193
NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Tano – Tarehe 11 Aprili, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae, Katibu! NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, swali letu la kwanza leo Ofisi ya Rais, TAMISEMI litaulizwa na Mheshimiwa Lameck Okambo Airo. Na. 35 Hitaji la Jengo la Upasuaji Kata ya Koryo - Rorya MHE. KISWAGA B. DESTERY (K.n.y. MHE. LAMECK O. AIRO) aliuliza:- Wananchi wa Kata ya Koryo kwa kushirikiana na Mbunge wao na wananchi wa Rorya wanaoishi Mwanza, Arusha na Dar es Salaam wamejenga wodi ya akina mama na watoto pamoja na kununua jokofu lakini mapungufu yaliyopo sasa ni Jengo la upasuaji.

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1493275419-11 APRILI 2017.pdf · MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti,

  • Upload
    others

  • View
    1

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE___________

MKUTANO WA SABA

Kikao cha Tano – Tarehe 11 Aprili, 2017

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua

MWENYEKITI: Tukae, Katibu!

NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, swali letu lakwanza leo Ofisi ya Rais, TAMISEMI litaulizwa na MheshimiwaLameck Okambo Airo.

Na. 35

Hitaji la Jengo la Upasuaji Kata ya Koryo - Rorya

MHE. KISWAGA B. DESTERY (K.n.y. MHE. LAMECK O.AIRO) aliuliza:-

Wananchi wa Kata ya Koryo kwa kushirikiana naMbunge wao na wananchi wa Rorya wanaoishi Mwanza,Arusha na Dar es Salaam wamejenga wodi ya akina mamana watoto pamoja na kununua jokofu lakini mapungufuyaliyopo sasa ni Jengo la upasuaji.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

Je, Serikali sasa haioni ipo haja ya kusaidia jengo hilopamoja na vifaa vyake?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Lameck Okambo Airo, Mbunge wa Rorya, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Bajeti ya mwaka wafedha 2016/2017 mradi uliidhinishiwa shilingi milioni 30 kwaajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la upasuaji. Fedha zotezimepokelewa na tayari Halmashauri imeanza taratibu zakumpata mkandarasi. Aidha, katika mwaka wa fedha2017/2018 Serikali imepanga kutumia shilingi milioni 25 kwaajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa jengo hilo.

MHE. KISWAGA B. DESTERY: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, je, Serikali inampango gani wa kuzielekeza Halmashauri kutumia forceaccount i l i miradi midogo midogo kama hii iwezekutengenezwa kwa fedha ndogo na iweze kuleta impact?

Swali la pili, kwa kuwa jambo hili linafanana kabisana vituo vya afya vilivyoko Jimbo la Magu katika kituo chaafya Lugeye pamoja na Nyanguge. Serikali ina mpango ganiwa kuvijengea majengo ya upasuaji ili wananchi wawezekupata huduma karibu? Ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango waSerikali hivi sasa si kutoa maelekezo, tayari tumeshatoamaelekezo hivi sasa na Halmashauri mbalimbali zinaendelea

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

kutumia force account na tumepata mafanikio makubwasana, kwa sababu maeneo mbalimbali unapopita hivi sasamradi ambao zamani ulikuwa saa nyingine ulikuwaunagharimu shilingi milioni 150 utakuta sasa hivi milioni 70mradi umekamilika tena upo katika ubora unaokusudiwa.

Kwahiyo Mheshimiwa Kiswaga ni kwamba sasa hivijambo hilo linaendelea na linaendelea kwa ufanisi mkubwa,na nipende kuwashukuru sana Wenyeviti wa Halmashauri naWakurugenzi ambao wanasimamia jambo hili kwa uzuri zaidina hasa Waheshimiwa Wabunge katika Majimbo yenu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, katika sualazima la Jimbo la Magu ambalo Mheshimiwa Mbungeumesema na ni kweli, katika harakati za Serikali tuna mpangoambao si muda mrefu sana tutakuja kuuanza katika kituochako kimoja cha afya tutakuja kujenga jengo la upasuajina kuweka vifaa tiba vyote. Kwa hiyo, naomba nikushauriMheshimiwa Mbunge kwamba usiwe na wasiwasi Serikaliyako kama kila siku inavyopiga kelele hapa Bungeniitaendelea kushirikiana nanyi na ujenzi huo Mungu akijaaliautaanza hata kabla ya mwezi wa sita.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Paresso.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekitiahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Katika Mkoa wa Arusha kuna majimbo saba na katikamajimbo hayo majimbo mawili yana jiografia ngumu sanaikiwemo Jimbo la Longido na Jimbo la Ngorongoro. Je, Serikaliiko tayari sasa katika bajeti tunayoiendea kutazama majimbohaya kwa mujibu wa jiografia yao ili wananchi wanaoishikatika maeneo hayo waweze kupata huduma za afya kwaurahisi na kwa wakati?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

Serikali inapeleka nguvu kubwa sana katika eneo hilo, nandiyo maana juzi juzi nilikuwa katika Wilaya hizo zote mbili;Wilaya ya Longido pamoja na Wilaya ya Ngorongoro, katikaWilaya ya Ngorongoro siyo muda mrefu sana Mungu akijaaliakatika kipindi hiki cha katikati tutakwenda kuwekeza nguvukubwa sana kwa kupeleka takribani milioni 700. Lengo kubwani kwamba maeneo yale yana jiografia tata sana wananchiwaweze kupata huduma kujua kwamba Serikali yao ipovitani katika kuhakikisha kwamba wananchi wanapatahuduma hiyo inayokusudiwa.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri yaMheshimiwa Naibu Waziri, kuna wilaya nyingi mpya ambazozina matatizo sana ya hata kutokuwa na Hospitali za Wilaya.Na kwa kuwa majibu yake anasema kwamba kuna fedhaambazo zimetengwa, je, Mheshimiwa Naibu Waziri anawezakunihakikishia kwamba katika Wilaya ya Busega kituo chaNasa hizo fedha zitapatikana lini?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Dkt.Chegeni unafahamu na wewe kule kwako umenikaribisha,nakushukuru sana. Hicho kituo cha afya ulichokisemamiongoni mwa maeneo ambayo yana changamoto, naakina mama wanapata shida kubwa sana kupata hudumaza upasuaji. Nilikueleza wazi kwamba katika kipindi cha huumwaka tutafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwambatunajenga jengo la upasuaji kama nilivyosema katikamaeneo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kuwa na imani,kwamba Serikali kwa kupitia Wizara ya afya tuna mkakatimpana sana kuhakikisha kwamba tunapelekea hudumakatika maeneo hayo na Mungu akijaalia kabla ya mwezi wasita tunaweza tukaenda kuweka jiwe la msingi sawa sawana kituo cha afya cha Malya kule kwa ndugu yangu Ndassa.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Kiwelu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

MHE. GRACE S. KIWELU: Mheshimiwa Mwenyekitinakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti katika hospitali yetu ya Wilayaya Siha hatuna hatuna jokofu na imekuwa inaleta usumbufusana kwenye kuhifadhi miili ya marehemu wetu.

Je, ni lini Serikali itatuletea jokofu kupunguza upungufuhuo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwakifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Hospitaliya Siha takribani wiki sita zilizopita nilikuwa pale Siha nanamshukuru sana Mbunge tulikuwepo pamoja natulitembelea hospitali ile na kipindi kilichopita hapa nilitoamaelekezo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nil ivyofika pale Siha,kutokana na changamoto tuliyobaini pale, kwambatumepeleka fedha lakini matumizi yale ya fedha tumeonahayaelekezwi sawa sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kabla ya jokofukuanza kuna suala zima la fedha tulizozipeleka pale lazimazitumike vizuri na tumeshatoa maelekezo hayo. Lengo letuni kwamba lile jengo, floor ya juu iweze kukamilika vizuri lakinihatuachi hapo kwa sababu changamoto kubwa ya palelazima tuhakikishe hospitali ile inafanya kazi vizuri na Serikaliitaweka nguvu za kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulishapeleka zaidi ya milioni250, inafanya kazi lakini suala la jokofu litakuwa ni kipaumbelechetu ili kuhakikisha, lengo kubwa hospitali ile inafanya vizurikwa wananchi wa Siha.

MWENYEKITI: Ahsante, waheshimiwa tunaendelea,Mheshimiwa Anatropia.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

Na. 36

Kyerwa Kuwa Makao Makuu ya Wilaya

MHE. PAULINE P. GEKUL (K.n.y. MHE. ANATROPIA L.THEONEST aliluiza:-

Mkao Makuu ya Wilaya ya Kyerwa yamewekwakatika Kata ya Kyerwa.

Je, ni mchakato gani ulifanyika mpaka Kata yaKyerwa kuwa Makao Makuu ya Wilaya?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Anatropia Lwehikila Theonest, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili eneo liwe na makaomakuu ya Wilaya lazima wananchi washirikishwe kupitiamikutano mikuu ya Vijiji na Halmashauri za Vijiji, Kamati zaMaendeleo za Kata, Mabaraza ya Madiwani, Kamati yaUshauri ya Wilaya na Kamati ya Ushauri ya Mikoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uamuzi wa kuifanya Kata yaKyerwa kuwa Makao Makuu ya Wilaya ya Kyerwa ulitolewabaada ya kupitishwa na Baraza la Madiwani katika kikao chatarehe 30 hadi 31 Oktoba, 2012 na Kamati ya Ushauri ya Mkoawa Kagera katika kikao chake cha tarehe 15 Machi, 2013hivyo uamuzi wa mwisho kuhusu eneo la Rubwera katikaKata ya Kyerwa kuwa Makao Makuu ya Wilaya Kyerwaulizingatia mapendekezo ya vikao hivyo vya kisheria.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekitinikushukuru kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili yanyongeza.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

Kwanza, kwa kuwa michakato hii inachukua mudamrefu sana ambayo inaanzia kwenye ngazi za vijiji mpakajuu kama Naibu Waziri alivyosema.

Je, endapo michakato hii katika ngazi za chiniitakamilika mapema, nini kauli ya Serikali Kuu ili na waowaharakishe na wananachi hawa wapate haki zao?

Swali la pili, kwa kuwa tunapokaribia wakati waUchaguzi Mkuu, Serikali imekuwa na hali ya kugawa kata zetuna vijiji ili kuhakikisha kwamba wananchi wanapata hudumakwa karibu. Naomba nifahamu Serikali ina mpango ganikuanza mchakato huo mapema kuelekea Uchaguzi waSerikali za Mitaa ili kuondoa usumbufu na maandalizi pia yamuhimu kwa wananchi hawa ambao maeneo yao nimakubwa na Kata zao ni kubwa?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti kwanza katiasehemu ya kwanza ni kwamba mchakato umekamilika naMakao Makuu ya Halmashauri imeshathibitishwa ndiyo ileambayo imetajwa pale isipokuwa Mheshimiwa Mbungealikuwa na utata katika hayo Makao Makuu mapya, kwahiyo mchakato huo ulishakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala zima la kugawawakati wa kuelekea kwenye uchaguzi nadhani hii sasa nimamlaka zetu katika Ward Council zetu, vikao vyetu vile vyakisheria kama nilivyovisema, ambapo inaonesha baadayejambo hili litaenda katika Tume ya Uchaguzi kupita Ofisi yaWaziri Mkuu.

Kwa hiyo, hakuna shaka naamini kwamba kila mtukatika maeneo yake anabaini changamoto zinazokabili eneohilo na tutafaya maandalizi ya awali ilimradi kuepushaukakasi kwamba maeneo yanagawiwa muda mfupi kablaya uchaguzi.

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

Kwa kuwa Wilaya ya Ngorongoro ni kubwa kulikoMkoa wa Kilimanjaro, hali inayopelekea jiografia ya Wilayahiyo kuwa ngumu. Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafakawa kugawa Wilaya hii ya Ngorongoro au kuwekaHalmashauri mbili ili kuwasogezea wananchi wa Ngorongorohuduma kwa karibu?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli naMheshimiwa Mbunge pale wa Jimbo hio la Ngorongoroambalo Naibu Waziri wa Kilimo na yeye alinialika niwezekufika kule jimboni kwake juzi juzi hapa nilikuwepo kule. Kwaumbali kweli jiografia ya Ngorongoro ina changamotokubwa sana kwa sababu ukianzia hapa getini ukitoka hapaKaratu mpaka unafika Makao Makuu kule Loliondo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nilipata fursa yakutembelea mpaka Ziwa Natron kwenda shule ya sekondariya Ziwa Natron. Jiografia ya Ngorongoro kweli ni kubwa zaidi,lakini mara nyingi sana maeneo haya yanagawanywakutokana na population.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia eneo kubwa laNgorongoro ni hifadhi, lakini kama kutakuwa na haja yakuweza kugawanya basi kwa mchako ule ule wa kisheriawananchi wa aeneo hilo watafanya hivyo na Serikaliitaangalia kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini inawezekanatunaweza tukaangalia mbali kwa sababu Ngorongoro naSerengeti ukiangalia jiografia yao ina changamoto kubwasana. Hili sasa tuwaachie wenye maeneo hayo mkawezakufanya maamuzi sahihi kama ulivyo Mheshimiwa CatherineMagige unavyokuwa na wazo hilo, basi na Serikali itaangalianini cha kufanya kwa maamuzi sahihi kwa maslahi mapanakwa wananchi wa Ngorongoro.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea,Mheshimiwa Qambalo Willy Qulwi, Mbunge wa Karatu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

Na. 37

Kupandisha Hadhi Kituo cha Afya cha Karatu

MHE. QAMBALO W. QULWI aliluliza:-

Wilaya ya karatu ina umri wa zaidi ya mika 20 lakinibado haina Hospitali ya Wilaya jambo ambalo linawatesawakazi wengi hasa wazee, akinamama na watoto.

Je, ni lini Serikali itapandisha hadhi Kituo cha Afya chaKaratu kuwa Hospitali ya Wilaya?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Qambalo Qulwi, Mbunge wa Karatu kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapendekezo yakupandisha hadhi kituo cha afya kuwa hospitali yanaanzakatika Halmashauri yenyewe kupitia Baraza la Madiwani,Kamati ya Ushauri ya Wilaya na Mkoa. Taratibu hizi zikikamilikaWizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watotoinatoa kibali baada ya kujiridhisha kupitia timu ya ukaguzihivyo Halmashauri unashauriwa kuanzisha mchakato wakujadili suala hilo katika vikao vya kisheria na kuwasilisha katikamamlaka husika kwa maamuzi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Qambalo.

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Mwenyekitinakushukuru kwa kunipa nafasi tena naomba niulize maswalimawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili la kupandishwahadhi kituo hiki limekwisha kujadilikwa katika mamlaka zilizopopale wilayani na hata mkoani, kwa hiyo kama ni suala la

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

mamlaka iliyobaki kushughulikia jambo hili ni mamlakailiyoko juu ya hizo mbili. Je, ni lini sasa timu hiyo ya ukaguziitatumwa ili upandishwaji hadhi wa kituo hiki uwezekukamilika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa safariya kuelekea kupata Hospitali ya Wilaya ya Karatu imeanza,Mheshimiwa Waziri yuko tayari sasa kutenga fedha katikabajeti ya kuanzia mwaka huu na kuendelea ili miundombinumichache iliyobakia iweze kukamilika? Ahsante

MWENYEKITI: Mheshimiwa waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nili-cross checkmpaka jana kuangalia taarifa hizi status zikoje, lakini kwataarifa nilizozipata kule inaonekana mchakato ulikuwahaujakamilika vizuri. Kwa hiyo, naomba tushauriane tu,tutaangalia jinsi gani tutafanya ili wenzetu wa Halmashauriili kama lile jambo limekwama halijafika katika mamlakahusika, hasa katika Wizara ya Afya waweze kufanya hivyo iliWaziri wa Afya aweze kufanya maamuzi, nadhani jambo hilolitakuwa halina shida kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Wizara kuwezakutenga fedha, ni kweli, na unakumbuka nilikuja pale jimbonikwako na nilitoa maelekezo kadhaa ambapo nilikuasijaridhika na kufika pale nilikuta watu wamefunikwa ma-blanket ambayo yametolewa store baada ya kusikia NaibuWaziri anakuja pale; kwa hiyo nimegundua changamotombalimbali pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mchakato wa ujenziwa Hospitali ya Wilaya tutaendelea kufanya hivyo. Naombaniwasihi hasa ndugu zetu wa Halmashauri, anzeni mpangohuo sasa kuanzia bajeti zenu za Halmashauri ikifika kwetu sisiWizarani jambo letu kubwa liwe ni ku-compile vizuri nakufanya taratibu vizuri ili mchakato wa ujenzi wa hospitaliufanyike. Hoja yako ni hoja ya msingi na bahati nzuri eneolile ni eneo la kitalii lazima tuwekeze vya kutosha tuwe na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

hospitali yenye maana pale hata mgeni akija aweze kupatahuduma nzuri.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Chatanda,Mwamoto na Mbatia

MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Mwenyekitinashukuru kunipa nafasi ili na mimi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti tatizo la Karatu linafananana tatizo la Korogwe Mjini. Korogwe Mjini haina hospitali,kwa maana ya Halmashauri ya Mji, na Wilaya yetutumeamua kwa makusudi kabisa kujenga kwanza kituo chaafya ambacho tutakifanya kiwe hospitali.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuweza kutusaidiakutupiga jeki kwa sababu tunajenga kituo cha afya chenyeghorofa tatu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwakifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanzanaomba niweke kumbukumbu sawa ni kwamba nipendekumshukuru Mama Mary Chatanda, Profesa Maji Marefupamoja na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe kwa kazi kubwaambayo wanaifanya ambapo nimetembelea mara kadhaakatika eneo li le. Nil ivyofika pale nimekuta initiativembalimbali wanazozifanya hasa katika suala zima la sektaya elimu na sekta aya afya na bahati nzuri wanatumiahospitali ya ndugu yangu Profesa Maji Marefu, iko vijijini lakiniobvious kijiografia iko mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kwa sababummeanza harakati za ujenzi, na kile kituo cha afya ni kituocha afya makini inaonekana kuna viongozi makini eneo lile,Serikali itachukua wazo lile jema kuangalia wapi mmeishia,tukishirikiana nanyi kwa pamoja tufanyeje, kwa kuangaliaresource tulizo nazo tusukume ili eneo la pale ambalo ni

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

katikati; watu wanaotoka Arusha hata ikipatikana ajalilazima watakimbizwa pale, tuweze le tuweze kushirikianakwa pamoja tujenge Hospitali ya Wilaya pale.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwamoto.

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: MheshimiwaMwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri,nianze kwanza kwa kuishukuru Serikali kwa kusikiliza kilio chawatu wa Kilolo kwa ujenzi wa hospitali. Pamoja na hiyo,Mheshimiwa Waziri, itachukua muda mrefu hiyo hospitalikuweza kuisha. Lakini tatizo ambalo lipo ni kwambaWagonjwa inabidi wapelekwe Kituo cha Afya Kidabagaambacho hakijakamilika, hakina wodi ya watoto, wodi yawazazi wala upasuaji, lakini inabidi sasa wasafirishwe waendekwenye hospitali ambayo iko zaidi ya kilometa 120. Tatizohakuna gari Mheshimiwa Naibu Waziri kwa hiyo utatusaidiajeilituweze either kukarabatiwa vizuri kituo cha Kidabaga autupate gari?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, kwa kifupi. Wakowengi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, MheshimiwaMbunge anafahamu tulifanya ziara pamoja na tukakutahospitali yao ya Wilaya pale iko taabani. Tukafanya mawazoya pamoja, na bahati nzuri ndani ya muda mfupi wakapaashilingi bilioni 1.2. Lakini, kama hiyo haitoshi niwapongeze;kwasababu wameshafanya harakati na ujenzi unaendeleakule site na Mungu akitujaalia ndani ya wiki mbili hizi wakatituko Bungeni nitakwenda kutembelea ili kuona ni jinsi ganiujenzi unaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Kituo cha Afya chaKidabaga nadhani unafahamu kwamba Serikali tutawezakuweka nguvu kubwa pale kwasababu tukiangalia jiografiayake ni tata sana, tutaangalia namna ya kufanya. Tutapelekafedha kwa ajili ya kujenga theatre ikiwezekana na wodi ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

wazazi. Lengo kubwa wananchi wa eneo lile waweze kupatahuduma bora. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante! Mheshimiwa Mbatia. JiandaeMheshimiwa Saumu.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Hospitali nyingi za Wilaya zina mkataba kati yaSerikali na mashirika hasa ya dini, Hospitali ya Kilema ikiwamoja wapo. Tunajenga maabara ya kisasa, nini commitmentya Serikali katika hospitali ya Kilema ili iweze ikatoa hudumazilizo bora katika Taifa hili?

MWENYEKITI: Waziri kwa kifupi sana.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nisemeujenzi wa maabara ni jambo jema sana na sisi Seriali tuna-appreciate hiyo juhudi kubwa inayofanyika na ukiona hivyomaana yake tunasaidia juhudi za Serikali jinsi gani iwezekusaidia wananchi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juu ya commitment yaSerikali katika hilo naomba tuangalie jinsi gani tutafanyakatika suala zima la mikataba hata suala zima la watendaji;kwa sababu wakati mwingine tunaweza tukawa namaabara lakini tukawa na watu ambao hawawezikuendesha vizuri ile maabara. Kwa hiyo, commitment yaSerikali ni kuangalia jinsi gani tutafanya ili maaabaraikikamilika tuweze ku-deploy watu wazuri pale wa kuwezakufanya analysis ya maabara, wananchi wetu wakienda palewaweze kupata huduma bora hata magonjwa yao yawezekudundulika vizuri zaidi.

MHE. SAUMU H. SAKALA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru, nina swali moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo cha afya ambachokiko katika kijiji cha Mwera, Kata ya Mwera ni kituo ambachokwa muda mrefu sana kimepandishwa hadhi ya kuwa kituo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

cha afya; lakini kituo kile hakina huduma zinazokidhi kuwakaama kituo cha afya. Hakina gari la wagonjwa, lakini piavipimo vya damu salama bado havipo katika hospitali ile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kujua ni liniSerikali itakipa hadhi sahihi kituo kile ya kuwa kituo cha afyakatika Wilaya ya Pangani?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, ni lini tu anatakakujua.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kusema linikwanza naomba tuweke rekodi sawa za MheshimiwaMbunge kwamba kipindi kile mlinialika na MheshimiwaAweso tumefika pale Mwera na nikatoa maagizo kwambakituo kile kutokana na yule mwekezaji pale japo anawekezaaweze kujenga theatre.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwashukuru kwa sababuwodi ya wazazi imeedelea kujengwa, lakini hata hivyo Serikalikuufanya kuwe kituo cha afya lazima miundombinu ikamilikevizuri, ndiyo maana tukaona sasa hivi tujenge jengo latheatre pale kubwa lakini pia kujenga na wodi zingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na ndiyo maananikamuelekeza Mheshimiwa Aweso kwamba awaambiewatu waiandae mapema ile BOQ. Tuta deploy pesa pale,kwa sababu watu wa pale wakikosa huduma, suala lakuvuka Mto Pangani ni changamoto kubwa sana na usikuvivbuko hakuna. Kwa ajil i ya kuwaokoa Watanzaniatumeamua kuweka nguvu kubwa za kutosha, fedha zakutosha kujenga jengo lile litakamilika huenda kabla yamwezi wa saba mwaka huu ujenzi utakuwa umeshaanza.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa tunaendelea.Wizara ya Viwanda na Biashara, Mheshimiwa FakhariaShomar Khamis.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

Na. 38

Kushamiri kwa Biashara ya Vyuma Chakavu

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS Aliuliza:-

Biashara ya vyuma chakavu imeshamiri sana TanzaniaBara na Visiwani na imesababisha madhara ya kuharibiwana kuibiwa kwa miundombinu yakiwemo mifuniko ya chembana majitaka.

(a) Je, Serikali imejipangaje kupambana na wizi nauharibifu huo wa mali za Serikali na wakati walinzi wa maeneohusika wanashuhudia hayo?

(b) Je, Serikali haioni kwamba hata usalama wa raiana mali zao uko mashakani?

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJIAlijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali laMheshimiwa Fakharia Shomar Khamis, Mbunge wa VitiMaalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na MheshimiwaFakharia Shomar Khamis kuwa biashara ya chuma chakavuimeshamiri hapa nchini na duniani kwa ujumla. Kuongezekakwa mahitaji (demand) ya vyuma chakavu kulitumiwa nawahalifu kuharibu miundombinu iliyojengwa kwa vyuma kwania ya kupata chuma ili waiuze kama chuma chakavu.Maeneo yaliyoathirika sana ni mifumo ya kusafirisha umeme,reli, barabara kwa kutaja baadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kukabiliana na hujuma hizimamlaka husika yaani TANESCO, TANROADS na RAHCOwamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na Jeshi la Polisiikiwemo kutumia walinzi wa taasisi husika kulinda rasilimali hizo.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kupata suluhu ya kudumu,Wizara yangu imekwishaandaa rasimu ya muswada washeria itakayoweka bayana taratibu na mfumo wa usimamizina udhibiti wa biashara ya chuma chakavu katika hatuambalimbali za uzalishaji, ukusanyaji, usambazaji, uuzaji nauyeyushaji wake kwa kuzingatia uhifadhi na usimamizi wamazingira kwa manufaa ya Taifa. Aidha, muswada huoumeweka bayana adhabu itakayotolewa kwa mtu yeyoteatakayebainika kuharibu miundombinu kwa sababu yakuchukua chuma chakavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimtoe hofuMheshimiwa Mbunge na Watanzania kwa ujumla usalamawao na mali zao ziko salama. Aidha, nitumie fursa hiikuwaomba wananchi wote kutoa taarifa pindi wawaonapomtu anayehujumu miundombinu kwa namna yoyote ile kwalengo la kuchukua chuma chakavu au chuma. Kwa wenyeviwanda na wafanyabiashara wa vyuma chakavu jiepushenina ununuzi wa vyuma ambavyo asili yake inatia mashaka.Kama nilivyoeleza awali, tutaharakisha sheria ambayo kwakiasi kikubwa itasaidia kutatua tatizo hili.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Fakharia.

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Nashukuru Mheshimiwa Wazirialivyonijibu vizuri na kwa ufasaha swali langu, lakini nitakuwana maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Waziri, je, kwa nini Serikali haioniumuhimu wa kuwepo vyombo vya awali vya kuhakiki ainaau bidhaa mbalimbali ya vyuma chakavu kabla havijafikasokoni?

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kwa nini usiwepoutaratibu wa kutofautisha biashara ya vyuma chakavu kablaya kuharibu miundombinu ya Serikali ambayo sasa hiviimeenea nchi nzima kila mahali vinang’olewa? Kungekuwana uhakiki kabla ya hivyo vyuma chakavu kuweza kufikasokoni na kuweza kuuzwa? Ahsante.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, ile dhana ya kutumia vyumachakavu ambavyo kimsingi vinakuwa havitakiwi kwendakuviyeyusha na kutengeneza chuma ni wazo zuri. Tatizolililopo ni kwamba watu wenye tamaa, wahalifu ndiyowanaharibu ile dhana nzuri, hawa ni wahalifu kama wahalifuwengine. Sasa chombo cha awali cha kuweza kuzuia watuhawa ni wananchi, kama inavyosema Katiba ya nchi yetu,ulinzi wan chi hii ni jukumu la wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwenye ilemiundombinu mikubwa kama ile ya TANESCO nilivyosema,TANESCO anaweka ulinzi akisaidiana na wananchi waliowema. Nina imani huo ndio mfumo mzuri wa kuweza kulindamiundombinu yetu Tanzania nzima, Wizara yangu au Serikalihaiwezi kutengeneza polisi wa kulinda vyuma kuanzia vilevya taasisi mpaka vyetu binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa kutofautisha,kama ilivyo kwa wale wanaoharibu miundombinu kwendakujipatia pesa wapo hata wenye viwanda ambaowanapokea vyuma ambavyo wazi kabisa vinaonekanavimetoka kwenye miundombinu ya Serikali au ya watu, haomimi ndio nakula nao sahani moja. Ma-inspector wanguwanatembelea viwanda hivyo na ni vichache vinajulikanana naendelea kuwapa elimu, atakayebainika atajutakwanini alifanya hivyo. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Sugu. JiandaeMheshimiwa Mwakasaka, jiandae Mheshimiwa Raymond.

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Suala la biashara ya vyuma chakavu inaonesha niwazi kuna soko zuri la chuma nchini na nje ya nchi. Sasa kifupitu, sijui mradi wa chuma Liganga na Mchuchuma umefikiawapi ili nchi ifaidike na soko hilo? Ahsante.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Mchuchuma na Liganga;katika mpango wa Serikali wa miaka mitano wa ujenzi wa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

uchumi wa viwanda, mchuma na Liganga ipo. Nilipofikiamimi; hili suala liko mezani kwangu. Nimepitia vivutio vyotevya mwekezaji alivyoweka, nimevikamilisha, vinakwendakwenye mamlaka kusudi waweke sahihi, mwekezaji yukotayari kuweka fidia na kuweza kuanza. Nikipata sahihi yamamlaka tunaanza kazi.

MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali mojala nyongeza.

Kwa kuwa hii biashara ya vyuma chakavu inavikumbapia viwanda vilivyobinafsishwa kwa muda mrefu sasakikiwemo Kiwanda cha Nyuzi Tabora, na kwa kuwa kunataarifa kwamba mashine nyingi mle ndani zimeuzwa kamachuma chakavu na kimefungwa kile kiwanda, je,Mheshimiwa Waziri, kwa sababu nimewahi kulalamika hapaBungeni na kutoa taarifa kuhusu kufanyika kwa vyumachakavu, ni lini tunaweza tukaenda tukakagua kile kiwandakwa sababu sasa hivi umetoka kusema utakula nao sahanimoja, tuweze kujua kama vile zile mashine hazijauzwa kamavyuma chakavu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, kwa kifupi.Mheshimiwa Raymond jiandae baadae.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiwanda cha Nyuzi cha Tabora kinamwenye nacho (owner) kwa hiyo, mwenye mali anapoibiwamimi siwezi kwenda kuangalia mali yake yule, lakini taarifanilizonazo kutoka kwa mwenye kiwanda ameniambiaamepata soko la nyuzi na kiwanda hicho kitaanza kazi.

Kwa hiyo, mimi naweza kumbana yule kwa kupitiamsajili wa hazina kwamba aanze kazi na ndio wajibu wangu.Sasa kama alizembea, mali ikaibiwa mle hilo nadhani ni sualala kila abiria achunge mzigo wake.

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa fursa hii. Ni takribani miaka kumi sasa toka hili

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

swali linaulizwa. Nakumbuka lile Bunge la Tisa niliuliza hili swalimwaka 2007 na Bunge la Kumi aliuliza Mheshimiwa Maida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jibu la Serikali siku zote nikwamba muswada unaandaliwa. Ni lini sasa muswada huoutaletwa hapa Bungeni ili uweze kupitishwa kama sheria?

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mbunge najua una imani na mimi. Sasa upeleumepata mkunaji, safari hii unaletwa chini ya uongoziwangu. (Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa tunaendelea,Wizara ya ujenzi, Mheshimiwa Mussa Ramadhani Sima.

Na. 39

Ujenzi wa Uwanja wa Ndege – Kijiji cha Manga

MHE. MUSSA R. SIMA Aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa uwanja wa ndegekatika eneo lililotengwa katika Kijiji cha Manga kwa msaadawa Benki ya Dunia?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO Alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano naomba kujibu swali laMheshimiwa Mussa Ramadhani Sima, Mbunge wa SingidaMjini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilipata mkopo kutokaBenki ya Dunia ambapo sehemu ya mkopo huo imetumikakufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa viwanja 11vya ndege vya Iringa, Njombe, Songea, Lindi, Kilwa Msoko,Tanga, Moshi, Lake Manyara, Musoma, kiwanja kipya katikaMkoa wa Simiyu na Singida kwa ajili ya ukarabati, upanuzina ujenzi wa viwanja hivyo kwa kiwango cha lami.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

Ninapenda kumtaarifu Mheshimiwa Mbunge kuwa upembuziyakinifu na usanifu wa kina kwa kiwanja cha Singidaunafanyika katika eneo la kiwanja cha sasa na si katika eneojipya la Manga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utafutaji wa fedha za kaziza ukarabati, upanuzi na ujenzi kutoka vyanzo mbalimbaliutaanza baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu nausanifu wa kina ambao kwa sasa upo katika hatua zamwisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati kazi hii ya usanifuikiendelea, Wizara yangu ilipata maombi ya Mkoa wa Singidaya kutaka wataalam kwenda kufanya tathmini ya awali yaeneo jipya linalopendekezwa katika eneo la Uhamaka karibuna kijiji cha Manga kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja cha ndegecha Mkoa wa Singida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo hilo la Uhamakalimependekezwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja kipya chandege cha Mkoa wa Singida katika mpango kabambe wauendelezaji wa Manispaa ya Singida kwa mwaka 2015 – 2035.Tathmini ya awali iliyofanywa na Mamlaka ya Viwanja vyaNdege mnamo Februari, 2016 kuhusu eneo hilo lenye ukubwawa hekta 2400 (kilometa sita kwa kilometa nne) imeoneshakuwa eneo pendekezwa linafaa kwa ujenzi wa kiwanja chandege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia matokeo yatathmini, hatua zitakazofuata ni utwaaji rasmi wa eneo hilounaohusisha ulipaji fidia ya mali za wananchi waliomo ndaniupimaji wa eneo kwa aji l i ya hatimiliki, usanifu wamiundombinu ya kiwanja, utafutaji wa fedha za ujenzi wakiwanja na hatimaye ujenzi wenyewe.

MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nishukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri,kwa kuwa Singida Mjini ni mji ambao unakua kwa kasi sanakwa sababu Serikali imehamia Dodoma, Serikali haioni hajasasa ya kutenga fedha kwenye bajeti ya mwaka huu ili uweze

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

kuwalipa fidia wananchi wa kwenye hilo eneo la Manga naUhamaka ilitoe hilo eneo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwaSerikali imeanza ukarabati kwenye uwanja wa ndege wasasa, je, Serikali itamaliza ukarabati huo lini ili na sisi tuwezekuutumia uwanja huo kwa kupanda ndege? Ahsante sana.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuombeMheshimiwa Sima na wananchi wa Mji wa Singida wawe nasubira, tupate taarifa ya mwisho ya kazi ya upembuzi yakinifuna usanifu wa kina ili hatua ya pili ifuate. Si rahisi tukaanzakutenga fedha kwa mwaka huu na hasa vipaumbeleambavyo tulipitisha mwaka huu, mtakumbuka ambavyotulipitisha katika mpango wa mwaka huu wa fedha, vinahitajirasilimali fedha nyingi na hivyo hii kazi tutaifanya mara badaaya kazi hii ya upembuzi yakinifu kukamilika. Itakuwa sio rahisikwa mwaka huu, mnafahamu kwamba bajeti ya mwakahuu tumeshaipitisha katika ngazi ya Kamati na hivi sasatunaanza kuingiza katika hatua za Bunge Zima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kuhusu ukarabati;nimhakikishie Mheshimiwa Sima kwamba kazi hii ya upembuziyakinifu na usanifu wa kina itakapokamilika suala la ukarabatilitafuata.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bobali, atafuatiaMheshimiwa Bura.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Nishukuru kwamba uwanja wa ndege wa Lindiupo kwenye mapendekezo ya Serikali ya kutaka kuufanyiaukarabati lakini kwa sasa wananchi wa Lindi tunakosahuduma ya ndege mpaka twende Mtwara kwa kuwa uwanjaule sasa hivi umekuwa ni chakavu sana. Nataka commitmentya Serikali, ni lini itakamilisha ukarabati wa uwanja wa ndegewa Lindi ili ndege zianze kutua kama kawaida?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli uwanja waLindi ni kati ya viwanja 11 vinavyofanyiwa upembuzi yakinifuna usanifu wa kina kwa kutumia fedha za mkopo kutokaBenki ya Dunia. Kimsingi kazi hii itakapokamilika ndipotutapata ratiba kamili ya tuanze wapi na tumalizie wapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda tu nimkakishieMheshimiwa Bobali, kwamba kutokana na umuhimu wakuhakikisha wananchi wa Lindi nao wanakuwa na kiwanjacha ndege, tutahakikisha katika kuangalia priority, na linditutaiangalia kwa macho matatu. (Makofi)

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo lanyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaishukuru sana Serikalikwa kupanua uwanja wa ndege wa Dodoma, lakini upanuzihuo umeathiri sana barabara ya Area D round about yaShabiby, na wananchi wanaotoka Area D na Majengo Mapyahurudi mpaka Kisasa kuja mjini kilometa nyingi.

Je, Serikali iko tayari kujenga barabara nyingine yalami kuwapunguzia safari ndefu wananchi wanaokaamaeneo ya Area D na Majengo Mapya? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Waziri!

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwambatunahitaji kuangalia upya namna Area C na Area Dinavyoweza kufikika ukitokea Dar es Salaam bila mzungukohuo mkubwa kwa kuhakikisha tutapata barabara nyinginebadala ya ile ambayo sasa hivi imefungwa kwa ajili yakiwanja cha ndege. Kwa hiyo, namhakikishia Serikali nayoinalifikiria na tutalifanyia kazi kwa haraka hilo.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Sokombi, halafuMheshimiwa Kangi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Kwa sababu pia uwanja wa Musoma upo kwenyeajenda hiyo na kwamba upembuzi yakinifu umeshafanywa.Kwa sababu kutengwa fedha ni kitu kingine na ujenzi ni kitukingine, je, ni lini Serikali itaanza ujenzi katika uwanja waMusoma?

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Waziri majibu kwakifupi.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naombanimhakikishie Mheshimiwa Sokombi na wananchi wote waMji wa Musoma na viunga vyake ambao kwa kawaidawamezoea kutumia uwanja wa ndege wa Musoma kwasafari zao kwamba Serikali iko makini na katika muda wahivi karibuni kama mtakumbuka tuliwaambia katika viwanjavitatu vya mwanzo tutakavyohakikisha kwamba ujenzi wakeunaanza haraka ni pamoja na Musoma, Nduli na Mtwara.

Naomba nimhakikishie Serikali ipo mbioni kuhakikishaviwanja hivi vitatu vinapata fedha na uzuri wake fedha zaviwanja hivi vitatu vinatarajia ataketupa fedha maana siomfadhili ni mkopehsaji hivi karibuni.

MHE. KANGI A. N. LUGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kunipa fursa niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa MheshimiwaNaibu Waziri katika majibu yake ya msingi ametamka nenofidia, kuhusiana na kuwafidia wale watakaoathirika na ujenziwa kiwanja cha ndege Singida. Kwa kuwa neno hilo fidiaamewatonesha na kuwakumbusha wananchi wa Mwibaraambao barabara ya Bunda, Kisoria na Nasio kwa miakamingi hawajafidiwa. Je, wananchi hao wanataka kumsikiaMheshimiwa Naibu Waziri, ni lini watafidiwa au kwenyemwelekeo wa bajeti fidia ya Mwibara ipo? Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupisana.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Lugolaamekuwa akifatilia sana suala la fidia katika eneo lake, nanaomba nitumie fursa hii kumdhihirishia yale ambayotumekuwa tukimwambia ofisini na maeneo mengine ambakoamekuwa akituuliza swali hili ni sahihi, kwamba tunatafutafedha kwa ajili ya kulipa fidia na kwa kweli nimhakikishiemara tutakapopata hizo fedha suala la fidia hilotutalishughulikia kwa kazi sana.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Kwa kuwa Manispaa ya Iringa na kiwanja chandege cha Nduli kimekaa kimkakati, ukizingatia kwambaWizara ya Maliasili na Utalii inaboresha Southen Sackett kwaajili ya kuimarisha utalii Kusini mwa Tanzania. Ni lini sasa Serikaliilikuwa imeahidi kwamba kiwanja hiki kitaboreshwa kamaambavyo Waziri amesema kwamba ni miongoni mwaviwanja 11 ili Manispaa ya Iringa iweze kukua kiuchumi nakimkakati kwa ajili ya ku-boost uchumi wa Taifa ambaokimsingi uchumi unaenda chini?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyonilijibu swali la Mheshimiwa Sokombi, kwamba katika viwanjaambavyo tunatarajia kupata mkopo hivi karibuni ni kiwanjacha Musoma, Nduli na Mtwara. Kwa hiyo, naombanimhakikishie Mheshimiwa Msigwa kwamba kiwanja chaNduli nacho kipo katika mtazamo wa mbele sana ilikuhakikisha kwamba utalii unaongezeka katika mbuga yetuile ya Ruaha na kuleta mapato makubwa kwa Serikali.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kabati, ajiandaeMheshimiwa Waitara ambaye atakuwa wa mwisho.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali dogo lanyongeza.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niko kwenye Kamatiya Miundombinu; kwa kuwa uwanja huo huo wa Nduli tayarikuna pesa zimetengwa kwa ajili ya ukarabati huo lakini piamradi huu umeshakubaliwa na wananchi kwa sababuSerikali tayari ilishakaa na wananchi waliopo katika eneolile. Sasa naomba jibu kutoka kwa Serikali, kwa sababu kunawananchi ambao wamekuwa wakiendeleza maeneoambayo yataguswa sasa ni lini itaweka alama na iliwasiyaendeleze maeneo yale ili wakati wa kulipa fidia pesaiwe kidogo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi,jiandae Mheshimiwa Waitara!

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa RittaKabati amekuwa akihoji haya masuala ndani ya Kamati yaMiundombimu na mimi niendelee kumpongeza kwa namnaanavyochukua hatua kuwatetea wananchi na kuhakikishakwamba maslahi yao yanazingatiwa na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu kamaambavyo nimekuwa nikimhakikishia mara nyingi katika Vikaovya Kamati, kwamba kazi hii ya kuweka alama tutaifanyahivi karibuni. Naongelea si zaidi ya miezi mitatu, minne ijayokazi hii itakuwa imekamilika ili kuhakikisha kwamba wananchiwa pale wanajua mipaka ya maeneo tutakayotumia katikakukarabati na kupanua ule uwanja wa Nduli.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Tunaunga mkono juhudi ambayoinafanyika ya kuboresha Uwanja wa Ndege wa Kimataifawa Dar es Salaam. Lakini kuna malalamiko ya muda mrefuya wananchi wa Kata ya Kipawa, Ukonga - Kipunguni,Kigiragira kule Buyuni, wanadai fidia Serikali mpaka leo nawameshindwa kufanya shughuli za kimaendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kujua ni linimgogoro huo utamalizwa na Serikali ili uwanja ukamilike nawananchi wakaendelea kuwa na amani na kuishi maisha

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

ambayo na wenyewe wanapaswa kuishi kama binadamuwa kawaida hapa Tanzania? Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tenakumthibitishia Mheshimiwa Waitara pamoja na jirani yakeMheshimiwa Bonnah Kaluwa, Mbunge wa Segerea kwambakazi mlioifanya, mtakumbuka mimi ndio Mbunge wa Segereaalinileta kukutana na wale wananchi wa Kipunguni,kuhusiana na suala hili. Niwaombe kwamba tulidhamiria sualahili tutalimaliza katika miaka hii mitano. Mnafahamu baadhiya maeneo tumeshaanza kulipa fidia, Mheshimiwa BonnahKaluwa unalifahamu hilo na umelifuatilia kwa kasi sana naninakuhakikishia pamoja na Mheshimiwa Waitara kwambawananchi wale watalipwa fidia katika miaka hii mitano. Kunamatatizo ambayo yapo katika suala hili la fidia.

MWENYEKITI: Order please!

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivitunashughulikia matatizo yaliyoingiliwa katika suala hili lafidia, kuna wajanja wachache walitumia fursa wakatumiafedha vibaya na tumepelekea PCCB wanafanya kazi,tutakapopata taarifa PCCB tutakuja kulimaliza hili suala lafidia katika wale ambao wamebakia kulipa.

MWENYEKIT: Ashante Waheshimiwa tunaendeleaWizara ya Maji, Mheshimiwa Kigola.

Na. 40

Mradi wa Maji Mufindi

MHE. MENDRAD L. KIGOLA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itamaliza kujenga mradi wa maji waSawala, Mtwango, Rufuna na Kibao?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Majina Umwagiliaji naomba kujibu swali la mheshimiwa MendradLutengano Kigola, Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa maji wa Sawala -Kibao ambao utahudumia vijiji vya Sawala, Mtwango, Rufunana Kibao vilivyopo katika Kata ya Mtwango ulianzakutekelezwa tarehe 01/06/2015 na ulitarajiwa kukamilikatarehe 01/06/2016 kwa gharama ya shilingi bilioni 2.55.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa mradi huoulipangwa kufanyika kwa awamu tatu ambazo ni kujengaintake na kupeleka maji kijiji cha Sawala, kujenga mfumowa bomba kuu kutoka kijiji cha Sawala hadi Kibao nakujenga mtandao wa kusambaza maji katika vijiji vyaMtwango, Rufuna na Kibao. Awamu ya kwanza utekelezajiumefanyika katika kijiji cha Sawala kwa mkataba wagharama ya shilingi milioni 644.21.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi sasa, jumla ya shilingimilioni 261.64 zimetumika kwenye mradi. Kazi zilizotekelezwahadi sasa ni pamoja na ujenzi wa intake, sump well, pumphouse, ulazaji wa bomba kuu, ujenzi wa tenki la mita za ujazo200, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 16 na sehemu yamabomba ya usambazaji kilometa 3.4; kwa wastani kaziiliyofanyika imefikia asilimia 50 kwa kijiji cha Sawala tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huo haukuwezakukamilika kwa wakati kutokana na mkandarasi kushindwakukamilisha kazi kwa mujibu wa mkataba. Mwezi Novemba,2016 Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ilivunja mkataba namkandarasi huyo, na kuamua kuutangaza upya tarehe07/02/2017 ili kuweza kupata mkandarasii mwingine wakumalizia kazi zilizobaki. Mkandarasi anatarajiwa kupatikanamwezi Juni, 2017 na kazi itakamilika katika mwaka wa fedha2017/2018.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kigola.

Waheshimiwa Wabunge, leo kipindi cha bajetimaswali ni saa moja tu tumebakiwa na dakika saba tu zamaswali. Maswali ambayo tutayachukua sasa ni ya msingipeke yake, kwa sababu ili tuwe na wachangiaji wengikwenye bajeti. Mheshimiwa Kigola.

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na majibu mazuri ya Naibu WazirI ninaomba niulizemaswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza kutangazana kutafuta mkandarasi sasa hivi imeanza muda mrefu tokamwezi wa pili na imechukua karibu miezi sita sasa, ukisemampaka Juni itachukua miezi sita. Swali langu, je, kutafutamkandarasi kisheria inatakiwa miezi mingapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Jimbo langu laMufindi Kusini tuna tatizo kubwa sana la maji, ukizingatiaSerikali ilijenga matenki ya maji katika kijiji cha Igowole,Nyororo, Idunda, Itandula, Kiyowela matenki haya yoteyameharibika sasa hivi yana miaka karibu sita, je, Serikali inamkakati gani kuhakikisha watu wa Igowole na Nyororo navijiji nilivyotaja vinaweza kupata maji na kukarabati mitandaoambayo imeharibika?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupisana.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, moja anasema muda au mchakatowa kumpata Mkandarasi unakuwa mrefu sana unatumiamuda gani; upo kwa mujibu wa sheria. Muda wa manunuziupo kwa mujibu wa sheria ambayo ilipitishwa katika Bungehili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni kuna matenki11 yaliyojengwa na sasa hayana maji, ni kweli tatizo hilinilikuta pia Nanyamba, kuna matenki zaidi ya saba ambayo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

yalijengwa na AMREF na yalikuwa hayana maji. Matenki yaleyalikuwa yamejengwa pamoja na visima. Sasa jumuiya zawatumiaji maji ambazo tuliziunda tumekuta changamotoziko nyingi unakuta kulikuwa na pump, pump imekufa, kunajenereta, jeneretaimekufa. Wakati mwingine kisima kinakuwakimekosa maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa sasa nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba tunachokifanya sasa hivitumefanya uchunguzi tukakuta kwamba hzi jumuiyazinaelekea kushindwa kufanya hii kazi; lakini sio kwamba nikwa sababu yao tu, hapana; i la ni kwa sababu yamiundombinu iliyowekwa hawana uwezo wa kuiendesha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tumechukuautaratibu wa kuweka solar na visima vilivyopo tutavisafishamaeneo yaliyokuwa na mtiririko tutayaweka vizuri kuhakikishakwamba wananchi wanapata huduma na yele matankiyanafanya kazi iliyotarajiwa.

MWENYEKITI: Ahsante Waheshimiwa tunaendeleaWizara hiyo hiyo Mheshimiwa Hawa Ghasia kwa niabaMheshimiwa Chikota.

Na. 41

Kilimo cha Umwagiliaji Bonde la Mto Ruvuma

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA (K.n.y. MHE. HAWA A.GHASIA) Aliuliza:-

Wananchi wa Kitere na Bonde la Mto Ruvumawamekuwa wakijishughulisha na kilimo cha mpunga kwamiaka mingi.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwawezeshawakulima hao kuwa na kilimo cha umwagiliaji katikamaeneo hayo?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Maji na Umwagiliaji, naomba kujibu swali laMheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Jimbola Mtwara Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Umwagiliaji waKitere ulianza kutekelezwa mwanzoni mwa miaka ya 2000ambapo shughuli zilihusisha ujenzi wa bwawa, mifereji navigawa maji mashambani. Ujenzi huu ulifanyika kwa awamukulingana na upatikanaji wa fedha na kukamilika Disemba,2015. Mradi una jumla ya eneo la hekta 270 na wananchiwanaonufaika ni takribani 3,300 ambao kwa sasawanajihusisha na kilimo cha mpunga na mbogamboga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu matumizi ya Bondela Mto Ruvuma, mwaka 2012 Serikali kwa kushirikiana naSADC iliajiri mtaalam mshauri Kampuni ya SWECO tokaSweden aliyepewa kazi ya kuainisha matumizi mbalimbaliya Bonde la Mto Ruvuma ikiwa ni pamoja na uzalishaji waumeme, umwagiliaji na uhifadhi wa mazingira. Kazi hii tayariimekwishafanyika na taarifa ya mtaalamu mshauri imeainishamaeneo yote ambayo yatafanyiwa upembuzi yakinifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Umwagiliaji waKitere na ile iliyopo katika Bonde la Mto Ruvuma tayariimekwisha ingizwa katika Mpango wa Taifa wa Umwagiliajiwa mwaka 2002 ambao hivi sasa unafanyiwa mapitio iliuendane na hali halisi ya sasa.

Aidha, katika mwaka wa fedha 2017/2018 Wizarayangu imeyaweka maeneo hayo katika bajeti kwa ajili yakuanza kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwalengo la kuendeleza maeneo hayo.

MWENYEKITI: Ahsante Waheshimiwa tunaendelea.

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,swali la nyongeza.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninamaswali mawili ya nyongeza.

Mosi, kuhusu Mradi wa Kitere pamoja kwamba majibuya Mheshimiwa Naibu Waziri yanasema mradi umekamilika,lakini mradi huo umekamilika lakini haufanyi kazi kamaunavyotakiwa na mwenyewe Mheshimiwa Naibu Wazirishahidi amepita pale na hakuona hizi ekari 3,000 zimelimwa.Kwa hiyo, naomba kauli ya Serikali kwamba, kuna mkakatigani wa kukamilisha mapungufu yaliyopo ili mradi huo sasauweze kufanya kazi pasavyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kupitia Ofisi zaUmwagiliaji Kanda, kuna miradi mingi hapa nchini ambayohaifanyi kazi. Juzi Kamati yetu ya LAAC ilikuwa Tabora, kunamradi haufanyi kazi, kuna mradi Liwale, kuna mradi Mkurangana miradi mingine. Sasa Serikali ina kauli gani kuhusu ushauriunaotolewa na ofisi hizi za umwagiliaji kanda ambazo miradimingi ambayo inabuniwa na ofisi hizi huwa haifanyi kaziipasavyo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, kwa kifupi nendatu moja kwa moja kwenye hoja yake.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili yaMheshimiwa Mbunge Chikota, ambayo yote ni kama swalimoja kwamba, miradi hii haifanyi kazi vizuri. Lakini piaameonesha kuwa na utata kidogo katika ushauri wa taasisiyetu inayohusika na umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyozungumzakatika swali la msingi, Mheshimiwa Mbunge, ni kwamba sasahivi miradi yote hii ya umwagiliaji tunaifanyia mapitio. Natulichokibaini ni kwamba tulijenga skimu za umwagiliaji, lakinikutokana na mabadiliko ya tabianchi zile skimu za umwagiliajizimekuwa ama zinafanya kazi mara moja kwa mwaka nawala sio mara mbili kutokana na ukosefu wa huduma yamaji kwa kuwa miradi hiyo hatukuijengea mabwawa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutapitia katika mpangohuu kabambe wa mwaka 2002 tuhakikishe kwamba, miradihii sasa inafanyiwa usanifu na kutekelezwa kuhakikishakwamba, inafanya kazi ile iliyotarajiwa. Lakini mapungufupia yaliyojitokeza katika miradi hiyo tutayapitia, ikiwa nipamoja na kuimarisha tume yetu ambayo WaheshimiwaWabunge ninyi wenyewe mmeunda Tume ya Umwagiliaji kwaajili ya kusimamia moja kwa moja shughuli ya umwagiliaji.

Na. 42

Tanzania Kupeleka Vikosi vya Kulinda AmaniNdani na Nje ya Afrika

MHE. ALLY SALEH ALLY Aliuliza:-

Tanzania imekuwa ikipeleka vikosi vya kulinda amanindani ya Afrika na sehemu nyingine duniani kadri mahitaji nahali inavyoruhusu na kutimiza dhima ya duniani.

(a) Je, mazoezi kama haya yanaimarisha jina laTanzania kiasi gani katika jukumu hili?

(b) Kama miaka kumi iliyopita Tanzania imepelekavikosi maeneo gani na kwa misingi gani?

(c) Changamoto gani zinakuwepo katika kukusanyavikosi hivyo kabla havijapelekwa nje ya nchi kwa kzi kamahizo?

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA Alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali laMheshimiwa Ally Saleh Ally, lenye sehemu (a), (b) na (c), kamaifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania nimwanachama wa Umoja wa Mataifa na inatimiza wajibuwake wa kuzisaidia nchi zenye migogoro ili kuleta amanipale inapoombwa kufanya hivyo. Ushiriki wetu umetuletea

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

heshima kubwa duniani kwa mara zote kuonesha utayariwetu wa kutoa msaada kwa ulinzi wa amani pamoja nakazi nzuri unayofanywa na jeshi letu katika kutekeleza jukumuhili.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika miaka kumiiliyopita Tanzania imepeleka vikundi vya ulinzi wa amanikatika maeneo yafuatayo;

(i) Lebanon, kombania mbili toka mwaka 2008;(ii) Darfur, Sudan, kikosi kimoja toka mwaka 2009; na(iii) DRC zaidi ya kikosi kimoja toka mwaka 2013.

(c) Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto zilizopokatika kukusanya vikundi kabla ya kupelekwa nje ya nchikwenye majukumu ya ulinzi wa amani ni zifuatazo:-

(i) Gharama za kuvihudumia vikosi hivyo vikiwakwenye mafunzo;

(ii) Gharama ya vifaa vya wanajeshi vitakavyotumikaeneo la uwajibikaji; na

(iii) Ugumu wa kupata mafunzo ya uhalisia wamaeneo wanakokwenda kwa mfano jangwani, misituni nakadhalika.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Albeto.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Wanaokwenda kwenye maeneo hayo ambako nikwa kulinda amani mara nyingi hukutana na kujeruhiwa aukufariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na hapa Tanzaniatumeshuhudia wanajeshi hao wakirudi wakiwa wamefarikina wengine wakijeruhiwa. Je, Serikali, hasa kwenye watuwaliofariki, ina utaratibu gani ambao unafanya familia zawanajeshi hao, wapiganaji haokuendelea na maisha baadaya bread winner wao kufariki? Hilo la kwanza.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, MheshimiwaWaziri umezungumza hapa kuna matatizo wakati wakutayarisha vikosi, lakini mimi naona hii ni fursa.

Je, Serikali haioni kwamba, kuna haja ya kujifunza nakutafuta utaalamu kutoka nchi ambazo zime-specializekatika masuala ya kulinda amani, ili iwe ni fursa ya kufunguakituo (centre) ya ku-train watu kwa ajili ya kulinda amani kwaajili ya eneo hili la Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika?Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba katika baadhi yamaeneo ya ulinzi wa amani huwa vinatokea vifo na penginepia huwa watu wanajeruhiwa, lakini upo utaratibu madhubutiwa kuwafidia kwa yote mawili. Nitoe tu taarifa kwamba kwawale ambao wamepoteza maisha katika ulinzi wa amaniUmoja wa Mataifa wenyewe unafidia na wanaporudishwahapa familia zao zinapata maslahi yao yote kwa mujibu wautumishi ambao mhusika alikuwa ameutekeleza hapa nchini.

Kwa hiyo, katika hili hakuna mgogoro, fidia huwazinatolewa kama utaratibu unavyotaka kwa wotewaliojeruhiwa pamoja na wale waliopoteza maisha kwapande zote mbili, Umoja wa Mataifa na Serikali na Jeshi laWananachi wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kujifunzakutoka maeneo mengine juu ya ulinzi wa amani; natakanimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba, hapa Tanzaniatunacho chuo cha ulinzi wa amani. Tumepata msaadakutoka kwa Serikali ya Canada, wamekijenga na mara nyingitunatoa mafunzo, si kwa Watanzania peke yao, ikiwemo nanchi nyingine za Afrika Mashariki wanakuja hapa kujifunzamafunzo haya ya ulinzi wa amani kwa hiyo, hili halina tatizo,tunaendelea vizuri.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jibu langu la msingi,nililosema ni upungufu wa fedha za matayarisho, si suala lamafunzo, mafunzo yapo na chuo tunacho na mafunzoyanaendelea pale kama kawaida.

Na. 43

Mpango wa Kuunda Bodi Mpya ya Tumbaku (TTB)

MHE. MARGARET S. SITTA Aliuliza:-

Pamoja na hatua mbalimbali zinazochukuliwa naSerikali katika kutatua matatizo ya wakulima wa tumbakukatika Mkoa wa Tabora akiwemo wa Wilaya ya Urambo.

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuunda Bodi yaTumbaku (TTB) nyingine ili ianze kazi haraka iwezekanavyobaada ya Bodi ya Tumbaku iliyovunjwa?

(b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikishapembejeo za msimu ujao zinamfikia mkulima wa tumbakumapema wakati huu ambapo bodi husika imevunjwa?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI Alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waKilimo, Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la MheshimiwaMargaret Simwanza Sitta, Mbunge wa Urambo, lenye Sehemu(a) na (b), kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, A, ni kweli kuwa Serikaliimevunja Bodi ya Tumbaku Tanzania kwa lengo la kufanyamarekebisho katika utendaji kazi wa bodi. Hatua hii yakuvunja Bodi ya Wakurugenzi haihusu kusitisha shughulizinazotekelezwa katika tasnia hii ya tumbaku kwani wapowataalam wanaoendeleza utekelezaji wa mpango uliopona kuendeleza soko la tumbaku nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia umuhimuwa uwepo wa Bodi ya Tumbaku nchini kwa maendeleo ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

tasnia hii ya tumbaku, utaratibu unaandaliwa wa kuundaBodi mpya ya Wakurugenzi haraka iwezekanavyo nawananchi watataarifiwa kupitia tamko la Serikali marabaada ya taratibu kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pembejeo za muhimukwenye zao la tumbaku ni pamoja na mbolea aina ya NPK,mbolea aina ya CAN, nyuzi za kufungia tumbaku wakati wakuvuna na wakati wa masoko, vipande vya magunia namadawa. Pembejeo hizo huagizwa kupitia vyama vikuu vyaushirika kwa kila eneo kwa kupitia mchakato wa zabuniunaosimamiwa na kuratibiwa na vyama vikuu vya ushirika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia kuwawakulima wanahitaji huduma muda wote hasa kipindi hikicha kuelekea masoko ya tumbaku kwa msimu wa 2017/2018,Serikali kupitia Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchiniameshateuwa timu nyingine ambayo ipo Mkoani Taboraikiendelea kuratibu na kusimamia masuala mbalimbali yawakulima, ikiwa ni pamoja na kuandaa upatikanaji wapembejeo kwa msimu ujao. Hivyo, naomba kumhakikishiaMheshimiwa Mbunge kuwa, pamoja na Bodi ya WETCUkuvunjwa, lakini kazi za chama kikuu zinaendelea kamakawaida.

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu. Pamoja namajibu yako na jit ihada kubwa inayochukuliwa naMheshimiwa Waziri Mkuu katika kutatua changamoto za zaola tumbaku, naomba niulize maswli ya nyongeza kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, msimu wa kuuzatumbaku, yaani msimu wa masoko ya tumbaku ni sasa, nimwezi huu wa nne, Serikali inatoa kauli gani kuhusuyafuatayo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza uongozi wa AMCOSambao umefutwa kutokana na agizo la Serikali nakuwaacha bila uongozi kipindi hiki ambacho masoko

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

yanaanza? Serikali inasema nini kuhusu suala hili? IkiwemoAMCOS ya Utenge na Nsenga ambazo hazina uongozi hadisasa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pil i, Serikaliinasemaje kuhusu kuwasaidia wakulima ambaowamejitahidi wao wenyewe kutokukopa, lakini hatimayewamejikuta wanabebeshwa madeni yasiyowahusu nakuwaacha hoi kiuchumi. Serikali inatoa kauli gani? Ahsante.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI:Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uuzaji wa tumbaku katikamazingira ambayo uongozi wa AMCOS umefutwa auumesimamishwa; taratibu zitaendelea kushughulikiwa kwakupitia Chama Kikuu katika maana hiyo WETCU na kamanilivyokwishsema tayari WETCU imewekewa utaratibu wampito, ili kuweza kufanya kazi zake kama kawaida. Kwa hiyo,kama kuna AMCOS ambazo hazina uongozi uuzaji watumbaku utaendelea kushughulikiwa na chama kikuu chaushirika, lakini vilevile kwa kushirikiana na vyombo vinginekama Maafisa Ushirika, lakini vilevile kwa kupitia watendajiambao bado wapo kwenye Bodi ya Tumbaku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Mheshimiwa Mbungeameuliza kuhusu wakulima ambao wanalazimika kubebamzigo wa madeni ambayo yametokana na wao kuwepokwenye vyama vya ushirika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kati ya sababuzilizosababisha Mheshimiwa Waziri Mkuu kuchukua maamuzimazito kuhusiana na WETCU na Bodi ya Tumbaku ni kwasababu kulikuwa na usimamizi mbovu sana kuhusiana namadeni ya vyama vya ushirika, hali ambayo ilisababishawakulima kimsingi kubebeshwa madeni ambayo kwa kiasikikubwa hata matumizi ya fedha ambazo zimekopwautaratibu wake haufahamiki sawasawa. Kwa hiyo, hatuaambazo zinachukuliwa ni ili kuondoa hiyo hali, ni ili ifahamike

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

kwamba, mikopo ambayo inachukuliwa inafanya kazi gani,lakini vilevile ni kuwawajibisha wale ambao wamekopafedha na kuzitumia kwa njia ambazo ni kinyume na taratibu.

Na. 44

Wanafunzi Wanaopata Mikopo ya Elimu

MHE. MATTAR ALI SALUM Aliuliza:-

Kuna malalamiko makubwa kwa upande waZanzibar kuhusu idadi ndogo ya wanafunzi wanaopataMkopo wa Elimu ya Juu jambo ambalo linapunguza idadiya wataalamu kwa upande wa Zanzibar, hivyo kuingiakatika soko la ajira katika Afrika ya Mashariki na Kati nakuijenga nchi yetu kwa ujumla.

(a) Je, Serikali haioni kuwa Bodi ya Mfuko wa Elimu yaJuu inatakiwa kutenga asilimia maalum kwa wanafunzikutoka Tanzania Zanzibar?

(b) Je, bajeti iliyotengwa kwa mwaka huo wa2015/2016 ni kiasi gani?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAAlijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali laMheshimiwa Matta Ali Salum, Mbunge wa Shaurimoyo, lenyeSehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, utoaji wa mikopo kwawanafunzi wa elimu ya juu huzingatia matakwa ya sheria,kanuni, vigezo na miongozo itolewayo mara kwa mara naSerikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.Vigezo muhimu vinavyozingatiwa ni pamoja na kwambamuombaji awe ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,awe mhitaji, mlemavu au yatima. Aidha, muombajianatakiwa kuwa amedahiliwa katika taasisi ya elimu ya juu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

na awe anachukua programu za vipaumbele vya taifaambavyo ni ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa gesina mafuta, sayansi za afya na uhandisi wa kilimo na maji.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2015/2016 kiasi cha shilingi 480,599,067,500 kilitumika kwa ajiliya kugharamia mikopo pamoja na ruzuku kwa ajili yawanafunzi 124,358.

MHE. MATTAR ALI SALUM: Mheshimiwa Mweyekiti,ahsante sana kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili yanyongeza. Kwanza nisawazishe jina langu, mimi naitwaMattar Ali Salum, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri akilijibu alijibuvizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sanaMheshimiwa Waziri kwa majibu yake ambayo ameyatoa.Mheshimiwa Waziri, wapo wanafunzi wanaendelea kupatamikopo ya Serikali kwa kima kidogo hadi sasa, husababishakukosa kukidhi mahitaji ya vyuo husika ambavyowamepangiwa. Je, Serikali ni kwa nini isiwaongezee fedhawanafunzi hawa ili waweze kukidhi mahitaji ya vyuo husika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wako wanafunziwalikuwa wakipata mikopo kwa kipindi kirefu, ghafla Serikaliimewafutia mikopo yao, sijui ni kwa nini. Je, MheshimiwaWaziri, Serikali ina mpango gani wa kuwarejeshea mikopohawa wanafunzi ili waweze kukidhi na kuendelea na masomoyao vizuri? Ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba nijibu swali laMheshimiwa Mbunge, kama alivyorekebisha jina lake, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba kiuhalisiatulingependa kutoa mikopo kwa wanafunzi wengi zaidi,lakini vilevile ingewezekana hata kila mwanafunzi akapata

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

mkopo kwa kadiri ya mahitaji ya chuo anachosoma; lakinikwa sababu fedha hazitoshi inakuwa ni vigumu kufanya hivyona tunaangalia zaidi ni uhitaji wa kiasi gani upo.

Kwa hiyo, kwa misingi hiyo niseme tu kwamba, Serikaliitaendelea kutenga fedha ya kuona kwamba, inawasaidiawanafunzi wengi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kuhusu kufuta mikopo.Ni kweli kuna baadhi ya wanafunzi walifutiwa mikopokutokana na kutokuwa na vigezo vinavyostahili. Hata hivyoSerikali imeendelea kulifanyia kazi suala hilo ili kuona kwamba,anayefutiwa mkopo iwe kweli ni mtu ambaye hana uhitaji.Kwa yule mwenye uhitaji na kwamba vigezo vyote vimetimiabasi, baadhi yao tumeweza pia kuwarejeshea.

MWENYEKITI: Waheshimiwa maswali yoteyamekwisha.

Wageni waliopo Bungeni asubuhi hii. Wageni waliokoJukwaa la Spika; tunao Waheshimiwa Wajumbe wanane waBaraza la Wawakilishi Zanzibar ambao ni Wajumbe waKamati ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti MheshimiwaMohammed Said Mohammed, karibuni Bungeni. Hawawamekuja kwenye mafunzo, watakutana na Kamati ya Bajetimuda huu ili wabadilishane mawazo kwa nia njema ya nchiyetu. (Makofi)

Pia tunao wageni mbalimbali wa WaheshimiwaWabunge pamoja na wageni waliokuja kutembea Bungekwa ajili ya mafunzo Bungeni, pamoja na Madiwani ambaoni Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii wakiongozwana Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga,Mheshimiwa Charles Makoga na hawa ni wageni waMheshimiwa Chumi, karibuni Bungeni. Mbunge wenuanawapenda, sasa tena na ninyi mumpende (Makofi)

Tangazo la semina; naomba kuwatangaziaWaheshimiwa Wabunge kuwa kesho, Jumatano, tarehe 12mwezi huu, mwaka huu, kutakuwa na semina kwa Wabunge

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

wote kuhusu masuala ya hisa. Semina hiyo ambayoitaratibiwa na taasisi ya Vodacom, Dar es Salaam StockExchange na Capital Market Security Authority itafanyikakatika Ukumbi wa Bunge kuanzia saa 7:00 mchana. Aidha,katika semina hiyo Wabunge watapata fursa ya kununua hisaza Vodacom. Katibu!

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mwongozo wa Spika!

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mwongozo wa Spika!

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa, hebu soma…unayo Kanuni hapo eeh? Soma Kanuni ya 52. MheshimiwaSugu kaa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,52 inasema; “Shughuli za Serikali zitaanza wakati Spikaatakapomwita Waziri au Mwanasheria Mkuu wa Serikalialiyetoa taarifa ya kuwasilisha Muswada au ya kutoa hojaBungeni baada ya Katibu kusoma jambo linalohusika kwenyeOrodha ya Shughuli.”

MWENYEKITI: Endelea.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: (2) Baada ya Spika kutoawito huo Mbunge yeyote binafsi hataruhusiwa kutoa hoja yakuahirisha shughuli za Bunge wala kuuliza swali.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, hizi kanunituzisome. Nikishamwita Katibu…Subirini, nikishamwitaKatibu, naanza shughuli zangu. Nataka mniwahi, siyo miminiwawahi ninyi.

WABUNGE FULANI: Aaaaaah!

MWENYEKITI: Kwa vile mlikuwa hamjui na sasamnajua…

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Tulikuwahi.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

42

MWENYEKITI: Subiri basi Sugu! Mheshimiwa Msigwakaa kwanza. Kwa vile mlikuwa hamjui, sasa nimewajulisha,nawapa fursa leo Mheshimiwa Mchungaji Msigwa naMheshimiwa Sugu. (Makofi)

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,na Sixtus Mapunda.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti,niko kwenye Kanuni ya 68(7), naomba mwongozo wako wakikanuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana Mheshimiwa Bilago,Mbunge wa CHADEMA na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMATaifa ambaye pia anawakilisha UKAWA, aliomba mwongozokuhusu matusi ya Mbunge wa CCM, Mheshimiwa Mlinga dhidiya Upinzani ambapo alieleza namna ambavyo Mbunge huyuanatoa matusi Bungeni, lakini anaachwa bila kuchukuliwahatua zozote with impunity na ameshazoea. Lakini NaibuSpika alikuwa amekalia Kiti akamjibu Mheshimiwa Bilago,Mjumbe wa Kamati Kuu kwamba suala hilo kwa kuwalilitokea jana yake, kanuni hairuhusu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wiki i l iyopita, akinaMheshimiwa Kangi Lugola wa CCM waliomba mwongozokuhusu jambo lililotokea siku tatu zilizopita kwenye uchaguziEALA, tena nje kwenye press. Japokuwa zilikuwa zimepitatakribani siku tatu, mwongozo wao ulifanyiwa kazi, hatimayeKiongozi wa Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Mbowe ambayealihukumiwa kwa kuzungumza kwenye press na MheshimiwaMdee wakaitwa katika Kamati ya Maadili, tena kwa mkwarawa kukamatwa na polisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hii ni double standardya hali ya juu na inaligawa Bunge. Unapoligawa Bunge, kwakuwa humu kuna wawakilishi wa Taifa, maana yakeunaligawa Taifa kule nje bila kujijua.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

43

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba mwongozowako, kwa nini kiti kinakuwa na double standard ya hali hiyohasa anapokalia Naibu Spika? Kwa sababu Kanuni ya 64(7)inahusu jambo lililotokea mapema, lakini haisemi jambolililotokea mapema leo, inaweza kuwa mapema leo, jana,juzi hata mapema mwezi uliopita kwa mujibu wa kanuni ile.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mwongozo wako.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Nasimama kwa kanuni hiyo hiyo ya 68(7).

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Wabunge ni wawakilishiwa wananchi na ni ukweli usiopingika kwamba katika kipindicha hivi karibuni wananchi pamoja na sisi Wabunge tukokwenye taharuki kubwa kwa vitendo vinavyofanyika katikanchi yetu vya watu kutekwa na watu ambao hawajapewamamlaka ya ku-arrest au ku-interrogate kufanya kazi hizo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku mbili hizi kuna baadhiya Wabunge wa pande zote mbili wameomba mwongozoili Bunge liweze kujadili kwa manufaa ya Wabunge wenyewena Taifa kwa ujumla kwa sababu sisi ndio wawakilishi wawananchi lakini mwongozo huo umekataliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Spikajana amekataa, yeye ana walinzi, ana ma-bodyguard. SisiWabunge hatuna walinzi katika nchi hii. Watanzania wengihuko mitaani wanaishi kwa hofu na sisi ndio wasemaji wao.Masuala makubwa kama haya ninavyojua, mimi siomwanasheria lakini chombo pekee kinachoruhusiwa ku-arrestna ku-interrogate ni Jeshi la Polisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yametokea matukiomakubwa ya kutisha; tumeona watu ambao hata Wizara

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

44

ya Mambo ya Ndani inayohusika, inasema mtualiyemnyooshea bastola Mheshimiwa Nape, sio Polisi, lakinimpaka sasa yupo kwenye custody, hajakamatwa. Watuwalioenda kuteka tv ya Clouds, Jeshi la Polisi limesemahawakuwa polisi. Hawa watu hawajawa arrested. Sasachombo kikubwa kama Bunge, tumekaa kimya, business asusual na Serikali katika kipindi chote hiki haijatoa tamkololote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaye Waziri wa Sheriahapa amekaa kimya, hasemi chochote kuhusu sheriainasemaje? Sasa hili ni Bunge gani ambalo tutaka kimya,mambo makubwa kama haya katika nchi yanatokea?Tunafanya nini hapa? Nilikuwa naomba mwongozo wako.(Makofi)

MBUNGE FULANI: Roma bado…

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Roma kisaikolojia inaonekana bado ametekwa. Mtu kamayule huwezi kum-parade kwenye vyombo vya habari;anatakiwa akutane na psychologist am-counsel kwanza.Sasa mnampeleka pale anatumika kama stepping stone.Bunge kazi yake ni kujadili mambo haya, tutakaa tunafanyanini? Huu ni mkutano wa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mwongozo wako,kazi yetu ni nini kama tunaomba haya mambo halafu Wazirianayehusika hasemi, Waziri wa Mambo ya Ndani amekaakimya, haya mambo yanatokea katika nchi? Sasa tufanyejekama Wabunge? Na sisi Wabunge tunanyamazishwa.Mheshimiwa Mwakyembe Wizara haimhusu, kasimama paleanatoa matangazo. Sasa sisi kama Wabunge tufanyeje?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mwongozo wako.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chief Whip.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

45

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni unayo nafasi na sitakikuingilia utaratibu wako wa kikanuni wa kuweza kutoaufafanuzi wa miongozo ambayo Waheshimiwa Wabungewameiweka mbele yako kwa mujibu wa kanuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda tu wewe sasakama Mwenyekiti wa Bunge hili na kwa kuwa mambo hayayameendelea kuzungumzwa, nadhani itakuwa vizuriWaheshimiwa Wabunge ambao wanazungumza jambo hilina kama wana ushahidi wa kutosha wa mambo haya...(Makofi)

WABUNGE FULANI: Aaah!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU): …MheshimiwaMwenyekiti wa Bunge, wafanye utaratibu ili tuweze kulimalizajambo lenyewe vizuri kwa kuzingatia maamuzi yaliyotokea,lakini kwa kuzingatia utaratibu pia wa kimfumo na wakisheria. Kuna haja sisi Waheshimiwa Wabunge wote kwapamoja tupate nafasi nzuri ya kupata uthibitisho wa mambohaya kupitia taratibu zinazotakiwa na hatua stahiki ziwezekuchukuliwa na jambo hili liweze kufikia mwisho kwa kufuatasheria na taratibu zilizopo. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sana,kwetu sisi Waheshimiwa Wabunge ambao tumekuwatukilieleza jambo hili toka jana nadhani…

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Ah, wewe kaa chini!

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Kaa chini!

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

46

MHE. MWITA M. WAITARA: Huyu anaingilia mamlakaya kiti.

MWENYEKITI: Kaa chini.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, nafikiri ifike mahali sasa tuchukue nafasi yetukama Wawakilishi wa Wananchi kulisaidia Taifa tuleteuthibitisho mbele ya meza yako na hatua ziweze kuchukuliwakwa kufuata kanuni, taratibu na sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,niliomba mwongozo, nilikuwa wa kwanza.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, haya mamboyanazungumzwa…

MBUNGE FULANI: Mwenyekiti unayumba.

MWENYEKITI: Mimi nayumba? Unataka nikutoe njeujue ninavyoyumba? Aah, unataka nikutoe nje ujueninavyoyumba? (Makofi/Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, kama alivyosema ChiefWhip hili suala kiti inalichukua na tutalifanyia maamuzibaadaye. Katibu!

NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka2017/2018 - Ofisi ya Waziri Mkuu

(Majadiliano yanaendelea)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza na

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

47

Mheshimiwa Esther Matiko, atafuatia Mheshimiwa RashidAbdallah, Mheshimiwa Munde Tambwe Abdallah naMheshimiwa William Ngeleja.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kuweza kunipatia fursa hii nami niwezekuchangia kwenye hotuba ya Waziri Mkuu. NaombaWaheshimiwa Wabunge kama tunatambua ni nini wananchiwametutuma kufanya kwenye Bunge hili Tukufu, basituwatendee haki kwa kufanya yale ambayo wametutumakufanya na kutokujitoa ufahamu na kufanya kinyume naambavyo tumetumwa na wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kuunga mkonohotuba ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni na ninaombaWaheshimiwa Wabunge msome hotuba zote pamoja nakwamba mtakuwa mnayo mengine kichwani, lakini hotubaya Upinzani kwa kweli imeeleza mengi na mazuri kwa Taifaletu, tuweze kuishauri vema Serikali ili tuweze kusonga mbelekama nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2016 nilisema kabisawakati wa bajeti imepitishwa na niliandika kwenye mtandaowa Bunge, nikasema hii bajeti ikitekelezwa hata kwa asilimia70 tu, nikatwe kichwa changu. Mbunge mmoja, ndugu yanguMheshimiwa Chegeni akaingia inbox akaniambiaunamaanisha nini? Sasa napenda nimwambienilichokimaanisha ndiyo tunachokiona leo, kwamba mpakaleo bajeti ya maendeleo hata asilimia 40 hatujafika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nishauri kwambakuliko kuja na bajeti ambazo hazina uhalisia, kama mpakaleo hatujafika asilimia 40, ile bajeti ya mwaka jana, tuchukuenusu yake ndiyo tuilete. Tulete bajeti ambazo zinatekelezeka.Tusiandike matumaini kwenye makaratasi mwisho wa sikuhata asilimia 50 tu hamfikishi. Tuwe na uhalisia ili hataunapokuwa umeelezwa kwamba mathalan Mkoa wa MaraJimbo la Tarime Mjini kwenye maendeleo kwa mwaka wafedha 2017/2018 tutaleta shilingi bilioni moja, basi na hiyoshilingi bilioni moja tuweze kuitekeleza. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

48

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambaloningezungumzia tuliondoa duty free kwa majeshi kwa maanaJeshi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Polisi, Askari waUhamiaji, Askari wa Majini na Magereza. Cha ajabu mpakaleo kumekuwa na double standard. Kuna wenginewameshalipwa mara mbili, kwa maana ya kila mwezi laki,laki; wameshalipwa shilingi laki sita. Jeshi la Wananchi waTanzania na Askari Polisi, lakini Askari wa Uhamiaji, Majini naMagereza mpaka leo hawajalipwa. Ndugu zangu, tunatakakujua ni kwa nini kunakuwa na double standard?

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba kabisaMheshimiwa Waziri Mkuu awaangalie ndugu zetu Magereza,wamekuwa wakionewa sana. Unakuta Askari Magereza anadegree lakini bado analipwa mshahara kama yule askari wakidato cha nne. Leo mnawalipa hawa wengine, lakini hawaAskari Magereza niliowatja mpaka leo hamjawalipa. Walewatu ni muhimu sana na ikizingatiwa kuna watumnawapeleka kwa kesi za kubambikwa kule Magereza.Hawa watu wakiamua kugoma, wale watu waliopomagerezani kule kutakuwa hakukaliki. Kwanza mngekuwamnatumia busara zaidi, mngewalipa wale kabla hatahamjawalipa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Naombamzingatie hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna madeni wanadaiya mwaka 2012/2013; 2013/2014 mpaka leo hawajalipwa. Leomfungwa akitoroka, hawa ndugu zetu wanapewa adhabukutokwenda masomoni, wanapewa adhabu ya kukatwafedha, maisha wanayoishi ni duni na kipato chao ni duni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu naWaziri husika tunaomba hawa ndugu zetu muazingatie nawenyewe waweze kupata hiyo package ambayo mliiondoaya duty free nao waweze kupata stahiki zao kamamnavyowapa Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi waTanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hotuba ya WaziriMkuu ametanabaisha kwamba wamejitahidi sana katika

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

49

kuwawezesha wananchi, lakini ukisoma ameainisha kwambakuna shilingi bilioni moja sijui pointi ngapi wamewapa vijanakwa mfuko wa vijana na shil ingi bil ioni 4.6 kupitiaHalmashauri, kwamba ndiyo hapo wamewezeshawananchi. Hatuko serious na Serikali hampo serious.Mlituambia mmetenga milioni 50 kwa kila kijiji au mtaa,mpaka leo mtuambie mmetekeleza vipi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Waziri Mkuu akijaakasema kwamba Halmashauri zimejitahidi kupeleka 4.6billion kuwezesha wananchi ilhali mkijua kuna Halmashaurinyingine hazina kipato cha kutosha, mathalan Halmashauriya Mji wa Tarime, tumejitahidi, hapo zamani walikuwa hatahawatoi hela. Kwa mwaka huu, tumejitahidi tumetoa tenmill ion. Ten mill ion only; leo mnasema tunawezakuwawezesha wananchi kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali itekeleze ile ahadiyao ya shilingi milioni 50 kila mtaa na kijiji; tumehamasishawananchi wameunda vikundi mbalimbali na SACCOStunazihitaji hizo shilingi milioni 50. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye elimu.Mheshimiwa Waziri Mkuu, ndugu yangu amesema kabisatumejitahidi kutoa elimu bure na vitu kama hivyo. Ni dhahiribaada ya kuja hii elimu bure sijui, wakasema kwambausipopeleka motto, unafungwa; kweli tumeandikisha watotowengi sana mashuleni, lakini hatuangalii idadi. Tunatakiwatuangalie quality ya ile elimu ambayo tunaitoa. Leo mmesajiliwanafunzi wengi, lakini walimu wanadai madeni mengi nahamjawapa mazingira mazuri ya kuwafanya wafundishewatoto wetu waweze kuelewa, hawana motisha yoyote ile,leo mnategemea kutakuwa na ufaulu mzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mmesema mmerekebishamadawati. Sawa, madawati kwanza kuna sehemu nyinginebado hayajatosheleza, madarasa hayatoshi. Wananchiwanajenga, Serikali inashindwa kwenda kuezeka, vitabuhamna pamoja na kwamba TWAWEZA jana wamesema rationi moja kwa tatu, lakini mimi kwangu darasa la kwanza na

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

50

la pili ni moja kwa tano; darasa la tatu mpaka la saba,kitabu kimoja; wanafunzi 50 mpaka wanafunzi 100. Hapotunategemea elimu bure itatoka wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuwe serious, kama tunatakatutoe elimu ambayo ni nzuri kwa wanafunzi wetu, elimu bora,tuwekeze na walimu wawe na motisha, wapewe fedhastahiki, walipwe madeni yao na wawe na mazingira mazuriya kufundishia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee afya. Hospitali yaMji wa Tarime mmeandika kwamba bado ni Hospitali yaWilaya ya Tarime, lakini mnaleta OC na basket fund ambazozinatumika idadi ya wananchi wa Mji wa Tarime, wakatikiuhalisia wanahudumia wananchi wa Wilaya nzima yaTarime, watumishi mmepunguza idadi wakati wanahudumiawananchi wa Wilaya nzima ya Tarime, wengine wanatokaRorya na wengine Serengeti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwepo na vigezostahiki. Kama mnaona ni vyema hospitali ile iwe ya Wilaya,basi tunaomba OC na basket funds zije kwa idadi yawananchi wa Wilaya ya Tarime na siyo idadi ya wananchiwa Mji wa Tarime. Mnawapa kazi kubwa watumishi, unakutadaktari anafanya masaa zaidi ya 30 wakati alitakiwa awekazini kwa saa nane tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye maji. Kunamradi wa kutoa maji Ziwa Victoria ambao usanifuulishafanyika na Benki ya Maendeleo ya Ufaransa wapotayari ku-sponsor huo mradi ambao unaanzia Shirati, Ingili Juu,Utegi, Tarime mpaka Sirari. Kuanzia mwaka 2011 watuwamefanya design mpaka leo haujatekelezwa. Napendakujua ili kutatua tatizo la maji Tarime, ni lini huu mradi utaanzakufanya kazi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, fidia ya ardhi yawananchi ambao Jeshi la Wananchi wa Tanzaniawamechukua. Nimekuwa nikiimba sana hapa Bungeni naMheshimiwa Waziri Mkuu, naomba unisikilize katika hili.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

51

Mheshimiwa Mama Ritta Kabati mwache Waziri Mkuuanisikilize, maana nimekuwa nikiimba hii kuanzia mwaka 2007.Jeshi la Wananchi wa Tanzania limechukua maeneo yawananchi wa Nyandoto, Nyamisangula na Nkende mpakaleo hawajalipwa. Kama… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Rashid AliAbdallah, ajiandae Mheshimiwa Munde.

MHE. RASHID ALI ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Kwanza sina budi kumshukuru MwenyeziMungu kwa kunipa uwezo leo hii kusimama hapa. Pianakushukuru wewe kwa kunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana nakupongeza hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani kwa jinsiilivyoelekeza Serikali kwa mwelekeo wa mwaka 2017/2018.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii nitazunguka katikamaeneo machache kabisa kuhusu ulinzi na usalama wataifa, utawala bora na uchumi wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yoyote dunianiinaongozwa kwa kutegemea Katiba na Sheria. Ni hatarikubwa sana kuona Katiba na Sheria za nchi zinavunjwawakati watawala wanasaidia na kufurahia. Narejea, Katibana Sheria zinavunjwa katika nchi hii, watawala wanasaidialakini pia wanafurahia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mzuri zaidi niuchaguzi haramu wa Zanzibar wa Machi, 2015. Uchaguzi huuulivunja Katiba ya nchi, viongozi walifurahia na wamesaidia,lakini tunasema mapambano yanaendelea, haki ya Zanzibartutaidai na tunaendelea kuidai na itapatikana kwa haliyoyote. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

52

Mheshimiwa Mwenyekiti, vitendo vya uvunjaji washeria kwa Msajili wa Vyama Siasa, Kamati ya Katiba, Sheriana Utawala ni Kamati ya Bunge, inapofanya kazi Kamati yaBunge ina maana Bunge zima linafanya kazi. Taarifa zaKamati ya Katiba na Sheria inaweka wazi kwamba Msajiliwa Vyama vya Siasa amevunja Sheria za Vyama vya Siasana kuingilia uhuru wa vyama vya siasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni taarifa ya Bunge nataarifa ya Bunge inakemea kitendo hiki cha Msajili wa Vyamavya Siasa. Kauli hii ni ya Bunge, siyo Kamati ya Katiba na Sheria.Waheshimiwa Wabunge wote lazima mwone hili lipo nalimekemewa na Kamati ya Katiba na Sheria. Kwenda kinyumekwa Msajili kwa vitendo hivi, atakwenda kinyume na taarifaza Bunge. (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa!

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chief Whip.

TAARIFA

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kutumia Kanuni ya 68(8) kumpa Taarifamchangiaji wa hoja. Ukisoma Taarifa ya Kamati ya Katibana Sheria hakuna kifungu chochote katika Taarifa hiyoambacho kimesema kwamba Msajili wa Vyama amevunjasheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa ya Kamati imetoaushauri kwenye Ofisi ya Msajili wa Vyama, imetoa ushauri kwaMsajili wa Vyama kuvilea na kuvishauri vyama na haijasemaMsajili wa Vyama amevunja sheria. Kwa hiyo, naomba nimpeTaarifa Mheshimiwa Mbunge asiiwekee Kamati ya Bungemaneno ambayo hayamo kwenye taarifa ya Kamati yaBunge. (Makofi)

MWENYEKITI: Taarifa hiyo Mheshimiwa Rashid.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

53

MHE. RASHID ALI ABDALLAH: MheshimiwaMwenyekiti…

MBUNGE FULANI: (Aliongea nje ya kipaza sauti).

MWENYEKITI: Sasa mpaka mumfundishe!

MHE. RASHID ALI ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa hiyo siikubali na Kamati ya Sheria ilimwita Msajili,ikamhoji (ukurasa wa 30 naendelea kusoma) na ikamwonyaMsajili huyo. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba masikitikoyangu na nitaendelea kusikitika sana kuona Jeshi la Polisilinashiriki kisiasa wazi wazi na kuleta hujuma na kuvunja sheriawakati Jeshi la Polisi linalinda uvunjaji wa sheria. Nalaani sanavitendo hivi. Watu wote mnafahamu, mnajua na mnaona,halihitaji ushahidi, Serikali imenyamaza kimya. Hii nasema nimkakati wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi la Polisi limepotezamwelekeo kwa wananchi na litaendelea kupotezamwelekeo kwa wananchi kwa sura hii, tutakuwa hatunaimani kabisa na Jeshi la Polisi. Na mimi nilishasema, sitakikuchangia Jeshi la Polisi, sina imani kabisa na Jeshi la Polisi.Baadhi ya Jeshi la Polisi wanavunja sheria, Serikali ipoinayamaza kimya, wanashiriki uvunjaji wa majengo yachama, Jeshi linalinda na linaangalia tu bila kuchukua hatuayoyote. Kitendo hiki ni kibaya sana kwa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Msajili pamoja na washirikawake mlivunja Katiba ya Vyama vya Siasa na mlivunja Sheriaza Usajili. Kwa kufanya hivyo, amevunja msingi mkubwa wautawala bora na kwa misingi hiyo, amevunja demokrasianchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba Msajili ajue,matokeo yake ni nini? Matokeo yake ataliingiza Taifa hilikatika mgogoro mkubwa kwa Muungano wetu, lakiniatahatarisha amani ya Taifa hili, la tatu, ataingiza Taifa hili

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

54

katika mgogoro wa kiuchumi. Mnalifurahia lakini matokeoyake mtayaona mbele tunakokwenda. Kwa kufanya haya,uchumi wetu utadorora, ndani na nje ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende haraka harakakuhusiana na masuala ya uchumi. Sekta za uzalishaji maranyingi zinakuwa ni sekta za kiuchumi na kwa maana hiyokuna nchi nyingi ambazo zimejikita katika maeneo mahsusiya kiuchumi, kwa mfano, nchi ya Afrika Kusini imejikita katikabiashara, madini na utalii; Algeria mafuta na uzalishaji;Nigeria mafuta na mawasiliano, Morocco utalii, viwandavya nguo pamoja na kilimo. Tanzania kuna msururu kabisa,series!

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa!

MWENYEKITI: Taarifa.

TAARIFA

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,Waziri wa Nchi aliposimama hapa dakika chache zilizopitaalinukuu ripoti ya Kamati kwamba Kamati…

MWENYEKITI: Mheshimiwa, sasa unampa nani taarifa?

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nampa taarifa msemaji.

MWENYEKITI: Hapana Mheshimiwa, kaa.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Ningemwomba…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Rashid, endelea.

MHE. RASHID ALI ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti,Tanzania kuna series za mambo ya kiuchumi, kuna kilimo,viwanda, maliasili, madini, gesi, usafirishaji and so on and soforth. Kilimo kinawakilishwa kwa asilimia 75 na Watanzania,

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

55

kilimo kinabeba Watanzania wengi sana, lakini awamu hiiinaelekea kana kwamba kilimo siyo kipaumbele chake hasa,kina viashiria hivyo. Nasema hivyo kwa sababu mwaka2015/2016 Serikali iliyopita ilitoa pembejeo za kiasi cha shilingibilioni 78, lakini Serikali hii hadi kufika hapa imetoa pembejeoza shilingi bilioni 10. Kutoka shilingi bilioni 78 mpaka shilingibilioni 10, hivi kweli Serikali hii inawaambia nini wakulima?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kusema kwamba kilimokinaanza kushuka na kwa sababu hakuna mbolea ya kutoshaambayo imetolewa na Serikali, tutegemee upungufumkubwa wa mazao katika kipindi kinachofuata. Hili litakuwani tatizo kubwa kweli kwa wananchi walio wengi waTanzania.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. RASHID ALI ABDALLAH: MheshimiwaMwenyekiti,…

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Munde Tambwe.Mheshimiwa Ngeleja, Mheshimiwa Chikota na MheshimiwaNkamia wajiandae.

MHE. MUNDE T. ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa fursa hii na mimi niweze kuchangiahotuba ya Waziri Mkuu.

Kwanza kabisa niapongeza Serikali yangu ya Chamacha Mapinduzi, nampongeza Waziri Mkuu pamoja naMawaziri wake, Mheshimiwa Jenista, Mheshimiwa Mavundepamoja na Baraza zima la Mawaziri kwa kazi nzuriwanayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naungana na Wabungewenzangu wa Tabora kumpongeza kwa dhati MheshimiwaWaziri Mkuu kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutatua keroya tumbaku Mkoani Tabora. Mheshimiwa Waziri Mkuutunakuombea kila la heri, Mwenyezi Mungu akuwezeshe ili

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

56

umalize kero hii ya tumbaku ambayo imetukabili kwa miakamingi sana. Tunakuamini, tunajua utaimaliza naumedhamiria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile naipongeza Ofisi yaWaziri Mkuu kwa kazi kubwa wanayoifanya, wameanzishaprogramu maalum ya kuhakikisha wanafuatilia Ilani yaChama cha Mapinduzi itekelezeke, lakini kufuatilia ahadi zoteza viongozi wakuu. Nawapongeza pia kwa kuhamiaDodoma, wamefanya kazi kubwa. Tulikuwa tunasikia tokatukiwa wadogo kwamba Serikali inaenda Dodoma, lakiniimeenda Dodoma leo hii. Tunaipongeza sana Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napongeza Kitengo chaBaraza la Uwezeshaji ambacho kipo chini ya Ofisi ya WaziriMkuu. Baraza la Uwezeshaji limefanya kazi kubwa yakuwatambua, kuwabaini wajasiriamali wadogo ambao kwaMkoa wa Tabora wameianza kazi hiyo na kuwawezeshakuwapa mitaji ili waweze kusonga mbele na huu ndiyouchumi wa kati ambao tunautaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri tu Serikali yangu,naishauri Ofisi ya Waziri Mkuu kwamba hili Baraza laUwezeshaji lingeungana na watu wa SIDO likaungana naWizara ya Viwanda ili kuwawezesha hawa wajasiriamaliwadogo sasa waweze kuingia kwenye viwanda vidogovidogo, mkiungana nadhani itakuwa vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongee kuhusubajeti. Nimesikia wenzangu wanasema kwamba kulikuwa nabajeti hewa, nimesikia jana kuna neno linaitwa bajeti hewaambapo mimi kama Mbunge wa Tabora sikubaliani na hikikitu cha bajeti hewa na sababu ninazo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa ukiniambiabajeti hewa, mimi nimeingia hapa Bungeni mwaka 2011,nilikuwa nahangaika kila siku kugombana kuhusu maji yamradi wa Ziwa Victoria, leo hii mkandarasi yuko site tokamwaka 2016. Kwa hiyo, ukiniambia bajeti hewa, siwezikukuelewa. Tulikuwa tunahangaika na barabara ya lami ya

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

57

Chaya – Tula ambayo inaunganisha kutoka Dar es Salaam -Tabora mpaka Urambo kwa lami, leo hii mkandarasi yukosite. Pia tulikuwa tunahangaika kwamba uwanja wetu wandege unatua ndege ndogo tu, leo hii mkandarasi yuko siteanafanya matengeneza ya kupanua uwanja wa Tabora.Kwa hiyo, sikubaliani kabisa na kuniambia kwamba kunabajeti hewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, punda hasifiwi kwa rangizake, anasifiwa kwa kazi anazozifanya na mzigo anaobeba.Hii Serikali ya Hapa Kazi Tu inafanya kazi sana, Rais wanguMheshimwia Dkt. Magufuli anafanya kazi sana. WamwacheMheshimiwa Rais afanye kazi! Toka nikiwa mdogo nikiwaTabora nasikia Waheshimiwa Wabunge wa Taborawanalalamika kuhusu reli ya kisasa, lakini leo hii minara yareli ya umeme imeanza kutengenezwa. Reli ya standardgauge inajengwa. Leo mtu ananiambia kuna bajeti hewa,sitakaa nikubali. Huu ni uongo na niwaombe Wabungewenzangu, tuseme Serikali inapofanya mambo mazuri,tusinyamaze, tusiogope, tuseme. Nimetoka kifua mbele,nasema Serikali yangu imefanya mambo makubwa sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa humu Bungenikipindi kilichopita, kaka yangu Mheshimiwa Zitto kama yupoatasema. Tulikuwa tukisimama tukiungana kulilia ndege,wanasema nchi gani hii, inashindwa hata na Rwanda, hainahata ndege moja. Leo tuna ndege, watu wanasema kwanini tumenunua ndege? Wamwache Mheshimiwa Rais afanyekazi, waiache Serikali ifanye kazi. Tukifanya kazi, mnasema,tusipofanya kazi, mnasema. Tunajua binadamu hata ufanyenini, hawezi kukusifia kwa asilimia 100, tufanye kazi kamatulivyojipangia. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaongelea elimu bure.Kuna mtu labda ana hela watoto wake hawasomi shule hizianaona utani. Leo hii shule zimejaa, madarasa yamejaa,watoto wanasoma, hakuna ma-house girl vijijini. Yote hii nijuhudi ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi na MheshimiwaRais, Waziri Mkuu na Serikali yake. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

58

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tumeona juzi, mwaka2016 hii bajeti hewa UDSM, leo hii watoto 4,000 watakaakwenye mabweni UDSM, yamejengwa kwa muda wa harakasana. Leo unaniambia Serikali haijafanya chochote,sitakubali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, REA, tumemwonaMheshimiwa Muhongo huko, umeme unawaka vijijini. Leo hiitunashindwa kusifia Serikali yetu. Nawaomba Wabungewenzangu, tusiingie baridi, tutoke tuseme memayaliyofanywa na Serikali yetu. Watu wanasema viwanda,viwanda gani? Vitajengwa lini? Viwanda hewa. Mpaka hapaninapoongea, tunajenga viwanda 2,160 na hii issue yaviwanda tumeanza juzi mwaka 2016, Magufuli kaingiamwaka mmoja. Mimi niwaulize Wabunge wenzangu, ninyikwenye Majimbo yenu mwaka mmoja mmefanya mangapi?(Makofi)

MBUNGE FULANI: Kweli!

MHE. MUNDE T. ABDALLAH: Mbona mnaisema Serikalitu! Kuna watu hapa hawajawahi kufanya chochote.Akimwona DC ameenda kwenye mkutano wa DC, nayeanakwenda kama Mbunge. Lako wewe kama Mbunge likowapi? Tuoneshe. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Sema, sema.

MHE. MUNDE T. ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti,naishukuru sana Serikali yangu, nampongeze MheshimiwaRais, Mheshimiwa Waziri Mkuu na Mawaziri wake, wanafanyakazi. Hii nchi ni kubwa jamani, kazi ni ngumu. Ni rahisi sanakukosoa, lakini ukiambiwa kafanye wewe, hiki kitu ni kigumujamani, tuwatie moyo, tuwaombee kwa Mwenyezi Munguwaweze kutekeleza walioyaahidi. Ni faida yetu sisi wote.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunajisifu Tanzania nikisiwa cha amani, Tanzania ina amani, Tanzania ina utulivu,nani aliyetuletea utulivu? Ni Usalama wa Taifa. Leo tumo

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

59

humu, tuna amani tu. Leo tukitoka tutaenda Club, tunaendatunarudi hata saa 9.00 usiku, tuna amani. Kama kuna madoamadogo madogo, basi yatashughulikiwa, lakini tusisemeUsalama wote hawafanyi kazi. Hiki kitu nakataa nanitaendelea kukataa. Tuko hapa kwa sababu ya amani.Tunajisifu, tuna sifa dunia nzima, kisiwa cha amani. Amaniinatengenezwa, kuna watu hawalali kwa ajili ya amani hiituliyonayo, ni lazima tuwatie moyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukifuga mbwa ukionahabweki, bweka mwenyewe. Leo nimeamua kusemamwenyewe. Wenzetu hawa kama hawayaoni haya, leonimeamua kuyasema mimi niliyeyaona. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongezee kidogokuhusu Msajili wa Vyama vya Siasa (Registrar), amekuwaakishambuliwa sana. Nasema vyama vingi ni tatizo, ni kazikubwa. Sheria zake anazozisimamia, ndiyo maana leotumekaa Wabunge wa CUF, wa CCM, wa CHADEMAtunaongea kwa sababu wa usimamizi mzuri wa Registrar.Tulishuhudia watu walitaka kupigana viti kule Ubungo kwenyemikutano yao, lakini Registrar kwa kazi yake kubwaaliyoifanya, ndiyo leo CUF kuna amani na utulivu. Ndiyo leowameweza kukaa pale wote wakiwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napata shida sanatunapokuwa tunawashambulia wataalam, tuwatie moyokwa kazi wanazozifanya. Pale kwenye upungufu tusiachekusema; tuseme. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nirudie kusema,naipongeza sana Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi,nampongeza sana Rais, Mheshimiwa Dkt. Magufuli na sisitumwambie tupo, tutasema. Sisi ni wanasiasa, kazi yetu nikusema. Tutasema na tunamuunga mkono kwa asilimia miamoja kwa kazi anazozifanya. CCM oyee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwakunisikiliza. (Makofi/Kicheko)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

60

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Ngeleja.Mheshimiwa Chikota na Mheshimiwa Nkamia wajiandae.

MHE. WILLIAM M. NGELEJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana, nakushukuru sana. Na mimi naungana nawenzangu kumshukuru sana na kumpongeza MheshimiwaWaziri Mkuu kwa hotuba yake nzuri sana, yeye pamoja nawasaidizi wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijazungumzia mambomanne ambayo nimepanga kuyazungumzia, nina salamu zapongezi kutoka kwa wananchi wa Jimbo la Sengerema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, tunaipongezaSerikali, lakini kwa hapa tunazungumza mbele ya MheshimiwaWaziri Mkuu, tufikie salamu kwa viongozi wote wakuu wanchi yetu pamoja na wewe Mheshimiwa Waziri Mkuu kwanamna ambavyo mnaratibu shughuli za maendeleo ya Taifaletu. Tunazungumza kama Wabunge tukiwa tumejumuikakutoka katika maeneo mbalimbali. Yapo maeneo ambayosisi wenyewe kutoka kwenye maeneo tunayofanyia kazi nimashahidi kwa namna ambavyo shughuli za maendeleozinafanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaipongeza Serikali kwanamna ambavyo imeshughulikia jambo moja kubwa ambalolilishakuwa kidonda ndugu kwa Taifa letu nalo ni nidhamuya kazi. Taifa lilikuwa limefikia mahali pabaya. Sisi wote nimashahidi, tumekuwa tukifika kwenye taasisi za umma nakuona namna ambavyo huduma zimekuwa zikitolewa miakailiyopita, lakini tuseme kweli kabisa, katika hii Awamu ya Tano,tumeshuhudia mageuzi makubwa ya uwajibikaji kwaWatendaji wetu. Kwa hilo tunamshukuru sana MheshimiwaRais, lakini kiranja mkuu katika usimamizi wa Serikali,Mheshimiwa Waziri Mkuu. Shukrani za pekee kwa namnaambavyo unalifuatilia hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kule Sengerema tunamambo makubwa yamefanyika, moja, namshukuru sanaWaziri wa Afya, Mheshimiwa Ummy pamoja na Mheshimiwa

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

61

Dkt. Kigwangalla kwa namna ambavyo mnatusaidia katikaJimbo la Sengerema. TAMISEMI pale, Mheshimiwa Jafo naMheshimiwa Waziri Simbachawene, kile Kituo cha Afya chaNgoma A ambacho mmekitengea fedha, wananchi waSengerema wamenituma nifikishe salamu zenu kwa shukranikwa namna ambavyo mnatufanyia kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Engineer Lwenge na msaidizi wako NaibuWaziri, ule mradi mkubwa kabisa katika nchi za Jumuiya yaAfrika Mashariki kwa ngazi ya Halmashauri na Wilayaunaofanyika Sengerema, sasa uko katika hatua za mwishokabisa. Shukrani kwenu pamoja na Serikali nzima kwa namnaambavyo mmesimamia mradi huo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Simbachawenetuna kiporo. Tumezungumza miezi michache iliyopita. Kwenyehesabu za Mfuko wa Jimbo zilizofanywa hivi karibuni, yapobaadhi ya Majimbo ambayo tulipunjwa. Halmashauri yaSengerema ni mojawapo hali iliyotokana na makosa yakimahesabu. Mmetuahidi kwamba kufikia mwisho wa mwezihuu fedha zile zitakuwa zimeshafika, lile salio. NaombaMheshimiwa Simbachawene na Serikali kwa ujmla, jambo lamapunjo ya Mfuko wa Jimbo mlifanyie kazi, fedha zifikemahali pake, zifanye kazi kwa ajili ya wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizamie kwenye mchango,la kwanza, Mheshimiwa Waziri Mkuu tunaanzia kwenyeukurasa wa 43. Umeanzishwa mfumo wa wazi wakielektroniki kufuatilia uwajibikaji na utendaji wa Serikali,jambo hili ni kubwa sana. Ni muhimu tuipongeze Serikali.Wamesema, kwa kupitia utaratibu huu, wata-trackutekelezaji wa ahadi ambazo zimefanywa na Serikali kupitiaIlani ya Chama cha Mapinduzi, matamko, ahadi za viongoziwakuu wa Serikali akiwepo Mheshimiwa Rais, Makamu waRais pamoja na Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Serikalikatika hili ni kwamba kwa sababu hatuna mashaka yoyotekuhusu umakini na Serikali yetu, lakini pia kwa kutambuakwamba sisi Wabunge ndio daraja la wananchi na Serikali,

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

62

nilikuwa naomba uandaliwe utaratibu ambao Serikali kupitiaOfisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, watakuwa wanatushirikishaWabunge, tujiridhishe kujua yale ambayo tunaya-track katikamaeneo yetu ya kazi ni yapi? Miradi gani ambayo inaonekanakatika ule mfumo? Mahali ambapo pamesahaulika, sisituwakumbushe kwa kusema hili nalo ni sehemu ya yalemambo yaliyokusudiwa, yafanyiwe kazi kupitia huu mfumowa kielektroniki ambao utawasaidia Watanzania kufahamushughuli ambazo zinafanywa na Serikali.

Kwa hiyo, naomba na nilikuwa naamini kwambaatakapokuwa anafanya majumuisho Mheshimiwa WaziriMkuu pamoja na wasaidizi wake, atatusaidia kuona umuhimuwa kutushirikisha sisi Wabunge tujue miradi ambayo uki-google ama ukibonyeza ule mfumo unakuletea miradiiliyotekelezwa katika maeneo yetu. Tusipofanya hivyo,narudia tena kusema kwamba, sina mashaka na utendajiwa Watumishi wa Serikali, lakini binadamu ni binadamu. Sisini jicho la pili kusaidia kufikia yale yaliyokusudiwa katikakuyasimamia yaliyotekelezwa kwa namna ambayotunakusudia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumezungumzia jambomoja la kufanya maendeleo katika maeneo yetu ya kazi.Tunapanga bajeti, kila mwaka tunaipitisha hapa. Tumekuwana changamoto ambayo sijapata jibu lake, tutasaidianakadri ambavyo siku zinaendelea. Suala la disbursement,kufikisha pesa ambazo tunazipitisha hapa kwenye bajetikwenda kwenye maeneo yetu. Ninazungumzia kutotimizajukumu hili ama wajibu huu ambao sisi tunaufanya Kikatiba,tumekuwa tukipitisha bajeti kila mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninavyozungumza hapaSengerema kwenye OC ambazo ndizo fedha ambazozimeidhinishwa kufutil ia miradi mbalimbali ambayotunazungumzia hapa tuna asilimia 20 tu, lakini shughuli zamaendeleo tuna asilimia 30. Nafahamu WaheshimiwaWabunge wengi wanalalamika. Hilo siyo la kumnyoosheamkono mtu yeyote, lakini ushauri wangu kwa Serikali,

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

63

tusaidiane kupitia chombo hiki cha uwakilishi wa wananchituone namna bora zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumejifunza na mwaka 2016tumeshauriana hapa, yapo mambo tulikubaliana kwambayako mambo hayakunyooka sana, lakini tutumie nafasi hiikatika Bunge hili tuelewane vizuri kwa mfumo huu wa bajetitulionao, tuone namna ambavyo tunaweza kutekeleza bajetiambazo tunazipeleka kule. Haina maana yoyote kupitishamafungu hapa kwa kiwango fulani halafu utekelezaji wakeunakuwa chini ya asilimia 50. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachozungumza, hili niletu sote, halina itikadi ya vyama kwa sababu tunazungumziautekelezaji wa mambo ambayo kwa pamoja tumekubalianakuyatekeleza. Kwa hiyo, nashauri sana Kamati ya Bajetipamoja na Serikali kwa ujumla, tushauriane namna bora yakuhakikisha kwamba mafungu tunayoyapitisha, fedhazilizokusudiwa zinafika mahali pake palipokusudiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mweyekiti, ukisoma Mkataba wa Nchiza Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo sasa ziko sita, ukisomaIbara ya 49 inayozungumzia namna ambavyo tunawezakuimarisha mtengamano wa nchi za Jumuiya ya AfrikaMashariki. Inazungumzia habari ya Bunge Sports Club ikiwani chombo mahsusi kutoka Bunge la Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kushiriki katika michezo hiyo ambayoinafahamika kutokana na Mkataba wa Jumuiya ya Nchi zaAfrika ya Mashariki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumzia jambo hili kwasababu ninaona kuna masuala yanaingiliana na hii hotubaya Mheshimiwa Waziri Mkuu na hasa lile Fungu la Mfuko waBunge. Bajeti ya Bunge Sports Club inatokana na huo mfuko.

Naomba Bunge pamoja na Serikali kwa ujumla tuonekwamba ushiriki wa Bunge Sports Club katika michezo siyojambo la anasa ama la kwenda kutumia pesa hovyo, bali ninyenzo ya utekelezaji wa Mkataba wa Jumuiya ya AfrikaMashariki. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

64

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sanaMheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Spika, MheshimiwaWaziri Mkuu, Watendaji wote wa Serikali na Bunge kwanamna ambavyo mliwezesha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2016 tulikwendakwenye mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,Mombasa; tuliondoka katika mazingira magumu kidogo,lakini ninavyozungumza sasa hivi mambo yote yako level seat.Shukrani za pekee kwa Mheshimiwa Spika na Naibu Spikapamoja na Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa namna ambavyomliwezesha jambo hilo. Tunasema ahsanteni sana. naimeandikwa katika maandiko matakatifu, asiyeshukuru kwakidogo hatashukuru kwa kikubwa. Sisi tumepata kikubwa,kwa nini tusishukuru? Ahsanteni sana. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Moto, moto, moto.

MHE. WILLIAM M. NGELEJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,mwisho, lakini siyo kwa umuhimu, mimi ni Mjumbe wa Kamatiya Sheria Ndogo inayoongozwa na Mheshimiwa MtemiChenge. Unapozungumzia fedha nyingi ambazo tunazipitishahapa, utekelezaji wake unakwenda kutekelezwa kutokanana miongozo na sheria zilizotungwa katika Halmashauri, Taasisizetu mbalimbali zikiwemo Wizara za Serikali. Ninachotakakuzungumza hapa ni kwamba tunapozungumzia Sheriazinazotungwa na Halmashauri zetu, ndiyo mpango wa fedhawenyewe. Tumeshuhudia wote kama Taifa, wakati mwingineviongozi wakuu wa Serikali wamekuwa wakitamkamatamko ambayo wakati mwingine katikati ya safariwanaamua kuondoa tozo ambazo zimeshakubalika kwautaratibu wa kisheria kwa namna ambavyo tumekasimumadaraka kwenye Halmashauri zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, silaumu katika hilo kwasababu kama kuna kero ni lazima ishughulikiwe hapo hapo,lakini ninachosema, tuboreshe utaratibu wa namnaambavyo tunaweza kukatiza katikati ya safari, kwa sababuhizi Sheria Ndogo ndiyo zinaongoza mafungu ya kuleHalmashauri na hasa mafao yale ambayo yanakwenda

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

65

kuwawezesha hata Madiwani wetu ambao sisi tulioko hapatunawategemea na ni Madiwani wenzetu kutekeleza miradimbalimbali ambako fedha nyingi zinakwenda. Tusiwakatishekatikati ya safari. (MakofI)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya bajeti hizi, kuwena utaratibu mzuri wa kukaa pamoja tuelewane kwambamwaka huu tutaondoa tozo hizi na hizi ili wasizifuate kwenyebajeti zao wanazoziweka. Tukikatisha katikati tutakujakuwalaumu hawa wawakilishi wa wananchi wenzetukwamba hawatimizi wajibu wao, lakini kwa kweli mazingiraambayo yamesababisha kumbe nasi tumeyachangia. (Maiofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa hili narudiakusema, simlaumu mtu yeyote lakini naomba tulifanyie kazikwa uzuri kwa namna ambavyo tutaweza kuwa… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Chikota.Mheshimiwa Nkamia na Mheshimiwa Shangazi wajiandae.

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,na mimi naungana na wenzangu kumpongeza MheshimiwaRais kwa kazi kubwa anayofanya katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni MheshimiwaRais alifanya ziara Mkoani Mtwara na ametufanyia kazikubwa sana, mojawapo ikiwa ni kutatua changamotoambayo ilikuwa inakabili Kiwanda cha Dangote. Hapa janakuna mchangiaji mmoja alitoa maelezo ambayo penginealichokifanya Rais kule Mtwara hakukielewa, anasemaDangote amepewa eneo la mgodi kwa ajili ya kuchimbamakaa na maamuzi yale yatakuwa na athari kamatutakavyofanya mchanga kutoka kwenye migodi ya almasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilichofanyika Mtwara nitofauti na hicho alichokisema mchangiaji kwa sababuMheshimiwa Rais ametatua changamoto mbili kuu ambazo

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

66

Kiwanda cha Dangote kil ikuwa kinakabiliwa nayo.Changamoto ya kwanza ilikuwa ni upatikanaji wa Makaana alisema tunaamua hapa hapa. Mheshimiwa Muhongona Mawaziri wengine walikuwepo na walipewa siku sabakwamba taratibu zote zifuatwe ili achimbe mkaa mwenyewena kodi zote stahili alipe ili apeleke kwenye kiwanda chakecha Mtwara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu cha pili, MheshimiwaRais alitatua tatizo la muda mrefu ambalo ni upatikanaji wagesi asilia kutoka Madimba. Tulikuwa tunalalamika hapakwamba wawekezaji wakubwa hawasikilizwi, kwa hiyo,Mheshimiwa Rais akatoa maamuzi pale kwamba TPDC impeumeme Dangote bila kupitia kwa mtu mwingine wa pili. Kwahiyo, maamuzi yale ni ya kumpongeza sana Mheshimiwa Raisna siyo ya kumkatisha tamaa kwamba alichofanya siyo sahihi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kwa niaba yaWabunge wa Mtwara na kwa niaba ya wananchi wa Mtwaratunamshukuru sana Rais wetu kwa maamuzi mazitoaliyoyafanya katika ziara yake Mkoani Mtwara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka nichangie hojanyingine ukurasa wa 23 wa hotuba ya Mheshimiwa WaziriMkuu.

Kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza MheshimiwaWaziri Mkuu kwa hatua alizochukua katika kusimamia zaola korosho. Wananchi wa Mtwara na wananchi wa Kusiniwanakupongeza kwa kile ulichokifanya mwaka huu. Kwanzahukusita kuvunja bodi pale uzembe ulipotokea, lakini pili,ulichukua hatua ya kusimamisha uendeshaji wa Mfuko waPembejeo na kazi hiyo sasa ikapelekwa kwenye Bodi yaKorosho na kusimamia kwa karibu kwa yale yanayoendeleakatika tasnia ya korosho katika msimu wote. Hata palezilipopotea tani 2,000 kwenye lile ghala la Masasi, ulichukuahatua za haraka na wale watuhumiwa sasa hiviwamefikishwa kwenye vyombo vya sheria. Tunakupongezasana. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

67

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na jitihada hizo,bado kwenye mfumo wetu wa Stakabadhi Ghalani kunachangamoto ambazo kwa usimamizi wako MheshimiwaWaziri Mkuu na Waziri wa Kil imo nafikiri msimu huumtazirekebisha ili bei ya korosho izidi kupaa, na sisi Wana-Mtwara tunategemea bei ya korosho mwaka huu itafika kiloshilingi 5,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto zilizopo nipamoja na wakulima kucheleweshewa malipo na hii ni kwasababu vyombo vingi havikujiandaa na ununuzi wa msimuwa mwaka huu na ule utaratibu wa mwaka huu. Tumeonapale ghala ya Benki Kuu ilikuwa inaingia Mtwara kila baadaya siku moja. Kwa hiyo, nafikiri kwa sababu sasa hivi Tawi laBenki Kuu limezinduliwa Mtwara, yale ambayo yalikuwayanatokea mwaka huu kwamba kila baada ya siku mojazinapelekwa fedha Mtwara, nafikiri msimu ujaohayatajitokeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kuna changamoto yausafirishaji. Tumeona pale zikitokea kauli mbili; Watendaji waBandari wanasema Bandari ya Mtwara inaweza kusafirishakorosho lakini Mkoa wa Lindi wanasema kwamba Mtwarahawana uwezo wa kupeleka korosho zote, kwa hiyo,tusafirishe kwa barabara. Yote kwa yote, kuna changamotopale zimejitokeza. Kwa hiyo, ni matarajio yangu kwambaMamlaka ya Bandari, Wizara husika na Wizara ya Kilimowataishughulikia hii changamoto ili mwakani korosho zotezisafirishwe kwa Bandari yetu ya Mtwara kwa sababu koroshozinaposafirishwa kwa Bandari ya Mtwara, tunawapa vijanawetu ajira, lakini vilevile tunadhibiti ununuzi wa korosho holelaule ambao unajulikana kwa jina la kangomba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo tunatakiwatulifanye katika mfumo wetu wa Stakabadhi Ghalani,tuongeze uwazi. Sasa hivi kuna malalamiko kwa wakulimakwamba mkulima anauza korosho yake kwenye mnada wapili, lakini amelipwa kwa bei ya mnada wa tano. Kwa hiyo,nafikiri hili Wizara ya kilimo italifanyia kazi. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

68

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, katika mfumo huuwa Stakabadhi Ghalani, kuna tozo moja. Kwanzatumshukuru na tumpongeze Mhesimiwa Waziri Mkuu, mwaka2016 kwa usimamizi wake walifanikiwa kuondoa tozo tanokwenye zao la korosho. Kwa hiyo, kuna tozo moja ambayoinalalamikiwa sana na wakulima, tozo ya uchangiaji wagunia. Ni matarajio yangu kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu,Wizara ya kilimo na wadau watalishughulikia suala hili ili guniazinunuliwe na Bodi ya Korosho au Mfuko wa Kuendeleza Zaola Korosho ili wakulima wasichajiwe ile fedha ya kuchangiaununuzi wa gunia kila kilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende ukurasa wa 36ambao unahusu elimu na mimi nakubaliana kauli ya WaziriMkuu kwamba uchumi wa viwanda lazima unahitaji rasilimaliwatu yenye weledi, lakini rasilimali watu yenye welediinapatikana kukiwa na mfumo bora wa elimu. Lazima hapatukubaliane kwamba tunapozungumzia mfumo bora waelimu au tunapozungumzia elimu bora, hatuwezi kusahaumahitaji na kero za walimu.

Kwa hiyo, naomba sana Serikali yangu ya Awamu yaTano ijikite katika kuondoa changamoto zinazowakabiliWalimu. Walimu bado wana malalamiko kwamba wanamadai, bado hatujaandaa incetive package kwa Walimuwapewe motisha; lakini Walimu vile vile wanahitaji mafunzokazini. Kwa hiyo, naomba Serikali chini ya Mheshimiwa ProfesaNdalichako na Mheshimiwa Simbachawene, basiwalishughulikie hili suala la matatizo ya walimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie mchango wangukuhusu suala la maji. Kwanza naipongeza Wizara ya Maji kwakazi kubwa ambayo wanaifanya na katika Jimbo langu kunaharakati ambazo zinaonekana, za kuongeza kiwango chaupatikanaji wa maji kutoka asilimia 40 kwenda kwenyemalengo yetu ya kufika asilimia 85, lakini bado kunachangamoto nyingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ya kwanzakuna ule mradi ambao tunatarajia kupata mkopo kutoka

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

69

Benki ya India, miradi 17 ambapo ni pamoja na mradi waMuheza, ule mradi wa Makonde. Kwa kweli ni muda mrefusasa hivi tunataka mradi huu uanze kutekelezwa. Kila sikumnasema kwamba tunamalizia financial agreement, lakinisasa hivi natarajia Wizara ya Maji itaongeza speed ili mradihuu uanze kutekelezwa. Mradi huu ukianza kutekelezwa kwamiradi ile 17, tuna uhakika kwamba asilimia ya watu wetuambao wanapata maji vijijini itaongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hivyo tu, kwa sisi Wana-Mtwara kuna mradi wa kutoa maji Mto Ruvuma na kupelekaManispaa ya Mtwara. Mradi huu ni tegemeo kwetu nautaongeza upatikanaji wa maji katika Jimbo langu laNanyamba. Kwa hiyo, naomba pia na utekelezaji wa mradihuu usimamiwe kwa karibu na fedha zipatikane ili utekelezajiwake uanze mara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja na yaleyote ambayo yapo katika kitabu cha Waziri Mkuuyakitekelezwa, tuna uhakika kwamba nchi yetu tunakwendakule ambako tunatarajia. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Nkamia.Mheshimiwa Shangazi na Mheshimiwa Kikwete mtotowajiandae. (Makofi)

MHE. JUMA S. NKAMIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu,lakini pia nawapongeza sana wachezaji wa Simba, janakidogo watulaze na viatu, lakini kwa kweli kazi waliyoifanyani nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina machache tu, lakwanza nachukua nafasi hii kwa dhati kabisa ya moyowangu kumpongeza sana Mheshimiwa Rais, Dkt. John PombeMagufuli, Mheshimiwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwakazi nzuri wanayoifanya ya kuleta maendeleo ya Taifa letu.Wakati mwingine maneno haya ni kwa sababu mnafanyakazi nzuri. Ukiona mtu anakushambulia hivi, ujue unafanya

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

70

kazi nzuri sana. Na mimi niwatie shime kwamba endeleenina kazi hiyo ili Taifa letu liweze kusonga mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekeekabisa, nawapongeza watu wa TAMISEMI vilevile na Wizaraya Afya kwa kutupatia fedha kwa ajili ya Kituo cha Afya chaHamai ambacho kwa leo ndiyo tunakitumia kama Hospitaliya Wilaya ya Chemba. Nawashukuruni sana na ninaombakazi hiyo ya kujenga wodi, nyumba za waganga iwezekufanyika kwa haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nizungumzie maji. TunaMradi wa Maji wa Ntomoko, alisimama Mbunge mmoja hapaakasema ufutwe, lakini mimi nasema ashindwe tu, kwa jinala Yesu. Ni kama amedandia gari katikati, kwa sababu hajuichanzo chake na hajui mwisho wake. Mradi huu unachangamoto zake ndogo ndogo, lakini mimi namshukuruMheshimiwa Waziri Mkuu kwa kukubali kwenda, kama Munguakijaalia wiki ijayo ili na wewe ujionee kwa namna mojaama nyingine changamoto zilizopo kwenye mradi huu iliziweze kutatuliwa na watu wapate maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu ni suala la kuhamiaDodoma. Kwa namna ya kipekee kabisa sisi Wabunge waDodoma tulikuwa na mkakati kabla ya tamko la MheshimiwaRais kuleta muswada binafsi hapa Bungeni ili Serikali ihamieDodoma, lakini namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwakuamua kwa dhati ya moyo wake kuhamia Dodoma, lakinisuala hili halipo kisheria. Naiomba Serikali sasa ilete muswadaBungeni hapa ili iwe sheria. Anaweza kuja mtu mwinginekesho akasema Makao Makuu ya nchi anayapeleka kwingine.Kwa hiyo, niwakumbushe hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile pamoja na kuhamiaDodoma, harakisheni ujenzi wa mradi wa maji wa bwawala Farkwa ambao pia utaongeza maji Dodoma, Chemba,Chamwino na Bahi. Leo tathmini imeanza kule Farkwa,Mombose na Bubutole, vile vijiji vinahama basi wale watuwalipwe fidia zao mapema.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

71

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la nne, Serikali lazimaiwe active, lakini siyo kuwa active kwa kukosea. Nitoe mfano,samahani sana, jana nilikuwa naangalia mkutano wawaandishi wa habari (press conference) na yule Bwanaanaitwa sijui nani yule…

MBUNGE FULANI: Roma.

MHE. JUMA S. NKAMIA: Roma Mkatoliki. Hivi Waziriwa Habari alikwenda kufanya nini? Unajua wakati mwingineunaweza kuambiwa ukweli ukachukia, lakini ni afadhaliuambiwe ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Habariamekwenda kwenye mkutano wa Roma Mkatoliki,anampisha na kiti, anayeongoza press conference ile niZamaradi Kawawa, Afisa wa Serikali. Hivi kesho, mtuakikwambia wewe ndio ulimteka Roma, utakataaje? Ni vizuriuchukue ukweli hata kama unauma, lakini take it. At theend of the day unaweza ukafanya marekebisho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati mwinginemnamgombanisha Mheshimiwa Rais na wananchi bilasababu ya msingi. Mimi sikuona logic kabisa. Mimi siyomwanasheria, nimesoma uandishi wa habari na nimesomauhusiano wa kimataifa, lakini this is wrong. Is not applicable!

Kwa hiyo, Serikali wakati mwingine mnaingia kwenyemtego wenyewe bila kujua. Hebu liangalieni hili, ilitokea wapimpaka Mheshimiwa Waziri anakosa kiti, anahama, halafuhuyu mtu binafsi anafanya press conference, weweunakwenda kufanya nini? What were you doing there? Halafuleo akina Nkamia wakisema ukweli humu, kuna watuwanasema, aah, unajua labda kwa sababu alikosa Uwaziri.No, we have to tell you the reality! This is a principle! (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuhusu sualala kuongeza maeneo ya utawala. Hapo nyuma tumeongezasana maeneo ya utawala lakini bado tunashindwa

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

72

kuhudumia yale maeneo tuliyoyaongeza. Hebu angalieni,malizeni kwanza tatizo la yale maeneo mliyoyaongeza yautawala ndiyo muanze kuongeza maeneo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfuko wa Jimbo ulipoletwa,idadi ya watu ilikuwa tofauti na sasa. Fanyeni review, Chembailikuwa na watu 160,000, leo tuko watu 250,000, lakini badokiwango cha Mfuko wa Jimbo kinachotolewa ni kile kile chawakati ule na wakati mwingine kinapunguzwa, amesemaNgeleja hapa. Hebu angalieni namna gani mnawezakuongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kil imo. Janaamesema hapa Mbunge wa Kiteto, kuna tatizo kubwa katiya Wilaya ya Chemba, Kiteto, Kongwa na Gairo. Watu waKiteto wanafikiri kama ni Jamhuri ya Wamasai hivi ndani yaTanzania. Baadhi ya viongozi wanaopelekwa katika maeneohaya, nao ni shida. Hebu tusaidieni, mtaniwia radhi. RAS waManyara, DC wa Kiteto, DC wa Chemba, kabila moja nawanawasiliana vizuri sana. Matokeo yake kumekuwa na crisiskatika Wilaya hizi kwa sababu Wagogo, Wakaguru, Warangihawatakiwi Kiteto. Amekaa miaka 30 anaambiwa ondokaleo. Hivi leo na sisi tukaamua Mrijo tukafunga mpaka, hakunaMmasai kuingia Chemba…

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

TAARIFA

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: MheshimiwaMwenyekiti, nilitaka tu kumweleza mwenzetu kwambawakati mwingine kuna mambo magumu yanatokea ambayoviongozi tunayaona, lakini wakati mwingine unaangaliamaneno ya kutumia kwa ajili ya umoja wa utaifa wetu hatakama una uchungu wa jambo fulani, cha kwanza ni kufikiriaTanzania iliyo moja na kuchagua maneno ya kutumia nakutafuta namna ya kiuongozi ya kupeleka hoja yako naikaeleweka. Ahsante.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

73

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nkamia, taarifa.

MHE. JUMA S. NKAMIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, huoni ushauri, wala siyo taarifa tu. Kwanza hawa niliowasema, niwatani zangu wote, hawa Wakurya wote watani zangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachosema,tunazungumza leadership credibility. Wapo watu wanapewavitu vidogo vidogo kuwaumiza baadhi ya watu. Mtu amekaamiaka 30, unamwambia ondoka leo, acha nyumba yako,wewe ni Mrangi nenda Chemba. Wewe ni Mgogo toka,nenda Kongwa, wewe ni Mkaguru toka nenda Gairo. Tukaekimya! This is a problem. Ni ndani ya Tanzania hii kaka yanguanayoisema pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tufike wakati sasatuwe serious ili tuendelee kuishi kwa umoja na amani yetu.Namshukuru kaka yangu pale, namheshimu sana kwa ushauriwake, nimeupokea, lakini pia kwa wakati mwingine nanyiupande wa pili muwe mnaangalia maneno ya kutumia, isiweupande mmoja tu. Kisu kikate kote kote. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie la mwisho, mimi nimwana michezo. Naomba sisi Wabunge tuiunge mkono timuya Serengeti Boys kwa nia njema kabisa na Serikali nayo iwekemkono wake ili timu yetu ikafanye vizuri, badala ya kulaumutu wachezaji, na sisi tuoneshe moyo wa upendo kwa timuzetu ili tupate vijana walete heshima kwa Taifa letu. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Shangazi jiandae,Mheshimiwa Kikwete na Mheshimiwa Nsanzugwankoutachukua nafasi ya Mheshimiwa Shangazi.

MHE. RIDHIWANI J. KIKWETE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kwanza nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungukwa kunijaalia afya njema na kunipa nafasi leo hii yakuzungumza. Pia nimpongeze sana Mheshimiwa Mama

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

74

Salma Kikwete kwa kuapishwa kuwa Mbunge wa Bunge laJamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kipindi kirefu sanaamekuwa anahangaika na masuala yanayohusu watoto,hasa yatima, wasio na uwezo na akina mama. Nina uhakikakabisa kwa kupata nafasi ya kuwa Mbunge, Mheshimiwa Raisamefanya jambo jema sana kwa makundi haya na sasawatapata mtetezi wa kweli ambaye anayaishi yaleatakayokuwa anayaongea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo,namwombea pia kwa Mwenyezi Mungu Rais wetu apeweafya njema sana aendelee kuhudumia Taifa hili ambalolinamhitaji sana kipindi hiki kuliko muda mwingine wowote.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo, pianamwombea heri mzee wangu, Mzee Chrisant MajiyatangaMzindakaya ambaye anaugua pale Dar es Salaam,Mwenyezi Mungu ampe afya njema na apone mapema iliaendelee kuwa mshauri katika maisha yetu sisi vijana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo, napendasana pia niwape pole wananchi wenzangu wa Jimbo laChalinze na Halmashauri ya Chalinze hasa kwa tatizo kubwalililotupata ndani ya siku mbili au tatu, kutokana na mvuakubwa ambazo zinanyesha sasa katika maeneo yetu.Tumeshuhudia barabara zikikatika, tumeshuhudia magariyakisimamishwa, safari zinasimama lakini baya zaidi niuharibifu mkubwa wa miundombinu na nyumba zetu ambaoumetokea katika Halmashauri yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampa tu taarifaMheshimiwa Waziri Mkuu kwamba hapa ninaposimama leohii kuzungumza, zaidi ya kaya 150 hazina mahali pa kulalawala hazijui zitakula nini kutokana na tatizo kubwa lamafuriko lililokumba eneo letu lile. Ninachomwomba yeyepamoja na Serikali ni kuangalia njia za haraka zitakazofanyikahasa katika kile chakula cha msaada ili wananchi wanguwa Halmashauri yetu ya Chalinze wapate chakula kwanza

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

75

wakati tunajipanga kuona mambo mengine tunayafanyavipi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo pia kipekeekabisa, naomba sana wananchi wenzangu wa Jimbo laChalinze kwamba Mbunge wao niko pamoja nao sana nakatika kipindi hiki kigumu mimi baada ya kumaliza kuchangialeo hii, nitarudi tena kukaa nao na kushauriana nao. Piatumeomba tukutane kama Madiwani kupitia Kamati yetu yaFedha ili tuweze kuona tunaweza kuchanga kipi au kutoakipi katika Halmashauri yetu ili kukabiliana na hali hiyo ngumuambayo wananchi wenzangu wanaikabili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, sasanirudi katika mchango wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu nanitapenda nianze na eneo la maji na viwanda. MheshimiwaWaziri Mkuu, tunatambua kwamba Serikali yetu imewekamsisitizo mkubwa sana katika kuhakikisha kwamba viwandavinajengwa katika eneo hili la Tanzania na katika kipindi hikikifupi tumeshuhudia mabadiliko makubwa sana katika ujenziwa viwanda. Waziri Mkuu mwenyewe anaweza kuwa shahidina Serikali inaweza kuwa shahidi juu ya jinsi wananchi waJimbo la Chalinze au wananchi wa Halmashauri ya Chalinzewalivyotoa maeneo yao kwa ajili ya kujenga viwanda.Viwanda takriban sita vikubwa vimekwishaanza ujenzi ndaniya Halmashauri yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na viwanda hivyovinavyojengwa, tatizo kubwa sana lililokuwepo ni upatikanajiwa maji. Tulizungumza na hata juzi alipokuja Waziri Mkuukufanya ziara katika Halmashauri yetu, aliona juu ya shidakubwa ambayo wananchi wanavyokabiliana na maji lakinipili alipata taarifa ya kina juu ya viwanda vile ambavyovinaweza vikashindwa kuanza kutokana na matatizo ya maji.Tumezungumza mengi, lakini kubwa zaidi tulimwomba WaziriMkuu kupitia Wizara ya Maji atoe kibali kwa wale wawekezajiwanaojenga kiwanda kikubwa cha tiles pale Pingo iliwaweze kupata access ya kutumia maji ya Ruvu na siyo majiya Wami ili waweze kujenga kiwanda. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

76

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutoa maji Ruvu mpakakwenye kiwanda pale Pingo ni kilometa zisizopungua 16;lakini kutoa maji Wami mpaka Pingo ni kilometa zaidi ya 26.Tunachoangalia hapa ni upatikanaji rahisi wa maji hayo naninashukuru kwamba Waziri Mkuu alinikubalia. Nimeonaniseme hapa leo kwa sababu hii ni mikakati ambayoikiingizwa kwenye bajeti itakaa vizuri. Tunachosubiri kutokakwake ni kusikia neno kwamba kibali kile kimetoka nakwamba ujenzi wa miundombinu hiyo umeanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini siyo hili tu, maji hayayatasaidia pia hata wananchi wa Mji wa Chalinze kwanamna moja au nyingine kwa sababu makubaliano yetu siyotu maji yaende kwenye kiwanda, lakini pia yaende mpakapale Chalinze Mjini ili kupunguza tatizo la maji tunalokabiliananalo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo pia,kiwanda kikubwa kingine kinachojengwa kule Mboga chakuchakata matunda nacho kinahitaji maji. Tumezungumzana Mheshimiwa Waziri Mwijage, tunamshukuru kwa jinsi alivyotayari kukabiliana na changamoto hiyo, lakini piakinachohitajika zaidi ni ule Mradi wa Maji wa Wami ukamilikemapema ili maji yapate kupelekwa pale na wananchi waChalinze wapate kazi, wananchi wa Tanzania wapatematunda kwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi katika kipindihiki cha miaka mitano hii inayoanza mwaka 2015 mpaka2020. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo, nije katikajambo la vita ya dawa ya kulevya. Katika vita ya dawa zakulevya tunashuhudia mamlaka mbili zenye nguvu tofautizikifanya kazi moja. Mimi ni mwanasheria, katika utafiti wanguau ujuzi wangu wa sheria, haiwezekani kazi moja ikafanywana vyombo viwili na ndiyo maana katika mgawanyiko wakazi hizi, mambo yanagawanyika kutokana na mihimili nakutokana na ofisi. Leo hii tunashuhudia, wako watu wanaitwana Bwana Siro lakini pia wako watu wanaoitwa na BwanaSianga. Matokeo yake sasa haieleweki, kumekuwa na doublestandards katika treatment ya watu hawa.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

77

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachokiomba kwa kuwanatambua Sheria ya Dawa za Kulevya inayompa nguvuBwana Sianga ya kuita, kukamata na kufanya inspection,hiyo sheria pia inaingiliwa na Jeshi la Polisi. NaombaMheshimiwa Waziri Mkuu atakaposimama hapa awaelezeni jinsi gani vyombo hivi viwili vinaweza vikatenganishautendaji ili kutoharibu mlolongo mzima wa upelelezi naupatikanaji wa watuhumiwa hawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo pia,Mheshimiwa Waziri Mkuu alikuja kule kwetu na akaendakatika mbuga yetu ya Saadani, ameona jinsi mamboyanavyokwenda na ameona hali ilivyo. Naomba sanaMheshimiwa Waziri Mkuu, wakati anakuja kufanyamajumuisho ya hotuba yake azungumzie vizuri juu ya jinsi ganitunaweza ku-promote utalii katika mbuga yetu ya Saadani,lakini pia azungumzie ni jinsi gani Serikai imeweza kukabilianana vile vilio vya wananchi wanaozunguka mbuga yetu yaSaadani juu ya matatizo ya migogoro ya mipaka iliyopo bainaya mbuga yetu na makazi au vijiji vilivyo jirani hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilio vimekuwa vikubwasana, vimefika kwenye Ofisi ya Mbunge, lakini pia vimefikakwenye Ofisi ya Waziri Mkuu na Waziri Mkuu mwenyeweameshuhudia watu wakigaragara kumzuia asitoke katikambuga ya Saadani kwa sababu ya taabu kubwawanayoipata hasa wenzetu hawa wanaosimamia mbugawanapoamua kuchukua sheria katika mikono yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo pia,niendelee kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa hatuakubwa anazozifanya. Sisi tulikutana naye, niliongea naye nabaada ya kuzungumza naye, siku tatu baadaye akaja WaziriMkuu kuzungumza juu ya kero ambazo zinawakabiliwananchi wa Chalinze. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba yangu na kwaniaba ya wananchi wa Chalinze, namshukuru sanaMheshimiwa Rais kwa jinsi alivyomwepesi kukabiliana nachangamoto. Katika wepesi huo, naomba niishauri Serikali

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

78

yangu, kumekuwa na malalamiko mengi sana. Tumeshuhudiamalalamiko mengine ambayo yanahitaji majawabu kamasiyo majibu ya haraka ili kuondoa hizi sintofahamu walizonazowananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba sana, hakunasababu ya mtu kama Mheshimiwa Waziri Mwigulu kuendeleakukaa kimya wakati wananchi wanalalamika juu ya hali yakiusalama katika maisha yao. Mimi binafsi naishauri Serikaliyangu kwamba unapojibu jambo lolote lile unatoa hali yawasiwasi na wananchi wanapata… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Sasa ni Mheshimiwa DanielNsanzugwako. Mheshimiwa Zitto na Mheshimiwa Riziki SaidLulida wajiandae.

MHE. RIDHIWANI J. KIKWETE: Mheshimiwa Mwenyekitinaunga mkono hoja. (Makofi)

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: MheshimiwaMwenyekiti, na mimi nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Kablasijasema mengi, kwanza niunge mkono hoja hii ambayoimeletwa mbele yetu toka Ofisi ya Waziri Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuwa na machachesana, lakini moja kubwa naomba tu kwa namna ya pekeeniwapongeze wenzetu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri nawatendaji wake, timu nzima ya Serikali, mmefanya kazi nzurisana na hasa hii kazi ya kurejesha nidhamu Serikalini,hongereni sana. Hili ni jambo jema na kila mmoja anaonatofauti iliyokuwepo siku za nyuma na siku za sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado niendelee kuwashauri,kama ilivyo kazi yetu Wabunge ni kuwashauri Serikali,kwamba tunaomba utaratibu huu wa nidhamu ya watumishiwa Serikali ujikite katika kulinda misingi ya sheria. Tafadhalinisana, endelezeni nidhamu ya watumishi wa umma,

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

79

tuwaheshimu watumishi wa umma kwa kuzingatia sheriazilizopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kwa namna ya pekeenaipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kumaliza ligi hii yaWakuu wa Mikoa na Wilaya ya kuwaweka ndani watumishiwa umma hovyo hovyo. Kwa kweli juhudi zimekuwa nzuri,sasa tunaona mashindano haya hayapo tena, maana hukonyuma ilikuwa Mkuu wa Mkoa akijisikia, Mkuu wa Wilayaakijisikia anaweza kumweka ndani ofisa yeyote wa Serikalibila utaratibu. Tunashukuru sana, jambo hili wenzetu waUtumishi, TAMISEMI na Ofisi ya Waziri Mkuu mmelisimamiavizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya pekee,Mheshimiwa Simbachawene najua amefanya vizuri katikajambo hil i, na tunakupongeza sana kwa kazi nzurianayoifanya. Lazima Wakuu wetu wa Wilaya na Mikoawafuate sheria kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalonapenda nilisemee limeainishwa ukurasa wa 31 na 32 wahotuba ya Waziri Mkuu ni ujenzi wa reli ya kati kwa kiwangocha standard gauge. Tunaishukuru sana Serikali kwa jitihadahizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwakumbushe,Mheshimiwa Jenista, reli ya kati tafsiri yake ni reli inayotokaKigoma kwenda Dar es Salaam ikiwa na matawi ya kutokaTabora kwenda Mwanza na matawi kutoka Kaliua kwendaMpanda, ndiyo reli ya kati hiyo. Sasa nimeona kwenye kitabucha Waziri Mkuu, kuna juhudi kubwa zimefanyika katika ujenziwa reli ya kati na hususan kuanza kufanya feasibility studieskatika matawi haya ya reli ya kati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwashaurikwamba ili reli hii iweze kuwa ya kiuchumi, maadamu inaanzakujengwa kwa kiwango cha standard gauge ni vizuri reli hiiikatoka Dar es Salaam ikaenda Kigoma kwa sababu yamzigo mkubwa, tani milioni nne zilizoko katika Jamhuri ya

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

80

Demokrasia ya Kongo ambayo zinahitaji njia kwenda kwenyemasoko ya Kimataifa. Tusipofanya hivyo, tutajikuta mbeleya safari, hii reli haitakuwa na faida za kiuchumi mbali nakusafirisha abiria peke yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonapenda niliseme ni uwiano wa maendeleo katika Mikoayetu. Waheshimiwa Mawaziri mlioko hapa nadhani Waziri waTAMISEMI unanisikia, nchi yetu hii ina mikoa takribani 25.Uwiano wa Mikoa hii umetofautiana katika sekta mbalimbali,ni vyema sasa Serikali yenyewe kama ambavyo mwaka wa2016 mlitupa takwimu za hali ya umaskini katika nchi yetutukawa na utaratibu wa kuiinua mikoa ambayo iko nyuma,mikoa hiyo iko nyuma kwa sababu za kihistoria tu. Mikoakama Kigoma, Dodoma, Singida, Katavi, iko nyuma kwasababu za kihistoria. Ni jukumu la Serikali kuweka uwianosawa wa mikoa hii katika sekta mbalimbali kama elimu, maji,afya, kilimo, barabara na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maeneo mengineyana nafuu kidogo na maeneo mengine yana shida kubwasana na wananchi wote hawa ni Watanzania hawa hawa.Kwa mfano, Mkoa wetu wa Kigoma mpaka leo bado ni mkoahaujaunganishwa na Tabora kikamilifu, haujaunganishwa naKatavi, haujaunganishwa na Geita, haujaunganishwa naKagera, haujaunganishwa na Shinyanga, hali ni mbaya sana.Sasa naomba sana TAMISEMI mko hapa, Ofisi ya Waziri Mkuu,angalieni uwiano ambao una afya katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania hawa wanahaki sawa. Maeneo mengine yana unafuu na mengine yanashida kubwa. Kwa hiyo, naomba kama ushauri Serikalinikwamba ni muhimu sana kuweka uwiano wa maendeleokatika mikoa ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambaloningependa niishauri Serikali ni suala la kilimo. Katika nchiyetu kuna maeneo yanapata mvua, Mwenyezi Munguameyabariki tu, yanapata mvua za kutosha na tunalo tatizokubwa sana hata la kuzalisha mbegu.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

81

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu kwa kweli kwamiaka yote hii, miaka 50 ya uhuru sasa hatuwezei kujitoshelezahata kwa mbegu za mazao ya nafaka. Nilikuwa nafikiri niwakati muafaka wenzetu wa kilimo na Serikali, yale maeneoyanayopata mvua za kutosha kwa mwaka mzima tuyapekipaumbele ili tuweze kuzalisha mbegu za kutosha ilitujitosheleze kwa mbegu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaoneshakwamba mpaka sasa nchi yetu tunazalisha mbegu asilimia40 ya mbegu zilizobaki zinatoka nchi jirani kama Kenya, Zim-babwe na mataifa mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho nizungumzie juuya umeme wa Malagarasi. Niwapongeze wenzetu wa nishatiwamefanya kazi kubwa na taarifa niliyonayo ni kwambawenzetu wa Benki ya Dunia na African Development Bankwametoa fedha kwa ajili ya kuanza kujenga umeme waMalagarasi. Huo umeme ni muhimu sana kwa maendeleoya watu wa Kigoma na ni dhahiri umeme huo utaingizwapia kwenye Gridi ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisanizungumzie suala la maji, maji ni uhai na ni dhahiri kwambamaeneo yenye vyanzo vya maji vingi na mikoa ambayo inavyanzo vya maji vingi tu sasa kwa sababu ya matatizo yatabia ya nchi, uharibifu wa mazingira, naishauri Serikalikwamba wakati umefika maeneo yenye vyanzo vya majituyalinde, kuwe na mkakati wa kitaifa wa kulinda vyanzovya maji. Kwa mfano, katika Mkoa wa Kigoma, katika Wilayaya Kasulu peke yake tuna vyanzo vya maji takribani 600ambavyo havikatiki mwaka mzima. Vyanzo hivi vinapelekamaji yake katika Mto Malagarasi kwa kiwango kikubwa namaji hayo hatimaye yanakwenda kwenye Ziwa Tanganyika.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna huu mpangokabambe wa kupeleka maji Malagarasi, Urambo, Kaliua nakwingineko kama hakuna mkakati endelevu wa Serikali ninahakika tutafika mahali maji ya Mto Malagarasi yatakuwa

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

82

hayatutoshi, hayataweza kuzalisha umeme na kufanyashughuli za kilimo. Kwa hiyo, nashauri strongly kabisa kwambawenzetu wa Serikali hata kama ni mwakani tuleteeni acomprehensive plan ya kulinda vyanzo vya maji. Iko mikoayenye vyanzo vingi, Morogoro wana vyanzo vingi, Kataviwana vyanzo vingi tuwe na mpango mkakati kabisa kitaifawa kulinda vyanzo vya maji katika maeneo ambayo majihayakauki mwaka mzima. Ni kweli yako maeneo yenye shidalakini tukiwa na mkakati endelevu nina hakika maji hayahatimaye yatatusaidia sisi wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, MheshimiwaSimbachawene ulitembelea Kigoma, ulitumwa naMheshimiwa Rais kule Kigoma…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na MheshimiwaZitto na Mheshimiwa Riziki Lulida, Mheshimiwa Koshuma,Mheshimiwa Mgimwa, Mheshimiwa Aeshi Hilaly wajiandae.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangiahotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, kuhusiana na mapitiona mwelekeo wa kazi za Serikali tukifahamu kwamba WaziriMkuu kwa mujibu wa Katiba ndiyo mwenye udhibiti nausimamiaji wa ujumla wa shughuli za Serikali. Nina mambomanne kama nitapata muda wa kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ambalonataka kulizungumzia ni hali ya uchumi. Kwa mujibu wa taarifaya Waziri Mkuu anaonesha kwamba hali ya uchumi ni nzuri,mfumuko wa bei uko chini asilimia 5.2 lakini jana tu NBSwametoa taarifa mpya ya mfumuko wa bei ambaoumepanda kwa kasi sana. Sasa hivi hali ya wananchi kwakweli ni ya kupoteza matumaini, bei za vyakula zimepanda,sukari imefika mpaka shilingi 2,500 kwa kilo, maharageyamefika mpaka shilingi 3,000 kwa kilo, unga kuna maeneoya nchi umefika mpaka shilingi 2,200 kwa kilo. Kwa hiyo, kuna

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

83

haja ya kuweza kuangalia taarifa ambazo Wizara zinapelekaOfisi ya Waziri Mkuu kwa sababu inaonesha kwamba taarifaambazo Waziri Mkuu amezitoa katika ibara ya 20 ya hotubayake ni outdated, siyo taarifa za sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, Waziri Mkuu katika ibaraya 26 ya hotuba yake ameongelea ajira na kusema kwambatumeingiza ajira mpya 418,000 lakini naomba ifahamikekwamba kwa mwaka Tanzania watu wanaoingia kwenyesoko la ajira ni milioni 1.6. Kwa hiyo, kuingiza watu 418,000maana yake ni kwamba kuna zaidi ya watu milioni 1.2ambao hawajapata ajira na wako nje ya shughuli za kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hata hivyo kuna ajirazimepotea. Ndani ya Manispaa yako Mwenyekiti, Manispaaya Ilala jumla ya biashara 2,900 zimefungwa. Maana yake nikwamba leo Ilala hamuwezi kupata service levy, leo Ilalahamuwezi kupata leseni za biashara, kwa sababu biasharazimefungwa kulingana na sera za Serikali ambazo siyo rafikikwa watu kuweza kufanya biashara inavyotakiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia matamko kwa mfanoya viongozi yanasababisha upotevu mkubwa wa mapato.Mimi nafahamu na natambua juhudi ambazo Raisanazifanya, anataka tukusanye mapato zaidi kwenye madini,lakini Rais hafahamu na wasaidizi wa Rais pia hawafahamukwamba tamko lake alilolitoa Mkuranga kuhusiana namchanga limepoteza mapato ya Serikali kuliko mapatoyoyote ambayo tungeweza kuyakusanya kwa miaka 20iliyopita na nitawapa takwimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya mwaka 1998tulipoanza uchimbaji mkubwa wa dhahabu mpaka mwaka2016 tumeuza nje dhahabu ya Dola za Kimarekani bilioni 18na makusanyo yetu kwa miaka yote hiyo ya kodi ni dola zaKimarekani milioni 833. Tamko alilotoa Rais Mkuranga, kwasababu kulikuwa na mazungumzo ya kuuza Kampuni yaAcacia ambayo ingeingiza mapato mengi sana Serikalinikupitia capital gain tax ambapo tulipitisha sheria hapa,

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

84

tumepoteza Dola za Kimarekani milioni mia nane themaninina nane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Rais anazungumzakukusanya mapato, Rais huyu huyu anaipotezea nchimapato. Haya ni mambo ambayo tunapaswa tuwe makininayo sana na ningeomba viongozi hasa Mawaziri wajaribukumshauri. Tunajua ana dhamira njema, lakini tuifanye kwanamna ambayo haiathiri maslahi ya Taifa kama ambavyoimefanyika sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo asubuhi hapa kulikuwakuna mwongozo ambao umeombwa na Chief Whip waSerikali ametoa maelekezo ambayo wewe umeyakubali.Maelekezo ambayo Chief Whip ameyatoa na weweumeyakubali hayaendani na Kanuni za Bunge. Suala laMtanzania aliyepotea Ben Sanane, ni suala ambalolinapaswa kuchukuliwa kwa uzito wa hali ya juu sana, sio sualalinalopaswa kuchukuliwa kisiasa. Sio suala linalopasaWabunge wabebe uthibitisho waulete mezani kwako kwasababu taarifa ambazo ziko sasa hivi na zipo Jeshi la Polisizinaonesha kwamba Novemba 15, Ben Sanane kwenyemawasiliano yake ya simu kuanzia asubuhi alikuwa maeneoya Tabata, akaenda maeneo ya Mikocheni, akatumia mudamwingi sana maeneo ya Mwenge, akapelekwa au akaendaMburahati, saa nne usiku tarehe 15 Novemba, simu yakeikapoteza mawasiliano na toka hapo hajawahi kuwa tracedtena na haya maelezo yako polisi. Ukifuatilia Jeshi la Polisiwanakwambia sisi tumefikia mwisho, lakini mwelekeo wetuunaonesha kwamba waliomchukua Ben Sanane ni Usalamawa Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ume-save kwenyeKamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama na Mambo ya Nje,unafahamu sheria ya Usalama wa Taifa, kifungu cha 5(2)kinaipiga marufuku Usalama wa Taifa ku-enforce laws.Usalama wa Taifa hawana mamlaka ya kukamata, hatawakimwona mwizi hivi, sheria inawakataza, kwa sababu yakuepuka haya mambo ambayo tunayo. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

85

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kumekuwa namatukio hatuyapatii ufumbuzi. Ninyi mnafahamu namnakumbuka aliyekuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri,Absalom Kibanda, alikamatwa, akateswa, akaumizwa naleo jicho lake moja, halioni lakini mpaka leo hakuna hatamtu mmoja aliyekamatwa kulingana na tukio kama hilo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa katika mazingira kamahaya, hatuna namna na siyo kawaida ya Bunge hili ninyiwenyewe ni mashahidi ambao mmekaa Bungeni muda mrefukujadili Usalama wa Taifa. Kwa mara ya kwanza tunaivukahiyo taboo kwa sababu watu wamechoka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa mujibu waKanuni ya 120 ya Bunge, natoa taarifa rasmi kwamba nitaletaHoja Binafsi ndani ya Bunge ili Bunge liunde Kamati Teule yakufanya uchunguzi wa matukio yote ya upoteaji, mauaji namatukio ambayo yanaweza kujenga taswira hasi dhidi yaIdara ya Usalama wa Taifa katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizikumbusheKamati za Bunge, kuna masuala ambayo Kamati za Bungehazipaswi kupelekewa na Spika, zinapaswa kufanyazenyewe, ndiyo maana Bunge lina utaratibu wa taarifamaalum.

Mimi ningetarajia Kamati ya Bunge ya Ulinzi naUsalama ingetuletea taarifa maalum kuhusu mambo hayabadala ya kusubiri mpaka Wabunge wazungumze, tuanzekujianika na kama nilivyoeleza it was a taboo kuongeleaUsalama wa Taifa ndani ya Bunge lakini leo tunaongelea kwasababu ya utendaji mbovu ambao unaendelea.

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Kuhusu Utaratibu.

MWENYEKITI: Kuhusu Utaratibu.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

86

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafahamukwamba Mheshimiwa Zitto anafahamu Kanuni vizuri sanalakini nafahamu kwamba ni mtu mwenye uwezo mkubwawa kusoma vitu vingi na anafahamu kwamba hili analolijadilihaliruhusiwi kujadiliwa humu, anazungumzia suala la Usalamawa Taifa ambalo hawezi kulijadili humu. Pia Mheshimiwa Zittoanautuhumu Usalama wa Taifa kwamba umeshiriki kukamatawatu, je, anaweza akalithibitishia Bunge hili? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Zittoanafahamu kwamba ni makosa kufanya hivyo, it is a taboolakini anasema imebidi tuvuke mipaka na sasa anauingizaUsalama wa Taifa katika kuutuhumu kwa jambo ambalo sinahakika kama anao ushahidi wa kutosha. Kwa hiyo, miminimuombe tu kwa ruhusa ya Kiti chako Mheshimiwa Zitto aleteushahidi wa kulithibitishia Bunge hili kwamba Usalama waTaifa ndio waliomshikilia Ben Sanane.

TAARIFA

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bashe.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimpe taarifa Waziri, Mheshimiwa Simbachawenekwamba mimi Hussein Mohamed Bashe nilikamatwa naMaafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, acheni unafiki, weare all Tanzanians in this country. Hamjawahi kunyanyaswaninyi, acheni.

Mimi ni mwana CCM, I don’t care mkitaka nifukuzeniUbunge. Mimi nimekamatwa na Usalama, nimeonewa in thiscountry, acheni unafiki, tunavumilia mambo mengi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Bashe,umeshaeleweka.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

87

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Acheni, hamjawahi kuwahumiliated.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bashe, umeshaeleweka,ahsante.

(Hapa Mhe. Hussein M. Bashe aliendelea kuongea bilakipaza sauti)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bashe umeshaeleweka,ahsante. Mheshimiwa Zitto. (Makofi)

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Zitto, hebu kaa kidogomuda wako tutakupa. Kufuatana na mjadala wako nakuanza kuzungumzia habari ya Kiti, Kiti kilishachukua maamuziya kulichukua jambo hili na kulipeleka mbele likajadiliwe kwakina kabisa ndani ya Bunge lenyewe kwenye uongozi huko.Sasa sijui unalalamika kitu gani, ulitaka hapa watu muanzekuimbaimba tu bila kuwa na jambo lolote? Haya endelea.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, miminimetoa taarifa kwa mujibu wa Kanuni ya 120 ya kuundaKamati Teule na ndiyo taarifa ambayo inapaswa kufanyiwakazi kwa mujibu wa Kanuni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nataka nimkumbusheMheshimiwa George anafahamu, ni rafiki yangu, ni nduguyangu yaani ndugu kabisa, waliokwenda kuvamia CloudsMedia ni Kikosi cha Ulinzi wa Rais na ninaweza kuthibitisha,aliyemtolea bastola Mbunge wa Mtama ni Afisa Usalama waTaifa na ninaweza kuthibitisha. Kwa hiyo, kama Bungelinaweza likaunda chombo cha kutaka nikathibitishe hayo,niko tayari kuthibitisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie,Mheshimiwa Waziri Mkuu ibara ya 31 ya hotuba yakoimezungumzia kilimo na umezungumzia mavuno ambayotumeyapata msimu uliopita wa 2014/2015. Naomba

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

88

nikukumbushe Mheshimiwa Waziri Mkuu kwamba, taarifa yaBenki Kuu ya Quarterly Economic Review inaonesha kwambakilimo kimekua kwa asilimia 0.3 tu. Kwa hiyo, maana yake nikwamba, wananchi wetu vij i j ini mwaka 2016, wengiwamekuwa maskini kwa sababu ya ukuaji mdogo katikasekta ya kilimo.

Mheshimiwa Mweyekiti, lakini Mheshimiwa Waziri Mkuuamezungumzia mbolea ambayo Serikali imenunua tani30,000. Ni kazi nzuri sana mbolea imenunuliwa lakini naombanikufahamishe katika kila mfuko wa mbolea ambaoumenunuliwa kwa shilingi bilioni 10 Serikali ilizotoa, watu wakoama ni watendaji wa Wizara ya Kilimo au TFC wameongezashilingi 15,000 kinyemela. Mnunuzi wa kawaida akinunuambolea Dar es Salaam ananunua kwa shilingi 55,000 mpakaifike kwa mfano Rukwa, Kigoma au Katavi mbolea ileinauzwa kwa shilingi 60,000. Leo hii mbolea ambayoimenunuliwa kwa fedha za Serikali, kwa kampuni ya Serikaliikifika Sumbawanga, Mpanda, Kigoma ni shilingi 75,000.Nakuomba Mheshimiwa Waziri Mkuu, jana nimekuonaumechukua uamuzi katika mambo kama haya ya pembejeo,nakuomba umwagize CAG akague…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Zitto, nakuongezea dakikambili.

WABUNGE FULANI: Anakuongezea dakika mbili.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana. Nimeweka pia kwa maandishi nitayaleta iliiweze kufanyiwa kazi kwa uzuri zaidi. Naomba Ofisi yakoimwagize CAG akague manunuzi ya mbolea ya shilingi bilioni10 yaliyofanywa na kusambazwa katika msimu huu na taarifahiyo uweze kuifanyia kazi, kwa sababu kuna shilingi 15,000zimeongezwa kwenye mbolea zote zilizonunuliwa ile ya DAPna ile nyingine ya kukuzia. Kwa hiyo, naomba jambo hilouweze kuliangalia.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

89

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa MheshimiwaWaziri Mkuu ibara ya 17 ameongea maneno mazuri sanakwamba tufanye siasa na naomba nimnukuu, ni manenomazuri sana, anasema; “Ninatoa rai kwa wadau wa siasakote nchini kujenga utamaduni wa masikil izano nakuendesha siasa za maendeleo badala ya siasa zamalumbano; siasa za kuunganisha watu wetu badala yakuwagawa; na siasa za uwajibikaji badala ya siasa zamazoea.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Mheshimiwa WaziriMkuu mmetufungia kufanya siasa. Tunafanyaje siasa zakuwaunganisha watu wakati hatufanyi mikutano yahadhara? Tunafanyaje siasa za maendeleo wakati hatufanyimikutano ya hadhara? Tunafanyaje siasa za uwajibikaji wakatihatufanyi mikutano ya hadhara na mnafahamu kabisakwamba ni kinyume cha Katiba. Namwomba MheshimiwaWaziri Mkuu kama Waziri ambaye unahusika na suala lavyama vya siasa umshauri Rais. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Riziki Said Lulidaajiandae Mheshimiwa Koshuma, Mheshimiwa Mgimwa naMheshimiwa Aeshi.

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikushukuru sana na nimshukuru Mwenyezi Mungu kunijaliaafya njema na kuwepo katika kuchangia hii hoja ya WaziriMkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitoe pole kwafamilia ya Mheshimiwa Dkt. Macha ambaye MwenyeziMungu amempenda zaidi. Kwa muda mfupi niliokaa naMheshimiwa Dkt. Macha nimejifunza vitu vingi sana na nikikaana Waheshimiwa Wabunge wenzangu huwa nawaambiaMama Macha alikuwa na kipaji maalum kwa walemavuhasa. Hivyo Mwenyezi Mungu amrehemu amuweke katikanjia iliyokuwa sahihi na ampe pepo.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

90

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,napenda nitoe pongezi za dhati kwa Waziri Mkuu, WaziriMkuu ni mtu mnyenyekevu, huruma, na mwenye upole.Nataka nimpe usia mmoja kama ndugu yangu, tulichukuaQurani na Biblia tukasema tutatenda haki kwa Watanzania.Nina imani kwa unyenyekevu na upole wake atawatendeahaki Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania sasa hivitunasimama kutaka kutatua migogoro ya Burundi, tunaiachaZanzibar iko katika mgogoro, Zanzibar ni mwiba. Mwiba ulekwa unyenyekevu kabisa, nakuomba Waziri Mkuu uliapakutenda haki na kuwatetea Watanzania, basi lile unalolionawewe litakuwa haki ulisimamie kwa vile Qurani hii itakujakutuadhibu siku moja. Qurani na Biblia zetu hizi zitakujakutuadhibu siku moja tutende haki kwa waislam, wakristona wote wanaopenda haki katika Tanzania hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hilo,nataka nimshukuru tena Waziri Mkuu, nilitoa hoja yakumuomba Waziri Mkuu ashughulikie suala la koroshokuhusiana na tozo. Napenda kumshukuru Mheshimiwa WaziriMkuu nikiwakilisha wananchi wa Mtwara, Lindi na walimakorosho wote kwamba ameweza kulitatua tatizo lile kwaasilimia kubwa sana, sasa hivi tuko katika neema. Neema hiitunaomba iende katika mazao ya tumbaku, pamba nakahawa. Naamini Mheshimiwa Waziri Mkuu una uwezomkubwa, ahsante sana na Mwenyezi Mungu atakujalia.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi natoka katika Mkoawa Lindi. Mkoa wa Lindi ni wa mwisho katika maendeleolakini ni wa kwanza kwa kuwa na resource nzuri, lakini badokeki ya kugawiwa Lindi inapelekwa ndogo sana. Natakaniongelee tatizo la maji Lindi na ni karibu miaka 10tunazungumzia, leo Manispaa ya Lindi imetumia shilingi bilioni51 lakini hakuna maji. Hata hivyo, nataka nitoe sababu yamsingi inayosababisha miradi ya maji kufeli. Tunawapawakandarasi kutoka India na hela zinapelekwa shilingi bilioni51, mkopo wa Watanzania, mkopo wa walipa kodi, kwa

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

91

nini zipelekwe India? Tunaagalia mradi wa maji wa Chalinze,shilingi bilioni 51 hela zote kunapelekwa katika Benki ya Indiasio Bank of Tanzania. Tujiulize, maji hakuna tayari mabilioniyanakwenda India, kwa faida ya nani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu anameno na macho ya kuangalia, nashauri akaangalie hili sualala maji Tanzania nzima. Kila ukija humu ndani watuwanalalamikia maji lakini mabilioni ya pesa ya majiyamepotea kwa ajili ya wazembe wachache ambaowamefanya wanawake wanatoboka utosi kwa ajili yakutafuta maji kisa wao wananufaika na kuzichukua zile pesakuzipeleka India. Inakuwaje mkopo wa World Bankunachukua pesa za Mtanzania, zinawekwa Benki ya Indiana sisi wenyewe tumenyamaza? Cha kushangaza miradi hiiyote wamepewa Wahindi, kuna syndicate hapa. NaombaMheshimiwa Waziri Mkuu kabla hujamaliza kuhitimishauandae Tume ujiulize ni akaunti ngapi za maji zimepelekwanje? Akaunti ngapi za ujenzi wa barabara zimepelekwa njena kwa faida ya nani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa maji wa Lindimpaka leo haujafika hata shilingi bilioni mbili lakini tayarishilingi bilioni 51, nilikuwa Mjumbe wa Bodi ya Maji, alipewaMS Jandu shilingi bilioni 13.7 maji hayakupatikana Lindi.Akapewa tena shilingi bilioni 16 maji hayakupatikana Lindi.Amepewa shilingi bilioni 29 maji Lindi hamna. Je, hizi hela zawalipa kodi tunazifanya nini? Ni madeni ambayo yangewezakuzuilika lakini haiwezekani kutokana na watu wachachewanaifanya hii nchi isitawalike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze MheshimiwaWaziri Mkuu kwa kazi kubwa anayoifanya ya kusimamiauhifadhi wa wanyamapori. Mimi ni mdau wa wanyamapori,ni Mwenyekiti wa Kupambana na Ujangili. Kwa idhini yako,nataka nimuombe ahakikishe mpaka wa Gorogonja ambaounaunganisha Serengeti na Masai Mara usifunguliwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri WaheshimiwaWabunge wengi hawaelewi ni wapya, nashauri wapewe

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

92

semina wajue kwa nini mpaka wa Gorogonja usifunguliwe.Mtalii akija Tanzania atarudi kwenda kulala Kenya, uchumiwote utapelekwa Kenya. Ni lazima tuhakikishe kuwatunajitambua kuwa ule mpaka ni sumu kwa Watanzania.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa na mzigo mudamrefu nataka niutue, lakini leo nataka nimtulie Waziri Mkuumzigo huu. Mjusi ameanza na Mheshimiwa Mudhihirakashindwa mahali pa kuupeleka yule mjusi. AkajaMheshimiwa Mama Mikidadi na Mheshimiwa Riziki, dinosaurambaye yuko Ujerumani nimeshindwa kulitua. Hapa simtuliiMnyamwezi wala Mndengereko mzigo huu namtulia WaziriMkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapato yanayopatikana nadinosaur yule ni makubwa sio ya kubeza ndani ya Bunge hili.Leo watu wa Lindi hatuna mirahaba ya TANAPA, hatupatitozo yoyote ya Ngorongoro lakini tungepata pato la mjusi,shule za Mipingo, Matakwa, Namapwia, tungepatabarabara, tunajiuliza kigugumizi kiko wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nasema tena,sitamuuliza swali hili Mheshimiwa Maghembe, nitauliza Ofisiya Waziri Mkuu mpaka Mwenyezi Mungu aniondoe katikaBunge hili, suala la mjusi limefikia wapi? Naomba suala la mjusihuyu ulipokee wewe na unijibu wewe siyo mtu mwingine tena.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja tena katika masualaya uwiano wa maendeleo katika Mikoa ya Kusini, Lindi naMtwara. Mradi ambao ni mwiba katika Mkoa wa Lindi nihuu Mradi wa TASAF. Bahati nzuri nilimpelekea documentkuonesha shule zilizojengwa Lindi ziko chini ya viwango,hospitali zilizojengwa Lindi ziko chini ya viwango, vyoovilivyojengwa Lindi viko chini ya viwango, maji yaliyopelekwaLindi hayapatikani, yote ilikuwa ni miradi ya TASAF, lakininataka nitoe sababu na yeye kwa vile yuko humu ndaniakalisimamie, tuko pamoja kwa ajili hiyo.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

93

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna baadhi ya viongoziwamekuwa miungu watu ndani ya Wilaya zetu, hawawanaitwa Makatibu na Wenyeviti. Wale wanawatishaMadiwani wasifanye kazi zao, wasikague miradi, matokeoyake nafikiri umeona. Choo cha TASAF kimejengwa kwakaribu shilingi milioni 100 hakuna choo. Darasa limejengwalimeshaanguka. Je, tutaendelea na TASAF III wakati TASAFI…

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Kuhusu Utaratibu.

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Haya, ahsante.

MWENYEKITI: Kuhusu Utaratibu, Mheshimiwa Waitara.

KUHUSU UTARATIBU

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ulitolewa mwongozo hapa juzi na Kiti kikaamua kwambatunapochangia hapa tunam-address Waziri Mkuu na hii nihotuba yake. Katibu wa CCM, Mheshimiwa Ulega amehamakwake karibu saa nzima yupo pale, Mheshimiwa Mama Rizikianalazimisha Waziri Mkuu amsikilize lakini hasikilizi anampigishastory.

MWENYEKITI: Mbona mimi sioni mtu hapa?

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,tunaomba Waziri Mkuu asikilize ili aweze kujibu hoja. Ni hilotu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara, mimi sioni mtuhapa.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MWENYEKITI: Kiti hakijaona mtu. Endelea MheshimiwaLulida.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

94

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MWENYEKITI: Kaa chini wewe.

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba uniongezee muda wangu.

Mheshimiwa Waziri Mkuu mjusi namhamisha kutokakwa Mheshimiwa Riziki, Mheshimiwa Bobali, nakukabidhitupate mapato na tozo liende Namapwiya, Mipingo naNangaro. Wakati Mheshimiwa Rais anakuja Nangaro alisemaatatuletea mapato katika maeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema nashukuru nanawapenda Watanzania wote, Mungu ibariki Tanzania naMungu mbariki Waziri Mkuu. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na MheshimiwaKoshuma. Wajiandae Mheshimiwa Mahmoud Mgimwa,Mheshimiwa Aeshi Hilaly na Mheshimiwa Cosato Chumi.

MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Pia naombanimshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ambayeameweza kunijalia afya njema ili niweze kuendelea kutoamichango yangu katika Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwanza nianzekuongelea suala zima la uwezeshaji wananchi kiuchumi.Katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ukurasa wa 15ameongelea suala la uwezeshaji wanawake kiuchumi naukisoma pale ndani ameandika kuhusiana na maendeleoya wanawake kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Wanawakewa mwaka 2007 ambao unalenga kuwawezesha wanawakekiuchumi ili waweze kukopesheka. Lakini kwenye bajeti yamwaka 2016/2017 Mfuko huu wa Maendeleo ya Wanawakehaukutengewa fedha zozote. Naomba niiombe Serikaliitusaidie kutenga fedha kwa ajili ya kuuwezesha huu Mfukowa Maendeleo ya Wanawake ili wanawake wawezekukopesheka. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

95

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nilikuwa nina kikao nawanawake wa Mkoa wa Mwanza, kwa kweli swali zitoambalo nilikumbana nalo ni huu Mfuko wa Maendeleo yaWanawake. Wanauliza Mfuko huu wa Maendeleo yaWanawake unawasaidiaje wanawake il i wawezekujishughulisha na masuala mazima ya uchumi? Ukiangaliawanawake wengi wa Mkoa wa Mwanza wanajishughulishana shughuli mbalimbali kama vile mama lishe hatawamachinga pia wapo ambao ni wanawake lakini kamaMfuko huu wa Wanawake usipotengewa fedha, ni jinsi ganiwanawake wataweza kujikwamua kiuchumi? Hivyo, naombasana katika bajeti ya Waziri Mkuu basi suala hili la wanawakeliweze kuangaliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia katika mataifamakubwa duniani na hata yale ya nchi jirani kama vileZimbabwe, Malawi na Msumbiji na nchi nyingine hata Kenyatu hapo jirani, wamekuwa wakiliangalia suala zima lawanawake katika kutenga bajeti. Ukiangalia hapa Tanzaniakatika bajeti zote ambazo zimekuwa zikitengwa suala lamwanamke limekuwa liki-lag behind. Unakuta mwanamkeanatajwa katika maeneo machache sana. Sisi wanawaketumeamua sasa kuiambia Serikali, lakini kuiomba kwaunyenyekevu mkubwa sana kwamba sasa ianze kuangaliasuala zima linalowahusu wanawake. Kwa sababu wanawakendiyo ambao wanachangia katika pato la Taifa na hivyobasi naomba wasiachwe nyuma. Hivyo basi, naendelea kuisihiSerikali yangu kuuangalia mfuko huu na kuweza kutengafedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia Wizara hii ya Afyainayoshughulika na wanawake, huyu mama ambaye ndiyoameshikilia hii Wizara, dada yangu Mheshimiwa UmmyMwalimu, tunapomuweka kuwa yeye ndiyo mshika dhamanaya wanawake hapa Tanzania halafu mfuko ulehaujatengewa fedha, ina maana tunamdhoofisha huyu dadakatika kuisimamia hii Wizara ya wanawake. Kwa hiyo,naendelea kusisitiza na kuiomba Serikali, kwa mwaka huuwa fedha iweze kutoa fedha na kuweka kwenye mfuko uleili kuweza kuwasaidia wanawake kwenye VICOBA ambavyo

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

96

wamevianzisha waweze kujikopesha na kuweza kujikwamuakiuchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa niongeleesuala la afya. Katika hotuba ya Waziri Mkuu ukiangaliaameongelea suala zima la afya na amesisitiza kwa kusemakwamba Serikali inaendelea kujenga vituo vya afya ilikuhakikisha wanawake nchini wanapata huduma za kiafyavizuri. Ukiangalia katika afya kuna pillars tatu, yaani zahanati,vituo vya afya pamoja na hospitali za Wilaya. Kule ndikoambako zile basic needs za afya zinaanzia. Katika Mkoa waMwanza tunavyo vituo vya afya vya Serikali 46 tu ukiunganishana vituo vingine vya binafsi jumla ni vituo 388.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hivi vituo 46 va Serikalini vituo vinne tu katika mkoa wa Mwanza ndivyo ambavyovinatoa huduma ya upasuaji. Wanawake wengi wamekuwawakipoteza maisha wakati wa kuleta watoto hapa duniani.Ukiangalia idadi ya vifo vya akina mama Mkoa wa Mwanzani 21% na hiyo inatokana na kukosa huduma za upasuajikatika vituo vyetu vya afya. Hivyo basi, naiomba Serikali iwezekutusaidia katika Mkoa wa Mwanza kuwezesha kutupa vituovya afya ambavyo vinaweza vikatoa huduma za afya iliviweze kuongezeka kutoka vituo vinne tufikie hata vituo 15kwa kuanzia ili wanawake wasiweze kuendelea kupotezamaisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia katikaSustainable Development Goals, goal mojawapo nikuhakikisha huduma za mama na mtoto na za wajawazitozinapatikana kwa urahisi na kuendelea kuondoa vile vifo vyamama na mtoto. Kwa hiyo, kama tumeingia mkataba huuwa kwenye Sustaibale Development Goals, naiomba Serikaliiweze kutusaidia katika Mkoa wa Mwanza kutuboreshea vituovyetu vya afya ili viweze kutoa huduma ya upasuaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utakumbuka siku moja hapanilipokuwa nikiuliza swali langu la nyongeza niliuliza suala lawanawake wanavyopata huduma za upasuaji lakinihawapati huduma za upasuaji kwa kupangiwa. Nilipokuwa

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

97

naongea kile kitu nafahamu kwa sababu mama anapopataujauzito kuna matatizo ambayo huwa yanaonekana kwenyescan kabla hata muda wake wa kujifungua haujafika. Kwahiyo, kama tatizo limeshaonekana na kwenye kituo cha afyakuna huduma ya upasuaji, mama huyu anatakiwa apangiweni lini na siku gani atakayofanyiwa upasuaji ili kuweza kuokoamaisha yake yeye kama mama lakini pia na maisha ya mtotoyule ambaye anamleta duniani. Kina mama wengi sanawamekuwa wakipoteza maisha yao lakini mtoto anabaki kwasababu ya kutoa damu nyingi na matatizo menginembalimbali ambayo yanawakumba akina mama wakati wakujifungua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia katika hotuba yaWaziri Mkuu wameeleza ni namna gani bajeti ya vifaa tibapamoja na dawa imeongezeka kutoka shilingi bilioni 31 hadishilingi bilioni 251. Katika kuongezeka kule sisi Mkoa waMwanza naiomba tu Serikali katika bajeti hii ya mwaka huuiweze kutusaidia CT Scan, Mkoa wa Mwanza hatuna CT Scan.Ukiangalia CT Scan inasaidia katika mambo mengi sana si tuwanawake. Kuna watoto wanazaliwa kule na vichwavikubwa Mkoa wa Mwanza lakini na Kanda ya Ziwa kwaujumla…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na MheshimiwaMahmoud Mgimwa, ajiandae Mheshimiwa Aeshi.

MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Naunga mkono hoja. (Makofi)

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisanaunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hiikumpongeza sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri yaMuungano, Dkt. John Pombe Magufuli, lakini kwa namna ya

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

98

kipekee, naomba nimshukuru sana na kumpongezaMheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba yake. Pia niwapongezendugu yangu Waziri, Mheshimiwa Jenista Mhagama na Naibuwake kwa kazi nzuri wanayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangunitauelekeza katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza kuwawezeshawananchi kiuchumi. Katika kampeni yetu ya uchaguzi yamwaka 2015, Ilani ya Chama cha Mapinduzi tuliahidikupeleka shilingi milioni 50 kwenye kila kijiji na kwenye kilaSerikali ya Mtaa. Huu ni mwaka wa pili sasa toka tulipotoaahadi ile. Ni vyema tukatekeleza ile ahadi. Tumebakia namwaka mmoja tu wa kufanya kazi, mwaka 2018, 2019tutaenda kwenye uchaguzi, tusipotimiza ahadi ambazotumeziahidi wenyewe itakuwa vigumu sana mwaka 2019kuomba kura hasa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri Mkuu nakuomba, kupitiakwenye Serikali yetu ya Chama chetu cha Mapinduzitutekeleze ahadi hii muhimu kwa sababu wananchiwaliokuwa wengi kule vijijini na kule kwenye Serikali zetu zamtaa walikuwa wanategemea wapate shilingi milioni 50 hizikusudi ziweze kuwatoa kwenye stage moja kwenda kwenyestage nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili ambalo natakakuchangia ni suala la kilimo. Watanzania kati ya 67% mpaka70% wameajiriwa katika eneo hili. Tumekusudia kwendakwenye uchumi wa viwanda, lakini hawa wananchi ambaowameajiriwa kwenye eneo hili hatuwapi facilities za kutosha.Ukiangalia pembejeo sasa hivi ni ghali sana kuliko siku zanyuma. Kwa hiyo, ule uchumi wa viwanda ambaotumekusudia kwenda utakuwa mgumu sana kwa sababumalighafi ambazo tumekusudia kuzipata hatutazipata kwasababu wakulima hawa watakuwa hawana uwezo wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namuomba sanaMheshimiwa Waziri Mkuu aliangalie sana hili eneo la

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

99

pembejeo hasa mbolea kwa wakulima wetu zisiendeleekupanda bei. Mheshimiwa Waziri Mwigulu kipindi kilichopitaalituahidi kwamba mbolea itauzwa bei rahisi, itauzwa kamasoda, lakini haya yaliyokuwa tumeahidiwa hayafanyiki nahatuyaoni. Kwa hiyo, tunaiomba Serikali iliangalie sana eneohili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo hili hili la kilimoMheshimiwa Waziri Mkuu kuna hawa wenzetu mawakala wapembejeo ambao wanaidai Serikali takribani shilingi bilioni68. Huu ni mwaka wa nne wanadai hela zao na hawajalipwampaka leo. Kuna baadhi ya watu wameshaanza kuuziwanyumba zao na wengine wanakufa. Kwa hiyo, tunamuombasana Mheshimiwa Waziri Mkuu atengeneze utaratibu wakuhakikisha hawa watu wanaodaiwa hela zao katikamaeneo haya wanalipwa baada ya kuwa wamehakikiwavizuri. Kuendelea kuwaacha na madeni, watakufa na halizao zitaendelea kuwa mbaya. Serikali yetu ni sikivu, ninauhakika hawa watu watalipwa hela zao harakaiwezekanavyo baada ya uhakiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo natakakuchangia ni suala la maji. Maji ni tatizo kubwa na kulekwenye jimbo langu kuna tatizo kubwa sana la maji. Chakusikitisha ni kwamba tatizo hili l imekuwa kubwa nalinaendelea kuwa kubwa siku baada ya siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi kubwa ya Bunge nikuishauri na kuisimamia Serikali. Mwaka jana katika mambomengi ambayo sisi Wabunge tuliishauri Serikali kwenye bajetiiliyopita hayakutekelezwa likiwepo la kuongeza tozo yakutoka shilingi 50 kwenda shilingi 100. Tulikuwa na uhakikakama tungeweza kuongeza tozo kwenye eneo hili Mfuko waMaji ungeendelea kuwa mkubwa na hatimaye watu wengiwangepata huduma ya maji katika maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sanakupitia Waziri Mkuu, muwe mnatusikiliza na sisi Wabunge.Hakuna Mbunge ambaye anataka kero ya maji iwepo katikamaeneo yake. Kwa hiyo, tunaomba sana Waziri Mkuu kwenye

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

100

jambo hili atusikilize na sisi Wabunge. Sisi Wabunge wenyewetumekubali kwamba ile shilingi 50 iende kwenye shilingi 100na tutatolea majibu kwa wananchi kwa nini tumeamuakuongeza tozo katika eneo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nilitakakuchangia katika sehemu ya maji ni kwamba katika Jimbolangu la Mufindi Kaskazini kuna vyanzo vikubwa viwili vya maji.Katika Tarafa ya Sadani kuna vyanzo vya maji vya Mto Kihata.Hili eneo linahitaji shilingi bilioni mbili tu ili eneo hili liwezekusaidia kutoa maji katika vijiji 19. Tumeshaleta maombi marakwa mara katika Wizara ya Maji lakini mpaka leohalijashughulikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini eneo lingine la pili niTarafa ya Ifwagi. Tuna taasisi ya RDO ya watu binafsiimetusaidia kutoa maji kwa kata takribani tano na wanalishavijiji takribani 30. Serikali haijatia mkono wake wowote katikaeneo hili. Ni wakati umefika sasa kwa Serikali yetu kutia mkono.Kwa masikitiko makubwa kwenye eneo hili inafika wakatihawa wanatozwa VAT, kwa hiyo, badala ya kuwapa moyowanakosa moyo wa kushughulikia eneo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo natakakulizungumzia ni barabara. Tuna barabara kubwa mbili katikaJimbo langu la Mufindi Kaskazini ambazo nataka mziangaliekwa macho mawili. Barabara moja ni kutoka Kinambo A –Isalavanu – Saadani - Madibila - Lujewa. Mwaka 2010 na 2015barabara hii iliingia kwenye Ilani ya uchaguzi, kwa maanaya vipindi vyote vitano imeingia kwenye Ilani ya Uchaguzilakini hata kilometa moja haijawahi kutengenezwa. Kwa hiyo,tunakosa majibu ya kuwajibu wananchi kwenye maeneoyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamuomba sana WaziriMkuu kwenye jambo hili aliangalie. Nakuomba Waziri Mkuuufanye ziara katika Wilaya ya Mufindi kwa sababu hakunakiongozi yeyote wa kitaifa ambaye amekuja katika Wilayaya Mufindi kujionea hali halisi. Nataka nikuambie miongonimwa maeneo ambayo tunapata kura nyingi CCM ni Wilaya

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

101

ya Mufindi. Wananchi wa Wilaya ya Mufindi wasije wakakatatamaa kwa sababu yale mambo ambayo tumeyaahidihayafanyiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine tulilokuwatunaomba mtusaidie ni barabara ya kutoka Johns Corner -Mgololo na barabara ya kutoka Mchili – Ifwagi – Mdabulo –Ihanu - Tazara - Mlimba. Barabara hii inaunganisha Wilayambili na mikoa miwili. Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi hainauwezo wa kuitengeneza barabara hii.

Kwa hiyo, tunaomba sana ipandishwe hadhi natumejitahidi kadri ya uwezo wetu kupeleka barua kupitiakwenye Road Board ya Mkoa, lakini kwa bahati mbayampaka leo Waziri mhusika hajawahi kutujibu kwenye eneohili. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Aeshi, ajiandaeMheshimiwa Chumi.

MHE. KHALFAN H. AESHI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi hii na mimi niweze kuchangiakatika bajeti ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa naombanimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa na nzurianayoifanya. Pili, nimpongeze Mheshimiwa Waziri Mkuu kwakazi na uwajibikaji mzuri na kila Mbunge ndani Bunge laJamhuri ya Muungano wa Tanzania anakuamini kwa asilimiamia kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuchangia maeneomachache sana katika bajeti hii na kwanza, ni suala la maji.Ndani ya Mji wa Sumbawanga Mjini tuna mradi mkubwa sanawa maji ambao napenda sana kwa niaba ya wananchiniwashukuruni sana kwa mradi ule. Sumbawanga sio mji pekeyake pale mjini, Sumbawanga imezungukwa na vijiji vingi

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

102

sana. Naomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu mliangalie hili,mtusaidie kupata fedha za kuwezesha miradi ile midogomidogo ili wananchi wanaozunguka Mji wa Sumbawangawaweze kupata maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pil i ni lawafanyabiashara. Nataka kuongelea sana wafanyabiasharahususan wa Jimbo la Sumbawanga Mjini wengi niwakandarasi na wengi wamefanya kazi ndani ya Serikali,lakini ni muda mrefu sana hawajapata malipo yao. Hao watuwanaumia sana kwa sababu wanadaiwa kodi, kwenyemabenki na kwenye maeneo mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ambalolinanishangaza Mheshimiwa Waziri Mkuu tumeunda kamatikila Mkoa ya kudai madeni ya wafanyabiashara ambaohawajalipa kodi. Kamati hiyo wameandika barua sehemumbalimbali pamoja na kuzuia fedha ambazo wakandarasiwamefanyia kazi Manispaa au taasisi nyingine, wakizuiafedha zile zote hawa watu wanakwama. NikuombeMheshimiwa Waziri Mkuu hili suala la kamati ambazommeziunda mikoani ziongozwe na watu wa TRA kwa sababuwao ni wataalam na wamesomea kazi hiyo. Nilikuwa natakanizungumzie hili ili mliangalie kwa uzito wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pembejeo,wameongea Wabunge wengi na jana nimekusikil izaukiongea na hawa mawakala wa pembejeo na umeahidikwamba ifikapo tarehe 26 at least wachache watakuwawameshaanza kulipwa wale ambao wamehakikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili linaumiza sana,watu hawa wamekopa kwenye mabenki na watu hawakama mnakumbuka, nataka niweke kumbukumbu sawawafanyabiashara au mawakala wakubwa walikataakuikopesha Serikali. Wafanyabiashara wadogo wadogo haowakaenda kukopa fedha benki wakaenda ku-supplypembejeo na bahati nzuri tukapita kwenye uchaguzi vizurisana, lakini baada ya uchaguzi kupita hawa watuhatujawakumbuka.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

103

Nikuombe Mheshimiwa Waziri Mkuu wananchi wanaimani kubwa sana na Serikali hii, liangalieni hili kwa jicholingine watu wanaumia sana, watu wamekufa, watu wanapresha na wengine wamejinyonga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, l ingine ambalo ni lakusikitisha, mwaka jana kwenye bajeti wakati tunapitishahapa masuala ya pembejeo na kutoa ruzuku kwenye mboleatukaichagua TFC iwe mwakilishi wetu. TFC ndiyo wamekuwawalanguzi wakubwa. Mheshimiwa Zitto amechangia hapaamesema umtume CAG, nikuombe kabla hujamtuma CAGmsimamishe huyu Mkurugenzi wa TFC ana miaka 20 yupopale, ana kampuni binafsi ya kwake. Mheshimiwa Waziri Mkuunikuombe sana kabla hujamtuma CAG kwenda kuhakiki aukuchunguza, kwanza huyu Mkurugenzi wa TFC mumsimamishekazi. Jana mmemsimamisha mmoja, lakini huyu ni wa pili iliakae pembeni uchunguzi ufanyike. Nikuombe sana nanaamini hili unalisikia ulichukulie kwa uzito wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine ni uwanja wandege. Uwanja wa ndege tumepata bajeti, tumeshatafutamwekezaji, uwanja wa ndege utajengwa ndani ya Mji waSumbawanga Mjini, shida kubwa nayoiona ni wale wananchiwanaouzunguka uwanja wa ndege. Wale wananchiwanaozunguka uwanja ule walifanyiwa tathmini miaka sitaau saba iliyopita, gharama za ujenzi zimeongezeka nagharama za viwanja zimeongezeka. Nikuombe MheshimiwaWaziri Mkuu na Mheshimiwa Simbachawene yuko hapa kwasababu wanaotakiwa kuwalipa fidia sio Idara ya Ujenzi,hapana, wanotakiwa kuwalipa fidia wananchi ni sisi TAMISEMIkupitia Manispaa. Naomba tufanye tathmini upya kulinganana wakati uliopo. Nafikiri hil i Mheshimiwa utakuwaumelichukua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine ni kuhusiana naumeme. Sumbawanga Mjini tumebahatika tuna umeme nahatuna mgao wowote lakini Sumbawanga imezungukwa navijiji mbalimbali. Kwa bahati nzuri vijiji vingine vyote vimepataumeme tatizo kubwa ambalo naliona na nilishamwambiaMheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini na ameahidi

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

104

kunisaidia ni vijiji ambavyo vinatoka nje ya barabara kilometatano kutoka barabarani, wale watu hawakubahatika kupataumeme. Hata hivyo, kwenye REA III nimeona baadhi ya vijijivipo na niishukuru sana Serikali katika hilo. Niombe tuMheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini naye aje azinduemradi huo wa REA III ndani ya Jimbo la Sumbawanga Mjini.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine nataka kuongeleakuhusiana na minara ya simu. Minara hii ya simu ni michachesana. Yapo baadhi ya maeneo hayana kabisa network.Niwaombe Wizara inayohusika na jambo hili lichukulie kwauangalifu mkubwa na kwa nguvu kubwa kuhakikisha sasaTanzania nzima inafikika na Tanzania nzima mawasilianoyanapatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine katika hili hili nikuomba tu Serikali iwekeze TTCL, iache maeneo mengineiongeze nguvu TTCL ili na yenyewe iwe kama kampuni nyinginetulizonazo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa na mengi yakuongea lakini mengine nimeamua kuyaacha kwa sababumaalum. Nimalizie tu na suala la Bunge Sport Club.Mheshimiwa Waziri Mkuu ulikua kocha wetu. Kwenye bajetiya mwaka huu tumeona mmetujali kidogo lakini ikumbukwesisi tuna ugeni mwaka huu kwa sababu sisi ni wenyeji wamashindano hayo.

Mheshimiwa Mwenyeki, nikuombe sana bajetituliyonayo japokuwa mmetuongeza haitutoshi kulingana naugeni mkubwa ambao tutakuwa tumeupokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama taifatusiingie aibu. Nikuombe sana Mheshimiwa Waziri Mkuuuliangalie hili kwa sababu wewe ulikuwa kocha wetu.Mashindano yakianza tutakuomba rasmi uombe likizo kidogouwe kocha ili tuweze kuchukua kikombe kwa sababu kidogotumeshuka kiwango baada ya wewe kutoka ndani yamashindano haya. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

105

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema kwamba kunamengine nimeyaacha lakini kuna kitu ambacho kinaniumalazima nikiseme. Mimi ni miongoni mwa watu waliotishwatena mimi sikutishwa kwa maneno nimemuona yeyemwenyewe, nimekutana naye uso kwa uso vis a vis,akiniambia…

MBUNGE FULANI: Nani?

MHE. KHALFAN H. AESHI: Nitamtaja mwisho.Akiniambia kwamba Wabunge mmezidi unafiki na baya zaidimaneno haya ameyatamka mbele ya Mkuu wa Wilaya yaKinondoni. Alisema hivi; “Wabunge mmezidi unafiki na nita-deal na nyie nikianza na wewe.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi leo Dar es Salaamsikanyagi na naiogopa yaani nilikuwa nimei-miss mno lakinibaada ya kutishwa nimeogopa inabidi nikae Dodoma naSumbawanga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka niliarifuBunge na familia yangu ijue kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam miongoni mwa watu wanaowatisha watu ikiwani pamoja na nini. Mengine mabaya siyasemi wala mazuriyake siyasemi nasemea hili kwa usalama wa nafsi yangu.Najua yapo mazuri aliyoyafanya na yapo mabayaaliyoyafanya, lakini mimi naomba niseme hilo moja tukwamba ni bora tukaliangalia kwa makini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nipo tayari kuhojiwa,nipo tayari kuja kusema na nitatoa ushahidi kwa sababunilikuwa kwenye hoteli inaitwa Colosseum, niliitwa mbele yaMkuu wa Wilaya na akanitisha. Sasa mimi sisemi mengi,naomba hili niseme kulitaarifu Bunge kwamba na mimi nimiongoni mwa watu ambao tunatafutwa na Mkuu wa Mkoawa Dar es Salaam. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayomachache nakushukuru kwa kunipa nafasi hii, naunga mkonohoja. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

106

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Chumi,wajiandae Mheshimiwa Benardetha Mushashu naMheshimiwa Constantine Kanyasu.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kushukuru kwa kupata nafasi na pia nipendekuwapongeza Mawaziri wanaofanya kazi katika Ofisi ya WaziriMkuu. Mheshimiwa Jenista alifika mpaka kule JimboniMafinga akazungumza na wajasiriamali na akina mamakuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana kupitia Baraza laUwezeshaji, pia ndugu yangu Mheshimiwa Mavunde hakuwana ziara rasmi lakini alivyopita pale akasimama standakaongea na vijana kuwatia moyo, kwa hiyo, nawapongezasana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa tunajadili hotubaya Waziri Mkuu ambayo ndani yake kuna Bunge, moja kwamoja nizungumzie kuhusiana na ufanisi wa ufanyaji kazi waBunge. Tumeshuhudia siku zilizopita badala ya kukutana wikitatu tumekutana wiki mbili. Kwa mujibu wa Katiba, wajibuwa Bunge ni kuisimamia na kuishauri Serikali na sehemumojawapo ya kuisimamia ni kupitia tunavyokutana kwenyeKamati, lakini pia tunavyokagua miradi mbalimbaliinayotekelezwa na Serikali. Niombe bajeti hii pamoja na jinsiambavyo tumeambiwa imeongezwa, iliangalie Bunge katikanamna ambayo italiwezesha kufanya kazi kwa ufanisi kwamujibu wa Katiba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Aeshiamezungumza hapa kuhusu Bunge Sports Club, sisi tulioendaMombasa kwenye mashindano ya Bunge tunajuakilichotokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi tumechagua Wabungewa EALA ni sehemu ya ushiriki wa Tanzania katika masualamazima ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo suala lamichezo. Tumekwenda kule kuna watu tulikuwa tunapandakwenye karandinga, huu ni ukweli mpaka kuna watuwametuuliza ninyi ni Wabunge kweli maana we were seenlike a second citizen wa Bunge. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

107

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi niombe kwa niaya kufanya kazi kwa ufanisi, tumeona hapa wakati wakukagua miradi Wabunge wanasafiri na double coasterzinaharibika njiani. Hata security yao, pamoja na kuwawanakuwa na maaskari mle ndani lakini kuna healthysecurity, afya yao katika kusafiri kwenye mazingira ya magariambayo basically yamejengwa kwa ajili kuwa school bus siojambo jema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi naomba iliBunge lifanye kazi kwa ufanisi hebu kile kinachotengwakipatikane. Kwa sababu sisi hatufanyi kwa kujipendekeza,tunafanya kazi kwa mujibu wa Katiba iliyowekwa. Naombahilo tulitizame sana…

TAARIFA

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nilindie muda wangu.

MWENYEKITI: Taarifa, Mheshimiwa Keissy.

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, hiimambo ya Wabunge, sisi kule kwetu Namanyere wananchiwangu wanasafiri kwa shida sana wengine kwa mguu,wengine kwenye Noah na kwenye daladala wanasimama.Nashangaa Wabunge wanadai kuwa na hadhi kuliko watuwengine wa kawaida. Ndugu zangu tuwafikirie na wanakijijikule kwetu majimboni.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Cosato.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa yake siipokei kwa sababu naamini amepokea mkopowa Bunge kwa ajili ya gari, hii siyo luxury ni ili kutuwezeshakufanya kazi kwa ufanisi, that is my point. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

108

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusupembejeo. Wamezungumza Waheshimiwa hapa na kakayangu Mgimwa amesema. Tumesikia kwamba MheshimiwaWaziri Mkuu amekutana na watu waliokopesha pembejeo,ni kweli matajir i wakubwa walikataa kuwahudumiawakulima wetu, wafanyabiashara wadogo wadogowakajitokeza. Kwa hiyo, mimi niombe baada ya uhakiki watuhawa walipwe pesa zao. Kwa sababu ni kupitia kilimo watuwetu kwa mfano mimi kule Mafinga kuanzia Bumilaingampaka Itimbo watu wale hawana shida, wewe wapembolea tu ni wapiga kazi wazuri. Vijiji vyote Isalamanu naKitelewasi watu wanalima mwaka mzima lakini wapete tumbolea kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hata hawa ambaowamekopeshwa wapewe fedha zao kwa wakati ili kusudiwakati ujao waweze kuwa na moyo wa kushirikiana na Serikalikatika kuwahudumia wananchi wetu. Kwa hiyo, niombe sanaOfisi zinazohusika, najua itakuja Wizara ya Kilimo tutalisemea,lakini suala la pembejeo ni suala linalogusa maisha ya watu.Kwanza, mbolea zifike kwa wakati kwa sababu msimuunajulikana. Sasa mbolea ya kupandia iende mwezi wa pilisio jambo zuri, wananchi wanaona kama tumewatelekeza.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ukurasa nadhani wa16 wa hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu umezungumziakuhusu kutenga maeneo kwa ajili ya biashara. Mimi niombemamlaka zinazohusika, Halmashauri zetu kwa hali ilivyobaada ya kutoa ule utaratibu wa retention haziwezi kuwana fedha kwa ajili ya kutenga maeneo, kwa sababutunaposema kutenga haiishii tu kutenga ni pamoja nakuyapima maeneo yale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa kuwaHalmashauri hazina nguvu hii tena tuje na utaratibu ambaotunaweza tukazisaidia, zikatenga maeneo yakapimwayakajulikana haya ni maeneo ya biashara, haya ni maeneoya wafanyabiashara wadogo wadogo na yakajengewamiundombinu yake. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

109

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sambamba na hiloMheshimiwa Waziri Mkuu kwenye hotuba yakeamempongeza Alphonce Simbu, huyu ni mwana michezo.Sasa katika kutenga maeneo pia tuzisaidie Halmashaurizitenge maeneo kwa ajili ya michezo. Kwa sababu ni kupitiamichezo vijana wanapata ajira na kupitia michezo tunapataakina Samatta na hawa akina Simbu. Bila kuwa namiundombinu kwa maana ya viwanja hatuwezi kufanikiwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kupitia michezotumeona hapa utalii umeongezeka kwa asilimia 12 lakinikupitia michezo tunaweza tukafanya promotion kwa wepesizaidi. Leo hii Simbu ameshinda Mumbai Marathon ni Wahindiwangapi India wameweza kuifahamu Tanzania? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, l ingine ni kwambaHalmashauri bado hazijaweza kuwa na nguvu especiallykama ya Mji wa Mafinga. Wananchi wamejitahidiwamejenga zahanati, juzi tunashukuru Ubalozi wa Japanumetusaidia tujenge theatre. Kwa hiyo, niiombe Serikalikwenye Halmashauri kama hizi ambazo ni mpya na wananchiwamejenga maboma itie nguvu yake katika kuhakikishakwamba zahanati zinakamilika. Vilevile kama ambavyoSerikali imefanya kwenye utaratibu wa kuwapata walimu wasayansi na hesabu pia tuweke utaratibu na tupate vibali ilikusudi watumishi wa kada ya afya nao waweze kuongezwakatika maeneo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa haya yotetunayoyasema na kuyatekeleza na tutakayoyatekelezayatafanikiwa tu ikiwa Serikali kwa macho mawili itaangaliawelfare ya watumishi wa umma. Chochote tutakachofanyakama watumishi wa umma morale wako chini nadhanikwamba hatuwezi kufanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuwatutazungumza kwenye Wizara husika lakini Serikali iangaliekama wamepata promotion, waweze kulipwa zile haki zaozinazoendana na promotion zao na welfare yao kwa ujumla

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

110

watumishi wa umma. Kwa sababu hawa pamoja narasilimali fedha ni watu muhimu kuhakikisha kwambatumefanikisha mipango tuliyoipanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mushashu,ajiandae Mheshimiwa Constantine Kanyasu.

MHE. BENARDETHA K. MUSHASHU: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa,nampongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba yake nzuripamoja na Mheshimiwa Jenista Mhagama na MheshimiwaAntony Mavunde kwa kazi nzuri wanayofanya katika shughulizao za kumsaidia Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Raiswetu, Mheshimiwa Dkt. Magufuli pamoja na Waziri Mkuu,Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa kazi nzuri mnayofanya. Nimwaka mmoja tu tangu mmeingia madarakani lakini mambomnayofanya ni mazuri sana, uchumi wa nchi hii umeendeleakuwa mzuri hadi sasa hivi viashiria vyote vya uchumivinaonekana kwamba tunafanya vizuri sana kwenye uchumi.Pato la Taifa limeendelea kukua hadi sasa hivi linaendeleakukua kwa asilimia saba na mmeweza kuu-contain mfumukowa bei ukaendelea kukaa kwenye tarakimu moja. Vilevile nifuraha ilioje niliposikia kwamba Tanzania iko kati ya nchi sitathe best in Africa ambao uchumi wao unakuwa kwa kiasikikubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunayo mengi ya kujivunia,tumeambiwa TRA sasa hivi makusanyo yameongezekakutoka kwenye shilingi bilioni 850 mpaka kwenye shilingi trilioni1.2 ndiyo maana mmeweza kuyafanya mambo makubwakama kununua ndege. Anayependa apende, asiyetakaasitake lakini makubwa yanafanyika ndani ya Serikali yaChama cha Mapinduzi. Mmeweza kuwa mnapeleka shilingibilioni 18.77 kwenye shule kwa ajili ya elimu bure kila mwezi,hongereni sana. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

111

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba yakeMheshimiwa Waziri Mkuu amezungumzia kwamba mabenkiyako salama, mitaji na ukwasi upo wa kutosha. Hapa ninawasiwasi kidogo kwa sababu tukienda kule chini, tukiendamijini na vijijini tunaona kwamba mabenki ya biasharayamepunguza kutoa mikopo. Tunahamasisha wajasiriamaliwengi wajitokeze wafanye shughuli mbalimbali, wafanyeshughuli za kilimo, biashara ndogo ndogo, tunahamasishawananchi waanzishe viwanda vidogo na vikubwa, hivi kamamabenki hayatoi mikopo hawa mitaji watapata wapi?Niombe Mheshimiwa Waziri Mkuu atusaidie ili Serikali sasaiweke mpango wa makusudi wa kuziwezesha hizi benki ilizianze kutoa mikopo kama walivyokuwa wanatoa kwa ajiliya wajasiriamali wadogo wadogo waliopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nitajikita kwenye sualala kahawa. Kahawa ni zao la muhimu sana katika nchi yetuya Tanzania, lakini lina umuhimu wa pekee kwa sababutunaliuza nje linatuletea fedha za kigeni. Bei ya kahawaimeendelea kuwa chini kiasi ambacho inakatisha tamaa naukilinganisha bei ya kahawa ya Tanzania na nchi jirani yaUganda unakuta bei ya kahawa ya Uganda iko juu pamojana kwamba nchi hizi zimepakana, ndiyo kitu kinachoshawishiwatu wauze kahawa ya magendo kuitoa Tanzania kuipelekaUganda. Bei ya kahawa kuwa chini ni kwa sababu bei yakahawa ya Tanzania imegubikwa na tozo nyingi, ada nyingi,kodi nyingi. Wataalam wanasema hizi kodi na tozo zinafikiahadi 26. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mfano, kuna kodina tozo za zimamoto, OSHA, land rent, crop cess pamoja nakwamba sheria inasema crop cess inaweza kuwa kati yaasilimia tatu mpaka tano, sisi halmashauri zinatoza maximum,five percent. Kuna income tax, cooperate tax, VAT kwenyeinputs zote zinazoingaia kwenye kahawa, research cess,Coffee Development Fund ambapo hela zinakatwa kwenyekila kilo, lakini sijawahi kuona huu mfuko unakwendakumuendeleza au kuendeleza kilimo cha kahawa. Kunalabour charge, service levy, property tax, coffee bags duties,coffee industry licence et cetera mpaka zinafika 26. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

112

Mheshimiwa Mwenyekiti, tozo hizi ziko kwenye ngazimbalimbali za uzalishaji pamoja na pale wanapouza nje.Ukienda pale mkulima anapouza kahawa kwenye chamacha msingi, kwenye chama kikuu cha ushirika, kule kwenyemnada Moshi ambapo wana-export kahawa kote kuna tozokila mahali, lakini mzigo mzima anaubeba mkulima. Tozohizi ndiyo zinasababisha bei ya kahawa inakuwa chini sana.Kwa msimu huu Mheshimiwa Waziri Mkuu, bei ya kahawakwa Mkoa wa Kagera ni shilingi1,300, mtu anatunza ule mbunikwa miezi tisa anapalilia, anakatia na kadhalika lakinianakuja kuishia kupata kati ya shilingi 1,100 na shilingi 1,300.

Mheshimiwa Mwenyekti, tukijilinganisha na nchi jiraniambazo ni washindani wetu katika hili zao la kahawa kamaEthiopia wao wanakata 0.04% kama exchange rate sale price,Uganda wanakatwa 1% export levy, Kenya wanakata 3% tukwa ajili ya cess, lakini Tanzania tuna different cess’s, licencefees, taxes na tozo mbalimbali zinazofikia zaidi ya 26 nakuifanya hiyo bei iwe chini sana na kuwafanya wakulima wakahawa wakate tamaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuuamefanya mambo mazuri sana kwenye korosho,tumemuona. Ameweza kuifanya bei ya korosho ikapandakutoka kwenye kilo moja shilingi 1,200 mpaka shilingi 3,800.Tumuombe chondechonde, mimi kama mwakilishi wawakulima wa Mkoa wa Kagera na nyuma yangu wakiwaWabunge wote wa Mkoa wa Kagera, tunamuomba hebuaangalie kwenye hili zao la kahawa, watu wamelia ni kiliocha siku nyingi. Hebu aangalie tunatoa ada, tozo na feesgani ili kumwezesha huyu mkulima na yeye mwenyewe awezekufaidi jasho lake aweze kupata bei ya juu ili angalau kilomoja isiteremke chini ya shilingi 3,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati namalizia,unakumbuka kwamba watu wa Mkoa wa Kagera naMwanza wanafanya biashara na Uganda kwa kupitia ZiwaVictoria. Meli ya Mv Bukoba ilizama, Victoria imezeekainakarabatiwa kila kukicha lakini wafanyabiashara wanapatamatatizo kwa sababu ili waweze kupeleka mazao yale ina…

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

113

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Kanyasu.

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana.

Naomba na mimi nimshukuru Mwenyezi Mungu kwakunipa afya njema na kupata nafasi ya kusema machachekuhusu hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, lakini pia naKamati ambazo ziliwasilisha maoni yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze na kwenyehiki kitabu cha Mheshimiwa Waziri Mkuu ukurasa wa 21. WaziriMkuu ametoa takwimu za upatikanaji wa chakula kwamwaka uliopita na akagusia kwamba mwaka huu kunamaeneo ambapo hali ya hewa haikuwa nzuri sana.Nilichokuwa nakitegemea hapa kidogo na nitoe ushauri nikwamba kutokana na hali hiyo kutokuwa nzuri, kwanzanilitarajia nione hapa kama kuna akiba kiasi gani sasa yachakula lakini tunakitumia kwa namna gani ku-control beiinayoendelea kupanda kwenye soko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi ninavyozungumza janaMwanza gunia la mahindi lilikuwa shilingi 125,000 na wakatikelele za uhaba wa chakula zinaanza gunia la mahindilil ikuwa shilingi 80,000. Hii maana yake ni nini? Kadritunavyokwenda kuja kufikia mwezi wa kumi kama hakunamechanism ya Serikali ku-control bei ya mahindi yatafikashilingi 160,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachozungumza hapa sionjaa, hatuzungumzi njaa tunazungumzia kwamba bei yachakula inapanda kwa sababu Serikali ni kama haijachukuaposition yake ya ku-control bei ya chakula kwenye soko.Wakati tunazungumza wakati ule bei ya mchele ilikuwashilingi 1,200 leo ni shilingi 2,500, Mwanza ni shilingi 1,800.Maeneo yote haya ninayoyazungumzia hawakulima kwasababu mvua hazikuwepo. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

114

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ombi languMheshimiwa Waziri Mkuu, kama tunayo stock ya chakulakwenye godowns, Wizara ichukue position yake, chakulakingie kwenye masoko na bei elekezi itolewe ili kisiendeleekupanda, vinginevyo purchasing power ya wananchiinapungua. Wananchi kipato ni kilekile, chakula kinapanda,matokeo yake watajikuta hata hiyo shilingi 2,000 ya kula kwasiku inakosekana. Hilo ndiyo lilikuwa ombi langu kwenye huuukurasa wa 21.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hotuba hii yaMheshimiwa Waziri Mkuu ukurasa wa 25 amezungumziakuhusu hekta 38,567 za wachimbaji wa madini. Tatizo langumimi sio utengaji wa maeneo, nilimwambia Waziri wa Nishatina Madini, alikuja Geita akazungumza takwimu kubwa zakuwapa watu maeneo ya kuchimba. Nikamwambia tatizokubwa lililoko hapa wanaopewa ni walewale. Ukiingiakwenye database utamkuta Kanyasu huyu ana-appearkwenye karibu kila eneo dhahabu inapotokea wale ambaowanatakiwa kabisa wapewe maeneo haya hawapewi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi ninavyozungumza nawewe tuna vikundi zaidi ya 100 Geita vimejiandikishavinasubiri maeneo ya kuchimba havipewi, lakini ukiendakwenye takwimu za Wizara atakutajia kubwa ya watu ambaokimsingi ni walewale wachimbaji wakubwa ambaowanahama toka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Kwa hiyo, nilikuwa naomba sana, ni ahadi yetukwenye Ilani ya CCM, tutawapa watu maeneo ya kuchimba,lini? Huu ni mwaka wa pili sasa. Kama yapo tunaombayaanze kutolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye ukurasa wa 28limeongelewa suala la umeme. Geita kila siku umemeunakatika. Hivi ninavyozungumza na wewe umeme hakuna,unakatika zaidi ya mara nne. Nimezungumza na Waziri naNaibu Waziri, wana matengenezo ya kutoka Busisi kwendaGeita karibu miaka miwili hayaishi. Nataka kufahamu hilitatizo la umeme Geita linakwisha lini?

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

115

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hata hivyo, kunamaeneo tumepeleka umeme wa REA baada ya umeme waREA kufika kazi imeisha, jirani akiomba umeme TANESCOhakuna vifaa. Ina maana REA peke yake ndiyo sasa inafanyakazi ya kusambaza umeme, TANESCO wenyewe hawanauwezo? Naomba sana eneo hili lifanyiwe kazi vizuri kwasababu linakatisha tamaa, kama umeme umefika kijijini, kunawatu wanne wamepewa umeme, jirani hapewi umeme kwasababu TANESCO hana vifaa, nadhani hapa kuna mipangomibovu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye suala la faola kujitoa. Mimi natoka Geita na naomba WaheshimiwaWabunge wote wanisikilize vizuri sana. Geita pale karibu nusuya watu wanaofanya kazi pale Geita Mjini ni watumishi wamgodi. Kinachotokea kwenye mgodi pale ni kwambahakuna mwenye ajira ya kudumu. Kuna watu palewanafanya kazi kwa mikataba ya miezi sita, miaka miwili,miaka mitatu. Anapofukuzwa kazi hawezi kupata kazi ya ainaile tena katika nchi hii, kuna wengi ni vibarua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa watu wanafukuzwakazi, kwa sababu kandarasi iliyokuwa imempa kazi mkatabawake umekwisha, imeondoka imekwenda South Africa.Akienda kufuata pesa zake NSSF anaambiwa hizo pesahawezi kupewa mpaka afike umri uliolezwa. Mtu leo anamiaka 25 au 30 asubiri pesa hizi mpaka afikishe miaka 55ndiyo aweze kulipwa na hana kazi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana kuna MheshimiwaMbunge mmoja ametoa hoja kwamba wapewe asilimia 25,hapana. Ziko kada ambazo wanaweza wakasubiri,ukimwambia mwalimu, polisi, daktari asubiri sawa. Palemgodini kuna tabia supervisor akikuchukia anaku-blacklist,akiku-blacklist huwezi kuajiriwa mgodi wowote duniani. Sasaunakaa unasubiri hiyo pesa mpaka utakapofikisha miaka 60unaendelea kuwa maskini kwa misingi gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kushauri, sekta yamadini iangaliwe kwa jicho tofauti. Kuna watu pale

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

116

wanaacha kazi kwa sababu ni wagonjwa. Mgodi ulehauchukui watu wagonjwa, ukitibiwa mara mbili unaumwakifua wanakufukuza, Mheshimiwa Jenista unafahamunilikuletea watu wanaumwa, walipokuwa vilema walifukuzwakwenye kazi, wana miaka 25, 30 halafu wananyimwa zile pesawanaambiwa wasubiri mpaka watakapozeeka, anazeekahizo pesa aje atumie nani? Ushauri wangu ni kwamba sektaya madini ichukuliwe kwa namna tofauti, hatuwezi kuwa najibu moja kwenye maswali yote magumu, lazima tuliangaliehili suala tofauti. Kama tuna nia ya kuwekeza NSSF wana mitajimikubwa waangalie sehemu nyingine, lakini haya maisha yawatu kwa pale Geita tutawafanya kuwa maskini zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna gereza pale Geita Mjini,uwezo wake ni kuchukua watu 100 na zaidi, hivi sasa linawatu 800, sababu kubwa ni wachimbaji wadogo wadogoambao wanatafuta pesa ndogo ndogo ya kula, akikamatwaanarundikwa pale. Kuna tatizo sasa hivi kwenye Jeshi la Polisina watu wa Idara ya Sheria, kesi ya madai inageuzwainakuwa jinai wanarundikwa mle, matokeo yake watuwanalala wamesimama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu MheshimiwaWaziri Mkuu na nafikiri nilizungumza na wewe, pale kunatatizo tuna OC-CID hafanyi kazi yake vizuri, kazi yake nikukusanya pesa, anachokifanya yeye ni kuhakikisha kwambakila anayetuhumiwa pale, iwe ni jinai, iwe ni civil lazimaabambikwe kesi ambayo itamuweka magereza zaidi ya miezimitatu, gereza limejaa. Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe alikujaaliona, Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ulikuja uliona,tunaomba mtusaidie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna hizi kesi ndogondogo za kupita tu mgodini anakamatwa mtu anawekwandani miezi sita. Unapita tu na baiskeli unakamatwaunawekwa ndani miezi sita. Serikali ina pesa za kuchezea,kwa nini hizi pesa ambazo zinakwenda kulisha watu humowasipewe hawa wanasheria wakapeleka hizi kesiharaka? Mimi nadhani kuna haja ya kuisaidia Wilaya ya Geita.(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

117

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo lingine ni uwepo wamigodi mingi sana kwenye Mkoa wa Geita na tatizo lahuduma za afya. Wilaya ya Geita peke yake ina watu 800,000kwa sensa ya mwaka 2012, lakini hospitali yetu iliyokuwa yaWilaya tuliigeuza kuwa ya Mkoa, matokeo yake hatuna tenaHospitali ya Wilaya. Sasa ufikirie population ya watu 800,000wa Wilaya moja na ile hospitali imegeuka kuwa ya mkoa,watu milioni mbili matokeo yake ile hospitali imezidiwa kabisauwezo. Tuna vituo viwili vya afya tumeanza kuvitengeneza,tunaomba support yako Mheshimiwa Waziri wa Afya,tunakushukuru ulitupa gari lakini hatuna madaktari. Daktarialiyepo pale kuna specialist mmoja ambaye ni surgeonwaliobaki wote ni AMO.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niishukuru sanaSerikali, tulitaka kuleta muswada hapa wa kuwaondoaMadaktari Wasaidizi kwenye mfumo wa madaktari, lilikuwani kosa kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kule vijijini madaktariwetu ni ma-AMO na ndiyo wanaofanya kazi usiku namchana. Ukiwaondoa wale kwenye mfumo wa madaktariwaliobaki wengine wote ni mabosi wakienda kwenye wilayakazi yao ni research, hawakai kwenye ofisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi namuombasana Mheshimiwa Waziri Mkuu mtusaidie sana Hosptali yetuya Mkoa wa Geita ianze ili Hospitali ya Wilaya irudishweWilayani ili gharama za matibabu ziweze kupungua. Hivi sasanavyozungumza na wewe gharama za matibabu ziko juusana kwa sababu tunalipa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana na naunga mkono hoja.(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

118

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, muda wetuumekwisha na wachangiaji waliopangwa muda huu wamchana wametimia kwa uhakika.

Waheshimiwa Wabunge, tuna utaratibu wa mambomahsusi yanayojadiliwa humu kwenda kwenye Kamati yaBajeti. Naelekeza Kamati ya Bajeti kushughulikia suala la TTCLna wakae na Serikali, Wizara ya Mawasiliano, TCRA nawenyewe TTCL.

Waheshimiwa Wabunge, Ethiopia chombo cha simukinakusanya almost 1.7 billion dollars kwa mwaka. Njia yakuondokana na matatizo haya ya maji, barabara ni chombochetu kipewe nafasi kubwa nchini kiweze kufanya kazi. Kwamaana hiyo, tutaiomba Kamati ya Bajeti baadaye naWabunge wote wawe mabalozi wa TTCL. Sidhani kamaWaheshimiwa Wabunge hapa wana kadi za TTCL. Lazimawote tuingie TTCL na tuhakikishe by december subscribers waTTCL wako milioni 30 na Serikali iwekeze ili minara na umemeupatikane maeneo yote na TTCL iwe number one Tanzania.

Waheshimiwa Wabunge, nina tangazo dogo,Wabunge wote wa CCM leo wanatakiwa kwenye caucussaa mbili baada tu ya Bunge kuahirishwa. Tangazo lingine,Waheshimiwa Wabunge wote wanatangaziwa kuhudhuriaibada katika chapel iliyopo Jengo la Pius Msekwa, ghorofaya pili leo, leo siku ya Jumanne, tarehe 11 Aprili, 2017 marabaada ya kusitisha shughuli za Bunge saa saba mchana.Aidha, wanamaombi wa Mkoa wa Dodoma watahudhuriaibada hiyo. Waheshimiwa Wabunge wote mnakaribishwa.

Waheshimiwa Wabunge, jioni mchangiaji wetu wakwanza atakuwa Mheshimiwa Zubeda Sakuru, wa piliMheshimiwa Joyce Mukya na wa tatu Mheshimiwa MwanneMchemba.

Waheshimiwa Wabunge, nasitisha shughuli za Bungempaka saa 11.00 jioni.

(Saa 7.00 Mchana Bunge lilisitishwa hadi Saa 11.00 Jioni)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

119

(Saa 11.00 Jioni Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Tukae.

Waheshimiwa Wabunge, majadiliano yanaendelea.Mchangiaji wetu wa mwanzo jioni hii ni Mheshimiwa ZubedaHassan Sakuru, jiandae Mheshimiwa Joyce Mukya naMheshimiwa Mwanne Ismail Mchemba ajiandae.Mheshimiwa Zubeda.

MHE. ZUBEDA H. SAKURU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kuweza kunipa nafasi hii kujadili hotubaya Waziri Mkuu katika kupitia mwelekeo wa kazi za Serikalina makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi yaWaziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka huu wa fedha wa2017/2018. Pia nitoe pole kwa familia ya Mbunge mwenzetuDkt. Elly Macha aliyefariki nchini Uingereza na naungana nawana CHADEMA wote kufikisha salamu hizi kwa familia yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuweka wazikuwa naunga mkono kwa asilimia mia moja maoni yaMsemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani MheshimiwaFreeman Aikaeli Mbowe na naamini kwamba Serikali itaendakuyafanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Baba wa Taifa alipatakusema maneno yafuatayo naomba niyanukuu: “tunatakakuona katika Taifa hili vijana jeuri na wenye kujiamini siyovijana waoga akina ndiyo Bwana Mkubwa, vijana wenyeujasiri wa kuhoji na kupiga vita mfumo wa jamiiisiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii yaKitanzania na tunataka kuona vijana waasi dhidi ya mfumokandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa”. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kijana nauliza swaliambalo vijana wenzangu wa Tanzania wanauliza where isBen Saanane? Tunapozungumza leo hii kijana aliyezaliwa namwanamke na Watanzania tunajua usemi wa Kiswahiliunaosema “uchungu wa mwana aujuae mzazi” kijana wa

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

120

watu Ben Saanane ana takribani miezi sita haonekani,hajulikani alipo, itakuwa ni kosa kubwa kama Bungetukinyamaza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna taarifa mbalimbalizimeletwa mbele yetu, katika mijadala hii kunaonekanakwamba kulikuwa kuna namba 0768-797982 iliyosajiliwa kwajina la Emmanuel Joseph, ndiyo iliyotuma ujumbe wa vitishokwa Ben Saanane. Wasiwasi wangu kama kijana ambayeleo hii nipo katika siasa lakini siasa za upinzani na wasiwasialionao Mama yangu Doris Harold Mboni alipo ni kwambaje, nini hatma yangu kesho?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumza mweziOktoba, 2016 kulitokea uvumi wa aliyekuwa Mkuu wa MajeshiNchini Devis Mwamunyange kwamba amelishwa sumu.Uvumi huu ulianza tarehe 2 Oktoba, 2016 lakini ukajakufupishwa kwa kumpata kijana aliyetuma na kuanzishaujumbe huu kupitia TCRA na Jeshi la Polisi, tunachouliza nikitu gani kifanyike, ni aina gani ya hasira na maumivu yawazazi wa Ben Saanane waliyonayo wayafanye ili TCRA naJeshi la Polisi liseme huyo aliyetuma ujumbe ni nani? yukowapi na wamechukua hatua gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu zangu wana CCMpamoja na wana CHADEMA na wana CUF hakuna dhambikubwa duniani kama dhambi ya uoga, uoga huanzakumtafuna mmoja baada ya mwingine. Tumeimbiwa juzihapa na kijana mwenzangu Diamond anasema tupigekimya, mimi kama tunda la aliloliacha Baba wa Taifa sitokaakimya nikiwa kijana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini Waziri Mkuu kwasababu tunapozungumzia hali ya kisiasa nchini ni lazimatuzungumzie tension iliyosambaa. Mimi kama Mbungenaweza nikajihakikishia usalama wangu lakini kwawanaonipenda, familia yangu, jamaa zangu nawahakikishianini? Tunapokaa hapa sasa hivi tunaongelea hali ya kisiasakuwa nzuri nchini lakini kuna video zinatapakaa za Mkuu waMkoa wa Dar es Salaama akivamia kituo cha Television

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

121

(Clouds Media) Waziri Mkuu hajazungumzia kitu chochote.Pamoja na kwamba hawa ni wateule wa Rais lakini ipo hajaWaziri Mkuu kuzungumza haya kama Msimamizi Mkuu washughuli za Serikali hapa Bungeni na tulitegemea kwambahili litaonekana hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalolinasikitisha sana ni kuhusu pension ya Wazee ambayo ikochini ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Mwaka 2010 hii Mifuko yaHifadhi ya Jamii na kwa kuwa ilikuwa katika ilani ya Chamacha Mapinduzi, wazee waliahidiwa pensheni, leo miaka 15baadaye hakuna anayezungumzia pension ya wazeeambayo ilisemwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.Mwaka 2005 na 2010 ni dhahiri kuwa, waliokuwa wapigajikura wakubwa walikuwa ni wazee, sasa leo tunawaachaje?Itakuwa dhambi kubwa sana kuhitimisha mjadala huu bilakuhakikisha Serikali inatekeleza ahadi yake ya kuhakikishawazee wote nchini wanapata pension. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa piakuzungumzia kuhusu watu wenye ulemavu. Ni haki na wajibuwa walemavu kupata huduma zote za kijamii kamaambavyo tunapata sisi wengi lakini hali ikoje? Tukijiangaliana kufanya tathmini katika sekta mbalimbali za huduma zajamii, je, walemavu wamewekewa mazingira rafiki,kuwawezesha kupata haki zao za msingi kama tunavyopatawengine? Ukienda hospitalini, hakuna hata kitu kimojakinachoonesha kwamba haya mazingira ni rafiki kwawalemavu, ukienda katika sekta ya elimu huwezi kukutamazingira rafiki kwa ajili ya walemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kuna mikakatiimewekwa ambayo Serikali inasema kwamba imejaribukuyajibu haya lakini kwa kiwango kikubwa mtu mlemavuanayezaliwa katika familia ya kimaskini anakuwa ameachwakama alivyo. Sasa ni wajibu wetu kama Wabunge kuendeleakuikumbusha Serikali kuhakikisha inajenga mazingira wezeshikwa watu wenye ulemavu.(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

122

Mheshimiwa Mwenyekiti, mazingira rafiki au mazingirawezeshi kwa wafanyabiashara; tarehe 2 Februari, 2017, WaziriMkuu alitoa katazo la uuzaji wa viroba. Hakuna asiyepingamatumizi ya viroba nchini, lakini je, hili katazo lilikuja kwawakati na je, l i l ikuwa rafiki kwa wafanyabiashara?Mfanyabiashara wa Dodoma tulioneshwa hapa amejipigarisasi shambani kwake kwa sababu alichukua mkopo.Tunasemaje kwamba tunajenga mazingira wezeshi wakatiSerikali inatoa matamko bila kufikiria athari zake mbadalazinazojengwa kwa wafanyabiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa kwa ubaya ganikwa Waziri Mkuu kuzuia uzalishaji wa viroba nchini halafuwawape muda au grace period hawa wafanyabiasharawarudishe viroba viwandani vifanyiwe packaginginayotakiwa ili kuhakikisha kwamba hawa watu wanawezakurejesha mikopo yao. Leo hii mtu amejiua kwa hasara yakaribu bilioni mbili, bilioni tatu, Waziri Mkuu anasemaje kuhusuhicho kitu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna mtu ambayeanapenda matumizi ya viroba hapa, kwa sababu mwishowa siku hivi viroba mnavyokataza vinaenda kutengenezwaupya katika ujazo mwingine na mnasema kwamba matumiziyake wanatumia vijana, hapana. Leo ukienda kwenyemaduka ya reja reja mtoto wa miaka saba, nane anatumwakwenda kununua sigara, kuna mtu anayezungumzia hiki kituau kwa sababu sigara imeandikwa ni hatari kwa maishayako? Ni lazima tuhakikishe kwamba, tunawawezeshawawekezaji na wafanyabiashara nchini kwetu mazingira yakubadilisha maisha kwa kupitia matamko yatakayowajengana siyo kuwabomoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine tumeonakwamba kuna baadhi ya makampuni nchini ambayoyanawafanyisha watu kazi bila ya kuwa na mikataba ya ajira.Je, Serikali inaliona hili? Kamati ya Miundombinu tulipitakatika makampuni mengi ya simu na tukaona kwamba kunawafanyakazi ambao wanafanya kazi nchini lakini hawapewimikataba ya ajira na hii mwisho wake inasababisha wao

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

123

kushindwa kupata stahiki zao za kazi. Naamini kwambaSerikali inaweka mkakati wa kuhakikisha kwamba mikatabaya kazi katika sehemu za ajira inapewa kipaumbele naWatanzania hasa wazawa wanapata stahiki zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nije kwenye jambomoja la msingi; Tanzania ni yetu sote, Tanzania haitojengwana CHADEMA peke yake, haitojengwa na CCM peke yake,ndiyo maana leo hii fedha za miradi ya maendeleo hazitokiLumumba, mnakusanya kwa Watanzania waliowachaguana wasiowachagua, mnakusanya kutoka kwa wanaCHADEMA na wasio wana CHADEMA, sasa tunapokujatunajinasibu kwamba hii ni mikakati ya Serikali, hata TLPingepewa dhamana ya Serikali, ingesimamia kwa sababu niwajibu wa kila Chama kusimamia….(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Sakuru.Mheshimiwa Joyce Mukya.

MHE. JOYCE J. MUKYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimipia nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia katikahotuba hii ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendeleealipoishia mwenzangu Mheshimiwa Zubeda kuhusuwalemavu. Walemavu wamekuwa wakidhalilishwa sana,walemavu wamekuwa hawasaidiwi kimatendo. Kwenyehotuba ya Waziri Mkuu katika ukurasa wa 47 amezungumziasuala la walemavu lakini hakuna mkakati wowoteunaoonesha kwamba walemavu watasaidiwa kimatendo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niishauri Serikalikama ambavyo tunatoa asilimia 10 kwenye Halmashauri zetukutoka kwenye own source, naomba kwenye asilimia hizohizo 10 iwe ni lazima kwa wanawake asilimia tano wawepowalemavu at least watano au 10 kwenye watu 30 na

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

124

walemavu wengine watano kwenye watu 30 ambao nivijana. Naomba sana kwa sababu walemavu hawawanaonekana kwa macho tofauti na wanawake na vijanaambao mara nyingi wamekuwa wakitumika kisiasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wanasiasa mara nyingiwamekuwa wakiwatumia wanawake na vijana kwa ajili yakuwatafutia kura kwa vipindi vya uchaguzi vijavyo lakininaomba sana suala la walemavu wamekuwa hawanamsaada dhahiri unaoonekana. Naomba sana suala lawalemavu, aliliongelea sana Marehemu Dkt. Elly Macha,naomba tumuenzi marehemu Mheshimiwa Macha kwakuwasaidia walemavu wa nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hela za maendeleo; nidhahiri kwamba Serikali yetu imeshindwa kabisa kuisaidia nchihii kwa hela za maendeleo. Asilimia 34 tu mpaka bajetiinakwisha ya mwaka 2017, hakuna hela za maendeleoambazo zimeenda kwenye Halmashauri zetu ambazozinaenda kuwasaidia moja kwa moja wananchi kule chini.Ingekuwa hakuna own source katika Halmashauri zetu,mfano, Arusha Mjini tunaendesha Halmashauri kutokana naown source zetu wenyewe. Mpaka Februari mwaka 2017imeenda shilingi milioni 320 kati ya bilioni tatu ambayo niasilimia 11 tu iliyopendekezwa mwaka 2016. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sanatunavyoendelea hivi tunaenda kuua zile Halmashauri zetu,wananchi hawatapa maendeleo na kwa Halmashauriambazo ziko vij i j ini hawana own source za maana,wanashindwa kuendesha vikao, wanashindwa kulipana helaza vikao, wanashindwa kufika kwenye vikao kutokana naumbali ama distance kulipana mafuta na gharama za usafirikwa sababu tu Serikali haipeleki hela za maendeleo kule chini.Naomba sana hili mliangalie kwa jicho la pekee sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongele suala lautawala bora; kumekuwa na tabia mbaya sana Viongoziwa Serikali wanachukua madaraka mikononi na kuanza

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

125

kutumia hela za Halmashauri au hela za Mikoa na Wilayawalizopangiwa kuanza kutumia bila kuwashirikisha Kamatiza Fedha na Uchumi za Halmashauri husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili limetokea mwakajana Septemba. Mkuu wa Mkoa wa Arusha MheshimiwaMrisho Gambo aliita Walimu wa AICC pale Simba Hallakaongea nao, wakahojiana, Walimu 701 wakampa madaiyao akamuamuru Mkurugenzi wa Jiji, Ndugu Athuman J.Kihamia awalipe wale Walimu shilingi 169.8 milioni, hii siyosawa. Hata kama Walimu wale walikuwa wanatakiwawalipwe zile pesa lazima ilitakiwa vikae vikao vya Kamatiya Fedha na Uchumi, lazima vikae vikao lakini siyo Mkuu waMkoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Mkuu wa Mkoaalikuwa anaumia sana na wale Walimu angeingia kwenyeMfuko wake wa Mkoa na kutoa hela kwa ajili ya kuwalipawale walimu. Hilo alilofanya siyo sawa, alipoambiwaakasema nawakomesha na hapa nimeanza tu lakinimtakoma. Pesa zile zilikuwa kwa ajili ya kuwalipa Madiwani,ilikuwa ni stahiki za Madiwani kwa ajili ya vikao, kwa ajili yavocha, kwa aji l i ya usafiri lakini Madiwani ambaowanaongozwa na Chama cha CHADEMA walivumilia yotena leo wanaenda kwenye vikao wanalipwa sh. 40,000 mpakash. 60,000 mbali walivyokuwa wanalipwa sh.120,000 kwakikao kimoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee suala laFaru Fausta; Serikali hii imejitanabaisha kuwa inapunguzamatumizi na mpaka sasa hakuna mtu yeyote ambayeanalipwa milioni 17 kwa mwezi, lakini Faru Fausta analipwamilioni 64 kwa mwezi hiyo ni mara tatu. Gharama za FaruFausta huyo ambaye ni Mzee ana miaka 54 ni kwa ajili yagari lake ambalo linabeba chakula chake, kwa ajili yachakula kinachotoka nchini Kenya aina ya LASEMI, kwa ajiliya kulipa Walinzi 15 ambao wanamlinda kwa masaa 24 nanguvu za Kijeshi. Faru Fausta huyu ni Mzee lakini ukiongea naWizara ya Maliasili wanakwambia eti kwamba anaingizafedha nyingi za kigeni sawa na bilioni 70.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

126

Mheshimiwa Mwenyekiti, siamini kama Wazungu auWatalii wanakuja Tanzania kumuangalia Faru Fausta pekeyake. Naamini Watalii wanakuja Tanzania kuangalia utalii,kujifunza kutali i Tanzania lakini wakifika Tanzaniawanakutana na Faru Fausta. Naomba sana Serikali kwasababu inajidai kwamba inapunguza gharama na kutumbuamajipu, ianze kumtumbua Faru Fausta ambaye ni Mzee sanasasa hivi na wanasema kwamba nyumba yake ikishakamilikaatatumia milioni 20.4 tu sawa sawa na milioni 244 kwamwaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado gharama hizi ni kubwasana. Kule chini Ngorongoro wale Wamasai na wale wakaziwa Ngorongoro wanahangaika, hawana mahali pa kulishamifugo yao, Serikali imeshindwa hata kuwajengea majoshokule juu kwa ajili ya kulisha mifugo yao, Faru Fausta ambayeni Mzee anahudumiwa kwa milioni 64 kwa mwezi, hii siyohaki na siyo sawa kwa wananchi wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niingie katika sualala elimu bure; elimu bure ni kwenye makaratasi tu, ukiendakule chini elimu bure hakuna cha elimu bure zaidi ya kulipaile UPE. Walimu wamekuwa kwanza wanahangaika, hakunawalimu wa sayansi, hakuna walimu wa hisabati, imefikiawazazi wakae vikao na walimu na wanafunzi kutafutawalimu wa hisabati na walimu wa sayansi. Inabidi walimuwakae vikao na wanafunzi na wazazi kulipa walinzi, kulipamaji kwa ajili ya wanafunzi wao waweze kusoma, hii siyosawa kabisa hapa hakuna elimu bure. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana Ma-DC naMa-RC badala ya kupigana na Wapinzani kwenye Wilayazenu na Mikoa yenu, tafuteni njia mbadala ya kusaidia a elimubure ambayo ni sera ya Serikali yenu. Kama mnawezakuchangisha hela za Mwenge, Mheshimiwa Gambo Arushaalinunua pikipiki 200 kwa kusaidiana na wadau wa Mkoawa Arusha sasa Mheshimiwa Gambo fanya hili la elimu burekwa watoto ambao wanakua sasa hivi. Naomba sana hilimliangalie kwa jicho la pekee kabisa, hakuna elimu burehapa ni utapeli tu wa makaratasi. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

127

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niende katika sualala utalii; suala la utalii tangu kodi na tozo za utalii zipandelimekuwa halina faida kwa nchi yetu. Kama mnavyofahamunchi ya Kenya ndiyo imekuwa mpinzani mkubwa sana kwetukwa suala la utalii. Nchi ya Kenya imeondoa kodi ya VAT,nchi ya Tanzania imeweka kodi ya VAT, nchi ya Kenyaimeondoa kodi kwenye magari ya utali i wakati wamatengenezo, nchi ya Kenya imeondoa Visa kwa watotona kuwafanya watalii ambao wana familia waende Kenyana siyo Tanzania. Nchi ya Kenya imeondoa Park fees Tanzaniavyote hivyo mmeviweka, Tanzania mnataka utalii wa ainagani ninyi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Tanzania,naomba sana nchi yetu, naomba sana Waziri Mkuuanavyokuja kujibu utalii Tanzania umeshuka katika ukurasawa 20 amesema kwamba utalii umepanda kwa asilimia 1.2siyo kweli. Wageni hawa ambao wanaingia nchini ni wageniambao wanakuja kwenye mambo ya kibiashara namikutano lakini takwimu za utalii zinasema wageni wotewanaokuja Tanzania ni watalii siyo kweli, siyo watalii wavivutio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wageni wengi wanatokeaRwanda, wanatokea Burundi, wanatokea South Africa nahii ni kwa sababu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Naombasana Mheshimiwa Waziri Mkuu anapopewa takwimu zipitiena watu wako, anapokuja hapa kwenye Bunge ziletwetakwimu ambazo ni sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee mimeavamizi katika crater ya Ngorongoro. Kumekuwa na mimeavamizi sana katika crater ya Ngorongoro. crater yaNgorongoro kuna uoto wa asili. Mimea vamizi imeharibucrater ya Ngorongoro, Waziri January Makamba alienda lakinihali ni mbaya na mbaya zaidi mimea hii inakua kwa kasisana. Sehemu ambako mimea hii inakua, wanyamahawawezi kwenda kula. Sasa inaharibu uoto wa asili kule.Naomba sana Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Waziri Mkuuashirikiane… (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

128

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa MwanneMchemba, ajiandae Mheshimiwa Profesa Maji Marefu naMheshimiwa Joram Hongoli ajiandae.

MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru nami pia kwa kunipa nafasi nichangie hotuba yaWaziri Mkuu. Kwanza nianze na pongezi. Nimpongeze sanaMheshimiwa Rais wetu kwa kazi nzuri anayoifanya, asirudinyuma, ana uhakika na kitu anachokifanya nasi tunamuungamkono. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze MheshimiwaWaziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri Mkuu kazi aliyoifanya katikanchi hii ni kubwa sana, siyo hilo tu uamuzi wake wa kuhamiaDodoma inataka ujasiri, ametekeleza jinsi Mheshimiwa Raisalivyosema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze tena nduguyangu Mheshimiwa Jenista Mhagama, amesimamia vizurisana uanzishwaji wa Makao Makuu na Serikali kwa ujumlaakiambatana na Naibu wake Mheshimiwa Antony Mavunde.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sitatenda haki kama sitatoapongezi kwa Mheshimiwa Spika, Naibu Spika, weweMwenyekiti na Viongozi wote ambao wameweza kufanyakazi ya Bunge hadi sasa tuko vizuri ingawa Bunge lilikuwakatika hali ngumu. Nimpongeze sana Mheshimiwa Katibu waBunge Dkt. Thomas Kashil i l lah amefanya kazi nzuri,tumetembea, tumefanya kazi kwenye miradi na Kamatizimekwenda vizuri, niwapongeze sana kwa kazi nzuri ambayowanaifanya ya kuisimamia Bunge. Pia nimpongeze tena AGkwa kazi nzuri ya kusimamia sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya pongezi hizo,niwapongeze Mawaziri wote, wamezunguka Tanzania hiikuhakikisha Ilani ya Uchaguzi ya CCM inafanya kazi.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

129

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie hoja sasa yakuchangia Bajeti hii. Mimi nichangie moja kwa moja kuhusuviwanda, bahati nzuri au mbaya Waziri wa Viwanda hayupo.Tabora tuna matatizo makubwa sana ya viwanda, tulikuwana kiwanda cha nyuzi hakipo, nimpongeze Waziri waViwanda amesema kwamba wako njiani na yule Mwekezajianakuja kuzindua kiwanda hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwanda hicho kinasikitisha,kina historia kubwa sana katika Mkoa wa Tabora, kiliwezeshakuwapa ajira vijana wetu lakini sasa tumerudi kwenyeumaskini. Tuna kiwanda kingine cha Manonga, kila sikunazungumza na sitachoka kuzungumza. Kiwanda chaManonga cha Rajan mpaka sasa kina matatizo ambachokiko Wilaya ya Igunga. Naomba katika uwekezaji sasaiangalie suala zima la viwanda katika Mkoa wa Tabora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunasindika asali,tunarina asali nyingi sana katika Mkoa wa Tabora na zamanitulikuwa na kiwanda cha Kipalapala ambacho kilikuwakinasindika mpaka tunauza nchi za nje lakini kimekufa, kwahiyo natangaza soko na ombi la wawekezaji kama watakujakuwekeza ardhi ipo na ipo ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kidogo sualazima la afya. Tuna tatizo sana la hospitali za Wilaya, Manispaaya Tabora, Kaliua, Uyui mpaka sasa Hospitali za Wilaya hazipo.Niombe Serikali iangalie kwa jicho la huruma kwa sababutabu wanayopata wananchi wa maeneo hayo MheshimiwaWaziri Mkuu aiangalie. Wilaya ya Kaliua haina Hospitali yaWilaya, wanakwenda Urambo kutibiwa lakini wazingatie piakwamba kuna huduma ambayo inatakiwa akinamama namtoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Igunga kuna kituocha Afya ambacho ni cha Jimbo la Manonga. Kimekamilika,kilikuwa kimefadhiliwa na ADB mpaka sasa hakifanyi kazi,hakuna vifaa vya kufanyia kazi, hakuna gari la wagonjwa.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

130

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala zima lamaendeleo kwenye maeneo yetu. Serikali imefanya kazikubwa sana kuondoa umaskini kwenye kaya maskini hususanTASAF, imefanya kazi nzuri sana. Imezunguka na imesaidiamiradi ya awamu ya kwanza na ya pili ambayo haijakamilikatungeomba sasa awamu ya tatu Serikali iangalie na ikamilishemiradi yote hususan vituo vya afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niiombe sana Serikalikusimamia na kuhakikisha mradi wa MKURABITA unakwendavizuri na wanapewa pesa za kutosha ili angalau wapunguzeumaskini kwenye kaya ambazo ziko chini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzieasilimia 10 ya Wanawake na Vijana, Serikali imefanya vizuri.Niwapongeze Wakuu wa Mikoa, niwapongeze Halmashaurina Majiji nchi nzima, kwa sababu naomba nichangie kamaMakamu Mwenyekiti, nina uhakika na ninachokizungumzakwa sababu wamekuja kwenye Kamati yetu, tumeona bajetiwaliyopanga na mafanikio yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, karibu Halmashauri zotezimetenga asilimia 10 kwa sababu mwaka 2016/2017tuliwapa masharti kama Kamati, wamefanya kazi nzuri,nawapongeza na kwenye bajeti wameonesha. Kwa hiyo,kazi wanaifanya, hatuwezi kusema hawafanyi, asilimia 10 ipo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna baadhi yaHalmashauri imeweza kutenga katika asilimia 10 imesaidiamakundi maalum. Kwa mfano, Tanga tumekuta walewenzetu kwenye makundi maalum wasiosikiawametengewa fedha. Kwa hiyo, niiombe Serikali iangalie jinsigani ya kutenga asilimia 10 angalau asilimia mbili wawezekupata wenye makundi maalum. Ukurasa wa kumi na sitaMheshimiwa Waziri Mkuu amesema, naungana naye na nikweli hii fedha imetolewa, tuombe tu Serikali iangalie ni jinsigani sasa ya kusaidia kuhakikisha fedha zile zinaongezeka.(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

131

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni barabaraniipongeze sana Serikali, barabara ya kutoka Itigi kwendaTabora imetengewa fedha, lakini bado kazi ile inasuasua.Kwa hiyo niombe barabara ya kutoka Chaya kwenda Taboraipewe kipaumbele. Niombe tena barabara ya kutoka Pugekwenda Ndala, Nkinga hatimaye Manonga, hii barabaratumeiombea sana iweze kutengenezwa, Nkinga kunahospitali kubwa sana ambayo inasaidia wananchi wa Mkoawa Tabora kwa ujumla. (Makofi)

Kwa hiyo, niombe sana Serikali iangalie…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Maji Marefu,ajiandae Mheshimiwa Hongoli na Mheshimiwa Kakosaajiandae.

MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nianze kwa kuunga mkono hoja ya Bajeti ya WaziriMkuu, vilevile nitoe pole sana kwa familia ya Dkt. Machakwa msiba mkubwa ambao umewapata. Nawapa pole.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile niendelee kutoashukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Rais wetu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa PombeMagufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuilinda nchi hii.Wote sasa tumekuwa kitu kimoja na wote tumekuwa sawa.Vilevile nisiache kumshukuru Waziri Mkuu, Spika, Naibu Spika,Katibu wa Bunge pamoja na Wizara ya Afya pamoja naWabunge wote bila kujali Vyama vyao kwa msaadamkubwa walionipitia wakati naumwa pale, hawakujalivyama wala itikadi za vyama vyao, walikuja wakaniona nawalinipa faraja sana. Nawashukuru sana ndugu zanguWaheshimiwa Wabunge, haya mambo msiyafanye kwangutu, myafanye kwa kila Mbunge msijali vyama vyao. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

132

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya,nianze kwanza kwa kuongelea Mfuko wa Jimbo. Mfuko waJimbo toka tumeanza kuupata Mfuko huu wa Jimbo tokamwaka 2009 haujafanyiwa marekebisho ya aina yeyote. Mfukowa Jimbo umekuwa ni kichocheo cha Wabunge katika kilaWilaya na kila Jimbo ili pale wananchi wanapojitolea sisitunaongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfuko huu umekuwahauwasaidii sana Wabunge kwa sababu unakuwa namlolongo mrefu kiasi ambacho Mbunge hana uwezo nao,yeye kazi yake ni Mwenyekiti tu, lakini inapofika kutoa fedhakwa ajili ya kusaidia maendeleo yaliyoanzishwa na wananchi,Mfuko huu unakuwa ni mgumu sana kama vile ni mfukoambao tumepewa kama mtego. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba MheshimiwaWaziri Mkuu, huu Mfuko wa Jimbo usiishie tu kwa Wabungewenye Majimbo. Hata hawa Wabunge wa Viti Maalumwangekuwa wanapewa kiwango kiasi kwa sababu wengiwa Viti Maalum hawakai katika Majimbo peke yake,wanazunguka katika mikoa yote. Wanapozunguka katikamikoa wanafika mahali akinamama wanawaambia tunashida, utatoa wapi hela? Hela yenyewe ndiyo hii yakuchanganya changanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ningeomba naohawa Wabunge wa Viti Maalum watengewe kiwangokidogo kisilingane na cha kwetu lakini kiwasaidie kuzungukakatika mikoa yao ili itusaidie Wabunge wa Majimbo ili iweinatupa nguvu zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kujua MheshimiwaWaziri Mkuu akija atuambie sisi sasa hivi tuko wapi, kwasababu mara nyingi tulikuwa tunaambiwa vifaa vyaWabunge katika Majimbo hasa zile furniture tunapewa naOfisi ya Bunge, jambo la kushangaza hii taarifa kwa Warakawa mwaka 2010 inaonesha kabisa kwamba Mfuko huu ukochini ya Mkuu wa Mkoa, toka Wakuu wa Mikoa wamepewa

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

133

huu mfuko kwa ajili ya kuwasaidia Wabunge, hakuna hataMbunge mmoja ambaye amejengewa ofisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakuja kwenye Ofisi yaBunge tunaomba vitendea kazi lakini tunaambiwa viko kwaWakuu wa Mikoa, Wakuu wa Mikoa hawatuelezi ukweli.Naomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu atakapokuja kutoahitimisho lake atuelekeze vizuri Wabunge tusisumbue Bunge.Tukisumbua Bunge wakati kitu hiki kishatengwa kwambakwenye Waraka wa Rais wa mwaka 2010 unaoneshakwamba Mfuko huu uko chini ya Mkuu wa Mkoa na sisi tukijahapa tunaendelea kuwasumbua wenzetu ili tuonekanekwamba tunafanya kazi nzuri lakini kule vijijini watu hawajui.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tusijitetee sisi tu. Hapatuko katika mazingira mazuri kufuatana na utendaji mzuriwa Rais wetu, lakini kuna Watendaji ndani ya Bunge hiliwanafika wakati wao wenzetu ambao wanatusaidia kwakila kitu hata mishahara wakati mwingine wanakaa miezimitatu hawapati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wabunge hakuna Mbungeana mazingira magumu. Tulizoea raha sana ndiyo leotunaona kwamba kuna ukata. Watu wanakwenda kwenyevyombo vya habari kusema kwamba kuna mazingiramagumu, mazingira magumu hakuna. Ukiangalia bajeti yetuni ile ile, ila siku za nyuma Wabunge tuli-relax sana tukajisahaundiyo maana inafika mahali mtu anakimbilia kwenyeVyombo vya Habari kusema Bunge baya, Bunge gumu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia mazingira yamwaka 2010 hakuna kilichopungua ila utendaji wetu, rahazetu, maisha yetu, ndiyo tunakimbilia kusema kwambamaisha magumu. Hela tunapata kwa wakati, hela ni ile ile.Tulikuwa tunapata sh. 80,000, lakini sasa hivi tunapata karibush. 120,000 na tunapata sh. 200,000. Sasa tukianza kuyasemahaya hatutendi haki. Naomba tuwe wawazi..

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

134

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: MheshimiwaMwenyekiti, hapana! Niacheni niseme, kila mtu anasema kwawakati wake, kila mtu yuko huru kusema. Tusiwe tu watu wakulalamika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niliona niyaseme hayamapema kwa sababu inafika mahali tunakimbilia vyombovya habari, tukae wenyewe, tuna uongozi wetu, tukae chini,tuangalie upungufu uko wapi, turekebishe kuliko kukimbiliakulalamika, kama sisi tunalalamika na wapiga kura naowatamlalamikia nani? Nimekosea eeh?

MBUNGE FULANI: Ndiyo.

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Kumbe imefika mahalipake?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusumatibabu ya Wabunge.

T A A R I F A

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS , TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, natakanimtaarifu Mheshimiwa Ngonyani mzungumzajianayezungumza sasa kwamba, kwa taarifa tunazozijua sisini kwamba hakuna Mbunge yeyote anayedai, anayedaiposho, anayedai sitting allowance. Kwa hiyo, unavyosemani sawa kabisa kwamba hapa mambo ni safi isipokuwamazoea ya watu ndiyo tatizo. (Kicheko)

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Ahsante sanaMheshimiwa Waziri nimeipokea taarifa yako na naendeleakuongea. ..

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kwenye suala lamatibabu ya Wabunge. Tungeomba ikiwezekana Waziri Mkuuamshauri Rais, matibabu ya Wabunge yarudi kwaMheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania. Kwa sababu yalikuwa….

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

135

MBUNGE FULANI: Taarifa

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ngonyani, ngoja kidogotaarifa.

T A A R I F A

MHE. JULIUS K. LAIZER: Mheshimiwa Mwenyekiti,nataka tu nimpe taarifa mzungumzaji kwambatunavyozungumza maslahi ya Bunge, tunazungumza Bungekama Taasisi ili Wabunge wafanye kazi zao katika mazingiraambayo ni rafiki ikiwemo na Kamati. Hatuzungumzi habariya maslahi ya Mbunge mmoja mmoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa yake siipokei, kama yeye alikuja kufuata maslahi...

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, sasa sipokeitaarifa kutoka upande wowote.

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninachojua kilichotuleta hapa siyo maslahi ya Wabunge nimaslahi ya wapiga kura waliotuchagua kuja kutetea Bungehili. Kama watu walifuata maslahi basi wakabadilishe kaziambayo itakuwa na maslahi juu yao lakini ninachokumbukakilichotuleta hapa ni kutetea wanyonge waliotuchagua ilituwape maslahi mazuri waendelee kutuchagua kwa namnayoyote ile. Kwa hiyo, taarifa yake siipokei akatafute sehemunyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuzungumzia sualala matibabu ya Wabunge, naomba mzigo mkubwa…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. ALLY K MOHAMED: Bima ya Afya inatosha..

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

136

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, MheshimiwaEster Bulaya, tuwe na order ndani ya Bunge.

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba ulinde muda wangu, naona kuna mahalinimewagonga kidogo ndugu zangu. Kama kuna mahalinimewakosea ndugu zangu Wabunge basi kawaida ya mtuhuwa tunasameheana basi tugange yanayokuja, ahsanteni.(Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa endelea.

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naendelea na suala la matibabu. Siku za nyuma suala lamatibabu yalikuwa yanapitia Ofisi ya Spika na yeye alikuwaanajua huyu anaumwa au huyu haumwi, inategemea sasahivi tumeona kwamba Rais anafanya kazi nzuri sana lakinibaadhi ya watumishi wake wanaweza kuchelewesha kitukwa makusudi na kumfanya mgonjwa azidiwe. Hapaningeomba Mheshimiwa Rais ambakishie madaraka Spikawa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili aendeleekutusaidia katika kututibu au kwenda kuzungumzia suala laaina yoyote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nizungumziemambo machache naona taarifa zinakuwa nyingi kwasababu nimegusa maslahi ya Wabunge, nilichokuwa natakakujali ni kwamba kauli aliyosema MheshimiwaSimbachawene kwamba hakuna tunachokidai mambo yoteyako sawa, kwa hiyo naunga mkono hoja asilimia mia kwamia na kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuukatika hoja zangu zote alinisaidia kunisafirisha India kwakunilipia watu zaidi ya wawili. Kwa hiyo, namshukuru sanaMheshimiwa Waziri Mkuu kwa msaada wako mkubwa,usifanye kwangu tu, fanya na kwa hawa wengine ambaomaslahi yao wanaona kama yamebanwa banwa, Munguawasaidie sana.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

137

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Hongoli, MheshimiwaKakoso nafikiri hayupo, ajiandae Mheshimiwa Dkt. Kafumuna Mheshimiwa Ritta Kabati.

MHE. JORAM I. HONGOLI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nami nichukue nafasi hii kukushukuru kwa kunipa hii nafasi.Kwa namna ya pekee naomba nimshukuru Mheshimiwa Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi anazofanyahasa za kuiongoza nchi yetu Tanzania. Niwashukuru Mawaziriwote kwa namna ya pekee nimshukuru Waziri Mkuu kwa kazikubwa anazozifanya na Mheshimiwa Jenister Mhagama naNaibu Waziri wake kwa kazi kubwa wanazofanya usiku namchana kuhakikisha kwamba Watanzania tunapatamaendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kuipongezaSerikali kwa kazi kubwa walioifanya kwa kuimarisha viashiriavya kukua kwa uchumi, hasa kwenye upande wa ujenzi wabarabara. Lengo la Serikali ilikuwa ni kujenga na kukarabatibarabara kilomita 692, lakini tumefanikiwa kukarabati nakujenga barabara kilomita 430 ambayo ni sawa na asilimia62. Naipongeza sana Serikali yangu inayosimamiwa na JohnPombe Magufuli na inayoongozwa na Chama chaMapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongee kidogo kidogo juuya barabara yetu, hasa barabara yetu ya Lupembe. Barabaraya Kibena, Lupembe, Madeke ni miongoni mwa barabarazilizopangwa kutengenezwa kwa kiwango cha lami, mwakajana kwenye Bunge la Bajeti tulipitisha shilingi bilioni nanekwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hii kwa kiwango chalami, mpaka sasa bado tenda ya ujenzi wa barabara hiihaijatangazwa, nimwombe Waziri mwenye dhamana naWaziri Mkuu mwenyewe aliona ile barabara jinsi ilivyo angalautuweze kutangaza tender na ianze kujengwa.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

138

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii ni muhimu sana,ile barabara ya Lupembe kwanza inatuunganisha watu waMkoa wa Njombe na Mkoa wa Morogoro kupitia Jimbo laMlimba. Barabara hii imekuwa ni barabara muhimu ambayowananchi wetu wa Lupembe wanasafirisha mazao yao.Lupembe tunalima chai, Lupembe tunazalisha mbao,tunazalisha nguzo za umeme, tunazalisha maharage,mahindi, viazi na kila aina ya matunda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi ninavyoongeabarabara ile kutokana na mvua zinazoendelea sasa hivihaipitiki tena, imekuwa-blocked, kuna eneo kubwa garizimekuwa zikikwama na hivyo wananchi kupoteza uchumimkubwa sana kwa mazao yao kuozea barabarani kwakutoweza kusafirisha au kupitisha kupitia ile njia, kwa mtindohuo maana yake tunakwamisha uchumi wa wananchi waLupembe. Naiomba Serikali yangu sikivu itenge hizi fedha ilituweze kupata uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tunavyojua Mkoawetu wa Njombe ni moja ya mikoa ambayo tunaitegemeasana katika uzalishaji wa mazao ya chakula, pia nguzo kamanilivyosema na zao hili la chai. Sasa kama tutakuwa badohatuna barabara nzuri, itakuwa ni vigumu wananchiwanazalisha kwa wingi, lakini hawatoweza kuuza au mazaohaya hayataweza kufikia soko kwa sababu barabara yetusiyo nzuri na haipitiki wakati wa kifuku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naombaatakavyokuja kusimama baadaye niweze kujua ni lini sasaSerikali itatangaza tender ili barabara hii ianze kujengwa kwakiwango cha lami kadri ilivyokuwa tumekubaliana katikaIlani yetu ya Chama cha Mapinduzi pia katika bajeti yamwaka jana, kwa hizo fedha tulizotenga bilioni nane.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa kilimo, Mkoawetu wa Njombe ni moja ya mikoa ambayo inategemewasana katika uzalishaji. Mikoa mingine inapopata njaa sisindiyo watu tunaohusika katika kutoa chakula au wananchiwa Njombe ndiyo wanaosambaza chakula katika mikoa

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

139

mingine tukishirikiana na Mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Rukwa.Mikoa hii pia iweze kupewa consideration maalum katikakuhakikisha kwamba tunaipatia kipaumbele hasa kwenyeupande wa pembejeo. Mara nyingi pembejeo zimekuwazikija kwa kuchelewa, zinafika wakati tumepanda, sasa beiyenyewe iko juu, wananchi wetu hawawezi kununua kwabei hiyo kwa sababu kipato chao ni kidogo, tunaomba beiya mbolea ipungue, pia iwahi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Njombe huwatunalima mara mbili, tunalima mwezi wa Sita kwenye bustanibaadaye mwezi wa Kumi tunalima sehemu za milimaniambako kunazalisha magunia ya kutosha au mazao yakutosha. Kwa hiyo, tuombe mbolea zije mapema naikiwezekana zianze kuja mapema mwezi wa Sita ili wananchiwetu waweze kutumia mbolea vizuri na hatimaye wawezekupata mazao vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niongelee zao moja lachai ambalo tunalima hasa maeneo ya Lupembe na maeneoya Luponde. Zao hili limekuwa likiuzwa kwa bei ndogo sanaukilinganisha na gharama za uzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi ukipiga hesabu yambolea inayotumika shambani, kuhudumia ule mmeampaka unapofikia kuanza kutoa chai, kilo moja ya chaiinagharimu takribani shilingi 450 na zaidi, lakini bado tunauzakwa shilingi 250, sielewi ni kwa nini zao hili limekuwa likiachwatofauti na mazao mengine kwa hiyo tuombe wananchi wetuili wasiendelee kuzalisha kwa hasara, angalau tupunguzebaadhi ya kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze Serikalimmeshapunguza tozo la moto na uokoaji, nipongeze sanaSerikali kwa jitihada hizo lakini bado bei ya kuuzia wananchihaijapanda, pamoja na kwamba baadhi ya kodi imepungua,bado bei imebaki palepale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kama kuna kodinyingine ambazo zinafanya hili zao liuzwe kwa bei ndogo

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

140

basi nazo tuziondoe ili waweze kunufaika na kilimo cha chai.Wote tunajua chai tunaitegemea sana hakuna mtu ambayehatumii chai hapa ndani na ni zao ambalo kila mmojalinamgusa hasa kwenye matumizi ya majani ya chai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niipongeze Serikalikwenye upande wa elimu, kwa kutoa elimu bure hasakupeleka fedha kwenye shule zetu za sekondari na msingikwa ajili ya kugharamia elimu bure. Ni kweli kabisa baadaya kuanza kutoa fedha hizi idadi ya wanafunzi wanaoingiadarasa la kwanza imeongezeka, hata watoto wa sekondariwanaoacha yaani drop out zimepungua baada ya kuanzakupeleka hizi fedha. Wazazi wengi walikuwa wakishindwakutoa…

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge upande huu,tuko Bungeni Waheshimiwa. Mtu anacheka kama yukonyumbani kwake. Endelea!

MHE. JORAM I. HONGOLI: Mheshimiwa Mwenyekiti,wazazi wengi walikuwa wanashindwa kulipa hizi ada nahatimaye kuwaondoa watoto shuleni na kuwarudishanyumbani, hasa watoto wa sekondari na shule za msingi,baada ya hii elimu bure tumeona shule nyingi zinakuwa nawatoto wengi pia shule za msingi wanaoingia darasa lakwanza wameongezeka sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tatizo lipo kwenyewalimu wa sayansi, pamoja na kwamba tumeajiri walimuelfu mbili na kitu, tuombe basi hao walimu wasambazwekwenye hizi shule za sekondari ili tuwe na mkakati na ni lazimatuwe na mkakati wa kudumu wa kuhakikisha kwambatunawapata walimu wa sayansi wa kutosha, mkakati huulazima tuanze mapema, tuwe na mkakati wa muda mrefuna wa muda mfupi. Tulichofanya sasa hivi ni kama mudamfupi, ni lazima tuanze kuandaa watu wetu hasa kuanziashule za msingi kupenda masomo ya sayansi na wakiendasekondari wachukue masomo ya sayansi.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

141

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutawezaje kufanya hivi, nilazima sasa kule sekondari tusiweke option, tunapowaambiawatoto wachague kuchukua combination za sayansi aukutosoma hasa chemistry na physics, tunafanya hawa watotosasa waanze kukata tamaa mapema. Hivi sasa ukiendakwenye shule hizi za msingi, ukiuliza mtoto wa darasa la tano,utapenda kusoma masomo gani sekondari, atakwambiamimi nitasoma art. Nataka kuwa Mwanasiasa nataka kuwaMwanasheria, ni lazima tutengeneze mazingira, tuwa-motivate kwa kuhakikisha kwamba watoto wotewanapokwenda kidato cha kwanza…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Kakoso hayupo,Dkt. Kafumu yupo?

MBUNGE FULANI: Yupo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Kafumu.

MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Nianze kwakumshukuru Mungu kwa kupata nafasi hii tena ya kuchangiahoja hii iliyoko mbele yetu ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.Namshukuru sana Waziri Mkuu kwa speech yake nzuri yenyemaelekezo mazuri. Naipongeza Serikali kwa kazi nzurimnazofanya, kazi zenye changamoto nyingi sasa hivi, kwakweli mna changamoto nyingi lakini endeleeni kuzifanya,endeleeni kulisaidia Taifa hili tuweze kufika mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kutoa mchangowangu, naomba nitoe ushauri mdogo, ushauri unaotuhusubaadhi yetu sisi. Tuna bahati nzuri sana katika nchi yetu katikakipindi hiki cha Awamu ya Tano, tumepata Rais mwenye sifakubwa tatu, hizi sifa tulizihitaji muda mrefu. Sifa ya kwanzaana nia thabiti ya kuleta maendeleo kwa wanyonge. Sifa ya

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

142

pili, anaamua papo kwa papo, hacheleweshi na sifa ya tatuanataka watu wafanye kazi, ndiyo maana ya msemo waHapa Kazi Tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sifa hizi baadhi yetutumezitumia vibaya, tumeshindwa kuzitumia kuzi-harness ilinchi yetu isonge mbele. Nasema hivyo kwa sababu baadhiyetu Wabunge wa Upinzani, Chama cha Mapinduzi, baadhiyetu Mawaziri siyo wote na baadhi yetu Wasaidizi wa Raistumeshindwa kusema kweli. Tumeshindwa kushauri kwaukweli, tumekuwa wanafiki, hili jambo litatuua sana, badalaya kutengeneza ushauri uliokamilika, unatengeneza ushaurinusu nusu, unampelekea Rais anaamua palepale unafikirikitatokea nini? Tunahitaji uchambue ushauri wako uupime,uutengeneze uende umekamilika na Rais wetu huyuanayefanya papo kwa papo akiamua nchi inasonga mbele.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi haya yotetunayoyaona ni kwa sababu unafiki umezidi miongonimwetu, nasema kweli. Mimi ni mwathirika wa mambo haya,mtu anaenda kusema anasema Dkt. Kafumu, Kafumu,Kafumu, jambo hili siyo zuri sana. Tumsaidie Rais kusongambele tutafika, tukifanya vinginevyo kwa kweli tutarudinyuma. Ushauri wangu jamani tumsaidie Rais, tumshauritumshike mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Baba wa Taifa aliaminikatika ujamaa lakini waliomzunguka hawakuamini,tumeufikisha ujamaa wapi, Mzee amekufa ameondokaanaamini peke yake na sasa tuna bahati hii, hebu tuitumie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maneno hayo,naomba nitoe mchango wangu sasa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kama ilivyo kwaWabunge wa Tabora nakushukuru sana Mheshimiwa WaziriMkuu, suala la tumbaku lilikuwa linatusumbua kweli lakini

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

143

umelimaliza ahsante sana. Tunakushukuru sana endelea kujaTabora kwa watani zako utusaidie na mambo mengine.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba ya MheshimiwaWaziri Mkuu, Kifungu cha 46 kinazungumzia miundombinu,haya ninayoyasema nayaleta kwa Waziri Mkuu ili anisaidiekumwambia Waziri wa Miundombinu, Wilaya ya Igunga naJimbo la Igunga, tuweze kupata miundombinu, tuwezekupata barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo langu sinabarabara kabisa, unajua ni kwa sababu za kijiolojia. Miaka60,000 Kabla ya Kristo Igunga asilimia 80 ilikuwa ni ziwa naziwa hilo lilipokauka limeacha tope, ukifika Igunga ni mbugaambayo ukitaka kujenga barabara ni lazima uweke tuta zitokubwa la juu. Halmashauri haina uwezo, tunajikuta hatuwezikujenga barabara. Ukikwangua hiyo barabara ni ya kiangazitu, wakati wa masika barabara hakuna kabisa na hasa Jimbola Igunga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Igunga halinabarabara ya TANROADS, kuna kipande cha kilomita nadhanikumi kutoka Itunduru kwenda Igurubi. Hakuna barabara yaTANROADS kwenye Jimbo la Igunga, wakati wa masika lileJimbo halipitiki kabisa. Naleta hili kwa Mheshimiwa WaziriMkuu, uwatume wataalam wakaangalie na hasa wakati wamasika wakienda, hatuwezi kabisa. Mimi huwa sifanyi kaziwakati wa masika, nasubiri kiangazi ndiyo niweze kuwafikiawananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumzia barabaraJimbo la Igunga tunazungumzia, Kata 16 za Wilaya ya Igungaambazo hakuna barabara ya TANROADS na wakati wamasika hakuna barabara. Nataka nizungumze habari zabarabara Wilaya ya Igunga na nimwombe Mheshimiwa WaziriMkuu, anisaidie kabisa ikiwezekana atume wataalamwakatembee sasa Igunga. Kwa kweli hakuna barabara nawale waliofika Igunga waliofanya kampeni wanajua hakunabarabara. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

144

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Mheshimiwatunatumia ‘mapanda ya ng’ombe’, ni njia za ng’ombehatuna barabara kabisa. Wakati wote nimeomba kunabarabara ya kutoka Shinyanga, kupitia Igurubi mpaka Igunga,na inapita inaenda mpaka Loya kwa ndugu yangu Mbungewa Igalula. Hiyo barabara tumeomba ipandishwe hadhimpaka leo angalau tupate barabara moja ambayoitatusaidia kwa ajili ya wananchi wa Igunga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sitaongelea kitu kinginechochote, nataka niongelee barabara tu, namwomba sanaMheshimiwa Waziri Mkuu, tukimaliza Bunge hili, atumewataalam wakaangalie barabara Wilaya ya Igunga hususanJimbo la Igunga. Kwa kweli kuna shida kubwa sana nanitaomba akiwa hapo akimaliza hii nitaenda hapo pembenilabda kesho kutwa niende kumwonesha vizuri MheshimiwaWaziri Mkuu. Naomba sana sitaki kusema mambo menginenasema barabara. Barabara Igunga ni mbaya, barabaraIgunga hakuna, barabara Jimbo la Igunga hakuna kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mliofanya kampeni Upinzanihuku na huku CCM, mliona barabara hamna mapanda duwanasema Wasukuma, kwa hiyo ni kazi kubwa kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nirudie tena,ningeweza kusema mambo mengi, mambo ya maji lakininaomba barabara, hiki ni kilio cha wananchi na najuawanasikiliza, tuna shida kubwa kweli tusaidieni. MheshimiwaWaziri Mkuu, naona majirani zangu wananiambianizungumzie Ziwa Victoria lakini sitaki, naomba barabara,barabara, barabara, barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naombabarabara Mheshimiwa Waziri Mkuu tafadhali sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mipata jiandaeMheshimiwa Ugando.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

145

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,namshukuru Mwenyezi Mungu na nakushukuru wewe kunipanafasi. Naomba nichukue nafasi hii kutoa shukrani za dhatikwa Ofisi ya Spika, Waziri Mkuu, Wabunge wenzangu, kwasalamu za faraja mlizotupatia tulipompoteza Mama yetumwezi wa Pili. Tulipokea msaada mkubwa sana tunashukurusana, hasa ule mfuko wa faraja Mungu awabariki natunamwombea mama yetu apate mapumziko ya milele.Amina.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kabisa kuungamkono hoja na nina sababu; kwanza natambua kazi nzurizinazofanywa na Serikali hii ambazo ni kushughulika namambo mengi ambayo yalisuasua zamani. Tumeonawahenga wanasema kila zama na kitabu chake, ni hakikakitabu cha Awamu ya Tano kitakuwa cha pekee kidogo naupekee wake ni namna Serikali ilivyojipanga kushughulikiamatatizo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona suala la madawatililikuwa sugu mashuleni limepata ufumbuzi wa haraka kabisa.Tumeona ubadhirifu Serikalini umepata ufumbuzi wa harakakabisa ingawaje unaendelea, Utumishi wa Serikali umekuwana nidhamu, uamuzi wa kuhamia Dodoma wa harakakabisa, umesuasua miaka mingi. Tumeona dawa za kulevyazikishughulikiwa kwa haraka. Kwa hakika wananchi waJimbo la Nkasi Kusini wameniambia niunge mkono juhudizote zinazofanywa na Serikali hii kama mabosi wanguwalionileta hapa kuwawakilisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ajenda yetu sasa ni viwandana katika Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ukurasa wa19, Ibara ya 28, imezungumza suala la uchumi wa viwanda.Katika uchumi huu wa viwanda, historia inatuambia mahaliambapo viwanda vilianzia kulikuwa na maandalizi muhimusana kwanza na mojawapo ni elimu. Elimu lazima iwe namsisitizo wa sayansi na teknolojia, masomo ya kisayansilazima yawekewe msisitizo mkubwa.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

146

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ninavyozungumza hapaWilaya yangu ya Nkasi, Walimu wa Sayansi wako 14 tu katikashule 22, kati ya hizo nyingine zina kidato cha kwanza mpakacha sita. Kwa hiyo, hatuwezi kufanikiwa kama walimu wasayansi hatuwapati, walimu wa ufundi hatuwapati, hatuwezi.Kwa hiyo, naomba tuleteeni walimu ili tushiriki katika uchumiambayo ni ajenda yetu ya sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile hatutaweza kufanyavizuri katika kilimo. Kilimo kinahitaji elimu, kilimo kinahitajisayansi na jinsi kilimo kinavyosukumwa katika nchi hii, nikomiaka sita sasa Bungeni, sijaridhika. Naona kilimo kamakinasuasua kila siku, kinaenda ili mradi kiende, wakati kilimomchango wake kwa pato la Taifa ni mkubwa, mchangowake kwa ajira ya Watanzania ni mkubwa na kilimo ndichokitakachoendeleza ajenda hii ya viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika uanzishwaji waviwanda Ulaya, kitu cha kwanza ilikuwa mapinduzi katikakilimo ili kutengeneza ready market. Maana watu wakilimavizuri watakula chakula, watazaliana, watakuwa sasawananunua chakula hicho, bidhaa mtakazozalisha kwenyeviwanda, watakuwa na afya na nguvukazi itakuwepo. Sasakwa nini kilimo kinasuasua miaka yote na kinabeba watuwote wanyonge? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeshauri watuwanaopelekwa kwenye kil imo kusimamia wawewakakamavu na hatua zichukuliwe. Kwa nini mkulima apatembolea kwa kuchelewa? Sababu zinakuwa zinatolewa lakinizote hazitoshi zote. Naomba ufike wakati tuchukue hatuakakamavu, hasa katika suala la ucheleweshaji wapembejeo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mchezo pia katikautoaji wa pembejeo zinakuwa fake, wenzangu wamesema.Mwaka huu mimi ni mmojawapo wa watu walioathirika,nilinunua madawa fake ya kupalilia, ya magugu, jambo hilisi jema sana na wasimamizi mpo, vitu hivi vinarudishawakulima nyuma. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

147

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maeneo ya utafiti wamambo ya kilimo, ukurasa wa 21; Wilaya ya Nkasi tuna Kituocha Utafiti Mirundikwa, hakijasaidiwa vya kutosha, hakinapesa ya kutosha. Naomba tusaidiwe ili tuweze kujitahidikupata mbegu kwa karibu, sasa hivi mbegu tunaagiza njebila sababu za kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni nilikuja hapanikatoa kilio changu juu ya kunyang’anywa Shule yaMirundikwa! Leo hii nipende kuishukuru Serikali, nimepata pesazaidi ya milioni 259 kwa ajili ya kujenga bweni na kuendelezamadarasa. Niikumbushe Serikali, nil isema wakati ulekwamba, miundombinu iliyokuwepo wakati ule ilikuwa nazaidi ya thamani ya milioni 871 kwa mujibu wa Mthamini waSerikali kwa hiyo, bado kuna safari ya kutosha ingawa si haba,lazima tushukuru. Ninaposema Serikali hii ikiambiwa jamboinatekeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nililia hapa kila mtu aliniona,sauti yangu nil i ipaza, nikapata nafasi ya kumwonaMheshimiwa Rais na kumweleza kwa nafasi mbalimbali, lakinisasa napata matokeo chanya. Sasa kwa nini niseme hafanyikazi? Kwa nini niseme hashughulikii matatizo ya wananchi?Nitakuwa mtu wa ajabu sana. Kwa hiyo, anafanya kazi vizurisana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa katikamaeneo niliyoyasema waangalie, Mawaziri watusaidie. Waziriwa Elimu upungufu wa walimu kwangu ni 647, hatunawalimu 647. Upungufu wa nyumba na vyumba vya madarasani 1,100. Upungufu wa nyumba za walimu 900, ni mkoa nawilaya iliyo pembezoni kabisa! Mtutupie macho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho Mji wa Namanyereumeshakua vya kutosha, tunaomba uwe ni Halmashauri yaMji. Mheshimiwa Malocha amekuwa akizungumza upandewake na wenyewe huko. Hiyo inatakiwa iwe wilaya nisehemu kubwa. Mwisho zaidi tunaidai NFRA zaidi ya milioni200 kwenye Halmashauri yetu. Halmashauri yetu sasa haiwezikufanya kazi kwa sababu, mapato hayatoshelezi. Kwa hiyo,

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

148

kama mtatusaidia mtusukumie hili jambo liwezekane iliHalmashauri ipate nguvu na uwezo wa kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niungane na wenzanguwote waliozungumzia juu ya asilimia 10 kwamba, hazitoki.Kama kuna mtu aliziona basi labda ni kwa sababu kwetuhazitoki. Tunaiomba Serikali ihakikishe kwamba asilimia 10zinatoka ili ziende kwa vijana na akinamama kwa mwakahuu. Kwenye bajeti ya mwaka huu zimeingizwa, lakini sasatulikuwa hatuzipati na hatuzipati kwa sababu ya mapatomachache ya Halmashauri, wanaona vipaumbelewanavyokuwanavyo vinawafanya wasizitumie pesa hizikupeleka kwa vijana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikia wanamsifu sanaMheshimiwa Mavunde. Hiyo habari yako ya mikopo kwavijana kuwezesha vikundi mbalimbali kwetu haijafika.Tusaidie au tupe namna ambavyo tutaweza kushiriki twendekwa pamoja na wenzetu ambao wanasifia kwambaunafanya vizuri katika eneo hili. Binafsi, kwangu mimi badoelimu haijafika na vijana wangu wote ni wachapa kaziwanahitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho niongelee sualazima la uchapaji kazi, kama ilivyo Serikalini muangalie nakwenye kilimo. Kilimo, kuna watu wanajiita wakulima, lakinini wazururaji tu na hakuna mtu anayewaangalia! Hili haiwezikutuletea tija! Wasimamizi, hasa watawala, tujitahidikuhakikisha kwamba, kila mtu katika eneo lake aweanafanya kazi inayotambulika na kufanya kazi kwa bidii kwamasaa mengi. Isiwe kama ni ajenda ambayo hainamsimamizi; tutakuwa tunazungumza kila wakati kwambatunaondoka hapa tulipo kiuchumi, kumbe tunafuga watuambao…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Ugando, jiandaeMheshimiwa Yusuf Kaizer Makame.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

149

MHE. ALLY S. UNGANDO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii na mimi leo nichangiehotuba ya Waziri Mkuu. Awali ya yote itabidi kumshukuruMwenyezi Mungu kwa kunipa afya njema ili nichangie hotubahii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naunga mkonohoja kwa asilimia mia moja; sababu, hotuba hii imejalimaslahi ya wananchi wa vipato vya aina zote. Pili, niwezekumshukuru kwa kazi nzuri anayofanya Mheshimiwa WaziriMkuu na Baraza lake kwa ujumla. Hii kauli ya Hapa Kazi kwakweli inaonekana kwa vitendo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya yangu ya Kibititakriban Mawaziri watano wamefika ndani ya mwezi mmoja.Hata wananchi wa Rufiji kwa ujumla wamesema kwa kweliSerikali hii ya Awamu ya Tano inakwenda na wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende sasa katika afya.Nashukuru kwamba Idara ya Afya imetugawia kila kituoshilingi milioni 10 ambazo tumekarabati, kila penye mafanikiohapakosi kuwa na changamoto. Tuna upungufu mkubwawa watumishi katika Idara ya Afya. Kuna baadhi ya zahanatiina watumishi mmoja-mmoja ikiwemo Kiomboni, Kechuru,Msalale…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge, hebu badilisha hiyomicrophone nenda sehemu nyingine.

MBUNGE FULANI: Mwambie ndivyo nilivyo.

MWENYEKITI: Aah ok, basi endelea.

MHE. ALLY S. UNGANDO: Mheshimiwa Mwenyekiti,mimi ndivyo nilivyo. Nikupe taarifa tu nina kigugumizi, ninakilema ambacho amenipa Mwenyezi Mungu, hata hii micukiibadilisha hutaweza kunibadilisha, haya ni maumbilealiyonipa Mwenyezi Mungu. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

150

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niongelee suala lakilimo. Wananchi wangu wa Jimbo la Kibiti bado wanalimakilimo cha Nungu abile, yaani ina maana Mungu yupo, watuwanalima ili kusubiria mvua wakati sasa hali ya hewaimebadilika. Ninachoomba Waziri anayehusika atuleteemiundombinu ya umwagiliaji Kibiti ili wananchi walime kilimochenye tija. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unavyozungumzia kilimochenye tija kwa sisi wananchi wa Kibiti lazima tuzungumziemasuala ya korosho. Korosho bado Chama Kikuu cha Msingikina matatizo, kwa sababu wananchi wanalima korosho zao,wanapopeleka katika hayo masoko bado makato yaoyanachukua muda mrefu katika kulipwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende katika suala zima laelimu. Tunafahamu Serikali yetu imeweka mfumo wa elimubure, lakini kila penye mafanikio hapakosi kuwa nachangamoto, katika Wilaya yangu ya Kibiti kuna upungufumkubwa hasa wa watumishi, majengo na nyumba zawalimu. Kwa hiyo, naiomba Serikali yangu huu ni upungufuiliangalie Kibiti kwa jicho la huruma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Benki ya Maendeleoya Akinamama; sote tunafahamu bila ya akinamamahatuwezi tukasonga mbele. Hawa akinamama lazimatuwaboreshee mazingira yao kwa sababu muda mwingi wanyumbani akinamama ndio wanalea familia. Tuna kilasababu ya kuangalia kwa jicho la huruma ili katika vile vikundivyao wapewe mikopo ya bei nafuu. Jambo la kushangazani kwamba benki hizi zimekaa mijini tu, je, kule vijijini watafikalini ili na kule akinamama wetu wa vijijini nao wakafaidike?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nimalizie na sualala miundombinu kwa sababu, barabara yetu ya Bungulukwenda Nyamisati haipitiki. Tunaomba Mheshimiwa Wazirimwenye dhamana aiangalie barabara hii kwa sababu

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

151

barabara hii inafaidisha wananchi wa Kibiti na wananchiwa Mafia kwa ujumla. Mbali ya barabara upo ujenzi wa Gati– Nyamisati, ujenzi huo wa Gati Nyamisati likirekebishwanaamini kwamba wananchi wa Mafia na wananchi wa Kibitiwatafaidika na gati hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nimalizie kwamba,Wilaya ya Kibiti ina Kata 16, lakini ziko baadhi ya Kata zikoDelta. Kwa hiyo, Delta iangaliwe kwa jicho la huruma kwasababu miundombinu ya Delta siyo rafiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuunga hojaasilimia mia kwa mia. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana kwa mchango mzuri.Mheshimiwa Yussuf Kaizer Machame na Mheshimiwa MbaroukSalim Ally.

MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Kwanza namshukuru MwenyeziMungu, pili nakushukuru wewe kwa kunipa fursa na mimi yakuchangia hotuba hii ya Waziri Mkuu. Kabla ya kusemachochote naomba kwanza niunge mkono Hotuba yaMsemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusiana na Ofisi hii ya WaziriMkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaenda kwenye maeneomatatu mpaka manne. Suala la kwanza nitazungumziamasuala ya general ya Bunge, nitazungumzia unit ya BungeSports, nitazungumzia masuala ya misaada ya Wahisani kwaSerikali ya Tanzania, nitazungumzia Ofisi ya Msajili kwa sababuhii haiwezekani kutokuizungumza kwa yeyote anayesimamaupande huu kwa sasa inavyotekeleza majukumu yake, lakinina nne kama nitapata muda nitazungumza suala lauanzishwaji wa Baraza la Vijana la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwenye issue yaBunge. Mimi ni Mbunge wa awamu ya kwanza hii 2015/2020,

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

152

wakati tunakuja hapa kwenye briefing ya kuapishwa mweziwa Novemba, 2015 nilidhani kwamba Bunge linaloyasemalinayasimamia. Tuliambiwa kwamba issue ya vitabu itakuwamwisho kwenye meza zetu Mkutano ujao kwenye Bunge hilituliloanza. Mwezi Novemba, tuliambiwa maneno hayo naSpika wa Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matarajio yangu nikwamba, sasa hivi sisi tungekuwa tunatumia zile computermpakato. Hizi siyo kwa mantiki ya kujionesha sisi tunatumiani kwa usiri wa siri za Serikali, nyaraka hizi ni muhimu na kilakitu, lakini mpaka leo tunaenda mwaka wa pili, lile nenobaada ya kulisikia kwenye Briefing ya Bunge halijawahikuzungumzwa tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, MheshimiwaWaziri Mkuu atakapokuja kuhitimisha haya makabrashayanajaa humu, hebu tujitahidi basi, kwenye hili atakapokujakuhitimisha atuambie Bunge letu linaenda electronicallytechnological whatever! Atambie tunaenda kwenyecomputer mpakato au tunaendelea na hili mpaka tumalizeBunge hili la 11? Hilo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nataka kuzungumzakwenye maslahi ya Wabunge. Wabunge kituo chao cha kazini Dodoma na ndiyo mmeamua kwamba, kituo cha kazikiwe Dodoma. Wabunge wanapotoka Majimboni wanakujaDodoma asilimia kubwa ya Wabunge ni watu wanaoishikatika hoteli ama Guest hapa Dodoma.

Tunapotoka kuja hapa tunapanga kwenye vyumbavyetu vya hoteli, sasa tukitoka kwenda kukagua miradi yamaendeleo ya Serikali tunakuwa tayari tumepanga kwenyevyumba vya hoteli, lakini bajeti tunayotengewa ni ile ya kukaaDodoma. Kwa hiyo, kimsingi kwenye hili tuache itikadi zetuza vyama na mambo mengine, Mheshimiwa Waziri Mkuu,tunahitaji stahiki za mtu anayetoka kituo chake cha kazikwenda sehemu nyingine. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

153

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa utaratibu tu kwasababu tukienda Geita, huku tuna chumba, kule tunachumba, cost zinaongezeka, otherwise mliangalie kwanamna nyingine suala hili kwa ajili ya Wabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Bunge Sports Club,limeongelewa sana. Tutaliongelea kwa umuhimu wake, hasamwaka huu ambao tutapokea ugeni. Ninayeongea nimchezaji wa Bunge Sports Club wa kutegemewa tena. Sasatuliyoyapata hatutarajii tuyaone tena. Tunakushukuru WaziriMkuu kwamba mambo yetu yamekua vizuri Kurwa ametokakama Doto alivyotoka, lakini ilikuwa ni kusuguana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi ni stahiki zetu kamaWabunge hatuombi. Tunapotoka nje ya nchi ni stahiki zetutunazopaswa kulipwa siyo kwamba ni maombi au ni hurumaya Bunge kutufanyia hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachoomba sasatunapanga bajeti hapa, mara nyingi tukiongea na Spikaanasema bajeti mliipitisha ninyi na nini. Tuliangalie kwa kinasuala la Bunge Sports Club hasa tukitilia umuhimu kwambamwaka huu tutakuwa na ugeni wa East Africa kwenyemashindano hayo ya East Africa, pia Rais wa Jamhuri yaMuungano ndiye Mwenyekiti wa East Africa. Kwa hiyo, itakuwaaibu kuja kuyapata yale tuliyoyakuta Mombasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wengine, walisema akinaMheshimiwa Cosato Chumi hapa kwamba tulikuwatunaingia kwenye magari ya Askari! Wabunge!Wanatushangaa Wakenya, eeh! Wewe Mbunge kweli? Kwahiyo, tunatarajia mambo haya myarekebishe yakae vizuri,kwa sababu tukipata aibu Wabunge wa michezo linapataaibu Bunge na linapata aibu Taifa kimsingi. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

154

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalonilisema nitazungumzia ni suala la misaada. Wakati Serikalihii inaingia madarakani mlikuwa mnazungumza kwa kinakwamba tutaenda kwenye kujitegemea na suala la misaadahalitakuwa muhimu sana kwa Serikali hii. Tumemaliza mwakahuu wa bajeti asilimia 30 ya bajeti ya maendeleo ndioiliyopatikana na sababu zilizoandikwa kwenye mpango nimbili tu; kubwa kwamba kuchelewa kwa mazungumzo yawahisani ambayo kwa kumwambia Mbunge mwenye akilikama mimi hiyo haiingii akilini ndio iliyoandikwa kwenyempango wa bajeti 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kwamba miradi yamaendeleo iliyoandikwa haikukidhi vigezo. Kwa hiyo, ilikuwahaina maana kwangu, sio hoja za kimantiki zinazoingia kwaMbunge; tuangalie kwa kina kwa nini Serikali yetu ilikosamisaada na fedha za bure kama za MCC, za bure kabisa.Tuangalie kwa kina tusitoe hoja dhaifu kama hizi kwenyevitabu vyetu vya maandishi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Msajili; suala la Msajililimezungumzwa vizuri kwenye hiki kitabu cha Bunge chaKamati ya Katiba na Sheria. Hii ni taarifa ya Bunge imeiagizaOfisi ya Msajili ukurasa wa 30 imeiagiza Ofisi ya Msajili kwambaifuate sheria, taratibu na kanuni. Kwa maana ya kwambaBunge limeona kwamba Ofisi ya Msajili inakiuka sheria nataratibu hasa kwenye mgogoro wa Chama cha WananchiCUF na suala la kutolewa kwa ruzuku isiyofuata utaratibu wakiserikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa suala hili limeletamjadala; msidhani kwamba hapa tukijadili tunafurahishana,Watanzania wanaona what is going on kwenye CUF. Huumgogoro wanaujua what is going on, nini kilichopandikizwana nini kinachofanywa. Lipumba humu ana genge lake lawatu wawili tu and we are forty MPs from CUF. Hatuungimkono kwa Lipumba, why tunafanya hivi vitu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hili suala ni lakuangaliwa kwa kina na Ofisi ya Msajili siyo Ofisi ya kutoa

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

155

haki kama mtu amefukuzwa anaenda mahakamani na hukondio kwenye kutoa haki wala hawezi ku… (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Yussuf.Mheshimiwa Mbarouk Salim Ally.

MHE. MBAROUK SALIM ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru…

MWENYEKITI: Jiandae Mheshimiwa Pascal Haonga

MHE. MABROUK SALIM ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa fursa hii. Kwanza nianze kwa kumshukuruMwenyezi Mungu kunijalia fursa hii ya kuweza kuchangiakatika hoja hii ya bajeti ya Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongezekiongozi wangu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF)kwa ziara ambazo anaendelea kuzifanya za kuimarishachama katika visiwa vya Unguja na Pemba na Tanzania kwaujumla. Lakini pia nimpongeze kwa hotuba yake ya tarehetisa pale Lamada hotel Dar es Salaam kwa kweli ilikuwahotuba nzuri sana, nampongeza sana Mwenyezi Munguamjalie na amfanyie wepesi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kusemakwamba Inna-Lillahi Wainna-Ilayhi Rajiun na nasema hivyokwa sababu mwelekeo wa nchi yetu kwa kweli unasikitishasana. Unasikitisha kwa sababu inawezekana tunacheza naMungu; binadamu hatakiwi kucheza na Mungu, tunachezana Mungu na kwa sababu mwanzoni katika kipindi chakampeni tulikuwa tunaomba sana dua tunawaombaWatanzania watuombee dua na Watanzania wamefanyahivyo na viongozi wa dini wote wamefanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa unapomwombaMwenyezi Mungu akusaidie na akakusaidia, lakini badalayake ukarudi sasa ukafanya mambo ya kimaajabu ajabu yakutesa watu, kunyanyasa watu na kudhulumu watu kwa kweli

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

156

hapo Mwenyezi Mungu anakuwa hayupo. Kwa hiyo, hilijambo la kucheza na Mungu ni baya sana na hil ihalitotupeleka pazuri Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndio maana kwambahakuna linalokwenda, hali ya uchumi ni mbaya, hakuna ajira,kila linalopangwa halienda na hapa tulifanya fanya tu kidogokwa sababu kulikuwa na pesa za kuokota za madawati ndioikaonekana kwamba tulijitahidi tukafanya kidogo lakinihakuna lolote ambalo linafanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye issue yaMuungano; Waziri Mkuu katika hotuba yake amesifu sanavikao vinavyofanyika baina ya SMT na SMZ kuhusu kero zaMuungano. Niseme tu kwamba kwa kweli tumechoka nakuona idadi ya vikao; wananchi wameona idadi ya vikaovinavyofanyika baina ya SMT na SMZ lakini hatuoni matokeo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu Muungano sio waviongozi, sio wa Mawaziri; waasisi wa Muungano walikusudiakwamba Muungano ni wa watu wa Zanzibar na watu waTanganyika. Sasa inapotokea kwamba kuna vikao vinakaalakini haijulikani linalotatuliwa wala linalozungumzwa hilo nitatizo na hatuwezi tukaenda hivyo kwa sababu kero zipo palepale. Kila siku vikao 13, 16, 20 lakini huoni jambo ambalolinatatuliwa, kwa hiyo hili ni tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kusikitisha zaidi ni kwambahata zile mamlaka ambazo zinahusika na zile kero ukiendawanakwambia sisi hatujui, kama wametatua, wametatuawao juu. Sasa wanasiasa tunatatua kero lakini watendajihawajui; kwa hiyo kero zinabaki zipo pale pale. Kwa hiyo, hilikwa kweli halitendeki vizuri hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonataka nilizungumzie ni kuhusu Msajili. Kwa kweli hatuwezikuidhinisha pesa kwa ajili ya kwenda kufanya au kutumia mtuanavyotaka. Kama hatukupata maelezo mazuri ya Ofisi yaWaziri Mku ya pesa milioni 369 zilivyotumika kwa kweli hapa

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

157

patachimbika, hatuwezi kuruhusu hiyo kitu, kwa sababutunakaa hapa tunaidhinisha pesa kwa matumizi ambayotunakubaliana halafu anatokea mtu tu wakati yeyemwenyewe ameshaandika barua kumpelekea Katibu Mkuuwa CUF kwamba Chama cha Wananchi CUF kwa sababuya mgogoro tunakizuia ruzuku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa iweje tena urudiuipitishe ruzuku kwa mtu ambaye ameshafukuzwa, siomwanachama lakini pia ruzuku hiyo hiyo ikatembea mpakakwenye akaunti za watu binafsi, hatuwezi kufanya upumbavuwa aina hiyo. Kwa kweli hatukubali; hii ni lazima tupatemaelezo ya kutosha na vinginevyo hatuwezi kupitisha hiibajeti, lazima pachimbike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonataka nilizungumzie ni kuhusu Mfuko wa Jimbo hususan kwasisi Wazanzibari. Pamoja na kwamba Mfuko wa Jimbo badopesa ni ndogo sana yaani pesa ambazo zilikuwa zinatolewakwa idadi ya watu kidogo sana ndio zile zile mpaka leohaubadiliki; nafikiri kuna mjumbe mwenzangu aliwahi kusemahilo. Lakini tatizo kubwa la Zanzibar hizi pesa zinachelewasana; ile Serikali yenu ya Zanzibar inazikopa pesa kwa shereheza Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kila zikitolewa Disembawanazichelewesha mpaka Juni ndio pesa tunazipata.Tunashindwa kufanya mambo ambayo tumeahidi kufanyasasa naomba patafutwe utatuzi wa tatizo hilo, sio mara mojamara mbili wala mara tatu, kila siku pesa hizi zinachelewa.Wenzetu huku wanatumia pesa wanamaliza sisi bado kuletunaulizia kila siku; tumechoka kuja kuulizia pesa hii. Hili jambohebu litafutiwe ufumbuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, natakanizungumzie kidogo kuhusu Bandari ya Wete. Bandari ya Wetepana kaofisi kidogo kabanda tu; hicho hicho wanatumiawavuvi na hilo hilo wanatumia wasafiri na hilo hilo wanatumiaOfisi ya Uhamiaji. Kwa kifupi ni kwamba pale pana movementkubwa sana ya wasafiri baina ya Pemba na Mombasa Kenya

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

158

lakini kuna tatizo kubwa hakuna Ofisi ya Uhamiaji, forodhawala Ofisi yoyote. Kwa hivyo, inawezekana kuna upotevumkubwa wa mapato. Namwomba Waziri Mkuu hili jambotuliangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika awamu iliyopitailisemekana kwamba pesa za ujenzi wa Ofisi pale tayarizilishatoka kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini lakusikitisha mpaka leo hatujaona lolote ambalo limetendeka.Hili Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba tulipatie majibu sijuilimefikia wapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Pascal Haonga,ajiandae Mheshimiwa Sokombi.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Naomba kuchangia hii hotuba ya Waziri Mkuu.Awali ya yote niweze kwanza kumpongeza Rais mpya waTLS ndugu yangu Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu kwakuchaguliwa kwa kura nyingi sana. Kwa hiyo, pongezi sanajapokuwa mchakato huu ndugu yangu Mwakyembe alitakakuingilia, bahati mbaya akawa amelemewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuzungumza hayonaomba sasa niweze kujikita kwenye hotuba ya Waziri Mkuuna naomba nianze na suala moja la wakulima wa zao lakahawa. Mheshimiwa Waziri Mkuu wakati yupo kule kusinialifanya mambo mazuri sana kwenye suala la watu wakorosho akapunguza tozo kwenye korosho na mambo mengisana, lakini kiukweli kabisa amewasahau wakulima wa zaola kahawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wa Mbozi pamoja naMkoa wa Songwe na Mikoa yote ya Kanda ya Nyanda zaJuu Kusini wanaolima kahawa wana maeneo menginewanasema kwamba kama Waziri Mkuu hatapunguza tozona kodi kwenye zao la kahawa maana yake Waziri Mkuuatakuwa ameonesha upendeleo wa hali ya juu sana na

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

159

atakuwa amefanya ubaguzi ambao kwa kweli hatutegemeikuuona. Wao pia wanasema kwamba amefanya hivyo kwasababu kule ni nyumbani kwao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa wakulima wa zao lakahawa wanasema kwamba wanategemea kusikiaatakapokuwa anahitimisha na hapa nimepokea meseji kama200 hivi kutoka Jimboni kwangu; wanategemea kusikiaanapunguza kodi na tozo mbalimbali kwenye zao la kahawa.Zipo tozo nyingi sana; kuna ushuru Bodi ya Kahawa, iko tozokwenye TaCRI na iko tozo kwenye Halmashauri kule asilimia0.5.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo wanaombatafadhali suala hil i Mheshimiwa Waziri Mkuu awezekulichukulia kwa umakini sana maana kule kwake nadhaniameshamaliza sijui ndio alikuwa anatengeneza mazingiralakini kwa kusema ule ukweli kwenye mazao mengine kamakahawa nahitaji kuona anapunguza tozo na kodi mbalimbalikwenye zao la kahawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kwetu Mbozi kahawandio dhahabu yetu; kahawa ndio kila kitu, mtotoanapokwenda shule lazima unaangalia kwenye kahawa namtoto anapotaka kuoa unaangalia kwenye shamba lakahawa, kila kitu kahawa. Kwa hiyo, tafadhali suala hili ajaribukuliangalia Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu wakulimawetu wa kahawa sasa wamefika mahali wamekata tamaana wameanza kung’oa miche ya kahawa kwa sababu beikwanza ni ndogo na hizo tozo na kodi zimekuwa nyingi hivyowanategemea atatoa majibu mazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuukama hatozungumza lolote kuhusu kahawa mimi naWabunge wengine tunaotoka kwenye Majimbo na maeneowanayolima kahawa tutahamasishana kuwaleta wote hapaDodoma ili waje kupewa majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine naombakuzungumzia kidogo suala la maafa amegusa kwenye

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

160

ukurasa wa 48. Suala la maafa tunajua ndugu zetu wa paleBukoba tetemeko lilitokea wakapata matatizo makubwasana. Cha kusikitisha Rais wa nchi hii amechukua muda mrefukwenda pale kuwafariji wananchi wale. Kibaya zaidi zipofedha ambazo zilichangwa bilioni sita kutoka EU na lakini zikopesa ambazo tulikatwa hapa Bungeni kwa ajili ya ndugu zetuwa Bukoba, hizi pesa zimeliwa Mheshimiwa Waziri Mkuu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatujui hatujaambiwa hadileo lakini inaonekana fedha hizi zimepigwa. Tulifanya mechipale Dar es Salaam uwanja wa Taifa; Wabunge tumechezamechi hadi miguu imeuma, tumepata zaidi ya milioni miambili na kitu pesa hizi zinaonekana kama mmeshazipiga. Sasahatujui kwa nini watu wanapata matatizo badala ya Serikalikuchukua fedha zile kuwasaidia, mnaamua kuzitumiakinyume na matarajio, kinyume na ile kazi ambayo tulikuwatunategemea zifanye. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunategemea kabisakwamba pale wananchi wanapopata matatizo, Rais wanchi, Serikali iweze kutoa lugha nzuri. Leo kama Rais wa nchianasema mimi sikuleta tetemeko, hatutawasaidia chakulaina maana kwamba Taifa hili tumekosa Rais. Nadhani sualahili tujaribu kuliangalia sana. Naomba niwe muwazi kabisakwamba Rais wetu lugha anazozitoa watu wanapopatamatatizo…

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusuutaratibu.

MWENYEKITI: utaratibu

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Hujaruhusiwa naombaukae Simbachawene kwa sababu hujaruhusiwa. (Kicheko/Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

161

MWENYEKITI: Ameruhusiwa, Mheshimiwa Pascal kaachini.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Simbachawenetumeambiwa tusiingiliane, naomba ukae basi hujaruhusiwa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Pascal kaa chini.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafahamukwamba Mbunge anaeongea ni Mbunge mgeni na kwahivyo anaweza akawa hazifahamu vizuri kanuni. Kanuniinasema haturuhusiwi humu ndani na naomba niinukuuhaturuhusiwi humu ndani kuzungumzia mwenendo wa watufulani fulani. Sasa naomba nisome ile kanuni aliyoivunja katikakifungu cha 64 cha kanuni zetu inasema

“Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 100, ibarainayolinda na kuhifadhi uhuru na mawazo au majadilianokatika Bunge:-

(e) Mbunge hatazungumzia mwenendo wa Rais,Spika, Mbunge, Jaji, Hakimu au mtu mwingine yeyoteanayeshughulikia utoaji wa haki isipokuwa tu kamakumetolewa hoja mahsusi kuhusu jambo husika.” (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kanuni hii iko very clear;tukitaka tuzungumzie personality huruma ya mtu, tukitakatuzungumzie namna mtu anavyofanya mambo, tunakuwatunaingilia uhuru wa watu wengine pia na kanuni hiiinakukataza hivyo hata kwa Mbunge mwenzio. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Kwa sababu hiyo basi namwombaMheshimiwa…

MWENYEKITI: Amekuelewa ahsante.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

162

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Bado sijamazilia na kwa sababu hiyobasi namwomba Mheshimiwa Mbunge aondoe manenohayo katika kauli yake.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,anatumalizia muda wetu naomba akae tu.

MWENYEKITI: Mheshimwa Pascal kama ni Mbungemgeni hujui kanuni…

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Nimeshakuwa mwenyejitayari maana yake ni muda mrefu sasa…

MWENYEKITI: Nimeshaelewa sasa hiyo ni kadi ya njanoumepewa, tuendelee.

MHE.PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba niseme tu kwamba, mara ya kwanza ulisema kuwahutatoa taarifa yoyote ila nasikitika umetoa taarifa kwa huyobwana. Labda inawezekana il ikuwa kasoro kwaSimbachawene tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo nil i lokuwanalizungumza hapa ni kwamba watu wanapopata matatizowananchi wakipata maafa, Serikali inatakiwa ikae karibu nawananchi. Sasa kama Serikali fedha zinachangwa inafikamahali fedha zile zinatumika kinyume ni lazima tuhoji, lazimatuulize. Sasa leo hii tusipouliza unategemea nani atauliza sualahili sisi ndio tunaowakilisha wananchi; tumekaa hapa huu nimkutano wa hadhara wa wananchi nchi nzima hawawezikukusanyika wote hapa. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

163

TAARIFA

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa!

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa nchi.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nimpe Taarifa Mheshimiwa Mbunge,mimi ni Waziri ambaye nasimamia masuala ya maafa nchini.Si kweli kwamba fedha tulizozipokea kutoka Ubalozi waUingereza fedha zile zimeliwa na Serikali, hiyo sio kweli nafedha zile zimetumika kujenga Shule ya Sekondari ya Ihungona akienda leo na nitakapokuwa nahitimisha hoja hiiMheshimiwa Waziri Mkuu na Ofisi yake tutawaeleza Wabungekazi nzuri iliyofanywa na Serikali katika kurudisha miundombinuya Serikali katika Mkoa wa Kagera. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naombaMheshimiwa Mbunge kama hana taarifa za matumizi yafedha hizo asifanye generalization kwamba fedha hizozimeliwa na Serikali, taarifa hiyo sio sahihi na Serikali haijalafedha hizo na kazi iliyofanyika kule imefanyika na inaonekana.Kwa hiyo naomba kumpa taarifa Mheshimiwa Mbungeasipotoshe umma wa Watanzania kwamba fedha hizozimeliwa na Serikali. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante!

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Kuhusu utaratibu!

MWENYEKITI: Mheshimiwa, no research, no right tospeak.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Kuhusu utaratibu!

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mchungaji Msigwa!

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

164

KUHUSU UTARATIBU

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Mheshimiwa Simbachawene amesoma Ibaraya 64 kuhusu suala la kujadili mwenendo wa Rais, lakini kamawote tunavyojua, kipengele alichokisoma kinazungumzakwamba bila kuathiri Ibara husika ya uhuru wa mawazo,Katiba iko juu inayompa uhuru mwananchi wa Tanzaniakuzungumza bila kubugudhiwa na mtu yeyote. Kipengeleanachokisema kinaeleza wazi, bila kuathiri Katiba mama,uhuru wa mawazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo anachozungumzahuyu haathiri uhuru wake wa kujadili mawazo, kwa hiyokipengele alichosema Mheshimiwa Simbachawenekinatufunga kwenye Katiba mama ambayo inaturuhusukujadili na anachokijadili ni kujadili maendeleo ya nchi na sisindio wawakilishi wa wananchi. Kama kiongozi hafanyi vizuri,tuna haki ya kujadili na ndiyo uhuru tunaopewa. Kwa hiyonaona anapotosha Bunge kwa kusema kile kipengelekinatuzuia… (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mchungaji Msigwa kaachini, Mheshimiwa Simbachawene kaa chini, MheshimiwaPascal endelea. (Makofi)

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba uweze kulinda muda wangu na najua bado ninadakika kama saba hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa niendekuzungumzia suala lingine, suala ambalo Waziri Mkuuamelizungumzia kwenye ukurasa ule wa 11 kuhusu kufanyasiasa za kutuunganisha badala ya kufanya siasa za kutugawa.Naomba sitanukuu sana kile alichokisoma pale Waziri Mkuu,naomba niseme tu kwamba nchi yetu ilipofikia siasa zakuwagawa Watanzania zimeasisiwa na Mwenyekiti wa CCMTaifa.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

165

Mheshimiwa Mwenyekiti, siasa hizi zimeasisiwa juzijuzihapa kwenye vyombo vya habari, imeripotiwa tu Mwenyekitiwa CCM Taifa anasema kwamba Wabunge wa Chama chaMapinduzi ni marufuku kwenda kumwona Mbunge mwenzaoMheshimiwa Godbless Lema aliyekuwa amewekwa ndani.Siasa hizi za kutugawa Watanzania…

TAARIFA

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, Taarifa!

MHE. PASCAL Y. HAONGA: …Ni siasa ambazo kwakweli tukiziangalia hazitufikishi popote pale.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Pascal, kaa chini.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nimpe Taarifa Mheshimiwa Mbunge,anachotaka kufanya hapa ni kucheza na lugha za kisiasakuwapotosha tu Watanzania kwenye manenoanayoyasema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpe taarifaMheshimiwa Mbunge; Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzianayo nafasi yake ya kukaa na Wabunge wake wa Chamacha Mapinduzi wakati wowote lakini atakayetoa taarifa zamjadala wa kikao cha Mwenyekiti wa Chama na Wabungewake wa chama ni mamlaka zinazohusika ndani ya caucusya Wabunge wa Chama cha Mapinduzi na sio mtu mwingineyeyote. Sasa naomba nimpe Taarifa Mheshimiwa Mbungehayo aliyoyachukua huko sisi hatuyajui na asituletee humundani… (Makofi)

MHE. ESTER A. BULAYA: Taarifa!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: Kama ni

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

166

mambo ambayo yalijadiliwa na Mwenyekiti wa Chama chaMapinduzi na Wabunge wa Chama cha Mapinduzi. Kwa hiyonaomba kumpa Taarifa, tunaendelea kuwa na vikao vyetu…

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Taarifa!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: …lakini vikaovyetu vya kikanuni ambavyo vinakidhi maslahi ya Wabungewa chama na maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania yakutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Pascal…

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Taarifa!

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bulaya, kaa kwanza. KaaMheshimiwa Bulaya. Mheshimiwa Bulaya unadharaumamlaka ya Kiti?

Mheshimiwa Haonga, kuna hoja muhimu sana mbeleyetu ya maendeleo ya wananchi ambayo yanafanywa vizurisana na Serikali hii. Wewe ni wajibu wako kuhoji maji,barabara, shule kwenye kambi yako…

WABUNGE FULANI: Aaaah!

MWENYEKITI: …unapotaka kuleta mambo ambayohuyajui, unapotaka kuleta mambo ya vyama vingineambavyo wewe si mjumbe wa vyama hivyo na unapotakakuleta mambo ya mitaani ambayo humu ndani hamnautajitia katika matatizo makubwa sana. Nakuomba,umesamehewa mara ya kwanza kwa sababu ni Mbungemgeni, wakilisha wananchi wako kwa hoja za msingi zamaendeleo ya jimbo lako. Mambo ambayo hayakuhusuyaache hukohuko yalipo. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

167

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba ulinde muda wangu na naomba niseme kwambaninachochangia hapa sichangii kitu ambacho hakipo,nachangia Hotuba ya Waziri Mkuu ukurasa wa 11.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba wale ambaolabda hawajasoma hotuba hii vizuri wangepata mudawaweze kusoma vizuri, hapa kwenye ukurasa wa 11amezungumza vizuri sana Waziri Mkuu, kwamba tufanye siasaza kutuunganisha badala ya kufanya siasa za kutugawa nanilichokizungumza mimi, siku ambayo Mwenyekiti wa CCMTaifa amewaasa baadhi ya Wabunge wasiendekumtembelea Mbunge mwenzao vyombo vya habarivilitangaza, magazeti yaliandika, Kituo cha Utangazaji chaTBC kilitangaza, ITV walitangaza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sasa nashangaa sana,labda inawezekana kuna wengine ambao inawezekanahawafuatilii vyombo vya habari, labda hawajasoma naHotuba ya Waziri Mkuu. Kwa hiyo, naomba tafadhali usiingiekwenye mtego, hii Hotuba ya Waziri Mkuu naichangia vizurisana, hii ninayo hapa, ni ukurasa ule wa 11. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine naombanizungumze; wapo ndugu zetu wengi ambao walifukuzwasiku za hivi karibuni Msumbiji, Mheshimiwa Waziri Mkuunadhani anakumbuka na Wabunge wote mnakumbukakwenye Bunge hili. Wale Watanzania wamefukuzwa Msumbijiwamepelekwa mpakani pale wengine wamepoteza maisha,wengine wamebakwa. Rais wa nchi, naomba niseme tukwamba kiongozi mkuu wa nchi, maana yake mmesematusimtajetaje, sijajua tatizo ni nini, anasema kwambawalikwenda kwa njia za panya warudi kwa njia za panya.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunategemea viongoziwetu, watu wetu wanapopata matatizo tuwe wa kwanzakwenda kuwasaidia, tuwe wa kwanza kwenda kuwatia

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

168

moyo. Watanzania wengi wanaoondoka nchini hawaendinchi za huko mbali kwa ajili ya kwenda kutalii, wanatafutamaisha, wanatafuta fursa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkuu wa mkoa alipojaribukupeleka hata gari lile la jeshi kwenda kuwabeba wale watualikatazwa akaambiwa kwamba usiwabebe, waache kamawalivyo, walikwenda kwa njia za panya warudi kwa njia zapanya. Suala hili kwa kweli linasikitisha sana na kwa jinsi haliilivyo kwenye nchi yetu kama tutaendelea kwenda hivi, miminaamini kabisa kwamba tutakuwa hatuwatendei hakiWatanzania ambao wametuchagua sisi Wabunge naambao wamemchagua Rais wa Jamhuri wa Muungano waTanzania na ambao wametuchagua sisi wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naomba tukwamba ifike mahali sisi viongozi ambao ndio tumaini laWatanzania tufanye kazi ya kuwawakilisha wananchi wetuvizuri na tufanye kazi ya kuwatetea, tufanye kazi yakuwasemea, lakini inapofika mahali unasema kwambasikuwatuma mimi kwa kweli hatuwatendei haki hata kidogo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumze sualalingine ambalo linapatikana ukurasa ule wa 21 wa Hotubaya Waziri Mkuu kuhusu ziada ya chakula ambayoameizungumza kwenye hotuba hii. Mheshimiwa Waziri Mkuuanafahamu yeye na Wabunge wote wanafahamu kwambatakribani halmashauri 55 zina tatizo la njaa japokuwa sasahatujaambiwa, hatujaletewa taarifa rasmi Bungeni kwambakwa sasa tumefikia wapi, lakini taarifa iliyokuwepo siku zanyuma ni kwamba halmashauri 55 zina njaa. Imefika mahalitunaambiwa kwamba chakula hakitapelekwa, sasa watuwaliotuchagua leo tu…

MWENYEKITI: Nakuongeza dakika moja!

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante, dakika zangu nadhani umenipunja kidogo.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

169

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo natakanizungumze tu kwamba sasa tuulize, wakati Watanzaniawanapata njaa kipindi cha Nyerere alikipata wapi chakulacha kuwapelekea, wakati Watanzania wamepata njaakipindi cha Mkapa, kipindi cha Mwinyi, kipindi cha Kikwete,chakula kilitoka wapi na hii Serikali leo kwa nini inashindwakuwapelekea Watanzania chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo hili la njaa halinabaunsa, mtu yeyote anaweza akapata njaa kutokana nakwamba inaweza kuwa mvua labda haijanyesha, kumetokeaukame, kumetokea matatizo mbalimbali, sasa leo Serikaliinasema kwamba sisi hatutapeleka chakula kwenye maeneoya njaa, hii ni fedheha kubwa sana kwa Taifa letu na nina…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Sokombi, jiandaeMheshimiwa Chegeni, Mheshimiwa Mayenga, MheshimiwaAlly Keissy, Mheshimiwa Bashungwa.

Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla, please kaa chini.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa, kuhusuutaratibu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kigwangalla, please kaachini.

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Kwanza kabisa nipende kumshukuru MwenyeziMungu, pili nipende kumshukuru pia Mwenyekiti wangu waChama cha CHADEMA na nipende kumpongeza kwa hotubayake nzuri iliyoletwa hapa Bungeni yenye kuonesha dira namdororo wa uchumi wa Tanzania juu ya bajeti yetu iliyoletwahapa Bungeni. Bajeti iliyoletwa hapa Bungeni ni bajeti hewa,na nitaendelea kusema kwamba ni bajeti hewa. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

170

Mheshimiwa Mwenyekiti, nayasema haya kwa sababumoja. Ukiangalia Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani ukurasawa 35, kwenye Wizara ya Kilimo, zimetengwa asilimia 2.22,Wizara ya Viwanda na Biashara imetengwa asilimia nane,Wizara ya Afya asilimia 25. Mheshimiwa Waziri Mkuu, hii asilimia25 unazipenda kweli afya za Watanzania, maana hii asilimia25 ndiyo imebeba maisha ya afya zote za Watanzania juu yamatibabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nianze kwa kuchangiajuu ya hii Wizara ya Afya; Serikali ya CCM iliahidi kujengazahanati kwenye kila kijiji na kata na vituo vya afya. Swali lakujiuliza; kwa bajeti hii ya asilimia 25 fedha hizi zitakidhi kwelivigezo vya afya katika Tanzania yetu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikienda katika Mkoawangu wa Mara, Hospitali ya Mkoa wa Mara ni jambo lakusikitisha na ni aibu, tena mahali ambapo anatoka Babawa Taifa, hospitali haina hadhi kwamba ni hospitali ya mkoa.Mfano mdogo, CT scan, ile hospitali haina CT scan na mtuakitaka kufanyiwa hicho kipimo ni mpaka wampe rufaakwenda Bugando, Mwanza na Bugando hiki kipimo hakipo,hakipo Bugando wala Sekou Toure, ni aibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipimo cha CT scan kipokwenye hospitali moja tu tena ni dispensary ya mtu binafsi,inakuwaje mtu binafsi anaweza kununua hii mashine lakiniSerikali inashindwa, ni jambo la kujiuliza na ni jambo lakusikitisha. Pia wanapokwenda kufanya hicho kipimo kwenyehiyo dispensary gharama yake ni kuanzia 290,000 kuendelea,je, mwananchi mwenye kipato cha chini hiyo 290,000 ataitoawapi? Moja kwa moja inaonesha kwamba Serikali haina nianzuri juu ya afya ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakwenda katika Hospitaliya Wilaya ya Bunda. Hospitali hii ni hospitali inayohudumiawilaya tatu, lakini ile hospitali imeandikwa Hospitali ya Wilayaya Bunda lakini yale madawa yanayopelekwa pale ni ya kituocha afya. Hakuna madaktari bingwa kisa tu hakuna mortuary.Ndugu zangu tambueni zile wilaya tatu ni wilaya zenye

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

171

wananchi wengi na hakikisheni kwamba msipoiweka katikahadhi nzuri ile Hospitali ya Bunda mnahatarisha maisha yawatu wa Mwibara, Musoma Vijijini na Bunda yenyewe na uzuriMheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, MheshimiwaBulaya ameshalisemea sana suala la Hospitali ya Wilaya yaBunda. Kwa hiyo basi, ninachoomba, Serikali iseme kwambani lini itaipa hadhi Hospitali hiyo ya Wilaya ya Bunda iliwananchi wa Wilaya ya Bunda na wao wawe na hali nzurikwa kuona kwamba wilaya yao ina hospitali ya wilaya,inaleta sifa pia kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitazungumzia kuhusiana nasuala la maji Bunda; sasa hivi ni takribani miaka 10 Wilaya yaBunda kila siku wanasema maji yataletwa matokeo yakempaka sasa maji bado hayajaletwa. Kila siku mnasemachujio, hilo chujio litatengenezwa lini ili wananchi wa Bundawapate maji salama. Tunaomba mradi wa maji Bundaukamilike ili wananchi wale na hasa upande wa akinamama,akinamama wanateseka sana Mheshimiwa Waziri Mkuu,kwenda kuhangaika kutafuta maji na wakati maji yapo shidani chujio. Kwa hiyo, tunachohitaji Wilaya ya Bunda inahitajiipate maji salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaenda upande wa elimubure. Naomba tu niseme ukweli, mshaurini tu MheshimiwaMtukufu kwamba hili suala tayari sasa hivi limeshashindikanaili liwe wazi kwa wananchi na ikiwezekana pia aombe tumsamaha kwa wananchi kwamba hil i sualalimeshashindikana ili wananchi wenyewe waweze kuchangiakusomesha watoto wao. (Makofi)

TAARIFA

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa!

MWENYEKITI: Taarifa!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasimama

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

172

kutoa Taarifa kwa sababu ya aina ya maneno yanayotumika.Naomba tu nimuarifu mzungumzaji kwamba Serikali inatengashilingi bilioni 22.5 kila mwezi kwa ajili ya kulipia mitihani, kwaajili ya kulipia uendeshaji wa shule, kwa ajili ya kulipia mambomadogomadogo yanayotumika pale katika shule kwa ajiliya uendeshaji.

Pia Serikali kupitia makubaliano iliyofanya na Chamacha Walimu Tanzania na mapendekezo yakawa tutoe poshoya madaraka, tunatoa shilingi 200,000 kwa kila mratibu waelimu kata, mwalimu mkuu na wakuu wa shule, shilingi 200,000.Hata hivyo, kupitia uandikishaji ambao sasa hivi wazazihawatoi gharama yoyote katika kuandikisha watoto,tumeweza kuandikisha watoto wengi mara mbili ya waletuliokuwa tumewatarajia, matarajio ilikuwa tuandikishe750,000 tumeandikisha 1,849,000… (Makofi)

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, Taarifa!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: …idadi hii inatokana na utaratibu waelimu…

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, Taarifa!

MWENYEKITI: Hebu kaa chini kwanza.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: …hakuna Taarifa juu ya Taarifa mzee…

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, Taarifa!

MWENYEKITI: Hapana, kaa chini, hebu kaa chinikwanza.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

173

nataka tu tuwe wakweli, dhana na kufikiri kwamba elimubure basi wazazi wasifanye chochote hata watoto waowasiwanunulie uniform, watoto wao watakula hukohukoshuleni, watapata kila kitu shuleni inakuzwa na wenzetu wasiona nia njema na jambo hili, lakini suala la elimu bila malipolimesaidia sana nchi hii na watoto wengi wamekwenda shulena wazazi wengi wamepata nafuu hiyo. (Makofi)

MWENYEKITI: Hapana! Waheshimiwa…

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, Taarifa!

MWENYEKITI: Hapana, hebu kaeni chini, subirini. Hebukaa chini…

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, anapotosha.

MWENYEKITI: Kaa chini, na wewe kaa chini.Niliyemsimamisha ndiye mwenye instrument ya elimu.Mheshimiwa Matiko kaa chini! Nimemsimamisha Wazirimwenye instrument, mnatakiwa mjenge hoja, Serikali inalipazaidi ya mabilioni every month na pesa zinakwenda shulenizinafika na kama una mchango wa ziada changia kwamaandishi na utajibiwa na sekta inayohusika. (Makofi)

Mheshimiwa Sokombi, endelea.

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru lakini sitaipokea kwa sababu najua Waziri Mkuuatakuja kujibu hoja, tuseme tu ukweli elimu sio bure,Mheshimiwa Simbachawene.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaenda upande wa hilisuala lililopo Tanzania sasa hivi, ni hali ya kutisha hili suala lautekaji. (Makofi)

Mheshimwa Mwenyekiti, kusema ukweli…

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

174

MWENYEKITI: Vipi umeishiwa? (Kicheko)

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Siwezi kuishiwa na badonaendelea.

MWENYEKITI: Tuendelee!

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti,suala la utekaji kwa kweli ni suala ambalo linatisha juu yamaisha yetu na juu ya maisha ya Watanzania. Kila mtuanasimama hapa anaongelea juu ya utekaji, naomba wewekama Mwenyekiti uliyekalia hiki kiti hapo mjiulize ni kwa ninikila mtu anasimama na kuongelea suala la utekaji? HalafuWaziri mwenye dhamana, Waziri Mkuu hajatamka kituchochote mpaka dakika hii, kusema ukweli inasikitisha na nijambo la aibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachoomba, BenSaanane amepotea ni muda mrefu sasa umepita, Serikaliimekaa kimya. Msanii Roma alitekwa lakini cha ajabu yulemtu kapatikana kwenda kujieleza matokeo yake Waziri waMichezo eti anamsindikiza, unategemea yule msaniiataongea kitu gani cha ukweli? Ina maana Serikali inajua nikitu gani kilicho nyuma yake.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Chegeni,Mheshimiwa Mayenga, Mheshimiwa Ally Keissy, MheshimiwaBashungwa.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana nami napenda kuunga mkonohotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu jinsi ambavyo amewezakuiwasilisha nikiangalia inakidhi kwa kiwango kikubwamahitaji ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni rahisi sana kukosoa lakininaomba niwarejeshe Watanzania na Waheshimiwa

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

175

Wabunge wenzangu kwamba ukiangalia Serikali ya Awamuya Tano, kwa muda mfupi imefanya mambo mengi namakubwa kwa Watanzania. Tukikumbuka kwamba Serikaliya Awamu ya tano imeingia ikirithi madeni ya awamu iliyopitakitu ambacho ukikiangalia na hata katika maelezo yampango wa Waziri wa fedha, sasa hivi tunalipia karibu trilionimoja, deni la Taifa kwa kila mwezi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ukiangalia kwambaMheshimiwa Rais pamoja na ubinadamu wake hebu tumpesifa kwa kile anachokifanya kwa ajili ya Watanzania natumuunge mkono kama Watanzania na kama WaheshimiwaWabunge ndani ya Bunge hili. Nchi hii tunaiongoza sisi sote,sitegemei kwamba kwa vile uko upande mmoja wewe nikusema mabaya siku zote. Hebu tuwajenge Watanzaniawajue kwamba chombo hiki kinafanya kazi kama mhimilimmojawapo wa utawala hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa ku-registerkidogo kwamba kwa kipindi ambacho tumeanza kipindi chabajeti kuna dosari zimejitokeza lazima tuzikubali. Mhimili huuuna heshima yake na heshima yake hii lazima ilindwe naMhimili wenyewe. Vile vile kwa mujibu wa kanuni za Mabungeya Jumuiya ya Madola, mimi kama Mwenyekiti wa CPA kwatawi la Tanzania ningeomba sana Mheshimiwa Spika na kitichake walinde maslahi ya Bunge hili na mustakabali waBunge hili kwa sababu haiwezekani tukawa kila siku tunatupalawama kwa Serikali, tujiulize sisi Kama mhimili tumefanya nini?Haiwezekani kila siku tunasema Serikali, Serikali, Serikali. Bajetiya Bunge inawezesha Bunge hili lifanye kazi zake kuisimamiaSerikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi za Mbunge ni tatu; yakwanza ni kutunga Sheria, ya pili ni kuwawakilisha watuwaliomchagua kwenye chombo hiki na tatu ni kusimamiana kuishauri Serikali, haya ndiyo majukumu ya msingi yaMbunge ndani ya Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumejitokeza manenoyanazungumza hayatii afya kwa Bunge hili. Tunahitaji kauli

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

176

za Serikali zitoke zikieleza bayana kama kuna tatizo liainishwe.Sitarajii kwamba yamezungumzwa hapa na WaheshimiwaWabunge wa pande zote mbili lakini kuna Mawaziri wenyedhamana wamekaa kimya. Huku ni kutokuwajibika ndani yachombo hiki lazima watoe kauli wawaondolee hofuWatanzania ili wajue kwamba Serikali yao wanachofanyandicho hicho Watanzania wanachokitaka lakini tunapokaakimya tunaleta a lot of speculations, watu wanakuwahawaelewi sisi kama Wabunge tunafanya nini. Wananchiwanalalamika, Wabunge wanalalamika, Serikali inalalamikatunakwenda wapi? Kwa hiyo ningeomba sana hiisintofahamu hii, niiombe Serikali, Mheshimiwa Waziri Mkuukama Kiongozi wa Shughuli za Serikali ndani ya Bunge nivyema ukatusaidia kuondoa sintofahamu hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo nikiangaliakwamba Serikali ya Awamu ya Tano imefanya mambo mazurisana na lazima tujenge msingi wa uchumi ili tuwezekuendelea. Huku nyuma ukiangalia watu wanalalamikauchumi umebadilika, mdororo wa uchumi siyo kwa Tanzaniapeke yake, dunia nzima sasa iko kwenye mdororo wakiuchumi. Tusipofikiria nje ya box nadhani sisi Watanzania nikama kisiwa ndani ya dunia haiwezekani lakini yanayofanyikatuyapongeze na tuyape jitihada kubwa zaidi ya kuya-support,angalia miundombinu inayofanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi, ndani ya mudamfupi tumeona uanzishwaji wa ujenzi wa reli ya kati kwastandard gauge, historia, miradi ya maji inayoendelea nihistoria. Upande wa elimu nawasikitikia ambao wanabezakwamba eti hakuna elimu bure, jamani nawasikitikia sana,labda hawajui wanachosema. Haijatokea katika historia yanchi hii kwamba kila mwezi zaidi ya bilioni 18.7 zinatengwakwa ajili ya elimu bure kwa mtoto wa Kitanzania. Hayatunapaswa kuyapongeza na Mheshimiwa Rais ukiangaliaanachokifanya na naomba Watanzania tujue kwambadhamira yake ni nyeupe, dhamira yake ni kwa ajili yakuwatumikia Watanzania, tumpeni support hii tusim-discourage. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

177

Mheshimiwa Mwenyekiti, sijaona kiongozi, mimi nimgeni ndani ya Bunge lakini ni mwenyeji kidogo. Kaziinayofanyika sasa hivi ni kazi nzuri sana lakini kuna vitu vyakushauriana. Mfano; katika suala zima la kiuchumi, kwelifedha ndani ya uchumi imepungua, ni suala la Waziri waFedha. Hii ni issue ya Micro-economics, mambo ya MonetaryPolicy na mambo ya Fiscal Policy atusaidie namna gani yakurudisha fedha katika mzunguko na leo nimesikia kwambaBenki Kuu wameamua kushusha riba ile ya kuwekeza unajuakuna Central Mineral Reserves ambayo ni asilimia 10 yaMabenki kuwekeza na Benki Kuu wameshusha mpaka asilimianane. Hii italeta msukumo wa fedha ndani ya mzunguko wauchumi, nakushukuru Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwakuchukua Monetary Policy ya namna hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tukumbuke kwambajamani tunasafiri kwenye ngalawa moja. Sisi Wabunge bilakujali vyama vyetu nchi hii ni ya kwetu sote, uchumi huu niwa kwetu wote tufanye kazi kwa pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namalizia, naipongezaSerikali. Huko Busega mimi nasema kwamba nina mradi wamaji mkubwa umeshaanza kutekelezwa, sasa niseme ninizaidi ya hili jamani. Umeme wa REA keshokutwa tunaendakuzindua, mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Tanokwa nini niikosoe kwa kitu ambacho naona kuna faida kwaWatanzania? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kama haitoshi leo hiiwatoto wameongezeka katika kusajiliwa darasa la kwanzani historia katika nchi hii. Hivi wewe unayelalamika kwambaSerikali haijafanya kitu unataka ikufanyie nini? IkuleteeKitanda nyumbani kwako?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mayenga,wajiandae Mheshimiwa Ally Keissy na MheshimiwaBashungwa.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

178

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kutoamchango wangu. Nianze kwa kutoa shukrani zangu nyingisana kwa Waheshimiwa Wabunge wote walioko katikaBunge hili kwa support kubwa waliyonipa na hatimaye sasanimekuwa Mrs. Jamal, ahsanteni sana. Haya makofi naombayaendelee mpaka mwisho najua kuna sehemu yatagoma.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpe pongezi zadhati sana Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na MheshimiwaJenista Mhagama na Naibu wake Mheshimiwa Mavunde,wanafanya kazi nzuri sana na kazi kubwa sana. Leonimesimama hapa, kwanza kwa kweli nina hasira kwasababu kuna baadhi ya vitu ambavyo havijanifurahisha hatakidogo na kuna baadhi ya vitu ambavyo nikiviangaliaunamwangalia mtu halafu unasema; hivi huyu anategemeanini? Unakosa majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa nafasi yakipekee nimpe pongezi zangu za dhati sana Mheshimiwa Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa sanaambayo anaifanya yeye pamoja na Baraza lake la Mawaziri,wanafanya kazi kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi ambayo asilimia32 ya mapato ya ndani yanakwenda kulipa madeni, katikanchi ambayo malimbikizo ya madeni yapo asilimia sita, katikanchi ambayo Mheshimiwa Rais anapozunguka au WaziriMkuu au Mawaziri wanapozunguka Rais anaanza kuombwakuanzia vidonge kwenye hospitali mpaka kwenye ndegewatu wanalalamika, Rais huyu kwa kazi hizi anazozifanya kwakipindi hiki kifupi alichofanya kazi, anastahili pongezi kubwasana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaweza tukakaa hapakukaanza kuongea kirahisi rahisi kwamba Rais huyu amefanyahivi, Rais huyu hafai, Rais huyu sijui amefanya hivi ni rahisi sanakuongea namna hiyo, lakini Wabunge baadhiwamezungumza; hivi sisi Waheshimiwa Wabunge maana

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

179

nianze hata na mimi mwenyewe kwa sababu nipo humundani; katika kipindi hiki cha 2016 mpaka sasa hivi mmefanyanini kwenye Majimbo yenu? Hivi kila mtu akisema akae hapaaanze kuulizwa orodhesha ulichokifanya atasema amefanyanini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema makofiyaendelee najua yatagoma; mimi nimekaa hapa Bungenikwa kipindi cha miaka 12 kuanzia mwaka 2005 mpaka leo hiiniliingia hapa Bungeni nikiwa mdogo sana. Naomba kutoatahadhari kubwa sana kwa Wabunge ambao ni wapya nahasa Waheshimiwa Wabunge ambao ni vijana. Wako watuambao ni Genuine kabisa kutoka pande zote mbili; kutokaupinzani na pia na huku. Kuna watu ambao wakiongeaunajua kabisa huyu anaongea ni kwa kutoka kwenyedhamira yake lakini kwa experience yangu kuna watunimeshuhudia tangu nimeingia hapa Bungeni miaka 12 hiikuna watu wananunuliwa na ni Wabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wana interest zaonyuma, mambo yao yameharibika, wanakuja hapawanataka kutuvuruga. Kuna mtu anakuja hapa anasimamakwa sababu mume wake alikuwa fisadi ameondolewakwenye madaraka anasimama hapa anataka kutuvuruga.Kuna mtu anakuja anasimama hapa kwa sababu alikuwaanapewa pesa na mafisadi, mambo yamekuwa magumuanakuja hapa anataka kutuvuruga, kila saa Serikali mbaya,Rais mbaya, sijui vitu gani vibaya; tunaomba samahanini sanahayo maneno yenu mnyamaze mkaongee huko barabarani.Hapa tunataka tukae tuongee masuala ya maana, masualaya wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeishi Rwanda kwa kipindicha miaka kadhaa siwezi kusema ni miaka mingapi na kulewalikuwa wanajua mimi ni Mnyarwanda. Nimeishi uswahiliniya Rwanda na nimeishi Masaki ya Rwanda; watu ambao niviongozi wanakuwa wazalendo, kuna mambo ambayo ni yamsingi, mtu anakaa nazungumza kwa ajili ya nchi yao. Watuwanakaa wana-discuss issues ambazo ni za maana leo hii

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

180

tumekuwa viongozi ni mambo ya Twitter, sijui Whatsapp,meseji za kipumbavu pumbavu ni aibu kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, inatakiwa tutumie mudaambao huu tunao kukaa, kufanya mambo ambayo ni yamaana. Kwa nini hatukai tukashauriana kwamba jamanihebu tufundishane ujasiriamali tunafanyaje, hebu jamanitwende tukamfuate Mheshimiwa Waziri wa Fedha, jamaniMheshimiwa hebu tusaidie, tunataka tujiunge Wabunge 20tufungue kiwanda, Mheshimiwa Waziri wa viwanda hebutusaidie Wabunge 50 tunataka tukae tuweke mitaji yetu,tunataka tufanye biashara ya maana, matokeo yake watumnakaa mnaanza kuchanganyikiwa, mnakuwa hamna helamkitoka hapa maisha magumu, mmekaa wengine hapamnapiga makelele, mnapata hizo nguvu kwa sababu mpondani ya vyama vyenu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inatakiwa watu muwezekukaa kila mtu amekuja hapa kwa nguvu yake na kila mtuamekuja hapa kwa moyo wake na anajua yeye mwenyewenini kilichomleta. Sasa msikae hapa mnaanza ku-insight otherMembers of Parliament to turn against the Government hii niadabu mbaya, mbaya, mbaya kupita kiasi. Kama mnamambo yenu huko pembeni nendeni mkayamalize, kamamna jambo lenu huko pembeni nendeni mkakae mkaongeehuko, lakini siyo mnakuja hapa eti Bunge zima likae liongeemambo ya ajabu ajabu…

MHE. SAID A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti..

MHE. SAID A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekititaarifa.

MWENYEKITI: Taarifa

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti…

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

181

MHE. SAID A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekititaarifa.

MWENYEKITI: Taarifa

MHE. LUCY T. MAYENGA: Naomba kuzungumza hayayafuatayo.

MWENYEKITI: Taarifa, Taarifa

MHE. LUCY T. MAYENGA: ….naomba MheshimiwaWaziri Mkuu kwa sababu upo hapa...

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mayenga hebu subiri.

MHE. SAID A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekititaarifa. Nimesimama kwa kanuni ya 64 ambayo inamtakaMbunge asizungumze lugha ya kuudhi ndani ya Bunge,asizungumze lugha ya matusi ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti Mbunge anayezungumzasasa ametumia lugha ya maudhi ndani ya Bunge, amesemakuna watu ndani ya Bunge hili wamenunuliwa na kwambawaume zao au wake zao walikuwa ni mafisadi nawapumbavu na haya maneno siyo maneno ya Bunge, nimaneno ya kuudhi na Mbunge hawezi kuyathibitisha. Kwahiyo, tunaomba kwa mwongozo wako ayafute au athibitishekwamba kuna Wabunge humu ndani wamenunuliwa naaseme wamenunuliwa na nani na wamelipwa kiasi gani nalini. Hao mafisadi anaowataja ni akina nani, wako wapi naleo wako wapi na walimnunua nani. Ahsante (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, nitaagizia Hansard baadayenihakikishe hayo maneno endelea Mheshimiwa.

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nilichokisema nilisema kwamba, katika kipindi ambachonimekaa hapa Bungeni nimeshuhudia Wabunge wa aina hiyowapo.

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

182

(Hapa kuna Mheshimiwa alikuwa akiongeana mzungumzaji bila kufuata utaratibu)

MHE. LUCY T. MAYENGA: Usitake kunipigia makelelena wewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba MheshimiwaWaziri Mkuu afikishe salamu zetu kwa Mheshimiwa Rais aendeakamwambie kwamba tuko nyuma yake, tunajua kazi kubwaambazo anazifanya, tunajua Serikali hii kazi kubwa ambayoinaifanya na tuko nyuma yake kwa njia yoyote ile. Hatuwezikunyamazishwa lakini ninachoweza kuwaambia, hawaambao wanaweza kupambana naye, yupo mpaka 2025ambao wanadhani kwamba 2020 ni mwisho, they are verywrong na wanajidanganya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuwaambia hatabaadhi ya Wabunge ambao tuko huku kwenye Chamachetu, kila siku nasema na kuna mtu mmoja nimeshawahikumwambia; You cannot win the fight with your Boss, youare messing up with the very wrong person katika Awamu hiiya Tano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwepo hapa Bungeni,kipindi cha uchaguzi uliopita, wote tulikuwepo hapa labdahawa wengine wageni ambao hawakuwepo lakini walikuwawanafuatilia. Baadhi ya Wabunge tulikuwa tunaona tabiaza ajabu ajabu walizozifanya ukiwa humu ndani, watu naheshima zao. Mimi nimeingia hapa kwa mara ya kwanzaulikuwa unamwona Mheshimiwa Mbunge unadhani kwasababu ya umri wake ni mtu mzima, ‘shikamoo Mheshimiwa’baadaye unakuja kukaa baada ya mwaka mmoja, baadaya miaka miwili, unasema kumbe hata ‘mambo’ hastahili kwasababu ya jinsi vitu anavyovifanya vya aibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wote tunajua na wala siyosiri, tulikuwa tumekaa hapa, watu wakati wa uchaguzi,makundi yaliyokuwepo, sasa mimi nasema hivi; kama yalemakundi yalikuwepo, kama ni masuala ya interest nyingineambazo tunazo tuachane na hizo biashara sasa hivi tukae

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

183

tujenge nchi yetu. Tukae tufanye kazi, tukae tuanze kuangaliamaendeleo ya nchi yetu yanakwendaje, wengine hapakwanza hata muda wenyewe wa kuuliza maswali hatuna kwasababu unawaza biashara tu sasa unamshangaa mtumwingine kila saa amekaa ‘Serikali hii sijui imefanya hizi’ miminasemaga hivi hawa watu wanatoa wapi muda? Mwishomtakosa Ubunge mrudi nyumbani kule maisha yaanze kuwamagumu, shauri zenu. Ndiyo ukweli wenyewe si nyie mnajijua?Niliwaambieni haya makofi yatafika mwisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata siku moja SimbaWazungu wana msemo kwamba; “The lion does not turnaround when a small Dog barks” Kwa hiyo, naombaMheshimiwa Waziri Mkuu wala msihangaike na hawa watuambao wanapiga makelele ya ajabu ajabu, maneno yaajabu ajabu, wanasema vitu vya ajabu ajabu, ninyi kaeni,fanyeni kazi mwendelee kuwepo kwenye mstari na tukopamoja, tunaowaunga mkono ndani ya hili Bunge ni wengizaidi kuliko hawa wachache ambao wanapiga makelele.Tuwaache waendelee kupiga makelele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nataka niseme;watakuja siku moja kula matapishi yao, wapo watu ambaotumewashuhudia leo mtu anasema hivi kesho anakujaunamshangaa huyo huyo anasimama Serikali hii nzuri sana.Unashangaa haya maneno ametolea wapi, watakuja kurudikula matapishi yao lakini wakati huo tutakuwa tayaritumeshawajua.

Mheshimimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nina hasirasana. Naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Ally Keissy. JiandaeMheshimiwa Bashungwa.

MHE. ALLY M. KEISSY: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa fursa hii nichangie kidogo kuhusuOfisi ya Waziri Mkuu. Kwanza kabisa namshukuru MheshimiwaWaziri Mkuu, kwa muda mfupi aliokuwa Waziri Mkuu alikujaNamanyere akafanya ziara katika Jimbo langu la Wilaya ya

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

184

Nkasi akatembelea mpaka vyanzo vya maji ambavyonilikuwa napiga kelele hapa kila mwaka habari ya shida yamaji Namanyere. Sasa mwaka huu tatizo la maji Namanyerelitakuwa historia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile namshukuru Waziriwa Maji, alifika Namanyere mpaka kwenye vyanzo vya majina akaahidi kusaidia mitambo ya kusukumia maji.Namshukuru vile vile Waziri wa Mambo ya Ndani alifikaNamanyere, pia Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Makambaalitembelea Namanyere. Mawaziri wote walitembeleaNamanyere.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa dhati kabisanamshukuru Mheshimiwa Magufuli. Mimi nilikuwa Bunge laNne hapa ndugu zangu, nilikuwa msumari nazungumza ukwelikuhusu mafisadi, wezi wa mali ya umma, nilizungumza mpakamakaburi yao yafukuliwe wafungwe minyonyoro kwenyemakaburi. Nilizungumza vile vile safari za Wabunge kwendanje hazina manufaa, tunapishana airport kama wakimbizi.Nilizungumza hapa kabla Mheshimiwa Magufuli hajawa Rais,nilisema hizi safari hazifai! Hebu niambieni Mbunge hatammoja aliyekwenda nje alete tija hapa kama sio ubadhirifuwa hela humu. Wengine walikuwa wanarudia airport,nimezungumza hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ushahidi wakamatehata passport zao waangalie, kama walipewa helawakaenda, passport zitaonesha. Wengine wanapewa sikukumi wanakaa siku mbili wanarudi. Ndugu zangu tumsifuMagufuli amedhibiti nchi! Nilimwambia Rais Magufuli Kinyerezikwenye kuzindua mtambo wa umeme nikasema; spidi yakobado sijaiona, bado spidi ni ndogo. Nchi hii bado mafisadiwengi, wanatuibia! Juzi juzi tu tender ya EWURA wanatakakutuingiza kutuibia bilioni sita kwa mwaka, shilingi bilioni kumina tatu za Kitanzania kwa miaka mitatu mkataba huotutaibiwa bilioni 40 wakati hatuna zahanati, hatunamadawati, hatuna kila kitu. Ndugu zangu bado watuhawaogopi Serikali, wapo! Hao wanataka wabanweikiwezekana kunyongwa! (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

185

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfuko wa Jimbo.Nimezungumza, Mfuko wa Jimbo kwanza usimame. Wapitieupya majimbo sio sahihi. Uchaguzi uliopita safari hiitumezidishiwa Kata kutoka Kusini kwenda Kaskazini, majimboyameongezeka. Jimbo langu kata nzima imehamia kwangulakini Napata mfuko wa jimbo ule ule, nitahudumiaje kata ilenyingine?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilimwambia MheshimiwaSimbachawene nikampelekea na taarifa kwamba katanzima imekuja kwangu. Haiwezekani niendelee kupata mfukowa jimbo ule ule. Simamisha kwanza nchi nzima, fanyamchakato upya. Wabunge wengi wamelalamika hapa.Halmashauri ya Mji wa Namanyere ina vigezo vyote chaajabu wamekwenda kutoa halmashauri zingine hazinavigezo! Ushahidi tunao, upendeleo wa hali ya juu na ugawajiwa majimbo vile vile kwa upendeleo. Haiwezekani! Nchi nimoja hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna majimbo kama kwandugu yangu huyu hapa, Sikonge square kilometers 27,000,kwa Malocha, 15,000, kuna majimbo mengine square metre1,000 humu, kuna mengine 200! Haiwezekani! Hatuwezikwenda hivyo. Lazima twende sambamba, haiwezekaniMbunge yule yule anapata pesa ile ile, gari ile ile, mafutayale yale, jimbo lake linakuwa kubwa kama Rwanda, kamaBurundi, haiwezekani! Hii ni kuoneana. Lazima Namanyeresisi tupate halmashauri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mikoa imeanza juzi juzihalmashauri tano, sita. Cheki Mkoa wa Rukwa, Mkoa mkubwakabisa halmashauri zile zile nne, haiwezekani! Ni maonezihatuwezi kwenda. Ahadi ya Rais alituahidi alipokuja,barabara ya lami kilometa tatu tunaitaka Namanyere,alituahidi kilometa tatu za lami, tunazitaka!

Mheshimwa Mwenyekiti, hospitali Namanyere. Tunamiaka 40 Wilaya ya Namanyere haina hospitali ya wilaya,miaka 40! Watu wanasema miaka 20, miaka mitano mpewe

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

186

hospitali. Kuna wilaya zimeanzishwa juzi zina hospitali yawilaya, sisi miaka 40 hamna hospitali ya wilaya. Haiwezekani,haya maonezi!

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu DC wetu wa Nkasi.Tangu ameanza hana gari, hana usafiri. Anahudumia wilayasquare kilometers 13,500 hana gari! Leo kasimamia shule 105kujenga madarasa matatu shule ya msingi katika kila shulekuhamasisha wananchi na anajenga, anasimamiaje? Hanagari DC, anaombaomba magari. Polisi Namanyere hawanahata matairi. Ndugu zangu tuoneane huruma, kuna wilayazingine zinapewa magari matatu, manne hata hadhi yawilaya hazina, ziko humu humu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Wabunge hataukubwa wa Kata kama Kata yangu hakuna! Wanapewa kilakitu. Lazima tufanye mchakato upya. Ikiwezekana RaisMagufuli aangalie, kama majimbo mengine ayafute!Ayavunje majimbo na halmashauri zingine. Hatutaki mamboya kuoneana. Kupanua halmashauri ambazo hazina hatauwezo, hazikusanyi chochote! Mzigo kwa Serikali. Tuambizaneukweli hata kama unauma. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, usafiri wa ziwa Tanganyika;Awamu ya Nne tumeahidiwa meli mbili katika ziwaTanganyika lakini nakuja kusoma tena ni utengenezaji waLiemba ina miaka 113. Ndugu zangu, tunataka usafiri waziwa Tanganyika, meli mpya! Liemba itengenezwe maanabado inafaa, bado ni nzuri ikarabatiwe, lakini meli mpyatunaitaka katika Ziwa Tanganyika, wananchi wanapatamatatizo sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu pembejeo. Haowanaogawa ruzuku ya pembejeo, ndugu zangu haiwezekanimtu anasema ana deni milioni 360 wakati tukipiga hesabu nimbolea bil ioni 1.8 alipeleka katika jimbo langu.Wanachakachua, lazima wafuatiliwe. Nimemwambia hataWaziri wa Kilimo, Waziri Mkuu nimemwambia, katika Jimbolangu la Nkasi kuna kata kadhaa, hakuna kuwapa pesawamechakachuka, ni wezi wa hali ya juu. Ndiyo hawa Rais

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

187

Magufuli anawatafuta awafunge mara moja hao. Hawahawafai katika nchi yetu, haiwezekani anakuja mtu nabriefcase anapewa kuleta mbolea, analeta gari moja lambolea anataka milioni 360, huu ni wizi wa hali ya juu. Hawani watu wabaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo ya mboleandugu zangu bora iuzwe bei chini, mambo ya pembejeohakuna tena ruzuku waache ruzuku, kila mtu anunue kamavile ananunua vocha ya simu, mambo yaishe! Wametajirikawatu kwa hela za vocha hizi, nchi hii ni wezi wa hali ya juu.Waaminifu ni wachache! Kwa hiyo, agenda zangu ni hizi hizi;nataka Namanyere kuwa Halmashauri ya Mji. MheshimiwaWaziri Mkuu uliona Namanyere ilivyokuwa, kuna halmashaurizingine ukitembelea hakuna lolote, mnawapa halmashauri,ni uonezi!

Mheshimiwa Mwenyekiti, usafiri Ziwa Tanganyika;namwomba Rais Mheshimiwa Magufuli aendeleze, azidishemara mbili. Asionee huruma mtu yeyote anayeiba hela zawalipa kodi. Wananchi wetu, ndugu zangu majimbonikwangu kuna matatizo. Nazungumza habari ya usafiri kutokaKilado kwenda Kazovu miaka 50, tangu uhuru hatujaona gari!Nashukuru Ofisi ya Rais imenipatia pesa, mwaka huuwananchi wa Kazovu wataona gari! Niseme nini sasa? Nikosekumshukuru? Nilikuwa napiga kelele hapa wananchihawajona gari, hawajaona bajaji lakini mwaka huu wananchiwataona gari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba na Waziri waUjenzi aniongezee tena hela nipasue ile barabara Kazovukwenda Korongwe, wananchi wafurahie uhuru katika nchiyao. Rais asikate tamaa aendelee kupambana na watukama hawa. Hakuna kuoneana aibu!

Haiwezekani ndugu zangu katika nchi zingine, mtuanaimba wimbo wa matusi kumtukana Rais mwanzo mwishoanaachiwa! Nchi gani hii? Utawala gani huu? Wewe mtuunamtukana Rais unaachiwa? Aende Rwanda kuleakaangalie au nchi za Kiarabu, watakunyonga! Wewe

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

188

unamtukana Rais wa nchi, wewe umekuwa nani? Uhurugani? Demokrasia gani hii? Unaimba nyimbo, wewe nyimbona mtu wa studio anarekodi nyimbo, ama kweli sio utawalahuu! (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wangeniachia mimi dakikambili niwaoneshe hawa! Haiwezekani! Kiongozi wa nchianatukanwa na nyimbo, ukiisikia hiyo nyimbo ya Roma sijuiMkatoliki, ndugu zangu nyimbo ya aibu. Haiwezekani mtuunasikiliza nyimbo kama ile. Halafu unamshabikia mtu!Haiwezekani! Kusema kweli ni makosa, ni kukosa adabu. Raiswa nchi hatukanwi popote pale. Haiwezekani! Nendeni nchizingine, nenda Rwanda hapo, nenda Burundi, nenda DRCukaangalie, watakushughulikia! Nyie mnacheka cheka hapa,haiwezekani kumchezea Rais namna hii. Huu ni utovu wanidhamu. Huyu Rais anaheshimika, dunia nzima wanamsifuMagufuli. Leo nyie wenyewe ndiyo mnamwona hafai kwenu,kote ukienda wanamsifu, Uarabuni wanamsifu, Ulayawanamsifu, sijui ukienda…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Ahsante kwa mchango wako.(Makofi)

Mheshimiwa Bashungwa.

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niwezekuchangia hotuba hii muhimu ya Ofisi ya Mheshimiwa WaziriMkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongezaMheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba nzuri pia nimpongezeMheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na Mheshimiwa WaziriJenista na kaka yangu Mavunde kwa kazi nzuriwanayoifanya. Tunawashukuru kwa kutupa ushirikiano mzurikatika kuwahudumia Watanzania. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

189

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nitumie nafasi hiikumpongeza Mheshimiwa Rais Magufuli, MheshimiwaMakamu wa Rais mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kazinzuri wanayoifanya katika kutekeleza Ilani ya Chama chaMapinduzi na dira ya miaka mitano ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya pongezi nianzekwa kusema kwamba naunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mawili katika hotubaya Mheshimiwa Waziri Mkuu kipengele cha hali ya uchuminchini ukurasa wa 13 mpaka 40 kuna mambo ambayohotuba imeyazungumzia ningependa kuchangia mambomawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na suala; kwenyemjadala sasa hivi kuna mjadala kuhusu size ya Bajeti yaSerikali. Katika Mwaka wa Fedha wa 2016/2017, Serikaliilitenga trilioni 29.5 na katika mwaka ambao unakuja waMwaka wa Fedha 2017/2018, bajeti hii itapanda kutoka 29.5kwenda kwenye trilioni 31.7.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mijadala kuhususize ya Bajeti ya Serikali naona Serikali kwa sababu dhamirayake na nia yake ni kutatua changamoto za Watanzaniakwa kasi, si mbaya kuwa na malengo marefu na kwa vileSerikali ya Awamu ya Tano tunajua ina dhamira ya kuhakikishainatumia vizuri fedha za umma, nadhani WaheshimiwaWabunge tujikite kwenye kusimamia kile ambacho Serikaliinakikusanya kama kinaenda kwenye kutekeleza miradi yamaendeleo. Sio mbaya kuwa na malengo if you aim higherna ukaweka jitihada ya ufanya kazi ili kwenda kwenye hayomalengo mapana ni jambo la kupongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Serikali ya Awamu yaTano inaingia madarakani TRA ilikuwa inakusanya takribanbilioni 800, lakini Serikali ingependa ikae kwenye kusifiwakwamba inatimiza malengo ya kila mwezi, basi tungejiwekeatarget za bilioni 800, tunaendelea kupongezana kila mwezilakini Serikali ikajipa challenge ikasema tujivute twende

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

190

kwenye trilioni 1.2. Kwa hiyo, unaona kwamba ni hatua nzuri,unakuwa na malengo marefu, lakini unajitahidi kwendakwenye hayo malengo marefu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ambayonaiona kwenye uandaaji wa bajeti ni kwamba asilimia kubwaya Watanzania, kikundi cha wananchi ambao wako vijijini,asilimia kubwa ya wale Watanzania ni kwamba uchumiunakua lakini hauwagusi wale asilimia kubwa. Kwa mfano,katika mpango wa maendeleo wa 2017/2018 na katikahotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ukiangalia kwa upandewa kilimo kwanza kwenye ukuaji wa Sekta ya Kilimo 1.7% nikidogo mno. Hatuwezi kuona social economic transformationkwenye Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Sekta hizi ambazozinaajiri Watanzania walio wengi kama tutaendelea kupataukuaji wa 1.7%. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nipende kuiomba Serikalikatika Bajeti za Kisekta ambazo zinakuja, tuone bajeti yakutosha imetengwa kwa ajili ya pembejeo, tuone kunampango wa kupata maafisa ugani wa kutosha ili vijiji vyetuvipate maafisa ugani, tuone bajeti ya kutosha kwenye kilimocha umwagiliaji. Mwaka wa Bajeti wa 2017 ilitengwa helakidogo sana kwenye kilimo cha umwagiliaji. Katika Bunge hilibaada ya ukame ambao ulitupata kule Karagwe, niliombaSerikali ije kwenye kata kumi ambazo zina vyanzo vya majitutathmini kuona kama tunaweza kufanya kilimo chaumwagiliaji, lakini mpaka hivi sasa sijapata timu ya wataalamkufanya hii tathmini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ili tuweze kwendakwenye uchumi wa viwanda na kwenda kwenye middleincome country status lazima tufike mahali tuone jitihada zakibajeti zinazolenga kutoa bajeti ya kutosha kwenye Sektaya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili Watanzania wengi hawa ambaowanajishughulisha kwenye hii sekta tuweze kuwasaidiakujikwamua kutoka kwenye umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye mazao ya biashara,kodi kero 27 kwenye zao la kahawa tumeondoa kodi moja

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

191

tu ya ada ya leseni ya kusindika kahawa ya dola 250 tu. Tukokwenye rekodi, kwenye Ilani tumeahidi kwamba tutaondoahizi kodi kero kwenye zao la kahawa. Mheshimiwa Rais alikujaKagera akaahidi kwamba kwenye bajeti hii ya 2017/2018tutaziondoa hizi kodi kero. Mheshimiwa Waziri Mkuunakushukuru ulikuja Karagwe tukaahidi lakini sijaona jitihadaya Serikali kuondoa hizi kero kwa sababu kwenye hotuba yaWaziri Mkuu hazitatajwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kwenye kusaidia yalemakundi ya wananchi ambao wako vijijini pia kuna haja yakuangalia wajasiriamali wadogo na wa kati na kuwekamazingira wezeshi ili kuwasaidia kukua. Kwenye hotuba yaMheshimiwa Waziri Mkuu inatambua kwamba 56% yawananchi ni nguvu kazi ya vijana, lakini kwa sababutumekuwa na malengo ya kukusanya mapato ya kila mwezikwa mfano, kumekuwa na aggressive behavior katikakukusanya mapato kiasi kwamba haya makundi ambayotunategemea kuwasaidia kuwakwamua kutoka kwenyeumaskini tunajikuta zile aggressive behavior za kukusanya kodikwa mfano upande wa bodaboda, ukija Karagwe,bodaboda awe kwenye gulio, msiba au shambani, pikipikizinawindwa na askari wa usalama barabarani kwa sababuwana target ya mapato kiasi fulani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo matokeo yakeunakuta badala ya kumsaidia yule kijana ambayetumeshindwa kumpatia ajira kwa sababu tatizo la ajira ni lanchi nzima na si Tanzania tu ni Afrika na dunia nzima, walevijana ambao wanajiajiri tunatakiwa kuwawekea mazingirawezeshi ya kukua. Kama amejiajiri kama bodaboda basitumsaidie ili aweze kukua. Kwa hiyo, matokeo yake, kwasababu ya target za mapato unakuta tunawaathiri yalemakundi maalum ambayo tulitakiwa kuwasaidia kuwawekeamazingira wezeshi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayosasa, niende kwenye changamoto zlizoko kwenye Jimbo la

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

192

Karagwe na nimezileta kwenye hotuba ya Mheshimiwa WaziriMkuu ili nimwombe aweze kunisaidia yapate attentioninayostahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na mradi wa maji waRwakajunju. Huu mradi ni ahadi ya muda mrefu, MheshimiwaRais wakati wa kampeni tuliwaahidi wana Karagwe katikahii Serikali ya Awamu ya Tano tutatekeleza mradi huu. Serikaliikatenga dola milioni 30 kwenye Mwaka wa Fedha 2016/2017,lakini nashangaa kwenye bajeti ya mwaka huu 2017/2018,fedha hizi sizioni sasa sijui zimeenda wapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuunakumbuka ulivyokuja karagwe tuliwaahidi wana Karagwekwa vile zilikuwa zimeshatengwa kwenye bajeti ya mwakauliopita, tukawaahidi pale tulikofanya Mkutano pale Kihangatena ukamwomba Mkurugenzi wa Halmashauri aje kwenyejukwaa awaambie kwamba wananchi wa Kata ile yaKihanga na wenyewe watapata huduma ile ya maji kutokakwenye mradi wa Rwakajunju. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mradi huuusipotekelezwa kwa kweli kuna hali ya hatari huko mbeleni.Namwomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu anisaidie katikahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la elimu.Naipongeza Serikali katika elimu ya bila malipo, tunakwendavizuri na Serikali inaendelea kurekebisha pale ambapotunakwama lakini ili tuweze kwenda vizuri, naomba Bajeti ya2017/2018, tutenge fedha za kutosha kwa ajili ya kuajiriwalimu. Wilaya ya Karagwe peke yake tuna deficit ya walimu840 wa shule za msingi, tuna deficit ya walimu wa sayansi 96.

Mheshimiwa Mwenyekiti,…

MWENYEKITI: Nakuongezea dakika moja.

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: MheshimiwaMwenyekiti, nizungumzie suala la afya. Katika malengo ya

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

193

Serikali ya kuwa na kituo cha afya kila kata nadhani nimalengo mazuri lakini hatuwezi kuyatimiza kwa muda mfupi.Nipende kuishauri Serikali angalau tulenge kuwa na kituo chaafya kwa kila tarafa ili katika kipindi cha miaka mitano tuwezekuonesha kwamba tuna malengo ya muda mrefu lakini katikakipindi cha miaka mitano tumeweza kuwa na kituo cha afyacha kila tarafa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie na migogoro yaardhi. Pale Kihanga tulipofanya mkutano, zile hekta 2000ambazo Mheshimiwa Waziri Mkuu alielekeza Serikali irudishekwa wananchi mpaka hivi sasa bado. Walienda palewakasema tunawapa hekta 2000 lakini zimelenga sehemuambapo wananchi tayari wanakaa, hazijatolewa kutokakwenye ranch ya Kitengule na wenye ma-block, kwa hiyo,namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu asiingilie katika hili sualaili tuweze kurudisha hekta 2000 kwa wananchi kamatulivyowaahidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, orodha yawachangiaji wa vyama vyote imekwisha na wotewamechangia. Wengine wataendelea kesho naahirishashughuli za Bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi.

(Saa 1.40 Usiku Bunge liliahirishwa hadi Siku ya Jumatano,Tarehe 12 Aprili, 2017 Saa Tatu Asubuhi)