BULLETIN 96 PRINT.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

  • 7/23/2019 BULLETIN 96 PRINT.pdf

    1/9

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali

    kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizar a ya Nishati na MadiniWasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263

    au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    HABARI ZA

    NISHATI &MADINI

    Toleo No. 96 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Desemba 4 - 10, 2015Bulletinews

    http://www.mem.go.tz

    SomahabariUk.2

    Serikali yatenga zaidi ya Dola milioni 3 kwa Wachimbaji Wadogo

    No ENEO LA UCHIMBAJI MKOA WILAYA

    1 Mererani Block I-V Manyara Simanjiro

    2 Kilindi Tanga Kilindi

    3 Maganzo Shinyanga Kishapu

    4 Mihama Mwanza Misungwi

    5 Winza Dodoma Mpwapwa

    6 Ibaga Singida Iramba

    7 Mpambaa Singida Iramba

    8 Nyakunguru Mara Tarime

    9 Mbesa Ruvuma Tunduru

    10 Vianzi-Mindevu Pwani Kibaha

    11 Lugweni- Mwanadilatu Pwani Kibaha

    12 Ilagala Kigoma Kigoma

    13 Melela Morogoro Mvomero

    14 Dete-Mwalazi Pwani Mkuranga

    15 Nyangwale Shinyanga Kahama

    16 Itumbi B Mbeya Chunya

    17 Makanya Kilimanjaro Same

    18 Mwajanga Manyara Simanjiro

    19 Nyamwironge Kigoma Kakonko

    20 Saza Mbeya Chunya

    21 Kalela Kigoma Kigoma

    22 Ilujamate Mwanza Misungwi

    23 Viziwaziwa Pwani Mkuranga

    24 Kwa Mpa Pwani Kibaha

    25 Nyangalata Shinyanga Kahama

    26 Maguja Lindi Nachingwea

    27 Buzwagi Shinyanga Kahama

    28 Kinamiyuba Shinyanga Kahama

    29 Selemi Tabora Nzega

    30 Mumba Tabora Nzega

    31 Bukene Tabora Nzega

    32 Ibologelo Tabora Igunga

    34 Nyamongo Mara Tarime

    No ENEO LA UCHIMBAJI MKOA WILAYA

    Neema kwaWachimbajiWadogo Serikaliyatenga zaidi yaekari 190,000

    uchimbaji madini

  • 7/23/2019 BULLETIN 96 PRINT.pdf

    2/9

    2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Rhoda James

    Serikali kupitia Wizara yaNishati na Madini imetengamaeneo 34 katika sehemumbalimbali nchini yenyeukubwa wa ekari 197,432

    kwa ajili ya uchimbaji madini kwawachimbaji wadogo nchini.

    Hayo yameelezwa na Msemajiwa Wizara ya Nishati na Madini,Badra Masoud hivi karibuni wakatiakizungumza na vyombo vya habari

    jijini Dar es Salaam.Masoud alisema kuwa dhamana ya

    kutenga maeneo hayo, hupewa Waziriwa Nishati na Madini kwa mujibuwa Sheria ya Madini ya mwaka 2010,kifungu cha 16 ambacho kinampamamlaka Waziri husika kutenga eneolililo wazi na lenye madini kwa ajili yauchimbaji madini mdogo.

    Masoud aliongeza kuwa zoezi la

    kutenga maeneo hayo 34 ni kielelezocha Serikali kuendelea kuwajaliwachimbaji wadogo ili kuufanyauchimbaji huo kuwa wenye tija nahivyo kusaidia kukuza uchumi wa mtummoja mmoja na serikali kwa ujumla.

    Aliitaja baadhi ya mikoa yenyemaeneo hayo kuwa ni pamoja na;Mwanza, Tanga, Shinyanga, Manyara,Dodoma, Singida, Mara, Ruvuma,Pwani, Kigoma, Morogoro, Mbeya,Lindi, Kilimajaro na Tabora.

    Pia alisisitiza kuwa Wizara yaNishati na Madini itawawezeshawachimbaji hao wadogo kuendeshashughuli zao kwa kutumia teknolojiaya kisasa na yenye tija zaidi kwenyemaeneo hayo tengefu.

    Vilevile aliwaasa wachimbajiwadogo kuzingatia sheria zilizopo ilikuepukana na uchimbaji holela ambaohupelekea wachimbaji hao kuhatarishamaisha yao.

    Neema kwa Wachimbaji Wadogo

    Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud akitoa taarifaya utengaji maeneo ya wachimbaji wadogo wa madini mbele yawaandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawapo pichani).

    Serikali yatenga zaidi ya Dolamilioni 3 kwa Wachimbaji Wadogo

    Na Remija Salvatory

    Serikali kwa kushirikiana naBenki ya Dunia imetenga kiasicha Dola za Marekani Milioni3 kwa miaka mitatu kuanziamwaka huu wa fedha 2015/16

    kwa ajili ya kuwawezesha wachimbajimadini wadogo kwa kuwapatia ruzukukwa awamu ya tatu ili waweze kuchimbakisasa na kujikwamua na umaskini.

    Akizungumza na waandishi wahabari, Msemaji wa Wizara ya Nishatina Madini, Badra Masoud alisema,Awamu ya Kwanza ya Ruzuku ilitolewamwaka wa fedha 2013/14 na ilikuwajumla ya Dola za Marekani 500,000ambapo vikundi vya wachimbaji wadogovipatavyo 11 vilinufaika.

    Masoud aliongeza kuwa awamu ya piliilitolewa katika mwaka wa fedha 2014/15ambapo jumla ya Bilioni 7.2 zilitolewakwa vikundi 111 vya wachimbaji wadogopamoja na watoa huduma, wengi waowakiwa ni vikundi vya akina mamakwenye migodi ya wachimbaji madiniwadogo.

    Akizungumzia utaratibu wakutoa fedha hizo, Masoud alisema, ilikuhakikisha fedha hizo zinawafikiawalengwa, Serikali imeandaa mpangomadhubuti ambapo mchimbaji mdogolazima awe na leseni ya uchimbaji wamadini, atachukua fomu za kuombaruzuku na kuwasilisha katika Ofisi yaMadini.

    Aliendelea kusema kuwa, Afisa wa

    Madini wa Kanda atakagua eneo lamchimbaji na kubaini hatua aliyofikia,kisha fomu itapelekwa Benki ya

    Uwekezaji ya Tanzania (TIB) na baada yakuhakikiwa utaratibu wa kuwawezeshautaandaliwa.

    Alisema hatua hiyo ya utoaji ruzukuimekuja baada ya Serikali kubainikwamba wachimbaji wadogo wa madiniwalio wengi huchimba kwa kutumia zanana vifaa duni kutokana na kutokuwa nafedha za kununulia vifaa vya kisasa hukuwengi wao wakiwa hawawezi kukidhimasharti ya kupata mikopo katika Benkiza Biashara nchini.

    Alisisitiza kuwa, Serikali kupitia ofisizote za madini nchini inatoa Elimu kwawachimbaji wadogo ili kuhakikisha kuwakuna usalama katika maeneo yao ya kazi,wanalinda afya zao na kutumia vifaavinavyotakiwa katika shughuli zao.

    Alitumia fursa hiyo kuwaasawachimbaji wadogo kufuata

    sheria,taratibu na kanuni za uchimbajiwa madini ili kulinda usalama waona kuzingatia elimu wanayoipata ilikudumisha amani na kukuza kipato chao.

    Alisema endapo itabainika kuwawahusika wameshindwa kutekeleza nakufikia malengo ya mradi, Wizara kwakushirikiana na TIB itatoa notisi ya sikuThelathini kwa mhusika juu ya kusudiola kusitisha mkataba na iwapo atatumiafedha ya ruzuku kinyume na malengoyaliyokusudiwa na ikagundulika kuwakuna udanganyifu wakati wa utekelezajiwa mradi mfano kughushi nyarakamuhusika hatapata fidia yoyote.

    Alifafanua kuwa Serikali imewekautaratibu husika ili kuwajengeauwezo wachimbaji wadogo waweze

    kukopesheka, kuondokana na umaskinina kuepukana na vifo vinavyotokea kwakutokufuata taratibu wakati wa uchimbaji.

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINI

    TAHADHARI YA UTAPELI

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI INAWATAARIFU WANANCHI

    KUJIHADHARI NA WATU WANAOTUMIA JINA LA KATIBU MKUUWIZARA YA NISHATI NA MADINI MHANDISI OMAR CHAMBOKUTAPELI WANANCHI NA WATUMISHI KATIKA TAASISI ZA SERIKALI.

    WATU HAO WAMEKUWA WAKIWAPIGIA SIMU BAADHI YAWATUMISHI WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI NA TAASISI ZAKEWAKIJITAMBULISHA KWA JINA LA MHANDISI OMAR CHAMBO NAKUTOA MAAGIZO MBALIMBALI ILI YAFANYIWE UTEKELEZAJI.

    VILEVILE WATU HAO HUTOA MAAGIZO YA KUTUMIWA FEDHA KWANJIA YA SIMU, NA MOJA YA NAMBA INAYOTUMIKA NI 0676 856 862.

    TUNATOA ONYO KALI KWA WATU WANAOTUMIA VIBAYA JINALA MHANDISI OMAR CHAMBO KUWA HATUA KALI ZA KISHERIAZITACHUKULIWA DHIDI YAO.

    IMETOLEWA NA;KITENGO CHA MAWASILIANO,

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

  • 7/23/2019 BULLETIN 96 PRINT.pdf

    3/9

    3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    FIVEPILLARS OFREFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMUKITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI

    MHARIRI MKUU:Badra MasoudMSANIFU: Lucas Gordon

    WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, GreysonMwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,

    Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

    INCREASE EFFICIENCY

    QUALITY DELIVERYOF GOODS/SERVICE

    SATISFACTION OFTHE CLIENT

    SATISFACTION OFBUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OFSHAREHOLDERS

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Kwa Ruzuku hii, Hapa kazi Tu,

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Maji ya Mtera yatunzwe- Chambo

    Wiki hii Wizara ya Nishati na Madini imetoa taarifakwa wananchi kuwa Serikali kwa kushirikiana na Benkiya Dunia imetenga kiasi cha Dola za Marekani milioni 3kwa miaka mitatu kuanzia mwaka huu wa fedha 2015/16kwa ajili ya ruzuku kwa wachimbaji madini wadogo nchinina watoa huduma.

    Hii ni kusema kwamba Serikali inaendelea kutekelezaahadi yake ya kutoa Ruzuku kwa wachimbaji wadogoambapo Ruzuku hii ya Awamu ya Tatu itawawezeshawachimbaji hao kuchimba madini kisasa, kujiongezeavipato vyao na pia kuchangia katika Pato la Taifa.

    Awamu ya Kwanza ya Ruzuku ilitolewa katika mwakawa Fedha 2013/14 ambapo jumla ya Dola za Marekani500,000 sawa na shilingi za kitanzania takribani BilioniMoja zilitolewa kwa vikundi vya wachimbaji wadogo 11.

    Aidha, Awamu ya Pili ilitolewa katika mwaka wa Fedha2014/15 ambapo jumla ya shilingi bilioni 7.2 zilitolewakwa vikundi 111 vya wachimbaji wadogo pamoja nawatoa huduma (wengi wao wakiwa ni vikundi vya akinamama) kwenye migodi ya wachimbaji madini wadogo.

    Hatua hii ya Serikali imekuja baada ya kubainikwamba wachimbaji wengi wadogo huchimba madinikwa kutumia zana na vifaa duni kutokana na kutokuwana fedha za kununulia vifaa vya kisasa huku wengi waowakiwa hawawezi kukidhi masharti ya kupata mikopokatika Taasisi za Fedha.

    Hakika Serikali imeamua kuwajengea uwezowachimbaji wadogo ili nao wafikie hatua ya kuwezakukopesheka katika benki za kibiashara na Taasisi zaFedha.

    Pamoja na kuwapatia wachimbaji hao ruzuku; Serikaliitaendelea kuwapatia elimu ya uchimbaji wa kisasa nanamna ya kuepukana na ajali ndani ya migodi pamoja nautunzaji wa mazingira katika maeneo wanayofanyia kazi.

    Vilevile ili kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumikakwa kazi iliyokusudiwa, Serikali itaendelea kuwa karibuna wachimbaji wadogo hususan wale wote waliopatiwaruzuku ili uchimbaji huo uwe wenye tija kama lilivyo lengola Serikali.

    Ikumbukwe kwamba ili kupata Ruzuku husika ni

    lazima mchimbaji awe na leseni ya uchimbaji, ajaze fomuza kuomba ruzuku, na mchimbaji kutoa ushirikiano kwaMaofisa Madini wa Kanda na Maofisa wa ofisi za AfisaMadini Wakazi kukagua eneo la mchimbaji anayeombaruzuku.

    Vilevile iwapo mchimbaji au wachimbaji wa madiniwadogo waliopewa Ruzuku hawatatumia fedha hizokama ombi lao lilivyoainisha, Benki ya Maendeleo ya(TIB) ambayo ndiyo iliyopewa dhamana ya kusimamiamalipo hayo inaweza kusitisha mkataba huo baada yakushauriana na Wizara ya Nishati na Madini.

    Hakika ni juhudi za kupongezwa kwa Wizara yaNishati na Madini na Serikali kwa ujumla kwa kuamuakuendeleza wachimbaji wadogo nchini. Tunatoa witokwa wote wanaopata ruzuku hizi, kutumia fedha hizo

    kama inavyoelekezwa ili kuwezesha wachimbaji na watoahuduma wengine kunufaika na Ruzuku zinazotolewa.

    Na Teresia Mhagama

    K

    atibu Mkuu wa Wizara ya Nishatina Madini, Mhandisi OmarChambo amewataka wataalamwa Shirika la Umeme nchini(TANESCO) kuhakikisha maji

    yanayoingia katika Bwawa hilo yanatunzwakatika kipindi chote cha mwaka ili kuwezakuzalisha umeme kwa mwaka mzima.

    Katibu Mkuu aliyasema hayo wakatialipofanya ziara ya kukagua Bwawa hilolililopo mpakani mwa mikoa ya Iringana Dodoma pamoja na kuzungumza nawataalam wa TANESCO wanaosimamiaBwawa husika.

    Kweli tumeona Bwawa limekauka lakiniwataalam mnao uwezo wa kutunza majimwaka mzima kwa kutumia utaalam wenukuhakikisha kwamba maji huko yanakotokahayatumiwi vibaya, lazima kuna utaalam waugawaji bora wa maji, nyinyi wataalam ndiomuwasaidie wakulima suala hili ili kusiwena upungufu wa maji ya kuzalisha umeme,

    alisema Mhandisi Chambo. Pia aliiagiza TANESCO kuunda timu

    ya wataalam itakayohusisha wadau kutokasekta mbalimbali ikiwemo kilimo, mifugo,maliasili, mazingira, Serikali za Mitaa naTaasisi zisizokuwa za Serikali ili kuweza kujana njia mbadala itakayowezesha nchi kuwana matumizi endelevu ya maji kutoka katikavyanzo vinavyopeleka maji katika Bwawahilo la Mtera.

    Mmekabidhiwa dhamana hii,

    msibweteke na kusubiri matokeo, undenitimu za kutatua changamoto za maji, sisi niwataalam hivyo lazima tushauri.Tumepotezamegawati 80 kutokana na Bwawa hili kuzimamitambo ya uzalishaji umeme, hizi nimegawati nyingi sana kupotea katika gridi ya

    Taifa hivyo tusifanye mzaha katika utatuzi wajambo hili, alisema Chambo.

    Aidha, Katibu Mkuu Chambo aliwatakawataalam hao kuzingatia maadili katikautekelezaji wa majukumu yao ya kila sikukatika Bwawa hilo na kutumia utaalam waokatika kusaidia nchi na si vinginevyo.

    Awali akitoa taarifa ya kituo hicho, MenejaUzalishaji Umeme wa Maji nchini, MhandisiAntony Mbushi alieleza kuwa maji katikaBwawa la Mtera hukauka kutokana nasababu mbalimbali ikiwemo upatikanaji wamvua kidogo, na kuongezeka kwa matumiziya maji ambayo si endelevu akitolea mfanokuongezeka kwa shughuli za kilimo ambapompaka sasa jumla ya ekari 21,000 zinatumiamaji hayo kwa umwagiliaji.

    Alitaja sababu nyingine kuwa ni mvuke

    ambao huchangia asilimia 25 ya upotevuwa maji hayo na kueleza kuwa Bwawa hilohupata maji kutoka mto Ruaha mkubwa,Mto Ruaha Mdogo na mto Kisigo.

    Bwawa la Mtera linalozalisha umeme wakiasi cha megawati 80 lilisimamisha uzalishajitarehe 7 Oktoba, 2015 baada ya kiwangocha maji katika Bwawa hilo kufika chini yamita 690. Endapo umeme utazalishwa chiniya kiwango hicho upepo huweza kuingiakatika mitambo ya uzalishaji umeme na hivyokusababisha uharibifu.

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo

    BWAWA LA MTERA

  • 7/23/2019 BULLETIN 96 PRINT.pdf

    4/9

    4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Nuru Mwasampeta na RemijaSalvatory

    Wizara ya Nishatina Madini naKampuni ya

    PriceWaterhouseCoopers (PWC)inayojishughulisha na masuala ya tafitimbalimbali zimesaini mkataba wakufanya tathmini ya utendaji kazi wakena utoaji wa huduma kwa wateja.

    Zoezi la kusaini mkataba huo

    lilifanyika hivi karibuni jijini Dar esSalaam kati ya Naibu Katibu Mkuuwa Wizara, Mhandisi Paul Masanjana Mkurugenzi wa Kampuni ya PWC,Maryanne Massawe.

    Mhandisi Masanja aliitaka kampunihiyo kufanya kazi kwa wakati ili kwendasambamba na kasi ya utendaji waSerikali iliyopo madarakani ili kufikiakwa malengo na kuiwezesha Wizarakuboresha utendaji kazi wake pamojana kufahamu namna ambavyo hudumazake zinapokelewa na wananchi katikamaeneo mbalimbali.

    Aidha, Mhandisi Masanjaaliwaeleza wataalamu hao kwambaanahitaji taarifa sahihi na zenyevielelezo vya kutosha na kuongeza

    kuwa katika kazi hiyo asingependakazi iliyonakiliwa kutoka kwenye kazinyingine za aina hiyo zilizofanywakatika kipindi cha nyuma.

    Wataalamu hao walimhakikishiakuwa kazi hiyo itafanyika kwa umakinimkubwa kama makubaliano yalivyokatika mkataba uliosainiwa.

    Akizungumzia muda uliopangwakatika utekelezaji wa kazi hiyo,Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu yaUfuatiliaji na Tathmini katika Idara yaSera na Mipango, Wizara ya Nishati naMadini, James Mganga alisema utafitihuo unatarajiwa kukamilika ndani yasiku 45.

    Aidha, Mganga alisema utafiti huoutaanzia Makao Makuu ya Wizara

    pamoja na Ofisi zote za Madini zaKanda ambazo alizitaja kuwa ni Kandaya Mashariki - Dar es Salaam, Kandaya Magharibi- Mpanda, Kanda ya ZiwaViktoria Magharibi - Mwanza, Kandaya Ziwa Victoria Mashariki Musoma,Kanda ya Kaskazini Arusha, Kandaya Kusini Mtwara, Kanda ya KatiMagharibi Shinyanga, Kanda ya Kati- Singida, Kanda ya Kusini Magharibi

    Mbeya, na Kanda ya Ziwa Nyasa Songea.

    Vilevile, Mganga alisema utafitihuo utazihusisha taasisi zote zilizopochini ya Wizara ya Nishati na Madiniambazo ni Wakala wa Nishati Vijiji(REA), Shirika la Maendeleo ya Petroli(TPDC), Kampuni ya Uendelezaji

    Jotoardhi Tanzania (TGDC), Wakalawa Ukaguzi wa Madini Tanzania(TMAA), Wakala wa Jiolojia Tanzania

    Wajumbe walioshiriki kikao cha kusaini Mkataba waUtafiti wa kiutendaji na huduma zinazotolewa na Wizaraya Nishati na Madini wakiongozwa na Naibu KatibuMkuu Mhandisi Paul Masanja (wa kwanza kushoto).

    Mkurugenzi Mkuu wa PriceWaterhouseCoopers Bimal Ghathi (kulia) akitoamaelezo kwa watendaji wa Wizara(hawapo pichani) juu ya hatuazitakazofuatwa wakati wa utekelezajiwa kazi hiyo. Kulia kwake ni MkurugenziMtendaji wa Kampuni hiyo MaryanneMassawe.

    Naibu KatibuMkuu wa Wizaraya Nishati naMadini MhandisiPaul Masanjaakipeanamkono naMkurugenziMtendaji waPricewaterhouseCoopers

    MaryanneMassawe baadaya kubadilishanaMpango kazi naMakubaliano yakazi wakati wautafiti.

    (GST), Shirika la Madini la Taifa(STAMICO) na Chuo cha MadiniDodoma (MRI).

    Kwa upande wake MshauriMwelekezi wa kampuni hiyo BimalGatha alipotakiwa kuelezea hatuazitakazofuatwa katika utekelezaji wakazi hiyo alisema kazi hiyo itafuatampango kazi uliokubaliwa baina yawizara na kampuni jinsi ilivyosainiwa.

    Gatha alisema ndani ya wiki mojabaada ya kusainiwa kwa mkatabawatawasilisha maswali/madodosoyaliyoandaliwa kwa ajili ya utafiti iliWizara iweze kujiridhisha endapo

    maswali hayo hayana utata na

    yataweza kueleweka kwa wananchiwa kawaida.

    Aidha, wataelezea maeneoyaliyopendekezwa katika kufanyautafiti huo na kwamba wanakadiriakuhusisha watu 500 hadi 700watakaojibu maswali hayo.

    Baada ya hapo kazi ya utafiti itaanzaambapo itachukua siku 30 baadaya mkataba kusainiwa na baadayekufanyiwa uchambuzi na kuja namajibu yatakayowasilishwa wizarani.Taarifa hiyo ya utafiti itapitiwa naWizara ambapo watawasilisha maoniyao yatakayotumika katika uandishi

    wa Taarifa ya mwisho ambayo

    itawasilishwa si zaidi ya siku nanebaada ya kufanyiwa kazi kwa maoniyaliyotolewa na wizara.

    Akifafanua Zaidi, Gathaalisema kuwa utafiti huo utafanyikaukiongozwa na Taarifa na Nyaraka

    mbalimbali za wizara kama vileMpango Mkakati wa Wizara waMwaka 2011/2012 - 2015/2016, Seraya Taifa ya Madini ya Mwaka 2009,Mpango wa Maendeleo wa MiakaMitano, Hotuba za Bajeti za Mwaka2011/2012 - 2014/2015 na taarifazozote zitakazofaa kutumika katikakazi hiyo.

    Mara ya mwisho, Utafiti kama huoulifanyika katika mwaka wa fedha2003/2004 - 2005/2006 ambapoulisaidia katika uandaaji wa MpangoMkakati wa kwanza wa Wizara waMwaka 2011/2012 - 2015/2016 nautafiti utakaofanyika sasa utasaidiakukamilisha Mpango Mkakati waWizara kwa Mwaka 2016/2017

    2020/2021.

    Wizara yasaini mkataba

    kuboresha utendaji

  • 7/23/2019 BULLETIN 96 PRINT.pdf

    5/9

    5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    MKATABA JOTOARDHI

    Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Tanzu ya Uendelezaji Jotoardhi (TGDC), MhandisiBoniface Njombe (Wa pili kushoto), akieleza jambo wakati wa kikao cha kusainiMkataba wa Makubaliano utakaowezesha Tanzania kunufaika na msaada wa kiasi chaDola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tatikatika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi; kuwajengea uwezo wataalam wa ndanikatika tasnia hiyo ikiwemo pia kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya utati wa nishatihiyo. Wengine wanafuatilia ni Meneja wa Sheria wa TGDC, Meshil Kivuyo (katikati), NaMtaalamu kutoka TGDC.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (katikati),akijadiliana jambo na Asa Sheria wa Wizara Yese Malolela wakati wa kusaini Mkatabawa Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tatikatika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi. Kushoto ni Mkurugenzi wa ICEIDA,Engilbert Gudmundsson akisaini Mkataba huo, akishuhudiwa na Meneja Mipangowa ICEIDA, David Bjarnason, kulia mbele ni Mkurugenzi Mkuu wa TGDC, MhandisiBoniface Njombe akijadiliana jambo na Meneja wa Sheria TGDC, Marshil Kivuyo,wengine wanaofuatilia ni Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia nishati Jadidifu,Edward Ishengoma.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi Paul Masanja (katikati) na Wataalamu kutokaWizara ya Nishati na Madini, TGDC na ICEIDAwakimsikiliza, Mkurugenzi wa ICEIDA, EngilbertGudmundsson (wa kwanza kushoto).

    Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Tanzu ya UendelezajiJotoardhi (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (Wakwanza kushoto mbele), akichukua matukio ya pichawakati wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishatina Madini, Mhandisi Paul Masanja na Mkurugenzi waICEIDA, Engilbert Gudmundsson (hawapo pichani)wakisaini Mkataba kwa ajili ya kupata MtaalamMwelekezi kufanya tati katika maeneo yenye viashiriavya Jotoardhi; kuwajengea uwezo wataalam wa ndanikatika tasnia hiyo ikiwemo pia kuwezesha upatikanajiwa vifaa vya utati wa nishati hiyo. Wanafuatilia niWatalaamu kutoka TGDC na Kamishna MsaidiziNishati anayeshughulikia nishati Jadidifu, EdwardIshengoma.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi Paul Masanja ( katikati), akibadilishanaMkataba na Mkurugenzi wa ICEIDA, EngilbertGudmundsson (Wa kwanza kushoto). Kulia niwataalam kutoka TGDC na Wizara wakifuhia jambomara baada ya tukio la kusaini Mkataba huo.

  • 7/23/2019 BULLETIN 96 PRINT.pdf

    6/9

    6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Iceland yawezesha TGDC kutafti JotoardhiNa Asteria Muhozya,Dar es Salaam

    Serikali kupitia Kampuni Tanzuya Uendelezaji JotoardhiTanzania, (TGDC) na Shirikala Kimataifa la Maendeleola Iceland (ICEIDA),

    wamesaini Mkataba wa Makubalianoutakaowezesha Tanzania kunufaikana msaada wa kiasi cha Dola zaMarekani 1,565,000 kwa ajili ya kupataMtaalam mwelekezi kufanya tafiti katikamaeneo yenye viashiria vya Jotoardhi;kuwajengea uwezo wataalam wandani katika tasnia hiyo ikiwemo piakuwezesha upatikanaji wa vifaa vyautafiti wa nishati hiyo.

    Makubaliano hayo yalifikiwa hivikaribuni jijini Dar es Salaam, MakaoMakuu ya Wizara ya Nishati naMadini hivi karibuni, kati ya NaibuKatibu Mkuu wa Wizara ya Nishatina Madini, Mhandisi Paul Masanjana Mkurugenzi Mkuu wa ICEIDA,Engilbert Gudmundsson, ambapotukio hilo lilishuhudiwa na MenejaMkuu wa TGDC, Mhandisi BonifaceNjombe, Kamishna Msaidizi wa Nishatianayeshughulikia Uendelezaji waNishati Jadidifu, Edward Ishengoma,

    baadhi ya Maafisa kutoka TGDC naWizara ya Nishati na Madini.

    Akizungumza wakati wa tukio hilo,Naibu Katibu Mkuu Mhandisi PaulMasanja alisema kuwa, matarajio yaTanzania ni kuzalisha kiasi cha megawati200 za umeme unaotokana na nishati ya

    jotoardhi ifikapo mwaka 2020 ambapo

    taarifa za awali zinaeleza kuwa, hazinailiyopo kupitia nishati hiyo ina uwezo wakuzalisha zaidi ya megawati elfu tano zaumeme (5,000), unaotokana na nishatiya jotoardhi .

    Aidha, Mhandisi Masanja aliongezakuwa, utayari na ushirikiano iliyouonesha

    nchi ya Iceland kupitia ICEIDA itakuwakichocheo kikubwa kufikia malengo yaSerikali ya kuwa na nishati ya kutosha yaumeme kutoka vyanzo mbalimbali.

    Tuna malengo yetu mengi kupitianishati hii, utafiti ndio njia itakayotufanyakufikia malengo yetu hivyo, ushirikiano

    huu ni mwanzo mzuri kwa upande wetu.Nafahamu Iceland mlianzia katika hatuaza chini kabisa lakini sasa mko mbali.Naamini uzoefu wenu utatuwezeshakuweza kufika mahali tunapotarajia,aliongeza Mhandisi Masanja.

    Aidha, Masanja aliitaka Kampuni ya

    TGDC, kuhakikisha inashirikiana vizurina nchi ya Iceland ikiwemo shirika laICEIDA kuhakikisha linafuata ushaurimzuri wa kitaalamu unaotolewa nashirika hilo ili kuweza kupata uzoefu,

    jambo ambalo litawezesha sekta yajotoadhi nchini kupiga hatua na hivyokuifanya jotoardhi kuwa chanzo kinginecha nishati ya umeme.

    Kwa upande wake, MkurugenziMkuu wa TGDC, Mhandisi BonifaceNjombe, alishukuru utayari wa ICEIDAkatika kuhakikisha kwamba Tanzaniainafikia malengo yake ya kuendelezanishati hiyo, utayari ambao utasaidiakufanyika kwa tafiti katika maeneoyenye viashiria vya jotoardhi ya Luhoi,na Kibiti, Mkoa wa Pwani.

    Vilevile, Mhandisi Njombe alielezakuwa, kutokana na utafiti utakaofanywa,utawezesha upatikanaji wa takwimusahihi ambazo zitafungua njia ya kupatamsaada zaidi kutoka katika taasisiambazo zimejikita katika masuala yenyeuhusiano na nishati ya jotoardhi, jamboambalo pia litawezesha uendelezaji wanishati hiyo nchini.

    Aidha, Mhandisi Njombealitumia fursa hiyo pia kueleza hatuambalimbali ambazo tayari zimefanywana kampuni hiyo katika kuhakikishakwamba, jotoardhi inakuwa chanzokingine cha uzalishaji umeme nchini nakuongeza kuwa, kupitia makubalianohayo, ICEIDA itawezesha wataalamwa ndani wa TGDC kupata ujuzi na

    uzoefu utakaowezesha kufanyika kwatafiti nyingine katika maeneo ya Kiejo/

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (katikati), sambamba na MkurugenziMkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Iceland (ICEIDA), Engilbert Gudmundsson, wakisaini Mkatabawa Makubaliano utakaowezesha Tanzania kunufaika na msaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwaajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tati katika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi katika maeneo yaLuhoi na Kibiti, Mkoa wa Pwani na Kiejo/Mbaka Mkoa wa Mbeya. Wanaoshuhudia ni Meneja Mkuu wa TGDC,Mhandisi Boniface Njombe na Asa Sheria kutoka Wizara ya Nishati na Madini Yese Malolela.

    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Iceland (ICEIDA), Engilbert Gudmundsson,(aliyenyoosha mkono), akieleza jambo wakati wa kikao cha kusaini Mkataba wa Makubaliano utakaowezeshaTanzania kunufaika na msaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata Mtaalam Mwelekezikufanya tati katika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi katika maeneo ya Luhoi na Kibiti, Mkoa waPwani na Kiejo/Mbaka Mkoa wa Mbeya; kuwajengea uwezo wataalam wa ndani katika tasnia hiyo ikiwemopia kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya utati wa nishati hiyo. Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (katikati), wanaoshuhudia ni Meneja Mipango wa ICEIDA (kushoto),David Bjarnason, kulia ni Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni ya TGDC .

    >> Inaendelea Uk. 7

  • 7/23/2019 BULLETIN 96 PRINT.pdf

    7/9

    7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Iceland yawezesha TGDC kutafti JotoardhiMbaka, Mkoa wa Mbeya.

    Naye, Mkurugenzi wa ICEIDA, Engilbert

    Gudmundsson alieleza umuhimu wa nishati hiyo naunafuu wake wa gharama ikilinganishwa na nishatinyingine na kueleza kuwa, asilimia 25 ya umemeunaozalishwa nchini Iceland unatokana na nishati yaotoardhi.

    Ilituchukua kipindi cha miaka 25 kufikia mafanikiotuliyonayo katika nishati ya jotoardhi. Kutokana naubobezi huu ni vema kwetu kutoa uzoefu kwa TGDCkuhakikisha inafakia malengo tarajiwa na kwambaotoardhi inakuwa chanzo kingine cha umeme

    kwa Tanzania ambao ni rahisi na nafuu,aliongezaEngilbert.

    Jotoardhi ni mojawapo ya chanzo cha nishatikitokanacho na mvuke unaotoka ardhini, hususankatika maeneo yaliyo katika Bonde la Ufa (Rift Valley).Nchi zilizo katika bonde la Ufa (African Rift GeothemalFacility ARGeo) ni pamoja na Djibouti, Eritrea,

    Ethiopia, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.Tayari Tanzania imefanya jitihada kadhaa zakuendeleza Jotoardhi ikiwemo uanzishwaji waKampuni ya TGDC, ambayo ni Kampuni Tanzu yaShirika la Umeme nchini (TANESCO), iliyoanzishwamwezi Juni, 2014. TGDC inatajwa kuwa kichocheomuhimu cha uendelezaji wa nishati ya jotoardhi.Aidha, mwishoni mwa mwezi Oktoba hadi mwanzonimwa Novemba 2014, Tanzania ilikuwa Mwenyejiwa Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Jotoardhiuliofanyika Jijini Arusha.

    Mkutano wa Jotoardhi unatajwa kuinufaishaTanzania katika kuhamasisha matumizi ya nishatiadidifu ili kuchangia upatikanaji wa nishati hiyo nchini;

    kubadilishana uzoefu na uelewa na wataalamu kutokanchi mbalimbali duniani; ikiwemo pia kuharakishauendelezaji wa jotoardhi.

    >> Inatoka Uk. 6

    Mkurugenzi Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe (wa nne kutoka kulia) akisaini Mkatabawa Makubaliano sambamba na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Iceland(ICEIDA), Engilbert Gudmundsson. Mkataba huo utawezesha Tanzania kunufaika na msaada wakiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tati katikamaeneo yenye viashiria vya Jotoardhi katika maeneo ya Luhoi na Kibiti, Mkoa wa Pwani naKiejo/Mbaka Mkoa wa Mbeya. Vilevile msaada huo utawezesha pia kuwajengea uwezo wataalamwa ndani katika tasnia hiyo ikiwemo kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya utati wa nishati hiyo.Wanaoshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja(katikati), Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshugulikia Nishati Jadidifu Edward Ishengoma (Wakwanza kulia) na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na ICEIDA

    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleoa Iceland (ICEIDA), Engilbert Gudmundsson (kushoto)na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na MadiniMhandisi Paul Masanja (kulia) wakibadilishana Mkataba

    wa Makubaliano utakaowezesha Tanzania kunufaika namsaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwaajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tati katikamaeneo yenye viashiria vya Jotoardhi katika maeneo yaLuhoi na Kibiti, Mkoa wa Pwani na Kiejo/Mbaka Mkoawa Mbeya. Vilevile, Mkataba huo utawezesha kuwajengeauwezo wataalam wa ndani katika tasnia hiyo ikiwemo

    na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya utati wa nishatihiyo. Katikati ni Asa Sheria kutoka Wizara ya Nishati naMadini, Yese Malolela.

    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Iceland (ICEIDA), EngilbertGudmundsson (Wa tatu kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati naMadini , Mhandisi Paul Masanja (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mkuuwa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe (Wan ne kulia) Kamishna Msaidizi wa Nishati

    anayeshughulikia Uendelezaji wa Nishati Jadidifu, Edward Ishengoma,(Wa kwanza kushoto),Meneja Mipango wa ICEIDA, David Bjarnason, na baadhi ya Maasa kutoka TGDC naWizara ya Nishati na Madini.

  • 7/23/2019 BULLETIN 96 PRINT.pdf

    8/9

    8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    ziara ya KATIBU MKUU chambo

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wakwanza kulia) akizungumza na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madinina Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mara baada ya kuwasili katikakituo cha kuzalisha umeme wa maji cha Mtera ili kukagua maendeleo yauzalishaji ya kituo hicho na kuzungumza na wataalam.Wa tatu kutokakulia ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi HoseaMbise) na wa nne kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria Wizaraya Nishati na Madini, Justus Mulokozi.

    Katibu Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi Omar Chambo (watatu kutoka kulia) akiangalia kima cha maji kilichopo katika Bwawa la Kidatumkoani Morogoro ambapo kimepungua kutoka mita 450.00 hadi mita439.48 kukia tarehe 27 Novemba 2015.Wa kwanza kulia ni Kamishna waNishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Hosea Mbise.

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wanne kushoto) akiwa katika mgodi wenye mitambo ya kuzalisha umemekatika kituo cha Kidatu mkoani Morogoro mara baada ya kukaguamitambo ya uzalishaji umeme na bwawa la kuhifadhia maji ya kuzalishaumeme katika kituo hicho.Wengine katika picha ni Kamishna wa Nishatina Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Hosea Mbise (wa tatu kushoto),Meneja wa Kituo cha Kidatu, Eng. Justus Mtolera (kushoto kwa KatibuMkuu), na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO.

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo(katikati) akikagua kituo cha kuzalisha umeme wa maji cha Mtera marabaada ya kufanya mazungumzo na watendaji wa Tanesco wanaosimamiakituo hicho. Wa Kwanza Kushoto ni Kaimu Meneja wa Kituo cha Mtera,Mhandisi Manfred Mbyallu na kulia ni Meneja Uzalishaji Umeme wa Majinchini, Antony Mbushi.

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishatina Madini, Mhandisi OmarChambo (wa kwanza kushoto)akipata maelezo kuhusu kipimokinachoonesha kima cha majikatika bwawa la kuzalisha umemela Mtera. Bwawa hilo lilisimamishauzalishaji tarehe 7 Oktoba 2015kutokana na kima cha maji kuwachini ya kiasi kinachoruhusiwakuzalisha umeme.Anayetoamaelezo ni Kaimu Meneja waKituo hicho, Mhandisi ManfredMbyallu (wa pili kutoka kulia).

  • 7/23/2019 BULLETIN 96 PRINT.pdf

    9/9

    9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    ziara ya KATIBU MKUU chambo

    Mwonekano waBwawa la Kidatu marabaada ya kima chamaji katika bwawahilo kupungua kutokamita 450.00 hadi mita439.48 kukia tarehe27 Novemba 2015na hivyo kupelekeakiwango cha uzalishajiumeme katika kituocha Kidatu kupunguakutoka megawati204 hadi 27.3 kukiatarehe 27 Novemba2015.

    Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo(kulia) akikagua kituo cha uzalishaji wa umeme cha Kidatu mkoaniMorogoro, wakati alipofanya ziara katika vituo vya kuzalisha umeme wamaji vya Mtera na Kidatu. Pamoja naye ni Meneja wa Kituo cha Kidatu,Mhandisi Justus Mtolera.

    Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (aliyevaa suti)

    akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa umeme katika bwawa la Kidatu mkoaniMorogoro, wakati alipofanya ziara katika bwawa hilo. Anayetoa maelezo ni Menejawa Kituo cha Kidatu, Mhandisi Justus Mtolera.

    Kaimu Meneja Mwandamizi Uzalishaji Umeme wa Maji Nchini,Lewanga Tesha (aliyesimama) akitoa maelezo kwa Katibu MkuuWizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa

    kwanza kulia) kuhusu uzalishaji umeme wa maji nchini katikaziara ya Katibu Mkuu kwenye vituo vya Kidatu na Mtera.Wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa Kituo cha Mtera,Mhandisi Manfred Mbyallu.

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wakwanza kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika chumba cha kuongozeamitambo ya uzalishaji umeme katika kituo cha kuzalisha umeme chaKidatu mkoani Morogoro wakati alipofanya ziara katika kituo hicho.Katikati (waliokaa) ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli,Mhandisi Hosea Mbise na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa SheriaWizara ya Nishati na Madini, Justus Mulokozi.