Azimio La Tabora 2015

Embed Size (px)

Citation preview

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    1/88

     AZIMIO LA TABORA  

     Juu ya Siasa ya Ujamaa wa

    KiDemokrasia 

     Juni 2015

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    2/88

     AZIMIO LA TABORA 1 

     Juu ya Siasa ya Ujamaawa KiDemokrasia 

    Limetolewa na 

    HALMASHAURI KUU YACHAMA CHA ACT - WAZALENDO

     Juni 2015

    1 Linalohuisha Azimio la Arusha lililotolewa na Chama cha TANU mnamo mweziFebruari mwaka 1967 na kutangaza rasmi siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    3/88

    NDOTO YETU YA TANZANIA NI

    aifa lenye kujitegemea kiuchumi nakiutamaduni, na ambalo linalinda na kudumishausawa, ustawi wa jamii, uwajibikaji, demokrasia,na uongozi bora.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    4/88

     YALIYOMODIBAJI .….….….….….….….….….….….…. i

    SEHEMU YA KWANZA ….….….….….….…. 1

    1.1 Itikadi, Falsafa, Misingi na Madhumuni ya

     ACT-Wazalendo ….….….….….….…. 1

    SEHEMU YA PILI .….….….….….….…. 13

     2.1 Siasa ya Ujamaa wa kidemokrasia na ndoto ya Tanzania .….….….….….….….… 13

    SEHEMU YA TATU .….….….….….….…. 17 3.1 Hali ya nchi na Matamko ya kisera .… 17 

     3.1.1 Kumomonyoka kwa umoja na kukithirikwa rushwa na umaskini .….….….…17 

     3.1.2 Mfumo wa uchumi unaonyonya wanavijijini ….….….….….….….….….… 19 

     3.1.3 Tusisahau jambo hili, Azimio lilisema 26 

     3.1.4 Ufisadi unatengeneza makumi yamabilionea na kufukarisha mamilioni 28 

     3.2 Maono ya ACT-Wazalendo ….….….… 34 

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    5/88

     3.2.1 Kuweka Akiba (Savings) na Ukuaji waUchumi .….….….….….….….….…40 

     3.2.2 Kupambana na mfumo wa unyonyaji naufisadi ….….….….….….….….….… 44 

     3.2.3 Kilimo ….….….….….….….….….…47 

     3.2.4 Viwanda .….….….….….….….….… 51

     3.2.5 Utalii .….….….….….….….….….…53

     3.2.6 Madini, Mafuta na Gesi Asilia .….… 55 

     3.2.7 Hitimisho ….….….….….….….….… 57 

    SEHEMU YA NNE .….….….….….….…. 61

    4.1 Miiko ya Uongozi .….….….….….…61

    4.1.1 Miiko ya viongozi .….….….….….…61

    4.1.2 Tafsiri ya kiongozi .….….….….….… 63

    NYONGEZA .….….….….….….….….…. 64

    Hotuba ya kiongozi wa chama Ndugu Zitto

    Ruyagwa Z. Kabwe aliyoitoa katika uzinduzi waChama cha AC-Wazalendo siku ya Jumapilitarehe 29 Machi 2015 katika ukumbi waDiamond Jubilee, Dar es Salaam.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    6/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA i

    DIBAJIMnamo tarehe 26-28 Januari 1967, HalmashauriKuu ya ANU ilikutana Mjini Arusha. Pamojana mambo mengine, Mkutano huu ulipitisha

     Azimio la Arusha. Lengo la Azimio hilo lilikuwa

    ni kusimika misingi ya ujamaa yenye kuzingatiaudugu, umoja, uzalendo, uadilifu na uwajibikaji wa taasisi za umma. Ujamaa huu ulilenga kuujazaumma ujasiri wa kupambana na maadui wakuu

     watatu, yaani ujinga, maradhi na umaskini.

    Mapambano dhidi ya maadui tuliowataja hapo juu yalififishwa na viongozi wa kisiasa kwakushindwa kuhimili na kukabiliana na wimbila utandawazi lililokuja na imani ya soko hurialisilozingatia maslahi mapana ya jamii na umma.

     Aidha, viongozi wa kisiasa na umma kwa ujumla

     walitumia mwanya wa siasa za utandawazikujiimarisha katika maslahi binafsi dhidi yamaslahi ya umma na hivyo kuzima ndoto zaujenzi wa siasa na jamii ya kijamaa.

    Kwa sababu ya kuzikana siasa za ujamaa nakukumbatia siasa za kibepari, tena ubepari

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    7/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIAii

    uchwara unaosambaratisha mfumo wa jamiina kuvunja misingi ya utawala bora na sheria,mfumo wa ufisadi, rushwa na unyonyaji unazidi

    kujikita nchini mwetu. Kutokana na kutamalakikwa mfumo wa ufisadi, rushwa na unyonyanji,taifa limejikuta linazalisha matajiri wachachena mamilioni ya watanzania kuendelea kuwamafukara.

    Pamoja na kwamba nchi yetu imejaliwa rasilimalinyingi ambazo, raia wake kwa umoja waohawafaidiki na rasilimali hizi. Badala yake, uwepo

     wa rasilimali hizi umechochea migogoro kati yamakundi mbalimbali ya jamii yetu, ikiwemo

    migogoro kati ya wakulima na wafugaji; migogorokati ya wanaoitwa wawekezaji na wananchi nahata kati ya serikali na wananchi katika maeneo yauwekezaji. Mazingira haya yanachangia kuligawataifa, kulikata vipande vipande na kulinyang’anyaumoja na udugu uliojenga misingi ya taifa hili.

     AC – Wazalendo tunaamini kuwa taifa letulinahitaji kurejea katika misingi mama iliyojengataifa hili, ikiwemo misingi ya umoja, udugu,uzalendo, uadilifu na uwajibikaji wa viongozi nataasisi za umma.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    8/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA iii

    Hivyo basi, Azimio hili la abora linalengakuhuisha misingi mama ya aifa hili, ikiwemosiasa ya Ujamaa. Hata hivyo, kwa kutambua

    umuhimu wa demokrasia na haki za binadamukatika mazingira ya dunia ya leo, na kwa kuzingatiamapungufu ya msingi ya kisera katika utekelezaji

     wa toleo la kwanza la Azimio la Arusha, Azimiohili limezingatia, pamoja na mambo mengine,umuhimu wa demokrasia na mchango wa sektabinafsi katika maendeleo ya kijamii na kiuchumihapa nchini.

    Mama Anna Mghwira 

    Mwenyekiti wa AC – Wazalendo aifa 

     Juni 2015

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    9/88

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    10/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 1

    SEHEMU YA KWANZA 1.1 Itikadi, Falsafa, Misingi na

    Madhumuni ya ACT-Wazalendo

    Lengo kuu la siasa ya ujamaa wakidemokrasia ni kujenga jamii inayozingatiausawa. Ili kujenga jamii yenye kuzingatia nakuishi usawa, chama cha AC-Wazalendokitachukua hatua tatu mahsusi zifuatazo:

    i) Kuweka mazingira ya kiserayatakayohakikisha kwamba

    tunapunguza pengo la kipato kati yamtu na mtu, na kati ya jamii moja nanyingine.

    ii) Kuhakikisha kwamba kila mwananchianakuwa na fursa ya kupata huduma

    za jamii, ikiwemo elimu na afya 

    iii) Kuhakikisha kwamba wananchi wanakuwa na fursa kikamilifu zakushiriki katika kufanya maamuzi juuya mambo yanawagusa na kuwakabilibinafsi na jamii kwa ujumla.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    11/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA2

     Aidha, ujenzi wa siasa ya Ujamaa wakiDemokrasia utazingatia ngao nnezifuatazo:

    i) Udugu ni hifadhi ya jamii ya asili kwa Waafrika, na hivyo kila mtanzaniana kila mwafrika ana jukumu lakumsaidia mwenzake anayekabiliwana tatizo au janga popote alipo bila

    kutarajia malipo ya aina yoyote. AC-Wazalendo itahimiza wananchikushirikiana kidugu katika kukabilianana changamoto mbalimbali zakibinadamu, kijamii na kiuchumi

    na serikali itaweka mazingira yakufanikisha ushirikiano huo hususanikwamba kila mtu atakuwa na hakisawa ya kupata elimu bora bila malipoyeyote na afya bora kupitia mfumomadhubuti wa Hifadhi ya Jamii;

    ii) Serikali kusimamia maendeleo yanchi kwa kuwa na haki na wajibu wakuendesha moja kwa moja sekta nyetikatika jamii zenye maslahi mapanaya kiusalama na kiuchumi kwa nchi

    bila kuathiri nafasi ya sekta binafsi

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    12/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 3

    kuendesha shughuli za uzalishaji malina utoaji wa huduma;

    iii)  Viongozi na watumishi wa ummawana  wajibu wa kuhakikisha kwamba

     wanaishi na kuenenda katika misingiinayolinda heshima ya ofisi za ummana kwamba hawatumii nafasi zao kwamanufaa yao binafsi na jamaa zao. Ili

    kuwasaidia na kuwawezesha viongozina watumishi wa umma kuenendakatika misingi ya uadilifu, Miiko yaViongozi itakuwa ni kanuni ya lazimakufuatwa na kila mtu wenye dhamana

    ya umma.iv) Demokrasia   ndiyo msingi wa

    maendeleo ya kijamii, kiutamaduni,kiuchumi na kisiasa na kwambademokrasia ndiyo msingi wa ujenzi

     wa taifa huru na linaloheshimu nakuzingatia utawala wa sheria.

    Falsafa ya AC-Wazalendo ni UNYERERE,ikiwa ni dhamira ya kurudisha, kuhuishana kupigania misingi mama iliyoasisi aifa

    la anzania, kama ilivyoainishwa katika

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    13/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA4

     Azimio la Arusha ambalo lilipitishwa naHalmashauri Kuu ya ANU mwaka 1967na kama lilivyohuishwa na Chama cha

     AC-Wazalendo kwa mazingira ya anzaniaya sasa, ikiwa na imani kwamba:

    i) Binadamu wote ni sawa;

    ii) Kila mtu anastahili heshima;

    iii) Kila raia ana uhuru kamili wa kutoamawazo yake, kwenda anakotaka nakuamini dini anayotaka na kukutanana watu wengine bila kuvunja sheria;

    iv) Kila mtu ana haki ya kupata kutoka

    katika jamii hifadhi ya maisha yake namali yake aliyo nayo kwa mujibu washeria;

    v) Kila mtu anayo haki ya kupata malipoya haki kutokana na kazi yake;

    vi) Raia wote kwa pamoja wanamilikiutajiri wa asili wa nchi hii ukiwa kamadhamana kwa vizazi vyao na vizazivijavyo; na 

    vii) Serikali ina mamlaka na wajibu wa

    kusimamia njia muhimu za kukuzauchumi.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    14/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 5

     AC-Wazalendo itaongozwa na msingikumi ifuatayo:

    i) UzalendoSisi wananchi wa anzania tunaipenda nchiyetu. Uzalendo ndio moyo wa kuanzishwakwa AC-Wazalendo. Zaidi ya kuipendanchi yetu, uzalendo ni juu ya kile ambacho

    tunadhamiria kukifanya na kujitoa katikakuitumikia na kuilinda nchi yetu. Hivyobasi, ubora na umakini wa maamuzi yetukama chama utapimwa kwa kuangalia ninamna gani maamuzi hayo yana faida kwataifa letu na wananchi wake kwa leo na

    kesho.

    ii) Utu 

    Sambamba na Katiba ya nchi yetu naamko la Kimataifa la Haki za Binadamu

    ambalo nchi yetu imeliridhia, utu nimsingi mama kwa chama cha AC- Wazalendo. unatambua thamani ya asiliya ubinadamu na haki za msingi na zaasili ambazo binadamu wamepewa tanguuumbaji. unaamini kwamba utu ndio

    msingi wa uhuru, haki, amani na ustawi wa

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    15/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA6

     jamii. umedhamiria kupigania, kulinda nakuendeleza maendeleo ya jamii na ustawi

     wa watu wote na tutapigania na kuheshimu

    haki za kiuchumi, kisiasa, kijamii nakiutamaduni kwa watu wote.

    iii) Kupinga ubaguzi 

    Ubaguzi ni adui wa utu na tutaupinga

    kwa nguvu zote wakati wote na mahalapopote. unaamini kwamba kilabinadamu anastahili heshima na hastahilikubaguliwa kwa sababu ya kabila, rangi,

     jinsi, lugha, dini, chama cha siasa, utaifa,hali ya kiuchumi, familia anayotoka, afya,

    ulemavu, n.k. unaamini kwamba kila mtuanastahili kupata haki na kwamba maslahiya makundi yote lazima yazingatiwe katikautungaji wa sera na sheria. Kutokuwa naubaguzi ni msingi muhimu katika kujengautaifa na maendeleo shirikishi.

    iv) Usawa

    Kutokana na miaka mingi ya ubaguzi wakiuchumi na kijinsia, nchi yetu kwa sasainapita katika wakati ambao kuna pengo

    kubwa la kipato katika hali ya kimaisha na

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    16/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 7

    kijamii kati ya maskini, ambao ni kundikubwa, na matajiri wakiwakilishwa nakundi dogo. Bila kuchukua hatua stahiki

     wakati huu wa sasa basi maskini watazidikuwa maskini zaidi. Chama cha AC-

     Wazalendo kimeundwa katika msingi wakuamini kwamba kila mtu ana haki yakufurahia matunda ya bidii yake katikakazi, na kwamba bidii, umakini na weledikatika kazi ndiyo shina la maendeleo.unaamini kwamba tunahitaji kuhuishamisingi ya usawa kwa kuweka mazingirasawa na kuwekeza katika kundi la watuambao wameachwa nyuma na kunyimwa

    fursa za kujiendeleza. unaamini ni jukumuna wajibu wa serikali kuhakikisha usawakatika jamii kwa kuchukua hatua stahiki zakuwainua wale ambao wapo nje ya mstarina hawafaidiki na ukuaji wa uchumi wataifa.

    v) Demokrasia

    Msingi mama wa demokrasia ni kuhakikishakuwa sauti za watu zinasikika na kuzingatiwakatika mipango ya maendeleo ya nchi.

    unaamini kwamba ni wananchi pekee

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    17/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA8

     wenye uhalali wa kuamua nani awaongozena aina ya viongozi wanaowataka. Kamachama, kwetu dhana ya demokrasia

    inakwenda zaidi ya chaguzi za mara kwamara. Dhana ya demokrasia kwa chamacha AC-Wazalendo ni sehemu ya mfumo

     wa uendeshaji wa chama ambapo kilamwanachama anayo nafasi, wajibu na fursaya kuchangia katika maamuzi ya chama nanchi, na anayo haki ya kuomba kuchaguliwakatika ngazi yoyote ya uchaguzi.

    vi) Uhuru wa Mawazo na Matendo

     Jamii yoyote ya kidemokrasia inategemea

    uwepo wa uhuru wa kutofautiana kimawazona fursa ya kila mtu kutoa maoni yake bila

     woga. unaamini kwamba watu wanapaswakuwa na uhuru wa matendo ili mraditu matendo yao hayaingilii haki za watu

     wengine wala kuvunja sheria. unaaminikwamba ubunifu ni zao la mchango wamawazo tofauti kutoka kwa watu tofauti.Hivyo, chama kitalea na kuhamasishautamaduni wa uhuru wa mawazo kama njiaya kuendelea kujifunza njia bora zaidi za

    kuboresha maisha ya watanzania.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    18/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 9

    vii) Uadilifu 

    unaamini kwamba kura ni tendo la imani

    linaloonyeshwa na mwananchi kwa viongozianaowachagua. Uaminifu wa wananchiunapaswa kuheshimiwa kwa kuonyeshauadilifu wa hali ya juu kutoka kwa viongozi.Sisi kama chama tutasimamia uadilifu kwaumakini mkubwa kama njia muhimu ya

    kujenga imani na kuwapa heshima wale wanaotuamini katika kuwatumikia. Ilikuhakikisha kwamba tunatekeleza msingihuu kikamilifu, tumetengeneza kanuniza mwenendo wa maadili na miiko yauongozi ambayo kila kiongozi wa chama

    cha AC-Wazalendo na serikali itokanayoatasaini kukubali kuwa tayari kuwajibika nakuwajibishwa kwayo. Maadili na miiko yauongozi itakuwa ndiyo dira ya mwenendo

     wa viongozi wote wa chama cha AC- Wazalendo katika utumishi wa umma naambao tungependa umma wa watanzaniautuwajibishe nao.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    19/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA10

    viii) Uwazi 

    Ili wananchi waweze kuwawajibisha

    viongozi wao ni lazima wawe na taarifasahihi na kwa wakati unaofaa. unaaminikwamba wananchi wana haki ya kupatataarifa sahihi na kwa wakati kutoka kwaviongozi wao na ofisi zote za ummakwa kuwa viongozi wanafanya kazi na

    kusimamia raslimali za chama na taifa kwaniaba ya wananchi. Katika kutekeleza msingihuu, viongozi wote wa AC watapaswakueleza wanachama na wananchi kuhusumali wanazomiliki katika maeneo yao yauongozi, kabla na baada ya kuchaguliwa au

    kuteuliwa. Aidha, programu zote za chamapamoja na mapato na matumizi zitawekwa

     wazi kwa umma na wanachama na wananchi wataruhusiwa kuzikagua wakati wowote.

    ix) Uwajibikaji 

    Bila kujenga utamaduni wa kuwajibishanahatutaweza kama taifa kujenga jamiiambayo kila mtu anaheshimiwa nakuheshimu sheria ambazo tumejiwekea.Uwajibikaji unapaswa kuanza na viongozi

     waliopewa dhamana ya kuongoza harakati

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    20/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 11

    za mabadiliko katika nchi. Katika chamacha AC-Wazalendo, tunaamini kwambakila mtu anayetupigia kura ametuamini na

    kuweka matumaini yake kwetu kwambatunaweza kutekeleza kile tunachosema.unaamini pia kwamba wanachamana viongozi wanapaswa kuwajibishwakwa matendo na ahadi wanazozitoa kwa

     wananchi.

    x) Umoja

    Umoja ndiyo nyenzo muhimu ya kukabilianana changamoto ambazo zinatukabili leo nakesho. Kama nchi ambayo imejaliwa utajiri

    na tofauti za kijamii mbalimbali kama vileutamaduni, makabila, dini, lugha, na siasa,tunahitaji kusimama pamoja ili kuwezakujenga taifa moja la anzania ambalokila mmoja anafurahia kuwa sehemu yake.Kwa hiyo mapambano na shida za kundimoja ni mapambano na shida zetu sote.Kwa kuzingatia historia yetu ya kupiganiaumoja na maelewano katika bara la Afrikana duniani kwa ujumla, chama cha AC-

     Wazalendo kinatambua umuhimu wa

    umoja na ushirikiano na majirani zetu na

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    21/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA12

    hivyo itashirikiana na nchi nyingine katikakusukuma mbele ajenda ya Umoja wa

     Afrika ili kuweza kujenga nguvu za pamoja

    katika kujiendeleza kiuchumi, kiutamadunina kisiasa.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    22/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 13

    SEHEMU YA PILI2.1 Siasa ya Ujamaa wa kidemokrasia na

    ndoto ya Tanzania 

    anzania ni zaidi ya mkusanyiko wa watuna vitu vilivyomo. Msingi wa ujenzi waaifa ni UZALENDO unaochochewa naitikadi, falsafa na imani imara. Hata hivyo,katika siku za karibuni utaifa wa aifa laanzania umetikiswa. Nchi sasa imeanzakugeuka kuwa mkusanyiko tu wa watu

     wanaohangaika kutafuta vitu na ambao wanatumia muda mwingi kuimarisha‘vitaifa’ vyao kupitia vyama vyao vya siasa,dini zao na hata makabila yao. Hii inatokanana kukosekana kwa itikadi moja ya kitaifayenye kuweza kuunganisha makabila zaidi

    ya 124 yaliyopo nchini na wafuasi wa dinizote.

    Hivyo basi, chama cha AC-Wazalendokinalenga kuhuisha misingi iliyoimarishataifa na sera zake zitalenga kufufua

    uzalendo, upendo, umoja na mshikamano

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    23/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA14

     wa watanzania wote bila kujali rangi,kabila, dini, jinsia na wala ufuasi wa chamacha siasa. Chama cha AC-Wazalendo

    kinalenga kufufua utaifa wa anzania ilikila Mtanzania aone kuwa ana wajibu

     wa kujenga nchi yake ili kutimiza ndotoya kuwa na Taifa lenye kujitegemeakiuchumi na kiutamaduni, na ambalolinalinda na kudumisha usawa, ustawiwa jamii, uwajibikaji, demokrasia, nauongozi bora. 

    Ili ndoto hii itimie, ni sharti kuzingatiakwamba:

    i) Hakuna unyonyaji 

    Nchi yenye Ujamaa wa kidemokrasia hainaunyonyaji maana kila mtu huwajibikakufanya kazi na kupata malipo anayostahilikulingana na kazi yake. Katika Nchi

    ya aina ya ujamaa tunaotaka kujenga,Serikali kwa kupitia sera za kodi na seraza nchi hurekebisha tofauti ya kipato katiya walionacho na wasio nacho. Nchi yetuhivi sasa imekuwa na matabaka makubwakiasi kwamba wakulima, wafanyakazi,

     wavuvi, wafugaji na wafanyabiashara ndogo

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    24/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 15

    ndogo wananyonywa na watu wenye mitajimikubwa na wawekezaji wa nje. Ili kujengamfumo wa ujamaa wa kidemokrasia ni

    lazima kuondoa vikundi maslahi vyakinyonyaji (cartels) katika uchumi na

     wajibu huu ni wajibu wa Dola. Vile vileni lazima kuwezesha wananchi kufanyashughuli za uzalishaji mali kwa uhuru nabila bugudha kwa kuweka sera zinazozuia

     watu wa kati (middlemen) na kuhakikishaupatikanaji wa mitaji kwa wananchi wakawaida.

    ii) Uchumi imara, shirikishi na

    unaosimamiwa na dola Watawala walipoamua kulizika amko la Arusha na Azimio la Arusha walielekezataifa katika sera za kiliberali na kibwanyeyeambapo uchumi uliendeshwa na soko holela.Hii ilirejesha umiliki wa uchumi kwa watu

     wachache wenye mitaji. Viwanda, Mabenki,Njia za Usafirishaji, Bima, Biashara yandani na ya kigeni vyote vilimilikishwa kwa

     watu binafsi. Madhara yake ni kwamba watu wachache na hasa wageni wameshika

    uchumi wa nchi na wanafanya watakalo.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    25/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA16

     Wakati mwishoni mwa miaka ya sabini,anzania ilikuwa na uwezo wa kubanguakorosho zote zinazozalishwa nchini, hivi

    sasa korosho yote inauzwa nje ikiwa ghafina kukosesha aifa mapato mengi ya fedhaza kigeni. Mabenki yameshikwa na wagenina hivyo aifa kushindwa kusimamia serazake za fedha za kigeni ipasavyo.

    Namna pekee ya kujenga na kudumishaujamaa wa kidemokrasia ni kubomoa‘cartels’ na kuwezesha wananchi wengizaidi kumiliki uchumi kupitia Serikali yaoau vyama vyao vya ushirika na jumuiya

    za wananchi. Dola inapaswa kusimamiauchumi ipasavyo kwa kutunga sera zamakusudi zenye kuwezesha uzalishajimkubwa wa ndani. Vile vile iwe ni marufukukwa watu binafsi kumiliki miundombinukama barabara, reli, bandari, viwanja vya

    ndege, mifereji ya umwagiliaji, nguvu zaumeme, mkonga wa aifa na viwandamama kama vile chuma na makaa ya mawena visima vya mafuta na gesi. Watu namakampuni binafsi wanaweza kuhusikakwenye uendeshaji (operatorship) kwa

    makubaliano maalumu na Serikali.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    26/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 17

    SEHEMU YA TATU3.1 Hali ya nchi na Matamko ya kisera 

    3.1.1 Kumomonyoka kwa umoja na kukithirikwa rushwa na umaskini 

    Ni dhahiri kwamba nchi yetu hivi sasa inanyufa na hasa nyufa katika umoja wetuna kuporomoka kwa maadili. Udugu nautu unazidi kumomonyolewa. Leo hii,kwa mfano, ikitokea mtu amepata ajalibarabarani, badala ya watu kumsaidia,

     watu wengi humuongezea maumivukwa kumpora na kumnyang’anya vitualivyokuwa navyo. Huko nyuma jamiinzima iliweza kuwajibika kumlea mtotoyeyote popote alipo, lakini leo anzaniainazalisha watoto wa mitaani kila siku kwakuwa tu hawana wazazi wa kubailojia au

     wazazi waliopo hawana uwezo wa kiuchumi wa kuwatunza. Undugu na udugu umefifiana uko hatarini kutoweka.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    27/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA18

    Hatuamini tena kwamba mafanikiohutokana na kujitegemea na bidii katikakazi. umegeuka kuwa taifa la ombaomba

    na kuishi kwa ujanjaujanja. Wezi wa mali zaumma wanasifiwa na kuchekewa. Uongozina utumishi wa umma umekuwa ndiyo njiaya kujipatia utajiri badala ya kutumikia

     wananchi. Uongozi na utumishi wa ummaumegeuka kuwa tiketi ya kujitajirishakupitia kujilipa posho kubwa na mishaharamikubwa na stahili kadha wa kadha bilakujali hali ya nchi yetu kiuchumi. AC-

     Wazalendo tunasema hali hii haikubalikina lazima turudi katika misingi!

    anzania hivi sasa ni moja ya nchi masikinizaidi duniani licha ya utajiri mkubwa

     wa watu, maliasili na eneo la kijiografia.akwimu za maendeleo ya binadamuzinaonyesha kuwa anzania ni nchi ya

    159 kwa umasikini kati ya nchi 187duniani. AC-Wazalendo tunasema hali hii haikubaliki!

    Baadhi ya wanazuoni wamewagawa Watanzania katika madaraja matatu:

     Walalahoi, Walalaheri na Walalahai

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    28/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 19

     wakimaanisha watu wenye kuishi kwenyedimbwi la umasikini, watu wenye ahuenina matajiri. Pia kuna daraja jipya la

    ‘wakeshahoi’. Hawa wa mwisho ndio hao wanaitwa ‘masikini wa kutupwa’ kwalugha ya mtaani. Watanzania ni masikinikwa sababu watawala wetu wameamuahivyo kwa kutunga na kutekeleza serana mikakati ambayo inanufaisha watu

     wachache katika tabaka la juu la maishaambao wengi wanaishi mijini na kuacha

     watu wengi wanaoishi vijijini wakiwamasikini zaidi. AC-Wazalendo tunasemahali hii haikubaliki na lazima turudi

    katika msingi wa kukifanya kila kijijikuwa kitovu cha maendeleo ya taifa!

    3.1.2 Mfumo wa uchumi unaonyonyawananchi vijijini

    Mfumo wa uchumi wa nchi yetu bado ni

     wa kinyonyaji. Kwamba wakazi wa mijini wanafaidi zaidi rasilimali za nchi kuliko wakazi wa vijijini. Mfumo wa uchumi wa anzania ni wa kifisadi na ufisadiunafaidisha kikundi kidogo cha watumijini au wenye tabia za kimjini na hivyo

    kukosesha huduma za msingi za wananchi

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    29/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA20

     wengi waishio vijijini. azama mifano hiihapa chini:

    • Kuongezeka kwa kasi kwa tofautiya kipato kati ya walionacho na

     wasionacho ambapo sasa kunakundi dogo la watu matajiri sana nakundi kubwa sana ni la watu fukarasana. akwimu zinaonyesha kuwa

    asilimia 30 ya Watanzania wanamilikiasilimia 75 ya Pato la aifa. Kwakutumia vigezo mbalimbali vyakupima kiwango cha Umasikini (MPI2013), asilimia 64 ya Watanzania ni

    masikini na asilimia 31.3 wanaishikatika umasikini uliokithiri. Kwahiyo ni asilimia takribani tano (5%)ya watanzania ndiyo wenye maishaahueni au matajiri.

    • Kasi ya kupunguza umasikini nchiniinaonekana mijini kuliko vijijiniambapo katika kipindi cha miaka16, umasikini wa watu wa Dar esSalaam, kwa mfano, umepungua kwaasilimia 12 wakati umasikini vijijini

    umepungua kwa asilimia 2 tu. Ripoti

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    30/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 21

    ya Maendeleo ya Binadamu ya aifaya Mwaka 2014 kuhusu anzaniainaonyesha kuwa Watanzania masikini

    zaidi wanaishi mikoa ya Kigoma,Singida, Dodoma, Kagera, abora,Shinyanga na Pwani.

    • Kasi ya ukuaji wa uchumi wa vijijiniipo chini ya wastani wa ukuaji wa

    uchumi wa aifa kutokana na sekta yakilimo, ambayo inaajiri asilimia 75 ya

     Watanzania, kuwa na ukuaji mdogomno wa asilimia 4 wakati uchumi wanchi umekuwa ukikua kwa wastani

     wa asilimia 7 katika muongo mmojauliopita. Asilimia 67 ya kaya nchinikwetu zinaishi katika makazi yenyesakafu za udongo, mchanga au kinyesicha ng’ombe. Asilimia 63 ya kaya zaanzania hazipati maji ya bomba.

    Hali hii inasababishwa na ukweli kwambafursa nyingi za kiuchumi na maendeleokwa ujumla zimekuwa zikitolewa kwa watu

     wa mijini zaidi kuliko vijijini na kwambamfumo wetu wa maendeleo ya uchumi na

    kijamii umewanyima fursa watu waliopo

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    31/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA22

    vijijini. Hali hii ilijitokeza pia wakati Azimio la Arusha linapitishwa mwaka 1967pale ambapo Mwalimu Nyerere alisema,

    tunanukuu:

    “Vile vile mkazo wa fedha na wa viwandaunatufanya tukazanie zaidi maendeleo yamijini. Tunatambua kuwa hatuwezi kupata

     fedha za kutosha kuleta maendeleo katika kila

    kijiji na ambayo yatamfaa kila mwananchi.Tunajua pia kuwa hatuwezi kujenga kiwandakatika kila kijiji ili kisaidie kuleta maendeleo

     ya fedha na viwanda katika kila kijiji; jamboambalo tunajua kuwa haliwezekani. Kwa

    ajili hiyo, basi, fedha zetu huzitumia zaidikatika miji na viwanda vyetu pia hujengwakatika miji. Na zaidi ya fedha hizi huwa nimikopo na hatimaye lazima zilipwe.

    Lakini ni dhahiri kwamba haziwezi kulipwa

    kwa fedha zinazotokana na maendeleo yamijini au maendeleo ya viwanda. Hazinabudi zilipwe kwa fedha tunazopata kutokanana vitu tunavyouza katika nchi za nje.Kutokana na viwanda vyetu hatuuzi na kwamuda mrefu sana hatutauza vitu vingi katika

    nchi za nje. Viwanda vyetu zaidi ni vya

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    32/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 23

    kutusaidia kupata vitu hapa hapa ambavyompaka sasa tunaviagiza kutoka nchi zanje. Itapita miaka mingi kabla ya kuweza

    kuuza katika nchi za nje vitu vinavyotokanana viwanda vyetu. Kwa hiyo ni dhahirikwamba fedha tutakazotumia kulipa madenihaya ya mikopo ya fedha kwa maendeleo naviwanda mijini hazitatoka mijini na walahazitatokana na viwanda. Zitatoka wapi,basi? Zitatoka vijijini na zitatokana naKILIMO. Maana ya ukweli huu ni nini?Ni kwamba wale wanaofaidi maendeleo

     yanayotokana na fedha tunazokopa sio kwakweli watakaozilipa. Fedha zitatumika zaidi

    katika miji lakini walipaji watakuwa zaidini wakulima.

     Jambo hili linafaa kukumbukwa sana, maanakuna njia nyingi za kunyonyana. Tusisahauhata kidogo kwamba wakaaji wa mijini

    wanaweza wakawa wanyonyaji wa jasho lawakulima wa vijijini. Hospitali zetu kubwazote ziko katika miji. Zinafaidia sehemundogo sana ya wananchi wa Tanzania. Lakinikama tumezijenga kwa fedha za mkopowalipaji wa mkopo huo ni wakulima, yaani

    wale ambao hawafaidiwi sana na hospitali

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    33/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA24

    hizo. Mabarabara ya lami yako katika miji,kwa faida ya wakaaji wa mijini na hasawenye magari. Kama mabarabaraba hayo

    tumeyajenga kwa fedha za mikopo walipajini wakulima; na fedha zilizonunua magari

     yenyewe zilitokana na mazao ya wakulima.Taa za umeme, maji ya mabomba, mahotelina maendeleo mengine yote ya kisasa yakozaidi katika miji. Karibu yote yametokana na

     fedha za mikopo na karibu yote hayana faidakubwa kwa mkulima, lakini yatalipwa kwa

     fedha zitakazotokana na jasho la mkulima.

    Tusisahau jambo hili. Japo tunapotaja

    unyonyaji hufikiria mabepari, tusisahaukuwa bahari ina samaki wengi. Naohutafunana. Mkubwa humtafuna mdogo namdogo naye humtafuna mdogo zaidi. Katikanchi yetu twaweza kugawa wananchi kwanjia mbili. Mabepari na Makabaila upande

    mmoja; na wafanyakazi na wakulima upandemwingine. Pia twaweza tukagawa wakaajiwa mijini upande mmoja na wakulima wavijijini upande mwingine. Tusipoangaliatutakuja kugundua kuwa wakaaji wa mijininao ni wanyonyaji wa wakulima.” Azimio la

     Arusha,1967. (msisitizo ni wetu).

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    34/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 25

     Azimio la Arusha limerudia zaidi ya maramoja “usisahau jambo hili” ama “Jambohili linapaswa kukumbukwa sana”. Ni

    dhahiri kuwa tumesahau jambo hili nahivyo maendeleo vijijini kuwa ni hadithi tuza wanasiasa.

    Licha ya kwamba wanasiasa wa kisasa wanaona Azimio la Arusha ni nyaraka

    iliyopitwa na wakati, sisi AC-Wazalendotunaamini kwamba maana ya kurudi katikamisingi ni kurudi katika misingi ya Azimiola Arusha. Mwangwi wa “tusisahau jambohili” lazima uendelee kutuonyesha kuwa

    kuna kazi ya kufanya kuhusu mafukaramamilioni wanaoishi kwenye vijiji vyetu. Watanzania hawa wa vijijini hawana fursa zabarabara, maji, umeme na hata huduma za

     jamii kama wenzao wa mijini. Kwa mfano,aarifa ya aifa ya Maendeleo ya Binadamu

    ya Mwaka 2014 inaonyesha kwambani asilimia 8 tu ya kaya za vijijini zenyeumeme kwa ajili ya mwanga, wakati mijinini asilimia 49. AC –Wazalendo tunasemahili halikubaliki na lazima turudi katikamisingi!

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    35/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA26

    Ukiangalia Bajeti ya nchi yetu anzaniahivi sasa utaona namna ambavyo rasilimalikubwa ya nchi inatumika kutatua

    changamoto za watu wa mijini na hasaDar es Salaam. Wabunge (ambao wengi

     wanatumia muda mwingi sana Dar esSalaam) bila kujali majimbo au mikoa yaohukasirikia sana, kwa mfano, foleni Dares Salaam na kuisukuma Serikali kutengafedha zaidi za kujenga barabara za Dar esSalaam. Umeme ukikatika Dar es Salaam,

     waandishi wa habari wanaandika ‘nchigizani’ bila kujali kuwa Watanzania waUrughu kule Iramba na wengine asilimia

    92 ya Watanzania wapo kwenye gizala kudumu. Zaidi ya fursa walizonazo,masikini wa mijini pia sauti zao zinasikika.Mafukara wa vijijini nadra kuwasikia nahuishia tu kukugumia shida zao.

    3.1.3 Tusisahau jambo hili, Azimio lilisemaMasikini wanaoishi vijijini licha ya kufanyakazi kwa bidii na hasa kazi za kilimohawana fursa za kuondokana na umasikini.Mfumo wa uchumi wa nchi umejengwa

    kwa misingi kwamba watu wa vijijini

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    36/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 27

    hupokea bei za kuuza mazao yao kutokamijini na vilevile hupokea bei za kununuabidhaa zinazotengenezwa mijini kutoka

    huko huko. Mkulima wa Peramiho huuzamahindi yake kwa bei ya kijijini iliyo chini(tena kwa mkopo) na anapotaka kununuasukari hulipa bei kubwa kuliko hata bei yaSongea Mjini.

    Barabara za vijijini zina hali mbaya auhazipo kabisa. Huduma za jamii kamaelimu, maji na afya ni mbaya. Hudumaza nishati ya umeme hazipo kabisa katikanyumba 92 kati ya 100 za vijijini hapa

    nchini. Masikini wa vijijini ni mafukara. Wamefukarishwa kutokana na serazinazonyonya jasho la kazi yao kwa upandemmoja na sera zinazowanyima maendeleoya miundombinu kwa upande mwingine.

    Kufunguliwa kwa miundombinu ya vijijinikama barabara, maji na nishati ya umemekunaweza kuwaondoa watu wa vijijinikwenye minyororo ya ufukara. Hudumabora za elimu, afya na uhakika wa masokoya mazao na hifadhi ya jamii vinaweza

    hatimaye kutokomeza kabisa umaskini.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    37/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA28

    Lakini, watawala wanaogawa rasilimali yanchi hawataki. Wanasema hakuna rasilimalifedha za kutosha kusambaza umeme

    vijijini ili kukuza viwanda vidogo vidogona kuongeza thamani ya mazao ya kilimo,kusambaza maji safi na salama ili kuboreshaafya na kumpunguzia mwanamke wakijijini muda wa kutafuta maji na kujengabarabara za vijijini ili wakulima wafikishemazao yao sokoni. Ikifika kujenga shulena zahanati na vituo vya afya, wananchi

     wa vijijini wanaambiwa wajenge wenyewe, wajitolee. AC-Wazalendo tunasema halihii haikubaliki na lazima turudi katika

    misingi!

    3.1.4 Ufisadi unatengeneza makumi yamabilionea na kufukarisha mamilioni 

    Kwa vipindi tofauti katika miaka yakaribuni, Bunge la Jamhuri ya Muungano

     wa anzania limekuwa likiibua kashfambalimbali zinazoonesha namna ambavyofedha za nchi zinavyoibwa na wachache.umeshuhudia, kwa mfano:

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    38/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 29

    • Ufisadi uliofanywa Benki Kuu yaanzania kwa kuibwa kwa zaidi yashilingi bilioni 133 za Akaunti ya

    Malipo ya Nje (EPA),

    • Utoroshaji mkubwa wa fedhazilizofikia dola za Kimarekani milioni136 kupitia mradi wa Meremetauliokuwa chini ya Jeshi la Wananchi

     wa anzania (PDF),

    • Uingiaji wa mkataba wa madiniya dhahabu wa Buzwagi uliokuwana thamani ya dola za Kimarekanimilioni 400 bila kuzingatia uhitaji wakuboresha mazingira ya nchi kufaidikana utajiri wa madini; na

    • Wizi mkubwa wa fedha za msaada wa kuagiza bidhaa kutoka Serikali ya

     Japan (Commodity Import Support)ambapo zaidi za shilingi bilioni 40ziligawiwa kwa viongozi kadhaa waserikali na wafanyabiashara.

    • Kashfa kubwa ya Mkataba wa Umeme

     wa Richmond ambayo ilipelekea nchi

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    39/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA30

    kukaa gizani kwa muda mrefu nakuzorotesha shughuli za uzalishajimali na kuathiri uchumi.

    • Kashfa kubwa sana ya egeta Escrow Account ambapo zaidi ya shilingibilioni 306 zilichotwa kutoka BenkiKuu ya anzania.

    • aarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuendeleakuonyesha namna ubadhirifuulivyokithiri katika matumizi yafedha za Umma. akribani asilimia 30ya bajeti kwenye manunuzi ya ummahuishia kwenye mikono ya watu

     wachache.

    • Kashfa kubwa ya Watanzania wanaoficha fedha katika benki za

    nje ya nchi ambapo Benki Kuuya Shirikisho la Uswisi ilitangazakwamba Watanzania wamehifadhizaidi ya shilingi bilioni 334 katikafedha za kigeni kwenye mabenki yanchi hiyo.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    40/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 31

    Katika Kitabu cha ‘Africa’s Odious debts: Howforeign loans and capital flight bled a continent’,

     waandishi Leonce Ndikumana na James Boyce,

     wameonyesha kwamba katika kipindi chamiaka 40 jumla ya dola za Kimarekani 11.4bilioni zimetoroshwa kutoka anzania kwa njiambalimbali. Hizi ni sawa na wastani wa dola zaKimarekani 285 milioni kutoroshwa kila mwakakuanzia mwaka 1970 mpaka 2010. Sehemukubwa ya fedha hizi zinatoroshwa na makampunimakubwa ya kigeni yanayofanya biashara nakuwekeza hapa nchini (utoroshaji mkubwaumefanyika mara baada ya anzania kuanzakuzalisha dhahabu kwa wingi na makampuni

    makubwa ya nje kuanza kutafuta mafuta na gesiasilia kwenye bahari ya anzania) na sehemunyingine ni bakshishi wanayopewa viongozi namaafisa wa serikali wanaofanikisha utoroshajihuu.

    Utafiti uliofanywa na Africa Progress Panel nakikosi kazi kilichoongozwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Bwana Tabo Mbeki unaonyeshakuwa Afrika hupoteza zaidi ya dola za kimarekani50 bilioni kila mwaka kutokana na utoroshajiunaofanywa na makundi haya. Huu ni mtaji

    mkubwa unaotumika na mataifa ya magharibi

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    41/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA32

    kuendeleza nchi zao na kuendelea kuzinyonya nchiza Kiafrika. Makampuni makubwa ya kimataifakwa kushirikiana na wananchi hutorosha fedha

    hizi na kulikosesha bara la Afrika na anzaniachanzo kikubwa cha mitaji katika soko la mitaji.

     Watanzania hawa (wanasiasa, watendaji, maafisa wa Jeshi na Usalama wa aifa na wafanyabiashara)huficha fedha hizi chafu kwenye mabenki

    ughaibuni na hasa Uswisi, Dubai, Mauritius, Afrika Kusini na maeneo mengine (ax Havens/Offshore/reasure Islands). Wengine wamewekezakwenye mali zisizohamishika kama majumba nazinazohamishika kama hisa kwenye makampuni

    mbalimbali duniani.Rushwa na ufisadi vinatengeneza Watanzania

     wachache kuwa mabilionea. Mabilionea hawaambao wana ushawishi mkubwa katika kuundasera za nchi na utekelezaji wake wanasababisha

    kuundwa kwa sera na sheria zinazolinda utajiri wa walionacho na kuendelea kuhakikisha maskini wanaendelea kuwa mafukara.

    Rasilimali za nchi zinaboresha maeneo ambayomabilionea na wasaidizi wao wanaishi na kusahau

    kabisa kwamba Watanzania wengi wanaishi vijijini

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    42/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 33

    na huko ndiko kuna umaskini mkubwa. Umaskini wa vijijini kwa kiasi kikubwa unatokana na serana matendo yanayofukarisha wananchi wengi.

    Ukuaji wa uchumi unaoambatana na ufisadi wakiwango kinachotokea anzania unawafanya

     wenye nacho kupata zaidi na masikini kuwamafukara zaidi. AC-Wazalendo tunasema hilihalikubaliki na lazima turudi katika misingi!

    unaweza kujenga taifa la watu sawa kwa kufanyamaamuzi ya kubomoa mfumo wa kiuchumi wakinyonyaji ambao umejengwa tangu kupatauhuru. Juhudi za kujenga taifa lenye watu sawaziliyeyuka mara baada ya kuamua kutelekeza

     Azimio la Arusha na kufuata sera za ubinafsishajiambapo zilitafsiriwa kwa kukabidhi mali za taifakwa kundi dogo la watu na hivyo kutengenezamfumo wa kifisadi ambao sasa umeota mizizi.Kazi iliyofanywa kwa miaka ishirini ya kujengauchumi wa viwanda ziliyeyushwa katika kipindi

    cha miaka mitano tu ambapo viwanda vyoteviligawanywa kwa watu binafsi na vingi leo nimaghala tu ya kuhifadhia bidhaa nyingine.

    Kutochukua maamuzi madhubuti ya kutokomezaufisadi na mfumo wake ni kufukarisha Watanzania

    kwa sababu rasilimali ambayo inapotea kupitia

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    43/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA34

    vitendo vya kifisadi ingeweza kuwekezwa katikamaendeleo ya watu wa vijijini, kwa kukuzashughuli za kiuchumi na kupanua mapato ya

     wananchi.

    3.2 Maono ya ACT-Wazalendo

     Jambo moja la msingi la kuzingatiatunapohuisha Azimio la Arusha ni kwamba

    mazingira yamebadilika. Mwalimu Nyererena wenzake walifanya tathmini ya hali yakipindi ambacho aifa lilitegemea sanamazao ya kilimo kwenye mauzo ya nje.Ndio maana mara kadhaa MwalimuNyerere alipata kusema ‘tunanunua trekta

    moja kwa tani 15 za chai’ akilinganishaurari wa biashara kati ya tunachouza nje natunachonunua kutoka nje. Hivi sasa haliimebadilika na hivyo Azimio lililohuishwani vema lizingatie muundo wa sasa wakiuchumi na kuufanyia mageuzi makubwa(transformation) ili kujenga uchumishirikishi (inclusive economy).

    Ni muhimu kuwa tayari kubadilikakulingana na mabadiliko katika dunia nanchini kwetu. Ujamaa wa kiDemokrasia

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    44/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 35

    wenye kuelekea kujenga dola lakimaendeleo (developmental state) nawenye kuzingatia mila na utamaduni wa

    kitanzania ndio njia tunayopaswa kwendahivi sasa. Swali muhimu la kujiuliza wakati

     wote ni kama njia tunayochukua itajibuchangamoto zetu za Maendeleo? ukishachagua njia tunayotaka ni lazima tuwe naimani thabiti kwa njia hiyo na kuhakikishakuwa maamuzi yetu yanatokana na ukwelina ukweli huo lazima ujaribiwe kwa vitendo.Hatuna budi kubomoa mfumo uliopo sasana kujenga mfumo madhubuti utakaokuwanjia ya msingi tuliyochagua kwa ajili ya

    kujenga Dola la Kimaendeleo ili kutimizandoto yetu.

    Mazingira ya sasa yanataka sekta binafsikushiriki kikamilifu katika kuendeshauchumi na Serikali kusimamia na kudhibiti

    njia kuu za uchumi na kuendesha hudumaza msingi kama Elimu na Afya, Maji,Umeme na miundombinu.

     Azimio la Arusha lilitafsiri kuwa ujasiriamali(entrepreneurship) ni unyonyaji; Kwamba

    mtu mwenye kiwanda akifanyiwa kazi na

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    45/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA36

     watu aliowaajiri ni mnyonyaji; Kwambamtu mwenye shamba akilimiwa na vibaruaaliowaajiri ni mnyonyaji. Kwa AC –

     Wazalendo, unyonyaji ni kutompa mtu ujirastahiki kulingana na kazi yake. Uchumi nilazima uwe na watu wanaofikiria na kubunishughuli za uzalishaji na walipwe kulinganana ujasiriamali wao bila ya kunyonywakwa kazi zao. Kama ambavyo nguvu kazi(labour force) hulipwa kwa mshahara, mtajihulipwa kwa riba na ardhi hulipwa kwatozo (rent), ndivyo ujasiriamali hulipwakwa faida. Ni wajibu wa Dola kudhibitiulimbikaji wa mali kupitia mfumo wa kodi

    kama ilivyo kwa nchi za Skandinavia siokuzuia wajasiriamali kubuni biashara nakupata faida (reward) kulingana na ubunifuna usimamizi wa biashara zao.

    Mazingira ya sasa ya nchi kama Tanzania

     yanataka ongezeko la uzalishaji mali natija katika uzalishaji ili kuongeza uwezowa Taifa kuhudumia wananchi wake.Mazingira ya sasa yanahitaji kujengauwezo mkubwa wa kujiwekea akiba ilikuhimiza ukuzaji wa mitaji ya ndani

    ili kuongeza uwezo wa kuzalisha mali,

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    46/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 37

    ubunifu na maendeleo ya teknolojia.Mazingira ya sasa sio ya kutaifishana kubinafsisha kila kitu, bali ni ya

    kumilikisha wananchi uchumi wao nakuuondoa kwenye mikono ya wachache.anzania ya sasa inataka soko la mitajikumilikiwa na wananchi wengi kwa msaada

     wa dola. Ni vema kuzingatia jambo hilikila wakati tunapohuisha Azimio la Arusha.

     Jambo jingine ni kwamba Azimiolililohuishwa lazima lizingatie uzalishajimali badala ya kujikita kwenye mgawanyo

     wa kidogo kilichozalishwa. Mwaka

    1977 Mwalimu Nyerere alisema “Kwamiaka kumi tumefanya vizuri sana katikakusambaza huduma za msingi za kijamiikwa watu wengi vijijini. Bado kuna kazizaidi ya kufanya; lakini tunaweza kufanyahivyo iwapo tu tutazalisha zaidi mali.

    Hatujaweza kufanya hivyo”.

    Mwaka 1967 sekta ya Kilimo (ikiwemouwindaji, ufugaji na misitu) ilikuwainachangia 80% ya Pato la aifa (GDP),viwanda na huduma vilichangia kiwango

    kilichobakia. Kipindi hicho zao moja tu

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    47/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA38

    la Mkonge lilikuwa linaingiza takribanitheluthi mbili ya fedha za kigeni kutokanana mauzo ya nje ya nchi.

    Mwaka 2014 sekta za kilimo na viwandavimechangia 50% ya Pato la aifa (Kilimo26%, Viwanda 24%), wakati sekta yahuduma inachangia nusu iliyobakia.Mapato ya fedha za kigeni yanachangiwa

    na utalii kwa zaidi ya dola za kimarekanibilioni mbili, viwanda dola bilioni mojana nusu na dhahabu dola bilioni moja namilioni mia mbili. Biashara ya bandari(transit trade) inaingiza fedha nyingi zaidi

    za kigeni kuliko mazao yote ya kilimoambayo yanaingiza dola milioni mia sabatu.

    Changamoto kubwa ya anzania nikutokubadilika kimaendeleo kwa sekta ya

    kilimo wakati bado inaajiri watu wengi sananchini. Hiki ndicho kiini cha umasikini waanzania. Azimio la Arusha linalohuishwalazima lijibu changamoto hii kwa kuelekezauundwaji wa sera zitakazoongeza uzalishajinchini kwenye sekta zote na maradufu

    kwenye sekta ya kilimo na viwanda vya

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    48/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 39

    bidhaa za kilimo. Hili litawezekana iwapotaifa litawekeza vya kutosha kwenye kilimona ili kupata fedha za kuwekeza hatuna

    budi kuongeza uwekaji akiba nchini.

    Hifadhi ya Jamii kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wote walio katika sekta isiyo rasmini moja ya njia ya kuongeza uwekaji akibanchini na kuwalinda watu kwenye makundi

    hayo dhidi ya majanga ya kiuchumi nakijamii. Shirika la Kazi la Dunia (ILO)linathibitisha kwamba “Nchi zilizofanikiwasana kwenye kuongeza tija kukiwa namifumo ya hifadhi ya jamii ziliongeza

    kasi ya ukuaji uchumi kwa nukta mojazaidi kuliko nchi nyingine zinazoendelea”.Uwekaji akiba nchini hivi sasa ni mdogokwa kiwango cha 16% tu ya Pato la aifa

     wakati nchi kama Uchina wananchi waohuweka akiba mpaka 50% ya Pato la aifa.

    Ili kuhimiza uwekaji akiba nchini inabidikuweka vivutio kwa Serikali kuchangiatheluthi ya kiwango cha chini cha mchangoambao mwananchi (Mkulima, Mfugaji,Mvuvi, Mfanyabiashara ndogondogona yeyote asiye kwenye sekta rasmi)

    anachangia kwenye mfumo wa Hifadhi ya

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    49/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA40

     Jamii, kuweka fao la Bima ya Afya kwa kilamchangiaji na fao la Bei kwa Mazao (PriceStabilization Benefit) kwa wakulima.

    Ili aifa letu liweze kujitegemea kiuchumi,hatua zifuatazo zitachukuliwa:

    3.2.1 Kuweka Akiba ( Savings ) na Ukuaji waUchumi 

    Kwa miaka takribani kumi na mitano(2000 – 2015) anzania imekuwa nauchumi unaokua kwa kasi ya wastani wa7% kwa mwaka. Hata hivyo kasi hii yakukua kwa uchumi imeshindwa kuondoa

    umasikini wa wananchi kwani kwa kiasikikubwa kasi hii imesukumwa na mitajikutoka nje ambayo imewekezwa kwenyesekta ambazo haziwanufaishi wananchimoja kwa moja kama vile Madini, Mafutana Gesi, Mawasiliano ya Simu na Uchuuzi.Ni muhimu kasi ya ukuaji wa uchumiiendane na kiwango cha uwekaji akibacha aifa (National savings rates). Wakatiuwekaji akiba anzania upo katika kiwangocha 16%, nadharia za uchumi zinaelekeza

    kuwa “Nchi zenye malengo ya kukua kwa

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    50/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 41

    7% kwa mwaka inabidi ziwe na uwekaji wa akiba wa 35% ya pato la aifa” (Pinto,2014). Kwa uwekaji akiba nchini ni wa

    chini na duni, uhuru wa nchi unahatarishwakwa kutegemea sana mitaji kutoka nje. Ilikuondokana na mrija huu wa mitaji ya nje,Chama cha Wazalendo kinataka kuhimizauwekaji akiba kupitia mfumo wa hifadhi ya

     jamii ( Social Security Systems).

    Licha ya Hifadhi ya Jamii kuwa ni kwaajili ya pensheni, AC-Wazalendo itatumiahifadhi ya jamii kama nyenzo (instrument)ya kukuza uwekaji akiba nchini ili kuweza

    kuwa na vyanzo vya mitaji ya uwekezaji wa ndani. Moja ya sababu kubwa ya kuwana mporomoko wa thamani ya sarafuya anzania ni nakisi ya uwekaji akibamaana ‘nchi yenye nakisi ya akiba, sarafuyake hushuka thamani mpaka pale mali

    zake zinapokuwa rahisi sana kiwango chakuvutia akiba za nje kuingizwa nchini’. Bilaya kuwa na uwekaji akiba mkubwa nchini,nchi yetu itakuwa kwenye mnyororo wamitaji kutoka nje ambayo inahatarishauhuru wa nchi yetu katika kuamua namna

    ya kuwekeza na maeneo gani ya kuwekeza.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    51/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA42

    Uwekezaji wa miradi mikubwa yenyefaida kwa nchi kama miundombinu yaumwagiliaji, viwanda vya kusindika mazao

    ya kilimo, barabara kuu, reli, bandari,viwanja vya ndege, vyuo vikuu na vyuo vyaufundi utafanywa na akiba kwenye mifukoya hifadhi ya jamii kwani kwa uasili wakemadai dhidi ya mifuko (liabilities) ni yamuda mrefu. Iwapo Watanzania milionitano tu kati ya Watanzania milioni ishirinina mbili waliopo kwenye nguvu kazi

     wakiweka akiba ya shilingi thelathini elfutu kwa mwezi (shilingi 20,000 itachangiwana mwananchi na shilingi 10,000 na

    Serikali kwa kila mwananchi mchangiaji),akiba itakayowekwa itakuwa ni shilingi1.8 trilioni kwa mwaka, sawa na 2.5% yaPato la aifa. Fedha hizi ni sawa na jumlaya Fedha zote anzania imeingiza kamaForeign Direct Investments kutoka nje

    mwaka 2013. Fedha hizi ni mtaji tosha kwauwekezaji kwenye miradi ya muda mrefuna yenye kuweza kulipa vizuri na kufaidisha

     wanachama wa hifadhi ya jamii.

    Kuna ugumu kwa watu masikini kujiwekea

    akiba kwa sababu ama ya kipato kiduchu

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    52/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 43

    au kutokuwa na nidhamu ya kuweka akiba.Hata hivyo, watu masikini wengi katikanchi yetu ni wanachama wa vyama vya

    kuweka na kukopa (SACCOS) ili kuwezakufikia akiba yao wanapokuwa na mahitajikama vile matibabu, elimu ya watoto waona kupata mikopo ya gharama nafuu ilikuanzisha biashara ndogondogo. Mfumo

     wa Hifadhi ya Jamii utamwezesha masikinikuweka akiba kupitia vyama vyao vya hiarivya SACCOS na kupata mikopo nafuuili kuongeza kipato chao. Muhimu kulikoyote mwanachama atapata Bima ya Afya nahivyo kuweza kupata matibabu bure bila

    ya kuathiri michango yake katika mfuko wa hifadhi ya Jamii. Hifadhi ya Jamii kwa wote itakuwa nguzo muhimu katika Sera zaChama cha AC-Wazalendo na nyongezamuhimu sana katika kuhuisha Azimio la

     Arusha.

    Katika kutekeleza Azimio la Arusha,Serikali ya wakati huo ilianza kampeniya wananchi kuhamia kwenye vijiji vyaujamaa. Msukumo mkubwa pamoja namambo mengine ulikuwa ni kuiwezesha

    Serikali kutoa huduma za kijamii kwa

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    53/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA44

    urahisi. Vilevile wananchi walilima kwenyemashamba ya ujamaa kwa kutumia kaulimbiu nyingi ikiwemo kilimo cha bega kwa

    bega. Chama cha AC- Wazalendo kitakanataka Serikali kuwafuata wananchi huko

     walipo vijijini na kuwawezesha kulimamashamba yao binafsi wenyewe kwa tijakwa kupitia ushirika wa msingi ili kuongezauzalishaji, kufungua viwanda vidogovidogo vya kuongeza thamani ya mazao yakilimo vijijini na kuunganisha uchumi wavijijini na uchumi wa aifa. Ujamaa wakidemokrasia unaosimamiwa na ACT-

     Wazalendo ni ujamaa wa kuzalisha na sio

    ujamaa wa kugawana tu.

    3.2.2 Kupambana na mfumo wa unyonyaji naufisadi 

    Hata uchumi ukue kwa kasi ya namna ganiiwapo ukuaji huo unanufaisha kikundi

    kidogo cha watu hauna maana na ni hatarikwa uwepo wa taifa lenyewe. Ni lazimakuchukua maamuzi ya kujenga taasisi zenyenguvu ambazo zitaondoa hali hii ya uchumikutajirisha wachache na kufukarisha wengi.Lazima kupambana na rushwa kwa vitendona bila huruma wala kuoneana aibu.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    54/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 45

    Ufisadi utaondoshwa kwa kujenga mifumomadhubuti ya uwajibikaji na taasisizake. aasisi na mfumo utakaohakikisha

    kuwa watawala wanawajibika kwa ummakwa wanayoyatenda na wasiyoyatenda.Mfumo utakaohakikisha kuwa rasilimaliza nchi zinarudi kwa wananchi ili kujengamiundombinu vijijini ikiwemo barabara,maji, nishati ya umeme na kuboreshahuduma za kijamii hasa elimu na afya.Vinginevyo tutaendelea kuwa taifa vipandevipande kutokana na tofauti kubwa ya kipatona fursa ndani ya jamii.  ACT-Wazalendotunasema Tanzania yenye watu fukara

    milioni thelathini na bilionea thelathinihaikubaliki. 

    Hapa nchini kwetu anzania, ufisadiunasukumwa na mambo makuu manne.Moja, ni rushwa ndogo ndogo zinazotokana

    na huduma mbovu za kijamii kama kwenyemahospitali, mashuleni na kwenye idara zaSerikali kama polisi, mahakama na ardhi.Hizi hongo Mwalimu Nyerere alipatakuziita “little chai” ili kuharakisha huduma.Hongo za namna hii zinawaathiri sana

     wananchi masikini kabisa vijijini.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    55/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA46

     Jambo la pili ni fedha zinazotumika kwenyesiasa, ambapo vyama vya siasa hupewafedha na matajiri ili kulinda maslahi yao.

    Hapa anzania tunashuhudia vyama vyasiasa vikitumia vibaya ruzuku wanazopewana Serikali lakini pia vikifadhiliwa fedhanyingi sana na matajiri ili kulinda matendoyao na haswa ukwepaji mkubwa wakodi. Vyama vikishinda na kuunda dolavinaunda Serikali yenye sera zinazolindamatajiri hawa. Jambo la tatu ni makampunimakubwa ya kimataifa ambayo hutumia njiaza kitaalamu kukwepa kodi na kutoroshafedha kwenda ughaibuni. Jambo la nne ni

    makundi ya kiharamia yanayojihusisha namadawa ya kulevya, ujangili na ujambazi.Kiasi fulani makundi haya huwa ni mtandaommoja wenye lengo la kuhifadhi tabakala Watawala na wenye nacho waendeleekunyonya wananchi.

    Katika kupambana na ufisadi, hatuna budiya kuvunja mfumo wa sasa unaokumbatiaufisadi. Mfumo wa siasa na uchumi tulionaosasa unazaa ubinafsi na hivyo ufisadi. Miakaya hivi karibuni tumeshuhudia minyukano

    ya wanasiasa dhidi ya rushwa, hata hivyo

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    56/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 47

    hakuna chama hata kimoja cha siasaambacho kinazungumzia kubomoa mfumounaozaa ufisadi. AC-Wazalendo inataka

    kujenga Ujamaa wa kiDemokrasia ambaounaojengwa juu ya misingi ya Azimiola Arusha na haswa Miiko ya Uongozi.Ni lazima kupiga marufuku viongozi wakisiasa kujilimbikizia mali. Ni lazima kuwa

     wazi kabisa kuhusu maamuzi ya kiserayanayopelekea kubomoa mfumo ulioposasa na kujenga mfumo mpya wa uchumi.

    Masuala ya kiuchumi na hasa umasikini,afya, elimu na masuala ya rushwa ni mambo

    makuu ambayo Watanzania wanayaonakama changamoto kubwa zinazowakabili.Hivyo shabaha kubwa ya serazitakazotekeleza Ujamaa wa kiDemokrasiani kutokomeza umasikini na kuumilikishauchumi kwa wananchi wenyewe.

    3.2.3 Kilimo

    Ili kujenga uchumi shirikishi, ni muhimukufanya jitihada za makusudi katikakuhakikisha kwamba kilimo chetu kinaanzakuchangia vya kutosha katika ukuaji wa

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    57/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA48

    uchumi. Shabaha ya muda wa kati katikasekta ya kilimo ni kuongeza Mapato yafedha za kigeni kutokana na kilimo ikiwemo

    kilimo cha maua na mbogamboga hadikufikia dola za kimarekani bilioni mbili kwamwaka ifikapo mwaka 2025. Shabaha yamuda mrefu ni kujitosheleza kwa chakulana ziada kuuza nje na kuongoza katika nchiza Afrika Mashariki kwa kuuza nje Sukarina Mchele; Kurejea kuwa nchi ya kwanzaduniani kwa kuuza nje Katani na bidhaaza Katani; Kuongoza Afrika kwa kuuza njeKorosho zilizokobolewa na Wakulima wote

     wa anzania kuwa na hifadhi ya jamii.

    Chama cha ACT-Wazalendo kitaagizaserikali kuchukua hatua mahususizifuatazo kuhusu kiilimo:

    1) Kilimo ndio shughuli kiongozi katika

    kutokomeza umasikini. Shughuliza Kilimo lazima ziendeshwe na wananchi wenyewe kwa kuwawezeshakumiliki ardhi, kuongeza tija na hivyouzalishaji na kupata mitaji kwa kupitiamfumo wa hifadhi ya jamii.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    58/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 49

    2) Mfumo wa Hifadhi ya Jamii uwekeweutaratibu wa kuwepo kwa fao la Beiya Mazao (Price Stabilization Benefit),

    Bima ya Mazao na Mifugo na mikopoya gharama nafuu kwa vikundi vya

     wakulima ili kununua pembejeo zakilimo na ufugaji kwa lengo la kuhamimwananchi asitumbukie kwenyeufukara.

    3) Ardhi na mashamba yote yaliyokuwa yaMashirika ya Umma na kubinafsishwayarejeshwe kwa wananchi wasio naardhi kwa kuwagawia na kushiriki

    katika uzalishaji kwa kutumia mfumo wa ‘outgrowers’ scheme’.

    4) Mashamba makubwa ya kibiasharayatakapohitajika itakuwa ni jumlaya mashamba madogo madogo

    ya wananchi na pale uwekezajiutakapohitaji basi wananchi watamiliki theluthi mbili ya shambahusika na mwekezaji wa ndani au wanje atamiliki theluthi moja tu.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    59/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA50

    5) Serikali itunge mfumo wa kodiunaoeleweka na usiotetereka (stablefiscal regime) katika sekta ya kilimo ili

    kuhakikisha kuwa mkulima anabakiana sehemu kubwa ya mapato yake.

    6) Serikali iunde Mamlaka ya Kilimo ilikusimamia sekta ya kilimo. Wajibu

     wa kuhakikisha mazao ya kilimo

    ya wananchi yote yamenunuliwakwa bei nzuri utakuwa wajibu waSerikali kupitia Shirika la Ummalitakaloundwa mahususi kwa kazihiyo.

    7) Dola kuhusika kikamilifu kwenyehifadhi ya mazao na kuanzishamfumo wa soko kupitia soko la bidhaa(commodities exchange) ambaoutashirikisha vyama vya wakulima

    na hivyo kufuta kabisa watu wa kati(middlemen).

    8) Mfumo wa usambazaji wa pembejeoza kilimo utapaswa kurekebishwa ilikutoa nguvu kwa vyama vya msingi

    vya wakulima kununua pembejeo zao

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    60/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 51

     wenyewe kwa wakati. Serikali itakuwana wajibu wa usambazaji wa pembejeokwa wakulima kupitia Shirika la

    Umma litakalokuwa na wajibu huopekee.

    3.2.4 Viwanda

    Shabaha ya muda wa kati ni kuhakikisha

    kuwa bidhaa za viwanda zinaliingizia aifamapato ya fedha za kigeni zaidi ya dolaza kimarekani bilioni tatu kwa mwaka.Msukumo uwekwe kwenye bidhaa zanguo kwani zinaajiri watu wengi zaidina mnyororo wake wa thamani ni mrefu

    mpaka kwa wakulima wa pamba nchini.Itakuwa ni marufuku kuuza nje malighafi(raw materials) isipokuwa kwa mazingiramaalumu ikiwemo inapothibitika kuwauwezo wa ndani wa nchi ni mdogo.

    Chama cha ACT-Wazalendo kitaagizaserikali kuchukua hatua mahususizifuatazo kuhusu viwanda: 

    1) Viwanda, vikiwemo vya kuongezathamani ya mazao ya kilimo, mifugona uvuvi vipewe kipaumbele kikubwa

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    61/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA52

    kwa kuwekewa vivutio vya kodiikiwemo ruzuku za kufidia gharamaza uzalishaji kama umeme (mfano

    viwanda vya kuzalisha sukari, saruji,ngozi, korosho na nyuzi za Pamba) nazawadi za kodi (exports tax credits) ilikuchochea mauzo ya nje.

    2) Serikali ishiriki katika umiliki wa

    viwanda vya msingi kama vile viwandavya chuma cha pua na kusimamiakikamilifu ushiriki wa sekta binafsikatika kuongeza uzalishaji viwandani.

    3) Viwanda vya anzania vina fursa yakuuza ndani ya Afrika Mashariki,Kati na Maziwa Makuu bidhaakama unga, plastiki, saruji, sukari navinywaji maradufu ya mauzo ya sasa.Hivyo serikali ihakikishe kwamba

    soko la kanda linakuwa ni kipaumbelecha kwanza katika uimarishaji waviwanda.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    62/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 53

    3.2.5 Utalii 

    Shabaha ya muda wa kati ni anzania

    iwe na uwezo wa kuingiza na kuhudumia watalii milioni 5 kwa mwaka na kuingizamapato ya fedha za kigeni yasiyopunguadola za kimarekani bilioni 8 kwa mwaka.Makusudio ya Serikali katika sekta yautalii isiwe ni kukusanya kodi tu bali iwe

    ni kuzalisha ajira na kuongeza mapato yafedha za kigeni.

    Sekta ya utalii ina nafasi kubwa sana yakuzalisha ajira kwa vijana na wananchi kwaujumla. Pia mnyororo wa thamani wa sekta

    utalii ni mrefu na kwa kuwa nchi imejaaliwavivutio vingi vya utalii inaweza kuleta fedhanyingi za kigeni kuweza kununua mashinena vipuri tusivyoweza kuzalisha wenyewekatika kipindi cha mpito. Tamani ya fedhaza kigeni katika utalii lazima ziendane na

    thamani ya manunuzi yetu nje ya nchi nahasa mafuta ambayo yanatumia sehemukubwa ya akiba yetu ya fedha za kigeni.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    63/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA54

    Chama cha ACT-Wazalendo kitaagizaserikali kuchukua hatua mahususizifuatazo kuhusu utalii: 

    1) Kuweka mfumo rahisi wa kikodikatika sekta ikiwemo urahisi wakupanua vyumba vya wageni vyamahoteli.

    2) Utalii wa kitamaduni udumishweikiwemo kuboresha michezo kamariadha, mpira wa miguu, sanaa nk ilikutangaza nchi.

    3) Shirika la ndege la taifa ni lazima

    liundwe upya na liwe chachu yakuongeza mapato ya fedha za kigeninchini.

    4) imu ya taifa ya mpira wa miguuitumike kutangaza nchi kwa

    kuwekewa lengo la kufika kombela dunia kabla ya mwaka 2025 kwakujenga shule za michezo katika kilamkoa wa anzania, Mashirika yaUmma kuwa na timu za michezo namashindano ya michezo mashulenikurejeshwa.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    64/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 55

    5) Sanaa kama vile nyimbo na filamu ziwenyenzo za kutangaza nchi, kuongezaajira kwa vijana kupitia vipaji vyao na

    kuongeza mapato ya fedha za kigeni.

    3.2.6 Madini, Mafuta na Gesi Asilia

    Sekta za Madini, Mafuta na Gesi Asilia nisekta za maliasili ya nchi yetu. Sekta hizi

    zinaweza kuzalisha mapato ya kutosha yaSerikali ili kuboresha sekta nyingine kamavile Kilimo na uwekezaji katika Afya, Elimuna Hifadhi ya Jamii.

    Chama cha ACT-Wazalendo kitaielekeza

    serikali kuchochea mabadiliko makubwakatika sekta hizi za uvunaji wa maliasili

     ya nchi kwa kuchukua hatua zifuatazo:

    1) Maliasili zote za madini, mafutana gesi asilia ziw mali ya wananchi

    KIKAIBA na uchimbaji wake lazimauwe na kibali cha wananchi (free priorinformed consent).

    2) Mfumo wa uchimbaji wa maliasilihizi ubadilike kutoka mfumo wa

    sasa wa kutoa leseni na kukusanya

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    65/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA56

    kodi na mrahaba kwenda mfumo waumiliki na ukandarasi. Mwekezaji awemkandarasi, arejeshe gharama zake na

    faida iliyobakia kugawana na Serikalikwa makubaliano maalumu. Haki(Mineral Rights) iwe ya Shirika laUmma linalomilikiwa na Serikali na

     wananchi kwa asilimia 100. Wenyemitaji wawe wakandarasi wa Shirikahilo la Umma kwa mujibu wa mikataba(Revenue Sharing Agreements).

    3) Mikataba yote ya uvunaji wa maliasiliiwe wazi kwa wananchi. Mapato

    yatokanayo na mrahaba yagawiwe kwamaeneo yenye shughuli za uchimbajikwa uwiano maalumu utakaowekwa.Mapato yatokanayo na mali asiliya nchi yawekwe kwenye mfumomaalumu na kutumika kwa ajili ya

    ujenzi wa miundombinu, upanuzi wahuduma za afya na elimu, akiba kwavizazi vijavyo na kuimarisha mfumo

     wa hifadhi ya jamii nchini.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    66/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 57

    3.2.7 HitimishoSera za AC-Wazalendo zinalengakuelekeza nguvu kwenye uchumi na

    kujenga mazingira ya kufanya mageuzimakubwa (transformation) ya kiuchumi,kuwezesha kasi ya ukuaji uchumi kwa zaidiya wastani wa asilimia 10 kwa muongomzima na kujenga jamii ya watu walio sawana huru. Sekta msukumo za uzalishaji niKilimo, Viwanda, Usafiri wa kimataifa(transit trade) na Utalii. Sekta msukumoza matumizi/uwekezaji ni Elimu, Afya,miundombonu ya usafiri/usafirishaji naHifadhi ya Jamii.

    Hata hivyo, yote haya hayatakuwa namaana iwapo mfumo wa fedha kupitiamabenki utakuwa umeshikwa na wageni.Nchi yetu haiwezi kuendelea iwapomabenki makubwa yote yanamilikiwa na

     watu kutoka nje. Utaifishaji wa Mabenkiuliofanyika mwaka 1967 na kuundwakwa Benki ya aifa ya Biashara, Benki yaNyumba na Benki ya Maendeleo Vijijiniilikuwa ni maamuzi ya msingi sana kwamaendeleo ya nchi yetu. Ubinafsishaji wa

    Benki ya aifa ya Biashara na kufilisiwa kwa

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    67/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA58

    Benki ya Nyumba ilikuwa ni maamuzi yahovyo kabisa kupata kutokea katika nchiyetu.

    Malengo ya kujenga uchumi shirikishi wenye uhuru mkubwa katika soko lamitaji hayawezi kufikiwa bila ya kuwana Benki zinazomilikiwa na Watanzania

     wenyewe. Hivyo, Chama cha AC-

     Wazalendo kitahimiza kuwa Benki ya aifaya Biashara irejeshwe kwenye mikono ya

     Watanzania kwa kumilikiwa na Serikali50% na Wananchi na taasisi za wananchikupitia soko la mitaji nusu iliyobakia.

     AC-Wazalendo itahimiza pia Benki yaMaendeleo na Benki ya Kilimo kuwa namuundo wa umiliki kama wa Benki yaaifa ya Biashara.

    Mashirika yanayoendesha sekta nyeti katika

    uchumi kama Umeme, Reli, Bandari,Mkonga wa aifa, Mafuta na Gesi Asilia,Bima ya Maisha, Benki ya aifa ya Biashara,Madini ya msingi kama Chuma yataendeswamoja kwa moja na serikali na kwa ubia na

     wananchi, na kamwe hayatamilikishwa kwa

     wageni.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    68/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 59

    Shabaha yetu katika muda wa kati ni kuwana Pato la aifa la dola za kimarekanibilioni 90, uwekaji akiba usiopungua

    asilimia 30 ya Pato la aifa na makusanyoya kodi yasiyopungua asilimia 25 ya Pato laaifa. Tunalenga kuwa Tanzania itakuwanchi ya 5 kwa ukubwa wa uchumi barani

     Afrika na ya kwanza katika AfrikaMashariki ifikapo mwaka 2030. 

     AC-Wazalendo tunataka kufufua utaifa wa anzania ili kila Mtanzania aone kuwaana wajibu wa kujenga nchi yake kwaajili ya leo na vizazi vijavyo. unataka

    kufufua uzalendo wa aifa kwa kurejeshaimani ya wananchi kwa viongozi waokwa kutokomeza ufisadi kupitia Miikoya Viongozi. Kujenga uchumi shirikishi

     wenye mfumo madhubuti wa uwajibikajina unaowezesha kila mtu mwenye uwezo

     wa kufanya kazi afanye kazi na kupata ujiraunaotosha ni moja ya njia bora zaidi yakujenga uzalendo miongoni mwa wananchina viongozi wa aifa hili. unatakaanzania ambayo kila raia ana haki sawa yakupata Elimu bora na Afya bora. unataka

    anzania ambayo kila raia ana Hifadhi ya

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    69/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA60

     Jamii. unataka anzania yenye usawa. Tunataka kujenga Taifa lenye kujitegemeakiuchumi na kiutamaduni, na ambalo

    linalinda na kudumisha usawa, ustawiwa jamii, uwajibikaji, demokrasia, nauongozi bora. Hii ndio ndoto yetu wana

     ACT - Wazalendo.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    70/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 61

    SEHEMU YA NNE4.1 Miiko ya Uongozi

    Ili kubomoa mfumo wa kinyonyaji nakifisadi, Chama cha Wazalendo (AC-

     Wazalendo) kimeamua kurejesha miiko

    ya Uongozi na Kuiishi. Ni wazi kuwakama chama tumejiwekea misingi mizitoambayo itahitaji kujitoa kikamilifu katikakuisimamia. Jukumu kubwa la usimamizi

     wa Itikadi, Falsafa na Misingi ya chamalipo mikononi mwa viongozi. unahitajiviongozi watakaojitoa kwa dhati kusimamiamisingi hii. Hivyo basi, miiko hii ya uongoziimewekwa iwe dira ya viongozi wa AC-

     Wazalendo na serikali itakayotokana nayokatika kuwatumikia wananchi.

    4.1.1 Miiko ya viongozi 

    1. Kiongozi wa AC-Wazalendo au waSerikali itokanayo na chama chetuau akiwa katika chombo chochotecha dola, katika Serikali za Mitaa na

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    71/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA62

    Serikali Kuu sharti awe ni mtu mwenyeshughuli halali inayompa kipatohalali na asishiriki katika jambo lolote

    litakalomuweka katika mgongano wakimaslahi unaompelekea yeye binafsi,familia yake, rafiki zake au jamii yakekufaidika kifedha au kwa namnanyingine.

    2. Kiongozi sharti aweke wazi shughulizake za biashara na nyakati zote akiwakiongozi kwenye ofisi ya umma na awehaendeshi moja kwa moja shughulihizo yeye mwenyewe.

    3. Akiwa katika uongozi wa umma,kiongozi asiwe mkurugenzi katikakampuni yeyote binafsi au shirika laumma.

    4. Kiongozi sharti aweke wazi vyanzovyake vya mapato na mali zitokanazokwa kuzingatia utaratibu wa sheriaza nchi na Kanuni za Mwenendona Maadili ya Viongozi wa AC-

     Wazalendo na miongozo mingine ya

    chama.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    72/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 63

    5. Kiongozi asifanye biashara ya ainayeyote ile na chama na serikaliitokanayo na AC-Wazalendo wakati

    akiwa katika nafasi ya uongozi wachama na/au serikali.

    4.1.2 Tafsiri ya kiongozi 

    Viongozi wanaotajwa hapa ni Viongozi

     wa Kitaifa wa chama, Rais, Mawaziri, Wabunge na Madiwani wanaotokana na AC – Wazalendo. Kwa mujibu wa kifunguhiki kiongozi ni mtu peke yake, au mtu namkewe au mke na mumewe.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    73/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA64

    NYONGEZA Hotuba ya kiongozi wa chama Ndugu ZittoRuyagwa Z. Kabwe aliyoitoa katika uzinduzi waChama cha AC-Wazalendo siku ya Jumapilitarehe 29 Machi 2015 katika ukumbi waDiamond Jubilee, Dar es Salaam

    _____________________________________

    Turejeshe nchi yetu Tanzania! 

     Watanzania wenzangu, wageni waalikwa

    Nawashukuru kwa kuwa pamoja nasi siku hii yakihistoria.

    Karibu Miaka 54 iliyopita tulipopata uhuru,Muasisi na Baba wa aifa Mwalimu Julius

    Kambarage Nyerere alikuwa kijana mwenye umri wa miaka 39, mwenye matumaini makubwana taifa jipya na alikuwa na ndoto! Ndoto yakeilikuwa imejikita katika kuhakikisha taifa letulitakuwa taifa lisilo na umaskini, dhiki, ufukara;taifa lisilo na tofauti kubwa kati ya maskini na

    tajiri; taifa lenye usawa, haki na maendeleo,

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    74/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 65

    ambapo watoto wote wanasoma shule bila kujalikipato cha mzazi; taifa ambalo wananchi wake

     wanamiliki uchumi wao.

    Ndoto hii aliiamini kwa dhati na wananchi wote walikubali na kuota nae ndoto hii. Alilisimamiakwa maneno na vitendo kupitia Azimio la Arusha,sera zake na uongozi wake wa kizalendo. Mpakamauti ilipomkuta aliamini katika misingi hii

    aliyojitahidi kuturithisha. Lakini miaka 16 baadaya kifo chake, ndoto yake imeyeyuka! ulilonaloni jinamizi alilolihofu Nyerere.

    Leo hii:

    Watanzania wachache wameondoka katika unyongena dhiki.

    Watanzania wengi bado wapo katika hali ya dhiki.

    Watanzania wachache wameshikilia uchumi:Warasimu, Wanasiasa na Matajiri wachache wenyemitaji.

    Watanzania wengi bado kama Mwalimu Nyererealivyosema “wananyonywa kiasi cha kutosha;wanapuuzwa kiasi cha kutosha”.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    75/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA66

    Ndoto ya Mwalimu Nyerere bado haijawafikiawananchi.

    Sasa ndio wakati wa mabadiliko ya kimapinduzi.Sasa ndio wakati wa kujenga Uchumi shirikishiambao utaruhusu kila mwananchi kupata fursaya kuboresha maisha yake. Sasa ndio wakati dolaimara ipate nafasi ya kusimamia uchumi. Sasa

    ndio wakati kwa wananchi kuwa na uhuru wakweli wa mawazo, fikra, kushirikiana na kuabudu.Sasa ndio wakati wananchi kuwa na nguvu yakuwawajibisha viongozi wao. Sasa ndio wakati

     wetu watanzania kujirithisha upya nchi yetu!

    Huu ndio wakati wa kubomoa uchumi wakinyonyaji na kifisadi na kujenga uchumi wa wananchi. Haya ndio mabadiliko ya kimapinduzitunayoyataka. Hii ndiyo ilikuwa ndoto yaMwalimu Nyerere, na muda umefika wananchiturejeshe nchi mikononi mwetu!

    Haya yamekuwa mawazo yangu kwa muda mrefukwa sababu mimi ni zao la ndoto ya MwalimuNyerere. Nililelewa na mama yangu mzazi pekeemwenye ulemavu; nimeanza kusoma shule yamsingi nikiwa naenda peku. Lakini kutokanana kufaulu mitihani vizuri, sikuhitaji kuwa tajiri

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    76/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 67

    kusoma mpaka Chuo Kikuu. Leo hii kutokana naelimu bora niliyoipata bure, nimesafiri na kufikakatika nchi zaidi ya 70; nikiwa kama kiongozi

    nimekutana na kubadilishana mawazo na watumuhimu duniani kama vile wakuu wa nchi. Siomimi peke yangu bali tupo maelfu tuliofaidikana mfumo huu. Lakini muhimu kupita yote,nimeweza kutumikia wananchi wa Kigoma na

     watanzania bungeni kwa miaka 10. Kama hii sindoto iliyokuja kuwa kweli, ni nini?

    Zitto Ruyagwa Z. Kabwe angezaliwa mwaka2000, angekuwa kijana ambaye hajakamilishaelimu yake, haelewi lugha za kigeni kama

    kiingereza, hana ujuzi wowote na kama Munguangeendelea kuninyima kipaji cha kuimba kamasasa ningeshindwa hata kutoka kama Diamondna Mwana FA! Mwalimu Nyerere asingepiganiandoto yake miaka ya 60 na 70, ningekuwa kamamamilioni ya vijana leo ambao wanahangaika

    kutafuta ajira na kipato bila ujuzi na elimu.

    Na ndiyo maana siku ya leo ni muhimukwangu. Nina furaha na heshima kubwa kuwakatika familia yangu mpya ya kisiasa. Familiainayoaamini katika itikadi, misingi na tunu

    ninazoziamini.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    77/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA68

    Nimezungumza mara kadhaa kuhusu sababuza kujiunga na chama hiki. Chama cha

     Wazalendo AC-anzania inaongozwa na

    misingi ya Uzalendo, Demokarsia, Uhuru wa fikra na matendo, Utu, Usawa, Uadilifu,Uwazi, Uwajibikaji na Umoja katika kila kitu.Chama hiki ni cha wananchi si wenyenchi wasasa waliojimilikisha taifa. Chama hiki ni cha

     watanzania wote bila kujali kabila, dini, jinsia,rangi ya ngozi au hali ya ulemavu!

    unapojadili wananchi kujimilikisha upyanchi yetu ni kupitia usimamizi wa sheriautakaohakikisha kuwa kuna uwazi na uwajibikaji

     wa viongozi. Uwazi tunaouamini ni uleutakaohakikisha kila mwananchi anapata taarifaza fedha zao, mikataba ambayo Serikali inaingiakwa niaba yao na taarifa za maslahi, mali namadeni ya viongozi wao. unataka uwazi katikauendeshaji wa Serikali na sisi tutaanza na uwazi

    katika uendeshaji wa chama chetu. unataka wananchi sio tu wajione kuwa sehemu yauendeshaji wa nchi yao, bali pia wawe sehemu yauendeshaji wa nchi yao.

    unataka uwazi utakaoruhusu uhuru wa mawazo

    na uhuru wa wananchi kujieleza bila kuhofu

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    78/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 69

    Serikali kuwachukulia hatua kwa kutoa mawazoyao. Ndio maana AC-Wazalendo tunapingavikali miswada ya sheria ambayo Serikali ya

    CCM imeiwasilisha bungeni katika mkutanounaoendelea. Miswada hii kama vile muswada

     wa Haki ya kupata taarifa, vyombo vya habarina ule wa makosa ya mtandao inalenga kuminyana kunyima haki za wananchi kuwasiliana kwauhuru na kutoa mawazo yao kama inavyoainishwakatika katiba ya nchi.

    unapojadili wananchi kurejesha taifa mikononimwao tunazungumzia uwajibikaji. Ripoti yaume ya Marekebisho ya Katiba ilieleza moja

    ya sababu kubwa ya kushamiri rushwa, ufisadina ubadhirifu nchini ni nanukuu ‘kukosekanakwa mfumo madhubuti wa uwajibikaji’ nchinikwetu. Sababu kubwa ya AC-Wazalendo kupingaKatiba inayopendekezwa ni kwamba, Katibahiyo imechakachua nia hii ya kuweka mfumo wa

    uwajibikaji. Ndio maana tunawaambia wananchi waikatae Katiba hiyo kwa nguvu zao zote! Katibainayoepndekezwa inastahili kadi nyekundu,tuikatae na kura ya hapana!

    Iwapo wananchi hawawezi kuwawajibisha

    viongozi kwa matendo yao hatuwezi kujenga

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    79/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA70

     jamii ya watu wanaoheshimiana na kutii sheria zanchi. Kila Mtanzania bila ya kujali cheo chake nilazima awe chini ya sheria. Uwajibikaji ni lazima

    uanze na viongozi. Mnajua kuwa katika maishayangu ya kisiasa hili ndio limekuwa jukwaa langu.

    Kwa bahati mbaya tunaishi katika kipindi ambacho wanasiasa wengi wamekuwa wakikumbwa nakashfa mbalimbali za kifisadi na matokeo yake

    inajengwa picha kuwa kila mwanasiasa ni fisadi.Mfumo wa Uwajibikaji wenye uwazi utasaidia

     wananchi kutofautisha wanasiasa wanaosimamiamaslahi ya umma na wale wanaosimamia maslahiyao binafsi na vyama vyao vya siasa. Mwungwana

    ni vitendo; nimewajibisha watu kwenye Buzwagina mikataba ya madini, kwenye matumizimabaya ya fedha za umma na juzi juzi kwenyeakaunti ya egeta Escrow. Lakini matukio hayamachache hayatoshi kujenga mfumo madhubuti

     wa Uwajibikaji. Ni lazima kufanya mapinduzi

    ya mfumo mzima wa uchumi wa nchi yetuna kujenga mfumo mpya unaohudumia kilaMtanzania na ambao kila Mtanzania anajivuniakuujenga. Hatuwezi kuwa aifa linaloshikiliwana vikundi vya wafanyabishara wachache na

     wanasiasa wanaofadhiliwa na wafanyabishara hao.

     AC-Wazalendo inataka kujenga aifa ambalo

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    80/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 71

    viongozi wake wanawajibika kwa wananchi.Hii ndio fikra tunayotaka kurejesha. Hizi ndizosiasa zilizoasisi aifa letu. Hatuna budi, ni lazima

    kurudi kwenye misingi na kuanza upya!

    Kwa sababu AC-Wazalendo imejikita kwenyemisingi hii, tumelihuisha Azimio la Arusha.Sio tu tumeweka miiko ya uongozi lakini piatumetunga kanuni za kutekeleza miiko hiyo na

    kuifanya kuwa sehemu ya Katiba ya chama chetu.Hitaji moja kubwa la Kanuni zetu za Maadili nikutaka kila Kiongozi wa AC-Wazalendo kuwekahadharani Maslahi yake, Mali na Madeni yake.Katika chama hiki huo ndio utamaduni wa kisiasa

    tunaotaka kuujenga. Kutenda tunachohubiri hatakabla ya kuingia kwenye uongozi wa Dola.

    Chama cha AC-Wazalendo kimeelekezakikanuni kwamba kila Kiongozi wa chama lazimaatangaze Mali zake na Madeni yake. Kila Kiongozi

    lazima aweke wazi maslahi yake ya kibiashara namengineyo wazi ili kila anapotenda au kusema jambo wananchi wajue maslahi aliyonayo au lakatika suala husika. Viongozi wote wa kitaifa wa

     AC-Wazalendo watalazimika kufanya hivyo nakwa kuanzia leo hii mimi na Katibu Mkuu wetu

    tutaweka saini zetu mbele yenu kama mashahidi.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    81/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA72

    Naomba Mwanasheria wetu aje hapa tutekelezematakwa haya ya kikanuni.

    Fomu hizi zitakuwa kwenye tovuti ya chama ndaniya muda mfupi ujao ili kila mtanzania aone. KilaKiongozi wa Chama ambaye Miiko ya Uongoziinamtaja anapaswa kuwa amejaza fomu hizi nakuziwasilisha kwa Katibu wa Kamati ya Uadilifuifikapo tarehe 30 Juni 2015. unapopinga

    Viongozi wa Umma kufanya Biashara na Serikalina hivyo kuwa na mgongano wa kimaslahi nakushamiri kwa ufisadi, hivyo hivyo tunapingaViongozi wa Chama chetu kufanya Biashara naChama. Ni Marufuku Serikali kugeuzwa kuwa

    genge la watu wachache wanaopora rasilimali zaUmma. Uadilifu tunaoutaka Serikalini ni lazimauanzie kwetu tunaohubiri.

    utafanya haya kwa kubadilisha siasa zetu kuelekeakwenye masuala yanayowahusu wananchi;

     Wakulima, Wafanyakazi, Wafanyabiasharandogo ndogo, Vijana, Wanawake na Wazee wetu. unataka kurejesha nchi yetu anzaniakwa kujenga uchumi wa wote. unaporejeakwenye Azimio, hatusemi tunakwenda kutaifishakila kitu na Serikali kuendesha shughuli zote za

    kiuchumi kama ilivyofanyika mwaka 1967 kwa

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    82/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 73

    sababu za mazingira ya wakati huo. unaheshimuna kuthamini sekta binafsi na mchango wakekatika kukuza uchumi na kuleta maendeleo.

    unamaanisha kuwa ni lazima Dola isimamieuchumi. Sio kazi ya Serikali kufanya biashara.Lakini tunamaanisha kuwa ni lazima kurekebishabaadhi ya makosa yaliyofanyika kwenyeubinafsishaji na hususan ubinafsishaji holelauliofanyika kwenye sekta ya Kilimo na kuporaardhi ya wananchi wetu na kuwageuza kuwamanamba kwenye ardhi yao wenyewe.

    unataka kutomokeza ukwepaji kodi. anzaniainapoteza 15% ya makusanyo katika forodha

    kwa sababu ya ukwepaji wa kodi. Hii ni sawa nashilingi za kitanzania 490 bilioni kwa mwaka,fedha ambazo zingeweza kuchangia wananchimilioni 4 kwenye hifadhi ya Jamii. anzaniainapoteza takribani shilingi 2 trilioni kila mwakakwenye misamaha ya kodi. Hii ni fedha ambayo

    ingeweza kujenga reli mpya ya kati ya kisasakutoka Dar mpaka Mwanza na Kigoma ndaniya miaka mitatu. Ili kuondoa upotevu huuni lazima kupanua wigo wa kodi, kurahisishakodi, kupunguza baadhi ya kodi kama vile kodi

     wanaotozwa wafanyakazi (PAYE) na kutumia

    teknolojia kuziba mianya ya ukwepaji wa kodi.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    83/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA74

     Aidha ni muhimu kuimarisha mfumo wetu wakodi za kimataifa ili kuzuia utoroshaji mkubwaunaofanywa na makampuni ya kigeni. Ili

    tujitegemee kama aifa ni lazima kukusanyamapato ya ndani ya kutosha. Ili kukusanya mapatoya ndani ya kutosha ni lazima kuweka mazingiramazuri ya biashara hasa kwa wafanyabisharandogo ndogo kwani ndio wazalishaji wakubwa

     wa ajira.

    Kwa Vijana,  aifa hili ni lenu. Asilimia 75 ya Watanzania wapo chini ya miaka 40. Asilimia65 ya wapiga kura wapo chini ya miaka 40.Nusu ya Watanzania ni watoto chini ya miaka

    18. Kurejesha nchi kwenye misingi ni wajibu wa kujenga maisha yenu. Haikubaliki Vijanakuwa mzigo kwa wazazi kwa sababu tu uchumihauzalishi ajira za kutosha. AC-Wazalendondio jukwaa lenu la kufanya mapinduzi yamfumo wa uchumi ili kujenga uchumi shirikishi

    unaozalisha ajira. AC-Wazalendo inatakakuwajengea mfumo wa hifadhi ya jamii ambapomtakapokuwa Wazee msipate tabu za penshenina matibabu wanazopata wazee wetu hivi sasa.Shiriki kujijengea aifa litakalohakikisha maishayako ya sasa, baadae na ya kizazi kijacho.

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    84/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 75

    Kwa Wanawake, Ninyi ndio mhimili wa aifahili, wazalishaji wakuu na walezi wa aifa letu.Kurejesha nchi kwenye misingi ni wajibu wa

    kutambua nafasi yenu stahili katika jamii. Nikiwanimelelewa na Mwanamke mwenye ulemavu nampiganaji wa kweli wa haki za wananchi waliopembezoni, sina namna kutoa heshima yanguzaidi ya kuongoza chama chenye misingi thabitiya kumkomboa mwanamke. Msitarajie watu

     wengine kuwapigania mnapaswa kuchukua hatuakupitia jukwaa hili la AC-Wazalendo.

    Kwa wafanyabishara,  ninyi ndio mnachocheashughuli za Uchumi na kuzalisha ajira. Kuanzia

    kwa wamiliki wa maduka madogo mitaanimpaka kwa mameneja wa maduka makubwa;kutoka kwa wachuuzi na mama lishe mpaka kwa

     wamiliki wa viwanda na biashara; mnaamka kilasiku asubuhi kujenga aifa hili kwa kuzalishamali na huduma. Baadhi yenu ambao mnamiliki

    viwanda, mashirika makubwa na kutoa ajira kwamaelfu ya wananchi, mmeanza mkiwa mnashonaviatu na sare za shule, au mkitengeneza na kuuzamkate. Mmepata utajiri wenu na mali zenu kwa

     juhudi na jasho lenu na kutokana na fursa zakiuchumi zilizokuwepo kipindi hicho ambacho

    hakikuangalia dini, kabila, uwezo wa kifedha

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    85/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA76

    au rangi ya ngozi. AC-Wazalendo inatakakuwawekea mazingira bora ya biashara halali lakinipia kuhakikisha mnalipa kodi zenu na kutonyonya

     wafanyakazi wenu. unataka kuwawekea mfumorahisi wa kodi, wenye kueleweka na unaowapamotisha kuzalisha zaidi ili kuongeza ajira zaidi nakupanua Pato la aifa. Msipotimiza wajibu wenubiashara zenu hazitashamiri. Kurudi kwenyemisingi ya aifa hili ni kurejesha maadili katikabiashara zenu.

    Kwa Wakulima,  Wafugaji na Wavuvi, ninyindio mnaolilisha aifa letu na kuleta fedhanyingi za kigeni kupitia mauzo nje. Kwa miongo

    mitatu sera za nchi zimewaweka pembeni nahivyo uchumi wenu kusinyaa. Viwanda vyotevya kusindika mazao yenu vimeuzwa kwa beiya kutupwa licha ya kwamba jasho lenu ndiolilitumika kuvijenga. Miundombinu ya barabara,maji, umeme na mawasiliano haiwafikii ili

    muweze kupata masoko. Hamna hifadhi ya jamii wala bima ya mazao yenu. Ardhi yenu wamepewa wawekezaji na mnakodishiwa, mnapanga kwenyeardhi yenu wenyewe. Mmeachwa mkijihangaikia.Kurejesha nchi kwenye misingi kutawarudishiaheshima yenu katika nchi yetu. AC-Wazalendo

    ndio jukwaa sahihi kwenu kuhakikisha kuwa

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    86/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA 77

    tunajenga uchumi shirikishi ambao mtafaidikana jasho lenu. Hamna cha kupoteza isipokuwaminyororo ya kinyonyaji.

    Kwa Watanzania wote,  mnaonisikiliza leo,katika ukumbi huu na popote mlipo kupitiavyombo vya habari, mnamo mwaka 1978 Baba

     wa aifa Mwalimu Julius Kambarage Nyererealitangaza vita dhidi ya nduli Idi Amini na kusema:

    “Tutampiga. Sababu za kumpiga tunazo. Niatunayo. Uwezo wa kumpiga tunao”.

    anzania ipo katika vita hivi sasa: Vita dhidi yaUfisadi; Vita dhidi ya uporaji wa rasilimali zetu ;Vita dhidi ya Siasa chafu ; Vita dhidi ya Uchumi

     wa kinyonyaji. Vita dhidi ya kuporomoka kwaUtaifa wetu.

    unapaswa kufanya jambo moja tu, nalo nikupigana vita hizi. Ni vita kwa ajili ya kurejesha

    ndoto tuliyoota miaka 54 iliyopita na Muasisi wetu Mwalimu Julius Nyerere. unataka kurejeshanchi kwa wananchi, tunataka kujimilikisha nchiyetu. Wananchi wawe WENYE nchi! utimizendoto yetu ya kuona;

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    87/88

     AZIMIO LA TABORA JUU YA SIASA YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA78

    anzania yenye Dola madhubuti,

    anzania yenye Wananchi wenye mwamko,

    anzania yenye sekta binafsi iliyochangamka,anzania yenye uchumi unaonufaisha watu wote.

    Sababu tunazo. Nia tunayo. Uwezo tunao. wendeni tukajenge Chama kitakachorejeshamisingi ya aifa letu.

     Asanteni sana

  • 8/21/2019 Azimio La Tabora 2015

    88/88