3
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI IDARA YA UHAMIAJI OFISI YA UHAMIAJI (M) S.L.P 369 MUSOMA AFISA UHAMIAJI MKOA S.L.P 369 MUSOMA. YAH: TAARIFA YA UCHUNGUZI WA URAIA WA WATU WAFUATAO:- PENDO GAWEDA MBOGO NA NYAMBAGA GAWEDA MBOGO Mnamo tarehe 06/07/2012 tulikwenda katika Kijiji cha Salama A, Tarafa ya Chamriho Wilaya ya Bunda kufuatia ombi la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mwanza kututaka tushirikiane na Afisa wake katika kufanya kazi ya uchunguzi wa uraia wa watajwa hapo juu. Maafisa Uhamiaji walioshiriki katika kazi ya uchunguzi majina yao ni kama ifuatavyo:- (i) Konstebo. Benny N. Sanga - Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Bunda. (ii) Koplo. Mbaraka Kh. Vuai - Ofisi ya Uhamiaji Mkoa, Mwanza. Katika kazi hii, tulimpata Ndg. Gaweda Mbogo ambaye ni kaka mkubwa wa familia ya Mzee Mbogo ambaye ni baba mzazi wa watajwa, ambao tulikuwa tunawafanyia uchunguzi kuhusu uraia wao. Aidha tulifanya naye mahojiano ya kina kuhusu historia ya watoto wake Anuani ya Simu: “UHAMIAJI” NUKUSHI: SIMU: +255 282622426 OFISI YA UHAMIAJI WILAYA S.L.P 417 BUNDA Sunday, 21 August 2022

Barua Ya Uchunguzi Gaweda

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Barua Ya Uchunguzi Gaweda

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

IDARA YA UHAMIAJI

OFISI YA UHAMIAJI (M)S.L.P 369MUSOMA

AFISA UHAMIAJI MKOA

S.L.P 369

MUSOMA.

YAH: TAARIFA YA UCHUNGUZI WA URAIA WA WATU WAFUATAO:- PENDO GAWEDA MBOGO NA NYAMBAGA GAWEDA MBOGO

Mnamo tarehe 06/07/2012 tulikwenda katika Kijiji cha Salama A, Tarafa ya Chamriho Wilaya ya Bunda kufuatia ombi la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mwanza kututaka tushirikiane na Afisa wake katika kufanya kazi ya uchunguzi wa uraia wa watajwa hapo juu.

Maafisa Uhamiaji walioshiriki katika kazi ya uchunguzi majina yao ni kama ifuatavyo:-(i) Konstebo. Benny N. Sanga - Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Bunda.(ii) Koplo. Mbaraka Kh. Vuai - Ofisi ya Uhamiaji Mkoa, Mwanza.

Katika kazi hii, tulimpata Ndg. Gaweda Mbogo ambaye ni kaka mkubwa wa familia ya Mzee Mbogo ambaye ni baba mzazi wa watajwa, ambao tulikuwa tunawafanyia uchunguzi kuhusu uraia wao. Aidha tulifanya naye mahojiano ya kina kuhusu historia ya watoto wake ikiwa ni pamoja na kujaza fomu ya maelezo ya Mzee Gaweda Mbogo, ambaye ni baba yao mzazi.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mzee Gaweda Mbogo alizaliwa mwaka 1930 katika Kijiji cha Salama A, Kata ya Salama, Tarafa ya Chamriho, Wilaya ya Bunda, Mkoa wa Mara. Baba yake aliitwa Mbogo Nyakara pia ni mzaliwa wa Kijiji cha Salama A ambaye alifariki mwaka 1984 na kuzikwa Kijiji cha Salama A. Aidha mama yake aliitwa Nyambaga Mathaba ambaye alizaliwa kijiji cha Salama A na kuzikwa hapo hapo kijijini.

Anuani ya Simu: “UHAMIAJI”NUKUSHI:

SIMU: +255 282622426

KUMB .NA.BND/IMM//INV/VOL.11/01/13

/1/1105

OFISI YA UHAMIAJI WILAYAS.L.P 417BUNDAThursday, 27 April 2023

Page 2: Barua Ya Uchunguzi Gaweda

Mzee Mbogo alibahatika kupata watoto ishirini na nne (24) kwa wanawake wawili. Mke wake wa kwanza aliitwa Wathato Mahuza (Mtanzania) alifanikiwa kupata watoto kumi na mbili (12). Hata hivyo, alifariki mwaka 1984 na kuzikwa katika kijiji cha Salama A. Mke wa pili aliitwa Kurwa Zagara (Mtanzania) ambaye alifanikiwa kupata watoto kumi na mbili (12); miongoni mwao ni Pendo Gaweda Mbogo ambaye kwa sasa anaishi Mwanza. Na wa pili anaitwa Nyambaga Gaweda Mbogo ambaye pia anaishi Mwanza.

Kwa mujibu wa uchunguzi tulibaini kuwa maelezo yaliyotolewa na wahusika yalikuwa ni ya kweli kulingana na taarifa alizotoa baba mzazi wa wahusika, Mzee Gaweda Mbogo.

Naomba kuwasilisha.

…......................................... CONST. BENNY N. SANGA