280

Click here to load reader

3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

  • Upload
    lamthuan

  • View
    1.615

  • Download
    270

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

1

3 MEI, 2013

BUNGE LA TANZANIA_____________

MAJADILIANO YA BUNGE________________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Kumi na Saba – Tarehe 3 Mei, 2013

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati Zifuatayo Ziliwasilishwa Mezani na:-

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:

Randama ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzina Jeshi la Kujenga Taifa, kwa mwaka wa Fedha 2013/2014.

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA:

Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwaMwaka wa Fedha 2013/2014.

Page 2: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

2

3 MEI, 2013

MHE. GOSBERT B. BLANDES (K.n.y. MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA, SHERIA NAUTAWALA):

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala, Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu yaWizara ya Katiba na Sheria, kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2013/2014.

MHE. TUNDU A. M. LISSU - MSEMAJI MKUU WA KAMBIYA UPINZANI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA:

Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni wa Wizara ya Katiba na Sheria Kuhusu Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha2013/2014.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunapowasilishaMezani lazima vitu vile viwepo. Hapa nina kitabu cha Hotubaya Waziri wa Katiba na Sheria, kitabu cha Kamati ya Katiba,Sheria na Utawala, lakini ya kwenu Upinzani haipo. Iko wapi?Zilizowasilishwa hizi hapa, ya kwenu iko wapi?

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Spika, hili nijambo geni kidogo. Sijawahi kuona katika Bunge lako Tukufuukitoa matamshi kama haya. Naomba nilieleze Bunge lakoTukufu kwamba, kama Kanuni zinavyosema, maoni ya KambiRasmi ya Upinzani Bungeni yatawasilishwa kwenye Bunge lakona Wabunge watapata nakala zao kama ilivyo kawaida sikuzote.

SPIKA: Si mnasema tufuate Kanuni, ninachokisema nikwamba mnaponiwasilishia mezani zipo hizi, sasa hizo zenuziko wapi? Siyo kwamba ni kitu kigeni, nauliza iko wapi? Kanuniya 99(5). Sasa nyie mnang’aka, mimi nauliza iko wapi? Kwaninihamjibu? Iko wapi?

Page 3: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3

3 MEI, 2013

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Spika, hotubayetu inapelekwa kwenye Idara ya Uchapaji sasa hivi, shidaiko wapi?

SPIKA: Sasa hivi haipo! Kwa hiyo, naomba ku- withdrawile, haijawasilishwa. (Makofi)

Tunaendelea, Katibu.

MASWALI NA MAJIBU

Na. 135

Ujenzi wa Barabara za Lami Kawe

MHE. EUGEN E. MWAIPOSA (K.n.y. MHE. RITA L. MLAKI)aliuliza:-

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kujengabarabara kwa kiwango cha lami katika Jimbo la Kawehususan barabara za Mikocheni, Mbezi Beach na Tegetaambako kuna mali za thamani kubwa.

(b) Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga nakupanua barabara ya Old Bagamoyo kutoka makutano yabarabara ya Kawawa hadi round about ya Kawe ambakohutokea mafuriko eneo la Mayfair na kuna msongamanomkubwa wa magari.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu,naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rita Louise Mlaki, Mbungewa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Page 4: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

4

3 MEI, 2013

(a) Mheshimiwa Spika, barabara za Mikocheni,Mbezi Beach na Tegeta zipo katika Jimbo la Uchaguzi laKawe. Katika mwaka wa fedha 2012/2013 Halmashauri yaManispaa ya Kinondoni inaendelea kujenga barabara zalami ikiwa ni pamoja na barabara ya Journalism iliyopoMikocheni yenye urefu wa kilomita 1.1 pamoja na daraja laMto Feza kwa gharama ya shilingi milioni 840. Vilevile ujenziwa barabara ya Tegeta Soko la Nyuki iliyopo Tegeta yenyeurefu wa kilomita 1.0 kwa kiwango cha lami kwa gharamaya shilingi milioni 512.7.

Aidha, daraja la Ndumbwi lililoko Mbezi Beach nalolinajengwa ili kupunguza foleni katika eneo hilo ambalolinagharimu kiasi cha shilingi milioni 325.9. Pamoja na kazi hizo,Serikali imetenga shilingi milioni 700.0 katika mwaka 2012/2013kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya ITV hadi kwa Wariobayenye urefu wa kilomita 1.6 kwa kiwango cha lami.Mkandarasi ameishapatikana na ujenzi utaanza Mei, 2013.

Mheshimiwa Spika, sambamba na mipango hiyo,Serikali imeandaa mpango muda mrefu wa kujengabarabara za Jiji la Dar es Salaam unaojulikana kama Dar esSalaam Metropolitan Development Project ambaoutahusisha pia ujenzi wa barabara za Jimbo la Kawe ikiwemobarabara ya TANESCO – Msasani – Msasani Soko la Samakiyenye urefu wa kilomita 1.5. jumla ya kilomita 25.25 zitajengwakupitia mpango huu katika Halmashauri ya Manispaa yaKinondoni.

(b) Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala waBarabara (TANROADS) iliajiri kampuni ya NORPLAN (T) Ltd.,kufanya usanifu wa barabara ya Old Bagamoyo (MwaiKibaki Road) yenye urefu wa kilomita 5.3 na barabara yaGarden yenye urefu wa kilomita 1.2 kwa ajili ya kupanuliwakwa kiwango cha njia mbili ili kupunguza msongamano wamagari katika barabara hiyo.

Hata hivyo, kabla ya kuanza upanuzi wa barabarahiyo, Serikali imepanga kuanza na ujenzi wa mfereji wa majiambao utapeleka maji ya mvua baharini ili kuepuka mafuriko

Page 5: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

5

3 MEI, 2013

ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara katika eneola Mayfair hadi TMJ. Katika Bajeti ya mwaka 2012/2013zimetengwa jumla ya shilingi bilioni 6.0 kwa ajili ya kazi hiyo.Serikali inaendelea na tathmini ya malipo ya fidia kwa wakaziwa eneo hilo ambao nyumba zao zitaathiriwa na zoezi hili.

Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilika kwa ujenziwa mfereji huo, Serikali itaweka katika mpango kuhusuupanuzi wa barabara hiyo kuwa njia mbili ili kuondoamsongamano wa magari uliopo. (Makofi)

MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa nafasi hii. Naomba sasa niulize maswali mawiliya nyongeza.

(a) Kwa kuwa, tayari Serikali ina mpango wakupanua barabara ya Old Bagamoyo na kwa kuwa tayarikuna mpango pia wa kujenga mifereji ambao utawezeshamaji kuelekea baharini ili kuweza kuepusha mafuriko pamojana msongamano wa magari.

Je, Serikali iko tayari sasa kuwaambia wananchi waKawe ni lini zoezi hilo litaanza?

(b) Kwa kuwa, asilimia kubwa sana ya barabaraza Jiji la Dar es Salaam ni za changarawe na kwa kuwa Serikalikwa kipindi kirefu imekuwa inatumia fedha nyingi sanakukarabati barabara hizi mara kwa mara zikiwemo za jimbola Ukonga ambazo asilimia 98 ni za changarawe?

Je, Serikali iko tayari sasa kuanza mpango wa kujengabarabara za lami katika jiji la Dar er Salaam ili kuepushagharama nyingi pamoja na changamoto wanazozipatawananchi kwa barabara hizi kuwa mbovu mara kwa mara?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwa niabaya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu maswali mawiliya nyongeza ya Mheshimiwa Eugine Mwaiposa, kamaifuatavyo.

Page 6: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

6

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, kwanza hil i analolisemaMheshimiwa Mwaiposa la kuweka mkondo wa kutolea majikwa maana ya drainage system ndiyo tatizo la msingi lililokokatika eneo lile.

Ujenzi mwingi umefanyika pale, jana nilikuwanazungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa eneo li le,nikamwambia nataka pia kujua ni nini kilichotokea mpakawatu wamejijengea kiasi hicho. Hili ni tatizo ambalo tunalonchi nzima. Maji yakiishajaa pale basi ndiyo unaona kelelezinakuwa nyingi hapo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nilitaka niseme kwambahii kazi itafanyika. Lini itaanza, nimesema hapa kwamba, kunahawa wenzetu wa NORPLAN halafu kuna feasibility studyambayo inafanyika sasa hivi. Barabara haijengwi tu hivi hivi,ni lazima uwe na watu ambao wanakwenda pale kucheki ilikujua kinachohitajika, mahitaji yaliyoko pale na nini.

Kwa hiyo, nilitaka nimhakikishie Mheshimiwa MbungeMwaiposa kwamba, kazi hii tunapozungumza sasa hiviinaendelea kwa sababu ni kero kubwa sana. Hili tatizolinalotokea Dar es Salaam sasa hivi limesababishwa na hilijambo ambalo anali- address Mheshimiwa Mbunge.

Sasa kuhusu barabara za chanagarawe ni kwelikabisa kwamba, ukijenga barabara za changarawe, keshoasubuhi mvua inaweza ikanyesha ukakuta imesomba yoteikaenda. Sasa tunachofanya hapa ni kwamba, hii Dar esSalaam Metropolitan Development Project ambayotumeweka pale inakwenda pia Manispaa ya Ilala, hiyo planiko kule.

Hizi ni fedha ambazo mnaona tunajenga mijimbalimbali kama Arusha, Dodoma hapa, kule Kigoma,tukaitengea Dar es Salaam utaratibu wake kwa sababuilionekana inakomba fedha zote zile, ndiyo maana tukawekahuu mpango. Huo mpango tunao, sasa ni suala la kipaumbelekwamba, wanapopelekewa fedha wao wapange nakusema hizi fedha ziende katika eneo gani.

Page 7: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

7

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie MheshimiwaMwaiposa kwamba tuko tayari kukaa nae tumsaidie kwasababu mpango huu tayari upo huko.

MHE. ZARINA Z. MADABIDA: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kuniona.

Manispaa ya Dar es Salaam hususan wilaya yaKinondoni imebadilisha barabara zake nyingi sana ambazozilikuwa za changarawe na kuzifanya lami nyepesi. Lakini kwasababu ya huu msongamano malori makubwa yanayotokamikoani yanapita na kuziharibu hizi barabara katika kipindikifupi sana.

Je, Waziri anasemaje, yuko tayari tukitoka hapatwende Dar es Salaam tukapite kwenye zile barabara naatwambie atatusaidiaje kuzirudisha hizi barabara zetuambazo tumezijenga kwa kiwango cha changarawe nakuharibika haraka sana?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwa niabaya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la nyongezala Mheshimiwa Zarina Madabida kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, nilipata shida kidogo alipoanzaalisema lami nyepesi baadaye alipomalizia akasemabarabara za changarawe, lakini nahani pia…

MHE. ZARINA Z. MADABIDA: Mheshimiwa Spika, ni laminyepesi.

SPIKA: Unasema pale unapoitwa, siyo unasema tuunavyotaka.

Page 8: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

8

3 MEI, 2013

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, sawa.

Ni kweli kwamba tunachofanya sasa hivi, kwanzakabisa hizo lami nyepesi ukipitisha haya malori makubwa,mizigo haibebwi na malori. Ukienda nchi hizi kubwa kubwakama Marekani, Uingereza, mizigo inabebwa kwa treni. Ndiyomaana atakapokuja Waziri anayehusika na eneo hili lausafirishaji, mtaona mpango wake mkubwa pale nikuimarisha njia ya treni. Ukiishaona mizigo inabebwa na trenibasi umeondokana na tatizo la msingi katika maeneo haya.

Hata hivyo, kwa vile bado tunatumia barabara hapa,ni kweli kabisa kama anavyosema Mheshimiwa Madabidakama barabara zetu zitaendelea kutumika hivyo na magarimakubwa yanapita, maana yake ni kwamba tatizo hililitaendelea kuwepo.

Mheshimiwa Spika, sisi tunashirikiana na TANROADS,tunaweka mizani barabarani ili kupima mizigo ili kujua ina uzitokiasi gani. Sasa yeye ametaka tufuatane twende Dar esSalaam. Waziri wangu yuko hapa anasikia wala hana tatizo,mimi nitaondoka akihitaji tutakwenda kule tukaziangalie hizobarabara.

Lakini kubwa ambalo tunalifanya sasa hivi katikabarabara hizi zote zinazozungumzwa hapa ni pamoja nakuhakikisha kwamba, tunazielekeza katika ile Dar es SalaamRapid Transport. Ndiko tunakokimbilia ili watu wetu wawezeku-access kuingia katika hii barabara ambayo sasawatakuwa wanakwenda kwa haraka.

Mheshimiwa Spika, tuko tayari kufuatana naye.

SPIKA: Namwona Mheshimiwa Halima anasimamamara elfu kumi. Haya swali la nyongeza Mheshimiwa Halima.

Page 9: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

9

3 MEI, 2013

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, nashukuru.Kwanza Mheshimiwa Madabida awe anakuja kwenye vikaovya halmashauri, hayo mambo huwa haji, halafu anaulizahapa.

SPIKA: Aah, uliza swali, hizo habari. Naomba uondoemaneno yako ya mwanzo.

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, sawasawa.

Wakati Naibu Waziri anajibu swali amezungumziasuala la mfereji wa six billion. Vilevile ikumbukwe Serikaliinagharamia six billion kwa sababu iliuza maeneo ambayoyalikuwa mkondo wa maji kwa wale Warabu. Swali langu nihivi, eneo ambalo linaathirika sana ambalo haliko katika huumpango wa six billion ni barabara ya Mandazi (MandaziRoad) ambayo inaunganisha Old Bagamoyo Road naKimweri.

Hii ni barabara muhimu sana kwa watu ambaowanakaa bonde la Mpunga. Sasa nilitaka Serikali iniambiekwa sababu tokea mwezi wa Pili Manispaa ya Kinondoniimeandika barua kwa TAMISEMI kuwaomba hii barabaraiingizwe katika huu mpango wa Dar es Salaam MetropolitanProject, mpaka sasa hakuna jibu. Nilitaka Serikali iniambie inamkakati gani kuhusiana na barabara muhimu sana yaMandazi Road ambayo kwa miaka mitatu mfululizokumekuwa kuna ahadi ambazo hazitekelezeki. Kwa hiyo,nataka nipate jibu makini kutoka kwenye Serikali.

SPIKA: Swali la nyongeza, kama ungekuwa makiniungeleta. Haya naomba Waziri ujibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwa niabaya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali lanyongeza la Mheshimiwa Halima Mdee.

Page 10: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

10

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, barabara ambazo ziko katikamradi huu zil ichaguliwa na Halmashauri husika. Sisitulichofanya tuliwapa menu tu, wao wenyewe ndiyowalichagua. Sasa baada ya kuwa wamepanga, haiwezekanitena wakawa wanachomekea chomekea njiani. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Tunaendelea na swali linalofuata.Mheshimiwa Aliko Kibona anapaswa kuuliza swali hilo. Kwaniaba yake Mheshimiwa Mchungaji Mwanjale.

Na. 136

Posho kwa Wenyeviti wa Vijiji

MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE (K.n.y. MHE. ALIKON. KIBONA) aliuliza :-

Kwa muda mrefu Serikali iliishaahidi kuangaliauwezekano wa kuwalipa posho Wenyeviti wa Vijiji kutokanana kazi kubwa wanayofanya ya kusimamia shughuli zamaendeleo ya Taifa:-

Je, viongozi hao wataanza kulipwa lini posho hiyomuhimu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa WaziriMkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Aliko NikusumaKibona, Mbunge wa Ileje, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kazi kubwazinazofanywa na Wenyeviti wa Viji j i na Mitaa katikakusimamia shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao.Majukumu hayo yameongezeka kutokana na utekelezaji wa

Page 11: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

11

3 MEI, 2013

Sera ya Ugatuaji wa Madaraka kwa Wananchi ambapoSerikali inapeleka raslimali fedha, vifaa na raslimali watu kwawingi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Uamuzi huu wa Serikali umesaidia kuwapa fursawananchi kujiwekea vipaumbele vya utekelezaji wa miradiya maendeleo kwa kuzingatia fursa na vikwazo vilivyopo.

Mheshimiwa Spika, kwa mantiki hii, viongozi wa ngaziza msingi za Serikali za Mitaa wanayo majukumu mengiambayo ni kuhamasisha ushiriki wa wananchi katikauchangiaji wa mirad ya maendeleo na kusimamiautekelezaji wa miradi hiyo kupitia Kamati za Maendeleo zaVijiji.

Kwa kutambua hilo Serikali kupitia kila Halmashauriimeweka utaratibu wa kuwalipa posho Wenyeviti wa vijiji namitaa kutokana na vyanzo vya mapato ya ndani ambavyoni asilimia 20. Mgawanyo wa fedha hizi ni kwamba asilimia3 hutumika kwa ajili ya maendeleo na asilimia 17 hutumikakwa ajili ya utawala ikiwemo kulipa posho hizi za Wenyevitiwa Viji j i. Hata hivyo, viwango ambavyo hulipwavinatofautiana kati ya Halmashauri moja na nyinginekulingana na makusanyo ya mapato ya ndani katika vyanzovilivyopo.

Mheshimiwa Spika, changamoto kubwa inayoikabiliSerikali, ni ufinyu wa Bajeti pamoja na makusanyo kidogokatika Halmashauri. Aidha, mkazo umekuwa ukitolewa kwaHalmashauri zote chini kuhakikisha kuwa asilimia 20 hiyo yamapato ya ndani ya Halmashauri zinapelekwa katika vijiji,kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kubunivyanzo vipya vya mapato.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kulipa posho hiyo,Serikal imeweka utaratibu wa kuwajengea uwezo Wenyevitiwa vijiji na Mitaa ambapo kila Halmashauri hutenga nakuidhinishiwa fedha za kujenga uwezo katika Bajeti ya kilamwaka.

Page 12: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

12

3 MEI, 2013

Kati ya fedha hizo, asilimia 40 hupelekwa katika ngaziya kijiji/mtaa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ofisi na mafunzokwa viongozi hao. Lengo ni kuwajengea uwezo wa kusimamiamajukumu yao kwa ufanisi. Napenda kutumia fursa hiikuzielekeza Halmashauri zote kuhakikisha fedha ambazo niasilimia 20 ya mapato ya ndani ya Halmashauri zinapelekwakatika vijiji ili sehemu ya fedha hizo zitumike kulipa posho yaviongozi hao lakini pia kuhakikisha asilimia 40 ya fedha zakujenga uwezo zinazotengwa kila mwaka zinapelekwakatika ngazi ya Kata na Vijiji/Mtaa ili kuwajengea uwezoviongozi hao kupitia katika Chuo cha Serikali za Mitaa chaHombolo. (Makofi)

MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE: MheshimiwaSpika, asilimia 20 ya pesa ambazo zinapelekwa katika vijijihazibainishwi wazi kwamba zinalipa posho za Wenyevitiisipokuwa mikutano ndiyo inaendeshwa.

La kwanza, Sasa naiuliza Serikali ni lini itabainishawazi kwamba labda asilimia 10 au 15 itakuwa ni posho kwaajili ya Wenyeviti?

La pili, kwa kuwa, Wenyeviti ndiyo vinara kabisa wamaendeleo vijijini ni lini Serikali sasa itatoa fedha kwa ajili yaWenyeviti kutoka katika Serikali Kuu na siyo Serikali za Mitaa?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika,hili ainisho nililolitoa hapa ni ainisho linalotokana na ushuruambao ungekusanywa kule katika Halmashauri.

Kuna kitu kinaitwa nuisance taxes yaani tax ambayoinaleta kero vitumbua, samaki wa kukaanga, mandazi,mchicha mchicha, vile vitu vinavyopita wanasema hayadagaa, haya dagaa tena, haya dagaa, wanasema dagaa.

Page 13: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

13

3 MEI, 2013

Hiyo Serikali ikafuta, Serikali ilipofuta ikasema hivi sisitutaleta kitu kinachoitwa fidia na ndiyo maana Bunge lakohapa kujibu swali la pili, ikaja na kitu kinachoitwa generalpurpose grant na katika hii Bajeti tunayokwenda nayo bilioni63 zikatengwa.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Manjale alikuwepohapa na sisi wote tulikuwepo hapa ikarudishwa tena ilikuwabilioni 10 ikarudishwa ikaja bilioni 63. Kwa hiyo msuli wa SerikaliKuu unauona pale. Tunachosema hapa tunatoa maagizokwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Kwa hiyo ni kwelianavyosema Mchungaji hapa wapo watu wenginewanakusanya pale kwenye Halmashauri zinakaa pale.

Waheshimiwa Wabunge kama mnaijua Halmashauriambayo haipeleki hii posho kwa Wenyeviti wa vijiji naVitongoji tuleteni majina yao, tuleteni sisi hapa halafu sisitushuke nao jumla jumla hizi fedha zinatengwa. (Makofi/Kicheko)

SPIKA: Naona tuendelee sasa. Wizara ya Maliasili naUtalii, Mheshimiwa Betty Machangu. Watu mpaka wameuzadagaa. Naibu Waziri mpaka ameuza dagaa hapa.

Na. 137

Ulinzi wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro

MHE. BETTY E. MACHANGU aliuliza:-

Miti iliyoko katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro nimirefu zaidi ya mita 30 na kufanya doria zinazofanywaKINAPA kubaini uharibifu wa vyanzo vya maji na wakataomiti kuelekea kugonga mwamba:-

(a) Katika mazingira ya miti mirefu kiasi hicho kwa ninidoria za Helikopta zisitumike ili kuleta ufanisi wa kuwakamatawaharibifu wa hifadhi hiyo?

Page 14: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

14

3 MEI, 2013

(b) Kwa sababu Jeshi la Wananchi wa Tanzania hufanyamazoezi ya kijeshi/kivita mara kwa mara kwenye maeneombalimbali nchini, na ili kuleta ufanisi katika kulinda hifadhizetu za Taifa nchini. Je, ni kwa nini Serikali l isiliagize Jeshikufanya mazoezi yao ya kawaida katika maeneo ya hifadhinchini ili liweze kupambana na kuwakamata waharibifu wahifadhi zetu?

(c) Kwa kutumia “water gauges” ni rahisi kufahamu kiasicha mtiririko wa maji kutoka vyanzo vya maji hasa katikavyanzo vya mito itokayo mlimani, kwamba “rate of flow”ikipungua ni dhahiri vyanzo vya maji vimeharibiwa hivyodoria itiliwe mkazo. Je, Serikali inatumia “water gauges”katika vyanzo vya mito inayoanzia Msitu wa Hifadhi yaKilimanjaro ili kudhibiti kwa ufanisi uharibifu wa vyanzo vyahivyo?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziriwa Maliasili na Utalii, naomba kujibu swali la MheshimiwaBetty Eliezer Machangu, Mbunge wa Viti Maalum, lenyesehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Doria za anga kwa kutumia helikopta hufanyikakatika maeneo ya Mlima Kilimanjaro katika kipindi ambachohali ya hewa inaruhusu. Mafanikio ya doria kama hizi siyomakubwa kutokana na msitu mnene uliofunga kuzungukaMlima Kilimanjaro na miteremko, makorongo na mito, nahivyo kusababisha ugumu wa kuwaona wahalifu wa chini.Hali ambayo husababisha helikopta kushindwa kutua katikasehemu nyingi za msitu.

Mheshimiwa Spika, doria nyingi zinazofanyika katikaMlima Kilimanjaro ni zile za miguu ambapo magarihuwapeleka askari jirani na maeneo tarajiwa ya doria. Hiiimekuwa na ufanisi na mafanikio makubwa na imesaidiasana kudhibiti uhalifu katika hifadhi.

Page 15: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

15

3 MEI, 2013

Pamoja na doria za miguu na magari, Shirika la Hifadhiza Taifa litaendelea kutumia helikopta katika kudhibiti uhalifukwenye maeneo ya wazi katika hifadhi ya Mlima Kilimanjarona kwenye Hifadhi zingine nchini.

(b) Serikali haina mpango wa kuliagiza Jeshi la WananchiTanzania kufanya mazoezi yao ya kawaida katika maeneoya Hifadhi nchini kwa sababu zifuatazo:-

(i) Mafunzo wanayofanya ni ya utumiaji wasilaha za kivita;

(ii) Mazoezi ya kijeshi kwa kawaida hayafanyikikatika maeneo ya Hifadhi za wanyamapori; na

(iii) Mazoezi haya yakifanyika hifadhini yataathiriutalii.

Aidha, Serikali itaendelea kushirikiana na wadauwengine katika kukomesha ujangili.

(c) Shirika la Hifadhi za Taifa lina Idara ya ikolojiaambayo pamoja na mambo mengine hufuatilia nakukusanya takwimu za hali ya hewa na kupima ubora wawingi wa maji katika hifadhi ili kushauri na kupendekeza njiaza kitaalum za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mheshimiwa Spika, Hifadhi ya Kilimanjaro imekuwaikishirikiana na wataalam wa Bonde la Pangani kupimawingi wa ubora wa maji katika maeneo kumi na tano (15)yaliyopo ndani ya Hifadhi kwa kutumia vifaa vya kisasa kamavile Advanced Stream Flow Meter na Multi-parameterExpech water Quality Meter wakati wa kiangazi na masikana kushauri hatua za kuchukua. (Makofi)

MHE. BETTY E. MACHANGU: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa majibu ya Naibu Waziri, naomba kuulizamaswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu utaratibu wa kutumiaPolisi katika check points katika hifadhi zetu na hususani

Page 16: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

16

3 MEI, 2013

Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro hazijazaa matunda kwa sababuya uchache wa Polisi. Je, Serikali ipo tayari sasa kutumiawanafunzi wa Chuo cha Polisi yaani CCP angalau kwenyemazoezi yao yaani field attachment ili kunusuru tatizo hili?

La pili, ili kuendeleza utalii, utafiti na uhai wa ndegena wanyama katika hifadhi zetu kuna haja ya kutunza nakila mara kurejesha bionwai yaani bio- diversity iliyopo.

Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kugawiawananchi wa vijiji jirani na hifadhi zetu miti yote ya asili iliwapande kwenye maeneo yao na hivyo kuwaondoa tamaakuingia msituni kukataa miti, lakini hasa hasa kurudishabionwai katika yale maeneo ambayo yameharibika sana?

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri naomba ujibu kwakifupi.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, moja, tunamshukuru sana Mheshimiwa Betty kwakuendelea kuwa na Serikali katika jitihada zake za kuhakikishakwamba Mlima Kilimanjaro na integrity yake inaendeleakulindwa. Na nimjibu tu kwamba Serikali inalishukuru sanaJeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wizara yetu katika kuendeleakulinda maliasili na katika kuendelea kudhibiti wahalifuambao wanatusumbua nchi nzima.

Katika kuwatumia na kushirikiana na Jeshi la Polisilitakuwa ni Jeshi la Polisi lenyewe kuamua kuwatumiawanafunzi wake kama vile ambavyo sisi tunawatumiawanafunzi wa Mweka katika mazoezi mbalimbaliyanayoendelea na kufundisha kazi.

Mheshimiwa Spika, la pili, tunaendelea na kufanyaufatifi kwanza, TAWIRI kama Shirika letu muhimu katika utafitiwa wanyamapori, lakini vilevile utafiti ambao unafanywakwa kusimamiwa na Taasisi yetu ya Misitu TSF natunamhakikishia Mheshimiwa Betty Machangu na wananchi

Page 17: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

17

3 MEI, 2013

wa Kilimanjaro na wananchi wote wanaozunguka MlimaKilimanjaro tutaendelea kupanda miti, tutaendelea kutoamiche ya miti tukishirikiana na Halmashauri zinazozungukaMlima Kilimanjaro.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Spika, Misituwa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro unavunwa na wahalifuwakishirikiana na baadhi ya viongozi pamoja na wafanyakaziwa TANAPA na taarifa hii tulipewa katika RCC na Mkuu waMkoa katika utafiti ambao Taasisi moja isiyo ya Kiserikaliilifanya na kuikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa.

Mheshimiwa Spika, naiuliza Serikali lini tutaachakufanya siasa katika mambo mazito kama haya nakuchukulia hatua wahalifu ambao wanaharibu maliasili zetu?(Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba ujibu kwakifupi pia uzizungumze sana.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, Serikali inaendelea kupambana na wahalifu wa ainayoyote na endapo atagundulika mhalifu yoyote ambaye nimtumishi katika hifadhi zetu za Taifa hatutasita kabisakumchukulia hatua na wahifadhi wa Mlima Kilimanjarowanaendelea sana kushirikiana na Halmashauri ya Wilayaya Rombo na mimi mwenyewe nilifika na kuzungumza naMadiwani wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Tulizungumza na Mheshimiwa Selasini na katika tatizolao moja lililojitokeza la tembo kutoka Kenya kuvamia, kuuana kuathiri mazao na wananchi wa Rombo Serikali ilifanyauamuzi haraka tuka-de-employ kikosi ambacho kimeendeleakuzuia na wana technique za kuweza kuwazuia tembo nakuwafukuza badala ya kulazimika kuwaua. Nafikiri ushirikianohuo tunahitaji na sisi tutazingatia alichokisema MheshimiwaSelasini. (Makofi)

Page 18: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

18

3 MEI, 2013

Na. 138

Kuendeleza Kitalu cha Kigosi North

MHE. AUGUSTINO M. MASELE aliuliza:-

Kitalu cha Kigosi North kwenye Pori la Akiba Kigosikwa muda mrefu kimeachwa bila mwekezaji wakukiendeleza hivyo kutoa mwanya kwa ujangili na uharibifuwa mazingira:-

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kukiendelezakitalu hicho ili kiweze kufikia kiwango cha kuweza kuvutiawawekezaji?

(b) Huduma za utalii ni pamoja na kuwepo kwahuduma za hoteli za kitalii.

Je, Serikali itatoa kipaumbele cha mwekezaji wahoteli kwenye pori hilo la Kigosi North?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziriwa Maliasili na Utalii, naomba kujibu swali la MheshimiwaAugustino Manyanda Masele, Mbunge wa Mbogwe, lenyesehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inatambuakwamba kitalu cha Kigosi North hakijapata mwekezaji.Hata hivyo, ili kuimarisha ulinzi wa wanyamapori katika kitaluhicho, Serikali ilianzisha kituo cha Lwahika ambapo askariwasiopungua watano wafanya doria za kudhibiti ujangili nauharibifu wa mzingira katika eneo hilo.

Page 19: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

19

3 MEI, 2013

(a) Mheshimiwa Spika, Wizara imeendeleakuimarisha ulinzi wa eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuidadiwanyamapori ili kutambua mwenendo, aina na idadi yaokatika eneo hilo. Aidha, miundombinu ya eneo hiloimeendelea kuimarishwa ili kitalu hicho kiweze kufikiakiwango cha kuwavutia mwekezaji.

(b) Wizara inahamasisha wadau wa utaliikuwekeza katika ujenzi wa Loji na Hoteli katika maeneo yahifadhi na mapori ya akiba na ikiwemo Pori la Akiba laKigosi.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakininina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Kwanza, Sheria Namba 5 ya Hifadhi ya Wanyamaporikifungu 23 kinazuia utafiti wa madini mengine yoyoteisipokuwa madini ya Urani, mafuta na gesi.

Je, utafiti unaofanywa wa madini ya dhahabu katikakitalu hicho unafanyika kwa sheria namba ngapi? (Makofi)

La pili, kwa kuwa, shughuli zinazofanyika katika kitaluhiki hazifahamiki vyema na Madiwani wa Halmashauri yaBukombe na Mbogwe.

Je, Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari kufanyaziara katika Wilaya yetu ya Bukombe na Mbogwe ili kufafanuajambo hili?

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba ujibu wakifupi sana muda unakwenda.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, naomba nikubaliane na Mheshimiwa Maselle kwanzanitafanya ziara hiyo mapema iwezekanavyo baada yashughuli hizi za Bunge hili la Bajeti.

Page 20: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

20

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, swali lake la mwisho ambalolilikuwa kwanza ni kweli kitalu hicho ni eneo ambalolinafanyiwa utafiti na Kampuni ya Tanzania AmericanInternational Corporation 2000 Limited tangu tarehe26 Septemba, 2005 na Kampuni hii inazo leseni tatu za utafitiambazo ningeweza kumpa baadaye.

Lakini niseme tu kwamba kuna sheria ambayoimepitishwa na Bunge lako Tukufu kuruhusu utafiti wa ainakadhaa ya madini ikiwemo hiyo ambayo wanafanyaKampuni hii katika maeneo haya ya hifadhi za mapori yaakiba.

MHE. JAMES D. LEMBELI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Kwa kuwa, pori hili la Akiba la Kigosi Muyowosikwa upande wa Mashariki l inapakana na Wilaya zaBukombe, Mbogwe na Kahama na kwa kuwa, eneo hililimekuwa ni kichakaa cha majambazi na majangili. Ni liniSerikali sasa inafikiria kuipandisha hadhi eneo hili la Masharikikuwa Hifadhi ya Taifa ili liweze kuleta tija kwa Taifa badalaya lilivyo hivi sasa? Ahsante sana.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, ni kweli tuna changamoto kubwa sana ya ujangili namatukio mbalimbali katika maeneo haya aliyoyataja ikiwani pamoja na hili pori Kigosi ikiwa ni pamoja na wahamiajiharamu ambao wamekuwa wakitoka nchi za jirani nakujificha hapo. Serikali inalitambua hilo na juhudi za makusudimoja zinafanywa kuendelea kuhakikisha kwamba pori hililinadhibitiwa dhidi ya majangili.

Lakini la pili, utaratibu ambao tunautumia ili kupandahadhi pori kuwa sehemu ya Hifadhi za Taifa TANAPAunazingatia mambo mengi ya kisayansi na sisi tupo tayarikuendelea kufanya utafiti huo na endapo maeneo hayayatakidhi mahitaji au masharti ambayo yanakubaliwa nasheria ya Hifadhi za Taifa hatutasita kufanya hivyo.

Page 21: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

21

3 MEI, 2013

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Pamoja na nia nzuri ya Serikali ya kugawa vitalubaada ya marekebisho ya Sheria Namba 5 ya Mwaka 2009.Nil itaka kujua kwa kuwa, vitalu vingi vil ivyogawiwahavizingatia uhifadhi yaani ikoloji na inaleta usumbufu sanahasa kwa wanyama na usumbufu kwa baadhi ya wawindaji.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuangalia upya ilivitalu hivyo vizingatie uhifadhi.

SPIKA:Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba ujibu kwakifupi.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, ni kweli kuna maelezo mengi tofauti ambapotunaendelea kuyapata kutoka wadau ikiwa ni pamoja nahoja hii aliyoisema Mheshimiwa Mchungaji Msigwa kwambabaadhi ya vitalu ilikuwa ni kitalu kimoja vikagawiwa vikawavitalu vitatu, na kwa mantiki hiyo kama kitalu kilikuwa kimojana kinaruhusiwa kuvuna wanyama 30 kikigawiwa vikawavitalu vitatu kwa maana hiyo utavuna wanyama 90.

Ni suala ambalo Mheshimiwa Waziri analotunaendelea kuliangalia na hatutasita kabisa kuchukuahatua ambazo ni za makusudi kuweza kurekebisha dosariambazo zinaweza kujitokeza kutokana na ushauri ambaotunaupata na majadiliano ambayo yanaendelea katikaWizara na sehemu zingine.

Na. 139

Kuchimba Mabwawa ya Maji Nanyumbu

MHE. DUSTAN D. MKAPA aliuliza:-

Vijiji vingi vya Wilaya ya Nanyumbu havina maji safina salama:-

Page 22: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

22

3 MEI, 2013

Je, Serikali haioni kuwa ipo haja ya kuchimbamabwawa ili kuondoa tatizo hilo hasa katika maeneoyaliyoathirika zaidi katika Kata za Sengenya, Chipuputa,Mnanje, Likokona, Mikangaula na Nandete?

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziriwa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dustan DanielMkapa, Mbunge wa Nanyumbu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ili kuboresha huduma ya majikatika Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, Serikali imeanzautekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kuchimba visima virefuvyenye mtandao wa mabomba, kuvuna maji ya mvua kwakuchimba mabwawa na kuweka mifumo ya uvunaji wa majiya mvua kwenye mapaa ya nyumba.

Kupitia programu ya Sekta ya Maji, mwaka huu wa2012/2013, Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu imepangakutekeleza miradi ya maji katika vijiji vya Ndwika Kata yaMangaka, Nandembo Kata ya Lumesule, Chivirikiti Kata yaNandete, Holola Kata ya Mnanje na Chipuputa Kata yaChipuputa. Ujenzi wa mradi kwenye kijiji cha Ndwika umeanzana vijiji vya Nandembo, Chivirikiti, Chipuputa na Holola vikokatika hatua mbalimbali za manunuzi.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2013/2014, Serikali itajenga bwawa kubwa na kulaza mtandao wamabomba katika Kata ya Sengenya litakalohudumia vijiji viwili(2) vya Sengenya na Mara kwa gharama ya shilingi bilioni 1.

Serikali pia inaendelea na uhamasishaji wa uvunajiwa maji ya mvua kwa kutumia mapaa ya nyumba. Kwa sasa,Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu inaendelea kujengamifumo ya uvunaji maji ya mvua katika nyumba za watumishina jengo la Halmashauri ya Wilaya ili wananchi waweze kuigateknolojia hiyo.

Page 23: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

23

3 MEI, 2013

MHE. DUSTAN D. MKAPA: Mheshimiwa Spika, kwakuwa swali la msingi niliomba kujengewa mabwawa ya maji.Nashukuru kupata hilo moja katika Kata ya Sengenya.

Kwa kuwa hivi juzi Wizara ya Maji imeongezewa shilingibilioni 185. Je, inaweza kunihakikishia kujengewa mabwawaangalau mawili katika Wilaya yangu ya Nanyumbu?

Swali la pili, Serikali itayatumiaje maji ya mto Ruvumakuwasaidia wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu kupata majisafi na salama?

SPIKA: Ahsante kwa kuuliza maswali kwa kifupi naMheshimiwa Naibu Waziri na wewe ujibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kuhusukuongezewa fedha katika Wilaya ya Nanyumbu kutokanana ongezeko ambalo tumepata juzi nataka kumhakikishiakwamba kama alivyotamka Mheshimiwa Waziri kwamba kilaHalmashauri itapata vijiji viwili hii inamaanisha kwamba naNanyumbu itakuwepo na tutawashirikisha wao sasa wawezekuainisha ni mradi gani uweze kutekelezwa katika hivyo vijijiviwili.

Mheshimiwa Spika, kuhusu matumizi ya mto Ruvumanaweza nikasema kwamba ni wazo zuri na namshukuru, lakinikwa sasa vyanzo vilivyopo vinatosha kabisa kuwezakuwapatia maji wananchi wa Nanyumbu. Lakini vilevile tujuekwamba hii rasilimali ya maji ya Ruvuma ni rasilimali yakutumia sisi leo, kesho na baadaye.

Kwa hiyo itakapofikia muda wake tutaweza kufanyautafiti na kuona kama tutatumie yale maji ya mto Ruvuma.

SPIKA: Mheshimiwa Kilufi swali la nyongeza, sasausiende kuuliza swali la Mbarali, lazima liwe swali la kiserakwako.

Page 24: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

24

3 MEI, 2013

MHE. MODESTUS D. KILUFI: Mheshimiwa Spika,nashukuru sana kwa kunipa nafasi. Tatizo la wananchi waNanyumbu halitofautiani sana na tatizo la wananchi waMbarali.

Mheshimiwa Spika, mradi wa maji kutoka mtoMpeng’o kuelekea Wilayani Mbarali ni tumaini kubwa sanakwa kuhudumia Kata za Mawindi na Ipuani na baadayeIgava, Rujewa, Ubaruku na Songwe Malilo.

Je, ni lini utekelezaji wa mradi huu utaanza kwasababu upembuzi yakinifu ulishafanyika?

SPIKA: Sijui kama Waziri anakumbuka, kamahukumbuki ni swali geni kabisa.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwanzanimpongeze amekuwa akifuatil ia sana mradi huu.Nimhakikishie kwamba katika miradi iliyoombewa fedha naKamati ya Kudumu ya Bunge inahusisha mradi huu pia wakutoa maji kutoka Njombe kwenda Mbarali ambaoutafaidisha vijiji vya Wanging’ombe na vijiji vya Wilaya yaMbarali. (Makofi)

Na. 140

Tatizo la Maji – Kata ya Mbokomu

MHE. SUSAN A. J. LYIMO aliuliza:-

Tatizo la Maji katika Kata ya Mbokumu hususan Vijijivya Korini Kusini, Juu na Tema pamoja na Vitongoji vyakelimekuwa la muda mrefu sana hivyo kuathiri Wakazi hao:-

(a) Je, ni lini tatizo hili litakuwa historia?

(b) Kwa kuwa, vyanzo vya maji havikidhi mahitaji yawakazi wa maeneo hayo; Je, Serikali haioni uwezekano wakuwa na vyanzo mbadala vikiwemo vile vya maji ardhini?

Page 25: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

25

3 MEI, 2013

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwa niabaya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa SusanAnselm Jerome Lyimo, Mbunge wa Viti Maalum lenye sehemu(a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, vijiji vya Korini Kusini na Korini Juuni miongoni mwa vijiji vilivyowekwa kwenye utekelezaji wamiradi ya maji chini ya Programu ya Maji na Usafi wa MazingiraVijijini. Ujenzi wa miundombinu ya maji katika vijiji hivyoumeanza tarehe 14 Januari, 2013 na umepangwa kukamilikamwezi Septemba, 2013 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.027.

Aidha, hivi sasa kijiji cha Tema kinapata huduma yamaji kwa asilimia 75. Huduma ya maji kwa kijiji hichoitaongezeka baada ya mradi wa maji wa Korini Kusini na KoriniJuu kukamilika ambapo maji yote yaliyokuwa yakitumika kwavijiji vya Korini Kusini na Korin Juu yatatumika kwenye kijiji chaTema.

(b) Mheshimiwa Spika, kutokana na jiografia ya Kata yaMbokumu pamoja na aina ya miamba iliyopo, uwezekanowa kupata maji chini ya ardhi ni mdogo sana.

Hivyo, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini imetafutachanzo mbadala cha chemchem ya Mrusunga chenyeuwezo wa kutoa maji kiasi cha lita za ujazo 859,200 kwa siku.Kiwango hicho cha maji kinakidhi mahitaji ya maji kwa wakaziwa Korini Kusini na Korini Juu.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Spika, nashukuruna namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibuyake na nakubaliana naye kwa sababu nimetoka huko juzina nimekuta tayari wananchi wanachimba mitaro.

Mheshimiwa Spika, lakini ni kweli pia kwamba miambaya Kata ya Mbokumu ni migumu sana kwa ajili ya kutoa maji.Lakini tuna chanzo kingine kizuri sana cha maji katikachemchem ya Mangi pale Rau ambapo tayari wananchi

Page 26: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

26

3 MEI, 2013

wamechangishana zaidi ya shilingi milioni 20 na ilikuwaimebakia shilingi kama milioni 100 ili waweze kumaliza lakiniuwezo wao ndio huo.

Nilikuwa naomba Serikali itoe tamko kama inawezakuwasaidia wananchi wale shilingi hizo milioni 100 ili wawezekukamilisha mradi huo hasa ikizingatiwa kwamba idadi yawatu katika vijiji hivyo au Kata hiyo inazidi kuongezeka.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, katika Kata yaMakongo Dar es Salaam vilevile kuna tatizo kubwa sana lamaji na Serikali iliahidi mwaka jana kununua pampu kubwaili kuweza kusukuma maji katika mitaa ya Mbuyuni pamojana mtaa wa Makongo.

Nilikuwa naomba kujua ni lini Serikali itakamilisha ahadiyake hiyo ili wananchi waweze kupata maji safi na salama?(Makofi)

SPIKA: Sasa na Makongo imeingiaje haya.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika,nimpongeze na nimshukuru kwa kutupa shukrani kwambamradi ule umeanza. Lakini nimhakikishie kwamba Serikali hiiipo tayari kushirikiana na wananchi kwenye mradi ule ambaowao wameuanzisha. Kwa hiyo, tutalichukua, tutalifanyia kazina ni moja ya miradi ambayo inaweza ikaingizwa kwenyehivi vijiji viwili ambavyo tumetangaza kama mtapewa.

Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu mradi wa Makongohili ni swali jipya naomba Mheshimiwa Mbunge tuwasiliane ilikufuatilia vizuri na kumpa jibu sahihi kuhusu kinachoendeleaMakongo.

Page 27: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

27

3 MEI, 2013

Na. 141

Athari za Vituo Vingi Vya Mizani Kwa Wafanyabiashara

MHE. RASHID ALI ABDALLAH (K.n.y. MHE. MKIWA A.KIMWANGA) aliuliza:-

Kwa muda mrefu sana wadau wa usafirishaji nawafanyabiashara wa nchi jirani wanaotumia Bandari ya Dares Salaam wamekuwa wakilalamikia urasimu uliopobarabarani unaotokana na vituo vingi vya Mizani, TRA, nakusimamishwa mara kadhaa na Askari wa UsalamaBarabarani jambo linalowafanya kuchelewa Bandarini naama kuharibika kwa bidhaa walizobeba:-

Je, Serikali inachukua hatua gani kuondoa adha hiyo?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi,napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mkiwa AdamKimwanga, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kulingana na Sheria ya UsalamaBarabarani “The Road Traffic Act. 1973” (No. 30 of 1973) na“The Road Traffic Maximum Weight of Vehicles Regulations”ya mwaka 2001 magari yote yenye uzito kuanzia tani 3.5 nakuendelea yanatakiwa kuingia kwenye vituo vya mizani nakupima uzito wakati wa safari zao, hivyo Wizara inatekelezasheria katika kupima magari hayo.

Mheshimiwa Spika, lengo kuu la kupima magari nikulinda barabara na madaraja ambayo ujenzi wakeunaligharimu Taifa fedha nyingi sana.

Page 28: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

28

3 MEI, 2013

Hata hivyo uzoefu unaonyesha kuwa pamoja nawasafirishaji kufahamu tunayo mizani, zaidi ya asilimia 25 yamagari yanayopima kwenye mizani hubainika kuzidisha uzitona hivyo kuchangia katika kuharibu barabara. Bila shaka haliingekuwa mbaya zaidi endapo wasingekuwa na mizani iliwaweze kupima.

Mheshimiwa Spika, vituo vilivyopo vimewekwa kwakuangalia uwezekano wa kupima magari mengi kwa wakatimmoja. Vituo hivyo ni Central Corridor yenye kilometa 1297na vituo 7, Dar es Salaam Corridor (Tanzam Corridor) yenyekilometa 915 na vituo 5, South Coast Corridor yenye kilometa556 na vituo 3, Kaskazini Mashariki (Northern East) yenyekilometa 786 na vituo 3.

Hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kuongeza ufanisina kupunguza msongamano kwenye vituo vya mizani. Hii nipamoja na kuweka mizani pande zote mbili za barabarakwenye vituo ambavyo vilikuwa na mzani upande mmoja;kuajiri wafanyakazi wapya wa vituo vyote vya mizani waliona sifa zaidi na pia mpango wa kujenga mizani za kisasa (multideck and weigh in motion) kwa kuanzia na eneo la Vigwaza.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuwaelimishawasafirishaji mujibu wa kufuata sheria ili wajiepushe nauzidishaji wa mizigo katika magari yao ili kuepuka usumbufu.Aidha, Wizara itaanzisha mfumo wa kisasa zaidi wa kupimamagari hayo tukianzia na mizani itakaojengwa eneo laVigwaza.

MHE. RASHID ALI OMAR: Mheshimiwa Spika, pamojana majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri naomba niulizemaswala mawili ya nyongeza kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa ya nchi zaAfrika Mashariki, Tanzania ni nchi ya kwanza inayoongozakwa urasimu na rushwa barabarani. Hii inatokana kwa kuwaTanzania ina vituo vingi sana vya ukaguzi wa magari. Kwamfano kutoka Dar es Salaam hadi Lusumo ina vituo 30. Je,Mheshimiwa Waziri ni lini ataondoa usumbufu huu.

Page 29: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

29

3 MEI, 2013

Swali la pili, wafanyabiashara wengi wamekuwawanalalamika kwa kuchelewa mizigo yao kufika mahaliinapokwenda, kwa sababu ya vituo hivi vingi. Je,Mheshimiwa Waziri haoni itasababisha wafanyabiasharawahamie nchi nyingine na kuikosea mapato Tanzania?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kwanzakabisa sikubaliani naye kwamba kuna utafiti unaonyeshakwamba Tanzania tunaongoza kwa urasimu na rushwa. Sualala rushwa ni tabia ya watu na hiyo huwezi kusema Tanzaniatunaongozwa, kwa hiyo hiyo naikataa. Pia si kweli kwambatuna vituo vya mizani 30 kwenda Rusumo, tuna vituo 7 kwenyeCentral Corridor na tumeshaeleza.

Kwa hiyo vituo ambavyo katika suala la msingitunazungumzia vituo vya mizani, sasa hivyo vituo vingine 30mimi sivifahamu. Ndio najua kwamba kweli kuna haja yakuangalia muda ambao msafirishaji anatoka Bandarinikwenda kwa mfano Rusumo labda badala ya kuchukua siku3 iweze kuchukua siku 2.

Suala hili tunaliangalia na ndiyo maana nimesemakwamba tunajenga vituo na mizani ya kisasa zaidi ambayogari litakuwa halisimami linapita linapima huku linakwenda.Kwa hiyo kwa namna hiyo muda wa kusafiri utakuwa ni mfupizaidi na tutaweza kusafirisha mizigo kwa muda mfupi nakuongeza uchumi kwa haraka zaidi.

Na. 142

Kukabiliana na Tatizo la Usafiri Dar es Salaam

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU( K.n.y. MHE. FATUMAA. MIKIDADI) aliuliza:-

Pamoja na jitihada za Serikali za kuongeza barabarakatika bajeti hii kwa kuweka barabara za juu flyover katikaJiji la Dar es Salaam lakini bado msongamano wa magari nawatu katika Jiji hilo bado ni mkubwa:-

Page 30: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

30

3 MEI, 2013

Je, wakati Serikali ikiendelea na mpango wake wakuweka “flyover” haiwezekani kuweka mpango wa dharurawa usafirishaji wa abiria kutumia Reli kwenye maeneo yaUbungo, Tabata, Mabibo, Buguruni, Yombo Vituka na TabataRelini japo kwa asubuhi na jioni tu kama zinavyofanya nchiza Harare na Afrika Kusini?

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, kwaniaba ya Waziri wa Uchukuzi, naomba kujibu swali laMheshimiwa Fatma Abdallah Mikidadi, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Kwanza napenda nimshukuru Mheshimiwa Mbungekwa ushauri wake ambao hata hivyo Serikali ilikwishalionajambo hilo na katika mwaka huu wa fedha 2012/2013imeanzisha huduma za usafiri wa abiria kwa njia ya reli katikaJiji la Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza msongamanobarabarani na msongamano wa abiria ndani ya mabasi.

Katika kutekeleza mpango huo, Taasisi zinazohusika,yaani RAHCO, TRL na TAZARA ziliboresha miundombinu yareli iliyopo katika Jiji la Dar es Salaam kwa kuifanyia ukarabatipamoja na kuvifanyia matengenezo vichwa vya treni namabehewa ambavyo vinatumika katika kutoa huduma hiyo.Huduma za usafiri wa treni kwa reli zote mbili (TAZARA na TRL)katika Jiji la Dar es Salaam zilianza tarehe 29 Oktoba, 2012.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Reli ya Kati (TRL)huduma hiyo ni ya kuanzia Stesheni ya Ubungo Maziwa hadiStesheni ya Dar es Salaam. Usafiri huo una vituo vingine vyaabiria sita (6) katika sehemu za Kamata, Buguruni kwaMnyamani, Tabata Reli, Tabata Mwananchi, Makuburi naMabibo. Huduma zinatolewa kwanzia saa 12.20 hadi saa5.14 asubuhi na kutoka saa 10.00 jioni hadi saa 3.46 usiku.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa TAZARA, hudumahiyo ni ya kuanzia Stesheni ya Mwakanga hadi Kurasini naMwakanga hadi TAZARA Stesheni. Vituo vya kati vipo sehemuya Kwa Fundi Umeme, Yombo kwa Limboa, Lumo Kigilagila,barabara ya Kitunda, Kipunguni B, Moshi Bar, Majohe, Shule

Page 31: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31

3 MEI, 2013

ya Sekondari Magnus, Mwakanga, Chimwaga, Maputo,Mtoni Relini, Kwa Azizi Ali na Kurasini. Huduma zinatolewakuanzia saa 10.45 alfajiri hadi saa 5.04 asubuhi na kutoka saa10.00 jioni hadi saa 4.00 usiku.

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziriningependa nimwulize maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza kwamba huduma ya Reli ya Kati yaani(TRL) hakuna kutoka Pugu kwenda Jijini ambapo ingewezakuwasaidia wakazi wa Gongo la Mboto, Pugu pamoja nawakazi wa maeneo ya Ukonga. Nini mpango wa Serikali wakuanzisha huduma hii kutoka Pugu kwenda Jijini?

La pili, nini mpango wa Serikali kuboresha hudumaya reli ambayo itasaidia sana kupunguza traffic volumekutoka Bandarini kwenda katika maeneo mengine ya ndanina nje ya nchi hii ikiwa ni pamoja na mradi ule wa ujenzi waTruck Port pale Kisarawe ambao utasaidia sana kupunguzamizigo ambayo inatoka Bandarini na kuweza kuunganishwakwenye access ya barabara kuu kwenda katika nchi za jirani?

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kifupi ninadakika 5 tu kwa maswali matatu yaliyobaki.

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika,Serikali inao mpango wa kuweka usafiri wa treni pia katikahiyo njia ya Reli ya Kati kuanzia stesheni kuelekea Pugu naikiwezekana hadi Morogoro. Ziko treni maalum kwa ajili hiyoambazo tuko katika mchakato wa kutafuta fedha natukizipata hizo tutanunua diesel multiply units ambazozinaweza kutoa huduma hizo za kati ya Pugu Stesheni auMorogoro kwa urahisi zaidi, kwa hivyo huo mpango upo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu uimarishaji wa Reli ya Katikwa ujumla naomba Mheshimiwa Mbunge avute subiratarehe 16 Mei, 2013 tutatoa kwa urefu sana mkakati uliopowa Serikali wa kuboresha Reli ya Kati kwa ujumla hapa nchini.

Page 32: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

32

3 MEI, 2013

Na. 143

Ukarabati wa Viwanda Vya Nguo Nchini

MHE. HUSEIN N. AMAR aliuliza:-

Je, Serikali inachukua jukumu gani la kuvikarabati vyanguo kama vile Mwatex ili mkulima aweze kuuza pamba yakekwa bei yenye faida?

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Viwandana Biashara napenda kujibu swali la Mheshiwa Hussein NassorAmar, Mbunge wa Nyang’wale, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwea Spika, Serikali imekuwa ikitoa unafuu wakodi (Tax Remmision) kwa wawekezaji wanaoingiza mashinena mitambo kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa viwanda vyotevikiwemo viwanda vya nguo kama vile MWATEX (Mwanza)MUTEX (Musoma), 21 Century (Morogoro) Sunflag (Arusha)na kadhalika. Unafuu huo wa kodi unatoa fursa kwawawekezaji wenyewe kuweza kutumia teknolojia ya kisasa,kuzalisha kwa ubora kwa ajili ya mauzo ya ndani na nje yanchi na kuongeza ajira.

Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu waviwanda vya nguo nchini, Serikali kwa kupitia Mamlaka yakutenga maeneo huru ya uzalishaji kwa mauzo ya nje(EPZA),imetenga maeneo ya kipaumbele ambapo hadi hivisasa jumla ya viwanda 13 vya kutengeneza nguo (Textiles)vimejengwa.

Mheshimiwa Spika, kuanzishwa kwa viwanda hivyo,viwanda vitakuwa na uwezo wa kusindika na kuongezathamani ya pamba inayolimwa na wakulima wa hapa nchinina hivyo kuwawezesha kuuza pamba yao kwa bei yenyefaida.

Page 33: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

33

3 MEI, 2013

MHE. HUSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika,ninamshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yakemazuri ambayo yanatia matumaini kwa wakulima wapamba. Nina maswali mawili ya nyongeza.

(a) Je, Serikali ina mikakati gani wa viwanda hivikuvibaini ni viwanda vingapi mpaka sasa hivi vinafanya kazi.

(b) Viwanda hivi vikiwa vinafanyakazi inamaana vitaongeza ajira kwa Watanzania. Je, ni viwandavingapi mpaka sasa hivi vinafanya kazi?

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Swali la kwanza kuwa ni viwanda vingapivinavyofanya kazi. Kama nilivyosema katika jibu langu lamsingi kuwa MUTEX ya Musoma, MWATEX ya Mwanzaviwanda hivi vyote vinafanya kazi ingawa hapo mwanzovilikuwa vina suasua lakini kwa sasa hivi vinafanya kazi kwaukamilifu na wawekezaji wameonyesha nia kubwa sana nauwezo mkubwa sana wa kuviendeleza viwanda hivi ili viwezekufanya kazi.

Kwa takwimu kidogo ni kwamba MWATEX sasa hiviwanaweza kuajiri wafanyakazi baada ya kuwa umeme kuwaume - stabilize hadi kufikia 1000. MUTEX Wanaweza kuajirihadi 200, URAFIKI wanaweza kuajiri wafanyakazi 760 na hiiinaendana na teknolojia ya kisasa kama kiwanda kinatumiateknolojia ya zamani bado wale wafanyakazi wa zamaniwataendelea kuwepo lakini sehemu kubwa ya viwanda hivikwa kushirikiana na kilimo vinaendeshwa na vijana.

Mheshimiwa Spika, MWATEX sasa hivi ninapoongeawameanzisha training wing ambayo inayofundisha kwa ajiliya teknolojia ya kisasa katika viwanda hivi. Ajira kwa vijanakwa sasa hivi imeshika kasi hasa kwasababu ya teknolojia yakisasa na kama nilivyosema kwenye jibu la msingi ni kuwaviwanda hivi vinafanya kazi.

Page 34: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

34

3 MEI, 2013

Serikali kwa sasa inavifuatilia kwa karibu sanakuhakikisha kuwa viwanda hivi vinafanya kazi vikiwemo naviwanda vingine mbali na MWATEX, kuna URAFIKI kinafanyakazi, kuna TWENTY FIRST CENTURY cha Morogoro kinafanyakazi, AFRITEX cha Tanga kinafanyakazi pamoja na TaboraMills nayo inafanyakazi kwa kutumia pamba.

Na. 144

Ukarabati wa Bwawa la Ikowa

MHE. HEZEKIAH N. CHIBULUNJE aliuliza:-

Ukarabati wa skimu ya umwagiliaji ya Chalinzeunaoendelea hivi sasa umeshaanza kuwalea manufaabaadhi ya wakulima kwa kuwapatia mazao ya chakula nabiashara kwa kipindi kifupi cha msimu wa mwaka:-

Je, ni lini Serikali itatenga fedha za kutosha kwa ajiliya kulikarabati Bwawa la Ikowa linalotoa maji ya kutoshelezashughuli za kilimo cha umwagiliaji kwa mwaka mzima?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKAalijibu:-

Mheshimiwa spika, kabla ya kujibu swali la MheshimiwaHezekiah Ndahani Chibulunje Mbunge wa Chilonwa,naomba kutoa maelezo ya utangulizi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika,Bwawa la Ikowa lilijengwa kati yamwaka 1957 na 1958 kupitia Idara ya Maji na Umwagiliaji(WD&ID) kwa madhumuni ya kilimo cha umwagiliaji kwa eneola hekta 40 na kwa matumizi ya Mifugo na Binadamu. Baadaya bwawa hilo kutumika kwa takribani miaka 32, lilijaa topekutokana na uharibifu wa mazingira ulichangiwa kwa kiasikikubwa na shughuli za kibinadamu na mifugo na hivyokupunguza uwezo wake wa kuhifadhi maji.

Page 35: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

35

3 MEI, 2013

Aidha, katika kipindi hicho bwawa hilo lilikumbwa natatizo la kumomonyoka kwa tuta upande wa juu(Upstream)kutokana na kujaa na kupwa kwa maji (waterwave action)ambapo kujaa tope na kumomonyoka kwaudongo wa tuta kuendelea hadi sasa.

Mheshimiwa Spika, baada ya kufanya upembuzigharama inayohitjika kurejesha uhai wa bwawa hilo nitakribani shilingi bilioni 2.5. Kwa ajili ya kuongeza kimo cha labwawa kwa meta moja(1), wa tuta kwa km1, na kukarabatisehemu ya juu (upstream) ya tuta.

Mheshimiwa spika, baada maelezo hayo, naombakujibu swali la mheshimiwa Hezekiah Ndahani Chibulunjekama ifutavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia mfuko wakuendeleza kil imo cha umwagili j i ngazi ya Wilaya(DIDF)ilitenga shilingi milioni 300 kwa mwaka wa fedha 2010/2011, na shilingi milioni 300 mwaka 2011/2012. Hata hivyo,kutokana na gharama kubwa za kukarabati bwawa hilofedha hizo hazikutosha kukamilisha ukarabati huo.

Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu wa skim yaChalinze kwa wananchi wa Chilonwa fedha hizo zilielekezwakwenye ukarabati wa skim ya Chalinze ambayo maji yakeyanatokana na bwawa la Ikowa ambapo kazi zilizofanyikani pamoja na kusakafia mfereji mkuu wenye urefu wa kilomita4 na kuboresha barabara yenye urefu wa km 2.5, kujengavigawa maji 11 na kukarabati sehemu tuta inayokinga majiya mvua yasiharibu tuta la bwawa lililobomoka urefu wa meta64.

Mheshimiwa Spika, kutokana na gharama kubwa yaukarabati wa bawawa hilo, Serikali inaendelea kutafurafedha kwa ajili ya kukarabati bwawa hilo ikiwa ni pamojana kutenga fedha za kutosha katika bajeti ya Serikali nakuandaa maandiko ya kuombea fedha kutoka vyanzombalimbali vya fedha kama vile mfuko wa pamoja waMsaada wa Chakula unaosimamiawa na Serikali ya Tanzania

Page 36: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

36

3 MEI, 2013

na Japan (Food Aid Counterpart Fund (FACF) ili kupata fedhaza kutosha kwa ajili ya kumalisha ukarabati wa bwawa hilokwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Chilonwa na Mkoawa Dodoma.

MHE.HEZEKIAH N. CHIBULUNJE: Mheshimiwa Spika,ninakusuhukuru sana kwa nafasi hii, pamoja na majibu mazuriya Mheshimkwa Waziri, nina maswali mawili:-

(a) Mheshimiwa Waziri amesema kuwa Serikaliinaendelea kutafuta fedha kupitia Bajeti ya Serikaliningependa kujua mpaka sasa ni kiasi gani cha fedhakimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa Bwawa hili?

(b) La pili, amesema kuwa kuna utaratibu wa kupelelamaandiko katika vyombo mbalimbali ili kuombea fedha,ninapenda pia kujua maandiko haya yamepelekwa katikavyombo vipi na mchakato wake umefikia wapi?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, tumesema Serikali inaendelea kutafutafedha kwa ajili ya mradi huu wa Chalinze na gharama zaketumesema kwa kupata ukamilifu ili turudishe katika hali yazamani zinatakiwa bilioni 2.5 hizo ni hela nyingi sana.

Kwa hiyo, tunachofanya tunakadiria kuangalia kamatunaweza kufanya marekebisho kwa awamu ili wananchiwanaotumia skim ile wapate matumizi ambayo yanawezakusaidia katika kuongeza uzalishaji.

Mheshimiwa Spika, maandiko yanayofanyika,yanafanyika na kanda ya Umwagiliaji kwa maana ya ZonalDepartment kwa Kanda hii ya Katikati ambayo Makao Makuuyake yako Dodoma, maandiko haya yanajumuisha miradiambayo iko Wilaya ya Bahi, Kondoa, Chilonwa, Kongwa namaeneo yote haya. Jana tulikuwa Wilaya ya Bahi tumeanzkupitia miradi ya Wilaya ya Bahi tutafika mpaka miradi hiyoya Chilonwa Kondoa na kadhalika ili tupate tathimini yamiradi ya Umwagiliaji kwa Kanda hii ya kati kwa lengo lakuongeza uzalishaji wa chakula katika Kanda hii.

Page 37: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

37

3 MEI, 2013

SPIKA: Waheshimiwa Muda umekwisha natumechukua muda wa dakika zingine huko. Kwa namna yapekee sana, ninapenda kutambua uwepo wa MheshimiwaJaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohammed ChandeOthman. (Makofi)

Pia Jaji Kiongozi Mahalama Kuu ya TanzaniaMheshimiwa Faki Jundu ninaomba usimame wapo na Majajiwengine lakini pia kwa namna ya pekee nitambue uwepowa Maaskofu kumi wa Kanisa la Sabato Tanzania wako hapaDodoma kwa shughuli zao. Ninaomba wasimame Maaskofupale walipo asanteni sana na ninaomba muombee nchi hiiiendelee kuwa ni nchi ya Amani, nchi ya utulivu na nchi yaupendo kama inavyostahili na sisi humu mtuombee tu simnatujua mambo yetu? Ahsanteni sana na karibuni sana.

Waheshimiwa Wabunge, nitangaze shughuli za kazi.Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria naUtawala Mheshimiwa Pindi Chana anaomba niwatangazieWajumbe wa Kamati yake kuwa leo watakuwa na Kikao chaKamati saa saba mchana, kukutana na Tume ya Mipangona Kikao hicho kitafanyika katika Hoteli ya VETA. Kwa hiyo,wanakwenda VETA hawa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Ulinzi na UsalamaMheshimiwa Anna Margareth Abdallah, anaombaniwatangazie Wajumbe wa Kamati yake watakuwa na Kikaosaa saba mchana leo, katika ukumbi namba 227. Mwenyekitiwa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na MazingiraMheshimiwa James Lembeli anaomba niwatangazieWajumbe wa Kamati yake kuwa leo saa saba na robowatakuwa na Kikao katika Ukumbi wa Pius Msekwa.

Halafu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yaMaendeleo ya Jamii, Mheshimiwa Jenista Mhagama,anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamati kuwa leo saasaba mchana watakuwa na Kikao cha Kamati katika ukumbinamba 231. Kwa hiyo, hizo ndizo kazi zitakazofanyikamchana. (Makofi)

Page 38: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

38

3 MEI, 2013

KAULI ZA MAWAZIRI

Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA,URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya WaziriMkuu ninapenda kutoa Kauli ya Serikali Bungeni kuhusu taarifaya awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Matokeo ya Mtihaniwa Taifa wa Kidato cha nne mwaka, 2012.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 49 (1)yaKanuni za Kudumu za Bunge toleo la mwaka 2007 ninaombakuwasilisha taarifa ya awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguzamatokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2012.Waheshimiwa Wabunge watakumbuka kuwa matokeo yamtihani wa kidato cha nne mwaka 2012, yalionyesha kuwakiwango cha ufaulu kimeshuka kwa kiwango kikubwaikilinganishwa na miaka ya hivi karibuni.

Matokeo yaliyotangazwa mwezi Februari, 2012yalionyesha kuwa kati ya wanafunzi laki tatu na sitini na saba,mia saba hamsini na sita waliofanya mtihani huo, watahiniwalaki moja na ishirini na sita elfu, mia nane na arobaini na sabandiyo waliofaulu.

Katika idadi hii wanafunzi waliofaulu katika daraja lakwanza hadi la tatu ni ishirini na tatu elfu mia tano na ishirinisawa na 6.4% na daraja la nne ni laki moja na tatu, mia tatuishirini na saba sawa na 28.1%.

Mheshimiwa Spika, watahiniwa laki mbili na arobaini,mia tisa na tisa sawa na 65.5% ya wanafunzi wote waliofanyamtihani wa kidato cha nne mwaka 2012, walipata daraja lasifuri. Kushuka kwa kiwango cha ufaulu kulihusu shule za ainazote yaani sekondari za Serikali ikijumulisha zilizojengwa kwanguvu za wananchi, shule binafsi na Seminari na takwimuzinaonyesha kuwa ukilinganisha na matokeo ya kidato channe mwaka 2011 na mwaka 2012 shule za wananchi matokeoyao yameshuka kwa 1.82%, shule za umma zile za zamanizile kongwe yameshuka kwa 6.43%, shule binafsi yameshuka

Page 39: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

39

3 MEI, 2013

kwa 6.39%,na kwa shule za Seminari yameshuka kwa 7.29%hali hii inaonyesha kuwa matokeo katika shule za wananchiyameshuka kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na yale yashule za umma za zamani yaani zile kongwe.

Mheshimiwa Spika, shule binafsi na shule za Seminariambazo zilitegemewa kufanya vizuri zaidi ya zile za wananchiambazo matokeo yake yameshuka zaidi kwa 6.4% na 7.3%.Kutokana na matokeo hayo yasiyoridhisha na ambayo yakonje kabisa ya mwenendo wa ufaulu kwa miaka ya karibuniSerikali iliamua kuunda Tume ya kuchunguza kushuka kwakiwango cha ufaulu wa mtihani wa Taifa wa Kidatocha nnemwaka 2012, kwa madhumuni ya kupata ufumbuzi wakudumu.

Mheshimiwa Spika, Hadidu za Rejea. TumeyaUchunguzi ilipewa hadidu za Rejea zifuatazo:-

(1) Kubainisha sababu za matokeo mabaya yamitihani wa kidato cha nne mwaka 2012.

(2) Kubaini sababu za kushuka sababu za kushuka kwaufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2011/2012.

(3) Kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuakukabiliana na tatizo la mwenendo wa kushuka kwa kiwangocha elimu mara moja, kipindi cha muda mfupi, kati na kipindicha muda mrefu.

(4) kutathimini nafasi ya Halmashauri katika kusimamiaElimu ya Sekondari katika Halmashauri zake.

(5) Kuainisha sababu nyingine zinazoweza kuwazimechangia hali hii ya matokeo.

Mheshimiwa Spika, katika kutafakari Hadidu za Rejeahizo Tume imejikita katika kujibu maswali makuu matatu:-

Page 40: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

40

3 MEI, 2013

(1)Kwa nini matokeo ya kidato cha nne kuanziamwaka 2008 yamekuwa na mserereko wa kushuka kulikomiaka iliyotangulia?

(2) Kwa nini wanafunzi wa Kidato cha nne wa mwaka2012, matokeo yao yalikuwa mabaya kuliko ya wenzao yamwaka 2011, pamoja na kuwa ufaulu ulishuka tangu mwaka2008?

( 3) Nini kifanyike?

Mheshimiwa Spika, Wajumbe wa Tume ya Uchunguzi;Tume ya Uchunguzi iliongozwa na Professor Sifuni Mchomekutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania na ndiye alikuwaMwenyekiti, Wajumbe wengine walioteuliwa waliteuliwakutoka Baraza la Wawakilishi, Mashirika yasiyo ya Kiserikali,Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Madhehebuya Dini, Chama cha Walimu, Muungano wa wenye shulebinafsi na Muungano wa Walimu wa Sekondari. Orodha yaWajumbe wa Tume hii ni kama ifuatavyo:-

(1) Professor Sifuni Mchome – Tume ya Vyuo VikuuMwenyekiti.

(2) Mheshimiwa Bernadetha Mshashu- Bunge la Jamhuriya Muungano – Makamu Mwenyekiti.

(3) Mheshimiwa Abdul Marombwa – Mbunge na Mjumbe

(4) Mheshimiwa Suleiman Hamis - Mjumbe wa Baraza laWawakilishi Zanzibar.

(5) Mwalimu Honorata Chitanda – Chama chaWalimu Tanzania.

(6) Ndugu Rakesh Rajan- Twaweza.

(7) Mwalimu Daina wa Temu- Umoja wa Wakuuwa Shule za Sekondari.

Page 41: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

41

3 MEI, 2013

(8) Mwalimu Kizito Innocent Lawa – Taasisi yaElimu Tanzania.

(9) Mwalimu Mbarouk J. Makame- Baraza la ElimuZanzibar.

(10) Professor Mwajabu Posi- Chuo Kikuu cha Dares salaam.

(11) Mwalimu Nurdin Mohammed – Chuo chaUalimu cha Halmain.

(12) Ndugu Peter Maduki- Baraza la KikristoHuduma za Kijamii.

(13) Ndugu Mahmoud Mringo- Chama chaWamiliki na Mameneja shule na vyuo visivyo vya Kiserikali.

(14) Ndugu Abdalah Mohammed – Chuo KikuuTaifa Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, Taarifa ya Tume ya Uchunguzi.tarehe 28 Aprili, 2013, Tume ya Uchunguzi wa Matokeo yaKidato cha nne mwaka 2012, ilikamisha kazi yake katikaawamu ya kwanza na kutoa taarifa ya awali. Uchambuzi wataarifa hiyo ya awali unaonyesha kuwa kutokana naUchunguzi uliofanyika kwa muhtasari Tume imebaini mambomuhimu yafuatayo:-

Matokeo ya kidato cha nne kuanzia mwaka 2008,yamekuwa na mserereko wa kushuka kuliko miakailiyotanguliwa kwasababu mbalimbali ikiwemo changamotozinazotokana ya mafanikio yaliyopo sana ya kuongozekasana kwa idadi ya shule za msingi na sekondari hususani katikamwaka 2001 na sasa 2013, na hivyo kuwa na idadi kubwa yawanafunzi walioko shuleni kwa mfano; katika kipindi chamwaka 1961 hadi 2001 idadi ya wanafunzi wa shule ya msingiimeongezeka kutoka laki nne na themanini na sita elfu, mianne sabini mwaka 1961hadi milioni nne, laki nane sabini natano elfu, mia saba sitini na nne mwaka 2001.

Page 42: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

42

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, sawa na ongezeko la milioni nne, miatatu, themanini na tatu themanini na tisa elfu, mia mbili tisinina nne katika kipindi hicho cha takribani miaka arobaini,hatahivyo, kati ya mwaka 2001 hadi 2012 wanafunziwameongezeka kutoka milioni nne, laki nane na sabini natano elfu, mia saba sitini na nne mwaka 2001 hadi milioninane mia mbili arobaini na saba elfu mia nne sabini na mbilimwaka 2012, sawa na ongezeko la wanafunzi milioni tatulaki tatu na sabini na moja elfu mia saba na nane katikakipindi cha takribani miaka 11 na hivyo kufanya jumla yawanafunzi wote wa shule za msingi kuwa milioni nane, lakimbili na arobaini na saba elfu mia nne sabini na mbili mwaka2012.

Mheshimiwa Spika, idadi ya wanafunzi imeongezekakutoka elfu kumi na moja, mia nane thelathini na mbili mwaka1961, hadi laki mbili themanini na tisa elfu mia sita tisini na tisamwaka 2001, ambayo ni sawa na ongezeko la wanafunzilaki mbili sabini na nne elfu, mia nane sitini na saba katikakipindi hicho cha miaka arobaini. Lakini kati ya mwaka 2001hadi 2012 idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka laki mbilithemanini na tisa elfu, mia sita tisini na tisa mwaka 2001, hadimilioni moja laki nane na themanini na nne elfu mia mbilisabini, mwaka 2012, sawa na ongezeko la wanafunzi milionimoja laki tano tisini na nne elfu mia tano sabini na moja katikakipindi cha miaka kumi na moja tu.

Mheshimiwa Spika, juhudi hizi zimetokana na mpangoulioandaliwa chini ya mpango wa maendeleo ya Sekta yaElimu wa Mwaka 1999, mipango hii ni pamoja na:-

(i) Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya MsingiMMEM wa mwaka 2000 ambapo MMEM I ambayo ililengakatika kufungua shule zaidi ili wanafunzi wengi wa rika lengwawaweze kujiunga na elimu ya msingi. MMEM II ambayoililenga katika kuboresha ubora wa elimu iliyotolewa katikashule za elimu za msingi na MMEM III ambayo ililenga katikakuendelea kuimarisha ubora wa elimu ya msingi baada yamafanikio ya MMEM ya I na II.

Page 43: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

43

3 MEI, 2013

(ii) Mpango wa elimu ya sekondari MMES kwamwaka 2004 ambapo MMES I ambayo ililenga katikakufungua shule zaidi za sekondari katika ngazi za Kata iliwanafunzi wengi zaidi wanaomaliza elimu ya msingi wawezekujiunga na elimu ya sekondari kidato cha kwanza. MMES IIambayo ililenga katika kuendelea kuimarisha ubora wa elimuya sekondari kadri idadi ya wanafunzi wa elimu ya sekondariwanavyoendelea kuongezeka.

Mheshimiwa Spika, changamoto zinazoambatana namafanikio haya ni pamoja na mazingira yasiyoridhisha yakufundishia na kujifunzia ikiwemo upungufu wa miundombinumuhimu ya shule kama vile madarasa, maabara, madawati,maktaba, nyumba za walimu, hosteli na majengo menginemuhimu ya shule. Vilevile kuna tatizo la uhaba wa walimu,vitabu, zana za kufundishia na matatizo ya ukaguzi wa shule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile Tume imebaini kuwa,mfumo wa elimu ya msingi na sekondari unakabiliwa nachangamoto nyingine mbalimbali ambazo Taifa linapitia kwasasa ikiwemo masuala ya kisera, kisheria, kimfumo, kimuundopamoja na changamoto za uhaba wa rasilimali fedha narasilimali watu. Tume inaendelea kufanyia kazi maeneo hayakwa kushirikiana na watalaam na wadau wengine.

Mheshimiwa Spika, kuhusu matokeo ya kidato chaNne ya mwaka 2012, Tume imebaini kwamba pamoja nawanafunzi hawa kuwa katika mazingira yanayofanana nayale ya wenzao wa miaka iliyopita na kwamba ufanisi katikashule kwa ujumla umekuwa unashuka kwa sababumbalimbali, ufaulu wao umeshuka zaidi kwa sababu yamabadiliko ya mchakato wa kuandaa na kutoa matokeoya mtihani wa mwaka 2012. Mfumo uliotumika mwaka 2012katika kupanga matokeo ya madaraja ni tofauti na uleuliotumika mwaka 2011 na miaka iliyotangulia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchunguzi unaonesha kuwa,mwaka 2011 Baraza la Taifa la Mitihani lilikuwa linachakataalama za mwisho kwa kutumia mfumo ambao ulikuwaunabadilika kutegemea hali ya ufaulu wa wanafunzi ambao

Page 44: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

44

3 MEI, 2013

ni National Min Difference (NMD). Utaratibu huu ulitokanana tofauti ya wastani wa Kitaifa wa alama za maendeleokutoka alama za maendeleo endelevu Continuity Assessment(CA) na watahiniwa wote na wastani wa Kitaifa wa ufauluwa mitihani ya mwisho kwa somo husika. Kila mtahiniwaaliongezewa National Min Difference iliyokokotolewa katikaalama za mtihani wa mwisho ili kupata alama itakayotumikakatika daraja la ufaulu. Kimsingi kila somo lilikuwa na NMDyake kulingana na continuity assessment zilivyo katikamwaka husika. Lakini mwaka 2012 ilitumia mfumo mpya wakuwa na viwango maalum vya kutunuku fix grade range.Tume imebaini kwamba pamoja na kwamba mfumo huouliandaliwa kwa nia nzuri utaratibu huo mpya haukufanyiwautafiti na maandalizi ya kutosha kabla ya kutumika.

Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya awali ya Tume,kwa kuzingatia masuala mbalimbali yaliyojitokeza wakati wauchunguzi, Tume katika taarifa yake ya awali imetoamapendekezo mbalimbali yakiwemo yale yanayohitajikutekelezwa kwa haraka na kutokana na kuwepo namapendekezo hayo ambayo inabidi yafanyike kwa harakatarehe 29 Aprili, Baraza la Mawaziri lilipokea taarifa ya awaliya Tume na kuijadili ambapo liliridhia Mapendekezo hayoyaanze kutekelezwa mara moja.

Mheshimiwa Spika, maamuzi ya Baraza la Mawaziriyanalenga kutenda haki kwa Walimu na Wanafunzi ambaojuhudi zao za kufundisha na kujifunza zimepimwa kwa kutumiamfumo mpya ambao hawakupata fursa ya kushirikishwa nakuandaliwa. Mapendekezo hayo ni kama yafuatayo:

(i) Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibuuliotumika mwaka 2011. (Makofi)

(ii) Standardization ifanyike il i matokeo yawanafunzi yalingane na juhudi walizoziweka katika kusomakwa mazingira na hali halisi ya Tanzania na uamuzi wa Taifakuongeza Idadi ya shule na wanafunzi wakati wa uwekezajikatika ubora unaendelea.

Page 45: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

45

3 MEI, 2013

(iii) Baraza la Taifa la Mitihani limeelekezwakuzingatia kuwa pamoja na kwamba sheria ya kuanzishwakwake inawaruhusu kufanya marekebisho ya mchachato wamtihani lakini marekebisho yeyote ya kubadilisha utaratibuwa kupanga viwango vya ufaulu na madaraja ya matokeoya mtihani lazima yahusishe wadau wote wanaohusika namitaala, ufundishaji na mitihani.(Makofi)

(iv) Wakati Tume imeendelea kukamilisha kazi yakeuamuzi wa Baraza la Taifa la Mitihani la kutumia utaratibumpya wa kupanga viwango vya ufaulu madaraja yamatokeo ya mitihani uliotumika mwaka 2012 usitishwe nabadala yake Baraza la Mitihani litumie utaratibu wa mwaka2011 kwa kidato cha Nne na cha Sita kwa mitihani yoteukiwemo utaratibu wa standardization na kutoa matokeomapya kwa kuzingatia maelekezo haya.

(v) Aidha, mchakato wa mfumo wa Tuzo wa TaifaNational Qualification Framework na mfumo wa kutahiniwa,kutathmini maendeleo ya mwanafunzi katika masomo yakeNational Assessment Framework ukamilishwe harakaiwezekanavyo.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mapendekezo yaTume, kutokana na umuhimu wa mapendekezo haya Barazala Mawaziri limeamua kwamba utekelezaji wa mapendekezohayo uanze mara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Tume ya Uchunguzi itaendeleakukamilisha taarifa yake vizuri kwa kuhusisha wadaumbalimbali ili kupata maoni zaidi na ushauri wao juu yamambo mbalimbali yaliyobainika wakati wa uchunguzi kablaya kuikamilisha na kuitoa kwa matumizi ya Umma na vyombombalimbali.

Mheshimiwa Spika, hitimisho, Serikali inaipongeza sanaTume kwa kutoa mapendekezo ya awali ambayo Serikaliimeyaridhia. Aidha, Serikali inawashukuru wananchi wote nawadau mbalimbali wa sekta ya elimu wanaoendelea kutoamaoni na ushauri wao kwa Tume.

Page 46: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

46

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, Serikali inawahakikishia wananchikuwa itaendelea kuboresha elimu nchini ili kuwezesha watotowetu wapate mafanikio katika maisha na maendeleo yao,kwani wahenga wanasema: Elimu ni Ufunguo wa Maisha.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuunaomba kuwasilisha taarifa ya awali.(Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunategemea wakatiwowote kupewa nakala ya rasimu ya elimu na tumeshaurikwa nguvu sana Serikali ikae na Kamati yetu ya Huduma zaJamii lakini tutakuwa na semina kwa Wabunge wote lakinibaada ya kupewa hiyo nakala muwe mnasoma siyo tuendepale ukumbini tusikilize tu.

Kwa hiyo, tunaomba waandae nakala za kutoshakwa ajili ya Wabunge wote, lakini kazi kubwa itafanyika katikangazi ya Kamati, maana yake wenzetu wana utalaam nawana muda na wanaweza kudadisi na kufuatilia kwa nguvuzaidi. Kwa hiyo, tunashukuru kwa taarifa hiyo. Katibutuendelee.

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Matumizi ya Serikali Mwaka 2013/2014 Wizara ya Katiba na Sheria

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika,Utangulizi; Kutokana na taarifa yangu niliyoiwasilisha kwenyeKamati ya Katiba, Sheria na Utawala tulipokutana kwa lengola kujadili na hatimaye kupitisha maombi ya Mpango na Bajetiya Wizara yangu, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lakoTukufu likubali kupokea Mpango na Makadirio ya Mapatona Matumizi ya fedha ya Wizara Katiba na Sheria, uliopitishwana Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawalakwa Mwaka wa fedha 2013/2014.

SPIKA: Wale wanaoamua kutoka wawewanatoka kwa utulivu.

Page 47: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

47

3 MEI, 2013

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika,aidha, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Kamatina kwa kazi kubwa waliyoifanya na kwa ushauri waowalioutoa wakati wa kupitia Makadirio ya Wizara yangu.

Mheshimiwa Spika, Muundo wa Wizara na Majukumuyake; kulingana na Muundo wa Wizara yangu, majukumuyanayotekelezwa yanajumuisha: kuratibu mfumo wa utoajihaki nchini, kusimamia mambo ya katiba na utawala washeria, kuendesha mashtaka na kuitetea Serikalimahakamani, na kusimamia utaratibu wa kutoa huduma yamsaada wa sheria kwa jamii. Majukumu hayo yanatekelezwana Taasisi zifuatazo:-

(i) Mahakama ya Tanzania;

(ii) Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;

(iii) Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora;

(iv) Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania;

(v) Tume ya Utumishi wa Mahakama;

(vi) Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA);

(vii) Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo(Law School of Tanzania); na

(viii) Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto,(Institute of Judicial Admnistraion).

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge hebu msianzekuzungumza tunasikiliza hotuba.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika,Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Malengo kwa Mwakawa Fedha 2012/2013 na Malengo ya Mwaka 2012/2013.

Page 48: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

48

3 MEI, 2013

Katika mwaka 2012/2013, Wizara ilipanga kutekelezamalengo ya Muda wa Kati kwa kuzingatia maeneo yakipaumbele kama ifuatavyo:-

(i) Uratibu wa Mchakato wa Mabadiliko yaKatiba;

(ii). Usimamizi wa Usikilizaji na Uendeshaji waMashauri;

(iii) Uimarishaji wa Shughuli za Usajili, Ufilisi naUdhamini;

(iv) Uimarishaji na Uboreshaji wa Vyuo vyaMafunzo ya Sheria;

(v) Uimarishaji wa Utoaji wa Ushauri wa KisheriaNchini;

(vi) Kufanya tafiti, mapitio, uandishi wa Sheria,Kanuni na Hati Mbalimbali; na

(vii) Usimamizi wa Haki za Binadamu na UtawalaBora.

Mheshimiwa Spika, Uratibu wa Mchakato wa Mabadilikoya Katiba; katika Mwaka wa Fedha 2012/2013 Wizara yanguimeendelea kuratibu Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeanza kazi rasmi tarehe1 Mei, 2012. Madhumuni ya kuanzishwa kwa Tume ni kuratibu,kukusanya, kuchambua na kutathmini maoni ya wananchikuhusu mabadiliko ya Katiba. Kwa kuzingatia muda ambaoSheria imeelekeza, Tume imeweka malengo ya kuwezeshakupatikana kwa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano waTanzania ifikapo Aprili 26, 2014.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka waFedha 2012/2013, Tume ilitekeleza shughuli zake kamaifuatavyo:-

Page 49: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

49

3 MEI, 2013

(i) Kutoa elimu kwa umma na kuhamasisha wananchikushiriki katika hatua zote za mchakato wa mabadiliko yaKatiba kupitia vyombo vya habari (Redio, Luninga, Magazeti,Tovuti) machapisho mbalimbali na katika mikutano;

(ii) Kuandaa na kusambaza nakala 1,700,000 za Katibaya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, nakala 400,000 zaSheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83, Katiba ya Zanzibarnakala 19,000, Vipeperushi 800,000 vinavyoeleza majukumuya Tume, Vipeperushi 670,000 vyenye maswali yanayoulizwamara kwa mara na majibu yake nakala 588,600 za Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Mabadilikoya Katiba sura ya 83 kwa lugha nyepesi;

(iii) Kuandaa mifumo/njia mbalimbali ya ukusanyajiwa maoni ya wananchi kama vile mikutano ya hadharakatika Wilaya zote nchini, mikutano ya Makundi Maalum,tovuti na mitandao ya kijamii, barua kwa njia ya posta, baruapepe, nukushi, ujumbe wa simu, makala, kujaza fomu maalumza Tume pamoja na magazeti;

(iv) Kukusanya maoni ya wananchi kuhusuMabadiliko ya Katiba katika Wilaya zote nchini nakuyachambua maoni hayo;

(v) Kuandaa, kuchapisha na kusambaza nakala50,000 za Mwongozo kuhusu Muundo na Utaratibu wakuwapata Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya(Mamlaka ya Serikali za Mitaa);

(vi) Kutoa elimu kwa umma kuhusu utaratibu wauundwaji wa Mabaraza ya Katiba, majukumu ya Mabarazahayo na kuandaa ratiba ya uchaguzi wa Wajumbe waMabaraza ya Katiba (Mamlaka ya Serikali za Mitaa);

(vii) Kuunda Mabaraza ya Katiba ya Wilaya(Mamlaka ya Serikali za Mitaa;

Page 50: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

50

3 MEI, 2013

(viii) Kusimamia uchaguzi wa Wajumbe waMabaraza ya Katiba ya Wilaya (Mamlaka ya Serikali za Mtaa);

(ix) Kuandaa Mwongozo wa Mabaraza ya Katibaya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu; na

(x) Kuandaa Ripoti ya Awali na Rasimu ya Katiba.

Mheshimiwa Spika, Tume hii pia, inalo jukumukubwa la kusimamia Mabaraza ya Katiba. Tume imeyagawaMabaraza ya Katiba katika Makundi mawili; kundi la kwanzani Mabaraza yatakayosimamiwa na Tume (Mabaraza yaKatiba ya Wilaya – Ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa)na kundi la pili ni Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi naMakundi ya Watu wenye malengo yanayofanana.

Hadi sasa Tume imeweza kuwapata Wajumbe waMabaraza ya Katiba katika Ngazi ya Mamlaka ya Serikali zaMitaa kupitia chaguzi na taratibu mbalimbali ambapo jumlaya Wajumbe 10,932 wamepatikana katika Mikoa 17. Katikakufanikisha kupatikana kwa Wajumbe, Tume ilitumia Mfumowa Serikali za Mitaa na taratibu za Mikutano katika ngazi zaSerikali za Mitaa zilizopo sasa (Vijiji, Mitaa na Kata).

Utaratibu huu ndio ulioainishwa kwenye Sheriazinazosimamia Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Aidha, kwamujibu wa Ratiba ya shughuli za Tume, mikutano ya Mabarazaya Katiba itaanza mwezi Juni, 2013 na itaendelea hadi mweziAgosti, 2013.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kifungu cha 10 chaSheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, Tume yaMabadiliko ya Katiba inayo mamlaka na uhuru katikautekelezaji wa majukumu yake.

Aidha, Tume imekuwa na utaratibu wa kutoa taarifakuhusu jambo lolote linalopangwa kutekelezwa na kutoataarifa baada ya utekelezaji wake kupitia mikutano navyombo vya habari, magazeti, majadiliano katika redio,luninga na majarida ya kijamii.

Page 51: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

51

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, Usikilizaji wa Mashauri nchini katikaMwaka wa Fedha wa 2012/2013 Mahakama ya Tanzaniaimesikiliza mashauri katika ngazi mbalimbali kama ifuatavyo:-

(i) Mahakama ya Rufani ilianza Mwaka wa Fedha wa2012/2013 ikiwa na idadi ya mashauri 1,743 yaliyosalia kutokamiaka ya nyuma.

Aidha, Mahakama ya Rufani ilipokea mashauri mapya450 na hivyo kuwa na jumla ya mashauri 2,193. Katika kipindicha kuanzia Julai, 2012 hadi Machi, 2013 Mahakamaimesikiliza na kuyatolea maamuzi jumla ya mashauri 275 sawana asilimia 13 ya jumla ya mashauri yote na hivyo kubaki najumla ya mashauri 1,918.

Aidha, uwezo wa wastani wa uondoaji wa mashauri(Clearance Rate) katika Mahakama ya Rufani kwa tathminiya kipindi cha miezi sita iliyopita ni asilimia 61

(ii)Mahakama Kuu ilianza Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 ikiwa na idadi ya mashauri 9,737 yaliyosalia kutoka miakaya nyuma. Aidha, Mahakama Kuu ilipokea mashauri mapya7,547 na hivyo kuwa na jumla ya mashauri 17,284. Katikakipindi cha kuanzia Julai 2012 hadi Machi 2013 MahakamaKuu imesikiliza na kuyatolea maamuzi jumla ya mashauri 5,191sawa na asilimia 30 ya jumla ya mashauri yote na hivyo kubakina jumla ya mashauri 12,093. Aidha, uwezo wa wastani wauondoaji wa mashauri (Clearance Rate) katika Mahakamaya Kuu kwa tathmini ya kipindi cha miezi sita iliyopita ni asilimia70.

(iii) Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara, ilianzaMwaka wa Fedha wa 2012/2013 ikiwa na idadi ya mashauri285 yaliyosalia kutoka miaka ya nyuma. Aidha, Mahakamailipokea mashauri mapya 118 na hivyo kuwa na jumla yamashauri 403. Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2012 hadiMachi 2013 Mahakama ya Biashara imesikiliza na kuyatoleamaamuzi jumla ya mashauri 74 sawa na asilimia 18 ya jumlaya mashauri yote na hivyo kubaki na jumla ya mashauri 329.(Makofi)

Page 52: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

52

3 MEI, 2013

Aidha, uwezo wa wastani wa uondoaji wa mashauri(Clearance Rate) katika Mahakama ya Biashara kwa tathminiya kipindi cha miezi sita iliyopita ni asilimia 64.

(iv) Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, ilianza Mwakawa Fedha wa 2012/2013 ikiwa na idadi ya mashauri 1,597yaliyosalia kutoka miaka ya nyuma. Aidha, Mahakamailipokea mashauri mapya 674 na hivyo kuwa na jumla yamashauri 2,271. Katika kipindi cha kuanzia Julai 2012 hadiMachi 2013 Mahakama ya Kazi imesikiliza na kuyatoleamaamuzi jumla ya mashauri 491 sawa na asilimia 22 ya jumlaya mashauri yote na hivyo kubaki na jumla ya mashauri 1,780.Aidha, uwezo wastani wa uondoaji wa mashauri (ClearanceRate) katika Mahakama ya Kazi kwa tathmini ya kipindi chamiezi sita iliyopita ni asilimia 73.

(v) Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, ilianza Mwakawa Fedha wa 2012/2013 ikiwa na idadi ya mashauri 5,393yaliyosalia kutoka miaka ya nyuma. Aidha, Mahakama yaArdhi ilipokea mashauri mapya 427 na hivyo kuwa na jumlaya mashauri 5,820. Katika kipindi cha kuanzia Julai 2012 hadiMachi, 2013 Mahakama ya Ardhi imesikiliza na kuyatoleamaamuzi jumla ya mashauri 427 sawa na asilimia 7 ya jumlaya mashauri yote na hivyo kubaki na jumla ya mashauri 5,393.Aidha, uwezo wa wastani uondoaji wa mashauri (ClearanceRate) katika Mahakama ya Ardhi kwa tathmini ya kipindi chamiezi sita iliyopita ni asilimia 100.

(vi) Mahakama za Hakimu Mkazi, ilianza Mwaka waFedha wa 2012/2013 ikiwa na idadi ya mashauri 25,002yaliyosalia kutoka miaka ya nyuma. Aidha, Mahakamailipokea mashauri mapya 980 na hivyo kuwa na jumla yamashauri 25,982. Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2012 hadiMachi 2013 Mahakama imesikiliza na kuyatolea maamuzijumla ya mashauri 612 sawa na asilimia 2 ya jumla ya mashauriyote na hivyo kubaki na jumla ya mashauri 25,370. Aidha,uwezo wa wastani wa uondoaji wa mashauri (ClearanceRate) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa tathmini yakipindi cha miezi sita iliyopita ni asilimia 73.

Page 53: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

53

3 MEI, 2013

(vii) Mahakama za Wilaya, zilianza Mwaka wa Fedhawa 2012/2013 ikiwa na idadi ya mashauri 31,025 yaliyosaliakutoka miaka ya nyuma. Aidha, Mahakama za Wilayailipokea mashauri mapya 94,872 na hivyo kuwa na jumla yamashauri 125,897. Katika kipindi cha kuanzia Julai 2012 hadiMachi 2013 Mahakama za Wilaya imesikiliza na kuyatoleamaamuzi jumla ya mashauri 104,359 sawa na asilimia 83 yajumla ya mashauri yote na hivyo kubaki na jumla ya mashauri21,538. Aidha, uwezo wa wastani wa uondoaji wa mashauri(Clearance Rate) katika Mahakama za Wilaya kwa tathminiya kipindi cha miezi sita iliyopita ni asilimia 110.

(viii) Mahakama za Mwanzo, zilianza Mwaka wa Fedhawa 2012/2013 zikiwa na idadi ya mashauri 124,959 yaliyosaliakutoka miaka ya nyuma. Aidha, Mahakama za Mwanzozilipokea mashauri mapya 650,181 na hivyo kuwa na jumlaya mashauri 775,140. Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2012hadi Machi 2013 Mahakama imesikiliza na kuyatoleamaamuzi jumla ya mashauri 577,425 sawa na asilimia 74 yajumla ya mashauri yote na hivyo kubaki na jumla ya mashauri197,715. Aidha, uwezo wa wastani wa uondoaji wa mashauri(Clearance Rate) katika Mahakama za Mwanzo kwa tathminiya kipindi cha miezi sita iliyopita ni asilimia 89.

Mheshimiwa Spika, Uendeshaji wa Mashauri nchini;katika kutekeleza jukumu la kuiwakilisha Serikali katikamashauri mbalimbali ndani na nje ya nchi, Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali, imeendesha mashauri yaJinai, Madai na Katiba katika Mahakama ya Rufani,Mahakama Kuu na Mahakama zilizo chini ya Mahakama Kuuisipokuwa Mahakama za Mwanzo. Aidha, Ofisi piaimeendelea kuratibu mashauri ya usuluhishi (arbitration)ambapo manne (4) ya Mahakama Kuu na 11 ya Tume yaUsuluhushi (CMA). Hadi Machi, 2013 kulikuwa na jumla yamashauri ya madai 682 yakijumuisha mashauri mapya 132.Mashauri haya yote yalifunguliwa dhidi ya Serikali na Kesi moja(1) ya Madai ilifunguliwa na Serikali. Mashauri hayo yakokatika hatua mbalimbali za kusikilizwa na kutolewa maamuzina Mahakama Mashauri ya madai yaliyohitimishwa hadimwezi Machi, 2013 ni 40 na kubaki mashauri 642.

Page 54: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

54

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, aidha, kulikuwa na jumla yaMaombi ya madai 285 yaliyofunguliwa yakiwemo mapya 89yaliyopokelewa katika kipindi cha Julai 2012 hadi Machi 2013.Maombi haya ya madai yalifunguliwa dhidi ya Serikali. HadiMachi, 2013 maombi ya madai 63 yalihitimishwa na maombi222 yanaendelea kusikilizwa. Vilevile, palikuwepo na Rufaniza madai 46 zikijumuisha mpya saba (7). Kati ya hizi rufanimbili (2) zilihitimishwa na kubaki na rufani 44 ambazozinazoendelea kusikilizwa.

Mheshimiwa Spika, vilevile kuhusu masuala yaupatanishi (arbitration) mgogoro mmoja (1) unaohusu Serikaliulishughulikiwa kati ya Mashauri yaliyobakia. Hali kadhalika,Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeendeleakuendesha mashauri ya rufani za uchaguzi yatokanayo nauchaguzi Mkuu wa 2010 ambayo ni kutoka Kigoma (3), Tabora(2), Mara (1), Sumbawanga (1), Dar es Salaam (1), Mtwara(3), Kagera (1) na Arusha (2). Kati ya mashauri hayo, mashaurimatano (5) yamehitimishwa na mashauri tisa (9) yanaendeleakusikilizwa katika Mahakama ya Rufani.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali kupitia Kurugenzi ya Mashtaka iliendelea kutekelezajukumu lake la kuendesha mashauri ya jinai katika Mahakamaya Rufani, Mahakama Kuu na Mahakama zilizo chini yaMahakama Kuu na pia iliendelea kuratibu kazi za upeleleziunaofanywa na vyombo vya upelelezi isipokuwa Mahakamaza Mwanzo. Jumla ya mashauri 14,453 yaliyokuwepo namengine mapya 13,487 ya Mwaka 2012/2013 yaliendeleakuendeshwa Mahakamani.

Mashauri haya yanahusu kesi mbalimbali ikiwa nipamoja na mashauri yaliyohusisha mauaji ya watu wenyeulemavu wa ngozi, udanganyifu na utakatishaji wa fedhaharamu. Hadi mwezi Machi 2013 mashauri 5,257 yalihitimishwana kubaki mashauri 22,683 yatakayoendelea kuendeshwakatika ngazi mbalimbali za Mahakama pamoja na Mashaurimapya yatakayopokelewa.

Page 55: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

55

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, katika uendeshaji wa mashauriyanayohusu watu wenye ulemavu wa ngozi, jumla ya matukio60 yaliripotiwa na polisi nchi nzima. Mashauri 12 yanaendeleakusikilizwa, mashauri 14 yameondolewa mahakamani namashauri 10 yameamuliwa ambapo Jamhuri imeshindamashauri yote. Mashauri 24 yanaendelea kufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali kwa kushirikiana na vyombo vya upelelezi vyaTAKUKURU na Jeshi la Polisi ni mshiriki mkubwa katikamapambano dhidi ya rushwa. Hadi kufikia Mwaka 2012/2013Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepokea jumla yamajalada 317 yaliyohusu rushwa kubwa na ubadhirifu kutokavyombo vya upelelezi vya TAKUKURU na Jeshi la Polisi.

Kati ya Majalada hayo, 95 yaliandaliwa hati zaMashtaka na kupewa kibali cha kushtaki, jalada moja (1)lilifungwa na majalada 65 yalirudishwa kwa vyombo husikakwa ajili ya kufanyiwa upelelezi zaidi na majalada 156yanaendelea kufanyiwa kazi na Divisheni ya Mashtaka.

Mheshimiwa Spika, Vilevile, katika kuhakikishakwamba mali zilizopatikana kwa njia zisizo halali zinarejeshwa,Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inasimamia urejeshwajiwa mali na fedha (Asset Recovery and Forfeiture) katikamashauri mbalimbali.

Katika kipindi hiki mali zilizotaifishwa ni pamoja namagari manne (4) katika mikoa ya Morogoro (1), Dar esSalaam (1) na Tanga (2) na nyumba tatu (3) pamoja na fedhaShilingi bilioni saba (7) zinazotakiwa kurejeshwa baada yawatuhumiwa watano kutiwa hatiani katika shauri la madawaya kulevya. Watuhumiwa hao wamekata rufaa.

Page 56: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

56

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeendeleakuendesha mashauri 14 yanayohusu makosa ya wizi, kugushina kutakatisha fedha ambayo yaliyobaki katika kipindi chamwaka 2011/2012 katika Mahakama mbalimbali nchinizikiwemo Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Arushana Nzega. Mashauri haya yanahusu takribani kiasi cha ShilingiBilioni 48.

Hadi Machi, 2013 kulikuwa na jumla ya kesi tatu (3)zilizotolewa hukumu. Kesi moja (1) yenye kuhusisha kiasi chatakriban Shilingi Bilioni moja washtakiwa waliachiwa huru lakiniJamhuri imekata rufaa na kesi mbili (2) washtakiwa wametiwahatiani na wanatakiwa kurudisha fedha zipatazo ShilingiMilioni 960. Vilevile, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikaliimeendesha mashauri yanayohusu madawa ya kulevyaambapo katika kipindi cha Julai 2012 hadi Machi 2013 kesimoja (1) ya madawa ya kulevya ilihitimishwa kwa Mahakamakuwatia hatiani watu watano kwa kila mmoja kuhukumiwakifungo cha miaka 25.

Mheshimiwa Spika, Utenganishaji wa jukumu laUpelelezi na Mashtaka (Civilianisation of ProsecutionsService); katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali iliendelea na utekelezaji waMpango wa Kutenganisha Jukumu la Upelelezi na Mashtaka(Civilianisation of Prosecutions Service) ili kuondoa tatizo lahaki kuchelewa kutendeka, kesi kuchukua muda mrefuMahakamani kwa sababu ya muda mrefu unaotumika katikaupelelezi.

Hatua mbalimbali ziliendelea kuchukuliwa ikiwa nisehemu ya utekelezaji, uelimishaji na uenezaji wa utaratibuhuu katika Mikoa na Wilaya zote za Tanzania Bara. Hatua hizini pamoja na kuajiri Mawakili wa Serikali na kufungua ofisikatika Mikoa mitano (5) ya Morogoro, Manyara, Kigoma,Njombe na Pwani pamoja na Wilaya za Monduli na Temeke.Hadi sasa zipo Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali katikaMikoa 22 ya Tanzania Bara.

Page 57: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

57

3 MEI, 2013

Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, Iringa,Singida, Dodoma, Mtwara, Lindi, Mara, Kagera, Ruvuma,Rukwa, Mwanza, Kilimanjaro, Tanga, Tabora, Shinyanga,Morogoro, Pwani, Kigoma, Manyara na Njombe. Aidha, lengola kuwa na Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali katikaMikoa mitatu i l iyosalia ya Geita, Simiyu na Katavilitakamilishwa katika Mwaka wa Fedha wa 2013/2014.

Hadi Machi, 2013, Divisheni ya Mashtaka ilikuwainaendesha kesi katika Mahakama za Wilaya 22 za MakaoMakuu ya Mikoa na Wilaya zilizotajwa hapo juu. Lengo nikufikisha huduma za mashtaka karibu zaidi na wananchi.Aidha, Mpango huu wa kutenganishwa kwa shughuli zaupelelezi na mashtaka umesaidia sana kupunguza idadi yakesi zinazofunguliwa Mahakamani na msongamano wamahabusu na wafungwa magerezani. Idadi ya Mahabusuimepungua kutoka 17,932 kwa mwezi Julai, 2012 hadi kufikiamahabusu 16,973 mwezi Machi 2013. Vilevile, idadi yawafungwa imepungua kutoka 17,868 kwa mwezi Julai 2012hadi kufikia wafungwa 17,497 mwezi Machi, 2013.

Mheshimiwa Spika, lakini la msingi zaidi ni kuwa,utenganishaji huu unafanywa kwa misingi ya utawala bora.Si vyema kukipa chombo kimoja cha dola madaraka yakuhisia, kutuhumu, kukamata, kupeleleza na kushitaki bilaudhibiti wa chombo kingine.

Wataalam wa utawala wanasema “Regulation is thehallmark of Government” ndiyo maana kuna EWURA, TICRA,SSRA na kadhalika. Na ndani ya Serikali nako ni muhimu kuwana utaratibu huu wa “checks and balances”. Nchi nyingiambazo mifumo yao ya Sheria na Utawala inafanana na sisiwana utaratibu huu. Marekani mashtaka huendeshwa naMwanasheria Mkuu kupitia “District Attorneys”. Uingerezakuna “Crown Prosecution Agency” na kadhalika. Na hapakwetu ndiyo tuna Mwanasheria Mkuu kupitia Ofisi ya DPP.

Page 58: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

58

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Wizara yangu kwa kushirikiana na Asasi zisizo za Kiserikali,iliunda kikosi kazi kwa ajili ya kufanya utafiti na kuwasilishamapendekezo yatakayoisaidia Serikali kubuni utaratibu wautoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa watu wasiona uwezo wa kulipia gharama za kisheria. Kikosi kazi hichokimefanya utafiti na tayari mapendekezo ya kutunga sheriaitakayoratibu utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwaumma na kuwatambua watoa huduma za msaada wakisheria kwa umma, ikiwa ni pamoja na Wasaidizi wa Kisheria(Paralegals) yameshawasilishwa Serikalini. Taratibu za kupataSheria hiyo zinaendelea vizuri na ni matumaini yetu kwamba,Rasimu ya Sheria hii itawasilishwa katika Bunge hili Tukufukatika kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka waFedha wa 2011/2012, Wizara yangu ilianzisha Kamati ya Kitaifaya Kuzuia Mauaji ya Kimbari. Kamati hii imeanzishwakutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya NchiZinazozunguka au za Ukanda wa Maziwa Makuu (TheInternational Conference on the Great Lakes Region - ICGLR).Nchi husika zilifikia makubaliano katika Mkataba uliosainiwana nchi zote wanachama ya kuweka utaratibu wa kubainiviashiria vya uvunjifu wa amani na kusababisha vita katikaeneo la Maziwa Makuu. Tanzania imesaini Protocol for thePrevention and Punishment of the Crimes of Genocide, WarCrimes, Crimes Against Humanity and all Forms ofDiscrimination, ambayo pia yanaitaka Nchi Wanachamakuanzisha Kamati za Kitaifa za Kuzuia Mauaji ya Kimbari.

Nchini Tanzania, Kamati hiyo ilianzishwa mweziFebruari, 2012 na Kamati hii ina jukumu la kubaini dalili auviashiria vya uvunjifu wa amani ya nchi yetu, kuishauri Serikalipamoja na kujenga uelewa wa Wananchi kuhusu umuhimuwa kuzuia uvunjifu wa amani na mauaji na uhalifu dhidi yabinadamu nchini. Kamati hii ya Kitaifa ina Wajumbewafuatao: Ofisi ya Rais - Ikulu; Ofisi ya Mwanasheria Mkuuwa Serikali; Ofisi ya Waziri Mkuu; Wizara ya Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa; Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi; Wizaraya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa; Wizara ya

Page 59: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

59

3 MEI, 2013

Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Wizara ya Vijana, Habari,Utamaduni na Michezo; Wizara ya Elimu na Mafunzo yaUfundi; Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto;Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora; Chuo Kikuu chaDar es salaam; na Taasisi ya Wakfu ya Mwalimu Nyerere.

Mheshimiwa Spika, mapema mwezi Disemba, 2012,Wizara kupitia Kamati hii imefanya Mkutano na Viongozi waDini zote ambapo Viongozi wa Kidini walijadili nafasi yaokatika kulinda na kudumisha amani nchini. Mikutano yaKamati hii ni endelevu na ili iwe na tija, hutumika kuishauriSerikali na pia kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzuiamauaji na uhalifu dhidi ya binadamu nchini.

Katika utekelezaji wa Mpango huu, Wizara kwakushirikiana na Ofisi ya Mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusukuzuia Mauaji ya Kimbari, imeandaa Mkutano wa Kimataifautakaofanyika nchini Tanzania mwishoni mwa mwezi Mei,2013. Mada kuu ya mkutano huu itakuwa ni njia bora nafursa mpya katika kuzuia Mauaji ya Kimbari, Hatua za Kiserikalina Matumizi ya Kiteknolojia Kikanda (Best Practices in NewOpportunities in Genocide Prevention, Governmental Action,Technology in Regional Contexts).

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2012/2013, Wizara yangu imeratibu na kuandaa Mkutano waKimataifa wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kupambanana Ugaidi uliofanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 26 - 28Februari, 2013 na kuhudhuriwa na Wajumbe kutoka Nchi 36Duniani. Ujumbe au mada kuu katika Mkutano huo ulikuwani “Bringing Terrorists to Justice; Policy Challenges in theProsecution and Prevention of Terrorism”.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka waFedha wa 2012/2013, Wizara yangu imekamilisha tafiti kuhusuhali ya watoto wanaokinzana na Sheria na pia kuhusuupatikanaji wa haki sheria kwa watoto wenye umri wa chiniya miaka 18 kwa kushirikiana na UNICEF. Kutokana na utafitihuo, Wizara imeandaa Mpango Mkakati wa Miaka Mitanowa Haki Sheria kwa watoto. Mpango Mkakati huu utaboresha

Page 60: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

60

3 MEI, 2013

mfumo mzima wa upatikanaji wa ulinzi na haki kwa watotonchini. Vilevile, Mpango Mkakati huu utasaidia kuwekapamoja mikakati ya namna bora ya kushughulikia masualaya haki sheria kwa watoto nchini. Mpango Mkakati huuunaandaliwa Waraka wa Baraza la Mawaziri kwa ajili yakujadili na kupitisha Mpango Mkakati huu ili uweze kutumika.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka waFedha wa 2012/2013, Wizara yangu imeendelea kupokeamalalamiko ya aina mbalimbali toka kwa Wananchi nayameshughulikiwa. Malalamiko mengi yalielekezwa kwenyeTaasisi na Vyombo vya Serikali vinavyojishughulisha na utoajihaki na usimamizi wa Sheria. Malalamiko hayoyalishughulikiwa kwa kuwasiliana na Vyombo au Taasisi husikakama njia ya kuyatafutia utatuzi.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali, imeendelea kutekeleza jukumu la kuimarisha utoajiwa ushauri wa kisheria kuhusu masuala ya Mikataba yaKibiashara, Kimataifa, Katiba na Haki za Binadamu. Aidha,Ofisi pia imeshiriki katika mikutano mbalimbali ya Jumuiya yaAfrika Mashariki, Umoja wa Mataifa, Nchi Wanachama waKusini mwa Afrika (SADC) na Nchi za Umoja wa Afrika, kwaajili ya kufanya majadiliano na kutoa ushauri wa kisheria.Majadiliano ambayo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikaliimeshiriki ni ubia wa kibiashara kati ya Umoja wa Nchi za Ulayana Jumuiya ya Afrika Mashariki (EPA); kuanzishwa kwa Itifakiya Umoja wa Fedha; Itifaki ya Mahakama ya NchiWanachama wa Kusini mwa Afrika; kuanzisha Soko Hurubaina ya Nchi Wanachama wa Afrika Mashariki, SADC naCOMESA; kurekebisha Mkataba wa kuanzisha Mahakama yaUmoja wa Afrika; kurekebisha Mkataba ulioanzisha Bunge laAfrika; Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kuzuia kusambaakwa silaha ndogo; kurekebisha Itifaki ya Jumuiya ya AfrikaMashariki; na majadiliano ya mgogoro wa mpaka baina yaTanzania na Malawi. Vilevile, katika kipindi cha Mwaka waFedha wa 2012/2013, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikaliimeshughulikia na kutoa ushauri wa kisheria katika mikataba(Contracts) 330. Kati ya Mikataba hii, mikataba 295 ilihusumanunuzi ya umma na Mikataba 35 ilihusu masuala ya

Page 61: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

61

3 MEI, 2013

uwekezaji. Vilevile, Mikataba ya Makubaliano (MoU) 58ilishughulikiwa na makubaliano baina ya Nchi na Nchi(Bilateral Agreement) 21; mahudhurio ya vikao 185 vilivyohusuMajadiliano ya Mikataba na Mahusiano ya Kimataifa.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza mwaka janakatika Bunge lako Tukufu, Serikali imeendelea kutelekezaMpango wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi (OpenGovernment Partnership - OGP), ambao ulianzishwa tarehe21 Septemba, 2011. Mpango huu unasimamiwa na Wizarayangu na kuratibiwa na Kamati ya Kitaifa chini ya Uenyekitiwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu. Katika mwaka wafedha 2012/2013, Mpango huu umeendelea kutekelezwa naSekta tatu za kipaumbele za huduma za jamii ambazo ni Afya,Maji na Elimu. Mpango wa Serikali wazi unajikita katikamaeneo ya kuweka uwazi zaidi katika uendeshaji wa shughuliza Serikali, ushirikishwaji wa Wananchi katika mpango wautekelezaji, uwajibikaji na uadilifu, Utawala Bora, kupambanana rushwa na matumizi ya teknolojia na ubunifu. Malengo yaMpango huu ni kuimarisha usimamizi wa matumizi ya rasilimaliza umma, kuboresha utoaji wa huduma, kuongeza usalamawa nchi na kuongezeka kwa uwajibikaji wa kitaasisi.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Mpango huu,yafuatayo yamefanyika:-

(i) Mpango Kamili wa OGP Tanzaniaumeandaliwa na kuwasilishwa Makao Makuu ya OGP katikaMkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Nchi Wanachamawa OGP uliofanyika Brasilia Brazili tarehe 17 - 18 Aprili, 2012.

(ii) Road Map na Bango kitita ya Commitmentsya shughuli zitakazotekelezwa hadi kufikia Juni, 2013imeandaliwa na kusambazwa kwenye sekta husika.

(iii) Wizara nane zimeandaa Mipango Kazi yao nakuiwasilisha kwenye Kamati. Wizara hizi ni Ofisi ya Rais - Ikulu,Ofisi ya Rais - Tume ya Mipango, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawalaza Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Maji, Wizara ya Afyana Ustawi wa Jamii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Page 62: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

62

3 MEI, 2013

na Wizara ya Fedha. Aidha, kwa hivi sasa Kamati imeandaaMkakati wa Mawasiliano kuhusu utekelezaji wa Mpango waOGP Tanzania (Open Government PartnershipCommunication Strategy) na vilevile Kamati inashirikiana kwakaribu na Wakala wa Serikali Mtandao (e-GovernmentAgency) kuhakikisha Tovuti ya Wananchi (Citizen Portal)inaanza kazi mapema iwezekanavyo ili iweze kuhudumiaWananchi. Aidha, Waraka wa Mapendekezo ya KutungaSheria ya Uhuru wa Habari (Freedom of Information Law)unaandaliwa na Wizara husika ambayo ndiyo yenyedhamana ya masuala ya habari nchini, na utawasilishwakwenye ngazi za maamuzi na hatimaye sheria kutungwa nakuletwa katika Bunge lako Tukufu.

(iv) Kuhudhuria Kikao cha Mawaziri wa Nchizinazotekeleza Mpango wa Serikali Wazi (OGP) kilichofanyikaMjini London kuanzia tarehe 22 – 25 Aprili, 2013.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2013/2014, Wizara yangu itaendelea kusimamia Mipango Kazi yaSekta za kipaumbele na kuzipatia ufumbuzi changamotozinazoendelea kujitokeza katika utekelezaji wa Mpango waSerikali Wazi.

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Tume yaKurekebisha Sheria Tanzania, imekamilisha Taarifa ya Mfumowa Haki za Madai (Civil Justice System Review) na Taarifa yaMapitio ya Tamko la Sheria za Mila zinazofuata mkondo waukoo wa mama (Matril ineal Societies) . Taarifa hizizimewasilishwa kwangu ili ziweze kufanyiwa kazi zaidi naMwanasheria Mkuu wa Serikali na kutolewa kauli Bungeni yahatua zitazochukuliwa. Tume iko katika hatua za mwisho zakukamilisha Taarifa ya Mapitio ya Sheria zinazosimamiaUsuluhishi na Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi. Aidha, Rasimu yaAwali ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria zinazosimamia Hudumaza Jamii kwa Wazee imeandaliwa ili kuwezesha kufanya utafitikatika Mikoa 12 ya Tanzania ambayo ni Kagera, Shinyanga,Mara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Dodoma,Mbeya, Rukwa Ruvuma na Pwani. Kwa upande wa Mapitioya Mfumo wa Sheria unaosimamia Haki za Walaji (Consumer

Page 63: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

63

3 MEI, 2013

Protection), taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezizimeanza.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2012 hadiMachi, 2013 Tume imefanya uchambuzi wa hukumu za kesiza Mahakama ya Rufani ya Tanzania zipatazo 100 ili kuainishamisingi ya Kisheria (Legal Principles) na kuweka misingi hiyokatika tovuti yake ili kuwarahisishia wadau kuelewa tafsiri yamaamuzi ya Mahakama ya Rufani kuhusu vipengele vyakisheria vilivyotumika. Vilevile Tume imewasilisha kwaMwanasheria Mkuu wa Serikali, Rasimu tano za tafsiri za Sheriakatika Lugha ya Kiswahili. Pia Tume imeendelea kutoa elimuya Sheria kwa umma kupitia vipindi vya redio na runinga kwalengo la kuelimisha jamii kuhusu haki, wajibu na masualambalimbali ya Kisheria.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, iliendeleakutekeleza jukumu la kuandaa Miswada ya Sheria nakuiwasilisha mbele ya Bunge kwa ajili ya kujadiliwa nahatimaye kupitishwa na kuwa Sheria za Nchi. Hadi mweziMachi, 2013 jumla ya Miswada sita iliandaliwa; kati ya hiyo,Miswada minne ilipitishwa na kuwa Sheria, Miswada miwilibado haijapitishwa. Aidha, kazi ya kuzifanyia urekebu Sheriazilizopitishwa na Bunge iliendelea kufanyika ambapo Sheria14 zil ifanyiwa urekebu, jumla ya Sheria Ndogo 260zilitayarishwa na kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali naMaazimio 11 yaliwasilishwa Bungeni.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Ofisi ya Mwanasheria Mkuuwa Serikali ilitekeleza jukumu la kutafsiri Sheria kwa Lugha yaKiswahili na Kiingereza. Kwa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013,Ofisi imetafsiri jumla ya Sheria saba katika Lugha ya Kiswahili.

Mheshimiwa Spika, kuhusu usimamiaji wa Haki zaBinadamu, Utawala Bora na Masuala ya Katiba. Kwa upandewa masuala ya Katiba na Haki za Binadamu, Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali ilipokea maombi ya mashauriya Kikatiba na Haki za Binadamu 73 na kuhitimishwa 17; hivyo,kubaki mashauri 56 yanayoendelea kusikilizwa. Aidha, Ofisi

Page 64: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

64

3 MEI, 2013

ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliweza kushiriki vikaombalimbali kuhusiana na masuala ya haki za binadamu kamavile Kikao cha Kamati ya Haki za Binadamu inayosimamiaMkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii naKiutamaduni ambapo Taarifa ya Nchi ya Mkataba huoilijadiliwa Novemba, 2012 huko Geneva, Uswisi; Kikao chaBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa Marekani; na Kikao chaTume ya Haki za Binadamu na Watu (African Commission onHuman and People’s Rights) kilichofanyika Gambia Aprili,2013.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Ofisi ya Mwanasheria Mkuuwa Serikali imeshiriki kwenye wiki ya Maadhimisho ya Kitaifaya Haki za Binadamu ambayo hufikia kilele chake tarehe 10Desemba kila mwaka kwa kushirikiana na Tume ya Haki zaBinadamu na Utawala Bora na Wizara ya Katiba na Sheria.Katika maadhimisho hayo, taarifa mbalimbali za nchi kuhusuHaki za Binadamu na mapendekezo yanayotolewa naKamati au Tume zinazosimamia Mikataba husika ya Kimataifaya Haki za Binadamu kuhusu Tanzania zilitolewa kwaWananchi. Madhumuni ya maadhimisho hayo yalikuwa nikuwawezesha Wananchi kufahamu hali halisi ya Kitaifa katikamasuala ya Haki za Binadamu na jinsi Tanzaniainavyotekeleza shughuli za kulinda na kukuza Haki zaBinadamu.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Wizara ya Katiba na Sheria kupitia Tume ya Haki zaBinadamu na Utawala Bora, ilipanga kudumisha UtawalaBora nchini kwa kusimamia Utekelezaji wa Haki za Binadamukama zilivyoelezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Katiba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Tamko la Umoja wa Mataifa na Tamko la Afrika la Haki zaBinadamu. Katika kutekeleza hili, Tume imekamilisha kuandaaMpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu ambaoumewasilishwa Serikalini kwa ajili ya Kuidhinishwa na Barazala Mawaziri. Aidha, Tume iliendelea kushughulikia malalamikoya Wananchi kwa kupokea na kufuatilia malalamiko, kutoaushauri wa kisheria, kufanya uchunguzi na utafiti juu yamasuala yanayohusu haki za binadamu na Utawala Bora.

Page 65: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

65

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, Tume iliendelea kupokea nakushughulikia malalamiko mapya na ya zamani kulingana nauwezo uliokuwepo. Hadi kufikia mwezi Machi, 2013 Tumeilikuwa imeshughulikia jumla ya malalamiko 8,350. Kati yamalalamiko hayo, 7,165 ni ya miaka ya nyuma na 1,185 nimapya. Kati ya Malalamiko hayo 688 yalihitimishwa baadaya kupatiwa ufumbuzi na kubakia na malalamiko 7,662yanayoendelea kushughulikiwa.

Mheshimiwa Spika, Tume iliongeza juhudi za kuletaufumbuzi wa malalamiko ya Wananchi na migogoro ya ardhi.Vilevile, Tume ilikamilisha uchunguzi na kutoa mapendekezokwa mamlaka husika kuhusu ukiukwaji wa haki za Watumishiwa Mamlaka ya Maji Safi na Taka (DAWASCO), Mgogoro katiya Wafugaji na Wakulima wa Wilaya ya Rufiji na Mgogorowa Ardhi Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni. Aidha, Tumeiliitisha na kuendesha vikao vya kujadili taarifa za uchunguziwa hadharani kuhusu migogoro ya ardhi na uhamishwaji wawatu katika ardhi yao ulioshirikisha wadau mbalimbali kutokaTaasisi za Serikali na Binafsi. Vilevile Tume ilifanya kaguzi katikavituo 100 vya vizuizi (detention facilities) katika Wilaya 21 ilikupima na kutathmini hali na haki za watoto waliozuiwa katikavituo hivyo.

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Tume ya Haki zaBinadamu na Utawala Bora, imetoa elimu kwa umma kuhusuHaki za binadamu na Utawala Bora kupitia vipindi vya redio,runinga na machapisho mbalimbali. Jumla ya machapisho38,250 yalisambazwa na Wananchi 1,594 walipatiwa ushauriwa kisheria. Aidha, Tume ilitoa mafunzo kwa waandishi wahabari 112 katika Mikoa sita ya Tanzania Bara ya Iringa,Dodoma, Lindi, Morogoro, Mwanza, Tanga na Mjini Magharibikwa upande wa Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, Wakala wa Usajili, Ufilisi naUdhamini umeanza mazungumzo na wadau wa usajili wawatoto ambao ni Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Ofisiya Waziri Mkuu (TAMISEMI), juu ya namna ya kuboreshashughuli za usajili wa watoto. Rasimu ya Mkataba waMakubaliano kati ya RITA, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) na

Page 66: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

66

3 MEI, 2013

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhusu namna yakusogeza huduma za usajili wa vizazi na vifo kufikia ngazi yakata imekamilika na rasimu hiyo inatarajiwa kujadiliwa katikaKikao cha Wadau kitakachofanyika tarehe 3 Mei, 2013.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mpango wa kusajiliwatoto chini ya umri wa miaka mitano unaojulikana kama“U5BRI – Under 5 Birth Registration Initiative” ulianza kwamajaribio kwa kipindi cha wiki sita yaliyofanyika kuanziatarehe 4 Juni, 2012 katika Manispaa ya Temeke. Jumla yawatoto 15,513 walio na umri wa chini ya miaka mitanowalisaji l iwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa. Wakalaunaendelea kutekeleza Mpango huo ambao ni mkakati wakupunguza mlundikano wa vizazi ambavyo havijasajiliwa.Maandalizi ya kueneza mpango au mkakati huu yamefanyikakatika Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya kwa kufanya utafitiwa awali (Baseline Survey) na kutoa hamasa kwa makundimbalimbali ya Viongozi kama vile Kikao cha Kamati ya Ushauriya Mkoa (RCC), Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoawa Mbeya, Vikao vya Madiwani na Maafisa Maendeleo yaJamii wa Wilaya. Utekelezaji wa Mkakati huu unatarajiwakuanza mwezi Juni, 2013.

Mheshimiwa Spika, sanjari na Mkakati huo wa kusajiliwatoto walio na umri chini ya miaka mitano, Wakala piaunatekeleza mkakati wa kusajili watoto wa umri kati ya miaka6 hadi 18 (6 - 18 Birth Registration Initiative) waliopo mashuleniambao umefanyiwa majaribio katika Wilaya ya Igunga.Katika majaribio hayo, jumla ya watoto 1,499 walisajiliwakatika kipindi cha miezi miwili kuanzia tarehe 18 Februari, 2013na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.

Mheshimiwa Spika, Wakala wa RITA umeendeleakusogeza huduma za usajili kwa Wananchi, kwa kuendeshakampeni za uhamasishaji ambazo zilipelekea kusajili vizazi331,272, vifo 59,099, ndoa 6,094, talaka 42, uasili wa watoto23 na kufunga mirathi moja, kuandika na kuhifadhi wosia 37.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu yaufilisi, Wakala pia uliteuliwa na Mahakama kuwa mfilisi wa

Page 67: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

67

3 MEI, 2013

muda ili kusimamia mali za Kampuni ya Mitambo ya KufuaUmeme ya IPTL. Katika shauri namba 49 la mwaka 2003lillilohusu IPTL, Mahakama ya Rufani ilitoa maamuzi ya kufutaamri ya kuifilisi IPTL iliyotolewa tarehe 17 Disemba, 2012, hivyoWakala kubaki na jukumu la kuwa Mfilisi wa muda (ProvisionalLiquidator) wa Kampuni hiyo hadi shauri hilo litakapomalizika.

Mheshimiwa Spika, katika masuala ya udhamini,Wakala una jukumu la kusimamia mali zisizokuwa na uangalizimaalumu, mali zisizokuwa na mwenyewe na zile zinazopaswakumilikiwa na watoto walio chini ya umri wa miaka 18 ambaohawana waangalizi maalum (Guardians), kwa mujibu waSheria ya Mdhamini wa Serikali ambapo Wakala(Administrator General), huteuliwa na Mahakama kamaMdhamini wa Serikali (Public Trustee).

Mheshimiwa Spika, pia, Wakala husimamia mirathibaada ya kuombwa na ndugu wa marehemu au kuteuliwana Mahakama. Shughuli nyingine inayofanyika ni kusajiliMiunganisho ya Wadhamini ili kuwapatia nguvu ya kisheriaya kumiliki mali kwa niaba ya Taasisi zao. Wadhamini waTaasisi za Kijamii, Kidini, Mifuko ya Maendeleo ya Kijamii, Vilabuvya Michezo pamoja na Vyama vya Siasa husajiliwa kwamujibu wa Sheria ya Muunganisho wa Wadhamini, Sura ya318, Toleo la 2002. Hadi kufikia Machi, 2013, Wakala umesajiliMiunganisho ya Udhamini 204 na kutoa elimu kwamadhehebu ya dini mbalimbali na kutoa hati za usajili kwaWadhamini wa Vyama vya Siasa, Vikundi, Makanisa, Misikitina Mali zipatazo151. Pia, Wakala imetembelea Vikundi vyaUdhamini katika Wilaya ya Morogoro, Iringa na Arusha.

Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuboreshamazingira ya kazi, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini,unaendelea na ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Ofisi zaWakala lililopo katika Mtaa wa Makunganya Mjini Dar esSalaam ambao unatarajiwa kukamilika katika Mwaka waFedha wa 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, katika kuiimarisha Taasisi yaMafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School

Page 68: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

68

3 MEI, 2013

of Tanzania), Wizara yangu kupitia Programu ya Maboreshoya Sekta ya Sheria (Legal Sector Reform Programme),imekamilisha ujenzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi hiikatika kiwanja Na. 2005/2/1 Sam Nujoma/Mpakani, Sinza, Dares Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 16.1 zilitumika katika ujenzihuo. Kwa sasa Taasisi hii inaendesha mafunzo katika majengohayo baada ya kuhamia hapo Agosti, 2012. Kukamilika kwamajengo hayo kutaiwezesha Taasisi hii kuongeza udahili wawanafunzi kufikia 1,500 kwa mwaka.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2012 –Februari, 2013, Taasisi hii ilidahili wanafunzi wapya 736. Aidha,Taasisi hii imetoa mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo kwawanafunzi 585 waliosajiliwa katika Mwaka wa Fedha wa 2011/12, ambao walikuwa wanaendelea na mafunzo. Katikakipindi hicho, jumla ya wanafunzi 1,136 walifanya mitihani yamwisho na wanafunzi 409 walifaulu mitihani hiyo na kupatasifa ya kusajiliwa kuwa Mawakili wa Kujitegemea. Wanafunzi861 walitakiwa kurudia mitihani mbalimbali (SupplementaryExaminations) ya kukamilisha mafunzo yao wakati wanafunzi43 walishindwa mitihani.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kutoa fedhakupitia Wizara yangu kwa ajili ya kuwapa ruzuku wanafunziwahitaji wa Taasisi hii kwa ajili ya kugharamia mafunzo. TanguJulai, 2012 hadi sasa jumla ya Shilingi 2,232,558,500.00zimetolewa na Serikali kwa ajili ya ruzuku kwa wanafunzi hao.Aidha, mchakato wa kurejea Sheria ya Bodi ya Mikopo yaElimu ya Juu ya Mwaka 2004 umeanza ambapo suala laMikopo kwa Wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwaVitendo yamezingatiwa.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2012 hadiFebruari, 2013, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto(Institute of Judicial Administration), kilidahili wanafunzi 551wa Mwaka wa Kwanza wa Stashahada ya Sheria naWanafunzi 634 wa Cheti cha Sheria. Kulikuwa na Wanafunzi273 wa Mwaka wa Pili wa Stashahada ya Sheria waliokuwawanaendelea na mafunzo. Jumla ya wanafunzi 706walihitimu mafunzo, ambapo 223 walitunukiwa Stashahada

Page 69: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

69

3 MEI, 2013

ya Sheria na 483 walitunukiwa Cheti cha Sheria. Aidha, Chuokiliendesha mafunzo ya awali (Induction Course) kwa ajili yaMahakimu Wakazi wapya 290 waliokuwa wameajiriwakufanya kazi katika Mahakama za Mwanzo sehemumbalimbali hapa nchini. Mafunzo hayo ni sehemu ya MpangoMkakati wa Chuo ya kuanzisha na kuendesha mafunzomahususi na endelevu kwa Majaji, Mahakimu na Watumishiwengine wa Mahakama ya Tanzania. Vile vile, Chuo kimefikiaasilimia 50 ya ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kiume 300linalotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Juni, 2013.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali inahakikisha uboreshaji wa mfumo wa teknolojia yahabari, elimu na mawasiliano, unapewa umuhimu wakutosha. Katika kutekeleza azma hiyo, hatua ya kuunganishakwenye Mfumo mmoja wa mawasiliano (WAN), Makaomakuu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Divisheniya Mashtaka na Kanda ya Dar es Salaam imeanza. Katikakutekeleza hili, usimikaji wa Local Area Network (LAN),ambayo ni ya kisasa, yenye uwezo wa kusafirisha na kupokeasauti, picha na takwimu, imeanza kufungwa Makao Makuu.Lengo ni kurahisisha, kuboresha mawasiliano na kuongezaufanisi wa kazi. Aidha, Tovuti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuuwa Serikali (www.agctz.go.tz) imeendelea kufanya kazi ikiwani pamoja na kutoa taarifa mbalimbali kwa jamii. Pia,Software ya kutunza kumbukumbu za vitabu vya maktabaimekamilika na imeanza kutumika.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Ofisi imeendelea kutoaelimu kwa umma kwa njia mbalimbali ikiwemo kushiriki katikavipindi vya redio na runinga juu ya masuala ya Katiba naHaki za Binadamu, mikataba, uandishi wa sheria, uendeshajiwa mashauri ya madai na usuluhishi, masuala ya haki jinaipamoja na majukumu ya Ofisi kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali inaendelea kuandaa mtandao wa kompyutaujulikanao kama Case Docket Management System,utakaowezesha utunzaji wa nyaraka mbalimbali za mashaurinchini. Mfumo huu utakapokamilika, utaimarisha upatikanaji

Page 70: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

70

3 MEI, 2013

wa takwimu za kesi na masuala mengine ya uendeshajimashauri. Ofisi pia ipo katika hatua za usimikaji wa mfumowa eletroniki kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu za uendeshajimashauri katika ofisi zote za mikoa baada ya kazi ya kufungamfumo kukamilika katika Makao Makuu na Mkoa wa Dar esSalaam.

Mheshimiwa Spika, Wizara pia imekamilisha usimikajiwa mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu (Data Center), ambaolengo lake ni kuunganisha mifumo ya utunzaji kumbukumbuza Taasisi zilizo chini ya Wizara. Sambamba na uimarishaji wamifumo ya teknolojia, Wizara iliendelea na jukumu la kutoaelimu kwa umma kwa njia ya vipindi vya redio na runingakuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utoaji na usimamiziwa haki. Vilevile, Wizara imeingia Mkataba wa makubalianona Kampuni Tanzu ya Serikali ya China ya ZTE Corporation ilikufanya upembuzi yakinifu wa kusimika mfumo wa e-justicekatika Mahakama na Magereza ili kurahisisha usikilizaji wakesi. Upembuzi huo yakinifu umekwishaanza na unaendeleakufanyika. Mpango huu wa kusikiliza kesi kwa kutumia mfumomaalum wa e-justice i l ikuwa ni ahadi yangu wakatinikiwasilisha bajeti ya mwaka 2012/2013 Bungeni. Utaratibuwa kutekeleza Mradi huu unaendelea kwa kuratibiwa naWizara yangu.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2012/2013, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa Ufadhili waShirika la Umoja wa Mataifa (UNDP), iliwajengea uwezo wakitaalamu Mawakili kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali, Wanasheria na Wataalam wengine walio katikaWizara mbalimbali na Idara za Serikali.

Mafunzo haya yalihusu nyanja za kujadili, kuandikana kuhakiki mikataba kwa lengo la kuimarisha usimamizi wahatua zote za majadiliano ya mikataba ili kuweza kubainimatatizo kabla ya mikataba kusainiwa na hatimaye kuwana mikataba yenye maslahi kwa Taifa. Vilevile, Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali inatekeleza Mradi wa KujengaUwezo katika Mapambano Dhidi ya Rushwa (STACA). Kazizilizofanyika kwa Mwaka 2012/2013 kutokana na Mradi huu

Page 71: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

71

3 MEI, 2013

ni kufanya mapitio ya Sheria mbalimbali zinazokinzana,kufanya mapitio ya mafaili ya kesi za rushwa kwa kuzitoleaushauri, maandalizi ya Hadidu za Rejea kwa ajili ya kupatamtaalam mwelekezi wa kutengeneza mwongozo wa maadilikwa waendesha mashtaka na kuandaa majarida (journals)mbalimbali ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na jukumu lakuratibu na kutekeleza Programu ya Maboresho ya Sekta yaSheria kwa Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Sheria ambazo niMahakama ya Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Taasisi ya Mafunzoya Uanasheria kwa Vitendo, Tume ya Haki za Binadamu naUtawala Bora na Sekretarieti inayoratibu huduma ya msaadawa Kisheria (Legal Aid Secretariat).

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai hadiFebruari, 2013, Programu imetekeleza kazi zifuatazo:Kukamilisha ujenzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi yaMafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (Law School ofTanzania); Kuendesha mafunzo ya Jinsia kwa Watumishi tokaTaasisi zinazotekeleza Programu kwa lengo la kupatawakufunzi watakaoendelea kutoa mafunzo haya ndani yaTaasisi husika; na kutayarisha andiko la mchakato wakuandaa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria. Aidha,wahisani wamekubali kuongeza kipindi cha utekelezaji waProgramu hii kwa mwaka mmoja zaidi hadi Juni, 2014 ilikukamilisha malengo yaliyochelewa kufikiwa. Programu yaMaboresho ya Sekta ya Sheria ilipaswa kuisha Juni, 2013.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Mahakamaya Tanzania imekarabati na kujenga Mahakama kamaifuatavyo:-

(i) Ukarabati wa Jengo la Mahakama Kuu Dares Salaam na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutuunaendelea.

(ii) Ujenzi wa mabweni ya Chuo cha MahakamaLushoto unaendelea.

Page 72: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

72

3 MEI, 2013

(iii) Ujenzi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ukokatika hatua ya mwisho ambapo unategemewa kukamilikamwezi Juni, 2013.

(iv) Ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Kisaraweumekamilika.

(v) Ujenzi wa Mahakama Kuu Bukobaumekamilika na awamu ya pili ya ujenzi wa Jengo laMahakama Kuu Shinyanga unaendelea.

(vi) Magari 33 yamenunuliwa yakiwemo magari32 ya Waheshimiwa Majaji na basi moja kwa ajili ya Watumishiwa Wizara.

Mheshimiwa Spika, katika kuleta ufanisi na tija kazini,jumla ya watumishi 579 wa Wizara na Taasisi zakewamepatiwa mafunzo ya muda mrefu na mfupi katika fanimbalimbali nje na ndani ya nchi ikiwa ni pamoja na mafunzokazini (on job training). Watumishi 13 wamepandishwa vyeona watumishi 15 walihudhuria mikutano mbalimbali ya kitaifana kimataifa kuiwakilisha Wizara katika masuala mbalimbali.Aidha, Tume ya Utumishi wa Mahakama hadi kufikia mweziFebruari, 2013 imefanya vikao viwili vya kawaida na vikaoviwili vya dharura ambapo watumishi 17 waliajiriwa katikamasharti ya kudumu na malipo ya pensheni; Mahakimu 98walithibitishwa katika cheo pamoja na kuthibitisha kaziniHakimu mmoja. Tume kupitia vikao hivyo ilishughulikiamasuala saba ya kinidhamu ambapo sita walirejeshwa kazinina mmoja alifukuzwa kazi.

Mheshimiwa Spika, Tume ya Utumishi wa Mahakamailikamilisha mchakato wa kumpata Mtendaji Mkuu waMahakama, Msajil i Mkuu wa Mahakama, Msajil i waMahakama ya Rufani na Msajili wa Mahakama Kuu. Tumepia ilifanya ziara Katika Mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera,kwa lengo la kutoa elimu kwa Watumishi wa Mahakama naKamati za Maadili za Mikoa na za Wilaya kuhusu utendajiwake. Aidha, Tume imekagua Kamati za Maadili za Mikoana Wilaya katika Mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha,

Page 73: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

73

3 MEI, 2013

Manyara, Dodoma, Morogoro na Pwani. Lengo la ukaguzihuu ni kufuatilia uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibuzilizowekwa.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendeleakutekeleza majukumu yake ya msingi na kupata mafanikiombalimbali. Hata hivyo, Wizara pia imeendelea kukabiliwana changamoto. Baadhi ya Changamoto hizi ni kamaifuatavyo:-

(i) Baadhi ya Taasisi kukosa Ofisi zake za kudumuna hivyo kutumia gharama kubwa kwa ajili ya kulipia pango.

(ii) Bajeti inayotengwa kwenye Wizara na Taasisizake imeendelea kuwa pungufu ikilinganishwa na mahitajihalisi ya kutekeleza majukumu ya Wizara ambayo yamekuwayakiongezeka mwaka hadi mwaka.

(iii) Wizara inakabiliwa na upungufu wa rasilimaliwatu katika Taasisi zake, hali ambayo inaathiri ufanisi wa utoajihaki kwa Wananchi.

(iv) Baadhi ya Wananchi kukosa imani na vyombovya utoaji haki kutokana na baadhi ya watumishi wasiowaadilifu kuendelea kulalamikiwa kwa kujihusisha na vitendovya rushwa.

(v) Suala la mikopo kwa wanafunzi wa Taasisi yaMafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo limekuwa tatizo kubwakwa Wizara na kwa wanafunzi husika ambao ni wahitimu waShahada ya Kwanza. Hali hii inatokana na Sheria ya Bodi yaMikopo inayowaruhusu wanafunzi wa Shahada ya Kwanza(undergraduate) peke yake kupata mikopo hiyo.

(vi) Uwezo na uelewa mdogo wa Wananchi waliowengi kutumia vyombo vya kutoa haki na huduma za Kisheriakuhusu mfumo uliopo wa Sheria.

(vii) Mazingira ya kazi yasiyoridhisha kwa watumishi

Page 74: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

74

3 MEI, 2013

walio wengi yanayotokana na maslahi duni na uhaba wavitendea kazi ikiwa ni pamoja na vyombo vya usafiri.

Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuzipatia ufumbuzichangamoto nilizozielezea, Wizara pamoja na Taasisiinaendelea kuchukua hatua zifuatazo:-

(i) Kuendelea kuomba na kufuatilia vibali ilikujaza nafasi zilizo wazi katika Muundo na kurejea Miundo iliitosheleze mahitaji ya Taasisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

(ii) Kuboresha mazingira ya kazi kwa kujenga nakukarabati Majengo ya Mahakama na Ofisi za Wizara naTaasisi.

(iii) Kuendelea kuainisha vipaumbele vya Wizarana Taasisi zake na kujenga hoja ya kuongezewa Bajetikulingana na uwezo wa Serikali.

(iv) Kuwajengea watumishi uwezo na ujuzi wataaluma zao.

(v) Kuimarisha uwajibikaji na uadilifu kwakusimamia vyema Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo yautekelezaji wa majukumu.

(vi) Kufanya mawasiliano na Uongozi wa Bodi yaMikopo ya Elimu ya Juu na kupendekeza Marekebisho yaSheria iliyoanzisha Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwaVitendo ya Mwaka 2007 kufanyika ili kulipatia ufumbuzi tatizola Mikopo kwa Wanafunzi wenye Shahada ya Kwanza yaSheria.

(vii) Kuendelea kutoa elimu ya Sheria na kusogezahuduma za Kisheria kwa Wananchi.

(viii) Kuongeza idadi ya Mawakili wa Serikali, Majaji,Mahakimu na Watumishi wa kada nyingine ili kuongeza kasiya uendeshaji wa mashauri mbalimbali nchini. Lengo ni

Page 75: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

75

3 MEI, 2013

kulipatia ufumbuzi suala la mlundikano wa mashaurimahakamani na msongamano wa Mahabusu na WafungwaMagerezani.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuelezea utekelezaji wamajukumu ya Wizara yangu kwa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, sasa napenda kulielezea Bunge lako Tukufu Mpangona Malengo ya Wizara yangu kwa Mwaka 2013/2014 kamaifuatavyo:-

(i) Kutoa elimu na habari kuhusu utoaji wa hakikwa jamii.

(ii) Kuimarisha utoaji wa huduma za Kisheria.

(iii) Kuhakiki na kushiriki majadiliano ya mikatabambalimbali.

(iv) Kuboresha miundombinu ya utoaji haki.

(v) Kusikiliza na kuendesha Mashauri nchini.

(vi) Kufanya tafiti na tafasiri za Sheria.

(vii) Uandishi wa Sheria na Hati za Serikali.

(viii) Kuimarisha Taasisi za Mafunzo ya Sheria.

(ix) Kuimarisha shughuli za Usaji l i , Ufi l isi naUdhamini.

(x) Kuimarisha Haki za Binadamu na UtawalaBora.

(xi) Kuratibu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.

(xii) Uratibu na utekelezaji wa Programu yaMaboresho ya Sekta ya Sheria na Miradi ya Maendeleo.

Page 76: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

76

3 MEI, 2013

(xiii) Kuimarisha Usimamizi na Uwajibikaji katikarasilimali.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/2014 Wizaraitatekeleza Mpango na Malengo yake ambayo yamezingatiamaelekezo yaliyotolewa na Serikali katika Mwongozo wakewa Utayarishaji Mpango na Bajeti kwa kuzingatia Vipaumbelevya Taifa na Kisekta vilivyoainishwa katika Mpango waMaendeleo wa Miaka Mitano na Mpango wa Pili wa Mwakammoja mmoja, MKUKUTA II na Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2010– 2015). Wizara ya Katiba na Sheria ikiwa moja ya Wizarazilizo chini ya Nguzo ya Tatu ya MKUKUTA II ya Utawala Borana Uwajibikaji, mkazo na msukumo utawekwa katikakuhakikisha kunakuwa na rasilimali za kutosha na mikakatiya utekelezaji wa mpango vinawekwa ili kuimarisha UtawalaBora, Utawala wa Sheria na uwajibikaji katika kusimamiamatumizi ya rasilimali na upatikanaji wa haki kwa wakati ikiwani pamoja na kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya Katibakwa ufanisi.

Mheshimiwa Spika, aidha, Mpango na Malengo yaWizara yangu yamelenga kutoa kipaumbele cha kusogezahuduma za utoaji haki karibu na Wananchi kwa kuendeleakuimarisha na kujenga miundombinu muhimu ya utoaji haki,kujenga uwezo wa watumishi na kuongeza vitendea kazikatika Sekta ya Sheria. Malengo yafuatayo yatatekelezwa:-

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu itaendeleaKuboresha Mfumo wa matumizi ya TEHAMA katika usikilizajiwa mashauri na utunzaji kumbukumbu pamoja na takwimumbalimbali. Hivyo, kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014Wizara itatekeleza yafuatayo:-

(i) Kuendelea kupanua mtandao wa kielektronikikwa ajili ya kusikiliza au kuendesha Mashauri na shughulimbalimbali za kiofisi.

(ii) Kuandaa Sera na Mkakati wa TEHAMA kwa Wizarana Mahakama.

Page 77: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

77

3 MEI, 2013

(iii) Kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu kwa kutumiamtandao wa kompyuta.

(iv) Kuongeza matumizi ya kompyuta katika shughulimbalimbali za kiofisi;

(v) Kuimarisha mafunzo ya ujuzi wa TEHAMA.

(vi) Kutayarisha programu mbalimbali zitakazojadiliwakwenye vyombo vya habari kwa ajili ya kuelimisha ummakuhusu masuala ya Sheria, Haki za Binadamu na Utawala Borana majukumu ya Wizara pamoja na Taasisi zake kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea na mchakatowa kutunga Sheria itakayoratibu Utoaji wa Huduma zaKisheria kwa Umma na kutambua watoa huduma za msaadawa Kisheria kwa umma ikiwa ni pamoja na Wasaidizi waKisheria (Paralegals). Aidha, Wizara itaendelea kupokea nakushughulikia malalamiko mbalimbali toka kwa Wananchiyanayohusu upatikanaji wa haki zao.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali itahakikisha kuwa maslahi ya Taifa yanapewakipaumble katika mashirikiano ya Kitaifa, Kikanda naKimataifa. Aidha, mashirikiano haya yanakuwa na mchangomkubwa kwa maendeleo ya Wananchi kwa ujumla. Katikakutekeleza lengo hili, ofisi imepanga kutekeleza shughulizifuatazo:-

(i) Kushiriki katika masuala ya Mtangamano waKikanda kwa masilahi ya Taifa.

(ii) Kutoa ushauri wa kisheria na kufanyamajadiliano ya mikataba ya kibiashara na Mikataba yaMahusiano ya Kikanda na Kimataifa (Contracts & Treaties).

(iii) Kuimarisha uwezo wa kutayarisha taarifambalimbali zinazojadiliwa katika Mikutano ya Kikanda naKimataifa.

Page 78: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

78

3 MEI, 2013

(iv) Kushiriki katika mikutano ya Kamati mbalimbaliza uanachama wa vyombo mbalimbali vinavyohusika nauendeshaji wa mashauri ya jinai, madai, kikatiba na haki zabinadamu.

Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka 2013/2014, Wizarayangu kupitia Mahakama, imepanga kuendelea na ujenziwa Mahakama Kuu ya Shinyanga na kuanza ujenzi waMahakama Kuu katika Mikoa ya Kigoma, Mara, Lindi naMorogoro. Aidha, Kanda Maalum ya Mahakama Kuu Ilalana baadaye Temeke na Kinondoni, zitaanzishwa ili kuwezakusogeza huduma karibu zaidi na Wananchi.

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira yakazi, Mahakama itaanza ujenzi wa nyumba za Majaji katikaMkoa wa Dar es Salaam na pia kuboresha masjala zaMahakama Kuu, Mahakama za Hakimu Mkazi, Mahakamaza Wilaya na Mahakama za Mwanzo kwa kuanzia na zilezilizoko mijini. Aidha, Mahakama pia itafanya upanuzi waJengo la Mahakama Kuu Dodoma na kuanza ujenzi waMahakama za Mwanzo za Bunda, Ludewa, Bariadi, Kawe,Mkomazi, Mailimoja, Lukuledi, Gairo, Mangaka naNyamikoma.

Mheshimiwa Spika, Mahakama pia ipo katika hatuaza awali za kuanzisha Programu Maalum ya Ujenzi waMahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzo kwakushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Mikoa, Wilayana Halmashauri husika. Ni matumaini yangu makubwa kuwa,Programu hiyo itasaidia katika kufanikisha lengo kuu la Wizarala kusogeza huduma karibu na Wananchi.

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali, itaendelea kuimarisha Ofisimpya zilizoanzishwa katika Mikoa na Wilaya kwa kuzijengeauwezo wa kuendesha mashauri mbalimbali ili kuongezaufanisi katika utoaji haki kwa ujumla. Aidha, Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali itafungua Ofisi mpya katikaMikoa ya Geita, Simiyu, Katavi na Ofisi moja katika Wilaya yaTarime. Vilevile, Wizara itafanya ukarabati wa Jengo la Ofisi

Page 79: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

79

3 MEI, 2013

za Wizara (Makao Makuu) na kukamilisha ujenzi wa Jengo laMakao Makuu ya RITA. Tume ya Haki za Binadamu na UtawalaBora itaendelea kuimarisha Ofisi zake za Kanda na itaanzishaOfisi nyingine za Kanda za Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu itaendelea kusikilizana kuyatolea maamuzi mashauri katika ngazi mbalimbali zaMahakama, kupitia Programu Maalum ya KumalizaMlundikano wa Mashauri ya Nyuma 1,918 yaliyokoMahakama ya Rufani, 12,093 Mahakama Kuu, 329 yaliyokoMahakama Kuu - Divisheni ya Biashara, 1,780 yaliyokoMahakama Kuu - Divisheni ya Kazi, 5,393 yaliyoko MahakamaKuu - Divisheni ya Ardhi, 25,370 yaliyoko Mahakama za HakimuMkazi, 21,538 yaliyoko Mahakama za Wilaya na 197,715yaliyoko Mahakama za Mwanzo.

Mheshimiwa Spika, aidha, Mahakama pia itaongezakasi ya usikilizaji wa mashauri katika ngazi za Mahakama zaMikoa (RMs na Wilaya) kwa kutenganisha shughuli zaKimahakama na za Kiutawala. Vilevile, Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali itaendesha Mashauri ya Madai, Katiba naJinai na kushughulikia mashauri ya zamani na menginemapya yatakayopokelewa.

Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka 2013/2014 Wizarayangu itaendelea kufanya mapitio ya Mfumo wa sheriazinazosimamia huduma za jamii kwa wazee, sheriazinazomlinda mlaji na sheria za makosa ya jinai. Kutafsiri Sheriakutoka Lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili, kufanyauchambuzi wa hukumu za kesi za Mahakama ya Rufani ilikuainisha misingi ya kisheria na kuziweka kwenye Tovuti yaTume ya Kurekebisha Sheria. Aidha, Wizara yangu itafanyamapitio ya Sheria mbalimbali ili kuhakikisha kuwa hazikinzanina Katiba ya Nchi na Misingi ya Haki za Binadamu.

Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa kuwana Mfumo wa Sheria nchini unaokidhi mahitaji ya jamii katikakujiletea maendeleo kiuchumi, kijamii na kiteknolojia, Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali itatekeleza yafuatayo:-

Page 80: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

80

3 MEI, 2013

(i) Kusimamia uandishi, tafsiri na urekebu waSheria mbalimbali za Nchi.

(ii) Kutayarisha Maazimio mbalimbali yaKimataifa ambayo Nchi imeweka saini ili yaridhiwe na Bunge.

(iii) Kuwezesha upatikanaji wa Sheria mbalimbalizilizotungwa na Bunge.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu itaendeleakuimarisha Taasisi za Mafunzo ya Sheria kwa kuanzishaushirikiano maalum wa maendeleo ya watumishi kati yaMahakama, Chuo cha Uongozi wa Mahakama na Taasisi yaMafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendeleakuimarisha shughuli za Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) ili kuhakikisha kwamba, lengo la Taasisi hii la kuwaWakala linafikiwa kwa ufanisi. Katika Mwaka wa Fedha 2013/2014, Wakala unatarajia kuupeleka Mfumo wa Usajili wawatoto walio chini ya umri wa miaka mitano (Under 5 BirthsRegistration Initiative - U5BRI) hadi ngazi ya Serikali za Mitaa,ili kupunguza mlundikano wa vizazi ambavyo havijasajiliwana kumwezesha mtoto kupata cheti cha kuzaliwa ambachoni haki yake ya msingi. Mpango huu unatarajiwa kuanza rasmikatika Mkoa wa Mbeya na kuendelea kuutekeleza katikaMikoa ya Simiyu, Geita, Shinyanga na Mwanza. Katika Mfumohuu, utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa mara ya kwanzahutolewa bila tozo kwa watoto wote walio na umri wa chiniya miaka mitano. Aidha, Wakala pia utatekeleza mkakati wakusajili watoto wa umri kati ya miaka 6 hadi 18 (6 - 18 BirthRegistration Initiative) waliopo mashuleni kwa kutumia Bajetiya Serikali.

Mheshimiwa Spika, vilevile Wakala unatarajiakuanzisha mazungumzo kati yake na NIDA pamoja naUhamiaji, ili kuona namna ya kupunguza gharama za usajilikwa kutumia Mifumo ambayo tayari ipo kwa ajili yauandikishaji na uchapishaji wa vyeti.

Page 81: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

81

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali imedhamiria kuhakikisha kuwa Sheria na taratibuzil izowekwa na mamlaka mbalimbali kuhusu haki zabinadamu zinafuatwa wakati wote wa utekelezaji wamajukumu mbalimbali. Kwa kuzingatia hilo, Ofisi imedhamiriakufanya yafuatayo:-

(i) Kutoa ushauri wa kisheria ulio bora katikamasuala ya Katiba na Haki za Binadamu.

(ii) Kuandaa taarifa za utekelezaji wa masuala yahaki za binadamu nchini kwenye Mikataba ya Kikanda naKimataifa ya Haki za Binadamu ambayo Nchi imeridhia nakuziwasilisha kwenye vyombo husika kwa ajili ya majadiliano.

(iii) Kufanya ukaguzi katika maeneoyanayohifadhi mahabusu na wafungwa ili kutoa ushauri wanamna ya kuboresha.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Tume ya Hakiza Binadamu na Utawala Bora, itaendelea kulinda, kukuzana kuhifadhi Haki za Binadamu na Utawala Bora. Katikamwaka 2013/2014, Tume ya Haki za Binadamu na UtawalaBora, itaendelea kukamilisha uchunguzi wa mashauri yauvunjwaji wa Haki za Binadamu ambao haukukamilika;kufanya tafiti kuhusu Haki za Binadamu na Utawala Bora;kupitia Miswada na Sheria ili kuangalia kama zinakidhi vigezovya kimataifa na vya kikanda ili kulinda Haki za Binadamu naUtawala Bora; na kukagua Magereza na Vituo vya Polisi nasehemu nyinginezo wanamozuiliwa watu. Aidha, Tume yaHaki za Binadamu na Utawala Bora itaendelea kushughulikiamalalamiko yaliyosalia na yatakayopokelewa, yanayohusuuvunjwaji wa haki za binadamu.

Mheshimiwa Spika, katika kusimamia maadili yaMahakimu, Wizara yangu kupitia Tume ya Utumishi waMahakama, itaendelea kuzijengea uwezo Kamati za Maadiliza Mikoa na Wilaya kwa Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha,Manyara Tanga, Dodoma na Singida, kwa kuzipatia mafunzoili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Aidha, Tume

Page 82: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

82

3 MEI, 2013

itaendelea na kazi ya kukagua Kamati za Maadili za Mkoana Wilaya kwa Mikoa ya Mtwara, Lindi, Mbeya, Rukwa naKatavi. Lengo likiwa ni kuona kama zinatekeleza majukumuyake kwa misingi ya sheria na taratibu. Tume itaitisha vikaovinne vya kawaida kwa ajili ya kujadili na kuamua masualambalimbali ya watumishi.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu itaendelea kuratibujambo kubwa na la kihistoria nchini mwetu ambalo nimchakato wa mabadiliko ya Katiba. Awamu ya kwanza yaukusanyaji wa maoni ya Wananchi na Makundi mbalimbaliimekamilika. Hivi sasa Tume ya Mabadiliko ya Katibainaendelea na uchambuzi wa maoni hayo ili kuandaa Rasimuya Katiba itakayowasilishwa kwenye Mabaraza ya Katiba.Aidha, katika Mwaka wa Fedha wa 2013/2014, Wizara yangukupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba, inategemea kufanyamambo yafuatayo il i kukamilisha mchakato huu wamabadiliko ya Katiba:-

(i) Kusimamia Mikutano ya Mabaraza ya Katiba.

(ii) Kuchambua maoni yatakayotolewa na Wajumbewa Mabaraza ya Katiba.

(ii) Kuchapisha Ripoti na Rasimu ya Katiba.

(iv) Kuwasilisha Rasimu ya Katiba katika BungeMaalum la Katiba.

(v) Kutoa elimu na kuhamasisha Wananchi kushirikikatika Kura ya Maoni.

Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu wamchakato huu wa mabadiliko ya Katiba, kupitia kwenuWaheshimiwa Wabunge, ninaomba muwahamasisheWananchi wa Majimbo yenu ili waweze kujitokeza kwa wingikatika kutoa mawazo kuhusu Rasimu ya Katiba kupitia kwaWajumbe wanaounda Mabaraza ya Katiba.Nawahamasisha na kuziomba Taasisi, Asasi za Kiraia, Jumuiaza Kidini, Vyama vya Siasa na Makundi mengine yote, kuunda

Page 83: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

83

3 MEI, 2013

Mabaraza ya Katiba. Aidha, ninawaomba Wajumbe waMabaraza kutoa mawazo yao kwa uwazi, uhuru na bila yahofu yoyote. Pia nipende kuwahakikishia Wananchi kuwa,Tume inafanya kazi zake kwa uhuru na uwazi na kwamba,maoni yote yaliyotolewa na yatakayotolewa na Wananchi,Taasisi, Asasi za Kiraia na Makundi mengine, yanaheshimiwana kufanyiwa kazi ipasavyo.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu itaendeleakutekeleza Mpango Mkakati wa Muda wa Kati (Medium TermStrategy) wa Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria naMiradi ya Maendeleo, kwa kuendelea kuziwezesha Taasisizinazotekeleza Programu hii kuboresha Mfumo wa Sheria nakuimarisha mazingira ya kisheria yanayoongeza fursa yaWananchi ya kupata haki kwa wakati ili kuwezesha jamiikutumia muda wao mwingi katika kujihusisha na kazi zamaendeleo ya kiuchumi na kijamii, badala ya kupoteza mudahuo wakitafuta haki. Aidha, napenda kulitaarifu Bunge lakoTukufu kuwa, Wizara imekwishaanza kujiandaa kukamilishana hatimaye kufunga Programu kwa kuanza kutekeleza kaziya kufanya tathmini ya hali ya sasa ya Sekta hii (Legal SectorAssessment) ili kujua kiwango cha maendeleo kilichofikiwa,kubaini changamoto zinazoikabili Sekta hii na kutambua fursazilizopo na ambazo zinaweza kutumika kikamilifu katikamipango hiyo ya kuboresha sekta hii muhimu.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendelea kubunimbinu na kuanzisha Miradi mbalimbali ya Maendeleo yakuboresha huduma zitolewazo na Taasisi mbalimbali za Sheria,ili kuweza kufikia dira yetu ya ‘haki sawa kwa wote na kwawakati’. Kama ambavyo nililiarifu Bunge lako Tukufu mwakauliopita kwamba, Wizara yangu imebuni na itaanzisha Mradiwa e-justice; ninafurahi kulialifu Bunge lako Tukufu kwamba,tayari hatua za awali za Mradi huu zimekwishaanza na Serikaliya China imeridhia kufadhili Mradi huu. Tayari kazi yaupembuzi yakinifu wa Mradi huo inafanywa na Kampuni yaZTE Corporation, iliyokasimiwa kazi hiyo na Serikali ya China.Kutegemeana na taarifa ya upembuzi yakinifu wa Mradi huuitakayoandaliwa, Wizara yangu itatekeleza Mradi huu kwaawamu tatu. Awamu ya kwanza ikiwa ni majaribio (Pilot

Page 84: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

84

3 MEI, 2013

Study) kwa Mkoa wa Dar es Salaam, kisha kuhusisha Mikoayote yenye Kanda za Mahakama Kuu kwa awamu ya pili naawamu ya tatu kukamilisha Mradi kwa kufikia Mikoa yoteTanzania Bara.

Mheshimiwa Spika, katika kuzingatia umuhimu wakuwepo na Mikataba mizuri yenye maslahi kwa Taifa, Ofisiya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, itaendelea kuwajengeauwezo wa kitaalam Mawakili wa Serikali katika nyanja zakujadili, kuandika na kuhakiki mikataba kupitia Mradi waUNDP unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UNDP).Katika uendeshaji wa mashauri ya rushwa, Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali itaendelea kutekeleza Mradiwa Uimarishaji wa Mapambano Dhidi ya Rushwa Tanzania(STACA), kwa kuwajengea uwezo Mawakili wa Serikali katikauendeshaji wa mashauri ya rushwa, ununuzi wa vitendea kazi,uimarishaji wa mfumo wa utunzaji na usimamizi wakumbukumbu za mashauri kielektroniki (Case DocketManagement System).

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imezingatia lengohili katika mipango yake ili kuhakikisha kwamba kunakuwana usimamizi madhubuti wa rasilimali mbalimbali za Serikali.Katika kufanikisha lengo hili, mambo yafuatayo yatafanyika:-

(i) Kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha katika Ofisiza Makao Makuu na Mikoa kwa Taasisi zote za Wizara.

(ii) Kufanya ukaguzi wa vifaa mbalimbali vilivyopo navinavyonunuliwa katika Ofisi zote.

(iii) Kutayarisha ratiba ya utekelezaji wa mpango kaziwa malengo yaliyopangwa na Wizara na Taasisi zake ilikuwezesha utekelezaji na utoaji wa taarifa.

(iv) Kuimarisha uratibu, ufuatiliaji na tathmini yautekelezaji wa mipango ya Wizara.

(v) Kuimarisha uwajibikaji na uadilifu katika utendajiwa kazi katika ngazi mbalimbali.

Page 85: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

85

3 MEI, 2013

(vi) Kuwaongezea watumishi maarifa na ujuzi katikamaeneo yao ya kitaalam ili wawe na tija wakati wakutekeleza majukumu yao hasa katika maeneo ambayoyameonekana kuwa na changamoto nyingi katika kuletaufanisi wa utendaji.

(vii)Kuandaa Mpango thabiti wa rasilimali watu kwaWizara na Taasisi na kuchambua mahitaji ya ujuzi kwa kilaeneo la utekelezaji.

Mheshimiwa Spika, naomba nitumie nafasi hiikuwashukuru sana wadau wetu wa maendeleo kwakuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha Sekta yetuya Sheria. Kwa namna ya pekee, napenda kushukuru Nchiza Canada na Denmark ambazo kupitia Mashirika yao yaKimataifa ya Maendeleo ya CIDA na DANIDA, wameisaidiasana Wizara yangu katika kushawishi Mashirika na nchinyingine wahisani, kuelekeza misaada yao katika kuboreshaSekta ya Sheria. Nayashukuru pia Mashirika na Taasisisi zaKimataifa zifuatazo; Benki ya Dunia (WB), Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo ya Watoto (UNICEF), Shirika la Umojawa Mataifa la Maendeleo (UNDP) na Taasisi ya Maendeleoya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza (DFID).

Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani za pekeekwa wadau mbalimbali wa Sekta ya Sheria kwa ushirikianona ushauri uliowezesha kutekelezwa kwa majukumu ya Wizarakwa mwaka 2012/2013 kama yalivyobainishwa katika Hotubahii. Ninapenda kumshukuru Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mheshimiwa Angellah Kairuki (Mbunge), Jaji Mkuu -Mheshimiwa Othmani Chande, Mwanasheria Mkuu waSerikali - Mheshimiwa Frederick Mwita Werema, Jaji Kiongozi- Mheshimiwa Fakih A.R. Jundu, Katibu Mkuu wa Wizara yaKatiba na Sheria - Ndugu Fanuel E. Mbonde, Mtendaji Mkuuwa Mahakama ya Tanzania - Ndugu Hussein Kattanga, NaibuMwanasheria Mkuu wa Serikali - Ndugu George Masaju, MsajiliMkuu wa Mahakama ya Tanzania - Ndugu Ignas Paul Kitusi,Mkurugenzi wa Mashtaka - Dkt. Eliezer M. Feleshi, KatibuMtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria - Bi. Winifrida Korroso,Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Page 86: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

86

3 MEI, 2013

- Bi. Mary Massey, Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheriakwa Vitendo - Mheshimiwa Dkt. Gerald Ndika, Mtendaji Mkuuwa Wakala wa RITA - Ndugu Philip Saliboko, Wakurugenzi waIdara na Taasisi zilizo chini ya Wizara na Watumishi wote, kwaushirikiano na kazi kubwa waliyoifanya katika kuandaaMpango na Bajeti hii kwa wakati. Ni matarajio yangukwamba, Wizara itaendelea kupata ushirikiano wao katikamwaka 2013/2014 kama walivyofanya nitekeleze majukumuyangu na wajibu wangu kwa ufanisi hadi sasa. Mwisho, natoashukrani kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, kwa kufanikishauchapishaji wa Hotuba hii.

Mheshimiwa Spika, tukitambua kwamba, Sekta yaSheria ndiyo jiwe la msingi katika Utawala wa Serikali na kwakuzingatia umuhimu wa Sekta ya Sheria katika kuchocheamaendeleo ya nchi kiuchumi, kisiasa, kijamii, kisayansi nakiteknolojia, Wizara ya Katiba na Sheria inao wajibu mkubwawa kuhakikisha kwamba, inakuza, inaimarisha na inalindaamani na utulivu na kudumisha haki za binadamu na Utawalawa Sheria nchini.

Mheshimiwa Spika, napenda kutoa wito kwaWananchi wote na Waheshimiwa Wabunge, kuhakikishakuwa azma ya Serikali ya kulinda Amani, Utulivu na Haki zaBinadamu inazingatiwa, inaendelezwa na kupewakipaumbele kwa manufaa ya Taifa letu na kwa kizazi kijacho.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Wizara ya Katiba na Sheria ilitengewa jumla ya Sh.186,323,718,000. Hadi kufikia tarehe 28 Februari, 2013 jumlaya Sh. 86,005,210,966.19 zilikuwa zimekwishatumika. Ilikutekeleza majukumu yaliyopangwa kwa Mwaka wa Fedhawa 2013/2014. Wizara yangu inaomba kuidhinishiwa kiasi chaSh. 230,687,333,000 kwa ajili ya Taasisi, Idara na Vitengo vyaWizara. Matumizi ya Kawaida yanaombewa jumla yaSh.195,427,547,000. Kati ya fedha hizo, Sh.152,890,448,000 nikwa ajili ya Matumizi Mengineyo na Sh.42,537,099,000 ni kwaajili ya Mishahara. Miradi ya Maendeleo inaombewa jumlaya Sh. 35,259,786,000. Kati ya fedha hizi, Sh. 24,000,000,000 niza ndani na Sh.11,259,786,000 ni fedha za nje. Mchanganuo

Page 87: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

87

3 MEI, 2013

wa matumizi ya bajeti kwa mafungu ya Wizara ni kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Fungu 8 - Tume ya Mabadiliko yaKatiba: Matumizi Mengineyo Sh. 33,944,588,000.

Mheshimiwa Spika, Fungu 12 - Tume ya Utumishiwa Mahakama: Matumizi ya Mishahara Sh. 161,882,000,Matumizi Mengineyo Sh. 2,871,716,000. Jumla Sh.3,033,598,000.

Mheshimiwa Spika, Fungu 16 - Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali: Matumizi ya Mishahara Sh. 2,174,186,000,Matumizi Mengineyo Sh. 8,332,865,000, Matumizi yaMaendeleo (nje) Sh. 826,000,000. Jumla Sh. 11,333,051,000.

Mheshimiwa Spika, Fungu 35 - Mkurugenzi waMashtaka: Matumizi ya Mishahara Sh. 4,383,211,000, MatumiziMengineyo Sh. 6,460,826,000, Matumizi ya Maendeleo (nje)Sh. 2,167,759,000. Jumla Sh. 13,011,796,000.

Mheshimiwa Spika, Fungu 40 – Mahakama: Matumiziya Mishahara Sh. 30,980,157,000, Matumizi Mengineyo Sh.86,600,000,000, Matumizi ya Maendeleo (ndani) Sh.20,000,000,000, Matumizi ya Maendeleo (nje) Sh.2,716,668,000. Jumla Sh. 140,296,825,000.

Mheshimiwa Spika, Fungu 41 - Wizara ya Katiba naSheria: Matumizi ya Mishahara Sh. 2,447,110,000, MatumiziMengineyo Sh. 8,028,651,000, Matumizi ya Maendeleo (ndani)Sh. 4,000,000,000, Matumizi ya Maendeleo (nje) Sh.3,898,840,000. Jumla Sh. 18,374,601,000.

Mheshimiwa Spika, Fungu 55 - Tume ya Haki zaBinadamu na Utawala Bora: Matumizi ya Mishahara Sh.1,814,993,000, Matumizi Mengineyo Sh. 3,795,802,000, Matumiziya Maendeleo (nje) Sh. 1,034,169,000. Jumla Sh. 6,644,964,000.

Mheshimiwa Spika, Fungu 59 - Tume ya KurekebishaSheria: Matumizi ya Mishahara Sh. 575,560,000, Matumizi

Page 88: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

88

3 MEI, 2013

Mengineyo Sh. 2,856,000,000, Matumizi ya Maendeleo (nje) Sh.616,350,000. Jumla Sh. 4,047,910,000.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa mwaka 2013/2014 inatarajia kukusanya jumla ya kiasi cha Sh. 5,250,454,700kama maduhuli ya Serikali. Mchanganuo wa makusanyo kwamafungu husika ni kama ifuatavyo: Fungu 16 - Sh. 3,002,000;Fungu 40 - Sh. 2,261,303,900; Fungu 41 - Sh. 2,983,648,800; Fungu55 - Sh. 2,500,000. Jumla Sh. 5,250,454,700.

Mheshimiwa Spika, mchanganuo wa maombi yafedha kwa kila Fungu umeainishwa kwenye Randamazilizoandaliwa kwa kila Fungu na kuwasilishwa hapa Bungenirasmi. Hata hivyo, nitaleta pia mapendekezo ya nyongezakidogo ambayo tumepewa asubuhi hii ya shilingi bilioni 30ambazo tutaziweka kwenye mgawanyo unaohusika.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

SPIKA: Hoja hii imeungwa mkono, tunaendelea nahatua inayofuata.

Waheshimiwa Wabunge, asubuhi wakati Viongozimbalimbali walipokuwa wanaleta nyaraka zao Mezani, huwatunatumia Kifungu cha 99(5), ambacho kinasema hivi:“Asubuhi ya siku ambayo Waziri amepangiwa kuwasilisha hojaya makadirio ya Wizara yake, Waziri, Mwenyekiti wa Kamatiinayohusika au Mjumbe yeyote atakayeteuliwa kwa niabayake na Msemaji wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara husika,wataweka Mezani nakala ya taarifa zao kwa kuzingatiampangilio wa shughuli za Bunge. Ndiyo maana nikasemakwamba, vingine naviona hapa na vingine sivioni.

Mheshimiwa Tundu Lissu, ameniletea ingawa nimeonadistribution yake siyo nzuri, lakini tunakubali, naomba

Page 89: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

89

3 MEI, 2013

mzingatie hivyo. Kuweka Mezani ni pamoja na kuweka hapakwangu, mnaposema na mimi naiona. Siyo kuwekewa mbuzikwenye gunia halafu mnasema mnasema mmepatadocument.

Nashukuru sana. Sasa nimwite msemaji wa Kamatiiliyohusika na suala hili; Mheshimiwa Gosbert Blandes.

MHE. GOSBERT B. BLANDES (K.n.y. MWENYEKITI WAKAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA): Mheshimiwa Spika,kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge,Katiba, Sheria na Utawala, Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana,naomba kutoa Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge yaKatiba, Sheria na Utawala kuhusu utekelezaji wa majukumuya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa2012/2013, pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirioya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99(9)na 117(11), Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2013,naomba kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu, Taarifa yaKamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala,kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Katiba naSheria kwa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 na Maoni yaKamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwaMwaka wa Fedha wa 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Katiba na Sheriainahusisha Mafungu manane; Fungu 8 - Tume ya Mabadilikoya Katiba, Fungu 12 - Tume ya Utumishi wa Mahakama, Fungu16 - Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fungu 35 -Mkurugenzi wa Mashtaka, Fungu 40 - Mahakama, Fungu 41 -Wizara ya Katiba na Sheria, Fungu 55 - Tume ya Haki zaBinadamu na Utawala Bora na Fungu 59 - Tume yaKurekebisha Sheria.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipata muda wa kutoshawa kuchambua Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu yaWizara ya Katiba na Sheria pamoja na Taasisi zilizo chini yake

Page 90: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

90

3 MEI, 2013

kwa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 na Makadirio yaMapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014,yaliyowasilishwa na Mheshimiwa Mathias Chikawe - Waziriwa Katiba na Sheria, akishirikiana na Naibu Waziri -Mheshimiwa Angellah Kairuki. Katika maelezo yake, Wazirialiieleza Kamati kuhusu utekelezaji wa Maoni na Ushauri waKamati kwa kipindi cha mwaka 2012/2013.

Mheshimiwa Spika, wakati wa kuchambua Bajeti yaWizara hii kwa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Kamati ilitoaMaoni na Ushauri katika maeneo mbalimbali ili kuboreshautendaji kazi wa Wizara. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufukwamba, kwa kiasi kikubwa ushauri wa Kamati ulizingatiwa.Kwa yale maeneo ambayo utekelezaji upo katika hatua zaawali, Kamati inasisitiza Wizara ikamilishe utekelezaji wamaagizo hayo.

Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa majukumuyake kwa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Wizara ya Katibana Sheria inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa nipamoja na:-

Ukomo wa bajeti umeendelea kuwa changamotokubwa kwa Wizara kwani kiasi cha fedha kinachotengwakwa Wizara kimekuwa hakikidhi mahitaji halisi ya Wizara naTaasisi zilizo chini yake; Ucheleweshwaji wa mashaurimahakamani pia ni changamoto inayoendelea kuwakikwazo katika mfumo wa utoaji haki nchini; Vitendo vyarushwa kuendelea kujitokeza katika baadhi ya vyombo vyautoaji haki, hali ambayo inasababisha Wananchi kukosaimani na vyombo vya utoaji haki; Serikali kuchelewakuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Bodi yaMikopo kumeendelea kuwa kikwazo kikubwa kwa Wanafunziwa Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa vitendo (The Law Schoolof Tanzania), kwani sheria iliyounda Bodi ya Mikopo haiwapifursa ya kukopa wanafunzi waliomaliza Shahada ya Kwanzaya Sheria.

Mazingira duni ya kufanyia kazi kwa Watumishi waWizara pamoja na Taasisi zake hususan ukosefu wa majengo

Page 91: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

91

3 MEI, 2013

ya Mahakama za Mwanzo, Ofisi za Mawakili wa Serikalipamoja na Taasisi zingine; upungufu wa watumishi katikaTaasisi za Wizara ya Katiba na Sheria, bado ni changamotoinayotakiwa kufanyiwa kazi, upungufu huu unasababishaufanisi kupungua au baadhi ya kazi kutotekelezeka kwawakati; uwezo mdogo wa Wananchi walio wengi kutumiavyombo vya kutoa haki na huduma za kisheria na uelewamdogo wa Wananchi kuhusu mfumo uliopo wa Sheria naMahakama nchini; Serikali kupitia Mahakama kutotoamachapisho ya Ripoti za Maamuzi ya Mahakama kuanziamwaka 1998 – 2006 (The Tanzania Law Reports 1998 - 2006)kwa Umma na badala yake kutumika na Mahakama pekeyake, kumeendelea kuwa kikwazo kwa Mawakili ambaohushindwa kufanya rejea ya Maamuzi hayo kwa kuwamachapisho hayo hayajawekwa tayari ili yaweze kuuzwakwa Mawakili wa Kujitegemea kwa lengo la kuwarahisishiakufanya rejea; Wasaidizi wa Sheria wa Majaji kufanya kazibila kuapishwa kama Maafisa wa Mahakama (JudicialOfficers) kwa muda wa miaka mitatu mfululizo toka waajiriwemwaka 2010 huku wakiwa wanafanya kazi nyeti sanainayohusisha kuwasaidia Waheshimiwa Majaji katika kutoahaki. Kutoapishwa huko kumeendelea kuwanyima baadhiya haki na stahiki zingine ambazo Mahakimu na Maafisawengine wa mahakama wanazipata; hivyo, kuwafanyawajisikie wanyonge na kujihisi kuwa wao siyo sehemu yaMahakama na hivyo kupunguza ari ya kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia taarifazilizowasilishwa mbele ya Kamati na kwa kuzingatia majukumuya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zilizo chini yake,Kamati inatoa maoni na ushauri kwa Wizara na Taasisi zakekama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipata fursa ya kutembeleaTume ya Mabadiliko ya Katiba mnamo tarehe 7 Machi, 2013.Katika ziara hiyo, Kamati i l ielezwa kazi mbalimbalizinazofanywa na Tume na hatua ambayo Tume imefikiakatika ukusanyaji wa maoni ya Wananchi. Kamati inatambuakazi kubwa inayofanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katibakatika kuratibu mchakato mzima wa Mabadiliko ya Katiba.

Page 92: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

92

3 MEI, 2013

Kamati il ipotembelea Tume iliambiwa kuwa, zoezi laukusanyaji wa maoni ya Wananchi limekwishakamilika; hivyo,Tume kuendelea na zoezi la kutathmini na kuchambua maonihayo, kupitia na kuchambua michango, mawazo, taarifa namapendekezo yaliyokusanywa na kufanyiwa tathmini siku zanyuma kwa madhumuni ya kuandaa Rasimu ya Katiba Mpyaili iweze kuchambuliwa kwenye Mabaraza ya Katiba. Pamojana hayo, Kamati inashauri ifuatavyo:-

Moja, Kamati inashauri Serikali kufuatilia kwa makiniutendaji kazi wa Tume hii bila kuathiri uhuru wa Tume ilikuiwezesha nchi kufikia lengo la kupatikana kwa Katiba mpyaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wakati mwafaka.

Mbili, Kamati inashauri kwamba, bajeti ya Bunge laKatiba ifahamike na kuletwa Bungeni mapema kwa ajili yakujadiliwa na kupitishwa.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Tume ya Utumishi wa Mahakama - Fungu 12, ilitengewakiasi cha Sh. 977,101,000. Kufikia Februari, 2013, Tume ilikuwaimepokea kiasi cha Sh. 709,279,940, kiasi hiki cha fedhakimetumika kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwa ni pamojana kuiwezesha Tume kuajiri Mahakimu 17 kwa masharti yakudumu na malipo ya uzeeni. Aidha, Tume imeendelea najukumu lake kubwa la kumshauri Rais kuhusu uteuzi wa JajiMkuu na Majaji wengine wa Mahakama Kuu. Aidha, kwamwaka huu wa fedha wa 2013/2014, Tume ya Utumishi waMahakama imetengewa kiasi cha shilingi 1,471,716,000 kwaajili ya matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo, kiasi chashilingi 161,882,000 ni kwa ajili ya mishahara. Hakuna fedhazozote zilizotengwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo kamailivyokuwa mwaka jana, jambo ambalo Kamati inaona siyojema kwani kutenga fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaidakila mwaka hakutaisaidia Mahakama kupiga hatua zakimaendeleo.

Kamati katika majadiliano ya Makadirio ya Bajetiilishauri Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kuiongezeafedha Tume hii ili iweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi

Page 93: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

93

3 MEI, 2013

zaidi. Kiasi cha shilingi 1,471,716,000 kilichotengwa kwaMwaka wa Fedha wa 2013/2014 hakikidhi mahitajiukilinganisha na majukumu mazito iliyonayo Tume ya Utumishiwa Mahakama.

Kamati inatoa pongezi kwa Jaji Mkuu wa Tanzania,Mheshimiwa Othman Mohamed Chande, kwa kukubalianana ushauri wa Kamati kutekeleza maagizo ya kuiongezeaTume ya Utumishi wa Mahakama kiasi cha fedha hadi kufikiashilingi 2.9 bilioni ili kuiwezesha Tume kifedha kutoka Mfukowa Mahakama kwa lengo la kuziwezesha Kamati za Maadiliza Mikoa na Wilaya kufanya kazi zao kama inavyotakiwakupitia Barua yenye Kumb. Na. CAB.75/197/01 ya tarehe 8Aprili, 2013 iliyotumwa kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba naSheria na kunakiliwa kwa Katibu wa Bunge. Wizara iendeleekuwaelimisha Wananchi kuhusu uwepo wa Tume hii pamojana majukumu yake ili ifahamike na Wananchi wengi zaidi nahatimaye kuwawezesha Wananchi kutoa malalamiko palekunapotokea ukiukwaji wa maadili kwa baadhi ya Watendajiwa Mahakama.

Mheshimiwa Spika, wakati wa kupitia utekelezaji wamajukumu na makisio ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria,Kamati ilishauri ifuatavyo kuhusu Ofisi ya Mwanasheria Mkuuwa Serikali - Fungu 16:-

Moja, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iimarisheKitengo cha Mikataba kwa kuwajengea uwezo wa fedhana rasilimali watu ili Kitengo hiki kiweze kushiriki kikamilifu katikakuingia Mikataba mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.

Mbili, Kamati inashauri Kitengo cha Uandishi waMiswada kinapokuwa kinaandaa Miswada kwa lengo lakuileta Bungeni, kiandae Miswada kwa Lugha ya Kiswahili naKiingereza ili hatimaye inapokuwa imepitishwa na Bunge,kuwepo na sheria moja yenye Lugha ya Kiingereza naKiswahili ili kuwawezesha Wananchi wengi kunufaika naSheria hiyo kwa kiwango kikubwa.

Tatu, Kamati inashauri kwamba, kwa kuwa kasi ndogo

Page 94: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

94

3 MEI, 2013

ya kushughulikia mashauri inatokana na sababu mbalimbaliikiwemo uhaba wa watumishi, ni vyema Serikali ikaiwezeshaofisi hii kibajeti ili iweze kuajiri watumishi wa kutosha.

Nne, asilimia saba tu ya bajeti nzima ya mwaka 2013/2014 imetengwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo, ambayoni kidogo sana kuleta maendeleo katika Sekta ya Sheria.Fedha zilizotengwa kwa ajili ya mwaka 2013/2014 ni shilingi11,333,051,000 na kati ya hizo, shilingi 826,000,000 pekee ndizozilizotengwa kwa Miradi ya Maendeleo. Kamati inaishauriSerikali kuanza kutenga fedha nyingi zaidi ili kutekeleza Miradiya Maendeleo.

Tano, Serikali iboreshe maslahi ya watumishi katika Ofisiya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuwapa motishawatumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa.

Mheshimiwa Spika, katika kupitia bajeti ya Wizara,Kamati ilielezwa kazi zinazofanywa na Mkurugenzi waMashtaka ikiwa ni pamoja na kusimamia vyema uendeshajiwa mashauri ya jinai na uratibu wa kazi zinazofanywa naVyombo vya Upelelezi. Aidha, Kamati inaishauri Serikalikuongeza uwezo wa fedha kwa ajili ya kuiwezesha Kurugenziya Mashtaka kutekeleza vyema mpango wake wakutenganisha suala la upelelezi na uendeshaji wa mashtaka.

Mheshimiwa Spika, Kamati inatambua juhudizilizofanywa na Ofisi ya Kurugenzi ya Mashtaka kwa kufunguaofisi zake katika Kanda za Morogoro, Pwani na Njombe. Aidha,Kamati inaishauri Kurugenzi ya Mashtaka kuongeza kasi zaidikufungua Ofisi katika kila Wilaya, hasa katika Wilaya mpya ilikurahisisha uendeshaji wa Mashtaka nchini.

Kamati inashauri kwamba, Ofisi ya MwendeshaMashtaka wa Serikali iongezewe Mawakili wa Serikali kwaniMahakama inajitahidi kuongeza idadi ya Mahakimu, hivyoni vyema mawakili nao wakaongezwa ili kuwe na uwianowa kiutendaji kati ya Mawakili na Mahakimu.

Mheshimiwa Spika, katika kupitia utekelezaji wa

Page 95: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

95

3 MEI, 2013

majukumu ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zilizo chiniyake, Kamati ilibaini kuwa Wizara imejitahidi katika kujengana kukarabati mahakama zilizo katika maeneo mbalimbalihapa nchini.

Tarehe 18 Machi, 2013 Kamati ilifanya ziara katikaWilaya ya Kisarawe na kujionea Jengo la Kisasa la Mahakamaya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe. Kamatiinaipongeza Wizara kwa hatua hiyo. Aidha, Kamati inashauriWizara kununua vifaa vya kisasa kama kompyuta kulikokutumia typewriter na kununua samani za ndani kwa ajili yaMahakama zote nchini, kwani uzoefu unaonesha kwamba,samani zinazotengenezwa ndani ya nchi zinadumu mudamrefu zaidi kuliko zinazotengenezwa nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Kamati inasikitishwa kuona Serikalihaikupeleka kiasi chochote cha fedha za maendeleo katiya kiasi cha shilingi 17,213,116,000 zilizotengwa kwa Mwakawa Fedha wa 2012/2013 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.Suala hili linatia shaka kama kweli Serikali ina utashi wa dhatiwa kumaliza changamoto ya ukosefu wa majengo,uchakavu na upungufu wa vifaa katika mahakama. Aidha,Kamati imebaini kwamba, kitendo cha Serikali kutokutoafedha iliyokuwa imepangwa kwa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, kimekwamisha Miradi ya Ujenzi wa Mahakama zaMwanzo za Kawe, Bunda, Mangaka, Gairo, Bariadi, Lukuledina Mkomazi. Kamati inaishauri Serikali kuzitoa fedha hizomapema ili kuwezesha miradi ya ujenzi wa Mahakamakuendelea kama ilivyokuwa imepangwa.

Kamati inashauri Mahakama ipewe fedha za kujengamajengo ya Mahakama Kuu kwenye Mikoa ya Kigoma, Mara,Lindi, Morogoro, Singida, Manyara, Katavi, Njombe, Simiyu naPwani ambako Wananchi husafiri mwendo mrefu kwakutumia gharama nyingi kutafuta haki zao kwenye mikoamingine zilipo Kanda za Mahakama Kuu. Aidha, Mahakamainahitaji ongezeko la watumishi wa fani mbalimbaliwanaofikia 3455 ili kuweza kutoa huduma kwa ufanisi.

Mheshimiwa Spika, Kamati inatambua juhudi

Page 96: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

96

3 MEI, 2013

mbalimbali zinazofanywa na Uongozi wa Mahakama katikakupunguza mlundikano wa mashauri Mahakamani (Backlogs). Mahakama ya Mwanzo kwa mfano iliingia Mwaka waFedha wa 2012/2013 ikiwa na idadi ya mashauri 124,959yaliyosalia toka miaka ya nyuma na kusajili mashauri mapya650,140, hivyo kuwa na jumla ya mashauri 775,140. Katikakipindi cha kuanzia Julai hadi Disemba, 2012, Mahakama yaMwanzo ilisikiliza na kutolea uamuzi mashauri 577,425, sawana asilimia 89 ya mashauri yaliyofunguliwa na hivyo kubakina mashauri 197,715.

Kamati imeridhishwa sana na kasi hii na kuamini kuwakama itaendelea hivyo, inaweza kumaliza kabisa tatizo lamlundikano wa mashauri mahakamani. Pamoja na jitihadahizi, Kamati inashauri Mahakama ije na njia bora zaidi yaupimaji wa utendaji kazi wa Mahakimu na Majaji ili kuongezaufanisi na utendaji wa Mahakama kwenye kazi za msingi.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Serikalikukubaliana na ushauri uliotolewa na Kamati wa kuondokanana utaratibu wa uendeshaji wa mashauri mahakamani kwakuandika mwenendo wa mashauri kwa njia ya mkono nabadala yake kufikiria kutumia njia ya kisasa inayofanana naHansard katika baadhi ya divisheni za Mahakama. Kamatiil i julishwa kwamba, Wizara ya Katiba na Sheria kwakushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Watu Wa China,zinaendelea kufanya upembuzi yakinifu wa Mradi mkubwawa Tele-justice utakaoiwezesha Mahakama kuendeshaMashauri na kurekodi mienendo ya kesi kama ilivyo Hansard.

Kamati inaishauri Serikali kutilia mkazo na kusukumaupembuzi yakinifu kwa haraka zaidi ili Mahakama iwezekuondokana haraka na mfumo wa zamani wa kurekodimienendo ya kesi kwa njia ya mkono.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaishauri Serikalikuimarisha Mfuko wa Mahakama kibajeti ili Mfuko huo uwezekukidhi haja za mahitaji ya Mahakama. Aidha, Kamatiinaishauri Serikali itoe motisha kwa Mahakimu wanaofanyakazi katika mazingira mugumu.

Page 97: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

97

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu yakekwa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Wizara ya Katiba naSheria iliidhinishiwa jumla ya shilingi 12,986,298,000. Kati yafedha hizo, fedha za matumizi ya kawaida zilikuwa shilingi9,544,571,000 na shilingi 3,441,727,000 zilikuwa fedha za njekwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.

Hadi kufikia Februari, 2013, fedha zilizopokelewakutoka Hazina na kutumika zilikuwa shilingi 4,483,399,491.64,sawa na asilimia 47 ya bajeti nzima iliyopangwa; hivyo, Kamatiinashauri kama ifuatavyo:-

- Kasi ya utoaji wa fedha zinazotengwa naWizara na kupitishwa na Bunge zitolewe kwa wakati ilikuwezesha ufanikishaji wa utekelezaji wa shughuli hizo.

- Serikali kuweka kipaumbele Miradi yaMaendeleo na kutenga fedha za ndani kwa ajili hiyo kulikokutegemea fedha za nje.

Mheshimiwa Spika, Kamati inatambua kazi nzuriinayofanywa na Tume ya kurekebisha Sheria, ikiwa ni pamojana kukamilisha Taarifa ya Mfumo wa Haki za Madai (CivilJustice System), inayofanywa na Wizara kupitia Tume yaKurekebisha Sheria Tanzania. Aidha, Kamati inaona kwamba,taarifa hizo zitasaidia sana kuboresha mifumo ya utoaji hakinchini hasa katika nyanja ya madai lakini pia kuboreshamfumo wa Sheria za Kimila. Hata hivyo, Kamati inashaurikwamba, Serikali ikamilishe haraka taarifa ya mapitio ya sheriazinazosimamia usuluhishi na utatuzi wa migogoro ya ardhi,kwani migogoro ya ardhi imekuwa mingi na mfumo wakewa utatuzi haukidhi haja hivyo ni vyema mfumo wa utatuziwa migogoro ya ardhi ukarekebishwa. Aidha, Ibara ya 107ya Katiba inasema: “Mamlaka yenye kauli ya mwisho yautoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa niMahakama na hivyo Kamati inashauri Sera ya Mabaraza yaArdhi ya Vijijini kuwa chini ya Wizara ya Ardhi iangaliwe upyana ikiwezekana Mabaraza hayo yawe chini ya Mahakama.”

Mheshimiwa Spika, Tume ya Haki za Binadamu na

Page 98: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

98

3 MEI, 2013

Utawala Bora - Fungu 55. Kamati inashauri na kupendekezaifuatavyo:-

Kiasi cha shilingi shilingi 4,047,910,700 kilichotengewaTume ni kidogo sana kikilinganishwa na majukumu makubwailiyonayo kama yalivyoainishwa katika Ibara ya 130(1)(a) -(h) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaMwaka 1977 kama ilivyorekebishwa ikisomwa pamoja naKifungu Na. 6(1)(a) - (0) cha Sheria ya Tume ya Haki zaBinadamu na Utawala Bora Na. 7 ya Mwaka 2001, ambayopamoja na mambo mengine ni kuhamasisha uhifadhi wa hakiza binadamu na wajibu kwa jamii kwa mujibu wa Katiba naSheria za nchi.

Matukio ya uvunjwaji haki na vitendo vya kujichukuliasheria mkononi vinaongezeka; hivyo, ni vyema Tumeikaongeza jitihada zake za kutoa elimu kwa Umma juu yaumuhimu wa kuheshimu Sheria.

Tume iongeze kasi ya uchunguzi wa matukio yauvunjwaji wa haki na kutoa ripoti zake mapema il ikuwawezesha Wananchi kujua hali ya Haki za Binadamunchini. Aidha, Kamati inashauri Serikali kuipatia fedha zakutosha ili iweze kuchapa Ripoti za Haki za Binadamu za kilamwaka.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu yakeya kuisimamia na kuishauri Serikali, Kamati ilifanya ziara tarehe5 Aprili, 2013 kwenye Jengo la Wakala wa Usajili wa Vizazi,Vifo na Ufilisi (RITA TOWER), lililopo Mtaa wa Makunganya,Jijini Dar es Salaam. Kamati imetambua kazi nzuri inayofanywana Serikali kupitia Wakala kwani ujenzi umesimamiwa vizurina uko katika hatua nzuri. Jengo hili litapunguza kero yakupanga pamoja na uhaba wa ofisi. Aidha Jengolitauongezea Wakala kipato kwa kupangisha ofisi za ziada.Hata hivyo, Kamati inaomba Serikali kutoa fedha za ujenzikwa Wakala haraka kwani Jengo hilo linajengwa kwa ubiakati ya RITA na NSSF. Hadi sasa fedha zote kati ya shilingi bilioni35 zinazotakiwa kugharamia Mradi zimetolewa na NSSF, RITAwalipaswa kutoa shilingi bilioni 17 sawa na asilimia 69 ya

Page 99: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

99

3 MEI, 2013

gharama za mradi. Kamati inaitaka Serikali kuupatia Wakalafedha hizo mapema iwezekanavyo ili zilipwe, kukwepa ribakubwa itakayotekea endapo fedha zitachelewa kulipwa.

Mheshimiwa Spika, Kamati inashauri kwamba,utekelezaji wa Mpango wa Kusajili Watoto Chini ya Umri waMiaka Mitano unaojulikana kama U5BRI - Under Five BirthRegistration Initiative, ukilenga kupunguza mlundikano wavizazi ambavyo havijasajiliwa, usambazwe katika wilaya zotenchini ili kuhakikisha watoto wote chini ya miaka mitanoambao hawajasajiliwa wanasajiliwa. Aidha, Kamati inashauriSerikali kuuwezesha kibajeti Wakala wa Usajili, Ufilisi naUdhamini ili uweze kutekeleza mpango wake ilioubuni waU5BRI Underfive Birth Registration Initiatives ili kuongezakiwango cha usajili na kutoa vyeti hasa kwa watoto wenyeumri chini ya miaka mitano.

Mheshimiwa Spika, napenda kukushukuru wewebinafsi kwa kunipa fursa hii muhimu ili niweze kuwasilishataarifa hii mbele ya Bunge lako Tukufu. Pia, namshukuru Waziriwa Katiba na Sheria - Mheshimiwa Mathias M. Chikawe, NaibuWaziri - Mheshimiwa Angellah Jasmine Kairuki naMwanasheria Mkuu wa Serikali - Mheshimiwa Jaji FrederickWerema, kwa ushirikiano wao mkubwa walioutoa wakatiKamati ilipojadili Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizarahii. Vilevile, nawashukuru Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba naSheria na Wakuu wa Taasisi pamoja na Maafisa Waandamiziwa Wizara na Taasisi zake, kwa ushirikiano waliotupatia.

Mheshimiwa Spika, kipekee, nawashukuru Wajumbewa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, kwa kazinzuri ya kujadili na kuchambua Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Wizara hii kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014.Uzoefu wao wa muda mrefu katika masuala mbalimbalikuhusu Sekta ya Sheria, Haki za Binadamu na Utawala Bora,umesaidia kufanikisha kazi hii kwa ufanisi. Kwa heshimakubwa, naomba kuwatambua kwa majina kama ifuatavyo:-

SPIKA: Tulishaacha mchezo huo, sisi hatuna muda.(Kicheko/Makofi)

Page 100: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

100

3 MEI, 2013

MHE. GOSBERT B. BLANDES (K.n.y. MWENYEKITI WAKAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA): MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru, samahani sana.

1. Mhe. Dkt. Pindi Hazara Chana - Mwenyekiti2. Mhe. William Mganga Ngeleja - M/Mwenyekiti3. Mhe. Abbas Zuberi Mtemvu - Mjumbe4. Mhe. Nimrod Elirehema Mkono - Mjumbe5. Mhe. Halima James Mdee - Mjumbe6. Mhe. Fakharia Khamis Shomar - Mjumbe7. Mhe. Nyambari C. M. Nyangwine - Mjumbe8. Mhe. Jaku Hashim Ayoub - Mjumbe9. Mhe. Felix Francis Mkosamali - Mjumbe10. Mhe. Gosbert Begumisa Blandes - Mjumbe11. Mhe. Rukia Khasim Ahmed - Mjumbe12. Mhe. Mustapha Boay Akunaay - Mjumbe13. Mhe. Ramadhan Haji Saleh - Mjumbe14. Mhe. Tundu Antiphas Mughwai Lissu - Mjumbe15. Mhe. Deogratias Aloys Ntukamazina - Mjumbe16. Mhe. Jason Samson Rweikiza - Mjumbe17. Mhe. Ali Khamis Seif - Mjumbe18. Mhe. Abdallah Sharia Ameir - Mjumbe19. Mhe. Mariam R. Kasembe - Mjumbe

Aidha, napenda kuwashukuru kwa dhati Watumishiwa Ofisi ya Bunge, kwa kuisaidia Kamati kutekeleza majukumuyake. Kipekee, namshukuru Ndugu Haika Mtui na NduguMatamus Fungo, Makatibu wa Kamati hii, kwa kuratibu kaziza Kamati na kuhakikisha kuwa Taarifa hii inakamilika kwawakati uliopangwa.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, sasanaliomba Bunge lako Tukufu likubali kuidhinisha Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisizake, kama yalivyowasilishwa na mtoa hoja.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naungamkono hoja. (Makofi)

Page 101: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

101

3 MEI, 2013

SPIKA: Ahsante, hivyo hivyo hata Waziri wa Katiba naSheria, kuwashukuru watu wake, kawashukuru ofisini siyo hapakutumia muda wetu.

Sasa namwita Msemaji wa Kambi ya Upinzani.(Makofi)

MHE. TUNDU A. M. LISSU - MSEMAJI MKUU WA UPINZANIKWA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kupata fursa hii na kama inawezekana mudaambao Kamati haijaumalizia nikopeshwe mimi.

SPIKA: Hakuna cha kukopa hapa. (Kicheko)

MHE. TUNDU A. M. LISSU - MSEMAJI MKUU WA UPINZANIKWA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, kwaniaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako Tukufu,naomba kuwasilisha Maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni, Wizara ya Katiba na Sheria, kuhusuMpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha yaWizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/14 na ninaomba nifanye hivyo kwa mujibu wa Kanuni ya 99ya Kanuni za kudumu za Bunge lako Tukufu za mwaka 2013.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Waziri wa Katiba na Sheria,imeanzishwa kwa mujibu wa kipengele cha 12 cha Nyongezaya Waraka wa Rais uliochapishwa kama Tangazo la SerikaliNa. 494 la tarehe 17 Desemba, 2010. Majukumu ya Ofisi hiiyameainishwa katika Tangazo la Ukasimishaji wa Majukumuya Kiuwaziri la Mwaka 2010 (The Ministers [Assignment ofMinisterial Functions] Notice, 2010) lililochapishwa katikaGazeti la Serikali kama Tangazo la Serikali Na. 494A la tarehe17 Desemba, 2010.

Kwa mujibu wa Nyongeza ya Pili ya Tangazo hilo,pamoja na mengine, Ofisi ya Waziri wa Katiba na Sheriaimekasimiwa majukumu ya masuala ya kikatiba, uendeshajina utoaji wa haki, uendeshaji mashtaka na Haki za Binadamu.Kwa sababu ya matukio ya hivi karibuni yanayohusu utendajiwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mchakato wa

Page 102: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

102

3 MEI, 2013

Katiba Mpya na kwa kuzingatia umuhimu wake katikamustakbali wa Taifa letu, tunaomba kuanza na masualayanayoihusu Tume na uendeshaji wa mchakato huo.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliidhinishiwa jumla yashilingi bilioni 33.944 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yakekwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83ya Sheria za Tanzania. Kwa mujibu wa Maelezo ya Makadirioya Matumizi Mengineyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014yaliyoletwa mbele ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawalamwezi uliopita, hadi kufikia tarehe 25 Februari, 2013, Tumeilishapokea shil ingi bil ioni 18.473 kutoka Hazina nailikwishatumia shilingi bilioni 14.968, sawa na asilimia 81 yafedha zilizopokelewa.

Kwa mujibu wa maelezo hayo, shilingi bilioni 3.504ambazo hazijatumika zimetengwa kwa ajili ya kulipia madenikutokana na huduma za uchapishaji wa Mwongozo waMabaraza ya Katiba, uratibu wa mchakato wa kupatikanaWajumbe wa Mabaraza ya Katiba na gharama nyingine zauendeshaji wa Ofisi.

Maelezo ya Tume yanaonesha kwamba, shillingi bilioni15.471 ambazo hazijatolewa na Hazina zitatumika kwa ajiliya kusambaza nakala milioni moja za Rasimu ya Katiba Mpya(shilingi bilioni 3.848); elimu kwa umma juu ya Rasimu ya KatibaMpya (shilingi milioni 400); kuratibu na kuendesha Mabarazaya Katiba kwa nchi nzima (shilingi bilioni 4.734); na shilingibilioni 6.488 kwa ajili ya matumizi mengine pamoja na stahiliza Wajumbe na Sekretarieti.

Mheshimiwa Spika, katika Maoni yetu ya mwaka jana,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ililalamikia kile ilichokiita“... matumizi yasiyoelezeka na yasiyokubalika ya fedha zaumma hasa hasa katika mazingira ambayo Wananchiwanahubiriwa na Watawala kwamba miradi ya maendeleoyao ya kiuchumi na kijamii haitekelezeki kwa sababu ya ufinyuwa Bajeti ya Serikali.” Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniilidai kwamba, shilingi bilioni 14.633 zilizotengwa kwa ajili ya

Page 103: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

103

3 MEI, 2013

kuwalipa Wajumbe na Watendaji wa Tume poshombalimbali, zilikuwa zinatishia kuigeuza heshima ya kutumikiawaliyopewa Wajumbe wa Tume kuwa hongo ya Serikali.

Madai ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuitakaSerikali ilieleze Bunge hili Tukufu gharama zote za kila Mjumbewa Tume, Sekretarieti na Watumishi wengine wote wa Tumeili Wabunge na Wananchi wa Tanzania wafahamu kodiwanazolipa zinavyotumika katika mchakato wa Katiba Mpya,yalikataliwa na Serikali kwa hoja kwamba taarifa hizo ni sirikati ya mwajiri na mwajiriwa.

Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu linaombwakuidhinisha shilingi bilioni 33.944, kiasi kile kile kilichoidhinishwamwaka jana, kwa ajili ya matumizi ya Tume kwa Mwaka waFedha wa 2013/14. Kiasi hiki ni pamoja na shilingi bilioni 12.193kwa ajili ya kulipia posho za vikao kwa Wajumbe wa Tume 34na Sekretarieti 160; shilingi bilioni 1.728 ambazo zitalipia poshoya kujikimu kwa ajili ya Wajumbe na Sekretarieti wanaposafirindani ya nchi kikazi; na shilingi bilioni 1.650 kwa ajili ya kulipagharama za nyumba za Wajumbe na Sekretarieti wanaotokanje ya Dar es Salaam. Aidha, kuna shilingi milioni 18zinazoombwa kwa ajili ya kugharamia chakula kwa Wajumbewa Tume na Sekretarieti watakaokuwa wamepatamaambukizi ya UKIMWI; shilingi milioni 60 kwa ajili ya usafiriwa ndani; shilingi milioni 50 kwa ajili ya gharama za malazikwa Wajumbe wa Tume na Sekretarieti wanaposafiri kikazi;shilingi milioni 423 kwa ajili ya chai na vitafunwa; na shilingimilioni 50 kwa ajili ya wahudumu wanaosaidia kazi za Tumewakiwa mikoani wakati wa kushiriki kwenye Mabaraza yaKatiba na zoezi la upigaji kura ya maoni.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Bunge lako Tukufulinaombwa kuidhinisha shilingi milioni 60 za kulipia maji kwamatumizi ya Ofisi za Tume; shilingi milioni 30 kwa ajili ya kulipiagharama za usafiri wa basi na taxi kwa Wajumbe naSekretarieti watakaposafiri ndani ya nchi kikazi; na shilingimilioni 103 kwa ajili ya kulipia gharama za simu za mikononi.

Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu linaombwa

Page 104: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

104

3 MEI, 2013

kuidhinisha posho na ulaji zaidi ya huu kwa ajili ya Wajumbena Sekretarieti ya Tume. Ulaji huu mwingine unajumuishashilingi milioni 604 kwa ajili ya posho kwa Wajumbe wa Tumena Sekretarieti wakati wa Bunge Maalum la Katiba.

Maelezo ya Tume yamejaribu kuhalalisha matumizi yafedha hizi za ziada kwa kuzibatiza jina la hardship allowances,yaani posho ya mazingira magumu, wakati Vikao vya BungeMaalum la Katiba vitafanyika Dar es Salaam au hapaDodoma!

Vilevile, katika ulaji huu mpya zipo shilingi milioni 266zinazoombwa kwa ajili ya chakula na viburudisho wakati waVikao vya Bunge Maalum la Katiba; shilingi milioni 12 nyinginekwa ajili ya huduma za chakula na viburudisho kwa shughulizinazohusiana na Tume; na shilingi milioni 185 kwa ajili yakulipia usafiri wa basi na taxi. Aidha, kuna shilingi milioni 30za utengenezaji wa T-shirts na kofia kwa Wajumbe wa Tumena Sekretarieti wakati wa kushiriki kwenye zoezi lauhamasishaji kuelekea upigaji wa kura ya maoni; shilingimilioni 40 nyingine kwa ajili ya utengenezaji wa sare wakatiwa maadhimisho mbalimbali ya Kitaifa; na shilingi milioni 12kwa ajili ya posho za kujikimu kwa Watumishi wa Tumewatakaohudhuria kwenye maadhimisho mbalimbali yaKitaifa.

Zaidi ya hayo, kuna shilingi bilioni 1.307 zinazoombwakwa ajili ya posho za kujikimu kwa ajili ya Wajumbe naSekretarieti ya Tume wanaposafiri ndani ya nchi wakati wakushiriki kwenye zoezi la upigaji wa kura ya maoni; na shilingimilioni 218 kwa ajili ya ununuzi wa mafuta ya magari ya Tumewakati wa kushiriki zoezi la uhamasishaji kuelekea upigaji wakura ya maoni.

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla, Bunge lako Tukufulinaombwa kuidhinisha jumla ya shilingi bilioni 19.039 kwa ajiliya posho za aina mbalimbali na malipo mengineyanayowahusu Wajumbe na Sekretarieti ya Tume kwaMwaka wa Fedha wa 2013/14. Hii ni zaidi ya asilimia 56 yabajeti yote inayoombwa kwa ajili ya Tume. Kwa ulinganisho,

Page 105: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

105

3 MEI, 2013

posho na malipo mengine yanayowahusu Wajumbe naSekretarieti ya Tume yalikuwa shilingi bilioni 14.633 au asilimia43 ya bajeti yote ya Mwaka wa Fedha uliopita. Hii ina maanakwamba, gharama za moja kwa moja za Wajumbe naSekretarieti ya Tume zitaongezeka kwa zaidi ya shilingi bilioni4.406 au zaidi ya asilimia 30 ya gharama za mwaka jana kamaBunge lako Tukufu litaidhinisha maombi haya!

Mheshimiwa Spika, maombi haya ya mabilioni yafedha za Wananchi yanatoa uvundo na harufu mbaya yaufisadi na hayaelezeki na wala kukubalika kwa misingi yakisheria na kwa rekodi ya utendaji kazi wa Tume ya Mabadilikoya Katiba. Kwanza kabisa, kwa mujibu wa Kifungu cha 7(1)cha Sheria ya Mabadailiko ya Katiba, Tume ina Wajumbewasiozidi thelathini pamoja na Mwenyekiti na MakamuMwenyekiti wake.

Kwa maana hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinataka kujua uhalali wa maombi ya shilingi bilioni 12.193 kwaajili ya posho za vikao kwa Wajumbe 34 wa Tume wanaotajwakatika kijifungu 210321 cha kasma 210300 kwenye randamaya Fungu 08 linalohusu Tume.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kujuaWajumbe hawa wanne wa ziada ni akina nani nawameteuliwa lini kuwa Wajumbe wa Tume? Aidha, KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inataka kuelezwa, inakuwaje Tumeiwe na Wajumbe 34 wakati Sheria iliyoiunda inataka Tumeyenye Wajumbe wasiozidi thelathini?

Pili, kwa mujibu wa kazi za Tume kama zilivyoainishwakatika kifungu cha 9 cha Sheria; na kwa mujibu wa utaratibuwa utendaji kazi wa Tume kama ulivyofafanuliwa katikaSehemu ya Nne ya Sheria; na kwa kuzingatia masharti yakifungu cha 22(1) cha Sheria hiyo, Wajumbe na Sekretarietiya Tume siyo Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Badalayake, uhusiano pekee wa kisheria uliopo kati ya Tume naBunge Maalum ni ule uliotajwa katika Vifungu vya 20(3), 20(4)

Page 106: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

106

3 MEI, 2013

na 25(2) vya Sheria vinavyomruhusu Mwenyekiti wa Tumekuwasilisha Rasimu ya Katiba Mpya kwenye Bunge Maalumna kuwaruhusu Mwenyekiti na Wajumbe kutoa ufafanuziutakaohitajika wakati wa majadiliano katika Bunge Maalum.

Hii ina maana kwamba, mara baada ya kuwasilishaRasimu ya Katiba Mpya, Mwenyekiti wa Tume anakuwafunctus officio, yaani hana kazi nyingine yoyote ya kufanyakwenye Bunge Maalum. Aidha, Mwenyekiti na Wajumbe waTume hawana kazi nyingine yoyote ya kufanya katika BungeMaalum hadi hapo watakapohitajika na Bunge Maalum kwaajili ya kutoa ufafanuzi wa jambo lolote linalohusu Rasimu yaKatiba Mpya.

Wakishatoa ufafanuzi utakaohitajika walioitiwa, naopia wanakuwa functus officio. Kwa sababu hizo, Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni inataka kujua uhalali wa shilingi bilioni1.055 ambazo Bunge lako Tukufu linaombwa kuziidhinisha kwaajili ya posho, chakula na viburudisho na usafiri wa basi nataxi kwa Wajumbe wa Tume na Sekretarieti wakati wa Vikaovya Bunge Maalum la Katiba.

Tatu, kwa mujibu wa Kifungu cha 33(2) cha Sheria yaMabadiliko ya Katiba, jukumu pekee la Tume katika hatuaya uhalalishaji wa Katiba Mpya ni kutoa elimu ya uraia nauhamasishaji juu ya Katiba inayopendekezwa kwa mudausiozidi siku thelathini kuanzia siku ya kuchapishwa katikaGazeti la Serikali.

Kwa kazi ya mwezi mmoja tu, Wajumbe na Sekretarietiya Tume wanaombewa shilingi bilioni 1.307 kwa ajili ya poshoza kujikimu. Kwa mahesabu hayo, kila Mjumbe wa Tume,Katibu na Naibu Katibu pamoja na Wakuu wa Vitengo sabavya Tume na madereva wa kila mmoja wao, watalipwawastani wa shilingi milioni 16.756 kwa mwezi huo mmoja aushilingi 558,547 kama posho ya kujikimu kwa kila siku moja.

Page 107: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

107

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, katika nchi ambayo Wauguzikatika hospitali za umma wanalipwa mshahara wa kuanziawa takriban shilingi 360,000 kwa mwezi na Walimu wa shuleza msingi wanaanzia shilingi 250,000 na wale wa sekondarishilingi 325,000 kwa mwezi, malipo haya kwa Tume yaMabadiliko ya Katiba yana uvundo na harufu mbaya yarushwa kwa Wajumbe wa Tume. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivyo basi, kwa vile kifungu cha14(2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kinatamka kwambaWajumbe wa Tume na Sekretarieti “watalipwa kwa mujibuwa Sheria na Kanuni za nchi”, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inaitaka Serikali hii ya CCM iliambie Bunge lako Tukufuni Sheria na Kanuni zipi za nchi yetu ambazo zimetumikakuhalalisha malipo haya makubwa kwa Wajumbe naSekretarieti na Tume. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aidha, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inaitaka Serikali hii ya CCM itoe kauli rasmi mbele yaBunge lako Tukufu kama kuna uhalali wowote wa kutumiafedha za wananchi wa Tanzania ili kununua ‘chakulamaalum’ (special foods) kwa ajili ya Wajumbe na Sekretarietiya Tume watakaopata UKIMWI kwa sababu ya kuendekezangono zembe na starehe zao binafsi wakati wanatakiwawafanye kazi ya Tume. Vinginevyo, Bunge lako Tukufu lielezwekwa ufasaha ni kwa namna gani mchakato huu wa KatibaMpya unatazamiwa kusababisha maambukizi ya UKIMWI kwaWajumbe na Sekretarieti ya Tume. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa Serikali kujificha nyuma yapazia la ‘siri ya mwajiri na mwajiriwa’ hakutoshi tena, kwanini kulizuia Bunge lako Tukufu kutekeleza wajibu wake kikatibawa kuisimamia Serikali chini ya Ibara ya 63(2) ya Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sura ya 2 ya Sheria zaTanzania. Aidha, ni haki kwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungenikujua uhalali wa malipo haya kwani, kwa mujibu wa Ibaraya 63(3)(a) ya Katiba, Bunge lako Tukufu “laweza kumuulizaWaziri yeyote swali lolote kuhusu mambo ya umma katikaJamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake....”

Page 108: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

108

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinataka kujua shilingi milioni 218 kwa ajili ya ununuzi wamafuta ya magari ya Tume zitatumikaje ndani ya kipindi chasiku thelathini za uhamasishaji na kuelimisha wananchi kupigakura ya maoni kwa Katiba Mpya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii ina maana kwamba hata kamakila Mjumbe wa Tume, Katibu, Naibu Katibu na wakuu wavitengo saba vya Tume watapewa gari moja kwa kilammoja wao kwa kipindi hicho, kila gari itatumia wastaniwa shilingi 186,325 kwa siku kwa ajili ya mafuta tu! KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inataka kujua ni safari zipi hizo zaTume ambazo zitalazimu matumizi ya full tank ya mafutakila siku kwa mwezi mzima? Huu, kama Baba wa TaifaMwalimu Nyerere alivyowahi kusema, ni ‘wizi mtupu’! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, amlipaye mpiga zumari ndiyeachaguaye wimbo. Baada ya Tume kulipwa mabilioni yotetuliyoyapigia kelele kwenye Maoni yetu ya mwaka jana, kunaushahidi kwamba Tume imekuwa inacheza wimbouliochaguliwa na CCM na Serikali yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwezi Februari ya mwaka huu,Tume ilichapisha Mwongozo Kuhusu Muundo, Utaratibu waKuwapata Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya(Mamlaka za Serikali za Mitaa) na Uendeshaji Wake.Mwongozo huo ulisainiwa na Mwenyekiti wa Tume Jaji JosephSinde Warioba na ulianza kutumika tarehe 1 Machi, 2013.Ingawa Tume imedai kwamba Mwongozo huo ulitolewa kwakuzingatia matakwa ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwambaMwongozoulitolewa kinyume na matakwa ya Sheria hiyo nakwa lengo la kuinufaisha CCM na washirika wake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 17(8) cha Sheriakinailazimu Tume kubuni “... utaratibu unaofanana ambaoutatumika katika kila upande wa Jamhuri ya Muunganokatika ukusanyaji na uchambuzi wa maoni ya wananchi,uendeshaji wa Mabaraza na uandaaji wa ripoti.” Katikautekelezaji wa majukumu yake, Tume inatakiwa kufuata

Page 109: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

109

3 MEI, 2013

msingi huu mkuu “isipokuwa kama mazingira yatahitajivinginevyo....”. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatambuakwamba, kwa kiasi kikubwa, Tume il iweka utaratibuunaofanana ambao ulitumika katika hatua ya ukusanyaji wamaoni ya wananchi katika kila upande wa Jamhuri yaMuungano.

Mheshimiwa Spika, kwanza, Tume haikuwekautaratibu wowote wa maana wa kutoa elimu kwa wananchijuu ya masuala yote yanayohusu Katiba Mpya ili kuwaandaawananchi kuchangia maoni yao kwa Tume wakiwa nauelewa wa kutosha. Badala yake, wakati wa mikutano yaTume ya kupokea maoni ya wananchi, wajumbe wa Tumewalipewa jukumu la kuwaeleza wananchi juu ya Katiba Mpyakwa muda usiozidi nusu saa. Hii ilifanyika katika mikutanoyote ya Tume katika kila upande wa Jamhuri ya Muungano.

Mheshimiwa Spika, pili, muda uliowekwa na Tume wakukusanya maoni ya wananchi ulikuwa mdogo sanaukil inganisha na ukubwa wa nchi yetu na wingi waWatanzania. Katika Majimbo karibu yote ya uchaguzi, Tumeiliendesha wastani wa mikutano saba kwa kila Jimbo kwalengo la kukusanya maoni ya wananchi lakini huu ni wastanitu, katika Majimbo mengi, Tume ilifanya mikutano minne aumitano tu. Hili pia lilifanyika katika kila upande wa Jamhuriya Muungano.

Mheshimiwa Spika, tatu, katika mikutano yote yaukusanyaji maoni, wananchi walitakiwa kutoa maoni yaokuhusu Katiba Mpya kwa muda wa dakika tano kila mmojana mikutano yenyewe ilichukua muda wa masaa matatuikiwa ni pamoja na muda wa kutambulishana wajumbe waTume na mambo mengine yaliyo nje ya kuchukua maoni yawananchi. Hii ilifanyika hata kwa Wabunge wakati Tumeilipokuja kuchukua maoni ya Wabunge hapa Dodoma.Utaratibu huu ulitumika katika kila upande wa Jamhuri yaMuungano.

Aidha, utaratibu unaofanana katika kila upande waJamhuri ya Muungano ulitumika pia kukusanya maoni ya

Page 110: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

110

3 MEI, 2013

makundi maalum kama vile vyama vya siasa, taasisizisizokuwa za kiserikali, mashirika ya kidini na hata taasisi zakiserikali na viongozi wake, wa sasa na waliostaafu.

Mheshimiwa Spika, wakati Tume iliweka utaratibuunaofanana katika kila upande wa Jamhuri ya Muunganowakati wa zoezi la kukusanya maoni ya wananchi, Tumehiyohiyo iliweka utaratibu tofauti na wa kibaguzi katika hatuaya kuunda Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.

Kwanza, Tume iliweka ngazi mbili za uchaguzi wawajumbe wa Mabaraza kwa upande wa Tanzania Barawakati kwa upande wa Zanzibar Tume iliweka ngazi mojatu ya uchaguzi. Hivyo, kwa mfano, aya ya 6.1.4 ya Mwongozowa Tume imeweka Mkutano Mkuu Maalum wa Kijiji au Mtaa“ambao utakuwa na agenda moja tu ya kuwapendekezakwa kuwapigia kura watu wanne ambao majina yaoyatawasilishwa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata.” Hiini ngazi ya kwanza ya uchaguzi wa wajumbe wa Mabarazakwa upande wa Tanzania Bara na kazi yake ni kupendekezatu.

Baada ya hapo, majina ya watu walioshinda katikauchaguzi wa ngazi ya Kijiji au Mtaa yatawasilishwa kwa AfisaMtendaji wa Kata “ambaye ataitisha Kikao Maalum chaKamati ya Maendeleo ya Kata, ambacho ... kitachaguamajina manne ...” ya wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya.(aya ya 6.1.8, 6.1.9 na 6.1.10). Hii ni ngazi ya pili na ndiyoinayoamua nani awe mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilayakwa upande wa Tanzania Bara na nani asiwe.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Zanzibar, ngaziya uchaguzi ni moja tu, Mkutano wa Shehia ambao, kwamujibu wa aya 6.3.4 ya Mwongozo wa Tume, “... utakuwana agenda moja tu ya kuwapigia kura ya siri watu watatu ...ambao majina yao yatawasilishwa kwa Mkurugenzi waBaraza la Manispaa au Katibu wa Halmashauri ya Mji au Wilayaambapo Shehia hiyo ipo.” Kwa utaratibu huu, wajumbe waMabaraza ya Katiba ya Wilaya kwa upande wa TanzaniaBara wamechaguliwa na watu wanne au watano tu ambao

Page 111: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

111

3 MEI, 2013

ni wajumbe wa WDC wakati wajumbe wa Mabaraza ya hayokwa upande wa Zanzibar wamechaguliwa na watu wotewalioshiriki katika Mkutano wa Shehia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wajumbe wa Mabaraza ya Katibaya Wilaya kwa upande wa Zanzibar wana uhalali wa kisiasakwa sababu wanawakilisha matakwa ya wananchiwaliowachagua moja kwa moja bila mchujo, wakatiwajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kwa upandewa Tanzania Bara hawana uhalali wowote wa kisiasa kwasababu wanawakilisha maslahi ya CCM ambayo ndiyoinayotawala asilimia zaidi ya themanini ya WDC zote ambazondio zilizowachuja wajumbe hao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo la pili l inalothibitishakwamba utaratibu wa Tume ni wa kibaguzi ni katikauendeshaji wa mikutano ya uchaguzi wa wajumbe waMabaraza ya Katiba ya Wilaya. Kwa mujibu wa aya ya 6.1.4ya Mwongozo wa Tume, kwa upande wa Tanzania BaraMkutano Maalum wa Kijiji au Mtaa “... utaendeshwa naMwenyekiti wa Kijiji au Mtaa, ambapo Afisa Mtendaji wa Kijijiau Mtaa atakuwa Katibu wa Mkutano na ndiyeatakayewasilisha majina ya wananchi walioomba kuingiakwenye Baraza la Katiba la Wilaya.”

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kwa upande waZanzibar kwa mujibu wa aya ya 6.3.5 ya Mwongozo wa Tume,“Mkutano wa Shehia utachagua Mwenyekiti na Katibu waMkutano huo kutoka miongoni mwa wananchiwaliohudhuria Mkutano. Katibu ndiye atakayewasilishakwenye Mkutano majina ya wananchi wote walioomba kuwawajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya....” KaribuMaafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa wote wa Tanzania Barani wanachama na makada wa CCM, ilhali zaidi ya 90% yaWenyeviti wa Vijiji na Mitaa wote ni wanachama na makadawa chama hicho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo, mikutano yauchaguzi wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kwa upandewa Tanzania Bara imeendeshwa na makada wa CCM wakati

Page 112: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

112

3 MEI, 2013

kwa upande wa Zanzibar mikutano imeendeshwa naviongozi waliochaguliwa na wananchi walioshiriki katikamikutano hiyo bila kujali itikadi au uanachama wao katikavyama vya siasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana, karibu nchi nzimaukiacha Zanzibar, kwa mujibu wa taarifa ilizo nazo KambiRasmi ya Upinzani Bungeni, wananchi wengi wasiokuwawanachama wa CCM ambao walipata kura nyingi katikakura za mikutano ya uchaguzi ya Vijiji na Mitaa walienguliwakwenye michujo iliyofanyika katika Kamati za Maendeleo zaKata zilizowekwa kwa mujibu wa Mwongozo wa Tume.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata mahali ambapo wananchiwasiokuwa wana CCM walifanikiwa kupenyeza katikachekecheke la mchujo wa WDC, wamefanyiwa mizengwena wana CCM ili waondolewe katika orodha ya wajumbewa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mfano mzuri ni yaliyomkuta BwanaBeatus Kipeya aliyechaguliwa mjumbe wa Baraza la Katibala Wilaya ya Arusha Mjini kwa kupitia Kata ya Sombetini. Marabaada ya Bwana Kipeya kuchaguliwa kwenye kikao chaKamati ya Maendeleo ya Kata ya Sombetini cha tarehe 8Aprili, 2013, siku hiyo hiyo Katibu wa CCM Wilaya ya ArushaAllan G. Kingazi alimwandikia Mkuu wa Wilaya ya Arushabarua ya malalamiko juu ya kuchaguliwa kwa Bwana Kipeya.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kumpa Mkuu waWilaya ‘salaam za Chama’ chao, Katibu wa CCM Kingazialilalamika kwamba Afisa Mtendaji wa Kata ya Sombetiniamemruhusu “... raia wa Burundi Bwana Beatus NdanyahubwiKipea (ambaye katika kugombea ametumia jina la BeatusiKipea ili asijulikane kama ni Mrundi – ila mtu wa Kigoma yaaniMuha) kugombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Katiba laWilaya na akashinda, kinyume na maagizo ya Tume yaKatiba, kwamba Mjumbe ni lazima awe Raia wa Tanzania.”(Makofi)

Page 113: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

113

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo mengi kuhusu‘Urundi’ wa Bwana Kipeya, Katibu wa CCM Kingazianamwambia Mkuu wa Wilaya yafuatayo: “... (N)ashaurimatokeo ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Katibaufutwe na utangazwe upya. Aidha, Afisa Mtendaji huyoachukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvuruga kwa makusudiuchaguzi wa Muundo wa Baraza la Katiba la Wilaya.” (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitu cha kwanza cha kushangazakuhusu barua ya Katibu wa CCM Kingazi ni kwambaaliyetumiwa malalamiko ni Mkuu wa Wilaya ambaye, kwamujibu wa Ibara ya 42(3), 44(3) na 46(3) ya Katiba ya CCMToleo la 1982, Mkuu wa Wilaya ni mjumbe wa Mkutano Mkuuwa CCM Wilaya, Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya na Kamatiya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya. Kwa mujibu waSheria ya Mabadiliko ya Katiba na Mwongozo wa Tume, Mkuuwa Wilaya hana mamlaka yoyote kushughulikia jambo lolotelinalohusu uchaguzi wa Wajumbe wa Mabaraza ya Katibaya Wilaya. Kwa maana hiyo, sababu pekee ya Mkuu waWilaya ya Arusha kuandikiwa malalamiko haya ni kwasababu ni kada wa CCM! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiacha Afisa Uhamiaji wa Mkoawa Arusha, watu wengine wote walionakiliwa barua yamalalamiko ya Katibu wa CCM Kingazi ni makada wa CCM.Hivyo basi, nakala za malalamiko hayo zinaonyeshwakupelekwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Katibu wa CCMMkoa, Mkuu wa Mkoa (ambaye pia ni mjumbe wa vikaovyote vya kikatiba vya CCM katika ngazi ya Mkoa), Afisausalama wa Taifa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauriya Jiji la Arusha. Wote hawa hawahusiki kisheria kwa namnayoyote ile katika mchakato wa uundaji wa Mabaraza yaKatiba ya Wilaya. Chombo pekee ambacho kinahusikakisheria na mchakato wa kuunda Mabaraza hayo naambacho kilitoa Mwongozo wa namna ya kuyaunda, yaaniTume, hakikuandikiwa wala kunakiliwa barua ya malalamikoya Katibu wa CCM Kingazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mara tu baada ya Afisa UhamiajiMkoa wa Arusha Bwana R. Gowelle kupata nakala yake,

Page 114: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

114

3 MEI, 2013

alimwandikia Bwana Kipeya barua ya ‘wito wa kufika ofisiya uhamiaji Mkoa wa Arusha’, ambapo alimtaka kufika ofisinikwake ‘bila kukosa wala kutuma mwakilishi.’ Chakushangaza ni barua hiyo imenakiliwa kwa Afisa MtendajiKata ya Sombetini, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kirika A,Sombetini na Balozi wa Mtaa wa Zurich, Sombetini.

Mbali na Afisa Mtendaji Kata ambaye alikuwamlalamikiwa, wengine wote walionakiliwa barua ya AfisaUhamiaji Mkoa ni makada wa CCM na kwa taarifa za KambiRasmi ya Upinzani Bungeni, ndio walikuwa chanzo chamalalamiko ya Katibu wa CCM Kingazi. Kwa taarifa za KambiRasmi ya Upinzani Bungeni, Bwana Kipeya ni raia halali waTanzania anayetoka katika Jimbo la Muhambwe katikaWilaya ya Kasulu ya Mkoa wa Kigoma. Dhambi pekee nakubwa aliyoifanya na kustahili kusumbuliwa na Idara yaUhamiaji ni kugombea na kuchaguliwa kuwa mjumbe waBaraza la Katiba la Wilaya ya Arusha wakati yeye siomwanachama wa CCM. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniina ushahidi unaoonyesha kwamba njama za kuhakikishakwamba wanaCCM pekee ndio watakaochaguliwa kuwawajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kwa upandewa Tanzania Bara zilipangwa katika ngazi za juu kabisa zaCCM. Mnamo tarehe 3 Machi, 2013, siku mbili tu baada yaMwongozo wa Tume kuanza kutumika, Katibu wa NEC yaCCM, Uhusiano wa Kimataifa Dkt. Asha-Rose Migiro alitumabarua pepe kwa wajumbe na watendaji wa Sekretarieti yaNEC ya CCM yenye kichwa cha habari: ‘MUHIMU!! MABARAZAYA KATIBA YA WILAYA. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, barua pepe ya Dkt. Asha-RoseMigiro inasema: “Naandika kuhimiza kazi ya kuwatia hamasaMakatibu wa Mikoa wasimamie kikamilifu mchakato wakuundwa kwa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba. Kamamnavyofahamu Tume ya Katiba imeshatoa taarifa rasmikwenye vyombo vya habari ... kuhusu zoezi hili muhimu.Sambamba na hatua za awali tulizochukua baada ya kupatarasimu ya mwanzo ya Mwongozo wa Tume, hivi sasa

Page 115: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

115

3 MEI, 2013

tunatakiwa tuongeze juhudi za ushiriki wetu na kutayarishamakundi husika kama tulivyokwishaongea.” (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walipiga Makofikwa muda mrefu)

SPIKA: Inatosha.

MHE. TUNDU A. M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIYA UPINZANI KWA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA:Mheshimiwa Spika, baada ya kuagiza ‘mawasiliano kati yaSUKI na Makatibu wa Mikoa’ kuhusu mambo ya kufanya, Dkt.Asha-Rose Migiro alimalizia barua yake kwa manenoyafuatayo: “Tafadhali wanakaliwa msisite kutoa maoni,ushauri na mbinu bora zaidi za kutimiza azma yetu katikasuala hili muhimu.” (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wanakiliwa wa barua pepe yaDkt. Asha-Rose Migiro ni pamoja na Mheshimiwa MwiguluNchemba, Mheshimiwa Zakhia Meghji, Mheshimiwa MuhamedSeif Khatib na Bwana Nape Nnauye, Katibu Mwenezi wa NECya CCM. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, siku moja baadaye, Bwana NapeNnauye aliwaandikia ‘wanakiliwa’ wenzake kama ifuatavyo:“nashauri ikiwezekana kwa sababu ya unyeti wa swala hilitupate taarifa kila siku/au walau siku tatu ya hali halisiinavyoendelea katika kila Mkoa, ni vizuri idara ikaandaachecklist ya mambo muhimu ya kupima kama mchakatounakwenda vizuri au la! Mfano ... idadi ya walioandaliwakugombea katika kila eneo, idadi ya waliohamasishwakuhudhuria na kupiga kura, n.k.” (Makofi)

Mheshimiwa Spika, njama za CCM kuteka nyaramchakato wa Katiba Mpya zinahusu pia mchakato wauhalalishaji wa Katiba Mpya kwenye kura ya maoni. Mnamotarehe 18 Desemba mwaka jana, Katibu wa Sekretarieti yaHalmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Francis K. Mwonga,aliwaandikia barua Makatibu wote wa CCM wa Mikoakuwapa ‘Maelekezo ya Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri

Page 116: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

116

3 MEI, 2013

Kuu ya Taifa na Makatibu wa CCM wa Mikoa KilichofanyikaDar es Salaam Tarehe 10/12/2012.’ (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sehemu ya Maelekezo hayoinasema: “Wakati wa kupiga kura ya maoni kuhusu KatibaMpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mawasilianoyafanywe na wahusika ili vituo vya kupigia kura visiwe mbalisana na wananchi.” Maneno haya yameandikwa hata kablaTume haijamaliza zoezi la kukusanya maoni ya wananchi natayari Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM inawaelekezamakada wake mikoani kufanya mawasiliano na ‘wahusika’juu ya namna ya kupanga vituo vya kupigia kura. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kifungu cha 56(a)cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 ya Sheria zaTanzania, mamlaka inayohusika kupanga vituo vya kupigiakura ni Msimamizi wa Uchaguzi, yaani Mkurugenzi wa Jiji,Mkurugenzi wa Manispaa, Mkurugenzi wa Mji na MkurugenziMtendaji wa Halmashauri ya Wilaya. Wasimamizi hawa wauchaguzi wamelalamikiwa kwa miaka mingi na vyama vyaupinzani kwa kupendelea CCM na wagombea wake katikachaguzi mbalimbali. Hawa ndio wanaotakiwa wawasilianena Makatibu wa CCM Mikoa ili wapange vituo vya kupigiakura ya maoni juu ya Katiba Mpya! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mawasiliano haya ya viongozi wangazi za juu za CCM yanathibitisha kwamba mchakato waKatiba Mpya umeiingiliwa na kuhujumiwa kwa kiasi kikubwana CCM. Aidha, mawasiliano haya yanathibitisha kauliiliyotolewa mbele ya Bunge lako Tukufu na Kiongozi wa KambiRasmi ya Upinzani Bungeni wakati wa mjadala wa hoja yaOfisi ya Waziri Mkuu kwamba “...viongozi wa kiserikali kamavile Wakuu wa Wilaya na wa Mikoa waliwahamasishaWenyeviti wa Vijiji, Mitaa na Madiwani kuhakikisha kwambawagombea wote wasiokuwa wa CCM, hasa wa CHADEMA,wanaenguliwa katika chaguzi za Vijiji, Mitaa au Kata.” Aidha,mawasiliano haya yanathibitisha kauli ya Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni kwamba Mabaraza ya Katiba ya Wilayayaliyochaguliwa kwa utaratibu “...ni Mabaraza ya CCM nasio Mabaraza ya Katiba ya Watanzania wote.” (Makofi)

Page 117: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

117

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, yote ambayo tumeyasema hapayanathibitishwa pia na Tume yenyewe. Tarehe 29 Aprili, 2013,Mwenyekiti wa Tume Jaji Warioba alikiri kwenye mkutano wawaandishi habari kwamba “... sehemu kubwa ya matatizoyaliyojitokeza yalisababishwa na misukumo na misimamo yakisiasa na kidini.” Mwenyekiti Warioba amekiri kwamba kunawajumbe wamejazwa katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya:

“Hao waliojazana kwenye Mabaraza wanadhaniwanakuja kupiga kura, hapana.... Tume inazingatia uzito wahoja zilizotolewa na wananchi na si idadi ya watu waliotoamaoni.” Kwingineko, Mwenyekiti Warioba amekaririwa navyombo vya habari akikiri kwamba kulikuwa na rushwakatika mchakato wa uchaguzi wa Mabaraza ya Katiba yaWilaya. Hata hivyo, licha ya kukiri kuwepo kwa matatizomakubwa kama haya katika mchakato wa kuundaMabaraza hayo, Mwenyekiti Warioba na Tume yakewamekataa madai ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguziwa Mabaraza kwa hoja kwamba kufanya hivyokutachelewesha kupatikana kwa Katiba Mpya! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kauli ya Mwenyekiti wa Tume niya kinafiki na ya kujikosha kutokana na makosa ya Tumeyenyewe. Hii ni kwa sababu Tume yake ilitahadharishwamapema juu ya uwezekano mkubwa wa matatizo hayokujitokeza. Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kiliitahadharisha Tume mapema mwezi Februariya mwaka huu kwamba rasimu ya Mwongozo wa Tumeitazaa Mabaraza ya kiCCM na italeta manung’uniko mengiya wadau ambao wataenguliwa kwenye ngazi ya WDCambazo zinatawaliwa na CCM kwa kiasi kikubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, CHADEMA iliishauri Tume iachanena mapendekezo ya kuziweka WDC kuwa ni kikao chauchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilayana badala yake wajumbe wa Mabaraza wachaguliwe mojakwa moja na wananchi kama ilivyopendekezwa kwa upandewa Zanzibar. Jaji Warioba na Tume yake walikataa kata katamapendekezo haya ya CHADEMA. Kama alivyosema Kiongoziwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni: “... (L)icha ya Tume ya

Page 118: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

118

3 MEI, 2013

Mabadiliko ya Katiba kupatiwa maoni ya wadau kwambautaratibu huo utaharibu mchakato wa Katiba Mpya, Tumeilikataa kata kata kuubadilisha Muundo wa Mabaraza haya.Ni wazi kwamba Tume inafahamu inachokifanya. Ni wazivilevile kwamba Tume inafahamu matokeo ya hichoinachokifanya, yaani kuundwa kwa Mabaraza ya Katiba yaWilaya ambayo ni ya wanaCCM.”

Mheshimiwa Spika, Jaji Warioba na Tume yakehawawezi wakasikika sasa hivi wakisema kwamba vyamavya kisiasa na taasisi za kidini ndio zenye makosa kwakuvurugika kwa mchakato wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya!Aidha, Tume iliyotengeneza Mwongozo uliosababishawanachama wa CCM ‘kujazana’ katika Mabaraza ya Katibaya Wilaya haiwezi sasa ikalalama na kudai kwambahaitaangalia idadi ya waliotoa maoni bali itaangalia uzitowa hoja! Katika hili Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitakaSerikali iwaeleze Watanzania kama kuna uhalali wowotekutumia shilingi bilioni 4.734 kwa ajili ya kuratibu na kuendeshaMabaraza ambayo Tume imesema maoni ya wengi katikaMabaraza hayo hayatafuatwa.

Mheshimiwa Spika, zaidi ya hayo, kukataa kwa Tumekufuta matokeo ya uchaguzi wa Mabaraza ambayo Tumeyenyewe inakiri umevurugwa, ni uthibitisho tosha kwambandivyo Tume ilivyodhamiria tangu mwanzoni. Mabaraza hayaya kiCCM ni matunda ya moja kwa moja ya Tume kukiukautaratibu uliowekwa na kifungu cha 18(3) cha Sheriaulioilazimu Tume kuunda Mabaraza ambayo “... yatashirikishana kuwakutanisha wawakilishi toka makundi mbalimbali yawananchi katika jamii.”

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Serikali itoe kauli mbele ya Bunge lako Tukufu kamaCCM au viongozi na makada wake wamefanya mawasilianoyoyote na vyombo vitakavyosimamia kura ya maoni juu yaKatiba Mpya kama zinavyoashiria nyaraka za CCM ambazotumezielezea hapa. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Serikali hii ya CCM itoe kauli juu ya uhalali wamawasiliano haya wakati mchakato wa kutengeneza Katiba

Page 119: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

119

3 MEI, 2013

Mpya haujakamilika na wala Sheria husika za Uchaguzihazijafanyiwa marekebisho ili kuruhusu kura ya maonikufanyika kihalali, hasa kwa upande wa Tanzania Bara.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 10 cha Sheria yaMabadiliko ya Katiba kinafafanua kwamba “Tume itakuwana mamlaka na uhuru kwa kadri itakavyokuwa muhimu kwaajili ya utekelezaji wa majukumu na mamlaka yake chini yaSheria hii na haitaingiliwa na mtu au mamlaka yoyote.”(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nyaraka za CCM ambazotumezielezea hapa zinaonyesha dhahiri kwamba CCMimeingilia uhuru na mamlaka ya Tume. Kwa uchache kabisa,nyaraka hizi zinaonyesha viongozi wa ngazi za juu kabisawa Sekretarieti ya NEC ya CCM wamefanya makosa ya kulanjama kutwaa mamlaka ya Tume kwa kuwatumia Makatibuwa Mikoa wa CCM ‘kusimamia kikamilifu mchakato wakuundwa kwa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba.’ Kwa mujibuwa kifungu cha 21(2)(b) cha Sheria, “mtu yeyote ...atakayejifanya kuwa mjumbe wa Tume au Sekretarieti ...atakuwa ametenda kosa.”

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 21(3) kinaelekezaadhabu ya faini isiyopungua shilingi milioni mbili na isiyozidishilingi milioni tano au kifungo kwa muda usiopunguamwaka mmoja na usiozidi miaka mitatu au adhabu zotembili, kwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia na kosahilo.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali hiiya CCM itoe kauli mbele ya Bunge hili Tukufu kama iko tayarisasa kuwachukulia hatua tajwa za kisheria Dkt. Asha-RoseMigiro, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, Mheshimiwa ZakiaHamdani Meghji, Mheshimiwa Muhamed Seif Khatib, BwanaNape Nnauye na wengine wote waliotajwa katika nyarakaza CCM kwa uhalifu walioufanya dhidi ya Sheria yaMabadiliko ya Katiba.

Page 120: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

120

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, baada ya ushahidi wote huu,hakuwezi kuwa na ubishi kwamba utaratibu mzima wakuundwa kwa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ni haramu.Hakuwezi kuwa na ubishi tena kwamba uharamu huu unalengo moja tu: kuhakikisha kwamba Katiba Mpyaitakayopatikana kwa mchakato huu haramu “... itakuwa niKatiba Mpya kwa jina tu, mambo mengine ya msingi yatabakivilevile (yalivyo katika Katiba ya sasa). Kwa maneno mengine,itakuwa ni Katiba ile ile, ya watu wale wale, wa chama kilekile.

“Mheshimiwa Spika, kama alivyosema Kiongozi waKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni: “Katika mwaka wakwanza wa mchakato wa upatikanaji Katiba Mpya, Tumeya Mabadiliko ya Katiba imethibitisha hofu tuliyokuwa nayotoka mwanzo kwamba lengo la mchakato wa Katiba Mpyauliowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba nikuhakikisha kwamba mabadiliko pekee yakayokuwepo niyale yenye kulinda matakwa ya CCM na Serikali yake au yalepekee yatakayokuwa na baraka za “status quo.”

Mheshimiwa Spika, katika Maoni ya Kiongozi waKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu hoja ya Ofisi ya WaziriMkuu, tulitangaza kwamba CHADEMA itajitoa ushiriki wakekatika mchakato wa Katiba Mpya endapo mambo yafuatayohayatapatiwa ufumbuzi hadi kufikia mwisho wa mwezi huu,yaani tarehe 30 Aprili, 2013:-

(i) Kufutwa kwa uchaguzi wa Wajumbe waMabaraza ya Wilaya ya Katiba uliofanywa na Kamati zaMaendeleo za Kata na badala yake wajumbe wa Mabarazaya Katiba ya Wilaya wachaguliwe moja kwa moja nawananchi wa Kata husika bila kuchujwa na WDC;

(ii) Serikali ilete mbele ya Bunge hili TukufuMuswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadilikoya Katiba yatayofanyia maeneo yafuatayo marekebisho:

(a) Vifungu vyote vinavyohusu uwakilishi katikaBunge Maalum la Katiba wa taasisi zilizoainishwa katika Sheria

Page 121: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

121

3 MEI, 2013

ya Mabadiliko ya Katiba ili kuweka wazi namna wawakilishiwa taasisi hizo watakavyopatikana kutoka kila taasisi naidadi yao kwa kila taasisi;

(b) Vifungu vyote vinavyohusu ushirikishi wawajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Zanzibar katikamijadala inayohusu mambo yasiyokuwa ya Muungano yaTanzania Bara ili kuhakikisha kwamba wajumbe wa Zanzibarambao hawatakuwa pungufu ya theluthi moja ya wajumbewote watashiriki katika mijadala inayohusu mambo yaMuungano tu na sio mambo ya Tanzania Bara yasiyokuwaya Muungano;

(c) Vifungu vyote vinavyohusu mamlaka ya Raiskuitisha tena Bunge Maalum la Katiba baada ya Bunge hilokuwa limeshapitisha Rasimu ya Katiba Mpya kwa lengo lakufanya marekebisho katika Rasimu kabla haijapelekwakwenye kura ya maoni ili kumwondolea Rais uwezo wakubadilisha maamuzi yaliyopitishwa na Bunge Maalum;

(d) Vifungu vyote vinavyohusu mamlaka yaKikatiba na ya kisheria yatakayoiwezesha Tume ya Taifa yaUchaguzi kuendesha na kusimamia kura ya maoni ilikurekebisha hali ya sasa ambayo Katiba na Sheria za Uchaguziza nchi yetu hazitambui uwepo wa kura za maoni nautaratibu wa namna ya kuiratibu, kuisimamia na kuiendesha;

Mheshimiwa Spika, madai ya Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni hayajatimizwa hadi tunatoa Maoni haya. Mwenyekitiwa Tume Jaji Warioba amesema waziwazi kwambauchaguzi wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, ambayo Tumeinakiri ulivurugwa na mivutano ya kisiasa na kidini,hautarudiwa na Mabaraza hayo yataendelea. Aidha,Mwenyekiti wa Tume amewaasa wale wanaolalamikiauchaguzi wa Mabaraza hayo wapeleke malalamiko yaokwenye Tume ili yashughulikiwe. Ushauri huu wa Tume haunamaana yoyote kwa sababu Mwongozo uliotolewa na Tumeyenyewe haujaweka utaratibu wowote wa kufungua nakushughulikia malalamiko yoyote yanayotokana na uchaguziwa Mabaraza hayo!

Page 122: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

122

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Serikali, WaziriMkuu aliahidi – wakati wa kuhitimisha hoja ya Ofisi ya WaziriMkuu – kwamba Serikali italeta Muswada wa Marekebishoya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kabla ya mwisho waMkutano huu wa Bajeti. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniimetafakari sana ahadi hii ya Waziri Mkuu. Pamoja nakwamba ni ahadi ya maneno tu, kama ilivyokuwa ahadi yaMheshimiwa Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete kwambamarekebisho yote yanayohitajika katika Sheria hiyoyatakamilika hadi kufikia Novemba 2012, Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni imeona ni vema iipe muda Serikali wa kuletamarekebisho tajwa ndani ya Mkutano huu wa Bunge la Bajeti.Kipindi hiki pia kitaenda sambamba na Tume kutoa Rasimuya Kwanza ya Katiba Mpya kwa ajili ya kuanza kujadiliwa naWatanzania.

Mheshimiwa Spika, endapo hadi kufikia mwisho wakipindi hicho Serikali itakuwa haijaleta Muswada wamarekebisho yanayotakiwa; au endapo Muswadautakaoletwa hautakidhi matakwa ya kuboresha mchakatowa upatikanaji wa Katiba Mpya, basi CHADEMA itawaalikawanachama, wafuasi na mashabiki wake Tanzania nzima,pamoja na taasisi za kiraia na za kidini, vyama vya siasa naWatanzania wote wenye nia njema na Taifa hili kuhamasishaWatanzania kuikataa Rasimu ya Katiba Mpya kwenye kuraya maoni itakayofanyika kwa ajili ya kuihalalisha Katiba hiyo.

Mheshimiwa Spika, nchi ya Kenya imepata KatibaMpya mwezi Agosti 2010 baada ya mchakato uliochukuazaidi ya miaka kumi na moja. Kwa mujibu wa Dkt. PatriceL.O. Lumumba (Kenya’s Quest for a Constitution: ThePostponed Promised, The Jomo Kenyatta Foundation, Nairobi,2008) aliyekuwa Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba yaKenya, kwanza Serikali ya KANU chini ya Rais Daniel Arap Moina baadaye Serikali ya NARC chini ya Rais Mwai Kibaki,zilijaribu kuteka nyara mchakato wa Katiba Mpya ya Kenyakwa kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya ambayo ilipopelekwakwenye kura ya maoni mwaka 2005 ilikataliwa na wananchiwa Kenya.

Page 123: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

123

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, kama inavyojulikana, baadayeKenya ilifanya Uchaguzi Mkuu wa Desemba 2007 kwa mujibuwa Katiba ya zamani ya Kenya ya mwaka 1969. Matokeo yauchaguzi huo chini ya Katiba ya zamani yaliingiza Kenya katikamachafuko makubwa ya kisiasa yaliyosababisha mauaji yamaelfu ya Wakenya. Kwa sababu ya machafuko hayo, Kenyaimeingia katika vitabu vya historia kuwa nchi ya pili katikaBara la Afrika, baada ya Hassan al-Bashir wa Sudan, yenyeRais na Naibu Rais walioko madaraka lakini wanakabiliwana mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu (crimes againsthumanity) katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.

Mheshimiwa Spika, Jamhuri ya Zimbabwe nayoimepata Katiba Mpya mwezi Februari ya mwaka huu baadaya mchakato uliochukua zaidi ya miaka kumi na sita. Mwaka2000, Chama Tawala cha ZANU PF cha Rais Robert Mugabekiliwapelekea wananchi wa Zimbabwe Rasimu ya KatibaMpya iliyotokana na mchakato uliotawaliwa na chama hichokuanzia mwanzo hadi mwisho. Katika kura ya maoniiliyofanyika mwaka huo, Rasimu hiyo ya Katiba Mpyailikataliwa kwa kura nyingi na wananchi wa Zimbabwe.Matokeo yake, Zimbabwe il i ingia katika giza kuu lamachafuko ya kisiasa na kijamii yaliyopelekea ukiukwaji wakutisha wa haki za binadamu na hatimaye Zimbabwekutengwa kimataifa kwa kufukuzwa katika Jumuiya yaMadola na kuwekewa vikwazo vya kiuchumi nakidiplomasia.

Mheshimiwa Spika, baadaye, ZANU PF iliyofikiriakwamba inaweza kutawala kwa mabavu ya kijeshi, ilipotezawingi wake Bungeni na hatimaye ili lazimika kufanyamaridhiano na vyama vya upinzani na makundi mengine yakijamii yaliyopelekea kusainiwa kwa Makubaliano Makuu yaKisiasa (Global Political Agreement). Chini ya Makubalianohayo, Bunge la Zimbabwe liliunda Kamati ya Katiba ya Bungeiliyokuwa na wajumbe sawa kwa kila kimoja cha vyamavikuu vya kisiasa vya nchi hiyo. Kamati hiyo ya Bunge,iliyokuwa na Wenyeviti Wenza Watatu, Makamu WenyevitiWenza Watatu na wajumbe tisa kwa kila chama, ndiyoiliyoandaa Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Zimbabwe

Page 124: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

124

3 MEI, 2013

iliyopigiwa kura ya maoni na kupitishwa na wananchi waZimbabwe mwezi Februari ya mwaka huu. Baadhi yaWabunge wa Bunge lako Tukufu walishiriki katika kura yamaoni hiyo kama sehemu ya ujumbe wa waangalizi waChama cha Mabunge ya SADC.

Mheshimiwa Spika, mifano ya Kenya na Zimbabweinatosha kuwaonyesha kwamba wanajidanganya walewote wanaodhani kwamba kuwa chama tawala chenyeWabunge wengi na mabavu ya kijeshi inatosha kubakimadarakani hata kwa hila na uchakachuaji. Saa yamabadiliko inapogonga, hakuna mabavu ya kijeshi walaUsalama wa Taifa wala mapesa mengi wala ukatili wa ainayoyote unaoweza kuzuia wimbi la mabadiliko hayo! Bungelako Tukufu litafanya vema kujifunza kutokana na historia yawenzetu.

Mheshimiwa Spika, hifadhi ya Haki za Binadamu.Katiba ya nchi yetu inatambua na kuhifadhi haki zabinadamu na wajibu muhimu. Sehemu ya Tatu ya Katiba yetuimefafanua haki hizo kwa kirefu. Kama sehemu ya Jumuiyaya Kimataifa, Tanzania vilevile imeridhia mikatabambalimbali ya haki za binadamu kama vile Tangazo laUlimwengu la Haki za Binadamu (Universal Declaration ofHuman Rights – UDHR), 1948; Mkataba wa Kimataifa wa Hakiza Kiraia na Kisiasa (International Covenant on Civil andPolitical Rights – ICCPR), 1966 na Mkataba wa Kimataifa waHaki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (InternationalCovenant on Economic, Social and Cultural Rights – ICESCR),1966. Aidha, Tanzania ni mwanachama wa Mkataba waAfrika wa Haki za Binadamu na za Wananchi (African Charteron Human and Peoples Rights – ACHPR), 1981.

Mheshimiwa Spika, licha ya kuwepo kwa msingi huuwa kikatiba na kisheria, hali ya haki za binadamu imezidikuzorota kwa kiasi kikubwa katika nchi yetu kama ambavyoKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeelezea mara nyingikatika Bunge lako Tukufu. Kwenye Maoni haya, MheshimiwaSpika, tunaomba tufanye marejeo ya taarifa rasmi za kitafitiza mamlaka za umma za kiserikali na za taasisi zisizokuwa

Page 125: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

125

3 MEI, 2013

za kiserikali kuhusiana na matumizi ya nguvu za vyombo vyadola na jinsi ambavyo zinahatarisha haki za binadamuzilizohifadhiwa na Katiba yetu. Taarifa hizi rasmi zinahusuuchunguzi wa kifo au mauaji ya mwandishi wa habari DaudiMwangosi katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, MkoaniIringa mnamo tarehe 2 Septemba, 2012, wakati akifanya kaziya kukusanya habari kwa niaba ya Kituo cha Televisheni chaChannel Ten katika mkutano wa ndani ulioandaliwa naChama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 18(b) na (d) ya Katibainahifadhi haki ya kila mtu “... kutafuta, kupokea na kutoahabari bila ya kujali mipaka ya nchi”; na “... haki ya kupewataarifa wakati wowote kuhusu matukio mbali mbali muhimukwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masualamuhimu ya jamii.” Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 22(1)inatamka bayana kwamba “kila mtu anayo haki ya kufanyakazi.” Kwa misingi hii ya Kikatiba, Marehemu Daudi Mwangosialikuwa na haki zote kisheria kukusanya habari katikamkutano wa CHADEMA katika Kij i j i cha Nyololo sikualipouawa.

Mheshimiwa Spika, Katiba yetu pia inatambua nakuhifadhi “... uhuru wa kukutana na watu wengine kwa hiariyake na kwa amani, kuchanganyika, kushirikiana na watuwengine na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani nakuanzisha na kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwakwa madhumuni ya kuhifadhi na kuendeleza imani aumaslahi yake au maslahi mengineyo.” (Ibara ya 20(1), nimuhimu kutambua hapa kwamba ‘aya nyakuzi’ (clawbackclauses) zilizokuwa zinaweka masharti na vizingiti vya ‘kwamujibu wa sheria’ vilivyokuwa vinazuia raia kufaidi haki nauhuru unaotambuliwa na Ibara za 18 na 20 viliondolewa naSheria ya Marekebisho ya Katiba, Sheria Na. 1 ya 2005.

Kwa maana hiyo, hakuna sheria nyingine yoyoteinayoweza kufunga au kupunguza uhuru na haki zilizotolewana vifungu hivi isipokuwa masharti yaliyoko kwenye Ibara ya30 ya Katiba yenyewe.

Page 126: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

126

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, Sehemu ya Kwanza ya Sura ya Sitaya Katiba inaunda Tume ya Haki za Binadamu na UtawalaBora na kuipa majukumu na mamlaka ya kuyatekelezamajukumu hayo. Kwa mujibu wa ibara ya 130(1) ya Katiba,majukumu ya CHRAGG ni pamoja na kuhamasisha hifadhiya haki za binadamu na wajibu kwa jamii; kupokeamalalamiko ya uvunjaji wa haki za binadamu nakuyachunguza; na, kama itabidi, kufungua mashaurimahakamani ili kuzuia uvunjaji wa haki za binadamu.

Mara baada ya mauaji ya Marehemu Mwangosikutokea, Tume ya Haki za Binadamu ilifanya uchunguzi wamazingira na sababu za mauaji hayo. Baada ya uchunguzihuo, Tume iliandaa Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu naUtawala Bora ya Uchunguzi wa Tukio Lililopelekea Kifo chaDaudi Mwangosi Kilichotokea Septemba 2, 2012 KijijiniNyololo. Taarifa hiyo ilitolewa hadharani na kwa vyombo vyahabari tarehe 10 Oktoba, 2012.

Mheshimiwa Spika, Taarifa ya Uchunguzi inaelezakwamba “... Tume ilizingatia zaidi masuala ya uvunjwaji wahaki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.Hivyo basi, Tume ilitilia maanani Katiba ..., sheria mbalimbalina mikataba ya kimataifa na ya kikanda inayohusu haki zabinadamu ambayo Tanzania imeridhia.” Katika uchunguziwake Tume ilibaini mambo yafuatayo:-

(1) Tarehe 2 Septemba, 2012 CHADEMA kiliruhusiwana Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi kufanya mikutanoya ndani na kuzindua matawi mapya lakini jioni ya tarehe 1Septemba, 2012 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa IringaMichael Kamuhanda alizuia CHADEMA kufanya mikutanoiliyoruhusiwa. Kwa mujibu wa Tume ya Haki za Binadamu,Kamanda wa Polisi wa Wilaya ndiye ‘“Officer in charge” waPolisi wa eneo husika kama sheria inavyotaka.’

(2) Viongozi wa CHADEMA kilifanya mazungumzona Mkuu wa Upelelezi wa Jinai Mkoa wa Iringa “... nakuruhusiwa kufungua matawi yao bila ya kuwa na mikutanoya hadhara.”

Page 127: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

127

3 MEI, 2013

(3) Msajili wa Vyama vya Siasa aliwaandikiabarua viongozi wa vyama vya siasa kuwataka kusitishashughuli zao kwa sababu ya sensa ya watu na makaziiliyokuwa inafanyika wakati huo.

(4) Wakati shughuli ya uzinduzi wa tawi la Nyololoukiendelea, Kamanda Kamuhanda alifika eneo hilo nakuamuru viongozi wa CHADEMA wakamatwe na wafuasi waCHADEMA walipinga kukamatwa kwa viongozi wao.

(5) Kamanda Kamuhanda aliamuru kupigwakwa mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchiwaliokusanyika katika ofisi za tawi hilo la CHADEMA.

(6) Baada ya mabomu ya machozi kupigwa,wananchi walitawanyika na kukimbia ovyo, lakini MarehemuMwangosi “... alizingirwa na Askari, aliteswa na hatimayeinadaiwa alipigwa bomu na kufa papo hapo.

(7) Marehemu Mwangosi aliuawa umbali watakriban mita 100 kutoka ilipo Ofisi ya CHADEMA tawi laNyololo.

(8) Katika tukio hilo wananchi kadhaawalijeruhiwa kwa mabomu, wakiwemo mwandishi wahabari wa gazeti la Nipashe Godfrey Mushi, Mwenyekiti waJumuiya ya Wanawake CHADEMA Wilaya ya Mufindi, WinnieSanga na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mufindi AsseliMwampamba “aliyekuwa akifanya jitihada za kumuokoamarehemu Daudi Mwangosi.”

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Taarifa ya Tumeya Haki za Binadamu, “... Tume imejiridhisha kuwa tukio lalililopelekea kifo cha Daudi Mwangosi limegubikwa nauvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi yautawala bora.” Taarifa ya Tume inafafanua kuwa, “... Tumeimejiridhisha kuwa Jeshi la Polisi limevunja haki ... ya kuishi,haki ya kutoteswa na kupigwa, haki ya usawa mbele yasheria na haki ya kukusanyika na kutoa maoni.”

Page 128: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

128

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na amri ya KamandaKamuhanda ya kupiga marufuku mkutano wa CHADEMA,Taarifa ya Tume inasema kwamba katika utekelezaji wamajukumu yake, Kamanda Kamuhanda “... alikiuka Sheriaya Vyama vya Siasa ... kifungu cha 11(a) na (b) na Sheria ya(Jeshi la) Polisi ... kwa kuingilia kazi za OCD wa Mufindi nakutoa amri ya kuzuia shughuli za CHADEMA wakati yeyehakuwa ‘Officer in-charge’ wa polisi eneo husika. Kwa maanahiyo amri aliyoitoa haikuwa halali kwa kuwa ilitolewa namtu ambaye hakuwa na mamlaka kisheria kutoa amri hiyo.Haya ni matumizi mabaya ya madaraka, hivyo ni ukiukwajiwa misingi ya utawala bora.”

Mheshimiwa Spika, Tume ya Haki za Binadamu ilihojipia hatua ya Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwakuwaandikia barua viongozi wa vyama vya siasa kuwatakakusitisha shughuli zao kwa sababu ya sensa. Kwa mujibu waTaarifa ya Tume, hatua hiyo “... ilikiuka misingi ya utawalabora kwani maelekezo yaliyotolewa ndani ya barua hiyoyanakinzana na Sheria ya Takwimu, Na. 1 ya mwaka 2002inayotoa fursa kwa wananchi kuendelea na kazi zao wakatiwa sensa....” Barua hiyo pia “... ni kinyume na Sheria ya Vyamavya Siasa ... inayotoa fursa kwa vyama vya siasa kufanyashughuli zake bila kuingiliwa.”

Mheshimiwa Spika, katika hili ni muhimu kunukuumapendekezo ya Tume ya Haki za Binadamu kwa kirefu:“Jeshi la Polisi na Msajili wa Vyama vya Siasa waepukekufanya maamuzi au matendo yanayoibua hisia za ubaguziau upendeleo miongoni mwa jamii wakati wanapotekelezamajukumu yao kisheria. Mfano, Jeshi la Polisi lilizuia mikutanoya CHADEMA kwa sababu ya sensa wakati huo huo ... CCMwalikuwa wakifanya uzinduzi wa kampeni huko Zanzibar.

Aidha, rai ya Msajil i wa Vyama vya Siasahaikuzingatiwa kwa upande wa CCM Zanzibar hukuCHADEMA walishurutishwa na Polisi kutii rai hiyo.” Aidha,Taarifa ya Tume inasisitiza kwamba “demokrasia ya mfumowa vyama vingi iheshimiwe na kulindwa.”

Page 129: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

129

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, sio Tume ya Haki za Binadamupekee iliyofanya uchunguzi wa mauaji ya MarehemuMwangosi. Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa laWahariri Tanzania (TEF), taasisi mbili huru zinazojihusisha namasuala ya habari Tanzania, nazo zilifanya uchunguzi wapamoja. Taarifa yao inayojulikana kama Ripoti ya TimuMaalum ya Uchunguzi Iliyoteuliwa na Baraza la HabariTanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)Kuchunguza Mazingira Yaliyopelekea Kuuawa kwa Mwandishiwa Habari Daudi Mwangosi Septemba 2, 2012 Katika Kijijicha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa, imeungamkono Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu juu ya jambohili.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Ripoti ya MCT/TEF, matokeo ya uchunguzi wao “... yanadhihirisha bila wasiwasi kwamba Polisi kwa makusudi waliwavurumishaWaandishi waliotoka Iringa wakati wakikusanya habari zashughuli za CHADEMA katika kijiji cha Nyololo. Zaidi ya hapo,Daudi Mwangosi mwenyewe aliuawa akiwa mikononi mwaPolisi huku wakisimamiwa moja kwa moja na Kamanda ...Kamuhanda.” Ripoti inakubaliana na Taarifa ya Tume ya Hakiza Binadamu kabla ya Mwangosi kuuawa, “... maelewanoyalifikiwa katika ya RCO na maofisa wa CHADEMA nakamanda (RCO) (aliwa)amuru maofisa wake kutotumianguvu dhidi ya watu waliokusanyika kwenye ofisi ile.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, hali hiyo maelewanoilibadilika mara baada ya Kamanda Kamuhanda kufikakatika eneo la tukio. Kwa mujibu wa Ripoti ya MCT/TEF,“mashuhuda wanaeleza kuwa RPC alimwita RCO nakumuonya wazi kuhusu kushughulikia kwa amani masualaya CHADEMA katika eneo la awali la utulivu.” Baada ya hapo,“inaelekea RCO alijitoa kuelekea eneo la umwagaji damu... na hivyo usimamizi wa utoaji amri katika eneo laumwagaji damu ... ulibakia kwa mkuu wake ambaye ni RPCMichael Kamuhanda.”

Mheshimiwa Spika, sawa na Taarifa ya Tume, Ripotiya MCT/TEF inaweka lawama za vurugu zilizotokea Nyololo

Page 130: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

130

3 MEI, 2013

kwenye miguu ya Kamanda Kamuhanda: Vurugu zilianzapale Kamanda Kamuhanda alipoamuru kukamatwa kwaviongozi wa CHADEMA waliokuwepo. “Kufuatia amri hiyo ...Polisi ... waliingia kwa nguvu katika ofisi ya CHADEMAwakipiga mabomu ya machozi na kuwaamuru viongozi haowajisalimishe.” Kwa mujibu wa Ripoti ya MCT/TEF, viongoziwa CHADEMA walitii amri hiyo na “... kujisalimisha kwa kuketina kuinua mikono yao juu.” Hata hivyo, “... wakati makadawa CHADEMA walitii maagizo ya viongozi wao ya kuketi chinina kuinua mikono yao juu, Polisi walifyatua risasi na mabomuya machozi na kuwapiga makada hao na waandishi kwavirungu.”

Mheshimiwa Spika, Ripoti ya MCT/TEF inakubaliana naTaarifa ya Tume ya Haki za Binadamu juu ya jinsi MarehemuMwangosi alivyouawa. “Alipoangalia nyuma, DaudiMwangosi aliona kikundi cha Polisi wakimpiga mwandishimkuu wa gazeti la Nipashe wa Iringa, Godfrey Mushi....Wakati mwandishi Godfrey Mushi akiwa bado anapigwa naPolisi, marehemu Mwangosi aliwakimbilia akiwaombawaache kumdhuru zaidi Mushi kwa kuwa alikuwa Mwandishitu. Polisi hawakumsikiliza. Badala yake wakamburutamwandishi huyo ambaye tayari alikuwa amepoteza fahamuna kumweka kwenye gari lao na wakamgeukia DaudiMwangosi mwenyewe, wakampiga kwa nguvu mpakaakapoteza fahamu.”

Mheshimiwa Spika, hata amri ya Mkuu wa Kituo chaPolisi Mafinga Mwampamba kuwataka Askari Polisi waachekumpiga marehemu Mwangosi haikusikilizwa na Askari hao.Ili kujiokoa, marehemu Mwangosi alimkumbatia OCSMwampamba na “baadaye kumwangukia miguuni mwakekuepuka kipigo zaidi.” Kwa mujibu wa Ripoti ya MCT/TEF,“picha za mgando zinaonyesha Polisi mmoja akipiga bomula machozi tumboni mwa marehemu Mwangosi kwa karibukabisa.” Bomu hilo liliusambaratisha mwili wa marehemuMwangosi aliyekufa papohapo. Kwa sababu marehemuMwangosi alikuwa chini ya miguu ya OCS Mwampamba,“naye pia alijeruhiwa vibaya.”

Page 131: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

131

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, siku moja baada ya mauaji yaDaudi Mwangosi, Kamanda Kamuhanda alinukuliwa navyombo vya habari akidai kwamba marehemu Mwangosialifariki “kutokana na kitu kizito kil ichotupwa nawaandamanaji.” Aidha, siku il iyofuata Kamishna waOperesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja alidai kwambabaada ya ghasia kudhibitiwa, marehemu Mwangosialikimbilia walipokuwa Polisi na “kitu kama bomu kikarushwana kundi la watu wanaokimbia hovyo na kumlipuaMwangosi.”

Mheshimiwa Spika, madai haya yanakanushwa naRipoti ya MCT/TEF inayomnukuu shuhuda mwanamkealiyeshuhudia mauaji hayo na kubainisha kwamba marehemuMwangosi “aliuawa chini ya usimamizi wa moja kwa mojawa RPC Michael Kamuhanda.” Ripoti hiyo pia imeelezea kwakirefu jinsi Jeshi la Polisi lilivyotoa taarifa zinazokinzana juu yakuhusika kwake na mauaji ya Mwangosi. Hivyo, kwa mfano,wakati Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa EmmanuelNchimbi alidai tarehe 4 Septemba, 2012 kwamba marehemualiuawa na bomu la machozi ambalo ‘halikulipuliwakitaalamu na Polisi’, Kamanda Kamuhanda alitokea kwenyetelevisheni siku iliyofuata “akitangaza habari za kuwatupialawama wafuasi wa CHADEMA kwa kutupa kitu kizitokilicholipuka na kumuua Mwangosi....”

Mheshimiwa Spika, kwa miaka miwili mfululizo, KambiRasmi ya Upinzani Bungeni imezungumzia kwa kirefu vitendovya mauaji ya raia wasiokuwa na hatia ambavyo vimekuwavinafanywa na vyombo vya dola hasa Jeshi la Polisi. Kamatulivyowahi kusema kwa kunukuu matokeo ya utafitiuliofanywa katika nchi za Afrika Mashariki na Mradi wa Hakiza Binadamu wa Jumuia ya Madola na kuchapishwa mweziJuni, 2006, ‘“watu wa Tanzania … wanakabiliwa na tatizola kuwa na Jeshi la Polisi ambalo mara nyingi lina sifa ya ulajirushwa, matumizi ya mabavu na kuwa na chombo katili chaserikali.” Kwa mujibu wa utafiti huo, “aina hii ya uendeshajiwa shughuli za Polisi inapingana na madai ya kuwepo kwademokrasia yanayotolewa na Serikali ya Tanzania.”

Page 132: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

132

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, sasa Taarifa ya Uchunguzi wa Kifocha Mwandishi wa Habari wa Channel Ten Bwana DaudiMwangosi, i l iyoandaliwa na Kamati i l iyoundwa naMheshimiwa Nchimbi na kuchapishwa tarehe 9 Oktoba 2012imethibitisha ukweli wa kauli hii na ukweli wa madai ya KambiRasmi ya Upinzani Bungeni juu ya matumizi ya nguvu ya Jeshila Polisi.

Baada ya kuzunguka huku na huko ikijaribu kulisafishaJeshi la Polisi, Taarifa ya Kamati hiyo inasema: “Hapakuwepona uhalali wa kutumia Bomu la Kishindo kwani lengo laulipuaji wake ni ili watu waogope na kukimbia.” Aidha,Kamati hiyo iliyoongozwa na Jaji Mstaafu Stephen Ihema,inakiri kwamba “hapakuwepo umuhimu wa kutumia Bomula Kishindo kwa sababu hata ingekuwa ukamataji tayariAskari Polisi wapatao sita walikuwepo eneo la tukio.” Kwamisingi hiyo, “… Kamati imeona kwamba … tukio la kuuawaBwana Daudi Mwangosi na kuumizwa baadhi ya Askari Polisihalikustahili kabisa.”

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Serikali itoe kauli kama inakubaliana na matokeoya taarifa hizi tatu zilizoandaliwa na taasisi za kiserikali kamavile Tume ya Haki za Binadamu, Kamati ya Jaji Ihema na MCT/TEF juu ya kuhusika kwa Jeshi la Polisi na mauaji ya marehemuDaudi Mwangosi. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Serikali iteo kauli mbele ya Bunge lako tukufu kamainakubaliana na Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamukwamba kitendo cha Kamanda Kamuhanda kupigamarufuku mkutano halali wa CHADEMA kilikuwa ni kinyumecha Sheria ya Jeshi la Polisi, Sheria ya Vyama vya Siasa naukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inaitaka Serikali itoe kauli kama – baada ya ushahidiwa taarifa hizi tatu - iko tayari kuiomba radhi CHADEMA kwakuisingizia kuhusika na kifo cha marehemu Daudi Mwangosi.Mwisho, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikaliitoe kauli mbele ya Bunge lako Tukufu kama iko tayari kuilipafamilia ya marehemu Mwangosi fidia kwa mujibu wa sheria

Page 133: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

133

3 MEI, 2013

kwa kitendo cha Serikali kusababisha mauaji yake bila‘uhalali.’

Mheshimiwa Spika, Serikali na chama ambacho serazake zinakiuka haki za binadamu na misingi ya utawala borainapoteza uhalali (legitimacy) ya kuendelea kutawala. Hapandipo CCM na Serikali yake ilikoifikisha nchi yetu: Waandishiwa Habari wanauawa kwa sababu ya kufanya kazi yao halaliya kutafuta habari za mambo yanayohusu umma kamamikutano ya vyama vya siasa.

Watanzania hawastahili Serikali ya aina hii. Kamaalivyosema Baba wa Taifa katika kitabu chake Uongozi Wetuna Hatima ya Tanzania: “Hatulazimiki kuendelea na uongozimbovu wa Chama na Serikali. Wala tukiendelea na hali hii,bila kubadili uongozi wa Chama na Serikali, sina hakika kamatutafika huko salama. Masuala muhimu ya nchi yetuhayatashughulikiwa.... Na masuala mengine muhimu ...yataachwa yajitatue yenyewe.

Nasema katika hali kama hiyo sina hakika kamatutafika salama; na tukifika salama tukiwa na uongozi huuhuu wa Chama na Serikali mbele kutakuwa ni giza tupu.Majuto ni mjukuu, huja baadaye.”

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo haya marefu,naomba kukushukuru na wewe binafsi na naombakuwasilisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba ambayo sijayasemayaingizwe katika rekodi Rasmi za Bunge lako Tukufu,nashukuru. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Kwa maana hii, ni kwambawatakaoweza kuchangia asubuhi hii watakuwa kamawachangiaji wanne. Nitaanza na Mheshimiwa JassonRweikiza, atafuatiwa na Mheshimiwa Fakharia ShomarKhamis, Mheshimiwa Sabreena Sungura na Mheshimiwa RayaIbrahim na kisha atafuatia Mheshimiwa Pindi Chana.Tutaangalia itakavyokuwa, Mheshimiwa Rweikiza.

Page 134: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

134

3 MEI, 2013

MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa nafasi hii, nichangie katika hotuba yaWizara ya Katiba na Sheria.

Mheshimiwa Spika, nchi yetu inaendeshwa kwautawala wa sheria na huu ndiyo msingi wa utawala bora.Kwa hivyo, Wizara hii ni muhimu kama zile Wizara nyingine,lakini cha kushangaza tumesikia hotuba ya Waziri, hotubaya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, fedha inayopewaWizara hii haitoshi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa vile, muda wa dakika kuminil ionao ni mdogo sana, nizungumzie Mahakama.Mahakama ndiyo mhimili mkubwa wa kutenda haki katikanchi hii lakini inasikitisha sana kwamba Mahakama inafanyakazi katika mazingira magumu sana, haipati fedha kamainavyotakiwa. Tumemsikia aliyewasilisha maoni ya Kamatianasema mwaka wa fedha huu tunaomalizia sasa hivi, fedhailiyotengwa ni shilingi bilioni 17.2 kwa ajili ya maendeleo yaMahakama haikutolewa hata senti tano. Mahakamainafanya kazi kwa shida sana. Sasa katika hali kama hii nivigumu kutegemea kwamba utawala wa sheria utaonekanavizuri.

Mheshimiwa Spika, watu wanakwenda Mahakamanikesi zinachelewa kumalizika, haziishi upesi. Kule Bukoba mtuanakwenda Kituo cha Polisi kumlalamikia mtu kwambaamemwibia au amemtukana, anaambiwa mlete mshtakiwakwa gharama zako wewe mwenyewe, msafirishe. Akiwekwamahabusu au rumande pale ulimpie chakula. Sasa kama hiini bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani au Katiba na Sheria,sijui lakini ni katika mfumo mzima wa utendaji haki. Ukweli nikwamba fedha inayotengwa kwa ajili ya Wizara ya Katibana Sheria bado haitoshi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, matokeo yakewananchi hawaendi tena Mahakamani, wala Polisikulalamika, wanachukua sheria mkononi ile tunayoita mobjustice. Mtu ana manung’uniko dhidi ya mtu, anamtuhumuhata kama ni uongo, anatafuta ndugu na marafiki zake

Page 135: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

135

3 MEI, 2013

wanamuadhibu kwa kumpiga na wengine wanawaua kwasababu akienda kule Mahakamani anaambiwa agharamieyeye mwenyewe, uwezo huo hana. Kaonewa lakinianaambiwa agharamie hizo gharama za kumpeleka mtuMahakamani. Niiombe sana Serikali iongeze fedha kwenyemafungu ya Wizara ya Katiba na Sheria na hasa fungu laMahakama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika kutenda haki, kwa mfanoMahakamani pale kama nilivyosema, kuna Mahakamayenyewe, Waendesha Mashtaka ambao ni Polisi naMwanasheria Mkuu wa Serikali, ukiangalia zile Idara nyinginezina nafuu kidogo; Polisi wana magari, Mwanasheria Mkuuwa Serikali watu wake wana magari na vifaa vya kufanyiakazi, Mahakama haina vifaa hivyo. Mahakimu hawananyumba, hawana magari, hawana motisha, kwa kweli haliinakuwa ni mbaya sana. Niiombe sana Serikali itoe fedhakwenye idara ya mahakama na Wizara ya Katiba na Sheriakwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, isiwe kwamba tunatenga fedhahapa na tunapitisha bajeti inakuwa ni kama ukomo, ceiling.Tunasema kiasi fulani kimetolewa kwa Wizara fulani lakinihizo fedha haziendi, inakuwa ni kama tumeweka kiwangocha mwisho cha ukomo. Zile fedha ziende zitumike kufanyakazi iliyokusudiwa katika Idara iliyokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, nimemsikia Msemaji wa KambiRasmi ya CHADEMA, yeye anasema Kambi Rasmi ya Upinzani,mimi nasema siyo ya Upinzani ni ya CHADEMA. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, anazungumzia Mabaraza yaKatiba, Tume, ninamshangaa sana ni kwa nini anapendakupotosha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, anapenda kupotosha umma kwasababu wao walisema wakiingia madarakani siku 100 naKatiba Mpya, wangeipata wapi? Siku mpya wangeipatawapi Katiba? (Makofi)

Page 136: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

136

3 MEI, 2013

T A A R I F A

MHE. HALIMA J. MDEE: Taarifa!

MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Tumeanzisha mchakato wakutafuta Katiba Mpya…

MHE. HALIMA J. MDEE: Taarifa!

WABUNGE FULANI: Kaa chini.

SPIKA: Naomba uendelee Mheshimiwa. (Makofi)

MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Siyo jambo dogo hili!Tumepiga hatua kubwa sana kwenye mchakato huu.Wananchi wote wametoa maoni yao, wote waliotaka kutoamaoni yao wametoa maoni yao. Wamehudhuria vikao vilevilivyoandaliwa kwa uhuru na uwazi, wametoa maoni yao.Tume imeundwa na inafanya kazi yake vizuri. WanategemeaTume waende kwa miguu nchi nzima? Wajumbe thelathinina wangapi sijui, wazunguke nchi nzima kwa miguu? Nilazima watumie magari, walale hotelini, wafanye kazi yao,anatoa takwimu za uongo, sijui posho shilingi ngapi, zakubuni, si za kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka tu kusema kwambamchakato huu ni mkubwa, Mabaraza yameundwa, vilevileyamehusisha wananchi wote, kuanzia kwenye vijiji na mitaa,wananchi wote wamepiga kura kwa haki na uwazikuchangua wajumbe wa Mabaraza haya. Hakunaupendeleo wala kufichaficha, kila mwananchi amehusikakwenye Mabaraza haya, yatakaa yajadili Rasimu ya Katiba,tutakwenda hadi Bunge Maalum la Katiba, amelisema,tutakwenda hadi kwenye kura ya maoni, kuna tatizo gani?Wenyewe walitaka watoe Katiba ya kuweka tu Wabungewao, Tundu Lissu Mwanasheria atunge Katiba aseme ndiyoKatiba ya nchi! Katiba inatungwa na watu kwa ajili ya watu,lazima watu washiriki kuanzia mwanzo mpaka mwisho.(Makofi)

Page 137: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

137

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, namshangaa sanaanapolalamika kwamba sijui gharama gani, sasa alitegemeaifanyike namna gani, bila gharama? Lazima mchakato huuuwe na gharama kubwa na gharama hizi tunatoa wananchiwenyewe katika kodi, ndivyo ilivyotegemewa na ndivyoilivyo. Kwa hiyo, si vizuri kusimama pale na kupotoshawananchi kwamba, mchakato huu umetekwa na CCM, oohmchakato huu umekuwa sijui namna gani, siyo kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaunga mkono hojaya Waziri wa Katiba na Sheria lakini niombe kwamba Wizaraipewe fedha za kutosha na Mahakama iongezewe mafunguili iweze kufanya kazi zake vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Sasa namwita Mheshimiwa Fakharia ShomarKhamis atafuatiwa na Mheshimiwa Sabreena Sungura naMheshimiwa Raya.

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Spika,ahsante. Kwanza, naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitaanza kuzungumziaMahakama. Chombo cha Mahakama ni muhimu kwa nchiyoyote, siyo Tanzania peke yake lakini kuna mambonimeyaona ambayo kwa Mahakama yetu kidogo sijui nikwamba tuna Majaji wachache au umekuwa kama ndiyoutaratibu, kwa sababu ziko Mahakama kama nane;Mahakama ya Rufaa, Mahakama Kuu, Mahakama KuuDivisheni ya Biashara, Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi,Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mahakama ya HakimuMkazi, Mahakama ya Wilaya na Mahakama ya Mwanzo, zotehizi ukiziangalia utendaji wake hakuna hata Mahakama mojailiyomaliza mashauri au kesi. Kila mwaka zinalimbikizana,badala ya kesi kumalizika, zinazaa kesi nyingine.

Sasa najiuliza, hivi kweli tuko serious kama Mahakamakuwasaidia wananchi? Unapokuwa na kesi huwezi kulala,

Page 138: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

138

3 MEI, 2013

harakati zako zote zinakuwa haziko kwenye utaratibu mzuri.Sasa ningeona hiki chombo wakati kuna mfuko waMahakama, shilingi bilioni 20 zile walizopewa ambazowalisema watapunguza hizi kesi, nimuulize MheshimiwaWaziri, je, hili kweli linatendeka?

Mheshimiwa Spika, tunajua kuna utaratibu mmoja,mtu unapompa kazi umfuatil ie. Unajua Mahakimuhawafuatiliwi, kwa nini? Mtu anakuwa na kesi, hajui kwawiki mimi natakiwa amalize kesi ngapi, kwa mwezi amalizekesi ngapi, kwa mwaka amalize kesi ngapi? Sasa mtu huyukama hutamwekea utaratibu au Mkaguzi ambaye atakuwaakiwakagua Majaji kwa mujibu wa utaratibu wa kesiwanazopangiwa, ndio mambo yanakuwa hivi. MheshimiwaWaziri naona hawa Majaji lazima kuwe na utaratibu wakuangalia na kufuatilia ili kujua ni kesi ngapi wanazisikilizakwa wiki, mwezi na mwaka. Nafikiri huu utakuwa ushaurimzuri na hata Jaji atakuwa anajua kwamba wiki hii lazimanimalize idadi fulani ya kesi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakuja katika mabadiliko yaKatiba. Najua Tume wanatakiwa ifikapo Aprili, 2014 wawewamekamilisha mchakato mzima wa Katiba na tuwe naKatiba yetu. Siyo vibaya na Mwenyezi Mungu atawasaidia.Tume imepewa utaratibu wa kukusanya maoni na tumeonajinsi zoezi hilo lilivyokwenda. Wamepewa uwezo kuanziaMikoa, Wilaya, vikundi maalum na kadri watakavyojipangia.Utakuta utaratibu huu wa kura za maoni, wakati walipokujakule Zanzibar walikuwa wanafanya Kishehia. Mchakatomzima ule umekwenda, hasa tukichukua mfano wa Mkoaambao nilikuwepo mimi wa Mjini Magharibi, utakuta Tumewalikuwa wakifika pale wanapofanyia ile shughuli yamchakato ameachiwa Sheha.

Huyu Sheha maskini hajawezeshwa, uwezo wake nimdogo. Anatakiwa atafute sehemu ya mkutano, atafute vitivya wajumbe wa Tume, Sheha huyo huyo atafute kivuli chakukaa wajumbe wa Tume, Sheha huyohuyo uwezo hana,anaweza kutafuta vitu mahali popote, kama ni viti au nini,akipeleka inakuwa ni mvutano, aah kachukua viti au

Page 139: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

139

3 MEI, 2013

maturubai kwenye vyama. Sasa akachukue wapi na yeyeuwezo hana? Nyumbani kwake kitu hicho anaweza akawahana, akachukue wapi? Suala hil i nil ikuwa natakaniwatabanaishe Tume waangalie na kuhakikisha kwamba,wanapompa mtu kazi, wampe na uwezo wa kuitekelezakazi hiyo, najua vifungu hivyo Tume wanavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, isitoshe mchakato ule ulivamiwana vijana. Kwa nini ulivamiwa na vijana na ukakosa nguvu?Utakuta anakuja Mwenyekiti au mhusika wa Tume anasemakwamba, mtu yeyote anaweza kwenda Shehia yoyoteakavamia na akatoa maoni. Kweli watu wamevamia, watuwalewale walikuwa wanajirejea, mtu wa Shehia husikahawezi kufika pale, Masheha waliopewa kazi ya kusimamiawakawa wananung’unika.

Sasa ukakuta ule utaratibu badala ya kuwa mzuri,ukawa na vurugu. Wazee wanashindwa kwenda,walipowekwa watu hao wanaotoa maoni siyo pa heshima,mtu anawekwa chini, mahali pana vumbi, mvua inanyeshamahali pale unakuta pana maji, sasa utakuta mtu mzimana heshima zake hawezi kwenda, ikawa wanaokwenda nivijana. Huko mbele kuna kura za maoni, jamani tuangalie nivipi tutajipanga ili shughuli yetu iweze kuwa nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilikuwa nataka kuzungumza juuya RITA. Hapa nitazungumza kuhusu wosia. Watanzaniawengi bado hatujapata elimu ya kutayarisha wosia. Watuwanakufa, kesi zinakwenda kwenye Mahakama, watuwanacheleweshwa kupata haki zao, kesi zinachelewakumalizika. Nataka Mheshimiwa Waziri akifika hapa ajeanielezee, RITA na uhifadhi na uandikaji wa wosia ameuwekakwenye kiziba gani kwa sababu, RITA haijafanya kazi ya kupitakuelimisha na kuwafahamisha wananchi au kutoa elimukatika Vijiji, Miji na Mikoa.

Hili ni suala zuri kwa sababu tunakokwenda siku hiziumri wetu ni mdogo, siku hizi tunaona vijana wetu wanamilikimali nyingi, sasa kama hakutakuwa na wosia hapa katikatikutatokea vurugu, kutofahamiana au kuumizana. Naomba

Page 140: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

140

3 MEI, 2013

kitengo hiki kifanye bidii kupita kwenye Mikoa na jamii ili kutoaelimu itakayowasaidia Watanzania kuweza kujua jinsi yakuandika na kuhifadhi wosia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nije katika ofisi ya DPP. Ofisi yaDPP inafanya kazi nzuri na tunaipongeza lakini kuna mvutanoambao nilikuwa nataka Mheshimiwa Waziri akija hapaanifafanulie, juu ya ofisi ya DPP na ofisi ya TAKUKURU. TAKUKURUanasema kesi zangu za rushwa haziendi kwa sababu DPPhazitoi. DPP anasema kwamba mimi nafanya kazi kwa mujibuwa taratibu na sheria za nchi. Sasa ningeomba MheshimiwaWaziri aje kuifahamisha jamii huu mvutano uliopo katikatihapa unaashiria kitu gani? Kwa sababu Serikali inatakarushwa iondoke na DPP anafanya kazi kwa mujibu wa sheria,sasa jambo hili ili liweze kufanyika, kutendeka na kutoa hisiakwa wananchi ili waweze kuiamini Serikali yao, ni vipi Serikaliitalisimamia ili tumwone DPP anafanya kazi bila matatizona TAKUKURU anamuamini DPP kwa mujibu wa shughuli zake.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka kuzungumzia kidogo juuya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo. Katikaukurasa wa 45 wa hotuba ya Mheshimiwa Waziriamezungumza vizuri na tumemwelewa, lakini badochangamoto zipo kwa sababu hawa wanafunzi wapo,ruzuku inakwenda kwenye Wizara hiyo ninakubali, lakini nawanafunzi bado wanatakiwa kupata mikopo, bila ya mkopohuwezi kusoma. Kama kuna sheria inazuia wanafunzi hawawasiwezi kupata mikopo, iletwe hapa Bungeni, tuirekebisheili hawa wanafunzi na wao waweze kupata mikopo kamawanavyopata wanafunzi wenzao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia nakuja kwenyeTume ya Haki za Binadamu. Bado hii Tume yetu ya Haki zaBinadamu haijatusaidia kwa sababu imerundika mashauri6,891….

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

Page 141: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

141

3 MEI, 2013

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Spika,ahsante, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Haya, nitamwita Mheshimiwa Sabreena kwadakika tano na Mheshimiwa Raya dakika tano.

MHE. SABREENA H. SUNGURA: Mheshimiwa Spika,ahsante. Kwanza kabisa, napenda kuweka kumbukumbusawa kwamba, mchangiaji wa kwanza amepotosha ummakwa kusema Chama cha CHADEMA kilisema kitakamilishamchakato wa Katiba ndani ya siku 100. Sivyo, Ilani yaCHADEMA ilisema itaanza mchakato wa marekebisho yaKatiba ndani ya siku 100. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, naunga mkonohotuba ya Kambi ya Upinzani. Pili, ninapenda Serikaliitwambie, ilivyoamua kuweka shilingi milioni 18 kwa ajili yawajumbe wa Tume ambao wanaweza wakapatamaambukizi ya UKIMWI, mimi naona suala hili ni kuitabiriajamii yetu mabaya. Je, ulifanyika mchakato wa kuwapimaWajumbe hawa kabla hawajaingia kwenye kazi hiyo nawatajihakikishiaje kwamba ni wajumbe wangapiwamepatwa na dhoruba hiyo ndani ya mchakato huu?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niende moja kwa mojasasa kwenye suala zima la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu naWanasheria wa Wizara. Serikali imekuwa na double standard,Wanasheria ni haohao wenye same qualification lakini scaleza mishahara yao ni tofauti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunataka Serikali leo ije itwambieMwanasheria wa Wizara yupo pale kufanya kazi gani? Kesizote za Wizara zinazopelekwa pale, Mwanasheria wa Wizaraanabakia tu kama mshauri, wasimamizi wa kesi hizo niWanasheria wa Attorney General. Sasa wale watu wa Wizarapale tumewaweka wafanye kazi gani? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mikataba yote inayopelekwaWizarani inapita tu, inapelekwa kwa Attorney General. Kuna

Page 142: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

142

3 MEI, 2013

nini huko kwenye Ofisi ya Attorney General?Mnawacheleweshea Watanzania maendeleo. Mikatabainachelewa, kesi zinachelewa tunaambiwa zipo kwa AttorneyGeneral. Sasa wale Wanasheria waliopo katika Wizarawanafanya kazi gani jamani? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nafikiri sasa ni wakatimuafaka ndugu yangu Attorney General utaratibu wa zamaniurejeshwe kwamba Wanasheria wa Wizarani na Wanasheriawa Ofisi ya AG, wote wabakie kwamba ni ma-State Attorneysna wapewe mshahara unaolingana.

(Hapa Mwanasheria Mkuu wa Serikalialikuwa anatikisa kichwa)

MHE. SABREENA H. SUNGURA: Ndiyo unaweza ukatikisakichwa, lakini leo hii mtu ambaye ni Principal Legal Officerwa Wizara…

SPIKA: Kanuni inasema uzungumze na mimi sio nawatu wanaotikisa vichwa vyao. Zungumza na mimi. (Kicheko)

MHE. SABREENA H. SUNGURA: …anakuwa ni mdogokwa State Attorney hata kama ana-experience ya kutosha,ana uzoefu wa kazi wa muda mrefu wa kutosha,mnawaondolea watu morale, mnawakatisha tamaa. Kwahiyo, ni lazima mfikirie kurejea upya utaratibu wa zamaniambapo watu wote walikuwa wanaajiriwa kama StateAttorneys ili mambo yaweze kwenda sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ninalopenda kugusiani suala nzima la ucheleweshaji wa kesi kwenye Mahakamazetu. Kumekuwa kuna mlundikano mkubwa wa kesi nahatuelewi kwa nini, ni muda mrefu toka enzi na enzi kesizimekuwa zikichelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda tu kuwausia wenzanguwa DPP, ni vyema sasa tukaanza system ya pre-bargaining.Wenzetu wa USA, asilimia 96 ya kesi zao za criminal zinakuwasolved kwa kutumia mfumo wa pre-bargaining kwamba DPP

Page 143: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

143

3 MEI, 2013

anafanya mazungumzo na watuhumiwa, wanamaliza hiyokazi kabla ya kupoteza muda na pesa ya Mahakama,wanamaliza nje kabisa, wanapokwenda pale inakuwa tu nisuala la utekelezaji lakini sisi kesi zetu zimekuwa zinachukuamuda mrefu haziishi. Kwa hiyo, tungefanya hii system ya pre-bargaining kwamba mtu anakubali kosa mapema, in extentcharge zao zinakuwa reduced. Nafikiri suala hili litakuwa nisuala la msingi sana na la umuhimu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu, napenda moja kwa mojanigusie Tume ya Haki za Binadamu… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante muda umeisha, Mheshimiwa Raya.

MHE. RAYA IBRAHIM KHAMIS: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotuba hii.Najikita katika maeneo matatu ambayo nitayazungumziakatika Wizara hii na miongoni mwa hayo nil i jaribukuyazungumzia katika Bunge la Bajeti lililopita la mwaka jana,lakini bado inaonekana kuna uzito fulani katika utekelezajiau pamoja na jitihada hizo imekuwa ni changamoto nabado ni tatizo, ni suala zima la mashauri.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri katika hotubayake amelieleza vizuri, yaani hotuba yake imeonyeshamatumaini ya kushughulikia mashauri pamoja na kupunguzamsongamano wa kesi Mahakamani. Mashauri yana gharamanyingi yaani mtu mpaka shauri lake liishe ni gharama kubwasana na Watanzania wengi siyo wote wenye uwezo wakumudu kushughulikia mashauri yao kwa gharama ambayoSerikali imeweka.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali ama maoniyangu katika suala hili ni kupunguza gharama za mashauri.Mheshimiwa Waziri katika hotuba yake kurasa za 45 na 46ameeleza mikakati ya kukabiliana na changamoto hiiambapo ni pamoja na kuongeza idadi ya Mawakili na idadi

Page 144: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

144

3 MEI, 2013

ya watumishi lakini shauri wangu kwa hapa ni kuwa nalimitation ya time katika mashauri. Kesi inapofunguliwa basiangalau isizidi miaka miwili iwe imemalizika, nadhani hiyoitakuwa njia ya kupunguza msongamano wa mashaurimengi yaliyopo Mahakamani. Vilevile itasaidia Watanzaniawengi kupata haki zao kwa muda muafaka kama ambavyowanatarajia na siyo ambavyo wanavyopata kwa sasa. Kwahiyo, nashauri kuwe na limitation ya time katika mashauriyaani yasizidi miaka kadhaa katika kuendeshwaMahakamani. Nadhani hilo litakuwa ni suala zuri pamoja nakupunguza gharama kwa watu ambao wanatakiwawafanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la pili ambalo nitaliongeleani suala zima la rushwa katika Mahakama zetu. Tunaonabado rushwa ni tatizo kubwa, rushwa ni changamoto katikaMahakama zetu. Inafikia wakati judgement imetoka basiupewe ile judgement yako, haujakaa sana umekaa miezisita, yaani mtu chini ya miezi sita huwezi kupata judgementunless una undugu na mtu yeyote ama vinginevyo labdaumetoa pesa ili upatiwe judgement yako ambayo ni hakiyako unatakiwa uipate mara tu baada ya kutolewa na isizidimuda kadhaa lakini inafika miezi sita mtu bado hajapatajudgement.

Mheshimiwa Spika, vilevile katika Mahakama, ku-release order kutoka Mahakamani pia inachukua mudamrefu sana labada uwe unajuana na mtu ama vilevileutangulize pesa ndiyo upate haki yako.

Mheshimiwa Spika, aidha, ukija kwenye suala lakumpata Jaji bado inakuwa ni tatizo kubwa kwa watukuwapata Majaji, Mahakimu na Mawakili ambao watakujakuwasimamia katika kesi zao. Nakumbuka nil iwahikulizungumzia na kidogo limegusiwa katika hotuba ya Wazirikwa matumaini lakini bado tunataka kuona utekelezaji, jinsiambavyo Watanzania, wananchi ambao wanakabiliwa namashtaka yao, wanakabiliwa na kesi zao Mahakamani,Serikali inawasaidia kama katika Act ilivyoelezwa kwambainatakiwa Mtanzania ambaye hana uwezo basi Serikali

Page 145: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

145

3 MEI, 2013

imwone, imsaidie, impe Wakili na imueleweshe lakiniunakuta mtu hana uwezo, hakuna maelekezo yoyote, hajuiaanzie wapi, hajui amalizie wapi ili apate haki yake. Hakiinafinywa, haki inazuiwa, inatumiwa na watu ambaohawastahili kuitumia na inatumiwa na watu kwa kupeanatuseme. Mtu ambaye ni maskini hata anapokwendaMahakamani anaona tu anapoteza muda wake na pesa,haendi kupata haki yake kwa sababu kwa sasa hivi hakizinanunuliwa na siyo kutolewa Mahakamani. Kwa hiyo,tunashauri Serikali iliangalie sana hilo, kupitia Wizara hiiilitazama hilo suala la rushwa katika Mahakamani zetu nakuwapatia wananchi haki zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la tatu ambalo napendakuliongelea, ni kutofikiwa kwa Mahakama ama kuwa naMahakimu wachache. Hatuwezi kuwa na accessibility yajustices endapo tutakuwa na hali ambayo tunayo sasakwamba Hakimu anatoka Bagomoyo, Hakimu huyohuyoanasubiriwa Chalinze katika Mahakama ya Wilaya aendeakasikilize kesi nyingine, tunakwenda wapi, tunafanya nini?Kinachotakiwa, wasomi wapo wengi mitaani, vijana wengiwame-qualify kuwa Mahakimu, lakini ajira bado ni kikwazo,inakuwa ni tatizo kwa vijana hawa kupatiwa ajira. Hivyobasi, ili tuwe na accessibility ya justices katika Mahakamazetu, ni vizuri kuongeza Mahakimu, kuajiri watu na vilevilekuboresha mazingira ya wafanyakazi wetu hasa Majaji…(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante. Sasa nitamwita Rukia Kassim Ahmed,atafuatiwa na Mheshimiwa Pindi Chana.

MHE. RUKIA KASSIM AHMED: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia katikahotuba hii ya Wizara ya Katiba na Sheria.

Mheshimiwa Spika, Wizara hii ndiyo chanzo kikubwacha migogoro katika nchi hii kwa watu kutokuelewa sera

Page 146: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

146

3 MEI, 2013

na sheria zilizopo katika nchi hii. Sera na sheria zipo lakinizimefungiwa katika makabati tu, wananchi hawazielewihata wale wanaotakiwa kutekeleza zile sera basi piahawazielewi, hili ni tatizo kubwa ambalo linasababishwa naWizara hii.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, migogoro mikubwainayohusiana na Muungano, inatokana na watu kutokujuasera na sheria. Kwa mfano, katika Bunge hili, kuna baadhiya Waheshimiwa Wabunge humu hawajui hata maana yaJamhuri ya Muungano. Kuna Waheshimiwa Wabunge humuwamethubutu kusema kuwa sisi Wazanzibari hatupaswikuingia katika Bunge la Katiba kwa kujadili mamboyanayohusiana na Bara. Tena la kusikitisha hasa, watu hawani watu wakubwa, watu ambao wapo katika Chamakikubwa kinachojiita ni chama mbadala, wanafikia mahaliwanatwambia sisi Wazanzibar hatuna haki ya kuingia katikamchakato wa kujadili Katiba ya nchi hii, hii yote ni uelewamdogo wa sera na sheria zinazohusu Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna baadhi ya WaheshimiwaWabunge humu katika Bunge la Tisa walithubutu kusemaGeita kuna watu wanaozidi milioni moja na kidogowanawakilishwa na Wabunge wanne lakini pia Zanzibarkuna watu milioni moja na kidogo wanaowakilishwa nawatu zaidi ya 50. Hii yote ni uelewa mdogo wa sera na sheriaya Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wa kulaumiwa ni Wizara hii kwakutokutoa taaluma na wakawafanya Wabunge wa Bungehili kujua nini sera na sheria ya Muungano. Naomba Wizarahii itoe taaluma kwa Waheshimiwa Wabunge kabla ya Bungela Katiba ili isije ikatuletea matatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, sasanataka niende kwenye Mahakama. Ucheleweshaji wa kupatahaki, hilo ni tatizo kubwa na kwa kweli linaleta mzozomkubwa katika nchi. Ucheleweshaji wa kesi Mahakamani,watu kutopata haki yao mapema ni tatizo kubwa sana.

Page 147: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

147

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, katika hotuba, ukurasa wa nane,Waziri mwenyewe amesema Mahakama ya Rufaa imesikilizakesi kwa asilimia 13, Mahakama Kuu imesikiliza kesi asilimia30, Mahakama ya Biashara imesikiliza kesi asilimia 22, hili nitatizo. Kwa sababu haki inapochelewa kupatikana watuwanakosa imani hata na Serikali, watu wanakosa imani nachombo hiki cha Mahakama.

Kwa hiyo, hii milundikano wa kesi upungue. Kuna watuwamelundikana katika mahabusu au katika jela ambaowana kesi ndogo ndogo. Kwa mfano, kibaka pengineakampora mtu simu, pengine kuna mtu kaiba kukuanawekwa katika jela, hawa watolewe, waende Kariakookule wakasafirishe mitaro, wakasafishe soko lile ile pekee yakeni adhabu na ni aibu wataona haya.

Mheshimiwa Spika, wakipelekwa kule, wakaendakusafisha watu wakiwaona hawa wamekamatwa kwa kesipengine ya kuiba kitu kama hiki, mtu atakuwa na taharukimara ya pili haibi tena itakuwa funzo na mlundikano kwenyejela zetu utapungua. Hata katika mahabusu zetu, utakutavilevile kuna mlundikano kama huo.

Mimi nashauri Serikali iangalie zile kesi ndogo ndogowatu watolewe kwa njia kama hiyo. Katika Mikoa yetu hukokuna sehemu za kusafisha, wapelekwe wakasafishe pia iweni hukumu yao na tutapunguza ule mlundikano.

Mheshimiwa Spika, halafu pia katika haya Magerezayetu, kuna watoto wadogo ambao wamechanganywa nawatu wakubwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

SPIKA: Mheshimiwa Mbunge muda wako umekwisha.Msemaji wa mwisho mchana huu ni Mheshimiwa PindiChana.

Page 148: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

148

3 MEI, 2013

MHE. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, nichukuenafasi hii kukushukuru kupata nafasi.

Mheshimiwa Spika, mimi nitajikita kwenye Sheria yaMabadiliko ya Katiba. Wakati sheria hii inapitishwa miminilikuwa ni Mwenyekiti na ninashukuru Mungu bado niMwenyekiti, kwa hiyo, napenda kuielezea. Kwanza nianzena Bajeti ya Tume, Tume tumepitisha bajeti shilingi bilionitakribani 33. Hela hizi kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nindogo na nitatoa sababu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, walikuja mara ya kwanza, hii nibajeti ya pili, walituomba shilingi bilioni 40 na kulikuwa nakazi nyingi za kufanya. Kwenye Kamati tukasema baadhi yakazi zipunguzwe, tukaenda shilingi bilioni 33 na sasa hiviwamepewa ceiling ya kipindi kilichopita shilingi bilioni 33.Sasa wakati wa kujadili tulisema hawa wajumbe wa Tumewalipwe posho au mishahara? Tukachukua mifano ya nchiambazo zimebadilisha Katiba mfano wa Ghana na Kenya.Kenya walikuwa wanalipwa dollar na Tume ya Mabadilikoya Katiba ya Kenya walikuwa wanaruhusa donors kutia pesakwenye Tume, kwa hiyo, walikuwa na pesa za kutosha. Kwahiyo, sisi tukasema hii ni call kwa ajili ya nchi, tunaombamfanyeni kwa viwango na malipo wanayolipwayamepitishwa na Standing Orders kwa utaratibu maalum.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatujaanza leo kuwa na hizi Tume,tumewahi kuwa na Tume ya Kukusanya Maoni kutoka ChamaKimoja kwenda Vyama Vingi, tumewahi kuwa na Tume yaku-fast track East Africa Community kwenda kwenye PoliticalFederation, hebu tuangalie Tume mbalimbali zimekuwazinalipwa shilingi ngapi halafu tuangalie Tume ya Mabadilikoya Katiba inalipwa shilingi ngapi? Pale ndipo tuta-justifykama wanalipwa fedha nyingi ama hawalipwi lakini utaonawanajitolea kwa maslahi ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba Watanzaniawajue kwamba posho wanayolipwa Wajumbe wa Tume kwakweli ni kwa kujitolea. Kwa sababu taarifa hizi zipo wazi wala

Page 149: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

149

3 MEI, 2013

siyo za kificho angalieni Tume mbalimbali zimekuwazikilipwa kiasi gani ukilinganisha na Tume mbalimbaliambazo zimeshakuwepo hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niendelee kusema kwamba Tumeimekuwa inachukua maoni katika baadhi ya maeneo,inapofika kwenye Wilaya inachukua Kata kadhaa. Ni kwelitungetamani iende kwenye Kata zote. Kutokana na bajetituliyowapa, kwa kweli ni vigumu kufika katika Kata zote.

Aidha, katika kufanya tafiti au kukusanya maonitunafanya sampling, kuna purposeful sampling, snow ballsampling, random sampling na kuna wasomi wengi hapa,sasa leo tunataka Watanzania milioni 45 wote wakatoamaoni, sijui hiyo ripoti itakuwaje? Huwa tunafanya sampling!Kwa hiyo, maudhui ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwakweli yapo sawasawa na sheria hii ililetwa Bungeni na tulijadiliWabunge wote 357. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la elimu, sisi Wabungetukipitisha sheria hapa lazima tukawaelimishe watu wetu,tukawape feedback iwe ni bajeti, iwe sheria, ni jukumu letu.Tulipopitisha hii sheria tena tukasema isije under certificateof urgency, tukaambiwa twende tukawape elimu watu wetuMajimboni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, utaratibu huu wa kutoa elimuilikuwa ni jukumu la Wabunge, Taasisi za Kidini, NGO’s nawadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Vyama vya Siasa.Leo hii Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasiliana na wanachamawa CCM au Nape anaambiwa kwa nini umewasiliana nawanachama wako, hiyo sijapata kuona. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumeruhusu Vyama visajiliwe, leohii tuna vyama 18 vilivyosajiliwa, kila chama kina utaratibuwake. Kwa hiyo, mimi ninasema big up Nape, big up Dkt.Asha-Rose Migiro muwasiliane na mkishindwa hiyo kazi,tutasema mtupishe wataingia wengine. Kwa hiyo,nawapongeza sana. (Makofi)

Page 150: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

150

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, lipo suala wanalosema wadaukwamba Mabaraza yamechukuliwa wanaCCM. Mimi sielewi,Tanzania population ni milioni 45 leo hii tukisema tufanyestatistics wanaCCM ni wengi, haikwepiki na ndiyo maanahumu Bungeni CCM ni wengi maana yake waliotupa ridhaahuko nje CCM ni wengi. Sasa unashangaa nini kuonaMabaraza CCM ni wengi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumesema twende tukashindane,sasa mwenzio anakimbia wewe unasema mshike huyo, rudinyuma. Leo kuna Vyama vinasajiliwa, tumeruhusu. Sasa hivikuna vyama 18 vil ivyosaji l iwa, Chama kitachokuwakimesajiliwa leo, followers wake hawatafanana na Chamakilichosajiliwa miaka ya nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tuliposemawakachaguliwe wajumbe, wala hatukusema watokane navyama, wanachaguliwa Watanzania wajumbe kwendakwenye Mabaraza na uchaguzi huo umefanyika wazi kabisa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaunga mkono hojahii asilimia mia moja na suala hili la Katiba lije haraka nalifuate muda unaostahili. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MHE. PINDI H. CHANA: Nadhani ni kengele ya kwanza,tunaendelea. (Makofi)

SPIKA Naona ni kengele ya pili imeishagonga tayari.

Waheshimiwa Wabunge, tutakaporudi, tutakuwa nawachangiaji wachache na hii Wizara ni ya siku moja kwahiyo tutakuwa tunamaliza. Kwa hiyo, nasitisha shughuli zaBunge mpaka saa kumi na moja jioni.

(Saa 7.00 mchana Bunge lilisitishwa mpaka Saa 11.00 Jioni)

Page 151: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

151

3 MEI, 2013

(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tulipokuwatumesitisha Shughuli za Serikali mchana, nilikuwa nimwiteMheshimiwa Anna Abdallah, atafutiwa na MheshimiwaMwanasheria Mkuu, Mheshimiwa Naibu Waziri halafu mtoahoja. Mheshimiwa Anna Abdallah!

MHE. ANNA M. ABDALLAH: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia hojaya Waziri wa Katiba na Sheria. Awali ya yote, naombakuunga mkono hoja hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nianze na kuelezakwamba asubuhi hukuwa umepata taarifa hii ya Upinzanihapo Mezani, lakini baadaye ukatuambia kwambaumeipata. Sisi wengine tumeipata alipokuwa anachangiamtoa hoja wa mwisho ule mchana. Kwa hiyo, imebiditufanye kazi kweli ya haraka haraka kuisoma. Sasa nafikiri,tuelezane wazi kwamba tabia hii sio nzuri, hizi taarifa inabidituzipate wote mapema, tupate nafasi ya kuzisoma ili tuwezekuchangia vizuri.

Mheshimiwa Spika, mimi binafsi niliposikiliza palehotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani tangumwanzo mpaka mwisho wa hotuba yake amezungumziahabari ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpaka pale mwishoaliposema na hayo mengine yaliyoko humo basiyachukuliwe, baada ya kitabu kukipata nikaanza kuangalianikasema alaah, kumbe alikuwa na mengine ya kusema.Mimi nilidhani alikuwa na hilo tu moja la Tume ya Katiba.Nataka niseme kwamba wanatunyima na wanawanyimaWatanzania haki ya kujua yale yote yanayosemwa na KambiRasmi ya Upinzani kwa sababu tu ya kuchelewa kutupa hivivitabu.

Mheshimiwa Spika, lakini baada ya kusema hayo,naomba niseme, maelezo yaliyotolewa hasa kuhusu Tumehususan kumtaja binafsi Mheshimiwa Warioba, ninasemakwanza haikuwa haki na maneno yaliyotumiwa yalikuwa ni

Page 152: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

152

3 MEI, 2013

ya kumvunjia heshima na vilevile kwa umri wake MheshimiwaJaji Warioba ukilinganisha na umri wa Mheshimiwa TunduLissu, nataka kusema Mheshimiwa Jaji Warioba anastahiliheshima ya asili kutoka kwa Mheshimiwa Tundu Lissu. Kwakweli nasema Bunge hili lisitumike kudharau watu, kunyanyasawatu, kusema maneno ya kashfa kwa ajili ya watu, tena hasawatu hawa waliotuzidi umri, mimi nafikiri hatutendi haki hatakidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata wenzangu waliokuwawanasema tunaunga hotuba hii mkono, nasema kamawanaunga maudhui, lakini maneno yale ya kashfa sidhanikama hata Wabunge wanawake wanayaunga mkonomaneno yale. Kwa kweli si vyema kuvunjiana heshimatunapotaka kuweka pointi yoyote ili ieleweke. Tunawezatukaeleza maelezo yetu vizuri bila hata kumkashfu mtu nayakaeleweka na yakaingia. Hivi sasa mnawakimbiza watutu ambao pengine walikuwa wanadhani kwamba Chamahiki ni kizuri sana lakini kwa maneno ya namna hiimnawakimbiza tu watu ambao wangependa kujiunganacho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema maneno hayo,ninaomba nijikumbushe kwamba kwa rekodi tuliyonayo,Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria aliwahi kuwa Katibuwa Tume ya Kurekebisha Sheria kwa muda mrefu tu, lakinialipokuwa yeye Katibu mambo mengi waliyopendekezakuletwa Serikalini mpaka sasa hayajatekelezwa. Sasanatarajia kwamba maadam yeye sasa ndio yuko kwenyechungu basi yale yaliyoshindikana wakati yeye akiwa Katibukule kwenye Tume ya Kurekebisha Sheria yaletwe Bungeni.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, hapa nazungumzia hususan Sheriaya Ndoa ya Mwaka 1971. Sheria ya Ndoa imetolewa taarifana nina hakika na Tume ilizunguka sana kupata maoni yawatu na taarifa yao ipo tulikwisha kuisoma. Sheria ya Ndoainaruhusu mtoto wa miaka 15 kuolewa kwa ridhaa ya mzaziama mlezi lakini Sheria ya Mtoto tafsiri ya mtoto ni mtoto wamiaka 18, lakini kwa Sheria ya Ndoa inavunja hata Sheria ya

Page 153: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

153

3 MEI, 2013

Bunge yenyewe iliyoweka tafsiri ya mtoto. Mtoto wa miaka15 anaweza kuolewa eti kwa ruhusa ya mzazi lakini mtotohuyu wa miaka 15 akibakwa ni kesi lakini akibakwa kwaruhusa ya wazazi wake sio kesi. Sheria hii moja inawezajekuruhusu kubakwa halafu hapohapo inaruhusu mtumwingine atoe ridhaa ya mtoto wake kubakwa? Mimi nafikirihuku ni kutokumtendea mtoto wa kike haki, mtoto wa kikewa miaka 15 ni mtoto mdogo sana, hana uwezo kabisa wakufikiri wala kubeba majukumu ya unyumba, iwe kwa ruhusaau bila ruhusa, hii ni kinyume kabisa cha haki ya mtoto. Kwahiyo, namwomba Mheshimiwa Waziri, alilishughulikia hilitunaomba alete hapa Bungeni kurekebisha jambo hili.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kuzungumzia juu yaWabunge wa Viti Maalum. Katiba ya Nchi inaweka aina yaWabunge. Wako Wabunge kutoka kwenye Majimbo, wakoWabunge wa Kuteuliwa na Rais, wako Wabungewaliotokana na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, yukoMwanasheria Mkuu halafu wako Wabunge wa aina ya VitiMaalum. Mle ndani ya Katiba haijasema kwamba Wabungewa Viti hivi watakuwa hivi, isipokuwa sheria ndiozimefafanua. Sheria ya kwanza ya ubaguzi kabisa ambayonina hakika kabisa kwamba Tume ya Kurekebisha Sheriaitaiangalia, ni kule kusema Mbunge yeyote mwingineisipokuwa wa Jimbo tu ndio anaweza kuwa Waziri Mkuu,huu ni ubaguzi kwa sababu tunao akinamama ambao wanauwezo mkubwa tu lakini hawakutoka kwenye Majimbo. Hilola kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ubaguzi wa pili, Wabunge wa VitiMaalum hawapewi zile fedha kwa ajili ya kuendelezaMajimbo kwa maelezo kwamba ile fedha ni kwa ajili yaMajimbo. Sasa kwa nini Katiba ikaweka aina nyingine zaWabunge kama hili jambo lilikuwa hivyo? Ni matumainiyangu kwamba jambo hili sasa litaangaliwa na nina hakikakabisa huko tunakokwenda na hasa kwa kupitia Tume hii,jambo hili litarekebishwa.

Mheshimiwa Spika, ambalo nataka kulisemea ni

Page 154: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

154

3 MEI, 2013

namna ya kumpata Mbunge wa Viti Maalum. Wabunge waMajimbo wanaeleweka wanavyopatikana, Wabunge kutokaBaraza la Wawakilishi wanajulikana jinsi watakavyopatikana,wanaoteuliwa na Rais inajulikana atakavyowateua lakinicha kusikitisha kabisa katika Viti Maalum ni kwambaWabunge wa Viti Maalum ambao ni wanawakehawakuwekewa utaratibu ukiachia ule tu unaosema kilaChama kitapata kutokana na uwiano wa kura walizozipatakwenye Uchaguzi Mkuu, hakuna utaratibu wa namna yakuwapata. Kwa hiyo, kila Chama kimeweka utaratibu wakena mnawafanya sasa hivi wanawake wawe kama ni milikiya vyama vya siasa. Hili halifahi, hakuna mtu anayemmilikimwenzake hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunataka sheria itungwehata kama mnasema mtangoja Katiba, tunataka utaratibuwa kisheria ambao kila chama utaufuata, mtuanayechaguliwa achaguliwe sio kwa mapenzi ya mtu nawala sio kwa matakwa ya mtu au ya chama chake,achaguliwe kwa sababu amechaguliwa hata kama ni kwaViti Maalum. Kwa hiyo, tunapenda kabisa kwamba jambohili lisahihishwe kwa sababu linadhalilisha baadhi ya Wabungewanawake hasa Wabunge vijana wanawake. Kwa hiyo,napenda jambo hili lisahihishwe liwe mwisho kabisa kamatulikosea huko nyuma tulikosea lakini lazima utaratibu wakuwapata Wabunge hawa uwekwe vizuri na iwe utaratibuwa kisheria na ikiwezekana hao akinamama wotewakachaguliwe ili na wenyewe basi mtindo wa kuwabaguakwamba hawawezi kupata hiki na kile, hawezi kuwa WaziriMkuu litakuwa limekwisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini suala la kuwa na hakika yakuwa na akinamama ndani ya Bunge hili, hilo ni lazimalizingatiwe. Piga ua, akinamama ni asilimia 51.1 ya watuwote wa nchi hii. Sasa hivi huko tunakokwenda tunahitajiuwakilishi wa nusu kwa nusu. Tunachohitaji ni utaratibuutakaofanywa ili akinamama hawa waingie katika Bunge.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi ninasema kwa tafrani

Page 155: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

155

3 MEI, 2013

zinazotokea humu Bungeni za maneno na mipasho nakadhalika, kama Wabunge akinamama wasingekuwemohumu ndani ya Bunge, sijui kungekuwaje? Mimi natakakusema Wabunge wanawake ni mhimili wa amani humuBungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wanasemwa wamenyamaza,mara wasemwe hili tunanyamaza, kila jambo linalosemwakuhusu mwanamke humu ndani tungesimama wote,ingekuwa tafrani kubwa sana. Mimi napenda kuwapongezaakinamama, tuendelee na moyo huo, sisi ni mhimili waamani… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu waSerikali atafuatiwa na Mheshimiwa Naibu Waziri…

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mwongozo wa Spika.

SPIKA: Mwongozo wa Spika, Mheshimiwa Zambi.

MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Spika, naombaMwongozo wako kwa kutumia Kanuni ya 68(7) kwenye Kanunizetu za Bunge, sina sababu ya kukisoma kwa sababu kifungukile kinaeleweka vizuri 68(8) kuhusu Mwongozo.

Mheshimiwa Spika, kama alivyorejea kusemaMheshimiwa Anna Abdallah kwamba kulikuwa na sababuza kupata kitabu hiki mapema lakini bahati mbayahatukukipata mapema. Mimi nilivyokipata, nimejaribukusoma lakini ukisoma labda kitabu cha wengineMheshimiwa Spika, cha kwangu hakina ukurasa wa 19, kikowazi, kiko blank hapo kwenye ukurasa wa 19 lakini piaukurasa wa 26 hakuna kitu yaani zimerukwa.

Mheshimiwa Spika, Mwongozo ninaotaka kuomba,

Page 156: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

156

3 MEI, 2013

je, kama kurasa hizo zinazo-miss ziko taarifa ambazozimeandikwa inawezekana sio nzuri sana na zingepaswalabda ziondolewe kama tungekuwa tumeziona, lakini hazipokatika kumbukumbu zetu za Hansard kipi kinachoenda hikiau kile ambacho kimerukwa baadaye wanawezawakasema wanataka kukirudisha kiwe ni kumbukumbu zakudumu za Bunge. Kwa sababu pia ukisoma ukurasa wa 27pale, kuna maneno ambayo yanakuwa kama ya uchochezikiwango fulani, kwenye paragraph ya pili ukurasa 27. Sasanina wasiwasi na hizo kurasa zinazo-miss na ndiyo nasemanaomba Mwongozo wako kitabu hiki kwa kuwa naupungufu huo unaelekeza nini?

Mheshimiwa Spika, naomba Mwongozo.

SPIKA: Sawa. Tutakaa kwenye Kamati ya Kanunikuweza kuweka utaratibu ni wakati gani taarifa zinazopaswakuwekwa hapa Mezani ziwe zimemfikia Spika si wakati waasubuhi ingawa Kanuni ya 99(5) inaelekeza kwamba ziledocuments zinazowekwa Mezani ziwepo kwa Spika.

Kwa hizo kurasa unazosema naona kama labdawachapaji waliruka, ndio sasa zinasambazwa lakini ni kwelikwamba kumekuwa na kuleta taarifa ki-pressure, pressurenamna hii, nadhani hili tutalirekebisha katika siku zijazo.

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. SAID SULEIMAN SAID: Mheshimiwa Spika, hojayangu ni juu ya Hati ya Muungano. Wakati Watanzania tumokatika mchakato wa kuandika Katiba Mpya, bado kuna kiucha kutofahamika ilipo Hati ya Muungano iliyosainiwa naWaasisi Wakuu wa zile zilizokuwa Dola Mbili Huru; yaaniMwalimu Nyerere kwa Dola ya Tanganyika na Mzee Karumekwa dola ya Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, naungana na wale Watanzaniawenzangu waliotangulia kutaka kujua ni wapi ilipo Hati yaMuungano? Kuna wapo waliothubutu kwenda Mahakamanimwaka 2007 kuidai Hati kama ipo basi ioneshwe hadharani.

Page 157: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

157

3 MEI, 2013

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibaralipoitwa Mahakamani alisema hata yeye hajawahi kuionahati hiyo na akawataka walalamikaji washirikiane nayekuitafuta na kujua wapi ilipo Hati hiyo ya Muungano.

Mheshimiwa Spika, wakati huo huo Mheshimiwa AliAmeir Mohamed aliyewahi kuwa Waziri katika Serikali zotembili na Katibu Mwenezi wa CCM Zanzibar, aliwahi kuulizaswali hapa Bungeni akitaka kuelezwa wapi ilipo Hati yaMuungano. Jibu alopata ni kwamba nakala moja ipo Ofisiya Rais, Ikulu Dar es Salaam, lakini mpaka hii leo haijaoneshwahadharani. Sasa swali langu ni kuwa, kama Hati ya Muunganoipo, Serikali zetu zote mbili zinaogopa nini kuionyeshahadharani?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili ni kutokana naSheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, Toleo la mwaka2012, Sehemu ya Nne kuhusu utaratibu wa utendaji kazi waTume, Kifungu namba 17(4), kinachoeleza kuwa katikakutekeleza majukumu yake chini ya sheria hii, Tume itapitiana kuchambua michango, mawazo, maoni, taarifa namapendekezo yaliyokusanywa na kufanyiwa tathmini siku zanyuma ikiwemo kifungu 17(4)(e) Hati za Muungano waJamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, hizi ni baadhi ya hati zilizotajwana sheria hii kama Tume katika kutekeleza majukumu yakeitazitumia katika kutayarisha rasimu ya Katiba Mpya. Hapaswali langu ni je, Tume imeshaiona Hati hiyo auimeshakabidhiwa Hati hiyo ya Muungano? Ikiwa Hati hiyohaipo, uhalali wa Muungano wetu uko wapi? Hii si inaoneshakwamba, uundwaji wa Muungano wetu haukuwa wa Kisheriana hivyo kuwa msingi wake ulikuwa mbaya tokea mapemakabisa ulipoundwa mwaka 1964.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Spika, napendakutumia fursa hii kwa njia ya maandishi kuwapongezaMheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Mathias

Page 158: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

158

3 MEI, 2013

M. Chikawe; Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Katibu Mkuuwa Wizara, Mheshimiwa Jaji Kiongozi, Mheshimiwa Jaji Mkuu,Mtendaji Mkuu wa Mahakama Alhaji Husein Katanga pamojana watendaji wote walioshiriki kuandaa bajeti hii nzuri yenyemikakati mizuri ya kuboresha utoaji wa huduma kwawatendaji ulio bora zaidi. Nawaombea Mungu awatanguliemalengo yatekelezeke vema.

Mheshimiwa Spika, kuhusu uhaba wa Mahakimu waMahakama za Mwanzo Singida, napenda kuikumbushaSerikali pamoja na Mahakama za Mwanzo chache zilizopoMkoani Singida kwani sio Kata zote zina majengo yaMahakama za Mwanzo, bado kuna tatizo kubwa la upungufuwa Mahakimu Mahakama za Mwanzo.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mheshimiwa Chikaweamelieleza Bunge kuwa tayari anao Mahakimu wapya,napenda kujua kwa Mkoa wa Singida tumepewa Mahakimuwangapi ili kusaidia kuondoa mrundikano wa kesi nyingiambazo zinahitaji kusikilizwa. Vile vile kuwapunguzia kaziMahakimu waliopo kwani karibu kila Hakimu ana vituo viwiliau zaidi. Nasubiri majibu ya Serikali ili wananchi wa Singidawalionituma wasikie, pia nisiwasumbue kwenye vifungu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu majengo ya Mahakamaza Wilaya zote za Mkoa wa Singida; inasikitisha sana pamojana juhudi za kuikumbusha hapa Bungeni mara nyingi kuwaMahakama zote za Wilaya za Mkoa wa Singida zinatumiamajengo ya Mahakama za Mwanzo. Napenda kujua niWilaya ngapi za Mkoa wa Singida zimetengewa fedha zakujenga Mahakama za Wilaya tafadhali.

Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingikakuwatengenezea maeneo mazuri ya kufanyia kazi Mahakimuwa Wilaya ni kuwaongezea moyo wa kujituma. Nasubirimajibu ya Mheshimiwa Mathias Chikawe yenye kutia moyokwa Mahakimu wa Mahakama hizi, uongozi wa Mkoa waSingida na wananchi kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, kuhusu ujenzi wa Mahakama Kuu

Page 159: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

159

3 MEI, 2013

Mkoani Singida; napenda kuleta kilio cha wananchi waSingida ambacho hata Mheshimiwa Waziri wa Sheria naKatiba, Mheshimiwa Mathias Chikawe anafahamu vizuri.Naendelea kusikia ujenzi wa Mahakama Kuu mikoa yawenzetu ambayo iliomba baada ya sisi wa Singida, lakiniimeshatupita.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali inieleze kulikonikucheleweshwa Mradi huu kwa kiasi kikubwa. Kosa letu ninini ili tujirekebishe. Nasubiri majibu yenye faraja kutokaSerikalini.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Serikali kutambua juhudiza Mtendaji Mkuu wa Mahakama Husein Katanga;nimeshindwa kujizuia kusema ukweli kuwa kwa muda mfupiNdugu Husein Katanga ameonesha uwezo wa juu wakupanga mikakati ya utekelezaji wa majukumu yake. Tatizonililoligundua ni kwamba, Serikali haijamuunga mkonoipasavyo kwani fedha anazopewa ni ndogo sana.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali kuongeza fedhakatika Bajeti ya Idara hii muhimu sana kwa Watanzania,nitashukuru sana kupata majibu mazuri.

Mheshimiwa Spika, kuhusu nafasi ya Wabunge VitiMaalum; napenda kuishauri Serikali kutoa ushirikiano kwaTume ya Katiba ya Mheshimiwa Jaji Mstaafu Warioba, juu yakuangalia dirisha lenye heshima kwa Wabunge Viti Maalumkuingia Bungeni ili ifike mahali Wabunge Viti Maalum wapateheshima na haki kama Wabunge wa Majimbo. Suala hililichukuliwe kwa uzito wa pekee.

Mheshimiwa Spika, kuhusu posho za wazee waMahakama; pamoja na Serikali kuendelea kutangaza poshoza wazee wa Mahakama, lakini bado kiwango ni kidogosana. Ni vema sasa kiangaliwe kiwango ambacho kitadumumuda mrefu na kiwe kiwango cha kuwafanya wasinunuliweau kushawishika na rushwa ambayo ni adui wa haki.

Mheshimiwa Spika, mwisho, napenda nimalizie kwa

Page 160: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

160

3 MEI, 2013

kuwapongeza Mheshimiwa Mathias Chikawe, Waziri mwenyedhamana na Mheshimiwa Angellah Kariuki, Naibu Waziri kwamshikamano wao mzuri ambao umeongeza ufanisi ndaniya Wizara hii ya Katiba na Sheria. Hivyo, naunga mkonohoja hii Mungu awatangulie.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kuongezewa fedhaWakala wa Vizazi na Vifo (RITA); napenda kutoa niliyonayomoyoni kuhusu kitengo hiki cha vizazi na vifo (RITA) kwambaTaasisi hii inayo Mtendaji Mkuu chapakazi na mwadilifu mnona amejitahidi kutekeleza wajibu wake wakishirikiana nawasaidizi wake, bali bado hajafanikiwa vizuri kwa sababufedha anazotengewa kila Bajeti ni ndogo mno, zinampanafasi finyu ya kwenda mikoani ndiyo maana asilimia ya usajiliwa watoto chini ya miaka mitano bado ni mdogo sana nakuna Mikoa kama Mbeya, Shinyanga, Simiyu, Geita naMwanza bado uko chini sana.

Mheshimiwa Spika, hata Singida bado watoto wengiwanahitaji kusajiliwa. Ningependa kujua Serikali itafanyajitihada za kuwaongezea fedha Wakala wa RITA i l iwasiendelee kukaa ofisini wakati kazi ziko mikoani,tusiwavunje moyo watendaji kama hawa wenye ari ya kazi.Nasubiri majibu ya Serikali yenye afya.

Mheshimiwa Spika, kuhusu sheria ya uandikishaji waVizazi na Vifo kufanyiwa marekebisho; nimeona ni vemakuikumbusha Serikali kuwa Sheria ya Uandikishaji wa Vizazina Vifo imepitwa na wakati. Hivyo, napenda kujua ni liniSerikali italeta Muswada huu hapa Bungeni ili tuweze kuifanyiamarekebisho. Ni vema iwe ni Sheria kuwa kila anayesomaawe na cheti cha kuzaliwa, anayeomba kazi, na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, hii itasaidia kuondoa adha palekijana anapopata nafasi ya kwenda kusoma au kufanya kazinje ya nchi kupata Passport bila shida. Hivyo, sheria ifanyiwemarekebisho kila kijana awe na cheti cha kuzaliwa. Nasubirimaelezo yenye kuonesha uzito wa suala hili.

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, kuhusu

Page 161: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

161

3 MEI, 2013

ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Kawe; kwa miaka mitatumfululizo, Serikali imekuwa ikiahidi mbele ya Bunge lakoTukufu kwamba, itajenga upya Mahakama ya Mwanzokutokana na ile ya awali kuwa gofu hali iliyopelekea mashauriyote kusikil izwa katika Ofisi ya Mtendaji Kata. Haliinayosababisha usumbufu mkubwa! Naomba kupata kauliya mwisho kutoka Serikalini kwa maana ya Wizara ya Katibana Sheria. Ni lini, Mahakama hiyo itajengwa na kwa gharamakiasi gani?

Mheshimiwa Spika, kuhusu mchakato wa Katiba,nitazungumzia mambo mawili:-

Kwanza, idadi ya wananchi waliochangia/toa maoniya Katiba; wakati tukiwa katika mchakato muhimu waKatiba kumekuwa na sintofahamu nyingi juu ya ushiriki wawananchi. Naomba Serikali iliambie Bunge hili Tukufu, mpakasasa tukiwa tunaelekea katika mchakato wa Baraza,ambapo Tume itatoa Rasimu kwanza ya Katiba ili Mabarazayajadili kama ilivyoelekezwa na kifungu 18 (2).

Pili, kuhusu Bunge la Katiba; kwa mujibu ya Sheria yaMabadiliko ya Katiba, sura 83, Toleo la mwaka 2012, kifungunamba 29(1) na (2) gharama za Bunge maalum la Katibazitalipwa kutokea Mfuko Mkuu wa hazina ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, taarifa ambazo zimewasilishwambele ya Bunge lako Tukufu, kupitia Kamati ya Katiba, Sheriana Utawala, ambayo ndio ina jukumu la kupitisha Bajeti yaWizara ya Katiba na Sheria, ambayo pia fungu la Tume yaMabadiliko ya Katiba iko ndani yake, hazioneshi fedha hizoziko wapi na ni kiasi gani ambacho kimetengwa kwa mwakahuu wa fedha.

Mheshimiwa Spika, kuhusu The Law School ofTanzania; kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu sanakutoka kwa wanafunzi wa Taasisi ya Sheria kwa vitendo (TheLaw School of Tanzania) kutokana na kutowepo kwautaratibu unaoeleweka utakaotoa fursa kwa wanafunzi

Page 162: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

162

3 MEI, 2013

waliomaliza Shahada ya kwanza ya Sheria kukopa toka kwaBodi ya Mikopo.

Mheshimiwa Spika, hii inatokana na ukweli kwamba,Sheria iliyounda Bodi ya Mikopo haiwatambui. Utaratibupekee uliopo ni kwa Wizara ya Sheria na Katiba kwa kutumiamafungu yake na kwa vigezo inavyovijua yenyewe kutoaufadhili/msaada/mkopo kwa wanafunzi wa Law School.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hoja hii imejadiliwakwa kipindi kirefu sana, naomba Serikali iliambie Bunge hiliTukufu ni lini Serikali itawasilisha Muswada wa Marekebishoya Sheria ya Bodi ya Mikopo ili kuwezesha uwepo wa mfumoulio wazi na huru kwa wanafunzi wote wenye sifa za kupatamkopo.

Mheshimiwa Spika, mwisho lakini sio mwisho kwaumuhimu, naomba kupata kauli ya Serikali juu ya mchakatouliomalizika hivi karibuni, wa Mabaraza ya Katiba ambaoumelalamikiwa sana na wadau wengi.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Spika,pongezi kwa Mheshimiwa Waziri, Naibu wake na watendajiwote wa Wizara kwa kuandaa Hotuba hii na kuileta hapaBungeni.

Mheshimiwa Spika, Mahakama zote hapa nchinizimekithiri kwa rushwa. Haki za Watanzania wengi maskinizinapotea kwa sababu ya rushwa. Mahakimu wengiwamefanya Mahakama ni deal/kesi za wanyonge ni mtajiwa kupata fedha. Hii ni hatari kubwa sana kwani Mahakamani eneo pekee ambapo mwananchi anategemea kupatahaki yake. Serikali ina mpango gani mahususi kuondoarushwa kwenye chombo hiki muhimu?

Mheshimiwa Spika, kuna ukiukwaji mkubwa wa hakiza binadamu kwenye Ofisi za Serikali kuanzia ngazi za Vijiji,Kata, hadi Wilaya.

Page 163: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

163

3 MEI, 2013

Watendaji wa Vijiji na Kata wametumia nafasi zaokuwakamata wananchi wanaochelewa kutoa michango yamaendeleo na kuwafungia kwenye Ofisi za Vijiji na Kata kwazaidi ya siku tatu (3) hadi siku saba (7), wanachanganywawanawake na wanaume.

Mheshimiwa Spika, mfano halisi Kata ya Sungwa,Tarafa ya Uliyankuru, Wilaya ya Kaliua kila leo wananchiwananyanyaswa. Nimeongea na Mkurugenzi wa Urambo juuya jambo hili, lakini bado tatizo linaendelea. Serikali ielezeBunge ni Sheria gani inaruhusu Ofisi za Vijiji na Kata kutumikakama mahabusu?

Mheshimiwa Spika, mahabusu za Polisi zimekuwazikikiuka taratibu na Sheria na kuweka watu mahabusu bilachakula na mbaya zaidi wanakaa kule siku nne (4) hadi wikimoja. Sheria inasema ndani ya masaa 48 mahabusu afikishweMahakamani. Kituo cha Polisi Usinge, Kaliua; Ulyankuru, Wilayaya Kaliua wanawaweka watu pale wiki nzima hadi siku kumina nne (14 days) halafu wanawaachia bila hata kuwafikishaMahakamani.

Mheshimiwa Spika, kuhusu haki za watoto; Tanzaniatumesaini Mkataba wa Haki za Watoto tarehe 1 Juni, 1990na kuridhia 1991. Pia tumesaini mkataba wa Afrika juu yaHaki za Watoto mwaka 2003. Bado matukio mengi yakukiukwa kwa haki za watoto hapa nchini yanaongezekakila leo. Watoto wanabakwa, wanalawitiwa, wanapigwa,wanachomwa kwa moto katika maeneo mbalimbali ya miiliyao. Hata watoto wa mitaani wameongezeka kutokana nakuongezeka ukatili kwa watoto.

Mheshimiwa Spika, Serikali bado haijaweka utaratibumakini wa kukomesha ukatili kwa watoto. Kesi zinazohusuukatili wa watoto bado zinachelewa sana wakati huuwatuhumiwa wako mitaani wanaoendeleza vitendo vibayakwa jamii.

Mheshimiwa Spika, lipo dawati maalum kwa ajili ya

Page 164: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

164

3 MEI, 2013

watoto, lakini bado halijatoa suluhisho la kudumu kwaniwatendaji wanachukua rushwa na kuficha ukweli.

Mheshimiwa Spika, ni kwa nini Serikali haiweki kitengomaalum cha Mahakama/Mahakama ya dharurakushughulikia kesi zote zinazohusu haki za watoto ili haki zaozipatikane kwa wakati?

Mheshimiwa Spika, Tume ya haki za binaadamuinafanya kazi nzuri sana, lakini hawawezeshwi na Serikali kuwana rasilimali za kutosha kutimiza wajibu wake kwa ufanisi.Serikali ituambie kwenye Bajeti hii ni Ofisi ngapi za Tumezitafunguliwa kwenye Mikoa na Wilaya hapa nchini?

Mheshimiwa Spika, Tume ipatiwe vyombo vya usafiriwaweze kwenda vijijini kusaidia wananchi wanaonyimwahaki zao. Wapatiwe Wanasheria wa kutosha (Manpower)kushughulikia masuala wanayoyaibua kwenye jamii. Tumeipatiwe fedha za kukaa vij i j ini kuchunguza kesiwanazokutana nazo. Suala la uchunguzi linahitaji muda napesa ili haki iweze kupatikana kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, zipo kesi zimekaa Mahakamanimiaka zaidi ya kumi (10). Mashahidi wa kesi hizo wanafariki,watuhumiwa wanafariki bado kesi ipo Mahakamani. Serikaliiweke utaratibu wa dharura wa kuhakikisha kesi zote zilizokaaMahakamani zaidi ya miaka kumi (10 years) zifanywe kwadharura kwa muda maalum, ziishe haki za watu zipatikanekwani wamechoka kusubiri haki zao na wengine wamekatatamaa. Siyo haki ni ukiukwaji wa haki kwa wakati.

MHE. MUSTAPHA B. AKUNAAY: Mheshimiwa Spika, mimini mjumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria, naungana namaoni ya Kamati.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Ofisi na vyumba vyaMahakama; kutokana na kuongezeka kwa idadi ya Majaji,Mahakimu na watumishi wengine Ofisi za Majaji na Mahakimu(Chambers) hazitoshi. Mahakimu wanashirikiana maofisikama makarani. Serikali ikope fedha popote kuongeza

Page 165: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

165

3 MEI, 2013

majengo ya Mahakama. Katika mchango wangu wa 2011/2012 na 2012/2013 nilisema haya, sijui kama Serikali ilipokeaje?

Mheshimiwa Spika, kuhusu Mabaraza ya Ardhi; hakunasababu ya kuwa na Mabaraza haya, Mahakama inatosha.Mabaraza haya yafutwe, iwapo mashauri ya ardhi yenyethamani zaidi ya shilingi milioni 50 yanafanyika MahakamaKuu kwa nini ya chini hapa yasifanyike katika Mahakama zachini?

Mheshimiwa Spika, kuhusu Tele-justice; Mradiutakaoiwezesha Mahakama kuendesha mashauri na kurekodimienendo ya kesi kama ilivyo Hansard ili kuharakisha kumalizamashauri kwa muda mfupi. Kama mradi wa nchi ya Chinaunakuwa mgumu, kitafutwe chanzo nyingine.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mafunzo ya Mawakili; kwauwakili ni fani inayohitaji mafunzo ya vitendo ya kina, naonamafunzo yanayotolewa na Law School hayatoshi kwa ajilihiyo nashauri Ofisi ya AG iwe ndiyo inayotoa mafunzo yavitendo kama ilivyokuwa huko nyuma (in order to avoidcompromising legal professional standards).

Mheshimiwa Spika, kuhusu muda wa kukaaMahakamani; Mahakimu au Majaji kama hawatafanya kaziwasiwaweke watu bure Mahakamani, shauri liahirishwemapema.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, napendakuchangia Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwakawa fedha 2013/2014 kwa kuzungumzia mambo makuumawili; ucheleweshaji wa kesi na upungufu wa wafanyakazikatika ngazi ya Wilaya na Mkoa (Wanasheria – StateAttorneys).

Mheshimiwa Spika, tumekuwa tukishuhudia idadikubwa ya mahabusu hata kwa wale wenye kesi zenyekupewa dhamana, lakini wanapelekwa gerezani, hivyo,kupelekea mrundikano wa Mahabusu gerezani, mfano

Page 166: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

166

3 MEI, 2013

gereza la Wilaya ya Tarime ambalo hupokea watu tokaWilaya mbili Tarime na Rorya.

Mheshimiwa Spika, gereza hil i la Tarime linamrundikano mkubwa wa Mahabusu ambao wengi wao niwenye kesi zenye dhamana lakini wananyimwa kwa sababuza upungufu wa maadili kwa watendaji wa Mahakama. Vilevile kumekuwepo na ucheleweshaji mkubwa wa kesi na hatazile zisizo na ushahidi. Ikizingatiwa nature ya kesi wapewazowananchi wa Tarime/Rorya ambapo kwa kiasi kikubwa niubambikaji wa kesi unaofanywa na Jeshi la Polisi kwa maslahibinafsi na sio ya umma.

Mheshimiwa Spika, kuna kesi mtu/watuwamekamatwa kwa kosa la jinai, lakini ghafla unaombwafedha (rushwa). Mara wakosapo hubadilishiwa kesi na kuwaArmed Robbery /murder kitu ambacho si haki na ni kinyumena Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambapo inatuambiakila raia ana haki ya kuishi na kutenda kazi ndani ya nchi.

Mheshimiwa Spika, hivyo ni wakati muafaka sasaWizara ikemee kitendo hiki/hivi na kuhakikisha kesi zote zenyekutoa/pewa dhamana zipewe. Zile ambazo hazina basiupelelezi ufanyike haraka, maana kesi nyingi Tarime/Rorya niza kisiasa ambapo watu hubambikwa kesi.

Mheshimiwa Spika, sehemu nyingine ambayohupelekea kesi kuchelewesha ni kuchelewa kwa upelelezipamoja na upungufu wa wafanyakazi wenye kutoa haki zakisheria (Mahakimu na Mawakili) ni wachache sana ambaohawakidhi mahitaji na hivyo kupelekea ucheleweshaji wakesi. Vile vile kuna upungufu wa majengo (Mahakama zaMwanzo), Mahakama Kuu, Ofisi ni duni/chakavu ambazohazina hata vifaa vya kisasa.

Mheshimiwa Spika, mwisho, naomba uwezekano wakujengwa Mahakama katika Wilaya ya Rorya pamoja nagereza ili kuweza kupunguza mrundikano wa mahabusu/wafungwa katika gereza la Tarime kitu ambacho kinawezakupelekea maambukizo ya magonjwa mbalimbali.

Page 167: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

167

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa Spika,nichangie kuhusu suala la upatikanaji wa Katiba mpyaTanzania. Katiba ni suala la Watanzania wote, Katiba siosuala la Vyama vya Siasa Katiba. Suala la upatikanaji waKatiba mpya bado halijakaa sawa. Kuna malalamiko kwamakundi yaliyo pembezoni kwa mfano, walemavu,wanawake na hata Watanzania wasiojua kusoma nakuandika bado hawajaelimishwa kuhusu Katiba mpya. Nikwa nini Serikali isiongeze muda wa kutosha ili tupate Katibailiyokuwa bora na ambayo imewashirikisha Watanzaniawote?

Mheshimiwa Spika, suala la Mahakama na kerombalimbali zinazozikabili Mahakama zetu. Mahakimu wengiwanafanya kazi katika mazingira magumu, majengo mengiya Mahakama ni chakavu, pia kuna mrundikano wa kesi zamuda mrefu ambazo zinasababishwa na Bajeti ndogo yaWizara hii. Ni lini Serikali itahahakikisha Wizara hii ya Katibana Sheria inatengewa fedha za kutosha ili kukarabatimajengo ya Mahakama kama za Mwanzo na Mahakamaza Wilaya, na kadhalika na kununua vifaa vya kisasa?

Mheshimiwa Spika, baadhi ya Watanzania ambaowanafikisha kesi zao Mahakamani hasa walio pembezoniaidha, wameshtaki au wameshtakiwa baadhi yao hawajuiSheria, vile vile hawana uwezo wa kuweka mawakili. Wengiwamekuwa wakidhulumiwa haki zao kwa sababu hawajuiSheria.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hukumu zote za kesizinazotetewa na Mahakama zinatolewa kwa Lugha yaKiingereza na baadhi ya Watanzania hawajui Kiingereza. Nilini Serikali itahakikisha hukumu zote zinazotolewa naMahakama zinatolewa kwa lugha ya Kiswahili?

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Mawakili waSerikali; baadhi ya Mawakili wa Serikali wamekuwa wakifanyakazi katika mazingira magumu. Vile vile hata kuhatarisha

Page 168: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

168

3 MEI, 2013

maisha yao wamekuwa wakiendesha (kusikiliza) kesi zamauaji na kadhalika, lakini cha kushangaza Mawakili hawawa Serikali wanapomaliza kesi Mahakamani, wanatumiausafiri wa daladala kwa sababu hawana usafiri wao binafsi.Ni lini Serikali itaboresha maslahi ya Mawakili hawa wa Serikalikwa mfano, vitendea kazi, makazi bora ya kuishi (kisasa) nakadhalika?

MHE. ALI KHAMIS SEIF: Mheshimiwa Spika, Dolaimejengeka kwa mihimili mitatu (3) ambapo ni Bunge, Serikalina Mahakama.

Mheshimiwa Spika, Bunge kazi yake moja ya Kikatibani kutunga Sheria na Serikali wajibu wake ni kuzitekelezaSheria hizo. Kutunga Sheria ni suala moja na utekelezaji wakewa Sheria hilo ni jambo lingine.

Mheshimiwa Spika, haifanani hata kidogo Serikalikutozitekeleza baadhi ya Sheria wakati Miswada ya Sheriahizo inatoka Serikalini.

Mheshimiwa Spika, Bunge la tisa (9) kwenye Mkutanowake wa April i mwaka 2013 il itunga Sheria mbilizinazohusiana na Sekta ya Mifugo. Sheria hizo ni Sheria namba12 ya mwaka 10 inayoitwa Sheria ya Utambuzi, Usajili naUfuatiliaji ya mwaka 2010 (Time Live Stock IdentificationRegistration and Traceability Act 2010) na Sheria ya pili ni Sheriaya Maeneo ya Malisho na Rasilimali za Vyakula na MifugoNamba 13 ya mwaka 2010 (The Grazing Land and AnimalFeed Resources).

Mheshimiwa Spika, Sheria mbili hizo ni muhimu mnokwa ufugaji bora na uhifadhi wa mazingira yetu. Bahatimbaya mpaka leo karibu miaka mitatu (3) Sheria hizohazijatekelezwa. Namwomba Mheshimiwa Waziriatakapofanya majumuisho anieleze kwa nini Sheria hizohazijatekelezwa.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa kuna mrundikano

Page 169: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

169

3 MEI, 2013

mkubwa wa mashauri katika Mahakama zetu katika darajambalimbali.

Mheshimiwa Spika, Mahakama Kuu ya Divisheni yaArdhi ilichukua mashauri ya zamani na ya sasa, jumla 5393ambayo kwa kasi ya sasa ni mashauri 427 ndio yaliyotatuliwa.Kwa kasi hiyo mashauri 5393 yatachukua miaka sita (6) namiezi mitatu (3). Hali hiyo inatisha! Ipo haja hatua maalumzichukuliwe ili kuongeza kasi ya kuyatatua mashauri yaliyokoMahakamani.

Mheshimiwa Spika, mashauri yaliyoko Mahakamani,Mahakama za Hakimu Mkazi hivi sasa ni 25,370 na uwezo nimashauri 612 kwa miezi sita. Ili kuyamaliza mashauri 25,370itakuwa muda wa miaka 20 na miezi saba (7) bila yakuongezeka mashauri mengine.

Mheshimiwa Spika, ipo haja Serikali iziwezesheMahakama ili mashauri yaliyoko Mahakamani yaweze kupataufumbuzi wa haraka.

Mheshimiwa Spika, nashukuru.

MHE. DESDERIUS JOHN MIPATA: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja. Elimu juu ya Katiba ya Nchi ni muhimu,Wananchi wengi hawana uelewa wa kutosha juu ya Katibaya Nchi yao ambayo ni Sheria Mama na muhimu kwa kilaraia kuwa na uelewa wa kutosha. Nashauri pamoja nakuwepo kwenye masomo kama topic au mada mojawapo,tutenge fedha za kutosha kuhakikisha kunakuwepo makalaza mara kwa mara za rejea ama kila wiki au kila mwezi.Vilevile Katiba iwe inapatikana hivi sasa, Katiba ilikuwabidhaa adimu hadi pale tulipoanza kuandika Katiba mpya.

Mheshimiwa Spika, zimetungwa Sheria ili sote tuzifuatelakini Sheria ya Rushwa inavunjwa kwa kiwango kikubwa nawasimamizi wa Sheria Mahakamani na Polisi. Ni vizurikumaliza dosari hii. Lazima vyombo hivyo viwe na utaratibuwa kuheshimu Sheria wanazosimamia ama Wizarazinazohusika wahakikishe stadi au research zinafanyika kujua

Page 170: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

170

3 MEI, 2013

sababu ili kumaliza dosari hii. Wilaya ya Nkasi hatunaMahakama ya Wilaya kwa maana ya Jengo na Hakimu pia.

Mheshimiwa Spika, zoezi la Katiba linaenda vizuri namadai ya Wabunge hasa wa CHADEMA ni kuogopa kivulichao tu, hapajakuwa na dosari kubwa.

Mheshimiwa Spika, nashauri Wajumbe wa Tumewasipangwe kwenda kufanya kazi maeneo wanayotokea,wapangwe sehemu nyingine ili kuleta ufanisi.

MHE. UMMY ALLY MWALIMU: Mheshimiwa Spika, awaliya yote, naunga mkono hoja. Pili, nampongeza MheshimiwaWaziri, Naibu Waziri, kwa kusimamia vyema utekelezaji wamipango na malengo ya nchi katika utoaji haki, kusimamiaUtawala wa Katiba na Sheria Nchini. Hata hivyo, ningependakupata maelezo katika masuala yafuatayo:-

Je, ni lini tafrisi ya Kiswahili ya Sheria ya Mtoto Namba21 ya 2009 itakamilika?

Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilipitisha Sheriaya Mtoto mwaka 2009 kwa lengo la kulinda na kukuza hakiza mtoto Nchini kwetu. Hata hivyo, bado jamii haina uelewawa Sheria hii kutokana na sababu mbalimbali ikiwemouelewa mdogo wa Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyoimetumika kutengeneza Sheria hii. Hivyo, ninaombaMheshimiwa Waziri anipatie majibu ni lini Sheria hii itatafsiriwakutoka Kiingereza kwenda Kiswahili ili iweze kueleweka vizurina Wananchi hasa walio vijijini.

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Ndoa, Mirathi na Sherianyingine Kandamizaji Dhidi ya Wanawake; ni lini mchakatowa kuzifanyia marekebisho utakamilika?

Mheshimiwa Spika, Ilani ya Uchaguzi ya Chama chaMapinduzi (CCM), aya ya 186(f), inaelekeza Serikali kuzifanyiamarekebisho Sheria za Mirathi na zile zinazooenekanakuwakandamiza Wananchi wake.

Page 171: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

171

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, ni ukweli usipopingika kuwauwepo wa Sheria za Mirathi (za kimila) na Sheria ya Ndoa yamwaka 1971, bado wanawake wengi wanakabiliwa nachangamoto mbalimbali ikiwemo haki ya kurithi mali, tokakwa wazazi au waume pale wanapofariki. Sheria ya Ndoainayoruhusu mtoto wa kike wa umri wa chini ya miaka 18kuolewa inadidimiza jitihada za nchi katika kumpatia elimumtoto wa kike, kupunguza vifo vya wanawake wajawazitona pia jitihada za kumkomboa mwanamke kiuchumi. Hivyo,hakuna ubishi kuwa Wanawake wa Tanzania wangependasasa kupata kauli ya mwisho ya Wizara ni lini Sheria za Mirathi,Sheria za Kimila na Sheria ya Ndoa zitaletwa Bungeni ili ziwezekufanyiwa marekebisho na hivyo kuwezesha kulinda nakukuza haki za wanawake na wasichana nchini?

Je, ni kiasi gani cha fedha kimetengewa kwa mwaka2013/2014 kwa ajili ya mpango wa kusajili watoto chini yaumri wa miaka mitano? Kwa mujibu wa TDHS - TanzaniaDemographic and House Hold Survery ya mwaka 2010,inaonyesha kuwa ni asilimia 16 tu ya watoto wa umri wamiaka mitano waliosajiliwa na Mamlaka husika na kati yahao ni asilimia nane tu waliopata vyeti vya kuzaliwa.

Mheshimiwa Spika, hali hii hairidhishi kabisa, ni lazimatuongeze jitihada katika suala hili. Hivyo, ninaomba Wizarailieleze Bunge lako Tukufu ni kiasi gani kimetengwa kwa ajiliya kutekeleza Mpango wa Kusajili Watoto Chini ya Umri waMiaka Mitano kwa Mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. HAWA ABDULRAHMAN GHASIA: MheshimiwaSpika, naunga mkono hoja. Pia napenda kuipongeza Wizarakwa kuanzia na Waziri pamoja na Viongozi wote ambaowanaunda Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, majengo ya Mahakama KuuKanda ya Mtwara hayaridhishi; kwanza, eneo yalipo siyomazingira mazuri kufanyia kazi hata kidogo na majengoyenyewe yana nafasi finyu tena yapo kajificheni. Ningependa

Page 172: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

172

3 MEI, 2013

kufahamu kama kuna mkakati wowote wa kujenga majengomapya ya kisasa na kwenye mazingira wezeshi kwa shughulimuhimu kama za Mahakama kutoa haki.

Mheshimiwa Spika, kwa kawaida ni vizuri mfanyakaziyeyote kupongezwa pale anapofanya vizuri ili kumtia moyowa kuendelea kufanya vizuri na hivyo kuongeza ufanisi.

Mheshimiwa Spika, ni utaratibu kwa Watumishi waVyombo vya Ulinzi na Usalama kupewa Tuzo na Nishani kamaishara ya kuthaminiwa mchango wao kwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, sijawahi kuona hata siku mojaWatumishi wa Mahakama wakipongezwa kupitia Siku yaWafanyakazi Duniani au eneo lolote au katika mazingira yashughuli zozote. Ndiyo kusema Watumishi wa Mahakamahawana haki ya kupongezwa wanapofanya vizuri?

Kutokana na utaratibu huu wa kutotambuawanaofanya vizuri hamwoni kwamba unawakatisha tamaawafanyao vizuri na hivyo kupunguza ufanisi wa Mhimili huumuhimu kwa kutoa haki?

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwarani kubwa kuliko zote Mkoani Mtwara, lakini Halmashauri hiiina Mahakama za Mwanzo zisizozidi au chini ya tatuzinazofanya kazi. Je, lini Mahakama za Mwanzo zitajengwaHalmashauri ya Wilaya ya Mtwara ili kuwapunguzia Wananchiadha ya kwenda umbali mrefu kutafuta haki?

Mheshimiwa Spika, naunga mkono haja.

MHE. HAMOUD ABUU JUMAA: Mheshimiwa Spika,nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kunipa nafasihii, nami niweze kutoa mchango wangu katika Bajeti yaWizara ya Kabiba na Sheria ya mwaka 2013/2014. Napendapia kuchukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri, kwaBajeti yake nzuri, iliyoandaliwa kwa umakini mkubwa ilikukidhi mahitaji na kukabiliana na changamoto katika Sektahii.

Page 173: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

173

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, sote tunajua Taifa letu kwa sasatupo kwenye mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya,itakayokidhi matarajio ya wengi kwani mchakato huuumekabidhiwa kwa Wananchi ili watoe maoni yao kipikiwepo kwenye Katiba mpya. Kwa hali hiyo, napendakuipongeza Serikali kwa jitihada zake katika kusimamiamchakato mzima na kufikia hatua kubwa katika mchakatohuu. Pia naipongeza Serikali kwa jitihada kubwa za kuongezaMajaji katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani.Kufanya hivyo, kunaongeza ufanisi katika utendaji washughuli za Mahakama ngazi ya Mahakama Kuu na Rufani.

Mheshimiwa Spika, hali ya uendeleshaji wa mashaurimengi hapa nchini inasikitisha sana, kwani kesi nyingizimekuwa zikichelewa kusikilizwa na hivyo kuchukua mudamrefu kutolewa hukumu. Kwa namna hiyo, huwanyima hakipande zote mbili zinazohusika. Hali hii ni hatari sana kwamustakabali wa utoaji haki nchini kwani ikumbukwekwamba, haki inayocheleweshwa ni sawa na hakiiliyonyimwa (Justice Delayed is Justice Denied). NaishauriSerikali iongeze idadi ya Watumishi hasa Mahakimu naMawakili wa Serikali wa Kada mbalimbali ili kuongeza kasiya uendeshaji wa mashauri mbalimbali nchini kwa lengo lakulipatia ufumbuzi suala la mlundikano wa mashauriMahakamani l inalosababisha pia msongamano wawafungwa na mahabusu Magerezani.

Mheshimiwa Spika, bado kumekuwa na changamotokubwa kwa waajiriwa wapya waliopangiwa kutoa hudumakatika Mahakama za Mwanzo Nchini. Mageuzi hayo katikamfumo wa Mahakama yana changamoto zake kwani vijanahao wasomi walioajiriwa itabidi wakakae na kufanya kazikwenye maeneo ya vijijini ambako katika mazingira yakawaida, imekuwa ni vigumu kwa vijana wengi kuyaafiki.Nashauri Serikali iboreshe miundombinu ya Mahakama zaMwanzo, ikiwa ni pamoja na utoaji wa motisha kwaMahakimu hawa wapya ili waweze kutekeleza majukumuyao katika mazingira rafiki.

Mheshimiwa Spika, suala la Serikali kuingia mikataba

Page 174: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

174

3 MEI, 2013

mibovu na makampuni mbalimbali hasa ya kigeni, ni jambolinalosumbua Jamii ya Watanzania. Hali hii inatafsiriwa kuwaOfisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambayo imepewadhamana kuishauri Serikali kabla ya kuingia mikataba hiyokuwa, haipo makini ama inajihusisha na rushwa au watumishiwake hawana utaalam wa kutosha kuhusiana na Mikatabahii ya kigeni. Naishauri Serikali ilichukulie eneo hili kwaumuhimu wa kipekee, kwani lina athari hata kwenye uchumiwa nchi yetu. Aidha, Serikali izidi kutoa mafunzo ya kutoshakwa Mawakili waliopo ili kupunguza gharama kubwazinazotumika kulipia makampuni binafsi hasa katika maeneomapya ya makosa ya kutakatisha fedha (Money Laundry, AssetForfeiture and Recovery and Trans National Crimes).

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, bado kumekuwa nachangamoto katika Mahakama zetu. Jambo hilo hutokanana kuwa na watumishi wasiokuwa waadilifu katika utendajikazi wa kila siku. Hali hiyo imekuwa ikiwapa usumbufuWananchi kwa kiwango kikubwa sana na hufikia mahali hatakupoteza haki zao za msingi. Vilevile ni ukweli usiopingikakwamba, kumekuwa bado na manun’guniko upande waWananchi kwamba, kuna kasoro za uandishi wa kesi namashauri Mahakamani pamoja na utoaji wa hukumu zenyeutata mkubwa.

Tuhuma hizi japo hazina ushahidi wa moja kwa moja,bado haziwezi kubezwa na hivyo, napenda kuishauri Serikalihususan upande wa Mahakama, kutoa mafunzo ya marakwa mara hasa kwa Majaji au Mahakimu wapya kuhusunamna bora ya uendeshaji wa mashauri katika ngazi yaMahakama ili kudumisha imani kwa chombo hiki muhimukatika utoaji wa haki. Aidha, napenda kusisitiza kwamba,Serikali izidishe kasi ya ujenzi wa majengo ya Mahakama Kuuili kufikia lengo la kuwa na Mahakama Kuu kwa kila Mkoakuliko ilivyo kwa hivi sasa ambapo Mahakama Kuu yaTanzania ina Kanda 13 tu ambazo hazikidhi mahitaji yaWananchi. Hali hiyo huleta usumbufu na gharama kwaWananchi pindi wanapohitajika katika Mahakama hizokwani hutakiwa kusafiri kutoka mahali walipo.

Page 175: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

175

3 MEI, 2013

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, nashukurukupata nafasi ya kuchangia Hotuba hii. Naomba niseme wazikwamba, Serikali haijaitendea haki Wizara hii. Pesa ya Bajetiiliyotengwa ni ndogo ukilinganisha na changamoto nyingizinazoikabili Wizara.

Mheshimiwa Spika, mchango wangu utaanzakujielekeza katika upungufu mkubwa wa waendeshamashtaka nchini ukilinganisha na idadi ya Majaji na Mahakimuwaliopo ili kuleta ufanisi katika kuendesha. Jaji mmoja nilazima ahudumiwe na Mawakili wawili, vivyo hivyo kwaMahakimu ni vyema kuwe na uwiano katika kuajiri Mahakimuna Mawakili wa Serikali. Pale ambapo Mahakama inapewakibali cha kuajiri, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ipewekibali cha kuajiri Mawakili wawili.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa idadi ya wanafunziwanaohitimu Shahada ya Sheria imeongezeka, ni vyemaSerikali ikawa na dhamira ya dhati ya kuongeza ajira zaMawakili wa Serikali na Mahakimu.

Mheshimiwa Spika, pia naomba nitumie fursa hiikuishauri Serikali kuwa pale ambapo Serikali haitoi kibali chaajira ya Mawakili wa Serikali, ni vyema Ibara ya 59(b)(3) yaKatiba na kifungu cha 22 cha Sheria ya Usimamizi waMashtaka, vinavyomruhusu DPP kuteua WaendeshaMashtaka vikatumika ipasavyo. Ni vyema DPP atengewe pesaza kutosha kuwalipa waendesha mashtaka watakaowateua.Utaratibu huu utatuwezesha kuondokana na pengo laWaendesha Mashtaka linaloikabili Nchi hii kuimarisha mfumowa kutenganisha mashtaka na upelelezi.

Mheshimiwa Spika, ninamwomba Mheshimiwa Waziriatakapokuwa anafanya majumuisho, atuelezewamejipanga vipi kuongeza Waendesha Mashtaka nakuwapeleka katika Mahakama za Wilaya na Mwanzo ilikuendana na mfumo mpya wa ajira wa Mahakama ambaosasa inaajiri na kupeleka Mahakimu Wahitimu wa Shahadaya Sheria kuanzia ngazi ya Mahakama za Mwanzo.

Page 176: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

176

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Iringa una Wilaya tatuza Iringa, Mufindi na Iringa na Mkoa wa Njombe una Wilayanne za Makete, Ludewa na Wanging’ombe. Wilaya hizi zotesaba bado ziko chini ya Mahakama ya Mkoa wa Iringa kwakuwa bado Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombehaijaanzishwa Kisheria. Mpaka leo hii Wilaya ya Kilolo hakunaMahakama ya Mwanzo. Wananchi wa Kilolo wanapatahuduma hiyo kutoka Mahakama ya Wilaya ya Iringa. Hii yoteni kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu yakimahakama katika Wilaya hiyo.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Iringa, Mahakama yaMwanzo Mlolo, inatembelewa na Hakimu kutoka Mahakamanyingine ya Mwanzo. Pia Wilaya ya Kilolo, Mahakama yaMwanzo ya Mahenge inatembelewa na Hakimu kutokaMahakama nyingine.

Mheshimiwa Spika, ningeomba Mheshimiwa Waziriatakapojumuisha anieleze ni lini Mahakama hizo za Mwanzoza Mlolo na Mahenge na Wilaya ya Kilolo zitaongezewaMahakimu kwani hivi sasa wapo wachache sana nakusababisha mlundikano wa kesi.

Mheshimiwa Spika, pia Mahakama zetu nyingimajengo yake ni chakavu, hakuna vifaa vya kutosha, kamamashine ya chapa, computer na hakuna umeme. Uangaliweuwezekano wa kuweka solar.

Mheshimiwa Spika, pia Serikali iangalie uwezekanowa kuboresha mishahara na maslahi ya Majaji na Mahakimukwa kuwa ipo chini sana ukilinganisha na uzito wa majukumuyao.

Mheshimiwa Spika, pia naomba nichangie kuhusuposho za Wazee wa Baraza. Serikali ifikirie mpango wakuwaongezea posho na kuwaboreshea baadhi ya huduma.Wapatiwe ofisi wakati wanasubiri kesi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

Page 177: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

177

3 MEI, 2013

MHE. RAYA IBRAHIM KHAMIS: Mheshimiwa Spika,gharama za kukata shauri Mahakamani bado ni kubwa kiasiambacho si Wananchi wote wanaoweza kuzimudu na hivyo,hupelekea baadhi yao kukosa haki zao kwa kutokuwa napesa za kutosha katika kukata shauri. Vilevile mashaurihuchukua muda mrefu sana Mahakamani kwa kuchelewakusikilizwa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na jitihada zilizofanywana Wizara hii, bado speed ya uendeshaji wa mashauri katikaMahakama takriban zote ni ndogo sana na kupelekea zaidiya miaka miwili kwa kusikilizwa shauri. Muda mrefu katikakesi za mashauri Mahakamani hupelekea Wananchi kukosaimani na Mahakama zao na vilevile Wananchi hukosa hakizao kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, katika suala hili, maoni yangunaitaka Serikali kupunguza gharama za kukata shauri.

Mheshimiwa Spika, pia au Serikali kwa ujumla iwekemuda maalumu (time limitation) ya kusikiliza mashauri. Kwamfano, kesi za mashauri zisizidi miaka miwili Mahakamanikabla ya kutolewa hukumu.

Mheshimiwa Spika, suala la rushwa bado ni tatizokatika Mahakama zetu kwani imefikia wakati hadi kuitishafaili kwa karani jibu ni kwamba halionekani, lakini ukijulikanaau ukitoa pesa faili lako hupatikana. Hivyo basi, suala hilinalo huwanyima haki zao wasio na pesa na vilevilehupelekea kesi kuchukua muda mrefu. Mfano, kupata Orderya Mahakama pia issue; kupata judgement pia si chini yamiezi sita; na delay yote hii ni kwa kuwa wanataka pesa(rushwa).

Mheshimiwa Spika, Wizara iliangalie hili kunusuru hakiza watu wasio na pesa. Iboreshe mazingira ya kazi kwawafanyakazi na wala rushwa wawajibishwe ili wengine naowasiendelee.

Mheshimiwa Spika, bado hatuna Mahakimu wa

Page 178: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

178

3 MEI, 2013

kutosha katika Mahakama zetu, hali ya kuwa mtaani wapopia wenye sifa lakini hawana ajira; hivyo, ni vyema kuajiriMahakimu wa kutosha katika Mahakama zetu. Kwa mfano,Hakimu wa kutoka Bagamoyo ndiye huyo huyo anasubiriwana Mahakama ya Wilaya ya Chalinze. Ninashauri kuongezaMahakimu katika Mahakama za Wilaya kutapelekeaaccessibility to Justice.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwa Mkurugenzi waTAKUKURU atakuwa appointed na Mheshimiwa Rais, basi nivyema apitishwe na Bunge, yaani awe confirmed auapproved ndani ya Bunge kama njia inayotumika kuwapataau katika mchakato wa Mawaziri wa Kenya. Baada yakuteuliwa, Bunge nalo huwapitisha.

Mheshimiwa Spika, bado Wananchi wetu wengihawazijui Sheria na taratibu za kufungua kesi na jinsi yakumpata Wakili wa Serikali kwa wale wasiokuwa na uwezowa kuwalipa Mawakili.

Mheshimiwa Spika, nashauri Wizara iwe na utaratibumaalumu wa kuwaelewesha ambao watahitaji msaada waMawakili hali ya kuwa hawana uwezo wa kuwalipa.

MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Spika,bajeti haikidhi haja kwa kiwango kikubwa mno.

Mheshimiwa Spika, nitalipeleka jambo hili katikamjadala wa Bajeti ya Serikali itakapowasilishwa siku chachezijazo.

Mheshimiwa Spika, kutokana na changamoto zilizopokatika Wizara hasa juu ya usimamiaji wa haki na Sheria,tengeo la jumla ya shilingi bilioni 18.4 kwa miradi na matumiziya kawaida halitoshi hata kidogo.

Mheshimiwa Spika, mahitaji ya miundombinu ikiwemomajengo ya Mahakama na nyumba za Watumishi hayawezitena kufumbiwa macho kwani hadhi ya Mahakamainaendelea kupungua.

Page 179: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

179

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, vitendea kazi kama vyombo vyausafiri, samani na kadhalika, vina upungufu mkubwaunaochangia utendaji hafifu wa Mahakama nchini kwakiwango kikubwa.

Mheshimiwa Spika, uhaba wa watumishi,unaochangiwa na changamoto nyingine kama nilivyoainishahapo juu, nalo ni tatizo kubwa linalosababisha Mahakamanyingi kuelemewa na hivyo Magereza nyingi kuwa namsongamano wa watuhumiwa huku baadhi yao wakiwana makosa madogomadogo kama wizi wa mahindimabichi kadhaa na kadhalika. Kesi nyingi huchukua mudamrefu kabla ya hukumu (zikiwemo zile zinazohusu makosaya kawaida sana).

Mheshimiwa Spika, nashauri Serikali ione haja yakuongeza tengeo katika bajeti yake kwa ajili ya Wizara yaKatiba na Sheria.

Mheshimiwa Spika, ipo haja ya kuona namna boraya kuhusisha jamii katika kutatua kesi zinazotokana namakosa madogo na ya kati; kwa mfano, matumizi ya safuza uongozi wa kimila pale ambapo bado zina nguvu(chiefdom), uongozi wa kidini na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, vilevile utaratibu wa kitaalamujulikanao kama Alternative Dispute Resolutions (ADR), utiliwemkazo. Kiundwe chombo mahususi cha ku-compilechangamoto zote za Idara ya Mahakama na kutoamapendekezo ya ufumbuzi wake.

Mheshimiwa Spika, nina maombi maalum kwa ajiliya Tunduru. Kwanza, naomba gari la Mahakama. Jiografiaya Tunduru iwe kichocheo cha kuipa Tunduru kipaumbele;tunaomba sana.

Pili, naomba ajira za Mahakamu na Watumishi waMahakama; Tunduru is a disadvantaged district due toremoteness, poor accessibility et cetera. Tunaomba specialconsideration.

Page 180: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

180

3 MEI, 2013

Tatu, naomba tengeo la fedha kwa ajili ya majengohasa Mahakama ya Wilaya.

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Spika, katikamwaka 2011/2012, Serikali ilitenga zaidi ya shilingi milioni 400kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Machame.Ramani na eneo la ujenzi vyote vilikuwa tayari, lakini katikamazingira ya kutatanisha, Mahakama hii haikujengwaMachame, bali ilihamishiwa katika Mji wa Bomang‘ombe (HaiMjini).

Mheshimiwa Spika, eneo palipokusudiwa kujengwaMahakama hiyo ni eneo ambalo kihistoria na kimila, palikuwandipo penye Baraza la Kichifu lililosimamia masuala yote yautoaji haki katika Tarafa za Machame na Lyamungo. Jengolililopo limechakaa sana na ni hatari kutumika.

Mheshimiwa Spika, maadam awali palionekanaumuhimu wa kujenga Mahakama hii Machame, badoumuhimu huo upo na sana sana umeongezeka. Eneolinalotegemea Mahakama hii ni zaidi ya vijiji 25, kata sita naidadi ya wakazi zaidi ya 150,000.

Mheshimiwa Spika, ningependa kujua vilevile Statusya Project iliyohamishiwa Mji Mdogo wa Bomang‘ombeimefikia wapi na itakamilika vipi.

Mheshimiwa Spika, ninaomba sana Serikali ioneumuhimu wa kuirejesha Mahakama ya Mwanzo Machamekatika bajeti ya mwaka 2013/2014.

MHE. SABREENA H. SUNGURA: Mheshimiwa Spika,kwanza kabisa, napenda kuchukua fursa hii kuiomba Serikaliijaribu kuiangalia kwa umakini Tume ya Haki za Binadamuna Utawala Bora, kwa sababu chombo hiki ni chombo chaKikatiba, lakini bajeti yake haitoshelezi kabisa kusimamiamajukumu yake. Lakini cha ajabu, Serikali imekuwa haifanyiikazi mapendekezo ya Tume ya Haki za Binadamu na UtawalaBora. Mfano mzuri ni mapendekezo ya kesi ya DaudiMwangosi kuhusu kulipwa fidia kwa mkewe na kuwasomesha

Page 181: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

181

3 MEI, 2013

watoto wa Marehemu, lakini hakuna lililozingatiwa. SasaSerikali itueleze: Kwanini haizingatii ushauri wa chombokilichoundwa kikatiba?

Mheshimiwa Spika, nashauri utaratibu wa upatikanajiwa Majaji uwe wa kupigiwa kura, yaani nafasi ya Jaji Mkuuipatikane kwa kushindanishwa.

MHE. AMINA NASSORO MAKILAGI: Mheshimiwa Spika,pamoja na pongezi kwa Wizara, naomba kushauriyafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, sheria zinazowakandamizawanawake kama vile Sheria ya Ndoa, Mirathi na Sheria yaArdhi nilijua zitawasilishwa Bungeni ili ziweze kufanyiwamarekebisho ili tatizo la kuolewa watoto wadogo walio chiniya miaka 18, Mirathi, wanawake kumiliki ardhi, yapatiweufumbuzi.

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni, kumejitokeza tabiaya wananchi kuchukua sheria mkononi na kuchoma motonyumba za baadhi ya viongozi hasa wanawake, majengoya Serikali na Ofisi za Chama.

Mheshimiwa Spika, napenda kujua, ni hatua ganizilizochukuliwa kwa wale wote waliohusika ili kutoa fundishokwa wengine?

Mheshimiwa Spika, vile vile hivi karibuni kumejitokezavitendo vya mauaji ya wanawake Mkoa wa Mara Wilaya yaButiama na mauaji ya vikongwe Mkoa wa Geita.

Pia ningependa kujua ni hatua gani zimechukuliwaili kudhibiti vitendo hivyo na kuchukua hatua kali kwa walewote waliohusika na mauaji hayo ili kutoa fundisho kwawengine?

Je, ni hatua gani zilizochukuliwa kwa wale wotewanaomdhalil isha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri yaMuungano Bungeni?

Page 182: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

182

3 MEI, 2013

Pia ni hatua gani zinazochukuliwa juu ya Wanasiasawanaovunja Sheria kwa kuwapotosha wananchi kupitiaMikutano ya hadhara?

Mheshimiwa Spika, kuhusu ufinyu wa bajeti, nashauriSerikali ione uwezekano wa kuongeza fedha katika Wizarahii kwa ajili ya matumizi ya ujenzi na ukarabati wa Mahakama,kuajiri Mahakimu na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, kuhusu ucheleweshaji wa kesi, nivyema sheria hii ya mwendo wa kesi ikaangaliwa upya ilikuwa na ukomo wa kumaliza kesi Mahakamani kuliko ilivyosasa. Kesi zinachukua muda mrefu sana, hivyo wananchiwalio wengi hasa wanyonge kukata tamaa na kupoteza hakizao.

Mheshimiwa Spika, wapo baadhi ya Mahakimuambao ni wala rushwa. Ni vyema kufanya uchunguzi nawatakaobainika kuchukuliwa hatua zinazostahili.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. GOSBERT B.BLANDES: Mheshimiwa Spika, Serikaliiliamua kuajiri Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo wenyeShahada ya Sheria (LLB), jambo ambalo ni jema.Waheshimiwa Mahakimu hawa tangu waajiriwehawajapangiwa Vituo vya Kazi. Wapo wamekaa bila kazikatika Mahakama za Wilaya, hawajapangiwa kazi yoyote,hata hawaruhusiwi kuahirisha kesi Mahakamani, hatamishahara ya baadhi yao haijatumiwa karibia miezi kumi. Nijambo la kukatisha tamaa sana kupita maelezo. Vijana hawahawajui wafanye nini, wametelekezwa kama watoto yatimahadi wanajuta ni kwanini waliomba nafasi za Uhakimu. Nikwanini Serikali haichukui hatua za makusudi na za harakasana ili kunusuru mgogoro huu?

Mheshimiwa Spika, Nolle Prosequi(no furtherProsecution)

Mheshimiwa Spika, Sheria ya mwenendo wa makosa

Page 183: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

183

3 MEI, 2013

ya Jinai CPA, inampa madaraka Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kumfutia mashtaka mshitakiwa yeyote paleanaporidhika kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuendeleakumshitaki.

Mheshimiwa Spika, kwa siku za hivi karibuni Ofisi yaDPP imekuwa na kigugumizi cha hali ya juu sana cha kutumiamamlaka haya kwa kuogopa vyombo vya habari namasuala ya kisiasa.

Naomba nishauri Ofisi ya DPP ifanye kazi kwa mujibuwa Sheria, kwani kutofanya hivyo, raia wengi wasio na hatiawanateseka bila sababu ya msingi na hakuna fidia yoyotewanayolipwa. DPP Office, isiogope maneno ya Mtaani,maneno ya kisiasa, chuki binafsi kukomoana au jambo lolotela kumnyima mtuhumiwa haki yake ya Nolle Prosequi (nofurther Prosecution). DPP na timu yake wawe wepesi kutoaNolle Prosequi haraka iwezekanavyo ili mradi wahakikishehaki inatendeka na Nolle Prosequi haitolewi katika mazingiraya rushwa au shinikizo lolote.

MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Spika,naomba kuchukua fursa hii i l i kuchangia hotuba yaMheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi kubwazinazofanywa na Serikali, bado kuna changamoto kubwakatika Wizara hii hasa katika Kitengo cha Mahakama, uelewawa wananchi kuhusu mambo mbalimbali ya kisheria.

Mheshimiwa Spika, Mahakama imekuwainalalamikiwa sana kuhusu utoaji wa haki kwa wananchi.Wananchi wamekuwa wanabambikiwa kesi tofauti kabisana zao za awali. Hata hivyo, Taasisi hii imekuwa inatuhumiwasana kwa rushwa, jambo linaloifanya Taasisi kukosa imanikwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, naishauri Wizara na Serikali kwaujumla kutafuta njia nzuri ya kushughulikia kesi za wananchiili kurudisha imani za wananchi kwa Taasisi hii.

Page 184: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

184

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, pia kesi nyingi na ndogo ndogozimekuwa zinachukua muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzihuku watuhumiwa wakiachiwa ndani bila kupewadhamana; huku kutokuelewa sheria kwa wananchi hawakukichukuliwa kama faida kwa Watendaji wa Mahakamana Askari Polisi.

Mheshimiwa Spika, asilimia kubwa ya wananchihazijui sheria nyingi za msingi au muhimu katika maisha yaoya kila siku. Jambo hili limefanya kudhulumiwa haki zao marakwa mara. Nashauri Serikali kutafuta mfumo wakuwaelimisha wananchi kuzijua Sheria mbali mbali ilikuwaepusha na matatizo mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO: Mheshimiwa Spika,Katiba ndiyo sheria mama katika nchi yoyote inayofuatamisingi madhubuti ya Sheria. Sheria yoyote ni lazima izingatiemisingi ya Katiba ya Nchi. Nchi yetu ina Katiba, lakini Katibayetu ina utata ambao umeleta manung’uniko na malalamikokwa muda mrefu, jambo ambalo limepelekea leo kuletamjadala wa mabadiliko ya Katiba.

Mheshimiwa Spika, jambo hili la kuridhiwa kujadiliwakwa suala la Katiba, litasaidia sana kutatua baadhi ya kerozilizomo katika Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibarendapo nia thabiti ya marekebisho hayo yatafuata zaidimaoni ya walio wengi na siyo maamuzi ya mtu.

Mheshimiwa Spika, Mwenyekiti wa Tume ya KuratibuMaoni ya Wananchi amekuwa akitoa maelezo kupitiavyombo vya habari kwamba suala la mabadiliko ya Katibani jambo ambalo halitochukuliwa vile wanavyotaka watoajiwa maoni hayo.

Kauli hiyo ya Mwenyekiti haiashirii kuwepo kwa uadilifuna uaminifu juu ya uratibu huo wa maoni ya wananchi juuya mabadiliko ya Katiba. Wananchi walio wengi wanaonakwamba suala la utoaji wa maoni ni kama kiini macho, lakini

Page 185: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

185

3 MEI, 2013

Katiba iliyokusudiwa imeshatayarishwa zamani na ndiyoMwenyekiti anayeshughulikia suala hilo akadai kama yukotayari wakati wowote.

Mheshimiwa Spika, maelezo yaliyotolewa ni Waziri waKatiba na Sheria yanakinzana kabisa na maelezoyanayotolewa na Mwenyekiti anayesimamia uratibu wamaoni ya wananchi juu ya mabadiliko ya Katiba. Ni vyemabasi Mheshimiwa Jaji Warioba akajikita katika maoni yawananchi na siyo yale tu anayoona yeye kwamba yanafaabadala ya kuwasilisha maoni ya wananchi, jambo ambalolinaweza kuleta ufa mkubwa na vurugu zisizokwisha,ambapo baada ya kusonga mbele likaweza kuturejeshanyuma. Ni vyema maoni hayo yakaangalia Muungano wanchi zote mbili.

Mheshimiwa Spika, uendeshaji wa Mahakama katikautoaji haki hautoshi, unadhalilisha. Ni wazi kwamba Serikaliimeshindwa kabisa kulisimamia jambo hili ambapo maranyingi washukiwa wa makosa wanadhalilishwa. Lakinimwisho wake washukiwa huonekana kwamba hawanamakosa, na baadhi ya makosa kuonekana na sura za kisiasa.Ni maoni yangu kwamba kwa wale ambao watachukuwahatua kwa nia tu ya kuwadhalilisha wananchi wengine kwakutumia nafasi zao na ikathibitika kwamba hakuna uthibitishowa kosa, ni lazima aliyedhalilishwa alipwe fidia.

Mheshimiwa Spika, ni wazi kwamba Serikali haikomakini katika kuangalia na kuimarisha majengo ambayoyanatumika katika kutoa haki. Majengo ni dhaifu, hayatoshina hayaonyeshi sura kwamba ni sehemu ya kutolea haki.Majengo yanaonekana kama maeneo yasiyo na amani naimani na wananchi wake.

Mheshimiwa Spika, mihimili mitatu ambayo ni SerikaliBunge na Mahakama; muhimili wa tatu, yaani Mahakamahaujatumika vizuri katika kusimamia kazi zake. Hivyo ni wazisasa muhimili huu ufanye kazi zake il i utendaji huousiambatane na misingi ya rushwa.

Page 186: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

186

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, nashauri haki zitendeke,zitekelezwe. Kuna wajibu wa makusudi wa Serikalikuhakikisha kwamba imeajiri Mahakimu wengi ili iwezekusimamia kutoa haki kwa kesi nyingi ambazo zimelundikwakwa muda mrefu bila kutolewa maamuzi, na hivyokuwafanya washukiwa ama kukaa ndani kwa muda mrefuau kwa wale walio nje na wanaoendelea na kesi kukosakuendelea kufanya shughuli zao za kimaendeleo, kwanihawawezi kwenda popote katika shughuli zao kwa kuhofiakuonekana kwamba wamekimbia.

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaSpika, napenda kuchangia katika haya yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na utamaduni waMahakimu kuendesha kesi kwa muda wanaotaka wenyewena hivyo kesi kulundikana na kusababisha kuwepo kwamianya ya rushwa. Hivyo basi, ni vyema Serikali ikaangaliaupya kwa kupitia Wizara husika namna bora ya kuendeshakesi hizo. Aidha, kwa kuongeza idadi ya watumishiwakiwemo Mahakimu; upanuzi wa ukarabati wa Mahakamaili kuziwezesha kuwa za kisasa zaidi ili kufanya kazi kwa ufanisina tija; ukarabati ama ujenzi wa Mahakama mpya lazimauendane sambamba na uwekaji wa vifaa vya kisasa kamaComputer na vinavyofanana na hivyo ili kuziwezesha kufanyakazi kwa ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Spika, ni vyema kikatumika Kiswahiliwakati wa hukumu ili kumrahisishia mtuhumiwa kuelewamwenendo mzima wa shauri na hatima ya hukumu.

Mheshimiwa Spika, ni vyema sasa Wizara husika naSerikali ikaangalia namna ya utoaji elimu kwa Umma ili Ummauweze kuzitambua sheria mbalimbali na pia waweze kuzitiibila shuruti.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. SARA M. ALLY: Mheshimiwa Spika, nampongezaMheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwamba katika

Page 187: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

187

3 MEI, 2013

kipindi chake cha Utawala hadi sasa ameteua Majaji zaidiya 50 ambao wameweza kusikiliza kesi kwa haraka nakuwawezesha Watanzania kupata haki zao kwa wakati nakutekeleza kwa vitendo dira ya Mahakama ya kutoa hakikwa wote na kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, hii inaonyesha jinsi ambavyoMheshimiwa Rais anavyowajali Watanzania kwa kuona hakiza Watanzania zinapatikana na kuonekana katika jamii.

Mheshimiwa Spika, bajeti ya mwaka 2012/2013zilitengwa Shilingi bilioni moja na laki tatu kwa ajili ya ujenzina ukarabati wa Mahakama, lakini fedha hizo hazikutolewana Hazina. Katika bajeti hii Serikali imetenga Shilingi bilionimoja na laki tano kwa ajili ya kazi hiyo.

Mheshimiwa Spika, fedha hizo hazitoshi, kwani kwamujibu wa taratibu zilizowekwa, ujenzi wa Mahakama Vijijiniunagharimu zaidi ya Shilingi milioni nne na laki tano naMahakama za Mijini, ujenzi unagharimu Shilingi milioni miatano na laki tano. Hivyo kwa fedha iliyotengwa, ina maanatutajenga Mahakama tatu tu. Bila kufanya ukarabati wowotekatika Mahakama, mfano, Mkoa wa Morogoro kuna mahitajiya Mahakama 54 za Mwanzo na Mahakama za Wilaya.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali itafute fedha zakutosha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Mahakama zetuili wananchi waweze kufikiwa na huduma na kuweza kupatahaki zao.

Mheshimiwa Spika, hitaji la Mahakama limekuwakubwa sana, mfano kwenye Wilaya mpya 19 ikiwemo yaGairo – Morogoro hakuna Mahakama; Mikoa mipya ya Geita,Simiyu, Njombe na Katavi hazina kabisa Mahakama.

Mheshimiwa Spika, gazeti la Daily News 22/4/2013limetangaza tenda ya kujenga majengo ya Utawala ya Mikoana Wilaya mpya ambapo jumla ya majengo 23 yatajengwa,lakini katika majengo hayo, hakuna hata Mahakama mojainayojengwa wala vituo vya Polisi.

Page 188: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

188

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali itazame upyaiweze kuweka kipaumbele ili wananchi waweze kupatahuduma za Mahakama ili haki zao zisipotee hasa kwa akinamama ambao wamekuwa wakikata tamaa kufuatilia hakizao, kwani inawalazimu kusafiri umbali mrefu kufuatahuduma za Mahakama.

Mheshimiwa Spika, lingine ni kuhusu utawala bora.Mahakama za Wilaya ziko kwenye Ofisi na majengo yaMamlaka nyingine. Mahakama za Mwanzo ziko kwenye Ofisiza Kata, mfano Mahakama ya Mwanzo ya Mlali Mvomeroiko kwenye Ofisi za Serikali ya Kata. Sasa endapo inatokeakesi inawahusisha viongozi wa Serikali za Kata: Je, Hakimuataweza kusimamia sheria na kutenda haki, wakati ndiyowamempa jengo kuendesha shughuli za Mahakama?

Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na migogoro mingiya ardhi nchini kati ya wakulima na wafugaji, wananchi nawawekezji na migogoro ya Vyama vya Siasa hasawanapoendesha Mikutano ya hadhara, jambo ambalolimepelekea Serikali kuunda Tume mbalimbali katikakushughulikia migogoro hiyo.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Tume ya Haki zaBinadamu na Utawala Bora imepewa mamlaka kikatibakulinda kukuza na kutetea Haki za Binadamu na misingi yautawala bora ni vyema sasa Serikali ikaijengea uwezo Tumekwenye Rasilimali Fedha na Rasilimali Watu ili kupunguzagharama za Serikali kuunda Tume kila linapotokea tatizo lauvunjifu wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Tume ya Haki zabinadamu ina mamlaka kikatiba ya kutoa elimu nakusuluhisha migogoro, naamini kabisa Tume ikiwezeshwaitasaidia kutatua kero nyingi za wananchi na kupunguzamlundikano wa kesi mbalimbali katika Mahakama zetu,kwani Tume itakuwa imezipatia ufumbuzi kwa njia yausuluhishi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

Page 189: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

189

3 MEI, 2013

MHE. SUSAN L. A. KIWANGA: Mheshimiwa Spika,napenda kuunga mkono hotuba ya Kambi ya Upinzaniiliyowasilishwa na Mheshimiwa Tundu Lissu.

Mheshimiwa Spika, napenda kujua ni lini Serikali italipaWashauri wa Mahakama za Mwanzo posho zao nchini? Kwamfano hai, ni kama nilivyowasilisha kwako madai ya Washauriwa Mahakama za Mwanzo wa Ifakara pamoja na jitihadazao za kufuatilia kwa barua.

Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango gani wakuboresha Mahakama za Mwanzo ambazo ndizo zinakuwakimbilio za Watanzania asilimia 75 - 80 waishio Vijijini?

Mheshimiwa Spika, tumepitisha Sheria hapa Bungeniinayotaka Hakimu wa Mahakama za Mwanzo wawe nashahada lakini hizo Mahakama za Mwanzo hazina nyumbaza Watumishi, majengo ya Mahakama, lakini katikaMahakama nyingi nchini ndiko rushwa imekithiri. Vile vilewananchi wengi wanahukumiwa kwa kukosa Wanasheriawa kuwasaidia. Je, Serikali ina mpango gani wa msaadawa kisheria kwa wananchi wa Vijijini?

Mheshimiwa Spika, kuhusu ucheleweshwaji wa kesi,Magereza nchini zinajaa kutokana na watu wengi kubakimahabusu au kwa kufungiwa dhamana au masharti yadhamana kushindikana. Mfano, hati ya nyumba ambapomaeneo mengi Wilayani Serikali haijapima viwanja walahaijatoa hati za nyumba, hivyo sheria zirekebishwe ili kupatamasharti nafuu ya dhamana.

Mheshimiwa Spika, ni wakati sasa Serikali ipelekeelimu ya sheria kwa wananchi i l i waondokane nakuhukumiwa bila kujijua.

Mheshimiwa Spika, ni ukweli kwamba baada yawananchi mbalimbali kupigiwa kura kwenye Mikutano Mikuuya Kijiji, Mtaa na kuchaguliwa na kushinda kwa kura nyingina kuongeza, lakini majina yalipopelekwa kwenye kikao chaKata ambapo kwa kawaida Wajumbe wa Baraza la

Page 190: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

190

3 MEI, 2013

Maendeleo ya Kata ni Diwani na Madiwani, Mtendaji Kata,Wataalam katika Kata, Viongozi wa Vyama vya Siasa,Wawakilishi wa NGO’s na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji.

Sasa wananchi wanashangaa, kwa nini uchaguzi waWajumbe katika Kata waliohusika kuteua Wajumbe ni Diwanina Wenyeviti tu ambapo uteuzi huo umelalamikiwa mahalipengi? Ni vyema suala hilo lingeangaliwa upya.

Mheshimiwa Spika, nawasilisha.

MHE. JOHN S. MAGALLE: Mheshimiwa Spika,napongeza juhudi za Wizara na Taasisi zote kwa umoja wadhamira na azma ya kutenda na kusimamia hifadhi ya haki.Haki huzaa amani, upendo na mshikamano kwa kustawishaustawi wa maendeleo ya jamii, uchumi na uwajibikaji borawa utawala bora.

Mheshimiwa Spika, Wizara hii hutambulisha mazingiraya hamasa ya matarajio ya shabaha na malengo ya uhaiwa hatma ya kusadikika demokrasia na siasa kuwa zitazaauwakilishi wa hiyari ya jamii kujiongoza na kujisimamia.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2005 ulikuwa wa uchaguziwa Madiwani na Wabunge. Serikali ilitambua kasoro ya kaziza Ubunge kuhitaji muda wa nyongeza wa kusikilizwa nakuamuliwa madai ya malalamiko ya kasoro na hitilafu kwaKanuni za Uchaguzi.

Mheshimiwa Spika, pana kesi za madeni ya kasorona hitilafu zilizopo katika Mahakama za Mikoa. Hatima yakesi hizo ni vurugu za utashi wa maono yasiyo na mwongozo.Je, ni lini patatolewa muda wa nyongeza wa kuzaauvumbuzi kwa madai ya malalamiko ya hizo kesi za uchaguziza Madiwani.

Mheshimiwa Spika, bima ya uhai wa utulivu wa siasaza uchaguzi hujengwa na vitendo ya haki zilizotendeka katikachaguzi zilizopita.

Page 191: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

191

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, naomba kauli elekezi itolewekupitia Bunge hili kuhusu usalama na uendelevu. Je,utatekelezwa vipi na Mahakama ziahirishe kesi hizo badalaya kuzifuta.

Mheshimiwa Spika, kauli ya Serikali na kauli yaMahakama Kuu kwa umoja wake watadhibiti mwonekanowa fikra hasa dhidi ya Serikali na dhidi ya Mahakama kuwani Wakala wa kudhulumu haki za utawala bora wademokrasi na siasa kwa watu wa tabaka la chini laMadiwani.

Mheshimiwa Spika, naomba kukumbusha kwambaWizara hii ina mhimili wa Mahakama. Ni fursa chanya na niwajibu mtambuka wa kuondoa mapishi ya mizozo namigogoro ya kuegemewa na wanasiasa kuezua imani yaUmma kwa mafanikio ya wema mpana ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, naomba vile vile DPP apatiwefursa ya kutoa Bungeni semina ya utambulisho wa maanana wajibu wa Ofisini hii.

Mheshimiwa Spika, Ofisi hii ndiyo maono ya hekimana busara pana, hivyo tuepuke malipuko ya kuisuta kwadhana ya asiyejua maana, hana sifa ya kuzua jambo.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

MHE. VINCENT J. NYERERE: Mheshimiwa Spika,natanguliza sana shukrani zangu kwa kupata fursa hii yakuchangia kwa kifupi sana.

Mheshimiwa Spika, nasema kwa kifupi kwa kuwaninayoyaona mimi yanayohitaji marekebisho ni kidogo sanakwani yaliyo mengi yapo sawa, hii ni kadri nionavyo mimi.

Mheshimiwa Spika, napenda kwanza kuipongezaSerikali kwa jitihada za kuongeza idadi ya Mahakimu tofautina hapo mwanzo japo wanafanya kazi katika mazingira

Page 192: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

192

3 MEI, 2013

magumu kutokana na maeneo wanayofanyia kazi hasamaeneo ya vijijini.

Mheshimiwa Spika, ukomo kumaliza kesi kwa mwaka.Mbali na kuongeza idadi ya Mahakimu basi uwepo utaratibuwa kisheria wa Hakimu kumaliza angalau kesi kwa idadifulani ili kupunguza mlundikano wa kesi ili kuokoa fedha zawalipa kodi ambazo zinatumika kulisha mahabusu nawafungwa. Uwepo wa ukomo wa chini wa idadi ya kesi nimzuri japo una changamoto zake kulingana na aina ya kesi.

Mheshimiwa Spika, njia nyingine ya kupunguzamlundikano Magerezani, ni kuhesabu miaka au muda wamahabusu walioutumia Gerezani kabla ya hukumu iliwakihukumiwa basi ule muda walioutumia uingizwe katikamuda wa hukumu atakayopata.

Mheshimiwa Spika, majengo ya Mahakama nyingihapa Tanzania ni chakavu na bado hayajakidhi kabisa idadiya mashauri yaliyopo. Napenda kuishauri Serikali iliangaliekwa umakini suala hili ili mlundikano wa watu Magerezanina kesi Mahakamani zipatiwe ufumbuzi wa kudumu piaadhabu mbadala itiliwe mkazo.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. ANNAMARYSTELLA J. MALLAC: MheshimiwaSpika, nashukuru kupata nafasi ya kuchangia Hotuba yaWizara hii muhimu ya Katiba na Sheria ambayo inasimamiahaki, sheria na uhuru wa binadamu.

Mheshimiwa Spika, nianze na uboreshaji wa mazingiraya kazi na ujenzi wa majengo. Mhimili huu wa sheria nimuhimu sana lakini Serikali imekuwa haitoi fedha za kutoshakulingana na majukumu ya mhimili huu ulivyo. Miundombinubado iko nyuma sana kwa maana ya majengo ya Mahakamanyingi za Wilaya nchini ni mabovu, yamechakaa na kuwamakazi ya bundi (magofu). Usafiri kwa Mahakimu ni mgumu,hawana magari ya kufanyia kazi vya kutosha. Hawana vifaavya kisasa vya kufanyia kazi maofisini, kama computer, bado

Page 193: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

193

3 MEI, 2013

wanatumia typewriter kizamani ambazo hucheleweshakupatikana kwa taarifa za kazi na kuweka mlundikano piaupotevu wa taarifa.

Mheshimiwa Spika, Tume ya Kubadilisha SheriaTanzania. Tume hii ipiganie kubadilisha sheria nyingi zilizopitwana wakati kwani sheria kandamizi kama vile umiliki wa ardhikwa mwanamke bado ni tata na hasa vijijini.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali hawa paralegalwazunguke sana vijijini kutoa elimu ya sheria mbalimbali. Piakatika sheria au kusimamia masuala ya mashauri, lugha yaKiswahili itumike ili wananchi waelewe kwa ufasaha misingiya haki zao badala ya kuingia gharama ya kutafuta Mawakiliwa kuwasimamia kwa gharama kubwa au kukata tamaakabisa na kumuachia Mungu.

Mheshimiwa Spika, nawasilisha.

MHE. DKT. AUGUSTINE L. MREMA: Mheshimiwa Spika,Mji Mdogo wa Himo ulitangazwa rasmi na Serikali mwaka2000. Mwaka 2002, watu wenye nia mbaya kuzuia maendeleoya mji huo, kwa kutumia Mawakili ambao lengo lao nikutafuta fedha, wakaanzisha kesi Mahakamani kuzuia mjihuo usipimwe na wala usijengwe.

Mheshimiwa Spika, kitu kinachonisikitisha kamaMbunge ni kuona jinsi Mahakama inavyotumika kuzuiamaendeleo ya wananchi. Kesi hiyo imekaa Mahakamanikuanzia mwaka 2002 hadi leo mwaka 2013 zaidi ya miaka11, kesi haiongelewi, kesi haimaliziki, mji haupimwi walahaujengwi, kisa kuna kesi Mahakamani. ni maoni yangukwamba Mahakama zinatumika vibaya kwa manufaa yawatu wachache wenye nia ovu. Ni kwa nini kesi inayozuiamaendeleo ya wananchi ikae Mahakamani kwa miaka 11?Huu utawala wa sheria uko wapi? Wananchi wakidai kunarushwa Mahakamani inayozuia haki na maendeleo yaoyasipatikane tunasema nini? Ni lazima Serikali izuie utapelihuu. Nina majina ya wananchi 400 wanaotaka kupimiwaviwanja kwenye Mji wa Himo lakini imeshindikana kupimiwa

Page 194: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

194

3 MEI, 2013

viwanja hivo kisa kuna kesi Mahakamani, kesi iliyokoMahakamani kwa miaka 11.

Mheshimiwa Spika, suala hili nimelifikisha mbele yaMwanasheria Mkuu wa Serikali atoe msukumo wake kwakuwa halijamalizika. Hii kesi ya bandia inaidhalilisha sanaSerikali. Naomba Serikali itoe tamko juu ya kesi hii ya bandiainayozuia Mji wa Himo kupimwa na kujengwa.

MHE. MICHAEL L. LAIZER: Mheshimiwa Spika, napendakutanguliza kuunga mkono Hoja ya Waziri. Pamoja nakuunga mkono, nieleze changamoto kwenye Wizara hii napili nieleze kero kwenye Jimbo la Longido.

Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu Serikali haiipatiiWizara hii fedha za kutosha. Serikali inapogawa maeneo yautawala mfano Mikoa, Wilaya Mpya, yote yanahitajiMahakama za Mikoa na Mahakama za Wilaya. Kuna mahitajikatika maeneo mengi nchini. Tunashauri Serikali iitengeeWizara fedha za kutosha ili majengo ya Mahakama yajengwekwenye maeneo yanayohitajika.

Mheshimiwa Spika, suala l ingine ni usafiri waMahakimu. Tatizo hil i ni kubwa hasa kwa Wilaya zapembezoni. Hakimu anahitaji kuzunguka kwenye Tarafambalimbali jambo hili ni tatizo.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni muhimuMahakimu kujengewa nyumba za kuishi kama watumishiwengine.

Mheshimiwa Spika, napenda nieleze kero za Wilayaya Longido. Wilaya ya Longido imetengwa kwenye Wilayaya Monduli mwaka 2007. Huduma ya Mahakama iliyokoMonduli ni mbali sana, kilometa 150 jambo ambaloinawawia wananchi vigumu kutumia huduma hiyo.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Longido ina Tarafa nne(4) ambazo ni mbali na Makao Makuu mfano, Tarafa ya

Page 195: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

195

3 MEI, 2013

Enduimet ni km.75 toka Makao Makuu (W), Tarafa yaKetumbeine km.60, Tarafa ya Engarenaibor km.44.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Longido haina jengo laMahakama ya Wilaya. Haina Mahakama ya Mwanzo, badoMahakimu wanakosa eneo la kuendeshea mashauri yaMahakama pamoja na usafiri wa kufikia Tarafa nilizozitajahapo juu.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba Wilaya yaLongido ni ya zamani tofauti na Wilaya ambazozimegawanywa mwaka jana lakini bado tuna mahitajimakubwa kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, ombi langu, naomba Serikaliisikilize ombi hili kwani ni la muda mrefu kuanzia Waziri BakariMwapachu mpaka sasa kila Waziri anayeingia anatoa ahadina kuondoka bila kutekeleza ahadi hii, kwa sasa Serikaliiangalie tena kero hii ya Jimbo la Longido.

Mheshimiwa Spika, nawaombea mafanikio mema.

MHE. JOHN P. LWANJI: Mheshimiwa Spika, naungamkono hoja ya Wizara hii kuhusu bajeti ya mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali iharakisheukarabati wa Mahakama za Mwanzo za Mwamagembe naUkimbu (Kayui).

Mheshimiwa Spika, aidha, naiomba Serikali iangalieuwezekano wa kujenga Mahakama za Mwanzo kwa ajili yaKata za Idodyandole, Ipande, Aghondi, Rungwa, Kitarakana Saijaranda.

MHE. FAITH M. MITAMBO: Mheshimiwa Spika, kwanzanaunga mkono hotuba ya Waziri wa Katiba na Sheria.Mambo mengi yaliyopangwa ndani ya hotuba hii ni memaiwapo yatafuatwa na kutekelezwa kwa wakati muafaka.

Page 196: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

196

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, niendelee kutoa msisitizo tu,kwamba mchakato wa kuunda Katiba Mpya, ungefaa kamakufikia mwaka 2014, mchakato huu ungekamilika na KatibaMpya kupatikana.

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 59 wa hotuba yaMheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria, ametamka kwambaTume ya kukusanya maoni ya Katiba Mpya, itayaheshimu nakuyafanyia kazi ipasavyo maoni yote yaliyotolewa nayatakayotolewa na wananchi, Taasisi, Asasi za kiraia namakundi mengine. TGNP na Chama cha WabungeWanawake kimeshiriki kutoa maoni yake katika Tume yaKukusanya Maoni. Naomba maoni na mapendekezoyaliyotolewa yazingatiwe kwa faida ya wanawake woteTanzania.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa suala la uwakilishiBungeni, bado wanawake wanasisitiza uwakilishi wa asilimia50 kwa 50 upatikane/uwepo na sio ndani ya Bunge tu hatakatika vyombo vingine vya maamuzi ngazi ya juu Serikalini.Naiomba Tume ya maoni ya Katiba ijitahidi kukamilishamapema uundwaji na upatikanaji wa Katiba mpya ilimapendekezo mengine yaliyotolewa na TGNP na Chamacha Wabunge Wanawake, yaweze kutumika katika uchaguziwa mwaka 2015.

Mheshimiwa Spika, siyo maoni yote yaliyotolewayanajenga au yatajenga. Tuweke utaifa mbele, tuangalieamani ya nchi yetu na watu wake. Maoni yanayotolewaambayo hayajengi na hayatajenga nchi na Utaifa wa nchiyetu. Ni vyema yakaachwa, na kwa hili Tume inahitajikuchukua na kufanya maamuzi magumu pale inapoonamaoni yaliyotolewa hayatafaa.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Liwale hainaMahakama ya Wilaya. Mahakama inayotumika sasa hivi niMahakama ndogo ambayo ilikuwepo enzi za mkoloni kablaWilaya ya Liwale haijawa wilaya mwaka 1975. Mahakamahii ilikuwa ni Mahakama ya Tarafa ya Liwale, na mpaka sasaWilaya inaendelea kutumia kibanda hiki kidogo

Page 197: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

197

3 MEI, 2013

kinachofanana na Mahakama za Mwanzo. Katikamajumuisho ya Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria, nilini Wilaya ya Liwale itapata jengo kubwa la Mahakamalinalolingana na hadhi ya Wilaya?

Mheshimiwa Spika, siyo kitu chema sana kudai jengola Mahakama kubwa na zuri, kwani Mahakama siyo mahalipazuri. Lakini jengo hili chakavu la Mahakama liko katikatiya Mji na hivyo kuleta sura mbaya ya Mji wetu wa Liwale.

Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikilalamika kuhusujengo hili kuu kuu, ila Mahakama sasa ni mwaka wa tatu, nivyema Serikali itujengee jengo lingine jipya la Mahakama.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. SILYVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Spika, Wizarahii ina jukumu kubwa la kutoa haki kwa wananchi na sasajukumu kubwa la kusimamia na kuleta Katiba mpya.

Mheshimiwa Spika, katika Jimbo langu la Kibaha Mjini,tunayo kero kubwa sana ya Mahakama ya Mwanzo. Jengola Mahakama ya Mwanzo kwanza liko kwenye eneo labarabara likitizama uwanja wa bwawani pale Maili Moja.

Mheshimiwa Spika, kama hii haitoshi, jengo hili ni laudongo na miti na linavuja kiasi kwamba haiingii akilini kamakweli hili ni jengo la Serikali, tena Mahakama inayotakiwakusikiliza malalamiko, na makosa mbalimbali ya wananchina kuyatolea maamuzi ya haki. Hata watumishi katikaMahakama hii waweza kutoa maamuzi mabaya kwa ajiliya athari wanazopata kutokana na mazingira haya mabayaya jengo hili la Mahakama wanapotendea kazi zao.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa Serikali itoe majibukuwa ni lini jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo litajengwana kukamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi waKibaha Maili Moja. Naomba Waziri atolee jambo hili maelezo.

Page 198: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

198

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, pamoja na changamoto zakibajeti (yaani kifedha) tulizonazo, ni wazi kwamba sasa Idaraya Mahakama ni lazima nayo iendane na teknolojia ya kisasa.Kwa sasa hivi, maelezo ya watuhumiwa, watuhumu namashahidi huchukuliwa kwa kunukuliwa na kuandikwa naHakimu, tena kimuhtasari katika jalada husika. Jambo hilihuchangia katika mambo matatu. Kwanza, ni kazi ngumu,lakini Hakimu kuweza kurekodi tofauti na maelezo au maanahalisi ya maelezo ya wahusika; pili, ni rahisi kuruka au kukataamaelezo hayo na tatu ni rahisi kukaribisha rushwa kwakubadili maana halisia ya maelezo na hata kupotea aukupotezwa kwa maelezo na faili ya kesi husika.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa Serikali iwekemitambo ya kisasa ya kurekodi maelezo ya watuhumiwa,watuhumu, mashahidi na hata Mahakimu na Wazee waMabaraza au Mahakama ili ukweli wa maelezo ya wahusikayaweze kutunzwa na hata hapo hukumu inapoandikwaMahakimu waweze kuzingatia maelezo sahihi ya sauti yawahusika. Hii ni rahisi na ni mfano halisi wa jinsi Hansard yaBunge inavyorekodi majadiliano mbalimbali ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Spika, tunafahamu kuwa Wizara inajukumu kubwa la kusimamia mchakato wa Katiba mpyaambayo ndiyo sheria mama ya nchi yetu. Ninashauri uwepoumakini mkubwa il i nchi ipate Katiba itakayoletautengamano, amani na msukumo wa maendeleo kwawananchi, Katiba itakayotoa changamoto za kuipelekaTanzania katika hatua bora za kimaendeleo yenyekumwajibisha kila Mtanzania ashiriki katika ujenzi wa Taifahuku akihakikishiwa usalama na maisha bora.

Mheshimiwa Spika, niitakie Wizara kila la kheri. Naungamkono hoja.

MHE. PROF. KULIKOYELA K. KAHIGI: Mheshimiwa Spika,Kitabu cha hotuba ya Waziri kinaelezea vizuri changamotombalimbali na mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.Mojawapo ya changamoto hizo ni, uwezo na uelewamdogo wa wananchi walio wengi kutumia vyombo vya

Page 199: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

199

3 MEI, 2013

kutoa haki na huduma za kisheria kuhusu mfumo uliopo waSheria (ukurasa wa 45) na Wizara inapendekeza mkakati wakuendelea kutoa elimu ya Sheria na kusogeza huduma zakisheria kwa wananchi (ukurasa wa 46).

Mheshimiwa Spika, kwa maoni yangu, tatizo la msingizaidi kwa wananchi wengi Vijijini na Mijini ni kwamba raiawengi hawazifahamu haki zao za kikatiba na kisheria. Ujingawa raia wengi kuhusu haki zao mbalimbali ni chanzo kikuucha dhuluma na hujuma mbalimbali ambazo wananchi(hasa wa Vijijini) hufanyiwa na Polisi na vyombo vya kutoahaki. Wananchi wanapobambikiwa kesi au taratibu zautawala bora zinapovunjwa, wananchi wengi hawajuiwafanye nini kwa sababu aina ya haki i l iyovunjwahawaifahamu. Wizara ina mpango gani wa kuwaelimishawananchi kuhusu haki zao kama zinavyosimamiwa na Tumeya Haki za Binadamu na Utawala Bora?

Mheshimiwa Spika, miongoni mwa mambo ambayoWizara imejipangia kufanya mwaka 2013/2014, ni “KutafsiriSheria kutoka lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili” (ukurasawa 54). Naipongeza Wizara kuendelea na zoezi hili ambalolitasaidia kuondoa kikwazo cha lugha kwa uelewa wawananchi wa sheria. Ninavyokumbuka, tafsiri ya sheria zetukutoka Kiingereza kwenda Kiswahili ni pendekezo lililotolewapia katika Mkutano wa Bunge la Bajeti wa mwaka 2012/2013na baadhi ya Wabunge (pamoja na mimi). Naipongeza nakuihimiza Wizara iongeze juhudi zaidi katika shughuli hii ilihatimaye sheria zote ziwe katika lugha ya Kiswahili. Swalilangu hapa ni hili: Je, Wizara imepanga kutafsiri Sheria ngapikwa Kiswahili? Mwaka 2012 ilitafsiri sheria ngapi? Wizara inampango mkakati wowote wa kukamilisha zoezi la tafsiri lasheria zetu zote?

Mheshimiwa Spika, naunga mkono ushauri wa Kamatiya Katiba na Sheria kwamba Miswada yote mipya ya sheriainafaa iandaliwe kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Ushaurihuu ukitekelezwa, Serikali itakuwa imefanikiwa kuifanya sheriakuwa karibu na wananchi kwa kuwa itakuwa katika lughawanayoifahamu. Wizara ijipange ili itekeleze ushauri huu.

Page 200: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

200

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho nitakaloongeleani ucheleweshwaji wa mashauri ambao pia umetajwa nataarifa ya Kamati. Hotuba ya Mheshimiwa Waziri, ukurasawa 7 - 15, imetaja mashauri mbalimbali ambayoyanaonyesha kuwa kuna mashauri mengi ambayohayajashughulikiwa. Tatizo hasa ni nini?

Mheshimiwa Spika, mfano wa kutisha waucheleweshwaji wa mashauri niliuona katika Gereza laKahama nilipolitembelea mwaka 2012. Gereza hili linamahabusu kutoka Wilaya ya Mbogwe, Bukombe na Kahama.Mahabusu wengi wamo ndani kwa tuhuma ndogo ndogo,ingawa wengine wanakabiliwa na tuhuma za jinai.

Niliongea na Mahabusu na lalamiko lao kubwalilikuwa kucheleweshwa kwa kusikilizwa kwa mashauri.Baadhi ya mashauri hayajasikilizwa kwa zaidi mwaka au hatamiaka miwili. Ushauri wangu kuhusu ucheleweshwaji wamashauri ya mahabusu wa Bukombe na Mbogwe katikaGereza la Kahama ni huu ufuatao:-

(1) Pendekezo langu la mwaka 2012 kuhusuWizara kujipanga ili adhabu mbadala ianze kutumika,lifikiriwe haraka. Njia hii itasaidia kupunguza msongamanokatika Magereza kama ya Kahama.

(2) Tatizo linalowakabili mahabusu wa Bukombena Mbogwe ni kwamba mashauri yao yanasikilizwa katikaMahakama za Bukombe. Inabidi wasafirishwe kutokaKahama hadi Ushirombo. Tatizo ni kwamba kuna wakatiambapo gari lipo na wakati mwingi hakuna gari. Wizaraitawasaidiaje mahabusu hao ili mashauri yao yaharakishwekusikilizwa?

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Spika, Wilayaya Nkasi ilianzishwa, leo hii ina umri wa miaka 37, ajabuhatuna Hakimu wa Wilaya. Ina wakazi wapatao 420,000 naKata 17, Tarafa tano, Vijiji 98 Vitongoji 12. Wananchiwanapata taabu sana, wanafika Namanyere, Hakimu kutokaSumbawanga hafiki Namanyere, wananchi wanapoteza

Page 201: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

201

3 MEI, 2013

nauli zao na muda wao, acha gharama za chakula namalazi. Je, hii ni utawala bora?

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Nkasi imekamilika kwakila Idara, maana hakuna Idara haina Mkuu wake, kasoro nihuyo Hakimu wa Wilaya, Idara mpya kabisa ya TAKUKURU nayoina Bosi wa Wilaya, hata Uhamiaji, OCD Afisa Usalama waWilaya wote wako.

Mheshimiwa Spika, wananchi wanateseka, wenginewanatembea kwa miguu wafike Wilayani halafu Hakimuhayupo. Je, huo ni uungwana? Nauli yake ni juu sana, mfanomtu wa Kala, Wampembe lazima apitie Sumbawanga, Itindihakuna njia, ni mguu njiani. Kwa mfano, kutoka Kabwe hadiNamanyere Kilometa 67, kutoka Itindi hadi NamanyereKilometa 85, kutoka Kirando hadi Namanyere kilometa 60,kutoka Namanyere hadi Sumbawanga kilometa 100, kutokaWampembe hadi Namanyere kilometa 100 na kutoka Kalahadi Namanyere kilometa 150.

MHE. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, naungamkono hoja.

Mheshimiwa Spika, ni muhimu mhimili huu waMahakama ukaongezewa fedha za kutosha hususan zamiundombinu kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama za MwanzoWilaya na Mahakama Kuu.

Mheshimiwa Spika, aidha, maombi ya Mahakama yaMwanzo Ludewa na Manda Ludewa itajengwa lini? Kwanini Bajeti ya tatu sasa ninakumbushia.

Mheshimiwa Spika, huduma za RITA ni muhimu zikawaDecentralized. Ni lini maeneo ya Local Government yatapatahuduma hii ya Wakala RITA Vijijini na Wilaya zote nchini?

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu nilazima iwe na tafsiri ya Kiswahili kwa Sheria zote. Ni lini jambohili litafanyika?

Page 202: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

202

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, naipongeza Tume ya Mabadilikoya Katiba. Je, Bajeti ya Bunge la Katiba ipo wapi?

Mheshimiwa Spika, aidha, taarifa za Tume ya Haki zaBinadamu kwa mujibu wa kanuni zinapaswa kuwasilishwaBungeni: Ni lini taarifa hizi zitaletwa Bungeni?

Mheshimiwa Spika, aidha, napongeza uwaziuliotumika kuwapata Wajumbe 19,182 wa Baraza la Katiba.

Mheshimiwa Spika, usiki l izwaji wa mashaurinapongeza, ila unapaswa kuongeza kasi. Mahakama Kuutakwimu zinaonyesha kuwa Speed inapaswa kuongezeka.

Mheshimiwa Spika, napongeza suala la Paralegals nanaomba sheria ije haraka Bungeni.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Sheria za Migogoro yaArdhi, nashauri Mabaraza yawe chini ya Mahakama.

Mheshimiwa Spika, vile vile napendekeza kwambaLaw Reform Commission irekebishe Sheria zilizopitwa nawakati, mapema.

Mheshimiwa Spika, Maazimio, “InternationalConcentions” ni muhimu tukawa na Idara (department)inayoonyesha maazimio tuliyoridhia na utekelezaji wake. Hivisasa ni vigumu sana kufuatilia maazimio yaliyopitishwa.Aidha, tunahitaji Matrix, Vitabu na CD.

Mheshimiwa Spika, naipongeza sana huduma yaregistration USBRI na naomba isambazwe mapema sana. Je,wale ambao ni six years, inakuwaje?

Mheshimiwa Spika, lingine ni kuhusu uimarishaji wamafunzo kwa vitendo (Law School). Wanafunzi hawa nimuhimu sana wakazingatiwa katika Bodi ya Mikopo, hivyoningeomba kujua jitihada za Wizara.

Page 203: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

203

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Uongozi waMahakama Lushoto kiendelee kutoa elimu kwa wafanyakaziwengi, na kikidhi quality ya kufundisha Majaji na Mahakimu.Aidha, wakati umefika sasa wa kutoa huduma zaKimahakama kwa mitandao (E-Judiciary) na hivyo kuhamakutoka typewriter kwenda computer.

Mheshimiwa Spika, kodi ya pango imekuwa kubwana hivyo ipo haja ya kupata majengo ya Wizara ili yatumikekwa ajili ya Mahakama nchini.

Mheshimiwa Spika, kuhusu upungufu wa bajeti naraslimali watu, tunahitaji political will. Vile vile kuwepo naHouse Allowance kwa Mahakimu na Majaji ambao hawananyumba.

Mheshimiwa Spika, ni lini Kamati ya Maadili ya Mkoana Wilaya za Njombe zitapewa elimu?

Mheshimiwa Spika, Taarifa ya Kamati KSU ilishauriuwepo utaratibu wa OPRAS kwa Majaji – Open PerformanceApraisal System ili kupunguza back log. Je, Wizara imefikiawapi?

Mheshimiwa Spika, aidha, kutokana na kazi nzuriambazo Wizara na Taasisi yake wamekuwa wakifanya,Kamati ya KSU itahitaji kuonana na Law Reform Comission,LHRC na Kutembelea Chuo cha Mahakama Lushoto naMahakama ya Wilaya na Mwanzo Mkoani Dodoma katikakipindi hiki cha Bunge.

SPIKA: Mheshimiwa Mwenasheria Mkuu wa Serikali!

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika,najua kwamba umeshalitolea uamuzi jambo hilo, lakini kwakweli ni kinyume na Kanuni kwamba ili uweze kufahamukama taarifa hii inastahili kuwasilishwa Bungeni, ni lazimakwanza uwe umeiona na kuna Kanuni inasema ziwasilishwesiku mbili kabla ya kufika hapa. Hata hivyo, hili limefanyikalakini nafikiri kwenye Kamati ya Uongozi tulizungumze vizuri.

Page 204: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

204

3 MEI, 2013

Ninachosema ni kwamba nafikiri tuepuke kama Wabungekufanya mambo kama wanafunzi wanaoficha kazi zao kwaajili ya kuwashtukizia wenzao kwenye mitihani au kwenyesemina.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasiya kuchangia hoja ya Mheshimiwa Mathias MeinradChikawe, Waziri wa Katiba na Sheria ambaye ameiwekaMezani kwako asubuhi ya leo. Aidha, napenda kutumianafasi hii kufafanua baadhi ya hoja na kutoa majibu kwamaswali yaliyoulizwa kuhusu Ofisi ninayoiongoza ambayoWaziri ameiombea fedha.

Mheshimiwa Spika, awali ya yote niseme kwambaninaunga mkono hoja hii asilimia mia kwa mia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza kuna mambo ambayoyamesemwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ambayoinaongozwa na Dkt. Pindi Hazara Chana na ambayoilisomwa na Mheshimiwa Gosbert Begumisa Blandes, Mbungewa Karagwe. Nawashukuru sana, naishukuru sana Kamatikwa ushauri iliotoa, ushauri mahsusi kuhusu Ofisi yangu naDivisheni zake lakini pia kwa moyo waliotupa na tunaupokeaushauri wao kwa moyo mmoja kabisa.

Mheshimiwa Spika, kwanza, kuhusu suala la weledikwenye suala la mikataba, Wabunge wengine piawamechangia suala hili. Naomba kutoa taarifa Bungenikwamba tumeanza kutoa mafunzo mahsusi yaani specialisedtraining kwenye eneo la mikataba kwa ufanisi yaani badalaya kusoma tu, lakini tunatumia pia mikataba ya zamani kamani njia ya kujifunza namna ya kusonga mbele. Kwenyemaeneo ya gesiasilia, uchimbaji wa mafuta, mikataba yauchimbaji wa madini, yote hiyo tunaifanyia kazi nazimeshatengwa fedha kwa ajili hiyo, shilingi 2,340,211,000/=zimetengwa kwa ajili hiyo.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Waandishi waMiswada, tunapokea ushauri kwamba Miswada iandikwekwa lugha ya Kiswahili na kwa Kiingereza. Kazi hii imeanza

Page 205: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

205

3 MEI, 2013

isipokuwa tu niseme kwamba zipo changamoto za kibajetipamoja na mafunzo ambazo tumeamua na zenyewekuzishughulikia.

Mheshimiwa Spika, kwenye usimamizi wa Mashauri yaJinai, mafunzo yatatolewa. Tunashukuru kwambazimetengwa fedha za kutosha kwa ajili hiyo kwa mwaka wafedha ujao.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na hoja ya Muswadawa Marekebisho wa Sheria ya Bodi ya Mikopo, naomba kutoataarifa kwamba leo saa 4.30 asubuhi tulipokea Rasimukutoka kwenye Wizara inayohusika. Tunaahidi kwambatutaishughulikia na baada ya kupitia kwenye vyombo vyamaamuzi, tutaleta Muswada huo hapa Bungeni mapemaiwezekanavyo. Hili suala ni muhimu kwa kila Mbunge na kilaMtanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la lingine ni lile ambalo dadayangu Mheshimiwa Sabreena Sungura alikuwaanalizungumzia.

Kwanza, namshukuru sana, nilipokuwa natikisakichwa nil ikuwa nakumbuka kwamba WaheshimiwaWabunge walitunga sheria ambayo iliweka mahusiano katiya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Maafisa Sheriakatika Wizara na katika Serikali za Mitaa. Nampongeza sanakwa kutetea maslahi ya Wanasheria wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Bunge lilitunga Sheria Na. 4 yaMwaka 2005 na sheria hiyo inaweka mahusiano ya Mawakiliwa Serikali na Maofisa wengine wanatekeleza majukumu yasheria katika Wizara, Idara na Serikali za Mitaa.

Kama inavyofahamika, mamlaka haya yaMwanasheria Mkuu wa Serikali ni ya Kikatiba. Jukumu lakuishauri Serikali kwenye mambo ambayo yameainishwakwenye sheria hiyo ambayo Bunge lilitunga, ni mamlaka yaMwanasheria Mkuu wa Serikali.

Page 206: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

206

Mheshimiwa Spika, mtu yeyote anayetekelezamamlaka hayo, ni yule mtu ambaye kwa mujibu wa sheria,ameelekezwa kufanya hivyo na Mwanasheria Mkuu waSerikali.

Maafisa walioko Wizarani, kwa kweli naomba kutumianafasi hii kuwaomba kwamba Sheria inawataka kwenyeSheria ambayo imetungwa hapa Bungeni Kifungu cha 26 chaSheria ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wajiandikishekwenye daftari la Wanasheria na sisi wako wenginetunawatumia, siyo kwamba hatuwatumii, tunawatumia nawengine ni wazuri, isipokuwa katika suala la maslahi, yaanimishahara, ni vizuri tufanye tofauti. Tofauti ya msingi nikwamba mimi sihusiki na mishahara yao. Mishahara yaoinahusiika na sehemu ambayo wanafanyia kazi. Ila ninahimizakwamba suala hili na lenyewe tutaliangalia ili maslahi yaWanasheria hawa nayo yasiwe haba.

Mheshimiwa Spika, ukosefu wa majengo, ni kwelikuwa tuna tatizo na tunachukua hatua za kulikabili. Kwa kweliukosefu wa Ofisi za kukaa pamoja na majengo katika Wilayana katika Mikoa ni kweli yapo na tunashukuru kwamba safarihii fedha tulizozipata zinatuwezesha kusonga mbele. Hivyohivyo kwenye Watumishi wachache na kuongeza bajeti DPPpamoja na suala la kufungua Ofisi za Kanda, kwa bajetiambayo tumefanya, nafikiri tutaanza kuendelea.

Kuhusu suala la Mheshimiwa Shibuda la kuongezamuda wa kusikiliza mashauri ya kesi za Uchaguzi waMadiwani; kama mnavyofahamu Muswada wenyemapendekezo hayo ulishawasilishwa hapa Bungeni naukasomwa mara ya kwanza. Kwa hiyo, hili jambo bado likokwenye hatua hii.

Kuhusiana na suala la Mheshimiwa Tundu Lissukwamba Serikali itoe tamko kuhusu taarifa za uchunguzi wamauaji wa Mwandishi wa Habari, Marehemu DaudiMwangosi; ni kweli kuwa Tanzania imeridhia mikataba mingi,lakini mikataba ile siyo zaidi ya Katiba yetu. Ina-supplementKatiba. Katiba ni ya kwanza mikataba ile inafuata. Kwa

Page 207: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

207

mujibu wa Katiba yetu, hakuna mtu ambaye anaruhusiwakutoa uhai wa mtu mwingine bila kufuata utaratibu wakisheria. Kwa ajili hiyo, tukio ambalo linahusiana na MarehemuDaudi Mwangosi, ni kwamba upelelezi wake umekamilika nakwamba mtu atakayehusika atapelekwa Mahakamani.Nafikiri huo ndiyo utaratibu. Sasa kusema kwamba tutoetamko, nafikiri tusubiri kwanza utaratibu huo wa Kimahakama.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ni hili la ushauri waOfisi ya DPP.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa Mzungumzaji)

Mheshimiwa Spika, ninaomba kuunga hoja mkono naninashukuru kunipa nafasi hii. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaSpika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi niweze kutoaufafanuzi kwa baadhi ya hoja zil ichochangiwa naWaheshimiwa Wabunge kwa Taasisi mbalimbali zilizoko katikaWizara ya Katiba na Sheria. Yako maeneo mengiyaliyochangiwa, lakini kutokana na ufinyu wa muda, nitatoamajibu kwa maeneo machache na Mheshimiwa Waziriatajibia maeneo mengi zaidi kwa kina. Baada ya kusemahayo, naomba sasa kujibu hoja hizo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwanza na hojazilizotolewa na Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala,ambapo katika hoja ya kwanza Kamati ilieleza kuwa ni vyemataratibu za kuhakikisha kwamba wananchi walio wengiwanaipata haki kwa kupata huduma za kisheria zikamilishwemapema. Serikali imekwishafanya maamuzi, hivi sasa Wizaraya Katiba na Sheria inaandaa taratibu za kuandika Muswadawa Sheria ambao pindi utakapokamilika katika mwaka huuwa fedha utawasilishwa Bungeni kwa ajili ya kutungiwa Sheria.

Kamati pia imetutaka kutulia mkazo upembuzi yakinifuwa mradi mkubwa wa Tele- Justice na kama ambavyoMheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria kupitia hotuba yake

Page 208: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

208

ya asubuhi alivyokuwa ameeleza, hivi sasa zoezi la upembuziyakinifu linakaribia kukamilika, na hivi sasa Kamati ya Ufundiiko katika Mikoa mbalimbali ya Kanda zetu ili kuweza kufanyautafiti, lakini pia kuweza kupata takwimu sahihi kabla yakusimika mitambo hiyo ambayo itasaidia sana kuendeshamashauri Mahakamani kwa njia ya mtandao.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na Tume ya KurekebishaSheria, tumetakiwa kukamilisha haraka taarifa ya mapitio yasheria zinazosimamia usuluhishi na utatuzi wa migogoro yaardhi pamoja na Sera ya Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji, kwanihivi sasa ni Wizara zaidi ya tatu zinashughulikia utatauzi wamigogoro ya ardhi. Tumepokea ushauri huu, na taarifakuhusiana na sheria husika imekwishakamilika na tunatarajiawakati wowote katika mwezi huu wa Mei mwaka huu 2013itawasilishwa Serikalini kwa ajili ya hatua zaidi.

Mheshimiwa Spika, tumetakiwa pia kupitia Tume yaHaki za Binadamu, wametakiwa kuongeza jitihada za kutoaelimu kwa Umma kuhusiana na uelewa na kuheshimu sheria;tumepokea ushauri huu, tutazingatia na kuufanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Serikali iipatie fedha zakutosha Tume ya Haki za Binadamu ili waweze kuchapa ripotizao za kila mwaka; ushauri huu pia tumeupokea, lakini hivisasa kutokana na ufinyu wa bajeti ndiyo maana wamekuwawakishindwa kutekeleza kuchapisha ripoti zao kwa wakati.Lakini tutakuwa tukiendelea kujenga hoja ili fedha zaidi ziwezekutolewa na waweze kuendana na wakati.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana Wakala, Ufilisi naUdhamini (RITA), wametakiwa kuharakisha Mpango wa Usajiliwa Watoto Walio na Umri wa Chini ya Miaka Mitano nakwamba mpango huu usambazwe katika Wilaya zote nchiniili kuhakikisha kuwa watoto wote walio chini ya umri wa miakamitano ambao hawajasajiliwa waweze kupata usajili.Tumepokea ushauri huu na ndiyo maana hata katika hotubaya Mheshimiwa Waziri pia, kwenye hili alilisemea kuwa tunaompango mahsusi kabisa na kwa mwaka huu, tutaanza naMikoa mitano; Mkoa wa Mbeya, Shinyanga, Simiyu, Geita

Page 209: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

209

pamoja na Mwanza, kwani katika ripoti ya TanzaniaDemographic Household Surveyor ya mwaka 2010 ndiyoambayo iliainishwa kwamba ina kiwango cha chini kabisacha usajili; na kama mnavyofahamu ni 6.2% ya watoto waliochini ya umri wa miaka miatano ndiyo wamesajiliwa na umrimwingine zaidi ya miaka sita kwenda juu ni 7.7% tu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunalitilia mkazo, naukiangalia katika bajeti hii, tumetenga Shilingi bilioni mojakuhakikisha mpango huu unatekelezwa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Serikali ihakikishe inaipatiafedha RITA kiasi cha Shilingi bilioni 17 ili zilipwe kwa ujenzi waRITA linalojengwa kwa ubia na NSSF ili kukwepa riba kubwaitakayojitokeza endapo fedha hizo zitachelewa kulipwa.Ushauri huu wa Kamati tunaupokea. Hivi sasa Wizara yaKatiba na Sheria inafanya mawasiliano na Hazina ili kuwezakufanikisha azma hii.

Kuhusiana na hoja mbalimbali za Mbunge mmoja,mmoja Mheshimiwa Ali Khamis Seif yeye alitaka kasi yakumaliza mashauri ya ardhi iongezwe. Napendakumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa Mahakamaimekuwa ikijitahidi sana na kuanzia mwaka 2012 ambapoMajaji kumi walioteuliwa kwa mara ya mwisho mahsusi kabisa,Mheshimiwa Jaji Mkuu aliwapangia waweze kusikilizamashauri ya ardhi.

Mwaka 2012 waliweza kumaliza mashauri 908 ya ardhina hivi sasa wapo wanakamilisha mashauri mengine 131 nakasi kwa kweli imekuwa ikienda vizuri sana. Kwa hiyo,nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mashauri hayayatapungua na ni lengo la Mahakama kumaliza kabisamashauri haya ya ardhi ambayo mengi yao yamekuwa niya muda mrefu.

Mheshimiwa Augustine Mrema - Mbunge wa Vunjo,ameomba tuharakishe kesi ya ardhi inayomhusisha AugustinoTemu na wenzake 768 kwamba kesi hii imekaa muda mrefu,imechukua takribani miaka 11. Ni kweli kesi hii imechukua

Page 210: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

210

muda mrefu, lakini sababu kubwa iliyopelekea ucheleweshajini maombi mbalimbali ambayo yalikuwa yakitolewa nawadaawa waliotaka kujiunga kwenye kesi hii na pingamizimbalimbali za awali ambazo zilikuwa zimeandikishwa. Tunaompango mkakati na tumeiweka kesi hii katika mkakatimaalum wa Mahakama wa kuondoa mashauri ya zamanina tunaamini itamalizika haraka iwezekanavyo. Tuombe tuushirikiano wa pande zote ili kesi hii iweze kumalizika mapema.

Mheshimiwa Silvestry Koka pamoja na MheshimiwaMustapha Akunaay wameitaka Serikali kupitia Mahakamaijitahidi kuongeza matumizi ya TEHAMA katika kurekodimashauri. Ushauri huu tunaupokea na hivi sasa tulishaanzaawamu ya kwanza ambapo mitambo ilisimikwa katikaMahakama ya Rufani, Mahakama Kuu pamoja na Divisionzote tatu za Mahakama Kuu; Division ya Biashara, Division yaArdhi pamoja na Division ya Kazi. Kama ambavyo nimeelezaawali kupitia mradi wa Tele-Justice ambao tunao, tunaaminiazma hii itaweza kuzingatiwa na tutaikamilisha.

Mheshimiwa Diana Chilolo ametoa rai tuangalieuwezekano wa kuongeza posho za Wazee wa Baraza. Ushaurihuu tunaupokea na ndiyo maana hata mwaka 2012 poshoya Wazee wa Baraza iliongezwa. Lakini pia tunaangaliauwezekano wa kuwapatia vivutio vingine, mfano hudumaya afya kupitia Mfuko wa Jamii ili na wenyewe wawezekupata huduma hii ya afya, kwani tunaamini kiwango hikicha fedha wanachopatiwa bado hakitoshi kulinganisha nakazi kubwa na nzuri wanayoifanya kwa ajili ya Mahakama.

Mheshimiwa Keissy, Mbunge wa Nkasi Kaskaziniameelezea mahitaji ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya yaNkasi. Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge maramoja tutapeleka Hakimu katika Mahakama ya Wilaya yaNkasi.

Mheshimiwa Raya Khamis pamoja na MheshimiwaEsther Matiko, wameongelea masuala ya rushwa iliyokokatika Mahakama. Suala hil i kwa kweli tumekuwatukiliongelea mara kwa mara katika Bunge hili, tunatambua

Page 211: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

211

wote kwamba rushwa ni kosa la jinai, lakini pia zipo kanuni zaMaadili za Mahakimu wetu na Majaji ambazo wanaongozwanazo, na zipo Kamati za Maadili za Mikoa na Wilaya ambazozimekuwa mara zote zikifanya kazi nzuri. Pindi itakapothibitikakuwa kuna tuhuma za rushwa na kwamba kweli wametendavitendo hivyo, Tume imekuwa ikiwachukulia hatua wotewaliohusika na vitendo hivyo.

Kwa hiyo, nitoe tu rai kwa Waheshimiwa Wabunge,endapo watakuwa na ushahidi watakapokuwa wanasikia,basi waweze kufikisha malalamiko haya katika Kamati zaMaadili ngazi ya Wilaya kwa Mahakimu wa Mahakama zaMwanzo, lakini katika Kamati za Madili za Mikoa kwaMahakimu wa Wilaya pamoja na Mahakama za HakimuMkazi. Mheshimiwa Eugine Mwaiposa, ameelezea tatizo lawananchi wengi kukosa Elimu ya Sheria za Msingi, jambolinalopelekea wananchi hao kudhulumiwa haki zao.

Mheshimiwa Spika, tunapokea ushauri huu,tunaelewa tatizo hili. Lakini Serikali imekuwa ikiweka mikakatimbalimbali ya kuongeza uelewa wa Sheria kwa wananchi.Tume ya Kurekebisha Sheria pamoja na Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali imekuwa ikiendesha vipindi mbalimbalikatika runinga zetu, katika redio lakini pia tumekuwa tukitoamakala katika magazeti.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja.

SPIKA: Mheshimiwa Mtoa Hoja!

WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA: Mheshimiwa Spika,kwanza nashukuru sana kwa kunipatia nafasi ili niwezekuhitimisha hoja yangu ambayo nimeileta kwako leo asubuhi.Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru kwa dhati kabisawachangiaji wote waliotoa maoni, ushauri na mapendekezombalimbali ambayo wangependa Wizara yangu iyachukueili kuboresha utendaji katika Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, napenda kutoa maoni ya jumlatu hasa kuhusu hotuba ya Kambi ya Upinzani. Siyo hotuba

Page 212: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

212

mbaya, isipokuwa tu, kwa ujumla, lugha iliyotumika, kidogohairidhishi. Unapodhani kwamba Tume ya Marekebisho yaKatiba ni sehemu ya ulaji na unawatazama Wana-Tume wale,unasema Mzee Warioba ndio mlaji mwenyewe, au SalimAhmed Salim ndio mlaji, kwa kweli unasema ah, labdaangesema jambo lingine au lugha nyingine, kwani hawawazee tunawaheshimu sana. Ni wazee ambao wanafanyakazi hii kwa kujitolea tu. Hawapati kitu chochote ukiondoalabda sifa itakayotokana na kazi nzuri ambayo watakuwawamefanya mwisho, kwa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini nasema pengineMheshimiwa alitumia lugha hii kwa kuteleza tu. Sidhani kamaalikusudia kuwafikiria wazee wale ni walaji. Nina uhakikakabisa hilo halimo kichwani mwake. Lakini nafikiri katikaujumla tu wa kudhani Serikali basi ni walaji, basi akadhaniana Tume ni walaji. Tume ile ni ya watu makini sana, hawaweziwakaruhusu aina yoyote ya ufisadi utokee ndani ya Tume ile.(Makofi)

La pili, majibu yangu pia yatazingatia hoja na maoniambayo yametolewa huko nyuma katika michangoiliyotolewa kwenye hotuba ya Waziri Mkuu na hotubanyingine, nitajaribu kutoa majibu, maana menginehayakuelezwa vizuri, nitachukua nafasi hii kuyaeleza hayoyaliyotolewa katika hotuba hizo zilizopita. Lakini kabla sijaanzakutoa majibu kwenye hotuba ya Kambi ya Upinzani, naombanitoe majibu ya taarifa ilitolewa leo hapa na Mwenyekiti auMwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bungeya Katiba, Sheria na Utawala.

Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Mwenyekiti waKamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge, zilitolewa hojambalimbali. Moja il ikuwa ni juu ya changamoto yaucheleweshaji wa mashauri Mahakamani, inayoendeleaambayo wanasema ni kikwazo katika mfumo wa utoaji hakihapa nchini.

Kwanza, niseme, hiyo ni changamoto kubwa naWizara na Mahakama tunatambua kwamba idadi ya

Page 213: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

213

mashauri ni mengi sana Mahakamani na kesi yakuyashughulikia haijawa nzuri ya kuridhisha. Sasa tumechukuahatua mbalimbali ya kupambana na changamoto hii.

Moja, tunajaribu kuhakiki takwimu za mashauri katikaMahakama zote nchini na tumepitia katika Mahakamakadhaa, tumegundua kuwa kesi nyingine zilizoko palezinaitwa kesi lakini siyo kesi, kwenye majalada hakuna kitu.Kwa hiyo, tunapitia na kuhakiki na tutagundua baadayekwamba tuna kesi ngapi ambazo kweli zipo na zinahitajikushughulikiwa. Takwimu tulizonazo sasa zinaonyesha kamatuna kesi nyingi, lakini kwa utafiti huu wa Masjala chacheambazo tayari wataalamu wa Mahakama wamezipitia,wamegundua kwamba jambo hili siyo kweli, lakini tunangojataarifa yao kamili, ndiyo tutajua kwa uhakika zaidi kuwa nikesi ngapi zipo na mlundikano huu ni wa kiasi gani hasa, natutazidi kutafuta njia za kuukabili.

La pili tulilofanya, tumejaribu kuongeza idadi yaMahakama kwenye Extended Jurisdiction. Kwa kipindi hikikifupi, tumeongeza kama thelathini hivi ili waweze kujaribukusaidia kupunguza kesi ambazo zipo katika Mahakama zetukuu. Sasa tunaandaa Program Maalum tunaita CleanupProgram kwa ajili ya kupunguza kesi za zamani ambazozimelundikana katika Mahakama zetu. Maandalizi hayayamekwishakamilika, tulikuwa tunangoja bajeti hii naninaomba Waheshimiwa Wabunge mtupitishie bajeti hii ilituanze na na Cleanup Program yetu ya kuondoa mashauriyaliyopo katika Mahakama zetu ambayo hayajashughulikiwakwa muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, nimewatolea leo asubuhi takwimummeziona, siyo nzuri na wala haziridhishi. Kwa hiyo,nawaomba mtupitishie bajeti ili tuanze progaramu hii tufanyekazi. Pia tutajaribu sana kadri inavyowezekana, kutumia njiambadala za kumaliza mashauri. Kuna WaheshimiwaWabunge wamezungumza hapa, nafikiri alikuwa niMheshimiwa Akunaay, nafikiri amezungumza kuhudu ADR nani muhimu sana. Jambo hili siyo la kupenda, ni jambo lakisheria liko ndani ya sheria na sisi tutalitekeleza ipasavyo.

Page 214: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

214

Mheshimiwa Spika, changamoto nyingineiliyozungumzwa, Waheshimiwa Wabunge walisema kuwakuna vitendo vya rushwa vimeendelea kujitokeza na hali hiiinasababisha wananchi kukosa imani na Mahakama kamachombo cha utoaji haki. Ushauri huu tumeupokea. Tatizo larushwa katika nchi yetu, tatizo la rushwa duniani ni tatizokubwa sana. Katika nchi yetu tunazo hatua mbalimbaliambazo tumezichukua kupambana na tatizo hili. Tunachochombo cha TAKUKURU ambacho kinajitahidi natunaendelea kukiongezea nguvu mwaka hadi mwaka iliwaweze kupambana na jambo hili.

Mheshimiwa Spika, lakini Waheshimiwa Wabunge piamtakubali kuwa vitendo vya rushwa vimepungua katikaMahakama zetu kutokana na juhudi za makusudi ambazotumezifanya sasa hivi katika kupambana na tatizo hili.

Mheshimiwa Spika, tatizo la ukosefu wa majengo yaMahakama za Mwanzo na niseme Mahakama zote; Serikalitunalitambua tatizo hili, tuna upungufu mkubwa sana wamajengo ya Mahakama. Huko nyuma wakati wa Ukoloni,majengo haya yalikuwa yanajengwa na Halmashauri. SasaHalmashauri hazijengi tena, na kwa kipindi fulani tukasemaMahakama ndiyo itajenga. Sasa Mahakama bajeti yakeimekuwa finyu kila mwaka, na hata mwaka huu tumeomba,lakini bado ni finyu. Kwa hiyo, tutachukua hatua za makusudikupambana na jambo hili. Tumeeleza katika mikakati yetukwamba tunatakiwa kujenga Mahakama na tutajengaMahakama za Mikoa; kwanza High Courts katika Mikoaminne, halafu tutajenga Mahakama za Mwanzo naMahakama za Kati kwa kadiri uwezo utakavyoruhusu.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilizungumzia pia suala lamachapisho ya ripoti za maamuzi ya Mahakama, yaaniTanzania Law Reports kuanzia mwaka 1998 mpaka mwaka2006 kwa ajili ya Mawakili na kwa ajili ya Umma. Ni kweli,taarifa hizi hazipatikani, Mawakili wanapata taabu sanawakienda Mahakamani, sana sana akiwa na Hakimu au Jajirafiki, ndio anaweza akatoa kopi pale kwake, lakinihawajapata nafasi ya kuzinunua.

Page 215: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

215

Mheshimiwa Spika, sasa jambo hili, tunasemaMahakama inatengeneza kwa ajili ya watumishi wake. Badohatujaweka utaratibu ni jinsi gani tutazipata hizi. Nimeongeana wenzangu kwa kirefu sana, hizi Law Reports tuwaachiePrivate Sector wazitengeneze, waziuze, tumeona privatesector yetu kidogo kwa upande huu iko dhoofu, ni weak. Kwahiyo, tunadhani labda hapo baadaye Wizara itakaa tenana kujipima ubavu na kuona kama Wizara inaweza ika-undertake jukumu hili na baadaye basi vitabu hivi vikauzwakwa watu wote ambao watavihitaji ili kuvitumia.

Mheshimiwa Spika, issue nyingine iliyoletwa mbeleyetu ni kuhusu Wasaidizi wa Sheria wa Majaji kwambawanafanya kazi bila kuapishwa kama Maafisa waMahakama (Judicial Officers) toka walipoajiriwa. Sasatumeliona hili. Vijana hawa wanafanya kazi za kuwasaidiaMajaji, lakini katika kufanya kazi hiyo, wanakutana na mambomengi, wanaona mambo mengi mazito, na kwa kweliwangepashwa waapishwe ili waweze kutunza siri za mambohayo wanayoyaona. Baada ya kugundua hilo, tunasemakwamba kwa sasa hivi Mahakama ina jumla ya Wasaidizi waMajaji 70 na wamegawanywa kwenye Vituo kama 13 hivi.

Mheshimiwa Spika, Tume ya Utumishi il ishatoamaagizo kwamba watu hawa waapishwe. Kwa hiyo, taratibusasa hivi zimekwishaandaliwa na vijana hawa wataapishwana Jaji Kiongozi, atakwenda kuwafuata katika Vituo hivyo13, atawaapisha mmoja baada ya mwingine na tutakuwatumeondokana na tatizo hil i, tukiamini sasa watuwataheshimu viapo vyao na watafanya kazi kwa uaminifuzaidi.

Mheshimiwa Spika, Kamati pia ilituelekeza kwambaMahakama ya Tanzania ishughulikie ununuzi wa vifaa vyakisasa kama vile kompyuta kuliko kutumia typewriters na piakununua samani za Ofisi zinazotengenezwa nchini kwa ajiliya Mahakama zote Tanzania. Ushauri huu tumeupokea, niushauri mzuri. Hata hivyo, ipo changamoto ya Mahakamanyingi, kama mnavyofahamu Waheshimiwa Wabungetunaotoka Vijijini kule umeme hakuna, kwa hiyo, katika

Page 216: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

216

Mahakama za Mwanzo zile, ukisema sasa utapelekakompyuta, utategemea kuweka solar na hiyo solar yenyeweinabidi nayo iingie katika bajeti ya ujenzi wa hiyo Mahakama.Lakini hili ni jambo ambalo tunaweza kulitekeleza katikasehemu zile ambapo umeme unapatikana kwa urahisi nahakuna matatizo ya nishati hiyo.

Mheshimiwa Spika, Kamati pia ili-raise suala la kusemakwamba kitendo cha Serikali kutokutoa fedha zilizokuwazimetengwa mwaka wa fedha 2012/2013 kimekwamishamiradi ya ujenzi wa Mahakama za Mwanzo za Kawe, Bunda,Mangaka, Gairo, Bariadi, Lukuledi na Mkomazi. Kitendo hichokishughulikiwe kwa fedha hizo kutolewa mara moja.

Mheshimiwa Spika, napenda niamini kwa ahadiambayo tunaendelea kupewa na Wizara ya Fedha kwambamwaka bado haujakwisha; “ninyi kwanini mnakuwa hivyo?Subirini ndani ya mwaka huu tutatekeleza ahadi zetu.” Kwahiyo, nasi tunasubiri na tunaamini tukipata pesa hizo angalaututakwenda haraka haraka, tuwaweke ma-contractorwafanye kazi kwa sababu pesa hizi hazitakuwa nyingi,kusema tutashindwa kuzitumia kwa kipindi kifupi Ni suala tula kuweka watu waanze kazi. Kwa hiyo, tunategemea na sisitunasubiri kama mnavyosubiri Waheshimiwa Wabunge.Tuendelee kusubiri, na Hazina watatekeleza ahadi yao.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mahakama ya Tanzaniaishughulikie upatikanaji wa fedha za kujenga majengo yaMahakama Kuu katika Mikoa ya Kigoma, Mara, Lindi,Morogoro, Singida, Manyara, Katavi, Njombe, Simiyu naPwani. Kati ya Mikoa 26 ya Tanzania Bara, kuna MahakamaKuu katika Mikoa 13 tu. Mpango wa Serikali ni kuwa naMahakama Kuu katika kila Mkoa.

Mheshimiwa Spika, ili kutimiza dhamira hii, napendakuliarifu Bunge lako Tukufu, kwamba mwaka ujao wa fedha,yaani mwaka huu mkipitisha bajeti hii, na nimesema kwenyebajeti yangu kwamba Wizara yangu itakamilisha ujenzi waMahakama Kuu ya Shinyanga na kuanza kujenga

Page 217: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

217

Mahakama Kuu katika Mikoa ya Singida, Kigoma, Mara, Lindi,Manyara na Morogoro. Tutaendelea na ujenzi katika Mikoailiyobaki kwa awamu.

Mheshimiwa Spika, hili ni jambo ambalo Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania - Mheshimiwa Dkt. JakayaMrisho Kikwete amelisisitiza sana. Amesema katika miakamiwili ijayo, ni lazima tumalize ujenzi wa Mahakama Kuu katikaKanda zote na katika Mikoa yote. Kwa hiyo, sisi tutafuatiliana wenzetu wa Hazina nina hakika wataendelea kutuelewa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Mahakama ya Tanzaniaishughulikie upatikanaji wa Watumishi wa fani mbalimbaliwanaofikia 3,455 ili kuweza kutoa huduma kwa ufanisi; ushaurihuu umepokelewa. Mahakama tayari imepewa kibali chakuziba nafasi 139 zilizoachwa wazi, na Serikali itaendeleakuziba pengo hilo kadri uwezo wa kifedhautakavyoongezeka. Mawasiliano na Ofisi ya Rais, Menejimentiya Utumishi wa Umma yanaendelea.

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine iliyotolewa naKamati, inasema kwamba Mahakama ya Tanzaniaishughulikie namna bora zaidi ya upimaji wa utendaji kazi waMahakimu na Majaji ili kuongeza ufanisi wa utendaji waMahakama.

Nakubaliana na suala hili sana na toka awamu yakwanza nilipokuwa Waziri wa Katiba na Sheria mpaka awamuhii, jambo hil i l ipo moyoni mwangu na nimekuwaninalizungumza sana na wenzangu wa Mahakama nawenzangu bahati nzuri wamelikubali. Sasa wameandaautaratibu ambao utakuwa na uwezo wa kupima utendaji kaziwa kila Jaji anafanya kazi kiasi gani. Wale wanaosikiliza kesikumi kwa mwaka na wale wanaosikiliza kesi 100 kwa mwaka,sasa atajulikana, na hatua zitachukuliwa kwa yule ambayehatekelezi wajibu wake. Haya wamefanya wenyewe,wamekubaliana, sasa kilichobaki ni utekelezaji.

Mheshimiwa Spika, kwangu kama Kiongozi, nikutizama na kusukuma na kuhakikisha jambo hili linafanyika

Page 218: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

218

na kutekelezwa. Kwa sababu ni muhimu tujue, haiwezekaniMajaji ninyi wote mnapata mshahara sawa, wote mnapatamarupurupu sawa, halafu mmoja anafanya kazi kwa mwakaanaamua kesi 200, mwingine kwa mwaka anaamua kesi 10au hata chini ya hapo. Haiwezekani! Hatuwezi kufanya kazinamna hiyo! Ni lazima tuwe na njia ya kupima ni kitu ganikinafanyika. Wazungu wanasema, “what you can’t measure,does not exist. Kwa hiyo, ukishindwa kupima, ina maanahakuna. Kwa hiyo, ni lazima tuwe na uwezo wa kupima natutaendelea kuwasisitizia wenzetu ili waweze kufanya jambohili.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na suala la Mahakamakwamba itoe motisha kwa Mahakimu wanaofanya kazi katikamazingira magumu. Motisha hapa nina hakikainayozungumziwa labda ni pesa au mikopo mbalimbali nakadhalika. Sisi tunasema, ni Sera ya Serikali kutoa motisha kwawafanyakazi wote pamoja na Mahakimu wanaofanya kazikatika mazingira magumu. Lakini ushauri huu tunaupokea naSerikali imeanza kutoa motisha kwa wafanyakazi natutaendelea kufanya jambo hili.

Mheshimiwa Spika, Kamati pia ilikuwa na maonikuhusu Wizara ya Katiba na Sheria. Kamati inasema: “Serikaliifuatilie kwa makini utendaji kazi wa Tume ya Mabidiliko yaKatiba bila kuathiri uhuru wa Tume ili kuwezesha nchi kupataKatiba mpya kwa wakati.” Ushauri huu umepokelewa naunatekelezwa bila ya kuathiri uhuru wa Tume. Serikali kwamuda wote toka Tume hii imeundwa, imekuwa na sera yaEyes On, Hands Off. Tunatazama, tunawa-facilitate lakinihatuwaingilii.

Mheshimiwa Spika, mimi mwenyewe ni mfano,nimekwenda Tume kutembea kuangalia ni nini kinaendelea.Lakini siyo kukagua kazi, wala kuuliza mnafanya nini, aumtafanya nini? Sizungumzi nao, hawazungumzi na mimi namimi sitaki, kwa sababu mambo mengine usipoyajua ni borazaidi kuliko ukiyajua. Mimi nikiyajua, pengine ni matamu sana,nitayasema. Nikiyasema nitakuwa nimeshaharibu, afadhalinisiyajue na siyajui, ninashukuru. Kwa hiyo, nawapongeza

Page 219: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

219

Tume, wameendelea na msimamo wao wa kufanya kazikama Independent Board na ndiyo kitu pekeekinachowaletea heshima na kitakachoendelea kuwaleteaheshima katika kazi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine tulishauriwa kwambaSerikali ishughulikie utoaji wa fedha zinazotengwa kwamatumizi ya Wizara na kutolewa kwa wakati. Ushauri huuutazingatiwa. Pesa zinapotolewa, sisi tutazitumia kamatulivyopanga. Zisipotolewa, tunasikitika kama wengine.Mheshimiwa Spika, tulishauriwa kwamba Serikali iwekekipaumbele katika kutekeleza miradi ya maendeleo nakutenga fedha za ndani kwa ajili hiyo kuliko kutegemea fedhaza nje. Ushauri huu ni mzuri na mimi ninauzingatia sana.Ukitegemea mambo ya nje, huwezi kuwa na uhakika kamazitakuja, ama zitakuja lini. Ukiwa nazo mwenyewe ndani, basiuna hakika zaidi ya kufanya mambo yako kama ulivyopanga.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Tume ya Mabadiliko yaKatiba, Kamati ya Sheria ilikuwa na mambo yafuatayo;wanasema Bajeti ya Bunge la Katiba ifahamike mapema nakuletwa Bungeni. Hili nimeulizwa hata nilipoingia hapa,Mheshimiwa Machali ameniandikia ki-note anasemazungumza kuhusu bajeti ya Bunge la Katiba.

Mheshimiwa Spika, kwa utaratibu tuliojiwekea, bajetiya kuendesha Bunge la Katiba haiko Wizarani kwangu. Bajetihii itasimamiwa na Ofisi ya Bunge. Kwa hiyo, pesa zake sasahivi ziko kwenye Consolidated Fund, itakapofika wakatiwanazihitaji, watazitumia. Vivyo hivyo, kwenye uchaguzi, ilereferendum itakayofanyika, fedha zile haziko Ofisini kwangu,wala Ofisi ya Tume. Zitakuwepo kwenye Tume ya Uchaguziambayo ndiyo itasimamia hiyo referendum na hizo zenyewepia nazo ziko kwenye Consolidated Fund zitakapohitajikazitatolewa. Kwa hiyo, usipoziona kwenye bajeti hii ,ni kwambahazipaswi kuwepo humu na hazipo.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilikuwa na neno moja lakusema kuhusu Tume. Walisema Tume ya Utumishi waMahakama iendeleze juhudi za kuelimisha wananchi kuhusu

Page 220: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

220

uwepo wa Tume na majukumu yake ili kuwawezeshawananchi kutoa malalamiko yao juu ya ukiukwaji wa maadiliya Utumishi wa Mahakama. Nami nasema, Tume inaupokeaushauri huo na sisi tutaendelea kuwaasa waendeleekuzingatia ushauri huu mzuri.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuzungumza hayo,kabla zijakwenda kwenye hoja ya Mbunge mmoja mmoja,nirudi kwenye hoja ya Mheshimiwa wa Kambi ya Upinzanialiyoitoa hapa Bungeni asubuhi hii. Kama wengine, hotubahii imechelewa sana kutufikia, kwa hiyo, nasi tumeipatamchana ule, tumekwenda kuisoma kadri tulivyowezakuisoma. Tutajaribu kujibu hoja zote au nyingi zilizoletwa katikahotuba ile.

Bahati nzuri hotuba hii kuanzia ukurasa wa kwanzampaka 30 na hii ni kati ya kurasa 42 imezungumza kuhusuTume ya Katiba Mpya, na kurasa zilizobaki, imezungumziakuhusu haki za binadamu, lakini hususan kesi ya MarehemuMwangosi. Kwa hiyo, ni mambo mawili ya msingi, naminitajaribu kwenda nayo kama yalivyokuja.

Mheshimiwa Spika, niseme mapema kabisa kwambaumetumika muda mwingi sana na kurasa nyingi katika hotubaya Kambi ya Upinzani, ukurasa wa 14 - 17 ulikuwaukimzungumzia mtu anayeitwa Beatus Kipea kwambaameunguliwa katika Orodha ya Wajumbe waliochaguliwa,kutoka Kata ya Sembetini na kwamba imefanywa hivyo kwasababu yeye siyo mwana-CCM.

Kwanza niseme kwamba taarifa hii siyo sahihi. Sitakikusema ni ya uwongo, lakini nasema siyo sahihi. Aliyempataarifa hii au aliyeandika taarifa hii, hakumwambia ukweli,kwa hiyo, naye akafanya jambo ambalo siyo sahihi. BwanaBeatus ni Mjumbe halali. Hadi kufikia tarehe 25 Mwezi huuwa Mei, taarifa nilizonazo mimi, Bwana huyu ni Mjumbe halali,na bado ni Mjumbe, na katika matangazo ya Wajumbe wotewatakaokwenda kwenye Mabaraza ya Kata, jina lake limona litatangazwa.

Page 221: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

221

Mheshimiwa Spika, nashangaa kuambiwa kwambakafutwa, sijui kwa sababu gani. Ndiyo maana nasema jambohili siyo sahihi. Taarifa zangu hizi nimeletewa leo. Sina Kawaidaya Kuongea na Tume, lakini kwa hil i nimeziomba.Wakaniambia Mratibu wa Tume ameleta taarifa rasmikwamba Bwana huyo yumo na katika majinayatakayotolewa atakuwemo. Sasa inapoandikwa hapazimetumika page 14, 15, 16, na 17 kuzungumzia jamboambalo siyo sahihi.

Mheshimiwa Spika, unataka kujiuliza ukurasa wa 1 -30 umesema nini ambacho ni sahihi? Maana page hizi tatuzote siyo sahihi. Hizi nyingine zimesema nini cha sahihi? Lakinitutakwenda nazo taratibu, nami nitajaribu kujibu hoja kwahoja. Lakini hili suala la Bwana Beatus siyo la kweli, ni lauwongo. Wananchi mlijue hivyo! Bwana Beatus kama yupomwenyewe anaweza kuthibitisha, maana hili limethibitishwana Viongozi wa Tume, wanasema yumo katika majina yawale watu wa Mabaraza na atatangazwa rasmi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja ya kwanza ilikuwa ni uhalaliwa malipo ya Shilingi bilioni 12.1 kwa ajili ya posho ya vikaokwa ajili ya Wajumbe 34 wa Tume. Wajumbe wa Tumehawapo 34, Wajumbe wa Tume wapo 32. Wapo Wajumbe30, halafu wana Mwenyekiti wao na Makamu wake.Waliowekwa ngazi sawa na Wajumbe hawa, ni Katibu naNaibu wake, unapata watu 34. Lakini Wajumbe wa Tumehawapo 34. Kwa hiyo, kama ilitolewa picha hiyo, basi pichahiyo siyo sahihi ni picha potofu. Wajumbe wenyewe pamojana Mwenyekiti wao na Makamu ni 32, halafu wanaongezwajuu yao ambao wako katika level sawa, kwa maana yakulipwa posho sawa, ni Katibu na Naibu wake. Kwa hiyowanakuwa watu 34 katika ngazi sawa.

Sasa kama waliitwa wote ni Makamishna, basi nimakosa kwa sababu wote siyo Makamishna, ila sasa poshohizi ndiyo zile ambazo zimepangwa na kukubaliwa kimsingi,kwamba watalipwa posho hii. Zimekubalika na Sheria zaFedha na sisi wenyewe tumepitisha bajeti ya kwanza hivyohivyo, bajeti hii inaendelea tena, sasa hata sijui,

Page 222: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

222

hazijaongezwa! Ni posho zile zile tulizokubali last year na ndiyohizo hizo wanazopewa mwaka huu. Sasa kinachogomba ninini?

SPIKA: Naomba Waziri ujibu, hakuna kusikiliza mtuambaye hahusiki na maelezo haya. (Makofi/Kicheko)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, kwahiyo, ukweli ndiyo huo. Posho hizi ni za kuwalipa viongozi hawana viongozi hawa walilipwa posho za namna hii mwaka 2012,wataendelea kulipwa hivyo mpaka watakapomaliza kaziyao. Kama itakuwa ni Mwezi Aprili ama baadaye, basitutaona. Lakini tumeweka bajeti ya mwaka mzima, maanabajeti ni makadirio. Zitakapohitajika, zitalipwa; zisipohitajikahazilipwi.

Kuhusu uhalali wa kuwa na Wajumbe 34 badala ya30 kulingana na sheria hili ndiyo nimelieleza. Kwa kweli hakunaWajumbe 34, wapo Wajumbe 32, ukijumlisha Mwenyekiti naMakamu wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uhalali wa maombi ya fedhaza matumizi ya Shilingi bilioni 33.94 zilizoombwa kwa mwakawa fedha 2013/2014. Kama mtakumbuka na MheshimiwaPindi Chana ametukumbusha hapa, mwaka 2012 tulipoombakwenye Kamati Shilingi bilioni 40, zikapunguzwa zikafika Shilingibilioni 33. Mwaka huu ukomo wa bajeti tuliyopewa na watuwa Hazina na Mipango wakasema hizo hizo, na mtaumianazo, hizo hizo. Lakini sasa kwa kupewa hizi, kuna mamboyataathirika. Kubwa ni haya Mabaraza ya Kata ya Katiba.Kwa sababu vichwani mwetu tulikuwa tunafikiria tufanye sikunne, lakini haiwezekani. Kwa hiyo, tutafanya siku mbili badalayake, ili angalau kuwa ndani ya bajeti hii ya Shilingi bilioni33.9.

Mheshimiwa Spika, tuliomba zaidi, lakini tukaambiwaukomo ni huo huo. Kwa hiyo, sasa inabidi tuji-adjust. Kwa hiyo,tunaathirika na tutaathirika kiasi kwa sababu hatuna pesahizi tena za kuweza kufanya Mabaraza. Tungeweza kufanyaMabaraza siku nne labda, lakini inaongeza pesa nyingi.

Page 223: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

223

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la uhalali wamatumizi ya fedha wakati wa Bunge Maalum la Katiba. Kwamujibu wa Sheria, mnafahamu kwamba Mwenyekiti wa Tumendio atawasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalumla Katiba. Lakini Mwenyekiti wa Tume, anaweza kutoaufafanuzi unaohitajika wakati wa majadiliano kwenye BungeMaalum la Katiba. Kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu tajwa,Tume imetenga fedha hizo kwa ajili ya kuwalipa poshoWajumbe wa Tume na Sekretarieti wakati wa Bunge Maalumla Katiba, kuwezesha kuwasilisha Rasimu ya Katiba na kutoaufafanuzi kuhusu rasimu hiyo. Hivyo basi, siyo sahihi kusemakuwa Mwenyekiti akishawasilisha Rasimu ya Katiba, anakuwahana kazi nyingine ya kufanya kwamba, yeye sasa ni fanctusofisio.

Mheshimiwa Spika, process hii ya kuwasilisha, kwelianakwenda mle ndani, labda atakwenda peke yake, lakinianabebwa na wenzake. Wakati wote hii Tume ndiyoinayomsapoti. Iko naye, itamwacha siku ile wakishaambiwahaya, sasa referendum imefanyika na Katibaimeshapatikana, hatahitajika tena. Tutawafukuza siku hiyohiyo kweli! Kama ndiyo itakuwa tarehe 26 mwezi wa Nne,basi wajue kazi yao inakwisha tarehe 26 mwezi wa Nnemwakani. Kama haitakuwa siku hiyo, itakuwa siku hiyoambapo watakuwa wamekamilisha kazi hii. Hatuwezikuwalipa kama hawaendi kufanya kazi. Huo ndiyo utaratibuwetu! Hawawezi kulipwa kama hawaendi kufanya kazi. Kamanilivyosema mwanzo, hii siyo Tume ya Ulaji, hii ni ya kufanyakazi. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kuhusu uhalali wa matumizi yafedha wakati wa kutoa elimu ya uraia kabla ya kura za maoni;kwa mujibu wa Kifungu 33 (2), Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,Sura ya 83; Tume inawajibika kuhamasisha na kutoa elimukwa wananchi kuhusu Katiba inayopendekezwa kabla yakura ya maoni. Kwa msingi huo, Wajumbe wa Tume naSekretarieti wote watalazimika kuzunguka nchi nzima kutoaelimu katika kipindi hicho. Fedha zilizotengwa ni hizo, sasasijui hata kama zitatosha. Wataizunguka nchi hii yote kujaribukuwaeleza wananchi kwamba, jamani, Katiba ile ambayo

Page 224: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

224

tumezungukanayo sasa ni hiyo, itoleeni maamuzi; kamamnaitaka semeni ndiyo, kama hamuitaki semeni siyo. Basi.

Mheshimiwa Spika, lakini ni lazima wazunguke.Watafanya kazi hiyo na yale matangazo ya redio namagazeti na television na runinga, yataendelea. Lazimayaendelee. Sasa pesa hizi sina hata uhakika kama zitatosha,maana mwaka huu bajeti yenyewe imefinywa sana. Uhalaliupo kwa sababu kazi hii ni ya Tume. Nina hakika Vyamavitasimama, vitakwenda kuhamasisha wananchi wake kwanguvu sana kwenda kusema jambo hili. As it is, wenginewameshaanza, Mheshimiwa nimekuona; nilifurahi kweli,Katiba haipatikani wapi? Itapatikana wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Lissu anaifahamu. Kwa hiyo, kampenizitakuwepo na zinaendelea, zimeshaanza kama hivyo, bado!Mtaendelea kufanya na sisi na Chama cha Mapinduzikitafanya, lakini Tume ndiyo wenye kazi hii na hicho tunaingiliakazi ya Tume, lakini tuna wajibu wa kuwaelimisha wananchiwetu waelewe. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, uhalali wa matumizi ya fedha kwaajili ya chakula maalum kwa Wajumbe wa Sekretarietiwatakaokuwa wamepata UKIMWI, duh. Katika utungaji wabajeti kuna cluster tano. Cluster ya kwanza kabisa, inawekwainasema kuhudumia watumishi ambao wana UKIMWI, maanahili ni suala mtambuka kwa jamii. Sasa haina maana kwambaWana-Tume wale wana UKIMWI au Sekretarieti, hatujui, mimisijui. Lakini tunaweka bajeti, endapo wapo, watatumia iliwaweze kutufanyia kazi vizuri. Kwenye Wizara yangu mimiwapo na tunayo hiyo bajeti na tunawahudumia ipasavyokabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kila Wizara hapaukiangalia, kila Wizara ina bajeti hiyo kwa sababi, ni clustermojawapo katika zile cluster 5 za bajeti. Ni lazima iwekwe.Hawa ni watumishi, tunataka watuhudumie, lakini wanahitajihudumja ya Serikali na Serikali inaweka. Kwenye Tume, sijuikama wapo! Lakini bajeti tunaiweka, kama wapo watatumia.

Page 225: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

225

Hatuwezi kuyatangaza haya mambo hadharani, hata kamawangekuwepo, siwezi nikakwambia wapo watano au sita.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na suala kuhusu Tumekwmaba haikuweka utaratibu wowote wa maana wa kutoaelimu kwa wananchi juu ya masuala yote yanayohusu Katiba.Hili lilizungumzwa, sasa dah, hata sijui nisemeje. Lakini nisemeyafuatayo:-

Mheshimwa Spika, katika suala la kutoa elimu kwaumma kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, Tume iliandaaprogramu mbalimbali za elimu na tulitumia vyombo vyahabari kama redio, runinga na magazeti. Tulitoa machapishombalimbali yakiwemo Katiba ya Jamhuri ya Muunganoyenyewe, kwa lugha nyepesi na kwa lugha yake ilivyo, Sheriayenyewe ya Mabadiliko ya Katiba kwa lugha nyepesi na kwalugha yake ilivyokuwa, Sheria ya Mabadiliko ya Katibayenyewe, hadidu za rejea za Tume, kazi za Tume, maswaliyanayoulizwa mara kwa mara, yaani frequently askedquestions, tulichapisha tukagawa.

Mheshimiwa Spika, machapisho hayo pamoja naKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar,yalisambazwa nchi nzima kabla ya Tume haijafika kukusanyamaoni ya wananchi. Elimu kwa Umma ilikuwa inatolewa naWajumbe wa Tume kila walipofika kwenda kukusanya maoni.

Mheshimiwa Spika, lilikuja lingine, wanasema mudauliotolewa pia haukutosha, watu walipewa dakika tano-tanotu kuzungumza.

Mheshimiwa Spika, lakini nasema, pamoja na hizodakika tano, watu walipewa muda wa kuandika. Hili la watukusema sample ni ndogo, kwa kweli, siyo sawa. Hakunasample kubwa iliyoweza kutumika kama hii ya kwetu,nitakwambia namna gani. Pamoja na watu wale ambaomnasema walionekana wakapigwa picha, wakatoa;tulikuwa na makundi mbalimbali. Chama cha Mapinduzichenye Wanachama wasiopungua 6,000,000 kilitoa maonikikiwakilisha wanachama wale 6,000,000. Chama cha

Page 226: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

226

CHADEMA, kilikwenda kutoa maoni yake, sina uhakika wanawanachama wangapi waliowawakilisha kwenye maoniyale?

MBUNGE FULANI: Milioni kumi.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Milioni kumi.

WABUNGE FULANI: Aaaah!

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Kwa hiyo, hapo pekeyake kuna wananchi milioni 16, ambao maoni yaoyametolewa. Sasa unaposema sample ni ndogo, ulitaka watumilioni 40 wote waweze kutoa? Maana wengine ni watotowadogo, hawawezi kutoa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa Vyama hivyo viwilipeke yake, you have one of the largest samples. Acha Vyamavingine. CUF, sitaki kuuliza, mna wanachama wangapi, lakinina ninyi mlitoa maoni kwa niaba ya wanachama wenu.

MBUNGE FULANI: Milioni 11. (Kicheko)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Milioni 11! Sasa unamilioni 11 wa CUF, milioni 10 wa CHADEMA, milioni sita waCCM, una watu zaidi ya milioni 26 wametoa maoni. Ukisemasample ni ndogo, siyo sahihi. Ni sample kubwa haijapatakutokea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Tume iliweka utaratibu tofauti nawa kibaguzi katika hatua za kuunda Mabaraza. Hil ilimezungumzwa sana.

Mheshimiwa Spika, lakini niseme kwa mujibu waKifungu 17 (8), Tume imepewa mamlaka ya kubuni na kutumiataratibu tofauti katika utekelezaji wa majukumu yake katikapande mbili za Muungano. Siyo kweli kusema kwamba,wakati wa kukusanya maoni Tume ilikuwa na utaratibuunaofanana na pande zote za Muungano. Kwa upande waMabaraza ya Katiba, kulikuwa na tofauti katika ngazi za

Page 227: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

227

uchaguzi wa Wajumbe wa Mabaraza hayo. Kwa upande waTanzania Bara, ngazi ya msingi ilikuwa ni Kata, wakati kwaupande wa Zanzibar, ilikuwa ni Shehia.

Mheshimiwa Spika, katika chaguzi hizi, Tume ilikuwainatumia mifumo iliyopo kisheria ya Uchaguzi katika ngazi zaMamlaka ya Serikali za Mitaa. Kwa Zanzibar, hakuna mfumowa kiuchaguzi katika ngazi ya Wadi, ambayo ndiyoinayofanana na Kata kwa Tanzania Bara. Kwa Tanzania Bara,kuna mfumo wa uchaguzi katika ngazi ya Kijiji na ngazi yaMtaa. Pia Kamati za Maendeleo za Kata zimepewa mamlakaya kufanya maamuzi mbalimbali ya kimaendeleo na chaguziza Wajumbe wa Kamati mbalimbali katika ngazi ya Kata.

Mheshimiwa Spika, tusingeweza kufanya uchaguzikatika ngazi za Kata, haiwezekani! Kata ni kubwa mno!Hakuna Kikao cha Uchaguzi wa Kata, lakini wa Kijiji kipo nandiko tulikofanya. Tusingeweza kufanya kwenye Kata, hatakidogo! Uchaguzi huo sijui ungekuwaje? Wakazi wote waKata, isingewezekana. Kata zote, isingewezekana! Kwa hiyo,tukafanya kwenye Kijiji tukaja kwenye Kata. Kwenye Kata,tukatumia mfumo tu uliokuwepo wa Serikali za Mitaa, wakupata Wawakilishi wa wanne wa wananchi. Najuazimetokea kasoro sehemu mbalimbali, zipo na hizo Tumewenyewe wanajua jinsi ya kufanya.

Mheshimiwa Spika, kuna Kata imetokea imepelekawatu wa wanne, bahati mbaya watu watatu katika wanne,wale wanatoka nyumba moja. Baba mwenyewe Diwani, mkewake na mwanawe. Sasa Uwakilishi wa namna hiyo, Tumeinajua. Ikasema, hapana, hili tutaliangalia vizuri jamani.Hamwezi mkapata watu kutoka kwenye vijiji vinne, badalayake mnapata watu kutoka nyumba moja? Kwa hiyo, yapomatatizo madogo madogo. Lakini kimsingi utaratibuumekamilika na kama nil ivyosema asubuhi,tumekwishawapata Wajumbe wote katika Mikoa yoteambayo inahusika.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Mabaraza ya Katiba yaWilaya kutawaliwa na Wajumbe wengi kutoka CCM na

Page 228: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

228

kuondolewa Wajumbe ambao sio wa CCM, na hasa waCHADEMA. Kama nilivyoeleza, jambo hili siyo kweli, na misingiyake chaguzi hizi haikuwa Vyama. Uwakilishi katika Mabarazahaya, siyo wa Vyama. Hauna msingi wa Vyama. Vyamavimeingilia sana mchakato huu na vimekaribia kuuvuruga.Lakini uchaguzi huu siyo wa Vyama.

Misingi ya Mabaraza haya siyo Vyama, ni Wawakilishiwa wananchi wenyewe. Wakitokea wote ni CCM, basi labdani kwa sababu hapo mahali wengi ni CCM. Wakitokea woteni CHADEMA, basi labda hapo mahala wengi ni CHADEMA,lakini hakuna mfumo uliotungwa eti wakachaguliwewanachama fulani, hapana. Chama siyo sifa mojawapo yakuwa Mjumbe wa Mabaraza haya. Uwanachama waChama chochote kile, siyo sifa mojawapo ya kuwa Mjumbewa Mabaraza haya. Uwakilishi wake ulikuwa mzee mmoja,mwanamke mmoja, kijana mmoja na mtu mwingine mmoja,basi.

Mheshimiwa Spika, sasa mambo ya Vyama haya niuvurugaji. Nami ninavionya, kama vyama vimeingiliamchakato huu, vinaharibu, viache. Havihusiki na jambo hili!Siyo lao! Hili ni jambo la Tume, Tume inatafuta maoni yawananchi na maoni hayo hayategemei wewe unatokaChama gani. Ila wewe katika Kijiji, chako unawakilisha, watuwamekupenda kiasi gani, basi.

Mheshimiwa Spika, kutokuwa mwanachama au kuwamwanachama, siyo sifa mojawapo ya kuwa Mjumbe waBaraza. Hiyo ningependa ieleweke mapema na kwa hiyo,waliochaguliwa wamechaguliwa kwa sifa zao ambazozimetajwa katika ule Mwongozo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hil i la bwana Beatus,nimelizungumzia ipasavyo. Nafikiri limeeleweka.

Mheshimiwa Spika, Tume ya Mabadiliko ya Katiba,imepata Hati ya Muungano na kuitumia kama ilivyoelekezwana Sheria? Hili ni swali linaulizwa na Mheshimiwa SaidSuleiman, Mbunge wa Mtambwe.

Page 229: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

229

Mheshimiwa Spika, sina hakika Sheria ni Kifungu ganikimeelekeza jambo hili, sikumbuki. Sikumbuki na MwanasheriaMkuu hajanikumbusha kama kipo Kifungu kinachosemakwamba, lazima ipatikane Hati ya Muungano ndiyo Tume hiiifanye kazi. Kwa hiyo, jambo hil i, labda penginehatukumwelewa vizuri. Lakini kwa sababu yupo na baadayeatapata nafasi ya kusimama, anaweza akaliuliza. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, wananchi wametoa maoni mengiya Tume na Tume itayazingatia. Mimi nataka niwahakikishiekitu kimoja tu kwamba, Tume hii imepokea na itaendeleakupokea maoni kutoka kwa watu mbalimbali, hasa hayaMabaraza ya Kata, yatatoa maoni yao, lakini Mabarazamengine pia yale ambayo nimesema yanaweza kujiunda,kwa aina yoyote ile ya Vyama, ya Dini, ya NGOs, ya Asasimbalimbali, wajiunde, ili watoe maoni. Ninachowahakikishiamimi ni kwamba, Tume itayapokea maoni yote na itayafanyiakazi. Kitakachofanyiwa kazi ni uzito wa hoja inayotolewa.

Mheshimiwa Spika, Tume ile ndiyo maana ina watuwenye busara, watu wazito, watakaa wataangalia hoja.Suala la kusema watu wengi wamesema hivi, kwa hiyo, hivindiyo iwe, pengine wingi siyo hoja. Uzito wa hoja ni muhimuzaidi kuliko wingi wa watoa hoja hiyo. Kwa hiyo, Tumeitazingatia uzito wa na hoja, na hoja zote zikipelekwa kwaTume, basi tuzipeleke nyingi kadri inavyowezekana na wengituzipeleke ili Tume ipate uwanja mpana zaidi wa kuwezakutafakari na kutuletea Katiba ambayo itatufaa wote.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nijaribu kujibu hojambalimbali zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge, mmojammoja.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Ester NicholausMatiko, alizungumzia hoja ambayo pia ilizungumziwa naKamati ya Katiba, nikaijibu kwamba ucheleweshaji wamashauri Mahakamani ni kikwazo katika mfumo wa utoajihaki. Nilisema ni sawa, na sisi tumeliona hilo na tunaendeleana taratibu za kuboresha hali hiyo.

Page 230: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

230

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Hamad Abuu Jumaa,Mbunge wa Kibaha Vijijini, yeye alizungumzia kuhusu mafunzoya Mahakimu na Majaji.

Mheshimiwa Spika, Mahakama imeendelea kutoamafunzo kwa watumishi wa kada zote kadiri ambavyo bajetiinaruhusu. Kwa mwaka ujao, Mahakama inakusudia kutoamafunzo kwa watumishi wake zaidi ya 1,000 wa ngazimbalimbali. Kwa hiyo, suala hili tunalitilia umuhimu na sisitunaona umuhimu wa mafunzo, Wizara na Taasisi zoteambazo ziko chini yake.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Jumaa piaaliendelea kuzungumzia kuhusu nyumba kwa WaheshimiwaMajaji. Katika hotuba yangu, nimesema tuna mpango wakujenga nyumba kwa Waheshimiwa Majaji. Tumepatakiwanja pale Dar es Salaam, tutajenga nyumba zao katikakijiji kimoja. Kwa hiyo, tunategemea kufanya hivyo. Lakinikatika kila mahali ambapo tuna Mahakama Kuu, tunajenganyumba ya Jaji na tunaendelea kujenga nyumba zaMahakimu, kila tunapojenga Mahakama nyingine mpya.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Hawa AbdulrahmanGhasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini, amesema wafanyakazibora kupongezwa ni kutiwa moyo na kuendelea kufanyavizuri. Anachosema ni kwamba, toka aone Sherehe za Sikuya Mei Mosi, hajapata kuona Wafanyakazi Bora kutoka Sektaya Mahakama. Yeye anasema kupata Wafanyakazi Bora nikutiana moyo.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli na mimi nakubali, ndiyomaana sisi Sekta yetu hii ya Mahakama huwa inawapongezawatumishi wanaofanya kazi kwa bidii kila mwaka kwakuwapa zawadi ya kutambua juhudi zao. Hata hivyo,utaratibu huu wa kwenda huko kwenye May Day na sisi basitutaingia, lakini unafanyika, lakini unafanyika katika ngazi yaTaasisi.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Ramo Makani,Mbunge wa Tunduru, alizungumza kuhusu kuzingatia ADR.

Page 231: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

231

ADR ni Alternative Dispute Resolution Mechanism, ambayotunatakiwa kuizingatia. Mimi nasema, sisi tunaizingatia sana.Actually kama nilivyosema mwanzo, haya ni matakwa yasheria na yapo kwenye Sheria na sisi tunazingatia sana,kujaribu kutatua matatizo badala ya kwendanayo Mahakani.Lakini pia mnaweza mkaenda Mahakamani, badala yakufanya kesi, mkatumia utaratibu huu na mkajaribu kutatua.Hii itaongeza kazi ya kupunguza mashauri yanayokwendaMahakamani.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Gosbert Blandes,Mbunge wa Karagwe, ambaye ndiye aliyesoma pia Taarifaya Kamati, alikuwa na mengine ya kusema. AnasemaWaheshimiwa Mahakimu wapya, hawakupangiwa vituovipya vya kazi.

Mheshimiwa Spika, nataka kumhakikishia MheshimiwaMbunge kwamba, Mahakimu hao wapya wako kwenye vituosasa hivi. Wako kwenye vituo mbalimbali vya Mahakamawakijifunza kazi na kupata uzoefu zaidi kutoka kwa Mahakimuwenye uzoefu, na siyo kuwa wamekaa tu na hawafanyi kazi.Wako pale wanafanya internship na hawa Mahakimu ambaowako siku nyingi. Wao sasa tulikuwa tunasubiri tu Sheria ileipite, Sheria imepita na Mheshimiwa Rais, amekwishaisaini.Barua wamekwishapewa sasa hivi. Vijana hawa watapewaMahakama zao na sasa wameshapata uzoefu, watapewaMahakama zao ili waende sasa wakaanze kazi ya kuendeshaMahakama zao wao wenyewe peke yao. Lakini kwa sasawalikuwa wamepangwa na Mahakimu wengine wakijifunzakazi na kupata uzoefu kwa Mahakimu hao.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge pia alisemavilevile kwamba, mishahara ya Mahakimu wapyahaikutumwa kwa wahusika. Nataka kusema kwamba kati yaMahakimu wapya walioajiriwa mwaka 2012, ni 12 tu ambaohawakulipwa mishahara yao. Hawa hawakulipwa kutokanana kukiuka taratibu za utumishi, ambapo walikuwa watumishiwa Taasisi za Serikali na kuacha kazi badala ya kuombakuhamishwa. Hata hivyo, mawasiliano na Ofisi ya Rais –Utumishi, yanaendelea ili kumaliza tatizo lao.

Page 232: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

232

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Laizer na MheshimiwaMakani, waliomba huduma za usafiri kwa Mahakimu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu jambo hili, Watumishi waMahakama wakiwa Mahakimu katika mwaka ujao wa fedha,tutanunua mabasi madogo katika Mahakama za Mikoa kwaajili ya usafiri wa watumishi wa Mahakama, wakiwemoMahakimu.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Eugen Mwaiposa,Mheshimiwa Hamad Abuu Jumaa, Mheshimiwa KomboKhamis Kombo na Mheshimiwa Esther Matiko, walizungumziasuala la rushwa katika Taasisi hii ya Mahakama.

Mheshimiwa Spika, nasema ushauri huu tumeupokea.Lakini kama nilivyosema mwanzo, suala la rushwa halikoconfined kwa Mahakama peke yake, ni tatizo mtambukana tunapambana. Tunaendelea kupambana kwa kadiritunavyoweza, lakini ni tatizo gumu na ninyi mnafahamu. Lakinihata hivyo, Waheshimiwa Wabunge, kama nilivyosemamtakubaliana na mimi kwamba angalau vitendo vya rushwakwenye Mahakama sasa vimepungua sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Felix Mtambo,Mbunge wa Liwale, Mheshimiwa Michael Lekule Laizer,Mbunge wa Longido, Mheshimiwa Sylivester Koka, Mbungewa Kibaha walizungumzia kuhusu mahitaji ya majengo yaMahakama katika sehemu zao. Kwa kutambua upungufu huuna uchakavu na mahitaji kwa ujumla wa majengo katikaMahakama zetu, Serikali imeanzisha program maalum yaujenzi wa Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzokwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Mkoa,Wilaya na Halmashauri husika. Ni matumaini yangu kamanilivyosema kwenye bajeti yangu kuwa Serikali kwa programhii itasaidia kutupatia ufumbuzi wa changamoto hizi.

Mheshimiwa Spika, aidha, ongezeko la bajeti laMahakama litasaidia kukabiliana na changamoto hii mwakawa fedha huu ujao. Kama nilivyosema asubuhi, tuliongezewakatika Mahakama leo hii asubuhi kama Shilingi bilioni 20

Page 233: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

233

ambazo tunategemea nazo zitaingizwa katika ujenzi waMahakama hizi na kupunguza tatizo hili la mahitaji yamajengo ya Mahakama.

Mheshimiwa Spika, Dkt. Prudenciana Kikwembe yeyealizungumza kuhusu ucheleweshaji wa mashauri na amesemakuna kuongezeka sana kwa idadi ya watuhumiwa naakazungumzia upanuzi, yaani ukarabati wa ujenzi wamajengo ya Mahakama, mwenendo na tuhuma za mashauriya jinai ziwe za Kiswahili ili washtakiwa waelewe mwenendowa shauri na hatma yake.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa kweli mashauriyanaweza yakaendeshwa kwa Kiswahili, kinachoandikwaKiingereza ni ile hukumu, lakini mle ndani wanawezawakasema Kiswahili. Kwa hiyo, haimnyimi mtuhumiwakuelewa nini kinaendelea. Hilo linafanyika na kamakuongezeka kwa watuhumiwa, pia tukubaliane Watanzaniatumeongezeka, hali ya maisha imebadilika nature yamisuguano katika jamii pia imebadilika. Sasa hivi kwenye kesizangu Mahakamani kule kesi zilizopo nyingi utakuta ni zakijamii jamii, siyo za mtu mmoja mmoja kama zamani. Ukishtakisasa, unamshtaki mtu mmoja, lakini ana watu wengine kamamia pale wanakwenda kama mashabiki wake. (Kicheko)

Kwa hiyo, kesi ni nyingi. Nyingine za kidini, nyingine zakisiasa, ziko nyingi. Lakini tu ile conflicts ndani ya jamiiizimebadilika. Zamani ilikuwa ukimkamata kibaka mmoja, basiuna-deal na huyo huyo. Lakini sasa ukimkamata mtuhumiwammoja, unaweza uka-deal na Chama kizima cha siasa. Kwahiyo, nature ya conflicts katika jamii imebadilika sana. Hilitunalielewa na ni changamoto ambayo inatukabili. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie kwakuzungumzia hoja aliyoitoa Msemaji wa Kambi ya Upinzanikuhusu haki za binadamu kwa ujumla. Lakini sana sana yeyealizungumzia kesi ya Marehemu ambayo ipo Mahakamani.Nami kwa sababu ya kesi i le kuwepo Mahakamanisitaizungumzia hata kidogo. Nitazungumzia tu hali ya haki zabinadamu katika nchi yetu.

Page 234: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

234

Mheshimiwa Spika, katika nchi yetu ndani na njetumesifika vizuri sana kwa kuzingatia haki za binadamu.Tumesifika sana! Mimi mwenyewe nimewakilisha nchi yetusehemu nyingi ambapo kila tukisimama wanasema status yahaki za binadamu kwa Tanzania ni nzuri. Yapo matukioambayo yanaweza yakawa yanatutia doa, mengine ni ajali;lakini hakuna la makusudi. Siku moja kuna mtu alizungumza,nafikiri tulikuwa kwenye Kamati akasema kuna mauaji kamavile ya kupangwa na Serikali. Hakuna kitu cha namna hiyo!Siyo Serikali hii! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali hii haiwezi kupanga,haijawahi kupanga wala haitapanga mauaji ya raia wakeinaowalinda. Haiwezekani! Kwa hiyo, kama yametokeamatukio ambayo yameonyesha kama vile kuna uvunjifu wahaki za binadamu, matukio haya hayajapangwa na Serikaliwala hayapangiki. Hakuna kikao kinachoweza kufanya hivyondani ya Serikali hii ninayoijua mimi na naijua. Hii Serikalinimeitumikia miaka mingi sana, uhai wangu wote nimetumikiaSerikali hii. Kwa hiyo, naijua. Hakuna uwezekano wa jambokama hilo kutokea. Kwa hiyo, hali yetu ya haki za binadamuni nzuri, na ni nzuri sana.

Mheshimiwa Spika, zinapotokea fujo mahali za ainayoyote ile, wanapokwenda Polisi kwenda kujaribu kutuliza fujohiyo katika harakati zile akatokea raia akauawa amaakaumizwa, ukatoka pale ukasema Tanzania inavunja hakiza binadamu, kwa kweli unatuonea. Ulitaka tufanyaje? Tukaetu zile fujo ziendelee, wananchi waendelee kuumizana? Sasaikitokea hiyo, Wamarekani wenzetu wana neno lao linaitwaCollateral Damage. Sisi hatuwezi kutumia hilo. Sisitunasikitishwa na kila raia anapoumia, kila raia anapokufatunasikitishwa sana. Tunaumizwa sana!

Kwa hiyo, nimwambie tu Mheshimiwa Mbungekwamba ajaribu kutuangalia katika picha hiyo na asitu-pointkama sisi ni watu wabaya, tunapenda kuua, tunakwendamahali, basi Polisi ua! Hapana. Hatuko hivyo na yeyeanafahamu hatuko hivyo. Ofcourse kuna maneno ya kisiasa,lakini hayo siyo mahali pake hapa. Hapa ni Bungeni,

Page 235: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

235

tunaongea facts, hatuongei maneno ya uongo na hatutakikuongea maneno ya uongo.

Mheshimiwa Spika, nimejitahidi kujibu hoja zaWaheshimiwa Wabunge, sina hakika kama nimezimaliza zote.Zipo nyingi, lakini wenzangu walinisaidia pale mwanzo,wamezipunguza.

Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie tu kwakushukuru sana. Naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaSpika, naafiki.

(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

SPIKA: Hoja hiyo imeungwa mkono. MheshimiwaZambi.

MWONGOZO

MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Spika,nimesikitika kidogo hapa, natumia Kanuni ile ile ya mwongozouniwie radhi, lakini nimeona nisimame tu kwa sababu yakuweka mambo sawa.

Mheshimiwa Spika, wakati Mheshimiwa Waziri anajibuhoja hapa, limekuja suala la takwimu za wanachama waVyama vya Siasa ambao walihusika katika utoaji wa maoni,ikasemwa kwamba CCM wanachama milioni sita, naCHADEMA watu wakacheka cheka hapa wakasema milioni10 na baadaye CUF wakasema milioni 11. Ulikuwa kamautani, watu wanacheka.

Mheshimiwa Spika, concern yangu hapa, hizi nikumbukumbu sahihi za Hansard za Bunge. Vizazi vinavyokujakesho kutwa, wataona kwamba mwaka huu 2013 na tareheya leo Serikali i l ithibitisha kwamba kumbukumbu zawanachama wa Vyama hivi ndivyo zilivyokuwa jamboambalo siamini kama liko hivyo. (Makofi)

Page 236: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

236

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naiomba Serikali, autupe mwongozo wako, taarifa zinaposomwa Bungeni zakiutani utani na zinarekodiwa na Hansard: Je, tunaziachahivyo hivyo au tunazisahihisha, au tunathibitisha zipo sahihi?

Mheshimiwa Spika, naomba mwongozo wako.

SPIKA: Mheshimiwa Tundu Lissu kaa chini tumalizemoja kwanza.

Actually, kufuatana na kanuni zetu hapa, kama hunauhakika na kitu chochote, siyo sahihi kusema. Kwa hiyo,Hansard isomeke kwamba zile figure hazina usahihi wowote.(Makofi)

Mheshimiwa Tundu Lissu!

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Spika, ahsante.Naomba nikupatie taarifa, nikujulishe kwa mujibu ya kanuniya 77(2) ya kanuni zetu inayosema: “Mbunge yeyotealiyehudhuria anaweza kumjulisha Spika kwamba Wabungewaliopo ni pungufu ya akidi inayohitajika kwa ajili ya shughuliinayoendelea.”

Mheshimiwa Spika, ili shughuli ya Bunge lako Tukufuiwe halali, akidi kwa kila kikao cha Bunge wakati wa kufanyamaamuzi itakuwa ni nusu ya Wabunge wote. Tunakwendakwenye Kamati ya Matumizi na idadi ya Wabunge ambaowako humu kwa mahesabu yangu ya haraka haraka niWabunge kama 133, wakati nusu inatakiwa iwe 176. Kwamahesabu yangu, naomba kwa mujibu wa kanuni hizi,ujiridhishe kama tuna akidi ya kutosheleza kutupeleka kwenyeKamati ya Matumizi.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, mnajua humu ndanikuna watu wanapenda kuchelewesha tu mambo na kufanyahivi; mimi hapa huwezi kuniambia wangapi nimewaruhusukwenda kufanya nini. Najua idadi hii inatosha kabisa. Kwahiyo, tunaendelea, Katibu.

Page 237: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

237

KAMATI YA MATUMIZI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 8 – Tume ya Mabadiliko ya Katiba

Kif. 1001 – Administration and HRManagement……………………..Tshs. 19,596,543,000/=

SPIKA: Mheshimiwa Mnyika na Mheshimiwa HalimaMdee.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kasma 210300 ambayo mwaka wa fedhauliopita ilikuwa Shilingi bilioni 10.2, mwaka huu Shilingi bilioni10.1, Kambi Rasmi ya Upinzani inaomba ufafanuzi wamgawanyo wa fedha hizi kwa maana ya viwango vya poshovya Wajumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba.

Mheshimiwa Waziri katika majumuisho hakutajakabisa viwango vya posho vya Wajumbe, na Kambi Rasmiya Upinzani imeonyesha mashaka yake siyo mwaka huu tu,hata mwaka 2012 kuhusu viwango ambavyo Wajumbe waTume wanalipwa na kufikia hatua ya kuviona kama viwangohivyo ni ulaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kupataufafanuzi kutoka kwa Mheshimiwa Waziri, kwa Shilingi hizibilioni 12.1 zilizopo hapa, kiwango cha posho cha Mjumbekwa kikao kimoja kwa siku wa Tume ya Mabadiliko ya Katibani kiasi gani? Iwapo ufafanuzi utakaotolewa na Wazirihautaniridhisha, nitaomba nipewe nafasi ya kutoa hoja yakuhamisha sehemu ya fedha hizi kupeleka kwenye vifunguvingine ambavyo Mheshimiwa Waziri mwenyewe amekirikwamba vina pesa kidogo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti naomba ufafanuzi.

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kujibia swali alilouliza Mheshimiwa

Page 238: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

238

Mnyika kuhusiana na kasma ya 210300 ambapo ametakakujua mgawanyo wa fedha wanazolipwa Makamishna waTume.

Mheshimiwa Spika, tumekuwa tukirudia suala hili marakwa mara. Mwaka 2012 wakati tunapitisha bajeti ya Wizaraya Katiba na Sheria, lakini pia hata leo Mheshimiwa Waziriamelieleza hili, viwango vya posho anayolipwa Kamishna waTume ni stahili na ni siri ya Mjumbe mwenyewe wa Tume.

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, hojayangu ilikuwa ni kifungu hicho hicho cha Mheshimiwa Mnyika210300. Kuna nyongeza ya Shilingi bilioni mbili. Sasa natakanipate ufafanuzi, hiyo nyongeza ya Shilingi bilioni mbili, kwasababu tumeambiwa kwamba kilicholipwa mwaka 2012ndiyo ambacho kimelipwa huu.

Sasa kwanza kuna Shilingi bilioni hii mbili ya ziada. HiiShilingi bilioni mbili ya ziada ni kitu gani na nisisitize kwamba,watupe mchanganuo wa kila Mjumbe analipwa kiwangogani, hasa ukizingatia kwamba wamesema ni vijisenti tu, nakwamba wale Wazee wanajitolea?

SPIKA: Nilivyosikia mimi, mgao wa Tume unalingana.The total amount inalingana kama ule wa mwaka 2012. Hayamaswali mengine; Mheshimiwa Zubeir.

MHE. HALIMA J. MDEE: Haulingani, imeongezekaShilingi bilioni mbili.

MWENYEKITI: Ndiyo imeongezeka!

MHE. HALIMA J. MDEE: Sasa haulingani basi!

MHE. SAID MUSSA ZUBEIR: Swala langu Mheshimiwalimeshaulizwa, ni hilo lililoulizwa la kwanza.

Page 239: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

239

MWENYEKITI: Haya ahsante.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1002 – Finance and Account Unit …….Tshs. 40,250,000/=

Kif. 1003 – Internal Audit Unit …………..….Tshs. 64,200,000/=Kif. 1004 – Procurement Mgt Unit…………..Tshs. 97,480,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1005 – Inform. Comm. and Techn……Tshs. 487,000,000/=

MHE. MTUTURA A. MTUTURA: Mheshimiwa Mwenyekiti,subvote 1005 kifungu namba 410600 - Acquisition of Officeand General Equipments. Hapa mwaka 2012 inaonekanakulikuwa na Shilingi milioni 30 lakini mwaka huu kuna ongezekozaidi ya mara tatu, Shilingi milioni 102, hebu naomba Wizaraitueleze, ongezeko hili ni kwa ajili ya nini?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri maelezo! Mmekionakifungu anachosema Mheshimiwa, cha 410600?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, ningependa kujibu swali la Mheshimiwa Mtuturakuhusiana na kasma 410600. Fungu hili litatumika katikakununulia saver itakayotumika ku-back up maoni yawananchi kutokana na umuhimu wa usalama wa maoniyenyewe yanayokusanywa kwa ajili ya kumbukumbu zaKitaifa.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1006 – Comm. and Outreach….... Tshs. 10,310,195,000/=

Page 240: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

3 MEI, 2013

240

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lugola, Mheshimiwa VitaKawawa, Mheshimiwa Chilolo, Mheshimiwa Zubeir,Mheshimiwa Susan Lyimo, Mheshimiwa Susan Kiwanga,Mheshimiwa Sabreena; vifungu vyenyewe havitoshi nyiewote!

Haya, Mheshimiwa Mnyika, Mheshimiwa Sakaya,Mheshimiwa Paresso, Mheshimiwa Ngonyani na MheshimiwaMipata. Tuanze na Mheshimiwa Paresso.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Napenda kupata ufafanuzi katika subvote 1006kifungu kidogo 220100 - Office and General Supplies andServices. Mwaka 2012 ilikuwa Shilingi milioni 200, lakini safarihii imetengwa Shilingi bilioni nane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungeomba ufafanuzi, kwanini kiwango hicho kimekuwa kikubwa sana?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, fedha hizi zitatumika katika kuchapishia nakalamilioni moja za rasimu ya Katiba.

MHE. ALPHAXARD K. LUGOLA: MheshimiwaMwenyekiti, nilikuwa nataka ufafanuzi kwenye hiyo subvote1006 kifungu 221300 kinachohusiana na Educational MaterialSupplies and Services. Mwaka 2012 ilikuwa Sh. 182,500,000/=lakini mwaka huu naona imekwenda mpaka Sh.1,578,195,000/=. Naomba ufafanuzi.

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, fedha hizi zitatumika katika kutoa elimu kwaUmma hususan sasa hivi tunapoelekea katika Mabaraza yaKatiba, lakini baadaye katika Bunge Maalum na mwishokabisa kwenye Kura za Maoni.

Page 241: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

241

3 MEI, 2013

MWENYEKITI: Mheshimiwa Stephen H. Ngonyani!

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Spika,nashukuru. Mheshimiwa Lugola ameshanimaliza kwenye swalilangu.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Suzan Kiwanga!

MHE. SUZAN L.A. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nipo…

MWENYEKITI: Kama ni kifungu hicho wala msipotezemuda wa Spika hapa!

MHE. SUZAN L.A. KIWANGA: Nipo kwenye fungu hilohilo, 220600 wanasema clothing, bedding, footwear andservices. Miaka yote hakuna hela iliyopangwa, lakini mwakahuu shilingi milioni 40 ni za nini? Hawa watu wananunuliwatena hivyo vitu?

SPIKA: Wewe uliza ni za nini? Hawa watu, watu gani?(Kicheko)

Mheshimiwa Waziri majibu!

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, fedha hizi zitatumika katika kununulia sare kwaajil i ya wajumbe wa Sekretarieti ya Tume, pindiwanapokwenda katika sherehe mbalimbali za maazimishokwa ajili ya kutangaza kazi za Tume, lakini pia kuhamasishawananchi waweze kushiriki katika kutoa maoni yao kuhusianana Rasimu ya Katiba pamoja na hatua nyingine zinazofuata.

MWENYEKITI: Mheshimiwa nani pale! Diana Chilolo!

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Mwenyekitihoja yangu imeshajibiwa.

MHE. VITA R. M. KAWAWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kifungu 221000, travel in country. Mwaka jana ilikuwa sh.

Page 242: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

242

3 MEI, 2013

70,000,000/= mwaka huu ni sh. 12,000,000/=, swali langu kwanini zimepungua, na kifungu hiki kinahusiana na mawasilianoand outrich.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Katiba naSheria!

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, fedha hizi zimepungua kwa sababu fedha zinginetumeziweka katika kifungu cha utawala.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Zubeir!

MHE. SAID MUSSA ZUBEIR: Mheshimiwa Mwenyekiti,unaniweka wa mwisho mwisho, kwa kuwa swali langu lilikuwakwenye clothing, Bedding, Footwear and Services, ambalolimeshaulizwa.

MWENYEKITI: Tayari limeshaulizwa, MheshimiwaMipata!

MHE. DEUSDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kifungu 221200, Communications and Information,kimepanda karibu mara tatu, naomba ufafanuzi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Katiba naSheria!

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, fedha hizi zitatumika kama nilivyoeleza kwa ajiliya kutangaza shughuli za Tume, lakini pia kwa ajili ya kulipiavikundi mbalimbali vya sanaa na kwa ajili ya kuelimishawananchi kutoa maoni yao.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1007 – Review Coordination Unit … …sh. 3,348,920,000/=

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tundu A. Lissu!

Page 243: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

243

3 MEI, 2013

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nauliza kuhusu kijifungu 210400, Personnel Allowances –(Discretionary) – Optional sh. 604,800,000/=.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika randama ya Tumena maelezo yaliyoletwa Bungeni, hizi pesa zinasemekana niposho za kujikimu za wajumbe wa Tume wakati wa Bunge laKatiba. Mheshimiwa Waziri ametueleza hapa kwamba pesaza Bunge la Katiba ziko kwenye consolidated fund, haikokwenye bajeti hii. Sasa naomba ufafanuzi kama pesa zakuendeshea Bunge Maalum la Katiba ziko kwenyeconsolidated na hazijaidhinishwa na Bunge hili. Hizi sh.604,800,000/= ambazo ni posho za kujimu za wajumbe waTume wakati wa Bunge Maalum la Katiba zikoje hapa?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, pamoja na kwamba Bunge la Katiba litakuwalikihudumiwa na Bunge la Jamhuri wa Muungano waTanzania, lakini mwisho wa siku bado Wajumbe wale wa Tumeni waajiriwa wa Tume na watahitajika kuja katika Bunge laKatiba kutoa ufafanuzi mbalimbali, kwa hiyo badowanawajibika chini ya Tume.

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Mwenyekiti, swalilangu liko kwenye item namba 221200, Communications andInformation, mwaka huu wa fedha unaoisha walitengewashilingi bilioni mbili, lakini mwaka ujao wa fedha hakuna pesazilizotengwa. Naomba maelezo.

MWENYEKITI: Umepata hapo, item 221200! kwambahakuna fedha safari hii.

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, fedha hizi tumeziweka katika fungu la utawala.

MHE. RUKIA KASSIM AHMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,niko katika kifungu namba 221000 Travel in Country, mwakauliopita palitumika sh. 600,000,000/=, lakini mwaka huuzimeongezeka sana zimekuwa sh. 1,493,820,000/=. Je, kunanini hapa, tuambiwe.

Page 244: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

244

3 MEI, 2013

MWENYEKITI: Jamani lakini mjue hii Tume ni ya muda,inatakiwa ieneze, inatakiwa ifanye nini, naona mnaona kamani kitu cha kudumu. Naomba mwelewe mazingira yenyeweya ofisi. Haya Mheshimiwa Naibu Waziri!

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, fedha hizi zitatumika na wajumbe wa Tumewanapokuwa wakisafiri mikoani kikazi hasa katika kusimamiauendeshaji wa Mabaraza ya Katiba.

MHE. SUZAN A. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikokwenye kasma ndogo 220600, Clothing, Bedding, Footwearand Services. Mheshimiwa Naibu Waziri alijibu kwamba fedhahizo ni kwa ajili ya sare na mambo mengine, lakini kifunguhuku bado kina appear katika subvote 1007 na vile vile kinaappear kwenye subvote 1001, pamoja na ile aliyoulizaMheshimiwa Suzan Kiwanga. Naomba kupata maelezo kamabado sub-vote hii pia ni kwa ajili hiyo na ni kwa nini?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, katika muundo wa Tume, kipo kitengo chauratibu wa maoni ya wananchi. Kitengo hiki ni muhimu sanatutakapokuwa tukielekea katika mchakato wa kura yamaoni. Kwa hiyo, wao watakuwa wakichapisha T-shirt kwaajil i ya kuhamasisha wananchi tunapoelekea katikamchakato wa kura ya maoni.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 12 – Tume ya Utumishi wa Mahakama

Kif. 1001- Administration and Human Resource Management… … sh. 1,432,410,000/=

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kifungu 1001, kasma 220700, Rental Expenses, ambapo kwawastani kodi imekuwa ikiongezeka kila mwaka. Mwaka huukodi imefikia shilingi milioni 186. Mheshimiwa Waziri katika

Page 245: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

245

3 MEI, 2013

maelezo yake, ameeleza kwamba, kuna changamoto yakutokuwa na jengo kwa ajili ya Tume ya Utumishi waMahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa kuwa kodi inazidikuongezeka kila mwaka, ningependa kupata maelezo, nikwa nini kodi inazidi kuongezeka kila mwaka, wakati penginejengo ni lile lile na namna gani wanalinusuru Taifa kutokanana kuongezeka kwa kodi kila wakati kwenye jengo hilo?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, hivi sasa mahali ambapo Tume inafanyia kazizake pako finyu sana, lakini pia kama mnavyofahamutulipitisha Sheria ya Bunge, Sheria ya Uendeshaji waMahakama, Sheria namba 4 ya mwaka 2011. Tume itajipanuakatika majukumu yake. Kwa hiyo, tunatarajia Tume hii iwezekuhamia katika ofisi nyingine, lakini pia tutaajiri watumishiwengi zaidi, kwa hiyo basi, mahitaji yatakuwa yameongezekana gharama za kodi zitapanda.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi pamoja na marekebisho yake)

Kif. 1002 – Finance and Accounts … … … sh. 108,362,400/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1003 - Procurement Management Unit … … … … … … … ... ... ..sh. 55,155,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi pamoja na marekebisho yake)

Kif. 1004 - Internal Audit Unit … … … … … sh. 46,935,500/=Kif. 1005 – Recruitment, Appointment

and Confirmation… … … … ..sh. 318,038,400/=

(vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 246: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

246

3 MEI, 2013

Kif. 1006 – Ethics and Discipline Section… … … … … … … … sh. 837,146,500/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi pamoja na marekebisho yake)

Fungu 16- Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Kif. 1001 - Administration and Human Resource Management… … ..sh. 2,209,907,000/=Kif. 1002 – Finance and Accounts Unit… …sh. 715,142,000/=Kif. 1003 - Planning Division… … … … ...sh. 609,010,000/=Kif. 1004 - Internal Audit Unit… … … … ...sh. 430,806,000/=Kif. 1005 – Government Communication

Unit… … … … … … … … ... sh. 237,152,000/=Kif. 1006 – Legal Registry Unit… … … … …sh. 302,968,000/=Kif. 1007 – Procurement Management

Unit… … … … … … … … … sh. 355,777,000/=Kif. 1008 – Research and Library

Service Unit… … … … … … ...sh. 262,363,000/=Kif. 1009 – Information and Comm.

Technology Unit… … … … … sh. 478,873,000/=Kif. 2003 – Legislative Drafting… … … … sh. 1,321,096,000/=Kif. 3001 – Civil Litigation and Arbitration

Division… … … … … … … …sh. 1,210,649,000/=Kif. 3002 – Treaties and Contracts

Division… … … … … … … …sh. 1,341,946,000/=Kif. 4001 – Constitutional Affairs and

Human Rights… … … … … sh. 1, 031,362,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 35 – Mkurugenzi wa Mashtaka

Kif. 2002 - Public Prosecution Division… … sh. 9,195,519,000/=Kif. 2004 – Zonal Office Arusha… … ... ... ...sh. 912, 430,000/=

Page 247: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

247

3 MEI, 2013

Kif. 2005 – Zonal Office Dodoma… … … ..sh. 593,390,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi pamoja na mabadiliko yake)

Kif. 2006 – Zonal Office Dar es Salaam… .sh. 1,492,614,000/=

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekitinashukuru. Kifungu hiki kinahusu Ofisi ya MwendeshaMashtaka kwa upande wa Kanda ya Dar es Salaam, sasaningeomba kupata ufafanuzi kuhusina na kasma 220100 kwaajili ya kuweka kumbukumbu sawa kwa ajili ya ufuatiliaji wamatumizi ya hizi fedha. Hakuna maelezo yoyote kuhusianana matumizi ya hizo fedha kwenye kitabu ambacho ninachoukurasa 191, Fedha zimeongezeka kutoka shilingi milioni 34mpaka shilingi milioni 40, lakini hakuna maelezo yoyote hizipesa ni kwa ajili gani. Kwa ajili ya kuweka record sawa,naomba ufafanuzi hapa.

MWENYEKITI: Mmeona hakuna maandiko!

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, fedha hizi ni kwa ajili ya kuhudumia mahitajimbalimbali ya ofisi na imeongezeka kwa sababu mwaka janaOfisi hizi katika Wilaya ya Kinondoni, Ilala na Temekehazikuwepo, ni ofisi mpya.

MWENYEKITI: Shida yake ni hiyo kuongezeka, ilamaneno gani yanayofuatia hapo?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Wapi?

MWENYEKITI: Ukiangalia lile fungu litakuwa ni officeand general supplies and services. Kwa sababu 220100 katikamaeneo haya ndiyo sehemu yenyewe. Kwa hiyo, iandikweni office and general supplies and services.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 248: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

248

3 MEI, 2013

Kif. 2007 -Zonal Office Iringa… … … … … sh. 440,193,000/=Kif. 2008- Zonal Office Moshi… … … … … sh. 567,038,000/=Kif. 2009 -Zonal Office Kagera… … … … ...sh. 478,585,000/=Kif. 2010- Zonal Office Mbeya… … … … …sh. 577,608,000/=Kif. 2011-Zonal Office Mtwara… … … … …sh. 479,894,000/=Kif. 2012 -Zonal Office Mwanza… … … … sh. 885,305,000/=Kif. 2013 -Zonal Office Ruvuma… … … … sh. 460, 213,000/=Kif. 2014 -Zonal Office Sumbawanga… … sh. 354,705,000/=Kif. 2015-Zonal Office Tabora… … … … sh. 667,033,000/=Kif. 2016-Zonal Office Tanga… … … … …sh. 618,598,000/=Kif. 2017-Zonal Office Shinyanga… … … ..sh. 470,787,000/=Kif. 2018 - Zonal Office Singida… … … … sh. 347,589,000/=Kif. 2019- Zonal Office Lindi… … … … … sh. 284,233,000/=Kif. 2020 -Zonal Office Mara… … … … … sh. 383,532,000/=Kif. 2021 -Zonal Office Manyara… … … …sh. 313,904,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi pamoja na marekebisho yake)

Kif. 2022 - Zonal Office Kigoma… … … … sh. 313,096,000/=

MWENYEKITI: Mheshimiwa Sabreena Hamza Sungura!

MHE. SABREENA HAMZA SUNGURA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nipate ufafanuzi kwenye kifungu kidogocha 221100, Travel out of Country katika Mkoa wa Kigomakuna shilingi 250,000/=, nataka kujua kiwango hiki...

MWENYEKITI: Tuko Pwani sasa!

MHE. SABREENA HAMZA SUNGURA: Hapana ni Kigoma!

MWENYEKITI: Tuko Pwani sasa!

MHE. SABREENA HAMZA SUNGURA: Hapana ni Kigoma,kifungu 2022!

MWENYEKITI: Tumeshapita! Haya turudi, hebu simamaSabreena, endelea!

Page 249: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

249

3 MEI, 2013

MHE. SABREENA HAMZA SUNGURA: MheshimiwaMwenyekiti, niko sahihi. Nataka kuuliza kwa sababu hapakuna travel out of country Kigoma Zone ni shilingi 250,000/=,nataka kujua ni nchi gani ambayo watu watasafiri kwa sh.250,000/=

MWENYEKITI: Umeiona hiyo! Ni 221100, ni travel out ofcountry.

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, kutokana na ufinyu wa Bajeti, hii ilikuwa nikushikilia kifungu.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi pamoja na marekebisho yake)

Kif. 2023- Zonal Office Pwani… … … … … sh. 350,737,000/=Kif. 2024- Zonal Office Njombe… … … ... ...sh. 294,825,000/=Kif. 2025- Zonal Office Morogoro… … ... ...sh. 362,209,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi pamoja na marekebisho yake)

Fungu 40- Mahakama

Kif. 1001 - Administration and Human Resouces Management … … … … … … ..sh. 0

Kif. 1002 – Finance and Accounts Unit … … … … … ...sh. 0Kif. 1003 – Internal Audit Unit … … … … … … … … … sh. 0

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 2002 – Court of Appeal Dar es Salaam … … … … sh. 117,580,157,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi pamoja na marekebisho yake)

Page 250: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

250

3 MEI, 2013

Fungu 41- Wizara ya Katiba na Sheria

Kif. 1001- Administration and Human Resources Management … … sh. 7,677,431,000/=

MWENYEKITI: Haya mshahara wa Waziri. MheshimiwaSara Msafiri atafutiwa na Mheshimiwa Tundu Lissu,Mheshimiwa Said Mussa Zubeir, Mheshimiwa Kange Lugolana Mheshimiwa Magdalena Sakaya. Haya tuanze na Sara!

MHE. SARA M. ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsantesana kwa kunipa nafasi. Kumekuwa na migogoro ya ardhikati ya wakulima, wafugaji na wawekezaji, migogoro ambayoinapelekea uvunjifu wa haki za binadamu. Kwa vile Tume yaHaki za Binadamu na Utawala Bora ina mamlaka kikatibakushughulikia masuala yote ya uvunjifu wa haki za binadamuna wana kitengo maalum kwa ajili ya elimu kwa umma.

Je, kwa nini sasa Serikali isitoe fedha ya kutoshakwenye kitengo cha elimu kwa umma kwenye Tume ya Hakiza Binadamu ili kushughulikia migogoro hiyo na kuepushagharama zinazoendelea kutokea. Inapotokea migogoro,kunaundwa Tume zingine ndogo za kushughulika migogorohiyo?

MWENYEKITI: Naomba muwe mnaandika vizuri.Mheshimiwa Tundu Lissu!

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nijielekeze kwenye utaratibu mzima wa Mabarazaya Katiba ya Wilaya. Kama ambavyo tulisema katika maoniya Kambi, kumekuwa na utaratibu wa kibaguzi katika uteuzi,uchaguzi wa Baraza la Kikatiba, kati ya Tanzania Bara naZanzibar. Huku Bara, Wajumbe wa Mabaraza ya Katibawamechujwa na Kamati za Maendeleo za Kata, wakatiZanzibar Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba wamechaguliwamoja kwa moja na wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bara Wenyeviti wa Vijiji naWatendaji wa Vijiji na Mitaa ndiyo waliokuwa Wenyeviti wa

Page 251: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

251

3 MEI, 2013

mikutano ya uchaguzi wakati Zanzibar, Wenyeviti naMakatibu wa mikutano ya uchaguzi walichaguliwa na walewaliokuwa wanachagua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hoja imeletwakwamba, haya Mabaraza ya Kata yaliyofanya mchujo kwaTanzania Bara, ni vyombo vya kisheria vinatumika kwenyemambo mengi, lakini ni muhimu nieleze hapa, Mabaraza yaKata siyo vyombo vya kisheria, these are not statutory bodies,hazina kazi zilizoandikwa kwenye sheria zetu za Halmashauriza Mitaa. Hizi ni Kamati tu na hazina Mamlaka yoyote yakisheria kwa mujibu wa sheria. Kwa hiyo, hakukuwa nasababu yoyote ya kuzifanya kuwa Mamlaka za uchaguzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili kwenye sualahilo hilo, hata Zanzibar kuna Madiwani na kuna kwenye Ward,lakini Madiwani wa Zanzibar kwenye ngazi ya Wardhakukuwa na mchujo wa Wajumbe wa Mabaraza ya Kata,Mabaraza ya Wilaya, wamechagua moja kwa moja. SasaWaziri amesema kwamba ngazi ya Kata kwa Tanzania Barasiyo ngazi ya kiuchaguzi, vilevile hapa amekosea, ngazi yaKata ni ngazi ya uchaguzi, Madiwani wanachaguliwa kwenyengazi ya Kata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama suala ningazi ya kiuchaguzi, hata kwenye Kata zetu kulikuwa nauwezekano wa kuwachagua moja kwa moja Wajumbe waMabaraza ya Katiba ya Wilaya badala ya kuweka watuwanne au watano wao ndiyo waamue nani anayekwendakwenye Mabaraza ya Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba ufafanuziwa jambo hili na nitoe hoja kwamba, kama sitaridhika naufafanuzi wa Waziri, nitatoa shilingi kwenye mshahara waWaziri, ili jambo hili lijadiliwe kwa kirefu zaidi na Kamati hii yaMatumizi ya Bunge lako. Nashukuru.

MHE. ALPHAXARD K.N. LUGOLA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Suala langu liko kwenye ujenzi waMahakama za Wilaya na za Mwanzo katika nchi yetu.

Page 252: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

252

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Waziri kwenye ukurasa wa 52 amezungumziakuwepo kwa program maalum kwa ajili ya ujenzi wa hiziMahakama, lakini katika maelezo yake, ameelezea kijuu juutu, hakuliambia Bunge hili kwamba program hii wanatarajiaianze lini na itakwisha lini ili Watanzania wajue kwamba kerozinazotokana na Mahakama zitakuwa zimekwisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitembelea Mahakamanyingi za Wilaya, nitolee mfano Mahakama ya Wilaya yaBunda. Bunda ni Wilaya ambayo ni kongwe, ya siku nyingi,lakini mpaka leo wako kwenye jengo dogo la kukodi likokwenye barabara kuu, vumbi kila siku, makelele kila siku. Kwahiyo hata katika mazingira ambayo Mheshimiwa Wazirialikuwa anajaribu kulishawishi Bunge kwamba, huendakukawa na upimaji na wameanza na Majaji kupima utendajiwao, kesi ngapi wamehukumu, watakapokuwawamekwenda kwenye kupima Mahakimu kwenye Wilaya,nina uhakika Hakimu wa Wilaya ya Bunda ataonekanahafanyi kazi, kwa sababu mazingira ya kazi ni sehemu yaufanisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka kujua,Mahakama hizi za Tanzania na hususan Mahakama ya Wilayaya Bunda, kuiweka kwenye mpango huu ambao maandishiyanasema uko kwenye hatua za awali, hatua za awali miakanenda rudi. Naomba kuwe na juhudi za makusudi kwenyehii Mahakama ya Wilaya ya Bunda kwa sababu niMahakama ya Wilaya kongwe, sasa kuniambia kwamba ipokatika program maalum kwa kweli sijaridhishwa na maelezohayo.

Kwa hiyo, naomba nipate maelezo ya kina juu yaMahakama hii ya Wilaya ya Bunda. Ahsante.

MWENYEKITI: Nilifikiri umesema programs za kujengaMahakama zikoje, hiyo ndiyo sera, hiyo nyingine ni ya kwakobinafsi, uliza inavyostahili.

MHE. SAID MUSSA ZUBEIR: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Katika hotuba ya Waziri, ameelezea namna ya

Page 253: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

253

3 MEI, 2013

Bunge la Katiba litakavyokuwa, lakini naona kuna jamboamesahau. Hakutuelezea Bunge hili la Katiba litafanyikaZanzibar au litakuwa Dar es Salaam ama litakuwa Dodoma.Naomba sana atuelezee na kama hajapanga basinapendekeza safari hii lifanyikie Zanzibar, hivyo katikamaelezo yake naomba sana aeleze.

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,swali langu alishajibu Naibu Waziri, sina tatizo naye tena.

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. Wakati nachangianilipenda Serikali itoe ufafanuzi kuhusiana na ukiukwajimkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na Watendajiwa Kata na wa Kijiji katika maeneo mbalimbali hapa Tanzaniakwenye nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watendaji wa Vijiji na Katawametumia ofisi za vijiji kuvifanya kama ni mahabusu yakuweka wananchi. Nilitoa specific mifano ya Kata na VijijiWilayani Urambo na Kaliua ambapo Watendaji wa Katawanafungia wananchi ndani ya ofisi za Vijiji siku tatu mpakasaba, wale ambao wameshindwa kutoa michango kwamuda unaotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wamerundikwa kulewanawake kwa wanaume bila kujali hata utu, saa nyinginehawaletewi hata chakula ni tatizo kubwa. Naomba Serikaliiseme ni sheria gani inayoruhusu Mtendaji wa Kata au waKijiji kutumia Ofisi ya Kijiji kama Mahabusu kwa ajili ya kuwatesawananchi. Ahsante. (Makofi)

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Ningependa nipate kauli ya Serikali kuhusianana Mahakama za Wilaya zote nchini ambazo zimekuwazinaendesha mashauri kule ndani. Kwa maana kwamba,wananchi hawana fursa ya kuweza kusikiliza na nitoe tu casestudy mfano, ni Mahakama ya Wilaya ya Kasulu, ambayoina muda mrefu sana mashauri yake yanafanyikia ndani, kiasikwamba wananchi hawajui ni kitu gani ambacho

Page 254: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

254

3 MEI, 2013

kinaendelea. Nini kauli ya Serikali katika kuja kutatua matatizokama haya kutokana na majengo ambayo mengine nimabovu, hayatumiki, ambayo yalikuwa yakitumika na kesizikifanyika waziwazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa commitmentya Serikali katika hili na hasa nitoe mfano wa Mahakama yaWilaya ya Kasulu. Kama hakuna mkakati wowote basinaomba nitangaze kwamba, nitatoa shilingi kwenyemshahara wa Waziri, kama majibu yatakuwa hayajaridhisha.

MWENYEKITI: Ukiitolea Sera shilingi inakuwa shughuli,naomba mjibu moja moja.

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, katika swali lililoulizwa na Mheshimiwa Sara Msafirikuhusiana na migogoro ya ardhi na kwamba ni kwa nini sasaSerikali isitenge fedha za kutosha kwa ajili ya kuiwezezeshaTume ya Haki za Binadamu kutoa elimu kwa umma ili wawezekushughulikia migogoro ya ardhi.

Mheshimwa Mwenyekiti, tumetenga fedha hizokutokana na ufinyu wa Bajeti. Tungekuwa tuna fedha zakutosha, tungeweza kuongezea, lakini tunatambua umuhimuwalio nao na ndiyo maana tumekuwa tukijitahidi kira marakwa kadiri Bajeti inavyoruhusu kuongezea fedha za Tume.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili la MheshimiwaTundu Lissu, kuhusiana na utaratibu wa Mabaraza ya Katibaya Wilaya na alituhumu kwamba katika uteuzi wa Wajumbewa Mabaraza haya ya Katiba kulikuwa na ubaguzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa tukijibu marakwa mara, lakini pia siku mbili zil izopita MheshimiwaMwenyekiti wa Tume hii, Mheshimiwa Jaji Warioba, alilielezeahili kwa kina na endapo ana uthibitisho wa hayo, anawezaakaiwasilishia Tume ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ameelezea piawasiwasi wake ambao suala hili lilijitokeza katika Bajeti ya

Page 255: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

255

3 MEI, 2013

Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, kwamba kumekuwana double standard katika Tanzania Bara, hatua ya uchaguziwa Wajumbe ilikuwa ni hatua mbili wakati Tanzania Zanzibarwalikuwa na hatua moja tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia mwongozo waTume, katika aya ya pili, unaeleza kabisa bayana kwamba,utaratibu wa kuwapata Wajumbe wa Mabaraza ya Katibaya Wilaya hautafanana kwa pande zote za Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inatokana na sababukwamba tuna tofauti ya mfumo wa utawala. Pia katikamwongozo huu kwa Tanzania Bara, katika ngazi ya Kitongojiau Mtaa, walieleza kwamba, hatua ile ni ngazi yamapendekezo, ngazi ya kuchaguliwa au kuteuliwa ni ngaziya Kata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali la tatu, aliuliziapia ni kwa nini Wenyeviti kwa Tanzania Bara walikuwa niWenyeviti wa Mtaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo hataMheshimiwa Mwenyekiti wa Tume alivyoeleza, ilionekana ilikuwapa wananchi ushiriki mzuri, ili waweze kushiriki katikasuala hili, ngazi ya Mtaa kupitia Mamlaka ya Serikali ya Mtaa,ni vyema wao ndiyo washiriki katika kuchagua na hususankatika mikutano hii ya wananchi wote. Hii ni kwa mujibu waSheria ya Mamlaka za Serikali za Mtaa, Sheria namba 287 na288. Hii si mara ya kwanza kwa mikutano hii ya wananchikutumika katika kuamua masuala mbalimbali ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, il ionekanakwamba, ni vyema suala hili likaamuliwa katika ngazi ya Mtaana Vitongoji, lakini pia si mara ya kwanza katika masualambalimbali ya kuteua Wajumbe wa Kamati za Kata za Maji,Kamati za Shule, Kamati za Afya, wamekuwa wakitumika nawamekuwa wakifanya kazi nzuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, si vyemaalivyokuwa akituhumu kwamba si sahihi, lakini pia kwa

Page 256: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

256

3 MEI, 2013

upande wa Zanzibar alisema kwamba, kwa nini Wenyevitiwalichaguliwa na Wajumbe wa mkutano. Kama ambavyonimeeleza awali, hili limetokana na tofauti ya kimfumo wakiutawala, kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali laMheshimiwa Lugola, ambapo ameuliza kwamba, ni kwa ninihatujaelezea program hii ya ujenzi wa Mahakama za Mwanzona Wilaya utaanza lini na utakwisha lini. Suala hili ni programendelevu na kama ambavyo Wabunge wanafahamu, tunamahitaji makubwa ya Mahakama zetu, kwa hiyo, suala hilitutaendelea nalo kwa muda mrefu kwa kadri Bajetiikavyokuwa ikituruhusu. Tutakapomaliza basi tutaachananalo, lakini tunaamini kwamba tunakwenda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na Mahakama yaWilaya ya Bunda, kama akiangalia vizuri hotuba yaMheshimiwa Waziri, Mahakama hii imewekwa kwenyempango, itajengwa katika mwaka huu wa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MWENYEKITI: Kuna maswali mengine hayo.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nijaribu kujibu swali lililoletwa naMheshimwa Zubeir, alitaka kujua Mkutano huu wa BungeMaalum wa Katiba utafanyika wapi, kama ni Dar es Salaam,Dodoma ama Zanzibar na alikuwa anapendekeza kwambakama ikiwezekana basi ufanyike Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mahali ambapo Bunge hilila Katiba litakutana ni mahali pale ambapo atapatamkaatakayeliitisha Bunge hili. Bunge hili kisheria katika ile sheriatuliipitsha hapa sura ya 83, ni Rais ndiye atakayeliitisha Bungehili na atakapoliitisha basi atatamka likutanie wapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pendekezo lake ni zuri, ninahakika Mheshimiwa Rais atashauriwa ipasavyo, ni mahali ganipatafaa kufanyia mkutano huu kwa wakati huo.

Page 257: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

257

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nisahihishe mojatu la Mheshimiwa Tundu Lissu hapa, aliposema kwambaKamati za Maendeleo za Kata ni Kamati tu. Kamati hizizimetungwa kisheria kwa mujibu wa sheria namba saba (7)na namba nane (8) za mwaka 1982 na Kamati hizi zinafanyamaamuzi yake na maamuzi yake ni ya kisheria. Ni Kamati zakisheria, huwezi ukasema ni Kamati tu, ni Kamati tu zinafanyanini, zina kazi gani, Mheshimiwa Lissu, soma vizuri sheria.(Makofi)

Nafikiri yote sasa tayari.

MWENYEKIT: Bado Mheshimiwa Magdalena naMheshimiwa Machali.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, Mheshimwa Sakaya na Machali yes. MheshimiwaMachali alikuwa anataka kwamba Mahakama zote zifanyikewazi na ndivyo inavyotakiwa kwamba, kesi zisikilizwe kwenyeopen court. Sasa kama hilo halifanyiki, nitawaombawenzangu wa Mahakama na bahati nzuri wako hapawakubwa wao, watatoa maelekezo kwa hawa wa chiniambao hawataki kusikiliza kesi kwenye open court, ni wajibuwao, wanatakiwa kufanya hivyo ili wananchi wote waonehaki ikitendeka, siyo wasikie tu.

MWENYEKITI: Bado la Mheshimiwa MagdalenaSakaya. Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali!

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kutumia nafasi hii kuungana naMheshimiwa Magdalena Sakaya kukemea vitendo hivi vyauvunjaji wa sheria. Ni marufuku mtu yeyote, Mamlaka yoyoteya kijiji kufungia watu kwenye ma-godown. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge nafikiri tuungane pamojakukemea mambo haya na watu hao kama tukishawajuatuwachukulie hatua za kisheria. Kwa hiyo, nachukua nafasihii, kumwomba Mheshimiwa Sakaya, baada ya kutoka hapaanipe majina, nitayashughulikia. (Makofi)

Page 258: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

258

3 MEI, 2013

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,sijaridhika na maelezo ya Mheshimwa Waziri na kwa hiyo,naomba nitoe hoja ya kutoa shilingi kwenye mshahara wakena naomba niielezee.

MWENYEKITI: Iwe specific.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, hojayangu ni very specific, Mabaraza ya Katiba ya Wilayayalivyochaguliwa. Hoja ya Waziri ni kwamba, kuna taratibutofauti za kiutawala kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii hoja si sahihi, kwaniTanzania Bara ngazi ya msingi ni kijiji, lakini Zanzibar hakunavijiji bali wanaita Shehia. Baada ya kijiji kwa Tanzania Bara,ngazi inayofuata ni Kata na kwa upande wa Zanzibar inaitwaWadi. Ni majina tofauti tu lakini ngazi ni zile zile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwenye uchaguzi waMabaraza ya Katiba ya Wilaya upande wa Tanzania Barangazi ya kwanza ya kijiji imependekeza tu, wamepiga kurawote, wanakijiji wamehudhuria wote, lakini kura zao zotehazina maana, ni mapendekezo tu! Wanaochagua niwajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kata. Kamati yaMaendeleo ya Kata, nina Wajumbe wake ni Wenyeviti waVijiji na Diwani wa Kata, Kata nyingi zina vijiji vinne au vitano.Kwa hiyo, ni watu watano au sita ndiyo waliochaguawajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Kata za Tanzania Barawakati Zanzibar wamechaguliwa na wananchi wote. Kunadirect democracy Zanzibar, lakini kuna mchujo Bara na ndiyoubaguzi ninaouzungumzia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisingekuwa na shida kabisakama ngazi ya msingi ya Tanzania Bara, vijiji vingechaguamoja kwa moja bila mchujo sawa na Tanzania Bara kwasababu ni ngazi za msingi yaani Shehia Zanzibar na kijiji aumtaa Bara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hoja ni hiyokwamba, kwa nini wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya

Page 259: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

259

3 MEI, 2013

Tanzania Bara wamechujwa na Kamati ya watu wanne auwatano wakati wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilayaya Zanzibar wamechaguliwa na wananchi wote. Hiyo ndiyohoja na naomba hoja hii ijadiliwe kwa sababu tunatengezaKatiba, hatuwezi tukatengeneza Katiba ambayo wajumbewake watakaokwenda kuizungumzia kwenye Wilaya ni watuwaliopitishwa kwenye mchujo. Kama nilivyosema ni kwambaWard C za Tanzania Bara over 80% ni za CCM, ndiyo hali halisi!Sasa kama ukitumia utaratibu huo maana yake ni kwambawalipitishwa wote ni wana CCM.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho, kuhusianana hoja hii ni kwamba, Sheria imesema wazi, katika kifungucha 17(8) kilisema Tume itabuni utaratibu unaofananautakaotumika katika kila upande wa Jamhuri ya Muunganokatika ukusanyaji na uchambuzi wa maoni, uendeshaji waMabaraza na uandaaji wa report. Hii ndiyo mandate yaTume, Tume haikuambiwa itutengenezee utaratibu ambaowatu wanakwenda kuchujwa na kikundi cha watu wanneau watano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hoja hii naombaijadiliwe kwa mapana na marefu yake. Ahsante sana.(Makofi)

MWENYEKITI: Ukishatoa shilingi maana yake ijadiliwe,sasa tena unataka kujadili mara ngapi?

Mheshimiwa Simbachawene! Kuna wenginewameongea sana na wengine sijawasikia wakiongea.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti, napendaniseme tu kwamba, kwa kweli hoja ya mtoa hoja hata kwaformula yoyote ile utakayoifanya, kama msingi wake niuwiano wa vyama, matokeo yatakuwa yale yale. Lakinisiamini kama msingi wa Mabaraza haya ni uwiano wa Vyamana ukijaribu kui- transmute, ukaipekela kwa aspect hiyo, kwadirection hiyo ya Vyama utapata matokeo yale yale.(Makofi)

Page 260: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

260

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mtoa hoja anasemakwamba 80% ya Mabaraza haya ya Kata kwa maana yaWard C ni ya CCM, maana yake nini? Viongoziwaliochaguliwa na wananchi kule chini anakosema kwenyekijiji, kwa maana ya vitongoji na vijiji hivyo, ndiyo waliamuaiwe hivyo. (Makofi)

Kwa hiyo, kwa vyovyote utakavyofanya hata ukiendakwenye kijiwe, uwiano huo kama ni ratio kwa maana yakekwa 80 na 20 maana yake ni nane kwa mbili, popoteutakapokwenda nchi hii ukawakusanya hivi utapata uwianohuo huo hata ukienda kijiweni. Sasa sina hakika kama mtoahoja anataka ku-achieve nini, lakini kama anataka ku-achieve uwiano wa uwakilishi katika Taifa hili huwezi ukaiwekapembeni CCM, huwezi, kwa namna yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe tu MheshimiwaMjumbe pamoja na mawazo mazuri na dhamira nzuri na miminamheshimu sana, kwamba jambo hili alione katika mtazamohuo mpana. Anaweza akawa ana-drive kitu anachotakakukifikia, lakini si rahisi akakifikia hata kwa formula anayokujanayo. Naomba sana aunge mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ah! yeye ndiye mwenye hoja,Mheshimiwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani.

MHE. FREEMAN A. MBOWE – KIONGOZI WA KAMBI YAUPINZANI BUNGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tuna dealna Katiba...

MWENYEKITI: Dakika tatu hizi, mnasikia ninyi nyotemnaosimama.

MHE. FREEMAN A. MBOWE – KIONGOZI WA KAMBI YAUPINZANI BUNGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambomawili yanayojitokeza ambayo ni vema kama Wabungetuondoe ushindani wa kisiasa ku-address logic.

Mheshimiwa Mwenyekiti, anachokizungumzaMheshimiwa Tundu Lissu, Mnadhimu wetu, anazungumzia

Page 261: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

261

3 MEI, 2013

kuchagua Wajumbe wa Mabaraza kutokana na uchaguziwa wananchi na siyo uchaguzi wa Vyama vya Siasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wote tunajua hapa ndanikwamba Vyama vyetu vyote vikichanganywa members waVyama vyote hatufiki milioni kumi, lakini nchi hii wapiga kurawapo zaidi ya milioni 20. Kwa nini tunaogopa na tunashindwakuwapa wananchi fursa ya kuwachagua wawakilishi wao,wakiwa wa CCM hewala, wakiwa wa CHADEMA hewala nawakiwa hawana Chama pia hewala! Where is the problem?Hilo ni moja!

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pili, pamejitokezamazingira ya kujaribu kuchonganisha na kumchonganishaMheshimiwa Warioba, tunaacha ku-address issue, watuwanajaribu kujenga hoja kwamba, pengine sisi tukijenga hojadhidi ya Tume tunajenga hoja dhidi ya Mheshimiwa Warioba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme jambomoja la msingi kwamba, tunamheshimu Warioba,tunawaheshimu Makashna wote na tunawaheshimuWatanzania wote katika hii process ya Katiba. Ila tunapokuwatuna-address issue ambayo ni ya msingi, tusiondoe ile issueya msingi, tukarudisha kwenye personality.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake tumeona watuwengine wanasema, ooh tuna-question uwezo wa Warioba,hiyo siyo hoja! Mheshimiwa Warioba tukimtaja hapa ambayetunamheshimu sana ni kwamba, tunamtaja Mwenyekiti waTume na hatuwezi tukamtaja Mwenyekiti mwingine kwasababu Mheshimiwa Warioba ndiye ambaye ana-communicate na public.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunapokujakuzungumzia mambo ya Katiba tusitafute ushindi wa kisiasahapa. Hii process inahitaji tolerance, hii process inahitaji kuwainclusive na inahitaji kuheshimiana. Tukitafuta wingi kwasababu tupo ndani ya Bunge, Watanzania wanatusikiliza kwapande zote mbili. Tunatafuta Katiba ya kutu-unite, kama ninyimnataka kuleta Katiba ya kutu-divide, try and do it! (Makofi)

Page 262: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

262

3 MEI, 2013

MWENYEKITI: Nimsikilize ambaye hajazungumza,Mheshimiwa Deo Sanga!

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hawaWajumbe ambao anawazungumzia Mheshimiwa Tundu Lissukwamba wamechaguliwa kutoka kwenye Kata, wajumbewale waliochaguliwa kutoka kwenye Kata ni walewaliochaguliwa kutoka kila kijiji katika Kata hiyo. Kwa mfano,Kata ina Vijiji sita au saba, wametoka kila kijiji wajumbe wannewane. Wakaenda sasa kwenye Kata ambapo sasawakachaguliwa wanne na Baraza la Kata ambalo sasakwenye Kata pale wapo Wenyeviti wa Vijiji na wa Vitongojina ndiyo waliowachagua wale wale waliochaguliwa nawananchi kule. (Makofi)

MHE. CAPT. JOHN Z. CHILIGATI: MheshimiwaMwenyekiti, hoja kwamba Tume imefanya ubaguzi kwakutumia mfumo tofauti Bara na Zanzibar, Waziri ameelezavizuri kwamba, mifumo yetu ni tofauti. Kwa hiyo, utaratibuusingefanana katika hiyo mifumo tofauti na tofauti yenyeweiko hivi, huku Bara tuna kikao cha Kamati ya Maendeleo yaKata yaani Ward C, wajumbe wake wanatoka kwenye vijijindiyo wanakwenda kwenye Kata, kwenye Ward C na ndichokikao ambacho kilichotumika cha uwakilishi wa vijiji hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Zanzibar kikao kamahicho hakipo, Kamati ya Maendeleo ya Kata Zanzibar haipo.Kwa hiyo, usingetegemea kitu ambacho hakipo Zanzibarkifanye kazi hiyo. Hiyo ndiyo tofauti ambayo MheshimiwaWaziri ameieleza. Namwomba Mheshimiwa Lissu aikubali hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Niseme hivi, suala la Katiba ni la Taifa na si lavyama. Kuna ushahidi unaonesha kwamba wajumbewaliochaguliwa kwenye vijiji ama mitaa, wamepata kuranyingi na wamechaguliwa na wananchi wengi,wamekwenda kuchujwa na wamepewa uwakilishi watuwaliopata kura chache, hiyo ni moja. (Makofi)

Page 263: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

263

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pili, kuna ushahidi wadhahiri, sheria inakataza Vyama kuingilia kabla hatujafikahatua ya referendum baada ya Bunge la Katiba. Kunaushahidi wa barua ya Asha-Rose Migiro, wameingiliamchakato kuelekeza viongozi wa Wilaya na Vijiji kwendakuingilia mchakato na kuchagua machaguo ambayo siyosahihi kisheria. Lakini Waziri amekiri kwamba, Diwaniamejichagua yeye na familia yake, huo ni mfano mmojaambayo unaelezea mifano mipana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwenyekiti wa Tume amekirikuna tatizo, anasema watu ambao hawajaridhika wakaterufaa. Ukipitia mwongozo ambao wametoa, watueleze kunamechanism ya kukata rufaa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niungane na hojaya Mheshimiwa Lissu kwamba, kuna tatizo, Waziri amekubali,Mwenyekiti wa Tume amekubali, turekebishe kwa manufaaya nchi. Hii Katiba ni zaidi ya CCM, ni zaidi ya CHADEMA, nizaidi ya NCCR Mageuzi na hali kadhalika ni zaidi ya CUF.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe tuWaheshimiwa Wabunge wenzangu kwa maslahi ya nchikwamba, hili suala siyo jepesi na tukisema tujigawe hapatwende kwa wananchi tumwage sumu huko hamtatoshakwa sababu kabla ya mwaka...

MBUNGE FULANI: Kamwage sumu wewe, usimtishemtu!

MHE. HALIMA J. MDEE: Kabla ya uchaguzi wa mwaka2010 na CCM ya sasa siyo....

WABUNGE FULANI: Kamwage! Kamwage sumu!

MWENYEKITI: Dakika tatu zimekwisha, MheshimiwaWaziri wa TAMISEMI!

Page 264: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

264

3 MEI, 2013

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): MheshimiwaMwenyekiti, nami napenda kuchangia hii hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosema NaibuWaziri kwamba, mifumo ya utawala ya Tanzania Zanzibar naTanzania Bara inatofautiana, wenzetu wametumia Shehia nasisi tumetumia Kata kwa sababu sisi Kata zetu nyingine zinavijiji mpaka nane na kila Kata inahitaji watu wanne. Ndiyomaana waliamua kila kijiji kifanye uchaguzi wa watu wanne.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ngazi ya kij i j iwananchi wote walishirikishwa na walivyokuja katika ngaziya Kata, wajumbe wa Baraza la Kata ni Wenyeviti wa Vijijiambavyo vinaunda Kata au mitaa kwa mijini. Hao Wenyevitiaidha wa mitaa kwa mijini au wa vijiji kwa maeneo yaHalmashauri wanatokana na vyama vyao. Sasa kama Wilayaambayo CHADEMA haina kijiji hata kimoja wala haina Diwanihata mmoja nikichukulia Halmashauri ya Mtwara Vijijini,CHADEMA haina Diwani, Mwenyekiti hata mmoja walaMwenyekiti wa Kitongoji hata mmoja. Hivi unategemeakwenye Baraza la Kata huyo wa CHADEMA ataingiaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa maana yawananchi wameshirikishwa katika ngazi ya Kata na Vijiji, lakiniwanaotakiwa ni wanne na Kata zetu za Bara ni kubwa, huwezikuwakutanisha wananchi zaidi ya 20,000 katika eneo moja,tofauti na Zanzibar ambapo Shehia zao zina watu kati ya3,000 na 4,000. Kwa hiyo, hatuwezi kuwa na mfumo mmojawa uteuzi kwanza wao wapo pamoja…

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Waziri na kwamamlaka niliyonayo naongeza dakika 30 baada ya saa yakuahirisha Bunge.

Mwanasheria Mkuu!

MWANASHERIA MKUU WA SERIKA: MheshimiwaMwenyekiti, nilishasema na narudia tena kusema kwamba,sina Chama. (Kicheko)

Page 265: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

265

3 MEI, 2013

MWENYEKITI: Mbona ninyi mna midomo jamani, kha!

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Sijasema kuwasijawahi kuwa mwanachama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi, hoja ni nini?Kwa sababu lazima kuna mtu aseme na mtu mwingineaamue na nawaomba sana Wanasheria waliomo Bungenikama mmesoma vizuri sheria, ni lazima mheshimu maamuzina mjenge hoja kwa kuangalia hoja, hoja ni nini? Je, Tumeya Mabadiliko ya Katiba katika kuamua hili imekosea?

WABUNGE FULANI: Ndiyo!

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Na kama ni ndiyo,imekosea wapi?

WABUNGE FULANI: Hapa! (Kicheko)

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Samahani kidogo,siwezi kujua, lakini najua kwamba watu wastaarabu kama niwanaume, wakiona mwanaume mwingine amesimamawananyamaza. (Kicheko)

WABUNGE FULANI: Kama ni wanawake?

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Kama nimwanamke mstaarabu yaani katika English if is a lady not awoman, kama ni lady anatakiwa kufumba tu mdomo. Sasaukimwangalia mwanamke au lady, wakati unazungumzaanakuonyesha midomo, basi unashindwa kujua kama umwa-dress kama ni lady au gentleman. (Kicheko)

MBUNGE FULANI: Twende kwenye hoja!

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Naomba kwasababu kila mtu ana nyongo juu ya hilo.

Mheshimiwa Halima nashindwa kuku-address kamani gentleman au ni lady. (Kicheko)

Page 266: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

266

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu ambachoMheshimiwa Tundu Lissu amekielekeza kinachoipa mamlakaTume kufanya haya, ni kile kifungu kidogo cha nane chakifungu kikubwa cha kumi na saba na naomba nikisome kwaurefu kwa sababu Mheshimiwa Tundu Lissu amekisomakuanzia katikati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, amesema hivi: “Isipokuwakama mazingira yatahitaji vinginevyo katika utekelezaji wamajukumu yake, Tume itabuni utaratibu unaofanana ambaoutatumika katika kila upande wa Jamhuri ya Muunganokatika ukusanyaji na uchambuzi wa maoni ya wananchi,uendeshaji wa Mabaraza na uandaaji wa ripoti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, usianze kusomakatikati, mazingira yanayozungumzwa hapa ni yapi? Kwaupande wa Zanzibar ngazi za mitaa kuanzia Shehia na siyosheria bali ni Shehia ambapo ndipo Sheha ana mamlaka yakuitisha mikutano. Ngazi ya Wodi au Ward ambayo ni sawana Kata kwa Tanzania Bara haina mikutano ya kisheria kwamujibu wa sheria namba moja ya Mamlaka ya Tawala zaMikoa ya Zanzibar ya mwaka 1998. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa TanzaniaBara, kwa busara za Tume, kuna utaratibu wa Kiserikali nahuo ndiyo uliotumika. Sasa hapa hoja ni hii kwamba, je, katikakufanya hivi Tume ilifanya makosa? Jibu lenu ni kwamba nindiyo na ni kweli kwa sababu kila mtu ana kichwa na hapatupo wengi. Kama ungekuwa wewe ungefanya hivyo, lakiniTume siyo wewe, bali Tume imefanya vile ilivyofanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kurudia tenakwamba, kila mtu mwenye macho na naona wenzangumnayo, anajua wakati gani Tume ilitoa mwongozo huu nawatu wakatakiwa kutoa maoni yao.

MBUNGE FULANI: Na si lazima yakubaliwe!

Page 267: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

267

3 MEI, 2013

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Sasa akitoa maoni,kama Mheshimiwa Tundu Lissu anapokwenda kwenyeMahakama ana-submit mbele ya Jaji tofauti na anavyofanyakwa Mheshimiwa Spika...

MBUNGE FULANI: Anajibu kama nani?

MWENYEKITI: Anajibu kwa niaba ya Serikali kamautakavyopewa wewe. Someni kanuni!

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, kwa hiyo, naona kwamba, Tume haijafanya kosalolote na imefanya kazi hizi kwa mujibu wa sheria. Nafikirituache kutumia Bunge hili kama kituo cha malalamiko, kwasababu nimeona tunaanza kutumia Bunge hili kama kituocha Polisi, malalamiko yanayohusu mambo ya hujumayanaletwa hapa. (Kicheko/Makofi)

MHE. JOHN J. MNYIKA: Kuhusu utaratibu.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Hakuna chautaratibu. (Kicheko)

MWENYEKITI: Naomba uendelee kusema.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Naendelea,hakuna cha utaratibu hapa! Hakuna cha utaratibu kwasababu Tume imefanya kazi yake. Nasema kwa mujibu washeria hii, Tume haijafanya kosa lolote na sheria hii tumetungasisi wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tundu Lissu, mtoa hoja.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana. Naomba nijibu hoja mbalimbali ambazozimetolewa na Wajumbe kama ifuatavyo:-

Page 268: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

268

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja hapa siyo uwiano waVyama katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Hoja ni je,Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba wanachaguliwa moja kwamoja na wananchi au wanapita kwenye chekecheke fulani?(Makofi)

Kwa upande wa Zanzibar, Wajumbe wa Mabarazaya Katiba ya Wilaya za Zanzibar, wamechaguliwa moja kwamoja na wananchi bila kujali itikadi za Vyama vyao na bilakujali uchama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa TanzaniaBara, Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilayawamechaguliwa moja kwa moja na wananchi kwenye vijijina mitaa, halafu wakapelekwa kwenye chekecheke fulanilinaitwa Ward C. Hiki ni chombo cha wanasiasa, Mwenyekitiwake ni Diwani, Katibu wake ni Afisa Mtendaji wa Kata,Wajumbe wake ni Wenyeviti wa Vijiji au Mitaa. Wote hawa niwanachama wa Vyama vya Siasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hil i chekecheke kwaTanzania Bara siyo chombo kilichoundwa na Sheria yaHalmashauri za Mitaa, si chombo chenye mamlakayaliyowekwa kwenye sheria, ni Kamati na ndiyo maanainaitwa Kamati. Lakini utaratibu wa kupata Wajumbe waMabaraza ya Katiba kwa kuwapitisha kwenye Kamati hii yawatu wanne au watano, wao ndiyo wanaoamua nani aendekwenye Baraza la Katiba, nani asiende. Hiyo ndiyo hoja.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine imetolewakwamba mifumo iko tofauti. Kama nilivyosema Zanzibarhawaiti Vijiji, wanaita Shehia. Ndiyo ngazi ya msingi kamailivyo kijiji kwa Tanzania Bara. Huku Bara ukitoka kwenye kijijiunakwenda kwenye Kata, ukiwa Zanzibar unakwendakwenye Wadi. Wadi kuna Diwani na Kata kuna Diwani. Diwaniwa Wadi wa Zanzibar anachaguliwa, Diwani wa Kata waTanzania Bara anachaguliwa. Kwa hiyo, zinafanana. (Makofi)

Page 269: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

269

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hoja ni kwamba, kwanini hizi ngazi ambazo zinafanana ziwe na utaratibu tofauti?Kwenye mkutano wa Shehia Zanzibar, wale wotewaliokusanyika kufanya uchaguzi jambo la kwanzawanachagua Mwenyekiti na Katibu wao. Kwa hiyo,Mwenyekiti wa Mkutano wa Katiba, Zanzibar anachaguliwana wananchi, anasimamia uchaguzi wa watuwatakaokwenda moja kwa moja kwenye Baraza la Katibala Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa Bara,Mwenyekiti wa Kijiji au Mtaa hachaguliwi na ule mkutanopale, ni Mwenyekiti by virtue of sheria ya Serikali za Mitaa.Kwa nini utaratibu uko tofauti kwenye ngazi zinazofanana?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu ni moja, ukija BaraWard C nyingi kama ambavyo tumesema mara nyingi, ni zaCCM na kwa hiyo Tume imetumia utaratibu wa Ward C ilikuhakikisha kwamba, wajumbe watakaokwenda kwenyeMabaraza ya Katiba ya Wilaya ni wana-CCM. Ndivyoambavyo imetokea na ndiyo maana ya hizo barua zaMwalimu wangu Dkt. Migiro na akina Nape Nauye nawengine humu ndani. Utaratibu huu wa kibaguzi, ndiyotunaoupigia kelele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Tume imetumiabusara zake. Nasita kusema busara za Tume hazikuwa sahihi.Busara za Tume kwenye jambo hili si sahihi, kwa sababu Tumehaiwezi ikatengeneza utaratibu wa kibaguzi unaokiukamakatazo ya ubaguzi kwenye Katiba yetu, halafu ikasemaina busara. Hizi si busara sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, walipoleta rasimu yamwongozo, tulipeleka maoni, haya tunayoyazungumzatumeyapigia kelele tangu mwezi wa Pili. Tume imeziba masikiona imefumba macho. Inatengeneza utaratibu ambao kamaambavyo imetokea Mabaraza ya Katiba ya Wilaya niMabaraza ya CCM.

Page 270: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

270

3 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hoja ni kwamba, Bungelako Tukufu siyo kituo cha malalamiko na sitaki kumbishiaMheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bunge si mahalipa malalamiko, Bunge ni mahali pa kuisimamia Serikali nakuiwajibisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge hili ni mahali pakuisimamia Tume ya Katiba, ikikosea inatakiwa isemwe hapakama ambavyo tumeisema. Kwa hiyo, hatujageuza Bungekuwa mahali pa kulalamika, hili Bunge ni mahali pakuisimamia Serikali na hii ni vema na haki kwa mujibu waKatiba yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume yenyewe imekubalikwamba, utaratibu ulikuwa mbovu, imekiri kulikuwa narushwa, kulikuwa na misukumo ya kisiasa, siasa ambazohaizisemi, lakini misukumo ni siasa za CCM. Barua zile za akinaAsha Migiro, Mwalimu wangu, maelekezo ya akina Msome,Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Katibu wa CCM wa Wilayaya Arusha, Ndugu Kingazi. CCM imehujumu mchakato waMabaraza ya Katiba, ndicho tunachokilalamikia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunataka Katibaitakayoongoza nchi hii kwa miaka 200 ijayo, mimi na wewetutakuwa tumekufa. Tunataka watoto wetu siku mojawaseme, we are proud of our parents. They did us proud.Kwa utaratibu huu, tunaelekea njia ya Zimbabwe ambayoni njia mbaya. Kwa utaratibu huu, tunaelekea njia ya Kenyakabla ya mwaka 2010 na utaratibu huu unatupeleka kwenyemaafa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba WaheshimiwaWabunge tafadhali, tafadhali, tuokoe Taifa letu, tutengenezeKatiba itakayokuwa worthy our while here. Nashukuru.(Makofi)

MWENYEKITI: Haya sasa tutafanya maamuzi, naombatusikilizane.

Page 271: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

271

3 MEI, 2013

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kukataliwa)

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1002 - Finance and Accounts… … … Sh. 399,255,000/=Kif. 1003 - Policy and Information

Services… … … … … … … … Sh. 642,746,000/=Kif. 1004 - Internal Audit Unit… … … … … Sh. 215,657,000/=Kif. 1005 - Government Communication

Unit… … … … … … … … … Sh. 288,905,000/=Kif. 1006 - Procurement Management

Unit… … … … … … … … … Sh. 283,013,000/=Kif. 1007 - Management Information System

Unit… … … … … … … … …Sh. 265,587,000/=Kif. 2004 - Public Legal Services Unit… … ...Sh. 511,780,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 4001 - Constitutional Affairs … … … … Sh. 191,389,000/=

MWENYEKITI: Mheshimiwa Rashid ulisimama?

MHE. RASHID ALI ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti,Ndiyo. Niko kwenye kasma ya 221200, Communication andinformation. Mwaka jana ilikuwa sh. 6,480,000/= lakini marahii sijui hamna fedha. Je, mwaka huu hamna informationyoyote au ni vipi?

MWENYEKITI: Mmeipata sub-vote 4001,communication and information.

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, shughuli hizo zimehamishiwa katika sub-vote 1005ya Government Communication Unit.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 272: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

272

3 MEI, 2013

Fungu 55 – Tume ya Haki za Binadamuna Utawala Bora

Kif. 1001 - Administration and Human Resources Management… … Sh. 2,232,686,000/=

Kif. 1002 - Finance and Accounts… … … Sh. 234,343,000/=Kif. 1003 - Internal Audit Unit… … … … …Sh. 124,790,000/=Kif. 1004 - Legal Service Unit… … … … …Sh. 355,704,000/=Kif. 1005 - Procurement Unit… … … … … Sh. 177,280,000/=Kif. 1006 - Management Information

System Unit… … … … … … ...Sh. 213,307,000/=Kif. 2001 - Administrative Justice… … … …Sh. 850,337,000/=Kif. 2002 - Human Rights… … … … … … Sh. 595,448,000/=Kif. 2003 - Research and Documentation… Sh. 309,975,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 2004 – Public Education and Training… … … … … … … ..Sh. 273,933,000/=

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kifungu hicho 2004 cha Elimu kwa Umma pamoja na mafunzo,kasma 221200 Communication & Information. Kasma hiimwaka wa fedha uliopita ilitengewa shilingi milioni 19.6,mwaka huu kiwango cha fedha kimeshuka mpaka milioni1.2 peke yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana wakati wakupitishwa kwa kifungu hiki nilieleza kwamba, niliwasilishamalalamiko rasmi ya kimaandishi kwa niaba ya wananchiwa Kata ya Goba, kuhusiana na matatizo ya maji ya DAWASAna Manispaa ya Kinondoni, ambayo naamini Tume ya Hakiza Binadamu inaelewa vizuri jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kulikuwa kuna tatizo lanamna gani Tume inatoa elimu kwa umma na inawasilianana umma pale ambapo malalamiko yanatokea. Maelezoniliyokuwa nimepewa ni kwamba, kiwango cha fedhaambacho Tume inacho kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma

Page 273: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

273

3 MEI, 2013

ni kidogo sana, kwa wakati huo ikiwa shilingi milioni 19.6. Sasakile kiwango cha milioni 19.4 ambacho kilikuwa kinaonekanani kidogo, safari hii kimeshuka zaidi na kuwa shilingi milioni 1.2peke yake katika wakati ambapo Tume ina malalamikomengi, inahitaji kufanya mawasiliano na umma, ina mambomengi ambayo inayafanyia uchunguzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ningependakupata ufafanuzi kutoka kwenye Wizara, ni kwa nini kiwangohiki cha fedha kimeshuka na hakikisho la kwamba, kiwangohiki hakitaathiri uchunguzi wa tuhuma za ufisadi wa maji katikaKata ya Goba ambayo nilikuwa nimeishawasilisha kwenyeTume? Naomba maelezo.

MWENYEKITI: Maelezo mengine hayo hayahusiani nahapa. Kuuliza kwamba kwa nini fedha zimepungua, hiyo safi.Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba maelezo, umekionalakini?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, katika fungu la utawala, tumetenga shilingi milioni58 kwa ajili ya shughuli hiyo. Pia ningependa kumhakikishiaMheshimiwa Mbunge kwamba, haiwezi kuathiri utatuzi wamigogoro; elimu kwa umma ni elimu kwa umma, lakini piautatuzi wa migogoro na ushughulikiaji wa malalamiko ni kitukingine tofauti. Kwa hiyo, nimhakikishie kwamba, tutafuatiliana Tume itaweza kufanya kazi zake kwa umakini. Fungu laelimu kwa umma limewekwa katika Government andCommunication Unit, Idara ya Utawala.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 3001 - Zanzibar Office … … … … … Sh. 242,992,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi pamoja na marekebisho yake)

Page 274: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

274

3 MEI, 2013

Fungu 59 – Tume ya Kurekebisha Sheria

Kif. 1001 - Administration and Human Resources Management… … Sh. 3,431,560,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

MIPANGO YA MAENDELEO

Fungu 16 – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Kif. 3001 - Civil Litigation and Arbitration Division… … sh. 0Kif. 3002 - Treaties and Contracts

Division… … … … … … … … sh. 826,000,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 35 – Mkurugenzi wa Mashtaka

Kif. 2002 Public Prosecution Division… … sh. 2,167,759,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 40 – Mahakama

Kif. 1001 - Administration and Human Resources Management… … sh. 42,716,668,000/=

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbowe na MheshimiwaHalima nimekuona. Mheshimiwa Mbowe!

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimi Mwenyekiti, sub-vote 1001, kifungu 6312 Construction and Rehabilitation ofPrimary Court buildings.

Napenda tu kumuuliza Mheshimiwa Waziri kama ileMahakama ya Mwanzo ya Machame iko katika fungu hili.

Page 275: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

275

3 MEI, 2013

MWENYEKITI: Sawa! Sijui kama mnaweza kujibu.

NAIBU WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwa bahati mbaya haipo na hii inatokana na ukomo wabajeti. Kama ambavyo Mheshimiwa Waziri alieleza asubuhi,alitaja kabisa ni Mahakama zipi ambazo zitajengwa kupitiafedha hizi, zikiwemo Mahakama za Mwanzo za Gairo,Ludewa, Lukuledi, Mangaka, Bunda, Bariadi, Nyamikoma nanyinginezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti,kifungu kidogo hicho hicho cha 6312, Construction andRehabilitation of Primary Court buildings, nilitaka nipate kauliya mwisho ya Serikali.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Halima tukiishakijibu kilehuwezi kuuliza tena.

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti,hapana, inahusu Mahakama nyingine.

MWENYEKITI: Aah, sasa ndiyo kimejibiwa hapa.Mheshimiwa Waziri amejibu extensively.

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa… aah!

MWENYEKITI: Hapana!

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Bunge zima bila mabadiliko yoyote)

Fungu 41 – Wizara ya Katiba na Sheria

Kif. 1001 Administration and Human Resources Management… … sh. 3,017,560,000/=

Page 276: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

276

3 MEI, 2013

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: MheshimiwaMwenyekiti, niko kwenye kifungu kidogo 6210, kuhusiana nautekelezaji wa Mradi wa Kupambana na Rushwa...

MWENYEKITI: Ngoja kwanza, tuko ukurasa wa 53,kifungu cha 1001, mbona hicho cha kwako sisi hatukioni?

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Kuna marekebisho.

MWENYEKITI: Angalia vizuri labda ni kingine.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif . 1003 – Policy and Information Services… … … … … … … sh. 4,881,280,00/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 55 - Tume ya Haki za Binadamuna Utawala Bora

Kif. 1001- Administration and Human Resources Management… … … sh. 206,414,000/=

Kif. 1004 - Legal Services… … … … … … … … ... ..sh. 0Kif. 2001- Administration Justice… … … … sh. 52,000,000/=Kif. 2002 - Human Rights… … … … … … sh. 597,575,000/=Kif. 2003 - Research and Documentation… sh. 52,180,000/=Kif. 2004- Public Education and

Training… … … … … … … ...sh. 126,000,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 59 - Tume ya Kurekebisha Sheria

MWENYEKITI: Hapa mtaona mmegawiwa karatasiinasema, Tume ya Kurekebisha Sheria Fungu 59, idadi ya pesa

Page 277: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

277

3 MEI, 2013

pale mwanzo zil ikuwa hazipo zimerudishwa milioni616,350,000. Mmeona hiyo karatasi.

Kif. 1001 – Administration and Human Resources Management… … …sh. 616,350,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

(Bunge lilirudia)

TAARIFA

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika,naomba kutoa taarifa kwamba, Kamati ya Matumizi imepitiaMakadirio ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka waFedha 2013/2014, kifungu kwa kifungu na kuyapitisha pamojana mabadiliko yake. Hivyo, naomba kutoa hoja kwamba,Makadirio hayo sasa yakubaliwe na Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwe na Kuafikiwa)

(Makadirio ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwakawa Fedha 2013/2014 yalipitishwa na Bunge )

SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya WaziriMkuu.

HOJA YA KUTENGUA KANUNI

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBUNA BUNGE: Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja chini yaKanuni 153(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo 2013kama ifuatavyo:-

Page 278: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

278

3 MEI, 2013

KWA KUWA Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge wakushughulikia Bajeti ya Serikali pamoja na Shughuli nyingineza Bunge zilizopangwa umepangwa kumalizika tarehe 28Juni, 2013;

NA KWA KUWA ratiba ya Shughuli ya zote zilizopangwakufanyika katika Mkutano huu wa Kumi na Moja zimepangwakwa kuzingatia Kanuni 99(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge,Toleo 2013;

NA KWA KUWA tarehe 25 Aprili, 2013 MheshimiwaSpika, baada ya kuzingatia michango ya WaheshimiwaWabunge wakati wakichangia hotuba ya Bajeti ya Wizaraya Maji, alisitisha shughuli zilizokuwa zikiendelea na kuagizaSerikali kukaa na Kamati ya Bunge ya Bajeti ili kuonauwezekano wa kuongeza fedha kwa Bajeti ya Wizara ya Maji,jambo lililohitaji siku nyingine ya kuhitimisha hotuba ya bajetiya Wizara hiyo;

NA KWA KUWA majadiliano ya Bajeti ya Wizara hiyoyaliendelea siku ya Jumatatu tarehe 29 Aprili, 2013 ambayoawali ilipangwa kujadili hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maliasililna Utalii.

NA KWA KUWA katika Kikao cha Kamati ya Uongoziya Bunge kilichofanyika katika Ukumbi wa Spika, tarehe 2 Mei,2013, Wajumbe wote wa Kamati hiyo waliohudhuriawaliazimia kuliomba Bunge likubali kufanya kazi siku ya tarehe4 Mei, 2013 ili kujadili hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ulinzi naJeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka 2013/2014;

NA KWA KUWA kwa mujibu wa Kanuni ya 28(15) yaKanuni za Bunge, Toleo 2013 Bunge haliwezi kukutana nakufanya kazi siku ya Jumamosi, Jumapili au siku ya Mapumziko.

NA KWA KUWA ili kuliwezesha Bunge kuweza kukutanasiku ya Jumamosi tarehe 4 Mei, 2013 ni lazima Bunge litenguekanuni 28(15) ya Kanuni za Bunge, Toleo 2013 kwa mujibu waKanuni ya 153(1);

Page 279: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

279

3 MEI, 2013

HIVYO BASI Bunge linaazimia kwamba, kwamadhumuni ya utekelezaji bora wa Shughuli za Bunge katikaMkutano huu wa Kumi na Moja Kanuni 28(15) kitenguliwakama ifuatavyo:-

Kanuni 28(15) ambayo kwa ujumla wake kinaelekezakwamba Bunge halitakutana siku ya Jumamosi, Jumapili nasiku za Mapumziko itenguliwe na badala yake Bunge likutanesiku Jumamosi yaani kesho tarehe 4 Mei, 2013 kuanzia SaaTatu Asubuhi hadi Saa Nane Mchana isipokuwa kwamba sikuhiyo hakutakuwa na kipindi cha Maswali.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika,naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

SPIKA: Kwa hiyo, kesho Waheshimiwa Wabunge,tutakuwa na kikao cha Bunge na ni Wizara ya Ulinzi na Jeshila Kujenga Taifa na ni Wizara ambayo katika hali ya kawaidani ya siku moja. Kwa sababu sisi wenyewe tulipanga nakuchagua kuizungumza Wizara ya Maji kwa kirefu na kwaundani na kukawa na mafanikio, basi tukubali gharama yakenyingine ambayo ni kufanya kikao kesho.

La pili, Waheshimiwa Wabunge, naona kuna tabiaambayo siyo nzuri. Tukisoma Kanuni yetu ya 66(1)na(2)inasema hivi: “Wakati wa Vikao vya Bunge Spika anapokuwaanaingia au kutoka katika Ukumbi wa Bunge, Wabunge nawageni wote waliopo kwenye Ukumbi huo watasimama kwautulivu mahali pao na kubaki kimya hadi Spika atakapokuwaameketi katika kiti chake au atakapokuwa ametoka kwenyeUkumbi wa Bunge.” Yaani ninapoingia mnatakiwa msimamekimya na ninapotoka.

Waheshimiwa Wabunge, lakini ya pili, inasema:“Wakati Bunge linaingia kwenye Kamati ya Bunge Zima au

Page 280: 3 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

280

3 MEI, 2013

katika Kamati ya Matumizi, Wabunge na wageni wotewaliopo kwenye Ukumbi wa Bunge watasimama kwa utulivumahali pao na kubaki kimya ili kutoa heshima kwa mchakatowa Bunge kuingia kwenye Kamati ya Bunge Zima au kwenyeKamati ya Matumizi na baadaye Bunge Kurejea.”

Sasa naona wakati tunakwenda kubadilisha nguokule wengine wanaanza kuzungumza, huyu anaweka Siwahapo, Waheshimiwa wanaendelea kuzungumza sivyokinachozungumzwa. Waheshimiwa Wabunge hii ndiyo kaziyetu na ni mahali petu, tusiposhika adabu za humu ndani,tutakuwa kama mahali pengine popote pale pasipokuwahata na busara zozote. Tuelewane tujadiliane kwa hoja nasiyo kufanya vitu ambavyo vinakuwa ni sehemu ya fujo yakazi zetu. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, nadhani siku ya Jumapilikuna Kamati zingine zitakuwa na Semina, kwa hiyo, nadhaniwanaohusika watawaambieni. Lakini kesho tutakuwa naKikao cha Bunge Saa Tatu Asubuhi. Kwa hiyo, naahirisha Kikaocha Bunge mpaka Kesho Saa Tatu Asubuhi.

(Saa. 2.08 Usiku Bunge liliahirishwa mpaka Siku yaJumamosi, Tarehe 4 Mei, 2013 Saa Tatu Asubuhi)