12
ISSN 0856 - 3861 Na. 1016 RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 5 - 7, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Baraza la Mitihani labadili matokeo F6 Ni kweli Uamsho watageuka Al Qaidah Shein ajifunze yaliyomkuta Mzee Ruhsa ’Alisaliti’ Masheikh waliomuombea dua FBI haihitaji kibali cha JK kuingia Unguja IMEGUNDULIKA kuwa uchochezi mkubwa umefanyika na unaendelea kufanyika katika kinachoitwa vurugu za Uamsho Zanzibar. Uchochezi wa kutisha Zanzibar Magazeti Bara yatumia picha za kughushi Zilipigwa Morogoro mtu kalowa damu Ikadaiwa ni Uamsho wakiandamana Mhadhara mkubwa wafanyika Mbuyuni Na Bakari Mwakangwale Katika kuwapachika uhalifu na hata ugaidi Masheikh wa Uamsho, baadhi ya magazeti yalitoa picha iliyopigwa Morogoro mwezi Januari mwaka huu na kudai kuwa ni ya Inaendelea Uk. 2 Sasa larudisha A, B, C za Waislamu Waislam wakutana Diamond, wasema… Mwizi katema mkufu, asachiwe mfukoni Hawafanyi mtihani mpaka NECTA ivunjwe AMIR wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Mussa Kundecha. ALHAJ Ali Hassan Mwinyi RAIS Jakaya Kikwete. Waislam wataka sensa ifanywe kwa umakini Uk. 4

ANNUUR 116

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: ANNUUR 116

ISSN 0856 - 3861 Na. 1016 RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 5 - 7, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Baraza la Mitihani labadili matokeo F6

Ni kweli Uamsho watageuka Al Qaidah

Shein ajifunze yaliyomkuta Mzee Ruhsa’Alisaliti’ Masheikh waliomuombea duaFBI haihitaji kibali cha JK kuingia Unguja

IMEGUNDULIKA kuwa u c h o c h e z i m k u b w a umefanyika na unaendelea k u f a n y i k a k a t i k a kinachoitwa vurugu za Uamsho Zanzibar.

Uchochezi wa kutisha Zanzibar

Magazeti Bara yatumia picha za kughushiZilipigwa Morogoro mtu kalowa damuIkadaiwa ni Uamsho wakiandamanaMhadhara mkubwa wafanyika Mbuyuni

Na Bakari Mwakangwale Katika kuwapachika uhalifu na hata ugaidi Masheikh wa Uamsho, baadhi ya magazeti yalitoa picha iliyopigwa Morogoro mwezi Januari mwaka huu na kudai kuwa ni ya

Inaendelea Uk. 2

Sasa larudisha A, B, C za WaislamuWaislam wakutana Diamond, wasema…Mwizi katema mkufu, asachiwe mfukoniHawafanyi mtihani mpaka NECTA ivunjwe

AMIR wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Mussa Kundecha.

ALHAJ Ali Hassan Mwinyi RAIS Jakaya Kikwete.

Waislam wataka sensa ifanywe kwa umakini

Uk. 4

Page 2: ANNUUR 116

2 RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 5 - 7, 2012 AN-NUUR TAHARIRI/HABARI

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110148, 0755 260 087, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro,

D'Salaam

MAONI YETU

Uchochezi wa kutisha ZanzibarInatoka Uk. 2maandamano ya Uamsho wiki iliyopita.

K a t i k a p i c h a h i y o iliyopigwa Januari 20, 2012 mjini Morogoro, anaonekana mtu kashika ki tambaa ki l icholowa damu.

Hiyo ilikuwa ni katika yale maandamano yaliyofanywa na Waislamu wa Morogoro kuhusiana na sakata la wanafunzi Waislamu wa shule ya sekondari Ndanda waliokuwa wamefukuzwa kwa dhulma.

Hata h ivyo , ka t ika k u w a t a n g a z i a u b a y a Uamsho, gazeti la Nipashe, la Mei, 28, 2012, lilitoa picha hiyo ukurasa wa mbele na kudai kuwa ni maandamano ya Uamsho.

Likaandika maelezo chini ya picha hiyo (caption) yanayosomeka:

“ M m o j a w a waandamanaji wa kundi la Jumuiya ya Uamsho ya Kiislamu (Jumiki) ak ionyesha k i t ambaa chenye damu wakati akiwa kwenye maandamano jana Mj in i Zanzibar, ambako kulitokea vurugu na kusababisha wafanya b i a s h a r a k u s h i n d w a kufanya shughuli zao.”

Ama kwa upande wa gazeti la Tanzania Daima, lilionyesha picha hiyo hiyo ukuraza wa mbele kwa siku hiyo hiyo, na kuanisha kwa kuandika:

“ M m o j a w a waandamanaji akionyesha kitambaa kilicho na damu wakati wakiendelea na maandamano.”

Picha hiyo ambayo magazeti hayo yalikuwa nayo ka t ika maktaba zao, waliipiga siku ya maandamano Morogoro ambapo mtu aliyeshika kitambaa alikuwa akiongea na waandishi wa habari ak ionyesha k i t ambaa k i l i c h o l o w a d a m u akilalamika kuwa polisi wamemwaga damu ya Muislamu.

Hata hivyo, magazeti hayo hayakutoa maelezo ya mlalamikaji wala kutoa picha hiyo hapo Januari.

Wakaihifadhi katika maktaba zao na sasa ndio wakaona wakat i muafaka kuitumia kupiga

propaganda kuwa Uamsho ‘wana kiu ya kumwaga damu “ya Wakristo” mbali na kuchoma moto makanisa kama inavyodaiwa hivi sasa.

Ustadh Juma Kitunga anayeonekana katika picha hiyo, anasema, amestushwa picha yake kutumiwa na magazeti ya Nipashe na Tanzania Daima, siku moja baada ya vurugu z i l i zo tokea Vi s iwan i Zanzibar yakimtaja kuwa ni mmoja wa waandamanaji wa kundi la Uamsho, akiwa katika Maandamano Mei, 28, 2012, Visiwani humo.

A k i o n g e a n a A n n u u r , J i j i n i D a r e s Salaam, kwa masikitiko Kitunga, aliye mwenyeji wa Mj in i Morogoro , alisema amesikitishwa na magazeti hayo na licha ya kuwaeleza makosa hayo waliyoyafanya, lakini wahusika wameonyesha dharau.

Kituga alisema hali hiyo imemuathiri kwa kiasi kikubwa katika shughuli zake kwa ujumla kwa kuelezwa kuwa alikuwa Zanzibar na kushiriki kuchoma moto makanisa, ili hali hakuwa huko na

zaidi hajawahi kukanyaga Visiwa hivyo katika maisha yake.

Amesema, mbali na kuathirika yeye binafsi, lakini pia amedai kwamba magazeti hayo (Nipashe n a Ta n z a n i a D a i m a ) yameiathiri Dini yake ya Uislamu kwa kuionyesha jamii kuwa waumini wake ni watu wa vurugu na ndio walioshir iki kuchoma Makanisa, jambo ambalo si sahihi.

Akiwa na kopi za magazeti hayo mkononi, zilizotoka siku ya Jumatatu, Mei, 28, 2012, akimuonyesha Mwandishi wa habari hizi na kumthibitishia kuwa picha hizo zilichapishwa ukurasa wa mbele hazikuwa za tukio la Zanzibar.

Kitunga, alisema yupo Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuangalia hatua za kisheria dhidi ya magazeti hayo, baada ya kushindwa kuonyesha ushirikiano naye haswa baada ya kuwapigia simu wahusika siku ileile ya kwanza magazeti hayo yalipotoka na picha yake mitaani.

Kwa upande wa gazeti

Inaendelea Uk. 4

WIKI iliyopita Baraza la Mitihani lilitoa matokeo mapya ya mitihani ya kidato cha sita yaliyokuwa yametangazwa h iv i karibuni. Matokeo hayo m a p y a y a m e t o l e w a baada ya kufanyika marekebisho ambapo w a n a f u n z i w e n g i Wais lamu wal ipewa daraja F kinyume na a l a m a w a l i z o k u w a wamepata.

Marekeb i sho hayo yamefanyika na majibu kutolewa katika kipindi kisichozidi wiki mbili baada ya Wakuu wa Shule za Kiislamu kufikisha malalamiko yao.

Alama zilizofanyiwa marekebisho ni zile za mt ihan i wa somo la I s l a m i c K n o w l e d g e ambapo ma tokeo ya a w a l i y a l i o n y e s h a kufeli kwa kiwango cha kutisha kukiwa hakuna mwanafunzi zliyepata A, B, wala C.

Kwa nchi nzima ilikuwa ni D saba tu zilizokuwa zimepatikana huku mamia ya wanafunzi wakiambulia F.

Japo baadhi ya Wakuu wa Shule wamearifu kuwa bado wanafuatilia suala hili ambapo wanataka serikali iunde tume ya uchunguzi, l ak in i s i s i tunasema kuwa hatua zilizokwisha kuchukuliwa na Wizara ya Elimu pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mit ihani , z inastahiki kupongezwa.

Tunawapongeza kwa sababu baada ya kupokea malalamiko ya Wakuu wa Shule, hawakufanya ajizi. Waliyafanyia kazi kwa haraka ndio maana wakatoa majibu kwa muda huu mfupi.

Baraza la Mitihani linastahiki pongezi

Kwa hakika huu ndio mwenendo na utendaji makini unaotara j iwa kuonekana kwa watumishi wa umma. Lau watendaji na viongozi wote serikalini, wangekuwa makini kiasi hiki, hapana shaka hata maendeleo ya nchi hii yangekuwa makubwa sana kuliko ilivyo hivi sasa.

Ni ma ta ra j io ye tu kwamba kama ambavyo Wizara ya El imu na Mafunzo ya Ufund i imeweza kushughulikia jambo hili kwa haraka, ni matarajio yetu pia itakuwa tayari kupokea na kushughulika malalamiko na matatizo mengine yatakayof ikishwa na wananchi.

Ni matarajio yetu pia kwamba utendaji makini kama huu alioonyesha Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, Bi Joyce Ndalichako, utakuwa ndio utambulisho wake unaojenga haiba yake muda wote atakaokuwa akilitumikia Baraza hilo.

Anachopaswa kufahamu Ndalichako (Baraza la Mitihani, Wizara ya Elimu na serikali kwa ujumla) ni kuwa, kuna malalamiko ya msingi na kwamba imefikia mahali Waislamu hawana tena imani na Baraza hilo.

Sasa kwa u tendaj i huu makini wa kujali malalamiko ya Waislamu na kuyafanyika kazi aliyoonyesha Ndalichako na Wizara ya Elimu, hatuna wasiwasi kuwa hata katika suala la kuundwa tume ya uchunguzi, atatoa ushirikiano unaostahiki ili kulijengea heshma Baraza la Mitihani la Tanzania.

Ustadh Juma Kitunga

Page 3: ANNUUR 116

3RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 5 - 7, 2012AN-NUUR HABARI

Baraza la Mitihani labadili matokeo F6 BARAZA la Mi t ihan i Tanzania limebadili kimya kimya matokeo ya mitihani ya kidato cha sita iliyotangazwa hivi karibuni.

Baraza la Mitihani likifanya hayo, Waislamu wanasema kuwa itakuwa ni muhali kwao kufanya mitihani ya NECTA kabla ya Baraza hilo kufanyiwa marekebisho.

B a r a z a l i m e f a n y a mabadiliko hayo baada ya Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu kutuhumu kuwa huenda matokeo ya watoto wa Kiislamu yamechakachuliwa.

“Ilichofanya NECTA ni sawa na mwizi aliyekabwa akikataka kumeza mkufu a l io iba akau tema, sasa inabidi asachiwe mifukoni na chumbani kwake kutafuta vitu vingine vya wizi.”

“Ni jukumu la wazazi na wanafunzi Waislamu sasa kupanga kupiga kambi pale Wizara ya Elimu na Baraza la Mitihani mpaka iundwe tume kuchunguza hali ilivyo katika masomo mengine na Baraza la Mitihani kwa ujumla.”

Hayo ni maoni ya baadhi ya Waislamu nje ya ukumbi wa Diamond, mara baada ya kumalizika kongamano Jumapili.

“Uonevu hauwezi kuwepo k a t i k a s o m o m o j a t u , utakuwepo katika Kiingereza, Historia, Fizikia, Kemia, Elimu ya Viumbe na masomo mengine”.

Amesema muumini mmoja akitaka uchunguzi wa kina ufanyike na sio kutosheka na mabadiliko yaliyofanywa na Baraza katika somo moja huku akidai kuwa wapo wanaopewa alama kubwa zisizo kuwa zao na wengine wakipunjwa.

Maoni hayo yanaendana na yale maombi ya awali ambapo pamoja na kutaka kuundwa Tume huru ya kuchunguza matokeo hayo, Wakuu wa shule wanataka uchunguzi wa awali kufanywa katika somo la Islamic Knowledge ambalo matokeo yake ya awali yalionyesha kuwa kwa nchi nzima walikuwa wanafunzi 7 tu waliopata D huku asilimia zaidi ya 80 wakiambulia F.

Inanyoonekana, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, pamoja na Baraza la Mitihani, baada ya kupata malalamiko ya Wakuu wa Shule za Kiislamu, walifanyia kazi kwa haraka malalamiko hayo na kwa kipindi kisichozidi wiki moja likatoa majibu.

Na Mwandishi Wetu Majibu mapya yaliyotolewa na NECTA toka mwishoni mwa wiki iliyopita yanaonyesha kuwa, wakati katika matokeo ya awal i hapakuwa na mwanafunzi alipata A, B, wala C, matokeo yanaonyesha kuwepo A, B na C nyingi.

Kufuatia marekebisho hayo zipo shule kwa mfano Shule ya Kiislamu Kirinjiko, awali ilionyeshwa kuwa ni ya 105 kati ya shule 156 kitaifa, lakini sasa inakuwa ya 46 (katika shule zenye wanafunzi wasiozidi 30).

Ipo pia shule kama Nyasaka Islamic High School ambayo awali ilionyeshwa kuwa na F nyingi katika somo la Islamic Knowledge, lakini sasa inakuwa haina F hata moja.

Wakati Ubungo Islamic High School ilionyeshwa kuwa na D moja tu, hivi sasa baada ya marekebisho shule hiyo ina A moja, B nne, C kumi na tisa na D thelathini na tisa na kuwa shule ya 128 kati ya shule 326 kitaifa badala ya nafasi ya awali ambayo ilikuwa 237 (hii ni kwa zile shule zenye wanafunzi zaidi ya 30).

Kwa upande wa shule ya Kiislamu ya Wasichana, Kunduchi (Kunduchi Girls), katika matokeo ya awali walipewa Division 1 moja, Division 2 tano, Division 3 thelathini na tisa, Division 4 kumi na moja na zero mbili.

H i v i s a s a b a a d a y a marekebisho Kunduchi Girls wana Div.1 mbili, Div. 2 kumi na moja, Div. 3 thelathini na nane, Div 4 sita na zero mmoja.

Kwa mabadiliko hayo, hivi sasa shule hiyo ni ya 183 kitaifa badala ya nafasi ya 266 hapo awali.

Kwa upande wa shule ya Mudio, awali ilionyeshwa kuwa wana D moja tu, lakini sasa kuna B, C, na D tisa huku kukiwa hakuna F wakati awali walipewa F saba.

Shule hiyo sasa ni ya 28 kitaifa kati ya shule 156 zenye idadi ya wanafunzi chini ya 30 wakati awali ilikuwa ya 61.

Taarifa kutoka kwa baadhi ya wakuu wa shule zinafahamisha kuwa kuna wanafunzi wengi walikoseshwa sifa za kwenda Chuo Kikuu na sasa ndio wanahangaika ku ta fu ta fomu baada ya matokeo kubadilishwa.

Pamoja na mabadiliko haya, Wakuu kadhaa wa shule za Kiislamu walioongea na mwandishi, wanahimiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuharakisha kuunda

tume huru ya uchunguzi kwani kuna mengi ya kuchunguzwa katika Baraza la Mitihani la Tanzania.

Wa m e s e m a , h a k u n a namna ya kurejesha imani ya wananchi na hasa Waislamu, kwa Baraza hilo, isipokuwa kwa kufanyika uchunguzi makini na wa kina.

Tu h u m a z i l i z o p o n i kuwa Baraza hilo limekuwa l i k i d h i b i t i w a n a w a t u wa dini moja ambao nao wanatuhumiwa kuwahujumu Waislamu na kuwapendelea Wakaristo.

Iwapo madai hayo ni kweli au la na ni kwa namna gani Baraza la Mitihani huwapendelea Wakristo na kuwahujumu Waislamu, ndio mambo yanahitajika kuchunguzwa na tume hiyo.

Baadhia ya wakuu wa shule mbalimbali walioongewa na mwandishi wanaarifu kuwa wamekuwa wakishangazwa na matokeo ya baadhi ya watoto kutoka shule za seminari zinazodaiwa kutesa kila mwaka kwamba japo wanafunzi hao huingia kidato cha tano wakiwa na daraja la kwanza, lakini wengine wanaonekana kutojiweza kiasi cha kupitwa hata na wale walioingia na divisheni 3.

Wakati huo huo, Waislamu walikutana Diamond Jubilee J u m a p i l i n a k u p i t i s h a maazimio kadhaa kuhusu kadhia hii.

A k i o n g e a k a t i k a Kongamano hilo lililoandaliwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Amiri wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasis i za Kiis lamu Tanzania , Alhaj Mussa Yusuph Kundecha, aliwataka Waislamu kutokuwa wazito kufikiri na kujifunza kisha

kutoa maamuzi.Alisema, Waislamu siku

zote wamekuwa wakipiga kelele kuwa ipo dhulma katika sekta ya elimu kutokana na Baraza la Mitihani kujaa na kuongozwa na Wakristo tokea kuanzishwa kwake hadi hivi leo, lakini alidai wanaonekana ni watu wa kulalamika tu na kupuuzwa.

“Baraza la Mtihani ni sehemu ya mfano wa sekta nyingi tunazopigia kelele Wais lamu. Baraza l ina Wakristo kwa asilimia zaidi ya tisini tangu lianzishwe hadi hivi leo, wenyeviti, Makatibu watendaji na manaibu Katibu watendaji wote ni Wakristo tokea kuundwa.” Alisema Shkh. Kundecha.

A l i s e m a , w a k a t i wakishuhudia majigambo na sifa kila mwaka kuwa shule za Makanisa zinatesa, sasa leo hila zao zimebainika na kwamba siku za mwizi ni arobain.

Akionyesha kustaajabu, alisema baada ya Waislamu kubaini hujuma hizo, sasa Baraza limetoa matokeo mapya ambapo aliyepata ‘0’ sasa ana ‘A’, jambo la kujiuliza alisema, kutoka mtu kupata ‘0’ mpaka ‘A’,

“ H i v i h u y u m p a n g a matokeo alikuwa amepitiwa kwa kiasi gani”. Alihoji.

Kwa upande wake Katibu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Maulana Ramadhani Sanze, akianisha hali hiyo alisema, kwa muda mrefu Waislamu wamekuwa wakilaani dhulma dhidi ya Waislamu katika sekta mbalimbali Serikalini.

A l i s e m a w i n g i w a watendaji Wakristo katika sekta za Serikali ni athari kwa Waislamu huku akitolea mfano Baraza la Mitihani la Taifa.

Akirejea sakata la matokeo mwaka huu na kudai matokeo hayo yamewastua Waislamu na kulazimika wanafunzi kukata rufaa kutokukubaliana na matokeo hayo.

Alisema, hakuna mtu m b a y a d u n i a n i k a m a anayekunyima elimu, hivyo akasema, Waislamu hawana budi kupambana ili Serikali iweze kuwasikia na kulisafisha Baraza.

Alisema, ipo haja kwa Waislamu kubadilisha muundo wa kudai haki zao, kwani inaelekea muundo wanaotumia siku zote haueleweki kwa sababu siku zote (Waislamu) huwa wanasema haki zao lakini hawadai haki zao.

Alisema, matokeo mapya yamekuwa na athari kubwa kwa matokeo ya wanafunzi na Shule husika kama yalivyo ainishwa upya na Baraza hilo baada ya kuyapitia upya.

“Hii ni kashfa kubwa kwa Baraza la Mitihani na Serikali. Kwa kuzingatia historia na muundo na utendaji wa Baraza hilo, Waislamu wanayo kila sababu ya kuamini kwamba matokeo haya ni kielelezo cha hujuma ambazo wamekuwa wakifanyiwa kwa muda mrefu. Yawezekan uchunguzi wa kina ukifanyika kwa masomo yote itadhihirika kwamba dosari hizo haziishii katika somo moja tu.” Alisema Maulana Sanze.

Kufa t ia kadhia h iyo , Jumuiya na Taas i s i za Kiislamu Tanzania, imeitaka Serikali kuunda tume huru ya kuchunguza Baraza la Mitihani na utendaji wake wa kazi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita, kisha hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa watumishi watakaobainika na kashfa hiyo.

Page 4: ANNUUR 116

4 RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 5 - 7, 2012 AN-NUUR HABARI

Uchochezi wa kutisha Zanzibarla Tanzania Daima, Ust. Kitunga, alisema amlipigia simu mpiga picha mkuu wa gazeti hilo kupitia namba zilizokuwemo katika gazeti hilo, aliyemtaja kwa jina la Joseph Senga na kumueleza suala hilo.

Alisema, mpiga picha huyo al iwajibu kuwa wasimfundishe kazi na kumtukana, kisha alikata simu.

K i t u n g a a l i s e m a , alistushwa kuiona picha hiyo, siku ya Jumatatu, Mei 28, ambapo alijiuliza kabla ya kusogelea magazeti hayo, kuwa ina maana picha ile ya maandamano ya Januari ndiyo wameitoa sasa?

Al isema, baada ya kusoma chini maelezo ya p icha h izo ndipo alipostaajabu na kuona uchochezi na upotoshaji wa dhahiri wa vyombo vya habari, ambapo anadai walikusanya Waislamu na kuamua kuwapigia simu wahusika na kupata majibu kama alivyo ainisha hapo juu.

Akijibu swali picha hiyo ilikuwa ni ya tukio gani, na sababu kitambaa hicho kuwa na damu, Kitunga alisema, picha ile ilikuwa ni ya tukio la maandamano ya kupinga kufukuzwa shule wanafunzi wa sekondari ya Ndanda, ambapo polisi katika kuwazuia, walimpiga kirungu muumni mmoja na kumjeruhi.

Al i sema, baada ya mwenzao huyo kujeruhiwa na kutokwa na damu nyingi, al i lazimika kuchukua kilemba chake na kumfuta ili kuzuia damu isizidi kutoka, hivyo kitambaa kulowa damu.

Alisema, aliinua kitamba hicho juu walipofika waandishi wa habari na Polisi kuwaonyesha na kusema kwa sauti, “mmeona polisi mmemwaga damu ya Mwislamu”.

Alisema, alitegemea ujumbe ule na picha hiyo ingeonekana siku ya pili katika vyombo vya habari

Inatoka Uk. 2 na maelezo yake kwamba polisi walimwaga damu, lakini hakuona picha hiyo wala habari ya polisi kujeruhi Muislamu katika gazeti lolote.

Kitunga aliitaka Serikali kuwa makini na taarifa za vyombo vya habari h u s u s a n i y a p o i b u k a masuala ya Waislamu kwani kwa kiasi kikubwa vinapotosha.

K u c h a p i s h w a k w a picha hizo za uwongo ili kuwapakazia Waislamu Z a n z i b a r , k u n a t i l i a nguvu yale madai kuwa waliochoma makanisa ni watu waliopangwa na vyombo vya dola au maaskofu ili kipatikane kisingizio cha kuwahujumu Wazanzibari na Waislamu kwa ujumla.

Wa k a t i h u o h u o , Askofu wa Kanisa la Ki in j i l i l a Ki lu the r i

Tanzania (KKKT) mkoani Arusha, Thomas Laizer, anasema kikosi cha vijana wa Kiislamu wapatao 300 tayari wameandaliwa kwa kushambulia makanisa.

A s k o f u L a i z e r akinukuliwa na gazeti la HabariLeo la jana Jumatatu Juni 4, amesema kuwa kambi ya vijana hao wa Kiislamu ipo Arusha eneo la Unga Limited.

A s k o f u T h o m a s anasema, “anazo taarifa za kutosha na za uhakika kuwa kwa sasa kuna vijana zaidi ya 300 wa Kiislamu eneo la Unga Ltd katika msikiti mmoja wakifanya mazoezi ya kareti tayari kujiandaa kufanya uhalifu katika makanisa.”

Limenukuu gazeti la HabariLeo katika habari iliyoandikwa na mwandishi John Mhala.

W A I S L A M U wametahadharisha kuwa iwapo zoez i l a s ensa halitafanyika kwa umakini kubwa, basi litakuwa halina maana yoyote na itakuwa ni kupoteza fedha bure.

Wa k i o n g e a k a t i k a kongamano lililofanyika Jumapili juzi katika ukumbi wa Diamond, baadhi ya v iongoz i wa Ki i s l amu wametaka pamoja na mambo mengine kuwekwa kipengele cha dini katika dodoso za sensa hiyo.

Kwa upande mwingine wamesema kuwa, haitakuwa jambo la kukubalika kama watakaopewa ‘ajira’ ya muda kufanya zoezi hilo watakuwa watu wa dini moja pekee.

Msimamo huo umetolewa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, katika Kongamano lililofanyika katika ukumbi wa Diamond, Upanga Jijini Dar es Salaam, m w i s h o n i m w a w i k i

Waislam wataka sensa ifanywe kwa umakiniNa Bakari Mwakangwale iliyopita.

Akiongea kwa niaba ya Taasisi na Jumuiya hizo, Sheikh Ponda Issa Ponda wa Shura ya Maimam, alisema msimamo huo unakuja kutokana na kutokuwa na imani na Idara ya Takwimu ya Taifa.

“Tume hiyo iwe na w a w a k i l i s h i w a d i n i (Waislamu, Wakristo na Wapagani) ambao watahusika katika hatua zote za mchakato wa Sensa zikiwemo ukusanyaji wa takwimu, majumuisho na utangazwaji wa matokeo.” Alisema Sheikh Ponda.

Alisema, baada ya hatua hizo kipengele cha dini kirejeshwe rasmi katika sensa na idadi ya Waislamu, Wakr is to na Wapagani ionyeshwe, ili kuondoa utata na dhana ya idadi rasmi ya makundi hayo.

Aidha, alisema kwamba Waislamu hawana imani na Idara ya Takwimu ya Taifa, kuendelea kubeba dhamana kubwa ya takwimu inayogusa misingi ya haki za raia.

Awal i , Shkh. Ponda, alisema kwamba uzoefu u n a o n y e s h a k w a m b a baada ya Serikali kuondoa kipengele cha dini imekuwa ni fursa iliyoandaliwa kwa makundi yenye muelekeo maalum kuchukua nafasi ya kutoa na kuibua takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo

na wananchi wenye imani nyingine.

Alisema, ni dhahiri hali hii ya kila kundi kuibuka na takwimu zake, inaonyesha ipo haja kwa Serikali kurudisha kipengele cha dini katika sensa ya taifa, kwani ndiyo njia sahihi ya kupata takwimu sahihi.

SHEIKH Ponda Issa Ponda (kulia) akiteta jambo

DKT. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar.

Page 5: ANNUUR 116

5RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 5 - 7, 2012AN-NUUR HABARI ZA KIMATAIFA

H A K U N A n y a r a k a zozote zinazoonyesha k a m a A f r i c a n Associat ion i l ikuwa imetayarisha mpango wa kushughulikia hali ya siasa. Kuelewa mwelekeo wa siasa wakati ule inabidi mtu atazame mwenendo wa viongozi wa TAA na jinsi walivyokuwa w a k i y a s h u g h u l i k i a m a m b o t o f a u t i yaliyokuwa yakiwadhili wananchi. Jambo la kwanza walilofanya Dk. Kyaruzi na Abdulwahid Sykes mara tu baada ya kuingia madarakani ni kuunda TAA Political Subcommittee (Kamati Ndogo ya Siasa ya TAA) iliyomjumuisha Sheikh Hassan bin Amir kama Mufti wa Tanganyika na Zanzibar; Dk. Kyaruzi, M w a p a c h u , S a i d Chaurembo aliyekuwa Liwali wa mahakama ya Kariakoo; John Rupia na Stephen Mhando. Kazi ya kamati hii ilikuwa ni kushughul ika na masuala yote ya siasa kat ika Tanganyika . Kuundwa kwake ndiyo hasa ulikuwa mwanzo wa siasa za dhahiri katika Tanganyika na mwanzo wa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Kwa kipindi cha miaka ishirini na moja African Association ilifanya kazi chini ya katiba isiyokuwa ya siasa. Kwa mara ya kwanza mwaka 1950, TAA chini ya uongozi mpya, ilijipa hadhi ya chama cha siasa, siyo kwa kubadilisha katiba yake bali kwa kuunda kamati ya siasa ndani ya chama. Kamati hii ilikuwa na watu wenye kuwakilisha maslahi na uwezo tofauti, wakiwa halikadhalika wanatokana na uzoefu na hali tofauti. Sheikh Hassan bin Amir Muunguja alikuwa ndiye Mufti wa Tanganyika na aliwakilisha Waislamu a m b a o h a s a n d i y o waliokuwa wakiongoza mapambano dhidi ya serikali. Said Chaurembo aliwakilisha Wazaramo wa Dar es Salaam na vitongoji vyake . John Rup ia

Dk. Kyaruzi Katika Kamati Ndogo ya Siasa Ndani ya TAA, 1950 - 1951Na Mohamed Said kutoka Mission Quarter

alikuwa mfanya biashara taj ir i na mfadhil i wa chama. Stephen Mhando Mbondei kutoka Muheza alijulikana kwa misimamo mikali aliwawakilisha wasomi wa Makerere, D k . K y a r u z i a k i w a mmojawapo. Uongozi huu ndiyo ulioweka msingi wa kuundwa kwa TANU chama kilichokuja kung’oa ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika.

Baada ya kuunda kamati hii uongozi wa TAA ulianza kuyaandikia matawi ya TAA ili kuyahuisha. Jambo kubwa lililokabili TAA na ile kamati ya siasa ilikuwa ni hadhi ya Tanganyika kama nchi ya udhamini c h i n i y a U m o j a w a Mataifa. Uongozi wa TAA ulimuingiza katika kamati ya siasa Earle Seaton, mwanashe r i a ku toka Bermuda aliyekuwa akikaa Moshi ili aishauri kamati kuhusu mambo ya sheria ya katiba. Seaton alitakiwa kuishauri jinsi ya kuliendea

shauri la kutaka Uingereza itoe uhuru ili Tanganyika ijitawale yenyewe kwa kuwa nchi hiyo haikuwa koloni, bali nchi chini ya udhamini wa Umoja wa Mataifa. Mwaka wa 1948 Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa tayari lilikuwa limetuma ujumbe wake wa kwanza kuzuru Tanganyika. Lakini hakuna jambo lolote la manufaa lilipatikana kutoka kwa ujumbe huo. Makao Makuu ya TAA mjini Dar es Salaam chini ya Dk. Kyaruzi na Abdulwahid ikiungwa mkono na kamati ya siasa sasa i l ikuwa ikiamka kutoka kwenye usingizi mzito . Kil ichotakiwa ilikuwa ni kupata maswala ya kutoa changamoto kwa akili za wale wasomi vijana. Uongozi wa chama cha TAA haukuwa na haja ya kuangaza mbali. Changamoto ilikuja kwa sura ya Constitutional Development Committee (Kamati ya Mapendekezo ya Katiba) iliyoundwa na

Gavana Edward Twining na mgogoro wa ardhi ya Wameru.

U inge reza i l i kuwa iki tawala Tanganyika ch in i ya k i fungu 76 na 77 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Kama mamlaka tawala Uingereza ilitarajiwa kuanzisha na kuendeleza maendeleo ya siasa, uchumi na ya kijamii ya Tanganyika hadi kufikia wakati ambao watu wake wangekuwa tayari kujitawala. Lakini Waingereza walifanya khiyana na hawakutimiza ahadi hiyo. Walijihusisha na kulinda maslahi yao wenyewe ya kikoloni na yale ya watu weupe wachache na wakaendelea kuwapuuza Waafr ika waliokuwa wengi na wenye nchi. Labda kwa kuanua ngoma juani, Gavana Twining a l ikar ib isha mapendekezo kutoka kwa watu mashuhuri, vyama vya us tawi wa jamii na Native Authorities, ku taka mapendekezo

ya j i n s i Tangany ika itakavyotawaliwa. Kamati ya siasa ya TAA ilipeleka mapendekezo yake ambayo yalitiwa sahihi na wajumbe wote wa kamati ya siasa. Sheikh Hassan bin Amir, A b d u l w a h i d S y k e s , Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando na Said Chaurembo. Katika taarifa yake ya TAA ya mwaka ya 1950 Abdulwahid aliandika:

“Kwa ajili ya maslahi ya Waafrika na kulinda maslahi ya chama hiki na yale ya jumuiya ya Waafrika kwa ujumla, chama kimeweka wakili atakayeshauri juu ya mambo ya sheria. Wakili huyo ni Bwana E. E. Seaton wa Moshi. Mara kwa mara amekiandikia chama hiki juu ya masuala mbali mbali ya siasa, na kwa kiasi kikubwa ushauri wake umesaidia wakati chama hiki kilipokuwa kikitayarisha mapendekezo juu ya katiba.”

( I t a e n d e l e a t o l e o lijalo)

BAADHI ya viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu. Kulia Sheikh Ramadhani Sanze, Sheikh Mohamed Issa, Amir Kundecha pamoja na Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa katika kongamano lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jumapili iliyopita. (Picha na Bakari Mwakangwale)

Page 6: ANNUUR 116

6 RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 5 - 7, 2012 AN-NUUR MAKALA

Ni kweli Uamsho watageuka Al Qaidah

KWA busara zake, gazeti la HabariLeo ambalo ni gazeti la serikali, katika habari yake inayoongoza katika toleo la Ijumaa Juni 1, liliandika habari ikitahadharisha kuwa U a m s h o w a n a w e z a k u g e u k a n a k u w a ‘kikundi cha kigaidi’ kama ilivyo kile cha Al Shabaab cha Somalia.

H a b a r i h i y o iliyoandikwa na Theopista Nsanzugwanko ilimnukuu mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Shehe Sadik Godigodi akisema sio kweli kuwa uchomaji wa makanisa na uvunjaji wa baa na kupora masanduku ya b ia u l i fanywa na wahuni, bali ulifanywa na Masheikh wa Uamsho.

“Wamedai wanajua harakati za dini Zanzibar na kusema si kweli kuwa vurugu hizo zilifanywa na vikundi vya wahuni, bali wanachama wa kundi la Uamsho.”

Limeandika HabariLeo l ikimnukuu Godigodi ambaye ametajwa kuwa ni mkurugenzi wa taasisi inayoitwa Tanzania Islamic Peace Foundation (TIPF).

HabariLeo likipamba kauli ya TIPF lilisema kuwa Uamsho kazi yao imekuwa ni kujenga chuki miongoni mwa wananchi na Waislamu misikitini na kwamba TIPF ilishaitaka serikal i iwachunguze

Na Omar Msangi Uamsho lakini haikujali.“Sisi Waislamu tunajua

historia ya kundi la Al Shabab ambalo lilianza kwa kukiuka miiko ya dini na kuingiza kile wanachokipenda wao kwa mgongo wa dini, hivyo ni vema serikali ichukue hatua mapema kabla hayajatokea madhara zaidi.”

Alisema Sadiki huku akisisitiza kuwa, anatoa nasaha hizo kwa vile anaona kila ishara kuwa si muda mrefu, Uamsho wataanza harakati za kigaidi kama za Al Shabab.

Niseme na mapema kwamba ni kweli Waislamu wanajua chanzo cha Al Shabaab kama lilivyosema H a b a r i L e o n a k a m a nitakavyofafanua baadae. Lakini niseme pia kwamba ni Habar iLeo hi i h i i iliyowahi kutujia na ‘muvi’ ya viwango vya Hollywood kuhusu mtoto wa shule ya msingi a l iyeweza kupenya ngome ya ulinzi ya Ubalozi wa Marekani pale Msasani akiwa na “mabomu” tayari kulipua ubalozi huo. Kwa umahiri mkubwa kabisa, HabariLeo likadai kuwa mtoto huyo aliweza kuwapita FFU na askari wengine wanaolinda ubalozi huo, akaweza pia kuihadaa mitambo ya elektroniki mpaka akaingia ndani ya ngome ya ubalozi huo! Kwa hakika muvi za kiwango hiki hata kule Bo l lywood , Mumba i hazijaingia!

H a b a r i L e o k a t i k a

kukoleza habari yake ipate kunoga vizuri, likasema kuwa mtoto huyo alipata ‘mafunzo ya ugaidi’ kupitia msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa akisikiliza kanda na mawaidha ya Masheikh ‘wa ki-Al Qaida’.

Hiyo ndiyo HabariLeo gazeti la serikali! Pengine ingekuwa vyema akina Theopista wakatumalizia kwanza ‘ile muvi’ (filamu) ya mtoto gaidi Muislamu wa shu l e ya ms ing i kabla ya kuja na mkanda mwingine wa Uamsho Vs Al Shabab.

K i a s i w i k i m o j a iliyopita, Baraza la Uslama la Umoja wa Mataifa lilichemka. Ilikuwa pale ilipowasilishwa habari kwamba serikali ya Syria kwa kutumia jeshi likiwa na vifaru na silaha nzito nzito, limeuwa watu zaidi ya 100 wasio na hatia wakiwemo watoto zaidi ya 30 na wanawake wengi.

Habari hizo zilizopigiwa chapuo vya ku tosha k a t i k a v y o m b o v y a habari, zilipelekea nchi za Ulaya kupitisha uamuzi wa kuvunja uhusiano na serikali ya Bashar el Assad kwa kuwatimua wanadiplomasia wake katika nchi hizo.

I l i k u w a n i U r u s i peke yake iliyotoa kauli kwamba taarifa za mauwaji hayo zisichukuliwe kama zilivyo na kuanza kuilani serikali ya Assad pekee kwani huenda hata waasi

wakawa wanabeba lawama kubwa. Kwa msimamo h u o , U r u s i i l i j i k u t a ikishutumiwa kwamba ndiyo inamtia kiburi Assad na kwamba kwa msimamo wake huo itasababisha vita na maafa makubwa kwa watu wa Syria. Kwa upande mwingine akina Cameron, Obama, Hillary Clinton na wenzao wa Ufaransa na Ujerumani ndio wakawa wanatamba wakimshutumu Assad na kujinadi kuwa wao ndio watu wema, wapenda amani, wanaojali uhai, utu na kuwatakia heri watu wa Syria.

Waswahili wana msemo wao, njia ya mwongo fupi na mwizi zake arobaini. Haikuchukua hata siku tatu, ukweli ukafichuka. Waliofanya mauwaji yale hawakuwa askari wa jeshi la Syria. Shirika la Utangazaji l a U i n g e r e z a , B B C , wakajikuta wakiumbuka. Katika kutumiwa kupiga propaganda chafu i l i ipatikane sababu ya kuipiga

Syria, BBC ilirusha picha za watoto waliouliwa Iraq May 2003 wakadai kuwa waliuliwa juzi Syria na Rais Bashar el Assad.

Huu ndio uzuri wa utandawazi, picha zile watu wengi walikuwa nazo na zilikuwa katika mtandao. Lakini kwa upande mwingine, Marco Di Lauro a l iyekuwa amepiga picha zile bado yupo hai. Akashangaa na kushtuka kuona picha zake alizopiga Iraq zikirushwa na BBC na kudai kuwa ni watoto waliouliwa Syria wiki iliyopita.

Lakini wapo watu nyuso zao hazina haya. Ni ile kauli ya Qur’an kwamba wanapoambiwa msifanye ufisadi katika ardhi, husema sisi ndio watengezaji. Nchi za Ulaya badala ya kutahayari, zikaendelea kupiga propaganda ileile kuwa Jesh i l a Syr ia l i m e u w a w a t o t o n a wanawake na wakaanza kutimua wanadiplomasia katika nchi zao.

WAKATI tukio h i l i l i n a t i m u a v u m b i k a t i k a a n g a z a kimataifa, Zanzibar kulitokea zinazoitwa vurugu . Uchunguz i u n a o n y e s h a k u w a kilichotangulia vurugu hizo ni maandamano na mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI). Mada kuu katika yote haya il ikuwa kuhoji uhalali wa muungano na kutaka marekebisho. M a a n d a m a n o n a m k u t a n o u l i i s h a k w a s a l a m a w a t u wakatawanyika. Jioni yake, mara baada ya swala ya Magharibi, Sheikh Mussa Abdallah Juma akiwa msikitini kwake akiendesha darsa, polisi walikuja na kuingia msikitini, kumkamata kifedhuli na kumpeleka korokoroni. Waumini hawakuweza kuswali Isha na kwenda nyumbani kulala bila kujua nini

Kilichotokea Zanzibarkimemsibu Imam wao. Wa k a j i k u s a n y a n a kuelekea polisi. Polisi nao wakajibu kwa kurusha mabomu ovyo mitaani. Huo ndio ukweli na ndio chanzo cha tukio lenyewe, tukio ambalo li l isababisha vurugu mitaani , wakatokea wengine kuvamia baa kuvunja na kupora m a s a n d u k u y a b i a na wengine kuchoma makanisa na kuharibu mali.

Wakati hata serikali ha i j a toa kau l i yake , Uamsho wakatoa kauli wakisema hawahusiki na uhalifu wowote, iwe ni ule wa kuchoma makanisa au kuvamia baa na kuharibu mali. Tamko kama hilo likatolewa pia na Jumuiya ya Maimamu-JUMIKI.

Kauli ya TIPF kama ilivyopambwa na gazeti la HabariLeo, inabeba na kuendeleza kile kile alichosema Askofu Mkuu

Inaendelea Uk. 7

WAISLAMU wakiwa katika kongamano lililofanyika Diamond Jubilee.

Page 7: ANNUUR 116

7RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 5 - 7, 2012AN-NUUR MAKALA

Kilichotokea ZanzibarInatoka Uk. 6

wa Kanisa la Anglikana nchini Askofu Valentino Mokiwa pale alipompuuza Waziri Mohamed Aboud ki-aina. Wakati Waziri akizungumzia “wahuni” na kufanyika uchunguzi kujua waliochoma makanisa na kupora masanduku ya bia, Askofu Mokiwa anapuuza kauli hiyo mbele ya Waziri a k i o n y e s h a k w a m b a anachotaka kusikia ni serikali kutamka kwamba waliochoma makanisa na kuiba masanduku ya bia ni Masheikh wa Uamsho na kuwatia adabu haraka.

Kauli na mwelekeo huu wa Askofu Valentino Mokiwa ndio unakaririwa na kutiliwa nguvu na HabariLeo kwa kutumia jina la Muislamu Sadik na taasisi ya Kiislamu, Tanzania Islamic Peace Foundation (TIPF). Kauli na msimamo huo wa Askofu Mokiwa, ndio huo huo umeendelezwa katika magazeti ya juzi Jumapili ambapo vijana wa CCM walisema watajadili na kutoa msimamo. Lakini katika hali ya kutisha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete naye kakamata msimamo huo huo wa Asko fu Mokiwa. Pengine kwa uzito huo ambao mwelekeo wake ni kuwatangazia ugaidi Uamsho, ndio gaze t i l a Mtanzan ia Jumapili likaibuka na habari ikitaka makachero wa FBI waletwe Zanzibar. Likimnukuu Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa l i k a f a h a m i s h a k u w a anaombwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein wawatafute FBI kwani ndio wenye uwezo wa kuchunguza kadhia ya Uamsho.

N i s e m e k u w a , n i kweli yapo makanisa yamechomwa moto na ni kweli pia kwamba kuna baa zimevamiwa na kuporwa. Swali ni je, nani kafanya uhalifu huo? Ambalo halina utata ni kuwa Uamsho walifanya maandamano na muhadhara na kwenda polisi kwa wingi usiku baada ya Sheikh wao kukamatwa. Utata upo kwenye nani

kachoma makanisa na kupora masanduku ya bia katika vurumai zile. Hilo linahitaji uchunguzi na taratibu za kimahakama.

Sasa labda niul ize, k a m a R a i s w a n c h i anatoa kauli ya kuwatia hatiani Uamsho kwamba wamechoma makanisa na kupora masanduku ya bia, kazi ya IGP Mwema na Afande Manumba itakuwa nini? Kazi ya mahakama ni ipi? Je, kinachokusudiwa ni kukamata Masheikh na kuwaadhibu ‘kisiasa’ na kwa “shinikizo la A s k o f u M o k i w a n a m a a s k o f u w e n z a k e ” k a m a i l i v y o f a n y i k a al ipokamatwa Sheikh Kassim Juma na Sheikh Pazi wa Manzese Darajani? Je , k inachotakiwa ni kuona Masheikh Zanzibar wakikamatwa, kuwekwa rumande na kuteswa kama walivyofanyiwa Imam wa Msikiti wa Mtambani Sheikh Abdallah Chatta wakati wa mauwaji ya Mwembechai?

Kauli ya Rais Shein na ile ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika kadhia hii, wakati vyombo vya dola vipo kazini vinafanya kazi, lengo lake nini? Je, ni kulinyenyekea Kanisa, kama ilivyofanya serikali ya Mheshimiwa Benjamini William Mkapa kwa Paroko Lwambano, “kuamuru” kuuliwa Waislamu wasio na hatia na kisha kuwapongeza wauwaji na kuwanyima Waislamu japo haki ya uchunguzi na kusimama mahakamani?

Yalipovunjwa mabucha ya nyama ya nguruwe jijini Dar es Salaam mwaka 1993, Rais wakati huo Mzee Ali Hassan Mwinyi alikuwa Pemba. Baada ya kupata taarifa alitoa amri akiwa huko huko kwamba “rungu la dola” liwaangukie Waislamu. Wenye chuki na Waislamu wakatumia fursa hiyo vizuri sana. Walikamatwa Masheikh wasio na hatia wakateswa na kudhalilishwa sana. Katika Masheikh waliokamatwa, walikuwepo mpaka wale waliokuwa vipenzi wa A l i H a s s a n M w i n y i

waliokuwa wakifanya uradi na kumwombea Dua kila uchao.

Nimetangulia kusema kuwa ulimwengu mzima ulimlaani Bashar Assad na jeshi lake kutokana na picha za kutisha zilizorushwa na BBC za maiti za watoto waliouliwa wengine miili ikiwa imechanikachanika kutokana na risasi na mabomu ikidaiwa kuwa mauwaji hayo yamefanywa juzi na Assad. Kumbe ni picha za watoto waliouliwa na askari wa Marekani waliovamia Iraq mwaka

2003. Miaka 9 baadae ‘Marekani na mshirika wake Uingereza katika kuuwa watoto, wanawake na watu wasio na hatia Iraq, inatumia picha hizo hizo kumsingizia uhalifu Assad ili ipate kumpiga kama walivyompiga Muammar Gadhafi.

Katika tukio hili la Zanz iba r, baadh i ya vyombo vya habari, kwa kutumiwa au kwa utashi wao wenyewe, vimetumia picha za tukio la Morogoro la toka Januari mwaka huu na kudai kuwa ni Uamsho.

Pengine kilichokusudiwa kat ika p icha hiyo ni kupandikiza his ia na ushawishi kwamba Uamsho n i watu wanaopenda kumwaga damu. Nasema hivyo kwa sababu, picha iliyotumiwa inaonyesha mtu akiwa kashiki l ia k i l emba k i l i cho lowa damu.

Na baada ya kupiga propaganda hiyo, ameibuka Askofu Thomas Laizer akidai kuwa kuna ‘jeshi’ la Waislamu linaandaliwa kwa ajili ya kushambulia makanisa.

KAMA inavyofahamika kwa kila mtu, Somalia ilikaa bila serikali baada ya kupinduliwa Rais Siad Barre ikiwa ni vurugu mitaani, mauwaji na uporaji kila kona. Ilikuwa ni katika hali hiyo pakaibuka watu waliopewa jina la wababe wa kivita. Hawa walikuwa na majeshi, silaha na kila mmoja akidhibiti eneo fulani katika Somalia n a w a k i p a m b a n a kugombea maeneo ya kudhibiti. Umoja wa Afrika (OAU), Umoja wa Kikanda wa Igad na hata Umoja wa Mataifa (UN), kila walivyojitahidi kuleta amani, walijikuta wakikwama. Ilikuwa ni Umoja wa Mahkama za Kiislamu waliofanikiwa k u w a u n g a n i s h a Wasomali na kurejesha amani. Nchi ikatulia, biashara na harakati

Uamsho VS Al Shabaabza uchumi zikaanza kushamiri , watu wa nje wakaanza kuingia Somalia kuwekeza na Wasomali waliokimbia nch i yao wakaanza kurejea.

Hata hivyo, hali hiyo ya amani haikuchukua muda. Marekani ikaingilia kati na kuvuruga amani hiyo. Ilianza na kusaidia kuvipa vikundi vya wababe wa kivita silaha na fedha pamoja na habari za ki-inteli j isia kupambana na serikali ya Umoja wa Mahakama za Kiislamu. I l ipoona mbinu h iyo haifanikiwi ikaitumia Ethiopia kuvamia Somalia kuwaondoa Mahakama ya Kiislamu madarakani. Hii ni historia maarufu na ukweli ambao hakuna mtu anayeweza kuupinga. Kilichotokea nini? Ni kurejea ubabe wa kivita ule ule wa awali. Wananchi

wa Somalia wakarejeshwa katika taabu ile ile ya mauwaji. Al Shabab nao wakaibuka kutoka katika Umoja wa Mahakama za Kiislamu na kushika silaha wakipinga nchi yao kukaliwa na vibaraka wanaounda serikali kutokea Nairobi na wakifadhiliwa na Marekani na Ulaya. Ndio hao wanapambana mpaka leo. Hiyo ndio Al Shabab ambayo leo tunalazimishwa kuitizama kama Marekani inavyoitizama.

Lakini la kusikitisha zaidi, baada ya Marekani kutibua mambo, sasa nchi za Kiafrika zinatumiwa kama upawa wa kupoza uji wa moto mwenye uji wake apate kuunywa bila ya kuungua. Uganda, Burundi na sasa Kenya wana majeshi huko wanapambana na Al Shabab. Na tunasikia, haup i t i muda Kenya

Inaendelea Uk. 8

WAISLAMU wakiwa katika kongamano lililofanyika Diamond Jubilee.

Page 8: ANNUUR 116

8 RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 5 - 7, 2012 AN-NUUR MAKALA

Uamsho VS Al ShabaabInatoka Uk. 7

inapigwa bomu au guruneti. Likilipuka tunaambiwa hao ni Al Shabab. Juzi Sauti ya Amerika (Voice o f A m e r i c a - V O A ) imesema kuwa Al Shabab watashambulia majengo marefu yaliyo Nairobi katika muda wa wiki mbili zijazo. Habari hiyo haikueleza VOA au tuseme Marekani wao wamepataje habari hizo. Lakini niseme kuwa lililo la uhakika ni kuwa Kenya wataendelea kupigwa ndani ya Nairobi na Mombasa, wananchi wa Kenya wasio na hatia wataendelea kuul iwa kama walivyouliwa wale Waganda waki t izama fainali za kombe la dunia katika mgahawa Kampala ikasemwa ni shambulio la kigaidi la Al Shabab.

Kwa nini waendelee kuuliwa? Wataendelea kuuliwa ili kudumisha kitisho cha Al Shabaab ili serikali ya Kenya ipate kizingizio cha kuendelea kuweka jeshi Somalia. Kutokana na siasa za kiharamia zilivyo hivi sasa katika hii inayoitwa vita dhidi ya ugaidi, lau utafanyika uchunguzi huru, haitashangaza kuona kuwa mengi ya mashambulizi yanayofanywa Kenya na kuleta madhara kwa wananchi, ni ya kupangwa na makachero wa Kenya wakishirikiana na wale

wanaodaiwa kupambana na ugaidi ulimwenguni.

S a s a H a b a r i L e o imetahadharisha kuwa Uamsho watageuka kuwa Al Shabab, kwa maana kuwa magaidi. Maadhali Marekani haikuwa imetaka Umoja wa Mahakama za Kiislamu kutawala S o m a l i a , m a a d h a l i Marekani haikuwa imetaka ionekane kuwa Uislamu umeleta suluhu na amani Somalia, ilidai kuwa Umoja wa Mahkama za Kiislamu ni magaidi. Paropaganda ikapigwa tukaaminishwa hivyo.

K w a m a a n a h i y o , haitashangaza hivi leo mbinu hizo hizo chafu zikitumiwa kuwachafua Uamsho. Ni mbinu zile zile za kiharamia za kudai kuwa Saddam ana silaha za maangamizi upate kuvamia. Ni mbinu zile zile

za kishetani zilizotumika Marekani kutengeneza kimeta na kuwashambulia nacho raia mpaka watu muhimu kama wabunge na kusingizia ni Al Qaida ili Bush apate sababu ya kutengeneza sheria (Patriot Act) ya kupambana na Waislamu dunia nzima.

Qur’an inasema, “Enyi mlioamini! Kama fasiki ak iku j ien i na habar i (msimkubalie tu), bali pe le lezeni (kwanza) , msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mliyoyatenda.” (49:6)

Huu (Qur ’an 49:6) ndio ujumbe wangu kwa Rais Ali Mohamed Shein, Maalim Seif Sharif Hamad, Balozi Seif Idd, SMZ, CCM Zanzibar mpaka wale “wahafidhina wa Kisonge” na wananchi wa Zanzibar kwa ujumla.

A L I P O K U J A a l i y e k u w a R a i s wa Marekani , Bi l l C l i n t o n , A r u s h a , hakuwa Mheshimiwa Benjamin Wil l iam Mkapa wakati huo akiwa Rais aliyeomba FBI na CIA waje na mbwa wanuse gari lake ili kuhakikisha hakuna

FBI hawahitaji ruhusa ya JKgaidi atakaye hatarisha usalama. Hata pale alipokuja George W Bush, hakuwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete al iyetuma maombi kwamba makachero wa Marekani waingine mpaka chumbani ili kuhakikisha hakuna gaidi aliyejificha Ikulu.

Walikuja wenyewe kama walivyojipanga wakapanda mpaka darini Ikulu na kufanya kazi yao bila kusubiri kuombwa au kuomba ruhsa.

J o s e p h K o n n y amekuwepo kwa miaka mingi akileta maafa makubwa kwa wananchi wa Uganda. Marekani haikujali. Lakini juzi hapa mara tu baada ya kugunduliwa mafuta U g a n d a , M a r e k a n i imetafuta kisingizio kuwa sasa inakuja kumsaka Kony. Bila kusubiri Museveni kutuma barua ya maombi, jeshi la Marekani hivi sasa lipo Uganda.

S a s a k a m a h a w a akina Fahmi Dovutwa wanatamani zile ‘Drone” zinazowaporomoshea m a b o m u w a n a n c h i wasio na hatia kule Yemen na Pakis tan sasa zije Zanzibar, wala wasihangaike kutuma maombi kwa Obama. Marekani yenyewe ikiona

ina masilahi inataka kuyadhibiti kupitia jeshi na makachero wake, itatuma ‘mbweha’ wake wakifuatiwa na wanamaji (Marines). Wala haihitaji kusomeshwa, yenyewe ni fundi na bingwa wa kutafuta visingizio vya kutuma ndege zisizo na rubani kupiga madrasa na kuuwa watoto wakisoma Qur’an.

Ila tu ambalo pengine wanashangaa, kudharau na kutupuuza, ni kuona kuwa miaka 50 baada ya uhuru, bado tuna watu ndani ya jamii ya Watanzania ambao w a n a d h a n i k u w a serikali ya Tanzania haijawa na uwezo wa kuchunguza tukio kama hili la Uamsho.

Kwa hiyo wakiibuka watu kama akina Fahmi Dovutwa wakisema kuwa FBI waletwe Zanzibar, tunaona ni habari muhimu ya kuipa kipaumbele katika magazeti yetu ya kuheshimika!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

WAISLAMU wakiwa katika kongamano lililofanyika Diamond Jubilee.

Page 9: ANNUUR 116

9RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 5 - 7, 2012AN-NUUR MAKALA

S H U K U R A N I z o t e z imstahi l i Mwenyezi Mungu ambaye ameweka wema katika kila kitu, na rehema na amani zimfikie kwa yule ambaye amemleta zimfikie kwa yule ambaye amemleta Mwenyezi Mungu kuwa ni Rehema kwa viumbe wote, Mtume Mkweli muaminifu mwenye tabia nzuri na jamaa zake na masahaba zake watenda mema.

Ama baada ya utangulizi huu, Jua ndugu yangu msomaji kuwa Dini ya Uislamu ni Dini ambayo ameir idhia Mwenyezi Mungu kwa kila Mtume m d o g o n a m k u b w a . A m e s e m a M w e n y e z i Mungu na hatukumtuma (Mtume ila tulimwambia) hakuna apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa mimi basi niabuduni na hii ndio imani thabiti katika kila ujumbe wa Kisheria. Ama sheria ambayo hiyo ndio tawi la ibada hapo Mwenyezi Mungu hufanya ali takalo na uhukumu analoli taka. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu (kila Mtume tumempa sheria yake na Mwenendo wake).

Ama shina la tatu la Dini ni tabia na hii vile ni miongozi mwa vyanzo v i l i v y o m a d h u b u t i ambavyo ni tabia. Ni hiki vilevile ni vitu madhubuti katika Dini ya Kiislamu kwani mafunzo yake yote yanalingana katika kuwa na tabia nzuri bora na njema na kuacha tabia mbaya na mbovu. Na kwa hayo amesema Mtume (S.A.W) Hakika nimetumilizwa ili nije kutimiza tabia nzuri na vitu vinavyoshikamana kwa mshikamano wenye nguvu. Na hivyo utaikuta Qur’ani Tukufu inaungana na tabia na imani.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu (Jee,

Na DR. AHMAD MAHMOUD.

Nafasi ya tabia katika kueneza Uislamu

umemuona (Unamjua) yule anayekadhibisha dini (asiye amini malipo ya akhera?) huyo ni yule anayemsukuma yatima wala hajihimizi kuwalisha maskini (Wala hawahimizi w e n z i w e ) a y a h i z i anayekanusha vitendo na tabia ambaye anayekanusha D i n i k w a m b a y e y e hawakirimu mayatima na anawasukuma na anawafanyia roho mbaya na wala hawahurumii na wala hawaonei huruma masikini vile vile, na wala haimizi juu ya kuwahurumia. Na amesema Mtume (S.A.W) m w e n y e k u m u a m i n i Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho aseme maneno mazuri au anyamaze na M w e n y e k u m u a m i n i Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho na amkarimu mgeni.

Na Mwenye kumuuamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho amfanyie wema jirani yake) na katika hadithi nyingine haikamiliki imani ya mtu ambaye jirani yake hanusuriki na maudhui na maovu yake amepiga mchoro Mtume (S.A.W) wa njia na mwenendo ambao inampasa kila Muislamu ashikamane nao akasema (Mche Mwenyezi Mungu

popote ulipo na fanya jema pale unapofanya baya wema unafuta ubaya naishi na watu kwa tabia nzuri) na miongozo hii imekusanya mambo makuu matatu ya msingi nayi ni:-

1. Kumcha Mwenyezi Mungu na kuchunga mipaka siri na dhahiri sehemu yoyote na mahala popote.

2. Kufuatia kufanya mema pale unapofanya baya hapa shaka binadamu ni kiumbe dhifu anafanya makosa kwa kuteleza n a k u t e n d a m a m b o kinyume lakini hapana budi awe na tabia hii ili ajisafishe na kuteleza huku na mapungufu haya. Atakapofanya makosa hapana budi au uondoe uovu na ubaya huu. Kwa kufanya mema amesema Mwenyezi Mungu (hakika mema huondoa mabaya).

3. Kuchanganyika na watu kwa tabia nzuri na kuishi nao kwa msingi ya usawa na wema na hisani na kauli nzuri na maneno laini na upole na kauli nzuri na maneno laini na upole amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu. (kwa rehema za Mwenyezi Mungu umekuwa laini k w a o . N a l a u k a m a

ungelikuwa Mgumu na moyo wangekukimbia ulionao wasamehe na waombee msamaha na shuriana nao kat ika mambo) na amesema tena (na waambie watu wanene mazuri)

N a k u t o k a n a n a m u o n g o z o h u u wameishinao masahaba. M w e n y e z i M u n g u a w a r e h e m u n a w a l e w a l i o k u j a b a a d a y a masahaba kwa wema hadi siku ya kiama (mwisho) ukaenea uislamu kwa tabia zake na tabia za watu wake ambo wameulewa Uislamu vizuri wakaueneza Uislamu kwa hekima wema kwa kufanyia kazi maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu (lingania katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa wema)

Na ukaenea Uislamu kwa kufanyiana mambo mazuri watu wake kwa kufuata amri ya Mwenyezi Mungu isemayo ( Na kwa wazazi wawili uwafanyie wema na ndugu wa karibu na mayatima na majirani wa Dini moja na Majirani wa Dini nyingine na rafiki wa karibu na aliyeharibikiwa na safari) umeenea Kislamu kwa kutendea mambo kwa ukweli katika kuuza na

kununua nakuaminiana katka matendo mbali mbali.

N a k w a kutokudanganyana na k u d a n g a n y a n a k w a kufuata maneno ya Mtume (S.A.W) jilazimisheni na shikamaneni na ukweli na jiepusheni na uongo. Na umeenea Uislamu pia kwa kusamehe katita kuuza na kununua na kukopeshana kwa kuyafuata maneno y a m t u m e ( S . A . W ) ( M w e n y e z i M u n g u amsamehe mtu ambaye husamehe anapouza na anaponunua na husamehe anapokopesha)

U m e e n e a U i s l a m u k w a w a t u w a k e n a kuonekana maendeleo yao na utamaduni wao pale walipokuwa wanafunzi wakitafuta Elimu nautafiti na ufundi na biashara na kufanyakazi katika kila nyanja hadi ulimwengu wote unashuhudia juu ya maendeleo ya Uislamu. Na Uislamu wanajifunza elimu mbalimbali na wanatafsiri vitabu basi kwa Elimu na kufanyia kazi na tabia nzuri ndizo zinazoturudishia kwetu maendeleo na nguvu zake na utukufu wetu.

M w e n y e z i M u n g u ndiye muwezeshaji.

Page 10: ANNUUR 116

10 RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 5 - 7, 2012 AN-NUUR HABARI

KINACHODHIHI ni kwamba tangu asi l i na zama za Visiwa vya Waislamu, vya Unguja na Pemba, kumekuwapo na mpito wa mawimbi n a m i t i k i s i k o , n a unapochunguza utabaini sehemu kubwa imekuwa ikishawishiwa na watu, Wazalendo au hata nje yao, almuradi ni mamluki ama kwa jina la Vibaraka.

Usiulize tangu zama za utawala wa ukingoni wa Kisultani, hadi zile za Mfumo wa Chama Kushika Hatamu, hatimaye sasa wakati ambao tunaambiwa Demokrasia inakuwa, chini ya Mfumo wa Siasa za Vyama Vingi, pamoja na wakati huu Zanzibar ikitawaliwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Haya hayataki mwenge wala taa ya kumulika, bali kwa kila mwenye macho ya kuona mbali anabaini namna limbukeni na pia waliobebeshwa ajenda ya kuona daima Visiwa hivi vya Waungwana v i k i b a k i n y u m a y a shemere, mithili ya punda au ng’ombe aliyefungwa ujamu akifuata nyayo za mchunga wake hatua kwa hatua.

A m a w a z i w a z i tuungame, hiyo siyo hadhi ya watu waungwana wa Visiwa vya Unguja na Pemba, na Pwani yote ya Afrika Mashariki na kati, kwani asili yao si hiyo, bali waliheshimika kwa nuru na neema waliyopewa, ingawa hatimaye kutokana na h iz i changamoto tunazozijadili hapa hali yao ikawa si hali tena na heshima yao ikawa si lolote si chochote.

Historia ni shahidi kwamba Watawala wa Mwishoni tangu pale Sultani Ali bin Sayyid Said bin Sultani, mwanawe jabar i la Sul tani wa Awali, Sayyid Said bin Sultani, ambaye alikuwa kiboko wa Wazungu na Watawala wote wa Ulaya na Bara Arabu wa zama zake hata wakamuita „Said The Great“, tayari walishabebeshwa bendera ya Ajenda ya Wamagharibi na zaidi katika kulipa mwanya kanisa lianze k u j e n g a m i a n y a y a

Zanzibar na Changamoto ya vibarakaNa Mwandishi Maalum

fitna ndani ya himaya za Waislamu.

Ijapokuwa Sultani Ali a l iyekul ia Marekani , a l i l e t e w a M a n u w a r i y a K i h i s t o r i a h a p a ; waliomletea ni Wazungu wakiwamo Wajerumani na Wamarekani, ili aende Makka (Saudi Arabia) kutekeleza Ibada ya Hijja, ambayo ni Nguzo ya Tano ya Dini ya Kiislamu, matarajio yalikuwa kwamba akirejea aje kutekeleza muradi wa ukibaraka na umamluki, ndani ya Dola Huru ya Zanzibar, iliyoheshimika, hali ambayo asilan abadan, Babaye angelikuwako duniani asingeliridhia.

Tunajua hatimaye ajenda ziligeuza kibao Utawala na maslahi yakienda kwa

Wazungu, lakini matusi yakielekea kwa Waarabu na Masultani na hadi leo historia isiyokuwa historia inayanadi madhara yake.

Maana hapa utaambiwa Zanzibar ilipata Uhuru wake kutoka kwa Sultani, au zaidi ya Uongo kama huo, wakati ambapo haki ya Ulimwengu mzima inabaini kwamba hadi muda huo Watawala wa Kisultani walikuwapo kivuli tu au tuwaite chambao, na Nchi ikitawaliwa na Wazungu.

Tu n a c h o z u n g u m z a hapa ni watu wachache Wazalendo wa Zanzibar, au wengineo wanaoonekana tu kupita njia, na hatimaye w a k a a n g u k i w a n a dezo la madaraka, hata yale dhaifu, almuradi

wakatumikia maslahi ya upande mwingine, yawe ya kanisani au ya mataifa ya magharibi.

Ndani ya Zanzibar hadithi imebaki hiyo hiyo na kila mwenye macho, masikio, na akili ya kubaini haki na batili, anaelewa k w a m b a m w e n e n d o wa kuwaonjesha utamu wa madaraka baadhi ya Wazanzibari kwa malipo ya kuwashibisha machungu ya shubiri wananchi wote, ndiyo mchezo uliopo.

Usishangae kumuona Mzanzibar i amepewa f u r s a y a k u e n d e s h a hata gari ya mkokoteni, anavyoweza kubana meno na kuyakodoa macho yote, akisema „watakoma au tutawaonyesha.

Hutashangaa mwengine yeyote aliyeonjeshwa vijidaraka vya magwanda ijapokuwa yale wazee waliyokuwa wakiyaita ya papuliki, anavyoweza kula kiapo cha kumwaga damu au kupambana na umma wa Wazanzibari wenziwe, kwa gharama yoyote ya uhai.

Ni kweli shoka pekee isingeliweza kuiteketeza miti pasi na mashirikiano ya sehemu ya ile miti yenyewe, ambayo ni kama kwamba hatimaye ikawa ashadu ya kiama cha miti wenziwe, na huo ndio ubaya wa changamoto za umamluki au ukibaraka, unaoisibu Zanzibar na umma wake.

Zama zinashuhudia shari ya watu waliobeba dhana ya Kilemba cha Uongozi wa Waislamu, tena katika Taasisi za Umma za Kidini, walivyo tayari kuufifiliza Uislamu na Kuwatosa Waislamu wote na imani zao, kwa thamani tu ya soda ya kanisani au Tiketi ya Marekani.

W a p o a m b a o h a w a k u j i f i c h a , wakipita nyumba kwa nyumba, kuwashawishi Wazanzibari wasiunge mkono Maridhiano na pia wakatae Maoni ya kuja kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ambayo ingeliwapa ahuweni ya vipigo, mabomu ya machozi, kubakwa, na kuhujumiwa mali zao

bila sababu ya msingi. Hao walitekeleza muradi huo kwa ahadi ya kupewa utamu wa madaraka; na hatimaye wamepewa wapo madarakani ijapokuwa ya kueneza uongo; ndiyo maana mara tu baada ya taharuki ya hivi majuzi, walikuwa wa kwanza kuibuka na kuwaibulia Wazanzibari visingizio vya kila namna, ili kuwa salamu wanaowatumikia kwamba wameshawateke lezea wajibu.

U m m a u t a k u w a mashahidi wakati ule wa Kipindi cha Kipima Joto cha ITV, mwishoni mwa wiki, kilichoongozwa na Bw. Masako.

Wakati ambapo hata akina Mhe. Lissu na wenzake wakijaribu, kubainisha chanzo cha machafuko ya Zanzibar, wakisema tatizo si Uamsho wala Uchomaji wa Makanisa, ambayo ni viashiria vya kuwapo watu wachache tu wa kulaumiwa, bali vipo vyanzo vikiwamo Ukosefu wa Hikma kwa Dola, Jeshi la Polisi Zanzibar, na pia Sheria kandamizi, hasa zinazoambatana na ghilba ghilba hivi za kukabiliana na kile kinachotajwa kuwa ni Kero za Muungano; ndipo tulipoona pingamizi za pekee kutokana na hisia za ukibaraka na umamluki.

Haikushangaza kuona ujio wa ‘koti la kijani’ katika kipindi hicho, lakini yote hayo yalikuwa ni tisa, kumi ni pale ambapo m j u m b e w a k i p i n d i hicho, akiendeleza zile tunazosema ni Changamoto za ukibaraka na umamluki katika Zanzibar .

Ya a n i b i l a s h a k a Wa e n d e s h a k i p i n d i walimshangaa na kumtupia maswali ya kuthibitisha hoja zake zisizokuwa na kichwa wala miguu, ambazo hapo hazikuweza kuingia vichwani mwa wanaopendelea na hata wasiopendelea kusikia habari za Dola huru ya Zanzibar .

Kwa ujumla yatosha kuamini kuwa miongoni mwa yanayoidhoofisha azma ya Zanzibar kurejea katika hadhi yake, ni wachache walioonjeshwa ladha ya madaraka, na kwamba Nchi hii inateswa n a C h a n g a m o t o y a Vibaraka.

SHEIKH Abdallah Said Ally kutoka jumuiya ya UAMSHO Zanzibar.

Page 11: ANNUUR 116

11RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 5 - 7, 2012AN-NUUR SHAIRI/HABARI

Ndugu ulo mashakani, shaka ninakuondoa,Swali lako gazetini, jibu ninakupatia,Sensa TBC wani, nini wamekusudia,Ni dhuluma ya zamani, wamejihalalishia.

Ni mengi wanatamani, waweze kuyafikia,Kila kilicho nchini, iwe yao milkia, Umoja hawathamini, amani wala sheria,Haja yao kileleni, kwa hila uzushi pia.

Sensa iliyo na dini, hapa kwetu Tanzania,Iliishia sabini, nne bila kukosea,Idadi ya waumini, ‘lizidi asilimia,Kilotusibu ni nini, leo tuwe qalilia.

LengoTBC wani, sasa nakuelezea,Saidi wa Kiwalani, hili ndugu zingatia,Kama likuwa makini, siku chache baadia,Baraza ‘kawa hewani, Rais kalichagua.

Nia yao ‘mebaini, maswali kuyazuia,Wao wamezidi nini, nchi kujitawalia,Kuanzia Taifani, mikoa, wilaya pia.Ni dhuluma ya yaqini, bila shaka kutilia.

Nakuomba ikhiwani, nyuma kidogo rejea,Ile mbili ya tisini, nini walijifanyia,Mgao wa chinichini, ridhaa iso sheria, Chumo la serikalini, kanisa linalo shea.. Nashanga wahofu nini, data wakajipikia,Sera imeanza lini, wingi kuuzingatia,Kila kilichomo ndani, haki yao asilia,Wengine sote wageni, urithi wa malikia,

Ndugu yangu samahani, hapa ninaishilia,Ni mgeni kwenye fani, ila nimeingilia,Inanichoma moyoni, ndo mana nimeongea,Jibu kama si makini, wengine watalitoa.

Ally MtandeMUM-Morogoro.(0715-888360)

TAKWIMU YA SENSA (JIBU)

Tahamidi kwa Manani, Bwana wa ukamilifu,Mtukufu mwenye shani, asiye na upungufu,Japo moja nuksani, kwa mambo yake sufufu, RAJABU ni MTUKUFU, msojua tambueni. Ni yeye alobaini, mieziye iso zidifu,Ashara wa ithnani, idadiye kamilifu,I ndani ya QURAANI, TAUBA nenda kashufu, RAJABU ni MTUKUFU, msojua tambueni. Thathna sita ayani, arba mitakatifu,Ndipo utaibaini, yote kwa ukamilifu,Rajabu wa pili ndani, ya minne ile safu, RAJABU ni MTUKUFU, msojua tambueni. Adhimu yake thamani, zaidi ya maradufu,Aula tuuthamini, dhuluma si yake kufu,Ya ndanimwe tusikhini, tuyaenzi kwa insafu, RAJABU ni MTUKUFU, msojua tambueni. Maovu tuyaacheni, kwa ya Ilahi hawafu,Na mema tuzidisheni, katu yasije tukifu,Kesho yaje tuauni, baada ya wetu ufu, RAJABU ni MTUKUFU, msojua tambueni. Nimefika ukingoni, siwezi kujikalifu,Lengo kukumbusheni, mzidishe matukufu,Yatakayokufaeni, kesho mbele ya RAUFU, RAJABU ni MTUKUFU, msojua tambueni. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

KUMBE MWEZI MTUKUFU...!

‘Crusade’ imewadia ZanzibarInatoka Uk. 12ya Kiislamu iliyotapakaa damu nyingi ya roho na mali ya Waislamu ilipomwagwa katika mito ya Tigris na Euphrates nchini Iraki, hapo zamani; Vita na Hujuma katika Ardhi ya Mitune ya Palestina; Mauaji katika Mataifa ya Balkan; Mauaji ya hivi karibuni katika Mataifa ya Iraki, Afghanistan, Libya (na sasa Syria), Jimbo la Miandanao la Vietnamu; Uvamizi wa Somalia; Uchochezi wa Kuisambaratisha Jamhuri ya Sudan; pamoja na kile kinachoitwa Vita dhidi ya Ugaidi Duniani kupitia Visingizio vya Matukio ya Septemba 11, 2001, yaliyodaiwa kuongozwa na akina Osama bin Laden na kundi lake la Alqaeda.

Kufuatia mwenendo wenye kufanana wa utekelezaji wa hujuma hiyo dhidi ya Uislamu ndiyo maana hata ile Vita ya akina George Bush na wafuasi wake kuwamaliza Waislamu wa Iraq na Afghanistan tangu mwaka 1992 ilipewa jina la ‘Crusade’ ambapo Waislamu walibandikwa majina mbali mbal i pamoja na kesi za kubambikiziwa.

Hayo hayana tafauti yeyote na hali ilivyo sasa katika Ukanda wa Waislamu wa Afrika Mashariki na Kati na zaidi hali ilivyo sasa katika Visiwa vya Waislamu vya Unguja na Pemba ( Zanzibar ).

Kutokana na mwelekeo huo ambao tayari umma umebaini kuwa sasa ‘crusade’ imeshawasili Zanzibar , ni pamoja na yale yanayobainika kupitia midomo ya wenye mamlaka za utawala sambamba vipaza sauti vya mtandao wa vyombo vya habari, hasa vinavyoonekana kuwa sehemu ya harakati hiyo ya kihistoria dhidi ya Waislamu, Ulimwenguni juu ya namna wanavyoripoti na kugeuza pia kadiri siku zinavyokwenda kuhusiana na kile kilichojiri hivi karibuni kwa majina ya Machafuko ya Zanzibar, Vurugu za Zanzibar, au Uchomaji wa makanisa Zanzibar .

Pamoja na hayo pia mazingira yaliyopo sasa na hata kabla ya matukio hayo, ni wazi kwamba yanaashiria muda umetimu wa kutekeleza lengo hilo la muda mrefu na la makusudi kwa ule usemi kwamba ‘kamba hukatikia pabofu’, hali ambayo pia inawapa nafasi Waumini kuagua kwamba huu ni wakati wa ile ‘Dalili ya Kiama ya Mashud-Dajjaal’.

Hii ni kutokana pia na majina ambayo sasa Magazeti, Kanisa, na baadhi ya Viongozi, wamekuwa wakiyasogeza usoni mwa ‘crusade’, wakiwaita Waislamu, Viongozi wa Kiislamu, na hata Wakaazi wa Visiwa hivi kwamba ati ni ‘Wafuasi wa Alqaeda’, ‘Alshabaab’, au vinginevyo.

Hii tabaan ni pamoja na azma ya makusudi ya kuivuta hasira ya ‘crusade’ iwashukie Waislamu wa Zanzibar , ili kutekeleza lengo hilo .

Ta a r i f a z a h a l i h i y o zinathibitisha kutokana na ujio

wa moja kwa moja wa miongoni mwa Viongozi Waandamizi wa Bunge la Congress la Marekani na kushukia Ikulu za hapa nchini, kutokea New York, wakati ambao Viongozi Wakuu wa Kitaifa na wale wa Kanisa wakisikika wakitapika makaripio makali dhidi ya Waislamu na Viongozi wa Taasisi zao.

Mwenendo wa kuja kwa ‘crusade’ machoni mwa watu wenye upeo mkubwa wa harakati za kidiplomasia, ulibainika tangu pale Majeshi ya Marekani yalipokuja kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi, Zanzibar kwa Baraka zote za watawala wa Visiwani.

“Jamani Masheikh wetu waliyabaini haya kupitia ndotoni si mmoja si wawili si watatu umma ulielekea na utaendelea kuhiliki hapa kwa shari ya ‘crusade’, alisema Maalim Mussa kuwaambia Waislamu ili wachukue tahadhari, hivi karibuni, Mjini Zanzibar.

Pamoja na dalili hiyo, na kwamba Ukanda huu wa Afrika ya Mashariki ukizungukwa na Mameli ya Kivita kwa Visingizio mbali mbali vikiwamo vya Kukabiliana na Maharamia na pia Zoezi ati la Kumkamata Kiongozi wa Waasi wa Uganda Joseph Kony, pia bishara ya wazi ilikuwapo kwamba lazima Wazanzibari walishaelekea kutumia fursa ya kuyapinga yale ambayo hawakuyakubali katika Mswada wa Mwanzo

wa Marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo hadi sasa hatimaye, Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, haujayapitisha licha kuonekana kuja tena kinyemela, baada ya Bunge kuuvurumisha rasmi.

Pamoja na ishara hizo za ‘crusade’, huenda kwa mujibu wa uoni wa kitaalamu, majeshi na vikosi vyote vya ulinzi nchini, vilishajiweka tayari kwa kupiga au kulenga shabaha sambamba na mazoezi ya kivita ya kijeshi.

Hali hii ilionekana kuzidi hata ile ya maandalizi ya kijeshi nyakati za uchaguzi zama zile za Siasa za Chuki za Zanzibar .

Pia ujio wa sasa Majeshi ya Kivita nchini, yakiwemo ya Wanamaji kutoka nje ambao, kwa hapa Zanzibar wanaonekana wakiendesha mazoezi ya pamoja na baadhi ya vikosi vya ulinzi, kunazidi kuongeza shaka ya kuwadia kwa ‘crusade’, hususan kwamba harakati hiyo imekuja na maandalizi yake kabla ya hata hii fujo iliyopewa jina la Uamsho haijawadia.

Kwa mujibu wa dalili zote za ‘crusade’ hiyo, idadi kubwa ya Misikiti Ijumaa hii katika Maispaa ya Zanzibar , iliibuka na wito wa tahadhari kwa Waislamu, na pia kujitahidi kutumia hikma iwezekanavyo ikibainika kwamba tayari sasa maandalizi yote ya kuimaliza Nchi hii yametimia.

kutoka kwa Viongozi hao, ambazo ndiyo misimamo ya Serikali zao wanazoziongoza, kufuatia kile kilichoripotiwa kuwa Machafuko ya Zanzibar.

”Mbona wakubwa wamekuwa wakali namna hii au hawakuwapo wakati ule Kitabu Kitukufu cha Qur-an kilipochafuliwa“ alihoji Maalim Omar Haji wakati wa Mashauriano ya Waislamu katika Viwanja vya Msikiti wa Mbuyuni, mwanzoni mwa juma hili ambapo Waislamu walikaa kutafakari juu ya masaibu ya shari waliyoelekezewa sasa Wazanzibari kufuatia vurugu za hivi karibuni.

Walichohoji Waislamu ni kuona Maraisi wameibuka kwa kasi kubwa kama kwamba hazikuwahi kuwafikia taarifa za kuchomwa Misahafu na kupakwa kinyesi kwa makusudi, matukio ambayo kama siyo subra ya Waumini wa Nchi hii, ingelitosha kuyateketeza kila yanayomilikiwa na Dini nyingine, na kwa gharama yeyote ya kueleza hasira zao.

„ S i s i h a t u e l e w i h a w a wakubwa wetu wanayemkaripia ni nani na wanayemtetea ni nani almuradi wanakuwa wakali kwa mambo wasiyoyajuwa mwanzowe wala mwishowe“, ndivyo alivyoibuka Sheikh Suleiman katika Itkafu Maalum ya Masjid Afra iliyofanyika hivi karibuni Mjini Zanzibar.

K a t i k a k i l e a m b a c h o

w a m e k i b a i n i b a a d h i y a Wapembuzi wa Mambo ya Utawala na Kijamii ni kwamba haiwezekani ukali wa Watawala hao kukaripia na kuonya machafuko yaliyodaiwa ya kuchoma makanisa, bali ni kutokana na mang’ako kutoka kwa Wakubwa wa kanisa la Tanzania, ambao ghafla walikuja Zanzibar na kung’aka wakilaumu dola kwamba imekaa kimya na ati ilikuwa haijasema chochote mpaka muda huo.

„Nauliza mpaka Marais wetu wan’gakiwe na kanisa ndipo waibuke waonekane au ndiyo wameambiwa waseme’, alihoji Maalim Abdalla Haji, pale alipokuwa akichangia fikra ya hikma ya Waislamu juu ya kadhia ya hivi karibuni, pale Msikiti wa Darajani mara tu baada ya Swala ya Ijumaa iliyopita.

Walichoonekana kushauri wengi kati ya wadadisi wa mambo nchini, ni matumizi ya busara kwa kila upande wakiwamo Viongozi Wakuu pamoja na wa Vyombo vya Dola, juu ya kufuatilia kwa makini mfululizo wa matukio hayo, na pia namna yalivyobebwa na Vyombo vya Habari vya Kitaifa na vya Kimataifa, na zaidi vinavyolitumikia kanisa, katika kubaini asili na chanzo cha matukio ya namna hiyo, hasa wakati huu ambao Taifa linatafakari juu ya Mustakbali mpya, kupitia Marekebisho ya Katiba, yajayo.

Shein alikuwa wapiInatoka Uk. 12

Page 12: ANNUUR 116

RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 5 - 7, 2012

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagaration Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR Soma AN-NUUR

kila Ijumaa

‘Crusade’ imewadia ZanzibarWaislamu chonde chonde

ZIPO kila dalili kwamba shari imewadia ya kuikunjakunja na kuifikicha Zanzibar , na hatimaye kuitokomeza

Na Mwandishi Wetu kusikojulikana.Hii yasemekana ni katika

kutekeleza lile lengo lililobainika kuwapo tokea zamani.

Lengo hilo ambalo dalili zake zipo kwa muda mrefu na zimebainika, lina azma ya

kuhakikisha, madhali fursa imepatikana, kukomesha kila namna ya harakati za kuibua tena Zanzibar kutoka dahari ya udhalilifu na ukandamizaji, ikibidi zisiwezekane tena maishani.

‘Crusade’ maana yake ni hilaki dhidi ya kila walipo Waislamu duniani, ambako chimbuko lake tokea asili ni kumwaga damu, na kuuteketekeza Umma wa Kiislamu kwa namna yeyote, ikihusisha nguvu za pamoja za kanisa na Dola zinazotawala ulimwengu.

Harakati hiyo ilipamba moto tokea zama za kuangushwa Dola ya Kiislamu katika Mataifa ya Kostantania (Dola ya Othman) iliyodumu tangu zama za Maswahaba na Makhalifa Watukufu, katika ardhi ya Mataifa yanayotambulika sasa kwa majina Spain (Hispania) na Istambul (Uturuki).

Pamoja na hujuma kadhaa dhidi ya maisha na mali ya Waislamu, mbinu mbali mbali zimekuwa zikitumika zikiwamo za propaganda, visingizio, uzushi, na uchonganishi dhidi ya jamii za Kiislamu.

Yapo mengi yaliyojiri katika mwelekeo wa harakati hiyo kuanzia pale Hazina na Taaluma

FBI waanza Kazi Unguja?

Na Mwandishi Wetu

M I T A N D A O y a W a n a u s a l a m a w a K i m a t a i f a i m e a n z a harakati zao rasmi hapa nchini, na zaidi katika kubaini hali ya mambo ndani ya Visiwa vya Unguja na Pemba .

Baadhi ya wachunguzi wa mambo wanadai kuwa kumekuwepo kwa harakati za Mitandao hiyo kabla na baada ya kile kinachotajwa kuwa ni machafuko ya hivi karibuni yaliyoikumba Zanzibar .

K a t i k a m a d a i h a y o i n a t u h u m i w a k u w a makachero wanaodaiwa kupewa kazi ya kupambana na ugaidi duniani wakiwemo wale wa FBI, hivi sasa wanafuatilia kwa karibu kabisa taarifa na harakati za Viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu pamoja na zile za kijamii.

Macho ya Makachero hao yamekuwa yakiwaangazia zaidi Viongozi wa Jumuiya ya Maimamu ya Zanzibar (JUMAZA), Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI), sambamba na baadhi ya Waislamu wanaojengewa shaka kuwa na fungamano na harakati za taasisi hizo.

Harakati za makachero hao zinajumuisha upatikanaji wa taarifa muhimu za Viongozi wa Jumuiya na Taasisi hizo zikiwamo kumbukumbu zao za kihistoria ‘profiles’ na ‘CVs’, ambazo zinaelezwa k u w a n y e t i k a t i k a kubaini wapi pa kuanzia ili kukabiliana na ikibidi kufifiliza harakati.

Taarifa za Viongozi hao, zinazowindwa na Makachero z i n a g u s a z a i d i w a p i walipozaliwa, walipowahi kutembelea, walipojipatia elimu, ni zipi harakati zao za kikazi zikiwamo darsa za kitaaluma, na ni nani wanayesuhubiana naye kat ika mwenendo wao mzima wa kimaisha.

Shein alikuwa wapiQur-an ikinajisiwa?

Na Mwandishi WetuBAADHI ya Wananchi , wanaharakat i , wasomi , Waislamu, na hata Viongozi wa Vyama vya Siasa wameibuka na hoja nzito kwa Viongozi Wakuu wa Nchi hii, hasa

baada ya kile walichotaja kuwa ni busara inayohitajika kufuatia vurugu zilizotokea Zanzibar hivi karibuni.

Hoja za wenye kuhoj i zimewaelekea zaidi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete, na Rais wa Zanzibar

Dokta Ali Mohamed Shein. Hoja hizo zimekuja mara

tu baada ya umma kutafakari na kufuatilia kwa makini kile walichobaini kuwa ni kauli nzito za makaripio makali

Inaendelea Uk. 11 Inaendelea Uk. 11

Ustadh Juma Kitunga mkazi wa Morogoro aliyeelezwa kuwa ni mmoja wa waandamanaji katika vurugu za Zanzibar, akionyesha magazeti yaliyotoa picha yake akihusishwa na vurugu hizo, hali ya kuwa picha iliyochapishwa kwenye

magazeti hayo haihusisiani na tukio hilo. Habari kamili Uk. 1