321
NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Kumi na Mbili – Tarehe 25 Aprili, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae. Tunaendelea na shughuli zetu Mkutano wa Saba, Kikao cha Kumi na Mbili. Katibu! NDG. LAWRENCE MAKIGI – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI. Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2017/2018. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Hotuba ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1494660814-25 Aprili 2017.pdf · Wizara ya Katiba na Sheria juu ya Makadirio ya Mapato

  • Upload
    others

  • View
    1

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA

_____________

MAJADILIANO YA BUNGE_____________

MKUTANO WA SABA

Kikao cha Kumi na Mbili – Tarehe 25 Aprili, 2017

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua

MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae. Tunaendelea nashughuli zetu Mkutano wa Saba, Kikao cha Kumi na Mbili.

Katibu!

NDG. LAWRENCE MAKIGI – KATIBU MEZANI:

HATI ZA KUWASILISHA MEZANI.

Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO:

Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wafedha 2017/2018.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA:

Hotuba ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwamwaka wa fedha 2017/2018.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

MHE. JORAM I. HONGOLI (k.n.y MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA):

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba naSheria kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Katibana Sheria kwa mwaka wa fedha 2016/2017 pamoja na maoniya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/18.

MHE. SUBIRA K. MGALU (k.n.y MWENYEKITI WA KAMATIYA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI):

Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajetikuhusu Maoni ya Kamati hiyo juu ya Utekelezaji wa Bajeti yaMfuko wa Mahakama kwa mwaka wa fedha 2016/2017pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwakawa fedha 2017/2018.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA (k.n.y MSEMAJI MKUU WAKAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBANA SHERIA):

Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusuWizara ya Katiba na Sheria juu ya Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria mwaka wa fedha2017/2018.

MWENYEKITI: Ahsante, tunaendelea.

Katibu!

NDG. ZAINAB ISSA - KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

MWENYEKITI: Maswali na swali letu la kwanza, swalinamba 95 linaulizwa na Mbunge wa Biharamulo Magharibi,Mheshimiwa Oscar Rwegasira Mukasa na linaelekezwa Ofisiya Rais, TAMISEMI.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

Na.95

Kuwawezesha Waendesha Bodaboda

MHE.OSCAR R. MUKASA aliuliza:-

Ibara ya 57(b) ya Ilani ya CCM inaahidi kuweka mfumowa kuvitambua, kuvisajili na kuviwezesha vikundi vyotevyenye mwelekeo wa ushirika na ujasiriamali nchini. Kwakuwa kundi la waendeshaji wa vyombo vya usafiri wa abiriamaarufu kama bodaboda ni kundi la kijasiriamali, nainawezekana ndilo kundi lenye mwelekeo na fursa zakiushirika ambalo ni kubwa zaidi Wilayani Biharamulo na nchinikote kwa sasa.

Je, Serikali ina mpango gani mahususi juu ya kundihili?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Oscar Rwegasira Mukasa, Mbunge waBiharamulo Magharibi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuhakikisha Ibara ya57(b) ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015inatekelezwa kikamilifu kuhusu uwezeshaji, Halmashauri yaWilaya ya Biharamulo imeweza kuvitambua na kuvisajili jumlaya vikundi 1,940 vya wajasiriamali vikiwemo vikundi 34 vyavijana waendesha bodaboda. Aidha, waendesha bodaboda2,000 wametambuliwa kwa jitihada kubwa za MheshimiwaMbunge kwa kushirikiana na Halmashauri na wakawekewautaratibu wa utoaji huduma ya usafiri wa pikipiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri kwakushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Biharamuloimewezesha jumla ya waendesha bodaboda 410 kupata

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

mafunzo ya uendeshaji wa pikipiki na kupata leseni zakuendesha na kufanya biashara hiyo.

Natoa wito kwa Wakurugenzi wote wa Mamlaka zaSerikali za Mitaa kuhamasisha waendesha bodabodawajiunge kwenye vikundi na SACCOS ili watambulike kisheriana kupata fursa ya mikopo inayotolewa kupitia asilimia 10 yavijana na wanawake pamoja na Baraza la Taifa la UwezeshajiKiuchumi.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Mukasa.

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Mwenyekitiahsante, nakushukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu, lakininina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, kwa mujibu watakwimu tulizopewa kwenye majibu na Mheshimiwa Waziri,asilimia 80 ya waendesha bodaboda hawana leseni, jamboambalo linawafanya waishi kwenye mzunguko wakukimbizana na polisi badala ya kuzalisha mali kwa ajilikujenga uchumi wao na uchumi wa Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kumuulizaMheshimiwa Waziri, je, Serikali iko tayari kuwasaidia kwakuwawekea ruzuku ya kupunguza walau kwa mara moja kodiya kulipia leseni angalau kwa nusu ili waweze kupata lesenikama hatua ya kwanza ya kuwasaidia ili tuweze kushirikiananao kuongelea habari ya kuwahamisha kuwapeleka kwenyeushirika wa SACCOS na mambo mengine?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili; Mheshimiwa Waziri yukotayari kuambatana na mimi twende Biharamulo kuziona fursanyingine zaidi ya kuwaomba tu wajiunge kwenye SACCOSambazo Serikali Kuu ikishirikiana na sisi tunaweza kuzitumiakuwatoa kwenye yale waliyonayo ili Biharamulo iwe mfanowa kusambaza hatua kama hiyo maeneo mengine ili kundikubwa la bodaboda nchini tulisaidie liwe la ujasiriamali kwelikweli? Ahsante.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZAA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yaMheshimiwa Mbunge kama ikiwezekana Serikali ifanyeuwezeshaji, naomba nikiri wazi kwamba hatuwezi kusemakama Serikali tufanye uwezeshaji kwa watu wote, lakinitunakuwa na mikakati mbalimbali ya kufanya uwezeshaji.Mimi niwapongeze Wabunge wengi humu ndani ambaowamefanya initiatives katika Majimbo yao kuhakikisha vikundimbalimbali vinahamasishwa na wao wanasaidia ku-chip inhumo kwa ajili ya kuwasaidia vijana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo mimi ninajua wazikwamba kuna baadhi ya Halmashauri nyingine zina mipangombalimbali yenye lengo la kuwasidia hawa vijana ilihatimaye, kama ulivyofanya Mheshimiwa Mbunge katikaJimbo lako ambapo na sisi tume-recognise shughuli na juhudikubwa unazofanya katika Jimbo lako, nadhani tukifanyauhamasishaji sisi wengine tutafanya kwa kuangalia fursazilizopo katika maeneo yetu na hivyo tutaweza kuwasaidiahao vijana kwasababu lengo letu ni kwamba vijana wawezekukomboka katika jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kikubwa zaidi kamahatufahamu; bahati nzuri Ofisi ya Mama Jenista Mhagamakatika Baraza la Taifa la Uwezeshaji, hata jana nadhaniwalikuwa wanafunga mafunzo yao, wameona kwamba jinsivijana wengi wanavyokosa fursa hizi kwa kutokuwa naufahamu wa kutosha na ndiyo maana wamesema sasa hiviwanataka kuzifanya programu zao kupitia maeneombalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sehemu ya pilinaomba nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba miminipo radhi, nilifika Biharamulo mara ya kwanza, lakini kamakuna jambo lingine mahususi tutakwenda tena ili kuwasaidiavijana wetu waweze kufika mbele katika suala zima lamaendeleo.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

Mwenyekiti, kwanza naomba nimpongeze sana MheshimiwaJafo kwa majibu yake mazuri kwenye swali hili la msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbungeametaka kuiuliza Serikali ni kwa kiasi gani inaweza ikajipangakupeleka juhudi za ziada ili kuhakikisha kwamba vijana waTanzania, hasa vijana wa kule Biharamulo wanawezakufaidika na mikopo mbalimbali na kuweza kuwaboresheashughuli za ujasiriamali wakiwemo vijana wa bodaboda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikuhakikishiekwamba, Mheshimiwa Mbunge ni kati ya Wabunge ambaowalihudhuria maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji wananchikiuchumi, na tumeshakubaliana na Mheshimia Mbungekwamba baada ya shughuli hizi za Bunge kukamilika,Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja natimu ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi pamojana yeye Mheshimiwa Mbunge watakuwa na ziara maalumkule Biharamulo ili kuangalia Serikali inaweza ikafanya ninikwa ajili ya maendeleo ya vijana na sekta nyingine.

Nitoe wito kwa Waheshimiwa Wabunge wote,tumefunga maonesho ya mifuko ya uwezeshaji wananchikiuchumi, tunaomba sana tuendelee kuwasiliana ili fursazilizopo ndani ya Serikali ziweze kuwafikia Watanzania wengihasa wakipato cha chini na kipato cha kati wakiwemo vijanana kuweza kuwainua kiuchumi. Nakushukuru.

MWENYEKITI: Ahsante, Waheshimiwa tunaendelea,swali letu l inalofuata, swali namba 92 linaulizwa naMheshimiwa Ezekiel Magolyo Maige Mbunge wa Msalala.

Na. 96

Mradi wa Maji Kutoka Ziwa Victoria Hadi Kahama

MHE. EZEKIEL M. MAIGE aliuliza:-

Mwaka 2014/2015 Serikali iliahidi kuongeza usambazajimaji katika vijiji 100 vilivyoko umbali wa kilometa 12 kutoka

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

bomba kuu la Ziwa Victoria hadi Kahama na Shinyanga.Serikali ilitenga na Bunge kupitisha shilingi bilioni nne ilikutekeleza mradi huo.

(a) Je, ni vijiji vingapi vimeshapatiwa maji kati ya hivyovijiji 100 hadi sasa?

(b) Je, Serikali inafikisha lini maji ya Ziwa Victoria katikavijiji vya Mwakuzuka, Mwaningi, Kabondo, Ntundu, Busangi,Buchambaga, Nyamigege, Gula, Izuga, Buluma, Matinje naBubungu?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Majina Umwagiliaji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa EzekielMagolyo Maige, Mbunge wa Msalala, lenye sehemu (a) na(b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa kuunganisha vijijivilivyopo umbali wa kilometa 12 kutoka bomba kuu la ZiwaVictoria hadi Kahama na Shinyanga unatekelezwa chini yaprogramu ya maendeleo ya sekta ya maji. Katika awamu yakwanza ya utekelezaji vijiji 40 viliainishwa, kati ya hivyo vijiji 32vimefanyiwa usanifu. Hadi sasa jumla ya vijiji 13 uunganishajiumekamilika na vijiji hivyo ni Nyashimbi, Magobeko, Kakuluna Butegwa, hilo ni Jimbo la Msalala. Ng’homango, Kadoto,Jimondoli, Mwajiji, Ichongo, Lyabusalu na Bukamba hili niJimbo la Shinyanga Mjini na Runere na Gatuli hii ni Kwimba;na viji j i viwili vil ivyopo Shinyanga Viji j ini ambavyo niMwakatola na Mwasekagi uunganishaji unaendelea. Hadisasa kiasi cha shilingi bilioni 1.96 zimetumika kwa ajili yakuunganisha maji kwa vijiji hivyo kutoka bomba kuu la ZiwaVictoria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viji j i vya Mwakuzuka,Kabondo, Ntundu, Busangi, Nyamigenge na Gula vipo katikampango wa awamu ya kwanza na usanifu wakeumekamilika na ujenzi unatarajiwa kuanza mwaka wa fedha2017/2018. Aidha, Serikali itaendelea kuunganisha vijiji

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

vilivyobaki vikiwemo vijiji vya Mwaningi, Buchamba, Izuga,Buluma, Matinje na Bubungu kulingana na upatikanaji wafedha.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Maige

MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibuyake mazuri. Pamoja na hayo naomba kuuliza maswalimawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika vijiji hivi ambavyovimewekwa kwenye kundi la vijiji vilivyoko katika kilometa12, infact viko vijiji vingine ambavyo viko ndani kabisa yakilometa moja kwa maana kwamba vilisahaulika wakati wausanifu wa mradi mwanzo hasa vijiji kama Matinje na Izuga.Kwa mfano pale Izuga lile bomba limepita kabisa kwenyeuwanja wa shule ya msingi Izuga.

Sasa katika mazingira haya ambapo jibu linasemavitaunganishwa kutegemea upatikanaji wa fedha. Hivi nisawa katika mazingira hayo ambayo bomba limepita palepale kijijini halafu wanaendelea kukaa bila kujua? Nilitakakujua Mheshimiwa Waziri atuambie ni lini hasa vijiji hiviambavyo bomba limepita pale pale kijijini kama Izuga naMatinje vitafanyiwa angalau mpango wa dharura wakuunganishwa badala ya kusubiri mpango au lugha yakwamba fedha zitakapopatikana? Nilitaka kujua lini katikahali ya dharura.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; katika maeneohaya ambapo bomba kuu la Ziwa Victoria kutoka Mwanzakwenda Kahama na Shinyanga limepita hapakuwepoutaratibu wa kutengeneza mabirika ya kunyweshea mifugo(water traps); na mwaka 2014 tulikubaliana kwamba uwepompango wa kutengeneza water traps kwa ajili ya mifugo.(Makofi)

Je, ni lini Serikali sasa itafanya mpango huo ili maeneohaya pia mifugo iweze kupata maji?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Naibu Wazirimajibu kwa kifupi tu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, amesema ndani yakilometa 12 kuna baadhi ya vijiji ambavyo vimesahaulika.Nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hatutaachakijiji hata kimoja, tunachotaka ni ushirikiano na Halmashaurihusika kama kuna kiji j i ambacho kimesahaulika basitunaomba tupeane taarifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia umependa kujuani mpango gani wa haraka, kwa mfano kama kijiji chaMitinje, kijiji cha Izuga ambacho kina kilometa moja tu kutokakwenye bomba. Tushirikiane Mheshimiwa Mbunge, Wizara yaMaji na Umwagiliaji kila mwaka inatenga fedha kwa kilaHalmashauri. Basi ningeomba Halmashauri husika ijaribukuangalia uwezekano wa kuunganisha kutokana na fedhatuliyotenga Wizara ya Maji na kama wanaona hawawezi basiwawasiliane na Wizara ili tufanye hiyo kazi haraka kuhakikishakwamba wananchi wanapata huduma ya maji safi nasalama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kuhusu mabirika.Mimi tu niseme Mheshimiwa Mbunge kwamba haya Mabirikatumepokea hii tutalifanyia kazi ili kuona ni namna ganitunaweza tukatumia maji haya ili kuweza pia kusaidia mifugoiliyo karibu na hilo bomba.

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa, tuone wanaotokaukanda huo, Mheshimiwa Kwandikwa.

MHE. ELIAS J. KWANDIKWA: Mheshimiwa Mwenyekitiahsante sana kwa kuniona ili na mimi niweze kuuliza swalidogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mahitaji ya Jimbola Msalala yanafanana kabisa na mahitaji ya Jimbo la Ushetu,na kwa kuwa maji haya ya Ziwa Victoria yamefikishwaKahama Mjini na hayajawafikia kabisa wananchi wa Jimbo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

la Ushetu, je, Serikali inawaambia nini wananchi hawa ambaowanayasubiria maji haya?

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Naibu Waziri waMaji na Umwagiliaji, Injinia Isaac Kamwelwe.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari tuna bomba, na juzi tumesainimkataba tarehe 22 Aprili kwa ajili ya kufikisha maji Nzega,Igunga na Tabora. Kama bomba limeshapita karibu na eneolako, tutaendelea, na kama topography inaruhusututaendelea kuweka fedha ili kuhakikisha kwamba namaeneo kama haya ya Ushetu na nikuhakikishie tu kwambabado capacity ipo kubwa, yapo maji ya kutosha, tutaendeleakutenga fedha kuhakikisha kwamba na hili eneno la Ushetutuhakikishe tunalipatia maji. Na nikuombe MheshimiwaMbunge kwamba naomba tuwasiliane ili tuweze kupangatuone namna gani tunaweza tukahakikisha kwamba majiyanafika haraka Ushetu.

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Wazirikwa kazi nzuri anayofanya. Mimi nilikuwa nataka kujua uleMradi wa Vuga - Mlembule - Mombo ambao yeyeameutembelea kwa muda mrefu sana na kuona matatizoyake na kuwaahidi wananchi wa Mombo kwamba ikifikamwezi wa sita watapata maji. Ni lini Mradi huu utakuwaumekamilika na wananchi wale wafurahie mradi ule mkubwawa maji ambao unagharimu zaidi ya shilingi 900,000,000?

MWENYEKITI: Ahsante! Majibu Mheshimiwa NaibuWaziri Maji na Umwagiliaji.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuhakikishie kwamba wananchiwa Mombo watapata maji. Nilifanya ziara nimeenda Vuga,nimeongea nao na tumekubaliana kwamba sasa tuongezefedha pamoja na hiyo milioni mia tisa, tunaongeza fedhakatika bajeti ya 2017/2018. Na tumeweka utaratibu, eneololote lenye chanzo tunapofanya mradi lazima tuhakikishe

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

kwamba wananchi wanaozunguka hilo eneo wapate majikabla ya kupeleka Kijiji cha mbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunatenga fedhaitakayohakikisha kwamba wananchi wa Vuga wanapatamaji, na bomba lingine linakuja moja kwa moja mpaka eneola Mombo na maeneo mengine yatakayopitiwa na hilobomba. Kwa hiyo nikuhakikishie Mheshimiwa Mbungekwamba tunaendelea na juhudi kuhakikisha kwambawananchi wa Mombo wanapata maji kutoka Vuga.

MWENYEKITI: Ahsante, Waheshimiwa Wabunge kwasababu ya muda tunaendelea. Swali linalofuata, swalinamba 97 linaulizwa na Mheshimiwa Innocent LughaBashungwa, Mbunge wa Karagwe, na linaelekezwa Wizaraya Maji na Umwagiliaji. Mheshimiwa Bashughwa.

Na. 97

Ujenzi wa Mabwawa ya Maji

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA aliuliza:-

Serikali imeahidi kujenga mabwawa ya maji katikaKata za Kanoni, Igarwa, Ihanda na Chenyoyo ili kuwapatiawananchi wa kata hizo maji.

(a) Je, Serikali imefikia hatua gani katika kutekelezakazi hiyo?

(b) Je, Serikali inawahakikishiaje wananchi wa vijiji vyaKafunjo, Kijumbura na Bweranyange kwamba mradi wa majiwa Lyakajunju utakapotekelezwa utawaachia wananchimiundombinu ya maji ili kuwanusuru kuliwa na mambawanapofuata maji ziwani?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Majina Umwagiliaji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Innocent

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

Lugha Bashungwa, Mbunge wa Jimbo la Karagwe, lenyesehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza ujenzi wamabwawa, Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliajiimeziagiza Halmashauri zote nchini kuainisha maeneoyanayoweza kujengwa mabwawa na kutenga fedhakwenye bajeti zao za kujenga angalau bwawa moja kilamwaka. Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe imewezakuainisha maeneo yanayofaa kujengwa mabwawa kamaifuatavyo:-

Kata ya Kanoni eneo la Kabare na Omukigongo, Kataya Igurwa eneo la Omukalinzi (Kabulala A) na Kata yaNyakahanga eneo la Kashanda (Karazi). Mabwawa katikamaeneo hayo yatajengwa kulingana na upatikanaji wafedha baada ya kazi za usanifu, kuandaa michoro, kuainishagharama na nyaraka za zabuni kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ipo katika hatua zausanifu wa kina wa utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Bwawala Lwakajunju ambao kutekelezwa kwake kutavipatiahuduma ya maji vijiji vyote vitakavyopitiwa na bomba kuu lamaji katika umbali usiozidi kilometa 12 kutoka eneo la bombakuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya usanifu kukamilikaitaainisha iwapo vijiji vya Kafunjo, Kijumbura na Bweranyangevitakuwa ndani ya kilometa 12 kutoka eneo la Bomba Kuu.Mradi huo utavipatia maji na endapo havitakuwepo basiHalmashauri iweke kwenye vipaumbele vijiji hivyo katikabajeti inayotengwa na Wizara kila mwaka.

MWENYEKITI: Ahsante! Mheshimiwa Bashungwa.

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuulizamaswali ya nyongeza. Kwanza nianze kwa kumpongezaMheshimiwa Naibu Waziri na Mheshimiwa Waziri kwa kazi nzuriwanayofanya katika utendaji wao wa kazi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

Mheshimiwa Mwenyekiti, maswali yangu mawili yanyongeza ni kama yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa Lwakajunju,imekuwa ni ahadi ya muda mrefu sana zaidi ya miaka 15.Kwa maana hiyo tumewaahidi sana akina mama waKaragwe na wananchi kuwatua ndoo kichwani kwa mudamrefu sana. Kama unavyojua akina mama ule muda ambaowanautumia kwenda kuchota maji umbali mrefu ndio mudahuo huo ungeutumia kufanya kazi za maendeleo. Sasa swalila kwanza, Mheshimiwa Naibu Waziri naomba unipe comfort,je,huu mradi wa Lwakajunju utatekelezwa lini? Ni liniwananchi wa Karagwe watapata hii huduma ya maji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na changamotoza kibajeti za Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, je, Wizaraipo tayari kushirikianan na Halmashauri kuhakikisha fedhaambapo tunahitaji kwa ajili ya kuchimba mabwawa katikaKata za Kanoni, Igulwa Ihanda, Chonyonyo na Nyakahangazinapatikana ili wananchi wapate huduma ya maji?

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Naibu Waziri waMaji na Umwagiliaji kwa kifupi, muda si rafiki.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kuhusiana na Mradi waLwakajunju, ameomba apate confort na wananchi wakepia. Comfort ya kwanza ni kwamba mradi huu umetengewadola milioni 30 kutokana na mkopo wa India, ni mkopowenye uhakika na sasa hivi tupo kwenye taratibu zakukamilisha usanifu i l i tutangaze tender. Kwa hiyo,nikuhakikishie kwamba mradi huu unatekelezwa kwasababutayari una fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pil ilinalohusiana na ushirikiano na Halmashauri, MheshimiwaMbunge nikuhakikishie kwamba tutaendelea kushiriakana naHalmashauri zote kuhakikisha kwamba miradi ya majiinatekelezwa, mabwawa, mserereko, visima na mingine ilikuhakikisha kwamba wananchi wanapata maji. Kuhusu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

suala la fedha upungufu wa fedha tutaenda nalo sabamba,lakini suala la msingi ni kuhakikishe kwamba wananchiwanapata maji. (Makofi)

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekitinashukuru kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Katavi kunamiradi ya umwagiliaji ambayo imeanzishwa na Serikali naimetumia fedha nyingi sana. Miradi hiyo ni mradi wa Karema,Kabage na Mwamkulu. Miradi hii ya Serikali imetolewa fedhanyingi, bahati mbaya sana Serikali inapoanzisha haiwezikuikamilisha hiyo miradi. Nilikuwa nataka kujua ni lini Serikaliitakamilisha hiyo miradi ya Karema, Kabage na Mwamkuluili iweze kuwanufaisha wananchi?

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri Majina Umwagiliaji majibu, anauliza lini.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi hiyo ilianza, ni kweliilichelewa kukamilishwa lakini sasa hivi tumeandaa timuambayo inakwenda kupitia ili kuainisha changamotoambazo zimefanya isikalimike ili tuweze kutoa fedhatuhakikishe kwamba miradi hiyo yote mitatu Karema, Kabagena Mwamkulu inakamilika.

Kwa hiyo, nikuhakikishie kwamba tayari, na mimimwenyewe nimeshakwenda kutembelea Mradi mmojawapopale na huo mradi sasa hivi tayari kazi inaendeleamkandarasi amerudi site ili kuhakikisha kwamba miradi yotehii inakamilika.

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti,na mimi nilitaka nimuulize Mheshimiwa Waziri. Imekuwa nikero kubwa kwa wananchi wa Manispaa ya Mpandakuendelea kusubiri miradi ambayo haitekelezeki, lakini pia niwiki sasa maji hayatoki. Sasa ni nini tamko la Serikali ilikuhakikisha wananchi hao wanapata maji lakini piawasiendelee kulipa bili ambazo hawapati maji? (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, Mji wa Mpandamahitaji ya maji ni lita 10,200,000 kwa siku. Hadi sasa kwamradi uliopo unatoa maji lita 3,150,000 kwa siku. Sasa hivikuna miradi miwili ambayo wakati wowote itasainiwa, miradihiyo ikikamilika basi itaongeza kiwango cha maji hadi kufikialita 6,000,000. Kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Mbungekwamba utekelezaji unaendelea. Changamoto kama majihayajapatikana, kwanza tufahamu kwamba maji yaliyopoyanatosheleza kwa asilimia 30 tu. Kwa hiyo, si suala kwambamaji hayapo, hapana, ni kidogo. Serikali inaendelea kujitahidikuhakikisha kwamba yale mahitaji ya lita 10,200,000yanafikiwa na tatizo la maji kutokupatikana halitakuwepotena.

Na. 98

Kupunguza Ajali za Barabarani

MHE. SABREENA H. SUNGURA aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kupunguza ajali zabarabarani?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali laMheshimiwa Sabreena Hamza Sungura, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeandaa mkakatiwa kudhibiti makosa yanayosababisha madhara makubwaambayo hupelekea ajali za barabarani kuongezeka. Mamboyaliyolengwa katika mkakati pamoja na mambo mengineni:-

(1) Udhibiti wa madereva walevi na kuendesha kwauzembe;

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

(2) Udhibiti wa mwendokasi kwa madereva nawamiliki wa magari , kuwa na madereva wenza kwa mabasiya safari za zaidi ya masaa manane;

(3) Kuthibiti uendeshaji magari bila sifa/leseni zaudereva ama Bima;

(4) Kudhibiti usafirishaji wa abiria kutumia magarimadogo yenye muundo wa tairi moja nyuma;

(5) Kusimamia matumizi ya barabara kwa MakundiMaalum mfano watoto, wazee, walemavu na wasiotumiavyombo vya moto ikiwemo mikokoteni na baiskeli;

(6) Kudhibiti ajali za pikipiki za magurudumu mawili(bodaboda) na magurudumu dumumatatu (bajaji);

(7) Kuzishauri mamlaka husika kuweka alama zakudumu za utambulisho kwenye maeneo hatarishi ya ajali;

(8) Kusimamia utaratibu wa nukta (Point System)kwenye leseni za udereva;

(9) Marekebisho ya Sheria za Usalama Barabarani;

(10) Abiria kufunga mikanda ya usalamawanapotumia vyombo vya usafiri;

(11) Kubaini maeneo tete na hatarishi ya ajali zabarabarani;

(12) Kuthibiti utoaji na upokeaji rushwa barabarani;

(13)Motisha kwa askari wanaosimamia vizurimajukumu yao; na

(14) Kuwajengea uwezo wa kiutendaji askari wausalama barabarani.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

Mheshimiwa Mwenyekiti, nidhahiri kwamba suala lausalama barabarani siyo la kundi au taasisi moja tu ila ni letusote. Wabunge ni miongoni mwa wahusika wa suala lausalama barabarani, kwa maana kuwa nafasi yao kubwani katika kuelimisha umma na kusaidia katika ujenzi wautamaduni wa kuheshimu alama za usalama barabaraninchini. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Sabreena.

MHE. SABREENA H. SUNGURA: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru pamoja na majibu ya MheshimiwaNaibu Waziri lakini bado kuna mambo ya msingi ambayoyanapelekea ajali za barabarani kuendelea kutokeaambayo hayajakuwa mentioned katika majibu yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hususani njia inayoelekeaKigoma, kuanzia Itigi kwenda Tabora mpaka Kigoma,tumekuwa na railway cross nyingi sana katika eneo hilo, lakininyingi katika hizo hazijawekewa alama kiasi kwamba msafirianapokuwa anaendesha ama madereva wanapokuwawanaendesha wanashindwa kutambua. Ni kwa mita chachesana alama hizo zipo na maeneo mengine alama hizohakuna kabisa, kitu ambacho kinaweza kikapelekea sasamagari yetu na treni zije zisababishe ajali kubwa hapobaadaye. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikishakwamba wana-fix vibao vinavyoonesha railway crossbarabarani katika njia hiyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwakumekuwa na shida kubwa sana hasa ya wafugaji, hususaniwafugaji wa ng’ombe, hufuga maeneo ambayo nipembezoni mwa barabara na wakati mwingine ng’ombewale hupelekea ajili zisizokuwa za msingi na kwa kuwakumekuwa na tendence ya traffic hasa katibu miji mikubwakama Mwanza, Dar es Salaam, Dodoma na kadhalika,hususani Dar es Salaam ambapo taa za barabarani zinafanyakazi, hapo hapo na traffic wanafanya kazi, kitu ambachokinapelekea ku-confuse madereva barabarani na kuwezakusababisha ajali.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

Je, Serikali inatoa kauli gani juu ya mambo hayamawili?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tumekuwa tukikabiliana nachangamoto za kukosekana katika baadhi ya maeneo alamaza barabarani zinazotakiwa kuelekeza madereva kuonamaeneo ambayo ni hatarishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kulitambua hilo ndiyomaana katika jibu langu la msingi nilieleza kati ya mikakati14 moja katika eneo tulilokuwa tulifanyia kazi ni eneo hilo nakwamba tumejaribu kwa kiasi kikubwa sana kuwezakuwasiliana na kufanya kazi kwa karibu na mamlaka husikaili kuweza kudhibiti na kuweka hizo alama ambazo anasemakuwa zimekosekama. Bahati nzuri Makamu Mwenyekiti waBaraza letu la Usalama Barabani ni Mheshimiwa Naibu Waziriwa Uchukuzi, kwa hiyo tumelifanya hili kwa ufanisi mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tatizo kubwa ambalolinasababisha alama hizi kupotea. Mara nyingi ni kutokanana tabia mbaya za baadhi ya wananchi ambao wamekuwawaking’oa kwa makusudi alama za barabarani na kuvitumiavyuma hivi kama vyumba chakavu. Naomba nitoe wito kwawananchi kuacha tabia hiyo na kwamba mamlaka husikaziko macho kwa wale wote ambao watakiuka sheria za nchi,kwa kung’oa vibao vya alama hizi tutawachukulia hatuaza kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili lilikuwalinahusiana na askari wa barabarani pamoja na taa zabarabarani. Mara nyingi askari wa barabarani wanakaawakati ambao kuna msongamano wa magari barabarani,hasa wakati wa asubuhi wakati watu wanakwenda kazinina wakati wa jioni wanapokuwa watoka kazini. Hii ni kwasababu taa za barabarani zilipowekwa haziwezi kukidhimahitaji ya nyakati husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo kunawakati ambao kuna msafara mwingi unatokea katika

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

upande mmoja, kwa hiyo kutegemea taa za barabaranipeke yake kunaweza kusababisha msongamano mkubwa.Kwa maana hiyo hao traffic police wanakaa pale kwa lengola kudhibiti na kuzuia msongamano huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutaendelea kuhakikishakwamba askari hao wanaendelea kutumika kusaidiakupunguza msongamano wa magari hasa katika nyakatihizo za watu ambao wanakwenda kazini na kurudi kaziniasubuhi na jioni. (Makofi)

MHE. RICHARD P.MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante, nina swali dogo kuhusiana na makazi ya Katumba,yaliyokuwa makazi ya wakimbizi. Makazi haya ya Katumbayana barabara takribani nne ambazo zinaingia kwenye eneohilo. Tuna barabara kuu ya kijiji cha Msaginya ambako kunageti ambalo limekuwa ni usumbufu mkubwa kwa wananchiwa Katumba hususani kuanzia saa 12.00 jioni kutokana nasheria za wakimbizi. Sasa kwa kuwa wananchi wa eneo hilotakribani asilimia 90 wameshapewa uraia na wenginehawaishi ndani ya eneo hilo.

Je, Serikali haioni sasa ni muda muafaka kwa lile getila Msaginya kuendolewa au muda kuongezwa hata ikawasaa 24?

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Naibu Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake tumelichukua natutalitafakari tuone jinsi gani tutalifanyia kazi.

MWENYEKITI: Ahsante, Waheshimiwa tunaendelea naswali namba 99 linaloulizwa na Mheshimiwa HamidaMohamed Abdallah, Mbunge wa Viti Maalum nalinaelekezwa kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa naMichezo.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

Na. 99

Kuboresha Uwanja wa Mpira wa Miguu Lindi

MHE. HAMIDA M. ABDALLAH aliuliza:-

Uwanja wa mpira wa miguu Lindi ulijengwa tangumwaka 1957 wakati wa ukoloni wa Gavana Sir EdwardTwining na mpaka leo haujafanyiwa maboresho.

Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wakuukarabati na kuwa wa kisasa ukizingatiwa kwamba uwanjahuo ulikuwa ukitumika kwa ajili ya michezo ya AfrikaMashariki?

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waHabari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, napenda kujibu swalila Mheshimiwa Hamida Mohamed Abdallah, Mbunge VitiMaalum. kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli uwanja wa mpirawa miguu wa Lindi (Ilula) ni mkongwe ulijengwa wakati waukoloni wa Mwingereza na unahitaji ukarabati ili kuufanyakuwa wa kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya Maendeleo yaMichezo inahimiza kila taasisi yenye kiwanja au viwanja vyamichezo kuvitunza viwanja hivyo ili viweze kudumu. Uwanjahuu upo chini ya Halmashauri ya Lindi kama ilivyo kwa viwanjavingine vingi vilivyoko chini ya Halmashauri hapa nchini.Wizara yangu inashauri Halmashauri ya Lindi kuangaliauwezekano wa kuufanyia ukarabati uwanja huo kwakuwashirikisha wadau mbalimbali pamoja na wananchi waLindi wakiongozwa na Waheshimiwa Wabunge.

Aidha, Wizara yangu itakuwa tayari kutoa ushauri wakitaalamu ili kusaidia kukarabati uwanja huo na kuufanya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

kuwa wa kisasa na kutumiwa na wanamichezo wengi zaidiwa Mkoa huo na Taifa kwa ujumla.

MHE. HAMIDA M. ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Nimshukuru Mheshimiwa Mheshimiwa NaibuWaziri kwa majibu yake mazuri yenye matumaini. NinashukuruSerikali inatambua kwamba uwanja ule unahitajikukarabatiwa na kuwa uwanja wa kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwanja wa Lindiusifananishwe na viwanjwa vingine vilivyojengwa naHalmashauri. Uwanja wa Lindi ni miongoni mwa viwanjavitatu bora vilivyojengwa na wakoloni mana yake nikwamba tumerithi kutoka mikononi mwa wakoloni ikiwemokiwanja cha Mkwakwani - Tanga, kiwanja cha Dar es salaamna kiwanja cha Lindi Manispaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwanja ule umewahikutumika kwa michezo ya Afrika Mashariki, kwa hiyo uwanjaunahistoria ya kipekee kwamba timu za Afrika Masharikizimechezwa katika uwanja wa Lindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wana-Lindi sasa tunahitajikuona uwanja ule unabadilika na kuwa uwanja wa kisasa,tunaiomba Serikali ituambie itatusaidiaje kukarabati uwanjaule? Ninajua kwamba Halmashauri haina uwezo wa fedhawa kukarabati uwanja ule na kuwa uwanja wa kisasa, kwahiyo ninaiomba Serikali ituambie ni namna gani itawezaikatusaidia kukarabati uwanja na kuwa uwanja wa kisasa?

NAIBU WAZIRI, HABARI UTAMADUNI SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasihii kumpongeza sana Mheshimiwa Hamida kwa jinsialivyokuwa mstari wa mbele kufuatilia suala la ukarabatiwa uwanja huu wa mpira wa miguu wa Ilula (Lindi), kwakweli hii imekuwa ni chachu kubwa sana katika maendeleoya ukuaji wa soka katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niishauriHalmashauri ya Lindi kwamba iweke kipaumbele katika

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

kutenga bajeti kwa ajili ya ukarabati wa uwanja huu. Pili,napenda kuchukua nafasi hii kumjulisha Mheshimiwa Hamidakwamba Serikali inalitambua hili na kutokana na hiloimekuwa ikitoa ushauri kwa TFF kuzisaidia Halmashaurikufanya ukarabati wa viwanja kwa kutumia wadaumbalimbali au wafadhili wa ndani na nje ya nchi, na kwanamna hiyo basi TFF imekuwa ikiweka katika orodha kilamwaka walau viwanja katika Halmashauri mbili hadi tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hiikumtaarifu kwamba uwanja wa Ilula upo miongoni mwaorodha ambayo imewekwa na TFF kwa ajili ya ukarabati.Niseme tu kwamba TFF watakapotaka kufanya ukarabatiitabidi waweke mkataba na Halmashauri ya Lindi namkataba huo unasharti kwamba ni lazima kipaumbele chamatumizi kiwe katika mchezo wa mpira, ahsante sana.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Kwa kuwa Chama cha Mapinduzi kirithi viwanjavilivyokuwa mali ya Watanzania kutoka kwa wakoloniwakati sasa nchi imekuwa ya mfumo wa vyama vingi; nakwa vile Chama cha Mapinduzi kimeshindwa kuitunza malihii ya mayatima, ni lini Chama cha Mapinduzi kitarudishaviwanja hivi kwa Halmashauri au Serikali ili irudi mikononikwa Watanzania wote badala ya kuendelea kudhulumu hakihii ya watanzania?(Makofi) [Neno kudhulumu siyo sehemuya Taarifa Rasmi za Bunge]

MWENYEKITI: Mheshimiwa Haji, naomba ili nenodhulumu uliondoe halafu lijibiwe.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwaheshima napenda kuondoa neno kudhulumu na badala yakeliwe kuirejesha haki hii kwa Watanzania wote. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Naibu Waziri waHabari Utamaduni Sanaa na Michezo majibu.

NAIBU WAZIRI, HABARI UTAMADUNI SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa hakuna

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

hati yoyote inayoonekana kwamba Chama cha Mapinduzikimechukua viwanja kutoka kwa mmiliki yoyote, hati zotezinaonyesha ni miliki ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo basinapenda kulithibitisha Bunge lako Tufu kwamba Chama chaMapinduzi kinavifanyia ukarabati viwanja vyake kamazinavyofanya Halmashauri; kwa mfano uwanja wa Singida.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Singida MheshimiwaMartha Mlata anasimamia zoezi hili, upo uwanja wa Mbeyana wenyewe unafanyiwa ukarabati na Chama chaMapinduzi kwa kushirikiana na wadau. Ahsante.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Kwa sababu tunao uwanja wetu wa Taifa (Dares Salaam) ambao ni wa kimataifa na ili kuutangaza uwanjahuo, na ili kutangaza utalii na kuongeza ajira kwa nini Serikalisasa isije na mpango wa kuziomba Balozi zetu nje ili timuzao za Taifa huko ziliko zije kuutumia uwanja wetu wa mpirawa uwanja wa Taifa, na wakimaliza kucheza mpira aubaada ya kucheza mpira wachezaji hao waende kwenyehifadhi zetu ili watangaze utalii wa nchi yetu kupitia uwanjawa Taifa?

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri waHabari Utamaduni Sanaa na Michezo jibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, HABARI UTAMADUNI SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, wazo lakeni zuri, tumelichukua na tutakwenda kulifanyia kazi natutarejesha majibu, ahsante sana.

MWENYEKITI: Asante tunaendelea, swali letu namba100 linaulizwa na Mheshimiwa Albert Obama Ntabaliba,Mbunge wetu wa Buhingwe linaulizwa kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

Na. 100

Ujenzi wa Barabara ya Kasulu – Manyovu Kilometa 48.7

MHE. ALBERT O. NTABALIBA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lamibaraba Mnanila – Manyovu – Kasulu ili kuwasaidia wananchiwa maeneo hayo?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali laMheshimiwa Albert Obama Ntabaliba, Mbunge wa Buhigwe,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Kasulu hadiManyovu yenye urefu wa kilometa 48.7 ni barabara yakiwango cha changarawe na inahudumiwa na Wakala waBarabara (TANROADS) Mkoa wa Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Kasulu hadiManyovu ni sehemu ya mradi wa kikanda wa Barabara yaKibondo - Kasulu hadi Manyovu yenye urefu wa kilometa 250inayofanyiwa mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu wakina kupitia mpango wa NEPAD yaani New Partnership forAfrica’s Development kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleoya Afrika chini ya uratibu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya AfrikaMashariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa kiwango cha lamiwa barabara hii unatarajiwa kuanza baada ya kukamilikakwa mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.

MHE. ALBERT O. NTABALIBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kwanza niipongeze Wizara kwa majibu mazuri,baada ya hapo nina maswali mawili ya nyongeza.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii ya Manyovu -Kasulu imekuwa ni kero kubwa sana hasa wakati huu wamvua na sasa hivi nauli ya kutoka Manyovu - Kasulu imefikiampaka shilingi 10,000; na tunayo barabara nyingi ya lami yakutoka Kigoma mpaka Manyovu yenye urefu wa kilometa60 ambayo nauli yake ni shilingi 3,000. Kwa hiyo, umuhimuwa kujenga barabara hii na kuianza mapema inajionyeshakwa vigezo hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kujua, Wizara imekirikwamba inafanya upembuzi yakifu, wananchi wa Buhigwewanataka kujua upembuzi yakinifu unaisha lini na ujenziunaanza lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Mheshimiwa Raisalipokuwa akijinadi tuliita vijiji vya Mlela, Buhigwe, Kavomo,Nyankoloko, Bwelanka na akaahidi kwamba atajengabarabara ya kilometa tano katika Wilaya ya Buhigwe, je, nilini ahadi hiyo itatimizwa?

MWNEYEKITI: Ahsante, Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naombakumpongeza sana Mheshimiwa Ntabaliba kwa kazi kubwaanayoifanya ya kufuatilia miradi mbalimbali ya Miundombinukatika Wilaya yake na Jimbo lake, nikupongeze sana. Mimininakuhakikishia kama ambavyo tumekuwa tukiwahikishiakatika ofisi zetu mimi na Waziri wangu, kwambatutashirikiana na wewe kuhakikisha mambo yote ambayotuliyaahidi katika Wilaya yako yanatekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katika jibula msingi, ujenzi utaanza baada ya kukamilika upembuzi nausanifu wa kina, kwa maana unaofanywa na kufuatiliwa nawenzetu wa AfDB. Nikuombe tu kwa kuwa anayefanya siSerikali, kazi hii inafanya na AfDB chini ya Afrika Mashariki sualala lini ni gumu kukueleza isije ikaonekana tunasema uongohapa Bungeni. Nikuhakikishie suala hili litakamilika katika

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

kipindi kifupi kijacho na baada ya hapo shughuli za ujenzizitaanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa swali lake la pili,nimuhakikishie, kama ambavyo tulimuhakikishia ofisini,kwamba kilometa zake tano ambazo Mheshimiwa Rais waAwamu ya Tano aliahidi zitatekelezwa mara baada yamasuala haya ya miradi ambayo ni kiporo yatakapokamilika;na uzuri wake sehemu kubwa za viporo zinakamilika mwakahuu ujao wa fedha baada ya hapo tutakamilisha ahadizingine zote ambazo Mheshimiwa Rais aliziahidi hasa zakilometa tano, kilometa sita katika sehemu mbalimbali za Mijiya Tanzania hii.

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge,keshokutwa uwanja ni mpana kwa Wizara hii, leo kidogo,Mheshimiwa Msukuma.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Wananchi wa Jimbo la Geita Vijijinihususan Jimbo la Geita Vijijini ndilo Jimbo pekee linaloongozakwa kupata chakula kingi kila mwaka kwenye Kanda ya Ziwa;wamekuwa na kilio cha barabara yao kutoka Senga -Sungusila - Lubanga mpaka Iseni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wabunge watatuwalionitangulia wote wamekuwa wakiomba Serikalibarabara hii ichukuliwe angalau tu kwa kiwangochangalawe sio lami na Serikali imekuwa ikitoa ahadi kila sikutunafanya tunafanya, na mipango yote sisi kwenye RCCtumeshabariki. Sasa nataka kujua Waziri ni lini barabara hiiunaichukua na kuiweka kwenye angalau kiwango chamolami tu?

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Naibu WaziriUjenzi, Uchukuzi Mawasiliano ni lini utaichukua.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru sanaMheshimiwa Musukuma kwanza kwa kutukumbusha kuhusu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

barabara hii. Aliiongelea muda mrefu, kuanzia miaka yanyuma na sasa tunamuhakikishi kwamba hii barabaraitachukuliwa na TANROADS, kwa maana ya kukasimiwa.Barabara hii haijakidhi vigezo vya kupandishwa hadhi, lakiniWaziri ameshakubali na ameshaikasimu barabara hii ili iwezekutekelezwa na TANROADS Mkoa wa Geita.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Paresso.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa nashukuru kwakuniona Mheshimiwa kwa kuwa barabara ya Tanga -Pangani hadi Bagamoyo ….

MWENYEKITI: Mheshimiwa Paresso. (Kicheko)

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa sera ya masualaya ujenzi ni kuunganisha barabara ya mkoa mmoja namwingine kwa kiwango cha lami, na kumekuwa na ahadiya muda mrefu ya ujenzi kwa kiwango cha lami barabaraya Njiapanda - Karatu - Mang’ola mpaka Lalago, ambayoinaunganisha Mkoa wa Arusha na Mkoa wa Simiyu, je, ni linibarabara hii itajengwa kwa kiwango cha lami?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuombeMheshimiwa Paresso asubiri, ni keshokutwa tu bajeti yetuinakuja, na ramani yote ya shughuli za ujenzi wa barabarazote itakuwa imeanikwa wazi. Nisinge penda kwenda kwaundani kwa sababu ni sehemu ambayo Waziri wanguataishughulikia keshokutwa.

MWENYEKITI: Ahsante tunaendelea WaheshimiwaWabunge swali namba 101 linaulizwa na Mheshimiwa GimbiDotto Masaba, Mbunge wa Viti Maalum na linaelekezwa kwaWaziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji. MheshimiwaGimbi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

Na. 101

Hitaji la Viwanda Mkoa wa Simiyu

MHE. GIMBI D. MASABA aliuliza:-

Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa ambayohaina viwanda licha ya wananchi wake kuwa wakulima nawafugaji.

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga viwandavingi Mkoani Simiyu wikiwemo viwanda vya kusindika nyama,matunda, maziwa, ngozi, mafuta ya kula na nguo ilikuharakisha ukuaji wa uchumi na ongezeko la ajira kwavijana?

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJIalijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali laMheshimiwa Gimbi Dotto Masaba, Mbunge wa Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, azma ya Serikali ya ujenzi wauchumi wa viwanda imeainishwa vyema katika Mpango waPilli wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa mwaka 2016/2017mpaka 2020/2021 wenye dhima ya kujenga uchumi waviwanda ili kuleta mageuzi ya kiuchumi na maendeleo yawatu. Ili kufikia azma hiyo, ushiriki wa mchango wa mtummoja mmoja, makundi ya watu, taasisi za umma na taasisibinafsi unahitajika. Aidha, Serikali kwa kushirikiana na wadauwengine tumeanza kutekeleza mikakati minne ya ngozi,mafuta ya kula, nguo na mazao jamii ya kunde. Wakati huohuo mapango wa wilaya moja, zao moja na uhamasishajiwa ujenzi wa viwanda chini ya SIDO unaendelea nchini kote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kulijulisha Bungelako Tukufu na Watanzania kwa ujumla kuwa Mkoa wa Simiyuchini ya uongozi wa Komredi Anthony Mtaka umekuwa kinarawa kutekeleza mpango wa one district one product. Wilaya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

tano za Bariadi, Busega, Itilima, Maswa na Meatu katika Mkoawa Simiyu zimepangiwa kuzalisha mafuta ya alizeti. VilevileMkoa wa Simiyu una viwanda ambavyo vinaanzishwa kwakuzingatia upatikanaji wa malighafi, teknolojia na soko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Maswakimejengwa kiwanda cha chaki, Wilaya ya Bariadi na Itilimakitajengwa kiwandacha nyama na Wilaya ya Meatukimejengwa kiwanda cha Maziwa. Hizi ni kazi ya mwakammoja na naweza kusema ni mwanzo mzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa taasisi, Mfukowa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unakamilisha taratibu zakuwekeza kwenye kiwanda cha kuzalisha vifaa tibavitokanavyo na pamba na bidhaa za maji (drip). Gharamaza miradi hiyo inakadiriwa kufikia dola za kimarekani 36.5 nakutoa ajira za moja kwa moja 1,600 na zisizo kuwa moja kwamoja 5,000. Mradi huo unakadiriwa kutumia pamba tani50,000 kwa mwaka. Aidha, Serikali ya Mkoa inaendelea najitihada za kutenga maeneo ya uwekezaji kwa kuwalengawajasiriamali wadogo, wa kati mpaka wakubwa bila kujalikwamba wanatoka ndani ya nchi au nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshauri MheshimiwaMbunge tushirikiane katika kuhamasisha wawekezaji wandani na nje kuanzisha viwanda na kusindika mazao ya kilimokatika Mkoa wa Simiyu ili kuhakikisha ukuaji wa uchumi nakuongeza ajira kwa vijana.

MHE. GIMBI D. MASABA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili yanyongeza. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri, wakatiSerikali inahamasisha wadau na jamii kujenga viwanda hivi,je, Serikali inatoa kauli gani kwa viwanda ambavyoilivianzisha na imevitekeleza, kama vile kiwanda cha NasalGinnery, Ngasamwa Ginnery, Rugulu Ginnery, MalampakaGinnery na Solwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kukosekanakwa bei nzuri ya ng’ombe na wananchi wa Mkoa wa Simiyu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

kulazimika kusafirisha ng’ombe wao kupeleka Jiji la Dar esSalaam, je, Serikali inatoa kauli gani na mkakati madhubutiwa kuhakikisha kwamba wanajenga viwanda vya nyamakama alivyojibu kwenye swali lake la msingi, kwambawatajenga Bariadi na Itilima. Ni lini mkakati wa makusudiwa kuharakisha kujenga viwanda hivyo? (Makofi)

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na hili la pili, sehemu ya Mkoawa Simiyu ni maarufu kwa ufugaji wa ng’ombe na zao lapamba. Juzi Mkuu wa Mkoa, Mheshimiwa Anthony Mtakaalikutana na wataalam wangu wa uwekezaji katika jitihadaza kusaidiana kutafuta wawekezaji. Wawekezajiwanatafutwa, kwa hiyo, tunachofanya ni sekta binafsiitakayowekezwa kwa hiyo tunatafuta wawekezaji wajewawekeze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali langu la pilinilikuomba Mheshimiwa Mbunge na wewe uingie kwenyeboti hiyo hiyo ya kuwatafuta wawekezaji. Tunatafutawawekezaji i l i wawekeze, ndiyo namna ya kupatawawekezaji. Nitumie fursa hii, kuwashukuru Wabunge ambaommekwenda maili moja zaidi na kuwatafuta wawekezaji,ambapo mimi kazi yangu ni kuwaondolea vikwazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la kwanza,kwamba vipo viwanda ambavyo vilibinafsishwa, vipoviwanda ambavyo vimekwama, kauli ya Serikali ni kwambawale waliokuwa na viwanda vile, walio vinunua au vyakwao wavirudishe katika shughuli vifanye kazi. Tunachofanyasasa chini ya Treasure Registrar Wizara yangu na Wizara zakisekta zinazohusika tunawafuata wale kuwashawishikutumia nguvu zote ili warudi katika shughuli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuhusu viwanda vyapamba naomba niwatoe hofu watu wanaolima pamba,chini ya mkakati wa pamba mpaka mavazi tuna imanikwamba uzalishaji wa pamba kwa tija utalazimisha viwandavile vifufuke kwa sababu the supply itakuwa nyingi naviwanda vitafanya kazi, tuwe na subira. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

MWENYEKTI: Asante Mheshimiwa Stanslaus Nyongo namwingine ni Mheshimiwa Halima.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi na miminimuulize Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Maswa imekwishakutenga eneo kwa ajili ya uwekezaji (EPZA) zaidi ya heka 110,na Mheshimiwa Waziri tulishakuja kuleta barua na EPZAwalishakubali kuwekeza hapo, lakini mpaka sasa hivi hakunamkakati wowote unaoendelea. Naomba kauli yako nacommitment ya Serikali, je, ni lini Serikali sasa au EPZA watakaana Halmashauri ya Maswa na kuweza kuanzisha mradi huukatika maeneo haya? Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Waziri waViwanda, Biashara na Uwekezaji kwa kifupi tu.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimjibu MheshimiwaNyongo kuhusu eneo la uwekezaji la Maswa na tunashukurutumelipata eneo la Maswa na Mheshimiwa Nyongonimshukuru ni miongoni mwa Wabunge ambao wamejasiriakutafuta maeneo ya uwekezaji bila vikwazo. Kuna wenginemaeneo yao yanakuwa na vikwazo vikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kitakachofuata,kama nilivyofanya kwa Bunda, Bunda nimeishaitangazakuwa special economic zone; nitaitangaza Maswa halafusasa tutaanza kutafuta wawekezaji.

Nirudie Waheshimiwa Wabunge Wawekezajiwanatafutwa dunia nzima na Tanzania si destnation pekeyake, wana-move kutoka Asia kuja Afrika, Afrika si Tanzaniapeke yake. Kwa hiyo, tuweke mazingira wezeshi tuwewakalimu waje kusudi tutengeneze ajira.

MWENYEKITI: Ahsante, swali la mwisho MheshimiwaHalima.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

MHE. HALIMA ALI MOHAMMED MheshimiwaMwenyekiti, ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimuulizeMheshimiwa Waziri, je, Serikali ina mkakati gani mahsusi wakuhakikisha kwamba Sera ya Tanzania ya viwandainamkomboa kweli mwanamke wa Kitanzania?

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Waziri waViwanda, Biashara na Uwekezaji tumkomboe mwanamkekupitia Viwanda.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, unapozungumzia uwekezaji katikaviwanda unazungumzia akina mama; na nguvu kubwa yaujenzi wa uchumi wa viwanda, viwanda ambavyo nisustainable, viwanda ambavyo ni darasa, ni viwanda vidogosana, viwanda vidogo na vya kati. Katika shughuli zakuhamasisha viwanda hivi mimi ninaokutana nao watupu niakina mama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna shirika la akina mamala Food Processing liko Dar es Salaam, Binti Nasibu ndiyeMwenyekiti wake. Tunawatafuta akina mamatunawahamasisha kusudi muanze viwanda vidogo na vyakati ili kusudi mkue mfundishe na wazazi wenu. Mama akipatakiwanda na wajukuu wanapata kiwanda, na mama zaowanapata viwanda nchi yote inakuwa ya viwanda. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, tunaendelea.

MWENYEKITI: Swali linalofuata 102 linaulizwa naMheshimiwa Zuberi Mohamed Kuchauka Mbunge wa Liwalena linaelekezwa kwa Waziri wa Fedha na Mipango.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

Na. 102

Kuhusu Kubinafsifishwa kwa Shirika la Usagaji la Taifa(NMC)

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:-

Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC) lililokuwa namatawi karibu nchi nzima na assets mbalimbali lilibinafsishwakutokana na sera ya ubinasfishaji.

(a) Je, ni matawi mangapi yamebinafsishwa namangapi yamebaki mikononi mwa Serikali?

(b) Je, Serikali imepata fedha kiasi gani kutokana naubinafsishaji huo?

(c) Kati ya matawi yaliyobinafsishwa ni mangapiyanaendeshwa kwa ubia wa Serikali?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waFedha na Mipango napenda kujibu swali la MheshimiwaZuberi Mohamed Kuchauka, Mbunge wa Liwale, lenyevipengele (a) (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Idadi ya matawi ya Shirika la Taifa la Usagishajiyaliyobinafsishwa ni 22 na yaliyobaki mikononi mwa Serikalini matano;

(b) Katika kubinafsisha mali za NMC Serikali imepatafedha kiasi cha shilingi 7,491,611,000; na

(c) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika matawi yaliyobakihakuna tawi linaloendeshwa kwa ubia kati ya Serikali namwekezaji. Matawi hayo kwa sasa yanasimamiwa na Bodiya Nafaka na Mazao mchanganyiko. Hata hivyo, tawi laNMC - Arusha maarufu kama Unga Limited limekodishwakwa Kampuni ya Monaban Trading Company Limited.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Zuberi.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Niseme tu nasikitika kwa majibu ambayo ni rahisi,majibu mafupi, majibu ambayo hayaoneshi matumaini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyoMheshimiwa Naibu Waziri...

MWENYEKITI: Uliza swali.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: ...anasema ubinafsishajiwa matawi 22 yaliyokuwa National Milling tumepata shilingibilioni 7.4, ni masikitiko makubwa sana; na hii inaonyeshamoja kwa moja kwamba sisi huu umasikini umetuandama.kwa sababu kama tunaweza tukatupa…

MWENYEKITI: Uliza swali Mheshimiwa.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: ...ni masikitiko makubwasana. Msheshimiwa Mwenyekiti, najenga hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Muda.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kuna matawi kama Plot 33, Plot 5, Tangold yale matawi sasahivi yote ni ma-godawn. Watu walionunua matawi yaNational Milling ambayo yanafanya kazi ni Bakheresa naMohamed Enterprises peke yake, lakini matawi mengine yoteyaliyobaki yamekuwa ma-godawn na ninyi mnasemamnaenda kwenye viwanda, mimi hapa sijapata kuelewa.Nini hatima ya hayo mashirika ambayo sasa hivi ni ma-godawn badala ya kuwa viwanda? (Makofi)

(b) Kwanza niseme wazi kwamba na mimi ni mmojakwenye taaluma hii ya usindikaji wa nafaka. Nimefanya kaziNational Milling si chini ya miaka 10. Kwa upande wa Kurasinimnamo tarehe 31 Aprili, 2005 waliletewa barua aliyekuwaMeneja pale kwamba kiwanda hicho akabidhiwe Mohamed

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

Enterprises anayekaribia kununua, alikabidhiwa tu kwasababu anakaribia kununua. Si hivyo tu, wafanyakaziwaliokuwepo pale mpaka leo hii wanaidai Serikali hii zaidiya shilingi milioni 234.3, bado hatima yao haieleweki na kesiimekwisha. Vilevile si hivyo tu, tarehe 20…Hazina wameitwamahakamani hawataki kwenda, nini hatima ya wafanyakaziwale? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwakifupi tu, maswali haya mawili.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, swali lake la kwanza nini hatima ya hayoMashirika ambayo yalikodishiwa na sasa sio viwanda ni ma-godown. Naomba kumkumbusha Mheshimiwa Mbungekwamba Serikali ilishaanza mchakato wa kufanya tathiminiya viwanda vyote vilivyouzwa na ambavyo vimegeuzwamatumizi.

Mheshimiwa Waziri wa Viwanda alishasimama hapana kusema na ndiyo kauli ya Serikali, kwamba vyote hivyovitarejeshwa Serikalini na vitaendelea kufanya kazi, navitatafutiwa wawekezaji na wataendelea kuviendeshaviwanda hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili linalohusuhatima ya wafanyakazi, ameshasema kesi iko mahakamani,ikishakuwa mahakamani naomba nisiliongelee hapa na niimani yangu kwamba kesi hiyo itaendeshwa na itafika mwishomzuri. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Waheshimiwa tunaendela.Swali linalofuata swali namba 103 linaulizwa na MheshimiwaYahaya Massare, Mbunge wa Manyoni na linaelekezwa kwaWaziri wa Maliasili na Utalii.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

Na. 103

Sheria ya Usafirishaji wa Mazao ya Misitu

MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:-

Tanzania ni nchi yenye misitu mingi na Sheria yaUsafirishaji wa Mazao ya Misitu inazuia kusafirisha zaidi yasentimeta15 au inchi sita.

Je, Serikali imepata hasara kiasi gani kwa kuruhusuusafirishaji wa sentimeta 20 sawa na inchi nane ili kujengauwezo wa kiushindani na nchi nyingine katika soko?

MWENYEKITI: Ahsante, majibu Mheshimiwa NaibuWaziri wa Maliasili na Utalii Engineer Ramo Makani.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waMaliasili na Utalii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa YahayaOmary Massarem, Mbunge wa Manyoni Magharibi, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha 50 cha Kanuniza Sheria ya Misitu kinakataza kusafirisha magogo nje ya nchi.Sheria hiyo pia hairuhusu kuuza nje ya nchi mbao zote zenyeunene unaozidi inchi sita, uamuzi ambao azma yake kubwani kutoa fursa ya kukuza viwanda ndani ya nchi na kupanuawigo wa ajira kwa vijana nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kwa mujibu washeria, Serikali hairuhusu usafirishaji wa mbao zenye unenewa sentimeta 20 sawa na inchi nane ni dhahiri kwambahaiwezi kuwa na takwimu za hasara iliyoipata kwa kuruhusuusafirishaji wa mbao za unene huo.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Massare.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi hii, pia nashukuru kwa majibu yaMheshimiwa Naibu Waziri. Lakini pamoja na majibu hayomazuri nina maswali madogo tu ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ya Maliasili kupitiaTFS imekuwa ikitoa vibali vya kuvuna mazao ya misitu.Mvunaji anaanzia vijijini, Wilayani kwenye kanda na hadiWizara, lakini kabla ya kuruhusiwa kuvuna mazao ya misitu,Serikali imekuwa ikiwasajili wadau hawa na kuwatoza pesakila mwaka. Vilevile kumekuwepo na tatizo kubwa la Wizarahii kuwa ikishatoa vibali hivi inachukua muda mfupi tu kuvifutakama ilivyokuwa mwaka huu ambapo vilitolewa vibalizikiwemo approval za…

MWENYEKITI: Swali.

MHE. YAHAYA O. MASSARE: … kutoka nchi za nje nabaadae vilifutwa na Mheshimiwa Waziri, sasa swali.

(a) Je, ni lini Serikali itaacha utaratibu huu mbaya naambao unawatia hasara wadau wao?

(b) Serikali haioni sasa ni vyema isitoe approval hizihadi i j ir idhishe kwamba wananchi na wadau hawawakipewa vibali hivyo watafanya kazi kwa mwaka mzimakuliko kama hivi wanatoa na kufanya kazi kwa miezi miwilitu na kuwasimamisha?

MWENYEKITI: Ahsante, Naibu Waziri wa Maliasili naUtalii majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, kwa ufupi suala la uvunaji wa maliasili linatokanana ukweli kwamba nia na dhamira ya Serikali ni kuliwezeshaTaifa hil i kuweza kutekeleza mipango yake yote yamaendeleo kwa kutumia rasilimali za Taifa hili ikiwemomaliasili. Jambo la msingi ni kwamba tunatakiwa kutumiamaliasili hizo kwa namna ambayo ni endelevu. Kwa hiyo,udhibiti haumaanishi kwamba rasilimali hizi au maliasili hizo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

zisitumike kabisa, hapana, nia ya Serikali ni kuhakikishakwamba tunafanya matumizi endelevu ili tuweze kuendanahata na malengo ya Umoja wa Mataifa ya MaendeleoEndelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kuhusu swali lakemoja kwa moja la utaratibu wa utoaji wa vibali, huo niutaratibu ambao utatuwezesha kutoa fursa kwa kilamwananchi ya kuweza kushiriki katika uvunaji wa raslimalihizo. Lakini ikiwa kwamba, utaratibu huo unaonekanapengine una kasoro basi kwa kuwa ulikuwepo kwa mujibuwa sheria basi…

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naombautulivu Bungeni.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge anayo fursa ya kufuatautaratibu wa kawaida wa kuleta maoni ili tuweze kupitiaupya sheria hiyo.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na swali letu lamwisho, swali namba 104 linaulizwa na Mheshimiwa JosephGeorge Kakunda, Mbunge wa Sikonge kwa Wizara hiyo hiyoya Maliasili na Utalii.

Na. 104

Kumega Sehemu ya Hifadhi kuwapa Wananchi – Sikonge

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza:-

Kati ya mwaka 1954 na 1957 kulifanyika zoezi la upimajiwa maeneo ya Hifadhi za Misitu, Mapori ya Akiba na Hifadhikatika Wilaya ya Sikonge ambapo kulikuwa na wakazitakribani 16,000 na ng’ombe wapatao 2500. Kwa sasawakazi wameongezeka hadi kufikia takribani 300,000 nang’ombe wapo takribani 200,000 lakini eneo la kuishi, kulimana malisho ya mifugo na shughuli nyingine za kiuchumi ni lilelile la asilimia 3.7 ya eneo lote la Wilaya huku eneo la Hifadhi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

likibaki asilimia 96.3 na hali hii inasababisha migogoro katiya wakulima, wafugaji na warina asali dhidi ya MaafisaMaliasili.

(a) Je, ni lini Serikali itawaongezea wakazi wa Wilayaya Sikonge eneo la kuisha, kulima na kulishia mifugo kutokaasilimia 3.7 hadi angalau asilimia 25 ya eneo lote la Wilaya?

(b) Je, Serikali haioni kuwa kuongeza eneo la Wilayahiyo kwa asilimia 25 kutaepusha migogoro iliyopo sasa nahivyo wananchi watatekeleza shughuli zao kwa amani nautulivu huku wakilinda mazingira pamoja na hifadhi?

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu WaziriMaliasili na Utalii, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waMaliasili na Utalii naomba kujibu swali la Mheshimiwa JosephGeorge Kakunda, Mbunge wa Sikonge, lenye sehemu (a) na(b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulingana na takwimu zaTaasisi ya Takwimu ya Taifa (The National Bureau of Statistics)na Sensa ya mwaka 2012, Wilaya ya Sikonge ina ukubwa wakilometa za mraba 27,873 na idadi ya watu wapatao 179,883.Aidha, maeneo ya hifadhi za misitu na wanyamapori yanaukubwa kilometa za mraba 20,056.94 sawa na asilimia 72 yaeneo lote la Wilaya, hivyo kufanya eneo la makazi na shughulinyingine za binadamu kuwa sawa na asilimia 28.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hifadhi za misitu na maporiya akiba katika Wilaya ya Sikonge ni muhimu kwa uhifadhina maendeleo ya sekta nyingine, ikiwa ni pamoja na kuwavyanzo vya mto Ugalla, ziwa Sagara, Nyamagoma na ardhioevu ya Malagarasi - Moyowosi. Kwa mantiki hiyo, kugawamaeneo haya na kuruhusu shughuli za kibinadamukutahatarisha upatikanaji wa rasilimali za maji kwa ajili yashughuli za uvuvi, kilimo, ufugaji, matumizi ya nyumbani na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

mengineyo kwa kiasi kikubwa. Muhimu zaidi ni mchangomkubwa wa misitu hiyo katika hali ya hewa na udhibiti wamabadiliko hasi ya tabianchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imethibitika kwamba kilimocha kuhama hama, ikiwa ni pamoja na utumiaji wa maeneomakubwa ya ardhi; ufugaji wa kuhama hama ukijumuishauingizaji wa mifugo katika maeneo yaliyohifadhiwa, nimatumizi mabaya ya rasilimali ardhi na yasiyo na tija kwaTaifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi nitumie nafasi hiikuwakumbusha na kuwaomba wananchi kwa kushirikianana uongozi wa Halmashauri za Wilaya husika, kuchukua hatuaza makusudi kuandaa na kutekeleza mipango ya matumizibora ya ardhi; hatua ambazo zitasaidia kuondoachangamoto za mahitaji ya ardhi katika Wilaya zote nchiniikiwa ni pamoja na Wilaya ya Sikonge iliyoko Mkoani Tabora.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Joseph Kakundaswali la nyongeza.

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Mwenyekitinashukuru kunipa nafasi. Niseme wazi kabla sijauliza maswalimawili ya nyongeza kwamba wananchi wa Sikongewemesikitishwa sana na majibu ya Serikali. Ninayo maswalimawili ya nyongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kutumia takwimuza Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) za mwaka 2012 kama zilivyoni sahihi, lakini je, Serikali haioni kuwa kutumia takwimu hizobila kufanya projections kwa kutumia formular rasmi iliyokwenye taarifa ya uchambuzi ya NBS inaweza kusababishatakwimu zisizo sahihi kwa mwaka 2017 na hivyo kusababishaBunge hili pamoja na wananchi kuamini kuwa Serikaliimelidanganya Bunge pamoja na wananchi? Hilo la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kwa kuwa takwimurasmi zilizoko kwenye Halmashauri yetu ya Wilaya ya Sikongepamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, ambazo pia ndizo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

alizonazo Mkuu wa Idara ya Maliasili wa Halmashauriinaonyesha kwamba kati ya kilometa za mraba 27,873 zaWilaya ya Sikonge, kilometa za mraba 26,834 ambayo ni sawasawa na asilimia 96.3 ni hifadhi za misitu, wanyamapori,mapori ya akiba na maeneo mengine ya hifadhi ambayoyote hayo yako chini ya udhibiti na dhamana ya Kisheria yaWizara ya Maliasili na Utalii. Je, wananchi tumebaki nakilometa za mraba elfu moja na thelathini na...

(Hapa sauti ilikatika)

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: …hili la pili, Serikali itateualini timu yake ije kufanya kazi na timu yetu Sikonge, ili kusuditupate suluhisho la kudumu kuhusu takwimu hizo?

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tuwetunaenda moja kwa moja kwenye maswali. MheshimiwaNaibu Waziri Majibu.

NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, jambo la kwanza, takwimu huwa zina chanzo,na mara nyingi unapokuwa unataka kunukuu takwimu nilazima useme chanzo cha takwimu hizo yaani hizo takwimuni kwa mujibu wa nani aliyezifanya. Takwimu zina mwenyewena mwenye takwimu ni lazima awe ni mtu mwenye mamlakana kwa Taifa hili takwimu ni mali ya Mtakwimu Mkuu waSerikali. Kwa hiyo, takwimu nilizozitumia kwa kuwa ni zaMtakwimu Mkuu wa Serikali sina shaka kwamba takwimuhizi ni sahihi na hizi ndizo takwimu zinazotakiwa kutumika

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kufanya projectionskwamba ilitakiwa kuzitoa kutoka mwaka 2012 kuzileta leo,hiyo inaweza kuwa ni hoja, lakini ingekuwa ni hoja tu kamakweli hoja ya takwimu ingekuwa ni ya msingi kutokana naswali la msingi lililoulizwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ifahamike kabisakwamba nchi yetu ndio nchi inayoongoza duniani kwa kuwana eneo kubwa lililotengwa kwa ajili ya uhifadhi kwa ajili yawanyamapori, misitu na hifadhi nyingine. Sisi tumetenga

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

asilimia 25 ya eneo zima la nchi yetu, hiyo inatosha kutumaujumbe kwamba ni kweli tumehifadhi maeneo makubwa.Lakini hatukufanya hivyo kwa makosa, tulifanya hivyo kwasababu za msingi ambazo ndio zimekuwa zikitupa faidanyingi sana zinazotokana na uhifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pil i,tunapozungumzia uhifadhi kwenye eneo la Sikonge ifahamikekabisa kwamba uhifadhi huo sio kwa ajili ya Sikonge. Kila eneolililohifadhiwa hapa nchini limehifadhiwa kwa maslahi yaTaifa. Eneo hilo litaweza kupitiwa pale ambapo kama Taifatutaona kwamba kweli kuna haja ya kufanya mapitio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naombanimuombe Mheshimiwa Mbunge, pamoja na kumpongezakwamba yuko hodari wa kufuatilia masuala yanayohusuwananchi wake, na yeye atakumbuka vizuri kabisa kwambamwanzoni mwa mwaka huu tulikuwa wote Sikonge,tumepita kwenye maeneo yake, nami napenda wananchiwa Sikonge wajue kabisa kwamba wanao jembe, Mbungewao ni mfuatiliaji sana wa masuala yanayohusu wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini wakati huo huonataka nimuombe kwamba atumie fursa hiyo ya kuwakilishawananchi kwa kuwaambia ukweli kwamba akiba ni akibana tunatakiwa kuyahifadhi maeneo yale kama akiba.Tutaweza kuyatumia pale tu itakapotokea kwamba kunaulazima wa kuweza kufanya vinginevyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la Serikalikuteua timu, nirudie tu kwamba tayari timu ipo na iko kazinina inaendelea na kazi hiyo, kinachosubiriwa sasa hivi ni waona ile kazi yao kukamilika na kuweza kuleta mrejesho Serikalinikwa ajili ya kuweza kupiga hatua kutekeleza masuala hayayanayohusiana na upitiaji upya wa kile ambacho tunachohivi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la mwisho kabisaniseme kwamba kamwe Serikali haitaweza kufikia mahaliikaamua tu haraka haraka kuweza kuyaondoa maeneo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

yaliyohifadhiwa kwa matumizi mengine bila kufanya tathminiya kuangalia kwamba maeneo yasiyohifadhiwa yametumikakwa tija. Kwa hiyo, jambo la msingi ni kuhakikisha kwambamaeneo ambayo hatujahifadhi yanatumika kwa tija kwanzandipo tuanze kugusa maeneo ambayo yamehifadhiwa kwaajili ya akiba ya Taifa hili kwa ajili ya kizazi kijacho.

MWENYEKITI: Ahsante.

Waheshimiwa Wabunge maswali na majibu yetuyamekula muda mwingi wa shughuli nyingine za Bunge letu.Ninyi ni watu wazima mnanielewa ninachokisema. Ombilangu la kwanza, utulivu Bungeni. Leo kidogo WaheshimiwaWabunge mnamashauriano, sijui yanahusu nini. Mshaurianelakini kwa staha, hilo ndilo ombi langu.

Tangazo la wageni tulio nao hapa Bungeni, kwenyeJukwaa la Spika tuna wageni tisa ambao ni WaheshimiwaWabunge kutoka Bunge la Zambia. Please be up standing,ambao pia ni Wajumbe wa Kamati ya Miundombinu kutokaBunge hilo. Walikuja kujuana na kufanya majadiliano nawenzetu wa Kamati yetu ya Miundombinu. (Makofi)

Niwatambue sasa Wabunge hao ni MheshimiwaDouglas Syakalima, Mwenyekiti wa Kamati na kiongozi wamsafara, Mheshimiwa Robert Lihefu, Mbunge, MheshimwaGiven Kituta, Mbunge, Mheshimiwa Anthony Mumba,Mbunge, Mheshimiwa Gift Sialubalo, Mbunge, MheshimiwaYizukanji Siwanzi, Mbunge, Mheshimiwa Gerald Zimba,Mbunge, Mheshimiwa Peter Daka, Mbunge na NduguChitachu Mumba, Katibu wa msafara. Karibuni sana, we aregreat to have you with us from our sister Parliament of theRepublic of Zambia.(Makofi)

Wageni wengine wanne ambao tunao hapa niwageni wa Mheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi,Waziri wa Katiba na Sheria, ni wageni wanne ambao niNdugu Amon Mpanju, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara yaKatiba na Sheria, Jaji Kiongozi Mheshimiwa Jaji FerdinandWambali, karibuni sana. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

Pia tuna Jaji Mfawidhi Mheshimiwa Jaji MwanaishaKwariko, Jaji wa Mahakama Kuu, Jaji Latifah Mansoor;Mtendaji Mkuu wa Mahakama si mwingine ni ndugu yetuHussein Katanga. Karibuni sana, tunajua leo mpo hapa kwaajili ya shughuli kubwa. Hawa wameongozana na wakuuwa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria ambao niWakurugenzi na Maafisa mbalimbali katika Wizara ya Katibana Sheria. (Makofi)

Tuna mgeni wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaana Michezo ambaye ni Bi. Asha Ally Mabula, ambaye nimshindi wa kwanza wa Tanzania Miss Super Model mwaka2017 ambaye ataiwakilisha nchi yetu Tanzania katikamashindano ya World Super Model yatakayofanyika MjiniMacau, China tarehe 21 hadi 28 Mei, 2017. Yuko wapi? Huyohapo! Tunakutakia kila la kheri katika jukumu hili kwako, lakinini kwa Tanzania lakini pia. (Makofi)

Tuna wageni mbalimbali wa Waheshimiwa Wabungena pia waliokuja kwa shughuli za mafunzo, hilo ni kundi lakwanza. Pia mkiangalia upande huu wa jukwaa la wagenimnaona lilivyopendeza leo. (Makofi)

Sasa hawa vijana ni askari polisi, mnaona sura mpyaya Jeshi sasa hivi, vijana succession plan inaanza namna hiyona tutaendelea. Lakini ni wageni wa Mheshimiwa Waziri wetuwa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa MwiguluNchemba. Napenda tu niwahakikishieni vijana, simamenimko Bungeni. (Makofi)

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Lissu piga makofi!

MWENYEKITI: Tunashukuru, karibuni sana. Tutambuana tunathamini kazi nzuri mnayoifanya kwa niaba ya Taifahili, endeleeni, kazeni buti. Waziri wenu ni Waziri mahiri sanana Waziri timamu sana. Karibuni, kaeni.

Nina matangazo, nianze na tangazo linatoka kwaMheshimiwa Mwenyekiti Anna Lupembe, Mwenyekiti waIbada, anawatangazia Waheshimiwa Wabunge wote kwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

Imani ya Kikristu kuhudhuria Ibada katika chapel iliyopo jengola Pius Msekwa, ghorofa ya pili, leo siku ya Jumanne, tarehe25 Aprili mara baada ya kusitisha shughuli za Bunge saa sabamchana. Aidha, wanamaombi ya Mkoa wa Dodoma nakwaya ya New Jerusalem watahudhuria ibada hiyo.

Tangazo la pili linatoka kwa Mheshimiwa WilliamNgeleja, Mwenyekiti wa Bunge Sports Club. Anaombaawatangaziwe Waheshimiwa Wabunge kuwa keshoJumatano tarehe 26 Aprili, 2016 kutakuwa na mechi ya kirafikiya mpira wa miguu (football) na mpira wa pete (netball)kati ya Waheshimwa Wabunge na Wajumbe wa Baraza laWawakilishi kwenye uwanja wa Jamhuri hapa Dodomakatika sherehe za kutimiza miaka 53 ya Muungano waTanganyika na Zanzibar.

Mechi hiyo ya Waheshimiwa Wabunge na Wajumbewa Baraza la Wawakilishi itakayofanyika saa tisa alasiriitakuwa ni utangulizi kabla ya mechi kati ya timu ya Yangana timu ya Polisi Dodoma. Kwa hiyo, WaheshimiwaWabunge wote na wananchi mnaombwa kuhudhuria.(Makofi)

Tangazo la tatu, Mheshimiwa Mwenyekiti wa Umojawa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) MheshimiwaMargret Sitta (Mbunge) anaomba niwatangazie Wabungewanawake wote kuwa kesho tarehe 26 Aprili, 2017 kutakuwana semina kwa ajil i ya Wabunge wanawake woteitakayofanyika katika ukumbi wa zahanati ya zamani yaBunge (the old dispensary). Semina hiyo itafanyika saa nanemchana, kwa hiyo mnakaribishwa.

Waheshimiwa Wabunge, hayo ndiyo matangazotuliyo nayo. Baada ya hapo sasa tuanze mambo yetu.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiri,Mwongozo.

MBUNGE FULANI: Mwongozo.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiri,Mwongozo wa Spika.

MWENYEKITI: Si mniruhusu nikae.

MBUNGE FULANI: Si ndiyo tumekuruhusu Mheshimiwa.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MWENYEKITI: Mwongozo, naanza na MheshimiwaSitta.

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi…

MWENYEKITI: Ngoja niorodheshe kwanza!Mheshimiwa Chumi.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Msigwa.

MWENYEKITI: Huku wametosha mnaonaje tukichukuawawili wawili tu.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mheshimiwa Haonga.

MWENYEKITI: Ndiyo.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Msigwa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Haonga.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mheshimiwa Kuchauka.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mheshimiwa Haonga.

MWENYEKITI: Unajisemea tu wewe! Wawili wawiliinatosha kwa leo. (Kicheko)

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mwongozo Mheshimiwa.

MWENYEKITI: Haya.

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mheshimiwa Japhary.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MWENYEKITI: Basi kama ni hivyo tutende haki tu,Haonga.

MBUNGE FULANI: Eeh tenda haki tu, eeh Haonga eeh!

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Japhary tayari!

MWONGOZO WA SPIKA

MWENYEKITI: Sasa tunaanza na Mheshimiwa MargaretSitta. (Makofi)

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi yakutoa mwongozo kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, natumia kifungu 68, wakatihuo nikielewa kwamba inawezekana mwongozo ninaotakakutoa hauhusiani pengine na kanuni mojawapo maalum nawakati huo inawezekana pengine haihusiki moja kwa mojana matukio ya leo, lakini naomba mwongozo wako kuhusuBinti yetu Asha Ally Mabula aliyesimama hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naombamwongozo kuhusu kumpongeza kwa dhati kwa nafasi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

aliyopata, lakini kwa la pili ni kwamba, mwongozo wakoutusaidie, binti amefanya vizuri, tuna haja ya kumpongezakwanza; lakini la pili kumuwezesha aweze kusafiri ashirikikatika mashindano mengine. Kwanza atangaze jina laTanzania, lakini pili ajiendeleze naye mwenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mwongozo wakoili wapendwa Waheshimiwa Wabunge kutokana na moyowaliouonesha kwa Serengeti Boys tunaomba piawamwoneshe huyu binti kwa kumchangia angalau si chiniya shilingi 30,000. Naomba mwongozo wako MheshimiwaMwenyekiti. Naomba kutoa hoja wenzangu mniunge mkonoupande wote. (Makofi)

MWENYEKITI: Haya, kaeni tu. Tunaendelea,Mheshimiwa Haonga.

MHE. PASCHAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninaomba mwongozo wako kwa Kanuni ya 68(7) kuhusujambo lililotokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, gazeti la leo la Mtanzaniatoleo namba 8526 limeeleza habari za kufukuzwa kwaMkurugenzi Mkazi wa UNDP ambaye aliletwa na UN.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkurugenzi huyuamefukuzwa ndani ya saa 24 na ameambiwa aondoke chiniya ulinzi mkali sana, na wanadai kwamba anaingilia mamboya ndani ya Serikali ikiwa ni pamoja na suala la uchaguzi waZanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili naona linawezakuleta shida kubwa sana. Watanzania ambao nchi yetu niwanachama wa UN na suala hili la kumuondoa chini ya ulinzimkali tumemu-harass sana. Suala hili linaweza kutuletea shidasana kidiplomasia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kauli ya Serikalikuhusu suala hili ambalo limejitokeza kwa sababu binafsinaliona kama litatuletea shida kama nchi yetu, na kwa kweli

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

linapokuwa linaharibika jambo ninaamini kabisa kwambawanaoathirika ni nchi nzima, ni sisi Watanzania wote kwaujumla. Ninaomba kauli ya Serikali kuhusu jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Mwongozowako. Ahsante sana.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na MheshimiwaJaphary Michael.

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba Mwongozo wako kupitia Kanuni ya 68(7) ikiendana Kanuni ya 64(1)(d), kuhusu jambo ambalo linalotamkwalinaloweza likadhalilisha nafasi ya Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana wakati MheshimiwaWaziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI anajaribu kujibu Mwongozouliotolewa na Mheshimiwa Kubenea kuhusu tatizo la Wakuuwa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kujichukulia maamuzi dhidiya watumishi walio katika ngazi zao katika Halmashauri namaeneo mengine yaliyo chini yao, Mheshimiwa Wazirialisema kwamba Wakuu wa Mikoa na Wilaya ni Marais waMikoa na Wilaya zile. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba Mwongozowako, iwapo ni jambo sahihi kwa Wakuu wa Mikoa kuitwaMarais wa Mikoa yao, na kwamba ni sahihi kuvunja Katibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Mwongozo wakokatika hili, na kama ni kosa, basi Mheshimiwa Waziri aomberadhi na ajirekebishe na asifanyie mzaha kiti cha Rais. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Chumi.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Mwongozo wangu Mheshimiwa Mama Sittaameshaufilisi. Nakushukuru sana.

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Msigwa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikushukuru. Mwongozo wangu nauomba kupitia Kanuni ya64, lakini nitaisoma na Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania; 64.-(1) Bila kuathiri masharti ya Ibara ya 100 yaKatiba yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo namajadiliano katika Bunge, Mbunge:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 100 ya Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania moja inasema; 100.-(1)Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibukatika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa nachombo chochote katika Jamhuri ya Muungano au katikaMahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na Ibara ya 59(1) ya Katibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kutakuwana Mwanasheria Mkuu wa Serikali, inaeleza pale. Namba59(2) Mwanasheria Mkuu atateuliwa kutoka miongoni mwawatumishi wa umma wenye sifa ya kufanya kazi za uwakiliau watu wenye sifa ya kusajiliwa kuwa wakili na amekuwana sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi natano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namba mbili, Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania inaainisha majukumu yaMwansheria Mkuu wa Serikali, na inasema; 59(3) MwanasheriaMkuu atakuwa ndiye mshauri wa Serikali ya Jamhuri yaMuungano juu ya mambo ya sheria na, kwa ajili hiyo,atawajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri yaMuungano kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekelezashughuli nyinginezo zozote zenye asili au kuhusiana na sheriazitakazopelekwa kwake au atakazoagizwa na MheshimiwaRais, na inamalizia pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni kumekuwa namazoea au na utamaduni ambao Mwanasheria Mkuu waSerikali ambaye namheshimu sana amekuwa akifanya kaziza Chief Whip. Katiba ya Jamhuri ya Muungano inamuelekezakabisa majukumu yake ni yapi. Mwanasheria Mkuu wa Serikalihauwezi kutofautisha amesimama kama Waziri wa Sheria

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

au ni Chief Whip. Anaingilia hata mambo ya lugha, kwamfano jana kisu cha ngariba nalo anataka tafsiri, hii sio kaziya mwansheria! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na ningekuomba wewe nimtu uliyebobea katika sheria, una authority katika nchi hii naulikuwa Mwanasheria Mkuu na Katiba inasema huyuMwanasheria Mkuu anateuliwa kwa sababu anakuwa nauzoefu. Amekuwa mzoefu, Mabunge matatu yamepita,amewaona wanasheria wengine walivyokuwa wanafanyakazi hapa, ameyaona haya mambo yanavyofanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kitendo anachokifanyaMwanasheria katika Bunge hili; kwanza yeye ni mshauri waSerikali, anapaswa aishauri Serikali inapokosea inaletamiswada, kwanza anaishushia heshima ya Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ameaminiwa na Rais, sasaanafika mahali anashughulika mpaka na lugha, namna zauandishi. Kitendo anachokifanya Mwanasheria kina crippleBunge na Bunge tunashindwa kujadili mambo ya msingi. Sikumoja uliwahi kusema wewe mwenyewe MheshimiwaMwenyekiti kwamba tunatakiwa tuwe na wivu wa kulilindaBunge letu, hapa ni mahali ambapo tunatakiwa tutoemijadala, sisi kama wapinzani lakini matokeo yake anafanyakazi za Chief Whip.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Mwongozo wangu, je,Serikali ina Chief whip wawili? Ili tujue Chief Whip ni yupi kwasababu Mwanasheria hafanyi kazi ya Mwanasheria.Nimuombe Profesa Kabudi, anaheshima yake, nimwanasheria aliyebobea katika nchi hii. Hebu tulindeheshima ya Bunge, mhimili huu tuulinde. Sheria zitungwe,zifanyike vizuri badala ya kufanya kazi kama anavyofanyakazi mwanasheria. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MWENYEKITI: Umeeleweka.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,mnapiga kelele huko most of you are not bookish, you don’tread, that’s why you are making noise. Haya mambo ni yamsingi, ya kulinda Bunge letu. Naomba Mwongozo wako.

MBUNGE FULANI: Inatosha.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa, mimi nimekupanafasi, sasa unaanza kujibizana huko. Hapana, please alwaysaddress the chair. Mheshimiwa Zuberi Kuchauka.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi hii…

MWENYEKITI: Kwani nimekosea jina lako?

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Nasimama kwa Kanuniya 68(7) ikisomwa pamoja na 46(1) inayohusu kujibu maswalikwa ukamilifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati nimejibiwa swalilangu hapa, swali la nyongeza namba (b) halikujibiwa kwaukamilifu. Nilichokisema ni kwamba kesi hii imeisha 2007 nahukumu ikatolewa, wafanyakazi wale walipwe shilingi milioni234.3, kwa hiyo kesi hii imeisha. Mheshimiwa Waziri anasemakwamba kesi hii iko mahakamani hawezi kuongelea hapa,si kweli kwamba hii kesi iko mahakamani, kesi hii imekwishamwaka 2007. Naomba Mwongozo wako. (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nawashukurusana kwa maombi yenu ya Miongozo. Nianze na hili laMheshimiwa Zuberi Kuchauka.

Majibu ya Serikali, mimi haya ninayo na ninyimmeyasikia na yamechukuliwa vizuri na Hansard. Nadhanihoja hapa ndogo ni kwamba muuliza swali anaaminikwamba kesi iliyokuwepo mahakamani ilikwisha. Serikaliwanasema hawawezi kulisemea suala hilo kwa sababu lipo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

mahakamani. Sasa tunataka tuupate huo ukweli. Nilikuwanakutegemea wewe ungeenda zaidi kwa sababu ndiyemwenye swali, ndiye mwenye data. Ile hukumu ungekuwananakala yake ingesadia sana Serikali, kwamba ndiyo hiihapa, kesi ilishaisha, wananchi hawa waliokuwa watumishiwa National Milling wanastahili haki zao stahiki. Ndiyo hivyohoja hiyo.

Mwongozo wangu ili tuokoe muda ni kwamba ipatebasi hiyo nakala ya hukumu uikabidhi kwa Mheshimiwa Waziriwa Fedha na Mipango ili waone na tuanzie hapo sasa,maana tunatafuta haki za watumishi waliokuwa wa NationalMilling. Huo ndio Mwongozo wangu kwa hilo. Tusaidie tuipatekwa uhakika.

Mheshimiwa Msigwa, umetumia kifungu cha 64(1) nakukiunganisha na Katiba kwenye vifungu vya nafasi yaMwanasheria Mkuu. Umevisema na ndiyo Katiba inavyosema.Nianze na hili la 64(1), maneno yale bila kuathiri masharti yaKatiba ambayo inasema uhuru wa mawazo na majadiliano.

Waheshimiwa Wabunge, unakisoma hicho kwanza,Ibara ya 101 ya Katiba halafu unashuka kwenye Ibara ndogoya pili. Ninachotaka kuwaambia ni hivi; 64(1) inasema mnauhuru wote mpana kabisa wa kufanya majadiliano, kutoakile ulichonacho ulichotumwa na wananchi humu Bungeni,lakini bila ya kuathiri Katiba. Katiba ile unakuta imekuwekeamipaka ile, lakini uhuru wako ni kwamba hayo uliyoyasemahumu ndani huwezi ukaenda ukahojiwa au ukafikishwamahakamani au kwenye chombo kingine kile. Huo ndiomsingi wa maneno hayo.

Waheshimiwa Wabunge, lakini ukienda nje na ndiyomaana sasa nakuja; humu ndani Ibara ya 89 ya Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania inaliruhusu Bunge hilikutunga Kanuni na Bunge hili limeshatunga Kanuni hizo. Kunamakatazo fulani ukiwa ndani ya Bunge hili huwezi ukatumiakugha ambayo sio ya Kibunge. Huwezi ukatumia lugha yakuudhi wenzako. Makatazo hayo yote yanatokana na Katiba.(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

Waheshimiwa Wabunge, sasa tutumie vizuri vifunguhivi tunavyovisemea lakini nikija sasa kwa nafasi yaMwanasheria Mkuu, mimi najua Chief Whip wa Serikali nimmoja, lakini hakuna kinachomzuia Mwanasheria Mkuu,Waziri mwingine yeyote wa Serikali kusimama na kutoaufafanuzi au maelezo kwa masuala yaliyo mbele ya Bungewakati huo. Kwa hiyo, ndugu zangu, Mheshimiwa Msigwamimi nakusihi sana, wewe ni Mbunge wa siku nyingi sasahumu. Kidogo tusilete hisia kwa ofisi kama hii.

Mimi nakubali nimewahi kuwa kwenye nafasi hiyokwa kipindi kirefu, tumefanya kazi na Bunge, lakini jamanituwe na staha tunapo address office ya Mwanasheria Mkuu.Mwongozo wangu ni huo, anaweza akasimama wakatiwowote kusaidia Serikali na hiyo haimfanyi kuwa Chief Whip.Tunachotaka ni sisi tuwe na uelewa mzuri wa Kanuni au Sheriaza nchi kwa suala linalosemwa kwa wakati huo (Makofi)

Mheshimiwa Japhary Michael, najua umeniomba tumsamaha kwamba AG Mstaafu nisaidie maana yale ya janayamepita. Lakini unasema kwa huruma yako. Mimi nasemaKanuni ya 68(7) ni jambo ambalo limetokea mapema sikuhiyo, linaruhusiwa na Kanuni au haliruhusiwi. Sasa miminisingependa sana Bunge hili tuliingize katika hayo ambayounayatafuta. Mimi naamini kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania, kwa madaraka ambayo ma-RCna ma-DC wamekasimiwa na Rais kwenye maeneo yao yakiutendaji na ya kiusalama ni kamili, wanamwakilisha Raiskatika eneo hilo. (Makofi)

Sasa yawezekana mtu akajifikiria kwamba yeye kwasababu anamwakilisha Mheshimiwa Rais hapo kwa kipindihicho yeye ni Rais, haiwezekani. Rais ni mmoja tu, lakinianatekeleza majukumu ambayo yamekasimiwa kwake naRais. (Makofi)

Mheshimiwa Haonga, kwa heshima zote huu nimhimili kamili, Bunge na Serikali ni mhimili kamili kama ilivyoMahakama. Mhimili wa Serikali (Utawala) umeshaamuakuhusiana na huyu uliyemtaja kwa sababu inazofahamu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

mhimili huo. Sisi hatuwezi tena kama mhimili kwenda kuanzakuhoji ni nini kifanyike, hatuendi hivyo. Haya masualayatasimamia mahusiano yetu ya kimataifa, diplomasiaitatumika kama kuna mtu atalalamika huo ndiyo utaratibuambao utatumika, sisi hatufiki huko. Halafu nimalizie kwakusema hivi, taarifa za magazeti sisi huwa hatutumii kufanyamaamuzi, hapana; hatutumii magazeti kufanya maamuzi.(Makofi)

Mheshimiwa Sitta amelisemea vizuri sana suala la bintiyetu Asha Ally Mabula. Hapa mezani nililetewa moja yamiongoni mwa wageni alikuwepo amesimama,tumemtambua, mmepiga makofi sana. Sasa nilivyomuelewaMheshimiwa Sitta, Mwongozo wake anaoniomba niufikishekwenu kwa sababu ni tukio kubwa linalohusu nchi yetukwenda kujitangaza nje kupitia binti huyu, amependekezatumsaidie kumsafirisha anakoenda akaitangaze nchi yetulakini na yeye pia amependekeza iwapendeze WaheshimiwaWabunge kama tulivyofanya huko siku za nyuma tuchangie.Amependekeza shilingi 30,000…

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaMwenyekiti, watu wana mafuriko majimboni kwao.

MWENYEKITI: … mimi nilikuwa naomba… Ngojanimalize basi. Tujenge heshima kidogo.

MBUNGE FULANI: Mnatuonea.

MWENYEKITI: Sasa mimi nilikuwa nasema, hebu tuwena kamjadala dakika mbili, tatu tu kidogo. Mheshimiwa Sittawewe ndiye ulianzisha hii. Dakika moja, unapendekeza shilingingapi?

MBUNGE FULANI: Michango imezidi jamani ah!

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nisimame? Ahsante.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

MWENYEKITI: Tuchukue watatu huku, na huku watatu.Hoja hapa iko wazi. Ngoja basi twende vizuri jamani.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, twende vizuri.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Tunahamia huku, Khatibu. Lissu…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MWENYEKITI: Ally Saleh. Imetosha! WaheshimiwaWabunge, Margaret Sitta anza.

MHE. MARGARET S. SITTA; Mheshimiwa Mwenyekiti,kwa heshima na taadhima nawaomba WaheshimiwaWabunge, najua tuna majukumu mengi sana lakininimewaomba angalau si chini ya shilingi 30,000, sikusemanyingi. Nawaomba Waheshimiwa Wabunge, tumpe nafasibinti ya kueneza na kutangaza jina la Tanzania.

MBUNGE FULANI: Hatutoi!

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nawaomba pande zote mbili tuungane, si chini ya shilingi30,000. Ahsante sana.

MBUNGE FULANI: Tuna mafuriko.

MBUNGE FULANI: Tupige kura.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, lazimatuliamue suala hili, nilitegemea ninyi sasa msimame muungemkono hoja hii.

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naafiki.

(Hoja ilitolewa Iamuliwe)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

MWENYEKITI: Eeh, imeungwa mkono. TunaendeleaMheshimiwa Chumi.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwanza kwa kuniona, naomba kuungana naMheshimiwa Mama Margaret Sitta, walikuja hapa vijana waSerengeti Boys ambao wamefuzu kwenda kwenye AFCONya under 17 kule Gabon na tulikubaliana tukawachangia.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, juzi Ndugu Alphonce Simbuamekuwa namba tano katika London Marathon, hivi karibunikwa jitihada zake binafsi alikuwa pia mshindi MumbaiMarathon. Mambo kama haya siyo kwamba tumemsaidiaindividual, mtu huyu anapokwenda kule anatuwakilisha kamaTaifa, pia anatangaza Taifa na kwa kufanya hivyoanatusaidia kuvutia watalii ambao ni chanzo cha mapatoya Taifa. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Hatutoi.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba tumuunge mkono Mama Sitta ni utamaduni wakawaida kama tulivyofanya katika football na hiki pia ni kituambacho kinatangaza Taifa.

MBUNGE FULANI: Serikali itoe hela.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Martha Mlata.Waheshimiwa Wabunge, naomba utulivu.

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba niunge mkono hoja ya Mama Sitta, lakini naombaniseme jambo moja. Tuko hapa Bungeni, tumepata kadinyingi na vikao vingi vya watu ambao wanahitajituwachangie kwenye harusi na watoto wao na mambomengine na tunachanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili ambalo binti yetuanaenda kuliwakilisha Taifa, kwanza mimi kama Mama

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

ninajisikia vibaya sana kuona wanawake ndiyowanaoongoza kupinga jambo la kumchangia binti yetu,ninasikitika sana. Naomba nitoe ushauri wale ambaohawahitaji kuchanga wanyamaze, wanaotaka kuchangawatachanga. Ahsante sana.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Tunachanga wote.

MBUNGE FULAN: CCM tutachanga wote.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Keissy.

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,namuunga mkono moja kwa moja Dada yangu Mwenyekitiwa Mkoa wa Singida. Amesema kuchanga ni hiari, mwenyekutaka kuchanga achange, asiyetaka kuchanga asichange.Mchango ni hiari siyo lazima. Kwa hiyo, ndugu zangu hakunamjadala zaidi, anayetaka kuchanga achange, asiyetakaasichange. siyo kulazimishana hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, anayetaka kuchangaachange na asiyetaka asichange. Mmojawapo ni mimimwenyewe sichangi. (Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naombautulivu. Kwanza muda siyo rafiki, Mheshimiwa Lissu.

MHE. JAMAL KASSIM ALI: Mheshimiwa Jamal.

MHE. TUNDU A. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, hili nijambo jema sana, isipokuwa wananchi wa Jimbo languwanakabiliwa na njaa kweli kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali hii imekataakatakata kutoa msaada wa chakula. Sasa kama kuna jambolinalohitaji kutolewa mchango ni suala la kuponesha watuwetu njaa. Haya mambo ya walimbwende yasubiri wakatiwake na kama kuna watu wanafikiri ni jambo jema kunaWaziri ambaye amekabidhiwa mambo haya, mwalimuwangu wa sheria afanye kazi hii. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

Mheshimiwa Mwenyekiti, binafsi sitakubali kukatwahata senti kumi kwa ajili hii.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ally Saleh.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Kwanza nataka kuanza na mwenzetu mmoja hapaaliyesema kwamba yeye kama mzazi wa kike amesikiauchungu, imekuja issue ya Ben Saanane hapa uchungumbona… (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MWENYEKITI: Mheshimiwa hebu jielekeze tu kwenyehoja tuliyonayo hapa.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Sipokei taarifa kutoka upande wowote.

MHE. JUMA S. NKAMIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa kidogo tu…..

MWENYEKITI: Hapana nimekataa, kaa chini tu.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti,jambo la pili tuna utamaduni mbaya sana hapa, kamaalivyosema Mheshimiwa Lissu hili ni jambo jema, lakini hatunainsafu tukileta mambo mema mbona upande huu hatuungwimkono! Kwa hiyo, nahisi kwamba this is a cooperate world,mkinipa mimi tu challenge ya siku moja tu I can raise millionskutoka kwenye mashirika ambayo yanafanya kazi yaulimbwende, waacheni Wabunge washughulikie na mambomengine. Ahsante.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Khatib wa mwisho.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Namuunga mkono Mheshimiwa Keissy moja kwamoja.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulishuhudia hapa timu yetuya Bunge ilivyokwenda Mombasa ilivyorudi kwa dhiki namalori na Bunge hili halikufikiria kuichangia. Bunge hilihalikufikiria kuichangia timu ile walirudi Mombasa kwa maloriya lift. Tukirudi imani yangu huu ni mwezi wa Rajab mweziunaokuja ni mwezi wa Ramadhani…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,Zanzibar hakuna mashindano ya warembo. Serikali yaZanzibar imelikataa na hili linalokuja sasa kwa imani yetu yakidini ni dhambi kubwa kumchangia yule dada aendekuwakilisha hili.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, diniyetu inatusuta na nafsi zetu zinatusuta. Aliposimama palewengine tuliinamia mivunguni, hatukuweza kumwangalia,kwa imani yetu ya kidini inavyotusuta.(Makofi/Kicheko)

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,tusaidie huku.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge lazimamheshimu…

MHE. JUMA S. NKAMIA: Hilo povu lote ni kwa sababuya shilingi 30,000 tu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuhusu taarifa.

MWENYEKITI: Nimeshasema, sijakuruhusu kuongeaMheshimiwa.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Nkamia kaa chini.

MWENYEKITI: Nimeikataa sipokei taarifa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Umenisahau kwenye…

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, huo ndiomjadala, kwa hoja iliyotolewa na Mheshimiwa Margaret Sitta,kwa pendekezo la kumchangia huyu binti yetu

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,hatuwachangii walimbwende.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, sasa hojayoyote lazima iamuliwe..

MBUNGE FULANI: Hatutaki.

MWENYEKITI: Ndio, lazima niitoe kwenu.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MBUNGE: Dhambi, dhambi.

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,ukikata hela tutaenda mahakamani mzee.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, unatakakulazimisha.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naombatusikilizane, sitaki kuwataja ninaowaona sasa.

Mimi nimetumia Kanuni ili suala hili likae vizuri,haturuhusiwi kuanzisha mjadala, soma Kanuni ya 53, ndiyomaana nimemruhusu atoe hoja iungwe mkono. Sasanawahoji wanaoafiki pendekezo la mtoa hoja kwamba kilaMbunge achangie si chini ya shilingi 30,000 waseme ndiyo.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hatukubali.

(Hoja ilitolewa Iamuliwe)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, ninaaminiwalioafiki wameshinda.

(Hoja ya pendekezo la Mheshimiwa Margaret S. Sitta la kilaMbunge kuchangia shilingi 30,000 lilikubaliwa na Bunge)

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,mchango ni hiari, haikubaliki hata kidogo hiyo, tutakwendamahakamani.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Wasanii mnawatumiakwenye kampeni hamtaki kuchanga. Profesa Jay unawaonawenzako?

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naombautulivu, tumeshaamua mengine ni utekelezaji. Katibu.

NDG. LAWRANCE MAKIGI-KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Katiba na Sheria

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, kablasijamwita mtoa hoja, nimeletewa tangazo hapa naMheshimiwa Ngeleja, Mwenyekiti wa Bunge Sports Clubakinifahamisha kwamba kwenye gallery ya Spika tutambueuwepo wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wachezajiwa football na netball ambao wameingia sasa, karibuni sana.Nadhani mmekuja kwa matumaini ya ushindi lakini michezoni furaha, afya, pia hii timu ya Bunge ni kazi, karibuni sana.(Makofi)

Waheshimiwa wabunge, tunaendelea na mtoa hojaWaziri wa Katiba na Sheria, Profesa Kabudi una saa moja.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, kufuatia taarifa zilizowasilishwa leo katika Bungelako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bungeya Katiba na Sheria na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu yaBunge ya Bajeti, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lakosasa likubali kupokea, kujadili na kupitisha mpango wamakadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara yaKatiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote napendakumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniruzuku uhai na kunijaliaafya njema kuweza kusimama mbele ya Bunge lako Tukufukuwasilisha mpango na makadirio ya bajeti ya Wizara yaKatiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha napenda kutoashukrani nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwaheshima kubwa aliyonipa kwa kuniteua kuwa Mbunge nakushika wadhifa wa Waziri wa Katiba na Sheria. Kutokanana heshima hiyo, ninaahidi kuitumikia nafasi hii kwa hekima,uadilifu na uaminifu kwa kadri alivyonijalia Mwenyezi Mungu.Vivyo hivyo, ninaahidi kuwatumikia wananchi wote waTanzania bila kuwabagua kwa dini zao, rangi zao, kabilazao, vyama vyao, itikadi zao kwa kuwa wao ndio msingiwa mamlaka yote ya Serikali kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwanakupa pole wewe na Bunge lako Tukufu kwa kuondokewana Wabunge wenzetu waliotangulia mbele ya haki, ambaoni Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir aliyekuwa Mbunge wa Jimboka Dimani CCM na Mheshimiwa Dkt. Elly Marko Machaaliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum - CHADEMA. Pia, natoapole kwako na Watanzania wote, ndugu, jamaa na marafikikutoka na kifo cha Mheshimiwa Samuel John Sitta aliyekuwaSpika wa Bunge la Kumi la Jamhuri ya Muungano waTanzania. Nitumie fursa hii kuwapa pole ndugu, jamaa namarafiki pamoja na wananchi walioguswa na misiba hii kwanamna moja au nyingine, Mwenyezi Mungu azilaze roho zamarehemu mahali pema peponi, Amina.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nimpongezeMheshimiwa Spika kwa uongozi wake mahiri wa kuliongozaBunge letu na hivyo kudhihirisha uwezo na uzoefu alionaowa kuwatumikia Watanzania kupitia chombo hiki. Aidha,nitumie fursa hii kumpongeza Naibu Spika, Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson Mwansasu na Wenyeviti wote wa Bunge kwakuendelea kutekeleza majukumu yao vema kwa kuzingatiasheria, kanuni na taratibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nampongeza WaziriMkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MheshimiwaKassim Majaliwa Majaliwa (Mbunge), kwa hotuba yake nzuriambayo imetoa mwelekeo wa kisera katika utekelezaji washughuli za Serikali kwa kipindi cha mwaka wa fedha2017/2018. Vilevile nampongeza kwa uongozi wake thabitikatika kusimamia vema shughuli za Serikali ndani na nje yaBunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niruhusu sasa niwapongezeMwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba naSheria, Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa, Mbungewa Rufiji na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge yaBajeti Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge waMtwara Vijijini, kwa kuziongoza vema Kamati zao. Maoni naushauri wao umekuwa ni msaada mkubwa kwa Wizarayangu katika kutekeleza majukumu yake na kuwahudumiaWatanzania. Napenda niwahakikishie kuwa Wizara yanguinayo imani kubwa katika uongozi wao na itaendeleakuwapatia ushirikiano unaostahil i katika kipindiwatakachokuwa katika nyadhifa hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia natoa shukrani zangu zadhati kwa Kamati hizo kwa kazi kubwa ya kuchambuampango na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizaraya Katiba na Sheria pamoja na Mfuko wa Mahakama kwamwaka wa fedha 2017/2018. Hakika tunatambua nakuthamini mchango wa Kamati hizi katika kuhakikisha kuwasekta ya sheria inabaki kuwa kiungo muhimu kwa maendeleoya nchi yetu kiuchumi, kijamii, kisiasa, kimazingira nakiteknolojia.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

Mheshimiwa Mwenyekiti, niruhusu sasa niwapongezeWabunge wenzangu wote wa pande zote mbili za Bungehili kwa heshima waliyopewa ya kuwa Wabunge wa Bungelako Tukufu. Kwa namna ya pekee natoa pongezi zanguzadhati kwa Mheshimiwa Abdallah Majurah Bulembo(Mbunge), Mheshimiwa Anna Kilango Malecela (Mbunge),Mheshimiwa Juma Ali Juma (Mbunge), Mheshimiwa SalmaRashid Kikwete (Mbunge) na Mheshimiwa Getrude PangalileRwakatare (Mbunge), kwa heshima kubwa waliyopewa yakuitumikia Taifa letu kupitia chombo hiki kitukufu. Binafsi,ninawatakia heri na baraka za Mwenyezi Mungu katikakutekeleza majukumu yao ya Ubunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue pia fursa hii kwasababu ni mara yangu ya kwanza nasimama katika Bungehili kuwashukuru wazazi wangu, kuishukuru familia yangu,kuwashukuru walimu wangu na wahadhiri wote ambaowamenifikisha katika nafasi hii ambayo leo ninayo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, dira ya Wizara ya Katiba naSheria ni kuwa na Katiba na sheria wezeshi, kwa maendeleoya Taifa. Madhumuni ya dira hii ni kuweka mazingira rafikikisera na kisheria ya kuwezesha utekelezaji wa mpango wamaendeleo ya Taifa, kudumisha hali ya amani, utulivu nautengamano wa Kitaifa ambavyo vimeendelea kuweponchini. Aidha, dhima ya Wizara ni kuwa na mfumo madhubutiwa Kikatiba na kisheria katika kufanikisha mipango yamaendeleo ya Taifa. Dhima hii inahimiza kufanya kazi kwaweledi na ubunifu katika kuhakikisha kunakuwepo mazingirarafiki ya upatikanaji wa huduma muhimu za kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Katiba na Sheriainajumuisha Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Tumeya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Utumishi waMahakama, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini, Taasisi yaMafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo na Chuo cha Uongoziwa Mahakama - Lushoto. Kwa pamoja tumeendeleakutekeleza majukumu yetu ya kuwahudumia wananchi kwakutoa huduma mbalimbali za kisheria na kuhakikisha kuwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

wananchi wanaifikia na kupata haki kwa wakatiwanapoitafuta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu inayo wajibuwa kuhakikisha kuwa nchi inaongozwa kwa kuzingatiaKatiba, sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na vyombohalali na kwamba haki inaendelea kutawala katika jamiiwakati wote. Hivyo, kwa kutambua wajibu huo Wizara yanguimeendelea kutekeleza majukumu yake kama yalivyo kwenyehati ya mgawanyo wa majukumu kwa Mawaziri (Instrument),iliyotolewa kupitia Tangazo la Serikali Na. 144 la tarehe 22Aprili, 2016 ambayo ni kama ifuatavyo:-

i. Kuweka sera kuhusu masuala ya sheria na utekelezajiwake;

ii. Kushughulikia masuala ya katiba;

iii. Kusimamia haki na mfumo wa utoaji haki;

iv. Uandishi wa sheria;

v. Uendeshaji wa mashtaka;

vi. Kushughulikia mashauri ya madai, usuluhishi,mikataba na sheria za kimataifa;

vii. Kushughulikia masuala ya haki za binadamunamsaada wa kisheria;

viii. Kusimamia na kufanya utafiti wa maboresho yasheria;

ix. Kushughulikia urejeshwaji wa wahaalifu nakuendeleza ushirikiano na mataifa mbalimbali kwenyemakosa ya jinai;

x. Kusajili matukio muhimu ya binadamu yanayohusuvizazi, vifo, ndoa, talaka, na uasili wa watoto; pamoja nakusimamia masuala ya ufilisi na udhamini;

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

xi. Kuboresha utendaji na maendeleo ya rasilimali watukatika Wizara; na

xii. Kuratibu shughuli za taasisi, mipango na miradi yamaendeleo chini ya Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2016/2017 Wizara yangu ilipanga na kutekeleza majukumuyake kwa kubainisha maeneo mahsusi ya kipaumbeleyafuatayo:-

(i) Kuimarisha usimamizi na uratibu wa mfumo washeria;

(ii) Kuanzisha Division ya Mahakama Kuu ya Makosaya Rushwa na Uhujumu Uchumi;

(iii) Kuimarisha mfumo wa haki na utoaji haki;

(iv) Kuimarisha usimamizi wa miradi ya ujenzi naukarabati wa miundombinu ya Mahakama na Taasisinyingine zilizo chini ya Wizara yangu;

(v) Kuimarisha matumizi ya mfumo wa kielektronikiya kutunza kumbukumbu na nyaraka muhimu pamoja nakutolea huduma;

(vi) Kuimarisha shughuli za utafiti na uboreshaji washeria nchini;

(vii) Kuimarisha uandishi na urekebu wa sheria za nchi;

(viii) Kuboresha mazingira ya kufanyia kazi, maendeleona ustawi wa watumishi;

(ix) Kuimarisha mfumo wa mafunzo ya uwanasheriakwa vitendo kwa kuongza udahili wa wanafunzi na kupanuawigo wa utoaji wa huduma;

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

(x) Kuimarisha upatikanaji wa msaada wa kisheria kwawatu wasio na uwezo; na

(xi) Kuimarisha shughuli za usajili wa matukio muhimuya binadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia vipaumbelehivyo Wizara iliandaa na kuwasilisha mbele ya Bunge lakoTukufu Mpango na Bajeti na kupitishwa kwa utekelezaji. Kwaheshima na taadhima naomba sasa uniruhusu kuwasilishambele ya Bunge hili taarifa kuhusu hatua mbalimbalizilizochukuliwa katika kutekeleza mpango na bajeti kwamwaka wa fedha 2016, mafanikio yaliyopatikana nachangamoto mbalimbali ambazo Wizara ilikabiliananazokama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, maandalizi ya Sera ya Taifaya Sheria; Wizara iliendelea na juhudi za kuandika sera mahsusikuhusu masuala ya sheria kwa kuandaa Rasimu ya Taifa yaSheria ambayo kwa sasa inajadiliwa na makundi mbalimbaliya wadau ili kutoa fursa kwa Wizara kukusanya maoniyatakayofanya sera hiyo kukidhi mahitaji ya sasa ya sekta yasheria na Taifa kwa ujumla. Ni matarajio yangu kwambaSerikali ikishapitisha sera hii na kuanza kutumika itakuwa nihatua muhimu katika kuimarisha usimamizi na utekelezaji wamfumo wa sheria nchini kwa maendeleo ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu tathmini ya hali yautekelezaji wa sheria nchini; Wizara ya Katiba na Sheria inayodhamana ya kuimarisha na kusimamia Mfumo wa SheriaNchini. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 Wizarailifuatilia utekelezaji wa sheria mbalimbali kupitia Wizara,Idara, Wakala na Mamlaka nyingine za Serikali ili kutathminihali ya utekelezaji wa sheria nchini. Kukamilika kwa zoezi hilikutaiwezesha Wizara kutoa mwongozo wa namna yakuimarisha mfumo wa sheria nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sera na makubaliano yakimataifa ya kikanda; kwa muda mrefu nchi yetu imekuwamwanachama wa taasisi mbalimbali za Kikanda na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

Kimataifa kupitia Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika,Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya yaAfrika Mashariki na nyinginezo. Kupitia taasisi hizo Tanzaniaimeendelea kuridhia sera, malengo na mipango yamaendeleo inayopitishwa na taasisi husika ikiwemo:-

(a)Malengo ya Maendeleo Endelevu (SustainableDevelopment Goals);

(b)Mpango wa Maendeleo wa Afrika; na

(c) Mpango wa Kazi wa Afrika Kugharimia Shughuliza Maendeleo (The Addis Ababa Action Agenda).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua wajibu ilionao katika kufanikisha makubaliano hayo, Wizara yanguimefanya uchambuzi wa maeneo muhimu na kuwekamikakati ya kuiwezesha kutekeleza vyema wajibu huu wawakimataifa sanjari na mipango ya ndani ya sekta. Kutokanana uchambuzi huo Wizara imebainisha maeneo lengwa(thematic areas) manne ambayo kwa namna moja aunyingine yanaakisi Malengo ya Mpango wa Pili wa Taifa waMaendeleo wa Miaka Mitano na pia Mpango Mkakati waWizara. Maeneo hayo ni upatikanaji wa haki kwa wote nautawala wa sheria, amani na ushirikishwaji wananchi kwamaendeleo endelevu, usawa wa kij insia na haki zabinadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu haki na mfumo wautoaji haki; Katiba imeipa mamlaka Mahakama ya Tanzaniakuwa ndicho chombo pekee cha utoaji haki nchini. Katikakuhakikisha kuwa chombo hiki kinatekeleza majukumu yakeipasavyo na kwa ufanisi, sheria zimeweka mfumo rasmi wautatuzi wa migogoro unaojumuisha mfumo wa upelelezi wamakosa ya jinai, uendeshaji wa mashitaka, ushirikishaji wamashauri pamoja na mifumo ya usuluhishi.

Hivyo, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017Serikali ilichua hatua madhubuti za kuimarisha mfumo wautoaji haki nchini kwa kuanzisha Divisheni ya Mahakama Kuu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kuharakishausikilizaji wa mashauri na ujenzi wa miundombinu muhimukama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Divisheni ya Mahakama Kuuya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi. Katika kipindihicho Wizara imetekeleza kwa vitendo azma ya Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. JohnPombe Joseph Magufuli, ya kupambana na rushwa na ufisadinchini kwa nguvu zote kwa kuanzisha Divisheni ya MahakamaKuu ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi. Divisheniimeanza kufanya kazi katika majengo yaliyopo kwenye Taasisiya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo na kwamba kilaKanda ya Mahakama Kuu ni Masjala Ndogo ya Divisheni hiyo.Hatua muhimu zil izochukuliwani pamoja na kufanyamarekebisho ya sheria na kuandaa kanuni za uendeshaji wamahakama, kufanya ukarabati wa majengo, ununuzi wavifaa, kuajiri na kutoa mafunzo kwa watumishi wa divisheni.Hadi sasa divisheni hiyo imeweza kusajili jumla ya maombi25, kati ya hayo 20 yamesajiliwa Dar es Salaam, matatuMtwara, moja Iringa na moja Tabora. Aidha, kati ya maombi25 yaliyosajiliwa maombi 13 yametolewa uamuzi na mengineyanaendelea kufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, usikilizaji wa mashauriMahakamani; mwaka 2016 Mahakama ya Tanzania ilianzana jumla ya mashauri 59,477 na kusajili mashauri mapya276,147. Mashauri yaliyoamuliwa katika kipindi hicho yalikuwa278,226 sawa na asilimia 83 ya wastani wa uwezo wakumaliza mashauri yote yaliyokuwepo. Mafanikio hayoyalitokana na Mahakama kuendelea kubuni na kutekelezamikakati mbalimbali ikiwemo kufanya kazi kwa malengo nakupima utendaji kazi wa Majaji na Mahakimu. Pia Mahakamaya Tanzania imeendelea kusisitiza matumizi ya njia mbadalaza utatuzi wa migogoro na kuimarisha ushiriki wa wadaukatika kubuni na kutekeleza mikakati ya kuharakisha usikilizajiwa mashauri. Maelezo ya ufafanuzi kuhusu usikilizaji wamashauri ni kama yalivyo kwenye kiambatisho namba moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia matokeo ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 yalifunguliwa jumla yamashauri 53 yaliyohusu nafasi ya Ubunge, mashauri 196 yanafasi za Udiwani. Hadi kufikia mwezi Machi, 2017 mashauri52 ya Ubunge yaliamuliwa hivyo kubaki na shauri moja nakwamba hivi sasa kuna rufaa mbili katika Mahakama yaRufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu. Aidha, mashauriyote ya Udiwani yalisikilizwa na kuamuliwa katika kipindikilichowekwa kwa mujibu wa sheria yaani mwaka mmojakwa mashauri ya Ubunge na miezi sita kwa mashauri yaUdiwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ni mafanikio makubwana ya kihistoria kuwahi kufikiwa kwa mashauri ya uchaguzikusikilizwa na kutolewa uamuzi ndani ya muda uliowekwakisheria. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilitoa mchangomkubwa kwa kusimamia uendeshaji wa mashauri hayomahakamani ambapo katika mashauri yote isipokuwa shaurimoja Serikali ilipata ushindi.

Aidha, katika kuhakikisha kuwa tunaimarisha uwezowa Serikali kushughulikia kesi za uchaguzi, Mahakama yaTanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa laMaendeleo (UNDP) ilitengeneza vitabu vitatu ambavyo nikijitabu kinachoeleza utaratibu na mienendo iliyotumikakatika kuendesha kesi za uchaguzi, ripoti kuhusu namnaMahakama zilivyoshughulikia kesi za uchaguzi na mafunzoyatokanayo na mkusanyiko wa sheria na kanuni za uchaguzi.Vitabu hivi vilikabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania na kwa Mheshimiwa Spika tarehe2 Februari, 2017 wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala lamiundombinu ya Mahakama; Mahakama ya Tanzaniaimeendelea na utekelezaji wa mikakati ya kuboresha hudumaza Mahakama ikiwa ni pamoja na kufanya ujenzi naukarabati wa Mahakama mbalimbali nchini. Hadi kufikiamwezi Machi 2017, Mahakama ya Tanzania ilikamilishaukarabati wa majengo ya Mahakama Kuu Dar es Salaam naTanga na kuendelea na ukarabati wa Mahakama Kuu Kandaya Mbeya unaotarajiwa kukamilika hivi karibuni.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

Aidha, Mahakama ya Tanzania imekamilisha ujenziwa Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani naMahakama ya Wilaya Kibaha na inaendelea na ujenzi waMahakama za Wilaya za Bagamoyo, Mkuranga, Kigamboni,Kinyerezi na Mahakama ya Mwanzo Kawe ambazo zipokatika hatua mbalimbali za ujenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana nachangamoto ya miundombinu, Mahakama kwa kushirikianana Chuo Kikuu cha Ardhi na Baraza la Taifa la Ujenzi ilifanyautafiti wa teknolojia ya gharama nafuu ya ujenzi wa majengoambapo teknolojia ya moladi imeonesha unafuu wagharama, kupunguza muda unaotumika kwenye ujenzi naubora wa majengo. Kwa kutumia teknolojia hii Serikaliimeweza kuokoa takribani asilimia 50 ya gharama za ujenziambazo zingetumika kwa kutumia teknolojia ya kawaida.Chini ya utafiti huu Mahakama za Mwanzo sita zimejengwaambazo ni Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani na Hakimuya Wilaya Kibaha, Mahakama za Wilaya za Bagamoyo,Kigamboni, Mkuranga na Kinyerezi pamoja na Mahakamaya Mwanzo Kawe. Ni dhahiri kuwa kutokana na uzoefuuliopatikana katika mradi huu, Wizara itaweza kutumiateknolojia hiyo ya moladi katika maeneo mengine ya nchikwa gharama nafuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hatua nyingineMahakama ya Tanzania imeanza kazi ya kukamilisha ujenziwa Mahakama ya Mkoa wa Manyara na Mahakama zaMwanzo za Iguguno – Mkalama, Waso – Ngorongoro,Magoma – Korogwe, Bereko – Kondoa, Karatu Mjini – Karatu,Mvomero – Mvomero, Old Korogwe – Korogwe na KilwaMasoko – Kilwa, ambazo ujenzi wake ulisimama kwa mudamrefu kutokana na ukosefu wa fedha. Aidha, Mahakama yaTanzania imeendelea kuimarisha shughuli za usimamizi naukaguzi wa Mahakama kwa kununua na kusambaza jumlaya nakala 650 za vitabu vya mwongozo wa ukaguzi katikaMahakama mbalimbali nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uandishi wa sheria,Wizara yangu imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

kuwa sheria za nchi zinakuwa ni nyenzo ya kuharakishamaendeleo katika nyanja za kiuchumi, kijamii, kisiasa,kiutamaduni, kimazingira na kiteknolojia kupitia sera namipango mbalimbali ya maendeleo. Hivyo, katika mwakawa fedha 2016/2017, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikaliiliratibu maandalizi ya Miswada 12 ya sheria iliyowasilishwana kujadiliwa Bungeni, kutokana na Miswada hiyo sheriambalimbali zilitungwa ikiwa ni pamoja na Sheria ya Haki zaKupata Taarifa na Sheria ya Msaada wa Kisheria ambazo zikochini ya usimamizi ya Wizara yangu pamoja na Sheria yaMarekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 03 ya mwaka 2016 naSheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 04 ya mwaka2016 na Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 01ya mwaka 2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la uendeshaji wamashtaka, Mkurugenzi wa Mashtaka aliendelea kuratibushughuli za upelelezi wa makosa ya jinai, kufungua nakuendesha mashauri Mahakamani. Katika kipindi cha Julai2016 hadi Machi 2017 kulikuwa na jumla ya mashauri ya jinai31,723 yaliyoendeshwa katika Mahakama mbalimbali nchini.Kati ya hayo, mashauri 14,732 sawa na asilimia 46 yalitolewauamuzi na Mahakama na mengine 16,991 yanaendeleakusikilizwa. Aidha, kulikuwa na mashauri matano yanayohusuurejeshaji wa mali zilizotokana na uhalifu yaliyokamilikakusikilizwa na fedha taslimu shilingi 439,628,000 kurejeshwaSerikalini ikiwa ni pamoja na nyumba nane, magari 25, pikipiki10, boti nane na viwanja vinne. Aidha, jumla ya shilingi1,110,893,995 zililipwa kama faini kutokana na mashauri hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha Julai, 2016hadi Machi, 2017 kulikuwa na mashauri 463 ya ujangili, katiya hayo mashauri 158 yalihitimishwa kwa wastani, kutiwahatiani na kupewa adhabu za vifungo na kulipa faini yashilingi milioni 811 taslimu. Aidha, kulikuwa na mashauri 9,813ya dawa za kulevya yakiwemo mashauri 161 yanayohusukiwango kikubwa cha dawa za kulevya ambapo mashauritisa kati ya hayo yalihitimishwa. Katika mashauriyaliyohitimishwa washtakiwa 13 walihukumiwa vifungo vyakati ya miaka 20 na maisha jela.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

Aidha, kilo 279 za dawa za aina ya cocaine na herionna kilo 21 za mirungi ziliteketezwa kwa amri ya Mahakama.Pia Mkurugenzi wa Mashtaka alipokea jumla ya majalada510 ya tuhuma za rushwa kutoka TAKUKURU yakiwemomajalada mapya 306 na 204 yaliyorejeshwa tena baada yauchunguzi zaidi. Kati ya hayo, majalada 201 yaliandaliwahati za mashtaka, majalada 136 yalirejeshwa TAKUKURU kwahatua zaidi za uchunguzi, majalada 168 yanaendeleakufanyiwa uchambuzi wa kisheria na mengine matanoyalifungwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uendeshaji wamashauri ya madai, Katiba na haki za binadamu; Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali iliendesha jumla ya mashauri984 ya madai yanayohusisha Serikali katika Mahakama Kuuna Mahakama ya Rufani yakiwemo mashauri 883 ya zamanina mashauri 101 mapya. Kati ya hayo, mashauri 11 yalitolewauamuzi na mashauri mengi 973 yanaendelea kusikilizwa.Serikali ilishinda katika mashauri tisa na kushindwa katikamashauri mawili. Kutokana na mafanikio hayo Serikali iliwezakuokoa takribani shilingi bilioni 23.75 sawa na asilimia 99.87ya fedha zinazodaiwa katika mashauri yalioisha. Vilevilekulikuwa na maombi 48 mapya na 277 ya zamani na hivyokufanya maombi yote kuwa 325. Kati ya hayo maombi 12yamehitimishwa na maombi 313 yanaendelea kusikilizwa.Rufani za madai zilizokuwepo ni 59 ikiwemo rufani moja mpyana zote zinaendelea kusikilizwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na jumla yamashauri mapya 32 ya Kikatiba yaliyofunguliwa kwenyeMahakama Kuu ya Tanzania na kufanya jumla ya mashauriyaliyokuwepo kuwa 164 yakiwemo mashauri 132 ya zamaniambapo mashauri 19 yalihitimishwa na kubaki mashauri 145.Katika Mahakama ya Rufani kulikuwa na rufaa saba ambazozinaendelea. Aidha, katika Mahakama ya Afrika ya Haki zaBinadamu na Watu (The African Court on Human and PeoplesRights) kulifunguliwa jumla ya mashauri 104, kati ya hayomashauri 40 ni mapya na 64 ni ya zamani na yanaendeleakusikilizwa, hali kadhalika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali iliendesha jumla ya mashauri sita katika Mahakama

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (The East African Court ofJustice), kati ya hayo, shauri moja lilimalizika na mashaurimengine matano bado yanaendelea kusikilizwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uhakiki wa mikatabana usimamizi wa sheria za kimataifa; Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali iliendelea kutoa ushauri wa kisheria kwenyemikataba na makubaliano mbalimbali ambapo katikakipindi cha Julai, 2016 hadi Machi, 2017 ilifanya upekuzi nauhakiki wa jumla ya mikataba 1,473 yenye thamani ya shilingitrilioni 12.6, kati ya hizi ilihusisha mikataba ya ununuzi,ukarabati wa majengo, ujenzi wa barabara na hati zamakubaliano (MOU) kutoka Wizara, Idara na Taasisi za Serikalina Mamlaka za Serikali za Mitaa. Vilevile katika ngazi yaKikanda na Kimataifa ofisi hii ilishiriki katika mikutano 86 yaJumuiya ya Afrika Mashariki, Jumiya ya Maendeleo ya Nchiza Kusini mwa Afrika na Umoja wa Mataifa iliyojadili masualaya sheria na sera za sekta mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu haki za binadamuna msaada wa kisheria, usimamizi na hifadhi ya haki zabinadamu; Wizara iliendelea kuimarisha na kusimamiautekelezaji wa haki za binadamu kama ilivyoainishwa nakuhifadhiwa katika Katiba na sheria za nchi. Katika kipindicha mwaka wa fedha 2016/2017 Wizara iliandaa taarifa yanchi kuhusu utekelezaji wa haki za binadamu iliyowasilishwakwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifachini ya Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mapitio kwa KipindiMaalum (The Universal Periodic Review Mechanism). Taarifahiyo ilijadiliwa kwenye vikao vya 25 na 33 vya Baraza la Hakiza Binadamu vilivyofanyika Geneva, Uswis kati ya Mei naOktoba, 2016. Kupitia taarifa hiyo Serikali ilipata fursa yakufafanua mbele ya Jumuiya ya Kimataifa kuhusu hali yautekelezaji wa haki za binadamu nchini na kutoa msimamowa nchi kuhusiana na mapendekezo mbalimbaliyaliyotolewa na Baraza la Haki za Binadamu wakati wakujadiliwa kwa taarifa ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Haki za Binadamuna Utawala Bora ilifuatilia na kutoa ushauri kwa Serikali na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

taasisi zake kuhusu utekelezaji wa haki za binadamu namisingi ya utawala bora nchini. Hii ni pamoja na kufanyaufuatiliaji wa haki za binadamu kwa watu walio katikamakundi yenye mahitaji maalum, haki za mahabusu nawafungwa, kufanya uchunguzi wa tuhuma za uvunjaji wahaki za binadamu na ukiukaji wa misingi ya utawala borana kutoa elimu ya haki za binadamu na utawala bora kwajamii. Katika kipindi hicho Tume ilitembelea jumla yamagereza 41 katika Mikoa 15 ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya,Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Lindi, Pwani, Manyara, Mara,Kigoma, Mwanza, Iringa, Singida na Dodoma. Pia Tumeilikagua vituo vya polisi 59, mahabusu za watoto tano nashule ya maadilisho ili kujiridhisha na utekelezaji wa haki zabinadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ilipokea na kufanyauchunguzi wa malalamiko 7,101 yanayohusu ukiukwaji wahaki za binadamu na kuhitimisha uchunguzi katikamalalamiko 1,443 ambapo malalamiko mengine 5,658yanaendelea kuchunguzwa. Baadhi ya malalamiko yalihusukubambikiziwa kesi, ucheleweshaji wa upelelezi, uendeshajiwa mashauri mahakamani, utoaji wa nakala za hukumu nautekelezaji wa amri za Mahakama. Pia kulikuwepomalalamiko ya migogoro ya ardhi, rushwa katika vyombovya utoaji haki na katika masuala ya mirathi. Aidha, Tumeiliendelea na utekelezaji wa Mpango wa Kazi wa Taifa waHaki za Binadamu (NHRAP) kwa kutoa mafunzo kwa maafisawa Serikali kutoka katika mikoa mbalimbali, asasi za kiraia,watumishi wa mahakama pamoja na watumishi wa tumekwa lengo la kuwajengea uwezo kusimamia na kukuza hakiza binadamu katika maeneo yao ya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu huduma ya msaadawa sheria; kwa kutambua umuhimu wa msaada wa kisheriakatika kuimarisha upatikanaji wa haki nchini hususan kwawatu wasio na uwezo wa kumudu gharama za uwakili,Wizara ilichukua hatua ya kuzitambua na kuzisajili asasi zisizoza Kiserikali zinazojihusisha na utoaji wa msaada wa kisheria.Katika kipindi hicho, Wizara ilifanya utambuzi wa zaidi yaasasi 290 zinazotoa msaada wa kisheria nchini na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

kuwasimamia wasaidizi wa kisheria (paralegals) zaidi ya 5,000.Pia ilichukua hatua ya kuweka mwongozo wa kisheriaambapo Bunge lako Tukufu lilitunga Sheria ya Msaada waKisheria na hivyo kuweka mfumo rasmi wa kisheria kusimamiaupatikanaji wa utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchiwasio na uwezo wa kugharamia huduma za kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utafiti wa kisheria;Wizara inatambua nafasi ya utafiti katika maendeleo ya sheriaili kuwa na mfumo wenye kuakisi mahitaji halisi ya nchi kwamaendeleo na ustawi wa watu. Hivyo kwa kutambua hilo,Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imekamilisha utafiti wamfumo wa sheria zinazohusu hifadhi ya taarifa binafsi (reviewof legal framework on personal data protection in Tanzania),mfumo wa sheria kuhusu haki za walaji na watumiaji wabidhaa (review of legal framework on consumers’ protection)na sheria zinazohusu masuala ya usajili wa matukio muhimuya binadamu (review of the legal framework on civilregistration and vital statistics). Maendeleo ya kinakuhusu hali ya utafiti wa kisheria kwa mwaka wa fedha 2016/2017 yanapatikana katika kiambatisho namba mbili 2 A na 2B.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu urejeshwaji wawahalifu na ushirikiano na mataifa kwenye makosa ya jinai;Tanzania imeendelea kutekeleza wajibu wake Kimataifa kwakushirikiana katika kupambana na uhalifu wa Kimataifa kwakurejesha watuhumiwa wa uhalifu katika nchi walikofanyamakosa. Katika kutekeleza wajibu huu Tanzania ilipokeamaombi ya kuwarejesha watuhumiwa wanne katika nchiwanakotuhumiwa kutenda uhalifu. Maombi matatuyanaendelea kufanyiwa kazi na maombi mawili yalikataliwakutokana na kutokidhi matakwa ya dheria. Pia kwa mujibuya Sheria ya Ushikiriano katika Masuala ya Jinai (MutualAssistant Criminal Matters Act) nchi yetu ilipokea jumla yamaombi 12 ya kukusanya ushahidi na vielelezo. Maombimanne yalishughulikiwa na mengine Nane yanaendeleakufanyiwa uchambuzi. Aidha Tanzania ilipeleka nje ya nchimaombi mawili ya kukusanya ushahidi na vielelezo ambavyoyanaendelea kushughulikiwa kushughulikia wahusika.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu usajili, ufilisi naudhamini; usajili wa matukio muhimu ya mwanadamu.Wakala wa usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kipindi chaJulai 2016 mpaka Machi, 2017 umesajili matukio muhimu kamaifuatavyo:-

(i) Kusajili na kutoa vyeti kwa watoto 869,182 wa umriwa chini ya miaka mitano katika mikoa saba ya Iringa,Njombe, Mbeya, Songwe, Mwanza, Geita na Shinyanga.

(ii) Usajili wa watoto walioko shuleni 28,554 katikashule za msingi zilizopo kwenye Halmashauri ya Manispaa yaIlala, Temeke, Kinondoni na Iringa.

(iii) Kampeni ya Usajili ya katika Wilaya Nzega naTunduru ambapo jumla ya watu 23,160 walisajiliwa nakupewa vyeti.

(iv) Kufanya usajili wa kawaida wa vizazi laki 348,544.

(v) Matukio ya vifo 5,213, ndoa 21,057 na talaka 85.Aidha jumla ya leseni mpya 2,477 za kufungisha ndoazilizolewa na leseni 1,618 kuuhishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia RITA imeendelea kutoaelimu kwa umma kuhusu masuala ya usajili kuhusu matukiomuhimu ya binadamu kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu kupitia RITAimesajili jumla ya miunganisho 164 ya wadhamini vyamasiasa, makanisa, misikiti, na mali za vikundi vya kijamii,Kuendelea kusimamia mali sizizokuwa na wenyewe pamojana masuala ya mirathi kulingana na amri za Mahakama.Aidha, mapitio yamefanywa katika bodi za wadhamini zataasisi zilizosajiliwa ili kufahamu uhai wake, na jumla ya taasisi181 zilifutiwa usajili wake. Pia jumla ya wosia 50 ziliandikwana kuhifadhiwa na huduma ya Ushauri wa masuala ya wosiana mirathi imetolewa kwa wananchi kupitia kampenimaalum. Orodha ya Bodi za Wadhamini zi l izofutwainapatikana kwenye kiambatisho namba 3.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu taasisi za mafunzomipango na miradi ya maendeleo; Chuo cha Uongozi waMahakama - Lushoto. Chuo cha Uongozi wa Makama Lushotokatika kutekeleza jukumu la kutoa elimu endelevu kwawatumishi wa Mahakama na sekta ya sheria imeendeleakutoa mafunzo ya Astashahada na Stashahada kwawatumishi wa Mahakama na jamii nzima kwa ujumla.Katika mwaka wa fedha katika 2016/2017 Chuo kwakushirikiana na wadau wa maendeleo, UN Women naChama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) kiliandaakitabu cha kuratibu, kuendesha na kufundishia wakufunzi wamasuala ya haki za binadamu na mapambano dhidi yaukatili kwa wanawake na watoto na hadi sasa kitabu hichokimetumika kuendesha mafunzo kwa Majaji, Wasajili,Mahakimu, Askari Polisi, Askari Magereza pamoja naWahadhiri wa Chuo hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2016/2017 Chuo kiliendesha mafunzo kwa watumishi waMahakama zaidi ya 400 ikiwemo mafunzo maalum kwaMajaji 24 waliojengewa uwezo na weledi wa namna yakuendesha mashauri ya makosa ya rushwa na uhujumuuchumi. Vilevile kiliandaa na kuendesha mafunzo ya namnaya kufanya upelelezi na kuendesha namna ya kushughulikiamashauri ya ujangili kwa Mahakimu 30, Mawakili wa Serikali10, Askari Polisi watano na Askari wa Wanyama poriwatano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Taasisi ya Mafunzo yaUanasheria kwa Vitendo; taasisi imeendelea kuongeza uwezowake wa kudahili wanafunzi katika makundi yaani cohortsmbalimbali katika mwaka wa fedha 2016/2017 ilidahili jumlaya wanafunzi 1,680 katika makundi matatu kundi la 23, kundila 22, kundi la 23 na kundi la 24. Kwa sasa taasisi ina jumla yawanafunzi 2,234 ambao wamesajiliwa katika makundimanne yaliyo katika hatua tofauti za mafunzo. Taasisi hiiimeendelea kujiimarisha katika masuala ya utafiti, kutoahuduma za udahili kwa njia za kieletroniki na kuendeshahuduma za maktaba ya kisasa inayohifadhi zaidi ya nakala7,000 za vitabu na machapisho ya aina mbalimbali.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maendeleo yarasilimaliwatu; Wizara imeendelea kusimamia watumishiwake ili kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao kwa mujibuwa sheria, kanuni, na taratibu za utumishi wa umma. Wizaraimechukua hatua za kinidhamu dhidi ya watumishiwaliokiuka maandili ya kazi kwa baadhi yao kupewa onyokushushwa vyeo na wengine kufunzwa kazi. Aidha, Wizarailiajiri, kuthibitishwa kazini na kupandishwa vyeo kwawatumishi wote waliostahili. Natoa wito kwa watumishi wotekuzingatia nidhamu ya kazi na kutekeleza majukumu yao kwajuhudi maarifa na weledi ili kufanikisha malengo ya Wizaraya kuwatumikia wananchi kwa kutoa huduma zilizo bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mpango na miradiya maendeleo; ni dhamira za Wizara yangu kusongezahuduma za kisheria karibu nawananchi kwa kubuni nakutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kwakuimarisha ushirikiano na wadau wa maendeleo. Katikamwaka wa fedha 2016/2017 Wizara imetekeleza miradi naprogramu mpya za maendeleo zikiwemo:-

(a) Programu ya maboresho ya Mahakama.

(b) Mradi wa kuimarisha mfumo wa upatikanaji hakinchini (strength excess justice human rights protectionTanzania).

(c) Programu ya ulinzi na upatikanaji wa haki yamtoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maboresho ya Mahakamani program ya miaka mitano inayotekelezwa na Serikali yaTanzania kwa fedha kutoka Benki ya Dunia kwa madhuminiya kuimarisha mfumo wa Mahakama upatikanaji na uborawa huduma za Mahakama nchini. Programu inahusuupatikanaji wa haki nchini ni sehemu ya mpango waMaendeleo wa Umoja wa Mataifa unaojulikana kamaUNDAP II . Wizara kwa kushirikiana na UNDP imeandaa andikola mradi wa mpango kazi kwa kipindi cha mwaka wa fedha2017/2018 ambapo kupitia Programu ya UNDAP II Tanzania

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

inaendelea kutekeleza mradi wa usajili wa watoto wa umrichini ya miaka mitano, mradi wa kudhibiti vitendo vya ukatiliwa kijinsia kwa wanawake na watoto, kukuza na kulindahaki za binadamu pamoja na usimamizi wa mfumo wa utoajihaki nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mafankio yaliyopatikana;mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wavipaumbele vya Wizara kwa mwaka 2016/2017 ni pamojana kuanzishwa kwa Divisheni ya Mahakama Kuu ya Makosaya Rushwa na Uhujumu Uchumi, kukamilika kwa mfumo wakisheria wa kusimamia na kuratibu utoaji wa msaada wakisheria nchini, kutungwa kwa sheria ya upatikanaji wataarifa, kuendelea kusimamia mashauri yote ya jinai namadai, kumalizika kwa mashauri yote ya uchaguzi yote waUbunge na Udiwani kwa wakati kama ilivyotakwa la kisheria,kuweka mfumo wa usajili wa vizazi kwa watoto walio chiniya umri wa chini ya miaka mitano katika Mikoa saba yaGeita, Iringa, Mbeya Mwanza, Shinyanga na Songwe; ujenzina ukarabati wa majengo ya Mahakama katika ngazi yambalimbali, kufanya utafiti na kuhuisha sheria mbalimbali ilikuakisi mahitaji halisi kwa maendeleo ya watu, kuongezekakwa matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma katikautoaji wa huduma na ufuatiliaji wa hali za wafungwa namahabusu magerezani uliopelekea kufanyika kwamaboresho ya huduma kwa wafungwa na mahabusu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mafanikio mengine nipamoja na kukamilisha uhakiki wa watumishi wote waWizara, kuimarika kwa usimamizi wa rasilimaliwatu nahuduma kwa watumishi ikiwa ni pamoja na kuboreshamazingira ya kazi. Kuendelea kusimamia maadili yawatumishi, kukamilika kwa rasimu ya mkakati wa Kitaifa wausajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu,ambayo ipo katika hatua za maamuzi Serikalini, kukamilikakwa mfumo wa TEHAMA utakaowezesha ubadilishanaji wataarifa kati ya RITA, Tume ya Uchaguzi na Mamlaka yaVitambulisho vya Taifa, kukamilika kwa mfumo wa kisheriawa kusimamia na kuratibu huduma ya msaada wa kisheriana kuendelea kutoa mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

Nipende kusizitiza kuwa Wizara inatambua kwamba pamojana mafanikio yaliyopatikana yapo maeneleo badoyanahitaji kufanyiwa kazi ili kufikiwa malengo tuliyojiwekea.Hivyo Wizara yangu itahakikisha kuwa kazi mbalimbalizi l izosalia zitakamilishwa sanjari na utekelezaji wavipaumbele vya mwaka wa fedha 2017/2018.

Mtiririko wa mapato na maduhuli ya Serikali; katikamwaka wa fedha 2016/2017 Wizara ya Katiba na Sheriailiidhinishiwa jumla ya shilingi 155,192,263,000 kwa ajili yamatumizi ya kawaida na ya maendeleo. Kati ya fedha hizomishahara ni shilingi 67,328,697,000 na matumizi mengineyo(OC) ni shilingi 50,404,380,000. Fedha kwa ajili ya miradi yamaendeleo ni shilingi 37,459,186,000 Ambapo kati ya fedhahizo shilingi 13,919,000,000 ni fedha za ndani na shilingi23,550,186,000 ni fedha za nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi kufikia mweziSeptemba, 2017 Wizara ilipokea jumla ya shilingi 80,503,233,455sawa na asilimia 52 ya fedha zilizoidhinishwa kati ya hizoshilingi 45,545,485,311 ni mishahara ya watumishi na shilingi31,434,746,899 ni kwa matumizi mengineyo sawa na asilimia62. Fedha za maendeleo ni shilingi 3,523,001,645 sawa naasilimia tisa ya bajeti ya miradi ambavyo fedha za ndani nishilingi 246,882,000 na fedha za nje ni shilingi 3,276,119,645.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha katika mwaka wafedha 2016/2017, Wizara ilipanga na kukusanya jumla yashilingi 17,085,829,511 kama maduhuli ya Serikali kutoka vyanzombalimbali vinavyosimamiwa na Wizara. Kufikia mweziMachi, 2017 Wizara ilikusanya jumla ya shilingi bilioni10,976,126,511 sawa na asilimia 64 ya makadirio yote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto na mikakatiiliyopo; pamoja na mafanikio yaliyopatika katika utekelezajiwa bajeti ya mwaka 2016/2017, kumekuwepo nachangamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na upungufuwa rasilimali muhimu ikiwemo fedha, watu na vitendea kazi,uchakavu na uhaba wa miundombinu ya Mahakama,mahitaji ya TEHAMA katika usimamizi wa mashauri, uelewa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

mdogo wa jamii kuhusu haki na wajibu wa raia, kuwepokwa uhalifu unaotumia teknolojia za kisasa na kuhusisha nchizaidi ya moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, i l i kukabiliana nachangamoto hizo Wizara yangu iliendelea kubuni nakutekeleza mikakati mbalimbali ya kukabiliana nazo katikakuhakikisha kuwa nchi inakuwa na mfumo imara wa kikatibana kisheria ili kufanikisha mipango ya maendeleo ya Taifamikakati hiyo ni pamoja na:-

(a) Kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimentiya Utumishi wa Umma katika kuyapatia ufumbuzi matatizoyanayohusiana na upungufu wa watumishi ikiwa ni pamojana upatikanaji wa vibali vya ajira, kujaza nafasi zilizoachwawazi na kushughulikia maslahi ya watumishi.

(b) Kutafuta vyanzo vipya vya mapato ili kufanikishautekelezaji wa miradi ya maendeleo ukiwepo mradi wa e-justice na programu ya maboresho ya mfumo wamahakama.

(c) Kuendelea kubana matumizi na kuepukana namatumizi yasiyo ya lazima kufanyika kwa wakati uliopo.

(d) Kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wahuduma za kisheria na ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali.

(e) Kuwajengea uwezo watumishi wa sekta ya sheriakatika kukabiliana na aina mpya za uhalifu.

(f) Kuboresha huduma za mafunzo ya wanasheria kwavitendo.

(g) Kutumia teknolojia ya gharama nafuu katika ujenziwa miundombinu ya mahakama ili kukabiliana na ukubwawa gharama za utekelezaji wa mradi wa maendeleo.

(h) Kuimarisha mfumo wa usimamizi, ufuatiliaji natathmini ya kazi za Wizara.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

Mheshimiwa Mwenyekiti, mafanikio katika utekelezajiwa majukumu ya Wizara ya Katiba ya Sheria yamewezekanakutokana na ushirikiano thabiti wa wadau wa maendeleoambao wameendelea kutupatia katika utekelezaji waprogramu na miradi mbalimbali ya maendeleo. Kwa namnaya pekee nichukue fursa hii kuwashukuru Benki ya Dunia, Shirikala Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Shirika la Umojawa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Umojawa Mataifa la Kuhudumia Wanawake (UN Women), Shirikala Msaada wa Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID)na Taasisi ya Bloomberg Data for Health Initiative. Napendakuwahakikishia wote kwamba Wizara yangu inathamini sanamchango wao na tutaendelea kutoa ushirikiano wakuhakikisha kwamba mipango na melengo ya Serikali kuhususekta ya sheria yanafanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuwa mchoyo wafadhila nisipotambua kazi iliyofanywa na Viongozi wenzangukatika Wizara, hivyo kwa moyo wa dhati napendanimshukuru Profesa Sifuni Ernest Mchome, Katibu Mkuu naNdugu Amon Mpanju, Naibu Katibu Mkuu, viongozi wakuuna watalaam wa taasisi zote zilizo chini ya Wizara yangukwa ushirikiano mkubwa walionipa katika kutekelezamajukumu yangu ya kila siku.

Vilevile naishukuru sana kama nilivyosema familiayangu kwa kuendelea kunifariji na kunitia moyo wakati wotewa utekelezaji wa majukumu mazito yanayoambatana nawadhifa huu wa Waziri wa Katika na Sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango na bajeti ya Wizarakwa mwaka 2017/2018; na katika hawa wa kuwashukurunapenda leo kwa namna ya pekee kabisa nimshukurumwalimu wangu wa darasa la kwanza na la pili MwalimuPenina Mnyangwira aliyenifikisha hapa nilipofika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2017/2018Wizara yangu itaendelea na juhudi za kuimarisha utawalawa sheria na misingi ya haki za binadamu kwa kuhakikishakuwa wananchi wanapata huduma bora na za uhakikika.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

Katika kufanikisha azma hiyo Wizara imeainisha maeneomahsusi ya kipaumbele kwa mwaka kwa fedha ujao kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Katiba na Sheria:-

(i) Kukamilisha uhamishaji wa Makao Makuu ya Wizarakutoka Dar es Salaam kuja Dodoma.

(ii) Kuratibu masuala ya kisera katika Wizara na taasisizake.

(iii) Kuratibu na kusimamia huduma na msaada wakisheria nchini.

(iv) Kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa masualaya Katiba na Sheria.

(v) Kusimamia utekelezaji wa haki za binadamu Kitaifa,Kikanda na Kimataifa.

(vi) Kuwajengea uwezo watumishi kuendelezaubunifu, maarifa na weledi ili kuleta tija na ufanisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakama ya Tanzania:-

(i) Kuharakisha usikilizaji wa mashauri.

(ii) Kuimarisha utawala bora maadili na uwajibikaji.

(i i i) Kuboresha mazingira ya kufanyakazi kwakuongeza upatikanaji wa vitendea kazi muhimu.

(iv) Kujenga na kukarabati miundombinu katika ngazimbalimbali.

(v) Kuongeza matumizi ya TEHAMA ili kurahisishausikilizaji wa mashauri na shughuli za utawala ili kufikishahuduma kwa wananchi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

(vi) Kuimarisha uwezo katika ukaguzi na usimamiziwa shughuli za Kimahakama.

(vii) Kuendelea kuimarisha uwezo wa rasilimali watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Mwanasheria Mkuuwa Serikali:-

(i) Kuimarisha mfumo wa uandishi na urekebu washeria.

(ii) Kusimamia shughuli za uendeshaji wa mashauri yajinai madai Katiba na haki za binadamu.

(iii) Kuimarisha usimamizi wa masuala ya mikataba.

(iv) Kuongeza matumizi ya TEHAMA katika utoaji wahuduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Haki za Binadamuna Utawala Bora:-

(i) Kukuza nakutetea haki za binadamu hususani hakiza makundi yenye mahitaji maalum.

(ii) Kuongeza uelewa wa haki za binadamu, utawalabora na wajibu wa raia.

(iii) Kufanya uchunguzi wa malalamiko na kuyapatiaufumbuzi kwa njia ya upatanishi na usuluhishi.

(iv) Kushirikiana na wadau mbalimbali nchini Kikandana Kimataifa kwenye masuala ya haki za binadamu nautawala bora.

(v) Kujenga uwezo wa watumishi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Kurebisha SheriaTanzania:-

(i) Kukamilisha utafiti kuhusu mfumo wa sheria zausimamizi haki jinai (review of legal framework on criminaljustice administration).

(ii) Kufanya utafiti kuhusu sheria za mfumo wa ushahidiyaani (review of legal framework on law of evidence).

(iii) Kufanya utafiti kuhusu mfumo wa sheria zausuluhishi (review of legal framework on arbitration).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Usimamizi waMahakama:-

(i) Kuboresha utoaji wa huduma za Mahakama kwakuongeza idadi ya watumishi wa Mahakama wenye weledina sifa stahiki.

(ii) Kuboresha mazingira ya kazi kwa kununuavitendea kazi pamoja na samani za ofisi.

(iii) Kuimarisha nidhamu ya maadili ya watumishi waMahakama kwa kufanya ukaguzi wa Kamati za Maadili zaMahakama.

(iv) Kuwajengea uwezo wajumbe pamoja nawatumishi wa Tume kwa kuwawezesha kuhudhuria mafunzoya muda mfupi na muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala wa Usajili na Ufilisina Udhamini:-

(i) Kutekeleza mkakati wa kitaifa wa usajili wamatukio muhimu ya binadamu.

(ii) Kufanya mapitio ya sheria zinazohusu ufisili (reviewof legal framework on solvency).

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

(ii i) Kuimarisha matumizi ya teknolojia katikakuboresha utoaji wa huduma.

(iv) Kuimarisha ukusanyaji na usimamizi ya maduhuliya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taasisi ya Mafunzo yaWanasheria kwa Vitendo:-

(i) Kudahili na kutoa mafunzo kwa wananfunzi 1,800ili kuongeza idadi ya watalamu wa sheria nchini.

(ii) Kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa mawakili nawadau wengine; katika mambo mapya yanayojitokezakatika taaluma ya sharia (continuing legal education).

(iii)Kuendesha programu za mafunzo kwa Wasaidiziya Sheria (paralegals).

(iv) Kuimarisha miundombinu ya taasisi.

Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto:-

(i) Kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa Majaji naMahakimu.

(ii) Kuimarisha na kuendelea kutoa mafunzo endelevuya Kimahakama, pamoja na mafunzo kazini kwa watumishiwa Mahakama na watumishi wote wa sekta ya sheria kwaujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kufanikisha utekelezaji wavipaumbele hivi Wizara yangu inaomba kuidhinishiwa jumlaya shilingi 166,479,908,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaidana miradi ya maendeleo. Mchanganuo wa makadirio yaBageti kwa mafungu saba ya Wizara na taasisi zake ni kamaifuatavyo; mishahara ya watumishi ni shilingi 76,141,279,000;matumizi mengineyo ni shilingi 66,801,799,000; miradi yamaendeleo shilingi 23,236,830,000; na jumla ni shilingi166,479,908,000.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

Mheshimiwa Mwenyekiti, muhtasari wa matumizi;mchanganuo wa matumizi ya bajeti kwa kila fungu ni kamaifuatavyo:-

Fungu Namba 12 - Tume ya Utumishi wa Mahakama,matumizi ya mishahara ni shilingi 282,400,000;matumizimengineyo milioni 820,507,000;matumizi ya maendeleo yandani haikutengewa, matumizi ya maendeleo kutoka nje piahaikutengewa katika kifungu hicho na jumla ni shilingi1,102,911,000.

Fungu Namba 16 - Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali, matumizi ya mishahara ni 3,863,792,000, matumizimengineyo ni shilingi 3,418,731,000; matumizi ya maendeleoya ndani na matumizi ya maendeleo ya nje hayakutengewafedha katika kifungu hiki na jumla ni shilingi 7,282,523,000.

Fungu Namba 35 - Divisheni ya Mashtaka, matumiziya mishahara ni shilingi 9,478,238,000; matumizi mengineyoni shilingi 5,435,825,000; matumizi ya maendeleo ya ndani namatumizi ya maendeleo ya nje hayakutengewa fedha katikavifungu hivyo na jumla ni shilingi 14,914,063,000.

Fungu Namba 40 - Mfuko wa Mahakama, matumiziya mishahara ni shilingi 54,524,408,000; matumizi mengineyoni shilingi 52,434,610,000; matumizi ya maendeleo ya ndani nishilingi 17,000,000,000, matumizi ya maendeleo ya nje ni shilingi1,158,011,000 na jumla ni shilingi 125,117,029,000.

Fungu Namba 41 - Wizara ya Katiba na Sheria,matumizi ya mishahara ni shilingi 4,897,729,000; matumizimengineyo ni shilingi 2,158,317,000; matumizi ya maendeleoya ndani ni shilingi 1,000,000,000; matumizi ya maendeleo yanje ni shilingi 1,806,020,000 na jumla ni shilingi 9,862,066,000.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

Fungu Namba 55 - Tume ya Haki za Binadamu naUtawala Bora, matumizi ya mishahara ni shilingi 2,328,102,000;matumizi mengineyo ni shilingi 1,566,080,000; matumizi yamaendeleo ya ndani hayakutengewa fedha katika kifunguhiki, matumizi ya maendeleo ya nje ni shilingi 2,272,799,000na jumla ni shilingi 6,116,981,000.

Fungu Namba 59 - Tume ya Kurekebisha Sheria,Matumizi ya mishahara ni shilingi 1,066,606,000, matumizimengineyo ni shilingi 967,729,000, matumizi ya maendeleo yandani hayakutengewa fedha katika kifungu hiki na vivyohivyo maendeleo ya nje na jumla ni shilingi 2,034,355,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, makusanyo na maduhuli yaSerikali; katika mwaka wa fedha 2017/2018 Wizara yanguinatarajia kukusanya kiasi cha shilingi 24,087,507,200 ikiwa nimaduhuli ya Serikali kutokana na vyanzo mbalimbali vyamapato vinavyosimamiwa kama ilivyoainishwa kwenyejedwali hapa chini.

Fungu Namba 16 ni shilingi 3,002,000;Fungu 35 nishilingi 13,002,000; Fungu 40 ni shilingi 9,318,061,200; Fungu 41ni shilingi 14,753,299,000 na Fungu 59 ni shilingi 150,000. Jumlani shilingi 24,087,507,200.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchanganuo wa maombiya fedha za bajeti ya kila Fungu imeainishwa kwenye vitabuvya kasma za mafungu husika ambavyo Wajumbe wa Bungelako Tukufu wamegaiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

(Hoja ilitolewa Iamuliwe)

MWENYEKITI: Ahsante, hoja imetolewa na imeungwamkono.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

HOTUBA YA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, MHESHIMIWAPROF. PALAMAGAMBA JOHN AIDAN MWALUKO KABUDI

(MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YABAJETI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018

KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

A. UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa zilizowasilishwa leokatika Bunge lako tukufu na Mwenyekiti wa Kamati yaKudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria; na Mwenyekiti waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti naomba kutoa hojakwamba Bunge lako sasa likubali kupokea, kujadili nakupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi yaFedha ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha2017/2018.

Shukrani na Pole

2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuruMwenyezi Mungu kwa kuniruzuku uhai na kunijalia afyanjema kuweza kusimama mbele ya Bunge lako tukufukuwasilisha Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara yaKatiba na Sheria kwa Mwaka Fedha 2017/2018. Aidha,napenda kutoa shukurani nyingi kwa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John PombeJoseph Magufuli, kwa heshima kubwa aliyonipa kwa kuniteuakuwa Mbunge na kushika wadhifa wa Waziri wa Katiba naSheria. Kutokana na heshima hiyo, ninaahidi kuitumikia nafasihii kwa hekima, uadilifu na uaminifu kwa kadri alivyonijaliaMwenyezi Mungu. Vivyo hivyo, ninaahidi kuwatumikiawananchi wote nikitambua kuwa wao ndio msingi wamamlaka yote ya Serikali, kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

3. Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwanakupa pole wewe na Bunge lako tukufu kwa kuondokewana Wabunge wenzetu waliotangulia mbele ya haki, ambaoni Mheshimiwa Hafidh Ally Tahir aliyekuwa Mbunge wa Jimbola Dimani, CCM na Dkt. Elly Marko Macha aliyekuwa Mbungewa Viti Maalum, CHADEMA. Pia, natoa pole kwako na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

watanzania wote, ndugu, jamaa na marafiki kutokana nakifo cha Mheshimiwa Samwel John Sitta, aliyekuwa Spika waBunge la Kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nitumiefursa hii kuwapa pole ndugu, jamaa na marafiki pamoja nawananchi walioguswa na misiba hii kwa namna moja aunyingine. Mwenye Mungu azilaze roho za marehemu mahalipema peponi, Amina.

Salamu za Pongezi

4. Mheshimiwa Spika, napenda nikupongeze wewe binafsikwa uongozi wako mahiri wa kuliongoza Bunge letu na hivyokudhihirisha uwezo na uzoefu ulionao katika kuwatumikiawatanzania kupitia chombo hiki. Aidha, nitumie fursa hiikumpongeza Naibu Spika Mheshimiwa Dkt. Tulia AcksonMwansasu na Wenyeviti wote wa Bunge kwa kuendeleakutekeleza majukumu yao vema kwa kuzingatia sheria,kanuni na taratibu.

5. Mheshimiwa Spika, pia nampongeza Waziri Mkuu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim M.Majaliwa (Mb), kwa hotuba yake nzuri ambayo imetoamwelekeo wa kisera katika utekelezaji wa shughuli za Serikalikwa kipindi cha Mwaka wa Fedha 2017/2018. Vilevile,nampongeza kwa uongozi wake thabiti katika kusimamiavema shughuli za Serikali ndani na nje ya Bunge lako Tukufu.

6. Mheshimiwa Spika, niruhusu sasa niwapongezeMwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba naSheria, Mheshimiwa Mohamed Omari Mchengerwa, Mbungewa Rufiji na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge yaBajeti, Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge waMtwara Vijijini kwa kuziongoza vema Kamati zao. Maoni naushauri wao umekuwa ni msaada mkubwa kwa Wizarayangu katika kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumiaWatanzania. Napenda niwahakikishie kuwa Wizara yanguinayo imani kubwa katika uongozi wao na itaendeleakuwapatia ushirikiano unaostahil i katika kipindiwatakachokuwa katika nyadhifa hizo. Pia natoa shukranizangu za dhati kwa kamati hizo kwa kazi kubwa ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

kuchambua Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumiziya Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Mfuko waMahakama kwa mwaka wa fedha 2017/18. Hakikatunatambua na kuthamini mchango wa Kamati hizi katikakuhakikisha kuwa sekta ya sheria inabaki kuwa kiungomuhimu kwa maendeleo ya nchi yetu kiuchumi, kijamii,kisiasa, kimazingira na kiteknolojia.

7. Mheshimiwa Spika, niruhusu sasa niwapongezewabunge wenzangu wote kwa heshima waliyopewa yakuwa wabunge wa Bunge lako Tukufu. Kwa namna ya pekeenatoa pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa AbdallahMajura Bulembo (Mb), Mheshimiwa Anna Kilango Malecela(Mb), Mheshimiwa Juma Ali Juma (Mb), Mheshimiwa SalmaRashid Kikwete (Mb) na Mheshimiwa Getrude PangalileRwakatare (Mb) kwa heshima kubwa waliyopewa yakulitumikia Taifa letu kupitia chombo hiki kitukufu. Binafsi,ninawatakia kheri na Baraka za Mwenyezi Mungu katikakutekeleza majukumu yao ya Ubunge.

B. DIRA NA DHIMA

8. Mheshimiwa Spika, Dira ya Wizara ya Mambo ya Katibana Sheria ni kuwa na Katiba na Sheria Wezeshi kwaMaendeleo ya Taifa. Madhumuni ya Dira hii nikuwekamazingira rafiki kisera na kisheria ya kuwezesha utekelezajiwa mipango ya maendeleo ya Taifa, kudumisha hali ya amani,utulivu na utangamano wa kitaifa ambavyo vimeendeleakuwepo nchini. Aidha, Dhima ya Wizara ni Kuwa na MfumoMadhubuti wa kikatiba na kisheria katika KufanikishaMipango ya Maendeleo ya Taifa. Dhima hii inahimizakufanya kazi kwa weledi na ubunifu katika kuhakikishakunakuwepo mazingira rafiki ya upatikanaji wa hudumamuhimu za kisheria.

C. MUUNDO NA MAJUKUMU YA WIZARA

9. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Katiba na Sheriainajumuisha Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Tume

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Utumishi waMahakama, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini, Taasisi yaMafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo na Chuo cha Uongoziwa Mahakama-Lushoto. Kwa pamoja tumeendeleakutekeleza majukumu yetu ya kuwahudumia wananchi kwakutoa huduma mbalimbali za kisheria na kuhakikisha kuwawananchi wanaifikia na kupata haki kwa wakatiwanapoitafuta.

10. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inao wajibu wakuhakikisha kuwa nchi inaongozwa kwa kuzingatia Katiba,sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na vyombo halali nakwamba haki inaendelea kutawala katika jamii wakati wote.Hivyo, kwa kutambua wajibu huo Wizara yangu imeendeleakutekeleza majukumu yake kama yalivyo kwenye Hati yamgawanyo wa majukumu kwa mawaziri (Instrument),iliyotolewa kupitia Tangazo la Serikali Na.144 la tarehe 22Aprili, 2016, ambayo ni:

i. kuweka sera kuhusu masuala ya sheria nautekelezaji wake;

ii. kushughulikia masuala ya Katiba;

iii. kusimamia haki na mfumo wa utoaji haki;

iv. uandishi wa sheria;

v. uendeshaji wa mashtaka;

vi. Kushughulikia mashauri ya madai, usuluhishi,mikataba na sheria za kimataifa;

vii. kushughulikia masuala ya haki za binadamu namsaada wa kisheria;

viii. kusimamia na kufanya utafiti wa maboreshoya sheria;

ix. kushughulikia urejeshwaji wa wahalifu na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

kuendeleza ushirikiano na mataifa mbalimbalikwenye makosa ya jinai;

x. kusajili matukio muhimu ya binadamuyanayohusu vizazi, vifo, ndoa, talaka na uasiliwa watoto; pamoja na kusimamia masuala yaufilisi na udhamini;

xi. kuboresha utendaji na maendeleo ya rasilimaliwatu katika Wizara; na

xii. kuratibu shughuli za taasisi, mipango na miradiya maendeleo chini ya Wizara.

D. MAPITIO YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2016/2017

11. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha2016/2017 Wizara yangu ilipanga na kutekeleza majukumuyake kwa kubainisha maeneo mahsusi ya kipaumbeleyafuatayo:

i. Kuimarisha usimamizi na uratibu wa mfumowa sheria;

ii. Kuanzisha Divisheni ya Mahakama Kuu yaMakosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi;

iii. Kuimarisha Mfumo wa Haki na Utoaji Haki

iv. Kuimarisha usimamizi wa miradi ya ujenzi naukarabati wa miundombinu ya mahakamana taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara;

v. Kuimarisha matumizi ya mifumo yakielektroniki ya kutunza kumbukumbu nanyaraka muhimu pamoja na kutoleahuduma;

vi. Kuimarisha shughuli za utafiti na uboreshaji washeria nchini;

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

vii. Kuimarisha uandishi na urekebu wa sheria zanchi;

viii. Kuboresha mazingira ya kufanyia kazi,maendeleo na ustawi wa watumishi;

ix. Kuimarisha mfumo wa mafunzo ya uanasheriakwa vitendo kwa kuongeza udahili wawanafunzi na kupanua wigo wa utoaji wahuduma;

x. Kuimarisha upatikanaji wa msaada wakisheria kwa watu wasio na uwezo;

xi. Kuimarisha shughuli za usajili wa matukiomuhimu ya binadamu.

12. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia vipaumbele hivyo,Wizara iliandaa na kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu,Mpango na Bajeti na kupitishwa kwa utekelezaji. Kwaheshima na taadhima, naomba sasa uniruhusu kuwasilishambele ya Bunge hili taarifa kuhusu hatua mbalimbalizilizochukuliwa katika kutekeleza Mpango na Bajeti kwaMwaka wa Fedha 2016/17, mafanikio yaliyopatikana nachangamoto mbalimbali ambazo Wizara ilikabiliana nazo,kama ifuatavyo:-

Sera na Masuala ya SheriaMaandalizi ya Sera ya Taifa ya Sheria

13. Mheshimiwa Spika, Wizara iliendelea na juhudi zakuandika sera mahsusi kuhusu masuala ya sheria kwakuandaa Rasimu ya Sera yaTaifa ya Sheria ambayo kwa sasainajadiliwa na makundi mbalimbali ya wadau ili kutoa fursakwa Wizara kukusanya maoni yatakayofanya Sera hiyo kukidhimahitaji ya sasa ya sekta ya sheria na Taifa kwa ujumla. Nimatarajio yangu kwamba Serikali ikishapitisha Sera hii nakuanza kutumika itakuwa ni hatua muhimu katika kuimarishausimamizi na uendelezaji wa mfumo wa sheria nchini kwamaendeleo ya Taifa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

Tathimini ya Hali ya Utekelezaji wa Sheria Nchini

14. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Katiba na Sheria inayodhamana ya kuimarisha na kusimamia mfumo wa sherianchini. Katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2016/2017, Wizarailifuatilia utekelezaji wa sheria mbalimbali kupitia wizara,idara, wakala na mamlaka nyingine za Serikali ili kutathminihali ya utekelezaji wa sheria nchini. Kukamilika kwa zoezi hilikutaiwezesha Wizara kutoa mwongozo wa namna yakuimarisha mfumo wa sheria nchini.

Sera na Makubaliano ya Kimataifa na Kikanda

15. Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu nchi yetu imekuwamwanachama wa taasisi mbalimbali za kikanda nakimataifa kupitia Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika,Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya yaAfrika Mashariki na nyinginezo. Kupitia taasisi hizo, Tanzaniaimeendelea kuridhia Sera, Malengo na Mipango yaMaendeleo inayopitishwa na taasisi husika ikiwemo (a)Malengo ya Maendeleo Endelevu [Sustainable DevelopementGoals], (b) Mpango wa Maendeleo wa Afrika na (c) MpangoKazi wa Afrika wa Kugharamia Shughuli za Maendeleo [AddisAbaba Action Agenda]. Kwa kutambua wajibu ilionaokatika kufanikisha makubaliano hayo, Wizara yangu imefanyauchambuzi wa maeneo muhimu na kuweka mikakati yakuiwezesha kutekeleza vema wajibu huu wa kimataifa sanjarina mipango ya ndani ya sekta. Kutokana na uchambuzi huoWizara imebainisha maeneo lengwa (thematic areas) manneambayo kwa namna moja au nyingine yanaakisi malengoya Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano(FYDPII) na pia Mpango Mkakati wa Wizara. Maeneo hayoni, upatikanaji haki kwa wote na utawala wa sheria; amanina ushirikishaji wananchi kwa maendeleo endelevu; usawawa kijinsia; na haki za binadamu.

Haki na Mfumo wa Utoaji Haki

16. Mheshimwa Spika, Katiba imeipa mamlaka Mahakamaya Tanzania kuwa ndicho chombo pekee cha utoaji haki

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

nchini. Katika kuhakikisha kuwa chombo hiki kinatekelezamajukumu yake ipasavyo na kwa ufanisi, sheria zimewekamfumo rasmi wa utatuzi wa migogoro unaojumuisha mfumowa upelelezi wa makosa ya jinai, uendeshaji wa mashtaka,usikilizaji wa mashauri pamoja na mifumo ya usuluhishi. Hivyo,katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17, Serikali ilichukuahatua madhubuti za kuimarisha mfumo wa utoaji haki nchinikwa kuanzisha Divisheni ya Mahakama Kuu ya Makosa yaRushwa na Uhujumu Uchumi; kuharakisha usikilizaji wamashauri; na ujenzi wa miundombinu muhimu kamaifuatavyo:-

Divisheni ya Mahakama Kuu ya Makosa ya Rushwa naUhujumu Uchumi

17. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho Wizaraimetekeleza kwa vitendo azma ya Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John PombeJoseph Magufuli, ya kupambana na rushwa na ufisadi nchinikwa nguvu zote kwa kuanzisha Divisheni ya Mahakama Kuuya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi. Divisheni imeanzakufanya kazi katika majengo yaliyoko kwenye Taasisi yaMafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo; na kwamba kila Kandaya Mahakama Kuu ni Masjala Ndogo ya Divisheni hiyo. Hatuamuhimu zilizochukuliwa ni pamoja na kufanya marekebishoya sheria na kuandaa kanuni za uendeshaji wa Mahakama;kufanya ukarabati wa majengo, ununuzi wa vifaa, kuajiri nakutoa mafunzo kwa watumishi wa Divisheni. Hadi sasaDivisheni hiyo imeweza kusajili jumla ya maombi 25, kati yahayo, 20 yamesajiliwa Dar es Salaam, 3 Mtwara, 1 Iringa na 1Tabora. Aidha, kati ya maombi 25 yaliyosajiliwa maombi 13yametolewa uamuzi na mengine yanaendelea kufanyiwakazi.

Usikilizaji wa Mashauri Mahakamani

18. Mheshimiwa spika, mwaka 2016, Mahakama yaTanzania ilianza na jumla ya mashauri 59,477 na kusajilimashauri mapya 276,147. Mashauri yaliyoamuliwa katikakipindi hicho yalikuwa 278,226, sawa na asilimia 83 ya wastani

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

wa uwezo wa kumaliza mashauri yote yaliyokuwepo.Mafanikio hayo yalitokana na Mahakama kuendelea kubunina kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo kufanya kazi kwamalengo na kupima utendaji kazi wa majaji na mahakimu.Pia, Mahakama ya Tanzania imeendelea kusisitiza matumiziya njia mbadala za utatuzi wa migogoro na kuimarishaushiriki wa wadau katika kubuni na kutekeleza mikakati yakuharakisha usikilizaji wa mashauri. Maelezo ya ufafanuzikuhusu usikilizaji wa mashauri ni kama yalivyo kwenyekiambatanisho Na: 1.

Kesi za Uchaguzi Mkuu wa 201519. Mheshimiwa Spika, kufuatia matokeo ya UchaguziMkuu wa mwaka 2015, yalifunguliwa jumla ya mashauri 53yaliyohusu nafasi ya Ubunge na mashauri 196 ya nafasi zaUdiwani. Hadi kufikia mwezi Machi, 2017 mashauri 52 yaUbunge yaliamuliwa, hivyo kubaki na shauri moja (1) nakwamba hivi sasa kuna rufaa mbili katika Mahakama yaRufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu. Aidha, mashauriyote ya udiwani yalisikilizwa na kuamuliwa katika kipindikilichowekwa kwa mujibu wa Sheria, yaani, mwaka 1 kwamashauri ya Ubunge na miezi sita kwa mashauri ya Udiwani.Haya ni mafanikio makubwa na ya kihistoria kuwahi kufikiwakwa mashauri ya uchaguzi kusikilizwa na kutolewa uamuzindani ya muda uliowekwa kisheria. Ofisi ya Mwanasheria Mkuuwa Serikali i l itoa mchango mkubwa kwa kusimamiauendeshaji wa mashauri hayo mahakamani ambapo katikamashauri yote, isipokuwa shauri moja, Serikali ilipata ushindi.Aidha, katika kuhakikisha kuwa tunaimarisha uwezo waSerikali kushughulika kesi za uchaguzi, Mahakama ya Tanzania,kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo(UNDP), ilitengeneza vitabu vitatu, ambavyo ni kijitabukinachoelezea Utaratibu na Mienendo Iliyotumika KatikaKuendesha Kesi za Uchaguzi; Ripoti Kuhusu NamnaMahakama Zilivyoshughulikia Kesi za Uchaguzi na MafunzoYatokanayo na Mkusanyiko wa Sheria na Kanuni za Uchaguzi.Vitabu hivi vilikabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania na kwako wewe, MheshimiwaSpika, tarehe 2 Februari, 2017 wakati wa maadhimisho yaSiku ya Sheria.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

Miundombinu ya Mahakama

20. Mheshimiwa spika, Mahakama ya Tanzania imeendeleana utekelezaji wa mkakati wa kuboresha huduma zaMahakama ikiwa ni pamoja na kufanya ujenzi na ukarabatiwa mahakama mbalimbali nchini. Hadi kufikia mwezi Machi,2017, Mahakama ya Tanzania ilikamilisha ukarabati wamajengo ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam na Tanga nakuendelea na ukarabati wa Mahakama Kuu, Kanda yaMbeya, unaotarajiwa kukamilika hivi karibuni. Aidha,Mahakama ya Tanzania imekamilisha ujenzi wa jengo laMahakama ya Hakimu Mkazi Pwani na Mahakama ya WilayaKibaha; na inaendelea na ujenzi wa Mahakama za Wilayaza Bagamoyo, Mkuranga, Kigamboni, Kinyerezi naMahakama ya Mwanzo Kawe ambazo zipo katika hatuambalimbali za ujenzi.

21 Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamotoya miundombinu, Mahakama kwa kushirikiana na Chuo KikuuArdhi na Baraza la Taifa la Ujenzi ilifanya utafiti wa teknolojiaya gharama nafuu ya ujenzi wa majengo ambapo teknolojiaya Moladi imeonyesha unafuu wa gharama, kupunguzamuda unaotumika kwenye ujenzi na ubora wa majengo. Kwakutumia teknolojia hii, Serikali imeweza kuokoa takribanasilimia 50 ya gharama za ujenzi ambazo zingetumika kwakutumia teknolojia ya kawaida. Chini ya utafiti huu,Mahakama sita za mfano zimejengwa ambazo ni Mahakamaya Hakimu Mkazi Pwani na Hakimu wa Wilaya Kibaha,Mahakama za Wilaya za Bagamoyo, Kigamboni, Mkurangana Kinyerezi, pamoja na Mahakama ya Mwanzo Kawe. Nidhahiri kuwa kutokana na uzoefu ulioupatikana katika mradihuu, Wizara itaweza kutumia teknolojia hiyo katika maeneomengine ya nchi kwa gharama nafuu.

22. Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine Mahakamaya Tanzania imeanza kazi ya kukamilisha ujenzi waMahakama ya Mkoa wa Manyara na Mahakama za Mwanzoza Iguguno (Mkalama), Wasso (Ngorongoro), Magoma(Korogwe), Bereko (Kondoa), Karatu Mjini (Karatu), Mvomero(Mvomero), Old Korogwe (Korogwe) na Kilwa Masoko

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

(Kilwa), ambazo ujenzi wake ulisimama kwa muda mrefukutokana na ukosefu wa fedha. Aidha, Mahakama yaTanzania imeendelea kuimarisha shughuli za usimamizi naukaguzi wa Mahakama kwa kununua na kusambaza jumlaya nakala 650 za vitabu vya mwongozo wa ukaguzi katikaMahakama mbalimbali nchini.Uandishi wa Sheria

23. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu iliendelea kuchukuahatua mbalimbali za kuhakikisha kuwa sheria za nchizinakuwa ni nyenzo ya kuharakisha maendeleo katika nyanjaza kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiutamaduni, kimazingira nakiteknolojia kupitia sera na mipango mbalimbali yamaendeleo. Hivyo, katika Mwaka wa Fedha wa 2016/17, Ofisiya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliratibu maandalizi yamiswada 12 ya sheria iliyowasilishwa na kujadiliwa Bungeni.Kutokana na miswada hiyo, sheria mbalimbali zilitungwaikiwa ni pamoja na Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa na Sheriaya Msaada wa Kisheria, ambazo ziko chini ya usimamizi waWizara yangu pamoja na Sheria ya Marekebisho ya SheriaMbalimbali, Na. 3 ya Mwaka 2016, Sheria ya Marekebisho yaSheria Mbalimbali, Na.4 ya mwaka 2016 na Sheria yaMarekebisho ya Sheria Mbalimbali, Na.1 ya Mwaka 2017.

Uendeshaji wa Mashtaka

24. Mheshimiwa Spika, Mkurugenzi wa Mashtaka aliendeleakuratibu shughuli za upelelezi wa makosa ya jinai, kufunguana kuendesha mashauri mahakamani. Katika kipindi chaJulai, 2016 hadi Machi, 2017, kulikuwa na jumla ya mashauriya jinai 31,723 yaliyoendeshwa katika mahakama mbalimbalinchini. Kati ya hayo, mashauri 14,732, sawa na asilimia 46,yalitolewa uamuzi na mahakama na mengine 16,991yanaendelea kusikilizwa. Aidha, kulikuwa na mashaurimatano yanayohusu urejeshaji wa mali zilizotokana na uhalifuyaliyokamilika kusikilizwa na fedha taslimu Shilingi 439,628,000kurejeshwa Serikalini ikiwa ni pamoja na nyumba 8, magari25, pikipiki 10, boti nane (8) na viwanja vinne (4). Aidha, jumlaya shilingi 1,110,893,995 zililipwa kama faini kutokana namashauri hayo.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

25. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2016 hadiMachi, 2017 kulikuwa na mashauri 463 ya ujangili. Kati ya hayo,mashauri 158 yalihitimishwa kwa washtakiwa kutiwa hatianina kupewa adhabu za vifungo na kulipa faini ya Shilingimilioni 811 taslimu. Aidha, kulikuwa na mashauri 9,813 yadawa za kulevya yakiwemo mashauri 161 yanayohusukiwango kikubwa cha dawa za kulevya ambapo mashauritisa kati ya hayo yalihitimishwa. Katika mashauriyaliyohitimishwa washtakiwa 13 walihukumiwa vifungo vyakati ya miaka 20 na maisha jela. Aidha, kilo 279 za dawaaina ya cocaine na heroine; na kilo 21 za mirungi ziliteketezwakwa amri ya mahakama. Pia, Mkurugenzi wa Mashtakaalipokea jumla ya majalada 510 ya tuhuma za rushwa kutokaTAKUKURU yakiwemo majalada mapya 306 na 204yaliyorejeshwa tena baada ya uchunguzi zaidi. Kati ya hayo,majalada 201 yaliandaliwa hati za mashtaka, majalada 136yalirejeshwa TAKUKURU kwa hatua zaidi za uchunguzi;majalada 168 yanaendelea kufanyiwa uchambuzi wa kisheriana mengine matano yalifungwa.

Uendeshaji wa Mashauri ya Madai, Katiba na Haki zaBinadamu

26. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuuwa Serikali iliendesha jumla ya mashauri 984 ya madaiyaliyoihusisha Serikali katika Mahakama Kuu naMahakama ya Rufani, yakiwemo mashauri 883 ya zamanina mashauri 101 mapya. Kati ya hayo, mashauri 11 yalitolewauamuzi na mashauri mengine 973 yanaendelea kusikilizwa.Serikali ilishinda katika mashauri tisa na kushindwa katikamashauri mawili. Kutokana na mafanikio hayo, Serikali iliwezakuokoa takriban shilingi Bilioni 23.75 sawa na asilimia 99.87ya fedha zinazodaiwa katika mashauri yaliyoisha. Vilevile,kulikuwa na maombi 48 mapya na 277 ya zamani na hivyokufanya maombi yote kuwa 325. Kati ya hayo, maombi 12yamehitimishwa na maombi 313 yanaendelea kusikilizwa.Rufani za madai zilizokuwepo ni 59 ikiwemo rufani 1 mpya,na zote zinaendelea kusikilizwa.

27. Mheshimiwa Spika, kulikuwa na jumla ya mashauri

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

mapya 32 ya Kikatiba yalifunguliwa kwenye Mahakama Kuuya Tanzania na kufanya jumla ya mashauri yaliyokuwepokuwa 164 yakiwemo mashauri 132 ya zamani ambapomashauri 19 yalihitimishwa na kubaki mashauri 145. KatikaMahakama ya Rufani kulikuwa na rufaa 7 ambazo badozinaendelea. Aidha, katika Mahakama ya Afrika ya Haki zaBinadamu na Watu (African Court on Human and PeoplesRights) kulifunguliwa jumla ya mashauri 104, kati ya hayomashauri 40 ni mapya na 64 ni ya zamani na yanaendeleakusikilizwa. Hali kadhalika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuuiliendesha jumla ya mashauri 6 katika Mahakama ya Haki yaAfrika Mashariki (East African Court of Justice). Kati ya hayo,Shauri moja lilimalizika na mengine mashauri 5 badoyanaendelea kusikilizwa.

Uhakiki wa Mikataba na Usimamizi wa Sheria zaKimataifa

28. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali, iliendelea kutoa ushauri wa kisheria kwenye Mikatabana Makubaliano mbalimbali ambapo katika kipindi cha Julai2016 hadi Machi 2017 ilifanya upekuzi na uhakiki wa jumla yamikataba 1,473 yenye thamani ya shilingi trilioni 12.6. Kazi hiiilihusisha mikataba ya ununuzi, ukarabati wa majengo, ujenziwa barabara na hati za makubaliano (MOU) kutoka Wizara,Idara na Taasisi za Serikali na mamlaka za Serikali za Mitaa.Vilevile, katika ngazi ya kikanda na kimataifa, Ofisi hii ilishirikikatika mikutano 86 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiyaya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika na Umoja waMataifa iliyojadili masuala ya sheria na sera za sektambalimbali.

Haki za Binadamu na Msaada wa Kisheria

Usimamizi na Hifadhi ya Haki za Binadamu

29. Mheshimiwa Spika, Wizara iliendelea kuimarisha nakusimamia utekelezaji wa haki za binadamu kamazilivyoanishwa na kuhifadhiwa katika Katiba na Sheria za nchi.Katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2016/17, Wizara iliandaa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

Taarifa ya Nchi kuhusu utekelezaji wa haki za binadamuiliyowasilishwa kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umojawa Mataifa, chini ya Mfumo wa Umoja wa Mataifa waMapitio kwa Kipindi Maalum (The Universal Periodic ReviewMechanism).Taarifa hiyo ilijadiliwa kwenye vikao vya 25 na33 vya Baraza la Haki za Binadamu vilivyofanyika Geneva,Uswisi kati ya Mei na Oktoba 2016. Kupitia Taarifa hiyo, Serikaliilipata fursa ya kufafanua mbele ya Jumuiya ya Kimataifakuhusu hali ya utekelezaji wa haki za binadamu nchini nakutoa msimamo wa nchi kuhusiana na mapendekezombalimbali yaliyotolewa na Baraza la Haki za Binadamuwakati wa kujadiliwa kwa Taarifa ya nchi yetu.

30. Mheshimiwa Spika, Tume ya Haki za Binadamu naUtawala Bora ilifuatilia na kutoa ushauri kwa Serikali na taasisizake kuhusu utekelezaji wa haki za binadamu na misingi yautawala bora nchini. Hii ni pamoja na kufanya ufuatiliaji wahaki za binadamu kwa watu walio katika makundi yenyemahitaji maalum; haki za mahabusu na wafungwa; kufanyauchunguzi wa tuhuma za uvunjwaji wa haki za binadamuna ukiukwaji wa misingi ya utawala bora; na kutoa elimu yahaki za binadamu na utawala bora kwa jamii. Katika kipindihicho Tume ilitembelea jumla ya magereza 41 katika mikoa15 ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Dar es salaam, Tanga,Mtwara, Lindi, Pwani, Manyara, Mara, Kigoma, Mwanza,Iringa, Singida na Dodoma. Pia, Tume ilikagua vituo vya polisi59, mahabusu za watoto 5 na Shule ya Maadilisho ili kijiridhishana utekelezaji wa haki za binadamu.

31. Mheshimiwa Spika, Tume ilipokea na kufanya uchunguziwa malalamiko 7,101 yanayahusu ukiukwaji wa haki zabinadamu na kuhitimisha uchunguzi katika malalamiko 1,443ambapo malalamiko mengine 5,658 yanaendeleakuchunguzwa. Baadhi ya malalamiko yalihusukubambikiziwa kesi; ucheleweshaji wa upelelezi, uendeshajiwa mashauri mahakamani, utoaji wa nakala za hukumu nautekelezaji wa amri za mahakama. Pia, kulikuwepomalalamiko ya migogoro ya ardhi, rushwa katika vyombovya utoaji haki na katika masuala ya mirathi. Aidha, Tumeiliendelea na utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Haki

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

za Binadamu (NHRAP) kwa kutoa mafunzo kwa maafisa waSerikali kutoka katika mikoa mbalimbali, asasi za kiraia,watumishi wa Mahakama pamoja na watumishi wa Tume,kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kusimamia na kukuzahaki za binadamu katika maeneo yao ya kazi.

Huduma ya Msaada wa sharia

32. Mheshimiwa Spika, Kwa kutambua umuhimu wamsaada wa kisheria katika kuimarisha upatikanaji haki nchinihususan kwa watu wasio na uwezo wa kumudu gharamaza uwakili, Wizara ilichukua hatua ya kuzitambua na kuzisajiliasasi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na utoaji wa msaadawa kisheria. Katika kipindi hicho, Wizara ilifanya utambuziwa zaidi ya asasi 290 zinazotoa msaada wa kisheria nchinina kuwasimamia wasaidizi wa kisheria (paralegals) zaidi ya5,000. Pia, ilichukua hatua za kuweka mwongozo wa kisheriaambapo Bunge lako Tukufu lilitunga Sheria ya Msaada waKisheria na hivyo kuweka mfumo rasmi wa kisheria wakusimamia upatikanaji na utoaji wa msaada wa kisheria kwawananchi wasio na uwezo wa kugharamia huduma zakisheria

Utafiti wa Kisheria

33. Mheshimiwa Spika, Wizara inatambua nafasi ya utafitikatika maendeleo ya sheria ili kuwa na mfumo wenye kuakisimahitaji halisi ya nchi kwa maendeleo na ustawi wa watu.Hivyo, kwa kutambua hilo, Tume ya Kurekebisha SheriaTanzania imekamilisha utafiti wa Mfumo wa sheria zinazohusuhifadhi ya taarifa binafsi (review of legal framework onpersonal data protection in Tanzania); Mfumo wa sheriakuhusu haki za walaji na watumiaji wa bidhaa (review oflegal framework on consumers’ protection); na Sheriazinazohusu masuala ya usajili wa matukio muhimu yabinadamu (review of the legal framework on civil registrationand vital statistics). Maelezo ya kina kuhusu hali ya utafiti wakisheria kwa mwaka wa fedha 2016/17 yanapatikana katikakiambatisho Na. 2(a) & 2(b).

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

Urejeshwaji wa wahalifu na ushirikiano na mataifa kwenyemakosa ya jinai

34. Mheshimiwa Spika, Tanzania imeendelea kutekelezawajibu wake kimataifa wa kushirikiana katika kupambanana uhalifu wa kimataifa kwa kurejesha watuhumiwa wauhalifu katika nchi walikofanya makosa. Katika kutekelezawajibu huu, Tanzania ilipokea maombi ya kuwarejeshawatuhumiwa wanne katika nchi wanakotuhumiwa kutendauhalifu, maombi 3 yanaendelea kufanyiwa kazi na maombimengine 2 yalikataliwa kwa kutokidhi matakwa ya kisheria.Pia, kwa mujibu wa Sheria ya Ushirikiano katika Masuala yaJinai (Mutual Assistance in Criminal Matters Act) nchi yetuilipokea jumla maombi 12 ya kukusanya ushahidi na vielelezo.Maombi 4 yalishughulikiwa na mengine 8 yanaendeleakufanyiwa uchambuzi. Aidha, Tanzania ilipeleka nje ya nchimaombi 2 ya kukusanya ushahidi na vielelezo ambayoyanaendelea kushughulikiwa husika.

Usajili, Ufilisi na Udhamini

Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu

35. Mheshimiwa Spika, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA), kwa kipindi cha Julai 2016 mpaka Machi 2017 umesajilimatukio muhimu kama ifuatavyo:-

(i) Kusajili na kutoa vyeti kwa watoto 869,182 waumri wa chini ya miaka mitano katika mikoasaba ya Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe,Mwanza, Geita na Shinyanga;

(ii) Usajili wa watoto walio shuleni 28,554 katikashule za msingi zilizopo kwenye halmashauriza Manispaa ya Ilala, Temeke, Kinondoni naIringa,

(iii) Kampeni ya usajili katika wilaya za Nzega naTunduru ambapo jumla ya watu 23,160walisajiliwa na kupewa vyeti;

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

(iv) Kufanya usajili wa kawaida wa vizazi348,544; na

(v) Matukio ya vifo 50,213; ndoa 21,057 natalaka 85.

Aidha, jumla ya leseni mpya 2,877 za kufungishia ndoazilitolewa; na leseni 1,618 kuhuishwa. Pia, RITA umeendeleakutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya usajili wa matukiomuhimu ya binadamu kwa wananchi.

Miunganisho ya Wadhamini

36. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia RITA imesajilijumla ya miunganisho 164 ya wadhamini wa vyama vya siasa,Makanisa, Misikiti na Mali za vikundi vya kijamii na kuendeleakusimamia mali zisizokuwa na wenyewe pamoja na masualaya mirathi kulingana na amri za mahakama. Aidha, mapitioyamefanywa katika Bodi za Wadhamini za taasisi zilizosajiliwaili kufahamu uhai wake na jumla ya taasisi 181 zilifutiwa usajiliwake. Pia jumla ya wosia 50 zimeandikwa na kuhifadhiwana huduma ya ushauri wa masuala ya wosia na mirathiimetolewa kwa wananchi kupitia kampeni maalumu.Orodha kamili ya bodi za wadhamini zilizofutwa inapatikanakwenye kiambatisho Na.3.

Taasisi za Mafunzo, Mipango na Miradi ya Maendeleo

Chuo cha Uongozi wa Mahakama- Lushoto

37. Mheshimiwa Spika, Chuo cha Uongozi waMahakama – Lushoto katika kutekeleza jukumu la kutoa elimuendelevu kwa watumishi wa mahakama na sekta ya sheria,kimeendelea kutoa mafunzo ya Astashahada na Stashahadakwa watumishi wa mahakama na jamii nzima kwa ujumla.Katika mwaka wa fedha wa 2016/17 Chuo kwa kushirikianana wadau wa maendeleo (UN Women) na Chama cha MajajiWanawake Tanzania (TAWJA) kiliandaa kitabu cha kuratibu,kuendesha na kufundishia wakufunzi wa masuala ya Hakiza Binaadamu na Mapambano dhidi ya Ukatili kwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

Wanawake na Watoto na hadi sasa kitabu hicho kimetumikakuendesha mafunzo kwa majaji, wasajili, mahakimu, askaripolisi, askari magereza pamoja na wahadhiri wa Chuo hicho.

38. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2016/17, Chuo kiliendesha mafunzo kwa watumishi wa mahakamazaidi ya 400 ikiwemo mafunzo maalumu kwa majaji 24waliojengewa uwezo na weledi wa namna ya kuendeshamashauri ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi. Vilevile,kiliandaa na kuendesha mafunzo ya namna ya kufanyaupelelezi na kuendesha ya namna ya kushughulikia mashauriya ujangili kwa mahakimu 30, mawakili wa serikali 10, askaripolisi watano na askari wa wanyama pori watano.

Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo

39. Mheshimiwa Spika, Taasisi imeendelea kuongeza uwezowake wa kudahili wanafunzi katika makundi (cohorts)mbalimbali. Katika mwaka wa Fedha wa 2016/17 ilidahilijumla ya wanafunzi 1,680 katika makundi matatu, kundi la22, 23 na 24. Kwa sasa, Taasisi ina jumla ya wanafunzi 2,234ambao wamesajiliwa katika makundi manne (4) yaliyo katikahatua tofauti za mafunzo. Taasisi hii imeendelea kujiimarishakatika masuala ya utafiti, kutoa huduma za udahili kwa njiaza kielektroniki na kuendesha huduma za maktaba ya kisasainayohifadhi zaidi ya nakala 7,000 za vitabu na machapishoya aina mbalimbali.

Maendeleo ya Rasilimali Watu

40. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamiawatumishi wake ili kuhakikisha wanatekeleza wajibu waokwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi waumma. Wizara imechukua hatua za kinidhamu dhidi yawatumishi waliokiuka maadili ya kazi kwa baadhi yaokupewa onyo, kushushwa vyeo, na wengine kufukuzwa kazi.Aidha, Wizara iliajiri, kuthibitisha kazini na kupandisha vyeokwa watumishi wote waliostahil i. Ninatoa wito kwawatumishi wote kuzingatia nidhamu ya kazi na kutekelezamajukumu yao kwa juhudi, maarifa na weledi ili kufanikisha

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

malengo ya wizara ya kuwatumikia wananchi kwa kutoahuduma zilizo bora.

Mipango na Miradi ya Maendeleo

41. Mheshimiwa Spika, ni dhamira ya Wizara yangukusogeza huduma za kisheria karibu na wananchi kwa kubunina kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kwakuimarisha ushirikiano na wadau wa maendeleo. Katikamwaka wa fedha wa 2016/17, Wizara inatekeleza miradi naprogramu mpya za maendeleo zikiwemo (a) Programu yaMaboresho ya Mahakama, (b) Mradi wa Kuimarisha Mfumowa Upatikanaji Haki Nchini (Strengthening Access to Justiceand Human Rights Protection in Tanzania) na (c) Programuya Ulinzi na Upatikanaji wa Haki ya Mtoto. Maboresho yamahakama ni programu ya miaka mitano inayotekelezwana Serikali ya Tanzania kwa fedha kutoka Banki ya Dunia kwamadhumuni ya kuimarisha mfumo wa mahakama,upatikanaji na ubora wa huduma za mahakama nchini.42. Mheshimiwa Spika, Programu inayohusu upatikanaji hakinchini ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa Umoja waMataifa unaojulikana kama UNDAP II. Wizara kwa kushirikianana UNDP imeandaa Andiko la Mradi na Mpango Kazi kwakipindi cha mwaka wa fedha 2017/18 ambapo kupitiaprogramu ya UNDAP II, Tanzania itaendelea kutekeleza Mradiwa Usajili wa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano (U5BRI);Mradi wa Kudhibiti Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kwaWanawake na Watoto; kukuza na hulinda haki za binadamu;pamoja na usimamizi wa mfumo wa utoaji haki nchini.

E. MAFANIKIO YALIYOPATIKANA

43. Mheshimiwa Spika, mafanikio yaliyopatikana kutokanana utekelezaji wa vipaumbele vya Wizara kwa mwaka2016/2017 ni pamoja na, kuanzishwa kwa Divisheni yaMahakama Kuu ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi;kukamilika kwa mfumo wa kisheria wa kusimamia na kuratibuutoaji wa msaada wa kisheria nchini; kutungwa kwa kwasheria ya upatikanaji wa taarifa; kuendelea kusimamiamashauri yote ya jinai na madai; Kumalizika kwa mashauri

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

yote ya uchaguzi wa Ubunge na Udiwani kwa wakati kamailivyo takwa la kisheria; kuweka mfumo wa usajili wa vizazikwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano katikamikoa saba ya Geita, Iringa Mbeya, Mwanza, Njombe,Shinyanga, na Songwe; Ujenzi na ukarabati wa majengo yamahakama katika ngazi mbalimbali; Kufanya utafiti nakuhuisha sheria mbalimbali ili kuakisi mahitaji halisi kwamaendeleo na ustawi wa watu; Kuongezeka kwa matumiziya TEHAMA katika utoaji wa huduma; na Ufuatiliaji wa haliza wafungwa na mahabusu magerezani uliopelekeakufanyika kwa maboresho ya huduma kwa wafungwa namahabusu.

44. Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine ni pamoja nakukamilisha uhakiki wa watumishi wote wa Wizara; kuimarikakwa usimamizi wa rasilimali watu na huduma kwa watumishiikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya kazi; Kuendeleakusimamia maadili ya watumishi; Kukamilika kwa rasimu yamkakati wa kitaifa wa usajili wa matukio muhimu yabinadamu na takwimu ambayo ipo katika hatua za maamuziSerikalini; kukamilika kwa mfumo wa TEHAMA unaowezeshaubadilishanaji wa taarifa kati ya RITA, Tume ya Uchaguzi naMamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; na kuendelea kutoamafunzo ya uanasheria kwa vitendo. Nipende kusisitiza kuwaWizara inatambua kwamba pamoja na mafanikioyaliyopatikana, yapo maeneo ambayo bado yanahitajikufanyiwa kazi ili kufikia malengo tuliyojiwekea. Hivyo, Wizarayangu itahakikisha kuwa kazi mbalimbali zi l izosaliazinakamilishwa sanjari na utekelezaji wa vipaumbele vyamwaka wa fedha 2017/18.

F. MTIRIRIKO WA MAPATO NA MADUHULI YASERIKALI

45. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2016/17 Wizara ya Katiba na Sheria iliidhinishiwa jumla ya Shilingi155,192,263,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradiya maendeleo. Kati ya fedha hizo, mishahara ni Shilingi67,328,697,000 na matumizi mengineyo (OC) ni Shilingi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

50,404,380,000. Fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo niShilingi 37,459,186,000 ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi13,919,000,000 ni fedha za ndani na Shilingi 23,540,186,000 nifedha za nje.

46. Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia mwezi Machi, 2017,Wizara ilipokea jumla ya Shilingi 80,503,233,855 sawa naasilimia 52 ya fedha zilizoidhinishwa. Kati ya hizo Shilingi45,545,485,311 ni mishahara ya watumishi na Shilingi31,434,746,899 ni kwa matumizi mengineyo, sawa na asilimia62. Fedha za maendeleo ni Shilingi 3,523,001,645 sawa naasilimia 9 ya bajeti ya miradi, ambapo fedha za ndani niShilingi 246,882,000 na fedha za nje ni Shilingi 3,276,119,645.Aidha, katika mwaka wa fedha 2016/2017, Wizara ilipangakukusanya jumla ya Shilingi 17,085,829,511 kama maduhuli yaSerikali kutoka vyanzo mbalimbali vinavyosimamiwa naWizara. Kufikia mwezi Machi, 2017 Wizara ilikusanya jumla yaShilingi 10,976,126,511 sawa na asilimia 64 ya makadirio yote.

G. CHANGAMOTO NA MIKAKATI ILIYOPO

47. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio yaliyopatikanakatika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17,kumekuwepo na changamoto mbalimbali ambazo nipamoja na upungufu wa rasilimali muhimu ikiwemo fedha,watu na vitendea kazi; uchakavu na uhaba wamiundombinu ya mahakama; mahitaji ya TEHAMA katikausimamizi wa mashauri; uelewa mdogo wa jamii kuhusu hakina wajibu wa raia; kuwepo kwa uhalifu unaokutumiateknolojia za kisasa na kuhusisha nchi zaidi ya moja.

48. Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na changamotohizo, Wizara yangu iliendelea kubuni na kutekeleza mikakatimbalimbali ya kukabiliana nazo katika kuhakikisha kuwa nchiinakuwa na mfumo imara kikatiba na kisheria ili kufanikishamipango ya maendeleo ya Taifa. Mikakati hiyo ni pamojana:

(a) Kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma, katika

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayohusianana upungufu wa watumishi, ikiwa ni pamojana upatikanaji wa vibali vya ajira, kujazanafasi zilizoachwa wazi na kushughulikiamaslahi ya watumishi;

(b) Kutafuta vyanzo vipya vya mapato ilikufanikisha utekelezaji wa miradi yamaendeleo ukiwemo mradi wa e-Justice naProgramu ya Maboresho ya Mfumo waMahakama;

(c) Kuendelea kubana matumizi na kuepukanana matumizi yasiyo ya lazima kufanyika kwawakati uliopo;

(d) Kuimarisha matumizi ya TEHAMA katikautoajihuduma za kisheria na ukusanyaji wamaduhuli yaSerikali;

(e) Kuwajengea uwezo watumishi wa sekta yasheria katika kukabiliana na aina mpya zahalifu.

(f ) Kuboresha huduma za mafunzo yauanasheria kwa vitendo;

(g) Kutumia teknolojia ya gharama nafuukatika ujenzi wa miundombinu yamahakama ili kukabiliana na ukubwa wagharama za utekelezaji wa miradi yamaendeleo; na

(h) Kuimarisha mfumo wa usimamizi, ufuatiliajina tathmini ya kazi za Wizara.

49. Mheshimiwa Spika, mafaniko katika utekelezaji wamajukumu ya Wizara ya Katiba na Sheria yamewezekanakutokana na ushirikiano thabiti wa wadau wa maendeleoambao wameendelea kutupatia katika utekelezaji wa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

programu na miradi mbalimbali ya maendeleo. Kwa namnaya pekee, nichukuwe fursa hii kuwashukuru Benki ya Dunia(WB); Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP);Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF);Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wanawake (UNWomen); Shirika la Msaada wa Maendeleo la Kimataifa laUingereza (DfID) na Taasisi ya Bloomberg Data for HealthInitiative. Napenda kuwahakikishia wote kwamba, Wizarayangu inathamini sana michango wao na tutaendelea kutoaushirikiano na kuhakikisha kwamba mipango na malengoya Serikali kuhusu sekta ya sheria yanafikiwa.

50. Mheshimiwa Spika, nitakuwa mchoyo wafadhila nisipotambua kazi kubwa iliyofanywa na viongoziwenzangu katika Wizara. Hivyo, kwa moyo wa dhati,napenda nimshukuru Prof. Sifuni E. Mchome, Katibu Mkuuna Bw. Amon A. Mpanju, Naibu Katibu Mkuu; viongozi wakuuna wataalam wa taasisi zote zilizo chini ya Wizara yangukwa ushirikiano mkubwa wanaonipa katika kutekelezamajukumu yangu ya kila siku. Vilevile, naishukuru sana familiayangu kwa kuendelea kunifariji na kunitia moyo wakati wotewa utekelezaji wa majukumu mazito yanayoambatana nawadhifa wa uwaziri wa Katiba na Sheria.

H. MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA 2017/18

51. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/18 Wizara yangu itaendelea na juhudi za kuimarisha utawalawa sheria na misingi ya haki za binadamu kwa kuhakikishakuwa wananchi wanapata huduma bora na za uhakika.Katika kufanikisha azma hiyo, Wizara imeainisha maeneomahususi ya kipaumbele kwa mwaka wa fedha ujao, kamaifuatavyo:-

(a) Wizara ya Katiba na Sheria

i. Kukamilisha uhamishaji wa Makao Makuuya Wizara kutoka Dar es Salaam kwendaDodoma;

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

ii. Kuratibu masuala ya kisera katika Wizara nataasisi zake;

iii. Kuratibu na kusimamia utoaji wa hudumaya msaada wa kisheria nchini;

iv. Kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa masualaya Katiba na sheria;

v. Kusimamia utekelezaji wa haki za binadamukitaifa, kikanda na kimataifa; na

vi. Kuwajengea uwezo watumishi, kuendelezaubunifu, maarifa na weledi ili kuleta tija naufanisi.

(b) Mahakama ya Tanzania

i. Kuharakisha usikilizaji wa mashauri;

ii. Kuimarisha utawala bora, maadili nauwajibikaji;

iii. Kuboresha mazingira ya kufanyia kazikwa kuongeza upatikanaji wa vitendea kazimuhimu;

vii. Kujenga na kukarabati miundombinu katikangazi mbalimbali;

viii. Kuongeza matumizi ya TEHAMA ili kurahisishausikilizaji wa mashauri na shughuli za utawalaili kufikisha huduma kwa wananchi;

ix. Kuimarisha uwezo katika ukaguzi nausimamizi wa shughuli za kimahakama; na

x. Kuendelea kuimarisha uwezo wa rasilimaliwatu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

(c) Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

i. Kuimarisha mfumo wa uandishi naurekebu wa sheria;

ii. Kusimamia shughuli za uendeshaji wamashauri ya jinai, madai, katiba na haki zabinadamu;

iii. Kuimarisha usimamizi wa masuala yamikataba; na

iv. Kuongeza matumizi ya TEHAMA katka utoajiwa huduma.

(d) Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

i. Kukuza na kutetea haki za binadamuhususan haki za makundi yenye mahitajimaalum;

ii. Kuongeza uelewa wa haki za binadamu,utawala bora, na wajibu wa raia;

iii. Kufanya uchunguzi wa malalamiko nakuyapatia ufumbuzi kwa njia ya upatanishi nausuluhishi;

iv. Kushirikiana na wadau mbalimbali nchini,kikanda na kimataifa kwenye masuala ya hakiza binadamu na utawala bora; na

v. Kujenga Uwezo wa watumishi.

(e) Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

i. Kukamilisha utafiti kuhusu mfumo wa sheriaza usimamizi wa haki jinai (Review of Legal

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

Framework on Criminal JusticeAdministration);

ii. Kufanya utafiti kuhusu mfumo wa sheria zaushahidi (Review of Legal Framework on Lawof Evidence); na

iii. Kufanya utafiti kuhusu mfumo wa sheriaza usuluhishi (Review of Legal Frameworkon Arbitration).

(f) Tume ya Utumishi wa Mahakama

i. Kuboresha utoaji wa huduma za Mahakamakwa kuongeza idadi ya watumishi waMahakama wenye weledi na sifa stahiki;

ii. Kuboresha mazingira ya kazi kwa kununuavitendea kazi pamoja na samani za ofisi;

iii. Kuimarisha nidhamu na maadili ya watumishiwa Mahakama kwa kufanya ukaguzi waKamati za Maadili za Mahakama; na

iv. Kuwajengea uwezo wajumbe pamoja nawatumishi wa Tume kwa kuwawezeshakuhudhuria mafunzo ya muda mfupi na mudamrefu.

(g) Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini

i. Kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Usajili waMatukio Muhimu ya Binadamu.

ii. Kufanya mapitio ya sheria zinazohusu ufilisi(review of legal framework on insolvency);

iii. Kuimarisha matumizi ya teknolojia katikakuboresha utoaji wa huduma; na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

iv. Kuimarisha ukusanyaji na usimamizi wamaduhuli ya Serikali.

(h) Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo

i. Kudahili na kutoa mafunzo kwa wanafunzi1,800 ili kuongeza idadi ya wataalam washeria nchini;

ii. Kutoa mafunzo ya muda mfupi kwamawakili na wadau wengine katikamambo mapya yanaoyojitokeza katikataaluma ya sheria (Continuing LegalEducation),

iii. Kuendesha programu za mafunzo kwawasaidizi wa sheria (paralegals); na

iv. Kuimarisha miundombinu ya taasisi.

(i) Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto

i. Kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa majajina mahakimu; na

ii. Kuimarisha na kuendelea kutoa mafunzoendelevu ya kimahakama pamoja namafunzo kazini kwa watumishi wamahakama na watumishi wote wa sekta yasheria kwa ujumla.

52. Mheshimiwa Spika, ili kufanikisha utekelezaji wavipaumbele hivi, Wizara yangu inaomba kuidhinishiwa jumla

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

ya Shilingi 166,479,908,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaidana miradi ya maendeleo. Mchanganuo wa makadirio yabajeti kwa mafungu saba ya Wizara na taasisi zake ni kamaifuatayo:

Na. Fungu la Matumizi Bajeti 2017/18Mishahara yaWatumishi - Sh. 76,441,279,000Matumizi Mengineyo - Sh. 66,801,799,000Miradi ya Maendeleo - Sh. 23,236,830,000

JUMLA Sh. 166,479,908,000

53. Mheshimiwa Spika, kiasi hicho cha fedha kinaombwakupitia mafungu ya bajeti yaliyo chini ya Wizara kamainavyoainishwa hapa chini.

Fungu 12 - Tume ya Utumishi wa Mahakama

-

1,102,911,000 Fungu 16 - Ofisi ya Mwanasheria

Mkuu wa Serikali

-

7,282,523,000 Fungu 35 - Divisheni ya Mashtaka - 14,914,063,000 Fungu 40 - Mfuko wa Mahakama - 125,117,029,000

Fungu 41 Wizara ya Katiba na Sheria

-

9,862,066,000 Fungu 55 - Tume ya Haki za

Binadamu na Utawala Bora

-

6,166,981,000 Fungu 59 - Tume ya Kurekebisha

Sheria Tanzania

-

2,034,335,000 JUMLA 166,479,908,000

 

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

(a) Muhtasari wa Matumizi

54. Mheshimiwa Spika, mchanganuo wa matumizi ya bajetikwa kila Fungu ni kama ifuatavyo:-

(ii) Fungu 35: Divisheni ya Mashtaka

(i) Fungu 12: Tume ya Utumishi wa Mahakama Matumizi ya Mishahara - Sh. 282,404,000

Matumizi Mengineyo - Sh. 820,507,000 Matumizi ya Maendeleo (Ndani) - Sh. 0 Matumizi ya Maendeleo (Nje) - Sh. 0 Jumla - Sh. 1,102,911,000

 

Matumizi ya Mishahara - Sh. 3,863,792,000 Matumizi Mengineyo - Sh. 3,418,731,000 Matumizi ya Maendeleo (Ndani) - Sh. 0 Matumizi ya Maendeleo (Nje - Sh. 0 Jumla - Sh. 7,282,523,000

(iii) Fungu 35: Divisheni ya Mashtaka

Matumizi ya Mishahara - Sh. 9,478,238,000 Matumizi Mengineyo - Sh. 5,435,825,000

Matumizi ya Maendeleo (Ndani)

- 0

Matumizi ya Maendeleo (Nje

- 0

Jumla - 14,914,063,000

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

(iv) Fungu 40: Mfuko wa Mahakama Matumizi ya Mishahara - Sh. 54,524,408,000 Matumizi Mengineyo - Sh. 52,434,610,000 Matumizi ya Maendeleo (Ndani)

-

Sh. 17,000,000,000 Matumizi ya Maendeleo (Nje - Sh. 1,158,011,000 Jumla - Sh. 125,117,029,000

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

(b) Makusanyo ya Maduhuli ya Serikali

55. Mheshimwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2017/2018 Wizara yangu inatarajia kukusanya kiasi chaShilingi 24,087,507,200 ikiwa ni maduhuli ya Serikali kutokanana vyanzo mbalimbali vya mapato inavyovisimamia, kamainavyoainishwa kwenye jedwali hapa chini:-

56. Mheshimiwa Spika, mchanganuo wa maombi ya fedhaza bajeti ya kila Fungu umeainishwa kwenye vitabu vyaKASMA za mafungu husika ambavyo wajumbe wa Bunge lakoTukufu wamegawiwa.

57. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

(vii) Fungu 59: Tume ya Kurekebisha Sheria Matumizi ya Mishahara - Sh. 1,066,606,000 Matumizi Mengineyo - Sh. 967,729,000

Matumizi ya Maendeleo (Ndani) - Sh. 0 Matumizi ya Maendeleo (Nje - Sh. 0 Jumla - Sh. 2,034,335,000

Fungu 16 - Sh. 3,002,000 Fungu 35 - Sh. 13,002,000 Fungu 40 - Sh. 9,318,061,200 Fungu 41 - Sh. 14,753,292,000 Fungu 59 - Sh. 150,000 JUMLA Sh. 24,087,507,200

 

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

MWENYEKITI: Tunakushukuru Waziri. Namuita sasaMwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria, ambayo ndiyoimefanya kazi ya kuchambua utekelezaji wa bajeti ya sasana maombi ya mwaka ujao wa fedha. Namuona Mwenyekitimwenyewe Mheshimiwa Mchengerwa.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA – MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa hii ni mara yangu yakwanza kusoma taarifa hii ya Kamati ya Kudumu ya Bunge,kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheriakwa mwaka huu wa fedha 2016/2017, pamoja na maoni yaKamati kuhusu makadirio ya mapato na matumizi, niruhusukwanza nimshukuru sana Mwenyezi Mungu mwingi warehema kwa kunijaalia uhai, afya njema na kunipa fursa yakuwasilisha taarifa hii mbele ya Bunge lako Tukufu.

Pili, niendelee kuwapa pole wananchi wa Mkoa waPwani hususan Wilaya ya Rufiji, Mkuranga na Kibiti kwataharuki ya ujambazi na nina imani kubwa sana na Serikalikwamba matatizo haya yatakwisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mara nyingine tenanapenda kumpongeza aliyekuwa Mjumbe wa Kamati yanguhii ya Katiba na Sheria Profesa Palamagamba John AidanMwaluko Kabudi, ambaye ameteuliwa na kupewa dhamanaya kuongoza Wizara hii muhimu ya Katiba na Sheria. ProfesaKabudi ni jungu la sheria, Kamati inamtakia kila la kheri katikakutekeleza majukumu yake mapya.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni ya99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo Januari, 2016,naomba kuwasilisha taarifa sasa ya Kamati ya Kudumu yaBunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa bajeti yaWizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2016/2017pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizarahiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Muheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa kifungu cha6 (2) cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

Toleo Januari 2016, Kamati ya Katiba na Sheria ina jukumu lakusimamia Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria pamoja nataasisi zake sita zifuatazo:-

(i) Wizara ya Katiba na Sheria Fungu Na. 41;

(ii) Mwanasheria Mkuu wa Serikali Fungu Na. 16;

(iii) Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka Fungu Na. 35;

(iv) Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Fungu Na. 55;

(v) Tume ya Kurekebisha Sheria Fungu Na. 59; na

(vi) Tume ya Utumishi wa Mahakama Fungu Na. 12.

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa hii inatoa maelezokuhusu maeneo makubwa matano yafuatayo:-

(i) Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kwa mujibu waKanuni ya 98 Kanuni ndogo ya kwanza ya Kanuni za Kudumuza Bunge, Toleo Januari, 2016.

(ii) Utekelezaji wa mapendekezo na ushauri waKamati kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

(iii) Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti wa mwaka wafedha 2016/2017.

(iv) Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwamwaka wa fedha 2017/2018, pamoja na Taasisi zilizo chiniyake.

(v) Maoni na ushauri wa Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ukaguzi wa miradiiliyotengewa fedha kwa mwaka wa fedha 2016/2017; tarehe22 Machi, 2017, Kamati ilipata fursa ya kutembelea Ofisi zaHaki za Binadamu na Utawala Bora, Fungu Namba 55 zilizoko

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

Wete - Pemba na kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuliza Tume kwa upande wa Pemba. Mpaka kufikia Machi, 2017gharama za upangishaji na ukarabati wa jengo zilifikia shilingimilioni 40 ambazo zimekuwa zikitolewa kwa awamu,kuanzia mwaka wa fedha 2010 mpaka 2011. Baada yakufanya ziara hiyo, Kamati imeridhishwa na ukarabati na halihalisi ya mazingira ya ofisi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na Kamatikuridhishwa na hali halisi ya ukarabati na mazingira ya ofisi,kuna changamoto za kiutendaji kwa kuwa na watumishiwawili tu. Mmoja ni Afisa na mwingine ni Mlinzi ambao wapokatika ofisi hiyo toka ilipoanzishwa katika mwaka wa fedha2010/2011. Hivyo ofisi hii inaendelea kuwa na changamotonyingi za kiutendaji kutokana na upungufu wa watendaji.Changamoto hii kwa kiasi kikubwa imeathiri sana utekelezajiwa majukumu ya Tume kwa upande wa Pemba. Katikakutatua changamoto hiyo kiutendaji, Kamati imearifiwakwamba kutokana na ongezeko la fedha katika Bajeti yaTume katika mwaka wa fedha 2017/2018, watumishi wawiliwataongezwa katika ofisi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maoni ya jumlakuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo; Kamatihaijaridhishwa na kasi ya utoaji wa fedha zilizoidhinishwa kwaajili ya miradi ya maendeleo. Karibu miradi yote iliyotengewafedha imepokea sehemu tu ya fedha iliyoidhinishwa kwamwaka wa fedha 2016/2017.

Vilevile Kamati inasikitishwa sana na hatua ya Serikalikutotoa fedha za ndani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi yamaendeleo. Miradi mingi ya maedeleo imekuwa inategemeafedha za nje kwa kiasi kikubwa. Mfano, Wizara ya Katiba naSheria Fungu la 41 limepokea fedha za nje toka kwa ajili yamiradi Namba 6201 wa e-Justice kiasi cha shilingi bilioni mojana mradi namba 6517 UNICEF Support to MultisectoralProgram ilipokea shilingi 396,472,613 zote zikiwa ni fedha zanje. Hapakuwa na fedha ya ndani yoyote iliyotolewa kwaajili ya miradi hii yote. Hali hii pia imejitokeza kwenye Miradamingi katika taasisi zilizo chini ya Wizara hii.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

Mheshimiwa Mwenyekiti, i l i kukabiliana nachangamoto za ukosefu wa fedha za ndani za kutosha kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, upo umuhimukwa kila taasisi ya Serikali kubuni vyanzo vya mapatovitakavyosaidia kuongeza fedha za ndani ili kuepukautegemezi wa fedha za nje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni ya68 (2) Kanuni ya Kudumu ya Bunge iliyotolewa Januari, 2016,Kamati ilikutana Mjini Dodoma tarehe 31 Machi, 2017 mpakatarehe 1 Aprili, 2017 kwa ajili ya uchambuzi wa taarifa yautekelezaji wa mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha2016/2017, pamoja na uchambuzi wa makadirio ya mapatona matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wafedha 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika uchambuzi wautekelezaji mpango wa bajeti wa Wizara hii, Kamati ilizingatiaulinganisho wa kiasi cha fedha zilizoidhiniwa na Bunge lakoTukufu Mei mwaka 2016 na kiwango ambacho kimepokelewahadi kufikia Machi, 2017. Lengo la kufanya tathmini ya namnahii ni kufahamu mwelekeo wa mpango wa bajeti wamapato na matumizi ya Serikali katika mwaka wa fedha2016/2017 na kujua vipaumbele vya bajeti katika mwaka wafedha unaofuata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2016/2017 Wizara ya Katiba na Sheria kwa ujumla iliidhinishiwashilingi 191,450,901,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida namiradi ya maedeleo, kati ya fedha hizo shilingi 65,949,643,300,kwa ajili ya mishahara na shilingi 108,562,097,961, kwa ajili yamatumizi mengineyo. Hadi kufikia mwezi Disemba mwaka2016 Wizara ilipokea jumla ya shilingi 97,255,506,269, ikiwa niasilimia 51 zilizoidhinishwa katika Bunge lililopita kama jedwalinamba moja linaloonesha mlinganisho wa fedha iliyotengwana kupokelewa katika mwaka wa fedha 2016/2017.

Mhesmiwa Mwenyekiti, Kamati inatoa wito kwa ofisiya Hazina kutoa kiasi cha fedha kilichobaki ambachokiliidhinishwa na Bunge lako Tukufu kwa Wizara hii ya Katiba

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

na Sheria katika kipindi kilichobaki kwa mwaka wa fedhawa 2016/2017 ili Wizara iweze kumaliza kutekeleza majukumuyake kwa ufanisi kama ilivyopangwa.

Mchanganuo wa fedha zil izoidhinishwa nazilizopokelewa katika mwaka wa fedha 2016/2017 hadikufikia Machi, 2017 katika mafungu sita yaliyosimamiwa naWizara hii, Fungu Namba 41, Fungu Namba 16, Fungu Namba35, Fungu Namba 59, Fungu Namba 55 na Fungu Namba 12umeainishwa kwenye jedwali kama ilivyoorodheshwa hapochini jedwali namba mbili linaloonesha mlinganisho wa fedhailiyoidhinishwa na kupokelewa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 hadi kufikia mwezi Machi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mlinganishouliooneshwa katika jedwali namba mbili, inaonesha kwambaFungu Namba 35 ndilo lililotengewa fedha nyingi zaidiambayo ni shilingi 13,097, 619,000 kwa mwaka wa fedha2016/2017. Hata hivyo, hadi kufikia mwezi Machi, 2017 Funguhili limepokea kiasi cha shilingi 7,955,545,061. Ukiangalia kiasihicho cha fedha kilichotolewa ni pungufu ya asilimia 39 yafedha ambazo ziliidhinishwa na Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mlinganisho huo,Tume ya Utumishi wa Mahakama - Fungu Namba 12liliidhinishiwa fedha kidogo zaidi kuliko mafungu menginekwa kiasi cha shilingi 1,134,955,000, pamoja na kuidhinishiwafedha hizo kidogo hadi kufikia mwezi Machi, 2017 fungu hililimepokea shilingi 609,858,475 tu. Ukiangalia kiasi hiki chafedha kilichotolewa kinaashiria kwamba ni asilimia 53 tu yafedha ambayo imetolewa na pungufu ya asilimia 47 ambayoilitengwa na Bunge lako hili Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwenendo huu waupokeaji wa fedha kwa ujumla unadhihirisha kuwa, fedhainayotolewa ni kidogo sana ukilinganisha na kiasi cha fedhakilichoidhinishwa na Bunge lako Tukufu. Hivyo Taasisi hizizinashindwa kutekeleza majukumu yake kwa wakati naufanisi kutokana na ucheleweshwaji wa utoaji wa fedha kwaupande wa Hazina.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa uchambuziwa taarifa kuhusu ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka wafedha 2016/2017; kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Wizaraya Katiba na Sheria pamoja na Taasisi zake ilitarajiakukusanya kiasi cha shilingi 17,085,879,511, kama maduhuliya Serikali kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato, hadi kufikiaDisemba, 2016 Wizara ilikuwa imekusanya kiasi cha shilingi10,943,491,845 sawa na asil imia 64 ya makusanyoyaliyotarajiwa kama ilivyochanganuliwa kwenye jedwalinamba tatu. Makusanyo haya ni kutokana na adambalimbali za usajili wa matukio, ada za wanafunzi, uuzajiwa vitabu vya zabuni na huduma nyingine mbalimbalizilizotolewa na Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Katiba na SheriaFungu Namba 41, imeongoza katika ukusanyaji wa maduhulikwa kukusanya shilingi 5,599,313,845, ikifuatiwa na Idara yaMahakama Fungu Namba 40 il iyokusanya shil ingi5,344,178,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mafungu mengine yalikuwana matarajio ya kukusanya maduhuli lakini hayakuwa kamayalivyopangwa. Hii ni changamoto ambayo Wizara, taasisizote zenye vyanzo vya mapato zinazidi kuiangalia kwaumakini kwani matarajio siyo mapato, hivyo kuna umuhimuwa kubuni vyanzo vingine vya ukusanyaji wa maduhuli ilikuongeza upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wamajukumu ya Wizara hizi hasa kwa zile taasisi zilizokosamapato kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapitio ya utekelezaji waushauri wa Kamati ni kuwa wakati wa uwasilishwaji wamakadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba naSheria kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Kamati ilitoa ushaurina mapendekezo 16 kuhusiana na Bajeti ya Wizara ya Katibana Sheria pamoja na taasisi zake. Kamati imefurahishwa nautekelezaji wa maoni ya Kamati yaliyotolewa katika taarifaya uchambuzi wa bajeti kwa Wizara hii Mei, 2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo mahsusi ambalo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

Kamati imeridhika nalo ni ongezeko kidogo kwenye bajetina utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Haki za Binadamuna Utawala Bora, ambayo imetengewa shilingi 1,566,080,000,katika mwaka ujao wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya matumizimengineyo (OC) ikilinganishwa na mwaka wa fedha uliopitaambao Tume hii iliidhinishiwa shilingi 994,500,014, tu kwa ajiliya matumizi mengineyo ambayo ilikuwa ni ndogo nahaikulingana na uzito wa majukumu ya Tume kuhakikishaHaki ya Binadamu na Utawala Bora zinazingatiwa. Tofauti hiini ya ongezeko la asilimia 57 ya bajeti inayoombwakuidhinishwa kwa ajili ya Tume katika mwaka wa fedhaunaokuja. Hata hivyo, fedha iliyoidhinishwa haitosheleziikilinganishwa na majukumu yanayopaswa kutekelezwa naTume hii katika nchi yetu. Kamati inaishauri Serikali kuendeleakuongeza fedha za kutosha kwa ajili ya Tume ili kutekelezamajukumu yake kikamilifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la mpango wamakadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha2017/2018; kwa mwaka wa fedha 2017/2018, Wizara ya Katibana Sheria imejiwekea malengo saba ya utekelezaji ilikuongeza ufanisi na ubora katika utoaji huduma za kisheriana masuala ya Katiba yakiwemo:-

Kwanza, ni kuendelea na uhamasishaji wa shughuliza Serikali kutoka Dar es Salaam kwenda Makao Makuu yaNchi Dodoma.

Pili, ni kuimarisha mfumo wa Sheria na kuongezauwezo wa Wizara katika maeneo maalum ya sheria pamojana usimamizi wa utoaji haki.

Tatu, kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa masualaya Katiba na Sheria na jambo la nne ni kuimarisha misingi yahaki za binadamu na kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inakubaliana namalengo ya Wizara kwa ujumla kwani yanalenga katikakuboresha utekelezaji wa majukumu yake na kuleta ufanisizaidi katika suala zima la utoaji haki nchini.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu makadirio yamapato ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha2017/2018; kwa mwaka wa fedha 2017/2018, Wizara inatarajiakukusanya kiasi cha shilingi 24,087,507,200, ikiwa ni maduhuliya Serikali kama inavyoonekana katika jedwali namba nneambalo linazungumzia matarajio ya maduhuli kwa mwakawa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati imebaini kuwamakadirio ya mapato hayaendani na hali halisi yamakusanyo, hivyo Kamati inashauri kuwa ni vizuri kuwekamakadirio madogo yenye uhakika katika kukusanya kulikokuweka makadirio makubwa ya fedha ambayo hayanamatarajio makubwa katika kukusanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Haki za Binadamuna Utawa Bora - Fungu Namba 55, na Tume ya Utumishi waMahakama - Fungu Namba 12 hayana matarajio yoyote yakukusanya maduhuli kwa sababu ya kutokuwa na vyanzovya mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uchambuzi wamakadirio ya matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwamwaka wa fedha 2017/2018; katika mwaka wa fedha wa2017/2018, Wizara pamoja taasisi zake inaombakuidhinishiwa shilingi 159,331,822,000 kwa ajili ya matumizi yakawaida na miradi ya maendeleo ambayo ni upungufu waasilimi 4.4 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha2016/2017. Upungufu huu wa asilimia 4.4. unatokana naukomo wa bajeti ya fedha za maendeleo kupungua kwaasilimia 55 ikilinganishwa na fedha za miradi ya maendeleozilizoidhinishwa mwaka 2016/2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Katiba na Sheriapamoja na taasisi zake kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018inaomba fedha kama ilivyooneshwa katika mchanganuouliopo kwenye jedwali namba tano ambalo linaoneshauchambuzi wa makadirio ya matumizi ya Wizara ya Katibana Sheria kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ambapo Wizaraya Katiba na Sheria - Fungu Namba 41 inaomba shilingi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

9,862,066,000; Fungu Namba 16 - Ofisi ya Mwanasheria Mkuuwa Serikali inaomba shilingi 7,282,523,000 na Fungu Namba35 - Divisheni ya Mashtaka inaomba shilingi 14,914,063,000 naFungu Namba 12 - Tume ya Utumishi wa Mahakama inaombashilingi 1,102,911,000; Fungu Namba 59 - Tume ya KurekebishaSheria inaomba shilingi 2,052,757,000 na Fungu Namba 55 -Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inaomba shilingi6,166,981,000. Jumla ya fedha zinazoombwa ni shilingi41,381,301,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Divisheni ya Mashtaka -Fungu Namba 35 ina makadirio ya matumizi ya juu zaidiikilinganishwa na mafungu mengine. Bajeti inayoombwakwa ajili ya Fungu hili ni sawa na asilimia 37 ya bajeti ya Wizarakwa mwaka wa fedha 2017/2018. Tume ya Utumishi waMahakama Fungu Namba 12 ina makadirio ya matumizimadogo zaidi ikilinganishwa na mafungu mengine ikiwa nisawa na asilimia 3.2 ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wafedha 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maoni na ushauri waKamati; kwa kuzingatia taarifa zilizowasilishwa mbele yaKamati pamoja na majukumu ya Wizara ya Katiba na Sheriana taasisi zilizo chini yake, Kamati inatoa maoni na ushauriufuatao ili kuboresha utendaji wa kazi na ufanisi katikakutekeleza majukumu ya Wizara hii:-

(i) Kamati inaipongeza Serikali kwa kuongeza bajetiya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa fedhaza matumizi mengineyo (OC) kutoka shilingi 994,000,514,000katika mwaka wa fedha 2016/2017 hadi kufikia shilingi1,566,080,000 katika mwaka wa fedha ujao 2017/2018.Ongezeko hili ni sawa na asilimia 57.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, Kamati inatoarai kwa Wizara na taasisi zake kufanya rejea ya maagizoyaliyotolewa na Kamati katika taarifa ya mwaka wafedha 2016/2017 na kuendelea kuyatekeleza katika kipindicha robo ya mwisho wa mwaka huu unaoisha Juni, mwaka2017.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

(ii) Ofisi ya Hazina kutoa fedha zilizoidhinishwa naBunge kwa Wizara husika kwa wakati ili kuiwezesha Wizarakutekeleza majukumu yake kama yalivyopangwa katika kilamwaka wa fedha.

(iii) Wizara kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria kufanyamapitio ya maboresho yote ya msingi ya sheria zotezinazohitaji maboresho kutazama uwezekano wa kuhuishamchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya kwa wakatimuafaka. (Makofi)

(iv) Wizara pamoja na taasisi zake kukamilisha kwaharaka utekelezaji wa mpango wa kuhamia Dodomamapema iwezekanavyo ili kutekeleza uamuzi wa Serikali wakuhamishia Makao Makuu ya nchi Dodoma.

(v) Kamati inatoa wito kwa Serikali kuleta Bungenisheria mahsusi ambayo itahalalisha utekelezaji wa maamuziya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuufanya Mji wa Dodomakuwa Makao Makuu ya nchi.

(vi) Tume ya Kurekebisha Sheria kuendelea kufanyamapitio ya sheria mbalimbali kwa lengo la kuzirekebisha nakuziboresha il i kuendana na mabadiliko mbalimbalitulitonayo sasa. Kamati inatoa rai kwa Tume kushirikiana naWizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili kufanya mapitio yaSheria ya Elimu kwa mwaka 1978 na kutazama uwezekanowa kuirekebisha ili kufanya elimu ya sekondari kuwa lazimana kuwawezesha vijana wanaomaliza elimu ya msingikuendelea na elimu ya sekondari. Bila kusahau Tume piakuweza kupitia Sheria ya Usalama Barabarani ambayotunaona hatuelewi kuna kigugumizi gani, kwa nini sheria hiihailetwi Bungeni kwa ajili ya marekebisho. Sheria hii imepitwana wakati na ni sheria ya muda mrefu.

(vii) Serikali kuongeza ukomo wa bajeti kwa Wizarana taasisi zake katika mwaka ujao wa fedha ili ziweze kuanzautaratibu wa kujenga majengo ya ofisi zao katika Mji waKiserikali utakaojengwa Dodoma.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

(viii) Wizara kuendelea kusimamia kwa ufanisi masualayote ya haki za binadamu na upatikanaji wa haki nchini nakuhakikisha kwamba inachukua hatua za kutosha kupunguzawingi wa kesi mahakamani na wingi wa mahabusu katikarumande, jambo ambalo linavunja haki mbalimbali zawatuhumiwa ambao wanakaa rumande kwa muda mrefubila kesi zao zinazowahusu kusikilizwa na kumalizika kwawakati. (Makofi)

(ix) Serikali kuzingatia kwa umakini matakwa ya Ibaraya 13(6)(a) mpaka (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo inatoa haki za msingiza kuhusiana na watuhumiwa wa makosa ya jinai ikijumuishahaki ya kupata dhamana, kusikilizwa kesi zao na kukata rufaakwa wakati muafaka. Jambo hili ni la msingi sana kwa kuwaIbara ya 13 iwapo ikikiukwa tunamaanisha kwamba zilepresumptions zilizotolewa katika sheria zitakuwa zinakiukwana watuhumiwa sasa watakuwa wametiwa hatiani kablaya kusikilizwa kesi zao kama Ibara ya 13 inavyozungumza.(Makofi)

(x) Wizara na Mhimili wa Mahakama kwa ujumlakuzingatia matakwa ya kisheria kuhusu uendeshaji wa kesiza jinai na hususani taratibu za utoaji wa dhamana kwawatuhumiwa kama zilivyowekwa katika kifungu cha 148 chaSheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai iliyopitiwa kwa mwaka2002 katika Criminal Procedure Act. Kamati inasisitizakwamba dhamana ni haki ya mtuhumiwa na ni suala laKikatiba hivyo taasisi za utoaji haki zinapaswa kuzingatiasuala hil i i l i kutenda haki kwa watuhumiwa. Piatunawakumbusha Mahakimu matumizi ya kifungu cha 222mpaka 225 cha kesi ambazo zimekaa muda mrefu na nijukumu lao Mahakimu kutenda haki kama ambavyonimezungumza hapo. (Makofi)

(xi) Serikali kuridhia na kutekeleza Mikatabambalimbali ya Kimataifa iliyoridhiwa na nchi yetu ili iwezekutekelezwa, kama vile mkataba wa Kimataifa wa mwaka1984 unaopinga matumizi yote ya kikatili dhidi ya wanadamu(Convention Against Torture) sheria hii ya mwaka 1984.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

(xii) Wakala wa Usajili na Ufilisi na Udhamini (RITA)kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya sheria,taratibu na kanuni za uadilifu na weledi katika usajili waMabaraza ya Wadhamini wa vyama vya siasa au makundimengine ya kijamii kwa kusimamia sheria, kanuni na taratibuzilizopo, hivyo kuepuka kuwa sehemu ya migogoro ya vyamahivyo. (Makofi)

(xiii) Wizara kuanzisha na kukamilisha mchakato waupatikanaji wa Kanuni za Sheria za Utoaji wa Msaada waKisheria (The Legal Aid Act) iliyopitishwa na Bunge lako hiliTukufu katika Mkutano wa Sita wa Bunge uliofanyika mweziFebruari mwaka 2017. Hapa ninaipongeza Kamati ya Katibana Sheria kwa ku-pioneer uundwaji wa sheria hii ambayoitakwenda kuwasaidia Wabunge wote ndani ya Bunge lakoTukufu katika maeneo yetu huko tunakotoka. (Makofi)

(xiv) Tume ya Utumishi wa Mahakama kusimamia kwaumakini mkubwa maslahi ya Mahakimu wote na hasaupandishwaji wa vyeo na nyongeza ya mishahara kwaMahakimu waliopo kwenye Mahakama za mwanzo. Kamatiinafahamu kwamba wapo Mahakimu wa Mahakama zaMwanzo ambao hawajapandishwa vyeo kwa zaidi ya miakakumi sasa. Ni vema pia Waziri wa Katiba na Sheriaakaangalia marekebisho ya Sheria ya Magistrate Court Act,Marekebisho Namba Moja ya mwaka 2013 ambayoinakinzana na Waraka Namba Moja wa mwaka 2010, warakawa Katibu Mkuu Utumishi ambao unazungumzia watumishiwa Mahakama hususan katika suala zima la upandishwajiwa vyeo, Mahakimu wana zaidi ya miaka 10hawajapandishwa vyeo, hususan Mahakimu wa Mahakamaza Mwanzo. (Makofi)

(xv) Kamati inatoa wito kwa watendaji waMahakama wote kufanya kazi kwa weledi na kuzingatiasheria, taratibu na mipaka ya kazi zao na kutoingiliamajukumu ya msingi ya Mahakama katika utoaji nausimamiaji wa haki. (Makofi)

(xvi) Wizara na Mhimili wa Mahakama, Fungu Namba

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

40 kuendelea kuboresha mfumo wa utoaji haki nchini nakuendesha kesi kwa kutumia njia ya mfumo wa kisasa wamawasiliano (E-Justice). Kamati inawapongeza wadau wotewa maendeleo kama Shirika la Maendeleo la Umoja waMataifa (UNDP) na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa(UNICEF) ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kufadhilimiradi mbalimbali ya maendeleo iliyo chini ya Wizara yaKatiba na Sheria ikiwemo mradi huu wa E–Justice.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho napendakumshukuru Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Spika naWenyeviti wote wa Bunge lako Tukufu kwa busara na umakiniwa namna ambavyo mnaendesha Bunge letu hili Tukufu. Kwanamna ya kipekee kabisa napenda kumshukuru sanaMheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe aliyekuwa Waziri waKatiba na Sheria ambaye kwa zaidi ya mwaka mmojaalifanya kazi kwa weledi na kutoa ushirikiano mkubwa kwaKamati wakati wa utekelezaji wa majukumu yake, hasakatika wakati wa uchambuzi wa Sheria ya Huduma ya Utoajiwa Msaada wa Kisheria wa mwaka 2016. Niipongeze piaKamati, kama nilivyosema, kwa ku-pioneer sheria hii ambayoinakwenda kuwasaidia Wabunge wetu wote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nitumie nafasi hiipia kumshukuru Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria,Mheshimiwa Profesa Palamagamba John Aidan MwalukoKabudi (Mbunge), Katibu Mkuu Profesa Sifuni Ernest Mchome,Naibu Katibu Mku Ndugu Amon Mpanju na Watendaji wotewa Wizara ya Katiba na Sheria kwa ushirikiano wao mkubwawalioutoa wakati Kamati ilipojadili makadirio ya mapatona matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wafedha 2017/2018. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee nawashukuruWajumbe wa Kamati kwa kazi nzuri waliyoifanya wakati wakujadili na kuchambua makadirio ya mapato na matumiziya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha2017/2018. Uzalendo, uchapakazi pamoja na ushirikianomkubwa walionipa umesaidia kufanikisha kukamilika kwataarifa hii kwa wakati, ningependa majina haya niyasome

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

lakini kwa kuwa Kanuni haziruhusu, naomba majina yao yoteyaingie katika Hansard.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia niseme Kamati hiindiyo Kamati bora kuliko Kamati zote za Bunge lako hiliTukufu, kwa kuwa Kamati hii imefanyia marekebisho sherianyingi na imevunja rekodi ya Bunge hili Tukufu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napendakuwashukuru kwa dhati watumishi wote wa Ofisi ya Bunge,chini ya uongozi makini kabisa wa Dkt. Thomas Kashililah,Katibu wa Bunge kwa kusaidia kuiwezesha Kamati kutekelezamajukumu yake ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee namshukuruMkurugenzi wa Idara ya Kamati za Bunge, Ndugu AthumaniHussein, Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Angelina Sanga naMakatibu wa Kamati Ndugu Stella Bwimbo na kijana wetundugu Dunford Mpelumbe kwa kazi nzuri kabisawanayoifanya pamoja na Msaidizi wa Kamati Ndugu RachelMasima, Makatibu Muhtasi wa Idara ya Kamati za Bunge,Ndugu Chiku Ramadhani, Ndugu Grace Wambura, NduguIrene Makongoro kwa kuratibu vema kazi za Kamati nakuhakikisha kuwa taarifa hii inakamilika kwa wakatiuliopangwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo sasanaomba Bunge lako Tukufu likubali kuidhinisha makadirio yamapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwamwaka wa fedha 2017/2018 kama yalivyowasilishwa na mtoahoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha naninaunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Mwenyekiti waKatiba na Sheria kwa wasilisho lako.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

TAARIFA YA KAMATI YA KATIBA NA SHERIA KUHUSUUTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA YA KATIBA NASHERIA KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017 PAMOJA NAMAONI YA KAMATI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA

MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

1.0 UTANGULIZI

Mheshimwa Spika, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungumwingi wa rehema kwa kunijalia uhai, afya njema na kunipafursa ya kuwasilisha Taarifa hii mbele ya Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Spika, kwa mara nyingine tena, napendakumpongeza aliyekuwa Mjumbe wa Kamati hii, Prof.Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb), ambayeameteuliwa na kupewa dhamana ya kuongoza Wizara hiimuhimu ya Katiba na Sheria. Kamati inamtakia kila la herikatika kutekeleza majukumu yake mapya.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99 (9) ya Kanuniza Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016, naombakuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katibana Sheria kuhusu Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Katibana Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 pamoja naMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwakawa Fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kifungu cha 6 (2) chaNyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo laJanuari 2016, Kamati ya Katiba na Sheria ina jukumu lakusimamia Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria pamoja naTaasisi zake sita (6) zifuatazo:

i. Wizara ya Katiba na Sheria (Fungu 41)ii. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Fungu 16)iii. Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (Fungu 35)iv. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

(Fungu 55)v. Tume ya Kurekebisha Sheria (Fungu 59)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

vi. Tume ya Utumishi wa Mahakama (Fungu 12)

Mheshimiwa Spika, Taarifa hii inatoa maelezo kuhusumaeneo makubwa matano yafuatayo:

(i) Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kwa mujibuwa Kanuni ya 98 (1) ya Kanuni za Kudumu zaBunge, Toleo la Januari, 2016;

(ii) Utekelezaji wa mapendekezo na ushauri waKamati kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017;

(iii) Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti kwa Mwakawa Fedha 2016/2017;

(iv) Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizarakwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja naTaasisi zilizo chini yake; na

(v) Maoni na Ushauri wa Kamati.

2.0 UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO ILIYOTENGEWAFEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017

Mheshimiwa Spika, tarehe 22 Machi, 2017 Kamati ilipata fursaya kutembelea Ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na UtawalaBora (Fungu 55) zilizoko Wete - Pemba na kupokea Taarifa yaUtekelezaji wa Shughuli za Tume kwa upande wa Pemba.

Mheshimiwa Spika, mpaka kufikia Machi, 2017 gharama zaupangishaji na ukarabati wa jengo hili zilifikia Shilingi MilioniArobaini (40,000,000.00) ambazo zimekua zikitolewa kwaawamu kuanzia Mwaka wa Fedha 2010/2011. Baada yakufanya ziara hiyo, Kamati imeridhishwa na ukarabati na halihalisi ya mazingira ya Ofisi hiyo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na Kamati kuridhishwa na halihalisi ya ukarabati na mazingira ya Ofisi hii, kuna changamotoya kiutendaji kwa kuwa na Watumishi Wawili (2) tu, Mmoja(1) ni Afisa na mwingine ni Mlinzi ambao wapo katika Ofisi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

hiyo toka ilipoanzishwa katika Mwaka wa Fedha 2010/2011.Hivyo Ofisi hii inaendelea kuwa na changamoto nyingi zakiutendaji kutokana na upungufu wa Watendaji.Changamoto hii kwa kiasi kikubwa imeathiri sana utekelezajiwa majukumu ya Tume kwa upande wa Pemba.

Mheshimiwa Spika, katika kutatua changamoto hiyo yakiutendaji, Kamati imearifiwa kwamba, kutokana naongezeko la fedha katika bajeti ya Tume katika Mwaka waFedha 2017/2018, Watumishi Wawili (2) wataongezwa katikaOfisi hiyo.

2.1 MAONI YA JUMLA KUHUSU UTEKELEZAJI WA MIRADI YAMAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017

Mheshimiwa Spika, Kamati haijaridhishwa na kasi ya utoajiwa fedha zinazoidhinishwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.Karibu miradi yote iliyotengewa fedha imepokea sehemu tuya fedha iliyoidhinishwa katika Mwaka wa Fedha 2016/2017.Vilevile Kamati inasikitishwa na hatua ya Serikali kutotoa fedhaza ndani kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.Miradi mingi ya maendeleo imekuwa inategemea fedha zanje kwa kiasi kikubwa. Mfano, Wizara ya Katiba na Sheria(Fungu 41) ilipokea fedha za nje tu kwa ajili ya Mradi namba6201 (E-Justice) kiasi cha Shilingi Bilioni Moja (1,000,000.000.00)na Mradi namba 6517 (Unicef Multi-Sectoral Support Program)ilipokea Shilingi Milioni Mia Tatu Tisini na Sita, Laki Nne Sabinina Mbili Elfu, Mia Sita Kumi na Tatu (396,472,613.00) zote zikiwani fedha za nje. Hapakuwa na fedha yoyote ya ndaniiliyotolewa kwa ajili ya Miradi hii yote. Hali hii pia imejitokezakwenye miradi mingine katika Taasisi zilizo chini ya Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na changamoto ya ukosefuwa fedha za ndani za kutosha kwa ajili ya kutekeleza Miradiya Maendeleo, uko umuhimu kwa kila Taasisi ya Serikali kubunivyanzo vya mapato vitakavyosaidia kuongeza fedha zandani ili kuepuka utegemezi wa fedha za nje.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

3.0 UCHAMBUZI WA TAARIFA YA WIZARA YA KATIBA NASHERIA KUHUSU UTEKELEZAJI WA MPANGO WA BAJETI NAUZINGATIAJI WA MAONI YA KAMATI KWA MWAKA WA FEDHA2016/2017

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 98 (2) ya Kanuniza Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016, Kamati ilikutanaMjini Dodoma Tarehe 31 Machi na 01 Aprili, 2017 kwa ajili yauchambuzi wa Taarifa za Utekelezaji wa Mpango wa Bajetikwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 pamoja na uchambuzi waMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba naSheria kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, katika uchambuzi wa Utekelezaji waMpango wa Bajeti ya Wizara hii, Kamati ilizingatia mlinganishowa kiasi cha fedha kilichoidhinishwa na Bunge Mwezi Mei2016 na kiwango ambacho kimepokelewa hadi kufikia Machi2017.Mheshimiwa Spika, lengo la kufanya tathmini ya namna hiini kufahamu mwelekeo wa Mpango na Bajeti ya Mapato naMatumizi ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017 nakujua vipaumbele vya kibajeti katika Mwaka wa Fedhaunaofuata.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2016/2017Wizara ya Katiba na Sheria kwa ujumla, ilidhiinishiwa ShilingiBilioni Mia Moja Tisini na Moja, Milioni Mia Nne Hamsini, LakiTisa na Moja (191,450,900,001.00) kwa ajili ya matumizi yakawaida na Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo ShilingiBilioni Sitini na Tano, Milioni Mia Tisa Arobaini na Tisa, Laki SitaArobaini na Tatu Elfu na Mia Tatu (65,949,643,300.00) ni kwaajili ya Mishahara na Shilingi Bilioni Mia Moja na Nane, MilioniMia Tano Sitini na Mbili, Tisini na Saba Elfu, Mia Tisa Sitini naMoja (108,562,097,961.00) ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo.Hadi kufikia Mwezi Disemba 2016, Wizara ilipokea jumla yaShilingi Bilioni Tisini na Saba, Milioni Mia Mbili Hamsini na Tano,Laki Tano na Sita Elfu, Mia Mbili Thelathini na Tisa(97,255,506,239.00) sawa na asil imia 51 ya fedhazilizoidhinishwa kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali hapachini.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

Jedwali Namba 1: Mlinganisho wa Fedha iliyotengwa nakupokelewa katika Mwaka wa Fedha 2016/2017 Chini yaFungu 41 Hadi kufikia Disemba 2016.

Mheshimiwa Spika, Kamati inatoa wito kwa Ofisi ya Hazinakutoa kiasi cha fedha kilichobaki ambacho kiliidhinishwana Bunge kwa Wizara ya Katiba na Sheria katika kipindi hikikilichobaki cha Mwaka wa Fedha 2016/2017 ili Wizara iwezekumaliza utekeleza majukumu yake kwa Ufanisi kamailivyopanga.

Mheshimiwa Spika, mchanganuo wa fedha zilizoidhinishwana zilizopokelewa katika Mwaka wa Fedha 2016/2017 hadikufikia Machi 2017 katika Mafungu Sita yanayosimamiwa naWizara hii, yaani Fungu 41, 16, 35, 59,55 na 12 umeainishwakwenye jedwali hapa chini kwa kila Fungu.

Jedwali Namba 2: Mlinganisho wa Fedha Iliyoidhinishwa naKupokelewa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Hadi KufikiaMachi 2017

Fungu Fedha

Iliyoidhinishwa Sh.

Fedha Iliyopatikana Sh.

Tofauti Sh.

Asilimia Sh.

41 91,450,900,001.00 Sh.97,255,506,239.00 Sh.94,195,393,762 51

 

 

Fungu Taasisi Fedha Zilizoidhinishwa

Fedha Zilizopokelewa

Asilimia ya kiasi kilichopokelewa

41 Wizara ya Katiba na Sheria

Sh.9,141,681,000.00 Sh.3,883,679,000.00 42

16 Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Sh.6,997,324,000.00 Sh.5,306,378,890.89 76

35 Mkurugenzi wa Mashtaka

Sh.13,097,619,000.00 Sh.7,955,545,061.32 61

12 Tume ya Utumishi wa Mahakama

Sh. 1,134,955,000.00 Sh. 609,858,475.00 53.7

59 Tume ya Kurekebisha Sheria

Sh. 1,658,192,000.00 Sh.1,021,696,624.65 61

55 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Sh. 3,741,929,226.22 Sh.2,074,860,878.22 55.44

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

Mheshimiwa Spika, katika mlinganisho ulioonyeshwa kwenyejedwali namba 2 hapo juu, Fungu 35 (Divisheni ya Mashitaka)ndio lililotengewa fedha nyingi zaidi ambazo ni Shilingi BilioniKumi na Tatu, Milioni Tisini na Saba, Laki Sita Kumi na Tisa Elfu(13,097,619,000.00) kwa Mwaka 2016/2017. Hata hivyo hadikufikia Mwezi Machi, 2017 fungu hili limepokea Shilingi BilioniSaba, Milioni Mia Tisa Hamsini na Tano, Laki Tano Arobaini naTano Elfu Sitini na Moja (7,955,545,061.00).

Mheshimiwa Spika, katika mlinganisho huo, Tume ya Utumishiwa Mahakama (Fungu 12), liliidhinishiwa fedha kidogo zaidikuliko mafungu mengine, kwa kiasi cha Shilingi Bilioni Moja,Milioni Mia Moja Thelathini na Nne, Laki Tisa Hamsini na TanoElfu (1,134,955,000.00). Pamoja na kuidhinishiwa fedha hizokidogo, hadi kufikia Mwezi Machi, 2017 fungu hili limepokeaShilingi Milioni Mia Sita na Tisa, Laki Nane Hamsini na NaneElfu, Mia Nne Sabini na Tano (609,858,475.00).

Mheshimiwa Spika, mwenendo huu wa upokeaji fedha kwaujumla, unadhihirisha kuwa, fedha inayopokelewa ni ndogosana ukilinganisha na kiasi kinachoidhinishwa na Bunge lakoTukufu. Hivyo Taasisi hizi zinashindwa kutekeleza majukumuyake kwa wakati na ufanisi kutokana na ucheleweshaji wautoaji wa fedha kwa upande wa Hazina.

3.1 UCHAMBUZI WA TAARIFA KUHUSU UKUSANYAJIMADUHULI KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017

Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Wizaraya Katiba na Sheria pamoja na Taasisi zake, ilitarajiakukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni Kumi na Saba, MilioniThemanini na Tano, Laki Nane Ishirini na Tisa Elfu, Mia TanoKumi na Moja (17,085,829,511.00) kama maduhuli ya Serikalikutoka vyanzo mbalimbali vya mapato. Hadi kufikia MweziDisemba, 2016, Wizara ilikuwa imekusanya kiasi cha ShilingiBilioni Kumi, Milioni Mia Tisa Arobaini na Tatu, Laki Nne Tisinina Moja Elfu, Mia Nane Arobaini na Tano (10,943,491,845.00)sawa na asilimia 64 ya makusanyo yaliyotarajiwa kamailivyochanganuliwa kwenye jedwali hapa chini

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

Jedwali Namba 3: Mlinganisho wa Makadirio, Makusanyona Asilimia Kwa Mafungu yaliyo Chini ya Wizara ya Katibana Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Hadi KufikiaDisemba 2016

Mheshimiwa Spika, makusanyo haya ni kutokana na adambalimbali za Usajili wa Matukio, Ada za Wanafunzi, Uuzajiwa Vitabu vya Zabuni na Huduma nyingine mbalimbalizinazotolewa na Wizara.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Katiba na Sheria (Fungu 41)imeongoza katika ukusanyaji wa Maduhuli kwa kukusanyaShillingi Bilioni Tano, Milioni Mia Tano Tisini na Tisa, Laki TatuKumi na Tatu Elfu, Mia Nane Arobaini na Tano(5,599,313,845.00) ikifuatiwa na Idara ya Mahakama (Fungu40) iliyokusanya Shilingi Bilioni Tano, Milioni Mia Tatu Arobainina Nne, Laki Moja Sabini na Nane Elfu (5,344,178,000.00).

Mheshimiwa Spika, mafungu mengine yalikuwa na matarajioya kukusanya Maduhuli lakini matarajio hayakuwa kamayalivyopangwa. Hii ni changamoto ambayo Wizara na Taasisizote zenye vyanzo vya mapato zinabidi kuiangalia kwaumakini kwani matarajio sio mapato. Hivyo kuna umuhimuwa kubuni vyanzo vingine vya ukusanyaji wa Maduhuli ilikuongeza upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wamajukumu ya Wizara hasa kwa zile Taasisi zilizokosa mapatokabisa.

3.2 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA USHAURI WA KAMATI

Mheshimiwa Spika, wakati wa uwasilishaji wa Makadirio ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwaMwaka wa Fedha 2016/2017, Kamati ilitoa ushauri namapendekezo Kumi na Sita (16) kuhusiana na Bajeti ya Wizaraya Katiba na Sheria pamoja na Taasisi zake.

Mheshimiwa Spika, Kamati imefurahishwa na utekelezaji wamaoni ya Kamati yaliyotolewa katika Taarifa yake yaUchambuzi wa Bajeti kwa Wizara hii Mwezi Mei, 2016. Jambomahsusi ambalo Kamati imeridhika nalo, ni ongezeko kidogokwenye Bajeti ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Hakiza Binadamu na Utawala Bora, ambayo imetengewa ShilingiBilioni Moja, Milioni Mia Tano Sitini na Sita, Themanini Elfu(1,566,080,000.00) katika Mwaka ujao wa fedha (2017/2018)kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC), ikilinganishwa naMwaka wa Fedha uliopita ambapo Tume hii iliidhinishiwaShilingi Milioni Mia Tisa Tisini na Nne, Laki Tano Kumi na NneElfu (994,514,000.00) tu kwa ajili ya Matumizi Mengineyoambayo ilikuwa ni ndogo na haikulingana na uzito wamajukumu yake katika kuhakikisha Haki za Binadamu naUtawala Bora zinazingatiwa. Tofauti hii ni ongezeko la asilimia57 ya Bajeti inayoombwa kuidhinishwa kwa ajili ya Tumekatika Mwaka wa Fedha unaokuja. Hata hivyo fedhailiyoidhinishwa haitoshelezi ikilinganishwa na majukumuyanayopaswa kutekelezwa na Tume katika Nchi nzima.Kamati inaishauri Serikali kuendelea kuongeza fedha zakutosha kwa Tume hii ili itekeleze majukumu yake kikamilifu.

4.0 MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZIKWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018

Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Wizaraya Katiba na Sheria, imejiwekea malengo saba (7) yakutekeleza ili kuongeza ufanisi na ubora katika kutoa hudumaza Kisheria na masuala ya Katiba yakiwemo;

i) Kuendelea na uhamasishaji wa shughuli za Serikali kutokaDar es Salaam kwenda Makao Makuu ya Nchi, Dodoma;ii) Kuimarisha mfumo wa Sheria na kuongeza uwezo waWizara katika maeneo maalum ya Sheria, usimamizi na utoajihaki;

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

iii) Kuimarisha usimamizi na ufuatilaji wa masuala yaKikatiba na Sheria;

iv) Kuimarisha misingi ya haki za Binadamu na Kisheria;

Mheshimiwa Spika, Kamati inakubaliana na malengo yaWizara kwa ujumla kwani yanalenga katika kuboreshautekelezaji wa majukumu yake na kuleta ufanisi zaidi katikasuala zima la utoaji haki nchini.

4.1 MAKADIRIO YA MAPATO YA WIZARA YA KATIBA NASHERIA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018

Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018, Wizarainatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni Ishirini na Nne,Milioni Themanini na Saba, Laki Tano na Saba Elfu, Mia Mbili(24,087,507,200.00) ikiwa ni Maduhuli ya Serikali, kamainavyoonekana kwenye jedwali hapa chini:

Jedwali Namba 4: Matarajio ya Maduhuli kwa Mwaka waFedha 2017/2018

Mheshimiwa Spika, Kamati imebaini kuwa Makadirio yaMapato hayaendani na hali halisi ya makusanyo. HivyoKamati inashauri kuwa, ni vizuri kuweka makadirio madogoyenye uhakika katika kukusanya kuliko kuweka makadiriomakubwa ya fedha ambayo hayana matarajio makubwakatika ukusanyaji.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

Mheshimiwa Spika, Tume ya Haki za Binadamu na UtawalaBora (Fungu 55) na Tume ya Utumishi wa Mahakama (Fungu12) hayana matarajio yoyote ya kukusanya maduhuli kwasababu ya kutokuwa na vyanzo vya mapato.

4.2 UCHAMBUZI WA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA WIZARAYA KATIBA NA SHERIA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2017/2018,Wizara pamoja na Taasisi zake inaomba kuidhinishiwaShilingi Bilioni Mia Moja Hamsini na Tisa, Milioni Mia TatuThelathini na Moja, Laki Nane Ishirini na Mbili Elfu,(159,331,822,000.00) kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida naMiradi ya Maendeleo ambayo ni upungufu wa asilimia 4.4ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017.Upungufu huu wa asilimia 4.4 unatokana na ukomo wa Bajetiya fedha za maendeleo kupungua kwa wastani wa asilimia55 ikilinganishwa na fedha ya Miradi ya maendeleoiliyoidhinishwa Mwaka 2016/2017.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Katiba na Sheria pamoja naTaasisi zake, kwa Mwaka 2017/2018 inaomba fedha kamailivoonyeshwa katika mchanganuo uliopo kwenye jedwalihapa chini.

Jedwali Namba 5: Uchambuzi wa Makadirio ya Matumizikwa Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

Fungu Taasisi Kiasi 4 1 Wizara ya Katiba na Sheria 9,862,0 66,000.0 0 1 6 Of isi ya Mwanasher ia Mkuu wa Serikali 7,282,5 23,000.0 0

3 5 Divisheni ya Mashitaka 14,914,0 63,000 .00 1 2 Tume ya Utumish i wa Mahakama 1,102,91 1,000.0 0 5 9 Tume ya Kurekebisha sher ia 2,052,75 7,000.0 0 5 5 Tume ya Haki za Binadamu na Utaw ala

Bora

6,166,98 1,000.0 0

JUMLA 41,381 ,301,0 00.00

 

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

Mheshimiwa Spika, Divisheni ya Mashitaka (Fungu 35) linamakadirio ya matumizi ya juu zaidi ikilinganishwa na mafungumengine. Bajeti inayoombwa kwa ajili ya Fungu hili ni sawana asilimia 37% ya Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, Tume ya Utumishi wa Mahakama (Fungu12) lina Makadirio ya Matumizi madogo zaidi ikilinganishwana mafungu mengine ikiwa ni sawa na asilimia 3.2% ya Bajetiya Wizara kwa Mwaka 2017/2018.

5.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Taarifa zilizowasilishwambele ya Kamati pamoja na majukumu ya Wizara ya Katibana Sheria na Taasisi zilizo chini yake, Kamati inatoa maoni naushauri ufuatao ili kuboresha utendaji kazi na ufanisi katikautekelezaji wa majukumu ya Wizara hii.

i) Kamati inaipongeza Serikali kwa kuongeza bajeti ya Tumeya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa Fedha yaMatumizi Mengineyo (OC) kutoka Shilingi Milioni Mia TisaTisini na Nne, Laki Tano Kumi na Nne Elfu (994,514,000.00)katika Mwaka wa Fedha 2016/2017 mpaka Shilingi BilioniMoja, Milioni Mia Tano Sitini na Sita, Themanini Elfu(1,566,080,000.00) katika Mwaka wa Fedha ujao (2017/2018).Ongezeko hili ni sawa na asilimia 57. Hata hivyo, Kamati inatoarai kwa Wizara na Taasisi zake kufanya rejea ya maagizoyaliyotolewa na Kamati katika Taarifa ya Mwaka wa Fedha2016/2017 na kuendelea kuyatekeleza katika kipindi cha roboya mwisho ya mwaka huu wa Fedha unaoishia Mwezi Juni,2017;

ii) Ofisi ya Hazina kutoa fedha zinazoidhinishwa na Bunge kwaWizara husika kwa wakati ili kuiwezesha Wizara kutekelezamajukumu yake kama yalivyopangwa katika kila Mwaka waFedha;

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

iii) Wizara kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria kufanya mapitiona maboresho yote ya msingi ya Sheria zote zinazohitajimaboresho na kutazama uwezekano wa kuhuisha Mchakatowa Upatikanaji wa Katiba Mpya kwa wakati muafaka;

iv) Wizara pamoja na Taasisi zake kukamilisha kwa harakautekelezaji wa Mpango wa kuhamia Dodoma mapemaiwezekanavyo il i kutekeleza uamuzi wa Serikali wakuhamishia Makao Makuu ya Nchi Dodoma;

v) Kamati inatoa wito kwa Serikali kuleta Bungeni Sheriamahsusi ambayo itahalalisha utekelezaji wa maamuzi yaSerikali ya awamu ya Tano ya kuufanya Mji wa Dodoma kuwaMakao Makuu ya Nchi;

vi) Tume ya Kurekebisha Sheria kuendelea kufanya mapitioya Sheria mbalimbali kwa lengo la kuzirekebisha nakuziboresha il i kuendana na mabadiliko mbalimbalituliyonayo sasa. Kamati inatoa rai kwa Tume hii kushirikianana Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili kufanya mapitioya Sheria ya Elimu ya Mwaka 1978 na kutazama uwezekanowa kuirekebisha ili kufanya Elimu ya Sekondari kuwa ya lazimana kuwawezesha vijana wanaomaliza Elimu ya Msingikuendelea na Elimu ya Sekondari;

vii) Serikali kuongeza ukomo wa Bajeti kwa Wizara na Taasisizake katika mwaka ujao wa fedha ili ziweze kuanza utaratibuwa kujenga majengo ya Ofisi zao katika mji wa Kiserikaliutakaojengwa Dodoma;

viii) Wizara kuendelea kusimamia kwa ufanisi masuala yoteya haki za Binadamu na upatikanaji haki nchini nakuhakikisha kwamba inachukua hatua za kutosha kupunguzawingi wa kesi Mahakamani na wingi wa mahabusu katikarumande, jambo ambalo linavunja haki mbalimbali zawatuhumiwa ambao wanakaa rumande kwa muda mrefubila kesi zinazowahusu kusikilizwa na kumalizika kwa wakati;

ix) Serikali kuzingatia kwa umakini matakwa ya Ibara ya 13(6)(a-e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

Mwaka 19777 ambayo inatoa haki za msingi za kuhusianana watuhumiwa wa makosa ya Jinai ikijumuisha hakiyakupata dhamana, kusikilizwa kwa kesi zao na kukata rufaakwa wakati muafaka;

x) Wizara na Mhimili wa Mahakama kwa ujumla, kuzingatiamatakwa ya kisheria kuhusu uendeshaji wa kesi za jinai nahususani taratibu za utoaji wa dhamana kwa watuhumiwakama zilivyowekwa na kifungu cha 148 cha Sheria yaMwenendo wa Kesi za Jinai iliyopitiwa Mwaka 2002 (CriminalProcedure Act ). Kamati inasisitiza kwamba dhamana ni hakiya Mtuhumiwa na ni suala la Kikatiba. Hivyo Taasisi za utoajihaki zinapaswa kuzingatia suala hili ili kutenda haki kwawatuhumiwa;

xi) Serikali kuridhia na kutekeleza Mikataba mbalimbali yaKimataifa iliyoridhiwa na Nchi yetu ili iweze kutekelezwa kamavile Mkataba wa Kimataifa wa Mwaka 1984 unaopingamatendo yote ya kikatili dhidi ya mwanadamu (ConventionAgainst Torture, 1984);

xii) Wakala wa Usajili,Ufilisi na Udhamini (RITA) kuendeleakufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya Sheria, Taratibu,Kanuni, uadilifu na weledi katika usajili wa mabaraza yawadhamini wa vyama vya siasa au makundi mengine yakijamii kwa kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo,hivyo kuepuka kuwa sehemu ya migogoro ya vyama hivyo;

xii i) Wizara kuanzisha na kukamilisha mchakato waupatikanaji wa Kanuni za Sheria ya Utoaji wa Msaada waKisheria ( The Legal Aid Act ) iliyopitishwa na Bunge katikaMkutano wa Sita wa Bunge uliofanyika Mwezi Februari, 2017;

xiv) Tume ya Utumishi wa Mahakama kusimamia kwa umakinimkubwa maslahi ya Mahakimu wote na hasa upandishajiwa vyeo na nyongeza ya mishahara kwa mahakimu waliokokwenye Mahakama za Mwanzo. Kamati inafahamu kwambawapo mahakimu wa Mahakama za Mwanzo ambaohawajapandishwa vyeo kwa miaka zaidi ya Saba (7) kinyumekabisa na taratibu za kazi na ajira kwa Watumishi wa Umma;

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

xv) Kamati inatoa wito kwa Watendaji wa Mahakama waWilaya kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatiaSheria,Taratibu na Mipaka ya Kazi zao na kutokuingiliamajukumu ya msingi ya Mahakama katika kutoa naKusimamia Haki;

xvi) Wizara na Mhimili wa Mahakama (Fungu 40) kuendeleakuboresha mfumo wa utoaji haki nchini na uendeshaji wakesi kwa kutumia njia na mifumo ya Kisasa ya Mawasiliano(E-Justice). Kamati inawapongeza wadau wote waMaendeleo kama Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP) na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF)ambayo yamekuwa mstari wa mbele katika kufadhili Miradimbalimbali ya Maendeleo iliyo chini ya Wizara ya Katiba naSheria ukiwamo mradi huu wa E-Justice.

6.0 HITIMISHOMheshimiwa Spika, mwisho napenda kukushukuru wewebinafsi, Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi hii muhimukuwasilisha maoni ya Kamati yangu. Aidha, hatuna budikukupongeza wewe binafsi Mheshimiwa Spika, MheshimiwaNaibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuliongoza Bungeletu Tukufu kwa busara, umakini na umahiri mkubwa.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee, napendakumshukuru sana Mheshimiwa Dr. Harrison G.Mwakyembealiyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, ambaye kwa zaidi yamwaka mmoja alifanya kazi kwa weledi na kutoa ushirikianomkubwa kwa Kamati wakati wa utekelezaji wa majukumuyake, hasa katika wakati wa uchambuzi wa Sheria yaHuduma za Utoaji wa Msaada wa Kisheria ya Mwaka 2016.

Mheshimiwa Spika, napenda nitumie nafasi hii piakumshukuru Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb), KatibuMkuu Prof. Sifuni Ernest Mchome, Naibu Katibu Mkuu NduguAmon Mpanju na Watendaji wote wa Wizara ya Katiba naSheria kwa ushirikiano mkubwa walioutoa wakati Kamatiilipojadili Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yaKatiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

Mheshimiwa Spika, kipekee nawashukuru Wajumbe waKamati kwa kazi nzuri waliyoifanya wakati wa kujadili nakuchambua Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yaKatiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. Uzalendo,uchapakazi pamoja na ushirikiano mkubwa walionipaumesaidia kufanikisha kukamilika kwa Taarifa hii kwa wakati.Kwa ruhusa yako naomba majina yao yaingizwe kwenyeKumbukumbu Rasmi za Bunge kama yalivyo yaani Hansard.

(i) Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa, Mb, Mwenyekiti(ii) Mhe. Najma Mutraza Giga, Mb, Makamu Mwenyekiti(iii) Mhe. Ajali Rashid Akbar, Mb, Mjumbe(iv) Mhe. Ally Saleh Ally, Mb, Mjumbe(v) Mhe. Anna Joram Gidarya, Mb, Mjumbe(vi) Mhe. Asha Abdallah Juma, Mb, Mjumbe(vii) Mhe. Dkt Mathayo David Mathayo, Mb, Mjumbe(viii) Mhe. Gibson Blasius Meiseyeki, Mb, Mjumbe(ix) Mhe. Joram Ismael Hongoli, Mb, Mjumbe(x) Mhe. Joseph Kizito Mhagama, Mb, Mjumbe(xi) Mhe. Juma Hamadi Kombo,Mb,Mjumbe(xii) Mhe. Makame Mashaka Foum, Mb, Mjumbe(xiii) Mhe. Mboni Mohamed Mhita, Mb, Mjumbe(xiv) Mhe. Nassor Suleiman Omar, Mb, Mjumbe(xv) Mhe. Omary Ahmed Badwel, Mb, Mjumbe(xvi) Mhe. Rashid Abdallah Shangazi, Mb, Mjumbe(xvii) Mhe. Riziki Shahari Mngwali, Mb, Mjumbe(xviii) Mhe. Saumu Heri Sakala, Mb, Mjumbe(xix) Mhe. Seif Ungando Ally, Mb, Mjumbe(xx) Mhe. Selemani Jumanne Zedi, Mb, Mjumbe(xxi) Mhe. Suleiman Masoud Nchambi, Mb, Mjumbe(xxii) Mhe. Taska Restituta Mbogo, Mb, Mjumbe(xxiii) Mhe. Twahir Awesu Mohamed, Mb, Mjumbe(xxiv) Mhe. Wanou Hafidhi Ameir, Mb, Mjumbe(xxv) Ussi Pondeza, Mb, Mjumbe

Mheshimiwa Spika, vilevile napenda kuwashukuru kwa dhati,Watumishi wa Ofisi ya Bunge, chini ya Uongozi wa Dkt. ThomasD. Kashililah, Katibu wa Bunge, kwa kusaidia na kuiwezeshaKamati kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Kipekee,namshukuru Mkurugenzi wa Idara ya Kamati za Bunge Ndugu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

Athumani Hussein, Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Angelina Sangana Makatibu wa Kamati Ndugu Stella Bwimbo na NduguDunford Mpelumbe pamoja na Msaidizi wa Kamati, NduguRaheli Masima, Makatibu Muhtasi wa Idara ya Kamati zaBunge Ndugu Chiku Ramadhan, Ndg. Grace Wambura naNdg. Irene Makongoro kwa kuratibu vyema kazi za Kamatina kuhakikisha kuwa Taarifa hii inakamilika kwa wakatiuliopangwa.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, sasa naombaBunge lako Tukufu, likubali kuidhinisha Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka waFedha 2017/2018 kama yalivyowasilishwa na Mtoa Hoja.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkonoHoja.

Mohamed Omary Mchengerwa, Mb.MWENYEKITI,

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA25 Aprili, 2017

MWENYEKITI: Tunaendelea, sasa namuita Mwenyekitiwa Kamati ya Bajeti mwakilishi wake Mheshimiwa SubiraMgalu.

MHE. SUBIRA K. MGALU (K.n.y MWENYEKITI WA KAMATIYA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI): Mheshimiwa Mwenyekiti,awali naomba uniruhusu na mimi nichukue fursa hiikumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha afya njemakusimama mbele ya Bunge lako Tukufu na kuwasilisha maoniya Kamati.

Pia nichukue fursa hii kuwapa pole wananchiwenzangu wa Mkoa wa Pwani hususan Wilaya za Mkuranga,Kibiti na Rufiji kutokana na madhila mbalimbali yaliyojitokeza,lakini niishukuru sana Serikali kwa kufanya kila jitihadakurejesha hali ya usalama katika maeneo hayo na naombawananchi wenzangu tuendelee kutoa ushirikiano kwavyombo vya usalama ili kuweza wahalifu na kuwafikisha

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

kwenye vyombo vya sheria. Kwa mujibu wa Kanuni ya 99 yaKanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2016, naombakuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bajeti kuhusuutekelezaji wa bajeti ya Mfuko wa Mahakama kwa mwakawa 2016/2017 na makadirio ya mapato na matumizi kwamwaka 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilikutana na Waziriwa Fedha na Mipango, Waziri wa Katiba na Sheria pamojana Mtendaji Mkuu wa Mahakama na kujadiliana na kufanyamashauriano kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Mfuko waMahakama kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na makadirioya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/2018.Mashauriano haya yamefanyika kwa mujibu wa kifungu cha75 cha Sheria ya Bajeti Na. 11 mwaka 2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa majukumu yaMfuko wa Mahakama kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Kwamujibu wa Katiba jukumu kubwa la Mahakama ni kusimamiautoaji wa haki katika kutekelza hili Mahakama imefanikiwakutekeleza yafuatayo:-

(a) Mahakama imefanikiwa kuanzisha DivisionMaalum ya Mahakama Kuu inayoshughulikia makosa yarushwa na uhujumu uchumi.

(b) Watumishi 539 wamepata mafunzo ya mudamfupi ya ndani ya nchi baadhi yao Waheshimiwa Majaji 57Wasajili watatu, Naibu Wasajili tisa na Mahakimu 144.

(c) Imekarabati Mahakama Kuu ya Dar es Salaam,Tanga na ukarabati wa Makahama Kuu ya Mbeya upo katikahatua za mwisho.

(d) Imesambaza nakala mbalimbali za vitabu vyamwongozo wa usimamizi na ukaguzi wa shughuli zaMahakama ili kuwezesha Mahakama nchini kutoa hudumabora ziadi kwa wananchi.

(e) Imeendelea kukamilisha miradi yake ya maendeleo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

ikiwemo ujenzi na ukarabati wa majengo ya Mahakama kwagharama nafuu katika maeneo ya Kibaha, Bagamoyo,Kigamboni, Mkuranga, Kawe na Kinyerezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na utekelezaji wamajukumu haya bado Mfuko wa Mahakama unakabiliwana changamoto mbalimbali kama vile; moja, utolewaji wafedha usiondana na mpango kazi wa Mfuko wa Mahakama,pili, uhaba wa watumishi wenye sifa zinazotakiwa kwenyekada mbalimbali na tatu, bajeti ndogo ya Mfuko waMahakama isiyolingana na mahitaji halisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mapitio yautekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017; katikamwaka wa fedha 2016/2017 Mfuko wa Mahakama Fungu 40uliidhinishiwa jumla kiasi cha shilingi 131,627,043,504, kati yafedha hizo shilingi 50,345,775 ni kwa ajili ya mishahara, shilingi34,519,534 kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi46,761,734,504, kwa ajili ya mpango wa maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha Julai hadiFebruari, 2017 jumla ya shilingi 55,427,630,446.56 zilitolewa naWizara ya Fedha kwa Fungu 40 kwa ajili ya mishahara namatumizi mengineyo, hii ikiwa ni sawa na asilimia 42 ya bajetiiliyotengwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Aidha, kwaupande wa fedha za maendeleo jumla ya shilingi 829,593,993zilitolewa, hii ikiwa ni sawa na asilimia mbili ya bajetiiliyotengwa kwa mwaka 2016/2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kupokea fedhahizo bado kumeonakana kuna changamoto kubwa yakutotolewa fedha kwa wakati kwa Fungu husika na hivyokuathiri utekelezaji wa baadhi ya majukumu ya Mfuko waMahakama. Aidha, Kamati ya Bajeti ilifanya mashauriano naSerikali na kukubaliana kiasi cha fedha kilichobakia kwenyeFungu hili kitolewe kabla ya tarehe 30 Juni, 2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu makadirio yamapato na matumizi ya Mfuko wa Mahakama kwa mwakawa fedha 2016/2017; kwa mwaka wa fedha 2016/2017 fedha

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

zilizokasimiwa kwenye Mfuko wa Mahakama zimetengwakatika maeneo mbalimbai kwa aji l i ya kuhakikishaMahakama inatekeleza majukumu yake ya Kikatiba. Baadhiya majukumu ambayo yamepangwa kutekelezwa katikabajeti ya mwaka 2017/2018 ni kama yafuatayo:-

(a) Kuendelea kutoa huduma ya haki sawa kwa wotena kwa wakati.

(b) Kuimarisha uongozi, utawala bora na uwajibikajikwa Mahakama pamoja na kuongeza upatikanaji wa harakawa huduma za Mahakama wa Wananchi.

(c) Kuimarisha ufanisi wa kazi za Mahakama kwakutumia TEHAMA

(d) Kuongeza mahusiano baina ya wadau wan je nandani ya Mahakama.

(e) Kujenga taswira mpya ya Mahakama yenyemtazamo chanya

Mheshumiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2017/2018. Mfuko wa Mahakama umepanga kukusanyamaduhuli ya kiasi cha shilingi 9,318,061,200 ikilinganishwa namakadirio ya shilingi 6,504,132,435 ya mwaka 2016/2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2017/2018 Mfuko wa Mahakama umetengewa jumla yashilingi 125,117,029,000 baada ya Serikali kushauriana naKamati ya Bajeti na kuongeza fedha za matumizi mengineyokwa mfuko wa kiasi cha shilingi bilioni Sita na Kamati ya Bajetiinaipongeza Serikali. Kati ya fedha hizo zilizotengwa, shilingi56,477,636,000 ni kwa ajili ya mishahara, shilingi 50,481,382,000ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi 18,150,011.000ni kwa ajili ya maendeleo ambapo kati ya hizo shilingi bilioni17 ni fedha za ndani na shilingi 1,154,011,000 ni fedha za nje.Mchanganuo wa namna ya fedha za matumizi ya kawaidana maendeleo zitakavyotumika zimeainishwa katika jedwalinaomba isomeke kwenye Hansard.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

Mheshimiwa Mwenyekiti, maoni na ushauri waKamati; kwa kuwa tathmini ya utekelezaj wa bajeti ya mfukowa Mahakama kwa mwaka wa fedha 2016/2017 inaoneshakuwa hadi kufikia Machi, 2017 Mfuko huu unakabiliwa nachangamoto ya kutokupokea fedha kwa wakati pamojana kupokea fedha pungufu tofauti na ilivyoombwa na hivyokuathiri utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huu hasa kwaupande wa miradi ya maendeleo. Hivyo basi, Kamatiinaishauri Serikali kuhakikisha kwamba kwa mwaka wa fedha2017/2018 Mfuko wa Mahakama unapatiwa fedha kwawakati na kwa mujibu wa maelekezo ya Sheria ya Bajeti yamwaka 2015 kama zilivyoidhinishwa na Bunge.

Kwa kuwa Mfuko wa Mahakama unakabiliwa nauhaba wa watumishi wenye sifa zinazostahili katika kadambalimbali, hivyo basi Kamati inaishauri Serikali kuhakikishainaongeza idadi ya watumishi wanaohitajika kwenye kadambalimbali kwa awamu ili kusaidia utekelezaji wa majukumuya Mfuko huu.

Kwa kuwa mtiririko wa fedha kwenye Mfuko waMahakama umekuwa hauzingatii mpango kazi wa mfukohusika, hivyo basi Kamati inaishauri Serikali kuhakikishainazingatia maelekezo ya kifungu cha 48 cha Sheria ya BajetiNamba 11 ya mwaka 2015 kinachoitaka Hazina kutoa fedhakwenda Mfuko wa Mahakama kwa kila robo mwaka. PiaSerikali ihakikishe ukomo unaotolewa unazingatia hali halisiya mahitaji ya Mahakama. (Makofi)

Kwa kuwa bajeti iliyotolewa kwa mwaka 2016/2017haikidhi mahitaji ya msingi ya Mfuko wa Mahakama hadikupelekea Mfuko huu kukabiliwa na madeni mbalimbaliyanayohusu posho za Wazee wa Baraza, malipo ya pangoza nyumba wanazoishi Majaji, Ofisi za kuendesheaMahakama pamoja na madai mbalimbali ya watumishi,hivyo basi Kamati inaishauri Serikali kuhakikisha inamaliziakupeleka kwenye Mfuko wa Mahakama bakaa ya matumizimengineyo ya kiasi cha shilingi bilioni 20 katika bajeti yamwaka 2016/2017 ili Mfuko huu uweze kulipa baadhi yamadeni hayo. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

Mheshimiwa Mwenyekiti, hitimisho; naombanihitimishe kwa kumshukuru Spika, Mheshimiwa Job YustinoNdugai na Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, Naibu Spikapamoja na Wenyeviti wote wa Bunge kwa kuongoza vyemaBunge letu na pia kwa kuongoza vyema mashauriano katiya Kamati ya Bajeti na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru MheshimiwaDkt. Philipo Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango naMheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Fedha naMipango kwa ushirikiano wao kwa Kamati. Aidha, Kamatiinamshukuru na kumpongeza Profesa Palamagamba Kabudi,Waziri wa Katiba na Sheria na Mtendaji Mkuu wa Mahakamakwa kushirikiana na Kamati wakati wa majadiliano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuwashukuruwajumbe wa Kamati kwa umakini wao katika kujadili nakutoa maoni na mapendekezo mbalimbali kuhusu bajeti yaMfuko wa Makama. Ukurasa wa 15 umewatambua wajumbehawa na naomba Hansard inukuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, napenda kuchukuafursa hii kumshukuru Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas D.Kashilillah kwa kuiwezesha Kamati kutekeleza majukumu yakeipasavyo pamoja na Sekretarieti ya Kamati ya Bajeti kwakuipa ushauri wa kitaalam Kamati hadi kukamilika kwataarifa hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo haya,naliomba Bunge lako Tukufu sasa lijadili na kuidhinishamakadirio ya mapato na matumizi ya Mfuko wa Mahakama- Fungu 40 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kamayalivyowasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha nanaunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Tunakushukuru kwa wasilisho lako zuri.(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

MAONI YA KAMATI KUHUSU UTEKELEZAJI WA BAJETI YAMFUKO WA MAHAKAMA KWA MWAKA WA FEDHA 2016/17PAMOJA NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA

MWAKA WA FEDHA 2017/18 KAMAILIVYOWASILISHWA MEZANI

1.0 UTANGULIZI.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kanuni ya 99(9)ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2016, naombakuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bajeti, kuhusuutekelezaji wa Bajeti ya Mfuko wa Mahakama kwa Mwakawa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwaMwaka wa Fedha wa 2017/18.

Mheshimiwa Spika, kamati ilikutana na Waziri waFedha na Mipango, Waziri wa Katiba na Sheria pamoja naMtendaji Mkuu wa Mahakama na kujadiliana na kufanyamashauriano kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mfuko waMahakama kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio yaMapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18.Mashauriano haya yamefanyika kwa mujibu wa kifungu cha75 cha Sheria ya Bajeti Na. 11 ya Mwaka 2015.

2.0 UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA MFUKO WAMAHAKAMA KWA MWAKA 2016/17

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Katiba, jukumukubwa la Mahakama ni kusimamia utoaji wa haki. Katikakutekeleza hil i Mahakama imefanikiwa kutekelezayafuatayo:-

a) Mahakama imefanikiwa kuanzisha divisheniMaalum ya Mahakama Kuu inayoshughulikia makosa yarushwa na uhujumu uchumi;

b) Watumishi 539 wamepata mafunzo ya mudamfupi ya ndani ya nchi, baadhi yao ni Waheshimiwa Majaji57, Wasajili 3, Naibu Wasajili 9 na Mahakimu 144;

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

c) Imekarabati Mahakama Kuu Dar es Salaam,Tanga na Ukarabati wa Mahakama kuu ya Mbeya upo katikahatua za mwisho;

d) Imesambaza nakala mbalimbali za Vitabu vyamwongozo wa usimamizi na ukaguzi wa shughuli zaMahakama ili kuwezesha Mahakama nchini kutoa hudumabora zaidi kwa wananchi;

e) Imeendelea kukamilisha miradi yake yamaendeleo ikiwemo ujenzi na ukarabati wa majengo yaMahakama kwa gharama nafuu katika maeneo ya Kibaha,Bagamoyo, Kigamboni, Mkuranga, Kawe na Kinyerezi;

Mheshimiwa Spika, pamoja na utekelezaji wamajukumu haya, bado Mfuko wa Mahakama unakabiliwana changamoto mbalimbali kama vile:-

I. Utolewaji wa fedha na usioendana naMpango Kazi wa Mfuko wa Mahakama;

II. Uhaba wa watumishi wenye sifa zinazotakiwakwenya kada mbalimbali;

III. Bajeti ndogo ya Mfuko wa Mahakamaisiyolingana na mahitaji halisi.

3.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YAMWAKA WA FEDHA 2016/2017

Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2016/17Mfuko wa Mahakama – Fungu 40 uliidhinishiwa jumla ya kiasicha Sh.131,627,043,504 Kati ya fedha hizo Sh.50,345,775,000 nikwa ajili ya Mishahara (PE), Sh.34,519,534,000 kwa ajili yaMatumizi Mengineyo (OC), na Sh.46,761,734,504 kwa ajili yaMpango wa Maendeleo.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwezi Julai2016 hadi Februari 2017 jumla ya shilingi 55,427,630,446.56zilitolewa na Wizara ya Fedha kwa Fungu 40 kwa ajili ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

mishahara na matumizi mengineyo, hii ikiwa sawa naasilimia 42 ya fedha zilizotengwa kwa mwaka 2016/17. Aidha,kwa upande wa fedha za maendeleo jumla ya shilingi829,593,993 zilitolewa hii ikiwa sawa na asilimia 2 ya bajetiiliyotengwa kwa mwaka 2016/17 (shilingi 46,561,734,000).

Mheshimiwa Spika, Hata hivyo pamoja na kupokeafedha hizi bado kumeonekana kuna changamoto kubwaya kutokutolewa fedha kwa wakati kwa fungu husika nahivyo kuathiri utekelezaji wa baadhi ya majukumu ya Mfukowa Mahakama. Aidha, Kamati ya Bajeti ilifanya mashaurianona Serikali na kukubaliana kiasi cha fedha kilichobakiakwenye fungu hili kitolewe kabla ya tarehe 30 Juni 2017.

4.0 MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YAMFUKO WA MAHAKAMA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/18.

Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa Fedha 2017/18, fedha zilizokasimiwa kwenye Mfuko wa Mahakamazimetengwa katika maeneo mbalimbali kwa aji l i yakuhakikisha Mahakama inatekeleza majukumu yake yaKikatiba. Baadhi ya majukumu ambayo yamepangwakutekelezwa katika bajeti ya mwaka 2017/18 ni kamayafuatayo:

a) kuendelea kutoa hukumu ya haki sawa kwawote na kwa wakati;

b) kuimarisha uongozi, utawala bora nauwajibikaji kwa Mahakama pamoja na kuongeza upatikanajiwa haraka wa huduma za Mahakama kwa wananchi;

c) kuimarisha ufanisi katika kazi za Mahakamakwa kutumia TEHAMA;

d) Kuongeza mahusiano baina ya wadau wa njena ndani ya Mahakama;

e) kujenga taswira mpya ya Mahakama yenyemtazamo chanya;

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

4.1 Maduhuli

Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2017/18Mfuko wa Mahakama umepanga kukusanya maduhuli yakiasi cha Sh. 9,318,061,200 ikilinganishwa na makadirio yashilingi 6,504,132,435 mwaka 2016/17.

4.2 Matumizi ya Kawaida na Maendeleo

Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2017/18Mfuko wa Mahakama umetengewa jumla yaSh.125,117,029,000; baada ya Serikali kushauriana na Kamatiya Bajeti na kuongezea fedha za matumizi mengineyo (OC)kwa mfuko huu kiasi cha shilingi 6,000,000,000.

Mheshimiwa Spika, Kati ya fedha hizo zilizotengwa;Sh.56,477,636,000 ni kwa ajili ya Mishahara, Sh.50,481,382,000ni kwa aji l i ya Matumizi ya Mengineyo (OC) naSh.18,158,011,000 ni kwa ajili ya maendeleo ambapo kati yakiasi hicho Sh.17,000,000,000 ni fedha za ndani naSh.1,158,011,000 ni fedha za nje. Mchanganuo wa namnafedha za Matumizi ya Kawaida na maendeleozitakavyotumika zimeanishwa kwenye jedwali lifuatalo.

JEDWALI: Mchanganuo wa Makisio ya Bajeti kwa mwaka2017/18

NA.

MAELEZO

BAJETI YA MWAKA

2016/2017

MAKISIO YA MWAKA 2017/2018

1. Mishahara 50,345,775,000 56,477,636,000 2 Matumizi Mengineyo

(OC) 34,519,534,000 50,481,382,000

3 Matumizi Ya Maendeleo

46,761,734,504 18,158,011,000

Fedha za Ndani 24,000,000,000 17,000,000,000

Fedha za Nje 22,761,734,504 1,158,011,000

4 Jumla ya Matumizi ya Kawaida na Maendeleo

131,627,043,504 125,117,029,000

 

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

5.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI

5.1 Kwa kuwa, Tathmini ya utekelezaji wa Bajetiya Mfuko wa Mahakama kwa mwaka wa fedha 2016/2017inaonyesha kuwa hadi kufikia mwezi Machi 2017; mfuko huuunakabiliwa na changamoto ya kutopokea fedha kwawakati pamoja na kupokea fedha pungufu tofauti nailivyoombwa na hivyo kuathiri utekelezaji wa majukumu yaMfuko huu hasa kwa upande wa miradi ya maendeleo’

Hivyo basi, Kamati inaishauri Serikali kuhakikishakwamba kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 Mfuko waMahakama unapatiwa fedha kwa wakati na kwa mujibuwa maelekezo ya Sheria ya Bajeti (2015) kamazilivyoidhinishwa na Bunge.

5.2 Kwa kuwa, Mfuko wa Mahakama unakabiliwana uhaba wa watumishi wenye sifa zinazotakiwa katikakada mbalimbali,

Hivyo basi, Kamati inaishauri Serikali kuhakikishainaongeza idadi ya watumishi wanaohitajika kwenye kadambalimbali kwa awamu ili kusaidia kutekeleza majukumuya Mfuko huu;

5.3 Kwa kuwa, mtiririko wa utoaji fedha kwenyeMfuko wa Mahakama umekuwa hauzingatii Mpango Kaziwa Mfuko husika,

Hivyo basi, Kamati inaishauri Serikali kuhakikishainazingatia maelekezo ya kifungu cha 48 cha Sheria ya BajetiNa. 11 ya mwaka 2015 kinachoitaka Hazina kutoa fedhakwenda Mfuko wa Mahakama kwa kila robo mwaka. Pia,Serikali ihakikishe ukomo unaotolewa unazingatia hali halisiya mahitaji ya Mahakama,

5.4 Kwa kuwa, bajeti iliyotolewa kwa mwaka2016/17 haikidhi mahitaji ya msingi ya Mfuko wa Mahakamahadi kupelekea Mfuko huu kukabiliwa na madeni mbalimbaliyanayohusu posho ya wazee wa baraza, malipo ya pango

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

la nyumba za kuishi Majaji, ofisi za kuendesha Mahakamapamoja na madai mbalimbali ya watumishi,

Hivyo basi, Kamati inaishauri Serikali kuhakikishainamalizia kupeleka kwenye Mfuko wa Mahakama bakaaya matumizi mengineyo kiasi cha shilingi bilioni 20 katikabajeti ya mwaka 2016/17 ili Mfuko huu uweze kulipa baadhiya madeni hayo.

6.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, naomba nihitimishe kwakukushukuru wewe Mheshimiwa Spika na Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson (Mb), Naibu Spika kwa kuongoza vemamashauriano kati ya Kamati ya Bajeti na Serikali. NamshukuruMheshimiwa Dkt. Philip Mpango (Mb), Waziri wa Fedha naMipango na Mheshimiwa Dkt Ashatu Kijaji (Mb), Naibu Waziriwa Fedha na Mipango kwa ushirikiano wao kwa Kamati.Aidha, Kamati inamshukuru pia Mheshimiwa Proff.Palamagamba Kabudi , (Mb), Waziri wa Katiba na Sheria naMtendaji Mkuu wa Mahakama kwa kushirikiana na Kamatiwakati wa majadiliano.

Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuru wajumbewa Kamati hii kwa umakini wao katika kujadili na kutoamaoni na mapendekezo mbalimbali kuhusu Bajeti ya Mfukowa Mahakama. Naomba kuwatambua wajumbe hao kamaifuatavyo;

1) Mhe. Hawa Abdulrahman Ghasia, Mb – Mwenyekiti2) Mhe. Josephat Sinkamba Kandege, Mb - M/Mwenyekiti3) Mhe. Hamida Mohamedi Abdallah, Mb4) Mhe. David Ernest Silinde, Mb5) Mhe. Mbaraka Kitwana Dau, Mb6) Mhe. Mendrad Lutengano Kigola, Mb7) Mhe. Maria Ndilla Kangoye, Mb8) Mhe. Susan Peter Maselle, Mb9) Mhe. Agustino Manyanda Masele, Mb10) Mhe. Freeman AikaelMbowe, Mb11) Mhe. Flatei Gregory Massay, Mb

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

12) Mhe. Makame Kassim Makame, Mb13) Mhe. Janet ZebedayoMbene, Mb14) Mhe. Cecil David Mwambe, Mb15) Mhe. Susana Chogisasi Mgonukulima, Mb16) Mhe. Subira Khamis Mgalu, Mb17) Mhe. Juma Hamad Omar, Mb18) Mhe. Ali Hassan Omari, Mb19) Mhe. Martha Jachi Umbulla, Mb20) Mhe. Jerome Bwanausi, Mb21) Mhe. Jitu Vrajlal Soni, Mb22) Mhe. Abdallah M. Bulembo, Mb23) Mhe. Andrew John Chenge, Mb24) Mhe. Mussa A. Zungu, Mb25) Mhe. Japhet Ngalilonga Hasunga, Mb26) Mhe. Dalali Peter Kafumu, Mb27) Mhe. Albert Obama Ntabaliba, Mb

MheshimiwaSpika, napenda kuchukua fursa hii, piakumshukuru Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah kwakuiwezesha Kamati kutekeleza majukumu yake ipasavyo,pamoja na Sekretarieti ya Kamati ya Bajeti kwa kuipa ushauriwa kitaalamu Kamati hadi kukamilika kwa taarifa hii.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayonaliomba Bunge lako tukufu sasa lijadili na kuidhinishaMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Mfuko wa Mahakama– Fungu 40, kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 kamayalivyowasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naungamkono hoja hii.

Subira Khamis Mgalu, MbKny: MWENYEKITI

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI25 APRILI, 2017

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, sasa namwitaMsemaji wa Kambi ya Upinzani awasilishe taarifa, MheshimiwaTundu Lissu. (Makofi)

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Kambi Rasmiya Upinzani ya Bunge lako Tukufu, naomba kuwasilisha maoniya Kambi kuhusu Mpango na Makadirio ya mapato…

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Kuhusu Utaratibu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tundu Lissu, hebu ketikitako, naona kuna Kuhusu Utaratibu.

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Okay.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, Kuhusu Utaratibu, nakwenda na ile Kanuni ya68(1) lakini inakwenda kuzungumzia Kanuni ya 64(1) navifungu vyake vidogo. Kwanza nitasoma Kanuni ya 64(2)ambayo inasema:-

“Mbunge yoyote anayeamini kuwa Mbungemwingine amevunja au amekiuka masharti ya fasili ya (1) yaKanuni hii, atasimama mahali pake na kumwambiaMheshimiwa Spika “Kuhusu utaratibu”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuniruhusunizungumze maneno ya utaratibu. Nimekuwa nikipitiahotuba ya Kambi ya Upinzani…

WABUNGE FULANI: Umeitoa wapi?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, nimeipitia hotuba ya Kambi ya Upinzani nanaomba kusema kwamba, namheshimu sana MheshimiwaTundu Lissu kwa weledi mkubwa alionao na kwa kaziambazo amekuwa akizifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kupitia hotubahiyo, nataka kuzungumza maneno ya utaratibu ambayoyanajitokeza kwenye Kanuni ya 64(1). Jambo la kwanza lakiutaratibu ambalo nimeligundua kwenye hotuba hii, yapomaeneo mengi tu kwenye hiyo hotuba ambayo kwa kiasikikubwa yanahusiana na mienendo ya kesi ambazo zikomahakamani na hii ni kinyume na Kanuni ya 64(1)(c). (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, vilevile katika hotuba hii yapo mambo ambayoyanazungumzia mwenendo wa Rais ambayo ni kinyume naKanuni 64(1)(e). (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, vilevile ndani ya hotuba hii yamezungumziwamambo ambayo yanahusika na mwenendo wa watu ambaowanashughulikia masuala ya kutoa haki ambapo ni kinyumena Kanuni 64(1)(e). (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, yapo pia maeneo ambayo yanazungumziamambo ambayo tulikwishayafanyia maamuzi humu ndani.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, mambo hayo yalishawasilishwa wakati wahotuba pia ya Kiongozi ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungenina tulishayaondoa kwa mujibu ya Kanuni 64(1)(c). (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, kwa sababu hoja yenyewe imekiukwa Kanunihizo ambazo nilizisema, naomba unipe utaratibu ni kwa ninihoja hii isirudishwe Mezani kwako na maeneo ambayoyanakiuka Kanuni hizi yaweze kuondolewa na ndipo hoja hiiiweze kuwasilishwa ndani ya Bunge hili. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naombautulivu. Nimeombwa suala la utaratibu, amelielezea Waziriwa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu kwa sahihi kabisa. Kikanunindivyo hivyo zilivyokaa.

Waheshimiwa Wabunge, sasa kuhusiana na tukio,mimi mwenyewe hapa nina tatizo moja, naona ndiyonaletewa sasa…

WABUNGE FULANI: Ndiyo. (Makofi)

MWENYEKITI: Sasa uamuzi wangu kuhusu utaratibu,maeneo hayo ambayo Mheshimiwa Waziri Nchi ameyasema…

WABUNGE FULANI: Ameyapata wapi?

MWENYEKITI: Yeye ameyapata…

WABUNGE FULANI: Wapi?

MWENYEKITI: Hiyo sio hoja, tusibishane na Kiti.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

MBUNGE FULANI: Ni hoja.

MWENYEKITI: Kitu kimoja ambacho nimeambiwa nanilikuwa naulizia kwa nini sijaletewa hotuba hapa, nimepewamaelezo na Meza kwamba Kambi Rasmi ya Upinzaniwalichelewesha kupeleka kwenye uchapishaji, hilo ni la huko.

MBUNGE FULANI: Yeye ameipata wapi?

MWENYEKITI: Hata hivyo, ili twende vizuri sasa, maanataarifa hii lazima iwasilishwe hatua ya kwanza lakini kamayapo maeneo ambayo tayari yameshatolewa maamuzikwamba yasirudiwe hatuwezi kuyarudia. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Ninachomtaka Mheshimiwa Waziri yeyeanayajua maeneo hayo atuambie ibara…

MBUNGE FULANI: Siyo atuambie awasilishe kwanza.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, sasamnaongoza Bunge ninyi?

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Mniachie basi nitoe…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, mbonalinawasumbua sana suala hili?

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: (Hakutumia kipaza sauti)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa, nakuheshimu sana,tafadhali.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

MWENYEKITI: Mkiendelea hivi, mnajua nina madarakaya kuweza kutumia, sitaki kufika huko.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Sasa naongeza muda usiozidi dakika 30ili turuhusu shughuli hii ikamilike. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Hapo sawa.

MWENYEKITI: Ninachotaka sasa Serikali wanisaidie zileparaghaphs ambazo zina tatizo utasema …

MBUNGE FULANI: Asome zijulikane.

MWENYEKITI: Lakini Mheshimiwa Tundu Lissu uwasilishehotuba yako.

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekuwa nasoma kwa sikumbili zilizopita maandiko ya Walimu wangu, Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe (the Parliament and Electoral Process)na mwalimu wangu mwingine leo ni Waziri Katiba na Sheria,Profesa Pala Kabudi (the state and party). Kwa hikikinachoendelea katika Bunge hili linaloitwa la vyama vingiyanathibitisha kitu kimoja, hili litakuwa Bunge la hovyo kulikoBunge la wakati wa chama kimoja. Kama Bunge litaruhusuSerikali iwe inaamua namna ya kukosolewa hili halitakuwaBunge. (Makofi) [Maneno haya Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmiza Bunge]

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba niendelee.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

WABUNGE FULANI: Wewe endelea.

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni mara yangu ya sabakusimama mbele ya Bunge lako Tukufu …

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa.

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: ...na kutoa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tundu Lissu, wewe nimwanasheria mzuri tu na una uzoefu…

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Nafahamu.

MWENYEKITI: Huwezi ukatusomea taarifa hapaambayo ni tofauti na hiyo ambayo umetuandikia,haiwezekani! Kwa hiyo, maneno yako so called utangulizi,naagiza yafutwe kwenye Hansard sasa hivi. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Wewe nenda straight kwenye taarifayenu kama mlivyoiandika, niliyonayo hapa hayana manenohayo uliyoyasema sasa hivi.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MBUNGE FULANI: Afute.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni mara yangu ya sabakusimama mbele ya Bunge lako Tukufu na kutoa maoni yaKambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako Tukufu kuhusu Wizaraya Mambo ya Katiba na Sheria. Tangu mwaka 2010 hadimwezi uliopita, Wizara hii imeongoza kwa kuwa namabadiliko mengi ya Mawaziri kuliko Wizara nyingine yoyote.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, itakumbukwa kwanzaWizara hii mwaka 2010 ilianza na Waziri Mheshimiwa CelinaOmpeshi Kombani, Mheshimiwa Mathias Mendrad Chikawe,Mwalimu wangu Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mwalimuwangu wa pili Dkt. Harrison George Mwakyembe na sasakaka yangu na Mwalimu wangu wa tatu wa sheria,Mheshimiwa Profesa Palamagamba John Aidan MwalukoKabudi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ushahidi huu, tanguniwe Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lakoTukufu, tumekuwa na Mawaziri tofauti wa Mambo ya Katibana Sheria kwa takribani kila baada ya mwaka mmoja namiezi mitatu. Kwa vyovyote vile inavyoweza kuelezewa hiini rate of turn over kubwa sana katika uongozi wa Wizarayoyote ile. Kama nilivyosema mwanzoni katika kipindi hichohakuna Wizara nyingine yoyote katika Serikali hii ambayoimekuwa na mabadiliko ya mara kwa mara ya namna hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maoni ya Kambi Rasmiya Upinzani ya Bunge lako Tukufu mabadiliko haya ya marakwa mara ya Mawaziri ya Mambo ya Katiba na Sheriayanaashiria kitu kimoja kikubwa. Mawaziri husika walishindwaama kwa sababu zao binafsi, ama kwa sababu za mfumowetu wa kisiasa na kikatiba kuiongoza nchi yetu katikakutatua matatizo makubwa ya kisiasa na kikatiba ambayoyameikabili nchi yetu kwa miongo kadhaa. Tumeyazungumzamatatizo haya kwa kipindi chote ambacho nimekuwaMsemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Bunge lako Tukufu.(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Profesa Kabudianaweza kuwa mgeni katika Bunge lako Tukufu na katikaWizara ya Mambo ya Katiba na Sheria. Hata hivyo,Mheshimiwa Profesa Kabudi sio mgeni hata kidogo katikauelewa wa matatizo makubwa ya kisiasa na kikatiba ya nchiyetu. Mwaka 1984 Profesa Kabudi akiwa mwanafunzi waShahada ya Uzamili ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar esSalaam aliandika thesis yake kuhusu Muungano waTanganyika na Zanzibar (the International Law Examinationof the Union between Tanganyika and Zanzibar).

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika thesis yake,Mheshimiwa Profesa Kabudi alikuwa mtu wa kwanza kuwekahadharani ushahidi wa nyaraka wa chanzo cha kuchafukakwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar mwaka 1983/1984kulikopelekea kung’olewa madarakani kwa Rais wa pili waZanzibar Alhaj Aboud Jumbe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaalam wa MheshimiwaProfesa Kabudi haukuishia kwenye uelewa wake wa masualaya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mwaka 1985Profesa Kabudi na Dkt. Agrey Mlimuka walikuwa wasomi wakwanza kabisa kuelewa na kuelezea historia ya jinsi chamakimoja kwanza TANU na badaye CCM kil ivyotumikakulimbikiza madaraka makubwa kikatiba na kisheria kwaSerikali na ndani ya Serikali kwa Rais wa Jamhuri yaMuungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, makala yao The State andthe Party (Dola na Chama) katika The State and WorkingPeople in Tanzania kitabu kilichohaririwa na Profesa Issa Shivjina kuchapishwa mwaka 1985 lilikuwa andiko la kwanza lakisomi kuelezea dhana ya chama dola katika mfumo wetuwa kisiasa na kikatiba na jinsi chama dola hicho kilivyovunjanguvu ya Bunge kama chombo kikuu cha maamuzi katikanchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya utaalam nauelewa wake mkubwa wa masuala muhimu ya kikatiba nakisheria ya nchi yetu, mwaka 2012 Mheshimiwa Profesa Kabudi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

aliteuliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mjumbe waTume ya Mabadiliko ya Katiba maarufu kama Tume yaWarioba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama inavyofahamika,Tume hiyo ndiyo ilikusanya maoni ya Watanzania kuandaaripoti na rasimu ya Katiba mpya kwa ajili ya nchi yetu nakuiwasilisha mbele ya Bunge Maalum mnamo mwezi Februari2014. Kama mwanafunzi wake na mmoja wa wale ambaotumefuatilia maisha ya kitaaluma ya Mheshimiwa ProfesaKabudi kwa karibu, naweza kusema bila wasiwasi walashaka yoyote kwamba ripoti ya Tume ya Warioba na Rasimuya Katiba Mpya ina alama za vidole vya kitaaluma vyaMheshimiwa Profesa Kabudi kuliko pengine vya mjumbemwingine yeyote wa Tume hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kusema hivyo hakunamaana ya kudharau michango ya Wajumbe wengine wotewa Tume ya Warioba bali ni kutambua mchango mkubwawa Waziri wa sasa wa Mambo ya Katiba na Sheria katikamchakato huo wa kihistoria katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu zote hizi, wakatini halali kabisa kumpongeza Profesa Kabudi kwa kuteuliwakatika nafasi yake hii mpya, ni vizuri kumkumbusha juu yamajukumu makubwa na mazito ambao nafasi yake hiiinamlazimisha kuyabeba. Ni vizuri zaidi kumkumbushakwamba mazingira ya utekelezaji wa majukumu hayoyanamlazimisha kuchagua kati ya kusimamia maslahi ya kwelina ya kudumu ya nchi yetu ambayo yanajionesha katikamaandiko yake ya kitaaluma na katika ripoti ya Tume yaMabadiliko ya Katiba na maslahi ya muda ya kisiasa ambayomara nyingi hayana maisha marefu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutaanza na suala la KatibaMpya. Katika taarifa yake kwa Kamati ya Kudumu ya Katibana Sheria ya mwezi uliopita, Mheshimiwa Profesa Kabudiamezungumzia suala la Katiba Mpya kwa aya moja tu yenye

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

kichwa cha habari ‘mambo ya Katiba’ na nimeona kwenyehotuba yake ameifuta kabisa hiyo habari ya Katiba Mpya.(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa MheshimiwaWaziri, Serikali ya Awamu ya Tano inatambua umuhimu wanchi kuwa na Katiba Mpya. Hata hivyo, ikumbukwe kuwamara baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingiamadarakani ilianza kazi kwa kuunda Serikali na kufanyamabadiliko ya kina ya miundo na mifumo ya kiutendaji. Kwasasa baada ya kazi hiyo kukamilika Serikali inapitia sheriazinazohusika na mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwamadhumuni ya kubaini utaratibu mzuri wa kuendelea namchakato huo kutoka pale ulipoishia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa hiyo imeainishamambo saba ambayo Mheshimiwa Waziri ameyaita maeneomahsusi ya kipaumbele. Kati ya hayo, hakuna jambo hatamoja linalohusu Katiba Mpya ambayo hata haijatajwakabisa. Aidha, katika mchanganuo wa matumizi ya bajetikwa kila fungu hakuna fungu hata moja linalohusu KatibaMpya. Vilevile katika vitabu vya randama kwa mafungu yotesita yaliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheriahakuna kasma hata moja ambayo imetengwa kwa ajili yaKatiba Mpya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maneno menginemchakato wa Katiba Mpya ambayo Mheshimiwa Wazirianataka tuamini kwamba haujauawa na Serikali ya Awamuya Tano haujatengewa hata senti moja katika bajetiinayopendekezwa kwa Bunge lako Tukufu mwaka huu. Huuni mwendelezo wa bajeti ya mwaka jana ambayo nayohaikutenga hata senti moja kwa ajili ya mchakato wa KatibaMpya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maoni yangu juu yabajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2015/2016,nilielezea kwa kirefu jinsi ambavyo Katiba Mpya imekwama.Tarehe 26 Aprili, 2014 yaani the Golden Jubilee ya Muunganowa Tanganyika na Zanzibar ambayo Rais Dkt. Jakaya Kikwete

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

aliwaahidi Watanzania kuwa ndiyo tarehe ya nchi yetu kuwana Katiba Mpya ilifika na ikapita bila nchi yetu kuwa na Katibampya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 30 Aprili, 2015ambayo Rais Kikwete aliwaahidi wananchi kuwa ndiyoingekuwa siku ya kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu Katibainayopendekezwa, ahadi ambayo ilirudiwarudiwa na kilakiongozi wa CCM na Serikali yake ndani na nje ya Bunge hiliTukufu ilifika na kupita bila kura ya maoni kufanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo na kwakipindi kilichobakia cha utawala wa Rais Kikwete, viongoziwa CCM na Serikali waliendelea kusisitiza ijapo kwa sauti zakinyonge kwamba kura hiyo ya maoni ingefanyika katikatarehe ambayo hata hivyo hawakuwa tayari kuitaja tena.Haikufanyika hadi wakati Rais Kikwete anaondokamadarakani na Rais Magufuli anaingia madarakani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana nilisema katikamaoni yangu ya mwaka juzi kwamba kwenye signature issueya utawala wake yaani Katiba Mpya huyu ni Rais aliyeshindwana hii ni Serikali iliyoshindwa. (Makofi) [Maneno Haya SiyoSehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais John Pombe Magufulialisema…

KUHUSU UTARATIBU

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Kuhusu Utaratibu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa AG.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, Kanuni ya 64(2), kuhusu utaratibu, hayo manenoyanayosemwa, moja, Serikali haijashindwa wala Raishajashindwa…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

WABUNGE FULANI: Si una muda wa kujibu?

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Hapana!

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Hakuna hiyo kwasababu hata maneno yalivyoandikwa huwezi kuainisha niSerikali ipi na Serikali ni ileile ya Chama cha Mapinduzi.(Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MBUNGE FULANI: Katiba iko wapi, mnayo?

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Katiba hatujapigakura…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, maneno yalivyowekwa yamekaa vibaya haya,hayaweki mpaka lakini hata hayawezi kuweka mpaka kwasababu ni mwendelezo wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi.Naomba maneno haya yaondoke yanakiuka Kanuni ya 64.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tundu Lissu…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naombautulivu. Mheshimiwa Tundu Lissu, kwa haya manenoyanayosema kwenye signature issue ya utawala wake mpakaneno iliyoshindwa, naomba uyaondoe, uendelee tu namtiririko wako ili twende vizuri. Kwa hiyo na Hansard nayenyewe yawe expunged maneno haya yasiwepo. Endeleana hotuba yako.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo ni maneno ambayoyapo kwenye Hansard kwa miaka mitatu iliyopita, nimeyatoakwenye Hansard. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais Dkt. John PombeMagufuli ameshatangaza hadharani kwamba Katiba Mpyasiyo kipaumbele cha Serikali yake. Rais amedai kwambawakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2015 yeye hakutoaahadi yoyote kwa Watanzania kwamba atawaletea KatibaMpya akichaguliwa kuwa Rais. Kwa hiyo, kwa msimamo huowa Rais Magufuli, mchakato wa Katiba Mpya ambao hadiulipoishia kwa kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwaulikwisha kugharimu jumla ya shil ingi bil ioni 121.463,umekwishakufa na kuzikwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Profesa Kabudini mtu mwelewa sana wa siasa za kikatiba za Tanzania. Kwauelewa wake mkubwa wa masuala haya, MheshimiwaProfesa Kabudi anafahamu vyema kivuli kirefu cha urais wakifalme ambao ndio imekuwa the organizing principle yakatiba na siasa za Tanzania tangu mwaka 1962 ilipotungwaKatiba ya Jamhuri. Kwa uelewa wake huo, MheshimiwaProfesa Kabudi anafahamu au anatakiwa kufahamukwamba kwa katiba na sheria za Tanzania na kwa mila nadesturi za kisiasa na kikatiba Rais akishasema hawezikubishiwa na Waziri wake. Ni suala la kama wasemavyoWakatoliki Roma locuta, causa finita yaani Roma ikishasemandiyo mwisho wa mashauri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hiyo KambiRasmi ya Upinzani ya Bunge lako Tukufu inataka kujua kutokakwa Mheshimiwa Waziri Serikali ya Awamu ya Tanoinatambuaje umuhimu wa nchi yetu kuwa na Katiba Mpyawakati Rais Magufuli amekwishasema Katiba Mpya siokipaumbele cha Serikali yake. Je, kama kweli Serikali hii inampango wa kuundeleza mchakato wa Katiba kutoka paleulipoishia ni kwa nini Serikali hii haijatenga hata senti mojakwenye bajeti hii kwa ajili ya jambo hili muhimu? (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

Mheshimiwa Mwenyekiti, bila majibu ya kweli yamaswali haya, Waziri Mheshimiwa Kabudi atakuwaameangukia kwenye shimo lile lile waliloangukia watanguliziwake wanne la kushindwa kutekeleza matakwa na matarajioya Watanzania ya kupata Katiba Mpya na ya kidemokrasiaitakayokidhi mahitaji ya kizazi hiki na vizazi vijavyo. Sio ajabumaisha yake kama Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheriayakawa mafupi kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nizungumziemahakama…

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakama ya Tanzaniahaina kiongozi kamili yaani Jaji Mkuu…

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Hii ni kwa sababu tangu Jaji Mkuu Mohamed ChandeOthman astaafu tarehe 1 Januari, 2017, Rais John PombeMagufuli hajateua Jaji Mkuu mpya kuchukua nafasiiliyoachwa wazi na Jaji Mkuu Chande Othman. (Makofi)

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, Kuhusu Utaratibu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lissu subiri kidogo,Mheshimiwa Waziri wa Nchi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, kwanza tulikuwa tunamwomba sana Msemajiwa Kambi Rasmi ya Upinzani atupeleke kwa mujibu wakitabu chake cha …

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Ukurasa wa 29.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, atupeleke kwa mujibu wa kitabu chake…

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Ukurasa wa 29.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti …

MWENYEKITI: Nimekuelewa Mheshimiwa Waziri,Mheshimiwa Tundu Lissu kwa sababu hawa viongozi wanahii hotuba…

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Ndiyo.

MWENYEKITI: Wewe unapofanya summary usemekwamba naenda sasa ukurasa wa …

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Sawasawa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

MWENYEKITI: Itawasaidia ili wawe pamoja na wewe.(Makofi)

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, jambo la kiutaratibu…

MWENYEKITI: Ngoja kidogo Mheshimiwa Lissu,Mheshimiwa Waziri wa Nchi.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, naomba Waheshimiwa Wabunge tuelewane,Mheshimiwa Tundu Lissu nakuelewa. Mheshimiwa Tundu Lissuunatupeleka ukiwa umeacha maeneo mengine…

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Nitarudi.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Na unaendakutupeleka kwenye page…

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Nitarudi.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, naomba suala la utaratibu na utaratibu wanguni kwamba…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, pale ambapo anatakiwa kuanza sasa ni masualaya haki za binadamu. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, kama hatatusomea eneo hili la haki za binadamuina maana kwamba …

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Sijasema hivyo.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Utaratibuwangu…

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Sijasema hivyo.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Basi naomba …

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, vinginevyo basi utuambie utaratibu wa kusomahii…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. JOHN J. MNYIKA: Ni wajibu wako kufuatilia?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Kwa hiyo, kamatunaanza …

MHE. JOHN J. MNYIKA: Ni wajibu wako kufuatiliaanasoma wapi.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa hebu kaeni chini.Nakuomba Mheshimiwa Gekul kaa chini. Hoja ya MheshimiwaWaziri wa Nchi ni kwamba mtiririko wako usipokuwa wa waziutawachanganya watu.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Ndiyo maana nikasema kwa sababulazima ufanye summary…

MHE. JOHN J. MNYIKA: (Hakutumia kipaza sauti)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika mimi siyo mtu wakujaribiwa, nakuomba sana. (Makofi)

MHE. JOHN J. MNYIKA: Anayoyasoma yamo humuhumu.

MWENYEKITI: Mimi ndiyo naongoza shughuli humu.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Sawa, lakini anayoyasomayamo humu humu.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Hata MheshimiwaJanuary jana alifanya hivyo hivyo.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Sasa Mheshimiwa Tundu Lissu hebu somahotuba yako kwa mtiririko ambao tunataka kuuona. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

MHE. JOHN J. MNYIKA: Ni wajibu wao kufuatilia.

WABUNGE FULANI: Unapendelea.

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 29, wa KaimuJaji Mkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakama ya Tanzaniahaina kiongozi wake kamili yaani Jaji Mkuu. Hii ni kwa sababutangu Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman astaafu tarehe1 Januari, 2017, Rais John Pombe Magufuli hajateua Jaji Mkuumpya kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mkuu ChandeOthman. Badala yake Rais Magufuli amemteua Jaji wa RufaaProfesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 118(4) ya Katiba yetuRais anaruhusiwa kuteua Kaimu Jaji Mkuu iwapo itatokeakiti cha Jaji Mkuu kitakuwa wazi au kwa Jaji Mkuu kuwahayupo Tanzania au Jaji Mkuu atashindwa kutekeleza kaziyake kwa sababu yoyote na Rais ataona kuwa kwa mudawa tukio lolote kati ya hayo matatu inafaa kumteua KaimuJaji Mkuu. Kaimu Jaji Mkuu aliyeteuliwa kwa utaratibu huuatatekeleza kazi za Jaji Mkuu mpaka atakapoteuliwa JajiMkuu mwingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuwapo kwaIbara ya 118(4), Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako Tukufuinaamini kwamba Rais Magufuli anavunja Katiba ya nchi yetukwa kushindwa kuteua Jaji Mkuu kamili takribani miezi mitanotangu kustaafu. (Makofi) [Maneno Haya Siyo Sehemu yaTaarifa Rasmi za Bunge]

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE WALEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, Kuhusu Utaratibu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tundu Lissu, nenda ukakaetu, Kuhusu Utaratibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, nilishayasema haya mambo toka mwanzo nandiyo maana nilisema Kanuni ya 64(1) na maeneo niliyoyatajayameendelea kuvunjwa kwa kutumia hotuba hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipokuwa nasema hotubahii isomwe kwa mtiririko maana yangu ilikuwa twende eneomoja na lingine ili la kubaki libaki na la kuondoka liwezekuondoka.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa na jirani yako kaenichini, kaa chini.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, sasa nirudi kwenye hili la kikatiba. Ibara ya 118(3)na (4) imeeleza ni wakati gani Mheshimiwa Rais atateuaKaimu Jaji lakini Ibara hizo wala hazioneshi…

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Kuhusu Utaratibu.

MBUNGE FULANI: Atajibu, anapoteza muda.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Ni kwa mudagani…

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Huu ni utaratibu gani?

MBUNGE FULANI: Anapoteza muda.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Kuhusu Utaratibu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

MWENYEKITI: Mheshimiwa huwezi ukaomba utaratibujuu ya utaratibu.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Kwa sababu anachokisemakinavunja utaratibu. (Makofi)

MWENYEKITI: Kaa chini wewe.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Anachokisema kinavunjautaratibu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika kaa chini.

MBUNGE FULANI: Mtoe nje.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge tusiwadanganyeWatanzania…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. JOHN J. MNYIKA: Wewe unajibu kama nani?

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti …

MWENYEKITI: Jielekeze sasa kwenye hiyo ninayoitafutamimi.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, ninachotaka kusema ni kwamba manenoyanayosema Mheshimiwa Rais anavunja Katiba yaondokekwa sababu…

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

MHE. JOHN J. MNYIKA: Yaondoke kwa sababu gani?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Kwa sababu ibarandogo ya (5) inasema, Kaimu Jaji Mkuu atatekeleza kazi zaJaji Mkuu mpaka atakapoteuliwa Jaji Mkuu mwingine.Kipengele hiki hakisemi ni muda gani?

WABUNGE FULANI: Wewe.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Ni mpaka paleatakapoteuliwa Jaji Mkuu mwingine. Kwa hiyo, Raisamevunjaje Katiba hapo? (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Jenista,Waziri wa Nchi. Tafsiri hiyo ya Katiba kuhusiana na Jaji Mkuukipindi ambacho anakaimu uliyoyasema ndio sahihi. (Makofi)

Sasa kitu ambacho Mheshimiwa Tundu Lissu amekoseani pale aliposema Rais anavunja Katiba ya nchi. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Kweli.

MWENYEKITI: Sasa hizo sweeping statements mimisitaziruhusu humu…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: No, no. Masuala hayo kama una-feel verystrongly kwamba there is ukiukwaji wa Katiba, ninyiwanasheria mnajua cha kufanya. Humu Bungeni msituleteetaarifa ambazo zinapotosha wananchi. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Naagiza maneno yale ambayoyanasema, Rais kwa kufanya hivyo anakiuka Katiba…

MBUNGE FULANI: Ni kweli.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

MWENYEKITI: Yaondolewe kwenye Hansard. Endeleasasa Mheshimiwa. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Mheshimiwa nitakutoa nje sasa hivi,nakuheshimu sana.

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 118(4) ya Katibahaikutungwa kwa lengo la kumwezesha Rais kuteua KaimuJaji Mkuu bila kikomo cha muda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ilivyo kwa sheria zote,Ibara ya 118(4) ina sababu yake maalum. Ibara hiyoimewekwa kwa makusudi ya kuhakikisha kwamba kwamuda wote kunakuwa na kiongozi wa Mahakama ya Rufaniya Tanzania pamoja na kiongozi wa Mahakama ya Tanzaniawakati Jaji Mkuu kamili anasubiria kuteuliwa. Kaimu Jaji Mkuuni sawa na kile kinachoitwa na wanasheria an interlocutoryposition. Kaimu Jaji Mkuu ni nafasi ya muda inayoshikiliwana mtu mwenye sifa za kuwa Jaji Mkuu kabla nafasi hiyohaijajazwa na Jaji Mkuu kamili. Swali halali linalohitaji majibuni, je, Kaimu Jaji Mkuu anastahili kuwepo madarakani kwamuda gani? Hili ni suala la tafsiri ya Katiba linalohitaji kujibiwana Mahakama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maoni ya Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni, miezi mitano ni muda mrefu mno wakuwa na Kaimu Jaji Mkuu. Hii ni kwa sababu katika historiayetu yote tangu uhuru haijawahi kutokea Rais wa nchi yetuakashindwa kuteua Jaji Mkuu kamili kujaza nafasi iliyo waziya Jaji Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge lako Tukufu kamamojawapo ya mihimili mikuu ya dola Tanzania lina kiongoziwake mkuu muda wote, Spika au Naibu Spika. Serikali kamamhimili mwingine mkuu ina kiongozi wake mkuu muda wote,Rais au Makamu wa Rais. Kwa Mahakama ya Tanzania

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

mhimili mkuu wa tatu wa dola ya Tanzania kutokuwa nakiongozi wake kamili miezi mitano baada ya kustaafu kwaJaji Mkuu Chande Othman kunatoa taswira potofu kwambamahakama ina hadhi hafifu au ya chini ikilinganishwa namihimili mingine mikuu ya dola ya Tanzania.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Kitendo hiki vilevile kinatoa taswira potofu kwambamiongoni mwa Majaji wote wa Rufaa au wa MahakamaKuu…

MWENYEKITI: Naku-interrupt sasa, Mheshimiwa AG.

MBUNGE FULANI: Mlinde muda wake.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, hadhi ya mahakama na mihimili yote mitatu yadola imewekwa kikatiba, haiwezi kuwa kwa sababu huyuhajateuliwa. Kwa mujibu wa Sheria ya Tafsiri ya Sheria, TheInterpretation of Laws Act, Cap 1 inasema…

MBUNGE FULANI: Si utajibu bwana.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mwongozo.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, inasema kwamba anayekaimu…

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Kuhusu Utaratibu.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Atakuwa namamlaka sawa na mwenye cheo mwenyewe na kwasababu yapo kwenye Katiba…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

MHE. JOHN J. MNYIKA: Kuhusu utaratibu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu waSerikali, nimekuelewa. Nasema hivi kwa suala hili ambalolinahusu tafsiri naamini mtoa hoja Mheshimiwa Waziri waKatiba na Sheria atakapokuja kujibu kuna maeneo ambayoyanahitaji yanyooshwe. Nategemea hilo Profesa mtalifanyakwa ukamilifu. AG kwa sababu ya muda, tusiliendeleza, it isokay. (Makofi)

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kitendo hiki vilevile kinatoataswira potofu kwamba pengine Kaimu Jaji Mkuu wa sasahatoshelezi nafasi hiyo au kwamba miongoni mwa Majajiwote wa Rufaa au wa Mahakama Kuu ya Tanzania auMawakili na Wanasheria wengine wa nchi hii pamoja na walewa nchi za Jumuiya ya Madola hakuna hata mmoja waomwenye uwezo au sifa za kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzani yaBunge lako Tukufu inamtaka Mheshimiwa Waziri amshauri RaisMagufuli kwa heshima zote anazostahili amthibitishe KaimuJaji Mkuu Profesa Juma katika nafasi hiyo au vinginevyo ateuemwanasheria mwingine yeyote anayemuona anafaa na anasifa za kuwa Jaji Mkuu kamili wa Tanzania. Hali ilivyo sasainawatia aibu wanasheria wote wa Tanzania na inaitia aibunchi yetu katika Jumuiya ya Kimataifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kurudi kwenyeukurasa wa kumi, haki za binadamu. Katika taarifa yake kwaKamati Mheshimiwa Profesa Kabudi alidai kwamba Wizarainaendelea kuimarisha na kusimamia uzingatiwaji wa misingiya haki za binadamu kama ilivyoainishwa na kuhifadhiwakatika katiba na sheria za nchi. Madai haya hayaelezi halihalisi ya haki za binadamu katika nchi yetu. Ukweli ni kwambakauli ya Mheshimiwa Profesa Kabudi inapotosha ukweli juuya haki za binadamu katika nchi yetu. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

Mheshimiwa Mwenyekiti, badala ya kupunguamatukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa nahasa vyombo vya ulinzi na usalama…

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, Kuhusu Utaratibu.

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Ambayo Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lakoTukufu…

MWENYEKITI: Kuhusu Utaratibu, Mheshimiwa TunduLissu kuna suala la utaratibu hapa.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, hili ni suala la utaratibu. Kanuni ya 64(1)(c)inazungumzia mambo ambayo yalikwishakufanyiwamaamuzi hayatakiwi kurejewa tena. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo analotakakulisoma Mheshimiwa Tundu Lissu sasa.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, wakati wa uwasilishaji wa hotuba ya Kiongoziwa Kambi ya Upinzani Bungeni, jambo hili na yale yanayofuatatuliyaondoa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungenialiyaondoa kwa maneno yake. Ukifuatilia Hansard mambohaya yalishaondolewa kwa maamuzi ya Bunge. Ni suala lautaratibu mambo haya hayatakiwi kuendelea kubaki leo.(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

MHE. JOHN J. MNYIKA: Siyo jambo sahihi.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Tunaomba utusikilize nasisi.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Kuhusu Utaratibu kablahujatoa uamuzi.

MBUNGE FULANI: Unasikiliza upande mmoja?

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Hivi utalazimisha, kwanza sijakutambua.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kablahujatoa uamuzi ungetusikiliza nini…

MWENYEKITI: Sijakuruhusu kuongea, kaa kwanza,twende vizuri. Mheshimiwa Tundu Lissu nenda ukaketi.

MBUNGE FULANI: Muwe mnatenda haki.

MWENYEKITI: Hebu sema sasa, unaongelea point oforder, unaongelea nini?

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuhusu utaratibu kwamba hayo anayoyasema kwanzahakukuwa na uamuzi wowote wa Bunge juu ya mamboanayoyasema. Pili, mambo anayosema yaliondolewayaliondolewa kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, hayahusu hii Wizaraya Katiba na Sheria. Hapa ambapo yanazungumzwa sasandiyo mahali pake. Kwa hiyo, Serikali isikilize iweze kutoamajibu juu ya mambo haya. (Makofi)

MWENYEKITI: Kanuni ni kanuni tu, hatuwezi kujidaikwamba hatuzifahamu. Narudia uamuzi wa Kiti uliotolewawakati wa majadiliano kuhusu hoja ya Waziri Mkuu kwenyeeneo hili na ambalo Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

alikubali kuyaondoa ambayo yanahusu haki za binadamuna tukienda kuangalia Hansard ipo, tusibishane.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. JOHN J. MNYIKA: Anazungumzia haki zabinadamu na ana wajibu wa kujibiwa.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, uamuziukishachukuliwa na Bunge wewe kama unataka kubadilisha…

MHE. JOHN J. MNYIKA: Hapana, sio sahihi.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, yale ya Wazirialiyoyasema kwenye hotuba ndiyo maana nimeyaruhusulakini hayo unayoshuka nayo ambayo ndiyo moja ya hoja…

MHE. JOHN J. MNYIKA: Yapi sasa?

MWENYEKITI: Nasema hayo hayapo.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Yapi sasa?

MBUNGE FULANI: Muacheni asome.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nimelindasana muda wa Mheshimiwa Tundu Lissu, namuongezeadakika mbili tu halafu nasitisha shughuli za Bunge.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Hapana, muda wake ulindwe.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti…

MWENYEKITI: Usiendeleze malumbano.

MHE. TUNDU A.M. LISSU – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NASHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, wenye hatia huwa niwaoga. Wenye hatia na wenye madhambi ni waoga,ahsante sana. (Makofi/Vigelegele)

WABUNGE FULANI: Rais, Rais, Rais. (Makofi/Vigelegele)

WABUNGE FULANI: Waoga.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nawasihi sanakwa lugha zetu hizi.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Nawasihi sana kwa lugha zetu hiziambazo siyo za Kibunge. Hiyo ndiyo taarifa ya Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni. Mimi naamini kupitia mtoa hoja kunamaeneo mengi katika hotuba hii ambayo yanahitajikunyooshwa.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Haiwezekani tukapotosha wananchi.(Makofi)

MHE. JOHN J. MNYIKA: Kama unataka yanyooshweyazungumzwe basi.

MWENYEKITI: Sasa hiyo sio kazi yangu.

WABUNGE FULANI: Nyie waoga.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

MWENYEKITI: Hiyo siyo kazi yangu mimi kama Kiti, lakininaamini wakati muafaka ninyi mtakapoanza kuchangiampaka tutakapofika hatua ya kuhitimisha hoja hii kupitiamtoa hoja, kuna maeneo mengi yatanyooshwa tu.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Yazungumzwe sasa il iyanyooshwe.

MWENYEKITI: Na yatanyooshwa tu na ni lazimayanyooshwe. (Makofi)

MAONI YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANIBUNGENI, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA, MHESHIMIWA

TUNDU A.M. LISSU (MB.) KUHUSU MPANGO NAMAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YAFEDHA YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

KWA MWAKA 2017/2018 - KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

(Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016)

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,Hii ni mara yangu ya saba kusimama mbele ya Bunge lakotukufu na kutoa Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bungelako tukufu kuhusu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria.Tangu mwaka 2010 hadi mwezi uliopita, Wizara hiiimeongoza kwa kuwa na mabadiliko mengi ya mawazirikuliko Wizara nyingine yoyote. Kama utakavyokumbuka,Mheshimiwa Spika, mara baada ya Uchaguzi Mkuu wamwaka 2010, mtu wa kwanza kuteuliwa Waziri wa Mamboya Katiba na Sheria alikuwa marehemu Mheshimiwa CelinaOmpeshi Kombani. Hakumaliza mwaka mmoja, kwani nafasiyake ilikabidhiwa kwa mwanasheria Mathew MeindrardChikawe.

Mheshimiwa Chikawe alidumu kwenye nafasi hiyo kwatakriban miaka mitatu. Ilipofika mwezi Disemba 2014, WaziriChikawe aliondolewa na nafasi hiyo ikakasimishwa kwamwalimu wangu wa sheria, Mheshimiwa Dkt. Asha-Rose

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

Mtengeti-Migiro. Huyu alidumu kama Waziri wa Mambo yaKatiba na Sheria hadi mwezi Disemba, 2015, wakati nafasiyake ilipokasimishwa kwa mwalimu wangu mwingine washeria, Mheshimiwa Dkt. Harrison George Mwakyembe. Sasa,baada ya mwaka na miezi mitatu, nafasi ya Waziri waMambo ya Katiba na Sheria imekabidhiwa kwa kaka yanguna mwalimu wangu wa tatu wa sheria, Mheshimiwa Prof.Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.Kwa ushahidi huu, Mheshimiwa Spika, tangu niwe Msemajiwa Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu, tumekuwana Waziri tofauti wa Mambo ya Katiba na Sheria kwa takribankila baada ya mwaka mmoja na miezi mitatu. Kwa vyovyotevile inavyoweza kuelezewa, hii ni rate of turnover kubwa sanakatika uongozi wa Wizara yoyote ile. Na kama nilivyosemamwanzoni, katika kipindi hicho, hakuna Wizara nyingineyoyote katika Serikali hii ya CCM ambayo imekuwa namabadiliko ya mara kwa mara namna hii.

Mheshimiwa Spika,Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu,mabadiliko haya ya mara kwa mara ya Mawaziri wa Mamboya Katiba na Sheria yanaashiria kitu kimoja kikubwa: Mawazirihusika walishindwa, ama kwa sababu zao binafsi ama kwasababu za mfumo wetu wa kisiasa na kikatiba, kuiongozanchi yetu katika kutatua matatizo makubwa ya kisiasa nakikatiba ambayo yameikabili nchi yetu kwa miongo kadhaa.Tumeyazungumza matatizo haya kwa kipindi chote ambachonimekuwa Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bungelako tukufu.

Mheshimiwa Spika,Mheshimiwa Prof. Kabudi anaweza kuwa mgeni katika Bungelako tukufu na katika Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria.Hata hivyo, Mheshimiwa Prof. Kabudi sio mgeni hata kidogokatika uelewa wa matatizo makubwa ya kisiasa na yakikatiba ya nchi yetu. Mwaka 1984, Mheshimiwa Prof. Kabudiakiwa mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili ya Sheria ya ChuoKikuu cha Dar es Salaam, aliandika Thesis yake kuhusuMuungano wa Tanganyika na Zanzibar, The International LawExamination of the Union Between Tanganyika and Zanzibar.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

Katika Thesis yake, Prof. Kabudi alikuwa mtu wa kwanzakuweka hadharani ushahidi wa nyaraka wa chanzo cha‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar’ mwaka1983-84, kulikopelekea kung’olewa madarakani kwa Rais waPili wa Zanzibar, Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi.

Mheshimiwa Spika,Utaalamu wa Mheshimiwa Prof. Kabudi haukuishia kwenyeuelewa wake wa masuala ya Muungano wa Tanganyika naZanzibar. Mwaka 1985, Prof. Kabudi na Dkt. Aggrey K.L.J.Mlimuka walikuwa wasomi wa mwanzo kabisa kuelewa nakuelezea historia ya jinsi chama kimoja, kwanza TANU nabaadae CCM, kilivyotumika kulimbikiza madaraka makubwakikatiba na kisheria kwa Serikali na, ndani ya Serikali, kwaRais wa Jamhuri ya Muungano.Makala yao, ‘The State and the Party’, yaani ‘Dola naChama’, katika The State and the Working People in Tanzania,kitabu kilichohaririwa na Prof. Issa G. Shivji na kuchapishwamwaka 1985, ilikuwa andiko la kwanza la kisomi kuelezeadhana ya ‘chama-dola’ katika mfumo wetu wa kisiasa nakikatiba, na jinsi chama-dola hicho kilivyovunja nguvu yaBunge kama chombo kikuu cha maamuzi katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika,Kwa sababu ya utaalamu na uelewa wake mkubwa wamasuala muhimu ya kikatiba na kisheria ya nchi yetu, mwaka2012 Mheshimiwa Prof. Kabudi aliteuliwa na Rais JakayaKikwete kuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,maarufu kama Tume ya Warioba. Kama inavyofahamika,Tume hiyo ndiyo iliyokusanya maoni ya waTanzania, kuandaaRipoti na Rasimu ya Katiba Mpya kwa ajili ya nchi yetu nakuiwasilisha mbele ya Bunge Maalum mnamo mwezi Aprili,2014.

Kama mwanafunzi wake na mmoja wa wale ambaotumefuatilia maisha ya kitaaluma ya Mheshimiwa Prof.Palamagamba Kabudi kwa karibu, ninaweza kusema bilawasi wasi wala shaka yoyote kwamba Ripoti ya Tume yaWarioba na Rasimu ya Katiba Mpya ina alama za vidole vyakitaaluma vya Prof. Kabudi kuliko, pengine, vya mjumbe

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

mwingine yeyote wa Tume hiyo. Na kusema hivyo hakunamaana ya kudharau michango ya Wajumbe wengine wotewa Tume ya Warioba, bali ni kutambua mchango mkubwawa Waziri wa sasa wa Mambo ya Katiba na Sheria katikamchakato huo wa kihistoria katika nchi yetu.

Kwa sababu zote hizi, wakati ni halali kabisa kumpongezaMheshimiwa Prof. Kabudi kwa kuteuliwa katika nafasi yakehii mpya, ni vizuri kumkumbusha juu ya majukumu makubwana mazito ambayo nafasi yake hii inamlazimisha kuyabeba.Na ni vizuri zaidi kumkumbusha kwamba mazingira yautekelezaji wa majukumu hayo yanamlazimisha kuchaguakati ya kusimamia maslahi ya kweli na ya kudumu ya nchiyetu – ambayo yanajionyesha katika maandiko yake yakitaaluma na katika Ripoti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba– na maslahi ya muda ya kisiasa ambayo mara nyingi hayanana maisha marefu. Tutaanza na suala la Katiba Mpya.

YA KATIBA MPYA

Mheshimiwa Spika,Katika Taarifa yake kwa Kamati ya Kudumu ya Katiba naSheria ya mwezi uliopita, Mheshimiwa Prof. Kabudiamezungumzia suala la Katiba Mpya kwa aya moja tu yenyekichwa cha habari ‘Mambo ya Katiba.’ Kwa mujibu waMheshimiwa Waziri, “Serikali ya Awamu ya Tano inatambuaumuhimu wa nchi kuwa na Katiba Mpya. Hata hivyo,ikumbukwe kuwa mara baada ya Serikali ya Awamu ya Tanokuingia madarakani ilianza kazi kwa kuunda Serikali nakufanya mapitio ya kina ya miundo na mifumo ya kiutendaji.Kwa sasa, baada ya kazi hiyo kukamilika Serikali inapitia sheriazinazohusika na mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwamadhumuni ya kubaini utaratibu mzuri wa kuendelea namchakato huo kutoka pale ulipoishia.”1

1Taarifa ya Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (MB),Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Akiwasil isha Mpango naMakadirio ya Bajeti ya Wizara kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge yaKatiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/2018, Dodoma, Machi,2017, uk. 8

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

Mheshimiwa Spika,Taarifa hiyo imeainisha mambo saba ambayo MheshimiwaWaziri ameyaita ‘maeneo mahususi ya kipaumbele.’ Kati yahayo, hakuna jambo hata moja linalohusu Katiba Mpya,ambayo hata haijatajwa kabisa. Aidha, katika‘mchanganuo wa matumizi ya bajeti kwa kila Fungu’,hakuna Fungu hata moja linalohusu Katiba Mpya. Vile vile,katika vitabu vya Randama kwa Mafungu yote sita yaliyochini ya Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria, hakuna kasmahata moja ambayo imetengwa kwa ajili ya Katiba Mpya.

Kwa maneno mengine, Mheshimiwa Spika, mchakato waKatiba Mpya, ambayo Mheshimiwa Waziri anataka tuaminikwamba haujauawa na Serikali ya Awamu ya Tano,haujatengewa hata senti moja katika bajetiinayopendekezwa kwa Bunge lako tukufu mwaka huu. Nahuu ni mwendelezo wa bajeti ya mwaka jana ambayo nayohaikutenga hata senti moja kwa ajili ya mchakato wa KatibaMpya.

Mheshimiwa Spika,Katika Maoni yangu juu ya bajeti ya Wizara ya Katiba naSheria kwa mwaka 2015/2016, nilielezea kwa kirefu jinsiambavyo ‘Katiba Mpya imekwama.’ Tarehe 26 Aprili, 2014,yaani The Golden Jubilee ya Muungano wa Tanganyika naZanzibar, ambayo Rais Jakaya Kikwete aliwaahidiwaTanzania kuwa ndiyo tarehe ya nchi yetu kuwa na KatibaMpya, ilifika na ikapita bila ya nchi yetu kuwa na Katiba Mpya.

Tarehe 30 Aprili, 2015, ambayo Rais Kikwete aliwaahidiwananchi kuwa ndiyo ingekuwa siku ya kufanyika kwa kuraya maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa - ahadi ambayoilirudiwa rudiwa na kila kiongozi wa CCM na Serikali yakendani na nje ya Bunge hili tukufu – ilifika na kupita bila kuraya maoni kufanyika.Baada ya hapo, na kwa kipindi kilichobakia cha utawalawa Rais Kikwete, viongozi wa CCM na Serikali waliendeleakusisitiza, ijapo kwa sauti za kinyonge, kwamba kura hiyo yamaoni ingefanyika katika tarehe ambayo, hata hivyo,

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

hawakuwa tayari kuitaja tena. Haikufanyika hadi wakati RaisKikwete anaondoka madarakani na Rais Magufuli anaingiamadarakani. Ndio maana nilisema, katika Maoni yangu yamwaka juzi, kwamba

(Maneno ya mwisho ya aya hapo juu yalifutwa na Bunge)

Mheshimiwa Spika,Rais John Pombe Magufuli ameshatangaza hadharanikwamba Katiba Mpya sio kipaumbele cha Serikali yake. Raisamedai kwamba wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa2015, yeye hakutoa ahadi yoyote kwa waTanzania kwambaatawaletea Katiba Mpya akichaguliwa kuwa Rais. Kwa hiyo,kwa msimamo huo wa Rais Magufuli, mchakato wa KatibaMpya ambao, hadi ulipoishia kwa kupitishwa kwa KatibaInayopendekezwa, ulikwisha kugharimu jumla ya shilingibilioni 121.463, umekwishakufa na kuzikwa.

Mheshimiwa Prof. Kabudi ni mtu mwelewa sana wa siasa zakikatiba za Tanzania. Kwa uelewa wake mkubwa wamasuala haya, Prof. Kabudi anafahamu vema kivuli kirefucha ‘Urais wa Kifalme’, ambayo ndiyo imekuwa ‘theorganizing principle’ ya katiba na siasa za Tanzania tangumwaka 1962 ilipotungwa Katiba ya Jamhuri. Kwa uelewawake huo, Mheshimiwa Prof. Kabudi anafahamu, auanatakiwa kufahamu, kwamba, kwa Katiba na Sheria zaTanzania, na kwa mila na desturi zake za kisiasa na kikatiba,Rais akishasema hawezi kubishiwa na Waziri wake. Ni sualala – kama wasemavyo Wakatoliki - Roma locuta, causa finita,yaani Roma ikishasema, ndio mwisho wa mashauri!

Kwa sababu hiyo, Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi yaUpinzani ya Bunge lako tukufu inataka kujua kutoka kwaMheshimiwa Waziri, Serikali ya Awamu ya Tano inatambuajeumuhimu wa nchi yetu kuwa na Katiba Mpya wakati RaisMagufuli amekwishasema Katiba Mpya sio kipaumbele chaSerikali yake? Na, je, kama kweli Serikali hii ina mpango wakuuendeleza mchakato wa Katiba Mpya kutoka paleulipoishia, ni kwa nini Serikali hii haijatenga hata senti mojakwenye bajeti hii kwa ajili ya jambo hili muhimu?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

Bila majibu ya kweli kwa maswali haya, Waziri Kabudiatakuwa ameangukia kwenye shimo lile lile walimoangukiawatangulizi wake wanne: kushindwa kutekeleza matakwana matarajio ya waTanzania ya kupata Katiba Mpya na yakidemokrasia itakayokidhi mahitaji ya kizazi hiki na vizazivijavyo. Na sio ajabu, maisha yake kama Waziri wa Mamboya Katiba na Sheria, yakawa mafupi kama ilivyokuwa kwawatangulizi wake.

A HAKI ZA BINADAMUMheshimiwa Spika,

Katika Taarifa yake kwa Kamati, Mheshimiwa Prof. Kabudialidai kwamba “Wizara iliendelea kuimarisha na kusimamiauzingatiwaji wa misingi ya haki za binadamu kamailivyoainishwa na kuhifadhiwa katika Katiba na sheria zanchi....” Madai haya hayaelezi hali halisi ya haki za binadamukatika nchi yetu. Ukweli ni kwamba kauli ya Mheshimiwa Prof.Kabudi inapotosha ukweli juu ya haki za binadamu katikanchi yetu.

(Aya zinazofuata baada ya aya ya hapo juuzilifutwa na Bunge)

UENDESHAJI WA MASHTAKA YA JINAI

Mheshimiwa Spika,

Mamlaka ya uendeshaji wa mashtaka ya jinai imekasimiwakwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka kwa mujibu wa ibaraya 59B(2) ya Katiba. Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 59B(4),katika kutekeleza mamlaka yake, “Mkurugenzi wa Mashtakaatakuwa huru, hataingiliwa na mtu yeyote au na mamlakayeyote na atazingatia ... nia ya kutenda haki, kuzuia matumizimabaya ya taratibu za utoaji haki na maslahi ya umma.”Kanuni hii kuu imetamkwa pia na kifungu cha 8 cha Sheriaya Utumishi wa Mashtaka ya Taifa, Na. 27 ya 2008 (NationalProsecutions Service Act, 2008) ambayo pia imefafanua nakutilia nguvu mamlaka haya ya kikatiba.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

200

Kwa mujibu wa Sheria hii, Mkurugenzi wa Mashtaka anamamlaka sio tu ya kudhibiti mashtaka yote ya jinai bali piakuratibu shughuli za upelelezi wa makosa ya jinai [kifungucha 16(1)]. Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 17(1) na (3),Mkurugenzi ana uwezo wa kutoa maelekezo ya maandishikwa ofisa yeyote wa umma ili apatiwe taarifa yoyoteinayohusu upelelezi au uendeshaji wa mashtaka ya jinai naofisa huyo anatakiwa kutii maelekezo hayo.

Mheshimiwa Spika,Ili kumwezesha Mkurugenzi wa Mashtaka kutekeleza wajibuwake wa kikatiba kwa uhuru kamili na bila woga auupendeleo, Mkurugenzi wa Mashtaka amewekewa kinga yaajira yake. Kwa mujibu wa kifungu cha 19(1) na (2) cha Sheriaya Utumishi wa Mashtaka ya Taifa, sifa, masharti na mafaoya ajira ya Mkurugenzi wa Mashtaka yatakuwa sawa _ay a_eya ajira ya Jaji wa Mahakama Kuu.

Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 19(3), Mkurugenzi waMashtaka hawezi kuondolewa kwenye madaraka yakeisipokuwa kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kwa sababuya ugonjwa au kwa kukiuka Kanuni za Maadili ya Kitaalumaya Maafisa wa Sheria, Mawakili wa Serikali na WanasheriaWalioko kwenye Utumishi wa Umma chini ya Sheria yaUtekelezaji wa Mamlaka ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali, Sura ya 268 ya Sheria za Tanzania.Hii ndio kusema kwamba, kwa mujibu wa Sheria Na. 27 ya2008, utaratibu wa kumwondoa Mkurugenzi wa Mashtakakwenye ajira yake hauna tofauti na utaratibu wakumwondoa Jaji wa Mahakama Kuu kwenye ajira yake.

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba utaratibuhuu wa kikatiba na kisheria umempa Mkurugenzi waMashtaka nyenzo za kutosha kisheria za kupambana na uhalifumkubwa hapa nchini na vile vile kuzuia matumizi mabayaya mfumo wa uendeshaji na utoaji haki na hasa hasa yamfumo wa mashtaka ya jinai. Licha ya kuwa na mamlakana kinga hizi za kisheria, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtakaimeshindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

201

Hii inathibitishwa na kitendo cha kutowachukulia hatua zakijinai Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliasDavid Bashite kwa vitendo vya kijinai alivyofanya katikauvamizi wake wa Clouds Media Group. Inathibitishwa piana kitendo cha kushindwa kuwachukulia wale wotewaliteka waTanzania na kuwatesa kama ambavyotumeelezea humu kwa kirefu; na wale waliomtishiaMheshimiwa Nape Nnauye silaha hadharani mbele yawaandishi habari. Na hii inathibitishwa na kushindwa kwakekuchukua hatua za kijinai dhidi ya wale wote waliokulanjama za kumfungulia mashtaka ya uongo na kumfungaMheshimiwa Lijualikali.

Mheshimiwa Spika,Katika mazingira haya, Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bungelako tukufu inataka Mheshimiwa Waziri alieleze Bunge lakotukufu, kama bado Mkurugenzi wa Mashtaka anastahilikuendelea kushikilia nafasi hiyo muhimu wakati ni wazi hanauwezo wala nia ya kutekeleza majukumu yake ya kikatibana kisheria.

YA KAIMU JAJI MKUU

Mheshimiwa Spika,Mahakama ya Tanzania haina kiongozi wake kamili, yaaniJaji Mkuu. Hii ni kwa sababu, tangu Jaji Mkuu MohamedChande Othman astaafu tarehe Mosi Januari ya mwaka huu,Rais John Pombe Magufuli hajateua Jaji Mkuu mpya kuchukuanafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mkuu Chande Othman. Badalayake, Rais Magufuli amemteua Jaji wa Rufaa Prof. IbrahimHamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu.

Mheshimiwa Spika,Ibara ya 118(4) ya Katiba yetu, Rais anaruhusiwa kuteua KaimuJAji Mkuu iwapo itatokea kiti cha Jaji Mkuu kitakuwa wazi;au Jaji Mkuu hayupo Tanzania; na au Jaji Mkuu atashindwakutekeleza kazi yake kwa sababu yoyote, na Rais ataonakuwa kwa muda wa tukio lolote kati ya hayo matatu inafaakumteua Kaimu Jaji Mkuu. Kaimu Jaji Mkuu aliyeteuliwa kwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

202

utaratibu huu “... atatekeleza kazi za Jaji Mkuu mpakaatakapoteuliwa Jaji Mkuu mwingine....”3

Mheshimiwa Spika,Pamoja na kuwapo kwa ibara ya 118(4), Kambi Rasmi yaUpinzani ya Bunge lako tukufu inaamini kwamba Rais Magufulianavunja Katiba ya nchi yetu kwa kushindwa kuteua Jaji Mkuukamili takroban miezi mitano tangu kustaafu kwa Jaji MkuuChande Othman. Hii ni kwa sababu, ibara ya 118(4)haikutungwa kwa lengo la kumwezesha Rais kuteua KaimuJaji Mkuu bila kikomo cha muda.

Kama ilivyo kwa sheria zote, ibara ya 118(4) ina sababu yakemaalum. Ibara hiyo imewekwa kwa makusudi ya kuhakikishakwamba kwa muda wote kunakuwa na kiongozi waMahakama ya Rufani ya Tanzania pamoja na kiongozi waMahakama ya Tanzania, wakati Jaji Mkuu kamili anasubiriwakuteuliwa. Kaimu Jaji Mkuu ni sawa ni kile kinachoitwa nawanasheria ‘interlocutory position.’ Kaimu Jaji Mkuu ni nafasiya muda inayoshikiliwa na mtu mwenye sifa za kuwa JajiMkuu kabla nafasi hiyo haijajazwa na Jaji Mkuu kamili.

Swali halali linahitaji majibu ni, je, Kaimu Jaji Mkuu anastahilikuwapo madarakani kwa muda gani? Hili ni suala la tafsiriya Katiba linalohitaji kujibiwa na Mahakama. Kwa maoni yaKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, miezi mitano ni muda mrefumno wa kuwa na Kaimu Jaji Mkuu. Hii ni kwa sababu, katikahistoria yetu yote tangu uhuru, haijawahi kutokea Rais wanchi yetu akashindwa kuteua Jaji Mkuu kamili kujaza nafasiiliyo wazi ya Jaji Mkuu.

Mheshimiwa Spika,Bunge lako tukufu, kama mmojawapo wa mihimili mikuu yadola ya Tanzania, lina kiongozi wake mkuu muda wote: Spikaau Naibu Spika. Serikali, kama mhimili mwingine mkuu, inakiongozi wake mkuu muda wote: Rais au Makamu wa Rais.Kwa Mahakama ya Tanzania, mhimili mkuu wa tatu wa dolaya Tanzania, kutokuwa na kiongozi wake kamili miezi mitanobaada ya kustaafu kwa Jaji Mkuu Chande Othman, kunatoa

3Ibara ya 118(5) ya Katiba

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

203

taswira potofu kwamba Mahakama ina hadhi hafifu au yachini ikilinganishwa na mihimili mingine mikuu ya dola yaTanzania.

Kitendo hiki vile vile kinatoa taswira potofu kwamba pengineKaimu Jaji Mkuu wa sasa hatoshelezi nafasi hiyo; au kwambamiongoni mwa Majaji wote wa Rufaa au wa MahakamaKuu ya Tanzania au mawakili na wanasheria wengine wanchi hii pamoja na wale wa nchi za Jumuia ya Madola hakunahata mmoja wao mwenye uwezo au sifa za kuwa Jaji Mkuuwa Tanzania.

Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu inamtakaMheshimiwa Waziri amshauri Rais Magufuli, kwa heshima zoteanazostahili, amthibitishe Kaimu Jaji Mkuu Prof. Juma katikanafasi hiyo au, vinginevyo, ateue mwanasheria mwingineanayemwona ana sifa za kuwa Jaji Mkuu kamili wa Tanzania.Hali ilivyo hivi sasa inawatia aibu wanasheria wote waTanzania na inaitia aibu nchi yetu katika jumuia ya kimataifa.

Mheshimiwa Spika,Naomba nimalizie maoni yangu haya kwa kusemayafuatayo. Watanzania hawastahili Serikali ya aina hii. Kamaalivyosema Baba wa Taifa katika kitabu chake Uongozi Wetuna Hatima ya Tanzania: “Hatulazimiki kuendelea na uongozimbovu wa Chama na Serikali. Wala tukiendelea na hali hii,bila kubadili uongozi wa Chama na Serikali, sina hakika kamatutafika huko salama. Masuala muhimu ya nchi yetuhayatashughulikiwa.... Na masuala mengine muhimu ...yataachwa yajitatue yenyewe. Nasema katika hali kama hiyosina hakika kama tutafika salama; na tukifika salama tukiwana uongozi huu huu wa Chama na Serikali mbele kutakuwani giza tupu. Majuto ni mjukuu, huja baadaye.”

Tundu Antiphas Mughwai LissuMSEMAJI & WAZIRI KIVULI, SHERIA NA KATIBA

KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI25/04/17

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

204

MWENYEKITI: Sasa baada ya kusema hayo, nasitishashughuli za Bunge hadi saa 11.00 jioni.

(Saa 7.24 Mchana Bunge lilisitishwa hadi saa 11.00 Jioni)

(Saa 11.00 Jioni Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae.

Waheshimiwa Wabunge, ili kuweka mambo sawakwa madhumuni ya kumbukumbu za kudumu za Bunge letu.Nilitoa uamuzi kwamba katika hotuba iliyotolewa na Kambiya Upinzani maeneo yote ambayo mapema wakati wahotuba ya Waziri Mkuu yalikuwa yameondolewa nayamerudiwa tena katika hotuba hii yasiwepo. Kwa kuwahata mwasilishaji wa taarifa ya Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni wakati anahitimisha hoja yake hakusema kwambahotuba yake yote iingie kwenye Hansard, maelekezo yanguni kwamba maeneo yote ambayo yana ukakasi ambayoyanatokana na uamuzi huo hayataingia kwenye Hansardpamoja na yale aliyoanza nayo ya utangulizi ambayo nilisemamoja kwa moja hayataingia. (Makofi)

Baada ya kusema hayo, sasa tuendelee na hatuamuhimu ya ninyi kuijadili hoja hii. Naombeni tuongee kwastaha tu, unafahamu ninyi kama viongozi wa nchi hii,unaweza ukajenga hoja yako ujumbe ukafika kwa lugha yastaha tu bila hata kumtukana mtu au kufanya nini. Hilo ndiloombi langu kwenu Wabunge. Nashukuru sana.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuombamwongozo wako na kwa lugha hizohizo za staha na zautaratibu sana ndiyo najielekeza huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikumbukwe kwamba leowakati wa mchana hapa Mbunge alitoa hoja juu ya sualazima la kumchangia mrembo ambaye atatuwakilisha katika

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

205

shughuli huko anakokwenda. Hata hivyo, ikumbukwekwamba Wabunge wengi kabla ya kutuhoji tulioonesha hisiazetu tena kali kwamba sisi hatutaki tukatwe fedha hizi.Tumekwenda katika maelezo mbalimbali ya kukisihi Kiti,kukipembejea Kiti, kukiomba Kiti kwa lugha za staha sana,kwa wingi wa upande mwingine Kiti kikasema jambo hililimepita fedha hizi zitakatwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mwongozo wakokama mtu jambo hili limeingia ndani ya imani yake na halitakina hasa kipindi hiki ambacho hata Mheshimiwa Khatibalisema kwa nini tulazimishwe? Naomba mwongozo wako,hatupendi tuvutane katika mambo mengine maanatukienda hivi itakuwa hatufiki tunakokwenda. Wewemwenyewe umesema hapa tutumie lugha nzuri, lugha zastaha, lugha za kufahamiana kwa hil i tutakuwahatufahamiani lazima nikwambie kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mwongozo wakojambo hili uliondoe kabisa mtu kuchangia iwe ni hiari.Naomba Mwongozo wako wa ziada. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Masoud wewe ni mzoefuwa Kanuni, Bunge limehojiwa likaamua. Mimi naombatuheshimu uamuzi huo.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Mnisikilize basi, mnisikilize kwanza.

WABUNGE FULANI: Sawa.

MWENYEKITI: Kwamba uamuzi wa Bunge wa wengiutabaki kama ulivyo. Mbunge mmojammoja kwa viletunajua utaratibu unaofuata baada ya hapo uendeukamuone Katibu wa Bunge ukaelezee ya kwako maanatusiingize humu suala la imani ya dini kwa suala ambalotunajua tukifika huko tutaanza kutoka kila mmoja na njiayake humu. Kwa hiyo, nasema uamuzi unabaki palepale

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

206

lakini kama unadhani kwamba ni hiari ya moyo pamoja nauamuzi huo basi wewe fika kwa Ofisi ya Katibu wa Bungeukaelezee tatizo ulilonalo. Huo ndiyo uamuzi wangu. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, uwiano wa wachangiajiwote mnaujua kwa kambi na majina yako hapa,tusisingiziane muda wenyewe ndiyo huo. Naanza na hawawawili ambao wamekubaliana kugawana dakika zaotanotano, maana nafasi zilizopo hapa ni CHADEMA Mbungemmoja, CUF Mbunge mmoja, CCM Wabunge wanne, ndiyouwiano huu kwa mjadala huu. Kwa hiyo, nasema hawaambao wamegawana dakika zao kumi naanza naonimalizane nao. Mheshimiwa Sabreena, dakika tanoatafuatiwa na Mheshimiwa Kubenea dakika tano.

MHE. SABREENA H. SUNGURA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa dakika chache nilizopata, lakini namwombaMwenyezi Mungu niweze kuzitendea vyema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu napendakujielekeza kwenye suala zima la usafirishaji wa binadamuambao ni Watanzania kwenda nchi za nje kufanya kazi nawengi wao wamekuwa wakiuawa na clips zinatumwa hapanchini, zinazagaa kwenye mitandao ya kijamii, sisi kamaWabunge tunaona, Serikali imekaa kimya haisemi jambololote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali hii ni hatari kwa sababuhawa wanaofanya biashara hii ya kusafirisha binadamu kwamaana ya human trafficking na kuwapeleka hukowanakwenda kuuawa kinyama, kwa nini Serikali haifanyimsako maalum wa kuhakikisha inawakamata? Vijana wetutena vijana wa kike wanakwenda huko wanafanyiwaunyama lakini Serikali imekaa kimya. Tunataka tamko leolitoke, ni hatua gani zimechukuliwa kubainisha watuwanaosafirisha wasichana wa Kitanzania bila ridhaa amakwa ridhaa lakini kwa udanganyifu. Wanakwenda kwawazazi wanawahonga dola 200, 300 wanawaambia kijana

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

207

wako anakwenda huko atafanya kazi nzuri supermarket,wapi, akifika kule anadhalilika anauawa, Serikali inasemajijuu ya hili? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalonapenda kulizungumzia ni conflict of laws. Nchi yetu inatabaka za watu mbalimbali, kuna mila na desturi mbalimbali.Sheria zetu zimeingia kwenye mgongano, tuna Sheria yaMirathi lakini pia tuna Sheria ya Ndoa, tunayo IslamicRestatement Act lakini pia tunayo Sheria ya Kimila ambayoni Customary Declaration Order ya mwaka 1963.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi sheria zinakinzana, kunasheria ambayo inamtambua mtoto ni kuanzia umri wa miaka21 lakini kuna sheria inayosema mtoto mwisho wake itakuwani miaka 18, lakini kuna sheria za Kiislamu zinazosema mtotomwisho wake ni pale anapobalehe. Sasa linapokuja sualala mtoto aolewe ama aozeshwe kwenye umri gani ama aoekwenye umri gani kuna mwingiliano wa mila, desturi, dini nasheria. Je, mambo haya tunakwenda nayo vipi? Ni lazimamijadala ya kina ifanyike ili kuhakikisha kwamba pande zotezinabaki bila dukuduku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi siungi mkono ndoa zautotoni, naunga mkono wanaopendekeza watoto waolewekuanzia umri wa miaka 18. Hata hivyo, kuna watoto ambaona wenyewe wanaingia kwenye mapenzi kabla ya umri sualaambalo linapelekea ubebaji wa mimba. Sasa mtoto yulealivyopata mimba kwenye umri wa miaka 13, 14 ni mzazigani atakayekubali kuona mtoto wake mwenye umri huomdogo anakaa nyumbani na anazalishwa, hapohapo sheriazetu haziwaruhusu watoto hao kuendelea na shule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tukubaliane,kama tutaamua mtoto aanzie umri wa miaka 18 aweze kuoana kuolewa, je, mtoto anayepata ujauzito kabla ya miakahiyo status yake itakuwaje? Kama tutakubaliana miaka 18basi kuwe kuna exception, kama atapewa ujauzito kablaya hapo aruhusiwe kuozeshwa kwa sababu kuna watuambao mila zao kukaa na binti nyumbani mama yake mzazi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

208

anapata ujauzito na mtoto anapata ujauzito ni matusi.Naomba hili lifanyiwe kazi kwa namna ya kipekee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia napenda kuzungumziasuala moja, tunayo Sheria ya Probate and Administration ofEstate Act ya Tanzania ambayo inaunda Waqf Commission.Wenzetu wa Zanzibar tayari wana Waqf Commission na watuambao wanataka mali zao zigawanywe kwa mtindo huowanakwenda kwenye Waqf Commission wanapelekamapendekezo yao na yanafanyiwa kazi. Kwa upande wetuwa Tanzania Bara tume hii ipo kwenye sheria lakini haijawahikuundwa toka uhuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunataka majibu kutokakwa Mheshimiwa Waziri, ni l ini Serikali itaunda WaqfCommission kwa upande wa Tanzania Bara ili wale ambaowanajisikia kupeleka mali zao pale ambazo zitakuja kusaidiavizazi vinavyokuja basi waweze kuzingatiwa na wawezekufanya hivyo kwa mujibu wa sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, umuhimu wa hili ni nini?BAKWATA imekuwa na malalamiko mengi sana, watu wengihapa nchini hawana imani na BAKWATA hususan Waislamwengi hawana imani na BAKWATA. BAKWATA wanauza maliza Waislam, BAKWATA wanaingia kwenye migogorowamewauzia akina Yussuf Manji mali za Waislam, kesi, vita,ngumi kila siku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini sasa msitengenezehii Waqf Commission ambayo itatoa sasa mali hizi ambazozinawekwa kwenye mikono ya watu ambao kwa kiasi fulanihawaaminiki ziweze kuwa kwenye mfumo wa Serikali ili…

T A A R I F A

MHE. ALHAJ ABDALLAH M. BULEMBO: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Sabreena, taarifa, kaakidogo. Taarifa Mheshimiwa Alhaji Bulembo.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

209

MHE. ALHAJ ABDALLAH M. BULEMBO: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa, msemaji anasema Waislam hawanaimani na BAKWATA ana ushahidi gani? Ni Waislam wapi, niMsikiti gani, tunaomba ushahidi uwepo Mezani. BAKWATA nitaasisi iliyosajiliwa, BAKWATA ni taasisi ambayo ina Waislamwanaoamini, naomba aweke ushahidi Mezani asigonganishedini kwa imani yake yeye. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Kweli.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Sabreena taarifa hiyoumepewa.

MHE. SABREENA H. SUNGURA: Mheshimiwa Mwenyekiti,namsikitikia sana Mbunge mwenzangu aliyesimama, kamani Mtanzania ambaye anafuatilia vyombo vya habari naanafuatilia habari za kila siku katika nchi hii hawezi kuhojiBAKWATA kwamba haikubaliki na kundi kubwa la WaislamTanzania. Kwa hiyo, hilo ni jibu ambalo linamtosha kamahalijatosha aje nitampa research na mifano ya kesi ambazoBAKWATA wameuza mali za Waislam, kitu ambachokinapelekea vita nchi hii. (Makofi)

MWENYEKITI: Unaikubali au unaikata?

MHE. SABREENA H. SUNGURA: Kwa hiyo, napendekezakabisa kwamba Waqf Commission iundwe kama ilivyoZanzibar ili hawa waporaji ambao wamejificha kwa mgongowa BAKWATA suala hilo liweze kwisha na lipatiwe muafaka.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kugusia sualazima la migogoro ya kazi katika chombo chetu chaCommission of Mediation and Arbitration. Chombo kiletumekianzisha ili kiweze kupunguza mrundikano wa kesi zalabour hususan katika mahakama zetu kuu. Hata hivyo,nasikitika kusema kwamba, majengo yake hayatoshi ku-accommodate wateja wanaokwenda pale. Ukienda paleunakuta makundi ya watu yamekaa kwenye vyumbavidogovidogo, kelele, hata wale wanaosikiliza mashauri

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

210

hawawezi kuelewana, joto, giza, mrundikano wa watu,mpaka watu wengine wanafanya kupangiwa …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Kubenea.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nami nakushukuru kwa kunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri Mkuu, MheshimiwaKassim Majaliwa wakati anazungumza Bungeni akijibu swalila Kiongozi wa Upinzani, alisema Serikali yetu hii tuiamini sanaifanye uchunguzi wa mambo haya ya utekaji na utesaji nasisi humu ndani ukiuliza nani haiamini hii Serikali hayupoatakayetokea. Kwa sababu Serikali hii ni yetu sote ndiyomaana tuko hapa tunaisimamia Serikali, tuko hapatunaishauri Serikali, lakini Serikali inayotaka kuaminika nilazima iwe wazi. Hivi kwa mfano mtu aliyetaka kumpiga risasiMheshimiwa Nape hajulikani, Serikali haimjui, kama inamjuabasi ijitenge naye, kama haimjui iseme, lakini tunavyojuaSerikali inamjua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna makosa ya kijinaiyametendwa katika nchi hii na watendaji wa Serikali.Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameingiakwenye chumba cha habari akitumia silaha, kwa mujibu washeria zilizopo ule ni unyang’anyi, wizi wa nguvu. Amekwendakupora CD za chumba cha habari…

MBUNGE FULANI: Una ushahidi?

MBUNGE FULANI: Ndiyo.

MHE. SAED A. KUBENEA: Kamera zimeonesha, Tumeya Mheshimiwa Nape Nnauye imeripoti. Ripoti ya Tume yaMheshimiwa Nnauye imeundwa na waandishi wa habari naimekuwa submitted kwa Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

211

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu anayetenda jinai, DPPyuko pale, moja ya majukumu yake ni kuendesha kesi za jinaimahakamani, lakini pia kuangalia ni nani anayetenda jinaikuagiza DCI wafanye uchunguzi, hiyo ndiyo kazi ya DPP. SasaDPP yupo amenyamaza, polisi wapo wamenyamaza. Mtuanatumia jina ambalo sio lake, ametenda makosa mengineyenye adhabu ya zaidi ya miaka 30 gerezani. Watuwamekwenda mpaka Kolomije, wamekwenda nyumbanikwao kijijini kwake wamezungumza na mama yake, vyombovya habari vimefika huko, Waziri Mkuu anasema tuiaminiSerikali, tunaiamini kweli lakini Serikali lazima iwe wazi iachedouble standards. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watumishi wa ummakwenye nchi hii wamefukuzwa kazi wengine wameshtakiwawamefungwa lakini mtu mmoja anaitwa Paul Makonda jinalake Daudi Bashite anaachwa kwa sababu gani, who isMakonda? Mtu anaingia kwenye chumba cha habari akiwana silaha za moto na polisi, who is Makonda? Halafu Serikaliinasema iaminike, waandishi wa habari wanafanya kazikwenye mazingira magumu halafu Waziri wa Habariananyamaza, inasikitisha. Waziri wa Habari ananyamaza,ameona waandishi wa habari wananyanyasika kwenye nchihii anatetea uhalifu halafu anasema tuamini Serikali,tunaaminije? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna makosa zaidi ya nanewanasheria wanasema. Rais wa Chama cha Wanasheriayuko humu ndani, TLS haichukui hatua dhidi ya Makonda,Tume ya Haki za Binadamu haichukui hatua dhidi yaMakonda halafu mnasema Serikali tuiamini. Bungelimenyamaza linapigwa pini, linapigwa kufuli lisimzungumzieMakonda, jamani, halafu mnasema tuamini Serikali, Serikaliinaaminikaje ikiwa imejifunika kwenye blanketi. Kutoa silahahadharani ni kosa la jinai. Leo Kamishna Siro amesema nikosa la jinai, Mheshimiwa Nape ametolewa silaha hadharani.Juzi watu wametoa silaha hadharani, aliyetoa silahaMheshimiwa Nape anamjua, dunia inamjua, vyombo vyahabari vinamjua, waandishi wa habari ndio waliozuia…(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja ya Kambi ya Upinzani, nashukuru sana.(Makofi)

MWENYEKITI: Tunaendelea na msemaji wetu waChama cha Wananchi CUF, ni Mheshimiwa Riziki ShahariMngwali.

MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru na nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu,Muumba wa mbingu na ardhi ambaye kwa matakwa yakemwenyewe ametuchagua sisi kuwa miongoni mwa wajawake ambao amewatunuku uhai na uzima na akili timamuna akawajalia pia kufanya kile ambacho wamejipangiawenyewe kukifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa imani ya dini yangu,katika mambo ambayo tunaambiwa tuyafanye kwa wingisana ni kukumbushana kwa sababu katika kukumbushahutoa msaada kwa wale wenye kuamini. Nami nalifanya hilonikiamini kabisa kwa dhati ya moyo wangu kwamba nyumbahii imejaa wenye kuamini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kitabu ambacho kwadini yangu nakiamini, Kitabu cha Quran, kuna aya ya 54 ikokatika Sura ya 36 na sura hii kwa jina lake mahsusi inaitwa“Surat Yaseen” na kwa hadhi yake hii sura ndiyo inaitwa ndiyomoyo wa Quran. Katika hiyo aya ya 54 inasema:-

“Iangalieni i le siku ya hukumu ambapohaitadhulumiwa nafsi chochote na wala haitolipwaisipokuwa yale ambayo imeyatenda”. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niliseme hili kamatahadhari kwetu sisi sote, iko siku ambayo hakuna chochote

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

213

ambacho tutaulizwa isipokuwa kile ambacho tumekitendahapa. Kwa imani ya dini yangu, maisha ya kila siku,mahusiano yetu, kusoma kwetu, kuwa Wabunge kwetu yotehaya yataulizwa siku hiyo na hayo ndiyo katika hayo ambayotunayatenda. Kwa hiyo, naomba nitoe hiyo tahadhari nanimwombe Mwenyezi Mungu ashuhudie kwambanimewakumbusha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kuchangia kwakusema kwamba naunga mkono hoja hotuba hii ya WaziriKivuli wa Kambi ya Upinzani lakini pia mengi yaliyomo kwenyetaarifa ya Kamati ya Katiba na Sheria hususani yale ambayoyameelezwa ukurasa wa 18 na 19 kuhusu msisitizo wakuangalia masuala mazima ya haki za binadamu hasayakiendana na namna ambavyo vyombo vya kutoa sheriaikiwemo Mahakama vinavyotakiwa vitende haki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi sitaki kuhojiMahakama zinafanyaje kazi lakini nataka kuhoji sera za nchihii, sheria na taratibu kuhusu masuala ya haki za binadamu.Mheshimiwa Waziri amesema hili na Kamati imesema naWaziri Kivuli amesema namna gani kesi zinacheleweshwa,namna gani mahabusu na wafungwa wanateseka katikanchi hii lakini tumenyamaza kimya au hatuchukui hatuainavyostahiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Mashekhe ambaowanaoza mahabusu kwa miaka minne sasa ambapo sualalao linapigwa danadana hilo sijui kama siyo suala la haki zabinadamu au siyo katika zile kesi ambazo taarifa zote hizizimesema lazima masuala ya upelelezi yakamilishwe katikawakati ambao ni reasonable. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana Mheshimiwa Waziri huyuambaye yuko leo na hoja yake Mezani lakini jana alikuwaanatupa utaalam kama Profesa wa Sheria, alipokuwaanazungumzia Sheria ya Ndoa alisema kwamba, kuna kitukinaitwa legal anthropology. Ombi langu ni kwamba hii legalanthropology sipati maneno sahihi lakini ninachotaka

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

214

kusema ni kwamba isiangalie tu masuala ya abstract, zilevalues ambazo huzioni, lakini pia iangalie masuala ambayoni real and tangible, yale unayoyaona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili, inapokuja sualala dini, viongozi ni katika values hizo. Sasa tunapoonaviongozi wetu wa dini wanadhalilika, wananyanyasika kwamiaka nenda, rudi, mjue mnatukwaza kiimani namnateteresha hivyo vitu ambavyo mnasema legalanthropology inaviangalia kwa umakini sana. Kaka yanguMheshimiwa Profesa Kabudi utanisamehe huko mwishonikama nitashika shilingi ya mshahara wako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Profesa Kabudikama ambavyo Waziri Kivuli amesema hapa kwenye ukurasawa nne kwamba hakuna shaka yoyote kwamba Ripoti yaTume ya Warioba na Rasimu ya Katiba Mpya ina alama zavidole vya kitaalam vya Profesa Kabudi, ni kweli.Ninachoongeza tu ni kwamba alikuwa ana wasaidizi wakekama proof-readers wake, wanawake wawili, mmojanapenda nimtaje Mheshimiwa Kibibi Mwinyi Hassan,mwingine kwa leo nahifadhi jina lake, walifanya kazi ile kwakukesha, tukatoka na document zile na mimi nilibahatikakuwa katika Tume ya Warioba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ripoti ile haikuzumngumziatu pendekezo la Katiba Mpya lakini kuna masuala kadhaaya kijamii, kisheria, kitaratibu ambayo Tume ya Wariobailiandaa kwa volumes na zikakabidhiwa Serikalini. Laitimchakato ule ungefikishwa mwisho haya mambo yote hapatunayozongwazongwa nayo sasa hivi yasingekuwepo.Taratibu zingekaa sawa, Katiba Mpya ingepatikana masualayote haya tunayosema huyu asitajwe, huyu asifanywe hiviyalishajadiliwa na wananchi kwa kina kabisa mpaka sualala viroba na zile suruali ambazo vijana wetu wanavaa,wananchi walilisema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kamatungeupeleka mchakato mpaka mwisho wake yale yoteyasingekuwa issue sasa hivi, lakini imekuwa hivyo kwa sababu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

215

suala la Katiba Mpya limekuwa kizungumkuti, sasa sijuinikisema limepigwa kaputi nalo nitaambiwa msamiati siyo,lakini ni katika lahaja tu na nadhani Waziri anayehusika nautamaduni alisimamie hili. Lugha yetu ya Taifa ni Kiswahili,tutumie utajiri wa lugha hii, tutumie lahaja ambazo zinaletaladha masikioni, lugha ina ladha yake masikioni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala hilo la KatibaMpya masuala ya maadili ya kijamii, mila na desturi zetu,tunu hizi za Taifa ikiwemo lugha yetu, uongozi na mihimilihasa mihimili hii mitatu versus masuala ya vyama vya siasayamefanyiwa kazi vizuri kabisa. Wananchi walisema hatutakikumuona Spika ambaye ni m-NEC, hatutaki kumwona Raisambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Siasa na walitaja kwavitu specific lakini hatukulifanyia kazi sasa hivitunahangaishana hapa kila kinachosemwa kinaambiwasicho, kila kinachoandikwa kinaambiwa kifutwe, lakini kilekisu cha jana kile kwa bahati mbaya kimebaki humu nakinaendelea kutesa watu, mimi sijui kisu gani. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia humu asubuhihaki ya msingi kabisa ikitetereshwa ambayo ni haki yakujieleza. Hivi Mbunge, Waziri Kivuli anapozongwazongwa,anapokatazwa kueleza kile ambacho yeye ana imani nachoinashangaza. Mimi nitashangaa sana ikiwa Mawaziri Vivuliwa Kambi hii watarudia yale hotuba za Mawaziri wa upandeule itakuwa kituko! Yule Waziri akisema tumefanya kila kituna Waziri Kivuli naye aseme Serikali ile imefanya kila kitu,itakuwa kiini macho gani hicho? Hebu tupewe haki hiiambayo tunaizungumzia hapa, haki za binadamu, utawalawa sheria uachwe utekelezwe katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kaka yangu MheshimiwaProfesa Kabudi amevishwa viatu au sijui amevishwa kilembahiki ambacho inabidi akifanyie kazi sawasawa. Namshauriasisite kushauri mamlaka husika kuhusu utawala wa sheriaunavyotakiwa kufanya kazi kwa sababu sasa hivitumefikishwa mahali ambapo hatujui twende kwa sheria aukwa matamko.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

216

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria inasema, vyama vyasiasa vipewe ruzuku vifanye kazi, vifanye shughuli za kisiasaikiwemo mikutano ya hadhara. Matamko yanasema, hakunakufanya kazi za siasa, hakuna mikutano ya hadhara mpakatarehe fulani, kipi ni kipi? Hii haifai na haikubaliki katika nchiambayo tunasema tunafuata utawala wa sheria, tunademokrasia ya vyama vingi lakini zaidi tunasema kila sikutuombeane dua, tuombeane Mungu, hatuwezi … (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na wachangiajiwafuatao; Mheshimiwa Almas Athuman Maige atafuatiwana Mheshimiwa Kiteto Zawadi Koshuma na Mheshimiwa EsterMichael Mmasi ajiandae.

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa fursa ya kuchangia Wizara hiiya Sheria na Katiba. Kabla ya kuanza kuchangia, naombaku-declare interest kwamba mimi taaluma yangu ni ya ulinzina usalama katika sekta binafsi lakini vilevile nina kampunikubwa ya ulinzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipeleka kwa Katibu waBunge Muswada Binafsi kama ilivyo katika Kanuni yetu ya81(1)(2) na (3), Toleo la 2016. Baada ya kupeleka Muswadawangu binafsi katika Ofisi ya Katibu wa Bunge alinijibu rasmikwamba Muswada ule ulikuwa ni mzuri na Serikali iliuchukuaMuswada huo kwa nia ya kuuleta tena Bungeni baada yakutimiza kanuni za kuleta Muswada Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, makampuni binafsi ya ulinziyalianza mawili tu mwaka 1980 lakini leo yapo makampunikaribu 850, yameajiri askari walinzi wengi zaidi ya mara tanoau mara sita ya Jeshi la Polisi. Makampuni haya yanafanyakazi nzuri sana ya kulinda raia na mali zao lakini hayanamiongozo, kanuni, sheria na wala hayana mamlaka binafsiya kuongoza makampuni haya kama il ivyo kule njeyalikotokea.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

217

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilifungua milango yasekta ya ulinzi binafsi hapa nchini na ikafungia nje sheria zakuyaongoza makampuni haya. Suala hili limekuwa ni tatizokwani makampuni haya yana silaha, yanavaa sare kama zajeshi, yanacheza gwaride, yanafuata kanuni za kijeshi nayameajiri wataalam kutoka nje ya nchi wenye taalumakubwa ya kijeshi. Hatuwezi kuyazuia tena makampuni hayahapa nchini yasifanye kazi kwa sababu kila kwenye uwekezajimkubwa makampuni haya yapo na yanafanya kazi nzurisana, tunachoweza kufanya ni kuyadhibiti makampuni hayabinafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, makampuni haya hayawezikudhibitiwa bila sheria. Ni lazima Sheria inayoitwa PrivateSecurity Industry Act or Bill iletwe Bungeni ipitishwe. Hukoyalikotokea makampuni haya kote, wenzetu Kenya, Uganda,Afrika Kusini, Uingereza, Marekani, Ulaya ziko sheria namamlaka ya sekta ya ulinzi binafsi. Sheria ile niliyoleta mimikama Muswada Binafsi ilizingatia kuanzishwa kwa mamlakaya sekta binafsi ya ulinzi. Nia ile na sababu hiyo haijafutika.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda Mheshimiwa Waziriatakapokuja hapa, ajaribu kulieleza Bunge lako kamamaslahi na madhumuni ya kuwepo sheria sasa yamefutikaau mchakato wake umefikia wapi ili tujue tuweze kudhibitimakampuni haya ya ulinzi binafsi yaweze kulipa kodi navilevile yanaajiri watu kinyume na kanuni. Kule kwenyeMahakama ya Kazi, robo tatu ya kesi zote ni za makampuniya ulinzi, inakuwa kama ile Mahakama ya Kazi imeandaliwakwa sababu ya makampuni ya ulinzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile makampuni hayayanatumia sheria ya kiraia, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kaziniya mwaka 2004. Sheria hii ni ya kiraia na imepigwa marufukumajeshini kote. Hairuhusiwi kutumika Polisi, JWTZ, Magerezawala Immigration. Sheria hii kutumika katika sekta ya ulinzibinafsi inaenda kinyume na inashindwa kuyadhibitimakampuni hayo. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

218

Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria hii inaruhusu migomo.Hebu tufikirie ikatokea siku makampuni ya ulinzi yamegomaau wafanyakazi wa kampuni za ulinzi wamegoma,wakaacha malindo wazi na wana silaha mikononi,itakuwaje? Naomba Waziri atakapokuja hapa aeleze Bungelako hili amefika wapi na Sheria hiyo niliyoipendekeza yaSekta ya Ulinzi Binafsi yaani Private Security Industry Act or Billpamoja na pendekezo la kuanzishwa Private Security IndustryAuthority.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo niendekwenye Idara ya Mahakama. Waziri wa Sheria hapamwanzoni alisema kwamba wangependa kila Kata iwe naMahakama. Kule kwetu Tabora Kaskazini (Uyui) kunaMahakama ya Mwanzo ina kila kitu, Mahakama ipo, inamabenchi, jengo zuri la Mahakama, nyumba nane zawafanyakazi wa Mahakama lakini imetelekezwa, huu nimwaka wa 10 haifanyi kazi. Watu wameiba milango namadirisha yaliyojengwa kwa thamani kubwa na mpaka sasasijui sababu ni nini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu nimekuwa Mbunge,wananchi wananiuliza imetokea nini Mahakamaikatelekezwa na kuna kesi nyingi. Juzi juzi kumetokea kesi yamauaji kule Tabora, Uyui ndiyo inaongoza kwa kesi mbayaza mauaji, wizi na kadhalika lakini Mahakama ya Mwanzoimefungwa. Nimeona katika hotuba yake Mheshimiwa Wazirianaongelea kujenga Mahakama za Mwanzo katika maeneombalimbali, lakini Mahakama ya Mwanzo katika Kata yaUpuge, Wilaya ya Uyui, Mkoa wa Tabora imesimama nahaifanyi kazi na majengo yanabomolewa tu wananchiwanachukua kama shamba la bibi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba atakapokujaMheshimiwa Waziri kuhitimisha hoja yake ya bajeti, anielezekimetokea nini mpaka Mahakama ya Mwanzo inayotakiwasana kutelekezwa. Pia anieleze majengo yale yafanywejesasa, maana watu wanaingia na kuiba milango kama hainamwenyewe. Mimi ningeshukuru Mahakama ile ingeanzishwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

219

tena kwa sababu kesi za kutosha zipo, lakini kama kunasababu iliyofanya Mahakama ile ifungwe naomba nielezweili nikawaambie wananchi wangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuniruhusu kwaheshima kubwa, nakushukuru sana na niwaachie wenzanguwachangie. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Maige Almas.Mheshimiwa Kiteto Zawadi Koshuma na Mheshimiwa EsterMichael Mmasi ajiandae.

MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Mnamo tarehe 5 Mei, 2016nilisimama katika Bunge lako Tukufu kuwatetea watotoambao wanaolewa wakiwa na umri chini ya mika 15. Naminaomba niahidi kwamba nitaendelea na ari hii hii yakuwatetea watoto wa kike ambao wamekuwa wakipotezandoto zao wakiolewa katika umri mdogo sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na utangulizi huo,Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inaonekana ni sheria ambayoinambagua mtoto wa kike ambapo katika kifungu kile cha13 na 17, kinamtaka mtoto wa kike kuolewa akiwa na umriwa miaka 15 wakati mtoto wa kiume anaoa akiwa na umriwa miaka 18. Ukiangalia katika Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Ibara ya 13 nitanukuu, inasema:-

“(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayohaki bila ya ubaguzi wowote kulindwa na kupata haki sawambele ya sheria”.

(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa namamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakuweka sharti lolote ambalo lina ubaguzi wa dhahiri au kwataathira yake.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Sheria hii ya Ndoa yamwaka 1971 utaona ni kwa namna gani inakinzana naKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

220

kumbagua mtoto wa kike ambaye anatakiwa kuolewa naumri wa miaka 15 ilihali mtoto wa kiume anatakiwa kuoaakiwa na umri wa miaka 18 na kuendelea. Ni jukumu letusasa sisi kama wanawake na wawakilishi wa watoto wa kikena wanawake wote Tanzania nzima lakini tukishirikiana naWaheshimiwa Wabunge wote bila kujali rika na kujali jinsiakuwatetea watoto wa kike ili na wao pia waweze kutimizandoto zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaona madhara ya ndoayakiwemo ya kiafya. Watoto wengi wa kike wanapokuwawanaolewa na umri mdogo wa miaka 15, kiafya watotohawa wanakuwa hawajapevuka katika maumbile yao nahivyo basi kitu hiki kinasababisha watoto hawa wanapopataujauzito, hizo tunaziita ni mimba za utotoni kwa sababu zileni mimba ambazo bado yule mtoto hajapevuka maumbileyake na madhara makubwa ambayo yanatokea ni vifo vyaakinamama. Naamini kabisa Serikali haitapenda kuona vifovya wanawake vikiendelea kutokea ambavyovinasababishwa na sheria hii ya ndoa za utotoni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia madhara mengine yandoa za utotoni ni vifo vya watoto wachanga ambaowanazaliwa na akinamama ambao bado hawajapevuka.Kitu kingine, wasichana wanakosa elimu na kuna msemounaosema kwamba unapompa elimu mtoto wa kikeumesaidia jamii nzima, hili linaonekana wazi kabisa. WapoWaheshimiwa sasa hivi humu ndani wakiamua watoeshuhuda zao kwa kweli kila mtu atastaajabu. Basi ni jukumuletu sisi Waheshimiwa Wabunge kuiomba au kuishawishiSerikali iweze kutusaidia kurekebisha Sheria hii ya Ndoa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na madharaambayo yanawakuta wasichana, kwa sababu wasichanandiyo waathirika wakubwa, wanapoolewa na umri mdogo,kwa nini tunasema Sheria ya Ndoa ibadilishwe. Mchakatowa kuomba Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ifanyiwe

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

221

marekebisho haukuanza leo. Hivyo naamini kwamba Bungehili halitakuwa la kwanza kuishawishi Serikali kuletamabadiliko ya Sheria ya Ndoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchakato huu ulianzamwaka 1984 ambapo Umoja wa Wanawake Tanzaniawaliishauri Serikali kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria kwambaSerikali irekebishe Sheria hii ya Ndoa kwa sababu walizungukaTanzania nzima na wakaona kwamba watoto wengi wakike wanapata hasara kubwa sana wanapoolewa na umrimdogo. Kwa hiyo, utaona kwamba mchakato huuhaukuanza leo ulianza siku nyingi sana mwaka 1984 wakatisheria imeundwa mwaka 1971, mchakato huu ulianzamapema sana. Wanawake Tanzania waliona ni kwa namnagani watoto wa kike wanaathirika katika kuolewa na umrimdogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchakato huu pia mwaka1994 Tume ya Mabadiliko ya Sheria baada ya kupokea maonimbalimbali kutoka kwenye NGO’s mbalimbali walileta piamapendekezo yao. Kama ningepata nafasi ya kukuleteahapo mezani na wewe pia ukayapitia mapendekezo ya Tumehii ambayo ilishauri kwamba Serikali ifanyie marekebishoSheria hii ya Ndoa. Pamoja na changamoto zote ambazozinaonekana za kimila na za dini lakini bado Tume hii ilishauriSerikali kufanyia marekebisho Sheria hiyo ya Ndoa ilikuwanusuru watoto wa kike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia tumeingiamikataba mbalimbali ya kimataifa ukiwepo Mkataba waHaki za Watoto, Mkataba wa Kutokomeza Aina Zozote zileza Ubaguzi hapa Nchini Tanzania na kwingineko. PiaSustainable Development Goals inazingatia sanakutokomeza ndoa za utotoni ifikapo mwaka 2030. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, juzi juzi tu hapailitoka hukumu dada mmoja anayeitwa Rabeca Gyumialipeleka mapendekezo yake Mahakamani kuhusiana nakubadilishwa kwa Sheria hii ya Ndoa. Kama tunavyofahamuMahakama ndiyo sehemu pekee ambayo wanaweza

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

222

kutusaidia kutafsiri sheria na hapa ninayo nakala ya hukumu.Katika hukumu hii iliyotolewa na Mahakama inapendekezaSerikali kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali kubadilishaSheria hii ya Ndoa kile kifungu cha 13 na 17 ambachokinapendekeza umri wa mtoto wa kike kuolewa kuwa miaka15 na wa kiume kuoa akiwa na miaka 18. Kwa hiyo, hukumuimetoka ikieleza au ikiitaka Serikali kubadilisha vifungu hivyovya Sheria ya Ndoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa leo sina mengi sana yakuongea lakini naomba nihitimishe kwa kusema kwamba,sisi Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tukikaakimya bila kuwasemea watoto wa kike kwa kweli watuwengi huko nje watabaki wanatushangaa. Nasema hivi kwasababu nimekuwa nikifuatilia sana kwenye TV, wanawakewanalia na kutoa machozi tena wanabaki wanauliza, wakowapi wanawake wa Tanzania waweze kututetea watotowetu wasiolewe katika umri mdogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ndoa hiziwanaoathirika sana ni watoto wetu wa kike. Japokuwa kunajuhudi za Serikali ambazo kwa kweli zimeonekana na siwezikukataa kwamba juhudi za Serikali hazijaonekana. Tunaonamarekebisho ya Sheria ya Elimu ya mwaka 2016 ambayoinataka watoto wasiolewe chini ya umri wa miaka 15 auwakiwa wako shuleni. Hata hivyo, ukiangalia sheria hiiinawabagua wale ambao wapo nje ya mfumo wa elimu.Kwa hiyo, ni ombi langu kwa Serikali kutusaidia tu kutekelezahii hukumu ambayo imekwisha kutoka au la sivyo naombawanapokuja kuhitimisha hoja yao…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea, Mheshimiwa EsterMichael Mmasi na wa mwisho atakuwa MheshimiwaMohamed Mchengerwa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

223

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza kabisa nikushukuru kwa kunipa fursa hii adimu naminiweze kuchangia kwenye Bunge lako hili Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kabla sijaenda mbali,napenda sana kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kwa kutupa si tu Waziri lakini pia ametupaencyclopedia ya sheria katika Bunge hili. Si encyclopediaametupa guru wa masuala ya sheria katika muktadha huu.Nampongeza sana Mheshimiwa Rais, kwa kweliametutendea haki sisi Wabunge wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nichangie masualaya ajira kwa vijana kwa mlengo wa sheria. Kwa kuanzanaomba nichangie Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ni kwanamna gani inasigina fursa ya ajira kwa vijana wetu lakini sihivyo tu ni kwa namna gani sheria hii imetumika katikakupora rasilimali ya Tanzania na kusafirisha na hata wazawatumebaki kuwa watazamaji katika muktadha huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukianza na Sheria hii yaMadini ya mwaka 2010, ukiangalia Kanuni ya 16(1) inaruhusumgeni kusafirisha madini nje ya nchi. Tukienda kifungu cha16 tunaona kabisa hata kwenye maonyesho ya kibiashara,mgeni anaruhusiwa kununua madini na kusafirisha nje yanchi. Si hivyo tu, tunaambiwa kwamba mgeni ambayeamekuja kwa visa siku tatu nchini Tanzania anaruhusiwakusafirisha madini kwa kadri awezavyo lakini tu kama ata-comply kwenye requirement na miongozo ya kisheria. Nambamoja atalipa mrahaba unaotakiwa kwa kusafirisha madinihayo lakini pia Kamishna wa Madini atakapokuwa ametoakibali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini si hilo tu, inasikitishasana kuona kwamba mchimbaji mdogo ambaye ni brokerslicensed holders ananyimwa kibali cha kusafirisha madini njeya nchi. Hii hatutokubali hata siku moja, sisi ambao tunaaminivijana wetu vitovu vyao vilivyozikwa katika ardhi ya Tanzania,

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

224

kijana ambaye anajua kuongea lugha ya Kiingerezaananyimwa fursa ya kufanya biashara nje ya nchi kwa kigezoambacho hatukielewi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye Sheria yaMadini kifungu cha 18 unaona adhabu il iyotolewa,unaambiwa kwamba mtu atakapokuwa amefanya biasharaakakiuka haya yote katika muktadha wa sheria, adhabu nimiaka mitatu jela au shilingi milioni 10 tu, hii tunakataa.Tunakataa kwa sababu hata kwenye Ilani ya Chama chaMapinduzi tumeagizwa tutetee haya. Nitasoma ni kwanamna gani Ilani ya Chama cha Mapinduzi imesimamakuona kwamba imefika mwisho tuzuie biashara ya utoroshajiwa madini. Hili tulili-swear kwa wananchi wetu, naombanirejee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Ilani ya Chama chaMapinduzi, ukurasa wa 34, kipengele ‘K’ kinasema:-

“Katika kipindi cha 2015 hadi 2020, Chama chaMapinduzi kitaielekeza Serikali yake kutekeleza mamboyafuatayo: Kubuni na kutekeleza mikakati mahsusiitakayowezesha kupunguza au kukomesha kabisa vitendovya utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi na biasharaharamu ya madini nchini”. Hii ni Ilani ya Chama chaMapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nasema kwambaimefika mwisho, tunachotaka kuona ni kwamba viwandavya uchenjuaji wa madini vinajengwa nchini Tanzania.Kwenye sheria hii kwenye kifungu cha 52 wamewekaobligations za mwekezaji lakini hatujaona kipengelekinachomlazimisha mwekezaji kuweka plants katika nchi yaTanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili nalitetea kwa nguvu zotekwa sababu naamini kiwanda cha uchenjuaji wa madinikitakapojengwa Tanzania, kwanza tutatengeneza ajira kwavijana wetu lakini pili tutaongeza thamani ya madini na tatumimi kama mwana Kilimanjaro, ninyi ni mashahidi tulipoenda

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

225

juzi kwenye msiba Kilimanjaro, mliona Kilimanjaro hatunaardhi. Mkoa wa Kilimanjaro ardhi iliyobaki ni kwa ajili yamakaburi ya bibi na babu zetu, hatuna pa kulima. Mimininapotetea viwanda hivi vya uchenjuaji vijengwe ni kwasababu vijana wangu watapata ajira kwenye migodi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona nchi ya Botswanailivyopiga hatua. Miaka 40 wananchi wa pale wamebakikuwa watazamaji kwenye masuala haya ya uwekezaji wamadini lakini baada ya kubadilisha sheria na kusemakwamba viwanda vya uchenjuaji vijengwe katika nchi yaBotswana ndipo ambapo nchi hiyo imeweza kuchangiaasilimia 50 ya pato la ndani katika bajeti yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi vijana wa Chama chaMapinduzi, sisi Wabunge wa Chama cha Mapinduzi,tunasema kwamba tuna kila sababu viwanda hivi vijengwe.Tofauti na Mheshimiwa Kaka yangu wa Siha pale,Mheshimiwa Dkt. Mollel, nilishangaa sana tarehe 20 mwezihuu hapa Bungeni aliona hakuna mantiki lakini amesahauvijana hawa wa Kilimanjaro hawana pa kulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitasema hata kama Mwanrihayupo, nitatetea vijana wa Kilimanjaro, nitatetea Siha, Hai,Moshi Vijijini, Moshi Mjini, Same na Mwanga, nitasema bilakuogopa, msiogope vijana wangu mimi nipo. Nitasemanitapaza sauti kwa ajili yenu Kilimanjaro. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nayasema haya lakini pia tukumbuke dada yanguMheshimiwa Angellah Kairuki hata tungepitisha vifungu vyakemamia na maelfu, hana obsorption capacity ya kutengenezaajira hizi ni sisi tumsaidie. Mheshimiwa Waziri wa Katiba naSheria mimi na wewe ni mashahidi tulienda kufunguamabweni ya Chuo Kikuu pale lakini uliona juhudi zaMheshimiwa Rais, alitoka nje ya mikataba, alitoka nje ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

226

utaratibu akaona kwamba tutengeneze ajira kwa kufanyaTBA waweze kufanya kazi, vijana na akinamama waajiriweili tuweze kusonga mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumwambiaMheshimiwa Waziri tunadaiwa, Ilani hii tuliahidi watu, nasemakwamba ifike mahali tujenge viwanda. Nitasoma Ilani yaChama cha Mapinduzi maana imeniagiza niseme, ukurasawa 34 kwenye kipengele cha 10 tumeambiwa pamoja namajukumu haya Chama cha Mapinduzi kitafanya yafuatayo:-

“Kitasimamia na kuhamasisha uwekezaji katikashughuli za uongezaji thamani madini ili kukuza mchangowa sekta hiyo katika pato la Taifa”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasadiki hili na nitalisemasiyo leo tu, kesho na kesho kutwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika musuala haya ya ajiraukienda ukasoma Public Procurement Act ya Kenya utaonani kwa namna gani kijana anathaminika katika nchi ile.Katika sheria ile ya Kenya inasema asilimia 30 ya publicprocurement activities zinafanywa na vijana na kunakuwana dawati maalum katika Ofisi ya Rais. Mheshimiwa Wazirinaomba utusaidie, ulipokuwa Kitengo cha Sheria kama Deanwafanyakazi wako walikuwa na imani sana na wewe,ulikuwa mkali lakini ulikuwa tayari kutetea maslahi yaTanzania. Nakuomba Mheshimiwa Waziri usiishie kufundishapale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tunadaiwa ajira, Ilanihii imetuagiza tutengeneze ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kwa sababugani? Hata Bertha Soka, Mkurugenzi wa PPRA alikuwa hapaDodoma, kuna siku…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

227

MWENYEKITI: Ahsante sana. Haya tunaendelea naMheshimiwa Mohamed Mchengerwa.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, kwa niaba ya wana Rufiji wote duniani,nasimama hapa nami kuwasilisha ya kwangu lakini kwakuzingatia maelekezo yaliyowahi kutolewa katika kitabuchake Paul Flynn, mmoja wa Wabunge wazoefu nchiniUingereza kinachozungumzia how to be an MP. Pia ProfesaPhillip Collin naye katika kitabu chake aliwahi kuzungumziamambo ya msingi kabisa ambayo Mbunge anapaswakuyafanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kumshauridada yangu Mheshimiwa Sabreena atambue kwambaBAKWATA sasa ina uongozi ulio imara na wachapakazi sana.(Makofi)

MBUNGE FULANI: Aaah.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: Shekhe Mkuu wasasa, Shekhe Zuberi ni mchapakazi sana na mambo haya yadini tusiyalete kwenye Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu mmoja anaitwa K.Sachiarith mmoja kati ya wa washindi wa Global Award,katika Mkutano wa 136 wa Bunge wa Dunia uliofanyika kuleBangladesh, aliwahi kuzungumza maneno ambayo napendaniyazungumze katika Bunge lako hili Tukufu. Ndugu Sachiarithaliwahi kusema kwamba kama akinamamawangewezeshwa miaka 50 iliyopita basi dunia tungekuwana Taifa jema sana (if women were empowered in the lastfifty years we could have a better world).

Mheshimiwa Mwenyekiti, aliendelea kwa kusisitizakwamba iwapo vijana wangezaliwa na akinamamawaliowezeshwa miaka 50 iliyopita basi tungekuwa na vijanawazalendo wa Taifa, waadilifu na tungekuwa na Taifa lenyenguvu sana, Tanzania ingekuwa ni Taifa lenye nguvu sana.(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

228

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona niseme manenohaya kwa sababu tunaona kabisa kwamba vijana waadilifuutawakuta upande huu tuliokaa wengi. Hapa natakanimtofautishe ndugu yangu Bwana Tundu Lissu ni miongonimwa ignorant pan-politician. Nimeona niseme hivi kwasababu Tundu Lissu hana uzalendo wa Taifa hili, anaendekezaharakati, yeye ni mwanaharakati lakini si mwanasiasa. Kwahiyo, tunawaomba Watanzania kumuepuka na kuepukananaye kwani dhamira yake ni kuligawa Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jukumu la Bunge kwa mujibuwa Ibara ya 63 na 64 ni kutunga sheria na kuisimamia Serikali.

T A A R I F A

MHE. KHATIB SAID HAJI: Taarifa Mwenyekiti.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mchengerwa.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, wanasheria wote duniani wanatambuakwamba nchi hii inaendeshwa na Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mchengerwa taarifa.Mheshimiwa Khatib endelea.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nataka nimpe taarifa Mheshimiwa Mchengerwa…

MBUNGE FULANI: Kanuni ya ngapi?

MHE. KHATIB SAID HAJI: Kanuni waijua wewe.(Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, amemwambia MheshimiwaSabreena kwamba BAKWATA ya sasa hivi ina uongoziunaoaminika. Nataka nimpe taarifa MheshimiwaMchengerwa, BAKWATA ya Tanzania (Baraza Kuu la Waislamuwa Tanzania) ambapo pia mimi ni Mwislam, haijawahi,

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

229

haitawahi kuwa na uongozi unaoaminika. BAKWATA nichombo kinachotumika kuwakandamiza Waislam waTanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mchengerwa unaikubali aukuikataa taarifa hiyo?

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza naomba unitunzie muda na ikiwezekanaleo uniongezee dakika ishirini nina mambo mengi yakuzungumza.

WABUNGE FULANI: Aaah.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa hii naikataa kwa sababu Shekhe Zuberini Shekhe ambaye anatambua elimu ya dunia pamoja naya akhera. Ni mtu muadilifu na mchapakazi sana naameweza kui-transform BAKWATA kuwa ni chombo kizuri sanakwa Waislam. Niwaombe Waislam wote kuendelea kuiaminiBAKWATA. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanasheria wote dunianiwanatambua kwamba nchi inaongozwa na katiba, sheria,kanuni na taratibu. Vilevile inaongozwa na taratibu zaChama Tawala ambacho ndicho kimeiweka Serikalimadarakani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona niseme hili kwasababu upo upotoshaji mkubwa uliozungumzwa na TunduLindu kuhusu Rais kwamba haitaki Katiba Mpya. Naombanikumbushe Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi yamwaka 2015 ambayo katika ukurasa wake wa nne (4)inazungumzia mambo yatakayotekelezwa na Serikali yaChama cha Mapinduzi. Katika Sura ya Saba ya Ilani yaUchaguzi wa Chama cha Mapinduzi pamoja na manenomengine ukurasa 163 katika aya ya 144 inazungumzia mamboyafuatayo ambayo naomba niyanukuu hapa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

230

“Mchakato wa kutunga Katiba Mpya umeendeshwana umefikia hatua ya Katiba Inayopendekezwa iliyopitishwana Bunge Maalum la Katiba ambayo itapigiwa kura yamaoni”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni Ilani ya Chama chaMapinduzi ambayo nchi hii inaongozwa kwa mujibu wataratibu kama ambavyo nimezisema.

MHE. ANTONY C. KOMU: Taarifa MheshimiwaMwenyekiti.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, nirejee hapo…

T A A R I F A

MHE. ANTONY C. KOMU: Taarifa MheshimiwaMwenyekiti.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: Katika Ibara ya118…

MBUNGE FULANI: Uzalendo siyo uwoga.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge mnanielewamimi kuhusu mambo ya taarifa, lakini leo endelea taarifa.

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kwa Kanuni 68(7) naomba nimpe MheshimiwaMchengerwa taarifa kwamba Mheshimiwa Tundu Lissu yuposahihi kusema kwamba Rais hataki Katiba Mpya.

WABUNGE FULANI: Ndiyo.

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwasababu Rais alivyotimiza mwaka mmoja…

MBUNGE FULANI: Taarifa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

231

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Raisalipotimiza mwaka mmoja aliitisha vyombo vya habariakazungumza na wahariri

MBUNGE FULANI: Taarifa.

MHE. ANTONY C. KOMU: Na aliulizwa swali kuhusuKatiba Mpya akasema hajawahi kusema mahali popotekatika kampeni zake.

MBUNGE FULANI: Taarifa.

MHE. ANTONY C. KOMU: Kwa hiyo, Katiba Mpya sioajenda yake na ajenda peke yake aliyonayo yeye nikunyoosha nchi.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. ANTONY C. KOMU: Kwa hiyo Tundu Lissu yuposahihi.

MBUNGE FULANI: Taarifa.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, nitunzie muda.

MWENYEKITI: Muda wako unalindwa lakini unaikubaliau unaikataa taarifa hiyo?

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa hii naikataa kutoka kwa layman huyu nanaomba nimsaidie kwamba nchi inaongozwa na katiba,sheria na kanuni na taratibu ambazo Chama Tawala ndichokilichosimamisha dola madarakani. Chama cha Mapinduzikilikuwa na Ilani ya Uchaguzi ambayo wananchi walio wengiwaliiona na kuisoma wenzetu walikuwa na tovuti ambayoilikuwa ni vigumu kwa wananchi wa vijijini kuiona nakuisoma na kuikubali. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

232

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 118 ya Katibaambayo Tundu Lissu amepotosha hapa jamii kwa kusemakwamba Mheshimiwa Rais amevunja Katiba kwakutomchagua Jaji Mkuu wa Tanzania. Ibara ya 118haimlazimisha Rais kuchagua Jaji Mkuu wa Tanzania. Ibaraya 118 iko wazi kabisa. Mheshimiwa Tundu Lissu anaifahamusheria na anaijua Ibara hii imezungumza vizuri lakinianachofanya ni kupotosha Watanzania na kuleta taharukikatika nchi yetu hii ya Tanzania. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, yamezungumzwa masuala mengi kuhusudemokrasia na utawala bora. Chama cha Mapinduzikinaongozwa na Ilani na ukurasa wa 146 umezungumziademokrasia na utawala bora. Nataka niseme hapa kwambachama hiki kina demokrasia ya kutosha na unapomwonanyani anamtukana mwenzie ni vyema akajiangalia nyumanikwake. Chama hiki kimekuwa na Wenyeviti kadhaa kilabaada ya miaka kumi wenzetu wamekuwa na Mwenyekitiamekaa madarakani zaidi ya miaka 20. Hauwezikuzungumzia demokrasi wakati nyumbani kwako kunaungua.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi hii mwaka 1961 ilikuwana Rais wa kwanza alikuwa Mzanaki, Mheshimiwa MwalimuJulius Kambarage Nyerere. Baada ya Mwalimu Nyererewananchi walimchagua Rais wa Awamu ya Pili, Mzee wetuMheshimiwa Ally Hassan Mwinyi, alikuwa Mzaramo wa kutokaZanzibar.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, mwaka 1995 baada ya kupitishwa mfumo wavyama vingi 1992 tulimchagua Mheshimiwa Benjamin Mkapa,huyu alikuwa Mmakonde kutoka kule Kusini. Mwaka 2005tulimchagua Mheshimiwa Dokta Jakaya Mrisho Kikwete huyualikuwa Mkwere kutoka pale Pwani. Taifa letu leo hii

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

233

tunashuhudia kuwa na Rais Msukuma kutoka Kanda ya Ziwa.Hii ni demokrasia ya hali ya juu ambayo wenzetu hawana.(Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, ni vyema nyani akawa anaona kundule kulikokutukana wenzio wakati wewe mwenye una matatizo.(Makofi/ Kicheko)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, sasa naomba nijielekeze katika kuishauri Serikaliyangu njema ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi/Kicheko)

MBUNGE FULANI: Taarifa.

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimpe taarifa kwamba maneno anayoyatumiaMbunge…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naombautulivu Bungeni.

MHE. KASUKU S. BILAGO: Haya maneno ya nyani haonikundule sio maneno ya Kibunge ayafute.

MBUNGE FULANI: Jana mmelalamikia ngariba nyie.

MWENYEKITI: Taarifa unaikubali au unaikataMheshimiwa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

234

MBUNGE FULANI: Kundule na ngariba.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, mimi ni mtoto wa Pwani na neno hilo ni lakawaida tu kule kwetu Pwani. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika miaka ya 90…

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kuhusu utaratibu.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, miaka ya 90 katika moja ya mikutano yakeMheshimiwa Mwalimu Julius Nyerere…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Hebu subiri kidogo MheshimiwaMchengerwa.

Waheshimiwa Wabunge, upande wangu wa kushoto,mnisikilize, mimi siamini kwamba Bungeni humu kuna fisi.Haiwezekani watu wazima mnatoa milio ya wanyama wale,tafadhali tuvumiliane. (Makofi/Kicheko)

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA. Tumpe maji marefuawanyooshe mafisi hao.

MWENYEKITI: Kiswahili yawezekana wengine tunamatatizo nacho lakini as long as Mheshimiwa Mbungehajatumia lugha ya kutukana au ya kuudhi twende mbele.

MBUNGE FULANI: Ngariba je?

MWENYEKITI: Ngariba ni Kiswahili kinafahamika.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mchengerwa hebuhitimisha hoja yako dakika zako tumelinda.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

235

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, miaka ile ya 90….

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kuhusu utaratibu.

WABUNGE FULANI: Ahaaa.

MWENYEKITI: Haya kaa Mheshimiwa.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, miaka ile ya 90….

MBUNGE FULANI: Kaa wewe.

MWENYEKITI: Kanuni gani bwana?

MHE. MWITA M. WAITARA: Kanuni ya 68(1).

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba niulize kuhusu utaratibu na natumia Kanuni ya64(1)(a), (b) na (g). Kanuni ya 64(1)(a) inasema mchangiajihatatoa ndani ya Bunge taarifa ambazo hazina ukweli.Mheshimiwa Mchengerwa ambaye anaendelea kuchangiasasa anasema Mheshimiwa Tundu Lissu hana uzalendo.Tunaomba athibitishe kwenye Bunge hili ametumia vigezogani kumpima Mheshimiwa Tundu Lissu hana uzalendo katikanchi hii?

WABUNGE FULANI: Alete huyo.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba athibitishe vinginevyo afute maneno yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pil i wakatianachangia anaendelea kupotosha, anajadili jamboambalo halipo kwenye mjadala sasa. Hatuzungumzii uongoziwa vyama vya siasa, hatujauliza CCM wanachagua namnagani wala habari ya CHADEMA wala CUF. Hapa mjadala

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

236

uliopo mezani ni hoja ya mapato na makadirio ya Wizara yaMambo ya Katiba na Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu mchangiajianaendelea kutoa maneno ya kuudhi sana kadrianavyoendelea kuchangia. Kwa hiyo, naomba Meza yakoituongoze kuhusu utaratibu hapa Bungeni.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nimesemalugha inayotakiwa Bungeni ni lugha ya kibunge wala hakunamabishano hilo na ndiyo maana nilisema kama ametumianeno hilo ambalo halikubaliki, nimesema ngariba sio nenoambalo, ni Kiswahili tu…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Msibishane na mimi nasema huo ndioutaratibu wetu tutumie lugha ya kibunge. La pili…

MBUNGE FULANI: Tuvumiliane.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara sidhani kamaMheshimiwa anayechangia kwamba hajielekezi kwenye hojailiyo mbele yetu kwa sababu Wizara ya Katiba na Sheriaimebeba mambo mengi yakiwemo ya utawala bora nademokrasia. Kwa hiyo, hilo lisikusumbue hata kidogo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la uzalendo unampimajemtu? Unampima mtu kwa kauli zake na vitendo vyake.(Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, sisi tumeletwana Watanzania hawa, wana matumaini makubwa sanakwamba Bunge hili linaweza likatoa maamuzi na mwongozokwa faida wa mustakabali wa nchii hii. Sasa tukienda namnahii tunaanza kutoa taswira tofauti na matarajio ya wananchi.Mheshimiwa Mchengerwa nakuomba umalizie. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

237

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Nianzie hapo kwenye uzalendo,miaka ya 90 Mwalimu Nyerere aliwahi kumthibitisha Kawawakatika moja ya mikutano yake pale Mnazi mmoja kusemakwamba Kawawa ni muadilifu sana na alikuwa tayari kutoamachozi kuthibitisha kwamba Kawawa alikuwa ni muadilifu.Nami ndani ya Bunge lako Tukufu naomba kuthibitishakwamba iwapo siku moja Wabunge walio wengi wakasemakwamba mambo mazuri anayofanya Mheshimiwa Dkt. JohnPombe Joseph Magufuli kwa nchi hii si uzalendo, basinitaliomba Bunge lako hili Tukufu kufuta hili neno uzalendokatika dictionary ya Kiswahili. Kwa sababu mambo makubwaanayoyafanya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli niuzalendo wa hali ya juu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijielekeze kwamaneno mawili matatu ambayo nimeyaacha pembeni.Mheshimiwa Waziri nikuombe sana wakati unahitimisha hojayako hapa...

MBUNGE FULANI: Uteuzi umekwisha. (Kicheko)

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: Nikukumbushejambo moja, kwanza, tuiangalie kada ya Mahakimu waMahakama za Mwanzo ambao wamekuwa wakipatamishahara midogo. Zipo taarifa wako Mahakimu zaidi ya 118ambao hawajapandishwa vyeo na hao ni Mahakimu waMahakama za Mwanzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pili, kwa hali ya uchumituliyonayo ni vyema tukawaangalia Mahakimu pamoja naWanasheria wa Serikali ili kuwawezesha fedha kidogo kwaajili …

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, mwisho kabisa napenda niseme kwamba Taifahili linategemea Bunge na uzalendo wetu ndio utakaoliwekaBunge hili katika…

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

238

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba niunge mkono hoja na nampongezaMheshimiwa Waziri kwa kila jambo alilolifanya katika Bungehili. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MBUNGE FULANI: Uteuzi hamna, uteuzi umekwisha.

MBUNGE FULANI: Tukuteue wewe.

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema.Naanza kwa kuchangia Wizara hii ambayo inahusiana naKatiba na Sheria ambavyo vyote ndio msingi wa haki. Mfano;katika kitabu cha Hotuba ukurasa wa 36 kipengele cha Tumeya Haki za Binadamu na Utawala Bora:-

(i) Kukuza na kutetea haki za binadamu hususanmakundi yenye mahitaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maneno hayayameandikwa lakini hayafanyiwi kazi na ushahidi kunamahabusu na wafungwa wengi ambao wamefungwa bilakupatiwa haki za kisheria kwa kutetewa na wanasheria waSerikali, kutojua haki zao lakini pia kwa kesi za kubambikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wapo akinamamawajawazito wanaojifungulia Magerezani na pia wapowanaotiwa hatiani wakiwa na watoto wachanga ambaobado wananyonya maziwa ya mama zao na hawawezikuishi bila ya mama zao, wanakuwa wafungwa bila hatia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu; Serikaliitafute adhabu mbadala kuwaepusha watoto kuwawafungwa bila hatia.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

239

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Katiba na Sherianimeishangaa kwa kutoweka katika Bajeti yake Fungu laFedha kwa ajili ya kuendeleza mjadala wa Katiba mpyaambayo ndio haja ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali kupitiaWizara ya Katiba na Sheria itenge fedha kwa ajili yamwendelezo wa mjadala wa Katiba mpya ili kuondoa kiuya Katiba mpya kwa Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakimu kukaa katikaVituo vyao kwa muda mrefu wanazoeleka na wanazoea nakuwa wepesi kuweza kupokea rushwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakimu waongezewemishahara ili kuwaepusha katika suala zima la kupokearushwa.

MHE. DKT. HAJI H. MPONDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naanza kwa kuunga mkono Hoja. Wilaya ya Malinyi nimiongoni mwa wilaya mpya na zilizoko katika mazingiramagumu (pembezoni). Hivyo, wahitaji kupewa kipaumbelena jicho la kipekee. Wilaya ya Malinyi haina Mahakama yaWilaya hivyo, hutegemea Wilaya jirani (mama) Ulanga.Tumepeleka maombi ya kuanzisha au kujengewa majengoya Mahakama ya Wilaya ya Malinyi. Tunaomba Serikali kulipakipaumbele ombi hili la ujenzi wa Mahakama ya Wilaya kwakuwa huduma hiyo inapatikana mbali sana kilomita 200 hadi300 toka Wilayani Malinyi kwenda Ulanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Malinyi inaMahakama za Mwanzo mbili tu kuhudumia wilaya nzimayenye ukubwa wa kilomita za mraba 10,576 na idadi ya watukaribu 250,000. Hivyo tunaomba tuongezewe Mahakamaza Mwanzo. Aidha, Mahakimu waliopo wa Mahakama zaMwanzo wamekuwepo muda mrefu katika vituo vyao vyakazi; hivyo kuathiri sana utendaji/ufanisi wa majukumu yaoya kazi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

240

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara iweke nakumwezesha Hakimu wa Wilaya ya Ulanga ambaye piaanahudumia Wilaya ya Malinyi kuja kusikiliza mashtaka (kesi)katika Wilaya ya Malinyi ili kuepusha au kupunguza usumbufukwa watuhumiwa kwani wanapata adha kubwa sanakwenda na kurudi Mahenge (Ulanga). Ahsante.

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ukosefu wa Mahakama ya Wilaya ya Kakonko; Wilaya nimpya ina Mahakama za Mwanzo tatu, ambazo hata mojahakuna hakimu (aliyekuwepo yuko masomoni) kama Wilayatuna kiwanja cha kujenga Mahakama ya Wilaya. Ombinaomba kujengewa Mahakama; na mbili naombaMahakama ya Mwanzo Kakonko ipewe Hakimu ili kupunguzaumbali kwa wananchi kufuata huduma hiyo wilaya jirani yaKibondo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Burundikukamatwa ovyo na kufungwa bila kosa lolote. Polisiwanakuwa wakiwakamata warundi wanaokuja kufanyabiashara Kokonko (Jimbo la Buyungu) kwa kukutwa sokonikuwa ni wahamiaji haramu. Matokeo yake hata wanaokujakulima vijiji vya jirani Burundi na kurudi jioni kwao naohukamatwa na kufungwa vifungo bila kujadili ni nchi ya AfrikaMashariki. Wapo warundi wapatao 254 wamefungwagereza la Nyamisinyi- Kibondo kwa makosa kama hayo.Kimsingi Burundi na raia wake pamoja na sisi tunaopakananao hatufaidi kuwa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapendekezo, Warundiwaruhusiwe kuja Wilayani Kakonko kulima na kurudi kwao(uwekwe utaratibu). Warundi wanaokuja kufanya biasharawasikamatwe na kufungwa. Sheria ya kukamata ovyoiangaliwe upya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, polisi kubambikiza kesiwananchi, kesi nyingi ni za kubambikiza tu na hivyo kujazawafungwa gerezani wasio na hatia. Polisi Kakonko

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

241

wamekuwa wakiwabambikiza kesi wananchi, sheriazilizopitwa na wakati zifanyiwe marekebisho hapo Bungeni.Mfano Sheria ya Ndoa ya 1971.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mashauri kuchelewakupelekwa mahakamani. Kumekuwa na tatizo la mashaurikutopelekwa Mahakamani mapema hivyo kuwekwa polisizaidi ya saa 24.

MHE. TWAHIR AWESU MOHAMED: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwakunijalia na kuwezesha kupata fursa hii muhimu ya kutoamchango wangu huu katika hoja hii iliyopo mbele yenu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haki za binadamu,tumekuwa na tabia kwa Serikali yetu hii tukufu kuwekamaneno kwenye makaratasi mazuri yenye kuonesha kwambanchi inafuata taratibu nzuri za kisheria suala zima la utoajina utekelezaji wa haki za binadamu wakati haki hiyo haipona haipatikani badala yake Serikali na vyombo vyake vyadola vinatumia nguvu kupita uwezo kwa kuwakandamizana kuwanyanyasa raia zake kuwekwa magerezani nakuwapa vifungo kwa makosa ya kuwabambikiza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na watuhumiwawa makosa ya ugaidi zaidi ya miaka minne sasa Watanzaniawenzetu wamo wanateseka na kufanyiwa vitendo vyakinyama na kiudhalilishaji wako mbali na familia zao. Kesihadi leo inaelezwa ushahidi haujakamilika, naiomba Serikalikwanza itambue hapa duniani tunapita, iache kutesa raiazake, basi kama wanahatia ni vyema wakahukumiwa,wakapewa adhabu kulingana na ukubwa wa makosa yaona kama makosa hayakukidhi wakaachiwa huru wakarudina kuishi na familia zao ambazo hivi sasa zinateseka sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la katiba mpya, sualahili sasa si suala rahisi tena kutekeleza ni dhahiri Serikali halimokabisa katika mpango wake wa utekelezaji wake, pamojana Watanzania kuhitaji sana suala hili. Ni vyema kwa Serikalikuzingatia na kusikiliza maoni na matakwa ya wananchi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

242

wake kuepusha nchi yetu kuingia katika kutoelewana kituambacho kinaweza kuleta mgawanyiko mkubwa,utakaopelekea Taifa kusambaratika na kugombanawenyewe kwa wenyewe. Naiomba Serikali ikae na ilifikiriejambo hili kwa umakini mkubwa ili thamani ya kazi namichango waliyotoa Watanzania ionekane umuhimu wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. ELIAS J. KWANDIKWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwa kuwa tumehamia Makao Makuu ya Halmashauri yaUshetu, Makao Makuu katika Kijiji cha Nyamilangano (Jimbola Ushetu) na kwa kuwa Mahakama inayohudumia eneo hiliyako mbali na kwa kuwa tunayo Ofisi ya OCD – Ushetutuliyopewa hivi karibuni na ni muhimu mashauri mbalimbaliyanaelekezwa umbali mrefu kupata huduma zaKimahakama na kwa kuwa Halmashauri ya Ushetu iko tayarikutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama tunaombaSerikali itujengee Mahakama ya Mwanzo eneo hili la Kijiji chaNyamilangano (Makao Makuu ya Halmashauri ya WilayaUshetu) ili wananchi wapate huduma ya haki zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza napenda kukupongeza kwa hotuba yako nzuri. Pianaunga mkono kwa asilimia mia moja pamoja na kuungamkono hoja hii naomba kuchangia maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, upungufu wa Mahakimu waMahakama za Mwanzo. Mahakimu wa Mahakama yaMwanzo ni wachache sana hapa nchini. Wilaya yangu yaMpwapwa ina Kata 33 lakini PCM wapo wanne tu nahawana usafiri, angalau PCM wote nchini wangepata pikipikiau magari madogo ya kuwasaidia kutembelea Mahakamaza mbali kuliko ilivyo sasa PCM wengi wanapanda mabasiambapo ni hatari hasa PCM akiwa na mafaili ya kesianaweza kuporwa ndani ya basi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

243

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mahakimu waMahakama za Mwanzo wajengewe nyumba za kuishi badalaya kuishi mitaani ambapo ni hatari kwa maisha yao, bahatimbaya anaweza kupanga na mtu mwenye kesi katikaMahakama yake. Maslahi ya PCM ni duni sana waongezwemishahara ili kumudu mazingira wanayoishi au kuboreshamaisha yao kuliko hali ilivyo sasa. Wilaya ya Mpwapwatulijengewa jengo la Mahakama ya Wilaya lakini Rest Houseya Mheshimiwa Jaji haikujengwa mpaka sasa. Je, itajengwalini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kila Tarafa zijengweMahakama za Mwanzo nne ili kuwasogezea wananchihuduma ya Mahakama karibu kuliko hali ilivyo sasa wananchihutembea kilomita zaidi ya 100 kufuata huduma hiyo. Chuocha Mahakama Lushoto waongeze wanafunzi ili kuongezaidadi ya PCM hapa nchini.

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Mwenyekiti,coverage ya civil registration ni ndogo sana hapa nchini,inawezekana ni chini ya asilimia kumi. Kwa nini msitumiewatendaji wa Kata na Vijiji kama mawakala wa RITA kwakuwapa gawio kwa kila kizazi, kifo na ndoawanavyoorodhesha na kutumia taasisi za utafiti kwa kuhakikiubora.

MHE. ALLAN J. KIULA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nichukue fursa hii kuipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwakazi nzuri inayofanywa. Pamoja na kuwepo changamoto yaumuhimu wa kuboresha baadhi ya sheria ambazo amazimepitwa na wakati au zinahitaji kuweka mkazo/udhibitikatika baadhi ya maeneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesoma hotuba hiikikamilifu na kubaini kuwa ahadi iliyotolewa Bungeni naWaziri mtangulizi kuhusu Wilaya mpya ya Mkalama kutokuwana Mahakama ya Wilaya ilihali wananchi wakiifuata hakiWilaya ya Iramba Magharibi. Wakati jibu likitolewa katikaswali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Iramba MasharikiMheshimiwa Allan Kiula iliahidiwa kuwa bajeti ya Wizara ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

244

mwaka wa fedha 2017/2018 itaweka/itatenga fedha kwaajili ya ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Mkalama lakinisijaona utekelezaji wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Wizara itenge fedhakatika bajeti hii ili kuwasaidia wananchi wa Mkalama ambaowamewekwa wakihangaika kupata haki katika Wilayanyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru na naungamkono hoja.

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kuunga hoja mkono. Aidha, naombakuchangia katika maeneo mawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ucheleweshaji wa kesihususan za jinai Mahakamani ni tatizo kubwa sana ambalolinahusisha Wizara nyingine kuu za Mambo ya Ndani. Makosaya mauaji ni moja ya makosa ambayo watuhumiwa wakewanakaa muda mrefu mahabusu. Nashauri Serikali iangalieupya utaratibu wa High Court Session ili kesi hizo zisichukuemuda mrefu kama inavyochukua wakati huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mahabusu pia ambaowanahukumiwa kifo utekelezaji wake haufanyiki vizuri. Sualahilo l ikaangaliwe mawakil i wa Serikali maslahi yaoyaangaliwe upya. Mishahara na marupurupu yao ni midogosana ukilinganisha na kazi zinavyofanyika.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Sheria naKatiba Palamagamba Kabudi. Nianze na hali za Mahakamazetu nchini hususan Mahakama za Mwanzo. Hali za majengo,watumishi na vitendea kazi ni mbaya sana. Katika Wilaya yaMafia tuna Mahakama ya Mwanzo moja tu na imechakaana haina watumishi wa kutosha. Wananchi wa Mafiawanalazimika kusafiri masafa marefu kwenda kufuatahuduma za Mahakama.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

245

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kuiombaSerikali ituongezee Mahakama za Mwanzo angalau mbilikatika maeneo ya Utende na Vunjanazi sambamba nakuimarisha vitendea kazi na kuongeza watumishi waMahakama ya Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haki ya dhamana kuumahabusu kwenye rumande zetu kuna mahabusu wengiwanashikiliwa katika mahabusu zetu wakati wapo wenyekukidhi vigezo vya kumchukulia dhamana. NamwombaMheshimiwa Waziri wakati wa kuhitimisha hoja alitoleeufafanuzi hili jambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upo umuhimu wa Serikalikuongeza bajeti ya Wizara hii ili kuhakikisha suala la utoajiwa haki nchini linafanyika kwa weledi wa hali ya juu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana nanaomba kuunga mkono hoja.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,katiba mpya, Wizara haina muda tena wa kusubiri kuanzakumalizia mchakato wa kupata katiba mpya. Kama bajetihii ya 2017/2018 haitatenga pesa kwa ajili ya jambo hili,maana yake Watanzania wasitegemee tena kupata katibampya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, marekebisho ya sheria,Serikali ilete Muswada Bungeni kwa ajili ya kubadilisha sheriaya mabadiliko ya katiba ya 2011 na ile ya kura ya maoni ya3013 ili iendane na hali ya sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zuio la shughuli za kisiasa,Serikali itengue zuio lake la kuwakataza wanasiasa kufanyamikutano ya kisiasa kwani kwa kufanya hivyo inavunja sheriaya vyama vya siasa. Ni haki ya msingi ya vyama vya siasakufanya mikutano ya kisiasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, majengo chakavu, Wizaraitafute vyanzo vyake vingine ili ipate fedha za kujenga na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

246

kukarabati majengo ya mahakama hasa Mahakama yaMwanzo.

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kupata nafasi ya kuchangia. Ucheleweshwaji wakusikiliza kesi za mahabusu. Baada ya kesi zilizopo katikauchunguzi chini ya DPP zinachukua muda mrefu sana nawakati watuhumiwa wengine hawana hatia lakiniwanaweza kuwa gerezani kwa zaidi ya miezi sita. Je, kesihizi hazina kikomo cha uchunguzi? Inakuwa kamawanakomoa na kudhalilisha wengine na huu ni ukiukwajiwa haki za binadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ya Mfuko waMahakama, bado mfuko huu wa fedha zinazoainishwahazifiki kwa wakati na hata wakizipata zinakujazimechelewa na pungufu ambayo inakuwa ni vigumukutekeleza miradi ya maendeleo hii inajionesha mpaka Machi2017, fedha hazikutumwa kwa wakati. Chombo hiki nimuhimu sana nashauri fedha zipelekwe kwa wakati ikiwa nipamoja na kuhakikisha wapo watumishi wa kutosha,kuhakikisha posho za wazee wa mabaraza zinalipwa, wazeehawa wanaacha shughuli zao wengine inabidi watumienauli zao, hivyo, wana haki ya kupata stahili zao kwa wakati.

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuishauri Serikali kupitia upya sheria mbalimbali,naomba Serikali itafute utaratibu wa kila Tarafa nchini kuwana Mahakama za Mwanzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa kupata wazeewa Mahakama uboreshwe. Hivi sasa wazee wengi waMahakama wanakaa muda mrefu bila kuteuliwa kwakuzingatia jinsia na kutoka Kata au Tarafa kulingana na idadiyao, hata hivyo uteuzi haushirikishi Mamlaka za Serikali zaMitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mabaraza ya Ardhi baadhiyake yamejihusisha na rushwa kiasi kwamba wapokeahuduma toka Mabaraza mbalimbali nchini yanakosa imani.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

247

Kwa sasa kuna haja ya ufafanuzi wa Wizara kuhusu masualambalimbali ya wananchi kufahamu utaratibu wa kupata hakizao mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Wakuu wa Wilayandiyo Wenyeviti wa Kamati ya Maadili ya Mahakama. Kunahaja ya kuwa na ratiba ya vikao vya Kamati hiyo muhimukwa ustawi wa Mahakama nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku ya Maadhimisho yaMahakama nchini itumike kuwa siku ya wapokea hudumakutoa mawazo yao kuhusu huduma hiyo ili Watendaji waMahakama waweze kujijua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumo wa malipo ya Wazeewa Mahakama utazamwe ili kuleta tija, kwa sasa wazeewengi wanalalamikiwa kujihusisha na rushwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwe na kipindi chakuwahabarisha umma kuhusu huduma ya Wasaidizi waKisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali isaidie kutoa fedhaza ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Mbulu naJengo la nyumba ya Hakimu wa Wilaya. Kwa sasa majengoyaliyoko ni chakavu sana, hayafai kwa matumizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Wilaya ya Mbuluyenye Kata thelathini na tano ina Mahakama moja ya Wilayana Mahakama za Mwanzo tatu lakini Mahakama za Mwanzohaina Mahakimu wa kutosha na kesi nyingi huchelewa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba Wazirimwenye dhamana afanye ziara Wilayani Mbulu na kuonachangamoto ya Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha,naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. Ahsante

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

248

MHE. GIMBI D. MASABA: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kuchukua nafasi hii kuwasilisha mchango wanguwa maandishi kuhusu Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria.Ningependa kuzungumzia kuhusu suala la uwazi katikamchakato wa utoaji haki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu ni nchimwanachama wa OGP Open Government Partnershipambapo mojawapo ya misingi muhimu ni Serikali za nchihusika kutekeleza majukumu yao kwa uwazi wa hali ya juu iliwananchi wajue Serikali zao zinavyofanya kazi. Hata hivyokwa Tanzania hali ni tofauti kwa kuwa uhuru wa habariumeminywa kwa kiwango cha juu kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na usiri mkubwasana katika mchakato wa utoaji haki Mahakamani. Vyombovya habari vinazuiwa kuingia Mahakamani kuona mwenendowa kesi, jambo ambalo limesababisha kushamiri kwa vitendovya rushwa na wanyonge kudhulumiwa haki zao kutokanana usiri uliogubika Mhimili wa Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi jirani ya Kenya,kesi zote zenye maslahi kwa Taifa huwa zinarushwa moja kwamoja kwenye Televisheni na wananchi wanaona mwenendowa mchakato wa utoaji haki. Kesi za uchaguzi na katibakatika nchi ya Kenya zilirushwa moja kwa moja na CitizenTV. Aidha, kuhusu kesi ya BREXIT ya Uingereza juu ya nani katiya Bunge na Serikali ya Uingereza anatakiwa kuanzishamchakato wa kujitoa katika umoja wa Ulaya ilirushwa livemoja kwa moja na BBC na dunia nzima ilishuhudia na kuonamwenendo wa utoaji haki. Kwa kutumia mifano ya Kenyana Uingereza, nadhani Tanzania sasa inatakiwa kwenda levelnyingine kwa kuruhusu uwazi zaidi katika mchakato wa utoajihaki Mahakamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na vyombo vyahabari kuruhusiwa kuingia katika vyumba vya Mahakama ilikuripoti mwenendo wa mchakato wa utoaji haki, vyombohivyo pia viruhusiwe kuwatembelea wafungwa Magerezaniili wafungwa wapate haki ya kueleza fikra na mtazamo wao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

249

kuhusu maisha yao Magerezani. Kwa kufanya hivyo, tutakuwatumepiga hatua kubwa ya kudumisha uwazi katika utendajiwa Mahakama, lakini pia tutakuwa tumepiga hatua kubwakatika kujali haki za wafungwa ambazo ni miongoni mwahaki za binadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Wizara ya Katiba na Sheria ina wajibu wa kuiwezesha nchikuwa na mfumo mbalimbali wa Kikatiba na Kisheria katikakufanikisha Mipango ya Maendeleo ya Taifa. Pamoja nawajibu huu muhimu hotuba nzima ya Waziri haijazungumziakabisa kuhusu mchakato wa Katiba mpya. Aidha, katikavitabu vya bajeti hakujatengwa fedha zozote/kiasi chochotekwa ajili ya kuendeleza mchakato wa Katiba mpya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali inadhihirisha kwambaSerikali ya Rais Dkt. John Magufuli lazima dhamira yakuendeleza kwa wakati mchakato wa mabadiliko ya katiba.Hivyo ni vyema Serikali ikatoa kauli hii Bungeni ni kwa ninihaijatenga fedha kwa ajili ya mchakato huu muhimu kwamaslahi ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika aya ya 20, 21, 22,Waziri wa Katiba na Sheria amezungumzia kuhusuutekelezaji wa mkakati wa kuboresha huduma zaMahakama ikiwa ni pamoja na kufanya ujenzi na ukarabatiwa Mahakama mbalimbali nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika orodha hiyoimetajwa Wilaya mpya ya Kigamboni, hata hivyo Wilayampya ya Ubungo haijatajwa hivyo, Serikali itoe kauli nikwa nini Wilaya mpya ya Ubungo haijajumuishwa na liniMahakama ya Wilaya ya Ubungo itajengwa. Aidha,Mahakama hiyo ni vyema ikajengwa katika Jimbo laKibamba yalipo Makao Makuu ya Wilaya mpya ya Ubungokama ilivyopendekezwa kwa nyakati mbalimbali.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

250

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya kurekebisha Sheriaina wajibu na mpango muhimu ya maboresho ambayoyamependekezwa muda mrefu ni pamoja na matumizi yalugha ya Kiswahili katika mfumo mzima wa Mahakama nautungaji sheria nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Haki za Binadamuna Utawala Bora imeeleza kuwa imefanya uchaguzi kuhusumabadiliko yaliyowasilishwa katika THUB.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiwa Mbunge wa Ubungoniliwasilisha malalamiko na madai ya kutaka, uchunguzikuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi yake yautawala bora juu ya mgogoro wa muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu matatizo ya majikatika Kata ya Goba naomba kupatiwa majibu juu yahatua ambazo Tume imechukua na kupatiwa nakala yaripoti ya Tume kuhusu uchunguzi huo. Aidha pamoja nauwekezaji mkubwa wa Serikali juu ya miradi ya Ruvu juu naRuvu chini tume ielewe kwamba Goba bado imeachwakama kisiwa kwa kuwa haina mtaro wa mabomba.

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nichukue fursa hii kuipongeza Serikali na Waziri husika kwahotuba nzuri inayohusu makadirio na matumizi kwa mwakawa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi zimekuwa mahalimuhimu kwa ajili ya kutoa haki katika nchi yetu. Hata hivyo,nimesikitika sana kuona kuwa katika bajeti ya mwaka wafedha 2016/2017 Wizara ilitaja Wilaya 17 zitakazojengwaMahakama ya Wilaya na moja ya Wilaya hizo ni Kilindi.Naomba kupata majibu ya kuridhisha kwa nini Wilaya yaKilindi si miongoni mwa Wilaya zilizopo katika ujenzi kwamwaka huu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni takribani miaka 30 sasawakazi wa Wilaya ya Kilindi wamekuwa wakipata hudumaza Mahakama za Wilaya katika Wilaya jirani ya Handeni.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

251

Mheshimiwa Mwenyekiti, upo umbali mrefu sanakutoka Kilindi na Handeni hususani kwa Kata za Pagwi,Kikunde, Tunguli kata hizo zipo karibu kabisa na Wilaya yaGairo. Utaona kwa kiasi wananchi wa kilindi wanahitajiMahakama hii kwani kupata Mahakama ni sehemu yahaki za msingi kwa wananchi wa Kilindi. Halmashauri inaloeneo kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama. Niombe sasa Wizaraione umuhimu wa kuwapatia wananchi Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Uhaba wa Mahakama zaMwanzo; Mahakama za Mwanzo pia zimekuwa ni chombomuhimu sana katika kutoa haki kwa wananchi wetu, lakinimaeneo mengi hayana Mahakama za Mwanzo na hatakama zipo basi zimechakaa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano katika Jimbo langula Kilindi yote tarafa nne, kata 21 na vijiji 102 tunazoMahakama za Mwanzo zisizozidi tano, hali hii ni mbaya sana.Ningeomba kauli ya Wizara na Waziri mwenye dhamana yaMahakama hizi ni lini watu wa Kilindi watapata Mahakamaza Mwanzo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa na Mahakama zaMwanzo Kata za Kimbe, Mgora, Kwekiku, lakini Mahakamahizi zote majengo yake yote yamekuwa magofu na hakunaMahakimu, je, lini Mahakama hizi zitajengwa upya? NiombeWaziri alichukue jambo hili kwa uzito mkubwa unaostahiki

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianzena kumpongeza Waziri Profesa Kabudi na watendaji wotewa Wizara kwa kutuletea bajeti yao ili tuweze kuijadili. Kunamambo ambayo nataka kuyapatia ufafanuzi wake nakushauri pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ucheleweshaji wa kesi zaubakaji; Mkoa wetu wa Iringa ni kati ya mikoa inayokabiliwana idadi kubwa sana ya kesi ya ubakaji na ulawiti. Inasikitishasana Bunge lililopita nilileta swali langu hapa Bungeni na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

252

niliweza kutoa takwimu ya mwaka 2016 kesi 217 lakinizilizoweza kufikishwa Mahakamani ni kesi 27 tu lakini kilamwaka katika mkoa wetu matukio ya ubakaji yanazidikuongezeka. Napenda kujua mkakati wa Serikali kuhusianana jambo hili ni kwa nini kusiwepo na Mahakama Maalumya kushughulikia kesi hizi. Matukio haya yamekuwayakiwaathiri watoto wetu kiakili pamoja na mama zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ucheleweshaji wamabadiliko ya sheria zilizopitwa na wakati; baadhi ya sheriazetu hapa nchini zimekuwa ni za muda mrefu sana nazimepitwa na wakati na kusababisha baadhi ya sheria zetuhapa nchini kutoendana na mabadiliko na kasi yamaendeleo ya Taifa na kuonekana kuwa zimepitwa nawakati. Mara nyingi sana sisi Wabunge tumekuwa tukiletahoja zetu hapa Bungeni lakini bado hatupatiwi majibu yakuridhisha. Kwa mfano, 12 Aprili, 2017 nilileta swali kuhusianana Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 lakini bado majibu yakehayaridhishi. Je, ni lini sasa Serikali italeta hoja ya kufanyamarekebisho ya kuboresha baadhi ya sheria zilizopitwa nawakati?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ufinyu wa bajeti, Wizara hiini muhimu sana na imekuwa na malalamiko mengi kwawananchi kutomaliza kesi zao au kuchukua muda mrefusana. Pia miradi mingi kutokamilika kwa wakati pamoja nabajeti yao kuwa kidogo sana lakini pia pesa yao imekuwaikicheleweshwa sana na kusababisha miradi kutokamilikakwa wakati hivyo kusababisha miradi hiyo kutumia pesanyingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza naunga mkono Hoja ya Serikali au Wizara ya Katibana Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunayo malalamiko katikaeneo hili la Mahakama. Hatuna Mahakama katika eneo laHaydom ambapo pana watu zaidi ya hamsini elfu na wapo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

253

pembezoni na Halmashauri ya Mji wa Mbulu ni kilomita 86toka Makao Makuu ya Wilaya ambapo ipo Mahakama yaWilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunacho Kituo cha PolisiHaydom ambapo tunaomba tujengewe Mahakama hataya Mwanzo. Tumekwisha tenga kiwanja cha kujengaMahakama. Kituo cha Polisi kinafanya kazi ya kukamatawabadhirifu na kuwasafirisha Mbulu zaidi ya kilomita 86 hivyokuipa Serikali gharama kubwa sana ya kupeleka mahabusu/watuhumiwa zaidi ya kilometa nilizozitaja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tujengeweMahakama Haydom maana wakati mwingine Polisi hutumiamabasi kusafirisha watuhumiwa na wakati mwinginekutoroka na kupotea. Hivyo naomba sana.

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipatia fursa hiiya kutoa mchango kwa njia ya maandishi. Napendakumpongeza Waziri wa Katiba na Sheria yeye pamoja nawataalam wake kwa kuandaa hotuba hii yenye kuoneshaubora na utaalam mkubwa. Katika kuchangia hotuba hii,napenda kuchangia maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, urejeshwaji wa wahalifu naushirikiano na Mataifa kwenye makosa ya jinai, hili ni jambozuri ambalo linaongeza ushirikiano na mahusiano mazuri kwaMataifa ya nje. Uhalifu ni jambo baya ambalo linahitajikupigwa vita kwa nguvu zote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu katika sualahil i, Serikali iwe makini katika utekelezaji wake.Inapotokelezea ulazima wa kuwapeleka wananchi wetu(wahalifu) ni vyema tukaangalia usalama wa nchitunayotaka kuwapeleka. Kwa mfano; juzi imetokezeawahalifu wa biashara ya unga ambao wanafika kupelekwaMarekani lakini hivi sasa katika nchi ya Marekani kuna vita yamaneno kati ya Marekani na Korea ya Kaskazini.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

254

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali hii inatisha na ni vyematukachukulia tahadhari kubwa. Korea ya Kaskaziniwametishia na wanaendeleza vitisho la kuipiga Marekanikwa silaha za nuclear, hii ni hatari kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maendeleo ya rasilimaliwatu, rasilimali watu ni jambo jema katika sehemu zote zamaendeleo. Ushauri wangu katika jambo hili ni kwamba,Serikali ni vyema ikawatayarisha kwa kuwasomesha nakuwapatia elimu juu ya masuala ya kisheria ili kuendelezaufanisi katika Wizara hii nyeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. MGENI JADI KADIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya njemana kuniwezesha kuchangia hotuba hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiukwaji wa haki zabinadamu, kwanza kuna jambo la kusikitisha kuhusu vijanawanaokwenda kufanya kazi za ndani katika nchi ya Uarabuni-Dubai. Vijana hawa wanateswa, wananajisiwa, wanauliwalakini hawana watetezi. Je, ni kwa nini Balozi zetu wanakaakimya na kwa nini hawafuatilii matokeo haya? Huu niukiukwaji wa haki za kibinadamu kwa hiyo Serikali yetu yaTanzania ifuatilie tatizo hili ni kubwa, Watanzania wetuwanapotea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Masheikh wetu waupande wa Zanzibar walishikwa huku Bara sasa ni miakaminne wako mahabusu mpaka leo upelelezi haujapatikana,basi sasa waachiliwe huru wakaishi na familia zao kwasababu jambo hili linaonekana ni la kisiasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Mahakama ya Kadhi,Mahakama ya Kadhi ni chombo cha Kisheria kwa dini yaKiislam. Chombo hiki ndicho kinachosimamia mirathi nandoa. Ni kwa nini nchi hii ina Waislamu wengi na inazuiachombo hiki?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

255

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi nyingi duniani zinazoMahakama ya Kadhi kama vile Kenya, Uganda, Zanzibar nakadhalika. Je, ni lini chombo hiki kitafanya kazi hapa Tanzaniabara kwa faida ya Waislam wa nchi hii? Naomba Waziriatakapofanya majumuisho nipate ufafanuzi tafadhali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya mchango huu,naomba kuwasilisha.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na kuunga mkono Hotuba ya Kambi ya UpinzaniBungeni. Naomba Serikali ione haja ya kuwaokoaWatanzania wanaoishi Wilaya ya Kilombero, Jimbo la Mlimbaambako jimbo zima pamoja na kuwa na miundombinumibovu lakini hakuna huduma ya uhakika ya Mahakama.Hivyo kupelekea watu wengi kukaa mahabusu kwa kukosausafiri ama mashahidi kushindwa kufika mahakamani kutoaushahidi, zaidi ya kilometa 260 hadi Mahakama ya Wilayailiyopo Ifakara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu, naombaMheshimiwa Waziri atembelee Jimbo la Mlimba; pili, tupatiwemahakama Jimbo la Mlimba; na tatu Mahakimu waajiriweili haki zipatikane.

MHE. MARY D. MURO: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuchangia kama ifuatavyo:-

Nishauri Serikali kuweka bayana mambo ya kisheriana kuyatendea haki mfano haki ya kujieleza, haki ya kupatahabari, haki ya kuishi, ni vizuri Serikali ikatendea haki maeneohayo ili taifa liwe na Amani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali itambuekuwa amani haiwezi kuwepo bila haki ambayo inatokanana utawala wa Sheria. Sheria za Ndoa na mirathi zipo lakiniwananchi wa kawaida hawana elimu ya sheria. Pia nashauriSerikali kufanya juhudi ili kutoa elimu ya sheria kama ilivyokwa matangazo mengine ya UKIMWI na madawa ya kulevya.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

256

Nashauri Serikali kutembelea mahakama zetu zilivyo nawafanyakazi wanaoishi na kufanya kazi katika wakatimgumu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nishauri kuhusu upelekajiwa wafungwa kutoka mahabusu imekuwa shida, hivyoSerikali iangalie kwa nini kutokana na ukosefu wa usafiri, kesizao huahirishwa mara kwa mara hivyo kusababishamahabusu kutumikia vifungo vyao kabla ya hukumu. Mfanohalisi mtuhumiwa anakaa mahabusu miaka minne kabla yahukumu, hivyo Serikali inaingia hasara ya kulisha mahabusu.Pia kupunguza nguvu kazi ya Taifa kwa kuwaweka gerezani.Nashauri Serikali iongeze fedha kwa mahakama ili kuongezautendaji.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,usikilizaji wa mashauri mahakamani; pamoja na Serikalikueleza 80% ya mashauri yameweza kusikilizwa, kasi hii badoinahitaji kuwekewa nguvu zaidi ili kuendelea kupunguzamrundikano wa kesi zilizopo mahakamani. Serikali lazima itienguvu na mkazo katika Mahakama za Mwanzo naMahakama za Wilaya kwani huko ndiko kwenye mrundikanowa kesi nyingi, jambo ambalo linawafanya wananchi wenyekesi mbalimbali kuendelea kutumia muda mwingimahakamani. Hata hivyo, haki inayocheleweshwa ni sawana haki iliyonyimwa. Nashauri Serikali iendelee kujipangakuhakikisha mrundikano wa kesi katika mahakama za chinizinakwisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taasisi ya Mafunzo yaUanasheria kwa Vitendo; pamoja na umuhimu wa Taasisi hiiya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo, ipo haja ya kuongezachuo hiki katika kanda nyingine za nchi hii. Ni ukweli kuwanchi hii ni kubwa na wanafunzi wanaohitaji kupata mafunzohaya ni wengi. Hivyo basi, ni muhimu kwa Serikali kuongezavituo vya mafunzo hayo kwa angalau Kanda ya Kaskazini,Kanda ya Kati, Kusini na Magharibi. Kwa kuongeza vituo hivyoitasaidia wanafunzi kumudu gharama za mafunzo na hivyokuongeza wanafunzi zaidi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

257

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,katika nchi yetu kuna hali ya kutisha kwa sababu ya utekwajiwa watu (wananchi) lakini Serikali imenyamaza kimya, mfanokutekwa kwa Ben Saanane. Naiomba Serikali ishughulikiesuala hili na hasa kumleta Ben Saanane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria zetu za jinai zimesisitizakwamba utekaji nyara kwa lengo la kuua au kuumiza mtu nikosa kubwa la jinai. Chini ya Kifungu cha 248 cha Sheria yaKanuni ya Adhabu, kwa mfano;

“Mtu yeyote ambaye anamteka nyara au kumtoroshamtu yeyote ili mtu huyo auawe, au aweze kutupwa ilikuwekwa katika hatari ya kuuawa, atakuwa anatenda kosana anawajibika kwa adhabu ya kifungo cha miaka kumi”

Kwa mujibu wa kifungu cha 250 cha sheria hiyo, kutekanyara kwa lengo la kumuumiza mtekwa nyara ni kosa la jinaivilevile na adhabu yake ni kifungo jela kwa muda wa miakakumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kuwazuia watuwasiwe na uhuru wa mawazo ni kukiuka Katiba ya nchi Ibaraya 18(a) inayosema:-

“Kila mtu-

(a) Anao uhuru wa kuwa na maoni na kuelezafikra zake”

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwepo nakamatakamata ya baadhi ya Wabunge na wananchiwengine kwa sababu ya kueleza au kutoa mawazo yao yakuikosoa Serikali. Naishauri Serikali kusikiliza mawazo hayona kuyatendea kazi kwani ni kwa njia ya kukosolewa Serikaliinaweza kuboresha utendaji wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ndoa za utotoni,naiomba Serikali kurekebisha Sheria ya Ndoa ili kuwatendeahaki watoto wa kike.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

258

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuzuia mikutano ya hadhara,hapa naona Serikali inakiuka Katiba ya Jamhuri ya MuunganoIbara ya 20(1) inayosema:

“Kila mtu anao uhuru wa kukutana na watu wenginekwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika, kushirikianana watu wengine, na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yakehadharani na kuanzisha na kujiunga na vyama au mashirikayaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendelezaimani au maslahi yake au maslahi mengineyo.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali iruhusumikutano ya vyama vya siasa kwani hii ni kulingana naKatiba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana nami niweze kuchangia kidogo kwenyeWizara hii nyeti ya Sheria na Katiba. Kumekuwa namalalamiko na kilio cha muda mrefu sana cha wafanyakaziwalioachishwa kazi Kilombero Sugar Company mwaka 2,000.Wafanyakazi hao karibu 3,000 walipoachishwa kazihawakulipwa stahiki zao na wamekuwa wakidai stahiki zaohizo kwa muda mrefu sana, wengine wameshatanguliambele za haki na wengine bado wapo hai. Wafanyakazi haowalipoona hawatendewi haki walikwenda Mahakamani nakukawa na Jalada la Kesi Namba 50/2000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wafanyakazi haowamekwenda mara kadhaa Wizara ya Katiba na Sheriawakiomba wapewe nakala ya hukumu ya jalada lao la kesiNamba 50/2000 bila mafanikio. Pia, waliandika barua kwaWaziri wa Wizara ya Katiba na Sheria tarehe 24 Machi, 2016na nakala kupelekwa kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ambayemnamo tarehe 25 Julai, 2016 (Kumb. Na. PM/P/1/569/82),Katibu wa Waziri Mkuu alijibu kuwa ameipata na ataisisitizaWizara ya Katiba na Sheria ishughulikie kikamilifu kwa mujibuwa Sheria.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

259

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnamo mwaka 2014Mahakama Kuu iliwapatia tamko la kuvumilia na kwamba,walikuwa wakilifanyia kazi, mpaka sasa hakuna majibu.Ndipo walipoamua kulipeleka Wizara ya Katiba na Sheriamwezi Julai, 2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, kwa niaba yawafanyakazi walioachishwa kazi Kilombero Sugar Company2000, namwomba Waziri atakapokuja kwenye majumuishoyake aje atupe majibu kwamba, ni lini sasa wananchi haowatapata haki yao ya kupata nakala ya hukumu ya kesiNamba 50/2000. Ni matumaini yangu mtawasaidia kilio chawanyonge hawa, ili wapate haki yao ya kulipwa mafao yaowanayostahili ambayo wamekuwa wakiyapigania kwamuda mrefu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza naanza kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwahotuba yake nzuri na pili, naunga mkono hoja. Napendakujielekeza katika ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo hasakatika halmashauri mpya kama ilivyo Halmashauri yangu yaItigi. Pia, kuna upungufu mkubwa wa Mahakimu waMahakama za Mwanzo na hata watumishi katika mahakamahizi. Nashauri Wizara yake iajiri Mahakimu wa Mahakama zaMwanzo na hasa vijijini, kama ilivyo Jimbo langu la ManyoniMagharibi. Halmashauri za Wilaya zina hadhi sawa na wilayaya kiserikali, hivyo zipewe hadhi ya kuwa na Mahakama zaWilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Wazirialitazame Jimbo langu la Manyoni Magharibi kwa jicho lakipekee katika ujenzi wa Mahakama za Mwanzo kwani,zilizopo ni chakavu na hazina hadhi, kama ilivyo Wizara yakoilivyo na heshima kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha nanarudia tena naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

260

MHE. VEDASTUS M. MANYINYI: MheshimiwaMwenyekiti, Mheshimiwa Waziri nakupongeza kwa hotubayako nzuri, nami naunga mkono hoja. Pamoja na pongezihizo napenda kupata ufafanuzi mdogo, mwaka jana JajiMkuu alipokwenda Musoma pamoja na shida mbalimbalina hoja zilizotolewa mbele ya Jaji, moja ilikuwa posho zaWazee wa Baraza kulipwa 5,000/= kwa kesi, vilevilekucheleweshwa malipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jaji Mkuu aliwaahidi waleWazee wa Baraza kulipwa 10,000/= badala ya 5,000/=. Mpakasasa wale Wazee wa Baraza wanalipwa 5,000/= na cha ajabutoka mwaka jana mwezi Septemba hawajalipwa hadi leo.Mheshimiwa Waziri, ikumbukwe kwamba, wazee hawawanakwenda Mahakamani tangu asubuhi hadi mchana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ufafanuzi namajibu ya maslahi ya wazee hawa. Ahsante na naombakuwasilisha.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, sasanitamwita Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamuda wa dakika ishirini watagawana na mtoa hoja ili mtoahoja atumie dakika arobaini. Mheshimiwa Mwanasheria Mkuuwa Serikali.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kunipatia fursa hii ili naminiweze kuchangia. Kubwa nakushukuru kwa jinsiulivyoliongoza Bunge lako Tukufu asubuhi kwenye sala amadua. Wabunge tuna tabia tunapofika hapa asubuhi shughulizetu kabla hazijaanza tunaanza na sala au dua.Unapotafakari maneno mazuri yaliyopo kwenye ile salahakika huwezi kuamini kwamba baada ya muda mfupi tuule tunaweza kusahau commitment yetu kwa Mungutukaanza ku-behave kama watu ambao hatukutambuamamlaka ya Mungu tunayemwomba kila siku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili nimshukuru MwenyeziMungu kwa kunipa fursa ya kuchangia hapa na aendelee

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

261

kutukuzwa sana. Pia nimshukuru Waziri na kumpongezaMheshimiwa Profesa Kabudi kwa hotoba hii nzuri ya bajetiyake ambayo naiunga mkono. Kusema kweli imezungumzamambo ya msingi ambayo yanalihusu Taifa hili. Kwa sababuhiyo, naungana nawe Mwenyekiti kwa ushauri wako ulioutoambele ya Bunge lako Tukufu muda mfupi uliopita kwambahotuba hii imesheheneza mambo ya msingi kwa mustakabaliwa Taifa hili. Laiti Wabunge tungeelekeza michango yetukwenye mambo mazuri yanayosimamiwa na Wizara yaKatiba basi tungeweza kuishauri Serikali vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kitu ambachonapenda kusema hapa kwamba Bunge kama Bungetunapaswa tutambue wajibu wetu. Wakati fulani huwanakaa hapa nasikiliza sana kwa makini, lakini hatuwezikuligeuza Bunge hili kuwa sehemu ya burudani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati mambo ya msingiyanazungumzwa kwa mustakabali wa Taifa hili halafu baadhiyetu tunageuza Bunge hili kuwa sehemu ya burudani na watuwengine wanaleta sauti za wanyama kama ulivyosema fisi,wakati fulani najiuliza mimi kama Mshauri wa Sheria wa Serikalihii hivi tutumie Sheria ya Afya ya Akili? Maana tunayo Sheriaya Afya ya Akili ambayo tunaweza kuitumia kuangalia kamabaadhi yetu akili zetu ziko sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mtu ambaye akiliyake iko sawa na anashiriki mjadala kuna namna yakushughulika na mjadala, mjadala ama ni kwa kuzungumzaau kwa maandishi lakini siyo kwa kuzomea au kwa kupigakelele. Unapofika hatua hiyo katika mjadala sisi ambaotumeshiriki sana kwenye mjadala, mimi nilikuwa Mwenyekitidebating club shuleni, ujue huyu mtu ameishiwa hoja za msingina kwenye hotuba kama hii hamkupaswa kuishiwa hoja zamsingi yapo mambo mengi ambayo yalipaswa yazingatiwe.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimishiwaMwenyekiti, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

262

pamoja na mambo mengine inataja mihimili mitatu ya dolana mgawanyo wake katika Ibara ya 4; Bunge linatungasheria, Mahakama inatafsiri sheria na kutoa haki na Serikaliinasimamia utekelezaji wa sheria. Sasa humu ndaniyamezungumzwa mambo ambayo mengine yameingiliakwenye mihimili mingine kwa mfano yale mambo ambayoyako Mahakamani, hayo hayapaswi kuletwa hapa Bungeni.Moja, yamezungumzwa hapa mambo ya kesi ambazo zikoMahakamani.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Zipi?

MBUNGE FULANI: Usimjibu Msigwa.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Huyu Msemaji waKambi ya Upinzani yeye mwenyewe ana kesi nneMahakamani analeta hoja hapa kuhusu mambo yaMahakamani. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaGodbless Lema ana kesi mbili Mahakamani. Hawa ambaowanashtakiwa kwa sababu ya kukiuka Sheria ya Makosa yaMitandao wana kesi Mahakamani. Kwa hiyo, mambo yotehaya ambayo yako Mahakamani tuyaachie mhimili waMahakama iyashughulikie. Bunge haliwezi kugeuka kuwandiyo mtunga sheria, Jaji na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna tuhuma, Bungelinapotunga sheria hapa maana yake zifanyiwe kazi. Bungehili lilitunga Sheria ya Cyber Crimes Act, Electronic TransactionsAct na sheria chungu nzima, kama wapo watu ambaowamekiuka zile sheria, Serikali iliyopewa jukumu la kusimamiautekelezaji wa sheria lazima ichukue hatua ipasavyo. Watuhawa wanaposhtakiwa Serikali isichukuliwe kwamba nidikteta au inanyanyasa, ndiyo wajibu wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kushauri, katikahotuba hizi zote na michango yote hii yale mambo ambayo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

263

yako Mahakamani Kiti chako kisiyatilie maanani na wananchiwayapuuze kwa sababu upo mhimili mahsusi kwa ajili hiyo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Subira Sunguraamezungumza juu ya utata wa umri wa mtoto wa kikekuolewa. Hili pia limezungumzwa na Mheshimiwa KitetoKoshuma, ni hoja za msingi sana lakini Serikali imekuwaikichukua hatua. Jana Waziri wa Katiba na Sheria alizungumzana atazungumza lakini suala hil i j insi l i l ivyo Serikaliimeshachukua hatua. Moja, kuna kesi Mahakamani. Kwahiyo, kwa vile kuna kesi iko Mahakamani Kanuni zetu naKatiba vinakataza tusiyazungumze haya humu ndani jamani.Tuna prejudice Mahakama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katiba hii Ibara ya 30(2)(d)inasema kwamba:-

“Kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine aumaisha binafsi ya watu wanaohusika katika mashaurimahakamani; kuzuia kutoa habari za siri; kutunza heshima,mamlaka na uhuru wa mahakama”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, pamoja namichango yao mizuri kuhusu huu utata wa umri wa kuolewakwa sababu kuna kesi Mahakamani, naomba kulishauriBunge lako Tukufu Wabunge wavute subira, tuiachie fursaMahakama, Mahakama itaamua, tuishie tu pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini mimba za utotoni piaSerikali imeshachukua hatua. Kwanza, kuna Sheria ya Kanuniya Adhabu ambayo inapiga marufuku mtu kujamiana namtoto wa kike ambaye yuko chini ya umri wa miaka 18.Ukifanya kitendo hicho basi unakuwa umetenda kosa lakubaka na adhabu yake ni miaka 30 na kama yuko chini yamiaka 12 ni kifungo cha maisha.

MBUNGE FULANI: Uwiiii.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

264

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, pia tumerekebisha Sheria ya Elimu kamaalivyosema Mheshimiwa Koshuma, mwaka 2016 hapa,tukaweka kwenye kifungu cha 60A kwamba ikawa nimarufuku mtu kuoa au kuolewa na mwanafunzi au kuozeshaau kwa namna yoyote kumfanya mwanafunzi aachekusoma, ni kosa la jinai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi ya hapo, tuliwapajukumu wakuu wa shule kwamba kila robo wawe wanatoataarifa za incidences case za ndoa, za utoro kwa Afisa Elimuwa Wilaya. Kwa hiyo, Serikali kama Serikali imechukua hatuaza kisheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, licha ya hilo, Serikali piaimechukua hatua za kisera, moja, imejenga sekondari za Katakila sehemu; sekondari nyingine zipo mpaka vijijini. Piaikaifanya elimu hii ya msingi mpaka sekondari kuwa bure.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ukingo uleuliowekwa unamwezesha huyu mtoto asome. Ni wakati ganianapata umri wa kuolewa? Polisi hawezi kuwa kila wakati,lakini Sheria ya Mtoto (The Law of the Child, 2009) kifungu cha(8) na (9) kinatoa jukumu kwa mzazi kuhakikisha kwambamtoto wake anapata elimu. (Makofi)

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara kaa chini.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, kwa hiyo, kwa kuwa Serikali imeweka sera hizi zaelimu bure, imejenga shule, imetunga sheria, ombi langu kwawazazi sisi, tuipe Serikali ushirikiano ili tuisimamie hii sheria nawatoto wetu wapate elimu. Kwa hiyo, wazazi tuna jukumuhilo la msingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa SabreenaSungura amezungumzia juu ya Serikali… (Kicheko/Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

265

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza masuala ya kidini,Waheshimiwa Wabunge hatuwezi kutumia Bunge hili kuletamtafaruku wa kijamii kwa kutumia Bunge hili kuwafanya watuambao ni ndugu wasielewane. Unapozungumza, unailaumuBAKWATA hapa, sasa unatambua taasisi gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katiba yetu Ibara ya 19inasema, masuala ya kidini na ya imani hayawezi kuingiliwana Serikali. Eeh, hatuwezi kwenda huko. Katiba iko wazi,kama kuna mgogoro uende kwa Kabidhi Wasii Mkuu, ndivyosheria zinavyosema. Hamwezi kutumia Bunge hili kupandambegu za chuki kwa wananchi wa Tanzania. We cannotallow this. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninashangaa hatamnayoyaleta humu ndani, nawe Mheshimiwa Kubenea,unajua vitu vinazungumzwa hapa, ngoja nianze kuwashauri.Hili la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam lazima tuheshimuSheria na Katiba tulizozitunga.

WABUNGE FULANI: Aaaaah!

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, tunayo sheria hapa, inaitwa Sheria ya Maadili yaViongozi wa Umma. Sheria hii inatoa fursa kwa sisi viongoziwa umma tunaokiuka kushitakiwa kule. Meya wa Ubungoamefungua kesi dhidi ya huyo RC, iko pale. Kwa hiyo, tusiwena haraka. Mnavyoiharakisha, mnaiharibu.

WABUNGE FULANI: Aaaaah!

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, sasa mnataka Mheshimiwa Rais achukue hatuagani dhidi ya huyu mtu wakati tayari iko kwenye mamlakanyingine inashughulikiwa? Ile Tume ikiona kuna mambo yajinai, itapendekeza, kwa sababu ina mamlaka mle yakupeleka PCCB, kupeleka polisi. Eeh, msiwahishe hivi vitu.Mnajua mkiingilia hizi kesi Mahakamani, mnaziharibu. Sisitunaoendesha kesi, kuna kitu kinaitwa mis-trial; na miminaende kule tunasema bwana umeshahukumiwa, hiyo kesi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

266

unaiharibu. Kwa hiyo, isije ikawa ni mikakati ya kuharibu hizikesi. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, vuteni subira.Utawala wa Sheria mnaoutaka ni lazima mzingatie hamwezikuwa mnaisema Serikali tu, na ninyi hamtaki kuizingatia hiyokitu. Kwa hiyo, RC anayo mamlaka yake ya uteuzi na sasahivi sijui ametuhumiwa amevunja, amepelekwa kwenye hiyoSekretariati. Let us be patient, hatuwezi kuwa tunahukumutu hivi hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, aaah, Mheshimiwa Shahariamezungumza hili la mashehe. Hili suala liko mahakamanina ni ushauri wangu tu ni kwamba tuliache Mahakamaichukue hatua. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wetu sisi tutajitahidikuharakisha uendeshaji wa kesi hii, ama upelelezi ukamilikemapema hatima yake ijulikane, lakini hili siyo jambo lakuzungumzia humu ndani, unajua masuala ya kuzungumziakesi zilizopo Mahakamani, mnaziharibu halafu mnaingiliauhuru wa Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ya Mheshimiwa Maige naMuswada binafsi tuliupokea ule Muswada unashughulikiwana Serikali. Kwa wakati muafaka atashirikishwa, kwa hiyonaomba Mheshimiwa Maige uwe na subira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Ester Mmasiametushauri vizuri sana Serikali. Ushauri wa Mheshimiwa Mmasini mzuri sana, kuna kila sababu ya sisi Serikali kuchukuamambo mazuri anayoyatoa pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ambacho naweza kuahidi,moja, tunachoweza kufanya, Mheshimiwa Waziri wa Nishatina Madini atazungumza wakati wa Bajeti yake, kunaumuhimu wa kuirekebisha ile sheria ili nako tuweke fursa localcontent kwa maana ambayo itazingatia ajira, fursa nyingine,goods and services na kadhalika; na hapa Watanzaniaanaowazungumza watapata hizo fursa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

267

Mheshimiwa Mwenyekiti, siwezi kwenda kwa undani,lakini ninachoweza kusema ni kwamba ni ushauri mzuri,Serikali itautafakari na muda muafaka WaheshimiwaWabunge mtaona matokeo yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli niseme tukwamba Mheshimiwa Mchengerwa ambaye pia niMwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria amelisaidia sanaBunge hili. Kwa hiyo, sisi kwa upande wetu tumeunga mkonomchango wake katika hili na tuseme tu kwamba kamaWabunge wote mkiwa mnatoa michango ya aina hiiingetusaidia sana. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba, hayamambo ya kuzungumza viongozi wa mahakama yakome.Kambi yenu ya Upinzani na hasa Msemaji wenu wa Upinzaniana tabia sana ya kuwasema Majaji Wakuu. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Ndiyo.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, sisi tumekuwa hapa kwenye Bunge, kila akiwemoJaji Mkuu, alikuwa anamshambulia sana Jaji MohamedChande amekuja huyu, naye anamshambulia tu. Sasa uliwahikuona anaingia humu ndani? Kwa hiyo, acheni. Wananchi,muwapuuze hawa watu. Huyo anayekaimu ana mamlakasawa na Jaji mwenyewe in full. Ndivyo tafsiri ya sheriainavyosema na wananchi waendelee kuwa na imani namahakama yao. Hakuna kitu chochote kinachovurugwa.Kama ni mashauri waende mahakamani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine la ushauri, tuzingatiesana sheria. Haiwezekani Serikali ambayo imepewa jukumula kusimamia utekelezaji wa Sheria, inapochukua hatua zakusimamia zile sheria mliozitunga ninyi wenyewe, mnasemahii ni Serikali ya kidikiteta, haiwezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unavunja sheria,unashitakiwa. Huwezi kushitakiwa halafu ukasema ni dikiteta.Mwalimu Nyerere alisema hivi, Serikali ni sheria. Hakuna kitu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

268

kinaitwa Serikali bila sheria na sheria zikishatungwa ni lazimazifuatwe. Ndiyo msingi wa utawala wa sheria mnaousemaMheshimiwa Shahari na ndiyo msingi wa Ibara ya 26 ya Katibaya nchi yetu inayotaka kila mtu kuzingatia Katiba na sheriaza nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hapa hakuna chadikteta. Nchi hii inaongozwa kwa demokrasia na taasisi zakezote za kidola likiwemo Bunge, Mahakama na Executive,vinafanya kazi kwa ufanisi; na Ma-Rais walioko madarakani,wameingia madarakani kidemokrasia kwa Uchaguzi Mkuu.Eeh, Mheshimiwa Rais Magufuli na Mheshimiwa Rais Shein,wala hapa hakuna cha Udikteta. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, ile ya kubadilisha Mawaziri na yenyewe ni kitucha kawaida. Mheshimiwa Rais amepewa mamlaka yakuteua Mawaziri wake na hatukuweka sheria ya ukomokwamba huyu ata-serve kwa muda fulani na akimbadilishaanampeleka Wizara fulani. Msianze kuwatisha viongozi.(Makofi)

Mazingira hayo mnayojenga kwenye jamii ya watukwamba kuna hofu imetanda, mwache. Kwa sababu hukonyuma mliwahi kusema kwamba mtaifanya Serikaliisitawalike, haiwezekani. Mliwahi kusema mtafanya nchiisitawalike, haiwezekani. Wakati ule mlichukua vitendo, sasamnaleta hoja kwamba hofu hofu, wakati mamboyanaendelea hapa. Shughuli zote za kijamii, kiuchumi, kisiasazinaendelea kama kawaida, halafu mnasema eti kwambakuna hofu. Haya lazima tuyapuuze. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia kushauri, hayamambo yote ambayo yametajwa hapa kwamba kesi sijuina vitu gani, haiwezekani ninyi mnashabikia wenginewashitakiwe, ninyi mkishtakiwa mnasema sijui tunaonewa.That cannot be the case. Kesi nyingine mnayosemawalifikishwa mahakamani wakaachiwa…

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

269

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa Mzungumzaji)

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja hii. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa MwanasheriaMkuu wa Serikali kwa mchango wako mzuri, umetuelimisha,tunakushukuru sana. (Makofi)

Tunaendelea, sasa namwita mtoa hoja ahitimishehoja yake, Mheshimiwa Profesa Kabudi, Waziri wa Katiba naSheria na muda wako ni dakika zisizozidi 40.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, awali ya yote napenda kumshukuru MwenyeziMungu kwa kuniwezesha kutoa hotuba yangu leo asubuhina kuwawezesha Waheshimiwa Wabunge kuchangia hotubaya Wizara yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekee,nachukua fursa hii kukushukuru wewe binafsi, kwanza kwamchango wako mkubwa kwangu katika taaluma ya sheria.Mimi na Dkt. Harrison George Mwakyembe baada ya kuhitimuShahada ya Sheria wakati wa mafunzo ya sheria, tukiwa StateAttorney grade III Mheshimiwa Chenge ulikuwa Mkurugenziwa Mambo ya Kimataifa na ulitusaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru pia, kwa miakamitano niliyoazimwa katika Ofisi ya Makamu wa Raiskushughulikia mambo ya mazingira, ambapo tulifikatukatunga Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, wewe ulikuwamsaada kwangu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka, naombaniliseme ndani ya Bunge hili, kazi ya Muswada ule haikuwarahisi, ilinizulia watu wengi na maadui wengi, wenginewalioona husuda ya fedha niliyolipwa; na wengine ambaohawakuelewa kwa nini sheria ile itungwe. Kwenye kikaokimoja unakumbuka nil itolewa kwa hali i l iyokuwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

270

haikunifurahisha. Hata hivyo, wewe uliniambia jambo mojana leo nataka niliseme; “In public service, learn to swallowyour pride. In public service learn to suppress your eagle.” Kwelimambo hayo sasa naona umuhimu wake ndani ya jengohili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru MheshimiwaGeorge Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwaushirikiano alionipa katika kutekeleza majukumu yangu nakwa kuungana na mimi katika kujibu baadhi ya hojazilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mara nyingine,naishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge la Katiba, Sheria naUtawala pamoja na Kamati ya Bajeti kwa maoni na ushauriwao ambao wameipatia Wizara na Taasisi zake katikakutekeleza majukumu yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizihakikishieKamati na Waheshimiwa Wabunge wote kuwa tumepokeamaoni, hoja na ushauri mliotupa katika mjadala wa Bajetiyetu na tunaahidi kufanyia kazi masuala yote yaliyojitokezakatika mjadala huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Kambi ya Upinzani,nashukuru pia kwa maoni yenu yaliyotolewa na kukubaliwana Bunge hili kutoka kwa Msemaji wa Kambi ya Upinzani wamambo ya Katiba na Sheria; ni mdogo wangu, kaka yakeMheshimiwa Tundu Lissu, Ndugu Alute Mughwai na mimitumesoma pamoja Milambo. Kwa sababu hayupo, sipendikuleta mambo ya mila hapa ndani, lakini wale wotetunaotoka Singida mnajua mila yetu na heshima kwa watu,eeh, kwa neno lililokataliwa jana, waliotangulia kwa ngaribakabla ya wewe. (Makofi/Kicheko)

Mhesimiwa Mwenyekiti, niseme hili, nimeshangaa sanakuwa watu katika jengo hili kubagazana. WaheshimiwaWabunge kama ni kawaida, ni kawaida mbaya. Hatuwezikubagazana. Jengo hil i siyo la kubagazana; natunabagazana kwa sababu kwa bahati mbaya tumepoteza

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

271

pia uelewa mzuri wa lugha ya Kiswahili. TunazungumzaKiswahili kikavu kama alivyosema Mheshimiwa, Riziki ShahariMngwali, tumepoteza uelewa wa Kiswahili wa kutumia lughaya kumfanya mtu mpuuzi ajue ni mpuuzi bila kumwambiampuuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ukimsikia muingerezaanakwambia your stupid, siyo muingereza. Muingerezamstaarabu ndani ya Bunge, atakwambia I am sorry, your levelof appreciation of issues is diminishing, which means you arestupid! Yes. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ugeni una faida wakusema mambo ambayo hayakufurahishi. Nimefundishawanasheria, na mimi nimefundishwa. Mwanasheria yeyoteworth being called a lawyer, he must have sense of respectand more so, as officer of the court to the judiciary. Ndiyomaana naanza kuelewa kwa nini nchi nyingine Bajeti yaMahakama hailetwi Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa vituambavyo vinanisumbua na nilisema siku ya hotuba yaMheshimiwa Mbowe na ninamheshimu sana kwa maturityyake, niliomba tusii-drag judiciary in our mucky politics. It isabominable! It is flabbergasting! Tusii-drag Mahakama katikamazungumzo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nitaanza na suala lauteuzi wa Majaji, ikiwa ni pamoja na Jaji Mkuu na naombamnisikilize; na kama hamniheshimu kwa umri wangu, I amabove 60, mniheshimu kwa utu wangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unajua nafasi ya Raisinagombewa, anachaguliwa…

MBUNGE FULANI: Kama Wabunge. (Makofi)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, nafasi ambayo ndiye mkuu wa nchi, naombamnisikilize.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

272

MWENYEKITI: Waheshimiwa pale, MheshimiwaMsigwa, nawaombeni sana jamani. Nawaombeni sana.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, nafasi ya Rais tunayempigia kura, Rais waTanzania, Rais wa South Africa hapigiwi kura, anachaguliwana Wabunge kama alivyo Waziri Mkuu. Ndiyo maana SouthAfrica chama ni juu. Rais Zuma, chama kinawezakikamwondoa leo, ndiyo kama kilivyomwondoa Mbeki.Hapigiwi kura. Lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,anapigiwa kura. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Spika wa Bunge, anapigiwakura. Mtu pekee wa mhimili ambaye hapigiwi kura,anateuliwa, ni Jaji Mkuu. Mnajua kwa nini?

WABUNGE FULANI: Hatujui.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Ni msingi wakuhakikisha mtu huyu anayeteuliwa kushika nafasi hiyo,aachwe bila laumu ya mpumbavu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme hivi, katikauteuzi wa Jaji, nafasi ya Jaji katika hili, kwanza siyo kwelikwamba hapajawahi kuwa na Kaimu Jaji Mkuu kwa kipindi.Mara baada ya Jaji wa mwisho wa Tanzania, muingerezaWindham kumaliza muda wake, Tanzania 1965, Mwalimuhakuona sababu ya kuwa tena na Jaji Mzungu. Ndipo jitihadazilianza za kutafuta Jaji mwafrika na huyo Jaji alipatikanakutoka nchi ya Trinidad and Tobago Telford Philip Georgies.Ilichukua muda kwa sababu Majaji walikuwa wanasita kujakwa sababu ya elimu ya watoto wao. Ni mwafrika, tenaalikuwa mweusi kuliko wewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa vitunawasifu waafrika, wamekaa kule miaka 500, wengine niweusi kuliko sisi; na ni Waafrika kuliko sisi kwa sababuwameishi ugenini. Ndipo nafasi ile ilikaa kwa kipindi kirefuikisubiri Jaji Telford Philip Georgies afike nchini aapishwe. Theseare facts. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

273

Mheshimiwa Mwenyekiti, alichaguliwa mwingineakaimu kwa sababu daima nafasi ya Jaji Mkuu haiwezi kuwawazi hata kwa dakika moja. Ndiyo maana hata Jaji Mkuuakisafiri, akiteuliwa mwingine kukaimu, anaapishwa. HakunaKaimu Jaji Mkuu ambaye haapishwi, hata kama atakuwaKaimu Jaji Mkuu kwa siku mbili, ataapishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ukiangalia Katiba,iko wazi kabisa, inamruhusu Rais kuteua Kaimu Jaji Mkuu nahaiweki mipaka. Haiweki, haiweki.Ukienda kwenye Katibampaka mwaka 2000 wakati Mwenyekiti akiwa AttorneyGeneral kabla ya hii 2005 kufanya marekebisho kupunguzamaneno, niwasomee tafsiri ya Jaji Mkuu ilikuwa inasemaje.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jaji Mkuu maana yake ni JajiMkuu wa Mahakama ya Rufani aliyetajwa katika Ibara 115(1)ambayo sasa ni 118 ya Ibara hii, ambaye ameteuliwa kwamujibu wa masharti ya Ibara ndogo ya pili ya Ibara hiyo ya118 au iwapo Jaji Mkuu hayupo au anashindwa kutekelezakazi zake kwa sababu yoyote, Kaimu Jaji Mkuu aliyeteuliwakwa mujibu wa masharti ya Ibara 118(4) ya Katiba hii na KaimuJaji Mkuu naye hayupo au anashindwa kutekeleza kazi yake,Jaji Mkuu, Jaji wa Mahakama ya Rufani aliyeko kazini kwawakati huo na ambaye yuko kwenye daraja la juu zaidi lamadaraka kupitia Majaji wote wa Mahakama waliopo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiisoma ya sasa inaelezawazi kabisa Jaji Mkuu ni nani, maana yake ni Jaji Mkuuanayetajwa kuteuliwa na ambaye majukumu yakeyameelekezwa katika Ibara ya 118 ya Katiba. Ukiisoma hiyoni pamoja na Kaimu Jaji Mkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake nini? Watuwengine wote wanaoteuliwa kukaimu, hawaapishwi. Ni JajiMkuu tu. Kaimu Jaji Mkuu anaapishwa, peke yake.Maanayake, kitendo cha kumwapisha kinampa mamlaka na ulinzikamili wa cheo hicho. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

274

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uteuzi wa Jaji Mkuu,mimi nalisihi Bunge liheshimu Mamlaka ya Uteuzi. Rais anayomamlaka kamili ya uteuzi na Rais anavyo vigezo vingi vyauteuzi na Rais msidhani ni mtu anayetembea, ni taasisi. Hivyo,kwa sababu ni taasisi, haina macho mawili tu, ina zaidi yamacho mawili, tuiache ifanye kazi yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwasihi sana WaheshimiwaWabunge, tuache Kaimu Jaji Mkuu afanye kazi yake.Tusimfikishe mahali tukamtweza. Kwa sisi wanasheria,tuheshimu sana mhimili huo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo napendanilizungumzie ni kuhusu Rais. Ndiyo maana dada yanguMheshimiwa Riziki Shahari Mngwali ametoa, ni kwelialichokisema. Kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba tulikuwana Kamati tatu; Kamati ya Maadili na Haki za Binadamu chiniya Mzee Ussi, Mwenyekiti; Kamati ya Muungano, chini yaMzee Butiku, Mwenyekiti na Kamati ya Mihimili, mimi nikiwaMwenyekiti. Watu walionisaidia sana, nikiri ni Kibibi MwinyiHassan kutoka Unguja, Zanzibar na Mheshimiwa Riziki ShahariMngwali kutoka Tanzania Bara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa kuzunguka kuletulikuta nafasi ya Rais watu hawaielewi. Nimekuja na maonihapa na mengine nimeyaacha. Watu hawaelewi nafasi yaRais, yaani kama kuna nafasi ilikuwa inazungumzwa mpakatunashtuka, ni nafasi ya Rais, mpaka tukajiuliza hawaWatanzania kwa nini nafasi hii hawaielewi? Tukabaini,tunachanganya mambo mengi katika nafasi ya Rais. Ndiyomaana tukasema, ni vyema tukapambanua tuelewe nafasiya Rais na Rais ni nani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais anazo nafasi tatu; moja,ni Mkuu wa Nchi (Head of State); pili, ni Kiongozi wa Serikalina tatu ni Amiri Jeshi Mkuu. Sasa yako madaraka ya nafasi yaRais kama Mkuu wa Nchi na kama Amiri Jeshi Mkuuyanayompa hadhi tofauti ambayo haistahili kubezwa nandiyo maana Bunge kwa Kanuni limezuia. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

275

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, Rais ni taswira ya nchi.Kwa nafasi yake ya Mkuu wa Nchi Rais ni taswira ya nchi.Malkia wa Uingereza kwa nafasi yake ya ukuu wa nchi, nitaswira ya nchi (Head of State). Kwa maana hiyo, yeye ndiyoalama ya umoja, yeye ndio alama ya uhuru wa nchi namamlaka yake. Kumuonesha kwamba yeye ni alama ya uhuruwa nchi, ndiyo maana Rais peke yake anafuatana na mtuambaye tumezoea kumwita mpambe, ambaye amevaamavazi ya kijeshi. Maana yake ni kwamba anawaonyeshakwamba huyu ndiye alama ya Serikali yenu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hiyo Rais anadhamana ya kukuza na kuhifadhi umoja wa kitaifa, anadhamana hiyo. Sasa ukiangalia madaraka ya Mkuu wa Nchi,yale huwezi kuyapunguza; lakini ukiangalia mamlaka yakeya Amiri Jeshi Mkuu, huwezi kuyapunguza na ukiangaliamamlaka yake kama Mkuu wa Serikali, kwa mujibu waKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania majukumu yaRais kama Mkuu wa Serikali, akiwa Mkuu wa Serikali, hayounaweza kuyapunguza. Unaweza kuyasimamia, unawezakuyadhibiti. (Makofi)

Mdogo wangu Tundu Lissu asubuhi ameeleza zilemakala ya mimi na Mlimuka na ya Mheshimiwa Dkt. HarrisonMwakyembe tuliyoandika wakati wa mfumo wa chamakimoja, tena tukielekea mabadiliko makubwa ya Katiba yamwaka 1985. Niseme hivi, mwaka 1985 hii Katiba, MzeeChenge yuko hapa, kwa maudhui hii siyo Katiba ya mwaka1977, ni Katiba ya mwaka 1985. Iliandikwa yote upya. Kwanini ilitwa Katiba ya mwaka 1977, ni kwa sababu TheConstituent Assembly haikuwa convened. (Kicheko)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa tuheshimiane tu!

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, ni kwa sababu Constituent Assembly haikuwaconvened na kwa nini Mwalimu haku-convene ConstituentAssembly? Mimi na Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe…

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

276

MBUNGE FULANI: Tulieni mfundishwe! (Kicheko/Makofi)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, hii ni kwa sababu wapo watu wanaoamini theConstituent Assembly is only convened once. Only convenedonce. Ndiyo maana nilipokuwa amidi, Kiswahili cha dini niamidi. Nilipokuwa amidi wa Shule Kuu ya Sheria, nimeanzishacourse mpya ya Legal History na nimeifundisha mwenyewe.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nilianza course yaLegal History? Ni kwa sababu niligundua vijana wetu wengiwanaidhani Tanzania ni hii ilivyo leo. Hii ilivyo leo haikuwahivi. Kabla ya mabadiliko yale, Bunge hili Wabunge wengihumu ndani walikuwa ni wa kuteuliwa na siyo wakuchaguliwa, ndiyo! Tena nina fahari sana ya kuwa Mbungewa Kuteuliwa, ndiyo. (Kicheko/Makofi)

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Bora wewe umeteuliwakwa akili.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, nitawaambia kuwa sisi wasomi hakunaDoctorate unayoiheshimu kama Honorary (Honoris Causa),ndiyo. Unapokuwa Doctor Honoris Causa, tena ukiwa multi…

MBUNGE FULANI: Hebu ingia kwenye kampeni kama…

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Shauri yako, sikukutuma.(Kicheko/Makofi)

Wewe umejituma mwenyewe. Kwa hiyo, wakati huoWaziri Mkuu yuko hapa hakuwa Mbunge wa kuchaguliwa,walikuwa ni Wabunge wa kuteuliwa. Ndiyo. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Wape sumu hao.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, wakati huo, Bunge lilikuwa ni Kamati ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

277

Halmashauri Kuu ya Chama. Sasa mtu asiyejua historiaatabeza mafanikio yaliyofikiwa. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Tango pori eeh.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Ndiyo maanaWangazija wana msemo, ukitaka kujua mafanikio ya mtuusiangalie kimo alichofika, angalia shimo alikotokea.(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme mara baada ya kilekitabu kutoka, ndugu yangu Mheshimiwa Dkt. HarrisonGeorge Mwakyembe yupo, wako Mabalozi waliodhaniMwalimu angetutia kizuizini, yuko hapa. Leo ninyi mnaongeaSheria ya Kizuizini hayupo! Tuliongea wakati yupo. Don’t dareme, don’t dare me. We spoke when the law was law andwhen the President was President. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ndiyo maanaKatiba hii kwa mapendekezo ya wakati huo Mwalimuanaondoka ilikubaliwa kabisa, lazima madaraka ya Raisyapunguzwe. Someni mapendekezo ya Halmashauri Kuu yaTaifa ya mwaka 1983/1984 na yalipunguzwaje? Moja yakuyapunguza ilikuwa ni kuanzisha cheo cha Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Uwaziri Mkuu wetu huu,siyo kama wa Uingereza, huu ni kama wa Ufaransa. Kwasababu ni kama wa Ufaransa ambapo Mzee Joseph SindeWarioba alitumwa kwenda kujifunza, Mzee Msekwa alitumwaIndia na Canada, Waziri Mkuu wetu huyu mkisoma Katibaanatokana na chama chenye Wabunge wengi na anapigiwakura ndani ya Bunge. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, aina hii ya Katiba yetuambayo una Mkuu wa Nchi ambaye amechauguliwa nawananchi moja kwa moja, siyo kama wa Afrika Kusini na unaWaziri Mkuu anayetokana na chama chenye Wabunge wengiau anayeungwa mkono na wengi, kinaweza kukupa ainaya government inayoitwa kwa Kifaransa kohavision.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

278

MBUNGE FULANI: Eeh!

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, kwa namna hiyo, madaraka ya Rais yakawayamepunguzwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pil i kubwalililofanyika mwaka huo, ilikuwa ni kuweka ukomo wa Rais.Mwalimu alitawala kama Rais miaka 23, anaondokamadarakani sisi ilikuwa ndiyo nchi ya kwanza Barani Afrikakuweka ukomo wa Rais kuwa ni vipindi viwili vya miaka mitanomitano. Eeh, kule Cameroon, Rais Ahidjo; Wafaransawalipomchoka Rais Ahidjo, wakamwambia anaumwa;alipoondoka akagundua haumwi, hawezi kurudi. Rais SédarSenghor wa Senegal alikuwa ndiye Rais wa pili kung’atukana yeye kuweka term limit. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu muhimu ndaniya Katiba hii, lilikuwa ni kuweka sura ya haki za binadamu.Hazikuwepo wakati huo, hazikuwepo. Ndizo hizo leo, Ibaraya 12 mpaka ya 29, hazikuwemo. Hayo ndiyo maendeleo namapito ambayo nchi hii imeyapitia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mabadiliko ya mwaka 2005kuhusu haki za binadamu, yaliyondoa clawback clauses zote.Tena yalikwenda mbali, hayakuondoa tu clawback clauses,yaliondoa hata enabling clauses.

MBUNGE FULANI: Muda unaisha.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Acha uishe. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninachotakakusema katika mambo ya Katiba, eeh, lecture room, kwasababu Waswahili wana msemo, mwana wa muhunziasiposana hufukuta. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ndugu zangu,tumefika hapa tulipofika kwa sababu nchi hii imejaliwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

279

kuchukua maamuzi kwa wakati, lakini maamuzi hayo nilazima yajenge umoja wa Taifa, maamuzi hayo ni lazimayajenge mshikamano, ni lazima yajenge utu, ni lazimayalenge ustawi wa watu. Ndiyo maana katika Katiba hii kamakuna Ibara naisoma kila siku, ni Ibara ya nane. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, at the bottom line wananchindio source ya mamlaka yote, sio sisi. Kwa hali hiyo, nashaurisana tutunze heshima ya Rais akiwa Mkuu wa Nchi, tutunzeheshima ya Rais akiwa Amiri Jeshi, lakini inapokuja kwenyenafasi ya ukuu wa Serikali, isimamiwe na ishauriwe. Hapandani ni kupitia kwa Waziri Mkuu na Baraza la Mawazirilililomo humu ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja mbalimbalizimetolewa, jumla ya Waheshimiwa Wabunge 24wamechangia hotuba yetu ambapo Wabunge 17wamechangia kwa maandishi na Wabunge sabawamechangia kwa kuzungumza. Miongoni mwa mamboambayo yamezungumzwa, yako ambayo yamegusa vyombona mambo mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na hoja zilizotolewakuhusu Mahakama; hoja kubwa iliyotolewa na Mahakamani kuhusu ujenzi wa majengo ya Mahakama. Ujenzi wamajengo ya Mahakama Kuu, za Wilaya na za Mwanzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kueleza kwaujumla kwamba moja ya changamoto kubwa zinazoikabiliMahakama ya Tanzania ni uhaba na uchakavu wamiundombinu. Mathalani katika ngazo ya Mahakama zaWilaya, tuna majengo katika Wilaya 30 na Wilaya nyinginehuduma zinatolewa katika majengo ya kuazima kutoka taasisinyingine za Serikali. Aidha, tuna Wilaya 23 zinapata hudumaza Mahakama katika Wilaya za jirani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kwa upande waMahakama za Mwanzo kuna Mahakama 960 tu kati yaMahakama 3,963 zilizopo nchini. Sasa katika kukabiliana nachangamoto hii, Wizara kwa kushirikiana na Mahakama

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

280

imeanza kutekeleza mpango wa ujenzi katika ngazi zote zaMahakama. Kwa hiyo, kupitia mpango huo, katika kipindicha miaka mitano tumepanga kuhakikisha kwamba mikoayote itakuwa na majengo ya Mahakama, ndani ya miakamitano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika hiyo miakamitano, imepangwa kujenga Mahakama za Wilaya 109 naMahakama za Mwanzo 150 katika maeneo mbalimbalinchini. Kwa hiyo, kwa msingi huo ni matarajio yetu kuwahadi mwaka 2021 Wilaya zote nchini ziwe na majengo yaMahakama, huo ndiyo mpango. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika mpango huoyapo maeneo ambayo tunaomba msaada, moja likiwaJimbo la Mheshimiwa John Mnyika, tusaidiwe kupataviwanja, mahali ambapo tunaweza tukajenga Mahakamana pia Wilaya nyingine. Nimetaja yako Mheshimiwa Mnyikakwa sababu nimeona umeleta mchango wako kwamaandishi na nimeu-note. Sasa tukishapata viwanja hivyo,itatusaidia sisi kuweza kujenga Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalolimeelezwa na michango ya Waheshimiwa Wabunge wengini kuhusu Mahakimu wa Mahakama ya Mwanzo kukaa mudamrefu katika kituo kimoja. Sasa hili limechangiwa na gharamaza uhamisho na vituo vya kuhamishwa kwa watumishi wotewa Mahakama ambao ni pamoja na Mahakimu wa Mwanzo.Gharama ya zoezi hili inakwenda takriban shilingi bilioni 2.3.

Kwa hiyo, Wizara yangu kwa kuthamini kwamba nivyema Mahakimu au Mahakama za Mwanzo wakawawanapata uhamisho, kwa sababu kukaa mahali pamojamuda mrefu na wewe unakuwa sehemu ya ile jamii.

Kwa hiyo, tunashirikiana Wizara na Mahakamakuhakikisha kwamba tunaongea na Hazina ili kulifanyia sualala upatikanaji wa fedha za uhamisho wa watumishiwakiwemo Mahakimu waliokaa kituo kimoja kwa mudamrefu. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

281

Mheshimiwa Mwenyekiti, l ingine ambalolimezungumzwa kuhusu Mahakama ni juhudi za kuondoamlundikano wa mashauri katika ngazi zote za Mahakama.Sasa Mahakama ya Tanzania pia imeweka muda maalumwa mashauri kuwa mahakamani. Kwa Mahakama zaHakimu Mkazi na Mahakama za Wilaya, shauri linatakiwakukaa mahakamani kwa muda wa miezi 12. Mahakama zaMwanzo, shauri linatakiwa kukaa muda wa miezi sita tu. KwaMahakama za Mwanzo hazina mashauri yanayozidi miezi sita.Sasa kama ambavyo tumeeleza katika hotuba yetu namaelezo ya Mahakama, Mahakama ya Tanzania imejiwekeampango wa kuondoa mlundano wa mashauri katika ngazizote za Mahakama, iwe ni Mahakama ya Hakimu Mkazi auya Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia katikaMahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya zinamashauri 2,912 yanayoangukia kwenye mlundikano. Mashaurihayo yako katika Programu Maalum ya Uondoaji waMlundikano wa Mashauri inayoendelea nchi nzima.Nachukua fursa hii tena kuipongeza Mahakama kwa kazikubwa waliyoifanya katika kuhakikisha kwamba kesi zote zauchaguzi wa Wabunge na Madiwani zinamalizika ndani yamuda uliopangwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili ni la kihistoria nani vyema tukaipongeza Mahakama, kwa sababu ni mara yakwanza kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi zimemalizikakatika kipindi kifupi. Huko nyuma tunafahamu, mpaka kipindicha Bunge kilikwisha kesi bado zinaendelea Mahakamani.Kwa hiyo, ni imani yangu kwangu kwamba rasilimali fedhaikiongezeka, uhamisho wa Mahakimu utafanyika, ajira zaidizitapatikana na majengo ya Mahakama zaidi yatajengwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonapenda kulizungumzia ingawa Mwanasheria Mkuu waSerikali amelizungumzia na mimi pia napenda nilizungumzie.Suala lolote linamlohusu Mtanzania yeyote au mtu yeyotekufunguliwa mashtaka na kupelekwa Mahakamani au

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

282

kuwekwa mahabusu au rumande, siyo suala ambalo mtuyeyote angelifurahia. Tungependa uhalifu usiwepo,tungependa wahalifu wasiwepo, lakini hulka ya binadamu,tunatenda makosa. Makosa yakitendeka kwa mujibu washeria, lazima mtu aitwe, ahojiwe, kesi ifunguliwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimeanza na hilo,niliseme wazi. Serikali haifurahii kuona watu wako ndani.Ingetokea muujiza leo pakawa hakuna uhalifu na Magerezayakafungwa, lingekuwa ni jambo la furaha kubwa sana, lakinihuo ni utashi na mapenzi ambayo ni vigumu kuyatekeleza.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama alivyosemaMwanasheria Mkuu wa Serikali, moja ya mambo ambayoyamezungumzwa sana humu ndani, ni suala la kesi inayohusuMashehe wa Zanzibar ambao wameshitakiwa chini ya Sheriaya Kuzuia Ugaidi (Prevention of Terrorism Act) ambayoinatumika Tanzania Bara na Zanzibar. Sasa maadam sualahili liko mahakamani, kama alivyosema Mwanasheria Mkuuwa Serikali, sisi kazi yetu kubwa tuharakishe uchunguzi na kesiikamilike mahakamani. Sasa uchunguzi unategemea mambomengi ambayo pia siyo vyema kuanza kuyazungumza ndaniya Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosemaMwanasheria Mkuu wa Serikali kufanya hivyo tutakuwabadala ya kuisaidia kesi hii, labda tukaivuruga zaidi. Kwa hiyo,naomba tuendelee kuviachia vyombo vinavyofanya shughulihiyo pamoja na Mahakama na wachunguzi lakini kwa kadriinavyowezekana kesi hii kama kesi nyingine zozote zileimalizwe mapema iwezekanavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalolimezungumziwa na Waheshimiwa Wabunge ni suala zima laKatiba mpya. Napenda nirudie maelezo yale yaliyotolewa.Katika jambo hili niseme kama nilivyoeleza katika maelezoyangu kwenye Kamati nilipoulizwa, Serikali inatambuaumuhimu wa Katiba mpya, lakini Katiba siyo kitabu hiki tu.Ziko nchi hazina katiba iliyoandikwa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

283

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waingereza hawana Katibailiyoandikwa. Ukiwauliza Waingereza leo Katiba yao ni nini?Ni mila na desturi. Israel haina Katiba iliyoandikwa; na kwakuwakumbusha, Zanzibar toka mwaka 1964 baada yaMapinduzi mpaka mwaka 1979 haikuwa na Katibailiyoandikwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo, mimi naMheshimiwa Dkt. Harrison George Mwakyembetutamkumbuka Mwalimu wetu wa Katiba, Profesa Srivatavaaliyetuambia Katiba siyo hicho kitabu, ni ujumla wa maishayenu yote, matamanio yenu, matarajio yenu na shida zenu.Hii ambapo Waingereza wenyewe hawakuwa na Katiba yakuandika na mpaka leo hawataki, walituandikia sisi na sijuiniliseme maana yake nimekuwa Waziri, wakiamini kwambaninyi hamna uwezo wa kuwa na mila na desturi zinazostahilikuwa Katiba. Kwa hiyo, wawaandikie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana Katiba yetu yauhuru ya mwaka 1961, actually it was a schedule to an Act ofParliament which was passed by the House of Commons. TheTanganyika Order in council and accented by the Queen, notin Buckingham Palace, in St. George Chapel, Windsor . (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, maana yake kamaalivyosema dada, Mheshimiwa Riziki Shahari Mngwali, Tumeya Mabadiliko ya Katiba ilitoa siyo Rasimu tu; tuliangaliaRasimu tu na nimekutaja kwa kazi kubwa uliyofanya. TulitoaJuzuu hii, maoni ya wananchi kuhusu sera, sheria nautekelezaji, iwe sehemu ya hiyo Katiba inayoishi. Ndani yamambo hayo, niwasomee moja tu ambalo wananchiwalituambia, ni safari za viongozi, ukurasa wa 38 kwambasafari za viongozi ziwe na kikomo. (Makofi)

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Hatujasikia Mheshimiwa.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, sasa huyu anasafiri sana? Wakasema, malengoya safari za nje za viongozi yawe wazi kwa wananchi.Niwaambie jambo moja walilolisema, na mimi ningetamani

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

284

liwe, matumizi ya neno mheshimiwa, mapendekezo yawananchi. Mapendekezo ya wananchi kuhusu matumizi yaneno mheshimiwa yalikuwa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, neno mheshimiwa lisitumikekwa Wabunge na viongozi wengine wa umma, badala yakeneno ndugu litumike ili kuondoa matabaka na kuwakwezaviongozi juu ya wananchi ambao kimsingi ndiowaliowaweka madarakani. (Makofi/Kicheko)

MBUNGE FULANI: Tutakuwa tunaitana ndugu.

MBUNGE FULANI: Sasa unashangiliwa kila upande.

MBUNGE FULANI: Tuanzie kesho.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, lakini sehemu kubwa kama alivyosemaMheshimiwa Shahari Mngwali…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKTI: Mheshimiwa Waziri, malizia tu.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, kama alivyosema Mheshimiwa Shahari Mngwali,kitu kikubwa kilichozungumzwa na wananchi humu, ni maadiliya viongozi. Moja, wananchi walipendekeza viongozi wotewakiapishwa, waape maadili ya viongozi. Tunaapa auhatuapi?

WABUNGE FULANI: Tunaapa. (Makofi)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, kwa hiyo, mimi, mimi, mimi…

MBUNGE FULANI: Muongezee nusu saa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

285

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, mimi kitabu hiki nitakikisha tunakipa uzitounaostahili kwa sababu ndiyo maoni ya wananchi ya Katibainayoishi. Kwa hiyo, tayari matashi ya wananchi yameanzakutekelezwa. Ndiyo maana kwa sasa kama nilivyosemakwenye Kamati, kazi tunayoifanya ni kazi ya kuzichambuasheria, ndiyo maana haina kasma. Si ni kazi za siku zote, ndiyomaana haikutengewa fedha, kwa sababu ni kazitunayoifanya ndani ya Serikali. Ni kazi ya kila siku, tunaangaliasheria zote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hivyo tu, nawaambiamambo makubwa kama haya hayataki shinikizo. Mambomakubwa kama haya yanataka umuombe Mwenyezi Munguakufanye uwe mwerevu kama nyoka na mpole kama hua iliufikie unapotaka Taifa likiwa moja. (Makofi)

(Hapa kengele ya pili ililia kuashiria kwisha kwamuda wa Mzungumzaji)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, wananchi na Wabunge wametoa maoni mengina ninataka niwahakikishie kwamba maoni yotetumeyapokea na kwa utaratibu uliopangwa na Bunge,tutahakikisha kila aliyetoa hoja yake, jibu lake linapatikanakwa utaratibu uliopo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

MBUNGE FULANI: Muongezee muda.

MWENYEKITI: Ahsante. Hoja imetolewa, imeungwamkono. Profesa tunakushukuru sana kwa mchango wako nakwa elimu uliyotoa kwa Waheshimiwa Wabunge nawananchi. Endelea hivyo. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

286

MBUNGE FULANI: Sindano imewachoma.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, kablahatujaingia kwenye Kamati ya Matumizi, nachukua nafasi hiikutoa tangazo tu kwa sababu ya muda, tuna wageni hapaambao siyo lazima wakakaa na sisi mpaka mwisho, nao niwageni wa Mwenyekiti wa TWPG, Mheshimiwa Margaret Sittaambao ni wageni kutoka Taasisi ya Girl Guides Tanzaniawakiongozwa na Profesa Martha Qorro. Mko wapi?Msimame, simameni. Karibuni sana wageni wetu, mmejioneashughuli za Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.Karibuni sana. Katibu! (Makofi)

NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU MEZANI:

KAMATI YA MATUMIZI

MATUMIZI YA KAWAIDA

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae.

Fungu 41 – Wizara ya Katiba na Sheria

Kif. 1001- Admin. and HR Management... Shs. 5,484,469,000/=

MWENYEKITI: Huo ndiyo mshahara. Ndiyo, lakini ninyiWaheshimiwa Wabunge msifikirie kwamba kwa sababu tunautaratibu huu, eti hakuna kusimama. Shauri yenu, lazimamsimame kuandika. Eeh, sawa na msije mkashangaa.

Mheshimiwa Tundu Lissu, Mheshimiwa Abdallah AllyMtolea, Mheshimiwa Balozi Adadi Rajab, Mheshimiwa CosatoChumi na Mheshimiwa Amina Mollel.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mbogo.

MWENYEKITI: Kwa uwiano wetu, kwenye eneo hililazima nitende haki, ni matakwa ya kanuni. Tunaanza naMheshimiwa Amina Mollel.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

287

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi. Katika mshahara wa MheshimiwaWaziri, mimi narejea katika Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabungewamezungumza mengi, vilevile Mheshimiwa Waziriamezungumza mengi pamoja na AG, lakini hili ni sualaambalo kwa kweli kwa muda mrefu Waheshimiwa Wabungena jamii yote kwa ujumla imekuwa ikilizungumzia sana nalina madhara makubwa kwa watoto wa kike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumemsikia MheshimiwaWaziri jana/juzi katika mojawapo ya maswali alilielezea kwamapana na akaelezea mengi tu. Kubwa hasa tunalotakakujua na endapo sitaridhishwa na majibu ya MheshimiwaWaziri nitakamata mshahara wake. Tunataka kujua ni linisheria hii italetwa humu ndani i l i iweze kufanyiwamarekebisho, kwa sababu madhara wanayopata watotowa kike ni makubwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria hii inaruhusu mtotoaolewe chini ya miaka 18 na hapo hapo katika sheria hiitulipitisha sheria hapa mwaka 2016, inayosema kwambaukimpa mtoto wa kike mimba chini ya miaka 18 unafungwamiaka 30 jela. Kama unafungwa miaka 30, iweje mtoto huyuaolewe chini ya miaka 14? Kwa maana hiyo, sheria hizi mbilizinakinzana. Napenda tu kutoa mfano, katika Mkoa waShinyanga kati wa watoto 100, watoto 58 mpaka 59wanaolewa na sheria hii hamtaki kuileta hapa. (Makofi)

MWENYEKITI: Kwa nini umechukua Mkoa waShinyanga? (Kicheko)

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, niutafiti na pengine wewe ni mwanasheria mzuri na unatokahuko, sasa ushuhudie kwamba ni kwa jinsi gani pamoja nakwamba unatoka huko watoto 59 kati ya 100 wanaolewa.Siyo Shinyanga tu, ukienda Tabora 58 pia wanaolewa, ninayehapa mwanasheria pia…

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

288

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante, umeeleweka.

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,endapo sitaridhika na majibu ya Mheshimiwa Waziri, nitatoahoja ili basi Wabunge wote waweze kuchangia na tuwezekuomba ni lini sheria hiyo italetwa katika Bunge hili tufanyiemarekebisho. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri au AG.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nianze kwa kumshukuru sanaMheshimiwa Amina Mollel, Mbunge. Na mimi kujibu maswaliya akina Amina napata shida kwa sababu mke wanguanaitwa Amina na kwa maana hiyo ni lazima nilijibu kwaheshima sana ili nitunze jina la heshima la mama wa MtumeMuhammad Swalallahu-Alayhi Wasalam. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa kamanilivyosema jana, kama ni matashi yangu mimi ningekwendana maoni hayo, lakini kwa utaratibu wa Serikali yako mambomuhimu ambayo lazima yachukuliwe kabla ya hayotunayoyatamani kufanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa ambayo napendakuitoa ni kwamba tayari utaratibu wa ndani wa Wizara wakuipitia Sheria ya Ndoa umekamilika na nimeanza kuipitia ilina mimi niweze kutoa maoni yangu kuhusu taarifa hiyoambayo hatimaye kwa utaratibu unaotakiwa itafikishwakatika vyombo husika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda tu niseme kwambaSheria ya Ndoa ya mwaka 1971, ukiondoa huu upungufu wahapa na pale, ni sheria ya kimapinduzi. Sheria hii ni yakimapinduzi. Ni sheria ambayo katika Bara la Afrika Kusinimwa Sahara ilikuwa ya kwanza kupitishwa ambayo ililengakumkomboa mwanamke.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

289

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mifano tu michache.Moja, sheria hii ya 1971 kwa mara ya kwanza iliondoa tafsiriya cohabitation yaani maana ya wanandoa kuishi pamojakuwa na maana ya kuishi ndani ya nyumba moja na chumbakimoja. Leo hii kwa mujibu wa sheria yetu ya mwaka 1971,cohabitation sasa ni pamoja na whatsapp, mnapotumianawhatsapp na mkeo au mmeo, tayari mna-cohabit siyo lazimamuwe pamoja. Kabla ya hapo ilikuwa ni lazima muishipamoja. Matokeo yake ni nini? Wanawake wengiwalishindwa kupata madaraka makubwa, kwa sababuilikuwa ni lazima waishi walipo waume zao, leo siyo hivyo.(Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, l ingine zuri tu kabisaliliwekwa humu ndani, ni kuhusu suala zima la presumption ofmarriage. Presumption of marriage bahati mbayaimetafsiriwa isivyo, maana yake siyo ndoa ipo, ila inapotokeamwanamke ameishi na mwanaume na jamii imewachukuliakuwa ni mke na mume na hawana vizuizi vya ndoa na sasamahusiano hayo yanavunjika, Mahakama ita-presume therewas a marriage i l i mwanamke huyo na watoto haowasiondoke mikono mitupu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata ikitokea ikionekanakwamba pana kasoro kwamba hawa walikuwa ni maharimuyaani watu wasioruhusiwa kuoana, bado sheria hiyo inasemawale watoto wapewe haki na watunzwe.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, muhimu ni necessary of life. Sasa kwa sababuhiyo, yapo mambo mengi ambayo tunayapitia ikiwa nipamoja na kifungu cha umri wa mtoto ili kwa pamoja Serikaliitakapoleta mabadiliko ya Sheria ya Ndoa yasiwe tu yakipengele kimoja cha umri, bali na mambo mengine yoyote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, muipe Serikalimuda, iyapitie mapendekezo yote yaliyoletwa na hatimaye

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

290

tuone ni jinsi gani jambo hili tulilete, lakini kwa kulinda yalemazuri yaliyomo ndani ya ile sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeanza na hayo kwasababu tendency ni kui-dismiss sheria yote, inayo mazuri nainayo yaliyopungua, lakini tutafanya hivyo. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana. Mheshimiwa Mollel,baada ya assurance hiyo ya Serikali bado unataka tenakuongea?

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na majibu hayo mazuri ya Mheshimiwa Waziri, badonakamata mshahara wake na nina sababu za msingi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watoto wa kikewanalitegemea Bunge hili, watoto wa kike ndio Taifa la keshoambao tunapozungumza hapa hivi tafiti mbalimbali…

MWENYEKITI: Nenda moja kwa moja unakotaka.

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kutoa hoja ili Wabunge waweze kuzungumza,waweze kujadili na Serikali basi iweze kulifanyia kazi tujuekwamba ni lini sheria hiyo inaletwa humu ndani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hojaWaheshimiwa Wabunge.

MHE. ZAYNAB M. VULLU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naafiki.

(Hoja ilitolewa Iamuliwe)

MWENYEKITI: Haya. Tutachukua wawili tu; wawiliupande huu na wawili upande huu.

MBUNGE FULANI: Huku Mwenyekiti, kushoto kwako.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

291

MWENYEKITI: Mheshimiwa Vulu, MheshimiwaJacqueline, Mheshimiwa Salome na Mheshimiwa Dkt.Suleiman. Tunaanza na Mheshimiwa Dkt. Suleiman.

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona. Mimi siungi mkonohoja ya Mheshimiwa Bi. Amina. Siungi mkono kabisa kwasababu suala la ndoa linaambatana na masuala ya dini naimani. Kwa imani yetu ya kiislamu hatukuwekewa mudamaalum wa mtoto wa kiume kuoa au mtoto wa kikekuolewa. Kutokana na hali hiyo…

MBUNGE FULANI: Lete aya.

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF: Aya zipo nyingi,hakuna haja ya kuleta aya.

MBUNGE FULANI: Lete aya.

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF: Aya zipo nyingi.Mtume Swalallahu-Alayhi Wasalam kwa mfano, katuambiakatika mambo ambayo yanatakiwa yafanywe haraka nimtoto wa kike kuolewa anapofikia ukubwa. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF: MheshimiwaMwenyekiti, kutokana na hali hiyo, naomba uchunge mudawangu…

MBUNGE FULANI: Ongea, ongea.

MWENYEKITI: Ongea Mheshimiwa.

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF: MheshimiwaMwenyekiti, nilisema siungi mkono hoja hiyo na kama italetwahapa Bungeni, basi patachimbika, kabisa kabisa.

MBUNGE FULANI: Uamsho.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

292

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tumekuelewa!

MBUNGE FULANI: Msiingilie imani za dini. Msiingilieimani za dini.

MWENYEKITI: Waheshimiwa polepole! Tulielewa.Mheshimiwa Zaynabu Vulu.

MHE. ZAYNABU M. VULU: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Awali ya yote niseme Mheshimiwa Waziri amejitahidikuelezea vizuri, lakini hoja yangu iko pale pale; ni kwambatunapozungumzia suala la mtoto wa kike kuolewa, tunaingizaimani za dini, mila na tamaduni. Sidhani kama Serikaliinashindwa kusimamia yote hayo, ikatuletea hapa bilakuathiri mila za aina yoyote ile. Naomba niishie hapo. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa SalomeMakamba.

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangiasuala hili la muhimu la ndoa za utotoni. Naungana naMheshimiwa Amina Mollel kupinga ndoa za utotoni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mimba za utotonisiyo suala la kuleta mjadala mrefu hapa. Mahakama marazote tukikaa hapa, suala la ndoa za utotoni tunasematusiingilie maamuzi ya Mahakama. Mahakama ilikaa, kesiikafunguliwa na ikafikia hatima. Kesi iliyofunguliwa mwaka2016 imetolewa maamuzi na Jaji Kihiyo pamoja na Jaji Munisitarehe 8 Julai, 2016. Wamesema kwamba ndoa za chini yamiaka 18 ni marufuku. Jaji huyo akaenda mbali na kusemakuwa, ukisoma judgment, Mwanasheria Mkuu wa Serikalipamoja na Waziri wetu wa Sheria mtusaidie. (Makofi)

Mhehsimiwa Mwenyekiti, hukumu inasema ndani yamwaka mmoja Attorney General pamoja na Waziri wa Sheriawalete sheria hii Bungeni tuibadilishe. Haya ni maagizoyaliyotolewa na Mahakama. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,wakataka ku-dilly dally hili suala la kulipeleka kule wajifanye

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

293

wanataka kukataa rufaa, wakashindwa. Tunashikilia hukumuipi?

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ndoa za utotoni ni kinyume na katiba, miaka 18 ndiyo mtotoanatakiwa kuolewa… (Kicheko)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Muda wako umekwisha.

Waheshimiwa Wabunge, naongeza muda usiozididakika 30 tufanye majukumu yetu vizuri. MheshimiwaJacqueline Ngonyani.

(Hapa baadi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Naomba niungemkono hoja ya Mheshimiwa Amina Mollel kwa hoja zifuatazo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama unavyofahamukwamba umri wa mtoto wa kike na wa kiume kuwezakujitegemea wakati ambapo atakuwa anajitambua kujuazuri na baya ni umri wa miaka 18. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sioni sababu wa kuwahishashughuli, kumuozesha mtoto akiwa na miaka 14 kwa sababuakiwa na miaka 18 ndiyo atakuwa anajua barabara shughuliyenyewe namna ya kwenda. Kwa hiyo, niseme tu kumuozeshamtoto miaka 14 yaani hii ni sawasawa na mateso bila chuki.(Kicheko/Makofi)

Kwa hiyo, naona ni vizuri mtoto akiwa na umri wamiaka 18 ndiyo aweze kuozeshwa kwa mujibu wa sheriaambayo tunataka kuileta hapa kurekebishwa tena ileteharaka sana ili tuirekebishe na tutaisimamia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

294

MWENYEKITI: Mheshimiwa Simbachawene.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mtuyeyote aliyesoma sheria, jambo hili lazima lilimpasua kichwa.Nataka niwashawishi Waheshimiwa Wabunge, tukubalianena position ya Serikali. Sababu ni moja tu, kuna conflict ofinterest za jambo hili. Ili uweze kufanya uamuzi mzuri wakuzingatia makundi yote ni lazima ukubali kuna cha kutoana cha kuchukua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hiyo, Serikalitumesema jambo hili tunalijadili na tunazingitia mapendekezomengi. Hapa kuna mgogoro wa kidini, lakini nataka niwaulize,kuna mgogoro pia wa kibaiolojia, kimaumbile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi mtoto wa kike anavunjaungo akiwa na miaka kuanzia 12, 13, 14 mpaka 15. Siku hiziwanavunja ungo mpaka na miaka 10. (Kicheko/Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Naomba mnisikilize. Sasa kamahamnisikilizi…

MWENYEKITI: Haya, order, order!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kamatutasema kifungu cha 13 na 17 vya Sheria ya Ndoa; kifungucha 17 kinasema, mtoto ambaye ni chini ya umri wa miaka18 ataolewa endapo wazazi wake wataridhia. Sasa hililinazingatia nini? Tuchukue kwamba aliingia darasa lakwanza akiwa na miaka saba, anamaliza darasa la sabaakiwa na miaka 14, hahitaji kwenda hiyo sekondari yenu,hahitaji chochote yupo. Halafu sheria iseme, halafu amepatamchumba, halafu mchumba mwenyewe yuko vizuri, anatakakumuoa halafu sheria inamzuia…

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

295

MHE. KOSHUMA Z. KITETO: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, sheriainamzuia, inamtaka toka miaka 14 mpaka afike miaka 18 au19 au 20. Watakwenda kufungua kesi Mahakamani wapingesheria hii…

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mwanao wa kike anakuona.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo,naomba tukubaliane na position ya Serikali, acha tukae natutafakari yote haya kwa umoja tuone itakuwa katika positionya namna gani na itakuja Bungeni na Wabunge tutatungasheria.

MBUNGE FULANI: Taarifa.

MWENYEKITI: Nakuelewa.

Waheshimiwa Wabunge, mnaona jinsi huu mjadalaunavyonoga. Utakuja kuwa mtamu zaidi wakati Serikaliitakapoleta muswada.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti,hukumu ya Mahakama haijadiliwi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mollel, hitimisha tuamuesisi.

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaimani sana na Serikali. Nina imani sana na Waziri kwa sababundiyo ameingia tu katika Wizara hii…

WABUNGE FULANI: Aaaaaah!

MHE. AMINA S. MOLLEL: Tulieni.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

296

MBUNGE FULANI: Lakumnidukum Walyadin!

MHE. AMINA S. MOLLEL: Kwa sababu kamaalivyosema ndiyo ameingia tu kwenye Wizara hii, MheshimiwaWaziri umebeba dhamana ya watoto wa kike wa Taifa hili.Watoto wa kike wanakutegemea wewe. Pamoja nakuonesha kila mmoja anaegemea upande wake, lakinilazima tufike mahali tukubaliane wote ili kumnusuru mtotowa kike. (Makofi)

MWENYEKITI: Kwa kifupi.

MHE. AMINA S. MOLLEL: Kama alivyosemaMheshimiwa Waziri, mke wake ni Amina, mimi ni Amina,nakurudishia mshahara wako. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Balozi Adadi.

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: MheshimiwaMwenyekiti, katika mchango wangu wa maandishinilizungumzia suala kubwa la msongamano wa mahabusundani ya magereza zetu. Msongamano ni mkubwa sana naunachangiwa na mambo mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo mambomengi, ni kesi ambazo upelelezi wake umemalizika, lakinimahabusu wengi wanasubiri kitu kinaitwa High Court Session,hasa kwa kesi za mauaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, watuhumiwa wakesi za mauaji wengi wanasubiri High Court Session na wakondani ya mahabusu zaidi ya miaka minne, mitano wakatiwanasubiri session hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na session hiyo, hatakesi hizo zinaposikilizwa na hukumu ya kifo inapotolewa,utekelezaji wa adhabu hiyo haufanyiki. Tangu Awamu ya Tatuna ya Nne, karibu zaidi ya miaka 20 sasa hivi mahabusuambao ni condemned wanaotakiwa kunyonwawanagalagala kwenye mahabusu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

297

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka uthibitisho wa Serikalikwenye mambo mawili; kwanza, ni wataishauri mamlakainayohusika ili watuhumiwa wao ambao wanasubiri adhabuhiyo aidha itekelezwe au kama inashindwa kutekelezwa basiitolewe adhabu nyingine mbadala. (Makofi)

Pili, Serikali iangalie utaratibu sasa hivi wa kujaribukuboresha High Court Sessions ili kesi ambazo upelelezi wakeumemalizika mapema ziweze kusikilizwa kuondoa mlundikanowa mahabusu iliyoko magerezani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nisipopata majibumazuri kutoka kwa Mheshimiwa Waziri, nitachukua shilingiyake. Naomba kuwasilisha. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA: MheshimiwaMwenyekiti, pia nimshukuru Mheshimiwa Adadi Rajab,Mbunge wa Muheza kwa ushauri alioutoa kwetu. Ni kwelikabisa kumekuwa na msongamano wa mahabusu na sualazima la High Court Sessions.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya sababu imekuwani upungufu wa rasilimali fedha, lakini pia, inawezekanakabisa tatizo hilo linatokana pia na mfumo wenyewe. Kwahiyo, napenda nikubali ushauri huo ili Wizara pamoja namhimili wa Mahakama tuone ni njia gani bora zaidiinayoweza kutumika kuhakikisha kwamba mashauri hayana suala zima la High Court Session linafanyiwa kazi vizuri.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukichukua spirit ya sasa,iliyoko katika Mahakama Kuu kuhakikisha kwamba hizibacklog za kesi zinakwisha. Kwa kutumia hii justice na njianyingine, ninaamini kabisa tukikutana tena bajeti ijayotutakuwa tumekuja na jibu zuri kutoka mhimili waMahakama. Uzuri ndani ya ukumbi huu, ingawa siyo ndaniya Bunge, kule kwenye gallery, watu wa mhimili waMahakama wapo, ikiwa ni pamoja na Jaji Kiongozi ambao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

298

nadhani kwa pamoja na Mtendaji wa Mahakama tutaonajinsi ya kulifanya jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la watuwaliohukumiwa adhabu ya kifo na adhabu hiyohaijatekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati tunakusanya maoniya wananchi, mimi nilikusanya maoni ya wananchi katikaGereza la Ukonga, wengine wakaenda Segerea; tulitembeleakila magareza kwa sababu wafungwa pia ni Watanzania.Kweli pale Ukonga tulikuta watu ambao wamehukumiwakifo na adhabu hiyo haijatekelezwa. Miongoni mwa maoniyao yanafanana kabisa na ya Mheshimiwa Adadi Rajab.Wengi waliomba wapewe adhabu mbadala na hasa vijana;na wale watu wazima kwa umri, walisema basi miaka yoteimeishia humu si wanimalize tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, pia napendakukubali ushauri huu. Labda Serikali ione utaratibuikiwezekana hata kutumia Law Reform Commission kwasababu utafiti uliofanywa na Law Reform Commission ulihusuadhabu yenyewe ya kifo kuhusu nini kifanyike kwa walewaliohukumiwa. Kwa hiyo, tunalichukua na tutalipeleka hukoili tuone jinsi ya kuona nini kifanyike. (Makofi)

MWENYEKITI: Sawa kabisa. Mheshimiwa Balozi AdadiRajab.

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: MheshimiwaMwenyekiti, Mheshimiwa Waziri amejitahidi sana kujibumaswali yangu na hoja yangu. Naamini kwa sababu ya ugeniwake, ushauri huo atauchukua. Kama tusipoona mabadilikoyoyote, basi tutakutana kwenye bajeti ijayo. Nakushukurusana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Tutakutana tu, hata leo hii.(Kicheko)

Mheshimiwa Cosato Chumi!

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

299

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa kunipa nafasi. Nimepitia kitabu hiki chaMheshimiwa Waziri kutoka ukurasa wa kwanza mpaka wamwisho ukurasa wa 71 na nimepitia pia kitabu cha Maoni yaKamati, ukurasa wa 17 nadhani ni kipengele cha tatu, maoniya Kamati yanazungumzia kuhusu suala la kurekebisha sheriakwa ajili ya Katiba Mpya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Katiba Mpya katikanchi nyingi duniani ni jambo ambalo limechukua miaka mingina resource nyingi. Mfano mzuri ni wenzetu Kenya, walianzatakribani miaka ya 1990, wakaja kupata Katiba Mpya mwaka2010.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi yetu tumekuwana jambo hili na limechukua gharama kubwa, resourcekubwa kwa Taifa letu mpaka kufikia hatua ambayo ilikuwaimebaki, kwangu mimi noana ilikuwa imebaki kazi ndogo yakuelekea kwenye kupiga kura ya maoni. Wabunge wengikatika michango yao, wanazungumzia sana kuhusu kura yamaoni na namna gani bajeti itatengwa kwa ajili ya kura yamaoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwangu mimi pamoja nakuwa sio mwanasheria, mimi ni political scientist, ninafahamukwamba sheria inayohusiana na masuala ya Katiba Mpyailishakufa na kwa hiyo, inahitaji kuhuishwa upya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kitabu chaMheshimiwa Waziri pamoja na maoni yaliyomo kwenyeKamati, sijaona popote ambapo panaonesha kwamba kunadalili zozote za kuleta sheria hiyo ili kuweza kuhuisha mchakatohuu wa Katiba Mpya. Kwa sababu hiyo, napenda kupatamaelezo ya kujitosheleza kwa sababu hata wananchi wanahamu ya kuona jambo hili ambalo tulitumia fedha nyingikulifanyia kazi, kilichobaki ni kitu kidogo. Kama sitapatamaelezo ya kutosha, na mimi nitaingia kwenye mkumbo wakutoa shilingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

300

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waziri wa Katibana Sheria, maelezo tu.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, wakati wa majumuisho nililieleza jambo hili nabado napenda nirudie yale yale niliyoyasema; mchakato huuumefika mahali ulipofika na sheria mbalimbali zilihusika. Kwawakati muafaka, jambo hil i l itakapokuwa sasalinashughulikiwa, tutatoa maelezo ya jinsi kuhuishamchakato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme hivi, MheshimiwaCosato Chumi ni political scientist na mimi nawaheshimu ma-political scientist kwa sababu ilibidi miaka miwili nisomepolitical science. Nasema hivi, mchakato wowote wamabadiliko ya Katiba katika Taifa una mawanda ya ainambalimbali. Na mimi katika hili ningewasihi sana sisi sotetuvute subira kwa sababu hata hao Kenya walipokwamahawakujikwamua kwa njia ambayo labda tungependa nasisi tuipitie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba kusema,Wizara na Serikali inaendelea kuzipitia sheria, wakati muafakautakapofika hayo yote yatajadiliwa. Tukitaka kuyatoleamajibu sasa, tutakuwa tunatoa majibu wakati usiokuwamuafaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pil i, nampongezaMheshimiwa Rais kwa kusema kwamba jambo hili lisubiri. Kwanini lisubiri? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lisubiri kidogo kwa sababu,mnapokuwa katika hali ya vumbi, siyo vizuri kuja na jambokubwa kama hili. Linahitaji sote tutulie, tuwe wamoja; lakiniwakati huu mazingira ya kutufanya tuwe na huo utulivuyanaendelea na baadhi ya mambo tunayoyahitaji yanaanzakutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, muda ukifika,wala hayatakuwa na mjadala kwa sababu tayari yatakuwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

301

yameshatekelezwa, yamekubalika yamekuwa sehemu yautamaduni wetu wa kisheria. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Cosato, wewe siyo tu a political scientist,wewe ni mwanadiplomasia, nadhani umeelewaanachokisema Mheshimiwa Waziri.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naona umenivisha pia kofia ya ziada. Sioni kama nawezanikawa na nyongeza zaidi baada ya maelezo ya MheshimiwaWaziri, lakini napenda kufahamisha Bunge kwambawananchi wangependa jambo hili lifike wakati liwezekutendeka na kukamilika. Nashukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Nakushukuru sana Mheshimiwa.Mheshimiwa Tundu Lissu.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuzungumzia hoja ya Kaimu Jaji Mkuu na kwasababu Mheshimiwa Waziri hawezi akaniridhisha, nitaondoashilingi hili jambo lijadiliwe na Bunge. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemsikia MheshimiwaProfesa Kabudi na marembo mengi. Mheshimiwa ProfesaKabudi ni msomi kweli kweli, sijawahi kuwa na shaka kabisa,lakini kwa alichokisema leo kuhusu nafasi ya Kaimu Jaji Mkuukutokuwa ya ukomo, imenishangaza sana. Inanishangaza,naanza kufikiria alichokiandika yeye na Mlimuka kwambakuna wataalamu wasomi ambao wanatumika ku-justify theunjustifiable. A progressive rhetoric ili ku-justify mambo yahovyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katiba yetu, nilisema katikamaoni yangu kuna sababu kwa nini huyu anaitwa KaimuJaji Mkuu, kuna sababu. Kuna sababu ya Ibara ya 118(1)inayosema Jaji Mkuu. Kuna tofauti kati ya Jaji Mkuu na KaimuJaji Mkuu. Hoja yangu ni kwamba ukishasema kaimu (acting),ni interlocutory, ni interim, ni ya muda. Haiwezi ikawa haina

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

302

ukomo. Haiwezi ikawa haina ukomo, ndiyo maana inaitwakaimu, ndiyo maana inaitwa ya muda na ndiyo maanainaitwa interim. Pending substantive appointment.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Profesa anatakakutuaminisha kwamba kunaweza kukawa na Kaimu Jaji Mkuumiaka yote, haiwezekani! Haiwezekani, siyo kwa Katiba hii.Profesa Kabudi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Muda umekwisha.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Nitatoa shilingi yako.

MWENYEKITI: Wewe, hakuna haja.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimesema…

MWENYEKITI: Tulia tu.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Nimesema natoa shilingitujadiliane.

MWENYEKITI: Unatulia muda tu. Profesa, hebu lielezeekwa kifupi tu. Maana umeeleza sana.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, nirudie yale yale niliyoyasema kwamba nafasi yaKaimu Jaji Mkuu kama ni ukomo ni pale kwa mujibu wa Ibaraya 118, Rais atakapomteua Jaji Mkuu au Jaji Mkuuatakaporejea nchini au kama alikuwa hawezi kufanya kazianaumwa, amepona na amerudi kazini. Huo ndio ukomo.(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

303

Mheshimiwa Mwenyekiti, lini Rais atamteuwa Jajimwingine ili Kaimu Jaji Mkuu aache kuwa Jaji Mkuu, hilo ndilonililosema halijawekewa muda. Hajaambiwa miezi sita aumiezi mitano, hajawekewa, lakini mara akimteua huyo huyoau mwingine huo ndiyo ukomo wa Kaimu Jaji Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichokisema, ukija kwenyefunctions zake, ndiyo maana ukienda kwenye Ibara ya 151inayoeleza nani Jaji Mkuu, functions zake ni zile zile za JajiMkuu. Ana-enjoy mamlaka yote ya Jaji Mkuu na ana-enjoysecurity of tenure ambayo tayari ana-enjoy kwa sababu niJaji wa Mahakama ya Rufani. Katika maamuzi yake, yeyemwenyewe haingiliwi na yeye hawaingilii Majaji walaMahakimu wengine, hata Hakimu wa Mahakama yaMwanzo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, toka Kaimu Jaji Mkuu huyuateuliwe ni takribani miezi mitatu. Sasa Mheshimiwa TunduLissu, mdogo wangu hakuwepo hapa nilisihi na ninaendeleakusihi, mimi naanza kuzielewa nchi ambazo suala laMahakama na vote ya Mahakama haiji Bungeni. Sasanaelewa. Ziko nchi za commonwealth, mhimili wa Mahakamahela zake zinatolewa moja kwa moja kwenye CF na sasanaanza kuelewa. Kwa sababu, ni chombo ambachonisingependa kabisa tukijadili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unajua Mahakimu na Majajiwanasimama nafasi ya Mwenyezi Mungu, ndiyo. Ni MwenyeziMungu peke yake mwenye hukumu ya haki na ndiyo maanahukumu hiyo ya Mwenyezi Mungu haina rufaa za sisi wotebinadamu. Tunajitahidi, ndiyo maana tuna madaraja yarufaa. Sasa watu ambao Nabii Daudi kwenye Zaburi ya 15anawaita ni marafiki wa Mungu kwa sababu wanafanya kaziambayo yeye peke yake ndiyo mtoa haki, tuwaheshimukidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, napenda kusemakwamba mdogo wangu nirudishie shilingi, ili jambo hilitulijadili vizuri na tuiachie mamlaka husika kutekelezamajukumu yake. Kwenye hotuba yako umenisihi nitoe ushauri,

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

304

sasa kwa njia hii itakuwa vigumu kutoa ushauri. Kwa hiyo,nisaidie kutoa ushauri kwa kurudisha shilingi. (Makofi)

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,shilingi yangu hairudi, hili jambo tulijadili. (Kicheko)

Narudia tena, hizi hoja ni nyepesi sana. KweliMheshimiwa Profesa Kabudi anapenda sana kusema, TheChief Justice is primus inter pares, maneno umenifundisha sanaMwalimu wangu na Majaji wengine. Primus inter pares, anamamlaka yale yale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Spika wa Bunge naMwenyekiti wa Bunge, wewe Mwenyekiti unapokuwa hapo,kazi zako ziko sawa na za Spika. Wewe ni Spika? (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mwalimu wangu,Mheshimiwa Profesa Kabudi anasema kwa vile kazi za ChiefJustice zinafanana na kazi za Acting Chief Justice, then theActing Chief Justice is the Chief Justice, tafadhali.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kitu amekisemaMheshimiwa Profesa Kabudi kizuri sana. Nchi zinaishi kwa milana desturi za kikatiba na kisiasa. Mila za desturi za kikatibana kisiasa za nchi hii, kwenye suala la Jaji Mkuu tangu enzi zaPhilip Georges ni kwamba nafasi ya Chief Justice ikiwa wazi,anateuliwa immediately a substantive Chief Justice. Ithappened 1964 umesema, it happened 1973 with PhilipGeorges, it happened with Judge Agostino Said, it happenedwith Nyalali, it happened with Samata, it happened withAugustine Ramadhani, imetokea kwa Jaji Mohamed OthmaniChande utafikiri hamkujua kwamba Chande Othmanatastaafu mkajipanga. Utafikiri hamkujua. It was well known.(Makofi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini you are breakingwith our constitutional and judicial tradition? Tumekuwa naMajaji Wakuu substantive miaka yote, why now? Kwa hiyo,hili jambo lijadiliwe, nimeondoa shilingi na hairudi. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

305

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa hoja lijadiliwe.(Makofi)

MWENYEKITI: Haya, tunachukua majina. Mnaelewamaana yake? Mnanielewa eeh! Nachukua wawili huku nawawili huku. Naanza na Mheshimiwa Angellah Kairuki naMheshimiwa Kakunda Joseph, Mheshimiwa Mnyika naMheshimiwa Ally Saleh. Tunaanza na Mheshimiwa Ally Saleh.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Kwanza napenda kusema kwamba naunga mkonohoja iliyoletwa mezani na Mheshimiwa Tundu Lissu. Hoja zanguni zifuatazo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tunatengenezautamaduni mpya kabisa, utamaduni ambao tunaonyesha,kama alivyosema Mheshimiwa Tundu Lissu tangu asubuhikwamba hatuko tayari kwa kitu ambacho tulikuwa tuko tayarina tukajua kwamba kitatokezea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha pili, nataka MheshimiwaWaziri atuelezee ni wapi katika utamaduni wacommonwealth tunakaa muda wa miezi kama hiihatujampata Jaji mwingine? Ingekuwa angalau tuna systemya kumleta mwombaji katika panel kuhojiwa kupitia katikamfumo kama vile Marekani au kama vile Kenya angalautungesema imechukua muda; lakini bado tulikuwa tunajuamuda wake ni muda fulani, haikutekelezwa.

Suala la tatu, inaondoa confidence ya utawala wakisheria katika nchi, inaondoa confidence kwa wawekezajina marafiki zetu, kwamba nchi hii haipo stable, tunashindwakuamua katika jambo muhimu la nguzo ya kitaifa. Kwa hiyo,nahisi kwamba katika hil i hatupendi kusema, lakinitunapenda kusema kwamba Mheshimiwa Rais hakutekelezawajibu wake wa Kikatiba.

Kwa hiyo, naunga mkono hoja hii kwamba tuendeleekuijadili na tuamue katika njia nyingine, lakini siyo kupitishabajeti ya Waziri. Ahsante. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

306

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kariuki.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Niendeleekusimamia katika maelezo ya Waziri, Mheshimiwa ProfesaKabudi. Ameeleza kwa kina kabisa msingi mzima wa Ibara118(1). Ukiangalia ibara 118(4)(a) lakini zaidi katika ibarayenyewe 118(5).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi si jaona lolotelililoharibika, kwa kuwa anakaimu Jaji Mkuu mpaka sasa.Tumekuwa tushuhudia ufanisi wa Mahakama. Kesi kwa kiasikikubwa zaidi ya asilimia 85 unaona kuna completion ratena disposal rate zaidi ya asilimia 90 na wamekuwa wakifanyakazi kubwa kwa kweli tunawapongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ukiangalia Ibara ya 118(4)(a),nafasi ya Jaji Mkuu itakapokuwa wazi na imeeleza nimazingira gani inaweza ikatokea ikawa wazi na ninikinafanyika na ambacho amekifanya Mheshimiwa Rais,amemteua Kaimu Jaji Mkuu anatekeleza madaraka yakempaka hapo Mheshimiwa Rais atakapofanya uteuzi.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Malizia.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono maoni na maelezo yaMheshimiwa Profesa Kabudi. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kakunda.

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,imeletwa hoja hapa ya nchi za commonwealth, na miminaomba niongezee kwenye maelezo ya Mheshimiwa Wazirikwa kuongeza maelezo kumwambia mchangiaji mmoja

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

307

aliyetaka mfano kwenye nchi za commonwealth, Katiba yaIndia mwaka 1949 Ibara ya 126 kuhusu appointment of ActingChief Justice inasema: “When the office of the Chief Justiceof India is vacant or when the Chief Justice is by any reason orotherwise unable to perform the duties of his office, thePresident may appoint…”

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasoma kipengele chaKatiba na nanukuu; “The duties of the office shall be performedby such one of the other Judges of the Court as the Presidentmay appoint for the purpose.” Kwa hiyo, India wana kipengelecha kuteua Kaimu Jaji Mkuu. (Makofi)

MWENYEKITI: Sawa, Mheshimiwa Mnyika.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naminaunga mkono hoja iliyotolewa na Mheshimiwa Tundu Lissu.Mheshimiwa Waziri Kairuki alipokuwa anazungumza hapa,amesema hajaona tatizo lolote katika kipindi hiki ambachoJaji Mkuu amekaimu nafasi yake kwa kipindi chote hicho.Sasa kama Mheshimiwa Kairuki anaona hakujawa na tatizololote, kwa nini sasa asikubaliane na hoja ya Kambi yaUpinzani kwamba Rais amthibitishe huyu Kaimu Jaji Mkuu ilisasa awe Jaji Mkuu kamili ili kusiwe na utata tena? (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba sanaMheshimiwa Waziri wa Katiba na Mheshimiwa MwanasheriaMkuu wa Serikali, ninyi ndio Washauri Wakuu wa MheshimiwaRais katika masuala ya sheria. Ninyi washauri wakuu waMheshimiwa Rais katika masuala ya sheria mkichukuliamsimamo kwamba mamlaka ya Rais hayana kikomo katikakuachia nafasi ya ukaimu, ni wazi kwamba ninyi mnaongozakatika kumpotosha Mheshimiwa Rais na ili msiingie katikavitabu vya kumpotosha Mheshimiwa Rais ni vema mka…(Makofi/Kicheko)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

308

MWENYEKITI: Muda. Ahsante sana.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, Bunge hili linafanya kazi na linapaswa lifanyekazi kwa kuzingatia Katiba. Kwanza, imeletwa hoja hapaya Bunge kutaka kumshauri Mheshimiwa Rais amthibitisheKaimu Jaji Mkuu kitu ambacho hakipo. Kwa sababu tunayoIbara ya 37 inasema hivi, mbali na…

MBUNGE FULANI: (Hapa alizungumza bila kutumiakipaza sauti).

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Sasa kwa ninimnaleta hoja hapa? Mbali na kuzingatia masharti yaliyomokatika Katiba hii na Sheria za Jamhuri ya Muungano katikautekelezaji wa kazi nashughuli zake, Rais atakuwa huru nahatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyoteisipokuwa tu pale atakapotakiwa na katiba hii au na sherianyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushaurianaopewa na mtu au mamlaka yoyote.

Moja, Katiba haijatoa mamlaka kwa Bunge hilikumshauri Rais kuhusu uteuzi wa Jaji Mkuu; hilo la kwanza; lapili, katiba haijaweka kiasi cha ukomo wa mtu anayeteuliwakuwa Jaji Mkuu kukaimu. Kwa hiyo, muda wa kukaimu huyoJaji Mkuu huwezi kusema kwamba umeisha kwamba Raisamefungwa. Tumwachie Rais atekeleze wajibu wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hali ya kawaida, sisitulipaswa tushangilie kwamba mwenzetu anateuliwa kuwaKaimu ambaye ni njia ya kwenda pengine kuthibitishwa kulehalafu wewe unakasirika. How many people have beenappointed on the acting positions, then let one be confirmedaccordingly. (Makofi/Kicheko)

MBUNGE FULANI: Ruka baba, ruka!

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, nilisema hapa nilipochangia mara ya mwisho,hatuwezi kuwa na tabia ya kuwasakama…

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

309

MBUNGE FULANI: Chief Whip.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mmekuwa natabia ya kuwasakama viongozi wakuu wa mahakama. JajiMstaafu Chande mlikuwa mnamshambulia…

MHE. PAULINE P. GEKUL: Apunguze sauti, hatumsikiikabisa.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Halafu pia na huyumnamshambulia, why? We can ask ourself.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naunga mkonohoja ya Mheshimiwa Waziri na namwomba MheshimiwaTundu Lissu baada ya kusoma masharti haya ya Katibaakubali kumrudishia Mheshimiwa Waziri shilingi yake. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tundu Lissu, kwa kifupituhitimishe tu.

MHE. TUNDU A. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,hapana ni dakika zangu tatu.

MWENYEKITI: Siyo lazima utumie zote.

MHE. TUNDU A. LISSU: Muda wangu wa Kibungetafadhali!

Mheshimiwa Mwenyekiti, ya Masaju nitayaacha, kwasababu sasa tuna Mwanasheria Mkuu au tuna partyapparatchik? (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyeikiti, kuna hoja inajengwakwamba kuhoji mambo haya ni kuidharau Mahakama.Hapana, unaidharau Mahakama kwa kutofanya Mahakamaiwe na kiongozi wake kamili, hiyo ndiyo dharau yaMahakama. Siyo hawa wanaohoji kwa nini Judiciary hainaSubstantive Head? Ni ninyi ambao mnasababisha haina, ndiomnaodharau. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

310

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kuna hoja kwambahalijaharibika neno. Limeharibika neno vibaya sana. Judiciaryni mhimili wa dola, unaongozwa na Jaji Mkuu. Katibainasema ndiye Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Ukimfanyaakaimu, hana uhakika kama kesho atakuwa confirmed,hana hakika kama kesho ataondolewa, maana yake ninamna ya kuvuruga independence ya Judiciary.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na uzuri kabisa, nimesemauzuri wa walimu wangu hawa walipokuwa bado vijana nawakweli, sasa hivi wamekuwa wanatumikia tu,walizungumza vitu vya maana sana. Walizungumza vyamaana sana. Samahani mwalimu wangu, samahani kakayangu. (Kicheko/Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa. Muda ndiyo huo.(Makofi)

MBUNGE FULANI: Tumechoka pumba.

MHE. TUNDU A. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninachosema ni kwamba…

MWENYEKITI: Muda wako umekwisha. Mudaumekwisha Mheshimiwa.

MBUNGE FULANI: Muda wake umeisha.

MHE. TUNDU A. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikwamba…

MBUNGE FULANI: Tumechoka pumba.

MBUNGE FULANI: Kaa chini.

MHE. TUNDU A. LISSU: Tunataka Judiciay iheshimiwe,Mheshimiwa Waziri amshauri Rais ateue Jaji Mkuu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

311

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea.

Waheshimiwa Wabunge, nawahoji wale mnaoafikihoja ya Mheshimiwa Tundu Lissu ya kupunguza mshahara waWaziri kwa shilingi moja waseme ndiyo na wasioafiki wasemesiyo.

(Hoja ilitolewa Iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kukataliwa)

(Hoja ya kuondoa shilingi katika mshahara wa Waziri waKatiba na Sheria, iliyotolewa na Mhe. Tundu A. M. Lissu

ilikataliwa na Kamati ya Matumizi)

MWENYEKITI: Wasioafiki wameshinda.

Mheshimiwa Abdallah Mtolea muda haupo. Sema tuulichonacho, tutaenda mbele. (Kicheko/Makofi)

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Pamoja na muda haupo lakini kuna muda ulewa kanuni zetu za Kibunge, kwa hiyo, naamini huoutaheshimika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nil ikuwa natakakuzungumzia jambo dogo tu na lenyewe ni hili, kuzuiamikutano ya Vyama vya Siasa. Mheshimiwa Waziri kablahujajiunga na Serikali hii yalitoka matamko ya kuzuiamikutano ya kisiasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, wanasiasaunaotuona humu ndani, hatufanyi mikutano ya kisiasa. Nawewe umesema hapa kwamba unasoma sana Ibara yanane. Kama unasoma Ibara ya nane ambayo inaitajaJamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni nchi yaKidemokrasia, pia utakuwa unaisoma Ibara ya 18 ambayoinatoa uhuru wa mawazo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uhuru wa mawazo nakuijenga demokrasia inatutaka tuzungumze na wananchi,

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

312

inatutaka twende kwa jamii tukafanye mikutano tuwaelezeSerikali inafanya nini na Serikali haifanyi kitu gani? Ndiyomaana katika Awamu ya Nne wakati Chama cha Mapinduzikinaelelekea shimoni, Mheshimiwa Kinana na MheshimiwaNape Nnauye walizunguruka nchi nzima...(Makofi)

MBUNGE FULANI: Kuzunguruka?

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Kuelezea namna ganiSerikali inatekeleza majukumu yake na ikaweza kuinusuruCCM na hatimaye ikashinda kwenye uchaguzi wa mwaka2015.

MHE. AMINA N. MAKILAGI: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa!

MWENYEKITI: Muda Mheshimiwa.

MHE. AMINA N. MAKILAGI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nitoe taarifa.

MWENYEKITI: Hapana.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kama sikupata maelezo ya kina kutoka kwa Waziri, kwelinitaondoa shilingi katika eneo hili.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndaniya Nchi.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza naomba niweke kumbukumbu sawa.Mikutano ya vyama vya siasa haijafutwa wala haijazuiwa,bali imewekewa utaratibu. Duniani kote, hiyo ndiyo standard;mikutano ya hadhara inawekewa utaratibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, duniani kote mikutano yahadhara huwa inapangwa na Tume ya Uchaguzipanapokuwepo na majukumu ya masuala ya kisiasa. Hivimajuzi tulikuwa na chaguzi za marudio za Kata pamoja na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

313

Jimbo. Vyama vyote vya siasa viliruhusiwa, vilienda kufanyakampeni popote pale walipokuwa wanataka. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mazingira ya sasa hivi,hapa tulipo wachaguliwa wote ambao ni ninyi WaheshimiwaWabunge mnarusiwa kufanya mikutano ya hadhara na ninyini wanasiasa. Hakuna Mbunge hata mmoja ambaye siomwanasiasa na hakuna Mbunge hata mmoja ambayeanapokuwa kwenye Jimbo lake hatokani na chamachochote siasa. Kwa maana hiyo, mikutano ya hadharainaendelea kama kawaida, lakini kwa kuwekewa utaratibukutumia watu ambao wana anuani ya kuweza kuitishamikutano ya aina hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili limewasaidia sananinyi wenyewe Waheshimiwa Wabunge. Na mimi namshukurusana Mheshimiwa Rais. Nadhani kwa uzoefu wake wa kuwaMbunge kwa zaidi ya miaka 20 ametambua kwamba ni vizurikatika nchi kuweka utaratibu wa kufanya mikutano yahadhara ambao utakuwa unatumia watu ambaowanawajibika katika eneo ambalo wanafanya mikutano yahadhara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niliseme kwauwazi kabisa na wenzetu hawa watumie mifano hata yanchi hizo ambazo wanazitumia kwenye demokrasia, huondiyo utaratibu wanaoutumia.

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge kwamamlaka niliyonayo kwa mujibu wa Kanuni 104(2) sasatunaingia kwenye guillotine.

Fungu 41- Wizara ya Katiba na Sheria

Kif. 1001 - Admin.and HR Management ...Shs. 5,033,833,000/=Kif. 1002 - Finance and Accounts ………… Shs. 228,991,000/=Kif. 1003 - Police and Information Services.. Shs. 437,718,000/=Kif. 1004 - Internal Audit Unit...…………… Shs. 122,562,000/=Kif. 1005 - Government Comm. Unit..…… Shs. 107,736,000/=

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

314

Kif. 1006 - Procurement Mg’nt Unit.............. Shs. 131,204,000/=Kif. 1007 - Management Inform. Unit…… ....Shs. 141,758,000/=

(Vifungu vilivyojatwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 12 - Tume ya Utumishi wa Mahakama

Kif. 1001 - Admin. and HR Management..... Shs. 916,897,595/=Kif. 1002 - Finance and Accounts …........... Shs. 24,295,000/=Kif. 1003 - Procurement Mg’nt Unit.………….Shs. 14,260,000/=Kif. 1004 - Internal Audit Unit……………….. Shs. 12,440,000/=Kif. 1005 - Recruitment, Appointment & Confirmation............................. Shs.102,030,000/=Kif. 1006 - Ethics and Discipline Section……..Shs. 32,988,400/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 16 - Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Kif. 1001 - Admin. and HR Mg’nt...............Shs. 1,915,081,000/=Kif. 1002 - Finance and Accounts Unit ..……Shs. 408,964,000/=Kif. 1003 - Planning Division….………….….Shs. 513,080,000/=Kif. 1004 - Internal Audit Unit……………….Shs. 268,194,000/=Kif. 1005 - Government Commu. Unit…...…Shs. 98,150,000/=Kif. 1006 - Legal Registry Unit……………… Shs. 132,512,000/=Kif. 1007 - Procurement Mg’nt Unit.............. Shs. 216,304,000/=Kif. 1008 - Research and LibraryService Unit. Shs.100,824,000/=Kif. 1009 - Information and Comm. Unit…. Shs. 197,020,000/=Kif. 2003 - Legislative Drafting..……………..Shs. 976,016,000/=Kif. 3001 - Civil Litigation & Arbitration Division..................................Shs.1,100,573,000/=Kif. 3002 - Treaties and Contracts Div...…… Shs. 799,761,000/=Kif. 4001 - Constitutional Affairs and Human Rights……............…….Shs. 556,044,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

315

Fungu 35 - MKurugenzi wa Mashitaka

Kif. 2002 - Public Prosecutions Division……Shs. 4,106,416,000/=Kif. 2004 - Zonal Office Arusha ……………..Shs. 855,004,000/=Kif. 2005 - Zonal Office Dodoma ………… ..Shs. 492,634,000/=Kif. 2006 - Zonal Office Dar es Salaam.......Shs. 1,995,042,000/=Kif. 2007 - Zonal Office Iringa………………..Shs. 367,612,000/=Kif. 2008 - Zonal Office Moshi ……………... Shs. 422,073,000/=Kif. 2009 - Zonal Office Kagera…………….. Shs. 321,481,000/=Kif. 2010 - Zonal Office Mbeya …………..…Shs. 499,729,000/=Kif. 2011 - Zonal Office Mtwara .………….. Shs. 346,856,000/=Kif. 2012 - Zonal Office Mwanza ……………Shs. 891,419,000/=Kif. 2013 - Zonal Office Ruvuma …………… Shs. 300,269,000/=Kif. 2014 - Zonal Office Sumbawanga …….. Shs. 305,778,000/=Kif. 2015 - Zonal Office Tabora ……………..Shs. 501,312,000/=Kif. 2016 - Zonal Office Tanga ……………… Shs. 523,039,000/=Kif. 2017 - Zonal Office Shinyanga ………… Shs. 372,857,000/=Kif. 2018 - Zonal Office Singida .…………… Shs. 274,746,000/=Kif. 2019 - Zonal Office Lindi………………… Shs. 214,558,000/=Kif. 2020 - Zonal Office Mara ..…………….. Shs. 183,188,000/=Kif. 2021 - Zonal Office Manyara ……………Shs. 172,757,000/=Kif. 2022 - Zonal Office Kigoma ……………..Shs. 224,695,000/=Kif. 2023 - Zonal Office Pwani .……………..Shs. 358,741,000/=Kif. 2024 - Zonal Office Njombe …………....Shs. 283,623,000/=Kif. 2025 - Zonal Office Morogoro..…………Shs. 310,644,000/=Kif. 2026 - Zonal Office Geita ………………..Shs. 216,451,000/=Kif. 2027 - Zonal Office Simiyu ..……………..Shs. 180,821,000/=Kif. 2028 - Zonal Office Katavi ………………Shs. 192,318,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 40 - Mfuko wa Mahakama

Kif. 2002 - Court of Appeal D’Salaam…Shs.106,959,018,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi pamoja na Marekebisho yake)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

316

Fungu 55 – Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Kif. 1001 - Admin. and HR Mg’nt................Shs. 1,539,930,400/=Kif. 1002 - Finance and Accounts ………......Shs. 215,028,000/=Kif. 1003 - Internal Audit Unit ………..………Shs. 66,220,000/=Kif. 1004 - Legal Services ……………………Shs. 252,815,000/=Kif. 1005 - Procurement Unit……………….Shs. 46,840,000/=Kif. 1006 - Mg’nt Information Syst. Unit....…Shs. 47,070,000/=Kif. 2001 - Administrative Justice……....…..Shs. 650,063,000/=Kif. 2002 - Human Rights…………..….......…Shs. 502,021,600/=Kif. 2003 - Research and Documentation…Shs. 166,586,000/=Kif. 2004 - Public Education and Training…..Shs. 150,488,000/=Kif. 3001 - Zanzibar Office…………………....Shs. 180,912,000/=Kif. 3002 - Mwanza Office …………...………Shs. 45,638,000/=Kif. 3003 - Lindi Office ………………………Shs. 30,570,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 59 – Tume ya Kurekebisha Sheria

Kif. 1001 - Admin. and HR Mg’nt.…....…Shs. 2,034,335,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

MIPANGO YA MAENDELEO

Fungu 16 – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Kif. 1003 - Planning Division………………....….............Shs. 0Kif. 3002 - Treaties and Contract Division………...........Shs. 0

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

317

Fungu 35 - Public Prosecutions Division

Kif. 2002 - Public Prosecutions Division …………......…. Shs. 0

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 41 – Wizara ya Katiba na Sheria

Kif. 1003 - Policy and Inform. Services….....Shs. 2,806,020,000/=

(Kifungu Kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 55 – Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Kif. 2002 - Human Rights…………….….…Shs. 2,272,796,000/=Kif. 2003 - Research and Documentation……………… Sh. 0

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

NDG. JOSHUA CHAMWELA - KATIBU MEZANI:Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Matumizi imemaliza kaziyake.

MWENYEKITI: Bunge linarejea.

Waheshimiwa Wabunge, naomba utulivu. Tukae.

Mheshimiwa mtoa hoja, taarifa. (Makofi)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, Bunge lako lilikaa kama Kamati ya Matumizi,limekamilisha kazi zake. Naomba taarifa ya Kamati yaMatumizi ikubaliwe na Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

318

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

MWENYEKITI: Hoja imetolewa na imeungwa mkono.Sasa naitoa kwenu muiamue.

(Hoja ilitolewa Iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba naSheria kwa Mwaka 2017/2018 yalipitishwa na Bunge)

MWENYEKITI: Walioafiki wameshinda. Kwa hiyo,napenda kutamka rasmi kwamba maombi ya Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwamafungu yote ambayo yako chini ya Wizara hiyoyamepitishwa rasmi na Bunge. (Makofi)

Nachukua nafasi hii kumshukuru sana MheshimiwaProfesa Kabudi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Serikalinzima, uongozi wa Mahakama, Jaji Kiongozi na timu yake,Katibu Mkuu na wataalam wote ambao wenginehamuwaoni ambao wako nyuma hapa, wako wengi, kwakazi nzuri ambayo mmeifanya.

Bunge limeidhinisha maombi ya fedha kwa mwakaujao wa fedha, matarajio yetu ni kwamba yaliyosemwa,yaliyoshauriwa, fedha hizi kwa mafungu yote zitapatikanakwa mtiririko mzuri ili muweze kutekeleza majukumu yenu.Hongereni sana. Kwangu mimi kwa Wizara hii huwa najisikiakama ni chura mnamrejesha kwenye maji, nimefurahi sana.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, kabla sijaendelea, kunaombi moja ambalo nadhani mtanivumilia. Nilikuwa naongeana Katibu hapa Mezani, siku za usoni nadhani tuwe tuna-anticipate, mimi huwa sipendi kuvunja Kanuni na sidhanihata kiongozi yeyote anayekaa hapa anapenda kuvunjaKanuni. Suala la muda, tutakuwa tunawahi tunapoona hali

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

319

ilivyo maana dakika 30 tunaona hatuzitendei haki shughuliya Bunge. Kwa leo, Mheshimiwa Mdee, dakika tatu tu.

MAELEZO BINAFSI YA MBUNGE

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mosi,nakushukuru kwa kunipa fursa hii, lakini vilevile nilitamaniwakati ninasema maneno haya Mheshimiwa Spikaangekuwepo, lakini ninaamini kwamba uwepo wako weweunawakilisha Kiti cha Spika na atapata kusikia manenoambayo nilitaka kuyasema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 4 Aprili, 2017 wakatiwa uchaguzi wa EALA kuna matukio ambayo yalitokeayakanipelekea kuzungumza lugha ambayo kitamaduni zaBunge siyo sawa. Lugha husika ilimgusa pia Mheshimiwa Spikana Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla kwa namna moja aunyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Mbunge mzoefu,nilitumia jitihada kuzungumza na kuomba radhi wahusikakatika individual capacity, lakini vilevile nikaona ni busarakwa sababu haya maneno niliyasema Bungeni, kuzungumzapia hapa na kumwomba radhi Mheshimiwa Spika. Kwa hiyo,nil iomba huu muda specifically kumwomba radhi,kumwambia kwamba namheshimu na kwamba sitarudia.(Makofi)

Mheshimiwa Spika ni kiongozi wangu, lakini Spika nimwananchi wa Jimbo la Kawe. Kwa hiyo, nina kila sababuya kuyazingatia haya mawili kwa umakini mkubwa. Kwa hiyo,naomba radhi kwake, naomba radhi kwa Mheshimiwa Dkt.Kigwangalla, ninaomba radhi kwa Bunge na ninaombaradhi kwa wananchi wa Jimbo la Kawe ambao miongonimwenu ninyi asilimia kubwa ni wananchi wa Jimbo la Kawe.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niahidi tu nawananchi wa Tanzania najua kuna ambao nitakuwanimewakwaza, kwa hiyo, ninaomba radhi. Naahidi tu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

320

michango yangu ya Kibunge itaendelea kama ilivyo lakinikwa kutumia lugha za staha. (Makofi)

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Leo Halima kaokoka leo!(Kicheko/Makofi)

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Ameacha pombe. (Makofi)

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Halima ni wewe kweliHalima? (Makofi)

MBUNGE FULANI: Ameacha pombe?(Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naminamshukuru sana Mheshimiwa Halima Mdee kwa ukomavuwake aliouonesha. Huo ndiyo uongozi, hongera sana.(Makofi)

Tutazifikisha salamu zako na ombi lako tutalifikisha kwaMheshimiwa Spika pamoja na kwamba imo kwenye Hansard.

Nifanye sahihisho la Hansard kwa jina la MheshimiwaWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi waUmma na Utawala Bora, nilitaja jina Mheshimiwa AngellahKariuki, jina sahihi ni Mheshimiwa Angellah Kairuki, ikae vizuri.Ukisema hivyo, unaleta matatizo mengine.

Tangazo linatoka kwa Chief Whip wa SerikaliMheshimiwa Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya WaziriMkuu, kwa shughuli kubwa ya kesho ya Muungano.

Tangazo, tunaadhimisha miaka 53 ya Muungano waTanganyika na Zanzibar, kesho Jumatano tarehe 26 Aprili, 2017.Maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika katika Uwanja waJamhuri Dodoma. Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo,atakuwa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

321

wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama. Wabunge wote wa Bungela Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnaalikwa rasmikuhudhuria katika sherehe hizo. (Makofi)

Kutakuwa na usafiri wa pamoja kwa WaheshimiwaWabunge kuelekea Uwanja wa Jamhuri utakaoanzia katikaUwanja wa Mashujaa saa moja asubuhi, tuwahi. Usafiri huoutawarudisheni uwanja wa Mashujaa mara baada ya sherehekumalizika. Hii ni kutokana na kutokuwepo nafasi ya kuegeshamagari Uwanja wa Jamhuri. Kauli Mbiu ya Sherehe za kutimizamiaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Miaka53 ya Muungano, Tuulinde na Kuuimarisha, Tupige Vita Dawaza Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Hakuna usalama wa magari kule.

MWENYEKITI: Hilo ndilo tangazo. Kesho WaheshimiwaWabunge tuwahi saa moja eneo la Viwanja vya Mashujaa.

MBUNGE FULANI: (Hapa alizungumza bila kutumiakipaza sauti).

MWENYEKITI: Hayo mtauliza baadaye.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayo,niwashukuru sana kwa kazi nzuri mliyoifanya, ndiyo shughuliza Bunge. Tuendelee hivyo kushikamana.

Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, naliahirisha Bungehadi kesho kutwa siku ya Alhamisi tarehe 27 Aprili, 2017 saa3.00 asubuhi.

(Saa 2.32 Usiku Bunge liliahirishwa mpaka Siku ya Alhamisi,Tarehe 27 Aprili, 2017 Saa Tatu Asubuhi)