafanya wakumbuke na kuweka kipaumbele katika
mipango yao ya kazi
Vifaa: Bangokitita, kalamu rashaha, gundi utepe, video ya CPD
Kazi ya 1: Faida ya mafunzo endelevu kwa Afisa Elimu Kata dakika
10
Wagawanye washiriki katika makundi matatu; Waeleze kuwa kila kikundi kujadili ni faida
gani kuu tano zinazopatikana katika kushiriki kwenye mpango wa mafunzo endelevu
waandike mawazo yao kwenye bango kitita. Kikundi cha kwanza kumaliza kitasema kwa
8
sauti "BINGO". Kundi hili litabandika bangokitita lao ukutani. Endelea hadi makundi yote
matatu yakamilishe.
Kazi ya 2: Mrejesho wa Kikundi na Mjadala wa wote dakika 15
Kila kundi libandike Bangokitita lao kwenye ukuta. Yaambie makundi yasome orodha ya
faida za mafunzo endelevu waliyoainisha. Mwezeshaji sasa ongoza majumuisho ya mrejesho
kwa kutumia maswali yafuatayo:
Kwa jinsi gani mafunzo hayo yatafanikisha kazi zako za kila siku?
Unafikiri mabadiliko gani yanaweza kutokea kwenye shule endapo utashiriki katika
mafunzo endelevu kwa kikamilifu?
Ni vikwazo gani unafikiri vitakukwamisha katika safari yako ya mafunzo endelevu?
Nini kitakufanya uendelee na mafunzo endelevu?
Mambo ya Kusisitiza:
Waeleze umuhimu wa mafunzo endelevu na jinsi itakavyowasaidia kuinua utendaji
kazi wao wa kila siku.
Kazi ya 3: Kwa nini kuwe na mafunzo endelevu kwa Afisa Elimu Kata? dakika
15
Hakikisha kila kikundi kina karatasi ya bangokitita na kalamu rashasha. Yakumbushe
makundi kwamba wanapaswa kuchagua mtu mmoja ambaye ataandika maelezo na
kuwasilisha wakati wa mjadala wa wote.
Kwanini msisitizo wa mafunzo endelevu umeelekezwa kwa Afisa Elimu Kata?
Nini tofauti ya mafunzo endelevu na mafuzo yasiyoendelevu?
Kazi ya 4: Mrejesho wa wote dakika
15
Waambie kila kikundi kikuambie majibu yao (majibu yasizidi 2). Kisha zungukia tena
kuuliza majibu toka kwenye makundi mengine. Waambie wana kikundi wasirudie kile
kilichosemwa na wengine. Andika kwenye bango kitita mambo muhimu tu (siyo kila neno)
yaliyotolewa na vikundi.
9
KIPINDI CHA TATU: NJIA ZA KUPATA MAFUNZO ENDELEVU DAKIKA
60
Vifaa; Bangokitita, karamu rashaha, gundi utepe, Video ya CPD
Waratibu Elimu Kata waje na majibu ya kazi waliyopewa katika kipondi kilichopita
Kazi ya 1: Kila AEK awasilishe majibu ya kazi yake Dakika 20
Malego ya kipindi
Kutaja njia za kupata mafunzo endelevu na kupendekeza njia zinazofaa kulingana na
mazigira ya kazi na eneo.
Kazi ya 2: Shughuli za Mafunzo Endelevu Dakika
15
Waeleze washiriki kila aina ya shughuli za Mafunzo Endelevu
Mwezeshaji tambua kuwa kuna aina nyingi za utoaji mafunzo endelevu ambazo zitaendana
na mahitaji, kwa kuwa lengo ni kufanya mafunzo endelevu yahusishe wengi, njia hizi
zinazingatia gharama, muda na maudhui ya masomo ili kufanya Afisa Elimu Kata asilemewe
Faida za Mafunzo Endelevu
Kuwa mahiri kitaalamu kwenye taaluma uliyosomea na eneo la majukumu yako ya
kazi
Kuwa na mwendelezo wa kujifunza zaidi kwa utaratibu unaotekelezeka na
kuhakikisha kuwa ujuzi huo unatumika kuimarisha utendaji kazi wa kila siku
Kuhuisha ujuzi na maarifa ya mtu ili aendane sambamba na mahitaji/mabadiliko ya
utendaji kazi
kuongeza ufanisi katika utendaji kazi ili kupata matokeo yaliyotarajiwa
Kumuandaa mtu kwa ajili ya majukumu makubwa zaidi
kukuza weledi wa kitaalamu
kujitathmnini na kubaini maeneo yenye changamoto na kuyatafutia ufumbuzi
Fursa ya kujiendeleza kitaaluma na kiutalaam zaidi
Hutumia gharama ndogo kutekeleza mafunzo hayo
Mambo ya kusisitiza:
Eleza kwa ufupi juu ya mafunzo endelevu na taratibu zake
Waambie washiriki kuwa kila mmoja aeleze njia anayoona inafaa ili kupata mafunzo
endelevu. Na kila mmoja atawasilisha kipindi kijacho.
10
na mzigo wa majukumu yake ya kila siku na muda wa kujifunza. Zifuatazo ni njia mojawapo
zinazopendekezwa:
Mfumo wa kawaida wa mafunzo ya darasani (traditional training model)
Mafunzo elekezi
Mafunzo kwa njia ya mtandao
Mafunzo kwa njia ya kuwasilisha mada au kuhudhuria mikutano na kongamano
Kujifunza kwa kujitolea kufanya kazi bila malipo
Ongeza njia nyingine ambazo washiriki wameziongeza
Kazi ya 3: Kujadili njia zipi rahisi kuzitekeleza na kwa nini? dakika 10
Kwenye vikundi vya watu 6 hadi 8 waliochanganyika
Jadili njia gani za mafunzo endelevu ambazo ni rahisi kuzitekeleza na kwa nini?
Kazi ya 4: Mrejesho wa Jumla na mjadala dakika 10
Mwezeshaji waalike washiriki kufanya mjadala wa wazi kushirikishana majibu ya kazi ya 3
Hitimisho dakika 5
Mambo muhimu ya kusisitiza
Njia za kujifunza mafunzo endelevu hazina mipaka, ni muhimu kuangalia kuwa njia ipi
inaendana na malengo uliyojiwekea na kuleta mabadiliko katika utendaji wako wa kazi.
11
SEHEMU YA TATU
MAENEO YA KUJIFUNZA KATIKA MAFUNZO ENDELEVU
Maeneo ya kujifunza Kumwendeleza Afisa Elimu Kata
Mwezeshaji eleza kuwa Mafunzo endelevu yametokana na mahitaji ya mafunzo kutoka kwa
MaAfisaelimu Kata. Mahitaji ya mafunzo yamegawanyika katika makundi makubwa
matano: 1. Mafunzo Elekezi binafsi 2. Uongozi 3. Uelekezi na elimu elimishi 4. Uongozi
binafsi 5. TEHAMA
MAFUNZO ELEKEZI
Kipindi cha kwanza: Mwongozo kwa AEK Muda dakika:
Mada hii ni LAZIMA kufundishwa kwa kila mafunzo mapya yanapoanza hata kama
washiriki walishapata mafunzo mengine ili kuwa na uelewa wa pamoja.
Vifaa: Mwongozo wa Mafunzo Endelevu kwa AEK
Malengo ya somo: washiriki waeleze maana ya Mafunzo Endelevu na umuhimu wake katika
kazi zao za kila siku.
Utangulizi: Mafunzo endelevu ni nini? dakika 5
Waulize washiriki wachache waeleze wanafahamu nini kuhusu mafunzo endelevu: kisha
elezea maana ya Mafunzo Endelevu:
Ni mchakato endelevu wa kujifunza ili kuongeza maarifa, ujuzi, uzoefu na umahiri
unaofanyika kwa njia rasmi au isiyo rasmi kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utendaji
kazi wa kila siku.
Kisha waeleze washiriki kuhusu mwongozo kwa kifupi na kuwagawia kila mmoja nakala
yake.
Kazi ya 1:
iv. Wape muda wa dk 20 kila mmoja apitie muongozo
v. Baada ya dk 15 wagawe katika makundi matatu na kila kundi liandike maeneo
ambayo yanahitaji ufafanuzi zaidi
vi. Fafanua kulingana na maswali ya washiriki (dk 5)
AU:
Soma na washiriki hatua kwa hatua kitabu cha mwongozo wa mafunzo Endelevu na
fafanua toa nafasi ya maswali kabla hujaendelea hatua inayofuata.
12
Hitimisho: dakika 5
Hitimisha kipindi kwa kuwaalika washiriki katika kipindi kijacho, wape taarifa endapo kuna
vifaa vya kuchukua katika kipindi kijacho. Kabla ya kipindi kuisha, hakikisha kila mshiriki
amepata mwongozo.
Kipindi cha Pili: UMUHIMU WA MAFUNZO ENDELEVU
Vifaa: Bangokitita, kalamu rashaha, gundi utepe, video ya CPD
Utangulizi Mafunzo endelevu ni nini? dakika 5
Toa maswali machahe kuhusu mada ya kipindi kilichopita
Kazi ya 1: dakika 5
Faida ya mafunzo endelevu kwa Afisaelimu Kata
Wagawanye washiriki katika makundi matatu; Waeleze kuwa kila kikundi kujadili ni faida
gani kuu tano zinazopatikana katika kushiriki kwenye mpango wa mafunzo endelevu
waandike mawazo yao kwenye bango kitita. Kikundi cha kwanza kumaliza kitasema kwa
sauti "BINGO". Kundi hili litabandika bango kitita lao kwenye ukuta. Endelea hadi makundi
yote matatu yakamilishe.
Kazi ya 3 Mrejesho wa Kikundi na Mjadala wa wote dakika 10
Kila kundi wabandike bangokitita lao kwenye ukuta. Waambie kila kikundi kusoma orodha
ya faida za mafunzo endelevu waliyoyaainisha.
Ongoza majumuisho ya mrejesho kwa kutumia maswali yafuatayo:
Kwa jinsi gani mafunzo hayo yatafanikisha kazi zako za kila siku
Unafikiri mabadiliko gani yanaweza kutokea kwenye shule endapo utashiriki katika
mafunzo endelevu kwa kikamilifu
Ni vikwazo gani unafikiri vitakukwamisha katika safari yako ya mafunzo endelevu?
Nini kitakufanya uendelee na mafunzo endelevu?
13
Kipindi cha Tatu: NJIA ZA KUPATA MAFUNZO ENDELEVU
Vifaa: Bangokitita, karamu rashaha, gundi utepe, Video ya CPD
Utangulizi: Kila AEK asome majibu ya kazi waliyopewa Dakika 10
Malengo ya kipindi
Kutaja njia za kupata mafunzo endelevu na kupendekeza njia zinazofaa kulingana na
mazigira ya kazi na eneo.
Faida za Mafunzo Endelevu
Kuwa mahiri kitaalam katika fani husika
Kuhakikisha kuwa kujifunza zaidi kunaendelea katika utaratibu unaotekelezeka na
kuhakikisha kuwa ujuzi huo unatumika kuimarisha utendaji kazi wa kila siku
Kuhuisha ujuzi na maarifa ya mtu ili aendane sambamba na mahitaji/mabadiliko ya
utendaji kazi
kuongeza ufanisi katika utendaji kazi ili kupata matokeo yaliyotarajiwa
Kumuandaa mtu kwa ajili ya majukumu makubwa zaidi
kukuza weledi wa kitaalam
kujitathmnini na kubaini maeneo yenye changamoto na kuyatafutia ufumbuzi
Fursa ya kujiendelza zaidi
Hutumia gharama ndogo kutekeleza
Mambo ya kusisitiza:
Eleza kwa ufupi juu ya mafunzo endelevu na taratibu zake
Waeleze umuhimu wa mafunzo endelevu na jinsi itakavyowasaidia kuinua utendaji
wao wa kazi zao za kila siku.
Waambie washiriki kuwa kila mmoja akiwa nyumbani aeleze njia anayoona inafaa ili kupata
mafunzo endelevu. na kila mmoja atawasilisha kipindi kijacho.
14
Kazi ya 1: Shughuli za Mafunzo Endelevu Dakika 10
Baada ya kusikia majibu ya washiriki, waeleze washiriki kila aina ya shughuli za Mafunzo
Endelevu
Namna ya utoaji wa mafunzo
kuna aina nyingi za utoaji mafunzo endelevu ambazo zitaendana na mahitaji, kwa kuwa
lengo ni kufanya mafunzo endelevu yahusishe wengi, njia hizi zinazingatia gharama, muda
na maudhui ya masomo ili kufanya Afisaelimu asilemewe na mzigo wa majukumu yake ya
kila siku na muda wa kujifunza. Zifiatazo ni njia zilizopendekezwa
Mfumo wa kawaida wa mafunzo ya darasani (traditional training model)
Mafunzo elekezi (Coaching)
Mafunzo kwa njia ya mtandao (Online/ e-leaning)
Mafunzo kwa njia ya kuwasilisha mada au kuhudhuria mikutano na kongamano
(Presentation)
Kujifunza kwa kujitolea kufanya kazi bila malipo ( Volunteer)
Ongeza njia nyingine ambazo washiriki wameziongeza
Kazi ya 3: Njia zipi ni rahisi kuzitekeleza na kwa nini? Dakika 10
Kwenye vikundi vya watu 6 hadi 8 waliochanganyika
Jadili Njia gani za mafunzo endelevu ambazo ni rahisi kuzitekeleza na kwa nini?
Hitimisho: Ufupisho wa mada za kipindi dakika 5
Mambo muhimu ya kusisitiza
Njia za kujifunza mafunzo endelevu hazina mipaka, ni muhimu kuangalia kuwa njia ipi
inaendana na malengo uliyojiwekea na kuleta mabadiliko katika utendaji wa kazi.
Kipindi cha Nne : SIFA ZA WEO
VIFAA: Bango kitita, Nakala ya Sifa za WEO, Kalamu za rashasha nk
15
LENGO: Washiriki waweze kubainisha sifa zinazomfanya awe WEO
WEO waweze kujitathimini wao wenyewe kama wanazo sifa hizo
NJIA ZA KUFUNDISHIA
Igizodhima, kisa mkasa na majadiliano
Mwezeshaji achague njia mojawapo kati ya hizo hapo juu au zaidi ili kuwasilisha
somo lake
KAZI YA 1 DAKIKA 10
Hakikisha katika njia uliyotumia inagusa sifa za WEO kama zilivyooneshwa katika
mwongozo
Baada ya Igizodhima/kisa mkasa/majadiliano washiriki wbainishe sifa zilizo nzuri na
zilizo mbaya kawa WEO
Mwezeshaji awape washiriki kazi ya kuorodheresha sifa nzuri alizonazo
MMwezeshaji awape washiriki kazi ya kuorodheresha sifa mbaya alizonazo
Washiriki kila mmoja aeleze hadharani sifa nzuri na sifa mbaya aliyo nayo na
atafanya ninin kuiondoa sifa hiyo mbaya aliyonayo.
HITIMISHO/TATHIMINI:
Mwezeshaji waeke msisistizo katika kuacha sifa mabaya aliyo nayo na kila mmoja awe
msaada kwa mwenzake ili kusaidia kuicha sifa hiyo.
Tumia kila njia ya Ubunifu ili kuona kila mshiriki anataja sifa yake mbaya
Bandika stika mgongoni kwa kila mshiriki na washiriki wote waandike kwenye stika
hiyo sifa mabya alizonazo
Tumia njia ya mduara wa uaminifu.
16
Kipindi cha Tano: KAZI ZA WEO
VIFAA: Bango kitita, Nakala ya kazi za WEO, Kalamu za rashasha
LENGO: Washiriki waweze kuzibainisha na kuzitaja na kuzitekeleza kwa Ufanisi
NJIA ZA UFUNDISHAJI
Majadiliano – Dakika 40
Kazi ya kufanya
Mwezeshaji awaongoze washiriki waorodhodheshe kazi zaidi ya tano ambazo ni
muhimu kwa WEO.
Kisha kila mmoja azisome.
Mwezeshaji aandike majibu ya washiriki bila kurudia yaliyotajwa awali
Mwezeshaji awe na majukumu rasmi ya WEO ayasome na kujumuisha yale
yaliyotajwa awali
Washiriki wayanakili majukumu yaote rasimi yaliyo wasilishwa
Kazi zotezilizowasilishwa wazichukue kuwa vitendea kazi muhimu katika
maeneo yao ya kazi
Majadiliano
Mwezeshaji awape nafasi washiriki wajadili changamoto zinazojitokeza katika
Utendaji wao wa kazi
HITIMISHO/TATHIMINI
Mwezeshaji atoe majumuisho ya somo na kuangalia ushiriki wa kila mmoja
Kipindi cha Sita: MAJUKUMU YA WEO
VIFAA: Bango kitita, Nakala ya Majukumu ya WEO, Kalamu za rashasha nk
LENGO: Washiriki waweze kubaini majukumu yao na waweze kuyatekeleza kwa usahihi
Kazi ya 1: DAKIKA 15
Mwezeshaji awagawe washiriki kwenye makundi ya watu wanewanne na kisha
waandike majukumu yao ya kila siku
Kisha kila kundi liwasilishe kazi yao ubaoni
17
Kazi ya 2: DAKIKA 10
Mwezeshaji aeleze tofauti kati ya kazi na majukumu
Mwezeshaji awaongoze wanakikundi kuorodhesha kwa kutofautisha kazi na
majukumu yao kwenye bango kitita
Kazi ya 3: DAKIKA 25
Mwezeshaji awaongoze wanakikundi waeleze changamoto zinzojitokeza katika majukumu
yao na namna ya kuzitatua
JUKUMU CHANGAMOTO NJIA ZA UTATUZI
HITIMISHO/TATHIMINI: Majukumu, changamoto na utatuzi zilizoainishwa zitasaidia na
kutumika kama zana za kutendea kazi ili kuondoa changamoto zilizobainishwa na kuboresha
utendaji wa WEO
Kipindi cha saba: Nafasi (Madaraka) na Mipaka ya majukumu ya WEO
Zana/vifaa: Bangokitita, kiongozi cha mwezeshaji, kalamu rashasha, picha za matukio
MALENGO YA JUMLA
Kuwawezsha washiriki kuelewa nafasi/madaraka na mipaka ya majukumu ya Afisa
Elimu Kata.
MALENGO MAHUSUSI
Hadi mwisho wa kipindi washiriki wawe wameelewa:
Nafasi/madaraka waliyonayo Maafisa Elimu Kata
Mipaka ya majukumu ya WEO
NJIA ZA KUFUNDISHIA
Mwezeshaji atumie njia mbalimbali zitakazowesha washriki kuelewa mada, njia hizo ni
pamoja na;
Maswali na majibu
Majadiliano katika vikundi
18
Kisa mafunzo
Mwezeshaji waongoze washiriki kubunguabongo kwa kuwauliza maswali kuhusu
nafasi na mipaka ya majukumu ya WEO, andika majibu yao kwenye bango kitita.
Mwezeshaji awagawe washiriki kwenye makundi ya watu watano watano wajadili
kuhusu nafasi na mipaka ya majukumu ya WEO na waandike majibu yao katika
Bangokitita. Washiriki wawasilishe majibu yao waliyoandika kwenye Bangokitita.
Baada ya mawasilisho fanya majumuisho kwa kubainisha mambo muhimu kuhusu
nafasi ya WEO na mipaka ya majukumu yao
Mwezeshaji awagawe Washiriki kwenye makundi ya watu watano watano na kuwapa
kila kundi kupitia kisa-mafunzo aliyoiandaa inayohusu nafasi na mipaka ya WEO.
Baada ya kupitia Kisa-mafunzo iliyoandaliwa, Washiriki katika vikundi vyao
wabainishe upungufu wa Kiongozi huyo katika kutambua nafasi na mipaka yake.
Mwezeshaji afanye majumuisho kubainisha nafasi na mipaka ya WEO
Kisa-mafunzo: nafasi na mipaka ya majukumu ya WEO
Mwezi Novemba timu ya Wadau wa Elimu ilitembelea kata ya Mapinduzi kwenda kujifunza
namna uongozi wa kata unavyofanya kazi, na jinsi kata hiyo inavyopambana kujiletea
maendeleo katika sekta za elimu, afya na maji. Tulipokelewa na Mratibu Elimu Kata ambaye
alitoa taarifa fupi ya utenda kazi wake kwenye kata hiyo. Mratibu alisema hivi. Nanukuu;
‘’ kwenye Kata yangu huwa natekeleza majukumu yangu kwa kufuata sheria, Kanuni na
Taratibu za utumishi. Kila wiki huwa natemebelea shule moja iliyo ndani ya kata yangu.
Nikiwa shuleni hukagua kazi za walimu na kuongea na Mwalimu mkuu. Ninapogundua kuwa
kuna Mwalimu ambaye hatekelezi wajibu wake ipasavyo huwa namkemea na akiwa mbishi
namchapa viboko ili iwe fudisho kwa wengine. Mwalimu mkuu ambaye hasimamii vizuri
shule yake huwa napeleka taarifa zake kwa Afisa elimu mkoa na hata kumsimamisha kazi
kwa muda ili ajifunze. Mimi sina utani kwenye kazi! Mara nyingi huwa nakutana pia na
Wajumbe wa kamati za shule, kwasababu wengi hawana elimu ya kutosha juu ya majukumu
yao katika Shule zao, huwa natoa maelekezo kwao na kuwapangia majukumu yao. Pia
inapotokea Shule imepokea fedha Mwalimu mkuu ni lazima atoe taarifa kwangu na hawezi
kutumia fedha hadi ziidhinishwe na mimi. Na kila ninapotembelea Shule ni lazima Shule
husika waniandalie chai na mafuta ya pikipiki yangu ili niweze kufanya kazi zangu kwa
ufanisi. Mbinu hizi zimenisaidia sana kupata mafanikio mnayoyaona’’ Mwisho wa kunukuu.
Karibuni sana Kata ya Mapinduzi .
19
Kipindi cha Nane: RIPOTI NZURI YA AFISA ELIMU KATA (AEK) INA SIFA GANI?
Vifaa
Bango kitita, Kalamu rashasha na gundi utepe
Afisa Elimu Kata waje na ripoti zao zilizounganishwa
Kazi ya 1
Utangulizi Nini kinaifanya taarifa ya Afisa Elimu Kata iwe nzuri? dakika 10
Kila mshiriki aandike jibu la swali hili kwenye karatasi/daftari
Kazi ya 2: Muda dakika 20
Kila mshiriki asome majibu yake na mwezeshaji aandike majibu kwenye bango kitita,
hakikisha haurudii uliyoandika awali
Wote mpitie mambo ambayo umeyaandika na ongoza mjadala kwa nini mambo hayo ni
muhimu katika uandishi wa taarifa nzuri.
Hitimisho Dakika 5.
Wape zoezi la kufanya nyumbani, kila mshiriki aandike taarifa ya maendeleo ya shule zake
na kuileta katika kipindi kijacho. Wazingatie yale muhimu yaliyofundishwa katika kipindi
hiki
Kipindi cha Tisa: Kushirikishana Taarifa za Afisa Elimu Kata (AFISA ELIMU KATA)
Kazi ya 1 dakika 25
Waeleze washiriki wabadilishane taarifa walizoandika na kuja nazo na wachunguze ubora wa
ripoti kwa kutumia vigezo vifuatavyo.
Sentensi zina ujumbe mahususi unaoeleweka?
Je, unafahamu matatizo makuu ya shule ni nini?
Je, maendelao ya shule yameelezwa kwa ufasaha na yanaeleweka kwa urahisi?
Je, unafahamu shughuli gani zilikubaliwa kufanyika kwa ajili ya kuboresha shule?
Je, mpangilio wa taarifa unaeleweka?
Bainisha mambo yaliyosahauliwa kwenye taarifa hiyo.
Kazi ya 2 Mrejesho wa wote dakika 25
Kila mmoja awasilishe matokeo ya taarifa aliyokuwa anaifanyia kazi na washirikishane
20
Hitimisho dakika 10
Hitimisha somo kwa kusisitiza umuhimu wa kuandika taarifa nzuri na kwa wakati. Pia eleza
athari za kutokuandika taarifa nzuri na kwa wakti.
Toa nafasi ya maswali na fafanua pale panapohitaji maelekezo yako
Kipindi cha 10: MKUTANO WA ELIMU WA WILAYA
Vifaa: Bangokitita, kalamu rashaha, gundi utepe
Kazi ya 1:
Utangulizi Mkutano wa Elimu wa Wilaya (MEW) ni nini? dakika 5
Elezea
Mkutano wa Elimu wa Wilaya ni mkutano wa kila mwezi ambao unajumuisha Maafisa wa
Elimu kutoka Wilayani, Wathibiti Ubora wa shule na Afisa Elimu Kata.
MEW ni mkutano rasmi wa Wilaya unaozihusu Wizara za, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Elimu, wenye lengo la kuunganisha
mawazo na uzoefu ili kuweza kusaidia uboreshaji wa shule zetu.
Kazi ya 2: dakika 10
Wajibu na majukumu ya sasa kwenye uboreshaji wa shule wilayani
Wagawanye washiriki katika makundi matatu; Kundi la 1 litaigiza kama Afisa Elimu Kata,
kundi la 2 litajifanya kuwa Wathibiti Ubora (QAs) na kundi la 3 litakuwa la Maafisa. Lipatie
kila kundi bango kitita na kalamu rashasha.
Waambie kila kikundi kujadili jinsi wanavyowajibika kuboresha shule na waaandike mawazo
yao kwenye bango kitita. Kikundi cha kwanza kumaliza kitasema kwa sauti "BINGO".
Kundi hili litabandika bango kitita lao kwenye ukuta. Endelea hadi makundi yote matatu
yakamilishe.
Kazi ya 3: Mrejesho wa Kikundi na Mjadala wa wote dakika 10
Kila kundi libandike Bangokitita lao kwenye ukuta. Waambie wasome orodha ya majukumu
waliyoainisha.
Mwezeshaji sasa ongoza majumuisho ya mrejesho kwa kutumia maswali yafuatayo:
21
Jukumu lipi kati ya hayo linaathari kubwa kwenye uboreshaji wa shule?
Je, muda mwingi unatumia kufanya jukumu gani?
Jukumu na wajibu gani unakusaidia kutekeleza uboreshaji wa shule?
Ni majukumu gani yanayokusaidia kutekeleza uboreshaji wa shule yako?
Mambo ya Kusisitiza:
Kupitia jamii inayojifunza Wilaya ni lazima ihakikishe kuwa:
Ufundishaji na ujifunzaji unaboreshwa
Viwango na madaraja ya wanafunzi yanaimarika
Shule zinawajibika ipasavyo
Hoja za kifedha zinajadiliwa kama vile ruzuku ya Miradi ya shule (IGA)
Wananchi wanashiriki na kujihusisha na masuala ya shule zao
Taarifa zinapokelewa na kutolewa kwa wengine kupitia ripoti
Huu ni wajibu wa pamoja!
Kufanya kazi pamoja kunahitaji muda maalum uliotengwa, muda huo unaitwa
Mkutano wa Elimu wa Wilaya (MEW)
Unashughulikia masuala yanayohusu ufundishaji na ujifunzaji yanapoibuka
Kushirikishana na kuimarisha maboresho ya elimu wilayani
Unasaidia kuleta mawasiliano yenye ufanisi
Kazi ya 4: Faida za Mkutano wa Elimu wa Wilaya (MEW) ni zipi? dakika 10
Hakikisha kila kikundi kina karatasi ya bangokitita na kalamu rashasha. Yakumbushe
makundi kwamba wanapaswa kuchagua mtu mmoja ambaye ataandika maelezo na
kuwasilisha wakati wa mjadala wa wote.
Kuna faida zipi kwa Wathibiti Ubora wa Shule (QAs), Afisa Elimu Kata na Maafisa
wa Wilayani kukutana kila mwezi kuzungumzia suala la ubora wa elimu katika
wilaya yenu?
Kipi ni tofauti kuhusu Mkutano wa Elimu wa Wilaya (MEW)?
Kazi ya 5: Mrejesho wa wote dakika 15
22
Omba kila kikundi kikuambie majibu yao (majibu yasizidi 2). Kisha zunguukia tena kuuliza
majibu toka kwenye makundi mpaka pointi zote zitolewe. Waambie wana kikundi wasirudie
kile kilichosemwa na wengine.
Andika kwenye bango kitita pointi muhimu tu (siyo kila neno) zilizotolewa na vikundi.
Kipi cha tofauti kuhusu MEW?
Mikutano ya Afisa ELimu Wilaya (DEO) na Afisa Elimu Kata, itahusu, vipengele vingi
vikiwemo:
Wajibu wa kiutawala, kuendana na mahitaji na taratibu za Wizara
Kuwataarifu wafanyakazi kuhusu nyaraka na maagizo
Kujadili maendeleo na ufaulu wa wanafunzi
MEW ni chombo mahususi kwa ajili ya kuboresha utendaji wa shule:
Mijadala hujikita zaidi kwenye jinsi ya kuboresha elimu wilayani
Maamuzi hufanywa kwa pamoja kama ‘Jamii inayojifunza’
Ufumbuzi unapatikana, badala ya matatizo, Kwa Afisa Elimu Kata, Wathibiti Ubora
wa shule na Maafisa Elimu kufanyakazi pamoja
Dhamira na wajibu kwa ajili ya kuboresha shule vinashirikishwa kwa wote,
Faida za Mikutano ya Elimu ya Wilaya (MEW)
Mambo ya kusisitiza:
Uelewa wa pamoja wa michango iliyotolewa na kila mtu na kushirikishana mawazo
Kushirikishana masuala ya kufanya yaliyokubalika na wote kwa ajili ya kuboresha
kwa pamoja shule wilayani
Kuthamini na kujenga uwezo wa washiriki wote kwenye mkutano,
Kushirikisha mafanikio na ubunifu mpya
Umuhimu wa mahusiano ya Mkutano wa Elimu (MEW) na majukwaa mengine ya
jamii inayojifunza
Umuhimu wa kushirikishana ripoti za mikutano ya “Jamii inayojifunza”
Kuboresha utendaji wa shule ni kazi ya pamoja!
23
vinakubaliwa, na kufuatiliwa
Fursa kwa Wathibiti Ubora wa Shule na Maafisa kuwajengea uwezo AEK
Afisa Elimu Kata wanabeba jukumu la kutafuta ufumbuzi
Hitimisho dakika 10
Kwa ufupi elezea jinsi unavyoiona mikutano ya MEW:
Kujenga uelewa wa pamoja wa mbinu za kupandisha viwango na ubora wa elimu
wilaya nzima
o Kwa Wathibiti Ubora kuchangia utaalamu wao na kwa Maafisa Elimu kupata
taarifa kuhusu shule zao kwenye wilaya zao
o Kwa halmashauri kupokea taarifa ili kuandaa mipango yao ya kusaidia,
kuelekeza na kuhimiza shule kufanya vizuri, pamoja na kuweka vipaumbele
vya mipango yao kwa ajili ya kuboresha na kugharamia elimu
o Kwa mtiririko wa taarifa kati ya Wathibiti ubora, Maafisa Elimu na Afisa Elimu
Kata kuhusu shughuli za mwezi uliopita na shughuli zitakazopangwa kufanyika
mwezi ujao.
Kupitia maendeleo ya miradi ya Wilaya na kupata mrejesho
Kujikita kwenye masuala ya kuinua ubora wa elimu Wilayani: kupanga shughuli za
mafunzo na kusaidia utekelezaji wa mpango wa maemdeleo ya shule
Kutoa fursa kwa Wathibiti ubora, Maafisa Elimu na Afisa Elimu Kata kuwa na
mikutano ya kila mwezi ya ‘Jamii inayojifunza”, ili kuibua mawazo mapya na
kutafuta njia za kutatua matatizo kwa ajili ya kuboresha shule.
JAMII YA KUJIFUZA YA WALIMU WAKUU
Kipindi cha 11: Jamii ya kujifunza ya Walimu Wakuu ni nini?
Malengo ya kipindi:
Yafuatayo ni malengo ya kipindi hiki:
Kuelezea shabaha ya Jumuiya ya kujifunza ya walimu wakuu
24
Kutoa wasaa kwa washiriki kurejea uzoefu wao wa kuendeleza shule zao hadi sasa
Matokeo Mahsusi:
Mwisho wa kipindi hiki kila mshiriki:
Ataweza kueleza uhusiano uliopo kati Mpango wa maendeleo ya shule na jumuiya ya
kujifunza
Vifaa: Bango lenye maana na malengo ya jumuiya ya kujifunza kwa walimu wakuu
Pangilia ukumbi vizuri ili washiriki wakae kwenye nafasi nzuri ya kukaa na kujadili
1. Jumuiya ya kujifunza ya walimu wakuu (Dakika 10)
Kazi ya 1:
Uliza maswali machache kuhusu maana ya Jumuiya ya kujifunza , wape nafasi ya
kujibu mmoja mmoja.
Kisha waeleze maana ya jumuiya ya Kujifunza ya walimu wakuu
"Jumuiya ya kujifunza ya walimu wakuu ni kikundi cha walimu wakuu
wanaoshirikishana malengo, kusudi, hamu na mitazamo inayofanana, na wanaokutana
mara kwa mara ili kufanya kazi pamoja kwa ajili ya maendeleo ya shule zao".
Jumuiya ya kujifunza ya walimu wakuu inatoa fursa:
Kushirikishana ujuzi, uzoefu, hofu na mashaka
Kuwasaidia kujifunza yaliyo mazuri kutoka kwa kila mmoja
Kuboresha utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya shule
Kazi ya 2: Majadiliano ya vikundi (Dakika 10)
Kwanini Jumuiya ya kujifunza kwa walimu wakuu?,
Kwenye makundi yao washiriki wajadili umuhimu wa Jumuiya ya kujifunza ya walimu
wakuu, kwanini inafaa na ni muhimu. Waweke kumbukumbu ya mambo muhimu kwenye
bango na wamchague mmoja wao kwa ajili ya uwasilishaji.
Kazi ya 3: Mrejesho wa pamoja (Dakika 10)
Kila kundi libandike bango lao ukutani. Kila kundi liwasilishe mambo muhimu waliojadili
(Mwezeshaji ahakikishe makundi hayarudii jambo lililokwisha wasilishwa na kundi
lililotangulia).
25
Mambo ya kukazia: Kwa nini Jumuiya ya kujifunza kwa walimu wakuu
Hitimisho:
Waulize washiriki kama wana maswali na toa ufafanuzi juu ya suala lililoulizwa.
Kushirikishana uzoefu, ujuzi, maarifa, hofu na mashaka
Kusaidia ya Walimu Wakuu kujifunza mambo mazuri kutoka kwa kila mmoja
Kusaidia Walimu Wakuu kuwa na ufanisi katika kutekeleza mabadiliko
Kuboresha utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya shule
Jumuiya ya kujifunza itawasaidia walimu wakuu wajifunze kutoka kwa kila
mmoja, waweze kufanya jambo lisilo sahihi/sawa kuwa sahihi/sawa
Kipindi cha 12: SIFA ZA JAMII YA KUJIFUNZA YA WALIMU WAKUU
Vifaa: Bango kitita, kalamu za rashasha,
Njia za kufundishia: Maswali na majibu, majadiliano.
Kazi ya 1: Muda dakika 10
Wagawe washiriki katika makundi mawili na wajadili sifa kuu za jamii ya Kujifunza
zilizoainishwa hapa kila kundi wafanyie kazi sifa mbili
Kwenye jamii ya kujifunza hakuna madaraka
Wanachama wote wa jamii ya kujifunza ni wanafunzi
Jamii ya kujifunza huanzishwa kwa makusudi, ina mpangilio maalum na ina misingi
ya kuaminiana kati ya wanachama.
Jamii ya kujifunza huzingatia hamu ya kujifunza, wasi wasi, au changamoto ambazo
walimu wakuu wanataka kuzifanyia kazi kwa Pamoja
Kazi ya 2: Dakika 10
Kila kundi wawasilishe kazi yao na wengine wachangine mawazo yao.
Baada ya kuwasilisha kila kundi waongeze sifa kuu mbili.
Hitimisho: Dakika 10
Eleza umuhimu wa sifa hizo zilizoainishwa ili waweze kufahamu ni aina gani ya jamii ya
Kujifunza inayotakiwa kuundwa
26
Kipindi cha 9: Hatua nne za kuunda jamii ya kujifunza kwa walimu wakuu
Vifaa: Bango kitita, kalamu za rashasha,
Njia za kufundishia: Maswali na majibu, Igizodhima.
Kazi ya 1: Muda dakika 15
Eleza kwa kina maana ya kila hatua, kisha wagawe washirika katika makundi manne
kulingana na hatua zilizopo. Kisha waambie washirika kutengeneza igizodhima juu ya
kila hatua
Kujenga ushirika
Kutafuta kusudi la pamoja
Kutafuta njia ya kufikia mabadiliko na maboresho
Kubaini uwezo wa jamii ya kujifunza (ujuzi, maarifa na uzoefu wa wanajamii
Kazi ya 2: Dakika 20
Wape nafasi washiriki waoneshe igizo kulingana na hatua (waanze wa hatua ya kwanza)
Baada ya kuwasilisha wape nafasi ya kujadiliana juu ya maigizo hayo.
Kazi ya 3: Dakika 20
Chagua washiriki watatu na waigize kama Afisa Elimu Kata kwa zamu, na wengine wawe
ndio walimu wakuu. Washiriki watatu waliochaguliwa waunde jamii ya Kujifunza kwa
zamu, baada ya kundi la kwanza kuundwa, washiriki wajadili kama kuna Maeneo ya
kuyaimarisha zaidi. Wafanye hivyo hadi wote watatu watakapomaliza.
Hitimisho: Dakika 5
Waeleze washiriki kuwa sasa wanatakiwa kuunda jamii za Kujifunza za walimu wakuu
katika kata zao. Pia wanatakiwa kusimamia na kutoa msaada inapohitajika na kuona walimu
wakuu wanafanya vizuri katika masomo yao.
Kipindi cha 13: KUFANYAKAZI NA WADAU WENGINE WA ELIMU
Zana/vifaa: Bangokitita, kiongozi cha mwezeshaji, kalamu rashasha, chati ya wadau
wa elimu
MALENGO YA JUMLA: Kuwawezsha washiriki kuwatambua wadau muhimu wa elimu
na jinsi ya kufanya nao kazi ili kufanikisha malengo ya elimu.
27
MALENGO MAHUSUSI
Hadi mwisho wa kipindi Afisa Elimu awatambue wadau muhimu wa Elimu katika kata yake
anaopaswa kufanya naye kazi ili kufikia malengo ya elimu.
NJIA ZA KUFUNDISHIA
Mwezeshaji atumie njia mbalimbali zitakazowesha washriki kuelewa mada, njia hizo ni
pamoja na;
Maswali na majibu
Majadiliano katika vikundi
Igizodhima
Kazi ya 1: dakika 25
Mwezeshaji awagawe washiriki kwenye makundi ya watu watano watano , kila kikundi
waorodheshe wadau wa elimu ambao wanafanya nao kazi na wabainishe wengine wapya.
Kisha kila kikundi waoneshe ni jinsi gani watafanya kazi na kila mdau na kazi yake ni
nini
wajadili kuhusu jinsi wanavyopaswa kufanya kazi kwa kushirikiana na wadau wengine
wa elimu.
Washiriki wafanye mawasilisho kwa kutumia Bango kitita kwa Mfano uliooneshwa
Jina la mdau/mtu au
Taasisi
Shughuli anayofanya Utafanya nae kazi katika
Maeneo gani
Mfano: Visiga
foundation
Mchimbaji wa visima vya
maji
Kumshirikisha katika mkakati
wa upatikanaji wa maji shuleni
Hitimisho: dakika 5
Baada ya mawasilisho mwezeshaji afanye majumuisho kwa kuonesha chati iliyoandaliwa
inayofafanua wadau muhimu wa Elimu ambao WEO anapaswa kushirikiana nao katika
utekelezaji wa majukumu yake.
28
Kipindi cha 14: SHERIA, KANUNI, MIONGOZO NA NYARAKA ZINAZOHUSU
MASUALA YA ELIMU.
Zana/vifaa: Bangokitita, kiongozi cha mwezeshaji, nakala za; Sheria ya Utumishi wa
umma, utumishi wa waalimu na kanuni zake,Kanuni za kudumu za
utumishi wa umma za mwaka 2009,Miongozo na Nyaraka zinayohusu
masuala ya Elimu.
Muda: Dakika 120 (gawanya kipindi hiki katika vipindi/ Sehemu ndogondogo ili
washiriki waelewe kikamilifu)
MALENGO YA JUMLA
Kuwawezsha washiriki kuweza kubainisha sheria, kanuni, miongozo na nyaraka
mbalimbali wanazopaswa kuzitumia katika kutekeleza majukumu yao.
MALENGO MAHUSUSI
Hadi mwisho wa kipindi washiriki wazitambue;
Sheria Na.8 ya Utumishi wa umma ya mwaka 2003 na Na. 25 ya Utumishi wa Waalimu
ya mwaka 2015.
Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003 na za Utumishi wa Waalimu za mwaka
2016.
Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009.
Sera ya Elimu ya mwaka 2014
Waraka wa mishahara wa mwaka 2015
Waraka Na. 3 wa mwaka 2016 unaohusu Utakelezaji wa Elimu Msingi bila malipo
Waraka Na.1 wa Elimu 2013 wa kuchangia ngarama za ukaguzi wa shule kwa kiwango
cha shilingi 1,000 kwa kila mwanafunzi, kwa shule za sekondari zisizo za serikali.
Miongozo ya bajeti upande wa masuala ya Elimu, 2018-01-19
Muongozo wa Matumizi ya fedha za Ruzuku ya Uendeshaji (Capitation Grants) kwa
shule za Msingi za Serikali kufuatia uamuzi wa Serikali kutekeleza Elimu msingi bila
Malipo.
Muongozo wa fomu za kujiunga na kidato cha kwanza kwa shule za sekondari za serikali
Kumb. Na.DC.297/507/01/146/ ya 23/11/2015.
NJIA ZA KUFUNDISHIA
Mwezeshaji atumie njia mbalimbali zitakazowesha washiriki kuelewa mada, njia hizo ni
pamoja na;
29
Maswali na majibu
Majadiliano katika vikundi
Igizodhima
JINSI YA ZA KUFUNDISHA
Mwezeshaji awagawe washiriki kwenye makundi ya watu watano watano waandae
Igizodhima linalohusu uvunjwaji wa Sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa.
Igizodhima kuhusu uchangiaji wa Elimu msingi bila Malipo kinyume cha Sheria, Kanuni na
Miongozo iliyowekwa.
IGIZO DHIMA JUU YA UCHANGIAJI WA ELIMU MSINGI BILA MALIPO- KISA
MKASA.
Mkata Kicheko ni mkuu wa shule katika Shule ya Sekondari Asante Nyerere. Shule hii ipo
wilayani Katamajani katika Wilaya ya Mkonganje. Mkuu wa shule akishirikiana na
mwenyekiti wa Shule ndugu Kikombe badilisha, waliitisha kikao cha bodi ya shule na
kuwaeleza wajumbe changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo. Baadhi ya
changamoto hizo zilikuwa ni pamoja na shule kutokuwa na walimu wa masomo ya sayansi,
kutokuwa na mlinzi, uhaba wa fedha za kuendesha mitihani, uchache wa majengo, kutokuwa
na uzio na hivyo wananchi kukatiza hovyo katika mazingira ya shule na wakati mwingine
kuiba mali za shule, pamoja na changamoto zingine. Mwisho wa kikao mkuu wa shule
pamoja na bodi ya shule walikubaliana kuandaa fomu kwa ajili ya kuwaomba
wazazi/wananchi michango ya fedha ili kupunguza changamoto hizo. Fomu hiyo ilionesha
aina ya michango iliyokuwa inahitajika. Miongoni mwa michango hiyo ni kama ifuatavyo;-
michango kwa ajili ya waalimu wa Sayansi, ulinzi, mitahani/majaribio, ukarabati wa
madarasa, ununuzi wa samani, ujenzi wa uzio wa shule, mhafali ya kidato cha nne, ununuzi
wa t-shirt, uwekaji nembo, ziara za kitaaluma, vitambulisho na picha za kadi za maendeleo.
Baada ya hapo kikao kiliridhia na Mtendaji wa kata ambae pia ni mjumbe wa bodi katika
shule hiyo aliahidi kufanya kazi ya kukusanya michango akishirikiana na watendaji wake wa
vijiji baada tu ya kufanya kikao cha hadhara na wananchi wake.
Mwezeshaji awaongoze Washiriki waweze kubainisha mambo yanayoashiria uvunjaji
wa Sheria , Kanuni na Taratibu katika
kushughulikia masuala ya Elimu msingi bila malipo kwa mujibu wa habari
waliyoisoma.
Aidha, Washiriki wabainishe hatua zinazopaswa kufuatwa katika kuridhia michango
iliyotokana na wazazi/wananchi.
Mawasilisho yafanyike kwa kutumia bangokitita.
30
Baada ya mawasilisho mwezeshaji afanye majumuisho kwa kubainisha ukiukwaji wa
Sheria Kanuni,Taratibu na Miongozo uliofanywa na Mkuu wa Shule kwa Mujibu wa
kisa mkasa.
Mwezeshaji awaongoze washiriki kupitia Kanuni Na. 12(3) ya Kanuni za Utumishi
wa Walimu za mwaka 2016 ambayo imewapa Walimu Wakuu na Wakuu wa shule
mamlaka ya
Mwezeshaji awaongoze Washiriki kupitia Kanuni Na. 12 (3) cha Kanuni za Utumishi
wa Walimu za mwaka 2016 ambapo imetamkwa kuwa Mamlaka ya Nidhamu ya
Mwalimu katika ngazi ya Shule ni Mwalimu Mkuu au Mkuu wa Shule. Baada ya
kupitia Kanuni hiyo katika vikundi wabainishe aina ya makosa ambayo Mwalimu
anaweza kuyafanya na adhabu zinazoendana na makosa hayo.
Mwezeshaji awape washiri kazi ya vikundi inayohusu kesi ya Kinidhamu ya
Mwalimu ambaye hufika shuleni lakini hatimizi wajibu wake.
Kipindi cha 15: WAJIBU, MIIKO NA MAADILI YA KAZI YA UALIMU
Zana/vifaa: Bangokitita, kiongozi cha mwezeshaji, nakala ya Mkataba wa Ajira wa
Mwalimu.
MALENGO YA JUMLA
Kuwawezsha washiriki kuweza kubainisha Wajibu, Miiko na Maadili ya kazi ya
ualimu
MALENGO MAHUSUSI
Hadi mwisho wa kipindi washiriki wawe kutekeleza;
Wajibu wao
Miiko na Maadili ya Kazi ya Ualimu.
NJIA ZA KUFUNDISHIA
Mwezeshaji atumie njia mbalimbali zitakazowesha washiriki kuelewa mada, njia hizo ni
pamoja na;
Maswali na majibu
Majadiliano katika vikundi
31
Kazi ya 1: Dakika 20
Wagawe washiriki katika makundi ya watu wanne wanne, kila kundi waandike majuku
makuu 5 ya mwalimu mkuu au mkuu wa shule. Wape nafasi kubandika ukutani kazi yao
kisha wasomee zile zilizoandaliwa na washiriki waongezee zile wasizokuwa nazo.
Ni mtaaluma mkuu katika shule;
Kuhakikisha kuwa maagizo na miongozo yote inayohusu elimu inazingatiwa na
walimu na jamii pamoja na kusimamia utekelezaji wake;
Kuongoza jumuiya nzima ya shule;
Kusimamia shughuli zote za uendeshaji wa shule;
Ni kiungo kati ya shule na jumuia inayozunguka shule, viongozi wa Serikali, wazazi;
jamii na Taasisi mbalimbali;
Msimamizi wa raslimali zote za shule;
Kuhakikisha kuwa fedha zote za shule zikiwemo ruzuku toka serikalini au vyanzo
vya shule zinathibitiwa ipasavyo na kutumika kwa malengo kusudiwa tu;
Kuhakikisha kuwa walimu na watumishi wasio walimu wanashirikiana katika
uongozi na maendeleo ya shule;
Kuhakikisha kuwepo kwa uwazi juu ya mapato na matumizi ya fedha za shule kwa
walimu, wanafunzi na jamii husika; na
Kubuni mikakati ya kuboresha taaluma na maendeleo ya shule kulingana na
mazingira yake.
Kazi ya 2: Dakika 10
Wagawe washiriki katika jozi na kila jozi ijadili na kufafanua jukumu mojawapo la mwalimu
mkuu au mkuu wa shule. Hakikisha kila jozi imepata kazi.
Baada ya mawasilisho hitimisha kipindi kwa kusisitiza kuwa ni jukumu la Afisa Elimu Kata
anahakikisha kuwa mwalimu mkuu au mkuu wa shule anatekeleza majukumu yake
kikamilifu na anamsaidia pale anapopata tatizo katika utekelezaji.
32
SHERIA ZA UTUMISHI
Kipindi cha 16: MAADILI YA UONGOZI
VIFAA: Bango kitita, kalamu za rashasha, Maadili ya Uongozi,
LENGO: Washiriki waweze kubaini na kutekeleza maadili ya uongozi katika sehemu zao za
kazi
KAZI YA 1: DAKIKA 10
Mwezeshaji awagawe washiriki katika jozi na wajadili maana ya maadili
Mwezeshaji aunganishe jozi mbili na washirikishane majibu ya majadiliano yao
Washiriki waandike yale waliyokubaliana na wayawasilishe ubaoni kwenye bango
kitita
Mwezeshaji atoe nafasi kwa kila kikundi kuwasilisha kazi yake
Kazi ya 2: Dakika 10
Mwezeshaji awaongoze washiriki kuoroghesha maadili ya uongozi wanayo yafahamu
katika vikundi vya watu watano watano
Mwezeshaji awape nafasi wanakikundi kuwasilisha kazi zao
Kila kikundi kibandike kazi yake ukutanii mmoja atateuliwa kuwasilisha na wengine
watazungukia kazi za wenzao
Kazi ya 3: Dakika 30
Mwezeshaji awasilishe rasmi maadili ya uongozi kwa washiriki
Mwezeshaji awape nafasi washiriki wajadili yale waliyowasilisha
Mwezeshaji aandae maswali ya kuwaongoza washiriki katika majadiliano kwenye makundi
ya watu watano watano na wajibu maswali yafuatayo
1. Je viongozi wanayo maadili
2. Je wanayajua
3. Je wanayafuata, Kama hawayafuati ni changamoto gani zinazowafanya washindwe
kuyafuata
4. Wewe kiongozi (WEO) ni kwa jinsi gani maadili ya uongozi yanakusaidia kutekeleza
kazi zako za Kielimu
5. Wanakikundi watawasilisha majadiliano yao mbele ya washiriki
HITIMISHO/TATHIMINI: Mwezeshaji atawaambia washiriki wachukue nukuu za somo
kwa ajili ya rejea.
33
Kipindi cha 17: HAKI NA STAHIKI
VIFAA: Makala za haki na stahiki, bangokitita nk
LENGO: Washiriki wajue haki na stahiki wanazo stahili ili ziweze kuwasaidia katika
kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa ufanisi zaidi
NJIA ZA KUFUNDISHIA
Majadiliano
Mapitio ya nyaraka na uchambuzi wake
Jedwali la kutofautisha Haki na stahiki
S/N HAKI STAHIKI
KAZI YA 1: DAKIKA 40
Mwezeshaji awaongoze washiriki kubaini maana ya haki na stahiki (Rights and
Privileges
Washiriki waorodheshe haki na stahiki zao katika jedwali
Mwezeshaji awapitishe kwenye haki na stahiki kama zilivyoandikwa kwenye sheria
za utumishi
Washiriki wajadili utekelezaji wa haki na stahiki zao
KAZI YA 2: DAKIKA 10
ICE BREAKER – Ichukue muda wa dakika kumi kuhakikisha kuwa inahusisha mada
ya haki na stahiki
HITIMISHO NA TATHIMINI:
Mwezeshaji atoe majumuisho ya somo na kuangalia ushiriki wa kila mmoja pia na
kupokea maoni kutoka kwa washiriki.
Pia atafute nyaraka zifuatazo
34
1. Maadili ya uongozi
2. Haki za mtumishi
3. Stahiki za mtumishi
4. Kazi za weo
5. Sifa za weo
6. Majukumu ya weo
AINA ZA HAKI ZA MTUMISHI
Likizo..........(Zipo aina tofauti ...)
Haki ya kuacha kazi
Haki ya matibabu
Haki ya mazishi
Haki ya kuazimwa
Haki ya mafunzo/kujiendeleza
Haki ya kukata rufaa kutoka
mamlaka moja kwenda mamlaka
nyingine (Mamlaka ya nidhamu)
Haki ya kulipwa mashahara
Haki ya kupanda cheo...... vipo vitu
vya kuzingatia
Haki ya kuthibitishwa kazini
Haki ya ajira (Kuwa na mkataba wa
kaz
UONGOZI NA MENEJIMENT KATIKA ELIMU
Kipindi cha kwanza: MAANA YA UONGOZI
ZANA / VIFAA: Bango kitita, karatasi, na kalamu rashasha
MALENGO YA JUMLA
Kuwawezesha washiriki kuelewa dhana nzima ya uongozi na utekelezaji wake
kwa lengo la kufanikisha malengo ya taasisi husika.
MALENGO MAHUSUSI
Hadi mwisho wa kipindi washiriki wawe wamebainisha na kutambua:
NJIA ZA KUFUNDISHIA
Mwezeshaji atumie njia mbalimbali kuhakikisha washiriki wanaelewa dhana nzima ya
Uongozi. njia hizo ni pamoja na kumwalika mgeni, mapitio ya nyaraka, vitabu na
mitandao .
Kazi ya 1: Dakika 10
waambie washirika waandika kwenye daftari zao maana ya Uongozi kwa jinsi wanavyoelewa.
Wape nafasi kila mmoja kueleza maana ya Uongozi aliyoiandika.
Wapatie tafsisi ya Uongozi uliyoinandaa na kuwafafanulia zaidi.
35
Kazi ya 2: Dakika 10
Wagawe washilriki katika makundi matatu, na kila kundi waeleze kiongozi ni nani, na
majukumu yake ni nini katika shule kisha wawasilishe kazi yao.
Uliza maswali ya udadisi ili waweze kueleza zaidi.
Kazi ya 3: Dakika 20
Waambie kila mmoja andike katika daftari lake kwa nini anafikiri kuwa yeye
ni kiongozi katika kata.
Kisha kila mmoja ashirikishane na mwezake aliye upande wake wa kulia.
Waunganishe sifa zao na wawasilishe.
Washiriki wengine waulize maswali au juu ya yanayowasilishwa
Hitimisho
Hitimisha kwa kuelezea maana ya Uongozi na nani ni kiongozi.
Pia awakumbushe kuwa wao ni viongozi katka kata zao.
Kipindi cha 2: AINA ZA UONGOZI
Utangulizi: Dakika 5
Wakumbushe kwa njia ya maswali kiongozi ni nani na Uongozi ni nini?
Kazi ya 1: Dakika 20
Zana/vifaa Bangokitita, kiongozi cha mwezeshaji, kalamu rashasha, picha za viongozi mbalimbali.
Mwezeshaji abandike picha za viongozi mbalimbali ukutani na awatake washiriki
wabunguebongo katika jozi kwa kurejea picha hizo.
Mwezeshaji awatake washiriki kutoa mrejesho wa walichokibaini kutokana na picha hizo.
Mwezeshaji awagawe washiriki katika vikundi vya watu watano watano na kuwapa orodha ya
viongozi 20 wa Afrika na kuwataka wabainishe aina ya uongozi wao na sababu za ubainisho
huo.
Mwezeshaji aongoze washiriki kufanya majadiliano ya pamoja kubainisha aina za viongozi
kulingana na majadiliano ya vikundi.
Mwezeshaji, achague mshiriki mmoja aongoze zoezi la kuchangamsha mwili kwa vitendo.
Changamsha mwili inaweza kuwa kuimba, kucheza, au kufanya zoezi lolote kwa vitendo.
Hitimisha kwa kuwaeleza kuwa somo litaendelea kipindi kijacho
Kazi ya 2: Dakika 20
Waulize washiriki wataje aina za Uongozi wanazozifahamu kulingana na majadiliano ya
zoezi la kwanza.
Andika aina za Uongozi zilizotajwa
Wagawe washiriki kulingana na aina za Uongozi zilizotajwa na waeleze faida na hasara za
aina hizo na watoe angalau Mfano mmoja halisi. Kisha waeleze ni aina ipi ya Uongozi ni
bora zaidi?
Wape nafasi ya kuwasilisha
36
Hitimisho: Dakika 5
Hitimisha kipindi kwa kuwauliza mmoja mmoja je wao wanatumia aina gani ya Uongozi na kwa
nini
Kipindi cha Tatu: MAJUKUMU YA KIONGOZI
Utangulizi: Dakika 5
Wakumbushe washiriki juu ya aina za Uongozi na sifa zake.
Zana/vifaa Bangokitita, kiongozi cha mwezeshaji, kalamu rashasha, simulizi ya utendaji wa
kiongozi iliyoandaliwa.
Simulizi Mwezeshaji atafute simulizi inayohusiana na majukumu ya kiongozi
Kazi ya 1: Dakika 10
Mwezeshaji awagawe washiriki katika vikundi vya watu watano na kuwapa karatasi
inayosimulia utendaji wa Kiongozi. Baada ya kupitia habari hiyo, mwezeshaji awatake
kubainisha majukumu ya Kiongozi waliyoyabaini kutokana na habari waliyoisoma.
Mwezeshaji awaongoze washiriki kubainisha majukumu ya Kiongozi.
Wape nafasi ya kuwasilisha.
Kazi ya 2: Dakika 25
Kila mshiriki aandike majukumu yake makuu matano (hakikisha kila mmoja anaandika
majukuu yake na sio kuangalia kwa mwingine)
Kila mshiriki awasilishe majukumu yake
Andika majukumu ya kila mmoja kwenye bangokitita (usirudie lililotajwa)
Bandika majukumu ya AEK kama iliyoainishwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia
Wape nafasi washiriki wanakili majukumu yao rasmi.
Kazi ya 3: dakika 10
Ongoza majadiliano jinsi wanavyotekeleza majukumu yao, kuna changamoto gani na
wanazitatuaje? Je wakipata changamoto wanapata wa msaada?
Hitimisha kipindi kwa kuwaelezea umuhimu wa kujua majukumu yao na kuyatekeleza
Kipindi cha nne: SIFA ZA KIONGOZI
Utangulizi Dakika 15
Kila mshiriki amtaje amuelezee kiongozi anayemuhusudu na kwa sababu gani
Kazi ya 1: Dakika 10
37
Zana/vifaa Bangokitita, kiongozi cha mwezeshaji, kalamu rashasha, aeneo i ya utendaji wa
kiongozi iliyoandaliwa.
Mwezeshaji awagawe washiriki kwenye makundi ya watu watano watano wajadili na waandike
sifa za kiongozi bora wanazozifahamu na kutoa mifano halisi, na kuwasilisha majibu yao
waliyoandika kwenye Bangokitita.
Kazi ya 2: Dakika 15
Mwezeshaji awagawe washiriki katika vikundi vya watu watano, watano na kuwapa karatasi
inayosimulia utendaji wa Kiongozi. Baada ya kupitia aeneo hiyo, mwezeshaji awatake kuainisha
sifa za Kiongozi walizobaini kutokana na aeneo waliyoisoma.
Simulizi, Mwezeshaji: Andaa kisa mkasa au igizodhima kuhusu sifa za kiongozi
Kazi ya 3: Muda dakika 20
Mambo yanayofanya mtu kupoteza sifa za kiongozi bora.
Zana/vifaa: Bangokitita, kiongozi cha mwezeshaji, kalamu rashasha, picha za viongozi
mbalimbali.
Wagawe washiriki katika makundi matatu.
Mwezeshaji awatake washiriki wataje mambo yanayoweza kumfanya yeye akiwa ni kiongozi
apoteze sifa ya Uongozi watoe mifano halisi na athari zake kwa maendeleo ya kata/wilaya zao.
Hitimisho
Waambie washiriki wataje jambo moja walilojifunza kuhusu sifa na majukumu ya kiongozi
MENEJIMENT/USIMAMIZI
Kipindi cha 5: Kuelewa dhana ya Menejiment/Usimamizi
Zana/vifaa: Bangokitita, kiongozi cha mwezeshaji, kalamu rashasha,
Muda: Dakika 20
MALENGO YA JUMLA
Kuwawezsha washiriki kuelewa dhana nzima ya Menejimenti na utekelezaji wake
kwa lengo la kufanikisha malengo ya taasisi husika.
MALENGO MAHUSUSI
Hadi mwisho wa kipindi washiriki wawe wamebainisha:
Dhana ya Menejimenti
Umuhimu wa Taasisi kuwa na Menejimenti/Usimamizi
Kubainisha Kanuni za Menejimenti.
Kutathmini aina ya Menejiment zilizopo katika taasisi za elimu
NJIA ZA KUFUNDISHA
Majadiliano, maswali na majibu kazi za vikundi
38
Kazi ya 1: Umuhimu wa Menejiment muda dakika 40
Zana/vifaa Bangokitita, kiongozi cha mwezeshaji, kalamu rashasha, Kisa mafunzo
Mwezeshaji awagawe washiriki katika vikundi vya watu watano na kuwapa karatasi
inayosimulia menejimenti katika taasisi mbili tofauti. (Kisa mafunzo yameambatishwa-
Kiambatisho 1&2)
Baada ya kupitia habari hiyo, mwezeshaji awatake kuainisha umuhimuna athari za
kutokuwa na Menejimenti kwenye makundi hayo.
Hitimisho
Hitimisha kipindi kwa kuwapa zoezi la kufanya nyumbani kama kuna umuhimu wa kuwa na
menejimenti au uongozi katika shule, waeleze kuwa tutawasilisha mwanzo wa kipindi kijacho
Kipindi cha 6: Kanuni za Menejimenti/Usimamizi
Zana/vifaa Bangokitita, kiongozi cha mwezeshaji, kalamu rashasha
Utangulizi Dakika 5
Wakumbushe washiriki kusoma majibu ya kazi uliyowapatia kipindi kilichopita
Kazi ya 1: Dakika 20
Mwezeshaji awagawe washiriki kwenye makundi ya watu watano watano wajadili na waandike
Kanuni za Menejiment wanazozifahamu na kuwasilisha majibu yao waliyoandika kwenye
Bangokitita.
Mwezeshaji aongoze washiriki kufanya majadiliano ya pamoja kubainisha Kanuni za
Menejimenti kulingana na majadiliano ya vikundi.
Mwezeshaji kwa kukazia maarifa awatake washiriki watatu kusimulia kisa mkasa
kinachoashiria kufuatwa au kutokufuatwa kwa Kanuni za Menejimenti kama walivyoziainisha
kwenye makundi yao.
Kipindi cha Saba: UMUHIMU WA MENEJIMENTI KATIKA SHULE
VIFAA: Bango kitita, Igizo dhima, kalamu rashasha.
LENGO LA KIPINDI: Kuwezesha washiriki kupata umuhimu wa management katika Elimu.
NJIA ZA KUFUNDISHIA
Mwezeshaji atumie njia shirikishi kuwaongoza washiriki kutoa fasili mbalimbali kuhusu
menejimenti.
Wagawe washiriki wakae wawili wawili wajadiliane kisha wakupe fasihi moja
waliokubaliana
Mwezeshaji awaelekeze kuziandika kwenye bango kitita na kuzibandika ukutani
39
Mwezeshaji awaongoze washiriki kuzipitia fasili hizo na kisha kutoa fasili moja sahihi
ya wanakikundi watakayo kubaliana nayo.
Kazi ya 1 Muda Dk.40
Mwezeshaji ataunda kikundi cha watu watano watakaoigiza katika kuhusiana na umuhimu wa
menejiment na uongozi katika Elimu.
Washiriki wengine waliobakia watakuwa wanasikiliza na kufuatilia kwa makini mtiririko
mzima wa Igizodhima kisha watawasilisha kile walichokibaini kwenye igizodhima kutokana na
menegiment na uongozi katika Elimu.
Washiriki wagawanywe kwenye makundi matatu ya watu watano watano, kisha watoe
mrejesho.
HITIMISHO NA TATHIMINI dk 20
Mwezeshaji afanye majumuisho ya mada nzima ya umuhimu wa menejimenti na uongozi katika
Elimu. Atoe muda wa maswali. Pia aangalie ushiriki wa kila mmoja katika somo/kipindi kizima.
Kipindi cha Nane: TOFAUTI YA MENEJA NA UONGOZI
VIFAA: Bango kitita, Igizodhima, Kadi ndogo na kalamu za rashasha
Utangulizi: Dakika 5
Tengeneza mpira mdogo wa makaratasi na warushie, atakayeudaka aeleze sababu moja ya
umuhimu wa menejimenti na Uongozi, akimaliza amrushie mwingine, wafanye hivyo hadi wote
wamemalizika.
LENGO: Kuwawezesha washiriki kubaini tofauti zilizopo kati ya menejiment na uongozi katika
Elimu
Kazi ya 1: Dakika 10
Mwezeshaji abandika maneno mawili ukutani (Meneja na Kiongozi)
Mwezeshaji agawe stika kwa washiriki wote na kila mshiriki aandike sifa mbili mbili kwa
meneja na kiongozi
Mwezeshaji awaongoze kubandika stika chini ya neno meneja au kiongozi
Mwezeshaji awaongoze kuzipanga stika kulingana neno husika na kuzipitia ili kuonesha
utofauti
Mwisho mwezeshaji aawaleze tofauti kati ya meneja na kiongozi , kisha washiriki wapange
stika zao kulingana na maelezo ya mwezeshaji
40
KAZI YA 2: dakika 30
Wagawe washiriki katika makundi mawili, kundi moja waigize kama meneja , kundi la pili waigize
kuhusu kiongozi, wakionesha tofauti zake. Baada ya Kuonesha igizodhima, katika jozi wajibu
maswali yafuatayo:
1. Je umejifunza nini kutokana na igizodhima
2. Je kuna uwezekano wa mtu moja kuwa meneja na kiongozi kwa wakati moja? Ndio au Hapana
Eleza.
3. Wewe ni kiongozi au meneja?
4. Je mwalimu mkuu ni kiongozi au meneja?
Kazi ya 3: Dakina 10
Kila jozi iungane na jozi nyingine na kushirikishana majibu, yao, waandike majibu yao kwenye
bango kitita na kuyawasilisha
Waulize umuhimu wa kuwa na tofauti hizo, kama ndio au hapana ni kwa sababu gani
HITIMISHO dakika 5
Mwezeshaji afanye majumuisho kwenye mada nzima na aelezee umuhimu wa tofauti kati ya
menejiment na uongozi katika Elimu
UELEKEZI NA USHAURI ELIMISHI
Kipindi cha kwanza
UTANGULIZI: Wakaribishe washiriki katika kipindi waeleze mada itakayofundishwa .
Mada: Maana Ya Uelekezi Na Ushauri Elimishi Dakika 30
VIFAA: Bango Kitita, Kalamu za rashasha, gundi,
MALENGO: Washiriki waweze kuelezea kwa ufasaha maana ya uelekezi na Ushauri Elimishi
Kazi ya 1: Dk 10
Wagawe washiriki katika makundi manne kulingana na idadi ya washiriki. Kila kundi wajadili na
kuandika kwenye bango kitita maana ya uelekezi na Ushauri Elimishi –
Kazi ya 2: Dk 10
Waongoze washiriki kuwasilisha kazi za vikundi, toa nafasi ya kujadili kazi iliyowasilishwa.
HITIMISHO: Dk 10
Hitimisha mjadala kwa kutoa maana ya Uelekezi na ushauri elimishi washiriki wanakili maana
ulizotoa kwa kuongezea yale waliyowasilisha hapo awali.
41
Kipindi cha pili
Mada: umuhimu wa uelekezi na ushauri elimishi katika uongozi
VIFAA: Bango Kitita, Kalamu za rashasha, Igizodhima
Utangulizi: dakika 5
Waulize washiriki kurejea mada ya kipindi kilichopita kwa kuwauliza maana ya uelekezi na ushauri
elimishi na nini nafasi yake katika Uongozi
Malengo: Washiriki waweze kufahamu umuhimu wa kuwa na mwelekezaji na Mshauri Elimishi
katika uongozi
Njia za ufundishaji
Mwezeshaji atatumia njia ya maswali na majibu, kazi katika vikundi, Majadilianao, Igizo dhima.
Kazi ya 1: Igizodhima – Umuhimu wa uelekezi na ushauri elimishi Dakika 20
Chagua washiriki wachache na watengeneze igizo kulingana na kisa-mafunzo kifuatacho
Afisa elimu kata ya Mivumoni amepata walimu wa kuu watatu katika kata zake. Waalimu wakuu
hao ni mara yao ya kwanza kushika nyadhifa hizo. Jumatatu asubuhi, alikutana na walimu hao na
kuwaonesha shule zao zilipo na kuwatambulisha kwa walimu, aliwaambia walimu hao wasisite
kumtaarifu wakati wowote watakapopata tatizo linalohotaji msaada wake. Kisha aliondoka na
kuendelea na kazi zake za kila siku.
Wakati washiriki wengine wanajiandaa waulize washiriki waliobaki tofauti wanayoiona kati ya
uelekezi na ushauri elimishi.
Baada ya kuona igizodhima, wagawe washiriki katika makundi ya matatu kisha wajibu maswali
yafuatayo:
Kundi la 1: Je kama wewe ni Afisa Elimu kata huyo ungefanya nini tofauti kwa walimu wakuu
wapya hao? Kwa nini?
Kundi la 2: Eleza jinsi unavyotoa msaada kwa walimu wakuu wapya wanaohamia kwenye kata
yako
Kundi la 3: Changamoto gani za kiutendaji unazipata unapowapokea walimu wakuu au walimu
wapya katika kata yako: je unazitatuaje?
HITIMISHO: Dakika 5: Fanya majumuisho kwa kusisitiza mambo mawili muhimu kwa kiongozi
kutumia mbinu za uelekezi na ushauri elimishi
42
Kipindi cha Tatu
Mada: Kanuni za Uelekezi na Ushauri Elimishi Muda dk 60
MALENGO: Washiriki waweze kubainisha kanuni za uelekezi na ushauri elimishi na kuzitekeleza
katika majukukumu yao ya kila siku
VIFAA: Bango kitita, kalamu rashasha, nakala ya kitabu cha mwongozaji
NJIA ZA KUFUNDISHIA
Mwezeshaji atatumia njia mbalimbali katika kuendesha mada, kama vile Bongua bongo,
majadilianao, maswali na majibu.
Kazi ya 1: Dk 40
Wagawe washirika katika makundi mawili, wapatie kundi moja kanuni za uelekezi na
kundi la pili wapatie kanuni za ushauri elimishi.
Wape muda wa kujadili kisha wawasilishe jinsi walivyoelewa juu ya kanuni waliyoijadili.
Kipindi cha Nne kanuni za uelekezi na ushauri elimishi
Utangulizi: Wape maswali ya ufahamu juu ya kipidi kilichopita
Jambo gani kubwa Kujifunza juu ya kanuni za uelekezi na ushauri elimishi.
Kazi ya 2: Dk 45
i. Wagawe washiriki katika makundi Katika makundi mawili, waeleze washiriki kujadili
namna watakavyotumia kanuni za uelekezi na ushauri elimishi katika kazi zao.
Wape muda wa kuwasilisha kisha ruhusu majadiliano
Uliza maswali ya udadisi ili kuwafanya wahusika waeleze na kuelewa zaidi.
HITIMISHO:
Mwezeshaji atoe majumuisho ya somo na kutathimini ushiriki wa kila mshiriki
43
Kipindi Cha Tano: Changamoto Za Kufanya Uelekezi Na Ushauri Elimishi
Muda: dk 60
Vifaa: kalamu rashasha, bangokitita
Njia za kufundishia: Oneshombinu, majadiliano katika vikundi , maswali na majibu
Malengo: Kuainisha changamoto mbalimbali zitokanazo na kufanya uelekezi na kutoa ushauri
elimishi kwa mtu
kazi ya 1: dk 15
Mwezeshaji wagawe washiriki katika vikundi vya watu watatu watatu, kasha waongoze kujadili
changamoto za kufanya Uelekezi na kutoa ushauri elimishi. Baada ya kujadili kila kundi liandike
majibu yake kwenye bando kitita na kubandika ukutani, kasha liwasilishe majibu yao.
Kazi ya 2: dk 15
Mwezeshaji akusanye mambo muhimu na kuyafafanua kwa undani ili kila mshiriki aelewe
vizuri
Mwezeshaji ongoza washriki kujadili ufumbuzi wa changamoto zilizoainishwa
HITIMISHO: Mwezeshaji waongoze washriki kuchukua nukuu za somo kwa ajili ya rejea
Kipindi cha Sita: Changamoto za kufanya Uelekezi Muda: dakika 60
Mada: changamoto za kufanya uelekezi/kutoa mafunzo kwa vitendo na kutoa ushauri elimishi
Vifaa: kalamu rashasha, bangokitita
Njia za kufundishia: Oneshombinu, majadiliano katika vikundi , maswali na majibu
Malengo ya somo: Kuainisha changamoto mbalimbali zitokanazo na kufanya uelekezi na kutoa
ushauri elimishi kwa mtu
Ufunguzi: kulitambulisha somo
Kazi ya 1: dk 15
Mwezeshaji wagawe washiriki katika vikundi vya watu watatu watatu, kasha waongoze kujadili
changamoto za kufanya Uelekezi na kutoa ushauri elimishi. Baada ya kujadili kila kundi liandike
majibu yake kwenye bando kitita na kubandika ukutani, kisha liwasilishe majibu yao.
Kazi ya 2: dk 15
44
Eleza mambo muhimu na kuyafafanua kwa undani ili kila mshiriki aelewe vizuri
Mwezeshaji ongoza washriki kujadili ufumbuzi wa changamoto zilizoainishwa
Kazi ya 3: Dakika 30
Washiriki wasome kisa- mafunzo kifuatacho kisha wabainishe Changamoto zilizojitokeza na wape
nafasi wajadili namna ya kuzitatua Changamoto hizo.
Mwezeshaji aandae kisa mkasa
Hitimisho: Mwezeshaji ahitimishe kipindi kwa kutoa ufupisho wa mambo muhimu yaliyojitokeza.
Kipindi cha Saba: Namna ya kufanya uelekezi
Malengo: kuwezesha washiriki kutambua na kuelewa namna ya kufanya uelekezi na ushauri
elimishi
Malengo mahususi:
Afisa elimu kata kuwa na uwezo wa kufanya uelekezi katika kutekeleza majukkumu yake
Afisa elimu kata awe tayari kufanyiwa uelekezi pale inapohitajika
Zana/vifaa: bango kitika, kalamu za rashasha
Kazi ya 1: dk15
Kisa mafunzo: Uelekezi
Maria ni mkurugenzi wa shirika la watoto Tanzania, amefanya kazi mashairika mbalimbali
kwa muda mrefu na ameonesha mafanikio makubwa katika kufanikisha kuwaeleisha wazazi
kuhusu haki za watoto.
Maria anaona Grace ambaye amefanya kazi nae kwa muda mrefu na ana uwezo mkubwa wa
kiutendaji. Kwa kuwa Maria anatarajia kustaafu miaka mitatu ijayo, ameamua kumfanyia
uelekezi Grace ili aweze kushika majukumu makubwa zaidi siku zijazo.
Kila anapokwenda kuendesha mafunzo humpa jukumu grace la kuendesha mafunzo hayo na
kuangalia maeneo ya kuboresha na humshauri mara kwa mara.
Grace amefurahia sana utaratibu huo na anaona imemsaidia sana kujijenga kiutendaji pia
imekuza mahusiano mazuri ya kikazi kati yake na Maria.
Kazi ya 2: dk15
Baada ya washiriki Kuonesha igizo, wagawe washiriki katika makundi ya watu watano watano,
waeleze washiriki waigize kisa kilichoandaliwa na kisha wajadili:_
45
Kuna umuhimu gani wa kufanya uelekezi na ushauri elimishi
Mambo gani muhimu ya kuzingatia
Nani anastahili kufanyiwa uelekezi au ushauri elimishi
Mpango binafsi : dk 20
Wape nafasi washikiri wabainishe eneo moja ambalo watafanya uelekezi kwa mwalimu mkuu
katika shule mojawapo katika kata yake.
HITIMISHO DAKIKA 10
Hitimisha somo kwa kutoa mifano michache ya uelekezi na umuhimu wake katika kuletaufanisi
katika kazi. Kisha anakili eneo ambalo Afisa Elimu kata atatoa uelekezi kwa mwalimu mkuu[.
hakikisha unatunza kumbukumbu kwa ajili ya ufuatiliaji baadaye.
Kipindi cha 10: Elimu Elimishi
Malengo: Kuwezesha washiriki kutambua na kuelewa namna ya kufanya uelekezi na ushauri
elimishi
MALENGO MALENGO MAHUSUSI:
Afisa Elimu kata kuwa na uwezo wa kufanya ushauri elimishi katika kutekeleza
majukkumu yake
Afisa Elimu kata awe tayari kufanyiwa Uelekezi na ushauri elimishi pale inapohitajika
Zana/vifaa: Bango kitika, kalamu za rashasha ,
Kazi ya 1: Dakika 40
Bwana Miche ni AEK mgeni katika kat ya Ungwani ambayo ipo umbali wa kilomita 10 toka
kata ya Shura, kata hii ina AEK ambaye ni mzoefu na amefanya kazi kwa mudawa miaka 20.
Pia katika taaluma, kata ya Shura inafanya vizuri sana.
Afisa Elimu wilaya anamuunganisha Bwana Miche na AEK ya Shura ili aende kujifunza
kama AEK mpya lakini pia kupata uzoefu na kujifunza kutokana na utendaji wa AEK ya
Shura.
Washiriki wasome kisa-mafunzo kilichoandaliwa
Wagawe washiriki katika makundi mawili
Kila kundi watengeneze igizo Kuonesha ni jinsi gani watakavyotoa ushauri elimishi kwa
Afisa Elimu mpya.
Wape nafasi ya kila kundi Kuonesha igizo
Hitimisho dakika 10
Hitimisha somo kwa kutoa kufafanua zaidi juu ya namna ya kufanya uelekezi
Toa nafasi kwa maswali na majadiliano.
46
UONGOZI BINAFSI
Kipindi cha Kwanza: UONGOZI BINAFSI
Vifaa
Bango kitita, Kalamu za rashasha na gundi utepe
Kazi ya 1: Kila mmoja ajibu maswali haya na kisha wengine wamuulize maswa Dk 10
Toa nafasi kwa watu 4 wawili waliofikia ndoto za maisha yao na 2 ambao hawakufikia waeleze
uzoefu wao.
Wape nafasi washiriki kujadili kwa mida mfupi wa DK 5
Kazi ya 2: dk 15
Kila mmoja awe na kipande cha karatasi na aandike ni tabia na mwenendo gani ambao
unamtofautisha na wengine. wahamasishe wawe huru na kila mmoja awe mwaminifu kwake
mwenyewe
Bandika karatasi kubwa mbili ukutani na Kila mmoja (bila kuandika jina) aandike kwe tabia
ambazo anapenda kuziendeleza na anazotaka kutoziendeleza
Tabia ninazotaka kuziendeleza Tabia nisizotaka kuziendelza
Mfano: Kusoma vitabu Kuzungumzia Habari za watu wengine
Baada ya dk 15, wape nafasi washiriki waeleze maoni yao na kisha waongoze kuweka
mambo ambayo yametokea katika washiriki wote kisha
Ongoza mjadala kuhusu mambo yaliyojitokeza kwa wote na kutafuta njia /suluhisho/kauli
ya pamoja Dk 15
Je ulipokuwa mdogo ulitamani kuwa nani?
Sasa umekuwa mtu mzima umekuwa kama uliyotaka?
Kama ni jibu ni hapana kwa nini hukufikia malengo
Kama ni ndio umewezaje kufikia malengo?
47
Hitimisha kipindi kwa kufafanua mambo muhimu katika kufanikisha malengo binafsi
Dk 15
Uongozi binafsi ni kichocheo muhimu sana katika Kujifunza
Kujitathmini mwenyewe (unakotoka, uliko na unkokwenda)
Nguvu na udhaifu ulionao ili kufikia malengo yako (Imani ya kufikia lengo na thamani
uliyotoa kwa lengo lako)
Dhamira thabiti (Uzito gani unatoa katika kufikia lengo lako)
Dhamira (kulifikia lengo kwa Kujifunza zaidi na kukua kiutendaji) Kwa nini upo hapo
ulipo?
Kazi ya Kufanya nyumbani (wape washiriki maswali haya na waje na majibu yake kipindi
kijacho)
Malengo yako ni nini katika kazi yako?
Unahitaji nini kutimiza lengo lako?
Nini kinazuia kufika ulipotaka kufikia?
Kipindi cha pili: Mpango wa uongozi binafsi
Utangulizi: Dakika 10
waeleze washiriki mpango binafsi wa uongozi ni nini na umuhimu wake kwao kama viongozi
Malengo ya kipindi: washiriki waweze kutambua na kutengeneza mpango binafsi wa uongozi
Kazi ya 1: Dakika 5
Waeleze kila mshiriki aandike sifa ujuzi au maarifa matatu muhimu anayotaka kuyajua au
kuyaimarisha katika uongozi wake
Kazi ya 2: Dakika 40
Kila mmoja atengeneza mpango wake binafsi wa uongozi kwa kufuata mtiririko ufuatao
1. Taja mambo matatu yanayofanya mtu awe kiongozi mzuri
2. Ainisha angalau tabia tatu zinazokutambulisha wewe kama kiongozi
3. Andika maono yako katika safari ya uongozi
Unataka kuwa kiongozi wa aina gani
Unataka kufanikisha nini
48
Ni kwa jinsi gani utafanikisha
4. Wengine wanakuonaje, je kama ukiondoka wengine watasema nini juu yako?
5. Bainisha ujuzi unaohitaji katika kuimarisha uongozi wako
6. Tengeneza mpango wa uongozi binafsi
Hitimisho: waeleze kila mmoja kuwa afuatilie utekelezaji wa mpango aliouengeneza.
Kipindi cha Tatu: Uongozi wa mkakati
Lengo Kuu: washiriki waweze kufikia malengo ya kazi zao kwa ufanisi na mafanikio
Kazi ya 1: Wagawe washiriki katika makundi ya watu 3. Kisha wape swali lifuatalo na walifanya
ke kufanya igizo fupi la dk 10
Shule ya masige haina madarasa ya kutosha, wanafunzi wa darasa la nne hadi la saba, wanakaa
chini ya mti, shule ina vyoo viwili tu, na walimu hawana ofisi. Shule ina walimu sita tu ambao huto
mazoezi na kuondoka darasani, wachache husahihisha kazi za wanafunzi, kutokana na kulemewa na
vipindi. shule ina wanafunzi 600 wanaokaa umbali wa kilometa 5 hadi 14. Shule inafanya vibaya
katika matokeo ya darasa la saba. Wazazi hawajitolei katika maendeleo ya shule. Wanajamii
wamejenga katika eneo la shule hivyo wanafunzi hawana uwanja wa michezo. Je utafanya nini
kuifanya shule iwe shule bora na ya mfano wa kuigwa.
Kazi ya 2: Kuwasilisha (DK 10)
Kila kikundi kioneshe jinsi walivyoshughulikia tatizo hilo
Baada ya kuwasilisha wapatie muda wa kujadili maamuzi ya kila kikundi
Kazi ya 3: Uchambuzi wa uongozi wa kimkakati (Dk 20)
49
Wagawe washiriki katika makundi 4 na kila kundi lifanyie kazi sehemu moja ya mkakati bila
kuwaonesha sehemu zake kazi ya kufanya:
Ni mambo gani utayaangalia katika kutengeneza mkakati wa eneo la mkakati ulipopewa
Wawasilishe kazi zao na kisha uhitimishe kipindi
Hitimisho:
Waeleze washiriki kuwa uongozi wa kimkakati inakufanya uweze kufikiri ni kwa jinsi gani utafikia
malengo yako. Na katika muktadha wa elimu lengo letu kubwa ni kumfanya anayejifunza kupata
maarifa na ujuzi utakao mfaya amudu maisha yake kwa ufanisi.
Pia nyanja hii inasisitiza kufikiri kimkakati ua kufikiri kwa makini ili kupata suluhisho la
kudumu la tatizo au kufikia mafanikio yanayotakiwa.
eneo hili linaangalia pia ubora wa utoaji wa huduma na hapa tunaangalia ufundishaji na ubora wa
mtaala. Jambo la mwisho ni uongozi na utawala wa watu, rasilimali na mchakato wa kujifunza.
Ni muhimu kuyazingatima mambo haya ili uweze kufanikiwa katika usimamizi na uongozi wa
elimu katika kata.
Kipindi cha nne: UONGOZI WA KIKUNDI/TEAM KATIKA KATA
Utangulizi Muda: Dakika 5
Katika somo hili team au kikundi ni watu wanaongozwa na Afisaelimu kata ambao ni Waalimu,
Wanafunzi na Jamii au wengine walio chini yake kulingana na kazi au jukumu alilopewa.
Lengo la somo:
Afisaelimu Kata aweze kuongoza kikundi/team yake vizuri zaidi katika utekelezaji wa shughuli
zake za kila siku.
VIFAA: Picha, Bango kitita, Kalamu za rashasha
Kipindi cha Tano: KIONGOZI WA TIMU NI NANI
Kazi ya 1: dakila 10
Andika maswali kwenye bango kitita kisha washiriki wajibu kwa jozi na kuwasilisha
1. Nani ana jukumu la kuwaongoza walimu wakuu katika kutekeleza majukumu yao?
Afisa Elimu Kata Afis Elimu Wilaya
mwalimu mkuu Afisa wa ajira
50
2. Nani ana jukumu la kuhakikisha kuwa jukumu linatekelezwa shuleni?
3. Nini kazi ya kiongozi wa timu
4. Ukiwa ni kiongozi wa Kata je timu yako inatengenezwa na akina nani?
Kazi ya 2: Muda dakika 20
wagawe washiriki katika makundi mawili, kila kundi waeleze je ni mambo gani yanamfanya
kiongozi wa timu kufanikiwa katika kazi yake
Kazi ya 1: Dakika 5
waambie wasimame duara kisha warushie mpira mdogo na kila mmoja ataje sifa za
kuwa kiongozi wa timu
Andika majibu yao kwenye bango kitita
Kazi ya 2: DAKIKA 10
wape nafasi washiriki kusoma yaliyoandikwa kwenye bango kitita, kisha kila mmoja
abainishe sifa kuu tatu alizo nazo na sifa tatu ambazo hana.
Kazi ya 3: Dakika 20
Wagawe washiriki katika makundi mawili
kundi la kwanza washugulike sifa walizonazo kama viongozi wa timu mambo gani
watafanya kuhakikisha kuwa sifa hizo zinaendelezwa
na kundi la pili washughulike sifa wasizo nazo kama viongozi wa timu mambo gani
watafanya kuhakikisha kuwa zinarekebishwa
Hitimisho: dakika 5
Hitimisha kipindi kwa kuwaelezea umuhimu wa kuwa kiongozi wa timu mwenye sifa
zinazostahili.
Sifa za kiongozi bora wa timu
- Hufanya mawasiliano yenye tija - hupanga utaratibu wa kazi zake
- Anaiamini timu yake
- Ana heshimu wengine
- Anatoa maamuzi bila upendeleo
- Mwaminifu - Anawezesha kwa umahiri
- Anatoa nafasi kwa wengine
kutekeleza au kushika madaraka
51
KIPINDI CHA SITA: KUISAIDIA TIMU KUTEKELEZA JUKUMU
KAZI YA 1 MUDA: Dakika 10
MWEZESHAJI:
• Andika kwenye karatasi/kadi namba 1 hadi 4 kisha zibandike ukutani
• Waambie washiriki wote wasimame kwenye namba wanayoipenda
• Angalia kundi moja lisizidi washiriki watano
Waweke katika vikundi kulingana na namba walizochagua kisha wape swali lifuatalo walifanye
katika vikundi vyao. Zingatia muda uliowekwa
SWALI: Ni hatua gani tano muhimu utafuata ili kuwaongoza wenzako kutekeleza kazi
mliyopewa na mkuu wa Mkoa?
KAZI YA 2: Muda: Dk 20
Washiriki wasome habari hizi kisha wajibu maswali kulingana na visa mkasa
KISA: 1
Katika kata ya Mketo kuna shule 7 ambazo ziko chini ya uongozi wa Mratibu Elimu Kata
bwana Lifu. Katika uongozi wake aliamua kufanya kikao na walimu wakuu wote akieleza
taratibu na kuwakumbusha kuhusu Majukumu yao ya kila siku kazini. Baada ya kikao hicho
Walimu wakuu nao walienda kukaa na walimu shuleni na kuwakumbusha taratibu za kazi.
Hivyo walimu kwa pamoja walijipanga na kuamua kuongeza muda kidogo wa kutoka ili
wabaki kazini lakini wala wazazi na wanafunzi hawakuelezwa kuhusu mpango wa jitihada za
ziada. Mratibu akiwa kwenye pikipiki yake alipita shule mojawapo na akakuta walimu
hawajatoka alipowaona, yeye aliamini kuwa walimu wake wamebaki pale ili wawafundishe
wanafunzi. Baada ya hapo hakufuatilia tena akijua agizo lake litafanikiwa.
Matokeo ya mtihani yalipotoka wanafunzi wa shule za kata yake hawakufanya vizuri kama
aliyotarajia na kwani shule zote za kata zilifanya vibaya zaidi.
Kisa: 2
Fuli ni Afisaelimu kata wa kata ya Fulele, anashule zipatazo kumi anazozisimamia. Afisaelimu
wa wilaya amempa jukumu la kuwaongoza maafisa wengine wa kata kuandaa mpango wa
maendeleo ya elimu ya Mkoa wa Futa. Fuli aliwaita maAfisaelimu wenzake na kuaambia jukumu
walilopewa, aliwapa nafasi watoe mawazo jinsi gani watatekeleza kazi ya kwa muda wa wiki
moja waliopewa.
Baada ya majadiliano, Fuli aliwagawia kila mmoja kazi yake na pia aliwaambia kuwa wawe huru
kutumia njia mbalimbali za kutekeleza kazi hiyo. Baada ya siku mbili aliwatembelea kuona
maendeleo yao. Alitoa msaada wa maelekeao kwa wale waliohitaji msaada wake. Pia aligundua
52
kuwa kuna Afisaelimu kata mmoja amepatwa na dharula hivyo hataweza kushiriki katika
utekelezaji. Fuli ashika nafasi ya yule aliyepatwa na dharula ili kufanya kazi iendelee.
Baada ya wiki moja kazi ikawa imekwisha. Afisaelimu alikuja kuiangalia maendeleo ya kazi, Fuli
alimpa Afisaelimu kata wa Kole kuelezea jinsi mpango wa maendeleo ya elimu ya mkoa
utakavyotekelezwa. Afisaelimu alifurahi sana na kumpongeza Fuli kwa kazi nzuri. Fuli
alishukuru na kusema kuwa kazi kubwa imefanywa na maAfisaelimu wa wilaya yote hivyo sifa
ziwaendee wao.
SWALI:
• Je unajifunza nini kati ya uongozi wa Fuli na Lifu?
• Mambo gani unafikiri ni mazuri na mambo gani ambayo siyo mazuri? ni kwa nini
unafikiri hivyo?
Baada ya majadiliano, washiriki wawasilishe kazi zao (zingatia muda)
KAZI YA 3: Muda Dk. 15
Bandika picha ubaoni kisha waambie washiriki waiangalie kwa makini na kuandika maelezo
juu ya picha hiyo.
HITIMISHO: Muda: Dk.10
• Mwezeshaji hitimisha kwa kufanya majumuisho juu ya Uongozi wa Kikundi/Team
• Ruhusu maswali na majadiliano ya muda mfupi kuhusiana na somo.
Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA)
5. TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA)
Maudhui ya mafunzo kuhusu TEHEMA yanahusisha maeneo muhimu kuhusu maarifa na
ujuzi wa TEHEMA yenye lengo la kujenga wataalamu wenye ujuzi, utaalamu kwenye
TEHEMA utakaowasaidia kwenye shughuli nyingi za maendeleo ya kitaaluma na
kiuchumi. wataalamu hawa wataweza kufanya kazi kwa ufanisi kwa kutumia maarifa na
ujuzi waliopata wakati wa kozi. Vipengele vya TEHAMA ni pamoja na:
53
i. Uelewa kuhusu TEHAMA kwa ujumla
Vipengele muhimu ni:
TEHAMA ni nini
Mawanda ya TEHAMA kwenye elimu
Athari za TEHAMA katika elimu
ii. Jinsi ya kuitimia Kompyuta
Vipengele muhimu ni:
Kompyuta ni nini
Kompyuta inafanyaje kazi
Aina za kompyuta
Matumizi ya kumpyuta
Aina za mifumo ya utendajikazi wa kompyuta
Programu za mifumo ya utendajikazi wa Kompyuta
Sehemu mbali mbali za mifumo ya utendajikazi wa kompyuta na kazi zake
iii. Programu ya Ofisi
(a) Uuundaji na uandishi wa neno kwenye Kompyuta
Vipengele muhimu ni:
Kutengeneza na kuhifadhi
Kuchapa
Kuchagua herufi/neno/sentensi na kufanya mabadiliko tarajiwa
Utangulizi juu ya menu ya Kompyuta na sehemu zake
Njia za ufupisho (shortcuts)
Kuthibitisha usahihi wa maandishi (kuhakikisha usahihi wa herufi)
Jedwali (kutengeneza, kurekebisha, kufuta ‘safu’ au ‘mlalo’)
Mpangilio wa maneno na hati
Rangi na ‘watermark’
Kuchapisha
54
(b) Program ya kusadisi mahesabu (Ekseli)
Vipengele muhimu ni:
Utangulizi juu ya program ya kufanyia mahesabu-ekseli
Kutengeneza karatasi ya ukokotozi wa mahesabu na kuhifadhi
Utangulizi juu ya maeneo na zana mbali mbali za kutumia ekseli
Kuunda mtindo mbalimbali ya karatasi la mahesabu
Kokotozi mbali mbali
Kanuni mbali mbali na namna ya kuzitumia
Kuchapisha karatasi la mahesabu
Matumizi ya kila siku ya program ya mahesabu (kukokotoa matumizi, n.k)
(c) Programu za Kuandalia na Kuwasilisha mada
Vipengele muhimu ni:
Utangulizi juu ya uandaji mada na Powapointi
Kutengeneza mada ya kuwasilisha kwa kutumia powapointi
Jinsi ya kutengeneza slaidi
Kutengeneza maudhui na muonekano wa slaidi
Jinsi ya kuweka Madoido ya slaidi kwenye powapointi
Kutumia picha na vionjo mbalimbali kwenye kwenye wasilisho
Kuongeza maelezo kwenye slaidi
Kutengeneza Maombo mbali mbali
Kutumia powapointi kwenye Kuonesha picha jongefu
(d)Programu za Kuendesha kompyuta (Maunzilaini)
Vipengele muhimu ni:
Utangulizi juu ya dhana ya program (maunzilaini)
Kuingiza na kuitoa program kwenye kompyuta
Vitafutio vya intaneti
55
Programu za kuzuia virusi
Program za kucheza nyimbo na video
iv. Intaneti
Vipengele muhimu ni:
Utangulizi juu ya dhana ya intaneti
Namna ya kujiunganisha kwenye intaneti
Faida na matumizi ya intaneti
Vitafutio vya Intaneti
(a) vidokezo
(b) Menu
(c) Njia za mkato
Kurasa za tovuti, Viunganishi, tovuti
Injini za kutafutia taarifa kwenye mtandao
Tovuti za ndani ya nchi – tovuti za serikali, n.k.
Utangulizi juu ya mawasiliano ya barua pepe
Kutengeneza akaunti ya barua pepe
Vielekezi mbalimbali kwenye akaunti ya barua pepe, vipengele vya usalama
Kutuma, kupokea, kujibu na kufuta barua pepe
Kutumia intaneti/injini za kutafutia taarifa/zana za barua pepe kwenye simu ya
mkononi
Utangulizi juu ya mitandao ya kijamii
Kuweka na kupakua taarifa kwenye mitandao
Usalama mitandaoni (Cyber security)- namna ya kujiepusha nayo
Mambo yanayoruhusiwa kufanyika na yasiyoruhusiwa kwenye intaneti.
v. Mawasiliano: kwenye mtandao na kikazi
Vipengele muhimu ni:
Mapitio ya mawasiliano ya baruapepe
Utangulizi juu ya taratibu/kanuni za intaneti
56
Kuwasiliana na mwingine kwa kutumia baruapepe, mitandao ya kijamii na
vituma ujumbe mfupi
vi. Namna mbalimbali za kuwasilisha taarifa kwenye Kompyuta
Vipengele muhimu ni:
Utangulizi wa namna za kuwasilisha taarifa kwenye kompyuta
Vifaa mbalimbali vya kusanifia taarifa kwenye kompyuta
Program mbalimbali za kuendeshea taarifa zilizo kwenye maumbo tofauti
Njia mbalimbali za kuwasilisha taarifa kwenye mtandao (Mfano, Youtube)
57
VIAMBATISHO
MPANGILIO WA MADA ZA MAFUNZO
1. Mpangilio wa Mada za mafunzo
a. Utangulizi
Sehemu ya kwanza: Mafunzo Elekezi
Mada:
a. Maana na madhumuni ya Mafunzo Endelevu
b. Usimamizi na uthibiti wa ubora wa shule
i. Mwongozo mpya wa uthibiti ubora wa shule
ii. Jinsi ya kusaidia shule kujaza fomu ya kujipima
iii. Alama za ubora wa shule
iv. Utoaji wa taarifa
v. Mkutano wa elimu wa Wilaya
vi. Jamii za Kujifunza za walimu wakuu
c. Sheria, Kanuni na taratibu za Utumishi wa umma
i. Sifa za AEK
ii. Kazi na majukumu ya AEK
iii. Mipaka ya AEK
iv. Sheria, stahiki na haki ya mtumishi wa Umma
Sehemu ya pili: Uongozi na menejiment katika elimu
Mada
i. Maana ya Uongozi na menejimenti
ii. Tofauti kati ya uongozi na menejiment
iii. Misingi ya Uongozi
iv. Kanuni za Uongozi na menejiment
v. Sifa za kiongozi
vi. Umuhimu wa Uongozi na menejiment katika elimu
vii. Maadili ya Utumishi wa umma
viii. Kutengeneza mpango wa kazi
ix. Ufuatiliaji na utoaji wa taarifa
Sehemu ya Tatu : Uelekezi na Ushauri Elimishi
Mada
Maana ya Uelekezi na Ushauri Elimishi
umuhimu wa Uelekezi na Ushauri Elimishi katika uongozi
58
Ujuzi/ maarifa ya Uelekezi na Ushauri Elimishi
Namna ya kufanya Uelekezi na Ushauri Elimishi wenye tija
Kanuni za kufanya Uelekezi na Ushauri Elimishi
Changamoto za kufanya Uelekezi na Ushauri Elimishi katika Uongozi
Mahali na wakati wa kufanya Uelekezi na Ushauri Elimishi
Sehemu ya nne: Uongozi binafsi (Personal Leadership)
Mada
• Uhusiano wa kina wa malengo na dhamira
• Uelewa juu ya maadili, imani, uwezo na udhaifu wako
• Usimamizi wa mawazo yako na muda
• Uwazi wa maoni na changamoto
• Ujifunzaji na ukuaji endelevu
• Kuwa mfano kwa wengine
• Uongozi binafsi ni muonekano wa maadili yako, tabia na imani yako
• Uongozi binafsi ni chanzo cha ndani cha ufanisi wa kiongozi
i. Uongozi wa kimkakati (Strategic leadership)
• Kuangalia mambo kwa mtazamo mkubwa
• Kuwa na muda kwaajili ya kufikiri kimkakati
• Kupata ufafanuzi juu ya vipaumbele mkakati na matokeo
• Kufanya maamuzi kwa makusudi
ii. Uongozi wa Timu (Team Leadership)
• Kuhusisha mioyo na akili za wengine ili kufikia dira
• Kutoa wasaa kwa kila mmoja kuchangia kulingana na uwezo na vipaji vyao
• Uongozi wa timu unahitaji ushirikiano na ubunifu ili kufikia lengo la pamoja
Sehemu ya Tano: Teknolojia Ya Habari Na Mawasiliano (Tehama)
Maudhui ya mafunzo kuhusu TEHEMA yanahusisha maeneo muhimu kuhusu maarifa na
ujuzi wa TEHEMA yenye lengo la kujenga wataalamu wenye ujuzi, utaalamu kwenye
TEHEMA utakaowasaidia kwenye shughuli nyingi za maendeleo ya kitaaluma na
kiuchumi. wataalamu hawa wataweza kufanya kazi kwa ufanisi kwa kutumia maarifa na
ujuzi waliopata wakati wa kozi. Vipengele vya TEHAMA ni pamoja na:
Mada
59
vii. Uelewa kuhusu TEHAMA kwa ujumla
Vipengele muhimu ni:
TEHAMA ni nini
Mawanda ya TEHAMA kwenye elimu
Athari za TEHAMA katika elimu
viii. Jinsi ya kuitimia Kompyuta
Vipengele muhimu ni:
Kompyuta ni nini
Kompyuta inafanyaje kazi
Aina za kompyuta
Matumizi ya kumpyuta
Aina za mifumo ya utendajikazi wa kompyuta
Programu za mifumo ya utendajikazi wa Kompyuta
Sehemu mbali mbali za mifumo ya utendajikazi wa kompyuta na kazi zake
ix. Programu ya Ofisi
(a) Uuundaji na uandishi wa neno kwenye Kompyuta
Vipengele muhimu ni:
Kutengeneza na kuhifadhi
Kuchapa
Kuchagua herufi/neno/sentensi na kufanya mabadiliko tarajiwa
Utangulizi juu ya menu ya Kompyuta na sehemu zake
Njia za ufupisho (shortcuts)
Kuthibitisha usahihi wa maandishi (kuhakikisha usahihi wa herufi)
Jedwali (kutengeneza, kurekebisha, kufuta ‘safu’ au ‘mlalo’)
Mpangilio wa maneno na hati
Rangi na ‘watermark’
Kuchapisha
(b) Program ya kusadisi mahesabu (Ekseli)
Vipengele muhimu ni:
Utangulizi juu ya program ya kufanyia mahesabu-ekseli
Kutengeneza karatasi ya ukokotozi wa mahesabu na kuhifadhi
Utangulizi juu ya maeneo na zana mbali mbali za kutumia ekseli
60
Kuunda mtindo mbalimbali ya karatasi la mahesabu
Kokotozi mbali mbali
Kanuni mbali mbali na namna ya kuzitumia
Kuchapisha karatasi la mahesabu
Matumizi ya kila siku ya program ya mahesabu (kukokotoa matumizi, n.k)
(c) Programu za Kuandalia na Kuwasilisha mada
Vipengele muhimu ni:
Utangulizi juu ya uandaji mada na Powapointi
Kutengeneza mada ya kuwasilisha kwa kutumia powapointi
Jinsi ya kutengeneza slaidi
Kutengeneza maudhui na muonekano wa slaidi
Jinsi ya kuweka Madoido ya slaidi kwenye powapointi
Kutumia picha na vionjo mbalimbali kwenye kwenye wasilisho
Kuongeza maelezo kwenye slaidi
Kutengeneza Maombo mbali mbali
Kutumia powapointi kwenye Kuonesha picha jongefu
(d)Programu za Kuendesha kompyuta (Maunzilaini)
Vipengele muhimu ni:
Utangulizi juu ya dhana ya program (maunzilaini)
Kuingiza na kuitoa program kwenye kompyuta
Vitafutio vya intaneti
Programu za kuzuia virusi
Program za kucheza nyimbo na video
x. Intaneti
Vipengele muhimu ni:
Utangulizi juu ya dhana ya intaneti
Namna ya kujiunganisha kwenye intaneti
Faida na matumizi ya intaneti
Vitafutio vya Intaneti
(d) vidokezo
(e) Menu
(f) Njia za mkato
Kurasa za tovuti, Viunganishi, tovuti
61
Injini za kutafutia taarifa kwenye mtandao
Tovuti za ndani ya nchi – tovuti za serikali, n.k.
Utangulizi juu ya mawasiliano ya barua pepe
Kutengeneza akaunti ya barua pepe
Vielekezi mbalimbali kwenye akaunti ya barua pepe, vipengele vya usalama
Kutuma, kupokea, kujibu na kufuta barua pepe
Kutumia intaneti/injini za kutafutia taarifa/zana za barua pepe kwenye simu ya
mkononi
Utangulizi juu ya mitandao ya kijamii
Kuweka na kupakua taarifa kwenye mitandao
Usalama mitandaoni (Cyber security)- namna ya kujiepusha nayo
Mambo yanayoruhusiwa kufanyika na yasiyoruhusiwa kwenye intaneti.
xi. Mawasiliano: kwenye mtandao na kikazi
Vipengele muhimu ni:
Mapitio ya mawasiliano ya baruapepe
Utangulizi juu ya taratibu/kanuni za intaneti
Kuwasiliana na mwingine kwa kutumia baruapepe, mitandao ya kijamii na
vituma ujumbe mfupi
xii. Namna mbalimbali za kuwasilisha taarifa kwenye Kompyuta
Vipengele muhimu ni:
Utangulizi wa namna za kuwasilisha taarifa kwenye kompyuta
Vifaa mbalimbali vya kusanifia taarifa kwenye kompyuta
Program mbalimbali za kuendeshea taarifa zilizo kwenye maumbo tofauti
Njia mbalimbali za kuwasilisha taarifa kwenye mtandao (Mfano, Youtube)
62
VIAMBATISHO
F1
FOMU YA MPANGO WA KUJIENDELZA BINAFSI
Mkoa------------------------------ Wilaya -------------------------------------Kata------------
Maelezo binafsi
Jina: ___________________ Jinsi: Ke/Me ----------------Umri__________
Simu: ______________________________ Baruapepe
Muda Malengo Shughuli za mafunzo
Muda wa kukamilisha malengo
Matokeo tarajiwa
Mpango wa muda mfupi: KukIdhi mahitaji ya muda mfupi
Mpango wa muda wa kati (Medium) kukidhi mahitaji ya majukumu mapya
Mpango wa muda mrefu: kukidhi mahitaji ya kitalaamu
63
F2. FOMU YA KUJIUNGA NA MAFUNZO ENDELEVU
Mkoa------------------------------ Wilaya -------------------------------------Kata-------------------
Maelezo binafsi
Jina: __________________________ Jinsi: Ke/Me………………..Umri__________
Simu: ______________________________ Barua pepe--------------------------------------
Historia ya kazi
a) Miaka uliyofundisha shule ya msingi ---------------------------------------------- b) Muda uliofundisha sekondari -------------------------------------------------------- c) Muda uliofundisha vyuo vya ualimu-------------------------------------------------
Sifa za kitaaluma (v)
(i) Diploma ------------------------------------------- (ii) Shahada ya kwanza --------------------------- (iii) Shahada ya Uzamili -------------------------- (iv) Shahada ya Uzamivu --------------------------
Aina ya mafunzo unayoyaomba
i) -----------------------------------------------------------------------------------------------------
ii) ----------------------------------------------------------------------------------------------------- Mafunzo uliyowahi kupitia
Mafunzo
uliyohudhuria
Mwaka Muda wa
mafunzo
Taasisi iliyoandaa
mafunzo
64
Uthibitisho
Mimi -------------------------------------------- Afisa wa Elimu Kata ya------------------------ ni
naahidi kwamba nitajifunza kwa bidii na kutumia ujuzi wangu kwa kuongeza ufanisi katika
utendaji wangu wa kazi. Nitajituma na kufuata taratibu zote za mafunzo endelevu
Saini ya mwombaji ----------------------------------- tarehe -----------------------------------------------
Imepitishwa na: Jina-----------------------------------Cheo------------------------Saini --------------
Tarehe---- (Afisa wa Elimu wa Wilaya)
F3.
FOMU YA TATHMINI BINAFSI YA MAFUNZO
(Ijazwe kila baada ya kuhudhuria mafunzo)
Mkoa------------------------------ Wilaya -------------------------------------Kata--------------
Maelezo binafsi
Jina: __________________________ Jinsi: Ke/Me----------------- Umri__________
Simu: ______________________________ Barua pepe--------------------------------------------
Tarehe ya mafunzo Mfano: 2/02/2018
Mafunzo yalihusu nini Mfano: matumizi ya kompyuta
Namna gani mafunzo yaliyotolewa (Mfano: mkutano, kongamano, mafunzo darasani
Matokeo ya mafunzo (ujuzi na maarifa)
Matokeo katika utendaji
Uthibitisho wa mtoa mafunzo. (Jina, saini na tarehe)
65
F4.
FOMU YA KUJIUNGA NA MAFUNZO ENDELEVU
Mkoa------------------------------ Wilaya -------------------------------------Kata--------------
Ndugu Afisa Elimu Kata (Jina)…….......................................................………………………………
KUKUBALIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO ENDELEVU
66
Ofisi ya Uthibiti Ubora wa Shule wa wilaya, inayofuraha kukuarifu kuwa umechaguliwa
kujiunga na mafunzo endelevu kwa mwaka ---------------------------- katika eneo
….………………….ambayo yataanza………………………..hadi……………….............................……………..
Ni mategemeo yetu kuwa, kwa muda wote wa mafunzo utajifunza kwa bidii na kuonesha
mabadiliko ya kiutendaji na pia utaweka kumbukumbu ya maendeleo ya masomo yako
Tafadhali kubali au kataa kujiunga na mafunzo haya kwa maandishi ndani ya siku 14 tangu
kupokea kwa barua hii
Hongera!
Jina---------------------------------------------------- Saini------------------------------ Tarehe ------------
Ofisi ya Uthibiti Ubora wa Shule wa wilaya
Recommended