211
1 29 APRILI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kumi na Nne Tarehe 29 Aprili, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHA MEZANI Hati zifuatayo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII:- Hotuba ya Mpango na Makadirio ya Matumizi ya Fedha za Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE. JAMES D. LEMBELI – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

  • Upload
    others

  • View
    12

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

1

29 APRILI, 2013

BUNGE LA TANZANIA________________

MAJADILIANO YA BUNGE________________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Kumi na Nne – Tarehe 29 Aprili, 2013

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua

HATI ZILIZOWASILISHA MEZANI

Hati zifuatayo Ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII:-

Hotuba ya Mpango na Makadirio ya Matumizi yaFedha za Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa mwaka wa Fedha2013/2014.

MHE. JAMES D. LEMBELI – MWENYEKITI WA KAMATI YAKUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA:

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu yaWizara ya Maliasili na Utalii, kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio na Matumizi ya Wizarahiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

Page 2: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

2

29 APRILI, 2013

MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y. MSEMAJI MKUU WAKAMBI RASMI YA UPINZANI KWA WIZARA YA MALISILI NAUTALII):

Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzanikwa Wizara ya Maliasili na Utalii Kuhusu Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

MASWALI NA MAJIBU

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge Maswali leo tunaanzana Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, atakayeuliza swalila kwanza ni Mheshimiwa Lameck Okambo Airo.

Na. 110

Uhamishaji wa Kituo cha Uhamiaji Shirati kwenda Kirongwe

MHE. LAMECK O. AIRO aliuliza:-

Wilaya ya Rorya ina vituo viwili vya mipaka yaTanzania na Kenya ambavyo ni Shirati na Kogaja, lakini Serikaliya Kenya tayari imeishajenga kituo cha Mihuru Bay nakukamilika.

(a) Je, Serikali itahamishia kituo cha Shirati Kirongwesehemu waliyojenga Serikali ya Kenya?

(b) Je, ni lini Serikali itawafidia wananchi wa Kirongweambao wametoa maeneo yao kwa ajili ya kituo hichokuhamishiwa hapo?

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Lameck O. Airo, Mbunge wa Rorya, lenyesehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Page 3: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

3

29 APRILI, 2013

(a) Mheshimiwa Spika, suala la kuhamisha kituo chaUhamiaji cha Shirati kwenda Kirongwe limewekwa katikaMpango wa utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2013/2014ambapo Wizara kupitia Idara ya Uhamiaji inatarajia kuanzaujenzi wa ofisi katika kituo cha Kirongwe. Ujenzi huu unafuatiakutengwa kwa eneo la kutosha kwa madhumuni ya kujengaofisi za taasisi zote zinazotoa huduma mpakani.

(b) Mheshimiwa Spika, kwa kuwa eneo la Kirongwe lipochini ya Serikali ya Kijiji ambayo imelitoa kwa madhumuni yamatumizi ya kujenga ofisi za taasisi zinazotoa hudumamipakani, utaratibu wa kufidia wananchi waliotoa maeneoyao utafanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu za ulipajifidia baada ya maeneo husika kufanyiwa uthaminishaji.(Makofi)

MHE. LAMECK O. AIRO: Mheshimiwa Spika, Rorya niwilaya ambayo imekamilika; ina DC, Usalama wa TaifaWilaya, Mshauri wa Mgambo wa Wilaya, TAKUKURU nakadhalika.

Mheshimiwa Spika, Idara ya Uhamiaji mpaka sasahawajahamia katika eneo lao la wilaya na tayari DCamewahi kutoa nafasi ili Afisa Uhaniaji wa Wilaya awezekuhamia pale kwenye ofisi yake, lakini mpaka sasa AfisaUhamiaji hajahamia pale.

Kinachotokea ni Wanarorya kufuata huduma hiyoMusoma na Tarime wakati Afisa Uhamiaji wa WIlayaameishateuliwa, yuko Wilayani. Naomba majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaSpika, kwanza nizingatie kwa makini sana tatizo ambaloameliongelea. Lakini pia tunazingatia na kulifuatilia kwaukaribu. Naomba nimhakikishie kwamba tutachukua hatuaharaka inavyowezekana kuliondoa tatizo hilo. (Makofi)

Page 4: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

4

29 APRILI, 2013

Na. 111

Matatizo ya Kiulinzi YanayoikabiliMipaka Yetu

MHE. FAKI HAJI MAKAME aliuliza:-

Mipaka ya nchi ni eneo muhimu sana ambalo linajukumu la Ulinzi na Usalama kisiasa na kwa afya ya raia nanchi husika. Katika kutekeleza majukumu hayo walinzi naviongozi wao wamekuwa wakipata shida na matatizomakubwa ya kudhibiti mipaka yetu hasa katika mpaka waTanzania na Zambia.

Je, ni lini Serikali itamaliza matatizo yanayowakabiliwalinzi wetu hususan pale Tunduma katika ulinzi wa afya yaWatanzania?

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Faki Haji Makame, Mbunge wa Mtoni, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nimemwelewa vizuriMheshimiwa Mbunge ni kweli mazingira ya eneo la Tundumayanazifanya shughuli za ulinzi mpakani kuwa ngumu. Serikaliimekuwa ikilitafakari suala la kuzibomoa nyumba zilizojengwakiholela kwenye eneo la mpaka.

Hata hivyo, uamuzi huu una gharama kubwa sana.Kwa msingi huo Serikali imeviagiza Vyombo vya Ulinzi naUsalama viimarishe shughuli za ulinzi na ukaguzi wa eneo laTunduma ili kudumisha usalama wa nchi yetu wakatiikiendelea kulitafutia suala hili ufumbuzi wa kudumu.

Page 5: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

5

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wahalifu wanawezakujifanya wafanyabiashara wakati wanapotaka kutimizadhamira zao, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Jeshila Polisi na Idara ya Uhamiaji hushirikiana ili kuhakikishakwamba ulinzi na usalama katika maeneo ya mipakaniunalindwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kuwa Serikali italipatia ufumbuzi tatizola walinzi wetu pale Tunduma hali ya fedha itakapoimarika iliwaweze kutimiza wajibu wao kwa Taifa. (Makofi)

MHE. FAKI HAJI MAKAME: Mheshimiwa Spika, ahsantesana. Pamoja na majibu hayo mazuri katika fani ya uandishina usimulizi, naomba nimWulize Mheshimiwa Waziri maswalimawili kama ifuatavyo:-

(i) Kwa kuwa, Waziri ametueleza kuwa JKT, Polisina Uhamiaji wanashirikiana katika kusaidia ulinzi wa lile eneo,na Kamati ya Huduma za Jamii kipindi kilichomalizikatulipotembelea eneo lile tulioneshwa mpaka zile njia zapanya ambazo zinategewa kutumika kupitisha vitu kamadawa feki na biashara nyingine haramu. Mbona walewafanyakazi pale hawakutuonesha ule ushirikiano wenyewekwamba hapa katika uchochoro huu, njia za panya hizi, kunahuyu mlinzi wa usalama, huyu ni mlinzi labda wa JKT? Hilondiyo swali langu, hatukuwaona.

(ii) Kwa kuwa, TFDA wanajitahidi sana kukamatadawa kadhaa feki, vipodozi visivyofaa na dawa tiba ambazohazifai zinazoingia nchini hukamatwa.

Je, Serikali inaisaidiaje TFDA kuweza kuwa na nguvuya kuimarisha ulinzi zaidi kwa ajili ya usalama wa raia? (Makofi)

SPIKA: Haya, swali la kwanza Mheshimiwa Waziriunaweza kujibu. lakini hilo la pili sijui ni nani tena?Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Page 6: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

6

29 APRILI, 2013

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Faki HajiMakame, swali lake la nyongeza, kama ifuatavyo:-

Ushirikiano upo, si rahisi sana kama alivyoambiwa nawafanyakazi kwamba lazima wamwambie kuna ushirikianowa kiwango hiki. Kwa kadiri ninavyoelewa ushirikiano upo.Suala la kwamba zipo njia za uchochoro, nadhani ipo mipakaya majukumu hapa kwa sababu yapo majukumu ya ulinziwa mipaka na hili ni jukumu la Jeshi la Wananchi wa Tanzaniana siyo kama alivyosema yeye JKT, Jeshi la Wananchi laTanzania (JWTZ).

Lakini ziko shughuli hasa katika maeneo hayo yakwenye vichochoro ambazo zinatekelezwa na Jeshi la Polisi.Lakini kwa kuwa Serikali ni moja, tumesikia jambo hili,tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu kuimarisha ushirikiano uliopokati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la Polisi ilituweze kutekeleza wajibu wetu wa kulinda usalama na ulinziwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru.

SPIKA: Swali la pili Mheshimiwa Waziri wa Afya naUstawi wa Jamii.

WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: MheshimiwaSpika, napenda kujibu swali la nyongeza la MheshimiwaMbunge kama ifuatavyo.

Ni kweli kwamba TFDA wanafanya kazi nzuri kamaalivyosema Mheshimiwa Mbunge, tatizo lao ni uhaba wawafanyakazi na vitendea kazi. Kwa mfano zile zinazoitwamin- lab, maabara ndogo sehemu za mipaka. Kamamlivyosikia ni kwamba tunatarajia sasa kupata vibali vya ajira.Tutawaongezea wafanyakazi TFDA pamoja na hizo min-labili waweze kutoa huduma hiyo kwa uhakika zaidi. Tatizo laolilikuwa ni uhaba tu wa wafanyakazi.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Page 7: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

7

29 APRILI, 2013

MHE. SELEMAN S. JAFO: Mheshimiwa Spika, ahsantesana. Kwa kuwa Kambi ya JKT Bulombora kule mkoani Kigomaimekuwa katika mazingira magumu sana hasa kwa kukosanishati ya umeme ya uhakika. Kwa vile kambi hiyo imekuwaikisaidia suala zima la ulinzi hasa katika mpaka wetu na nchiyetu na Kongo?

Je Serikali ina mpango gani hasa Wizara ya Ulinzi naJeshi la Kujenga Taifa ikishirikiana na Wizara ya Nishati naMadini, kusaidia kambi ya Bulombora eneo lile kuwa naumeme wa uhakika ili hali ya ulinzi wa maeneo yale yawezekuimarika? (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri si unaijua hiyo Kambi? Huyualikuwa Tunduma.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza laMheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo.

Ni kweli kwa muda mrefu Kambi ya JKT Bulomboraimekuwa na tatizo la umeme. Wizara yangu inalijua tatizohilo, tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu kulifanyia kazi nakulitafutia ufumbuzi. Tatizo linalotukabili sasa hivi ni upungufuwa fedha na kambi ambazo bado hazina nishati ya umemeni nyingi. Lakini tutajitahidi kufanya hivyo kwa kadiri hali yafedha itakavyoruhusu ili katika kipindi kifupi kijacho kambi hiiya Bulombora nayo iweze kupata umeme wa uhakika ilihatimaye waweze kutekeleza jukumu lao la ulinzi katika eneohilo. (Makofi)

SPIKA: Swali hil i lakini l i l ikuwa jingine kabisa.Mheshimiwa Mama Sitta.

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi nami niongeze swali lanyongeza kama ifuatavyo.

Page 8: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

8

29 APRILI, 2013

Swali la msingi la Mheshimiwa Faki lilihusiana nausalama wa afya na kama alivyojibu Mheshimiwa Waziri waAfya na Ustawi wa Jamii, naomba niulize.

Je, tatizo la pale mpakani kuhusu afya ni idadi yawafanyakazi tu na si vitendea kazi hasa magari kutokana naurefu wa mpaka ili waweze kudhibiti dawa na vipodozi visivyohalali vinavyoingizwa nchini? (Makofi)

WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: MheshimiwaSpika, kama nilivyosema wakati najibu swali hili, tatizo letu niuhaba wa wafanyakazi pamoja na vitendea kazi. Lakinisiyo rahisi kuweka hizo zinazoitwa min-lab mpaka mzima, nilazima ziwe sehemu maalum. Tunachotegemea ni kwambavyombo vya ulinzi na usalama vitalinda hiyo mipaka ili kufanyawatu wote wapite katika sehemu rasmi ambazo ndipotutakapokuwa tuna wataalam wanaoshughulikia masualaya afya.

Kwa hiyo, anachosema Mheshimiwa Waziri wa Ulinzini kwamba kwa kushirikiana kati ya vyombo vya ulinzi nausalama na vile vyombo ambavyo vinatoa huduma za afyawakiwamo mabwana afya katika maeneo yale pamoja nawatu wa TFDA. Ni vyema tukahakikisha mipaka hiyoinalindwa na vyombo vya ulinzi na usalama ili watu wotewapite katika mipaka rasmi na bidhaa zao ziwezekukaguliwa.

SPIKA: Ahsante sana. Naomba tuendelee na Wizaraya Nishati na Madini, Mheshimiwa Murtaza Ali Mangungu,atauliza swali linalohusika.

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Pamoja na kuipongeza Yanga kwa Ubingwanaomba sasa swali langu Na. 112 lipatiwe majibu. (Makofi)

SPIKA: Sasa kuchomekea tu, Mheshimiwa Naibu Wazirimajibu. (Kicheko)

Page 9: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

9

29 APRILI, 2013

Na. 112

Agizo la Mheshimiwa Rais la kuwafungia UmemeWananchi wa Somanga

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU aliuliza:-

Eneo la Somanga ndipo mitambo ya kuzalishaumeme ilipo; na kwamba pamoja na agizo la MheshimiwaRais kuwa wananchi wa eno hilo wafungiwe umeme badohawajafungiwa:-

(a) Je, kwanini agizo hilo la Mheshimiwa Raishalijatekelezwa?

(b) Je, kwanini maeneo ya Banduka, Mtandago, Miteja,Sinza, Puyu, Matandu na Njenga hayapati umeme licha yaumeme kupitia kwenye maeneo hayo?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. CHAWENE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishatina Madini napenda kujibu swali la Mheshimiwa Murtaza A.Mangungu, Mbunge wa Kilwa Kaskazini, lenye sehemu (a)na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, ahadi ya Mheshimiwa Raisimekwishaanza kutekelezwa, ambapo tayari baadhi yamaeneo ya Somanga Fungu yana Umeme na wateja 200wameunganishwa. Kwa sasa Serikali inaendelea nautekelezaji wa mradi mdogo ambapo tunatarajiakuwaunganisha wateja wengine 50. Katika mradi huu, nguzo60 zimetengwa na tayari 40 zimekwishasimamishwa.

Aidha, wananchi wa eneo la Somanga Funguwanashauriwa kuanza kupeleka maombi ya kuwekewaumeme TANESCO Kilwa Masoko.

Page 10: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

10

29 APRILI, 2013

(b) Mheshimiwa Spika, kazi ya kupeleka umememaeneo ya Banduka, Mtandago, Miteja, Sinza, Puyu,Matandu na Njenga zimejumuishwa katika mpangokabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshajiwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Zabuni ya kuwapatawakandarasi wa kazi hizi ilitangazwa mwezi Desemba, 2012na kufunguliwa mwezi Julai Machi, 2013. Kazi za ujenzizinatarajiwa kuanza wakati wowote mwaka huu.

Mheshimiwa Spika, kazi za kufikisha umeme kwenyevijiji tajwa hapo juu zinajumuisha: -

(i) Ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kV 0.4urefu wa Km. 15.5;

(ii) Ufungaji wa transoforma saba (7) zote za kVA 50;na

(iii) Kuwanganishia umeme wateja wapatao 225.Gharama za kazi hizi zinakadiriwa kuwa shilingi za Kitanzaniamilioni 290.

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana na majibu ya Waziri yanawiana na ukwelihalisia. Ningependa kumwuliza Waziri maswali ya nyongezayafuatayo.

(a) Wananchi wameishapeleka maombi yaopale Kilwa Masoko na wataendelea kupeleka, lakini nilitakakujua kwamba utekelezaji wa miradi hii itaanza lini katikamaeneo kama kule Mkanyageni ambako ni kitongoji, ndaniya hiyo Somanga ambayo tunazungumzia? Vilevile Mitondoambako ni eneo hilo hilo la Somanga, nguzo zipo badohazijatandazwa.

Lini utaratibu huu wa utekelezaji wa miradiutafanyika? Siyo wakati wowote, tunataka kujua lini?

Page 11: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

11

29 APRILI, 2013

(b) TANESCO ina matatizo katika suala la uzalishajina ukusanyaji wa mapato. Nini mpango wa Serikali kuivunjaau kuiboresha pamoja na kuipa mtaji mwingine ili iwezekujiendesha kwa ufanisi?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. CHAWENE): Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katikajibu langu la msingi, nikisema wakati wowote ndani ya mwakahuu ninamaanisha ni logistics za utekelezaji utaratibu wakupata mkandarasi. Lakini pia mobilization na vitu vinginekwa sababu miradi hii ya umeme inahusisha karibu malighafikutoka nje, ikiwa ni transformers na vitu mbalimbali, tuna-dealna suppliers mbalimbali kwa hiyo ndiyo maana jibu langulinakuwa hivyo.

Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na WaheshimiwaWabunge wengine wote wenye miradi ya umeme hiiambayo tumeipanga toka mwaka jana kwamba, itaanzakutekelezwa wakati wowote ndani ya mwaka huu.

Mheshimiwa Spika, swali la pili ni juu ya utendaji kazina ufanisi wa Shirika letu la ugavi wa umeme TANESCOkwamba lenyewe ndilo linalozalisha umeme, kusafirishaumeme na kusambaza umeme.

Hii imekuwa ni ajenda kuu Serikalini na tumekuwatukilifikiria, lakini tumehusisha wadau mbalimbali.

Tumeweka katika Tovuti yetu ya Wizara natumepokea maoni ya watu mbalimbali wasomi na wadauwote kwa ujumla, katika nchi nzima na tumekuwa tukifanyahivyo hata tukipata mawazo ya watu mbalimbali na hatanje ya nchi.

Nia na dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kwambatunaiboresha na kuifanya TANESCO iwe na ufanisi na uamuziwake utatokana na maoni tuliyoyachukua na ushauri wakitaalam juu ya namna gani TANESCO iwe.

Page 12: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

12

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, tumepokea maoni mengi sana nasasa tunayapanga ili tuweze kujua nini tufanye na nini tuamuekulingana na hali ya uendeshaji wa Sekta hii ya nishati katikamaisha ya kisasa ya duniani. (Makofi)

MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMAZINA: MheshimiwaSpika, nakushukuru sana kwa kuniona. Mwaka jana Serikaliya Holland wasaini Mkataba na Serikali ya Tanzania kuenezaumeme Wilayani Ngara, Biharamulo na Mpanda.

Je, utekelezaji wa mradi huo utaanza lini WilayaniNgara?

SPIKA: Jamani hilo ni suala jipya lakini sijui unawezakujibu Mheshimiwa Naibu Waziri. Ni suala jipya sana.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna miradiya kufunga transformer mpya katika Wilaya za Ngara,Biharamulo na Mpanda.

Mheshimiwa Spika, nimtaarifu tu Mheshimiwa Mbungekwamba Kampuni itakayofanya kazi ile imekwishapatikanana shughuli ile itaanza kutekelezwa wakati wowote.Kampuni inaitwa Holiyon na shughuli zile nataka nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba wakati wowote kuanzia sasamnajua tukishaingia kwenye mikataba hii ya utendaji wakazi ni vigumu sana kusema sasa wamefikia wapi ili mradideadline ile tuliyokubaliana kwenye mikataba haijapita basisisi tunabakia kuamini kwamba atatekeleza kwa wakati, lakiniMkandarasi amepatikana.

Mheshimiwa Spika, naomba niwatoe wasiwasiwananchi wa Ngara, Biharamulo na Mpanda kwambatransformer zile zitafungwa mpya na watapata umeme wauhakika. (Makofi)

Page 13: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

13

29 APRILI, 2013

MHE. SUSAN A. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsantesana. Naomba kumwuliza Mheshimiwa Naibu Waziri kwambaWilaya ya Kilombero ina tatizo kubwa sana la kuwekewaumeme hasa katika Tarafa ya Mgeta kwenye uzalishajlimkubwa wa kilimo cha mpunga yenye Kata tano na Katanyingine.

Je, ni lini sasa Serikali itapeleke huduma ya umemekatika Tarafa hiyo ya Mgeta yenye Kata tano na vijiji vingineambavyo ndani ya Wilaya ya Kilombero havina umeme?

SPIKA: Mheshimiwa Mbunge unaamini kabisa hilo nisuala kabisa kabisa. Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati naMadini.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, pengine MheshimiwaSusan Kiwanga alitaka watu wa Kilombero wamsikie, lakinitunazo progamu mbalimbali ambazo Mheshimiwa Mbungeanazifahamu pengine tuwasiliane aweze kujua ni wapi nakuna mradi gani katika maeneo haya aliyoyataja.

Tunazo programu mbalimbali, TANESCOwanasambaza umeme na tuna miradi inayosambazwa naREA na yote karibu nchi nzima tumeweka basi MheshimiwaMbunge tuwasiliane ili aweze kujua programu gani itafanyikakupeleke umeme Kilombero.

SPIKA: Ahsante sana. Kazi kwako uwasiliane naNaibu Waziri huko.

Page 14: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

14

29 APRILI, 2013

Na. 113

Ujenzi wa Barabara ya Mbande – KongwaMpwapwa

MHE. FELISTER A. BURA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara yaMbande – Kongwa - Mpwawa, kwa kiwango cha lami?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziriwa Ujenzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Felister AloyceBura, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, barabara ya Mbande – Kongwa- Mpwapwa- Gulwe Kibakwe , yenye urefu wa Kilometa106.52 ni barabara ya Mkoa inayohudumiwa na Wizara yaUjenzi kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa waDodoma.

Mheshimiwa Spika, barabara hii kwa sasa inafanyiwaupembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Usanifu huuunafanywa na Mhandisi Mshauri aitwaye Inter consult Ltdkwa gharama ya shilingi milioni 499.9.

Kazi hii ilianza mwezi Oktoba, mwaka 2012 nainatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2013. Mara baada yakukamilika kwa usanifu huu, na makisio ya gharama zaujenzi wa barabara kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwaajilil ya kuanza ujenzi wa kiwango cha lami. (Makofi)

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa, barabara hii ahadiya Rais, narudia tena. Kwa kuwa barabara hii ni ahadi yaRais na kwa kuwa Barabara hii ina umuhimu wake kwasababu pale Godegode kuna madini mengi ya copper,kuna rubi na bado kuna gypsum Godegode.

Page 15: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

15

29 APRILI, 2013

Kwa hiyo, barabara hii ina umuhimu wake Kitaifa nakwa kuwa ni ahadi ya Rais naomba kujua kama Serikali ipotayari kuanza ujenzi wa barabara hii kwa mwaka ujao wafedha? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kwanzakabisa nimhakikishie kwa sababu kama anavyojua barabarahii ipo kwenye Ilani na ni ahadi ya Rais ya barabara muhimuna ndiyo maana tumeanza kufanya usanifu.

Kujenga barabara huwezi kuanza kabla hujafanyausanifu, ukishakamilisha usanifu ndiyo unaweza kuanzakujenga. Kwa hiyo, naomba niwape matumaini wananchiwa Mkoa wa Dodoma kwamba barabara hiyo itajengwakwa kiwango cha lami, siwezi kusema itaanza mwakaunaokuja wa fedha kwa sababu kazi bado haijakamilika yausanifu.

Tunatarajia Mkandarasi Mshauri amalize Mwezi Juni,hivyo ndivyo Mkataba ulivyo, lakini inaweza ikafika mweziJulai, inategemea na mazingira ya kazi yenyewe. Kwa hiyo,watakapomaliza Serikali inakuahidi kwamba itatafuta fedhana tutaanza kujenga kwa kiwango cha lami.

SPIKA: Barabara haifanani na nyingine yoyote.Mheshimiwa Laizer.

MHE. LEKULE M. LAIZER: Mheshimiwa Spika, nashukurusana kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa, barabara ya Kamwanga Sanya Juuimefanyia usanifu na kila Bajeti inapangiwa fedha. Je, katikakipindi hiki fedha zilizopangiwa zitaanza kazi au zitapelekwakatika maeneo mengine kama Bajeti zilizopita?

Page 16: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

16

29 APRILI, 2013

SPIKA: Utakumbuka hata hicho kijiji alichokisema.Mheshimiwa Waziri kwa sababu wewe ni fundi tu labda.Kama mtauliza maswali yasiyo yenyewe siwape nafasi yakujibiwa.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, naombanimhakikishie kama fedha ziliishawekwa kwa mwaka huu wafedha 2012 kwa ajili ya kazi ya usanifu hiyo kazi itatekelezwakama ilivyopangwa. Barabara hizi nyingi ambazo tunazifanyiausanifu ni nyingi. Kwa mfano, mpaka sasa kilomita 11,174zinaendelea kujengwa ndani ya nchi hii.

Kwa hiyo, kuna barabara zingine zinajengwa kwakiwango cha lami na nyingine zinafanyiwa usanifu.Tutakapomaliza kazi ya usanifu zote tutaziweka kwenye kundimoja tunazitafutia fedha tunaanza kujenga kwa kiwango chalami. (Makofi)

SPIKA: Haiwezi kufafana na mahali popote,tunaenda Wizara ya Elimu.

Na. 114

Mkataba wa Ajira kwa Nchi za Afrika Mashariki

MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA aliuliza:-

Nchi za Afrika Mashariki zimekubaliana kuridhiaMkataba wa pamoja wa ajira kwa wananchi wake hasavijana.

Je, Tanzania ina mkakati gani wa makusudi wakuwaandaa vijana wake kielimu ili waweze kushindanakatika soko la ajira la Jumuiya ya Afrika Mashariki?

Page 17: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

17

29 APRILI, 2013

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDIalijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimuna Mafunzo ya Ufundi, napenda kujibu swali la MheshimiwaChristowaja Gerson Mtinda, Mbunge wa Viti Maalum, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, naomba kulitaarifu Bunge lakoTukufu kwamba kilichoridhiwa ni Itifaki ya Soko la Pamoja laJumuiya ya Afrika Mashariki na siyo Mkataba wa Ajira waNchi za Afrika Mashariki.

Ndani ya Itafiki hii, sehemu “D” kipengele cha 10sehemu ya 8 kinahusu uhuru wa kufanya kazi nchi nyinginekwa mujibu wa Sheria, Taratibu za Mikataba na kiutawalakwa kila nchi husika.

Hivyo, inapaswa kuzingatiwa kuwa uhuru wa Ajirakwenye Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya AfrikaMashariki unahusu Sekta binafsi na siyo ajira kwenye sektaya umma, isipokuwa kama sheria za nchi husika zinaruhusu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza mikakatimbalimbali katika ngazi zote za elimu kwa nia ya kuwaandaavijana wetu waweze kushindana katika soko la Ajira laJumuiya ya Afrika Mashariki.

Pamoja na utekelezaji wa mipango ya MMEM naMMES, Serikali inatekeleza Mpango wa Maendeleo ya Elimuya Juu (MMEJU) 2010 – 2015 na Mpango wa Maendeleo yaElimu ya Ufundi (MMEU – 2013/2014 -2017/2018) ambapomipango hii kwa pamoja inalenga kuvijengea uwezo VyuoVikuu na Vyuo vya Ufundi ili viweze kuzalisha wataalamwengi ambao watakuwa na uwezo wa kitaaluma nakitaalam kwa kuingia kwenye soko la ajira ndani na nje yanchi. (Makofi)

Page 18: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

18

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, Serikali pia inatekeleza Mpangowa Sayansi na Teknolojia na Elimu ya Juu unaogharamiwana Benki ya Dunia (2009-2013) wenye lengo la kuvijengeauwezo Vyuo Vikuu vyote vya Umma katika maeneo yaRasilimali watu na Miundombinu ili viweze kuzalishawataalam wa Sayansi na Teknolojia wenye uwezo wakuingia kwenye soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Vilevile, Serikali imeanzisha Taasisi ya Teknolojia yaNelson Mandela, Mbeya University of Science andTechnology pamoja na kuimarisha Taasisi za Sayansi naTeknolojia za Dar es Salaam na Arusha. (Makofi)

MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA: Mheshimiwa Spika,ahsante. Pamoja na majibu ya Naibu Waziri, nina maswalimawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, katika jibu la msingi Serikaliimeonyesha mkakati mkubwa wa kuwaandaa wataalamwake hasa katika Vyuo Vikuu kwenye eneo la Sayansi kulikofani zingine.

Je, Serikali inawaambia nini Watanzania kwamba nikwa kiwango gani imewaandaa vijana wake katika fani zaUhasibu, uchumi, utalii na nyinginezo ili waweze kushindanana wenzao ukizingatia ukweli kwamba Bodi ya Mikopo haitoimikopo kwa wanafunzi waliochukua fani hizo?

Swali la pili, Serikali inaweza kuwaambia vijana waKitanzania ni maeneo gani ambayo imehifadhi ajira hizi katikasekta binafasi hasa ukizingatia ukweli kwamba katika sektaya Utalii hususan kwenye mahoteli makubwa ya Kitalii niWakenya tu ndiyo wamejaa wakifanya kazi hizo? Ahsantesana. (Makofi)

Page 19: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

19

29 APRILI, 2013

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, swali la kwanza Mheshimiwa Mbungeanauliza kwamba Serikali imejikita sana kufundisha programuza Sayansi na Teknolojia katika Vyuo Vikuu. Suala hili ni kwelikabisa kutokana na ulimwengu wenyewe jinsi unavyoendakwa sasa hivi. Wote hapa hata Waheshimiwa Wabungetunakubaliana kabisa kwamba tunahimiza kusoma masomoya Sayansi i l i tuweze kukimbizana na hali ya duniainavyoenda.

Lakini siyo kwamba tumeacha hizi programu zingine.Kwa sababu Vyuo Vikuu wanajiandalia Curriculum wenyewekwa hiyo, vyuo vingi tunavyo Vyuo Vikuu vya Uhasibu hatahapa Tanzania vinavyotoa programu hizo.

Lakini vilevile tunatoa programu za Kiuchumi, tunatoaprogramu za Kitalii kama ambavyo Mheshimiwa Mbungeamejaribu kuvi-mention. Lakini sasa sana sana niendeleekusisitiza kwamba bado tunatoa Sayansi na Teknolojia ndiyokitu kikubwa sana kinachoendana pamoja na nchi nyinginehapa duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunaandaa sera mpya ya elimuambapo tarehe 19 Mei, 2013 tutakuja tuwapitishe kwenyerasimu mpya ya Sera. Kwa hiyo mambo yote mtakujakuyaona humo.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mheshimiwa Mbungeanasema kwamba vijana wengi na hasa Sekta ya Utaliikwenye mahoteli makubwa wanaajiriwa kutoka Kenya tu nasiyo Tanzania. Linaweza kuwa na ukweli au lisiwe na ukweli.

Lakini ni kwamba kama nilivyosema kwenye swalilangu la msingi kwa sekta binafsi tumeridhia Itifaki kwambaWakenya wanaweza kufanya biashara Tanzania,Watanzania wanaweza wakafanya biashara Kenya, kwaWaganda wanaweza wakafanya biashara Rwanda,Warwanda wanaweza wakaenda Burundi.

Page 20: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

20

29 APRILI, 2013

Kwa hiyo, siyo ajabu sana kuwaona Wakenyawanakuja kufanya kazi Tanzania na hasa katika sekta binafsi.

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana. Kwa kuwa, umoja wetu wa Afrika Masharikitunashikiriana kwa mambo mbalimbali isipokuwa ajira zavijana kama alivyoeleza Mheshimiwa Naibu Waziri kwenyemajibu yake. Kwa kuwa, vijana wetu wengi wamesoma naajira nchini bado ni chache.

Je, Serikali haiwezi kuliweka hili mezani katika Umojawetu wa Afrika Mashariki ili waweze kulijadili kuona namnaya vijana wetu watapata ajira Afrika Mashariki kwa ujumla?

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika,alichokiongea Mheshimiwa Diana Chilolohapa ni kweli kabisa na katika vikao vyetu vya East AfricaCommunity vinaendelea kujadiliana na linaendeleakufanyiwa kazi. Lakini naomba vilevile tuchukue ushaurikwamba labda tulifanyie kazi kwa haraka zaidi. (Makofi)

Na. 115

Madai ya Fidia kwa Kampuni ya KamweneWoodworks

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA (K.n.y. MHE. JOYCE J.MUKYA) aliuliza:-

Kuwekuwepo na madai ya muda mrefu kwa Kampuniya Kamwene Woodworks kwa Wizara ya Maliasili na Utaliitangu mwaka 1979 juu ya fidia ya hasara iliyosababishwana Serikali, madai ambayo pamoja na Mamlaka za Serikalina Tume zilizoundwa kuafiki uhalali wa malipo hayo, badowahusika wameendelea kuzungushwa:-

Page 21: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

21

29 APRILI, 2013

Je, ni lini Serikali italipa madai ya Kampuni yaKamwene Woodworks?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, naombakujibu swali la Mheshimiwa Joyce John Mukya, Mbunge waViti Maalum, kama ifuatavyo:-

Kampuni ya Kamwene Woodworks ina nia yakuishtaki Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii wakidaijumla ya shilingi 556,510,000/= kama fidia ya magogo nambao vilivyotaifishwa na TANAPA mwaka 1979 hukoMorogoro baada ya kukamatwa ndani ya Hifadhi ya Taifaya Mikumi.

Mheshimiwa Spika, kimsingi, suala hili kwa upandewa Wizara lilishamalizika tangu mwaka 2000 baada ya madaiyao kufungwa na Kampuni hiyo kulipwa fidia ya jumla yashilingi 5,468,280/=.

Hivyo, ushauri uliotolewa na ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali kwa kampuni kulipwa “simple interest”pamoja na fidia ya magogo 65 na mbao vipande 4,100ulitolewa bila kupata maoni na mapendekezo ya Wizara.

Hata hivyo, Wizara ilishatoa msimamo kuwa madaiyao hayana msingi na hawastahili kulipwa fidia yoyote zaidiya malipo ambayo wamekwishalipwa.

Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 3(1) kikisomwakwa pamoja na sehemu ya kwanza ya jedwali ya sheria yaUkomo wa Muda (The Law of Limitation Act) Sura ya 89 R.E.2002 vinatoa mwongozo juu ya ufunguzi wa mashauri baadaya ukomo wa muda kupitia ambao ni miaka 3 tangu tareheya maamuzi kutolewa yawe dismissed.

Page 22: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

22

29 APRILI, 2013

Hivyo kwa vile maamuzi ya kulipwa kampuni husikayalishafanyika, walipaswa kutoa malalamiko yao yakutoridhika na fidia hiyo na kuonyesha nia yao ya kuishtakiSerikali ndani ya kipindi cha miaka mitatu na si vinginevyo.

Mheshimiwa Spika, Serikali haina mpango wa kuilipakampuni ya Kamwene Woodworks kwa vile kampuni hiyohaikufungua kesi ndani ya muda uliopo kisheria.

Hii ina maana waliridhika na msimamo wa Serikalibaada ya kulipwa kwa kiasi kilichotajwa hapo juu. Kwasasa kampuni inachojaribu kufanya ni kuleta usumbufuambao hauna tija yoyote kwani suala hilo lilishamalizwana Wizara. (Makofi)

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi. Nina maswali mawili yanyongeza.

Swali la kwanza, Naibu Waziri amesema kwambawalipata ushauri kutoka kwa Mwanasheria na kisha mnasemaMwanasheria hakupata maoni na mapendekezo kutokaWizarani. Mwanasheria alijuaje kama kuna tatizo laKamwene Woodworks kama hamkupelekea mapendekezomliyokuwa nayo?

Swali la pili, kwa kuwa, kipaumbele cha Serikaliyoyote ni maslahi ya watu wake, utu wa watu wao.

Je, Wizara haijaribu kutumia udhaifu wa wananchiwao ambao hawajui sheria kukwepa mwanya wa kuwalipamadai ambayo Kamwene Woodworks inadai?

Page 23: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

23

29 APRILI, 2013

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, moja, kwa mujibu wa Sheria ya Misitu, Sura Na. 323 yaMwaka 2002, maeneo yote ambayo yamehifadhiwa ikiwani pamoja na Hifadhi zote za Taifa na Misitu ya Lindimajiinajulikana kama Catchment Area kwa Kiingereza na hifadhiasilia (Natural Reserve) na ningeweza kutaja mojawapo kamaAmani, Uluguru, Kilombero na kadhalika; maeneo haya nimarufuku mtu yeyote kukata mti ndani ya maeneo ya hifadhi.Kimsingi, Serikali inapenda kusisitiza Kamwene Woodlandwalil ipwa kimakosa na ingekuwa sasa hivi badotusingewalipa na tunarudia mtu yeyote atakayekamatwaanakata miti katika Hifadhi zetu za Taifa, hata leotukimkamata tutamfungulia mashtaka na tutamfunga.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Serikali inajali sanawatu wake na ingependa matumizi ya rasilimali hizi tulizonazoziwe rasilimali endelevu. Nchi yetu miti inapotea, jangwalinaingia kwa kasi na hii ni kutokana na watu ambaowanavunja sheria makusudi, wanafanya wanavyofanya nawanarejea kwa Serikali iwalipe, hatuko tayari tena kufanyahivyo.

Na. 116

Kuanzisha Mamlaka ya Hifadhi ya Mapori ya Akiba

MHE. JOHN P. LWANJI aliuliza:-

Serikali ilishaahidi kuanzisha Mamlaka itakayosimamiaHifadhi ya Mapori ya Akiba ya Wanyamapori badala ya Idaraya Wanyamapori:-

Je, ahadi hiyo itatekelezwa lini?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasilina Utalii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa John Paul Lwanji,Mbunge wa Manyoni Magharibi, kama ifuatavyo:-

Page 24: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

24

29 APRILI, 2013

Ahadi ya Serikali ya kuanzisha Mamlaka yaWanyamapori iko palepale na kwa sasa Rasimu za Kwanzaya Sheria ya Uanzishwaji wa Mamlaka, Muundo na Majukumuya Mamlaka na Mapendekezo ya Marekebisho ya Sheria yaWanyamapori Na. 5 ya 2009 zimekamilika. Hatua iliyobaki niwadau kujadili na kutoa maoni yao kuhusu rasimu hizo.

Mheshimiwa Spika, katika Mkutano wa Nane waBunge hili, Serikali iliahidi kuwa ifikapo Desemba mwaka 2012,mchakato wa uanzishwaji wa Mamlaka ya Wanyamaporiutakuwa umekamilika. Hata hivyo, baada ya Kamati yaUanzishwaji wa Mamlaka kupata maoni ya wadau, iligunduauwepo wa mambo muhimu yaliyohitaji kujadiliwa kwa kina.Kufuatia hatua hiyo, mpango kazi ulipitiwa upya ili kupanuawigo wa majadiliano na kushirikisha wadau wengi zaidi katikakujadili rasimu za sheria hizo. Kutokana na kupanuka kwawigo wa wadau, kazi hii itakamilika ifikapo mwezi Novemba,2013.

MHE. PAUL J. LWANJI: Mheshimiwa Spika, ahsante.Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninamaswali mawili ya nyongeza.

(i) Ahadi hii imedumu muda mrefu toka Bungela Tisa na si Mkutano wa Nane tu na sasa hivi tunaambiwakwamba hii Kamati ya Uanzishwaji wa Mamlaka pamoja nawadau wanajadili mambo muhimu. Je, Naibu Wazirianaweza kutueleza mambo hayo muhimu ni nini kiasi chakuchelewesha mambo hayo kwa muda mrefu kiasi hicho?

(i) Kutokana na ucheleweshaji wa kuanzishaMamlaka hizo Mapori yetu ya Akiba hasa yale ya Rungwa,Kizigo na Muhesi, yanaendeshwa kwa tabu na Watumishi waIdara ya Wanyamapori. Licha ya Serikali kupata mapatomakubwa kutoka mapori hayo, lakini Watumishi wa Maporihaya wanashindwa kupata stahiki zao kama vile posho,hawana nyenzo za kufanyia kazi na mambo menginemuhimu. Je, katika kipindi hiki mpaka kufikia kuanzishwa kwaMamlaka haya Wizara au Serikali inachukua hatua gani za

Page 25: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

25

29 APRILI, 2013

dharura kujaribu kuwakwamua hawa watumishi wanaofanyakazi katika mazingira magumu kiasi hicho?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, ahadi hii ya Serikali tunafurahi kusema kwamba,pamoja na muda wote ambao imechukua, sasa inakwendakukamilika. I l ikuwa ni muhimu sana Serikali kupitiachangamoto zote zilizopo katika tasnia ya uhifadhi, ilikuwani muhimu sana kuwashirikisha wadau wote kwa undani ilituweze kuhakikisha kwamba, Sheria hii ambayo tutaianzishana Mamlaka hii ambayo tutaianzisha itakuwa Mamlakaendelevu, itakayoweza kujiendesha kimfumo, kifedha nakiutekelezaji kwa majukumu ambayo kwa kweli ni makubwasana.

Mheshimiwa Spika, la pili ni kweli kwamba, tunachangamoto ya watumishi wanaofanya kazi katika maporiya akiba nchi nzima. Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utaliiametembelea baadhi ya hayo mapori, amenituma miminimetembelea baadhi ya hayo mapori, tumezungumza naaskari, tumeona maisha ambayo wanaishi na Serikaliinachukua hatua zifuatazo za makusudi na za dharura wakatitunamalizia mchakato huu wa uanzishwaji wa Mamlaka:-

Kuanzia Julai, Wizara yangu imepata kibali cha kuajiriwafanyakazi wapya 400 katika tasnia hii ya uhifadhi natunategemea wafanyakazi hao wote watakuwa wawanyamapori. Kwa hiyo, kama ambavyo Mheshimiwa Wazirialiwaahidi vijana pale Pasiansi na kama alivyonitumanikawaahidi pale Mweka, tunategemea kufanya kilatuwezalo ili ajira hii ipatikane, vijana hawa washiriki katikaulinzi wa maeneo yetu ya hifadhi.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, kwanza,naomba turekebishe suala la kuanzishwa kwa Mamlaka yaWanyamapori siyo ahadi ya Serikali ni maamuzi ya Bungeambayo yalifikiwa kwenye mjadala wa kuandikwa kwa Sheriaya Wanyamapori mwaka 2009. Kwa hiyo, Serikaliinapochelewa kuanzisha Mamlaka haya maana yake nikwamba, inachelewa kutekeleza maamuzi ya Bunge.

Page 26: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

26

29 APRILI, 2013

Sasa napenda Mheshimiwa Waziri alieleze Bunge hilini lini Mamlaka hii itaanza kazi rasmi kwa sababu kutokuwepokwa Mamlaka hii ya Wanyamapori kunapelekea tembowengi sana kuuawa kwenye maeneo ambayo siyo ya hifadhi.Maeneo ambayo tembo wanakufa wengi ni ya nje ya hifadhizinazomilikiwa na TANAPA na kadhalika. Kwa hiyo, naombanijue ni lini sheria hii itakuja ili Mamlaka ianze kazi tulindetembo wetu?

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika,kwanza, nashukuru kwa majibu mazuri ambayo Naibu Waziriameyatoa. Kuhusu mamlaka ni kweli tunatambua kwambahilo...

SPIKA: Inaonekana husikiki labda usogee mbelemaana ni majibu yako. Sogea mbele hapa wanalalamika,ndiyo unayepaswa kujibu.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika,kwanza, namshukuru Naibu Waziri, kwa majibu mazurialiyoyatoa. Kuhusu suala hili la msingi niseme kwamba,tunatambua na tunazingatia kwamba haya yalikuwa nimaamuzi ya Bunge kwamba Mamlaka ya WanyamaporiTanzania iwepo. Kwa kweli nikiri kwamba, imechelewa, lakininataka nimhakikishie na nilihakikishie Bunge lako Tukufukwamba, azma yetu ifikapo Bunge la Novemba, tutailetahapa ili iweze kupitishwa na baada ya hapo iweze kufanyakazi.

MHE. KAIKA S. TELELE: Mheshimiwa Spika, ahsante.Kwa kuwa TANAPA imeendesha semina mbalimbali hivikaribuni katika Kanda mbalimbali hapa nchini; Kanda yaKaskazini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati na wadauwanaozungumzwa wamejadili sana suala hili la kuanzishwaMamlaka. Sasa ni wadau wengine gani tena wanasubiri ilijambo hili liweze kuanza?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, ni kweli Wizara imeshirikisha wadau wengi.Tumezungumza na Taasisi zetu ikiwa ni pamoja na TANAPA

Page 27: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

27

29 APRILI, 2013

na Wananchi ambao wanayazunguka maeneo ya uhifadhi.Niseme tu kwamba, wigo wa wadau ambao ni lazimakutokana na umuhimu wa hii sheria wafikiwe ni mkubwa natutakumbuka kwamba kuna baadhi ya mapori ya akibaambayo yanapakana; kwa mfano, na nchi ya Msumbiji natuna maeneo ambayo eco-systems zinaingiliana. Kwamfano, eco-systems kati ya Tanzania na Kenya, kati yaTanzania na Rwanda na tumeona kwa kufanya hivyo, sheriahii itakuwa yenye tija, itakuwa ina nguvu na ni matumainiyangu kwamba, kama alivyosema Mheshimiwa Waziri, sheriahii inakamilika mwaka huu mwezi Novemba na nimwombetu Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wote, tushirikianetuhakikishe tunaipitisha itakapokuja hapa Bungeni.

Na. 117

Vitambulisho vya Kupiga Kura Kutotambulika Zanzibar

MHE. RUKIA KASSIM AHMED aliuliza:-

Kwa kuwa Zanzibar na Tanganyika ndiyo vinafanyaJamhuri ya Muungano wa Tanzania:-

Je, kwa nini vitambulisho vya kupigia kura vya Jamhuriya Muungano wa Tanzania havikutumika Zanzibar katikaUchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muunganowa Tanzania?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBUNA BUNGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa WaziriMkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Rukia KassimAhmed, Mbunge wa Viti Maalum Zanzibar, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, sababu dhahiri i l iyofanyaVitambulisho vya Kupiga kura vya Jamhuri ya Muungano waTanzania kutotumika Zanzibar katika Uchaguzi wa Wabungewa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mashartiya Kifungu cha 12A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya

Page 28: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

28

29 APRILI, 2013

343, iliyorekebishwa mwaka 2010. Kifungu hicho kinaitakaTume ya Taifa ya Uchaguzi kutumia Daftari la Wapiga Kuralililoandaliwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa Uchaguziwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwaupande wa Tanzania Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, swali hili limekuwa likiulizwa marakwa mara hapa Bungeni na hata mwuliza swali amewahikuniuliza hata na mimi kwenye Kamati ya Katiba na Sheriana Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi alikuwepo na hatakwenye vikao mbalimbali vya Kamati ya Bunge. Napendakuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge kuwa, suala hilinaamini litaangaliwa upya mara baada ya kupitisha Katibaambayo itakuwa imeweka utaratibu wa kuunda Tume yaTaifa ya Uchaguzi.

MHE. RUKIA KASSIM AHMED: Mheshimiwa Spika,pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, lakini natakanimwulize:-

(i)Je; Mheshimiwa Waziri hii huioni kama inapinganana Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani sheriambili zinatawala suala la Muungano na ambapo Katiba yaZanzibar peke yake haiwezi kutumika kwa masuala yaMuungano; je, hili hujaliona?

(ii)Kwa kuwa Katiba zote mbili zipo na suala hili lipokaribu vipindi vinne vya Uchaguzi. Je, Mwanasheria Mkuualikuwepo wapi au linafanywa kwa makusudi na Serikali zotembili kuwanyima Wazanzibari haki yao ya kuwachaguaWabunge? (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBUNA BUNGE): Mheshimiwa Spika, kwa Zanzibar kwa wakati uleilikuwa ni lazima itumike Sheria hii kwa sababu Zanzibar wanaSheria zao nyingine. I l i mtu apige kura kule, wanaVitambulisho Maalum vya Uzanzibari. Uhalali wa kupiga kurakwanza lazima uwe Mzanzibari. Sasa sisi huku watu wa Barana Sheria hii ya Bara haiwezi ku-define nani Mzanzibari, Sheriaya Zanzibar ndiyo iliyo-define nani ni Mzanzibari.

Page 29: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29

29 APRILI, 2013

Kwa hiyo, ukiwa katika Territory ya Zanzibar, utapigakura kwa Sheria ya Zanzibar, kwa sababu Zanzibar ndiyo iliyo-define nani Mzanzibari mwenye haki ya kufanya uchaguzikwa chaguzi zote. Hivyo ndivyo ilivyo. Kwa hiyo, naombatena Mheshimiwa Mbunge kwamba, najua hili linawakwazasana, mngependa sheria zote mbili zitumike lakini sheria kwasheria kule na Katiba ya Zanzibar kule mnakoishi hairuhusuhili. Kule wanataka mpige kura zote za ndani ya Zanzibarkwa mujibu wa sheria ile na mwoneshe Vitambulisho vyaUzanzibari ndiyo masharti ya msingi.

Kwa kuwa Katiba sasa tunaiandika upya, tuvutesubira, Mheshimiwa Rukia Kassim Ahmed, mimi najua yotehaya yameshaonekana ndiyo mambo ambayo tutawezakuyarekebisha kwenye Katiba hiyo mpya.

Na. 118

Upigaji wa Kura Siku ya Jumapili

MHE. MCH. ASSUMPTER N. MSHAMA aliuliza:-

Je, Serikali haioni kuwa kitendo cha kupanga kupigakura katika Chaguzi za Kitaifa Siku za Jumapili kinasababishaWatanzania ambao ni waumini wanaoabudu siku hiyokushindwa kupiga kura kwa sababu wanakuwa kwenyeibada jambo linalowanyima haki yao ya Kikatiba?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBUNA BUNGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa WaziriMkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa MchungajiAssumpter Nshunju Mshama, Mbunge wa Nkenge, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Sheria za Uchaguzi pamoja naKanuni zake, hazitaji wala haziainishi siku maalum iliyoteuliwakwa ajili ya upigaji kura. Uamuzi wa Serikali kuteua Siku yaJumapili ulitokana na sababu kuwa ni siku ambayo

Page 30: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

30

29 APRILI, 2013

Watanzania walio wengi hawaendi makazini na hivyo kuwana fursa nzuri ya kushiriki katika zoezi la upigaji kura. Serikaliinatambua kwamba, Siku ya Jumapili waumini wengi waMadhehebu ya Kikristo huitumia kwenda kuabudu, lakini piahuweza kupata fursa ya kupiga kura kwa vile mudaunaotengwa kwa ajili ya zoezi la upigaji kura unachukua saachache kuanzia asubuhi inachukua kama saa tisa hadi kumikatika siku moja uchaguzi umeshakuwa umekamilika.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, swali hili la MheshimiwaMbunge limejitokeza sana. Sisi tumeshuhudia katika mijadalambalimbali iliyotolewa na watu mbalimbali wakiwemowaumini wa dini hizi, wametoa maoni yao katika marekebishoya Katiba. Kwa hiyo, tunaamini kwamba kutokana na maonimbalimbali yaliyotolewa na waumini na Watanzaniakwamba siku za ibada zisitumike, pengine Katiba mpyaitakuja kurekebishwa au Sheria ya Tume ya Uchaguzi itakujakurekebishwa kufuatia maoni ya Katiba mpyayatakavyoletwa na kupitiwa na Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, namwombaMheshimiwa Mshama, asubiri kwa sababu jambo hililimesemewa sana na waumini. Najua hata waumini waKiislam wasingependa Ijumaa itumike, waumini wa Kikristowasingependa itumike Jumapili. Kwa hiyo, tuvute subirapengine wakati wa marekebisho ya Sheria hii ya Uchaguziambayo itafuatiwa na mahitaji ya marekebisho ya KatibaMpya, hili nalo litaangaliwa ili angalau tutafute siku mwafakakwa Watanzania wote ya upigaji wa kura.

MHE. MCH. ASSUMPTER N. MSHAMA: MheshimiwaSpika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi niulize maswalimawili ya nyongeza.

(i)Kwa kuwa kupiga kura Jumapili siyo suala la Kikatibana ukiangalia katika Katiba yetu sidhani kama imeandikwa;bado ninaiuliza Serikali lini itafanya badiliko kusudi watu wengiwaweze kushiriki kupiga kura ukizingatia kwamba katikakupiga kura watu wanakuwa na mambo mawili muhimu;

Page 31: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

31

29 APRILI, 2013

kuabudu au kupiga kura; mtu anachagua jambo mojaanalifanya na lingine linakosa nafasi?

(ii)Kwa kuwa nchi jirani ya Kenya ambayo juzi tuimepiga kura siku ya kawaida na ikawa Public Holiday; haionini vyema tu kutamka kabisa kwamba hiyo siku iachwe kamaalivyokiri mwenyewe kwamba ni siku ambayo watu wengiwamelalamika ili watu wengi wapige kura ukizingatiawanaojiandikisha na wanaopiga kura ni vitu viwili tofauti?Naomba kuwasilisha.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBUNA BUNGE): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswalimawili ya nyongeza ya Wabunge wote waliosimama pamojana Mbunge wa Tunduru, najua anataka kuuliza nini nawengine wote waliosimama, napenda kujibu maswali yaokama ifuatavyo:-

Nataka kulihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba ...

SPIKA: Naomba mjibu Mheshimiwa Mshama tutafadhali.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBUNA BUNGE): Ehee!!! Nimeoteshwa maswali yao.

Napenda kumjibu Mheshimiwa Mbunge naWaheshimiwa Wabunge kwamba, Tume ya Uchaguziinaamini Katiba hii italazimisha kuandikwa upya Sheria yaTume ya Uchaguzi. Ingawa haya mambo anayoyasemahayapo kwenye Katiba, lakini kwa makubaliano na mawazoyanayoendelea ndani ya nchi hivi sasa, jambo hili tunaaminilitarekebishwa. Kwa hiyo, ni lini tutarekebisha ni pale wakatiukifika wa kuja kutunga au kurekebisha ya Tume ya Uchaguzina jambo hili tutalirekebisha pia.

Page 32: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

32

29 APRILI, 2013

Na. 119

Viwango Vinavyostahili Kulipwa na Wawekezaji wa Zao la Katani

MHE. HERBERT J. MNTANGI aliuliza:-

Kumekuwapo na utata juu ya wawekezaji wa Zao laKatani kulipa ushuru stahili kwa Halmashauri ya Wilaya yaMuheza;-

Je, ni viwango gani stahili ambavyo wawekezaji haowanapaswa kulipa kwa Halmashauri husika?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa WaziriMkuu, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Herbert Mntangi,Mbunge wa Muheza, kama ifuatavyo:-

Mamlaka za Serikali za Mitaa zimepewa madarakana Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290, Toleo la2002, kutoza ushuru na kodi mbalimbali kwa madhumuni yakuziwezesha Mamlaka hizo kutekeleza majukumu yakeipasavyo, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za jamii kwaWananchi walio katika maeneo yao. Kwa upande wa ushuruwa mazao, Halmashauri za Wilaya zimepewa madaraka yakutoza ushuru wa mazao chini ya kifungu cha 7(g) cha Sheriaya Serikali za Mitaa, Sura 290. Ushuru huu hulipwa na mnunuzina hutozwa mahali ambapo zao linazalishwa na kwa bei yamkulima, yaani bei ya zao kabla ya kuongezwa thamani.

Sheria hii ilifanyiwa marekebisho mwaka 2010/2011,ambapo sasa kiwango cha kutoza shuru wa mazao shambanikilipitishwa kuwa ni kuanzia asilimia tatu hadi asilimia tano yabei ya kuuza mazao shambani ili kuziwezesha Halmashaurikupata mapato ya ndani. Kwa upande wa ushuru wahuduma, yaani service levy, kifungu cha 7(z) cha Sheria yaFedha za Serikali za Mitaa, Sura 290, kinazipa uwezo

Page 33: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

33

29 APRILI, 2013

Halmashauri za Wilaya kutoza ushuru wa huduma kwawafanyabiashara kwa kiwango kisichozidi asilimia 0.3 yamauzo (turnover) ya mfanyabiashara baada ya kulipa kodiya ongezeko la thamani.

Mheshimiwa Spika, kwa mantiki hiyo,wafanyabiashara wote wa Zao la Mkonge wanatakiwakulipa ushuru wa mazao, yaani produce cess, ambao nikuanzia asilimia tatu hadi asilimia tano kwa mujibu wa Sheria.Aidha, wasindikaji wa Zao la Mkonge wanatakiwa kwa mujibuwa Sheria kulipa ushuru wa huduma ambao ni asilimia 0.3 yamauzo baada ya kulipa ongezeko la thamani na exerciseduty.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Spika,pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Waziri, ninamaswali mawili ya nyongeza:-

(a)Kwa kuwa tangu mwaka 2002 Wafanyabiasharawa Zao la Mkonge hawalipwi ushuru wa mazao kamaambavyo Sheria inahitaji; ni nini kauli ya Serikali kuhusiana nasuala hili?

(b)Kwa kuwa imethibitika bila shaka kuwawafanyabiashara hawa wamekuwa wakikiuka kulipa kodi nakwamba mashamba mengi sasa yametelekezwa. Je, Serikaliipo tayari kufanya uamuzi wa haraka wa kufuta hati zamashamba haya ili Wananchi waweze kupatiwa ardhi hii?

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Spika,mapendekezo ya Wilaya Mkingaya kufutwa Hati Miliki ya Maashamba yaliyotelekezwa katikaWilaya ya Muheza na Mkinga yamekwishapokelewa nabaada ya uhakiki kufanyika yamewasil ishwa kwaMheshimiwa Rais kwa ajili ya uchambuzi wa mwisho nahatima yake kupata kibali chake cha kufuta Hati Milikihizo.Tunafuatilia hilo kwa kushirikiana na watendaji wa Ikuluili kuweza kukamilisha taratibu zile ambazo zinatakiwa ili

Page 34: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

34

29 APRILI, 2013

kumuwezesha Mheshimiwa Rais kufuta Hati Miliki hizo nabaadae tutawasiliana na uongozi wa Mkoa baada yakupata kibali cha Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, tunaomba Mheshimiwa Mbuungepamoja na Wananchi wa Mkinga na wa Muheza waendeleekuwa na subira wakati taratibu hizo zinakamilishwa.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika,ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa DunstanKitandula, kama ifauatavyo:-

Alitaka kauli kwa kutokulipwa ushuru kwa wakulimawa Zao la Katani toka mwaka 2002, kwa mujibu wa Sheria,Halmashauri zinazo uwezo na haki ya kwenda Mahakamanina kuwashtaki wale wote ambao wamekataa kulipa ushuruambao ni haki kulipwa kwa Halmashauri husika.

MHE. JOHN M. CHEYO: Mheshimiwa Spika, kwa kuwakatika msimu wa pamba mwaka jana kule Bariadi Mkuu waMkoa aliwaambia Bariadi Council kuwa walipwe baada yamsimu na mpaka leo hii hawajalipwa karibu bilioni moja nalaki tisa. Je, Mheshimiwa Waziri unatoa ushauri gani sasa ilikuhakikisha kuwa ile amri ambayo imeleta hiyo hasarainafidiwa mara moja?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika,ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Cheyokuhusu ushuru wa Halmashauri ya Bariadi; ni kweli alipotoaamri ile niliwasiliana na Mkuu wa Mkoa na ninakamwambiakuwa ahakikishe ushuru huo unalipwa katika Halmashauri.

Ninaomba pia nichukue fursa hii kuwaagiza walewote kuwa ushuru wa Halmashauri ni haki na katu tusivunjeSheria, kwa mujibu wa maelekezo yaliyopo; na ninaombaMkuu wa Mkoa husika azisaidie Halmashauri kupata ushuruwake kama ilivyokusudiwa. Kwa sababu nilimtahadhalishamwanzo kuwa huenda kwa kuweka mwisho Halmashauri

Page 35: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

35

29 APRILI, 2013

zisipate ushuru na yeye mwenyewe alinihakikishia; kwa hiyo,ninaomba aendelee kusimamia ahadi yake aliyoitoa iliHalmashauri zipate ushuru wao.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, muda umekwisha,kwa hiyo, ninaomba nitoe matangazo ya kazi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikaliza Mitaa, Mheshimiwa Rajab Mohamed, anaombaniwatangazie Wajumbe wa Kamati yake kuwa, leo saa narobo mchana, watakuwa na kikao chao Ukumbi Namba 227.Mheshimiwa Mnyika.

MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.

SPIKA: Nilishamwita mtu mwingine.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Spika,ninashukuru. Ninaomba kutoa hoja kwa mujibu wa Kanuniya 55(3)(f) kuhusu jambo linalohusiana na haki za Bungeambazo ninaamini ...

SPIKA: Kanuni namba gani?

MHE. JOHN J. MNYIKA: Kanuni ya 55(3)(f) kuhusu jambolinalohusiana na haki za Bunge, ambalo ninaamini kwa kadiriya umuhimu wake, Waheshimiwa Wabunge wenzanguwataniunga mkono. Alhamisi, siku ya maswali kwa Waziri Mkuunilimwuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu.

SPIKA: Ujue kuwa hii haihusu haki za Mbunge, haihusikihiyo sasa uliza hoja yako.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Hoja yangu inahusu haki zaBunge kufuatia habari iliyoandikwa na gazeti la jana laJambo Leo, Sakata la Jairo, Serikali yakamilisha Ripoti yake,Bunge lachambuliwa kama karanga, Ripoti yaozea mikononimwa Spika, Serikali yakumbushwa ya RICHMOND, yaaniBunge lachambuliwa kama karanga na Ripoti yaozeamikononi mwa Spika.

Page 36: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

36

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, ninaamini jambo hili linahusu Hakiza Bunge kwa sababu nilipomwuliza swali Waziri Mkuu juu yaRipoti hii, Waziri Mkuu alitoa jibu kuwa, bado Ripotihaijawasilishwa kwa Bunge. Nilipomwuliza lini ripotiitawasilishwa kwa Bunge, Mheshimiwa Waziri Mkuu alijibuwakati wowote kuanzia sasa. Kwa mujibu wa gazeti hili,inaonesha Ripoti ilishawasilishwa kwa Spika muda mrefu sanana imekaliwa kwa Spika mpaka inaozea mikononi mwa Spikana kwamba Ripoti hiyo imelichambua Bunge kama karanga.Sasa ningependa kutoa hoja kuhusiana na haki ya Bungekupewa taarifa.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, alisema kuwa Bungehalijapewa taarifa; sasa ukweli ni upi hasa kwamba WaziriMkuu tarehe 25 hakusema taarifa ya ukweli kwamba alikuwaameshaleta taarifa kwako lakini haijafika kwa Wabunge?

Nia ya kutoa hoja hii ni ili Wabunge tujadili nahatimaye tupitishe Azimio la kuiwekea muda Serikali nakuuwekea muda Uongozi wa Bunge ili katika Mkutano huuwa Bunge katika kipindi cha tarehe saba mpaka tarehe kumina mbili Juni, ambayo shughuli za kawaida za Serikalizitasimama, shughuli za Bunge zitaendelea, basi taarifa hiiiweze kuwasilishwa Bungeni na Wabunge tuweze kuijadiliikiwemo kujadili hizi habari za kwamba taarifa hiyo tuone kwaukweli na uwazi.

Kama ni ukweli kuwa hiyo Taarifa imelichambuaBunge kama karanga, na kama ni ukweli vilevile kwambaTaarifa hiyo imekaliwa na Spika muda wote huo bilakuwasilishwa; ninaomba kutoa hoja kuwa jambo hili lijadilikama jambo la haki za Bunge na ninaomba WaheshimiwaWabunge mniunge mkono.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja.

SPIKA: Na hoja hii siikubali, naomba mkae chini.Siikubali kwa sababu hakuna wakati wowote Bunge linafanyakazi na magazeti; la kwanza. (Makofi)

Page 37: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

37

29 APRILI, 2013

Angefanya utaratibu huyu kuwa hilo gazeti namaamuzi yameshatolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu kuwaataitoa hiyo taarifa, mimi kama Spika, ninakataa sina taarifaya namna hiyo. Sasa mimi siwezi ku-operate na magazetiambayo mara nyingi yanasema uwongo juu ya mambomengi. Kwa hiyo, siwezi kufanya kazi kwa kufuata magazeti.(Makofi)

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2013/2014Wizara ya Maji

(Majadiliano yanaendelea)

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa,ninaomba kuwafahamisha Waheshimiwa Wabungekwamba, katika tatizo la maji na ufinyu wa bajetiulivyoelezwa, Serikali imelitizama tatizo hili na kuangalia kwaumakini hoja za Waheshimiwa Wabunge na kutazamaumuhimu wa maji kwa Wananchi wetu na kuungana na hojaza Waheshiwa Wabunge, kuwa tatizo la maji tulipekipaumbele zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, katika kutoa kipaumbele zaidikwa upande wa maji, Serikali imelifanyia kazi suala hilikiundani na kuangalia namna ya kuweza kupata fedha zaziada kwa kutazama mafungu mengine. Tumetazamakiundani na kuona mafungu mbalimbali ya posho ambayohayaathiri sana utendaji wa Serikali yakipunguzwa, basituyapungeze mafungu hayo tuongeze fedha katika Mfukowa Maji. (Makofi)

Tatu, katika kwenda kuitekeleza kazi hii, uchambuziwa ndani kwa maana ya details, Wizara ya Fedhanitawasilisha katika kipindi cha kuwasilisha Appropriation Billili maeneo yale ambayo yatapunguzwa yalete afueni kwaajili ya Bajeti ya Maji, details hizo nitazionesha kwenyeAppropriation Bill.

Page 38: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

38

29 APRILI, 2013

Nne, katika kutekeleza hiyo kazi details hizonitaziwakilisha kwa Kamati ya Bajeti husika ili Waheshimiwawahusika wa Kamati ya Bajeti waweze kuyaona maeneoambayo tutayagusa kwa ajili ya kusaidia kuongeza Vote yaMaji na katika hilo, tumezingatia ripoti iliyowasilishwa naMwenyekiti wa Kamati ya Maji na kiwango kile ndichotulichokizingatia.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha.

SPIKA: Unaweza kutaja kiwango chenyewe?

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, Mwenyekiti waKamati ya Maji, alieleza kwa undani jumla ya shilingi bilioni184.5 ndicho kiwango ambacho Kamati ilipendekeza naWaheshimiwa Wabunge waliunga mkono.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji, tulikuwatunapewa taarifa halafu tunaendelea.

MHE. KABWE Z. KABWE: Mwongozo wa Spika,kuhusiana na taarifa ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha.

SPIKA: Ninaomba mtulie kidogo halafu mtaulizamwongozo baadaye.

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. SELEMANI S. JAFO: Mheshimiwa Spika, kwanza,naiomba Serikali iIongezee pesa Wizara ya Maji ili kuwezakuwapatia maji Wananchi hususan walio vijijini.

Pili, Serikali ifute kabisa kodi katika madawa ya maji ilikupunguza gharama za uendeshaji kwa mamlaka za majina hivyo kupunguza gharama kwa mtumiaji.

Tatu, naiomba Serikali iendelee na mikakati yake yaujenzi wa Visima vya Kimbiji na Mipera ili Wilaya ya Kisarawepamoja na Mkuranga ziweze kunufaika na upatikanaji wamaji kutoka chanzo cha mipera.

Page 39: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

39

29 APRILI, 2013

Nne, naiomba Serikali iendeler kuiangalia Kisarawekwa jicho la karibu kwani tatizo la maji limekuwa kubwa sana.

Tano, naishukuru Serikali kupitia Wizara yake na Taasisiyake ya DAWASA kwa kuweka mikakati yenye kutia moyoya kuisaidia Kisarawe.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. ABDULSALAAM SELEMANI AMER: MheshimiwaSpika, napenda kuipongeza Hotuba ya Wizara ya Maji.Hotuba iliyojaa nia nzuri ya Wizara na mipango thabiti yakuweza kuwapatia Watanzania maji safi na salama.

Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hiikuunga mkono michango ya baadhi ya Wabunge kuhusukupunguza bajeti ya Serikali upande wa Other Charges (OC)kwa asilimia kumi na tano angalau itasaidia kuongezakwenye bajeti ya maji.

Mheshimiwa Spika, ningependa kuishauri Serikali iundeWakala wa Maji kama vile TANROAD. Naona ingewezakusaidia na kutoa lawama kwa Wizara moja kwa moja.

Mheshimiwa Spika, pamoja na bajeti hiyo finyu,ningeomba Wizara ya Fedha (Hazina), ipeleke pesa kwawakati ili iweze angalau kufanya kazi kwa wakati. Miradi yoteiliyopangwa bajeti iliyopita takriban robo tatu haijakamilikakutokana na kuchelewa kwa pesa toka Wizarani.

Mheshimiwa Spika, Mji Mdogo wa Mikumi unaendeleakukua kwa kasi. Kwenye Mradi wa Vijiji Kumi vya World Banktumepata katika Mji Mdogo wa Mikumi.

Mheshimiwa Spika, naomba kwa heshima nataadhima, Mheshimiwa Waziri aelekeze nguvu katikakumalizia Mradi huo. Visima viwili vimechimbwa na kufanyiwamajaribio na vinatoa maji safi na hayana chumvi. Naombachonde chonde mpeleke fedha kumalizia Mradi huo kwa

Page 40: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

40

29 APRILI, 2013

kujenga matanki na kufunga pump ili maji yatoke kumalizatatizo la maji katika Mji Mdogo wa Mikumi.

Mheshimiwa Spika, shukrani.

MHE. REBECCA M. MNGODO: Mheshimiwa Spika, Bajetiiliyoombwa na Wizara ya Maji kwa mwaka 2013/2014ambayo ni jumla ya Sh. 398,333,474,000; kati ya hizo matumiziya kawaida ni Sh. 18,890,254,000, Miradi ya Maendeleo ni Sh.379,443,220,000. Katika fedha hiyo ya Miradi ya Maendeleo,fedha inayotegemewa kutoka ndani ni Sh.138,266,164,000.

Mheshimiwa Spika, fedha inayotegemewa kutoka njeni Sh. 241,177,056,000. Fedha hii siyo ya kutegemewa kwanihivi karibuni tumeanza kusikia kwamba, Nchi za Ulaya nazozimepatwa na mtikisiko mkubwa wa kiuchumi kiasi kwamba,hakuna uhakika kwamba fedha hiyo kutoka nje itapatikanakama ilivyopangwa.

Mheshimiwa Spika, sote tu mashahidi wa jinsiambavyo Watanzania wengi waishivyo vij i j iniwanavyoendelea kuteseka kutokana na ukosefu wa majihasa wanawake na watoto wa kike, ambao hutumia mudamrefu kutafuta maji ambayo mwisho wa siku siyo safi nasalama.

Mheshimiwa Spika, Wizara hii iongezewe fedha zakutosha ili Miradi yote ya Maji ambayo ni ya muda mrefu;kwa mfano, Miradi ya Vijiji Kumi iweze kukamilishwa na hivyokuwaondolea adha Watanzania waishio vijijini ambao ndiyowengi.

Mheshimiwa Spika, Miradi ya Vijiji Kumi ilionekanaingewezekana kabisa kuwapatia Wananchi maji kwakuwachimbia visima. Haipendezi kwamba vipo visimavilivyochimbwa ambavyo havitoi maji.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tuna wataalam wa majiwaliosomeshwa kwa gharama kubwa kwa kodi zaWatanzania; na kwa kuwa kabla ya kuchimba visima utafiti

Page 41: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

41

29 APRILI, 2013

hufanyika kwanza ili kutambua kama eneo husika lina majiardhini na hivyo linafaa kwa kuchimbwa kisima; je, inakuwajefedha nyingi kupotezwa kwa kutumika kuchimba kisima eneoambalo halina maji kabisa?

Mheshimiwa Spika, katika maeneo ambayoyamechimbwa visima na matokeo yake maji hayapo, ni ninimpango wa Serikali katika kuwapatia maji Wananchi waishiokatika maeneo yenye visima visivyotoa maji?

Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache, naombakuwasilisha.

MHE. JITU VRAJLAL SONI: Mheshimiwa Spika, nashukurukupata fursa ya kuchangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Maji.

Mheshimiwa Spika, kwanza, naiomba Serikali yetuiangalie suala hili muhimu la maji, maji ni uhai. Bajetiiliyotengwa ni ndogo sana. Tunahitaji kuwa na Mfuko wa MajiKitaifa na pia uamuzi ufanyike kupunguza bajeti za Wizaranyingine na kuongeza katika Wizara ya Maji.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyochangia awali, Wizarazote husika zishirikiane kutatua matatizo ya maji. Maji katikamaeneo ambapo yapo yatunzwe, uharibifu wa vyanzo namaeneo ya kukinga (catchment area), maji yameendeleakuharibiwa sana na tunaendelea kuangalia bila kuchukuahatua. Nashauri maeneo yote ya vyanzo, maeneo oevu,maeneo yenye hifadhi ya chini ya ardhi pamoja napembezoni mwa mito na maziwa, yaendelee kuhifadhiwakwa nguvu zote, maji siyo endelevu kama hayatatunzwa.

Mheshimiwa Spika, nashauri mpango kabambeuandaliwe wa kuchimba mabwawa ya kuvuna maji. Idaraya uchimbaji mabwawa na visima iendelee kuboreshwa.Tupatiwe wataalam wa kuandaa michoro ya mabwawakitaalam, visima vipimwe ili hata halmashauri na wadauwaweze kutafuta fedha na wafadhili wakisaidiana na Wizaraau Serikali kuu.

Page 42: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

42

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, pia nashauri Serikali iangalienamna ya kuboresha kwa kurekebisha masuala machachekatika Sheria ya Manunuzi. Sheria hii ni kikwazo kikubwa katikakutekeleza Miradi ya Maji na miradi mingine ya maendeleo;kwanza, inachelewesha muda wa utekelezaji, gharamazinaongezeka sana za manunuzi na huduma ambayo ni zaidiya bei za kawaida sokoni.

Mheshimiwa Spika, nashauri kipengele cha bei yavifaa kitajwe katika tender na bei ya kutoa huduma katikaeneo hilo ili wakati wa kuchambua na kutoa maamuzi, Kamatiau Bodi za Zabuni waweze kulinganisha na bei iliyopo sokonikwa wakati huo. Pia baada ya hapo, hizo bei zibandikwe auzitolewe katika vikao vya maamuzi ya juu na fursa ya yeyoteanayetaka kuona apate.

Mheshimiwa Spika, nashauri kodi mbalimbaliziondolewe kwa Miradi ya Maji ili kupunguza gharama zautekelezaji kwa fedha kidogo iliyopo. Kwa mfano, Kodi yaOngezeko la Thamani (VAT) katika mabomba, viungo,pumps, mota za umeme, kwa anayetoa huduma, yaanimkandarasi. Mafuta ya vifaa vya ujenzi, matenki, sementi,nondo na kadhalika, itapunguza gharama kwa takribanasilimia 18 hadi 36. Maji iwe mjini au vijijini ni muhimu na majisiyo anasa (luxury) ni muhimu na hitaji kwa maisha (necessity).

Mheshimiwa Spika, nashauri Serikali pia ifute kabisakodi kwa madawa ya kutibu maji na madawa yoteyanatumiwa na Taasisi au Wakala wa Maji na kupunguzamatatizo ya kiafya na kwa kuondoa kodi hiyo pia gharamaya maji kwa mtumiaji wa mwisho itapungua.

Mheshimiwa Spika, nashauri Serikali iboreshe kwakuongeza uwezo wa ofisi zetu za mabonde. Mabonde mengihayana uwezo wa kujiendesha na kutoa huduma muhimukwa watumia maji kutokana na ufinyu wa bajeti zao hataudhibiti wa rasilimali maji unakuwa mgumu. Wapatiwe bajetiya nyongeza ili wapatiwe vifaa vya kupima maji kwausalama, vifaa vya kupima maji ya chini ya ardhi. Wakiwana vifaa hivyo vya kutosha wataweza kupima maeneo

Page 43: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

43

29 APRILI, 2013

mbalimbali na halmashauri, wadau wengine mbalimbaliwanaweza kutafuta fedha za kuchimba maji na kuwekamiundombinu ya kusambaza maji hayo.

Mheshimiwa Spika, narudia kushauri kuwa, Wizara zotezishirikiane na ngazi za Halmashauri, Idara zote ili wakati wakuandaa miradi na wakati wa utekelezaji, zipange pamojaili kupata ufanisi. Kila Idara isije na mpango wake; mfano,Babati, Idara ya Kilimo ilibuni Mradi wa Maji kwa ajili yaumwagiliaji Gichameda, Mradi ulitekelezwa kwa gharamakubwa. Mafanikio yapo na pia migogoro ipo ya watumiamaji wengine wa Mradi huo. Hapo hapo chanzo hichokinapeleka maji kwa matumizi ya kawaida ya binadamu kwaMji wa Magugu, Matufa na maeneo yote ya jirani. Sasa Mradimwingine mkubwa umeibuliwa na Idara ya Maji na tayariutaanza kutekelezwa, kupeleka maji ya matumizi yabinadamu kutoka chanzo hicho hicho kutoka Darakutakwenda Minjingo. Sasa kuna migogoro iliyopo kabla ya Mradihuu unaotegemewa kuanza, Mradi huu utaongeza kabisamigogoro. Sera yetu inasema maji ya kunywa ni kipaumbelecha kwanza, haya yote ni sababu ya kutoshirikishana katikaIdara mbalimbali wakati wa mchakato wa kuandaa Miradi.Huu Mradi wa pili ungeweza kutumia chanzo kingineambacho kipo jirani na hapo ambapo hakuna watumia majiwengine.

Mheshimiwa Spika, mwisho, naomba Serikali iangalieMiradi ya Maji Babati Vijijini, kuna tatizo kubwa huko. Sehemukubwa ya Tarafa ya Mwada maji ya chini hayafai kwamatumizi kwa sababu ya fluoride. Maeneo ya kanda ya juuBashnet, Ufana, Nar, Dabil maji ya chini ya ardhi yako mbalimita 125 hadi 200. Maeneo yote yanapata mvua za kutosha,tunashauri Serikali itusaidie kuchimba mabwawa ya kuvunamaji. Pia Serikali itusaidie wataalam wa kupima maji chini yaardhi na wataalam wa kusanifu na kuandaa michoro yamabwawa ili na sisi Viongozi wa Wilaya na Mkoa tuangaliepia namna ya kuomba msaada wa vifaa vya kuchimbavisima na kutengeneza mabwawa.

Page 44: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

44

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, kuna visima 15 vilipimwa nawataalam wa bonde la kati miaka michache iliyopita kwaajili ya maji ya matumizi ya binadamu na pia umwagiliaji,hadi leo haijapangiwa bajeti ya kuchimba na tayari Wizaraya Nishati imepeleka umeme maeneo jirani na hapo.Naomba mpange bajeti kwa visima hivyo.

MHE. AMOS G. MAKALLA: Mheshimiwa Spika, naombakujua Mradi wa Maji Mvomero na Turiani umefikia wapi? Nifedha kiasi gani imetengwa kwa mwaka huu wa fedha?

Nasikitika kuona mtaro tu pasipo mabombakutandazwa katika Mji wa Mvomero, Dibamba na kule Turiani.Nasikia Mkandarasi anadai fedha. Naomba sana Waziriatamke wazi ni lini Miradi hii itakamilika na kwa kutaja fedhazilizotengwa mwaka huu.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja.

MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, kwanini Shule zote za Serikali za Msingi na Sekondari hazina maji;mfano; Sekondari ya Manda, Luana, Msembe, Lugarwa,Livingstone na Ludewa zote hazina maji? Vilevile Shule zaMsingi watoto wengine wanaenda shule bila kunywa chaina shuleni hakuna hata maji ya kunywa?

Mheshimiwa Spika, wanawake wengi wanahangaika,hutumia muda mwingi sana kutafuta maji. Akina mama waNjombe, Ludewa na Makete, muda huo wangekuwawanazalisha hususan kil imo. Kwa kuwa wanawakewanatumia muda mrefu kutafuta maji umaskiniunaongezeka.

Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango gani wakutatua tatizo la maji Kata ya Amani, Mundindi? Naombamajibu Serikali ina mkakati gani wa kutatua tatizo la maji.

MHE. JOHN M. CHEYO: Mheshimiwa Spika, naombakuchangia kama ifuatavyo:-

Page 45: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

45

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, dhana ya kuchimba visima namabwawa bila miundombinu ya kutumia maji ni matumiziyasiyo na manufaa ya fedha za umma (NugatoryExpenditure). Mifano ipo mingi na hotuba imetaja visima namabwawa kumi bila kutaja Bwawa la Nkowa na Machari –Mugumu. Ushauri wangu ni kwamba, Wizara ikubali kugeuzamtazamo huu na makisio yote ya Miradi ya Maji iwe kuchimbachanzo pamoja na miundombinu ya matumizi ya majiambayo ni pamoja na miundombinu ya kupata maji safi nasalama.

Mheshimiwa Spika, Bwawa la Nkowa ni mfano wakuchimba chanzo cha maji bila miundombinu ya kusafirishamaji na kusambaza kwa vijiji kwa matumizi ya Hospitali yaMwalushu, vijiji na wanyama na ikiwezekana umwagiliaji wamashamba. Bwawa hili lina maji kwa miaka kumi na tatu sasa.Lil ifunguliwa na Rais mwaka 2006 na kila Kiongozinimemweleza juu ya hali hii ambayo ni pamoja na WaziriMkuu, Waziri wa Maji, Katibu Mkuu (TAMISEMI) na wa Maji.Tathmini ya gharama ni takriban shilingi bilioni 2.5, naombafedha hizi zitengwe kwa mwaka wa fedha 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, Lagangabili ni Makao Makuu yaWilaya mpya ya Hilima na kijiji hiki hakina maji na sioni jitihadayoyote ya kupata maji katika kijiji hiki. Mpango wa ZiwaVictoria ambao utachukua miaka mingi na mahitaji ni ya sasahivi, naomba kijiji hiki kichimbiwe kisima kirefu pamoja namiundombinu ya kusambaza hayo maji hayo na kuyasafirisha.

Mheshimiwa Spika, Bajeti kila mara inaahidiwa fedhalakini pesa haitolewi na Hazina. Jambo hili lazima litatuliwe,Bunge haliwezi kuamua kutoa kipaumbele kwa maji naWizara ya Fedha inabeza uamuzi wa Bunge. Serikali itoeuamuzi kuwa, fedha yote itakayotolewa na Bunge basiitolewe kama first charge, tusipopata commitment hii yaSerikali basi yote yanayoamuliwa na Bunge hayatasaidiakatika kilio cha maji.

Page 46: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

46

29 APRILI, 2013

MHE. KAIKA S. TELELE: Mheshimiwa Spika, nawapa poleWizara ya Maji kwa kazi kubwa ya kujaribu kutatua tatizo lamaji linalowakabili Watanzania.

Mheshimiwa Spika, Wakazi wa Ngorongoro wapatao270,000 ni sehemu ya Watanzania wanaokabiliwa na tatizola maji. Tulileta maombi ya fedha kwa nyakati tofauti (Tsh.200,000,000 na Tsh. 400,000,000) kwa ajili ya Mradi wa Majiwa Mji Mdogo wa Loliondo – Wasso. Tulikumbushia maombihayo mara kadhaa bila mafanikio licha ya mimi Mbungekuleta barua hizo hapa Bungeni na Wizarani na kuzungumzana Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri na pia Katibu MkuuSayi na kukabidhi barua hizo.

Mheshimiwa Spika, mahitaji ya maji kwa Wakazi waLoliondo – Wasso ni lita za ujazo 500,000 kwa siku. Fedhazinazoombwa ni kwa ajili ya kujenga tenki la lita za ujazo680,000 pamoja na kukarabati miundombinu ya majiiliyojengwa mwaka 1989. Tenki lingine la lita za ujazo 200,000litajengwa katika Kijiji cha Sakala ili kuhudumia Kituo cha Afyacha Sakala na Wananchi wa eneo hilo. Kwa heshima naunyenyekevu, naomba kupewa fedha hizo kwa madhumunihayo.

MHE. PROF. KULIKOYELA K. KAHIGI: Mheshimiwa Spika,tatizo la maji safi ni kubwa kuliko takwimu zinavyolifanyalionekane. Katika maeneo mengi, hasa vijijini na hata mijini,huduma ya maji safi ni adimu. Katika Wilaya nyingi, hasazilizo pembezoni kama Bukombe, huduma ya majisafi na hatamajitaka imebaki kuwa ni ndoto kwa watu wengi. KamaWabunge wengi walivyothibitisha, hali ni mbaya sana kwanimahali pengi watu wananunua maji kwa bei kubwa sanaau wanatumia maji ambayo siyo safi na salama ambayoyanapatikana kwa shida sana.

Mheshimiwa Spika, kwa maoni yangu, Serikaliimeshindwa kupeleka huduma ya majisafi kwa Wananchiwengi kwa sababu zifuatazo: Maji safi hayajapewakipaumbele na hivyo kwa muda mrefu bajeti ya maji imekuwandogo; na hakuna mpango mkakati ambao ungetekelezwa

Page 47: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

47

29 APRILI, 2013

hatua kwa hatua hadi matatizo ya maji yakaisha kabisa.Kilichopo sasa ni Miradi michache iliyotawanywa nchi nzimana mingi ya Miradi hii inasuasua.

Mheshimiwa Spika, lipo tatizo pia la Miradi mingikukabiliwa na ubadhirifu wa fedha za maji kwenye ngazi zote.Kwa kuzingatia umuhimu wa maji katika maisha ya binadamuna katika shughuli za kiuchumi, kwa nini Serikali isitoekipaumbele kwa maji na kuandaa mpango mkakati wakitaifa utakaolenga kumaliza kabisa tatizo la maji?

Mheshimiwa Spika, sasa nitajielekeza moja kwa mojakwenye matatizo ya maji yanayowakabili Wananchi waBukombe. Lengo ni kuonesha tatizo lilivyo kubwa. Bukombeni miongoni mwa Wilaya zinazokabiliwa na tatizo kubwa lamaji safi na salama. Hakuna maji katika Shule za Msingi naSekondari. Wanafunzi hutumia muda mwingi kutafuta majikwa ajili ya matumizi ya shuleni. Hakuna maji katika Zahanatina Vituo vya Afya.

Miradi ya Ushirombo na Uyovu inasuasua; Wananchiwamekuwa wakipewa ahadi hewa kwamba Serikali itatoafedha kwa ajili ya mtandao wa mabomba kwa miji midogohii.

Wanawake wengi wanahangaika kutafuta maji kilasiku badala ya kufanya shughuli nyingine za kiuchumi.Mathalani, Wananchi wa Kijiji cha Nalusunguti huendakutafuta maji katika Wilaya jirani ya Chato.

Mheshimiwa Spika, napenda kumalizia kwa kuunganana Wabunge wanaopendekeza kuwa na mpango mkakatiwa haraka wa kutatua tatizo la maji nchi nzima. Fedhaitafutwe kwa njia yoyote ili watu waache kuhangaika natatizo hili.

MHE. RIZIKI OMAR JUMA: Mheshimiwa Spika, tatizo laukosefu wa maji Tanzania ni kubwa sana, kiasi chakuwanyima raha Watanzania, kwani bila ya maji hakunamaisha, kwa kuwa maji ni uhai. Tatizo hili liko mjini na vijijini.

Page 48: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

48

29 APRILI, 2013

Mwathirika mkubwa wa ukosefu wa maji ni mwanamke namtoto. Wanawake wengi wanatumia muda wao mwingikutafuta maji katika masafa marefu. Mwanamke huyoanataka kujitafutia riziki kwa kujiajiri mwenyewe, huyohuyofamilia inamsubiri kutoa huduma za ndani kama vile watotona baba watoto pia. Hivyo basi, naiomba Serikali ifanye kilarai, watoe fedha katika fungu ambalo uzito wake haulinganina ule wa maji.

Mheshimiwa Spika, hali ya maisha ya Wananchi wetuni mbaya sana kiuchumi, sasa tunamwongezea na mzigo wakununua maji kila siku kwa ajili ya matumizi ama ya nyumbaniau hata akiamua kujenga bado badala ya kununua vifaavya ujenzi, analazimika kununua na maji. Huo ni mzigo mzitoukilinganisha na kipato chake; mlo mmoja unampa shida,je, maji atatoa wapi?

Mheshimiwa Spika, hili ni tatizo ambalo linahitajiumakini mkubwa sana kukabiliana nalo.

Mheshimiwa Spika, miradi ya Maji ambayo hupelekwakwa nini haitekelezwi, inaonekana kama vile kuna ujanjafulani unafanywa na Wananchi wanaendelea kuteseka,fedha zinatengwa lakini miradi haikamiliki; ni kwa nini?Naiomba Serikali ifuatilie kwa karibu sana ili kuhakikisha azmaya hotuba hii na malengo yanafikiwa ili watu waondokanena adha hii ya ukosefu wa maji ambao pia huchangia kupatamagonjwa ya milipuko kutokana na maji yasiyokuwa salama.

Mheshimiwa Spika, hotuba hii nzuri yenye matumainiisiwe pambo, itekelezwe kwa uhakika ili Wananchi wafaidike.

MHE. JOHN P. LWANJI: Mheshimiwa Spika, naungamkono hoja.

Mheshimiwa Spika, naomba majibu kwa mamboyafuatayo:-

(a) Ahadi ya Rais aliyoitoa mwaka jana Itigi,Manyoni kuhusu kuupatia mji huo maji ya kutosha.

Page 49: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

49

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Rais, alimsimamisha Mhandisi wa Maji wa Wilayana Mkurugenzi (DED) kwa muda wa nusu saa aelezeeWananchi kwenye mkutano wa hadhara mikakati ipiitachukuliwa kuupatia Mji wa Itigi maji ya kutosha. Walielezana kuhitimisha kwa kuiomba Serikali itenge fedha ili kazi hiyoifanyike. Mheshimiwa Rais, akaahidi Wananchi kuwa Serikaliyake itatekeleza katika kipindi kifupi ili Mji wa Itigi upate majiya kutosheleza mahitaji ya Wananchi.

Mheshimiwa Spika, sioni mpango huu kwenye bajetihii, napenda kupata majibu ni kwa nini mpango huu na ahadiya Rais, hakuna fedha zilizotengwa?

(b) Mheshimiwa Spika, nasikitika kwamba,mchakato wa kusaka maji ardhini na kuyapata kwa matumiziya binadamu na mifugo bado ni kitendawili. Mara nyingiwataalam wa kupima maji, wamekuwa wakikosea nakusababisha hasara pale wachimbaji wanapochimba nakukosa maji. Eneo kubwa la jimbo langu hasara hii imetokeamara kwa mara.

Napendekeza kuwa kazi ya kupima na kuchimba majiapewe mkandarasi mmoja ili atakapopima na kuchimbaakakosa maji, basi hasara iwe kwake na si kwa Serikali ilikuokoa fedha za Wananchi. Hatua hii itawafanya wawemakini zaidi katika kutafuta maji kuliko utaratibu wa sasaambapo mpimaji ni tofauti na mchimbaji ni tofauti. Fedhanyingi sana zinapotea kwenye mchezo huu.

Mheshimiwa Spika, Vijiji vyote vya Jimbo hili la ManyoniMagharibi wakazi wake ni wakulima na wafugaji. Maji yavisima virefu hayatoshelezi mahitaji. Naiomba Serikali ije namkakati wa kuchimba mabwawa. Hatua hii itatoa ufumbuziwa matatizo ya maji.

Mheshimiwa Spika, aidha, pamoja na ahadi ya Serikaliya kuchimba bwawa la Kijiji cha Rungwe, mpaka sasa ahadihiyo haijatekelezwa. Napenda kujua ni kwa nini hadi sasautekelezaji wa ahadi hiyo bado haujafanyika?

Page 50: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

50

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali ifanye utafiti wakutosha kwenye Kata za Idodya, Ndole, Aghondi, Ipande,Kitaraka, Mwamagembe na Rungwa ili kujua kina cha majimaeneo haya. Mara nyingi uchimbaji umeonesha kuwahamna maji ardhini. Aidha, nguvu zielekezwe zaidi kwenyeuchimbaji wa mabwawa na malambo.

Mheshimiwa Spika, nawasilisha.

MHE. NAMELOK E. M. SOKOINE: Mheshimiwa Spika,nashauri yafuatayo:-

(i) Miundombinu ya maji taka hasa kwa Wilayaya Arusha Mjini ishughulikiwe, kuna maji mengi na machafuyanazagaa wakati wa mvua kiasi kwamba inasababishamagonjwa ya mlipuko katika Mji huu na hata kugharimumaisha ya watu.

(ii) Mheshimiwa Spika, katika Mkoa wa Arusha,Wilaya ya Arumeru, kuna vyanzo vingi vya maji; mfano, MtoDututi, Mlima Meru, nashauri Wizara iende ikafanye utafiti ilimaji yaweze kupatikana na gharama yake itakuwa nafuu.

(iii) Mheshimiwa Spika, lipo tatizo la visima vingikutokutoa maji na hili ni kwa sababu ya visima hivyovilichimbwa wakati wa mvua na inapokuwa kiangazi majihayo hayatoki na hivyo kupoteza fedha nyingi za Serikali.Inasikitisha kuona tuna wataalam wengi wa kutosha namakosa kama haya yanatokea.

(iv) Mheshimiwa Spika, hali kadhalika tatizo hili lipokwenye mabwawa ya maji, yanachimbwa kwa gharamakubwa za ajabu, baada ya mvua mengi hubomoka nakukauka maji.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nashauri bajeti iongezwe,pia Wananchi waelimishwe kuvuna maji ya mvua.

Page 51: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

51

29 APRILI, 2013

MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Spika,naipongeza Serikali kwa utekelezaji wa kazi zake katika kipindicha 2012/2013.

Mheshimiwa Spika, matatizo ya maji ni mengi katikamaeneo ya vijijini na athari zake ni kubwa. Tarehe 14 Aprili,2013 Wabunge Wanawake tulipata fursa ya kushiriki katikaKongamano la Wanawake waliowakilisha Wanawake waKanda zote za Tanzania. Wanawake kutoka Mikoa ya Lindina Mtwara walitueleza yafuatayo:-

(i) Wananchi hasa akina mama wanatumiamuda mwingi kwa siku kutafuta maji ambayo yako mbali namaeneo wanayoishi. Wastani wa muda ni saa nane hadikumi. Hawana muda wa kufanya kazi za maendeleo.

(ii) Maji yanayopatikana siyo safi wala salamakwani ni kama tope kabisa. Chanzo cha maradhi.

(iii) Ili kupata maji akina mama wengi hutafutamaji nyakati za usiku.

(iv) Wanapotafuta maji usiku wakati mwinginehuumia kutokana na giza kwani hujikwaa kwenye visiki namawe au kuanguka katika mashimo, kukimbiawanapokutana na wanyama na wabakaji lakini maranyingine wanawake hawa hubakwa. Inasikitisha.

(v) Jambo baya zaidi ni pale mama anapoamkaalfajiri akiwa amemwacha mumewe nyumbani na kwendakutafuta maji. Inaposhindikana kabisa kupata majiwanawake hulazimika kufanya ngono ili wapate maji kutokakwa wanaume waliowahi kuchota maji usiku.

Kwa kweli inasikitisha sana na sasa tulipofikia kamaTaifa ni pabaya.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwa Serikali,iongeze fedha za ziada kwa ajili ya maji vijijini na ichukuehatua za dharura. Pale ambapo MIRADI ya Maji itaonekana

Page 52: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

52

29 APRILI, 2013

kuchukua muda mrefu ni vyema Serikali ijaribu kutumiamapaa ya Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Zahanatiili kuvuna maji ya mvua katika kipindi cha mvua za vuli mwakahuu 2013. Haitakuwa lazima kujenga matenki kwani yapomatenki ya plastiki yanauzwa kwa bei nzuri tu. Serikali ichukuehatua tafadhali kwani kuna kaya zinakosa mlo wa mchanakutokana na ukosefu wa maji. Mihogo na viazi vinachomwana si kupikwa kwani hakuna maji.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja, fedhazilizopo zitolewe na nyingine ziongezwe ili maji yapatikanenchi nzima.

MHE. NIMROD E. MKONO: Mheshimiwa Spika, kwaniaba ya Wananchi wa Musoma Vijijini, napenda kuchukuanafasi ili nichangie Bajeti hii kwa maandishi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nimekua Mbunge wa Jimbo laMusoma mfululizo toka mwaka 2000 hadi sasa. Kwa kipindichote Ubunge wangu, wamekuwa wakinituma Bungenikueleza shida yao kuhusu maji safi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba Jimbo kwakiasi kikubwa, takriban asilimia 60, limezingirwa na vyanzo vingivya maji kama vile Ziwa Victoria, Mto Mara, Mto Kyarano naMto Suguti, bado Wananchi wengi wanaishi bila kupatahuduma ya maji safi na hivyo kusababisha mlipuko wamaradhi mengi yatokanayo na maji wanayoyatumia.

Mheshimiwa Spika, kila Bajeti ya Maji ilipokuwa ikiletwahapa Bungeni, nimekuwa nikilia kwamba, Miradi mikubwaya Maji iliyobuniwa na Baba wa Taifa, Mwalimu JuliusKambarage Nyerere kwenye Awamu ya Kwanza, yaanimwaka 1974, ilibuni Miradi mikubwa mitatu ya maji WilayaniMusoma kama ifuatavyo: Trunk Route 1 ambayo ililengausambazaji wa maji kwenye maeneo kame ya maji ya Bunda;Trunk Route 2 ambayo ililenga usambazaji wa maji kuhudumiamaeneo ya …; Trunk Route 3 ambayo ililenga usambazaji wamaji kutoka Mto Mara sehemu ya Kirumi na kuhudumia Tarafanzima ya Kyagata yenye Kata tatu za Bwiregi, Buswahili na

Page 53: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

53

29 APRILI, 2013

Nyamimange; Trunk Route 3 ambayo ililenga kutoa majikutoka Mugango, Ziwani Lake Victoria na kuyasambazakwenye maeneo ya Nyang’oma, Kwikuba, Mwiringo, BwaiKwituru, Mugango, Kamugegi, Kyatungwe, Kyabakari, Buturu,Butiama, Muryaza, Bumangi, Busegwe, Tringati na Masaha.

Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa,nasikitika kurudia kuliambia Bunge hili Tukufu kwamba,imetelekeza Miradi hii yote mitatu hatua kwa hatua bila aibukwamba ilianzishwa na Hayati Baba wa Taifa. MheshimiwaNaibu Spika, tunalipeleka Taifa letu hili wapi?

Mheshimiwa Spika, leo hii nimeshangazwa kusikiaWabunge wenzangu waliopendelewa kujengewa Miradimikubwa eti kwamba hiyo miradi mipya ilikuwa ni utekelezajiwa ahadi za Rais wa Awamu ya Nne; sielewi!

Mheshimiwa Spika, mimi nilidhani kila Rais aliyepitaalitoa ahadi kwa Wananchi ili itekelezwe na kila Rais ajae.Je, sasa ndiyo kusema ahadi za Rais wa Awamu ya Kwanzazimefutiliwa mbali? Mimi nilidhani kwa kuwa ahadi alizozitoaHayati Baba wa Taifa zilitolewa na Rais wa Serikali ya CCM,CCM bado ipo madarakani kwa nini basi Miradi hii mitatuitelekezwe hivi hivi bila kujali mateso wanayopata Wananchiwa maeneo husika katika ukosefu wa maji.

Mheshimiwa Spika, katika Hotuba ya Waziri, ukurasawa 51, Waziri anatuambia hivi, ninanukuu: “Miradi mipyakatika eneo la Ziwa Victoria. Katika mwaka 2013/2014, Serikalikwa kushirikiana na AFD na European Investment Bank (EIB),itaanza utekelezaji wa Miradi ya Maji Safi na Usafi waMazingira katika Jiji la Mwanza. Vilevile Mradi huo utahusuuondoaji wa maji taka katika Manispaa za Bukoba naMusoma, pamoja Mradi wa majisafi na usafi wa mazingirakatika Miji ya Lamadi, Misungwi na Magu. Miradi hiyoitaongeza upatikanaji wa maji kutoka asilimia 35 hadi asilimia90 kwa Mji wa Magu, kutoka asilimia tano hadi asilimia 90kwa Mji wa Lamadi na kutoka asilimia 45 hadi asilimia 90 kwaMji wa Misungwi.

Page 54: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

54

29 APRILI, 2013

Mradi wa kuboresha usafi wa mazingira kwa Jiji laMwanza utahusisha kupanua mtandao wa maji taka kutokaasilimia 13 hadi asilimia 30. Mradi wa maji taka kwa Jiji laBukoba utahudumia asilimia 15 na Mji wa Musoma ni asilimia20 ya wakazi.” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, maeneo yote yaliyotajwa hapojuu yako kandokando ya Ziwa Victoria, Jimbo la MusomaVijijini nalo lote liko kandokando ya Ziwa Victoria. Kwa ninibasi Miradi mipya hiyo isingegusa pia maeneo sugu yaMugango, Buswahili na Wegero ambako mafuriko makubwaya maji ya Mto Mara yamiminikayo Ziwa Victoriayasingeingizwa kwenye Miradi mipya hiyo.

Mheshimiwa Spika, kwa muda wa miaka mingi MtoMara umekua kero kubwa kwa Wananchi wa Tarafa yaKiagata. Mwaka hadi mwaka Mto huo umekua ukifurika nakumeza maeneo ya wakulima na wafugaji waishio Kata yaBuswahili na Bwiregi. Wananchi hao wamekua wakiishi bilamaji safi kwa muda mrefu. Eneo kubwa la ardhi yaolimemezwa na maji ya Mto Mara, ambao sasa umejaamagugu maji mengi yanayo-emit gas nyingi mno ambayowataalam wanasema ni environmental disaster. Nini Serikaliinasema kuhusu janga hilo la Mto Mara?

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Trunk Route 3i l iyoahidiwa na Hayati Baba wa Taifa mwaka 1974imetelekezwa, Wananchi wa Kiagata sasa hawana maji safiwala mashamba ya kulima au maeneo ya kufuga. Wizaraya Maji iliwaahidi Rambo Wegero. Mwaka jana Serikali ilitumiakiasi cha fedha karibu shilingi bilioni moja. Kutokana na ufisadiuliofanywa kwa kubuni Mradi huo wa Rambo, muda mfupibaada ya kulijenga, Mto Mara ulifurika na kumeza Rambohilo. Je, Serikali inasema nini kuhusu ufisadi huo.

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, nasema katikamchango wangu wa kusema nilieleza kwa kifupi kwa ninisiungi mkono hoja hii. Sasa basi nimeeleza kwa kirefumasikitiko yangu kuhusu utelekezaji wa Miradi mitatu maarufuTrunk Route 1, 2, 3. Wilaya ya Butiama imenyimwa maji safi

Page 55: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

55

29 APRILI, 2013

kwa kipindi kirefu tangu Baba wa Taifa alipotuacha. Serikaliimeziba masikio; kwa nini basi niunge mkono hoja Bajeti hii.Narudia tena kusema siungi mkono hoja hii.

MHE. GRACE S. KIWELU: Mheshimiwa Spika, naombakutoa mchango wangu kidogo juu ya Wizara hii kamawalivyokwisha kusema wenzangu, maji ni uhai, kama hakunamaji hakuna maisha. Nchi yetu kwa ujumla ina tatizo kubwasana la maji na tatizo hili linawaumiza zaidi akina mamaambao hutumia muda mrefu kutafuta maji na kupotezamuda wa kufanya kazi zao za maendeleo. Mbali na kupotezamuda wa kufanya kazi, ndoa zao zimevunjika na watoto wetukupata mimba ambazo hazikutarajiwa kwa sababu tu yaukosefu wa maji.

Matatizo ni mengi sana hata ukiangalia katika shulezetu za bweni utoro unaongezeka kwa sababu ya ukosefuwa maji huwezi kumuweka mtoto wa kike siku mbili bila kuogahasa ukizingatia akiwa kwenye siku zake. Lazima hawawatoto watakimbia kama hatutaweza kufikiri kwa upanatatizo hili la maji basi maendeleo tunayoyatarajia na umaskinikupungua havitatekelezeka.

Mheshimiwa Spika, suala la Mradi wa Vijiji Kumi ninitatizo la Mradi huu; kila siku tumesikia ndani ya Bunge hili lakinihautekelezeki? Tunaomba majibu sahihi ya suala hili.

Mheshimiwa Spika, Wananchi wamechoka kunywamaji ya tope ambayo siyo salama na husababisha maradhikwa Wananchi wetu.

Mheshimiwa Spika, niiombe Serikali ya Chama chaMapinduzi ione umuhimu wa suala hil i la maji kwaWatanzania. Kama kweli tunataka maendeleo lazima tuanzena maji ili hayo maendeleo yaweze kupatikana; elimu inahitajimaji, afya inahitaji maji na kilimo kinahitaji maji. Maji nimuhimu sana kwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, Bajeti hii ni kidogo sana kuwezakutatua tatizo hili la maji; hivyo, naishauri Serikali kukaa chini

Page 56: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

56

29 APRILI, 2013

na kupitia upya bajeti hii ili iweze kuongeza fedha kwa ajiliya kutatua tatizo hili la maji. Tumesikia mipango mingi mizurilakini haitekelezeki, sasa tumechoka tunataka utekelezaji.

Mheshimiwa Spika, huo ndiyo mchango wangu,nategemea utafanyiwa kazi kwa maendeleo ya Taifa letu laTanzania.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, ni dhahirihamna kitu muhimu katika maisha ya binadamu na viumbevingine kama vile mimea na wanyama kama maji.

Mheshimiwa Spika, tangu tupate Uhuru hadi sasa nitakriban miaka 52, lakini tumeshuhudia adha kubwa ya majivijijini na mijini licha ya nchi yetu kujaliwa au kubarikiwa vyanzovingi vya maji. Tumeendelea kushuhudia akina mamawakitembea kilometa nyingi kutafuta huduma za maji, kituambacho kinadhoofisha uchumi wa nchi kwani akina mamawamepoteza muda mwingi wakitafuta maji hukuwakishindwa kufanya shughuli za maendeleo kama biasharaili kujipatia uchumi. Tumeshuhudia ndoa nyingi zikivunjikakutokana na adha ya maji, pia watoto wengi wamekufawakati wakiachwa majumbani na wazazi kwenda kutafutamaji.

Mheshimiwa Spika, sasa nizungumzie Mkoa wetu waMara. Mkoa ambao tumebarikiwa na vyanzo vingi vya majikwa maana ya mito na mabonde, hata ziwa. Kuna shida auuhitaji wa maji kwenye takriban wilaya zote za Mkoa wa Maraambapo tumeshuhudia akina mama wakitembea umbalimrefu kutafuta maji na hata maji yenyewe yanayopatikanasiyo salama wala masafi, mengi ni machafu, yenye rangi yakahawia, yenye matope na vijidudu. Hivi kweli kwa hali hiimagonjwa nyemelezi yatokanayo na maji machafu kamakichocho, minyoo, amoeba, kipindupindu yataepukika kweli.Serikali haioni kwa kuto-solve tatizo la maji inajiongezeagharama kubwa katika kutibu magonjwa na pia hupotezanguvukazi kwani hamna uzalishaji wenye tija kwenye Taifalililojaa Wananchi wenye maradhi, wenye kupoteza mudamwingi wakitafuta maji.

Page 57: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

57

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Tarime ni ya mwisho auni kati ya Wilaya zilizosahaulika kabisa. Hatuna Miradi yoyoteya mabwawa inayofanywa, hakuna Miradi ya visima vifupiau virefu, wala mbadala wowote ambao ndiyo suluhisho lamaji. Hata pale Tarime Mjini, kwenye Halmashauri ya Mji waTarime, wakazi wake wengi hawana maji safi na salama. PaleTarime Mjini maji yanatoka mchana tu na ni ya rangi yakahawia, udongo au chai. Usiku hakutoki maji kabisa naikizingatiwa Tarime tumepakana na Mto Mara, tuna Mto Mori,Mto Mlale na kadhalika, lakini Serikali inashindwa kutupatiahuduma ya maji.

Mwisho, Mradi wa Visima vya World Bank unaoneshakufeli kwani visima vingi vimechimbwa lakini havitoi maji.

Pia umuhimu wa maji katika miji na vijiji; ni aibu Jijikama Dar es Salaam kuna tatizo la maji. Mfano, eneo laGoba, Wananchi wake wanateseka sana kwa kukosa majina wananunua ndoo ya lita 20 kwa shilingi 500. Jamani huyuMtanzania wa kipato kidogo mfano cha shilingi 100,000, atoelabda shilingi 50,000 kwa maji au shilingi 2500 kwa maji, yaanindoo tano kwa siku ina maana kwa mwezi ni shilingi 75,000,hapo bado pango, bado chakula, bado matibabu, nauli hiyobalaa shilingi 25,000 itamtosha kweli?

Naomba Wizara pia iisaidie jamii ya Wana-Dar esSalaam, Goba, kuna miundombinu iliwekwa lakini hamnamaji, kisa eti hawa Goba Water User Association, sijui kunaubadhirifu au kuna kwa nukuu ya Nape Nnauye; eti walifungamaji kwa sababu Jimbo la Ubungo linaongozwa na Mnyika.Kama ni kweli hii, ni aibu kabisa kwa Serikali hii ya Chamacha Mapinduzi. Ninaomba Serikali ifanyie kazi.

MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO: Mheshimiwa Spika,nimesikiliza na kuisoma Hotuba ya Waziri wa Maji. Kazi kubwainaonekana kufanyika ili kuwapatia Watanzania maji safi nasalama. Kasoro kubwa, uwekezaji wa maji ni lopsided.Hauchukulii uwiano kwa maana ya vijiji vyote, wilaya zotena mikoa yote. Katika kitabu hiki, Mbinga hususan Jimbo la

Page 58: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

58

29 APRILI, 2013

Mbinga Mashariki, lina kijiji kimoja tu cha Mahande chenyeMradi unaotekelezwa.

Mheshimiwa Spika, licha ya majibu ya Wizara ya Majiya kusema itahakikisha maji yanapatikana kwa wingi zaidikatika Mji wa Mbinga, lakini dhamira hiyo haionekani katikabajeti hii. Maana yake Mbinga inayochangia sana uchumiwa nchi hii kwa mazao ya kahawa na mahindi, haitakuwana maji. Hili ni jambo lisilokubalika. Vipo pia Vijiji vya Paradiso,Ndongozi, Luhagali, Mabuni, Litumbandyasi na Kingoli, vinashida kubwa ya upatikanaji wa umeme!

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa 2013/14, Wilayana Halmashauri ya Nyasa itaanza. Katika utekelezaji wa VijijiKumi Mbinga ina vitatu. Naomba Wizara iangalie uwiano huoili vijiji hivyo vigawiwe sawa 5/5 kati ya Wilaya hizi Mbinga.Kwa upande wangu nitazungumza na Mkurugenzi ili achukuezifuatazo. Wakati wa mvua tunapoteza maji mengi na mengiyanaelekea ziwani. Ninaomba tupatiwe Mradi wa Mabwawaangalau mawili tu makubwa yatakayoweza kuhifadhi majina kuwa chanzo cha maji katika vijiji vile ambavyo vinamatatizo ya vyanzo vya maji.

Mheshimiwa Spika, nirudie tu juu ya kuifikiria Mbingahasa mjini pamoja na vijiji nilivyovitaja.

Mheshimiwa Spika, nawasilisha.

MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA: Mheshimiwa Spika,naomba kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, tatizo la maji lililokithiri katika taasisiza Serikali hususani shule, vyuo na hospitali. Maji ni tatizo sugusana katika shule zote za msingi na za sekondari zilizoko vijijini.Tatizo hili linapelekea wanafunzi badala ya kusoma kwamasaa yanayokubaliwa na Wizara ya Elimu wamekuwawakitumia nusu ya masaa yao kutafuta maji ambayohupatikana umbali mrefu sana. Bila maji shuleni tusitegemeeutulivu na ufundishaji wa amani katika shule zetu. NaishauriSerikali kufanya kila iwezalo kutoa kipaumbele kwa shule, vyuo

Page 59: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

59

29 APRILI, 2013

na hospitali ili kuepusha magonjwa ya mlipuko ukizingatiataasisi hizi zina mkusanyiko wa watu wengi.

Mheshimiwa Spika, kuna tatizo kubwa sana la majikatika Mkoa wa Singida hususani Singida vijijini mfano vijiji vyaSepuka, Mtunduru, Ighombwe, Mgungira, Msosa, Mhintini,Kinyampembee Itito katika Tarafa ya Ihanji na Sepuka.Naitaka Serikali itoe kipaumbele cha kuchimba visima ilikunusuru wananchi wa maeneo haya ambao wengi huishimaeneo yenye wanyama kama Tembo na huhatarishamaisha yao wanapokwenda kutafuta maji usiku na kwaumbali wa takribani kilomita 10-15.

Mheshimiwa Spika, mpango wa visima 10 kilaHalmashauri. Mpango huu umeonyesha kushindwa na kwakweli umewakatisha tamaa wananchi ambao walijitoleakuchangia ili kuweza kuchimbiwa visima. Katika Mkoa waSingida, kij i j i cha Puma, Kata ya Puma, wananchiwalishakamilisha michango yao tangu mwaka 2011 lakinimpaka sasa hakuna kinachoendelea kwenye visima hivyo.Serikali sasa itoe tamko ni kwa nini bado inaendelea kuwatesawananchi ilihali walishamaliza sehemu yao ya mchangokama walivyopangiwa? Ni kwa nini Serikali inaendeleakutegemea fedha za wahisani katika suala nyeti kama hili lamaji badala ya kuwa ni kipaumbele muhimu na kutengafedha za ndani ili kumaliza miradi ya maji nchi nzima?

Mheshimiwa Spika, uvunaji wa maji ya mvua. Pamojana maeneo mengi ya nchi kupata mvua za msimu, lakini kunawakati mvua hizi huja na mafuriko makubwa. Ni kwa niniSerikali haina mpango mkakati wa makusudi wa kuvuna majiya mvua ambayo hupotea kwa wingi wakati wa masika nabaada ya muda mfupi wananchi wanaanza kuhaha kutafutamaji?

Mheshimiwa Spika, ni kwa nini Serikali isione umuhimuwa kupunguza bei ya vifaa vya kuvunia maji ya mvua iliwananchi walio wengi waweze kumudu kununua nakurahisisha utunzaji wa maji?

Page 60: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

60

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, ni kwa nini Wizara isione umuhimuwa kushirikiana na Wizara zingine kama Elimu, Afya ili kupangamkakati wa kuvuna maji ya mvua katika idara na taasisi zotezilizo chini yake?

Mheshimiwa Spika, mfumo wa maji taka. Hili ni tatizola nchi nzima na hasa limekuwa sugu katika Jiji la Dar esSalaam. Hakuna udhibiti au mkakati mahususi wakutengeneza mfumo endelevu wa kudhibiti maji taka hasakatika kipindi cha mvua ambapo licha ya mafuriko makubwaambayo huharibu miundombinu ya barabara, pia wananchihutapisha vyoo vyao na uchafu hutapakaa barabarani nakwenye makazi ya watu, matokeo yake ni magonjwa yamlipuko kama kipindupindu na kuhara ambayo huua watukwa kiwango kikubwa. Hii pia ni aibu kwa Taifa lenye miaka51 ya kujitawala.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Spika, katikaukurasa wa 52 wa hotuba ya Waziri, kupatiwa Mji waNamanyere Dora za Marekani 1,900,000, naomba Wizaraitekeleze kama ilivyoahidi katika ukurasa 52 ili kuondoa adhaya maji Namanyere.

Mheshimiwa Spika, pia ukurasa wa 168, mpango wavisima kumi. Katika Wilaya ya Nkasi, vijiji vya Kabwe,Tambaruka na Mkinga hakuna chochote kinachofanyikakabisa na hakuna pesa kabisa zilizopelekwa.

Mheshimiwa Spika, mimi kama Mbunge wa Jimbo laNkasi Kaskazini na mzaliwa wa Mwambao mwa ZiwaTanganyika, nina mshangao mkubwa, katika kijiji chaKamwanda – Kirando, kuna matanki mawili makubwa ya majitangu enzi ya Mwalimu na maji ya Ziwa Tanganyika yako mita100. Cha kushangaa kabisa ni eti wameamua kuchukua majiya mto ambayo hayana uhakika sana yanaweza kukaukaau kuchafuka na mifugo na binadamu na huo mto sasatunategemea kwa umwagiliaji wa Bonde la Lwati, sasa hayomaji yako wapi kwa mradi huo? Mimi kama Mbunge nilishauri

Page 61: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

61

29 APRILI, 2013

wachukue maji Ziwa Tanganyika, jibu la ajabu eti maji ya Ziwasio salama, ajabu hayo ya mto yanaweza kuchafuka wakatiwowote ule. Wamekwenda kuchukua maji kilometa 8-9wakati maji yapo mita 100 tu. Je, huo si ubadhirifu wa pesaza umma? Wakazi wote wa mwambao mwa ZiwaTanganyika wanatumia maji hayo, iwe ajabu watuKamwanda. Naomba Wizara iingilie kati suala hili.

Mheshimiwa Spika, ajabu nyingine kijiji cha Mkingaeti hatuna maji wakati Ziwa Tanganyika liko mita 50 tu tokaZiwani, hii ni ajabu kabisa, inashangaza sana hawawataalamu wanatupeleka wapi? Wakazi wote wanaoishiMwambao mwa Ziwa Tanganyika, wanaoishi Zambia,Burundi, Congo wanatumia maji ya Ziwa waachekudanganya na kuitia Serikali hasara bure, maji ya kunywawashauriwe kuchemsha tu.

MHE. NAOMI A. M. KAIHULA: Mheshimiwa Spika,ninaomba nafasi nami nichangie katika hoja hii muhimu yamaji.

Mheshimiwa Spika, kama tujuavyo, kila mtuanafahamu kuwa maji ni uhai. Cha kusikitisha ni pale ambapoSerikali imeshindwa kuona kuwa suala la maji ni la kipaumbelekuliko jambo lolote. Maji ni zaidi ya barabara, sasa inakuwajekulundika mabilioni ya fedha kwenye barabara badala yamaji au ni kwa vile magari yanayomilikiwa na wanaumeyanahitaji kupita kwenye barabara?

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala la biashara yamaji. Hili ni tatizo kubwa. Serikali isikubaliane kabisa kulifanyasuala hili kuwa la kibiashara kwa vile maji ni haki ya msingi yabinadamu, hivyo kutowapatia maji wananchi tuliowapamatumaini ya maisha bora halafu tunawatosa sio haki. Majini mojawapo ya tatizo kuu la Taifa.

Mheshimiwa Spika, katika nchi ambayo imepataUhuru zaidi ya miaka 50 kushindwa kuwapatia maji watu wakeni fedheha. Inakuwaje nchi zilizo Jangwani mfano Libya,Misri na sehemu nyingine zenye majangwa ziweze kuwapatia

Page 62: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

62

29 APRILI, 2013

watu wake maji safi na salama, Tanzania ishindwe? Hiiinamaanisha Serikali haijapata kiini cha ukosefu wa majipamoja na tafiti zote zilizofanywa, Serikali ijizatiti upya.

Mheshimiwa Spika, maji yanazidi kupotea na Serikaliinaangalia tu, mambo mengine hayahitaji fedha bali nikujipanga tu. Iwapo Serikali za Mitaa zingechukulia jambohili kama ni la kufa na kupona kwa kutumia Sheriandogondogo za kudhibiti uharibifu wa mazingiraingewezekana tu. Nasema hivi kwa vile kwa umri wangunimeishi wakati wa Native Authority (NA), hizi zilijali sanamazingira pamoja na vyanzo vya maji. Watendaji wakewalikuwa waaminifu na walifanya kazi kwa uzalendomkubwa. Walizungukia maeneo yote muhimu na kukaguakwa umakini sana na kutoa adhabu papo kwa papo bilakupokea rushwa, kwa njia hii wakayaponya mabonde yamaji.

Mheshimiwa Spika, wameeleza WaheshimiwaWabunge wengi tu juu ya kuwapunguzia wanawake nawatoto wao adha ya maji. Kinachohitajika ni kupunguzamipango ya makaratasini na maneno bali tuweke katikavitendo, tutumie wataalamu kutoka NGO‘S walio na ujuziwa kuvuna (tap-water) maji kutokana na mvua zinyeshazoza msimu. Serikali iwatie moyo, matokeo mazuri yatapatikana.

Mheshimiwa Spika, tuwahi kuokoa mabondeyanayokauka sasa Wilaya ya Rungwe wakati yalikuwayamejaa maji yatiririkayo na chemchem za maji safi nasalama, sasa hamna tena, watu wameanza kuhangaika.Hebu Serikali yetu ifanyie kazi ushauri mdogomdogo tuwezekuwanusuru mama, dada na watoto wetu katika janga hilila kuzurura kutafuta maji.

Mheshimiwa Spika, mwisho naomba kusisitiza kuwatuache kushabikia Serikali kuwa imefanya vizuri wakati hayani maneno tu ya danganya toto mwaka hadi mwaka. Bali

Page 63: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

63

29 APRILI, 2013

tuitake Serikali kuongezewa bajeti na kuipa timeframe,kumaliza suala hili kabla ya bajeti nyingine ya 2014.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika,kwanza naanza kwa kumpongeza Mheshimiwa JumanneMaghembe (Waziri) kwa uwasilishaji wake mzuri na wenyeweledi wa hali ya juu kabisa.

Mheshimiwa Spika, pili, nampongeza kwa imani,uvumilivu na moyo wa kujitolea sana katika utendaji wakewa kila siku. Pia nampongeza Naibu Waziri Dkt. Mahengekwa uwezo mkubwa alioonyesha kwa kipindi kifupi tanguuteuzi.

Mheshimiwa Spika, katika uwasilishaji wa hotuba,tumeona kuwa wananchi wanasisitizwa kuvitunza vyanzo vyamaji, rasimali za maji na matumizi bora ya rasimali za majilakini kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Wizara yaMazingira ziweke mkakati wa wananchi kushiriki kulinda nakuelimishwa umuhimu wa uhifadhi. Ifike wakati sasa miti narasimali zote ziingizwe kuwa ni mali ya Taifa na ziwezinakabidhiwa kwa uongozi wa vijiji kama (assets) ambazozinafanyiwa inventory kila mwaka au kila baada ya mudafulani ambao utapangwa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kushukuru sana kwamradi wa maji Kandawale, Ngea na Njinjo, bado nasisitizakuwa miradi inayohusu World Bank hakika ni kero kwa maanakila eneo lina tatizo la aina yake. Ila katika Wilaya ya Kilwatatizo kubwa lipo katika uchangiaji wa asilimia kumi. NaiombaSerikali kwa maeneo ambayo yana hali duni kimaisha basiyenyewe ibebe jukumu la kuchangia kwa niaba yawananchi. Licha ya kuchangia pia Serikali iweke jitihadakatika usimamizi wa miradi maana yapo maeneo mengiambayo miradi imefanyika lakini hakuna mafanikio kwamaana maji hayakupatikana na Wakandarasiwameshalipwa stahili zao.

Page 64: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

64

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, eneo la Mtandango ambapotulipewa mradi wa World Bank kwa bahati mbaya majihayakupatikana. Hivyo, tunaiomba Serikali ikubali kubadilishachanzo cha maji kwenda Mikereng‘ende ambapo maji yapomengi na si ya kuchimba sababu eneo hili lina chemchem.

Mheshimiwa Spika, mfumo wa mgawanyo wa fedhaza maji uangaliwe upya maana maeneo ya mijiniyanapangiwa pesa nyingi bila sababu za msingi na marazote wao ndio wamekuwa chanzo cha matatizo kwa maanawalishindwa kulipia bills za maji katika mamlaka husika hadikupelekea mamlaka hizo kufilisika. Pia ukataji wa miti auuharibifu wa mazingira unachangiwa sana na mahitajio yamijini. Napendekeza katika mgawanyo wa miradi, licha yakubuniwa na Halmashauri au Wizara, tuweke mfumo ambaoviongozi kama Wabunge na Madiwani washiriki katikausimamizi wa miradi au mingine ipitie katika mifuko ya Jimbo.Hali ya wananchi kutokubaliana na vigezo vinavyotumikasasa kwa maana ya idadi ya watu, wananchi wa vijijini kamaKilwa wana mazingira hatarishi zaidi kuliko mijini lakini piaizingatiwe kuwa ukubwa wa eneo la Kilwa kama Wilaya nisawa na Mkoa mzima wa Kilimanjaro.

Mheshimiwa Spika, hatua madhubuti zichukuliwe ilikuimarisha ujenzi wa mabwawa ili kuhifadhi maji ambayomengi yanapotea bila kutumika huku ikifika wakati wakiangazi kunakuwa na upungufu mkubwa sana wa majikatika maeneo yote nchini haswa vij i j ini. Kamainavyoeleweka Tanzania haina tatizo la maji kwa maanavyanzo ni vingi mno, tatizo ni management ya maji haya.

Mheshimiwa Spika, lipo tatizo kubwa sasa katikamaeneo mengi haswa ambapo wananchi kwa nguvu zaowameamua kuchimba visima, lakini matokeo yakewanalazimishwa kulipia kila mwezi hali ya kuwa wametumiavyanzo vyao vya fedha kuanzishwa visima hivyo nawanatumia kwa matumizi yao binafsi.

Mheshimiwa Spika, napendekeza pia sasa kubunimbinu mpya za mapato ili kuweza kuimarisha huduma za maji

Page 65: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

65

29 APRILI, 2013

vijijini haswa kwa kutumia mamlaka za maji mijini kamaDAWASCO, DUWASA, MUWASA na kadhalika) ziwe zinatoagawio kwa mfuko maalum utakaoanzishwa ili kumaliza tatizola maji vijijini.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja, ahsante.

MHE. HENRY D. SHEKIFU: Mheshimiwa Spika, wakatiWaziri wa Maji akijibu swali langu namba 74 kwenye Mkutanowa Tatu, Kikao cha Tano, tarehe 12/4/2011, Serikali iliahidikuunga mkono juhudi za wananchi wa Tarafa ya Mlola kwakulipia michoro ya mradi wa maji unaoitwa Mtumbi WaterSupply ambao ungehudumia vijiji katika Kata tatu zaKwekanga, Malibwi na (Kilole) Makole. Kuanzia hapo mwaka2011 hadi hii leo ramani hazijachorwa na kukamilisha kazi hiyo,je, Serikali inatekeleza lini ahadi hii? Naomba ramani hiyoikamilike na liingizwe kwenye awamu ya pili ya miradi ya WorldBank.

Mheshimiwa Spika, maji mji wa Lushoto. Nashukuruziara za Manaibu Mawaziri wawili wa Wizara hii ya majiMheshimiwa Lwenge na Mheshimiwa Dkt. Mahengekutembelea Lushoto kujionea na kusikiliza vilio vya wananchiwa mji wa Lushoto kuhusu uhaba wa maji. Mawaziri wotewameahidi kusaidia katika kutafuta suluhu au ufumbuzi watatizo la maji. Naomba Wizara itutumie fedha tulizoombajapo shilingi milioni 200 kupunguza tatizo hilo la maji kwakujenga tank pale Magamba na kuunganisha maji kutokaMagamba kupelekwa kwenye matanki ya Kwembagon ilikupunguza tatizo hilo wakati tukisubiri mradi mkubwa wa majiutakaotekelezwa kwenye mpango wa maji mijini kupitia Benkiya Dunia. Nitasikitika sana kama sitapata msaada japo wahizo shilingi milioni 200 japo tumeomba shilingi milioni 400kama tulivyoandikia Wizara yake.

Mheshimiwa Spika, utunzaji wa vyanzo vya maji. Kwawananchi tunaoishi milimani, tunahitaji msaada wa SerikaliKuu katika kulinda na kusimamia vyanzo vya maji hasa katikamaeneo ambayo tunategemea maji ya mtiririko (gravity).Vyanzo vingi vimeharibika kutokana na usimamizi hafifu, maji

Page 66: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

66

29 APRILI, 2013

katika maeneo mengi ya milima hutoka kwenye chemchem,katika misitu. Tunaomba kama ikibidi Halmashauri itengewefedha mahususi za ulinzi wa vyanzo vya maji.

Mheshimiwa Spika, mifuko ya maji. Wananchiwameanzisha mifuko ya maji, nashauri mifuko ya maji igeuzweiwe Mamlaka ya Mfuko wa Taifa wa Maji – Serikali ichangiena wananchi wachangie katika mfuko wa Taifa wa Maji.Serikali ibuni vyanzo vingine vya kuimarisha mfuko huo, kamavile Road Fund inavyofanya kazi, Mfuko wa Maji ukianzishwakutakuwa na mtandao thabiti wa kuwafikishia wananchi majikama barabara zinavyojengwa.

MHE. IDDI M. AZZAN: Mheshimiwa Spika, hali ya majikatika Jiji la Dar es- Salaam bado hairidhishi. Pamoja namipango mizuri ya Serikali kutatua tatizo hili kubwa la majikatika Jiji la Dar es Salaam, tunaomba sana Serikali ihakikisheahadi ya kuondoa tatizo hili la maji ifikapo 2014/2015inatekelezwa kama mlivyoahidi wananchi wa Dar es- Salaamhususani Jimbo la Kinondoni wamevumilia kiasi cha kutoshana ahadi hizi.

Mheshimiwa Spika, ni matumaini ya wananchi waJimbo la Kinondoni na Dar es Salaam kuwa hayamliyowaahidi mtayatekeleza. Hata hivyo, wakatitunaendelea kusubiri mipango hiyo, tunaomba haya majikidogo yanayopatikana yagawanywe kwa wananchi bilaupendeleo.

Mheshimiwa Spika, pia Serikali idhibiti wauza majiambao wamefunga Water pump na maji yotewanayaelekeza kwenye matanki makubwa na visimavikubwa walivyochimba kuhifadhi maji hayo na kuyauza kwabei kubwa. Tena wanashirikiana na baadhi ya watumishiwa DAWASA, DAWASCO, tunaomba kuwe na udhibitimkubwa kwa hawa wanaouza maji.

Mheshimiwa Spika, mtandao wa majitaka katikamaeneo ya Mwenge, Kijitonyama ni kero kubwa, chembazinaziba, zinamwaga majitaka mitaani, kwenye makazi ya

Page 67: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

67

29 APRILI, 2013

watu lakini hakuna hatua za haraka zinazochukuliwa kuzibuaau kukarabati na kuleta usumbufu mkubwa kwa wananchi.Tunaomba Serikali ichukue hatua za haraka kukabiliana natatizo hilo la kuvuja majitaka.

Mheshimiwa Spika, maeneo ya Kinondoni, Block 41na Kinondoni Shamba hakuna kabisa mtandao wa maji takana eneo hilo ni oevu hivyo ni vigumu kuhifadhi majitakakwenye mashimo. Tunaomba maeneo hayo yaunganishwekwenye mtandao wa majitaka ambao unapita kandokandoya barabara ya Ally Hassan Mwinyi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. DKT. FESTUS B. LIMBU: Mheshimiwa Spika, kitabucha bajeti ya Wizara, ukurasa 54-55 kuhusu maji Magu Mjini,kinasema kwamba taratibu za kumpata Mtaalamu Mshauriatakayefanya upembuzi yakinifu, usanifu na uandaaji wamakabrasha ya zabuni na kwamba kazi hiyo itaanza mweziJulai, 2013.

Mheshimiwa Spika, kauli ya Wizara niliyoitaja hapo juuhailingani na kile kilichotendeka hadi sasa ukweli ni kwamba:Mtaalamu Mshauri alishafanya upembuzi na usanifu na kujana kiasi cha gharama zinazohitajika kutekeleza mradi huu.Mtaalamu Mshauri huyu alitumia takribani Tshs millioni 900.Niliuliza swali hapa Bungeni nikajibiwa na Wizara kwambazabuni imeshatangazwa. Leo anatamka kuwa anatafutatena Mtaalamu Mshauri afanye tena upembuzi yakinifuambao tayari ulishafanyika.

Mheshimiwa Spika, mimi naona Serikali haina niathabiti ya kuwapatia wana Magu maji kabla ya 2015.Matokeo ya kutotekelezwa mradi huu ni janga kwa CCM kwasababu: Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania aliwaahidi wana-Magu kuwa wasimuulize Mbungekuhusu maji wamuulize yeye. Mheshimiwa Waziri Mkuu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania alituhutubia Mkutano wahadhara mwaka jana na kusema kuwa angetoa (ndani yamuda mfupi toka siku hiyo) fedha (nafikiri million 800) ili

Page 68: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

68

29 APRILI, 2013

utekelezaji wa mradi uanze kutekelezwa kwa lengo la walaukupunguza kero za wana–Magu kuhusu maji. Mimi toka niweMbunge miaka 12 iliyopita kila awamu nimekuwa nikiwaahidiwana –Magu kuwa chagueni CCM ndiyo suluhisho la tatizola maji, waliniamini awamu tatu na nina mashaka tena iwapowataendelea kuwa na imani na CCM 2015.

Mheshimiwa Spika, Wizara ilikuja kuiunganisha Maguna Ngudu kabla ya bajeti hii na sasa Waziri anaiunganishatena Magu (kwenye ukurasa wa 54-55 wa hotuba ya bajeti)na Bariadi na Mwanhuzi. Hii inashangaza na inakatisha tama,wana-Magu tutaenda tuwaambie nini tena? Ningeombasana Mheshimiwa Waziri/Naibu Waziri/Katibu Mkuu mje Maguili muisaidie CCM kuelimisha wana Magu kuhusiana na hatimaya kero yao ya maji maana mimi sioni pa kuanzia.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa unyongesana.

MHE. RUKIA KASSIM AHMED: Mheshimiwa Spika,nashukuru sana kwa kupata nafasi hii ya kuweza kuchangiakatika Wizara hii ya Maji. Maji ni uhai, kiumbe chochotehakiwezi kuishi bila ya maji hivyo basi Serikali ni vyemaikaangalia ni namna gani ya kuweza kutatua tatizo hili sugundani ya Mikoa yetu, wanaoteseka zaidi ni wanawake nawatoto, wengi wao wanahangaika mpaka usiku na watotomigongoni wanatafuta maji wengine wanaliwa na simba nawanyama wakali wanapoteza maisha yao kwa sababu yakuhangaika kutafuta maji.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali iongeze fedhakatika Wizara hii ili iweze angalau kuongeza idadi ya visimakatika yale maeneo ambayo yana matatizo makubwa. Piakuwe na wataalamu ambao wanaweza kutoa elimu kwawananchi wetu waache tabia ya kulima katika vyanzo vyamaji. Hali hii ya wananchi kulima katika vyanzo vya majiinazidisha ongezeko la kupungua kwa maji katika maeneoyetu.

Page 69: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

69

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, kuna Ziwa Victoria, kuna ZiwaTanganyika ambayo yana maji mengi, hivyo basi naishauriSerikali isambaze maji angalau katika sehemu ambazo zikokaribu na Maziwa haya. Matatizo haya yapo hata katikamaeneo yaliyo karibu na Maziwa haya. Pia kuna Mito katikabaadhi ya maeneo yetu kwa mfano Mto Ruvu, MtoNanyumbu, Serikali iangalie namna ya kutafuta njia yakusambaza maji. Wananchi wanateseka sana na hililimekuwa ni tatizo la Kitaifa.

Mheshimiwa Spika, malalamiko makubwa ni kuwamiundombinu ni chakavu na baadhi ya wananchi wahalifuwanabomoa miundombinu na kuuza chuma chakavu.Naiomba Serikali itumie miundombinu isiyokuwa chuma,kama ni mabomba ya plastiki au mengineyo ili maji yawezekusambazwa bila ya wahalifu hawa kutokuweza kuharibumiundombinu hiyo.

Mheshimiwa Spika, pia Serikali itumie njia ya kuhifadhimaji ya mvua ili yaweze kutumika kipindi cha kiangazi.

MHE. VINCENT J. NYERERE: Mheshimiwa Spika,napenda kutoa shukrani za dhati kwa niaba ya wakazi waMusoma Mjini, kwa mradi wa maji ambao sasa unatekelezwa,japo imechukua muda mrefu sana kutekeleza mradi huu.

Mheshimiwa Spika, mbali na utekelezaji wa mradi huuila bado kuna matatizo katika Mamlaka hasa katika shughuliza uendeshaji na hii ipo kwenye Mamlaka karibu zote hapanchini. Mamlaka zimeajiri watu wa kukata maji kulikokuunganisha maji, hili ni jambo la msingi la kuangalia maanainachounganisha raia na Serikali yao.

Mheshimiwa Spika, Wizara bado ipo mbali naMamlaka za Maji za Miji ambapo utendaji wa baadhi yaMamlaka umekuwa wa kusuasua na wakati mwingineumekuwa mbaya sana. Wilaya ya Butiama ikumbukwe,maana kijiji kile mbali na kutangazwa kama Wilaya bado majiyanatoka mara tatu kwa mwezi na imepelekea baadhi yawatu kutolipa ankara zao za maji.

Page 70: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

70

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, bado kuna matatizo makubwasana ya maji pia Serengeti na Musoma Vijijini na Butiama.Ikumbukwe pia kuna mradi mkubwa sana unatekelezwaMusoma Mjini, kwa nini isiangaliwe namna ya kuyafikisha majiyale Musoma Vijijini, Butiama na Serengeti kama ilivyo mradiwa Ihelele unaotoa maji Ziwa Victoria kwenda Shinyangana Kahama kuelekea Tabora? Napenda sana kuona wakatiMheshimiwa Waziri anatoa majumuisho basi aje na majibumahususi yenye mikakati thabiti ya kupeleka maji Butiamana Serengeti kwa kutumia mradi unaotekelezwa.

Mheshimiwa Spika, pia najua mahitaji ya maji yapokwa aina tofauti, napenda kutoa rai yangu kwa Wizara kukaana Mamlaka za Maji za Miji au Halmashauri ili tuone ni jinsigani tunaweza kuweka fire hydrants kwa Miji inayokuwa iliitusaidie sana wakati wa uzimaji moto.

Mheshimiwa Spika, hujuma za miundombinu zipokatika maeneo ambayo mabomba ya maji yanapita na vijijihavina maji hapo hujaza hasira na kupasua mabomba.Nashauri sehemu zote zenye mikusanyiko zipatiwe maji kwabinadamu na mifugo yao ili angalau kupunguza sana hujumazinazotokea.

Mheshimiwa Spika, mengi yamesemwa na Wabungena wote kilio chao ni maji. Napenda sana kukupa shukranikwa mradi unaotekelezeka Musoma Mjini kwa ufadhili waAFD, tafadhali sana mradi huu huko mbele basi maji yafikeMusoma Vijijini, Butiama na Serengeti kama ulivyo mradi waIhelele.

MHE. BENEDICT N. OLE-NANGORO: Mheshimiwa Spika,kila Bonde na Mamlaka husika wabainishe vyanzo vyote vyamaji na mikakati ya kuvitunza na kuhakikisha sustainabilityya water resouces kwa nchi nzima.

Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Maji Mjini Kibayaijengewe uwezo zaidi ili iweze kutoa huduma kwa wakazi waKibaya wenye shida kubwa ya maji.

Page 71: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

71

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, usimamizi uboreshwe kwa ajili yamiradi hii ya vijiji 10 hali bado ni mbaya sawa na ilivyokuwakatika awamu ya kwanza ya mradi huu wa vijiji 10.

Mheshimiwa Spika, Wilaya zilizomo katika maeneokame ikiwemo Kiteto, zipewe kipaumbele kwa ajili yaprogramme ya maji kwa binadamu na mifugo.

Mheshimiwa Spika, Serikali itenge fedha ya kukarabatimabwawa yote yaliyovunjwa/bomolewa na maji katikamasika ya 2013. Bado gharama ya ukarabati ni ndogo kulikokujenga maeneo au mabwawa mapya.

Mheshimiwa Spika, Serikali ianzishe Mfuko wa Maji iliutumike kutekeleza miradi ya maji.

Mheshimiwa Spika, bajeti ya maji iongezewe fedhakatika msimu huu.

MHE. MCH. DKT. GERTUDE P. RWAKATARE: MheshimiwaSpika, naunga mkono hotuba hii kwa asilimia mia moja.

Mheshimiwa Spika, kero kubwa ya maji Wilaya yaKilombero. Tatizo sugu la maji Mji wa Kilombero, Ifakara,wananchi wanalia kwa kukosa maji safi. Tunaomba mradiwa maji wa Kiburuguto shilingi bilioni 213 ufanyiwe kazi, nikilio changu Bungeni maji kwa wakazi wa Ifakara na Wilayaya Kilombero.

Mheshimiwa Spika, mito 38 iko Wilaya ya Kilombero,kila kijiji kina Mto wake, kijiji cha Sonjo kuna Mto Sonjo, Idete– Mto Idete Kiberege – Mto Kiberege na kadhalika. Tatizo ninini? Mito hii mingi ni ya msimu. Tunategemea visima vyaMdundiko navyo ni vya msimu. Ahadi ya Rais daraja na maji2005/2010 lakini mpaka leo shilingi bilioni mbili mnasemanyingi. Tunaomba mtukumbuke Kilombero.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hotuba hii asilimiamia kwa mia.

Page 72: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

72

29 APRILI, 2013

MHE. MAJALI K. MAJALIWA: Mheshimiwa Spika,napenda kumkumbusha Mheshimiwa Waziri hali mbaya yamaji aliyoishuhudia akiwa ziarani na Mheshimiwa Rais kuleWilaya ya Ruangwa ambako aliona na kusikia wananchiwakilalamikia suala la ukosefu wa maji.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais aliahidi kujengamiundombinu ya maji kijiji cha Maudara, Makao Makuu yaWilaya ya Ruangwa, Rais na Mhandisi walitoa matumaini yakupata maji kutoka visima kumi (10) vya Kitandi ambavyoiliahidiwa kuunganishwa kwenye mtandao wa mabombayanayosambaza maji mjini Ruangwa. Sijaona mpango huokwenye bajeti ya mwaka 2012/2013.

Mheshimiwa Spika, kwenye orodha ya vij i j ivitakavyotekelezewa miradi ya maji vijijini, nashauri vijiji vyaNaudagala na Ngau vianze kwanza kwa sababu ya halimbaya iliyopo akilinganisha na vijiji vinavyoanza. Vijiji hivi vinamradi wa maji wa mwaka 1970 uliokuwa na mtandao wabomba ambao ulikuwa unahudumia vijiji vinne (Naudagala,Ngau, Chimbila B na Namahima). Mahitaji hapa ni kuwekaupya mtandao wa bomba ili maji yasafiri kwenye vijiji tajwa.

Mheshimiwa Spika, mgao wa fedha za Mfuko wa Majikwa Halmashauri ya Ruangwa hazitoshi kutokana na kuwepokwa matatizo makubwa ya maji kwenye vijiji vyetu. Naombamgao huo uangaliwe upya ili vijiji hivi navyo vipate maji kwanjia ya visima virefu.

Mheshimiwa Spika, ni matumaini yangu, nitapatamajibu ya hoja zangu, ahsante.

MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Spika,naomba Mheshimiwa Waziri wa Maji anifahamishe ni lini MjiMdogo wa Laela utapata maji? Nasema hivi kwa sababuMheshimiwa Waziri wa Maji alifanya ziara katika Mkoa waRukwa na ali j ionea mwenyewe namna wananchiwanavyopata shida ya maji katika Mji Mdogo wa Laela naalishauri vichimbwe visima vya maji badala ya maji yamserereko na akasema fedha ipo, hadi leo hii hakuna fedha

Page 73: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

73

29 APRILI, 2013

na Halmashauri inasubiri fedha hizo zipelekwe, je ni lini fedhahiyo itapelekwa? Maeneo ya kuchimba visimayameshaandaliwa, majibu ya Mheshimiwa Waziri wa Majiyanasubiriwa ikiwa ni pamoja na fedha. Ni l ini majiyatapatikana Mji Mdogo wa Laela? Namwomba sana Waziriatakapokuwa anatoa ufafanuzi wa hotuba yake, afafanuejuu ya tatizo la maji Mji Mdogo wa Laela na atoe kauli tatizoni fedha au nini?

MHE. HAWA A. GHASIA: Mheshimiwa Spika, naombakuanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Profesa JumanneMaghembe kwa hotuba nzuri yenye kuleta matumaini.

Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hizo, napendakuiomba Wizara ya Maji kuisaidia Mtwara Vijijini katikakuondoa tatizo la maji kwani zaidi ya 60% ya wananchi waHalmashauri ya Mtwara haipati maji kabisa (salama walayasiyo salama).

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwarainao mradi ambao AMREF/EU walionesha nia ya kusaidiakatika Kata za Mruma, Kiromba, Njengwa, Mtiniko, Kiyanga,Mtimbwilimbwi na Nitekela. Cha ksikitisha sasa ni zaidi yamiaka mitano mradi umeweza kufikisha maji chini ya 30%(thelathini). Kitu ambacho wananchi kinawashangaza nakuwasikitisha ni kitendo cha AMREF kuanza kujenga matenkina kutandaza mabomba katika maeneo hayo kabla hataya kuwa na uhakika wa chanzo cha maji. Mradi huuumekamilika kwa kukamilisha kujenga matenki nakuchimbisha wananchi mitaro na kuzika mabomba ardhinibaada ya hapo wananchi wanaambiwa wameshindwakupata chanzo cha maji. Namwomba Waziri au Naibu wakekutembelea Mtwara vijijini ili wakajione kiasi cha fedhakilivyotumika vibaya kwa kujenga miundombinu ambayo nimapambo tu kwa wananchi.

MHE. CELINA O. KOMBANI: Mheshimiwa Spika, Mji waMahenge, Wilaya ya Ulanga waliahidiwa na Mheshimiwa RaisDkt. Jakaya Kikwete mwaka 2008 kwamba atawapatiashilingi milioni 200 kwa ajili ya kumaliza tatizo la maji katika Mji

Page 74: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

74

29 APRILI, 2013

wa Mahenge. Napenda kuwashukuru sana Wizara ya Majiwamefanikisha zoezi hili kupitia MORUWASA wametekelezamradi huu kwa kiasi kikubwa, nawashukuru sana.

Mheshimiwa Spika, namwomba Mheshimiwa Wazirimradi huu umebakiza pampu ambayo inagharimu shilingizaidi ya milioni 300 na vifaa vingine shilingi karibuni 150.Naomba katika bajeti hii ya mwaka 2013/2014 watengefedha ili kumaliza mradi huu wa maji Mahenge.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja.

MHE. SHAFFIN A. SUMAR: Mheshimiwa Spika, awali yayote, niipongeze Serikali na Wizara ya Maji kwa kazi nzuriinayoifanya.

Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Waziri, jambolililonikwaza ni kwamba katika mwaka huu JICA itaendeleakusaidia lakini katika Jimbo langu la Tabora Kaskazini maeneoyaliyotajwa ni Mabama na Ufuluma lakini tayari Mabamamradi ulishaanza tangu mwaka juzi na Ufuluma walitoa ripotikwamba maji yameshindikana kupatikana, sasa kuna ninijipya katika bajeti ya mwaka huu? Naiomba Serikali ioneuwezekano wa kuongeza maeneo kwenye mradi huu waJICA katika Jimbo la Tabora Kaskazini.

Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2012/2013niliahidiwa kupewa shilingi 100 milioni ili kulinda vyanzo vyamaji ya Chemchem lakini hadi leo hata nusu haijatolewa navyanzo vinaendelea kuharibika. Naomba Serikali itusaidieharaka kutunza vyanzo vya maji ya Chemchem.

Mheshimiwa Spika, kuna mradi wa Bomba la Majikutoka Shinyanga – Nzega –Isikizya – Tabora ambalo nimkombozi kwa tatizo la maji Mkoani Tabora lakini bado tukombali sana na utekelezaji. Naiomba Serikali ione umuhimuwa kuanzisha mradi huu lakini pia ione uwezekano wakusambaza katika vijiji vinavyopitiwa na bomba la majikwenda zaidi ya kilomita 12 ili tuweze kusaidia wananchi waliowengi zaidi.

Page 75: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

75

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali ione namna yakuomba hela za World Bank zitoke kwa muda muafakamaana miradi ya World Bank katika Jimbo langu inasuasuasana.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika,naomba Waziri wa Maji, atakapojibu aseme kuhusu ombilangu la maji kijiji cha Mwandiga na Kibingo.

Mheshimiwa Spika, natanguliza shukrani.

MHE. BEATRICE M. SHELLUKINDO: Mheshimiwa Spika,mbona sijasikia wala kuona hela za kusambaza mabombaMakao Makuu Songe ambapo ni kero kubwa sana kamaulivyoona na inakimbiza sana Watendaji wazuri. Wazirialininong’oneza kuwa shilingi 400,000,000/= zimetengwa,nami jana nimewaambia kwenye Finance Kil indi nawakashangilia.

Mheshimiwa Spika, Bwawa la Kwamaligwa linahitajishilingi milioni 500 tu kujengwa upya baada ya kuvunjika namvua zinaelekea mwisho. Bwana linasaidia vijiji 15, Kata nne,ng’ombe zaidi ya milioni 12, mbuzi, uvuvi kilimo chaumwagiliaji na maji ya kunywa.

Mheshimiwa Spika, naomba majibu.

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika,nimejaribu kupitia mpango wa miradi ya 2013/2014 katikaukurasa 142, bado Halmashauri haikuweza kuleta maombiya fedha kwa ajili ya ule mradi wa Muhunga Heru Juu naKalunga, unaweza ukaona ni kwa kiasi gani hawajali. Hilowanalifahamu tangu last year please naomba wa-check lakufanya kwa project hiyo ya rehabilitation.

Mheshimiwa Spika, aidha vijiji vya Kidyama, Kigondohavina maji kabisa na havipo mbali na Mji wa Kasulu.Mhandisi haoni umuhimu wa watu hao kupata maji?

Page 76: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

76

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, naomba Waziri asahihishe katikakitabu chake ili walau ule mradi wa Muhunga Ward upatefedha mwaka huu.

MHE. AMINA N. MAKILAGI: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa nafasi ili niweze kutoa mchango wangukatika sekta hii muhimu ya maji kwa uhai wa Taifa.

Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kusema kuwamaji ni miongoni mwa changamoto ambayo inawakabiliwananchi hasa wanawake waishio vijijini. Kwa hiyo, badotunayo kazi kubwa ya kuhakikisha changamoto hii inaondokakwa gharama yoyote ile kwa uhai na uchumi wa Taifa.

Mheshimiwa Spika, huduma ya maji mijini, naombaniipongeze Serikali kwa kazi kubwa ya kuboresha hudumaya maji kwa kukarabati na kujenga miundombinu ya maji nakupunguza tatizo la maji kwa kiwango fulani. Naipongezapia mipango iliyopo ya kuhakikisha kuwa miji iliyobaki nayoinapata maji safi na salama.

Mheshimiwa Spika, huduma ya maji vijijini. Naombakuwasilisha kilio cha wanawake na wananchi waishio vijijinikuwa wanalo tatizo kubwa pamoja na jitihada zinazofanyikabado huduma ya maji iko chini sana. Naomba Serikali ijitahidikutafuta fedha za ziada katika mwaka huu wa fedha 2013/2014 ili ziweze kujenga miundombinu ya maji vijijini iliwanawake na wananchi waweze kuepukana na adha hiiya kushinda wanatembea umbali mrefu kutafuta maji.Nashauri wakati wa kuandaa bajeti 2014/2015 katikakuondokana na tatizo hili la ukosefu wa maji vijijini, Serikaliiweke mkazo kwa kutenga fedha za maji vijijini kuwakipaumbele cha kwanza.

Mheshimiwa Spika, kodi ya madawa ya maji.Nashukuru mpango wa kupunguza kodi ya madawa ya maji.Ombi langu kodi hii ifutwe kabisa kama tulivyoondoa kodinyingine kama hii ya maji ili Mamlaka za Maji ziweze kutoahuduma kikamilifu.

Page 77: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

77

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, Bodi ya Maji zote nchini ziwe nauwiano ulio sawa kati ya wanawake na wanaume ili kutoauongozi ulio bora.

Mheshimiwa Spika, upotevu wa maji na wizi wa majiudhibiti ufanyike kwa kujenga miundombinu ya majiisiyochakaa. Vilevile Serikali iwachukulie hatua kali wale wotewanaohujumu miundombinu ya maji na wizi wa maji.

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Spika,pongezi kwa Waziri, Naibu Waziri na Watendaji wake wotekwa kuandaa bajeti hii na kuileta hapa Bungeni.

Mheshimiwa Spika, mradi wa maji wa vijiji kumi kwakila Wilaya wa Benki ya Dunia ulipokelewa kwa matumainimakubwa sana kwa wananchi. Pamoja na umaskini waowaliuza mazao na mifugo yao wakachangia fedha asilimia20% iliyohitajika kama michango yao kwa mradi waliopewa.Asilimia hiyo 20 ya wananchi imekaa Benki na mpaka leohawaoni maji na hawaelewi nini kinaendelea. Wanaendeleakuteseka kwa maji wakitumia muda wao wa kuzalishashambani kwa ajili ya kufuata maji kilometa 8 - 10.

Mheshimiwa Spika, mradi huu umefeli, hakuna hataWilaya moja ambayo imekamilisha hata vijiji vinne na hatavisima vilivyochimbwa maji yakapatikana hayajasambazwa.Naomba Waziri aeleze Bunge visima ambayo majiyamepatikana na maji hayajasambazwa wala hakuna hatapump ya kuvuta maji wananchi wamebaki wanayaangaliatu, kwa nini maji haya hayanufaishi wananchi?

Wilaya ya Kaliua, kij i j i cha Ushokola, majiyamepatikana kwenye kisima tangu mwaka 2011 hadi leomkandarasi hakuwahi kurudi pale wananchi wakiulizaHalmashauri ya Wilaya hawana majibu wanayaangalia majihuku hayatumiki.

Mheshimiwa Spika, nini hatma ya vijiji tisa vya Kaliwana Urambo ambavyo mtafiti alipima akasoma kuna maji,wachimbaji wakaja kuchimba wakakosa maji? Tangu mwaka

Page 78: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

78

29 APRILI, 2013

2011 walipoondoa vyombo vyao hadi leo hawakurudi nahakuna majibu yoyote yanayotolewa kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, ni hatua gani zinachukuliwa kwawakandarasi waliopewa tender ya kutafiti maeneo yenyemaji, Urambo wakalipwa pesa zote na wachimbajiwalipokuja wakakosa maji? Halmashauri ya Wilaya wametuliakimya na hata kwenye vikao hakuna anayezungumzia swalahilo. Serikali inatoa maagizo gani kwa Halmashauri ya Wilayahiyo?

Mheshimiwa Spika, Tanzania tumezungukwa naBahari, tuna Mito, tuna Mabwawa, tuna Mabonde na tunaMisitu, Milima vyote hivi ni vyanzo vya maji. Kuna kila sababusasa Serikali ikabuni mbinu za kutumia maji ya Bahari kwa ajiliya matumizi ya watu. Nchi nyingine tena zilizoko Jangwanimfano Namibia, Dubai wanatumia Bahari inayowazungukakupata maji.

Mheshimiwa Spika, Serikali ifanye utafiti kwenye nchiza wenzetu wajue mbinu za kuchuja, kuondoa chumvi nakuondoa/kuua wadudu kwenye maji ya Bahari ili yawezekutumika ndani ya nchi kwa matumizi ya binadamu.

Mheshimiwa Spika, Serikali itoe elimu kwa wananchiili wavune maji ya mvua wakati wa mvua kwenye nyumbazao. Kutokana na wananchi kutojua umuhimu wa kuvunamaji hata wale wenye uwezo wa kuweka miundombinu yakuvuna maji na wao pia wanategemea maji ya Bomba naVisima.

Mheshimiwa Spika, miundombinu ya maji ya bombamaeneo mengi imechakaa sana na hivyo kusababisha kiasikikubwa cha maji kupotea. Serikali iweke mpango wakukarabati miundombinu kila baada ya muda fulanikutokana na uchakavu ili kuokoa maji yanayopotea chinihuku wananchi wanateseka.

Mheshimiwa Spika, tumeshuhudia miundombinu yamaji machafu Mkoa wa Dar es Salaam, maeneo mengi yapo

Page 79: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

79

29 APRILI, 2013

hatarini, chemba ziko wazi, mifuniko hakuna, uchafuunatapakaa barabarani, magonjwa ya tumbohayatapungua hata siku moja. Serikali inafumba macho hukuwanaona yanayofanyika kule maeneo ya Kariakoo. Miakaya nyuma zilijaa nyumba za kawaida za kuishi familia zakawaida na miundombinu ya maji machafu ilijengwa kwakuangalia majengo yale. Leo zile nyumba zotezimebomolewa yamejengwa magorofa ya floor 10 – 16,miundombinu ya maji machafu bado ni ile ya zamani.Matokeo yake, hali ni mbaya sana, Halmashauri na Manispaaya Ilala wanakusanya kodi ya soko kubwa la Kariakoo walahawawazi kupanua miundombinu, ile mifereji imejaa vinyesi.Serikali ieleze Bunge nini kimepangwa kufanyika kuhusianana miundombinu ya Kariakoo, Manzese na kwingineko?

MHE.ANNA MARYSTELLA J. MALLAC: MheshimiwaSpika, maji ni tatizo sugu sana katika nchi nzima na maji ndiyouhai, hakuna shughuli inayoweza kufanyika bila majikuhitajika. Tumekuwa tukishuhudia vifo vya Watanzaniavinavyotokana na magonjwa yanayosababishwa na majiyasiyo salama.

Mheshimiwa Spika, nikianza na Mkoa wa Katavi, halingumu ipo vijijini. Mwaka jana katika Bunge la bajetiniliongelea suala la maji vijijini na kuvitaja vijiji ambavyo havinamaji lakini Serikali hii wanayoita sikivu haisikii hata kidogo, shidani ileile vijijini, wananchi wanateseka bila sababu yoyote nawapo karibu na Ziwa Tanganyika au Mto Ugala lakini Serikaliimeshindwa hata kuvuta mabomba kutoa maji katika Ziwaau Mito iliyokaribu na vijiji ili wananchi waondokane na adhahii ya maji. Mpaka sasa wananchi wa vijiji vifuatavyo Ugala,Mbede, Chamalendi, Maji Moto, Iloba, Nkungwi, Kamsanga,Ngoma Lusambo, Ijenje na kadhalika wanaishi kwa kufukuakwa mikono ardhini kutafuta maji.

Mheshimiwa Spika, mpango wa maji katika vijiji kumikatika kila Halmashauri. Mpango huu haujatekelezeka kwanihata katika hotuba ya Waziri wa Maji mwaka 2012 iliongelewana vijiji vingi bado havina visima na wananchi wengiwanahangaika. Naiomba Serikali ielekeze macho vijijini kwa

Page 80: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

80

29 APRILI, 2013

kuwachimbia hata visima vifupi vyenye gharama ndogokwani tatizo la maji haliko Katavi tu bali kuna maeneo mengiambako wananchi wanakufa kwa magonjwa yanayotokanana maji yasiyo salama.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali kupitia Wizaraiwabane Wahandisi Wilayani kukagua miundombinu ya majikama mabomba ambayo yanakuwa yamepasuka nakumwaga maji hovyo huku wengine hawayapati. Ni upotevuwa fedha za Serikali.

Mheshimiwa Spika, katika suala la uboreshwaji wamiradi ya huduma ya maji katika Miji Mikuu ya Mikoa mipyakama Mpanda, Mkoa mpya wa Katavi, kama hotuba yaMheshimiwa Waziri wa Maji, ilivyoeleza ukurasa 52, tatizo hapasio mipango na maelezo mazuri ya Serikali bali tunamwombaMheshimiwa Waziri atueleze wananchi wa Katavi miradi hiiitakamilika lini? Maana muda ni mrefu umepita bila utendajikazi kuonekana hasa vijijini.

Mheshimiwa Spika, mwisho, ninaomba nitoe ushaurikwa Mheshimiwa Waziri wa Maji kuwa Mawaziriwanapofanya ziara za kikazi katika Wilaya au Mikoa wasiendekichama bali waende Kiserikali na kujionea wenyewe miradiinavyokwenda kuliko kuandaliwa Mezani taarifa hukuwananchi wanakufa kwa adha ya maji salama.

Mheshimiwa Spika, nawasilisha.

MHE. SALUM K. BARWANY: Mheshimiwa Spika,kumekuwepo na uzoefu mara nyingi juu ya mikataba yauchimbaji visima na utafiti wa maeneo ya upatikanaji majiambako kumepelekea kulitia hasara Taifa. Mfano ni mradiwa visima kumi (10) uliopo eneo la Kitunda ambao uliingiziaTaifa zaidi ya hasara ya shilingi bilioni saba. Serikali haioni kwasasa utafiti wa utafutaji maji uende sambamba na uchimbajiili mkandarasi anayepewa kazi hiyo akabidhi visima ambavyotayari vina uwezo wa kuzalisha maji? Mradi wa Kitunda nivisima viwili tu kati ya kumi ndivyo vyenye uwezo wa kutoamaji machache.

Page 81: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

81

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, mradi wa maji wa Kineng’eneuliopo Manispaa ya Lindi ambapo ulizinduliwa na Waziri waTAMISEMI, Mheshimiwa Aggrey Mwanri tarehe 27 Februari,2012, Mheshimiwa Waziri hakukubaliana na mashine yakusukuma maji iliyonunuliwa na Mkandarasi na kuagizaiundwe Kamati itakayofuatilia BOQ kuona ubora, lini na wapiimetoka mashine hiyo, mpaka leo Mkandarasi huyoameikatalia Kamati hiyo kutoa namba ya injini ya mashinehiyo kwa madai kwamba ipo chini na imeshajengewa kwazege.

Mheshimiwa Spika, aidha, Mkandarasi huyo alitakiwaachimbe mtaro wa bomba wenye urefu wa cm 100 lakinimpaka anaunganisha bomba urefu wa mitaro hiyo ni kati yacm 50 mpaka cm 60. Vilevile inaonekana hata ubora wamabomba sio sahihi kwani wakati maji yanasukumamabomba hayo yamepasuka hata katika maeneo yaviungio. Baya zaidi ni kuwa hata tenki alilojenga linavuja nataarifa nilizonazo ni kuwa anatafuta njia ya kuziba virakamaeneo yanayovuja haraka haraka.

Mheshimiwa Spika, namwomba Mheshimiwa Wazirialieleze Bunge hili na wananchi wa Jimbo langu kuwa hatuagani zitachukuliwa dhidi ya ukaidi wa Mkandarasi huyo kwakukataa kuonyesha BOQ za manunuzi ya mashine na vifaahivyo ili kunusuru fedha nyingi zitolewazo na Serikali kutokanana kodi za wananchi.

MHE. JOB Y. NDUGAI: Mheshimiwa Naibu Spika, tatizola maji ni kubwa sana katika Vijiji vya Kongwa. Matatizo nimengi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza uwezo wa MhandisiWilaya na Idara ya Maji ni mdogo mno.

Pili, Consultant A&O na Wakandarasi, baadhi hawafaina miradi ni ya hela nyingi sana (ya WB) Kijiji kimoja kati yaShilingi milioni 300 na Shilingi milioni 600. Tungekuwa namamlaka katika Halmashauri ya Wilaya tungetumia wastani

Page 82: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

82

29 APRILI, 2013

wa si zaidi ya Shilingi milioni 100 kila Kijiji kwa survey, kuchimbatenki, pampu na mashine .

Mheshimiwa Naibu Spika, Consultant wa Halmashauriya Wilaya zote Mkoa wa Dodoma ni O&A au A&O ni feki;hafai, hafai, hafai!

Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti ya Maji Vijijini kitaifani ndogo sana, hatukubali iongezeke.

Mheshimiwa Naibu Spika, toeni madaraka makubwakwa Halmashauri ya Wilaya Kongwa kuamua kiasi cha fedhacha kutumika kwa kila mradi kwa Kijiji ili tutumie helatunazopata kwa Vijiji vingi zaidi badala ya hela kutumika nama-consultants ambao hawana faida yoyote naMakandarasi feki.

MHE. SAID A. ARFI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninamambo mawili tu katika hoja hii kwa kujielekeza katika Jimbolangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Wizara kwakutenga pesa kiasi cha Shilingi bilioni 1.5 katika hotuba yaWaziri Ukurasa wa 52 na 53, kwa kuendeleza Mamlaka yaMaji ya Mji wa Mpanda. Ahsante sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, umekuwepo mradi waHalmashauri ya Mji, Mpanda wa maji wa Ikolongo ambaohivi sasa unaendelea, pamoja na kwamba haujatengewafedha Bajeti hii, isipokuwa, tayari Shilingi milioni 600 zimefikaMpanda kwa bajeti ya 2012/2013 na hazijatumika, na mwakawa fedha unaishia 30 Juni, 2013. Kwa sababu tu Wizarahaijatoa letter of objection ya kuridhia kusaini mikataba yakutandika bomba kwa vijiji ambavyo Waziri amevitaja katikajedwali no 11, naomba sasa Wizara itoe hiyo letter ofobjection mapema na nitashukuru kama nitaarifiwa kamabarua hiyo imetolewa au itakapotolewa ili kuharakishakupunguza tatizo la maji Mpanda Mjini.

Page 83: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

83

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, ni vyema sasaWizara ikaweka kipaumbele katika kuvuna maji ya mvua kilainapowezekana kwa matumizi ya binadamu na mifugo,kwani akiba ya maji katika sura ya dunia inapungua kwa kasikubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushuru sana.

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kutumia nafasi hii kwa njia ya maandishi kuipongezaSerikali kwa juhudi zake kubwa za kuwapelekea Watanzaniahuduma ya maji wakiwemo wananchi wa Singida, Manispaaya Singida hususan Mjini kulikuwa na kero kubwa ya maji. Sasamaji yamepatikana kupitia mradi wa maji wa World Bank naBADEA, wananchi, hususan akina mama, wanafurahiamatunda ya Serikali yao ya CCM. NinawapongezaMheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete - Rais wa Jamhuri yaMuungano ya Tanzania, Mheshimiwa Profesa Maghembe -Waziri wa Maji, Katibu Mkuu na Watendaji wote walioshirikikuibua na kutekeleza mradi huu. Vile vile nawapongeza kwakuandaa bajeti nzuri ingawa fedha ni ndogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasikitika kuieleza Serikalikuwa Jimbo hili lina upungufu mkubwa wa maji. NaaminiSerikali inatambua tatizo ambalo limetokana na siasa, kwanimiradi ya maji hutekelezwa kwa mpango shirikishi, wananchihuchangia fedha na kufungua akiba benki ndipo Serikalihuchangia pamoja na wahisani wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa wananchiwalikatazwa kuchangia mradi wowote, naishauri Serikalikuacha tabia ya kuwatesa wananchi hususan wanawakena vijana wanaotembea mwendo mrefu kutafuta maji. Hivyo,ni lazima kauli ya Serikali itumike ili wananchi wakubalianena Serikali, siyo mtu kwa maslahi yake. Nitashukuru kusikia kauliya Serikali yetu yenye kuwajali watu wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala hili siyo dogo, kwaniVijiji na Kata ambazo zina tatizo la maji, vingi lazima Serikaliichukue hatua.

Page 84: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

84

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile napenda kuijulishaSerikali yangu kuwa inatakiwa kutoa kipaumbele kwa Jimbohili la Iramba ya Mashariki kwani Vijiji na Kata, nyingi zina shidaya maji ili tusiwape Wapinzani nafasi. Naomba Serikai iombetaarifa ya tatizo la maji Wilaya mpya ya Mkalama ili nguvukubwa ielekezwe huko. Vile vile tuwe na huruma kwa Mbungewa Jimbo, Mheshimiwa Salome Mwambu ambaye amekuwana tatizo la kiafya muda mrefu. Nitashukuru endapo Waziriwakati wa majibu atasema kidogo kuhusu wananchi waJimbo la Iramba Mashariki wasikie, tafadhali. MfanoMatongo, ardhi ina mwamba, hivyo maji lazima yatokeMisenye. Vile vile Vijiji kumi tulivyopewa maji, yametobolewana kupatikana lakini bado hakuna miundombinu yakuunganishwa ili maji yaanze kupatikana Kata za Miganga,Nkalankala, Mwanga na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, maombi ya Halmashauri nikupatiwa fedha za Vijiji 30. Napenda kujua: Je, tumetengewafedha?

Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli usiyopingika kuwaDar es Salaam ndiyo Tanzania. Hivyo ni muhimu sanakuhakikisha ukarabati wa njia za maji unatiliwa mkazo, kwanihali ya maji Dar es Salaam siyo nzuri. Mfano mzuri ni MagomeniMwembe Chai na Magomeni Kagera Mtaa wa Pongwe,wakazi wengi wamechimba chini ili wafungue njia za majiwapate maji, jambo ambalo ni kosa kubwa. Ili kuondoa adhahii ambayo pia imechangiwa na ujenzi wa barabara mpya,ni Jiji la Dar es salaam litengewe fedha za kutosha nausimamizi madhubuti. Haya maji ya kuchimba chini pia siyosalama, wananchi wataugua maradhi ya matumbo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, napenda kumaliziakwa kuipongeza DAWASA kwa kazi zao nzuri za kusimamiamiradi mikubwa ya maji na DAWASCO kwa kusambaza, hivyowatiwe moyo kwa kuongezwa fedha. Bila fedha,tutawalaumu bure.

Page 85: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

85

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie kwa kuungamkono hoja hii.

MHE. BETTY E. MACHANGU: Mheshimiwa Naibu Spika,maji ni uhai. Bajeti ya Wizara hii ni ndogo hasa ukizingatianchi yetu imeanza kunyemelewa na mabadiliko ya tabianchi.Vyanzo vingi vya maji vimeharibika, ukame upo hasa katikaMikoa ya Kanda ya Kaskazini, mito imekauka na hivyo hatavisima vitakavyochimbwa vinaweza visitoe maji ya kutoshaau baada ya muda mfupi vitakauka.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Serikali isimamiemkakati wa kukemea na kulinda mifumo ya maji iliyowekwakatika Halmashauri ya Wilaya. Mfano, mradi wa Vijiji 10 katikakila Wilaya, lakini na miradi mingine yote inayotokana nafedha ya Wafadhili.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu wa Vijiji 10 ulianzatangu 2004 na hadi leo katika Halmashauri na Wilaya ya MoshiVijijini ni Vijiji viwili tu umeanza kutekelezwa vya Kovi Kaskazinina Kiriu Kusini ambavyo vilitengewa Shilingi bilioni 1.02. Vijijivingine vitatu vya Mawanjeni, Matala na Kilimo Makuyunigharama yake ni Shilingi bilioni 2.3, bado na hata mkatabahaujatiwa sahihi.

Mheshimiwa Naibu Spika, bado Vijiji vitano vitakuwahavijashughulikiwa, mfano Vijiji vya Machame Juu naMachame Chini vitakavyogharimu Shilingi milioni 704.Wananchi wa maeneo haya hawajawahi kupata maji yabomba, siku zote wameendelea kunywa maji ya mifereji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kero ya tatizo la maji katikaKij i j i cha Matala ni kubwa. Wanawake na watotowanatembea zaidi ya kilometa tano kutafuta maji, wenyematrekta na bodaboda wana-take advantage ya tatizo, kiasindoo moja ya maji inauzwa Sh. 1,500/= fedha ambazo ninyingi kwa mkulima wa kawaida.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata katika Vijiji vilivyo chiniya Mlima Kilimanjaro, mfano Kijiji cha Mwika Maring’a Chini

Page 86: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

86

29 APRILI, 2013

wanapata mgawo wa maji na mara mbili kwa wiki. NaiombaSerikali itekeleze mradi wa maji katika Vijiji vitatu vilivyobakina hasa Kijiji cha Matala kuondoa adha ya ukosefu wa maji,gharama kubwa ya kununua maji na unyanyasajiwanaopata wanawake na watoto wanaotembea mwendomrefu kutafuta maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, fedha iliyotengwa kwaMfuko wa Maendeleo katika Halmashauri ya Moshi mwaka2012/2013 ni Sh. 601,830,844/=. Mwaka 2013/2014 fedha hiyoimepungua kufikia Sh. 525,238,522/= kipindi ambacho Mkoawa Kilimanjaro unakabiliwa kwa kiasi kikubwa na ukame.

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali itekelezemradi katika miradi ya Vijiji tajwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Naibu Spika,kwa mara ya kwanza naanza kwa kutokuunga mkono hojailiyo mbele yetu na ninazo sababu za kwanini siungi mkonohoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, nalazimika kutokuungamkono hoja kutokana na hotuba ya Mheshimiwa Waziriukurasa wa 51 inayoanzia na kichwa cha habari miradi yamajisafi na usafi wa mazingira katika Miji inayozunguka ZiwaTanganyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni jambo lisiloingia akilinikuwa Wizara inaweza ikawa haifahamu Jiografia na kuwana uhakika Ziwa Tanganyika linagusa Wilaya za Kigoma,Mponda Vijijini, Nkansi na Kalambo na siyo Wilaya wala Mjiwa Kasulu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Kalambo yenyeMakao Makuu yake Matai ina Vijiji vifuatavyo ambavyovinategemea maji ya Ziwa Tanganyika kwa kunywa nashughuli zote za kibinadamu; Kipwa, Kapele, Kapozwa,Kilewani, Kasanga, Muzi, Somazi, Kipanga, Katil i na

Page 87: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

87

29 APRILI, 2013

Kantalamba, Vijiji hivi vyote vina matatizo makubwa sana yamaji na hivyo hukumbwa na kipindupindu kila kipindi chamvua kutokana na kunywa maji machafu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sielewi ni sababu zipizilizosababisha Mji wa Kasulu kuingizwa katika mpango huuna kusababisha pesa nyingi kiasi hiki cha Dola za Marekanimilioni 4.6 kutengewa Mji wa Kigoma Kasulu, dola za Marekanimilioni 2.3, Mpande 3.1 na Namanyere 1.9 na kuachwa Wilayaya Kalambo na Vijiji vyote huku ikiwa inapakana na nchi yaZambia. Ni sababu zipi zilizosababisha Mji wa Kasulu kuingizwakwenye huu mpango wakati hakuna eneo lolote la Wilayahii inapitiwa na Ziwa Tanganyika? Au ni kuaminisha kwambanafasi ya Kalambo kwa maana ya Matai na Vijiji vyamwambao wa Ziwa Tanganyika imeporwa na Wilaya yaKasulu ambayo haina sifa yoyote kuwa inanufaika na mradihuu?

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na upendeleowa dhahiri kwa miradi mingi inayotekelezwa mwambao mwaZiwa Tanganyika kuelekeza pesa nyingi Mkoa wa Kigoma nakuona maeneo mengine ya Mkoa wa Rukwa kamaApandage suala ambalo ni hatari.

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Wizara inapotoamajibu itoe ufafanuzi na kutenga pesa kwa Wilaya yaKalambo, kwani ndiyo yenye kustahili na siyo Mji wa Kasulu.

MHE. KULTHUM J. MCHUCHULI: Mheshimiwa NaibuSpika, namshukuru Waziri wa Maji na Naibu Waziri pamojana Watendaji wote kwa kuendelea kutambua uwepo wamradi wa maji ambao unatekelezwa katika Mji wa IkwiririWilayani Rufiji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri ni linimradi wa maji unaotekelezwa katika Mji wa Ikwirir iutakamilika? Kwa sababu umeahidiwa na uliahidiwakukamilika mwaka 2010/2011, haukukamilika; mwaka 2011/2012, haukukamilika; na leo tena mwaka 2013/2014 hotubainaonesha mradi umefikia asilimia 95%.

Page 88: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

88

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa Kijiji cha Ikwiririwamechoshwa na ahadi za Serikali ambazo zinatolewa kilamwaka na mradi haukamiliki. Wananchi wa Ikwirir iwanaomba mradi wao ukamilike ili waweze kupata maji safina salama kama Watanzania wengine wanavyopatahuduma hii muhimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mgawanyo wa fedha zaSerikali katika Wizara ya Maji hauoneshi kabisa dhamira yaSerikali hii ya CCM kutaka kuwapunguzia wananchi waTanzania hasa wanaoishi Vijiji adha ya kukosa maji safi nasalama ambayo wameyakosa kwa miaka mitano tangutupate uhuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2006/2007 Serikaliilipanga Shilingi bilioni 16.8 kwa Wizara na kufikia mwaka 2012/2013 Serikali ilitoa Shilingi bilioni 3.8. Hii inaonesha dhahiri kuwaSerikali hii haina nia ya kuwakomboa Watanzania kuwapatiamaji safi na salama kwa kuendelea kutegemea pesa zaWahisani kama ambavyo World Bank wanavyoyumbishautekelezaji wa miradi ya Vijiji kumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

MHE. LUCY P. OWENYA: Mheshimiwa Naibu Spika,kama tujuavyo, maji ni uhai. Bila maji hakuna maisha. VitaKuu ya Nne ya Dunia itatokana na kugombania maji. Majiyanahitajika katika kila kitu; binadamu, mifugo, kilimo, hatampaka magari tunayoendesha lazima yawe na maji ili uwezekuliendesha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Kilimanjaropamoja na kuwa na mlima wenye theluji ya kutosha, lakiniwakazi wa Kilimanjaro hususan Moshi Vijijini kuna uhabamkubwa wa maji. Miaka ya 1970 kulikuwa hakuna shida yamaji kabisa, wananchi wa Old-Moshi, Kibosho, Uru, TPC,Mabogini walikuwa na maji mengi yakitiririka kwa miferejikutoka Mlima Kilimanjaro. Walilima kilimo cha ndizi na kahawakwa umwagiliaji wa mifereji. Maji yalikuwa ni safi na salama,kulikuwa hakuna magonjwa. Je, Serikali imefanya utafiti

Page 89: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

89

29 APRILI, 2013

kuona tatizo ni nini? Sasa hivi wananchi wa Moshi Vijijiniwanapata maji kidogo tena kwa mgao.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa nini Sheria ndogo zaHalmashauri hazifuatwi? Kwa mfano, bado watu wanaharibuvyanzo vya maji, wanalima kando kando ya mito, wanakatamiti, kutokuwepo na maji ni kupoteza nguvu kazi. Mfano,akina mama Kata ya Mbokomu na kwingineko wanatembeazaidi ya kilometa tatu kutafuta maji, watoto wanasitishamasomo, wanakwenda kukinga maji badala ya kufanyashughuli za maendeleo kwa maana wanapoteza mudamwingi kuchota maji, watoto wanafeli kwa kukosa masomodarasani. Kwa sasa hivi maeneo kanda za chini Moshi, majiya Mto Kisasago/Mto Rau, yote yanaelekea kwenyemashamba ya watu na kuharibu mimea iliyopandwamahindi.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni kwa nini Serikali isijengeBwawa kubwa kule chini Mandaka wakavuna maji hayo nayakatumika baadaye kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji?

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri kwamba, kwakuwa shule nyingi za Serikali hazina maji, Serikali ifanye jitihadaShule ziwe na running woter ili kuepukana na magonjwa yamilipuko kama kuharisha, typhoid na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kila mtu aweze kuhifadhimaji, Serikali ipunguze kodi kwenye vifaa vya kuhifadhi majikama matenki (Simtank), ni ghali sana. Siyo hilo tu, pia bei yamaji haitofautiani na bei za soda na juice. Kodi zipunguzwe,maji ya chupa yapatikane kwa bei nafuu, kila mtu awezekununua. Hii itasaidia sana kuepuka magonjwa ya milipuko.Je, miradi ya maji kwa Vijiji kwa visima 10 kila Kijiji kwa Mkoawa Kilimanjaro vimetelekezwa kwa kiasi gani?

Mheshimiwa Naibu Spika, hotuba zote za Bajeti 2005– 2013 Serikali imekuwa inalieleza Bunge hili kuhusu miradi hii;ni lini Serikali itatenga fedha za ndani kwa ajili ya maji Vijijini?Hili ndilo tatizo la kutegemea wafadhali wa Wold Bank;

Page 90: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

90

29 APRILI, 2013

hawatoi fedha za maendeleo kwa wakati na wakitoahawatoi zote.

MHE. AMOS G. MAKALLA: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba nichangie Wizara ya Maji, nikijielekeza kwenye hojanilizouliza mwaka 2012 kwenye Bajeti ya mwaka 2012/2013.

Mheshimiwa Naibu Spika, kero ya maji katika Jimbola Mnvomero ni kubwa. Naomba kujua hatua za utekelezajiMradi wa Benki ya Dunia katika Vijiji vya Kipera, Mlali, Doma,Kwadoli, Hoza na Salawe. Baadhi ya Vijiji hivi, visimavilishachimbwa, lakini usambazaji mabomba bado. Naombamajibu, nini kilichokwamisha awamu ya pili ya utekelezaji?Je, lini Vijiji hivi wananchi watapata maji?

Mheshimiwa Naibu Spika, Vijiji vya Kipara na Mlaki,Kigugu na Bumu tunaelezwa kutakuwa na miradi ya majikutumia vyanzo vya mserereko. Je, miradi hii itatekelezwa lini?Kijiji cha Mlumbilo kinatajwa katika Mradi wa Benki ya Dunia,nataka kujua, ni lini wananchi wa Kijiji hiki watapata maji?

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2012 niliishauriWizara ikanijibu inayafanyia kazi maombi ya maji Kata yaHuale, Hagali, Buduki, Mgeta Tchengema, Kikeo na Nyandinawapatiwe maji kupitia vyanzo vya mserereko. Kwanini Wizarahaijapeleka wataalam Tarafa ya Mgeta kujionea vyanzo vyamaji ya mserereko ili kutatua tatizo la maji safi na salama?Wizara inatoa tamko gani juu ya maombi haya?

Mheshimiwa Naibu Spika, Kata za Maskati na Kindazina vyanzo vizuri vya maji ya mserereko. Naiomba Wizaraitafute wataam ili wananchi wa maeneo haya wapate majisafi na salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. DKT. BINILITH S. MAHENGE: Mheshimiwa NaibuSpika, namtakia baraka tele Mheshimiwa Waziri wa Majikatika kuwasilisha na kupitisha bajeti yao leo.

Page 91: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

91

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Vijiji vya Luhagara,Mabuni, Litumbandyosi, Kingoli na vingine ni Kijiji cha Paradisona Ndongozi, vipatiwe maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, DED ameniambia DDCA inamitambo yake, ipo Mbinga sasa. Napendekeza tutumienafasi hii, wakati mitambo hiyo inafika kwa shughuli hiyomaalum watuchimbie pia visima katika maeneo tuliyoongeana hayo mawili. Tukiwezeshwa kifedha, pia tutashukuru sana.

MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Naibu Spika,pamoja na hotuba nzuri, naomba kujua yafuatayo:-

(i) Ahadi ya kupeleka maji Kagongwa – Isaka(hadi Tinde na kadhalika), iliyotolewa na Mheshimiwa Raistangu mwaka 2008 imefikia wapi katika utekelezaji?

(ii) Ahadi ya Serikali ya kuweka birika za maji yamifugo (Cattle troughs) maeneo yaliyofikiwa na bomba kuula Victoria – Kahama, imefikia hatua gani katika utekelezaji?

(iii) Kuna Mradi wa Ubia baina ya Serikali naMgodi wa Bulyanhulu kupeleka maji Bulyankulu na Bugarama.Mgodi walishatoa fedha za utafiti (feasibility study), lakiniSerikali haijatoa commitment yoyote. Kwanini?

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi unahitaji Shilingi bilioni10. Mgodi uko tayari kutoa 50%, mbona Serikali iko kimya?Je, Serikali iko tayari kushiriki katika mradi huu?

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya ufafanuzi wamambo haya, naunga mkono hoja hii.

MHE. HAMOUD A. JUMAA: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa fursa hiiya kuchangia hutuba hii ya Bajeti ya Wizara ya Maji ya mwaka2013/2014. Maji ni uhai, hakuna asiyejua hilo, na kila kiumbekinategemea maji. Napenda kumpongeza MheshimiwaWaziri kwa hotuba yake nzuri na yenye mikakati mizuri kwaWatanzania. Mipango hii ikitekelezwa kama ilivyopangwa.

Page 92: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

92

29 APRILI, 2013

Basi matatizo ya kutokupatikana kwa maji yanayolikabili Taifahili yatapungua kama siyo kwisha kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia hojahii kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, tunatambua umuhimuuliopo katika Sekta ya Maji, kwani maji ni uhai, viumbe vyotehutegemea maji; bila maji hakuna uhai. Upatikanaji wa majihutegemea zaidi vyanzo vyake. Kutokana na hili, tusipokuwawaangalifu na kutunza mazingira na vyanzo vyetu vya maji,basi tatizo la upatikanaji wa maji halitakwisha na litakuwaendelevu. Hapa nazungumzia zaidi ukataji wa miti ovyo,kutotunza vyanzo vya maji. Ukataji huo wa miti husababishaukame. Kwa maana hiyo, vyanzo vya maji, mito, maziwahukauka, mifugo hufa na binadamu kukosa maji kutokanana kutotunza vyanzo vya maji na ukataji miti pembezoni mwamito na maziwa husababisha mmomonyoko wa ardhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda pia kuipongezaSerikali kwa jitihada zake katika Sekta hii ya Maji kujitahidi nakuhakikisha kupatikana kwa maji safi na salama kwawananchi wake ingawa changamoto ni nyingi na Serikalihaina budi kuzifanyia kazi changamoto hizo. Tatizo laupatikanaji wa maji safi kwa nchi nzima limezidi kukua sikuhadi siku, na tatizo hili hupelekea hasa wanawake kupatashida kwa kutembea umbali mrefu kufuata maji huku wakiwawamebeba watoto mgongoni na hata kukaa kwa mudamrefu kwenye foleni kwa kusubiri maji. Hali hiyo imepelekeawananchi kutumia maji yasiyokuwa salama na hatarishi kwaafya zao. Kwa Mijini, wananchi wamekuwa wakikesha usikukucha kwa kusubiri maji, kununua maji kwa bei ya juu sanana hali ya kipato chao ni kidogo. Hali hiyo imekuwa ikizidishaugumu wa maisha kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi mingi ya majiimekuwa ikifanyika na kwisha, lakini baadhi ya Miradi hiyohuishia kutokutoa huduma yoyote kwa wananchi.

Page 93: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

93

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna huu mradi wamabomba ya kichina ambayo yaliwekwa karibu sehemunyingi Jijini Dar es Salaam, lakini mpaka leo mradi huohaujaanza kutoa huduma yoyote ya maji. Mradi huuungeanza kusambaza maji kwa wananchi, basiungepunguza sana adha ya maji waipatayo wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba MheshimiwaWaziri atuambie, kwanini mradi huu mpaka leo haujaanzakufanya kazi kwa mabomba yake kuanza kutoa maji?

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo ni jambo lakusikitiksha sana pale Serikali inapojitahidi kutatua matatizohaya ya upatikanaji wa maji safi kwa kuanzisha miradi yakuchimba visima, lakini watumishi wasiokuwa waadilifuhuihujumu miradi hiyo na kuitia hasara Serikali. Nashauriwatumishi kama hao kuchukuliwa hatua kali za kisheria,kusimamishwa kazi, kufikishwa Mahakamani; wakikutwa nahatia, adhabu kali itolewe juu yao.

Vilevile nashauri Wizara iweke utaratibu wa kuwapaelimu ya kutosha wananchi jinsi ya kuvuna maji yatokanayona mvua. Hii itasaidia kwa zile sehemu ambazo bado tatizola maji ni kubwa, ili wapate mbinu hizo za uvunaji wa majihayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Kibaha Vijijini kiliochao kikubwa na cha muda mrefu katika Wizara hii niupatikanaji wa maji safi na salama. Wananchi hawawamekuwa wakipata shida ya upatikanaji wa maji safi, kwanibaadhi ya Vijij i wamekuwa wekitegemea visima vyakuchimba na mkono ambavyo ni vifupi sana, kwa hali hiyomaji yake siyo salama, lakini wanatumia maji hayo hivyo hivyo,kwani hawana namna nyingine ya kuishi bila maji. Ingawachanzo cha maji cha Mto Ruvu kiko kwao na wao ndiowatunzaji wa mazingira ya chanzo hicho kwa manufaa yaTaifa, lakini leo hii wao ndio wahanga wakubwa wa maji.Kwani maji ya Mto Ruvu yanapita Mlandizi kwenda kutumiwana watu wanaoishi Dar es Salaam.

Page 94: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

94

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili nimelizungumziasana katika Mabunge yaliyopita kuwa kilio changu kwaSerikali kupitia Wizara hii, ni kuwapatia wananchi wa KibahaVijijini maji ili na wao waondokane na adha hii. Leo hiiinashangaza kuona kwamba wananchi wa Kibaha Vijijinihawana maji wakati chanzo cha maji kimetoka kwao.Kiukweli inauma sana! Naomba Wizara husika iwaangaliewananchi hawa kwa jicho la huruma ili na wao waondokanena adha hii ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile Miradi mingiinasuasua katika utekelezaji wake. Kwa mfano, Mradi waChalinze Magindu hadi Lukenge hadi sasa utekelezaji wakeunasuasua. Pia na Mradi wa Ngeta ambao unatakiwaupeleke maji katika Vijiji vya Kikongo, Mwanabwito, Soga naKipangege. Pia kuna tatizo la mda mrefu la upatikajanji wamaji Kata ya Boko Mnemela Vijiji vya Kata ya Boko, Kijiji chapili na Kijiji cha Mkalambati na kadhalika; tunaomba maelezoya miradi hii kwa Wizara husika na ikibidi utekelezaji wakeuanze il i wananchi hawa waondokane na shida yakutokupata maji safi na salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo mazuri siku zotehuigwa na tusiwe wavivu wa kujifunza kutoka kwa wenzetuwaliopiga hatua katika Sekta hii ya maji, ni jinsi ganiwameweza kupambana na changamoto na kufanyawananchi wao kufurahia huduma hiyo na kupata maji pasiposhida.

Pia kuna matatizo katika Idara ya Usambazaji wa Maji,kwani inafika mahali maji hukatika pasipo taarifa yoyote zaidiya kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari, yaani Redio naMagazeti. Lakini siyo mara zote hufanya hivyo. Ikumbukwekwamba siyo kila mtumiaji wa huduma hii ya maji ana nafasiya kusikiliza redio ama kununua gazeti. Nashauri Serikali kupitiaWizara kuandaa utaratibu mzuri pale mitambo hiiinapotakiwa kufanyiwa ukarabati, basi kutoa taarifa za tatizola maji angalau siku tatu au nne kabla ya utekelezaji huo, ilikuwasaidia watumiaji wa huduma hiyo muhimu kujiandaakwa kutunza maji na kuweka akiba ya kutosha.

Page 95: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

95

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumalizia kwakuishauri Serikali kuzingatia na kutilia mkazo Sekta hii ya maji,kwani ni muhimu sana na itapunguza kero kwa wananchikuilaumu Serikali yao kwa kuona miradi mingi, lakini majiyenyewe hawayaoni.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. SILYVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Naibu Spika,huduma ya maji ndiyo huduma ya jamii mama kwa kilaMtanzania. Huduma ya maji safi na salama na hatakumhakikishia mwananchi uhai na kinga dhidi ya maradhimbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo langu la Kibaha Mjinipamoja na kupakana na chanzo kikuu cha maji yatumikayohadi Dar es Salaam, bado asilimia kubwa ya wananchihawapati maji ya bomba. Aidha, Miradi ya Benki ya Duniaya Vijiji kumi haijatoa matunda katika Jimbo hili, ukizingatiakuwa miamba ya ardhi ya Jimbo hili halihifadhi maji nayakipatikana ni machache na yana chumvi sana, hayafaikwa matumzi ya binadamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi mipya ya Benki yaDunia ambayo Serikali imekuwa inaahidi wananchi waKibaha, inachukua muda mrefu sana, licha ya kuhakikishiwakuwa sasa tayari fedha zipo katika Wizara husika na kwa sasaMradi huu wa Bomba Kubwa la Kipenyo cha 85 sentimita.Kutoka Ruvu hadi Kimara litajengwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mkanganyiko ya kuwasasa wananchi wa Kibaha watahudumiwa na bomba jipyaau yale ya zamani? Je, ni lini mradi huu utakamilika?Mheshimiwa Waziri alisema Pwani hatutaweza kuwa namamlaka ya maji, maana hatuna chanzo, lakini tutapewaUwakilishi kwenye Bodi, basi tunaomba sana Uwakilishi huuukamilike na usiishie kuwa maneno tu.

Page 96: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

96

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ni muda muafaka,Serikali itamke wazi: Ni lini mradi huu utakamilika na wananchiwa Kibaha wapata maji safi na salama na ya kutosha?

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli usiofichika kuwatatizo la maji ni kwa nchi nzima licha ya Tanzania kuwa namito, mabwawa na maziwa ya kutosha. Hii inaonyesha wazikuwa bado Serikali haijaweza kutumia vyema rasilimali hiiasilia tuliyopewa na Mungu ipasavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa Serikali kwamakusudi ijikite kwenye mpango maalum wa kuhakikishawananchi wanapata maji safi na salama. Kikubwa, Serikaliijikite katika mito, maziwa na hata mabwawa na sasa ikubalikwa makusudi kabisa uwekezaji binafsi au uwekezaji wakushirikiana (GPP) ili huduma hii iweze kuwafikia wananchikwa urahisi na kwa haraka.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni jambo la kusikitishakwamba bajeti ya Wizara hii huwa inapunguzwa. Kwa hakikakama hatutawekeza kwenye maji kwa wananchi,hatutamkomboa Mtanzania kutoka katika umasikini.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri bajeti ya majiipandishwe hadi kufikia angalau asilimia kumi ya bajeti.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie kwa kuiombaSerikali itamke rasmi kuwa ni lini sasa Mradi wa Maji Ruvu –Kimara kupitia Kibaha kwa ajili ya wananchi wa Kibahautakamilika?

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. MKIWA A. KIMWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,nami napenda kuchangia Wizara hii kwani maji ni uhai. Piamaji safi hupunguza maradhi na kupunguza wagonjwa wengiambao huugua kwa kukosa maji safi na salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda MheshimiwaWaziri aniambie kuhusu mpango wa maji katika Manispaa

Page 97: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

97

29 APRILI, 2013

ya Ilemela, kwani katika ukurasa wa 51 ameongelea miradimipya katika eneo la Ziwa Victoria, lakini Manispaa ya Ilemelahaipo kwenye Mradi huo. Nimeona Jiji la Mwanza, Manispaaya Bukoba na Musoma, pia ya Lamadi, Misungwi na Magu.Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa kujua nini hatma yaManispaa ya Ilemela katika Mradi huo?

Mheshimiwa Naibu Spika, pia napenda kujua baadaya Halmashauri ya Jiji la Mwanza kugawanywa kuwa na Jijila Mwanza na Manispaa ya Ilemela, ni chombo ganikinachosimamia Miradi ya Maji katika Manispaa ya Ilemela?Au kukosekana kwa chombo hicho, ndiyo kukosekana kwaManispaa ya Ilemela katika Wilaya ya Ilemela kutoonekanakwenye Miradi hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vyema kabisa Waziriakafahamu Tawala za Wilaya hizi mbili sasa ni tofauti.Nyamagana (Jiji) na Ilemela ambao ni Manispaa kwa fungula pamoja huleta utata. Mfano, Mfuko wa Barabara ambaohuja pamoja. Ni vyema mkatambua Manispaa ya Ilemelakama ilivyo. Au sisi ni watunza maji taka tu?

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kitabu chaMaendeleo (Volume IV) Sub Vote 4001 kasma ndogo 3341,Mradi huu unaonekana umetengewa fedha nyingi sana,kwani tumeshuhudia miradi mingi hutengewa fedha kwaawamu, na huu kutengewa fedha nyingi sana. Au kwakuwaMkuu wa Mradi huu ni Waziri; au ndiyo “chukua chakomapema”, au ndiyo mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake?Ni vyema fedha hizo zikapunguzwa na kupelekwa kwenyemiradi mingine ambayo imekwama kwa ajili ya malipo, kamaMradi wa Geita, au Jiji la Mwanza kwa Miradi midogo yandani.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuondokane na dhana yamwenye kisu kikali ndio hula nyama. Mheshimiwa Waziri ndiyemwenye kisu, hivyo ni busara akakubali kupunguza fedha hii

Page 98: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

98

29 APRILI, 2013

ili kurudisha heshima na kuondoa fikra zilizotujaa Wabungeya kujipendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

MHE. RECHEL M. ROBERT: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kuchangia hoja ya Wizara ya Maji kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na Maji ni Uhai. Ninamaana kuwa binadamu yeyote hawezi kuishi bila maji, nasiyo maji tu, bali maji safi na salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kinachonisikitisha, kamasiyo kunishangaza, ni Bajeti ya Wizara ya Maji kuendeleakupungua mwaka hadi mwaka, kana kwamba maji siyo uhai,huku mahitaji yake nayo yakizidi kuongezeka. Kuna haja sasaya Serikali kuongeza fedha katika Wizara hii ili iweze kwendana ongezeko la mahitaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na upungufu wabajeti ya Wizara, napenda kuipongeza Serikali kwa kuonaumuhimu sasa wa kutenga fedha kwa ajili ya Vijiji 100 vilivyokondani ya kilometa 12 kutoka bomba kuu la maji yanayotokaZiwa Victoria. Pamoja na pongezi hizo, wananchi wa maeneohaya wangependa kuona sasa kazi hii inafanyika na kwishakwa wakati kama hotuba ya Wazri ilivyosema.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziriameainisha maeneo ambayo upembuzi yakinifu utafanyika,pamoja na mtaalam mshauri kwa ajili ya Mradi wa Majikutoka Ziwa Victoria kwenda Miji ya Bariadi, Mwanhuzi,Lagangabilili, Magu na Ngudu. Lakini sijaona Mradi wa Majikwa ajili ya Mji wa Kishapu, Mhunze, Kolandoto, ambako kunaHospitali kubwa, na sasa ni Hospitali teule ya Mkoa pamojana Tinde Shinyanga Vijijini. Je, ni lini sasa maeneo hayayatapata maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria,ikizingatiwa kwamba maji tayari yameshafika Manispaa yaShinyanga na Wilaya ya Kahama?

Page 99: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

99

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo mengi katika Mkoawa Shinyaga na Simiyu yanapata mvua chache sana katikamwaka na hata zinapokuwa nyingi, hakuna sehemu ambapokumechimbwa mabwawa ya kuhifadhia maji pindi mvuazinapokuwa nyingi. Naomba Serikali iangalie haja yakuchimba mabwawa ya kuhifadhia maji ili yaweze kusaidiawananchi katika kipindi cha ukame, kwani akina mamahutembea mwendo mrefu sana kufuata maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kitabu cha hotubaya Mheshimiwa Waziri, nimeona kuna maeneo ambayonimeyataja hapo juu yapewe kipaumbele na baadhiyanatekelezwa na mengine yatatekelezwa katika Mkoa waShinyanga. Basi Serikali ifanye kama ilivyoahidi ili wananchiwa maeneo haya wapate maji safi na salama na hiiitaongeza watumiaji wa maji pamoja na kuongeza patokatika Mamlaka zote, yaani KASHWASA na SHUWASA.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna tatizo la miundombinumibovu katika maeneo mengi sana, hii inasababisha upotevumkubwa sana wa maji yakiwa yanasafiri kwenda kwamtumiaji. Pengine Serikali kupitia Wizara na hasa Mamlakakatika maeneo husika, wawe na utaratibu wa kufanyamarekebisho au replacement ya miundombinu ili majiyasipotee njiani na hivyo kuepuka hasara zitakazopataMamlaka husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kodi kwenye maji na hasaya kunywa, Serikali iangalie uwezekano wa kuondoa kodikatika maji ya chupa ili hata wanafunzi wanapokwenda shulewaweze kununua maji ya chupa ambayo kimsingi ni safi nasalama. Hii itapunguza magonjwa ya milipuko kamakipindupindu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Manispaa ya Shinyangakuna tatizo kubwa sana ambalo limekithiri ambapo wizi wamabomba kwa wateja umekuwa mkubwa sana, na hiiinasababishwa na biashara ya vyuma chakavu. Kila sikutakribani wateja 20 huibiwa vyuma hivyo na kuacha maji

Page 100: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

100

29 APRILI, 2013

yakitiririka hovyo Mtaani, hivyo kuiletea hasara Mamlaka yaMaji pamoja na mteja kununua bomba lingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara, ionesasa kuna haja ya kubadilisha mfumo wa mabombayanayounganishwa na Mita ili yatumike yale ya plastiki. Hiiitapunguza wizi huu ambao kimsingi umetia hasara Mamlakahusika.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, naomba Serikaliiangalie na kulinda sehemu zenye vyanzo vya majivisiharibiwe ili viendelee kusaidia maeneo husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuchangia hayomachache, naomba kuwasilisha.

MHE. RITA L. MLAKI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanzanichukue nafasi hii kumpongeza Waziri wa Maji na Wizarayake kwa ujumla kwa hutuba nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitapenda kuchangia juuya upatikanaji wa maji Mkoa wa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Dar es Salaamuna wakazi 4.5 - 5 milioni. Hawa ni watu wengi sana. Kunaumuhimu wa kuhakikisha kuwa kuna maji ya kutosha katikaJiji hil i. Maji yanahitajika kwa matumizi ya viwanda,majumbani kwetu, mahospitalini na umwagiliaji. Kukosa majiya kutosha ni kurudisha maendeleo ya nchi yetu nyuma.

Mheshimiwa Naibu Spika, upatikanaji wa maji katikaJiji la Dar es Salaam bado siyo zuri. Mpango au mkakati wakuboresha upatikanaji wa maji Jiji Dar es Salaam ulioanzatangu mwaka 2012, umesaidia kwa kiwango kidogo, lakinibado tunaiomba Serikali kuongeza juhudi.

Mheshimiwa Naibu Spika, miundombinu ya maji nimibovu na inapoteza maji mengi sana Mjini. Pia ukataji wamabomba hovyo unachangia sana upotevu wa maji nakuongeza tatizo kuwa kubwa zaidi.

Page 101: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

101

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali ichunguzena idhibiti upotevu huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunashukuru mkakati wadharura wa kupata maji katika Jiji la Dar es Salaam, lakininimependekeza Serikali ifikirie njia nyingine ya kupata majikutoka baharini kama kutengeneza desalination plant ili majiya bahari yatumike na kubaini kupunguza tatizo la maji Jiji laDar es Salaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. GOSBERT B. BLANDES: Mheshimiwa Naibu Spika,tatizo la maji katika nchi yetu ni kubwa sana. Mkoa wa Kageraumepakana na Ziwa Victoria. Wilaya ya Karagwe ipo ndaniya Mkoa wa Kagera. Pia Wilaya ya Karagwe inavyo vyanzovingi vya maji ikiwemo Ziwa Victoria, Mto Kagera, ZiwaKajunju, Ziwa Burigi, Ziwa Ngoma, Ziwa Kaberenge, ZiwaTanganyika, chemichemi nyingi sana zisizokauka kwa mwakamzima ikiwemo Chisulo Kata ya Ihembe, Kabagendela Kijijicha Ihembe I, Chitanga, Charuhanga nakadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na neema yote hiikutoka kwa Mwenyezi Mungu, Wilaya ya Karagwe inapatamaji chini ya asilimia 20.

Mheshimiwa Naibu Spika, mji mkongwe wa kibiasharawa Omurushaka wenye wakazi wengi unapata maji asilimiasifuri. Mji huu unapakana na chanzo cha maji chaCharuhanga umbali usiozidi kilomita tano. Ajabu Mji huuhauna maji. Mji huu unapakana na Vitongoji vyaNyakahanga, Bugene, Kishao na Ihanda. Vitongoji vyote hivivinapata maji asilimia sifuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na ufinyu wa bajetiya Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Serikali imejitahidi,imeshapeleka umeme kwenye chanzo hiki. Pia imenunuamashine ya kusukuma maji, bado inahitaji fedha kwa ajili yakutandaza mabomba (miundombinu) na kukarabati matankiya zamani ili kupeleka maji katika maeneo haya.

Page 102: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

102

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, nil ishamwandikiaMheshimiwa Waziri wa Maji, Katibu Mkuu, Naibu Waziri naMkurugenzi wa Maji. Pia nimepata ahadi kutoka kwaMkurugenzi wa Maji Ndugu Yohana kutupatia fedha kwa ajiliya mradi huu. Ni imani yangu kuwa ahadi ya Serikali yakuwapatia wananchi maji wa Omurushaka, Nyakahanga,Kishao, Bugene na Ihanda maji.

Ninaomba na kumsihi sana Mkurugenzi wa MajiNdugu Yohana, aguswe ndani ya moyo wake, usumbufuambao nimekuwa nikimpatia katika kipindi chote chakufuatilia maji ya Omurushaka. Naamini hataniangusha,kwani ahadi hii ni ya muda mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Miradi ya Benki yaDunia, utafiti uliofanywa na Mhandisi Mshauri, unaonyeshakuwa maji yalipatikana katika maeneo ya Vijiji vya Nyakakikana Kayungu katika Kata ya Nyakakika na Kata yaNyakabanga Wilayani Karagwe, lakini hatuoni juhudi zozoteza kusambaza maji haya kwa wananchi. Naomba nielezwe,kazi hii ya kupeleka maji katika vijiji hivi, itaanza na kukamilikalini?

Mheshimiwa Naibu Spika, nashuri kupendekezakwamba maji ya Ziwa Victoria yawanufaishe wananchi waMkoa wa Kagera na hasa Wilaya ya Karagwe kamayalivyopelekwa katika Mkoa wa Shinyanga. Kwa kuwa Wilayaya Karagwe ina jiografia ya milima na miinuko, jambolinaloifanya ikose maji bubujiko, naomba Serikali itenge fedhaza kutosha kupeleka mradi kabambe wa maji kutoka katikavyanzo vingi vya maji vilivyopo Wilayani Karagwe. Serikaliianze japo kidogo kidogo na itenge fedha mwaka hadimwaka mpaka mradi mzima ukamilike.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji wa Nile Basinupo katika nchi mbili za Rwanda na Tanzania. Kuna fununukuwa mradi huu unakusudia kujenga mradi wa maji nchiniTanzania katika Wilaya ya Karagwe Kata ya Nyakabangakwa ajili ya kusambaza maji Wilayani Karagwe. Mimi kamaMwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Karagwe, naomba

Page 103: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

103

29 APRILI, 2013

nieleweshwe kama jambo hili lipo au la. Kama lipo, litaanzalini?

Mheshimwa Naibu Spika, naunga mkondo hoja;

MHE. DEO H. FILIKUNJOMBE: Mheshimiwa Naibu Spika,Mji wa Ludewa ni Mji unaokua kwa kasi na watuwanaongezeka kila siku. Je, Wizara ya Maji ina mpango ganiwa kupeleka maji safi na salama na ya kutosha katika Mji waLudewa?

Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri wa Maji hajisikiivibaya kuona kwamba Makao Makuu ya Wilaya ya (Ludewa)hayana maji ya kutosha?

MHE. KHATIBU SAID HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda na mimi mchango wangu huu uzingatiwe katikajambo hili muhimu linalogusa maisha ya watu wetu wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa muda mrefu katika Jijila Dar es Salaam kumekuwa na tatizo lililopitiliza la upatikanajiwa maji. Hii tunaelewa kwamba moja ya sababu iliyopelekeahali hii ni ongezeko kubwa la mahitaji kutokana na idadi yawatu kuongezeka katika Jiji hilo. Pia suala la mfumo mbovuwa usambazaji wa maji unatokana na miundombinuiliyozidiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili linatokana naSerikali kutojiandaa katika muda uliostahili kukabiliana natatizo hili. Hivyo, pamoja na jitihada zinazoonekanakuchukuliwa, sasa ni budi Serikali kuongeza msukumo wamakusudi ili suala la upatikanaji wa maji safi na salamalipatiwe ufumbuzi wa kudumu na kuwapunguzia wananchishida kubwa wanayoipata.

Mheshimiwa Naibu Spika, nigependa piakuifahamisha Serikali kuwa ule Mradi wa Maji maarufu waMchina katika maeneo ya Mbezi/Kimara ni kwanini utendajiwake unaonekana ni wa kusuasua?

Page 104: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

104

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wengi wamaeneo yale waliweka matumaini makubwa na Mradi huu,na mpaka sasa bado hawajafuta imani hiyo. Hivyo ni jukumula Serikali kurekebisha kasoro zilizojitokeza ili lengo liwezekufikiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba Wizara yakoiangalie hujuma inayofanywa na baadhi ya wananchiwanaoweka pampu na kuhifadhi maji mengi katika matenkikwa ajili ya kufanya biashara, hali inayopelekea raia wenginekukosa huduma hii muhimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tafadhali Serikali iwafuatiliewatu hawa, kwani kisheria wanaruhusiwa kufanya biasharaya kusambaza maji ni DAWASCO peke yake na siyo mtu auTaasisi nyingine yoyote kwa sasa hivi. Hivyo jambo hili nimuhimu lishughulikiwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

MHE. REBECCA M. MNGODO: Mheshimiwa NaibuSpika, Wizara ya Maji ina jukumu la kuratibu uchimbaji wavisima vya maji nchini. Katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri,amesema kwamba uratibu huo unalenga kuhakikishakwamba taratibu za kitaalam zinafuatwa ili kuhakikisha visimavina ubora kwa matumizi endelevu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, jedwali Na. 8katika ukurasa wa 118 wa kitabu cha Hotuba ya Waziri waMaji - Mheshimiwa J. A. Maghembe, kuna orodha ya maeneoyenye visima ambavyo maji yake hayakidhi viwango.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mkoa wa Arusha,Wilaya ya Arumeru kuna maeneo yenye visima ambavyo majiyake hayakidhi viwango kutokana na maji ya maeneo hayokuwa na Chloride kiasi cha Mg/L (ppm) 5.0 - 41.7. Maeneohayo ni Kikatiti, Sawaria, Malula, Oleriani, Oldonyosambu,Ngongongare, Mbuguni, Olkun’gwado, Nsengony Owiro,Kisimirichini kwa Ugoro, Kikuletwa Nkwanekoli, MakibaMigungani, Lemong’o, Engareolmotony.

Page 105: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

105

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, je, baada ya Wizara ya Majikugundua kwamba maji ya maeneo hayo hapo juu hayakidhiviwango, ni hatua zipi zimechukuliwa na Wizara ili wananchiwaishio katika maeneo hayo wasiendelee kutumia maji hayoya visima na hivyo kuendelea kuathirika?

Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali kupitia Wizara hiiya Maji, ina mpango gani wa kuweka/kupeleka maji yabomba kutoka Ngerenanyuki kwenda maeneo hayo?

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Uongozi wa Awamuya Kwanza, chini ya uongozi wa Hayati Baba wa Taifa -Mwalimu Julius Kambalage Nyerere, kulikuwepo na maji yabomba kutokea Ngarenanyuki kupitia Kingori, Sakila hadiKikatiti na Samaria. Katika kila Kijiji nilichotaja hapo juu, yaaniKingori, Sakila, Kikatiti na Samaria kulikuwepo na tenki la majiyaliyokuwa yanatokea Ngarenanyuki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivi sasa, matenki hayoni matupu na hakuna maji yoyote yanayotoka Ngarenanyukitena kuja katika matenki hayo. Ningependa kujua: Je, majihayo yaliyotokea Ngarenanyuki kwa bomba, yalipatwa nanini? Wananchi waishio maeneo hayo wangependa kujua,maji yale ya bomba nini kilitokea kwamba sasa hayapatikanitena?

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwapo na desturi yaWatendaji wa Serikali kutokuwa waadilifu katika kusimamiavizuri miradi ya maendeleo ya wananchi ikiwemo mradi yamaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ichukue hatua kali zakinidhamu kwa wale wote wanaobainika kutumia kwaubadhirifu fedha zilizolengwa kwa miradi ya maji. Wananchiwengi waishio Vijijini kwa miaka mingi wameteseka kwakunywa maji yasiyo safi na salama, wao pamoja na mifugoyao.

Page 106: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

106

29 APRILI, 2013

MHE. AMINA MOHAMED MWIDAU: Mheshimiwa NaibuSpika, sote tunajua kuwa maji ni uhai, bila maji hakunamaisha. Hivyo Wizara hii ni muhimu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, upatikanaji wa maji salamani muhimu sana katika kupigana na umaskini na matatizo yaafya. Watu masikini ambao wengi wao huishi Vijijini, wananafasi finyu ya kupata maji safi kwa ajili ya matumizi yanyumbani na kwa ajili ya mazao na matumizi ya afya. Chakusikitisha zaidi, mbali na maji salama, hata hayo ambayosiyo salama hayapatikani.

Mheshimiwa Naibu Spika, japokuwa kuna adharikubwa ya mabadiliko ya tabianchi lakini Tanzania bado inavyanzo vya kutosha vya maji kukidhi mahitaji yake, tena majiyaliyo juu na chini ya ardhi, asilimia saba ya ardhi imefunikwana maziwa ya maji matamu ambayo yako mpakani licha yamaziwa mengine ambayo yako ndani ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli Tanzania Munguanatupenda, tuna maziwa makubwa, mito na mabwawa,lakini cha kusikitisha, hata wananchi wanaoishi karibu navyanzo hivyo vya maji hawanufaiki na neema hiyo. Wanamatatizo ya maji kama watu walio mbali na vyanzo hivyo.Mfano, Ziwa Victoria, japokuwa hotuba ya Mheshimiwa Waziriimeonesha mikakati mbalimbali ambayo inabidi tuiombeeMungu itekelezeke.

Mheshimiwa Naibu Spika, I am sorry to say this, butnina mashaka makubwa kuwa Serikali imeshindwakuwasaidia Watanzania kupata maji safi na salama. Miakazaidi ya 50 ya Uhuru mpaka leo Watanzania wanateseka namaji. Hivi kweli Serikali ina nia ya dhati ya kuwasaidiaWatanzania kujikwamua na janga hili?

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri, katikasakata hili la maji wanaoteseka kupindukia ni wanawake nawatoto. Wanawake wanateseka sana kwa kuchota majimbali na watoto afya zao zinakuwa mbovu, hawaogiinavyotakiwa na wanakunywa maji machafu.

Page 107: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

107

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitaje maeneomachache ambayo nimejionea mateso ya kukosa maji;mfano Igunga, kule ndiyo nilijionea maajabu. Wananchi wakule, maji wanayotumia huwezi kuamini! Maji wanayokunywabinadamu ni hayo hayo, wanakunywa n’gombe, mbuzi,mpaka mbwa ni hayo hayo! Kwa kweli maisha yao nimagumu na ya ajabu sana. Unaweza kudhani hawakoTanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Pangani Mkoawa Tanga kuna tatizo sugu la maji. Vijiji vyote vya Wilayanihuko vina matatizo ya maji. Naomba vile ambavyovinajitahidi kwa kushirikiana na Serikali za Vijiji mnawasaidiaje?Kwa mfano, kuna Kijiji kimoja cha Mwera Kata ya MweraWilaya ya Pangani, Serikali hiyo ya Kijiji inajitahidi sana,wamechimba kisima kwa pesa za Kijiji na nguzu za wananchikwa Shilingi milioni 10 walizokuwanazo kwenye akaunti. Sasahivi wanahitaji mabomba ya kutoa maji hayo kwenye kisimana kuunganishwa kwenye laini kubwa inayopeleka majikwenye tenki la maji lenye ukubwa wa milimita 20,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba MheshimiwaWaziri, nitakuja kuona ili Wizara yako iweze kuwaungawanakijiji hawa ambao wako tayari kujitolea kwa maendeleoyao.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

MHE. UMMY A. MWALIMU: Mheshimiwa Spika, nianzekuunga mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, pili, naishukuru sana Wizara ya Majikwa kutekeleza mipango mbalimbali ya kuhakikishaupatikanaji wa maji safi kwa wananchi hasa wa vijijini.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naishukuruWizara kwa kutenga kiasi cha shilingi milioni mia tatu(300,000,000/=) kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa uboreshajihuduma za maji safi Muheza na pia kutenga fedha za Miradimbalimbali ya maji katika Wilaya nyingine za Mkoa wa Tanga

Page 108: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

108

29 APRILI, 2013

hasa Korogwe, Handeni, Mkungu (Kasera) na Lushoto. Huuutakuwa ni ukombozi kwa wanawake wa Wilaya hizi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu maji na maendeleo yawanawake; suala la upatikanaji wa maji safi lina uhusianowa karibu sana na suala zima la usawa wa jinsia namaendeleo ya wanawake hasa walio vijijini hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kuwa jukumula kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani/familia nijukumu la wanawake na wasichana. Katika maeneo mengiya vij i j ini nchini, wanawake na watoto wamekuwawakikabiliwa na tatizo kubwa la kutafuta maji, mara nyingiwanatembea umbali mrefu kutafuta maji.

Mheshimiwa Spika, inasikitisha kuona wanawakewakitembea mwendo mrefu tena wakiwa na watotomgongoni, wanahangaika kutafuta maji.

Mheshimiwa Spika, naiomba Wizara kuwekeza fedhaza kutosha katika kuboresha huduma za upatikanaji majivijijini. Upatikanaji wa maji vijijini utachochea maendeleo yaelimu kwa watoto wa kike nchini. Hii itapelekea kuchocheamaendeleo ya familia, jamii na Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa maji vijijini piautachochea maendeleo ya wanawake kwani badala yawanawake kupoteza muda mwingi kutafuta maji watatumiamuda huo katika shughuli za uzalishaji mali kama vile kilimo,mifugo, biashara na pia kutumia muda huo kwa malezi yawatoto na familia.

Mheshimiwa Spika, kuwekeza katika uboreshaji wahuduma za maji vijijini kutasaidia kupunguza mimba kwawasichana wadogo na pia vitendo vya ukatili dhidi yawanawake hasa vitendo vya kubakwa na kudhalilishwakijinsia.

Mheshimiwa Spika, tunao ushahidi wa kuwepo kwavitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na ongezeko la mimba

Page 109: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

109

29 APRILI, 2013

kwa wasichana wadogo vijijini kutokana na tatizo hili laukosefu wa maji vijijini. Hivyo, napenda kuishauri Serikali/Wizara kuhakikisha mipango/mikakati iliyopo yenye lengo lakuhakikisha upatikanaji wa maji hasa vijijini inatekelezwaipasavyo. Huu ndio utakuwa ukombozi wa kweli wawanawake Tanzania hasa vijijini.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Sera ya kuvuna maji yamvua; wakati sehemu nyingi za nchi zinakabiliwa na ukosefuwa maji safi, inasikitisha kuona kuwa maji mengi ya mvuayanamwagika na kupotea ovyo. Maji haya yanatakiwakuhifadhiwa na kutumika wakati wa kiangazi. Hivyo, nitoe raikwa Wizara kuandaa sera/mkakati mahususi wa kuvuna nakuhifadhi maji ya mvua.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii.

MHE. HAROUB MUHAMMED SHAMIS: MheshimiwaSpika, awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu(Subhanah Wataala) kwa neema na rehema zake nyingikwangu, familia yangu na Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, Mwenyezi Mungu amesema katikakitabu chake kitukufu cha Qur-ani: “Tumeujaalia uhai wa kilakitu kutokana na maji.” Nini maana ya Aya hii? Ni kwamba,bila maji hakuna maisha, hakuna uhai, maisha hayawezekanina hapa ndipo tunapopata kipimo juu ya umuhimu wa maji..

Mheshimiwa Spika, kiasi kidogo cha fedhakinachotengwa kwa aji l i ya miradi ya maji na zaidiucheleweshwaji wa kuzitoa hizo fedha kidogo ni kufanyamzaha na maisha ya Watanzania.

Mheshimiwa Spika, Serikali kulalamika juu ya hujumaya miundombinu ya maji kwa sababu ya biashara ya chumachakavu ni kukwepa majukumu. Serikali ina dola, ina mkonomrefu, je, kuna yeyote aliyetiwa nguvuni na dola au Serikaliimelala? Au kuna ubia wa biashara hiyo kati ya watendajiwa Wizara na wabadhirifu hao wa miundombinu ya maji?

Page 110: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

110

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, haiwezekani tena haiwezekanikuwe na hujuma za namna hiyo bila ya wahujumukukamatwa. Bila shaka kuna namna hapo, Serikali itafakariupya isiwe nayo ni mlalamikaji baada ya kuwa ni mtatuzi wamatatizo haya!

Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo, kuna tatizo sugusana la watendaji au wasimamizi wa miradi ya maji hasamiradi ya visima ni walafi wa fedha za miradi hiyo.Wanafanya mchezo wa kuigiza kuwadanganya wananchi.

Mheshimiwa Spika, tatizo la maji Jijini Dar es Salaamlimeendelea kukua siku hadi siku. Ni jambo la aibu nakusikitisha sana Mji Mkuu wa nchi, Makao Makuu ya Serikalikuwa hakuna maji safi na salama. Pia majitaka ni tatizolinalokwenda sambamba na la maji safi Jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, wakazi wa Dar es Salaamwanategemea maji ya visima ambayo uhakika na usalamawake haujulikani. Biashara ya maji ya visima imeshamiri bilaya kuzingatia ubora wa maji yenyewe. Visima hivi vya majiDar es Salaam vina uwezekano mkubwa wa maji yakekuchafuliwa na maji taka ambayo yanatiririka ovyo kilamahali. Hii ni aibu!

Mheshimiwa Spika, hali ya ukosefu wa majisafihairidhishi hata kidogo, Serikali ni lazima sasa iwe na mkakatimadhubuti wa kumaliza kero ya maji kwa Watanzania. Niwakati sasa wa kutafuta fedha za ndani kwa mkakati maalumili kuondoa tatizo la maji.

Mheshimiwa Spika, bila ya utashi maalum wa kisiasajuu ya tatizo la maji safi hata juhudi za kupunguza vifo vyawatoto chini ya miaka mitano hazitofanikiwa; kwani maradhimengi hasa ya watoto na akinamama yanasababishwa kwaasilimia kubwa na maji yasiyo salama.

Mheshimiwa Spika, wakati haumsubiri mtu, Serikaliiache sasa, iamue na ifanye kazi ya kuondoa kero zawananchi ikianzia hii ya maji.

Page 111: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

111

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Mungu ibarikiTanzania, Mungu ibariki Afrika.

MHE. SAID A. ARFI: Mheshimiwa Spika, katika Ibara yakumi na mbili (xii), ukurasa wa 51 tunaomba ufafanuzi wamiradi ya maji safi na usafi wa mazingira Lake Tanganyika.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

MHE. JOHN M. CHEYO: Mheshimiwa Spika, katikamakadirio ya miundombinu ya mabwawa kumi (10),niliwaomba wataalam waongeze Bwawa la Nkoma,tafadhali.

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika, naombakumuuliza Mheshimiwa Waziri swali lifuatalo:-

Je, mnaposema Miradi ya maji safi na usafi wamazingira katika miji inayozunguka Ziwa Tanganyika,mnamaanisha nini? Kasulu mmeitengea milioni 2.3 nampanda milioni 3.1. Hatuelewi ni kwa ajili ya kutandazamtandao wa maji, yaani mabomba au ni uhifadhi wamazingira? Tusaidie ufafanuzi tuna kiu kweli ya kuelewa.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Spika,namwomba Mheshimiwa Waziri anipe ufafanuzi juu ya Mradiwa Maji Vijiji Vitano mwaka 2013/2014, vitakavyofadhiliwa naBenki ya Dunia. Vijiji vilivyo katika Jimbo la Mbogwe niLugunga, Iponya na Ilolangulu.

Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Waziriaangalie ukurasa wa 175 na anifafanulie kila kijiji kinatengewashilingi ngapi?

Mheshimiwa Spika, natanguliza shukrani kwaushirikiano.

MHE. DKT. ANTONY G. MBASSA: Mheshimiwa Spika,naomba nami kuchangia hoja ya Wizara ya Maji kamailivyoletwa mbele yetu. Nianze kwa kuunga mkono Hotuba

Page 112: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

112

29 APRILI, 2013

ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Wizara hii muhimu ya Maji.Hakika suala la maji ni muhimu kwa viumbe hai wote hapanchini. Hakika bila maji hakuna uhai wa kiumbe chochoteutakaowezekana na hakuna ustawi wa mji au jamii yoyoteutakaokuwa na ufanisi mahali popote.

Mheshimiwa Spika, suala hili la maji katika Hotuba hiiya Bajeti, umepewa au umetolewa umuhimu mkubwa sanamaeneo ya mjini na kuachwa maeneo ya vijijini ambako kunauhaba mkubwa sana wa maji. Ni suala ambalo halina ubishi,hili linatokana na ukosefu mkubwa wa miundombinu. Hiiinasikitisha sana. Hakika idadi kubwa sana ya wananchi wapovijijini ambao sasa kwao kupata maji safi na salama imekuwani ndoto isiyotekelezeka.

Mheshimiwa Spika, nikitaja baadhi ya maeneo katikaKata ya Nemba ambako wakazi wengi ni wafugaji nawakulima. Hakuna mabwawa ya kunyweshea mifugo namatumizi ya kawaida ya binadamu. Maeneo mengi katikaKata hiyo, suala la kuoga limekuwa la anasa na hivyokupelekea kuibuka kwa maradhi mbalimbali ya magonjwaya ngozi, kama si kuomba Mungu yasiibuke magonjwa yamilipuko maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, katika Kata ya Nyamigogo kunahali mbaya ya upatikanaji wa maji, bwawa lilipo halikidhi hajana bado ukarabati wake haukukidhi kiwango, sehemu nyingiwakati wa kiangazi ni matatizo makubwa sana. Shule zamsingi Nyanshimba, Nyamigogo bado hazina utaratibuambao angalau unaweza kumsaidia mtoto apate maji yakuosha mikono pale anapotoka chooni kama kanuni za afyazinavyotuongoza.

Mheshimiwa Spika, ni wakati sasa pamoja na juhudiza Halmashauri zetu, basi Serikali ione umuhimu wa maeneohususani pale penye mikusanyiko mingi na kambi zawatumishi mbalimbali ili wapatiwe huduma ya maji. NaiombaSerikali kutoa kipaumbele cha mgao au huduma yausambazaji maji vijijini na kubwa zaidi maeneo ya pembezoniambako huduma za jamii ni duni sana.

Page 113: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

113

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie mchangowangu kwa kuongelea suala la Mradi wa Maji wa Vijiji Kumi(10). Miradi hii imetekelezwa kwa kiwango cha chini sana aubila mafanikio. Yapo maeneo ambayo visima vilichimbwalakini maji haya hupatikana na bado imerukwa kwenyemaeneo ambayo miradi imetekelezwa. Naomba nishauriSerikali kuwa Wakandarasi hawa walipwe mara baada yakukamilisha mradi wote. Pesa zimelipwa lakini maji hakuna,hii ni dhambi kubwa sana kwa kuwadanganya na kuwatesawananchi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo, katika taarifazinazoletwa hakika hatupati taarifa za ujumla za miradimbalimbali ya maji inapotekelezwa katika maeneo yetu.Mfano Mradi wa CONCERN ambao umekuwa ukitekelezwakatika baadhi ya Kata mfano Kata ya Nyabusozi. Hakika majini uhai na maji ndio msingi wa maisha ya viumbe hai wote.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, pamoja naSerikali kutenga shilingi bilioni 398.3 ambayo ni asilimia mbili(2%) ya Bajeti nzima ya nchi.

Mheshimiwa Spika, ningeomba Serikali ingetuleteamkakati madhubuti wa kuhakikisha kuwa pesa ya ndaniinatengwa kiasi kikubwa zaidi kuliko kutegemea fedha yawafadhili. Miradi mingi sana katika Halmashauri zetu inakuwahaitekelezeki kwa wakati kwa sababu ya kutegemea pesaya wafadhili.

Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu wa Wizarahii kwa matatizo makubwa ya maji katika miji na vijiji vingivya nchi hii, Serikali ingetenga pesa nyingi zaidi za ndani kulikoza nje ili kuwa na uhakika kwa miradi ambayo imeainishwa.

Mheshimiwa Spika, Serikali pia iweke utaratibu mzuriwa kusimamia miradi hii ya wafadhili. Wahandisi wengi katikaHalmashauri zetu sio waaminifu kuanzia kwenye upembuziyakinifu, kwenye uchimbaji wa visima na kumekuwa naudanganyifu mkubwa. Hata tenda zinatolewa kwa kujuanampaka kusababisha miradi mingi kujengwa chini ya kiwango.

Page 114: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

114

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, naomba niunge mkono nanikubaliane na Wabunge wenzangu walioona umuhimu wahii Wizara kuwa na Mfuko wa Maji kama ilivyo Wizara ya Ujenzikuwa na Mfuko wa Barabara. Kuwepo kwa Mfuko huukutasaidia ujenzi wa miradi mingi kufanyika na pesakupelekwa kwa wakati kwa Halmashauri zetu.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mheshimiwa Rais alipitakatika maeneo mengi na kutoa ahadi nyingi za majiningependa kujua utekelezaji wake ukoje? Maana nimesikilizamichango mbalimbali ya Wabunge, pia maswali ya kila sikuinaonesha ahadi nyingi bado hazijatekelezeka. Ni vyemaWizara ingetambua idadi ya ahadi za Mheshimiwa Rais nazijulikane idadi ya ahadi zilitekelezwa na zile ambazohazijatekelezwa na Serikali ingeeleza mkakati wa utekelezajiwake.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. Kwenye Wilayayangu ya Korogwe Vijijini kuna kisima cha maji Mombomwisho wa shamba, Serikali ilisema kabla ya mwezi wa Sitamaji yawe yametoka na kwenye mpango wa maji hakunachochote.

Mheshimiwa Spika, kwenye Vijiji Kumi (10) vyaudhamini wa Benki ya Dunia ni Mradi mmoja tu wa Makumba,mingine yote haijaanza. Sasa naomba Serikali iseme hivi Vijijivingine vya Mashewa, Kwashemshi, Mmyuzi, Nugiri, Mwenga,Mlembule, Hale, Kwamkole na Changalikwa, Miradi hiyo yaBenki ya Dunia itaanza lini na wananchi wanalalamika.Naomba Serikali iangalie suala hilo kwa uhakika.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa asilimiamia moja.

MHE. CHARLES J.P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika,kupitia maandishi nichangie Bajeti ya Wizara ya Maji kamanilivyomalizia ushauri wangu wakati nikichangia Bajeti ya Ofisi

Page 115: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

115

29 APRILI, 2013

ya Waziri Mkuu, maji ni uhai. Hoja hapa ni kuwa kutokana naumuhimu wa sekta hii kwa maendeleo na ustawi wa nchiyetu, tunapaswa kuisimamia kwa makini.

Mheshimiwa Spika, Hotuba ya Wizara hii imeshindwakukidhi matakwa ya hoja hiyo hapo juu. Kiasi kinachotengwahakiwezi kukidhi mahitaji ya Miradi iliyoanishwa. Mbali namiradi iliyoanishwa kwa mwaka ujao vipo viporo ambavyohaieleweki ni kwa vipi vitaweza kukamilishwa. Kitendawili tatakatika sekta hii ni hata hiyo miradi inapochaguliwa nakupewa kipaumbele.

Mheshimiwa Spika, yapo maeneo mfano lile Jimbolangu ambayo yana shida kubwa sana ya maji hayajawahikufikiriwa, acha kupangwa. Katika eneo hilo hilo kunamaeneo yenye afadhali, yaani wanaweza kupata maji kwawastani wa mita 800, wamepewa hiyo miradi ya ahadi.

Mheshimiwa Spika, sambamba na maelekezo hayohapo juu nielezee tatizo la utekelezaji wa miradi. Mfumo wasasa ambapo Halmashauri za Wilaya hutumika kamamsimamiaji na mtekelezaji wa Mradi imekuwa na upungufuau udhaifu mkubwa sana. Miradi imekuwa na ucheleweshaji,utendaji usiokuwa na ubora, ugawaji wa miradi bila kuzingatiautaalam na ubadhirifu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu maendeleo, sekta ya majihasa vijijini kusikokuwa na Mamlaka nashauri yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kwa haraka kadri iwezekanavyomiradi ya maji isimamiwe na timu maalum katika ngazi yaMkoa. Timu hii isiwajibike kwa Mabaraza ya Madiwani,iongozwe na utaalam kwa kulenga mahitaji. Hii ni njia ausuluhu ya muda, mpango wa kati na baadaye ni kuanzishaTANWATER kama ilivyo TANROAD ambayo itakuwa nawatendaji, ngazi ya Mkoa.

Mheshimiwa Spika, chini ya utaratibu wa TANWATERitakuwa rahisi na haraka kupunguza kama si kumaliza tatizola maji nchini. Chini ya utaratibu huu tozo mbalimbali

Page 116: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

116

29 APRILI, 2013

zinaweza kuanzishwa chini ya Mfuko wa Maji wa 2009 nakutumiwa kujenga mifumo ya maji. Tukiwa na chombo hikikwa pamoja kama Taifa tunaweza kuandaa nguvu kazi watuili kuweza kumudu shughuli hizi.

Mheshimiwa Spika, mafanikio ya TANROAD pamojana mambo mengine yanachangiwa na nidhamu yawatendaji hasa Waandisi na Kada zote za kifundi kuwajibikakwa mamlaka moja. Hoja hapa ni kuanzisha mamlakaambayo itakusanya rasilimali (chini ya Mfuko wa Maji) nakusimamia rasilimali watu kwa weledi na uadilifu wa hali yajuu.

Mheshimiwa Spika, chini ya upungufu niliyoyaelezahapo juu niwasilishe kwa Serikali kilio cha wananchi wa Jimbolangu wenye shida ya maji kupindukia. Kata ya Rutoro vijijivyote vinne vinashida ya maji kupindukia. Kata ya Ngenge,Vijiji vya Kishuko, Ngenge na Kuzigembe matatizo yao ya majini kama maeneo aliyoyaelezea Mheshimiwa Ole Sendeka.

Mheshimiwa Spika, Kijiji cha Omulanazi, Kata yaMashabago mfumo wa maji uliofungwa umeshindwakufanya kazi. Suluhisho mojawapo la mfumo huo ni kuwekapampu inayoendeshwa na mfumo juu (Solar Energy). Kipatocha watu wa sehemu ile hakiwawezeshi kumudu gharamaya kununua Diesel kila watumiapo mfumo huo.

Mheshimiwa Spika, mwisho, niwakilishe kupitia Bajetiombi langu la kila mara juu ya Mradi wa Maji katika Mji Mdogowa Kamachumu. Mfumo wa maji uliojengwa mwaka 1958sasa umeshindwa kukidhi mahitaji ya wananchi. Watuwameongezeka sambamba na ongezeko la shughuli zakibinadamu zinazohitaji maji mengi na ya uhakika.

Mheshimiwa Spika, wananchi wa eneo laKamachumu chini ya uongozi wangu na Halmashauri yaWilaya wameanzisha Mradi wa kuboresha mfumo huu kwakupanga kutumia chemchemi za Kalinga. Mradi huuukifanikiwa Vijiji vya Bulembo, Bunywambele, Kanoni,Bushangara, Irogelo na Kafunyo vitanufaika. Mafanikio haya

Page 117: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

117

29 APRILI, 2013

gharama yake ni ndogo kuliko gharama ya miradi mingineambayo huduma yake kwa wananchi ni ndogo.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. ENG. RAMO MAKANI: Mheshimiwa Spika, kuhusuutekelezaji wa miradi ya maji. Nianze na matumizi yawataalam hasa Wahandisi Washauri; Serikali itumie kanzidatailiyopo Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) ili iajiri na kuwatumiawataalam hawa wenye sifa na uzoefu katika research,planning, design na kadhalika. Hali ilivyo sasa ni hatari nagharama kubwa kwa Serikali.

Mheshimiwa Spika, Halmashauri za Wilaya ambazondizo watekelezaji wa miradi katika ngazi ya ujenzi(construction) na matunzo/matengenezo (maintenance)ziwezeshwe kuwa na Wahandisi wa Maji, Mafundi Sanifu naMafundi Sadifu wa kutosha kwa idadi na utaalam (ujuzi). Paleambapo haitoshi, resource sharing itumike miongoni mwaHalmashauri.

2. Mheshimiwa Spika, kuhusu hali ya maji Tunduru;Tunduru Mjini, Mamlaka ya Maji Mji wa Tunduru ilianzishwana kukabidhiwa mtandao wa maji chakavu (almost uliokufa)na kwa hiyo kushindwa kuanza kazi kwa kukosa mtaji (initiallost).

Mheshimiwa Spika,Halmashauri hii haina fedha nahaiwezi kujiendesha kutokana na kukosa mapato kutokanana tozo ya huduma ya maji, maana hayapo, hivyo hakunawateja wa kuchangia.

Mheshimiwa Spika, naomba Mamlaka ya Maji,Tunduru ikamilishwe kimuundo, watumishi, ofisi, vifaa na Bajetiili ianze kazi seriously mara moja.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Maji Viji j ini; hali yaupatikanaji wa maji vijijini Wilayani Tunduru ni taabani.Takwimu zinaonesha idadi ya vijijini vyenye hali mbaya,

Page 118: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

118

29 APRILI, 2013

kuongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na kukosekanakwa maintenance culture.

Mheshimiwa Spika, naomba Wizara itembeleeTunduru kujionea na kuchukua hatua.

MHE. ASSUMPTER N. MSHAMA: Mheshimiwa Spika,napenda kuchangia Wizara ya Maji kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Ilani ya Chama cha Mapinduzi yamwaka 2010 iliwaeleza wananchi kuwa ifikapo 2015 maji safina salama yatakuwa yamewafikia wananchi kwa asilimiathemanini (80%), suala ambalo limekuwa kitendawili. Pia Seraya Maji ya mwaka 2012 ililenga katika kuhakikisha kuwa,wananchi vijijini wanapata maji safi na salama. Umbali usiozidimita 400, kutoka kwenye makazi yao. Jambo ambalo ni gumusana kutokea hata miaka ishirini (20) i jayo kamahakutafanyika mikakati ya makusudi.

Mheshimiwa Spika, mpaka Disemba, 2012 ndiokwanza waliopata maji ni milioni 20.6 ambayo haijafika hataasilimia hamsini. Je, mamilioni ya watu waliobaki watafikiwalini ili nao wapate maji safi na salama? Hii inakatisha tamaa,shida kubwa ni kutokuwa na vipaumbele na vikatekelezeka.

Mheshimiwa Spika, kuhusu uhifadhi wa mazingira navyanzo vya maji; mikakati ya kuhifadhi vyanzo muhimu vyamaji zoezi hili limekuwa halitekelezwi ipasavyo. Katika Wilayayangu ya Missenyi vyanzo vingi vya maji vimeharibiwa na haowanaojulikana kama wahifadhi, maana vyanzo vyetuvilitengwa na simenti, hivyo vimeziba chemchemi zetu namatokeo vimekauka hasa na ukweli walijenga chini yakiwango.

Mheshimiwa Spika, vyanzo vingi vya maji vya wilayaya Missenyi ni vya asili, kinachohitajika ni kuvisafisha nakuviacha kama vil ivyo maana kuvijengea kunazibachemchemi na hivyo vinakauka kabisa na kusababishausumbufu kwa kuwa vimebomoka na kuziba chemchemi.

Page 119: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

119

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, suala la Vijiji Kumi kupata maji kilaWilaya kweli hilo linaweza kuleta tija ya kufikia wananchi waTanzania kwa asilimia themanini (80%) ifikapo 2015? Jambohili sidhani kama linawezekana ukizingatia vijiji ni vingi sana,Missenyi tu kuna vijiji 74, na Serikali imeviwezesha vijiji kumi, hiisiyo hata robo. Je, Serikali inaweza kunieleza mpaka kufikia2015 vijiji vingapi vitafikiwa katika kupata maji salama?

Mheshimiwa Spika, kuhusu changamoto za visimakumi (10) kila Wilaya; vijiji kumi vya kila Wilaya vimekuwa nachangamoto nyingi.

(a) Watafiti walifanya mchakato na mwishowakatoa majibu sehemu za kuchimba maji, lakini wachimbajihawakupata maji katika maeneo mengi.

(b) Sehemu nyingi hawajaanza kuchimba kwasababu ya maelezo ya tofauti yaliyopelekwa Wilayani,kusema kuwa maji hayawezi kuchimbwa mpaka hiyo asilimiaitimie, sehemu nyingi wameambiwa asilimia ishirini (20%) yafedha za mradi, kitu ambacho siyo sahihi, matokeo yakemiradi imesimama.

Mheshimiwa Spika, je, Mheshimiwa Waziri anawezakutusaidia kujua taratibu zipi zifuatwe il i wananchiwachimbiwe maji safi na salama. Kama tulivyo waahidikwenye Ilani ya Uchaguzi wa CCM.

Mheshimiwa Spika, je, kwa wale waliochimba na majiyakakosekana, nani atafidia hasara, au ndio hasara kwaSerikali ukizingatia pia kuwa jukumu la kuratibu uchimbaji wavisima vya maji ni duni, na Mheshimiwa Waziri amesemautaratibu huo unalenga kuhakikisha kwamba taratibu zakitaalam zinafuatwa ili kuhakikisha visima vina ubora namatumizi endelevu.

Mheshimiwa Spika, Wizara iliwapa makapuni 131kuchimba visima na vikachimbwa visima 420, hakutwambiavingapi vimetoa maji na vingapi havikutoa maji na kamahavikutoa maji hasara ya nani?

Page 120: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

120

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, kuhusu Mradi wa Hifadhi yaMazingira ya Ziwa Victoria; awamu ya pili ya Mradi waUsimamizi na Hifadhi ya Mazingira Ziwa Victoria ilianza 2009,nchi husika ni Tanzania, Kenya na Uganda. Madhumuni yaMradi huu ni kuimarisha usimamizi wa pamoja wa rasilimaliza bonde la Ziwa Victoria kwa kudhibiti uharibifu wa mazingirakatika ziwa hilo. Kwa upande wa Tanzania, Mradi unalengakuimarisha Taasisi zinazohusika na hifadhi ya maji na samaki.

Mheshimiwa Spika, kumekuwepo uharibifu mkubwawa mazingira, kuvua samaki hata wasiofaa kuvuliwa naukizingatia kuwa utaratibu wa kuachia uvuvi wa muda ilisamaki wazaliane na wakue, ili kuzuia samaki wadogo nahivyo kufaidika kuvua samaki wenye kilo 29 kutosha na hivyokupata fedha za kutosha, lakini zoezi hili limekuwa halifanyikikwa nchi nyingine, Tanzania ikifunga uvuvi Uganda na Kenyawanaendelea kuvua.

Mheshimiwa Spika, kama Tanzania ndio imepewa kaziya kuimarisha Taasisi zinazohusika na hifadhi ya maji nasamaki, Wizara inatueleza nini kuhusu kuweka mkakati wakulinda ziwa hilo wakati wa zuio la kuvua ili kila nchi isivuewakati wa zuio na ikivua iwekwe faini au adhabu kubwa ilikukomesha uvunaji samaki kwa kipindi hicho.

Mheshimiwa Spika, kuhusu chanzo cha maji cha MtoKagera na Mto Ngono; Mto Kagera na Mto Ngono (Nkenge)ni mito ambayo inaweza kutoa maji ya kutosha na kumwagiliana hata kuzalisha mpunga kupitia mabonde ya mito hiyo nahivyo kuongeza kipato cha Wanamissenyi na kuchangia patola Taifa.

Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango gani wakuwapa maji ya mito hii kwa matumizi ya nyumbani yaliyosafi na salama ukizingatia Missenyi ni Wilaya mpya.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

Page 121: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

121

29 APRILI, 2013

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Spika, kilio chamaji licha ya kuwa ni cha nchi nzima, naomba kuweka mbeleyako kilio cha watu wa Rombo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, mradi wa visima kumi (10)hadi sasa haujazaa matunda. Ni mambo manne (4) tuambayo yameonesha dalili za kuwepo maji. Halmashauriinaomba fedha ambazo zimetengwa kwa ajili hiyo zitumikekwa ajili ya kujenga malambo kwa kukinga maji katika mitoya msimu.

Mheshimiwa Spika, ombi la kupatiwa malambolilitolewa pia kwa Mheshimiwa Rais wakati akizinduabarabara Jimboni. Mheshimiwa Rais aliahidi kwamba kablaya kumaliza kipindi chake cha uongozi atatupatia malambomawili. Wananchi wanasubiri kwa hamu utekelezaji wa ahadiya Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, pili, katika Bajeti ya mwaka huuunaomalizika, tuliomba maji ya Ziwa Chala yatumike kwa ajiliya wananchi. Jibu la Serikali lilikuwa kwamba, Mamlaka yaBonde la Pangani inachunguza kama maji hayo yanafaa kwamatumizi ya binadamu. Pamoja na kwamba majibuhayajapatikana, lakini wenzetu wa Kenya na Lake ChalaSafari Lodge wanayatumia. Jambo hili linawapa wananchihasira dhidi ya Serikali yao. Tunaomba mradi wa kusukumamaji hayo ili yawafae wananchi hasa wa ukanda wa chiniambao shida ya maji ni kubwa sana kwao.

Mheshimiwa Spika, mwisho, Kampuni ya Maji Kilwaterimethibitisha kwamba, imeshindwa kuwapa wananchihuduma ya maji kutokana na kushindwa kugawa maji kidogoyaliyopo kwa haki na kutawaliwa na rushwa.

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Rombo tunaiombaSerikali kuivunja Kampuni hiyo na badala yake kuanzishaKampuni nyingine au mamlaka ya maji ambayo itabunivyanzo vipya na kusambaza maji kidogo yaliyopo kwa haki.

Page 122: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

122

29 APRILI, 2013

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Spika, majini muhimu na Bajeti tuliyonayo ni ndogo. Naomba Serikaliizingatie maoni ya Kamati kwa kuiongezea Wizara hii fedhakiasi cha shilingi bilioni 185 ili kuweza kufikisha maji vijijini.

Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya mwaka 2012/2013,imepata pesa kidogo ikilinganishwa na pesa zilizopitishwa naBunge letu. Naiomba Serikali kuhakikisha katika Bajeti yamwaka huu ziende kama ilivyokusudiwa ili kutekeleza miradiiliyopangwa.

Mheshimiwa Spika, akinamama ni waathirikawakubwa sana wa tatizo la maji. Naiomba Serikali iupe mradiwa maji kipaumbele ili akinamama waondokane na adhahii.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, Mradiwa Maji kwa Vijiji Kumi (10) kwa kila Halmashauri nchiniumekuwa wa kusuasua bila mafanikio toka ulipoanza mwaka2003. Wananchi kwa upande wao wamefanikiwa kuchangiakiasi walichopaswa kuchangia kwa kila kijiji nchini. Hata hivyohaya yote yanatokea kwa kuwa Bajeti zetu zimebakikutegemea wafadhili ili miradi itekelezwe. Hili ni hatari sanakwa Taifa na hasa kwa suala muhimu kama hili la maji.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali ipunguzematumizi mengine na kuelekeza fedha nyingi katika miradiya maendeleo. Hata hivyo, udhibiti wa mianya ya rushwa,ufisadi ni muhimu sana ili fedha zielekee katika miradi yamaendeleo. Serikali kwa kusimamiwa na Bunge inapaswakufanya tathmini ya kina kwa Mradi huu wa Vijiji Kumi kablaya kuanza kwa programme hii kwa awamu ya pili.

Mheshimiwa Spika, kuhusu udhibiti wa maji taka;kulingana na ongezeko la watu nchini ndivyo ambavyo kunaongezeko la maji taka katika miji mikubwa na miji inayokuahapa nchini. Tumeshuhudia katika miji mikubwa wakati mvuakubwa zikinyesha hapa nchini, maji taka nayo hutiririka na

Page 123: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

123

29 APRILI, 2013

kusababisha magonjwa ya milipuko na kuathiri nguvu kazihapa nchini.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali kuzisimamiaMamlaka za Maji Mijini kuweka miundombinu bora na yauhakika itakayoweza kupitisha maji taka bila kuleta atharikwa jamii. Hata hivyo, elimu kwa wananchi inahitajika zaidiili uelewa wa masuala ya maji taka na athari zake uelewekekwa ufasaha.

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ukweli nikwamba tatizo la maji ni kubwa sana karibu nchi yote. KatikaJimbo la Nyang’hwale napenda kusema Jimbo hili linamatatizo sana kwa upatikanaji wa maji safi na salama karibuKata zote kama Bukwimba, Izunya, Kafita, Kharumwa,Nyugwa, Kakora, Shabakaba, Busolwa, Nyang’hwale,Nyijundu, Nyaburanda, Mwingiro.

Mheshimiwa Spika, tatizo hili la maji limesababishabaadhi ya mambo kama mimba kwa wasichana, kuvunjikakwa ndoa nyingi, akinamama kuota vipara, akinamamakutopata mapumziko vizuri, maradhi mbalimbali yatokanayona kunywa maji ambayo si safi na salama, vituo vya afya nazahanati kutofanyiwa usafi wa uhakika na wanafunzi wa shuleza msingi na sekondari kupoteza vipindi vingi vya masomoyao.

Mheshimiwa Spika, napenda kuipongeza Serikali kwajuhudi zake za kupambana na tatizo la maji Jimbo laNyang’hwale na kutuchimbia visima katika baadhi ya vijijikama Nyalubere, Kitongo, Izunya, Kayenze, Ikangala, Kakora,Kharumwa, Bukwimba na Nyamtukuza. Visima vyote nanehavitoi maji, kisima kimoja cha Kij i j i cha Kharumwahakijafungwa pampu zaidi ya miezi 18 tangu kichimbwe.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa ushauri wangukuwa, zitengwe pesa zaidi ili kufufua mtandao wa maji uliopoZiwani Nyamtukuza ambao ulisimama kutoa maji tangu 1975.Mtandao huo ulikuwa ukisambaza maji katika Vijiji vyaNyamtukuza, Kakora, Nyarubere, Kitongo, Ikangala,

Page 124: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

124

29 APRILI, 2013

Kharumwa, Izunya, Kayenze na Bukwimba, mtandao huo sasaufufuliwe ili kupanua zaidi usambazaji wa maji katika Katazote na vijiji vyote vya Jimbo la Nyang’hwale.

Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali kwa kutengafedha za maji katika Wilaya ya Nyang’hwale kiasi cha sh.316,590,593/= kwa mwaka wa 2013/2014. Pesa hizi ni kidogosana ukizingatia uhitaji wa maji Jimboni Nyang’hwale,naomba pesa zaidi ziongezwe.

Mheshimiwa Spika, pia naishauri Serikali ijengematenki ya kuvunia maji ya mvua kwenye mashule yote yasekondari, shule za msingi, zahanati, vituo vya afya na vituovya Polisi ili kupunguza tatizo la maji.

Mheshimiwa Spika, siungi mkono hoja hii mpakaSerikali iongeze Bajeti ya maji katika Jimbo la Nyang’hwale.

MHE. ISRAEL Y. NATSE: Mheshimiwa Spika, napendakutoa mchango wangu kuhusu hoja hii ya Wizara ya Maji.

Mheshimiwa Spika, kero ya maji ni kwa nchi nzima,hivyo napenda kuishauri Serikali katika mambo yafuatayo:-

Kwanza, utunzaji wa vyanzo vya maji; Serikali ihakikishekuwa vyanzo vya maji vinatunzwa kwa gharama yoyote ile.

Pili, kuchukua hatua kali kwa wale wote wanaoharibumazingira na vyanzo hovyo. Namwomba Mheshimiwa Waziriafike katika bonde la Eyasi na kuangalia uharibifu wa chanzocha Qanded, chanzo ambacho hutumika kwa kilimo chaumwagiliaji. Pia Serikali iboreshe skimu za umwagiliaji.

Mheshimiwa Spika, kuhusu uvunaji wa maji; Serikaliiwekeze katika kutengeneza miundombinu ya uvunaji wa majihasa katika Taasisi zote kwa shule zote za msingi/sekondarina kadhalika na kutengeneza mabwawa kwa matumizi yabinadamu na mifugo.

Page 125: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

125

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, napenda kushauri Serikali kuhusumpango wa maji wa vijiji kumi (10) kwa Halmashauri zote.Mpango huu unasuasua sana katika Halmashauri yangu yaKaratu, kati ya vijiji kumi, vijiji nane (8) maji yalipatikana, lakinichangamoto kubwa ni umeme. Nashauri Serikali iangaliempango wa matumizi ya nishati ya umeme wa jua (solar) naupepo ili kuweza kupampu maji hayo.

Mheshimiwa Spika, kero ya maji katika Mji wa Karatuni kubwa sana. Tarehe 18 Machi, 2013 Mheshimiwa Waziriwa maji Mheshimiwa Profesa Maghembe alifika Karatu nakutoa ufumbuzi wa dharura kwa wananchi wa Karatu.Mheshimiwa Profesa aliagiza kuwa ndani ya siku kumi (10)tayari Serikali itakuwa imeweka pump ya kuvuta maji nakuchimba visima viwili mpaka sasa hakuna kilichofanyika.

Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Wazirianiambie kama kauli ile ilikuwa ni ya kufurahisha wananchiwa Karatu tu au anamaanisha kweli na lini kazi hiyo itaanza?

Mheshimiwa Spika, naomba majibu ya Serikali.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, maji nimuhimu sana katika Uhai wa mwanadamu. Tunaiomba sanaSerikali hii iongeze bajeti ya Wizara hii kwani vijijini kunamatatizo makubwa sana ya maji. Kama Serikali haitawekezakuongeza fedha hasa kwa wananchi wa viji j ini nchihaitakuwa na maendeleo. Mradi wa vijiji kumi umeshindwakabisa kukidhi mahitaji ya wananchi, ni vyema tukawa namipango ya muda mfupi ya kutatua tatizo la maji.

Mheshimiwa Spika, katika Jimbo langu kuna Vijiji vyaNgomalusambo, Igagala, Kabungu, Kamsanga, Ifukutwa,Majalila, Vikonge, Katuma, Kasekese, Kabage, Sibwesa,Kapalamsenga, Isenga na Tarafa ya Mwese, kuna matatizomakubwa sana ya maji. Naiomba Serikali ipeleke hudumahiyo muhimu ya maji katika vijiji hivyo, tukipeleka huduma yamaji tutakuwa tumewasaidia wananchi na kukuza uchumikatika maeneo hayo.

Page 126: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

126

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, nitaunga mkono hoja kama miradihii itatekelezwa katika vijiji nilivyovitaja hapo juu.

MHE. REBECCA M. MNGODO: Mheshimiwa Spika,katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, ukurasa wa 85,kuna maelezo kwamba, miradi ya kipaumbele ambayoinatoa huduma kwa wananchi wengi zaidi imeendeleakujengwa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Mradi wa Maji waVijiji Kumi (10) kwa kila Halmashauri.

Mheshimiwa Spika, lakini pia katika kitabu hicho hichocha hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, jedwali Na. 11kuhusu mpango wa kutekeleza vijiji 10 kwa kila Halmashauri,ukurasa wa 130, vijiji vitano (5) vilivyopewa kipaumbele katikaHalmashauri ya Meru na vinavyotekelezwa kwa mwaka 2012/2013, ni Kasanumba, Kikuletwa, Mbunguni, kwa Ugoro naAmbureni Moivaro”.

Mheshimiwa Spika, ningependa kujua, je, ni kwakiwango gani mradi huo umetekelezwa katika vijiji hivyo? Je,kazi ya mradi huo imemalizika katika vijiji hivyo na hivyo kuwasababu ya kuongeza vijiji vingine vitano (5) kwa mwaka huuwa fedha 2013/2014 ambavyo ni Valeska, King‘ori, Majengo,Patanumbe, Nkoarisambu, Nshupu na Kasanumba?

Mheshimiwa Spika, ningependekeza kwamba,endapo kazi katika vijiji vitano (5) vinavyofanyiwa kazi/mradikwa mwaka 2012/2013 haijamalizika, basi ni bora mradiukamalizika kwanza na ndipo kuongeza mradi mwinginekatika vijiji vipya vitano (5) kwa mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, kimsingi wananchi wa maeneohayo katika Wilaya ya Meru wanapata adha kubwa ya majikwa miaka mingi. Eneo la King’ori Madukani ambalo linabomba la maji linalotokea maeneo ya Mlima Meru, wananchihupata maji kwa mgao. Cha kusikitisha ni kwamba mkazimmojawapo anauza maji ya bomba la Serikali katika eneohilo la King’ori madukani, je, Serikali imetoa kibali kwa mkazihuyo?

Page 127: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

127

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa maji ni rasilimaliinayotakiwa kufaidika kwa kila Mtanzania, ni kwa nini Serikaliinakaa kimya wakati baadhi ya wananchi wanajimilikishamaji ya bomba lililowekwa na Serikali kwa faida yaowenyewe kama ilivyo King’ori Madukani ?

Mheshimiwa Spika, nashauri Serikali ifuatilie suala hiloili kukomesha biashara hiyo ambayo inawaudhi wakaziwengine wa pale.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Mradi wa Vijiji Kumi (10),Serikali iweke umuhimu mkubwa kukamilisha miradi hiyo katikaWilaya ya Meru ikiwa ni ile inayoendelea ya 2012/2013pamoja na hiyo mipya ya 2013/2014. Hii itasaidia sana katikakuwapunguzia wanawake adha kubwa wanayoipata yakusafiri umbali mkubwa kutafuta maji.

MHE. KAPT. JOHN Z. CHILIGATI: Mheshimiwa Spika,awali ya yote naunga mkono hoja hii. Hata hivyo, pamojana kuunga mkono napenda kutoa hoja na maombiyafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusu upeo wa tatizo la majiKitaifa; kero kubwa ya Watanzania kuliko zote kwa sasa niupungufu wa maji, hasa vijijini. Takwimu za Wizara zinaoneshani 58% tu ya wananchi vijijini ndio wanapata maji safi nasalama. Wilaya ya Manyoni ni 53% tu, Serikali ikubali ushauriwa Wabunge kwamba tatizo la maji l isiendeleekushughulikiwa kwa utaratibu wa kawaida kupitia bajeti yakawaida (business as usual).

Mheshimiwa Spika, ushauri ni kwamba, iundweWakala wa Maji Vijijini mithili ya REA (umeme), ili bajeti yakeitoke Serikalini, Wahisani na mikopo ya nje na ndani,tusiendelee kutegemea fedha za mkopo wa World Bankpekee, lazima tuchukue hatua zingine nje ya miradi chini yamkopo wa World Bank.

Mheshimiwa Spika, tatizo la maji Wilaya ya Manyoni,hasa Kata nane zilizo katika eneo la Bonde la Ufa kuna ukame

Page 128: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

128

29 APRILI, 2013

na maji yakichimbwa chini ya ardhi ama hayapatikani nayakipatikana yana chumvi nyingi. Hivi sasa kuna mradi waWorld Bank katika Vijiji vya Kintinku na Lusilile, wataalamwamechimba visima, lakini wanakosa maji!

Mheshimiwa Spika, ushauri tunaoutoa kwa Wizara nikwamba, maji katika vijiji hivi yavutwe kutoka mwinuko waMbwasa (along Saranda escarpment). Eneo hili tayari linavisima visivyopungua vitatu (3) na vyote vina maji mengi. Majihayo tunaomba yawekewe bomba toka hapo kilipo chanzocha maji (Mbwasa) hadi Kintinku. Aidha, vijiji vya njianiambamo bomba litapita navyo vipatiwe maji, Vijiji hivyo niChelejeho, Maweni, Mvumi, Ngiti na Lusilile.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mipango ya kuvuna majiya mvua; maji ya mvua takribani yote hupotea kila mwaka.Hii ni dhambi kubwa. Tujisahihishe, Wizara iagize uwepo washeria, kila mtu anayejenga nyumba ya bati au vigae ajengetanki la chini la kuvuna maji kwa ajili ya familia yake.

Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara hiyo pamoja naHalmashauri za Wilaya ziweke fedha za kuvuna maji kwakuweka makinga maji katika Mito ili tupate Mabwawamadogo (Charcal dams) ambayo yatapunguza sana tatizola maji vijijini.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMAZINA: MheshimiwaSpika, nianze kwa kumpongeza Waziri, Naibu Waziri pamojana wataalam wote wa Wizara kwa kazi nzuri wanayoifanyakatika mazingira magumu ya bajeti finyu.

Mheshimiwa Spika, maji na umeme ni miundombinumuhimu katika kutukwamua kutoka katika dimbwi laumasikini. Kwa sababu hiyo, watumishi wa Wizara shartiwawajibike ipasavyo. Bahati mbaya Ngara tuna watendajiwabovu sana katika Idara ya Maji; Maji Mjini na Maji vijijini.Watendaji hao wanawaweka Wakandarasi ambao ni nduguzao na hivyo kukwamisha miradi.

Page 129: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

129

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, katika vijiji vitano (5) vya maji yaWorld Bank – ni Vijiji viwili tu vya Rulenge na Ngundusivimeanza kushughulikiwa, lakini kazi inakwama kwama kwasababu ya undugu wa Wakandarasi na Watendaji.

Mheshimiwa Spika, kuna Kijiji cha Mbuga ambachokilikuwa kwenye orodha ya vijiji vya maji ya World Bank, lakininaona hakiko kwenye orodha tena wakati wanakijij iwalichanga fedha zao. Kijiji hiki ni muhimu sana kwa sababukina Sekondari mbili na Dispensary moja, naomba sanakirudishwe kwenye orodha.

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla Ngara ina matatizomakubwa sana ya maji, karibu vijiji vyote 73 havina maji.Wilaya ya Ngara ina Mito mikubwa miwili ya Kagera naRuvubu lakini hatufaidiki na maji ya Mito hiyo.

Mheshimiwa Spika, tatizo kubwa sana kwa upandewa maji, kwetu Ngara ni watendaji wabovu na wabadhirifuna wanaotuchagulia Wakandarasi ndugu zao ambaohawakidhi viwango. Mwaka jana nilimtaja ndugu Rwegasiramaji vijijini, mwaka huu naongeza Mkuu wa Idara ya Maji Mjini,ndugu Magai. Hawa watu wawili bila kuondolewa Ngaratatizo la maji litabaki pale pale. Najua hakuna siri Serikalini,lakini wananchi wamechoka na Wakuu hao wa Idara, namisiogopi kuwataja.

Mheshimiwa Spika, naiomba Wizara ya Maji,Mheshimiwa Waziri awasiliane na TAMISEMI (Serikali ni moja),watuletee watu wazuri na waadilifu. Maafisa haowaondolewe.

Mheshimiwa Spika, Ngara iko pembezoni mwa nchi,hivyo maafisa wanaopelekwa huko wanakuwa miunguwadogo, kazi ni kujitajirisha tu.

Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kuwapongeza tenaMheshimiwa Waziri na Naibu wake na watendaji wote waWizara kwa kazi nzuri sana wanayoifanya. NamwombaMheshimiwa Waziri atembelee Wilaya yangu ya Ngara aone

Page 130: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

130

29 APRILI, 2013

ukubwa wa tatizo, Mji Mdogo wa Ngara una matatizomakubwa sana ya maji kwa sababu system ya Ngara Hightsimechoka, mabomba yamechoka kwani yaliwekwa miakaya 80.

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa Spika,kikosi 821 cha Bulombora kimezungukwa na Ziwa Tanganyika.Cha kushangaza kikosi hiki hakina maji ya kutumia na kikosihiki kinachukua wanafunzi ambao wanajiunga na JKT 3,000.Wanafunzi ambao wanajiunga na JKT pamoja na wakufunzina wake wa wakufunzi hawana maji ya kutumia. Wakihitajimaji mpaka waende Ziwa Tanganyika, cha kusikitisha ZiwaTanganyika kuna mamba na baadhi yao hupoteza maishakwa kuliwa na mamba.

Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itayavuta haya majikutoka Ziwa Tanganyika na kuingia kwenye kikosi 821 chaBulombora na kuepusha adha wanayoipata wakufunzipamoja na wanafunzi ambao wanakwenda kujiunga na JKT?

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la maji safi; Mkoa waDar es Salaam kumekuwa na tatizo la upatikanaji wa majisafi. Maji ambayo yanatoka DAWASCO yamekuwa si salamakwa kunywa. Wananchi wanalipia maji kila mwisho wamwezi, lakini hawapati maji safi, wenye uwezo wananunuamaji ya drop na kadhalika, kwa wasiokuwa na uwezo(hawawezi kununua maji ya drop) hutumia maji ambayo sisalama kwa afya zao.

Mheshimiwa Spika, hii inasababisha milipuko yamaradhi ya mara kwa mara kwa mfano, kipindupindu, taifodina kadhalika. Je, ni lini Serikali itahakikisha inasimamia vyanzovyote vya maji na kusambaza madawa ya kutosha katikavyanzo vyote vya maji ili wananchi wapate maji safi nasalama?

Mheshimiwa Spika, kuna baadhi ya Mitaa wanajenganyumba bila mpangilio, sehemu wanayojenga wananchi haoDAWASCO walikuwa wamepitisha mabomba ya maji safi namulemule wananchi hao wanapitisha mabomba ya maji

Page 131: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

131

29 APRILI, 2013

machafu, hii itaepusha wananchi kutopata maradhi yamlipuko!

Mheshimiwa Spika, ni kwa nini Serikali haiwachukuliihatua hao ambao wanapitisha mabomba ya maji machafukwenye vyanzo vya maji?

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la uchimbaji wavisima vya maji kwenye Mikoa mbalimbali; kuna hii miradi yauchimbaji visima, wamekuwa wakichimba visima vikubwa navipana kiasi ambacho hata walemavu wanashindwakwenda kuchota maji na kusababisha maafa. Vile vile kunabaadhi ya visima havina maji, ni kwa nini visifukiwe auvikajengewa uzio na hivyo vinavyotoa maji vijengewe uziomaalum. Hii itaepusha vifo vya watoto pamoja na walemavukwani kuna baadhi ya Mikoa imeweza kupata maafa kupitiavisima hivyo kama Tabora, Singida na kadhalika.

SPIKA: Sasa namwita Mheshimiwa Naibu Waziri waMaji.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninaombanichukue nafasi hii kwanza kuwashukuru sana WaheshimiwaWabunge, kwa michango yao mizuri iliyosheheni maonimbalimbali ya kuboresha Sekta hii ya Maji. Wabunge wotewaliochangia kwa maandishi, waliochangia kwa kuongeahapa Bungeni wameonesha kuguswa sana na tatizo la majikatika nchi yetu, mijini, vijijini na mahala pengine panapohitajihuduma ya maji. Wabunge wote kwa pamoja wamefikiamaamuzi yanayoonesha wazi kabisa kuwa, Sekta ya Majindiyo key determinant ya maeneo mengine zikiwemo Sektaza Afya, Sekta za Elimu na Sekta za Uzalishaji na wameoneshakuguswa kwao kuwa yale Malengo ya Milenia yakiwemokupunguza umaskini, kuwapeleka watoto shuleni nakupunguza maradhi haya ya kuambukiza au ya mlipukoyanayochangiwa sana na tatizo la maji kutokuwapo.

Kwa maana hiyo, ninataka kuwahakikishiaWaheshimiwa Wabunge kwamba, yale yote mliyoyasema sisikama Wizara tuliokabidhiwa dhamana hii, tutayafanyia kazi

Page 132: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

132

29 APRILI, 2013

na tutatoa ushirikiano yaweze kutekelezwa na Wananchiwaweze kupata maji kama ilivyopangwa kwenye Sera zetu.Katika michango hii, lipo suala ambalo limejitokeza nalimechangiwa na Wabunge mbalimbali, kwa hisia mbalimbalina hili ni la kupeleka Mradi wa Maji wa Same, Mwanga naKorogwe. Kweli katika hali tuliyo nayo ya ufinyu wa bajeti,katika hali ya kutokuwa na maji katika maeneo mengi yanchi, inatoa hisia kwa Wabunge mbalimbali kwamba,huenda Mradi ule unatekelezwa kwa upendeleo.

Mheshimiwa Spika, ninaelewa kabisa kama hisiaalizonazo Mheshimiwa Blandes, ambaye amekuwa akifuatiliaMiradi yake ya Maji, anaguswa na maji. Ninadhani issue hapasiyo nani kapewa nini, issue ni hali halisi kuwa maji yanahitajikasehemu nyingi katika miji yetu na ndiyo maana hisiazimetolewa kwa aina tofauti; wako waliotoa hisia kwakuonesha kuwa wao wanahitaji maji katika miji yao, lakiniwapo waliotoa hisia zao kwa kuonesha mbona hakakasungura kadogo kuna mtu kachukua sehemu kubwa zaidi!Tunalielewa hilo, lakini tatizo kubwa ni ufinyu wa bajetiilivyokuwa.

Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi kumshukuru sanaWaziri wa Fedha, ambaye sasa ameonesha mwanga kuwahaya yote tunaweza kuyachukua na kufanya sehemu kubwaya kutekeleza Miradi hii. Niseme tu kwamba, Serikali yetukuanzia awamu ya kwanza, imekuwa ikitekeleza Miradimbalimbali; ipo Miradi mikubwa hasa hii ya Miji ambayouwekezaji wake ni mkubwa sana. Kuanzia miaka ya 1974imejengwa Miradi ya Handeni Trunk Main ambayo nimikubwa inayohudumia vijiji vingi.

Tuliweza kujenga Mradi wa Makonde unaohudumiaWilaya tatu za Newala, Tandahimba na Mtwara Vijijini. Hayoyalikuwa ni maamuzi makubwa, haikuwa na maana kwambasehemu zote zina maji, lakini tuliamua kwamba ni lazimatuanze. Kwa kuzingatia misingi hiyo iliyowekwa na Baba waTaifa, Serikali ya Awamu ya Pili na Awamu ya Tatu imeendeleakutenga fedha kwenye Miradi mikubwa na mpaka sasa hivitumeweza kujenga Mradi mkubwa wa Mbwinji – Masasi –

Page 133: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

133

29 APRILI, 2013

Nachwingea, ambao uko katika hatua za mwisho kukamilikana unagharimu shilingi bilioni 31. Tunajenga Mradi mkubwawa Chalinze ambao unakaribia kukamilika na loti kati kaributisa na Mradi huu unagharimu karibu bilioni 56. Kwa hiyo, hiini Miradi mikubwa.

Mheshimiwa Spika, ipo Miradi mikubwa ambayo ipokatika hatua mbalimbali za manunuzi, ikiwemo ya kutoa majikutoka Shinyanga kwenda Tabora, kupeleka maji katika vijiji100 vya kwenye bomba kuu linalotoa maji kutoka ZiwaVictoria mpaka Shinyanga na Kahama. Kwa hiyo,kilichofanyika katika Mradi huu wa Same - Mwanga naKorogwe ni mwendelezo wa Miradi mingine ambayo ni azmaya Serikali ya kupeleka maji maeneo mengine yote.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba niwahakikishieWaheshimiwa Wabunge kwamba, maoni yaotumeyazingatia, lakini yote hii ni kwa sababu ya tatizo lafedha na haina maana kwamba kuna maeneo hatutafikiana kama ni lazima tuanze ili tuweze kuitekeleza Miradi hii yote.Ninawaomba sana muunge mkono hoja hii ili tuanzekutekeleza.

Mheshimiwa Spika, imejitokeza issue kwamba, katikaMradi huu umetengewa fedha nyingi haziwezi kutumika zotekwa wakati mmoja. Mradi huu tunaugawa kwa loti tatu nasababu ya kuugawa kwa loti tatu ni kwa sababu unatakiwautekelezwe kwa miezi 18, mwaka mmoja na nusu. Kwa hiyo,tutakuwa na wakandarasi watatu ambao mmoja atatoa majikutoka pale Nyumba ya Mungu mpaka Kisangani na wawiliwatatoa kutoka pale Kisangani kwenda Same na mwinginekwenda Mwanga. Kwa hiyo, hizo fedha zitatumika kwa jinsiilivyopangwa na kwa muda ambao tumeudhamiria.

Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa maelezomachache, nawaomba Wabunge watuunge na nilete tafsiriambayo siyo rasmi kwamba, tafsiri ya www.com tusemewaache Wananchi wanufaike.com. (Makofi/Kicheko)

Page 134: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

134

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo haya mafupi,niweze kupitia baadhi ya hoja za Wabunge ambazowamekuwa wakichangia hapa na kwa sababu ya muda,nitapitia chache na tumeandaa kitabu hoja zote zimejibiwana ufafanuzi wa kina umetolewa. Ipo hoja ya MheshimiwaAliko Nikusuma Kibona, aliyetoa pendekezo kwamba, Mradiwa Maji kutoka Ziwa Victoria umeonesha mafanikio kwa vilemaeneo ya Mbozi, Ileje na Momba, yana shida ya maji. Je,Serikali haioni umuhimu wa kuchukua maji Ziwa Rukwa kamailivyofanywa kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kutatua tatizo lamaji katika Miji ya Tunduma?

Mheshimiwa Spika, wazo la Mheshimiwa Mbunge nizuri, tunalipokea lakini kwa sasa tulichofanya ni upembuziyakinifu uliokamilika mwaka 2012 unaonesha kwamba, Mijiya Vwawa, Miji ya Tunduma, Miji ya Chunya na Miji mingineya Ileje kule Isongole, vyanzo vilivyopo vinajitosheleza kutoahuduma ya maji. Rasilimali ya maji ya Ziwa Rukwa inatakiwatuiendeleze ili baadaye itakapobidi au itakapoonekana idadiya watu imeongezeka, tuweze kutumia chanzo cha ZiwaRukwa.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mkiwa AdamKimwanga, alielezea ukosefu wa maji kwa Wananchi wa Jijila Mwanza wanaoishi maeneo ya milimani hasa ya Jimbo laIlemela.

Mheshimiwa Spika, Mwanza tunao Mradi wakuboresha huduma ya maji unafadhiliwa na EuropeanInvestment Bank (EIB) na Mradi huu utatoa huduma ya majimpaka kwenye maeneo ambayo watu wamejenga milimaniau juu ya usawa wa tenki ikiwemo Ilemela. Kwa hiyo,utakapokuwa umeanza kutekelezwa, Wananchi hawawatafaidika na huduma hiyo.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Selemani JumanneZedi, anaomba kasi iongozwe kukamilisha ahadi ya Rais yakupeleka maji Tabora kutokea Kahama ifikapo mwaka 2014.Wizara imeshakamilisha taratibu za kuwapata WahandisiWashauri wenye uwezo wa kufanya usanifu na uandaaji wa

Page 135: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

135

29 APRILI, 2013

makabrasha ya zabuni za ujenzi wa maji kutoka Ziwa Victoriahadi Mji wa Nzega – Igunga – Tabora, ambapo wahandisiwashauri hao wamewasilisha mapendekezo tarehe 25 Aprili,mwaka huu.

Mheshimiwa Ally Keissy Mohamed, Mbunge wa NkasiKaskazini, ameuliza ni lini maji yatapatikana Namanyere ilikutatua tatizo sugu la maji. Pia amesema Serikali itenge fedhakutoka vyanzo vyetu vya ndani badala ya kutegemeawafadhili. Mwaka jana tulipeleka Wilaya ya Namanyereshilingi milioni 100 na ile kazi ya kuboresha huduma paleimeanza kufanyika, tumefunga pampu, tunapelekamabomba na dira za maji, huduma hii itakuwa tayari mwezihuu wa tano, 2013.

Mheshimiwa Spika, kuhusu fedha za ndani, Serikalikama mlivyoona, itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya maji,kutumia hela zetu za ndani; na moja ya jambo ambalotumelifanya kubwa mwaka huu ni kuanzisha Mfuko wa Majiambao utaanza mwezi wa saba.

Mheshimiwa Nyambari Chacha Nyangwine, aliulizani lini Serikali itawapatia maji Wananchi wa Tarime kutokaMto Mara. Katika bajeti ya mwaka 2013/14, Serikali imetengashilingi milioni 500 zitakazotumika kwa ajili ya kutekeleza Mradiwa Matokeo ya Haraka. Aidha, Serikali imekamilisha usanifuna uandaaji makabrasha ya zabuni kwa ajili ya Mradi waMaji Safi. Ujenzi wa Mradi utafanyika katika Awamu ya Pili yaProgramu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Vick Paschal Kamata,aliuliza tatizo la maji litaisha lini. Hapa tunao Mradiunaotekelezwa hivi sasa na Kampuni ya Geita Gold Mine(GGM), ambao wanajenga chanzo cha maji kwenye ZiwaVictoria na wanajenga tenki kwa ajili ya kusambaza maji mjinina kulaza mabomba.

Mradi huu unagharimu dola milioni nne lakini sehemuya pili ni sehemu ya kuweka mtandao wa mabomba katikaMji wa Geita na kupanua mtandao ambao unafanywa na

Page 136: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

136

29 APRILI, 2013

African Development Bank (ADB) na Serikali yetu, ambao niMradi unaogharimu dola milioni sita. Utekelezaji wa Awamuya Kwanza ya GGM unakaribia kwisha na kwa sababusehemu ya pili ya kutanua pale mjini itachelewa, kwa sababuinafanyiwa upembuzi yakinifu, hii itakapokamilika ya GGMianze kutoa huduma ya maji kwa kutumia mtandao wa majiuliopo. Tumelazimika kurudia kufanya upembuzi yakinifu kwasababu imekuwa ni mahitaji ya wanaotoa fedha, ADB,wanataka wajiridhishe kwamba hata ile sehemuinayofanyiwa mtandao wa maji na GGM kama inafaa kwaajili ya kuwekeza zile fedha. Kwa hiyo, Mradi huu ukikamilika,Wananchi wa Geita watapata maji ya kutosha.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Maria Ibeshi Hewaamesema, Mwanza hawana maji wanahitaji mabombamapya ili wapate maji. Vilevile amesema, Waziri wa Majiafanye ziara Mkoani Mwanza kwani Wananchi wa Mwanzawanahitaji maji kutoka kwenye mabomba ya maji.

Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza Miradimbalimbali; kama nilivyosema, kuna huu Mradi wa kuboreshahuduma ya maji Mjini Mwanza, kuna Mradi wa kutoa majikutoka Ziwa Victoria kupeleka vijiji 100 Kahama na Shinyanga,kuna Miradi ya uboreshaji maji utakaojengwa kutokaMisungwi - Magu na Lamadi. Miradi hii ikitekelezwa,Wananchi watapata maji. Ombi la kwamba MheshimiwaWaziri afike, tuko tayari tumepokea maombi na tutafikaMwanza.

Mheshimiwa Kebwe Stephen Kebwe anasema, Mji waMugumu unapata huduma ya maji ambayo hayajatibiwatoka Bwawa la Manchila, tumelipokea na Serikali imetengakatika bajeti hii shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuanza ujenziwa mtambo wa kutibu maji katika Bwawa la Manchila.

Mheshimiwa Spika, mwingine aliyechangia niMheshimiwa Mariam Salum Mfaki, anasema Maji DodomaMjini yameongezeka; je, Serikali ina mpango gani kuhususuala la uondoshwaji wa majitaka? Serikali imekamilishausanifu wa kina wa mradi wa uboreshaji wa huduma ya

Page 137: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

137

29 APRILI, 2013

uondoshaji wa maji Mjini Dodoma. Jumla ya kilomita 250mitandao ya kukusanyia maji inatarajiwa kujengwa pamojana mabwawa ya kudumu ya kutibia maji (WSP). Jumla yashilingi bilioni 102 zitahitajika kutekeleza Mradi huu ambaoSerikali inatarajia kuanza kuutekeleza kwa awamu kupitiaProgramu ya Maendeleo Sekta ya WSDP.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Felister Aloyce Buraanasema, katika bajeti ya mwaka 2012/13 ilitengwa fedhakwa ajili ya Bwawa la Farkwa, bwawa hili lingehudumiaWananchi wa Wilaya ya Chemba na Bahi, mpaka leo hakunakazi yoyote iliyofanyika. Taratibu za ujenzi wa Bwawa laFarkwa kwenye Mto Bubu, Wilaya ya Kondoa katika Bondela Kati zinaendelea, Bwawa hilo litakuwa chanzo cha majikwa Manispaa ya Dodoma na Miji ya Wilaya ya Kondoa,Chamwino na Bahi.

Katika mwaka 2012/13 Mtaalamu Mshaurianayefanya upembuzi yakinifu, usanifu wa kina, kuandaavitabu vya zabuni, aliajiriwa na ameanza kazi na tayariameshaandaa inspection report. Kwa hiyo, matokeo ya kazihiyo yataainisha uwezekano wa maji kutoka kwenye bwawahilo kwa ajili ya umwagiliaji mifugo na matumizi ya nyumbani.

Mheshimiwa Beatrice Shellukindo anasema, Bwawala Kwamarigwe linahitaji shilingi milioni 500 kujengwa upyakwa kuwa mvua zinaelekea mwisho ambapo bwawa hililinasaidia vijiji 15 na ng’ombe zaidi ya milioni 12 wanapatahuduma hii.

Mheshimiwa Spika, ni kweli bwawa hili ni muhimukama alivyosema Mheshimiwa Mbunge na bahati nzuri miminimelitembelea. Serikali imelipokea hilo ombi na imetengafedha kwenye bajeti hii shilingi milioni 500 kwa ajili ya kwendakulifanyia ukarabati na kuona kama linaweza kuanzakutumika kwa madhumuni yaliyokuwa yamewekwa.

Mheshimiwa John Chiligati anasema, kuwepo kwamaji ya chumvi katika Bonde la Ufa na ushauri wa Mbungemaji yachukuliwe Milima ya Saranda katika visima vilivyopo

Page 138: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

138

29 APRILI, 2013

eneo la Ngwasa. Wizara itapeleka wataalam haraka kwendamaeneo yaliyopendekezwa na Mbunge kufanya tathmini nakushauri Wizara na Halmashauri ya Wilaya husika ili hatuaziweze kuchukuliwa.

Mheshimiwa Spika, mwingine ni Mheshimiwa NamelokSokoine amesema, ufanyike utafiti wa maji katika Milima yaMeru, kuna vyanzo vingi. Tumelichukua hili ni wazo zuri,tutashirikiana na Halmashauri na Wataalam wetu kwendakuona hivyo vyanzo na tuweze kuvitumia kwa ajili ya kutoahuduma ya maji kwa Wananchi.

Mheshimiwa John Lwanji alisema watafiti wa maji yavisima pia wahusike katika kuvichimba ili vikikosa majiwasilipwe. Hili ni wazo zuri na ndiyo ambalo limetokea katikaMiradi mingi ya uchimbaji visima kwamba, aliyefanya utafitini mtu mwingine, aliyechimba ni mtu mwingine na aliyekujakujenga miundombinu ni mtu mwingine.

Kwa maana hiyo, visima ambavyo vilikosa majitulishindwa kumpata aliyekuwa amefanya utafiti kwa sababuhawakuwa na mahusiano. Serikali kupitia Wizara ya Maji,tumesharekebisha hilo na Waziri atalisemea kwamba sasatutaunganisha anayefanya utafiti na anayechimba itakuwani kampuni moja na kwa maana hiyo atawajibika kwa kilealichokifanya.

Mheshimiwa Rebecca amesema kukosekana kwamaji baada ya utafiti ni kweli tatizo hili limekuwa likijitokeza,lakini kwa hivi sasa tutakachofanya ndiyo haya ambayonimesema, atapatikana mkandarasi mmoja atakayefanyakazi zote mbili. Yale maeneo ambayo utafiti ulionesha majihayapatikani kitaalam, tutafanya utafiti maeneo mengineau tutaangalia teknolojia nyingine ya kuwapatia maji ikiwemouvunaji wa maji ya mvua na teknolojia ya mabwawa.

Mheshimiwa Lekule Laizer alisema ni asilimia 15 tu yaWananchi wa Halmashauri ya Longido wanapata maji, Miradi

Page 139: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

139

29 APRILI, 2013

ya World Bank imeonekana kufeli na Serikali itatue tatizo lamaji katika Halmashauri ya Longido.

Mheshimiwa Spika, Miradi ya World Bank haijafeli,Serikali imeendelea kutekeleza Miradi katika Halmashauri zotenchini. Miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji,ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Longido inatekelezaMiradi katika Vijiji vya Longido, Sinya na Mndarara. Ujenzi wamiundombinu katika Kijiji cha Longido umekamilika kwaasilimia 55. Aidha, vijiji vingine navyo vitatengewa fedhakatika awamu ya pili ya utekelezaji wa programu hiiinayoanza mwaka 2014.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mahmoud HassanMgimwa, Mbunge wa Mufindi Kaskazini amesema, kuna vijijihavina maji ambavyo ni Katuo, Kikwea na Sadani. Kunashilingi bilioni moja na nusu ambazo wafadhili wako tayarikuzitoa kwa ajili ya miradi ya visima. Kwa hiyo, Serikali itusaidiekupata exemption. Tunamwomba Mheshimiwa Mbunge kwakupitia Halmashauri ya Mufindi, alete hayo maombi Wizaranitutayafanyia kazi ili hiyo exemption iweze kutolewa.

Mheshimiwa Suleiman Kakoso, Mbunge wa Jimbo laMpanda Vijijini anasema, maji ni tatizo katika Vijiji vya Igagala,Katuma na Kasekese, anaiomba Serikali iongeze bajeti kwanimaji ni uhai. Baada ya Serikali kukubali kuongeza bajeti yaWizara ya Maji, vijiji hivyo vimetengewa bajeti kama ifuatavyo:Igagala shilingi milioni 200.8, Kasekese shilingi milioni 368.2,Majalila shilingi milioni 267.8 na Katuma itatekelezwa katikabajeti inayofuata.

Mheshimiwa Juma Nkamia, Mbunge wa Kondoa,ametoa shukrani kwa Serikali kutenga shilingi bilioni mbili kwaajili ya Mradi wa Ntomoko na kwamba anasubiri ahadi hiyoitekelezwe. Ofisi ya Waziri Mkuu iliahidi kutoa shilingi bilioni3.03 kwa ajili ya ukarabati wa Maporomoko ya Ntomoko.Serikali kwa kupitia Bajeti ya Wizara ya Maji, mwaka 2013/14imetenga shilingi bilioni mbili kwa ajili ya Mradi wa Ntomokokatika Halmashauri ya Kondoa na Chemba. Fedha zilizobakizitakasimiwa katika bajeti ya mwaka 2014/15.

Page 140: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

140

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Hussein Nassor anasema kuna matatizoya maji Kanda ya Ziwa. Bajeti ya Maji izingatie kutatua tatizola maji Kanda ya Ziwa. Katika mwaka wa fedha 2013/14,Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 3.6 kwa ajili yakuvipatia maji vijiji 100 vilivyo kandokando ya bomba kuu laMradi wa Kahama – Shinyanga, kwa ajili ya kuboreshahuduma ya maji katika Wilaya za Mikoa ya Mwanza naShinyanga. Uboreshaji huduma ya maji nchini utaendeleakufanyika kulingana na upatikanaji wa rasilimali za fedha.

Mheshimiwa Spika, mwingine aliyetoa mchangowake ni Mheshimiwa Leticia Mageni Nyerere kwamba,Wanawake wa Kwimba wanahangaika kuchota maji usiku,hali hiyo inasababisha migogoro ya kifamilia.

Katika mwaka wa fedha 2012/13, Serikali ilipelekakwenye Halmashauri ya Kwimba jumla ya shilingi milioni 574.9kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji ambapoutekelezaji wa Miradi katika vijiji kumi unaendelea katika Vijijivya Mwabilanda ambapo umefikia asilimia 65, Ishingishaimefikia asilimia 40.

Katika mwaka wa 2013/14, Serikali imetenga kiasi chashilingi milioni 667.1 kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji waMiradi ya Vijiji vilivyobaki. Aidha, baada ya Wizara ya Majikuongezewa fedha, vijiji vitatu vya Wilaya ya Kwimba,vitajengewa Miradi ya Maji kama ifuatavyo: Lioma shilingimilioni 361.6, Igunguhya shilingi milioni 437.3 na Goloma shilingimilioni 414.4.

SPIKA: Ahsante muda umekwisha.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naombakuunga mkono hoja. (Makofi)

Page 141: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

141

29 APRILI, 2013

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa mtoa hoja.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Spika,Mwongozo.

SPIKA: Tuwasikilize kwanza, mwongozo unawezaukasubiri tu hauna tatizo. Unajua mwongozo ni kusema nisahihi au siyo sahihi. Kwa hiyo, naomba amalize Waziri kwanzahalafu nitakuita.

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, katika siku mbiliza majadiliano wiki iliyopita, michango mizuri sana ilitolewakatika kuchangia hoja ya maji ambayo niliiwasilisha Siku yaJumatano.

Mheshimiwa Spika, waliochangia waliisemea hoja hiikwa hisia kubwa na walitoa mawazo yao yaliyopo moyoni.Hata vyombo vya habari kama umeweza kuangalia naWabunge navyo vimetoa ya kwao na vimeongea jambo hilikwa hisia kubwa kwa sababu ya ukubwa wa tatizo lenyewe.

Mheshimiwa Spika, katika Hotuba za Wabunge,Wabunge 46 walichangia hoja hii kwa kuongea hapa ndaniya Bunge na Wabunge 81 walichangia kwa maandishi.Wakati wa hoja ya Waziri Mkuu, Wabunge 29 walichangiahoja ya Maji.

Kanuni zetu za sasa haziruhusu kuwatambua mmojammoja kama walivyochangia katika hoja hii, lakini napendanikuombe kwamba nawashukuru sana wote ambaowamechangia na kutoa mawazo ambayo yamejenga nakutuonesha njia ya kuelekea jinsi tunavyokwenda mbelekatika kutatua tatizo hili.

Page 142: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

142

Napenda niwashukuru sana wewe mwenyewe MheshimiwaSpika, nimshukuru sana Mheshimiwa Naibu Spika na niishukuruKamati ya Kilimo Mifugo na Maji. Niwashukuru WaheshimiwaWabunge na Wadau mbalimbali ambao wametoa maonikatika Hoja hii.

Mheshimiwa Spika, kutokana na wingi wawaliochangia hoja na maoni yaliyotolewa ni mengi naMheshimiwa Naibu Waziri amejaribu kujibu hoja mojamojakati ya hoja zaidi ya 96 ambazo zimetolewa. NinawaombaWaheshimiwa Wabunge, wakubali kwamba, zile ambazohatutaweza kuzijibu hivi sasa tutatoa kitabu cha majibu kablaBunge hili halijakamilika.

Mheshimiwa Spika, hoja kubwa ambazo zimetolewakatika Bunge hili ni ufinyu wa bajeti ya Wizara na Sekta yaMaji. Katika Hotuba yangu nililiomba Bunge lako Tukufu,liidhinishe shilingi bilioni 398.4 kwa ajili ya bajeti ya Wizara kwamwaka 2013/2014. Kati ya fedha hizo shilingi bilioni 18.9 kwaajili ya matumizi ya kawaida na zilizobaki, shilingi bilioni 379.4kwa ajili ya maendeleo. Hisia za Wabunge, zilioneshakwamba, bajeti hii haitoshi kukidhi mahitaji ambayo nimakubwa, hasa katika maeneo ya vijijini. Kwa hiyo, zilishawishiBunge lijadiliane na Serikali, kuongeza bajeti ya Wizara yaMaji, ili kutekeleza miradi zaidi katika sekta ndogo ya majivijijini.

Mheshimiwa Spika, chimbuko la mapendekezo hayoni kwamba, wananchi wanaopata maji safi na salama hukovijijini hivi leo ni 58% ya wananchi wote. Hii ikiwa na maanakwamba, 42% ya wananchi wetu hawapati maji safi nasalama na hili ni tatizo kubwa katika maendeleo ya nchi.Aidha, Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010 naMalengo ya Milenia, yanalenga kufikia 65% ya wananchiwote kupata maji mwaka 2015; hivi sasa tunatekeleza miradiya vijiji vitano katika Halmashauri zote. Fedha zote kwa ajiliya utekelezaji wa miradi hii huko vijijini imeshakwenda na zikokwenye Wilaya zetu. Hivyo, utekelezaji wa miradi hiiutakamilika mwezi Septemba, 2013.

Page 143: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

143

Mheshimiwa Spika, kazi nyingine katika miradi hiizimechelewa, lakini hatua ambazo nitazichukua hapa leo,zitaharakisha miradi hii na kuifanya iweze kukamilika katikakipindi hicho. Miradi hiyo itakapokamilika mwezi Septemba,mwaka huu, idadi ya watu ambao wataongezeka wenyemaji safi na salama katika nchi yetu ni watu milioni 1.7.

Mheshimiwa Spika, katika mapendekezo yetu yamwaka 2013/2014, tayari Serikali imetenga shilingi bilioni 105kwa ajili ya maji vijijini. Fedha hizo tumezipitisha hapa kupitiaMafungu ya Mikoa, shilingi bilioni 94.9 na shilingi bilioni 10.3tunaomba mkubali kuzipitisha katika Kikao hiki. Fedha hizokwa pamoja zitajenga miradi ya vijijini katika vijiji 480. Vijiji hivyovitakuwa ni wastani wa vijiji vitatu katika kila Halmashauri.Miradi hiyo itakapokamilika mwaka kesho, jumla ya watu1,200,000 watapata maji; ukishapata watu 1,200,000 na wale1,700,000 asilimia 60 ya Watanzania wanaoishi vijij iniwatakuwa na maji safi na salama. Sasa kwa speed hii,tutashindwa kufikia malengo ya Ilani ya Chama chaMapinduzi na Malengo ya Milenia.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naishukuru sana Kamatiya Kilimo, Mifugo na Maji kwa kutoa mapendekezo mahsusi,ambayo yalisomwa hapa mbele yetu siku ya tarehe 24,ambayo yamekubaliwa na Serikali na utekelezaji wakeutaongeza speed hii ya utekelezaji wa miradi ya vijijini naupatikanaji wa maji vijijini. Utatuweka vizuri katika kufikia nakupita malengo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi naMalengo ya Milenia na utaendana na Mpango wa Serikaliwa Big Results Now – Tenda Sasa kwa Matokeo Makubwa.Kwa hiyo, Kamati ilipendekeza nyongeza ya bajeti ya ziadaya shilingi bilioni 184.5. Baada ya majadiliano ndani ya Serikalina majadiliano kati ya Serikali na Kamati ya Bajeti namajadiliano kati ya Wizara yangu na Kamati ya Kilimo, Mifugona Maji; Serikali, imekubali kuiongezea Wizara ya Maji shilingibilioni 184.5 kama ilivyotangazwa na Mheshimiwa DoktaMgimwa, Waziri wa Fedha, hapa Bungeni hivi karibuni.(Makofi)

Page 144: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

144

Mheshimiwa Spika, fedha hizo zitatumika kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, shilingi bilioni 65, zitatumikakuongeza miradi ya maji ya vijiji viwili-viwili katika kilaHalmashauri na kufikia vijiji vitano katika kila Halmashaurimwaka 2013/2014 na hivyo, jumla ya vijiji 840 vitatekelezwanchi nzima katika mwaka huu wa fedha. Matokeo ya kazihiyo ni kwamba, watu 62% watapata maji Tanzania nzima.

Mheshimiwa Spika, eneo la pili litakalonufaika nafedha hizo ni kujenga miundombinu ya kusambaza maji katikamabwawa ambayo yamekwishajengwa tayari katika Wilayakame za Simanjiro, Bunda, Monduli, Rorya, Musoma Vijijini,Nkasi, Iringa Vijijini, Nzega, Kilindi, Chunya, Itimila na Sikonge.Jumla ya shilingi bilioni 13 zitatumika na kuwapatia maji watu480,000.

Mheshimiwa Spika, eneo la tatu litakalotumia fedhahizi ni kujenga miundombinu ya pampu na mabomba yakusambaza maji katika visima virefu ambavyovimeshachimbwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.Gharama za kutekeleza miradi hiyo itakuwa ni shilingi bilioni11.2 na mradi huu utawapatia wananchi 640,000 maji safi nasalama pamoja na kupatia mifugo mingi maji.

Mheshimiwa Spika, eneo la nne ni kupanua,kukarabati na kujenga miundombinu kwenye miradi katikaWilaya mbalimbali; miradi ambayo kwa sasa haitoi hudumaipasavyo kutokana na uchakavu, kwa gharama ya shilingibilioni 10.8 na kufaidisha watu 440,000.

Mheshimiwa Spika, eneo la tano, ni kujengamiundombinu ya kusambaza maji kwa wananchi kutokakatika miradi mikubwa ambayo usanifu umekamilika namiradi mikubwa inayohitaji ukarabati. Miradi hii inahitaji shilingibilioni nane na itafaidisha watu zaidi ya 500,000.

Mheshimiwa Spika, eneo la sita, ni kufanya usanifu naujenzi wa mradi wa Ugala, utakaopeleka maji katika Mji wa

Page 145: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

145

Urambo na Mji wa Kaliuwa na vijiji vilivyoko njiani MkoaniTabora. Mradi huu utagharimu shilingi bilioni 12.1.

Mheshimiwa Spika, eneo la saba, ni miradi ya majivijijini iliyoainishwa na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji kwenyeTaarifa yangu niliyoipeleka mbele ya Kamati hiyo. Miradi hiiya vijijini itakuwa katika kila Wilaya na itagharimu shilingi bilioni53.5 na miradi hiyo itafaidisha watu 614,780.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuongezewa fedha, nilazima tuchukue hatua mbalimbali ili kuhakikisha kwambamiradi hii inatekelezwa na tunapokuja kukutana hapa tenamwaka kesho mwezi wa sita, tuwe tuna ripoti ya kukamilikakwa miradi hii ambayo tunaitaja katika ripoti hii. Miradi yoteitawasilishwa kwenye Kamati ya Kilimo, Maji na MifugoWabunge watasambaziwa kabla ya mwisho wa Bunge hili.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kwamba miradi hiiinatekelezwa na ili kuhakikisha kwamba fedha ambazo zikohuko vijijini kwa kutekeleza miradi ya vijiji vitano na yenyeweinatumika haraka na miradi ya vijiji hivyo ikamilike nawananchi wapate maji, nachukua hatua zifuatazo:-

Mheshimiwa Spika, kuanzia leo tunafuta vibali vyotevya No Objection ambavyo vinangojewa huko katika Wilayambalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii. Miradiambayo inajulikana imeorodheshwa, imesanifiwa na Wilayazimepata fedha, ianze kutekelezwa mara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Ununuzi iweHalmashauri za Wilaya kuanzia sasa badala ya Mamlaka hiyokuwa kwenye Wizara ya Maji. Halmashauri itangaze, ifanyetathmini ya waombaji, ichague Mkandarasi na ihakikisheutekelezaji wa miradi. Waheshimiwa Wabunge, sisi wote niMadiwani na tunashiriki katika Kamati ya Uchumi na Fedha,tushiriki katika Kamati hizi kwa sababu fedha ambazozimepelekwa ziko huko tayari na fedha nyingi sana natumezionesha kwenye jedwali ambalo tumesambazapamoja na Kitabu cha Hotuba. (Makofi)

Page 146: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

146

Mheshimiwa Spika, tuhakikishe kweli, badala ya kujahapa kuuliza kwamba, mradi wangu umefikia wapi;tuhakikishe tunajua miradi yetu imefika wapi, utekelezaji wakeunakwendaje, ili tushauriane maeneo na hatua za kuchukuakabla ya kuulizana maswali humu ndani. Kama tunaulizanayawe ni maswali ya kimsingi, ambayo tukiyarekebishayatasaidia na Wabunge wenzetu wengi. Sekretarieti zaMikoa, Wizara ya Maji, watafuatilia utekelezaji wa miradi hii,watasimamia miradi hii kwa karibu na kutoa ripoti kila mwishowa mwezi ili tujue maendeleo ya kazi hizi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hizi, ninapendakusisitiza kwamba katika utekelezaji wa hatua ya manunuzi,lazima Sheria ya Manunuzi ifuatwe. Kuondoa vibali, hainamaana kwamba, tusifuate Sheria za Manunuzi, ni lazimaSheria zifuatwe na Sheria zile zikifuatwa kwa busara si lazimazichukue muda mrefu sana. Hivi sasa circle ya mradi wa majikuanzia mradi wa maji unapobuniwa, kuanzia unapofanyiwastudy, unaposanifiwa, unapotangazwa, mpaka Mkandarasiapatikane, inachukua wastani wa siku 234. Muda huu ni mrefusana na hatuwezi kutekeleza miradi hii kwa kufuata utaratibuhuo.

Mheshimiwa Spika, aidha, ninapendekeza hatua yanne hapa kwamba, Wilaya ziondoe vikwazo vyote vyautekelezaji wa miradi hii. Katika Wilaya zingine ambazozimepokea fedha na zimepokea labda asilimia 80, kati yakila shilingi 100, shilingi 20 hazijafika; uamuzi unafanywakwamba tungoje mpaka fedha zote ziletwe kutoka Hazinaau fedha zote ziletwe kutoka kwenye Halmashauri. Wilayaziendelee na utekelezaji wa miradi kwa hatua zile ambazozina fedha na wakati wanapofikia hatua ambazo sasa fedhazitakuwa na matatizo, watoe taarifa haraka, ili fedha hizozitafutwe na miradi isisimame. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, utaratibu wa miradi ni Serikalikutoa fedha au fedha za washirika wa maendeleo nawananchi wanahitajika kuchangia miradi hii, ili fedha zawananchi zinazochangiwa, zishiriki katika operation and

Page 147: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

147

maintenance, yaani zishiriki katika kuendesha na kukarabatimiradi kama inaharibika.

Mheshimiwa Spika, katika Wilaya zaidi ya 45, taarifanilizonazo ni kwamba, Viongozi wa Wilaya wanangojawananchi wengine wachangie 20% ya mradi au wachangie5% ya mradi au wachangie 2.5% za mradi. Ule msingi wakuchangia wananchi ni ili wananchi waone ushiriki wao namradi ukishakamilika, ukikabidhiwa kwa wananchi, wananchiwaweze kuwa na hela ya mbegu (Seed Money), ya kuanzakuendesha na kukarabati mradi wao, fedha zao sio kwa ajiliya ujenzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, fedha za wananchizinazochangwa sio kwa ajili ya ujenzi, fedha za wananchizinazochangwa ni kwa ajili ya kuendesha na kukarabati nakutengeneza miradi mahali ambapo imeharibika. Kwa hiyo,utekelezaji wa miradi katika Wilaya zote ufanywe harakaiwezekanavyo bila kuwa na visingizio ambavyo havinamaana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, itakapofika mweziSeptemba, tutazikagua hizi Wilaya zote kulingana na ahadizao za kutekeleza miradi hii. Zile ambazo hazitakuwazimetekeleza miradi hii, Maofisa wanaoshughulika nautekelezaji wa miradi hii, tutawachukulia hatua ikiwa nipamoja na kuwaondoa na kuweka watu wengine ambaowanaweza kufanya kazi hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hizi, Wizara,inaanzisha Ofisi kwenye Kanda. Madhumuni ya kuanzisha Ofisihizi kwenye Kanda ni kuhakikisha kwamba, ufuatiliaji wamiradi, usimamizi wa miradi na pale inapohitajika maeneoambayo Wilaya hazina Wahandisi, wanasaidia Wilaya hizokuhakikisha kwamba, miradi inaanza na kutekelezwa kwawakati. Kwa hiyo, wataalamu hawa watashirikiana nawataalamu kwenye Sekretarieti za Mikoa katika maeneo yakitaaluma pale inapobidi na katika kusimamia miradi.

Mheshimiwa Spika, eneo la nne ambalo ninataka

Page 148: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

148

kulichukulia hatua, nimeunda Kamati ya Wataalamu waUjenzi wa Miradi ya Maji itakayochambua gharama za ujenziwa maji vijijini na kutoa ukomo wa bei za utekelezaji wa miradihiyo. Katika miradi mingine huko vijijini gharama zake ni kubwasana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimeunda Kamati yaWataalamu, itakayoongozwa na Profesa Idrissa Mushoro waChuo Kikuu cha Ardhi na ina Wataalamu ambaowamebobea katika maeneo ya ujenzi na gharama za ujenzi.Kamati hii pia itahusu washirika wetu wa maendeleo ilikuhakikisha kwamba, kweli, tunapata thamani ya fedhaambazo tunaweka.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hii, ni vizuriWaheshimiwa Wabunge na Wananchi kwa ujumla, wajuekwamba, pale tunapochimba kisima na kuweka bomba lakwanza pale ili wananchi pale kisima kilipo wapate maji, siogharama peke yake katika kutekeleza miradi ya maji vijijini.Baada ya kuweka pampu na kuweka bomba pale, kunabomba la kusambaza maji kwenye vijiji na kwa kawaida kunaujenzi wa ma-tank, kuna usambazaji, ili kuwe na maeneo yakuchotea maji katika maeneo mbalimbali ya vijiji na gharamazote hizi ni muhimu mkazielewa, lakini ni muhimu kwambakila component ya gharama hizi inakuwa gharama ambayoinalingana na thamani ya kazi iliyofanywa na inalingana nauwezo wetu wa kupeleka maji vijijini. Kutokana na hatua hiiWilaya, zione umuhimu wa fedha zilizopo ziweze kuhudumiavijiji vingi zaidi. Wilaya ambazo zitakuja na innovation auubunifu huo, zitapewa ruhusa kutekeleza miradi hiyo nazitasaidiwa na Wataalamu ambao watakuwa kwenyemaeneo ya Kanda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, ningependa sana wale watuambao wanachimba visima kama Wakandarasi wawezekuwajibika zaidi. Katika mfumo wa mradi wa maendeleo yamaji awamu ya kwanza uliopo sasa Mtaalam Mshaurianakwenda aangalie atambue mahali pa kuchimba kisima,halafu Mkandarasi wa kuchimba kisima anaonyeshwaaambiwe chimba hapa ndipo mtaalam aliposema, Mshauri

Page 149: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

149

analipwa anakwenda zake. Mtaalam anakuja kamahakuona maji ni kosa la Mshauri ambaye ameshalipwaameondoka. Kuanzia sasa mtu ambaye anachimba visimalazima awe na ujuzi wa kujua mahali penye maji wapi nakwamba sisi tutalipa kisima kilicho na maji na wala siyo kisimakikavu na visingizio vinavyoungana na jambo hili tunatakatuviondoe ili tupate kweli wakandarasi ambao wana ujuzina uwezo wa kuchimba visima. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lakoTukufu kwamba tutawachukulia hatua kali wale wote ambaowatakuwa na visingizio mbalimbali vya kutoanza miradi hiina kutotekeleza miradi kwa wakati. Tumefikiria pia kwambatuwe na mashindano kati ya Wilaya na Wilaya ili zile Wilayaambazo zinatekeleza miradi yake kwa haraka na kwa uboraunaotakiwa ziweze kupewa kipaumbele katika utekelezaji wamiradi ya huko mbele.

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Kilimo, Mifugo na Majiimetoa mapendekezo mengine mbalimbali ambayo Wizarayangu itaendelea kuyatekeleza na kuyafanyia kazi ilikuboresha huduma ya maji katika maeneo mbalimbali ikiwani pamoja na mjini na vijijini. Maeneo hayo ni pamoja nakuendelea kujadiliana na Serikali ili kuondoa Kodi yaOngezeko la Thamani kwenye dawa za kusafisha maji.

Mheshimiwa Spika, pili kupitia Mpango Maalum waSerikali wa ‘Tekeleza Sasa kwa Maendeleo Makubwa’ (BigResults Now Program) ili kuongeza uwekezaji zaidi katika eneola maji vijijini.

Mheshimiwa Spika, Serikali itachukua hatuamadhubuti ya kutunza vyanzo vya maji kwa kuendeleakuviainisha na kuvitengea maeneo yake kisheria nawananchi watashirikishwa katika kutunza vyanzo vya maji.Serikali itahimiza Halmashauri ambazo bado hazijatungasheria ndogondogo za utunzaji wa maji na vyanzo namaeneo ya mito ili sheria hizo ziweze kutungwa na wananchiwatunze maeneo yao ya maji.

Page 150: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

150

Mheshimiwa Spika, Wizara itapitia tena utekelezaji wamradi katika vijiji kumi ili kuondoa changamoto zinazojitokeza.

Mheshimiwa Spika, sehemu ya changamotonimezieleza hapa na ninawaomba sana WaheshimiwaWabunge tuwe karibu sana na miradi hii na tuelewe kwambafedha tayari ziko kule kwenye vijiji zile ambazo zinahitajikakutekeleza miradi hii mpaka mwezi Septemba na kufikia nusuya vile vijiji kumi na baada ya fedha hizi za mwaka huu kuanzakupelekwa Wilayani, fedha zote ambazo zinahitajika kwa ajiliya utekelezaji wa vijiji vingine vile vilivyobaki vitano zitatolewana miradi hii ambayo nimeianisha hapa na itaelezwakinaganaga katika taarifa tutakayopeleka katika Kamati yaKilimo, Mifugo na Maji na vyenyewe vitekelezwe kwa harakaili tuweze kuwafikishia wananchi maji na kwamba fedha hiziambazo Serikali imetuamini imetupa, imesikiliza kilio chetutuweze kuzitumia vizuri na kusiwe na visingizio ambavyohavina maana.

Mheshimiwa Spika, nawashukuru Wabunge wote naninaishukuru Kamati kwa kazi ambayo imeifanya il ikuhakikisha kwamba kunakuwa na haya mabadiliko chanyakatika bajeti ambayo tumeiwasilisha.

Mheshimiwa Spika, moja ya changamoto ambazozilitolewa na Msemaji wa Kambi ya Upinzani ni kwambaEWURA inadhibiti zaidi sekta ya nishati kuliko inavyodhibitisekta ya maji. Kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha EWURA,EWURA inadhibiti utoaji wa huduma kwenye sekta za umeme,mafuta ya petroli, gesi asilia, maji na usafi wa Mazingira. Kaziza kudhibiti zilizofanywa na EWURA katika Sekta ya majizimeelezwa kwa kina katika hotuba yangu ya bajeti.

(Hapa Waziri alinyamaza kwa mudaakisoma karatasi aliyopatiwa)

SPIKA: Mkimpelekea barua muda huu atachanganyamambo, wewe endelea tu kusema yale uliyoyaandaa.

Page 151: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

151

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kazi za kudhibitizilizofanywa na EWURA katika sekta ya maji zimeelezwa kwakina katika hotuba ya bajeti kuanzia kifungu 139 hadi 148,kazi hizo ni:-

(i) Kufuatilia utendaji wa Mamlaka za Maji mijinina kuzitolea maboresho ya kufanya ili ziweze kutekelezamajukumu yake kwa ufanisi zaidi.

(ii) Kupitisha bei za maji katika miji mbalimbalikulingana na gharama ambazo zinatumika katika kuyazalishamaji hayo.

(iii) Kutatua malalamiko ya wateja kuhusuhuduma ya maji safi na maji taka itolewayo au na bill ambazowamepewa.

(iv) Kuanzisha utaratibu wa kudhibiti sekta binafsiya kutoa huduma ya maji kupitia magari ya maji yaani watertankers and water bowser na kuangalia ubora wa visimabinafsi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kudhibiti watoa hudumabinafsi, EWURA imetayarisha mwongozo wa udhibiti wabiashara ya maji kwa kutumia magari binafsi katika eneolinalosimamiwa DAWASA na utekelezaji wake umeanza.Udhibiti huu unahusisha EWURA kupitisha bei zilizoainishwa nakukagua magari ya maji ili ubora wa maji ulingane na ukwelikwamba maji ni chakula na hivyo lazima wapelekewewananchi yakiwa salama.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge wa Jiji laDar es Salaam, Kibaha, Bagamoyo wamechangia sana juuya huduma ya maji ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja naMheshimiwa Abuu Jumaa, Mheshimiwa Sylvestry Koka,Mheshimiwa Khatib Haji, Mheshimiwa Rita Mlaki, MheshimiwaAmina Amour, Mheshimiwa Kuruthum Mchuchuli naMheshimiwa John Mnyika. Katika jitihada za kutatua tatizo lamaji katika jiji la Dar es Salaam Serikali inatekeleza miradi yakuongeza maji ili maeneo yote yapate maji ikiwa ni pamoja

Page 152: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

152

na maeneo yenye mabomba ya mchina. Kazi zitazofanyikani pamoja na upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini ambaosasa umekamilika kwa zaidi ya 85% na unatazamiwakukabidhiwa mwezi Julai mwaka huu, upanuzi wa Ruvu Juuna ambao utaanza mwezi Julai mwaka huu na kukamilikamwezi Desemba mwaka 2014 na uchimbaji wa visima vyaKimbiji na Mpera ulioanza mwezi Machi mwaka 2003 naunategemewa kukamilika mwaka 2014.

Mheshimiwa Spika, katika bajeti hii pamoja na fedhaza kuchimba visima hivi, tumetenga shilingi bilioni 15 kwa ajiliya kuanza malipo ya wananchi ambao watapisha ujenzikatika maeneo haya. Miradi hii itaongeza uzalishaji wa majikutoka lita milioni 300 za sasa hadi kufikia lita milioni 756 kwasiku.

Mheshimiwa Spika, napenda kusisitiza sana na hilijambo nataka kulisema tena kwamba ujenzi wa bombakubwa la maji kutoka Ruvu Chini mpaka Dar es Salaam aukutoka Ruvu Juu mpaka Dar es Salaam au kujengamiundombinu kuleta maji kutoka Kimbiji kuleta Dar es Salaamsiyo kama kuweka chupa za soda kwenye production lineya kiwanda cha soda kwamba soda hizo baada ya dakikakumi na tano zitakuwa zimejazwa na zinatoka. Hii ni kazi yaujenzi wa miundombinu, inachukua mpaka miaka mitatu,minne. Tumeeleza rasmi hapa jinsi ambavyo tumewekezakama Serikali katika maeneo haya na nia yetu ya thabitikabisa ya kuleta maji Dar es Salaaam.

Mheshimiwa Spika, katika kazi hii, tusinyang’anyanefito, tunajenga nyumba moja hakuna mtu mmojaatakayepata credit ya kazi yote kwamba kazi hii isingekuwamimi isingefanywa, kazi hii inafanywa na Serikali ya Chamacha Mapinduzi haifanywi kwa ushabiki. Wananchimsidanganywe kuandamana kwamba bomba la majilinaweza kuwekwa siku ya Ijumaa likafika eti muende Wizaraya Maji muandamane mdai mpewe glasi ya maji. Majiyatakuja katika kipindi ambacho kimeelezwa na tumeelezajambo hili kwa kinaganaga sana. Wananchi tumewapelekahata nyinyi wenzangu Waheshimiwa Wabunge mmekwenda

Page 153: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

153

mkaangalia mkaona kazi inayotekelezwa. Tusifanye ushabiki,hii ni kazi ya kujenga nchi yetu, subirini maji yatakuja Dar esSalaam kama mwaka kesho miradi mingine haitakuwaimekamilika, tuulizeni lakini msiende kusumbua watu ambaowanajenga miradi kwa ajili ya ushabiki wa kisiasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilika miradi hiyomaeneo yote yasiyopata maji kwa sasa yatapata maji yakutosha ikiwa ni pamoja na Kiluvya, Kibamba, Mlonganzila,Kwembe, Mbezi Luis, Mbezi Msumi, Masakuzi, Makabe, Mpijina kadhalika. Maeneo haya yamewekwa katika taarifambalimbali ambazo tumezitoa hapa Bungeni.

Mheshimiwa Spika, tatizo la maji katika majimbo yaKibaha, Mjini na vijijini itakwisha baada ya kuongeza uzalishajikatika mtambo wa Ruvu Juu. Kazi ya upanuzi wa mtambowa ujenzi wa bomba itaanza mwezi Julai na itakamilikamwishoni mwa mwaka kesho. Fedha kwa ajili ya miradi hiizimetolewa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikaliya India.

Mheshimiwa Spika, kuhusu uwakilishi kwenye bodi yaDAWASA na DAWASCO, Mkoa wa Pwani unawakilishwakatika Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA. Wakati wa uteuziwa Bodi ya DAWASCO utakaofanywa hivi karibuni uwakilishiwa Mkoa wa Pwani utazingatiwa. Hata hivyo nimetoamaagizo kwamba Bodi iliyoko sasa ikitumia Sheria ile iwaalikeWajumbe watakaopendekezwa na Ofisi ya Mkoa wa Pwaniili waweze kuendelea kuwakilisha eneo lao katika Bodi hiyo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na desalination ya majiya bahari ili kutafuta ufumbuzi wa haraka wa maji ya Dar esSalaam, tulifanya uchunguzi wa vyanzo vipya vya maji kwaajili ya Dar es Salaam, teknolojia ya kutumia maji ya baharikwa aji l i ya matumizi ya kawaida il ikuwa moja yailiyochunguzwa. Matokeo ya awali yalionyesha kwamba majiambayo yanafanyiwa desalination gharama yake ni maratatu ya maji yanayotoka Ruvu Chini na Ruvu Juu, kwa hiyo

Page 154: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

154

wakati ule mradi ule ulisimama. Hivi sasa tumepata taarifakwamba kumekuwa na maendeleo katika teknolojia yakuondoa chumvi kwenye maji na kwa hiyo Serikali ikishirikianana mwekezaji binafsi, inafanya utafiti huo na kama shirikahilo binafsi litaweza kuonyesha kwamba linaweza ku-desalinate na kuingiza maji kwa bei ile ambayo imewekwana EWURA kwa kutumika kwa maji yanayotoka Ruvu Juu naRuvu Chini, Serikali haitasita kutoa ruhusa kwa kampuni hiyokuingiza mradi huo.

Mheshimiwa Spika, ukaguzi wa program ya maji,program ya maji hufanyiwa ukaguzi wa aina mbalimbaliikiwemo wa fedha, ununuzi, ufundi yaani technical, thamaniya kazi ikilinganishwa na fedha (value for money), ufanisi auperformance. Kazi hizi hufanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali na kwa mujibu wa Sheria na Mamlakaya Ununuzi Tanzania (PPRA) na Wakaguzi Binafsi auIndependent Auditors kulingana na makubaliano ya Serikalina washirika wetu wa maendeleo. Aidha, kila taasisizinazotekeleza program ya maji zinakaguliwa kwa utaratibuhuu.

Mheshimiwa Spika, mnamo mwaka 2010, ukaguzi wakiufundi ulifanywa ambao uliangalia utekelezaji wa programkwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2007/2008 hadi2009/2010 na kampuni binafsi ya M/S Artikines Internationalna CAG alifanya Ukaguzi Maalum yaani Special Audit katikakipindi hicho. Mwezi Desemba mwaka 2012, Mkaguzi wa njeM/S UPI Mark alianza ukaguzi wa kiufundi kwa kipindi chamiaka 2010/2011 na 2011/ 2012 na atawasilisha ripoti yaukaguzi huo mnamo mwezi Mei mwaka huu. Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hufanya ukaguzi waprogram kila mwaka ambapo taarifa ya mwisho wa mwakawa fedha 2011/2012 ilishajadiliwa na wadau kama rasimu nailiwasilishwa mwezi Februari mwaka 2013.

Mheshimiwa Spika, katika kaguzi zote hizi,haijagundulika ubadhirifu wa fedha za umma ikiwa ni pamojana mradi wa maji wa Dar es Salaam Water Supply andSanitation Project ambao kwa sasa ni sehemu ya program

Page 155: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

155

ya maji. Hata hivyo, tutaendelea kumkaribisha Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali ili aweze kuangalia na sehemu za miradihiyo kama sehemu ya mradi wa vijiji kumi, sehemu ya mradiwa Wachina huu ambao unasemwa kila siku ili kutuhakikishiakwamba fedha ya Serikali haikufujwa na kama kuna mtuambaye amehusika katika kufuja fedha hizi za Serikali awezekuchukuliwa hatua.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na malalamiko juu yaugawaji wa rasilimali katika utekelezaji wa sekta ya maji.Serikali kwa kutambua kuwa upatikanaji wa maji safi nasalama ni hitaji la msingi na haki kwa wananchi wote,inajaribu na inafanya hivyo, inagawanya fedha rasilimalikatika vijiji vyote 132. Mgao wa fedha katika Halmashauri zaWilaya, Miji na Manispaa za kuendeleza huduma ya maji nausafi wa mazingira vijijini hufuata kanuni au formula basedallocation ambayo ilikubaliwa kwa pamoja kati ya Serikali,washirika wa maendeleo, wadau wengine na sekta ya maji.Vigezo vya kugawa fedha kwa kila Halmashauri viliwekwakutokana na majadiliano na makubaliano yaliyofikiwa katikaWizara ya Maji, Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI na Wizara yaFedha. Vigezo hivyo ni idadi ya watu ambao hawajapatamaji katika Halmashauri, aina ya teknolojia itakayohitajikutumika katika Halmashauri hiyo kama ni mtiririko au ni visimavifupi au ni visima virefu na idadi ya wananchi katika kilaHalmashauri. Kigezo cha idadi ya watu ambao hawajapatahuduma ya maji, kina uzito mkubwa kuliko vigezo vingine.

Mheshimiwa Spika, katika kugawana fedha kwaMikoa kuanzia Julai mwaka 2007 hadi Machi mwaka 2013,Mikoa mbalimbali imepata fedha kwa ajili ya utekelezaji wamiradi vijiji vyake kama ifuatavyo; Arusha shilingi bilioni 11.9,Dar es Salaam shilingi bilioni 2.6, Dodoma shilingi bilioni 10.5,Iringa shilingi bilioni 13.4, Kagera shilingi 15.5, Kigoma shilingi10.2, Kilimanjaro shilingi bilioni 10.5, Lindi shilingi bilioni 11.3,Manyara shilingi bilioni 12.3, Mara shilingi bilioni 9.2, Mbeyashilingi bilioni 19.8, Morogoro shilingi bilioni 8.5, Mtwara shilingibilioni 12.7, Mwanza shilingi bilioni 14.5, Pwani shilingi bilioni11.8, Rukwa shilingi bilioni 9.7, Ruvuma shilingi bilioni 8.7,

Page 156: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

156

Shinyanga shilingi bilioni 19.8, Singida shilingi bilioni 11.8, Taborashilingi bilioni 11.6 na Tanga shilingi bilioni 15.1.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa miradi mikubwa naya Kitaifa na miradi ya maji mijini. Serikali imeendeleakutekeleza miradi mikubwa ya Kitaifa na miradi ya maji mijiniawamu kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.Mathalani ujenzi wa miradi mikubwa ya Kitaifa ya Makondehuko Mtwara, Wanging’ombe-Iringa, Mgangokyabakari-Mara, Chalinze-Pwani, Maswa- Shinyanga, HandeniTrackmen-Tanga na mradi wa Kahama -Shinyanga -Mwanzailijengwa kwa vipindi tofauti kwa ajili ya kuwahudumiawananchi katika maeneo ambayo yanashida kubwa za maji.

Mheshimiwa Spika, aidha, kutokana na gharama zaujenzi wa miradi ya maji mijini kuhitaji fedha nyingi, utekelezajiwa miradi hufanywa awamu kwa awamu kwa kuyapavipaumbele kwanza maeneo yenye uhaba wa huduma hiyo.Miradi ambayo imetekelezeka na kukamilika katika kipindicha hivi karibuni ni pamoja na maji safi katika Mamlaka yaMji wa Mbeya, Iringa, Songea, Mwanza, Shinyanga na Babatina miradi ya miji midogo ya Wilaya kama Kahama, Igunga,Kibiti, Mpwapwa, Utete na Kongwa. Kwa kipindi hiki, miradiinayoendelea kutekelezwa ni pamoja na Musoma, Lindi,Bukoba, Singida, Kigoma, Tabora, Sumbawanga, Dodoma,Mtwara, Dar es Salaam na Morogoro na baadhi ya Miji yaWilaya ikiwa ni pamoja na Mvomero, Turiani, Nansio, Masasi,Nachingwea, Kilosa, Sengerema, Kibaigwa, Orkesmet, Bunda,Namanyere, Bariadi, Muheza, Chalinze, Geita na miradimingine. Utekelezaji wa miradi hii unaendelea. Pia miradimingine kama alivyoitaja hapa Mheshimiwa Naibu Waziriinaendelea kutekelezwa.

Mheshimiwa Spika, niseme tu, maandalizi ya mradimpya mkubwa wenye thamani ya shilingi bilioni 105 katikamiji ya Ramadi, Magu, Mwanza na Misungwi, yanafanywakwa kushirikiana na European Investment Bank na Shirika laMaendeleo la Ufaransa. Mradi huu pia utajenga mfumo wakuondoa maji taka katika Mji wa Bukoba na Musoma. Kiasi

Page 157: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

157

cha fedha ambacho kinatumika kama nilivyosema ni Euro105 milioni na miradi hii itaanza kutekelezwa mwaka huu.

Mheshimiwa Spika, miradi mingine ambayo itaanzakutekelezwa ni katika makubaliano kati ya Serikali ya Tanzaniana Washirika ya Maendeleo kwamba washirika watapelekafedha zao moja kwa moja kwenye miradi na watateuamkandarasi na kusimamia ujenzi kwa kushirikiana na Wizaraya Maji.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa pia na malalamikokwamba fedha nyingi zinaenda mijini kuliko zile zinazokwendavijijini. Baada ya nyongeza ambayo Serikali imekubali kuipatiaWizara ya Maji, shilingi bilioni 184.5, hivi sasa fedha zamaendeleo za ndani kwa ajili ya vijijini katika Wizara ya Majizitafikia shilingi bilioni 315, ukilinganisha na shilingi bilioni 241za kutoka nje. Kwa hiyo, mwelekeo ni mzuri na Serikali inafanyakila iwezavyo kuhakikisha kwamba inaongeza uwekezajikatika sekta ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge wengiwaliongelea uwezekano wa kuanza Mfuko wa Maji.Tumeshatengeneza Kanuni na zinangojea kuchapishwakwenye Gazeti la Serikali na tumetengea mfuko huu shilingimilioni 100 kama seed money. Baada ya mfuko kuwepo,tutaleta mapendekezo mahsusi ili tuangalie vyanzo vya fedhakwa ajili ya mfuko huo ili sasa mfuko huu ukishakuwa navyanzo ambavyo ni kamili, sasa tuweze kuanza Shirika laTANWATER ili tuweze kutekeleza azma yetu ya kuwa na fedhaza kuaminika kabisa ambazo zitakamilisha na kumaliza shidaya maji ambayo inatukabili vijijini kwetu, katika miji yetu yaWilaya na katika Miji Mikuu ya Mikoa.

Mheshimiwa Spika, napenda kabla ya kumalizahotuba yangu hii, nieleze kwamba, pamoja na hatua hiziambazo tunazichukua kupeleka maji katika maeneo ya miji,katika vijiji na katika maeneo mengine mengi, ni muhimu sanatuhakikishe kwamba maji hayo yatakuwepo leo, kesho nakesho kutwa na kwamba rasilimali hii ya maji tuliyonayo sasa,tutaweza kuwakabidhi wajukuu zetu na wenyewe

Page 158: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

158

waendelee kuitumia. Yapo matatizo makubwa sana ambayoyanakabili rasilimali hizi za maji. Tatizo la kwanza, ni uharibifuwa mazingira. Tumekuwa tunakata sana miti katika maeneoyote. Ukaangalia kwenye ramani utakuta sehemu yote yakatikaki ya Tanzania imepakwa rangi ya kijani kwamba kunamiombo woodlands huko ndani, tuna misitu ya miombomikubwa kupita miombo yote Duniani kote. Hivi sasa ukiendahuko kwenye hiyo Miombo, miti yote imekatwa na mito navyanzo vya maji vingine vinavyotokea huko, vinaanza kuwani vya kipindi cha mwaka, wakati wa mvua maji yanapita,wakati wa kiangazi maji yanakauka. Kwa hiyo, ni lazimatuchukue hatua kubwa ya kuvihifadhi vyanzo hivi nakuhakikisha kwamba chanzo cha nishati ya kutumiamajumbani kinaondoka kutoka mkaa na kuwa chanzokingine.

Mheshimiwa Spika, Mwenyezi Mungu ametupatiagesi. Hatua ya kwanza ambayo tungeishughulikia nikuhakikisha kwamba wafanyakazi wote wa Tanzaniawanakopeshwa matenki yale madogo ya gesi na majiko yagesi ili wabadili mfumo wa nishati ya kupikia nyumbani namatumizi ya nyumbani kutoka mikaa na kwenda kutumia gesiili kuhifadhi misitu yetu na vyanzo vyetu vya maji. Tusipofanyahivyo hivi sasa, tutachelewa treni na tukifika station itakuwaimepita na sisi wote tutakuwa na matatizo makubwa sanaya maji.

Mheshimiwa Spika, ni muhimu pia tuangalie nakupambana na mabadiliko ya Tabianchi. Tuchukue hatuambalimbali kuwasaidia wananchi ambao wanatumia ardhioevu, waweze kuwa na maji mbadala ili kuweza ku-savevyanzo vyetu vya maji.

Mheshimiwa Spika, tunayo maoni mengi ambayotumeletewa na mengi yako kwenye book kubwa hapa, kamanilivyoleza, tutaleta kitabu ambacho tumeweka pamojamaoni yote haya na maswali na changamoto, tumezipatiamajibu kama ambavyo tunayaelewa ili wote tukiondokatuwe na uelewa wa pamoja.

Page 159: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

159

Mheshimiwa Spika, sasa nachukua fursa hii kuliombaBunge lako Tukufu watupitishie bajeti ambayotumependekeza ili tuweze kwenda kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

MWONGOZO WA SPIKA

SPIKA: Hoja hiyo imeungwa mkono, MheshimiwaKabwe Zitto kwanza!

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kunipa nafasi ya kutaka Mwongozo wako. Kabla Wizaraya Maji haijanza kueleza maelezo yake na kujibu hoja zaWaheshimiwa Wabunge, Waziri wa Fedha alisimama kutoaKauli ya Serikali kuhusiana na suala ambalo li l ikuwalimeahirishwa la utafutaji wa fedha kwa ajili ya Wizara ya Maji.Sasa ulimwomba Waziri wa Fedha aji-commit kusema ni kiasigani na Waziri wa Maji pia amesema ni kiasi gani ambachoSerikali imekitafuta. Kwa mujibu wa taratibu zetu za Bunge,Kauli ya Serikali ni lazima isambazwe kwa Wabunge. Waziriwa Fedha hakuwa sehemu ya wachangiaji katika Wizara yaMaji. Amekuja kulipa Bunge taarifa baada ya consultationsambazo zimefanyika katika kipindi cha weekend hii ambayoimepita. Naomba taarifa hii ili iwe rasmi, naomba nikumbushekwamba, mwaka juzi tulitaka fedha ziongezwe Wizara yaUsafirishaji na Bunge likapiga makofi sana hapa, fedha zilehazikuongezwa hata senti tano, pamoja na kwambatulipitisha hapa Bungeni. Hivyo, ni lazima kupata taarifa rasmiya Serikali, ya Wizara ya Fedha.

Mheshimiwa Spika, lakini pili lazima tuone mabadilikohaya kwenye vitabu, kama amendments za vitabu, tuonehizo fedha na tuweze kujua hizo fedha sasa zinakwenda wapi.Kwa sababu Kamati imeanisha maeneo ambayo tunatakafedha hizi ziende, yako wazi wazi, kwa Waziri wa Fedha katika

Page 160: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

160

taarifa yake alitakiwa kuanisha kama namna ambavyoKamati ya Maji imeanisha ili tukitoka hapa tuwe na taarifakamili ya Serikali na wasije wakatufanya kama walivyofanyawakati wa Wizara ya Usafirishaji, tulisema shilingi bilioni 94zimeongezwa lakini hazikuongezwa.

Mheshimiwa Spika, utakumbuka mwaka 2011, Bungehapa lilikubali kwamba nyongeza ya fedha ambazozitatokana na nyongeza ya ushuru wa mafuta ya taa, itaendakwenye miradi ya umeme vijijini. Fedha hizo hazikwendampaka leo. Kwa hiyo, ni lazima tupate commitment yauhakika na Waziri wa Fedha alete taarifa yake hapa,aiwasilishe kama Kauli na ipokelewe ili tuweze kuitumiakuwabana wasipopeleka fedha Wizara ya Maji, vinginevyohapa tutakuwa tunacheza. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Tundu Lissu!

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Spika, nashukuru.Langu linalingana kidogo na Mheshimiwa Zitto lakini naombaniweke mkazo kwenye Kanuni inayohusika. Kanuni ya 49(3),Waziri mwenye kutoa Kauli atawajibika kutoa nakala ya Kauliyake kwa Wabunge wote wakati inapowasilisha Bungeni.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa Fedhaametoa Kauli bila hata kusoma, hakuwa na chochotealichokuwa anakisoma wakati akitoa kauli ya Serikali. Maanayake ni kwamba hata wewe huna alichokuwa anakisema,achilia mbali Waheshimiwa Wabunge wote. NaombaMwongozo wako kama ni sahihi kwa Waziri kuja kutoa kauliya Serikali kwa maneno tu, wakati Kanuni zinaweka wazikwamba anatakiwa agawe nakala kwa Wabunge wotewakati anapoiwasilisha. Tuambiwe kama hii ni sahihi, kamasiyo sahihi tutaomba hatua stahiki zichukuliwe.

SPIKA: Mheshimiwa John Mnyika!

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Spika, naombaMwongozo wako, kwa mujibu wa Kanuni ya 57 (2) pamojana Kanuni ya 101 (1). Kanuni ya 57 (2) inahusu utaratibu wa

Page 161: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

161

kufanya mabadiliko kwenye hoja na Kanuni ya 101 inahusuutaratibu wa Bunge kupitisha Bajeti kifungu kwa kifungu.

Mheshimiwa Spika, sasa wakati mtoa hojaanahitimisha hoja yake, kufuatiwa Kauli iliyotolewa na Waziri,naungana mkono kabisa na Mheshimiwa Zitto Kabwe naMheshimiwa Tindu A. Lissu kuhusiana na ile kauli, lakini miminiko kwenye majumuisho ya Waziri. Katika majumuisho yakeMheshimiwa Waziri, akaanza kutaja miradi iliyofanyiwamarekebisho akianisha kiwango cha fedha kwa ile miradimbalimbali, bila sisi Wabunge kupewa nakala kama ilivyokawaida ya Jedwali la Marekebisho, kifungu kwa kifungu, kwamaeneo ambayo mabadiliko yamefanyika ili kupata hakikamarekebisho hayo yanahusu maeneo gani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa naomba Mwongozo wakokwa sababu kwa vyovyote vile maelezo yalitolewahayakufata utaratibu wa Kanuni wa kufanya mabadilikoyanayokusudiwa, ni kwa nini sasa Kanuni ya 69(1) isitumike, iliama Mbunge mmojawapo au wewe mwenyeweMheshimiwa Spika, uweze kuruhusu kutolewa kwa hoja yakuahirishwa kwa mjadala, ili Serikali ikakae tena, iwezekufanya mabadiliko kifungu kwa kifungu, kabla Bungehalijakaa kama Kamati tuletewe Jedwali la Marekebisho,tusiuziwe mbuzi kwenye gunia, ili hizi fedha kweli tuzione natuone kweli zinakwenda wapi na zinakwenda kufanya nini.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba Mwongozo wako kwamujibu wa Kanuni hizo.

SPIKA: Nashukuru kwa hiyo Miongozo, hivyo ndivyonilikuwa nategemea mtauliza kwa sababu utaratibu huu wakuwa na Kamati ya Bajeti ni mara yetu ya kwanza naassumption tuliyokuwa nayo kwa kuunda Kamati ya Bajeti nikukaa na Serikali kupitia vifungu kwa vifungu pale ambapotunafikiria kwamba, pengine tungependa nguvu zetuzielekee upande huu zaidi kuliko mahali pengine. Kwa hiyo,ndivyo walivyofanya wakati wa weekend tulipoachanahapa. Hizi hela zilizotolewa siyo kwamba zimepatikana

Page 162: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

162

nyingine, zimetoka kwenye baadhi ya vifungu, tenanaambiwa hata baadhi ya Wizara tulizopitisha, lakini yote hiini health. Kwa hiyo, mtatategemea kwamba tunafanyajuggling kuhamisha hapa, peleka huku, peleka hapa. Hiyokazi haikuwa rahisi, hivyo ndiyo maana nilisema nilikuwanategemea ninyi mtasema hivyo na ningeshangaa kamamsingesema hivyo. Kwa hiyo, ni kweli hata Wizara tulizopitishamafungu yao yamenyofolewa.

Waheshimiwa Wabunge, lakini sisi tunachokisema,bajeti tunayoizungumzia sisi ni ile ya Waziri wa Fedha, hiijuggling itaendelea, mnaweza kusema leo sisi maji hapashilingi bilioni 184.5, imefanyika kweli. Sasa tunachokisemakwa maana ya Wizara hii, itabidi tuletewe addendum kwasababu vinginevyo kifungu tutakachokuwa tunapitisha hapasiyo chenyewe lakini kwa maana ya kutazama bajeti nzimakufikia mwishoni ndiyo tutakwenda kwenye ile AppropriationBill, maana hiyo ndiyo itaanza kubadilisha hata mafungumengine. Kwa sababu ya muda tuliokuwa nao na ilibiditufanye hiyo kazi, bado tunaweza kuitaka Wizara ikawekemahali ambapo ilifikiria itaweka, kusudi tupate angalaumtazamo kwamba hii iliyosemwa ni kweli.

Kwa nini Waziri wa Fedha hakusambaza Kauli yaSerikali, ni kwa sababu tumemtaka asubuhi aweze kusema,kwani huyu asingeweza kusema kama hana manenomengine yoyote, lakini hiyo haizuii Waziri wa Fedha kuletaKauli iliyoandikwa.

Kwa maana hiyo, basi mimi ningependa tutumienafasi hii Waziri wa Maji na Waziri wa Fedha wajaribu kuonani maeneo gani ambayo wamefanyiwa mabadiliko ilitutakapokuja mchana kupitisha vifungu tuwe na hakikakwamba ni eneo linalohusika. (Makofi)

Kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge, kwa maana hiyo,naahirisha shughuli za Bunge mpaka saa 11 jioni.

(Saa 5.35 Asubuhi Bunge lilisitishwaMpaka Saa 11.00 Jioni)

Page 163: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

163

(Saa 11.00 jioni, Bunge lilirudia)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tulipositisha shughuliza Serikali asubuhi, tulikuwa na kazi mbili ambazo tulitaka tuwena uhakika nazo. Moja, ilikuwa ni kujaribu kupata maelezoya Waziri wa Fedha aliyokuwa ametoa hapa kwa maandishi.Ameleta na nakala aliyonipa mimi ina covering letter. Kwahiyo, msije mkaona kwamba aaah, mbona haijasainiwahapa? Ina covering letter, ndiyo hii ninayo. Kwa hiyo, ni yalealiyosema asubuhi, ndiyo yale ambayo ameandika.

Hiyo ya kwanza, ya pili, katika vitabu vyetu vyarecurrent expenditure na developments votes, kumefanyikaaddendums, maandiko ya kuweka humu ndani kubadilishavifungu fulani. Lakini kama tulivyoeleza, Bajeti kamili ya Serikalini ile atakayotoa Waziri wa Fedha. Hapa ni provisionary, hatatunapopitisha huwa ni provisionary, kwa sababu hatawaliponyofoa fedha nyingine kupata hizi, hata mafungumengine yamekuwa affected.

Kwa hiyo, yale yatakuwa yanaonekana paletutakapofika Wizara inayohusika, lakini mwisho wa jumla yafedha zote zilizopitishwa zitapitia kwenye Appropriation Bill.Kule ndipo tutakapokuwa tumesema nini kimetokea wapi.

Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, kama tungekuwatulianza vizuri na Bajeti Committee mapema, labda hayayangekuwa hayakutokea. Lakini nilishawaambia, wakatitulipokuwa tunafanya briefing kwamba utaratibutuliojianzishia wenyewe kwa siku za mwanzo tutakuwa nateething problems, utakuwa na matatizo ya hapa na pale.Lakini hayo siyo matatizo ya udhaifu wa utaratibu, ni namnayenyewe tu. Kwa mfano, sasa imekuwa jana na leo kuwezaku-fit in vifungu vile, siyo rahisi. Bado tunamwagiza Waziri waMaji akikaa vizuri na watu wake aweze kutoa tena maelezokwa kirefu kuhusu mradi mmoja baada ya mwingine kusudimuweze kuufanyiwa kazi mnakokwenda.

Kwa hiyo, naomba mwelewe hivyo kwambatumefanikiwa kupata nyongeza ya fedha, lakini ni katika

Page 164: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

164

kuchukua vifungu vingine. Sasa mtu asidhani kwambamchezo huu unaweza kuendelea indefinitely, kwa sababukwa mujibu wa Katiba yetu inatuzuia kufungua Bajeti Kuu.Tunaweza kugombana gombana humu ndani kwa ndanilakini siyo zaidi ya hapo.

Kwa hiyo, mimi nawashukuru sana Wizara kwa kuwezakufanya hayo, na ninaomba tunapojielekeza kwenye fungu,tutakwenda taratibu kusudi muweze kuelewa ninikinachoendelea.

KAMATI YA MATUMIZI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 49 - Wizara ya Maji

Kif. 1001 - Administration and HR Mgt......... Tsh 3,661,296,000/=

MWENYEKITI: Mshahara wa Waziri. Mheshimiwa JenistaMhagama. Wengine sikuwaona wamesimama.

MHE. JENISTA J. MHAGAMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kuniona na kunipa nafasi. Fungu nihilo hilo kama lilivyosemwa na ninasimama kwenye Mshaharawa Mheshimiwa Waziri na lengo langu ni jema tu, siyokwamba nataka kuondoa Mshahara. Maelezo yangu nikama yafuatayo:-

Kwanza kabisa nakubaliana na hoja iliyoletwa leo naMheshimiwa Waziri wa Fedha kwa kuhakikisha kwambaWizara hii ya Fedha inaongezewa fedha ili kwenda kutatuamatatizo ya maji katika nchi nzima kama Sera ya Majiinavyosema na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduziinavyosema. Nakubaliana na naipongeza sana Serikali yaChama cha Mapinduzi kwa kuwa sikivu na kuamua maamuzimagumu ya kuongeza fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini fedha hii itakwendakutatua tatizo la maji na hasa Vijijini kutoka asilimia 55 mpaka

Page 165: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

165

kwenda kwenye 66 kwa kuongeza idadi ya Vijiji. Lakini kwauzoefu tulionao, nataka sasa hapo Serikali inisikilize vizuri nainisaidie kujibu hapa Bungeni. Kwa uzoefu tulionao, miradi hiimikubwa yote katika nchi yetu ya Tanzania, pamoja na fedhahizi tunazoziongeza tukiamini zinakwenda kujibu matatizohaya, zinaathiriwa sana na tatizo la Sheria ya Manunuzituliyonayo mpaka sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ile isiporekebishwa,kazi hii nzuri ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi haitafanyikana wananchi wa Vijijini na Mijini hawatapata maji. Huo niuhakika nilionao. Sheria ile ina upungufu mkubwa, na unaonakabisa kwamba inasababisha utekelezaji wa miradikutokufanikiwa kwa sababu ya urasimu na udanganyifumkubwa ulioko katika eneo la manunuzi na hata ripoti yaMkaguzi Mkuu wa Serikali imesema hivyo.

Je, Serikali kupitia Waziri wa Maji leo, anatuambiajeWaheshimiwa Wabunge, lakini na Watanzania wotewanaofurahia maamuzi haya ya Serikali ya Chama chaMapinduzi ya kutatua tatizo la maji, ni lini watatuletea ileSheria ya Manunuzi yenye utata mkubwa na inayosaidiakutokufanikiwa kwa miradi mingi yenye nia njema ya Serikaliya Chama chetu ibadilishwe na kiu hii ya upatikanaji wa majina hasa maeneo ya Vijijini iweze kutekelezeka?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kupata maelezohayo kutoka kwa Serikali. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Mawazirimjiandae, mtajibu kwa pamoja baadaye. Mheshimiwa ClaraDiana Mwatuka.

Waheshimiwa Wabunge, tunatumia kifungu cha101(3).

MHE. CLARA D. MWATUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipatia nafasi nami niweze kutoa dukudukulangu nililonalo kutokana na Bajeti hii kwa lile ambalonililifikisha juzi katika kuchangia kwangu.

Page 166: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

166

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia kwangu,nilikuwa nimezungumzia au kulalamikia juu ya hali ya Kusinikulivyosahauliwa kwa kila mambo, na nikaelezea kwambamaji kule ni shida, akina mama wanalala visimani, Wilaya yaNewala, maji wanakunywa, wanamwomba Mungu kwambamvua inyeshe haraka hata kama wakati wa kifuku bado iliwapate maji kwa kuwa hawana maji mengine mbadala.Mabomba yamekuwa shida, na nikaeleza kwamba majiwanayokunywa kule, wageni mnapokwenda mnapewa yakwenye chupa, ya viwandani. Mgekuwa mnapewa yale,msingeyatumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikaomba vilevile kwambaafadhali wangepatiwa dawa wasafishe yale maji. Vilevilenikaomba kwamba kule Masasi miradi ndiyo, ilipelekwa yaVijiji kumi; visima vile kumi havitoi maji. Nikaeleza kwambavijana wanachimba na wanafanya miradi, visima vifupi tu.Sasa: Je, Serikali inasemaje juu ya hili? Iendelee kubaki vilevileKusini kama Kusini au kwa safari hii kwa Bajeti hiimtawarekebishia? Naomba jibu. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa John Mnyika!

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru, naomba ufafanuzi kupitia kifungu cha Mshaharawa Waziri na iwapo ufafanuzi hautaridhisha, nitaomba hojaya kuondoa Shilingi kwenye Mshahara wa Waziri ili hili jambonitakalolieleza liweze kujadiliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye maoni ya KambiRasmi ya Upinzani kwenye ukurasa wa tatu, ilipendekezakwamba Serikali itenge jumla ya Shilingi bilioni 529 kamamchango wa kutosha kwa mwaka huu wa fedha katikakupunguza ukubwa wa tatizo la maji nchini. Katikamajumuisho na katika kauli ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha,Serikali imekubali kutokana vilevile na maoni ya Kamatikuongeza kiasi cha Shilingi bilioni 184.5 ambayo ni hatua kiasi,lakini bado haijafikia kiwango ambacho Serikali ilipaswakutenga kwa mujibu wa Mpango wa Taifa wa Maendeleoambao umeridhiwa na Bunge hili.

Page 167: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

167

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa zaidi siyo tukutengwa kwa fedha, kwa mujibu wa hotuba ya Waziri,kwenye aya ya 188 ya hotuba ya Mheshimiwa Waziri, ukurasawa 88 wa Kitabu cha hotuba ya Mheshimiwa Waziri; mwaka2012 baada ya kutambua ukubwa wa tatizo la maji,kulitengwa Shilingi bilioni 140 za masuala ya maendeleokwenye miradi ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa mujibu wa hotubaya Waziri mwenyewe, mpaka ilipofikia mwezi Machi, 2013,ikiwa muda umepita takribani asilimia 75 ya muda wautekelezaji wa mwaka wa fedha, fedha ambazo zilikuwazimetolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo zilikuwa niShilingi bilioni 29 peke yake, ambazo kwa mujibu wa takwimuza Mheshimiwa Waziri mwenyewe ni asilimia 20.7 peke yakeya kiwango cha fedha ambacho kilipaswa kutengwa. Kwahiyo, hakikufikia hata robo kwa maana ya asilimia 25, wakatimpaka hatua hiyo, kama kweli tumedhamiria kuondoamatatizo ya maji ilipaswa kuwa zimetengwa angalau asilimia75 ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ningependa kupatahakikisho kutoka kwa Waziri wa Fedha ni kwa vipi safari hiiimejipanga kwamba fedha zitatolewa kwa wakati ili kwelituweze kutekeleza kwa vitendo adhima ya kuondoa matatizoya maji nchini?

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Ole-Sendeka.

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona. Pamoja na usikivu waSerikali wa kukubali kutenga Shilingi bilioni 184 katika miradiya maendeleo ya maji na kwa imani kwamba hii inawezakusaidia kutatua pia matatizo ya fedha zilizokuwa zinawekwakwenye bajeti kila mwaka na bahati mbaya fedha zilikuwahazipatikani, ikiwemo ile Shilingi bilioni 1.8 katika Vijiji vileambavyo vinalazimika kuhama kuanzia mwezi wa Sabakuhamia Wilaya nyingine za Simanjiro kwa ajili ya ukosefu wamaji na shule nyingine kulazimika kufungwa; nilikuwa nimetoapendekezo la kutumika kwa fedha za Benki ya Society

Page 168: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

168

General, mchakato ambao Mheshimiwa Waziri anaujuakabisa kwamba ulikuwa umefikia katika dakika za ukingoni,ili kuondoa adha ya watoto wanaopinda miguu paleMererani na katika Kata zinazozunguka za Naisinyai, Indiamtuna Shambarai pamoja na baadhi ya maeneo ya Wilaya yaHai na maeneo ya Wilaya ya Arumeru Mashariki, ili kuhakikishakwamba tunaokoa maisha ya watoto hawa ambao sasawanageuka kuwa vilema na kuzingatia kuwa tunawezakupata maji kutoka Mlima Kilimanjaro au Mlima Meru kwakutumia fedha hizo.

Nilitaka kujua, nini msimamo wa Serikali katikakuhakikisha kwamba adha hii ya watoto wanaopinda miguukutokana na maji yasiyofaa kwa matumizi ya binadamuinaweza kutumika? Inaweza kuchukua hatua gani zinapaswakuchukiliwa sasa ili kuondokana na adha hiyo na fedhehahiyo pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa IddI Azzan.

MHE. IDDI M. AZZAN: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi. Nami niungane tu na wenzangukuipongeza Serikali kwa ongezeko hili la Shilingi bilioni 184,nikiamini kabisa kwamba tatizo la maji angalau kwa kiasifulani litaondoka hapa nchini. Kwa sababu Sera ya Majiinataka kila mwananchi apate maji safi na salama, na kwakuwa Serikali imeshaanza kuchukua hatua za kukabiliana nahali hiyo kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama,naomba Serikali itueleze tu, yapo maeneo ambayo miradihii itakamilika mwaka 2014 na maeneo mengine itakamilikamwaka 2015, lakini kipindi hiki cha mpito yapo maji ambayoyanapatikana siyo kwa wingi, ni maji machache sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni jambo ambalo likokaribu nchi nzima lakini Dar es Salaam ni zaidi. Natakakufahamu Serikali inachukua hatua gani kwa wale ambaowanahujumu maji haya machache yasifike kwa wananchiama kwa mabomba kupasuka ama kwa kufanya biashara

Page 169: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

169

haramu ya kuuza maji, kufunga pampu kubwa na kuchukuamaji yote badala ya kwenda kwa wananchi yanakwendakwa hao wanaouza maji? Serikali inachukua hatua ganikukabiliana na hali hiyo katika kipindi hiki cha mpito kablaya miradi hii haijakamilika 2015?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Machali,nilikuona.

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Ninaamini kabisa kwamba siyo Sera ya Serikalikuwa na baadhi ya Watendaji ambao wana-lack integritykatika kuhakikisha miradi ambayo imekusudiwa na Serikaliinakwenda kama ilivyokusudiwa. Katika mchango wangunilichangia nikauliza juu ya mradi mmoja ambao umekuwaunasuasua, nimetoa kama mfano na maeneo mengineWaheshimiwa Wabunge wamekuwa wakichangia,wakionyesha kutokuridhishwa na hasa hii miradi ambayoinafadhiliwa na Benki ya Dunia.

Nilikuwa naomba kauli ya Serikali isaidie kuwezakufahamu, Serikali iko tayari kumsimamisha yule Mkandarasiambaye kuna mradi mmoja niliutaja hapa, kule Kasuluambaye ameonekana kwa kipindi cha miezi sita nainakwenda kwisha mwezi ujao itakapofika tarehe tisa, kwakuwa hajafanya kazi ambayo kwa kweli kwa kiwango kilena Mhandisi wa maji ameonyesha mfano mbaya wakushindwa kuweza kusimamia mradi ule?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa nipateufafanuzi kwa kuwa nimezungumzia hilo na hiyo nimeitoa tukama case study, lakini ni concern ya Wabunge wengi. Ninihatima ya Serikali katika kuweza kumwondoa Mkandarasiyule, pamoja na kuwachukulia Watendaji wote ambaowameonyesha utovu wa nidhamu katika kusimamia miradiya maji ambayo inatekelezwa hapa nchini ili kuweza kuletaufanisi?

Page 170: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

170

MWENYEKITI: Makandarasi kama huyo, siyo necessarilyhuyo, hilo litakuwa Sera. Ukiona unakwenda pake yakonyumbani, haiwezekani.

Mheshimiwa Suleiman Nchambi!

MHE. SULEIMAN M. N. SULEIMAN: MheshimiwaMwenyekiti, kwa kuwa Sera ya Maji ni kuhakikisha kilaMtanzania anapata maji safi...

MWENYEKITI: Naona ungehama huo mstari wa hukonyuma, husikiki. Naomba usogee mbele.

MHE. SULEIMAN M. N. SULEIMAN: MheshimiwaMwenyekiti, kwa kuwa Sera ya Maji ni kuhakikisha kilaMtanzania anafikiwa na huduma ya maji safi na salama nakwa kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kuzingatiaSera hiyo iliona ni vyema kuanzisha miradi mikubwa ya majiitakayoweza kusaidia Watanzania wengi ambao watafikiwana huduma ya maji safi na salama, moja ya miradi hiyomikubwa ni mradi wa maji toka Ziwa Victoria ambaounahudumia wakazi wa Mji wa Shinyanga na Kahama nabaadaye maeneo mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mradi huo kwaawamu ya kwanza ulikamilika na wananchi wananufaika namaji hayo, na awamu ya pili ilikuwa ni mradi wa takiribanibilioni 13 ambao ungeweza kuwanufaisha wananchi waJimbo la Kishapu kwa kiasi kikubwa ili Sera ile ya Maji ambayoiliwekwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa nia njemakabisa ya kuwahudumia Watanzania wote iweze kukamilikana kuwafikia Watanzania wengi na baadaye wote; naombasasa nipate majibu kutoka kwa Mheshimiwa Waziri, kwa kuwaWatanzania hawa waliko Kishapu ni sawa na Watanzaniawaliokuwa Shinyanga na Kahama na maeneo mengineambao wanapata huduma ya maji safi na salama:-

Je, Mheshimiwa Waziri, yuko tayari kunihakikishiakatika marekebisho haya ya Bajeti yaliyofanyika mpango huo

Page 171: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

171

wa kuyapeleka maji ya Ziwa Victoria, utakamilika kwawananchi wa Jimbo la Kishapu?

MWENYEKITI: Naomba mjiwekeze kwenye Sera zaidikuliko kwenye maeneo yenu. Mheshimiwa Laizer!

MHE. LAIZER M. LEKULE: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza ningependa Serikali ielewe kwamba miradi yotenchini 10% inakwenda kwa ajili ya manunuzi. Kwa hiyo, hilijambo alilozungumzia Mheshimiwa Jenista, huo utaratibu nasheria ziletwe haraka sana kwa sababu fedha za Serikalizinakwenda kwa ajili ya manunuzi. (Makofi)

Suala la pili ni uwiano.....

MWENYEKITI: Kwa hiyo, ni moja tu. Sasa usizungumzela pili, kwani la kwanza lilishaulizwa.

MHE. LAIZER M. LEKULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, sualala uwiano nimelalamika sana hapa katika bajeti hii na bajetizilizopita, nikisema kwamba Wilaya ya Longido ina matatizomakubwa ya maji.

Serikali katika nyongeza hii haikutambua kabisaWilaya ya Longido kwamba tuna matatizo ya maji. Majiyameongeza maisha magumu kwa wananchi wa Longido.Sasa sijui Serikali inatusubiri na sisi tuandamane kama watuwa Ubungo ndiyo tufikiriwe! Kwa sababu kwanza Ubungo inamatatizo madogo kuliko Longido.

Sasa kama ni maandamano ya wananchi waLongido na sisi tuanze kuandamana ndiyo tupate maji;naomba katika bajeti hii na sisi Longido tukumbukwe kwasababu sikuona popote kwamba jibu la wananchi waLongido wanapata ufumbuzi wa maji. Sisi ni watu kama watuwengine ambao wamewekewa pesa kwenye bajeti hii.(Makofi)

MWENYEKITI: Haya, kama mnaendelea kudai miradiya kwenu, basi nitaifunga orodha hii. Mheshimiwa Zitto!

Page 172: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

172

MHE. KABWE ZUBERI ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,wakati Kamati inatoa taarifa yake hapa, ilionyesha tofautikubwa iliyopo katika mgawanyo wa rasilimali kwa ajili yaWizara ya Maji kati ya maeneo ya Mijini na Vijijini, na Kamatiikawa imeomba Serikali iweze kuangalia ni namna gani yakuweza kurekebisha jambo hili.

Napenda Waheshimiwa Wabunge niwaonyeshekwamba kabla ya mabadiliko haya ambayo Bungelimeyawezesha kupatikana, maeneo ya Vijijini ambayo ndiyoyana 74% ya Watanzania wote, fedha zilizokuwa zimetengwaza miradi ya maji zilikuwa ni Shilingi bilioni 75 tu na ninaombaWaheshimiwa Wabunge wa Vijijini wanisikilize kwa makinisana. Mijini zilikuwa zimetengwa Shilingi bilioni 254.

Baada ya marekebisho haya na kuongezeka kwafedha hizi kidogo ambazo tumezipata, tungepaswa kupatazaidi kama jinsi ambavyo Kambi ya Upinzani ilivyokuwaimependekeza, sasa hivi fedha ambayo imetengwa kwa ajiliya Mijini ni Shilingi bilioni 266, fedha ambayo imetengwa kwaajili ya Vijijini baada ya nyongeza ni Shilingi bilioni 237. Asilimia74 ya Watanzania wanaoishi Vijijini wametengewa takribanisawa na 24% ya wananchi ambao wanaishi Mijini.

Napenda Waziri atoe kauli hapa kwa sababu trendhii imeendelea miaka yote. Watu wote tunafanya kazi,tunatoa kodi na kodi zinakusanywa, lakini fedha zinakwendaMijini kwa sababu watu wa Mijini wanajua kupiga kelele zaidikuliko sisi wa Vijijini. Trend hii tusipoiuzuia, maendeleo Vijijinihayatakuwepo. (Makofi)

Nawaomba Waheshimiwa Wabunge wenzangutukubaliane hapa na Waziri atoe commitment yake kwasababu hili ni suala la kisera, kwamba mgawanyo wowotewa fedha za bajeti unaokuja, uhakikishe Vijijini wanapata 70%na Mijijini wanapata 30% ya mgawo wa maji.

MWENYEKITI: Ahsante, hoja imeeleweka. Tunaendeleana mwisho ni Mheshimiwa Blandes!

Page 173: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

173

MHE. GOSBERT B. BLANDES: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Mimi nataka kuzungumzia kwamba kwenyemchango wangu nilijitahidi sana kuzungumzia tofauti kubwasana ya mgawanyo wa fedha hizi za maji na kusema kwelinilizungumzia miradi ya maji inayokwenda kwa MheshimiwaWaziri, nikazungumzia kwamba ni fedha nyingi, yaani nilisemaShilingi bilioni 30 lakini leo katika mabadiliko haya zinasomekaShilingi bilioni 32.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niliomba sana kwambakatika Shilingi bilioni 32 hizi amege kiasi fulani kiende katikaJimbo la Karagwe. Nataka majibu, kwa nini sioni Karagwehapa?

MWENYEKITI: Sasa hilo suala la siyo la kisera. Naonanifunge. Waheshimiwa Mawaziri mwanze kujibu hoja mojamoja na unaweza kusaidiana na Naibu wako. Aanze Waziriwa Fedha kuhusu Sheria ya Manunuzi.

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Waheshimiwa Wabunge kwa umakini wao wameelezanamna ambapo bajeti ikishaidhinishwa, miradi mingiinachelewa. Inaelekea kwamba Sheria ya Manunuzi haikidhikuhakikisha kwamba tunakuwa na value for money. Katikahilo Serikali inachukua nafasi ya kupitia Sheria ya Manunuzi ilituelekee kuwa na sheria inayokidhi manunuzi ambayobaadaye tunapata value for money, yaani thamani yamanunuzi ifanane na fedha tuliyotoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali itachukuauamuzi wa kuipitia ile sheria na tutaileta hapa Bungeni.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MWENYEKITI: Mawaziri!

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kumjibu Mheshimiwa Diana Mwatuka swali lakekama ifuatavyo:-

Page 174: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

174

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mwatuka,anaonesha kwamba tumesahau Mikoa ya Kusini na nilidhanihii siyo sahihi sana ikajulikana hivyo kwa Watanzania, kwasababu hata katika maelezo yetu leo tumeeleza kwambamoja ya mradi mikubwa ambayo Serikali imewekeza ni Mradiwa Mbwinji Masasi Nachingwea unaogharimu Shilingi bilioni31 na utahudumia wananchi wa Vijiji vya Wilaya hizo mbili.Nikaeleza pia kwamba kuna mradi mkubwa uliojengwamwaka 1957 wa Makonde unaohudumia Wilaya tatu, yaaniMtwara Vijijini, Newala na Tandahimba.

Sasa ni kweli tatizo la maji lipo na niseme tu kwambatunalichukua, tutaendelea kuboresha huduma kwenye Vijijialivyovisema na katika huu mgawo tulioongezewa fedhatutahakikisha vile Vijiji alivyovitamka Mheshimiwa Mbungevinapata maji.

Pia niendelee na jambo lingine kisha nimwachieMheshimiwa Waziri. Kuna hili suala la Mheshimiwa Azzankuhusu upotevu wa maji Dar es Salaam na kwamba nimikakati gani ya muda mfupi wakati tukisubiri ile miradimikubwa ya Ruvu Juu na Ruvu Chini ili kuona kwambawananchi wanapata maji. Imeonekana kwamba upotefu wamaji ambao unafikia 50% Dar es Salaam, kati ya 50%, basi30% zinatokana na watu kuiba maji. Kwa hiyo, MheshimiwaWaziri.....

MWENYEKITI: Ongeza sauti au sijui vipi!

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Nasema hivi, imeonekanakwamba katika 50% za upotevu wa maji Dar es Salaam, basi30% kati yake zinatokana na watu kujiunganishia kiholela, wizi,kuweka mabomba ndani ya nyumba, kuweka matenki nakuuza bila vibali. Kwa hiyo, tulianzisha Kampeni ya kusakawezi wote hawa na inakwenda vizuri sana na mpaka sasahivi tumekamata watu zaidi ya 86 ambao baadhi yaowamefikishwa Mahakamani na taratibu za kusikiliza kesi zaozinaendelea.

Page 175: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

175

Kwa hiyo, ninachotaka kusema ni kwamba naombasana Watanzania na Wanasiasa kwamba wakati tunatakamaji yaongezeke kwa wananchi wa Dar es Salaam, basitusaidiane pia kuhakikisha kwamba wananchi wetuwanalinda miundombinu hii wala hawaibi wala kubomoa iliwananchi wengi waweze kupata maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mwisho ni laMheshimiwa Blandes. Nafahamu kwamba anapata shidakwake kwenye Mji wa Omurushek kuhusu maji na ndiyomaana anafikia hatua kwamba pengine tungemega hiziShilingi bilioni 32 ili ziende kwake. Nataka kumhakikishiakwamba tumesikia kilio chake na kwa kuanzia tayari kwenyeawamu ya kwanza kuna Shilingi milioni 150 kwa ule Mji waOmurushek na katika mgawo huu wa pili tutamwongezeatena fedha kwa ajili ya Mji huo wa Omurusheki na Vijiji vingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri!

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanzanakushukuru sana kwa kutupa nafasi hii. Maelekezo yoteambayo mfumo huu mpya umetupa yanasaidia kujengahistoria ya Bunge letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mnyikaamesema kwamba Serikali iliombwa itenge fedha kufikiaShilingi bilioni 509.

Napenda kusema kwamba hivi sasa tunavyokwenda,fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo baada ya ongezekohili, imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 379.4 na kufika Shilingibilioni 553.2, na fedha za ndani zimeongezeka kutoka Shilingibilioni 138.2 kufika Shilingi bilioni 312.066.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ni vizuri ijulikane kwambafedha za nje katika bajeti hii sasa ni Shilingi bilioni 241.2ukilinganisha na fedha za ndani Shilingi bilioni 312.1. Kwa hiyo,kwa hali ya bajeti tuliyonayo, Serikali imefanya juhudi kubwa

Page 176: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

176

kutafuta fedha na kubadilisha hali ya bajeti ambayo tunayosasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imeulizwa hapa kuhusianana swali la Mheshimiwa Ole- Sendeka kuhusu fedha za ELIPS.Tulitafuta fedha za BADEA na OFID kwa ajili ya kujenga mradiwa Orkesmet na ule mradi wa Mwanga. Fedha hizozimepatikana na Serikali imetiliana sahihi na wafadhili haokwa ajili ya utoaji wa fedha hizo. Wakati tunafanya hivyo,suala hili limechukua muda mrefu tangu mwaka 2006 na kwahiyo, kulikuwa na haki kabisa kwa Serikali kuanza kutafutanjia mbadala za kupata fedha ya mradi huo, na wakati huoSerikali pamoja na Mheshimiwa Mbunge nami napendanimshukuru sana Mheshimiwa Ole-Sendeka kwa kufanya kazikubwa sana ya kushirikiana na kumleta huyo mwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua tuliyofikia sasamwekezaji huo hatutamtumia kwenye mradi wa Orkesmet.Lakini nakubaliana sana na Mheshimiwa Ole-Sendekakwamba ni vizuri tuendelee kuongea na huyo mwekezaji iliikiwezekana aweze kujenga mradi wa maji unaokwendaMererani na maeneo yale ya Kilimanjaro International Airportna Wilaya ya Meru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Machali aliulizaswali hapa kuhusu mradi unaotekelezwa kule Kasulu kwenyekijiji kimoja. Nitakachoweza kufanya, nitatuma wataalamuwaende kule waukague ule mradi ili watupe report yautekelezaji wa yule Mkandarasi na kama amezembea, sitasitakumwondoa na wafanyakazi kama wamezembea,wanafanya kazi kwa mazoea na wenyewe tutashirikiana naMheshimiwa Waziri Mkuu leo yuko hapa anasikia. Kama kunaMhandisi ambaye hatekelezi wajibu wake na Waziri waTAMISEMI yuko hapa tutamshughulikia haraka iwezekanavyo.Kufanya kazi kwa mazoea katika hali hii ya utekelezaji wamiradi ya maji hakutavumilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna swali la MheshimiwaSuleiman Nchambi juu ya mradi wa maji kutoka Shinyangakwenda Kishapu. Ni kweli mradi huu umeshasanifiwa na uko

Page 177: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

177

tayari kwa utekelezaji. Mradi huu ulikuwa utekelezwe pamojana miradi ya Tinde, Nzega, Tabora na miradi ile badoinasanifiwa. Mradi huu umekamilika na ninachoweza kusemani kwamba tutaendelea kuutafutia fedha na inshalahtutapata fedha ili mradi huo uweze kutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kuna swali hili la uwianowa Mijini na Vijijini. Ni kweli kwamba kwa muda mrefukumekuwa na uwekezaji mkubwa katika Miji na hivi sasakama nilivyoeleza kwenye majibu yangu hapa kwamba kunaMiji mingi ambayo miradi imekamilika, lakini pia ipo Miji mingiambayo miradi inaendelea kutekelezwa. Kwa mfano,tunatekeleza Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Singida,Tabora mpaka Kigoma; tunatekeleza mradi Bukoba, Musomana tunatekeleza miradi ya Lindi, Mtwara, Babati na maeneomengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kupanga ni kuchagua.Sasa eneo hilo nadhani tumefika mahali ambapo tunaelekeakulikamilisha na huku Mijini uwiano wa upatikanaji wa majisiyo kwa watu wanaokaa, lakini pia na viwanda, hospitalizetu na huduma nyingine muhimu ambazo na zenyewe nilazima zipatiwe maji na ni muhimu kwa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa tumefikia mahaliambapo baada ya uwekezaji unaoendelea kukamilika,upatikanaji wa maji Mijini utafikia 95% kwa Miji mikubwa, lakinibado tutakuwa na Miji Mikuu ya Wilaya, tutakuwa na Mijimidogo ambayo kwa ukweli na yenyewe ni sawasawa naVijiji. Kwa hiyo, uwekezaji katika maeneo haya pamoja naVijiji ndiyo yatakuwa makubwa katika uwekezaji wa maji naSerikali imeamua katika big results now, kwamba uwekezajikatika maji au kipaumbele katika uwekezaji wa maji kitakuwaMaji Vijijini. Kwa hiyo, tuimbeni wote “Maji Vijijini,” tupelekenimaji Vijijini, tuungane mkono ili tupitishe bajeti hii ili tupelekemaji Vijijini. Huko ndiko tunakokwenda. Ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la Mheshimiwa LekuleLaizer; katika marekebisho haya ambayo leo ndiyotunaongea juu ya marekebisho haya kwa mara ya kwanza,

Page 178: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

178

yatakapokuwa yametekelezwa, Wilaya ya Longido itakuwaimeangaliwa kwa undani sana. Kwa hiyo, namwombaMheshimiwa Lekule Laizer avute subira tu, kazi ya ukokotoajiwa miradi ambayo itatekelezwa ikikamilika, kila Mbungeatapewa nakala hiyo ili ajue miradi ambayo itakuwainatekelezwa katika Wilaya yake ni mradi gani.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika, unataka nyongezaya maelezo? Mheshimiwa Mnyika, kwanza samahani kidogo!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBUNA BUNGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kumwongezeatu Mheshimiwa Mnyika, kuomba ile Shilingi yake abaki nayoMfukoni.

Pamoja na bajeti ya Maji iliyosomwa na MheshimiwaWaziri leo kutoka kwenye Wizara, nilitaka kumkumbushaMheshimiwa Mnyika kwamba akichukua randama yaTAMISEMI, kuna fedha zimetengwa za usimamizi wa maji zaidiya Shilingi bilioni 12. Lakini ukichukua kitabu hiki chamaendeleo Mkoa kwa Mkoa, kuna fedha nyingi za maji tayariambazo zimeshapitishwa kupitia Mkondo wa TAMISEMI,kwenda kwenye Mikoa.

Kwa hiyo, akijumlisha hizi; bahati mbaya sikuwa nanafasi ya kujumlisha, lakini ukijumlisha hizi Shilingi bilioni 12 nahizi zilizopo kwenye miradi Mkoa kwa Mkoa na hizi zinazisi zileambazo mlifikiria kwamba ndiyo kiwe kiwango cha juu.

MWENYEKITI: Haya, Mheshimiwa Mnyika!

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,sijaridhika na ufafanuzi uliotolewa na nitaomba WaheshimiwaWabunge wenzangu tulijadajili hili jambo.

MWENYEKITI: Sema naondoa Shilingi tukuelewe!

MHE. JOHN J. MNYIKA: Naondoa Shilingi!

MWENYEKITI: Haya!

Page 179: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

179

MHE. JOHN J. MNYIKA: Kuna eneo moja ambaloMheshimiwa Waziri hakujibu kabisa. Kwenye ukurasa wa 88wa hotuba yake inaeleza wazi, mwaka 2012 Bunge hilililipitisha Shilingi bilioni 140 kwa ajili ya miradi ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka tunafikia mweziMachi, 2013 ikiwa imebaki miezi mitatu tu kuelekea mweziJuni ambapo ndiyo mwisho wa utekelezaji wa Serikali, fedhazilizotolewa ni Shilingi bilioni 29 peke yake, sawasawa naasilimia 20.7 peke yake. Yaani ni chini ya robo ya fedha,wakati mpaka kipindi hiki zilipaswa ziwe zimetolewa angalauasilimia 75 ya fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafsiri yake ni nini? Hatakama tukiwa na matumaini sana ya kiwango cha fedhakilichoongezwa, kama fedha hazitatolewa kwenda kwenyemiradi ya maji, hata ziongezwe kiasi gani, bado miradi yamaji haitatekelezwa kwa sababu fedha zitakuwa hazijafika.Sasa hili eneo Mheshimiwa Waziri hajasema neno lolotekwamba, sasa kuna mkakati gani wa kuhakikisha fedhazinazotengwa na Bunge kwenye miradi ya maendeleo;ukienda kwenye vifungu vya posho, utakuta fedha zimetokakwa asil imia 70, asil imia 90, lakini kwenye miradi yamaendeleo fedha zimetoka kwa asilimia 20.7. Hili ni jambozito ambalo linahitaji mjadala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwenye hili suala lanyongeza ya fedha, Mheshimiwa Waziri ni vizuri akarejeakwenye hotuba yake.

MWENYEKITI: Mheshimiwa ukitaka tukusaidie kwenyeShilingi ni hoja. Kwa hiyo, uwe precise.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Shilingi moja hii kwa masuala niliyahoji, nilihoji kiwango chafedha kilichoongezwa kwamba ni kiwango kinachofurahisha,lakini bado hakijakidhi mahitaji. Vilevile nikahoji kwamba hatahicho kidogo hakitatolewa kwa wakati, nataka commitmentkama zile fedha zinakuwa ringfenced au unatumika mkakatigani?

Page 180: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

180

Sasa kwenye hiki kiwango sisi tunazungumzia fedhaza ndani. Mheshimiwa Waziri kwenye hotuba yake ukurasawa 43, aya ya 94 ya hotuba yake kwenye program ya BigResults Now inasema kwamba ili kuweza kutafuta ufumbuziwa matatizo ya maji, fedha zinazohitajika ni Shilingi trilioni 1.45.Sasa Shilingi trillioni 1.45 kwa miaka michache iliyobaki,unaweza kujua ni kiwango gani cha fedha za ndanikinachohitajika kuweza kutimiza lengo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo ni muhimuWabunge wakatafakari kwa sababu wanazungumzia Ilaniya CCM. Ilani ya CCM ya mwaka 2005 – 2010 ilisema kwambaifikapo mwaka 2010 asilimia 65 ya wananchi Vijijini watakuwana maji, asilimia 90 ya wananchi Mijini watakuwa na maji.Mwaka 2010 umefika, I lani haijatekelezwa, asil imiahazijafikiwa. Sasa kama safari hii hatutakuwa wakalikukubaliana kwa pamoja, tuone kweli hizi fedha zinatoka nakwa kiwango kinachostahili, ni wazi hata hiyo ilani ambayommerudia tena, yaani Ilani ya 2005 – 2010 mmerudia kwenye2010 – 2015.

MWENYEKITI: Naomba uniambie mimi.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Nashukuru. NakwambiaMheshimiwa Mwenyekiti kwamba Ilani imerudia tenamalengo yale yale yaliyopaswa kutekelezwa mwaka 2010.Kwa hiyo, ninachokisema hapa ni kwamba kama hakunacommitment, naomba kutoa hoja kwamba jambo hililijadiliwe ili Serikali iweke commitment kwamba, kweli hizifedha zitatolewa na zitatolewa kwa wakati. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki!

MWENYEKITI: Eeh, sawa mnajadili. Waache wajadilikwanza, dakika tatu tatu. Mheshimiwa Ole-Sendeka,Mheshimiwa Akunaay, Mheshimiwa Nkumba na MheshimiwaMwijage.

Page 181: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

181

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: MheshimiwaMwenyekiti, kuna hoja moja ya msingi kubwa sanailiyozungumzwa na Mheshimiwa Mnyika, nayo ni kiasi chafedha kinachotolewa baada ya Bunge kupitisha bajeti.Kupanga bajeti na kupitisha kwenye Bunge ni jambo moja,lakini kutolewa kwa fedha nako ni jambo tofauti. (Makofi)

Hoja ya Mheshimiwa Mbunge ambayo natakakuiunga mkono ni vipaumbele. Mwalimu alisema Kupangani Kuchagua. Yawezekana ukapitisha bajeti kubwa, lakinimatumizi yakawa ni makubwa, zikajitokeza disastersmbalimbali na zikatumia fedha nyingi na pengine sektanyingine zikawa zinakosa fedha. Lakini kama wotetunakubaliana kwamba maji ni uhai na kwamba bila majihakuna uhai, na tunakubaliana kabisa kwamba ipo haja yakuweka kipaumbele kwenye Sekta ya Maji, nataka tukuiomba Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi, Serikali sikivu,na Mheshimiwa Mnyika namshukuru sana kwa kusoma Ilaniya Uchaguzi ya CCM japo amesoma kinyume nyume kidogo,kwamba katika mipango ya mwaka huu fedha nyingi katikakipindi cha bajeti ya mwaka uliokwisha imeelekezwa mnokwenye barabara na mitambo ya kukodi ya umeme. Safarihii elekezeni fedha nyingi kwenye maji na maji Vijijini.

Kwa hiyo, tunataka commitment ya Serikali katika hilina mimi naunga mkono pendekezo la kuhakikisha kwambaSerikali inatoa kauli ya kuhakikisha kwamba, Sekta ya Majiitapewa kipaumbele kuliko maeneo mengine ambayo ni yavipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Akunaay!

MHE. MUSTAPHA B. AKUNAAY: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja yaMheshimiwa Mnyika kwamba pamoja na kwamba bajeti yaawali ilikuwa ni Shilingi bilioni 365 na baada ya Wabunge

Page 182: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

182

kulalamika kwamba fedha hiyo haitoshi, imeongezwa mpakaShilingi bilioni mia tano na ushehe; hoja ni kwamba:-

Je, kuna uhakika gani kwamba fedha hizo zitafika auni kuondoa tu kwamba hii bajeti ipite kama ilivyotolewamfano kwamba iwapo mpaka mwaka huu mwezi wa Tatu,bajeti ya mwaka 2012 kwenye miradi imetekelezwa kwaasilimia chini ya 20? Je, bajeti hii ambayo imepita kwa ugumukiasi hiki, tuna uhakika gani kwamba fedha hizi zitafika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, issue ambayo iko mbele yetuni kuhusu uhai wa maji na kila siku tumetamka hapa kwambamaji ni uhai. Je, kwa hali hii, kweli maji ni uhai? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.

MWENYEKITI: Waziri!

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Maji ni uhai na hatuwezikuukabidhi uhai wetu kwa mtu yeyote.

Nakubaliana na hoja ya Mheshimiwa Mnyika na kwahoja hiyo napenda niipe ushauri Serikali yangu kwamba lilewazo letu la kuanzisha Mfuko wa Maji tulikazanie. Tutafutevyanzo, kama ni njia gani tutaweza kutoza tozo zozote, tuwena uhakika kwamba fedha itapatikana. Hatuwezi kuliachasuala la maji. (Makofi)

Pia niishauri Serikali yangu kwamba tuendeleekumwomba Mwenyezi Mungu, bomba la gesi lifike Dar esSalaam. Likishafika, ile saving ya fedha tunayotumia kwenyemafuta, trilioni karibu 1.6 tutakapokuwa tumefikia hapomwaka kesho mwezi Mei basi hiyo fedha yote tuiwekekwenye maji. Wasiwasi wa Mheshimiwa Mnyika kwambakipindi kimebaki kifupi, tutakwenda kwa speed kali natutaweza kumaliza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziriachukue ushauri wangu.

Page 183: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

183

MHE. JUMA S. NKUMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na kukubaliana na hoja ya Mheshimiwa Mnyika,niliomba nifanye marekebisho yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulipokuwa tunawasilishataarifa ya Kamati hapa Bungeni, takwimu alizozisemaMheshimiwa Mnyika zilikuwa zinahusiana na vikao vilivyokuwavinafanyika Dar es Salaam. Lakini tulipokuwa hapa, Serikalikwa maana ya Wizara ilikwishaingiza Shilingi za ziada nyingine,na kwa sasa Shilingi bilioni 104 ambazo ni sawa na asilimiakaribu 84, sisi kwenye Kamati tumekwisharidhika kwambazimeishakwenda katika kutekeleza shughuli hizi. Kwa hiyo, siyoile asilimia 29. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nataka kusema tukwamba pamoja na maelezo mazuri ya Mheshimiwa Mnyika,kupanga ni kuchagua kama walivyosema WaheshimiwaWabunge wenzangu; lakini nilikuwa naomba sana mambomengine yote yanahitaji mfuko mmoja tu wa Serikali na yoteni muhimu. Tunazo barabara zetu Mijini na Vijijini, umemeVijijini, Sekta ya Afya, Elimu; haya yote yanahitaji bajeti yetu.

Kwa hiyo, nilikuwa naomba sana, lazima tuanze. Yalemaombi ambayo yaliletwa na Kamati ya Shilingi bilioni 184.5ambayo Serikali imeyaridhia ni vizuri tukayaunga mkono,tukaanzia hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema kwambaSerikali ya Chama cha Mapinduzi itakuwa imesikia kilio chautofauti wa maji Vijijini na Mijini.

Maji Mijini kwa fedha hizi tunazoongeza, tumeongezaShilingi bilioni 12.1 peke yake. Lakini kwenye miradi ya Vijijinikwa fedha hizi zinazoongezwa, tumeongeza Shilingi bilioni161.7. Kwa hiyo, utaona jitihada za Serikali katika kuhakikishakwamba, sasa Sekta ya Maji maeneo ya Vijijini inapewakipaumbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, pamoja nakukubaliana na Mheshimiwa Mnyika, nilikuwa naomba tu hizi

Page 184: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

184

taarifa nazo zizingatiwe katika kuhakikisha kwamba Serikaliinafuatilia kikamilifu maelekezo ya Waheshimiwa Wabungewote hapa.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waziri wa Fedha.

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, lilealilosema Mheshimiwa Nkumba ndilo hilo nililotaka kusemakwamba, Serikali imeishatoa fedha ambayo ni juu zaidi kulikokiwango ambacho Mheshimiwa Mnyika anasema. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Maji.

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanzaniseme tu kwamba mradi wa Big Results Now utatekelezwakwa muda wa miaka mitatu. Kwa kiwango cha bajeti yamaendeleo kilichotengwa sasa, ukizidisha mara tatu unapataShilingi trilioni 1.659. Kwa hiyo, tuko kabisa njiani na kwenyekiwango cha utekelezaji wa mradi huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuunge mkonoMheshimiwa Said Nkumba na Waziri wa Fedha, kwambatangu mwezi Februari na mpaka early March, Serikali kuanziawakati ule mpaka mwisho wa mwezi Machi imepeleka Shilingibilioni 75 kwa Wizara ya Maji kwa fedha za ndani na Shilingibilioni 80 fedha za nje.

Kwa hiyo, katika utoaji wa fedha, Serikali imeendeleakutoa kama ambavyo imeahidi. Nategemea kwambampaka tufike mwisho wa mwaka wa fedha tutakuwatumepata fedha zote za maendeleo. Kwa vyovyote vile,fedha zote zinazohitajika kwa miradi ya maji Vij i j ini,zimeshatolewa kwa maana hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba baada yaMfuko wa Maji kuanzishwa, ni vizuri tuanze kufikiria vyanzovya fedha za uhakika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi yamaji. Namuunga mkono Mheshimiwa Mwijage naWaheshimiwa Wabunge wengine ambao wanapendekezajambo hili.

Page 185: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

185

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, napendekazakwamba, hoja ya Mheshimiwa Mnyika sasa ikataliwe kwasababu kila hatua iliyotaka kuchukuliwa, imechukuliwa nahakuna sababu tena ya kwenda katika hatua ile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,napata taabu kidogo kwa sababu kitabu hiki tumepewamwezi Aprili wiki iliyopita, Jumatano na ni cha MheshimiwaWaziri, na ameandika yeye mwenyewe kwenye aya ya 188ya hotuba yake kwamba: “Ilipofika mwezi Machi, mwaka2013 fedha ambazo zilikuwa zimetolewa ni Shilingi bilioni 29peke yake kati ya Shilingi bilioni 140, sawasawa na asilimia20.7.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maelezo yaliyotolewahapa, napata shida kidogo kuwa na hakika kwamba hizofedha zimetolewa kwa wakati. Lakini nilichokiomba zaidi nikwamba, tupate commitment ya Serikali kuwa hizi fedhazilizoongezwa sasa hivi, kuna mkakati wa kuhakikisha kwambazinatoka kwa wakati. Kuna baadhi ya wakati Bunge linaamuaku-ringfence baadhi ya fedha ili kuhakikisha kweli hizi fedhahazitatumika kwingine na zitatolewa kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini hii ni hoja yakawaida sana, haina sababu yoyote ya Mheshimiwa Wazirikuikataa. Kwa hiyo, nawaomba Wabunge wenzangu wapigekura kuikubali hii hoja.

MWENYEKITI: Aah, ngoja kwanza. Huo mkakati kwamfano wafanyaje? Hebu eleza vizuri hapo. Ili kukuhakikishiakabisa, wafanyaje?

MHE. JOHN J. MNYIKA: Hizi fedha ziwe ringfenced nakuwekewa kipaumbele cha kwanza katika fedha zamaendeleo.

MWENYEKITI: Waziri wa Fedha.

Page 186: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

186

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukuenafasi hii kusema kwamba Serikali inapoidhinishiwa fedha naWaheshimiwa Wabunge, inakuwa imepata mamlaka yakuzitumia katika maeneo ambayo imeomba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hali hiyo, nachukuanafasi hii kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge kwamba,fedha mnazoidhinisha zitatumika kule ambako mmeelekezana kwa kiwango ambacho mmeidhinisha.

MWENYEKITI: Haya, nitawahoji. Hakuna shida,ninawahoji tu, hakuna tatizo. Wanaosema kwamba hizi…

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa!

MWENYEKITI: Mheshimiwa ngoja kwanza tumalize.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Naomba nitoe taarifa kwa Waziriwa Fedha.

MWENYEKITI: Unajua, ngoja nisimame, wewe ukae.Ndiyo maana nakuuliza, ku-ringfence maana yake nini? Kwahiyo, haina tatizo, hii ni commitment ya Serikali. Kwa hiyo,suala kwamba mnaungana na Mheshimiwa Mnyika, ndivyowanavyofanya Serikali.

Sasa wanaosema kwamba Serikali i j ihakikishiekwamba, hizi fedha zinatumika, waseme ndiyo.

WABUNGE: Ndiyoooooo!

MWENYEKITI: Wanaosema siyo lazima kujihakikishia,waseme siyo. (Kicheko/Makofi)

Eeh, ninachojaribu kusema ni kwamba, anachosemaMheshimiwa Mnyika ndiyo maana ya bajeti. Asubuhitumesema hapa na Waziri wa Fedha hawezi kutueleza hivihivi, alete maandiko. Ameleta! Hili ni zoezi mojawapo yarinfencing. Tumekuja hapa tumesema aah, tuone kwenyevitabu, tumefanya. Kwa hiyo, anachokisema Mheshimiwa

Page 187: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

187

Mnyika ni kuongeza kwamba, jamani tuhakikishe fedhazinatolewa. Ndiyo hivyo! Kwa hiyo, mimi nadhani hakunanongwa.

Kwa hiyo, wanaosema hoja ya Mheshimiwa Mnyikaikubalike waseme ndiyo.

WABUNGE: Ndiyooooo.

MWENYEKITI: Wanaosema isikubalike.

WABUNGE: Siyooo.

MWENYEKITI: Waliokubali wameshinda.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi pamoja na marekebisho yake)

Kif. 1002 - Finance and Accounts ………..Tsh.1,383,129,000/=

MWENYEKITI: Naomba tukiwa kwenye stage hii,mjaribu kutulia ili niwaone wanaosimama. Mtaangaliakutakuwa na maandiko tofauti tofauti hapo na kuangaliaaddendum. Haya, Mheshimiwa Gekul!

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Katika hicho kifungu cha 1002 na katikamarekebisho tuliyopewa na Mheshimiwa Waziri, naombanipate ufafanuzi kuhusu fedha ambazo zimeongezwa Shilingimilioni 200. Katika fungu hili kwa ujumla zimeongezwa Sh.10,700,000,000/= na kwa specific kifungu hiki cha 1002 niShilingi milioni 200.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi fedha zinaonekanazimewekwa tu, lakini haijaoneshwa ni kasma gani ndogoambayo fedha hizi zinakwenda. Naomba Mheshimiwa Wazirianipe majibu ya kina, pamoja na kwamba ametuletea

Page 188: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

29 APRILI, 2013

188

marekebisho au ongezeko la fedha, lakini hata sasa hizi fedhawameziweka tu katika upande wa OC, haioneshi ni za usafiri,training au kitu gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama majibu hayataridhishakwa mujibu wa Kanuni ya 102 (2) nitoe hoja ya kuondoaShilingi kwa sababu hizi fedha Shilingi bilioni 10 ni nyingi.Nishauri Wabunge wenzangu tuziondoe fedha hizi tuzipelekeupande wa maendeleo badala ya kuziweka huku kwenyeOC.

MWENYEKITI: Naomba usikilize kwanza. Wewe uliza niza kazi gani? Halafu utajibiwa huwezi kenda mbele wakatinyuma hujafika. Mheshimiwa Waziri, umeliewa swali lake? Niile OC kwa ajili ya umeme. Unahitaji arudie? MheshimiwaNaibu Waziri!

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,mchanganuo wa fedha hizi Shilingi bilioni 10 unaoneshwakwenye jedwali la nyongeza ukurasa kwanza hadi ukurasawa pili na Idara ambazo zinaongezewa hizo fedha zimetajwapale ikiwemo Idara ya Utawala na Raslimali za Watu, Kitengocha Fedha na Uhasibu, Idara ya Sera na Mipango, Kitengocha Usimamizi na Ununuzi, Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani,halafu kuna Idara ya Usimamizi wa Raslimali za Maji, Idara yaHuduma za Majisafi na Uondoaji wa Majitaka Mijini, Idara yaHuduma za Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini na jumla yakeinaonesha pale kwamba ni Shilingi bilioni 10.7.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti,Naibu Waziri hakunijibu. Labda nirudie tu kwamba, nimeonawamepanga katika hizo Idara; Idara ya Sera na nyingineambazo amezitaja na jumla wakapata Sh. 10,700,000,000/=lakini katika hizo Idara kuna specific au sub votes. Kunatraining, allowances, mafuta na vitu kama hivyo.

Page 189: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

189

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupachika tu milioni 200katika Idara, haituoneshi sisi Wabunge kwamba, hizi fedhasasa zimeongezeka katika Sub-vote ipi. Ndiyo nikashaurikwamba, kwa sababu hizi fedha zinaonekana zina-hangtuzipeleke kwenye miradi ya maendeleo kuliko kupoteza hizibilioni 10,700,000,000/= wakati tu zimewekwa kwenye Idara,hazijulikani ni fedha za training au za mafuta au za kitu gani.

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, sasanimemwelewa Mheshimiwa Gekul. Fedha hizi kwa ujumlazitatumika si kwa ajili ya hiki kifungu pekee, lakini hizi shilingibilioni 10 zitatumika kwa ajili ya kulipia umeme katika miradiile mikubwa ya Taifa ambayo ni kama ule Mradi wa LakeVictoria-Shinyanga, Mradi wa Wanging’ombe, Mradi waMaswa, Mradi wa Handeni na Miji ile ambayo ipo kwenyegrade b au grade c ambayo umeme wake unalipwa naSerikali. Jumla ya shilingi bilioni 5.3 zinahitajika kwa jambohilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia haki za ajira au zinaitwastahili za ajira za wafanyakazi wa Wizara ya Maji ni shilingibil ioni 2.8. Hizi ni stahil i zao kwa mfano, kamawamepandishwa daraja na wamelipwa mshahara bilakulipwa arrears tangu siku ya kupandishwa au kila baada yamwaka mmoja wanapokwenda likizo wanalipiwa gharamaza kwenda likizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia na gharama zakuendesha Chuo cha Maji ambazo kila mwaka ni shilingibilioni 0.9 na fedha za kulipia mikataba ya Kimataifa ambayoWizara ya Maji inashirikiana kwa mfano, kama Nile BasinInitiative, kama Lake Victoria Equatorial Lakes na dhamanazingine za Kimataifa ambazo Serikali imeingia mikataba.Halafu pango la nyumba hapa Dodoma, gharama zakuendeshea ofisi na gharama za usimamizi wa miradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tutatenga fedha yamiradi peke yake, bila kuweza kwenda na kuhakikishakwamba inatekeleza, haiwezekani tukawa na uhakikakwamba kweli utekelezaji utakwenda kama tunavyofikiria.

Page 190: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

190

29 APRILI, 2013

MWENYEKITI: Naomba usome Addendum hii.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1003 – Policy and Planning... ... ... ... Sh. 2,320,332,000/=

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naulizia kifungu hicho kasma 270600 Current Grants to Non-Financial Public Agencies ambacho mwaka wa fedhauliopita kilikuwa billioni 1.9 na mwaka huu kimeshuka mpakashilingi bilioni 1.5. Hii ni kasma inayohusu kuiwezesha Taasisiya Uendelezaji Maji kwa maana ya Chuo cha Maji paleRwegarulila na kuwezesha wakala wa uchimbaji visima DDCAkwa ajili ya uchimbaji wa Visima.

Sasa ningependa kupata ufafanuzi kwa sababukiwango kinaonesha hapa kimeshuka, lakini kwenyeaddendum tuliyopewa kuna nyongeza ya kifungu cha 1003,Idara ya Sera na Mipango kwa ujumla wake imeongezewashilingi bilioni 1.2. Naomba kupata ufafanuzi iwapo hizi bilioni1.2 zimeelekezwa kwenye matumizi ya hicho Chuo cha Majipamoja na Wakala wa kwenda kuchimba visima auzimeelekezwa kwenye hivi vifungu vingine vya posho namatumizi mengine. Kwa hiyo, nahitaji commitment kwamba,zielekezwe pale ambapo zitakwenda kweli kusaidia hudumaya maji.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikweli kifungu hiki kwa mwaka 2012/2013, kilitumika kwa ajiliya kuendesha shughuli za DDCA yaani Wakala wa UchimbajiVisima na Ujenzi wa Mabwawa pamoja na Chuo cha Maji.Lakini mwaka huu DDCA wana kasma yake, kwa hiyo, hizifedha zilikuwa ni kwa ajili Chuo cha Maji na zilikuwazimepungua kwa sababu ya ufinyu wa bajeti. Sasa baadaya kuongezewa hizo fedha zingine ndiyo maanazimeonekana kwenye hii sehemu ya Mipango, Policy andPlanning kwamba kuna fedha za nyongeza ambazo zitakujatena kwenye shughuli hizi.

Page 191: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

191

29 APRILI, 2013

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1004 – Government Communication Unit ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... Sh. 160,010,944/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1005 – Legal Services Unit ... ... ... ... ... Sh. 224,033,008/=

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMED: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Naulizia item 221100, Travel out ofcountry ndani ya miaka miwili haikuwekewa fedha. Lakininashangaa kwamba safari hii imeweka milioni 1.5. Natakakujua hii safari ya nje ya milioni 1.5 ni safari gani?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,safari zote za nje zimekuwa centralized zipo kwenye kasmaya utawala. Hii milioni moja nadhani ni vitu vidogo vidogovya maandalizi kwenye hiyo Idara. Lakini sehemu kubwa yafedha zipo kwenye kasma ya Utawala ambayo tayaritumeshaipitisha.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1006 - Procurement Management Unit... ... ... ... ... ... ... ... ... ... Sh. 1,215,078,856/=

MHE. ESTER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Kwenye sub-vote 1006 ProcurementManagement Unit item 220800 Training domestic. Kwenyecolumn hiyo ya mwaka huu wa fedha hawajaweka figure ilaimeandika Mate of the na ukijaribu ku-totalize hizo unakutakwamba unapata jumla pamoja na nyongeza ya sasa nishilingi bilioni 1,211,078,856 inakuwa na pungufu na total aliyo-indicate hapa.

Page 192: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

192

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka kujua kwenyehiyo row ya Training domestic, hiyo mate of the ni amountgani ipo hapo. Kwa sababu ukijumlisha pia hiyo figureiliyotajwa kama jumla yake siyo sahihi.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kulikuwa na typing error hapo ni milioni nne.

MWENYEKITI: Wapi, kwenye mate of the. Tumiamicrophone.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimilioni nne pale palipoandikwa mate of the.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1007 – Management Information System ... ... ... ... ... ... ... ... ...Sh. 209,762,043/=

MHE. ESTER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Kwenye sub-vote 1007 sub- item 221000 Travel incountry ukisoma kwenye hiyo row kuna maneno na figureszimetolewa, inawezekana na typing error. Lakini kuna figureya 22,986,893, lakini pia nilivyojaribu kujumlisha zote na hiyomilioni 22, bado nilikuta kwamba figure ambayo wameitoaya mwisho ni tofauti. Ukijumlisha hapo pote unapata22,298,336. Sasa utaona kwamba, figure iliyowekwa hapo nipungufu na figure halisia ukijumlisha hizo items zote.

MWENYEKITI: Mmeiona hiyo. Umekiona kifunguanachosema travel in country, kuna maneno halafu nahesabu ndogo pale. Sasa according to her anasema hiihesabu ni ipi mbona huku kwenye total haifiki. Sub-vote 1007,lakini item 221000 pale kuna maneno maneno tu, Travel incountry.

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,tumejumlisha sana, hii discrepancies sijaiona.

Page 193: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

193

29 APRILI, 2013

MWENYEKITI: Hebu soma vizuri. Kuna maneno entAnd Pla 22,986,893, mmeiona lakini.

NAIBU WAZIRI MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ukijumlisha total inafika kwa sababu kuna 89, ukija 22, ukija50, ukija 30 inafika kwenye hiyo 200.

MWENYEKITI: 209?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Ndiyo 209.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1008 – Internal Audit Unit... ... ... ... ... Sh. 598,310,812/=

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nipatiwe ufafanuzi kwenye kasma ndogo ya otheroperating expenses, zimeongezeka kwa asilimia...

MWENYEKITI: Hebu taja item number.

MHE. PAULINE P. GEKUL: 229900. Zimeongezeka kutoka21,150,000 hadi 60,000,000, naomba nipate ufafanuzi kwa ninifedha hizo zimeongezeka kwa asilimia hizo?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kifungu cha other operating expenses ni kifungukinachoshughulikia shughuli kama za mazishi na shughuli zaushauri mbalimbali. Sasa mwaka uliopita kulikuwa namadeni, kwa hiyo kimeongezeka ili kiweza kulipa hayomadeni.

MHE. CHARLES P. J. MWIJAGE: MheshimiwaMwenyekiti, kwenye kifungu kizima, concern yangu ni kiasicha pesa nataka kujua kama Audit imezingatia ongezekola pesa. Kwa sababu concern yangu ni kwamba, hawa watuwa Audit wata-cover kazi ambazo tuna mashaka nazozilizopo kwenye Halmashauri zetu.

Page 194: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

194

29 APRILI, 2013

MWENYEKITI: Tafadhali, nenda kwenye item halafututakuelewa vizuri zaidi.

MHE. CHARLES P. J. MWIJAGE: MheshimiwaMwenyekiti, nitakuongoza twende 410700, kwa sababukwenye feasibility studies ndiyo mambo yanaharibikia hapo,ime-consider miradi mipya ambayo wataiongeza.

MWENYEKITI: Mmeiona hiyo?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ndiyo. Hii ni ya kuandaa miradi mbalimbali, makabrasha,documents mbalimbali za Idara. Kwa vyovyote vile fedhazilizoongezeka zitaongezeka kwenye kifungu hiki kwa sababukazi zitakuwa zimeongezeka.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 2001 - Water Resources Assessment and Exploration... ... ... ... ... ..Sh. 5,907,104,956/=

Kif. 2002 - Central Stores... ... ... ... ... ... ...Sh. 199,391,000/=Kif. 2003 – Water Laboratory ... ... ... ... .Sh. 2,041,429,048/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 3001 – Urban Water Supply and Sewerage ... ... ... ... ... Sh. 5,650,567,000/=

MHE. SUSAN L.A. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Sub-vote 3001, kifungu kidogo cha 229900 ionDepartment expenses yaani miaka yote iliyopita, kwa mfano,mwaka wa mwanzo kabisa ule ilikuwa milioni 1.9, unaofuatamilioni tano, lakini mwaka huu 61,508,000, kwa nini tofautiimepanda namna hiyo, kuna nini hapo?

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kifunguhiki kimeongezewa fedha katika nyongeza mpya. Kablakilikuwa na shilingi bilioni 1.6 kimeongezewa bilioni nne na

Page 195: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

195

29 APRILI, 2013

sasa kimekuwa bilioni 5. 6. Lakini ukiangalia trend ya kifunguhiki utakuta ilikuwa inashuka kutoka bilioni 2.7 mwaka wafedha unaokwisha kwenda bilioni 1.6.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo kubwa ambalo lilikuwalinatengewa fedha nyingi katika kifungu hiki ni basic salariesand Pensionable Posts ambapo imeshuka kutoka bilioni 2.4mpaka bilioni 1.2. Sasa nyongeza hii na hii ni Idara ya hudumaya maji safi na uondoaji wa maji taka Mijini. Nyongeza hii yabilioni nne inakwenda wapi, wanaajiri watu wapya,wanastaafu watu wapya na kama iliwekwa tu bila kuangaliahivyo, kwa nini sasa fedha zote hizi zisiende kuongezwakwenye maji vijijini ili ku-boost bajeti ile ya maji vijijini?

Swali hapa ni zile ulizouliza kwanza basi.

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katikamwaka huu...

MWENYEKITI: Bado tuna Mheshimiwa Mbunge mmoja.Mheshimiwa Felister Bura samahani!

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwenye sub-vote hiyo hiyo 3001, item namba 220200, Utilities,Supplies and services mwaka huu wa fedha walitengewamilioni 60, lakini mwaka ujao wa fedha kuna zero zero.Naomba Maelezo.

MWENYEKITI: Nina wasiwasi ni typing errors ausomething. Waheshimiwa Mawaziri mnaweza kuanza kujibuwa kwanza mpaka wa tatu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hiiutilities inachukuliwa na sehemu kubwa kwenye fungu lautawala kwa ajili ya kulipa gharama za simu, umeme na vituvingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye hii kasmaya 229900 kwamba kwa nini zimeongezeka kutoka milionitano mpaka milioni 61, Department expenses kama

Page 196: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

196

29 APRILI, 2013

nilivyoainisha ni kwamba, kwenye Idara kunakuwa nashughuli mbalimbali ambazo hizo services huwa wanazipatawakati mwingine bila kulipa. Kwa hiyo, kuna madeni na ndiyohiyo wameongeza ili waweze kulipa hayo madeni kwamwaka huu.

MWENYEKITI: Li le la Mheshimiwa Zitto, helazimesambazwa wapi?

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ningependa nimjibu Kabwe Zubeir Zitto kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka huu tutaanzisha Ofisiza Kanda, kwa hiyo, tutaajiri wafanyakazi wapya il ikuhakikisha kwamba usimamizi kule kwenye Wilaya unakujaharaka na Wilaya ambazo hazina Wahandisi zinapatamsaada wa kuandaa miradi haraka ili iweze kutekelezwakama ambavyo tumepanga, ndiyo maana kasma hiiimeongezewa fedha.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 4001 – Rural Water Supply ... ... ... ... .Sh. 4,012,567,332/=

MWENYEKITI: Lazima fedha zisomwe kwanza ndiyomnasimama, hata mkisimama kabla ya hapo no way.Mheshimiwa Riziki!

MHE. RIZIKI OMAR JUMA Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kupata ufafanuzi kidogo kwenye kifungu kidogo cha229900, other operating expenses, mwaka uliopita walikuwawametengewa 2,500,000. Safari hii ongezeko kubwa sanamilioni 34,750,000 naomba ufafanuzi.

MWENYEKITI: Naomba muwe mna-note. MheshimiwaParesso!

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante limeshaulizwa.

Page 197: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

197

29 APRILI, 2013

MWENYEKITI: Mheshimiwa Betty Machangu.

MHE. BETTY E. MACHANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante, limeshaulizwa.

MHE. ALPHAXARD K.N. LUGOLA: MheshimiwaMwenyekiti, niko kwenye kifungu kidogo cha 210100 kwenyeBasic Salaries and Pensionable Posts.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona nitafute ufafanuzikwenye kifungu hiki kwa sababu kinahusiana kabisa na sualala Rural Water Supply na kilio kikubwa cha Wabunge ni MajiVijijini.

MWENYEKITI: Ahaa! Mheshimiwa Lugola hii inahusianana Basic Salaries and Pensionable Posts, basi. Kwa hiyo, huwezikuuliza chochote kingine zaidi ya hapo, tafadhali. Hukutumeondoka kwenye mshahara wa Waziri, kwa hiyo, huwezikuuliza tu kwa sababu hiyo.

MHE. JENISTA J. MHAGAMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Niko kile kifungu 410700, Feasibility StudiesProject Preparation and Design.

Mheshimiwa Mwenyekiti, fungu hili ndio linahusika naRural Water Supply usambazaji wa Maji Vijijini na kifungu hichokidogo ndicho chenye wataalam wetu ambao wanatusaidiakusimamia upembuzi yakinifu na maandalizi ya miradi yoteya Maji Vijijini. Kwenye marekebisho hapa tunaona kwamba,Kurugenzi hii imeongezewa karibu shilingi bilioni nne.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kujua kitu kimoja,katika kifungu hiki, fedha iliyotengwa ni sh. 15,000,000/= tukwa hao wataalam ambao watakwenda kutayarisha hiyomipango yote ya miradi ya Maji Vijijini. Sasa fedha hiiMheshimiwa Waziri naomba akubaliane na mimi, kwenyefungu hilo dogo kwa fedha hii nyingi tuliyoiongeza iende naeneo hilo ili kuondoa matatizo ya ucheleweshaji ya mipango

Page 198: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

198

29 APRILI, 2013

ya miradi ya Maji Vijijini kama yanayovikuta vijiji vyotevikiwemo vijiji vyangu kule vya Igawisenga, Maweso nakwingineko.

MWENYEKITI: Hapana swali lenyewe unataka kuulizahiki kifungu kimeongezewa, sio tena wewe useme, maanayake laah!

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,swali langu limeulizwa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, naona maswali nimawili tu mtu wa kwanza na huyu wa mwisho.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hikikifungu, Other Operating Expenses. Idara hii ya Maji Vijijinitulishaanza kuiangalia kwamba tuiwekee fedha kwa wingi ilikuweza kusimamia miradi vizuri na ndiyo maana hizi fedhazikawa zimeongezeka kwa sababu lazima kuiangalia miradiyote katika Halmashauri zote na kuona hatua zake ilizofikiwa.Kwa hizi fedha ambazo zitakuwa zimeongezeka nazotutaongeza tena hapa ili tuweze kusimamia vizuri hii miradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hii Feasibility StudiesProject Preparations and Design, kwanza nakubali kwamba,katika fedha zilizoongezwa kama alivyosema MheshimiwaJenista Mhagama tutaongeza, lakini lengo kubwa la hapavile vile ni kuandaa documents mbalimbali za miradi hii katikangazi ya kiofisi.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 4002 - Water Sector Program Coordination Unit... ... ... ... ... ... Sh.196,758,000/=

Kif. 5001 - Water Development and Management Inst. ... ... ... ... ... Sh. 213,255,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 199: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

199

29 APRILI, 2013

Kif. 6001 - Drilling and Dam Construction Agency... ... ... ... ... ... ... ... ... Sh. 659,429,000/=

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: MheshimiwaMwenyekiti, nataka kufahamu au kupata ufafanuzi. Katikakifungu hiki inaonesha kwamba, fedha hizi zimetengwa kwaajili ya mishahara tu. Je, Kitengo hiki cha Drilling and Damhakina kazi zozote inayofanya?

MWENYEKITI: Mmeona hiyo kitu?

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hiki niKitengo kipya cha DDCA, ndio kimeanzishwa. Pamoja nafedha zil izoandikwa hapa chenyewe kinajiendeshakibiashara, kwa hiyo sehemu ya mapato yake yatatumikakwa kuendesha shughuli zake.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

MIPANGO YA MAENDELEO

Fungu 49 – Wizara ya Maji

Kif. 1001 – Administration and Management... ... ... ... ... ... Sh. 5,835,000,000/=

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru niko kwenye kifungu hicho cha 1001, kasma 3308,Water Sector Institutional Strengthening. Kifungu hiki mwakahuu wa fedha kinaombewa jumla ya shilingi bilioni 5.8, katiya hizo shilingi bilioni 3.5 zikiwa ni fedha za ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba ufafanuzi kuhusuhizi fedha za ndani. Kwa sababu naelewa katika hizi shilingibilioni 3.5 kati ya hizi fedha shilingi bilioni tatu ni kwa ajili yakuanza ujenzi wa jengo la Wizara. Shilingi bilioni tatu kwakule ambako wanachimba kisima kwa wastani wa shilingimilioni 30 kwa kisima kimoja ni sawa sawa na visima 100.Maana yake ni fedha za kuchimba visima vingi kweli kweli.

Page 200: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

200

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kupataufafanuzi sababu ya Wizara katika mazingira kama hayaambapo tunakimbizana idadi ya vijiji, ni kwa nini hizi shilingibilioni tatu za kujenga Ofisi ya Wizara zisingeondolewakwenye kujenga Ofisi ya Wizara, yenyewe ikasubiri na fedhahizi zikapelekwa kwenye miradi ya maji na kwa maana yakwenda kuchimba visima vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, iwapo ufafanuzihautaniridhisha, kwa nini hasa tutenge shilingi bilioni tatunitaomba nitumie kanuni ya 102 kutoa hoja ya kuwezakuhamisha hizi fedha kutoka kwenye kifungu hiki cha kujengaOfisi ya Wizara na kuzielekeza kwenda kuchimba visima katikavijiji mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ufafanuzi.

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yaMaji haiko yenyewe, inafanya kazi na jamii pamoja na Serikalikwa ujumla. Pale Wizara ya Maji ilipo pamepimwa kwa ajiliya kujenga flyover ya ule mradi wa Mabasi ya Mwendo wakasi na kuondoa msongamano wa magari pale Ubungo. Kwahiyo, Wizara ya Maji lazima iondoke, iandae Ofisi mahalipengine na kulingana na fedha za kodi za pango zilivyo sasa,ni rahisi zaidi kwa Serikali in the long time itenge fedha ijengemahali pengine pa kukaa, badala ya kwenda kupanga.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kutoa hoja kwa kutumia kanuni 102 kuhamishashilingi bilioni tatu kutoka kwenye kasma hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mbunge wa Jimbola Ubungo na naelewa kwamba flyover inajengwa pale,naelewa kipande ambacho kitachukuliwa na flyover nanaelewa kwamba Wizara ya Maji katika lile eneo ina ofisimbalimbali. Kuna Ofisi za Wakala wa Visima, kuna Ofisi yaChuo cha Maji, kuna ofisi za miradi na kuna ofisi za Wizarayenyewe. Naamini kabisa na kwa ujenzi wa mradiunavyoendelea tukiamua kuacha kutenga hizi shilingi bilioni3 safari hii Ofisi ya Wizara ya Maji itaendelea kufanya kazi.

Page 201: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

201

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa kuwa tuna tatizohapa la visima, tuna tatizo la maji na tuna tatizo la fedhakwa ajili ya wananchi kupata huduma ya maji ningeombaWabunge wenzangu tukubaliane kwamba, nitoe hoja ilifedha hizi zihamishwe kutoka kwenye hiki kifungu cha 1001zipelekwe kwenye kifungu cha 4001, Rural Water Supply andSanitation kwenye mradi ule wa 3216, Mradi wa Kupanua naKukarabati Miradi ya Maji Vijijini ambayo inaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Miradi hii imesambaakwenye Halmashauri nyingi ikiwemo baadhi ya hiyo miradiiko ndani ya Jimbo la Ubungo lenyewe maeneo yapembezoni kama ya Goba, Msumi, lakini kwenye kilaHalmashauri hapa nchini kuna hilo tatizo la kwamba kunamiradi inaendelea lakini haijakamilika. Kwa hiyo, tuzichukuehizi shilingi bilioni tatu ziende kule, zikaongeze idadi ya vijijiambavyo vitachimbiwa visima badala ya kwenda kujengaOfisi ya Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini Wabunge wa CCMwataunga mkono hili jambo kwa sababu Serikali hii ilisema...

MWENYEKITI: Achana na Wabunge.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Kwa sababu Serikali hii ilisemaitahamia Dodoma, sasa ni kwa nini kuendelea kujengamajengo ya Wizara Dar es Salaam wakati ambapo Serikaliilisema inahamia Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba kutoahoja kwamba, kifungu hiki kihamishwe, kipelekwe kwenyekifungu nilichokisema.

MWENYEKITI: Na mwaka gani wajenge ofisi?

MHE. JOHN J. MNYIKA: Waanze kujenga ofisi kuanziamwaka wa fedha unaofuata.

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, labdaingekuwa rahisi kuelewa kwamba, kama itabidi tusianze

Page 202: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

202

29 APRILI, 2013

ujenzi sasa kila mwaka itabidi tulipe shilingi bilioni moja nanusu mpaka bilioni mbili kwa ajili ya malipo mpaka hapotutakapokuwa na mahali pa kukaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo...

MWENYEKITI: Shilingi bilioni moja unalipa kwa nini?

WAZIRI WA MAJI: Kwa ajili ya pango.

MWENYEKITI: Rent.

WAZIRI WA MAJI: Ndiyo. Anachosema MheshimiwaMnyika kwamba yeye anajua, kwa bahati mbayaMheshimiwa Mnyika hatoki Wizara ya Ujenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeletewa michoro,inalazimu tuondoke pale. Naomba Waheshimiwa Wabungewakatae hoja ya Mheshimiwa Mnyika kwa sababu...

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kukataliwa)

(Hoja ya Mheshimiwa Mnyika ya kuondoa fedha zaujenzi wa Ofisi ya Wizara ya Maji na kupeleka katika

Miradi ya Maji Vijijini ilikataliwa na Bunge)

MWENYEKITI: Jamani Maji Vijijini ni Maji Vijijini, lakinitukianza kutafuta Maji Vijijini wala tusile na tusinywe, basi tenaMaji Vijijini litakuwa tatizo.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1003 – Policy and Planning... ... ... ... Sh. 20,114,100,000/=

MHE. ALPHAXARD K.N. LUGOLA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba ufafanuzi kwenye kifungu kidogo cha3436, kinachohusiana na Monitoring and Coordination ofWSDP. Kuna shilingi bilioni 11,257,000,000/=.

Page 203: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

203

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ufafanuzi hapokwa sababu juzi juzi hapa tumepitisha fedha za kufuatiliamiradi ambapo tulisema tuanzishe Presidential DeliveryBureau kwenye Ofisi ya Rais. Sasa na hapa naona kuna shilingibilioni nyingi sana ambazo zimetengwa kwa ajili ya ufuatiliaji.Mimi niliomba fedha za maji...

MWENYEKITI: Ahaa! Unaharibu hoja yako. Kwa ninisasa na hapa zimetengwa, basi.

MHE. ALPHAXARD K. N. LUGOLA: Sawa, kwa ninizimetengwa? Naomba maelezo vinginevyo hapa nitaondoashilingi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, tunaombamtusaidie kujibu hapo. Mheshimiwa Waziri, mna hojamnatakiwa kujibu hapa.

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi yafedha zile za PEMADU sio kukagua miradi ya maji ina kazi zakezingine na zilielezwa wakati wa mjadala wa bajeti ile. Fedhahizi tunazotenga hapa ni kwa ajili ya ufuatiliaji na ukaguzi wamiradi ya maji.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 2001 - Water Resource Assessment and Exploration... ... ... ... ... ..Sh. 19,465,143,000/=

Kif. 2003 - Water Laboratory... ... ... ... ... Sh. 4,483,000,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 3001 - Urban Water Supply and Sewerage... ... ... ... ... ... ... Sh. 266,196,615,000/=

MHE. IDDI M. AZZAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, katikakifungu hicho 3001 kuna mradi namba 3438, ujenzi wa Bwawala Kidunda. Zimetengwa hapa shilingi bilioni sita, jumla; shilingi

Page 204: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

204

29 APRILI, 2013

bilioni tatu za ndani na shilingi bilioni tatu za nje kwa ajili ujenzihuo. Napenda kufahamu kwa sababu ili Dar es Salaam iwesalama kwa maji na tupate maji ya kutosha ni lazima tuwena bwawa hili la Kidunda na kuna mgogoro mkubwa sanawa wananchi wa Kidunda kuhusu fidia kabla mradi huuhaujaanza. Nataka kufahamu wananchi wa Kidunda tayariwameshalipwa fidia ili mradi huu uweze kuanza?

MWENYEKITI: Mwambie watalipwa fidia. Naomba m-note maswali wanayoulizwa.

MHE. DKT. FESTUS B. LIMBU: Mheshimiwa Mwenyekiti,niko kwenye sub-vote 3001, item 3306, Rehabilitation andExpansion of Urban Water Supply. Nauliza, hizi fedhazilizotengwa hapa shilingi bilioni 86,656,615,000 ndiozitakazojenga maji pale Magu au ni fungu linalofuata la sub-vote 4001? Ahsante?

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kifungu hicho hicho, kasma 3437 DWSSP.

MWENYEKITI: Aliuliza mwenzio, hajajibiwa.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Ni kifungu tofauti aliulizaKidunda.

MWENYEKITI: Ahaa 3437, kimeshaulizwa.

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Nitajielekeza kwenye item 3307, Expansion ofUrbarn Water Supply. Naona kuna fedha nyingi tu ambazozimetengwa, jambo ambalo ni zuri.

Nina swali moja kwa Mheshimiwa Waziri. MheshimiwaWaziri upo tayari kuweza kutueleza kwamba ni miji ganiambayo fedha hizi zimekusudiwa kwenda kufanya kazi?

MWENYEKITI: Nimempata anasema ni UN Habitant

Page 205: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

205

29 APRILI, 2013

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nyongeza ya hizi fedha ambazo zimepatikana baada yamajadiliano kati ya Wabunge na Serikali inaonesha kwambamradi Na. 3307 kukarabati na kupanua miradi ya Maji Mijinichini ya WSDP imeongezewa shilingi bilioni nane nakuipelekea kuwa na shilingi bilioni 62.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda MheshimiwaWaziri anifafanulie kwamba, ni sawa kweli kuongeza hapaau fedha hii ingeweza kwenda kwenye sub-vote inayofuataya vijijini, kwa sababu already mijini kuna fedha nyingi sanaambazo zimetengwa?

MWENYEKITI: Naomba ujibu swali la MheshimiwaMachali, la Mheshimiwa Zitto ni hilo hilo katika sub-vote hiyohiyo. Mheshimiwa Mnyika tayari umeshauliza. MheshimiwaWaziri niliokuwa nao wamemalizika, naomba uwajibuMheshimiwa Iddi Azzan, Mheshimiwa Dkt. Limbu naMheshimiwa Machali.

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanzaningependa nijibu swali la Mheshimiwa Iddi Mohamed Azzan,Mbunge wa Kinondoni juu ya suala la bwawa la Kidunda.Tunaelewa kwamba, kuna mgogoro wa kulipa fidia kuleKidunda, lakini fedha kwa ajili ya kulipa wananchi wa Kidundazimeshatengwa na zimepelekwa ili wananchi hao walipwemwezi huu unaoanza kesho kutwa. Kwa hiyo, hiyo ni hatuaya kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hapa pia kunawananchi ambao watahitaji kulipwa wakati wa kujengabarabara inayounganisha bwawa la Kidunda na barabarakuu. Fedha hizi zimetengwa pia katika bajeti hii inayokujaambayo tunapitisha na ndizo hizo ambazo zipo hapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Dkt. Limbu ameulizakwamba, fedha za Magu ziko wapi. Fedha za Magu zikokwenye kasma 3306. Nataka nimhakikishie MheshimiwaLimbu kwamba mradi wa Magu uko pamoja katika Mradi

Page 206: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

206

29 APRILI, 2013

wa Magu, Lamadi, Misungwi na Mwanza na kwa ajili yakuondoa majitaka, mradi wa Mwanza, Bukoba na Musoma.

MWENYEKITI: Bado swali lingine la MheshimiwaMachali.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hilila Mheshimiwa Machali kwamba, ni miji gani, kamaalivyosema Mheshimiwa Waziri katika hotuba yake kwambatutaiainisha na tutaleta kwa ajili ya Wabunge kujiridhishakwamba ni miji gani itakayokuwa imepewa fedha kutokakwenye kasma hii.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 4001 - Rural Water Supply... ... ... ... Sh. 237,149,362,000/=

SPIKA: Ngoja niwaandikeni, Mheshimiwa John Cheyo,Mheshimiwa Zitto, Mheshimiwa Mbowe, Mheshimiwa Rajabna Mheshimiwa Muhagama.

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi kidogo nimuulize Waziri jambomoja la msingi sana. Katika mchango wangu wa msinginilizungumzia...

SPIKA: Kiongozi wa Kambi ya Upinzani tuko kwenyeKamati ya Matumizi, kwa hiyo tunaomba uwe very specific.

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Nakwenda katika sub-vote 4001, katika mradi 3216 kupanua na kukarabati miradiya maji vijijini ambayo inaendelea. Pia katika michangoyangu huko awali nilizungumzia maafa yanayopatikanaJimboni langu katika Vijiji vya Zarau na Mtakuja ambako majiyaliyoko sasa hivi yalipimwa na kujulikana yana sumu kwamaana ya fluoride na maafa haya yamesababisha watotokulemaa, kwa kupinda miguu na mifupa. Je, katika hili funguambalo limeongezewa Mheshimiwa Waziri anatoa

Page 207: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

207

29 APRILI, 2013

commitment gani kwa wananchi wa Vijiji vya Mtakuja,Tindigani, Zarau na Sanya Station kuwa vijiji hivi vitakuwakatika fungu hili?

SPIKA: Hatuulizi swali namna hiyo. Tunauliza hizi helakatika kifungu ulichosema ni za kufanyia nini? Je, hayomambo yako humo? Basi. Mheshimiwa John Cheyo!

MHE. JOHN M. CHEYO: Mheshimiwa Spika, 3223Borehole Drilling hii pia imeongezewa fedha karibu bilioni24. Sasa nauliza kusambaza maji ya Bwawa la Nkomaambalo limekaa zaidi ya miaka 13, je, baadhi ya fedhazitatatumika kutoka hapa?

MHE.ROSE K. SUKUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa fursa. Naomba nizungumzie sub-vote4001, item 3341 inahusu ujenzi wa Same–Mwanga-Korogwe.Ninachoomba ni Waziri atoe ufafanuzi ambao kwa kwelinitauelewa kwamba, ujenzi wa Same- Mwanga – Korogwekwa awamu kwa mara ya kwanza alisema ni bilioni 56.1,fedha ambazo wachangiaji wake ni OPEC ambao wametoaUSD mil ioni 12 na BADEA USD mil ioni 10 na Serikali20,900,000,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ufafanuzi utoleweambao utaeleweka kwa Wabunge kwamba hizi fedha zaOPEC ziko wapi kwa sababu hazionekani kwenye hiki kitabu,zinazoonekana ni za BADEA ambazo ni 11,400,000 na bilioni20,900,000,000 ya Serikali. Sasa hebu tuambieni mmewekawapi hizo za OPEC na Mheshimiwa Waziri mwenyeweamezungumza hapa kuwa tayari mmesainiana na wenzetuwa OPEC kuhusu uchangiaji wa Dola milioni 12 ambayo nikama bilioni kumi na tisa na point. Wakati wameshatangazakwenye gazeti la tarehe 24 kwa ajili ya kufanya tenda.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante, hiyo kengele umepigiwa wewe.Mheshimiwa Rajab!

Page 208: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

208

29 APRILI, 2013

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED: MheshimiwaMwenyekiti, japokuwa kifungu hiki tayari kilishatajwa, lakininakwenda katika maeneo mengine.

SPIKA: Taja, tukusikie.

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED: MheshimiwaMwenyekiti, 3223, nataka kujua fedha hizi zilizotengwa ni zilezile fedha ambazo itapewa ile agency mpya?

SPIKA: Naomba ukae, Kanuni hairuhusu hatujibuhicho. Mwingine ni nani, Mheshimiwa Kamili tayari,Mheshimiwa Mbowe tayari, Mheshimiwa Cheyo tayari. Sasanamwita Mheshimiwa Zitto kwanza.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kasmahiyo hiyo, kifungu 3280, Maji Vijijini na Usafi wa Mazingiraambacho kimeongezewa shilingi bilioni 118, napendaMheshimiwa Waziri anifafanulie katika fedha hizi ndiyo nafedha za Mradi wa Kijiji cha Mwandiga zimo?

MHE.MURTAZA A. MANGUNGU: MheshimiwaMwenyekiti, swali ambalo niliuliza lilikuwa ni kifungu namba3216 na tayari lilishaulizwa, kwa hiyo, ninazingatia Kanuni.

MHE.JENISTA J. MHAGAMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Niko kwenye ile sub- vote 3216 ambayo ni kwafedha zilizoongezwa leo...

SPIKA: Limeshaulizwa hilo, Mheshimiwa Waziri majibu!

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nitoe ufafanuzi kuhusu huu mradi wa Same -Mwanga – Korogwe. Kama tulivyosema kwenye maelezoyetu kwamba, mradi unagharimu dola milioni 56.1,zimetengwa bilioni 32 na Serikali yetu inatakiwa ichangie dolamilioni 34. Sasa ule mradi umegawanywa katika loti tatu nahizo loti tatu ndizo zinazochukua hizo fedha bilioni 32 kwakazi zinazoanza sasa hivi.

Page 209: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

209

29 APRILI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi kutoa fedha zote,fedha zinatengwa kulingana na kazi zinazofanyika. Mradiumepangwa kujengwa kwa miezi 18, kwa hiyo, hata hizozingine ambazo anasema zipo, zitaingizwa kwenye vifunguhapa kulingana na kazi ambazo zitakuwa zimepangwa kwamwaka huo unaokuja.

SPIKA: Kuna lingine, Mheshimiwa Waziri wa Maji!

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanzanimjibu mtani wangu hapa anasema swali la msingi na mimininamjibu jibu la msingi, ni mtani wangu huyu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilieleza wakati namjibuMheshimiwa Ole-Sendeka kuhusu azma yetu ya kuangaliakama eneo lile ambalo lina maji hayo mabaya linawezakupatiwa maji kutoka Mlima Kilimanjaro au Mlima Meru kwaajili ya maeneo yale ambayo tatizo hili la fluoride ni kubwasana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayotumeanzisha Kituo cha Utafiti pale Ngurdoto na hivi sasawana test membrane ambazo zina filter fluoride katikamolecule zile ambazo zinapatikana eneo lile na inaelekeakuwa kazi hiyo inaonesha matumaini. Labda baada ya miezimiwili au mitatu, tunaweza kutoa matokeo ya kazi hiyo kwaundani zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Bwawa la Nkoma,lipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vijiji ambavyo vikokwenye hiyo Miradi ya Vijiji vya Kutoa Matokeo ya Harakasinavyo hapa, isipokuwa niseme jambo moja; kwanza vijijivyote vilivyokuwa kwenye Miradi ya Vijiji Kumi vyote kamaMwandiga ipo for sure na yenyewe iko hapo na itatekelezwa.Utekelezaji huu utahusu pia vijiji vingine ambavyo vitagawiwashilingi bilioni 53.3 kwa uwiano ambao ni wa kawaidaunaofuatwa. Nashukuru sana.

Page 210: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

210

29 APRILI, 2013

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Bunge zima bila mabadiliko yoyote)

(Bunge lilirudia)

T A A R I F A

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kutoataarifa kuwa, Kamati ya matumizi baada ya kujadili taarifaya Makadirio na matumizi ya fedha ya Wizara yangu kwamwaka 2013/2014, kifungu kwa kifungu na kukubali nyongezailiyopendekezwa, hivyo basi, naomba sasa Bunge lako Tukufuliyakubali Makadirio hayo.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na kuafikiwa)

(Makadirio ya matumizi ya Wizara ya Maji kwamwaka 2013/2014 yalipitishwa na Bunge)

SPIKA: Naomba nichukue nafasi hii kuwapongezaWizara ya Maji na wataalam wao, lakini na WaheshimiwaWabunge wa Budget Committee, Kamati ya Sekta ya Majina pia Waheshimiwa Wabunge kwa kuelewa kwenu. Sasamjue huu ndiyo mwanzo, lakini siyo kwamba fedhazilizoongezwa zimetoka nje ya bajeti ambayo tunayo, ni hiyohiyo tuliyo nayo. Naomba Waheshimiwa Wabunge muelewehivyo.

Pia muelewe kuwa tunapopita Wizara kwa Wizara,hii ni provisional, tutakapofika kwenye Appropriation Bill ndiyotutakuwa na bajeti ya Waziri wa Fedha. Kwa hiyo,nawaomba msije mkajenga hoja kuwa tunadai tu ndiyomaana sisi tulijaribu kuangalia namna ambavyo tunawezakuishauri Serikali namna gani ambayo tunaweza kuongezamapato.

Page 211: 29 APRILI, 2013 MREMA 1 - Parliamentparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461917142-HS...2013/11/14  · kabambe wa Umeme Vijijini awamu ya pili chini ya uwezeshaji wa Wakala wa

211

29 APRILI, 2013

Waheshimiwa Wabunge kazi hii hatujaifanya vizuri yanamna ya kuishauri Serikali kuongeza mapato, kwa sababusiku zote tutakuwa na haya, lakini ukweli ni kuwa kamamapato hayaongezeki tutakuwa na matatizo.

Kwa hiyo, niwashukuru sana kwa kazi mliyoifanya ninzuri sana na nadhani tunakwenda vizuri.

Kwa kuwa muda uliopo hautoshi kwa Waziri kusomahotuba yake kwa sababu anahitaji saa nzima na hapahaiwezi kutosha, sasa naahirisha shughuli za Bunge mpakakesho saa tatu asubuhi.

(Saa 12.50 jioni Bunge liliahirishwa mpaka Siku yaJumanne, Tarehe 30 Aprili, 2013, saa Tatu Asubuhi)