Mkombozi wa Kweli - DCB Commercial Bank Plc · 2015-11-22 · kutoa mikopo ya jumla ya Shs....

Preview:

Citation preview

Historia ya Benki ya Biashara DCB

1

Benki ya Biashara DCB ambayozamani ilijulikana kama ‘Benki yaWananchi wa Dar-es-Salaam’ilisajiliwa rasmi mwaka 2001 chini yaSheria ya Makampuni ya mwaka2002, na kuruhusiwa kufanyabiashara ya kibenki chini ya sheria yaMabenki na Taasisi za Fedha yamwaka 2006 kama Benki inayotoahuduma za kifedha kwawafanyabiashara wa kipato cha chinina kati.

Benki hii ilianzishwa kufuatia agizoalilolitoa Rais mtaafu wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania wa awamu yatatu, Mhe. Benjamin William Mkapa,alipokuwa akifungua mkutano wa 10wa mabenki na vyombo vya fedhamwezi Disemba mwaka 1995. Raisalirudia tena wito huo wakatialipokuwa anakagua shughuli zawafanyabiashara ndogondogomkoani Dar es salaam mwaka 1999,ambao walimlalamikia juu ya ukosefuwa mitaji ya kuboresha biashara zao.

Kufuatia wito huo wa Rais, Tumeya Jiji la Dar es Salaam (wakati huo)ilitoa kandalasi kwa kampuni yaCommodities Finance & ConsultingLtd (CFC) ili kufanya upembuzi

yakinifu wa kuanzishwa kwa Benkimkoani Dar es Salaam. Taarifa yautafiti huo ilikamilika na kuwasilishwakwa Tume ya Jiji la Dar es SalaamJanuari 10, 2000. Taarifa hiyo

ilionyesha kuwa mradi wakuanzishwa kwa Benki ni wenye faidana kupendekeza kuanzishwa kwaBenki Wananchi mkoani Dar esSalaam.

Wiki hii, Benki ya Biashara DCBinaadhimisha miaka kumi ya mafanikio yautoaji huduma kwa wananchi. Benki hii nimiongoni mwa benki zinazokua kwa harakanchini. Tangu benki hii ifungue milangoyake kwa wananchi, imeendelea kutekelezadira na Dhima ya kuanzishwa kwake yakuwahudumia wateja wadogo na wakati,hasa wajasiriamali kwa kuwapatia hudumaza kibenki ili kukuza biashara zao na kuinuahali ya kipato cha maisha yao. Watejawaliokusuduwa ni watu wlioonekanakwamba hawakopesheki au kuaminiwa namabenki makubwa ambao kwa sasa,kupitia DCB wamethibitisha kwambawanakopesheka na kuaminika.

Katika kipindi cha Miaka 10, Benki hiiimepata mafanikio makubwa katika fanizote za shughuli zake na kutoa faidailiyowezesha kulipa gawio kwa wanahisa

wake kwa miaka sita mfululizo tangumwaka 2006. Kutokana na kuongezeka kwamtaji wa Benki hadi kufikia Shilingi Bilioni16, Benki imeamua kupanua wigo wautoaji huduma zake kwa kubadili hadhi naleseni mwaka huu wa 2012 kutoka Benkiya wananchi na kuwa Benki kamili ya

biashara. Pia Jina la Benki limebadilika nakuwa Benki ya Biashara DCB.

Mafanikio haya yasingewezekana bila yamsaada kutoka serikalini, wateja wetu,wanahisa wetu, washirika wetu wabiashara, waajiri wa makampunimbalimbali ya umma na binafsi, mifuko yahifadhi ya jamii na umma kwa ujumla wakeambao umekuwa mstari wa mbele kwamaendeleo ya benki yetu.

Menejimenti pamoja na wafanyakazi waDCB Commercial Bank Plc wanatoashukrani zao za dhati kwa watu wotewaliotuunga mkono kwa kushirikiana nasi.

Tuko tayari kuendeleza mafanikio hayayaliyokwishapatikana ili tuweze kuimarikazaidi katika kipindi kingine cha miaka 10ijayo. Ni jukumu letu kuihudumia kwaufanisi jamii ya Tanzania chini ya jina jipyala DCB Commercial Bank Plc ilikuwakomboa wananchi waondokane naumaskini. Ni jukumu letu sisi wenyewe,kwa taifa, kwa wanahisa, na kusema kweli,kwa Mwenyezi Mungu mwenyewe.

Mkombozi wa Kweli

Amb. Paul

Rupia

Edmund P.

Mkwawa

Ikifuata Dira na Dhima yakuanzishwa kwake, benki ilianzashughuli zake miaka 10 iliyopitaikiwa na mtaji wa shiling bilioni1.1. Halmashauri ya Jiji la Dares Salaam na Manispaa za Ilala,Kinondoni na Temeke ndizozilizochangia mtaji huo kwaasilimia mia moja.

Hadi kufikia Desemba 30,2011, mtaji wa benki ulifikiashilingi bilioni 8.1 uliokuzwakutokana na mauzo ya hisa kwasoko la awali, hisa za haki (IPO)na kujiunga Soko la Hisa la Dares Salaam mwaka 2008.

Tunajivunia kuona kwambaDCB ni benki ya kwanza nchinikujiungana na soko la hisa.Thamani ya hisa zake kwenyesoko imeongezeka kutokashiling 275 (thamani yakuandikisha) Septemba 16,2008 hadi shilingi 620 kufikiaAgosti 30, 2012. DCB imekuwaKampuni inayofanya vizurikatika soko la hisa barani Africamwaka 2011 na kushika nafasiya 5 kati ya kampuni 10 bora naya kwanza katika nchi za AfrikaMashariki. Kwetu sisitunafarijika sana na hatua hii yamaendeleo, na tumejipangakukabiriana na changamotokubwa iliyopo mbele yetukuendeleza mafanikio haya.

Pia tunatoa wito kwa wadauna wanahisa wa benki hiikushiriki kikamilifu katika zoezila kununua hisa za haki ilikuweza kukuza mtaji wa benki.

WIGO MPANAWA KUWAFIKIA

WAJASIRIAMALIWADOGO NA WA KATITANZANIA

Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Benjamin William

Mkapa akitembelea Tawi la DCB Arnautoglu eneo la Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam

mwaka 2002 katika ufunguzi wa Benki hiyo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa

DCB Bw. Edmund P. Mkwawa, na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa zamani wa

Dar es Salaam, Yusuf Makamba.

Miaka Kumi ya Ukombozi. Imara Zaidi, Mbele Daima

Ujumbe waMwenyekiti

Benki ya Biashara DCB

OKTOBA 5

2012

Ujumbe wa MkurugenziMtendaji

DCB-INSERT SWA.qxd:Layout 1 10/3/12 8:25 PM Page 1

Dira, Dhima na

misingi imara,

na shUghULi KUU

Za BEnKi

DIRA

Dira ya DCB ni kuwa Benki inayoongoza katikakusaidia wajasiriamali nchini Tanzania.

DHIMA

Dhima ya DCB ni kuainisha makundi, taasisi nawatu binafsi wenye kipato cha chini, kati na chajuu, wenye vipaji na kuwa washirika wazuri waBenki kibiashara, watakaoweza kukopa fedha nakuzifanyia kazi kikamilifu, kurejesha mikopo,kuweka akiba Benki mara kwa mara na kujengauwezo wakupanua biashara. DCB inalenga katikakujenga taratibu, mifumo, uwezo na mitandao yautendaji itakayoweza kuhimili utoaji wa hudumamakini na za ufanisi kwa idadi kubwa ya watejawa kipato cha chini, kati na cha juu nchiniTanzania.

MISINGI IMARA

• Utaalam• Uaminifu• Ubunifu• Utendaji wa pamoja• Dhamira• Heshima• Utawala bora

Shughuli kuu za Benki

• Kukusanya nguvu na uwezo wa kifedha kutokakwa watu binafsi, taasisi na wafadhili kwamadhumuni ya kutoa mikopo kwa sekta isiyorasmi ili kuunga mkono jitihada za Serikalikatika kutokomeza umasikini.

• Kutengeneza mazingira muafaka ya shughulibinafsi na kupunguza tatizo la ukosefu wa kazinchini Tanzania.

• Kutoa huduma za kibiashara kwa walengwakwa kuweka kiwango cha faida‘kitakachoiwezesha Benki kurudisha gharamaza uendendeshaji na kupata faida’ ilikuiwezesha benki kujiimarisha yenyewe nakuongeza gawio kwa wanahisa wake.

• Kutoa mikopo kwa wajasiriamali.

Benki ya biashara DCB, zamaniikijulikana kama Benki ya wananchi waDar es Salaam ilisajiliwa na msajili waMakampuni tarehe 6 Septemba 2001na hatimaye kupewa leseni ya kibenkikama Benki ya Wananchi. Ilianza kutoahuduma kwa wananchi tarehe15/4/2002 na tawi moja la Arnautoglulililopo Mnazi Mmoja katika manispaaya Ilala, Dar es Salaam.

Usajili na ufunguziwa biashara

2

Umiliki wa hisa hadi kufikia Disemba 2011Jina

Halmashauri ya Jiji

Manispaa ya Ilala

Manispaa ya Kinondoni

Manispaa ya Temeke

Unit Trust Of Tanzania (UTT)

Umoja Unit Trust Scheme

Wananchi (4,621

(2010: 5,036)

Idadi ya hisa

2,870,628

2,671,188

2,626,060

2,396,536

3,088,148

3,308,870

15,431,806

32,393,236

Thamani ya hisa TZS

717,657,000

667,797,000

656,515,000

599,134,000

772,037,000

827,217,500

3,857,951,500

8,098,309,000

Asilimia

8.86%

8.25%

8.11%

7.40%

9.53%

10.21%

47.64%

100%

Mkurugenzi Mkuu wa UTT Dk. Hamis Kibola akipokea mfano wa hundi ya gawio la 2010 yenye thamani ya Sh 140.8

millioni kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Theresia Mmbando.

Mfumo wa Hisa katika Asilimia

Benki ya Biashara DCB

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania wa Awamu ya Tatu Mhe. Ben-

jamin William Mkapa (aliyekaa) akizindua

Benki ya DCB tawi la Arnautoglu - Mnazi

Mmoja mwaka 2002.

OKTOBA 5

2012

DCB-INSERT SWA.qxd:Layout 1 10/3/12 8:25 PM Page 2

Katika kipindi cha miaka kumi, Benki

imeweza kujiendesha kibiashara na

kupata mafanikio makubwa katika

fani zote za shughuli zake kama

ifuatavyo:

Idadi ya Wateja na AmanaMwaka 2002, benki ilianza na

wateja 12,141 wa kuweka na kukopawenye amana ya Shs. Bilioni 1.76. Leotunafuraha kuwajulisha kuwa tunazaidi ya wateja 179,482 wenyeamana ya Shs. Bilioni 81.1; Disemba2011.

MikopoDCB imewezesha wananchi

kuboresha hali za maisha yao kwakutoa mikopo ya jumla ya Shs. Bilioni

222. 51 hadi Disemba 2011ikilinganishwa na Shs. Milioni 999iliyotolewa mwaka 2002 . Mikopohiyo imetolewa kupitia huduma yamikopo kwa njia ya Mshahara,Mikopo Binafsi, Mikopo ya Vikundi namikopo ya nyumba kwa watu wakipato cha chini na kati.

Mikopo ya vikundiMikopo ya vikundi imeendelea

kupewa kipaumbele. Katika kipindicha miaka kumi, jumla ya Shs. Bilioni31.07 zimekopeshwa kwa walengwa107,160 wengi wakiwa ni wanawakewaishio katika manispaa zote zaMkoa wa Dar es Salaam. Mikopo hiiimesaidia kuendeleza miradi yaomidogo midogo ambayo

imewawezesha kuinua hali ya maisha.Na hili ndilo hasa jukumu la Benki hiikwani jumla ya vikundi 2,143vimeanzishwa mwaka 2011ikilinganishwa na 316 vilivyoanzishwamwaka 2005 kama inavyoonekanakwenye jedwali.

FaidaTangu kuanzishwa kwake, DCB

imefanikiwa kutoa faida kila mwakana kutoa gawio kwa wanahisa wake

Maendeleo ya Benki

Baada ya kuendesha shughuli zakekwa mafanikio Jijini Dar es Salaamkwa miaka 10 na kuongezeka kwamtaji, tuna kila sababu ya kujivuna nakutangaza kwamba benki yetuimebadili jina lake kutoka ‘Benki ya

Wananchi wa Dar es Salaam’ nakuwa ‘Benki ya Biashara DCB’

kufuatia kubadili hadhi yake kutokaBenki ya Wananchi na kuwa Benkikamili ya Biashara.

Leseni yake pia imebadilika nakwamba benki hii sasa itaendeshashughuli zake nchi nzima hivyokupanua wigo wa kibiashara nahuduma kwa wateja. Hata hivyo, Dirana Dhima ya benki hii itabaki kamailivyo. Kwa kuendesha benki yakibiashara, DCB itapata faidazifuatazo:-• Kufungua dirisha kwa wateja

wakubwa (Corporate customers)-

hii itaboresha ukuaji wa benkikimtaji na kutumia fursa nyingizaidi ambazo benki hapo awalihaikuwa na nafasi kuzitumia

• Kujitanua kimtandao- Benki yetuitakuwa na fursa ya kufunguamatawi mikoani kila inapobidi nahivyo kuongeza mapato kwa benki

• Kutoa huduma zaidi za kibenkiambazo hapo awali benki haikuwana fursa ya kuzitoa.

• Kuongeza thamani kwa benki nakwa wanahisa.

Hafla ya uzinduzi wa DCB kujiunga na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) mwaka 2008

Manispaa

Ilala

Kinondoni

Temeke

Jumla

Mikopo ya vikundi kwa manispaa za Dar es Salaam hadi kufikia

Disemba 31, 2011

Idadi ya vituo

709

897

537

2,143

Idadi ya wateja

35464

44839

26857

107,160

JUMLA

Kiasi cha mkopo (TZS)

8,530,795,300

13,409,277,850

9,135,850,351

31,075,923,501

Faida/(hasara) kwa mwaka

Mwaka

Miaka Kumi ya Ukombozi. Imara Zaidi, Mbele Daima

3Benki ya Biashara DCB

OKTOBA 5

2012

kwa kipindi cha miaka sita mfululizotangu mwaka 2006.

Mwaka 2002 benki ilipata hasaraya Sh. Milioni 535.19 zilizotumikakatika kufidia gharama za kuanzishwakwa benki. Baada ya hapo tokamwaka 2005 faida ya benki imekuamwaka hadi mwaka na kufikia Sh.Bilioni 4.4 (kabla ya kodi) mwaka2011.

MABADIlIKO yA JINA NA leSeNI

Sh billioni 4.4Faida kabla ya kodi

mwaka 2011; ililipa gawio kwa wadau kwa

miaka 6 mfululizo tangumwaka 2006

DCB-INSERT SWA.qxd:Layout 1 10/3/12 8:25 PM Page 3

Huduma za BenkiBenki yetu inatoa huduma ya

akaunti mbalimbali kutokana namahitaji ya mteja zikiwemo akauntiya akiba, watoto, wanafunzi, vyamavya ushirika (SACCOS), Akaunti zapamoja, Akaunti za muda Maalum naCall account, Akaunti za hundi kwawatu binafsi, Taasisi, Makampuni naakaunti muhimu kwa ajili watejawalio katika vikundi, Huduma zafedha za kigeni, Huduma yakusafirisha fedha ya Western Union,Wakala mkubwa wa M-pesa, Hudumaza ATM ya UmojaSwitch na hudumaza mikopo kwa njia ya Mshahara,Mikopo ya vikundi, Mikopo yaNyumba kwa watu wa kipato chachini na Mikopo binafsi kwa SME,SMEs na wateja wakubwa.

Mchango wa Benki kwa Pato laTaifa.

Ajira:Hadi kufikia tarehe 31 Desemba

2011, Benki ilikuwa imeajiriwafanyakazi 155 Kati yao wanawakewalikuwa 66 (42.6%) na wanaume 66(57.4%). Aidha, Benki iliendeleakuwawezesha kitaaluma ambapowafanyakazi walipatiwa mafunzondani na nje ya nchi.

Mchango wa benki ya wananchiwa dar es salaam kwa pato la taifa

Kwa kipindi cha kuanzia mwaka2002 hadi 2011, benki ililipa kodi yamapato ya Shi. 4.98 bilioni nakukusanya kodi iliyoshikiliwa(withholding tax) ya Sh 1,229 milioni.Pia benki ililipa kodi ya makato yamishahara kwa wafanyakazi (PAYE) yaShi. 1,613.59 milioni, na ushuru waelimu (Skills Development Levy) waShi. 537.07milioni.

Aidha Benki iliwasilisha mafao yawafanyakazi kwenye mifuko ya jamiiyenye thamani ya kiasi cha Sh1,911.43milioni.

Matokeo kwa uchumi na jamiiTathmini iliyofanywa ilionyesha

kuwa mikopo iliyotolewa kati yamwaka 2002 na 2005 ilitumika kwashughuli za kiuchumi zifuatazo;• Asilimia 78 sawa na wateja 46,506

walitumia mikopo kwa ajili yaujenzi na ukarabati wa nyumbapamoja na kununulia viwanja nashughuli zinginezo.

• Asilimia 16 sawa na wateja 9,540walitumia mikopo kwa ajili yakulipia ada katika ngazi mbalimbaliza kielimu.

• Asilimia 6 sawa na wateja 3,577walitumia mikopo kwa ajili yakuanzisha miradi midogo midogona kujiongezea kipato. Kati yahawa wateja 52 walitumia mikopokuchimba visima vya maji kwa ajiliya matumizi ya nyumbani nabiashara.

Tunafarijika kuona kwamba hudumaza mikopo ya DCB iliyotolewa katikakipindi cha miaka kumi, imesaidiakubadili hali za maisha ya Wananchiwa Dar s Salaam na Tanzania kwaUjumla.

Matawi ya BenkiBenki ina jumla ya matawi matano

yaliyopo katika Manispaa za Dar esSalaam zikiwa zimeunganishwa namtandao wa ATM ya UmojaSwitch.➢ Tawi la Arnautoglu, Mnazi Mmoja ➢ Tawi la Magomeni katika jengo la

DCB, Magomeni Mwembechai ➢ Tawi la Temeke linatazamana na

Mahakama ya mwanzo Temekekwenye makutano ya barabara yaEvereth na Temeke.

➢ Tawi la Tabata, eneo la Tabatadampo

➢ Tawi la Ukonga katika Jengo laMamlaka ya Anga, Ukonga-Banana-makutano ya barabara yaKitunda na Nyerere.Benki iko katika hatua za mwisho

kufungua tawi eneo la Chanikamwaka huu katika manispaa ya Ilala.Hivyo Benki itakuwa na matawi sita.

Shuhuda za wateja jinsiwalivyonufaika na DCB

— Benki ya Biashara DCB

imenipatia mkopo wenye masharti

nafuu na hii imeniwezesha kukuza

biashara yangu, nimeweza kupeleka

watoto shule, na hivi sasa nina

mpango wa kuchukua mkopo

mwingine ili niweze kuanzisha

biashara nyingine. DCB ni ‘Mkombozi

wa Kweli’. – Vivian Shirima

— Nikiwa kama mteja wa DCB,

biashara yangu imeweza kukua na

kujulikana na watu wengi zaidi

kutokana na kuchukua mkopo na

kushiriki kwenye maonyesho ya

kibiashara kwa msaada wa DCB. Hii

imeniwezesha kujikwamua kiuchumi

na hata kusomesha watoto.

Naishukuru sana Benki ya Biashara

DCB. – Isack Ibrahim

Mipango/Matarajio ya baadaye• Benki inatakiwa ikuze mtaji wake ili

kuwezesha kupanuka kwa wigo wautoaji wa huduma zake.

• Kwenye Mkutano Mkuu wa 10 wamwaka,wadau walipendekezakukuza mtaji kwa kuuzaa hisa zahaki kwa kiwango cha 1:1 chashilingi 380/- ikiwa ni punguzo laasilimia 40 kutokana na bei ya hisaya sasa ya shilingi 640.

• Zoezi la kuuza hisa za hakilitazinduliwa rasmi na Rais Mstaafuwa Awamu Tatu MheshimiwaBenjamin William Mkapa, Oktoba5, 2012 kwenye viwanja vya MnaziMmoja.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibarikiTanzania, Mungu ibariki Benki yaBiashara DCB.

Kuhamia kwa Makao Makuu ya

Benki eneo la Magomeni

Makao Makuu ya Benki pamoja na

tawi la Magomeni vilihamishwa kutoka

jingo la Arnautoglu na Hoteli ya

Travertine kwenda jengo la DCB lililopo

Magomeni Mwembe Chai Januari 14

mwaka jana. Jengo la DCB lilifunguliwa

rasmi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Januari 14, 2011.

Huduma kwa jamiiTangu mwaka 2002 DCB imetoa

zaidi ya shilingi milioni 36 kwa ajilimiradi mbalimbali ya kijamii, ikiwemokuwafariji wananchi wa Mbagala naGongolamboto walioathiriwa namilipuko ya mabomu, kutoa madawatina viti kwa shule za sekondari, kugawa

vyandarua, vitanda na magodoro kwahospitali za manispaa mkoani Dar esSalaam, Hospitali ya Kijeshi ya Lugalo,Unguja na Pemba, ujenzi wa majengoya shulie, usambazaji wa vifaa vyaelimu pamoja na sare kwa wanafunziwalioathiriwa na mafuriko Jijini Dar esSalaam Desemba mwaka 2011.

Jengo la Makao Makuu ya Benki ya Biashara DCB na tawi la Magomeni lililopo

Magomeni Mwembechai, Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Bw. Edmund P. Mkwawa (kushoto) akitoa madawati

100 pamoja na viti kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Leonidas Gama. Madawati na viti

hivyo vilikabidhiwa Shule ya Sekondari ya Kivule, Manispaa ya Ilala.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda

(MB), akizindua jengo jipya la Makao Makuu ya Benki ya DCB, Januari 14, 2011.

Miaka Kumi ya Ukombozi. Imara Zaidi, Mbele Daima

4 Benki ya Biashara DCB

OKTOBA 5 2012

DCB-INSERT SWA.qxd:Layout 1 10/3/12 8:25 PM Page 4