MUHTASARI WA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA JUKWAA LA

Preview:

Citation preview

MUHTASARI WA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA JUKWAA LA UTAFITI KWA MAENDELEO WILAYA YA BABATI (JUMBA) ULIOFANYIKA TAREHE 22/10/2014 KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA WHITEROSE BABATI- MKOA WA MANYARA

MAHUDHURIO

S/N

JINA KAMILI WADHIFA KITUO/TAASISI

EMAIL ADDRESS TELEPHONE

1 NICODEMUS TARMO

MWENYEKITI HW BABATI tarmonicodemu@yahoo.com

0784452260

2 HASSAN LUGENDO MKITI JUKWAA BBT DC hjlugendo@yahoo.com 0784-4461233 MARY MASHINGO MTAFITI TALIRI K’JARO Mariahenry.58@gmail.co

m0754-204847

4 MATEETE BEKUNDA MSIMAMIZI AFRICA RISING/IITA

m.bekunda@cgiar.org 0687-516825

5 MARTIN PIUS MRATIBU MVIWATA Mpius@mviwata.org +255752367959

6 SIMON GLAWAY MKULIMA HALLU - 0786 -3029027 SHUFAA MSANGI AFISA UGANI

MIFUGOMAWEMAIRO - 0788 -802012

8 BERNARD SAMBALI

AFISA UGANI MIFUGO

LONG sambalibernard@yahoo.com

0784-393779

9 MAKERE L .S. AFISA UGANI MIFUGO

MWADA - O687-041947

10 ISSA A. MZAVA AFISA MIFUGO RS-MANYARA Issaally67@yahoo.com 0784-70500711 JACKSON

MBWAMBOAFISA MAZAO DAREDA - 0784-620173

12 ALEXANDER MPOGOLO

DAKTARI MIFUGO

RS-MANYARA alexmpogolo@gmail.com 0784-302088

13 FRANCIS MICHAEL MKULIMA SELOTO 0786-18723314 ELIYA DEUS MFUGAJI SHAURIMOYO 0785-36484815 F.S NGULU MTAFITI AFRICA RISING ngulufsale@gmail.com 0784-71249516 GONAMEN NAIMAN AFISA MRADI WORLD VISION

TZgodamen_naiman@wvi.org

0787-045452

17 STEPHEN LYIMO MTAFITI SARI-ARUSHA sdnlyimo@yahoo.com 0754-38011518 PER HILLBUR MTAFITI IITA ,ibadan per,hillbur@mah.se 0688-78091619 ISRAEL PETRO MFUGAJI SABILO 0769-40127820 PAULO JOAKIM MKULIMA SABILO - 0769-92569921 ROSE LOINA MTAFITI TALIRI-TANGA rloina@yahoo.com 0717-53938322 FELICIAN FRANCIS MKULIMA MATUFA - 0685-30727323 LUHENDA

YANGOLEMTAFITI SARI-ARUSHA yangoleluheda@yahoo.co

m0767-328710

24 LEONARD MARWA MTAFITI AFRICA RISING-ARUSHA

leonardmarwa@yahoo.com

0784-705134

25 COLLETA SHAYO AFISA KILIMO RS-MANYARA Shayo_colleta@yahoo.co.uk

0784-725907

26 PATRICE GWASIMA MKURUGENZI COSITA-NGO cositango@gmail.com 0784-64902527 MARK LWAKATARE MTAFITI IITA-DAR marqlw@yahoo.co.uk 0754-03362228 HILARY CHIWANGU MTAFITI IITA-DAR - 071220736529 ABDALLAH

MPANDASHALOMTAFITI IITA-DAR ampandashalo@gmail.co

m0754-063405

30 JUMA MSOGOTI AFISA MRADI BRAC jumamsogoti@gmail.com 0788-05544031 MARIAM CHRISTIAN MKULIMA MATUFA - 0785-65373232 ZAINABU MNUBI AFISA KILIMO BABATI DC Zainabumnubi@yahoo.co

m0784-586400

33 MSEMO .E. STANLEY

MCHUMI BBT DC stanleymsemo@gmail.com

0784-476728

34 A.KASINDEI MJUMBE TOBRA - 0784-39259835 MASAMU JONAS AFISA KILIMO BBT DC jonajuly@yahoo.com 0753-89112336 ROSE A.

PALLANGYOAFISA KILIMO BABATI DC Rose_anael@yahoo.com 0784-431161

37 JUDITH .E.MANZI AFISA KILIMO HALLU manzijudith@yahoo.com 0787-41546438 AINGICK .T.SHOO AFISA MIFUGO BBT DC aingick.shoo@yahoo.com 0784-96100839 NAOMI NASHON AFISA MIFUGO BBT DC naomieliakim@yahoo.co

m0759-920125

40 JAMES .B. DAVID AFISA VIJANA BBT DC jamesbubelwa@yahoo.com

0878-483586

41 LILIAN .O. LYIMO AFISA MIFUGO BBT DC lyimolilian@yahoo.co.uk 0784-52530842 PRISCA PETER MAENDELEO

JAMIIBBT DC pripea@yahoo.com 0765-855833

43 ANNA ROMAN AFISA KILIMO MATUFA Annaroman07@yahoo.cm 0786-81498244 ZAHORO

MADONGOAFISA KILIMO LONG zmodongo@gmail.com 0683-698567

45 CHACHA NYANGI MTAFITI IITA-DAR nyangichacha@yahoo.com

0764-775727

46 SAMSON LYIMO MTAFITI NM-AIST ARUSHA

samlyimo@yahoo.com 0755-767166

47 CLARA MOLLAY MTAFITI NM-AIST ARUSHA

- 0758-010308

48 JAPHARY B. MPELEMBWA

AFISA ARDHI BBT DC japharybm@gmail.com 0788-138617

49 IDA KAVISHE AFISA MRADI BRACK idahkavishe@gmil.com 0757-47711450 GILBERT MBESERE AFISA MIFUGO BBT DC mbesere@gmail.com 0784-45901751 ALPHONCE I.

HAULEMTAFITI AFRICA RISING mkulima@yahoo.com 0784-395950

52 CHRISTOPHER LYAMUYA

AFISA MIFUGO SABILO - 0784-725658

53 PASCHAL MAHETU MKULIMA SABILO - 0784-74367354 ANDREA MAYI MFUGAJI SELOTO - 0784-811025

55 PATRICK KISAMO AFISA MIFUGO SELOTO - 0782-72118156 JOHN .S.

KHALUNGUAFISA KILIMO SHAURIMOYO - 0788-707551

57 LUCIAN K. QAMARA MFUGAJI LONG - 0682-08347158 MUHIDINI .R.

MBELWAAFISA MIFUGO HALLU - 0782-758866

59 ISRAEL SANKA MFUGAJI HALLU - 0686-50907560 DANIEL SHADRACK MTAFITI IITA DSM dmssjut@gmail.com 0713696089

WAALIKWA WASIOHUDHURIA:

1. Dr. Hurbert Lyimo –Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mjumbe Menejimenti) : Kwa taarifa2. Kheri Kitenge – Selian Agriculture Research Institute (Mjumbe Menejimenti): Kwa taarifa3. Danny Manyangu- MVIWATA (Mjumbe Menejimenti): Kwa taarifa4. Mkurugenzi Ujasiriamaisha (JSBC ) Babati-Mdau : Bila taarifa5. Mkurugenzi FIDE- Mdau: Bila taarifa

6. Mkurugenzi Kiwanda cha Mbolea Minjingu-Mdau: Bila taarifa7. Mwenyekiti Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira Halmashauri Wilaya Babati - Bila taarifa8. Mratibu FARMAFRICA – Babati: Bila taarifa9. Mratibu Tuboreshe Chakula Babati- Bila taarifa10. Mwakilishi wa Wauza pembejeo Babati: Bila taarifa11. Mkurugenzi Kituo cha Mafunzo BACCHO IATC Dareda: Bila taarifa12. Mratibu Mradi wa Vit A Shirika la MEDA-Babati bila taarifa

AGENDA ZA MKUTANO

1. UFUNGUZI WA MKUTANO

2. TAARIFA FUPI ZA UTAFITI WILAYA YA BABATI

3. KUJADILI RASIMU YA KATIBA

4. MASWALI YA UJUMLA KUTOKA KWA WASHIRIKI

5. KAZI ZA VIKUNDI

6. MENGINEYO

7. KUFUNGA MKUTANO

MUHT 01/ MM/ 2014 : KUFUNGUA MKUTANO WA JUMBAMwenyekiti wa Jukwaa la Utafiti aliwakaribisha wajumbe wote waliohudhuria Mkutano wa JUMBA na kuwaomba kujitambulisha baadae alimuomba Mjumbe wa Kamati ya Menejimenti Dr. Mary Mashingo kwa niaba ya Kamati ya Menejimenti kutoa utangulizi na taarifa maalum za Jukwaa kuanzia uanzishwaji wake.

Baada ya Mjumbe wa Kamati kutoa taarifa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu, Mwenyekiti wa Jukwaa alimuomba na kumkaribisha Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Africa RISING Profesa Mateete Bekunda kuwasalimia washiriki.

Msimamizi wa Mradi alianza kwa kuwashukuru wajumbe kwa Kuhudhuria kwao na akasema atahakikisha kuwa Miradi mingi itakuja Wilaya ya Babati na akaendelea kusema kuwa ameandika andiko la Mradi na limepata fedha, na alisisitiza kwamba wajumbe wayafanyie kazi matokeo chanya ya Utafiti ili yaenezwe na kuleta mabadiliko kwa Babati na Nchi nzima.

Baada ya salam za Msimamizi wa Mradi, Mwenyekiti wa Jukwaa alimkaribisha Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati ili aweze kufungua mkutano.

Mgeni rasmi aliwasalimia na kuwakaribisha wajumbe wote na kushukuru Africa RISING kwa kuchagua Wilaya ya Babati kuwa miongoni mwa sehemu ya utafiti kwa Maendeleo ya Wakazi wa Babati.

Mgeni Rasmi alielezea kuwa Halmashauri inalikubali swala hili na ipo tayari kutoa ushirikiano pale inapohitajika na kuwasisisitiza Maafisa Ugani ngazi zote kutunza yale yote yaliyofanyiwa utafiti si kwa vile vijiji sita ( 6 ) ambavyo vipo kwenye utafiti bali katika vijiji 100 vya Halmashauri ya Wilaya ya Babati.

Baada ya utangulizi huo Mgeni Rasmi alifungua rasmi mkutano mnamo saa 05:11 asubuhi na kuwatakia wajumbe baraka za Halmashauri ya Wilaya.

Mwenyekiti wa Jukwaa alitoa shukrani kwa Mgeni Rasmi baada ya ufunguzi kwa kukubali kwake kuwa mgeni rasmi na kushiriki katika Mkutano Mkuu na mwisho aliwaomba wajumbe kupiga picha ya pamoja kama ishara ya kumbukumbu ya siku hii muhimu.

MUHT. 02/MM/2014: TAARIFA FUPI YA UTAFITI WILAYA YA BABATI

Mkutano uliendelea kwa washiriki kupokea taarifa juu ya shughuli za tafiti mbalimbali kutoka kwa wataalam wa Idara za Kilimo na Mifugo katika Halmashauri shughuli zinazofanyika kwa kushirikiana na Africa RISING kama inavyooneshwa:-

A:MADA YA KWANZA: UTAFITI JUU YA UBORESHAJI WA KUKU WA ASILI

Shughuli zilizofanyika za Uboreshaji uzalishaji wa kuku wa asili katika Halmashauri ya Wilaya Babati uliwasilishwa na Mtaalam wa Mifugo wa Halmashauri Bi.Lillian Lyimo kwa kuelezea maeneo yafuatayo:-

1.NJIA ZINAZOTUMIKA KATIKA UFUGAJI WA KUKU

Ufugaji Huria ambao kuku hujitafutia chakula wenyewe Ufugaji Nusu huria. Ufugaji wa ndani.

2. CHANGAMOTO ZA UFUGAJI WA KUKU WA ASILI

Magonjwa ya kuku Vyakula vya kuku visivyokidhi viwango. Mabanda ya kufugia kuku. Kuzaliana kwa kuku ( inbreeding ) Soko la kuku na mayai. Wafugaji kutokuona kama ufugaji wa kuku wa asili kama ni chanzo cha kipato. Dawa za kuku zisizokuwa na kiwango na uelewa mdogo wa matumizi ya chanjo . Vifungashio vya chanjo vinabeba kuku wengi kulingana na idadi ya kuku wanaofuga

kwenye kaya. Ongezeko la matukio ya wizi wa kuku, wanyama na ndege walao vifaranga vya kuku.

3.FURSA ZILIZOPO Kuku wa asili. Mabaki ya nafaka. Vifaa vya ujenzi/Eneo Maafisa ugani Watafiti mbalimbali. Mashine za kutotolesha vifaranga na bruda. Walaji wa kuku na mayai wameongezeka. Kuwepo kwa chanjo mbalimbali.

4..MATOKEO YANAYOTEGEMEWA BAADA YA KUFANYA UTAFITI Ongezeko la kuku. Ongezeko la kipato. Soko la kuku Utengenezaji wa vyakula vya kuku kufuatana mazao yanayolimwa. Kutakuwepo na mnyororo wa wadau katika kuinuia uzalishaji wa kuku na

kufikia mlaji. Kaya zilizo maskini kufuga kuku kwa wingi. Ongezeko la uelewa katika Nyanja za ufugaji wa kuku.

MADA YA PILI: UBORESHAJI WA MALISHO YA MIFUGO

Uboreshaji malisho ya mifugo kama fursa ya uendelezaji mfumo wa kilimo na ufugaji Babati iliyowasilishwa na Mtaalam wa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya Babati Bi.Lillian Lyimo kwa kuelezea kuwa Shirika la Utafiti (Africa RISING) wakishirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Babati wanafanya utafiti wa malisho ya mifugo katika vijiji vya Seloto, Sabilo na Long.

CHANGAMOTO KWA UFUGAJI

- Malisho hayana virutubisho vya kutosha - Malisho yanayotumika ni yale yanayopatikana msimu wa mvua tu- Hakuna eneo la Kijiji lililotengwa kwa ajili ya kukuza malisho.- Upatikanaji wa mbegu za aina bora za malisho- Kiwango cha maziwa ni kidogo - Afya mbaya za mifugo kutokana na lishe duni.- Upotevu wa malisho wakati wa kulisha mifugo- Wafugaji kutoona umuhimu wa kupanda na kutunza malisho.

FURSA ZILIZOKO

- Makinga maji- Mashamba ya wafugaji- Maeneo ya mipaka - Mifugo - Wafugaji wakufunzi - Utafiti wa aina za malisho na ubora.- Mabaki ya mazao

Matokeo ya utafiti yanayotarajiwa

- Aina bora za malisho yatakayochaguliwa kutokana na maeneo - Njia bora za hifadhi ya malisho- Maandalizi bora ya malisho kabla ya kulisha kuepuka upotevu (Ukatakataji)- Ongezeko la uzalishaji wa mazao yatokanayo na mifugo.- Ongezeko la malisho.- Upatikanaji wa mbegu bora za malisho ikiwepo majani na miti aina ya mikunde.- Hifadhi na matumizi bora ya ardhi kutokana na maeneo yatakayopandwa malisho.

MADA YA TATU: UBORESHAJI KILIMO CHA MBOGA

Mada hii iliwasilishwa na Bi.Zainab Mnubi kwa kuelezea yafuatayo:-

Utafiti wa tatizo

Ufumbuzi:

Kutumia mbinu za uzalishaji mboga salama na endelevu.

Kutumia udhibiti husishi wa visumbufu (udhibiti sango, kinzani, kibaiologia na kemikali)

Kutumia mbinu sahihi za kuhifadhi maji ya umwagiliaji wakati wa masika na kiangazi.

Kutumia mbegu bora

Shughuli zilizofanyika Mikutano ya uhamasishaji ilifanyika kwa wakulima wanaolima mahindi/mikunde. Mafunzo yametolewa kwa wakulima 71 (55 wanaume, 16 wanawake).

Kujengea uwezo wakulima kwa kuwapa mbegu bora kutoka AVRDC: Mchicha (Madira I and Madira II); Nyanya (Tengeru 2010, Tengeru 97 na Tanya); Nyanya chungu (DB3Pilipili hoho (PP 0042.68);

Kuanzisha mashamba ya majaribio, majaribio yalikuwa na sehemu 2 kila kituo – uzoefu wa mkulima na utafiti, wakulima 140 walishiriki, ambao waliweza kuchagua mazao/mbegu zilizokuwa na matokeo mazuri.

Kuendesha siku za wakulima Bermi, Matufa na Gallapo ambapo wakulima 162 walihudhuria.

Jumuisho Kwa kuwa walaji wa mboga za majani huongezeka kwa kuzaliwa kila siku ni dhahiri biashara yake itaendelea kukua. Hapa basi ndipo mahali pazuri pa kujiajiri vijana wengi na chanzo kizuri cha biashara isiyohitaji mtaji mkubwa. Mwanzo huu hatimaye humvusha na kumuingiza mfanyibiashara katika eneo zuri zaidi la biashara.

MADA YA NNE: HIFADHI YA MAZAO KABLA NA BAADA YA MAVUNOMada hii iliwasilishwa na Mtaalam wa Kilimo Bw.Masamu kwa kuongeza uhakika wa chakula kwa kupunguza hasara kabla na baada ya mavuno kama ifuatavyo:-

• Matokeo ya awali yalijielekeza kwenye mambo manne muhimu yakushughulikia kwenye hatua za kupunguza hasara kwa wakulima;

Yakiwa shambani.

Mahindi yakiwa shambani hasara zinakadiriwa kuwa ni asilimia ishirini ( 20%) zinasababishwa na Panya, wadudu na kutokuvunwa kwa usahihi.

Wakati wa kuyaandaa/kumenya na kupukuchua

Hasara zinazojitokeza ni asilimia tano ( 5% ) na shughuli hii inafanywa zaidi na wakina mama na inatumia muda mrefu.

Kuhifadhi

Kuhifadhi kunachangia hasara kwa zaidi ya asilimia tisini ( 90%) kwa wadudu wakubwa walao mahindi (Prostephanus truncutus) na asilimia kumi natano hadi ishirini na tano ( 15-25%) kwa wadudu wadogo walao nafaka (Sitophilus granarium) na kuna hasara zinazosababishwa na wadudu walao unga wa mahindi (Tribolium confusum) na (Rhyzopertha dominica

Virutubisha mwili

Virutubisha mwili kwenye jamii ni vya wastani navyo vilihiitaji kufanyiwa kazi

Hatua zilizochukuliwa kutatua changamoto hizi Sehemu ya hatua zilizochukuliwa kutatua changamoto hizi ni wakulima 80 kutoka

kila kijiji walifundishwa kuhifadhi mazao ya chakula Mashine ya kupukuchua Mahindi Kutumia makaratasi maalumu ya kuanikia mahindi yenye uwezo wa kupunguza

unyevu hadi asilimia kumi na tatu ( 13% ) kabla ya kuhifadhi. Karatasi Maalumu la Kuanikia mahindi (GrainPro Collapsible Dryer Case )

MADA YA TANO: MATUMIZI YA MBOLEAMada hii iliwasilishwa na Mtaalam wa Kilimo Bi.Rose Pallangyo kama ifuatavyo:-

o Shughuli za kilimo ndani ya Halmashauri.

o Uwezo wa uzalishaji wa udongo (soil productivity

o Kazi zilizofanyika

Tafiti za udongo kutambua rutuba ya udongo. Tafiti za sampuli za mbolea za asili. Tafiti za kikemia za udongo. Majaribio ya aina tofauti za mbolea za viwandani na mbegu bora za mahindi. Mbolea

zilizohusika ni pamoja na mbolea za Minjingu,(Minjingu chenga chenga na Minjingu Mazao), DAP, TSP Muriate of Potash na UREA. Katika majaribio haya mahindi yalipandwa na mbaazi au na maharage kwa nyanda za juu.

o matokeo yaliyopatikana kufikia sasa Tafiti za rutuba ya udongo zimethibitisha kuwa ukanda wa juu katika kijiji cha Long

udongo wake una kiasi kikubwa cha Nitrogen ukilinganisha na vijiji vya ukanda wa chini na hii inatokana na hali ya joto kuwa ndogo katika ukanda huu na hivyo upotevu mdogo wa kiini lishe hiki. Ukanda wa chini unaonyesha kuwa Nitrogen ni pungufu zaidi kwa sababu ya hali ya hewa ya joto kali. Virutubisho vingine vipo kwa viwango tofauti katika maeneo tofauti.

Sifa za mbolea za asili zilifanana kwa sampuli zote zilizochukuliwa. Kwa ujumla mbolea za asili zina uwezo mdogo wa kuongeza rutuba ya udongo. Hii inatokana na njia zisizo sahihi za hifadhi na matumizi ya mbolea hizi zinazotumiwa na wakulima wengi wa Babati.

Kwa ujumla matokeo ya tafiti za mbolea na mbegu za mahindi yalionyesha matokeo chanya kwa maeneo yote ya utafiti. Matokeo mazuri zaidi yalikuwa katika vijiji vya Hallu na Sabilo ambapo tafiti za rutuba ya udongo mwanzoni zilionyesha kuwa na kiwango cha chini sana cha rutuba na hivyo matumizi ya mbolea katika maeneo haya yalileta tofauti kubwa katika mavuno.

Katika siku za wakulima shambani ambazo zimefanyika katika vijiji vya utafiti

wakulima wengi walifurahia matokeo ya mbolea ya DAP kuliko mbolea nyingine za viwandani. Kutokana na gharama za mbolea wengi wao walikubali matumizi ya Minjingu mazao ambayo inapatikana kwa urahisi na bei nafuu zaidi. Hata hivyo mbolea hii inahitaji kuwa na unyevu wa kutosha shambani

o Nini cha kufanya:

Wakulima walioshiriki katika tafiti hizi wamejionea matokeo ya teknolojia zilizojaribiwa katika maeneo yao na kuzikubali.

Ni muhimu kutawanyisha matokeo haya katika maeneo mengine kwa manufaa ya wakulima wengi. Ieleweke bado wapo wakulima wenye mtazamo hasi wa matumizi ya mbolea hasa za viwandani.

Zipo mbinu za awali na za asili za wakulima zilizothibitika kuwa na manufaa ya hifadhi ya udongo (rutuba na maji) mfano uchanganyaji wa mahindi na mbaazi shambani matumizi ya matandazo na uchimbaji wa matuta.Hizi hazina budi kuendelea kusisitizwa.

Elimu ya usindikaji, hifadhi na matumizi ya mbolea za asili inahitajika kwa wakulima ili kuwa na matumizi mazuri yenye faida ya mabaki ya mazao na mifugo kurutubisha udongo.

Aina za mbolea zinazopendekezwa kwa wakulima zinapaswa kuzingatia hali halisi ya eneo husika kutokana na hali ya udongo. Mbolea ya aina moja haiwezi kuwa sahihi kwa maeneo yanayotofautiana.

MADA YA SITA: UGONJWA MPYA WA MAHINDI

Mada hii iliwasilishwa na Mtaalam wa Kilimo Bw.Edgar Lyakurwa kwa kueleza yafuatayo:-

Namna ugonjwa ulivyoingia nchini

o Hatua zilizofanyika katika kukabiliana na ugonjwa wa MLND Halmashauri ya Wilaya ya Babati

o Matokeo ya mbegu bora pamoja na mbegu za kienyeji

MADA YA SUMU KUVU

Mada hii iliwasilishwa na Mtaalam Mtafiti Bw.Mark kutoka IITA Dar kwa kuelezea kuwa:-

Sumu kuvu ni sumu inayotokana na ukungu kwenye mahindi na inaweza kuleta madhara kwa binadamu na mifugo. Shirika la IITA inafanya utafiti:-

1. kutathmini aina ya mbegu zinazotumika

2. Kutathmini aina ya mbolea inayotumika

MUHT. 03/MM/2014: KUJADILI RASIMU YA KATIBA YA JUKWAA

Rasimu ya Katiba ya Jukwaa iliwasilishwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ili kuweza kuijadili na kuidhinishwa.

Mjumbe wa Kamati ya Menejimenti aliwasilisha kwa kusoma kabrasha yote ukurusa kwa kurasa kisha kupitia masahihisho kwa rasimu yote yaliyopitiwa na wajumbe kwa pamoja.

Masahihisho yalipendekezwa kufanyika kwa kupitia kila kurasa iliyoonekana inahitaji masahihisho kama inavyoonekana kwenye jedwali

UKURASA WA KWANZA

Ukurasa

Neno kosewa marekebisho

1. Jukwaa la utafiti kwa Maendeleo Wilaya ya Babati

Liwe maandishi yaliyolezwa wino

1. 22nd Octoba ,2014 Iandikwe Mwaka

1. Manayara Manyara

2. Tafsiri Maneno magumu yatafsiriwe

2 Yaliyomo Kuwe na dira na dhamira ya JUMBA kabla ya Malengo

2. Yaliyomo na.7& 8 Iwe ibara moja ya Uongozi yenye vipengele A & B

2. Yaliyomo na .10,11, na 12

Iwe ibara moja ya mikutano yenye vipengele A,B & C na herufi ziendane Mfano Mm

3. 1.3 Email ,Web site na Namba ya simu viongezeke

3 4.Malengo Liwe lengo kuu 1

3 5.Majukumu Liandikwe malengo mhususi

5 b Iongezeke sekta binafsi (PPP)

4. 6.(1) Uanachama wa kudumu wa jukwaa utakuwa wazi kwa

Liandikwe sifa za uanachama wa kudumu

4 6.neno yeyote Liandikwe Mdau

4 6.Shirika lolote linalofanya shughuli

Shughli ziwe za sekta ya Mifugo na Kilimo ndani na nje ya Wiaya ya Babati

4 Namba 6 (1,2,..) Namba 6 (3) iongezwe iwe Namna/ jinsi ya kujiunga

4 6 Bullet ziondolewe

4 6 (2) bullet na.1 Uanachama aina hii

Uanchama wa aina hii

4. 6.Haki na Wajibu bullet na.2

Bullet na 2 iandikwe kwenye ukomo wa wanachama

4 6. Bullet na 4.Kuchagua na kuchaguliwa kwa nafasi ya uongozi

Kuchagua au kuchaguliwa katika nafasi ya uongozi

4. 6.Bullet na 7.Kuhudhuri mikutano

Kuhudhuria na kushiriki mikutano

4. 6.(2).bullet na 5 yanayotakiwa ndani ya miaka miwili

yaondolewe

5. 6.1 b) Liongezeke Ndani na nje ya wilaya ya Babati

5. 6.1.e) Kujiuzuru Kujiuzulu

5 7 a Muundo wa jukwaa 7a Muundo

b.Ukomo wa Uongozi

5 7.c) Ingalau Angalau

5 7.f)Maamuzi ya kumtoa mwanachama

Yafanywe na mkutano mkuu na si Kamati ya menejimenti.

6. Na 7.h.i. & j Vipengele hivyo viingie kwanye majukumu ya Kamati ya Menejimenti na kiongezwe kipengele cha kuainisha maeneo ya utafiti katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati pia majukumu yawekwe sehemu moja

6. 8.a bullet namba 3 Pale inapolazimu

Liondolewe

6 8.b.bullet na 1 mihtasari Mihutasari

7 9.8 watia saini Waweka saini

7 10 C) bullet na 4 amuriwa

amliwa

8 12 mkutano Maalum usiwe na siku 14

Usiwe na maaandalizi ya muda mrefu

9. 15. Kuwepo na majina saini na Nafasi zao

MUHT. 04/MM/2014: MASWALI KUTOKA KWA WASHIRIKI

Mwenyekiti wa Jukwaa alitoa nafasi kwa wajumbe kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa mawasilisho yote yaliyotolewa na mambo mengine yahusianayo na shughuli za Jukwaa.

Mjumbe kutoka shirika la COSITA alitoa ushauri kuwa Ufugaji wa ndani na ufugaji wa huria kwa Wafugaji ufanyiwe utafiti pia, na aliwashukuru sana walioandaa JUMBA.

Mjumbe kutoka Shirika la WORLD VISON alishauri kuwepo na utaratibu wa kutoa chanjo ya dhidi ya ugonjwa wa kideri kwa kuku.

Mjumbe pia aliuliza juu ya upatikanaji na bei ya Mifuko ya kuhifadhia Mazao bila kutumia dawa ya kuhifadhia mazao.

Majibu yalitolewa kuwa Mifuko ipo na itapatikana baada ya mkutano huu na kuomba iwapo watapatikana mawakala wanaoweza kuipokea na kuiuza kwa wahitaji utaratibu wa makubaliano unaweza kufanyika.

Mjumbe mwingine aliuliza ni mbegu ipi ya mahindi inafaa kwa kustahimili ugonjwa hatari wa mahindi baada ya kufanya utafiti katika maeneo ya Vijiji vya Babati?

Mjumbe alijibiwa kuwa kuhusiana na mbegu gani inafaa bado watafiti hawajafikia kutoa majibu na kazi ya utafiti inaendelea.

MUHT. 05/MM/2014: KAZI ZA VIKUNDI

Wawezeshaji wa Mkutano walitambulisha mada nne (4 ) zitakazojadiliwa na Vikundi na baadaye vikundi vinne vya majadiliano viliundwa.

MADA YA UTAFITI KUNDI LA KWANZA:

1: A changamoto zilizopo katika kuendesha shughuli za utafiti wa Mazao na mifugo zikigusia maeneo ya watafiti, wagani, wakulima/wafugaji, Uongozi wa Kijiji, Kata na Wilaya

1.B Mapendekezo ya ufumbuzi wa changamoto zilizojitokeza

MADA YA PEMBEJEO KUNDI LA PILI:

2:A Changamoto zilizopo kuhusiana na upatikanaji na Matumizi ya pembejeo katika uzalishaji wa Mazao na Mifugo katika Wilaya

2:B Mapendekezo ya ufumbuzi wa changamoto zihusikanazo na pembejeo

MADA YA MASOKO KUNDI LA TATU

3:A changamoto zilizoko kuhusiana na masoko ya Mazao baada ya uzalishaji mashambani

3:B Mapendekezo ya ufumbuzi wa changamoto

MADA YA SERA KUNDI LA NNE

4:A Changamoto zilizopo kuhusiana na sera katika Uendeshaji Shughuli za Kilimo na Ufugaji

4:B Mapendekezo ya ufumbuzi wa changamoto

Baada ya kuzitaja mada, Mada ziligawanywa kwa makundi ya wajumbe kwa Majadiliano.

MAJADILIANO YALIFANYIKA NA UWASILISHAJI ULIKUWA KAMA IFUATAVYO;

MADA YA UTAFITI KUNDI LA KWANZA:

1:A Changamoto

Watafiti

-upungufu wa fedha za kufanyia tafiti hasa fedha toka serikalini

-Elimu na ushirikiano hafifu kati ya wadau na Wataalam

-Magonjwa ya Mazao/Mifugo yanayojitokeza wakati wa utafiti

-Mrejesho wa teknolojia kwenda kwa wakulima unakuwa hafifu

Maafisa ugani

-Lugha

-Rushwa

-vibali vya Uhamiaji kuchelewa

Wakulima/Wafugaji

-Mrejesho hafifu wa tafiti

-Mahudhurio hafifu ya watafiti kwa wakulima

-Mlipuko wa magonjwa ya Mifugo/Mazao kwa wakulima

-Mabadiliko ya hali ya hewa

Uongozi wa Kijiji/kata/Wilaya

- Mahusiano ya watafiti na viongozi wakati mwingine sio mazuri

-Muda wa Kuhudhuria ni hafifu kwa sababu ya majukumu mengi

1:BMapendekezo ya ufumbuzi wa changamoto

- Elimu ya umuhimu wa tafiti itolewe kwa wadau kwa wakati

- Serikali iwekeze zaidi kwenye tafiti

MADA YA PEMBEJEO KUNDI LA PILI:

2:A Changamoto

Upatikanaji

- Pembejeo nyingi hazipatikani kwa wakati

- Baadhi ya pembejeo zinauzwa bei ghali kiasi kwamba mkulima peke yake anashindwa kumudu zile gharama

- Wataalam wa Ugani hawatoshelezi

- Pembejeo nyingine zinauzwa kiholela hivyo inazuia upatikanaji wa pembejeo zenye ubora

Matumizi

-Wakulima wengi hawataki kutumia pembejeo na wamejijengea dhana potofu juu ya Matumizi.

-Baadhi ya wakulima kutokufuata maelekezo ya namna ya utumiaji wa pembejeo

-Pembejeo nyingi hazina ubora

Mapendekezo

-JUMBA lishauri wasambazaji wa pembejeo wazifikishe mahali husika kwa wakati

-Wakulima washauriwe kujiunga kwenye vikundi ili waweze kumudu bei ya pembejeo iliyoko sokoni pamoja na Mafunzo ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa Wataalam wa ugani

-Pembejeo Mfano chanjo zirudishwe Idarani/Serikalini

-Wasimamizi wa Sheria wachukue hatua kwa wauzaji holela wa pembejeo Mfano minadani

MADA YA MASOKO KUNDI LA TATU

3:A Changamoto

-Ukosefu wa Taarifa za masoko

- Ukosefu wa ubora wa Mazao ya Kilimo/Mifugo

- Kukosa ushirikiano wa kutosha toka Serikalini

- Ujuzi mdogo wa kuhifadhi Mazao ya Kilimo/Mifugo

- Miundombinu duni ya usafirishaji wa Mazao

- Sera kandamizi

3:B Mapendekezo ya ufumbuzi

-Kuimarisha ushirika

-Uzalishaji kwa Mkataba

-Elimu kwa wakulima kuhusu kusindika Mazao kwa ubora

-Serikali ifanye utafiti wa kutosha kabla ya Kuweka Sera

-Serikali kuboresha miundombinu

MADA YA SERA KUNDI LA NNE

4: A CHANGAMOTO Sera hazifiki kwa wadau husika Sera kinzana (Pigana) Kilimo na Mifugo Utekelezaji wa Sera za Kilimo na Mifugo umekwama kwa kutokuwa na mpango

bora wa Matumizi bora ya ardhi Usimamizi, utekelezaji na Ufuatiliaji wa Sera haupo

4.B: UFUMBUZIo Serikali iweke mkakati maalum wa kutoa elimu, kusimamia na Kufuatilia Sera zote

zinazohusu Kilimo na Mifugoo Sera zifanyiwe marekebisho mara kwa mara kwa kuhusisha wadau wa ngazi zoteo Sera zinazorekebishwa zitolewe mapema mfano Sera ya Kilimo ya mwaka 1997

iliyorekebishwa mwaka 2007 haijatolewa hadi leoo Utungaji wa sera ushirikishe Idara zingine (Mtambuka) Mfano Misitu,Wanyama pori

na Ardhi ili kuondoa ukinzanio Serikali iweke mkakati wa Kitaifa wa kuweka mipango bora ya Matumizi ya ardhi

MUHT.06/MM/2014: MENGINEYOMwenyekiti alikuwa na mengineyo ya kujaza nafasi za Mtunza Hazina na Katibu katika safu ya Uongozi wa Kamati ya Menejimenti na wajumbe walishauri kwa kuwa Viongozi wanatokana na wajumbe wa Kamati ya Menejimenti inabidi Kamati yenyewe ifanye mchakato wa kuwapata hao Viongozi miongoni mwa wajumbe waliomo.

MUHT. 07/MM/2014: KUFUNGA MKUTANO

Mwenyekiti aliwashukuru wajumbe kwa uvumilivu wao na mchango mzuri wa mawazo pia alilishukuru Shirika la AfricaRISING kwa kufadhili na kufanikisha Mkutano huu Mkuu kwani JUMBA halina mapato yoyote kwa ajili ya kuweza kujiendesha. Mwisho Mwenyekiti alifunga Mkutano mnamo saa 11:12 jioni na kuwatakia wajumbe wote utekelezaji mwema wa maazimio yote na safari njema warejeapo makwao.

Umethibitishwa

…………………………….. …………………………………...

Katibu Mwenyekiti

…….…………………………

Tarehe

Recommended