6
Arafa ya Sera Ili kuwe na Mgao bora wa Idadi ya Watu nchini Kenya, ni lazima kuwe na uwekezaji kimkakati kupitia njia zifuatayo: Uwekezaji katika upangaji wa uzazi, maisha ya watoto na elimu ya wasichana: ili kuwe na mabadiliko kwa Idadi ya Watu Uboreshaji wa afya ya wananchi: Watoto walio na afya nzuri hufanya vyema shuleni. Mafanikio yao shuleni pia huchangia kwa upatikanaji wa wafanyikazi nchini wenye ujuzi mwingi. Huduma za afya kwa vijana na kwa watu wazima pia ni muhimu katika uboreshaji na maendeleo ya kiuchumi. Uwekezaji katika elimu : Mifumo ya elimu lazima ihakikishe kwamba vijana wote wanahitimu katika kila kiwango cha elimu, na kwamba wanaohitimu wana ujuzi wa kutosha na ufaao katika soko la ajira linalobadilika kila wakati. Utekelezaji wa sera za uchumi na utawala bora: Sera za kiuchumi na za utawala lazima zikuze sekta za ajira na uwekezaji katika sekta hizo kubwa za ajira na pia zilenge upanuzi wa miundo mbinu, ukuzaji wa biashara, kwa kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya kimataifa, na kujenga mazingira salama na motisha kwa uwekezaji wa kigeni moja kwa moja. Jinsi Vile Mabadiliko ya Watu Yanawezaleta Maendeleo nchini Kenya Arafa hii ya sera inaeleza jinsi vile Kenya inaweza kunufaika na mabadiliko haya kwa kuwekeza katika mipango ya afya, upangaji wa uzazi kwa hiari, elimu, na usawa wa kijinsia, pamoja na sera zitakazo saidia kizazi kipya cha vijana kufanya kazi. Nchi nyingi zinazoendelea zina idadi ya watu walio na umri wa chini kwa sababu katika miongo ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko katika wastani wa idadi ya watoto kwa kila mwanamke pamoja na boresho katika maisha ya watoto. Kushuka kwa wastani wa idadi ya watoto kwa kila mwanamke kunaweza badilisha mfumo wa umri nchini na kuathiri sana uchumi. Wakati nchi ina watu wazima wengi zaidi katika kiwango cha umri wa kufanya kazi kuliko watoto na wazee, hao watu wanaofanya kazi hawategemewi na watu wengi, na hivyo basi kiwango cha mapato na mali yao kitaenda juu. Hapo ndipo kutakuwa na fursa ya kuendeleza uchumi. Nchi katika bara la Asia, Amerika ya Kusini, na Afrika Kaskazini ambazo zilipata mabadiliko miongoni mwa waakazi, zilifanya uwekezaji ili kuboresha afya na elimu na kunufaika kutokana na mgao wa idadi ya watu. Nchi hizi pia zilivutia uwekezaji wa kigeni na zikatunga sera za kiuchumi zilizoongeza nafasi za ajira na kusababisha ukuaji wa uchumi huku zikupunguza matatizo ya umaskini na ukosefu wa usawa katika jamii. i vijana nchini Kenya watakaoboresha na kuleta maendeleo ya kiuchumi katika miongo yajayo, ikiwa sera na mipango yatabuniwa na kutekelezwa kwa lengo lakuhamasisha familia ndogo. Itakuwa bora kama kutakuwa na ongezeko la wafanyikazi wenye elimu bora zaidi na ambao wana watoto wachache wa kulinda watoto ambao kwa upande wao watapata elimu bora na walio na uwezo wa kuajiriwa, mradi tu kuwe na uboreshaji wa taasisi na sera nzuri za kiuchumi nchini. N Taasisi Zilizoshirikiana: Shirika la Taifa la Idadi ya Watu na Maendeleo, Chuo cha Masomo na Utafiti wa Idadi ya Watu, na Taasisi ya Kumbukumbu za Idadi ya Watu. Nambari 44 Julai 2014

Arafa ya Sera...Huduma za afya kwa vijana na kwa watu wazima pia ni muhimu katika uboreshaji na maendeleo ya kiuchumi. • Uwekezaji katika elimu : Mifumo ya elimu lazima ihakikishe

  • Upload
    others

  • View
    32

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Arafa ya Sera...Huduma za afya kwa vijana na kwa watu wazima pia ni muhimu katika uboreshaji na maendeleo ya kiuchumi. • Uwekezaji katika elimu : Mifumo ya elimu lazima ihakikishe

Arafa ya Sera

Ili kuwe na Mgao bora wa Idadi ya Watu nchini Kenya, ni lazima kuwe na uwekezajikimkakati kupitia njia zifuatayo:

• Uwekezaji katika upangaji wa uzazi, maisha ya watoto na elimu ya wasichana: ili kuwe na mabadiliko kwa Idadi ya Watu

• Uboreshaji wa afya ya wananchi: Watoto walio na afya nzuri hufanya vyema shuleni. Mafanikio yao shuleni pia huchangia kwa upatikanaji wa wafanyikazi nchini wenye ujuzi mwingi. Huduma za afya kwa vijana na kwa watu wazima pia ni muhimu katika uboreshaji na maendeleo ya kiuchumi.

• Uwekezaji katika elimu : Mifumo ya elimu lazima ihakikishe kwamba vijana wote wanahitimu katika kila kiwango cha elimu, na kwamba wanaohitimu wana ujuzi wa kutosha na ufaao katika soko la ajira linalobadilika kila wakati. • Utekelezaji wa sera za uchumi na utawala bora: Sera za kiuchumi na za utawala lazima zikuze sekta za ajira na uwekezaji katika sekta hizo kubwa za ajira na pia zilenge upanuzi wa miundo mbinu, ukuzaji wa biashara, kwa kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya kimataifa, na kujenga mazingira salama na motisha kwa uwekezaji wa kigeni moja kwa moja.

Jinsi Vile Mabadiliko ya Watu Yanawezaleta Maendeleo nchini Kenya

Arafa hii ya sera inaeleza jinsi vile Kenya inaweza kunufaika na mabadiliko haya kwa kuwekeza katika mipango ya afya, upangaji wa uzazi kwa hiari, elimu, na usawa wa kijinsia, pamoja na sera zitakazo saidia kizazi kipya cha vijana kufanya kazi.

Nchi nyingi zinazoendelea zina idadi ya watu walio na umri wa chini kwa sababu katika miongo ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko katika wastani wa idadi ya watoto kwa kila mwanamke pamoja na boresho katika maisha ya watoto. Kushuka kwa wastani wa idadi ya watoto kwa kila mwanamke kunaweza badilisha mfumo wa umri nchini na kuathiri sana uchumi.

Wakati nchi ina watu wazima wengi zaidi katika kiwango cha umri wa kufanya kazi kuliko watoto na wazee, hao watu wanaofanya kazi hawategemewi na watu wengi, na hivyo basi kiwango cha mapato na mali yao kitaenda juu. Hapo ndipo kutakuwa na fursa ya kuendeleza uchumi.

Nchi katika bara la Asia, Amerika ya Kusini, na Afrika Kaskazini ambazo zilipata mabadiliko miongoni mwa waakazi, zilifanya uwekezaji ili kuboresha afya na elimu na kunufaika kutokana na mgao wa idadi ya watu. Nchi hizi pia zilivutia uwekezaji wa kigeni na zikatunga sera za kiuchumi zilizoongeza nafasi za ajira na kusababisha ukuaji wa uchumi huku zikupunguza matatizo ya umaskini na ukosefu wa usawa katika jamii.

i vijana nchini Kenya watakaoboresha na kuleta maendeleo ya kiuchumi katika miongo yajayo, ikiwa sera na mipango yatabuniwa na kutekelezwa kwa lengo lakuhamasisha familia ndogo. Itakuwa bora kama kutakuwa na ongezeko la wafanyikazi wenye elimu bora zaidi na ambao wana watoto wachache wa kulinda watoto ambao kwa upande wao watapata elimu bora na walio na uwezo wa kuajiriwa, mradi tu kuwe na uboreshaji wa taasisi na sera nzuri za kiuchumi nchini.

N

Taasisi Zilizoshirikiana: Shirika la Taifa la Idadi ya Watu na Maendeleo, Chuo cha Masomo na Utafiti wa Idadi ya Watu, na Taasisi ya Kumbukumbu za Idadi ya Watu.

Nambari 44 Julai 2014

Page 2: Arafa ya Sera...Huduma za afya kwa vijana na kwa watu wazima pia ni muhimu katika uboreshaji na maendeleo ya kiuchumi. • Uwekezaji katika elimu : Mifumo ya elimu lazima ihakikishe

Ni jinsi gani Kenya itafaidika kutoka Mgao huu?

Kielelezo 1: Jinsi Vile Kenya Itapata Mgao Bora Wa Idadi ya Watu

© 2010 JHUCCP, courtesy of Photoshare

Kenya sasa inaweza kupata ukuaji wa haraka katika uchumi kupitia uwekezaji uliopangiwa vyema. Wakati huu, asilimia 43 ya wakaazi wa Kenya wako chini ya umri wa miaka 15 (angalia takwimu / kijisanduku),2 na ingawa Kenya imepiga hatua kubwa katika lengo lake la kupunguza vifo vya watoto wachanga, na kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa nchini, kiwango chawastani wa idadi yawatoto kwa kila mwanamke kwa ujumla bado kiko juu. Wanawake hupata, kwa wastani, watoto 4.6 maishani mwao, kwa mujibu wa uta�iti wa hivi karibuni kuhusu idadi ya watu na afya.3 Uta�iti huo pia ulionyesha kwamba moja kati ya wanawake wanne wanapendelea kuahirisha upataji wa mimba au kuacha kuzaa kabisa, lakini wao hawatumii mbinu yoyote ya kupanga uzazi ili kuzuia mimba zisizotarajiwa.4 Wanawake hawa wana "haja ambalo halijatimizwa" kwa upande wa upangaji wa uzazi.

Ikiwa wanawake wataendelea kupata watoto wengi zaidi ya wanaotarajiwa, viwango vya ukuaji wa idadi ya watu vitabaki juu na hivyo basi kutakuwa na ongezeko la idadi ya watu chini ya umri wa miaka 15. Hii inamaanisha kuwa watu hao watakuwa wengi kuliko wale ambao wanafanya kazi na kwa hivyo hakutakuwa na mgao bora kwa sababu serikali na familia zitashughulikia uwekezaji katika afya na elimu ya watoto na katika miundombinu inayohitajika kuongeza nafasi za ajira na ukuaji wa uchumi. Kwa hivyo kuna haja ya serikali kuwekeza katika huduma na mipango ya kuhakikisha kwamba wanawake na wanandoa

wana idadi ifaayo ya watoto. Maelezo kuhusu baadhi ya uwekezaji muhimu na mabadiliko katika sera ni kama ifuatayo hapo chini.

Kielelezo 2: Mafunzo kutoka Mgao wa Idadi ya Watu Thailand

Thailand ni mfano wa nchi zilizopata mafanikio wa mgao wa idadi ya watu. Kupitia uwekezaji muhimu katika upangaji wa uzazi kwa hiari, kiwango cha uzazi kwa kila mwanamke kilishuka na hivyo basi kukawa na mabadiliko katika muundo wa umri na idadi ya watu. Ili ku�ikia mafanikio haya, Thailand kwanza ilipunguza kasi ya ukuaji wa idadi ya watu kwa kupanua upatikanaji na matumizi ya huduma za upangaji wa uzazi. Kati ya 1970 na 1990,

NCPD Sera Nambari 44 - Julai 2014

Page 3: Arafa ya Sera...Huduma za afya kwa vijana na kwa watu wazima pia ni muhimu katika uboreshaji na maendeleo ya kiuchumi. • Uwekezaji katika elimu : Mifumo ya elimu lazima ihakikishe

Asili: United Nations Population Division, World Population Prospects: The 2010

Revision, low variant (New York: UNFPA, 2011); United Nations Population Fund,

Impact of Demographic Change in Thailand (Bangkok: UNFPA, 2011);

and United Nations Population Division, World Population

Prospects: The 2012 Revision, low variant (New York: UNFPA, 2012)

Kielelezo 3: Mgao wa Idadi ya Watu Kenya (2010)

Mnamo mwaka wa 2010, Kenya ilikuwa na muundo wa idadi ya watu sawa na ule wa Thailand mwaka wa 1970, wenye idadi kubwa ya vijana. Kwa wakati wa miaka 40, kiwango cha uzazi kilipungua kwa watoto 4 kwa kila mwanamke nchini Thailand, na muundo wa idadi ya watu ukabadilika na kukawa na idadi kubwa ya watu wenye umri wa kufanya kazi. Kukiwa na upangaji wa uzazi kwa hiari nchini Kenya, kiwango cha uzazi miongoni mwa wakazi wa Kenya kitarudi chini na nchi hii itakuwa na uwezo wa kuleta mafanikio kupitia mgao wa idadi ya watu.

kiwango cha uzazi kwa kila mwanamke kilipungua kutoka kwa watoto 5.5 hadi 2.2 – mafanikio wa kipekee nchini Thailand kwa sababu watu wawili kwa wananchi watatu Thailand walikuwa wakiishi vijijini.

Mwaka 1970, Thailand ilikuwa na muundo sawa na mfumo wa Kenya sasa wa idadi ya watu: wigo mpana unaowakilisha idadi kubwa ya watoto kulingana na watu wenye umri wa kufanya kazi. Ku�ikia mwaka wa 2010 - miaka 40 tu baadaye –upungufu endelevu wa kiwango cha uzazi ulisababisha muundo wa idadi ya watu ambao kikundi cha wakazi wa umri wa miaka 25-64 ni kikubwa kuliko idadi ya watu chini ya miaka 25. Ongezeko katika matumizi ya huduma za upangaji wa uzazi lilipunguza kiwango cha uzazi nchini Thailand - kutoka asilimia 15 mwaka wa 1970 hadi takriban asilimia 80 mwaka wa 2010. Matokeo yake: idadi ya watu wazee imeongezeka, uboreshaji wa elimu katika ngazi za juu na afya bora kwa wananchi.

Mafanikio ya kishindo nchini Thailand ambayo ni matokeo ya uvumbuzi na jitihada za Wizara ya Afya ya Umma kuhakikisha upangaji wa uzazi kwa hiari, ni mfano wa hatua ambazo zinahitajika nchini Kenya, nchi ambayo mpito wa idadi ya wakazi wake haujakamilika. Ingawa Kenya na Thailand ni nchi tofauti sana, Kenya inaweza kunufaika kutokana na mafunzo haya: uvumbuzi na kujitolea katika juhudi za upangaji wa uzazi kwa hiari, ni hatua ya kwanza muhimu ya kupunguza kiwango cha uzazi. Uwekezaji katika utoaji wa huduma za upangaji wa uzazi unapaswa kuwa pamoja na maboresho katika afya, uwekezaji katika elimu na utekelezaji wa sera sahihi za uchumi ili ku�ikia mgao bora wa idadi ya watu.

Ongezeko la fedha na matumizi kwa ajili ya upangaji wa uzazi ni muhimu Mipango bora kuhusu upangaji wa uzazi itahakikisha kwamba wanandoa wanapata habari na huduma wanaozihitaji kwa mujibu wakuzuia mimba zisizotarajiwa na kupata watoto kwa wakati unaofaa. Kuzaa watoto wachache na kwa wakati unaofaa, kutawezesha wanawake kuchangia katika uboreshaji wa maendeleo ya kiuchumi kwa sababu watapunguza wakati wao wa kulea watoto wachanga na watakuwa na nafasi bora ya kufanya kazi.5

Inakadiriwa na wata�iti kwamba Kenya inaweza kuongeza zaidi kipato cha kila mwananchi ku�ikia mwaka wa 2050 kama itaongeza juhudi zake za uwekezaji katika upangaji wa uzazi.6 Kuna haja ya elimu na utoaji wa habari kuhusu upangaji wa uzazi ili kufutilia mbali vikwazo kwa matumizi ya mbinu ya kisasa ya upangaji wa uzazi. Vikwazo hivyo ni kama vile wasiwasi kuhusu madhara ya madawa au vifaa vya

NCPD Sera Nambari 44 - Julai 2014

Page 4: Arafa ya Sera...Huduma za afya kwa vijana na kwa watu wazima pia ni muhimu katika uboreshaji na maendeleo ya kiuchumi. • Uwekezaji katika elimu : Mifumo ya elimu lazima ihakikishe

sababu mipango hii huchangia pakubwa katika upungufu wa kiwango cha uwezo wa kuzaana katika ukuzaji wa maendeleo ya kiuchumi.

Wakati wavulana na wasichana wanapata elimu bora na ya kiwango cha juu, kuna ukuaji wa haraka katika uchumi. Ni wazi kwamba kuna uhusiano kati ya elimu na maendeleo ya kiuchumi, na matokeo ya ta�iti mbalimbali yanadhibitisha kwamba kuna uhusiano kati ya viwango vya juu vya elimu na viashiria vya maendeleo kama vile ukuaji katika Pato la Taifa, tija na utawala bora.12

Lazima kuwe na ubunifu wa sera mpya za elimu nchini Kenya ili kukabiliana na mabadiliko kwa mahitaji ya soko la ajira. Pia ni lazima kuboresha mfumo wa elimu na kutoa mafunzo zaidi ya ufundi ili kuendeleza ujuzi muhimu miongoni mwa wafanyikazi. Mipango bora ya elimu inaweza kuandaa ustawishaji wa wafanyakazi katika sekta mbalimbali za kazi kama vile katika ujenzi, miundombinu, viwanda, ajira ya kijani kibichi katika kilimo na nishati, na katika sekta ya huduma kama vile utalii.

Sera za kiuchumi zinapaswa kulenga ongezeko la ajira

Ili kufaidika kutoka kwa idadi kubwa ya vijana wanao�ika umri wa kufanya kazi, Kenya lazima ibuni na kutekeleza sera zinazolenga ongezeko la ajira. Hatua muhimu ni pamoja na kuimarisha taasisi za serikali, kuwekeza katika sekta ya kazi yenye ajira ya kiwango cha juu, na ubunifu wa sera za kuboresha uwekezaji wa kigeni. Changamoto nchini Kenya ni kuongeza ajira mpya katika sekta rasmi ili kukidhi idadi ya wafanyakazi. Takriban 659,000 za ajira mpya zilipatikana mwaka wa 2012, lakini asilimia 90 ya ajira hizo zinapatikana katika sekta isiyo rasmi, na ambako kuna viwango vya chini katika tija na ukuwaji.14

upangaji wa uzazi, maoni na kanuni za kijamii, upinzani kutoka kwa waume, na matatizo ya upatikanaji wa huduma.7

Uwekezaji katika afya huboresha uzalishaji wa baadayeUwekezaji katika afya ya watoto ni uwekezaji katika ujuzi, uwezo, na maendeleo ya watu, na husababisha uboreshaji wa elimu na matokeo mazuri ya kazi. Mipango ya afya kama vile utoaji wa huduma za chanjo na matibabu ya magonjwa, itasaidia watoto kufanya vyema shuleni, na kwa kupata elimu bora, watakuwa wafanyikazi wenye ujuzi unaohitajika. Watoto wanapokuwa kutoka utotoni hadi ku�ikia ujana wao, wanahitaji aina mbalimbali za huduma za afya. Lazima wapate habari kuhusu afya ya uzazi na ufahamu wa kutosha juu ya huduma zinazopatikana, ili waepukane na mimba zisizotarajiwa na magonjwa ya zinaa, ikiwa ni pamoja na virusi vya ukimwi (yote haya yanaweza kudhoo�isha fursa za elimu, hasa kwa wasichana).

Elimu ni muhimu kwa uanzishaji wa mgao bora wa idadi ya watu

Elimu kwa wasichana, hasa katika shule za upili, ni uwekezaji muhimu utakaoanzisha mabadiliko, kwa sababu wasichana ambao wana elimu ya juu hawahusiki kwa urahisi na ndoa za mapema na hupata fursa ya kuajiriwa kazini.8 Pia, wanawake walio na elimu na ambao hawaolewi mapema hupata watoto wachache kuliko wanawake ambao wanaolewa wakiwa na umri mdogo.

Ingawa wakenya wengi wamehitimu elimu ya msingi, kiwango cha ukamilishaji wa masomo ya shule ya upili ni ya chini, na kuna tofauti wazi kati ya viwango vya elimu ya wanaume na wanawake. Takriban asilimia 25 ya wanawake wa umri kati ya 20 na 24 wamekamilisha masomo ya shule ya upili (au zaidi) ikilinganishwa na asilimia 37 ya wanaume.9

Wanawake nchini Kenya waliokamilisha elimu ya shule ya upili au ya juu, huolewa wakiwa na umri kwa wastani miaka 22.4, karibu miaka mitano baada ya wanawake wasio na elimu.10 Kwa kuchelewesha ndoa na kuzaa miaka mitano baadaye, wanawake wana fursa ya kukamilisha masomo yao na kuanza kazi. Kwa jinsi hii, kutakuwa na familia ndogo na upunguzaji wa ongezeko la watu.11

Ni vizuri kuzingatia umuhimu wa kutilia maanani mipango ya elimu na upangaji wa uzazi miongoni mwa wanawake na wasichana kwa

NCPD Sera Nambari 44 - Julai 2014

Page 5: Arafa ya Sera...Huduma za afya kwa vijana na kwa watu wazima pia ni muhimu katika uboreshaji na maendeleo ya kiuchumi. • Uwekezaji katika elimu : Mifumo ya elimu lazima ihakikishe

Hatua Zinazopendekezwa

Ili kuwe na Mgao wa watu ulio bora na unaochangia pakubwa kwa ukuzaji wa uchumi na kwa maendeleo, viongozi nchini Kenya wanastahili kuchukua kwa haraka hatua muhimu zifuatazo:

• Utekelezaji wa mipango ya kuelimisha jamii kuhusu upangaji wa uzazi: Kuna haja ya kuimarisha elimu na kueneza habari kuhusu upangaji wa uzazi kote nchini. Ni muhimu pia kuhakikisha kwamba huduma za upangaji wa uzazi zinapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu kulingana na mahitaji na chaguo tofauti za wanawake, hasa wale maskini au wa umri mdogo, ambao hupata watoto wengi lakini hawana rasilimali ya kutosha ili kuwekeza katika afya na elimu ya watoto wao. • Uwekezaji bora katika maisha na afya ya watoto: Uboreshaji wa huduma za afya kama vile huduma za kliniki, utoaji na huduma wakati na baada ya kujifungua na hakikisho la chanjo, utapunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga. Aidha huduma hizi zitaamasisha wanawake na wanandoa kuwa na familia ndogo na afya njema. Wanawake hao na waume zao watapata fursa ya kuwekeza zaidi katika afya na elimu ya kila mtoto.

• Uboreshaji wa elimu hasa elimu ya wasichana katika shule za upili: Wasichana waliokamilisha masomo ya shule ya upili huchelewesha ndoa na si rahisi wapate mimba wakiwa na umri mdogo. Pia kupitia elimu, vijana wanaweza kupata ujuzi unaofaa na unaoleta mafanikio kazini.Mbali na kupunguza kiwango cha tofauti ya kijinsia katika elimu ya shule ya upili, serikali inapaswa kutekeleza mipango bora ya elimu ili wanafunzi waandaliwe vyema kulingana na mahitaji ya soko la kazi la karne ya 21.

• Ubunifu na utekelezaji wa sera za kiuchumi na uimarishaji wa utawala ili kuongeza nafasi za ajira na uwekezaji wa kigeni: Sera za uchumi na utawala lazima ziendeleze ukuaji katika sekta ya ajira, na uwekezaji katika sekta zilizo na viwango vikubwa vya ajira kama vile sekta ya kilimo, uvuvi, ufugaji wa mifugo, viwanda na biashara. Uboreshaji wa ufanisi wa taasisi mbalimbali, utawezesha uwekezaji katika sekta ya kibinafsi nchini Kenya. Mabadiliko ya idadi watu ni sababu moja tu baadhi ya mambo yanayochangia maendeleo nchini Kenya. Ni vizuri kutilia maanani faida ipatikanayo kutoka mgao huu. Ubunifu na utetezi wa sera hizi kwa umma utaleta mafanikio makubwa.Asili: Mradi ya Sera ya Afya na Shirika la Kitaifa la Idadi ya Watu na

Maendeleo

y

x

Taasisi bora za umma huboresha ukuaji wa uchumi.

Kuna haja ya kuendelea kuboresha ufanisi wa taasisi za serikali nchini Kenya. Utawala dhaifu mara nyingi hujulikana na sheria zisizotosheleza, urasimu bila ufanisi, ukosefu wa utulivu serikalini, na rushwa. Kulingana na viashiria vya Benki ya Dunia vinavyohusu “urahisi wa kufanya biashara” nchi ya Kenya imechukuwa nafasi ya nambari 121. Kenya ina lengo la kuwa miongoni mwa nchi 50 bora zaidi.15

Ili kuwezesha uwekezaji katika sekta za kibinafsi na katika miundombinu na ili kuongeza uwazi na uwajibikaji – mambo mawili muhimu katika uboreshaji wa huduma- ipo haja ya kutekeleza mipango ilivyoainishwa katika dira ya serikali na ya Ruwaza ya mwaka 2030. Pia ni sharti kutekeleza sheria iliyo tungwa na kuidhinishwa mwaka 2013, kuhusu Ushirikiano wa mashirika ya umma na za kibinafsi, pamoja na Mkakati wa mageuzi katika usimamizi wa fedha za umma.

Ili kuboresha mazingira ya biashara nchini Kenya, lazima kuwe na utekelezaji wa mageuzi ya kifedha na sera, kwa lengo la kutoa vikwazo (kama vile kanuni lazima, urasimu, na rushwa ambayo huongeza gharama za kufanya biashara).

Kielelezo 4: Matokeo ya Uwekezaji - Mapato Kwa Kila Mtu Mmoja

NCPD Sera Nambari 44 - Julai 2014

Page 6: Arafa ya Sera...Huduma za afya kwa vijana na kwa watu wazima pia ni muhimu katika uboreshaji na maendeleo ya kiuchumi. • Uwekezaji katika elimu : Mifumo ya elimu lazima ihakikishe

Shukrani

Jarida hili liliandaliwa na O�isi ya Kumbukumbu na Takwimu za Idadi ya Watu (PRB) pamoja na Baraza la Kitaifa la Idadi ya Watu na Maendeleo (NCPD), na kwa msaada wa Watu wa Marekani kupitia Shirika la Ustawi na Maendeleo ya Kimataifa (USAID), chini ya masharti yamradi wao –IDEA-Informing DEcisionmakers to Act- (Nambari AID-0AA-A-10-00,009), unalosimamiwa na PRB.NCPD pamoja na PRB zinawajibika kwa yaliyomo katika jarida hili na hayaangazii maoni ya shirika la USAID wala Serikali ya Marekani.

@2014National Council for Population and Development

PRB INFORMEMPOWERADVANCE

IDEAIMFORMINGDECISIONMAKERSTO ACT

USAIDFROM THE AMERICAN PEOPLE

KENYA

Kumbukumbu

Shirika la Kitaifa la Idadi ya Watu na MaendeleoS.L.P. 48994 - 00100, Nairobi, Kenya.Simu: 254-20-271-1600/01Kipepesi 254-20-271-6508Baruapepe:[email protected]

www.ncpd-ke.org

NCPD ni shirika la Serikali linalobuni na kuimarisha sera za idadi ya watu na kushirikisha shughuli zinahusiana kwa ustawi wa maendeleo nchini Kenya.