183

Click here to load reader

31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

  • Upload
    phamlien

  • View
    1.213

  • Download
    142

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

1

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

BUNGE LA TANZANIA______________

MAJADILIANO YA BUNGE_____________

MKUTANO WA KUMI NA TATU

Kikao cha Tatu – Tarehe 31 Oktoba, 2013

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Anna S. Makinda) Alisoma Dua

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge mnajua mashine zakuzuia simu zisiweze kufanya kazi ndani hazifanyi kazi vizurisasa. Kwa mujibu wa Kanuni zetu naomba mzime simu zenu.Katibu tuendelee.

MASWALI NA MAJIBU

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kama nilivyosemamaswali kwa Waziri Mkuu hayapo Kwa hiyo, tunaanzamaswali na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa JosephatSinkamba Kandege, atauliza swali la kwanza. Kwa niabayake Mheshimiwa Malocha.

Page 2: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

2

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Na. 30

Kasoro Zilizoko Kwenye Sekondari za Kata

MHE. IGNAS A. MALOCHA (K.n.y. MHE. JOSEPHAT S.KANDEGE) aliuliza:-

Wazo la Serikali kujenga Sekondari za Kata nchi nzimani wazo zuri na limefanikiwa kujenga sekondari hizo lakinizinakabiliwa na kasoro au changamoto mbalimbali kama vileukosefu wa madawati, maabara, upungufu wa walimu,nyumba za kuishi walimu na hata hosteli za wanafunzi:-

(a) Je, Serikali ina mpango gani mahsusi wa kuondoakasoro hizo na kuziboresha zaidi hasa kwa Sekondari za Mkoawa Rukwa Jimbo la Kalambo?

(b) Sheria ya Elimu imemtaka mzazi/mlezi kuhakikishakuwa mtoto anayepaswa kwenda shule anakwenda shule,lakini sheria haisemi chochote kuhusiana na mwanafunzi wasekondari. Je, kuna udhati wa kukuza elimu katika hali kamahiyo?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) (ELIMU) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa WaziriMkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa JosephatSinkamba Kandege, Mbunge wa Kalambo, lenye sehemu (a)na (b) kama ifuatavyo:-

Page 3: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

3

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

(a) Mheshimiwa Spika, Serikali imeendeleakuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na changamotohizi kwa kupeleka fedha za ununuzi wa madawati ujenzi wamaabara, nyumba za walimu ukarabati wa shule kongwena kuajiri walimu wapya. Mwaka wa fedha 2010/2011.

Serikali ilitoa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wamaabara, kati ya fedha hizo mkoa wa Rukwa ulipelekewamilioni 160 na shilingi bilioni 2.6 zilitolewa pia kwa ajili yaukarabati wa shule kongwe na mkoa wa Rukwa ulipewashilingi milioni 150 kwa ukarabati wa shule za sekondari zaMpanga, Nkasi na Kantalamba. Mwaka wa fedha 2011/2012 Serikali ilitoa shilingi milioni 600 kwa ajili ya maabarahamishika mobile laboratory, mkoa wa Rukwa ulipata shilingimilioni 24.

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013Serikali iliidhinisha shilingi bilioni 3.4 kwa ajili ya ujenzi wamadarasa na ununuzi wa madawati ambapo kati ya hizomkoa wa Rukwa ulipata shilingi bilioni 130.9.

Aidha, katika mpango wa uboreshaji wamiundombinu ya sekondari, ikiwemo maabara nyumba zawalimu na madarasa tayari shilingi bilioni 26.4 zimetolewa kwamwaka wa fedha 2012/2013, katika kufanikisha uboreshaji washule 264 ambapo mkoa wa Rukwa umepatiwa jumla shilingimilioni 687.4 na katika robo ya mwaka wa fedha 2013/2014Serikali imetoa shilingi bilioni 8 ambazo zinatumika katika ujenziwa nyumba za walimu, na mkoa Rukwa umepata shilingimilioni 200.

Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kukabiliana nachangamoto hizi, mwezi Machi, 2013 Serikali iliajiri walimu washule za sekondari, 14,096 wakiwemo 4,176 wa stashahada,9920 wa Shahada, Rukwa ilipata walimu 276 wakiwemo wastashahada 180 na shahada 96 kwa mwaka wa 2013/2014tayari mipango ya kuajiri walimu wapya imekamilika baada

[NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU]

Page 4: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

4

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ya kibali cha ajira kutoka walimu wapya watakaopangwatena nchi nzima ikiwemo mkoa Rukwa na halmashauri yaWilaya ya Kalambo.

(b) Mheshimiwa Spika, kutokana na ugatuaji washule za sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo yaUfundi kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, tunahitajikufanya marekebisho ya sera ya sheria na elimu ili kuwezakukidhi mahitaji ya sasa. Katika marekesho hayo suala lakumlinda mwanafunzi litazingatiwa.

Kwa sasa sera ya Serikali ni kwamba walau asilimia50 ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi wajiunge nashule za sekondari. Hivyo Serikali inatoa utaratibuunaowalinda wanafunzi hawa ukiwemo waraka namba 6wa mwaka 2004 ambao unatoa maelekezo kuhusu adhabuinayotakiwa kutolewa kwa wanafunzi kwa wale wanaowapamimba wanafunzi wasichana.

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kuniona, pamoja na majibu mazurisana ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba niulize swali mojala nyongeza kama ifuatavyo.

Ni ukweli usipingika kwamba jiografia ya Kalamboukilinganisha na maeneo mengine ya Tanzania yana utofautimkubwa sana. Je, Serikali kwa kuzingatia uhalisia wa wilayahii na jiografia yake, itaekeleza mpango mahususi kuhakikishakwamba tatizo hili mahususi kwa Kalambo linatatuliwa?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) (ELIMU):Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua jiografia ya maeneoyale ya Sumbawanga na ndiyo sababu pia Ofisi ya WaziriMkuu TAMISEMI iliridhia ombi la wananchi wale kuanzishwakwa Halmashauri ya Kalambo ili kupata huduma kwa ukaribuzaidi na migao yote ninayoitamka hapa wilaya ya Kalamboinapata share yake na kwa hiyo huduma kwa halmashauriya Kalambo inapata kwa ukaribu zaidi.

[NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU]

Page 5: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

5

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Huo ndiyo utaratibu ambao tumeutumia maeneoyote makubwa yenye mazingira makubwa magumutumeyapa mamlaka ya kuwa na halmashauri za wilaya ilikuwasogezea huduma zote hizi. Kwa hiyo mikakati ya elimuiliyopo pamoja na mikakati mingine yote ya Serikali ni kwaajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi walioko kwenyemaeneo haya.

MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Spika,nashukuru pamoja na jitihada hizo za Serikali lipo tatizo kubwala wanafunzi ambao wanashindwa kuendelea na masomongazi za juu na mkoa wa Rukwa hauna chuo kimoja chaufundi cha VETA.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuharakisha kujengachuo cha ufundi VETA ili kuokoa kundi kubwa la watoto hao?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, kama tunavyoongea kila siku mpangowa kujenga vyuo vya VETA kwa kila mkoa hii mikoa mipyaminne na kwa kila wilaya.

Lakini kwa upande wa Rukwa tayari kuna Chuo chaVETA Mpanda, mkoa wa Katavi, ambao ni mkoa mpya tayarikuna Chuo cha VETA pale Mpanda. Lakini mkoa wa Rukwazamani tulikuwa tunasema kwamba kuna Chuo cha mkoawa Rukwa kwa sababu sasa baada ya kugawanywa ndiyoikaenda kule Mpanda kwa hiyo, tunatambua kwamba hiimikoa minne mipya ikiwemo na mkoa wa Rukwa tutajengaChuo cha VETA kwa mipango iliyopo.

Mheshimiwa Malocha, ni jana tulikuwa tunazungumzana wewe pamoja na Mheshimiwa Mipata kwamba wakatihawa wakandarasi walikuwa wanajenga barabara yakutoka Tunduma mpaka Rukwa tayari kuna majengoyameachwa pale na tayari tumeshawaagiza kwambamuandike barua RCC waweze kutuandikia barua Wizara yaElimu ili majengo yale mkitupatia tuweze kutoa mafunzo yaVETA kwenye yale majengo.

[NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU],

Page 6: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

6

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana, kati ya Wilaya zilizofanikiwa sana katikaujenzi wa shule za Kata ni pamoja na wilaya ya Rombo,ambapo karibu kila kata ina shule mbili za sekondari. Sasakumekuwa na ongezeko kubwa sana la vijana waliomalizaelimu ya sekondari lakini hawana nafasi ya kuendelea mbeleili lengo lao la kujitegemea liweze kufikiwa.

Sasa Serikali haioni kwamba ili kuharakisha ujenzi wahizi shule za kata baadhi ya wilaya kama Rombo ambayoina shule nyingi baadhi ya shule zikageuzwa na kufanywavyuo vya ufundi ili kuweza kuwachukua hao vijana ambaosasa baada ya form four wanazagaa mtaani?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, labda ni kutoa tu elimu juu ya neno Vyuovya Ufundi, kuna Vyuo vya Ufundi vya aina mbili, kuna Vyuovya Ufundi ambavyo vinakuwa credited na NACTE, Barazala Elimu la Taifa la Ufundi, kuna vyuo vya ufundi ambavyovinakuwa credited na VETA.

Sasa hapa kidogo nina swali baadayelinalochanganua mambo haya na ningeomba MheshimiwaMbunge aweze kusubiri na kama swali la nyongeza litakuwalimejumuishwa na hili nitaweza kumjibu ipasavyo.

Na. 31

Posho na Mishahara kwa Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji

MHE. JAMES F. MBATIA (K.n.y. MHE. DKT. AUGUSTINE L.MREMA) aliuliza:-

Ni sera ya Serikali kuhakikisha kuwa wenyeviti wa vijijina vitongoji wanalipwa mishahara na posho zao na kwambaWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) alitangazaBungeni kwamba Halmashauri ambazo hazilipi posho hizowapeleke majina ya Halmashauri husika.

Page 7: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

7

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Je, katika Jimbo la Vunjo ni Wenyeviti wa Vijiji naVitongoji wangapi wamelipwa mishahara na posho hizotangu 2010/2013?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) (ELIMU) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa WaziriMkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. AugustineLyatonga Mrema kwa kuanza kutoa maelezo mafupi yaufafanuzi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, wenyeviti wa vijiji na vitongojihawalipwi mishahara isipokuwa viongozi hao hulipwa poshoya mwezi kutokana na makusanyo ya mapato ya ndani yaHalmashauri pamoja na ruzuku ya fidia ya vyazo vya mapatovilivyofutwa baada kuonekana kuwa ni kero.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo mafupi,sasa naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kwapamoja kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kazi kubwazinazofanywa na wenyeviti wa vijiji na vitongoji katikakusimamia shughuli zote za maendeleo kwenye maeneo yao.katika bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2014 Serikaliimepeleka fedha ya fidia ya vyanzo vilivyofutwa sawa nashilingi bilioni 63.5 na halmashauri ya Wilaya ya Moshi, imepatashilingi 499,673,000 za fidia.

Halmashauri inatakiwa kupeleka katika Serikali za vijijiasilimia 20 ya fedha kama ilivyo kwa halmashuari zote nchini,matumizi ya fedha hizi ni kwamba asilimia tatu ya hizozinatakiwa kutumika kwa ajili ya maendeleo na asilimia 17kwa ajili ya utawala ikiwemo kulipa posho za wenyeviti wavijiji na vitongoji.

[MHE. JAMES F. MBATIA]

Page 8: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

8

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, kati ya mwaka 2010/2013,halmashauri ya wilaya ya Moshi, imepeleka ruzuku ya fidiakwenye Serikali za vijiji kiasi cha shilingi milioni 207,485,400ambapo sehemu ya fedha hizo zilikuwa ni kwa ajili ya kulipaposho za viongozi hao. Viwango vya posho vinavyolipwahutofautiana kati ya halmashauri moja na nyingine kulinganana makusanyo ya mapato ya ndani na fidia inayopelekwa.

Mheshimiwa Spika, changamoto kubwa iliyopo nikwamba kwa baadhi ya halmashauri kutopeleka fedha hizikatika Serikali za vijiji. Hivyo, napenda kutumia fursa hiikuzikumbusha tena halmashauri zote nchini kuhakikishakwamba fedha hizo zinapelekwa katika vijiji na ufuatiliajiufanyike ili kuhakikisha kuwa zinatumika kwa malengoyaliyokusudiwa.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwahalmashauri ya Wilaya ya Moshi na hususan jimbo la Vunjolina vijiji 84 na vitongoji 384 na mpaka sasa hivi jambo fedhahizo zinaonekana zimeenda kwenye halmashauri ya Wilayaya Moshi, hakuna Mwenyekiti yoyote wa kijiji ameshalipwaposho hizo navyozungumza leo hapa.

Serikali inaonaje ili utekelezaji uwe ni endelevu kwavijiji vyote nchi nzima watoe circular kwa Wakurugenzi naWabunge wapate kopi ili ufuatiliaji uweze ukawa ni wakaribuzaidi?

La pili, kwa kuwa wenyeviti hawa wamefanya kazikwa miaka minne sasa na wanaenda mwaka wa tano, hakizao za huko nyuma ambako hawajalipwa, Serikali inatoatamko gani kwa halmashauri zote ili haki zao zipatikane,hususan jimbo la Vunjo ambako ndiko anakotoka muulizaswali la msingi?

[NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU]

Page 9: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

9

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) (ELIMU):Mheshimiwa Spika, kwanza nasikitika kusikia kwambawaheshimiwa Wenyeviti wa vijiji na vitongoji kule Moshihawajalipwa kwa sababu kwa utaratibu ambao ofisi ya Waziritunaona, na kwa utaratibu ambao tumeelekeza Halmashaurizetu nchi kote kupitia mapato ya ndani kwamba kila kijijikijidhatiti katika kufanya makusanyo yake na makusanyo zileasilimia nilizozitaja yanaweza kufanyiwa matumizi, lakinilazima uripoti kwa halmashauri.

Lakini kwa vyanzo vyote ambavyo tulivifuta ambavyosasa ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI inapeleka kama ruzukukwenye halmashauri maana yake fedha ile sasa itumike naimeenda kama ruzuku kwenye halmashauri maana yakefedha ile sasa itumike na imeenda pale kama badala yafedha ambayo wangekusanya wao na kwa hiyo inatoshakufanya zoezi.

Kwa hiyo, ni wajibu wa kila halmashauri nawakurugenzi nchini kuhakikisha kwamba wenyeviti wote wetuwa vijiji wanalipwa fedha zao kwa wakati. Inaweza piatunapeleka kwa robo mwaka lakini bado ndani ya miezimitatu wenyeviti wangeweza kulipwa.

Sasa hili ya kwamba hawajalipwa, tunakuahidikufanya ufuatiliaji wa kina, hii sasa ikiwemo na ile miaka yoteambayo wenyeviti wa maeneo haya hawajalipwa nakuwaahidi kwamba nitafanya ufuatiliaji tupate sababukwanini wenyeviti kwa eneo lile hawajalipwa kwa miaka yoteminne halafu nitakupa taarifa.

Sasa tutaandaa utaratibu wa kuwashirikishaWaheshimiwa Wabunge ili mtusaidie kufanya ufuatiliajikwenye halmashauri zetu kwa sababu Serikali inapelekakwenye halmashauri na wakurugenzi nao wanapata zilefedha sasa namna ambavyo wanatumia na kwa kuwa sasaWaheshimiwa Wabunge ni wajumbe wa mabaraza yamadiwani kwenye maeneo.

Page 10: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

10

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Moja kati ya maswali ambayo mngepaswa kuyaulizana ambayo sasa nashauri myafanyie ufuatiliaji ni pamoja namatumizi ya fedha hizi kwa wenyeviti wa vijiji.

MHE. ASSUMPTER N. MSHAMA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kunipatia nafasi kwanza mimi nasikia hatakutetemeka kusikia neno alilolisema Mheshimiwa Waziri,tumekuwa tukizunguka majimboni mimi huu mwaka wa tatu,nazunguka kila mahali mimi nadhani sasa Mheshimiwaunataka kugombanisha Wakurugenzi na wenyeviti wa vijijikwa sababu hakuna mahali popote ambako imeandikwaSerikali inapeleka fedha yoyote katika vijiji? Kwa hiyo,naomba ieleweke vizuri ili kusudi wakurugenzi wasipatematatizo na wenyeviti wa vijiji ahsante. (Makofi)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) (ELIMU):Mheshimiwa Spika, analosema Mheshimiwa Mbungeanaweza kuwa ni la ukweli kwa baadhi ya halmashauri kamaMkurugenzi hawezi kutekeleza haya ambayo nimeyaeleza.Kwa sababu vyanzo vyote ambavyo tumevizuia kwenyehalmashauri kuvikusanya ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMIinapeleka fedha zile kama fidia ya fedha ambayo ilitakiwaikusanywe na halmashauri zake. Ndiyo hiyo hiyo ambayoinatakiwa igawiwe kwa asilimia hizo.

Kwa hiyo, kama ambavyo nimeahidi kwamba jambohili sasa kama limezungumzwa kwa upana huo sasa ni wajibuwetu sasa kufanya ufuatiliaji na naahidi tutawapa taarifaWaheshimiwa Wabunge.

MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Spika,nishukuru sana kupata nafasi ili niweze kuuliza swali kwa kuwawenyeviti hawa ni watu muhimu kama alivyoelezaMheshimiwa Waziri na kwa kuwa posho zao aidha haziendilakini pia kama zinaenda haziendi kwa wakati. Kumekuwepopia na tatizo la Waheshimiwa hawa Wenyeviti wa Serikali za

[NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU]

Page 11: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

11

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mitaa na vitongoji kutokuwa na sehemu kama ofisi yakufanyia kazi wamekuwa wengine wanapanga lakiniwamekuwa wanaomba omba sana fedha kwa ajili yapango.

Je, Serikali inaonaje suala hili ili kuweza kuhakikishakwamba watu hawa wanaweza kupata sehemu za kufanyiakazi ama fedha za kulipia pango ya ofisi wanazokodisha?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) (ELIMU):Mheshimiwa Spika, ni kweli tunavyo vijiji vingi nchini na katikakuboresha utendaji ilikuwa inapaswa kila kijiji kiwe na ofisi yakekwa ajili ya kufanya mawasailiano na wananchi wakekwenye maeneo yake.

Lakini tunatambua ziko ofisi ambazo kwa jitihada zakezenyewe zimejenga ofisi, lakini pia, Ofisi ya Waziri MkuuTAMISEMi inapeleka ruzuku kwenye Halmashauri ingawa sinyingi kwa ajili ya kutosheleza vijiji vyote; lakini viko vijijiambavyo sasa vinajenga ofisi zake ni pamoja na ofisi za Kata.

Kwa hiyo, tutaendelea na zoezi hilo la kuboreshaujenzi wa ofisi za vijiji kwenye maeneo yale ambayoyanaelekezwa zile fedha ili kuweza kutoshereza kuwa namaeneo ya kufanyia kazi maeneo haya. Kwa hiyo, wajibuwetu sasa ni kuona uwezekano wa kibajeti zaidi, ili kuongezaeneo hilo tuweze kuwezesha vijiji kuwa na eneo hilo kuwa naofisi za kufanyia kazi.

SPIKA: Ahsante, hili swali la mishahara kwa wenyeviti,Mheshimiwa Waziri mukalifanyie kazi vizuri. Mkalifanyie kazivizuri, tekinolojia ipo munaweza kupata maelezo kilaHalmashauri wanafanya nini na pengine mkaleta taarifahapa watu wakaridhika. (Makofi)

[NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU]

Page 12: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

12

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Tunaendelea na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Mahusiano na Uratibu, Mheshimiwa Dkt. Tatus Kamanaatauliza swali hilo.

Na. 32

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)

MHE. DKT. TITUS MLENGEYA KAMANI aliuliza:-

Kijiji cha Ngasamo Wilayani Busega kilipatiwa maji yabomba kupitia mradi wa TASAF na Serikali iliahidi kupanuamradi huo kwenda vijiji vya Ngunga, Malili na Nyamikoma:-

(a) Je, ni lini utekelezaji wa upanuzi huo utaanza?

(b) Je, ni lini kwa uhakika wakazi wa vijiji hivyowataanza kunufaika na huduma ya maji ya uhakika?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MAHUSIANO NAURATIBU alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Dkt. Titus M. Kamani, Mbunge wa Busega, lenyesehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Vijiji vya Ngasamo,Ngunga na Malili ulianza kutekelezwa mwaka 2003 kwa fedhatoka TASAF 1 kwa gharama ya shilingi 193,894,666. Huu nimradi mkubwa unaotegemea chanzo cha maji kilichopokatika kijiji cha Ngasamo.

Kazi zilizofanyika ni pamoja na Ujenzi wa Tenki lakusambaza maji kwenye kilima kilichopo karibu na kijiji chaNgasamo. Kuchimba mtaro na kulaza Mabomba ya majikutoka kwenye chanzo cha maji hadi kwenye tenki juu yamlima; ununuzi wa pampu wa pampu ya kusukuma maji naUjenzi wa nyumba ya pampu.

[SPIKA]

Page 13: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

13

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, mradi huu haukuweza kukamilikakwa wakati kutokana na fedha zilizotolewa ma TASAF 1kushindwa kukidhi mahitaji yote ya mradi huu mkubwa, hivyokusababisha mradi kusimama kwa muda wa miaka sita.Wakati wa utekelezaji wa awamu ya pili ya TASAF, tathiminiya kitaalamu ya mahitaji ya mradi uliofanyika mwaka 2009ilionesha kuwa zinahitajika fedha shilingi 168,835,000kukamilisha shughuli zote za mradi na kuwezesha vijiji vyotevitatu vilivyokuiwa vimelengwa kupata maji.

Hata hivyo, kulingana na taratibu za TASAF 2 mradiulipatiwa kiasi cha shilingi 53,531,500 ambapo wananchiwalichangia shilingi milioni 7,500,000 pamoja na nguvu kazikwa ajili ya kukamilisha mradi wa kuwezesha upatikanaji wamaji kwa kijiji cha Ngasamo kwa wakazi wake wapatao 3,100.

Aidha, mradi huu ulijumuisha miradi midogo midogondani yake ukiwemo ujenzi wa tanki la maji kijiji cha Ngungalita 22,000 na umekamilika, ujenzi wa barabara ya Ngasamohadi kijiji cha Nyangoka Km 2.5 umekamilika. Ufungaji wamabomba ya kushusha na kusambaza maji kwenye vituoyaani DP mita 1,300 umekamilika na ujenzi wa vituo saba vyakusambaza maji (DPs), na vitatu vipo kijiji cha Ngasamo, viwilikijiji cha Ngunga na viwili kijiji cha Malili, ila maji badohayajaunganishwa.

Mheshimiwa Spika, wananchi wa vijiji vya Ngunga naMalili bado hawajanufaika na huduma ya maji ya mradi huukwa kuwa maji bado hayajaunganishwa kwenye Vituo vyausambazaji maji (DPs) vilivyojengwa kwa sababu ya upungufuwa fedha. Kijiji cha Nyangoka hakikulengwa kwa mradi wamaji, ila wananchi wake walinufaika na barabara yenye urefuwa km 2.4 waliyoijenga kwa kushirikiana na TASAF.

Mheshimiwa Spika, muda wa utekelezaji wa mradi waTASAF awamu ya pili ulikwisha, Halmashauri zote zilijulishwana kushauriwa kukamilisha miradi ya wananchi ambayohaikuweza kukamilika kwa sababu mbalimbali kwa kutafutavyanzo vya fedha, ikiwemo miradi ya maji ya vijiji vya Ngungana Malili.

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MAHUSIANO NA URATIBU]

Page 14: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

14

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. DKT. TITUS MLENGEYA KAMANI: MheshimiwaSpika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi.

Mheshimiwa Spika, mradi huu uliwapa matumainimakubwa sana wananchi wa vij i j i vya maeneoyanayozunguka. Vilevile maji yaliyoko kwenye kile kisima nimengi sana kwa sababu ni kisima cha asili, chenye uwezowa kuhudumia eneo kubwa. Hata hivyo, Wilaya ya Busegandiyo juzi juzi tu imeanza, haina vyanzo vya mapato. Sasasijui Mheshimiwa Waziri anaweza kusemaje?

Serikali haoni kuna haja ya kuuchukua tena huumradi, kwa sababu Halmashauri hii mpya haina vyanzo vyakutekeleza mradi mkubwa wa namna hii?

Swali la pili ni kwamba, mradi huu mabomba sasayemepasuka kwa sababu kama nilivyosema maji ni mengina yana nguvu nyingi. Mabomba yaliyowekwa yamepasuka,lakini Wilaya ya Busega haina mratibu wa TASAF, mratibuanatoka Wilaya nyingine ambayo iko Mkoa mwingine tofautina Busega. Sasa ni lini Serikali italeta mratibu wa TASAF katikaWilaya hii ili aweze kufuatilia mradi huu na mambombayaliyopasuka yaweze kutengenezwa?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MAHUSIANO NAURATIBU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali yanyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nakubaliana naye kabisakwamba mradi huu ni muhimu na unawapa matumainimakubwa wananchi wote wa vijiji vyote vya Ngunga na Malilipamoja kama Ngasamo.

Kama nilivyoelezwa tatizo lililotokea ni la kifedha zaidikuliko la imuhimu. Kwa hiyo, nakubaliana na MheshimiwaMbunge kwamba, tutashauriana na Wizara ya Maji, pamojana Halmashauri ya Wilaya Busega ili kuona ya kwamba Serikaliinaendeleza kazi nzuri iliyoanzwa na TASAF pale, kuhakikishakwamba makusudio ya kuwapatia maji wananchi wa vijijihivi yanafikiwa.

Page 15: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

15

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Naujua mradi huu nimewahi kuutembelea,nilishaenda mpaka kwenye chanzo nimetembelea vijiji vyotevinavyozunguka pale mahali. Kwa hiyo, nakubaliana nayekwamba tutashirikiana kuhahakikisha kwamba hudumailiyokusudiwa inapatikana badala ya kuuacha kama ilivyosasa.

SPIKA: Mheshimiwa Chiku A. Abwao, nimekuonaumesimama?

MHE. CHIKU A. ABWAO: Mheshimiwa Spika, samahanisijakusikia vizuri. Kwa kuwa wananchi wa Isimani wanamatatizo makubwa sana ya maji na kwa kuwa kuna visimavingi ambavyo vilichibwa kwa bahati mbaya havitoi maji.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wananchiwa Jimbo la Isimani, kuhakikisha wanapata maji yaliyo safina salama?

SPIKA: Ninyi munapiga makofi mpaka hatukusikiamwishoni, umemaliziaje? Hebu simama useme tena,hatukukusikia mwishoni.

MHE. CHIKU A. ABWAO: Mheshimiwa Spika, nilikuwanapenda kujua Serikali ina mpango gani wa kuhakikishakwamba wananchi wa Isimani wanapata Maji yaliyo safi naSalama?

SPIKA:Jipya kweli kweli, Mheshimiwa Waziri wa nchinaomba majibu!

WA NCHI, OFISI YA RAIS, MAHUSIANO NA URATIBU:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyingeza laMheshimiwa Chiku A. Abwao, kama ifuatavyo:-

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MAHUSIANO NA URATIBU]

Page 16: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

16

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Tatizo la maji haliko Isimani peke yake, lipo katikaHalamsahauri nyingi nchini na kama tunakumbuka wakatiMbunge hili linajadili tatizo hili, tuliongeza fedha kwa ajili yakusaidia kuongeza kiwango cha maji na tukatilia mkazokwamba, maji haya yataenda katika maeneo ya vijijini nakazi ya kutekeleza imeshaanza na miradi mingi inatekelezwasasa vijijini.

Contractors wamekwisha ajiliwa kwa ajili ya kuongezakiwango cha maji na hiyo itahusu vilevile Wilaya ya Isimani.Hili ni suala la nchi nzima halitakuwa la Isimani peke yake.Lakini kama Isimani kuna tatizo kubwa na Mbunge wa Isimaniyuko hapa, tutashirikiana naye kuona namna ya kusaidiakupunguza tatizo hilo.

(Hapa Waheshimiwa Wabunge walishangilia)

SPIKA: Mbunge wa Isimani! (Makofi/Kicheko)

MHE. WILLIAM V. LUKUVI: Aaah! Mimi ni Waziri. (Makofi/Kicheko)

SPIKA: Mbunge wa Isimani! (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBUNA BUNGE: Mheshimiwa Spika, mimi nazungumza kwa niaba,mimi ni mtu wa Serikali na ndiyo mratibu wa shughuli zaSerikali, nina uwezo wa kutoa majibu yoyote humu ndani.Kama hamjui!(Vicheko)

Kwa hiyo, kwa niaba ya mheshimiwa Waziri wa nchi,Uratibu na Mawasiliano nataka kutoa jibu la nyongeza kwaswali ali louliza dada yangu Mheshimiwa ChikuAbwao.(Vicheko)

Serikali inafahamu tatizo la maji Isimani, MheshimiwaRais mwenyewe alipotembelea mara mbili Isimani alijuajambo hilo na hivi sasa kuna mradi mkubwa wa kufufuachanzo cha maji na kurekebisha, ambacho kinatoa majiMbigiri kwa Professor wenye thamani ya shilingi bilioni tatu.

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MAHUSIANO NA URATIBU]

Page 17: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

17

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Hivi ninavyozungumza Mbunge wa Isimani kwakutumia vyanzo mbalimbali, ameshachimba visima 25, visima25 vya maji na hivi sasa tunamalizia visima vingine 10. (Makofi)

Nia ni kuwa na kisima cha maji ya akiba katika kilakijiji cha Isimani, badala ya wananchi kuendelea kusubirimradi ule mkubwa wa bomba, kila kijiji kitachimbiwa kisimakwa jitiada anazofanya Mheshimiwa Mbunge kwakushirikiana na Serikali. (Makofi)

SPIKA: Wala huhitaji kusema, maana yake hapa mtuanaruhusa ya kujibu. Kwa hiyo, wewe mwenyewe kamaMbunge peke yake ungeweza kujibu tu, eeh kwa sababuwewe ndiyo unayejua jimbo lako.

Tunaendelea na swali linalofuata, Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Naona Chiku Abwaoanalitaka hilo Jimbo eeh! (Makofi/Kicheko)

Kwa hiyo, tunaendelea, Mheshimiwa Abdallah S.Ameir!

Na. 33

Shamba la Uvikuta – Chamazi

MHE. ABDALLAH SHARIA AMEIR aliuliza:-

Katika Wilaya ya Temeke, Jimbo la Kigamboni, Kataya Chamazi kuna Shamba la UVUKUTA lenye eneo kubwasana na mpaka sasa ni theluthi moja tu ya shamba hilolinatumika na eneo lililobaki ni pori kubwa linalohifadhiwanayama hatari pamoja na kuwa kimbilio la vibakawanapofanya uhalifu maeneo mengine:-

(a) Je, Serikali inalijua hilo?

(b) Je, eneo hilo lina ukubwa wa ekari ngapi?

(c) Je, eneo hilo lilitolewa kwa madhumuni gani?

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU]

Page 18: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

18

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEOYA MAKAZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Abdallah Sharia Ameir, Mbunge wa Dimani,lenye sehemu (a) (b) na (c) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, napenda kulijulisha Bunge lakoTukufu kwamba, Serikali inatambua uwepo wa ShambaNamba 2820 lenye barua ya toleo yaani letter of Offer, Kumb.Na. LD/177113/17 ya tarehe 25 Aprili, 2001 lenye ukubwa waekari 893 linalomilikiwa na umoja wa Vijana wa KikristoUzalishaji Tanzania (UVIKUTA) lililopo eneo la Chamazi katikaManispaa ya Temeke Jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa Spika, shamba hili lilitolewa kwa matumiziya makazi, kilimo na ufugaji. Kwa sasa eneo hilo lipo kwenyemchakato wa kuandaliwa matumizi bora ambayoyatajumuisha maeneo ya makazi, miradi ya elimu na mafunzoyaani Education and Vocational Training biashara, viwanjavya michezo na huduma za kijamii kama zahanati pamojana viwanda na kadhalika.

MHE. ABDALLAH SHARIA AMEIR: Mheshimiwa Spika,ahsante, pamoja na majibu mazuri yaliyotolewa naMheshimiwa Waziri, naomba kuuliza maswali mawili yanyongeza.

Mheshimiwa Spika, majibu ya Mheshimiwa Waziriameeleza kwamba liko katika mchakato wa shamba hilokufanyiwa hayo aliyoeleza.

Je, mchakato huo unaanza lini na utamalizika lini?Swali la pili, Mheshimiwa Waziri atakuwa yuko tayari

kufanya vikao na wananchi ambao wanazunguka eneo hiloili kuelezea azima hiyo kwa ajili ya kuondoa malalamiko?Ahsante sana.

Page 19: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

19

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEOYA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusu mchakato kwambaunaanza lini na kumalizika lini, Mchakato umekwishaanza.Kwa kawaida, mmiliki wa eneo, pale ambapo ataonaameshindwa kufikia yale malengo yaliyokuwa yamepangwaawali, au mamlaka ya upangaji ikiona kwamba mmiliki waardhi ameshindwa kutimiza masharti yaliyomo kwenye hatiau mpango wa matumizi ya ardhi, inayo mamlaka ya kuingiliana kupendekeza ardhi ile ipangiwe matumizi mbadala.

Hivyo, kwa sasa hivi tumekwishapokea maombi yakubadilisha matumizi kutoka yale ya makazi kilimo na ufugajipekee na kupima viwanja upya, kupanga matumizi ilikujumuisha yale ambayo nimeyataja katika jibu la swali lamsingi.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, napenda nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba ndiyo nitakuwa tayari kwakushirikiana na Mbunge wa Jimbo linalohusika, pamoja nauongozi wa Mkoa na Wilaya kwenda pale kukutana nawananchi na kuzungumza juu ya mstakabali wa eneo hilo.

SPIKA : Nakupongeza kwa majibu mafupi.Tunaendelea na Wizara ya Nishati na Madini, MheshimiwaProfessor Mahamudu Msolla, atauliza swali linalofuata.

Na. 34

Utafiti wa Madini ya Chokaa Kijiji cha Vitono – Kilolo

MHE. PROF. PETER MAHAMUDU MSOLLA aliuliza:-

Kampuni ya Kastan Mining Ltd. ya Dar es salaam ilipewaleseni ya Utafiti wa Madini ya Chokaa (Prospecting LicenceNo. PL 6528/2010) ya terehe 13 Agosti, 2010 kwa kipindi cha

Page 20: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

20

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

miezi thelathini na sita (36) ya tarehe 13 Agosti, 2010 kwakipindi cha miezi thelathini na sita (36) katika kijiji cha Vitino,Wilayani Kilolo. Kampuni hiyo imekuwa ikichimba chokaakwa wingi na kuisafirisha na malori kupeleka mahalikusikojulikana:-

(a) Je, utafiti huo umefikia wapi kwa sasa?

(b) Je, wananchi wa Vitono na Halmasahauri yaKilolo kwa ujumla wananufaika na uchimbaji huo waChokaa?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishatina Madini, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Prof. PeterMahamudu Msolla lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa Kampuni ya KastanMining Ltd. ya Dar es salaam, ilipewa leseni ya utafutaji yamadini ya Viwandani yaani, Prospecting Licence No. Pl 6528/2010 ya tarehe 13 Agosti, 2010 kwa kipindi cha miezi 36. Lesenihiyo, yenye ukubwa wa kilometa za mraba 198.8, ilitolewakatika Wilaya ya Kilolo na uhai wake ulikoma tangu tarehe12 Agosti, 2013. Utafutaji wa madini ndani ya leseni uliendeleana haukufikia hatua ya kuanzisha mgodi.

Aidha, baada ya uhai wa leseni hiyo, kumalizikatarehe 11 Agosti, 2013 na kwa kuwa mwenye leseni hiyohajawasilisha maombi ya kuihuisha, eneo hilo kwa sasa likochini ya Mamlaka ya leseni kwa muda wa miezi minneambapo baada ya hapo itakuwa wazi kwa waombajiwengine wapya.

Mheshimiwa Spika, Wizara pia, ilitoa leseni nyinginenne za uchimbaji mdogo katika eneo la Vitono za tarehe 27/

[MHE. PROF. PETER MAHAMUDU MSOLLA]

Page 21: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

21

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

6/2011 kwa Bwana Salim Abdallah Zagar na kuna uchumbajiwa madini ya chokaa unaeoendelea katika leseni hizo.Aidha, kufuatia uchimbaji huo Serikali ilipata jumla ya dolaza Marekani 977.63 ikiwa ni mrahaba, ikijumlisha na adhabuya 25% ya ucheleweshaji wa kulipa mrahaba, ilipouza tani896 kama mbolea ya chokaa. Kiasi hicho cha fedha kilipwakatika ofisi yetu ya madini Mbeya.

(b) Mheshimiwa Spika, manufaa ya wazi kwa kijiji na kwaHalmashauri ya Wilaya ya Kilolo ni ajira kwa wananchi wamaeneo hayo. Aidha, kampuni hizi zinapaswa kushiriki katikakuchangia shughuli za kijamii katika maeneo hayo, pomojana kulipa ushuru wa huduma kwa Halmashauri ya Kiloloambayo ni asilimia 0.3% ya mapato yatokanayo na madiniwanayochimba.

MHE. PROF. PETER MAHAMUDU MSOLLA: MheshimiwaSpika, pamoja na majibu ya Serikali ninayo maswali mawilimadogo ya nyongeza.

Je, Serikali ina utaratibu gani wa kufuatilia makampuniambayo yamepewa prospecting Licence, kuhakikishakwamba kweli bado wanendelea kufanya utafiti na kwambahawachimbi madini. Ninasema hivyo kwa sababumuwekezaji huyu amechimba madini, amekuwa akisombakwa malori mengi kwa siku, kiasi cha kuharibu hata barabara.

Je, huo bado ni utafiti tu, ama ameanza kuchimba?(Makofi)

Pili, manufaa kwa wananchi kwa Vitono, pamoja naHalmsahauri ya Kilolo hayajawahi kupatikana. Hajashughulikakwenye mambo ya cooperate resiponsibility yeyote nabadala yeke amechimba kwenye mashamba ya wananchina aliahidi kwamba angelipa fidia na mpaka leo hii hakunamwananchi yeyote ambaye amelipwa fidia hiyo.

[NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI]

Page 22: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

22

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Je, serikali itasaidiaje ili wananchi ambao mashambayao yamechukuliwa waweze kulipwa fidia stahiki?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, kwa niabaya Waziri wa Nishati na Madini, naomba kujibu maswalimawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Prof. Peter M. Msolla,kama ifuatavyo:-

Kwanza nimpongeze kwa kuuliza maswali mazuriambayo kwa kweli yamekuwa yana mgogoro mkubwakatika sekta hii ya uchimbaji wa Madini katika maeneo mengina hasa Vijijini.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, utaratibu wautafiti unaofanywa na Makampuni haya, na kwambamatokeo yake yanapokuwa tayari je, tunajua wakati ganikwamba sasa wanaanza kuchimba au bado wanafanyautafiti.

Uko utafiti wa aina tofauti tofauti, uko utafiti unaowezaukaishia palepale, lakini uko utafiti ambao unawezaukapaswa kumaliziwa au kukamilika kwa kutumia nje ya eneolile kwa sababu ya teknolojia. Hata hivyo, Sheria inatakaWizara ikague maeneo hayo na huwa tunakagua kila baadaya muda fulani, na tunao Maafisa wa Madini katika maeneohaya.

Sasa kama imetoakea basi jambo hili likafanyikakama anavyosema Mheshimiwa Mbunge, basi pengine niuzembe wa mtaalam wetu ambaye tumemweka kule, lakininaamini kwamba mambo haya yanavyotokea wakatimwingine huwa ni kwa siri au kwa kificho. Tutajitahidi kuwekamsisitizo mkubwa katika kuangalia suala hili wakati wote kwasababu ni kweli Mheshimiwa Mbunge na eneo hili miminilipita, yako madhara ambayo yametokea na wao

Page 23: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

23

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

hawajapata kitu chochote na huyu bwana akafunga leseniyake na kuiachia ili tuweze kutoa kwa watu wengine.

Mheshimiwa Spika, la pil i, manufaa ambayowananchi wamepata wa Kitono, ni kwamba ni hakuna, nikweli. Jambo la kwanza kabisa ambalo nataka niliseme hapa,na ninawaomba wachimbaji wa madini wote walielewe nawananchi, kwa maana ya Serikali zote, kwa maana ya Serikaliza Mitaa na za Vijiji kuelewa ni kwamba uchimbaji wa madinihauendi kiholela kama ambavyo wachimbaji wanataka.

Ni lazima huyu mchimbaji afike kwenye Halmashari,aripoti, aelekezwe anakokwenda kule kwenye Kijiji, aripoti iliwaweze kukubaliana mambo fulani fulani ya msingi nauchimbaji huu hauwezi ukaanza mpaka kwa kibali cha Waziri.

Kwa hiyo, nichukiue nafasi hii kuwaomba sana,kwamba Serikali za Mitaa zinahusika katika uchimbaji waMadini, na zinatambulika na zinatajwa kisheria kwamba nilazima zilidhie, na washirikiane ili kuweza kuruhusu huouchimbaji. Pia suala la fidia, ni suala la msingi sana, leseni yauchimbaji haiwezi ukatolewa mpaka pale Waziriatakapojiridhisha kwamba fidia zimelipwa, hali ya mazingiraimetizamwa, ndipo uchimbaji uweze kuendelea.

Nichukue nafasi hii kuwaomba Viongozi wetu waHalmashauri wasiwe wanyonge, wanapoona mtuanachimba, wachukue hatua, wamwulize kama ana kibalina ikibidi wawasiliane na Wizara ili kuweza kupata uhakikawa jambo hilo.

MHE. MUSTAPHA B. AKUNAAY: Mheshimiwa Spika,nashukuru. Je, badala ya Wizara ya Nishati na Madini kumpaMtafiti wa Madini leseni na baadaye aje kwenye Halmashauri,siyo bora kwamba anayeomba leseni hiyo apitie kwenye

[NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI]

Page 24: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

24

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Halmashauri ili Ardhi hiyo ijulikane kwamba haina watukatika maeneo hayo?

SPIKA: Ahsante, Mheshimiwa Naibu Waziri majibukwa kifupi.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGE B.SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Mustapha B. Akunaay, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kimsingi ziko haki mbili, iko miningright ambayo iko chini ya Ardhi, lakini pia kuna surface right.Kwenye Sheria ya Madini yenyewe inazungumzia mining rightambayo iko chini ya Ardhi, lakini haimtengi mwenye surfaceright. Halmashauri hizi zinamiliki surface right, lakini huwezeuka access mining right kama hujapata surface right.

Hapa ndipo kuna fidia na mambo mengine. Kwahiyo, ni ukweli kwamba mchimbaji wa Madini, hata kamaana leseni kutoka Wizarani, hataruhusiwa kuendeshauchimbaji, mpaka apate surface right ambayo inamilikiwana Mamlaka zilizoko pale chini.

Kwa hiyo, nichukue nafasi hii kuwaomba wachimbaji,wasidharau haki ya surface, haki ya hapa juu ya ardhi, hiihaki ina watu ambao wameiipata kisheria. Ardhi ya Tanzaniahakuna iliyo wazi, ardhi inamilikiwa na Mamlaka za Umma,za Vijiji, na Serikali Kuu.

Kwa hiyo, hakuna ardhi iliyo wazi, kwa hiyo, wakipatahaki ya kuchimba wasidharau haki za watu wenginewanaomiliki hapa juu.

MHE. JENISTA J. MHAGAMA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali dogo

Page 25: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

25

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

la nyongeza. Kwa kuwa kwa sasa Serikali imefanya kazi nzurisana ya kujenga Barabara nyingi katika maeneo mbalimbalinchini ikiwemo katika Jimbo la Peramiho na Makampuniyanayojenga Barabara hizo yamekuwa yakichimba vifusina kupata maliasili za kutengenezea Barabara hizo kutokakatika Vijij i, lakini wanavijij i wale hawafaidiki na kituchochote badala yake wanaachiwa mashimo, makorongomakubwa bila kupata faida yoyote ile. (Makofi)

Je, Wizara hii haioni kwamba sasa ni wakati muafakawa kuhesabu changarawe na kokoto na kila kitukinachochimbwa katika maeneo ya wananchi pia ni ainamojawapo ya madini na wananchi hao wakapata fidia amamrahaba kwa namna moja ama nyingine? (Makofi)

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGE B.SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swalila nyongeza zuri sana la Mheshimiwa Jenista J. Mhagamaambalo nalo huwa ni chanzo cha migogoro mikubwainayotokea kwenye Vijiji na Sekta hii ya uchimbaji wa Madinikama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Sheria yetu inatambua kwamba,Mchanga, Mawe, ni Madini. Kwa hiyo, isionekane kwambasiyo Madini, na kwamba utengenezaji wa barabara aushughuli zozote zinazo involve uchukuaji wa rasilimali hiyo nilazima watu wa maeneo yale wanufaike, hili liko wazi katikaSheria, lakini maendeleo ni ubia, tunahitaji barabarawenyewe, tunahitaji kupata mambo mengine wenyewe.

Barabara nazo hizi ni msingi, na fedhazinazotengeneza barabara ni fedha za Serikali, tunapowekahivyo maana yake tunaongeza gharama ya utengenezajibarabara, itakuwa kubwa, na sijui tutapata kipi, lakini nisemeni suala la kukubaliana, tunataka kipi katika hivi.

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi nimwulize swali moja dogo lanyongeza. Mheshimiwa Naibu Waziri unafahamu kwambawananchi wanaopatikaka katika Wilaya ya Kasulu, kule

[MHE. JENISTA J. MHAGAMA]

Page 26: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

26

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

katika Kijiji cha Makele hivi karibuni kupitia oparesheniKimbunga, baadhi yao Migodi yao ya chokaa ililipuliwa namoja ya sababu ambayo imepelekea ni kwa sababu Serikaliimekuwa inaona kwamba wale watu ni wachimbaji haramu.

Jambo ambalo siyo kweli kwa sababu Wizaraimewapa leseni, lakini wanazungushwa sana na Wizara yaMaliasili na Utalii kwenye kupewa vibali vya kuingia kwenyemaeneo yale ambayo Serikali imeiita ni Hifadhi. Ningependanipate kauli ya Serikali, ni lini contradiction hii ya Wizara yaNishati na Madini ya kutoa leseni, halafu Wizara nyinginewanakuja wanawazuia tena, hii contradiction itaisha lini?

Mheshimiwas Spika, ni serikali moja au ni serikalimbili?

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGE B.SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swalila Mheshimiwa Moses Machali kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli eneo hili la Makele nisehemu ya Hifadhi ya Taifa, na kama nilivyosema, haki yakuchimba Madini, ukishaipata ile haki siyo kwamba haki yamtu anayemiliki surface right inapotea, taratibu zinapaswazifuatwe, na yako maeneo ya mfano ambayo imetokea hivyona Wizara hii ya Maliasili na Utalii ikatoa vibali, lakini taratibulazima zifuatwe.

Siyo tu ukiwa na ile leseni, basi una access mining kwaurahisi, hapana, lazima uhakikishe umelipa fidia, lazimautambue haki za watu walioko wanaomiliki hapa juu. Kamakuna watu wa Mashamba, kama kuna watu wana Nyumba,ni lazima kutambua.

Mimi nadhani na nichukue nafasi hii kuwaomba sanana kuwashauri wachimbaji hawa, ambao MheshimiwaMachali anawatetea leo kwa sababu ni wachimbajiwadogo, lakini naamini ingekuwa ni mchimbaji mkubwaasingefanya hivyo.

[MHE. MOSES J. MACHALI]

Page 27: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

27

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Kwa Kanuni na Sheria iko palepale, kwamba lazimakutambua surface right, na haki hii iko chini ya Wizara yaMaliasili na Utalii. Kwa hiyo, tujaribu kufuata taratibu tuonenamna ya kusaidia, na sisi Wizara yetu iko tayari kusaidiapale ambapo pataonekana msaada wetu unahitajika wasababu ndiyo tuliotoa leseni ya kuchimba.

SPIKA: Swali la mwisho katika hili, Mheshimiwa Telele.

MHE. KAIKA S. TELELE: Mheshimiwa Spika, ahsante,mimi nilitaka kuuliza tu kama aina hii ya leseni wanapewapia wageni au ni wazalendo tu peke yake.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGE B.SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swalila Mheshimiwa Telele kama ifuatavyo:-

Ingawa siyo rahisi kujua swali alivyoliuliza, lakini zipoleseni za aina mbalimbali, ziko leseni za wachimbaji wadogo(Primary Mining License) ambazo zinatolewa kwa wazalendotu na ziko zile za kati na kubwa ambazo zinatolewa eitherkwa wageni hata kwa wazalendo. Kwa hiyo, kwa leseni hiziambazo tumesema hapa ni zile ambazo ni Primary MiningLicense ambazo zinatolewa kwa wazawa tu.

SPIKA: Tunaendelea na Wizara ya Fedha, MheshimiwaHamad Rashid Mohamed, atauliza swali hilo.

Na. 35.

Kampuni Zilizomaliza Muda wa Kusamehewa Kodi

MHE. HAMAD RASHID MOHAMED aliuliza:-

Je, ni Kampuni ngapi zimemaliza ule muda wakusamehewa kodi na wanadaiwa kiasi gani katika benkiwalimokopa?

[WAZIRI WA NISHATI NA MADINI]

Page 28: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

28

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYASALUM) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziriwa Fedha, naomba kujibu swali la Mheshimiwa HamadRashid Mohamed, Mbunge wa Wawi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Uwekezaji ya mwaka1997 inatoa muda wa mpaka miaka mitano kwa ajili yakuanzisha miradi ya uwekezaji na katika kipindi hicho, miradihiyo hupata misamaha ya kodi kwenye vifaa vya mitaji(capital goods) . Toka mwaka 1997 – 2007 jumla yamakampuni 5,002 ya uwekezaji yalikamilisha ujenzi wa miradiyao na hivyo hayapatiwi misamaha ya kodi.

Mheshimiwa Spika, miradi iliyo katika hatua yauanzishwaji na inayopata misamaha ya kodi kwa sasa ni ileiliyosajiliwa mwaka 2008 – 2013. Nafuu ya misamaha ya kodiinayotolewa ni ile ya forodha kwa asilimia 75 na VAT asilimia10.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mikopo, hivi sasaTIC kwa kushirkiana na BOT na NBS inafanya utafiti kwa ajiliya kupata mitaji iliyoingizwa nchini na makampuni yauwekezaji kutoka nje (capital inflows) ili Serikali iweze kubainikiasi cha mitaji kilichoingizwa kama “equity” na mikopo.

Aidha, sambamba na utafiti huu, pia TIC kwakushirikiana na NBS na UNIDO inafanya utafiti mwingine kwasample ya makampuni 500 ya ndani ili kujua kiasi cha mitaji.Matokeo ya tafiti hizi yatatolewa kwa wadau baada yakukamilika.

MHE. HAMAD RASHID MOHAMED: Mheshimiwa Spika,nakushukuru, maswali mawili madogo ya nyongeza. Mwaka2007 ambapo Waziri anasema walisamehe, misamaha ileilifutwa, lakini bado kiwango cha misamaha ya kodi ilibaki ileile asilimia 3.5, ni kwa sababu zipi kama makampuni 5000

[NAIBU WAZIRI WA FEDHA]

Page 29: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

29

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

yalifutwa misamaha yake, lakini bado kiwango chamisamaha ilibaki pale pale.

Swali la pili, kutokana na survey iliyofanywa naInvestors Motivations Survey ya mwaka 2012 kwa nchi yaRwanda, Tanzania na Burundi, kati ya wawekezaji 450, ni 139tu, walisema wao kama hawakupata misamahahawatawekeza, lakini 413 hawana tatizo bila ya misamahawangeweza kuwekeza. Kwa nini Serikali inaendelea kutoamisamaha wakati wawekezaji walio wengi kwa kutokana navivutio vya Tanzania wako tayari kuwekeza bila yamisamaha?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYASALUM): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawiliya nyongeza ya Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli misamaha inafutwa lakiniutaona kwamba level imebaki pale pale, ni kwa sababu,wakati miradi mingine inamaliza misamaha ya kodi, kunamiradi mingine inaingia.

Vilevile nayo inapata hizi exemptions. Kwa data tukwamba , kuanzaia mwaka 2011 inflow, investors ambaowamekuja na miradi yao inafikia thamani ya dola milioni1229.4, lakini mwaka 2012 kumeingina dola 1706.9 milioni,mwaka 2003 kumeingia dola 1852.9. Utaona kwambakwamba kuna kuwa inflow nayo inazidi, wakati tunaondoa,lakini wengine nao wanarudi.

Swali lake lingine, ni kweli hiyo ni survey iliyofanywa,lakini vilevile sisi kama Wizara ya Fedha tume commission astudy, peer tax exemption study ambayo ina study maeneoya excemption. Katika study ile utaona kwamba wawekezajikweli wasingependa kupata exemption, lakini iwapo tutaimprove investment climate. Kwa sasa investment climate

[MHE. HAMAD RASHID MOHAMED]

Page 30: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

30

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ya Tanzania bado iko chini, na hiyo tuna compensate withexemption.

Utaona kwamba wawekezaji wanakuja,wanachopenda kwanza ni market potential ambayo sisikwa Tanzania tunayo, lakini ukienda kwenye mrorongowanahitaji roads. Kwa Tanzania maeneo mengi roads zakehaziko katika hali nzuri, wanahitaji competitive labour,Tanzania bado labour yetu iko katika chini and is not thatcompetitive.

Kwa hiyo, wakisema kwamba hawahitaji exemption,lakini provided kwamba, mambo haya yote yamewekwakatika hali nzuri. Si kweli kwamba wanakuja and they don’tneed any exemption, lakini kama tukijaribu ku-address issueshizi nyingine, tuki improve climate investment yetu hapaTanzania, basi naamini hata misamaha ya kodi itarudi chini,ahsante. (Makofi)

MHE. DAVID Z. KAFULILA: Mheshimiwa Spika, ahsante,Serikali hii ina tatizo kubwa sana la kutoa misamaha ya kodipasipo utaratibu na ambayo kwa kiasi kikubwa haina tija, naushahidi wa hilo ni taarifa ya TRA ambayo imesema kwambamisamaha ya kodi ambayo imetolewa kwenye uagizaji waSukari na Mchele, haikuwa na tija kwa sababu bei ilehaikushuka kama ambavyo ilitarajiwa.

Naomba kupata majibu ya Serikali, ilizingatia hojagani kutoa misamaha ya kodi kwenye uagizaji wa Mchelena Sukari na wakati TRA inasisitiza kwamba hakuna tija kwasababu impact yake kwenye bei haionekani?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYASALUM): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongezala Mheshimiwa David Kafulila kama ifuatavyo:-

Siwezi kukubaliana naye kwamba TRAwamezungumza kwamba hiyo misamaha haina tija, kwasababu wakati misamaha ya Mchele na Sukari ilipokuwa

[NAIBU WAZIRI WA FEDHA]

Page 31: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

31

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ikitolewa, Tanzania tulikuwa tume-face high food inflationrates, kulikuwa tu hiyo ndiyo sababu ambayo imeingia kwaajili ya kutoa hizo exceptions. Inawezekana sehemu nyinginehakukuwa na ile impact kwa ajili ya inflow, Dar es Salaamtumeona na sasa hivi tunajua kwamba food inflation ikochini kwa sababu bei za Sukari pamoja na Mchelezimeendelea kuwa stable, lakini kwa sehemu nyingine kwasababu tu ya ubovu wa infrastructure kweli ule msamahawa Sukari na Chakula ulipoingia haujaweza kufika sehemunyingine kutokana na ubovu tu wa infrastructures zilizopo.

Hiyo misamaha ya Mchele na Sukari ilipotolewakulikuwa kuna sababu muhimu na maalum kwa wananchiwa Taifa hili.

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kuniona, kwamba Serikali imekili kwambainatoa incentives kwa makampuni ya nje kuja kuwekezahapa. Kwa kuwa Serikali inapoteza kwa kutoa zile incentivesambao wao wange-claim kama ni taxes.

Je, Serikali inaweka kama hii ni uwekezaji kwa hawawawekezaji wanaokuja kama sehemu ya uwekezaji waoSerikali ni kutoa zile incentives na exemptions kwa kampuniambazo zinakuja kuwekeza. Kwa nini sasa ibakie kuwa nisehemu ya uwekezaji peke yake wakati Serikali imeshatoasehemu yake ya kodi kwenye kuwekeza huko?

SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Uwekezaji naUwezeshaji.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJINA UWEZESHAJI: Mheshimiwa Spika, naomba nimshukuru nakumpongeza Naibu Waziri kwa majibu mazuri na kwa niabaya Waziri wa Fedha, naomba nijibu swali la nyongeza laMheshimiwa Mangungu, kama ifuatavyo:-

[NAIBU WAZIRI WA FEDHA]

Page 32: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

32

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, tunavyoongea, misamaha kwaajili ya mitaji au uwekezaji, hakuna kodi ambayo tayariimeshalipwa, ila tunatoa incentives kwa wale waje.

Pili, mitaji inashindaniwa nchi zote siyo Tanzania tu.Kwa hivyo, wale wenye mitaji, wanapotaka kuwekezawanaona ni wapi ambapo mazingira ni bora zaidi, ikiwemona hii misamaha ya kodi, lakini tusingependelea sana kutoamisamaha wakati ambapo si lazima.

Mheshimiwa Spika, ninaomba Watanzania waonekwamba bila ya uwekezaji hakuna maendeleo. (Makofi)

Misamaha haitolewi kwa makampuni ya nje tu,inatolewa kwa makampuni ya ndani vilevile, na kamatunakubali hivyo, naomba niwaonyeshe kwamba uzoefuumeonyesha, kila tunapofuta misamaha hiyo ya kuvutia, siyoya kuondoa kodi ambayo ipo, ya kuvutia, uwekezajiunatelemka na takwimu zipo, na tutawapeni.

Ninaomba Watanzania wapende wawekezaji kwasababu ya kuendeleza maendeleo ya nchi yetu na ukuajiwa uchumi.

Na. 36

Matumizi ya Fedha za Kigeni Nchini

MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:-

Kumekuwepo na matumizi makubwa ya fehda za kigenihususan Dola za Marekani katika kununua bidhaa na hudumambalimbali katika masoko hapa nchini.

(a) Je, kwa kufanya hivyo kuna athari gani katika uchumiwa nchi yetu?

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI]

Page 33: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

33

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

(b) Kama kuna athari. Je, Serikali imechukua hatua ganikatika kurekebisha tatizo hilo?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYASALUM) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa ni ya Waziri wa Fedhanaomba kujibu swali Mheshimiwa Cecilia Daniel Pareso,lenye vipengele viwili kwa pamoja kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, endapo matumizi ya fedha zakigeni yatakithiri yanaweza kusababisha athari mbalimbalizikiwemo kupungu ufanisi wa sera za fedha, kupunguzauwezo wa Benki Kuu kutimiza wajibu wake kama mkopeshajiwa mwisho katika uchumi, yaani lender of last resolt, na kuwakero endapo watu watalazimika kufanya malipo kwa njia zakigeni.

Mheshimiwa Spika, kiwango cha matumizi ya Dolakatika uchumi wetu bado hatujafikia mahala pa kuwezakuwa na madhara ambayo tumeyataja. Uwiano kati yaamana za fedha za kigeni na ujazo wa fedha, ambapouliwahi kupanda hadi kufukia asilimia 34 mwaka 2003 kwasasa umeshuka hadi kufikia asilimia 27.2 mwezi Juni 2013.

Aidha kiwango cha amana za fedha za kigeniambacho kinazidi rasilimali za fedha za kigeni za Mabenkikil ikuwa asil imia 23 tu ya hazina ya fedha za kigeniinayotunzwa na Benki Kuu, hivyo tatizo la Benki Kuu kushindwakutekeleza wajibu wake wa mkopeshaji wa Mwisho badohalijaweza kutokea.

Mheshimiwa Spika, mnamo mwezi agosti 2007 Serikaliilitoa tamko rasmi kuhusu matumizi ya fedha za kigeni katikakulipia bidhaa na huduma katika soko la ndani. Katika tamkohilo Serikali i l iagiza kuwa mkazi yeyote wa Tanzaniaasilazimishwe kulipia bidhaa au huduma yeyote hapa nchinikwa fedha za kigeni isipokuwa tu mtu akiamua kwa hiari yakemwenyewe kulipia kwa kutumie fedha ya kigeni. Aidha

Page 34: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

34

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006 sehemu ya 3 kipengelecha 26 nayo imeweka wazi kuwa Shilingi ya Tanzania ndiyofedha halali kwa malipo ya bidhaa na huduma nchini.

Mheshimiwa Spika, sheria ya usimamizi wa fedhaza kigeni ya mwaka 1992 na kanuni zake za mwaka 1998zinatamka wazi kwamba Watanzania wanaruhusiwakupokea, kumiliki na kutumia fedha za kigeni kwa shughulizao za kiuchumi hapa nchini.

Aidha baada ya kuanza kutumika kwa sheria hii, akibaya fedha za kigeni inayotunzwa na Benki kuu iliongezekakutoka Dola za Kimarekani milioni 228.3 mwaka 1993 sawana asilimia 6 ya pato la taifa hadi kufikia Dola za KimarekaniMilioni 4,069 ambayo ni sawa na asilimia 14 ya pato la Taifakwa mwaka 2012.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, ahsante,naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006imeweka wazi kuwa Shilingi ya Tanzania ndiyo fedha halilikwa malipo ya bidhaa na huduma hapa nchini, na kwa kuwaSerikali ilitoa tamko mwaka 2007 kwamba Mtanzaniaasilazimishwe kulipa huduma hizo kwa fedha za kigeni, nakwa tamko hilo Serikali imetoa mwanya unaokinzana nasheria.

Je Serikali kwa kuweka matamko laini kiasi hichokutaifanya exchange rate ya Dola kuwa kubwa dhidi yaShilingi na ukizingatia demand motive ya fedha hizo mbiliyaani Shilingi na Dola?

Swali la pili, kwa kuwa Serikali imeacha hali iwe ilivyo,na baadhi ya bidhaa na huduma kupatikana kwa rate yaDola jambo ambalo linafanya gharama ya bidhaa nahuduma kuwa kubwa, nini kauli ya Serikali?

[NAIBU WAZIRI WA FEDHA]

Page 35: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

35

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYASALUM): Mheshimiwa Spika kwa niaba ya Mheshimiwa Waziriwa Fedha naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza yaMheshimiwa Pareso kama ifuatavyo.

Wakati tunatoa tamko hilo tuliweka wazi kwambakweli mwananchi asilazimishwe, asilazimiswe kutumia pesaya kigeni hususan Dola katika kupata huduma na bidhaa. Atthe same time tunamtaka mwananchi huyo huyo anawezakutumia fedha hiyo ya kigeni kwa shughuli zake za kiuchumi.Kwa hiyo hayo ni maeneo mawili tofauti. Ikiwa mtu labdahana shughuli zake za kiuchumi, anataka kununua bidhaakama ni capita kwa ajili ya shughuli zake za uchumi na bidhaahiyo haipatikani labda isipokuwa kwa fedha nyingine yakigeni basi hapo anaruhusiwa. Lengo ni kuweza tukumrahisishia mwananchi kuweza ku-invest na kuweza vilevile kutoa investment kwa kutumia fedha ya kigeni. Kwa hivyo,wakati tuna-control matumizi haya kiholela at the same timetunampa mwananchi fursa ya kuweza kujishajiisha kiuchumikwa kupata bidhaa kwa njia hiyo hiyo ya kigeni. Kwa hivyokumekuwa hakuna contradictory.

Swala la pili kwamba kama nilivyosema katika jibulangu la msingi kwamba kumekuwa hakuna athari mpakasasa hivi. Ili athari ya kiuchumi itokee basi, level ya fedha yandani, fedha yako ya local currency pamoja na fedha yakigeni iwe asilimia 50 hapo ndipo uchumi utaweza kuwadistorted.

Lakini sasa hivi kwa sababu ya control measuresamba zo Benki Kuu ya Tanzania imeweza kuzichukua kwaKuruhusu, lakini at the same time kwa ku-control matumizihaya tumeweze ku-stabilize na sasa tumeshuka asilimia 27 tuya fedha za kigeni katika mzunguko huu wa kiuchumi. Kwahivyo naomba tu mkumhakikishia Mheshimiwa Mbungekwamba kwa sasa hivi hiyo athari haijaweza kuathiri sanamzunguko wetu wa fedha hapa nchini.

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo.

[NAIBU WAZIRI WA FEDHA]

Page 36: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

36

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, pamoja na matumizi makubwaya Dola, hali ya pesa ya Tanzania imeimarika dhidi ya Dola.Je, ni sababu zipi mahsusi ambazo zimesababisha kuimarikakwa Shilingi hii?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYASALUM): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa fedha naomba kujibu swali la nyongeza laMheshimiwa Kadege kama ifuatavyo.

Sababu ziko nyingi, kwanza tukiangalia sera za fedhaambazo tunazi-implement hapa nchini zimesababisha fedhayetu iweze ku-stabilize. Lakini kuna measures za kiuchumiambazo zimechukuliwa, kwamba sasa hivi tunajitahidi at leastkuweza kuzalisha.

Sasa kwa sababu bidhaa nyingi zinapatikana ndanikwa hivyo ile motion ya kununua Dola, demand ya kununuaDola imekuwa imeshuka kwa sababu bidhaa nyingiwanaweza kuzipata humu ndani.

Kwa hivyo, sababu nyingi Mheshimiwa Spikatunaweza tukachukua muda mrefu sana kuanza kuzielezea,lakini kiufupi tu kwamba sera zetu za fedha pamoja na seraza matumizi pamoja na sera za kiuchumi ambazo tumewezakuzi-implement zimesababisha kwa njia moja ama nyinginekuweza ku-stabilize Shilingi yetu against Doa. Ahsante sana.

No. 37

Utaratibu wa Kuwawezesha Vijana wenye UlemavuKujiunga na VETA

MHE. MARGARETH A. MKANGA aliuliza:-

Page 37: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

37

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Serikali imedhamiria kujenga Vyuo vya Ufundi (VETA)kwenye kila Wilaya nchini ili kuwawezesha vijana kupatamafunzo ya fani mbali mbali ya kuwawezesha kujiajiri.

Je, kuna utaratibu gani mahususi umewekwa ilikuwawezesha vijana wenye ulemavu kujiunga?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDIalijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu naMafunzo ya Ufundi, napenda kujibu swali la MheshimiwaMargareth Agnes Mkanga, Mbunge wa Viti Maalum, kamaifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, Sera ya Elimu na Mafunzo yamwaka 1995, katika kipengele cha tatu kinazungumzia utoajiwa elimu na upatikanaji wa nafasi kwa makundi maalumkama vile walemavu, yatima na watoto wa mitaani. Hivyo,Serikali inatambua umuhimu wa kila mtoto kuwa na haki yakupata elimu bila ya ubaguzi wowote.Kwa msingi huo huo vijana wenye ulemavu wanaoombanafasi za kujiunga na vyuo vya ufunsi stadi huchaguliwa bilaubaguzi.

Matangazo ya kuomba nafasi za kujiunga na vyuovya ufundi stadi hutolewa kupitia vyombo mbalimbali vyahabari ikiwa ni pamoja na mbao za matangazo. Hivyo, vijanawanaoomba nafasi za kujiunga na vyuo vya ufundi stadihujaza form hizo ambazo zina kipengele cha kuainisha ainaya ulemavu ili kuweza kupata huduma kutokana na aina yaulemavu walio nao.

Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha Januari 2009 hadiDesemba, 2012 vijana wapatao 578 wakiwemo wavulana345 na wasichana 233, wenye aina mbalimbali za ulemavuwalihitimu mafunzo ya ufundi stadi katika fani mbalimbalihapa nchini.

Page 38: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

38

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Aidha, kwa kutambua mahitaji maalum yawalemavu, vyuo vya ufundi stadi vimeweka miundombinurafiki kwa walemavu a wa aina zote ili kuwawezeshakujifunza kwa urahisi. Hivyo, natoa rai kwa wazazi na waleziwote wenye vijana wenye ulemavu kuomba nafasi zakujiunga na vyuo vya ufundi stadi pale matangazo yakuomba nafasi hizo yanapotolewa.

MHE. MARGARETH A. MKANGA: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi.

Pamoja na majibu mazuri yaliyotolewa na Serikali,nikiamini kwamba kweli hivi vitu ni kweli kwa baadhi ya vyuolakini vyuo vingine bado hawajarekebisha masuala hayo,nina swali moja tu la nyongeza.

Kwa kuwa wazazi walio wengi wenye vijana haowenye ulemavu, wao kiuchumi hali zao zinakuwa hali dhoofu,masikini kutokana na kuwa na shughuli ya hawa watotokuwaangalia. Serikali inasemaje kuona uwezekano wakuwalipia gharama za mafunzo haya vijana hawa ambaowanaomba wenye ulemavu kwenye hivyo vyuo vya VETA?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa ELimu na Mafunzoya Ufundi, napenda kujibu swali moja la nyongeza laMheshimiwa Margareth Mkanga, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, anachosema hapa MheshimiwaMbunge ni kweli kwamba kama nilivyosema kwamba kunayatima, kuna walemavu na wengine wasiojiweza.

Mheshimiwa Spika, lakini ukienda kwenye vyuo vyaVETA nchini pote, ada ya kulipa mavunzo hayo ni Shilingi lakimoja na ishirini (120,000/=) tu. Hapa sisi tulikuwa tumewekasera hii kwa sababu ya kuhakikisha kwamba vijana wengiwanaokosa elimu ya sekondari na hata wale wanaopataelimu ya sekondari wakitaka kwenda kujifunza ufundi waendewakasome mafunzo hayo; kwa sababu gharama zakuwalipia waalimu na hata mchakato wa kupata karakana

Page 39: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

39

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

na mashine zile zinazoendesha vyuo ni ghali sana, lakiniada hii ni ndogo sana.

Lakini wazo la Mheshimiwa Mbunge bado ni wazo zurisana tutalifanyia kazi namna ya kupunguza ada kwa vijanahawa walemavu. (Makofi)

MHE. SUSAN L. A. KIWANGA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana.

Kwa kuwa suala la walemavu ni pana sana, naonaMheshimiwa Naibu Waziri anajibu kwa walemavu sijui wa ainagani; lakini kuna walemavu ambao ni viziwi, mabubu,wengine wana mtindio kama wa ubongo lakini wanawezakwenda shule. Kwa kuchukulia kwa mfano Wilaya yaKilombero kuna walemavu wasiopungua 400, hawa ambaowako mitaani, na hakuna chuo chochote katika mkoa waMorogoro ama Wilaya ya Kilombero, ambacho kinasaidiahawa walemavu kwa ajili ya kupata ufundi ili wajitegemeemaisha yao.

Je, Wizara ina mpango gani wa kuweka Kitengo chawanafunzi wenye ulemavu katika chuo cha Maendeleo yaWilaya ya Kilombero ili watoto hao wapate elimu ya Ufundina Kujitegemea kimaisha?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzoya Ufundi napenda kujibu swali la Mheshimiwa SusanKiwanga, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, aina za walemavu, labda siku-mention kwenye swali langu la msingi, lakini ni aina yawalemavu wote ambao wanapenda kwenda kusoma vyuovya ufundi.

Ndiyo maana nimesema kuna form ambazo huwazinatoka kila mwaka mwezi wa nane, kuomba kwendakusoma mafunzo haya ya ufundi. Siyo suala tu la kuweka chuo

Page 40: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

40

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

pale Kilombero lakini vyuo vya VETA kama nilivyosema vipokila Mkoa; hata pale Morogoro fani hizi zinatolewa.

Kwa hiyo nilikuwa naomba wale vijana wa Kilomberowaombe tu, na wakienda pale chuo cha VETA Morogoro,ama Dakawa pale watakuta kuna form kabisa, na hapanimekuja nayo form maalum, na mheshimiwa tunawezatukawasiliana hata nikakuchapia, bado ukapeleka kuleKilombero ukawapa vijana wanaotaka kwenda kujifunzahaya mafunzo ya VETA.

Suala hili ni kwa nchi nzima wala hakuna upendeleo.Wapo walemavu wa ngozi , albino wanachukua form nawanasoma, wapo blind, wale wasioona kabisa na wapo waledeaf wasiosikia, lakini vile vile kuna wale mchanganyikoambao tunawaita blind-deaf yaani wasioona na kusikia, nawale vile vile walemavu wa viongo. Wote hawa ni walemavuambao nimesema wako 578, tayari kwa trend ya miakamitatu wamemaliza vyuo vya ualimu.

Kwa hiyo, hakuna upendeleo wowote. Kamanilivyosema hata kwa Waheshimiwa Wabunge wengine,kama wapo majimboni basi tuwasiliane na mimi niwezekuwapa form waweze kujaza. Pale kwenye form wamesemakwamba chagua chuo unachotaka kwenda. Kwa hiyo siyolazima wawe wanasoma Kilombero, anaweza akatokaKilombero anaenda Dar es Salaam, akatoka Kilomberoakaenda Mbeya.

MHE. MICHAEL LEKULE LAIZER: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.

Kwa kuwa ni kilio cha Wana Longido wanalia kwamuda mrefu wanalia kwamba wanahitaji Chuo cha VETA,Waziri akatuambia tutenge eneo na tumekwishatenga eneokwa muda mrefu sana.

Je, ni lini Serikali itajenga Chuo Cha VETA katika Wilayaya Longido ili vijana wa aina zote wanaotaka kujiunga na

[NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI]

Page 41: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

41

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

VETA waende kusoma huko kuliko kuzunguka kulindanyumba za watu?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzoya Ufundi, napenda kujibu swali moja la nyongeza laMheshimiwa Mbunge Laizer, Mbunge wa Longido, kamaifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, ni kweli, kama tunavyoendeleakuahidi kuanzia mwaka 2011, 2012 hata mwaka huu majibuni yale yale kwamba katika ilani ya Chama cha Mapinduzitumedhamiria kwamba tutajenga vyuo vya VETA kila Wilaya.

Mpango huo ndivyo unavyoendelea na kamaninavyosema kila siku kwamba tumeshsaanza, Chuo chaMakete kimeshamalizika na Wanafunzi wameshaanzakusoma pale, na Mheshimiwa Rais wiki iliyopita alikuwa kulena amekizindua Chuo cha Makete na mambo yanaendavizuri. Baada ya hapo tunahami kwenye vile vyuo vinginevitano vya wilaya; Ludewa, Kilindi, Ukerewe, Chunya naNamtumbo. Baada ya hapo tutafuata Wilaya nyingine.

Mheshimiwa Spika, lakini baada ya kuona kwambamlolongo wa kila mwaka vyuo vinne vinne ama vitano nimlolongo mrefu sana, na tunaweza tukafika mpaka mwaka2020 hapa tusimalize Wilaya zote, tuliamua kwamba popotepale penye Chuo cha Maendeleo ya Jamii (FDCs)tuanzekutoa mafunzo ya VETA.

Kwa hiyo kwa mwaka wa jana tumebadilisha amatumeweka mafunzo ya vyuo vya ufundi vya VETA kwenyevyuo 25, ambavyo kwa sababu sikujua ungeuliza ningewezakuja kusoma hapa, kwa hiyo tumebakiza vyuo 30 ambapo

[NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI]

Page 42: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

42

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ndiyo trend kwa mwaka huu kwamba tutavibadilishatuanze kuingiza mafunzo ya VETA.

Kwa upande wa Longido kule hakuna chuo chochotekwa FDCs wala VETA. Kwa hiyo Longido iko kwenye kati yaWilaya 28 ambazo baada ya kupata fedha tumeshaandikamaandiko mbalimbali, tukishapata fedha tu tayari Wilaya yaLongido iko kwenye mpango wa kujengewa Chuo cha VETA.

No. 38

Vyuo vya VETA Kutoa Mafunzo kwa Madereva waMatrekta

MHE. ABDULSALAAM S. AMER aliuliza:-

Pamoja na Serikali kujenga Vyuo vingi vya VETA nchinilakini bado kuna uhaba mkubwa wa Madereva wa matrekta.

(a) Je, kwa nini Vyuo vya VETA visitumike kutoa taalumaya Udereva wa Matrekta na jinsi ya kutumia vyombohivyo?

(b) Je, kwa nini Vyuo hivyo pia visitoe elimu ya jinsi yakuvifanyia matengenezo vyombo hivyo?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu naMafunzo ya Ufundi, napenda kujibu swali la MheshimiwaAbdulsalaam S. Amer, Mbunge wa Mikumi, lenye sehemu(a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Sera ya Kilimo,Serikali imekipa kilimo umuhimu wa pekee kwa kutenga Vyuovitano (5) nchini vya Ufundi Stadi, chini wa usimamizi wa VETA

Page 43: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

43

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kwa lengo la kutoa mafunzo ya udereva wa Matrekta naStadi za kilimo kwa wanaohitaji.

Vyuo vinavyotoa mafunzo hayo ni Chuo cha VETA,Kihonda na Dakawa kwa pamoja viko mkoa wa Morogoro,Chuo cha VETA Mpanda mkoani Katavi, Chuo cha VETAOljoro mkoani Arusha na Chuo cha VETA Manyara kilichopomkoa wa Manyara. Mafunzo yanayotolewa yanahusishaudereva wa matrekta na jinsi ya kutumia matrekta hayo, lakinivile vile na jinsi ya kuvifanyia matengenezo vifaa hivyo.

Jumla ya vijana waliohitimu mafunzo hayo kuanziamwaka 2010 hadi mwaka wa jana 2012, kwa kozi yaudereva wa matrekta kwa muda mrefu ni vijana 252 nakozi ya udereva wa matrekta muda mfupi ni 85.

Aidha, jumla ya wanachuo wanaoendelea namafunzo kwa mwaka huu kwa kozi ndefu ya udereva wamatrekta ni vijana 158 na mafunzo ya kozi ya muda mfupi nivijana 14.

Mheshimiwa Spika, kutokana na gharama kubwa yakuendesha mafunzo hayo, Serikali ilitenga vyuo vitano tu ilikuweza kutoa mafunzo kwa ufanisi zaidi. Serikali itaendeleakuviimarisha vyuo hivyo kwa ununuzi wa matrekta nakuongeza wataalam. Hivyo, natoa rai kwa wananjamii wenyekuhitaji kupata taaluma hiyo na ujuzi katika vyuo hivyowapeleke maombi yao katika vyuo vinavyotajwa kwani hatanafasi za mafunzo bado ni nyingi kuliko wanaoomba.

MHE. ABDULSALAAM S. AMER: Mheshimiwa Spika, ninamaswali mawili ya kuongeza.

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri yaMheshimiwa Waziri, sasa hivi mahitaji ya Matrektayameongezeka nchini. Kama Waziri alivyosema ameruhusu

[NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI]

Page 44: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

44

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Vyuo vitano (5) kutoa mafunzo hayo, ninaona haiwezikutekeleza kauli mbiu ya kilimo kwanza. Mahitaji ya Matrektana Madereva wa hayo na Matrekta ni mengi.

Je, kwa nini, Serikali isione huu ni wakati muafaka wakuruhusu vyuo vyote kutoa mafunzo hayo ya Udereva waTrekta nchini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukitaka kuongeza ajira kwa vijanawetu vijijini, na kupunguza ongezeko la vijana kwa ajili yakutafuta kazi za ajira.

Je, Serikali haioni ni wakati muafaka wa kuruhusukupunguza gharama ya mafunzo ya Trekta au kutoa kabisaada kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya Udereva wa Matrektavijana wetu waliopo vijijini? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Abdulsalaam Selemani Ameir,Mbunge wa Mikumi, kama hivi ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kuhusu idadi yavijana wanaoomba kujiunga na VETA kwa kuja kuchukua fanihii ya Udereva wa Matrekta. Ninachoweza kusema hapalabda sisi Wabunge tukahamasishe huko kwenye Majimboyetu ili vijana hawa wajitokeze.

Lakini ukweli ni kwamba baada ya kuona kwambakwanza gharama ya kuendesha yale Matrekta na kununua,maana yake ili kuendeshe hii kozi, ya Agro Mechanics, upateMatrekta pamoja na vile vyombo vyake na vifaa vyake.

Ni gharama ya shilingi milioni 193. Kwa hiyo tuliamuakama Serikali kutenga vyuo hivi vitano kwa ajili ya kuendesheamafunzo hayo. Lakini mpaka hivi ninavyosema vijanawanaojiunga ni wachache kuliko vyuo. Kwa hiyoWaheshimiwa Wabunge kama mtahamasisha vijana waje

[MHE. ABDULSALAAM S. AMER]

Page 45: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

45

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wasome kozi hii bado tunaweza tukaongeza na kupanuakwenye vyuo vingine.

Swali la pili, kuhusu kupunguza gharama za mafunzo.Kama nilivyosema hata kwenye jibu la swali la MheshimiwaMagareth Agnes Mkanga. Mafunzo ya vyuo vya VETAyanatolewa kwa ada ndogo sana. Tena hata ukimchukuamtoto wa Sekondari anayesoma miaka minne, naukimchukua na kijana wa VETA anayekwenda kujifunza iliajiajiri, unakuta hapa kwa mwaka kijana analipa shilingi120,000/= tu. Lakini chakula anapata pale na ada yamasomo.

Kwa hiyo, ni ada ndogo sana Mheshimiwa Mbunge.Nilikuwa ninaomba kwa hili tukubaliane na hali halisi kwambashilingi 120,000/= kwa mwaka mtoto anapata chakula pale,maji, umeme na kulipa mishahara na gharama nyingine zaMafunzo, na kama nilivyosema vyombo hivi bado gharamahii ni ndogo sana. (Makofi)

MHE. SUSAN A. LYIMO: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Spika, Ufundi bila ya vitendo ni kazi bure,yaani practicals. Kumekuwa kuna malalamiko makubwasana kwamba Wanafunzi wanaosoma katika vyuo hivi vyaufundi, hawapati fedha kwa ajili ya kufanya practicals.Matokeo yake wanamaliza bila kuwa na ufundi stahili na hiiinatokana na kwamba tengeo, au ruzuku inayopelekwakatika Vyuo vya VETA, ni ndogo sana, ukilinganisha na ileasilimia inayotakiwa kwenda.

Je, nilitaka kujua kutoka Wizarani. Ni lini wataongezafedha katika vyuo hivi ili wanafunzi waweze kumaliza wakiwana ufundi wa uhakika na waweze kuajiriwa sehemu zozotezile wanazokwenda?

[NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI]

Page 46: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

46

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UNFUNDI:Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Susan A. Lyimo, ni Waziri Kivuliwa Wizara yetu.

Kwa hiyo, nisingelipenda swali hili nimjibu kinamnaambavyo sintakuwa na ufahamu nalo sana. Lakini ni swalizuri. Mimi nilikuwa ninaomba kwa sababu sijawahi kupatamalalamiko yoyote kutoka kwa vijana wakilalamika kwambahatupati fedha kwa ajili ya practical kwenye vyuo vya ufundi.

Mheshimiwa Spika, mimi nilikuwa ninaomba aliwekeliwe swali la msingi ili niweze kulijibu kwa ufasaha zaidi.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Spika, Serikaliimejenga Chuo chenye hadhi sana cha VETA katika Jiji laArusha. Lakini miundombinu kufika kwenye Chuo hicho, hasabarabara wakati wa masika, imekuwa inaleta shida sanahata walimu kutokufika kwa wakati,, ama wakati mwinginekutokufika chuoni kabisa. Lakini vile vile kuna tatizo kubwa lamaji katika chuo kile na wamechimba visima mara mbili,ninafikiri bila kupata maji ya kutosha.

Je, Serikali ina mpango gani kwenye chuo hicho kizurisana, ili kiweze kuwa na hadhi ya wanafunzi kusoma bila yamatatizo.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali moja la nyongezala Mheshimiwa Mbunge wa Arusha Mjini Ndugu yetu Lemakama hivi ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, swali hili liko very specific, kwambalinagusa miundombinu ya chuo husika cha pale Arusha Mjini.Mimi ninaomba nifanye mawasiliano na Mamlaka husika ilinipate majibu kamili ya swali hili na tuweze kujua kwambamiundombinu na mambo mengine kama alivyosema yamaji, halafu tuweze kuwasiliana na Mheshimiwa Mbungenitampatia majibu yaliyokamilika.

Page 47: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

47

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

SPIKA: Ahsanteni sana.

Waheshimiwa Wabunge, muda wa Maswaliumekwisha. Mmeona tume relax katika maswali ya Nyongezakwa sababu tulikuwa hatuna Maswali ya Waziri Mkuu, lakinisiyo kwamba hiyo ndiyo kawaida. Kawaida uliza maswalimafupi ili tuweze kupata nafasi kwa wachangiaji wengi.Ninashukuru Mawaziri wanaendelea kujibu maswali yao kwakifupi na hiyo inatusaidia kuongeza muda wa kujadili. Kwahiyo, ninawaomba muendelee na utaratibu huo.

Waheshimiwa Wabunge ninapenda kuchukua fursahii kuwatambua Wageni waliopo. Bahati mbaya waliokaakwenye Speakers Gallery sijapata majina yao. I am sure niwageni wetu, but I did not have the name, so I will do it in theafternoon.

Tunao Wanafunzi 40 na Walimu wanne (4) kutokaShule ya Sekondari ya Kiwanja cha Ndege Dodoma.Wanafunzi wa Shule ya Sekodnari wako wapi ninawaombawasimame.

Ahsanteni sana. Karibuni sana. Tunao Wanamichezo24 kutoka Halmashauri ya Mji Mpanda Mkoa wa Katavi.Wakiongozwa na Ndugu Bahati Mwaikafu. Ninawaombamsimame hapo mlipo.

Wanamichezo ahsanteni. Tunao viongozi 14 wa Timuya Mchezo wa Pull Table Tanzania ambao ni washindi watatu (3) barani Afrika, wakiongozwa na Fred Mushi.Ninawaomba hao wanamichezo wasimame hapo walipo.

Wanamichezo hao kama mlivyowaona,wameambata na na viongozi wao yupo, Mheshimiwa FredMushi – Makamu Mwenyekiti. Wengine mkae ili viongoziwaliosimama tuweze kuwaona. Yuko Ndugu Patrick Nyagusi,mshindi wa Afrika. Hongera sana. Ndugu Patrick kamamlivyoomuona ndiye mshindi wa Afrika katika mchezo ya PullTable. Hongera sana Bwana Patrick. Tunao wageni watatu

[SPIKA]

Page 48: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

48

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ambao ni Wanafunzi kutoka katika Chuo Kikuu cha St.John’s. Wako wapi hao wanafunzi wa St. John’s. karibunisana. (Makofi)

Ninao wageni niliokuwa ninasema sijapata majinaya. Nimeyapata, yuko Balozi wa Norway hapa nchiniMheshimiwa Ingunn Klepsvick. Karibu Mheshimiwa Balozi,welcome to Tanzania, yuko na msaidizi wake Bi. ElizabethSchwabe-Hansen, welcome. I am sure I going to see you inthe afternoon. Thank you very much. Tunao wageni waliofikaBungeni kwa ajili ya mafunzo. Ahsanteni sana na wageniwengine ambao hatukuwataja pia wanakaribishwa.

Waheshimwia Wabunge, Mwenyekiti, wa Kamati yaBunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara MheshimiwaMahmoud H. Mgimwa, anaomba niwatangazie wajumbe waKamati yake kwamba leo hii saa tano (5.00) kutakuwa nakikao cha Kamati. Kikao hicho kitafanyika katika Ukumbi waPius Msekwa B.

Lakini wanaomba kabla ya Saa Saba. Wanatakiwawamuarifu Spika, kwa nini wanaomba kukutana muda huona wapewe ruhusa. Mikutano yote inatakiwa ifanyike saasaba. Kama unabadilisha muda unatakiwa mumuarifu Spika.Kwa hiyo ninaagiza Kamati hii nayo ikutane saa saba.

Halafu Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu zaSerikali, Mheshmiwa Deo Fil ikunjombe anaombaniwatangazie wajumbe wa Kamati yake kuwa leo mchanasaa saba na robo (07.15) watakuwa na kikao katika ukumbinambari 219.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo yaJamii, Mheshimiwa Jenista J. Mhagama, anaombaniwatangazie wajumbe wa Kamati yake kunako majira yasaa saba mchana watakuwa na kikao katika Ukumbi waMsekwa C. Mheshimiwa Pindi H. Chana – Mwenyekiti waKamati ya Katiba Sheria na Utawala, ameniomba

[SPIKA]

Page 49: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

49

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

niwatangazie wajumbe wa Kamati yake ya kwamba leosaa saba mchana watakuwa na kikao chao katika Ukumbiwa Msekwa D.

Halafu Mkurugenzi wa Mambo ya Bunge ameniombaniwatangazie Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati ya Uongozi,nafikiri Spika, mwenyewe kuwa tutakuwa na kikao cha Kamatiya Uongozi leo baada ya kipindi hiki cha maswali. YaaniKamati ya Uongozi ile ya Bunge tutakuwa na kikao sasa hivibaada ya kumaliza kipindi cha Maswali.

Waheshimiwa Wabunge kama tulivyoahidi jana,kulikuwa kuna hoja mbili za Waheshimiwa Wabunge. Hojaya Mheshimiwa Said J. Nkumba na Mheshimiwa Lugola, kwahiyo ndiyo maana ninaomba Kamati ya Uongozi twendetukutane kule tukaweza kuona namna nzuri ya kuendeshashughuli nzima.

Kwa hiyo, kwa sababu hiyo nitamwomba Mwenyekitiwa Bunge Mheshimiwa Zungu, aweze kuendelea na shughuliinayofuata baada ya kuingia kwenye kipindi kingine. (Makofi)

HOJA ZA SERIKALI

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa TaifaKwa Mwaka 2014/2015

(Majadiliano yanaendelea)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge ninaomba muwebrief. Kwa sababu kama mnavyoona muda umetutupamkono.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Spika,ninaomba mwongozo wako kwa mujibu wa Kanuni ya 39(i), ambayo ninaomba niisome. “Waziri anaweza kuulizwa

[SPIKA]

Page 50: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

50

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Maswali kuhusu masuala yoyote ya Umma, au jambo linginelolote, ambalo linasimamiwa na ofisi yake.

Vile vile Mbunge yeyote anaweza kuulizwa Mawalikuhusu mambo yoyote anayohusika nayo, kutokana nakuteuliwa na Bunge kushughulikia mambo hayo.”

Mheshimiwa Spika, mapema wakati wa kipindi chaMaswali, wakati majibu yanatolewa kwa Swali Nambari 32,Swali hili lilielekezwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Mahusiano na Uratibu na Mheshimiwa Stephen Wasiraakatoa majibu ya swali hili. Lakini baada ya kutoa majibu.Mheshimiwa Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge akasimama,kuongeza majibu ya Serikali na ilikuwa ni haki kusimama kwasehemu ya kwanza ya Kanuni, kwamba Waziri mwingineawaweza kutoa nyongeza ya majibu.

Lakini wakati akitoa majibu hayo akawa anatoamajibu akizungumzia kama Mbunge, akisema Mbunge,Mbunge, Mbunge, akirudia, katika jambo ambalo swali lamwuliza swali la nyongeza Mheshimiwa Chiku Abwao, lilihusuJimbo ambalo ni la Waziri mwenyewe.

Mheshimiwa Spika, alifanya hivyo, na alipokuwaakiendelea na alipomaliza ikaonekana kama vile ni sahihikujibu kama Mbunge, lakini Kanuni ya Wabunge wenginekujibu maswali inahusu (i) Wabunge walioulizwa, yeye kamaMbunge hakuulizwa swali kuhusu lile swali lililokuwa likiulizwa.Lakini pili, inahusu Wabunge walioteuliwa na Bunge kwa ajiliya kazi maalum, yeye hakuteuliwa na Bunge kwa ajili ya kazialiyokuwa akiifanya hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa vyovyote vile kilichotokea leoni ushahidi wa namna ambavyo mchanganyiko wa vyeo katiya Uwaziri na Ubunge unathari katika usimamizi wa Serikali.Ninaomba mwongozo wako ili jambo hili lisijitokeze tena.Waziri atakiwa kuepuka kutumia nafasi yake ya Uwazirikujibu masuala ya Jimboni kwake kama ambavyoalivyofanya.

[MHE. JOHN J. MNYIKA]

Page 51: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

51

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, ninaomba Mwongozo wako.(Makofi)

SPIKA: Mpaka mtakapobadilisha Katiba.Kilichotokea ni sahihi.

(Hapa Mheshimiwa John J. Mnyika Alisimama)

SPIKA: Mheshimiwa ninakuomba tafadhali ukae.Mheshimiwa John J. Mnyika ninakuomba ukae. Kwa niniunakuwa mbishi? Kanuni umeishika mwenye unatakiwakunisikiliza na mimi pia.

Alichokisema Waziri, Mbunge yeyote anayo haki yakujibu kitu kinachomhusu. Soma Kanuni nyingine. Anayokanuni.

Tusibishane Kanuni zetu ziko wazi, hata weweungeliguswa kwenye eneo lako kama unahusika, utasimamana mimi nitakuruhusu, power of replying ni wajibu wako.Power of replying ni haki ya Mbunge yeyote hapaatakayeguswa.

MBUNGE FULANI: Hata kama ni Waziri?

SPIKA: Waziri ni Mbunge, hiyo ya kwanza. Tuendeleena Mheshimiwa Mbunge mwingine. Mheshimiwa DavidKafulila, uwe brief.

MHE. DAVID Z. KAFULILA: Mheshimiwa Spika,nimesimama kuomba Mwongozo wako kwa mujibu waKanuni ya 68(vii) kufuatia tukio ambalo limejitokeza wakatiMaswali yakijibwa. Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed,aliuliza kuhusiana na tatizo la misamaha ya kodi.

Ukanipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongezaambapo nilitaka majibu ya Serikali kufuatia taarifa ya TRA,inayoonyesha kwamba misamaha inayotolewa kwenyesukari na mchele haina tija kwa walaji, ambao kimsingi ndiyomakusudio ya Serikali. Nikataka maelezo ya Serikali. Majibu

[MHE. JOHN J. MNYIKA]

Page 52: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

52

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

niliyojibiwa, Wizara ya Fedha ikaonyesha kwamba taarifahiyo siyo kweli. Lakini pia ikaonyesha kwamba jambo hiloau uamuzi huo wa misamaha ya kodi kwenye mchele nasukari ina tija.

Mheshimiwa Spika, mimi ni mjumbe wa Kamati yaUchumi, Viwanda na Biashara. TRA wanatoa taarifa zaokwenye Kamati yetu. Taarifa ninayo hapa, labda kwa maslahiya Bunge lako Tukufu niseme kwamba.

SPIKA: Ninakuomba Mheshimiwa Mbunge, jinsiunavyoelekeza hoja zako utaratibu siyo huo. Kwa sababukama ni suala la issue ya swali, hatuwezi kuanza ku-debateswali lililojibiwa. Kama una hoja yoyote andika maelezo sisitupate majibu. Kwa sababu hatuwezi kubishania maswali.Wabunge ninaomba msikilize hizi ni Kanuni, siyo kwambamnaenda kama tunaendesha Club ya pombe.

Ninachomuagiza Mheshimiwa Kafuli la, aendeakaandike, kusudi lije kwa utaratibu wake, hatuwezikubishana maswali yote hapa. Kaandike leta ije kwautaratibu unaohusika. Mheshimiwa Mbunge yulealiyesimama alikuwa ni nani?

(Hapa Mheshimiwa David Z. Kafulila Alisimama Tena)

SPIKA: Mheshimiwa Kafulila nimeishakuagiza tayariukafanye nilichokuagiza. Waheshimiwa wengine ni nanialiyesimama?

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika,nimesimama kuomba mwongozo wako kwa mujibu waKanuni ya 64(i)(a). Ambayo inasema kwamba: “Bila kuathirimasharti ya Ibara 100 ya Katiba yanayolinda na kuhifadhiuhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge. Mbungehatatoa ndani ya Bunge taarifa ambazo hazina ukweli.”

Mheshimiwa Spika, wakati nimeuliza swali lanyongeza kutokana na swali ambalo liliulizwa na MbungeMheshimiwa Profesa Peter M. Msola, swali nambari 34.

[MHE. DAVID Z. KAFULILA]

Page 53: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

53

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Naibu Waziri katika majibu yake, kuna statement ambazoamezitoa kidogo zinaashiri kama kwamba yeye ni Nabii,anajua ambacho mimi ningelieweza kufanya jambo ambalohalina ukweli. Alizungumza. “Suppose ingelikuwa niMakampuni makubwa ya uchumbaji wa Madini, mimiMbunge nisingeliweza kuwatetea. Lakini kwa sababu niwachimbaji wadogo wadogo ambao wanaopatikana kuleMakere, wachimbaji wa chokaa, ninawatetea.”

Mheshimiwa Spika, nilikuwa ninaomba MheshimiwaNaibu Waziri aweze kunithibitishia, amepata wapi ithibati auushahidi kwa kusema kwamba nisingeliweza kuwateteawachimbaji wakubwa wakubwa. Watu baadhi ya Mawaziriwamekuwa wanajibu kiainaaina, hovyo hovyo tuwanavyofikiria majibu ya kubeza Wabunge.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa ninaomba kwa sababualichokizungumza hayupo akilini mwangu, na wala hayupondani ya utashi wangu, na mimi ni Mbunge wa wote.Wachimbaji wakubwa na wachimbaji wadogo.

Ninaomba mwongozo wako ni kwa nini, MheshimiwaWaziri asiweze kuniomba radhi. Ndiyo aniombe radhi, kwasababu alichokizungumza sikuwa katika perspective hiyokabisa Mheshimiwa Spika.

Mheshimiwa Spika, ninaomba mwongozo wako juuya hili. Kwa sababu baadhi wamekuwa wanajibu maswalikiaina aina tu ambavyo wanavyojisikia na Bungelimeonekana ni mahali pa kuweza kuzungumza vyovyotevile.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, ninawaomba mkaechini wote. Ninaomba mkae chini wote. Waheshimiwa ndiyomaana nimemwambia Mheshimiwa David Kafulila. Utaratibuwa kama hujaridhika kuhusiana na jinsi maswaliyaliyvyojibiwa. Hatuwezi kuanza kubishana hapa. Kila

[MHE. MOSES J. MACHALI]

Page 54: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

54

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mbunge aliyeuliza hapa, akitaka kubishana swali lakeatabishana hapa, ndiyo maana nikasema tuna Kifungukinachosema utatoa maelezo binafsi. Katika maelezobinafsi tunafanya kabla ya kuahirisha kikao jioni, yeyote yuleambaye anafikiria hakupendezwa na jambo fulani, anaomuda wa kuandika na kusoma, tutampa dakika zake zoteza kusoma. Halafu pale utaratibu wetu unachukua nafasiyake. Vinginevyo kila mtu tukimruhusu katika pindi chamaswali asimame na kusema mimi sikuridhika. Itakuwa siyoBunge.

Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo ninawaagizaMheshimiwa David Kafulila, kafanye hivyo. MheshimiwaMoses Machali, kafanye hivyo. Mimi nitawapeni mudawakati muafaka muweze kueleza hayo mnayotaka kujieleza.Vinginevyo haiwezikani kama hivyo mnavyotaka. Wenginewanaona uvivu kufanya hivyo. Huu ni utaratibu, andikenimkaeleze mtapewa muda fuateni Kanuni ya 28 na Kanunizinginezo zile.

MBUNGE FULANI: Hakusikika

SPIKA: Kitu gani?

MBUNGE FULANI: Hakusikika.

SPIKA: Nani Mbunge gani?

Mheshimiwa unajua tatizo la Wabungemnachanganya kila kitu. Power of replying hata wewe kamaumekuta mtu amekusemea eneo lako unayo, una haki yakujibu, Mbunge yeyote anayo haki ya kujibu. Mbungealijibu kama Waziri wakati wa maswali alisimama.

(Hapa Waziri fulani alisimama)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri, ninakuomba na wewepia ukae na unyamaze. Mheshimiwa Waziri communicationmnayoifanya mnaleta fujo katika Bunge.

[SPIKA]

Page 55: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

55

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Waheshimiwa Wabunge, naomba tuwe na order,tatizo lenu ninyi mnafikiri kwamba humu tunaweza kuongozatunavyotaka, hapana, kila kitu kina Kanuni zake na naombamjifunze hivyo, siyo suala la kuzomea au kufanya nini, sio point,someni Kanuni. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, kwa sababu nilizoeleza,tunasimama kwa ajili ya Kamati ya Mipango.

KAMATI YA MIPANGO

Mwenyekiti (Mhe. Mussa Z. Azzan) Alikalia Kiti

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, sasatunaendelea na uchangiaji kwenye Mapendekezo yaMpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2014/2015.Mchangiaji wetu wa kwanza ni Mheshimiwa MahmoudHassan Mgimwa, ajiandae Mheshimiwa Stephen Ngonyanina Mheshimiwa Mbatia. Mheshimiwa Mgimwa!

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kukushukuru kwakunipa nafasi ya kuchangia Mpango wa Maendeleo wamwaka 2014/2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaenda kwenyeMpango, kwanza nataka nizungumzie habari ya bajeti yamwaka 2013/2014. Makusanyo ya bajeti ya mwaka 2013/2014ya robo ya mwaka ni 85.7% kwa makusanyo ya ndani na34.2% kwa makusanyo ya nje. Makusanyo hayo yanatoa dirakwamba uwezo wa Serikali kutekeleza miradi ya maendeleoni tatizo kwa sababu mpaka sasa tumepata 32.4% tu kutokakwenye misaada ya nje, kuna pengo la 68%, hili ni tatizo. Kwahiyo, Serikali inatakiwa ijiangalie upya ili kusudi tuwezekuji imarisha katika makusanyo ya ndani i l i tuwezekushughulikia miradi ya maendeleo hapa nchini. Kwa mfano,tulikuwa tunataka tujielekeze kwenye Wizara ya Maji kwakipindi cha robo mwaka kwa shilingi bilioni 157 lakini mpakasasa hivi imetolewa shilingi bilioni 43. Kwa maana hiyo ni

[SPIKA]

Page 56: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

56

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kwamba miradi mingi ya maji vijijini haijatekelezwa. Kwa hiyo,Serikali tunatakiwa tujiangalie upya katika maeneo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2012/2013, Serikaliilipanga matumizi ya bajeti ya shilingi trilioni 15 na mwaka2013/2014, Serikali ilipanga matumizi ya bajeti ya shilingi trilioni18 na mwaka 2014/2015, Serikali imepanga matumizi ya bajetiya shilingi trilioni 20, kila siku Serikali inaonyesha kwamba kunaongezeko la matumizi lakini ukiangalia hali halisi Serikali huwahaina uwezo wa kufikia, kwa mfano mwaka 2012/2013, Serikalihaikuweza kuwa na uwezo wa kukusanya shilingi trilioni 15na mwaka 2014, nina uhakika kabisa Serikali itakuwa hainauwezo wa kukusanya shilingi trilioni 18. Kwa hiyo, ni vemaSerikali inapotuletea Mpango huu wa Maendeleoikatuonyesha na source, wapi tutapata pesa hizo hasatukijiekeleza katika maeneo ya ndani kuliko kutuwekeamipango mikubwa ya matumizi wakati uwezo wa kukusanyapesa hizo kwa ajili ya matumizi hatuna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nizungumziekuhusu Tume ya Mipango, lakini kabla sijazungumzia Tumeya Mipango, naomba nisome kidogo mapendekezo yaKamati ya Bajeti. Kamati ya Bajeti inasema kwamba Tumeya Mipango ina majukumu ya kusimamia utekelezaji wamiradi ya kitaifa nchi nzima. Nchi yetu ni kubwa na miradimingi hutekelezwa kwa wakati mmoja. Kamati inasita kuaminikwamba Tume ya Mipango katika hali yake ya sasa inawezakutekeleza majukumu haya. Mimi sikubaliani na hoja hii yaKamati. Tume ya Mipango ni thinking tank ya Serikali kwahiyo kazi yake kama thinking tank ni kuelekeza tu na siyokusimamia miradi ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea ku-quote,Kamati inasema kwamba; aidha Maafisa Mipango wa Wizarana Halmashauri hutakiwa kuandaa maandiko ya miradi nakuwasilisha Tume ya Mipango kabla ya kuidhinishwa nakutolewa idhini ya fedha. Hata hivyo, Kamati imearifiwa kuwawengi wa Maafisa wana uwezo mdogo wa kuandaamaandiko ya miradi. Sasa kama thinking tank inakuwa haina

[MHE. M.H. MGIMWA]

Page 57: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

57

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

watu wenye uwezo basi hilo ni tatizo. Naomba tuliangalieeneo hili, kwa hiyo, Tume ya Mipango inatakiwa iwe na watuwenye uwezo wa kuisaidia Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Mipango imekuwana tatizo, kuna baadhi ya maeneo imetuletea matatizo.Wabunge tunaamua katika bajeti na Wizara ya Fedhainaamua, ikifika wakati wa uidhinishaji wa fedha lazima Tumeya Mipango ipitie, kwa hiyo, inakuja kutucheki mara ya pilisisi Wabunge tumefanya nini. Hili jambo siyo zuri na matokeoyake miradi mingi ya maendeleo inachelewa na kuchelewakwa miradi ya maendeleo kunasababisha cost ya ile miradikuwa mikubwa zaidi. Kwenye jambo hili mimi sikubaliani nahilo jambo, baada ya sisi Wabunge kupitisha bajeti kamafedha zipo zipitishwe na ziende kwenye miradi inayohusika.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo natakakulizungumzia ni Sheria ya Manunuzi. Sheria ya Manunuziimepitwa na wakati. Sheria ya Manunuzi inasababishagharama nyingi, imekuwa na mianya mingi ya rushwa na piakumekuwa na udanganyifu mkubwa. Kwa hiyo, Bunge lakoTukufu na Serikali zinatakiwa ziangalie utaratibu mpya wakurekebisha sheria hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuwa mtovu wa fadhilanisiposema kwamba Serikali kuna baadhi ya maeneoimefanya vizuri na hakuna eneo kubwa ambalo Serikaliimefanya vizuri kama katika eneo la barabara. Miundombinuya barabara hapa nchini ni mizuri, ni ukweli usiopingika lakinibado kama Serikali tunatakiwa tuendelee kufanya vizurikatika kurekebisha uchumi wetu, tunatakiwa tujiwekeemikakati katika eneo la reli. Kama kweli tutajiimarisha kwenyereli automatically cost of production zitashuka hapa nchinina kusababisha hali ya uchumi kubadilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo natakakuchangia ni ukusanyaji wa pato la taifa. Wenzetu Serikaliwanatuambia pato la taifa kwa mwaka uliopita lilikuwa ni6.9% na safari hii ni 7.0. Ni kweli katika nusu mwaka hali ya

[MHE. M.H. MGIMWA]

Page 58: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

58

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mapato imebadilika, lakini hali ya mapato imebadilikambona haiendi sambamba na kuondoa hali ya umaskini?Pato la Tanzania limebadilika lakini hali ya umaskini ikopalepale. Kwa hiyo, ukituambia pato la Taifa limekua hapasi kweli na mimi sikubaliani na hoja hii. Kwa hiyo, natakaniseme kwamba kama tunataka tuzungumzie hali ya mapatoni lazima iende sambamba na ukuaji wa uchumi wa mtummojammoja kwa ujumla. Matabaka kati ya watu maskinina matajiri limezidi kuwa kubwa zaidi kuliko hapo awali, kwahiyo, tunatakiwa tujiangalie kwenye eneo hili. Tukitaka kujuakama uchumi umekuwa lazima gap l ipungue lawaliokuwanacho na wasiokuwanacho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo natakakuzungumzia ni mfumuko wa bei. Ni kweli mfumuko wa beiumeshuka lakini mfumuko wa bei ungeshuka zaidi kamatungeangalia eneo la umeme, kama umeme ungepunguabei zaidi, nina hakika kabisa mfumuko wa bei ungeshuka. Lapili, ni eneo la reli, kama usafiri wa reli ungekuwa wa uhakikanina uhakika kabisa cost of production ingeshuka namfumukowa bei ungeendelea kushuka. La mwisho, hivi nisababu zipi zinazotufanya sisi Watanzania tuendelee kuagizamchele nchi za nje wakati mchele upo mwingi kwenye ma-godown? Hii ni aibu na tunaendelea kuongeza cost ambazohazina thamani yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Waziri mhusikana Serikali, inieleze mikakati iliyoiweka ya kuwalipa wazabuniwa ndani. Tumekuwa tunawatesa wazabuni wa ndani,wananchi wa Tanzania wanazidi kujitahidi kutaka kujiimarishakiuchumi lakini Serikali ndiyo inakuwa inawaangusha watuwake wenyewe. Tunataka mikakati ya uhakika, Serikaliimejipanga kiasi gani kuwalipa...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Mgimwa,muda wako umekwisha. Sasa namwita Mheshimiwa StephenNgonyani, ajiandae Mheshimiwa Mbatia na Mheshimiwa

[MHE. M.H. MGIMWA]

Page 59: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

59

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mwaiposa pia ajiandae. Naona Mheshimiwa StephenNgonyani hayupo na sasa namwita Mheshimiwa Mbatia!

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili nami nichangie hojahii ya mapendekezo ya mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana Mheshimiwa Spikaalitoa agizo kwa Serikali kwamba Mpango huu ni wa Serikalinzima lakini sasa hivi kuna full Ministers wapo wanne tu. Sasasijui tunafanya kitu gani hapa jamani! Full Ministers wapowanne tu kati ya Mawaziri 29 yaani sijui tumechoka, kunamchokomchoko fulani hivi katika jamii ambao unasikitishasana, sijui tunakwenda wapi? Wa tano ndiyo anaingia sasahivi Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo letu kubwa, ni umakiniwa mipango tunayopanga hapa. Mapendekezo ya mpangohuu yana kurasa 62, zaidi ya kurasa 47 ni kama copy andpaste za mwaka jana na kurasa 13 au 14 ndiyo mpangowenyewe tunaotegemea wa mwaka ujao wa fedha. Kurasa62 kwa Wabunge na makabrasha mengine kusoma inakuwani kujirudiarudia sana. Naomba tu kusema kwamba, duniaya leo kuna kitu kinachoitwa KISS (Keep It Short and Simple),waweke kwenye majedwali ambayo yanarahisishaWaheshimiwa Wabunge kuweza kufuatilia kwa umakini naurahisi kuliko hii vuta nikuvute.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mjumbe wa Kamatiya Bajeti, tumechambua kwa makini na niseme kabisamawazo yetu ya Kamati ya Bajeti nayaunga mkono natuangalie vipaumbele ambavyo ni muhim. Nizungumzievipambaumbele viwili yaani bandari pamoja na reli kwaMheshimiwa Dkt. Mwakyembe ambaye ameingia hapa sasahivi. Kama tunataka uchumi wetu uweze kuingia kwenyekarne ya 21, ukaingia kwenye kipato cha kati, hatuna budikuwekeza kwa kiwango kikubwa kwenye bandari na reli.Bandari zetu zote zinahitaji kama dola bilioni tatu. Bandari ya

[MWENYEKITI]

Page 60: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

60

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Dar es Salaam dola bilioni 1.5 na reli inahitaji kama dola bilioni7. Jumla tukitafuta dola bilioni 10 tutaondokana na huuwasiwasi tunalionao, tutafungua lango kuu la reli ya kati aulango kuu la uchumi na usafiri ambao ni rahisi kuliko woteduniani kwanza ni wa maji, pili ni wa reli. Ujenzi wa barabaraambao tunausifia sana, usafirishaji wa zaidi ya kilomita 600huwa ni hasara. Angalia haya malori makubwa yanavyozidikuharibu barabara zetu kwa hiyo tunarudia kwenye umaskiniuleule yaani tunajenga barabara ya kuja Dodoma, yakwenda Kaskazini hata ya kwenda Kusini. Kwa hiyo, bila kurana reli ambayo itasafirisha mizigo na kwa urahisi ambao nicheap, tutakuwa hapa tunajidanganya tu kwambabarabara zimejengwa lakini tunazunguka kwenye umaskiniuleule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napendekeza kwa Serikali,wanasema deni ni himilivu lakini kwa mapana zaidi, timu iweni ya maabara au ni ya wapi, fedha zipatikane, generationhii iwekeze kwenye bandari, geographically tupo vizuri,tuwekeze kwenye reli vizuri ili tuondokane na hizo ngonjeraza vuta nikuvute za kukopa dola 100,000, 200,000 au 1,000,000lakini tukope heavily na tuwekeze, mikopo hii duniani ipo nasiyo lazima tufuate masharti ya IMF na World Bank tu, sisi niTaifa ambalo tukiamua tunaweza. Sisi nchi yetu hii ambayoimekuwa ni kiongozi katika Bara la Afrika, mbona tunakuwana majibu mepesimepesi kwa maswali ambayo ni magumu?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka tarehe 9/4/2013tulivyokwenda kumwapisha Uhuru Kenyatta nilikuwepo naWaziri Sitta alikuwepo na Mheshimiwa Lowassa na wengine.Wimbo wa Afrika uliopigwa, beti ya kwanza ni wimbo waTanzania, ni wimbo wa Afrika leo kwamba Mungu ibarikiAfrika, ndiyo wimbo wa Afrika. Sasa kama tumepewa heshimahiyo na Bara la Afrika, sisi Tanzania tunafanya nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiangalia ngonjerazilizotokea jana hapa kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki,hakuna kosa kuwa na ushirikiano kati ya Kenya na Tanzaniawala Kenya na Uganda, ukiangalia nchi zote za Afrika Kenya

[MHE. J. F. MBATIA]

Page 61: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

61

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ni ya kwanza kwa uwekezaji wa Tanzania FDI yaani ForeignDirect Investment, kwa dunia ni ya pili, lakini majibu hapanani kampa talaka huyu, nani kamuoa huyu, economicdiplomacy ipo wapi? Let us be sincere! Kauli hizi zinaletamaafa makubwa kwa Taifa hili. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa uongozi wetu wa Taifala Tanzania sawa, tuna kilomita za mraba zaidi ya 945,000,Kenya 581,000, Uganda 236,000, Burundi 27,000 na Rwandani 26,000, sawa sisi tumewazidi kwa zaidi ya kilomita za mraba73,000 lakini tumewazidi hivyo, tunaitumiaje fursa tuliyonayokatika kuonyesha kweli tunaongoza katika ukanda huu?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuangalie kwenye sekta yautalii, Tanzania ni ya pili kwa vivutio vya utalii duniani baadaya Brazil lakini ukiangalia tupo nafasi ya ngapi kwenye vivutiohivi katika kuleta mapato kwenye Taifa hili katika ushindani?Sisi ni wa pili duniani lakini tunashika nafasi ya 110 kati ya nchi133. Mauritius ni ya 131 kwa vivutio vya utalii duniani kati ya133 lakini ni ya 53 katika sekta ya utalii. Sasa ukiangalia hiisekta ya utalii leo hii, wenzetu wa Kenya ni wa 28 kwa vivutiovya utalii lakini in terms ya uingizaji wake wa pato la Taifa ni103 imeishinda Tanzania, sisi ni wa pili duniani. Sasa sekta hiiya utalii mbona kigugumizi? Mwaka jana hapa kwenye bajetina tusingependa itokee tena kwenye bajeti inayokujakwamba tunaanza tena kukamua watalii hawa wakatitunajaribu kuikuza sekta hii ya utalii, tunajaribu tuangalie sektaya anga itakuwa namna gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, angalia leo hii KLM kutokaAmsterdam kuja Kilimanjaro, kuja Dar es Salaam ni aghalikuliko kutoka Amsterdam kwenda Nairobi. Sasa kwenye utaliihumu tunawekezaje? Costal line yenye kilomita 1,424,mahoteli ya kitalii yapo wapi? Wazawa watalii wanaowekezahumu ndani, mzawa anapewa nafasi ya kujenga hoteli lakinihapewi eneo la kujenga hoteli, inakuwa ni urasimu tu. Wizaraya Ardhi na Wizara ya Utali i wanatenga maeneo,wanakubaliana mwekezaji amekuja immediately anapewa

[MHE. J. F. MBATIA]

Page 62: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

62

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

eneo ili kuondokana na huu urasimu, urasimu, urasimu,urasimu!

Mheshimiwa Mwenyekiti, inasikitisha sana kwa kweli,tujitahidi tuone ni namna gani badala ya kusikiliza upandemmoja tu kuhusu hili sokomoko lililotokea tarehe 24 na 25mwezi wa Juni kule Kampala na 28 Agosti, 2013, Jumatano,kule Mombasa kuhusu Rwanda, Uganda na Kenya.Tumesikiliza upande mmoja wa Serikali lakini ukiangaliaWakenya walivyowekeza hapa waweza kutuacha hivihivi,hapana! Tuone hii ni changamoto chanya na sisi tuamketuwekeze seriously kwenye bandari yetu, tuwekeze seriouslykwenye reli yetu na kutoka Dar es Salaam kwendaBunjumbura na kwenda Congo ni karibu zaidi na ni punguzola zaidi ya kilomita 1000 kwa hiyo economicallymfanyabiashara yeyote atakuja kwenye bandari ya Dar esSalaam. Sasa tusilalamikelalamike tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna nguzo kuu sita zaumaskini wa fikra. Nguzo ya kwanza ni majungu, ya pili ni fitina,ya tatu ni umbeya, ya nne ni kusema uwngo, ya tanoukishasema uwngo unajenga chuki katika jamii na ya sita niuvivu wa kufikiri. Let us be sincere, tujiulize tunaongea nini nanani, mahali gani, wakati halafu athari yake itakuwa ni nini?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuwe Taifa linaloongoza Barala Afrika. Uwezo huo tunao, tusiangalie wazo limetoka kwanani, angalia quality ya wazo lenyewe, angalia fikra zenyewe,tushirikiane wote. Naamini pamoja tukiamua Taifa la Tanzaniatunaweza, uwezo tunao ilimradi tuachane na hizi tofautindogondogo za kiitikadi kwenye mpango wa kitaifatunawekeza fikra zetu zote kwa pamoja kwa kuwa Taifa hilini letu sote kwa maslahi mapana ya Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatiamuda huu. (Makofi)

[MHE. J. F. MBATIA]

Page 63: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

63

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana kwa kutunza muda.Sasa namwita Mheshimiwa Mwaiposa, ajiandae MheshimiwaJenista Mhagama na atafuatiwa na Mheshimiwa AssumpterMshama.

MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza kabisa nashukuru kupata nafasi ili na mimi niwezekutoa mawazo yangu kuhusiana na Mpango ambao ukombele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisaniwapongeze waandaaji, lakini la pili nitake kusema kwambani mara yangu ya pili kusimama hapa Bungeni kuongeleasuala la vipaumbele. Nakumbuka mwaka jana wakatininachangia, niliishauri Serikali ijaribu kuja na vipaumbelevichache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia mpango huu,umekuja na vipaumbele Sita. Hata hivyo, mbali navipaumbele hivyo umekuja tena na sehemu nyingine kumina mbili ambazo pia zitapewa vipaumbele. Tukiangaliamaana ya hilo neno vipaumbele, maana yake ni mpangoambao unatakiwa utoe fursa kwa maeneo machache lakinimaeneo mengine yakiwa yameachwa. Hata hivyo,ukiangalia kwenye mpango huu kiuchumi hakuna hata eneomoja ambalo limeachwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napata wasiwasi sana kwasababu tukienda kwa jinsi tunavyokwenda na vipaumbelesita na maeneo mengine kumi na mbili, tutamaliza mwakakama ilivyo kawaida, tutashindwa kufuatilia, tutashindwakufanya monitoring, tutashindwa ku- evaluate na mambomengine yanayofanana na hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe tu mfano, naonaSerikali ya awamu hii imejitahidi sana kuelekeza nguvu nyingikwenye barabara na hilo limeonekana. Laiti tungewezakuchukua vipaumbele vichache kwa mwaka mmoja tu, hatatukachukua tu hiyo miundombinu, tukaweza kuhakikishakwamba mambo ya umeme yamekaa vizuri, mambo ya

Page 64: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

64

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kilimo yamekaa vizuri, mambo ya viwanda yamekaa vizuri,nadhani hii ingeweza ikasaidia sana nchi kuona kwamba niwapi inakwenda vizuri au ni wapi imekwenda vibaya. Kwampango huu, nadhani tunaweza tukafikisha mwaka kamailivyo kawaida tukashindwa ku- evaluate kwamba tumefanyavizuri namna gani katika sekta hii lakini pia ni wapi tulikwamatusifanye vizuri katika sekta hii. Kwa hiyo, bado naiombaSerikali, hebu iangalie ni namna gani inaweza ikaja navipaumbele vichache ili tuweze sasa kuhakikisha tuna-concentrate kwenye zile raslimali chache za kifedhatulizonazo na impact iweze kuonekana kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yako maeneo mengineambayo napenda sana kuyazungumzia kwa mfano, elimu.Tukienda kwa mwenendo huu wa vipaumbele vingi lakini piatukikumbuka ule mradi wa Matokeo Makubwa Sasa na hayamatokeo makubwa yakajikita kwenye vipaumbele vyote hivi,nina wasiwasi kabisa kwamba tunaweza tusifanye vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu nimepata nafasiya kuzungumza na Walimu katika shule zao za primary katikaKata sita kati ya nane nilizonazo katika Jimbo la Ukonga.Lengo lilikuwa ni kuangalia zile changamoto walizonazo, lakinipia ni namna gani wamejipanga kupokea mpango huu waMatokeo Makubwa Sasa. Changamoto ziko nyingi mno, lakinikama tutakwenda kwa mtindo huu tunaokwenda nao, hatakatika elimu hatutaweza kufika mahali kwa sababu zikochangamoto za uchakavu wa madarasa, madarasahayatoshi, madawati hakuna, Walimu hawatoshi nakadhalika. Pia nilipata tena nafasi ya kuongea na MaafisaElimu katika Kata husika. Wale wenyewe wanasema kwambawanausikia huo mpango wa Matokeo Makubwa Sasa, lakiniwana changamoto lukuki ambazo zitawafanya waowashindwe kusaidia mpango huu ili uweze kufanikiwa hasakatika nyanja ya elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatana labda na jiografiaya maeneo mbalimbali ya Tanzania yalivyo, hususani yaJimbo la Ukonga, unajikuta kwamba Afisa Elimu ambaye nimsimamizi mkuu wa shughuli za elimu katika Kata nzima,

[MHE. E.E. MWAIPOSA]

Page 65: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

65

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kutokana na jiografia anashindwa kufikia shule mbili kwa siku.Hiyo ni changamoto. Ssasa wao wanasema mpangoumekuja, lakini sisi vitendea kazi bado havijafika. Huo ni mfanotu ambao nimesema niutoe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali kamaimekuja na vipaumbele vingi kiasi hiki basi hebu iangalie sasaMpango huu wa Matokeo Makubwa tusije tukauelekezakwenye vipaumbele vyote na maeneo yote ya kiuchumi yaTanzania. Tungechagua maeneo machache, hata matatuau manne tu, tukaweza kuelekeza huko huu mpango ilikwanza tuweze kuusimamia vizuri, lakini pia tuweze kuja ku-evaluate ni namna gani katika hizi sekta ambazotumejielekeza kwa sababu ya kuwa na rasilimali chache zakifedha tumefanikiwa na pia namna gani hatukufanikiwa nakwa sababu gani. Hayo ndiyo mawazo yangu katika kuishauriSerikali kwenye jambo zima la kuchagua vipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye eneo la reli.Nakumbuka hata mwaka jana eneo hili lilizungumziwa sana.Hili ni eneo ambalo kama likitumika vizuri linaweza likasaidiasana kunyanyua uchumi wa nchi hii na lingeweza pialikasaidia kuhakikisha kwamba bei za bidhaa nyingizinapungua. Hata hivyo, cha kusikitisha nimesoma mpangohuu nikakuta kwamba mwaka jana, kati ya mambo ambayoyalikuwa yafanyike kwenye reli, ni upembuzi yakinifu. Hiyoilikuwa ni mwaka 2012/2013 ndivyo ilivyoandikwa kwenyempango, mwaka 2013/2014 hiyo haijazungumzwa lakinimwaka 2014/2015 ndiyo sasa inakuja na kitu gani kitafanyikakwenye eneo hili la reli. Naona pia wamerudia kwambawataendelea kumalizia upembuzi yakinifu pamoja nakutafuta wakandarasi watakaofanya kazi hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukienda kamatunavyokwenda, ni wazi tutachelewa kufika, kwamba kwamiaka mitatu tunafanya upembuzi yakinifu. Hii itafanyamaendeleo yachelewe sana. Naomba eneo hili la reli lipewekipaumbele ili ujenzi wa reli uweze kuanza hasa zilezinazochukua mizigo kwa sababu kwanza malori mengiyanaharibu sana barabara. Kama ambavyo Waheshimiwa

[MHE. E.E. MWAIPOSA]

Page 66: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

66

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Wabunge wameona, hasa wale waliotokea Dar es Salaam,barabara nyingi zimeharibika kwa sababu ya kubeba mizigoambayo ni mikubwa zaidi kwenye malori. Kwa hiyo naombapamoja na maeneo hayo, basi kwenye eneo hili la reliMheshimiwa Waziri aangalie ni namna gani anawezakuharakisha na kuhakikisha mizigo mikubwa yote inaelekezwakwenye usafiri wa reli ili iwezeshe reli kujiendesha yenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kidogo eneo laviwanda. Mpango ni mzuri, umezungumzia viwanda lakininisikitike kusema kwamba sijaona kama tulivyoongea mwakajana, tuliomba Serikali ianze kufuatilia viwanda vile vya zamaniambavyo walipewa wawekezaji ili waviendeleze kwa mujibuwa utaratibu ambao ulikuwa umewekwa. Vipo viwanda vyakatani, viwanda vya kutengeneza magunia, viwanda vyangozi ambavyo vimekufa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukizungumza kuanzishaviwanda vipya wakati vipo viwanda vya zamani ambavyovil ikuwa vinatakiwa vifufuliwe kwanza il i viweze ku-accommodate vijana wetu na watu wengine ambaohawana kazi, tutapoteza rasilimali.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana MheshimiwaMwaiposa, kengele yako ya pili.

MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Sasa namwita Mheshimiwa AssumpterMshama, wajiandae Mheshimiwa Peter Msigwa naMheshimiwa Zainabu Vullu.

[MHE. E.E. MWAIPOSA]

Page 67: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

67

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. ASSUMPTER N. MSHAMA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi na miminiweze kuchangia katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ambalonapenda niliongelee ni kwamba, labda tungeondoa nenokipaumbele katika mpango huu kwa sababu unaposemakipaumbele, ndani ya kipaumbele hakuna kipaumbele. Kwahiyo, kusema kuna vipaumbele lingeweza kuondokatukatumia neno mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na Mpango waMaendeleo wa mwaka huu, mpango huu wa mwaka 2014/2015 hauna tofauti na mpango wa mwaka 2012/2013. Kwamaana nyingine kama kungekuwepo na kipaumbele, inamaana vipaumbele vilivyokuwa vimekuja, vilikuja vitano, kituwalichokifanya leo wamechukua kile kipaumbele chamwisho wakakitenga vikawa viwili, mwaka huu vikawa sita.Pale ambapo anasema huduma za utalii na fedha, mwakajana vilikuwa vimeunganika lakini mwaka huu imekuwa nikipengele cha tano, huduma za fedha na kipengele cha sitani utalii. Kwa hiyo, ni kwamba hakuna kipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende moja kwa mojakatika tatizo ninaloliona linalosababisha Mpango wetu waMaendeleo wa Tanzania usifanyike. Kama mtu angekuwana mpango, nakumbuka tena hata nilipochangia mara yamwisho nilisema kabisa kwamba, mpango mzuri upo lakiniwatekelezaji ni akina nani? Mfano kama unataka kusemauna mipango sita, tungesema ni ya miaka mitano, tungekujana mipango kama ninavyofikiri, labda mwaka 2011 ukawekamiundombinu na kilimo, mwaka 2012/2013 maendeleo yarasilimali watu na huduma za fedha, mwaka 2014/2015ukaenda viwanda na huduma za utalii. Mwaka unaofuataungechomoa kimoja kwamba hiki sasa kimekuwa tayari,tunaingiza kipaumbele kingine. Kwa hiyo, ndiyo maananinasema hakuna kipaumbele, kuna mipango yamaendeleo.

Page 68: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

68

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niende kwenyeniliyoyachunguza na kuyaona yanayosababisha mipangoyetu isitekelezeke. Jambo la kwanza ni kuwa na vipaumbeleau mipango mingi kwa wakati mmoja bila kuwa na fedha zakutosha kufanyia kazi hizo. Ukiwa unatumia cash budget,yaani wewe unaandaa, kwa mfano hiyo staili inayotumikahata harusi ina nafuu. Mtu anapoandaa harusi anakuwaanaandika vitu na analeta bajeti kwamba tunategemeakupata wageni mia nne (400) na tunategemea kuwa na kituhiki na hiki, lakini kwenye Serikali huwezi ukandaa bajeti wakatihuna hata senti tano mfukoni, unategemea watu auMipango au makusanyo yatakayotokea. Kwa hiyo, huwezikufikia malengo hata siku moja. Kwa mfano, unategemeabia, watu wakiokoka wakaacha kunywa bia huwezi kupatafedha. Ulikuwa unategemea kupata kodi, bila kutumiacapital budget hatuwezi kutimiza mipango yetu hata sikumoja. Kwa hiyo, suala la kwanza lazima tu-deal na cashbudget, tusipange mambo kama kwenye harusi. Hata walewanaoandaa mpango hawafahamu fedha watazitoa wapi.Wanaandaa mpango, wanauleta kwetu, ukiwauliza hizifedha utapata wapi hawana majibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kufanya kazikwa mazoea. Mpango huu tunasema tumekuja na staili mpyaya Matokeo Makubwa Sasa, lakini kwa watu wapi?Watanzania hawa ambao wamezoea kufanya vitu kamawanavyotaka, siyo rahisi kutimiza utaratibu huo. Kukosawasimamizi walio makini, walio na mzigo wa kulisaidia Taifahili, bila hivyo hiyo Big Results Now haiwezi kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulindana kazini. Mtuanakosea, anaendelea kuwepo kazini, unategemea kupatamatokeo makubwa kwa sasa, siyo rahisi! Halafu chuki, fitinana ugomvi, watu wengine hawamwambii Rais ukweli. Kunamtu tulimwita katika Kamati yetu, wakati anajieleza, alituelezalabda fulani awepo. Alipokuja huyo mtu akasema, aahmbona mnatugombanisha? Aah, wewe si ulisema akiwepohuyu na sisi tukiwepo tutaweza kufanya mambo sawasawa?Tukamwambia wewe ndiye unatakiwa sasa hivi kumshauri

[MHE. A.N. MSHAMA]

Page 69: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

69

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Rais, utamshauri nini wakati amekuja mtu mmojaumebabaika na umesema vitu tofauti? Kwa hiyo, hata fitina,kutomwambia Rais ukweli, watu hawamwambii Rais ukwelina matokeo yake mambo hayaendi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutotathmini kazi iliyofanyika.Kuna miradi, kwa mfano ukiangalia kwenye mpango wamwaka jana miradi ile imebeba mambo muhimu 18. Hivi leoamekuja Bwana Mpango na mpango uleule wa mwaka jana,unawezaje kutathmini? Huwezi kupata impact. Kwa hiyo,kinachokosekana ni watu kutojua kwamba hivi vyotetunapeleka vitaweza kufanyika kwa wakati huu kulinganana uwezo wetu wa kifedha?

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu hawaogopi mtuawaye yeyote. Mtu anaweza kufanya kitu chochote, kwawakati wowote na asiulizwe chochote, na hata akiulizwahakuna kitu kitakachofanyika. Huwezi kupata matunda aumajibu ya kusema ‘Big Results Now’ kwa sababu watuhawaogopi kitu chochote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uzembe wa hali ya juu kazini.Kwa mfano, mtu ametengeneza barabara ameiharibu badoanapewa muda tu irudie, irudie, irudie, uzembe wa hali yajuu! Kwa nini mtu huyu asifilisiwe tukaweka mtu mwingineakatengeneza barabara ikawa tayari?

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi zaidi ya mapato.Hivi kweli Wabunge tunafika mahali hatujapata mshahara,tunapata tarehe 30 kama tunafanya kazi kwa Mhindi, maanaMhindi ndiye ana mpaka tarehe 34 au kwa mtu binafsi!Kusema kweli ni matumizi mabaya, matumizi yanayozidimapato. Ukipiga matumizi yetu, eti unategemea mtu kutokaChina ndiyo atusaidie katika matumizi, kwa nini tusikusanye?Tungefanya kama wanavyofanya watu wengine,anakusanya fedha za miezi mitatu, kama hujakusanyaunakopa zinakuwepo, kwa hiyo, unapanga mambokulingana na kilicho kwenye kikapu, lakini watu wanaandaavitu wakati kwenye kapu hakuna kitu. (Makofi)

[MHE. A.N. MSHAMA]

Page 70: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

70

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufanya kazi bila malengo.Mtu yuko kazini ameajiriwa, hajawekewa malengo kwambaifikapo tarehe 30 tunataka utuletee moja, mbili, tatu.Anafanya kazi, anaweza kwenda Kariakoo, akazurura mjini,tarehe 30 lazima alipwe. Kwa nini watu wasiwekewe malengoya kutimiza ili mtu alipwe kulingana na kile alichokifanya?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni maneno mengikuliko matendo. Sisi tulipoletewa huu mpango kuuangaliakama bajeti, tuliuliza kitu, hivi tumebadili budget cycle,imetuletea mabadiliko gani katika nchi hii? Mimi naona ndiyoimekuwa worse, yaani tumekuja na mpango, tumekuja nabajeti hapa tukasema kuanzia tarehe 1 Julai, mamboyatakuwa sawa, lakini mpaka leo katika Wilaya yangu yaMisenyi fedha ya maendeleo, hakuna! Sasa tulikuwa nasababu gani ya kubadili budget cycle? Mimi naona kwambawatu maneno ni mengi kuliko matendo, tukiweka nguvukwenye matendo lazima tutapata Big Results Now.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi mipya kabla yazamani kuisha. Una mradi huu haujaisha umeanzishamwingine, matokeo yake unajikuta una miradi chungumbovu ambayo haitimiliki. Kwa hiyo, naomba sana tuangalie,hayo ndiyo nil iyoona yanayosababisha mpangokutotekelezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vyanzo vya mapato yandani. Mheshimiwa Waziri ameeleza katika maelezo yakekwamba wanakwenda kuangalia vyanzo vipya. Naombaatakapohitimisha atueleze ni vyanzo vipya vipi ambavyotunaweza tukaongeza mapato. Uko ushauri mwingiWabunge wanautoa, lakini kila siku tunarudishiwa maji, soda,sigara na bia. Tunaomba tuone ni namna gani wamegunduavyanzo vipya na tunataka kuviona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kazi na ajira. Tunavijana wako mitaani, watu wengi hawana kazi. Hiyo yote nikwa sababu hata wanapokwenda shuleni wanasomawanajua wakimaliza shule ni kuajiriwa. Kwa nini kwenye

[MHE. A.N. MSHAMA]

Page 71: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

71

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mitaala tusiweke mtu kujua kwamba unapomaliza shuleukiajiriwa ni sawa lakini bado kuna kujitegemea. Pili, Serikaliikaandaa utaratibu mzuri wa vijana wanapomaliza shulewanakuwa wanaweza kwenda kujiajiri, lakini mazingiramazuri ya kujiajiri yaweze kufanyika na hivyo tunawezatukawasaidia. Vijana wengi wana vyeti vyao, wanahitajicollateral katika benki, kwa nini tusiwe na benki ya vijana yakuwasaidia? Wao wakijulikana na matatizo yao na kwamaana hiyo misingi ya kukopa itakuwa tofauti na misingimingine. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ninakushukuru sana MheshimiwaMshama na sasa ninamwita Mheshimiwa Msigwa,Mheshimiwa Vullu, Mheshimiwa Ntukamazina na MheshimiwaSelasini wajiandae.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ili na mimi nitoe mchangowangu kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kitabu hiki, ukurasawa 48 unasema kuwa, inapendekezwa kwamba maandaliziya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2014/2015 yazingatieyafuatayo:-

(i) Kudumisha amani na utawala bora kwa kuwani misingi muhimu na kuwezesha uzalishaji mali, uwekezaji,ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka niguse kwenye eneomuhimu sana la utawala bora. Katika siku za hivi karibuniimekuwa ni lugha ya viongozi kusisitiza kuwa wanaombaAmani na Utulivu kila mahali kila kiongozi akisimama anasemaamani na utulivu. Naomba nikumbushe tu kuwa amani nitunda la haki. Haki inapokuwa imewekwa mahali pakehatuhitaji kugombana, hakutatokea fujo. Amani ya nchi hii

[MHE. A.N. MSHAMA]

Page 72: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

72

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

haitalindwa na vifaru vingi, haitalindwa kwa kuongezaWanajeshi wengi, amani ya nchi hii itatokana na palewananchi wanapopata haki zao, wananchiwanapotendewa haki, wananchi wanapopata huduma zileambazo wanastahili kuzipata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati mbaya sana,kwa muda mrefu tumekuwa na mfumo wa chama kimoja,pamoja na kuwa kwenye vitabu tumebadilisha, tunasematuna mfumo wa vingi, kuna watu kwenye fikra zao hawaaminikuwa tuko kwenye mfumo wa vyama vingi kwa hiyowanaona watu wengine ambao hawana imani kama yakwao ni watu wanaoleta vurugu. Nataka niwakumbushewalioko madarakani kwamba we are here to stay na tukohapa kwa mujibu wa Katiba, sisi siyo intruders, ni Watanzania,watawala mnatakiwa ku-accommodate mawazotunayoyaleta hapa kwa ajili ya mustakabali wa Taifa letu.Aidha, let us perish together as fools au tuishi pamoja kamaWatanzania na kujenga Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua watu wengineKagame hawampendi lakini kuna nukuu yake mojaninaomba niisome. Anasema, Africa is lagging behind andthere is no good reason for that. We have everything toenable us to move from where we are, to where we want togo. It should be leadership commitment and transform thelives of our people across the continent”. Aliyasema hayakwenye Summit mwaka huu kwamba Afrika tuna kila kituhakuna sababu yoyote kwamba tuwe nyuma katikamaendeleo isipokuwa ni tatizo la uongozi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbatiaamezungumza hapa kuwa tunazungumza Mpango waMaendeleo na Serikali ndiyo wanaosimamia mpango huo,angalia Mawaziri wako wapi? Spika jana amezungumzahapa, hawapo, ambao mnatakiwa mchukue mawazo yetuili mkaya-accommodate kwenye mpango huu lakini hampo!Hatuelewi mko wapi, mko wawili, watatu, hamtoshi, hatamkijielezea hampo. Hii inaonyesha kuwa hampo serious na

[MHE. MCH. P. S. MSIGWA]

Page 73: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

73

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ndiyo maana Serikali hii leo Waziri Magufuli anasema wenyemalori wasimamishwe barabarani analeta hasara kwenyeTaifa karibu shilingi bilioni ishirini, anakuja Waziri Mkuuanasimamisha, the same government. Waziri wa Maliasilianasema sijui watu wa Loliondo waondoke, anakuja WaziriMkuu anasimamisha, the same government. Utawala wenuumefitinika. Hatuwezi tukawa na mipango mizuri wakatinyumba yenu hamjaiweka vizuri. Ndiyo maana nimesema weare here to stay, either mtu-accommodate or let us perishtogether as fools kwa sababu mnahitaji mawazo yetu tukohuku, hamwezi mkatupuuza. Mawaziri Vivuli na Mawazirihusika ambao mna dhamana wengi wanawaona MawaziriVivuli kama ni maadui.

MHE. ESTER A. BULAYA: Taarifa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Hamuwezi kukaapamoja, tukashirikiana tukapanga mipango pamoja…

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Kaa chini, endelea Msigwa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Hatuwezi tukakaa pamoja tukajadiliana kwambahili ni Taifa la pamoja, tunaweka mipango ambayohaitekelezeki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali hii ambayoimepewa dhamana kama nilivyosema, mlianza mwanzonina Kauli Mbiu nyingi, mkasema Ari Mpya, Nguvu Mpya nakama vile haitoshi mkasema Kasi Zaidi. Ngoja niwaambie kitukimoja, Kasi, if you are heading the wrong direction is uselesskuongeza kasi. Mtu kama anapotea hum-motivate kuongezakasi unampa education akae kwenye drawing board namnagani aende kwenye mwelekeo sahihi. Kwa hiyo, Kasi Zaidimliyosema ni kasi ambayo imefanya uchumi wa nchi yetuushuke chini badala ya kuendelea mbele. (Makofi)

[MHE. MCH. P. S. MSIGWA]

Page 74: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

74

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mzungumzaji aliyepitaamesema tumebadilisha utaratibu wa budget cycle lakinimatunda yake hayapo. Tunatoka kwenye Majimbo yetu hukompaka leo hata nusu ya ile hela tuliyojadili mwaka jana haipo,leo tunakuja na mpango mpya, hii ni business as usual.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda katika ukurasa wathelathini, kwa mfano katika kipengele cha maliasili, Wizaraya Maliasili ni ya pili baada ya Wizara ya Nishati na Madinikuleta fedha za kigeni lakini hapa imewekwa utadhani Chuocha Mkwawa, imeelezwa kidogo tu. Mipango ambayohaionyeshi mazingira ya kuiwekea Wizara ya Maliasilikuongeza utalii katika nchi hii, mazingira ambayo Serikali hiiiliwawekea wawekezaji wale wa madini ambao kimsingimadini yanayochimbwa Tanzania mikono yake imejaa damu,kwa sababu kuna watu wamekufa na baada ya hapowanaondoka wanatuachia mashimo. Wizara hii ya Maliasili,mazingira ambayo Serikali ilitengeneza kwenye Nishati naMadini, sioni mkakati mkubwa ambao mnaitengenezeaWizara hii ambayo uchumi wake ni sustainable ambapowananchi watapata ajira, tutalinda wanyama wetu lakinimazingira hayo hayajatengenezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nenda kwa mfano kwenyeviwanja vya ndege, mmesema mnaweka mpango ambaoni strategic. Mmesema mtatengeneza kiwanja cha ndegecha Songwe, naunga mkono, pale ni pazuri. Mnasemakiwanja cha ndege Mwanza nakubaliana. Kuna kiwanja chandege Bukoba, kuna kiwanja cha ndege Kigoma, kunakiwanja cha ndege Mafia, kuna kiwanja cha ndege cha JuliusNyerere, ninakubaliana na kiwanja cha ndege Tabora. Hatahivyo, mnawezaje kwenye mpango huu, Mkoa wa Iringahapa katikati tuna mbuga kubwa ya wanyama na tunatakatukuze uchumi katika masuala haya ya utalii, tuna mbugaya wanyama ya Ruaha National Park, kubwa na ni kivutiokikubwa, uwanja wa ndege wa Nduli mmeutenga. Hii nimipango gani ambayo unaweza kuacha hapa katikatihakuna uwanja wa ndege na Mji wa Iringa ni moja ya vivutio,

[MHE. MCH. P. S. MSIGWA]

Page 75: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

75

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ni Mji Mkongwe pamoja na historia ya Mkwawa, mnawezajekuuacha katika Mpango huu wa Maendeleo kwa ajili yakukuza uchumi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema Wizara hii yaMaliasili ni ya pili baada ya Nishati na Madini. Haya ni mamboambayo tulitegemea wataalamu mkikaa ni lazima tuwe nastrategic, tuangalie ni centers zipi ambazo zitaongezauchumi, una-deal kwanza na primary contradiction ndiyounaenda kwenye secondary ambayo itajishughulikiayenyewe baada ya kumaliza hapa chini. Ya kwanza,niliyozungumza ni utawala bora. Utawala bora kama haupo,haya mambo yote hata tupange hayatakuwepo.Mtaongeza mabomu ya machozi, mtaongeza Maaskari,mtaongeza bunduki lakini kama wananchi hawatapata hakiyao, watapiga kelele tu. Mtafanya mikutano mingi,Mheshimiwa Rais amewaambia kabisa kuwa mjiandaekisaikolojia, mtasema wembe ni uleule lakini utawachanawenyewe kwa sababu hampangi mipango mizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuko hapa kwa ajili yakutetea Taifa letu kwa pamoja. Nachotaka kusema hata kuleAfrika ya Kusini waliandika kwenye makabrasha kuwa ubaguziwa rangi umeisha lakini mioyoni mwa watu ubaguzi wa rangiulibaki, and this is what happening here. Tunaimba utawalabora, tunaimba amani na utulivu lakini ndani ya watuwengine wana chuki, wakiona mpinzani wanamchukia,wanaona kama hastahili kuwepo mahali hapa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ninakushukuru Mheshimiwa Msigwa.Namwita Mheshimiwa Vullu na Mheshimiwa Ntukamazina naMheshimiwa Rita Mlaki wajiandae.

[MHE. MCH. P. S. MSIGWA]

Page 76: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

76

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMAZINA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na miminichangie Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2014/2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana kwa kuwa nilijuanitachangia, nilimpigia simu Mwenyekiti wa Council ya Ngaranikimuuliza kama wameshapata fedha za maendeleo kwamwaka 2013/2014? Akasema wamepata kidogo lakiniakaniambia kuwa kwa miaka mingi hawajawahi kupatafedha za maendeleo, wamekuwa wakipata fedha zamaendeleo chini ya 40%. Sasa hiyo inaonyesha kuwa tunamipango mizuri lakini utekelezaji bado ni mbaya. Tatizo letuwe talk miles and act centimetres. We do not work the talks.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu ni nini? Kwakuwa sasa tumeweka vipaumbele vizuri, Serikali ijitahidi kubunina kutafuta vyanzo vipya vya mapato. Siku zote nimekuwanikizungumzia kuwa sekta isiyo rasmi au the informal sector isa sleeping giant ambayo bado hatujai-tap. Najua kuwampango wa MKURABITA ulianzishwa ili kurasimisha mali nabiashara za wanyonge ili waweze kutozwa kodi. Kwa hiyo,nashauri kuwa tuiangalie informal sector na Serikali isaidieMKURABITA ili iweze kufanya kazi yake ya kurasimisha mali nabiashara za wanyonge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, ni makusanyo,tuimarishe makusanyo. Nimekuwa nikizungumza naCommissioner General wa TRA, Bwana Kitilya, namuuliza vipimakusanyo? Anasema wao wanavuka viwango ambavyowanapewa na Treasury lakini inawezekana Treasurywanawapa viwango vidogo. Katika bajeti iliyopita, nilisemakuwa the Treasury must put its house in order. Nikaawambiawataalamu wa Benki Kuu na watalaamu wa TRA, niwatalaamu zaidi kule wale Treasury kwa sababu mambo yamonetary policy ambayo yanahusu interest rates pamoja naInflation watalaamu wako Benki Kuu. Mambo ya fiscal policyambayo inahusu mambo ya Taxation na mambo yaGovernment spending wataalamu wako TRA, pale Treasurywanatakiwawawepo wataalamu wa fiscal policy na

Page 77: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

77

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

monetary policy ili waweze ku-control hata matumizi yaSerikali. Kwa hiyo, tuyaangalie makusanyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonapenda kulizungumzia ni Big Results Now, hata bajeti iliyopitanilisema ili tufanikiwe na hii mbinu ya Big Results Now lazimatu-address zile prerequisites. Prerequisites maana yake ni nini?Ni kwamba watendaji wa Serikali bado mtizamo wao siyomzuri, we need change of mind set, wawe na mtizamochanya kusudi waweze kuwa watendaji wazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ni kuwezeshaTume ya Mipango. Mimi nina imani na Waziri Wasira, bahatinzuri we went to the same very good school, AmericanUniversity, ni mtalaamu sana. Aidha, nina imani na Tume.Tume ina watalaamu wa fiscal policy na monetary policylakini nchi hii ni kubwa sana, kama tunawapa kazi yautekelezaji pamoja na kuwa think tanks, ni lazima tujengecapacity yao, tuwawezeshe kwa kuwapa watalaamu wengizaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ubia kati ya sekta binafsi nasekta ya umma, ni jambo zuri sana na tunaweka mazingiramazuri kwa ajili ya wawekezaji lakini we must at the sametime kuhakikisha kwamba hii sekta binafsi inatozwa kodiipasavyo kusudi tuweze ku-finance mradi wetu. Jambomuhimu ambalo nataka kulisisitiza, wakati tunazungumziaprivate sector kuwa mhimuli wa uchumi bado sekta ya ummaiwe ni kiongozi wa uchumi, micro-economic managementni kazi ya Serikali. Kwa hiyo, the Government must regulatethe private sector bila kuikaba roho. Kwa hiyo, ni jambomuhimu sana tunapozungumzia partnership lakini Serikali nilazima iwe ni kiongozi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo lingine ambalonimekuwa nikilizungumzia ni procrastination, kigugumizi chakufanya maamuzi muhimu. Nilizungumza wakati wa bajetiiliyopita kuwa tulichelewa sana kujenga reli ya Isaka- Keza-Msongati- Burundi, Keza- Kigali Rwanda. Sijui katika hali hii yamahusiano yetu na Rwanda kama hiyo reli tutaijenga kwa

[MHE. D. A. NTUKAMAZINA]

Page 78: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

78

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

sababu hiyo reli ilikuwa ijengwe na nchi tatu ya Burundi,Rwanda na Tanzania. Ninachozungumzia hapa ni kwambatuachane na procrastination, kigugumizi cha maamuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni equitabledistribution of resources. Nimelizungumzia wakati wa bajetiiliyopita kuwa tunao mpango mzuri lakini hizi fedha ndogotulizonazo tuzigawe na kuangalia nchi nzima. Ngara ikopembezoni tusije tukaisahau kwa sababu iko pembezoni,equitable distribution of resources.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwezeshaji wa wazawa,nilizungumzia sana katika bajeti iliyopita na pia nilizungumzana Katibu Mtendaji na Mheshimiwa Wasira kuwa katikampango, msiwe mnasahau kuweka sera ya upendeleo kwaajili ya wazawa. Wakati wa bajeti nilitoa mfano sera ya uzawaya Malaysia. Juzi nimekwenda Zimbambwe, wana sera yaindigenization na they are very serious about sera yao yaindigenization. South Africa they are very serious about blackempowerment. Hapa kwetu mimi si jaona the exactequivalent ya sera ya aina hiyo. With all due respect kwaMheshimiwa Nagu, lile Baraza la Uwezeshaji lakini haitoi seraya upendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonapenda kulizungumzia ni kituo cha wagonjwa wa moyo.Hapa nimefurahi sana na ninaipongeza sana Serikali kwakuanzisha kituo kizuri cha magonjwa ya moyo pamoja na figo.Serikali inatumia fedha nyingi sana kuwapeleka wagonjwanje ikiwa ni pamoja na mimi nimekuwa nikienda India.Naomba tuimarishe hiki kitengo cha magonjwa ya moyopamoja na figo ili tuokoe fedha za Serikali kwa ajili ya kupelekawatu nje ya nchi. Pia tuwape motisha Madaktari wetu iliwasitoroke kwenda Afika Kusini kutafuta green pasture nakadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonapenda kulizungumzia ni nidhamu katika matumizi. Serikaliijitahidi, tuwe na nidhamu zaidi katika matumizi ili tuokoe

[MHE. D. A. NTUKAMAZINA]

Page 79: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

79

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

fedha za matumizi ya kawaida ziende kwenye matumizi yamaendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni usafiri wa anga.Mimi nina imani sana na Waziri Mheshimiwa Dkt. Mwakyembekwamba ataifufua bandari na reli lakini naomba sana afufueAir Tanzania. Ni aibu kwa vinchi vidogo kama Rwandainakuwa na ndege saba, three Boeings na mimi hizo huwaninazitumia kwa sababu ni karibu na kwangu, Burundi wanandege ndogo, Swaziland kanchi kadogo wana ndege. SasaMheshimiwa Dkt. Mwakyembe, hii ni changamoto yako,tafadhali naomba tuwe na ndege yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri nimemaliza, ahsantesana.

MWENYEKITI: Nakushukuru sana MheshimiwaDeogratias. Sasa namwita Mheshimiwa Rita Mlaki,Mheshimiwa Selasini na Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalawajiandae.

MHE. RITA L. MLAKI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii i l i kuchangiamapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2014/2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeusoma sana mpangohuu kwa makini na ni mpango mzuri kusema ukweli lakinibado ninaona kuna tatizo kubwa katika utekelezaji, ufuatiliajina tathmini. Naona nipendekeze mwanzo kabla ya kusemahoja zangu ili nisikose nafasi ya kusema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niishauri Serikaliianzishe kitu kinaitwa Economic Intelligence Unit. Nchi nyingizilizoendelea zina hiki kitengo. Naomba Serikali waende hataUingereza kwanza watizame jinsi wanavyofanya kazi, kuanziamwanzo wa kupanga mpango wanakuwa na hawa watu.Hawa watu wanakuwa na composition ya Wachumi,Wahandisi, Ma-geologist, watu wa kilimo, Wahasibu nawataalamu mbalimbali ambao wataisaidia Serikali katika

[MHE. D. A. NTUKAMAZINA]

Page 80: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

80

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mpango kuwa realistic na ule mpango. Wanafanya feasibilitystudy kabla na unapouweka hapo, unajua kabisa huumpango unatekelezeka. Baada ya hapo, hiki kitengokinasimamia utekelezaji. Sisi tutajuaje kama walitekeleza,tutarudia tena mwaka mwingine na mwingine ambapo siyokitu ambacho kinatusaidia na wanafanya tathimini kwambampango huu ulifika wapi. Naheshimu sana Tume ya Mipangopamoja na ngazi zote waliotengeneza mpango huu lakinitunaomba tuboreshe kwa kuwasaidia sana katika kuandaampango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuipongeza sanaSerikali kwa kusaidia sana katika mambo ya growth rate yauchumi wa nchi yetu. Pato la Taifa limekua kwa 7%, ninatoapongezi sana na vilevile inflation kushuka kutoka 10.6% mpakakufikia 6.1% katika kipindi cha miezi tisa, ni kazi kubwa na nzurikwa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kushauri kwaharaka kabisa mpango huu napendekeza uweje.Napendekeza mfumo au mpangilio wa huu mpangoubadilike kidogo. Nikianza na kipaumbele ambachotulipewa, labda nichukue mpango wa 2012/2013 halafuniulinganishe na 2013/2014. Nikitizama mpango huo,kipaumbele cha kwanza kama viwanda, kule iliongelea kuwatutajitahidi sana kushughulika na mambo ya Mchuchuma,tukaongelea mambo ya kuchoronga mashimo kule Engarukakwa ajili ya magadi na kadhalika. Mwaka huu ikarudia lakiniangalau ikatusaidia kidogo, ikaongelea kuwa tutahakikishaviwanda vilivyopo vinavyotumia rasilimali inayopatikananchini angalau tunaweza kusindika mazao na kuongezathamani ya hayo mazao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango ufafanue zaidi,badala ya kusema tu kuwa tutasimamia usindikaji hebutubadilishe sasa tuandike kuwa tutasimamia kwa mfano zaola ngozi, tamkeni tu mtasimamia kiwanda hata kimoja kamakile cha Mwanza ambacho kimekaa idle na kuna ng’ombenyingi katika Kanda ya Ziwa na nchi yetu ikiwa ya pili au yatatu kwa ng’ombe hapa Afrika. Tukitaje halafu tukifuatilie na

[MHE. R. L. MLAKI]

Page 81: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

81

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Serikali ihakikishe inafanya kila mbinu kuhakikisha kwambakweli hiki kiwanda kinajengwa. Hali kadhalika na kusindikamazao ya kilimo. Tunaweza tukachagua mazao mawili,tukasema korosho labda na maharagwe, hebu twendenikwa mpango unaotekelezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda sana nikumbushekwamba tumepitisha Sheria hapa ya PPP (Private SectorPartnership). Sheria hii itatusaidia, kama Serikali imesemainajitoa kufanya biashara, basi tutumie sheria hii, tujaribukuhamasisha ili tuweze kuanzisha hivi viwanda. Ni muhimusana nchi yetu ikawa na viwanda. Kwenye mpango huusikuona kabisa wapi imezingatia uanzishwaji wa viwanda.Tumegusagusa tu, kweli tunaongelea kuchoronga mashimo,mpango huu na mpango unaofuata? Naomba tuliangaliesuala hili kwa makini zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda vilevile kuongeleasana kuhusu reli kama wenzangu walivyofanya. Mpangouliopita umeongelea reli ya Dar es Salaam – Isaka - Kigali naupembuzi yakinifu umekamilika. Mwaka huu tumeongeleareli ya kati na tutajitahidi kujenga reli mpya. Mafanikioyalikuwa kwamba tumeweza kufanya upembuzi yakinifu wagati namba 1 - 7 na vilevile tukasema kwamba tutajengampya. Naomba katika mpango wa sasa, tuweze kufafanua.Sasa hivi katika upande wa bandari ambao nimerukia, hiituliyosema kwamba tutajenga zile gati ambazo tayariupembuzi yakinifu umefanyika, je, ndizo ambazotutazirekebisha mwaka huu katika mpango wa sasa? Je, huompango wa bandari mpya itakayojengwa ni i le yaBagamoyo ambayo tuliongelea mpango uliopita? Tufafanuezaidi, ndicho ninachotaka kusema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee sasakuhusu utalii. Mpango mzima wa utalii ambao unasaidiauchumi wa nchi yetu, kweli niseme bila kusita kwambahaukuingia kwa kina. Mwaka jana tunaongelea jinsi ambavyotutaingiza tozo ile inaitwa bed night levy, tunaongeleatutakavyonunua furniture za chuo, tunaongeleatutakavyopandisha star hotel, iwe two star, three star na

[MHE. R. L. MLAKI]

Page 82: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

82

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kuendelea katika mpango? Angalau mwaka huu umeborekakidogo unaongelea kuboresha vituo vya utalii lakini tuwebado specific, tuseme tunataka kuongeza hoteli tano hatambili basi kama tano ni nyingi na tusimamie zijengwe, angalaututakuwa na uhakika tumesogea hatua moja kuliko twendekatika hivi vitu ambavyo ni supporting badala ya kuwaphyical na kuhakikisha kwamba tumeweza kupata katikasekta hii ya utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana hiziterminology za kuzingatia, kuhamasisha, kuboresha hazipimiki.Kwa hiyo, tungejitahidi sana tuweke vitu concrete katika huumpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuongelea kuhususekta ya madini. Utekelezaji wa mpango uliopita, umeelezeakukamilika ukarabati wa ofisi za madini. Mpango unasemajinsi utakavyofanya ukaguzi, mambo ya afya kwa walewachimbaji wadogo wadogo, usalama wao, mara utajengamtaro! Mpango wa mwaka huu angalau unaongeleakuimarisha rasilimali watu, kuendeleza shughuli za kuongezathamani za madini na kadhalika. Hata hivyo, Watanzaniawanachotaka kusikia, ni j insi ambavyo mpangoutamwezesha Mtanzania kushiriki katika biashara ya madini.Tusiwafanye Watanzania ni wachimbaji wadogowadogo,twende nao wachimbe kwenye migodi mikubwa. Madinipamoja na gesi, tuwatengeze wafanyabiashara wetuwenyewe, inahitaji mitaji mikubwa lakini Serikali iwekemikakati katika hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungependa kuona katikampango jinsi ambavyo Serikali itaimarisha STAMICO ili iwezekuingia katika uchimbaji huu. Vilevile tungependa kuona jinsiambavyo Serikali itavyoimarisha TPDC lakini kwenye mpangomzima mimi naona kama imeachwa na haionekani jinsiambavyo itakavyotusaidia. Hii ni rasilimali ya nchi yetu natunaitaka isaidie nchi yetu sana hasa kwa sisi wenyewekubakia na resource kubwa ya hivi vitu. (Makofi)

[MHE. R. L. MLAKI]

Page 83: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

83

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo ni maeneo machachenimegusia katika mapendekezo na nachosisitiza ni mpangouwe specific zaidi na kuoainisha vitu vitakavyofanyika kwauwazi zaidi. Aidha, mpango uweke vitu vichache kutokanana uwezo wa nchi na sio mambo mengi ambayoyatashindwa kutekelezeka kutokana na kutokuwa na fedha.Mwisho, mpango uwezekane kupimika. Kama kwelitumeweza kuutekeleza, tuepuke na hiyo misemo yakuhamasisha na nini. Watu wa Economic Unit ambayoitakuwa formed, ndio waweze kupima na kutusaidia katikahilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia,napendekeza mpango uwe na continuation. Kwa mfano,tukisema mwaka huu tuna kitu fulani, tuhakikishe mwaka ujaotunafuatilia sio tunaanza kingine kabisa na kile ambachotulisema tutakifanya hatujakimaliza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya marekebishohayo, naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana. Sasa namwitaMheshimiwa Selasini ajiandae Mheshimiwa DoktaKigwangalla, Mheshimiwa Mabumba na Mheshimiwa Kilufi.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nami nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kutoa mawazoyangu katika hoja iliyo mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninavyofahamu, mpangoulio mbele yetu ni sehemu ya mpango ule wa miaka 25ambao tuliupitisha hapa Bungeni. Huu tulionao sasa, niawamu ya nne ya utekelezaji wa ule mpango wa awali. Miminil itegemea kwamba Serikali ingetuletea jedwali lautekelezaji kwamba ile awamu ya kwanza tulipanga mambokadhaa haya na tumeyatekeleza kiasi fulani. Vilevilenilitegemea kwamba haya yaliyoletwa, yangekuwa na mudamaalumu wa utekelezaji kwamba tunasema tutashughulikiareli, lini tunategemea tutakamilisha lengo hili. Yanapoletwajumlajumla tu namna hii, wazo ambalo linaloingia ni siasa.

[MHE. R. L. MLAKI]

Page 84: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

84

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Wabunge wengi wanachokisema ni kwamba huu mpangouna mambo mengi sana ambayo kulingana na uwezo wetuwa kifedha ni kazi sana, haiwezekani kutekeleza yote. Kwahiyo, tutabaki tunadonoadonoa tu mwishoni tubakihapahapa tulipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, pendekezo langula kwanza, mimi ningeshauri tuangalie katika huu mpango,yale mambo muhimu ambayo yanaweza kusaidia kupelekauchumi wetu kwa haraka zaidi na tuyatekeleze hayo.Tumezungumza kwa mfano reli na hili litarudiwarudiwa sanana wachangiaji wengi kwa sababu reli ikitengenezwaitafungua bandari yetu. Reli ikitengenezwa barabara zetuzitalindwa, reli ikitengenezwa ajira zitaongezeka. Kwa hiyo,tuangalie ni namna gani kwa mfano, tunaweza kuchukuajambo hilo moja, tukalipa msisitizo na tukaweka mudamaalumu wa kulitekeleza baada ya huo muda ni rahisi hataBunge kuangalia kwamba mliahidi jambo hili kwa mwakamoja litashughulikiwa sasa tumefikia mahali hapa nakadhalika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiacha wazo hilo ambaloni la ujumla. Mimi napenda sana kuzungumzia habari yautawala bora. Tunaweza tukawa na mipango mizuri sanalakini utekelezaji wake ukawa mgumu kwa sababu ya hilisuala la utawala bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kamati tulilamikiwakuhusu urasimu ndani ya Serikali kwamba wako wawekezajiau wapo wananchi ambao wana tamaa ya kuwekeza, lakinimiradi yao inachukua muda mrefu sana kuidhinishwa. Imefikiahatua kwamba hata barua, kwa baadhi ya Taasisi za Serikalihazijibiwi. Sasa uzembe huu, unatukimbizia wawekezaji,wanakata tamaa wanakwenda kuwekeza nchi nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambasamba na hilo, kunauzembe tu wa kutofanyia mambo kazi. Watu wanatakakuwekeza lakini inaingia hisia ndani ya watendaji labda mradiuna rushwa kitu kama hiki, kwa hiyo, watu wanazungushwatu ofisi hii, ofisi hii, ofisi ile matokeo yake watu wanakata tama,

[MHE. J. R. SELASINI]

Page 85: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

85

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wanakwenda kuwekeza nchi za wenzetu na mafanikioyanaonekana makubwa tu. Kwa hiyo, ningeshauri Serikali,kama kweli tunataka kwenda, mambo ya urasimu tuyaache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mtu mmoja alikuwaanatuambia kuna supermarket moja ilikuwa ijengwe hapa,lakini watu wakazungushana hapa wakaenda Uganda, Raisakaita wale wote wanaohusika wakakaa kikao, siku moja kilakitu kikamalliza. Sisi jambo moja litazungushwa kwenye maofisimwaka mmoja, miaka miwili, hakuna uamuzi, hakunaanayezungumza, sasa hata hao wawekezaji tunaotaka wajehawatakuja, wanakwenda kwingine. Kwa hiyo, tuacheurasimu na tufanye kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tatizo pia la kutokuwana procurement plan katika Wizara, Idara za Serikali nakadhalika. Watu walishajua kwamba kuna mpango wautendaji lakini hakuna kitu chochote kinachoandaliwa. Kwahiyo, wanasubiri mpaka fedha zinapopatikana ndiowanakurupuka kuanza kufanya kazi. Sasa mimi nashaurikwamba kuwe na huo mpango wa manunuzi kwa sababuprocess yenyewe ya manunuzi inachukua muda mrefu. Nivizuri Wizara za Serikali, Taasisi za Serikali na kadhalika zikawana plan za manunuzi mapema kabisa wakati tunasubiriupatikanaji wa pesa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine kuhusu utawala bora,viongozi na sisi wenyewe Watanzania hatufanyi kazi.Tunaenda kwenye nchi za wenzetu, tunaona wenzetuwanavyofanya kazi. Sasa haiwezekani, hatuwezi tukaendeleabila kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya ofisi za Serikali,ukiingia hukuti watu na unaowakuta hakuna majibu, hakunauamuzi. Sasa ukija huku mtaani, mimi nashangaa hata fedhatunapata wapi. Nchi yetu ni kama imegeuzwa kuwa nchi yawalevi tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ni Mbunge Dar-Es –Salaam, hebu nenda Sinza unyoooshe mpaka Bunju ni baa

[MHE. J. R. SELASINI]

Page 86: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

86

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

tu, watu wanakunywa kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saanane usiku, watu wanakunywa tu. Hawataki kufanya kaziwakati tunataka maendeleo, hili halitawezekana. Ni lazimaifikie mahali tubadilishe mindset. Serikali itengeneze utaratibumadhubuti wa kupima utendaji wa watumishi wake naihakikishe kwamba sheria zilizopo zinafanya kazi sawasawa.Vipi watu wanakaa kutwa nzima wanakunywa hawafanyikazi, halafu wanaachwa tu hivi? Watu hawa wanapaswakufanya kazi ili nchi iendelee, kodi ipatikane na mambo kamahayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo napendakuzungumza ni kuhusu utalii. Nchi yetu ni ya pili kwa vivutiovya utali duniani baada ya Brazil. Hata hivyo, patotunalolipata kwenye utali i sio sawasawa na vivutiotulivyonavyo. Nafikiri hatuweki mkazo na wa kutosha katikakutangaza vivutio vyetu na kulinda baadhi ya vivutio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze kuhusu MlimaKilimanjaro. Mimi naupigia kelele sana hapa Bungeni. Sasahivi ukienda pale Kilimanjaro, hususani katika Jimbo langu laRombo, watu wote wanakimbizana na wananchiwaliopanda miti yao zamani na sasa wanataka kuivuna kwaajili ya kujenga nyumba zao na shughuli mbalimbaliwanakatazwa, wengine wanapigwa, wenginewananyang’anywa mbao zao. Nimeshasema kama ilivyokwenye pembe za ndovu, pale mlimani, msitu ule wa asili,miti ile inavunwa usiku, malori yanashusha mbao katika ulemsitu, hayana taa na mengine yanalindwa. Sasa hililinawaudhi wananchi! Unakwenda kumzuia namna gani mtukukata mti aliopanda mwenyewe kwa miaka labda 20 naanautunza? Leo anataka kuezeka nyumba yake unamkatalialakini msitu ule unavunwa, watu wanaona tu, watuwanaangalia tu. Sasa itafika mahali theluji pale mlimaniitakwisha. Watalii hawaji kuangalia ule mlima kwa sababuya urefu wake, wanakuja kuangalia theluji katika nchi zatropical. Sasa hili nimelisema sana, nisikilizeni jamani. Kamahii operesheni ya meno ya tembo inaendelea, pelekenioperesheni pale mlimani kuzuia miti kuvunwa na siokukimbizana na mwananchi mmoja mmoja ambao kwa kweli

[MHE. J. R. SELASINI]

Page 87: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

87

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wanavuna kilicho chao. Watu wa Rombo hawafundishwikupanda miti, ni desturi yao. Watu wa Rombo wanajuaukikata mti mmoja unapanda kumi na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, paleMoshi pana kiwanja cha ndege ambacho kilikuwa kinaletautalii pale kiurahisi...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Nakushukuru Mheshimiwa Selasini, nikengele ya pili.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Msemaji anayefuata ni MheshimiwaDokta Hamisi Kigwangalla, hayupo. Mheshimiwa Mabumbaatafuatiwa na Mheshimiwa Modestus Dickson Kilufi naMheshimiwa Kombo.

MHE. SYLVESTER MASSELE MABUMBA: MheshimiwaMwenyekiti, nikushukuru. Awali ya yote, napenda kuchukuanafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi yaRais, Mahusiano, kwa mapendekezo ya mpango ambaoamewasilisha katika Bunge lake Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapojadili mapendekezohaya, matarajio yangu yalikuwa kuonyesha ni kiwango ganiutekelezaji wa bajeti tuliyoipitisha, Serikali imewezakuitekeleza kwa kutoa rasilimali fedha, ili kutekeleza kaziambazo Bunge hili zilipitisha hapa. Kwa bahati mbaya,mambo haya sijaona katika mapendekezo ya mpango huu.Waziri ameelezea baadhi ya sekta ambazo kwa maoni yaSerikali tumefanya vizuri. Ni kweli tumefanya vizuri kwakudokoa sehemu ndogondogo sana kwa sababu mambo nimengi, wakati wenyewe hautoshi. Maoni yangu, naona Taifaletu halijawa na vipaumbele ambavyo tunavijua kwambatukivitekeleza hivi, uchumi wetu utakuwa lakini vilevile

[MHE. J. R. SELASINI]

Page 88: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

88

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wananchi wetu tutawaondolea umaskini na pia tutawezakuongeza ajira kwa watu wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano sekta moja hii yakilimo ambapo Serikali ilikuwa na kauli mbiu ya Kilimo Kwanza.Mimi nilitarajia kuona hapa tunaambiwa kwenye utekelezajiwa sera ya Kilimo Kwanza, nchi yetu imepiga hatua kiasi ganikuondokana na shida ya kuwa na uhakika wa chakula. Kunamaeneo tunapozungumza hapa yametajwa kwamba yanashida ya chakula. Sasa nilitarajia tuambiwe hapa, sera yaKilimo kwanza katika Mikoa mbalimbali, Serikali imefanikiwamambo gani? Mfano kwenye eneo moja la kuhakikishakwamba tuna kilimo cha umwagiliaji, ni mabwawa mangapiyamechimbwa ili watu wetu wasitegemee tena kilimo chamvua ambacho hakina uhakika? Naelewa Mikoa ile yaShinyanga, Simiyu, Tabora, kilimo chao ni cha kutegemeamvua. Wanatumia nguvu nyingi sana lakini mavuno ni kidogosana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tumeambiwakwenye sekta ya barabara kwamba tumefanikiwa sana. Miminadhani Serikali ingeweka nguvu zake kutatua kero katikaMiji mikubwa hii ambayo leo traffic jam inasumbua hatauzalishaji wenyewe unashuka. Tunaambiwa barabaraza kupita juu, fly overs Dar-es-Salaam, utekelezaji wake ukoje?Leo Dar-es-Salaam imekuwa ni karaha sana, eneo la kwendakwa saa moja unakwenda kwa saa tatu au nne, uzalishajiuko wapi? Wafanyakazi wanaishi katika hali ya mateso kwasababu analazimika afike asubuhi saa moja na nusu, kwahiyo, aamke saa kumi na moja au saa kumi na anapaswakuondoka saa tisa na nusu anafika kwake saa tano usiku.Nilitarajia kuona ni namna gani kwenye mpango huu, kerohii kwenye eneo la barabara, kwenye Miji mikubwa kamaDar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Tanga, Serikaliinatuambia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kwenye eneo la reli,taarifa ambayo imetolewa hapa, mimi sijaifurahia sana.Kama kweli tunataka kujenga uchumi imara na endelevu nawa kasi, ni lazima Serikali iangalie reli. Mfano sasa hivi wakati

[MHE. S.M. MABUMBA]

Page 89: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

89

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanapoitengaTanzania basi kumbe ni wakati muafaka Tanzania kuimarishareli mpaka Kigoma wananchi wa nchi ya Burundi na DRCambao kwa kweli kama sisi tutaweka miundombinu mzuri,watatumia na hata hawa ambao wanajaribu kuunda ushirikamwingine, wao watakuwa wamepotea sana kwa sababuhaiwezekani uzunguke kama tulivyoambiwa kilomita mia tisaza ziada. Mtu wa Burundi hatatumia hiyo alternative nyingine,mtu wa DRC hatatumia hiyo alternative hiyo nyingine, hawaambao wanataka kwenda kule ni kwa ushabiki lakini uhalisiahaupo, kibiashara hailipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali yanguiimarishe reli. Hata hizi barabara ambazo tunajenga kwagharama kubwa sana, tutaweza kuzilinda. Waziri wa Ujenzialisema hapa, uzito wa malori yanayopita kwenye barabarazetu wakati mwingine ni mkubwa sana, kwa hiyo, usalamawa barabara haupo. Kwa hiyo, kwenye eneo hili, naombaSerikali yetu ijenge sasa reli kwa ajili ya kuhakikisha kwambatunanufaika na fursa ambazo zipo DRC na Burundi lakini piawananchi wa maeneo yale ya Kigoma na Tabora.

Mheshimwa Mwenyekiti, tunapozungumzia Mpangowa Maendeleo, vilevile ni lazima tuzungumzie habari ya ulinzina usalama wa nchi yetu. Sijaona kwenye kitabu hiki wapiwanaelezea habari ya ulinzi na usalama ili kuhakikishakwamba hata huu uchumi tunaotaka kuujenga, tuwezekuufanikisha. Kwa mfano, usipowekeza kwenye ulinzi nausalama, ambapo sekta ya utalii kutokana na upana wakeinaweza kuchochea sana ukuaji wa uchumi wetu kwasababu sekta hii inatoa ajira na unaleta fedha za kigeni.Naomba sana kwenye mpango huu, suala hili la ulinzi nausalama wa nchi yetu na hata haya matukio ambayoyametokea leo, watu wengine ndani ya Jamhuri yaMuungano tunatembea hatuna uhakika na maisha yetu.Upande wa pili wa Zanzibar kule ambako kila siku watuwanamwagiwa tindikali, watu wanadhalilika, mpango wetuhuu kwa sababu naamini ni moja katika mandate yaMuungano kuhakikisha kwamba amani inapatikana katikamipaka yote. Sisi kule tunamwagiwa tindikali, maisha yetu

[MHE. S.M. MABUMBA]

Page 90: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

90

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

yapo hatarini, tuna hofu, hatuna amani. Sitaki kusema sanakwa sababu wote mmeona Padri yule mtu mzima miaka sitinialivyodhalilika, leo tunaambiwa hata kuona haoni, jicho lakelimekufa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ni lazima iwekezekwenye amani, kwenye usalama, kwenye ulinzi, vinginevyounapowavamia watu wenye ushawishi katika jamii, mfanosisi hapa tunaitwa Waheshimiwa, Ubunge wetu ni miakamitano, baada ya miaka mitano wananchi wanawezawakapoteza ladha ya kukuchagua tena, ukawa mwananchiwa kawaida, lakini viongozi wa dini wanakufa na uongoziwao. Kwa hiyo, wana ushawishi mkubwa katika jamii, ni lazimatuwalinde ili tuhakikishe kwamba wanasaidia pia kushawishiwatu wanaowaongoza kuunga mkono sera zetu.Tunapowaachia wakawa wanadhalilika, haitusaidii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye eneo mojaambalo Waziri amezungumzia kuhusu viwanja vya ndege.Nipongeze kazi imefanyika pale Kigoma lakini kamanilivyosema, uwanja wa ndege wa Kigoma tuupanue uwezekuhudumia DRC na Burundi. DRC na Burundi wawe washirikawakubwa na Tanzania na wengine wata-regret katikamaamuzi yao na wakiendelea, fursa ya DRC inatosha sanakuachana na wengine ambao wanaibeza Tanzania.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana kengele ya pili.

MHE. SYLVESTER MASSELE MABUMBA: Ya kwanza!

MWENYEKITI: Ni kengele ya pili.

MHE. SYLVESTER MASSELE MABUMBA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Sasa nitamwita Mheshimiwa ModestusKilufi na Mheshimiwa Kombo Khamis Kombo ajiandae.

[MHE. S.M. MABUMBA]

Page 91: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

91

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. MODESTUS D. KILUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kupewa nafasi hii il i na mimi niwezekuchangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2014/2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi kuzungumzia uhai waTaifa kama Taifa halina uchumi mzuri. Mipango yote hiiinategemea uchumi mzuri. Nimefurahishwa sana na mipangomingi ambayo imeoneshwa humu na mimi niseme kwambatu watu wazuri sana katika kupanga lakini napata taabu sanatunapokuja kwenye utekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazo rasilimali nyingi sanawala si za kusema tubuni, tunavyo vyanzo vingi sana vyakiuchumi ambavyo vinaweza kusababisha uchumi wetuukapanda. Tatizo tulilonalo ni namna gani tunasimamiavyanzo hivi, ni namna gani tunajipanga vizuri kucheza vizurina wawekezaji ambao tunasema sasa hivi tuelekeze nguvuzetu kwenye sekta binafsi ili iweze kusaidia kwenye utekelezajiwa miradi yetu ya maendeleo au kuchangia kwenye miradiyetu ya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasikitika sana kwamba leoWabunge tupo hapa tunachangia lakini napata taabukuona kwamba sijui ni nani anayeratibu haya tunayoyasemakwa sababu ukiangalia idadi ya Mawaziri waliopo, kwa kwelihairidhishi. Sijaelewa hapa tunapozungumza, anayeratibu ninani kwa sababu leo hapa Serikali imetuletea mpangotunatakiwa tuujadili lakini wale waliotuletea mpango ili tujadiliwaratibu na wakafanye vizuri zaidi, hawapo, sasa inakuwaje?Nadhani hapa kuna utani kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mengi wameyasemawenzangu, lakini siku zote nimekuwa nikizungumza humuBungeni kwamba nchi hii haina miiko ya kulinda uchumi wanchi, hatuwezi kwenda hata kidogo, haiwezekani! Tunajifunzakwa wenzetu ambao wameendelea wana miiko. Nchi ganiambayo watu wanafanyakazi bila woga. Haiwezekani kabisaWaziri anajua tunajadili hapa mambo ya msingi ambayoanatakiwa arekebishe hayupo. Kwani kama ni safari kwa ninizisipangwe wakati ambao siyo wa kipindi cha Bunge?

Page 92: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

92

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Unapangaje safari wakati Wabunge wanaendeleakuchangia hoja na wewe tunakutegemea utusaidiekurekebisha, wapo wachache tunawashukuru mliopo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo matatizo mengiambayo yanatokana na uwajibikaji. Nchi hii haiwezi kwendakama Serikali haitasimamia watendaji mbalimbali ambaowanatakiwa watekeleze miradi hii na mipango hii mizuriambayo imewekwa mezani kwetu. Nina mifano mizuri tu yakuonesha ni namna gani hatupo serious katika kusimamiauwajibaki na utekelezaji na usimamizi wa mipangombalimbali ya nchi yetu. Kwa mfano, hivi Halmashauri nyingiambazo zimesababisha upotevu wa pesa nyingi natukategemea hatua zitachukuliwa kwa watu waliosababishaupotevu huo lakini mpaka leo wanasuasua, hawachukuliwihatua, tunategemea nini tupeleke fedha zetu huku kwa ajiliya mipango ya maendeleo. Mfano mzuri ni Halmashauri yaWilaya ya Mbarari, imepata hati chafu na nchi nzimatunasemwa. Mimi nimekuwa nikisema kila siku juu yaubadhirifu uliopo pale lakini leo waliochukuliwa hatua nikichekesho, ni watu wawili, watatu tu, wengine wapo wapiwaliopoteza mabilioni ya fedha za maendeleo ya wananchiwa Mbarali? Kitendo hiki cha kutokuchukua hatua kwa watuwanaofanya vibaya nchi hii haiwezi kuendelea hata kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, China tunasema sasa hiviinaenda vizuri, lakini ina mipango mizuri ya kudhibiti wale wotewanaofanya vibaya. Wabunge kama tungekubaliana,ilitakiwa tuwe na sheria kali ya kusimamia uchumi wa nchi hiiikiwa ni pamoja na kuwapima Mawaziri utendajikazi wao,kwa sababu Waziri angeendelea kuwa Waziri kutokana nakuendelea na ku-perform kwa Wizara yake. Sasa weweunaongoza Wizara, Wizara inaenda vibaya unaendeleakuwa Waziri, unafanya nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, ni siku mbili, tatu hizitumeshuhudia wafugaji wakipata shida na kuhangaika katikanchi hii, lakini Wizara ipo na Waziri yupo! Hivi hawa wafugajiwanawezaje kuhangaika hivi? Hivi tuseme Serikali imeshindwa

[MHE. M. D. KILUFI]

Page 93: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

93

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kubuni ni namna gani mifugo inaweza ikawa ni chanzo chauchumi katika nchi hii? Kwa nini tuache wafugajiwanahangaika tu, wanapata shida, wanakuja hapawanalialia. Haya tunaambiwa kuna ng’ombe zao zimeshikwazipo mahali fulani lakini mwenye kutoa kauli kwambawapigwe faini, waachiwe tutengeneze utaratibu mzurihayupo, ng’ombe zinauzwa. Wafugaji wapo hapa na Serikaliipo hapa inaona. Ushauri wangu kwa Serikali yangu nikwamba operesheni ni nzuri na nia yake ni nzuri, lakini kitendokinachofanyika na kuona watu hawa wanahangaika, sijambo jema hata kidogo. Tunajivunia nini kama mifugoambayo tayari wafugaji wetu wanaitunza tumeachainaachwa hovyo ovyo, tunawafilisi watu badala ya kuwekautaratibu mzuri ambao utawasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya vyanzo ambavyomimi nilitegemea kama Serikali itaweka mipango yake vizuri,mifugo ni chanzo kizuri cha uchumi wa nchi hii. Badala yahizi ranchi za Taifa kugawiwa kwa wawekezaji, tungewezatukawapa wafugaji hawa na wakapewa masharti yaleyalewakaweza kumudu kutimiza il i kusudi nchi hii kamatunategemea ranchi kama sehemu ya uchumi basi tutapatakutoka kwa wafugaji wetu. Tunashindwa nini leo kutengamaeneo ya wafugaji hata wakayalipia kuliko ilivyo sasawanahangaika. Tukaboresha miundombinu ya maji nakadhalika ili wafugaji hawa nao wakawa ni sehemu ya patola Taifa. Hata hivyo, tumewaacha wanahangaika ni chanzokizuri cha mapato, ni afadhali hata kama tungesema wawewanalipia ile mifugo lakini tuwatengee maeneo mazuri kulikokuwaacha wanavyohangaika hivi sasa. Hicho ni chanzoambacho naona hatujakiwekea mikakati mizuri ambayoingeweza kuongeza pato la Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji kuimarishaviwanda ili kuzalisha ajira nyingi kwa Watanzania wengiambao hawana ajira. Tunahitaji kuimarisha kilimo ili kusudivijana wengi na wananchi wengi wa Tanzania ambaowamejiajir i kwenye kil imo waweze kulima kwa tija.Tunazungumza Kilimo Kwanza sijaona mkakati kamaambavyo wenzangu wamesema labda ni kitu gani

[MHE. M. D. KILUFI]

Page 94: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

94

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kinafanyika au tunatarajia kifanyike ili tuweze kutengenezascheme nyingi za umwagiliaji na vijana waweze kujiajiri huko.Sijaona mpango huo ambao unaonesha haya, nimeona tukwamba kuna maeneo fulani yataendelezwa kwa kilimo,lakini ni mikakati gani tutaitumia hii nguvukazi kubwa ambayoimekaa tu Mjini, vijana wanazurura ili waweze kwendakujiunga kwenye miradi hiyo muhimu, viwanda havipo, mimisiwalaumu, wafanye nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali hatujawekamipango mizuri ya kuweza kujiajiri kwa hawa wananchiwanaozurura mjini. Nguvukazi kubwa hii ambayo inakaahaina kazi kubwa, mtu anauza tu vifulana, anatembea sikunzima unategemea alete uchumi kwenye Taifa lake, atatoawapi, kama hatujampa mipango mizuri? Hawa vijanahawapendi kuzurura, lakini tungewekeza kwenye kilimo namimi nasema kwenye kilimo kuwaachia wawekezaji pekeyake bila sisi kuweka nguvu yetu na kuonesha mipango yetubado hii sekta haitaweza kutukomboa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, tumewekawawekezaji lakini hatujaonesha ni namna gani wawekezajiwatashirikiana na wananchi wa maeneo yale ili wananchiwale nao waweze kunufaika na uwekezaji huo. Tunategemeawawekezaji kuwepo mahali pale wananchi wa maeneo yalenao wanufaike na uchumi wao upande, lakini hatujawekamiiko wala taratibu zozote. Mwekezaji anaambiwaunawekeza hapa endelea, matokeo yake ni ugomvi nawananchi wa maeneo yale, ni taabu, ni kero, wale wananchiwanaona kama wamepelekwa jehanamu katika eneo laoambalo walikuwa wanaishi kwa raha na mustarehe. Je, huuni uwekezaji kweli? Je, asilimia wanazochangia Serikalini nikiasi gani? Tumefanya utafiti kiasi gani kuona mafanikio yauwekezaji katika nchi hii? (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Nashukuru sana, ni kengele ya pili. Sasanamwita Mheshimiwa Kombo.

[MHE. M. D. KILUFI]

Page 95: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

95

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kupata fursa hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niseme kwambaMpango wa Maendeleo ya Taifa, ni chombo ambachokinazihusu Wizara zote za Serikali. Mimi nilitegemea nakutazamia kwamba kwa sababu tunajadili masuala yampango, basi Waheshimiwa Mawaziri na Manaibu waopamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara wangekuwepo katikakujadili suala hili. Hata hivyo, kwa sababu tuna utamaduniwa kusema na kusoma bila ya kutenda, ndiyo leo ukaonakwamba Mawaziri na Manaibu waliopo ni wachache na sihivyo tu hata Makatibu Wakuu wa Wizara husika hawapo,pamoja na agizo la Spika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, nisemekwamba tuna sera inayosema kwamba Tanzania ni nchi yawakulima na wafanyakazi. Kama Tanzania ni nchi yawakulima na wafanyakazi, tujiulize ni kwa kiasi gani tunaitumiaardhi yetu katika masuala ya kilimo? Tumepeleka kipaumbelegani katika masuala ya kukuza kilimo? Tuna hekta ngapi zakilimo? Mimi nasema kwamba bado tamko la Tanzaniakwamba ni nchi ya wakulima na wafanyakazi litaendeleakuwa ni tamko ndani ya vinywa vyetu na ndani ya maandishilakini hatujaweza kutekeleza sera ya kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika masuala yaufugaji ambayo wengi wameyaongelea, nakubali kwambaTanzania tuna utajiri mkubwa wa mifugo. Hata hivyo, mpangohuu haujaeleza ni kwa kiasi gani Tanzania tuna bahari, mitona maziwa ambayo yana samaki wengi, tuna wavuvi wengitu, lakini suala hili halijaguswa. Niseme kwamba hii ni kinyumena Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa sababu sekta yauvuvi ipo kwa asilimia kubwa ndani ya nchi yetu. Tunamaeneo makubwa ya bahari, tuna samaki wengi, tunamaziwa mengi yenye samaki wengi, tuna mito mingi yenyesamaki wengi, je, tunazitumia vipi rasilimali hizi kwa uchumiwa Taifa? Kama si maneno ya usanii yaliyomo kwenye vitabu,rasilimali hizi tunazitumia vipi? (Makofi)

Page 96: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

96

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu wameendeleakatika masuala ya ufugaji wa samaki. Ni mara nyingi sanakumsikia Mheshimiwa Kitandula akizungumzia masuala yaufugaji wa samaki, lakini yanazungumziwa humu yanawekwakwenye madroo ya meza, hayafanyiwi kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna wataalam wengi wauvuvi. Je, hawa wamepewa nyenzo gani za kuweza kufanyiakazi. Wamepewa uwezo gani wa kuweza kuwaelimishawenzao ili tuondokane na umaskini. Wamepewa uwezo ganiwa kuwaelimisha wenzao ili waweze kufanya kazi kwa kujiajirikatika Sekta ya Uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya yote yanaachwa nahayashughulikiwi. Sasa Mpango huu ni mzuri na nawashukuruKamati ya Bajeti na pia Kambi ya Upinzani kwa namnaambavyo waliweza kuwasilisha hoja zao. Hoja zao zilikuwana msingi. Kamati ya Bajeti hoja zao zilikuwa za msingi naitabidi Wizara izifanyie kazi, isiwe wameshatoa kazi, lakiniikachukuliwa kama kinanda kinachopigwa kwenye taarabu.Ikimalizika taarabu na kazi imekwisha. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile Mpango ulipaswakuangalia mabadiliko ya tabianchi kwa uchumi wa Taifa laTanzania. Je, Mpango wa mwaka 2014/2015, umeangaliaangalia vipi athari za mabadiliko ya tabianchi kwa uchumiwa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini vile vile kuna suala zimala viwanda. Niseme kwamba, viwanda ni sehemu ya ajirakwa vijana, lakini tujiulize hivi kweli viwanda vipo? Viwandaambavyo vilikufa vimefufuliwa? Vinafanya kazi? Vimeajirivijana wangapi? Kwa sababu viwanda vitakapokuwa haina vikawa vinafanya kazi, vitaweza kuajiri vijana wetu wengina kwa hivyo lile suala tulilosema la vijana kukaa vijiwenilitaweza kuondoka kwa kiasi kikubwa na vile vile tutawezakuongeza pato la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, l ingine, ni suala labarabara...

[MHE. K. K. KOMBO]

Page 97: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

97

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Kombo.Sasa namwita Mheshimiwa Rage.

MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO: MheshimiwaMwenyekiti, ni ya kwanza.

MWENYEKITI: Ya pili.

MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO: Ahsante.

MWENYEKITI: Sasa namwita Mheshimiwa Rage,ajiandae Mheshimiwa Dkt. Kikwembe na MheshimiwaMwijage.

MHE. ISMAIL A. RAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, awaliya yote, napenda kukushukuru kwa kunipa nafasi hii yakuchangia. Kwanza, napenda kupongeza mapendekezo yaMpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2014/2015 navile vile…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Rage, hebu hamia kwenyemicrophone nyingine.

MHE. ISMAIL A. RAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Baada ya kuunga mkono napenda vile vilekuipongeza Serikali yangu ya CCM kwa kazi nzuri iliyofanyakatika kuhakikisha kuna mabadiliko katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajikita katika maeneomakubwa manne; maji, reli, kilimo na umeme. Napendakuanza na reli kwa sababu tumekuwa tunaongea kwa mudamrefu sana katika Bunge letu hili. Tunapenda kuwakumbushatu Serikali yetu kwamba, sasa wabadili na kuongeza speed iliwaweze kwenda mwendo wa kasi. Bahati nzuri Wazirimwenye dhamana ya masuala ya reli Mwenyezi Munguamekuja na hekima mpya na nguvu mpya, lakini nadhani

Page 98: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

98

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

tusipomwezesha kifedha, nguvu zake na hekima yakeitapotea bila sababu yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo kwa sababukwa zaidi ya miaka 25, tulikuwa hatujawahi kuthubutukununua mabehewa. Mheshimiwa Waziri huyu kwenyehotuba yake ya bajeti ametuhakikishia tutapata mabehewa15 ya vichwa vya treni na tutapa mabehewa 276 kwa ajili yakubeba mizigo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, azma hii kama itatekelezwa,kwa bahati mbaya ilikuwa kwenye Mipango wa Mwaka 2012/2013, lakini haikutekelezwa. Mimi nipo kwenye Kamati yaPAC, taarifa tuliyokuwa nayo ni kwamba, malipo ya awaliyamelipwa wiki chache tu zilizopita, kwa maana hiyomabehewa haya hayatafika nchini mpaka mwakani tena,2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kukuhakikishia,Mwenyezi Mungu akijalia mabehewa haya tukayapata,uchumi wetu utabadilika kwa sababu mizigo mingi itawezakubebwa kwenye reli na malalamiko ambayo kama uliyasikiajana kwa Waziri wa Ujenzi barabara zetu zimeanza kuharibikani kwa sababu tunatumia sana barabara kuliko reli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu za Benki Kuuzinaonesha kwamba, zao la tumbaku ndilo linaingiza fedhaza kigeni kuliko zao lolote, lakini mkulima hafaidiki kwa sababuanalipa gharama za kusafirisha kwa njia ya barabaratumbaku kwenda Morogoro, mbolea kutoka Dar es Salaamkuja Tabora au katika mikoa mingine, yote inakwenda kwabarabara. Kwa hiyo, gharama hii itakuwa kubwa. Lakiniendapo mabehewa Dkt. Harrison Mwakyembe tukiyapata,gharama ya usafirishaji itapungua sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuongelea suala lamaji. Vita ya tatu ilishakwisha. Watabiri wanatabiri kwambakama itatokea vita ya nne basi itatokea kwa ajili ya maji.Sijui kwa nini Serikali yetu katika Sekta hii bado inazembea.

[MHE. I. A. RAGE]

Page 99: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

99

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Nina ushahidi wa kutosha kabisa na nitatoa mfano wa mradiwa KASHIWASA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi huu unanikera sana,una uwezo wa kuzalisha maji milioni 1.2 litres kwa siku moja,lakini maji yanayotumika sasa ni lita milioni 17 tu asilimia 9.2.Asilimia 91 ya yale maji yamekaa idle pale Ihelela, kwa nini?Kwa kipindi cha miaka mitano sasa Serikali imepitisha pesazaidi ya bilioni 4.7 kwa ajili ya kulipa gharama za umeme nakuendesha mradi wa KASHIWASA. Kinachohitajika majiyamefika Kahama wapelekewe wananchi wa Maswa,Bariadi, Nzega, Igunga, Tabora, Urambo na Sikonge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, KASHIWASA watapata kuuzamaji lita milioni 57 kwa siku moja. Maana yake nini? Sasahivi KASHIWASA wanauza cubic meter moja ya maji shilingi505. Lakini ukiweza kupeleka maji haya yakafika mpakaTabora maji yatakuwa shilingi 249. Je, uchumi haujabadilikahapo? Utakuwa umempa mwananchi nafuu na Serikaliitapata nafuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu umeme; Waswahiliwanasema mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Wizarahii tangu imefanyiwa mabadiliko, Mawaziri wale watatuwanastahili sifa kubwa sana. Ni aghalabu sasa hivi kupataumeme wa masaa machache, umeme uko throughout now.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu tupate uhuru miaka52 mpaka mwaka 2005 wananchi waliokuwa wanapataumeme ilikuwa ni asilimia tisa tu, lakini sasa wananchi ambaowanapata umeme wa uhakika inafikia takribani asilimia 26mpaka 28. Kwa maana hiyo, kuna uwezekano kabisa Ilaniya Chama cha Mapinduzi kabla ya 2015, asilimia 45 mpaka50 ya wananchi kupata umeme itawezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo kwa sababuninazo taarifa za uhakika kwamba, sasa hivi pipes zimeanzakuwekwa kutoka kule inakotoka gesi kwenda Dar es Salaam.Kwa uchunguzi niliofanya, nimegundua kwamba, bei ya

[MHE. I. A. RAGE]

Page 100: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

100

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

umeme itashuka kutoka senti 45 za Marekani mpaka kati yasenti sita mpaka 10 za Marekani. Hii maana yake nini? Maanayake uchumi wa nchi utabadilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa rai kwaWaziri mwenye dhamana, atuletee mabadiliko ya Sheria yaRoad Toll. Reli wananunua mafuta mengi sana. Sasa waowanatakiwa tuwasamehe zile pesa wanazolipa kwa ajili yaRoad Toll zingerudi kwenye reli ili tuimarishe reli ya Kati na relizingine. Kinyume chake habari ya mipango au kuendelezauchumi wa nchi hii, tutakwama tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, nataka kushaurikwamba, Wizara ya Fedha sasa ibadilike katika kutoamaamuzi yake inapokuwa Bunge hili linaidhinisha Bajeti nawatoe pesa katika miradi ambayo tumeshapitisha ili tuwezekutekeleza kwa wakati unaotakikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mfano wa Kampunimoja inaitwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wamzungumzaji)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Rage.

MHE. ISMAIL A. RAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono mpango huu mia kwa mia. (Makofi)

MWENYEKITI: Namwita Mheshimiwa Dkt. Kikwembe naMheshimiwa Mwijage ajiandae.

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi nami niwezekuchangia katika Mpango huu wa Maendeleo wa Taifa kwakipindi kijacho cha mwaka 2014/2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napendanitoe pole kwa ndugu zangu wana Katavi walioko Wilaya yaMlele, Kata ya Kibaoni, kutokana na operesheni hii

[MHE. I. A. RAGE]

Page 101: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

101

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

inayoendelea ya upambanaji wa majangili; tumepotezamwanakijiji mmoja ambaye amepigwa risasi na MheshimiwaDiwani ambaye alikwenda kwenye msiba huo, yalimkutamasahibu na sasa hivi yuko hospitali anaumwa. NamwombaMungu ampe afya, arudi kuendelea na majukumu yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, napenda niishukuruSerikali kwa namna ambavyo imeweza kujitahidi kupangamipango ambayo mara nyingi tumekuwa tunaiona nainatuletea mabadiliko katika nchi. Sisi wote ni mashahidi,tumeona namna ambavyo Tanzania yetu inabadilika, hasasisi tunaotembea kwa barabara, tunashukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia upande waviwanja vya ndege tumejenga. Nashukuru Mkoa wetu waKatavi tumepata kimoja. Japokuwa katika mpango huuvinaonekana kama vimekamilika, hapana. Niiombe Serikalikatika kupanga mipangilio hii, sikatai kupanga ni kuchagua,lakini tupange mipango ambayo nafikiri tutaitekeleza kwawakati unaofaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa sana na huuutaratibu wa kusubiri, tukusanye kwanza, tunapanga,tunakusanya halafu ndiyo tunaanza kutekeleza. Kituambacho sidhani kama ni sahihi katika kupanga. Kwa hiyo,lazima Serikali ikubali sasa kubadilisha mfumo wa bajeti tutokekwenye cash budget twende kwenye capital budget.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ngumu sana kupanga kituambacho sinacho mkononi. Kwa mfano, nasema kwambanikipata milioni 10 ndipo nitafanya moja, mbili, tatu. Je,nisipopata ama nikapata robo. Ina maana yale malengomengine sitayatekeleza. Kwa hiyo, naishauri Serikali kupangamipango kutokana na rasilimali tulizonazo ili hii miradi ambayotunapanga kuitekeleza, tuitekeleze kwa wakati na tuwezekuimaliza na wakati ujao ndipo tuweze kupanga kitu kingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba niungane nandugu yangu Rage aliyeongelea suala la reli. Kwa kweli relindiyo mkombozi, tukubali tusikubali. Ukweli ubaki kuwa ukweli.

[MHE. DKT. P. W. KIKWEMBE]

Page 102: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

102

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Hatuwezi kusema tutaendelea bila reli. Kwa hiyo, reli ya katilazima tuipe kipaumbele. Tukubali tusikubali, Serikali ifanyejuu chini kuhakikisha kama tulivyoongea kwenye bajetiiliyopita, basi mpango wetu unakwenda vile vile na tujipimekatika kutekeleza hii miradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, hata Mwalimudarasani, ukiwa darasani huwezi kusema leo nitafundishahapa kidogo hapa kidogo, hapa kidogo, hapana. Utakuwana malengo ya jumla and then utakuwa na malengomahususi kwamba, lengo langu la jumla ni hili, sasa ndani yadakika hizi nitatimiza hiki. Siyo ndani ya dakika hizi nitatimizamoja, mbili, tatu, nne, tano, haiwezekani! Kwa hiyo, lazimatufike mahali, tuangalie namna gani tunapanga mipangiliioyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niende moja kwamoja kwenye elimu. Natoa mapendekezo katika mpangohuu, tuwekeze vya kutosha kwenye elimu. Tumeongeleasuala la rasilimali watu kuwaendeleza, tunawaendeleza vipi?Tunawaendeleza vipi, kwamba tutaendelea kuwaongezeamafunzo, ama semina, watumishi au wafanyakazi katikaSekta labda ya Uranium au kwenye makaa ya mawe, kivipi,kama kwenye elimu ya msingi na sekondari hatujatengeneza.Kwa hiyo, naiomba Serikali, kama kweli tuna niaya kuikomboa nchi yetu lazima tuwekeze kwenye elimu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependekeza zifanyikejitihada za makusudi katika kuhakikisha elimu ya sekondariau ikiwezekana tufanye basi kutoka elimu ya darasa lakwanza mpaka kidato cha nne iwe elimu bure na iwe ni yalazima. Sasa tuwekeze kwenye maabara tuwekeze kwaWalimu, tuwekeze kwenye nyumba za Walimu, maana yakemwanafunzi atapataje elimu bora na tutaendeleaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutakuwaje na rasilimali yawatu ambao tunasema wanakwenda kwenye gesi, ambao,jamani, si tunataka haya makampuni yaje na wataalam

[MHE. DKT. P. W. KIKWEMBE]

Page 103: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

103

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wao? Ndio maana yake? Sasa sisi tutaendelea kuwa vibaruakwenye yale makampuni mpaka lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba katikahilo, Serikali iliangalie sana, namna ya utekelezaji wa miradi.Sheria zipo, wazembe wachukuliwe hatua, kwa ninitunaonekana aibu? Ni kwa nini tunaoneana aibu?Wanaozembea kutekeleza wachukuliwe hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine tunawezatukawa tunalaumu wasimamizi, kumbe ndio haya hayatunayosema, kwamba, tunapanga kabla ya kuwa na pesa.Pesa inachelewa kufika, tunalipa mishahara watu wakusimamia miradi kabla ya pesa za miradi hazijatoka, maanayake ni nini? Maana yake ni hela ya mishahara inaendeleakwenda, lakini hela ya miradi haipo. Tunalipa watuwasiofanya kazi; kwa hiyo, tunazidi kupata hasara, badalaya kusonga mbele tutazidi kurudi nyuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, katika hilonaomba sana. Pia, naomba Kitengo cha Usimamizi naUfuatiliaji kiimarishwe, hii biashara ya kuwa mnatoa helamnaacha, haiwezekani hata kidogo. Narudia tena, hapamajibu yamejibiwa kwa mfano, swali la Mheshimiwa Kandegelilivyojibiwa, kwa kweli, hatuwatendei haki wananchiwanaosikiliza; naomba Serikali ijaribu kutoa maelezo ya kina,pia kwenye masuala ya msingi ambayo wananchi wanauliza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge,tusisubiri kuja humu ndani na kuuliza miradi imefikia wapi?Niliwahi kuuliza kwenye kikao, mimi ni Mjumbe wa Kamati yaMiundombinu. Niliwahi kuwauliza watu wa TANROAD MakaoMakuu; nikauliza, hizi taarifa mnazileta, mnakwenda kwenyeeneo ama mnaletewa tu makaratasi Wizarani and thenmnakuja kutusomea hapa? Wakaelezaeleza pale, kwasababu mimi sio engineer ilibidi nikubaliane nao tu. Sasa ndiohaya tunayosema kwamba, ni lazima sasa tuone namna ganitunawekeza kwenye elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nirudi niipongeze

[MHE. DKT. P. W. KIKWEMBE]

Page 104: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

104

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Serikali kwa kuanzisha mkongo huu wa Taifa wa Mawasilianoambao unahusisha pia mambo ya TEHAMA ambao kwawakati mwingine itaenda moja kwa moja kuunganishakwenye mashule. Niiombe Serikali, vile vifaa ambavyo niwezeshi kwa hii TEHAMA, kwa mfano labda, mambo yainternet, package za data na nini, nafikiri vile viwezeshi vyahii teknolojia, viweze kupunguziwa kodi ili kurahisisha aukupanua wigo wa watu wengi kutumia huduma hiyo nawewe ili uweze kukusanya kwa wingi kuliko ukiweka kodikubwa. Ina maana watumiaji watakuwa ni wachache namapato yako yatakuwa ni machache, kwa hiyo, hatutawezakupata mapato ya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni la ukusanyajiwa mapato, kama tunayumba hapa naomba paangaliweupya. Eneo la ukusanyaji wa mapato na lenyewelichunguzwe upya, inawezekana kuna uzembe mahaliambao unasababisha haya yote kutokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine napenda kuongeleahizi riba za benki. Kwa kweli, zimekuwa juu sana kiasi chakumfanya mwananchi wa kima cha kati ama kima cha chinikuogopa kwenda kukopa benki na hivyo kuwa ngumu kwakekujikwamua kutoka kwenye umaskini na sisi lengo letu nimaisha bora kwa kila Mtanzania, kwa kila mwananchi. Kwahiyo, basi waangalie upya ni namna gani mtumishi wa katiama mwananchi wa kima cha chini anavyowezakuwezeshwa, ili aweze kukopa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niongelee hili la Benkiya Wanawake. Katika bajeti iliyopita, tuliongelea angalaubasi ziwafikie wanawake vijijini; tukajaribu kueleza na namnaambazo zinaweza kuwafikia, lakini bado inaonekana kamahata kiwango chake bado ni kidogo kinachotolewa naSerikali. Kwa hiyo, tunaomba pia Serikali iangalie namna ganikwa sababu, vijijini hakuna mabenki. Mpaka utoke kule Kijijinikwenda benki kutafuta ni ngumu, basi tunaomba waangalienamna ambavyo Serikali itaongeza hela katika hii Benki yaWanawake ili wanawake wa vijijini hasa wanaotoka Mkoawa Katavi na Rukwa, Kigoma, Songea, Mtwara, waweze

[MHE. DKT. P. W. KIKWEMBE]

Page 105: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

105

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kupata huduma hizi. Sio tu wanawake wa mjini, fursa nyingizinakuwa kwa watu wa mjini. Kwa hiyo, hili naomba katikamipango hii mzingatie sana hilo, lakini la msingi kabisa lakuzingatia naomba uwekezaji mkubwa ufanywe na Serikalikatika sekta ya elimu. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Dkt.Kikwembe. Sasa namwita Mheshimiwa Mwijage, nadhanindiye atakayekuwa mchangiaji wetu wa mwisho kwamchana huu.

MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipatia nafasi ya kuchangiamapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2014/2015, labda nina mambo matatu ya kuzungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, ni lazima niliseme;wakati ilipoanzishwa operation Kimbunga, nilipokutana natajiri mwenye nchi, baadaye akatangaza operation, rafikiyangu mmoja Mtendaji wa Serikali, aliniambia nyie Wanasiasamsituingilie tufanye Kimbunga. Wakafanya Kimbunga huko,sikuwaingilia; juzi uzalendo umenishinda, nimekwenda kwaWaziri wa Ulinzi leo asubuhi nikaenda kwa Naibu Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kata ya Rutoro,Operation Kimbunga haikufanyika, ng’ombe wote walifichwapale na watu wa kutoka nchi fulani wakajificha pale, leowameamua kuvamia migomba ya wananchi, basi wananchiwanalia. Sasa rafiki yangu nimeamua kuingilia na bilakukuuliza wewe nimeshamwambia Waziri na Serikalinimeiambia. Kwa hiyo, Kimbunga ilipofika pale Rutoro ilirukajuu, haikufanya kazi. Sasa mkuu wa operation kaeleze kwawakubwa zako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, ambalo natakakuzungumzia ni kuhusu huu mpango. Niishukuru Kamati yaMheshimiwa Chenge, mmefanya tafakuri nzuri; maelezo yenukama kweli tutatenda haki tuyazingatie. Kamati ile yaMipango unaweza kuwa na jambo nao, lakini kazi iliyofanyikani nzuri. (Makofi)

[MHE. DKT. P. W. KIKWEMBE]

Page 106: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

106

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu, nizungumzekuhusu hawa Watendaji wa Serikali. Watendaji wa Serikaliwatatushangaa, na nadhani ndio maana leo wameamuawasije, sio Mawaziri tu hata Watendaji kule wanakokaahawapo, wameamua wasije. Watendaji wa Serikalimnafanya kazi, lakini kwa sababu na sisi kazi mnazofanyatunazijua, mnapaswa kufanya kazi zaidi ya mnavyofanyasasa; mna mgomo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye suala linginela nishati, niende kwenye Mpango, Mpango unasemautapeleka watu kujifunza gesi na nini. Hoja na suala siokujifunza gesi, tulivyokubaliana tangu tufike Bungeni 2010,tulisema Watanzania waajiriwe katika sekta ya gesi namafuta, waanze ku-understudy makampuni yanayoendeshashughuli, ili hawa Wazungu au wageni wanapokuwawanamaliza, wana-graduate, watu wetu waweze.Waheshimiwa Wabunge, ngoja niwachongee hawa watu waSerikali; najua ule mpango wa ku-train Watanzaniawamekataa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasikia tajiri mwenye nchi,Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, anasemaWatanzania waajiriwe, Mheshimiwa Muhongo anasemawaajiriwe, Waziri wa Utumishi anasema waajiriwe; ndani yaWizara ya Utumishi kuna watu wanakataa. Kama ningeulizwanje, ningesema wanalipwa, na nikiambiwa wanalipwa nanani, naweza nikamsema. Wanalipwa na mbaya wetu kwasababu si kila mtu anatutakia mema. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwa nini Serikali imekataakuchukua vijana wa Kitanzania kwenda kuwa-understudyWachina wanaochomea bomba? Mimi ni Pipeline Operator,kazi yangu niliyoanza kufanya ni Pipeline Operator niki-primematenki na kusukuma mafuta. Nikatoka hapo nikaendampaka nikafikia hapa nilipo, nimesoma shule nyingi kweli,lakini core job niliyojifunzia ni Pipeline Operator; kwa ninimnakataa kuwaruhusu watoto waanze kujifunza?

[MHE. C. J. MWIJAGE]

Page 107: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

107

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasikia Mchina ameanzakufanya kazi. Waziri wa Utumishi nina habari zako, umesemawaajiriwe, kuna watu wamekataa kwako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi zile pesa nilipokuwanaiongoza ile Kamati, tulipoibiwa Dola milioni 100, hamjui kesitulishindwa vipi. Katika Mkataba walikuwa wanasema niwajibu wenu kufanya auditing. Kumbe sisi tulipigwa changala macho kwa sababu, hatukufanya auditing, tukaamuawaajiriwe watu kwenda kufanya auditing; Utumishiwamekataa, Waziri umekubali nasikia, Mheshimiwa Muhongoamekubali, tajiri mwenye nchi amekataa, Utumishi kuna watuwamekataa. You don’t need restructuring, huhitaji kufanyarestructuring ya TPDC kusudi kuajiri Auditor; umwajiri Auditor,utakapotaka wa kumpeleka wakati huo utampeleka popote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wachina wanalaza bombakilometa tano kwa siku. By the time unapeleka watoto wetuWasukuma, Wanyamwezi wa Tanzania kwenda kujifunzaMchina atakuwa amenyanyua virago ameondoka. Watuwanasema mtaani kuna kampuni mnaiandaa kuipa hilobomba. Ndugu zangu niwaambie, mkiipa kaziwataandamana na sitakubali kuwa Mwenyekiti wa Kamatiwakati huo, eeh. Watanzania hawataridhika, you are notdoing fair to the country. Nimependa niliseme hilo ili rohoyangu iridhike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, makusudi mazima kunagenge la Watanzania limekataa kutekeleza maelekezo yaBunge, kuwaajiri wale vijana tuliosema wakawa-understudyWachina, nothing has been done, nimeamua kulisema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye viwanja vyandege, Mpango unazungumzia Viwanja vya Ndege.Nawapongeza, lakini Mpango ubadilike, kujenga mazingirawezeshi ya wawekezaji kuja kutengeneza Airline, aaa,tumeshindwa, tumesubiri muda mrefu; The Governmentshould take the lead law kuhakikisha tunayo National Airline,hatuwezi kuendelea kuwa nchi ambayo haina National

[MHE. C. J. MWIJAGE]

Page 108: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

108

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Airline. Kuna nchi zimefanya hivyo na sisi twende kule;mazingira wezeshi hamwezi kuyatengeneza, tunakaa kwenyevikao mno, vikao vinakuwa vingi mno. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema nimeunga mkonokazi ya Kamati ya Bwana Chenge, imefanya kazi nzuri.Niongezee kidogo kwenye suala la chakula.Ninachowaomba, pamoja na kujenga Silos, mtuelezekwamba, mtajenga maghala ya chakula angalau yakuhifadhi chakukula cha miaka kama minne, kujenga Silos sihoja ni silo za kutunza chakula cha miaka mingapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Silo moja Shinyangakwa ajili ya Kanda ya Ziwa, hamtutendei haki. Economicshazikubali kutoa chakula Peramiho, hata kama wangekuwawanatupenda namna gani, kutoa chakula Peramihokukipeleka Kagera; tunataka jitihada za Serikali zifanyikekusudi na sisi Kanda ya Ziwa tuzalishe big time. Tunayomabonde ya maji mengi, tunayo maeneo mazuri,muwawezeshe watu kulekule, pamoja na kuzalisha chakula,lakini mnatusaidia ku-retain nguvukazi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamezungumza mambomengi kwenye elimu. Mimi nina moja tu kwenye elimu,mnifanyie hilo nitaridhika. Nenda katafute pesa popote, kopamahali popote, walipe Walimu madai yao; mmeyahakiki,hamkuyahakiki, umekuwa wimbo wa kila siku, what is 57billion? Walipe waende wafanye kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama watu wanahisikwamba, watoto wanashindwa kwa sababu, Walimuhawajalipwa madeni, sasa muwalipe muwaachie ngomawao. Nyie malizeni kazi tuwahukumu wao wenyewe,mtufanyie hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika rasilimali watummeainisha maeneo ya kufundisha watu zaidi; mfundishewatu zaidi kwenye tiba, hiyo hamkuisema. Watu wengiwakifundishwa mambo ya tiba itatusaidia nini? Tunajengazahanati kila Kij i j i, sasa atafanya kazi nani mle? Sisi

[MHE. C. J. MWIJAGE]

Page 109: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

109

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

tunaendelea kujenga kule, mtengeneze Wataalam wengiwa ku-man zile zahanati na hospitali za Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninapomalizia,nimweke sawa rafiki yangu mmoja aliyesema mpango huusio shirikishi. Mpango huu ni shirikishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimetoka Jimboni siku30, nimetembea Kijiji kwa Kijiji, vijiji 62, nikizungumza nawananchi kuhusu Mpango na vipaumbele. Ni wajibu wa kilaDiwani, bahati mbaya kwa wale Wabunge ambao sioMadiwani, lakini Mbunge yeyote ambaye ni Diwani, unawajibu wa kwenda kukaa na watu wako kuwauliza je ikijaSerikali inauliza hapa, utachagua nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo langunimefanya hivyo siku 30, Vijiji 62 matawi ya Chama chaMapinduzi 75. Nilikuwa naanzia kwenye Chama najengahoja, naingia ndani ya umma nasukuma mambo. Kwa hiyo,ndugu zangu Wabunge, mpango huu ni shirikishi na ni jukumuletu sisi kama Madiwani kuwaongoza wananchi. Kwa sababu,kuna mtu mwingine unaweza kumuuliza unachagua nini,akamwambia mimi nachagua gari; unalo gari la kumpa nagari lenyewe anachagua Vogue? Kwa hiyo, ndugu zangutukubaliane ni jukumu letu sisi kuwaongoza wananchi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa ndugu zanguWatendaji, nimemwona rafiki yangu kwenye Wizara fulani,nimseme; watu wa Bandari mnatuangusha, Port Communityhaijafanya kazi vizuri. Nilimwona Waziri mmoja rafiki yanguanalalamika nikasikitika kweli, unajua katika vitu sitaki kusikianchi hii ni kuona Waziri analalamika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna ushirikiano mzuri waPort Community kati ya watu wa TRA, watu wa Madawa,watu wa Container sijui nini na nini, hamfanyi kazi pamoja,ongezeni kasi. Niwambie, Afrika Mashariki haitakufa kwasababu, mimi kwangu Gosba napakana na Kenya napakana

[MHE. C. J. MWIJAGE]

Page 110: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

110

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

na Uganda, sasa itakufa waondoke waende wapi? Kwa hiyo,tutaendelea kuwa nao, lakini ili tuwe nao ni ufanisi na siasani uchumi. Watu wa Kenya wako kwenye uchumi.

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Mwijage.

MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana na naunga mkono hoja.

MWENYEKITI: Sasa namwita Kaimu Waziri Mkuu,Mheshimiwa Mwandosya.

KAIMU WAZIRI MKUU - WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS,ASIYE NA WIZARA MAALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimeona nitumie nafasi ya kuwa karibu na hiki Kiti muhimusana ili niweze kutoa mchango katika haya yanayoendelea.Mchango wangu, najielekeza kwenye mawazo na michangoya Waheshimiwa Wabunge, iliyoelekezwa kuhusu kuwepo aukutokuwepo kwa Mawaziri wakati wa majadiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu na kwa niaba ya Serikali, naomba kuwahakikishiaWaheshimiwa Wabunge kwamba, tuwepo tusipokuwepo,tunathamini sana sana yale ambayo yanazungumzwa naWaheshimiwa Wabunge. Nasema hivi kwa uhakika kabisakwamba, macho na masikio ya Serikali wakati wa Mikutanoya Bunge yanakuwa Dodoma kwa njia mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tumeulizwambona Makatibu Wakuu hawapo? Napenda kuwathibitishiaWaheshimiwa Wabunge kwamba, hivi mnavyozungumza kilaOfisi ya Serikali katika ngazi za Katibu Mkuu au Naibu KatibuMkuu hata Wakurugenzi, kuna runinga na macho yao namasikio yao yameelekezwa Dodoma. Mnaweza msimwone,kwa mfano hapa Gavana wa Benki Kuu, nina uhakikaGavana wa Benki Kuu sasa hivi, Makamu wa Gavana, wotewanasikiliza yanayoendelea katika majadiliano muhimukama haya, ndivyo Serikali inavyofanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unaweza kuwaona nyuma

[MHE. C. J. MWIJAGE]

Page 111: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

111

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

yetu kule Maafisa wawili au watatu, lakini wanachukua kilakitu. Kile kinachowahusu wao, kinachowahusu vile vileMawaziri wengine, tutakipata leo hii hii na Mawaziri watajuani nini kimezungumzwa na watatakiwa, kwa taratibu zetu zaSerikali, kuandaa majibu ili kuweza kumsaidia MheshimiwaWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naombakuwathibitishia Waheshimiwa Wabunge kwamba, Serikalihufanya kazi kwa taarifa. Taarifa muhimu katika kipindi hikini zile zinazotoka Dodoma na yale ambayo wanazungumzaWaheshimiwa Wabunge. Kwa hiyo, tunaheshimu sanamichango, tunasikiliza, hata wale ambao hawapo, sisi tuliopotunasikiliza kwa niaba yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii haimaanishi kwamba,tusiwepo, lakini kwa kweli naamini, jana imezungumzwa, leoimezungumzwa vilevile na pale ambapo hakuna sababu yamuhimu ya kutokuwepo Waheshimiwa Mawaziriwatakuwepo, lakini pale ambapo kuna sababu za msingi,naamini kabisa kwamba, wanakuwa na sababu ambazozinawafanya wasiwepo, lakini sisi tuliokuwepo tunachukuakila kitu kwa niaba yao. Ningependa kuwahakikishiaWaheshimiwa Wabunge na wananchi kwamba, hilo ndilolinalofanyika. Serikali, inafanya kazi kwa...

MWENYEKITI: Nakushukuru sana.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, ASIYE NA WIZARAMAALUM – KAIMU WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Sasa Waheshimiwa Wabunge, jionitunaendelea na michango. Tutaanza na Mheshimiwa PeterSerukamba, Mheshimiwa Hamad Rashid, MheshimiwaCaptain Komba, Mheshimiwa Yussuf Salim, MheshimiwaKidawa Saleh, Mheshimiwa Freeman Mbowe, MheshimiwaMaige, Mheshimiwa Zambi na Mheshimiwa Lwanji.

Bunge linarejea.

[KAIMU WAZIRI MKUU - WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS,ASIYE NA WIZARA MAALUM]

Page 112: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

112

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

(Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae.Nasitisha Bunge, mpaka saa 11.00 jioni.(Saa 7.00 Mchana, Bunge lilisitishwa mpaka saa 11.00 Jioni)

(Saa 11.00 Jioni Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea.Nilitangaza majina ya watu watakaochangia jioni hii, sasanitaanza na Mheshimiwa Serukamba.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nishukuru kwa kunipa nafasi jioni hii kuwa wa kwanzakuchangia Mpango wetu wa Maendeleo wa 2014/2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati tunapitisha MpangoMkuu ule wa Miaka Mitano, tulisema tutakuwa tunatumia 8.5trilioni kila mwaka kwa ajili ya shughuli za miradi mikubwa yamaendeleo. Ningependa labda watu wa Serikali watuambie,tunakwenda mwaka wa tatu sasa, naamini mwaka janahatukutumia 8.5; mwaka wa kwanza walisema ndiyotunaanza na ukiangalia hata huu mwaka huioni 8.5 trilionikwenye mipango ya maendeleo, sasa tunajiulizatunafanyaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na kilimo; kwa miakahamsini iliyopita, tumeendesha kilimo chetu kama wanasiasa.Kila kitu tulikuwa tunafanya siasa kwenye kilimo, nadhaniumefika wakati sasa kama nchi, kilimo tukifanye kuwa nibiashara. This is the moment lazima kama Taifa, miaka hamsiniijayo sasa, tufanye kilimo ni biashara ili kichangie kwenyeuchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini tufanye hivyo?Tuamue kwanza tuzalishe chakula cha kutosha hapa nchini,lakini tukishafanya ni kilimo cha biashara kila mtu atakwendakulima kwa sababu anajua mwisho wa siku ukishakifanya

Page 113: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

113

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kibiashara maana yake hata bei utakazopata za mazao yakoni bei ambazo ziko kwenye soko la biashara. Baada ya hapotuanze kulima mazao ambayo ni demand driven duniani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia ili tuweze kufanyahaya yote, lazima tuweke sasa legal framework yenye clarity,tuwe na commodity stock marketing in Tanzania.Tukishakuwa na commodity stock market, kila mtu anajuaatakuwa analima kulingana na bei anazoweza kuzipatahapa ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili tunalofanya sisi siyo wakwanza, wenzetu wamefanya, Vietnam wamefanya,Thailand wamefanya, South Afrika wamefanya na Kenyawamefanya. Wamegeuza kilimo ni biashara ndiyo maanaleo mpunga wa Thailand na mpunga wa Vietnam unaliwadunia nzima na sisi tukiamua tiumnaweza kwa sababutumepewa ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini umefika wakatitumeongea sana, Wazungu wanasema; we have beentalking miles, we are doing centimeters. Tumekuwatunaongelea ma-mile na ma-mile lakini kwenye kutendatunakwenda sentimita kwa sentimita. Nadhani wakatiumefika tuache maneno, maneno tumesema sanayanatosha, kwa miaka hamsini ijayo tugeuze kilimo nibiashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, sasa hivi tunaambiwatumepata muarobaini wa matatizo yetu, ni mtu anaiwa BRN(Big Result Now), sasa hivi kila mtu wa Serikali anakwambiasasa tuna BRN, matatizo ya nchi hii yataondoka, mimi nasemahapana. Nataka tuambiwe clearly, source ya revenue ya hiiBRN iko wapi? Iletwe hapa tuione source of envelopeambayo tunasema BRN na miradi yake yote fedha ni hizihapa, zitapatikanaje na Wabunge waweze kuziona nakuzipitisha, otherwise itakuwa ni talk show.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikubaliana kwenye BRNkwamba, baada ya BRN kumaliza tu, tuondoe vizingiti

[MHE. P. J. SERUKAMBA]

Page 114: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

114

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

barabarani kwenda Rwanda, kwenda Tunduma, vizingitihavijaondoka na havihitaji bajeti. Sasa tunasema BRN hiiinakuja kufanya nini kama hatuwezi kuamua sasa, BRNhaiwezi kutuelewa tunachotaka kusema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha tatu, ni reli ya kati,jamani reli ya kati tumefanya siasa, inatosha. Tumeongeakuhusu reli ya kati, siasa imefanyaje, imetosha. Tukiamua leotunaanza kujenga standard gauge tunaweza na tunawezaje;tufanye kwa miaka mitano, unasema naanzia Dar es Salaammpaka Morogoro nitang’oa reli, wakati unafanya Dar esSalaam mpaka Morogoro hii reli ya zamani inafanya mpakaMorogoro; wakati huo unafanya study kutoka Morogorompaka Dodoma, unamaliza huku unakuja huku. UnatokaDodoma unakwenda Tabora, toka Tabora unakwendaKigoma, unatoka Tabora unakwenda Mwanza ndani yamiaka mitano tutakuwa na standard gauge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kama hatuwezikuamua na kutenda, kila siku tunasema, hapa watakujawatatuambia kuna Wachina, kuna Wajapan, kunaWamarekani, tunafanya study, tunafanya study kwa miakamingapi? Wenzetu wanafanya, leo Wakenya wanajengastandard gauge, tunapiga kelele hapa Wakenya, Wakenya,wenzetu wanaamua wanakwenda mbele. Wakati umefikatupunguze kusema sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu msongamano waDar es Salaam. Msongamano wa Dar es Salaam tusihangaikekuvunja nyumba, wako watu wanaweza wakafanya,unaweza ukaamua kutokea hapo Serena Hotel ukawekahighway, ukapanda juu, ukasema barabara ya juu huku niya watu wenye haraka watalipia, barabara ya chini ni yaWatanzania ambao wanakwenda bure, people will do it.Unaweza ukatoka pale ukajenga juu ukaenda mpakaUbungo, ukajenga juu ukaenda mpaka Airport, ukajenga juuukaenda mpaka Mwenge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, wale wenyeharaka watapanda juu watalipa, watakwenda; wale

[MHE. P. J. SERUKAMBA]

Page 115: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

115

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wanaosema hapana, lazima Serikali itujengee barabara,watapita kwenye barabara yetu ya chini. Hujambomoleamtu, lakini bado utakuwa umemaliza tatizo la Dar es Salaam.Kwa nini hatufanyi, mimi sijui Mungu ndiye anajua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la madeni;ukisoma kwenye vitabu deni letu la Taifa limepanda kutokadola bilioni 12 mpaka dola bilioni 16 maana yake kwa mwakahuu mmoja tu, kuna dola bilioni nne za deni la Taifazimeongezeka. Nataka Serikali ituambie tumefanya miradigani kwa dola bilioni nne kwa sababu dola bilioni nne byany standard hizo ni trilioni karibu sita, basi tungeziona kwenyemiradi ya maendeleo, otherwise tunakopa kwenda kula, kituambacho sidhani kama ni sahihi. Kwa hiyo, naomba wakatitunaambiwa, unless tunakopa tunakwenda kulipia mafutaya umeme ambayo nayo ni hatari kwa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba Waziriatakapokuwa anajieleza atuambie four billion dollarszilizoongezeka kwa mwaka huu za deni la Taifa zimefanyamiradi gani, otherwise Wabunge tutakuwa tunakaa hapa,tunapiga maneno, lakini hatuoni kinachokwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, madeni ya ndani.Kama tunataka kuendelea lazima tulipe madeni ya ndani.Madeni ya ndani ndiyo wafanyabiashara hawa walioajiriwatu wetu ambao hawajaajiriwa na tukiwalipa hawainashamihisha kwenye uchumi wetu. Kwa hiyo, naomba sana,nenda kwenye Halmashauri watu wanadai, nenda kwenyeMawizara watu wanadai, nenda Jeshini watu wanadai,everywhere watu wanadai. Sasa tunafanyaje kulipa madeniya ndani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, lazima sasa tuondokekwenye cash budget, tutoke kwenye cash budget twendesasa kwenye accrual basis na twende kwenye InternationalStandard katika kuripoti kwenye Mawizara yetu ili hao MaafisaMasuuli wasiwe wanafanya vitu, halafu kwenye bajetihawajaziweka zile fedha za madeni, ile fedha ya bajeti ya

[MHE. P. J. SERUKAMBA]

Page 116: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

116

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mwaka unaofuata wanalipia madeni ya mwaka uliopitaambao hawayakuya-provide. Nadhani umefika wakatituanze kutenda badala ya kusema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, naomba kuungamkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Nashukuru sana. Sasa namwitaMheshimiwa Hamad Rashid, atafuatiwa na MheshimiwaYussuf Salim na Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla ajiandae.

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kupata nafasi jioni hii ya kutoa mawazo yangukatika mada iliyopo mbele yetu katika Mpango huu wa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba kwanza sotetuliomo humu ndani kila mmoja ajiulize kwa nini tupo hapa,kwa nini tumechaguliwa na wananchi kuja kuwawakilishahapa, kwa nini tumeteuliwa na vyama kuja hapa na kwanini tumeteuliwa kuwa Mawaziri au Manaibu Mawaziri.Tukishajiuliza hili neno kwa nini tupo hapa, basi tutapatamajibu ya haya matatizo ambayo wenzangu wengiwamekuwa wakiyapigia kelele hapa kwamba utendaji auutawala bora unakuwa ni tatizo katika maendeleo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili nadhani ubinafsindiyo umetawala zaidi na ndiyo unaochangia kuonekanakwamba nchi yetu haiendi mbele. Kila siku Watanzaniatunaimba wimbo kwamba tuna rasilimali nyingi kuliko wenzetuwa Afrika; tuna vivutio vingi vya utalii, tuna bahari, tuna mito,tuna mabonde, tuna maziwa, lakini bado nchi hii ni maskinikupindukia, kwa nini? Ni kwa sababu ya ubinafsi nahatujakuwa committed katika ile nafasi ambayo mtuameiomba au amepewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baya zaidi ni kwamba,tunakula kiapo hapa na badala ya kiapo unamwombaMungu nisaidie. Sasa Mungu atusaidie nini kama ametupa

[MHE. P. J. SERUKAMBA]

Page 117: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

117

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

neema zote hizi alizotupa, akatupa na elimu, akatupa nauzima, lakini bado leo tunakuwa maskini na tunasema tu, tunahivi, tuna hivi, lakini bado ni maskini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu sasa imekuwakama ni pambo la jeneza, nje utaiona ni nzuri, lakini ndanikuna uozo kama huu; kila Mbunge anayesimama hapa,anapiga kelele tuna rasilimali lakini ni maskini sana. Kwa hiyo,nadhani kila mmoja ajiulize na ni wakati sasa wa kubadilika,ni wakati sasa wa kuamua kuwa committed, kila mtu kwanafasi yake aliyopewa kuona kwamba, nchi yetu inakwendambele na hizi hadithi za kwamba uchumi, uchumi, tukomaskini, ziishie kwa sababu nani atakuja kutufanyia nawafanyaji ni sisi, hilo la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa katika hili naiombaSerikali basi ichague miradi michache katika utitiri huu wamiradi ambao umeelezwa hapa. Ichague miradi michacheambayo tunaweza kuitekeleza, tuitekeleze imalizike, hayamambo ya kuwa na miradi mingi halafu hatuwezi kuitekeleza,hili ni tatizo ambalo baadaye litatugharimu; mtaka nyinginasaba hupata mwingi msiba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutayataka mambo hayayatatushinda, halafu 2015 yatatugharimu lakini hatuishii 2015kwamba labda utakosa Ubunge tu na nini, lakini umekulakiapo, umechukua ahadi kwamba utayatekeleza haya, kwaMungu tutajibu nini na tumeshindwa kuyatekeleza natumeandika wenyewe kwamba tutatekeleza haya. Kwa hiyo,lazima tujielewe, ni lazima sasa tujitambue, kwamba tumeji-commit na lazima tuwe committed katika yale ambayotumeji-commit wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya hatuwezi kuyafikia kwasababu ni mambo mengi yanahitaji fedha nyingi na uwezowetu wa kulipa kodi au wa kukusanya kodi ni mdogo. Sasanataka watu wa Wizara ya Fedha wanisikilize vizuri hapa,nataka nitoe rai katika suala la kodi, vipi tunawezatukakusanya kodi nyingi na tukaweza kufanikisha miradi mingituwezavyo. Tunajitahidi sasa hivi kukusanya kodi kwa kiwango

[MHE. Y. S. HUSSEIN]

Page 118: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

118

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kizuri, lakini pia tukubali kwamba, ni fedha nyingi vile viletunaipoteza katika kukusanya kodi, kivipi? Bado kuna mianyaambayo walipa kodi au walipisha kodi, fedha nyinginezinaingia katika njia nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mfano, Tanzania leomtu kama anaingiza gari la mwaka 2001, akiendaMheshimiwa Barwany gari hilo hilo la 2001, aina hiyo hiyo, cchizo hizo ataambiwa lipa tax milioni tatu. Akienda mwinginegari hilo hilo la mwaka huo huo lipa milioni mbili na nusu, sasakwa nini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naiomba Wizaraya Fedha kwa sababu tunajua bidhaa zote ambazo zinaingianchini na kwa sababu tunajua bidhaa zote ambazo tunatoakupeleka kuuza nje, kwa nini hatuweki bei moja, ikawamfanyabiashara wetu akiwa kule nje, anajua nanunuakhanga hii kwa bei hii, nitaisafirisha kwa bei hii, nitalipa ushuruhuu na nitauza kwa bei hii, nitapata faida hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwanzaitawasaidia wafanyabiashara wetu kuweza kujua kwambabiashara hii ninayoifanya nitapata faida ama nitapatahasara. Hilo la kwanza, lakini tujifunze mazuri kwa wenzetu.Katika nchi za Scandinavian, Sweden wameweka utaratibuhuu, kila kitu kinaeleweka, kwa hiyo, wako very transparentkatika biashara na wao kwa sababu wameweka hilo katikabiashara, kila kitu kinajulikana hamna ukifika pale unafanyanegotiation na mtu wa TRA, hakuna! Unajua nimechukua kiasihiki cha mzigo, tax yangu ninayopaswa kulipa ni hii, hakunaurasimu, hakuna kupoteza muda, unalipa, unachukua mzigowako, unaondoka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa wamefanya hilowamefanikiwa na wafanyabiashara wa Sweden, baada yakuona Serikali yao kweli imekuwa committed, imekuwa verytransparent, wameamua wanaisaidia Serikali yao 20% yafaida anayopata mtu. Kwa hiyo, kiwango kile kinatoshelezabajeti ya Sweden na surplus na ndiyo maana utakuta sasayale makusanyo yao ya kodi na njia nyingine ndiyo wanapata

[MHE. Y. S. HUSSEIN]

Page 119: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

119

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

fedha kutusaidia sisi. Tanzania tunashindwa nini kuiga hili,hadi leo tunaacha mianya ya rushwa, mianya ambayo inamifereji mingi ya kuingia fedha za kodi, tunashindwa ninikuliweka hili. Nadhani mambo mazuri tuige ili na sisi twendembele. Hilo moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije katika suala la uvuvi;katika maelezo yote yaliyotajwa katika vitabu hivi, suala lauvuvi halijazungumzwa vya kutosha pamoja na kwamba tunaeneo kubwa la bahari kuanzia Mtwara mpaka Dar es Salam,Zanzibar, Pemba, Tanga, wapi haijazungumzwa, tuna MaziwaTanganyika, Lake Victoria, tuna mito na mabwawa lakinisuala la uvuvi halijazungumzwa, halijapewa kipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia hatujaweza kuzitumiabandari zetu kama Dar es Salaam, Tanga, Mtwara naZanzibar kwa ajili ya uchumi wetu, wenzetu Dubai bandaritu, Malaysia bandari tu, lakini wako mbele, sisi MwenyeziMungu ametupa rasilimali hizo tunazitumia vipi? Ubinafsiumetawala ndani ya nafsi zetu, kila anayepewa nafasi basianaona yeye tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kila Mtanzaniaamelewa na gesi na mafuta ya Mtwara. Kwa hiyo, sotetumegeukia huko, tunaacha mambo yetu mengine yotehaya kuona kwamba haba na haba hujaza kibaba, hayotumeyaacha, tunakuja kuiangalia gesi tu, jamani tunaungakimo kwa kinu hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani tungeziangaliabandari zetu tukazitumia bahari tulizonazo na mabwawa namito tukaimarisha uvuvi, nchi kama Malaysia uvuvi unaingizaasilimia kubwa sana katika pato lao la Taifa, sisi hatuna kitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho natakakuishauri Wizara inayohusika na mambo ya Uvuvi sualalinaloendelea hili la uchimbaji wa gesi na mafuta kunamazingira yanaharibika, lakini pia kuna vyanzo ambavyotunaweza tukatengeneza…

[MHE. Y. S. HUSSEIN]

Page 120: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

120

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Yussuf, nakushukuru sana.

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana.

MWENYEKITI: Sasa namwita Dokta Kigwangalla,wajiandae Mheshimiwa Maige, Mheshimiwa Kidawa naMheshimiwa Zambi.

MHE. DKT. HAMISI A. KIGWANGALLA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa hii ili nami nitoemchango wangu kwenye hoja iliyoko mbele yetu. Awali yayote, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi kwa kutujalia afyanjema siku hii ya leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nimpongeze Waziriangalau kwa kuweka vipaumbele vichache kwenye Mpangohuu wa Big Result Now. Tulizoea kuona taarifa ama mipangomikakati ya Serikali ikiwa na vipaumbele vingi sana.Nakumbuka mwaka wa kwanza nilipokuwa Mbunge, kwamara ya kwanza kulikuwa na vipaumbele 13, mwaka huuangalau viko sita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe rai kwamba hata sitanafikiri ni vingi sana. Kweli tunashindwa tuache kipi, tushikekipi, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba, ukiwa navipaumbe vingi sana unashindwa ku-focus na katika mambohaya ya maendeleo the power of focus is very important,unahitaji ku-concentrate efforts zako, japokuwa ni chache,u-concentrate, uzi-focus kwenye eneo moja maalum ili uwezekuona matokeo katika muda fulani, lakini pia ili uweze kuwana excellence.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hil i jambo la kuwaexcellence lina tafsiri katika sura ya kuwa na utamaduni waexcellence. Kwa mfano, nafahamu pale Chuo Kikuu cha Dares Salaam hii culture ya excellence inapatikana sana kwenyeuwezo wa ku-generate graduates ambao wana

Page 121: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

121

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

independent thinking, ambao wako opened minded, wanauwezo mkubwa wa kufikiria na kuchambua mambo, ambaowanaweza kuwa tayari kwa open debate.

Mheshimiwa Mwenyekiti, chuo hicho toka kinaanzampaka leo hii huo ni utamaduni wa chuo kile, ni utamaduniwa excellence kwenye kuzalisha graduates ambao wanauwezo mkubwa wa kupambanua mambo, wana uwezomkubwa wa kuhoji na ndiyo maana wale viongozi wa zamaniwalikuwa wako huru sana walikuwa na uwezo wa kufikiri, waku-debate bila kukorofishana, bila kukasirikiana, kumbe niutamaduni ambao waliupata kwenye Chuo chao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia napata swali kwamba,hivi taasisi kwa mfano kama Bunge la Jamhuri ya Muunganowa Tanzania ama kama Baraza la Mawaziri lina excellencekwenye nini hasa. Hili ni jambo ambalo pia tunatakiwatulitazame, maana yake tunaweza tukawa tunaongeleamaendeleo tu, lakini kumbe tunasahau ingredients ndogondogo ambazo zingeweza kutupelekea kupata maendeleo,mojawapo ni kama hiyo tu ya kuwa na culture ya excellence,kuwa na mindset ambayo inawafanya watu wanapendakuendelea, wanapenda kuwa progressive. Hiyo tu nimojawapo ambayo ingeweza kutusaidia kupiga hatua, kulikokila siku tunaongea mikakati, lakini haitekelezeki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa namsikiliza kwamakini sana ndugu yangu Mheshimiwa Peter Serukamba,anaelezea mikakati kwa uchungu kweli kwamba, tunasemazaidi kuliko kutenda, lakini ukweli utabaki pale pale kamahatutaki ku-focus, kama hatutaki ku-concentrate efforts zetukwenye mambo machache, tuka-develop excellence,tukayafanya mpaka tukayakamilisha, hatuwezi kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutakuwa kila sikutunapanga mambo mengi, lakini mwisho wa siku hatuonimatokeo ya mipango yetu. Huo sasa mekuwa kama niwimbo kwa Watanzania, kiasi kwamba hata kama tunajaribukuweka mipango mizuri hapa, Watanzania wanakuwawameshatuzoea kwamba aah! The same business, kama

[MHE. DKT. H. A. KIGWANGALLA]

Page 122: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

122

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kawaida wanavyofanya Bungeni pale, wanaongea mikakatimizuri, lakini hatuoni matokeo. Kwa hiyo, nilipenda nisemeekwenye hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, leo hii sisi tunaexcellence kama Taifa kwenye mipango, kwenye kuandikadocuments, kwenye kuleta mikakati, kwenye kuja na slogansnzuri nzuri, lakini hatuna excellence hata kidogo kwenyekuchukua hatua na kwenye kutekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu Kenya wako shapukwenye ku-grasp opportunities kuzitafsiri kwenda kwenyematokeo mazuri kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa watuwao, sisi huko hatuko kabisa. Ndiyo maana leo hii tuna kilio,wenzetu wanakimbilia wanaona opportunity ya kuchukuasoko la South Sudan na Ethiopia, sisi bado tunahangaika namambo yale yale ya kila siku, wakati sisi tungeweza kuwagate ya kuingilia Afrika Mashariki na Afrika ya Kati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba tujifunzeku-focus, tu-develop culture ya excellence ili tuwezekujulikana kwamba Watanzania, kwa mfano, Bunge hili nimakini kwenye kitu gani, ni makini kwenye nini? Kamatungekuwa makini kwenye usimamizi, basi tungeonekanatunawawajibisha watu hapa. Kwa mfano, kama excellenceyetu ni oversight, mtu akikosea anakuwa responsible, lakinihilo pia hatuliwezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana leo hii, mambohaya tunayoyaongelea hapa, kwa mfano, hoja ya kukuzaajira kwa vijana, mambo ya kilimo ambayo yapo kwenyekipaumbele namba moja, tulipitisha hoja, tukasema kila mkoautaandaa ardhi, tukasema Serikali itatenga fedha, itaanzishaMfuko Maalum wa Kukuza Ajira kwa Vijana, pesa zitawekwamle, graduates wetu watakwenda kulima, lakini hakuna pesailiyopelekwa mpaka leo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Bunge lingetakiwalije liwa-task Serikali hapa kwamba, kwa nini hawajatekelezaAzimio, lakini tupo kimya, kwa hiyo hatuna excellence kwenye

[MHE. DKT. H. A. KIGWANGALLA]

Page 123: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

123

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kuwahoji watu responsible na kuwahoji watu accountable,tunanyamaza, mambo yanakwenda kama kawaida na hilondiyo tatizo kubwa ambalo tunalo kama Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye hoja yanguya pili na ya mwisho kwamba, tunapozungumzia Tanzaniaya kesho, wengi tuna-focus kwenye mambo ambayoyanapatikana leo, kwa mfano, tunazungumzia sanakuwekeza kwenye nishati na madini, tunazungumzia zaidimambo ya gesi sasa hivi, utafiti kwenye mafuta na tayariWizara ya Nishati na Madini inagawa vitalu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba iingie kwenyerekodi leo hii kwamba, siungi mkono jitihada zotezinazofanywa na Serikali za kwenda kugawa vitalu vyetuwakati hatuna Sera ya Gesi inayoeleweka, hatuna Sera yaLocal Content Initiatives, hatuna Sera ya Uwekezajiinayoeleweka, hatuna Sera ya Kutajirisha Makampuni yetukama TPDC na STAMICO kwenye madini, tunakwendatunagawa tu vitalu, watu wanachukua, sisi hatujajipangahata kama tuna sera gani na mle ndani tunafaidika vipi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tungekuwakama tuna excellence kwenye kupanga mipango yetu,tungeweza kusema kwamba kila kampuni itakayokuja freecarried interest kwenye kampuni hiyo inayowekeza palelazima TPDC ichukue 40 percent na ingekuwa kwenye serana ingekuwa kwenye sheria na kila Mtanzania angekuwaanajua hivyo lakini leo haiko hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba iingiekwenye rekodi kwamba, siungi mkono jitihada hizo nanaomba kama kweli Serikali hii inasikia isikie kilio changu nakilio cha Watanzania walio wengi zaidi, tusimamishe utaratibuwa kugawa vitalu vya gesi mpaka pale tutakapokuwa tayarikuliwezesha Shirika letu wenyewe la Kitanzania kamawalivyofanya Norway kwenye ile kampuni yao ya Start Oil.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Start Oil leo hii inakuja

[MHE. DKT. H. A. KIGWANGALLA]

Page 124: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

124

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kuwekeza Tanzania. Lakini miaka 20 au 30 iliyopita Start Oililikuwa maskini lakini wakawekeza wao wenyewe mtaji wao,wakaweka mikakati mizuri, wakajijengea uwezo, leo hii StartOil ni matajiri na nchi yao imetajirika kutokana na gesi. Lakinisisi tunakwenda kuwekeza hatujui TPDC ama kampuni yoyoteile ya Kitanzania, itakuwa inapata hisa kiasi gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbali na hivyo LocalContent Policy hatuna, kwa mfano, wale watu Mtwarawatafaidika vipi na uwepo wa uwekezaji huu mkubwa wagesi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungekuwa tuna Seratungeijadili Sera kama Watanzania, tukakubaliana kwamba,kwenye kila uwekezaji unaofanyika, may be asilimia 60 yakila kitakachouzwa kama raw materials and supplies kwenyehii migodi ya gesi, kitoke maeneo ya pembezoni ya migodihiyo, labda Mtwara na Lindi. Tungekuwa tuna sera ya namnahiyo ambayo inawa-task wale, tayari Serikali yetuingekwenda kuwekeza kwa wananchi ili wazalishe bidhaaambazo zinakidhi viwango vya ku-supply kwenye hayamakampuni makubwa ya Kimataifa, lakini sisi hatujajipangana hatuna sera yoyote, lakini tunaendelea kugawa vitalu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nirudie kusema naiingie kwenye kumbukumbu kwamba, Hamis Kigwangalla,mtoto wa Nzega anapinga uwekezaji wa kuendelea kugawavitalu kwenye gesi na ieleweke hivyo na wajukuu zanguwatakuja kulikuta hilo hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli mambo mengineyanasikitisha, kwa mfano, leo tunapata kauli ya Serikalikwamba, Watanzania hawawezi kuwekeza kwenye gesi,wanaweza biashara ndogo ndogo za kuuza juice na maji.Hizi ni kauli za aibu, akizitoa statesman, mtu ambayeamepewa majukumu ya kuwa Minister inakuwa ni aibukubwa zaidi, kwamba sisi hatuwezi kweli kuwekeza kwenyegesi, kwa nini tunashindwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wale Wazungu

[MHE. DKT. H. A. KIGWANGALLA]

Page 125: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

125

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wanachokifanya ni nini? Wanakuja hapa wanafanya utafiti,wakishapata wanakwenda kutafuta mitaji kwenye masokoya hisa huko duniani. Wakipata ile mitaji wanakuja kuwekeza,wanazalisha, wanatajirika, kwani Watanzania wetu hawanaelimu ya kuweza kufanya hivyo, naaamini wanaweza, lakinikatika hali ya kusikitisha hatuwaungi mkono.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba haya mambotuyaweke sawa, tutengeneze sera vizuri, tuandae wasomiwetu watakaokuja kutusaidia ku-exploit hizi resources kablahatujaendelea kuzigawa, maana yake tutakuja tutengenezesasa hiyo Sera ya Gesi wakati gesi yenyewe ilishakwisha. Kwahiyo, sheria inakuwa iko lakini haina maslahi yoyote walahaina faida yoyote kwa Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii nanashukuru kwa kunipa fursa hii. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana. NamwitaMheshimiwa Maige, wajiandae Mheshimiwa Kidawa naMheshimiwa Zambi.

MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Mpangohuu, Mpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2014/2015.Kwanza niseme tu kwamba, sina uhakika sana kama uandaajiwa mpango huu unajaribu kufanya slice ya mwaka mmojaya ilani yetu ya CCM ya miaka mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina wasiwasi kama focusni hiyo kwa sababu ukiangalia sasa miaka mitatu imekwisha,imebaki miaka miwili kufikia hatua ya mwisho ya kufanyiwatathmini ya kazi tulizofanya. Nitoe mfano tu wa maeneoambayo naona kama vile utekelezaji wake na taarifailiyotolewa, hauendi kwenye focus ambayo tunaitarajiakwenye ilani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, kwenye sualala maji, ukiangalia taarifa kwenye ukurasa ule wa 25, kifungucha (E), kinaeleza upanuzi wa Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria

[MHE. DKT. H. A. KIGWANGALLA]

Page 126: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

126

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

hadi Miji ya Igunga, Nzega na kadhalika. Niseme kwanza sinauhakika kwamba aliyeandika kifungu hicho sidhani kamaanatoka Mkoa wa Shinyanga! Kwa sababu ukiangaliagenesis ya wazo lenyewe lilianza mwaka 2008, MheshimiwaRais alipokuja kuzindua mradi ule, wananchi wa Kahamawakamwomba na Mheshimiwa Profesa Mwandosya bahatinzuri yuko hapa, wakati ule akiwa Waziri wa Maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awamu ya kwanza ya mradiule ulikusudiwa ufike Isaka, kwa maana ya kupata majiKagongwa na Isaka. Baada ya hapo mradi umeendeleakupanuliwa bila kutekeleza chochote. Sasa hivitunazungumzia kupeleka maji Nzega, Igunga hadi Tabora nahatuna hata hatua moja iliyofanyika. Wako waliozungumziakwamba tunazungumza miles na tunatekeleza inches na hilindiyo linalojitokeza kwenye suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, itafika mwaka 2015,tunazungumzia kwamba mradi tupeleke hadi Shelui, kwasababu tunachokifanya ni kuendelea kuongeza maeneo bilakutekeleza angalau kidogo. Kwa hiyo, naomba sana katikautekelezaji tuwe focused angalau mwaka huu au mwakauliopita tungekuwa tumefikisha maji Isaka, ili tunapokujakuzungumzia mwaka huu kwamba, sasa leo hii maji yamefikaIsaka mwakani tunayapeleka Tinde, ingeeleweka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka kuiombasana Serikali katika utekelezaji wa mpango, ikumbukwe sanakwamba tuna suala la Ilani na muda unakwenda na tathminiitakuja kufanyika kwa kuangalia utekelezaji ambao tutakuwatumefanya kwenye yale tuliyoyaahidi. Mfano huo mmojakwenye maji niutumie tu ku-emphasize kwamba, tatizo la majiIsaka na Kagongwa ni kubwa. Tathmini na uamuziutakaokuja kufanyika, wananchi wataangalia ni kwa kiasigani tumetatua eneo hilo na si kwa kiasi gani tumetajamaeneo mengi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili, ambalo natakakulizungumzia ni suala la madini, kwenye Ilani tumekusudiakupunguza matatizo ya wananchi na kunufaisha wananchi

[MHE. E. M. MAIGE]

Page 127: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

127

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wanaozunguka maeneo ya migodi. Mwaka 2010tulitengeneza Sheria ya Madini ambayo ililenga kupunguzamigogoro baini ya wananchi wanaoishi jirani na migodipamoja na wawekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati mbaya sanavifungu au utekelezaji wa eneo hili nalo hauridhishi.Nimeangalia taarifa kwa kweli nikashangaa, nikajiuliza hivimwaka mzima kilichofanyika, ukiangalia ule ukurasa wa 39kwenye suala madini, taarifa ya utekelezaji hasa kwenyesuala hilo maeneo yanayozunguka mgodi, wanasema kaziiliyofanyika ni kukamilisha uchambuzi na udhihirishaji wamipango wa ufungaji wa migodi ya Tulawaka, Bulyankulu,North Mara, Buzwagi na kadhalika. Nikasema hivi ahadituliyotoa ilikuwa ni kufanya tathmini ya ufungaji migodi aukunufaisha wananchi wanaozunguka migodi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Sheria ya Madini yamwaka 2010, kifungu cha 52(f) kinazungumzia migodi kuajirina ku-train Watanzania. Kwenye eneo hili tulitegemea mpakasasa hivi angalau kungekuwa na hatua kubwa imefanyikaangalau Chuo kimoja cha VETA kimejengwa Kahama, Geitaau eneo fulani ili kuwajengea uwezo wananchi wa maeneohayo waweze kuajiriwa migodini, hili halijafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilichofanyika kwa mwakamzima kwa mujibu wa taarifa hii niliyonukuu, ni kwendakuangalia na kukaa na wale jamaa wakatufanyiapresentation wakiangalia namna gani wanajiandaa kufungamigodi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa approach hii sidhanikama wananchi wale watatuelewa na sidhani kamawataendelea kutupa ridhaa ya kuendelea kuwatumikia.Nikutaadharishe sana Mheshimiwa Waziri kwamba, kwenyeeneo hili jambo hilo ni la muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni suala lawachimbaji wadogo wadogo. Kifungu cha 16 cha Sheria yaMadini, kinampa nafasi Waziri kufanya uamuzi ili eneo fulani

[MHE. E. M. MAIGE]

Page 128: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

128

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

liwe designated kwa ajili ya wachimbaji wadogo wadogo.Kasi ya utekelezaji wa eneo hili ni ndogo sana na matatizobado ni makubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nilitegemeakwenye taarifa tungeambiwa kitu gani kimefanyika nakwenye Mpango tungeambiwa sasa tumetekeleza angalauasilimia 30 ya lengo hili. Tuna wachimbaji wadogo wadogozaidi ya milioni nne kwenye nchi, angalau sasa wachimbajiwadogo milioni 2.5 wamepata maeneo, angalauingeeleweka. Kwa hivyo, focus iwe ni kutekeleza ahadi zetuna si vinginevyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la mwishokwa mujibu wa vipaumbele vyangu; suala la migogoro yawafugaji na jamii zingine za watumiaji wa ardhi. NaaminiSerikali yetu ipo kwa ajili ya kutatua matizo ya wananchi, tatizoya migogoro ya wafugaji na wakulima, migogoro ya wafugajipamoja na wahifadhi kwa upande mwingine imekuwa yamuda mrefu. Tatizo kubwa lililoko ni ukosefu wa ardhi, lakinimbaya zaidi kwa sasa hivi ni hujuma ambazo zinafanyika kwamakusudi kabisa kinyume cha sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka mwaka 2011tulianza mpango kwenye Wizara ya Maliasili na Utalii yakuyaangalia upya maeneo ya hifadhi na tuliunda Tume kwaajili ya kupunguza migogoro baina ya wananchi nawahifadhi. Tukaanza kukagua maeneo ili tuangalie maeneoambayo ama yamebaki hifadhi kwenye makaratasi ilimaamuzi yafanyike ili ya ku-degazette ili yaweze kutumikakwa shughuli nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka katika kazi hiyoyako maeneo ambayo naamini yalikwisha kuwasilishwaSerikalini na ukweli upo wazi kwamba, kwa mfano, misitukama ya Geita Forest Reserve, Nyantakala Forest Reserve,maeneo ya Game Reserve kama Uwanda, maeneo mengiambayo ukisoma kwenye karatasi yanaonekana ni hifadhi,hivi sasa ni makazi ya watu. Kinachoonekana hapa sasa hivini biashara na hujuma inayofanyika kwa makusudi kabisa kwa

[MHE. E. M. MAIGE]

Page 129: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

129

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wafugaji, kwa sababu kwa upande mmoja Serikali au Wizarahaichukui hatua ya ku-legalize makazi ambayo alreadywananchi wako pale kwa zaidi ya miaka kumi, badala yakeinaendelea kung’ang’ania kwamba yaendelee kubakihifadhi wakati kimsingi yalishabadilika kuwa makazi, lakinimbaya zaidi sasa kinachofanyika ni wizi wa ajabu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Sheria yaWanyamapori, kifungu cha 18 kinaelezea au kuzuia vituambavyo haviruhusiwi kufanyika kwenye Game Reserve,mojawapo kifungu cha 18(2) ni kuzuia kuchunga mifugohifadhini na kifungu kidogo cha (4) kwenye hicho kifungukinasema: “Mtu akikutwa na mifugo hifadhini anatozwa fainikati ya sh. 300,000 hadi milioni tano, has a maximum bila kujaliidadi ya mifugo aliyonayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati mbaya sana,ukiangalia taarifa ambazo zipo kwa sasa hivi, mifugoinatozwa kwa mfugo mmoja mmoja na kuna taarifazinaonesha mtu anatozwa mpaka milioni 30 na kitu ambachoni kinyume kabisa cha sheria. Matatizo haya yameanzakutokea toka miaka miwili mitatu iliyopita na kwa bahatimbaya sana ukiangalia mwaka jana tulipozungumza kuhususuala hili, hakuna hatua zilizochukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbaya zaidi sasa hiviimeongezwa sheria nyingine au adhabu nyingine ambayohaiko kwenye sheria ya kupiga risasi mifugo. Ni kinyumekabisa cha haki za mifugo, ni kinyume cha haki kwa kweli zakistaarabu cha jamii yoyote ambayo imeendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe sana katikamipango yetu, tuwe na mpango maalum kwenye Wizara yaMifugo, Wizara ya Maliasili pamoja na Wizara ya Ardhi kwaajili ya kupata ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la wafugaji,ambalo kwa sasa hivi ni tatizo kubwa na naamini kwa taarifailiyowasilishwa jana itabidi yafanyike maamuzi magumu yakuweza kukabiliana na hali iliyoko hivi sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda kuwa

[MHE. E. M. MAIGE]

Page 130: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

130

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

umekwenda sana, niombe tu kwamba pia katika utekelezajiwa Mpango wa MMAM wa kujenga zahanati na vituo vyaafya kwenye maeneo mbalimbali, utekelezaji wake naosidhani kama unaendana na Ilani, kwa sababu mpaka sasahivi miaka minne inakaribia kwisha, bajeti zinazoletwa kwenyeWilaya kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hazifiki zahanati tanokwa mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati malengo unakutakwenye maeneo mengine ni zahanati karibia 70 au 80 kwahesabu ya zahanati tano kwa mwaka, maana yake itafikamwaka 2015 kuna zahanati 15 au 25 na hatutakuwa tumefikialengo. Wananchi bahati nzuri sasa hivi ni wasomi, wanatunzakumbukumbu, wanaturekodi kwenye mikutano yetu nautakapofika wakati tutasema jamani tulikuwa tunasema yakwenye Ilani. Kwa hiyo, tunaomba tuelewe kwamba, is atotal failure of all of us na siyo ya mtu mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe sana, Serikali ndiyoinayotekeleza yale tuliyoyaahidi, na Serikali ndiyoinayokusanya kodi itekeleze kama tulivyokubaliana.

MWENYEKITI: Nakushukuru.

MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana. Sasa namwitaMheshimiwa Kidawa, ajiandae Mheshimiwa Zambi naMheshimiwa Kapteni Komba.

MHE. KIDAWA HAMID SALEHE: MheshimiwaMwenyekiti, nakushuru kwa kunipa nafasi nami kuchangiahoja iliyokuwa mezani sasa hivi. Nchi yoyote makini ni lazimaiwe na mipango makini kwa sababu mipango ndiyoinayoonesha tunataka kuiondoa nchi wapi na tunatakakuipeleka wapi. Kwa hiyo, tunaipongeza Serikali kwa kuletaMipango hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua mipango ya nchi iko

[MHE. E. M. MAIGE]

Page 131: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

131

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ya muda mrefu, miaka 20 na kwenda mbele; muda wa katiya miaka mitano, na muda wa mwaka mmoja ambayoinatafsiri au inafanyia kazi yale malengo yaliyowekwa yamiaka mitano. Baada ya miaka mitano tunajipima kuona je,tumefikia malengo au hatukufikia malengo na kamahatukufikia kuna changamoto zipi zilizotukwaza ili kutowezakufikia hayo malengo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu ina utaalam mzuriwa kuandaa mipango mizuri, lakini kuna changamoto nyingisana zinazozuia utekelezaji wa mipango hiyo. Mipangoimepangwa mizuri, lakini utekelezaji wake unakuwa mgumuna hasa hasa linalosababisha hivyo ni uhaba wa rasilimalifedha. Mipango inapangwa lakini hakuna mpango mzuri wakuona ni vyanzo gani vya mapato vya uhakika ambavyovinaweza kusaidia kutekeleza mipango hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mipango ya kifedhaambayo iko juu juu tu. Labda tunategemea fedha zaidikutoka kwa wafadhili, kutoka sekta binafsi na mchango yamapato ya ndani unakuwa ni mdogo sana. Kwa mfano,katika Mpango wa Mwaka, imeanishwa pale, trilioni 8.6zitahitajika kutumika kwa mwaka kutekeleza mpango huouliowekwa; lakini kwa bahati mbaya sana ni trilioni 2.9 ndiyomapato ya ndani. Mapato yenyewe ambayo hayapatikanikwa uhakika vilevile, lakini ni trilioni sita zimepangwa zitokanena sekta binafsi na Wafadhili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najiuliza sekta binafsi ni hiihii ya Tanzania au sekta binafsi ipi? Kwa sababu uelewa wetu,sekta binafsi ya Tanzania bado haijawa pevu, haijawa imarakusaidia kutoa fedha trilioni sita. Je, Serikali ilikaa na sektabinafsi wakaongea, wakakubaliana kama uwezo huu upo?Au Serikali imekaa ikawapangia watu wengine bila ya waowenyewe kushiriki katika huu mchakato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa wafadhili sasa hivi,yaonekana nao wanaendelea kutuchoka. Kwa sababuukichukua trilioni sita kwa mwaka, ukigawa kwa quarter,inategemewa zipatikane angalau trilioni 1.5, kwa robo

[MHE. K. H. SALEHE]

Page 132: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

132

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mwaka. Katika robo mwaka hii, mwaka huu tulionao takwimuzinasema kilichopatikana ni bilioni 50.7 tu. Kati ya zile zotezilizopangwa za misaada na mikopo za bilioni 291, ambapokilichopatikana ni 94.1 kwa ujumla wake sawa na asilimia 32.Ni kitu ambacho hakina uhakika. Kwa hiyo, mipangoitaendelea kuwa mizuri, wenzetu wa nchi nyinginewataichukua waifanyie kazi, lakini sisi katu haitatekelezeka.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri tujaribu kuletamiradi michache ya kipaumbele na vilevile iletwe pamojana vyanzo vyake vya mapato. Kwa mfano, kama tunaamuakipaumbele namba moja baada ya kufanyiwa tathmini nautafiti, ambacho kitakuza uchumi haraka haraka, ni reli yakati. Kwa hiyo, iangaliwe reli ya kati, itagharamiwa na chanzogani cha mapato. Kwa hiyo, Serikali ije na vyanzo vipya vyamapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano; reli ya Katiitagharamiwa na chanzo X, mfano uvuvi wa bahari kuu aumapato ya bahari kuu. Kwa hiyo, chanzo kile kisitumike kwamambo mengine yoyote, kitumike kwa kugharamia mradiule tu, wanaita merging principle. Chanzo hiki cha mapatokinaambatanishwa na mradi huu fulani na hii inakuwa ring-fanced, kuliko sasa kila kitu kinatua kwenye pool, hatimayefedha zinatumika katika matumizi ya kawaida zaidi, kulikomatumizi ya maendeleo na hatimaye miradi ile hakuna hatammoja unaokwenda mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo lingine ambaloni baya sana linafanyika, ni kwamba, Serikali hawakubaliani,zinakusanywa pesa chache katika robo mwaka, lakini kilaWaziri katika kila Wizara anataka na yeye apate kidogokidogo. Kwa hiyo, zile fedha zinakuwa zinagawiwa kidogokidogo, hazileti impact, haziwezi zikatumika kufadhili mradiwowote ule wa maana ambao unaleta athari ya kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali ikubaliane,kwa hiki kidogo kinachokusanywa sasa, basi mradi namba

[MHE. K. H. SALEHE]

Page 133: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

133

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

moja huu, upatiwe fedha za kutosha u-take off; uendeleena ile miradi mingine isubiri kipindi kingine kuliko kugawiwakidogo kidogo na hakuna lolote linalokwenda mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikubaliana hapakwamba, mgawanyo wa fedha za maendeleo na fedha zamatumizi ya maendeleo na matumizi ya kawaida; yawe kwaasilimia sitini na tano kwa matumizi ya kawaida na asilimiathelathini na tano ni matumizi ya maendeleo. Hilolimesahauliwa kabisa, fedha zikipatikana moja kwa mojaasilimia kubwa inakwenda kwenye matumizi ya kawaida,huku matumizi ya maendeleo yanasahauliwa kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tusipobadilika hatutayapatamaendeleo ambayo tunategemea kuyapata, ya kuhamishanchi yetu kutoka hali ya umaskini kwenda katika hadhi yakipato cha kati, haitawezekana, tutakuwa tuna mark timehapo hapo hatuendi mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo l inginelimezungumziwa ni la aibu kulisema, kwamba, wafadhiliwanashindwa kuchangia wakati mwingine, kutokana nakuwa wataalam wetu wanashindwa kuandika maandiko yamiradi yanayokidhi matakwa ya wafadhili hao. Huu mwakawa 50 tangu tupate uhuru, wataalam kila sikuwanasomeshwa, kuambiwa hilo bado ni tatizo sugu, wenginehatuelewi. Hivyo, Serikali iweke nia safi, ifundishe wataalamwetu, tusikose fedha kwa sababu ya maandiko. Karne hii niya sayansi na teknolojia na watu wetu wana akili, wakifunzwa,miradi itapatikana tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani bado watuhawajaweka msisitizo huo, pengine ni jambo lililokuja juu juutu, tuanzisheni miradi, lakini hatukujipanga vizuri katikamambo madogo madogo kama hayo; kwa sababu hilonaliona ni jambo dogo kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kurudia utaratibuwetu wa capital bajeti na tukaachana na cash bajeti,limezungumzwa na wengi sana. Tulifanyie utafiti wa kina na

[MHE. K. H. SALEHE]

Page 134: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

134

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)[MHE. K. H. SALEHE]

kuona ipo haja sasa ya kubadilika. Tusibakie pale pale,tumeshaona panatutia matatizoni, kwa nini tusirudie kulekwenye utaratibu wa cash bajeti? Zikatafutwa fedha mwakahuu, ambazo zitatumika kwa mwaka ujao, kwa utaratibuwowote ule utakaoonekana ni muafaka; tunaweza kukopaau tunaweza kufanya utaratibu wowote; Serikali ipo, fanyeniutafiti tuone, hili kila mmoja analiona kuwa linawezalikatusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni ukomo wa kukopa.Ukomo wa kukopa tumewekewa na taasisi za IMF, World Bank,kwamba tusizidi, lakini na Wizara ya Fedha inaweka vikomohata kwa taasisi ambazo zinajitegemea, waondoe huoukomo kwa hizo taasisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.(Makofi)

MWENYEKITI: Sasa namwita Mheshimiwa KapteniKomba na Mheshimiwa Riziki Lulida ajiandae.

MHE. KAPT. JOHN D. KOMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nitoe pongezi kwa Mpango huu ambao tumeletewa hapa,lakini ninavyoona hapa, watu wengine wakisimama ni kubezatu, kubeza tu! Inafika mahali mpaka mtu anamlinganishaRais wetu anayeongoza karibu watu milioni 50 na mtuambaye ana watu milioni tisa au milioni kumi na nchi yakeinaingia kwenye nchi yetu zaidi ya mara kumi na tano,kwamba huyu ndiye kaweza ila wa kwetu hakuweza. Kwakweli hapa hatutendi haki, mnyonge mnyongeni lakini hakiyake mpeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukubwa wa Tanzaniajumlisha nchi tano inazozizunguka, jumlisha Kenya, Uganda,Burudi, Burundi, Rwanda na Malawi. Hizo zote zinaundaasilimia 48% tu, lakini bado tumeweza kufanya vitu ambavyohata wengine hawawezi kufanya. Leo ukichukua umemeulioko Tanzania, ukausambaze Rwanda, haki ya Munguutakwenda mpaka vyooni, mpaka makaburini watatembea

Page 135: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

135

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kwa lami. Peleka mashule yaliyopo Tanzania, uyapelekeBurundi, mengine yatakaa angani. Peleka chochoteunachokifikiri wewe, tumefanya, watu wanasahau!

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati nasoma Sekondari,nilikuwa nasoma Songea Boys, miaka kama 40 iliyopita.Unatoka Songea unakwenda Tabora likizo unatumia sikusaba. Siku nne mpaka Dodoma, siku tatu mpaka Tabora. Leoukifiwa Mwanza unatoka Songea unatumia siku moja na nusu,unafika kuzika kama ndugu yako amekufa Mwanza. Hayasiyo maendeleo haya? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuyaseme, tumefanya lakinikuna upungufu, moja, mbili, tatu, hiyo ni sawa, hakunamkamilifu bwana. Mkamilifu ni yule aliyezikwa futi sita chini,hafufuki mpaka Yesu Kristo atakapokuja tena, huyo ndiyokakamilika, otherwise hakuna mkamilifu hapa. Sasa upoupungufu, kwa mfano, huu Mpango ambao tumeletewahapa, ningefikiri kwamba, ungetueleza katika vipaumbelevya mwaka jana, katika miundombinu tumekamilisha asilimiakadhaa, katika elimu asilimia kadhaa, katika afya asilimiakadhaa, katika hiki asilimia kadhaa. Sasa mpango huutunauleta kwa ajili ya kuboresha haya ya mwanzo na kuletamengine mapya. Hii sijaiona, kwa hiyo, hapa kuna upungufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia sisi wanasiasatunasimamia sera, lakini tatizo linapokwenda kwa watumishiwa Serikali kule, ni yule yule aliyekuwa tangu mwaka 60, huyohuyo anaendelea mwaka 70, 80, 90, mpaka 2000na uzoefuwake ni huo huo wa mwaka huo. Kwa hiyo, tunaangushwana watumishi wa Serikali, hawa walioko Serikalini. Tunapangamambo vizuri, lakini yakifika anatumia uzoefu tu, tunafanyamipango mizuri, lakini ukifika kwake anafanya uzoefu, hilo nitatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo sikulionakwenye mpango ni kuhusu Mtwara Corridor. Mtwara Corridorni kama sasa umekufa, hauzunguzwi chochote, yaanihauzungumzwi kwamba kuna mradi mkubwa ambaoutatukomboa sisi Watanzania na wenzetu wa Kusini mwa

[MHE. KAPT. J. D. KOMBA]

Page 136: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

136

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Afrika. Kidogo kuna barabara zinatengenezwa, ndiyo, lakiniBandari ya Mtwara imezungumzwa tu lakini kwa kweli sionijuhudi kubwa ya kuitengeneza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bandari ya Mbaba Bayimezungumzwa tu lakini ukifika Mbaba Bay ni kichekeshokitupu. Kwa hiyo, Mbamba Bay haiwezi kuwa kiungo kati yaTanzania na Malawi na nchi nyingine za Kusini mwa Afrika.Kwa hiyo, kwa kweli naomba katika mambo ya bandari,jambo hilo lingetiliwa mkazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maziwa, naonabahari imezungumzwa, lakini kwenye maziwa hakunakilichozungumzwa hasa katika mambo ya usafiri. Mpaka leoZiwa Nyasa linatumia usafiri wa Malawi, mpaka leo usafiri waMalawi, lakini mpango wa kunusuru Watanzania wale iliwajione kwamba wako Tanzania, mpango huo tumeusomamwaka jana na nimeusoma mwaka huu, haupo. Sasa sisi niwa Malawi au Watanzania bado?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sanaWaziri atakaposimama atueleze mpango huu wa kutunususisi wengine kuitwa Wamalawi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kilimo; nilipongezesana Shirika la SUMA ambalo mwaka jana lilipoleta matrektaangalau kilimo chetu kiliinuka kidogo, kutoka pale tulipokuwampaka hapa tulipofika. Hata hivyo katika Mpangonimeangalia hapa kuinua Shirika la SUMA liendelee kuletamatrekta ili kilimo chetu kipande juu, sijaona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachokijua ni kwamba,SUMA wanalalamika sana, viongozi wetu wanakwenda pale,ndiyo wamehamasisha kilimo, lakini wanakopa matrekta,fedha hazirudi, wanasema aah, sisi tulikuwa tunahamasishana matrekta haya ni kwa ajili ya kuhamasisha, SUMA

[MHE. KAPT. J. D. KOMBA]

Page 137: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

137

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wanaomba zile fedha mlizokopa mrudishe ili SUMA ipate uhai.Rudisheni zile fedha za matrekta ambazo viongozi mmekopa,wanalalamika sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie uvuvi;nimeangalia katika Mpango kuna uvuvi wa Bahari Kuu tu,uvuvi wa Maziwa na Mito hakuna. Sasa samaki wengiwanaovuliwa na kupelekwa nje, wanatoka kwenye maziwana hasa Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa kwa upande wa Malawi,lakini halizungumzwi katika mipango yetu, tunafanyaje uvuvikatika maziwa haya makubwa? Mpango huo hauko kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesoma kwenye Mpangowenyewe hakuna, nimesoma kwenye hotuba ya Wazirimhusika hakuna. Sasa naomba sana, tukitaka kukuza uvuvindiyo bahari ipo, lakini pia mito na maziwa yamesaidia sanakatika kujenga uchumi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni kivuko. Vimetajwavivuko vingi mle ndani, kuongeza na kufanikisha vivuko, lakinikipo kivuko kimoja ambacho kipo kwenye Ilani ya Uchaguzi,kivuko cha Mto Ruhuhu ambacho kinaunganisha mikoamitatu; watu hawawezi kwenda Iringa, Njombe wala sehemuyoyote wakitokea Ruvuma. Kwa hiyo, sehemu ile imekuwakama vile imefungwa, ni land locked.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana katika vivukovile na kwa kuwa Ruhuhu ilikuwa kwenye Ilani ya Uchaguzina bado tuna miaka miwili tu au mmoja na nusu, naombasana jambo hili litekelezwe tuliweke katika mpango wamwaka huu ili mikoa ile ambayo inazalisha mahindi nachakula kwa wingi waweze kutumia daraja hilo la Mto Ruhuhukuvusha vyakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, nipongeze Mpangohuu na niwaombe watumishi wa Serikali waupokee vizuri,wakifanya vizuri nina hakika kabisa tutaondoka hapa tulipo.Wasalaam allaykum, naunga mkono hoja. (Makofi)

[MHE. KAPT. J. D. KOMBA]

Page 138: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

138

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Komba.Sasa ni Mheshimiwa Riziki Lulida, ajiandae MheshimiwaMeshack Opulukwa.

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaliakuwa katika afya njema, hivyo kuweza kuchangia katika hojail iyopo mezani. Sera tunazo nzuri, lakini tunapaswakuzisimamia ili tupate mafanikio katika hizi sera ambazotunaziweka mezani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitazungumzia suala lakilimo. Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ilisema,mikoa il iyoko pembezoni itapewa kipaumbele chamaendeleo. Nilitarajia katika mikoa hiyo yote ya pembezonimmojawapo ukiwa ni Lindi, Mtwara na mikoa ya Rukwawakati ule na Kigoma, ndiyo mikoa ambayo ilikuwa nyumakwa kiasi fulani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoona sasa hivi, mikoamingine angalau inaonesha kufuatiliwa na kusimamiwawanaendelea. Mikoa mingine imegawanywa na katikakufanya hivyo maendeleo yamezidi kuboreshwa na wenzetuwanaendelea, lakini Mkoa wa Lindi bado uko nyumakimaendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimuunge mkonoMbunge aliyemaliza kuchangia sasa hivi kuhusu MtwaraCorridor. Tulitegemea Mtwara Corridor ingetusaidiawananchi wa Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma, lakiniMtwara Corridor haipo. Kwa vile haipo tukategemea SAGCOTitasimamia Mikoa ya Kusini ambayo imeingia katika mradiule; Lindi, Mtwara haipo. Sasa je, tunataka tulete maendeleoya kilimo, mikoa hiyo hatupo popote, tunayumbayumba tu,tunategemea sera hii ya maendeleo ya kilimo mtausaidiavipi Mkoa wa Lindi?

Page 139: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

139

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, zao la korosho katika Mkoawa Lindi lilikuwa la kwanza kuingiza fedha za kigeni katikamiaka ya sitini na mpaka sasa hivi korosho inaingiza fedha zakigeni, lakini Viwanda vyote vya Korosho viliingia katikauwekezaji na mpaka leo hatujajibiwa na Serikali uwekezajiwa viwanda vile unafanya nini hata kiwanda kimoja hakifanyikazi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijana wa Lindi hawana kazi,wanakimbilia Dar es Salaam, huko wanakimbizwa kimbizwahawana pa kwenda. Waziri mwenye dhamana, awe ni waKilimo, Viwanda na Biashara aseme vijana wale tuwapelekewapi ili na wao waondokane na umaskini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Lindi wanalima ufuta,lakini soko la ufuta hatuna. Usimamizi wa soko la ufuta haupo,korosho ndiyo zimekaa majumbani, hawajui watazipelekawapi, lakini ukiangalia nje, soko la korosho ni kubwa na hataukiingia ndani ya ndege unakula korosho kwa bei ya juu. Hiiina maana usimamizi wa sera zetu za maendeleo ya masokoumekuwa mgumu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja upande wa ardhi,nyumba na makazi. Tunakuja katika miji mipya new cities,programs zake ziko wapi? Mipango miji ya miji mipya ikowapi? Nitoe mfano ambao nataka nione pengine tukipigahesabu hizo Serikali italiona, kuna Kigoma nauona kamaunawekwa katika miji mipya una uwezekano wa kufika katikamaendeleo ya miji mipya, kwa vile uta-link na Burundi,Rwanda na Kongo, pale pakitengenezwa mji mpyapataweza ku-link katika masuala mengi ya maendeleo.

[MHE. RIZIKI S. LULIDA]

Page 140: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

140

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Kilwa, katika historia ya miaka ya 1690 ilikuwa MakaoMakuu ya East Africa na sasa hivi kuna madini, kunaMbuga ya Selous, mbili ya tatu ipo Kilwa; lakini je, Mpangowa Kilwa uko wapi?

Tuna kiwanda cha Songosongo. Ukienda pale Kilwaukaambiwa inatolewa gesi huwezi kukubali kamapametolewa gesi; watu ni maskini. Je, tumejipanga katikamipango bora ya maendeleo ya Wananchi wa Kilwa?

Tunafika mahali tunajiuliza, kama Mipango hiiitakuwa ni ya work and see attitude hatuendi; tutakuwatunapiga porojo za kuongea hapa lakini maendeleoyatakayotoa tafsiri hayapo. Leo najiuliza, Sera ya Madini,inabidi ije hapa ili ikishafika hapa Wananchi ambaowataondolewa katika maeneo yao watapata nafasi yakufaidika na maendeleo ya madini, lakini Sera hakuna!

Kama Sera hakuna watu hawa watafanya nini,wataondolewa kwa shilingi 400,000 halafu watafanya ninina shilingi 400,000, akiondolewa kwa milioni mbili atafanyanini na miloni mbili! Tunataka yule mtu anayekutana namadini katika eneo lake afaidike. Nataka nitoe mfano,Wachina kwao wanatetea uchumi wao, lakini wakija kwetuwanaongoza katika kuvuruga uchumi wa Tanzania. Sisemiwote, lakini majority ya Wachina na Waasia wamekujaTanzania hapa siyo kutusaidia katika maendeleo, wengiwao wamekuja hapa kutuvurugia maendeleo. Ndiyomaana tunajikuta wamepewa nafasi kila eneo wamejaa;ukienda Vijijini kila maeneo wamejaa, lakini hawajakuja namazingira ya kutusaidia, wamekuja katika mazingira yakupora uchumi wetu kwa nguvu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini ninawataja Watuwa Asia? Ninataka nichuke sehemu ndogo sana ya Utaliiwa Tanzania; Utalii wa Tanzania upo katika asilimia 18.7,lakini leo hii wao wanakuja kumaliza Tembo kwa faida yao.Ukienda kule Asia, Tembo anatunzwa, inakuwa kama nikivutio kikubwa. Sasa je, kwa nini tunaendelea kuwaacha

[MHE. R. S. LULIDA]

Page 141: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

141

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

hawa watu wakitufanyia fujo na sisi hatuna action ya ainayoyote?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo taarifa ambayo nisahihi na baadhi ya Wabunge nilikwenda nao Katavi,Mchina alikutwa na lori limejaa pembe. AlipopelekwaMahakamani wakasema huyu hajui Kiingereza na Kiswahili,anashindwa kuchukuliwa action yoyote! Leo tumefikia utaliiwa Tanzania ni wa Wildlife, ni wa Mifugo ya Wanyamaporina wanafanya fujo sasa hivi kupeleka sumu katikaMabwawa, bwawa lile Simba na Nyati wanakufa nawanyama wote wanaokwenda kunywa maji. Sasa je,survival ya utalii Tanzania itafikia wapi?

Are we serious? Are we committed? Are wemonitoring wanavyofanyiwa wanyama wetu au tuko hapatunaangalia tu? Tunahitaji sasa hivi juhudi ya pamoja naWabunge wenzangu naomba tuunge mkono suala hili lafujo ya wanyamapori limekuwa critical, ni janga la Taifa.

Napenda ku-declare interest, kwanza, mimi niMwenyekiti wa Kusimamia Mauaji ya Tembo na Vifaru ndaniya Bunge la Jamhuri. Pili, bado ninaupenda utalii wanguwa Tanzania ukue, lakini kama haukui ina maana wataliiwatakuja kufanya nini Tanzania! Kama Tembo hamna,kama Kifaru hamna, kama Nyati hamna, pana utalii hapo?Hamna utalii, usimamizi bora wa utalii wetu uwe mazingirabora kwa kila Mtanzania, asimamie utalii. Kwa nini ninasemahivyo? Kuna Vijiji vinazunguka Mbuga zetu za Wanyama,lakini maeneo yale wamepewa vitalu, watu wanawindakipindi cha corridor ya wanyama wanatembea. (Makofi)

Natoa mfano wa Miasa, Mozambique, pale panavitalu karibu sita karibu na eneo la Tunduru, wanapewawatu kuwinda kipindi kile wanyama wanapita kwa fujo.Kipindi cha neema zao, wao wanawindwa, wanauawa nabado tunaiona Asia kama ni sehemu ya kuisaidia. NaombaWabunge, tujumuike kwa pamoja, tuone janga la Taifa letula Utalii linauawa na Asia. Wamekuwa ni watu waharibifukatika nchi yetu, kwao wanatangaza utalii. Tumefikia mahali

[MHE. R. S. LULIDA]

Page 142: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

142

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

tunajiuliza, kama utalii unaingiza pato kubwa namna ile,bado wao wanaamua kutuhangaisha tunawachukuliaaction gani ya kina?

Mnasema, tutafute siku tuandae maandamano yamshikamano wa kupinga Asia kuharibu utalii wetu Tanzania.Tupeleke malalamiko yetu UN, hili suala la hunting lifetusiendelee nalo tena.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Nakushukuru. Mheshimiwa Riziki!

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante.

MWENYEKITI: Sasa namwita Mheshimiwa Opulukwa,ajiandae Mheshimiwa Zambi na Mheshimiwa Leticia Nyererepia ajiandae!

MHE. MESHACK J. OPOLUKWA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi hii nami niwezekuchangia Mpango wa Maendelo wa Taifa. Ningependanianze na barabara za kupunguza msongamano wa watuna magari kwenye Jiji la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mpango huuimeelezwa kwamba, kutakuwa na flyover moja kwenyeeneo la TAZARA. Kwa bahati mbaya sana, aliyekuwaanaandaa Mpango, either alipitiwa au hakuona umuhimu;anaweka flyover eneo la TAZARA, lakini kuna barabarainayojengwa ya mabasi yaendayo kasi kutoka Kimarampaka City Centre, hakuna flyover iliyoandaliwa kwa ajiliya Ubungo, hakuna flyover iliyoandalia au iliyoko kwenyeMpango kwa ajili ya Magomeni na kwa ajili ya Fire. Sasahaya mabasi yatakayokuwa yanakwenda kwa kasi,yatakwenda kwa kasi ipi wakati yakifika kwenye junctionnayo yana-stack?

[MHE. R. S. LULIDA]

Page 143: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

143

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Kwa hiyo, naomba sambamba na flyover ambayoitakuwa inajengwa pale TAZARA au ule Mpango ambaoumeandaliwa kwa ajili ya flyover ya TAZARA, basi hizi flyovernyingine tatu ambazo nimezitaja, ziingizwe kwenye Mpangohuu ili kuweza kuufanya Mradi wa Mabasi YanayokwendaKasi uweze kuwa na mafanikio na ufanisi mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuongelea sualala Mji wa Kingamboni. Mpango unasema maandalizi yaujenzi wa Mji wa Kigamboni yanaendelea, lakini kwa mstarimmoja tu na nusu, hakuna maelezo ya kujitosheleza kabisakatika Mpango huu ambao tunauongelea hapa ili kuwezakuupitisha. Wananchi wa Kigamboni, zaidi ya miaka minnesasa wamekuwa wakiishi kwa matumaini, wamekuwawakiishi wakiwa ICU, hawajui wafanye nini, hawajui waishivipi. Wameanza kuzaliana tangu wakiwa wanakaachumba kimoja, mwaka au miaka minne iliyopita mpakaleo bado chumba ni kile kile, hawaruhusiwi kuendeleza lakiniSerikali imekaa kimya!

Sasa kumeanza minong’ono mingine ambayoinaendelea kuhusu Mji wa Kigamboni inasema naningependa Waziri mwenye dhamana, alitolee ufafanuzikwamba; itakapofikia muda wa fidia, Serikali imepangakulipa shilingi 35,000 kwa square metre moja kama fidia kwawale ambao watahamishwa, lakini shilingi 700,000 kwasquare metre moja kwenye eneo ambalo ni built up area.Kwa maana hii hakuna nyumba ambayo italipwa chini yashilingi milioni 70 na kuendelea.

Wananchi walikuwa wanataka kujua; bahatimbaya sana hata Mbunge wao, Mheshimiwa Ndungulile,hayupo hapa, inabidi niwasemee kwa sababu hawana mtuwa kuwasemea. Serikali itafute fedha kwa ajili ya kulimalizatatizo la Kigamboni, kwa sababu Wananchi wamekuwawakiishi kwa matumaini kwa muda mrefu, hawajui hatimayao, hawajui kama ni fidia italipwa lini na ni shilingi ngapikwa square metre moja. Naomba wakati Mheshimiwa Wazirimwenye dhamana anahitimisha, basi awaambie Wananchi

[MHE. M. J. OPOLUKWA]

Page 144: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

144

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wa Kigamboni waweze kujua hatima yao na mamboyatakwisha lini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la utalii, kunamaeneo mawili ambayo nimeona leo ni bora niyazungumzie.Tunasema utalii unaingiza fedha nyingi sana kwenye Serikaliyetu, lakini kuna maeneo ambayo yamesahaulika ambayonapenda Serikali iweze kuyafanyia kazi. Kuna eneo mojaambalo liko pale Mkarama, pale kulikuwa na Wajerumaniwalioishi miaka ya zamani, kuna magofu ambayo yako pale,ambayo Serikali ingeweza kuyawekea mkakati wakuyatengeneza na kuyalinda, nadhani yatakuwa kivutiokikubwa sana kama malikale kwa ajili ya watu ambaowangependa kwenda maeneo yale kuangalia j insiambavyo Wajerumani waliweza kuishi na kufanya kazi zao.Kuna magofu ambayo yanavutia kuzidi hata yale ambayonimeyaona kule Bagamoyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiacha eneo la Mkarama,kuna eneo lingine ambapo aliwahi kuishi Baba wa Taifa,Mwalimu Nyerere, eneo la Gezaulole Kigamboni. Eneo hilililikuwa ni root ya Watumwa waliokuwa wakitoka interior,wanafikia maeneo ya Kigamboni halafu wanasafirishwawanakwenda maeneo ya Bagamoyo kabla ya kupelekwamaeneo mengine. Ukifika kwenye eneo hil i, majiyanapokuwa yameondoka katika eneo lile utakuta kunamagofu yako pale ndani ya maji.

Ninadhani ingekuwa ni wakati mwafaka sana kwawatu wa archaeology kufika pale ku-study magofu yaliyokopale. Wangeweza kupata mambo mengine mazuri,ambayo yangeweza kuwa hazina kubwa kwa ajili ya watuwanaojifunza historia, kwa wanaikolojia pamoja na watuwengine wanaokuja kufanya utafiti kuhusu maisha yaWatanzania hapo zamani wakati wa biashara yawatumwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna issue ya TASAF; TASAFwamekuwa wakilalamika muda mrefu kwamba, hawapatifedha za kutosha, lakini maeneo ambayo wamekuwa

[MHE. M. J. OPOLUKWA]

Page 145: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

145

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wakipata fedha za kutosha, zile fedha zimekuwa misused,au zinakuwa mismanaged.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 7 Julai, pale Meatu,TASAF walikuwa wanagawa vyerehani kwa ajili ya vikundivya wajasiriamali. Kwa bahati mbaya sana TASAF Meatuwanatumika kama chombo cha Chama cha Mapinduzi.Alikuja Mwenyekiti wa Mkoa wa Simiyu, ambaye pia niMbunge katika Bunge lako Tukufu, wakachukua vyerehanivilivyokuwa vinagawiwa na TASAF, vikapigwa rangi ya kijanivikaandikwa CCM, halafu kwenye mkutano wa hadhara,wakaenda kuzigawa kwamba hii ni mali ya Chama chaMapinduzi. Hii ni aibu na suala hili halikubaliki. NinaombaViongozi wenzangu ambao pia ni Wabunge pamoja naViongozi wa Serikali kama DCs na watu wengine, tuiacheTASAF ifanye kazi yake kama ambavyo inaelekezwa katikamiongozo ya utendaji wa kazi zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuongeleaukurasa wa 26 kuhusu ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti. Hauwezikuongelea ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti bila kuongeleabarabara ambazo zinaelekea ambako daraja linajengwa.Daraja hili ni kiungo kikubwa sana kwa Mkoa wa Singida,Shinyanga, Simiyu mpaka wanaotokea Mara na nchi za jirani.

Ninaomba katika Mpango unaokuja, pamoja nakwamba, barabara ipo kwenye upembuzi yakinifu kwa ajiliya kuwekwa lami, lakini sasa yale madaraja ambayo ni yachini, madaja yote ambayo yamewekwa kalvati yajengweyawe ya juu ili daraja lile litakapokamilika hata kamaitakuwa bado haijawekwa, basi magari yaweze kupita juuna Mkoa wa Simiyu, Shinyanga, Singida, pamoja na Mara,waweze kufaidika na ujenzi wa daraja hili pamoja nabarabara zake zinazoingia katika Daraja hili la Mto Sibiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuongelea sualala Pamba. Kipindi hiki ni cha msimu wa kuanza kilimo chapamba, lakini nimepata taarifa kwamba, Wananchiwameanza kulazimishwa kujiunga kwenye vikundi ili wawezekuuziwa mbegu za pamba. Yule ambaye hatajiunga

[MHE. M. J. OPOLUKWA]

Page 146: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

146

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kwenye kikundi hatapata mbegu na kwa hiyo hatawezakulima Pamba katika msimu huu unaoanza sasa. NinaombaSerikali itoe tamko kwa watu wote ambao wanalimapamba Tanzania, kama ni kweli ili mtu aweze kupatambegu ya pamba ni lazima awe amejiunga kwenye kikundi,kwa sababu Wananchi tayari wameshaanza kukwazika.

Ninaamini Serikali ikishirikiana na wadau, kwakuandaa mbegu bora ya pamba ambayo ni UK 91iliyotolewa manyoya, ni kwamba inaweza ikazalisha ileproductivity ikawa kubwa sana. Wananchi wameshaanzakukwazika kwamba kama productivity inakwenda kuwakubwa kiasi hiki; kwa nini kuanze kuwa na vikwazo vingineambavyo Wananchi wanaona kwamba hili ni tatizo!

Kwa hiyo, naomba wakati Mheshimiwa Waziriatakapokuwa anahitimisha hoja hii, awaambie Wananchiwa maeneo yanayolima pamba kwamba, siyo lazima aukama ni lazima mtu ajiunge kwenye kikundi ili aweze kupatahiyo mbegu ya pamba ambayo ni pamba bora ya UK 91.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, nilishangaa sanaaliposimama aliyekuwa Waziri wa Maliasil i na Utali i,Mheshimiwa Maige, akiwa analalamika na anashangaa,anasema Wananchi wanaonewa, wafugaji wanaonewa,wanatozwa shilingi 500,000 mpaka milioni 32 wakati yeyendiyo alikuwa Waziri mwenye dhamana na haya yoteyametokea kwenye kipindi chake! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli mkuki kwaNguruwe, kwa binadamu mchungu. Leo yuko back bencherhuku, sasa ameanza kuona machungu ya Wananchi wakewanavyoteseka. Mambo yanayofanywa na Serikali yaChama cha Mapinduzi, aliyokuwa anayafanya yeyemwenyewe, tayari ameshaanza kuona limekuwa tatizo. Hilinadhani ni mfano mzuri kwa Waheshimiwa Mawaziri mliokohapa; mnapokuwa mbele hapo, hebu fanyeni yale ambayoWananchi wanawategemea.

Mheshimiwa Mweyekiti, ahsante. (Makofi)

[MHE. M. J. OPOLUKWA]

Page 147: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

147

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nami nashukuru kwa kunipatia nafasi ili niweze kuchangiaMpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2014/2015,kama ulivyowasilishwa na Mheshimiwa Wasira, Waziri waNchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, naomba nisemekwamba, Watanzania tumekuwa wazuri sana kwenyeMipango, tunaandika Mipango mizuri, lakini tunafeli katikautekelezaji kwa sehemu kubwa sana. Sasa naiomba sanaSerikali, wakati imetuletea Mpango na maeneotunayoshauri ihakikishe yanakwenda kutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na suala la kilimo.Kwa vyovyote vile ili nchi yetu iweze kuendelea ni lazimatuhakikishe Mipango yetu ya Kilimo inawekwa vizuri, lakinipia inatekelezeka. Vinginevyo, tutaendelea kuzungumzahapa lakini hatutaweza kupiga hatua au kuondoa umaskiniwa Watanzania tunaotegemea hasa tukizingatia kwamba,zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania ni wakulima au wafugaji.Kwa hiyo, naomba Serikali ielekeze nguvu huko.

Ninasema hili, sijaona Mpango unaozungumzia. Kwamfano, tunazungumza hapa suala la uanzishwaji wa benkihususan Benki ya Wananchi, suala hili lilishaingia kwenyeMipango muda mrefu sasa, lakini utekelezaji wakehauonekani. Maana yake, tunazungumza kwenye Mpangoukisoma amesema kwamba, tunaendelea na tijihada zakuanzisha Benki ya Wananchi ya Kilimo, mpaka leo tukokwenye Dirisha la Kilimo ndani ya Benki ya TIB; lakini tijihadazenyewe za kuanza kujenga benki yenyewe ziko wapi?Tunazungumza Serikali imetenga fedha, lakini badotunaendelea kutoa huduma ndani ya Benki ya TIB.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hivyo haitoshi, sualala riba kwa mikopo hiyo ambayo inatolewa ndani ya Benkiya Rasilimali ya Taifa lakini Dirisha la Kilimo, bado mikopo ilehaiwanufaishi Wananchi walio wengi, ambao ndiyowanaweza pia wakasaidia sana kuchangia uchumi waTaifa. Leo ukiangalia hata waliokopa kwenye Benki ile, bado

Page 148: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

148

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ni watu wakubwa wenye uwezo wao, lakini angaliaWatanzania wa kawaida ambao wamekopa.Ninachosema hapa, hata masharti ya mikopo, hayakofavorable hata kidogo kwa wakulima wadogo.

Kwa hiyo, tunataka wanapotuandikia waje naMpango ni kiasi gani wakulima wadogo wadogowatafaidika na bajeti hii tunayoitegemea ya mwaka 2014/2015; vinginevyo, sioni namna.

La pili, tumezungumzia pia suala la kuwa na matumizisahihi ya mbolea, sioni tunapozungumzia ujenzi hasa.Ninajua Serikali inasema hatufanyi biashara, lakini kunamaeneo ambayo lazima ije na Mpango sawa sawa wakujenga viwanda vya mbolea. Leo tuna Kiwanda chaMinjingu, tumeambiwa na imendikwa kwenye Ilani yauchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, ujenzi wa kiwandakingine cha mbolea kule Mtwara. Sioni kuna mpango ganiambao wanatuambia Kiwanda cha mboleakinachotarajiwa kujengwa kule Mtwara kinakamilika lini iliWananchi wa Tanzania wawe na matumaini kwambawanaweza kupata mbolea hivi karibuni? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie na hilo; hivitunakuwa na Mipango gani; sisi Mbeya tulishazungumza,jamani mbolea ya Minjingu haiwafai Wananchi wale kwaajili ya uzalishaji wa mahindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inashangaza na hil initaomba Serikali ilijibu, kwenye Mipango tena kuanziamwaka 2008, tulishazungumza Mkoa wa Mbeya maeneomengi mbolea ya Minjingu haifai na kwa kweli hata katikamaeneo mengine katika nchi hii, mbolea ya Minjingu haifai.Serikali ikasema haina virutubisho vya kutosha tutairutubisha,tumetengeneza Minjingu Mazao, Minjingu Mazao imetumikamwaka jana, lakini matokeo bado yamekuwa mabaya.

Ninashangaa na nitaishangaa Serikali ya Chamachangu kama itaendelea kuwalazimisha Wananchiwaendelee kutumia mbolea ya Minjingu ambayo haina tija.

[MHE. G. W. ZAMBI]

Page 149: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

149

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Aliyekuwa wakala wa mbolea ile kule Mbozi mwaka jana,mwaka huu amekataa kwamba hataisambaza tena kwasababu mpaka leo Wananchi hawajaitumia ipo kwenyeghala, amepata hasara. Mwaka huu Serikali inatuleteambolea hiyo hiyo Wananchi waendelee kuitumia!

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wananchi wa Mbozi, Ileje,Momba na Wananchi wa Mbeya Vijijini, wamesema hiyombolea hawatakuwa tayari kuitumia; na kwa maana hiyo,tutegemee ruzuku ya Serikali, kama tutaendeleakuwang’ang’aniza mbolea ya Minjingu hawatakuwa tayarikuitumia. Bahati nzuri nimeongea na Mheshimiwa WaziriChiza, kama ananisikia popote alipo, basi wahakikishekwamba, ili kuendeleza Mipango mizuri ya kilimo nakuhakikisha Wananchi wale wanaweza kulima vizuri tenakwa tija, basi watuletee mbolea ya kupandia ya DAPambayo Wananchi walishaizoea. Serikali ikifanya hivyo,nadhani Mipango yote tunayoipanga kwenye Sekta yaKilimo na ustawi wa Wananchi basi unaweza ukapatikanakwa uzuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pil i ambaloningependa nil izungumze ni la Kiwira. Inasikitishatunavyopanga Mipango ya nchi hii; kwenye mipango yanchi tuna maeneo mengi, lakini nizungumzie hili la makaaya mawe, mengine Waziri ameyazungumza Mipangoinaonekana. Suala linalosikitisha ni la Makaa ya maweKiwira. Makaa ya Mawe Kiwira, alipokuwa WaziriMheshimiwa Ngeleja alituambia kwamba, mipango yoteimekamilika, tumeshamaliza na tunasubiri mwekezaji pale.Amekuja Waziri wa sasa Mheshimiwa Profesa Muhongo,akatuambia tumeshamaliza tunachosubiri ni utekelezaji. JuziMheshimiwa Waziri Mkuu amefanya ziara ya Uchina ndiyonimefahamu kwamba kumbe Mpango ule badohaujakamilika na Serikali inaendelea kufanya mazungumzo;na kwenye Mpango ndivyo wanavyozungumza Serikaliinaendelea kufanya mazungumzo. TunawadanganyaWatanzania, tunawapa matumaini na mambo ambayohayajakamilika.

[MHE. G. W. ZAMBI]

Page 150: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

150

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba hebutunapokuja na Mipango tuweke na time frame; Mpangohuu tunaouleta utekelezaji wake unachukua muda gani.Ukiweka Mipango ambayo ni open-ended, hatuwezi kufikahata kidogo. Wenzetu waliofanikiwa wanapokuja naMpango wanaweka na time frame, kila jambo linakuwana time frame yake; lakini ukiacha hivi hivi hatutawezakujua tunatekeleza lipi na tunaacha lipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambaloningependa nil izungumzie ni la elimu. Kwanza, hil ilimenichanganya kidogo na ukisoma kwenye Mpangowenyewe, inaonekana elimu kama vile haipewi kipaumbelekinachotakiwa. Kwenye yale maeneo sita ya mwanzoyanayozungumzwa, elimu haizungumzwi kwa ujumla wake.Nataka nijue tuna mipango gani inayotekelezeka hasakatika suala la ujenzi wa maabara, kumaliza madeni yawalimu na pia kuhakikisha madawati yanakuwepo shulenina kuhakikisha walimu wanakuwepo wa kutosha?

Mipango hii iweke wazi ni lini hasa tunamalizamatatizo ya walimu katika shule za msingi na shule zasekondari. Tunajua Serikali inafanya jitihada, lakini tuwe natime frame, tusiseme tu kwamba tunajua by 2014/2015inawezekana tukamaliza. Tuwe na time frameinayoeleweka kwamba, tutamaliza matatizo haya yaWananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni Mipangoya Maji. Kama kuna maeneo ambayo tutafeli ni pamojana suala la maji. Leo ukifuatilia bajeti iliyopitishwa ya majiya zaidi ya shilingi bilioni 500, haijaanza kutekelezeka mpakaninavyozungumza. Tulikuwa na Mpango tunasema lazimatuhakikishe Watanzania walio wengi wanapata maji, sasakama leo ndiyo tunaanza quarter ya pili pesa za majihazijaanza kutoka tunategemea nini? Nilikuwa nasomadocuments za Serikali, kwamba Serikali au Idara mbalimbalindiyo zimeanza kupata pesa sasa hivi, lakini quarter nzimaya kwanza hazikupata. Sasa hii Mipango tunayoipangautaitekeleza namna gani kama pesa hazitoki?

[MHE. G. W. ZAMBI]

Page 151: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

151

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Serikali tujaribu kuangalia, kama kuna tatizo kwenyeukusanyaji wa pesa Serikali iweke Mpango unaoelewekakwenye ukusanyaji wa pesa. Vinginevyo, tutakuwatunatwanga maji kwenye kinu. Tunaweka Mipango pesahazipo za kuitekeleza.

Wizara karibu zote, hakuna Mradi wowote wamwaka wa fedha ambao umeanza kutekelezwa kwasababu pesa hazitolewi. Kama tatizo liko Wizara ya Fedha,Serikali mje na tujue kabisa kwamba, tunahangaika namnagani katika kuhakikisha pesa zinapatikana za kutosha. Miminafikiri liko tatizo la matumizi au la ukusanyaji wa pesa,linalotokana na Wizara ya Fedha kwa ujumla. NadhaniWizara ya Fedha bado kuna matatizo, panapaswakutafuta utaratibu tuhakikishe pesa zinakusanywa mapemana ziende.

Pia ni vizuri Serikali ikatueleza kwa nini quarter yakwanza yote imepita Wizara hazijaanza kupewa fedha kwaajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo katika maeneoyao?

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Zambi.

MHE. GODFREY W. ZAMBI: Ahsante MheshimiwaMwenyekiti.

MWENYEKITI: Sasa namwita Mheshimiwa LeticiaNyerere, ajiandae Mheshimiwa Masoud Salim naMheshimiwa Jenista Mhagama!

MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipatia nafasi na mimi nichangie katikaMpango huu wa Maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze na Patola Taifa. Kwa uelewa wangu, unapotafuta pato la wastani

[MHE. G. W. ZAMBI]

Page 152: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

152

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

la kila Mtanzania ni lazima ujue idadi ya watu Tanzanianzima. Cha kushangaza kwenye hiki kitabu wameoneshaidadi ya watu kwa Tanzania Bara bila kuonesha idadi yawatu kwa Zanzibar. Sasa nashindwa kuelewa penginelabda nitahitaji ufafanuzi; tunapozungumzia Taifa, Zanzibarhaiingii kwenye Taifa au inakuwaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumziemasuala ya uchumi. Inaonekana uchumi umepanda kwaasilimia 0.1, jambo ambalo ni la kusikitisha lakini kuna baadhiya watu wanafikiri it’s a progress, lakini ni jambo la aibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika miaka ya 60, Babawa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,alisema yafuatayo: “Maendeleo si ya vitu bali ya watu.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapaswa sasa kuzingatiahilo, kwa sababu tumejikita kwenye maendeleo ya vitu nawala si maendeleo ya watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jambo la aibu tunajadiliMpango wa Maendeleo wakati Wananchi wa Kwimbahawana maji. Ni jambo la aibu tunajadili Mpango waMaendeleo wakati wafugaji wananyanyasika nchi nzima.Ni jambo la kutia aibu tunajadili Mpango wa Maendeleowakati wanafunzi wa Wilaya ya Kwimba na kwinginekoTanzania wanakalia mawe. Ni jambo la kusikitisha kujadiliMpango wa Maendeleo wakati akina mama wajawazitowanapoteza maisha yao kila kukicha kwa kukosa hudumaambazo ni basic. Ni aibu kujadili Mpango wa Maendeleowakati hatuna barabara. Nasema ni aibu kujadili Mpangowa Maendeleo wakati Wamachinga wanazagaa mijinihawana maeneo ya kufanyia biashara.

Vilevile ni aibu kujadili Mpango huu ambao haunatija kwa Taifa na Wananchi wake wakati wakulima wapamba wananyimwa bei ya pamba yao. Nasema ni aibukujadili Mpango huu wakati wakulima hawana pembejeo.Ni jambo la aibu na la kusikitisha, kukaa tunajadili Mipangoisiyokuwa na ukomo wakati kwenye hospitali zetu hakuna

[MHE. L. M. NYERERE]

Page 153: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

153

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

vifaa vya kutendea kazi ikiwemo Hospitali ya Ngudu Mjini,Kwimba. Ni aibu tunajadil i Mpango usiowanufaishaWananchi wa Tanzania wakiwemo akina mama wauzamboga wa Ngudu ambao wanatozwa ushuru usiolinganana kufanana na kipato chao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni masikitiko makubwa,tumejikuta tuko hapa tunajadili Mpango unaosemekanawa maendeleo, ambao umewaacha nyuma Watanzania.Ni aibu kubwa kujadili Mpango wakati tukienda mijini kwetuwatoto wa mitaani wamezagaa kila kona. Nasema ni aibukujadili Mpango usiokuwa na tija, Mpango usiowajaliwanafunzi wa Taifa hili ambao unawanyima mikopo yao yashule ambayo wanastahili kuipata ili wajiendeleze nahatimaye wajenge Taifa letu. Ni aibu kubwa; narudia tenani aibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna usemi unaosemakwamba, sasa hivi tuanze kuchukulia matatizo kamayalivyo na siyo kuyachukulia kama tulivyo. Ni aibu sanakuona tumeshindwa kujirekebisha, tumeshindwa kuwaserious. Ni aibu mifugo ya wafugaji inauawa; hatuoni aibukukaa humu ndani tunajadili Mpango wa Maendeleo?Tunajadili Mpango wa Maendeleo ya nani? TunajadiliMpango wa kitu gani kama siyo Watanzania wetu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasema kwa masikitikona ninawaomba wenye dhamana ya kuongoza nchi hii,tubadilishe utaratibu wa kuendesha nchi. Ni jambo lakusikitisha, ni jambo la aibu kubwa, Wananchi wa Kwimbawanachangia maji na ng’ombe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina ushahidi, leonimeletewa ujumbe hapa, Wananchi wa Ngudu Mjinihawajapata maji kwa siku saba na wanachota maji yenyetope kwenye Bwawa la Mwamasululu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni aibu kujadili Mpangoambao unawadidimiza Watanzania. Ni aibu kujadiliMpango wakati Wananchi wa Jimbo la Kwimba, wakiwemo

[MHE. L. M. NYERERE]

Page 154: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

154

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wale wa Hungumalwa, Mwamashimba, Jojiro, Hunge naNgudu Mjini, hawana barabara na hata njia tu za kupitiahazijapaliliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unadhani hawawatapelekaje mazao yao? Hawa Wananchi wa Kwimbaambao wananyanyasika wana-future gani katika Taifa hili?Ni aibu, ni aibu, ni aibu, kujadili huu Mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

T A A R I F A

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Kaa chini Mheshimiwa!

Nakushukuru Mheshimiwa Leticia.

Waheshimiwa Wabunge, lengo la mjadala huu lipokatika Kanuni ya 94. Naomba mfungue Kanuni ya 94mtapata mwongozo wa namna gani Serikali inahitajimsaada wa Bunge hili. Sehemu kubwa ambayo Serikaliinahitaji msaada au ushauri ni vitu vitatu; kupokea kujadilina kutoa maoni na ushauri kuhusu vyanzo vya mapato yaSerikali. Sasa tutoe maoni kuhusu vyanzo vya mapato iliSerikali iweze kutoa hiyo aibu.

Mheshimiwa Masoud, ajiandae MheshimiwaMhagama!

MHE. MASOUD ABDALLA SALUM: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Awali ya yote, namshukuruMwenyezi Mungu, Subhanahu Wataala, aliyenijalia uzimana afya njema na kuweza kujadili Mapendekezo yaMpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2014/2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna Mpango, tunamaneno yasiyoonesha dira wala mwelekeo utakaowezakuwanusuru Watanzania kuondokana na umaskini. Sifikirii

[MHE. L. M. NYERERE]

Page 155: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

155

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kwa utaalamu na Wataalamu wa Serikali mkatuandikiamaandishi haya mkasema huu ni Mpango! Ni kwelitutaendelea kuangalia mikakati ya Serikali au tupendekezemapendekezo ambayo yataweza kusaidia kuboreshauchumi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na pendekezo langukatika Mpango wa Kilimo cha Mwani Ukanda wa Pwani.Wakulima wa Mwani wanahangaika; hawana masoko yauhakika, bei ya mwani imekuwa ndogo, wanatangatanga,hawajaandaliwa mazingira mazuri katika Ukanda wa Pwani.Hii ni aibu nyingine ya Taifa hili. Hatutaacha kusema aibu hiikwa sababu mlipowasahau Wananchi wa Mtwara na Lindi,Dar es Salaam, Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba naVisiwa vingine vidogo vidogo, mkasahau mikakati ya Serikaliya kuboresha kilimo cha mwani ni aibu nyingine. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani Serikali iandaemikakati madhubuti ya kuhakikisha Zao la Mwanilinaboreshwa katika dhana nzima ya MKUKUTA kama kweliSerikali ina nia hiyo ya MKUKUTA. Kama ni maneno tuyaliyoandikwa kwenye kitabu hiki ambacho kinasemakimetolewa na wataalamu; funika kombe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo langu laMtambile, kuna eneo la Kangani, Shehia hiyo na Kuu Kuuwanalima mwani. Bei yao wanayouza kule ni shilingi 400; nindogo sana. Ukiuliza maeneo ya Bagamoyo nao ni hivyohivyo. Mimi ninaiomba Serikali iandae mazingira yaliyo mazurijuu ya kilimo hiki cha mwani. Masoko yatafutwe, ukitafutamasoko na masoko ni sehemu ya Mpango, Serikali ilielewehilo, masoko ni sehemu ya Mpango. Kwa hiyo, kamahutafuti masoko ina maana Mpango huo ni Mpango gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni uvuvi. Sektaya Uvuvi tunajua inaingiza Pato la Taifa kwa asilimia mbili.Uvuvi unaajiri watu wengi; iwe wa baharini, kwenye maziwana mito, watu karibu milioni nne tulionao Tanzania wanajiajirikatika sekta hii ya uvuvi. Mpango huu tulioletewa hauoneshi

[MHE. M. A. SALUM]

Page 156: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

156

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

namna ya kuboresha maisha ya wavuvi hasa wavuviwadogo wadogo wa kwenye bahari na kwenye maziwa.Hakuna kitu humu, Mpango huu ni fedheha nyingine.(Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wavuvi katika maeneo yaPwani, ningetegemea katika Mpango huu basiwangelikopeshwa zana za kisasa, wakapewa mitaji na siyoSerikali ikawa mabingwa wa kuchoma nyavu zao moto; niaibu nyingine. Mpango hauoneshi hapa. Ninadhani Serikaliikae iandae mazingira yaliyo mazuri, kama kweli kuna dhanaya kweli ya kuboresha wavuvi wetu, tuandae mazingirayaliyo bora waondokane na umaskini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni aibu nyingine, tunaagizasamaki tunaletewa samaki wabovu hapa kutoka Japani,kutoka China, Afrika Kusini, wakati wavuvi wetutumewaacha wanahangaika, hatuwakopeshi mitaji,tumekuwa mabingwa wa kuchoma nyavu moto tu; ni aibunyingine. Ninaishangaa Serikali, nadhani tuwe makini sana;ni vyema tujipange katika mazao ya bahari, mazao yakwenye maeneo ya maziwa ambapo sasa hivi magugu majiyanaendelea, mito hii au maziwa haya siku za mbeleyanaweza kutoweka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo la bahari linatupatiamapato mengi. Kwenye maziwa kama tunavyojua, asilimiakubwa ya uchumi wetu, sasa mikakati ya uchumi iangaliejambo lingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango huu tulioletewana Wataalam hawa, dhana ya diplomasia ya kiuchumi,Mpango hauoneshi kabisa namna Serikali itakavyoongezakipato na kutoa ajira kwa vijana wetu katika dhana nzimaya diplomasia ya kiuchumi. Hili linasikitisha sana kwamba,mpaka sasa sisi kama Tanzania tumekuwa na Mabaloziwetu na tunajipanga kuinua uchumi wetu, lakini haditunatoa maeneo au Serikali imekuwa na Ubalozi wake,hatujazifikia baadhi ya nchi. Hati za Uwakilishi, to presentcredentials; mfano, pale Abuja, sisi eneo letu la uwakilishi

[MHE. M. A. SALUM]

Page 157: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

157

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ni Nigeria, Benin, Togo, Cote d’Ivoire, Ghana, Guinea,Senegal, Burkina Fasso, Mali, Sierra Leone, Liberia, GuineaBissau, Mauritania na maeneo mengine; lakini mpaka kufikahivi sasa hati ambazo ziliwasilishwa ku-present credentialhakuna.

Maeneo ambayo hatujayafikia i l i watu wetuwaweze kutangaza vivutio vya utalii, kwenda kutoamaelezo kujitambulisha, ni maeneo mengi; Benin hatujafika,Togo hatujafika, Cote d’Ivoire hatujafika, Ghana hatuna,Guinea hatuna, Senegal hakuna kitu, Mali hakuna, SierraLeone, Liberia, Buinea Bissau na Mauritania. Hii ni aibunyingine. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhana ya EconomicDiplomacy ni kubwa, watu hujawafikia unataka utangazevivutio vyako vya utalii. Tunazo fukwe zilizo nzuri na vivutiovingi vya utalii kama vile Ngorongoro na maeneo menginemengi; hii kama siyo aibu ni nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Berlin pale Ujerumani,hatujafikia kutangaza au kuwasil isha Hati zetu zaUtambulisho kwa Jamhuri ya Czech, Slovakia, Holland,Hungary, Bulgaria na Romania; hii ni aibu nyingine. Miakana miaka, maana mlituahidi hapa mtakwenda hukompeleke mpaka leo; hii ni aibu nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, Rome paleItalia hatujafika Croatia, Marcedonia, Slovenia, Albania,Bosnia, Hesgovina na Serbia hatujafika. Kule StockholmSweden nako hatujafika Finland, Iceland, Latavia naLithuania. Tumekuwa mabingwa wa kutembea na mikasitu ya kukata utepe na makelele, amekata utepe; tutafikawapi? (Kicheko/Makofi)

Mheshimwia Mwenyekiti, dhana ya economicdiplomacy ni kubwa, tusiwe mabingwa, tuna maboksi yamikasi, anakuja Mheshimiwa anakata utepe makofi.Tunatafuta kura mwaka 2015 wembe ni ule ule, hatufiki niaibu. (Kicheko)

[MHE. M. A. SALUM]

Page 158: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

158

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimalizie kwa kusemakwamba, katika jambo ambalo silikubali hata kidogo katikaMpango huu, ukurasa wa 41 unazungumzia usafiri wa majini.Serikali haioneshi Mpango wa kuwanusuru Wananchiwalioko katika visiwa vidogo vidogo. Katika Bonde la MtoRufiji kuna visiwa vidogo vidogo kila siku watu wanakufakule. Kila wakifa ninyi mnakwenda kutoa ubani na salamuza rambirambi huku mkitoa machozi kumbe muwaongo. Hiini aibu, mngeliandaa boti za uhakika ambazo mtawanusuruwanafunzi wanaokufa kila wakati kule. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mpango huuhakuna chochote kinachoonekana; sijui tatizo ni wataalamau ni nani! Hii ni aibu nyingine kama siyo fedheha. Kamakatika visiwa vile wanafunzi wale wataendelea kufa nahatutaki kuwanusuru; hili ni tatizo lingine. Serikali iandaeMpango wa kweli hasa usio huu wa maneno haya kwahawa tunaowaita wataalam, ili kuwanusuru wanafunziambao wako katika visiwa vidogo vidogo wasipotezemaisha. Ubani wenu watu hawautaki tena, risala zenu zakufuta machozi, machozi siyo ya kweli ni ya uongo; hii niaibu nyingine na fedheha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushuru sana. Ahsante.(Kicheko/Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mhagama, wajiandaeMheshimiwa Chombo na Mheshimiwa Malocha!

MHE. JENISTA J. MHAGAMA: MheshimiwaMwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi yakuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati watu wenginewakisema ni aibu, lakini mimi ninaomba niseme ni farajakwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi na Wananchi waTanzania, kwa kushuhudia hata Kiongozi wa Kambi yaUpinzani Bungeni akiishukuru Serikali kwa mtandao mzuri wabarabara za lami hapa nchini na ambazo nyingi zimejengwa

[MHE. M. A. SALUM]

Page 159: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

159

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

hata kule kwenye Jimbo lake; kwa kweli ni faraja kubwasana kwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Vilevile ni faraja kubwa sana kwa Serikali ya Chamahiki cha Mapinduzi kwa kuona kwamba, kwa takribanimuda mrefu sana katika nchi yetu ya Tanzania. Nchi hiihaikuwa na Vyuo Vikuu, lakini Serikali hii kwa mfano mzurisana mwingine imejenga Chuo Kikuu kikubwa sana hatahapa Dodoma; hiyo ni faraja kubwa sana kwa Serikali hiiya Chama cha Mapinduzi na ni faraja sana kwa Wananchiwa Tanzania. Watoto wanaosoma pale ni wa Watanzaniawote bila kujali wa Chama gani wala wa Serikali gani. Hii nifaraja kubwa sana kwa Serikali ya Chama cha Mapinduzina ni faraja sana kwa Watanzania wa nchi hii ya Tanzania.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wenginewakilalamika ni aibu lakini mimi ninaendelea kusemakwamba ni faraja kubwa sana kwa Wananchi wa Tanzania;kwa sababu unaona kwa takribani miaka yote hii ya Uhuru,sasa hivi Serikali imeweka nguvu kupeleka umeme vijijini namifano ipo mingi. Mifano iko mizuri katika nchi hii ya Tanzaniampaka Pemba kuna Mradi mkubwa sana wa Umeme. Kwahiyo, nchi hii mimi ninasema mkitulia, Serikali ya Chama chaMapinduzi Mipango hii tukitulia nayo ni faraja kubwa na niheshima kubwa kwa Serikali hii ya Chama cha Mapinduzi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nikutaarifu; juzitarehe 29 Oktoba, nilikuwa nina mkutano mkubwa sanaPeramiho, umeme unasambazwa pale Peramiho pote.Katika Kijiji cha Maposeni kote unapatikana umeme.Umeme unataka kwenda mpaka Mpitimbi, kule vijjini kote.Nilikuwa Wizarani tu hapa kwenye Wizara ya Nishati naMadini. Umeme huu wa Gridi ya Taifa njia ya Makambako,unapita Igawisenga, Wino, Maweso, Mkongotema, yaanimimi ninasema kule ni faraja tu. Mbunge Jenista na Serikalihii, ninajisikia faraja sana kwa Serikali hii ya Chama chaMapinduzi. Kwa hiyo, wakati watu wengine wakisema niaibu mimi ninasema ni faraja kubwa sana, kwa sababu

[MHE. J. J. MHAGAMA]

Page 160: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

160

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

haya maendeleo, hata huo umeme ninaousema unakujakwenye Vijiji vya Jimbo la Peramiho, unaenda hata kwenyevijiji vingi vya Waheshimiwa Wabunge wa Upinzani, waChama Tawala, katika nchi nzima ya Tanzania. Kwa hiyo,ninasema hii ni faraja kwa Serikali hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati nilipoanza Ubunge,watumiaji wa simu katika nchi hii ya Tanzania walikuwawachache sana, lakini leo hii wanafika Wananchi karibumilioni 28. Kwa hiyo, unaona kabisa kwamba yapomaendeleo.

Ninachotaka kusema, ipo haja ya kutazamamambo haya sasa kwa ukubwa wake. Ninaombakumshauri sana Waziri wetu anayesimamia Mipango, kupitiaKiti chako, shida kubwa hapa ipo kwenye rasilimali fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye rasilimali fedhalazima tufanye kazi ya ziada. Tumejenga hivi Vyuo Vikuuvingi lakini, watoto wetu hawana mikopo. MheshimiwaWasira sasa hapo ndiyo tuseme kwamba pana kazi yakufanya. Ninasema hivyo na ninawashukuru sana Wabungewote, kwa umoja wao wananipigia makofi, kwa sababuwanajua mafanikio yanahitaji kupewa changamotonyingine ambazo zitakwenda kutatua haya mafanikio. Kwasababu karibu katika kila mafanikio lazima panakuwa nachangamoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninafikiri sasa tushughulikierasil imali fedha. Tumejenga Vyuo Vikuu, watotowatasomaje, lazima tuwe na fedha za kuwasomesha.Tumesema kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa letu la Tanzania.Hapo sasa Mheshimiwa Wasira kwenye Mipango yakoninategemea wewe na vichwa vyako vya Mipango,mtuondoe kabisa kwenye kuendelea na migogoro ya Sektahii ya Kil imo. Kwa mfano, tunasema uchumi wetuunakwenda mbele lakini hali ya kipato kwa Wananchi badoiko chini. Sasa hapo ndiyo mahali tunapotakiwa kutafutatatizo kubwa ni nini. Hapo lazima tujue; kwa mfano namimi nillikuwa ninafikiri Mheshimiwa Wasira utakapokuwa

[MHE. J. J. MHAGAMA]

Page 161: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

161

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

unajibu hoja yangu, umshirikishe sana Mheshimiwa Waziriwa Kilimo, Chakula na Ushirika, angalau mtuambie kwenyeMpango wa mwaka huu, tulikubaliana kwamba tunaanzakupunguza matumizi ya pembejeo kupitia kwa mawakala,kwa sababu tuligundua mawakala wametuangusha sana.Tukakubaliana tunaunda vikundi, nina mfano mimi wakikundi kimoja kutoka kwenye Kata ya Muukulu kinachoitwaUsenga, kimeshafungua akaunti, kimeishaweka hisa karibushilingi 900,000 na vikundi vingine. Tunavyo vikundi kamamia tatu thelathini na kitu kwenye Jimbo la Peramiho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivyo ndivyomtuambie, rasilimali fedha, Wananchi wale wapate zilepesa kupitia kwenye vikundi tuondokane na mfumo wapembejeo kupitia kwa mawakala. Katika hilo lazima tusemevizuri na mfumo huo utawakomboa sana Wananchi wetuwa Tanzania na hasa wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nikwambie kitu;unajua sisi tunafikiri sana haya mambo ya kilimo kwa kuwana Miradi mikubwa mikubwa, lakini ukiisoma Taarifa ya Haliya Uchumi ya mwaka 2012, unaona kilimo kilisonga mbelekwa sababu ya kupeleka pembejeo, kupeleka mbegu borana kwa sababu ya kutafuta namna na mbinu za kuwasaidiawakulima kuuza mazao yao. Haya ndiyo matatizo yakimsingi ambayo nadhani rasilimali fedha itafutwe; kilimokiwe cha kutumia zana bora za kilimo, mbegu ziende kwawakati, mbolea ipatikane kwa wakati. Hilo likifanyika, sasanitaona kabisa kwamba, yale tuliyoyafanya na ambayoyametupa heshima bado tukiongeza na hayoninayoyasema, tutakuwa tumekwenda mbele zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaweza kufanya nini?Tunachoweza kufanya bado niishauri Serikali ya Chama chaMapinduzi; hivi ni kwa nini inaendelea kupata kigugumizikupunguza misamaha ya kodi kwenye madini? Hapo panamatatizo. Katika Mpango huu namwomba MheshimiwaWaziri atuambie, sasa hivi tunazo rasilimali nyingi katika nchiyetu, tuna tatizo la rasilimali fedha, tunaendelea kutoa

[MHE. J. J. MHAGAMA]

Page 162: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

162

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

misamaha na hasa kwenye eneo la madini; je, hali hiiitaendelea mpaka lini?

Ninaomba hali hiyo iondoke, ikiondoka hiyo tutapatafedha na tukishapata fedha haya mafanikio niliyoyasemaambayo ni faraja kwa Watanzania, jumlisha na hiyo fedhanyingine, tutafika mbali sana. Tutatatua matatizo ya majiambayo tumeshaanza kuyawekea mikakati mizuri;Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe unajua. Tutaendeleakusambaza umeme vijijini ambacho ni kipaumbele kikubwa.Tufanye Miradi ambayo inawagusa Wananchi moja kwamoja na Miradi inayowagusa Wananchi moja kwa moja niya kihuduma zaidi.

Miradi ya kihuduma zaidi ni kama hiyo ya kuwasaidiawapate pembejeo kwa wakati, wapate zana bora zakilimo, wapate masoko kwa ajili ya mazao yao, wapatemaji ya kutosha na wapate umeme mpaka kule vijijini.Tukishafanya hayo, hiyo itakuwa inaendelea kuifanya Serikaliyetu ya Chama cha Mapinduzi, ione kabisa kwambainatekeleza Ilani yake kwa imani iliyopewa na Wananchiwa nchi hii ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa kutengenezavipaumbele, lakini utaratibu wa Bunge hil i kujadil ivipaumbele na Mpango wa Taifa ni kitu chema. Naminiseme, Mheshimiwa Waziri akae na atusikilize vizuri sana,hatutapenda kuona maneno haya ambayo Wabungewamekuwa wakiyashauri, tena maneno ya msingi namaneno ya kwenda kuboresha kabisa Mipango yaMaendeleo katika nchi yetu, yafanyiwe kazi. Wakatimwingine inasikitisha kuona mambo tunayoshauri hayaendikusimamiwa vizuri kiutekelezaji. Kwa hiyo, ninaomba sanahilo lizingatiwe na Serikali iwe makini na ione umuhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasema hivyo kwasababu ipo Miradi ambayo inaweza kutuokoa. KatikaMkoa wa Ruvuma sasa hivi tunayo machimbo ya makaaya mawe kule Ngaka. Makaa mawe yale kama kweliyatafanyiwa kazi ya kutosha, hapa tunaambiwa bado

[MHE. J. J. MHAGAMA]

Page 163: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

163

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kuna majadiliano kati ya TANESCO na Wawekezaji(TANCOM). Tunaomba hayo majadiliano yaishe, utekelezajiuanze, halafu basi tuone matokeo ya haraka. Hayomatokeo ya haraka tuweze kuyaona sasa. Tukiona hayomatokeo ya haraka yatatusaidia. Tuone matokeo yaharaka katika kuwasaidia wakulima, wakiwemo Wakulimawa Jimbo la Peramiho. Tuone matokeo ya haraka kamahaya ya barabara yalivyotokea haraka, tuyaone nakwenye maeneo mengine. Maeneo ya elimu na afya, ndiyosekta za huduma ambazo zitamwondoa Mtanzania kutokakatika janga hili la kuhangaika na umaskini wa kipato nakuweza kujikimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maendeleo ya Ulaya,yalitokana na watekelezaji wa shughuli wadogo wadogona wala siyo viwanda vikubwa vikubwa; vil ikuwa niviwanda vidogo vidogo na wakulima wadogo wadogo.Kwa hiyo, tukiendelea kufikiria sana Miradi mikubwa,tunapoteza muda. Turudi kwa wafanyabiashara wadogo,turudi kwa wakulima wadogo, tukiwafanyia hawa woteMipango mizuri, watatusaidia sana kutuvusha katikamaendeleo kwenye nchi yetu ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nikushukuru kwakunipa nafasi na ninaunga mkono hoja hii na MheshimiwaWaziri atusaidie kuyazingatia hayo. (Makofi)

MWENYEKITI: Ninakushukuru sana. Sasa ninamwitaMheshimiwa Chombo na Mheshimiwa Malocha ajiandae!

MHE. MUHAMMAD AMOUR CHOMBOH: MheshimiwaMwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi jioni hii niwezekuchangia katika hoja iliyopo mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina matatizo na Mpangoau Mipango ambayo Serikali imeleta kwa ajili ya kuijadilihapa. Hii siyo mara ya kwanza na wala haitakuwa maraya mwisho kuleta Mipango mizuri namna hii. Tatizo letuWatanzania ni utekelezaji wa Mipango yetu tunayoipanga.Hii inatokana na kutosimamia vizuri sheria ambazo Bunge

[MHE. J. J. MHAGAMA]

Page 164: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

164

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

hili Tukufu huwa linazipitisha katika utekelezaji wa mambombalimbali ambayo tumepanga kutekeleza nakuyasimamia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa tulilonalokatika utekelezaji wa Mipango yetu ni kwamba, sisi watuna ninafikiri nisiseme sisi watu niseme hivi; unakumbuka Babawa Taifa, Mwalimu Nyerere, alituambia kitu kimoja; alisemaili tuendelee tunahitaji vitu vine; Ardhi, Watu, Siasa Safi naUongozi Bora. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwenyezi Mungu katujaliatuna ardhi nzuri sana na kaipamba kwa kila kitu ambayonchi nyingi sana hawana. Tatizo tulilonalo sasa hivi hasawakati huu ni watu. Sensa il iyopita il ionesha tunaoWatanzania karibu 44,000,000 au 45,000,000, lakini hao nibinadamu, tuna uchache wa watu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchache wetu ni watu.Nikisema mtu au watu siyo Bodi. Utu ni kutofautisha bainaya mnyama, miti na viumbe vingine baina ya binadamu.Utu ni vitendo ambavyo binadamu mwenye umbo labinadamu anavitenda kwa masilahi ya binadamu wenzake,lakini pia kwa nchi yake, siyo kwa ubinafsi wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuna watu na kwa kuwahatuna watu wa kutosha tunao wachache, watu wakutosheleza hasa tukatimiza Mipango yetu hii ni wachachesana, waliokuwepo wameshaondoka na wanaendeleakuondoka, tukitaka kubadilika lazima turudi kwenye utu.Utu ule ambao aliusema Mwalimu Nyerere, kwamba; lazimatupate watu, uumwe na nchi, uumwe na wenzako. Ubinafsiumetuzidi, hatuwezi kuitekeleza Mipango hii. Mifano ipomingi sana; tunazungumza vitu mdomoni tofauti na vitendoambavyo tunatakiwa tuvifanye, hatuna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, kuna Sheriaya Mazingira imepitishwa hapa, anakuja mtu anavunjaSheria kwa makusudi halafu anakimbilia Mahakamani kuzuiaSheria ambayo ilipitishwa na Bunge hili na kusainiwa na

[MHE. M. A. CHOMBOH]

Page 165: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

165

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Rais isitekelezwe. Yeye kwa makusudianaivunja halafu anakwenda kuweka kizingiti Mahakamaniisitekelezwe na Mahakama inachukua hatua; huo ni utukweli? Huo siyo utu ni ubinafsi. Huo ni mfano mdogo sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kitu kingine; kwamfano, juzi kuna mtu mmoja, huyo ni mtu, alitekeleza Sheriaya Usimamizi wa Magari makubwa ambayo yanaharibubarabara zetu, l imekuwa zogo mji mzima, wakatianasimamia sheria ambayo yeye ni msimamizi mkubwa!Kuna mwingine alikwenda kusimamia Sheria kule Bandariniili tupate masilahi ya nchi mambo yaende vizuri, kila mmojaanamwona yule ni mbaya. Tunataka watu kama hawaambao wako committed ndiyo tunaweza kufanikisha kitukama hiki kwa kila sehemu. Lazima tusimamie sheria ambazotumezipanga wenyewe na tutekeleze ndiyo tutavukakatika kutekeleza Mpango huu. Serikali yetu imefika wakatisasa hivi inaajiri watu, inaajiri binadamu, maana wenginesiyo watu ni binadamu, kwa kupata mshahara tu, lakini siyokufanya kazi. Anaajiriwa mtu kwa kukusudia kupatamshahara siyo kufanya kazi.

Kuna vyama ambavyo vinasimamia masilahi yawafanyakazi au haki za wafanyakazi, lakini hakuna Chamaambacho kinasimamia wajibu wa mfanyakazi. Wale wenyevyama vinavyosimamia masilahi ya mfanyakazi ni kweliwana-trace au wanakwenda kufuatilia kwamba hawaninaowatetea haki zao wanatimiza wajibu wao?Wanatetea kweli hilo na kuna haki gani inayopatikana bilawajibu; lakini Tanzania tunakwenda hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeajiri watu auimeajiri binadamu kwa ajili ya kupata mshahara siyo kufanyakazi. Saa nane au saa kumi za kufanya kazi, basi mtuanakwenda kufanya kazi kwa saa tatu au nne tu, mudamwingine wote yuko kwenye shughuli zake; hatuwezikwenda. Nchi zinazoendelea zinafanya kazi zaidi.Tumeumbwa kufanya kazi, hatukuumbwa sisi kuja kustarehetu hapa. (Makofi)

[MHE. M. A. CHOMBOH]

Page 166: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

166

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika saa 24 ujipangiewewe upumzike saa ngapi, lakini muda uliobakia woteunatakiwa ufanye kazi. Sisi tunaamini kwamba, kazi ni ibada.Mimi ni Mwislamu, lakini kazi ni ibada na ninafikiri vitabuvyote vya dini vinasema asiyefanya kazi huyo na asile. Sasajamani ni watu sisi?

Tunakula bure bila kufanya kazi na bila kuwajibika;tukijipima sisi ni watu kweli? Tunataka tujirekebishe, tu-change mind zetu turudi kwenye utu ndiyo tutaweza kufikakwenye lengo ambalo tulisema ili tuendelee tunahitaji ardhina ardhi tunayo na watu tuwepo, tukiwa na watu tutapataSiasa Safi na Uongozi Bora. Lazima tufanye hivyo ndiyotutafika tunakotaka na ndiyo hapo tutakapowezakutekeleza Mipango hii na mingine na mingine.

Inafika hadi sasa hivi watu wanatuambia ni aibuwanasahau angalau kidogo kidogo ndugu yangu palealisema ni aibu, lakini sasa hivi kule Pemba kuna umemempaka chooni, barabara za lami kila kona, hakuna tatizola maji sehemu zote Pemba maji ni safi na salama. Hiyonafikiri siyo aibu isipokuwa alikuwa anasherehesha mambo,ni wajibu kila mmoja ana haki ya kusherehesha. Kwaupande huo ndugu zangu ninachokisema, ili tuwezekufanikiwa mambo haya na kuweza kutekeleza Mpangohuu ni lazima turudi kwenye utu, utu ni vitendo, utu ni imanina utu ni moyo wa kuweza kufanya jambo hili likafanikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haya machache mimisina zaidi. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Malocha!

MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangiakatika Mpango huu wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka2014/2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu imejaaliwamambo mengi sana; imejaaliwa rasilimali nyingi ambazo

[MHE. M. A. CHOMBOH]

Page 167: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

167

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

zinatosha kabisa kutuendeleza, kutusukuma na kutufikishambali katika suala zima la maendeleo. Nchi yetu ina rasilimalina rasilimali namba moja ni ardhi. Ardhi ambayo imeshehenimali nyingi; madini, maji yakiwemo maziwa, mito, mabwawana kadhalika. Imesheheni ardhi nzuri ya kilimo, imeshehenimifugo mingi ambayo wengine wanaanza kuirarua baadaya kukosa maarifa ya kuitumia wanairarua kwa kuipiga risasina pia imesheheni misitu mingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazo kila aina ya rasilimalizinazoweza kutuwezesha kuiendeleza nchi hii na Watanzaniatukaishi maisha bora kwa kila Mtanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shida tuliyonayo katika nchihii ni ukosefu wa wasimamizi wazuri, ambao wamekosauadilifu, wamekosa uwajibikaji, wamekosa uzalendo nawamekosa ubunifu. Hata kama nchi ingekuwa na rasilimalikiasi gani, kama baadhi ya wasimamizi wake siyo waadilifu,siyo wachapakazi, siyo wabunifu na siyo wazalendo ni bure.Kwa hiyo, namba moja katika jambo lolote lile ni uadilifu,uwajibikaji, uzalendo na ubunifu na ndiyo maana utakutaWizara ambazo zina watu wa namna hiyo ndiyozinaonekana zinaipa sifa nchi hii.

Mimi nashangaa Wizara ambazo hazitaki kuigamifano ya Wizara ambazo zinasemwa kila kona kwa mazuri;maana yake hiyo ni dalili ya kushindwa kazi na wanapaswakujiuliza kwa nini Wizara fulani inasemwa kila mahali; je, miminiliyepewa mamlaka kwa nini nisioneshe uwezo wangu?Mambo hayo yanapaswa kujiuliza kwa mtu yeyotealiyepewa dhamana; nafasi hii nil iyopewa watuwanasemaje juu yangu? Ukiwa na mawazo haya utafanyakazi kwa uadilifu mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu karibu asilimiakubwa ya Watanzania wanategemea kilimo, lakini miminataka kuzungumzia wakulima wadogowadogo. Wakulimawadogowadogo kwa sehemu kubwa ndiyo wanaolibebaTaifa hili katika kulilisha japokuwa nchi haijawatazama.Wakulima wadogowadogo ndiyo wanaoibeba nchi hii

[MHE. I. A. MALOCHA]

Page 168: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

168

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

katika kuilisha pamoja na mitaji yao midogo na kutumianguvukazi yao.

Ninachotaka kuzungumza na ambacho Serikaliinapaswa kuliangalia ni kwamba, wapo wakulimawadogowadogo ambao wanakosa mahali pa kulima,hawana kabisa sehemu ya kulima na nchi yetu tunatakiwakufanya utafiti kuangalia ni Watanzania wangapi ambaowanategemea kilimo hawana ardhi ya kulima wakati tukiwana ardhi ambayo imekaa na mapori, imemilikiwa na watuambao hawaiendelezi wamekaa nayo tu sanasanawanafanya kazi katika kuikodisha badala ya kuendelezakile walichokusudia. Kwa hiyo, jambo hili tunapaswakuliangalia kwa umakini sana vinginevyo litafutikishapabaya.

Tunashuhudia migogoro ya wakulima na wafugaji,wakulima na wawekezaji na kadhalika. Jambo hili Serikaliinapaswa kulitafutia majibu ya haraka kwa sababu kwahivi sasa kila kona unakuta kuna migogoro kati ya wakulimana wafugaji na wakulima na wawekezaji. Sasa nani atatuemigogoro hiyo kama siyo Mawaziri waliopewa dhamanaya kusimamia mambo hayo?

Utakuta kila kona ni matatizo ya ardhi na migogoroya ardhi kati ya wafugaji na wakulima na wawekezaji, nimigogoro na maeneo mengine yanaleta mauaji makubwa.Lazima Serikali iangalie ni namna gani inaweza kutatuamatatizo hayo; bila kufanya hivyo tutashuhudia migogoromikubwa sana huko tunakokwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami ninataka kutoa mfanommoja; jambo la kusikitisha ni kwamba, hata pale ambapoRais anatoa maagizo kwa Waziri kwamba nataka tatizohili lishughulikiwe haraka, Waziri hashituki! Sasa watuwasipomheshimu Rais nani ataheshimiwa katika nchi hii?Rais akitoa agizo maana yake ni agizo la kuvalia njuga,watu wote mliopewa dhamana mnapaswa kulishughulikia.

[MHE. I. A. MALOCHA]

Page 169: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

169

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kutoa mfano;mwezi wa sita, Mheshimiwa Rais alitoa agizo namna yaWaziri kushughulikia mgogoro wa Shamba la Malonje naakasema kwa namna yoyote ile lazima ardhi ile irudishwekwa Wananchi! Nami sheria inaniruhusu kama msimamizi waardhi, kama kuna tatizo lolote naomba Waziri aniletee,akiniletea saa moja basi saa tatu nitakuwa nimetatua. Chaajabu mpaka sasa hivi suala hili halina majibu walahalishughulikiwi, pamoja na jitihada za Mkoa kukumbushamara kwa mara. Kwa hiyo, mnachotaka kuona, Serikaliinataka kushughulikia mauaji huko baadaye, maanammezowea kuendesha kwa dharura za kuvamia matatizo.

Matatizo yanapoibuka ndiyo Serikali inaonekanakupeleka utatuzi, jambo ambalo siyo jema. Naishauri Serikalijambo hili lishughulikiwe haraka; vinginevyo, hali ninayoionainaweza ikatuletea matatizo huko mbele. Naomba Wazirimwenye dhamana, arudie agizo la Mheshimiwa Raiskushughulikia jambo hili haraka. Mimi naliona ni la hatarina ninazungumza ili Wananchi wasikie kwamba, wajibuwangu nimeutimiza, sasa kama tatizo linatokea ni suala laSerikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuzungumzia Miradiya Umwagiliaji. Sisi sote tumekubali kwamba, ili nchi hii iwezekuleta tija katika suala la kilimo ni lazima tuboreshe Miradiya Umwagiliaji. Kilimo cha umwagiliaji ni kilimo cha uhakika,lakini inashangaza toka mwaka 2005 ipo Miradi ambayoimeanza lakini mpaka sasa haijakamilika. Kama kuna Miradimitano au minne unakuta hata mmoja ulioanzahaujakamilika. Sasa tunakwenda wapi?

Nataka tujiulize kama tunaona uwezo wetu nimdogo kwa nini tuna-prolong Miradi mingi ambayotunashindwa kuitekeleza halafu baadaye tunaaza kupimwakwa Mipango ambayo tuliisema sisi wenyewe halafuutekelezaji wake umekwama? Kwa hiyo, lazima turuditujisahihishe tuhakikishe Miradi ile tuliyoipanga tunaisimamiabarabara.

[MHE. I. A. MALOCHA]

Page 170: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

170

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe mfano; katikaJimbo langu tuna Miradi kama mine; Mradi wa Sakalilo,Maleza, Ng’ongo na Zia, lakini hakuna hata Mradi mmojaambao umekamilika, hata ule ulioanza Sakalilo mwaka 2006mpaka sasa hivi haujakamilika; tunategemea nini? Mipangohii tunayoipanga mbona naona kama tunairudia ileiletuliyoipanga utekelezaji wake haujakamilika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha zinapotolewanusunusu ni lini Miradi hiyo itamalizika? Na hata ikimalizikabasi itamalizika kwa kiwango ambacho siyo kizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nizungumzie sualala miundombinu ya barabara. Kwanza, naishukuru Serikalikwa kazi nzuri na kubwa ambayo imejitahidi kuunganishaMikoa katika suala la barabara za lami mipakani. Nitoerai, yapo maeneo ambayo yanahitaji kuwa na barabaranzuri ili kuweza kuharakisha kukuza uchumi. Zipo kandambalimbali ambazo zinatakiwa Serikali iangalie kuboreshabarabara katika Kanda zile na hasa Kanda za Maziwa.Kanda za Maziwa zinabeba idadi kubwa sana ya watu;watu wanatoka mikoa mbalimbali wanakimbilia maeneoyale kwa sababu ya uvuvi, rutuba nzuri na maeneo mazuriya kushughulika na Miradi mbalimbali. Kwa hiyo, Kandakama hizo inatakiwa Serikali iboreshe barabara zake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe mfano; ipobarabara ya kutoka Kilimetundu – Muze – Stalike – Kibaonimpaka Mpanda, Ukanda ule wa Ziwa Rukwa rasilimali yakeni kubwa sana kwa upande wa ardhi, ni ardhi nzuri na yenyerutuba nyingi, hakuna zao linalokataa na yanakomaa kwaharaka. Vilevile ni eneo ambalo lina mito mingi sanaambayo ingeweza kutumika katika suala zima la umwagiliaji,ina mito zaidi ya 40 ambayo haikauki. Serikali inapaswakuangalia njia ya kuwekeza katika kuitumia ile mito ili kuwezakukuza uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ninalotakakulizungumzia ni umeme. Umeme ni ajira na ni uchumi.Tunapozungumzia suala la uchumi, kwanza, niipongeze

[MHE. I. A. MALOCHA]

Page 171: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

171

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Serikali kwamba imeanza vizuri katika suala hili, lakini lazimatuangalie ni maeneo gani ambayo tunapaswa kuwahishaumeme kulingana na utayari wa Wananchi katika kuutumiaumeme ili kuweza kukuza uchumi na kusaidia maeneomengine. Maeneo mengine unapeleka umeme lakiniWananchi hawako tayari wanauangalia tu na wanaangalianguzo. Yapo maeneo ambayo Wananchi wako tayari nawalishajiandaa kupokea umeme katika suala zima lakuendeleza uchumi wao. Kwa mfano, nawezakuuzungumzia Mkoa wa Rukwa; Wananchi wa Mkoa waRukwa ni wachapakazi, wanazalisha kwa kiasi kikubwasana na wanasaidia nchi hii katika suala la kilimo, lakiniumeme umeishia mjini tu, vijijini hakuna. Mpango wakupeleka umeme vijijini naona kama unasuasua, unaanzakuelekezwa maeneo ambayo ukiangalia hayana tija hataya uzalishaji. Hakuna kitu utakacho-gain kwa muda mfupiili kuleta maendeleo katika suala zima la uchumi. Kwa hiyo,pamoja na kupeleka umeme ni lazima tuangalie maeneoambayo yanaweza kutoa majibu ya haraka katika kukuzauchumi na siyo suala tu la kupeleka, maana umeme nigharama, tunategemea ukienda kwenye maeneo uwezekuleta impact ya uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nami ningewezakuishauri Serikali kuwa, kwa Mkoa wa Rukwa harakishenikupeleka umeme vijijini kwani Wananchi wanahitaji umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,nashukuru sana na ninaunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Sasa namwita Mheshimiwa Mbowe,ajiandae Mheshimiwa Vullu, tutamalizia na MheshimiwaMurtaza Mangungu.

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuwa mmojawapoya wachangiaji wa mwisho kwa jioni ya leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikisikiliza mazungumzo yaWaheshimiwa Wabunge, kinachogombaniwa hapa ni

[MHE. I. A. MALOCHA]

Page 172: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

172

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

namna ya ugawaji wa Keki ya Taifa. Cha msingi zaidi nikwamba, hii Keki ya Taifa kama hakuna uzalishaji wakutosha, kugawa kwake kunakuwa ni matatizo siku zote.Hilo la kwanza.

La pili, Mpango huu haujaweka mkakati wowotewa namna ya kupunguza matumizi makubwa ya Serikali.Hata tukirumbana na tukapanga Mipango mizuri, kamakile cha kugawa kwenye Mipango ya Maendeleotumeshakitumia katika uendeshaji wa Serikali, ni dhahiritutaendelea kurumbana kila siku na haitatusaidia sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Mpangowa Miaka Mitano, ratio ya matumizi ya kawaida ya Serikalina matumizi ya maendeleo, ilikuwa imekusudiwa iwe asilimia65 kwa 35. Kwa mtazamo wetu nafikiri ingeweza ikabanwavilevile zaidi ikawa ratio ya matumizi ya kawaida ya Serikaliikawa asil imia 60 na asil imia 40 ikapelekwa kwenyemaendeleo. Tungeweza kufanya hivyo kwa kujibana katikamatumizi ya Serikali, tungekuwa tuna resources nyingi zakupeleka kwenye shughuli za maendeleo. Nina hakikamarumbano na ugomvi unaoelekea kujitokeza mahali hapausingekuwa na sababu yoyote ya kuwepo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi ya Serikaliyameendelea kuwa makubwa sana. Ukiangalia historia,kwa miaka 15 iliyopita, mimi niliingia Bunge hili kwa mara yakwanza kabisa mwaka 2000; mwaka 2000 GovernmentBudget ilikuta shilingi trilioni 1.6, lakini leo tunakimbilia trilioni30. Tunazidi kupanua wigo na ukubwa wa Serikali,tunapanua Wilaya, Mikoa, Kata na Vijiji. Pamoja na nianjema ya kupeleka utawala karibu na Wananchi, lakinimaana yake ni kwamba, tunaongeza ukubwa wa matumizikatika masuala ya administration na tunapunguza funguambalo lingeweza kwenda kwenye maendeleo yakuwasaidia Wananchi moja kwa moja. Kwa hiyo, napendakuzungumza kwamba, kuna umuhimu sana wa kuliangaliahili.

[MHE. F. A. MBOWE]

Page 173: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

173

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia mtazamo wamuda mrefu na mitazamo ya kiuchumi, lazima tuangalietunagawaje hii Keki ya Taifa, tunatawala vipi rasilimali zaTaifa hili. Bado tunaendelea kupanga kila kitu Dar esSalaam, kila kitu kinapangwa na Baraza la Mawaziri Dar esSalaam, ndiyo wenye maamuzi makubwa ya mwisho.Watanzania wote sasa hivi wanaiangalia Dar es Salaam,wanamwangalia Mheshimiwa Rais, wanamwangalia WaziriMkuu na wanaiangalia Serikali kuomba.

Hebu tufikirie tunapokwenda kuandika Katibampya, umuhimu wa sisi kama Taifa kufikiria upya suala ladecentralization. Tuna uwezo mkubwa sana kama Taifaku-manage resources zetu kama tutaacha utaratibu wakutegemea centre moja ndiyo ikae na kapu lenye mayaiyote ya Taifa hili. Tufikirie upya mfumo wa utawala wauchumi wetu ili kuwasaidia Watanzania kuwa beggarskatika nchi yao. Hilo lilikuwa jambo la kwanza ambalonimeona nilizungumze siku ya leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalonapenda kulizungumza, nimeangalia Mpango waMaendeleo wa mwaka huu ambao tunakwenda nao sasa;yamefanyika mambo mengi, lakini nisikitike tu kusemakwamba, nimejaribu kuangalia kuna Mpango gani waMaendeleo mkubwa ambao umefanyika katika Mkoawangu wa Kilimanjaro, kwa bahati mbaya sikuuona.

Kuna jambo moja ambalo ninapenda nilizungumze;nimezungumza kwenye bajeti ya mwaka jana,nimezungumza kwenye bajeti ya mwaka juzi na ninaonabado haijaingia kwenye akili ya wenzetu, pengine naombahili mlitafakari kwa kina sana. Hili liko vipi?

Mlima Kilimanjaro ni chanzo kikubwa sana chamapato ya utalii na mapato ya Taifa letu. Mlima Kilimanjarounaliingizia Taifa hili mapato ya zaidi ya Dola za Marekanimilioni 50 kila mwaka na dhahiri unatoa ajira kwa watuwengine wengi sana. Kwa hiyo, kunakuwa na multiplier

[MHE. F. A. MBOWE]

Page 174: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

174

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

effect kubwa sana kwa upande wa utalii katika NorthernCircuit.

Nikiangalia Serikali inauangaliaje Mlima huu,inautunzaje na mazingira yanayouzunguka, ile KilimanjaroEcosystem yote inaendelezwa vipi i l i kuhakikishaunaendelea kuwa na barafu ambayo itaendeleakuwavutia wawekezaji na kuwavutia watalii kwendakuupanda. Ni kama vile tunachuma kwenye MlimaKilimanjaro, hatujali mazingira ya Kilimanjaro, hatujali thelujiya Kil imanjaro, ni kama tunataka kumchinja bataanayetaga mayai ya dhahabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mpango wetu waTaifa kwa mwaka ujao ninaomba sana wanaohusikawakaangalie uwezekano wa kufikiria kuhusu kitukinachoitwa Kilimanjaro Ecosystem. Nimelizungumza hilimwaka jana, nimelizungumza na Waziri wa Utalii, tumeundana Kamati ambayo haikufanya lolote mpaka leo; matokeoyake theluji inazidi kupotea, mazingira yanazidi kukauka namaji yanapotea Kilimanjaro.

Ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge, majiyanayoteremka katika Mlima Kilimanjaro yako katikaManagement ya Pangani Water Basin. Sasa hivitunashuhudia vita kati ya wakulima na wafugaji, katikamiaka michache iyajo tutakuwa na vita ya maji. KatikaMikoa ya Kanda ya Kaskazini na kipekee Mkoa waKilimanjaro, Arusha na Manyara, tunakwenda kuwa na vitaya maji kwa watu walioko milimani (upstream) na watuwalioko mabondeni (downstream).

Leo tunapozungumza watu waliopo upstreamhawaruhusiwi kutumia maji kwa sababu maji yaleyanatakiwa yaende downstream yakawasaidie watuwanaoishi downstream na watu hawa hawana kilimo kwasababu hakuna ardhi, watu hawa hawana mining kwasababu hakuna madini, watu hawa hawana uvuvi kwasababu hakuna mahali pa kuvua na hawana mifugo kwasababu hakuna ardhi ya kufugia.

[MHE. F. A. MBOWE]

Page 175: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

175

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Sasa, kama hatukufanya utaratibu maalum wawater management katika mabonde kama ya Pangani,Arusha na Meru Basins, tunakwenda kusababisha vituambavyo ninahisi vitakuwa na hatari sana kwa Wananchi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze jambo lingine;ni kwamba, maeneo haya ninayoyazungumza yana udongoambao ni mzuri mno, kuna infrastructure ambayoingeendelezwa kidogo ingeweza kuwa eneo zuri sana lauzalishaji na kutengeneza kilimo ambacho ni high yield, yaanikilimo ambacho kinazalisha mazao yenye bei kubwa kwaajili ya kuuza kwenye masoko ya nchi za nje.

Tuna Kilimanjaro International Airport, Uwanjaambao haujatumika effectively kusafirisha horticulture, kwasababu hakuna maji ya kuwezesha kufanya horticultureKilimanjaro na Arusha. Ninachoomba kifanyike; iwepomikakati ya makusudi ya kuvuna maji ya mvua ili kutoaugomvi wa maji na kuvuna maji ya mvua; ni infrastructurerahisi sana wala hatuhitaji rocket science. Sijui ni kwa sababugani wakati wa masika maji yanakimbilia baharini, tunaliamafuriko, kikija kiangazi tunaomba chakula.

Serikali inaweza kujenga miundombinu rahisi sanakatika mabonde ya Mlima Kilimanjaro. Imezungumzwa maranyingi, kuna mabonde makubwa mno, ni kujenga dykes tuupstream halafu tunafanya gravity irrigation. Tunawezatukanywesha chini Wananchi wale wakazalisha mwakamzima bila kungojea mahindi ya msaada au misaadamingine yoyote. Hii ni Economic Management, naombawatu wa Planning walisikie suala hili na waone watasaidiavipi kwa sababu Zone ya Kilimanjaro, Arusha, Manyarampaka Tanga, ina uwezo mkubwa sana wa kufanyaproduction kwa sababu ya export na KilimanjaroInternational Airport tunayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambaloningependa kulizungumza na hili ninaomba WaheshimiwaWabunge mnielewe vizuri sana, ni kauli zetu wanasiasa. Ni

[MHE. F. A. MBOWE]

Page 176: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

176

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

jambo la kusikitisha sana kwamba, tunataka kuua kituambacho tumekilea wenyewe, tumekijenga wenyewe,kimefikia hatua tunataka kukiachia kidondoke bila sababuza msingi kwa sababu ya kauli. Siyo tabia nzuri zakidiplomasia kubeza nchi za wenzetu, whether ni nchi ndogoama ni nchi kubwa. Impact ya kuvunjika kwa AfrikaMashariki itaathiri Uchumi wa Tanzania kuanzia Mwanza,Mara, Kilimanjaro, Manyara, Arusha na maeneo menginembalimbali. Tunahitaji kutafuta suluhu na majirani zetu,hatuhitaji kutafuta ugomvi na majirani zetu, wala hatunasababu ya kubeza. Tanzania tuna heshima, tuna mazoeaya kuwa wanadiplomasia. Huu utamaduni wa kuanzakuwadharau na kuwadhalilisha wenzetu tunaupata wapi?Siyo utamaduni wa Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoomba, hili jambolifikiriwe kwa makini sana, tunahitaji kutafakari mahusianoyetu badala ya kuyaangamiza.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mbowe,muda wako umeisha.

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Sasa namwita Mheshimiwa ZaynabVullu, tutamalizia na Mheshimiwa Murtaza Mangungu!

MHE. ZAYNAB M. VULLU: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi nami nichangie Mpangohuu wa Maendeleo. Kabla sijaanza kuchangia,nimpongeze kaka yangu Mheshimiwa Mbowe, kwa kauliyake aliyoibaini kwamba, kauli zetu wanasiasa zakudharauliana na kubezana si za kujenga. Hilo kwa kwelinampongeza ameliona na nishauri tu kwamba, tusione kwanchi za jirani, tuanze kuona kwetu wenyewe Watanzania ilituweze kujenga nchi yenye amani na upendo. (Makofi)

[MHE. F. A. MBOWE]

Page 177: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

177

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naomba sasa nijikite katika hoja ya msingi iliyotuweka humundani. Niipongeze Serikali kwa kufanya kazi zake kamailivyokuwa imepanga, kwa kuhakikisha maendeleoyanawafikia Wananchi. Hakuna Mbunge yeyote humundani atakayesema kwenye Jimbo lake au Wilaya yakehakuna maendeleo ambayo yamefika. Hatuwezi kuijenganchi nzima kwa siku moja, tunajenga kwa awamu. Sotetumeona barabara, maji, umeme na tumetangaziwa humundani, majimbo karibu vijiji vyote kama siyo robo au roboya tatu ya vijiji umeme utakwenda. Siyo mtu atoke hapaajidai kwamba, yeye ndiye amepeleka umeme, umeme huuumeletwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,haukuletwa na Mbunge, aseme mimi nimeenda kuletaumeme. Kwa hiyo, hili ni letu wote kwa ujumla na ni lakujivunia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waswahili wana msemowao wanasema kwamba: “Ili jambo liwe zuri, lazima kuwena mabaya au kuwe na upungufu ambao unahitajikuboreshwa.” Naomba yafuatayo; kwanza, kuna mgogorowa wakulima na wafugaji. Tunazungumzia hali ya uchumiimeongezeka, lakini Wananchi wa kule vijijini sidhani kamahili wanalijua kwamba, hali ya uchumi imeongezeka kwasababu mkulima analia na mazao yake, mfugaji analia nang’ombe wake. Watu hawa tuliambiwa hapa na Serikalikwamba, tutapeleka maendeleo pale hawa ng’ombewanapopelekwa kwenye Halmashauri zetu, lakini hadi hiileo Halmashauri zetu hazijawezeshwa hata senti tano;tunategemea nini?

Tunategemea wafugaji wale watatengenezewavipi miundombinu? Sote tunafahamu jinsi gani Halmashaurizetu hazina kipato cha kutosha, hiyo miradi ya kawaida tumingine inasuasua, sasa sikwambii wameongezewa najukumu la kuandaa mahali pa kuweka mifugo. Ombi langukwa Serikali; nimeona Mpango, Mheshimiwa Waziriatakapokuja kujibu hoja atueleze Serikali ina mkakati ganiwa kuziwezesha Halmashauri i l i ziweze kujipangakutengeneza miundombinu, malambo, majosho na maeneo

[MHE. Z. M. VULLU]

Page 178: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

178

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ambayo watalishia wale ng’ombe badala ya kuwafanyawafugaji wadhalil ike na mifugo yao, halikadhalikawanawadhalil isha wakulima kwa sababu mkulimaanategemea mazao yake na mfugaji anategemeang’ombe wake, sasa watu hawa wanapigana.

Naomba nijibiwe, mwisho wa siku watu hawawatakuwa na kipato chochote? Mfugaji mwisho wa sikuatakuwa hawezi kuuza ng’ombe kwani ng’ombe wakewatakuwa wamepigwa na yeye mwenyewe kapigwa.Halikadhalika, mkulima mwisho wa siku mazao yakeyameliwa na yeye mwenyewe amepigwa. TunaombaSerikali itusaidie kutatua hii migogoro kwa kuziwezeshaHalmashauri zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mifugo na mgogorowa wakulima linaweza likaharibu hata miundombinu ya maji.Sasa hivi Mto Rufiji tumepewa kivuko kule Utete, lakinihakifanyi kazi kwa sababu maji yamekauka. Mto Rufiji haunaasili ya kukauka, lakini sasa hivi Mto huu umekuwa wa msimuna tatizo kubwa ni wafugaji. Wakulima wakiona wafugajiwamewavamia wanahama kutoka eneo moja kwendalingine. Wafugaji wakiona majani yameisha pale na hawanamaji ya kunywesha mifugo yao, wanakwenda kule ambakowenzao wapo. Sasa hii migogoro mingine, Serikali iwekemikakati ya kuhakikisha haitakuwepo tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo nyuma hatukusikiamfugaji yeyote akilalamika wala ng’ombe wakidhalilika, kwasababu wale nao ni viumbe, lakini bahati mbaya hawawezikusema. Tumeshuhudia kwenye maeneo yetu wanapigana,zile Kamati zetu za Usalama za Wilaya na Mikoa zinaishiwanguvu kwa sababu hazina nyenzo, ziwezeshwe il ilinapotokea tatizo waende; lakini unakuta askari wana garilakini petroli hakuna au gari lipo lakini matairi matatu nimazima, moja ni bovu, wanakokwenda mitandao haifanyikazi, hawana radio call; tunawasaidia nini hapo wakulimana wafanyakazi? Ningeomba sana hilo nalo tuliangalie.(Makofi)

[MHE. Z. M. VULLU]

Page 179: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

179

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema maendeleo,maendeleo yanaletwa na maji na umeme. Nitoe kilio chaWanakisarawe, Kisarawe hatuna viwanda, tumebahatikakupata kiwanda kimoja cha Saruji lakini nacho kinashindwakufanya kazi. Naiomba Wizara ya Nishati na Madini naWizara ya Maliasili na Utalii, wakae pamoja na watusaidielile eneo la Pugu mpaka Kazimzumbwi, wamekataa nguzoza umeme zisipite. Tunaomba Wizara hizi mbili zikaezijadiliane, wapitishe nguzo za umeme ili na Wanakisarawewaweze kupata umeme, kiwanda kile kifanye kazi namaeneo mengine yaweze kupata umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hapo tu, na maeneomengine ya Wilaya za Mkoa wa Pwani. TunapozungumziaMkoa wa Pwani ni lazima utaje Wilaya zote kwa masilahiya Wilaya. Naomba hilo Wizara ilifuatilie ili tuweze kuonatunasaidiana vipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,nitoe nafasi kwa wengine, lakini naomba mwisho wa sikunipate majibu. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru. Sasa MheshimiwaMangungu!

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii na miminiweze kuchangia kwenye hoja iliyo mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwakustajabu kidogo. Nimestaajabu sana baadhi yawachangiaji hapa wamekuwa wakilaumu, kushutumu nakuweka wimbo wa kusema kwamba ni aibu, lakini mtuyeyote mwenye fikra na akili timamu, kufagia unaanziauliposimama. Wenzetu hawa ambao wamekuwawakilalamika sana, wameshindwa hata kujenga kulenyumbani, maghorofa yanamiminwa Kariakoo na maeneomengine ya Ilala. Sasa hili ni jambo ambalo inabidi ujiulizesana, mkataa kwao ni mtumwa. (Makofi/Kicheko)

[MHE. Z. M. VULLU]

Page 180: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

180

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

WABUNGE FULANI: Aibu!

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: MheshimiwaMwenyekiti, lakini wapo wengine ambao wamekuwawakisomesha watoto nje ya nchi kutokana na fursa namiundombinu iliyowekwa na Serikali hii inayowatia wao aibu,lakini katika kuudanganya umma, wanakuja hapa kusemani aibu. Sasa inabidi tujiulize! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchangiaji wa Wabungeniliamini sana tusimame pia katika jambo linalohusu ukweli,kwa sababu sisi ni watu ambao tumepewa dhamana katikanchi hii na tunao wajibu wa kuwawakilisha waliotuchagua.Wakati wa uchangiaji, yuko Mbunge mmoja ambayealisema mpaka leo TPDC inaingia mikataba bila kuangaliana hakuna masilahi yoyote ambayo Watanzaniawanayapata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mjumbe kwenyeKamati ya Nishati na Madini, na ni mtu ambayeninamwamini sana Mungu, siwezi nikakubali niingie ndaniya Bunge hili nikatamka kitu ambacho hakina ukweli.Ukiangalia Sheria ya Uchimbaji na Utafutaji Mafuta na Gesiya mwaka 1980 ambayo inafanya kazi hadi sasa, mapatona mgawanyo kutokana na ile Production SharingAgreement (PSA), Serikali kupitia TPDC inapata asilimia katiya 65 hadi 75. Sasa leo hii tunaposema TPDC ipate japoasilimia 40; mbona tunapata zaidi ya hapo? Huweziukamulika tochi unakotokea, lazima umulike unakoelekeaili uweze kupata mwanga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba MheshimiwaWaziri wa Mipango na Mawaziri wengine wote, lazimatukubaline; haiwezekani ikawa mimi ndiye ninaumwa homahalafu akatibiwa mtu mwingine il i nipone mimi. Hilohaliwezekani na ni jambo ambalo halina mantiki na haliingiiakilini.

Tumekuwa na malalamiko katika Mipango yetuambayo tunaiandaa. Wabunge wengi wamechangia

Page 181: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

181

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

hapa kwamba, fedha nyingi zinapelekwa katika maeneoya mijini, maeneo ya vijijini ambapo sisi wengine tunatokahakuna fedha zinazopelekwa kutekeleza Miradi.

Tunasema kwamba, uchumi unakua kwa asilimiasaba, ukisoma aya ya 1.2 ya kitabu hiki inasema, uchumiumekuwa ukikua kwa asil imia saba lakini Wananchihawanufaiki kwa sababu uchumi huu umejengwa katikamaeneo machache. Hatujakuza kil imo, Wananchiwanazalisha mazao hayafiki sokoni yanaharibika. Wananchiwanazalisha, lakini umeme wa kuweza kuzalisha kuongezathamani ya mazao haya hakuna. Leo hii mpaka vijijini watuwanaishi kwa kutegemea kwenda dukani. Mapatoyanatokana na nini? Kila siku asubuhi atoe fedha akanunuesukari, unga, mchele, hali ya kuwa ardhi na maeneo yakuweza kuzalisha mazao haya yote tunayo lakini badohatujafikia kuweza kuboresha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona katika Mipangoambayo imeandaliwa na Serikali, lakini niseme tu kwamba,hatuwezi kufanikiwa haya yote kama kuna urasimu. Leo hiiWizara na Wizara zinaweza zikawasiliana kwa muda wamiaka mitatu barua hazijajibiwa. Tumekaa hapa tunajadilivyanzo vipya vya mapato ya Serikali, bandari hatuitumii.Leo hii kuna ugonjwa ambao ni lazima upatiwe dawa naufumbuzi wa kudumu, mitandao. Ukienda Halmashauriunaambiwa mtandao haufanyi kazi watu hawawezi kulipwafedha EPICAR imekwama. Ukienda TRA unaambiwa leomtandao uko down hatuwezi ku-process, mizigo ya watuinakwama bandarini. Bandari vilevile wanakwambiamtandao haufanyi kazi; sasa huyu mtandao ni nani?

Leo hii mnakuja hapa mnatuambia Mipango yamaendeleo Serikali iongeze mapato; unaongeza vipimapato bila kuwa na efficiency kwenye utekelezaji wako?Haya hayawezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, limekuwa tatizo kubwasana kukosa consistence kwenye Mipango ya Serikali. Tunachuma na makaa ya mawe Liganga, tuna Nickel ambayo

[MHE. M. A. MANGUNGU]

Page 182: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

182

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

imeshafanyiwa utafiti na imegundulika Nachingwea,Ruangwa na maeneo ya Nakiu kule Kilwa, tunaisafirishajekuifikisha Bandarini? Bandari ya Mtwara unaambiwamipango inaendelea, itafanyika itakuja pale; chuma kiletunakisafirishaje? Kitasafirishwa na barabara? Mipango yareli haipo, aah! Hili tuliangalie kwa makini, lazima Mipangoyetu iwiane na utekelezaji na mahitajio halisi kwa wakatitulio nao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma ukurasa wa 54 ileaya ya 3.3.4 imesema, Misitu na Wanyamapori. Hawawanyama kwa tafsiri niliyo nayo mimi sasa hivi wanayo hakiya kuishi kuliko binadamu. Wananchi wa maeneo ya Njinjo,Miguruwe, Kandawale, Mitole, Miteja, Nanjil inji nakwingineko Kilwa, wanapigwa bila sababu, bila kufikishwamahakamani, hukumu zinatolewa na Wananchi haowamekosa haki ya kuishi; hil i ni tatizo kubwa sana.Nashukuru nimezungumza na Mheshimiwa Waziri, amenipamajibu ambayo yanawiana na kulipatia ufumbuzi wakudumu, lakini hili ni tatizo kubwa na lazima tuliangalie. Hizioperesheni zisitumike kwa ajili ya kunyanyasa na kuwatesaWananchi wasiokuwa na hatia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa kutokanana muda ni madeni ya ndani. Kila mwaka tunapanga bajetikwa ajili ya kulipa madeni ya ndani, wafanyabiashara hawawanakopa kwenye benki kwa mikopo ambayo ina riba yahali ya juu kabisa. Wakishakopa Serikali baada ya kupewahuduma inachukua muda mrefu, watu wengine wana zaidiya miaka minane, tisa, hawajalipwa, nyumba zinauzwa, malizao zinanadiwa bila sababu.

(Hapa kengele ililia kushiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mangungu, nakushukuru,kaa chini. (Kicheko)

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)

[MHE. M. A. MANGUNGU]

Page 183: 31 OKTOBA, 2013 MREMA 1.pmd

183

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, Bungelinarejea.

(Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naahirishaBunge mpaka kesho Saa Tatu Asubuhi. (Kicheko)

(Saa 1. 35 jioni Bunge liliahirishwa hadi Siku ya Ijumaa,Tarehe 1 Novemba, 2013 Saa Tatu Asubuhi)