Upload
others
View
132
Download
36
Embed Size (px)
Citation preview
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
HUDUMA YA KUWAIMARISHA VIONGOZI WA KANISA
AFRIKA MASHARIKI
THEOLOJIA YA KI-BIBLIA
na
Jonathan M. Menn
B.A., University of Wisconsin-Madison, 1974
J.D., Cornell Law School, 1977
M.Div., Trinity Evangelical Divinity School, 2007
Equipping Church Leaders-East Africa
3701 N. Gillett St., Appleton, WI 54914
(920) 731-5523
www.eclea.net
December 2009; revised February 2015.
Theolojia ya Ki-Biblia ni mkondo wa maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji wa nchi na mwanadamu katika Mwanzo, kupitia
anguko la mwanadamu na matokeo yake, na historia ya ukombozi wa Mungu kwa mwanadamu, hata utimilifu wa mbingu
mpya na nchi mpya katika Ufunuo. Biblia inaeleza ksimulizi inayofungamana, huku Yesu Kristo akiwa ndiye moyo wake.
Theolojia ya Ki-Biblia huangalia dhana kuu ambazo zinazopitia katika Biblia nzima, zinazolenga juu ya uhusiano wa
Mungu na mwanadamu. Pia huonyesha jinsi Kristo na kanisa ndio utimilizo wa maagano, ahadi, unabii, na taasisi
zilizoanzishwa katika Agano la Kale. Ramani za nyakati, na Dibaji zimeambatanishwa kama nyenzo za kusaidia.
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
1
ORODHA YA YALIYOMO
THEOLOJIA YA KI-BIBLIA: UTANGULIZI…………………………………………………………..........................4
I. Tabia ya Theolojia ya Ki-Biblia...…………………………………………………………………….............................4
A. Maelezo ya Theolojia ya Ki-Biblia……………………………………………………………..….....…………………..4
B. Fikira za Theolojia yaKi-Biblia...………………………………………………………………...….…………………...4
II. Mtazamo wa Mkondo wa Simulizi na Dhana za Theolojia ya Ki-Biblia….……………………................................5
A. Msingi wa mkondo wa simulizi za Biblia..…………………………………………………………...…………………..5
B. Dhana za Theolojia ya Ki-Biblia.…..………………………………………………………………..…………………...5
MSINGI WA SIMULIZI YA MKONDO WA BIBLIA ………………………………………….…................................6
I. Uumbaji (Mwanzo 1-2)………………………………………………………...................................................................6
A. Simulizi ya mkondo wa Biblia huanzia na Mungu (Mwa 1:1) ………………………………………............................7
B. Mungu aliumba kila kitu bila kutumia chochote.…………………..………………………………...............................7
C. Mungu alimuumba mwanadamu ili atawale viumbe vingine vyote (Mwa 1:26-28) …………………………………..7
II. Anguko la Mwanadamu Katika Dhambi na Matokeo Yake (Mwanzo 3-11:26)……………….…………………....8
A. Ukuu wa Mungu, wajibu wa mwanadamu, na kuwepo kwa dhambi..…………………………….................................8
B. Adamu na Hawa watenda dhambi na kufukuzwa kutoka bustani ya Edeni (Mwanzo 3) …………………………....14
C. Matokeo ya Anguko—kutoka kwa Kaini hadi Mnara wa Babeli (Mwanzo 4-11:26)…………….…………………...16
III. Tukio la Ukombozi—Mungu aita Watu Kwa Ajili Yake Mwenyewe (Mwa 11:27-Ufunuo 20)………………….19
A. Mwanzo mpya wa Mungu—Kutoka Ibrahimu hadi Yusufu (Mwa 11:27-50:26)……………………………………..19
B. Kuanza kwa taifa la Israeli—Kutoka Misri kwenda nchi ya ahadi (Kutoka-Kumbu-kumbu)…..................................21
C. Israeli ndani ya hiyo nchi (Yoshua-1 Samueli 7)…………………………………………………….............................23
D. Israeli kama ufalme ulioungana (1 Samueli 8-1 Wafalme 11; 1 Nyakati 1-2 Nyakati 9;
Zaburi-Wimbo ulio bora)……………………………………………………………………………………….....23
E. Israeli kama ufalme uliogawanyika (1 Wafalme 12-2 Wafalme 17; 2 Nyakati 10-31; Isaya na Mika
[utabiri kwa Israeli na Yuda]; Yoeli [utabiri kwa Yuda]; Hosea na Amosi
[utabiri kwa Israeli]; Obadia [utabiri kwa Edomu]; Yona [utabiri kwa Ninawi])………….…………………..24
F. Kuwepo, kushuka, na kuanguka, kwa ufalme wa Kusini (2 Wafalme 18-25; 2 Nyak 32-36:21;
Isaya-Danieli; Nahumu-Zefania)………………………………………………………………………….……..24
G. Kurejeshwa kwa ufalme wa Kusini (2 Nyak 36:22-Esta; Hagai-Malaki)…………………………………….…….....26
H. Kutimizwa kwa mpango wa Mungu wa ukombozi katika Yesu Kristo (Mathayo-Ufunuo 20)……………………….27
I. Ufunuo wa Yesu wa Masihi wa kweli, ufalme wa Mungu, na kanisa……………………………..……………….......28
IV. Mbingu Mpya na Nchi Mpya (Ufunuo 21-22)…………………………………………..……………………….…..30
A. Uumbaji mpya wa Ufunuo unaendana na uumbaji wa awali wa Mwanzo…………………………………………...30
B. Uumbaji mpya wa Ufunuo unapita uumbaji wa awali wa Mwanzo …………………………………………………..30
DHANA MBILI ZA KI-BIBLIA KUHUSU UHUSIANO WA MUNGU NA MWANADAMU.…………………......31
I. Hekalu na Nchi: Maskani ya Mungu na Mwanadamu…………………………………………………………….....31
A. Bustani ya Edeni (Mwanzo 2-3; ona pia Ezek 28:13-16)………………………………….………………………......31
B. Hema ya kukutania (Kutoka 25-31, 35-40)……………………………………………………………...……………..32
C. Hekalu (2 Sam 7:1-17; 1 Waf 6; 8:1-11; 1 Nyak 17:1-15; 22:1-16; 28:1-29:9; 2 Nyak 3-5)……..............................34
D. Maono ya Ezekiel ya Hekalu Jipya (Ezekieli 40-48)…………… …………………………………………………….35
E. Mbingu Mpya na Nchi Mpya (Ufunuo 21-22)…………………………………………………………........................40
II. Uhusiano wa Mungu na Watu Wake Kuhusu Ndoa…………………………………………………………….......43
A. Mwa 2:23-24 (mwanamke kuumbwa rasmi kwa ajili ya mwanaume; mwanaume kuwaacha babaye na
mamaye na kuunganishwa na mkewe na kuwa “mwili moja” naye) ni mfano unaoelezea uhusiano
ambao Mungu anautaka kwa watu.…………………………..……………………………………………….....43
B. Katika AK kiungo cha ndoa kati ya Mungu na watu wake kiliwekwa, lakini Israeli hakuwa mwaminifu.………....43
C. Katika AJ muktadha wa kindoa umetanuka na kufanyika rasmi kati ya Kristo na kanisa ………………………....45
D. Katika Ufunuo, picha ya Ki-Biblia kuhusu uhusiano wa kindoa kati ya Mungu na watu wake huja
kutimilika katika Kristo, bibi arusi (kanisa), na Nchi Mpya……………………………………………………46
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
2
KRISTO NA KANISA KAMA UTIMILIZO WA AK……………….……….………………………………………...47
I. Biblia Kimsingi ni Kumhusu Yesu Kristo—Yeye Ndiye Mtu Aliye Kiungo na Dhana Iunganishayo Yote.…......47
A. Zinapotazamwa peke yao, simulizi za AK na nabii zake hazimtaji moja kwa moja Yesu Kristo, bali huwa na
Nguzo ya kusimamia, na hutumia lugha zinazolenga, na kumwelekea mlengwa wa kuibukia taifa la
Israeli.………………………………………………………………………………………………………….....48
B. Yesu na waandishi wa AJ wote walitumia AK kumhusu Yesu na kwa Injili..…………………………………….....48
II. Agano la Ibrahimu, la Daudi, na Jipya Yalielekea Kwake na Kutimilizwa Katika Kristo na Kanisa.………….49
A. Agano la Ibrahimu limetimizwa katika Kristo na Kanisa…………………….………………..…………….………..50
B. Agano la Daudi limetimizwa katika Kristo na Kanisa…………………………………..…….…………………….....53
C. Agano Jipya limetimizwa katika Kristo na Kanisa………………………………………….…………………………57
III. Yesu Ndiye Israeli Mpya, wa Kweli, na Mwaminifu.……………………………………………………………....60
A. Yesu ageuza historia ya Israeli…………………………………………………………………………………………60
B. AJ lamwonyesha Yesu kama Musa mpya, aliye mkuu zaidi, awakomboaye watu siyo tu kutokana na
vifungo vya kimwili, bali kutoka utumwa wa kiroho, dhambi na mauti (Yohana 1:29; Rumi 6:3-23)……....61
C. AJ hutumia lugha na majina ya Israeli ya AK kwa Yesu………………………….………………………………...62
D. Katika Yesu ahadi za AK za marejesho kwa Israeli zatimizwa…………………………………………………….....62
IV. Kwa vile Kanisa liko “Katika Kristo,” Kanisa ndilo Israeli Mpya, wa Kweli na wa Kiroho.………………......68
A. Israeli ya AK na kanisa: neema za kimwili na za kiroho, kuchaguliwa, na imani katika AK………………………68
B. Uhusiano kati ya Israeli ya AK na kanisa …………………………………………………………………………….70
C. Yesu alilikataa taifa la Israeli kama chombo cha kujengea ufalme wa Mungu, na kuwapa jukumu hilo
wafuasi wake mwenyewe, kanisa .……………………….………………………………….…………………..71
D. Kanisa ndio watu wapya, wa kweli, wa Mungu—Israeli wa kiroho………………………………………..………...74
E. Kama Israeli mpya, wa kweli na wa kiroho, kanisa linakabiliwa na mitihani ile ile ya uaminifu ambayo
Israeli ya AK ya kimwili ilikumbana nayo…………………………………………….………..………………78
V. Kristo na Kanisa Watimiliza na Kuchukua Nafasi na Hekalu……………………………………………………..78
A. Yesu ndiye hekalu la kweli ………………………………………………………………………………………….…78
B. Kama mwawakilishi wa Kristo aonekanaye kwa macho hapa duniani, kanisa ni “Helaku” la Mungu duniani......83
VI. Yesu Alitimiliza na Kubadilisha Sikukuu za Kiyahudi.……………………………………………………………86
A. Kalenda ya Israeli ya AK……………………………………………………………………………………….………86
B. Mifumo ya AK ya Israeli ya Sikukuu.…………………………………………………………………………..……...87
C. Yesu alitimiza Pasaka na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu..……………………………………………………88
D. Yesu alitimiza Sikukuu ya Malimbuko na ya Majuma..………………………………………………………………89
E. Yesu alitimiza Sikukuu ya Mabaragumu.…………………………………………………….………………………. 90
F. Yesu alitimiza Siku ya Utakaso……………………..…………………………………………………………………..91
G. Yesu alitimiza Sikukuu ya Vibanda……………………………………………......…………………………………..92
H. Yesu alitimiza Mwaka wa Yubile………………………………………………………………………………….…....94
VII. Yesu Alitimiza na Kuchukua Nafasi ya Israeli ya Mfumo Mzima wa AK wa Utoaji Dhabihu
na Ukuhani……………………………………………………………………………………………………….95
A. Mifumo ya AK ya Israeli ya utoaji dhabihu…………………………………………………………………………....95
B. Yesu alitimiza mfumo mzima wa utoaji dhabihu wa Israeli wa AK ………………………….………………………96
C. Yesu alitimiza na kusimamisha ukuhani mzima wa AK………………………………………………..……………..96
D. Waebrania hutofautisha mfumo mzima wa desturi za dhabihu, na ukuhani wa Israeli na Kristo………………….97
VIII. Yesu Alitimiza na Kuibadilisha Sheria ya AK.……………………………………………………………………98
A. Sheria ya AK ilikuwa sehemu ya Agano la Musa (la Kale)……………………………………………………............98
B. Sheria ya AK ilikuwa ni mfano tu………………………………………………………………………………………98
C. Sheria ya AK ilikuwa ya kitambo ………………………………………………….………..........................................99
D. Yesu alikuja kuitimiliza sheria…………………………………………………………………………………….......100
E. Yesu alionyesha na kuthibitisha mamlaka yake juu ya sheria yote ya AK ……………………………….................101
F. Yesu alisshi chini ya Agano la Kale, bali alikuwa mjumbe wa Agano Jipya…………………………………..….....101
G. Wakristo hawafungwi na Agano la Musa wala sheria yoyote ya AK, bali wako chini ya “Sheria ya Kristo”……..102
IX. Yesu Aliitimiza na Kuibadilisha Sabato ya AK…………………………………………………………………….103
A. Yesu alionyesha na kuthibitisha mamlaka yake juu ya Sabato…………………………………………………........103
B. AJ linabadilisha umuhimu wa Sabato………………………………………………………………………………..104
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
3
C. Kutimizwa kwa Sabato katika Kristo kunamaanisha kuwa Jumapili siyo tu ni “Sabato ya Ki-Kristo” ya
mapumziko sawa sawa na Jumamosi ilivyokuwa Sabato ya Kiyahudi……………….....................................104
X. Kristo na Kanisa ndiyo “Mtumishi wa Bwana” aliyetabiriwa…………………………………………………...105
A. Yesu ndiye “Mtumishi wa Bwana” aliyetabiriwa .…………………………………………………………………...105
B. Kanisa ndilo kwa ujumla ni “Mtumishi wa Bwana,” kama vile Yesu alivyokuwa kibinafsi
“Mtumishi wa Bwana”………………………………..………………………………………………………..106
DIBAJI 1—VIFUPISHO KWA UCHACHE VYA VITABU VYA BIBLIA ……………………………………….107
DIBAJI 2—MIPANGILIO YA MUDA WA HISTORIA YA BIBLIA.…………………………………………......110
DIBAJI 3—BIBLIA KATIKA MPANGILIO UNAOONGOZANA.………………………………………………..112
DIBAJI 4—MPANGILIO WA MUDA WA WAFALME NA MANABII WA ISRAELI NA YUDA………….…114
DIBAJI 5—NABII CHACHE ZA KIMASIHI NA KUTIMIZWA KWAKE………………………………………116
DIBAJI 6—YESU NI MUNGU KAMILI NA MWANADAMU KAMILI.………………….....…………………...117
DIBAJI 7—YESU NA “ISHARA YA YONA” (MATH 12:38-41; 16:1-4; LUKA 11:29-32)……………………...126
DIBAJI 8—RAMANI ZA HIMAYA ZA ASHURU, BABELI, NA UAJEMI...…………………………………….130
DIBAJI 9—RAMANI YA HIMAYA YA RUMI & MAJIMBO YAKE...…………………………………………..130
DIBAJI 10—RAMANI YA KANAANI: SEHEMU 12 ZA MAKABILA..………………………………………….131
DIBAJI 11—RAMANI YA UFALME ULIOUNGANA WA ISRAELI..…………………………………………....131
DIBAJI 12—RAMANI YA FALME ZILIZOGAWANYIKANA ZA YUDA NA ISRAELI……………………....132
DIBAJI 13—RAMANI YA ISRAELI NYAKATI ZA AGANO JIPYA……………………………………………..132
NUKUU ZILIZOTOLEWA…………………………………………………………………………………………….133
KUHUSU MWANDISHI……………………………………………………………………………………………….140
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
4
THEOLOJIA YA KI-BIBLIA: UTANGULIZI
I. Tabia ya Theolojia ya Ki-Biblia
A. Maelezo ya Theolojia ya Ki-Biblia
1. Theolojia ya Ki-Biblia (TK) ni masomo yahusuyo kuweka bayana mkondo wa simulizi za Biblia kuanzia
mwanzoni (Mwanzo) hadi mwisho (Ufunuo). Ni “kutafuta unganiko la ndani la Biblia” (Bartholomew 2005: 84).
2. Theolojia ya Ki-Biblia “Hufuatia hatua za ufunuo tangu neno la kwanza la Mungu kwa mwanadamu
kupitia kupambanuliwa kwa utukufu kamili wa Kristo. Huchunguza hatua mbali mbali za historia ya
Biblia na mahusiano kati yao. Kwa hiyo, hutoa msingi wa kuelewa jinsi vifungu vya sehemu moja ya
Biblia vinavyohusiana na vifungu vingine vyote. Tafsiri iliyo safi ya Biblia hutegemeana na yapatikanayo
katika [TK].” (Goldsworthy 1991: 32)
3. Kwa vile inajihusisha kuelezea kiunganisho cha ndani cha Biblia kwa namna yake yenyewe, ni “ya
kujieleza na ya kihistoria kiasi kwamba tafsiri ya kitheolojia na theolojia ya ki-mfumo haiwezi kuwa
hivyo” (Bartholomew 2005: 86). Ingawaje TK ni nidhamu ya kimaelezo na kihistoria, Biblia inachagua
katika undani wa kihistoria inaoelezea. Uchaguzi huo msingi wake ni theolojia yote kiujumla ambayo
Biblia inaweka bayana. “Umoja wa historia ya Kibiblia huegemea katika njia ya uchaguzi ambavyo
simulizi huelezwa katika uelekeo fulani na siyo kwa mikondo mingine iwezekanayo. Kuna mwendelezo
kwenye mkondo wa simulizi ambao unakataa kugeukia kwenye makorongo yenye upofu. Hivyo
tunamfuata Seti, siyo Kaini; Shemu, siyo Hamu; Ibrahimu, siyo Lutu; Israeli, siyo Edomu; Daudid, siyo
Sauli; Yuda, siyo Samaria; Yerusalemu, siyo Babeli. Mwishowe, uchaguzi muhimu ni ule wa Yesu kama
Masihi halisi kinyume na hali ya sasa ya kumkana Yeye. Agano Jipya huona mwendelezo halisi wa
kihistoria wa taifa la Israeli kama watu wa Mungu wapatikanao katika Yesu Kristo. Mnyambuo huo wa
historia ni wa kitheolojia ya ndani na siyo wa kujaribisha.” (Goldsworthy 2000: 69)
B. Fikira za Theolojia ya Ki-Biblia
1. Biblia inaelezea simulizi inayoshikamana, na Yesu Kristo ndiye moyo wa simulizi hiyo (Luka 24:25-
27, 44-47; Yoh 5:39). Kila kitabu cha Biblia kinachangia kitu fulani kwenye simulizi hiyo, na ujumla wa
simulizi nzima hutoa mpangilio ambao kila kitabu kilichomo kinaweza kutafsiriwa vizuri zaidi.
2. Ingawaje Biblia inaelezea simulizi iliyounganika, ufunuo wa Mungu ni hatua kwa hatua—hujifunua
kila mahali katika Biblia yote. Kanuni kadhaa muhimu huibuka kutokana na kweli hizi.
a. Andiko halitalipinga Andiko. Vifungu viwili vinavyoonekana vinapingana, vitakuja kuonyesha
havipingani pale vitakapochunguzwa kwa umakini zaidi. Kifungu kimoja kinaweza kurekebisha
au kuongezea sifa ya kingine, lakini hakitakipinga.
b. Yote mawili hatua za ukombozi na “kusudi lote la Mungu” (Mdo 20:27) lazima yaangaliwe
ili kuelewa kiusahihi kifungu chochote kile. Mafundisho ya “ufunuo wa hatua kwa hatua”
hutueleza kwamba hatua za ukombozi lazima zizingatiwe wakati wa kutafakari kifungu chochote
kile. Biblia ni muunganiko unaoelezea simulizi ya kisa kilichoungan. Hata hivyo, kweli za Biblia
hazifunuliwi zote kwa mkupuo moja, bali hufunuliwa hatua kwa hatua. Maana kamili ya kifungu
chochote husika au fundisho la Ki-Biblia laweza lisiwe wazi hadi Biblia nzima iwe
imezingatiwa.
c. Agano Jipya linavyolitafsiri Agano la Kale.
(1) Maandishi yoyote ya Ki-Biblia yanapaswa kusomwa ndani ya muundo wa maneno
yaliyotumiwa (lugha na mfumo wa maandishi husika) na mazingira ya kihistoria
yalipoandikwa mara ya kwanza. Agano Jipya limeandikwa kwa misingi ya Agano la
Kale. Miktadha mingi ya Agano Jipya husimamia Agano la Kale. Uelewa wetu wa
Agano Jipya hutajirishwa kwa kiwango kikubwa kwa kulielewa Agano la Kale. Wakati
huo huo, hatupaswi kulisoma Agano la Kale kama kwamba Jipya halipo. Yote mawili
yapo – kutokuendeleza na mwendelezo kati ya Agano la Kale na Agano Jipya. Agano
Jipya hujengwa juu ya miktadha ya Agano la Kale, mara nyingi katika namna za
kushangaza. Hilo ni kweli zaidi kuhusu jinsi Agano Jipya linavyohusisha unabii wa
Agano la Kale.
(2) Lazima tukumbuke kwamba sheria za Agano la Kale, sikukuu, na taratibu nyingine
zimetimilizwa na kukamilishwa katika Kristo (Math 5:17; Rum 10:4; 2 Wakor 3:12-
16; Wagal 3:23-4:7). Kwa namna nyingi, Israeli ya kimwili ya Agano la kale, sheria
zake, sikukuu zake, na taratibu nyingine, zilikuwa “aina,” “vivuli,” au “mifano” ya
uhalisi wa Agano Jipya (1 Wakor 10:1-6; Wakol 2:16-17; Waeb 8; 10:1). Kwa hiyo,
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
5
tunapoiangalia picha nzima, hasa tunapotumia Maandiko, tunapaswa “kuyasoma
Maandiko ya Agano la Kale kwa kupitia miwani ya Maandiko ya Agano Jipya” (Lehrer
2006: 177). Kama ilivyosemwa, “Hili Jipya, ni lile la Kale lililotimilika; la Kale ni Jipya
lililofunuliwa.”
II. Mtazamo wa Mkondo wa Simulizi na Dhana za Theolojia ya Ki-Biblia
A. Msingi wa mkondo wa simulizi za Biblia
1. Katika mtazamo wa kawaida zaidi, Biblia ni simulizi ya uumbaji, historia, na hatima ya ulimwengu na
mwanadamu, kama ielezwavyo kimsingi kwa mtazamo wa kitheolojia. Mungu aliumba ulimwengu wa
kupendeza sana na wanadamu kuishi kwa furaha, na maisha yaliyotimilika katika ushirika na yeye.
Kupitia dhambi zetu tulipoteza ushirika ule na kuleta uovu na uharibifu na mauti duniani. Hata hivyo,
Mungu hakutuacha katika dhambi zetu na mauti. Kwa njia ya mpango mahususi uliohusisha kumwita
Ibrahimu na taifa la Israeli, aliandaa njia kwa ajili ya kuja ndani ya mwanadamu kwaYesu Kristo ili
kuleta msamaha wa dhambi na kurejesha ushirika na yeye. Anakuja tena, kumaliza dhambi kabisa na
mauti pasipo kutuangamiza sisi. Atakwenda kutimiliza kurejeshwa kwetu na uhusiano wetu na yeye. Na
pia ataifanya upya nchi, hata iwe ya utukufu zaidi ya ilivyoumbwa mara ya kwanza. Katika muundo huo,
mkondo wa simulizi hii ungeonekana namna hii: uumbaji (Mwanzo 1-2)=>Anguko na madhara yake
(Mwanzo 3-11:26)=>Ukombozi (Mwanzo 11:27-Ufunuo 20)=>Uumbaji mpya (Ufunuo 21-22).
Mungu mwenyewe ndiye yote mawili -mtunzi wa simulizi na ndiye mhusika mkuu wake.
2. Biblia ni ufunuo wa Mungu kuhusu jinsi alivyo na mpango wake (Injili) kwa mwanadamu.
a. Kiungo cha katikati cha ufunuo huo—yeye aliye kiungo mtendaji wa uumbaji, njia ya
ukombozi, na chanzo na utimilifu wa uumbaji mpya—ni Yesu Kristo (ona 2 Wakor 1:20; Waef
1:9-10; Wafil 2:6-11; Waeb 1:1-3).
b. Kwa hiyo, Agano la Kale ni maandalizi ya Injili, Injlili zile ni udhihirisho wa Injili; Matendo
ya Mitume ni upanuzi wa Injlili; Nyaraka ni maelezo ya Injili; na Ufunuo ni utimilifu wa Injili.
3. Biblia ni simulizi ya uhusiano na mwanadamu, tangu uumbaji hadi uumbaji mpya. Wanenaji
mbalimbali wameielezea simulizi kwa njia nyingine zinazotofautiana kidogo:
a. “Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na
mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi, hadi
kuutwaa mwili, kusulubiwa, ufufuo na kupaa; na mwafaka ni hukumu ya mwisho, mbingu na
jehanamu” (Sykes 1997: 14).
b. “Theolojia ya Ki-Biblia ni Mungu kuuleta ufalme wake ambamo mahusiano yote yanakuwa
yamerejeshwa kwenye ukamilifu” (Goldsworthy 1991: 76).
c. “Watu wa Mungu, katika nafasi ya Mungu, chini ya utawala wa Mungu, wakiishi kwa njia ya
ki-Mungu, katika uwepo mtakatifu na wa upendo wa Mungu, kama familia” (Cole 2006: n.p.).
B. Dhana za Theolojia ya Ki-Bibia
TK yaweza kukabiliwa kwa njia mbali mbali. Mtu moja aweza kuikabili TK kwa kujaribu kuelezea
mpangilio mzima wa mtiririko wa mkondo wa simulizi ya Biblia kiutaratibu kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Ndani ya mtiririko wa mkondo wa simulizi hiyo, dhana na miktadha muhimu hujitokeza mara kwa mara kila
mahali katika Biblia, ambayo husaidia kukazia na “kuimarisha upya” mkondo wa simulizi nzima ya Biblia.
mwishowe, dhana hizi, na Biblia yenyewe, huhusishwa, na huweza kutimilizwa, katika Yesu Kristo (ona Luka
24:25-27; Yoh 5:39, 46). Baadhi ya dhana muhimu zaidi na miktadha ni:
1. Ahadi na Kutimizwa. Mungu ni mwaminifu kutimiza ahadi zake. Lakini mara zote ahadi zake
hutimizwa kwa njia za kushangaza. Utimilifu wa mwisho wa ahadi za Mungu hupatikana katika Yesu
Kristo. Kama asemavyo Paulo katika Waef 1:9-10, “Akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa
na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo. Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu
atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia, naam, katika yeye
huyo.”
2. Agano la Mungu. Mungu alifanya Maagano kadhaa (mapatano maalum) kipindi chote cha historia ya
Biblia. Maagano makuu ni: Agano la Nuhu (Mwa 8:20-9:17); Agano la Ibrahimu (Mwa 12:1-3; 13:14-
17; 15:1-21; 17:1-21; na 22:15-18); Agano la Musa (Kutoka 19-24), pia hujulikana kama Agano la
Kale (2 Wakor 3:14; Waeb 8:6, 13); Agano la Daudi (2 Sam 7:8-17; Zab 89:1-4); na Agano Jipya
(Yer 31:31-34; 32:40; Ezek 36:22-28; 37:15-28; Luka 22:20; 1 Wakor 11:25; 2 Wakor 3:6; Waeb
8:6-13; 10:15-17). Kwa namna nyingi, mpango mzima wa Mungu wa ukombozi waweza kuonekana
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
6
kama ni kutenda kazi kwa Agano la Ibrahimu. Kama simulizi ya ukombozi inavyoendelea, Maagano ya
Ibrahimu, Musa, na Daudi, yote hupata utimilifu wake katika Agano Jipya, na Agano hilo hupata
utimilifu wake katika Kristo na watu wake, na kanisa.
3. Aina husika-Aina-Kinyume; Kivuli-Kitu halisi. Kadiri mpango wa Mungu ulivyoendelea na wakati,
kwanza alimwita Ibrahimu, kisha Isaka, kisha Yakobo, ambaye kupitia yeye alianzisha taifa la Israeli,
kuwa chombo ambacho kwacho mpango wake ulifanyika uhalisi. Hata hivyo katika mtazamo wa
kitheolojia na wa kiroho, mifano yote ya Agano la Kale au taasisi zake—kama vile Madhabahu na Hema,
mifumo ya utoaji dhabihu. Sikukuu, Sheria, na Nchi ya Ahadi. Ufalme, Sayuni, Yerusalemu, na Israeli
yenyewe—viliwakilisha “vielelezo” au “vivuli” vya kuonekana au vya kidunia, ambavyo vilielekeza
kwenye Agano Jipya, na uhalisi wa kiroho wa siku za mbeleni (Wagal 4:21-31; Wakol 2:16-17; Waeb
8:5; 9:15-10:22; 12:18-24). Uhalisi wa kweli ambao aina na vivuli vya Agano la Kale (AK) vilielekeza,
viko katika Kristo, kanisa, mbingu, Yerusalemu mpya, na mbingu mpya na nchi mpya.
4. Mkondo wa Mungu wa Uhusiano: Mungu huanzisha na hutenda kwa neema yake, watu wake
wanatakiwa kuonyesha mwitikio kwa imani.
a. Mungu siku zote ametafuta watu kwa ajili yake. Hivyo, kauli inayojirudia mara zote katika
Biblia nzima (ikitumia maneno tofauti) ni, “Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu
wangu” (ona Mwa 17:8; Kut 6:7; 29:45; Wal 26:12; Yer 7:23; 11:4; 24:7; 30:22; 31:1, 33;
32:38; Ezek 11:19-20; 14:10-11; 36:28; 37:23, 27; Hos 2:23; Zek 8:8; 13:9; 2 Wakor 6:16;
Waeb 8:10; Ufu 21:3).
b. Mkondo unaojirudia mara kwa mara katika Biblia nzima kwa ajili ya watu kuwa na uhusiano
mzuri na Mungu ni kwamba, Mungu huanzisha, na watu wake huonyesha mwitikio kwa imani
(ambayo kimsingi humaanisha “kutumaini na kutii kutoka moyoni”).
(1) Mungu hutenda kwa neema kwa watu; hata katika kuhukumu na kuwaadhibu makosa
huonyesha neema yake. Mungu alianza mchakato kwa kumuumba Adamu na Hawa na
alizungumza nao katika bustani ya Edeni (Mwa 2:7, 15-25; 3:8). Baada ya Adamu na
Hawa kuanguka dhambini, kwa neema Mungu alianzisha mpango wa ukombozi kwa
kuahidi mwokozi (Mwa 3:15) na kutoa sadaka ya wanyama ili kuwavika mavazi (Mwa
3:21). Kwa neema, Mungu alimchagua Nuhu na familia yake waokolewe wakati
alipoiangamiza dunia yote kwa Gharika Kuu, na Nuhu aliitikia kwa imani (Mwa 6:5-
22). Mungu akamchagua Ibrahimu, aliyeitikia kwa imani (Mwa 12:1-5; 15:5-6). Kwa
neema yake, Mungu alituma manabii wake kuwaonya Israeli juu ya maafa ya dhambi
zake na kuwaita warudi kwenye uaminifu tena. Mwishowe, kwa neema yake, Mungu
mwenyewe akafanyika mwili katika mwanadamu aitwaye Yesu Kristokuwaokoa watu
wake na dhambi zao na kurejeza mahusiano mazuri kati ya Mungu na wanadamu.
(2) Kwa vile wanadamu kiasili ni wadhambi, hawawezi “kustahili” au “kufanyia kazi”
mbinu iwawezeshayo kuwa na mahusiano mazuri na Mungu (Mdo 13:39; Wagal 2:16;
3:11; Waef 2:1-3, 12). Njia pekee ya watu kuwa na mahusiano mazuri na Mungu ni tu
kama wataitikia kwa imani kile Mungu, kwa neema yake, alichokifanya kwa ajili yao.
Kwa sababu hiyo, muktadha wa imani na uaminifu kwa Mungu—“mwenye haki ataishi
kwa imani”—hujirudia kila mahali katika Biblia (Hab 2:4; War 1:17; Wagal 3:11;
Waeb 10:38; ona pia Yoh 6:27-29; 20:26-29; 1 Yoh 3:23). Bahati mbaya, mkondo
umekuwa mara nyingi watu wengi hawaweki imani zao kwa Mungu, ingawaje daima
wamekuwako “mabaki wachache waaminifu” ambao wamefanya hivyo (1 Waf 19:11-
18; Rum 11:1-5; ona pia Luka 18:8).
MSINGI WA SIMULIZI YA MKONDO WA BIBLIA
I. Uumbaji (Mwanzo 1-2)
“Uumbaji si swala tu la vyanzo, bali la kusudi na mahusiano” (Goldsworthy 1991: 92). Katika uumbaji,
twamwona Mungu kama chanzo cha kila kitu. Zaidi ya hapo, kama kila kitu kilivyoumbwa mwanzoni, twaona
“kila kitu kuwa chema” (Mwa 1:31)—m.y., Mungu, mwanadamu, wanyama, mimea, na maumbile mengine yote
kutimiza makusudi ya kuumbwa kwao katika mahusiano mazuri kila kimoja kwa kingine. “Wasomi wamegundua
kwamba Sura za mwanzo za kitabu cha Mwanzo . . . zimeandaliwa ili kujibu swali la kwa nini mambo yako jinsi
yalivyo. Seti moja ya maswali ambayo sura za mwanzo za kitabu cha Mwanzo ni, ‘Kwa nini wanadamu wako
jinsi hii? Kwa nini wanadamu hutafuta maarifa zaidi? Kwa nini wanadamu hutafuta utawala mkubwa zaidi juu ya
dunia? Kwa nini daima hujaribu kuvumbua vitu vipya, kutafuta matumizi mapya ya rasilimali za “asili”? Kwa
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
7
nini wanadamu hupaka rangi, huchonga sanamu, huchora picha, hujenga majengo, hutunga nyimbo na mashairi?
Kwa nini wanadamu mara kwa mara na kwa namna tofauti hujihusisha na utamaduni wa kisanii, sayansi, na
teknolojia?’ Jawabu la Mwanzo 1 ni kwamba Mungu alimfanya mwanadamu awe hivyo. Mwanadamu ni mfano
wa Mungu. Mungu ni Muumbaji na ni Mfalme. Kama mfano wake, mwanadamu hubuni na kutawala.” (Leithart
n.d.: n.p.)
A. Simulizi ya mkondo wa Biblia huanzia na Mungu (Mwa 1:1).
1. Mungu pekee ni wa milele na anaishi kwa kujitegemea. Mungu si sehemu ya ulimwengu wala si
kinyume chake pia. Kila kitu kilichopo kumwacha Mungu (vitu; malaika; wanadamu, nk) viliumbwa na
Mungu, na humtegemea Mungu kwa kuwepo kwao (Mdo 17:28; Wakol 1:17; Waeb 1:3). Ukweli huu
huonyesha kwamba Mungu wa kweli, wa Ki-Biblia hafanani na “miungu” ya dini nyingine. Mungu si
kama wazo la Mashariki (n.k., Wahindu; Wabudha) kwamba Mungu na maumbile yote ni kitu “kimoja”
(m.y; muktadha wa muunganiko katika kimoja). Mungu pia si wa dini za kiutamaduni (zikiwamo zile za
Mashariki ya Karibu ya kale wakati Biblia ilipoandikwa), ambazo huamini kwamba vitu vilivyokufa vina
“roho”, na wanadamu wa kwanza walikuwa kwa sehemu moja ni wanadamu na sehemu nyingine
miungu.
2. Mungu peke yake anajitosheleza. Yuko Mungu moja tu, lakini ni mwenye hali isiyoelezeka kabisa,
tofauti na kila kitu kingine. Kwa hiyo, ingawaje yuko Mungu moja tu, anaishi katika nafsi tatu (Utatu):
Baba; Mwana; na Roho Mtakatifu. Hili ni muhimu. Kama Mungu angekuwa ni wa nafsi moja (kama
dhana ya Allah wa Ki-Islam), na si Mungu wa Utatu, Mungu asingekuwa anajitosheleza: m.y., angekuwa
anawajibika aviumbe viumbe vingine ili awe na uhusiano navyo. Hata hivyo, Mungu hakuhitaji aumbe
chochote (ona Mdo 17:24-26)—tayari alishaumba ulimwengu, alishakuwa na upendo kamili wa
kiuhusiano kati ya zile nafsi tatu za Utatu kabla hajaumba ulimwengu. Kwa hiyo, Biblia (tofauti na
Qur’an) hutueleza kwamba “Mungu ni upendo” (1 Yoh 4:8).
B. Mungu aliumba kila kitu bila kutumia chochote.
1. Ulimwengu haukuwa na kitu kilichokuweko kabla ambacho kwacho Mungu aliumbia nyota au mimea
au wanyama. Badala yake, Mungu alifanya tu kutamka au kutangaza, na ulimwengu ukatokea pasipo
kutumia chochote (Mwa 1:1, 3, 6-7, 9, 11, 14-16, 20-21, 24, 26-27). Sehemu nyingine, kote katika AK
na AJ, Biblia inakazia kitu hicho hicho (ona Kut 20:11; 31:17; Zab 8:3-5; 33:6; Math 19:4; Yoh 1:3;
Mdo 14:15; Rum 11:36; 1 Wakor 8:6; Wakol 1:16; Waeb 11:3; Ufu 4:11).1
2. Mwanadamu alikuwa ni tukio la kilele katika uumbaji wa Mungu. Ni wanadamu pekee wanasemekana
kuwa wameumbwa “kwa mfano wa Mungu” (Mwa 1:26-27); Mungu akambariki mwanaume na
mwanamke (Mwa 1:28); na Mungu akawaambia atakuwa na ushirika nao (Mwa 1:28-30; 2:16-17, 19;
3:8-9). Zaidi ya hapo, wakati kila siku baada ya kuumba vitu visivyo hai, mimea, au wanyama, Mungu
aliuita uumbaji wake kuwa “mzuri (njema)” (Mwa 1:4, 10, 12, 18, 21, 25), baada ya kuumba
wanadamu, Mungu akaona kwamba uumbaji ule ni “mwema sana” (Mwa 1:31).
3. Tukio la uumbaji la Mwa 2:4-25 ni sambamba au nyongeza ya tukio la kiuumbaji lililoko katika Mwa
1:1-2:3. Tukio la Mwa 2:4-25 hurudi nyuma na kujazia undani wa yaliopo katika Mwa 1:26-27
kuhusiana na jinsi Mungu alivyoumba wanadamu. Wote wawili mwanaume na mwanamke walikuwa
sehemu ya mpango wa Mungu tangu mwanzo (ona Mwa 1:27), ingawaje Mungu alimuumba Adamu
kwanza na kisha Hawa baadaye ili awe msaidizi na mwenzi wake (ona Mwa 2:18-25). Hii inaonyesha
kwamba tabia na majukumu ya mwanaume na mwanamke kwa kiwango fulani ni nyongeza, siyo ya
kubadilishana kabisa (ona 1 Wakor 11:3-15; Waef 5:28-32; 1 Tim 2:11-13), ingawaje ni kwa kiwango
gani yanaweza kuwa hivyo bado yanajadiliwa.
4. Wote wawili mwanaume na mwanamke wana mfano wa Mungu. Maana ya msingi ya “mtu”
(Kiebrania, adam) ni neno la kiujumla “mwanadamu, watu,” ambalo hujumlisha wote wanaume na
wanawake. Hilo linawekwa bayana katika Mwa 1:26, panaposema, “Na tumfanye mtu kwa mfano wetu .
. . wakatawale.” Mwa 1:27 likieleza wazi kwamba wote wawili mwanaume na mwanamke wanahusika
kiusawa, kwani panasema, “Mungu akaumba mtu [Adamu] kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu
alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” Zaidi, katika Mwa 1:28 Mungu akawabariki
“hao” (mwanamume na mwanamke) kiusawa na Mungu alisema “nao”. Katika Mwa 1:29, wakati
Mungu anasema “Nimewapa kila mche utoao mbegu,” hiyo “wa” ni uwingi, siyo umoja.
1 Kama zile siku sita za uumbaji zitajwazo katika Mwanzo 1 ni za kweli au za kitaswira ni swala la kujadika. Ona David G. Hagopian,
ed., David G. Hagopian, ed., The Genesis Debate: Three Views on the Days of Creation (Mission Viejo, CA: Crux, 2001).
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
8
C. Mungu alimuumba mwanadamu ili atawale viumbe vingine vyote (Mwa 1:26-28).
1. Adamu na Hawa wakiishi mbele za Mungu katika bustani ya Eden hutupatia mkondo wa ufalme wa
Mungu. “Mkondo wa ufalme wa Mungu ni huu: Mungu huanzisha uumbaji ulio kamili ambao
anaupenda na ambao yeye hutawala. Heshima kuu kabisa inatolewa kwa mwanadamu kama sehemu
pekee ya uumbaji uliofanywa kwa mfano wa Mungu. Ufalme unamaanisha kwamba kila kitu kilichomo
katika uumbaji kishirikiane vizuri, hiyo maana yake, kama Mungu alivyokusudia kiwe, kwa kingine
chochote na kwa Mungu mwenyewe.” (Goldsworthy 1991: 99)
2. Adamu na Hawa waliagizwa “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha dunia” (Mwa 1:26-
28). Kwa vile wanadamu wameumbwa kiajabu “kwa mfano wa Mungu,” kwa kuenea duniani wakitii
maagizo ya Mungu, watu wangekuwa wanaukuza utukufu wa Mungu, kwa kueneza sura yake, juu ya
dunia yote. Hali hiyo ya “dhana ya wajibu wa kutawala” huendelea kuonyesha kwamba walitakiwa
kupanua mipaka ya kijiografia ya Edeni hadi ienee dunia nzima. Kwa kupanua Edeni hadi kuenea dunia
nzima, Adamu na Hawa na vizazi vyao wangekuwa wanaigeuza dunia kuwa kioo cha mbinguni: m.y;
kuifanya dunia nzima kuwa paradiso imfaayo Mungu na mwanadamu, iliyojaa watu watakatifu.
3. Ni kwa kutegemea Neno la Mungu peke yake kwamwezesha mwanadamu kutimiliza ile dhana ya
wajibu wa kutawala sawa-sawa. “Pale Adamu alipowapa majina wanyama, alianza mchakato wa
uchunguzi, kupanga makundi, na maelezo toshelevu, ambayo ndiyo moyo wa uchunguzi wa maarifa ya
kisayansi. Lakini hangeweza kamwe kufanikisha uhusiano wake mwenyewe kwa Mungu au hata kwa
ulimwengu kwa kutegemea uchunguzi peke yake. Badala yake, lilikuwa ni Neno la Mungu lililokuja kwa
Adamu kumwambia jinsi ya kuhusiana na Mungu na kwa ulimwengu. Ni Neno la Mungu linalomjulisha
mwanadamu kwamba awe mwanasayansi na mwenye kuutunza kiupendo ulimwengu, badala ya kufanya
uchawi na kuwa mtu mharibifu asukumwaye na kutaka madaraka katika dunia.” (Goldsworthy 1991: 99)
II. Anguko la Mwanadamu Katika Dhambi na Matokeo Yake (Mwanzo 3-11:26)
A. Ukuu wa Mungu, wajibu wa mwanadamu, na kuwepo kwa dhambi
1. Mungu ni mkuu juu ya kila kitu, naye yuko kazini kukamilisha mpango wake (ona 1 Nyak 29:11-12;
Ayub 12:13-25; Isa 40:21-26; Mdo 4:27-28; Rum 9:14-24; Ufu 17:14-17). “Hakuna kitu chochote
‘cha asilia’ kuhusu dunia katika Theolojia ya Ki-Biblia. Hii haimaanishi kupendekeza kuwa Mungu
huitawala dunia kimaficho, bali anajihusisha kikamilifu na utendaji na matukio ya dunia.” (Walton 2009:
8) Kwa hiyo, Biblia humwona Mungu kama mtendaji na anayejihusisha na vipengele vyote vya maisha
ya duniani. Kwa mfano, Huumba milima, huumba upepo, na hufanya asubuhi kuwa usiku (Amosi 4:13);
Hufanya upepo uvume na kufanya maji yatiririke (Zab 147:18); Hutawala jua, mwezina nyota, na
aichafua bahari (Yer 31:35); Hutawala ukuaji wa mimea (Isa 41:19-20); Hutawala wanyama (Ayub 39).
Mungu pia ni mkuu na hutawala pia maswala ya wanadamu. Kwa mfano, Husimamia uhai na mausi,
kukiwamo pia matatizo ya kiuzazi, magonjwa, na mauti, vikiwamo vifo vya “wasio na hatia” (Mwa
20:17-18; Kut 4:11; 2 Sam 12:15; Neh 9:6; Ayub 12:9-10; Isa 44:24; Ezek 24:15-18); Huwainua
watu juu na kuwashusha wengine chini (1 Sam 2:7); Hutawala mataifa (2 Nyak 20:6; Zab33:10-11; Isa
40:23-25); Huamsha roho za watu, huingiza mawazo ndani yao, na kugeuza mioyo yao (Ezra 6:22; Neh
2:12; 7:5; Zab 105:25; Hag 1:14).
Wakati huo huo, Mungu huheshimu unyofu wao kama wanadamu; hawatawali wato kama vile ni
vikaragosi au kuwapangilia mambo kama vile roboti zinavyoongozwa kwa programu. Watu wana uwezo
wa kufikiri mawazo yao wenyewe na kufanya maamuzi yao. Kwa hiyo, Biblia kwa kurudia–rudia imetoa
maelezo ya pande tofauti za matukio: Mungu ni mkuu na ameanzisha matukio yote (hilo, kwa upande
moja, ni maelezo kamili kwa matukio yote); hata hivyo, hilo linaendana na, na kinamna yoyote
haliondoshi, wajibu wa watu kwa maamuzi wanayoyafanya na mambo wanayoyafanya (hilo, kwa upande
mwingine, ni maelezo kamili kwa matukio yote). Kinamna fulani, Mungu hufanya kazi ndani ya, na
kupitia viumbe vyake (wote, wanadamu na roho) kukamilisha mpango wake. Terrence Fretheim anaeleza
hivi: “Uhusiano wa Mungu na dunia ni wa uwanda mkamilifu: Mungu yupo na hutenda popote ilipo
dunia. Mungu haiumbi duniana kisha kuiacha, bali Mungu huiumba dunia na kisha huingia ndani yake,
huishi ndani yake, kama Mungu. . . . Mungu yuko katika kila tukio na mtendaji katika kila tukio. Kuanzia
ulimwengu wa juu hadi ulimwengu wa chini, hakuna kukwepa uwepo wa Mungu. Mungu hawezi
akaamshwa kutoka duniani au kutokana na maisha ya kiumbe. Wakati huo huo, uwepo wa Mungu
haumaanishi ama mwingilio wa kiungu wa kiutawala wala mapenzi ya kiungu yasiyozuilika. . . . Dunia
hudumisha unyofu wake kama kiumbe hata wakati imejawa na uwepo wa Muumba . . . . Mungu—aliye
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
9
tofauti na dunia—hutenda kimahusiano kutokea ndani ya dunia, na si juu ya dunia kana kwamba kutokea
nje. . . . Hiyo maana yake, wote wawili, Mungu na viumbe wana uhusiano muhimu katika mradi wa
kiumbaji, na maeneo ya kiutendaji yanaingiliana kwa maana ya kazi na matokeo. . . . Bali, zaidi kabisa,
Mungu huwapa wanadamu nguvu na wajibu katika namna ambayo humwajibisha Mungu kwa aina fulani
cha uhusiano nao. Uwajibikaji huu huhitaji usimamizi na udhibiti wa ki-ungu katika kuwepo kwa
mamlaka ndani ya uumbaji. Kwa mfano, Mungu hatafanya hatua za kutungisha kuumbika wanyama au
kuzalika kwa mbegu za matunda kwa njia isiyohusisha kuunganika.. La kukutisha zaidi wanadamu
wamepewa uhuru wa kuangamizana wenyewe, ingawaje hili linasimama kinyume na mapenzi ya Mungu
kwao. Huku kujidhatiti kutoa mamlaka ya wajibu kwa kiumbe husababisha kuendelea kutegemea
uongozi wa ki-ungu kwa viumbe ambavyo kwa kupitia hivyo, Mungu atatenda kazi kwa uhai wa dunia.”
(Fretheim 2005: 23-24, 26, 27)
Maoni mengine mawili ya kufanyika kuhusu kutegemeana huku kwa mahusiano ya Uungu-
uanadamu: (1) “Haya ni mahusiano ya wasiolingana; Ni uhusiano usiowiana. Mungu ni Mungu, na sisi
hatuko vile.” (Ibid.: 16) na (2) Ni ukweli unaokinzana unaoelezea tafsiri au uelewa kamilifu. Hata hivyo,
kuwepo kwa Mungu mwenye enzi yote, mwenye maarifa yote, aliyeko kote, aliye na mpango kwa dunia,
aliye mkuu, na anautimiliza mpango wake, na amewapa viumbe walio na uwezo wa kufanya maamuzi
halisi na kutenda mambo kihalisia ambayo wanawajibika nayo, uhusiano kati ya Mungu na viumbe Wake
kama ulivyoelezwa hapo juu usingeweza kuwa vinginevyo.
2. Ukuu wa Mungu juu ya kila tukio unahusisha ukuu juu ya dhambi na uovu, lakini si kwa namna
ambayo inamfanya Yeye kuwa mdhambi au mwovu. Ingawaje watu wengi wanajaribu kumwekea kinga
Mungu mbali na kila dhambi (huyahusisha maovu yote ama na Shetani au kwa dhambi binafsi), Biblia
inaonyesha picha iliyo na vidokezo na utata zaidi. D. A. Carson anaonyesha kwamba waandishi wa
Biblia “hawamwonei aibu kumhusisha Yahwe mwenyewe kwa njia ya siri (usiri ambao humlinda
kutohusishwa na uovu) chanzo ‘kikuu’ cha maovu mengi. . . . Mungu hasimami nyuma ya tendo ovu
kwa namna thabiti kama asimamiavyo matendo mema. Waandishi wa [Ki-Biblia] huelewa Mungu uwa
mtakatifu, asiye na upendeleo, mwenye haki, mema, mvumilivu (Mwa. 18.25; Law. 11.44; Isa. 6.3;
61.8; Zefania. 3.5; Zab. 5.4; 11.5; 145.17; Ayub 34.10-15; nk.). Kila kitu Mungu alichokifanya kilikuwa
‘chema sana ’ (Mwa 1.31). Umbali fulani huwekwa kati ya Mungu na watu pale wanapofanya dhambi.”
(Carson 1994: 28) Ingawaje Mungu, kwa njia fulani, husimama nyuma ya dhambi na uovu, wakati huo
huo vilevile “husimama kinyume nayo, kiasi kwamba neno hufanyika kondoo wa Mungu aichukuaye
dhambi ya dunia, na ghadhabu ya Mungu hudhihirika juu yake ([Yohana] 1.29; 3.36)” (Ibid.: 160-61).
“Kwa kifupi, ingawaje tunaweza kupungukiwa makundi ya maelezo kamili ya matatizo, hata hivyo ni
lazima tusisitize kwamba nguvu ya Uungu inasimama nyuma ya mema na mabaya mtindo moja.” (Ibid.:
36-37) Hilo linamaanisha kwamba, kwa mtazamo huo huo,kimsingi Mungu ndiye anayewajibika kwa
maovu kwa maana kwamba Yeye ndiye mkuu juu ya kila kitu, atangazaye “mwisho tangu mwanzo” (Isa
46:10), na ameanzisha mpango mpango kamili wa uumbaji wote , ukiwamo uovu, ambao anautimimiliza
(Mith 16:4; Isa 46:8-11). Hata hivyo Mungu, hahusiki na uovu kwa namna ambayo anakuwa chanzo
cha uovu wa uharibifu ule (ona Mwa 4:1-7; Isa 10:5-16; Hab 1:1-11; Mdo 2:22-24). Uhusikaji wa
Mungu “wa pande mbili ” nyuma ya mema na maovu humaanisha kuwa “Mungu husimama nyuma ya
uovu kwa jinsi ambayo uovu ule hautatokea nje ya mipaka ya ukuu wake, na kuwa uovu ule usihusishwe
kimaadili kwake: uwe daima unawajibishwa kwa vitendea kazi vingine, vyanzo vingine. Kwa upande
mwingine,Mungu husimamia mema kwa namna ambayo siyo tu hutendeka ndani ya mipaka ya ukuu
wake, bali daima huhusishwa kwake na daima hutendwa na vitendea kazi vingine.” (Carson 1990: 213)
Mfano wa hili huonekana katika Yakobo 1. Yak 1:2, 12 palizungumzia kuhusu watu
waliokabiliwa na “majaribu” mbali mbali.” Yak 1:13-14 ndipo pakasema, “Mtu ajaribiwapo, asiseme
Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu
mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.” Neno
“jaribu” na “shawishi” ni vitambulishi, m.y, jina na kitenzi cha neno lilelile la mzizi moja katika
Kiyunani la neno (peirasmos [jaribu] na peirazō [shawishi]). Muktadha huonyesha utofauti wake :
Mungu hutuweka sisi katika mazingira ya kutupima kutujaribu—ikiwa ni pamoja na mazingira ambayo
anajua tunaweza, kusema ukweli, kutenda dhambi—hata hivyo hatushawishi tutende dhambi. Mungu
huruhusu na kuanzisha dhambi, si kwa sababu za uovu au udhambi wa dhambi yenyewe, bali sababu ya
miisho na makusudi yaliyo “ya hekima, matakatifu, na yaliyo bora zaidi” (Edwards 1984, Freedom, §IX:
76; ona pia Piper 2000: 107-31). Kwa mazingira haya, Randy Alcorn anasema kwamba Mungu
“alikusudia kuanzia mwanzo kuruhusu uovu, kisha kugeuza uovu juu ya kichwa chake, kuchukua
malaika na watu waovu waliokusudiwa kwa ajili ya uovu na kuutumia kwa ajili ya uzuri. . . .
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
10
Inawezekana kujipanga kwa ajili ya jambo ujualo kuwa linakuja pasipo kulilazimisha litokee. Mungu
hakumlazimisha Adamu na Hawa kutenda uovu, bali aliwaumba wakiwa na uamuzi, na aliruhusu uwepo
wa Shetani katika ile bustani, akijua kabisa watachagua uovu na akijua atakachokifanya katika mpango
wake wa okombozi kitaleta matokeo mazuri zaidi.” (Alcorn 2009: 226-27) Hakika, watu wanaweza kuwa
na msukumo moja kwa watakalolifanya (k.m., kutenda uovu), bali Mungu anaweza kuwa na msukumo
mwingine kwa kuanzisha tukio lilelile (k.m., ili kuletesha uzuri). Mungu anao uwezo wa kufanya kazi
ndani na kupitia viumbe vyake, pasipo kuvilazimisha kutenda nje ya mapenzi yao au shauku zao (hata
wakati kusudio lake au nia yake ni tofauti na wa kwao) na pasipo Yeye mwenyewe kutenda dhambi
(hata wakati viumbe vyake vinatenda, kusema ukweli, dhambi) (ona Mith 16:2). Kuuzwa kwa Yusufu
kwenda Misri (Mwa 45:4-8; 50:20; Zab 105:17), kuvamiwa kwa Israeli na Ashuru (2 Waf 19:20-31;
Isa 10:5-16), kuangamizwa kwa Yuda na Babeli (Ezek 11:5-12; Hab 1:5-11), kusalitiwa kwa Yesu na
Yuda (Math 26:20-24; Yoh 6:64), hila ya Kayafa, kuhani wakuu, na Mafarisayo kumuua Yesu (Yoh
11:47-53), na kusulubiwa kwa Yesu na Herodi, Pilato, Wamataifa, na watu wa Israeli (Isa 53:3-10; Mdo
2:22-23; 4:27-28), ni mifano ya hili.
Hii ni siri ambayo sisi hatuwezi kuieleweka kikamilifu, kwa sababu uhusiano wa Mungu
muumba—asiye na mwisho, mwenye kujua yote, mwenye uweza wote—na viumbe vyenye mwisho si wa
kawaida (m.y., hakuna tena kama hivyo) na si sawa na uhusiano ulivyo kati ya kiumbe na kiumbe
mwingine. (Talbot 2005: audio message)2 Zaidi ya hayo, Mungu anajua kiundani kabisa hatima ya
yote—kuchanganya na mwisho, na madhara ya moja kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja ya muda
mfupi, na ya muda mrefu ya kila neno, tendo, na matukio mengine. Kila kitu ni sehemu ya mpango
mzima wa Mungu. Kwa hiyo Yeye kipekee kabisa ana sifa kujua lini kuanzisha na kuruhusu uovu na
mateso na lini kutofanya hivyo. Matokeo yake, Yeye peke yake ndiye anayefaa kuruhusu uovu na mateso
ambayo mtu aliye mwema (asiye na ufahamu mpana wa Mungu) atajaribu kuuzuia.
Huenda siri kuu kuliko zote ihusuyo uovu na mateso, hata hivyo, ni kuwa Mungu alichagua kuja
duniani na kibinafsi kukumbana na uovu na mateso ndani ya mwanadamu Yesu Kristo. Ingawaje Yesu
mwenyewe alikuwa mwema na hakutenda dhambi, aliamua kuichukua dhambi na hatia, na kulipa
gharama ya kudumu kwa ajili ya dhambi na hatia,yaw engine. “Katika upendo wake kwetu, Mungu
alijihukumu mwenyewe mauti kwa niaba yetu. Kitu kimoja tusichopaswa kamwe kusema kuhusu
Mungu—ni kusema haelewi jinsi ilivyo kuhusu kukataliwa vibaya, mateso mazito, na kufa kwa aibu. . . .
Watu wengine hawaamini Mungu angeliumba dunia ambamo ndani yake watu wangeliteseka kiasi hiki.
Je haishangazi zaidi kwamba Mungu angeliumba dunia ambayo hakuna mtu yeyote aliyeteseka zaidi
kuliko yeye mwenyewe?” (Alcorn 2009: 214-15)3
3. Ifuatayo ni mifano mingine ya Ki-Biblia inayoonyesha jinsi wote wawili, Mungu na visababisho
vingine vinavyohusika katika uwanja moja, yakiwamo matukio yanayohusiana na dhambi na uovu:
TUKIO LILILOFANYWA NA
MUNGU
LILILOFANYWA NA
VITENDEA KAZI VINGINE
Uumbaji wa wanyama
Sara kupata mimba & kuzaliwa kwa Isaka
Kufanikiwa kwa Yusufu akiwa mtumwa
Mwa 1:25
Mwa 21:1
Mwa 39:3, 23
Mwa 1:24
Mwa 21:2, 5
Mwa 39:3, 23
2 Kifalsafa, neno linaloelezea uhusiano wa Mungu-mwanadamu ni “kuchukuliana”: Mungu kiuhakika ni mwenye enzi yote,
bali uenzi wake hautendi kazi kwa jinsi ambayo majukumu ya kianadamu yanapotezwa au kuondoshwa (m.y., wanadamu
hawageuzwi kuwa maroboti, au vinyago); vivyo hivyo, wanadamu ni viumbe vyenye kuwajibika kimaadili wawezao
kufanya maamuzi na matendo halisi, yakiwamo kuasi kinyume na mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa, nao wanawajibishwa
kisahihi kutokana na maamuzi na matendo hayo, lakini haya hayafanyiki kumfanya Mungu ni wa udharura kivile. Kwa
maneno mengine, Mungu anao uwezo wa kujua kabla kwa uhakika kabisa; wanadamu, wao hutenda kile wakitakacho na
wakichaguacho (m.y., Mungu hawalazimishi kufanya kinyume na matamanio yao na kutaka kwao), ila hawana uwezo kamili
wa kutenda kinyume na mpango wa Mungu uliopangwa kabla . (Ona Carson 1994: 163-67, 201-22; Carson 1990: 199-227;
Feinberg 2001: 625-796; Alcorn 2009: 258-69) 3 Kusulubiwa kwa Kristo pia huonyesha kiukamilifu kwamba mfungamano lazima uwe kweli ikiwa Mungu ni yote mawili
mwenye enzi yote na ni mwema na watu wanao wajibu ki- haki kwa matendo yao. D. A. Carson anaelezea: “Ikiwa
kisababisho kilikuwa mia kwa mia cha wala njama, na Mungu alikuja tu dakika za mwisho kujitwalia utukufu kutoka
magego ya kushindwa kulikokuwa kunatarajiwa, basi msalaba haukuwa mpango Wake, makusudi yake, sababu hasa kwa
nini Alimtuma Mwanaye duniani —na hayo hayafikiriki. Ikiwa kwa upande mwingine Mungu alikuwa akipangilia sana
mambo kiasi kwamba maajenti wote wa kianadamu walikuwa vikaragosi, basi ni ujinga kuzungumzia mkakati, au hata
dhambi—ambao kwamba hakuna dhambi za Kristo kuziondoa kwa kifo chake, basi kwa nini alipaswa afe? Mungu ki-enzi
alikuwa kazini katika kifo cha Yesu; wanadamu walikuwa waovu katika kumuua Yesu, hata walipokamilisha mapenzi ya
Baba; na Mungu mwenyewe akawa mwema kikamilifu.” (Carson 1990: 212)
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
11
Kurudishiwa fedha kwa ndugu zake Yusufu
Safari ya Israeli kutoka Misri
Ugumu wa moyo wa Farao
Israeli kuingia nchi ya ahadi
Ndama wa dhahabu & Israeli kuabudu sanamu
Utakaso wa Israeli & kuwa wakfu
Kumshinda Sihoni
Kumshinda Bashani
Ushindi wa Yoshua
Uwezo wa watu kupata utajiri
Gideoni kuwashinda Wamidiani
Samsoni kumuoa mwanamke wa Kifilisti
Samsoni kuua Wafilisti 1000
Benjamini kushindwa naIsraeli
Watoto wa Eli kutomsikiliza
Sauli awashinda Waamaleki
Abigaili amwombea Nabali
Ushauri wa Hushai wakubalika
Daudi kuwashinda adui zake
Daudi afanya dhambi kwa kuwahesabu watu
Kifo cha Yoabu
Kugawanyika kwa Israeli na Yuda
Ahabu kwenda vitani & kumshinda Aramu
Ahabu kwenda vitani auawa
Kurudi kwa Rabshakehi kwao na kifo chake
Kifo cha Sauli
Kuvamiwa kwa Yuda na Wafilisti &Waarabu
Kushindwa kwa Yuda & kifo chaAmazia
Maandalizi ya hekalu kwa ibada mpya
Kushindwa kwa Yuda & kifo cha Yosia
Mungu kunena kupitia manabii wake
Kuangamizwa kwa Yuda na Babeli
Kutangazwa Wayahudi waweza kurudi
Yerusalemu na kujenga upya hekalu
Ezra apata kibali
Nehemia apata kibali
Mipango ya adui za Wayahudi kuharibika
Kujengwa upya kuta za Yerusalemu
Majaribu ya Ayubu
Kuumbwa kwa watu
Kushindwa kwa adui za Daudi
Kukua kwa mimea
Kujenga nyumba au tukio lolote
Kulinda mji
Mipango ya watu, maneno, na matendo
Maamuzi ya wanadamu
Kuvamiwa kwa Yuda na Waashuri
Kuangamizwa kwa Israeli
Kuangamizwa kwa Babeli
Kuangamizwa kwa Misri
Kufanikiwa kwa Tiro
Baruki & Yeremia wamkwepa mfalme
Gogi avamia Israeli
Kutupwa kwa Yona baharini
Kujengwa upya hekalu Yerusalemu
Kuandikwa & ushuhuda wa Biblia
Watu kuja kwa Kristo kwa wokovu
Matendo ya haki ya waamini
Wokovu kwa watu wa Korintho
Mwa 42:27-28
Kut 3:7-8
Kut 4:21;7:3; 9:12; 10:1, 20,
27
Kut 23:23, 29-30; Kumb 7:1-2
Kut 32:1-8; Mdo 7:39-41
Law 20:8
Kumb 2:30-31, 33, 36
Kumb 3:2-3
Kumb 3:21-22
Kumb 8:18
Waamuzi 7:7, 9, 14-15
Waamuzi 14:4
Waamuzi 15:18
Waamuzi 20:28
1 Sam 2:25
1 Sam 15:2
1 Sam 25:32
2 Sam 17:14
2 Sam 22:18-20, 40-42, 48-49
2 Sam 24:1
1 Waf 2:32-33
1 Waf 12:22-24
1 Waf 20:13, 28
1 Waf 22:19-23
2 Waf 19:6-7
1 Nyak 10:14
2 Nyak 21:12-16a
2 Nyak 25:14-16
2 Nyak 29:36
2 Nyak 35:20-21
2 Nyak 15-16
2 Nyak 36:15-17; Yer 21:8-10
2 Nyak 36:22; Ezra 1:1; 6:14
Ezra 7:6, 9-10, 27-28
Neh 2:8
Neh 4:15
Neh 6:16
Ayubu 1:12, 21-22; 2:6
Ayubu 10:8; 31:15;
Zab 18:17-19, 43a, 47-48
Zab 104:14a-b
Zab 1271a
Zab 127:1c
Mith 16:1b, 9b
Mith 16:33b
Isa 7:17-20; 8:5-8
Isa 9:8-21
Isa 13:1-5
Isa 19:1, 2a, 4a
Isa 45:1-7
Yer 36:26
Ezek 38:1-6, 16
Yona 2:3
Hag 1:14
Yoh 5:37-39; 2 Tim 3:16
Yoh 6:37, 44, 65; Mdo 13:38
Yoh 3:21; Waef 2:10; Wafil
2:13
Mwa 42:25
Kut 3:10
Kut 7:14, 22-23; 8:15; 9:34
Kut 23:24, 31; Kumb 7:2
Mdo7:42
Law 20:7-8
Kumb 2:32-36
Kumb 3:1, 3-6
Kumb 3:28
Kumb 8:18
Waamuzi 7:16-22
Waamuzi 14:1-3
Waamuzi 15:14-16
Waamuzi 20:29-48
1 Sam 2:22-25
1 sam 15:3-6
1 Sam 25:14-31
2 Sam 17:5-14
2 Sam 22:38-39, 43
2 Sam 24:10, 17; 1 Nyak 21:1-4
1 Waf 2:31, 34
1 Waf 12:16-20
1 Waf 20:14-21, 29-30
1 Kgs 22:29-37
2 Waf 19:7
1 Nyak 10:4
2 Nyak 21:16b-17
2 Nyak 25:17-28
2 Nyak 29:5-35
2Waf 23:29; 2 Nyak 35:22-24
2 Nyak 15-16
2 Nyak 36:17-19; Yer 21:8-10
2 Nyak 36:22-23; Ezra 1:1; 6:14
Ezra 7:6, 9-10, 27-28
Neh 2:7-9
Neh 4:11-14
Neh 3:1-32; 4:6, 21-22; 6:3, 15
Ayubu 1:13-19; 2:7
Mwa4:1; 5:3; Ayu 14:1; Zab 51:5
Zab 18:37
Zab 104:14c
Zab 127:1b
Zab 127:1d
Mith 16:1a, 9a
Mith 16:33a
Isa 7:17-20; 8:5-8
Isa 9:8-21
Isa 13:1-5
Isa 19:2b-3, 4b
Isa 45:1-7
Yer 36:19
Ezek 38:7-16
Yona 1:15
Hag 1:14
Yoh 5:46-47
Yoh 6:37, 44, 65; Mdo 13:38
Yoh 3:21; Waef 2:10; Wafil 2:12
Mdo 18:9-10a
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
12
Kuokoka kwa Sauli & manahodha katika meli
Kuhubiri Injili
Kuteswa kwa Wakristo
“Miiba ya” Paulo katika mwili
Kuhifadhiwa kwa watakatifu
Watu wafuatao “watu waovu”
Watu wapendako kwenda & na yale
wayafanyayo
Matendo ya “kahaba,” “wafalme kumi,” na
“mnyama” wa Ufunuo
Mdo 18:10b
Mdo 27:21-44
1 Wakor 2:4
1 Wakor 4:7-11; Rev 6:9-11
2 Wakor 12:7-9
1 Wathes 5:23-24
2 Wathes 2:11
Yak 4:13-15
Ufu 17:17
Mdo 27:21-44
1 Wakor 2:4
1 Wakor 4:7-11; Ufu 6:9-11
2 Wakor 12:7
1 Wathes 5:12-22
2 Wathes 2:9-10, 12
Yak 4:13-15
Ufu 17:1-16
4. Mtu mwingine anaweza kutazama swala la Mungu kuruhusu dhambi na uovu kutokea kwa mantiki ya
uhusiano wa jua na giza na baridi. “Kuna tofauti kubwa kwa Mungu kuhusiana na hivyo, kwa ruhusa,
yake katika tukio au tendo, ambalo, kwa jinsi lilivyo na sura yake, ni dhambi, (ingawaje tukio hilo bila
shaka litafuatana na ruhusa yake,) na kwa yeye kuhusika katika hilo kwa kulizalisha na kuongoza tendo
la dhambi; au katika ya yeye kuamuru kitu fulani kiwepo, kwa kutokukizuia, katika mazingira fulani, na
kwa yeye kuwa mtendaji au mmiliki astahiliye, kwa kutumika kiuzuri au kiuwezeshwaji. . . . Kama
kulivyo na utofauti mkubwa kati ya jua kuwa chanzo cha ile nuru na ujoto wa anga, na uangavu wa
dhahabu na almasi, kwa uwepo wake na athari njema za kuwepo kwake; na kwa kuhusiana na hiho hilo
kunakuja giza na baridi kali, usiku, kwa mwenendo wake, itokeapo linazama kwenye miisho ya dunia.
Mwenendo wa jua ni sababisho la aina ya matukio yanayofuatia baadaye; lakini silo sababu halisi,
uwezeshwaji, au mzalishaji wa hayo; ingawaje lazima yatokee kutokana na mwenendo wake, katika
mazingira hayo: hakuna tena tendo lolote la Ki-Uungu kuwa ndiyo sababu ya uovu wa mapenzi ya
kianadamu. Kama jua lingekuwa ndiyo chemchemi ya mambo hayo, kama lilivyo chemchem ya nuru na
joto: na kisha kitu chaweza kujadiliwa kutokana na tabia ya ubaridi na giza, kwa kulinganisha na sifa za
jua; na pia inaweza kabisa kukubalika kwamba, jua lenyewe ni giza na baridi, na ya kuwa miali yake ni
myeusi na yenye ukungu. Lakini kwa kufanyika sababu si kwa vinginevyo zaidi ya kutokuwepo kwake,
hakuna kitu kama hicho kiwezacho kuhusishwa, isipokuwa kinyume chake; yawezekana kiusahihi kabisa
ukadai, kwamba jua ni angavu na lenye joto kali, ikiwa baridi na giza ni matokeo ya kutokuwepo kwake;
na kadiri matokeo haya yanavyounganishwa na kuwajibishwa zaidi mara kwa mara na kutokuwepo
kwake, ndivyo inavyotia nguvu zaidi hoja kwamba jua ni chemchemi ya nuru na joto. Kwa hiyo, kama
ambavyo dhambi si tunda litokanalo kwa jinsi yoyote ile na utendaji mwema au uvuvio mzuri wa Aliye
Juu sana, bali, kinyume chake, hutokana na kuzuilia matendo yake na nguvu, na katika mazingira fulani,
hufuatia ulazima wa athari ya utendaji wake; hili si hoja kusema kuwa yeye ni wa dhambi, au utendaji
wake ni wa uovu, au una lolote la asili ya uovu; bali kinyume chake, ni kuwa Yeye, na utendaji wake,
pamoja ni mzuri na wa utakatifu, na kwamba yeye ni chemchemi ya utakatifu wote. Itakuwa ni hoja ya
kustaajabisha, tena sana, kusema wanadamu hawafanyi dhambi, isipokuwa tu pale Mungu anapowaachia
wenyewe, na kulazimika kutenda dhambi afanyapo hivyo, kwamba Mungu lazima awe wa asili ya
dhambi: ndivyo itakavyokuwa hoja ya kustaajabisha, kwani siku zote ni giza jua linapokuwa limezama,
na kamwe hakuwi giza wakati jua likiwapo, hivyo basi, giza lote latokana na jua, na kwamba mduara
wake na miale yake lazima iwe myeusi.” (Edwards 1984, Freedom, §IX: 77)
5. Mungu anaweza kuagiza jambo kwa mapenzi yake ya siri (au “ki-mamlaka”) ambayo mapenzi yake
yaliyofunuliwa (au “mtazamo”) wake unakataza. “Mungu anao uwezo wa kuitazama dunia kwa vioo
viwili. Anaweza kuiangalia kupitia kioo cha upeo mwembamba au kupitia kioo cha upeo mpana. Mungu
atazamapo tukio lenye kuumiza au lililo ovu kupitia kioo cha upeo mwembamba, huona maafa au
dhambi ilivyo yenyewe na huchukizwa na kuhuzunika. ‘Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye,
asema Bwana Mungu’ (Ezek. 18:32). Lakini Mungu anapoliangalia tukio lenye kuumiza au lililo ovu
kwa kupitia kioo chake chenye upeo mpana, huona maafa, au ile dhambi kuhusisha na kila kitu
kilichosababisha na kitakachotokea kutokana nayo. Huona inavyounganika na mpangilio kuelekea
umilele. Mpangilio huo, pamoja na sehemu zake zote (nzuri na mbaya) anazotaka ziwe (Zab 115:3).”
(Piper 2000: 126) Kwa mfano, Ayubu alielewa kwamba mabaya yote yaliyompata kiuhalisia yalikuwa
yamepangwa na kuruhusiwa na Mungu; kwa hiyo alimwelekezea kilio na kumbariki Mungu, ingawaje
aliyesababisha moja kwa moja uovu ule alikuwa ni Shetani (Ayub 1:21-22). Mungu aliwatumia
Waashuri kwa kuwaadhibu Waisraeli kwa dhambi yao, bali baadaye aliwaadhibu Waashuri kwa kiburi
chao (Isa 10:5-19). Matokeo muhimu ya hili ni kuwa hugongana na wazo la falsafa ya majaliwa. Randy
Alcorn states, “Ikiwa Mungu anaruhusu ubaguzi wa rangi, utumwa, na biashara za watoto kwa mambo ya
ngono, basi kwa nini tupambane nayo? Sababu ni hii: Biblia hunena kwa kiwango kikubwa kuhusu uenzi
wa umiliki wa Mungu, lakini bado mara kwa mara huhimiza watu kuchukua hatua, pia kuongelea na
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
13
kuwasaidia masikini na wahitaji (ona, kwa mfano, Mithali 31:8-9)—hii ndiyo kona kinyume katika
falsafa ya majaliwa.” (Alcorn 2009: 263)
6. Uovu wote ambao Mungu anauruhusu na anauagiza hatima yake hutumika au kuleta wema mkubwa
zaidi kwa uumbaji wenyewe. Paulo alisema, “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya
kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake”
(Rum 8:28). “Hakuna mantiki yoyote kufikiria, kwamba anaweza kukichukia kitu kama kilivyo, na
kukiona tu kuwa kiovu, na bado ikawa ni mapenzi yake kitokee, akijua maafa yake yote. . . . Wanadamu
hupenda dhambi kama dhambi, kwa hiyo ndio waanzilishi na watendaji wake: wanaipenda kama
dhambi, na kwa makusudio mabaya na matokeo mabaya. Mungu hakusudii dhambi kama dhambi, au
kwa kusudio la kitu chochote cha ubaya; ingawaje huwa ni furaha yake kuagiza mambo, ambayo, kwa
kuyaruhusu, dhambi itakuja kutendeka, kwa makusudio ya uzuri au wema mkubwa zaidi, ambao kwa
kutimia kwake yatakuwa ndio lengo. Kule kukubali kuachia mambo ili uovu uweze kutendeka, kama
uovu: na kama ndivyo, basi hakuna sababu kwa nini asiweze kiuzuri tu kuuzuia uovu kama uovu, na
kuuadhibu kama ulivyo.” (Edwards 1984, Freedom, §IX: 78-79; ona pia Piper 2000: 107-31; Edwards,
Remarks, ch. 3: 525-43). Kwa mfano, Yusufu aliuzwa utumwani na ndugu zake lakini baadaye
aliwaambia, “nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa
taifa kubwa, kama ilivyo leo” (Mwa 50:20). Huenda mfano mkubwa zaidi kuliko yote ni kusulubiwa
kwa Kristo. Yuda, Herodi, Pilato, na watu wengine wasiomcha Mungu walimsaliti, kumlaani, na
kumsulubisha Kristo asiyekuwa na dhambi, na bado alikuwa ndiye Mungu aliyeagiza tukio hilo lifanyike
kama njia ya kuleta masamaha ya dhambi, mabadiliko ya maisha, na upatanisho wa mwanadamu kwa
Mungu (Mdo 2:22-23; 4:27-28). Kusema ukweli, Mungu huchukua huzuni zetu na kuzigeuza kuwa
kuwa furaha (Zab 30:11; Yer 31:13; Yoh 16:20). Mateso yote ya dunia hii hayawezi kufananishwa na
utukufu mkuu, usio na mwisho ambao Mungu atauleta nyakati za miisho (Rum 8:18-21; 2 Wakor 4:16-
18; Ufu 21:1-4). “Tutakapoishi kwa amani kuu katika Nchi Mpya, ambako furaha itatawala anga la hewa
tutakayoivuta, tutazama nyuma kuangalia dunia hii iliyopo na kuthibitisha si kwa imani, bali kwa kuona
kwamba uovu na mateso yote yalistahili kabisa—na kwamba Kristo kutwaa mwili na ukombozi wake
umeufanya ulimwengu kuwa bora milele” (Alcorn 2009: 195).
7. Kwa vile Mungu ndiye wema mkuu zaidi ya wote uwezekanao kuweko, dhambi na uovu ni vya
lazima ili hali zote za Uungu na tabia za Mungu ziweze kufunuliwa vizuri. Hatimaye, kila kitu
alichokianzisha Mungu—zikiwamo dhambi na uovu—ni sehemu ya mpango mkuu, ulioandaliwa kabla
ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, kudhihirisha utukufu wa Mungu, utukufu wa Kristo, na utukufu wa
neema ya Mungu katika Kristo (ona, k.m., Zab 24:1-10; 148:1-13; Yoh 11:1-4; 13:31-32; 17:1-5, 22-
24; Rum 5:12-21; 8:28-29; 9:19-23; 11:32-36; Waef 1:3-6; Wafil 2:6-11; 2 Tim 1:8-9; Heb 2:9-10;
Ufu 13:8; 15:3). “Ni jambo jema na zuri kabisa kwa utukufu wa Ki-Ungu kung’ara; na kwa sababu hiyo
hiyo, ni vyema kwamba uangavu huo wa utukufu wa Mungu uwe kamili; yaani, sehemu zote za utukufu
wake zing’are, kwamba uzuri wote uwe kimlingano unaangaza, kwamba mhusika awe na sura halisi ya
Mungu. Si vyema kwamba utukufu moja udhihirishwe kupita kiasi, na mwingine usiwepo kabisa; maana
hapo, kule kung’ara hakutaleta uhalisia. Kwa sababu hiyo hiyo si sahihi moja udhihirishwe kupita kiasi,
na mwingine kidogo sana. Ni vyema sana ule uangavu wa Mungu utoe majibu ya unyofu wake wenyewe;
kwamba ile enzi ya kiutukufu iwajibike kwa utukufu halisi na ulio muhimu, kwa sababu hiyo hiyo ni
vyema na bora kabisa kwa Mungu kujitukuza mwenyewe kabisa. Kwa hiyo ni lazima, kwamba ukuu wa
Mungu usioneneka, mamlaka yake na enzi yake ya kutisha, haki yake, na utakatifu, udhihirishwe. . . .
Kama isingelikuwa ni vyema kwamba Mungu aagize na kuruhusu na kuiadhibu dhambi, kusingekuwa na
udhihirisho wa utakatifu wa Mungu katika kuchukia dhambi, au katika kuonyesha lile alipendalo, katika
upaji wake, katika uchaji mbele zake. Kusingekuwa na udhihirisho wowote wa neema ya Mungu au ucha
Mungu wa kweli, kama kusingekuwa na dhambi za kusamehewa, hakuna maafa ya kuokolewa kwayo. . .
. Huwa tunajali kidogo mno kiasi gani hisia ya wema inavyoinuliwa kutumia hisia ya uovu, kwa yote
mawili–kihamasa na kiasili. Na kama ilivyo lazima kuwe na uovu, kwa sababu kuonekana kwa utukufu
wa Mungu kusingelikuwepo na kusingekamilika, kama uovu usingalikuwepo, kwa hiyo uovu ni wa
lazima, ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha furaha ya kiumbe, na kukamilika mawasiliano ya Mungu,
ambayo kwayo aliuumba ulimwengu, kwa sababu furaha ya kiumbe hujumuishwa katika kumjua Mungu,
na hisia ya upendo wake. Na ikiwa kumjua yeye kutakuwa hakujakamilika, furaha ya kiumbe lazima iwe
haina uwiano kimlingano.” (Edwards 1986, Remarks, ch. 3: 528; ona pia Piper 1997: n.p.; Erlandson
1991: n.p.; Edwards 1984, The End: 94-121; Piper 2003a: 17-50; Piper 2003b: 17-35)
B. Adamu na Hawa watenda dhambi na kufukuzwa kutoka bustani ya Edeni (Mwanzo 3).
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
14
1. Biblia inaweka bayana kwamba Shetani “alianguka” kabla ya dhambi ya Adamu na Hawa, kwa vile
Shetani ndiye aliyewajaribu Adamun a Hawa na kuwadanganya kuhusu sababu na matokeo ya kula tunda
la mti wa ujuzi wa mema na mabaya (fananisha Mwa 2:16-17 na Mwa 3:1-4). Kwa hiyo, Yesu alimwita
Shetani yote mawili, “muuaji tangu mwanzo” na “mwongo na baba wa huo” (Yoh 8:44-45).
2. “Ujuzi wa mema na mabaya” (Mwa 2:17) huwakilisha uhuru wa kimaadili na kujitawala.
a. Ule “mti wa ujuzi wa mema na mabaya” haukuwa mti wa kiuchawi ambao ulizaa ujuzi wa
mema na mabaya kwa kila mtu aliyeula. “Inaelekea sana kwamba Mungu aliuandaa huo mti
kama uwigo wa mpaka, kama njia ya kuonyesha tofauti kati ya mema na mabaya. Kwa maneno
mengine, uchaguzi wa Adamu na Hawa haukuwa kati ya kutokujua na kujua mema na mabaya,
bali katika kubakia wema na wenyewe kuwa wabaya. Sura ya mtihani ilikuwa kwamba lolote
watakalolichagua, watakuja kujua mema na mabaya. Walikuwa viumbe vya kimaadili ambavyo
vingejua yaliyo sahihi na yasiyo sahihi kwa kutumia mwitikio wao binafsi kwa Mungu.”
(Goldsworthy 1991: 98) Kama wangefaulu mtihani huo, kule kumtegemea na kumtii Mungu
kungeliuthibitisha wema wao, na wangelilijua hilo. Kama wangelishindwa mtihani huo,
kutomtegemea na kutokumtii Mungu kungeliwageuza kuwa watu wenye uovu kwenye kiini
kabisa cha uanadamu wao, na wangelilijua hilo pia.
b. Katika vifungu Fulani vya AK (2 Sam 4:17; 1 Waf 3:9) maneno “mema na mabaya”
huzungumzia kimsingi uwezo wa kuchukua hatua kisheria. Kwa hiyo, kilichokuwa kimekatazwa
kwa mwanadamu kilikuwa ni ule uwezo wa kuamua nini kiwe kwa ajili ya manufaa yake na nini
kisiwe hivyo. Mungu hakutoa maamuzi ya aina hiyo kwa mwanadamu, kwa sababu ni Mungu
pekee ndiye ajuaye yote, mwenye hekima yote, na mwenye upendo wote. Kwa hiyo, ni Mungu
pekee anaweza kufanya uamuzi sahihi na wenye upendo kwa ajili ya manufaa ya mwanadamu
ya kweli, wakati wote. Mwanadamu atendapo katika hali ya kujitawala mwenyewe, hujiweka
nafsi yake mwenyewe kuwa mhimili wa kati kwa miongozo yake ya kimaadili na hujiamulia nini
chema na nini kibaya. Hivyo hujaribu kuwa “kama Mungu” (ona Mwa 3:5, 22). Hata hivyo,
kwa vile mwanadamu hajui yote, hana hekima yote, na hana upendo wote, juhudi zake za kuwa
kama Mungu ni dhahiri zitashindwa. Badala yake, ataishia kutenda zaidi kama “mungu wa dunia
hii” (2 Wakor 4:4), na matokeo yanayofanana nayo.
3. Shetani alimwingia nyoka na kumdanganya Hawa (Yoh 8:44; 2 Wakor 11:3; Ufu 12:9). Adamu
alikuwapo pamoja naye, hakufanya lolote kujaribu kumzuia, na, yeye pasipo kudanganywa, alikubali kwa
hiari kabisa kumfuata mkewe katika dhambi (Mwa 3:6; 1 Tim 2:14). Kama James Boice
anavyobainisha, “Ikiwa Adamu hakudanganywa, kama 1 Timothy 2:14 pasemavyo bayana, basi ni lazima
awe alifanya dhambi kwa kujua kikamilifu kile alichokuwa anakifanya. Hilo maana yake, aliamua kula
kwa kukusudia kabisa kutomtii Mungu.” (Boice 1986: 196) Hilo laweza kuwa sababu kwa nini dhambi
ya Adamu ni kubwa zaidi, na kwa nini matokeo yaliyowajia wanadamu wote baadaye husemekana
kutokana na dhambi ya Adamu na siyo ya Hawa (ona Rum 5:12-14, 17-21; 1 Wakor 15:21-22).
4. Mbinu ya Shetani ni kielelezo cha majaribu yanayotukabili.
a. Alimjia Hawa kwanza. Huo ulikuwa ni ujanja wa juhudi za kujaribu kumdanganya mtu
ambaye hakupokea maagizo moja kwa moja kutoka kwa Mungu, na kumgonganisha mtu moja na
mwingine
b. Alilenga jambo pekee ambalo Mungu alikuwa amelikataza. Licha ya Mungu kutoa mahitaji
yote kwa wingi mkuu, kwa kule kukazia kitu pekee ambacho hawakutakiwa kukifanya, Shetani
ndipo kama matokeo yake alipandikiza wazo ambalo limepotoka au lililokengeuka kuhusu
uhalisi katika akili zao.
c. Alitafuta kuingiza mashaka kwenye kweli ya Neno la Mungu (3:1). Kwa kuuliza “ati Mungu
[kweli] alisema, ‘msile matunda ya miti yote ya bustani?’” Shetani alitafuta kuingiza mashaka na
kupandikiza kuchanganyikiwa kuhusu kile ambacho alikitaka Mungu.
d. Alidanganya na kuligeuza Neno la Mungu (3:4). La kushangaza, ukweli mmoja ndio Shetani
aliushambulia kuhusiana na ghadhabu ya Mungu na madhara ya dhambi. Kama ilivyokuwa kwa
Adamu na Hawa, tunakabiliwa na uamuzi: nani tumwamini? Kwa mbinu za Shetani (na za
kidunia), Neno la Mungu halikubaliwi tena kama kweli inayojieleza yenyewe, bali limefanywa
kuwa ngazi ya neno la kiumbe. Yote mawili–Mungu na Neno lake huonekana kuwa na mamlaka
ya chini zaidi ambayo lazima yapimwe na mamlaka iliyo juu zaidi. Kwa mara nyingine, ujanja
wa nyoka: haupendekezi wanadamu wamwachie Mungu enzi yake mwenyewe, bali wao
wenyewe tu waangalie na kutathmini madai ya Mungu kuhusu kweli. Matokeo ya mwisho
yalikuwa sawa tu na kumweka Shetani awe Bwana, lakini hayo hufanyika pasipo mwanadamu
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
15
kuelewa.” (Goldsworthy 1991: 104)
e. Ailzijumuisha sifa za Mungu mwenyewe (3:5). Kimsingi, Shetani alikuwa anasema kwamba
Mungu alikuwa hana upendo kwa kuwazuia Adamu na Hawa vitu vya kula, na alikuwa hana
upendo kwa kuvitaka viumbe vyake kumtegemea yeye kwa maarifa ya mema na mabaya, badala
ya kufanya maamuzi hayo wenyewe.
f. Alichochea kiburi cha kianadamu. Shetani alimwahidi Hawa kwamba kwa kumuasi Mungu
angelikuwa na uzima (“hakika hutakufa”), maarifa (“na macho yako yatafumbuka”), furaha
kutokana na hali ya kuinuka (“utakuwa kama Mungu”), na ukuu wa kujitawa kimaadili (“kujua
mema na mabaya”). Kinyume chake, hata hivyo, kwa Adamu na Hawa kufanya maamuzi kwa
njia yao wenyewe (m.y., kujitawala kimaadili) ni sura ya kifo kwa sababu ni kutengwa mbali na
Mungu. Kwa hiyo, kiini cha dhambi yao kilikuwa kutokuamini (m.y., kukosa imani na tumaini
kwa Mungu, kunakodhihirishwa kwa kumtii Mungu). Hata tangu mwanzo, mpango wa Mungu
ulikuwa kwamba watu wamwangalie yeye na kumtumaini yeye kwa ajili ya kweli kuhusu nini ni
chema na nini kibaya, na kwa vipi tunatakiwa kuishi maisha yetu—m.y., “mwenye haki ataishi
kwa imani” (Hab 2:4; Rum 1:17; Wagal 3:11; Waeb 10:38).
5. Dhambi ya Adamu na Hawa iliwadhuru si wao tu, bali kila mtu katika historia yote.
a. Badala ya kuleta furaha na utoshelevu, Adamu na Hawa walileta hukumu, aibu, hofu,
kufarakana na Mungu, uumbaji wote, wao kwa wao, na hatimaye mauti. (Mwa 3:7-19). Adamu
na Hawa walitaka kujitawala (m.y., uhuru; kutengwa na Mungu), na wakapata hayo. Hata hivyo,
kujitenga huko na Mungu ni sura ya kifo na mauti. Kutokana na kile walichokifanya, Adamu na
Hawa kwanza walijikuta na aibu kuhusiana na hali yao ya kuwa uchi (Mwa 3:7-10). Hali yao ya
kijinsia ingeliwakumbusha kwamba wao hawakuwa kama Mungu: hawakuwa na uwezo wa
kuumba pasipo kutumia chochote (kama Mungu), bali tu waliweza kuzaa. “Hivyo hali yao ya
ujinsia ilikuwa iwakumbushe [au ingepaswa iwakumbushe] juu ya uhuru wao na changamoto
zake [au ingetoa changamoto] kwa fikira zao za uhuru na hali yao ya kuwa kama Mungu”
(Goldsworthy 1991: 105).4 Kama matokeo ya mkondo ulioanzishwa bustanini, Mungu mara zote
huwaachia watu waamue wenyewe njia zao na kisha kubeba madhara yao wenyewe (ona Kut
16:1-20; Hes 11:18-20, 31-34; Rum 1:24, 26, 28).
b. Adhabu ambayo Mungu aliiagiza (Mwa 3:16-19) kwa mwanaume (kazi inafanyika ngumut)
na mwanamke kuzaa watoto kunakuwa kwa uchungu) zote zahusiana na uwajibikazi kimaisha
kwa wanaume na wanawake. Zaidi ya hapo, Mwa 3:16b panaonyesha mwanzo wa mgongano
wa kindoa na/au mvutano wa madaraka ya kindoa—tangu sasa na kuendelea, uhusiano kati ya
waume na wake utakuwa una harufu ya dhambi (ona, k.m., kufuatia kwa mawazo mbali mbali
yahusuyo namna ya mwingiliano kati ya “kutamani” na “kutawala” katika 3:16: Busenitz 1986:
203-12; Cassuto 1961: 165-66; Walton 2001: 227-28; Stitzinger 1981: 41-42; Foh 1974-75: 376-
83).
c. Dhambi ya Adamu huathiri uumbaji wote. “Uumbaji upo hapo kwa ajili ya manufaa yetu.
Unyenyekevu ni uwakilishi wa uumbaji wote ili kwamba Mungu aushughulikie uumbaji kwa
msingi wa anavyoshughulika na wanadamu. . . . Mwanadamu aangukapo kwa sababu ya dhambi,
uumbaji hufanywa kuanguka pamoja naye.” (Goldsworthy 1991: 96) Zaidi ya hapo, Adamu
hupata baadhi ya dawa zake: kama tu jinsi alivyoasi kinyume na utawala wa Mungu, sasa
uumbaji wote, ambao anatakiwa kuutawala, utamwasi kinyume naye. “Laana ardhini kusema
kweli ni laana kwa Adamu. Mfalme wa dunia sasa hana mtumishi anayemtii ardhini. Uhuru wa
kula miti yote katika bustani unabadilishwa na kwa masumbufu kuifanya dunia itoe mkate
unaolazimika kila siku. . . . Mwisho wa mwanadamu ni kuipa ardhi mbolea kwa yeye kuurudia
mavumbi ambako alitokea.” (Ibid.: 106)
d. Biblia huona watu wote kuwa kama moja na Adamu (“katika Adamu”), Adamu akitenda
kama kichwa chetu au mwakilishi wetu (ona Rum 5:12-19; 1 Wakor 15:21-22; nk., Waeb 7:9-
10). Hatimaye, kama matokeo ya dhambi ya Adamu, kizazi chote cha mwanadamu kinapokea:
“uhalali” wa kuwa na hatia dunia nzima, kunakoongoza kwenye kuharibika kimaadili dunia
nzima (Zab 51:5; Yer 17:9; Rum 3:9; 7:14-25), kunakoongoza kwenye dhambi ya mtu moja
moja dunia nzima (Rum 3:10-18, 23), kunakoongoza kwenye hatia ya mtu moja moja. Jinsi
kamili ya namna ilivyokuwa na kwa nini na vizazi vya Adamu vimehesabiwa hatia na kuwa na
4 Baada ya Hawa “kutwaa na kula” (Mwa 3:6), Yesu kristo ilibidi aonje umasikini na mauti kabla ya maneno “twaa, kula”
(Math 26:26) kufanyika maneno ya wokovu badala ya mauti.
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
16
uharibifu mkubwa kutokana na dhambi ya Adamu, ni swala la mjadala. Zifuatazo ni baadhi ya
fikira zifikiriwazo:
(1) Biblia siku zote hutazama makundi ya watu kama mtu “moja aliyekamilika” (ona
Yosh 7:10-26; Rum 5:12-19; 1 Wakor 15:21-22). Hii ni sawa na kumtazama Adamu
kama mbegu au mzizi wa mti, na uzao wake kama matawi na majani: Vyote ni mti moja;
matawi na majani hupokea yote mawili - uzima na sura kutoka kwa ile mbegu na mzizi.
Adamu, kama kichwa cha kizazi chote, huzalisha viumbe vilivyoanguka, vyenye uasi,
kama vile yeye alivyifanya dhambi. Hali ya Adamu kama kichwa “huhusisha fursa za
ndani zaidi kuliko ubaba wa kikawaida. Huhusisha utukuzaji wa kuelezea nini
kinamaanisha kuwa mwanadamu [ona Mwa 5:3; 1 Wakor 15:49]. . . . Ikiwa wahusika
wanataka kuasi, je wasimamie wapi ili kufanya hilo? Sioni msingi wowote wa wao
kusimamia, hakuna kitovu cha madai yao, uhuru wao binafsi hauko huru, mshabihiano
wenye kujitegemea. Mungu ndiye aliyeuumba kama vile alivyowaumba, ndani na kupitia
Adamu, kama sehemu ya sifa za Adamu.” (Blocher 1997: 130)
(2) Kwa vile Adamu aliumbwa pasipo dhambi na alikuwa na kila fursa na mazingira
yake binafsi, hakukuwa na mtu bora zaidi yake wa kuwakilisha wanadamu katika ujumla
wao. Kama mwakilishi wetu, dhambi ya Adamu, na hivyo hata kukosa kwake,
kuliwekezwa kwetu (ona Johnson 1974: 298-316). Hali ilivyo ni kama taifa: “itokeapo
mkuu wa nchi akitangaza vita na taifa jingine, watoto wote wanao zaliwa wakati huo wa
vita huwa wako vitani na taifa jingine. Katika swala la Adamu, maafa hutenda kazi kwa
kina cha ndani zaidi, kwa sababu mshikamano wetu wa ki-Adamu (yaani, uanadamu) ni
muhimu zaidi na, kwa vile uhusiano ni kwa Mungu ‘ambaye tunaishi na kuenenda na
kuwa na uhalisi ndani yake’.” (Blocher 1997: 129).
(3) Ilikuwa lazima kabisa kwa Mungu kufanya kitu fulani kwa watu wote ili wawe na
uharibifu kama matokeo ya dhambi ya Adamu. “Ni kutoa katika yaliyojitokeza, kama
ilivyokuwa sahihi na lazima kwa kiwango cha juu sana afanye hivyo, kutoka kwa huyo
mwanadamu mwasi, na kanuni zake za kiasili zikiwa zimeachwa zenyewe, kwatosha
kumfanya awe mharibifu kabisa na aliyepindana kutenda dhambi kinyume na Mungu”
(Edwards, 1984, Original Sin: 219).
e. Matokeo ya anguko, na utu wetu “katika Adamu,”ni kwamba kwa jinsi yetu wenyewe, pasipo
Kristo, tunakuwa “wafu katika makosa na dhambi zetu” (Waef 2:1). Hii inamaanisha kwamba
kuna upungufu kupita kiasi au uharibifu kuhusiana na kila mtu (pia huitwa nguvu ya dhambi
ikaayo ndani) ambayo huathiri kila kitu ndani yetu, kuchanganya hata jinsi tunavyofikiri,
kuwaza, kuongea, kutenda, kujisikia, na mahusiano na watu na kwa Mungu. Matokeo ya
uharibifu huu ni kuwa, nje ya msaada wa Kristo, tunakuwa: hatuna uwezo kabisa kumjia Kristo
na kumwamini yeye (Yoh 6:44, 65; Waef 2:8-9); hatuwezi kabisa hata kuuona ufalme wa
Mungu (Yoh 3:3, 5); hatuwezi kabisa kujitoa kwa sheria ya Mungu na kumtii (Rum 8:6- 8);
hatuwezi kabisa kuelewa kweli za kiroho kumhusu Mungu (1 Wakor 2:14); hatuwezi kabisa
kumpendeza Mungu (Waeb 11:6); tunakuwa watumwa wa dhambi, dunia, mwili, na Ibilisi,
hatuna kabisa uzima wowote ule, na tunapaswa ghadhabu ya Mungu na hukumu yake (Rum
6:16-17; Waef 2:1-3) (ona pia Edwards, 1984, Original Sin: 143-233; Owen 1979: passim).
6. Hata katika hukumu yake kwa Adamu na Hawa, Mungu alidhihirisha neema yake.
a. Alitengeneza mavazi ya kuwatosha ya ngozi ya wanyama ili kuwavika Adamu na Hawa (Mwa
3:21).
b. Ingawaje Mungu alimfukuza Adamu na Hawa kutoka bustanini (Mwa 3:22-24),
hakuuondolea uwakili wao juu ya hii dunia (fananisha Mwa 2:15 na 3:23). Bila shaka,
kufukuzwa kwao kutoka bustanini kulisaidia kukamilika kwa mpango wa Mungu wa
mwanadamu kuijaza na kuimiliki dunia (Mwa 1:28).
c. Katika Mwa 3:15 alitoa tamko la kwanza la mpango wake wa wokovu kwa dunia: “Nami
nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo
utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.” Mtu fulani kati ya uzao wa mwanamke
(amekuwa akitajwa kama mzao wa Ibrahimu [Kristo]) atatoa pigo la kichwa na kuleta ushindi
kwa Shetani msalabani, wakati Shetani atamponda kisigino, au kumsababisha ateseke. Tamko
hili limetekelezeka hatua kwa hatua katika Biblia nzima yote. Bila shaka, tamko hilo,
likijumuishwa na swala kwamba Adamu na Hawa wasile kutoka katika mti wa uzima (Mwa
3:22), kuliwahakikishia kuwa wasingeweza kuishi milele wakiwa katika dhambi. Badala yake,
Copyright © 2009-2015 by Jonathan Menn. All rights reserved.
17
kama Mungu alivyofunua hatua kwa hatua mpango wake, wale waishio kwa imani katika Kristo
wataweza kula kutoka kwenye mti wa uzima katika nchi mpya milele katika haki (Ufu 22:2).
C. Matokeo ya Anguko—kutoka kwa Kaini hadi Mnara wa Babeli (Mwanzo 4-11:26)
“Baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi, uzao uliowafuatia uliendelea kuitawala dunia. Tatizo
halikuwa kama walikuwa hawatawali. Kinyume chake, Mwanzo 4 panaonyesha michango yao katika ubunifu wa
muziki, ufuaji vyuma, ufugaji, ustadi wa ujenzi, na siasa (‘Kaini akajenga mji, mst. 17). Tatizo kuu la
mwanadamu mwenye dhambi halijawahi kuwa kukataa kwake kuitawala dunia. Tatizo lake kuu ni kwamba
huitawala dunia katika namna isiyomcha Mungu. Mwanadamu huyu wa asili ya ki-Adamu hutawala ili kujifanyia
jina mwenyewe, siyo kwa kulitukuza jina la Bwana. Wanadamu wadhambi hujaribu kutawala wakati wao
wenyewe ni watumwa wa dhambi na Shetani. Mungu aliwaumba Adamu na Hawa ili wajenge nakala ya ule Mji
Wake hapa duniani. Wazao wao wakajenga mji uliopotoka wa Mwanadamu.” (Leithart n.d.: n.p.)
1. Kaini na uzao wake (Mwa 4:1-24).
a. Kwa Kaini twaona kuongezeka kwa dhambi: kukufuru5 (4:3); hasira (4:5); wivu, udanganyifu,
na mauaji (4:7-8); uongo (4:9); kujitafutia binafsi na kujihurumia (4:13-14); kukengeuka kutoka
kwa Mungu (4:14, 16). Kuongezeka kwa dhambi pia kunaonekana kwamba Kaini siyo tu
hakumuua kila mtu, bali alimuua ndugu yake mwenyewe ambaye alikuwa mtu “mwenye haki”
(Math 23:35; Waeb 11:4). Pia, hata hivyo, angalia neema ya Mungu kwa Kaini katika kumlinda
ili asiuawe na ndugu zake wengine wa kike na wa kiume (Mwa 4:15).
b. Uzao wa baadaye wa Kaini, Lameki (4:18-19, 23-24) apelekea uharibifu kimaadili kuwa
kiwango cha chini kabisa: ana kiburi na majivuno; ageuza mgongo wake kwa mpango wa
Mungu wa mke moja (Mwa 2:23-24; Math 19:3-6). Wake wengi siyo mpango sahihi wa
Mungu. Katika Biblia kuwa na wake wengi mara zote kumeonekana kuwa siyo sahihi, na
kuliongoza kuletesha matokeo mabaya. Kwa hiyo, haishangazi kwamba hata aliyeanzisha kuwa
na wake zaidi ya moja, Lameki, ni mtu mkali aliyejipatia uhuru wake kamili kutoka kwa Mungu
kwa kuua watu kwa visasi vya maswala madogo madogo na kudai haki ya Mungu ya kulipa
kisasi (ona Kumb 32:35). Madai yake makali ya kutaka kulipa kisasi kwa wengine “mara sabini
na saba” (Mwa 4:24) hupata mkondo mwenza katika kauli ya Kristo kuwa tunatakiwa
kuwasamehe wengine “mara sabini na saba” (Math 18:21-22).
2. Tangu Seti hadi Nuhu (Mwa 4:25-6:8).
a. Moja ya sifa kuu za kitabu cha Mwanzo ni matumizi ya vichwa vinavyofanana katika
kutambulisha simulizi na vizazi ambavyo hubadilishana katika Kitabu kizima. “Hivyo hutokea
katika 2:4; 5:1; 6:9; 10:1; 11:10, 27; 25:12, 19; 36:1, 9; 37:2. Kitu kinachofanana kote katika
vichwa hivi vyote ni neno la Kiebrania [Toledot—ambalo kikawaida hutafsiriwa kama “kizazi
(vizazi); uzao; hesabu; orodha; kumbu-kumbu”]. . . . Hivyo vichwa [Toledot] hutenda kazi mbili.
Kwanza, huwa kama vichwa vya sura katika vitabu vya kisasa. Baadhi yao hutambulisha sehemu
kuu za simulizi, kuonyesha hatua mpya ya kukua kwa mpango. . . . [Pili, hivyo vichwa vya
Toledot] hukazia mtazamo wa msomaji kwa mtu maalum na watoto wake aliowazaa.
Humwezesha mwandishi wa Mwanzo kufuatilia mema ya mkondo mzima wa familia kuu pasipo
kulazimika kufuatilia kwa kina maisha ya ndugu zao wengine.” (Alexander 1993: 258, 259)
b. Kuanzia Mwa 4:25 mpango wa kitabu unageukia mkondo wa Seti. Kwa hiyo, hivyo Toledot
vya Adamu, kuanzia Mwa 5:1 hukazia kwa Seti na kIsha kwa wazao fulani wa Seti. Biblia
hufanya hilo kwa makusudi, kwa sababu watu inaowakazia ndio kitovu cha kuanikwa wazi kwa
simulizi nzima.6
5 Dhabihu ya Habili ilikuwa kwa imani (Waeb 11:4); Ile ya Kaini bila shaka haikuwa hivyo. Ni lazima, bila shak