177
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Hamsini na Tatu – Tarehe 19 Juni, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. PAMELA PALLANGYO – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU (K.n.y. WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO): Taarifa ya mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Bodi ya Mfuko wa Barabara kwa mwaka wa fedha 2014/2015 (The Annual Report and Audited Accounts of the Roads Fund Board for the Financial Year 2014/2015). NAIBU SPIKA: Katibu.

parliament.go.tzparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1540620857-19...NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO

  • Upload
    others

  • View
    2

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE____________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Hamsini na Tatu – Tarehe 19 Juni, 2018

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu.

NDG. PAMELA PALLANGYO – KATIBU MEZANI:

HATI ZA KUWASILISHA MEZANI

Hati ifuatayo iliwasilishwa mezani na:-

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU (K.n.y. WAZIRI WAUJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO):

Taarifa ya mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Bodiya Mfuko wa Barabara kwa mwaka wa fedha 2014/2015 (TheAnnual Report and Audited Accounts of the Roads FundBoard for the Financial Year 2014/2015).

NAIBU SPIKA: Katibu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

NDG. PAMELA PALLANGYO – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

Na. 447

Kupandisha Hadhi Kituo cha Afya SinzaKuwa Hospitali ya Wilaya

MHE. JOSEPH R. SELASINI (K.n.y. MHE. SAED A.KUBENEA) aliuliza:-

Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne alipotembeleaKituo cha Afya cha Palestina kilichopo Kata ya Sinzaalitangaza kukipandisha hadhi kuwa Hospitali ya Wilaya. Hatahivyo, bado Serikali inaendelea kuipatia fedha hospitali hiyokama Kituo cha Afya.

Je, ni lini Serikali itaitambua hospitali hiyo kamaHospitali ya Wilaya kwa kuipa fedha na vitendea kazivinavyofanana na hadhi yake?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Saed Ahmed Kubenea, Mbunge wa Ubungo,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya cha Palestinakimekuwa kinafanya kazi kama Hospitali ya Wilaya kufuatiatamko la Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne la tarehe 11Disemba, 2012.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya tamko hilo,ukaguzi ulifanyika na kubaini uhitaji wa kuongezewa eneokwa ajili ya upanuzi wa huduma. Ifahamike wazi kuwa kituohiki kilianzishwa ili kitoe huduma kama Kituo cha Afya, hivyohakiwezi kuwa Hospitali ya Wilaya. Kwa kutambua umuhimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

wa kituo hiki, hatua zifuatazo zimechukuliwa kutatua baadhiya changamoto:-

(i) Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ruzuku ya ununuziwa dawa, vifaatiba na vitendanishi kutoka Bohari Kuu yaDawa (MSD) imeongezeka hadi kufikia shilingi milioni 69kutoka shilingi milioni 57.4 kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

(ii) Madaktari Bingwa watatu wameshapelekwakatika kituo hiki kati ya watano wanaohitajika, kwa maanaya Madaktari Bingwa wa Watoto, wawili na Daktari waMagonjwa ya Wanawake na Uzazi mmoja.

(iii) Katika mwaka wa fedha 2018/2019, kiasi chashilingi milioni 160 kimetengwa kwa ajili ya kuendeleza ujenziwa jengo la ghorofa moja ambalo lina wodi ya wanaume,wanawake na watoto.

(iv) Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kituokimetengewa asilimia 25 ya fedha za Mfuko wa Pamoja waWafadhili (Health Sector Basket Fund) ambayo ni sawa nashilingi milioni 357.73 ya mgao wa Manispaa ya Ubungoambayo ni shilingi bilioni 1.43. Fedha hizi ni kwa ajili ya utawalana ununuzi wa dawa na vifaa tiba.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia Bunge lako tukufu,napenda kuelekeza Halmashauri ya Ubungo kutenga eneolisilopungua ekari 25 litakalowezesha kuwepo katika eneomoja majengo yote ya msingi ya Hospitali ya Wilaya. Aidha,Serikali itaendelea kupeleka Madaktari Bingwa na kuboreshahuduma zaidi katika kituo hiki kadri bajeti itakavyokuwaikiruhusu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Joseph Selasini, swali lanyongeza.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. Mara nyingi Mawaziri wetu hapa Bungeniwamekuwa wakituambia kwamba ahadi ya Rais ni sheriana lazima itekelezwe. Sasa kupandisha hadhi Kituo cha Afya

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

cha Palestina kuwa Hospitali ni ahadi na agizo la MheshimiwaRais. Sasa ni kwa sababu gani badala ya Serikali kutekelezaahadi hii, inafanya maboresho?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Kituo cha Afyacha Tarakea katika Wilaya ya Rombo kinachukua wagonjwawengi sana kutokana na eneo kubwa na wagonjwa wenginekutoka nchi jirani ya Kenya, lakini hakina incinerator, hakinamortuary, vilevile kilikuwa hakina uzio lakini Mbungeakajitahidi kwa fedha za Mfuko wa Jimbo kujenga uzio.

Sasa je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kufika Rombokutembelea kituo kile ili tushauriane naye namna yakukiboresha kiweze kuhimili idadi kubwa ya wagonjwaambao wanakwenda kwenye kile kituo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu kwa maswali hayo.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaNaibu Spika, kama ambavyo nimejibu katika jibu langu lamsingi, Serikali tunakiri juu ya umuhimu wa Kituo cha Afyacha Sinza pale Palestina, lakini ni ukweli usiopingika kwambaili Kituo cha Afya kiwe Hospitali ya Wilaya kuna suala zima laeneo ambalo katika jibu langu la msingi nimemwambiakwamba tunahitaji ekari 25. Sasa ukienda katika kile Kituocha Afya cha Palestina, eneo hilo halipo na ndiyo maanakatika maboresho ambayo yanaendelea ni pamoja nakutenga shilingi milioni 160 ili kuweza kuwa na hadhi yakufanana na Kituo cha Afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli usiopingikakwamba tunapata changamoto katika Vituo vya Afya vilivyoMijini, kitu ambacho kinakosekana ni jina lipi tutumie? Kwasababu vinakuwa na hadhi zaidi ya Vituo vya Afya, lakinivinakuwa havijafikia kuwa Hospitali za Wilaya. Ndiyo maananimesema kwamba ni vizuri Manispaa wakatenga eneo kwaajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya. Kwa hiyo, kama Serikalituko tayari na wala hatupingani na kile ambacho

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

Mheshimiwa Rais alielekeza kwa wakati ule, lakinichangamoto ya ardhi ndiyo inayotusababisha tusemekwamba ni vizuri likatengwa eneo lingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili,Mheshimiwa Selasini anataka utayari wangu kwendakutazama Kituo cha Afya Tarakea. Naomba nimhakikishie,kama ambavyo nimefanya ziara kwenda Kituo cha Afya chaKiaseri kule, niko tayari kufika hata Tarakea kwa kadri mudaunavyokuwa umeruhusu.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, niwasihi kablasijaanza kuwaita kwa ajili ya maswali ya nyongeza, maswaliyawe mafupi. Ukiuliza marefu, unawanyima wenzio fursa yakuuliza maswali.

Mheshimiwa Flatei Massay, swali la nyongeza.

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto iliyopoUbungo inafanana kabisa na changamoto iliyopo Jimbo laMbulu Vijijini. Tuna kituo kimoja tu cha afya Jimbo zima; je,Serikali ina mpango gani sasa wa kutuongezea angalau kituokimoja ili katika huduma za afya jimboni, pakawa na hali yakuwasaidia wananchi?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu kwa swali hilo.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaNaibu Spika, changamoto iliyopo kwenye Kituo cha Afyakatika swali la msingi, ni suala la eneo, lakini kwake yeye eneosiyo tatizo kama ambavyo iko Sinza, Palestina pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba kwa dhatikabisa ya moyo wangu nimpongeze Mheshimiwa Flatei

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

Massay kwa jinsi ambavyo amekuwa akilipigania Jimbo lake,amehakikisha kwamba Halmashauri inajengwa lakini pia nimiongoni mwa maeneo ambayo yanakwenda kujengewaHospitali za Wilaya. Naomba nimhakikishie kwa dhati hiyo hiyoambayo Serikali imeonesha kuhakikisha kwamba tunajengaHospitali za Wilaya, ni azma yetu pia kuhakikisha kwambatunajenga Vituo vya Afya vya kutosha na kwa kadri bajetiitakavyokuwa imeruhusu hakika hatutasahau eneo la kwake.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Qulwi Qambalo, swali lanyongeza.

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Katika mwaka wa fedha unaokuja, Serikaliimetenga fedha za kujenga Hospitali za Wilaya kwenyemaeneo 67, lakini pia ni wazi zipo Wilaya nyingi ambazo badohazina Hospitali ya Wilaya ikiwemo Wilaya yangu ya Karatu.Ni lini sasa wananchi wa Karatu wategemee kujengewaHospitali ya Wilaya?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaNaibu Spika, kama ambavyo nimekuwa nikijibu hapa,kuanza na Hospitali za Wilaya 67 tafsiri yake ni kwambazikikamilika hizo tutakwenda kujenga nyingine. Ni azma yaSerikali inayoongozwa na CCM kuhakikisha kwamba Wilayazote ambazo hazina Hospitali za Wilaya baada ya kumalizahizi 67 tutakwenda hatua nyingine ya kwenda kuzijengea.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba MheshimiwaMbunge avute subira, bajeti ndiyo imepita, tumwombeMwenyezi Mungu makusanyo yetu yaende vizuri, tukimaliza67 tutakwenda hatua ya pili.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Daimu Mpakate, swali lanyongeza.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante.

Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne, mwaka 2014alipotembelea Jimbo la Tunduru Kusini alitembelea katikaKijiji cha Mbesa ambapo kuna Hospitali ya Mission pale.Hospitali ile inatoa huduma kubwa kuliko Hospitali ya Wilayana Mheshimiwa Rais aliahidi kuipandisha daraja hospitali ilekuwa Hospitali Teule. Je, ni lini hospitali ile itapewa hadhi yakuwa Hospitali Teule ili iweze kuendelea kutoa huduma vizuri?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaNaibu Spika, samahani, sikusikia vizuri hospitali inaitwaje,naomba arudie nisikie.

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Naibu Spika, niHospitali ya Mission ya Mbesa.

NAIBU SPIKA: Huyo ni Mbunge wa Tunduru, kwa hiyo,itakuwa iko Tunduru hiyo.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaNaibu Spika, kama ambavyo nimekuwa nikijibu na ambavyonimejibu leo, ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba maeneoambayo hakuna Hospitali za Wilaya zinakwenda kujengwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ni azma ya Serikali kwakushirikiana na Taasisi za Dini na Mashirika mengine paleambapo sasa hivi hatuna Hospitali Teule, tunatumia zileambazo zipo ili zifanye kazi kwa muda tu kama Hospitali Teule.Ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba tunakuwa nahospitali zetu za Serikali na zile za Mashirika ya Dini paleambapo tutakuwa tumejenga za Serikali wabakiwakiendesha kwao na sisi Serikali tuwe na za kwetu tukifanyakazi kama Serikali. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea.Mheshimiwa Waziri wa Afya, majibu ya nyongeza.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanzanamshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka tu kumshauriMheshimiwa Mpakate, ili hospitali binafsi au ya Shirika la Diniifanywe kuwa DDH sasa hivi tumeshusha madaraka hayakwenye Halmashauri husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Halmashauri ndiyoitafanya majadiliano na makubaliano na hospitali ile natumeelekeza kuwe na mkataba wa muda maalum, kwambaHalmashauri ya Tunduru inaamua kuingia makubaliano nahospitali hii i l i iwe Hospitali Teule ya Halmashauri namkishakubaliana ndiyo mnaleta taarifa hizi TAMISEMI naWizara ya Afya. Kwa hiyo, tutazitambua rasmi sasa kuwa niHospitali Teule ya Halmashauri husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, niseme tunatokakwenye Hospitali za Wilaya, tunakwenda kwenye Hospitaliya Halmashauri. Kwa hiyo, sasa hivi kila Halmashauri itakuwana Hospitali badala ya kuwa Hospitali ya Wilaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kama kuna Wilayazina Halmashauri mbili, zote zinapaswa kuwa na Hospitaliya Halmashauri ambayo ni ngazi ya kwanza ya Hospitali.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Ofisi ya Rais, Muungano na Mazingira, MheshimiwaMwantum Dau Haji, Mbunge wa Viti Maalum sasa aulize swalilake.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

Na. 448

Athari za Mabadiliko ya Tabianchi

MHE. MWATUM DAU HAJI aliuliza:-

Kilimo cha Tanzania hutegemea mvua za msimuambazo kwa kiasi kikubwa zimeathiriwa na mabadiliko yatabianchi na hivyo kuathiri shughuli za uzalishaji.

Je, Serikali ina mpango gani wa kukabiliana na athariza mabadiliko ya tabianchi?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,(MUUNGANO NA MAZINGIRA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira),napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mwatum Dau Haji,Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, i l i kukabiliana namabadiliko ya tabianchi katika Sekta ya Kilimo, Ofisi yaMakamu wa Rais iliandaa Mpango wa Taifa wa KuhimiliMabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 2007 na Mkakati wa Taifawa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 2012katika sekta mbalimbali ikiwemo na sekta ya kilimo. Mipangohii kwa sekta ya kilimo imejikita katika kuendeleza kilimo chaumwagiliaji ikiwa ni pamoja na kutumia teknolojiazinazopunguza upotevu wa maji ili kuepuka kilimo chakutegemea mvua.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, mipango hiiinaelezea namna ya kubadili vipindi vya upandaji mazao yamisimu ili kuendana na mabadiliko ya misimu ikiwa ni pamojana kupanda mazao na mbegu zinazohimili ukame,kuboresha mbinu za kudhibiti wadudu waharibifu wa mazaona kuweka mifumo mbadala ya kilimo ili kuongeza uzalishaji.Aidha, Ofisi ya Makamu wa Rais ipo katika mchakato wakukamilisha kuandaa mpango endelevu wa Kitaifa wa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (National Adaptation Plans).Mpango huu utakapokamilika utawezesha nchi kuwa namipango itakayowezesha kukabiliana na mabadiliko yatabianchi katika sekta muhimu ikiwemo sekta ya kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Makamu wa Raisimekuwa inashirikiana na Wizara ya Kilimo pamoja na Wizaraya Maji na Umwagiliaji katika kuandaa mipango yakukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika Sekta ya Kilimo.Mipango iliyoandaliwa ni pamoja na:-

Moja, Mpango Mahususi wa Sekta ya Kilimo katikaKukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Tanzania AgricultureClimate Resilience Plan); pili, Mpango wa Kitaifa wa KilimoRafiki cha Mabadiliko ya Tabianchi (National Climate SmartAgriculture) na programu mbalimbali za uendelezaji wakilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika utekelezaji wamipango na programu hizi katika sekta ya kilimo, suala lakuhimili mabadiliko ya tabianchi katika kilimo imezingatiwahasa kwa kusisitiza uwekezaji katika miundombinu ya kilimo(suala la kuongeza kilimo cha umwagiliaji).

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwantum Dau Haji swalila nyongeza.

MHE. MWATUM DAU HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. Kwanza namshukuru Mheshimiwa Waziri kwamajibu yake mazuri aliyoyatoa yenye kila aina ya vinjonjo.Napenda kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa programu hizikatika sekta ya kilimo linahusiana na suala la kuhimilimabadiliko ya tabianchi; je, Serikali ina mkakati gani kutoaelimu kwa wakulima ili waende sambamba na mabadilikoya tabianchi? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi yaMakamu wa Rais (Muungano na Mazingira) majibu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,(MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza kabisa nampongeza Mheshimiwa Mwatum ambayeamekuwa akifuatilia sana masuala ya mazingira na hasamambo haya ya mabadiliko ya tabianchi. Namhakikishiakwamba pamoja na mipango hii ambayo Serikali tumekuwatukiifanya, hata kule Unguja na Pemba tunashirikiana naTaasisi za Kimataifa USAID pamoja na FAO katika miradi yakilimo ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa kutoaelimu, nimhakikishie Mheshimiwa Mwantum tayari mpakasasa Serikali ilishatoa mwongozo pamoja na mafunzo kwawatu wapatao 192 wakiwemo Maafisa Kilimo, Maafisa Uvuvi,Maafisa Mifugo pamoja na Maafisa Mipango kutoka kwenyeHalmashauri za Wilaya na kuwaelekeza kwamba katikamipango wanayoipanga Wilayani pamoja na bajeti wawezekushirikisha mipango hiyo ya kilimo himilivu cha mabadilikoya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, elimu hii tayaritulishaipeleka kwa wananchi na bado tunaendelea katikampango huu tuliosema endelevu wa kuhimili mabadiliko yatabianchi, ni element ambayo pia inahusishwa. Pamoja nakwamba Mheshimiwa Rais alizindua juzi hapa ASDP II, vilevilekuna element ya kutoa mafunzo ya kilimo himilivu kutokanana mabadiliko ya tabianchi.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nawaonammesimama, lakini niwakumbushe kuuliza maswali yenyeuhusiano na swali la msingi. Mnaipa Serikali wakati mgumumnapouliza maswali yasiyohusiana kabisa na ninyi mnaonana mnataka majibu yaliyokamilika. Mheshimiwa AlexGashaza swali la nyongeza.

MHE. ALEX R. GASHAZA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali.

Mheshimiwa Naibu Spika, mapema mwaka 2017niliwasilisha andiko la mradi ujulikanao kama Commitment

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

Bush Fire Management and Livehood Improvement kwa lengola kudhibiti uchomaji moto ovyo. Ni lini Wizara yenyedhamana itaweza kuwezesha mradi huu kwa kutoa fedhaili tuweze kutekeleza kikamilifu kwa kuanzisha zao ambaloni rafiki na mazingira lakini pia na ufugaji wa nyuki? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi yaMakamu wa Rais (Muungano na Mazingira) majibu.

NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,(MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Naibu Spika,mapema katika Mkutano uliopita Mheshimiwa Gashazaaliuliza swali la nyongeza kuhusiana na mradi wake huu.

Napenda nimhakikishie kwamba sasa hivi Ofisi yaMakamu wa Rais inaandaa maandiko mbalimbali kwa ajiliya kuomba fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tunahamasishaHalmashauri za Wilaya waweze kuandika maandiko ambayowatayaleta Ofisi ya Makamu wa Rais ili tuweze kuwatafutiafedha katika kutekeleza miradi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie MheshimiwaGashaza, andiko lake tumelipitia ni muhimu sana. Pia aliwezakuwahusisha wananchi wa Jimboni kwake kupitia michezowakiwa na kauli mbiu ya kwamba mazingira ni uchumi iliwaweze kucheza ligi i le na kauli mbiu hiyo wawezekuhakikisha kwamba wanajihusisha na ufugaji wa nyukipamoja na kilimo ili wasiendelee kuchoma misitu ambayoinaendeleza uharibu wa mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishieMheshimiwa Gashaza kwamba hata hiyo ligi yake, baadaya kupata fedha mimi mwenyewe nitaenda kumsaidiakuizindua ili iwe kichocheo kwa nchi nzima ili wananchiwengine nao wafanye hivyo. Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Yussuf swali la nyongeza.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi. Nasikitika kwamba MheshimiwaNaibu Waziri hajajibu hili swali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuathirika kwa kilimo nimatokeo ya athari za tabianchi. Tuambie Serikali ina mikakatigani ya kukabiliana na athari hizi? Maziwa yanakauka, mitoinakauka, misitu inapotea. Mna mkakati gani mliouchukuaau ndiyo mko kwenye mipango tu? Ndiyo jibu tunalolitakakutoka kwako. Nakushukuru.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi yaMakamu wa Rais, (Muungano na Mazingira), majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,(MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Naibu Spika,kama nilivyojibu kwenye swali la msingi ambalo MheshimiwaMwantum Dau Haji alitaka kujua Serikali tuna mipango namikakati gani; nimeeleza kwamba mkakati wa kwanzatulionao tuliuandaa mwaka 2007 ambao unahusu uhimilivukatika mabadiliko ya tabianchi kwenye suala la kilimo.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nimejibu hapa kwambamwaka 2012 tuliandaa mpango mwingine wa mabadilikoya tabianchi tofauti na ule wa mwanzo. Vilevile nimejibuhapa kwamba mpaka sasa Serikali kupitia Ofisi ya Makamuwa Rais na kupitia wataalam tunaandaa na tunakaribiakumaliza kupata sasa mpango mkakati endelevu wakukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwenye suala lakilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, siyo kwambamikakati haipo, nimeieleza hapa. Pia nimeelezea hapakwamba hata juzi Mheshimiwa Rais amezindua ASDP Awamuya Pili ambamo ndani mwake pia kuna mikakati mingi sanaimezungumziwa. Pia mikakati na mwongozo niliousemaambao tumepeleka kwenye Halmashauri ambapo MaafisaMipango wanatakiwa kuweka kwenye bajeti zao,tumeelezea kuhusu utafiti wa mbegu ambayo inahimili

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

kwenye ukame pamoja na kilimo cha umwagiliaji naumwagiliaji wa matone.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mikakati hii ipo,Mheshimiwa Yussuf mtani wangu wa kisiasa, naomba ueleweSerikali ya Mheshimiwa Dkt. Magufuli ni Serikali makini, niSerikali ambayo inaongoza kwa kuwa na mikakati, tenamikakati ambayo inatekelezeka. Ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Sware Semesi, swalifupi.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru kwa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Makamu wa Raisimekuwa ikipokea fedha mbalimbali kutoka kwa wafadhiliili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kila mwaka. Miakamiwili iliyopita walikabidhiwa takribani shilingi bilioni 224 kwaajili ya shughuli hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Naibu Wazirianaongelea kuhusu mikakati; je, kuna utekelezeji wowotewa mikakati hii ya kuhusisha mabadiliko ya tabianchi nakuboresha kilimo chetu kwa kutumia hizi fedha za wafadhiliambazo zinagusa hususan mabadiliko ya tabianchi? Ahsante.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi yaMakamu wa Rais, (Muungano na Mazingira) majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,(MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza, namshukuru Mheshimiwa Dkt. Sware nimwanamazingira na ni kweli anafahamu kabisa kwamba Ofisiya Makamu wa Rais tumekuwa tukipata fedha ambazozinasaidia miradi mbalimbali ya kuhimili mabadiliko yatabianchi. Amesema sasa mbali na mikakati, fedha hizinamna gani tunazi-link.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimhakikishiekwamba mojawapo ya miradi ambayo tumeihusianisha nahiki kilimo kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi,ukienda kule Rufiji tayari katika Halmashauri ya Wilaya ya Rufijitulikuwa tunatekeleza mradi ukiwa ni pamoja na kupandamikoko na kuwawezesha wananchi wahimili mabadiliko yatabianchi kwa kilimo cha mboga pamoja na matunda.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, ukiendakule Pemba Kisiwa Panza mbali na kujenga ukuta, vileviletulikuwa tunawasaidia wananchi waweze kuhimili mabadilikoya tabianchi kwa kilimo cha mboga na matunda.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hayo sasa hivituna Mikoa kama Tabora, Singida, Kagera, Morogoro, Tangaambako tayari tunatekeleza miradi mbalimbali ya kutumiafedha hizi ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wakulimawa namna wanavyoweza kuhimili mabadiliko ya tabianchi,ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba wanatumia zilefedha katika kilimo cha mboga pamoja na matunda.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo ni pamoja pia na Bondela Kihansi kule Kilombero, vilevile tumeweza kutoa fedha iliwananchi wahimili athari za mabadiliko ya tabianchi kwakilimo katika lile mbonde.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishieMheshimiwa Sware kwamba siyo mikakati tu ambayo Serikaliinaishia, ni pamoja na fedha hizi. Tumetoa fedha nyingineshilingi milioni 200 sasa ambazo zinapeleka maji kuleShinyanga na yale maji yatatumika pia katika kusaidiaumwagiliaji kwenye kilimo. Hiyo ni katika kuhimili mabadilikoya tabianchi. Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaendeleana Wizara ya Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. JasmineTisekwa Bunga, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swalilake.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

Na. 449

Kujenga Hoteli Kubwa za Kitalii - Mikumi

MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA aliuliza:-

Mkoa wa Morogoro una vivutio vingi sana vya utaliiambavyo vikitumika vizuri vinaweza kuchangia pato la Taifana wananchi kwa ujumla; moja kati ya vivutio hivyo ni pamojana Mbunga za Hifadhi ya Wanyama Mikumi ambayoinaongeza mapato mengi, lakini mbuga hizo hazina hotelinzuri za kitalii zenye kukidhi viwango vya kimataifa, kutokanana kuungua kwa Hoteli ya Kitalii ya Mikumi.

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga hoteli kubwaza kitalii ndani ya Mbuga ya Mikumi ili kuvutia watalii wengi?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMaliasili na Utalii naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt.Jasmine Tisekwa Bunga, Mbunge wa Viti Maalum, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa kuwa Mkoawa Morogoro una vivutio vingi vya utalii ikiwemo Hifadhi yaMikumi. Baada ya kuungua kwa lodge ya Mikumi, Serikalikupitia TANAPA imeendelea na juhudi mbalimbali zakuhamasisha uwekezaji katika hifadhi hiyo, ambao fursa zauwekezaji hususan huduma za malazi zimekuwa zikitangazwa.Aidha, mwekezaji wa kuifufua lodge ya Mikumi alishapatikanana kazi ya ukarabati inaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, watalii wanaotembeleaHifadhi ya Mikumi kwa sasa wanatumia kambi tatu zamahema (tented camps) zilizoko ndani ya hifadhi, lodge nahoteli kumi zilizopo Mikumi Mjini. Wizara kupitia TANAPAimetenga maeneo saba kwa ajili ya uwekezaji wa hoteli nalodge ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi zenye hadhi na

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

viwango vya kimataifa ili kuleta watalii wengi na kuongezamapato.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuchocheamaendeleo ya sekta ya utalii katika Ukanda wa Kusini kwaujumla, Serikali ilizindua rasmi mradi wa kuendeleza utaliiUkanda wa Kusini wa Tanzania ujulikanao kama REGROWtarehe 12 Februari, 2018 Mjini Iringa. Lengo la mradi huu nikuwezesha maendeleo ya utali i kwa kuboreshamiundombinu, kuhifadhi maliasili na mazingira katika hifadhiya Ukanda wa Kusini ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo,napenda kutumia fursa hii kumwomba Mheshimiwa Mbunge,uongozi pamoja na wakazi wa Mikumi kwa ujumla kutengamaeneo ya uwekezaji wa huduma za malazi na utalii ilikunufaika na biashara ya utalii nje ya Hifadhi ya Taifa yaMikumi. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Jasmine TisekwaBunga, swali la nyongeza.

MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kunipa nafasi ya swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli majibu yaMheshimiwa Naibu Waziri bado kidogo ayajaniridhisha kwasababu mimi nilitembelea Mikumi pale 2016 na majibuniliyopewa ni haya haya kwamba mwekezaji amepatikanana ukarabati unaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa namwombaMheshimiwa Naibu Waziri anihakikishie hapa huu ukarabatiutamalizika lini ili tuweze kupata mapato ya uhakikika?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili ni kwambambuga hii ya Mikumi ipo katikati ya barabara ambayoinaenda mikoani na nje ya Tanzania. Kulikuwa na mpangowa kuanzisha road toll ili kuweza kupata mapato zaidi katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

mbuga hii ambayo inakumbana na changamoto nyingi,miundombinu na hata magari ya kuzuia ujangili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kujua, ni lini Serikaliitaanzisha ushuru huu kwa sababu mchakato ulishaanza, sasakuna kigugumizi gani? Hii itasaidia mbuga hii iweze kupatamapato na kukabiliana na changamoto ili iweze kuboreshana kuongeza mapato zaidi? Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Maliasili naUtalii, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, kwanza naomba nichukue nafasi hiikumpongeza kwa jinsi ambavyo amekuwa akifuatilia na nikweli kabisa kwamba mwaka 2016 alifika pale kuangalia ninamna gani hoteli zinaweza kuongezeka katika lile eneo ilikukabiliana na hii changamoto ya uhaba wa vyumba vyawatalii kulala pale Mikumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishiekwamba ni kweli kabisa kwamba yule mwekezaji alipatikanasiku nyingi toka mwaka 2016, lakini baada ya kupatikana,kwa mujibu wa taratibu za uwekezaji, lazima kwanza EIAifanyike ili aweze kuendelea na huo mradi. Huo mradi baadaya kufanya hiyo tathimini ya mazingira, imekamilika mweziNovemba, 2017. Baada ya kukamilika, mwezi Februari, 2018ndipo mwekezaji amekabidhiwa rasmi lile eneo.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kukabidhiwa lileeneo, sasa hivi ametoa mpango kazi, na mimi mwenyewenilienda pale nikaona, sasa hoteli yenyewe inategemeakukamilika mwezi Novemba mwaka ujao yaani mwaka 2019.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la kuwekaroad toll kule Mikumi, ni kweli hili suala limekuwepo natumekuwa tukiliangalia ndani ya Serikali kuona kama kwelilinaweza likatusaidia na kama linaweza likafanya kazi. Badotuko kwenye hatua za majadiliano na kuona namna bora

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

ya kuweza kulitekeleza hilo ili kusudi tusilete usumbufu kwawananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, wazo la MheshimiwaMbunge ni zuri na ninaomba niseme kwamba Serikali badoinaendelea kulifanyia kazi.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbarouk, swali lanyongeza.

MHE. MBAROUK SALIM ALI: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu nyingi ambazo zinavivutio vya utalii utakuta miundombinu yake ni mibovu sana.Hii ndiyo sababu kubwa ambayo inasababisha wawekezajiwarudi nyuma na washindwe kuwekeza katika maeneoambayo yana vivutio na hivyo kushusha utalii.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwambawanaboresha miundombinu katika maeneo hayo ya utalii?Nashukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kabisa kumekuwa na maeneo ya namnahiyo na bado kumekuwa na changamoto ya uwekezaji. Kazikubwa tunayoifanya kama Serikali ni kuhakikisha kwambatunaboresha kwanza mazingira ya uwekezaji nakuwahamasisha wawekezaji ili kusudi waweze kuwekezakatika maeneo yote hayo na yaweze kuchangia katikashughuli mbalimbali za utalii.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niseme tukwamba tutakaa na Mheshimiwa Mbunge ili tuone namnagani tunaweza tukafanya hiyo kazi ili kusudi wananchi waeneo lile waweze kufaidika na matunda ya hiyo kazi.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

NAIBU SIPKA: Mheshimiwa Janet Mbene, swali lanyongeza.

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ya utalii ni sektaambayo ina fursa nyingi sana na kubwa za kulisaidia Taifakimapato. Suala la Mikumi kama ambavyo limejibiwa sasahivi, tunapoteza fursa kubwa sana. Mikumi ilikuwa ni kivutiokatika vivutio vya mwanzo kabisa vya utalii nchi hii. Ilikuwainatoa fursa kubwa sana kwa utalii wa ndani hasa kwavijana, wanafunzi na taasisi mbalimbali wanaotaka kwendakuangalia mambo ya utalii. Jinsi ilivyo sasa hivi imekwamakwa muda mrefu na hii sawa na sehemu nyingine nyingi tu.

Je, Serikali sasa hivi iko tayari kuja na mkakati mahususiunaohakikisha kuwa sehemu zote za kitalii zinaendelezwa kwakutumia sekta binafsi? Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasili naUtalii, majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kabisa kwamba Mikumi ilikuwa ni mojaya hifadhi ambayo ilikuwa inatoa mchango mkubwa sanakatika pato la Taifa, lakini kumekuwa na changamoto ya hivikaribuni kwamba mchango ule kidogo umeshuka sanakutokana na mambo mbalimbali. Ndiyo maana kwakutambua hilo, Serikali tumekuja na mradi mkubwa wakuboresha utalii Kusini. Katika mradi huo, moja ya maeneoambayo yamepewa uzito ni pamoja na hifadhi ya Mikumi,kwa sababu ule mradi wa kukuza utali i wa Kusini,tunahudumia Selous upande wa Kaskazini, Udzungwa, Mikumina Ruaha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, katika huo mraditunaboresha miundombinu yote, tutatangaza ipasavyokuhakikisha kwamba tunawavutia watalii mbalimbali wandani na nje ya nchi ili waweze kuingiza mapato na Serikali

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

iweze kupata mapato ya kutosha na kuweza kuendelezanchi yetu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Felister Bura, swali lanyongeza.

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza Swali la nyongeza.Kama ilivyo Morogoro kwamba kuna vivutio kwa wataliindivyo ilivyo kwa Mkoa wa Dodoma ambako WilayaniKondoa kuna michoro ambayo haipo Tanzania na michoroile iko katika mapango ya Kolo na Pahi, lakini vivutio vilehavijawahi kutangazwa na Serikali.

Je, Serikali ina mkakati gani? Pamoja na Wabungewa Kondoa kuhangaika kuleta watalii, lakini badohaitoshelezi kama Serikali haitatia mkazo kutangaza vilevivutio.

Je ni lini sasa au Serikali ina mkakati gani kutangazamichoro ile ya mapango ya Kolo, Pahi na maeneo menginekatika Wilaya ya Kondoa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii,naomba nichukue nafasi hii kwanza nimpongeze sanaMheshimiwa Felister Bura na Wabunge wote wa Mkoa waDodoma kwa jinis ambavyo wamekuwa wakilifanyia kazi hilisuala. Hivi sasa tunajua kabisa kwamba Dadoma ndiyoMakao Makuu ya nchi na kweli lazima tuziimarishe hizi hifadhizetu na maeneo maengine ya Utalii ili kuweza kuvutia watumbalimbali kuja kuwekeza katika Mkoa huu wa Dodoma.

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu ambacho tunategemeakukifanya katika kutangaza yale maeneo ya michoro yaMiambani kule Kondoa; yaani Kolo na pale Pahi; jitihadaambazo tunaweka kuanzia tarehe 1 Julai, 2018 tunategemea

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

kuanzisha studio ya kutangaza utalii yaani kutangaza vivutiovyote nchi nzima. Hiyo ni pamoja na hilo eneo, tutalitangazavizuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, tunategemeakuanzisha channel maalum kupitia TBC ambayo itakuwainahusiana na masuala ya utalii. Kwa kutumia hilo basi,tunaamini kwamba basi matangazo, wananchi wengi wandani na wa nje wataweza kupata fursa ya kuweza kujuavivutio vyote tulivyonavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, la tatu, tunategemeakutumia viongozi mbalimbali mashuhuri pamoja na mambomengine mengi kutangaza ndani ya nchi na nje ya nchi kwakutumia mitandao ya facebook, twitter na mambomengineyo ili kusudi vivutio vyote vieleweke kwa watanzanialakini kwa watu wote walioko nchi za nje waweze kuijuaTanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitumie nafasi hiiniseme kwamba sasa hivi Tanzania tumepata taarifakwamba sasa imekuwa ni nchi inayoongoza kwa safari Afrikakupitia Serengeti. Kwa kweli huu ni ufahari mkubwa naDodoma nayo itafaidika sana na haya mambo ambayotunakwenda kuyafanya.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ally Keissy, swali lanyongeza.

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa naibu Spika,ahsante sana. Kuhusu Hoteli ya Kitalii ya Mikumi: Je,Mheshimiwa Naibu Waziri anafahamu kwamba mwekezajiwa kwanza alifanya hujuma makusudi baada ya kuchukuashilingi bilioni nne na mpaka leo akaichoma hoteli ile?

Je, Serikali imechukua hatua gani kwa yule mwekezajiwa kwanza? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii, majibu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, kwa kweli kama Serikali hatuna taarifa kamakweli ile ilichomwa kama hujuma, lakini tunachojua nikwamba ilipata janga la moto mwaka 2009 na ikaunguayote. Yule aliyekuwa amekabidhiwa baada ya hapo,alishindwa kuendeleza. Baada ya kuona ameshindwakuendeleza, ndiyo maana Serikali tukaamua tena kuchukuahatua kuhakikisha kwamba tunamtafuta mwekezajimwingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwekezaji huyu sasaliyepatikana amekuja na michoro mizuri sana na design nzurisana ambazo ninazo hata baaadaye Mheshimiwa Keissynaweza nikamwonyesha hapa jinsi i l ivyo ambapotunategemea itakapofika mwaka 2019 hoteli yenyeweitakuwaje? Kwa hiyo hilo tunalo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hilo la kusema kwambaalifanya hujuma, hizo taarifa hatunazo kama Serikali.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana swali la Mheshimiwa Ester Alexander Mahawe, Mbungewa Viti Maalum, swali lake litaulizwa kwa niaba naMheshimiwa Innocent Bashungwa.

Na. 450

Kuboresha Miundombinu katikaHifadhi za Taifa

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA (K.n.y. MHE. ESTER A.MAHAWE) aliuliza:-

Sekta ya utalii inachangia pato kubwa la fedha zakigeni katika nchi yetu.

Je, ni lini Serikali itatengeneza barabara ya Serengetiambayo ni mbovu kiasi cha kufanya watalii kukataa kupitahuko?

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMaliasili na Utalii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa EsterAlexander Mahawe, Mbunge wa Viti Maalum kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa naibu Spika, Hifadhi ya Taifa yaKilimanjaro na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ndiyozinachangia zaidi katika mapato ya fedha za kigenizitokanazo na shunguli za utalii hapa nchini. Hifadhi ya Taifaya Serengeti ina ukubwa wa kilometa za mraba 14,763 nabarabara zenye urefu wa kilometa 3,155. Barabara hizo nipamoja na barabara kuu zinazounganisha Hifadhi na Mikoaya Arusha, Mara na Simiyu. Barabara nyingine ni zile zamizunguko ya utalii na nyingine ni za utawala na doria.Barabara zote hizo ni za kiwango cha changarawe.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara zenye matumizimakubwa ni zile kuanzia mpaka unaotenganisha Hifadhi yaTaifa ya Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongorohadi Kituo cha Seronera yenye urefu wa kilometa 60 nakilometa 30 kutoka Seronera hadi lango na Ikoma. Barabarahizi wakati wa msimu wa watalii wengi zinatumiwa namagari zaidi ya 300 kwa siku. Kutokana na matumizimakubwa kiasi hicho, barabara hiyo yenye kiwango chachangarawe uchakavu wake huongezeka kwa kasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuanzia mwezi Agosti, 2016hifadhi inaendelea kuelekeza nguvu za ziada kuhudumiabarabara hizi wakati wote wa msimu wa watalii.

Mheshimiwa Naibu Spika, juhudi zinazoendeleazinahusisha kufanya matengenezo ya barabara hizo kwakutumia nyenzo mbalimbali ikiwemo mitambo miwili yabarabara yaani motor graders pamoja na malori. Ili kupataufumbuzi wa muda mrefu kukabiliana na changamoto hiyoya ubovu wa barabara, Shirika la Hifadhi za Taifa linaendeleakutafuta teknolojia mbadala il i kuwa na barabarazitakazodumu bila kuathiri ikolojia ya wanyamapori.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Innocent Bashungwa, swalila nyongeza.

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: Mheshimiwa NaibuSpika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Wazirinina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto zamiundombinu katika hifadhi ya Serengeti zinafanana nachangamoto za Hifadhi mpya ya Kimisi na Burigi.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuweka miundombinukatika hifadhi mpya ya Kimisi na Burigi ili hifadhi hii iwezekuchangia mapato katika Halmashauri zetu za Wilaya zilizopokatika Mkoa wa Kagera pamoja na kuchangia pato la Taifa?

Swali la pil i, Mheshimiwa Waziri yupo tayarikuambatana na mimi kwenda kwenye Kata za Bweranyange,Rugu, Nyakasimbi, Nyakabanga na Nyakakika ili kutatuamigogoro ya mipaka kati ya vijiji kwenye Kata hizi na Hifadhi?Ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, kwanza nichukue nafasi hii kuwapongeza sanaWabunge wa Mkoa wa Kagera kwa jinsi ambavyowameshirikiana na Serikali kuhakikisha kwamba maeneo yaleyanapandishwa hadhi na sasa Burigi na Kimisi yatakuwa nimojawapo ya Hifadhi za Taifa. Kwa hiyo, itakuwa ni hadhi yajuu kabisa ya uhifadhi katika nchi yetu. Kwa kweli hongerenisana.

Mheshimiwa Spika, sasa baada ya kupandisha hadhimaeneo hayo, hatua inayofuata sasa ni kuhakikisha kwambamiundombinu ya maeneo yote yale inaimarishwa, barabarazipitike wakati wote ili kusudi watalii waweze kutembeleakatika yale maeneo na Serikali iweze kupata fedha nyingizinazotokana na mapato ya utalii. Kwa hiyo, hilo litafanyika.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

Swali la pili, kuhusu kuambatana naye kwenda katikamaeneo hayo, naomba nimhakikishie tu kwamba marabaada ya Mkutano huu wa Bunge tutaambatana pamoja,kwa sababu tunataka kwenda kuangalia sasa baada yakupandisha hadhi mapori yetu yote yale matano, tuone je,nini kinatakiwa kufanyika? Tufanyeje kuhakikisha kwambautalii sasa unakua katika ile Kanda ya Magharibi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli hilo lote,tutalifanya vizuri kabisa na ninaomba tushirikiane ili tuwezekufanyakazi vizuri zaidi.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Abdallah Bulembo, swalila nyongeza.

MHE. ABDALLAH M. BULEMBO: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana.

Kutokana na swali la msingi la ubovu wa barabaraya Serengeti, Wizara ya Maliasili inaniambiaje; kwa sababubarabara zimekuwa mbovu, Hoteli ya Seronera, Lobo,Ngorongoro na Lake Manyara zilikuwa ni hoteli katika nchihii katika Hifadhi ya Serengeti? Leo hii watalii wakienda,wanabebewa maji kwenye ndoo. Wizara inayajua hayo?Inazirudisha lini hoteli hizi Serikalini? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kabisa kwamba tulikuwa na hoteliambazo zilikuwa zinamilikiwa na Serikali katika miaka yanyuma na hoteli hizi nyingi zilibinafsishwa. Kati ya hoteli 17ambazo zilikuwa zimebinafsishwa ilionekana karibu hoteli 11zilikuwa hazifanyi vizuri ikiwemo hizi hoteli chache ambazoMheshimiwa Mbunge amezitaja.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali tumeliona hilo,tumeanza kufuatilia kupitia mikataba ile ambayo walipewaili kuhakikisha kwamba kama tumeona kwamba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

hawakufanya yale waliyostahili kuyafanya na uwekezajiwaliotakiwa kuufanya, Serikali iweze kuzichukua hizo hotelina kuwapa wawekezaji wengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba baadhi ya hoteli sasa hivizimechukua hatua, zinaboresha huduma zao. Hili analolisemala maji, kwa kweli sasa litaendelea kupungua hasa baadaya kuanza kutekeleza miradi mbalimbali ya kuhakikisha majiyanakuwepo katika maeneo hayo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Aida Khenani, swali lanyongeza.

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Katika Mkoa wetu wa Rukwa tumejaaliwa kuwana maporomoko ya Kalambo ambayo kama Mkoa sisitumejipanga.

Sasa napenda kujua katika Wizara ya Maliasili na Utaliimmejipangaje katika kutengeneza mazingira rafiki ili kuwezakuwavutia watalii?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kabisa kwamba katika Mkoa wa Rukwatunalo eneo lile la maporomoko ya Kalambo ambayo nimaporomoko ya aina yake ambayo tena ni urithi wa dunia.Kwa kweli lile eneo ni zuri sana. Baada ya kuona hivyo, mimimwenyewe nimefika pale kuangalia mazingira yalivyo,tumechukua hatua ya kuanza kujenga ngazi kubwa ambayoinatoka kule juu kushuka kule chini ambayo ni mita karibu230. Tunatarajia lile daraja litasaidia sana katika kuboreshana kuvutia watalii kuweza kutembelea yale maporomoko.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua ya pili, tumewaagizaWakala wa Misitu Tanzania (TFS) kuhakikisha kwambawanawekeza katika lile eneo; wanaweka hoteli ambayo

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

itakuwa ndiyo kivutio kizuri cha kuwavutia watalii katika lileeneo kusudi waweze kutumia muda mrefu wa kukaa katikalile eneo. Ni tofauti na sasa hivi ambapo unakuta kwambawenzetu wa Zambia wameweka hoteli upande wao, lakiniupande wetu huduma hizi zimekuwa hazipo. Hivyotumekuwa tukikosa watalii. Nina imani baada ya kuchukuahizi hatua, sasa watalii wataongezeka sana kwa upande waTanzania kwa sababu ndiyo sehemu pakee unayowezaukaiona Kalambo vizuri kuliko maeneo mengine.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Richard Mbogo, swali lanyongeza.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa nafasi. Changamoto zilizopo maeneo yaSerengeti na kwingine, zinafanana kabisa na Mbuga yetuya Katavi ambayo inakosa watalii kutokana na miundombinumibovu.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuboreshamiundombinu ndani ya Mbuga ya Katavi ili kuvutia watalii?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kabisa kwamba tunayo hifadhi kubwaya Katavi ambayo ina wanyama wa kila aina.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa Setikali imechukuahatua mbalimbali za kuhakikisha kwamba kwanzatunaboresha miundombinu iliyopo ndani ya ile hifadhi ilituweze kuwavutia watalii wengi kutoka maeneo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua nyingine ni kwasababu ule uwanja wa Ndege wa Katavi umekuwa mzurikabisa na tunaamini katika hizi jitihada ambazo Serikaliimechukua za kuongeza ndege, basi safari za ndege zikianzakutumia uwanja ule wa Katavi basi ina maana wataliiwataongezeka sana katika lile eneo na hivyo miundombinu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

ikiwa inapitika, watalii wengi sana wataweza kuvutiwa nakutembelea katika ile mbuga ya Katavi.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana swali la Mheshimiwa Marwa Ryoba Chacha, Mbunge waSerengeti.

Na. 451

Ukatili Wanaofanyiwa Wananchi WanaouzungukaMbuga ya Serengeti

MHE. MARWA R. CHACHA aliuliza:-

Kumekuwepo na tabia ya askari wa SENAPAkuwakamata wananchi ndani ya hifadhi na wakati mwinginewasipouawa huwapeleka mbali na Mahakama za Wilayaya Serengeti.

(a) Je, ni l ini vitendo vya mauaji ya watuwanaozunguka Hifadhi ya Serengeti vitakoma?

(b) Je, ni lini askari wa SENAPA wataacha kuwapelekawatuhumiwa waliokamatwa ndani ya hifadhi nje yaMahakama za Wilaya?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMaliasili na Utalii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa MarwaRyoba Chacha, Mbunge wa Serengeti, lenye sehemu (a) na(b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Askari wa Hifadhi ya Taifaya Serengeti wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali iliyopo. Ni kweli kwambabaadhi ya wananchi wamekuwa wakikamatwa na kufanyashughuli au kuingia kwenye hifadhi bila ya kufuata taratibuzilizopo. Wengi wamekuwa wakijihusisha na ujangili ndaniya hifadhi. Kwa msingi huo, Askari wa Hifadhi huwakamatawatuhumiwa wote na kuwafikisha katika Jeshi la Polisi na

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

hatimaye Mahakamani kwa hatua zaidi. Jumla ya kesi 437zimefunguliwa na zipo katika hatua mbalimbali za usikilizaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Hifadhi ya Taifa ya Serengetiimepakana na Wilaya nane tofauti. Mtuhumiwaanapokamatwa ndani ya hifadhi, anapelekwa katika Kituocha Polisi ki l icho jirani kwa hatua zaidi. Baadhi yawatuhumiwa wamekuwa na tabia ya kufanya uhalifu kwakufuata mienendo ya wanyamapori wahamao. Kwa mfano,kati ya mwezi Mei na Juni ya kila mwaka, wanyama wengiwanahamia maeneo ya Kusini na Magharibi mwa Hifadhiambapo kiutawala yako Wilaya ya Bariadi na Bunda.

Hivyo baadhi ya watuhumiwa kutoka Wilaya yaSerengeti huenda katika Wilaya nyingine kufanya ujangili wawanyamapori ambapo kwa kipindi hicho hawapatikanikirahisi katika aneo la Wilaya zao. Kutokana na hali hiyo,watuhumiwa wamekuwa wakikamatwa na kushitakiwakatika Mahakama za eneo au Wilaya waliyokamatwawakifanya uhalifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vyema wananchiwakazingatia taratibu zote za Hifadhi na niwaase wananchihao kuachana na ujangili ili kuepuka adhabu hizo nakuwataka washirikiane na Serikali kulinda hifadhi za Taifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Marwa Ryoba Chacha,swali la nyongeza.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Waziri,wananchi wa vijiji vya Merenga, Machochwe, Nyamakendo,Mbalibali, Tamkeri, Bisarara, Mbilikili, Bonchugu, Miseke naPakinyigoti wamenituma nimwombe Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli aende akawasikil ize matatizo yao, lakiniMheshimiwa Rais, Dkt. Magufuli wa Wizara ya Maliasili na Utaliini Mheshimiwa Waziri.

Je, uko tayari baada ya Bunge hili kuambatana namimi kwenda kusikiliza matatizo yao? (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Wananchi wavijiji vilivyopo kando kando ya Hifadhi ya Serengeti, maporiya akiba ya Ikorongo na Gurumeti pamoja na Ikoo na WMAkazi yao kubwa ilikuwa ni uwindaji, ufugaji na kilimo. Uwindajisasa hivi hawawindi, maana wakienda kuwinda hawarudi;mifugo yao imetaifishwa; mazao yao ya kilimo tembowanakula; ninyi kama Wizara, nini mbadala mnaowasaidiawananchi wa maeneo haya ili waweze kujikimu kiuchumi?(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii, majibu kwa maswali hayo.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kabisa kwamba kwanza naombanimhakikishie tu kwamba niko tayari wakati wowote paleambapo muda utaruhusu tutapanga, lazima twendetukatembelee katika yale maeneo. Hiyo inatokana nakwamba sasa hivi tuna mpango kabambe wa kuhakikishakwamba maeneo yote yanayopakana na Hifadhi za Taifa,lazima vijiji vyote vile vipimwe vizuri, tuweke mipaka vizuri lakinipia tuimarishe ule ulinzi katika yale maeneo hasa kule ambakokumekuwa na changamoto nyingi ambapo wanyamaporiwamekuwa wakiharibu mazao na shughuli za wananchiwanazofanya katika yale maeneo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, pia tutawekaminara, pamoja na kutumia ndege zisizokuwa na Rubani. Kwahiyo, mambo mengi tutayafanya kuhakikisha kwamba hayayanafanyika. Ili kufanya hayo, lazima tufike na tuone kwambawananchi wanaondokana na hizi changamoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu hatua mbadala;sasa hivi tunatoa elimu ni nini kinaweza kufanyika katika yalemaeneo yaliyo jirani na hifadhi? Kwa sababu ukipanda yalemazao ambayo wanyamapori wanayapenda, ni wazi kabisakwamba yataliwa na wanyamapori. Ukipanda yale mazaoambayo wanyamapori hawayapendi, wanayaogopa, basikidogo hii itasaidia.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

Mheshimiwa Naibu Spika, tutakwenda kukaa pamojana Mheshimiwa Mbunge na wananchi kwa pamoja,tutashauriana kuona ni aina gani ya mazao ambayowananchi wa maeneo yale watashauriwa kwambawayapande ili kuondokana na hii migogoro ambayoimekuwa ikijitokeza katika hayo maeneo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zacharia Issaay swali lanyongeza.

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. Kwanza naishukuru Serikali kwa kutoa kifutamachozi takribani milioni nane kwa ajili ya wananchiwaliopoteza maisha yao na wale walioathiriwa na wanyamawakali.

Mheshimiwa Naibu Spika, mnamo mwaka 2016 Serikaliiliahidi kufanya ziara katika Tarafa ya Daudi na Tarafa yaNdekoti kwa ajili ya wananchi ambao mali zao na mazaoyameharibiwa na wanyama wakali, lakini hadi sasa Serikalihaijatimiza ahadi yake hiyo kwa kuwa wale waliokuwakwenye Wizara walibadilishwa.

Je, ni lini Serikali itafanya ziara katika Tarafa ya Daudina Tarafa ya Ndekoti kwa ajili ya wananchi ambao mali zaozimeathiriwa na wanyama ikiwemo mazao na hawajapatakufidiwa hadi sasa? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kabisa kwamba inawezekana kulikuwana ahadi ya kwamba viongozi wa Kitaifa wataendakutembelea katika lile eneo.

Naomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbungekwamba hata kama viongozi wa kitaifa hawajafika, badowapo Watendaji wetu ambao lazima wafike katika yalemaeneo na wahakikishe kwamba wanahakiki mali

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

zilizopotea, wanahakiki uharibifu uliofanyika kusudi walewananchi wanaostahili kupewa kile kifuta jasho au kifutamachozi, waweze kulipwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwa nafasi hii,naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba leo hiinitawaagiza watendaji wafike katika lile eneo ili wakutanena hao wananchi, wafanye tathmini na tuone ni kiasi ganiwananchi wale wanastahili kulipwa kwa mujibu wa kanunizetu tulizonazo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utayari, naombanimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutakuwa tayari,tutakuja pia kuhakikisha kwamba haya yote yanatekelezekana wananchi waweze kuona kwamba Serikali yao inawajalivizuri. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. PudencianaKikwembe, swali la nyongeza.

MHE. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kunipatia nafasi na mimi niweze kuulizaswali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa matatizoyaliyopo katika Jimbo la Serengeti yanafanana kabisa namatatizo yaliyopo katika Jimbo la Kavuu hasa katika Kataza Chamalendi, Mwamapuli, Majimoto na vitongoji vyake;kumekuwa na matatizo ambayo wananchi hasa wafugajiwamekuwa wakisukumizwa na askari wa wanyamaporindani ya Mbuga ya Katavi na wamekuwa wakipotea namara nyingi wakiwa wakitafutwa na ndugu zao ni nguo tuzinapatikana:-

Je, Serikali inasema nini sasa kwa ujumla kuhusu askariwote wa wanyamapori wanaofanya kazi katika mbuga zoteza National Park katika kuhakikisha usalama wa walewanaowaita majangili wakati sio majangili? Kwa sababu tuwanakuwa wameingia kwenye mbuga, kwa hiyo, wataitwamajangili.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

Je, Serikali inasema nini kuhusu Askari hao ambaowamekuwa wakiwateka wananchi na kuwapora ng’ombezao na mali…

NAIBU SPIKA: Ameshakuelewa Mheshimiwa.Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwa swali hilo.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, kwanza naomba niseme tu kwamba sina taarifakamili kwamba askari wetu wamekuwa wakiwakamatawatu na kuwaingiza kwenye hifadhi halafu wanapotea mojakwa moja. Hizo taarifa hatunazo kama Serikali na kamaMheshimiwa Mbunge anazo na anao ushahidi wa namnahiyo, basi nitaomba nikae naye ili aweze kunipa hayo majinaya watu ambao wamepotea kusudi Serikali iweze kuchukuahatua zinazostahili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu namna yakuboresha yale maeneo, naomba nitumie nafasi hiikuwaomba wananchi wote wanaopakana na hifadhi zetukuhakikisha kwamba wanazingatia taratibu, sheria, kanunina miongozo iliyopo. Hawaruhusiwi kuingia bila kibali kwenyehifadhi. Kwa kawaida ukiingia kwenye hifadhi bila kibali, nivigumu sana kujua yupi ni jangili, yupi sio jangili. Kwa hiyo, ilikuweza kuondokana na hilo, ni kuwaomba wananchikutoingia katika maeneo ya hifadhi ili kusudi tuondokane nahilo tatizo.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tunaendelea na Wizaraya Nishati. Mheshimiwa Alfredina Apolinary Kahigi, Mbungewa Viti Maalum, sasa aulize swali lake. (Makofi)

Na. 452

Hitaji la Umeme kwa Wananchi wa Kagera

MHE. ALFREDINA A. KAHIGI aliuliza:-

Wananchi wa Kagera wana tatizo la umeme naumeme wa REA II umeingia katika center za vijiji tu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

Je, ni lini wananchi hao watapatiwa umeme iliwaondokane na adha ya kutumia vibatari?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNishati, napenda kujibu swali la Mheshimiwa AlfredinaAporinary Kahigi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, awamu ya pili ya utekelezajiwa miradi ya kusambaza umeme vijijini ililenga pamoja namambo mengine kufikisha umeme katika maeneo ya njia kuu,baadhi ya maeneo muhimu katika vijiji na katika taasisi zaumma. Utekelezaji wa miradi ya REA Awamu ya Pili ulikamilikamwezi Desemba, 2016.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala waNishati Vijijini (REA) ilianza kutekeleza Mradi wa REA Awamuya Tatu mzunguko wa kwanza tangu mwezi Julai, 2017.Katika Mkoa wa Kagera vijiji vipatavyo 141 vinatarajiakupatiwa umeme kupitia mradi huu. Mradi huu utakamilikamwezi Juni, 2019. Kazi ya kupeleka umeme katika vijiji hiviinahusisha ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovoti33 yenye urefu wa kilometa 299, njia ya umeme wa msongowa kilovoti 0.4 yenye urefu wa kilometa 574, ufungaji watransfoma 287 za KVA 50 na 100 pamoja na kuunganishiaumeme wateja wa awali 9,136. Gharama za mradi ni shilingibilioni 38.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia mwezi Aprili,2018 mkandarasi Kampuni ya Nakuroi Investment Ltd.aliyepewa kazi ya ujenzi wa miundombinu ya kusambazaumeme katika Wilaya zote za Mkoa wa Kagera alikuwaameshakamilisha kazi ya upimaji wa maeneoyatakayopelekewa umeme. Kazi zinazofanyika sasa nikusambaza nguzo katika maeneo ya mradi na kujengamiundombinu, pamoja na kusambaza umeme.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kahigi swali la nyongeza.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

MHE. ALFREDINA A. KAHIGI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi nyingine. Nina maswalimawili ya nyongeza, naomba kuyauliza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, katikaWilaya yetu ya Bukoba Vijijini kuna baadhi ya kata nitazisemajapokuwa ni nyingi. Katika Kata ya Rubafu -Kijiji chaBwendangabo, Kata ya Buma - Kijiji cha Bushasha, Kata yaBwendangabo - Kijiji cha Kashozi, Kata ya Nyakato - Kijiji chaIbosa; hizo ni baadhi ya Kata ambazo nimezitaja, lakini nikata nyingi sana katika Wilaya yetu ya Buboka Vijijini au nisemeMkoa mzima wa Kagera tuna shida ya umeme.

Je, Serikali inaona umuhimu wa kuwapa kipaumbelecha kuweza kuwawekea umeme haraka iwezekanavyo? Hiloni swali la kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, wananchi wa katahizo hizo nilizozitaja wamenunua solar. Solar hizo tayarizimeshaharibika. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakiki hizosolar kabla hazijaingia sokoni? Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishatimajibu kwa maswali hayo.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika,swali lake la kwanza, amezitaja kata mbalimbali katikaWilaya yake ya Bukoba Vijijini na amewakilisha Mkoa mzimana ameeleza ni namna gani Serikali itaweka kipaumbele.Nataka nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge kuwa Serikali yaAwamu ya Tano chini ya Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. JohnPombe Magufuli katika Mkoa huo wa Kagera kwa awamuhii ya tatu inayoendelea jumla ya vijiji 141 vitapatiwa umeme.Katika Wilaya yake ya Bukoba Vijijini, Kijiji cha Burugokimeshasambaziwa nguzo na kazi zinaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimthibitishieMheshimiwa Mbunge kuwa Kata zile alizozitaja na vijijialivyovitaja, kwa awamu hii ya kwanza vijiji kwa Bukobavijijini ni 22, lakini kwa awamu ambayo itaendelea mzunguko

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

wa pili unaoanza Julai vijiji vyote vilivyosalia vitapatiwaumeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, ameulizamasuala ya sola ambazo zimewekwa katika maeneo hayoya Bukoba Vijijini na maeneo mengine ya Mkoa wakekwamba nyingi zimeharibika. Serikali ina utaratibu ndani yaSerikali na kwa Taasisi mbalimbali. Kwa mfano, kuna masualaya TBS yanavyoangalia viwango na taasisi nyingine za kiserikaliza kuangalia bidhaa zinazoingia ndani ya nchi zisiwe bidhaaambazo kwa kweli ni fake.

Mheshimwia Naibu Spika, kwa hiyo, naombanimthibitishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali yetuitaendelea kuziimarisha zile taasisi zinazohusika na kuzuiabidhaa feki ndani ya nchi ili kujiridhisha na vifaa hususani vyamasuala ya nishati viingie vifaa bora na wananchi wapatehuduma bora. (Makofi)

Mheshimwia Naibu Spika, nakushuruku Mheshimiwa.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hongoli, swali fupi.

MHE. JORAM A. HONGOLI: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la umeme lililopoWilaya ya Kagera linafanana kabisa na tatizo la umememradi ule wa Makambako - Songea. Ule mradi umepitakatika Kata tatu; Kata ya Kichiwa, Kata ya Igongoro na Kataya Ikuna. Kwenye maeneo hayo kuna baadhi ya maeneoyana huduma muhimu kama shule, zahanati na vituo vyaafya umeme haujapelekwa huko. Nini kauli ya Serikali kwamkandarasi aliyesambaza umeme kwenye maeneo haya,kuhakikisha kwamba umeme unaenda kwenye maeneoyenye huduma muhimu? Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati,majibu kwa kifupi.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi. Katika mradi unaoendeleaMakambako - Songea kwa kweli tunarajia mwezi Septembamradi ule utakamilika na kuzinduliwa rasmi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi inayoendelea yakusambaza umeme katika maeneo ambayo yameainisha,nataka nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwakuwa miradi hii ya kupeleka umeme vijiji ipo ya ainambalimbali, kuna mradi wa Makambako - Songea ambaounalenga vijiji 121, lakini sambamba na hilo kuna mradiambao unaendelea wa densification kwa maeneo ya Mkoawa Njombe na Mkoa wa Iringa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mradi huu,densification ya awamu ya kwanza ina vijiji kama 305 namradi umekamilika umefikia asilimia 98.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, maeneo ambayohajasalia kama ambavyo tunafahamu mradi wa REA Awamuya Tatu unaendelea na maeneo yale na maelekezo yetukama Serikali, tumesema taasisi za umma iwe shule, iwezahanati, iwe miradi ya maji na taasisi zote kwambakipaumbele kwa wakandarasi waelekeze kwenye maeneohayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kama Serikalitunaendelea kusisitiza hayo maelekezo na yaendeleekutekelezwa na Wakandarasi wote. NimthibitishieMheshimiwa Mbunge, kwa kweli kwa awamu inayoendelea,changamoto hizi hazitakuwepo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa, tunaendelea na Wizaraya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mheshimiwa Hassan EliasMasala, Mbunge wa Nachingwea, sasa aulize swali lake.(Kicheko)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

Na. 453

Viwanda vya Kukamua Mafuta Nachingwea

MHE. HASSAN E. MASALA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani juu ya wawekezajiwalioshindwa kuendeleza Viwanda vya Kukamua Mafuta vyaIlulu na Kiwanda cha Mamlaka ya Korosho WilayaniNachingwea?

NAIBU WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJIalijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waViwanda, Biashara na Uwekezaji naomba kujibu swali laMheshimiwa Hassan Elias Masala, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza napenda kulitaarifuBunge lako tukufu kwamba Serikali inafuatilia kwa karibu ilikuhakikisha kuwa waliobinafsishiwa viwanda wanatimizawajibu wao ipasavyo na kwamba viwanda hivyo vinafanyakazi kama ilivyokusudiwa kwa mujibu wa mkataba wao naSerikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Kiwandacha Mafuta Ilulu, kiwanda hicho kiliuzwa kwa njia ya ufilisi.Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina imekuwaikimfuatilia mwekezaji ili kiwanda kilichonunuliwa kichangiekatika uchumi wa Taifa letu. Kutokana na ufuatiliaji huo,tarehe 6 Juni, 2018, mmiliki wa Kiwanda cha Mafuta cha Ilulu,alitoa taarifa rasmi kurejesha kiwanda hicho cha Serikalinikwa kuwa ameshindwa kukiendeleza. Taratibu za kisheriazinafuatwa ili kukamilisha makabidhiano hayo rasmi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Msajili itaendeleakuona matumizi bora zaidi ya kiwanda au eneo hilo. Aidha,kwa upande wa Kiwanda cha Korosho Nachingwea,kilibinafsishwa kwa kuuza hisa asilimia 100. Hivyo, uendeshajiwote wa kiwanda upo chini ya mwekezaji binafsi.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

Mheshimiwa Naibu Spika, kiwanda kinaendelea nazoezi la kufunga mitambo ya kubangua korosho na sehemuya maghala inatumika kuuzia na kuhifadhia korosho zawakulima na wanunuzi. Mpango wa Serikali ni kuhakikishakuwa kiwanda hicho kinakamilisha ufungaji mitambo nakuanza uzalishaji haraka ifikapo msimu ujao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nilikuwanimeahidi hapo awali, narudia kusema tena mara baadaya Bunge hili nitatembelea viwanda vyote vilivyobinafsishwaMkoani Lindi na Mtwara pamoja na maeneo mengine kwaajili ya ufuatiliaji na tathmini ya viwanda hivyo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hassan Elias Masala, swalila nyongeza.

MHE. HASSAN E. MASALA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri, lakinipamoja na majibu hayo naomba niulize maswali mawili yanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, nilitakanijue Serikali imejipanga vipi au imejiandaa vipi? Kwa sababuwakati Kiwanda hiki cha Mafuta Ilulu kinabinafsishwa, kilikuwana majengo pamoja na mitambo yake, lakini ukaguzinilioufanya kwa awamu ya mwisho mpaka sasa hivi huyumwekezaji anatangaza kukirudisha, kiwanda kile hakinamashine hata moja na amesema kwamba anakirudisha. Ninikauli ya Serikali juu ya mashine ambazo zilifungwa katikaKiwanda kile cha Mafuta cha Ilulu?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, nilikuwanataka nijue; kwa sababu Serikali imetoa hisa asilimia 100 kwawawekezaji kwa ajili ya Kiwanda cha Korosho, ambapowawekezaji waliopewa ni Sunshine na mashine walizozifungapale hazioneshi kama zinaweza zikafanya kazi ambayotunaikusudia. Kwa nini Serikali isichukue angalau asilimia 51ya hisa zile ili Serikali iweze kupata gawio lake la moja kwamoja badala ya kutegemea mwekezaji? Ahsante.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, majibu.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NAUWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa upandewa Kiwanda cha Mafuta cha Ilulu ambacho anadai kwambamashine zake zimeshaondolewa na kiko katika hali mbayana kinarejeshwa, ndiyo maana tumesema kwambatutakipokea kufuatana na taratibu za kisheria. Kwa hiyo,tutaangalia masuala yote ya kisheria pale tutakapoonakwamba mwekezaji huyu anabanwa na masharti hayo, basihatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa kiwandacha korosho, niseme tu kwamba Serikali ilikuwa imeshajitoakatika kufanya shughuli za uwekezaji na hiyo ndiyo sera yetu.Tunachofanya zaidi ni kuwahamasisha wawekezaji, wao ndiowawekeze na mitaji mingi zaidi iweze kufika na kuwekezakatika nchi. Ila tu katika maeneo yale ambayo tunaaminikwamba pengine kwa mwekezaji binafsi ataona hakuna tija,lakini wakati huo kwa upande wa Serikali tunaona kwambasuala hilo lina manufaa makubwa kwa Watanzania au jamiikwa ujumla, ndipo Serikali inapoingilia na kuweza kuonaumuhimu wa kuwekeza.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Wizara ya Kilimo. Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota,Mbunge wa Nanyamba, sasa aulize swali lake.

Na. 454

Kuporomoka kwa Bei ya Mbaazi Nchini

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:-

Wakulima wa mbaazi Mikoa ya Mtwara na Lindiwameshuhudia kuporomoka kwa bei katika msimu wamwaka huu pamoja na kwamba walihamasika kulima kwawingi.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

(a) Je, ni nini kilisababisha kuporomoka kwa bei yambaazi?

(b) Je, Serikali inachukua hatua gani ili kuhakikishahali hiyo haijitokezi msimu ujao?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waKilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah DadiChikota, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli bei ya mbaaziiliporomoka kutoka wastani wa bei ya shilingi 2,750 kwa kilomwaka 2014/2015 hadi shilingi 700 kwa msimu wa mwaka2016/2017 na kufikia wastani huo na katika mikoa mbalimbalihapa nchini. Hali hii imesababishwa na ongezeko la uzalishajiwa mbaazi katika nchi za India, China, Brazil, Myanmar,Canada, Msumbiji, Sudan na Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na ongezeko hilola uzalishaji, mwezi Agosti, 2017 nchi ya India ambayo ndiowanunuzi wakuu wa mbaazi zetu ilizuia uingizaji wa mbaazikutoka nje ya nchi hiyo kwa kuwa walikuwa na uzalishajimkubwa wa kukidhi mahitaji yao na hivyo kusababishaukosefu wa soko la uhakika kwa mbaazi zilizozalishwa nchinimsimu wa 2016/2017.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuhakikisha wakulimawanapata masoko ya uhakika, Serikali imeandaa mikakatimbalimbali ya muda mfupi na muda mrefu kuimarishaupatikanaji wa masoko ya mazao hususan mbaazi. Mikakatiya muda mfupi ni pamoja na Wizara kupitia Bodi ya Nafakana Mazao Mchanganyiko kwamba itaongeza idadi yamazao yatakayonunuliwa ambayo ni pamoja na mazao yajamii ya mikunde (mbaazi, choroko na dengu), mbegu zamafuta (ufuta, alizeti na karanga) na nafaka kwa (mtama,ulezi na uwele) katika mwaka 2018/2019. Kwa sasa bodi hiyoimepata soko la tani 100,000 za soya, tani 20,000 za ufuta natani 3,500 za mbaazi ambazo zitauzwa kwa wadau ndani

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

ya nje ya nchi. Pia itanunua tani 6,000 za alizeti kwa ajili yakukamua mafuta katika kiwanda chake kilichopo Kizota, JijiniDodoma.

Mheshimiwa Naibu Spika, mkakati mwingine wamuda mfupi ni kuuza zao la mbaazi katika soko la bidhaakwa maana ya commodity exchange na kuhamasishautumiaji wa mbaazi hapa nchini katika maeneo mbalimbalihususan katika mashule na majeshi yetu (Magereza na JKT).Aidha, Serikali kupitia Maafisa Lishe waliopo katikaHalmashauri zote nchini, watatoa mafunzo ya namna boraya kuandaa vyakula vinavyotokana na mbaazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mikakati ya muda mrefu nipamoja na kampuni kutoka India kujenga Kiwanda chakiitwacho Mahashree Agro Processing Ltd kitakachosindikaaina zote za mazao jamii ya mikunde, korosho na ufuta katikaKijiji cha Mtego wa Simba, Kata ya Mkambarani, WilayaniMorogoro kitakachokuwa na uwezo wa kusindika tani 200 zaaina mbalimbali ya mikunde kwa siku na kuuza katika sokola ndani na nje. Kiwanda hicho kitasaidia wakulima kupatabei nzuri na soko la uhakika mara kitakapoanza uzalishajimwaka 2019.

SPIKA: Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, swali lanyongeza.

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru, pamoja na majibu mazuri ya MheshimiwaNaibu Waziri, naomba kuulizwa maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tulitegemeakwamba baada ya kuanzisha Bodi ya Nafaka na MazaoMchanganyiko ingekuwa Mkombozi wa mazao mengineambayo hayana bodi, lakini kuna changamoto ya fedhakwenye bodi hii.

Je, Serikali ina mpango gani wa kutenga fedha nyingiza kutosha ili Bodi ya Nafaka na Mazao iweze kununuamazao mengine pamoja na mbaazi? (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa sokola India limeonesha kulegalega na kwenye zao la koroshotulipoachana na soko la India tumeona kuna mafanikiobaada ya kuja Waturuki na Wavietinam; Serikali ina mpangogani wa kuingia kwenye masoko mengine ili kuachautegemezi wa soko la India?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo,majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kumjibu Mheshimiwa Mbunge RAS Mstaafu na kakayangu Mheshimiwa Chikota maswali yake madogo mawiliya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, kama Serikalini kwamba tumeielekeza na kusisimamia Bodi yetu ya MazaoMchanganyiko kwamba kuanzia sasa wajikite zaidi katikakufanya biashara ile ya kilimo cha ushindani. Tayaritumeshaanza kufanya mazungumzo na NSSF na mazungumzohayo yamefanikiwa na tayari tumeshapata shilingi bilioni 3.6kwa ajili ya kununua mashine zile kwa ajili ya viwanda vyamahindi na alizeti kwa maana ya mashine mbili na tayarizimeshafika bandarini.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili lanyongeza, ni kwamba ni vyema sisi kama Serikali; naombaniwaase Halmashauri zote nchini kwamba tutoe elimu kwawakulima wetu kuweza kufanya kilimo cha kibiashara(commercial farming) kwa sababu unapokuwa kwenyecommercial farming, utaweza kujua ulime kilimo cha ainagani? Mazao gani? Kwa bei gani? Utauza wapi? Kwa maanahiyo, hakutakuwa na hasara yoyote.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile naomba niwaelezeWaheshimiwa Wabunge kwamba mbaazi ni chakula kamavyakula vingine, tena ina protini zaidi kuliko maharage nainaongeza damu mwilini kuliko maharage. Vilevilenawaomba hata wale wanaofanya vyakula vya mifugo, ni

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

kwamba hizi mbaazi zetu pia zinatumika vizuri sana katikavyakula vya mifugo kama ilivyokuwa soya. Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea,Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa Mbunge waRufiji, sasa aulize swali lake.

Na. 455

Mradi wa Kilimo katika Bonde la Mto Rufiji

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA aliuliza:-

Mradi wa Kilimo wa RUBADA - Rufiji, umekuwa mradiwa kitapeli ambao watu wachache wanajinufaisha narasilimali za Rufiji bila ya Wana-Rufiji kupata maendeleoyoyote.

Je, ni lini Serikali itafikiria kuleta mradi wa kilimo katikaBonde la Mto Rufiji ambalo kwa miaka mingi liko tupu bilashughuli yoyote ya kilimo hasa ikizingatiwa kuwa bonde hilolina kila kitu?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waKilimo, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed OmaryMchengerwa, Mbunge wa Rufiji, lenye sehemu mbili, naombanianze kutoa maelezo ya utangulizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Rubada siyo mradi, baliilikuwa ni Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Rufiji kwamaana ya Rufiji Basin Development Authority.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo haya,sasa naomba nianze kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vema nikiri tu kwambakulikuwepo upungufu wa kiutendaji ndani ya RUBADA.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

Kutokana na hali hiyo, Wizara ilifanya uchunguzi mwezi ulewa Oktoba, 2014 na tarehe 8 Aprili, 2015 Wakurugenzi watatuwa RUBADA walisimamishwa kazi na hatimaye tarehe 21Januari, 2016 Bodi ya RUBADA i l iwafukuza kazi rasmiWakurugenzi wawili.

Aidha, kutokana na mabadiliko ya kisera, kisheria nakimfumo, imeonekana kuwa RUBADA imekosa uhalali wakuendelea kuwepo. Hivyo Serikali mnamo mwezi Septemba,2017 ilileta Muswada wa Sheria Bungeni ukipendekeza kuifutaRUBADA. Bunge liliridhia kuifuta RUBADA na shughuli zakekuhamishiwa taasisi nyingine za kiserikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaelewa fursazilizopo katika Bonde la Rufiji. Hatua kadhaa zimechukuliwakutumia vizuri fursa hizi. Mathalani, Serikali inatekeleza mradimkubwa wa Bwawa Stiegler’s Gorge kwa ajili ya umemewa megawati 2,100. Bwawa hili pia litawezesha kuhifadhimaji kwa ajili ya umwagiliaji, mifugo na uvuvi. Pia upo mradiwa Bwawa la Maji la Kidunda ambalo pamoja na kutoauhakika wa maji ya kunywa kwa Jiji la Dar es Salaamlitatumika pia kwa umwagiliaji, mifugo na uvuvi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya kilimo kwakushirikiana na Wizara ya sekta ya kilimo imeandaa programuya kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili kwa maana ya(ASDP II) ambapo ina maeneo ya kipaumbele 23 na jumla yamiradi ya uwekezaji kwa maana ya Investment Projects 56ya kipaumbele ambayo inajumuisha miradi iliyopo katikaBonde la Mto Rufiji ambayo ilikuwa ikiratibiwa na RUBADAchini ya uliokuwa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).Miradi hiyo ni kama vile iliyopo maeneo ya Muhoro, Tawi,Bumba na Msoro. ASDP II inalenga kuendeleza miradi hiyoiliyopo Bonde la Mto Rufiji kama kuweka miundombinu yaumwagiliaji ambapo wananchi wengi watanufaika kupitiaprogramu hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nimhakikishieMheshimiwa Mbunge, kaka yangu kuwa miradi hii ikikamilikaitalifanya Bonde la Mto Rufiji kuwa lulu ya maendeleo. Kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

maana hiyo, namwomba kaka yangu MheshimiwaMchengerwa avute subira kidogo kuona mabadiliko hayatarajiwa na yenye matokeo chanya.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa,swali la nyongeza.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaNaibu Spika, napongeza majibu mazuri ya dada yanguMheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa, mchapa kazi na ninaonakabisa anakwenda kuchukua Jimbo la mtu huko Mbeya.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili yanyongeza; kwanza kabisa Rufiji tunatambua jitihadaanazofanya Mheshimiwa Rais za ujenzi wa bwawa la Stiegler’sGorge kama ambavyo amelisema Mheshimiwa Naibu Wazirina kwamba tunatambua Serikali inapelekea zaidi ya shilingitrilioni mbili kwenye mradi huu na kuifanya Rufiji kuwa motomoto kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu wa Stiegler’sGorge una zaidi ya ekari 150,000 ambazo zimetengwa kwaajili ya kilimo. Swali langu kwa Mheshimiwa Naibu Waziri waKilimo: Je, Serikali inawaandaaje Warufiji sasa ili kuwezakupokea fursa hizi za eneo hili la kilimo zaidi ya ekari 150,000katika kuweka miradi mbalimbali ikiwemo na ule mradi wakiwanda kikubwa cha sukari kule Rufiji? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pil i,Watanzania wa Rufiji kwa asilimia 90 wanategemea kilimona RUBADA ilikuwa katika Kata ya Mkongo pale Rufiji; na hiindiyo kata iliyoathirika sana kwa wafugaji kuingiza mifugoyao eneo la wakulima; je, Serikali inajipangaje kuwasaidiawakulima hususan katika vijiji vya Mbunju, Ruwe pamoja naMkongo Kusini ambao wameathirika sana kwa mazao yaokuliwa na wafugaji? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo,majibu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kwanzakipekee kabisa naomba nimpongeze sana MheshimiwaMchengerwa, Mbunge wa Rufiji kwa dhati kabisa kwa maanayeye alikuwa ni sehemu mojawapo ya watu ambaowalishatueleza na wakatuambia kabisa kwamba mradi huuwa RUBADA ni non-starter na yeye alikuwa ni sehemu kamaMwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria, kuleta nakupendekeza kwamba mradi huu wa RUBADA haufanyi kazivizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya utangulizi huo,sasa naomba naiende moja kwa moja kumjibu maswali yakemadogo sana ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa kwamba sisikama Serikali katika Bonde hili la Rufiji ni hekta 1,350 kwa ajiliya mradi wa Stiegler’s Gorge. Naomba niseme kwambaeneo la hekta 300,000 limetengwa kwa ajili ya kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba hizo hekta 300,000zilizotengwa kwa ajili ya kilimo, ni kwa ajili ya irrigation scheme.Kwa maana hiyo, naomba nimhakikishie kwamba wananchiwa Rufiji na maeneo mengine yote watanufaika kwenyekilimo kupitia mradi huu ambao unaitwa irrigation scheme.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine lile la (b) ni kuhususuala zima la migogoro aliyoizungumzia kuhusu ardhi. Nikwamba Serikali tumejipanga na mpaka sasa hivi sheriainaandaliwa; tunaangalia suala zima la migogoro hii ya ardhina maandalizi tayari yameshafanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naombaMheshimiwa Mbunge avute subira, Serikali inaandaa sualazima la ardhi kwa sababu tumegundua kwamba kunamigogoro mingi sana kati ya wakulima na wafugaji.Nakushukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunamaliziaswali la mwisho Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Mheshimiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

Josephine Johnson Genzabuke, Mbunge wa Viti Maalum, sasaaulize swali lake.

Na. 456

Chujio la Maji Katika Mji wa Kasulu

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:-

Upatikanaji wa maji safi na salama katika Mji waKasulu bado ni changamoto kubwa sana, kwani majiyanayotoka kwenye mabomba ni machafu.

Je, ni lini Serikali itatoa pesa kwa ajili ya kununua chujiola maji ili wananchi waweze kupata maji safi na salama?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMaji na umwagiliaji naomba kujibu swali la MheshimiwaJosephine Johnson Genzabuke, Mbunge wa Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua tatizo lamaji katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu ikiwa ni pamoja namiradi ya maji kutokuwa na miundombinu ya kutibu majikatika bajeti ya mwaka 2017/2018. Kupitia Programu yaMaendeleo ya Sekta ya Maji, Halmashauri ya Mji wa Kasuluimetengewa shilingi bilioni 3.35 kwa ajili ya ujenzi wamiundombinu ya maji ikiwemo ujenzi wa miundombinu yakusafisha na kutibu maji. Hadi sasa usanifu wa miradi minneya Muganza, Marumba, Muhunga na Kimobwa katikaHalmashauri ya Mji wa Kasulu umekamilika na taratibu zakuwapata Wakandarasi watakaotekeleza ujenzi wa miradihiyo zinaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa miundombinuya kutibu maji ni sehemu ya mradi wa maji wa Kimobwaambao utaambaatana na uchimbaji wa visima virefu vitano,usambazaji wa bomba la kilometa 14, ujenzi wa tenki lenye

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

ukubwa wa mita za ujazo 225 na ukarabati wa vyanzo vitatuvya maji kwa ajili ya eneo la mji wa Kasulu.

Mheshimiwa Naibu Spika, miundombinu ya kutibu nakusafisha maji itasaidia kuondoa kero ya ubora duni wa majiyanayotumika hivi sasa hususan maji yanayotoka katikavyanzo vya maji vya Miseno, Nyanka, Nyankatoke na MtoChai. Hivyo ubora wa maji, uzalishaji na usambaji wa majikwa pamoja utaongezeka. Lengo ni kuhakikisha majiyanayosambazwa kwa wananchi ni safi, salama nayanayokidhi mahitaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, zabuni kwa ajili ya kazi hiyoimetangazwa tarehe 24 Machi, 2018 na utekelezaji wakeutaanza mara tu baada ya mikataba ya ujenzi kusainiwa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Josephine Genzabuke,swali la nyongeza.

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa NaibuSpika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri,nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; katikaKata ya Mwilamvya ndipo yalipo machinjio ya ng’ombe,mbuzi na kondoo. Eneo hilo hupata maji mara mbili kwawiki au mara tatu, lakini hivi sasa ninavyoongea eneo hilohalina maji na ni muda wa mwezi mzima maji hayapatikanikatika eneo hilo.

Je, Serikali iko tayari kutoa pesa kwa mpango wadharura ili eneo hilo la machinjio liweze kupatiwa maji?(Makofi)

Swali langu la pili, katika Halmashauri ya Wilaya yaKasulu DC ipo miradi ya maji ambayo haijakamilika, imefikiaasilimia 85 mpaka 95 lakini imekwama kwa ajili ya ukosefuwa pesa; je, ni lini sasa Serikali itamalizia miradi hiyo kwakupeleka pesa ili miradi hiyo iweze kukamilika na wanawakewaweze kuondolewa adha ya upatikanaji wa maji? (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji naUmwagiliaji, majibu kwa maswali hayo. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Awali ya yotenampongeza sana Mheshimiwa Mbunge, ni mama shupavu,jasiri, mfuatiliaji na mhangaikaji wa matatizo ya wananchiwa Kigoma hasa katika suala zima la maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Wizara ya Majihatutakuwa kikwazo kwa wananchi wako wa Mwilamvyahususan katika eneo hilo la Machinjio katika kuhakikishawanapata maji safi ili waendelee na usafi, wakati mwingineusafi ni uhai wa mwanadamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili kuhususuala zima la miradi ambayo haijakamilika, nitumie nafasihii kulishukuru Bunge lako tukufu na wewe mwenyewe kwaWizara yetu ya Maji kuidhinishiwa fedha na katika Mji huowa Kasulu umetengewa kiasi cha shilingi 1,466,000,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba MheshimiwaMbunge kwa kushirikiana na sisi Wizara na viongozi katikakuhakikisha tunasimamia fedha zile ili ziende zikamilishe miradiambayo haijakamilika ili wananchi wake waweze kupatamaji, salama na yenye kuwatosheleza.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaishiahapo kwa kipindi cha maswali na majibu. Nilete matangazotuliyonayo hapa mezani. Kwanza, ni matangazo ya wageni.Tutaanza na wageni walioko Jukwaa la Mheshimiwa Spika.

Tutaanza na wageni tisa ambao ni WaheshimiwaWabunge sita, Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Jamii(Committee on Community Safety) na Maafisa watatu kutokaBunge la Jimbo la Gauteng la nchini Afrika ya Kusini. Nao nihawa wafuatao; Mheshimiwa Sochayile Khanyile ambaye niMwenyekiti (Committee Chairperson) please stand up andwave to the house. Thank you very much. Honorable MikeMadladla (Committee Member), Honorable Godfrey Tsotetsi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

(Committee Member), Honorable Mafika Mgcina (CommitteeMember), Honorable Kate Lorimer (Committee Member),Honorable Michele Clarke (Committee Member), Mr. SizweMayoli (First Secretary Political South African High Commission),Ms. Thabile Malumane (Committee Coordinator) and Ms.Nthabiseng Mofokeng (Committee Administrator), you areall welcome to the House. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, pia tunao wageni watatuwa Mheshimiwa Dkt. Harrison Geoge Mwakyembe ambayeni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutokaKanisa la Kingdom Embassy ambaye ni Nabii Clear Malisaambaye ameambatana na mke wake Bi. Lisa Malisa. Karibunisana Nabii Malisa na mke wako. Nabii Clear Malisa, maanaMalisa wako wengi. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunao pia wageni waWaheshimiwa Wabunge mbalimbali tutaanza na wageni 45wa Mheshimiwa Anna Lupembe ambao ni Wanamaombikutoka Jijini Dar es Salaam. Karibuni sana wageni wetu. Tunaopia wageni watatu wa Mheshimiwa Marwa Ryoba Chacha,Mbunge wa Serengeti ambao ni watoto wake, Ndugu EstherChacha, Ndugu Victory Chacha na Ndugu StephenMwasanga kutoka Serengeti, Mkoani Mara, karibuni sana.(Makofi)

Tunaye pia mgeni wa Mheshimiwa Halima Bulemboambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, NduguBadru Shuza, karibu sana. Tunaye pia mgeni wa MheshimiwaAlex Gashaza ambaye ni rafiki yake kutoka Bukoba Vijijini,Mkoani Kagera na huyu ni Ndugu Khalifa Mutabuzi, karibusana. Pia nawatambua wageni 42 wa Mheshimiwa LolesiaBukwimba ambao ni Wanakwaya wa AICT Vijana Kanisa laDVC kutoka Ipagala Mkoani Dodoma wakiongozwa naMchungaji Daudi Samweli, karibuni sana. (Makofi)

Vilevile tunao pia wageni wanne wa MheshimiwaAntony Komu ambao ni familia yake kutoka Moshi MkoaniKilimanjaro akiongozwa na ndugu Jacqueline Antony Komu,karibuni sana.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Tunao pia wageni watatu wa Mheshimiwa AugustinoManyanda Masele ambao ni rafiki zake kutoka Wilaya yaMbogwe, Mkoa wa Geita, karibuni sana. (Makofi)

Tunao pia wageni watatu wa Mheshimiwa James OleMillya, ambao ni viongozi kutoka Jimboni kwake SimanjiroMkoani Arusha, karibuni sana. Tunao vilevile wageni nanewa Mheshimiwa Mahmoud Mgimwa ambao ni familia yakena wapiga kura wake kutoka Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa,karibuni sana. (Makofi)

Wengine ni wageni nane wa Mheshimiwa SelemaniMoshi Kakoso ambao ni viongozi wa Kampuni ya Maxmalipokutoka Jijini Dar es Salaam wakiongozwa na mwanzilishi wakampuni hiyo Ndugu Juma Rajabu, karibuni sana. Pia wapowageni watano wa Mheshimiwa Constantine Kanyasuambao ni familia yake kutoka Mkoani Geita wakiongozwana mke wake Ndugu Christina Bunini, karibuni sana. (Makofi)

Naona Waheshimiwa Wabunge wanamkaribisha wifiyao hapa na wengine ni shemeji. (Makofi)

Wageni Saba wa Mheshimiwa Mendrad L. Kigolaambao ni Wajumbe kutoka Peace Cop Tanzania ya MufindiMkoa wa Iringa, karibuni sana and you are welcome. Tunaopia Wageni Watatu wa Mheshimiwa Joram Hongoli ambaoni wapiga Kura wake kutoka Lupembe Mkoani Njombewakiongozwa na Katibu wa CCM Kata ya Kichiwa NduguBarton Makweta, karibuni sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunao pia wageniwaliotembelea Bunge kwa ajili ya mafunzo na hawa niWanafunzi 66 kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA)kilichopo Mkoani Morogoro. Naona hawapo penginewataingia baadae kidogo. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, ninayo matangazomengine, tangazo lingine linatoka kwa Katibu wa Bungeanawatangazia Waheshimiwa Wabunge kwamba mweziFebruari, 2018 Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

wa Umma iliwaandikia barua baadhi ya Wabunge kuwatakawawasilishe vielelezo vinavyothibitisha umiliki halali wa maliwalizoziainisha kwenye fomu ya Tamko la Viongozi wa Ummakwa ajili ya uhakiki. Waheshimiwa Wabunge ningewasihimsikilize kwa makini hili tangazo ni muhimu.

Kwa kuwa Wabunge wengi hawakutekeleza rai hiyo,sasa Sekretarieti ya Viongozi wa Umma inawakumbushakufanya hivyo kabla ya siku ya Jumatatu tarehe 25 Juni, 2018.Taarifa zinazotakiwa kuwasilishwa kwa ajili ya uhakiki huo ninyaraka zinazohusu fedha zilizoko benki au taasisi nyingineza fedha, hisa, gawio, nyumba, majengo, mashamba,mifugo, madini, mashine, viwanda na mitambo, magari naaina nyingine za usafiri, rasilimali au maslahi mengine yakibiashara, madeni na mikopo kwa mali zote zilizopo ndanina nje ya Tanzania. Mwakilishi wa Kamishna wa Sekretarietiya maadili atafika ofisini kwa Katibu wa Bunge kuchukuataarifa hizo. Aidha, kwa Waheshimiwa Wabunge ambaohawakuwahi kupokea wito huo wanatakiwa kuwasilishavielelezo vya taarifa kama hizo kwenye ofisi za Sekretarietiza Kanda kama ifuatavyo:

Kanda ya Dar es Salaam Ofisi ya Kanda ya Dar esSalam Mikoa inayohudumiwa ni Dar es Salaam na Zanzibar,Kanda ya Mashariki Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pwani- Kibahainahudumia Mikoa ya Pwani, Morogoro na Tanga. Kanda yaKaskazini Arusha AICC itahudumia Arusha, Kilimanjaro naManyara. Kanda ya Kati Dodoma Kilimani itahudumiaDodoma na Singida. Kanda ya Magharibi Tabora itahudumiaTabora, Kigoma na Simiyu. Kanda ya Ziwa Mwanza,itahudumia Mwanza, Geita, Kagera, Shinyanga na Mara.Kanda ya Kusini Mtwara itahudumia, Mtwara, Lindi naRuvuma. Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya NBC Houseitahudumia Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Songwe naRukwa.

Waheshimiwa Wabunge waliokuwa wamepata witohuo wapeleke hizo taarifa na hata ambao hawakupata witohuo wanaombwa kuwasilisha vielelezo vya mali walizonazona madeni waliyonayo. Ndiyo maana nil iwaambia

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

Waheshimiwa Wabunge tusikilize kwa makini na tarehe yamwisho ni tarehe 25 Juni, 2018.

Waheshimiwa Wabunge ninalo tangazo linginekutoka kwa Katibu wa Bunge, anawatangazia WaheshimiwaWabunge kwamba kesho siku ya Jumaatano tarehe 20 Juni,2018 kutakuwa na kongamano kuhusiana na masuala ya VVU(UKIMWI), hususani wajibu wa viongozi katika kufikia malengoya 909090 ifikapo mwaka 2020. Kongamano hilo litafanyikakatika Ukumbi wa Msekwa kuanzia saa 7:00 mchana hadisaa 10:00 alasiri ambapo mgeni rasmi atakuwa MheshimiwaSpika.

Waheshimiwa Wabunge, naomba tusikilizane kidogowengi mnaongea sana na mimi nimesimama na ninyimnafahamu Kanuni zinasemaje, naomba tusikilizane kidogoWaheshimiwa Wabunge tafadhali. Aidha, kuanzia saa 3:00usiku kutakuwa na majadiliano (round table discussion)kuhusu maudhui hayo ambayo yatahudhuliwa naMheshimiwa Spika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Waziriwa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Waziriwa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, mwakilishi wa wadau wamaendeleo na mwakilishi wa AZAKI.

Vilevile siku ya Alhamis tarehe 21 Juni, 2018 kutakuwana maonesho ya shughuli zinazofanywa na AZAKI mbalimbalikatika kufikia malengo ya 909090, maonesho hayoyatafanyika nyuma ya Ukumbi wa Msekwa sambamba nazoezi la upimaji wa virusi vya UKIMWI kwa hiari. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge ninalo pia tangazo kutokakwa Mheshimiwa Anna Lupembe ambaye ni Mwenyekiti waIbada, Chapel ya Bunge, anawatangazia WaheshimiwaWabunge wote wa imani ya kikristo kwamba leo kutakuwana ibada katika eneo la wazi la basement mara baada yakuahirisha shughuli za Bunge saa 7:00 mchana. Katika ibadahiyo kutakuwa na Mtumishi wa Mungu Prophet Clear Malisawa Kanisa la Ubungo Kibangu, Dar es Salaam na kwaya ya

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

AICT Vijana kutoka Dodoma itahudumu. WaheshimiwaWabunge wote mnakaribishwa kwenye ibada hii muhimu.

Waheshimiwa Wabunge, mtakumbuka MheshimiwaSpika jana alitangaza kwamba Uwanja wa Jamhuri leokutakuwa na pamoja na mambo mengine kutakuwa naupimaji wa Waheshimiwa Wabunge wa hiari wa Virusi vyaUKIMWI na Waheshimiwa Wabunge wengine walioendakwenye mazoezi walishaanza kuonesha mfano, na mfanohuu wa leo umeonyeshwa na Mheshimiwa Ali Keissy naMheshimiwa Daimu Mpakate wao wameshapima.Tutawauliza baadae kama wamechukua na majibu maanakupima ni suala moja, kuchukua majibu ni la pili, kwa hiyotutawauliza baadae. (Makofi/Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayotutaendelea.

MWONGOZO WA SPIKA

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Abdallah Bulembo naMheshimiwa Goodluck Mlinga. Wote mliosimama nimiongozo? Waheshimiwa Wabunge nawakumbusha sikuzote tukae anapoanza mwenzio kuzungumza Mwongozoisome vizuri ile Kanuni, ili usije ukajisikia vibaya nitakapokujibuhapa namna unavyoleta Mwongozo wako. MheshimiwaAbdallah Bulembo.

MHE. ABDALLAH M. BULEMBO: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana. Ninaomba Mwongozo wangu ni Kanuniya 68 (7) tukio la leo ni kwenye swali namba 454 linalohusianana mazao lililoulizwa na Mheshimiwa Abdallah Chikota.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mwongozo wakokwa sababu ya wakulima wa pamba wa Mkoa wa Mara naWilaya zake wamekumbwa na tatizo ambalo Wizara yaKilimo walishajibu hapa kwamba siyo lazima mkulima waPamba aende kufungua akaunti ndiyo aweze kuuza pambayake. Mikoa ya Shinyanga, Geita, Simiyu wao wanaendelea,lakini Mkoa wa Mara Wakuu wa Wilaya wamekataa,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

kwamba lazima wale wakulima wakafungue akaunti ndiowaweze kuuza pamba yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mwongozo waSerikali wakulima wa Mkoa wa Mara dhambi yao ni ipi? Kwanini wanatofautishwa na wakulima wa Mikoa mingine?Naomba Serikali itolee tamko na iweze kutoa agizo iliwakulima hawa waache kuteseka na pamba yao.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Goodluck Mlinga.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana. Naomba Mwongozo kupitia Kanuni ya68(7) ambao unatokana na tangazo lako ulilotangaza sasahivi.

Kwanza naomba niipongeze Serikali yetu kwa uhakikiwa mali za Wabunge na kutaka nyaraka il i kutakakuthibitihsha kuwa mali walizonazo ni kweli za kwao. Pianiipongeze Serikali kwa kuhakiki watumishi hewa nawatumishi ambao hawana sifa kulingana na kazi zao.

Naomba Mwongozo wako huu uhakiki usiishie tukwenye mali, kwa sababu sifa za Mbunge mojawapo ni kujuakusoma na kuandika. Tumeshuhudia katika Bunge lako hilitangu Bunge la Bajeti lianze Wabunge wa Kambi Rasmi yaUpinzani wameshindwa kuwasilisha hotuba zao kwa sababuhawana mtu wa kuwaandika.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mwongozo wako,kwa sababu wamelithibitisha hili wao wenyewe jana kuwawamepata mtu wa kuwaandikia, ndiyo maana wameletahotuba yao. Nilikuwa naomba Mheshimiwa Spika atengueteuzi zao Wabunge wote wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwasababu hawajui kuandika ili uchaguzi ufanyike tena. Pianilikuwa naomba uhakiki sasa uanze kwa Wabunge na miminimewasaidia nilikuwa ninamhakiki Mheshimiwa Musukumaasubuhi na ameweza kuniandikia majina matatu ya Spikakuwa nimethitibisha kuwa anaweza kusoma na kuandika.(Makofi/Kicheko)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba mwongozo wako.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Frank Mwakajoka.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa NaibuSpika, naomba mwongozo wako kwa Kanuni ya 68(7)ninataka mwongozo wako kwa watu ambao wanafanyamzaha, Wabunge ambao wanatumia nafasi hiyo kufanyamzaha ndani ya Bunge wakati hiki ni chombo muhimu sanana ni mkutano wa wananchi na wananchi wengi wanatakakusikiliza nini kinachozungumzwa kuhusiana na masualamuhimu ya kitaifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wapo Wabunge humundani ya Bunge wanafanya mzaha wanatumia Bunge hilikufanya mzaha kama michezo, michezo ambayo wanafanyahuko nje na wanalipwa na Bunge na hizi fedha ni fedha zawananchi. Lakini kilichozungumzwa leo na MheshimiwaGoodluck Mlinga kwamba Wapinzani wameshindwakuandika hotuba yao, nataka nimkumbushe pia kwambaujue kabisa kwamba hata Mawaziri wote hawa hawajawahikuandika hata siku moja hotuba zaowanaandikiwa, piawapo masekretari wanaandika. Kwa hiyo, hicho alichokuwaanakizungumza Mheshimiwa Goodluck Mlinga ni kituambacho hakifahamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunataka tumkumbushekwamba Sekretarieti ya Katibu wa Bunge wanafanyakazikubwa ya kuhakikisha kwamba wanaandaa hotuba zoteza Mawaziri.

MBUNGE FULANI: Sekretarieti ya Wizara.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Spika,Sekretarieti za Wizara wanafanyakazi kubwa kuhakikishawanaandaa hotuba, pia zote zilizowasilisha hapa...

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Frank Mwakajokaunaniomba Mwongozo mimi ukianza kumjibu yule maanayake wewe unachukua nguvu zangu mimi. Wewe omba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

mwongozo wa hilo jambo unalotaka kulisema hoja yako nanadhani umekwisha kueleweka. Unataka mwongozo juu yaalichokisema hapa ndani kwamba watu wanafanya mzahasi ndiyo? Nadhani hiyo ndiyo hoja yako, kwa hivyo kaaumeshaeleweka.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa NaibuSpika, ni mzaha kwa kweli mzaha umezidi ndani ya Bunge.

NAIBU SPIKA: Sawa umeshaeleweka. MheshimiwaKitwanga.

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa NaibuSpika, natumia Kanuni ya 68(7) Mwongozo wangu unahusumaelezo uliyoyatoa kuhusiana na uhakiki wa mali zetu. Kwawale ambao tulikuwa hatujapata barua, vithibitisho/vihakikivyetu viko katika maeneo yetu kule nyumbani. Tarehe 25 Junini karibu sana ukizingatia kwamba tarehe 26 Juni tunatakiwakuwepo Bungeni kupitisha bajeti ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mwongozo wakoje, haiwezi kutolewa nafasi zaidi ili tuweze kupeleka hiviviambatanisho baadae? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nimeombwamiongozo minne. Kwanza ni Mwongozo niliombwa naMheshimiwa Abdallah Bulembo, amehusianisha Mwongozowake na swali namba 454, amezungumzia wakulima wapamba kwamba wapo wakulima ambao wanalazimishwakufungua akaunti benki wakati maeneo menginewanaruhusiwa kuendelea kuuza pamba yao.

Sasa ametaja Mkoa wa Mara kwambawanalazimishwa kufungua akaunti wakati sehemu nyinginewanaruhusiwa kuuza pamba. Kwa sababu namna hata yeyealivyolizungumza ni kwamba Serikali ilishatoa maelekezokwamba hiyo siyo moja wapo ya mambo ambayo wakulimawanatakiwa kulazimishwa, kwa sababu benki kuna maeneoya vijijini ambapo hayajafika. Mwongozo wangu kwenyejambo hili ni kwamba watendaji walioko huko Mara ambao

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

wanalazimisha hawa watu kufungua akaunti waache,maana Serikali ilishasema jambo hilo.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, pia nimeombwaMwongozo na Mheshimiwa Goodluck Mlinga, akisemakwamba tangazo lililotoka kuhusu uhakiki wa mali tuendeleena hilo zoezi lisiishie kwenye kuhakiki mali, pia tuendelee nakuhakiki Waheshimiwa Wabunge kujua kusoma na kuandika.Ameeleza habari ambayo imetokea jana hapa naamelihusisha na hili tangazo la kuhakiki mali.

Waheshimiwa Wabunge, tangazo hili linahusu uhakikiwa mali haliwezi kuhusishwa na uhakiki wa sifa zaWaheshimiwa Wabunge kujua kusoma na kuandika. Kwasababu uhakiki huo huwa unafanywa kabla ya huyo Mbungekuwa na sifa za kugombea. Kwa hiyo, wakati akija hapamaana yake lazima atakuwa anazo hizo sifa ambazozimeainishwa Kikatiba na Kisheria.

Waheshimiwa Wabunge, nimeombwa Mwongozo naMheshimiwa Frank Mwakajoka naye anatoa hoja yakekwamba anataka kujua mzaha ambao hutokea mara nyingihumu ndani na kwamba Waheshimiwa Wabunge maranyingine tunatumia muda huo kufanya mzaha badala yakufanya mambo ya msingi.

Waheshimiwa Wabunge, wakati akitoa maelezoyake ameelekeza mzaha huo kwa Mheshimiwa GoodluckMlinga, ni wazi kwamba Mwongozo aliokuwa anauombaalikuwa amesimama hata kabla Mheshimiwa Mlingahajapewa fursa ya kuzungumza. Kwa hiyo, WaheshimiwaWabunge kwenye jambo hili la mzaha anaodhaniwakwamba amefanya Mheshimiwa Mlinga kwa kutumia mudahapa ndani ni namna ile ile ambayo Mbunge mwingineanakuwa amesimama na kuzungumza mambo ambayohayana uhusiano na jambo ambalo linakuwa lipo mbeleyetu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

Waheshimiwa Wabunge, hivyo mnakumbushwaWaheshimiwa Wabunge kuzingatia kanuni zetu zinachosemaili tusifanye mzaha na hasa pale ambapo wanakuwepowageni, hii haimaanishi kwamba Mheshimiwa Mlingaalichokifanya ndiyo mzaha.

Waheshimiwa Wabunge, nimeombwa Mwongozo naMheshimiwa Charles Kitwanga akielezea kuhusu tangazonililolitoa lililotoka kwa Katibu wa Bunge kuhusu tarehe yamwisho ambayo Waheshimiwa Wabunge mnatakiwakuwasilisha taarifa zinazohusu uthibitisho wa mali zenu amavielelezo vya mali na madeni yaliyoko nje na ndani ya nchi,ili Tume yetu iweze kufanyakazi yake kwa ukamilifu naMheshimiwa Kitwanga ameeleza kwamba kwa mudauliotolewa kwa wale ambao hawakupewa taarifa na Tume,inaweza ikawa ngumu kuwasilisha vielelezo hivyo maanamtakuwa bado mpo Dodoma na hamjapata nafasi yakwenda kuvifuatilia.

Waheshimiwa Wabunge, yako makundi mawili hapa,kundi ambalo walishaambiwa wawasilishe hivyo vyeti,wawasilishe vielelezo vya mali zao basi wao wafanye hivyo.Kwa hili kundi la pili ambalo halikuwa na hizi taarifatutaangalia namna ya kuwasiliana nao ili pengine vielelezohivyo viweze kuwasil ishwa katika muda ambaoWaheshimiwa Wabunge mtakuwa mmesharudi Majimbonikwenu na kuweza kuvikusanya na kuvipeleka.

Kwa hiyo, hoja hii ya hili kundi la pili ambalohalikupata hizo taarifa basi tunalifanyia kazi na nadhanimtapata tangazo kwamba sasa mnatakiwa kupeleka linikwenye hiyo Tume.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya hayotunaendelea, Katibu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

NDG. PAMELA PALLANGYO - KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2017 na Mpango waMaendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Na

Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirioya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa

Fedha 2018/2019

(Majadiliano yanaendelea)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, majadilianoambayo tulianza jana yanaendelea leo. Kwa hiyo, ninayoorodha ya majina hapa ya wachangiaji kutoka kwenyevyama vyetu. Tutaanza na Mheshimiwa Mussa Mbarouk,atafuatiwa na Mheshimiwa Zuberi Kuchauka na MheshimiwaRichard Mganga Ndassa ajiandae.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuruMwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya njema na kuwezakuchangia katika hotuba hii ya Wizara ya Fedha. Pili,ninawashukuru wapiga kura wangu wa Jimbo la Tanga kwaushirikiano ambao wananipa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza kuchangia kwenyeMpango. Katika kitabu cha mpango, ukurasa wa tisa,limeelezwa kwamba pato halisi la Serikali limefikia trilioni 50vilevile pia ni ongezeko la karibu trilioni 3.35 ukilinganisha namwaka 2016.

Sasa hapa naona kuna marekebisho kidogo kwasababu ukipiga hesabu vizuri, mgawanyo wa pato la Taifakwa kipato cha kila Mtanzania kupata shilingi 2,275,601,000

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

kutoka shilingi 2,086,168,000 za mwaka 2016 naona panahitajimarekebisho kidogo. Namuomba Waziri alifanyiemarekebisho hili ili kusudi hesabu hizi zikae sawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikija kwenye suala lamfumuko wa bei. Katika Mpango ukurasa wa 12 kwenyekitabu kimeeleza kwamba mwenendo wa mfumuko wa beiulikuwa tulivu. Sasa ukisema kwamba mfumuko wa beiulikuwa tulivu wakati tuna mifano hai katika mwezi Mtukufutu wa Ramadhani uliopita juzi ambapo leo ni siku nne tanguumemalizika, naona sio sawasawa. Kwa nini nasema hivyo?Kwa sababu ukiangalia bei ya kio moja ya tambi kutokashilingi 1,800 ilipanda mpaka shilingi 2,500 vilevile pia sukarikutoka kilo moja shilingi 2,000 ilipanda mpaka shilingi 2,500,ngano kutoka 1,200 ilipanda mpaka shilingi 1,800, vilevile piamafuta ya kula kutoka shilingi 2,200 kwa lita yalipanda mpakashilingi 3,000. Sasa tukisema kwamba eti mfumuko wa beiulikuwa tulivu naona hilo haliko sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalonataka kulizungumza katika kitabu chetu hiki cha Mpangoni katika ukurasa wa 55 kuna ubia kati ya Sekta ya umma nasekta binafsi. Nimeona kwamba wamezungumzia zaidikatika masuala ya viwanda kwamba sekta ya ummaishirikiane au iwe na ubia na Serikali lakini kuna vyanzo vingineambavyo vingeweza kuisaidia Serikali kimapato. Kwamfano, kama Serikali ingeweza kuingia ubia na sekta binafsina kuweza kujenga viwanja vya michezo kama vile michezoya football, basketball, golf na tennis, angalau pia tungekuwahapo tumeweka mazingira mazuri kati ya Serikali na sektabinafsi na ingeweza kutupatia kipato kwa sababu katikamipango hiyo sikuiona katika kitabu, sasa nashauri mipangohiyo nayo iingizwe katika Mpango wa Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni uandaaji wawachezaji wetu. Nchi za wenzetu nyingi zimekuwazinanufaika baada ya wachezaji wao kuwa wanachezakatika nchi za Ulaya. Kwa mfano, nchi kama Nigeria, Senegal,Mali, Tunisia, Algeria na nyinginezo, wameweza kukusanyamapato, hata Brazil Serikali inakusanya kodi kutoka kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

wachezaji kwa sababu kunakuwa na maandalizi maalum,lakini katika kitabu hiki sijaona kama kuna mpango wakuiendeleza sekta ya michezo kupitia hivyo viwanja hata kwawachezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ambalonataka kulizungumzia sasa niende moja kwa moja kwenyebajeti yetu. Katika bajeti kuna kitu ambacho ninakionahakiko sawa, kwa mfano, katika bajeti ya Wizara ya Kilimotumeona hapa kuna upungufu wa karibu asilimia 23 ambayoni sawasawa na karibu kwa mfano katika fedha za koroshokuna pesa ambazo zilikuwa ni shilingi bilioni 211 za Mikoa yaKusini, hizi zimeleta mkanganyiko, hazijapelekwa nahazijulikani ziko wapi.

Sasa atakapokuja Waziri hapa atueleze pia kwaninininagusa kwenye zao la korosho kwa sababu na sisi Tangakatika baadhi ya maeneo korosho zinalimwa. Sasa ikiwaimeguswa Mikoa ya Kusini maana yake na Tanga piaimeguswa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni katikakupunguza kodi kwa taulo za kike. Mimi naipongeza Serikalikwamba imepunguza kodi, lakini katika siku za karibuni miminilichangia nikatoa mfano wa nchi ya Kenya. Rais UhuruKenyatta alitia saini sheria ambayo Kenya watazitoa taulobure badala ya kusema wanapunguza kodi. Kwa ninininalisema hili? Kenya wameondoa kodi lakini wakaamuapia zitolewe bure, hapa katika viwanda ambavyo vinazalishahizo taulo za kike, baadhi ya viwanda vimepunguziwa tukodi, lakini baadhi ya kodi zipo. Kwa hiyo, tufikirie walewatoto wa kike ambao wako maeneo ya vijijini, hiyo tauloya kike iliyokuwa inauzwa shilingi 3,500 hata ikiuzwa shilingi1,500 bado kwao itakuwa ni tatizo kwa sababu hawana njiaza kipato ambazo zitawawezesha kulipia taulo hizo za kike.Kwa hiyo, naishauri Serikali badala ya kuondoa kodi, zitolewebure kwa watoto wa kike. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ambalonapenda kulichangia ni kuhusu wastaafu. Serikali yetu kwanza

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

katika kipindi cha miaka miwili hii tumeshindwa kuongezamishahara ya wafanyakazi. Sasa bado pamoja na kushindwakuongeza mishahara, kuna tatizo la wastaafu, walewaliokuwa watumishi wa Serikali waliongezewa kutokashilingi 50,000 mpaka shilingi 100,000 tena wanalipwa kilamwezi, lakini wale waliokuwa watumishi wa mashirika yaumma bado wako pale pale katika kiwango cha shilingi50,000 na wanaendelea kulipwa shilingi 50,000 tena kwamalimbikizo baada ya kila miezi mitatu.

Kwa hiyo, naishauri Serikali kwanza hawa wastaafuwaliokuwa katika Mashirika ya Umma nao waongezewewafikie shilingi 100,000 lakini walipwe kila mwezi na isiwewanalipwa kila baada ya miezi mitatu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ninalopendakulizungumza ni deni la ndani tumeambiwa ni himilivu, lakinibado kuna wazabuni ambao wana-supply vyakula katikamagereza, katika shule na taasisi nyingine ambazo zinahitajivyakula kama vile hospitali. Wazabuni hawa wenginewanapelekwa mahakamani, wanadaiwa kwa muda mrefuna kila mwaka imekuwa inatolewa ahadi tu kwambawataanza kulipwa.

Kwa hiyo, nashauri Serikali ituambie hapa/Waziriatakapokuja atuambie ni lini wataanza kuwalipa wazabuniambao wanaidai Serikali. Kwa mfano, katika Jiji letu la Tangawapo wazabuni wengi tu ambao wanadai ambao wame-supply vyakula magerezani, hospitalini na shuleni, lakininimeshuhudia wengine wanataka kufilisiwa, walichukuamikopo kwenye benki, wanashindwa kulipa mikopo ile lakiniSerikali inaendelea kuwapa ahadi. Naitaka Serikali ijibukwamba ni lini wazabuni wale watalipwa fedha zao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni katikamiradi. Miradi bado inapelekewa fedha kwa kuchelewa nafedha hizi zinakuwa hazitoshi na bahati mbaya mara nyingizinapelekwa katika robo ya mwisho ya mwaka wa fedhawa Serikali matokeo yake sasa miradi baada ya kuwa fedhazimeshafika Wakurugenzi, wataalam na wanaohusika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

wengine inapelekwa haraka haraka matokeo yake inakuwachini ya viwango. Kwa hiyo, naishauri Serikali iendeleekupeleka fedha mapema lakini pia namtaka Waziri wa FedhaTanga katika Halmashauri yetu tumetenga shilingi milioni 300kwa jengo la Hospitali ya Wilaya na tulikwishaanzakipindikilichopita (mwaka jana) tukajenga administrationblock kwa takriban shilingi milioni 400 lakini sasa hatujapatafedha kwa ajili ya kuweka hii OPD, kwa hiyo naiomba Serikaliituongezee fedha ili tuweze kujenga jengo la OPD.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo jingine ni kuhusuwastaafu wanaotarajiwa kustaafu, kama Serikaliimeshindwa kuwalipa wafanyakazi au kuwaongezeamishahara katika miaka miwili hii, je hawa watakaostaafumwaka huu, Serikali ina fedha za kuwalipa? Naombaatuthibitishie Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwamba hatawatakaostaafu waweze kulipwa fedha zao. Kwa nininalisema hili? Naogopa kwamba Watanzania wataendeleakuwa maskini na mtu baada ya kustaafu anakuwa hana umrimrefu, anapoteza maisha kwa sababu anakuwa hanakipato. Kwa hiyo, ninamtaka Waziri atakapokuja hapa ajeatuambie kwamba wamejiandaa vipi kuwalipa wastaafuwanaotarajiwa kwa sababu watumishi wengi wa Serikali niwastaafu watarajiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mwisho…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda waMzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa muda wakoumekwisha.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zuberi Kuchauka,atafuatiwa na Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa,Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu ajiandae.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante na mimi kunipa nafasi nitoe mchango wangukwenye hii bajeti iliyoko mbele yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niombe tu kusemakwamba hii bajeti tatizo kubwa haiakisi maisha ya wananchiwetu wa kawaida na ndiyo maana kuna baadhi ya watuwengine wanasema hii bajeti ni bajeti hewa, kwa sababuukiangalia kwenye vipaumbele vilivyoandikwa hapahaijaakisi kabisa maisha ya wananchi wetu wa chini. Kwamfano, kwenye miradi hii ya kipaumbele, ukiiangalia hatakwenye bajeti wamesema kwamba hailetewi fedha zakutosha, hakuna fedha ambazo zimeenda huko fedha zakutosha. Kwa mfano, wamesema kwamba miradi yakipaumbele kama vile Rufiji. Rufiji mwaka jana ilitengewashilingi bilioni 220 hivi lakini wakaipeleka shilingi bilioni tatu,sasa unashindwa kuoanisha tatizo liko wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo kubwa ambalonaliona bajeti hii inaanza kuharibika tangu kwenye mipango.Mipango tunayopanga na tunapokwenda kutekelezatunatengeneza vitu tofauti. Niwatolee mfano, kwenyemipango utakuta kuna miradi ya LNG, Mkuza, kuna huomradi wa Rufiji, kuna Special Economic Zone, kuna makaaya mawe, kuna General Tyre, mambo ya barabara nakufungamanisha kwamba uchumi na maisha ya wananchi.Lakini tunapokwenda kutekeleza, tunatekeleza vitu vingineambavyo havimo kwenye mpango.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano kwenye bajetiiliyopita hapa nimesikia kuna majengo ya Chuo Kikuuambayo hayakuwemo kwenye mpango, lakini yamejengwa,kuna ujenzi ule wa Magomeni Quarter umeanza kujengwalakini kwenye mpango haukuwemo, kwenye ukuta pamojana kwamba ni jambo zuri kwenye huo ukuta wa Tanzanite,haukuwemo kwenye mpango lakini umejengwa. Kwa hiyo,utakuta kuna miradi ambayo inakamilika ujenzi wake, haimokwenye mpango, lakini ile miradi ambayo imo kwenyempango hailetewi fedha. Kwa hiyo, kufeli kwa bajeti hiikunaanzia tangu kwenye mipango yetu kwa sababu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

tunachokipanga sicho tunachokitekeleza. Tunapanga kamaTaasisi, kama mpango, Wachumi wanakaa wanapangalakini inapokuja kwenye utekelezaji mtu anatoa matamkomengine yanafanyika mambo mengine, matokeo yake zilefedha ambazo zilitakiwa ziende huku, zinaenda huku. Kwahiyo kwa msingi huu, nasema kabisa kwamba bajeti hiihaiwezei kukidhi matakwa ya wananchi wetu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi tunaingia kwenyenchi ya viwanda na uchumi wa kati, hivi kweli kamatunakisahau kilimo, hatutaki kuwekeza kwenye kilimo tunadhamira kweli ya kwenda kwenye viwanda? Haiwezekanikwenye bajeti ukapanga asilimia 0.4 ziende kwenye kilimo,kilimo ambacho kinaajiri zaidi ya asilimia 65 ya Watanzaniahalafu mkasema kweli tuna nia thabiti, mimi siwezi kuungamkono jambo hili. Kwa mfano, unaona kwamba mifugoimepangiwa 0.1, uvuvi ndiyo kabisa, mmeua mmepangia0.06 maana yake tuendelee kula wale samaki wa Chinaambao wanakuja miaka mitatu iliyopita. Sasa tunaposemakwamba hii haiakisi maisha ya wananchi tunamaanisha hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano mimi natokaLiwale, wananchi wangu kule ni wakulima siyo wafugaji,wale ni wakulima lakini sasa naomba nimuulize MheshimiwaWaziri, wakulima wale mimi nikawaambie nini kwenye bajetihii? Sisi zao letu la uchumi kule ni zao la korosho,mmeshalihujumu, zile export levy zimeshapotea, mpaka leohii hatujui mbolea, pembejeo tunapataje! Hivi mimiwatakaponiuliza kwamba bwana eeh! umekaa Dodomamiezi mitatu unachangia bajeti, hivi kama wananchi waLiwale tumeletewa nini wakulima? Sasa hivi hawanauhakika wa ufuta, yaani bei za ufuta hazijulikani, masokohayajulikani.

Mheshimiwa Naibu Spika, juzi hapa mmetangazakwamba zao la ufuta litanunuliwa kwa stakabadhi ghalani,mmewapa Bodi ya Maghala ndiyo washughulikie hilo, lakinimpaka leo hawajaandaa chochote na ufuta sasa hivi ndiyouko sokoni, kwa hiyo, mipango hii tuanyopanga haiakisimaisha ya wananchi wetu. Tunaposema hii bajeti siyo rafiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

kwa watu wetu tunamaanisha hiyo kwa sababu wenginemipango hii hatunufaiki nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano nakuja kwenyehoja ya kufungamanisha, mnasema kwamba mnaendakuandaa akaunti moja (collection account) kwambamapato yote ya nchi hii yakusanywe kwenye akaunti mojahalafu Serikali au Hazina ndiyo wagawe. Jambo hili siyo sahihisana pamoja na kwamba nia yenu ilikuwa ni nzuri. Kwamwenendo wa upelekaji wa fedha za mafungu haya kwenyeHalmashauri zetu au kwenye Taasisi husika na hii sasamnakwenda kuua. Mmeshaiua Halmashauri, tumejua vyanzovyote vya Halmashauri mmevichukua mkavipeleka Hazinana hamrudishi, sasa hivi mnaenda kuua mifuko, hii mifukoambayo ilitengewa fedha maalum.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo sababu juzi nilikuwanachangia, Waziri wa Fedha nilikuwa nachangia kwambaSerikali hii ya Awamu ya Tano hatuoni fedha zile ambazozilikuwa za mafungu maalum zamani kiingereza wanaita,kuna fedha ambazo zilikuwa ring fenced, sasa hivi kwenyeAwamu ya Tano hizo fedha hazipo tena na sasa hivi ndiyomaana mnaleta hii sera kwamba mnataka kuweka akauntimoja ili muendelee kuua hiyo mifuko na mnapoua hiyo mifukomaana yake, kwanza mlitakiwa mjiulize kwa nini hii mifukoiliundwa, je, yale mahitaji ya hii mifuko imeondoka? Na kamamahitaji ya hiyo mifuko bado ipo kwa nini sasa mnaiondoa?Kuiondoa hii mifuko maana yake sasa mnakwenda kuuamalengo yaliyopangwa kwenye hiyo mifuko. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa kodi ndiyomaana bajeti zetu zinashindwa kutekelezeka, kwa mfanokwenye miradi ya maendeleo hatujawahi kufika asilimia 50ya utekelezaji wa bajeti yetu. Pamoja na kwambammeongeza, walipa kodi wameongezeka mkumbukekwamba walipakodi wameongezeka lakini kiwango chakodi kinachokusanywa kinazidi kupungua. Kwa mfano,kwenye page ya tano ya kitabu cha Mwenyekiti amesema;tatizo la kupungua kwa shughuli za uwekezaji nchini ndiyosababu inayosababisha uchumi wetu kudorora wameeleza

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

kabisa kwamba shughuli za uwekezaji zimepungua. Sababunyingine wamesema mitaji inahamishwa na hapa tulishawahikuwaambia kwamba wafanyabiashara kwa mazingira hayamliyowawekea sasa hivi wafanyabiashara wanahamishamitaji. Wafanyabiashara wanahama, tukiwaambiamnakataa, matokeo yake ndiyo haya kwamba watu mitajiwanahamisha na mazingira ya uwekezaji bado siyo mazuri,kodi zimekuwa nyingi hazielewekina usumbufu vilevile. Kwahiyo, haya mambo yote haya tunashindwa kuelewa,mipango yetu hii inatupeleka wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano kama mnazohizo mnazoita Economic Zones, pesa hampeleki! HalafuEconomic Zone zingine ambazo tayari watu wamelipwa ilikuacha uwekezaji pale uendelee halafu uwekezaji hakuna,maana yake pale kwanza wamepoteza fedha za kulipa watufidia halafu hatuna mipango. Hatuna mpango ambaotunaweza kwenda kuutekeleza.

Sasa hii mimi nashindwa kuelewa, hasammeshindwaje ninyi kama Serikali kufungamanisha kilimo naviwanda? Msitegemee hizi nyanya ambazo mnazikuta hapoMorogoro, hizi nyanya watu wachache wanaweka palebarabarani ndizo ambazo mnataka kuvijengea viwanda.Hebu fungueni milango watu wawekeze kwenye kilimo, watuwakija kuwekeza kwenye kilimo ndipo mtaweza sasakuendeleza hivyo viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nitolee mfano mmoja,jana Spika alisema hapa anashangaa kwa nini bajeti ya Kenyaiko juu kuliko ya kwetu, sababu wenzetu wa Kenyawamejiwekeza kwenye kilimo, sisi tumekataa kuwekezakwenye kilimo. Asilimia 60 ya nafaka inayosindikwa Kenya niya kwao wenyewe lakini sisi asil imia 98 ya nafakainayosindikwa Tanzania ni kutoka nje. Mfano mzuri miminilikuwa msindikaji wa nafaka wa aina ya ngano, asilimia 90ya ngano inayosindikwa Tanzania ni ya kutoka nje, kwa nini?Ardhi tunayo, tena ardhi nzuri lakini hakuna uwekezaji na walahamfikirii kutafuta wawekezaji kwenye kilimo cha kisasa,kilimo cha kibiashara.(Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

(Hapa kengele ililia kuashiria kumalizika kwa muda waMzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa, kengele ya pili ilishagonga.Nilikuwa nasubiri umalizie sentensi, naona unaendelea nakwa mfano mwingine. Ahsante sana.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa,atafuatiwa na Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu, MheshimiwaDavid Silinde ajiandae.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa nafasi hii nami niweze kuchangiamapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato namatumizi kwa mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kusemakwamba naunga mkono mapendekezo haya ya Serikali kwaasilimia mia moja, lakini nimpongeze sana MheshimiwaWaziri, Naibu Waziri pamoja na wafanyakazi wake kwamaandalizi mazuri kwa kweli ya hotuba hii. Nina ushauriambao ningependa kuutoa, lakini kwa sababu tukienda kwawenzetu hawa wa TRA kwa sababu yote tunayozungumzahumu ndani lazima pesa zipatikane, wala siyo vinginevyo,wala sio maneno. Sasa ni namna gani ofisi yako MheshimiwaWaziri wa Fedha inaweza ikapata hizi shilingi trilioni 18ambazo tumeipa jukumu la kuzitafuta TRA. Sasa ni lazimakwanza ile mianya ya upotevu lazima tuizibe. Lakiniwafanyakazi wenyewe wa TRA ambao wanafanya kazi nzurisana, sina mashaka na TRA wanafanya kazi nzuri sana nandiyo maana mapato kila mwaka kila mwezi yanaongezeka.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ni wajibu wetu sasa,Mheshimiwa Waziri hakikisha hakuna shilingi hata mojainayolala nje, pesa ya Serikali hata senti moja inayolala nje,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

hakikisha kwamba kila shilingi inayokusanywa lazima iingiendani.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukija kwenye nidhamu yamatumizi ya fedha, yapo matumizi mengine kwa kwelihayafanani, hayafai. Ili tuwe na pesa nyingi za kutosha nilazima tunapozipokea, tunapozikusanya, lazima tuwe nanidhamu ya kuzitunza na kuzitumia. Ipo miradi mikubwa,naomba kwa sababu tunacho Kitengo chetu cha TISS kwenyeile miradi mikubwa ili kwenda kui-verify kama kweli hiyo pesaimetumika kama inavyotakiwa. Nashauri Mheshimiwa Waziriwa Fedha watu hawa kwa sababu wapo na kazi yao ni mojani kuangalia upande wa pili, je, pesa hii imetumika vizuri?

Mheshimiwa Naibu Spika, nimuombe MheshimiwaWaziri wa Fedha, moja ya eneo ambalo mapato ya Serikalihuwezi kuyapima, kuyaona vizuri na eneo hilo kila mwakatumekuwa tukilalamika na ukiuliza watu wanatupiana mpirani pale bandarini.

Mheshimiwa Naibu Spika, floor meter watakwambiaimepona, lakini ukienda kwenye uhalisia Mheshimiwa Waziriwa Fedha eneo lile ni eneo muhimu kweli kweli kamalitasimamiwa, kwa sababu mimi nia yangu ni kupata mapatomengi siyo vinginevyo, tupate mapato mengi ili kusudi pesahizo ziweze kwenda kusaidia mambo mengine huko.

Sasa pale kwenye floor meter Mheshimiwa Waziri waFedha hebu pelekeni timu pale, TISS waingilie kati liko tatizo.Watakwambia wamechelewesha kushusha sijui, kuna linkagesijui, kuna temperature sijui, maneno matupu yale, liko tatizokubwa sana pesa nyingi zinapotea pale. Ni lazima tufanyeutaratibu Mheshimiwa Waziri wa Fedha, pesa hizi ziwezekukusanywa kama inavyotakiwa. Lakini ili tukusanye kamainavyotakiwa lazima pale watu wa TISS waendewakaangalie upya.

Mheshimiwa Naibu Spika, jamb la pili nikushukuru sanaMheshimiwa Waziri wa Fedha, mwaka jana tuli letamapendekezo kwako kuhusu hii michezo ya kubahatisha.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

Mwanzo nafikiri hukuwa unanielewa vizuri, kama nilivyosemamimi nia yangu kwa kweli ni kutafuta namna ya kukusaidiawewe kutafuta vyanzo vingine vya mapato. Hata ukipatashilingi mbili, shilingi tatu, shilingi nne, ukiziongezea kwenyezingine ukakusanya huku na huku chungu chako kitajaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sanaMheshimiwa Waziri wa Fedha mwaka jana ulikubali, nanimeambiwa kwamba kutoka kwenye bilioni 27 ambayozilikuwa zimekadiriwa mpaka juzi hapa mmeweza kupatashilingi bilioni 64. Sasa kama tukisimamia vizuri na yalemapendekezo niliyokuletea kwa nia njema kabisa wala siyovinginevyo, nia ni kukusanya lile eneo likisimamiwa vizuri eneolile utatoka kwenye shilingi bilioni 64, shilingi bilioni 70utakwenda mpaka kwenye shilingi bilioni 100 au zaidi. Lakinini lazima hayo mapendekezo uyapitie vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo hili ni technical kidogona mtu anaweza akafikiri kwamba hivi hii Gaming Board ninini, hivi nayo ina hela? Lakini ukienda Marekani, Las Vegaspale wanaishi lile Jimbo ni kwa sababu ya casino tu. Kwahiyo, eneo hili Mheshimiwa Waziri wa Fedha nikuombe sanayale mapendekezo ambayo tumekuletea, uyaainishe vizuriili yaje kwenye Finance Bill. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikuombe tena hapo,michezo hii ili wote tupate kwa maana ya mchezaji, Serikalina Mwekezaji lazima zile asilimia uziweke vizuri. Kwa sababuutakuta kwa mfano, BIKO, TatuMzuka na mwingine Bethawako kwenye Gross Gaming kwenye GGR, sasa kwa niniunawatenganisha wakati wao wote wanafanya mchezommoja. Kwa hiyo, nikuombe sana Mheshimiwa Waziri ilitupate pesa nyingi za kutosha na ziende zikafanye kazikwenye maeneo yetu hili eneo nalo nafikiri ungelitazama vizurizaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nije kwenye suala la mwishokabla kengele haijalia. Naunga mkono mapendekezo yaKamati ya Bajeti, lakini mimi hasa kwenye hii skipper hii siyombaya sana kwa sababu itatupeleka kuzuri. Lakini liko tatizo

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

hebu litazameni vizuri tusije tukafika pahala MheshimiwaWaziri wa Fedha tukaanza kuulizana maswali kwa sababutender yake ilitangazwa mwaka 2016, ikagota pahaliikapelekwa kwa AG ndiyo sasa imekuja tena sina tatizo nao,lakini kwa nini ilipelekwa kwa AG, AG alishauri nini lakiniuwekezaji wao nani anaujua kweli kama ni shilingi bilioni 44nani anaujua. Maana yake mtu anaweza akasema miminiwekeza shilingi bilioni 44 na hapa nikikaa nitakusanya 66nani anajua kwamba ni kweli uwekezaji wake ni shilingi bilioni44. Ni jambo jema lakini ni vizuri Mheshimiwa Waziri wa Fedhaukajiridhisha zaidi ili kusudi yasije yakajitokeza kama yale yaEFDs.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sanaMheshimiwa Waziri wa Fedha, naunga mkono. Huo ndiyoulikuwa ushauri wangu. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Mussa AzzanZungu, atafuatiwa na Mheshimiwa David Ernest Silinde,Mheshimiwa Ibrahim Hassanali Raza ajiandae.

MHE. MUSSA A. ZUNGU: Mheshimiwa Naibu Spika,awali ya yote nikushukuru kwa kunipa nafasi, nimshukuruMheshimiwa Waziri na Naibu wake na wataalam wote waWizara kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa maslahi ya Taifaletu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nipongeze mwongozo waMheshimiwa Rais kwa kuongoza nchi iwe na mwelekeo waviwanda, iwe na mwelekeo wa kizalendo kwa watu wote.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ina-introduceElectronic Tax Stamp (ETS) ni jambo ambalo zuri sana naukitizama tumechelewa, lakini uhakika wa source ya revenueya Serikali utapatikana kwa utaratibu wa mfumo huu waElectronic Tax System (ETS). Lakini nilitaka kujiridhisha tu auSerikali imejiridhisha vipi na huyu aliyepewa kazi hii, duediligence ilifanywa na nani? Kwenye semina tumeambiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

wamefanya Mabalozi, lakini ukitizama taarifa mbalimbali,hii kampuni ina matatizo makubwa. Hii kampuni ina kesiMorocco, wamefanya price offering mara kumi zaidi ya nchizingine walizofanya kazi hii. Kampuni hii inachunguzwa naBunge la Kenya, kwa malpractice. Kampuni hii imeziangushaSerikali zingine kutokana na mfumo wake wa malpracticena corruption. Sasa Mabalozi hawa waliofanya due diligenceya kampuni hii, mimi nitapenda waitwe waje waulizwetaarifa zao walizipata wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tulifanya semina; TRA naWabunge na hoja zilizoulizwa na Wabunge kwenye seminaSerikali walizi-defer, walishindwa kuzijibu. Kutokana na hojaza msingi za kizalendo ambazo Wabunge wameuliza.

Mheshimiwa Naibu Spika, TTCL chombo cha umma,kwa gharama za mradi huu wa bilioni 48, mimi binafsinaomba Serikali i-revisit mpango wake wa kuajiri watu wanje kusimamia makusanyo ya kodi nchini Tanzania. Unapo-surrender sovereign ya tax regime ya nchi kwa kampuniambayo tayari ina matatizo makubwa kama haya dunianina sever ya kampuni hii ni mali ya vendor mwenyewe.Naiomba Serikali tena na nia njema ku-support mpango huuwa ETS, lakini bado ningeomba shughuli hii ifanywe na TTCLambacho kina uwezo, chombo cha umma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, unaposema information zavendor huyu zitakwenda kwenye data center, kuna njia nyingisana za ku-under declare traffic kwenda kwenye data centerya Serikali. Kuna command nyingi sana za mitandaounaweza uka-hide information zingine. Kwa hiyo, mpangohuu ni mzuri naunga mkono asilimia 100, lakini naombaSerikali i-revisit jambo la ku-surrender regime ya tax kwaKampuni ya nje ambayo tayari ina misuguano kwenye nchinyingi sana. Kwa hiyo, naomba kazihii nzuri, ni muhimu kwaTaifa letu lakini wapewe TTCL.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2008 tulishauriSerikali kuhusu masuala ya wizi wa declaration za traffic

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

kwenye mitandao ya simu. Serikali ikanunua mtambo,walituambia walinunua mwaka 2008 kumbe hawakununua,walimuweka Mwekezaji ambaye kaja na mtambo wake wagharama za 50 billion wakaingia mkataba wa miaka 15,which was very wrong. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, masuala ya mitandao serverkama ni mali ya vendor utapigwa tu na tumepigwa natunaendelea kupigwa. Kwa hiyo, hoja yangu tulihoji hatagharama ya mtambo wenyewe na huu mkataba kwenyesemina tumeambiwa ni miaka mitano. Miaka mitano mtuanasimamia sovereign ya regime ya kodi nchini na hakunapopote ambapo tumepewa comfort ya forensic audit yamtambo wake atafanya nani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna nchi nyingi wamewekahii system, kuna kitu kinaitwa new generation quickly response,hoja kubwa ni makusanyo lakini ku-cub na kuzuia elicit goodskatika soko ambalo ni jambo zuri sana. Mitambo hiiinayowekwa sasa hivi huu sijui, kwa new generation mimi nawewe ukienda dukani unatumia app yako ya simu kuwezakuona stamp ile na goods ambazo ziko mitaani ni genuine.Sababu stamp za mitaani ambazo siyo genuine hazitakosaku-have return ili kuthibitisha unatumia simu yako una-logkwenye ile code ya stamp inakwambia hii ni genuine au siyogenuine. Sasa tulitaka kujiuliza mtambo huu ambao Serikaliwanatuambia walishainigia mkataba unayo app kama hiiambayo kujiridhisha mfanyabiashara, consumer kuweza kujuahii stamp iliyowekwa hapa ni kweli stamp ya Serikali namwananchi wa kawaida anaisaidia Serikali kwa kwendakatika maduka au katika supermarket aki-log in pale palena simu yake na yeye anapewa majibu kuwa hii ni stamp yaSerikali au ni stamp ya mitaani, nilitaka kujua hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, server inapokuwa ni maliya vendor si rahisi kwa TRA au Serikali kujua under declarationya ripoti yoyote ya vendor, siyo rahisi. Kwa hiyo, nilikuwanaomba, naunga mkono mpango huu naunga sana 100percent. Ombi langu uwekezaji huu ni mdogo sana,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

tuiwezeshe TTCL ifanye hii kazi siyo chombo kutoka nje.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Bombardier mpyazinatolewa Q400 New Generations, abiria 96 (96 passengers)flies Dar es Salaam - Dodoma siku zote watu wanakosa nafasi.Huduma nzuri, performance nzuri, tukipata Bombardier Q400New Generations ya abiria 96 gharama za uendeshajizitashuka, tutakuwa na abiria wengi kwenye ndege. Kwahiyo naomba Waziri wa Fedha hili nalo alitizime, kuwezakununua New Generation Bombardier Q400 ili tuwezekupunguza gharama za uendeshaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na Taarifa yaKamati ukurasa wa 47 chombo hiki kiendeshwe na mamlakaya umma ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Zungu.Mheshimiwa David Ernest Silinde atafuatiwa na MheshimiwaIbrahim Hassanali Raza, Mheshimiwa Mendrad Kigolaajiandae.

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipatia fursa hii na mimi nichangiehotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka jana tukiwa ndaniya Bunge lako tukufu kipindi tunapitisha bajeti humu ndanikama hii Bajeti Kuu, nakumbuka makofi yaliyokuwayanapigwa humu ndani kwamba bajeti hii haijawahi kutokeayaani haina mfano! Mwaka jana tukajenga hojatukaonekana sisi kama vile mwaka jana hatueleweki. Sasamwaka huu siku ya Alhamis wakati Waziri Mpangoanawasilisha bajeti yake, nakumbukua maneno ya Spikamwishoni ana-windup anasema jamani haya ni mapendekezoya bajeti, siyo bajeti haijawahi kutokea ni mapendekezo. Kwasababu gani, kwa sababu yale yote waliyoyaahidi mwaka

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

jana with confidence, hayajatekelezeka. Kwa kifupi kwa maraya kwanza ukisoma hotuba yake yaani unaona kabisa nibajeti ya kukiri kushindwa, bajeti ya kuomba msaadaanaomba Simon wa Kirene kwenye bajeti aje ashuke, abebemsalaba wa zege humu ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma ukurasa wa 81wametajwa viongozi humu ndani, mashuhuri. Alipowatajamimi nilikuwa nawakumbuka ikabidi nirudi tena nisome upya,ili niainishe hawa viongozi waliotajwa kwenye dunia, viongozimashuhuri na uchumi wetu wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mtu wa kwanzaaliyewekwa Deng Xiaoping, Rais wa Pili wa Jamhuri ya China,wakati anaingia madarakani alisema, to embrace peopleto be rich (kuwafanya wananchi kuwa mtajiri). To be rich issomething to be glorious, Deng Xiaoping. Haya yapo kwenyehotuba ya Mheshimiwa Mpango haya kayasema, sasa tu-compare na kwetu, sisi tunataka watu wetu wawe matajiri?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna kauli tumezisikia wote,tunataka matajiri waishi kama mashetani. Akatajwa Rais waPili, Lee Kuan Yew wa Singapore, huyu aliibadilisha Singaporekutoka dunia ya tatu kuwa dunia ya kwanza. Jambo lakwanza baada ya kupata madaraka, alifanya jambo moja,alisema lazima tuhakikishe watu wetu wanapata ajira (topromote stable employment jobs) kwa sababu Singaporeunemployment ilikuwa iko juu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo ya msingi yakujifunza kwa huyu Rais wa Pili wa Korea, moja yeye ali-promote private sector, Singapore uchumi wake ni privatesector. Sisi angalia private sector inavyolia leo, inalia siyokawaida. Nenda kwenye mabenki angalia uchumi wakekule, mabenki yameporomoka, tumekaa na NBCwanakwambia imeshuka mpaka faida, dividend ya Serikalihakuna. Tumekaa na NMB, tumekaa na watu wa privatesector wanailalamikia Serikali kwamba hatuwekezi kwaprivate sector. Haya aliyasema Rais wa Pili huyu ambaye

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

amekuwa compared hapa, hizi sifa hizi yeye ali-promoteprivate sector. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Lee alikujaTanzania mwaka 1973 pale UDSM, miaka hiyo akinaMheshimiwa Chenge walikuwepo pale, akaja pale naMwalimu Nyerere akamwambia Mwalimu hii sera yako yaujamaa na kujitegemea njia hii siyo sawasawa, alizomewakweli na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakatihuo. Alipozomewa akasema mimi nilichokisema ndiyo hiki,hii njia mliyochukua siyo sawasawa. Juzi nikamsikia KatibuMkuu wako wa chama anasema turudi ujamaa nakujitegemea! Mnakotupeleka siko. Kama unatumia mifanoya watu ambao waliwajali watu wa chini kuinua uchumihalafu comparison how? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Dkt. Mahathir Mohamed waMalaysia, unajua kabisa Malaysia imeendelea kwa mfumowa PPP (Public Private Partnership). Haya tueleze sisi publicprivate, tunasema reli tutajenga wenyewe, ndege tutanunuawenyewe, Stieglers’ Gorge tutanunua wenyewe, kwa nini,tutakopa, mwisho wa siku huu mfumo unaotumika sasa ukoTanzania tu. Duniani kote miradi mikubwa Serikali ina engagemiradi mikubwa ya kiuchumi pamoja na private sector, lengoili gharama zinazobakia, baadhi ya gharama ziende kusaidiawananchi. Sasa mikopo tunayochukua ni ipi, mikopo yakibiashara na hii mikopo ya kibiashara tunayoichukua unajuamaturity yake ni ndani ya muda mfupi miezi sita. Nilizungumzawakati wa Wizara ya Fedha kwamba, jambo la reli (standardgauge) siyo baya, lakini matokeo yake reli kabla haijaishatunaanza kulipa mkopo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii nakueleza ukweli, Waziriwa Fedha asipodhibiti Deni la Taifa tunakwisha. Kwa sababu,mwisho wa siku angalia kwenye hotuba yake kwenye uleukurasa ambao ameainisha ile bajeti yake nafikiri ni kamaukurasa wa 78, soma mapato anayoyapata. Mapato yaSerikali Kuu ya ndani anategemea kupata trilioni 20, lakinikwa miaka yote hawajawahi kuzidi trilioni 14, hapo ni kama

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

amekusanya asilimia 100. Ukija ukiangalia kwenye matumizi,Deni la Taifa, trilioni 10, mishahara trilioni saba, matumizimengineyo trilioni tatu, trilioni 20, hayo ni first and secondcharge, jukumu la kwanza na jukumu la pili, wana uhakikawa kukamilisha? Kuna miradi ya maendeleo, hakuna?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana ukipitia bajetinzima mwaka huu trilioni 10 hawajakusanya, miradi yamaendeleo haijafanyika, Halmashauri zina-suffocate! Hayatunawaambia kwa nia njema. Sasa unamgusa mtu kamaNelson Mandela amekaa jela miaka 27, mtu wa kwanza,hebu fikiria mtu aliyekufunga ndiyo unamuweka kuwaMakamu wako wa Rais, Frederik Willem de Klerk. Halafu yulealiyekuwa anamtesa Mandela ndiyo alikuwa bodyguardwake mpaka anakwenda kabirini, ndiyo alikuwa Chiefbodyguard, yule gerezani aliyekuwa anamtesa miaka 27,anayemfanyisha Mandela kazi ngumu mpaka akaumwa TBndio alikuwa bodyguard wa Mandela. Niambie wa kwetuangefungwa hata miezi sita ingekuwaje? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati fulani mnakimbiavitu. Hebu kwa mfano unataka umuige Mandela,tumekuletea hotuba ya kurasa 521 unakimbia hotuba,mtaweza tabia za Mandela? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, unajua wakati mwinginekama unakimbia maoni halafu unataka kuwa Mandela, hizindio tunaita nadharia. Utekelezaji ni tofauti na nadharia.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mwalimu Nyerere huyu sifazake hazielezeki, ana sifa kweli na mimi ninakiri kwambaMwalimu Nyerere anapaswa kuwa Mwenye Heri kama KanisaKatoliki wanavyotaka, kwa sababu gani, aliunganisha Taifa.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, akina Mtei wale waKaskazini walikuwa Magavana wake. Watu wale wa Usalamawa Taifa, Mkuu wa Usalama walikuwa ndiyo watu wake

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

waliokuwa wanamsaidia, akina Ndugu Kombe wale na akinanani, leo huwezi kusema Taifa moja la upande huu, sijuiKaskazini wasubiri, hawa hivi, haiwezekani! (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Naibu Spika,nilipewa dakika 15 na nimeweka stop watch hapa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Silinde, nadhani unayonakala ya Kanuni zako hapo, Kanuni ya 99(12) uchangiajikwenye bajeti ni dakika 10 siyo 15. Hata ukipewa zile dakika10 ndiyo unaweza kugawanya kwa watu wawili, Kanuni ikowazi kabisa. Kwa hiyo, huwezi kuwa na dakika 15, maliziasentensi uliyokuwa unazungumza.

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Naibu Spika, it isok. Sina shida na suala la ETS, mkitaka kushughulika nendenimpaka kwenye simenti, sigara na mafuta, lakini mfano wakewa mwisho wa Park Chung Hee wa South Korea, yule…

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Silinde.(Makofi)

Tunaendelea na Mheshimiwa Ibrahim Hassanali Raza,atafuatiwa na Mheshimiwa Mendrad Kigola, MheshimiwaMahmoud Mgimwa ajiandae.

MHE. IBRAHIM HASSANALI MOHAMMEDALI RAZA:Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasihii. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uwezo napumzi yake kusimama hapa kuchangia bajeti hii muhimusana katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwakumshukuru Mheshimiwa Waziri na Naibu wake, MheshimiwaDkt. Ashatu Kijaji, pamoja na timu yake nzima kwa jinsiwalivyoandaa hii bajeti ya fedha ambayo itatusukuma

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

mpaka 2019. Hongereni sana Mheshimiwa Waziri na timunzima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile niwashukuruwenzetu wa TRA. Unajua tunapozungumzia masuala ya bajetiya Serikali lazima tuwashukuru na wenzetu wa TRA namnawanavyohangaika kutafuta mapato ambayo yanatusaidiawananchi. Bila TRA kukusanya mapato leo hapa tusingewezakuzungumzia bajeti hii. Kwa hiyo, nimshukuru sana KamishnaCharles Kichere na timu yake nzima ya TRA kwa jinsiwanavyofanya kazi nzuri ya kukusanya mapato. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naweza kusema sasa hivikwa kiasi fulani TRA wamekuwa marafiki sana kwawafanyabiashara na wameweza angalau kukaa kwenyemeza kumaliza yale matatizo ambayo wafanyabiasharawamekuwa wanahangaika nayo. Kwa hiyo, lazima tuwapesifa TRA tofauti na miaka ya nyuma hawakujenga mahusianomazuri na wafanyabiashara lakini sasa hivi wamekuwawasikivu na wenye nidhamu ila baadhi yao bado siyowaaminifu lakini kwa asilimia kubwa wanafanya kazi nzuri.Nawapongeza sana TRA. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue nafasi hiikumpongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufulikwa sababu bila nguvu zake tusingefika hapa tulipo. Watuambao wanataka tusimsifu Rais, hivi jamani kwenye Bungehili tumsifu Uhuru Kenyata au tumsifu Museveni? Sisi tuko hapakumsifu Rais John Pombe Magufuli, hatuko hapa kuwasifiaMarais wa nchi nyingine, huo ndiyo ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kiongozi yeyote anapofanyamazuri usitegemee wapinzani kukusifu sana hiyo ni kawaida.Nchi zote duniani hakuna chama kinachoongoza wananchihalafu wapinzani wakakisifu, si India, Ulaya hata hukoMarekani. Kwa hiyo, nimwambie tu Mheshimiwa Raisasivunjike nguvu, aendelee na katika miaka yake miwili nanusu tumeona mambo makubwa aliyofanya RaisMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kushirikiana naWaziri Mkuu na Mawaziri. Mawaziri wa Awamu hii ya Tano

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

wamekuwa ni Mawaziri ambao wanafanya kazi usiku namchana, kwa hiyo, niipongeze Serikali nzima ya MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nizungumzie bajeti hii.Kwanza niipongeze Wizara kwa kuondoa VAT katika masualahaya ya taulo kwa sababu kweli yatawasaidia akina mamana wanafunzi kwa kiasi kikubwa sana, nimpongeze sanaMheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuzungumziakuongezea ushuru baadhi ya bidhaa kwa nia ya kuvilindaviwanda vya ndani. Kwa kweli, tulikuwa tunawafanyiabiashara kubwa wenzetu wa nchi jirani, wao wanatuleteahapa sisi tunafanya manunuzi tu, tunawachumia wao, ajirazinakwenda nchi za jirani, nchini kwetu viwanda vinaumiana wafanyakazi wakati mwingine wanapunguzwa. Katikakuongeza Ushuru wa Bidhaa katika bidhaa mbalimbali hatuahiyo itavilinda viwanda vyetu vya ndani. Namshukuru sanaMheshimiwa Waziri na timu yake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikija katika masuala yanguo zetu za mitumba, naomba Wizara hii iangalie kwa jichola huruma hizi nguo za mitumba kwa sababu huwazinatumiwa na wananchi wa hali ya chini kabisa Tanzaniahii. Nguo za mitumba zinauzwa rahisi, kila mmoja wetuanajua zinakwenda mpaka vijijini na mikoani. Sasa hivicontainer moja la mitumba linatozwa shilingi milioni 40.Naomba tu Wizara, kama kuna uwezekano wa kupunguzaangalau kidogo tukawapa nguvu hawa wananchi wa chiniambao hawawezi wakanunua shati la Sh.40,000 au Sh.50,000wajipatie mashati hayo kwa bei rahisi na hii itatusaidiakujenga uhusiano mzuri na watu wa chini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile niombe Waziriaangalie sana sekta ya kilimo kwa sababu ni sekta mojamuhimu sana katika nchi yetu ya Tanzania na asilimia 70 yaWatanzania wanategemea kilimo. Kwa hiyo, namwombasana wakulima wawezeshwe, wapatiwe mikopo, wapewe

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

initiative ambayo itawasaidia kuwekeza katika kilimo. Kilimokikiwa kizuri Tanzania tutapata foreign exchange. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nchini India wanategemeasana agriculture, wana-export kwa hali ya juu. Serikali ya Indiainapata pesa nyingi sana katika kwa ku-export bidhaa zaagriculture. Hata wenzetu wa Thailand kwa kiasi kikubwacha fedha wanategemea export ya agriculture. Kwa hiyo,siyo vibaya nasi tukaipa umuhimu sana sekta hii ya kilimoambayo kwa kiasi fulani itatusaidia kupata foreign exchangekwa sababu, njia kubwa ya kupata foreign exchange ni kuuzamazao yetu nje. Sisi Tanzania Mungu ametupa ardhi kubwasana ambayo mimi naweza kusema asilimia kama 40hazijatumika, bado tunayo ardhi ya kuwekeza katika kilimo.Tukikipa umuhimu kilimo basi Serikali yetu itapata foreignexchange. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna kasoro kidogoimejitokeza, wafanyabiashara wengi Dar-es-Salaam hawanamashine za EFD, wanatumia receipt book. Serikali inakosamapato, TRA inakosa mapato na naona hawawatendei hakiwafanyabiashara wengine wanaotumia mashine za EFD. Kwahiyo, naomba TRA kupitia Wizara yako ihakikishe katika kipindicha miezi miwili kila mfanyabiashara anatumia mashine yaEFD.

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa, muda wakoumekwisha.

MHE. IBRAHIM HASSANALI RAZA: Mheshimiwa NaibuSpika, naunga mkono asilimia 110. Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Mendrad Kigola, atafuatiwa na MheshimiwaMahmoud Mgimwa na Mheshimiwa Murad Saddiq ajiandae.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii na mimi niwezekutoa mchango wangu kwenye mapendekezo ya Serikali.Nianze na kuipongeza Serikali kwa kuleta mapendekezoambayo yanalenga sisi Wabunge tutoe mapendekezo yetuili bajeti itoke vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna maeneo mengineSerikali imefanya vizuri sana, kwa mfano, ku-promoteviwanda vya ndani na ili uweze ku-promote viwanda vyandani lazima udhibiti bidhaa zinazotoka nje. Kwa hiyo,kupunguza kodi kwenye baadhi ya bidhaa ambazo tunawezatukazalisha sisi wenyewe ni mpango mzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeona hata kwenyemafuta ambayo tunaweza tukazalisha, tunalima alizeti natuna viwanda vya alizeti, ili ku-promote hivi viwanda vifanyekazi vizuri wamepandisha kodi kwenye mafuta yanayotokanje, hiyo ni sawa, lakini lazima tuhakikishe tunapata soko lauhakika la ndani ili wazalishaji wafanye vizuri. Kwa hiyo, hilona mimi nakubaliana nalo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, halafu la pili ni bajeti. Bajetiya mwaka huu 2018/2019 tumeenda na shilingi trilioni 32.5mwaka jana tulikuwa na shilingi trilioni 31.6. Kuongezeka kwabajeti ni kitu kizuri sana kwa sababu inalingana na mahitajiambayo tunayo. Hatuwezi kusema mahitaji ya mwaka janani sawa na mahitaji ya mwaka huu. Kila mwaka mahitajiyanaongezeka na bajeti inaongezeka, huo ni mtizamo nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, mikakati ya Serikalikukusanya mapato siyo mibaya isipokuwa kwa sababutumesema tunataka ku-promote vitu ambavyo tuna uwezowa kufanya wenyewe ni jambo zuri sana. Kwenye ukusanyajikwa mfano kuna Electronic Stamping Tax System, kamaalivyoongea Mheshimiwa Zungu ni system nzuri sana kwa ajiliya kuongeza mapato ndani ya nchi yetu. Hapo naunga

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

mkono kwa mtazamo wa kudhibiti mianya ya ukwepaji kodini suala zuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna issue ambayoWabunge wengi tunajiuliza, hivi hatuna wataalam pale TRA,vijana wetu ambao wanasoma vyuo vikuu nje wakashindwakusoma hii system, tukaidhibiti wenyewe, tukaanzisha ndaniya nchi na tukaitumia kukusanya, kwa hiyo, tumeshindwakabisa? Kwa sababu unapofanya investment ukionaanaweza aka-recover within one year, atapata faida kubwasana. Kwa mfano, yeye atawekeza kwa thamani ya shilingibilioni 48 lakini katika hesabu za haraka haraka wamefanyaanalysis kwa mwaka mmoja anaweza akapata shilingi bilioni66, tofauti yake ni shilingi bilioni 18 ambayo yote inaendanje.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikawa ninajiuliza kamakuna zaidi ya shilingi bilioni 18 ndani ya mwaka mmoja,recoverage ya costs ikafanyika mwaka mmoja, kwa ninitusingesomesha vijana tukachukua hata shilingi bilioni 5wakaenda kusoma nje wakarudi wakafanya kazi TRAwakakusanya kodi? Hili ni suala la kujiuliza sana. Hivi kunaumuhimu gani kuchukua makampuni ya nje waje wakusanyefedha yetu halafu wapeleke pale, sisi tukawa tumeshindwa.Mwaka wa pili kuna- possibility ya shilingi bilioni 66 zikaendanje. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakumbuka siku mojatulifanya semina hapa, vijana wetu MaxMalipo vijana wetuwasomi wa hapa hapa Tanzania siku ile Wabunge tuliwapigiamakofi sana pale ukumbuni wali-present issue za kukusanyakodi na wakasema kwamba wako worldwide sasa hivi. Hawavijana wa MaxMalipo wameshindwa kufanya utafiti wakukusanya kodi? Labda tuwaite, tuwaulize itakuwajewameshindwa kufanya makusanyo ya humu ndani nawakienda kwenye nchi nyingine wanafanya vizuri na kusifiwa,lazima tuangalie sana. Halafu ule mkataba tumeweka mrefusana ni mpaka miaka mitano. Tungeweka labda hata miaka

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

mmoja au miwili ili tuangalie matazamio lakini miaka mitano,nadhani hii lazima iangaliwe vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ya Bajetitumependekeza vizuri sana, tumesema system siyo mbaya ninzuri nia ni kudhibiti na tunataka tudhibiti hata uzalishaji wamaji. Tunajua maji ni muhimu, tulikuwa tunafikiria kufanyaexemption kwenye product za maji ili watu waweze kupatamaji, watumie maji safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naongea na Nduguyangu hapa Mheshimiwa Charles Kitwanga, yeye alishafanyakazi Benki Kuu na utaalamu wa masuala ya electronics,nikamuuliza hivi wewe kama Mbunge mtaalamumeshindwaje ku-advise tuangalie hii system, kweli nimem-challenge hapa. Amefanya kazi BoT karibu miaka kumi nasystem ya tax collection anaijua. Ameshindwa kunijibu vizurilakini naendelea kumuuliza lazima Wabunge wataalamwatusaidie katika collection ya tax katika nchi hii na tunatakatax revenue iwe juu. Ndiyo maana kuna Wabungewanachaguliwa wataalam. Kwa hiyo, nimeona hili suala nila msingi sana nilielezee hapa ili siku nyingine tusianzekulalamika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine natakaniipongeze Serikali kwenye mgao wa fedha hasa ile ya vijanana wanawake. Point ambayo nimeipenda pale, ile asilimia5 kwa vijana na asilimia 5 kwa akina mama Serikali imesemahakuna interest, cha msingi ni usimamizi mzuri, hilo ni jambozuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ambalo nichallenge hasa Wizara ya Fedha, ule Mfuko Mkuu fedha yotemtakusanya kutoka Halmashauri, kutoka Serikali za Mitaa,na sehemu zote mtakusanya pale, halafu Halmashauri ikitakakutumia itaomba kufuatana na mahitaji. Challenge ambayoipo pale urudishwaji wa fedha unachukua muda mrefu sana.Lazima tuwe makini, Wizara ya Fedha lazima iwe active

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

katika kurudisha fedha Halmashauri. Tunaweza tukawa tunasystem nzuri ya kuweka kwenye akaunti moja lakiniHalmashauri inaweza ikatuma maombi ya kupewa fedha iliwatumie mkachelewesha. Hili lazima tutoe angalizo kwaSerikali, kwamba kama Halmashauri zimeeomba fedha ontime basi wapewe fedha on time. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Halmashauri yanguya Wilaya ya Mufindi kuna fedha ya maji na Waziri wa Majialiahidi kwamba mwezi Mei angeweza kuipeleka ile fedha.Wameomba kuanzia Machi tunaenda Julai ile fedhahawajapewa mpaka leo. Ni mradi wa maji mmoja tu. Sasanajiuliza kama mradi mmoja Mkurugenzi wa Halmashauriakishirikiana na Engineer ameandika request, vigezo vyoteviko pale, tena ni shilingi milioni 270 mpaka leo Juni mradiwa maji kule umesimama Kata ya Mtwango wananchihawana maji. Kupeleka shilingi milioni 200 ni kazi ya siku mojatu, mimi nikikaa kwenye komputa just a minutenimeshapeleka transfer ya hela zile, lakini mpaka leohazijapelekwa. Je, tukisema wapeleke shilingi trilioni kadhaakwenye Halmashauri itachukua muda gani? Hii ni bajeti yamwaka mmoja mmoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, sasa hivi Wizaraya Fedha ina shilingi trilioni 12 ambazo nyingi ni miradizinapitia pale. Naomba Serikali, system ni nzuri ndiyo maananaiunga mkono, lakini utendaji kazi lazima tuongeze juhudi,lazima tuende na muda. Bahati mbaya sana sisi huwa hatujalimuda.

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa, kengele mbilizimeshagonga.

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Mahmoud Mgimwa atafuatiwa na MheshimiwaMurad Saddiq na Mheshimiwa Lucy Magereli ajiandae.

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hiikwa kumpongeza ndugu yangu Mheshimiwa Dkt. Mpangopamoja na dada yangu Mheshimiwa Dkt. Ashatu. Kwanamna ya kipekee, nimpongeze sana Mheshimiwa Dkt. JohnPombe Magufuli kwa kazi nzuri na ya kizalendo anayoifanyakatika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimwambie Nduguyangu Mheshimiwa Silinde namheshimu na najua wakatimwingine anachangia vizuri, lakini kuna watu katika nchizingine wanampongeza Mheshimiwa Dkt. Magufuli anafanyavizuri. Profesa Patrick Lumumba mpaka amembandika jinana kumuita Magufulification kutokana na performance yake.Kuna watu wanataka kujifunza the way Mheshimiwa Dkt.Magufuli anavyofanya kazi nzuri katika nchi ya Tanzania. Kwahiyo, mnyonge mnyongeni lakini kuna maeneo tunafanyavizuri. Katika nchi za Afrika Mashariki na Kati hata wenzetuwa Kenya wanatamani Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli awe Rais wao. Ameweza kusimamia matumizi yapesa kwa nidhamu na kuna baadhi ya mambo makubwaambayo tumeweza kuyafanya kwa hela yetu hiyo ya ndani.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni rasimu ya bajeti nasiyo bajeti. Sisi Wabunge ni wajibu wetu kuikosoa nakuielekeza Serikali kwenye maeneo ambayo tunaona kunaupungufu. Kwa hiyo, tukikataa kabisa kwamba hakunajambo la maana lililofanywa kwenye hii rasimu ya bajetitutakuwa tunakosea. Yapo mambo mazuri Mheshimiwa Dkt.Mpango amekuja nayo nasi lazima tuyaunge mkono.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi ni viongozi wa wananchi,tumetoka kwenye Majimbo yetu, pamoja na uzuri wa rasimuhii ya bajeti lakini kuna maeneo Mheshimiwa Dkt. Mpangoalitakwa ayaangalie kwa ukaribu sana kwa sababuyanawagusa watu direct. Kwa mfano, eneo la kilimo linaajiriWatanzania wasiopungua asilimia 66.6 na yeye anajua, lakiniukiangalia bajeti iliyokwenda kwenye eneo hili hairidhishikabisa. Tunaomba aliangalie maana tulitakiwa tuweke bajetiya kutosha kwa sababu kwenye eneo hili kuna ajira, kunausalama wa chakula, kuna malighafi ya viwanda ambapotunataka twende kwenye uchumi wa viwanda. Sasatusipowekeza vizuri kwenye eneo la kilimo tunategemea nini,tutaendaje kwenye uchumi wa viwanda? Kwa hiyo,namwomba sana Mheshimiwa Dkt. Mpango tuliangalie marambili eneo hili la kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia wenzentuambao tumesoma bajeti pamoja nchi za Afrika Masharikina Kati, asilimia 10 ya bajeti nzima ndiyo wametenga kwenyebajeti ya kilimo, lakini bajeti yetu haifiki hata asilimia 3. Sasatujiangalietutafika huko. Shilingi bilioni 170 against shilingitriolioni 32 wapi na wapi? Tutakwenda kwenye uchumi waviwanda kweli? Kwa hiyo, Mheshimia Dkt. Mpango naombasana eneo hilo tuliangalie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni Benki yaMaendeleo ya Kilimo ambayo anaiongoza mwenyewe. Walewatu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo hawapeleki hela kwawakulima. Walianza na mtaji wa shilingi bilioni 60, ukakuaukafika shilingi bilioni 67, wakakopa mpaka wakafika shilingibilioni 287, lakini tujiulize kwenye shilingi bilioni 287 ni kiasi ganiwamewakopesha wakulima? Utakuta hela zile wanazokopana wenyewe wanaenda kuweka dhamana kwenye mabenkimengine, ndiyo madhumuni ya kufungwa hiyo benki? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Dkt.Mpango kwenye jambo hili nataka awaambie tumeanzishaBenki ya Maendeleo ya Kilimo kwa ajili ya kuwasaidia

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

wakulima siyo kwa ajili kufanya biashara. Wafanye yaleambayo tumekubaliana katika uanzishaji wa Benki hii yaKil imo, kwenye jambo hil i hatuko sawa. Mahitaji yaWatanzania kwenye eneo hili ni shilingi bilioni 800 lakini hatashilingi bilioni 287 zingekuwa zinakwenda direct kwawakulima sasa hivi wakulima wangekuwa wamebadilikakwenye eneo hili. Kwa hiyo, naomba eneo hili tuliangaliesana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ambaloamelizungumzia ni suala la Bodi ya Mazao Mchanganyiko,amesema wanataka kuunganisha Bodi. Mheshimiwa Dkt.Mpango, hawa wananchi ndiyo wanatengeneza hela zaopale, mnataka mfanye nini pale, interest yenu ni ipi? Kamakuna watu wana ubadhirifu wa hela si wapelekweMahakamani. Wamelalamika kwenye maeneo ya korosholakini hakuna hata mtu mmoja mpaka leo amepelekwamahakamani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, sikubaliani na hojaya kutaka kuunganisha Bodi, kwenye eneo hili siwezikukubaliana hata kidogo. Mkitaka kwenda vizuri kwenyeeneo hili angalieni Bodi za Udhibiti (Regulatory Board) zinatozo mbalimbali ambazo hazina ti ja na tozo hizozinawagandamiza sana wakulima na kuwaongezeagharama. Kwa hiyo, naomba tuangalie sana kwenyemaeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wana shida ya majina Wabunge wote tulikuwa tunasema hapa tunataka majina mpaka tukasema tuko tayari kuwashawishi watu wetukuongeza tozo la shilingi hamsini, lakini hakuna respond yoyotetuliyopata. Mwaka jana collection ya ndani iliyokuwainatakiwa iende kwenye maji ilikuwa shilingi bilioni 250 lakinimpaka tunakuja kwenye bajeti ni shilingi bilioni 26 tu ambayoni asilima 11 ya collection ya ndani ambayo ilikwenda kwenyemaji. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye bajeti ambayoilikuwa inatokana na Mfuko wa Maji ya shilingi bilioni 158 helazote karibu zimekwenda kwenye miradi ya maji. Kwa hiyo,tukiongeza kwenye eneo hili tutafika mbali. Sasa Wazirihajakubaliana na shilingi hamsini angesema basi niwafikiriehawa Wabunge hata niwape shilingi thelathini au shilingiishirini, akituacha hivi anatuacha solemba. Kazi ya Wabungeni kuishauri na kuisimamia Serikali, lakini inawezekana ikawakila siku tunashauri hakuna hata siku moja mmewahikuchukua mawazo ya Wabunge mkaamua kuyafanyia kazi.Kwa hiyo, tunaomba eneo hili mliangalie.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine MheshimiwaDkt. Mpango amezungumza vizuri sana kuhusu kusamehekodi kwenye chakula cha mifugo, yuko sahihi. Kamaunasamehe kodi kwenye chakula cha mifugo halafu unatozakodi kwenye mashudu umesamehe wapi sasa hapo?Unasamehe kushoto kulia unachukua hela ya wananchi.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, sikubaliani na hiyohoja, hujasamehe hapo. Umetuvisha blanketi hapo, kwambanimesamehe kodi kwenye chakula cha mifugo halafuunasema mashudu yatozwe VAT, haiwezekani. Kamatumeamua kusamehe kodi, iwe ni kwenye maeneo yote ilikusudi tupate tija kwenye eneo la kilimo.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ambalonapenda kuchangia ni suala la viwanda vya maziwa nanyama. Mheshimiwa Waziri yuko sahihi, ameamua kuvilindaviwanda vya ndani kwa kuongeza kodi ya mazao ya mifugokwa maana ya mazao ya nyama na maziwa yanayotokanje ya nchi, lakini tunavisaidiaje viwanda vya ndani hapa.Namwomba ili kusudi twende kwenye ushindani halali,maana sasa hivi maziwa yetu ukilinganisha na maziwa yaKenya na yanayotoka Uganda maziwa ya Tanzania gharamazaidi.

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mahmoud, kengele ya piliimegonga, malizia hiyo sentensi.

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru, naunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Murad Saddiq atafuatiwa na Lucy Magereli naMheshimiwa Rose Kamili ajiandae.

MHE. SULEIMAN A. SADDIQ: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba nikushukuru sana asubuhi ya leo na mimi kunipatianafasi niweze kuchangia mawili, matatu katika bajeti hii yaTanzania kwa mwaka 2018/2019. Naomba niseme naungamkono hoja asilimia mia kwa mia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianze kwakusema, sasa hivi tuna kaulimbiu ya Tanzania ya Viwanda.Katika kauli mbiu hii naomba nimpongeze sana MheshimiwaRais anaisimamia kauli yake hii kwa vitendo. Sisi kama Kamatiya Viwanda na Biashara tulipata changamoto mbalimbaliza wadau katika maeneo mbalimbali. Katika bajeti yamwaka huu, naomba nimpongeze sana Waziri wa Fedhachangamoto nyingi zimefanyiwa kazi na Serikali, zimefanyiwakazi na TRA kwa maana hiyo Rais wetu anatekeleza kwavitendo kauli yake ya Tanzania ya Viwanda. MheshimiwaWaziri, Naibu Waziri na TRA wote nawapongeza sanakwamba sasa tunakwenda vizuri sana katika eneo hili laTanzania ya Viwanda.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naanza na suala hili laelectronic stamp. Naunga mkono hoja, sina matatizo kwanimapato yataongezeka, uhakiki wa uzalishaji utafanyika lakiniwasiwasi wangu ni eneo moja la gharama. Kampuniambayo mnaingia nayo ubia TRA na Serikali kuna viwangowameeleza, kuna dola 6, 10 na 13. Unapozungumzia dola 6unazungumzia soft drinks, unapozungumzia dola 10unazungumzia alcohol, unapozungumzia dola 13unazungumzia spirit, sigara na vitu vingine.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu haina coins yaSh.10, 20 au 30, tuna coins ya Sh.50 na 100 ambazo nazo nichache sana. Mimi ni mdau nina Super Market, tuna shidakubwa sana ya coins ya Sh.100 na 200. Leo tunaposema dola6, huyu bwana atanunua stamp Sh.1,000 atazalisha chupa1,000, ina maana kila chupa moja imepanda Sh.13. Sodaleo inauzwa Sh.500 kwa kutumia utaratibu wa electronicstamp, anatakiwa auze Sh.513, tunapata wapi coins Sh.13?Maana yake ni kwamba wafanyabiashara watauza Sh.550,ile stamp sasa itatoka Sh.13 ya ukweli itakwenda kwenye Sh.50.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye bia wanasema dola10 sawasawa na Sh.23. Hatuna coins ya Sh.23, atatoka kwenyeSh.23 ataenda kwenye Sh.50 kwa maana stamp sasa pale niSh.50. Naomba TRA na Serikali mlifanyie kazi hili, gharamaziko juu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi naomba kidogo niulizeswali, je, wakati mna-bargain na hii kampuni, mliwaelezaukweli wa uzalishaji wa volume za chupa Tanzania? Leotunazalisha chupa zaidi ya bilioni 10 za soda, juisi, bia navinywaji mbalimbali, viwanda vimekuwa vingi. Unapofanyabiashara na mtu unatakiwa ufanye bargain, volume ya bilioni10 chupa si volume ndogo. Kama ni dola 6 lazimawapunguze wafanye dola 2 au 3, volume ni kubwa sana yahizi chupa.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, TRA walikwenda navolume halisi? Walifanya uhakiki kwenye viwanda? Mbonawenye viwanda wanasema hawajafanya uhakiki huo auuhakiki wanatumia uwakilishi wa return zao kwenye TRA?Kama wanatumia uwakilishi wa return za TRA bado liko tatizo.Kwa sababu kuna viwanda vinazalisha lakini hawapelekireturn za ukweli TRA, wanadanganya na Kamati tuliwashauriwafanyabiashara wawe wakweli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mimi kwenyeupande wa ETS (Electronic Tax Stamp) sina tatizo. Tatizo langu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

hizo gharama ambazo zipo mwisho zitamwangukia mlaji,Tanzania hatuna coins hesabu zake tutazifanyaje? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, upande wa mashine za EFDtumeanza kupata matatizo. Mwezi mmoja nyuma serveriliharibika, wafanyabiashara siku nne, tano tulishindwakupelekea returns reports zetu matokeo yake mapato kidogoyalipungua. Hata leo napozungumza mimi hapa bado ileserver haijakaa sawa, EFD bado inasumbua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri waFedha amefanya juhudi kubwa, mimi na Mheshimiwa Ndassatulimwona na tulimpa na ushahidi na tunawasifu sana naNaibu Waziri walifanya kazi kubwa lakini bado server ya EFDhaijatengemaa, je, imehujumiwa? Leo Mheshimiwa Waziriameondoa kodi ya EFD, je, server iko sawasawa? Kamakwenye EFD mashine ndogo hizi tunachemka, je, kwenyeelectronic stamp tutakuwa na hali gani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ushauri wangutuangalie upande wa gharama. Naunga mkono, itaongezamapato, itafanya uhakiki, hatutaibiwa lakini tunali-handlevipi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niende kwenyeeneo la pili la industrial sugar. Sisi Kamati yetu ya Viwandatulipata malalamiko mengi kuhusu refund ya VAT na ile ya15%. Wafanyabiashara ambao ni Big Five: Cocacola KwanzaPepsi, Azam, Nyanza Bottlers na Bonite wanaidai Serikali zaidiya shilingi bilioni 35. Fedha hizi ni mitaji yao ya ndani,hawajapata ile return yao ya 15%. Kamati imewashauriwaendelee kuvumilia, Serikali inalifanyia kazi suala lao.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu katika eneohilo, nia ya Serikali ya kudhibiti watu ambao si waaminifu ninjema, ndiyo maana tunawatoza 15% . Sasa tubadilike,badala ya kutoza 15% tuweke penalt, faini ambazozitasababisha Serikali kupata mapato ya moja kwa moja.Hizi fedha si zetu ni zao, tunatakiwa tufanye refund. Tuweke

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

audit team maalum, kila miezi mitatu iende kwenye viwandahivi ihakiki Industry sugar imetumika kiasi gani, industry sugarambayo haikutumika viwandani, wapigwe faini na penaltna ikiwekana wakirudia makosa wafutiwe leseni. Kwautaratibu huu wa kuchukua refund zao tunawanyima mitajiyao. Leo mitaji mingi imelala Serikalini na wanalalamika sana.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niingie eneo la kilimo (agri-business), nazungumizia kilimo cha biashara. Tanzania tunaeneo kubwa na ardhi nzuri sana, maji ni mengi lakini badoSerikali haijawapanga wananchi na wakulima wake waingiekwenye agri-business. Leo nenda Dubai wana kila aina yamatunda duniani lakini wale supplier wanafanya packagingnzuri, wanaweka matunda yao katika hali ya usafiwanafanya export. Matunda ya Dubai yanatoka Malaysia,Indonesia, India ns Vietnam. Embe linatoka maeneo ambayomaembe ya Tanzania ni mazuri zaidi. Twende kwenye agri-business tuwahamasishe watu wetu ili tusonge mbele zaidi.Katika maeneo ambayo yana ardhi nzuri, rutuba nzuri, mfanoMikoa wa Mbeya na Morogoro, tuna maeneo mazuri yaMpunga, kwa nini Serikali isihamasishe watu wawekezekwenye maeneo hayo?

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. SULEIMAN A. SADDIQ: Mheshimiwa Naibu Spika,najua ni kengele ya kwanza.

WABUNGE FULANI: Ya pili.

MHE. SULEIMAN A. SADDIQ: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba nimalizie kwa kusema naunga mkono hoja, yangumengine yote nitayaandika kwa maandishi. Ahsante sana.(Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Lucy Magereli, atafuatiwa na MheshimiwaConchesta Rwamlaza, Mheshimiwa Fakharia Shomar Khamis ajiandae.

MHE. LUCY S. MAGERELI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru nami kupata fursa kuchangia Bajeti Kuu yaSerikali mwaka 2018/2019. Nianze tu kwa maelezo ya awaliambayo ningetaka niyaweke katika utaratibu ambaotumeutumia wakati wote kama Wabunge wa Kambi yaUpinzani, kama Kamati za Bunge tunapokuwa tunatekelezamajukumu yetu ya kuishauri Serikali, kama wadau wamaendeleo ya nchi hii tunapotaka kutoa ushauri wetu kwaSerikali na pia kwa wananchi wetu ambao ndio picha halisiya kazi ambayo inafanywa na Serikali ya Chama chaMapinduzi na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Biblia, Kitabu chaYeremia 33:3, neno linasema hivi:-

“Niite nami nitakuitikia na nitakuonesha mambomakuu, magumu usiyoyajua.” (Makofi)

WABUNGE FULANI: Ameen.

MHE. LUCY S. MAGERELI: Mheshimiwa Naibu Spika,kutokana na maelezo yangu ya awali kwamba kamaWabunge, kama Kamati, kama wadau wa maendeleotumekuwa tukiishauri Serikali hii lakini bado imeendeleakutuletea mipango ambayo ni copy and paste, yenyemambo yale yale ambayo hayatekelezeki, basi nimefikirilabda we need God’s intervation. Labda tusali sasa, kwasababu kwa maneno tu kwa kusema kwa kuandika, kwakuhubiri tumesema sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilitamani nikuletee memokwenye Kiti chako nikuombe labda leo Bunge hili tulibadilisheliwe nyumba ya Ibada halafu niongoze maombi, halafu naWabunge wanijibu kwa kusema twakuomba utusikie. Kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

sababu sijaomba, basi naomba tu muwe wasikivu, mnisikilizeniombe.

Mwenyezi Mungu nakuomba uwakumbushe Serikaliya CCM kwamba wananchi wanataka huduma za maji,afya, elimu bora na sio ndege ambazo hawatozipandampaka wanakufa. (Makofi)

Mwenyezi Mungu nakuomba uwakumbushe Serikaliya CCM waache kutuletea mipango ya maendeleo hewa.(Makofi)

Mwenyezi Mungu ninakuomba uwakubushe Serikali yaCCM kwamba wananchi wa Simanjiro walihitaji maji kwasababu sasa hivi wanakunywa maji katika bwawa moja nang’ombe, hawakutaka ukuta Mungu wakumbushe hilo.

Mwenyezi Mungu naomba uwasaidie kuwakumbushaSerikali ya CCM...

T A A R I F A

MHE. MARTHA J. UMBULLA: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kumpa taarifa Mheshimiwa Mbunge.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Magereli pamoja nakwamba unasali naona kuna Mbunge anataka kukupataarifa hapo. Kwa hiyo, unajua Mungu ni msikivu sana kwahiyo usitie shaka. Mheshimiwa Martha Umbulla.

MHE. MARTHA J. UMBULLA: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kumpa taarifa mzungumzaji aliyezungumza hivipunde kwamba wananchi wa Simanjiro hususan Mereraniwaliojengewa ukuta Mheshimiwa Rais huyohuyo amewaleteamradi mkubwa wa shilingi milioni 780 na umeanza kazi nasasa hivi wananchi wale karibia wanaachana na tatizo lamaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilitaka kumpa taarifa hiyo.(Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Magereli, kabla sijakuulizakama unaikubali taarifa hiyo, naona wanakwaya wanatokakwenda kujiandaa kabisa kwa ajili ya maombi. Kwa hiyo,naamini yule Nabii aliyekuwepo hapo basement leo,atatupata Wabunge wote hapa tuungane jamani naMheshimiwa Magereli twende kwenye maombi. (Makofi)

Mheshimiwa Magereli, unaipokea taarifa yaMheshimiwa Martha Umbulla?

MHE. LUCY S. MAGERELI: Mheshimiwa Naibu Spika,nimemsikia Mheshimiwa Umbulla lakini mambo haya huwani maneno yanayosemwa tu, ni tarakimu zinazotajwa tu.Hata bajeti zimekuwa zikitajwa kwa tarakimu hivyo hivyomwisho wa siku asilimia moja, mbili, kumi na moja, tunangojakuona hilo la Simanjiro litachukua muda gani.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee namaombi yangu. (Kicheko)

Mwenyezi Mungu nakuomba uwaambie Serikali yaCCM ya kwamba uchumi wanaouhubiri unakua kwa kasiwao peke yao ndiyo wanaouona, wananchi wetu hawauonina sisi Wabunge pia hatuuoni. (Makofi)

T A A R I F A

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NAUWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Magereli, naomba usubiri,kuna Chief Whip amesimama hapa.

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa NaibuSpika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kitwanga, Chief Whipamesimama.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NAUWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Sina niaya kukataa kwamba Mwenyezi Mungu hatumheshimu, lakinini vema akakuelekeza wewe kwa sababu kwa mujibu wataratibu zetu humu si sawa kutumia nafasi ya Mwenyezi Mungukatika sura kama hiyo.

(Hapa baadhi ya WaheshimiwaWabunge waliongea bila mpangilio)

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NAUWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, namwombamzungumzaji a-address Kiti, ndiyo utaratibu.

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa NaibuSpika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kitwanga, kikanuni kwakuwa Waziri ameshazungumza inabidi nimpe nafasi kwanzaMheshimiwa Magereli.

Mheshimiwa Magereli ulikuwa unapewa ushauri,kwamba kwa kuwa inabidi uzungumze na mimi sasa itabidimimi ndiye nikusaidie kupeleka labda hayo maombi. Kikanuniinabidi uni-address mimi, nadhani hilo limekaa vizuri.Mheshimiwa Magereli. (Kicheko)

MHE. LUCY S. MAGERELI: Mheshimiwa Naibu Spika,wakati naanza mchango wangu niliomba idhini ya Kiti, kwahiyo, naamini na wewe unamwamini Mwenyezi Mungu nahili wala halikupi shida, naomba niendelee na mchangowangu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Magereli, maombitulishaomba asubuhi, ndiyo utaratibu wa Bunge, kwa hiyo,wewe endelea na mchango wako huo lakini address Kitikama kanuni zinavyosema, hapo ilikuwa unakumbushwa tu.Kwa hiyo, wewe endelea na mchango wako lakini addressKiti.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

MHE. LUCY S. MAGERELI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa maelekezo yako. Naomba basiniwakumbushe mimi kwa sababu tayari Mungu ameshaonadhamira niliyonayo moyoni kwangu, basi atayajibu maombihayo kwa ileile dhamira yangu kwamba …

T A A R I F A

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa NaibuSpika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Magereli, kuna taarifa yaMheshimiwa Kitwanga.

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa NaibuSpika, naomba nimpe taarifa mzungumzaji kwamba,Watanzania wanahitaji ndege za ATC si kwa sababu ya waokuzipanda. Ndege hizi zitakapokuwa zikiruka zikileta watalii,watalii wataleta pesa, pesa hizo zitakuwa nyingi natutakapozipata zitatumika katika maji, elimu na afya.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lucy Magereli, unaipokeataarifa hiyo kutoka kwa Mheshimiwa Kitwanga?

MHE. LUCY S. MAGERELI: Mheshimiwa Naibu Spika,namshukuru Mheshimiwa Kitwanga kwa taarifa yake, lakinimngewapa fursa Watanzania wakachagua nini wanataka,kati ya ndege au nini ambacho kitaleta madhara kwenyemaisha yao, wangekuambieni wanataka X-Rays, CT-Scan,MRI kwa ajili ya afya zao kwa sababu mpaka sasa hivyo nivitu ambavyo vinaonekana ni vya kupatikana Ulaya na siTanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa nimaliziekwanza kwenye ile hoja yangu ya sala, kwamba namshukurusana Mwenyezi Mungu kwa kuwa amejidhihirisha yupo naanatenda miujiza katika maisha ya Mheshimiwa TunduAntiphas Mughwai Lissu. Yule ambaye mlimtesa, mkampiga

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

risasi 18, mkakataa kupeleleza nani alifanya hivyo,mkashindwa kumtibu, navyozungumza …

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Magereli, unafahamumaana ya ‘m’ kwenye hicho usemacho? Ukisema ‘mli’, niakina nani na wewe upo ama mimi? Kwa sababu unani-address mimi, ukisema mlitesa, maana yake mimi ni sehemuya watesaji. Sasa tusiende huko Mheshimiwa, naombajielekeze kwenye mchango uliokuwa umejipangakuuchangia, tusiende kwenye haya maneno mengineambayo yanaleta ukakasi ambao hauna maana yoyote kwasasa. Mheshimiwa Magereli.

MHE. LUCY S. MAGERELI: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba nimshukuru Waziri wa Maji, kwa kazi nzurialiyoifanya, baada ya malalamiko ya wananchi na wakazi…

T A A R I F A

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika,taarifa.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, hii itakuwataarifa ya mwisho kwa asubuhi hii. Mheshimiwa Musukuma.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana. Nilitaka tu kutoa taarifa kwamba,mzungumzaji anayezungumza amesema Mbunge mwenzetualipigwa risasi 18 lakini taarifa za mwanzo zilizotolewa naMsemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwamba amepigwarisasi 38. Sasa inaonekana wenzetu wanajua mpigaji ni nanikwa nini wasilithibitishie Bunge ili hii hoja ikajiondoa kabisaWabunge tukaacha kujadili suala la Lissu?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lucy Magereli, unaipokeataarifa hiyo?

MHE. LUCY S. MAGERELI: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba niendelee na mchango wangu. Naomba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

nimshukuru Mheshimiwa Waziri wa Maji kwa kazi nzurialiyoifanya baada ya malalamiko ya sisi wadau na wakaziwa Kigamboni kuhusu mradi wa visima 20 vya maji vyaKimbiji na Mpera ambavyo hata juzi wakati nauliza swali kwaniaba ya Mheshimiwa Mwita Waitara nilieleza kwamba vilevisima havijakamilika, kwa hiyo, Serikali inatudanganyakutuambia kwamba visima vimeshakamilika kinachofanyikani kutafuta fedha kwa ajili ya usambazaji. Kwa taarifa rasmizilizotolewa na Serikali juzi nimeona amevunja Bodi yaDUWASA na kuwawajibisha waliohusika wote kwa sababuya ubadhirifu uliofanywa katika vile visima 20 na kwambampaka leo havijakamilika. Kwa hilo, naomba nimpongezeMheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna jambo lingine ambalona mimi nataka nil izungumzie kwa kina ambalo niunyanyasaji na matendo yasiyo sawa kwa wafanyabiashara,watu wa sekta binafsi na wawekezaji. Ukitaka kuwekezaTanzania, unaandamwa na ada, tozo, kodi, ushuru, leseni,na vibali visivyopungua 30. Tunasema tunakwenda kwenyeTanzania ya Viwanda, tunafikaje huko? Sisi tunaikimbia PPP,hatutaki kufanya miradi ya ushirikiano, wawekezajiwanaotaka kuwekeza nchini kwetu tunawaandama kwamilolongo ya kodi, ada na tozo zisizomithilika, tunafikajeTanzania ya Viwanda? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukitaka kuwekeza katikakiwanda au katika sekta ya kilimo kwa ujumla, unatakiwakulipia kibali cha BRELA, TBS, TPRI, TOSC, NEMC, Fire, Bima, OSHA,Zimamoto, TIN/VRN, Leseni ya Biashara, Vibali vya KusafirishaMazao, Ushuru wa Kusafirisha Mazao, Usajili wa Mbegu,Mabango, Bodi ya Usajili na Mizani na Vipimo. Ukiwamwekezaji ukafika nchini ukapewa orodha ya kwamba hayandiyo matakwa unayotakiwa kukamilisha ndiyo hatimayeusajiliwe na kufanya biashara Tanzania, naamini hata kamaungekuwa ni wewe ungekimbia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie swali linginela mipango inayoendelea ya kutaka kuuwa Serikali za Mitaa.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

Mipango yote tuliyonayo sasa hivi kiukweli na ukitazama halihalisi i l ivyo tunamaanisha tunataka kurudi kwenyeCentralization na si Decentralization ambayo ndiyo mfumoambao tumekuwa tunautumia wakati wote. (Makofi)

Mheshimiwa Naisu Spika, tumechukua vyanzo vyamapato vyote vya Serikali za Mitaa. Majukumu ambayoyalikuwa yakitekelezwa na Serikali za Mitaa mengi sasa naonayapigiwa upatu kwamba yarudishwe Serikali Kuu. Majukumukama ya ujenzi wa barabara za vijijini tukaanzisha mamlakainaitwa TARURA. Leo Serikali za Mitaa zinakwenda kukutanana aina ngumu kabisa ya mateso kwa sababu hata fedhaza utekelezaji wa shughuli zake zitatakiwa kuombwa kutokaSerikali Kuu. Mmeshaona kwa miaka miwili hii iliyopitaunaomba fedha inachukua muda mrefu sana hata kupatiwahizo fedha kwa ajili ya matumizi mengineyo ya Serikali zaMitaa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, fahamuni kwamba katikaSerikali za Mitaa ndiko kwenye umma mkubwa waWatanzania na ndiko wanakopata huduma kwa maeneoya karibu. Sasa tunapofikiri kwamba lazima tupangemlolongo mrefu kusubiri fedha kutoka Serikali Kuu, nadhanihili ni kosa kubwa tunalolifanya na Mheshimiwa Waziriaangalie namna ya kulirekebisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala ambalonimeliona kwenye bajeti kwamba kuna mpango wa kulindaviwanda vya ndani kwa kuongeza import duty. Miminadhani ambacho tunapaswa kufanya si kuongeza importduty kwa bidhaa zinazotoka nje ni kuangalia mazingira yetuyanavyoweza kuwa rafiki ili tuboreshe kilimo chetu lakinituzalishe kwa wingi tutosheleze soko letu na tuwezekuwahudumia Watanzania bila kufikiri kuwakandamiza watuwengine ambao wanatakiwa kutuhudumiwa ambapo kwawakati huo hatujaweza kuzalisha hizo bidhaa toshelevu kiasitunachotaka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye kitabu cha Kamatina kabla sijasoma maoni hayo niliyoya-quote kisehemu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

kidogo, niipongeze Kamati ya Bajeti wamefanya kazi nzuri,wamechambua vizuri na wamekuwa honest, wamekujakwenye Bunge na wamesema ukweli kuhusu wanachokionakuhusu mwenendo wa bajeti ya nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika ukurasa wa 30,Kamati wanasema kwamba, Kamati inajiuliza kuwaupungufu huu mkubwa wa mikopo na misaada kutoka njeunatokana na nini? Naomba nisaidie kuijibu Kamati kwambaupungufu wa misaada na mikopo kutoka nje inaletwa naukanywagaji wa Katiba katika maeneo ya utawala wa sheria,utawala bora, uhuru wa kupata habari, uhuru wa kujieleza,uchaguzi wa Zanzibar na mauaji ya raia ambayo mpaka sasahayachunguzwi na hatupati majibu yake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika…

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Kengele ya pil i imeshagongaMheshimiwa, ahsante sana.

Tunaendelea na Mheshimiwa Conchesta Rwamlaza,atafuatiwa na Mheshimiwa Fakharia Shomar Khamis kamamuda utaruhusu Mheshimiwa Mansoor.

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili na mimi niwezekuchangia kidogo kuhusu hoja iliyo mbele yetu ya bajeti yaSerikali mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Naibu Spika, navyoelewa mimi nikwamba hapa tunachojadili ni mipango yetu ya maendeleotunaitafsiri kwa minajili ya pesa. Tunapanga bajeti, tunatoapesa au sisi kama Bunge tunaidhinisha ili Serikali iwezekutekeleza ile mipango ambayo imeletwa hapa naimepitishwa na Bunge.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

Mheshimiwa Naibu Spika, kinachonisikitisha nikwamba Bunge hapa linakaa linapanga bajeti lakini Serikalihii iliyoko madarakani kusema ukweli haina nidhamu yakusimamia matumizi jinsi bajeti ilivyopitishwa. Tunapitishabajeti Serikali inakwenda kutumia pesa bila hata kulishirikishaBunge. Si makosa Serikali kuomba bajeti au supplementarybudget pale ambapo kumelazimika kuwa na matumizi yalazima na hayakuwepo kwenye bajeti lakini Serikali hailetiinatumia inavyoona kitu ambacho nakiona ni dharau kwaBunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nije kwenye uhalisia wabajeti. Nchi yoyote inapanga bajeti kulingana na uwezo namakusanyo yake. Ukiangalia mwaka jana, tulipitisha bajetizaidi ya shilingi trilioni 31 lakini haikutekelezeka kwa sababumakusanyo hayakuweza kutosheleza. Mwaka huu piatunakwenda kwenye bajeti ya shilingi trilion 32, je, tunauhakika wa kukusanya ili bajeti iweze kutekelezeka?Nachoshauri Serikali wala isione aibu, pale ambapo wanaonamakusanyo hayatoshelezi na hayatapatikana leteni bajetiambayo inalingana na uwezo wa nchi yetu ili tusifanye kwakuonesha wananchi kwamba Serikali inaweza kukusanyamapato makubwa na hatuwezi kufanya jinsi wananchiwanavyotegemea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niongelee kuhusuHalmashauri. Wengi sana wamesema kuhusu D by D, lakinimara nyingi nikisimama huwa nairejesha Serikali hii katikakitu kilichotendeka mwaka 1972 – 1982, kile kilichokuwakinaitwa madaraka mikoani, walikuwa wanasemadecentralization, sijui kama ilikuwa D by D. Zoezi hili lilishindwakwa sababu naona Serikali hii inapenda kuongoza nchi hiikwa trial and error. Tunajaribu tunashindwa halafu sijui tuna-retreat halafu tunaenda kuanza upya. Kwa hiyo, nchi inakaakatika kupanga na kupangua tu, ni kama tunafanyaexperiment kwamba tujaribu hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali sasa inarudi kwenyecentralization kwa sababu inachukua pesa yote inawekakatika mfuko mmoja. Dhana ya kuanzisha halmashauri hizi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

ni ipi? Kama zilianzishwa kwa ajili ya kutoa huduma kwawananchi na kwa kuzingatia kwamba nchi hii ni kubwa,huwezi kuiendesha ukisimama Dar es Salaam peke yake,haiwezekani. Kama tulijaribu tukashindwa ni kwa nini sasaSerikali inataka kuturudisha kule. Hizi halmashauri kama Serikaliiliyoko madarakani haizitaki leteni sheria hapa tubadilishe,tubaki na madaraka kule makao makuu ya Serikali halafupesa zote ziwe zinatoka huko zinakuja kule chini, kituambacho hakitawezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vyanzo vyote vyahalmashauri, kama walivyosema wengine na wewe unavijuavimekwenda Serikali Kuu. Kitu ambacho kimenisikitisha nihata ardhi, maana halmashauri nyingi zinategemea ardhi leya wilaya lakini hata ile asilimia 30 ambayo ilikuwa inabakiau inapaswa irudishwe kule katika halmashauri kusaidia kwasababu inatokana na ushuru au tozo mbalimbali ambazozinatokana ardhi na yenyewe mmebeba mmepelekaWizarani sijui Hazina na pesa hizi hazirudishwi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hebu tutazame ile LocalGovernment Development Grant mpaka sasa hivihakujatolewa hata senti tano. Kibaya zaidi hata kipindi hikiSerikali haijaweka bajeti ya pesa hizo kurudi katikahalmashauri. Kama pesa hizo hazirudi miradi yote ambayoilikuwa imepangwa kufanywa na halmashauri madarasa,zahanati, imekwama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama Serikali imeshindwakurudisha hicho kidogo tu, je, ikiwa na mfuko mkubwamaana yake ni nini? Labda Serikali inachotaka kutuoneshani kwamba imeweza kukusanya, siyo hivyo, la hasha,haijakusanya ni kwamba wamepora vyanzo vya halmashaurina halmashauri ziko mahututi na hatutegemei kwamba kweliwananchi wa Tanzania wataweza kupata hudumawanazostahili kama barabara.

Mheshimiwa Naibu Spika, mnaona barabarawanazotengeneza TARURA hata hapa Dodoma nendenihuku tunakokaa mitaani, wanatengeneza barabara ambazo

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

hata ma-engineer hawafiki. Mmechukua ma-engineer wotewa halmashauri wameenda TARURA, halmashauri zimebakihivi hivi zina wayawaya, ni kwamba hata barabarazinazotengenezwa hazipo. TARURA haiwezi kutengenezabarabara nzuri kwa sababu haipati pesa, watafanya gradingtu lakini hawawezi kutengeneza barabara ambazo zitawezakupitika ili wananchi waweze kusafirisha mazao yao. Hatahuduma nyingine za afya, elimu hazitaweza kutekelezekakama halmashauri hazipati pesa na Serikali Kuu inazikaliahaipeleki pesa katika halmashauri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nije kwenye kilimo. Ni jambojema kwamba Serikali imeleta bajeti ambayo kipaumbelechake ni kilimo. Ila mimi ninajiuliza kipaumbele hiki mmewekakatika makaratasi, je, utekelezaji wake ukoje?

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi ambao tuna umri kidogounawazidi walio wengi hapa, hebu turudi nyuma tuangalieile Awamu ya Kwanza ya Hayati Mwalimu Nyerere aliwezajekufanikiwa kutengeneza kilimo kikasaidia nchi yetu. Si vibayana wala si dhambi kuangalia kule nyuma huyu bwanaalifanyaje kwani makaratasi hayapo, mafaili hayapo,mipango haipo? Naiomba Serikali irudi nyuma ione ni kitugani ambacho Awamu ile ilifanya (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza walikuwa naextension officers, sasa hivi kilimo kinasemwa lakini hakunaelimu inayotolewa kwa wakulima. Hata yale mashambadarasa mnayoyasema hayapo na kama yapoyametelekezwa. Sisi tunakaa vijijini huko, mimi nikiendanakaa kijiji sijawahi kumwona extension officer wa kata nahata hao waliopo hawana huduma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi niko kwenye kamatiya LAAC kuna siku moja tumemwambia CAG hebu nendakafanye performance auditing ya hawa ma-extension officers,kwa kweli wanapata mishahara ya bure, atuoneshewanalipwa nini na wanafanya nini. Kama hawastahilikuwepo basi waondoke wakulima wajitegemee wenyewe

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

wanavyoona yaani bora liende kila mkulima anafanyaanavyoona. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi nchi yetu ina vijijizaidi ya 19,000, je, wako ma-extension officer kiasi gani ambaowanaweza kusaidia kuongoza wakulima? Mimi nakumbukababa yangu alikuwa analima kahama na kwenye kilimo chakahawa walikuwa wanakuja extension officers wiki mara mbilina pikipiki sasa hivi hawana hata usafiri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nije kwenye kahawa.Niongezee kwa mchango wa Benardetha Mushashu jana …

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Muda wako umeisha Mheshimiwa,ahsante sana. (Makofi)

Tunaendelea na Mheshimiwa Fakharia ShomarKhamis.

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kupata nafasi hii na mimi kuchangia hojaya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza lazima nifurahiekwamba sasa hivi Tanzania inaelekea katika viwanda, inamaana Tanzania ya Viwanda. Bajeti aliyoileta MheshimiwaWaziri imepangika, ina vionjo vya kutendea kazi nainatekelezeka. Hongera Mheshimiwa Waziri, MheshimiwaNaibu na watendaji wote wa Serikali katika Wizara hii.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kujielekeza katikaviwanda lazima tuwaangalie wakulima. Bila ya kuwa nawakulima hodari wakaweza kutupatia malighafi viwandavitakosa malighafi na amesema kwamba viwanda vya ndanivitapata malighafi hapa hapa Tanzania.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa wakulima,kama kweli watajielekeza kwenye kulima ina maana sasa nimwaka wao nao wa kufarijika katika maisha. Kwa sababuwataweza kuongeza mashamba, watakuwa na ushindanikatika bidhaa zao watakazokuwa wanalima, watakuwa namasoko kwamba watapeleka mazao yao katika viwandavyetu. Naomba wakulima waangaliwe ili kupata malighafiili viwanda vyetu viweze kujiendesha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukija kwa upande wa pili,tukumbuke kwamba Wizara ya Fedha wanatumia cashbudget kwa maana makusanyo mnayoyapata ndiyomnayoyatumia. Sasa inabidi lazima wajitahidi kupata kodiili kupata pesa za kutosha, bila ya kukusanya haitawezekanakutumia. Baadhi ya watendaji wetu wanaweza wakazembeakatika kukusanya huruma isiwepo, mtu anazembea kwenyekazi unamuondoa kwenye nafasi yake kwa sababuakizembea yeye ameifanya Serikali yote mapato. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuchukulie mfano, siku zahivi karibuni zile mashine zetu za kukusanya mapato EFDzimeharibika, Wabunge wanapiga kelele, jawabutunalolipata halitoshi kwa sababu mpaka leo ukweli hasahatujaupata. Sasa tuangalie, tatizo lilikuwa kwa wenyemashine au uzembe wa wafanyakazi au kuna kitu ganikilichojitokeza mpaka leo hakuna suluhisho? Kuna Mbungemmoja pia hapa kalizungumza hili kwa sababu sasa hivi watuwanatumia risiti na kama tunatumia risiti tayari tunapigwa.Mheshimiwa Waziri akija na hilo lazima alizungumzie ili tuwezekufarijika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, malalamiko mengiyanatokea hapa kuhusu malipo ya kodi mara mbili katikabandari zetu kwa vitu vinavyotoka Zanzibar. Suala hilil imezungumzwa, nakumbuka Naibu Waziri wa Fedhaalil itolea ufafanuzi kwamba wanakaa sasa hiviwanalizungumza na wakati wowote watafikia muafaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mimi nina ushauri, kwasababu jambo lolote linataka elimu, Wizara ya Muungano

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

iko inashughulikia Bara na Visiwani, ipeni majukumu piaWizara hii kutoa elimu. Taasisi za Zanzibar na na Barazinazoshughulika na mambo ya fedha wapewe elimu iliwaelewe kwa nini huu mvutano unatokea, kwa sababusheria mnajua ziko vipi na mwelekeo uko vipi ili huu mvutanouzidi kupungua. Nendeni kwenye media mtoe maelezo kunanini na baadaye mkubali watu wapige simu nao watoetaarifa au malalamiko yao, myapokee na myajibu. Haya nimambo madogo tu yanazungumzika. Jambo hili linachukuamuda mrefu ilhali si refu. Tunalifanya liwe refu ili tuwekemvutano hapa usio na maana ilhali jambo hil ilinazungumzika na ni rahisi kumalizika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakuja na suala lingineambalo liko katika ukurasa wa 46(v), kuhusu kusamehe Kodiya Ongezeko la Thamani kwenye taulo za kike ili isaidie vijanawetu wa kike na akina mama katika matatizo yao yakawaida. Nakubali Mheshimiwa Waziri alivyosema kwambawamepunguza kodi, ni sawa lakini kupunguza huko kusiwekwa mwaka huu na mwakani upunguze tena il i iwewanapunguza kidogo kidogo mpaka ifikie sawasawa kamamtu anakwenda kununua karanga haoni shida tena bei yakeitakuwa rahisi tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda vya ndanivinazalisha, itakuwa kila wakiteremsha bei na bei ya dukaniitakuwa inashuka na itakuwa rahisi kila mmoja kununua hatamtoto wa chini atanunua. Inaweza ikafika mpaka Sh.500;inategemea jinsi Wizara itakavyokuwa inashusha na malighafihiyo itakavyokuwa inauzwa madukani ili vijana na akinamama wetu wamudu kununua bidhaa hiyo. Baadaye itafikiampaka kupata bure, maana unaenda kununua kituunaambiwa Sh.200 au Sh.500, si bure hiyo? NaombaMheshimiwa hili aliangalie kila akija anapunguza bei mpakatufikie katika malengo tuliyoyakusudia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niongelee kuhusuhalmashauri, ukurasa wa 54. Marekebisho ya Sheria ya FedhaSerikali za Mitaa, Sura Namba 290 kwa kuongeza kifungu cha

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

37A. Nakubaliana na maelezo ya Mheshimiwa Waziri, ni sahihikwa sababu hii asilimia 10 inayokwenda kwa vijana nawanawake ilikuwa haina sheria lakini mtakapotungia sheriaitakuwa ni lazima itendeke. Kwa hiyo, nawaomba TAMISEMIwatengeneze kanuni haraka ili ziweze kutengenezewa sheriaije Bungeni ili tuwe na uhakika kwamba 10% ya vijana nawanawake ipo kisheria. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, shida tunayoipa mkaonahalmashauri hawatoi ni kwa sababu wanaona hawanapanapombana ni maelezo tu ya maandishi. Isitoshehalmashauri zinajipangia miradi ambayo haina prioritynyingi… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Fakharia, muda wakoumekwisha.

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante, mengine nitachangia kwa maandishi.Naunga mkono hoja na Mheshimiwa hapa kazi tu, endeleana majukumu yako kama yalivyo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Fakharia.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tumefika mwisho wa kipindichetu cha asubuhi. Nilete tangazo moja kwenu kabla sijatajamajina ya Waheshimiwa Wabunge tutakaoanza naomchana, kuna miwani ilishaulika kwenye kiti cha MheshimiwaMartha Mlata, ameileta hapa mbele imeandikwa Carol kwamaana ya wale watengenezaji wa hii miwani. Kwa hiyo,kama kuna mtu amepoteza miwani yake haioni atawaonaMakatibu watamkadhi miwani hii iliyosahaulika hapo.

Waheshimiwa Wabunge tutakaoanza naotutakaporejea ni Mheshimiwa Mansoor Shanif, MheshimiwaDaniel Nsanzugwanko, Mheshimiwa Leah Komanya,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

Mheshimiwa Magdalena Sakaya, Mheshimiwa MasoudAbdallah Salim, Mheshimiwa Cecilia Paresso, MheshimiwaSusan Kiwanga na wengine tutaendelea kuwataja kadritutakavyokuwa tukiendelea na michango yetu.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayo,nasitisha shughuli za Bunge mpaka saa 11.00 jioni leo.

(Saa 7.00 Mchana Bunge Lilisitishwa hadi Saa 11.00 Jioni)

(Saa 11.00 Jioni Bunge lilirudia)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,Mwongozo wa Spika.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Peter Serukamba.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba mwongozo kwa kutumia Kanuni ya 47(3) ambayoinasema:-

“Hoja itatolewa na Mbunge kwa kusimama mahalipake kuomba idhini ya Spika kutoa hoja ya kuahirisha Shughuliza Bunge kwa madhumuni ya kujadili jambo halisi la dharurana muhimu kwa umma”.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kukuombaunikubalie nitoe hoja tuahirishe shughuli za Serikali ili tuwezekujadili jambo la dharura lililotokea Bungeni leo.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, MheshimiwaPeter Serukamba amesimama akisema anaombamwongozo na ametaja Kanuni ya 47. Sasa mwongozounaombwa kwa mujibu wa Kanuni ya 68(7) lakini yeyeanasema anayo hoja ambayo anataka kuileta chini yaKanuni ya 47. Nitampa fursa aeleze maelezo yake ili niweze

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

kuona kama hiyo hoja ni ya dharura ama hapana.Mheshimiwa Peter Serukamba.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kutoa hojaili Bunge lako liweze kujadili hoja hii kama itawapendeza,kwangu mimi naona ni hoja ya dharura.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hapa Bungeniwamekuja maafisa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakaendakwenye kantini ya Bunge, jikoni, wakaanza kupima samakiambao wameshaandaliwa. Cha ajabu zaidi hawa maafisawamekuja Bungeni hawakumwambia Spika,hawakumwambia Katibu wa Bunge, hawakuiambia Serikali,hawakukwambia wewe Naibu Spika, maana yake ni nini?Maana yake ni kwamba Bunge hili sasa hatuko salama nakantini ile wanaokula ni Waheshimiwa Wabunge. Hivi huyuanayekuja tunajua amekuja kwa sababu gani? Pia mtuyeyote anayekuja nyumbani kwako si anapiga hodi, anakujana jambo mahsusi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hili natakaniwaombe Wabunge wenzangu tulijadili ili tuone hawamaafisa uvuvi, maafisa samaki nguvu hii ya kutaka kujakulishusha hadhi Bunge lako Tukufu wameipata wapi? Maanaleo wamekuja kwa ajili ya samaki kesho watakuja kwajambo lingine. Naomba Wabunge wenzangu tuwe na wivuna Ubunge wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja sasaili tuweze kuahirisha Bunge tuweze kujadili jambo hili.Naomba kutoa hoja. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Waheshimiwa WabungeWalisimama Kuunga Mkono Hoja)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naombamkae kidogo kwa aji l i ya utaratibu il i kanuni zetutusizipungukie.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

Waheshimiwa Wabunge, Kanuni ya 47(4),nitawasomea, inasema:-

“Iwapo Spika ataridhika kwamba jambo hilo ni ladharura, halisi na lina maslahi kwa umma, basi ataruhusuhoja hiyo itolewe kwa muda usiozidi dakika tano na mjadalajuu ya hoja hiyo utaendelea kwa muda ambao Spika ataonaunafaa kwa kuzingatia mazingira ya suala linalojadiliwa”

Sasa Mheshimiwa Peter Serukamba ametoa maelezoyake na yeye akafika mahali pa kutaka kuitoa hoja hiyo iliWaheshimiwa Wabunge muiunge mkono. Kwa maelezoaliyotoa na kwa masharti tuliyonayo kwenye Kanuni ya 47jambo hili alilolieleza Mheshimiwa Peter Serukamba halinautaratibu mahsusi ambao linaweza kushughulikiwa, kwahivyo tutalijadili hapa Bungeni. Sasa nitakaa ili nimruhusuatoe hiyo hoja yake muiunge mkono kama itaungwa mkono,kama haitaungwa mkono basi tutaendelea na ratiba iliyombele yetu.

Mheshimiwa Peter Serukamba kwa sababu ulishatoamaelezo mwanzo huna haja ya kurudia hayo maelezo, utoehoja ili tuendelee. (Makofi)

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Sasa Waheshimiwa Wabunge wenzangu,naomba kutoa hoja ili tuweze kuahirisha Shughuli za Bungetuweze kujadili jambo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa NaibuSpika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, hoja yaMheshimiwa Peter Serukamba imeungwa mkono. Mimi kwakuzingatia ratiba iliyo mbele yetu, nitatoa muda usiozidi nusu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

saa ili tulijadili jambo hili halafu nitatoa maelekezo kulinganana michango yenu Waheshimiwa Wabunge.

Waheshimiwa Wabunge, wanaotaka kuchangia hojaya Mheshimiwa Peter Serukamba sasa wasimame il iniorodheshe majina yao. Nitachukua Wabunge 10 na dakikazitakuwa tatu tatu ili muda wetu tuweze kwenda nao vizuri.Mheshimiwa Mtolea, Mheshimiwa Paresso, MheshimiwaSelasini, Mheshimiwa Dunstan Kitandula, MheshimiwaMwamoto, Mheshimiwa Rashid Shangazi, Mheshimiwa AlmasMaige, Mheshimiwa Kadutu, Mheshimiwa Kuchauka naMheshimiwa Sware Semesi. Tunaanza na MheshimiwaAbdallah Mtolea.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi nichangie hoja hiimaalum na mahsusi kwa jambo hili maalum kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mara kadhaa tumekuwatukilalamika namna ambavyo watendaji wa Serikaliwanavyowanyanyasa wananchi. Achilia mbali leo kuingiakatika Ofisi za Bunge kwenye kantini ya Bunge na kuanzakunusa vyungu na kuangalia kama kuna samaki wadogotumekuwa tukiona askari wa wanyamapori pia wakipitamitaani kwenye nyumba za watu wakikuta jembe lina mpinimpya wanakwambia wewe umeenda kukata mti, wakikutachungu chako zimebaki nyama mbili, tatu wanasema hiinyama inanukia nyama ya porini ulienda msituni na watuwamekuwa wakikamatwa kwa namna hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Mungu si Athumani leotumeletewa ndani kabisa tuone manyanyaso yalivyo,kwamba hata wasingewakuta hao samaki wangekuta miibabado wangesema hii miiba kwa ukubwa huu huyu samakialivuliwa kabla ya muda wake. Hivi, watendaji wa Serikaliwameishiwa mbinu kabisa za kuwakamata watu ambaowanavua samaki mpaka tunakuja kunusa vyungu, tunakujakukaguana kwenye majiko? Hili haliwezekani. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pili lazima tujue kamaleo mtu anaweza kuja na kuingia mpaka kwenye kantiniambayo Waheshimiwa Wabunge wanakula, usalama waWabunge uko wapi? Kwa hiyo, tunakula vyakula ambavyomtu mwingine anaweza akaingia, huyu mtu kabla hajaendakwenye kuwakagua hawa samaki, yeye kakaguliwa wapikama hana sumu, hana kitu chochote ambacho kinawezakuwazuru Wabunge? Jambo hili halikubaliki na ni lazimahawa watu washughulikiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Paresso.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia katikahoja iliyowasilishwa na Mheshimiwa Serukamba na miminaunga mkono hoja hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama alivyosemaMheshimiwa Mtolea labda inawezekana leo yalikuwa tu nimakusudi ya Mwenyezi Mungu hili likatokea ndani ya Bunge.Kwa sababu changamoto hizi na manyanyaso hayawamekuwa wakipata wananchi katika mambo mbalimbaliukiacha hili lililoko mbele yetu leo la Wizara ya Mifugo naUvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaokula kantini pale,tunaotumia wale samaki ni mlaji wa mwisho wa bidhaayoyote. Sasa unajiuliza hawa watumishi kama kweli niwaadilifu na wanajua utaratibu, inakuwaje unamfuatamtumiaji wa mwisho? Samaki tayari ameshakaangwa,ameshaandaliwa unachukua rula unampima, kwa ninihukudhibiti tangu kule mwanzo ambako samaki huyuanavuliwa? Kwa hiyo, huu ni ukiukwaji mkubwa wa sheriana taratibu na ni kuingilia kwa kiwango kikubwa uhuru wamtumiaji wa mwisho. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

Mheshimiwa Naibu Spika, ofisi yako sasa lazimaiangalie usalama wa Wabunge. Kama leo watu walidirikiwakaingia mpaka kantini bila taarifa, utaratibu au kibali,akaenda anachukua rula anapima samaki, kesho kutwaitakuwa nini? Ni lazima jambo hili sasa lituamshe, lituhakikishieusalama wa Wabunge lakini haya manyanyaso ambayowanapata wananchi katika maeneo mbalimbali yawezekuchukuliwa hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu, watumishiwa ambao wamefanya kitendo hiki ni lazima wachukuliwehatua za kisheria, kwa nini wamefanya jambo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naunga mkonohoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Joseph Selasini.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Naibu Spika,niseme moja kwa moja kwamba naunga mkono hoja yaMheshimiwa Serukamba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeacha wenyeweheshima ya mhimili huu ikamomonyoka na sasa tusipoangaliaitaporomoka itakwisha kabisa. Walianza polisi, wanakujakuwakamata Wabunge hapa bila taarifa kwa Spika, bilataarifa kwa Uongozi wa Bunge. Tulilalamika Spika akatoautaratibu kwamba asingependa Mbunge wake yeyoteachukuliwe tukiwa kwenye session bila yeye kuarifiwa.Wamekuwa wakiachwa wakiendelea, sasa taasisi zinginezimeona ni uchochoro. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la afya, mashinezetu zina uwezo wa kupima vyuma na silaha hazina uwezowa kupima sumu ndani ya mifuko ya watu. Hatujui walesamaki wamewashika katika mazingira gani ya kiafya. Siyohivyo tu, yaani samaki wameshapikwa, wapo kwa mlaji wamwisho ndiyo wanapimwa, hapa tulipofikia ni pakushangaza.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba MheshimiwaSerukamba atakapokuwa anafanya majumuisho ya hojayake, Bunge hili liazimie watu hawa waitwe kwenye Kamatiya Maadili, wahojiwe, ijulikane kwanza waliingiaje humu,walieleza wanakuja kufanya nini humu, walieleza mwenyejiwao ni nani ili tujue huo mlolongo na utaratibu waliotumiampaka wakafika hapo walipofika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa DunstanKitandula.

MHE. DUSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa fursa hii. Nianze kusema manenohaya. Kama kweli kuna mtu ameweza kuingia kwenye Bungelako Tukufu bila kupata ruhusa, Bunge lichukue hatua stahikiharaka. Hatuwezi kuuacha mhimili huu muhimu ukachezewahovyo hovyo namna hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa miaka kadhaanimekuwa nikipiga kelele kuhusu sekta ya ufugaji wa samaki,jinsi ambavyo tumeshindwa kama Taifa kuwekeza kwenyesekta hii. Leo tunashuhudia nguvu kubwa inatumika kwenyekudhibiti unaoitwa uvuvi haramu. Ningetegemea nguvu hiyokubwa kiasi hicho tuiweke kwenye kuhakikisha wananchi waUkanda wa Pwani ambao wanaangamia kwa umaskiniwananufaika na rasilimali yao iliyopo ambayo haitumiki kwakuwekeza kwenye ufugaji wa samaki. Badala ya nguvu hiyokuipeleka kule tunaipeleka kwenye vitu trivial, hii haikubaliki.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilitegemea nguvu hiyo leotungekuwa tunaielekeza kwenye kuangalia incentivepackage ambayo ingewezesha ufugaji wa samaki ukaibukakatika nchi hii. Tungehakikisha vyakula vya kufugia samakivinazalishwa kwa wingi nchini, mashine za kuweka oxygenkwenye ufugaji wa samaki zingeingia kwa bei ambayo nirahisi ya kuwawezesha wafugaji lakini nguvu hizi tunazionazinapelekwa kwenye vitu trivial. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

Mheshimiwa Naibu Spika, hili halikubaliki na naombaWabunge wenzangu tuoneshe hasira yetu kwa kuhakikishawote waliohusika kuja kufanya mchezo huu katika Bunge letuwanachukuliwa hatua.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa VenanceMwamoto.

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa NaibuSpika, niunge mkono hoja ya Mheshimiwa Serukamba.Niseme tu kwamba utaratibu wa wageni kuingia ndani yaBunge letu unafahamika na utaratibu ambao huwaunatumika mtu anapokosa nidhamu kwa Wabunge au kwachombo hiki cha Bunge unafahamika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bahati nzuri waliofanyakosa wanafahamika aidha kwa makusudi au kwa kutakakuchafua Serikali yetu. Sasa ni vyema wakachukuliwa hatuana wakaitwa kwenye Kamati yetu ya Maadili ya Bunge nakushughulikiwa kama wahalifu wengine. Walichokifanyawangeweza hata kuleta kitu kibaya kikawadhuru Wabungendani ya Bunge. Kwa hiyo, jambo hil i ni seriouswashughulikiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika,taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Heche, Mbunge uliyetakakumpa taarifa ameshamaliza kuzungumza. MheshimiwaRashid Shangazi.

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa nafasi hii. Naomba niunge mkono hojaya Mheshimiwa Serukamba lakini nataka nitofautiane kidogona Waheshimiwa Wabunge wenzangu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

Mheshimiwa Naibu Spika, hawa watu sidhani kamawamekuja tu wenyewe hapa ndani ya viwanja vya Bunge.Kwa mujibu wa clip ile ambayo inazunguka inaonyesha kabisakwamba Waziri mwenye dhamana ndiye aliyewapigia simu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani kwamba Mawaziriwetu kuna viburi vingine sijui wanavitoa wapi. Kwa sababuWaziri huyu angekuwa na ujasiri huu ambao ameufanya leoangeenda kuanzia kwenye mipaka na kule bandarini,ambako nyavu zinaingia na kuna maafisa wotewanaokagua halafu unaenda kuchoma za wavuvi kulekwenye maziwa. Nyavu hizo zinapita bandarini, nyavu hizozinapita mpaka wa Sirari kama zimeingilia Mombasahatujawahi kuona hata siku moja anawajibishwa Afisa Uvuvikwa kuruhusu nyavu ambazo ziko chini ya kiwango nakuchukuliwa hatua. Mara zote tumeona kwambawanaonyanyasika ni wavuvi wadogo na raia wa kawaida.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hili ni jambo ambalotunapaswa kulichukulia kwa umakini mzito na kwa namnayoyote ile tusingependa…

T A A R I F A

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika,Taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Shangazi, kaa kidogo.Waheshimiwa Wabunge, nitaruhusu taarifa hii moja tu kwasababu nilikuwa nimetoa nusu saa na bado kuna wachangijiwanahitaji kuchangia. Mheshimiwa Ryoba Chacha.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kumpa taarifa msemaji kwamba hili jambolimetendeka hapa lakini huko mtaani ni very worse. Kamatunachukua hatua isiishie hapa Bungeni, tutaonekana vibayakwa wale watu wetu wanaoonewa kule, ana samaki wawili

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

anakamatwa. Mimi naomba jambo hili lisiishie hapa, liendempaka chini.

Mheshimiwa Naibu Spika, yule mwenye clip amesemakatumwa na Waziri, huyu Waziri ana shida.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Rashid Shangazi,unaipokea taarifa hiyo?

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika,naipokea kwa sababu ndilo jambo ambalo limetufikishahapa tulipo na kwa msisitizo zaidi niseme tu kwambatunasikitika kwamba sisi kama vijana tunapopewa dhamanahizi tunatakiwa tuoneshe ubunifu na si kufanya mambo hayaambayo yanaweza kufanywa hata na mgambo ambayeameishia darasa la saba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nil itarajiakwamba kwa kupewa nafasi hizi vijana tungeonesha ubunifu,tungetafuta namna ya kuongeza uzalishaji wa samakimaeneo mbalimbali, tungezalisha vitalu vya samaki maeneoambayo hayana hata mito na maziwa. Kwa kuendeleakukumbatia maziwa tu haya inaonekana kabisa kwambanchi hii isingekuwa na maziwa na bahari basi tusingekuwana Mawaziri ambao wana dhamana hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Kuchauka.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi ili nami nichangie.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi kwa tendo hili ni iliWaheshimiwa Wabunge wajue uwepo wa Mwenyezi Mungu.Mwenyezi Mungu sisi ametupa uwezo wa kulinda haki zawatu lakini kwa vile tumeshindwa kuzilinda leo MwenyeziMungu amelileta hapa ili mlione mfanye maamuzi. Kwasababu jambo hili Waheshimiwa Wabunge wengi hapawalishawahi kuomba miongozo kwa mateso wanayoyapata

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

wananchi wetu huko majimboni na aidha wanyamapori nawatu wengine kama askari polisi na lilionekana kamangonjera, lakini leo Mwenyezi Mungu amelileta hapa ndaniili ninyi mlione, limo kwenye mhimili wenu ili mpate uchunguna ndiyo maana mmeibuka na hoja hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, natakaniwaambie Waheshimiwa Wabunge kwamba MwenyeziMungu ana makusudi yake kulileta jambo hili hapa. Kwasababu siku za nyuma mpaka vitanda vimeshatolewakwenye mabasi, mboga zimeondolewa kwenye majiko, leohii Mwenyezi Mungu amelileta ndani ya Bunge hili Tukufu ilimuone ni jinsi gani wananchi wetu wanavyonyanyasika nauongozi huu na hawa watu ambao wamepewa madarakayasiyo na ukomo, wajue Mwenyezi Mungu naye ana ukomo,watakwama kwa amri za Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, hayamaamuzi mnayoyachukua hapa leo mjue kwambaMwenyezi Mungu yupo na wale wanaonyanyaswa mudawote na mjue kwamba jambo hili ni zito. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi inawezekana vipi mtuaingie Bungeni? Hivi Dodoma kuna hoteli ngapi? Kwa ninihawajaenda kwenye hizi hoteli nyingine, hawapiki samaki,wanapika Bungeni pekee? Naomba hawa watu waletwekwenye Kamati yako ya Bunge ya Maadili kwa kuwa lengolao lilikuwa ni kulidhalilisha Bunge. Kama kufuata samakiwangeweza kwenda hata kwenye hoteli kubwa huko,wangekwenda Morena lakini walikuwa na lengo lakulinyanyasa Bunge na Mwenyezi Mungu anatakakuwaonesha Wabunge ni j insi gani wananchi wakewananyanyaswa ndiyo maana limekuja hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu ni huo.

MHE. MARWA R. CHACHA: Huyo Waziri aondoke.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa AlmasMaige.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Naibu Spika,kawaida mimi sichangii michango inayotolewa kwa dharuranamna hii lakini leo limefikia pabaya sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, zoezi la kupima samakindani ya kantini ya Bunge na wafanyakazi wa Serikali, niwafanyakazi wa mhimili mwingine kuingilia mhimili mwinginemakao makuu. Haiwezekani akatumwa mtu kutoka Bungenikwenda kupima samaki Ikulu na haiwezekani mtu akaendakupima samaki mahakamani. Imekuwaje Serikali wakajakupima samaki kwenye kantini ya Makao Makuu ya Bunge?Huku ni kuvuana nguo kupita kiasi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja hii yandugu yangu Mheshimiwa Serukamba kwa sababu imegusasehemu mbaya ya usalama wa Wabunge, usalama wetuleo umeguswa katika hali mbaya. Mimi nafikiri kama ni kweliwametumwa na Waziri kama ambavyo watu wanasemabasi Waziri huyu ana bidii lakini hana busara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile mimi nadhani Wazirihuyu hayuko na Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Rais hatakimambo ya hivi. Mheshimiwa Rais hataki watu wanyanyaswe,hataki watu wakate miti ya bangi badala ya kupanda. Waziriwa Mheshimiwa Magufuli ninayemfahamu hawezi kujakupima samaki kantini.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile imekuwajeusalama wamejaa mlangoni kote kule, wameingiaje?Wamedanganya nini mpaka …

KUHUSU UTARATIBU

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika,kuhusu utaratibu.

MHE. ALMAS A. MAIGE: Walikuwa wamevaa badgeza wageni, walidanganya vipi…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Almas Maige, kuhusuutaratibu, kanuni iliyovunjwa Mheshimiwa.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika,Kanuni ya 64(1)(g), anatumia lugha ya kuudhi dhidi yaMheshimiwa Waziri, kwamba Mheshimiwa Waziri ana bidiilakini hana busara.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Lugha mbaya sana.

MHE. JOHN W. HECHE: Anapimaje kwamba WaziriMpina hana busara? Afute kauli yake dhini Mheshimiwa Waziri,Mheshimiwa Waziri, chapa kazi. (Makofi/Kicheko)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, MheshimiwaHeche amesimama kwa mujibu wa Kanuni ya 64(1)(g),akisema kwamba Mheshimiwa Mbunge aliyekuwaanachangia ametumia lugha ya kuudhi na inayodhalilishakwa kuzungumzia busara na bidii.

Waheshimiwa Wabunge, matumizi ya maneno hayo,hayo ni maneno ya Kiswahili, ya kawaida kabisa wala simatusi.

WABUNGE FULANI: Aaaa.

NAIBU SPIKA: Kwa hiyo, kwa mchango anaoutoaMheshimiwa Almas Maige...

Waheshimiwa ninyi tena mkikaa wote hapo wawili,Mheshimiwa Heche na Mheshimiwa Mchunguji Msigwa yaanimnatusumbua sasa tunashindwa kuendelea na mamboambayo yako mbele yetu hapa. Aidha, mmoja wetu atokehapo au mtulizane tafadhali maana mkikaa hapomnaongea kila wakati. (Kicheko/Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Almas Maigeyuko sawasawa. Mheshimiwa Maige malizia mchango wako.

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa kulinyoosha hilo. Kwanza sikusemaMheshimiwa Waziri ana kosa, nimesema kama hawa watuwametumwa, maana hatujathibitisha kama walitumwa au

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

wamekuja wenyewe, basi aliyewatuma ana bidii ya kufanyakazi lakini busara hana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, mimi nadhanikama amewatuma huyu mtu hayuko kabisa na mawazo yaMheshimiwa Rais wetu Mtukufu. Nafikiri watu hawawaliotumwa waeleze wameingiaje Bungeni, walipita mlangogani, walitumia mbinu gani za kuingia ambazo zimeshindwakulinda usalama wa Waheshimiwa Wabunge?

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha,ahsante na naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Serukamba.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Dkt. SwareSemesi.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru kwa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nami naunga mkono hojaya Mheshimiwa Serukamba. Ni sheria ipi hiyo waliyoitumiahao maafisa wa fisheries kuja kufanya inspection, kuja kusemakwamba wanaangalia size ya samaki au wanaangaliaquality ya samaki? Namba moja, kama unaangalia size yasamaki kuna maeneo mahsusi ya kuangalia size za samakina akiwa katika hali gani. Samaki wale waliokwendakupimwa walishakuwa wamepikwa. Sasa sentimeta ya yulesamaki unai-judge vipi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namba mbili, unajuaje yulesamaki amevuliwa wapi? Kama una wasiwasi na hao samakiwanaokuwa saved hapa kwenye Bunge lako kwa niniusimhoji yule mwenye kile kitengo ni nani supplier wa walesamaki? Halafu from there unakwenda ku-trace back sourcezinatoka wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza huku ni kuudharaumhimili. Wamefuata kanuni zipi na sheria zipi ku-ambushBunge lako? Pili, wamekwenda ku-risk afya zetu kwa sababuhata hao wapimaji wamekwenda jikoni na kuepua samaki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

waliopikwa bila hata kuvaa gloves na kuanza kumpima nasisi ku-risk afya zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bahati mbaya huyu mhusikawa mgahawa amepigwa faini ya shil ingi laki tatu.Warudishiwe hela zao kwa sababu hawakufuata utaratibuule unaotakiwa. Kwa sababu huyu fish na fishery productinspector alitakiwa aandike ripoti iende kwa director wake,wenyewe wamekaa hapa hardly half an hour wamepelekakwenye news media kwamba Bunge ni hivi na hivi, huu niudhalilishaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wiki kadhaa zilizopita tuliliahapa kuhusu Operesheni Sangara kwamba wananchiwananyanyasika na operation ile, sasa imetukuta sisi hapa.Mungu si Athuman wamekuja hapa hapa kutudhalilishakwenye Bunge letu, kile kilio cha wananchi kimeletwa katikaBunge lako. Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mchangiaji wa mwishoni Mheshimiwa John Peter Kadutu.

MHE. JOHN P. KADUTU: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii. Mungu ni mwema,watu wote wenye viburi huwa wanaonekana mapema.(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa bahati nzuri jambo hililimefanyika na mimi nikiwepo pale. Nilikuwa na MheshimiwaMbogo, tukaulizana, kamera zinaingia jikoni na watuwanaingia jikoni. Kwa kifupi ni kwamba jambo hil ilimeandaliwa, Mheshimiwa Waziri hawezi kukwepa lawama,jambo hili limeandaliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi sipendi kabisa watuwenye kiburi, pepo kiburi ni mbaya kuliko kila kitu. MheshimiwaWaziri tumeongea hapa mjadala wa Wizara yako, ukaombakwamba tuwe na utulivu, hivi ni utulivu huu? Unakuja ku-testmitambo hapa Bungeni? Haifai. (Makofi/Vigelegele/Kicheko)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

Mheshimiwa Naibu Spika, wadogo zanguMheshimiwa Mpina na mtani wangu Mheshimiwa Ulega,hapa mmetukosea, muombe radhi hapa Bungeni na hililipeleke kwenye Maadili. Wapo watu tuliwajadili hivi hivitukawapeleka kwenye Maadili na viburi vyao vikateremka.Hivi ninyi Wabunge wenzetu mnakuja kutu-test sisi? Haifai,tuache. Mwaka 2020 unakuja, hivi tukikutana mtaani? Mimisiwaombei mabaya lakini viburi hivi. Tumewaona wengiwenye viburi, yaani ukishatoka hapa ni matatizo, kiburi chotekitakwisha. Kwa nini mtufanyie hivi? Hivi tunakula samakihalafu watu wanatupiga picha na kamera, kiko wapi? Hukomtaani wanasema ahaa, sasa ninyi huwa mnajifanyakututetea mbona mmeshindwa kujitetea? Hili jambo si zuri,hebu tuwe na busara, busara si lazima uwe na umri mkubwa,ukiwa mdogo na busara watu watakuheshimu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa hawahawawezi kukwepa jambo hili limepangwa. Ni kamamnapanga mashambulizi kwenda kukomboa mateka paleEntebe, ni jambo limepangwa, hawawezi kukwepa. Twendekwenye Maadili na tuone hatua nyingine zinachukuliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, halafu jambo hili kwa ninilimetokea na walinzi wa Bunge wako wapi? Kwa sababukila anayeingia hapa ana sababu maalum. Sisitunavyokaguliwa hapa, mtu anavyoingia si lazima asemenakwenda ku-search, nakwenda kutafuta hiki, kwa niniwaruhusiwe waingie mpaka kwenye kantini ya Wabungempaka tunapigwa picha sisi Wabunge tunakula samakiambao wamezuiwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, tutaendelea kuwaombeaili viburi viondoke. Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa mtoa hoja, MheshimiwaPeter Serukamba, hitimisha hoja yako.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,Waheshimiwa Wabunge, Bunge letu leo liko majaribuni.Kama kuna jambo Waheshimiwa Wabunge tutajua kwamba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

tunauheshimu mhimili huu ni kwenye hili jambo. Maana kamamtu anaweza akaja, amepanga na TV, lakini hayo yoteamepanga asimwambie Spika, Katibu wa Bunge, NaibuSpika, maana yake yeye yuko juu ya Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeshukuru sanaMheshimiwa Waziri Mkuu yupo, tunakuomba ufanye maamuzikwa kiongozi huyu wa Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi niombe Waziri huyuna wale maafisa wake waende kwenye Kamati ya Maadiliya Bunge ili atuambie alikuwa anatekeleza sheria ipi na Bungehili lifanye maamuzi. Leo Waheshimiwa Wabunge msipofanyamaamuzi kwenye jambo hili niwaambieni hatutaheshimiwatena na Serikali hapa mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, maana kuna ile hataheshima tu kwamba hawa ni wenzangu. Samaki amekujakupimwa mtu hajavaa gloves; na unajua kilichotokea?Wamemaliza kupima, wamechukua Sh.300,000wamewaruhusu samaki waendelee kuuzwa. Mnatakatudharauliwe kiasi gani? (Makofi)

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Risiti ya mashine wametoa?(Kicheko)

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,baada ya kusema hayo, naomba Bunge lako Tukufu,nakuomba wewe kwa sababu tuna Kamati yetu ya Maadili,jambo hili liendeke kwenye Kamati ya Maadili na itatuambiatufanye nini kama Bunge lakini tunalo jukumu. Amesemahapa Mheshimiwa Almas Maige, nataka kujiuliza, hivi kweliafisa wa samaki anaweza kwenda nyumbani kwaMheshimiwa Waziri Mkuu kupima samaki anaokula?Tuambiane ukweli hapa. Anaweza akaenda Ikulu kupimasamaki anaokula Mheshimiwa Rais? Hawezi hata kidogo.(Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ninaliachia Bungebusara yake. Nakushukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, imeletwa hojana Mheshimiwa Peter Serukamba kupitia Kanuni ya 47 kamaHoja ya Dharura. Waheshimiwa Wabunge, wameungamkono hoja hiyo na baadhi yetu wamepata fursa ya kuijadili.Kwa mjadala ulivyokuwa na mtoa hoja ameshahitimisha,jambo hili ni zito kwa nafasi yake na kati mazingira hayoyametajwa mambo mengi ambayo si kusudi langu kuyarudia;mambo ya afya na usalama wa Waheshimiwa Wabunge nanamna watu hawa walivyoingia hapa Bungeni.

Waheshimiwa Wabunge, kwa sababu taarifa hii,ukiacha Mheshimiwa Kadutu ambaye anasema alikuwepolakini naye si kwamba alikwenda mpaka jikoni labda na hizokamera pengine naye akajua wamepima na rula, lakini kwasababu Mheshimiwa Waziri Mkuu yuko hapa ndani sasa,naiagiza Serikali ilete taarifa ya jambo hilo kesho hapaBungeni. Baada ya kuleta taarifa hiyo, sasa tutapata pichakama jambo hili liamuliwe hapa ndani ama liende kwenyeKamati ili wale watu wapate fursa ya kusikilizwa, kulinganana taarifa ambayo itakuwa imeletwa kesho. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, kwa hivyo, kesho Serikaliilete taarifa Bungeni kuhusu mazingira ya jambo hili, namnalilivyotokea ili Bunge liweze kufanya maamuzi juu ya jambohili. Wakati huo Waheshimiwa Wabunge tutapata sasa fursaya kuazimia kama Bunge ama kupeleka jambo hili kwenyeKamati ili Kamati ije kutushauri namna ya kwenda nalo. Kwahiyo, kwa leo tutahitimisha jambo hili hivi kwa leo, lakinitutasikia kesho baada ya hiyo taarifa na kuchukua hatuazinazotakiwa.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kuyasema hayo,tutaendelea na ratiba yetu, Katibu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

NDG. PAMELA PALLANGYO - KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2017 na Mpango waMaendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Na

Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirioya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa

Fedha 2018/2019

(Majadiliano yanaendelea)

NAIBU SPIKA: Ahsante. Tutaendelea na michango yaWaheshimiwa Wabunge na tutaanza na Mheshimiwa MasoorShanif atafuatiwa na Mheshimiwa Daniel Nsanzugwanko,Mheshimiwa Leah Komanya ajiandae.

MHE. MANSOOR S. HIRAN: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia hoja ambayo ikombele yetu. Kwanza kabisa, naomba nichukue nafasi hiikumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya njema iliniweze kusimama mbele yako.

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue nafasi hii piakuwashukuru wananchi wa Kwimba kwa kunipa ushirikianomzuri ili niweze kutimiza wajibu wangu wa kuwatumikia.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue nafasihii pia kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri waFedha, Katibu Mkuu na watendaji wote wa Wizara ya Fedhakwa bajeti nzuri sana ambayo wamependekeza. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

Mheshimiwa Naibu Spika, sababu ya kusema bajetihii ni nzuri ni kwa sababu mimi kwa mara ya kwanza kwenyehistoria ya bajeti yetu nimekutana na bajeti ambayohaijapandisha kodi kwenye mafuta ya dizeli na petroli. Nibusara nzuri sana ambayo Mheshimiwa Waziri ametumiakuhakikisha kwamba mafuta hayapandi bei. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesema hivyo kwasababu unapotaka kupata uchumi wa viwanda unatakiwauhakikishe nishati ya mafuta ni bei nafuu. Nampongeza kwahilo na kama tukienda hivi Mheshimiwa Waziri nina uhakikauchumi wa viwanda ataweza kuufikia vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nichukue nafasi hiikumpongeza Mheshimiwa Waziri kwenye historia ya nchi yetukwa mara ya kwanza mwaka huu tumekutana na riba zabenki kushushwa. Riba za kukopa zimeshuka, hiyo ni maraya kwanza imetokea kwenye historia. Pia amewezakupambana na inflation ambayo iko tarakimu moja,nampongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa kazi nzuri ambayoanafanya yeye na Wizara yake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nij ielekeze kwenyemchango wa bajeti iliyowasilishwa. Naomba nijielekezekwenye hotuba ukurasa wa 46, paragraph ya kwanza.Naipongeza Wizara kwa kuleta mapendekezo ya kupunguzaCorporate Tax kwenye viwanda vipya vya dawa zabinadamu na ngozi. Nachoomba kwa Mheshimiwa Waziriasibague, viwanda vyote vinavyotengeneza dawa zabinadamu na ngozi ambavyo vipo na ambavyo zitakujavyote azipe incentive ya corporate tax asil imia 20.Atakapowabagua, wale wenye viwanda sasa hiviwatashindwa kushindana na viwanda vipya ambavyovitafika. Kwa hiyo, ni vizuri kuwe na Corporate Tax ambayoinafanana kwa wote. Pia nashauri Waziri asiishie kwenyedawa za binadamu, naomba pia viwanda vya dawa zamifugo na kil imo vihusishwe kwenye hil i punguzo laCorporate Tax. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu nyinginenayopenda kuelekeza mchango wangu ni kwenye ukurasawa 51, paragraph 12 ambayo inazungumzia Ushuru waBidhaa kwenye sigara zisizo na kichungi. Naomba ni-declareinterest kuwa mimi ni mdau. Nimesoma hotuba vizuri,amesema kwamba sigara ambazo zinatengenezwa kwatumbaku inayozalishwa hapa Tanzania kwa asilimia 75 nazaidi ambazo hazitumii kichungi atazichaji Excise Duty yaSh.12,447 na zile nyingine ambazo zinatumia kichungiatazichaji Sh.29,425.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi sikuelewa sababu yakuweka tofauti hiyo kwa sababu kwanza kabisa mtuanayevuta sigara ambayo haina kichungi anapata madharamakubwa zaidi kuliko yule anayevuta sigara ambayo inakichungi. Kwa hiyo, mimi nashauri ingekuwa opposite;kwamba zile za Sh.12,000 angeziwekea Sh.29,000 ili watuwavute sigara ambayo ina kichungi kwa sababu ile ambayohaina kichungi maana yake anaivuta tumbaku moja kwamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo ukienda sokoni sigaraambayo ina kichungi au haina kichungi zote zinauzwa kwaSh.100 mpaka Sh.150 kwa sigara moja. Ukichukua hizi sigaraambazo hazina kichungi zinazotozwa Sh.12,447, sigara hiyoinatakiwa iuzwe kwa Sh.60 mpaka Sh.65 kwenye soko, lakinisasa hivi inauzwa kwa Sh.100 kwa sababu sisi hatuna coinsza Sh.20 na Sh.30. Kwa hiyo, alichotaka Waziri ni kupunguzabei ya sigara ili mwananchi wa kawaida apate faida yakupata sigara ya bei nafuu, hiyo faida haipo, anayefaidikani mwenye kiwanda, mwananchi analipa ileile Sh.100. Kwahiyo, kuna karibu Sh.40 ambayo inapotea kama kodi kwasababu ya kutokuchaji hiyo bei. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri Waziri aendekuangalia suala hili kwa undani zaidi. Asilimia 70 yaWatanzania wanavuta sigara bila kichungi. Ni vizuri ku-

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

discourage suala hilo na ku-encourage watu waende kwenyeile yenye kichungi ili angalau madhara yapungue.

Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu nyingine ambayonapenda kupeleka mchango wangu ni ukurasa wa 52,paragraph 48 inayohusiana na stempu za kodi za kielektroniki.Mimi napongeza Wizara kwa maamuzi haya mazuri sana,naunga mkono maamuzi haya mia kwa mia. Shida yangu nimoja tu, ni gharama ya hiyo huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo gharama ya kununuastempu moja ya kuweka kwenye boksi la sigara unanunuakwa Sh.13. Naomba nirudie ili Mheshimiwa Waziri anisikievizuri, leo gharama ya kununua stempu ya sigara kwenyeboksi unalipa Sh.13, huyu SCIPA ambaye mmemteua kuwandiye atakayetoa huduma hii ataitoa kwa Sh.29.75, maratatu ya bei ya sasa hivi ambayo tunalipa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mimi sielewi hiyohesabu imefikaje mpaka mmekubaliana na hii Sh.29.75wakati sasa hivi tunalipa Sh.13. Ningetegemea tungepatahiyo huduma kwa bei nafuu zaidi kwa sababu ni electronictax stamps si tena karatasi , maana yake gharamazingepungua zaidi kuliko kupanda, ningetegemea ingekuwaSh.10 au Sh.5. Kwa hiyo, ningependa hili suala mliangalie kwaundani zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia kwa hesabu yaharaka haraka, mwekezaji anawekeza shilingi bilioni 44, anamkataba wa miaka mitano, kwenye taarifa ya Kamati yaBajeti imesema kwamba kwa mwaka atakuwa anafanyabiashara ya bilioni 66. Kwa hiyo, kwa miaka mitano mtuamewekeza bilioni 44 anachukua bilioni 330 kwa nchi yetu,kweli hesabu ya wapi ndugu zangu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri pia Ofisi yaAttorney General iangalie mkataba huu kwa sababu taarifanilizonazo ni kwamba huu mkataba alishapata huyu bwana

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

mwaka 2016 lakini ulikuwa na matatizo ndiyo maana ulikuwaumechelewa kutoka sasa hivi ndiyo umetoka. Kwa hiyo,naomba Serikali iangalie upya hili suala kwani ni zito.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabla sijamalizanichukue nafasi hii pia kumpongeza Commissioner Generalwa TRA kwa kazi nzuri wanayofanya yeye na timu yake maanabila makusanyo tusingeongea mambo ya bajeti hapa. Kwahiyo, naomba nichukue nafasi hii pia kuwapongeza TRA naWizara ya Fedha kwa kazi nzuri ambazo wanafanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja,ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa DanielNsanzugwanko atafuatiwa na Mheshimiwa Leah Komanya,Mheshimiwa Masoud Abdallah Salim ajiandae.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa NaibuSpika, naomba kwa namna ya pekee niunge mkono hoja hiina mapendekezo ya Waziri wa Fedha. Hata hivyo, naombaniwape hongera nyingi sana Waziri wa Fedha na timu yakekwa kazi nzuri wanayoifanya na hasa sera hizi za kodi zakuja na mkakati wa kulinda viwanda vya ndani nakuchochea uwekezaji katika Taifa letu, hilo ni jambo jema,hongereni sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini naomba pia kuwapahongera sana wenzetu wa TRA kwa kubadilisha mtazamo(attitudes), wameanza kuwa tax friendly kwa walipa kodi. Nikitu chema sana na Ndugu Kichere na wenzake hongerenikwa kazi nzuri, songeni mbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na hili la mfumompya wa stempu za kodi za kielektroniki. Kwanza ni jambojema, kama alivyosema ndugu yangu yule wa Kwimba naMheshimiwa Waziri nadhani cha msingi hapa hebu rudini

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

kwenye meza tena muangalie hizo economics zake, hayayanayozungumzwa yana ukweli kiasi gani?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia ni vyemaWatanzania tusiogope mambo mapya. Mzee Dkt. Kikwetealiwahi kutueleza hapa kwamba ili ule lazima uliwe. Kwahiyo, utaratibu huo wa stempu za kielectroniki uendelee lakininimwombe tu Waziri wa Fedha na wenzake, warudi kwenyemeza ya mazungumzo (drawing board) waangalieeconomics zake hizo. Hicho kinachosemwa kwambawatatupiga sana ni kitu cha kweli ili wajiridhishe na jambohilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina ushauri katika sualahili la mifumo ya kutoza kodi. Wakati kampuni hiyo inafanyakazi hizi mngeifungamanisha na kampuni ya Kitanzania, hiiKampuni ya Maxicom Africa, hawa ni Watanzania, niWaafrika wanaofanya kazi nzuri. Wamekubalika Uganda,Zambia, Rwanda na Kenya kwa washindani wetu wakubwawa kibiashara. Kwa hiyo, ingekuwa jambo jema kwa miakahii mitano muwafungamanishe na hii local company ilibaadaye kazi hii iweze kufanywa na kampuni yaWatanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,nitakuwa na machache tu. Jambo ambalo napenda nilisemeni nidhamu ya kibajeti. Pamoja na mambo mazuri hayaambayo yamekuja kwenye bajeti hii ambayo ameyaainishana mengine akayazungumza hata kwenye hali ya uchumi,nizungumzie nidhamu ya utekelezaji wa bajeti, hili ni jambokubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukurasa wa 29 MheshimiwaWaziri mwenyewe amebainisha kwamba kipaumbelekitakuwa ni ukamilishaji wa miradi inayoendelea. Sasanimwombe sana miradi mipya isimame kwanza tukamilishe

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

miradi ya kielelezo ambayo imekwama il i tuwe naconsistency.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini siyo hilo tu, kwenyehotuba pia ameainisha juu ya Waraka wa Hazina Na. 01 wamwaka 2018/2019 ambapo anawaagiza Maafisa Masuuliwote watenge fedha za kutosha kwenye miradiinayoendelea. Narudia tena, miradi inayoendelea kabla yakuanza mingine mipya. Sasa ipo miradi tunaijua ya kielelezo,miradi ya kipaumbele tangu bajeti ya mwaka jana, hiyomiradi haijakamilika. Moja ya miradi hiyo muhimu ni miradihii ya barabara ya kuunganisha mkoa na mkoa mwingine.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika nchi yetu mikoaambayo haijaunganishwa kati ya mkoa mmoja na mwingineni pamoja na Mkoa wa Kigoma. Mkoa wa Kigomahaujaunganishwa na Tabora, Katavi, Mwanza walaShinyanga. Niombe sana kupitia Waraka Na. 01 aliouainishaWaziri kwenye hotuba yake katika ukurasa wa 29 basi miradihii ambayo ina wakandarasi tayari kwenye maeneombalimbali ipewe kipaumbele na fedha ili ikamilike. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimkumbushe MheshimiwaWaziri barabara muhimu sana katika nchi hii inayoitwa yaKigoma – Kidahwe – Nyakanazi, hiyo ni barabara ya kielelezoimekaa miaka 20, bajeti zinakuja zinatoka barabara hiihaijakamilika. Nimwombe Mheshimiwa Waziri naye aachelegacy sasa kwamba barabara hii muhimu na kubwa katikanchi yetu inayotoka Kigoma - Nyakanazi haijakamilika.Nashauri Waziri akae na TANROADS na Katibu Mkuu waHazina, barabara hii ipewe fedha kwa sababu ni muhimusana.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalonapenda nilizungumze ni umeme. Umeme ni muhimu sanakwa maendeleo ya viwanda na hata hizi juhudizinazofanywa za kujenga Stiegler’s Gorge maana yake

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

umeme huu utaingizwa kwenye Gridi ya Taifa. Mimi natakanimkumbushe Waziri kuna mikoa iko off grid na inahitajikuendelea kiviwanda na moja ya mikoa hiyo ni pamoja naMikoa wa Kigoma na Katavi. Napenda sana MheshimiwaWaziri atakapokuja atueleze ule mkakati ambao Waziri waFedha mwenyewe alikwenda Korea kusaini pesa kwa ajili yakitu kinachoitwa North West Grid, umeishia wapi? Kwa mradiule Mikoa ya Geita, Kigoma, Katavi na Rukwaingeunganishwa kwa Gridi ya Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, zaidi ya hayo, sisi ambaotuko off grid kuna Mradi mkubwa wa Kielelezo wa MalagarasiHydro Power ambao una uwezo wa kuzalisha megawati 45.Naomba nimueleze Mheshimiwa Waziri wa Fedha, mradi huuni muhimu sana na hii mikoa ambayo sisi tuko off grid lazimatupate treatment sawasawa kama mikoa ambayo ipokwenye Gridi ya Taifa. Haiingii akilini mikoa ambayo ipokwenye Gridi ya Taifa inanufaika na umeme mwingi wakiviwanda lakini kuna mikoa ipo off grid. Bahati nzuri sanasisi Mkoa wa Kigoma tuna umeme wetu huu wa Malagarasiwa megawati 45.4, nina uhakika umeme huu utasaidia sanapia kuchochea maendeleo ya viwanda katika Mkoa waKigoma na maeneo ya jirani.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, naombanizungumzie uimarishaji wa ushirikiano na washirika wamaendeleo. Liko jambo ambalo ningependa MheshimiwaWaziri atueleze, washirika wa maendeleo, Jumuiya ya Nchiza Ulaya, USAID na World Bank wana malalamiko makubwana wamekuja kwenye Kamati zetu kutueleza kwamba Serikalimpaka tarehe 12 Juni kulikuwa na fedha shilingi bilioni 700ambazo ni sawa na USD milioni 300, Serikali imeshindwakusaini MoU. Mheshimiwa Waziri wa Fedha, ni kitu gani hiki?Naomba aje atueleze tatizo l iko wapi? Mfumo wamajadiliano ni wa kimkakati, kisera na kisiasa, zungumzenina watu hawa tupate fedha hizi.

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Nsanzugwanko, mudawako umekwisha.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru, naunga mkono hoja lakini Waziri ajeatueleze juu ya jambo hili muhimu sana, ahsante sana.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Leah Komanya atafuatiwana Mheshimiwa Masoud Abdallah Salim na MheshimiwaMagdalena Sakaya ajiandae.

MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipatia nafasi na mimi niweze kutoa maoniyangu katika mpango wa bajeti.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, napendakuipongeza Wizara ya Fedha kwa namna ilivyotuleteampango na kwa jinsi ilivyojikita zaidi kufuta tozo au kodizilizokuwa kero kwa wananchi, naipongeza sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya kuanza mchangowangu, naipongeza Serikali kwa namna ilivyoanza kulifufuazao la pamba kiasi kwamba sasa kumeanza kuwepomatumaini kwa wakulima wa pamba katika Mkoa wa Simiyuna Kanda ya Ziwa kwa ujumla. Naipongeza Serikali kwakufuta mchango uliokuwa ukitozwa, Sh.30 kwa kila kilo kwaajili ya kuendeleza zao la pamba. Mchango huu haukuwana tija kwa sababu Mfuko huu ambao unajulikana kamaCDTF haukuwa na tija yoyote, haukuweza kumsaidia mkulimana badala yake uliendelea kuleta pembejeo hafifu nauzalishaji uliendelea kupungua. Kwa mfano, takwimu zamsimu 2015/2016, zilikuwa tani 149,000 na kupungua zaidikatika msimu wa 2016/2017 ambapo zilivunwa tani 121,000.Kwa hiyo, hakukua na tija yoyote kuwepo kwa mfuko huu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

Mheshimiwa Naibu Spika, naamini kazi zilizokuwazinafanywa na Mfuko huu zitafanywa na Bodi ya Pamba kwakushirikiana na Maafisa Kilimo walioko katika halmashaurizetu. Kwa sababu muda wote ule kulikuwa na mgonganowa maslahi, mkulima alikuwa anamfahamu tu Bodi ya Pambapamoja na Mfuko ule kwa sababu ndo uliokuwa unapelekeapembejeo ya mbegu na dawa kiasi kwamba Afisa Kilimohakupewa nguvu yoyote au hakuthaminika kwa mkulimakuweza kulisimamia zao hilo kikamilifu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nina shauri sasa Serikalikupitia halmashauri iwawezeshe Maafisa Kilimo kikamilifu kwasababu kila Kata kuna Afisa Kilimo. Iwawezeshe usafiri naiwawezeshe kwa namna yoyote ili waweze kulisimamia lilezao badala ya Bodi ya Pamba ambayo ina mtu mmoja tukatika Wilaya ndiyo aliyekuwa anasimamia zao hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee kuipongezaSerikali kwa kufufua ushirika na kwa msimu huu imeanzakununua pamba kupitia vyama vya ushirika. Nafahamumwanzo ni mgumu, sisi Wabunge tuko nyuma yenu,tunamshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa jitihadazote anazozifanya kulisimamia hili zao. Mheshimiwa WaziriMkuu mimi niko nyuma yako nitaendelea kukupa ushirikianoambao ninaweza kukupa ili kuweza kufikia malengo ambayoSerikali inatoa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naamini sasa zao hililinaenda kuwa mikononi mwa Serikali, Serikali itakuwa nauwezo wa kuweza kulitolea maamuzi yoyote tofauti nailivyokuwa mwanzo. Naamini sasa vile vyama vinaibuka nakutoza hela kwenye ushuru huo sasa vinaenda kujifutavyenyewe kupitia ushirika. Halmashauri za Wilaya zinaendakupata takwimu sahihi kwa ajili ya kutoza ushuru wa pamba.Nachoshauri vile vitabu vinavyotumika Wakurugenzi waonekwamba ni nyaraka muhimu kwa sababu zinaenda kutumikakukokotoa kupata takwimu sahihi badala ya ule mgonganouliokuwepo baina ya Halmashauri na Bodi ya Pamba.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tatizo lililopo hatunaMaafisa Ushirika wa kutosha. Halmashauri zetu zina AfisaUshirika mmoja mmoja wengine wanaenda kustaafu mweziwa sita. Kwa kipindi hiki cha mpito Maafisa Ushirika ni waumuhimu kwa ajili ya kufufua ushirika, kwa sababu mara tubaada ya msimu ukaguzi unatakiwa ufanyike mara moja ilivyama vya ushirika vijiendeshe kwa faida. Bila Maafisa Ushikatunaenda kurudi nyuma, mapato yanayotokana na ushirikakwa vyama vya ushirika hayatajulikana badala yaketutaendelea kutengeneza hasara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi hiki ni muhimusasa kuwezesha kuwepo kwa COASCO kwa ajili ya ukaguzi ilibaadaye tusirudi kule tulikotoka. Kwa mfano, Wilaya yaMeatu ina AMCOS 80, ina vituo vya kununulia pamba 200,lakini Afisa Ushirika aliyepo ni mmoja. Je, ni nani anaendakukagua mapato na matumizi ya vyama vya ushirika?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee kuipongezaSerikali kwa kufuta Kodi ya Ongezeko la Thamani katika taulozinazotumiwa na akina mama na wasichana wakati wahedhi,. Kufuta tozo hiyo inaenda kumpunguzia mwanamkemzigo kwa kiasi fulani. Naishauri Serikali bado ina nafasi kubwaya kumsaidia mwanamke kupunguziwa bei ya taulo hizo.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, nikiangalia pedinyingi zinatoka nje, sisi Tanzania tunatumika kamawasambazaji, pamba inayozalishwa asilimia 30 tu ndioinayotumika nchini asilimia 70 inaenda nje. Hii inamaanishakwamba hatuna viwanda vya kutosha vinavyoweza piakutengeneza pedi. Hata pedi tunazotengeneza nchinipamba inayotumika inaenda nje kwanza ndipo inarudiTanzania kwa ajili ya kutengeneza. Kwa hiyo, Serikali inalojukumu kubwa la kuhakikisha sasa tunakuwa na viwanda vyakutosha ili sasa asilimia kubwa ya pamba iweze kutumikanchini. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Serikali katikaukurasa wa 85 umesema kwamba unaongeza uzalishaji wambegu bora za pamba aina ya UKM09 tani 40,000. Pia,inaenda kutenga maeneo kwa ajili ya uzalishaji wa mbeguhiyo; kutoa elimu kwa ajili ya wakulima; na kutoa vitendeakazi na kuhamasisha wakulima. Ukiangalia mikoa iliyotajwaSimiyu haijatajwa kama inaenda kuwezeshwa na hapo hapoSerikali imepanga shilingi bilioni 6.1 kwa ajili ya kutekeleza zoezihilo. Ukiangalia Mkoa wa Simiyu pia asilimia 60 ya pambainayozalishwa nchini inatoka Mkoa wa Simiyu. Kwa hiyo,naiomba Serikali Mkoa wa Simiyu na wenyewe uwemo katikakuwezeshwa kwa namna Serikali ilivyojipanga kuwezesha.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Simiyu unachokituo…

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha Mheshimiwa.

MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Naibu Spika,naunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa MasoudAbdalla Salim, atafuatiwa na Mheshimiwa MagdalenaSakaya, Mheshimiwa Cecilia Paresso ajiandae.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushuru, kama Serikali inataka kuambiwa ukweli iliijirekebishe bajeti ya 2018/2019 ni bajeti ya kuwadanganyaWatanzania, ya kufikirika, ya kusadikika na isiyo tekelezeka.Ni bajeti ambayo kwa kweli imewahadaa Watanzania nahasa wakulima. Ikiwa leo wakulima wametengewa asilimia0.4 ya fedha za maendeleo ndani ya fedha za bajeti yamaendeleo ya shilingi trilioni 12 ukiachia shilingi trilioni 2.1fedha za nje, hivi Tanzania ya viwanda kuelekea uchumi wakati ni kweli inawezekana? Mnawadharau wakulima tangubajeti iliyopita mwaka 2017/2018 walitengewa shilingi bilioni

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

150.2 mkapeleka shilingi bilioni 16.5 hadi mwezi Machi sawana asil imia 11, Tanzania ya viwanda iko wapi?Mmewatelekeza wavuvi, leo wavuvi bajeti ya maendeleokwa mwaka huu mmetenga 0.06 ndani ya shilingi trilioni hizoambazo nimezitaja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli Serikali kamainataka kuambiwa ukweli ni kwamba wavuviwametelekezwa, wakulima wametelekezwa na mifugoimetelekezwa. Sasa nauliza mkakati wenu wa Serikali wakuboresha uvuvi uko wapi, hauonekani. Wananchi waMtwara, Lindi, Dar es Salaam mpaka Tanga mkakati wakuboresha maisha yao uko wapi? Kwenye maziwa nakovilevile, Mikoa ambayo iko katika Ziwa Viktoria, ZiwaTanganyika na maziwa mengine, yote hakuna mkakati, bajetiyao ni 0.06 ya fedha za maendeleo, ina maana Serikali hainamkakati. Mkakati mkubwa unaojulikana ni kuchoma nyavumoto na kupeleka wapimaji wa samaki kantini, tutafika kweli?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nashangaa kweli kweli,ukiangalia Vote 99, Ministry of Livestock Development andFisheries Livestock, Subvote 1001, item 22010 Travel-In-Country,hii ndiyo Waziri mwenyewe, wametoka kwenye Sh.108,960,000hadi shilingi milioni 300 safari za ndani kumbe ni za kuchomanyavu moto na kupima kantini samaki wa Bunge. Hilihalikubaliki lazima tubadilike tuendane na wakati ulivyokwamba wavuvi mmewaacha kuendelea kuwa maskini, nchinyingine duniani wanaandaa mazingira mazuri kuwawezeshawavuvi wadogo wadogo kutafuta vyombo mbalimbalibaadaye wanakwenda kuvua bahari kuu na Serikali inapatamapato, lakini nyie mkiambiwa mnasema sisi siyo wazalendo,hatuwezi kufika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nigusie jambo lingine,nimesema bajeti hii ni kiini macho, ni kizungumkuti kwasababu kwenye ukurasa 78 hakuna uhalisia wa ukweli wamatumizi ya lazima yanayoendana na mapato. Deni la Taifani shilingi trilioni 10 kwa hivyo kwa kila mwezi zinatakiwazipatikane shilingi bilioni 833, ukienda kwenye mishahara

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

shilingi trilioni 7.4 kwa kila mwezi lazima zipatakine shiling bilioni617, matumizi mengineyo ni shilingi bilioni 3, kila mweziipatikane shilingi bilioni 254, shilingi trilioni 1.7 mtaipata wapina hamna makusanyo? Tukisema vyanzo chukueni vyanzohamtaki, hamueleweki. Amesema Mheshimiwa mmoja paleMheshimiwa Mgimwa, kwamba Waziri usiwe mgumu ukubaliushauri wa Waheshimiwa Wabunge. Ikiwa makusanyo yamwisho ni shilingi trilioni 1.2 mpaka 3, leo mnataka ipatikaneshilingi trilioni 1.7 ya lazima, hamna kitu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tena basi angalia ukurasawa 74 wa kitabu chao kuna shilingi trilioni 12 hizi ni fedha zamaendeleo ukiachia shilingi trilioni 2.1 ya fedha za nje. Badohaijakuja hapo, nazo zikusanywe shughuli iende. Ukiangaliakitabu cha Mheshimiwa Mpango na mwenzake Naibu Waziripicha ya juu hapa wanasema, uzinduzi wa mfumo waukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielekitroniki, uzinduzi lakinihawawezi kumuonesha Rais, tena Rais yupo hapaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, muonesheni Raisvyanzo vipya vya mapato mbona hamumuoneshi? Kunapicha hapa, nawashangaa kweli kweli, andaeni mazingira,njia mpya ya mapato iko wapi, uzinduzi wa vyanzo vipya vyamapato iko wapi? Ni vilevile vya siku zote hivyo ni kuwaumizawananchi, hamsomeki hamueleweke shauri yenu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalolinanikera Serikali hii hakuna ongezeko la mshahara, bajetihii haijagusa kabisa wafanyakazi, hakuna nyongeza yao.Hata lile takwa la kisheria la nyongeza ya kila mwezi nalohaliko, annual increment hakuna. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo baya zaidi nikwamba ukiangalia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waSerikali mbali na kwamba mishahara haikupandishwa,hakuna ile annual increment ile ya mfanyakazi ambayo niya kisheria haipo lakini hata pale wanapostaafu hawawafanyakazi wanapunjwa, wanadhulumiwa na kunyonywanakupa ushahidi. Ripoti ya Mdhibiti ninayo hapa, ripoti yaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

wa fedha unaoishia 30 Juni, 2017, ukurasa wa 71 sikiliza uovuna ubaya walionao hawa jamaa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukurasa wa 71, majaladayanayokaguliwa wastaafu 406 asilimia 11 ya majalada,majalada hayo 176 yamepunjwa yakiwa pungufu kwaSh.516,078,816. Hiyo ndiyo ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi waHesabu za Serikali, mishahara haipandishi, hakuna ongezekola mwaka la kisheria na wale wanaostaafu nao wanapunjwamnataka nini kwa Mungu, mkaseme nini? Nawashangaajamani mwogopeni Mwenyezi Mungu, nyie tumewapa kaziya kusimamia kwamba hata wastaafu nao kumbe maslahiyao wanayopata mafao yao siyo, mwaka mbaya kweli.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaambie Waheshimiwawenzangu hapa kwamba jukumu mlilopewa ni kubwa sanana kama jukumu mlilopewa ni kubwa sana muandaemazingira kwamba mtende haki. Siyo hiyo tu, huu wizi naubadhirifu katika nidhamu ya matumizi ya fedha umekuwamkubwa sana na inaelekea kwamba Mawaziriwameshindwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia kitabu hiki hapakuna wizi na ubadhirifu unaonekana. La kwanza, naombanianze na kwenye ukurasa wa 291 wa ripoti na Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Katika ukurasa huuinaonekana kwamba hata Hazina yenyewe chomboambacho wanakisimamia, Idara ya Hazina Fungu 21 kunaubadhirifu mkubwa wa fedha umeonekana na wao ndiyowasimamizi. Ukurasa wa 291 Naibu Waziri fungua uangalielakini ukusara wa 290 pia mmepata hati isiyo na shaka, ripotiya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kumbe ukiona kilembakimeloa uchafu sijui shuka inakuwaje? Mtihani, tumewapadhamana lakini hakuna kitu. Maisha yamekuwa magumu,mzunguko wa pesa hakuna. Mwaka 2017 baya zaidi, hii hapahotuba ya Mheshimiwa Dkt. Mpango alituambia kwambalengo lake ni kuwatoa wale wanaokula mlo mmoja kutoka

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

asilimia 9.7 mpaka asilimia 5, nendeni Majimbo Wabungewote hapa tuandae vikundi twende Mikoa yote TanzaniaBara tukachunguze wanaokula mlo mmoja wameongezekaau wamepungua?

WABUNGE FULANI: Hawajapungua.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Hali mbaya kupitakiasi. Sasa yale maelezo ambayo mnatupa siye tunayasomana tunayo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri akubalikwamba bado hali ya maisha ya Tanzania ni mbaya sanana Watanzania wana matumaini makubwa sana lakinihakuna kinachoeleweka, mpaka sasa hakunakinachokwenda. Ushauri wangu kwa Mheshimiwa Waziri,akae na wataalam wa kweli ambao wataweza kusadia hiiWizara angalau maisha ya Watanzania yabadilike lakini kwahali tunayokwenda nayo Watanzania tumepigika. Bajeti hiini mbaya, mbovu, ya kusadikika, funika kombe. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Masoud, hata ile asilimiakaribia 70 ya mwaka jana haujaiona kabisa, ni zero?

Tunaendelea na Mheshimiwa Magdalena Sakayaatafuatiwa na Mheshimiwa Cecilia Paresso, MheshimiwaSusan Kiwanga ajiandae.

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa NaibuSpika, nami nakushukuru sana kunipa nafasi niwezekuchangia kidogo kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri,hotuba ya Serikali ambayo iko mbele yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye vitabu vyote vyaMheshimiwa Waziri; kitabu cha hotuba hata kitabu cha haliya uchumi wa Taifa, uchumi wa Tanzania umekua kwa asilimia7.1 tofauti na mwaka 2017 ambapo ulikua kwa asilimia 7

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

mwaka 2016. Ukijaribu kuangalia hivi vitabu vinavyosema naukienda kwenye actual ground kule chini kwenye maisha yawatu ni tofauti sana. Uchumi tunaosema kwamba umekuakwenye vitabu kule chini bado hauendani. Nami nakubalianakabisa na hotuba ya Kamati kwamba tumeshindwakuoanisha uchumi na hali ya wananchi kule chini,tumeshindwa kuoanisha kukua kwa uchumi kwakufungamanisha na hali ya maisha ya Watanzania kule walikochini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi tunavyoongea kilo yadagaa Sh.10,000 tena wa Mwanza. Hivi tunavyoongea janasato Sh.10,000 kilo moja hata hapa kantini tunakula haijalishini mdogo au mkubwa. Ukiondoa mazao ya nafaka, mazaomengine yote gharama ni juu. Kwa hiyo, kwa mwananchiwa kawaida ukimwambia uchumi umekua hakuelewi.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tukienda pia kwenyevifaa vya ujenzi, cement wiki iliyopita ilikuwa Sh.14,500 leoasubuhi ni Sh.15,500. Sasa uchumi umekua umekuaje? Miezimiwili iliyopita nondo milimita 16 ilikuwa Sh.19,500 mpakaSh.20,000 leo nenda duka la dawa vifaa vya ujenzi ni Sh.38,000imepanda almost mara mbili. Nashindwa kuelewa, mimi siyomchumi ni mtu wa maliasili na mazingira, Waziri atuambieuchumi ukikua unaupima wapi? Unaupima juu au kule kwawananchi walioko kule chini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Serikali lazimatuhakikishe kukua kwa uchumi kunaendana na hali kule chini.Hivi tunavyoongea watu wanazidi kuuza mashamba naviwanja vyao, mabenki yanatangaza kila siku kapiga minadanyumba za watu, watu wameacha kukaa kwenye nyumbazao walizokuwa wamejenga wameziuza wameendakupanga nyumba, sasa hii kusema uchumi umepandaumepandaje? Kiukweli kusema uchumi umepanda wakatihatuuoni huko chini tunaoishi na wananchi bado kunawalakini mkubwa sana. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni uzalishaji wamazao. Ukienda kwenye Kitabu cha Hali ya Uchumi kwenyepage 134, kuna baadhi ya mazao ambayo siku za nyumandiyo yalisaidia uchumi wa Taifa hili kukua ikiwemo kahawa,pareto, katani, tumbaku, mkonge, pamba, korosho na chai .Leo ukisoma kitabu kinasema mazao haya yamepunguatena kwa asilimia kubwa na sababu zilizotolewa hapa nikwamba, kwanza mvua za kutosha zimekosekana lakini pili,wakulima wameshindwa kununua pembejeo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunazungumzia habari yauchumi wa viwanda, bado tunategemea mvua ambazohazina uhakika. Hatuwezi kuzungumzia uchumi wa viwandawakati mazao ambayo yalikuwa yanainua uchumi wa Taifahili, ukisikia Kagera wameendelea ujue ilikuwa ni ndizi nakahawa; Kilimanjaro wameendelea ni kahawa, kule Mbeyacocoa, Tanga viwanda vilikuwa zaidi ya mia ni katani ilisaidiasasa leo yale mazao hayapo, yamekuwa ni mapori,tunazungumzia habari ya uchumi wa viwanda, vinatoka wapihivyo viwanda? Kwa hiyo, tukitaka kwenda kwenye uchumiwa viwanda lazima tujizatiti kwenye kilimo cha umwagiliaji.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tulikubaliana miaka mitanoiliyopita kwamba tutahakikisha tuna angalau hekta 1,000 zaumwagiliaji. Kwenye hotuba ya Waziri wa sekta nilisomampaka sasa hivi ni hekta 460,000 hata nusu kwa miaka mitanohatujafika, hatuwezi kwenda na leo tena mabadiliko yatabianchi, global warming na mambo mengine mengi. Kwahiyo, hatuwezi kwenda kwenye uchumi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sababu ya pilitumeambiwa ni wakulima kushindwa kutumia pambejeo. Zaokama kahawa leo ukisema mkulima anunue pembejeohawezi, ni very expensive. Kwa hiyo, kwenye mzao kama hayalazima Serikali itoe ruzuku kuwaachia wakulima ni vigumu.Wengine wanang’oa wanapanda maharage, migomba kwasababu hawawezi kuendelea kumudu kununua pambejeo.Kwa hiyo, naomba tuangalie hisotoria ya nyuma, Mwalimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

Nyerere alifanya kazi kubwa sana, mazao ambayo ndiyoyalikuwa kielelezo cha Taifa letu tusiyaache. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hata kwa mazaoambayo yapo sasa hivi, kwa mfano, suala la tumbaku Mkoawa Tabora tunalima lakini bado wakulima wakewameendelea kuwa maskini. Bei za mazao yetu bado nitatizo. Hivi navyoongea masoko ya jana na juzi bei imeshukakutoka Sh.4,000 mpaka Sh.4,500 kwa kila sasa wanauza kilonzima ya tumbaku kwa Sh.181, hayo ni masoko ya jana. Sasamkulima kama huyu ambaye amenunua pembejeo kwaSh.90,000 mfuko mmoja wa kilo 50 mpaka Sh.140,000 kwa walewaliokosa ruzuku lakini bei ya Serikali Sh.90,000, mkulima huyuakauze tumbaku Sh.181 wakati amekwensda kukopa benki,anadaiwa kwenye taasisi za fedha, ananyanyukaje huyu?Kwa hiyo, hata kwa mazao ambayo yanasaidia bado Serikalihatujaweza kusimamia bei nzuri ya mazao yetu, hili ni tatizokubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine, Mkoa waTabora umelima tumbaku lakini bado kiwanda kipoMorogoro. Tumepiga kelele sana hapa kwa nini Kiwanda chaTumbaku hakijengwi Mkoa wa Tabora? Majibu tunaambiwakwamba tunatafuta wawekezaji lakini juzi mwaka uliopitaamekuja mwekezaji wa Kiwanda kingine cha Tumbakuamejenga Morogoro. Naomba Serikali na Waziri aje namajibu, tunataka Kiwanda cha Tumbaku kiende kikajengweMkoa wa Tabora na mtuambie namna gani mtafanyakiwanda kile kiweze kujengwa vinginevyo kiukweli vijana walehawana ajira lakini tumbaku inalimwa kwao tena asilimia 60ya tumbaku ya Tanzania inalimwa pale Mkoa wa Tabora.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda kwenye kitabu piacha Mheshimiwa Waziri ukurasa wa 92 utaona namna ganiambapo tunaingiza sana bidhaa ndani kuliko kupeleka njekwa hiyo, tunauza kidogo, tunaingiza sana, hili ni tatizo. Kunavitu vingine ambavyo hatuhitaji kuingiza kutoka nje, kwamfano, toothpick, pamba za kwenye masikio, viberiti lakini

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

tuna-import kutoka nje, fedha tunayokusanya tunapeleka njekutengeneza ajira kwa vijana wao, sisi tunabaki ni masokoya bidhaa za wenzetu, hatuwezi kupiga hatua, hili ni tatizokubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Tabora tunalimambao, tena quality mbao, mninga na mpogo safi unaupataTabora. Serikali ilisema itahakikisha samani zote za Serikalizinatoka ndani ya nchi lakini leo tunapeleka magogo, mbao,Wachina wanakwenda kuchukua, tunakwenda kununuabidhaa za Kichina very weak, hazina ubora kwa gharamakubwa. Kwa nini Serikali inashindwa kusimamia vitu ambavyotunaweza kutengeneza hapa ndani ya nchi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi kweli kwa ule Msitu waSao Hill pale Iringa, kuna haja ya kwenda kununua kiberitinje? Hata mtoto wa darasa la saba anatengeneza kiberiti,hata mtoto wa darasa la pili anatengeneza toothpick, tunayopamba, vitu vingine ni sisi tunajitakia. Fedha ambayotunaipeleka nje inakwenda kujenga kule nje kumbetunaweza tukaitumia ndani ya nchi yetu ikazunguka humuhumu, tuka-invest ndani ya nchi yetu. Kitendo cha Serikalikuruhusu hata vitu vidogo vidogo vikaingizwa ndani ya nchini kushindwa kusimamia nchi yetu lakini pia ni kushindwakusimamia namna gani vijana wetu wapate ajira, tuna-create ajira kwa Wachina na kwa wengine huku vijana wetuwakiwa watanga tanga bila ya kuwa na ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika…

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha Mheshimiwa,ahsante.

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa CeciliaParesso atafuatiwa na Mheshimiwa Susan Kiwanga,Mheshimiwa Mwita Mwikabe Waitara ajiandae.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuchangia katika hojailiyoletwa mezani kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeelezavipaumbele vitatu ikiwemo kilimo, viwanda, huduma za jamiikwa maana ya maji, elimu na afya. Mimi nitachangia katikasuala la kilimo na elimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya CCM tokatumepata uhuru wananchi hii imekuwa na kaulimbiu namikakati mingi kuhusiana na sekta ya kilimo. Tulikuwa nakaulimbiu na mikakati mingi ikiwemo, Siasa ni Kilimo ya mwaka1974, Azimio la Arusha la mwaka 1967, Azimio la Iringa mwaka1974 lakini hata mwaka 2009 tulikuja na Kilimo Kwanza naSerikali ya Awamu ya Nne pia katika Big Results Now, sektaya kilimo na yenyewe iliongezewa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna ambaye anapingaumuhimu wa sekta ya kilimo kwa Watanzania. NilipochangiaWizara ya Kilimo hapa nilieleza umuhimu wa sekta ya kilimokwamba inaajiri nguvu kazi asilimia 65 ya Watanzania,inachangia asilimia 30 kwenye pato la Taifa, malighafiviwandani asilimia 65 inatoka sekta ya kilimo na asilimia 100ya chakula hapa nchini inatoka kwenye sekta ya kilimo.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika malengo yaMKUKUTA ya miaka 10, ilijiwekea mkakati wa ukuaji wa sektaya kilimo angalau kwa asilimia 6 mpaka asilimia 8. Ukuaji wasekta ya kilimo kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2011mpaka 2015 umekua kwa asilimia 3.4 tu. Hata hivyo, tokaSerikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, Serikali ya HapaKazi, Serikali ambayo inataka kutupeleka kwenye uchumi waKati, Serikali inayojiita ya viwanda, ukuaji wa sekta ya kilimo

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

pamoja na umuhimu wake wote umeshuka ukilinganisha naSerikali ya Awamu ya Nne ilivyokuwa madarakani. Ukuaji wasekta ya kilimo umekua kwa asilimia 1.9 tu toka mwaka 2016mpaka 2017. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, bajeti ambazotumekuwa tukizipitisha hapa Bungeni kwenye sekta ya kilimoimekuwa haifiki kwenye Wizara, hazitolewi kwa wakati.Mwaka 2016/2017 tulipitisha Bungeni hapa shilingi bilioni 100zilizotolewa ni shilingi bilioni 2 tu fedha za maendeleo nisawasawa na asilimia 2.2. Mwaka 2017/2018 sekta ya kilimoilitengewa shilingi bilioni 150 zilizotolewa ni shilingi bilioni 16.5sawasawa na asilimia 11 na mwaka huu fedha zilizoombwakwenye sekta ya kilimo kwa maana ya Wizara ya Kilimozitakazotekeleza miradi ya maendeleo ni shilingi bilioni 98.1.Tunawashangaa sana kila siku Serikali iliyoko madarakani,pamoja na kaulimbiu zenu na mikakati yenu mnayosemakwenye vitabu lakini sekta ya kilimo ambayo tunaitegemeasisi Watanzania tulio wengi, mmeendelea kutoipa kipaumbelena kutoona umuhimu wa sekta ya kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukifanya uwiano kati yabajeti kuu ya Serikali na sekta ya kilimo, mwaka 2016/2017uwiano kati ya bajeti kuu na sekta ya kilimo kama ambavyommesaini Maazimio mbalimbali ya Kimataifa ni asilimia 0.93,mwaka 2017/2018 ni asilimia 0.85, mwaka 2018/2019 ni asilimia0.52 na mwaka huu imeshuka zaidi ukilinganisha na miakamingine. Sasa tunajiuliza mmesema mtaweka kipaumbelechenu cha kwanza ni sekta ya kilimo lakini sekta hiyo hiyo yakilimo hamuipi fedha, mmewasahau Watanzania wakulimawalio wengi, tutawaaminije? Mbona mmetudanganya miakamingi sana? Mmekuwa wazuri kwenye maandishi, kwenyevitabu lakini kuja kwenye utekelezaji mmekuwa tofauti kabisa.Kwa kweli nirudie kusema, wakulima wa nchi hii adui yenunamba moja ni Serikai iliyopo madarakani kwa mikakati nasera mbovu ambazo hazitekelezeki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kutuambiakwamba kwenye bajeti hii kipaumbele ni kilimo lakini miaka

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

iliyopita, mavuno ya mwaka juzi, wakulima mbaazi tuimewasumbua mpaka leo, kupata masoko ya wakulima wetumbaazi ni mtihani, korosho ni mtihani, pamba ni mtihani yaanihakuna ambako afadhali, tumbaku ni mtihani, mahindiimewasumbua mwaka mzima yanawahangaishamnakataza vibali, mnageuka kwa nyuma mnaruhusu vibali.Kahawa imewasumbua, pamba, mkonge, mazaomchanganyiko hakuna mkulima wa nchi anayelima zaololote ambaye ana uhakika wa soko. Sasa mnasemakipaumbele ni kilimo mnawahakikishiaje Watanzaniawakulima kuwa na uhakika wa masoko? Nini mkakati kwenyebajeti hii kuhakikisha wakulima wana masoko ya kutosha?Tunaomba majibu Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie kuhusu sektaya elimu. Serikali ya Awamu ya Tano mmesema mnatoa elimubure na Serikali ya Awamu ya Nne iliona kutoa elimu bure nichangamoto, ikaona namna bora ni kusaidiana na wazazikuhakikisha wanakabiliana na upungufu mbalimbali kwenyesekta ya elimu ikiwemo miundombinu na changamoto nyingikatika shule zetu za msingi na sekondari hapa nchini. Ninyimmekuja, mmefuta michango, mnasema elimu ni bure,Mheshimiwa Waziri kwenye mambo yako 10 uliyoyataja hapaya kumsifia Rais Magufuli umeelezea suala la elimu bure,nataka nikwambie elimu bure imekuwa na changamotokubwa, mnaua sekta ya elimu kuliko hata Serikali ya Awamuya Nne ilivyokuwa madarakani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe takwimu,upungufu wa walimu, shule za msingi, mwaka 2016 upungufuulikuwa 191,772 mwaka 2017 upungufu umeongezekaumefika 179,291; shule za awali, upungufu wa walimuumekuwa 1,948; shule za sekondari masomo ya hisabatiupungufu wa walimu ni 7,000, baiolojia 5,000, kemia 5,000,na fizikia 6,000. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, upungufu wa miundombinu;upungufu wa maktaba…

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

T A A R I F A

NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE):Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa

MHE. CECILIA D. PARESSO: Umeongezeka…

NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE):Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa

WABUNGE FULANI: Mheshimiwa Kandege, si utajibubaadaye.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Paresso, kuna taarifa.

NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE):Mheshimiwa Naibu Spika, naheshimu sana mchango waMheshimiwa lakini ni vizuri tukapeana taarifa; angekuwaanakwenda na takwimu walikuwa wanafunzi wangapi naongezeko limekuwa kiasi gani ndiyo unafanya comparison.Ukitazama ongezeko la wanafunzi huwezi ukasema kwambakuna pungufu, ni vizuri akaenda na hiyo taarifa ili asijeakawapotosha wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Cecilia Paresso, unaipokeataarifa hiyo?

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika,siipokei hiyo taarifa na kitu ambacho nafikiri Serikali mnakoseasana, mnapima mafanikio ya elimu bora na idadi yauandikishwaji siyo quality na hiki kitu mmekuwa mnakisemasiku nyingi. Pia idadi ya wanafunzi wanaondikishwainawezekana ikaongezeka kwa sababu ya uzao, birth ratenayo inawezekana ikawa inaongezeka, populationinaongezeka, sasa mnapimaje hayo? Mheshimiwa Naibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

Waziri utapata nafasi baadaye na wewe utasema ya kwako.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, upungufu wa maktaba;mwaka 2016 upungufu ulikuwa ni asilimia 88, mwaka 2017upungufu umekuwa ni asilimia 91. Maana yake badala yakwenda mbele kupunguza changamoto mbalimbali zakimiundombinu tunarudi nyuma hatua kadhaa haya matatizoyanazidi kuongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, maabara; upungufu wamaabara ya baiolojia ni asilimia 51, fizikia 54 na kemia 53.Upungufu wa madawati ni milioni 1,170,000 na upungufu wawalimu ni 186,000. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunajiuliza, mnatuambiaelimu bure, elimu hii siyo bure, mnakwenda kuua Taifa lakesho. Badala tuliandae Taifa la kesho, mnajua umuhimu waelimu ni kuandaa rasilimali watu, kuliandaa Taifa, tuwe nawataalam na wajuzi wa kutosha, tuandae mazingira yakufikia haya, tunatengeneza mazingira mabovu ya kuwa naelimu mbovu ya kuiangamiza nchi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa SusanKiwanga atafuatiwa na Mheshimiwa Mwita Waitara,Mheshimiwa Mussa Ramadhan Sima ajiande.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi hii adhimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na kitabu hiki chaWaziri, ukurasa wa 11 anazungumzia wastani wa pato la Taifala kila mtu, anasema kwamba wastani wa kila mtu kwamwaka 2017 ni sawa na dola za Kimarekani 1,021ukilinganishana na mwaka 2016 ni dola 958 kwa mwaka, kwahiyo anasema umekua. Sasa swali langu, mlishawahikupandisha mishahara? Hawa watumishi katika nchi hiiwastani wao wa pato la Taifa umepanda au umesimama

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

pale pale? Kwa hiyo, hapa kipato chako kinatudanganya?Hawa watumishi ambao hamuwapandishi mishaharapamoja na sisi Wabunge mnasema wastani kwa dola yaKimarekani 1,021 badala ya dola 958 huo ni uwongo wamchana kweupe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, watumishiwanapata wapi hela nyingine, wanakula rushwa mpakamnawapima wastani wao wa kipato kwa mwaka?Tusidanganyane. Yaani ninyi wataalam wa kuandika hivivitabu, mnaandika peke yenu halafu mnatuletea hapa,mnawadanganya Watanzania, wastani haujakua, hivyo nivitabu tu lakini hali halisi sifuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naenda sasa kwenye bajetikuhusu kilimo maana mimi ni mtoto wa mkulima na naishikwa kutegemea kilimo. Bajeti ya mwaka 2016/2017, Bungehili tuliidhinisha bajeti ya kilimo shilingi bilioni 100.5 lakini helazilizotolewa kwenye kilimo ni shilingi bilioni 2.252 halafuunasema pato limekua, limekua kwa nani? Labda kwakowewe lakini kwa Watanzania wa kawaida na wananchi waMlimba halijakua chochote, bado wanarudi nyuma badalaya kusonga mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Kilimo mwaka2017/2018, Bunge hili tuliidhinisha kwenye bajeti shilingi bilioni150.25 na sifuri sifuri huko, lakini hadi kufikia Machi mwakahuu pesa zilizotoka za miradi ya maendeleo ni shilingi bilioni16.5 sawasawa na asilimia 11 tu, leo unasema pato laMtanzania limeongezeka, limeongezeka wapi wakati miradiya kilimo ni shida?

Mheshimiwa Naibu Spika, kule kwetu na karibuTanzania nzima hivi ninavyosema ni wakati wa mavuno,wananchi sasa wanavuma pumba kwa sababu mipungapanya waliingia, mahindi panya waliingia wakahangaikawakulima mpaka sasa wakati wa mavuno watu hawavunitena, halafu tunaambiwa ikitokea njaa Mkuu wa Wilaya, sasakama panya wamekula halafu kilimo hamjawapa hela zakutoa wale panya hivi unadhani watu hawataomba tena

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

msaada? Mjiandae Wizara ya Fedha kuweka fungu maalumkwa ajili ya kuwasaidia Watanzania ambao wamekosakuvuna sasa hivi mazao yao yote yaliliwa na panya. Siyokwamba wavivu wamelima lakini uwezo wa kuvuna tenahaupo, hiyo ni hali mbaya, sijui watu wengine kamawamevuna lakini kwangu hali ni mbaya sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hali hii imeendelea katikamiradi yote, tumepiga kelele hapa Bunge zima, Serikaliilitenga shilingi bilioni 251 kwenye Miradi ya Maendeleo Vijijini,(Local Government Development Grants, kwenye mwakahuu tunaomaliza, Wakurugenzi wote Tanzania nzima naWenyeviti wa Halmashauri wakapuliza magari mafutawakaharibu bajeti zao wakaja Dodoma, wakaambiwamnapewa hela, leteni miradi ya mikakati, mkishaweka tumkirudi pesa zinaingia. Mpaka leo hakuna senti tano iliyoingia.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkurugenzi wetu naMwenyekiti wa Halmashauri alirudi Kilombero tukakaa vikaowakatumia pesa kwa ajili ya kuidhinisha miradi ya kimkakati,wananchi wamejenga madarasa, maabara, zahanati,mmesema mtaleta hela na mvua zitaingia ile miradiitakwenda kubomoka, nguvu za wananchi zitakwenda bure,halafu leo mnasema bajeti iko sawasawa, sawasawa ganininyi? Acheni mambo yenu bajeti hewa hizo. Kwanitunaposema bajeti hewa ni zipi? Si ndiyo hizo zakudanganyana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa leo mnatuambiatupitishe tena bajeti, haya hii bajeti tunayoipitishamtaitekelezaje wakati hii bajeti ya mwaka huu tunaoendakuumaliza mwezi huu hakuna kitu, hewa. Mnaharibu karatasitu hapa hamna lolote, bora mngesema tu kwamba, hatunahela, eti ninyi mnasema mna hela pato la Taifa limekua kwaasilimia 7.1 limekuakua vipi, mmekusanya wapi? Ninimmekusanya mpaka leo? Cash budget, mmekusanyaje hiyobajeti, mnaishia kulipa madeni lakini kibaya zaidi mnaendakukopa kwa biashara, halafu mnalipa madeni, nyie vipi? Nyie

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

mnadhani hatujui siri zenu mnazofanya? Mnajikazakaza tu,mnatumbua watu kila kukicha hamtaki kusema ukweliWatanzania huku wanaumia, watu hawalipwi mishahara yao.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona wenzetu waUganda walimu tu hawakupandishwa mishaharawametangaza mgomo, hapa Tanzania, yaani si juitumelogwa na nani? Ni haki kabisa ya kila mfanyakazikupandishwa mshahara lakini mpaka leo hata senti tano,mnavunja sheria, kwa nini mnavunja sheria? Kama ninyi kwelimnakusanya pesa na mna pesa kwa nini mnashindwakupandisha mishahara ya watu kwa mujibu wa sheria? Leomnajitamba hapa tuna pesa, pesa ziko wapi? Pesa hamna,mkiambiwa ooh, mnakopa kopa tu. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wapandisheni wafanyakazimishahara yao kwa mujibu wa sheria zilizowekwa. Hii Serikaliya Awamu ya Tano ni hatari kuliko Serikali zote zilizopita,nawaambia. Halafu leo vitabu unasema uchumi umekua,umekua kwa nani, labda umekua kwa ninyi mnaoshikashikahela huko Benki Kuu. Hela siyo zenu ni zetu halafu mnakujahapa mnatudanganyadanganya. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi hii tulipofikia hali nihatari hata wewe unajua, Waziri anajua kila mmoja anajua,lakini kwa vile mnailinda Serikali ndiyo mnasema hayahamtaki tu kusema hali mbaya. Kama hali nzuri lipenimishahara kwa Watanzania wanaolitumikia Taifa hili, kutwamnatumbuatumbua. Kama pato la Mtanzania limekua, walewafanyakazi waliotumbuliwa mpaka leo hawajui hatma yaopato lao limekua au limeondoka? Watanzania ganiwanaowazungumzia? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata ukiwa na kiwanjawakati wa JK utauza shilingi milioni 5 sasa hivi mpaka milioni 1hupati mnunuzi. Ninyi nini ninyi! Eti pato limekua limekulia wapiwakati watanzania wako hoi. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Hapo sasa.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwenye kitabu chake amezungumzia Tume ya Taifa yaUchaguzi waliidhinishia hela kidogo wakafika mpaka asilimia300, acheni ubabaishaji, kwa nini kutumia hela nyingi zauchaguzi? Kwa sababu kazi yenu Awamu ya Tano kununuaMadiwani na Wabunge halafu mnaenda mnafanyauchaguzi matokeo yake Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeendakutumia mpaka asilimia 300, acheni hizo. (Makofi)

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa NaibuSpika, kuhusu utaratibu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Susan Kiwanga Mchumikutoka Mlimba, naona Chief Whip amesimama hapa.(Kicheko)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa NaibuSpika, kuhusu utaratibu, pamoja na kumsikiliza sana Mchumikama ulivyosema kutoka Mlimba, Mheshimiwa Susan hapaanasema tulichobakia hapa ni kununua Madiwani badalaya kushughulikia masuala ya msingi ya maendeleo yawananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nafahamu kabisa kwamba,hata yeye anafahamu ni kwa kiasi gani Serikali hii ilivyowezakuboresha huduma nyingi ikiwemo huduma za afya katikanchi yetu ya Tanzania. Hata hivyo, nafahamu utaratibu wauchaguzi katika nchi yetu ya Tanzania unazingatia sheria nataratibu zilizokuwepo na zilizowekwa. Kama kuna mtu anaonakabisa amedhulumiwa na katika uchaguzi hajashinda ukoutaratibu wa kisheria wa kudai madai halisia kwa mujibu washeria. Kama hajafanya hivyo, nataka kumthibitishia kwambahakuna Diwani ambaye ameshinda eti kwa sababu labdammoja alinunuliwa na mwingine hakununuliwa.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba kwa mujibuwa utaratibu Mheshimiwa Susan atuthibitishie kama anauhakika wa Diwani aliyenunuliwa na kama hana uhakikaafute kauli hizo ili aweze kuendelea na mchango wake.

(Hapa baadhi ya WaheshimiwaWabunge walikuwa wakiongea bila mpangilio)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Chief Whip tusaidie kanuniuliyokuwa unaisoma.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa NaibuSpika, ni Kanuni ya 64(1)(a), Mbunge hatatoa ndani ya Bungetaarifa ambazo hazina ukweli.

(Hapa baadhi ya WaheshimiwaWabunge walikuwa wakiongea bila mpangilio)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Heche, yaani kila sikuunapenda jina lako liingie kwenye Taarifa Rasmi za Bungekwamba, unapenda sana kuongeaongea. Tafadhali, tuwetunasikilizana, lazima utajwe kwa sababu unavurugu zakuzungumza bila kusikiliza wenzako, kila wakati ni habari yakowewe tu, tafadhali.

Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa JenistaMhagama amesimama kwa mujibu wa Kanuni ya 64akimtaka Mheshimiwa Susan Kiwanga aliyekuwa akichangiakwa mujibu wa fasili ya (1)(a) ambayo inamtaka Mbungeasitoe taarifa Bungeni ambazo hazina ukweli, lakini pia fasiliya (2) ndiyo inayotaka Mbunge huyo atakiwe kufuta kauliyake.

Waheshimiwa Wabunge, hil i ni jambo kuhusuutaratibu na Mheshimiwa anaomba jambo hili lithibitishweama lifutwe kwenye Taarifa Rasmi za Bunge. Mambo haya siya leo yalishawahi kutolewa utaratibu siku za nyuma. Tuhumaza namna hii zimeshawahi kuzungumzwa hapa ndani maranyingi na tuhuma hizi zilishatolewa utaratibu. Kwa hivyo,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

tunapokuwa tukitoa michango yetu tujielekeze kwenye yalemambo ambayo yanaruhusiwa kwa maamuzi ya kitiyaliyopita lakini pia kwa Kanuni zetu. Ndio maana mara zoteWaheshimiwa Wabunge Kiti kinaposimama huwa nawasihisana tusikilizane ili usirudie makosa yale yale kila wakati.

Waheshimiwa Wabunge, mnafahamu wote kwambavyama vyote vinapokea wanachama kila wakati, watuwakitoka huku, wakielekea huku na wengine wakitoka hukukuelekea kule. Tusilete mambo humu ndani yanayotupotezeawakati wetu sisi wenyewe. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, kwenye hil i la hayoaliyoyasema Mheshimiwa Susan Kiwanga kwa sababu ndiyealiyekuwa anachangia nitamtaka afute hiyo kauli kwasababu uamuzi wa hili jambo ulishatolewa siku za nyumahakuna uamuzi mpya kuhusu jambo hili na ulitolewa humundani, kwa hivyo tujielekeze huko. Mheshimiwa SusanKiwanga, jambo hil i l i l ishazungumzwa humu ndani,lilishatolewa maamuzi kwa hivyo ufute kauli yako ili tuwezekuendelea mbele. Mheshimiwa Susan Kiwanga.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,sijui dakika zangu umenilindia maana mara nyingi hawaMakatibu wako huwa wanasema na za Mheshimiwa Jenistatumeingiza mle mle, tutakuja kuonana wabaya.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa wewe futa halafutuendelee na mengineyo, futa hiyo kauli yako.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,nafuta kauli kwa sababu Watanzania wengi wanajua hilo.

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Taarifa MheshimiwaNaibu Spika.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Susan Kiwanga, naombauifute kauli yako kwa unavyofahamu kikanuni na wewe sioMbunge mpya humu ndani, futa kwa kadri kanunizinavyokutaka, usianze message sent, sijui kitu gani, sijui

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

Watanzania wamefanya nini, futa kadri kanunizinavyokutaka, tafadhali Mheshimiwa Susan. MheshimiwaHawa Mwaifunga tafadhali.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,nafuta kauli ili maisha yaendelee. (Makofi)

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Taarifa MheshimiwaNaibu Spika.

(Hapa baadhi ya Waheshimiwa Wabungewalikuwa wakiongea bila mpangilio)

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,wamenitoa kwenye reli ndio hao akina Shika hao,unamwona. (Kicheko)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Susan, hapa nilikuwanakusifia Mchumi wa Mlimba kwani kuna tabu gani hukoMlimba, leo umekujaje humu ndani mwenzetu, malizia mudawako.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba nimalizie muda wangu kama alivyosema nduguyangu hapa Mheshimiwa Nsanzugwanko pamoja namipango yenu basi muangalie na sera ya nchi hii kuunganishamikoa. Mimi natokea Mkoa wa Morogoro, kuna Mkoa waNjombe unaunganika kwenye barabara Jimbo la Mlimbalakini tangu nil ivyoanza kusema mpaka leo, okay,wamefanya upembuzi kiasi mpaka Mlimba lakini kutokaMlimba mpaka Madeke Njombe hakuna upembuzi, hakunakinachoendelea. Kwenye vitabu vyao vya Serikali sioni hatamafungu yanayotengwa kujenga barabara angalau waanzekidogo ili Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Njombe kupitiaMlimba ile barabara iunganishwe. Ndio maana wakatimwingine tunachangia hapa tunaona uchumi haujakuwakwa sababu wananchi wa maeneo yale bado wanatesekana sera hazitekelezwi. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Naambiwa muda wako umekwishaMheshimiwa.

WABUNGE FULANI: Aaaaa.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,Makatibu hawa ni tatizo.

WABUNGE FULANI: Hajamaliza muda wake.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwita Waitara, atafuatiwana Mheshimiwa Mussa Ramadhan Sima, Mheshimiwa AidaKhenani atachangia dakika tano, tutamaliza na MheshimiwaEmmanuel Papian John.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Nimepiga kelele sana humu ndani, nachangiakwa nguvu mno lakini mambo ni yale yale mpaka koolimeharibika sasa, leo nitachangia taratibu sitapiga kelelesana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye taarifa yaMheshimiwa ndugu yangu Mheshimiwa Dkt. Mipango,ukurasa wa 81 alikuwa anamlinganisha Mheshimiwa Magufulina watu maarufu waliofanya mambo makubwa duniani. Sasana mimi nimeingia kwenye Google hapa nikajaribukuangalia, amemtaja mtu anaitwa Park Chung Hee, huyuamezaliwa mwaka 1917 na amekufa mwaka 1979 lakinialikuwa assassinated maana yake aliuwawa. Alikuwamwanajeshi tangu mwaka 1944 mpaka 1945 na alikuwa cheocha Jenerali halafu alikuwa ni Dikteta. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mtoto wake pia wakwanza alikuja akawa mwanamke wa kwanza kuwa Rais waKorea. Kwenye historia inaonyesha tarehe 10 Machi, 2017aliondolewa madarakani kwa kupinduliwa kwa tuhuma zarushwa. Historia inaonesha pia tarehe 6 Aprili, 2018, huyu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

mwana mama aliyekuwa Rais wa Korea (South Korea)amefungwa jela miaka 24 kwa tuhuma za rushwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilipoangaliahistoria hii nikasema haya maneno inabidi Mheshimiwa Dkt.Mpango ayafute kwa sababu Mheshimiwa Rais wetuhafanani na mambo ya namna hii. Afute maneno haya siosawasawa. Nadhani Mheshimiwa Dkt. Mpango atakuwalabda ame-quote vibaya lakini hii uindoe historia imekaavibaya, nilikuwa nataka nianze hapo. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitatumia kitabu chaMheshimiwa Mpango, ukiacha hilo andishi moja tu ambalonimeona lina shida, ameandika maneno mazuri kwa sababuamekiri vizuri na nitapitia maeneo machache aliyosemaukweli. Nampongeza sana Mheshimiwa Mpango kwa kusemaukweli.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mpango yeyeni msomi mchumi, mimi ni mwalimu sielewi, ni mwanasayansitu wa kawaida lakini 2016 uchumi ulikua kwa asilimia 7,mwaka 2017 ulikua kwa asilimia 7.1, mwaka2018 ulikua kwaasilimia 7.2. Mimi naomba Mheshimiwa Dkt. Mpango atusaidiehivi ukimueleza mtu wa kawaida yaani miezi hii kwa mwakahuu kwamba uchumi umekua ataelewa yaani Mbunge wakesielewi, atusaidie Watanzania waelewe, yaani hii ina-reflectvipi maisha ya kawaida ya wananchi? Kwa kweli hii napatanayo shida sana, unaweza ukaeleza hapa na fomulaumeandika, wananchi wa kawaida wanataka kuona kamaunasema uchumi unakua, mzunguko wa fedha mtaani uwemkubwa uonekane, bidhaa ipatikane, watu wapate mahitajiya kawaida. Sasa hiyo lugha hapa mimi siioni kwa kweliunisaidie Mheshimiwa Dkt. Mpango kwa utalaam wako.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Bajeti ya Serikali2016/2017 zilitengwa shilingi trilioni 29.5 hazikufika asilimia 80katika utekelezaji wake. Mwaka 2017/2018 tulipitisha bajetiya shilingi trilioni 31.7 sasa hivi taarifa inaonyesha ni asilimia69 labda imeongezeka kabla ripoti haijaandaliwa. Hii bajetiya sasa hivi ni shilingi trilioni 32.5, naomba unisaidie ni kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

nini tusiende na bajeti halisi? Tumeshatenga bajeti miakakadhaa iliyopita tumeona fedha yetu ya ndani ni kiasi gani,tumeona misaada ikoje na mingine inakwama halafu tusemehapa sisi uwezo wetu ni shilingi trilioni 20, tupange mipangoya shilingi trilioni 20. Hapa ndipo malalamiko yanapokujakwamba tunawapa watu matumaini makubwa, bajetikubwa, mambo mengi lakini hayafanyiki, inaonekanatunadanganya, nadhani hili pia lifanyiwe kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini lingine ni kwenyeukurasa wa 14, Mheshimiwa Mpango amesema kiwangokikubwa cha umaskini kimekuwepo kwa Watanzania, nimaneno kwenye kitabu hiki cha hotuba. Anasema ukosefuwa ajira, sasa naomba unisaidie kwa hapa Mheshimiwa Dkt.Mpango. Maduka mengi yamefungwa huo ndio ukweli, watuwamefungwa biashara zao. Kama biashara zinafungwamaana yake mzunguko wa fedha unapungua, wananchi wakawaida wale ambao waliokuwa wamepata ajira hawanaajira tena, uchumi unakuwaje hapa? Kwa hiyo, katika hili piamliangalie.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna usafi wa kilaJumamosi, nimeona tu mahesabu ya kawaida, Watanzaniawanaambiwa wafunge biashara zao kila Jumamosi asubuhiwanafungua saa nne haijalishi kama kuna famasi, kunawagonjwa lakini wale mama lishe ambao wanapika chapati,wanaopika supu, huo ndiyo muda wa kupata hiyo hudumana hao wamejiajiri, sasa tunafanyaje hapa. Kwa hiyo,naomba mtuambie hii ratibu ya kila Jumamosi kufanya usafitumepata faida kiasi gani na hasara kiasi gani ili tuwezekuamua maamuzi mengine tofauti na haya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine bar za Tanzaniazinafunguliwa saa kumi zinafungwa saa tano usiku. Kule kunaMa-barmaid walikopata ajira zao lakini kuna biasharazinafanyika wanalipa kodi. Kwa mfano, Dar es Salaam kunafoleni kweli kweli kama wewe umetoka mjini unafikanyumbani saa tatu, yaani unafika mtaani kwetu Kivule,Gongo la Mboto ni saa tatu usiku kwa mazingira ya Dar esSalaam, mwendo kasi haijafika. Maana yake hawa watakaa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

pale saa mawili wanazungumza bar inafugwa na ma-defender yanakamata watu kweli kweli, hawa watuwanalalamika. Kama kuna sheria ilikuwepo siku nyingi kwanini isibadilishwe twende na wakati? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wenzetu Kenya hapa haoUsalama wa Taifa, Polisi wanatakiwa kuhangaika na watuambao vipato vyao havijulikani wamepataje. Kama kunamtu anakunywa, anakula, anavaa vizuri, ana magari mazurihatujui kazi yake, hiyo ndiyo kazi ya Usalama wa Taifakuwatafuta watu ambao wana vipato ambavyo havieleweki.Kenya hapo Nairobi huduma ni saa 24, biashara inazunguka,kila mtu anafanya kazi yake, watu wawajibike. Kwa hiyo,tusitengeneze mazingira ya kutisha watu, wafundishweustaarabu na wajitegemee na wafanye maamuzi sahihi.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukurasa wa 15amezungumza habari ya kilimo, mifugo na uvuvi na amesemamwenyewe hizi sekta tatu zinawaajiri Watanzania asilimia 66.Sasa nimuulize Mheshimiwa Dkt. Mpango kwenye bajeti hiimalalamiko yote ambayo Wabunge wamesema kwenyekilimo watu wamelima mazao ya pamba, tumshukuruMheshimiwa Waziri Mkuu amechukua hatua lakini hatamahindi mpaka unaenda kwenye msimu mwingine hayamazao bado yapo mtaani. Mifugo imepigwa, imeteswahakuna malisho, hakuna sehemu ya kuchungia, ugomvi nawakulima, Operesheni Sangara, leo mmezungumza habariya samaki, haya mambo Mheshimiwa Mpangomngeyachukua mkakae pamoja mkayafanyia kazimkatengeneza Taifa ambalo tunataka kwenda mbelebadala ya kurudi nyuma tusirudie mambo yaleyale ya kilasiku.

Mheshimiwa Naibu Spika, iko hoja hapa MheshimiwaJenista ametoka nje, tulipokuwa tunajadili habari yakuunganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii tulilalamika hapakwamba ile formula iingizwe kwenye sheria. WaheshimiwaWabunge ile formula haijaingizwa, sasa hivi kuna ugomvimkubwa kati TUCTA na Serikali na wameshusha, ilikuwa 1/540

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

sasa imeenda 1/580. Mafao kwa mkupuo ilikuwa asilimia 50kwa formula hii ambayo inalazimishwa wataalipwa asilimia25,. Kwa mkupuo walikuwa wanalipwa asilimia 50 imeshukazaidi ya nusu kwa yale mafao na kuna ugomvi mkubwa.Tulilalamika sheria iingizwe haijaingizwa wametunga kanuni.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ina madhara kwasababu hawa watumishi ambao, kwa mfano watu wa LAPF,PSPF wanaidai Serikali siyo chini ya shilingi bilioni 600 za madenihayajalipwa na huu mzigo ni wa Serikali, hawa wastaafuwanachama wa vyama hivi ndiyo wataingia kwenye mzigohuu na hili ni janga la Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kama hauongezimshahara Mheshimiwa Dkt. Mpango hawa wakiendakustaafu calculation ya mafao yao mwishoni inategemeaincrement ya kila mwezi. Ndiyo maana tunasema fuatenitaratibu watu waongezwe pesa zao zitawasaidia siku zambele katika maisha yao. Watu wanakufa haraka kwasababu ya kukosa huduma nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nishauri jambomuhimu sana hapa, kwa mfano, kwenye Wizara ya Elimuametaja data ndugu yangu Mheshimiwa Paresso sitakikurudia yaani ukiangalia figure ya matundu ya vyoo,madarasa, nyumba za walimu, upungufu wa walimu, miminadhani Mheshimiwa Dkt. Mpango akija atuambie kwenyebajeti hii haya mambo yatatekelezwa kwa kiasi gani.Wabunge wamelalamika mmechukua kodi ya majengo, kodiya mabango kwenye maeneo mbalimbali tumeathirika,haujarudisha asilimia Mheshimiwa Mpango, ungetuambiafedha hii imerudishwa kwa kiasi gani, haya mamboyangefanyika ingetusaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nishauri jambomuhimu sana, kuna maneno mengi sana yanaendelea nakwa sababu mambo yanafanyika kwa haraka haraka sanakwa mazingira fulani hisia zinakuwa nyingi sana mtaani. Kwamfano, mimi nimesoma ule Waraka wa Watumishi wa Mungu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

wa Waislam na Wakristu, mambo ambayo yametajwa,wanashauri hivi, tuwe na utawala bora, tufuate sheria, hii nchihaiongozwi kwa Ilani za vyama na matumizi mabaya ya dola.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, hivi hayamambo ya kutishiana, haya mambo ya kufuata utaratibukuna kosa gani, Taifa hili humu ndani tumebaguana sanakivyama. Wabunge wa CCM, Wabunge wapinzani wakijadiliwanadhani wengine wana haki zaidi kuliko wenzao kumbeTaifa ni la kwetu sisi wote. Tungeona tu kwamba hawa watuwanashauri, mimi nikitoa hoja ingepokelewa kwa nia njemakabisa kwa kujenga Taifa. Hii bajeti ni ya kwetu na ikipita siyoya CCM ni bajeti ya Watanzania, iwe tumeunga mkono auhatujaunga, tusaidieni kupeleka Taifa mbele kwakutuunganisha. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiriakwisha kwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa muda wakoumekwisha, ahsante sana.

Tunaendelea na Mheshimiwa Mussa Ramadhan Sima,atafuatiwa na Mheshimiwa Aida Khenani dakika tano,Mheshimiwa Emmanuel Papian John ajiandae.

MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Naibu Spika,nichukue fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu lakinipia niwapongeze Mheshimiwa Waziri na Naibu wake kwabajeti hii ambayo mipango yake imekaa vizuri, yapo maeneoambayo tunapaswa kuishauri Serikali vizuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuliweke jambo moja sawa,unajua mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, MheshimiwaDkt. Mpango alisema vizuri sana, amesoma vitabu vyaviongozi hawa amejifunza best practice na worse practicesasa afute nini? Mheshimiwa Dkt. Mpango nikupongeze sana.Nadhani mimi nilikuelewa vizuri wakati umezungumza na hiyo

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

itakuwa imetusaidia sana lazima ujifunze sehemu zote mbili.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imejikita katikauchumi wa viwanda utakaochochea ajira na ustawiendelevu kwa jamii. Likisemwa hivi kwenye bajeti maanayake lazima tuone indicator za kuelekea kwenye uchumi waviwanda. Serikali imeeleza vizuri imepunguza Corporate Taxkwenye kilimo lakini kwenye bidhaa za ngozi, natakanijielekeze kwenye bidhaa za ngozi. Tukizungumzia bidhaaza ngozi ni lazima tujue kama viwanda vyenyewe vyakutengeneza ngozi vipo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka hapa tujielekezevizuri sana, tulikuwa na viwanda vya ngozi mimi sidhani kamavipo. Leo Mwanza hatuna kiwanda cha ngozi, ile MwanzaTannery imebaki kuwa go-down. Ukienda Arusha kipokiwanda kimoja kazi yake kubwa ni kutengeneza wet blue,inalainisha tu ile ngozi na kuisafirisha kwenda nje. Tuna HimoTannery na tuna Kiwanda cha Moshi Leather ambachokimefungwa. Morogoro tulikuwa na kiwanda pale nachenyewe kimefungwa kilikuwa kinafanya temporary.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nataka kujiulizatumepunguza kodi kutoka asilimia 30 kwenda 20 kwenyebidhaa za ngozi wakati viwanda hamna. Nataka Serikaliitusaidie hapa na nishauri vizuri, leo bidhaa ya ngozi hiitunayoizungumza ngozi yenyewe imeshuka thamani. Ngozileo kilo moja inauzwa Sh.200 mpaka Sh.500 lakini hivyoviwanda viwili vinavyofanya finishing kwa maana ya Himona Moshi Tannery, Himo tu kinaweza kununua ngozi tani 100peke yake, Dar es Salaam peke yake inazalisha kwa siku ngozitani 45 maana yake Dar es Salaam peke yake inawezaikalisha hivi viwanda viwili basi, kwa hiyo, mikoa yote hiiikiwemo na Singida ngozi yetu imekosa thamani.

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa lazima tuishauri Serikalivizuri na iwe makini kwenye jambo hili. Tunapotaka kuoneshaindicator kwenda kwenye viwanda kuna eneo la muhimusana, tunataka mashine ziingie humu lakini kwenye Customs

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

Duty ni lazima tuondoe Import Duty na VAT asilimia 18.Itakuwa imetusaida mno kwenye eneo hili ili viwanda namashine ziingie ili tuweze kuanzisha hivi viwanda tofauti nahapo hatuwezi kuwa na uchumi wa viwanda lakini bidhaatunazo. Ngozi hii tunayoizungumza ukitaka kuitoa nje unalipakodi asilimia 80 maana yake ngozi ambayo umeinunua kiloSh.500 unalipa kodi Sh.1,200 utaenda kuiuza wapi lakini ngoziinateseka leo. Nataka niiombe Serikali wakati tunajiandaakuweka viwanda hivi iruhusu ngozi hii iuzwe ili Serikali ipatemapato na wananchi waweze ku- survive. Kwenye eneo hilinilikuwa nataka niombe Serikali iliweke vizuri sana taarifa hiihaiko sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hata kwenye kilimo,nchi yetu leo kilimo ni uti wa mgongo kuondoa CorporateTax kwa asilimia 10 peke yake haitoshi. Nashauri tuweke zerotu kabisa walau kwa miaka miwili itatusaidia sana ku-promoteeneo hili la kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ziko Regulatory AuthorityTFDA, TBS, TPRI, NEMC, Vipimo na wengine wengi.Tumezungumza sana kwenye bajeti iliyopita kwamba ifikemahali tu-harmonize hizi Regulatory Authority zote zinafanyakazi moja. Kila mmoja anakwenda kwa mfanyabiasharaanatoza ada. Sasa tukaomba tufanye One Shop Stop Centernataka kusema leo hii nayo haiwezekani hawa wotewanafanya kazi ya Serikali, niiombe Serikali ilipwe ada mojatu ya mfanyabiashara kulingana na kiwango; kamamfanyabiashara ana mtaji wake wa Sh.100,000 mpakaSh.10,000,000 whatever alipe ada moja tu hawa kazi yaowaende wakatoe certificate, basi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, aende kwenye kiwandakwa mfanyabiashara akague atoe taarifa Serikalini siyo nayeye aende akatoze faini na yeye anataka ada, hatuwezikufika. Tunataka indicator hizi ziwekwe sawa. Kama tunatakauchumi wa viwanda hizi Regulatory Authority ni sehemu yakumomonyoa hatuwezi kufika, ilipwe ada moja tu Serikalini.Mtu akilipa ada moja hawa kazi yao waende wakafanyeauditing kuangalia kama hiyo bidhaa ni halali ama sio halali

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

watoe taarifa Serikalini. Wanalipwa mshahara na Serikali lakinihawana sababu ya wao kuanzisha vyanzo vya mapato.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niipongeze Serikali kwenyeeneo moja la betting, amezungumzia Sheria ya Michezo yaKubahatisha (sport betting) imeongeza kodi kutoka asilimia6 mpaka 10 lakini kwenye slot mashine Sh.35,000 mpakaSh.100,000. Tukizungumzia sport betting maana yaketunazungumzia Watanzania sasa wameamka na mwamkohuu ni wa eneo la soka, wapenzi na wanachama wa sokawameona sasa kuna haja ya kuingia kwenye eneo hili naSerikali inapata mapato.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa isiishie hapo, natakanioneshe na eneo lingine kila mchezo wa soka unaochezwaTanzania kwenye viwanja vyetu tunalipa VAT baada ya kutoayale mapato yote get collection wanatoa asilimia 18inayobaki ndiyo wanaita asilimia 100 wanaanza kugawana.Naiomba Serikali kwenye eneo hili tunataka kuboreshamichezo Tanzania na tuboreshe mchezo huu wa soka ilitupate mapato zaidi maana yake hii asilimia 4 na hii shilingisabini na kitu inayoongezeka tuwape Baraza la Michezo laTaifa ili liweze kujielekeza kuhakikisha kwamba tunapataviwanja na kuboresha mchezo huu wa soka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania hii leo hataukipewa msaada wa vifaa vya michezo kutoka nje maanayake unalipa kodi. Sasa niiombe Serikali vifaa vya michezohivi hebu viingie bure hatuna sababu ya kulipa Import Dutywala VAT sababu tunaboresha michezo Tanzania. Natakaniiombe sana Serikali eneo hili iliangalie vizuri sana. Hata ileasilimia 18 ya get collection ambayo inapatikana kwenyeviwanja wapeni Baraza la Michezo waweze kuboreshamichezo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna eneo lingine lawafanyakazi hapa, niipongeze Serikali kwa kuweka singledigit kwenye Income Tax lakini single digit tunayoizungumzahapa inazungumzika kwenye eneo la kima cha chini, hao

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

wengine inaendelea kama kawaida. Serikali izungumze singledigit kwenye Income Tax kwenye mshahara wote bila kujalikima cha mshahara cha mtu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimpongezeMheshimiwa Waziri Mkuu alifafanua vizuri sana kuhusumishahara ya wafanyakazi, sina sababu ya kurudia eneo hilikwa sababu ya muda lakini nataka niombe eneo mojamuhimu sana. Tangu Serikali imeingia madarakani mwaka2015 tulianza zoezi la uhakiki la wafanyakazi tukasimamishamadaraja ya watumishi wakiwemo walimu, madaraja hayayamesimama mpaka leo. Maana yake mtu aliyeanza kazi2015 na 2012, 2018 tutawakusanya pamoja waweze kulipwadaraja moja, this is unfair, halitakubalika. Niombe kamaalistahili kupanda daraja 2015 kama anaenda daraja D,mwaka 2018 alipaswa kuwa daraja E apewe daraja lake lasasa E na tusirudi huko kumpa daraja D, tutakuwatumemuonea. Nataka niiombe sana Serikali kwenye eneohili itusaidie ihakikishe watumishi wetu wanapata haki yao.Hawa watumishi hawana kosa lolote, uhakiki ulikuwa ni wakwetu wenyewe Serikali siyo wa watumishi, tutoe mwongozohuu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie eneo linginela PPP (Public Private Partnership). Nataka niende harakahapa nitolee mfano, leo eneo la UDART pale Dar es Salaamkwenye usafirishaji mwendokasi mradi ule unakufa lakiniSerikali tuna asilimia 49, mtu anaye-hold share na sisi anaasilimia 51, mradi unakufa. Mradi unakufa kwa sababu ganina Serikali imekaa kimya?

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi mingi tunaendeleanayo, juzi Mheshimiwa Rais amezindua Agricultural SectorDevelopment Program Phase II lakini Phase I hatujaitathminiikoje. Hapa tunazungumzia PPP, hata tunapokwenda kwenyestandard gauge tunatarajia kwenda kwenye PPPtutakwendaje? Niombe Serikali ituletee taarifa kuhakikishamiradi hii ya PPP inatusaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Aida Khenan dakika tano, tutamalizia naMheshimiwa Emmanuel Papian John.

MHE. AIDA J. KHENAN: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Kwa kuwa dakika tano ni chache sana kunamambo nategemea Waziri atakuja kutoa ufafanuzi ili tuwezekuelewa. Unapozungumzia kukua kwa uchumi leo katikakilimo wakulima wa mahindi ambao mwaka jana waliwezakuuza mahindi yao gunia Sh.60,000 leo ni Sh.24,000. Kwa hiyo,unapozungumzia kukua kwa uchumi mtuambie umekuasehemu gani.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo katika Taifa hili nimekaanimefanya tafakari kubwa ni nani ana amani, mfanyakazihana utulivu kwa sababu alitegemea sheria itamlindakuongezeka kwa mshahara wake leo mshahara hauongezwi,mkulima hana amani kwenye Taifa hili, hali ya kilimo ni mbaya,njoo kwa wavuvi, njoo kwa wafanyabiashara, nani ana utulivukwenye Taifa hili. Mheshimiwa Waziri wa Fedha wewe ndiyounaweza kumshauri Rais vizuri kama unaweza kusikilizamawazo ya Wabunge tunayozungumza humu ndani.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo mfanyabiasharaanajiona ni kama mkimbizi ndani ya Taifa lake. Ni kwa ninimmeshindwa kutengeneza mazingira rafiki kwawafanyabiashara ni kutoza kodi zisizokuwa na sababu. LeoTRA wanajua hali ya uchumi ni mbaya lakini wakiamuakufunga wanafunga, huwezi kukamua maziwa ng’ombeusiyemlisha, unategemea wao wanapata wapi pesa. Taifahili tunategemea wakulima, wavuvi, wafanyakazi, leo watuhawa wote wako kwenye wakati mgumu Taifatunaliendeshaje? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sera ya kulinda uchumi waTaifa. Tuliopo humu ndani siyo kwamba wote tumesomauchumi tuko kwenye facult tofauti tofauti lakini ni paleambapo unaweza kuchukua mawazo yetu ukaoanisha na

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

taaluma yako kuweza kulipeleka Taifa mbele. Kamautachukua mawazo yako binafsi ndiyo haya tunarudi tenakuzungumza ndani ya Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vijana kama mimi wanawakati mgumu kwenye Taifa hili, ajira ni shida, wamejiingizakwenye kilimo, kilimo hicho ndiyo imekuwa taabani hili Taifatunalipeleka wapi? Waziri wa Fedha ukisema uchumi unakuawewe ndiyo unayempotosha Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania hali ni mbaya kuliko hiki unachokiandika, hii halini nzuri kwa nani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapozungumza mazingirawezeshi kwa wafanyabiashara ni lazima tuangalie hawawafanyabiashara wanapolipa kodi wanategemea wayaonematokeo ya kodi wanayoilipa. Leo hakuna matokeo yoyoteambayo yanaweza yakawaletea tija na wao kujisukumakuweza kulipa kodi. Leo wanaona ukiwa mfanyabiashara nibora ukae nyumbani. Hili suala ambalo tunazungumzakwamba mfanyabiashara ukimuelimisha akajua umuhimu wakodi na akayaona matokeo hakuna ugomvi utakaotokeakwa sababu faida ya kulipa kodi anaiona. Leo mnatumianguvu kuliko kutumia busara na maarifa inatuweka kwenyewakati mgumu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hili Taifa sio la Waziri waFedha ni Taifa la Watanzania, hiki unachokiandikaunategemea kodi za Watanzania wakiwemo wakulima,wafanyakazi pamoja na wafanyabiashara. Ukijifungiamwenyewe ukaja na hizi takwimu unazozileta hapa zitaishakwenye kitabu na haitakusaidia. Kwa sababu ulipoteuliwana Rais aliamini ukija humu ndani utasikiliza mawazo yaWabunge na sio mawazo yako. Haya mawazotunayokwambia sisi kwamba unapozungumza hali ya uchumiumepima kwenye kipimo gani, ni kipimo gani ambachoumekitumia, wafanyakazi wanalia, wakulima wanalia,wafanyabiashara wanalia, wewe hizi takwimu unazipatawapi? (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

Mheshimiwa Naibu Spika, ndani ya Bunge pia tunawakati mgumu na ndiyo maana tunasema MheshimiwaWaziri wa Fedha zungumza ukweli. Ni lazima mbadilisheapproach na Taifa lolote makini linakuwa na vipaumbele nakipaumbele sio cha kwako ni kipaumbele ambachokinawagusa Watanzania na maisha halisi ya watanzania. Leoukienda kwenye uhalisia hiki ulichokiandika haujaoneshamkakati wowote…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha Mheshimiwa,ahsante sana. Mheshimiwa Emmanuel Papian John atakuwandio mchangiaji wetu wa mwisho.

WABUNGE FULANI: Hayupo.

NAIBU SPIKA: Nadhani ametoka kidogo.

Waheshimiwa Wabunge, tumefika mwisho wauchangiaji wetu kwa leo. Nitaleta matangazo niliyonayohapa halafu nitatoa taarifa kuhusu mwongozo uliokuwaumeombwa na Mheshimiwa Charles Kitwanga asubuhi.

Waheshimiwa Wabunge wote wa Chama chaMapinduzi wanatangaziwa na Mheshimiwa Jasson Rweikiza,Katibu wa Wabunge hao kwamba mara baada ya Bungekuahirishwa jioni hii wanatakiwa kufika Morena Hotel. Naaminiwanakaribishwa na wale wanaotaka kuhamia labda.(Makofi/Kicheko)

MAJIBU YA MWONGOZO

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, niliombwamwongozo leo asubuhi na Mheshimiwa Charles Kitwangakuhusu tangazo nil i lokuwa nimelitoa kuhusu taarifazinazotakiwa na Sekretarieti ya Tume ya Madili za uthibitishowa mali na madeni ya Waheshimiwa Wabunge yaliyoko

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

ndani ya nchi na pia nje ya nchi. Wakati nikisoma tangazolile nilitoa taarifa kwamba tarehe ya mwisho iliyotolewa kwawale ambao walikuwa wamepata taarifa mapema zakutakiwa kuwasilisha uthibitisho huo itakuwa ni tarehe 25 Juni,2018. Sasa nilisema baadaye tutatoa taarifa kuhusu waleambao walikuwa hawajapewa taarifa kuhusu kutakiwakupeleka uthibitisho huo na kwamba tarehe yao tungeitajabaadaye baada ya kufanya mawasiliano na wenzetu wamaadili.

Waheshimiwa Wabunge, sasa nimeletewa taarifa naWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi waUmma na Utawala Bora kuwa kama tulivyokuwa tumesemaasubuhi kwa wale ambao mwezi Januari, 2018 walitakiwakuwasilisha vielelezo na ambao hawajaviwasilisha mpakasasa wafanye hivyo kabla ya tarehe 25 Juni, 2018. Kwa waleambao hawakutakiwa kufanya hivyo ama hawakupewataarifa hiyo Januari sasa watapeleka vielelezo vyao katikaOfisi zao za Kanda kabla ya tarehe 31 Agosti 218. Hawawanaweza sasa kupeleka taarifa zao kwenye Ofisi za Kandana ili tuende vizuri Ofisi za Kanda nitazirudia kuzisoma kwaharaka ili Waheshimiwa Wabunge mmpeleke huko taarifabaada ya kurudi majimboni na kupata hivyo vielelezo.

Kwa upande wa Dar es Salaam, Ofisi ya Kanda yaDar es Salaam itahudumia Dar es Salaam na Zanzibar.Upande wa Kanda ya Mashariki, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waPwani Kibaha itahudumia Pwani, Morogoro na Tanga. Kandaya Kaskazini Arusha AICC itahudumia Arusha, Kilimanjaro naManyara. Kanda ya Kati Dodoma Kilimani itahudumiaDodoma na Singida. Kanda ya Magharibi Tabora itahudumiaTabora, Kigoma na Simiyu. Kanda ya Ziwa (Mwanza)itahudumia Mwanza, Geita, Kagera, Shinyanga na Mara.Kanda ya Kusini (Mtwara), itahudumia Mtwara, Lindi, Ruvuma.Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya NBC House)itahudumia Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Songwe naRukwa. Naamini Kanda ya Ziwa itahudumia pia Wabungewanaotoka Simiyu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kuyasema haya,naahirisha shughuli za Bunge mpaka siku ya kesho, tarehe 20saa tatu asubuhi.

(Saa 01.20 Usiku Bunge LiliahirishwaHadi Siku ya Jumatano, Tarehe 20 Juni, 2018)