20
Soma Uk. 12 Propaganda imekaa vizuuri Lakini ujumbe sio wenyewe Salamu za Maulid, Krismasi: Haya ndiyo majipu ya kutumbuliwa Isidingo ya kesi za Waislamu… Mwaka wa pili sasa bado Polisi wanatafuta ushahidi, upelelezi Mahakama yataka waharakishe! SHEIKH Msellem. IGP Mangu. Soma Uk. 20 ISSN 0856 - 3861 Na. 1209 RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA , DESEMBA 25-31, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected] UAMUZI wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kubatilisha uchaguzi hauna msingi wowote wa kisheria. Ni batili tangu mwanzo. Ni uamuzi uliofanywa kwa matakwa binafsi Diapora waandamana New York Uchaguzi haufutwi kama kufuta ubao ili kulinda maslahi ya watawala. Hauwezi kufuta uchaguzi kirahisi kama kufuta ubao. Hata Umiss wa Sii Mtemvu haukufutwa kirahisi namna hiyo. (Habari Uk. 11) Hawa ndio wanaharakati RAIS Magufuli alipokutana na Maalim Seif Ikulu jijini DSM. ANNUUR NEW.indd 1 12/24/2015 1:43:05 PM

ANNUUR 1209aaa

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: ANNUUR 1209aaa

Soma Uk. 12

Propaganda imekaa vizuuriLakini ujumbe sio wenyewe

Salamu za Maulid, Krismasi:

Haya ndiyo majipu ya kutumbuliwa

Isidingo ya kesi za Waislamu…Mwaka wa pili sasa bado Polisi wanatafuta ushahidi, upelelezi

Mahakama yataka waharakishe!SHEIKH Msellem. IGP Mangu.Soma Uk. 20

ISSN 0856 - 3861 Na. 1209 RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA , DESEMBA 25-31, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected]

UAMUZI wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kubatilisha uchaguzi hauna msingi wowote wa kisheria. Ni batili tangu mwanzo.

Ni uamuzi uliofanywa kwa matakwa binafsi

Diapora waandamana New York

Uchaguzi haufutwi kama kufuta ubao

ili kulinda maslahi ya watawala.

H a u w e z i k u f u t a uchaguzi kirahisi kama kufuta ubao. Hata Umiss wa Sitti Mtemvu haukufutwa kirahis i namna hiyo. (Habari Uk. 11)

Hawa ndio wanaharakati

RAIS Magufuli alipokutana na Maalim Seif Ikulu jijini DSM.

ANNUUR NEW.indd 1 12/24/2015 1:43:05 PM

Page 2: ANNUUR 1209aaa

2 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

Aal Imran: 102

Fethullah-Gulen“ E N Y I w a l e a m b a o m m e a m i n i , m c h e n i Mwenyezi Mungu ukweli wa kumcha kwake na msife isipokuwa hali ya kuwa nyinyi ni Waislamu”. [Aali-Imran 102]

K u m c h a M w e n y e z i Mungu ukweli wa kumcha k w a k e k u n a k w e n d a sambamba, moja kwa moja na kumjuwa Mwenyezi M u n g u m t u k u f u . K wa sababu hii kunawezekana kusema kwamba maarifa yote ambayo hayatusaidii juu ya nyongeza ya maarifa haya, hayakuwa isipokuwa ni maarifa ya nje tu. Na ni msemo unaoeleza kuwa maarifa hayo ni porojo tu. Ni hivyo hivyo, mazungumzo yoyote au makumbushano yoyote au maswali na majibu ambayo hayasaidii juu ya kuyajua maarifa haya, huko

ni kuutumia vibaya wakati na kuvuka mpaka katika maneno.

A m e a s h i r i a M t u m e (s.a.w.) kwenye hakika hii wakati aliposema “kwa hakika Mwenyezi Mungu amechukua kwenu mambo matatu na katika mapokezi mengine: Hakika Mwenyezi Mungu ameharamisha juu yenu (mambo matatu)” akataja katika mambo hayo, kufanya wingi kuuliza na akataja mfano wa maswali hayo luwa ni kama, “Nani aliyeumba kitu kadha ni nani aliyeumba kitu kadha mpaka akasema: Ni nani aliyemuumba Bwana wako”.

Tunaona kuwa ni jambo lenye faida, tuulete kwa mtiririko mtazamo wetu, kuhusiana na jambo la m w i s h o . K w a h a k i k a zilitupitia zama walituambia katika zama hizo, kuhusu s a b a b u k a n a k wa m b a Mwenyezi Mungu mtukufu (kutakasika ni kwake) ni m w e n y e k u s h i n d w a n a k w a m b a s a b a b u ndizo z inazofanyakazi n a k u t e k e l e z a m a m b o mbalimbali, na zinapatisha kila kitu, wakati wanapoutaja u g o n j w a w a s a r a t a n i wanasema: huu ni ugonjwa ambao hauna t iba . Na wakati ulipodhihiri ugonjwa

wa UKIMWI, walisema: Hapatarajiwi kwa ugonjwa huu kupona. Ehee ni kama hivyo, wamebomoa mbele za muumini msingi wa kumtegemea Mwenyezi Mungu na kujisalimisha kwake. Na jambo hili lipo hivi sasa kwa uchache au kwa wingi mbele za watu wote. Ninaona kwamba kunapasa juu yetu kwa njia ya kutafiti na kufuatilia kufika kutoka katika athari na kwenda kwa mwenye kuathiri. Ili kupata utulivu wa moyo, na kuelewa kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu ndiye mwenye kuzisababisha hizo sababu zote, na kwamba yeye ndiye aliyezipa hizo sababu uwezo wake na sifa zake na kukumbuka siku zote kwamba yeye ana uwezo wa kuumba na kupatisha nje ya duara ya sababu. Tutafanya upya kuendelea kwa fikra zetu za kiimani.

Hakika kuhangaika na kutoa juhudi kwa ajili ya kumcha Mwenyezi Mungu ukweli wa kumcha kwake maana ni kukumbuka kumcha na kumuogopa wakati wote na katika hali zote na kuipa umuhimu kila nyenzo na sababu inayopelekea kwenye hisia hii ya kweli na kutoa nafasi kupatikana myanya yoyote, kati ya maisha na kati ya lengo la maisha haya na shabaha zake na kutokezea katika maneno yoyote au t u k i o a u m a z u n g u m z o ambayo kunawezekana kumvuta na kumbadilisha kwa ajili ya kumkumbusha lengo hilo na kudumisha kumsifu na kumshukuru juu ya neema zake nyingi ambazo hazihesabiki na hazidhibitiki.

Ni jambo la lazima kwa ajili ya kuanzia kwenye njia ya uchaji iliyo ya kweli. Na jambo hili wakati huo huo ni dhamana kwa muumini, pindi atakapokufa afe juu ya imani na hiyo ni hali yenye kuridhiwa na hasa kwa Mitume watukufu na warithi wa Mitume katika watu wenye hali na sifa pekee. Na walikuwa maswahaba watukufu, wanamwabudu Mwenyezi Mungu mpaka inavimba miguu yao na zinadhoofika nafsi zao kwa ajili ya kupata daraja la uchaji na kufika kwenye lengo hili na kwa hakika katika uwezo wao juu ya msingi wa “mcheni Mwenyezi Mungu kiasi mnachoweza”. [Al-Haghabun 16] na hilo walilifanya maisha yao yote.

Jee Unajua?

MASUALA1.Mwaka waliozaliwa Mtume Muhammad (SAW). Jawabu: 5702.Mwaka aliohama Mtume Muhammad (SAW) kwenda Madina. Jawabu: 6223.Mwaka aliofariki Muhammad (SAW). Jawabu: 6324.Ukoo wa Mtume Muhammad (SAW). Jawabu: Bani Hashim5.Mamake Mtume Muhammad (SAW) alimpa jina gani? Mohammed, Ahmad, Abass. Jawabu: Mohammed6.Muhammad (SAW) alivyokwenda Syria alifwatana na nani katika ukoo wake? Abu Talib, Abdul Mutalib, Abubakar. Jawabu: Abu Talib7.Kwanini Bibi KHadija alitaka aolewe na Mtume Muhammad (SAW) Uzuri, Uaminifu, Umaarufu. Jawabu: Uaminifu8.Majina aliokuwa akijulikana Mtume Muhamad (SAW) Jawabu: Ahmad9.Mtume Muhammad (SAW) kabla ya kupewa Utume akijitenga katika eneo gani? Jawabu: Pango la Hira.10.Idadi ya Waislamu wa mwanzo kusilimu walikuwa wangapi? Jawabu: 40

JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 31

CHEMSHA BONGO: 32Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.

MASUALA1.Mtume Muhammad (SAW) alikufa akiwa na umri wa miaka mingapi? 53, 63, 732.Sahaba yupi akiitwa Al-Farooq?3.Sahaba gani akiitwa upanga wa Mungu?4.Sura ipi ukiendeleza kuisoma katika nyakati za Al-Asri utaondokewa na umaskini?5.Sahaba gani alimshauri Mtume Muhammad (SAW) kuchimba Khandaki katika vita vya Khandaq?6.Mji wa Madina kabla ya kuhamia Mtume Muhammad (SAW) ukiitwaje?7.Alipokuwa Mtume Muhammad (SAW) anaumwa nani akiongoza Sala, akiwa Imamu?8.Msikiti unaoitwaje alioujenga Mtume Muhammad (SAW) mara tu alipowasili Madina?9.Jina la mwanzo la Imam Abu Hanifa?10.Mtume gani alirembewa kwenye moto?

1.Kuwa kuna miripuko ya Volcano ambayo bado yanaendela na kuripuka mara kwa mara baadhi yao ni Yellow Stone Caldera ya Marekani, Mt. Vesuvius, Italy,Popocatapel ya Mexico, Sakurajima ya Japan: http://www.curiosityaroused.com/nature/10-most-dangerous-active-volcanoes-around-the-world/

2.Miji nchini Marekani ilio na uhalifu wa hali ya juu, ukitembelea huko ujihadhari na miji hio ikiwa ni East St. Louis uliopo Illinois, Canden katika mji wa New Jersey, Flint uliopo Michigan, West Memphis uliopo Arkansas, Saginow uliopo Michigan: http://www.curiosityaroused.com/world/the-10-most-dangerous-cities-in-america-in-2013/

3.Nyoka wenye sumu ni wengi kati ya hao ni Mkunga aonekaye baharini nyoka huyu akitoa sumu yake kwa milligram ndogo tu inaweza kuuwa watu alfu na zaidi: http://www.curiosityaroused.com/nature/10-most-dangerous-snakes-in-the-world/

4.Nchi inayoongoza kuwa na wanajeshi wengi ni China ikiwa ina wanajeshi 2,285,00, Marekani 1,429,995, India 1,325,000, Korea ya Kaskazini 1,106,000, Urusi 1,027,000, Korea ya Kusini 687,000, Pakistan 617,000, Iraq 578,269, Iran 523,000, Uturuki 510,000: http://www.curiosityaroused.com/world/the-10-largest-armies-in-the-world/

5.Wanamapinduzi waliokuja kuleta mabadiliko katika dunia hii? Namba moja ni Che Guevera wa Cuba, akifwatiwa na Martin Luther King Junior wa Marekani, George Washington wa Marekani, Bibi Eva Peron wa Argentina, Malcolm X wa Marekani, Adolf Hitler wa Ujerumani, T.E. Lawrence, Isaac Newton wa Uiengereza, Galileo Galilei wa Utaliano, Henry Ford wa Marekani, : http://www.curiosityaroused.com/history/10-most-famous-revolutionaries-in-history/

6.Mtu aliosajiliwa kuwa mfupi kuliko wote anaishi Nepal aitwaye Chandra Bahadur Dangi akiwa na urefu wa Centimeter 21.5: http://www.curiosityaroused.com/culture/who-is-the-smallest-person-in-the-world/

7.Ikulu ya Marekani ijulikanao kwa jina la White House ina vyumba 132, sehemu za kukogea 35, ngazi za kupandia kama 8, maeneo 28 ya kuepukana na moto, madirisha 147 milango 412, kiwanja cha kuchezea Tennis, kufanya mazowezi ya Jogging, Chumba cha Snema, Bwawa la kuogolea: http://www.curiosityaroused.com/politics/how-many-rooms-are-in-the-white-house/

8. Mlima Matterhon uliopo Switzerland ni Mlima wenye haiba na kupendeza: http://www.curiosityaroused.com/nature/10-of-the-most-beautiful-mountains-in-the-world/

A L A M E E N 40 50 60 70 80 100 200

U A M I N I F S A H A B A I

A L S A D I Q U M A Y A A A

A B A S I M U A W I Y A U I

A W S K H A R J I H I J R A

P A N G O L A H I R A I S H

A L F A J R I S H A A S R I

B A N I H A S H I M H I S H

A M I N A B I N T W A H A B

570 A H M A D 576 635 632 621 767 555 622 435

U T H M A N M U A D H K N U

I B R A H I M A D D U L U M

J A M A L U R W A S A D M A

K H A L D U N R I D H A A R

S U L E M A N F A R S Y A A

A B U B A K A R J A M A N L

W A A Q I Y A H M I K I D I

M A S J I D Q U B A A A M U

K H A L I D B I N W A L I D

63 73 P Y A T H R I B 53 N U R

ANNUUR NEW.indd 2 12/24/2015 1:43:13 PM

Page 3: ANNUUR 1209aaa

3 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015

Habari/Makala

TAREHE 7 Machi 1965, mamia ya Wamarekani Weusi na Weupe

wenye msimamo wa haki sawa kwa raia wote wa taifa hilo walikusanyika kwenye kitongoji kiitwacho Selma katika jimbo la Alabama kwa nia ya kuandamana hadi makao makuu ya jimbo hilo Montgomery kwa lengo la kupigania haki ya Mmarekani Mweusi kutumia haki yake ya kikatiba ya kupiga kura. Mfumo uliokuwapo Marekani wakati huo ulikuwa unawazuwia Wamarekani Weusi kutumia haki hiyo, ingawa ilishawekwa kwenye katiba ya nchi takribani miaka 100 nyuma kupitia kile kiitwacho Marekebisho ya 15 ya Katiba ya Marekani. Lakini wakati wanafika kwenye Daraja la Edmud Pettus, vyombo vya usalama vikawashambulia na kuwajeruhi vibaya wengi wao.

Siku mbili baadaye, mpigania haki Dk. Martin Luther King, akawakusanya watu wengine wapatao 2,500 kurudi tena kwenye Daraja la Edmund Pettus kabla ya kugeuza na kurejea nyuma kwa kuheshimu amri ya mahakama iliyowazuia kufanya maandamano kamili.

Tarehe 21 Machi, waandamanaji wanaokisiwa kufikia 25,000 wakaungana kuelekea Montgomery na wakafanikiwa kuingia kwenye mji huo mkuu wa Alabama. Siku nne baadaye, waandamanaji hao wakaingia kwenye lango la makao makuu ya serikali ya Alabama wakiwa wamesaini barua dhidi ya Gavana George Wallace.

Miezi michache baadaye, bunge la Marekani (Congress) likapitisha mswaada wa Sheria ya Haki ya Kupiga Kura ambayo Rais wa wakati huo, Lyndon B. Johnson, aliisaini kuwa sheria kamili tarehe 6 Agosti 1965. Sheria hiyo ilikusudiwa kuondosha vikwazo ambavyo aliwekewa Mmarekani Mweusi katika ngazi zote – tangu serikali za mitaa hadi majimbo – kumzuia kutumia haki yake ya

Siasa ya Selma na ya ZanzibarNa Mohamed Ghassany

WAMAREKANI Weusi wakiandamana kudai haki zao za kiraia nchini humo Machi, 1965.

kupiga kura akiwa kama raia na kama anavyopewa haki hiyo na katiba karne nzima nyuma.

Mkasa huu maarufu kama Maandamano ya Selma kwenda Montgomery umesimuliwa tarehe 7 Machi 2015 kwa muhtasari kwenye mtandao wa Ikulu ya Marekani, White House. Hapa nimeukariri na kuutafsiri kwa lengo maalum la kueleza mshabihiano baina ya Marekani ya miaka 50 nyuma na Zanzibar ya leo kwa kutumia hadithi yangu binafsi. Nitaisimulia.

Uchaguzi wa kwanza kabisa wa vyama vingi tangu baada ya Mapinduzi ya 1964 uliofanyika Zanzibar mwaka 1995, ulinikuta nikiwa na miaka 18 na nikiwa kijijini kwetu nilikozaliwa na kukulia kisiwani Pemba. Huo ndio uchaguzi pekee nilioweza kupiga kura hadi sasa. Chaguzi nyengine mbili – ule wa 2000 na 2005 nilizuiwa na masheha – na uchaguzi wa 2010 ulifanyika nikiwa sipo tena Zanzibar. Hapo katikati yake pia palifanyika upigaji kura mara mbili, ambao pia sikuruhusiwa na masheha. Nitafafanua.

Uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 ulinikuta kisiwani Unguja, ambako nilihamia tangu mwaka 1996 kwa ajili ya masomo. Nilianza maisha nikiwa dakhalia ya Tumekuja, kisha nikachukuliwa na jamaa yangu kukaa naye Mkunazini, kisha nikahamia Mtendeni. Mote humo muna shehia tafauti, ingawa ni jimbo

moja kwa sasa.Kwa hivyo wakati

uchaguzi unakuja, nilikuwa nimeshahama na kuhamia shehia tatu ndani ya kipindi cha miaka minne. Licha ya kwamba kila nilipohama na kuhamia nilichukuwa barua ya sheha mmoja kwenda kwa mwengine, hakuna sheha aliyenikubali kuwa mimi ni mkaazi wake kwa kipindi nilichotakiwa kujiandikisha kupiga kura.

Kama ilivyokuwa kwa Mmarekani Mweusi wa kabla ya mwaka 1965, ndivyo ilivyokuwa kwangu. Katiba ya nchi inaniruhusu kupiga kura, lakini kuna kanuni na sheria za kuwa mpiga kura zinazosimamiwa na mamlaka za kati na chini, ambazo zilinizuwia kupiga kura.

Baina ya mwaka 2001 na 2003 niliishi shehia ya Mpendae na uchaguzi wa 2005 ulifanyika nikiwa mkaazi wa kudumu wa shehia ya Kibweni, ambako hadi leo ndipo yalipo maskani yangu, lakini nilikuwa nimehamia hapo mwanzoni mwa mwaka 2004. Si sheha Haji Seti wa Mpendae wala Bi Asha wa Kibweni waliokuwa tayari kunipa haki yangu ya kupiga kura. Kwa wote wawili, mimi sikuwa na sifa za kutosha kuwa mpiga kura.

Hata kura ya maoni ya mwaka 2010, ambayo ilinikuta nikiwa mkaazi wa kudumu wa shehia ya Kibweni kwa miaka sita, hali ilikuwa hiyo hiyo. Sheha alisema hajui ikiwa kwenye nyumba

Na. SK/108 munakaa watu, na kama wanakaa hajui ikiwa jina langu ni miongoni mwa yaliyomo kwenye daftari lake. Nyumba hiyo niliijenga kwa jasho langu na katika kila hatua ya ujenzi wake ilipatiwa na ililipiwa vibali vya serikali.

Miradi na shughuli nyengine zote za kiserikali huwa inahusishwa kama vile kampeni ya kupambana na malaria, sensa na nyenginezo. Watoto wangu wanne walizaliwa kwenye nyumba hiyo baina ya mwaka 2004 na 2010. Lakini baba yao hakuwahi kustahiki kuwa mpigakura halali kwa mujibu wa sheha na nguvu alizopewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mwaka jana katika nchi hii niliyopo sasa palikuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa na mabaraza ya miji. Siku moja nimerudi nyumbani kwangu kutoka kazini, nikakuta barua kutoka baraza la mji wa Bonn ikiniarifu kwamba kuna kampeni za uchaguzi wa vyama zinafanyika na ikiwa ningependelea kushiriki.

Siku nyengine nikakuta barua kutoka kwa wagombea mbalimbali wakinishawishi kuwapigia kura. Siku nyengine nikakuta karatasi ya kura imetumwa na jina la kituo ninachoweza kupiga kura, tarehe na saa kwa ajili ya kumchagua mwakilishi wangu kwenye baraza la mji ambaye atatetea maslahi ya kundi langu la wahamiaji. Nikamuonesha

mke wangu barua. Hatukuweza kujizuwia. Mimi na yeye, sote kama tumeambiana tukajikuta tunalia. Machozi hayakauki.

Nchi iliyonizaa na kunilea kwa miaka 33 ya uhai wangu ilininyima haki yangu ya kikatiba ya kupiga kura takribani mara nne ndani ya kipindi cha miaka 15. Nchi niliyohamia kwa dharura ya miaka michache, inanipa haki hiyo ndani ya kipindi cha miaka minne.

Zanzibar sasa inaelekea kwenye uchaguzi mwengine mkuu (ushafanyika tayari). Ni bahati mbaya kwamba sipo ndani ya nchi, lakini kwa hakika kabisa ningelirejea tena kituoni kwenda kujiandikisha, hata kama sheha wangu angelisimama tena kunipinga. Na najua siko wala nisingelikuwa peke yangu.

Wa Selma waliandamana watu wasiofikia 1,000 tarehe 7 Machi 1965. Waliposhambuliwa na vyombo vya dola, wakarudi wiki moja baadaye wakiwa 2,500. Walipozuiwa na mahakama, wakarudi wiki mbili baadaye wakiwa 25,000. Miezi michache baadaye, wakaibadilisha historia nzima ya Marekani panapohusika haki ya Mmarekani Mweusi kupiga kura. Wazanzibari wanaweza kufanya hivyo hivyo panapohusika haki yao hiyo ya kupiga kura.

RAIS wa zamani wa M a r e k a n i , L y n d o n B . Johnson.

ANNUUR NEW.indd 3 12/24/2015 1:43:15 PM

Page 4: ANNUUR 1209aaa

4 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015

SHEIKH Ponda Issa Ponda (katikati mwenye kofia) na baadhi ya Waislamu wakisoma dua nyumbani kwake Ubungo, Dar es Salaam hivi karibuni.

Tahariri/Matukio

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

JA N A i l i k u w a n i siku ya Maulid, siku ambayo Waislamu

walisherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW), aliyezaliwa miaka 1436 iliyopita.

Wa i s l a m u h u m t a j a M t u m e M u h a m m a d (SAW), kwa sifa ya mtu na Mtume aliyetumwa na Mwenyezi Mungu kuleta Dini ya haki, ustaarabu, amani na haki duniani. Katika kufanya kazi hiyo akapewa Qur’an iwe Mwongozo wa Maisha kwa waumini.

Mtume Muhammad (Saw) alizaliwa baada ya kuaga dunia baba yake Abdul lah b in Abdi l -Mutwalib. Mama yake Bi. Amina alifariki Mtume akiwa bado mchanga na kulelewa na Ummu Ayman (Mama Halima b i n S a ’a d i a ) . H a t a hivyo wanahistoria wa Kiislamu wametofautiana k u h u s u m w a k a n a mwezi aliozaliwa Mtume Muhammad (saw).

S a f i - u r - R a h m a a n M u b a r a k p u r i , mwanachuoni aliyepata zawadi ya kwanza katika mashindano ya kuandika historia ya Mtume (Saw) ameandika yafuatayo katika kitabu chake:

“Muhammad (Saw) b w a n a w a M i t u m e , alizaliwa katika mtaa wa Bani Haashim katika mji wa Makkah, Jumatatu, tarehe 9 Rabiul Awwal, mwaka ule ule wa ndovu na miaka arobaini baada ya utawala wa Kisra, yaani tarehe 20 au 22 Aprili 571 BI (Baada ya kuzaliwa ‘Issa), kulingana n a a l i v y o h a k i k i s h a m w a n a c h u o n i Muhammad Suleiman al-Mansourpuri na mwana-falaki Mahmud Pasha” (Ar-Rahiqul Makhtuum, Uk. 62).

S i r a j u r R a h m a a n k a t i k a k i t a b u c h a k e amesema: “Tukio hili la ndovu lilitokea mwezi wa Muharram kabla ya kuzaliwa kwa Mtume ( S a w ) k wa s i k u 5 5 , kama wanavyothibitisha wa n a v y u o n i w e n g i .

Tuzingatie Ujumbe aliokuja nao Mtume wetu Muhammad (s.a.w)

Wakati huo nao unaafiki mwisho wa mwezi wa Februari au mwanzo wa Machi mwaka 571 BI” (Al-Mustafa, nakala ya Ansaar Muslim Youth Organisation, 1993, Uk. 11).

Kutokana na mapokezi hayo mawili, tunaweza k u i w e k a t a r e h e y a kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (Saw) baina ya tarehe 25 Swafar na tarehe 25 Rabiul Awwal na Mwenyezi Mungu anajua zaidi.

Afif Abdul-Fattaah at-Twabbarah na Abul Hasan Ali Nadwi wamesema katika vitabu vyao kuwa: “Amina alizaa alfajiri siku ya Jumatatu tarehe 9 au 12 ya Rabiul Awwal, mwaka wa Ndovu. Mahmuud Pasha, maarufu kutoka Misri amefanya hesabu ya tarehe ya kuzaliwa na kupata kuwa ni Jumatatu tarehe 20 Aprili mwaka 571 BI , inayokwenda sambamba na tarehe 9 Rabiul Awwal” (Ma‘al Ambiyaa Fil Qur’anl Karim, Uk. 338 na Muhammad Rasul Llaah, Uk. 91).

I n a o n e k a n a k u w a wanavyuoni na wana-historia wa wakati huu wamechukua tarehe 9 ya Rabiul Awwal kuwa ndiyo aliyozaliwa Mtume M u h a m m a d ( S a w ) (Allamah Shibli Nu‘mani, Seeratun Nabi na Prof. ‘Abdul-Hameed Siddiq, The Life of the Prophet).

H a t a h i v y o j a m b o a m b a l o l i n a j u l i k a n a kwa uhakika bi la ya utata wowote ni siku aliyozaliwa.

Imepokewa kwa Abu Qatadah (Ra) kwamba Mtume (Saw) aliulizwa juu ya kufunga (Swaum) ya Jumatatu. Akasema: “Hiyo ilikuwa ni siku niliyozaliwa na ndio siku niliyopatiwa Utume au niliyoteremshiwa Wahyi” (Muslim).

Na ili tuwe tumemfuata v i l i v y o M t u m e w a Mwenyezi Mungu katika Sunna zake, inatakiwa kufunga siku ya Jumatatu kila wiki na bila shaka j ambo h i lo l i t akuwa

l i n a w a k u r u b i s h a Waislamu na Mwenyezi Mungu na ni kumbukumbu muhimu kwa Mtume.

Kutajwa sifa za Mtume (SAW), katika siku hiyo na hata nyinginezo, siyo tu ni tanbihi kwa waumini wa dini ya Kiislamu katika masuala ya kiroho, bali ni mawaidha ambayo wanapaswa kuyatumia vyema katika maisha yao ya kila siku hasa katika kuimarisha umoja wao katika Imani na kufikia lengo la kuumbwa kwao.

K a t i k a v i t a b u mbalimbali vya Maulid, M t u m e M u h a m m a d (SAW), anatajwa kwa sifa ya mtu aliyejitolea kuleta amani na haki miongoni mwa watu, kwa mfano katika miji ya Makka na

Madina ambako dola ya Kiislamu iliweza kuishi pamoja na Mayahudi na kuwatendea haki.

Mtume Muhammad (SAW), alipinga dhuluma, ubaguzi, unyonyaji na ki la a ina ya maovu. Tunaposherehekea Siku ya Maulid, haya ni miongoni mwa mambo muhimu yanayohitaji tafakuri ya hali ya juu. Waislamu hawana budi kuitumia Sikukuu hii ya Maulid kusahau tofauti zao na kuwa mwanzo mpya wa kuelekea kupinga na uhalifu na maovu mbalimbali. Waamrishe m e m a n a k u k a t a z a mabaya. Wanafikaje hapo? Hilo ni jambo la kupanga na kuweka mikakati . Lakini angalau waanze

na kutambua kuwa wana wajibu huo na wataulizwa. Na kwamba kusherehekea kwao Maulid hakutakuwa n a m a a n a i w a p o h a w a t e k e l e z i y a l e waliyoagizwa na Mtume Muhammad (s.a.w).

Tufungue ukurasa mpya kwa kuyapa Mafundisho ya dini yetu kipaumbele na tuyatumie kukuza maadili mema katika jamii.

Tunawatakia Waislamu na Watanzania wote kwa jumla, mapumziko mema katika siku hii ya Mazazi ya Mtume (SAW), tukiwakumbusha kuwa huyu ndiye Mtume wa M w i s h o n a k wa m b a hakuna salama katika ulimwengu wa leo bila kushika njia yake.

HILI ndio Hijab sahihi inayotakiwa kuvaliwa na wanafunzi wa kike na sio vilemba vinavyofunika vichwa tu kama inavyodaiwa na baadhi ya wakuu wa shule. Kulia ni Mzee Mikidadi Khalfan ambaye ni Mratibu wa vazi hilo kwa wanafunzi.

ANNUUR NEW.indd 4 12/24/2015 1:43:17 PM

Page 5: ANNUUR 1209aaa

5 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015Habari za Kimataifa

KA M A N D A wa Hizbullah, Samir Qantar, aliyeuawa katika shambulizi

lililofanywa na ndege za kivita za Israel nchini Syria, amezikwa Jumanne wiki hii katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

S a m i r Q a n t w a r , amezikwa katika makaburi ya mashahidi wa Hadharat Zainab mjini Beirut, mahali ambapo mashahidi na wapiganaji wa Hizbullah huzikwa.

Maelfu ya wananchi, viongozi mbalimbali wa nchi, wanasiasa pamoja na wanajeshi wa Hizbullah walijitokeza walishirikiana katika mazishi ya kamanda huyo.

Akihutubia kwa njia ya televisheni umati mkubwa uliohudhuria mazishi ya kamanda huyo mjini Beirut Jumanne wiki hii, Katibu Mkuu wa Hizbul lah , Sayyid Hassan Nasrullah, alisema Hezbullah wana haki ya kujibu mapigo ya mauaji hayo na kwamba, h a wa n a s h a k a k u wa mauaji hayo yalitekelezwa na makombora ya ndege za utawala haramu wa Israel.

Kiongozi huyo Mkuu wa Hizbullah aliongeza kuwa Israel imemuua kamanda Samir Qantwar, sasa ni zamu ya Hizbullah kujibu uchokozi huo.

Alisisitiza kuwa hakuna shaka kwamba Hizbullah ina haki ya kulipa kisasi na italipa kisasi kwa muda inaotaka, mahali inapotaka na namna itakavyotaka.

Ta ya r i v i k u n d i ya wapiganaji wa Kipalestina navyo vimeahidi kulipa k i s a s i k u f u a t i a k i f o cha kamanda huyo wa Hizbullah, ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wa Palestina.

Siku chache baada ya ndege za Israel kuvuka m p a k a wa S y r i a n a kumuua kamanda huyo wa Hizbollah, viongozi wa Hizbullah walisema bado hawajaanza kujibu mapigo ya kulipa kisasi na kudai kuwa bado wanajipanga kulipa kisasi.

Hata hivyo kuliripotiwa kuwa kuna makombora matatu kutoka Lebanon kwenda Israel.

Lakini viongozi wa H i z b u l l a h wa l i s e m a kuwa makombora hayo hajarushwa na kikosi cha Hizbullah na kusisitiza kwamba, Hizbullah bado hawajaanza kujibu kisasi

JUMUIYA ya Nchi za Kiarabu (Arab L e a g u e ) i m e o n ya

kuhusu hatari za vituo vya televisheni vinavyorusha matangazo yake kwa kutumia satalaiti dhidi ya Waislamu na kusema kuwa, televisheni hizo zinaeneza upotofu dhidi ya Waislamu duniani.

Mtandao wa habari wa al Bawabah News nchini Misri umemnukuu Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Hayfa Abu Ghazala , ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Jumuiya hiyo, akisema Jumapili iliyopita katika kikao cha wataalamu cha Jumuiya hiyo kwamba, baadhi

VITA VYANUKIA

Baada ya kamanda wa Hizbullah kuuliwaHizbullah waapa kulipa kisasi

n a k u a h i d i k wa m b a wakianza zoezi la kulipa kisasi itafahamika tu kwani lazima kitaitetemesha Israel.

Hadi anauliwa, Bw. Samiri Qantar, alikuwa Syria akiongoza vita dhidi ya magaidi wa Daesh ambao wanaungwa mkono

na nchi za Magharibi na Israel.

Waziri wa Ujenzi wa Israel Yoav Galant kufuatia tukio hilo lilifanywa na nchi yake alinukuliwa akisema, “Kwa mtazamo wangu watu hatari kama Samir Qantwar ni bora watoweke duniani”.

Samir Qantwar aliuliwa na ndege za kivita za utawala wa Israel usiku wa kuamkia Jumapili baada ya kuvuka mpaka wa Israel na Syria na k u s h a m b u l i a j e n g o alilokuwemo kiongozi huyo wa Hizbullah katika mji wa Jaramana huko

Kusini mwa Damascus, mji mkuu wa Syria na kumuua.

Ndege hizo za kivita z i l i m u u a B w . S a m i r Qantwar katika kitongoji cha Humeh kilichopo mji mkuu wa Syria Damascus.

S h a m b u l i o h i l o p i a l imedaiwa kuuwa watu wengine takriban 10 na wengine wengi kujeruhiwa.

Samir Qantar, alishawahi kutumikia kifungo katika gereza za Israel kwa kipindi kirefu, lakini aliachiwa huru katika tukio la kubadilishana mateka baina ya Israel na kundi la Hizbullah, baada ya kundi la Hizbul lah kupigana vita dhidi ya Israel na hatimaye kuteka askari kadhaa wa Israel na baadae vita kusimama. Hii ilikuwa ni mwaka 2006.

S e r i k a l i y a I s r a e l i l i m h u k u m u S a m i r Qantwar kifungo cha maisha mara tano kwa t u h u m a z a k u w a u a wanajeshi watano wa Israel.

Wananchi wa Israel w a m e a n z a k u h a m a makazi yao kuhofia majibu ya Hizbullah.

Tayari kifo cha Samir kimeleta hofu kubwa sana kwa wakazi wa Israel na kulazimika kusimamisha kazi zao na kuhama makazi yao kwa kuhofia mashambulizi ya kulipa kisasi. ABNA.

KAMANDA Samir Qantwar (kushoto) enzi za uhai wake akiwa na Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah.

Nchi za Kiarabu zashtukia hatari ya televisheni za satalaitiYatoa tahadhari kwa Waislamu

ya vituo vya televisheni za nje vimeweka ajenda maalumu ya kuwapotosha Waislamu na Waarabu na kuwatuhumu kuwa ni magaidi.

Alisema hatari ya siasa

hizo ni kubwa kwa sasa kiasi kwamba hata baadhi ya vituo vya televisheni za Kiarabu, nazo zinafuata mkumbo huo huo wa kueneza fitna na mizozo ya kikabila.

Kikao hicho kilifanyika kwa lengo la kutafuta njia za kiutaalamu za kukabiliana na wimbi hilo la upotoshaji linalofanywa n a v i t u o h i v y o v ya televisheni.

ANNUUR NEW.indd 5 12/24/2015 1:43:18 PM

Page 6: ANNUUR 1209aaa

6 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015Hoja ya Juma Kilaghai

KATIKA miaka hii ni vigumu sana kukuta

tangazo lolote la ajira ambalo haliweki mkazo wa kipekee kwenye vigezo vya kitaaluma na uzoefu wa kazi wa miaka kadhaa. Japokuwa huu ni utaratibu mwepesi wa kuchuja na kupata waombaji wa kazi, uchambuzi wa watu wengi wenye mafanikio, wa zamani na wa sasa unaonyesha kuwa huenda utaratibu huu hauna ufanisi sana.

Nia ya mwajiri ni kupata mfanyakazi ambaye ataongeza thamani kwenye taasisi na kuyafanya malengo ya taasisi kufikiwa au hata kupitwa kwa wepesi zaidi. Hata hivyo uzoefu unaonyesha kuwa wafanyakazi wanaoajiriwa kwa vigezo vya taaluma na uzoefu wa miaka, mara nyingi hawaongezi thamani ya kutosha kiasi cha kuifanya taasisi ifikie malengo na kung’ara.

Kwa upande mwingine, wafanyakazi walioajiriwa kwa sifa nyingine, hasa uwezo wa ushawishi na kuongoza, bila kujali viwango vyao vya taaluma na uzoefu kwenye kazi, huongeza thamani kubwa kwenye taasisi na kuifanya taasisi ing'are kwa mafanikio. Wafanyakazi hawa ni wale ambao wanatajwa kuwa na kiwango cha juu cha uwezo wa kutambua kwa uhakika na kushughulikia kwa namna bora hisia zilizomo ndani mwao na ndani ya watu wengine wenye mahusiano nao ya kikazi. Kitaalamu uwezo huu hujulikana kama Emotional Intelligence (EI) au Emotional Quotient

Waajiri badilikeni!Taaluma, uzoefu sio vigezo pekee

John MayerDaniel Goleman Charles Schwab

(EQ).Kuna miundo

(models) miwili inayotumika kuutafsiri huu uwezo. Muundo wa kwanza ni ule uliopendekezwa na Konstantin Vasily Petrides mnamo mwaka 2001. Muundo huu, ambao kitaalamu huitwa trait model, unajumuisha mielekeo mbalimbali ya kitabia inayoonyeshwa na mtu, pamoja na uwezo na vipaji mhusika anavyojiona kuwa navyo. Muundo wa pili ni ule uliopendekezwa na mabwana Peter Salovey na John Mayer mnamo mwaka 2004. Muundo huu ambao kitaalamu huitwa ability model, huweka mkazo juu ya uwezo wa mtu kufanyia kazi taarifa zinazohusu maono/hisia za watu mbalimbali na jinsi ya kuzitumia taarifa hizo kwa weledi katika mazingira ya jamii aliyomo.

Tafiti zinaonyesha kuwa watu wenye EI kubwa huwa pia na kiwango cha juu cha ubora katika siha ya akili, wana utendaji kazi uliotukuka, na pia wana maarifa mkubwa ya kuongoza. Kwa mfano, kwa mujibu

wa utafiti uliofanywa na Daniel Goleman na kuchapishwa katika kitabu chake kinachoitwa ‘Working With Emotional Intelligence’, EI inachangia kiasi cha 67% ya vigezo vyote vya lazima vinavyohitajika ili mtu aweze kuwa na utendaji uliotukuka katika uongozi. Aidha, kwa mujibu wa utafiti huu, umuhimu EI ulibainika kuwa mara mbili zaidi ukilinganisha na akili ya kiufundi (IQ) katika kuleta mafanikio ya kiuongozi.

Hebu tuangalie mfano wa Bwana Charles Schwab katika kuthibitisha ukweli wa umuhimu wa EI katika uongozi. Huyu alizaliwa mwaka 1862 kule Williamsburg, Pennsylvania na kufariki mwaka 1939. Charles Schwab hakumaliza elimu ya chuo. Baada ya kuhudhuria chuo cha St. Fransis (sasa kinaitwa Chuo Kikuu cha St. Fransis) kwa miaka miwili aliacha na kuelekea katika jiji la Pittsburgh kutafuta kazi.

Moja ya sifa kubwa za Charles Schwab ilikuwa ni

uwezo mkubwa wa kushawishi. Kutokana na uwezo wake mkubwa mwaka 1897 akiwa na miaka 35 alifanywa kuwa Rais wa kampuni ya kutengeneza chuma ya Carnegie Steel. Mwaka 1901 alisaidia kufanikisha majadiliano ya siri ya kuuzwa kwa kampuni hii, ambapo iliuzwa kwa kundi la wawekezaji kutoka New York waliokuwa chini ya J.P. Morgan. Kampuni hii ilibadilishwa jina na kuwa U.S. Steel Corporation na Charles Schwab akawa Rais wake wa kwanza.

Hata hivyo mwaka 1903 Charles Schwab aliondoka U.S. Steel baada ya kutoelewana na Morgan, na kujiunga na Bethlehem Ship building and Steel Company. Chini ya uongozi wake kampuni hii ilikuwa haraka haraka na kuwa ya pili kwa ukubwa duniani miongoni mwa makampuni ya chuma. Kutokana na uwezo wake mkubwa mpaka mwanzoni mwa miaka ya 1920 Charles Schwab alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wanapata mishahara mikubwa ya kutisha.

Peter SaloveyKwa mujibu wa Dale Carnegie, mwandishi mashuhuri wa vitabu vya kufundisha mahusiano, wakati huo Charles Schwab alikuwa akipata mshahara wa dola za kimarekani milioni 1 kwa mwaka, sawa na dola 2,740 kwa siku!

Pamoja na uwezo wa kushawishi, Charles Shwab alikuwa pia ni muumini wa kutoa motisha moja kwa moja kwa mtu aliyefanya vizuri, na siyo kuoanisha motisha ya mtu mmoja mmoja na utendaji wa kampuni. Imani hii ilifanya wafanyakazi wake wawe wabunifu na wenye kujitoa kwa hali na mali kwa sababu watu walijua kuwa mwisho wa siku jitihada zao zitawalipa.

Bila ya shaka waajiri wetu wa leo wana mengi wanayoweza kujifunza kutoka kwa Charles Shwab. Mafunzo watakayopata yatasaidia kugeuza maeneo mengi ya kazi kuwa maeneo yenye ufanisi zaidi!

(Kwa maoni, mawasiliano 0754 281 131)

ANNUUR NEW.indd 6 12/24/2015 1:43:23 PM

Page 7: ANNUUR 1209aaa

7 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015MAKALA/T

NAPENDA nianze kwa kutoa shukrani

zangu kwa Serikali kutokana na agizo lake la kutoa viwango vya ada elekezi kwa shule binafsi. Inaonesha kuwa inawahurumia wazazi na watoto na Watanzania wanaosomesha watoto katika shule za Mashirika ya dini na za binafsi. Na hakuna mtu anayependa kitu cha ghali bila sababu. Kila mmoja anapenda nafuu na rahisi, lakini inayokidhi haja na malengo.

Hata hivyo, si mara nyingi tumeona na kusikia malalamiko ya walimu au wanafunzi wa shule za binafsi kuhusu kuchelewa posho zao, au chakula kibaya.

Kuna mashirika ya dini ambayo serikali imeyapendelea, kwa kuweka makubaliano ya kuyapa fungu la pesa ili kuendeshea miradi yao; na kuna mashirika ya dini ambayo hayapewi fungu kama hilo. Na hili ni tangu utawala wa wakoloni; na kuna mashirika ya dini yaliyofunguliwa milango ya wafadhili, na mashirika ya nje na ya kimataifa kuingiza misaada ya aina mbalimbali tangu mkoloni. Na kuna mashirika ya dini yamefungiwa milango kwa mashirika ya kimataifa na wafadhili wa nje.

Mashirika ya Kanisa yote yamefunguliwa milango hiyo, na mashirika ya Kiislamu yamefungiwa milango japo si kisheria au bali kwa mazingira na kiutendaji.

“Tunu za Kikristo katika sera na bajeti zimekuwa ndio kupe mkubwa anayefyonza nguvu yote ya wananchi kupitia mikataba mikubwa ya MoU, ruzuku na misamaha ya kodi. Kutunga sera, kubuni na kuratibu program kwa ajili ya kutoa, kupanua, kuboresha na kukarabati huduma muhimu za jamii ikiwemo ya Elimu ni jukumu la serikali.

Utaratibu huu umezingatia utendekaji

Ada elekezi za shule

DKT. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.wa haki kwa raia wote na ubora wa huduma. Hapa Tanzania mawakala wa Kanisa na dani ya serikali wamekasimu wajibu huo kwa Makanisa. Mkataba wa MoU kifungu cha 5 (Article V) kina maelezo ya utaratibu huo:

“Tume itaunda chombo chini yake kitakachoitwa Bodi ya Kikristo ya Elimu Tanzania (ambayo humu itajulikana kama ‘Bodi ya Elimu’) kwa minajili ya kuunganisha, kutoa na kupanua na kukarabati huduma za Elimu Tanzania.”

Kwa utaratibu huo uadilifu wa serikali kwa mashirika haya ya dini uko wapi?

“Elimu ni sekta muhimu sana ndiyo maana makundi mawili makuu ya kidini nchini, yaani Waislamu na Wakristo, wanajenga mashule yao. Hata hivyo bado wanahitajia sana msaada wa serikali. Tofauti na Waislamu, Wakristo kupitia mkataba wa Makanisa na Serikali huwezeshwa kusomesha wataalamu wao kwa gharama za Umma. Kifungu cha 11 cha MoU Kinaelezea:

“Serikali itatoa nafasi za masomo katika vyuo vya ualimu kwa ajili ya kufundishia wananchi watakao hitimu kama walimu kwa ajili ya kufundisha shule za

Kanisa.” Hakuna utaratibu

kama huo kwa Waislamu. Pamoja na kutokea mabadiliko ya kisiasa Waislamu wamenyimwa haki ya kurejeshewa shule zao wakati sehemu kubwa ya shule za Wakristo zimerejeshewa na kuhakikishiwa usalama:

“Serikali haitotaifisha shule, hospitali au taasisi yoyote ile ya elimu au Afya inayomilikiwa na makanisa.” (MoU, kifungu cha 12).

Kwa maana hiyo, ni kuwa mashule ya Waislamu waliyo anzisha na wanayoanzisha, yanaweza kufutwa au kutaifishwa kwa sababu wao hawakushirikishwa katika makubaliano hayo. Yalifanywa kinyemela kati ya serikali na Makanisa. Na kwa maana hiyo, wako walimu na madaktari waliosomeshwa kwa kodi za Watanzania wakiwemo Waislamu, wanaofanya kazi katika shule na hospitali za Makanisa, lakini wameajiriwa na kulipwa mishahara na serikali, hivyo kwa kupunguzwa karo katika mashule ya Mashirika ya dini watakaoathirika ni mashirika ya Kiislamu sio ya Kikristo.

Serikali imeyawezesha mashirika ya Kanisa na viongozi wa Kanisa kiuchumi, bila shaka ni uwezeshwaji mkubwa sana kupitia MoU na misamaha ya kodi.

Kwa hiyo Mashirika ya Kanisa yamejilimbikizia utajiri na mikataba na serikali itakayowezesha mashule ya Kanisa kuendelea hata kama karo itapunguzwa, lakini mashirika ya Kiislamu na watu

binafsi ndio shule zao zita athirika kama si kufungwa kabisa. Na hiyo ndiyo dhuluma iliyo na inayo endelezwa bila soni mpaka sasa.

Nimalizie makala yangu kwa kumpongeza Rais Mh. John Pombe Magufuli kwa aliyokwisha yafanya kwa huu muda mchache alioingia Ikulu. Lakini nimwambie kuwa kama vile kuna watu waliowadhulumu Watanzania kwa kupitisha makontena bila kodi zao kuingia serikalini, na sasa amewaambia kuwa walipe, ndivyo hivyo Waislamu waliwekwa pembeni katika makubaliano ya serikali na Makanisa MoU, ambapo Makanisa yanachotewa mamilioni ya pesa za kodi za Watanzania wakiwemo Waislamu, kila mwaka nakupewa kuendesha miradi yao. Ni vizuri uadilifu ukawepo, kwa Mashirika ya dini ya Kiislamu yakapewa haki yao tangu Serikali ilipo kubaliana na Makania mwaka 1992.

(Mwandishi wa Makala ni msomaji wa An nuur wa muda mrefu Khatibu Juma Mziray 0757013344.

Ni Duka lililopo Kariakoo Mtaa wa Livingstone na Tandamti karibu na Benki ya NMB.

Fika na upate mahitaji ya Kanzu za aina mbalimbali za kisasa, za mikono mifupi na mirefu ikiwemo Daffa, Al-Asil, Al-wasif, hanawai na Saddaf. Pamoja na Kanzu za kushona aina ya Emarat (Silk na Cotton).

Pia tunauza mafuta ya kunukia (Perfume), Udi na Body Sray za aina mbalimbali zenye marashi ya Udi.

Pia utapata Sandals, Kofia na bidhaa zingine mbalimbali.Unaweza kuwasiliana nasi kwa Namba:- 0658 500 201.

Wote mnakaribishwa.

AlhidAyA ColleCtion loCAtion

ANNUUR NEW.indd 7 12/24/2015 1:43:24 PM

Page 8: ANNUUR 1209aaa

8 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015Makala

WAKRISTO, labda kwa vile wanajiita Wakristo na

wanaamini Ukristo, wanapenda kudai wanamhodhi Kristo. Lakini taadhima ya Waislamu kwa Yesu ilianza wakati wa uhai wa Mtume wa Uislamu (Muhammad s.a.w). Labda kinachoshadidia jambo hilo Zaidi, ni maelezo ya jadi ya maisha ya Muhammad, ambaye akiingia jiji la Mecca akiwa mshindi mwaka 630 (AD, baada ya Kristo), haraka alienda katika Kaaba kusafisha maashera kutoka madhabahu hiyo takatifu. Alipokuwa akizunguka eneo hilo, akiamrisha kuteketezwa picha na sanamu za miungu takriban 360 wa kipagani, alifikia picha ya kuchorwa ukutani inayomwonyesha Bikira na Mwanae. Anasemekana aliifunika kwa heshima kubwa na joho lake na kutoa ilani kuwa michoro yote mingine ifutwe ila huo hapo.

Yesu, au Issa kama anavyojulikana kwa Kiarabu, anatajwa na Uislamu kuwa ni nabii wa Kiislamu badala ya kuwa Mwana wa Mungu, au Mungu aliyekuwa duniani. Anatajwa kwa jina mara 25 katika maeneo tofauti ya Kurani na mara sita kwa cheo cha Masihi (au Kristo, kulingana na tafsiri ya Kurani ambayo inatumika). Pia anatajwa kama Mjumbe, na Nabii, lakini, zaidi ya yote, kama Neno, na Roho wa Mungu. Hakuna mtume mwingine katika Kurani, hata Muhammad, anapewa heshima hii. Kusema kweli, kati ya manabii 124,000 ambao wanasemekana kutambuliwa na Uislamu - tarakimu ambayo ni pamoja na manabii wote wa Kiyahudi katika Agano la Kale - Yesu anaonekana ni wa pili kutoka kwa Muhammad peke yake, na anaaminika ndiye mtangulizi wa Mtume wa Uislamu.

Katika kitabu chake cha kufurahisha, Yesu Muislamu, Profesa wa zamani wa Kiarabu na Uislamu katika 'Chuo Kikuu cha Cambridge, Tarif Khalidi, anaunganisha pamoja, kutoka vianzio maridhawa, hadithi 303, misemo na jadi kuhusu Yesu ambayo inaonekana katika maandishi ya Kiislamu,

Yesu: Nabii wa WaislamuUKRISTO una mizizi katika imani kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu. Hivyo ufahamu wa Uislamu kuhusu Kristo, ni chanzo cha kutoelewana, au ni njia ya kujenga madaraja kati ya dini hizi mbili kuu za dunia?

Na Mehdi Hasan

kuanzia karne za kwanza za historia ya Uislamu. Hizi zinamwonyesha Yesu asiyetofautiana na Kristo wa Injili. Yesu wa Uislamu ni mlinzi mtakatifu wa kujinyima, bwana wa maumbile, mfanya miujiza, mponyaji, mfano bora wa maadili, na maisha ya kiimani na kijamii.

"Yesu alikuwa akila majani ya miti," hadithi moja inasema, "akivaa nguo ya manyoya, na kulala popote ambako usiku utamkuta. Hakuwa na mtoto ambaye angekufa, nyumba ambayo ingeweza kuharibika; wala hakuweka akiba chakula chake cha mchana kwa ajili ya kula jioni. Alikuwa akisema "kila siku inaleta riziki yake."

Kwa mujibu wa mafundisho ya kina ya Uislamu, Yesu hakuleta sheria mpya iliyofunuliwa, au kutengeneza upya sheria ya awali. Lakini alileta njia mpya (tariqah) kwa msingi wa kumpenda Mungu.

Labda ni kwa sababu hiyo amekubaliwa na wapania siri, au Wasufi, wa Uislamu. Mfikiriaji wa ki-Sufi, Al Ghazali, alimtaja Yesu kuwa "nabii wa roho" na bingwa wa ki-Sufi Ibn Arabi alimwita "muhuri wa manabii." Yesu wa u-Sufi wa Kiislamu, kama Khalidi anavyoainisha, ni mtu "asiyekuwa rahisi kumtofautisha" na Yesu wa Injili.

Nini kilimfanya Khalidi aandike kitabu hicho cha uchokozi? "Tunahitaji kukumbushwa historia ambayo ilitoa maelezo tofauti kabisa: jinsi dini moja, Uislamu, ulivyomchukua Yesu katika imani yake ya kiroho na bado ikambakiza kama shujaa aliye huru katika mapambano kati ya dhamira ya sheria na sheria yenyewe," aliniambia. "Kwa njia nyingi ni habari ya kustaajabisha ya makutano ya dini, ya dini moja kujenga hisia yake ya imani kwa kutwaa

na kuthamini kielelezo kikuu cha dini nyingine."

Uislamu unamtukuza Yesu pamoja na mama yake, Maria. (Yusufu haonekani kokote katika maelezo ya Uislamu ya kuzaliwa kwa Kristo). "Tofauti na Injili rasmi, Kurani inaegemea nyuma kuelekea kwa kuzaliwa kwake kimuujiza badala ya kuangalia kusulubiwa kwake," anaandika Khalidi. "Ndiyo maana anatajwa mara kadhaa kama mwana wa Maria, na ndiyo maana yeye na mama yake wanaonekana pamoja mara kwa mara." Kusema kweli, Bikira Maria, au Mariamu, kama anavyojulikana katika Kurani, anaonekana kwa Waislamu kuwa aliyetukuka zaidi kiimani miongoni mwa wanawake. Ndiye mwanamke peke yake anayetajwa katika kitabu kitakatifu cha Uislamu kwa jina lake na sura moja ya Kurani imepewa jina lake.-Katika mapokeo yanayotajwa kila mara, Mtume Muhammad alimwelezea kama mmoja wa wanawake wanne waliokamilika kabisa katika historia ya binadamu.

Lakini umuhimu halisi wa Maria ni kuwa Uislamu unamtambua kama bikira na kuafiki dhana ya Kikristo ya bikira kutwaa mimba. "Alikuwa ndiye mwanamke aliyechaguliwa, aliyechaguliwa kumzaa Yesu, bila mume," anasema Sheikh Ibrahim Mogra, Imamu wa Leicester na Katibu Mkuu Msaidizi wa Baraza la Waislamu la Uingereza (MCB). Huu ndiyo msimamo rasmi wa Uislamu miaka yote na, katika hali ya kushangaza, Sayyid Hossein Nasr anaandika katika 'Moyo wa Uislamu' "heshima kwa mafundisho kama hayo ni kubwa miongoni mwa Waislamu kiasi kwamba katika mikutano ya mazungumzo ya kidini na Wakristo, Waislamu mara nyingi wanaachwa wakitetea mafundisho ya jadi ya Kikristo kwa mfano kuzaliwa kimuujiza kwa Kristo

mbele ya watafsiri wa kisasa wanaosema hiyo ni mifano tu."

Walati Uislamu na Ukristo vimeshonwa kwa pamoja, inaweza kuwa jambo la maana kwa jumuia za Kiislamu kote barani Ulaya, wakiwa katika kusakamwa, kupigiwa makelele na mara nyingi tu kuzungukwa, kujitahidi kuelezea urithi huu wa pamoja wa kidini, na hasa upendo wa pamoja kwa Yesu na Maria. Kuna utangulizi maarufu kwa jambo hili katika maisha ya Mtume. Mwaka 616, miaka sita baada ya kuanza kazi ya utume huko Makka, Muhammad alitaka kupata hifadhi salama kwa baadhi ya wafuasi wake ambao walikuwa wameingia katika kusakamwa na kutishiwa maisha kutoka kwa wapinzani wake miongoni mwa makabila ya kipagani ya Kuraishi. Alimwomba Negus, mfalme wa Kikristo wa Abyssinia (baadaye Ethiopia) kuwachukua. Alikubali, na zaidi ya Waislamu 80 waliondoka Makka na familia zao. Mapokezi ya kirafiki waliyoyopata walipofika Abyssinia yaliwastua wa-Kuraishi kiasi kwamba, wakihofia Waislamu wa Muhammad kupata washirika wengi zaidi ng'ambo, walipeleka wajumbe wawili kwa Negus kumwambia awarudishe Makka. Wakimbizi hao Waislamu, wa-Kuraishi hao walisema, ni watu wa makufuru na wanaokimbia hukumu. Negus alimwita Jafari, binamu wa Muhammad na kiongozi wa kundi hilo la Waislamu, kujibu mashitaka hayo. Jafari akaeleza kuwa Muhammad ni mtume wa Mungu huyo huyo ambaye alikuwa ametoa ufunuo wake kwa Yesu, akatoa maelezo ya Kurani ya kuzaliwa kimuujiza kwa Yesu katika tumbo la Maria. Akamtaja Maria katika maandiko, akiwa ameondoka miongoni mwa watu wake akakaa katika chumba kinachoangalia mashariki, na alikuwa ameona ni vyema kujitenga nao. Ndipo tukampelekea roho kutoka kwetu ambaye alionekana kwake kama mwanaume aliyekamilika kwa wema. Akasema: "Tazama! Natafuta hifadhi kwa Aliye Mwema kutoka kwako, kama wewe unamwogopa Mungu."

Inaendelea Uk. 15

ANNUUR NEW.indd 8 12/24/2015 1:43:25 PM

Page 9: ANNUUR 1209aaa

9 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015Makala

IKIWA imepita karibuni miezi miwili tangu kumalizika kwa

Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muundo wa vyombo vya utendaji kukaribia kupata sura kamili kwa upande wa Bara, hali bado ni tete kwa upande wa Visiwani, na hadi leo bado matokeo ya uchaguzi hayajatangazwa.

Hali hiyo imepelekea mtafaruku wa kisiasa visiwani Zanzibar, na juhudi za nje na ndani zimekuwa zikiendelea katika kuupatia ufumbuzi mzozo huo.

Katika muqtadha wa juhudi hizo, Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani (ZADIA), mnamo tarehe 18 mwezi huu ilifanya maandamano kwenye viunga vya Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Akizungumza kwenye maandamano hayo, Mwenyekiti wa ZADIA Bwana Omar Haji Ali, alisema kuwa maandamano hayo yanakuja katika juhudi za Jumuiya hiyo za kutafuta uingiliaji kati wa jamii ya kimataifa katika kuukwamua mgando wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Bwana Omar H. Ali alisema kuwa wapenda amani wote ulimwenguni ikiwemo jumuiya yake walishangazwa na kushtushwa na hatua ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya kuufuta uchaguzi wote Visiwani humo.

“Wazanzibari, Watanzania na wapenda amani wote ulimwenguni ikiwemo Jumuiya yetu, walishtushwa na kushangazwa na tangazo lisilokuwa la kisheria la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Bwana Jecha S. Jecha la kufutwa Uchaguzi wa Zanzibar”, alisema Bwana Ali na kuongeza kuwa Wataalamu wote

Diapora waandamana New YorkBaada ya Obama, kumvaa Ban Ki-moon

Na Mwandishi wetu Washington

ili kuhakikisha kuwa sauti za Wazanzibari zinasikilizwa na kuheshimiwa”

Itafaa kukumbusha kuwa mnamo tarehe 21 mwezi uliopita, ZADIA iliandaa maandamano kama hayo kwenye Ikulu ya Marekani ya kumtaka Rais Barack Obama wa nchi hiyo kutekeleza ahadi yake aliyoitoa kwenye hotuba yake katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika jijini Adis Ababa, Ethiopia, mapema mwaka huu.

“Katika hotuba yake hiyo, Rais Obama alisema ‘pale ambapo raia hawawezi kutekeleza haki zao, basi ulimwengu una jukumu la kukemea. Na Marekani itafanya hivyo, hata kama wakati mwengine itakuwa inauma.”

Tayari serikali ya Marekani imesitisha baadhi ya misaada yake kwa Tanzania, zikiwemo fedha za Changamoto za Milenia mpaka pale serikali ya nchi hiyo itakapoutatua mgogoro wa kisiasa Visiwani Zanzibar.

Kufuatia maandamano hayo, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo alidokeza kuwa, iwapo hali itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwenye Umoja wa Mataifa. Katika maelezo yake kwenye maandamano ya jijini New York, Kiongozi wa ZADIA alielezea kushangazwa kwake na sifa kemkem alizojichotea Rais mpya wa Tanzania kwa mwanzo mzuri wa Urais wake.

“Rais mpya wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amejizolea sifa nyingi kutoka kila pembe ya Dunia kwa mwanzo mzuri wa Urais wake, lakini linapokuja swala la mzozo wa kisiasa Zanzibar, amekaa kimya na hajachukua hatua yoyote” alisisitiza Bwana Ali.

Katika maandamano hayo yaliyowashirikisha pia wapenda amani na demokrasia kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni, waandamanaji walibeba

Inaendelea Uk. 10

wa Kisheria waliuelezea uamuzi huo kuwa hauna mashiko ya Kisheria.

Akimnukuu Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Cha Zanzibar Bwana Awadha Said Ali, mwenyekiti wa ZADIA alisema:

“Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu cha 119 (10), ili maamuzi ya ZEC yawe sahihi, ni lazima pawepo na kikao cha Tume hiyo, chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa Tume au Naibu wake, pamoja na wajumbe wasiopungua wanne”. “lakini hilo halikufanyika”, alisisitiza Bwana Ali.

“Maelezo hayo yanatiliwa nguvu na maelezo ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Bwana Othman Masoud Othman ambaye alikuwa na mchango mkubwa katika marekebisho ya Sheria na kanuni za Uchaguzi za Zanzibar kwa mujibu wa Katiba ya Visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi ya 1984” , alifafanua Bwana Ali.

Aidha, alisema kwamba maandamano

hayo pia yana lengo la kumkumbusha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-moon ili kufuatilita zaidi hali inavyoendelea Visiwani Zanzibar.

“Katibu Mkuu wa Umaja wa Mataifa aliwapongeza viongozi na wananchi wa Watanzania kwa kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa njia za amani.

Wakati huo huo alielezea wasiwasi wake juu ya hali ilivyo Zanzibar, na kuwataka wadau wote kujizuia kuchukua hatua zozote zinazoweza kupelekea uvunjifu wa amani”, alidokeza Bwana Ali. Alisema kuwa, Wazanzibari wengi wameitikia wito huo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, hata hivyo matukio ya hapa na pale ya uvunjaji wa amani yamekuwa yakiripotiwa.

“Moja kati ya matukio hayo ni yale yaliyotokea usiku wa kuamkia tarehe 13 mwezi huu, ambapo makundi ya watu wenye silaha za moto na za kijadi yalivamia maeneo kadhaa katika Mji wa

Zanzibar na kusababisha hasara kubwa za mali”.

Halkadhalika Bwana Ali alinukuu baaadhi ya vipengele vya Mkataba wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, akisema kuwa hali inavyoendelea huko Zanzibar hivi sasa inakwenda kinyume na Mkataba huo, ikiwemo kuweko kwa wanajeshi mitaani, kitendo ambacho kinatia khofu raia na kuzorotesha harakati zao za kiuchumi.

Alitahadharisha kuwa iwapo hatua za mapema hazitochukuliwa, basi kuna hatari ya Ulimwengu kukabiliwa na janga la kiutu huko Zanzibar, kwani tayari kumekuweko na mfumko mkubwa wa bei za bidhaa muhimu hususan za chakula na kufikia zaidi ya 10% katika kipindi cha mwezi mmoja kufuatia Uchaguzi Mkuu Zanzibar.

Aliongeza kuwa “Wananchi wa Zanzibar wameshindwa kutekeleza haki yao kwa zaidi ya nusu karne sasa. Wakati umefika sasa kwa ulimwengu kuchukua jukumu lake kivitendo

JUMUIYA ya Wazanzibari waishio nchini Marekani (ZADIA), mnamo tarehe 18 mwezi huu ilifanya maandamano kwenye viunga vya Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

ANNUUR NEW.indd 9 12/24/2015 1:43:25 PM

Page 10: ANNUUR 1209aaa

10 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015

Makala

Diapora waandamana New YorkInatoka Uk. 9mabango yaliyokuwa na maneno kama vile “Mshindi wa uchaguzi atangazwe”, “maamuzi ya Wazanzibari yaheshimiwe”, “bila haki hakuna amani’, “tunahitaji mabadiliko”, “Wazanzibari wamechoshwa na ukandamizaji”, na mengineyo.

Aidha, waandamanaji hao walisikika wakipiga makelele wakidai “tunataka matokeo yetu ya uchaguzi.”

Itakumbukwa kuwa, wananchi wa Zanzibar walipiga kura mnamo tarehe 25 Oktoba mwaka huu, lakini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bwana Jecha Salum Jecha akatangaza kufutwa kwa uchaguzi huo Mkuu visiwani humo, kitendo ambacho wataalamu wa Sheria wamesema kuwa kinakwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar.

Wachambuzi wanaona kuwa hatua hiyo ya Bwana Jecha ilikuja wakati asilimia kubwa ya matokeo yaliyokuwa yametangazwa yalikuwa yanampa ushindi mgombea wa urais wa Zanzibar kutoka chama cha upinzani cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Shariff Hamad.

Kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi huo ambao wachunguzi wa nje na ndani waliulezea kuwa ulikuwa wa haki na huru, kimezua mtafaruku wa

kisiasa visiwani Zanzibar, na juhudi za ndani na nje zimekuwa zikifanyika ili kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani humo.

Kwa muda wa wiki kadhaa hivi sasa mazungumzo yamekuwa yakiendelea katika Ikulu ya Zanzibar kwa kuwashirikisha Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohammed Shein, Makamo wake wa kwanza Balozi Ali Seif Idd na Makamo wa Pili ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad.

Mazungumzo hayo ya siri pia yamewashirikisha Marais wastaafu wa Zanzibar, Bwana Ali Hassan Mwinyi, Dkt Salmin Amour na Dkt Aman Abeid Karume.

Usiri wa mazungumzo hayo umezaa tetesi kadha wa kadha katika mitandao ya kijamii, na kupelekea kuzaliwa kwa msimati mpya wa siasa za mitaani ujulikaonao kwa jina la “Drips”. Maandamano ya ZADIA ni katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kimataifa za kusaka suluhu za mgogoro huo kwa njia za amani.

Kufuatia maandamno hayo, Mwenyekiti wa ZADIA aliwashukuru wale wote walioshiriki kwa kuitakia kheri Zanzibar, na karamu maalum ya chakula cha Mchana iliandaliwa kwa ajili ya washiriki wa maandamano hayo.

AKIAMBIWA arudie maneno haya, hawezi kurudia.”

Alisema jamaa yangu mmoja tukiwa ndani ya gari jioni ya Jumanne wiki hii. Aliyasema hayo baada ya kusikiliza mahojiano baina ya mpasha habari wa BBC na mtu mmoja akijitambulisha kuwa ni katika majeruhi wa lililodaiwa kuwa shambulio la kigaidi la Al-Shabaab katika mji wa Mandera, Kenya.

Ufupi wa maneo kadiri ukisikiliza maneno ya jamaa huyo, unashindwa kupata ukweli wa anachosema. Kwanza anadai kuwa alipigwa risasi ikaingia upande mmoja wa mwili ikatokea kwingine. Anaulizwa, hali yako ikoje sasa, anajibu kuwa ni mbaya sana kwa sababu bado damu inatoka upande ilikoingilia risasi na

Salamu za Maulid, Krismasi:

Haya ndiyo majipu ya kupasuliwaNa Omar Msangi

BASI linalodaiwa kutekwa na Alshabab.

upande ilikotokea. Hata hivyo, ukisikiliza sauti yake, haikupi picha kuwa inatoka kwa mtu mahututi. Ni mtu mchangamfu ambapo wakati mwingine analeta na maneno ya mzaha.

Lakini jingie ni jinsi alivyokuwa akijiuma uma anapoulizwa maswali juu ya hali ilivyokuwa wakati Al-Shabaab wakitaka kuwatenganisha Waislamu na Wakristo, ili wapate kuwauwa Wakristo pekee.

Awali nilikuwa nimeisikia habari hiyo katika moja ya televisheni zetu na Redio nchini. Ikapambwa sana ikisisitizwa juu ya ushujaa wa Waislamu kuwahami ndugu zao Wakristo wasiuliwe na Al-Shabaab. Sikuwa nimedhamiria kuandika juu ya habari hiyo, kwa sababu kwangu ilikuwa wazi kabisa kwamba ni moja ya mizaha (hoaxes) ya

Inaendelea Uk. 16

Propaganda imekaa vizuuriLakini ujumbe sio wenyewe

ANNUUR NEW.indd 10 12/24/2015 1:43:30 PM

Page 11: ANNUUR 1209aaa

11 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 201511 AN-NUURMakala

MTU mmoja alinipigia simu Jumatatu kiasi saa tatu

usiku anakaniuliza, “mbona jamaa leo katoka Ikulu akiwa kafurahi sana?” Nikamwambia hata alipokutana na JK, walitoka pia wakicheka, lakini mpaka leo hakieleweki. Wala haijulikani waliongea nini na walikubaliana nini. Maana alikwenda kwa JK peke yake, kama anavyokutana na CCM peke yake Unguja na ndivyo alivyokuja peke yake kumuona JPM.

“Jamaa Kiboko. Hao ni watu waliokula viapo, na wanaonekana mabingwa wa kuchunga viapo vyao.” Alimalizia.

Jamaa yangu huyo alikuwa akizungumzia mazungumzo baina ya Rais Mheshimiwa John Pombe Magufuli na Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad yaliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam, Jumatatu wiki hii. Katika taarifa rasmi juu ya mazungumzo hayo ilielezwa kuwa hiyo ilitokana na maombi ya Maalim kukutana na Mheshimiwa Rais Magufuli. Na kama ilivyokuwa awali Maalim alipokutana na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, safari hii pia Maalim, hakuwa na timu aliyoongozana nayo (CUF/UKAWA). Alikuwa peke, huku Mheshimiwa Rais akiwa na Makamo wake Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Katika taarifa yake fupi kwa wandishi wa habari, Meshimiwa Rais Magufuli alipongeza mazungumzo ya kindugu yanayoendelea na kuhimiza kuwa yaendelee katika moyo huo huo maana udugu ni jambo muhimu. Mpaka sasa si rahisi kuelewa nini mwelekeo na hatma ya mazungumzo hayo. Suala la msingi hapa ni kuwa uchaguzi umefutwa. Kwa hiyo ilitarajiwa kwamba jambo la msingi kutizamwa ni iwapo ufutwaji huo wa uchaguzi, ni halali kikatiba na kisheria. Baada ya hapo itizamwe nini cha kufanya.

Juu ya uhalali wa tangazo la mwenyekiti wa Tume-ZEC, wanasheria wengi wamejaribu kuchambua sababu zilizotolewa na kuzipambanisha na sheria na kisha kufikia hitimisho kuwa uamuzi wa Tume ni batili.

Hatma ya mazungumzo!anajua Maalim Seif, CCM

Lakini ya Karume yanazingatiwa?

Na Mwandishi Maalum

Mmoja wa wanasheria aliyechambua uamuzi huo ni mwanasheria mwandamizi Bi Fatma Karume ambaye anasema kuwa tangazo la mwenyekiti wa ZEC kufuta uchaguzi ni batili.

Kabla ya kufikia hitimisho hilo, Fatma Karume amechambua sababu zilizotolewa na Jecha kisha kutizama sheria inasemaje. Katika kipengele cha kwanza anasema kuwa ZEC wanasema “kuna vijana walipeleka kura za mgombea fulani kwa kutumia fujo.” Kisha anahoji, sheria inasemaje katika mazingira hayo? Anajibu kuwa ukisoma kifungu cha 74 cha sheria ya ZEC kinaeleza kuwa “zikitokea fujo kwenye kituo cha kupigia kura, uchaguzi unaweza kuahirishwa mpaka siku inayofuata na Ofisa wa tume katika kituo hicho lazima atoe taarifa kwa tume”. Na kwa maana hiyo ZEC walifanya kinyume na sheria inavyotaka kwa sababu hakuna wakala aliyelalamika kwamba kulikua na fujo katika kituo chake wala hakuna ofisa wa tume aliyeripoti fujo hizo. Na kwamba hata waangalizi wa ndani na nje wanasema uchaguzi ulikuwa huru na haki. “Sasa ZEC imejuaje kulikuwa na Fujo? Pili hata kama zingefanyika fujo, isingekua kigezo cha uchaguzi kufutwa. Sheria inasema vituo vilivyoonesha fujo ingebidi zoezi la upigaji kura lisimame na liendelee kesho yake baada ya ulinzi kuimarishwa. Lakini hili

halikufanyika. Hivyo tume imevunja sheria.”

Katika kipengele cha pili, mwanasheria Karume anasema kuwa ZEC wamedai kulitokea fujo lakini hazikuripotiwa. Hata hivyo akasema kuwa Kifungu no.76 cha sheria kinatoa fursa kwa wakala kuwasilisha malalamiko kabla ya kufunga kituo. “Swali la kujiuliza, je, kuna fomu za mawakala kutoa hayo malalamiko zimejazwa!? Jibu ni hakuna. Kwahiyo ZEC wamejitungia hiyo sababu ili kuhalalisha ufutaji wa matokeo. ZEC wamevunja sheria.” Anasema.

Yapo madai pia kwamba idadi ya kura ilizidi idadi ya wapiga kura walioandikishwa. Kwa madai kama hayo Karume anasema kuwa “Kifungu cha 86 cha sheria (ya ZEC) kinatoa fursa kwa mawakala kujaza fomu maalumu ya malalamiko ikiwa wataona udanganyifu wowote ikiwa ni pamoja na kura kuzidi idadi ya waliojiandikisha.

Na ikitokea hivyo, ZEC haina Mamlaka ya kubatilisha matokeo bali kutoa barua kwa mgombea aliyewasilisha malalamiko ili aende mahakamani kupinga matokeo (isipokua ya Rais). Lakini Zanzibar haikufanyika hivyo. (Kwa hiyo) ZEC imevunja sheria.”

Ama kuhusu ya madai ya mwenyekiti Jecha kuwa matokeo yalijaa udanganyifu hivyo wameamua kufuta uchaguzi wote, wanasheria wanasema kuwa kwa mujibu wa vifungu 85 na 86 vya Sheria,

ZEC haina mamlaka ya “kuhoji” matokeo kwa sababu ZEC sio sehemu ya mgogoro katika hilo shauri (part of dispute). Anayetakiwa “kuchallenge” (kuhoji/kupinga) matokeo ni mgombea au chama chake sio ZEC. Na anatakiwa apeleke shauri lake mahakamani. Mahakama ndiyo itafanya maamuzi baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote. Na kwa msingi huo, ZEC kufuta uchaguzi wa Zanzibar ni kinyume cha sheria.

Katika jumla ya hoja na madai yaliyopelekea mwenyekiti wa ZEC kufuta matokeo ni pamoja na kile kilichodaiwa kuwa kulikua na kura hewa. Yaani hakukuwa na ulinganifu wa kura za kwenye maboxi na idadi iliyojazwa kwenye fomu. Kwa madai kama haya, wanasheria wanatwambia kuwa Kifungu 84 cha sheria kinasema “ikiwa kura zimehesabiwa kituoni na mawakala na wasimamizi wa uchaguzi wakakubaliana kuwa hakukuwa na dosari katika zoezi la kuhesabu kura, basi kura hizo zitahesabika kuwa halali.”

Kwa maana hiyo, kitendo cha ZEC kufanya uamuzi wa kukataa kura zilizokwishakubaliwa na wasimamizi, ni kuvunja sheria.

Katika kuhitimisha hoja zake, mwanasheria Fatma Karume anasema kuwa Mwenyekiti wa ZEC alipotangaza

kufuta uchaguzi alisema “Tume imeamua kufuta matokeo yote ya Zanzibar na hivyo uchaguzi utarudiwa ndani ya siku 90.”

Hata hivyo anasema kwamba, Sheria no.9 ya uanzishwaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 1992 (Zanzibar Electro Commission Act, 1992), inazungumzia uanzishwaji wa ZEC na mamlaka yake kisheria (Establishment and Mandate). Na kwamba Kifungu no.119 (1) cha Sheria hiyo kinasema “maamuzi yoyote ya Tume yatapata uhalali ikiwa mbili ya tatu (2/3) ya wajumbe watakuwa wameridhia.”

Baada ya kunukuu kifungu hicho anasema kuwa Mwenyekiti wa Tume hakushirikisha wajumbe wenzie katika kufanya maamuzi ya kufuta matokeo. Maamuzi hayo aliyafanya peke yake kinyume na sheria inavyotaka. Hivyo basi maamuzi hayo ni batili na hayatambuliki kisheria.

“Uamzi wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kubatilisha uchaguzi hauna msingi wowote wa kisheria. Ni uamuzi uliofanywa kwa matakwa binafsi ili kulinda maslahi ya watawala. Uamuzi huu ni batili tangu mwanzo. Hauwezi kufuta uchaguzi kirahisi kama kufuta ubao. Hata Umiss wa Sitti Mtemvu haukufutwa kirahisi namna hiyo.”

Ufupi wa maneno, maelezo na hoja hizi zinawakilisha maoni na msimamo wa wanasheria wengi juu ya suala hili la uchaguzi mkuu Zanzibar.

Ambacho ni vigumu mpaka sasa kufahamika, ni kitu gani kinajadiliwa katika hayo yanayodaiwa kuwa mazungumzo ya kindugu. Je, ni katika kutizama uhalali na uharamu wa tangazo la Jecha au ni kutizama namna ya kuhalalisha ‘haramu’ na namna ya kuifanya ikubalike kwa wananchi?

Wasiwasi uliopo ni kuwa, kama jambo hili lingekuwa likitizamwa kwa jicho la kuangalia uhalali wa uamuzi wa Jecha (ZEC?) na nini wananchi walifanya katika sanduku la kura, suala hili lisingechukua muda mrefu kiasi hiki. Lakini inavyoonekana pana ugumu wa kupata ufumbuzi na ugumu wenyewe ni namna ya kuhalalisha batili na kufanya ikubalike na kupata uhalali japo wa kisiasa hata kama itakosa wa uhalali wa kisheria na haki.

RAIS John Magufuli (kulia) akisalimiana na Maalim Seif Sharif Hamad Ikulu jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki hii.

ANNUUR NEW.indd 11 12/24/2015 1:43:31 PM

Page 12: ANNUUR 1209aaa

12 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 201512 Makala

YUPO Bwana mmoja kapiga hodi katika ofisi za An nuur wiki hii anataka kujua: ni sura gani na aya gani imewataka Waislamu kusoma Maulid. Wakati Bwana huyo anaingia ofisini, nilikuwa natizama taarifa za Shirika la Ndege la Malaysia, likijulikana kwa jina la Rayani (Rayani Air).

“Malaysia's first Islamic-compliant airline takes off”, kilikuwa ndio kichwa cha habari cha taarifa niliyokuwa nikisoma. Ni taarifa ambayo inaeleza kuwa Rayani, limekuwa Shirika la Kwanza la Ndege katika Malaysia kutoa huduma za usafiri wa anga kwa kuzingatia Sheria za Kiislamu. Ikafahamishwa kuwa, kwanza wahudumu wanawake ndani ya ndege (Flight attendants or cabin crew /air hostesses) watakuwa wakivaa Hijab na kwamba abiria atakuwa na uhakika kwamba vyakula vitakavyokuwa vikitolewa vitakuwa halali. Lakini pia hapatakuwa na pombe. Na kubwa zaidi, kabla ya rubani kuwasha injini kuanza safari, itasoma Dua ya Safari kama ilivyo mashuhuri katika mafundisho ya Uislamu.

“Sisi ni wa mwanzo katika Mashirika ya Ndege ya Malaysia kutoa huduma kwa kuzingatia Shariah. Kwa kweli tunapata faraja sana.” Anasema Mkurugezni Mtendaji wa Shirika hilo Bwana Jaffar Zamhari.

Kutokana na kukua kwa soko la abiria wanaohitaji huduma zenye kuzingatia Shariah, Shirika moja la ndege la Uingereza, Firnas Airways, nalo linapanga kuanzisha huduma hiyo mwakani.

“Nguruwe, ulevi na kila kilicho haramu kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, hakitaruhusiwa katika ‘flights’ hizo.” Inasisitizwa.

Mashirika mengine yanayotoa huduma za usafiri wa anga kwa kuzingatia Shariah ni pamoja na Royal Brunei Airlines, Iran Air na Shirika la Ndege la Saudia.

Tunapozungumzia harakati za Kiislamu, ni kufanya juhudi na program ambazo zitawaletea maendeleo Waislamu na kuupeleka mbele Uislamu. Kila

Maulid njema…

Hawa ndio wanaharakatiNa Omar Msangi

uchao Muislamu apate nafuu katika kutekeleza Uislamu wake kutokana na harakati zetu. Kwa mfano kwa kipindi kirefu, wafanyabiashara Waislamu na hata Waislamu wote tu kwa ujumla, walikuwa na tatizo la riba ya mabenki. Lakini watu wamelifanyia kazi suala hilo, zikaanza kufunguliwa ‘Windows’ za Islamic Banking mpaka sasa tuna Benki kamili. Na hii ni duniani kote. Hivi sasa zishafunguliwa mpaka kampuni za Bima za Kiislamu.

Nakumbuka siku moja nikisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Moscow zama za Mikhail Sergeyevich Gorbachev, na ndege ya Shirika la Ndege la Kirusi, Aeroflot, kilipopitishwa chakula ndani ya ndege bwana mmoja akamuuliza abiria mwenzake, ‘tusije tukalishwa khinziri hapa, hawana dini hawa.’ Mwenzake akamjibu kwa masikhara, ‘juu kote huku angani nguruwe atatoka wapi’.

Almuhimu, kwa wasafiri wa ndege au wanaofika mara kwa mara kupata huduma za malazi na vyakula katika mahoteli makubwa wanajua adha ya nyama ya nguruwe na pombe.

Sasa tunapozungumzia harakati za Kiislamu, ni pamoja na kutizama namna ya kuwaondolea Waislamu kero kama hizi. Lakini kama harakati zitakuwa ni za kutoa tu maneno makali katika mimbari za misikiti na katika makongamano, lakini mwisho wa siku Muislamu yupo pale pale na kero zake, hizo kwa hakika ni harakati tasa. Hazina maana.

Wiki iliyopita nilikutana na kijana mmoja wa Kiislamu ambaye yupo mwaka wa pili Chuo Kikuu akisomea ‘Medicine’ katika moja ya Vyuo Vikuu binafsi nchini. Ada ya chuo hicho kwa mwaka ni kiasi milioni sita na laki saba (6,700,000). Bodi imempa mkopo wa milioni 3 na laki mbili anatakiwa kulipa milioni 3 laki tano (3,500,000) zilizosalia. Wazazi, ndugu na jamaa hawana uwezo. Anahangaika kijana hajui la kufanya. Mwishowe itabidi akose masomo na udakitari.

Kutokana na ufinyu wa bajeti, serikali inajikuta kwamba inashindwa kutoa

mikopo kwa ajili ya wanafunzi wote wenye sifa za kwenda vyuo vikuu. Hii ni kero na tatizo kwa vijana wa Kiislamu na Watanzania kwa ujumla. Ukizingatia malalamiko ya muda mrefu ya Waislamu kwamba wamepunjwa na wamebaguliwa katika elimu, ulitarajia vijana wanaharakati wa Kiislamu walione tatizo hili la mikopo. Angalau liwashugushulishe. Ikiwezeka wakusanye nguvu waanzishe mfuko wa kuwasaidia vijana wa Kiislamu ambao watakosa mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ilihali wana sifa za kusoma. Lakini wapi, ndio kwanza wengine wanataka kujua, hii kupumzika siku ya Maulid imekuja katika Aya na Hadithi gani! Kwa hakika kuendelea kulalamika na kutoa maneno makali bila ya kutizama fursa kama hizi zilizopo na kuzitumia, haitatusaidia sana.

Niliwahi kusafiri kwa basi kutoka Istanbul, Uturuki hadi Isparta kupitia Ankara. Ni masafa marefu. Ukiacha miji na vituo vidogo vidogo ambapo mabasi yanasimama

kwa chakula na huduma nyingine, kila utakapopita utakuta vibanda vimejengwa porini au katika vijiji mnapopita kwa ajili ya ‘kuchimba dawa.’ Na ndivyo ilivyo kwa miji mingi kwa nchi zilizoendelea.

Sasa njoo hapa kwetu. Sheikh wangu Maalim Ally Bassaleh atakumbuka ile kauli yake “Alhamdulillah kwa Neema ya Uislamu” akishukuru kwa neema ya Uislamu baada ya watu kushuka katika basi wakikimbilia porini kuchuma dawa, bila kujali stara wala maji ya kujisafisha jambo ambalo Muislamu hawezi au tuseme ni vigumu kufanya. Ilitarajiwa wanaharakati sisi tuone kero inayowakabili Waislamu wanaposafiri safari ndefu na mabasi, tuchukue fursa hiyo kuwasiliana an mamlaka husika tukusanye nguvu tujenge sehemu za ‘kuchimba dawa’ na hata misikiti midogo ya kuswalia katika barabara zote kuu kila baada ya masafa kadhaa. Inakuwa mradi na huduma.

Katika toleo lililopita la gazeti hili, Juma Kilaghai akizungumzia nguvu ya wingi, alitoa mfano wa nyuki. Kwamba nyuki ana ‘mchale’ mmoja tu. Akishautumia kukuuma, hawezi tena kukufanya lolote. Lakini ni wingi wao unaowapa nguvu na kuwa hatari kwa anayewasogelea.

Pamoja na kuwa tunaweza kuleta hoja kuwa Waislamu walio wengi ni masikini, lakini kwa guvu ya wingi kama alivyoifafanua Kilaghai, shilingi mia moja tu kwa siku, inaweza kufanya maajabu. Asipatikane hata mwanafunzi mmoja Muislamu kukosa kusoma Chuo Kikuu kwa sababu hajapata mkopo kutoka Bodi au kapata pungufu na wazazi hawana uwezo.

Sasa pengine tutumie fursa ya wakati huu wa Maulid kutafakari namna ya kutumia nguvu ya wingi wetu katika harakati zetu kufanya mambo ya maana badala ya malumbano yasiyosaidia lolote katika kuwasogeza mbele Waislamu.

Tukiendelea kupiga kelele na kutoa maneno makali, huku Muislamu akitoka hapo anakwenda kutibiwa katika mazingira ambayo si rafiki na Uislamu wake, hizo sio harakati.

Maulid njema.

Ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia, (Rayani Air).

Ndege ya Shirika la ndege la Brunei ikiwa angani.

ANNUUR NEW.indd 12 12/24/2015 1:43:31 PM

Page 13: ANNUUR 1209aaa

13 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015Safu ya Ben Rijal

SAFU ya Mashekhe wetu waliopita leo itamuangalia

Sheikh Fatawi bin Issa na mchango wake alioutoa katika elimu ya dini ya Kiislamu. Jina lake kamili ni Fatawi Issa Mussa Hassan bin Haji bin Khatib. Sheikh Fatawi ni mzaliwa na Nganani, Makunduchi katika kijiji ambacho amezaliwa na kukulia hapo. Alianza masomo yake ya Chuwoni kwa mzee Choko.

Wazazi wake walijitahidi

Sheikh Fatawi bin Issa -9NAMTANGULIZA kumzungumzia Sheikh Fatawi bin Issa kabla ya kumchambua Sheikh Abdallah Saleh Farsy. Sheikh Fatawy bin Issa ndio Kadhi wa mwanzo visiwani Zanzibar akiwa ametokea maeneo ya Shamba. Alikuwa kati ya Masheikhe wachache waliobaki mara tu baada ya Mapinduzi ikiwa wengi waliihama nchi akiwemo Syd Umar bin Sumeyt, Sheikh Umar bin Abdallah, Sheikh Abdallah Saleh Farsy na wengineo. Alichaguliwa Ukadhi kuziba pengo aliloliwacha Sheikh Abdallah Saleh Farsy

kumsomesha mwanawao elimu ya dini na ya dunia, alipelekwa skuli kujifunza masomo ya Kizungu akiwa kati ya watoto wa mwanzo kujiunga na elimu ya skuli katika Makunduchi.

Kujiunga kwake na skuli kulikuja kumsaidia siku za baadaye juu ya kufanya hesabu na kuandika kwa Kiswahili. Kwa hio masuala ya Mirathi ilikuwa ikimrahisishia kuweza kuyafutu. Masheikhe wengi

walikuwa wakipata tabu kuusomesha mlango wa Mirathi kutokana na uzito wake wa kuwa unataka kuwa na ueledi wa hesabu na wanafunzi huchukua muda mrefu kuukamilisha mlango huu.

Sheikhe Fatawi alikuwa mwanafunzi mahiri. Alikuwa akiyamudu masomo yake vilivyo. Ilifika wenzake wa hirimu moja kumuheshimu na kumsogeza mbele kuliko wenzao wote na walikuwa siku zote

wakimfurahikia kwani alikuwa kila suala gumu yeye akilijibu. Wenzake walikuwa wakicheza mara zote na kuimba “Usi Mcha (Fatawi Issa) ngaia kidogo” na huku wakidemka kama ngoma ya msembwe. Nyimbo hio waliokuwa wakiimba wenzake ni kutamani kwao na wao wawe mahodari kama Fatawi bin Issa na kutaka akili yake awagaie walau kidogo.

Masheha wa siku hizo walikuwa ni watu wenye hadhi ya hali ya juu na kuheshimika. Sheha huchaguliwa kuwa ni mtu mwenye umri mkubwa, mwenye kuheshimika, ajuaye elimu ya akhera na ya dunia vile vile mtu mwenye hikma ya hali ya juu na asiyekuwa na upendeleo katika

masuala ya kazi yake.Ili Sheha wa siku

hizo ajisikie alikuwa akifanya juu chini kuwaelimisha watoto wao ili na wao wafike kuwa ni watu wenye hadhi. Sheikhe Fatawi alisoma na mtoto wa Sheha, Saleh Hijja, ambaye baadaye alihamishiwa mjini ili aweze kuelimika vya kutosha na kuja kumrithi baba yake au kuweza kupata nafasi ya juu katika Serikali. Mtoto wa Sheha kuelekea mjini kulimuathiri sana Sheikhe Fatawi na kutaka na yeye kwenda mjini akasome dini na masomo ya skuli ali aweze kutoa ushindani kwa mtoto wa Sheha.

Mtaa wa Nganani ulikuwa na bahati ya kuetembelewa na Masheikhe mbalimbali akiwemo Syd Abal Hassan, Sheikh Abdalla Bakathir na Sheikh Muhamd

Inaendelea Uk. 14

TAREHE 9 December, 2015 yale mazowea tuliokuwa yametuzowea ya sherehe kuu ya kitaifa kusheherekewa kwa Magwaride na shamra shamra za kila jazanda, safari hii hazikuwepo na mbadala wake ulikuwa ni kusafisha na kukusanya taka Tanzania bara nzima. Yaliojiri safari hii yameukinza msemo u l i y o k u w a u k i s e m a , “ L i p u l i z wa p o z u m a r i visiwani , watu mpaka kwenye maeneo ya maziwa huhemkwa.” Safari hii lilizwa Tanzania Bara na visiwani nako wakahemkwa. Aliyepuliza zumari safari hii sio mwanamuziki, lakini alikuwa Rais wa nchi naye ni Daktari. John Pombe Magufuli. Hakika kitendo hicho hakijawashajiisha na kuwafurahisha walioko Tanzania tu lakini hata nje ya mipaka ya Tanzania kilivuliwa kofia, kilemba na kupewa heko.

Suala z ima l i l ikuwa ni taka na kuzidhibiti ili kuweza kuuweka mji safi na kuepukana na maradhi a m b a y o h u t o k e a n a kusambazwa na vijidudu kutokana na taka, ziwe taka ngumu au maji machafu. Taka ni usumbufu na taka kila kukicha huzalishwa w a l a h a k u n a n j i a y a kuzisitisha kuzalishwa kwa

Yawe Endelevu - 1Na Ben Rijal

kuwa mwanadamu anaishi naye ndio chanzo cha taka kuzalishwa taka na kuzagaa.

Taka ni chochote kile utachokitumia kisha ukawa h u n a h a j a n a c h o t e n a ukaamua kukitupa huwa ni taka. Mwanzo kitu hicho huwa cha matumizi kisha kinageuka kinakuwa ni taka. Mfano ukakata ndizi ukaipika maganda ya ndizi hugeuka taka, machicha nayo huwa taka, na maji ulioshea sufuria nayo huwa maji machafu, samaki huwa ni chakula ukimpara na ukisafisha na ukamtengeneza miba ukiyatupa na matumbo wakati wa kutengeneza hapo hayo mabaki huwa taka, dawa imo ndani ya chupa yake ikimalizika ukiitupa chupa huwa ni taka. Aidha chupa ya maji huwa unaitumia ukimaliza kuitumia. Ukiitupa mwishowe huwa taka.

Taka ni taka na haitokuwa taka ni kukaa nazo lazima uzitupe kisha uzidhibiti. Sehemu ya pili ya makala hii itazungumzia namna sasa baadhi ya nchi, taka sio taka tena au tuite uchafu, lakini taka ni mali ni nyezo ya matumizi

Kuna aina mbili kuu za taka nazo taka ngumu (solid

waste) na maji machafu au lugha ya kimambo leo imetafsiriwa kutokana na neno la Kizungu (liquid waste) nakuitwa maji taka.

Taka zimegawiwa kwa mgawanyiko ufwatao: (a) Taka za kawaida (ordinary was te ) z inazoza l i shwa majumbani , madukani , taasisi mbalimbali za kijamii n.k. (b) Taka zinazotokana na mahospitali (medical waste). Taka hizi wingi wake zinakuwa za hatari na zinahitajia uangalifu katika utupwaji wake. (c) Taka maalumu (special waste), taka hizi huwa zina mchanganyiko na zinahitajia h a d h a r i k u b wa k a t i k a ukusanywaji wake pamoja na kutupwa kwake. (d) Taka za kilimo (agriculture waste) taka hizo hutokana na kilimo kutoka mabaki ya kilimo pamoja na madawa yanayotumiwa. (e) Taka zinazotokana na viwanda (industrial waste) hizi ni taka ambazo baadhi yake huwa ni za hatari.

T a k a h u h i t a j i w a k u d h i b i t i wa k wa n j i a mbalimbali bila ya kufanya hivyo taka huwa ni mashaka. Ukweli hakuna atakaye kukaa na taka, kwahio taka

zitupwe, kutupwa kwake zitupwe pasi kuleta athari (processing treatment).

Dondoo juu ya TakaKabla ya kuzama katika

mada hii hebu tuangalie namna ya mzigo wa taka ulivyo duniani na taka zilivyo kwa jumla. Inakadiriwa kila mwaka hutupwa tani milioni 50 za vi tu vya umeme ulimwenguni kote zikiwemo TV, zana za jikoni n.k. Kila mwaka duniani kote inakisiwa kumwagwa kwa chakula kinachofikia tani milioni 7.2 na nusu ya chakula hicho kinachotupwa kinaweza kutumiwa na kuliwa baada ya kutupwa. Katika kila watu 7 waliopo katika dunia hii tuliomo, kuna mtu mmoja hana chakula cha kula. Wenye maduka makubwa yanayojulikana kwa jina la Supper market hupelekewa vyakula ya matunda na mboga. Makisio yanaonyesha kuwa baina ya asilimia 20 na 40 hukataliwa na maduka hayo na mwisho wake huwajibika kutupwa.

Uingereza ni moja kati ya nchi zilizoendelea na watu wake wanaishi katika maisha ya anasa. Inakadiriwa kuwa taka zinazozalishwa Uiengereza zinaweza kulijaza

ziwa kubwa liliopo nchi hio lijulikanalo kama Lake Windermere kwa kipindi cha miezi 8 tu na zinaweza kulijaza ukumbi maarufu ujulikanalo Albert Hall kwa kipindi cha saa mbili tu kukawa hapana pa kutia mguu. Mifuko ya plastiki ifikayo milioni 500 hutumika na hununuliwa kila wiki kwa nchi ya Uiengereza. (Rejea: https://www.ovoenergy.com/blog/green/10-shocking-facts-about-waste.html).

Wa k a z i wa n c h i ya Marekani kwa mwaka hutupa madaipa 16,000,000,000, kalamu bilioni 1.6, vimwembe vya kunyolea bilioni 2 na mipira ya gari milioni 220. Wapanga hesabu na takwimu wamekuja kugundua kuwa kijana wa miaka 7 wa nchi ya Canada atakuwa ametumia rasilimali sawa na mkazi mtu mzima wa nchi zinazoendelea katika maisha yake yote.

Mbinu za kuzidhibiti TakaKatika somo la Mazingira

kuna R3 kwa Kiengereza zinahitajiwa kuzingatiwa nazo hutamkwa “ Reduce“ Punguza, “Reuse“, Tumia tena na “Recycle“ Kuzirejesha taka katika matumizi yake. R3 hizi zinahitajika pakubwa kuweza kuzitumia katika upunguzwaji wa uzalishaji wa taka ambazo tunazizalisha kila siku.

Tu z i a n g a l i e t a k a n a uzalishwaji wake katika

Inaendelea Uk. 19

ANNUUR NEW.indd 13 12/24/2015 1:43:32 PM

Page 14: ANNUUR 1209aaa

14 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015

MAKALA/MASHAIRI

Mhariri muadhamu, nipokee hodi hodi, Janibu japo nikumu, ya gazetilo suudi, Ndaniye abra nikimu, nitoe wito saidi,Kwa habari zenye nuru, tusomeni AN-NUUR. Naibtadi nudhumu, kwa Allah kumhimidi, Thuma swala na salamu, kwa rasuli Muhammadi, Kadhalika taadhimu, kwa swahaba murshidi, Kwa habari zenye nuru, tusomeni AN-NUUR. Baada ya taadhimu, sina budi kulinadi,Gazeti letu adhimu, ndani lenye irishadi,Kadhalika taalimu, na mzomzo suudi,Kwa habari zenye nuru, tusomeni AN-NUUR. Limesimama kawimu, pamwe na kutabaradi, Lengole hasa ikumu, ya Ilahi Tauhidi,Na zende zote kuzimu, za rajimu itikadi,Kwa habari zenye nuru, tusomeni AN-NUUR.

wa makalaze adhimu, za kisomi na weledi,Latujaza ufahamu, wa mengi yaso idadi,Kwa habari na elimu, kwalo tunastafidi,Kwa habari za yakini, tusomeni AN-NUUR.

Latetea madhulumu, kwa uvumba na kwa udi,Ukweli lauadhimu, na urongo kuurudi,Kwa yake mastakimu, kulisoma yatubidi,Kwa habari za yakini, tusomeni AN-NUUR. Daima dumu dawamu, kwalo nyuma tusirudi,IJUMAA 'napotimu, sote tufanze juhudi,Nakalaye tujihimu, japo moja kwa nakidi,Kwa habari za yakini, tusomeni AN-NUUR.

Kaditamati nudhumu, sitozisha idadi,Thamaniya zimetimu, za wito bila inadi,Naweka chini kalamu, AN-NUUR 'tuliridi',Tusomeni AN-NUUR, kwa habari za yakini.

KUMBUKUMBU YA UZAWA WA MTUME (S.A.W)(KUMSIFU SI HOJA!)

Kalamu i mkononi, kunena kwa uchechefu, Kwa beti zenye mizani, pamwe vina linganifu,Ndani nuni kasirani, nje vya fee dhumefu,Kumsifuye si hoja, hoja kugeza mwendowe !

Mada adhimu mezani, ni ya Tumwa kumsifu,Sifa zake Qur-ani, ishatujuza lufufu,Tamamu ziso kifani, siioni yake kufu,Kumsifuye si hoja, hoja kugeza mwendowe!

Si baidi karibuni, vyombo vimetuarifu,Jumatano waumini, Dar twende kumsifu,Rasuli maulidini, kwa twarika isohifu,Kumsifuye si hoja, hoja kugeza mwendowe !

Twarindima maidani, pasipo hata hawafu,Kwa zumari na maghani, kadhalika na madufu,Kwa nyenzozo pasi soni, twazuumu kumsifu,Kumsifuye si hoja, hoja kugeza mwendowe !

Bilhaki kwa yakini, na kwa dhati nakashifu,Jambo hili silioni, kwenye nususi sharifu,Si Sunnah yake Amini, wala Qurani tukufu,Kumsifuye si hoja, hoja kugeza mwendowe !

Niwombe kwa tamakuni, na kwa mtima kunjufu,Wenye dalili yakini, za hili waniarifu,Nitoke upotovuni, niupate uongofu,Kumsifuye si hoja, hoja kugeza mwendowe !

Mwisho nakushaurini, kwa lengo la uzindufu,Wahidu wa ishirini, AHZABU muishufu,Rasuli mtabaini, wa kugezwa si kusifu,Hoja kumgeza yeye, na wala si kumsifu.

ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

Tusomeni AN-NUUR

Sheikh Fatawi bin Issa -9Inatoka Uk. 13Bakathiri wa Fujoni na wengine ambao kila wakipata nafasi hufika Nganani. Masheikhe hao wote wanapofika Nganani hulahakiwa na mwenyeji wao akiwa Sheikh Issa baba wa Mohammed Issa ambaye huyu alikuja kutokea kuwa alim mkubwa katika zama hizo.

Sheikh Fatawi alipata fursa kusoma kwa vigogo hao ambao walikuwa magwiji katika fani ya Kiarabu na Sheria ya Kiislamu pamoja na tafsiri ya Qur’an na tarekhe. Sheikhe Fatawi alikuwa na fahamu pana na Masheikhe hao niliokwisha kuwataja walitokea kumpenda na kumiminia kila walichokuwa nacho, kwa kuwa walikuwa washamuona kuwa kijana huyo atakuja kuwa mtu muhimu katika siku za badaye.

Sheikh Muhammad wa Fujoni alimchukua Sheikh Fatawi na baada ya wazazi wake kukubali kumpeleka mtoto wao kwa Sheikh huyo na huko nako alifanikiwa kujifunza mengi.

Jina Fatawi alipewa kutokana na uwezo wake wa kuyafutu masuala mazito mazito wakati akiwa ni mdogo. Maana ya halisi ya Fatawi ni kuweza kujibu masuala kwa urahisi. Jina lake khasa ambalo alilopewa na wazazi wake lilikuwa ni Ussi. ghafla jina hilo likapotea alipokuwa madrasa anasoma.

Mzee Ussi kwa jina jengine mzee Kidagaa alikuwa ni mmoja wa wana familia ya Sheikh Fatawi alikasirishwa sana kusikia kuwa Ussi sasa kawa Fatawi. Mzee Ussi na wenziwe

walimpelekea Sheikh Issa salamu kutaka kujua lilopelekea Ussi Mcha kuitwa Fatawi. Ghadhabu zao zilikuwa hazina kifani.

Mzee Ussi alitulizwa nambari zake mara mmoja kuwa jina la Fatawi ndio hilo hilo Ussi na Ussi kawa Fatawi kwa kuwa amekuwa mahiri wa kujibu masuala mazito mazito. Mzee Ussi alitosheka na maelezo hayo na akamuombea dua, Mola amzidishie ilimu na iwe pana. Tena hapo ukatiwa ubani na mzee Ussi ndio aliokoleza chetezo na kuomba dua zote azijuwazo.

Sheikh Fatawi alisoma na kukaa kwa Sheikh Mohammed kwa kipindi kisichopungua miaka 9. Sheikh Ali alikuwa ni Sheha wa Fujoni akiwa na nasaba ya Kitumbatu alikuwa sio kama Sheha tu lakini alikuwa alim. Sheha huyo alipomuona Sheikh Fatawi uwezo wake wa ilimu, alimuomba Sheikh Mohammed akae naye aweze kumsomesha na kumsaidia katika kazi zake za Usheha.

Wakati wa Vita vya mwanzo vya dunia, wakati huo Sheikhe Fatawi alikuwa akiishi Fujoni na kazi yake kubwa ambayo ilikuwa ya hatari akipelekea watu chakula waliokuwa mafichoni wakiukimbia mkono wa Serikali kuwataka kwenda vitani. Sheikhe Fatawi alikuwa jasiri na kujitolea kufanya hivyo ambacho kitendo hicho hakikuwa rahisi.

Baada ya kuwepo Fujoni kwa takriban muongo mmoja, aliamua kurudi kwao Makunduchi akiwa ameelimika

vizuri na alipotua tu hapo, alikabidhiwa kuendesha darsa zote zile ambazo zilikuwa zikisomeshwa. Kati ya wale waliokuwa wakihudhuria darsa zake walikuwa ni walimu wake Sheikhe Issa na Sheikhe Hafidh bin Ameir. Baadhi ya Masheikhe aliosoma kwake ni Sheikh Mohammed wa Fujoni, Sheikh Abdulrahim wa Chwaka, Sheikh Hassan bin Ameir wa Makunduchi, Syd Abal Hassan na Syd Umar bin Sumeyt.

Katika kazi ambazo aliwahi kuzifanya alikuwa mwalimu wa skuli akisomesha Kiarabu, dini na tarekhe. Aidha alipewa Ukadhi wa eneo lote la Wilaya ya Kusini.

Mara tu bada ya Mapinduzi ya mwaka wa 1964 katika mwaka wa 1968 Sheikh maarufu aliokuwa Kadhi wakati huo Sheikh Abdalla Saleh Farsy alihajiri Zanzibar na kuhamia Mombasa, Kenya na nafasi alioiwacha ilikuwa haina mtu mwengine munasaba zaidi ya Sheikh Fatawi bin Issa na Rais wa Zanzibar akamteua Sheikh Fatawi kushikilia nafasi hii. Aliishikilia nafasi hio na kufanya kazi kwa juhudi zote, lakini uzee uliposonga mbele na nguvu kumpungukia aliamua kustaafu.

Sheikh Fatawi alifunga macho mwaka wa 1987 baada ya kuugua kwa kipindi cha mwaka mmoja na kukatwa mguu.

(Makala hii nimeiandika kutokana na msaada mkubwa wa Sheikh Salmin Hafidh. Kwa maoni mawasiliano tumia 0777 43 69 49)

ANNUUR NEW.indd 14 12/24/2015 1:43:32 PM

Page 15: ANNUUR 1209aaa

15 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015Makala

Yesu: Nabii wa WaislamuInatoka Uk. 8Akasema; Mimi ni

mjumbe tu wa Bwana wako, kuwa niweke kwako mwana asiye na waa. Maria akasema: Nawezaje kuwa na mwana wakati hakuna mtu anayeishi ambaye amenigusa, na wala sijawahi kuishi kwa uharibifu? Akasema: Ndivyo itakavyokuwa. Bwana wako anasema, Ni rahisi kwangu na rehema kutoka kwetu, na ni kitu ambacho kimeamriwa (Kurani 19:16-21).

Karen Armstrong anaandika, katika kitabu chake cha maisha ya Muhammad, kuwa "Jafari alipomaliza, ubora wa Kurani ulikuwa umefanya kazi yake. Negus alikuwa akilia kwa nguvu kiasi kwamba ndevu zake zilikuwa zimelowa, na machozi yaliteremka katika mashavu ya maaskofu wake na wasaidizi wake kwa wingi kiasi ambacho mavazi yao shingoni yalikuwa yamelowa." Waislamu hao walibaki Abyssinia, chini ya ulinzi wa Negus, na waliweza kushiriki dini yao bila kizuizi.

Hata hivyo, kwa Waislamu, bikira kutwaa mimba siyo ushahidi wa uungu wa Yesu, ila umuhimu wake maalum kama nabii na masihi. Utatu Mtakatifu unakataliwa na Uislamu pamoja na kupigiliwa msalabani na ufufuo wa Yesu. Msingi wa pamoja wa kitheolojia unaonekana kuminywa katika eneo hili - kama Jonathan Bartley, mkurugenzi mshirika wa kundi la uchambuzi wa Kikristo liitwalo Ekklesia (Mhubiri) anavyosititiza, kuamini katika ufufuo ndiyo 'kinachovunja makubaliano.' Anaongeza: 'Kuna mvutano wa kina katika moyo wa mazungumzo kati ya imani hizi mbili ambako hakuna upande ulio tayari kulikabili suala hilo, na hili ni mtazamo wa jadi wa Ukristo kuhusu Yesu ambao ni kufuru kwa Waislamu na kuwa mtazamo wa jadi wa Uislamu kuhusu Yesu ni kufuru kwa Wakristo."

Anayo hoja. Kurani inautaja Ukristo kuwa ndiyo umetunga dhana ya Utatu:

“Usiseme, 'Utatu,' Acha! Hilo ni jema zaidi kwako. Mungu ni Mmoja. Utukufu uwe kwake (utukufu alio nao) ni zaidi ya kuwa na mwana.” (Kurani 4:171)

Inaukosoa Ukristo kwa mazoea yaliyoenea

miongoni mwa madhehebu yake yakimwabudu Yesu na Maria na inaweka ukosoaji huo katika hali ya hojaji kwa Yesu kutoka kwa Mungu:

“Na pale Mungu atakaposema: "Ewe Yesu, mwana wa Maria, uliwaambia watu, 'Nichukueni mimi na mama yangu kuwa ni miungu nje ya Mungu'? Atasema, "utukufu uwe nawe, haikuwa kwangu kusema kile ambacho sikuwa na haki ya kusema! Kama ningesema, ungelifahamu jambo hilo.” (Kurani 5:116)

Yesu, kama Khalidi anavyoonyesha, "ni nabii mtata. Ndiye nabii pekee katika Kurani ambaye kwa makusudi kabisa anafanywa kujitenga na jinsi ambavyo jumuia yake inasemekana kumfahamu." Kwa mfano, Waislamu wanaamini kuwa Yesu hakusulubiwa ila aliinuliwa kimwili hadi mbinguni na Mungu.

Hata hivyo wanazuoni wengi wa Kiislamu wamesisitiza kuwa dhana ya Uislamu ya Yesu - bila uungu, nje ya Utatu, nabii - inaendana na imani na mafundisho ya baadhi ya madhehebu ya kwanza ya Wayahudi Wakristo, kama wa-Eboni na wa-Nazareni, ambao waliamini kuwa Yesu ndiye Masihi, ila hana uungu. Waislamu wanadai Yesu wa Waislamu ndiye Yesu wa kihistoria, akiwa ameondolewa fikra ya kuundwa na watu baadaye, ya Ukristo-mantiki. "Yesu kama ambavyo angekuwa bila Mtume Paulo, Mtakatifu Augustine au Baraza la Nicea," kumnukuu msomi wa Chuo Kikuu cha Cambridge, John Casey.

Au, kama A.N. Wilson alivyoandika katika gazeti la Daily Express muongo mmoja uliopita, "Uislamu ni itikadi ya kukiri utukufu wa Mungu kimaadili na kwa ufahamu bila kubeba mzigo wa mapokeo ya Kikristo.... Ndiyo maana Ukristo utapoteza nguvu katika karne (na zama) inayokuja, na njaa ya dini ya moyo wa binadamu itajibiwa na Mwezi Mchanga, si Msalaba." Licha ya tofauti kubwa za mapokeo, bado kuna maeneo ya kushabihiana kwa dhati, kwa mfano ujio wa pili wa Kristo.

Waislamu na Wakristo kwa pamoja wanakiri imani kuwa dunia itamalizika Yesu atakaporudi kwa ushindi dhidi ya Mpinga Kristo, ambao Waislamu wanamwita Dajjal. Dhana ya Yesu Muislamu, katika hali yoyote ya mapokeo, inaweeza kusaidia kujenga dhamira ya wanazuoni ambao wanaongelea haja ya kuunda upya nadharia ya ustaarabu wa kipekee wa Uyahudi-Ukristo. Hii inaweza kuwa haikubaliki katu kwa Wakristo wa Injili pambanaji - hasa katika Marekani, ambako wahubiri masifa kama Franklin Graham wanauona Uislamu kama "dini ya uovu yenye mabaya mengi" - lakini, kama Khalidi anavyoainisha, wakati mapokeo ya Kiyahudi kwa jumla yanamkataa Yesu, mapokeo ya Kiislamu, na hasa Usufi au Uislamu wa ufahamu roho, unajenga mahali pale katika kina kabisa cha mihimili yake ya utii."

Hata hivyo, Yesu anabaki kuwa sehemu ya imani ya kina na wanayofanya Waislamu. Wapi, kwa mfano, kuna kinachofanana na Krismasi katika Uislamu? Kwanini Waislamu wanasherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad na siyo kwa Nabii Issa? "Sisi pia, kwa njia yetu wenyewe tusherehekee kuzaliwa kwa Yesu.... (kwani) ni muhimu sana kwetu,: anasema Mogra. "Lakini nadhani kila jumuia ya kidini ina maadhimisho yake. hivyo Waislamu watafanya sherehe zao na Wakristo za kwao."

Katika miaka ya karibuni, magazeti ya kihafidhina nchini Uingereza yamepinga vikali kinachodaiwa ni juhudi za serikali za mitaa za kujali itikadi kushushua na hata kukataza Krismasi. Jaribio la jiji la Birmingham kuita sikukuu zake za msimu (Krismasi) kuwa ni 'Winterval' na mifumo ya taa inayoendana na sinema za mtoto mchawi Harry Porter au 'Luminos" (mwanga) ni mifano iliyochukiza. Kuna hisia mara nyingi kuwa maamuzi kama hayo kunasukumwa na woga kuwa kuonyesha waziwazi ishara za imani ya Kikristo kunaweza

kuchukiza hisia za Waislamu Waingereza, lakini, ukizingatia umuhimu wa Yesu katika Uislamu, woga kama huo unaokenana kuvuka mpaka, (Kwa undani wa suala hilo, majaribio hayo yanatumia tu Uislamu nchini Uingereza kama kisingizio, ila ni juhudi za Uyahudi wa siri, ambao kwa karne nyingi ndiyo unaitwa pia u-Freemason, kuvuruga imani ya Kikristo kwa ajili ya mapokeo ya kishetani kuwa imani zote ni sawa, na hakuna kitu kama upagani, n.k.-Mtafsiri).

Mogra, ambaye anaongoza kamati ya uhusiano na dini nyingine ya MCB, anakubali: "Ni upuuzi kubadili jina Krismasi, akiongeza: Uingereza ina sifa kubwa inapokuja katika suala la kusherehekea sikukuu za jamii zetu za dini tofauti. Zibaki kuitwa zilivyo, na tuzisherehekee zote."

Mogra anadiriki kuwahimiza Waislamu kuingia katika uwazi na mbele za watu kumsherehekea Yesu, hasa kuzaliwa kwake, ili kufikia taadhima ya ndani ambayo Waislamu wanayo kwake. Hivi kuna hatari, hata hivyo, kuwa majaribio ya Waislamu kuinua upya umuhimu wa Yesu ndani ya Uislamu na kama sehemu adhimu ya imani yao na mapokeo inaweza kueleweka vibaya? Wanaweza kueleweka vibaya kuwa ni sehemu ya Uislamu unaodaiwa kujizatiti na kutwaa itikadi ya kisiasa kujaribu kuiteka taswira ya Yesu, katika ulimwengu wa nchi za Magharibi ambako Ukristo wa kitaasisi unaonekana kufifia? Inaweza kuwa ni hatua ya kuumiza mazungumzo baina ya makundi ya imani tofauti? Viongozi wa Kanisa, kwa bahati nzuri, wanaonekana kukataa. "Nimefurahi wakati wote kuchukua muda na marafiki zangu Waislamu, ambao sisi kama Wakristo tunayo mengi ya pamoja, pamoja na Wayahudi, kwani tunaifuatilia imani yetu wote kwa kurudi nyuma hadi kwa Ibrahimu. Aliyekuwa Askofu Mkuu wa York, Dk. John Sentamu (marehemu) aliniambia:

"Ninapotembelea msikiti, nikiwa nimealikwa kwa jina la Allah na Mtume Wake Muhammad, amani iwe kwake, najibu na salaam katika jina la Yesu, ambaye ninyi Waislamu mnamkiri kama nabii, na ambaye mimi namfahamu kama Mwokozi wa Dunia, Mfalme wa Amani."

Wakati huu wa mvutano kati ya magharibi ya Kikristo na mashariki ya Kiislamu, kumwangalia Yesu kwa pamoja - na kile Khalidi anachoita ukumbushaji "adhimu" wa enzi ambako Ukristo na Uislamu vilikuwa na uwazi zaidi mmoja kwa mwingine na kuwa tayari kutegemea mashahidi wa upande mwingine - kunaweza kusaidia kujaza pengo linalozidi kupanuka kati ya imani hizi mbili kubwa zaidi duniani. Mogra anakubali: "Hatuna haja ya kupigana kuhusu Yesu. Ni muhimu kwa Wakristo na Waislamu. Kimo chake kinazidi maisha ya kawaida. Tunaweza kuwa naye kwa pamoja."

Mchungaji David Marshall, mmoja kati ya wataalamu wa Kanisa la Uingereza kuhusu Uislamu, ananukuu hitimisho la aliyekuwa Askofu Mkuu wa Cantebury, Rowan Williams, katika semina ya wanazuoni wa Kikristo na Kiislamu. Anasemekana aliguswa na "umakini wa tofauti zetu." "Wakristo na Waislamu wanapingana katika maeneo mengi na wataendelea kupingana - lakini kiwango tunachotofautiana hakikupangwa milele," anasema Marshall. "Waislamu wanahimizwa na Kurani wajadili kwa njia iliyo bora tu na Watu wa Kitabu,' (Kurani 29:46) na Wakristo wanahimizwa kueleza tumaini ambalo liko ndani yao "kwa uungwana na taadhima" (1 Petro 3:15).Kama tuaweza kufanya haya, hatuna sababu ya kuingiwa na hofu."

('Yesu Muislamu,' na Tarif Khalidi kinachapishwa na Chuo Kikuu cha Harvard (bei pauni 14.95). Mehdi Hasan ni mhariri mwandamizi (siasa) wa jarida la New Statesman la Uingereza.)

ANNUUR NEW.indd 15 12/24/2015 1:43:33 PM

Page 16: ANNUUR 1209aaa

16 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015Makala

Haya ndiyo majipu ya kupasuliwaInatoka Uk. 10vita dhidi ya ugaidi.

Hata hivyo niliposikiliza mahojiano hayo ya BBC na kusikia ile kauli ya Waziri Joseph Nkaisery akiwapongeza Waislamu kwa kitendo chao cha ujasiri, uzalendo, udugu na upendo, nikaona kuna haja ya kusema neno kwa sababu hapa kuna tatizo la “wrong message”, kwa maana ya ujumbe sio.

Tukio lenyewe linaelezwa hivi: Basi moja lililokuwa linasafiri kutoka Nirobi kwenda Mandera likiwa na abiria 62 mnamo Desemba 21, 2015 lilivamiwa na magaidi wa Al-Shabaab wapatao 15 wakiwa na silaja nzito za AK-47. Baada ya kusimamisha basi, baadhi ya magaidi waliingia katika basi na kuanza kuwatenganisha Waislamu na Wakristo ili wapate kuwauwa Wakristo pekee.

Kwa mujibu wa taarifa za BBC, Associated Press, Agence France-Presse (AFP) na Reuters, Waislamu walikataa kujitenga. Lakini zaidi akinamama Waislamu waliokuwa wamevaa hijabu wakawa wanavua hijabu zao na kuwapa Wakristo wavae, huku wakiwaficha Wakristo wengine chini ya viti na hata kuwafunika na kanzu zao. Al-Shabaab kuona hivyo, wakaona zoezi limekwama wakakimbia. Hizo ndio taarifa ambazo gazeti la Mwananchi likiripoti lilisema:

“Waislamu waliokuwa wakisafiri katika basi kutoka Nairobi kuelekea mji wa Mandera waliwalinda abiria Wakristo baada ya waasi wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab kusimamisha basi hilo na kuwaamuru kugawanyika katika makundi mawili (Waislamu na Wakristo.)”

Mwananchi likamalizia kwa kusema, “Waziri wa Usalama Kenya, Joseph Nkaisery alisifia kitendo hicho cha Waislamu akisema kuwa ni cha kijasiri.”

Ili kutafiti zaidi kujua ukweli nini kilitokea, nilijitahidi kupitia vipande vya habari hiyo vya taarifa za habari za televisheni za Kenya ambavyo bado vilikuwa vikipatikana katika mtandao. Ukitizama

NTV, KTN, CITIZEN tv na televisheni nyingine, mpaka ile ya BBC, unakuta kuwa ‘kipande’ ni hicho hicho kilichotumiwa na televisheni zote.

Kinachoonekana katika ‘screen’, ni basi viti vikiwa vitupu, inapita picha ya Al-Shabaab wakipiga kwata, kisha zinaletwa taarifa walivyovamia basi. Wakati taarifa zinaendelea yanakuja maandishi:

“Muslims reportedly shielded Christians from an attack by Al-Shabaab in Kenya.”

Ikiwa na maana kuwa inasemekana Waislamu wamewanusuru Wakristo kutokana na shambulio la Al-Shabaab.

Kisha yanakuja maandishi mengine: “A-Shabaab militants ambushed a bus travelling from Nairobi to Mandera.”

Halafu inakuja: “Muslim women gave Christian women hijabs and others were hidden inside the bus.”

Ikiwa na maana kuwa akina mama wa Kiislamu waliokuwa wamevaa hijabu walitoa hijabu zao na kuwapa akina mama wa Kikristo wavae!!!(?)

“We even gave some non-Muslims our religious attire to wear in the bus so that they would not be identified easily. Finally they gave up and left but warned that they would be back.”

Ndivyo walivyoripoti Reuters na Washington Post, wakimnukuu mtu mmoja akijitambulisha kwa jina la Abdi Mohamud Abdi, akidai kuwa alikuwa mmoja wa abiria.

Hebu fikiri na utumie

akili japo kidogo tu: basi limevamiwa na magaidi 15 wakiwa na silaha nzito. Waswahili wanasema ghafula mbaya, hiyo akili na huo muda wa kuamua uvue hijabu yako umpe Mkristo avae, ni jambo linalowezekana? Magaidi wame-‘ambush’ gari, wameingia ndani ya basi, inamaana wao ni vipofu hawatawaona Waislamu wakivua hijabu na kuwapa Wakristo?

Baada ya maelezo hayo kwamba akina mama walivua hijabu zao na kuwapa Wakristo huku wanaume nao wakivua kanzu, kofia na ‘hegeli’ zao kuwapa abiria Wakristo, mbele ya macho ya Al-Shabaab, sasa TV zinakuletea kauli ya Waziri wa Ulinzi Bwana Joseph Nkaissery akisema maneno yafuatayo:

“We are all Kenyans. We are not separated by religion. And that is a very good message from my brothers and sisters from the Muslim community.”

Kwamba, Wakenya ni wamoja bila kujali dini zao. Na kwamba anawapongeza Waislamu kwa kufikisha ujumbe huo kwa Al-Shabaab. Mahali pengine Waziri Joseph Nkaissery ananukuliwa akisema:

“These Muslims sent a very important message of the unity of purpose, that we are all Kenyans and that we are not separated by religion. Everybody can profess their own religion, but we are still one country and one people.”

Basi hii ndiyo habari iliyopigiwa sana debe wiki hii katika BBC jamaa yangu akasema,

huyu mtu akiambiwa arudie maneno aliyosema hawezi.

Kipropaganda, maneno haya ya Waziri Nkaissery, yamekaa vizuri sana. Kisiasa yanapiga debe la ukweli kuwa Wakenya ni wamoja. Na kwa Waislamu pengine pia wataona limekaa vizuri kwa sababu linawasafisha kuwa hawapo pamoja na Al Shabaab. Maana kama akina mama waliweza kuvua hijabu zao na akina baba wakavua kanzu na vilemba vyao wakawapa Wakristo wavae ili wasiuliwe na Al Shabaab, unataka ushahidi gani tena zaidi kuonyesha kuwa Waislamu wa Kenya sio Al Shabaab? Na ndio hapa Waziri wa Usalama Joseph Nkaissery anawapongeza Waislamu akisema:

“These Muslims sent a very important message of the unity of purpose, that we are all Kenyans and that we are not separated by religion.”

Na mimi hapa ndio ninaposema, tukielewa hivyo na kujipongeza, hiyo ni “wrong message.” Walichokusudia waliopanga ‘mchezo’ huo ni kingine kabisa, na kwa uelewa huo, wao watakuwa wamefanikiwa.

Suala hapa ni kudumisha hofu na kitisho hewa cha ugaidi. Kila wakati lazima Wakenya (na sisi huku) wakumbushwe kuwa kuna magaidi wa Al-Shabaab/Al-Qaida na sasa IS. Sasa ikipita muda hayajatokea ya Garissa na Westgate, mzaha (hoax) kama huu wa kutekwa basi, abiria Wakristo wakapewa hijabu ili wasitambulike, lazima uje.

Hata ukiwasifu wale abiria waliodaiwa kuvua hijabu zao, bado haiondoshi hisia za hofu na kitisho kilichohuishwa na tukio hilo. Na tukienda na “wrong message” kama hii, tunakwepa jambo muhimu: kufuatilia na kujua ukweli wa nini kilitokea, na nani wanahusika.

Katika tukio la mauwaji ya

Mwembechai, japo asili ya tafrani ile ni ‘uwongo’ na uchochezi wa Paroko, lakini Waislamu hawakuonyesha chuki kwa Wakristo. Kuna makanisa yapo jirani na msikiti wa Mwembechai, lakini hakuna lililoguswa.

Ukija Kenya, wameuliwa Masheikh na Waislamu wengi sana katika hii inayoitwa vita dhidi ya ugaidi na wengi katika jeshi na polisi kwa Kenya ni Wakristo, pamoja na viongozi wa kisiasa. Lakini Waislamu hawajamgusa Mkristo.

Kwa hiyo suala hapa sio Waisamu kutambua kuwa Wakristo ni ndugu zao na wananchi wenzao. Huko ni kubadili agenda na kuleta “wrong message” nyingine. Suala hapa ni je, kwa nini akina Joseph hawaonyeshi undugu, upendo na uadilifu kwa Waislamu?

Kama alivyosema Robert Finlayson Cook, huyu Bwana Joseph Nkaissery kwa nafasi yake kama afisa wa ngazi za juu wa jeshi (Retired Major-General), na sasa Waziri wa Usalama, hakosi kujua kuwa hiki kinachoitwa vita dhidi ya ugaidi na akina Al-Qaida, Boko Haram na majina kama hayo, ni “mambo ya watu” katika kufanikisha “The Global Spread Of US Military And Intelligence Bases” ili kufikia malengo ya kudhibiti dunia (global hegemony).

Sasa kama wanajua hivyo, kwa nini watumiwe kuwauwa Waislamu kwa kisingizio cha ugaidi?

Hili ndio suala la kuzungumzwa na kuhoji. Sio habari ya uzalendo, udugu na upendo wa Waislamu kwa Wakristo.

Tunaamini kuwa maadhali serikali ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli sasa imo katika safisha safisha, basi iyatambue na ‘majipu’ yatakayojaribu kutuletea propaganda na mizaha ya ugaidi. Haya yasipotumbuliwa, kila yanapobainika, tujue ni msiba kwetu sote.

ANNUUR NEW.indd 16 12/24/2015 1:43:33 PM

Page 17: ANNUUR 1209aaa

17 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015

MAKALA/TANGAZO

NI jambo la kutia moyo k u wa a n g a l a u k a t i k a k i l a S wa l a M a i m a m u wetu wanapata nafasi ya kutukumbusha juu ya mambo haya ya kunyoosha swafu, kuzikamilisha na kutoacha mapengo baina ya mtu na mtu. Kwa hivyo leo nimeona ipo haja ya mimi kujikita katika maeneo haya ya upangaji wa swafu zetu wakati tunaposwali hasa swala za kawaida (Swala Tano za Fardhi).

T u n a s o m a k a t i k a historia kwamba, Mtumwe wetu Mtukufu (SAW) na Maswahaba zake (Mungu awawie Radhi) walilipa uzito mkubwa jambo la kupanga swafu wakati wa kuswali, hadi Mtume (SAW) akafikia kusema kuwa, hakika ya Mwenyeezi Mungu haangalii swafu iliyopinda pinda au hakika kukamilika kwa swafu ndio ukamilifu wa swala yenyewe.

Maneno haya ni muhimu sana kwetu. Ni maneno ya kuyazingatia na ni maneno ya kuyabeba kwa uzito wake uliostahiki, alimradi tu tuwakweli na tunategemea chochote katika hizo swala zetu tunazoziswali kila siku kutwa mara tano.

N i m e p a t a k u s i k i a kwamba Mtume (SAW) alikuwa akitumia fimbo yake katika kuhakikisha kuwa swafu kweli zimekaa vile zinavyotakiwa/zimevyooka. Kwa hakika hayo ni mafunzo m e m a k w e t u a m b a y o yatatusaidia sisi wenyewe p i n d i p o t u k a ya s o m a , tukayajua na tukayafuata kwa ukamilifu wake.

Somo la kuonyoosha/ kukamilisha swafu wakati wa kuswali kwetu sisi hivi leo bado halijakaa sawa sawa, bado halijatuingia vichwani mwetu, bado tunazembea kwa kiasi kikubwa katika kupanga swafu zetu. Misikiti mingi niliyowahi kuswali nimeona kuwa pamoja na Imamu kuimba wimbo wa kupanga swafu katika utaratibu unaofaa wimbo huo hupita sikio moja na kutokea jengine, bila hata chembe ya kuzingatiwa, watu hawana habari nao kama kwamba hawakuimbiwa wao, wamegeuka yule “mbuzi anaepigiwa gitaa”.

U k i t o k e a k w a m b a umetilia maanani maneno hayo ya Imamu, unabaki na masikitiko makubwa moyoni ambayo hayana mliwazi. Ndio, kwa maana Imamu tayari ametimiza wajibu wake wa kukumbusha lakini Je! Wanaokumbushwa wanayo mazingatio angalau kidogo juu ya wanachokumbushwa?

Kwa hakika hawanayo hawana habari na hata hawajali. Ni kana kwamba wamekuja kuondoa wajibu tu sio kutekeleza wajibu na jukumu lao la kuswali.

Tu j a a l i e M u a d h i n i a n a k i m u k wa a j i l i ya k u s wa l i , u t a o n a wa t u wanavyo jikokota kwenda kupanga swafu zao, kila mtu amekuwa mzito utadhani labda anakokwenda kuna shimo la moto anaogopa kutumbukia. Inachukua dakika tano nzima Imamu anasubiri watu wajipange katika swafu hata kama Imamu atawahimiza wao

maamuma ndo kwanza wanajikongoja kama vizee vya miaka 100 – mpaka Imamu anaamua kutoa Takbira ya kufungua swala na kuwaachia maamuma wake wakiendelea kujiburura na kupanga swafu kivivu wanavyotaka wenyewe.

Wengine wao wanakuja kuswali wakati tayari watu wameanza ama rakaa ya kwanza na kuendelea , badala ya kuangalia wapi wanatakiwa kuunga swafu kiutaratibu, utaona mtu anajipanga popote tu bila ya kujali swafu imejaa au la, hilo yeye halimhusu na wala hana habari nalo anachokijua yeye ni kufungua swala tu na kuanza kuswali potelea mbali kukamilika au kutokamilika kwa swafu.

Mtume (SAW) anasema k a t i k a m a f h u m u y a Hadithi yake kwamba, jambo la mwanzo atakalo hesab iwa mtu s iku ya Kiama ni swala yake/ zake, zikiwa zimekamilika basi zimekamilika amali zake zote na zikiwa zimefisidika basi zimefisidika amali zake zote.

Kwa hivyo, tukae tukijua kuwa kuna mambo (factors) m e n g i a m b a y o h a y o yakipatikana au yakikamilika ndio tunasema kuwa na swala nayo imekamilika. Kwa mfano, usafi (kwa maana ya twahara) wa nguo, usafi wa mwili, kuchukua udhu vizuri, swala kuiswali kwa wakati stahiki, kuelekea kibla, na mengineyo mengi.

Sasa mambo hayo yote yatakapo kamilika, pamoja na kukamilika swafu vizuri, ndio swala zetu zinapo hesabiwa kuwa zimekamilika na zitakuwa na thamani siku ya hesabu. La kama ndio tunaswali ili usemwe kuwa - si tunaswali, basi hasara itakuwa ni yetu wenyewe na hatutakuwa na wa kumlaumu isipokuwa nafsi zetu.

Kwa hakika tunapaswa kuyaona haya na umuhimu wa k e i l i t u ya t e k e l e z e

na kuyachukulia masuala ya dini yetu kwa mazoea n a mch e z o mch e zo t u pasina kuyatekeleza kwa njia ambazo zinastahiki kutekelezwa.

Nimalizie kwa kusema kwamba dunia hii sio yetu, dini hii sio yetu na maisha haya tunayoishi pia sio yetu, kilicho cha kwetu sisi ni hizi amali tunazozifanya, t u n a p o z i f a n ya z i k a wa njema basi ndizo ambazo k wa R e h e m a z a A l l a h zitakazotuokoa na moto na tukizifanya kwa kuondoa kinu juani tu (zikiwa amali mbaya Allah asizoziridhia), b a s i n d i z o a m b a z o zitatuangamiza. Tuwe na hadhari na utekelezaji wa amali zetu. Mtume wetu (SAW) anatuambia kuwa kwa hakika wema hauozi na uovu hausahauliki na mlipaji (Allah SW) hafi milele. Basi fanya upendavyo utakacho kitenda ndicho utakachol ipwa. Aidha , Mtume (SAW) anasema mwenye akili sawasawa ni yule anaeihesabu nafsi yake na akatenda yale yatakayomfaa baada ya kufa kwake….

Wamaa Taufiq Illa Billahi(Imeandikwa na: Suluhu A.

Hamza, Mbweni, Zanzibar. 0776 720 588)

kwa nguvu zetu zote. Ni mambo ambayo tunaweza kuyatekeleza kwa asilimia

mia moja kwani sio mazito kiasi hicho. Tatizo ni kuwa bado imani zetu ni hafifu

MWANAFUNZI wa Madrasat Firdaus, Mukhtar Musa, akiwaongoza wanafunzi wenzake katika ibada ya swala kwa vitendo, mbele ya mgeni rasmi.

Upangaji swafu katika Swala

Inawatanganzia Waislam wote kuwa imeandaa safari ya Hijja mwaka 2016 sawa na mwaka 1437 Hijria kwa Dola US$ 3,555

Kutakuwa na punguzo la asilimia 16% kuanzia muda huu mpaka Feb 29/2016. Itakuwa Dola $2986 tu.

Kuanzia mwezi Machi 01-2016 mpaka Juni 12-2016 kutakuwa na punguzo la asilimia 6% sawa na Dola $3,341 tu.

MAMBO YATAKAYOGHARAMIWA1. Semina za Hija, 2. Huduma za afya na kuchinja 3.Airport Charge na ticket

za Ndege 4.Nyumba Makkah na Madina 5.Irham na Kuchinja kwa ajili ya Tama-tuu 6.Chakula wakati wote 7.Usafiri na ziara Makkah na Madina 8.Mahema Mina na Arafa.UMRA MWEZI WA RAMADHANI ITAKUWA NI DOLA US $1995

Fomu zinapatikana sehemu zifuatazo:-1.Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es Salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini nyumba Namba 26 mkabala na Showroom ya magari Tell. 0713 730 444, 0773 804 101 ,0785 930 444 au 0773 930 444.2. Ofisi ya Ahlu Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484 982, 0777 413 987.3. Abubakr Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es Salaam, Tel: 0784 453 8384. Abdallah Salehe Mazrui (Hoko) Dar es Salaam, Tel: 0715 724 444 5. Abdallah Hafidh Mazrui, Wete Pemba Tel: 0777 482 6656. Mohammed Hafidh Mazrui Mkoani Pemba 0777 456 9117. Sheikh Daud Khamis Shekha Tel: 0777 679 6928. Maalim Seif Humoud Hamed (Kijichi Zanzibar) 0777 417 736WAHI KULIPIA1. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Tel: 0713 730444, 0773

804101,0785 930444.2. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484982, 0777 413

987.Maalim Seif Humoud Hamed (Kijichi Zanzibar) Tel: 0777 417 736

TANBIH(a) Atakaemaliza taratibu zote mwanzo ndie atakayeshughulikiwa

mwanzo(b) Ili uwemo katika fungu la kwanza unatakiwa umalize taratibu

zote kabla ya punguzo (c) Kumbuka kikundi cha Ahlul Daawa kwa bei nafuu kuliko wote

na huduma kuliko wengi.Wabillah Tawfiq

Ahlu Daawa Hajj and Travel Agency

ANNUUR NEW.indd 17 12/24/2015 1:43:36 PM

Page 18: ANNUUR 1209aaa

18 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015

MAKALA/TANGAZO

SHUKRAN zote njema anastahiki Allah, Mola Mlezi wa Ulimwengu wote. Rehma na Amani zimuendee kipenzi chetu m t u m e M u h a m m a d (saw), sahaba zake, aali zake na wote waliofuata sunnah yake mpaka siku ya malipo.

Leo ni Sikukuu ya Krismas (Christmass) kwa baadhi ya madhehebu ya Kikristo kote duniani. Siku hii inanasibishwa na siku “aliyozaliwa” Yesu Kristo. Hata hivyo, yapo madhehebu ya Kikristo ambayo hayakubaliani na wala hayaungani katika kusherehekea sikukuu hii. Hii siyo mada yangu ya leo.

Wakati haya yakijiri, bado tungali na wiki moja mbele kukutana na kinachoitwa mwaka mpya. Hapo ndipo yanapojikita maudhui ya makala yetu ya leo. Kama tunavyojua, kwamba mwaka mmoja ni sawa na miezi kumi na mbili (12) sawia. Kwa maana nyingine, tunaweza kusema kwamba, hupati mwaka ila itimie miezi kumi na mbili. Hata hivyo, ifahamike kwamba mwezi ni mjumuisho wa siku 28 hadi 31 kwa mujibu wa kalenda inayotumiwa hivi sasa duniani kote. Lakini kalenda ya Kiis lamu inaanzia siku 29 hadi 30. Ukweli ulivyo ni kwamba, hakuna mwezi wenye siku 28 wala 31. Uchache ni siku 29 na wingi wake ni siku 30.

Tarehe 01 Januari kila mwaka, walimwengu wa huadhimisha kinachoitwa ‘mwaka mpya’ . Kwa wataalamu wa hesabu naomba muwe makini zaidi kusoma makala hii ili mpate kuwaelimisha we n g i n e wa s i o k u wa na ujuzi wa kutosha. Kwenye hesabu kuna kitu kinaitwa Dependent na Independent Variables. K wa m b a , k u n a v i t u a m b a v y o k u t o k e a ama kutotokea kwake kunategemea moja kwa moja kutokea/kutotokea kwa kitu kingine. Lakini vipo ambavyo vyenyewe

Sherehe za mwaka mpya mtumba!haviathiriwi na kingine, b a l i v i n a j i t e g e m e a vyenyewe.

Mathalani, mavuno mazuri yana uwiano wa moja kwa moja na mvua inayokidhi haja ya zao husika. Kuna m a z a o ya n a y o h i t a j i mvua nyingi na mengine mvua ya wastani. Kwa munasaba huu tunaweza k u s e m a , m a v u n o n i dependent wakati mvua ni independent. Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema mavuno yanategemea mvua.

Halikadhalika, kwa mfano huo huo, tuangalie mahusiano ya mwezi na tarehe kwa mitizamo m i w i l i , m t a z a m o uliozoeleka na mtazamo wa Kiislamu. Kwa kalenda ya Kiislamu, unaposema tarehe moja maana ya yake ni siku ya kwanza ya mwezi husika. Kwa mfano tulioona hapo juu ni kwamba, tarehe ni dependent wakati mwezi ni independent. Hii ina maana kwamba, haiwi tarehe ila kwa kutegemea mwezi.

Kalenda ya Kiislamu inafuata mfumo alioweka Allah mtukufu. Mwezi na tarehe haviachani lakini tarehe inategemea kuandama kwa mwezi. Ni kama mtu anapotaka kula, kawaida ni lazima anawe kwanza ndipo ale. Huwezi kula ndipo unawe. Au ni kama mtu anapokwenda kujisaidia, atajisaidia kwanza amalize ndipo achambe. Ni jambo la kushangaza kuona mtu anachamba kwanza ndipo aingie kujisaidia na ikatosha asirudie baada ya kujisaidia!!? Au mtu ale bila kunawa lakini mara amalizapo kula ndipo anawe.

Kwa upande mwingine, kalenda ya Papa Gregory i n a f u a t a h a w a a z a watu. Inaendeshwa na watu, wala haitegemei m p a n g o a l i o w e k a Mwenyezi Mungu kama t u t a k a v y o o n a h a p o baadaye. Katika kalenda hii , tarehe na mwezi havina mafungamano

yanayotegemeana. Kila kimoja kinajiendesha chenyewe. Mathalani, i n a w e z a i k a s o m e k a tarehe moja leo lakini tayari mwezi husika una siku takriban 10 au zaidi mbele!! Yako wapi mahusiano hapa kati ya mwezi na tarehe!? Nani anamtegemea mwenzake hapa!? Mnataka njia ipi isiyokuwa ya Allah?

Kwa mantiki hiyo, tunaona kwamba mwezi unaweza ukawa na siku nyingi mbele lakini tarehe zinajiendea tu zenyewe mpaka zitimize idadi ya siku za mwezi husika kwa mfumo walioweka wanadamu. Hii ndio kalenda ya Mzee Gregory!!

Sasa nikuulize ndugu m s o m a j i wa m a k a l a hii uwe ni Muislam au

Mkristo: kinachosubiriwa kusherehekewa tarehe 01.01.2016 na ambacho ni kawaida kwa miaka nenda, miaka rudi ni mwaka mpya au siku mpya!? Nauliza hivi kwa sababu, inawezekanaje kusherehekea mwaka mpya wakat i mwaka u n a t e g e m e a m w e z i na mwezi wa mwaka mpya tayari una siku zaidi ya kumi!? Au ndio kusema tunapenda sana “mitumba” au ‘used’ kama wanavyoita wenyewe!

M i t u m b a n g u o , mitumba s ikukuu na mitumba mwaka mpya! Lakini si ajabu kwa sababu ndivyo tulivyoaminishwa hivyo nasi tukakubali kumeza nzima nzima, hata kwenye kuoa tunatumiana kwanza mpaka tunakuwa

used. Tunakuja kufunga n d o a t u k i wa ‘ u s e d ’ , tukiwa ‘mitumba’. Lakini tukijipamba, tunaonekana wapya kumbe tumechakaa kuliko maelezo.

Kwa kumalizia niwausie ndugu zangu Waislamu kwamba, leo ni Krismasi na wik i mo ja mbe le itakuwa siku mpya ndani ya mwaka na mwezi ambavyo ni ‘used’. Ukitaka kujua namna nzuri ya kushiriki kwenye sikukuu hiyo, rejea An-nuur toleo nambari 1208 la Disemba 18-24, 2015 ukurasa wa nne. Hapo utakutana na “Nyinyi mna dini yenu nami nina dini yangu”.

Wabillah Tawfiiq!(Juma Jumanne, Katesh,

M A N YA R A . S I M U : 0659789468.)

Uongozi wa Shule ya SOTELE SEKONDARI (iliyochini ya TAMPO) iliyopo kata ya Dondo Tarafa ya kisiju wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

Inawatangazia waislamu wote nafasi za masomo kwa mwaka mpya wa masomo 2016 kwa kidato cha II,III,IV fomu zinapatikana katika mikoa ifuatayo: -

Mkoa wa DSM Imamu Jafari TIC, Magomeni Kichangani, Juma Nchia Ununio College Boko, Tampro Magomeni Usalama, Imamu Shaabani Masjid Tungi Temeke.Imamu Mkadam Masjid Haqa Buguruni, Imamu Yusufu kwa mwalimu Daudi Masjid Mtambani Kinondoni mkoa wa Pwani Rufiji Mwl Sodungu 0719 402695 sotele shuleni mkuranga.

Mkoani Tanga Sheikh Koja mtihani wa Usajili utafanyika tarehe 26/12/2015 siku ya Jumamosi katika shule ya Sotele Sekondari mkuranga Pwani. Saa 4:00 Asubuhi kwa maelezo wasiliana na Amir wa Tampro Hashim Saiboko 0784 299945, Makam Amir Tampro Pilly 0784 657216 Mwl. Pazi Mwinyimvua 0655 654 900, Yusufu Shaabani 0715 818187 Mwinyimvua Omar Tampro makao makuu 0714 151532

Nafasi za Masomo Sotele Sekondari 2016

ANNUUR NEW.indd 18 12/24/2015 1:43:37 PM

Page 19: ANNUUR 1209aaa

19 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015

MAKALA

Yawe Endelevu - 1Inatoka Uk. 13

GARI ya Manispaa imeamua kumwaga taka kwenye konde ya kilimo.

TAKA kutoka mahoteli zimemwagwa kwenye chaka.

Kandoni mwa makazi taka zimemwagwa

kisiwa cha Zanzibar kisha tuangalie R3 tutawezaje k u z i t u m i a t u k a p a t a mafanikio? Kis iwa cha Zanzibar kina visiwa viwili vikubwa navyo Unguja na Pemba vikiwa na masafa ya Kilomita za mraba 1,464 (Kilométer square) kwa Unguja na kilomita za mraba 868 kwa Pemba. Mwaka wa 1963-64 Idadi ya wakazi wa Zanzibar ilikuwa ni watu 300,000, ikiwa laki mbili ikionekana kisiwani Unguja na laki mmoja kisiwani Pemba. Hivi sasa idadi ya wakazi wa Zanzibar ni watu 1,211,486 ikiwa inaongezeko la ukuwaji wa watu wa asilimia 3.1( annual growth rate).

Zanzibar inazalisha taka ambazo wingi wake ni zile taka zinazooza lakini udhibiti wake hauridhishi. Najaribu kutoa taswira ndogo kwa kisiwa cha Zanzibar kisha tuje katika sura kubwa kwa nchi ya Tanzania bara i l i tuweze kuona kuwa k inachohi ta j ika ka t ika suala zima la ukusanyaji na kufanya usafi liwe jambo endelevu lisilosita.

Katika mwaka wa 2002 mtaalamu wa Kimazingira aliojariwa na mradi wa SMOLE alikuja na takwimu hizi zifwatazo kuwa kwa mtu mmoja visiwani Zanzibar atakuwa anazalisha taka kwa kiwango cha kilo 0.80 kwa siku na idadi ya watu ni milioni moja. Kwa hio kisiwa cha Zanzibar kitakuwa kinazalisha tani 800 kwa siku (kilo 800,000). Hio sawa na kusema Unguja wanazalisha taka kwa wastani wa tani 500 (kilo 453,592) na Pemba watakuwa wanazal isha tani 290 (kilo 263,083). Taka hizo ni mchanganyiko na inakadiriwa kuwa asilimia ya taka zote zinazozalishwa katika Manispaa na Zanzibar kwa jumla, asilimia ifikiao 80 ni za taka zinazooza (Organic waste). Uwezo wa ukusanywaji wa taka hizo ni asilimia 45 na asilimia zaidi ya 50 ya taka hizo hutupwa ovyo. Nyengine hutupwa katika sehemu za bahari kama pale Maruhubi, Kinazini na kwengineko. Nyengine hutupwa katika misingi ya maji (mitaro), baadhi hufukiwa na nyenginezo huchomwa moto. Zanzibar ni mmoja wa zile nchi ambazo zinazalisha taka zinazooza kwa wingi kwa asilimia 80. Jiji la Dar-es-Salaam asilimia 50, nchi ya Vietnam asilimia 53 na jiji la Nairobi asilimia 54.

Taka zinazooza ni rahisi kutengeneza mbolea na mbolea hio ni nzuri na yenye kukubalika kuliko mbolea inayotoka viwandani.

Majaa ambayo yalio rasmi ni machache na majaa yalio sio rasmi yamezagaa kila sehemu. Inakisiwa kuwa majaa yasio rasmi yapo zaidi ya asilimia 80 kinyume na zile sehemu za kukusanya taka na jaa kubwa lilio rasmi ambayo yapo kama asilimia 19. Kwa mtizamo huo mdogo, utaona kwenye idadi ya watu milioni 4 katika jiji la Dar es Salaam, uzalishwaji wa taka utakuwa mkubwa kwa kila siku. Uzalishaji wa taka

katika jiji la Dar es Salaam utakuwa zaidi ya mara tano ya taka zinazozalishwa visiwani. Ukusanywaji wake haupishani na ndio mana taka zimezagaa mitaani na maeneo mbalimbali.

Nini kifanyike kudhibiti taka?R 3 n i m o j a ya n j i a

madhubuti kudhibiti taka kisha elimu kwa jamii au Umma na maskuli juu ya suala la udhibiti wa taka unahitajika katika suala zima la taka. Kuna haja ya kupanga siku moja maalumu ya kujititimua katika udhibiti wa taka, lakini kufanya kazi kwa siku mmoja ikawa basi, inakuwa sawa na kujaza maji katika pakacha au kujaza maji katika ndoo iliotoboka.

R3, “ Reduce“ Punguza, “Reuse“, Tumia tena na “Recycle“ kuzire jesha t a k a k a t i k a m a t u m i z i yake. Reduce-Kupunguza tunahitajia kujitahidi kuwa

tunatumia vitu vya lazima na sio kununua vitu ovyo kisha tukawa tunavitupa. Katika mukhtadha huo utaona Reuse-Tumia tena hapo hapo, chupa ya maji uliokwisha kuitumia itumie kwa kutilia vitu mbalimbali, mfano itumie kwa kutilia mafuta ya taa, achari, mafuta ya nazi au Recycle-kuirejeza, kwa kuirejeza na hio ni kurejeshwa kiwandani kwa kuweza kutengenezwa chupa nyengine. Huo ni mfano wa chupa lakini hata kwa vibati au makopo ya soda na juisi na vitu vyengine. R3 zikiwa zimo kichwani mwetu, basi uzalishwaji wa taka unaweza kupungua kwa asilimia 15 hadi 20. Mfano mwengine unapokwenda sokoni au katika maduka makubwa Supper market, haina haja kuwa utavyonunua uwe unapewa mifuko ya plastiki badala yake utafute mfuko

wa kienyeji uwe mkoba wa ukili au mkoba wa kigunia uwe ndio unaokwenda nao madukani. Inaa maana ikiwa mifuko 300 katika duka moja inaokolewa bila ya watu kupewa, ni hapo itakuwa kupunguza matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kiwango kikubwa na mzigo wa uchafu kupungua katika mazingira.

Elimu na kushajiishwa watu ni jambo linalohitajika kuenezwa kwa kiwango c h a j u u , k wa n i u m m a unataka kuelimshwa na u n a p o f a h a m u , h u i t i k a kama walivyoitika tarehe 9 December 2015 katika suala zima la usafi wa mazingira kwa kukusanya taka. Elimu itolewe kwa njia mbalimbali kuanzia katika skuli, Shehia/kaya, Wilaya, maeneo ya kazi n.k. Aidha kutakuwa kuna haja ya watu kuhakikisha wao wanafanya usafi kila wiki kwa kujigawa kutokana na idadi yao katika maeneo yao.

Ukusanyaji ni kitu rahisi, utupwaji ni ngondo na hilo ndilo linaloleta kizungumkuti n a k u j i o n a t u n a k u wa tunatambarirwa na taka. Balaa iliyotuvaa sasa ni hizi taka zitokanazo na vitu vya elektroniki na vya umeme (e-waste). Makala zilizopita nishalielezea hilo. Wingi wa taka za e-waste zinakuwa na madini ya hatari kwa hivyo ni muhimu kukusanywa kwa njia zilizo makini pamoja na utupwaji wake.

Mada ya leo nimeipa jina Yawe endelevu yaani

yawe ya kudumu wala yasiwe ya kukurupuka na tukiyazingatia yakudumu k w a p a n d e m b i l i z a Muungano wa Tanzania, tutaweza kuorodheshwa katika nchi zilizokuwa juu katika usafi na mandhari ya kupendeza, ikiwa kwa sasa tumewekwa katika mkumbo wa nchi zilizokuwa na miji michafu.

Hadithi ya Mtume (SAW) inasema “Uislamu ni unadhifu kwa hio tu j inadhif ishe kwani hatoingia Peponi ila yule aliokuwa msafi.” Hapa unadhifu wa aina tatu unahitajika : kwanza wa nafsi ya mtu mwenyewe, usafi wake wa kuanzia kiwiliwili kisha usafi wa mazingira yaliomzunguka. Lau Waislamu watapoweza kuielewa hadithi hii ya Mtume (SAW) na ikiwa idadi yao ni nusu ya wakazi wa mwahali popote pale mfano Zanzibar, kwa mfano huo basi watakuwa na uwezo wa kupunguza mzigo wa uzalishwaji taka sio chini ya asikimia 40.

Sasa sisi Waislamu katika miji ambayo tupo kwa wingi mfano Unguja, Pemba, Kilwa, Bagamoyo, Tanga, Tabora, Kigoma, haiwi changamoto kwetu na miji yetu ikawa ya mfano?

Inawezekana na tutimize wajibu wetu ikiwa waumini wa Kiislamu na raia wema na muumini thabiti hutekeleza maelekezo ya imani yake na atakaye Pepo nikujikita katika kila yale tuliyoamrishwa.

Fatwana na mie katika makala i fwatayo yawe e n d e l e v u w i k i i j a y o , Insha’Allah.

(Kwa maoni, maswali, mawasiliano 0777 43 69 49)

ANNUUR NEW.indd 19 12/24/2015 1:43:38 PM

Page 20: ANNUUR 1209aaa

20 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 201520 MAKALA AN-NUUR

20

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 25-31, 2015

Changia damu okoa maisha kwani sote ni wagonjwa watarajiwa.

Tunaomba watu wote kuchangia damu kwa hiari siku ya Jumamosi tarehe 19/12/2015 katika Hospitali za Temeke na Mbagala Rangi tatu iliyopo Zakheem kuanzia saa 1:00 asubuhi.

Nyote mnakaribishwaLimetolewa na Jumuiya ya JAE-Temeke.

JAE JAE JAE

NI zaidi ya miaka miwili sasa, bado upande wa Jamhuri haukamilisha upepelezi w a k e n a k u k u s a n y a ushahidi ili kuwezesha kesi inayomkabili Sheikh M s e l l e m n a we n z a k e kuzungumzwa.

K a t i k a h a l i h i y o , M a h a k a m a ya H a k i m Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, imeamuru upande wa mashitaka kukamilisha uchunguzi huo wa tuhuma za Ugaidi dhidi ya Masheikh na Waislamu hao.

Amri hiyo imetolewa na Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo Alhamisi ya wiki iliyopita, kabla ya kuiahirisha hadi Desemba 31, 2015, baada ya upande wa mashitaka (Serikali) kueleza Mahakama kuwa ushahidi bado haujakamilika na kuna Rufaa katika Mahakama ya Rufaa.

Akiongea na An nuur, Wakil i wa upande wa utetezi Mh. Abdulfattah Abdallah, alisema kufuatia maelezo hayo ya upande

Isidingo ya kesi za Waislamu…Mwaka wa pili sasa bado Polisi wanatafuta ushahidi, upelelezi Na Bakari Mwakangwale

HAIIBA TIMAMU TEA CHAI YA AJABU KWA AJILI YA KUKABILIANA NA

SHINIKIZO LA DAMU (HYPERTENSION/HIGH BLOOD PRESSURE)

UGONJWA WA MOYO KIHARUSI JONGO (GOUT) MAUMIVU YA VIUNGO (RHEUMATISM) MAUMIVU SUGU YA KICHWA BAWASIR (PILES/HEMORRHOIDS) MAGONJWA YA INI SARATANI MBALIMBALI UOTO/UVIMBE MBALIMBALI KATIKA VIUNGO VYA UZAZI VYA MWANAMKE (FIBROIDS, POLYPS NA CYSTS)

KUSHINDWA KUZUIA MKOJO (URINARY INCONTINENCE)

ATHARI ZA KISUKARI CHA UKUBWANI PUMU UPUNGUFU WA KINGA ZA MWILI KASI YA KUZEEKA MATATIZO YA MFUMO WA MZUNGUKO WA DAMU

MKAKAMO WA NGOZI; UDHAIFU WA MACHO KUPOTEZA KUMBUKUMBU KASI NDOGO YA KUPONA MAJERAHA MAKOVU KWENYE MAPAFU UGONJWA WA NGOZI KUCHUJA RANGI, YAANI, VITILIGO

HAIIBA TIMAMU TEA INAPATIKANA

HERBAL IMPACT

MOSQUE STREET, NO. 1574/144 (MKABALA NA MSIKITI WA SUNNI), KITUMBINI, DAR ES

SALAAM

TUTEMBELEE AU TUPIGIE SIMU NAMBA:

0754281131/0655281131/0686281131/0779281131

HAIIBA TIMAMU TEA IMENIREJESHEA MAISHA YANGU!

Na. Salim Kajenge

Miaka michache iliyopita nilikumbwa na ugonjwa mbaya sana wa kushindwa kuzuia mkojo. Ilikuwa nikijisikia tu haja ya kukojoa na mkojo huo unafuata! Hali hii ilinilazimisha kuacha kabisa kuondoka na kwenda mbali na maeneo ya nyumbani. Ukweli wa mambo ni kwamba nilikwazika sana. Jitihada zote za kutafuta tiba hazikuzaa matunda. Mwezi wa Desemba 2014 nilisoma kwenye gazeti la Annur kuhusu dawa moja iliyokuwa inaitwa chai ya ajabu. Niliamua niijaribu japo sikuwa na matumaini sana. He! Nilishangaa kuwa baada ya kuitumia kwa siku chache hali yangu ilianza kubadilika. Niliitumia hii chai kwa majuma matano na baada ya hapo nikasitisha baada ya kuona kuwa nimepona kabisa!

https://www.facebook.com/Herbal-Impact-157972014402705/

wa mashitaka, upande wa utetezi waliieleza Mahakama kuwa licha uwepo wa Rufaa katika Mahakama ya Rufaa, lakini upande wa mashitaka uliahidi Mahakamani hapo kuwa uchunguzi ungekuwa umekamilika tokea mwezi wa tatu.

“ K w a u p a n d e w e t u tumeiambia Mahakama kuwa licha ya Rufaa kuwa katika Mahakama ya Rufaa, lakini vilevile waliahidi toka mwezi wa tatu uchunguzi ungekuwa umekamilika lakini mpaka leo bado.” Alisema Wakili Abdallah.

Kufuatia maelezo hayo, Wakili Abdallaha, alisema Hakimu alitoa ufafanuzi suala hilo akiueleza upande wa Jamhuri kwamba, licha ya kuwepo kwa Rufaa katika Mahakama ya Rufaa, wanatakiwa wahakikishe kuwa uchunguzi unakamilika isije ikawa Rufaa imekamilika huku uchunguzi unakuwa bado haujakamilika.

Wakili Abdallah, alisema wateja wake walifika wote Mahakamani, kasoro wawili ambao wanaumwa.

A k a wa t a j a k u wa n i mshitakiwa namba 14, Salumu Ally Salumu na mshitakiwa namba 19, Qasim Salumu Nassoro.

Wakatio huo huo, kesi zinazowakabili Waislamu katika mikoa mbalimbali z imekuwa z ik iendelea kuunguruma.

A l h a m i s i k a t i k a Mahakama ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam, ilitajwa kesi ya Ustadhi Haruna Lugeye na Mkewe Bi. Mwajumbe Wendo Bakari , pamoja na kundi la Waislamu 23, wa Mbagala, Jijini Dar es Salaam.

Jijini Mwanza, Desemba 2 8 , 2 0 1 5 , M a h a k a m a inayosikiliza kesi ya Imamu Hamza Omari, imepanga kusikiliza hukumu ya kesi hiyo baada ya kukamilika kwa ushahidi wa pande zote.

Aidha, Desemba 21, 2015, Waislamu wengine zaidi ya 20, wa tuhuma za Ugaidi waliopo katika Gereza la Butimba Jijini Mwanza, ambao wamewekwa katika makundi manne, katika kundi la Ustadhi Amin Msharaba, walifikishwa

mahakamani mapema wiki hii na kesi yao imeahirishwa hadi Januari 4, 2016.

A m a J i j i n i A r u s h a , Waislamu wenye tuhuma kama hizo wapatao 61, walifikishwa Mahakamani, Desemba 17, 2015, na kesi yao kuahirishwa.

Hao imeelezwa kuwa kila Alhamisi hufikishwa Mahakamani na kurejeshwa mahabusu.

K a t i k a M j i w a Sengerema, kuna Waislamu watatu akiwemo Ustadi Muhammadi, ambaye ni Mwalimu wa masomo ya dini katika Shule ya Tabasamu

Sengerema, ambao wapo mahabusu Jijini Mwanza.

H a o w a l i f i k i s h w a Mahakamani Jumatano ya wiki iliyopita.

Ama Jijini Morogoro kuna kesi ya Ugaidi inayowakabili Wa i s l a m u 2 9 , k a t i k a makundi mawili tofauti waliopo katika gereza la Mahabusu la Morogoro.

K e s i y a o i m e k u w a ikiahirishwa mara kwa mara, ambapo kundi moja kesi yake ilikuwa Mahakamani Desemba 23 na kundi la pili kesi imepangwa Desemba 29, mwaka huu.

SHEIKH Msellem. IGP Mangu.

ANNUUR NEW.indd 20 12/24/2015 1:43:41 PM