192

Click here to load reader

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

  • Upload
    dangkhue

  • View
    1.043

  • Download
    235

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE___________

MKUTANO WA SABA

Kikao cha Thelathini na Tano – Tarehe 26 Mei, 2017

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua

MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae, Katibu.

NDG. LAWRENCE MAKIGI - KATIBU MEZANI:

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANOWA AFRIKA MASHARIKI:

Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikikwa mwaka wa fedha 2017/2018.

MWENYEKITI: Ahsante sana Naibu Waziri wa Mamboya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Katibu.

NDG. NEEMA MSANGI - KATIBU MEZANI:

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

MASWALI NA MAJIBU

Na. 278

Tatizo la Maji Musoma Vijijini

MHE. JOYCE B. SOKOMBI aliuliza:-

Kumekuwa na tatizo kubwa la maji katika Wilaya yaMusoma Vijijini hasa vijiji vya Kabulabula, Bugoji, Kangetutyana Saragana. Aidha, visima vilivyochimbwa na wanakijiji haovinakauka wakati wa kiangazi.

Je, ni lini Serikali itahakikisha programu za majizinapelekwa na zinatekelezwa kwa umakini katika Wilayaya Musoma Vijijini?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Joyce Bita Sokombi, Mbunge wa Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli visima vingi hasavilivyochimbwa na kufungiwa pampu hukauka wakati wakiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katikamaeneo husika. Sababu kubwa ni mabadiliko ya tabianchihali inayosababisha maji kupatikana katika kina kirefu zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambuachangamoto hiyo, Serikali kupitia Programu ya Uendelezajiwa Sekta ya Maji (WSDP II) imeanza kufanya usanifu wa mradimpya utakaotumia Ziwa Victoria kama chanzo cha maji chauhakika. Vijiji vitakavyoingizwa katika mpango huo niKabulabula, Bugoji na Saragana.

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Sokombi swali lanyongeza kama unalo.

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Mweyekiti,ahsante. Nasikitika sana kwa majibu ya Waziri ambayoyamekuwa ni hayo hayo yakijirudia. Tumeona wenzetu waKahama na Shinyanga wananufaika kwa kiasi kikubwa sanana mradi huu wa maji kutoka Ziwa Victoria. Ni kwa niniSerikali imeviacha vijiji hivi ambavyo viko karibu kabisa naZiwa Victoria kuvipatia maji muda mrefu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, zoezi la usanifu limekuwalikichukua muda mrefu sana kabla miradi kuanzakutekelezwa. Je, ni lini usanifu wa mradi huu utakamilika?Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwaufupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafahamuconcern ya Mheshimiwa Mbunge kwa changamoto hii yamaji na ame-compare na mradi wa maji unaokuja Kahamasasa hivi unakwenda Tabora mpaka Sikonge. Ni kweli, katikanchi yetu na maeneo mbalimbali kuna changamoto ya majilakini siyo kwamba watu wa vijiji vile wamesahaulika ndiyomaana katika jibu langu nilizungumzia mpango wa majikatika Ziwa Victoria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipofika Musoma jamboambalo tulielekezana na wataalam ni kwamba siyo vyemawatu wa mji kwa mfano ukianzia hapa Bunda mpakaunafika kule Musoma ambako ukiangalia wana utajirimkubwa wa Ziwa Victoria halafu wakaendelea kupata shidaya maji. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika Programuya Uendelezaji wa Sekta ya Maji Awamu ya Pili ni commitmentya Serikali katika kipindi hiki cha miaka hii, tutahakikishausanifu unakamilika lakini siyo usanifu peke yake bali mradimkubwa huu wa maji lengo ni kuwasaidia wananchi wa

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

eneo lile kwa sababu wakikosa maji hata huduma za uchumizinakwama.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Susan Lyimo na MheshimiwaNdassa.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Tatizo la maji salama na maji safi katikanchi hii ni kubwa sana na Mheshimiwa Naibu Waziri waTAMISEMI na Naibu Waziri wa Maji hivi majuzi walikuwakwenye semina maalum ya programu ya maji inayoitwa “UkoTayari?” Takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 70ya wagonjwa katika hospitali wanaugua magonjwayanayotokana na maji machafu. Je, Serikali kupitia Wizarazote (TAMISEMI na Maji) zina mkakati gani kuhakikishakwamba wananchi wanapata maji safi na salama hasakatika Awamu hii ya Tano?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji,majibu kwa ufupi.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yake amedai kwamba kunamagonjwa mengi mahospitalini ambayo yanatokana nakutokuwepo kwa maji safi na salama. Kuanzia bajeti yamwaka 2006/2007 tulianzisha Programu ya Utekelezaji waMiradi ya Maji ambayo ilikwenda kwa muda wa miakamitano, imekwisha Juni, 2016 sasa hivi tumeingia programuya pili. Malengo yetu ni kuhakikisha kwamba tunaweka fedhaya kutosha na miradi mingi sasa inatekelezwa kuhakikishakwamba wananchi wanapata maji safi na salama na kwakaribu zaidi.

Kwa hiyo, tumeshaanzisha na tumelenga kwambaitakapofika mwaka 2020 vijijini tuwe tumeshakwenda zaidiya asilimia 85 na mijini twende asilimia 95. Kwa hiyo, tupo natumeshaanza siyo kwamba tumekaa, tunaendelea natutahakikisha kwamba wananchi hawapati shida yamagonjwa yanayotokana na maji. (Makofi)

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini zaidi ya hapo, sasa hivitume-centralize kuhusiana na ununuzi wa dawa za kutibumaji. Utaratibu uliokuwepo ni kila Mamlaka inanunua dawahizo kivyake sasa tutanunua kutoka center moja kwambaSerikali sasa itakuwa inafanya bulk purchase ya dawa za kutibumaji ili tuhakikishe kwamba maeneo yote tunakuwa na majisafi na salama. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ndassa.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Naomba niiulize Serikali, katika Wilaya yaKwimba visima 188 vimeharibika, havifanyi kazi kutokana nakuzeeka lakini vingine vimechakaa na vimekauka.

Sasa naomba kuuliza, kwa sababu wananchi wa Kataza Mwabomba na hasa Nkalalo pale center wanashidakubwa sana ya maji kutokana na visima hivi kuharibika, je,Serikali sasa ina mpango gani wa kusaidia ili visima hivyoviweze kufanya kazi wakati tunasubiri mradi mkubwa wamaji ya Ziwa Victoria? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwaufupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli hoja yaMheshimiwa Ndassa inakwenda katika maeneo mbalimbalina tumekuwa na changamoto kubwa sana katika visimavya maji na ndiyo maana tumekuwa tukitoa maelekezomaeneo mbalimbali kwamba hivi visima vya maji rechargingcapacity wakati mwingine inashuka kutokana na uharibifuwa mazingira. Hata hivyo, naomba nimhakikishieMheshimiwa Ndassa kwamba katika mpango wa Serikali wasasa hivi kuna mashindano maalum tumeyatoa kwa kilaHalmashauri ya jinsi gani mipango yao mikakatiwatakavyozindua kuhakikisha miradi ambayo mwanzoilikuwa haifanyi vizuri wanafanya ukarabati wa visima hivyona kuweza kuvisimamia. Kuna mpango maalum ambaotumepata fedha kutoka World Bank ambapo zinasaidia sana

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

katika suala zima la kuongeza nguvu za Halmashauri. Kwahiyo, naomba nimhakikishie kwamba kupitia Halmashaurizetu, ni mpango siyo wa Halmashauri ya Kwimba peke yakeisipokuwa ni katika Halmashauri mbalimbali tumewaelekezawataalam wetu wahakikishe sasa wanavikarabati visimambalimbali viweze kutoa maji, lakini hata hivyo kuwezakusimamia vizuri kwa sababu baada ya kufanya hivyowatapata fedha nyingine zaidi kwa ajili ya kuhakikishawanakarabati vituo vyao vya maji. Kwa hiyo, naamini Wilayaya Kwimba itafanya hili ili wananchi wa maeneo yale wawezekuondokana na shida ya maji katika maeneo yao.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na MheshimiwaGeorge Malima Lubeleje, Mbunge wa Mpwapwa sasa aulizeswali lake.

Na. 279

Mradi wa Kuchimba Mabwawa Katika Vijiji vya Mpwapwa

MHE. GEORGE M. LUBELEJE aliuliza:-

Serikali ilikuwa na mpango wa kuchimba mabwawakatika vijiji vya Msagali, Bumila, Makutupa, Lupeta, Inzomvu,Vibelewele, Kimagai, Chunyu na Ng’ambi ambayoyatahudumia wananchi pamoja na mifugo na kilimo chaumwagiliaji.

Je, Serikali imefikia hatua gani ya utekelezaji wampango huo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa George Malima Lubeleje, Mbunge waMpwapwa, kama ifuatavyo:-

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia TASAF IIIimekamilisha uchimbaji wa malambo sita katika vijiji vyaBumila, Msagali, Lupeta, Chunyu, Kazania na Nzogole kwagharama ya shilingi 83,194,200. Wananchi 19,304 watapatahuduma ya maji kupitia vyanzo hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upembuzi yakinifuumefanyika katika kijiji cha Chunyu kwa ajili ya kujengabwawa kubwa ambalo litahudumia vijiji vya Msagali, Berege,Kisokwe, Chunyu na Ng’ambi. Jumla ya shilingi bilioni 17zitahitajika kukamilisha kazi hii. Serikali inaendelea kutafutafedha ili kuanza ujenzi wa bwawa hilo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lubeleje, swali la nyongezakama unalo.

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nimshukuru sana Naibu Waziri kwa majibu mazuri,niipongeze sana TASAF kwa kazi nzuri, sasa nina maswalimawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza ni kwambakazi hii kweli imeanza Mheshimiwa Naibu Waziri lakini badohaijakamilika katika vijiji ulivyotaja. Ni lini kazi hii itakamilikaili maeneo haya yaweze kupata huduma ya maji kwa sababukuna shida kubwa sana ya maji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Serikali inampango gani wa kuongeza vij i j i katika mpango wakuchimbiwa mabwawa, katika vijiji vya Kisisi, Ngalamilo,Iwondo pamoja na Nana kwa sababu hawa nao wanamatatizo makubwa sana ya maji. Ni lini wataanza shughulihizi? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibuswali la Mheshimiwa Lubeleje, Senior MP kama ifuatavyo:-

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

Mheshimiwa Mwenyekiti, lini miradi hii itakamilika nakuweza kutoa huduma ya maji, kwanza naomba nimuahidikatika Bunge hili la bajeti linaloendelea nitaomba mimi naMheshimiwa Lubeleje twende katika miradi hii tukaiangaliekwanza halafu tushauriane vizuri tukiwa site kwa sababunajua Wilaya ya Mpwapwa ina tatizo kubwa sana la maji.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vijiji vingine ambavyoameviorodhesha ni kweli, nafahamu maeneo kwa mfanohata kule Tambi hali ya maji ni mbaya mpaka wanakuja hukuChamkoroma kutafuta maji. Kwa hiyo, tuna kila sababukuhakikisha kwamba Wilaya ya Mpwapwa tunaipakipaumbele. Pia katika ziara yangu hii nikiwa na MheshimiwaMbunge tutaambatana na wataalam kutoka kwenyeHalmashauri tuweze kufika maeneo mbalimbali ikiwa nipamoja na Makutupa ambako Mheshimiwa alikuwaanapigia kelele sana muda mrefu jinsi gani tutafanya kuwekamipango sahihi kusaidia shida ya maji katika Wilaya yetu yaMpwapwa.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na MheshimiwaNjalu Daudi Silanga, Mbunge wa Itilima, swali lake litaulizwana Mheshimiwa Mashimba Ndaki.

Na. 280

Kuunganisha Miundombinu ya Barabara Wilaya ya Itilima

MHE. MASHIMBA M. NDAKI (K.n.y. MHE. NJALU D.SILANGA) aliuliza:-

Wilaya ya Itilima ni mpya na ina eneo kubwalinalovutia kwa ajili ya makazi na shughuli za kilimo:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuunganishamiundombinu ya barabara ya Migato, Nkuyu,Longalombogo, Laini, Bulombeshi na Bumera ili kuvutia watukufanya biashara za mazao katika maeneo hayo?

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Njalu Daudi Silanga, Mbunge wa Jimbo la Itilima,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendeleakuunganisha maeneo ya Migato, Nkuyu, Longolombogo,Laini na Bulombeshi kwa uboreshaji wa mtandao wabarabara kama ifuatavyo:-

(i) Barabara ya Bumera - Bulombeshi na Bumera -Gaswa - Sagata - Laini ya kilometa 20, kwa mwaka wa fedha2015/2016 imefanyiwa matengenezo ya sehemu korofi kwakunyanyua tuta na kuweka changarawe kilometa 3 nakujenga Kalavati 9 katika barabara ya Bulombeshi – Bumera- Gaswa. Katika bajeti ya mwaka 2017/2018 zimetengwashilingi milioni 99.6 kwa ajili ya matengenezo ya mudamaalum urefu wa kilometa sita na matengenezo ya kawaidaurefu wa kilometa nane katika barabara ya Bumera - Gaswa- Laini.

(ii) Barabara ya Migato - Ndoleleji - Nkuyu yenyekilometa 22.9, mwaka wa fedha 2016/2017 imefanyiwamatengenezo katika maeneo korofi kwa kiwango chachangarawe na kujenga makalvati matatu katika barabaraya Migato - Ndoleleji yenye urefu wa kilometa 6.5.

(iii) Lagangabilili - Muhuze - Migato mpaka unapofikaLongolombogo yenye kilometa 40, kwa mwaka wa fedha2015/2016 barabara hiyo imefanyiwa matengenezo katikakipande cha Lagangabilili - Muhuze - Migato kilometa 11 nakujenga makalvati kumi. Katika bajeti ya 2016/2017yamejengwa makalvati sita na kuwekwa changarawebaadhi ya maeneo korofi yenye urefu wa kilometa 15. Aidha,katika bajeti ya 2017/2018, jumla ya shilingi milioni 49.18

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

zimetengwa kwa ajili ya kufanya matengenezo mbalimbalikatika barabara hii.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ndaki swali la nyongeza.

MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana na nashukuru pia kwa majibu mazuri yaSerikali kuhusiana na barabara hizi, lakini nina maswali mawiliya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kunamadaraja makubwa matatu kwenye barabara hizi ambazoMheshimiwa Naibu Waziri amezitaja na Halmashauri ya Wilayaya Itilima imekuwa ikileta bajeti yake ili iweze kuyajengamadaraja haya matatu lakini TAMISEMI wanapunguza bajetihiyo kiasi kwamba Halmashauri imeshindwa kujenga hayamadaraja matatu. Je, Serikali inasema nini juu ya madarajahaya kwa sababu yasipojengwa ni kikwazo kikubwa kwausafiri kwa wananchi wa Wilaya ya Itilima?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kuna ahadi yaMheshimiwa Rais ya kujenga daraja la Mwabasabi, ni yamwaka juzi. Serikali inasema nini juu ya ujenzi wa daraja hilo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli wakatimwingine bajeti zinakuja lakini kutokana na ukomo wa bajetimapendekezo mengine ya Halmashauri yanakuwayamekwama. Katika mchakato wa bajeti ya mwaka huutulivyokuwa tukipitisha hapa, tuliona ni jinsi gani Ofisi ya Rais,TAMISEMI itahakikisha inaangalia vipaumbele katika maeneokorofi hasa kuondoa vikwazo na ndiyo maana tumepitishabajeti ya shilingi bilioni 247.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naombanimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutajitahidikuangalia katika mpango wetu wa kuondoa vikwazomaeneo mbalimbali pale ambapo kuna vikwazo vya msingi

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

katika ujenzi wa madaraja tutatoa kipaumbele. Naombaniwasihi wataalam wetu kule site waanze kufanya designingna needs assessment katika maeneo mbalimbali ili kuonyeshani gharama kiasi gani zinahitajika katika ujenzi wa madarajahaya ambayo yatahusika. Kwa hiyo, naomba nisemekwamba kama Serikali tunalichukua hili lakini katika mpangowetu wa kuondoa vikwazo tutatoa kipaumbele katikamaeneo haya. Lakini suala la ahadi ya Mheshimiwa Rais,naomba niwahakikishie lengo kubwa la Serikali ya Awamuya Tano ni kuhakikisha kwamba ahadi hizi zotezinatekelezeka. Naomba nimhakikishie kwamba katikakipindi hiki cha utekelezaji wa Ilani 2015 - 2020 daraja hili nimiongoni mwa maeneo ambayo tunaenda kuyajenga, lengokubwa ni ili ahadi ya Mheshimiwa Rais iweze kutekeleza katikamaeneo hayo.

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Jafo.Tunaendelea na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,sasa Mheshimiwa Jamal Kasim Ali, Mbunge wa Magomeniaulize swali lake.

Na. 281

Kuwasaidia Wazawa kwenye Viwanda

MHE. JAMAL KASSIM ALI aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani katika kuwasaidiawafanyabiashara wa Kitanzania kuwekeza kwenye viwandanchini?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, majibu.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJIalijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali laMheshimiwa Jamal Kassim Ali, Mbunge wa Magomeni, kamaifuatavyo:-

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa viwanda nchiniunategemea zaidi mazingira ya uwekezaji yaliyopo ikiwa nipamoja na upatikanaji wa ardhi yenye miundombinuwezeshi, sera mbalimbali, mifumo ya kodi na mifumo yaupatikanaji wa vibali vinavyotakiwa kisheria ambayo nimajukumu ya Serikali. Baada ya kuwepo mazingira wezeshi,Serikali inabaki na majukumu ya kuhamasisha wawekezajiwakiwemo wa Kitanzania kuweza kuwekeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu ina mikakatimbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara waKitanzania ili kuwekeza kwenye viwanda hapa nchini.Miongoni mwa mikakati hiyo ni mafunzo yanayotolewa kwaWatanzania wenye nia ya kuwekeza katika viwanda juu yakuibua mawazo ya kibiashara, kuanzisha, kuendesha nakusimamia biashara kupitia SIDO, kutoa ushauri wa kitaalamuwa jinsi ya kuchagua teknolojia sahihi inayoendana na wazola ujenzi wa kiwanda alilonalo Mtanzania kupitia TIRDO,TEMDO na CAMARTEC na namna ya kupata ama kukuzamtaji wa ujenzi wa viwanda kupitia NEDF, SIDO na TIB.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuboresha utendaji,Wizara imeanzisha Dawati la Wepesi wa Kufanya Biashara(Easy of Doing Business) ambalo lina jukumu la kuondoaugumu wa kuanzisha na kuendesha biashara hapa nchini.Vilevile, imeandaa mwongozo kwa Mikoa, Wilaya, Kata naVijiji kutenga maeneo, kusimamia sheria, kanuni, taratibu nakutoa maelekezo kwa wawekezaji. Aidha, Watanzaniawanaotaka ama walio na mitaji mikubwa wanawezakuwekeza kupitia maeneo ya EPZA ambayo yametengwamahsusi kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zinazouzwa nje yanchi. Vilevile, wanaweza kuwasiliana na TIC kupata vivutiombalimbali vilivyowekwa na Serikali kwa ajili ya uwekezaji.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Jamal, swali la nyongezakama unalo.

MHE. JAMAL KASSIM ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawilimadogo ya nyongeza.

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza,Mheshimiwa Waziri katika jibu lake la msingi amekiri kwambamoja ya mambo muhimu kabisa ya Watanzania hawakwenda kuwekeza kwenye viwanda ni pamoja na kuwa namitaji. Watanzania hawa wamefanya biashara kubwa sanana Serikali na wana madeni makubwa ambayo wanaidaiSerikali.

Je, Serikali haioni ipo haja sasa madeni haya ambayowamekuwa wakidaiwa kwa muda mrefu kuyalipa kwaharaka ili Watanzania hawa nao sasa wapate fursa yakwenda kushiriki katika uchumi wa viwanda ambaoMheshimiwa Waziri ameeleza? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, je, Serikalihaioni ipo haja sasa ya kuja na sera maalum ambayo itatoaspecial incentive package kwa wawekezaji wazawaWatanzania ili nao waweze kushiriki kikamilifu katika uchumiwa viwanda kutokana na kuwa nyuma kiteknolojia, kifedhana mambo mengine ambayo ukiwaweka na wenzetu wamataifa mengine Watanzania hawa hawawezi ku-compete?Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo wapo wafanyabiashara,wakandarasi ambao wamefanya kazi na Serikali nawanadai stahiki yao, Serikali itawalipa. Utaratibu wa Serikaliunapitiwa na Mheshimiwa Waziri wa Fedha amekuwaakilisema mara kwa mara kwamba jambo kubwa ni kufanyauhakiki na kadri uhakiki unapofanyika hao watu wanalipwana niwahakikishie kwamba Serikali itawalipa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na vivutio, sasahivi kuna vivutio, suala la muhimu kwa wafanyabiashara waTanzania au kwa Watanzania ambao wangependa kupewavivutio maalum waone hivi vivutio vilivyopo watuambie niwapi sio vizuri. Hatuwezi kubadilisha vivutio, kwanza anzautuambie hiki siyo kizuri hiki ndiyo kizuri ndiyo tutabadilisha.

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nyongo na jirani yakeMheshimiwa Sakaya.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kuniona, naomba niulize swali lanyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kuna mfuko waNEDF ambao Mheshimiwa Waziri ameutaja yaani NationalEntrepreneur Development Fund, kwa mwaka huu pesa hizohazijatoka. Napenda kupata kauli ya Serikali, je, ni lini hizoshil ingi bil ioni 2.5 zitatolewa il i ziweze kuwawezeshaWatanzania wanaotaka kufungua biashara ndogondogo aukufungua viwanda vidogo vidogo waweze kuwezeshwa nakufanya hivyo? Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa ufupi.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfuko wa NEDF kama mlivyoonataarifa ambayo imekuja pekee ni mfuko ambaounawachangamsha wawekezaji ukitoa mikopo mbalimbali.Katika mwaka wa fedha tunaomaliza tulitengewa shilingibilioni 2.4, pesa hizo hazijatoka, lakini mwaka huu haujaisha.Nina imani hizo pesa zitakuja katika mwaka huu wa fedhana nimemkumbusha Waziri wa Fedha kwamba fedha hizoWabunge wanazihitaji haraka wazipeleke Majimbo. Ninaimani kabla jua halijazama pesa hizo zitapatikana.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa jirani yakeMheshimiwa Saumu.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Kwa sababu tunataka tuingie kwenye Tanzania yaviwanda na Tanzania ya viwanda ni lazima iende sambambana uwekezaji kwenye ardhi lakini uwekezaji kwenye ardhiunakumbwa na matatizo makubwa. Tatizo la kwanza vijijivyetu vingi havijaingia kwenye matumizi bora ya ardhi,

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

matokeo yake mwekezaji anakosa nafasi na hata paleambapo vijiji vimeshaingia kwenye matumizi bora ya ardhikuna tatizo kwenye Makamishna wa Kanda katikaupatikanaji wa ardhi lakini sio hivyo tu, hata kwenye Ofisi yaRais ambapo nako kuna matatizo...

MWENYEKITI: Mheshimiwa naomba ufupishe swalitafadhali.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Je, nini kauli ya Serikalikwa wawekezaji wanaohangaika kutafuta ardhi ya kufanyauwekezaji katika kilimo? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa ufupi.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa rafiki yangu Alhajametaka kujua kauli ya Serikali. Tunalitambua tatizo laupatikanaji wa ardhi, ndiyo maana si mara moja MheshimiwaWaziri Mkuu na Ofisi ya TAMISEMI wametoa maelekezo kwamamlaka za Mikoa na Wilaya, watenge maeneo kwa walewalio tayari waweze kuwekeza mara moja. Nirudie, Wakuuwa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, tengeni maeneo yuleanayetaka kuwekeza msimsubirishe.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na Wizara yaMambo ya Ndani, Mheshimiwa Magdalena Hamis Sakaya,Mbunge wa Kaliua sasa aulize swali lake.

Na. 282

Ajali za Pikipiki

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA aliuliza:-

Kwa kuwa lengo la Serikali kuruhusu vyombo vyausafiri wa pikipiki kubeba abiria na mizigo ni kusaidiakurahisisha usafiri na pia kutoa ajira kwa vijana hapa nchinilakini ajali zinazotokana na vyombo hivi kwa sasa ni nyingikuliko vyombo vingine.

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

(a) Je, Serikali inaweza kueleza ni ajali ngapi zabodaboda zimetokea kwa miaka mitatu toka mwaka 2015- 2017 na ni watu wangapi wamepoteza maisha kwenye ajalihizo na walemavu ni wangapi?

(b) Je, Serikali ina mikakati gani ya uhakika ya kuokoamaisha na nguvukazi ya Taifa inayopotea kwa usafiri huu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndaniya Nchi, majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali laMheshimiwa Magdalena Sakaya, Mbunge wa Kaliua, kamaifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha miakamitatu toka Januari, 2015 hadi Februari, 2017 jumla ya ajali5,418 za bodaboda zilitokea na kusababisha vifo vya watu1,945 na majeruhi 4,696.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Jeshi laPolisi inayo mikakati ya kukokoa maisha na nguvu kazi yaTaifa inayopotea kutokana na ajali za bodaboda. Mikakatihiyo ni pamoja na:-

(i) Kupitishwa kwa Kanuni ya Leseni za Pikipiki na Bajajiiliyopita mwaka 2009;

(ii) kutoa elimu ya Usalama Barabarani mashuleni nakupitia vipindi vya redio, televisheni pamoja na vipeperushi;

(ii i) Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwawaendesha bodaboda;

(iv) Kuimarisha usimamizi wa Sheria za Barabarani;

(v) Kusisitiza madereva wa bodaboda kuepukakuendesha kwa mwendo kasi;

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

(vi) Kuchukua hatua kwa vitendo vyote vya ulevi nakuweka viakisi mwanga (reflectors) ili kuonekana kwa urahisi;na

(vii) Kusisitiza matumizi ya kofia ngumu ili kupunguzamadhara punde ajali zinapojitokeza.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa MagdalenaSakaya, swali la nyongeza.

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu ya MheshimiwaWaziri, suala la ajali hizi kutokana na jibu la msingi imekuwani hatari kubwa na ukiangalia idadi ya watu waliopotezamaisha, waliopata ulemavu na majeruhi ni wengi. Vilevileajali hizi zinasababisha kuwepo kwa walemavu,wategemezi, wajane na wagane wengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hatua ambazozinachukuliwa na Wizara na Serikali kuona kwamba ajalizinapungua lakini bado ajali zinaongezeka.

Je, Serikali haioni sababu kubwa ya ajali hizi nikwamba madereva wa bodaboda hawafuati sheria zabarabarani ikiwepo ku-overtake kushoto badala ya kulia?Serikali haioni sababu ya kuendesha masomo au mafunzomaalum kila Wilaya kwa bodaboda wote waweze kuelewakanuni na sheria za barabarani na hivyo kuweza kupunguzaajali za barabarani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, baadhi yamaaskari barabarani badala ya kuwaelimisha bodabodawamefanya bodaboda ni vyanzo vya mapato, kilawakiwaona wanakimbizana nao barabarani matokeo yakewao wanakuwa ni kisababishi cha ajali badala yakupunguza ajali. Serikali inafanya nini na inachukua hatuagani kwa wale maaskari wote ambao wanakimbizana nabodaboda barabarani hajali amebeba abiria au hajabebaabiria i l i kupunguza ajali hizi na kuokoa maisha yaWatanzania wanaopoteza maisha? Ahsante.

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Mambo yaNdani, majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, nimpongeze Mbunge kwamba jambo hililinamgusa na ameongea kwa hisia kama mama na kamamwakilishi wa vijana wetu hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu Serikali imefanyajitihada kubwa kama ambavyo nimeelezea, jambo ambalolimesalia ni familia zetu kuanzia ngazi za familia na ngazi zavijiwe, kuliongea jambo hili kama moja ya jambo linalomalizamaisha ya vijana wetu. Kila tunapokaa tuambizane kwambaukienda mwendo kasi, usipofuata taratibu za uendeshaji wavifaa hivi vya moto, madhara yake ni kupoteza maisha yamwendeshaji mwenyewe ama yule aliyebebwa. Kwa hiyo,hili jambo likienea elimu yake itakuwa kubwa kuliko hii tuambayo mpaka sasa tunaendelea kuifanya ya kutoa seminaWilaya kwa Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuhusu vijana hawakukimbizwa na askari, niwaambie tu Waheshimiwa Wabungeukichukulia kwenye sura moja unaweza ukaona kama vijanawanaonewa sana lakini niseme kuna utaratibu ambaounakuwa unakosewa. Moja, vijana wanakuwawameshapewa leseni lakini inatokea wanapokuwa kulevijiweni wanakabidhiana bodaboda hizi kwa mtu ambayehana leseni, mtu ambaye hana mafunzo yaani amejaribishatu akaona pikipiki inatembea naye anabeba abiria, hili nikosa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimewaelekezaviongozi wa vijiwe vile vya bodaboda kwamba na wenyewewatimize majukumu ya kiuongozi kwamba akitokeamwenzao aliyekosea na wenyewe wawe tayari kumwambiaunatakiwa uripoti kistaarabu polisi ili uweze kumaliza jambolako la kisheria. Kama hawatafanya hivyo, polisi itakuwahaina njia nyingine zaidi ya kumtafuta kwa nguvu na kuwezakumkimbiza popote pale ambapo yupo aweze kufikishwakatika mkono wa sheria.

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabungetunawapenda sana vijana wetu lakini mapenzi yetu kwavijana wetu ni kuhakikisha tunaokoa maisha yao. Kwa hiyo,huruma tunayoweza kufanya ni kuhakikisha tunadhibitijambo hili na hamna njia mbadala zaidi ya kuwezakuhakikisha tunachukua hatua za kisheria kwa yule ambayeanaonekana anakiuka sheria. Kwa wale ambao kwenyevijiwe vyao watatimiza maelekezo haya, tumeelekeza askariwasikimbizane nao bali wamalize kistaarabu mamboambayo yanahusu sheria.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Asha Abdullah Jumaatafuatiwa na Mheshimiwa Waitara.

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi, napenda niulize swali moja lanyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mashaka,matatizo, huzuni na gharama kubwa za matibabuzinaendelea kuwakabili vijana wetu hawa kutokana na hiziajali za bodaboda. Je, ni lini Serikali itaongeza usimamizi naudhibiti wa kuhakikisha kwamba helmet na reflectorzinavaliwa na vilevile kudhibiti upakianaji wa kimishikakiambao unasababisha watu wengi zaidi kuumia kwa wakatimmoja? Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Mambo yaNdani, majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, niseme tu maelekezo tulishatoa na tunachukuahatua kwa maswali yote mawili aliyoyauliza. Moja likiwepohili la kuvaa kofia ngumu, tumeweka hiyo ni sheria natumeenda mbali zaidi tunataka si tu mwendesha bodabodatunataka hata abiria naye atimize wajibu huo wa kuvaa kofiangumu. Pamoja na hilo, hili lingine la ubebaji wa mishikakikama alivyoita, abiria zaidi ya moja na lenyewe tumeelekezapopote pale yanapotokea lichukuliwe kuwa ni kosa.

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema mwanzokwamba jambo hili ni vema likaongelewa kwa ngazi yakijamii na familia kwamba tuendelee kuwaelekeza vijanawetu. Mara nyingi vijana wetu wakielekezwa kwa mkonowa Serikali wanaona kama wanaonewa lakini wakielekezwakuanzia ngazi ya familia, tunapokaa tuwaambie vijana wetutunawapenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi mwenyewe niliwahikuwapa vijana bodaboda kule Jimboni, niliwahi kuwapawadogo zangu, watoto wa dada zangu lakini jambo lakwanza nililowaambia, niliwaambia nawapa chombo hikicha moto lakini chombo hiki kinauwa. Wakiambiwa mkonoambao usio wa kisheria ambao ni wa kifamilia linawakaazaidi kutambua kwamba ukikosea masharti ya uendeshajiukaenda kasi, ukakosea sheria za uendeshaji barabarani,gharama yake ni kupoteza maisha ya mwendeshajimwenyewe na abiria aliyebebwa kutoka kwenye hichochombo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Jimbo la Ukonga lina kata 13 na kata zotezina bodaboda karibu vijiwe zaidi ya kumi kila kata moja.Ukonga tumechangishana fedha tukajenga Kituo cha Polisikule Chanika na kingine kinataka kujengwa pale Kata yaKivule, lakini kwa hali ilivyo sasa, wananchi wa Ukonga nahasa bodaboda nikiwaambia wachangie fedhahawatachangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninavyozungumza usiku wakuamkia leo, wanakuja askari zaidi ya 20 wana bodaboda,walikuwa wanakuja na gari wanaificha, halafu wanapigawatu mpaka na marungu, wana-search kwenye wallet,kwenye pochi kila mahali wanaomba fedha. Sasa wanaendawanakusanya bodaboda zile wanaomba shilingi 10,000 kwalazima, kama huna zinapakiwa kwenye gari zinapelekwacentral.

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

Mheshimiwa Mwenyekiti, natakiwa nijue, ili kuletamahusiano mazuri kati ya vijana wa bodaboda na polisi,Waziri anatoa kauli gani kuhusiana na jambo hili? Hata hayamambo ya mauaji kama watu wana uhasama hawatoitaarifa. Wanawakimbia kwa sababu ukikamatwa na polisiwala hakuulizi leseni, wala hakuelekezi, kama huna pesaunatembea. Naomba Waziri atoe kauli hapa kusaidia vijanawa bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam na hasa Jimbo laUkonga. Ahsante Mwenyekiti.

MWENYEKETI: Mheshimiwa Waziri wa Mambo yaNdani, majibu kwa ufupi.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, niseme tu kwamba maelekezo ya Wizara tuliyotoani kwamba kuwa na bodaboda sio kosa na tumeelekezawatu wanaofanya makosa ndiyo wakamatwe. Kuwa tu nabodaboda haitoshi kuwa kosa kwa sababu hilo ni jamboambalo lipo kisheria. Kwa maana hiyo nimepokea tu hiyo yanyongeza aliyoisema ambayo yenyewe imekaa kituhumazaidi nitalifanyia kazi, kama kweli lipo tutachukua hatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini maelekezo yetutumesema kama vijana wamekosea wafikishwe kwenyemkono wa sheria lakini kama hawajakosea waachwewafanye kazi zao za kujitafutia maisha kwa uhuru na usalamana wala wasikimbie. Nilielekeza nikasema kuna wakatimwingine hata wanaweza wakawamata kwa bahati mbayana ikafika mpaka vituoni, niliwaambia wasione aibukumuachia yule ambaye walimkamata kimakosa ambayealikuwa hausiki.

Nilisema hata wamuombe radhi kwamba wewe situliyekuwa tunakutafuta nenda kaendelee na shughuli lakiniisiwe kosa kwamba yeyote ambaye ameshakamatwa akifikakituoni basi inakuwa kazi kutoka, tuwatendee haki kufuatanana kosa kama amefanya ama hajafanya.

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, tunaendelea na Wizara ya Maliasili

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

na Utalii na swali la Mheshimiwa Goodluck Mlinga, Mbungewa Ulanga litaulizwa na Mheshimiwa Sadiq Murad kwa niaba.

Na. 283

Wanyama Waharibifu wa Mazao

MHE. SULEIMAN A. SADDIQ (K.n.y. MHE. GOODLUCKA. MLINGA) aliuliza:-

Kumekuwa na ongezeko kubwa la wanyamawaharibifu kama vile viboko na tembo kwenye maeneo yamashamba katika Kata za Ruaha, Chilombola, Ilonga,Ketaketa, Mbuga ya Lukande na Lupilo.

Je, Serikali ina mpango gani kuzuia uharibifu huo wamazao?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali laMheshimiwa Goodluck Mlinga, Mbunge wa Ulanga, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwambakumekuwepo na ongezeko la wanyama wakali na waharibifukatika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo Kata ya Ruaha,Chilombola, Ilonga, Ketaketa, Mbuga ya Lukunde pamojana Lupilo. Kutokana na madhara yanayosababishwa nawanyama waharibifu hususan tembo na viboko, Serikaliinaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kunusurumaisha na mali za wananchi. Hatua hizo ni pamoja na:-

(i) Kufanya doria za wanyamapori wakali nawaharibifu ili kudhibiti madhara ya wanyamapori hao kwakutumia Askari Wanyamapori waliopo katika Pori la AkibaSelous eneo la Ilonga, Kikosi Dhidi ya Ujangili pamoja naAskari Wanyamapori katika Halmashauri ya Wilaya Mahenge;

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

(ii) Kutoa elimu ya uhifadhi kwa jamii kuhusu kujiukingana wanyamapori wakali na waharibu wakiwemo tembo naviboko;

(iii) Kuendelea na mbinu mbalimbali za kupunguzamadhara yatokanayo na uvamizi wa tembo na kukuzakipato kwa mfano matumizi ya mizinga wa nyuki, oil chafuna kilimo cha pilipili kuzunguka mashamba na kadhalika;na

(iv) Aidha, Wizara imekuwa inafanya majararibio yakutumia ndege zisizokuwa na rubani yaani drones kwa ajiliya kufukuza tembo pindi wanapovamia makazi namashamba ya wananchi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Saddiq Murad, swali lanyongeza.

MHE. SULEIMAN A. SADDIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi, nina maswali mawili madogoya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwaMikumi National Park imepakana na Wilaya ya Mvomero nakata za Doma, Msongozi, Melela, Malaka pamoja naMangaye; kwa kuwa wanyama waharibifu wanaingia sanakatika mashamba ya wakulima na wanaharibu sana mazaoya mahindi, mpunga, nyanya na kadhalika na kwa kuwatembo wengi sana wameshafanya uharibifu mkubwa, je,Serikali sasa iko tayari kuongeza Askari wa Wanyamaporikatika maeneo hayo angalau kila kata kuwe na askari mmojaili kuondoa tatizo ambalo wananchi wanakabiliana nalo?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwaWilaya ya Mvomero ina upungufu mkubwa wa vitendea kazi,je, Serikali iko tayari sasa kuisaidia Wilaya ya Mvomero vitendeakazi pamoja na masuala mengine ya usafiri ili tuwezekukabiliana na hali hiyo? (Makofi)

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli kwamba wanyama wakali na waharibifuwameongezeka katika maeneo mbalimbali hapa nchi nakatika eneo la Wilaya ya Mvomero wanyama hawawameongezeka sana katika maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali lanyongeza la Mheshimiwa Saddiq Murad Mbunge waMvomero, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi pamoja na Mkuu waWilaya na Mkurugenzi wa Wilaya tumetembelea hayomaeneo ambayo yamezidiwa sana na uvamizi wa wanyamawakali na waharibifu. Wizara itaongeza askari kusaidianana wale walioko katika Wilaya ya Mvomero ili kupambanana kadhia hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, Wizara itashirikiana naHalmashauri ya Mvomero kwa kuipa vitendea kazi zaidipamoja na kuwasaidia katika usafiri ili waweze kukabilianana tatizo hili ambalo limeongezeka sana katika Wilaya hiyo.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbaraka Dau hhalafuatafuata Mheshimiwa Bulaya.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Tatizo la viboko lililopo katika Jimbo laUlanga linafanana sana na tatizo la viboko lililopo KisiwaniMafia. Wananchi wa kata za Ndagoni, Baleni na Kirongwewameharibiwa mazao yao na ng’ombe wao wameuwawana viboko waharibifu. Kutokana na ongezeko kubwa sanala viboko hawa na Kisiwa cha Mafia ni eneo dogo, je,Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari kutoa ruhusa tuanzekuwavuna viboko hawa kwa sababu kule ni kitoweo pia?Ahsante. (Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nichukue fursa hii kumpa pole sanaMheshimiwa Dau na wananchi wake wa Mafia kwa kadhiahii ambayo imewakumba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua ambayo tutachukuani pamoja kutuma wataalamu waende wakafanye sensa ilitujue kwamba kuna viboko wangapi katika eneo hilo natuweze kuangalia kama kuna uwezekano wa kuwezakuwavuna hao viboko ili kupunguza madhara yake kwawananchi wa eneo la Mafia.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Bulaya.

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizola wanyama waharibifu ni kubwa sana katika Jimbo langula Bunda Mjini na Jimbo la kaka yangu Boni. Sisi wananchiwa Mkoa wa Mara hatuhitaji kuomba chakula na mwakajana Mheshimiwa Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge,Mheshimiwa Jenista alikuja akaliona tatizo hilo naMheshimiwa Waziri mwenyewe anajua, tatizo la tembokuharibu mazao ya wananchi, kuua wananchi pamoja namali zao. Sasa nataka kujua, ni lini Serikali mtahakikishamnakuwa na mkakati wa kudumu wa kumaliza tatizo hilikatika vijiji vyote vinavyozunguka hifadhi? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa ufupi.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli kwamba katika Mkoa wa Mara na hasaWilaya za Bunda, Serengeti, Tarime na Wilaya za maeneo yalekuna kadhia kubwa sana ya wanyama waharibifuwanaotoka hasa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuingiakatika mashamba na wakati huu ambapo mavunoyanakaribia ndiyo kadhia hii inaongezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua za muda mfupi,mwaka tutachukua hatua ya kuongeza askari na magari yapatrol i l i kuhakikisha kwamba kama mwaka janatunawaokoa wananchi na tatizo hili.

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

Pili, tunazungumza na washirika wetu wa maendeleokuona ni namna gani tunaweza kuweka fensi ya kilometa140 ili kuangalia kwa majaribio kama itakuwa ni suluhisho latatizo hili.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Ester AlexanderMahawe, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake.

Na. 284

Kero ya Kadi za Kulipia Hifadhi ya Ngorongoro

MHE. ESTER A. MAHAWE aliuliza:-

Kadi za kulipia Ngorongoro zimekuwa kero kwawageni na wahudumu kwani muda mwingi umekuwaukipotea wakati kufanya malipo.

Je, ni lini Serikali itafanya marekebisho ili kuwe namfumo wa kadi kama za TANAPA?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali laMheshimiwa Ester Alexander Mahawe, Mbunge wa VitiMaalum, Mkoa wa Manyara, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu kwakushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoroimebadilisha mfumo wa malipo na utoaji wa vibali vyakuingia katika Hifadhi ya Ngorongoro.

Mfumo huu mpya kabisa ujulikanao kamaNgorongoro Safari Portal ulianza kutumika tarehe 01 Februari,2017 na umeonyesha ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja nakuondoa kabisa msongamano wa wageni katika malangoya kuingia kwenye hifadhi na kuongeza ufanisi katikamakusanyo ya mapato.

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumo huu mpya ukokwenye mtandao wa internet na hivyo huwezesha wakalawa utalii kulipa na kupata vibali moja kwa moja kwa njia yamtandao bila kulazimika kufika katika ofisi, kwenda benkiau malango ya kuingia katika Hifadhi za Ngorongoro.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mahawe, swali la nyongeza.

MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziribaada ya kero hiyo kurekebishwa lakini bado driver guideswanapofika pale getini wanatakiwa kuandikisha majina yawageni ambao wanawapeleka Ngorongoro ama Serengeti.Kwa hiyo, hilo nalo bado linaleta usumbufu mkubwa kwasababu counter inayotumika katika uandikishwaji pamojana ku-submit zile risiti ni moja. Je, Mamlaka haioni kwambakuna ulazima sasa na umuhimu wa kuongeza madawati yaleya kutolea huduma hiyo ili kuokoa muda wa wageniunaopotea pale getini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwabiashara yoyote inahitaji huduma bora kwa wateja yaanicustomer care na hili limeonekana likikosekana maeneo yageti la Lodware na Naabi Hill. Je, Mamlaka haioni kwambawafanyakazi wale wanahitaji kupatiwa indoor training yamara kwa mara ili kuweza kufanya utalii wa ushindani nanchi jirani ambako customer care iko juu? Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nishukuru sana kwa maswali mazuriambayo Mheshimiwa Mahawe ameyauliza. Maswali haya nirelevance kabisa kwa kazi ambayo tunaifanya pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza suala la kuongezamadawati tumeliona na pale kwenye lango kuu kutokaKaratu unavyoingia Ngorongoro tumeongeza watendaji kazikwa ajili ya kuwatambua watu ambao wanataka kuingiandani ya hifadhi. Shughuli hii ni muhimu kwa sababu za

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

usalama, lakini pia kwa sababu ya kuweza kukagua mapatotuliyokusanya na watu ambao wameingia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini napenda nimuelezeMheshimiwa Mahawe kwenye swali lake la pili kwamba nikweli wafanyakazi wanahitaji kupatiwa mafunzo ya marakwa mara ili kuongeza ubora wao katika customer care, lakinipia katika kushirikisha na kutoa maelekezo kwa wageni. Kwahiyo, shughuli hii tutaendelea kuifanya kila siku natunategemea kwamba itaongeza ufanisi wa eneo hili.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Omary Badwel atafuatiwana Mheshimiwa Gidarya.

MHE. OMARY H. BADWEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo lanyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa utozaji huu waushuru na kodi mbalimbali kutoka Wizara hii ya Maliasili naUtalii katika maeneo mbalimbali mahali pengine umekuwaama haukufikiria vizuri au umekuwa kero. Kwa mfano katikamazao ya ubuyu na ukwaju, mazao ambayo yana bei ndogosana kwa maana ya shilingi 100 kwa kilo na katika masokoya Dar es Salaam na maeneo mengine ya miji yanauza kwashilingi 200. Mazao haya yamekuwa yakivunwa ama na kinamama wenye kipato cha chini au vijana na watu wengineambao wanapambana na umaskini.

Hata hivyo, Wizara hii kupitia Maliasili wanatozashilingi 350 kwa kilo na imewafanya sasa wafanyabiasharahawa washindwe kabisa kufanya hii biashara kwa sababubei yenyewe ni ndogo na sasa inafikia shilingi 500 baada yaushuru huu.

Je, Mheshimiwa Waziri anafikiria nini juu ya kufutaushuru huu ili kuwasaidia wale wafanyabiashara wadogowadogo waweze kupambana na umaskini? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa ufupi.

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli kwamba katika tozo za mazao ya misituna mazao katika sekta ya utalii zingine ni kero sana kwawananchi. Moja ya tozo hizo ambazo ni kero kwa wananchini tozo ya matunda ya ubuyu na matunda mengine yamisituni ambayo wananchi wanakusanya na kupeleka kuuza.Napenda kulihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba tozo hiziambazo ni kero zitafutwa pamoja na hii ya kutoza kodi yaubuyu. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Gidarya.

MHE. ANNA J. GIDARYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kumekuwa piana kero katika sekta ya uwindaji katika utoaji leseni hasakwa wazawa. Soko hili limemilikiwa zaidi kwa wageni kulikowazawa. Kwa mfano, leseni ya uwindaji kwa mwaka unalipadola 600 na tena unalipa dola 200.

Je, Wizara haioni umuhimu wa kuwapa wazawa zaidiili pia waweze kulinda hifadhi zetu? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa ufupi.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, katika mwaka uliopita wa uwindaji unaoishiamwezi Juni, 2017 vitalu vilivyokuwa vimetolewa asilimia 85walipewa wazawa na ni vitalu asilimia 15 tu ambavyowalipewa wageni. Kwa hiyo, siyo kweli kwamba utoaji wavitalu unawapendelea wageni.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na Wizara yaUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Mheshimiwa MendradLutengano Kigola, Mbunge wa Mufindi Kusini sasa aulize swalilake.

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

Na. 285

Ujenzi wa Barabara ya Nyololo- Igowole - Mtwango

MHE. MENDRAD L. KIGOLA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza kujenga barabara ya kilometa40 ya kutoka Nyololo - Igowole - Mtwango kwa kiwango chalami?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, napenda kujibu swali laMheshimiwa Mendrad Lutengano Kigola, Mbunge wa MufindiKusini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Nyololo-Igowole hadi Mtwango au hadi Kibao yenye urefu wakilometa 40.4 ni barabara ya Mkoa inayohudumiwa naWakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Maandalizi kwaajili ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lamiyanaendelea ambapo upembuzi yakinifu, usanifu wa kinana uandaaji wa nyaraka za zabuni kwa ajili ya ujenzi kwakiwango cha lami wa barabara hii yamekamilika. Kwa sasaSerikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi kwakiwango cha lami.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuifanyiamatengenezo ya aina mbalimbali barabara hii ili iwezekupitika katika majira yote ya mwaka wakati ikiendeleakutafuta fedha kwa ajilii ya ujenzi wa kiwango cha lami.Aidha, katika mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali imetengajumla ya shilingi milioni 450.077 na katika mwaka wa fedha2017/2018 Serikali imetenga jumla ya shilingi milioni 160.511kwa ajili ya kuifanyia matengenezo ya aina mbalimbalibarabara hii.

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kigola, swali la nyongeza.

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri, lakinihii barabara ina miaka minne sasa tangu upembuzi yakinifukukamilika. Naibu Waziri wa Ujenzi aliyepita aliwahi kuja kuleakaongea na wananchi akasema kwamba ujenzi wakiwango cha lami utaanza mara moja. Naibu Waziri naombaawaambie wananchi ni lini barabara hii itaanza kujengwakwa kiwango cha lami kwa sababu upembuzi yakinifuulishakamilika? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wananchi wakijiji cha Nyololo, Nziwi, Igowole, Mninga, Kibao, Lufuna naMtwango waliwekewa alama ya ‘X’ kwenye nyumba zaona Serikali iliahidi kwamba alama ya ‘X’ ambayo ni ya kijaniwatapewa fidia. Wananchi wameshindwa kuendelezanyumba za biashara kwa sababu zimewekewa alama ya‘X’. Ni lini Serikali italipa fidia wananchi wale ambaowanasubiria mpaka leo? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosemakwenye jibu la msingi barabara hii tutaanza kuijenga maratutakapoanza kupata fedha. Nimhakikishie tu MheshimiwaKigola kwamba Serikali itatumia kila aina ya nguvu zakekuhakikisha kwamba inapata fedha na kutekeleza ahadi audhamira ambayo Naibu Waziri aliyepita aliionyesha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ni kwambani kweli wote waliowekewa alama ya ‘X’ za kijani watalipwafidia na zitalipwa tutakapopata hizi fedha za ujenzi. Ulipajiwa fidia unaenda sambasamba na ujenzi wa barabarahusika. Kwa hiyo, fedha hizi tunazozitafuta tunazitafuta zote,za ujenzi na za kulipa fidia.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Devotha Minja naMheshimiwa Martha Mlata.

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa barabara yaKichangani - Tubuyu katika Manispaa ya Morogoro ambayoina urefu wa kilometa nne imejengwa kwa kilometa mojakwa shilingi bilioni tatu yaani kilometa nne imejengwa kwashilingi bilioni 12. Je, Serikali iko tayari kupeleka wataalamkwenda kubaini ubadhirifu wa ujenzi wa barabara hii ambayoimejengwa kwa Mfuko wa Benki ya Dunia? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwaufupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepataconcern hii kutoka kwa Wabunge hasa wa Mkoa waMorogoro na hasa barabara hizi zinazojengwa under StrategicCities Project pamoja na barabara zingine ambazozinajengwa katika Manispaa. Bahati nzuri kwa taarifa zaMorogoro tunazifanyia kazi, naomba nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba tutaenda kufanya verificationkuangalia value for money katika eneo lile lakini zoezi hilotutalifanya maeneo mbalimbali ikiwemo katika Mji wa Hai,Mkoa wa Kilimanjaro. Lengo letu ni kwamba thamani yafedha ipatikane ili wananchi waweze kupata hudumainayolingana na thamani ya fedha. Kwa hiyo, MheshimiwaMbunge kilio chake kimesikika tutaenda kulifanyia kazi eneohili.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mlata.

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Naiomba Serikali itoe tamko hapa kuwaelezawananchi wa Ilongelo, Mdida, Singa, Mtinko, Nkungi hadiHaydom kwa ahadi yao waliyoahidiwa na Rais wa Awamuya Nne kwamba barabara ya lami itajengwa kutoka Singidakupita maeneo hayo hadi Haydom lakini sasa hivi hakunakinachoendelea. Naomba Serikali iwaambie wananchi hao.Ahsante.

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwaufupi.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibuswali la nyongeza ya Mheshimiwa Martha Mlata, Mbunge waViti Maalum, Mkoa wa Singida na Mwenyekiti wa CCM waMkoa huo, kama ifuatavyo:- (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumhakikishiaMheshimiwa Mbunge kwamba juhudi zake za kufuatilia ujenziwa barabara hii kwa kiwango cha lami hatimaye zitazaamatunda kwa sababu ahadi ambayo ilitolewa na Rais waAwamu ya Nne tunayo na nimhakikishie kwamba ahadi hiyotutaitekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaenda kutekeleza ahadihizi awamu kwa awamu kama ambavyo nimekuwanikimueleza yeye pamoja na Wabunge wenzakewanaofuatilia sana barabara hii, barabara hii inaunganishaWabunge wengi sana.

MWENYEKITI: Tunaendelea na Wizara ya Nishati naMadini, Mheshimiwa Lolesia Jeremiah Bukwimba, Mbunge waBusanda sasa aulize swali lake.

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Kwanza nianze kutoa pole kwa wananchi waJimbo la Busanda hasa kule Nyamalimbe ambakowamepatwa na maafa, kwa watu kufukiwa na vifusi kwenyemgodi wa Nyamalimbe pale Magenge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naomba sasa swali langu namba 286 lipatiwe majibu.(Makofi)

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

Na. 286

Umeme wa REA Busanda

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA aliuliza:-

Je, ni l ini mradi wa umeme wa REA utaanzakutekelezwa katika Jimbo la Busanda?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNishati na Madini, napenda kujibu swali la Mheshimiwa LolesiaJeremia Bukwimba, Mbunge wa Busanda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa MradiKabambe wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatuumeanza rasmi nchi nzima tangu mwezi Machi, 2017. Mradihuu unajumuisha vipengele-mradi vya densification, gridextension na off-grid renewable. Mradi huu unalengakuongeza wigo wa usambazaji umeme katika vijiji vyotevilivyobaki nchi nzima, vitongoji vyote, taasisi zote za ummana sehemu za pembezoni ikiwa ni pamoja na maeneo vyavisiwa. Usambazaji wa umeme katika Jimbo la Busandautafanyika kupitia vipengele-mradi vya densification na gridextension utakaokamilika mwaka 2020/2021.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya kupeleka umemekatika Jimbo la Busanda pamoja na Wilaya yote ya Geitaitajumisha ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovoti 33yenye urefu wa kilometa 184.7; ujenzi wa njia ya umememsongo wa kilovoti 0.4 yenye urefu wa kilometa 582 naufungaji wa transfoma 109. Mradi huu utaunganisha watejawa awali 8,834. Gharama za mradi huu ni shilingi bilioni 25.6.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bukwimba, swali lanyongeza.

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasi hiikumshukuru Mheshimwia Naibu Waziri kwa majibu mazurilakini ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwakwa muda mrefu sana kuna baadhi ya sehemu kwa mfanondani ya Jimbo la Busanda wana umeme, lakini katika Taasisiza Serikali na za Umma hazijaweza kufikiwa na umeme huo.Nikitoa mfano, Kituo cha Afya Bukoli, Kituo cha AfyaLwamgasa, Shule ya Sekondari ya Bukoli, Shule ya SekondariLwamgasa, Shule ya Sekondari Chigunga na kwenye Zahanatiya Chigunga umeme huu haujafika.

Je, Serikali inasemaje sasa kuhusu mpango wakuhakikisha kwamba Taasisi zote za Umma pamoja nasehemu za kuabudia zinafikiwa na umeme wakati utekelezajiunapoendelea? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa tumeona katikavyombo vya habari katika mikoa mbalimbali umemeukizinduliwa ili Awamu ya Tatu ya REA iweze kuanza kufanyakazi lakini katika Mkoa wa Geita sijaona jambo hili likifanyika.(Makofi)

Je, ni lini sasa Serikali itazindua rasmi umeme wa REAAwamu ya Tatu katika Mkoa wa Geita ili wananchi wawezakuanza kuona utekelezaji wake? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwaufupi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, awali ya yote nianze kumpa pole sanaMheshimiwa Bukwimba kwa wananchi wake wannewalioangukiwa na kifusi kwenye machimbo ya kuleNyamalimbe, pole sana Mheshimiwa Bukwimba kwa niabaya wananchi wa Geita.

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyoulizaMheshimiwa Bukwimba, nianze kwanza kumpongezaanavyouatilia maendeleo ya umeme kwa wananchi waJimbo la Busanda. Hata hivyo, mradi kabambe wa REAAwamu ya Tatu, kama nilivyoeleza kwenye jibu langu la msingiunalenga kupeleka umeme katika vijiji vyote vilivyobaki lakinikatika vitongoji vyote vilivyobaki na taasisi za umma. Nisisitizekatika hili, Taasisi za Umma ninamaanisha vituo vya afya,shule, misikiti, masoko na kadhalika, haya yote yatafikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie MheshimiwaBukwimba, vijiji vyake vya Nyaluyeya ambavyo vituo vya afyahavina umeme sasa vitawekewa umeme. Kule Nyamalimbevituo vya afya pamoja na shule vitawekewa umeme. Shuleza Bukoli, shule za Kamena, Kaseme pamoja na vituo vyakwa Mheshimiwa Musukuma, kisiwa chake cha Izumacheletutaenda mpaka huko.

Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa wa Busandakwamba vitongoji vyote ambavyo vina zahanati tutawekeazahanati umeme pamoja na shule. Umeme mwinginembadala, kwenye taasisi za umma tutawawekea pia umemewa solar. Hii ni kwa sababu ikitokea kuna hitilafu ya umemebasi umeme wa solar uweze kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, ni lini sasatunazindua, nitumie nafasi hii kusema kwamba ni kwelitumezindua mikoa kumi tu nchi nzima, tunaendelea kuzinduamikoa yote 15 iliyobaki ya Tanzania Bara, mkoa mmoja hadimwingine na mahali pengine ikilazimika tutazindua kila wilayaili wananchi waweze kujua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hiikumueleza Mheshimiwa Lolesia Bukwimba kuanzia mwezi wasaba tutaanza uzinduzi, kwa hiyo, mwezi wa sabaMheshimiwa Bukwimba tufuatane ili tukazindue umeme waREA Awamu ya Tatu katika Jimbo lako.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Halima Bulembo halafuatafuatiwa na Mheshimiwa Sophia Mwakagenda.

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

MHE. HALIMA A. BULEMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera kuna vijijiambavyo vimewekwa katika mpango wa Rea Awamu waPili, vij i j i kama Songambele, Kitwe, Mulongo lakinihavikupatiwa umeme. Vijiji hivi hivi pia vimewekwa katikaMpango wa REA Awamu ya Tatu. Je, Serikali itahakikishakatika Mpango huu wa REA Awamu ya Tatu, vijiji hivihavitakosa umeme? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwaufupi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, vij i j i vya Kyerwa ambapo vimebakia 27vitapelekewa umeme vijiji vyote na siyo tu vijiji ambavyoumetaja vya Mulongo pamoja na Songambele lakini vikoviji j i na chuo vya ufundi pale Kyerwa na chenyewetutakipelekewa umeme. Kwa hiyo vijiji vyote 27 vilivyobakivitapelekewa umeme katika mradi wa REA Awamu ya Tatu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Sophia.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Natambua katika Mkoa wa Mbeyatayari REA Awamu ya Tatu imeishazinduliwa, lakini kunachangamoto kubwa sana katika Wilaya ya Rungwe katikavijiji vya Lupoto, Katabe na Ibungu mpaka sasa hawajapataumeme na hatujajua ni lini watapata. Naomba majibu yaSerikali tuweze kujua ni lini Wilaya hizi zitapata umeme waREA? Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwaufupi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza kabisa Mheshimiwa Mbunge nakushukuruulivyouliza, hapa tunapoongea katika kijiji cha Lugotawakandarasi wanaendelea na kazi, kwa hiyo wanaendeleakupata umeme, lakini vijiji vya jirani pia tutavitembeleaambavyo bado lakini vijiji vyote ulivyotaja kwenye eneo lako

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

vitapata umeme wa REA na umeanza mwezi wa tatu nakwako wewe utakamilika mwakani mwezi wa saba.

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunaendelea na swali lamwisho, Mheshimiwa Kasuku Samson Bilago, Mbunge waBuyungu sasa aulize swali lake.

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,kabla sijauliza swali langu naomba nitoe pole kwa raia waBurundi waliopigwa na wanajeshi wa Jeshi la WananchiTanzania katika Soko la Kabare, Kata ya Mwarama, Jimbola Buyungu. Naomba sasa kwa niaba ya wananchi wa Jimbola Buyungu swali namba 287 lipate majibu.

Na. 287

Uwepo wa Madini katika Wilaya ya Kakonko

MHE. KASUKU S. BILAGO aliuliza:-

Maeneo mengi ya Wilaya ya Kakonko yanaonyeshakuwepo kwa madini yenye thamani kama dhahabu naalmasi.

(a) Je, kuna tafiti zozote zil izofanyika kuhusuupatikanaji wa madini Wilaya ya Kakonko?

(b) Kama zipo, je, ni madini gani yanapatikana na nikatika maeneo yapi?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNishati na Madini, napenda kujibu swali la Mheshimiwa KasukuSamson Bilago, Mbunge wa Buyungu, lenye sehemu (a) na(b) kama ifuatavyo:-

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, kuanzia miaka ya 1970Serikali kupitia Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) imekuwaikifanya tafiti mbalimbali za kubaini uwepo na upatikanajiwa madini katika Wilaya ya Kakonko. Baadhi ya tafitizilizofanyika ni pamoja na upimaji na uchoraji wa ramani zakij iolojia katika eneo la Kakonko. Maeneo mengineyaliyofanyiwa kazi hiyo ni Kalenge na sehemu ya Kibondo.Aidha, kati ya mwaka 1980 na 1985, Serikali kwa kushirikianana Shirika la UNDP walifanya utafiti mwingine wa madini yachokaa katika eneo la Bumuli Wilayani Kakonko.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, tafiti hizo zilibaini uwepowa madini ya dhahabu katika maeneo ya Mwironge, Mwiruzina Nyakayenze; chokaa katika eneo la Bumuli na katika eneoya Keza, Kibingo, Nkuba pamoja na maeneo ya Kasanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafiti za kina zinahitajika ilikujua kina cha madini yaliyogunduliwa. Serikali inaendeleakuhamasisha makampuni mbalimbali binafsi ili kufanya utafitiwa kina na kuendeleza uchimbaji katika Jimbo la Kakonko.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nape atafuatiwa naMheshimiwa Rhoda Kunchela.

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti…

MBUNGE FULANI: Wewe si una maswali mawili.

MBUNGE FULANI: Endelea.

MWENYEKITI: Ndiyo, Mheshimiwa Bilago halafuMheshimiwa Nape. (Kicheko)

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante, ulitaka kupanua goli. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazurialiyotoa kwa swali hili, naomba kuuliza maswali mawili yanyongeza.

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, katika eneohili ambalo lina chokaa linaloitwa Bumuli maarufuNgongogwa liko katika Hifadhi ya Moyowosi - Kigosi.Wafanyabiashara wanaotaka kuchimba hiyo chokaawamekuwa wakikwamishwa na shughuli zinazofanyikakatika hifadhi na Mamlaka ya Hifadhi kuwazuia kufanyashughuli hiyo. Je, Serikali inaweza ikatoa utaratibu mahsusiwatakaofuata wananchi wa Kaknoko ili waweze kuchimbachokaa hiyo ambayo ni grade two? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo dhahabu ambayoimepatikana sehemu za Nyamwilonge na Nyakayenze namaeneo ya Ruhuli inayoendelea kuchimbwa na wachimbajiwadogo wadogo kwa kutumia zana hafifu. Je, Serikali ikotayari kutoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo wadogo katikamaeneo hayo? Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza namshukuru Mheshimiwa Bilago lakinipia namshukuru kwa sababu anafuatilia sana maeneo yawachimbaji katika maeneo yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imechukua hatuanyingi sana, lakini kulingana na Sheria ya Madini na Sheria yaHifadhi ya Mazingira, kifungu cha 95 cha Sheria ya Madinikinatoa utaratibu na utaratibu unaotumika hivi sasakuchimba madini katika maeneo mengine kwanza kabisamtu anaruhusiwa kupata leseni lakini akishapata leseni yauchimbaji anawaona watu wa maliasili ili apate kibali chamaandishi na huo ndiyo utaratibu unaotumika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshatoa leseni 70 katikamaeneo karibu na Hifadhi ya Moyowosi na hizo leseniwananchi wanachimba na kuna vikundi viwili vya ushirikaambapo wanafanya kazi hiyo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Bilagoutaratibu upo lakini ni vizuri tukaa zaidi ili nikueleweshe iliwananchi wa Jimbo lako wanufaike zaidi.

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la nyongeza la pili,maeneo ya Nyamwilonge na Nyakayenze pamoja na Makelena maeneo ya mbali, maeneo haya tumeshatoa leseni kwasababu kuna uchimbaji mzuri wa dhahabu. Mwaka 2012kuligunduliwa dhahabu na tukalitenga eneo hilo na hivi sasakuna leseni 76 katika maeneo hayo. Nimuombe MheshimiwaBilago awahamasishe wananchi wa Jimbo lake ili eneolililobaki tulilolitenga pia walitumie kwa manufaa ya maishayao.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nape.

MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo lanyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa chanzo kikubwacha migogoro kati ya wananchi na wawekezaji wanaoendakuwekeza kwenye sekta hii ya uchimbaji wa madini niutaratibu unaotumika wa kumalizana na wawekezaji kitaifana kutowashirikisha vizuri wale wa Wilayani na pale kijijinipenyewe ambapo utafiti au uchimbaji unakwenda kufanyikana mfano mzuri ni katika Jimbo langu la Mtama, Kata yaNamangale kuna utafiti unafanyika wa graphite na Kampuniya Nachi Resources lakini mgogoro uliopo ni kwambawananchi wa eneo lile hawaelewi kinachoendelea na hivyokubaki na malalamiko mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni l ini Serikaliitabadilisha huu utaratibu na kuwasaidia wananchi wanguwapate uelewa wa kinachoendelea ili waone ushiriki waoutakuwaje?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwaufupi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Napetumekuwa tukishirikiana sana katika hili na wananchi waMtama nadhani ni mashahidi.

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii nisemautaratibu unaotumika ni kwamba mwekezaji yeyoteanayepata leseni, hatua ya kwanza akishapata leseni nikuonana na uongozi wa Halmashauri au uongoziunaohusika wa wilaya na kama hilo halifanyiki ni uvunjivuwa sheria na sisi tutalisimamia.

Lakini pia nichukue nafasi hii kusema kwambatutapita katika maeneo ya kero, tumeshapanga utaratibu,kuanzia tarehe 02 Agosti, 2017 tunashughulikia matatizo hayo.Kwa hiyo, Mheshimiwa Nape hata kwake tutafika. Ahsantesana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Rhoda.

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kata ya Isulamilomo,Jimbo la Nsimbo katika Mkoa wa Katavi kuna mwekezajiyuko pale, hana leseni na kuna vijana zaidi ya 4,000 hawanaleseni, lakini mwekezaji huyu sijui anapata nguvu gani yakuwazuia hawa wachimbaji wadogo wadogo zaidi ya 4,000kuchimba lakini zaidi wanapigwa na wananyanyaswakwenye huu mgodi mpya ulioko katika Jimbo la Nsimbo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nini tamko la Serikali sasa ilitujue nani ni halali kuchimba katika mgodi huu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwaufupi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza ninamshukuru kwa kutupa taarifa, lakiniatusaidie zaidi mwekezaji huyu ni nani, utatusaidia sanaMheshimiwa Mbunge. Hebu tupatie huyo ni nani halafutukafanyie kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jibu la msingi ni kwambamaeneo yote ambayo wawekezaji wameyashikilia bila

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

kuyafanyia kazi Serikali sasa inayatwaa kwa mujibu wa sheriaili iwagawie wananchi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbungetutakaa pamoja tuone kero hiyo tuitatue kwa mujibu washeria, ikiwezekana kabisa tutachukua hatua za kisheria.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana, Mheshimiwa Naibu Wazirina Waheshimiwa Wabunge, muda wetu leo hautoshi, kwahivyo tumefikia mwisho katika maswali.

Waheshimiwa Wabunge, tunao wageni waliopoBungeni asubuhi hii ambao ni wanafunzi 25 na walimuwatano wa sule ya msingi Compassion kutoka Mkoa waNjombe ambao ni wageni wa Mheshimiwa Lucia Mlowe(Mbunge) karibuni sana.

Pia kuna wageni 40 wa Mheshimiwa Rashid Shangaziambao ni wachezaji viongozi wa benchi la ufundi la timu yaSimba Sports Club wakiongozwa na Mussa Hassan Mgosiambaye ni Meneja wa Timu hiyo.

Aidha tuna wanafunzi 60 wa Chuo cha BibliaSanjaranda kutoka Mkoani Singida ambao pia ni wageni waMheshimiwa Yahaya Massare Mbunge, wakiongozwa na Mkuuwa Chuo ndugu John Tuu. (Makofi)

Wapo wanafunzi 24 wageni wa Mheshimiwa JassonRweikiza ambao ni wanachama wa Shirikisho la Vyuo vyaElimu ya Juu kutoka Mkoa wa Arusha karibuni sana. Pia tunaowanafunzi 30 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kutokaMkoa wa Dodoma karibuni sana wanafunzi wetu, pia tunaowageni mbalimbali wa Waheshimiwa Wabunge waliokujakutembelea hapa Bungeni wote kwa pamojatunawakaribisha sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunalo tangazo kutoka kwaEmmanuel Mpanda - Msaidizi wa Katibu wa Bungeanawatangazia Waheshimiwa Wabunge kuwa kunamaonyesho ya vifaa na teknolojia ya kisasa ya upimaji ardhiyanayoratibiwa na wanachama wa Chama cha Wapima

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

Ardhi Tanzania (IST) katika viwanja vya Bunge, nyuma ya jengola Utawala, hivyo Waheshimiwa Wabunge mnaombwakufika katika viwanja vya maonesho ili kujifunza jinsi yakupunguza gharama za upimaji kwa kutumia vifaa nateknolojia ya kisasa.

Waheshimiwa Wabunge, tuendelee. Katibu.

MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.

MWENYEKITI: Katibu naomba tuendelee muda leohautoshi kwa hiyo hatutakuwa na miongozo.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,mwongozo.

MWENYEKITI: Katibu naomba tuendelee.

NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa

Mwaka wa Fedha 2017/2018

(Majadiliano yanaendelea)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, kablahatujaanza na wachangiaji wetu ninamkaribishaMheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, awezekutengua Kanuni.

HOJA YA KUTENGUA KANUNI

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kutoa maelezo ya hoja ya KutenguaKanuni za Bunge.

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa jana wakatinatoa hoja ya kutengua Kanuni, nilieleza kwamba sababuya utenguzi wa Kanuni hizo ni mfungo wa mwezi Mtukufuwa Ramadhani ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni nani muhimu sana kwa Waheshimiwa Wabunge waumini wadini ya kiislamu kufanya maandalizi ya kuanza mfungo huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi ninaomba tenakutoa hoja ya kwamba Kanuni ya 28(2) na (4) itenguliwe ilikatika kikao cha leo, badala ya Bunge kusitishwa saa sabamchana liendelee na mjadala wa hotuba ya Wizara ya ArdhiNyumba na Maendeleo ya Makazi na liahirishwe saa naneMchana, hadi siku ya Jumatatu tarehe 29 Mei, 2017 saa tatuasubuhi. Sababu zikiwa ni zile ambazo tulizitoa jana naWaheshimiwa Wabunge waliziunga mkono.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa, Mwenyekiti, naafiki.

(Hoja Ilitolewa Iamuliwe)(Hoja Iliamuliwa na Kuafikiwa)

MWENYEKITI: Hoja imeungwa mkono.

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa

Mwaka wa Fedha 2017/2018

(Majadiliano yanaendelea)

MWENYEKITI: Tunaanza na wachangiaji wetu ambaojana tuliwataja tunaanza na Mheshimiwa Yussuf atafuatiaMheshimiwa Martin tutaendelea na Mheshimiwa Mbowe.

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: Mheshimiwa Mwenyekiti,Bismillah Rahman Raheem, nakushukuru kunipa fursa ya kuwa

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

mchangiaji wa mwanzo kwa siku hii ya leo kwenye hotubailiyo mbele yetu. Nisiwe mwizi wa fadhila nami niungane nawenzangu kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri,Katibu Mkuu pamoja na Watendaji wote wa Wizara ya Ardhi.Pongezi hizi zinatolewa kwa usimamizi mkuu wa wawilihawa au watatu hawa lakini wameshirikiana vizuri nawatendaji wao ndiyo maana wakaweza kupongezwa nakila Mbunge anayesimama leo hii. Ni ombi langu kwao isijeikawa sifa ya mgema.

MBUNGE FULANI: Tembo akatia maji. (Kicheko)

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: Mheshimiwa Mwenyekiti,nianze na suala la migogoro ya ardhi, kuna migogoro mingisana ya ardhi hapa nchini, sina haja ya kuitaja lakini natakanimshauri tu Mheshimiwa Waziri pamoja na timu yake sasahizi sifa zao basi ziende katika kutatua haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama eneo la ardhi ndaniya nchi hii liliopimwa ni asilimia 15 ndiyo eneo ambalolimepimwa na kupangiwa matumizi ni dhahiri kwamba mnakazi kubwa ya kufanya ili kuweza kupima eneo kubwa zaidina kupangiwa matumizi ili kupunguza hii migogoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa faida za kupima ardhina kupanga matumizi zimeonekana wazi, mimi kamaMjumbe wa Kamati nilipoenda Kilombero pale imeonekanatumejifunza, tumeona na wananchi wanafaidika sana, kwasababu ile faida ya kupata Hati Miliki ya yale maeneo yaoinawafanya wao sasa kuenda mbele kiuchumi na kufaidi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili sasa tatizo liko wapi, sasahapa Mheshimiwa Waziri nadhani utanielewa weweunaelewa vizuri zaidi lakini kwa mtazamo wangu mimininawaomba katika Serikali ni vizuri Waziri Mkuu leo yupomkae katika Serikali, huu mkanganyiko wa kwambawatumishi wengi wa ardhi wako kwenye Halmashauri auwako chini ya Halmashauri ama TAMISEMI wako kule, nawewe sasa unataka kuipima ardhi ili wananchi wapate hati

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

miliki pamoja na kupanga mipango ya ardhi na hawa watusasa hawawajibiki moja kwa moja kwako, nani atawapatiavifaa vya kufanya hiyo kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri bajeti hiiiko kwako, bajeti hii iko TAMISEMI, bajeti hii iko wapi? Sasahili kama Serikali mkae ili kusiwe na conflict of interest hapakwenye hii Wizara ama katika eneo hili ili vifaa vya kupimiaardhi vipatikane, wataalam wapatikane, ardhi ipimwe ilikuondoa matatizo. Serikali mpo Waziri Mkuu yupo mkaekama Serikali muondoe haya mambo ya kupeleka hawaTAMISEMI, hawa wapi, hawa wapi, mimi kwa mtazamowangu ni mipango ya kiujanja ujanja iliyokuweko hapo,wekeni wazi hii Serikali ya Hapa Kazi Tu mfanye kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili niendeleekukupongeza kwa namna ambavyo umeweza kutumiabusara na hekima kubwa kuwahamasisha wamiliki wa ardhiwakaweza kulipa kodi ya pango, ni kitu kimoja kizuri sanakimeleta tija na kila mmoja ameona faida yake. Tunakuombauendelee kutumia approach hii ya kuwaelimisha na siyonguvu, wanaomiliki ardhi kama ambavyo unatumiawaendelee kulipa kwa faida ya nchi hii na pato la Taifaliongezeke. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa utakapokujakujumuisha utuambie wale ambao wanamiliki mashambamakubwa, wanamiliki ranchi lakini hawajaziendeleza,hawazifanyii kazi ni wangapi na je Serikali ina mpango gani?Pamoja na hayo nipendekeze kabisa kwamba mashambayale makubwa ambayo hayajaendelezwa pamoja na ranchiyatumike sasa kuwagawia au kuwaazima kwa muda hawawafugaji wakati mkiendelea kufikiria ili kupunguza migogorona vita vya wakulima na wafugaji wakati kuna maeneokama haya ambayo hayajaendelezwa na watuwanayamiliki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuongelea sualala Kigamboni, ni takribani miaka tisa sasa wananchi waKigamboni kwenye ule mradi wa Kigamboni nyumba zao

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

hawawezi kuziuza, hawawezi kutengeneza, hawawezikufanya kitu chochote wanasubiri mradi, lakini ni miaka tisamradi haujaanza, Mheshimiwa Waziri hatujui kwamba huumradi utaendelea kuwepo au hautakuwepo. Kamahautakuwepo wananchi wale kwa muda wa miaka tisammewazuia kufanya chochote mtawafidiaje na kamautakuwepo katika kipindi chote hiki mtawafidiaje. NaombaSerikali ijipange hapa ili wananchi wale muwaondoe katikaugumu ule ambao mmewapa hivi sasa, wanakaa wanasubirimradi, miaka tisa ni mingi sana kwa maendeleo ya mtubinafsi, kwa Serikali ni kidogo, lakini kwa maendeleo ya mtubinafsi ni miaka mingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la NationalHousing, ninaomba Serikali pia ipo, National Housing inafanyakazi moja kubwa sana na kila Mtanzania leo hii anaona kaziinayofanywa na National Housing, wanastahili sifa kweli,wanajitahidi sana. Kuna nyumba za gharama nafuu ambazowananchi maskini wanatakiwa wanunue zile nyumba lakiniukiziangalia siyo za gharama nafuu kulingana na patolmwananchi wa Tanzania uwezo wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyumba hizi siyo za gharamanafuu kwa sababu ya mambo mengi, moja kama kodi yaVAT kwa vifaa vya ujenzi itaondolewa kwa watu hawa waNational Housing wataweza kujenga nyumba hizo naMtanzania yeyote ataweza kununua, lakini kama kodi ya VAThaitaondolewa basi suala hili litaendelea kuwa gumu kwao.Vilevile gharama nyingine zinaongezeka wao wanapojengazile nyumba wanaweka gharama za kuweka maji, umeme,barabara ambazo wao wanapaswa kuweka wenyewe. SasaSerikali ipo, kama mmeamua kujenga nyumba hizo sehemufulani, kwa nini Serikali haipeleki maji, ikapeleka umeme,ikapeleka barabara kwenye eneo lile kabla ya watu waNational Housing hawajaanza kujenga? Serikali ni moja lakinikwa nini kunakuwa na conflict of interest?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nchi za wenzetuwanafanya hivyo, ukienda nchi zote za Arabuni na Ulayakabla ya lile eneo kuendelezwa huduma muhimu za barabara

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

maji na umeme zinapelekwa kwanza, barabara, maji,umeme, shule, masoko yanapelekwa kwanza halafu ndiyonyumba zinajengwa wananchi wanaenda kuhamia paleikiwa huduma zote muhimu zipo. Kwa nini kwenye nchi yetuinashindikana?

Kwa hiyo, nikuombe tu Mheshimiwa Waziri kwambahili nalo mliangalie katika Serikali ili watu hawa wafanye hiyokazi kwanza kabla ya kupeleka ujenzi katika eneo basihuduma hizi muhimu ziende ili kupunguza gharama.Mkiendelea kwamba watu wa National Housing walipegharama za kuvuta maji, walipe gharama za kuvuta umeme,walipe gharama za kutengeneza barabara, wananchi waTanzania kwa kipato chao wataendelea kushindwakuzinunua nyumba hizi na mtazijenga mtaziweka zitakuwahazileti ile faida iliyokusudiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,ninaunga mkono hoja ya Kambi Rasmi ya Upinzani, lakininiendelee kukupongeza Mheshimiwa Waziri nikuambie kazakamba, narudia isije kuwa sifa ya mgema, tunategemeakipindi kijacho tuendelee kukusifu zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Yussuf,tunaendela na Mheshimiwa Martin Msuha ambayeatagawana dakika zake na Mheshimiwa Dkt. ChristineIshengoma na baadae Mheshimiwa Mbowe ajiandae.

MHE. MARTIN M. MSUHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana nami kupata nafasi ya kuchangia Wizara hii yaArdhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ninayo mambomachache nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri,Naibu wake na watendaji wake wote katika Wizara kwakazi nzuri wanayoendelea kuifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, zoezi hili la upimaji wa ardhi,upangaji na urasimishaji wa makazi, wananchi wengiwalikuwa wanalisubiri kwa muda mrefu sana uliopita. Kule

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

kwetu Wilayani Mbinga zoezi hili limepokelewa kwa mikonomiwili kiasi kwamba ukiangalia kwenye makadirio yamapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbingawametoka kwenye shilingi bilioni tatu mpaka shilingi bilionitisa, lakini makusanyo yao mengi yanatoka kwenye upimajiwa mashamba, muitikio ni mkubwa kiasi kwambatunategemea pia kuboresha uchumi wetu wa Mbingakupitia mpango huu wa upimaji ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nichukue fursa hiikumpongeza Mkurugenzi wangu Gombo Samandito Gomboyeye ni mtaalamu pia wa Mipango Miji na ndiyo maana zoezihili linakwenda vizuri kule Mbinga. Ziko changamoto,changamoto ya kwanza ni elimu, mapokeo ya zoezi lenyewewananchi wengi walidhani wakipimiwa mashamba yaoSerikali inakwenda kunyang’anya mashamba hayo,inakwenda kumiliki mashamba hayo. Changamoto ya pilini ada za ardhi za mwaka, changamoto ya tatu ni namnaya kugharamia upimaji mpaka watu wakapata hati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa maranyingine Mkurugenzi wangu alifanya hesabu, Mbingatunapima kipande cha heka moja kwa shilingi 100,000 lakinibado kuna changamoto namna ya kwenda, mtu anamashamba ya heka kumi ishirini, tumeshirikisha sekta binafsiwale ni wafanyabiashara wamepata tender, wangependawapime kiasi kikubwa ili wapate zaidi. Kwa hiyo, unakutawale wakulima wamelimbikiziwa madeni katika eneo hili laupimaji. Nitoe shilingi milioni tatu kwa mkupuo hapana,tunaongeza umaskini kwa upande mmoja kwa hiyo iratibiwenamna ya kutengeneza malipo ya gharama hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika zoezi hili yakomaeneo ambayo watu waliona kama wanaonewa, kwamaana kwamba mapokeo yalikuwa watu wavunjiwenyumba baadhi ya maeneo, kwa hiyo likaleta shida. PaleMbinga Mjini maeneo ya Tangi la Maji kulitokea naMkanganyiko huo mlijenga holela kwa hiyo inabidi tuwavunjiekabla ya mipango miji kuwafikia, ikawa shida, mtu huyuamekaa hapa miaka yake hamsini unamvunjia leo nyumba

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

anakwenda wapi? Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Wazirihili litolee maelekezo vizuri. Kama mnaamua kurasimishamakazi ya watu basi elimu ishuke wale Watendaji kule chiniwaielewe ili, zoezi lenyewe litekelezwe namna gani,vinginevyo kuna kauonevu ndani yake na pengine utekelezajiwake sasa unasuasua kwa sababu hiyo watu wanasita kwasababu wanahisi sasa hapa nitavunjiwa, hapa nitahamishwa.Mheshimiwa Waziri kwa upande wa Mbinga mimi nilikuwanataka kusema hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, iko changamoto kwaupande wa upangiliaji, upimaji na urasimishaji wa miji, mimini Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msingwa kule Dar essalaam Kata ya Msigani. Tunalo zoezi hili, tunayo kampunibinafsi ambayo imepitia kwenu Wizarani, imepitiaHalmashauri, tumeshafanya mikutano kadhaa, mapokeo nimazuri sana na nitumie pia fursa hii kukualika MheshimiwaWaziri baada ya kumaliza mikutano hii nitakualika kwenyemtaa wangu tukazindue mpango wa upangiliaji miji kuleKata ya Msigani, tutaleta barua rasmi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapokeo ni mazuri,changamoto iliyoko kubwa ni gharama hizi za upimaji, beielekezi ni kweli Serikali imetoa lakini gharama za umilikishajini tatizo, Wizara hamjaziweka wazi, kuna tozo pale zipatazotisa mpaka uje upate hati mjini, ndiyo maana hati nyingihazijatolewa kwa sababu ya hizi gharama za umilikishaji.Ziko gharama pale zinahesabika, ziko tisa. Iko gharama yakuchukua form, premium, ada ya hati miliki, lakini iko ada yauandaaji wa hatimiliki, hati ya usajili na tunayo ada yauandikishaji. Sasa tulifanya ukokotoaji pale kwenye Mtaawangu wa Msingani Dar es Salaam…

MWENYEKITI: Mheshimiwa malizia sentensi yako,dakika zako zimeisha.

MHE. MARTIN M. MSUHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Kwenye kiwanja cha square metre 600 kinagharimushilingi 873,000 ada ya umilikishwaji, acha ile ya upimaji kwakampuni binafsi.

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

Kwa hiyo naomba Wizara muangalie upande huu,huo utatukwamisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja,ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Christine Ishengoma dakika tano.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii yakuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza natoa pongezi kwaMheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri na Wafanyakaziwote wa Wizara hii. Pili, naomba kutoa pongezi kwa kaziwanayoifanya nzuri hasa Mkoa wa Morogoro kuhusumigogoro ya wakulima na wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyote mnafahamu kuwaMkoa wa Morogoro ulikuwa na matatizo sana hasa kwaupande wa wakulima na wafugaji mpaka mapigano namauaji yakatokea kwa upande wa watu na mifugo.Nashukuru Serikali kwa sababu Mawaziri walifika kwakusaidiana na uongozi wa Mkoa pamoja na Wilaya waliwezakufanya kazi kadri walivyoweza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa sababudawa muhimu ya kumaliza hii migogoro ni upimaji wa ardhi.Upimaji wa ardhi ambao sasa hivi umefanyika kwenye Wilayaya Malinyi, Ulanga pamoja na Kilombero kwa baadhi,nashukuru kwa sababu wametoa hata hati miliki na hiyo ndiyoingekuwa mkombozi. Tufahamu kuwa hawa wanaopewahati miliki ni wachache, naomba kwa sababu tumepataufadhili kutoka Serikali ya Uingereza pamoja na Sweden naDenmark kupitia kwenye mashirika yao ya maendeleo yaDANIDA, DFID pamoja na SIDA nashauri Wizara kamainawezekana waweze hata watu wengine kupimiwa kwasababu hata registry ambayo ni masjala wameweza kujengalakini watu wangeweza kumilikishwa wote ingekuwa vizuri.

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mkoa wa Morogoroifahamike kuwa ni Wilaya zote zilikuwa na matatizo yamifugo. Wilaya zote Mvomero nashukuru mmeweza kupimakiasi, Kilosa mmeweza kupima kiasi, lakini mfahamu kuwawatu walikufa Mabwerebwere, watu walipigwa na hasawanawake ambao walikuwa wanalima mpunga wao,wengi walikimbizwa hawawezi kulima.

Naomba sana tena sana kwa kusaidiana jinsimlivyoweza kupata ufadhili kutoka kwa mashirika hayo,Mheshimiwa Waziri una wataalam wazuri ambao wanawezakuandika maandiko ya kuweza kuomba project pamoja nakusaidiana na Halmashauri zetu za Wilaya ya Gairo, Kilosa,Mvomero, Morogoro Vijijini hata Manispaa pamoja na kuleambako tayari mmeshaanza kupima tuweze kupatakupimiwa ardhi kwa sababu ni majaribio yaweze kuwamajaribio ya Mkoa mzima watu wote mlikuwa mnajua kuwaMkoa wa Morogoro ndiyo umeweka historia kwenyemigogoro ya wakulima na wafugaji, kuweza kupimiwa ardhikusudi tupate hatimiliki watu waweze kumiliki pamoja natuweke historia ya kumaliza migogoro ya wakulima nawafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nashauri kuwa kwaWilaya zingine Mikoa yote ya Tanzania ambayo inajulikanakwa migogoro hii ya wakulima na wafugaji pamoja namigogoro ya ardhi, dawa ni kupima ardhi, kupata hati miliki,hati miliki ambayo inaweza kukusaidia hata kupata mikopolakini kujua kuwa ni ardhi gani mifugo itaweza kuwa, ni ardhigani wakulima wataweza kuwa na ni ardhi gani wafugajiwataweza kuwa na hii tutakuwa tumepanga mipango mizuriya matumizi bora ya ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujua kuwa kwasababu wataalam ni wachache na kuna vyuo, Chuo Kikuucha Ardhi, Chuo cha Ardhi Morogoro pamoja na Chuo chaArdhi Tabora, udahili uweze kuongezwa ili kusudi tuwezekupata watumishi wengi wataalam wa ardhi huko kwenyeHalmashauri zetu.

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa niongeleakuhusu mipango ya miji. Bila ya kupanga miji itakuwa kunaujenzi holela kama tunaoushuhudia watu wanajenga mpakamilimani na ninyi Wizara mpo, naomba na hilo mliangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa kushukurusana nyumba za National Housing zimejengwa pamoja nanyumba za watumishi ardhi hata Mkoa wa Morogorotumepata lakini tatizo kama wenzangu wanavyosemagharama bado ni kubwa. Naomba muiangalie hiyogharama ili kusudi hata wale vijana wanaoanza kazi sasahivi, waweze kupata nyumba zao wakalipia kidogo kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naungamkono hoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. TunamkaribishaMheshimiwa Mbowe sasa na baadae Mheshimiwa SaddiqMurad na Mheshimiwa Nsanzugwanko wajiandae.

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi. Na mimi nafikiri nisiwemchawi, nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri Lukuvi naNaibu wake. Kwa kweli ni Wizara ambayo inafanya kazi bilaitikadi za kisiasa, inasimamia wajibu wake vizuri. MheshimiwaWaziri sifa unazopewa wewe na Naibu wako zinawastahilipamoja na Wizara yako yote, endeleeni kufanya kazi natutawapa ushirikiano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo manne tu yakuzungumza siku ya leo na yote naelekeza katika Jimbo langula Hai. Kwanza, japo nafahamu ni suala linalohusu Wakalawa Barabara yaani TANROADS lakini kwa sababu linagusaardhi nalizungumza ili Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, na ninahakika Mheshimiwa Profesa Mbarawa yuko hapa nayeatanisikiliza, kwa pamoja mnaweza mkaona mnawezakutupa vipi watu wa Hai ufumbuzi wa tatizo hili ambalo nikubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo hili linahusu barabara

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

ya Kilimanjaro Machine Tools - Machame Girls’. Barabarayenye urefu wa kilometa 26, barabara ambayo ilijengwawakati wa ukoloni na ni barabara kuu inayohudumia eneolote la Machame lenye wakazi zaidi ya 200,000. TANROADSwame-declare kupanua wigo wa barabara hii na waka-declare kwamba eneo la mita 60 linahitajika liwe reservedkwa ajili ya barabara. Sasa sisi hatuna tatizo na ulazima wakupanua na kuimarisha miundombinu yetu ya barabara. Nikweli sheria hizi inawezekana kuna sheria ambazozinasimamia mambo haya, lakini sheria hizi zinatungwa naBunge na tukitunga sheria mara nyingi tunatunga sheria kwakuangalia nchi nzima bila kuangalia mazingira mahsusi yaeneo moja baada ya jingine.

Mheshimiwa MWenyekiti, kwa eneo la Kilimanjaroambako makazi yana watu wengi sana, mashamba hakuna.Watu wenye miaka 50 kushuka chini hawana ardhi, kuchukuaeneo la barabara ya mita 60 ambayo inakwenda kwenyeforest pamoja na Kilimanjaro Gate (Machame gate) kwendakwenye National Park ni eneo kubwa sana. Tutambuekwamba kuna wakazi wamekaa kwenye maeneo haya kwazaidi ya miaka 100 iliyopita na kupanua barabara kwa upanahuu maana yake ni kwamba tutabomoa misikiti, shule,makanisa, makaburi, tutapoteza kabisa flow ya MtoWeruweru, tutakata mashamba ya wananchi, hili ni jambolenye ugomvi mkubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, upanuzi huuunazungumziwa kufanyika bila kulipa fidia. Ningependakuishauri Serikali katika kutekeleza sheria lazima tuangaliemazingira ya maeneo na historia ya maeneo. Hii barabarani muhimu ndiyo, lakini haijengwi reli, wala hatutegemeikwamba kweli mita zote 60 zitatumika katika kuipanuabarabara hii, kwa sababu inakwenda ndani kwa kilometa13 tu kuanzia maeneo ambayo wanakaa wakazi unaanzakukuta Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana Serikali,Waziri wa Barabara, Waziri anayeshughulika na mambo yamiundombinu pamoja na Waziri wa Ardhi tutafute ufumbuzi

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

na ikiwezekana tafadhali m-visit Wilaya ya Hai, mkaangaliehali halisi ninayoizungumzia mahali hapa, muelewe namnaambavyo vijiji vya Nshara, kijiji cha Uduru, Warisinde,Warindoo na Foo katika Kata ya Machame Kaskazini mpakakwenye Mronga na Mkuu wote hawa wanaathiriwa. Kwahiyo ni jambo ambao kwa kweli l inawakwaza sanawananchi. Bomoabomoa hii japo mnaona ni kilometa 13kwa Hai, inagusa zaidi ya wananchi 6,000, zaidi ya kaya 800zinaguswa katika jambo hili bila kuzungumzia hizo taasisiambazo nimezizungumzia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo ni jambo la kwanzaambalo ningependa kushauri Serikali na ningeomba sanaWaziri katika majibu yako, na pengine niombe WaziriMheshimiwa Mbarawa na timu yake nao vilevile penginewashirikiane katika kutupa ufumbuzi, tungependa tumalizehili tatizo bila kuleta mgogoro wa ziada na usumbufu usiowa lazima sana kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili MheshimiwaWaziri ni kuhusu hali nzima ya ardhi katika Mkoa waKilimanjaro. Tatizo kubwa la Mkoa wa Kilimanjaro ni ardhi.Tuna uhaba mkubwa sana wa ardhi, nitakiri kwamba niMkoa ambao idadi ya wakazi kwa kilometa za mraba nikubwa kuliko kijiji chochote katika Afrika Mashariki na ya Kati.

Tunapozungumzia Kilimanjaro, kilomita moja yamraba sehemu za milimani zina watu kuanzia, ikipungua sanani 650 mpaka 1,800 per square kilometer, hii density ni kubwakuliko eneo lolote katika Afrika ya Mashariki na Kati. Watuwenye umri wa miaka 50 kushuka hawana ardhi kabisa sasahivi na watu wameendelea kujenga, population imeendeleaku-increase kwa rate ya 1.9 people per annum ambayo siyokubwa sana ukilinganisha na maeneo mengine ya nchi, lakinikwamba kuna tatizo kubwa la ardhi ambayo inahitaji specialmanagement hili ni la lazima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo namuomba Waziriwa Ardhi mfanye land auditing ya Mkoa wa Kilimanjaro, siyoHai peke yake, Mkoa mzima wa Kilimanjaro. Kwa sababu

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

katika maeneo mengine sasa watu wamejenga nyumbampaka kumekuwa squatters, kuna squatter za vijijini. Sasasiyo kawaida sana kukuta squatter vijijini, kuna squatter zavijijini, kuna shida ya kupitisha huduma za barabara hizi feederroads, kuna tatizo kubwa sana ambalo linahitaji kwa kwelikufanyiwa intervention. Ningeomba Serikali Kuu ifanyeintervention na kama kawaida Mheshimiwa Wazirinakukaribisha ili uje na wengine kuangalia mnaweza kufanyajambo gani katika kutatua tatizo hili la wakazi wa Hai.(Makofi)

Jambo la tatu nizungumzie mashamba ya ushirika.Huko miaka ya nyuma wakati wa utawala wa Awamu yaKwanza ya Mwalimu Nyerere alitaifisha mashamba makubwayaliyokuwa ya wawekezaji wa kizungu na akakabidhi kwavijiji kadhaa vya Wilaya ya Hai na maeneo mengine ya Mkoawa Kilimanjaro. Baadae yale mashamba yakahamishwakupelekwa kwenye Vyama ya Msingi vya Ushirika, lakini baadaya Sheria ya Ushirika kubadilishwa yale mashamba hayakuwatena miliki za vijiji yakawa ni washirika wale wanaushirikaambao ni kundi katika kijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mashamba yame-holduchumi mkubwa sana wa Wilaya ya Hai na katika Mkoamzima wa Kilimanjaro. Ni ombi langu Mheshimiwa Waziri waKilimo na Waziri wa Ardhi mje tuyafanyie tathmini mashambahaya. Hivi kweli kuna economic value tunayopata kwenyemashamba yale ama yanatumika tu bila kutengeneza kileambacho kilikusudiwa. Kama ni lazima tubadilishe matumiziyake yaweze kurejeshwa kwa wananchi, yaweze kuwa natija zaidi katika kukuza uchumi wa Mkoa wa Kilimanjaro hasaukizingatia namna ambavyo ardhi imekuwa ni jambo adimu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mashamba makubwayamekodishiwa watu, hawalipi katika Vyama vya msingi vyaUshirika, wananchi hawafaidi chochote wakati wananchiwengine wa kawaida hawapati hata robo eka ya kulima.Kwa hiyo ni jambo ambalo linatakiwa kupatiwa ufumbuzi,ningeomba sana Waziri hili uliangalie. (Makofi)

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ambaloningependa kulizungumzia liko pale pale katika masuala yaardhi ni kuhusu mgogoro wa KIA. Naomba Mheshimiwa WaziriMkuu anisikilize vizuri kwa sababu Waziri Mkuu hili jamboamelisikiliza kwa muda mrefu. Mheshimiwa Waziri Mkuu,naomba Mkuu unisikilize sana katika hili unisaidie vilevile.Mheshimiwa Waziri Mkuu, unakumbuka bado mgogoro waKIA tumeushughulikia, nakushukuru sana kwa effort yoteuliyofanya, lakini bado hatujapata ufumbuzi, kwa sababulile eneo la mgogoro wa KADCO uwanja wa Kilimanjaro waKIA umegusa maeneo ya wananchi wa vijiji vitano vyaupande wa Wilaya ya Hai na vijiji kadhaa katika Wilaya yaArumeru kwa ndugu yangu hapa Mheshimiwa Nassari.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijiji vya Hai kama Mtakuja,Tindigani, Sanya Station, Rudugai, Chemka vimeathirika, kwakipindi chote hiki chenye mgogoro wananchi wamenyimwakufanya shughuli zozote za maendeleo katika maeneo yaompaka mgogoro huu utakapotatuliwa.

Kwa hiyo, kuchelewa kutatua mgogoro huu nakuwapa wale wananchi haki ya kuendelea kuishi katikamaeneo yao kunakwaza sana maendeleo na ujenzi wahuduma za kijamii kama shule, barabara, miundombinunyingine, umeme, maji na vitu kama hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Waziriwa Fedha ningeomba sana tusaidiane tumalize tatizo hili,kwa sababu kuna suala la mgogoro wa ardhi na kuna sualala KIA. Suala la KIA hilo ni suala lingine na Waziri Mbarawanaye amekuwa anashughulika na Waziri Mkuu, nawashukurusana, lakini ardhi kwa wale wananchi waliozunguka eneohili inakuwa ni tatizo kubwa kweli kweli. Kwa miaka kadhaasasa wananchi hawawezi kufanya chochote wamekaakwenye vij i j i vyao, hawaruhusiwi kujenga, kupanuamashamba, hawaruhusiwi kufanya chochote cha maendeleoya kudumu. Sasa jambo hili ni gumu kidogo hasa inapogusawananchi wengi sana katika Wilaya ya Arumeru na Wilayaya Hai ambayo wote wanagusa eneo la KIA. (Makofi)

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa WaziriMkuu nikuombe ile juhudi uliyokuwa umeianza uimalizie,Waziri Mbarawa atusaidie tumalizie jambo hili na Waziri Lukuvinae vilevile aje tuwa-relieve hawa wananchi. Kamatutaendelea na mazungumzo kuhusu uwanja wa KIAtuendelee, kuhusu uwekezaji wa uwanja wa KIA na KADCOtuache wananchi katika maeneo yao waweze kufanyashughuli zao za maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina imani Waziri Mkuuumelifanyia kazi vema jambo hili na nina hakika ukiamuawewe na Mheshimiwa Lukuvi na Mheshimiwa Mbarawamlimalize tatizo hili, mnao uwezo wa kulimaliza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuruni sana nanawatakia kheri. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mbowe.Tunaendelea na Mheshimiwa Saddiq Murad, dakika tano naMheshimiwa Nsanzugwanko dakika tano. BaadaeMheshimiwa Millya na Mheshimiwa Nassari wajiandae.

MHE. SULEIMAN A. SADDIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi asubuhi ya leo. Na mimi naombanianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, NaibuWaziri na wataalam wao, lakini salamu za kipekee kwaMheshimiwa Waziri, amefanya kazi kubwa sana katika Mkoawa Morogoro na Wilaya ya Mvomero. Mheshimiwa Waziri kaziuliyofanya Morogoro ni ya historia, migogoro ya ardhiimepungua, migogoro ya wakulima na wafugaji inaendeleakupungua. Tunaomba jicho lako la huruma liendeleekutusaidia wananchi wa Morogoro. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nielekeze matatizoyafuatayo kwa sababu muda wenyewe ni mdogo.Mheshimiwa Waziri, suala la kwanza tuna mgogoro wamipaka ya kiutawala kati ya Manispaa ya Morogoro naWilaya ya Mvomero, huu mgogoro ni mkubwa sana, naombasana utusaidie. Halmashauri ya Mvomero imeanzishwa kwaGN yake, Manispaa ina GN yake, lakini tunaomba sasa hivi

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

Mheshimiwa Waziri, Ofisi yako, wataalam wako waje watoetafsiri ya GN. Mgogoro unazidi kuendelea, mipaka inaingilianana wananchi wa Mvomero wanakosa haki kwasabbauManispaa wanaingilia eneo la Mvomero na wanaanzakugawa ardhi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri naomba kauliya Serikali katika suala hili na tunaomba sana uje utusaidieMkuu wa wilaya, wataalam wa Mvomero na wananchi piatumeanza zoezi hili lakini halina mafanikio kwa sababutunahitaji nguvu kubwa ya Serikali.

Mheshimiwa Waziri, jambo la pili ambalo ningependasana kulizungumza kwa sababu ya muda nao unakwendani kuhusu ardhi kubwa. Mvomero kuna ardhi ambazohazijaendelezwa, kuna ardhi inaitwa Katenda Group hawawana heka 12,500 tangu mwaka 2002 mpaka leo ardhihaijaendelezwa. Mheshimiwa Waziri tunaomba ofisi yako sasaitusaidie kutupatia ardhi hii ili wananchi wa Mvomero naWatanzania wengine waweze kufaidika na ardhi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu MheshimiwaWaziri ni upungufu wa wataalam. Mvomero tuna upungufumkubwa wa wataalam. Nimpongeze Mheshimiwa Raisamevunja CDA, wataalam wa CDA nawakaribisha Mvomero.Tusaidiane wataalam waje Mvomero, tunahitaji baadhi yawataalam katika maeneo yafuatayo. Tunahitaji Maafisa waMipango Miji wawili waaminifu, huo ndiyo upungufu wetuwa kwanza, wa pili tunahitaji Mthamini, na Mrasimu waRamani. Tunaomba Mheshimiwa Waziri kwa kuwa hayamambo mengine nitakuwa nayo kwa maandishi nitakuletea,tunaomba tupate watumishi hawa ili Mvomero sasa isongembele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la nne ni kutopatagawio la asilimia 30. Mvomero tunadai zaidi ya shilingi milioni178, gawio hili hatujalipata bado. Mheshimiwa Waziri, kunaahadi za Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa William Lukuvializozitoa Mvomero. Naomba kuzitaja ahadi zake, ahadi yakwanza aliahidi kutuletea vifaa vya upimaji (RTK) vifaa hadileo Mvomero hatujavipata. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziritunaomba utusaidie ahadi yako, tekeleza, tuletee vifaa vya

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

upimaji. Ahadi ya pili tunaomba kukamilisha uandaaji wamipango na matumizi ya ardhi kwa vijiji 52 kati ya vijiji 130.Ahadi ya tatu Mheshimiwa Waziri tunaomba ukamilishaji waupimaji wa mipaka ya kiutawala vijiji 32 kati ya vijiji 130.Mheshimiwa Waziri tunaomba sana utusaidie vifaa vyaupimaji ili Mvomero tusonge mbele zaidi na zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mvomero hatuna ofisi yaardhi, tunatumia ofisi ya Idara ya maji. Sasa umetoa ofisi tatuna unaendelea na mipango mizuri kwa maeneo mengineMvomero umeisahau, tunaomba kwenye mipango yakomizuri uweze kutusaidia ili na sisi tuwe na ofisi ya ardhi. Mwishoni kuhusu Ofisi ya Kanda ya Mashariki ambayo baada ya kutoatamko rasmi sasa kwamba Kanda ya Morogoro inaondokana badala yake tunahamia huku Dodoma. MheshimiwaWaziri kwanza nikupongeze ulianzisha Kanda mwaka 2015,ukajenga ofisi nzuri Morogoro, ofisi imefanya kazi nzuriwananchi wa Mikoa ya Pwani na Morogoro wamepata Hatizaidi ya 5,000; sasa kuondoa Kanda leo na kuturudisha tenaDodoma kwa kweli naona unaturudisha nyuma.

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Murad.

MHE. SULEIMAN A. SADDIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba Mheshimiwa Waziri masuala yangu menginenikuletee kwa maandishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Nsanzugwanko,hayupo. Tuendelee na Mheshimiwa Jitu Soni.

MHE. JITU V. SONI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsantesana naomba nichukue furasa hii kwanza kumpongezaWaziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na timu nzima ya Wizaraya Ardhi kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya na kuleta

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

matumaini makubwa. Migogoro mingi imeendeleakupungua na tunaendelea kuomba kwamba waendeleekufanya kazi hiyo kubwa ili migogoro ya ardhi sasa hapanchini iishe. Tunaomba ile migogoro hasa ile ya Babatiambayo Wabunge wenzangu wote tumekubaliana kilaanayepata fursa aisemee, ile ya vijiji vya Ayamango,Gedamar na Gidejabug wale wananchi wapatiwe maeneombadala kuna mapendekezo tumeshaleta, Serikali kupitiaOfisi ya Waziri Mkuu ifanyie kazi ili Wizara ya Ardhi iweze kutoavibali, lakini pia ile migogoro ya mashamba ya kule Kiruyafanyiwe kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, muhimu Mheshimiwa Wazirininaomba utuletee sheria mpya hapa ndani ya hii Sheria yaArdhi kipengele cha kuzuia matumizi ya ardhi ya kilimo ilindwekisheria ili ukitaka kubadilisha matumizi ya ardhi ya kilimo ijehapa Bungeni kwa sababu maeneo mengi yenye rutubaTanzania yamebadilika matumizi sasa yamekuwa makazi,viwanda na matumizi mengine ambapo hayo matumizimengine tungeweza kuyapangilia yakawa katika maeneombadala na italinda ardhi yetu ya kilimo, kwa sababu hatunauwezo kama Serikali kuandaa maeneo mapya ya kilimokatika maeneo ya jangwa au maeneo ambayo hayanarutuba kuwa ya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ningeomba kwamba laWabunge wote wamelalamikia suala la kupatiwa vifaa,mpango wenu mzuri wa kuweka vifaa vya kupima kwenyeKanda haitoshelezi, tunaomba muwe na mpango,mtukopeshe wala hatuhitaji kwamba Serikali iweke bajetiituletee bure, kila Halmashauri tukopeshwe vifaa ili sisitutaendelea kulipa hilo deni la vifaa vya kupimia ardhi zetu,ili tupime viwanja vya watu, mashamba ya watu lakini piavifaa vya kutolea hati miliki zile za kimila huko katikaHalmashauri zetu. Hiyo itatupunguzia sehemu kubwa yamatatizo ili wananchi wote waweze kupata huduma ilemuhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine hapo naombakwamba kuna ile asilimia ambayo kodi ya ardhi inapolipwa

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

ile Wizara basi iwe badala ya kufika Hazina na hukoHalmashauri iweze kukata moja kwa moja ili tuwezekuyapangia matumizi ya ile fedha ambayo tunawasaidiaWizara kukusanya ile kodi ya ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna migogoro mingiambayo sasa hivi kwa sababu Serikali haijatoa tamkomaalumu kwamba watu kuvamia maeneo ya hifadhi,kuvamia maeneo mbalimbali na katika mali za watu Serikaliiweke msimamo kwamba nini maamuzi ya Serikali na mahaliambapo Serikali huko nyuma tayari ilishakosea kwa kuanzishavijiji ndani ya maeneo ambapo ni hifadhi au ni mashambamengine ya lease, basi mgogoro huo utatuliwe mapema ilikila mmoja aweze kuishi kwa amani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine pia naombaiangaliwe namna kwa wale waliokuwa Watanzania ambaosasa wamebadilisha uraia wao kwenda nchi zingine ili hukowapate haki, pawe na mpango maalum. Najua Wizara yaArdhi mnao mpango masuala ya derivative rights, lakiniwaweze kurudi nyumbani angalau kama wanatakakuwekeza kujenga nyumba na kadhalika, waweze kuwa nahaki hiyo kwa sababu kuna diaspora kubwa ambao wanauraia wa kule lakini ni Watanzania kiasili na wao wawezekupata haki yao kuja kuwekeza hapa nyumbani bila kuwakupitia TIC. Labda anataka kuweka nyumba tu ya kuishi nanini na wengine wana ndugu zao ambao wapo hapa, lakiniwakirithishwa ile mali ni haki yake kurithi ya mzazi wake aubaba yake au babu yake, akija hapa inakuwa ni mgogorokwa sababu yeye tayari anao uraia wa nchi nyingine.Watanzania wengi wanakosa fursa hiyo naomba muangalienamna kwa wale ambao walikuwa Watanzania wameendawamebadilika sasa kuwa raia wa nchi nyingine aendeleekuwa na haki maalum, kuna haki zingine wasipewe lakiniangalau hii ya kwao ya kuja kuwekeza humu nchini basipawe na mfumo mzuri waweze kuja na kuwekeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, muhimu na ninaendeleakusisitiza kwamba hivi vifaa tumeona pale nje mmetuleteaaina nyingi, pawe na mpango maalum tuweze kukopa kila

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

Halmashauri kwanza itakuwa fursa ya kumaliza migogoroya watu kupatiwa hati miliki na hati za kimila, lakini piamaeneo mengi yatakuwa yamepimwa, muhimu nicoordination baina ya Halmashauri zetu na Wizara, namnaya kuelekeza Maafisa Mipango Miji na namna ya kupangamakazi hata huko vijijini tunahitaji kupanga matumizi boraya ardhi ili huko mbele tunakoelekea migogoro isiendelee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru na ninaungamkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Jitu Soni,tunaendelea na Mheshimiwa Millya, baadae atafuatiaMheshimiwa Nassari, Mheshimiwa Daniel Mtuka, MheshimiwaJoram Hongoli na baadaye Mheshimiwa Moshi Kakosiajiandae

MHE. JAMES K. MILLYA: Mheshimiwa Mwenyeiti, mudawa dakika tano ni mdogo sana nifanye mambo mawili, mojanimkaribishe sana Mheshimiwa Lukuvi Simanjiro, matatizo yaSimanjiro Wizara ina takwimu inaongoza Tanzania kwakuporwa kwa ardhi yake, lakini la pili kwa sababu Wizarayako imesogezwa tarehe, wananchi walikuwa wapo tayarikuja kukuletea matatizo yao, ninaomba hata baada yakupitisha bajeti yako wananchi wachache waje kukusalimia.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayomwaka 2005 nilikuwa kijana peke yake wa Wilaya nzima aliyegraduate degree ya kwanza, baada ya miaka mitatu baadaendio mwingine mmoja anapatikana. Kwa nini ninasemahivyo, Wilaya ya Simanjiro imejaa watu wengi ambaohawajasoma, wale wachache wanaojua kuandika nakusoma waliopewa Tarafa; waliopewa kuwa Wenyeviti vyaVijiji wame-take advantage ya hali ile na kuwaumizawananchi na kuwachukulia ardhi yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuomba MheshimiwaWaziri fika Simanjiro hali ni mbaya kweli kweli, lakini nisemetu kitu kimoja.

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mashambamakubwa, shamba namba 24 Lorbosoit ya aliyekuwa KatibuTarafa ya Emboreet Mzee Brown ambaye bahati mbaya aunzuri ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya, amechukua heka8,000 lakini kama haitoshi, baada ya kushindwa kulima nakufugia amebadilisha shamba lile anataka kufanya ni lawanyamapori na kuwauzia Wazungu. NinaombaMheshimiwa Waziri umetoa directives nakumbuka kamaWaziri ulisema hakuna kubadilisha ardhi yoyote, kubadilimatumizi yake bila idhini yako, huyo Mzee anafanya ujanjakutumia nafasi yake ya CCM kubadilisha mazingira hayo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna Muhindi mwingineKata ya Loiborsiret, Kijiji cha Loiborsiret eneo la Motio,ameamua kuchukua ardhi kubwa ya wananchi kununuamoja, moja heka mia, mia mbili lakini sheria zipo wazi,haiwezekani kijiji kikawa na uwezo wa kugawa zaidi ya heka50 haiwezekani, Mheshimiwa Waziri nakuomba usaidie hilo.Kuna kijiji kingine cha Narakauwo mtu anaitwa Jerry Hoopsamekuja ameingia kama mbia mwenzake na Mtanzaniammoja, alichukua heka 2,000, shamba lile lipimwe lina zaidiya hekta 10,000 mpaka sasa hivi naomba uliingilie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la Kilombero kuna zaidiya mashamba 50,000, maelfu na maelfu ya hekari ambayoyamechukuliwa. Mheshimiwa Waziri tatizo hili hatuwezikukusaidia kwa dakika hizi tano ninakuomba MheshimiwaWaziri ninakukaribisha uje Simanjiro, umeenda Arumeru,umeenda Monduli, umeenda Babati naomba uje Simanjirowanakusubiri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la Naberera kunaMwenyekiti wa Kijiji amekuwa ni mtu wa ajabu naombauangalie, kwa kweli mimi kwa ufupi niongee kwenye hilo tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo paleWizarani kwako una watu mahiri kweli, kuna mtu anaitwaNdugu Lwena ninamfamu ni mwanasheria mahiri kweli halirushwa ni mtu ambaye sijawahi kuona, nimeishi naye

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

nimefanya naye kazi mwaka 2009, anaweza kukusaidia. Kunakesi ya Lekengere, Faru Kamunyu and others versus Minister ofNatural Resources and Tourism ya mwaka 2002, Mahakamaya Rufani ilisema huwezi ukachukua ardhi inayomilikiwakimila bila kupata idhini ya Rais. Rais peke yake ndiye mwenyeuwezo wa kufanya hivyo. Ukisoma pamoja na Sheria ya LandAcquisition Act ya mwaka 1967, pamoja na kuwapawananchi fidia hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri naomba utusaidieSimanjiro imeoza, waliotutangulie wengine kwenyemadaraka hayo hawajatumia vizuri, ninaomba tusahihishehistoria, watu wangu wanaumia, ardhi inaumia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nirudiekwenye suala la ardhi Mkoa wa Arusha kwa ujumla. Kunawatu walioletwa na Mwalimu Nyerere kwa nia njema yakuwekeza, baada ya kumaliza uwekezaji na kuchukua ardhiyao, sasa wanayageuza mashamba yale kama mtaji.Inawezekanaje Mtanzania akanunua ardhi yake peke yake,sana Serikali muingile, kuna watu wakubwa wana mashambamakubwa pale Arusha, Arumeru na unafahamu. Mzunguanataka kwenda ulaya kwenda ku-retire kukaa kwenyenyumba ya wazee, anabadilisha ardhi yetu kama sehemuya kiinua mgongo chake, badala ya ninyi kusimamiaarudishiwe machinery na gharama ambazo ametumiakwenye shamba lile, anatuuzia mashamba yetu, NHCwalinunua kule Kisongo, ninampongeza Ndugu Msechu nikijana mzuri mwenzetu anafanya kazi kubwa ninaombatembelea Angola.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnamchanganya kamaSerikali, hamjui kama mpo kwenye ubepari, hamjui mpokwenye ujamaa you just confuse, philosophy mnaichanganyampeni afanye biashara ili atakapopata faida aendeleekusaidia watu maskini wengine, lakini mnamchanganya nimtu mzuri mwema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipanafasi ya kuchangia Mungu awabariki sana. (Makofi)

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Nassari.

MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru, nawashukuru waliotangulia kuchangiaMheshimiwa Mbowe na Mheshimiwa Millya angalauwamegusa kidogo masuala yetu na hili suala la KIA nawananchi wa vijiji vinavyozunguka nashukuru leo limesemewana Kiongozi wa Upinzani Bungeni kwa hiyo nina uhakikalimechukuliwa kwa uzito mkubwa zaidi kuliko ningelisemamimi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana niliongea sanahapa Bungeni, nililia sana, Mheshimiwa Lukuvi unakumbukaombi langu kubwa kwako lilikuwa ni kama ikiwezekana ujeMeru nikuambie nini cha kufanya kwenye mashamba yaliyokoMeru ambayo yaliachwa tangu enzi za waloweziwaliokuwepo Meru kwa wale mnaojua historia, nilisema hapamwaka 1952 watu wa Meru walimtuma Umoja wa MataifaNdugu Kiliro Japhet Ngura Ayo, miaka tisa kabla ya Uhurualikuwa ni Mtanganyika wa kwanza aliyekwenda Umoja waMataifa kwa sababu ya kudai ardhi la Meru, Meru land case.

Sasa nishukuru tu kwa Waziri Mkuu kwanza, pili kwaWaziri wa Ardhi ambao wote mlikuja kwa pamoja na WaziriMkuu alitoa yale maelekezo na Waziri ukaja na tukafanyakazi nzuri sana kwa pamoja, kwa kweli nikushukuru mno naniseme tu kwamba unapokuwa mpinzani siyo unapinga kilakitu kinapofanyika kitu kizuri huwa tunasema na leo mmeonakwa Waziri Lukuvi hapa amesifiwa mpaka na Kiongozi waUpinzani, kwa wale Mawaziri wengine ambao mna-ego,huwa mnajisikia na huwa hamsikii, jifunzeni kwa MheshimiwaLukuvi, nafikiri mtaweza kutengeneza Serikali nzuri sana, nanil iwakumbusha nikasema nikasema kuwa hii duniainazunguka leo Mheshimiwa Profesa Muhongo naye anaulizamaswali ya nyongeza humu ndani, juzi alikuwa huko.

Kwa hivyo ego siyo kitu kizuri sikilizeni Wabungewanaleta vilio gani kwenu, halafu muende kusikiliza msaidieWatanzania, kwa sababu dunia inazunguka kwa kasi niliwahikusema. (Makofi)

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya shukrani hizo,niseme tu baada ile baada ya ziara yako Mheshimiwa Wazirikule Meru, tulikubaliana kwamba Baraza la Madiwani nahususani Kamati, tufanye ziara kwenye mashamba yote nakujionea halafu tuandike mapendekezo ambayo yatakuwana consensus ili yaweze kupita Mkoani kuja kwako ili uwezekufanyia kazi. It is very unfortunate na nilikuambia siku ilenikiwa jukwaani pale nikasema kunaweza kuwa na mashakakwamba kusitokee consensus au siasa za kipuuzi ambazozimekuwa zikiendelea kwenye Wilaya nyingi nchi hii,zikafanyika na pale Meru zimefanyika kwenye ziara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yale mapendekezo ambayoyamekuja kwako nashukuru Mungu yamerudishwa nyuma kujakuanza upya hayakuwa na consensus hata kidogo nayatakayoletwa tena nakuomba ufanye verification utuulizewawakilishi wa wananchi, uwaulize Madiwani uwaulizeWenyeviti wa Vijiji, kwamba haya mapendekezo yamekuwana consensus au yametoka kwenye ofisi moja pale Wilayakuja moja kwa moja kwenye ofisi yako bila kuzingatia niniwawakil ishi wa wananchi kwa maana ya Madiwaniwalichokipindekeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hiyo ripoti ya kwanzailiyokuja kwako utaona ndani yake, vile vilio ambavyonimekuwa nikiongea hapa ndani havijasiki l izwa,havijaainishwa ndani yake kabisa, utaona kabisa inaandikwaripoti ya kuja kumnyang’anya mtu shamba heka 10, heka18, Meru hatulilii heka 10 na 18 tunalilia thousands of acres,hundred of acres. Mashamba ambayo yalikuwa yanamilikiwana Walowezi ambayo yalipata kibali cha Rais pia miaka yamwanzo ya tisini kufutwa, lakini usajili haukufanyika ambapoimerudi kwenye mikono ya baadhi ya watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Wazirinilikukumbusha nafikiri unafahamu vizuri kwa mfano, shambala Tanzania Plantation kwanza nikushukuru kwamba ulikubalikutoa hata fedha kutoka Wizarani kwako kwa ajili ya upimajina yule mtu alikuwa ameshakubali, mkakubaliana kwambaanabaki na kiasi gani na kiasi gani kiende kwa wananchi, it

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

is very unfortunate kwamba amekwenda Mahakamanikufunga mikono.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya watumishi waardhi kwenye Mkoa wetu Arusha siyo watu wazuri kwakonaomba nikuambie na ndiyo wanaokwenda kuwashawishihawa Wazungu kwamba nendeni mkafungue kesiMahakamani mfunge Wizara mikono, mfunge Halmashaurimikono, hakuna kinachoweza kufanyika. Ukweli ni kwambahuyu Mhindi wa Tanzania Plantation na sijui polisi wetu waInterpol wanafanya kazi gani hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu huyu bwanaana passport mbili, ana passport ya Tanzania na ana passportya Uingereza, na nchi hii haijaruhusu Dual Citizenship,tumefanya uchunguzi kabisa mara nyingi akiondoka nchinihuwa anakwenda Nairobi anaruka na passport yake yaUingereza, na huyu amekufunga mikono Mahakamani,naomba watu wa Mambo ya Ndani wakusaidie. It is veryeasy kum-capture huyu bwana, kwa sababu unaangaliarekodi zake za safari na unaangalia kwenye passport yakeziligongwa mihuri lini na lini na tarehe gani kwa sababu kunatarehe ambazo ameondoka ambapo passport yake yaTanzania haina hiyo mihuri kabisa, kwa hiyo huyu bwanaanatuibia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Waziri anakumbukakwenye ile list tuliweka hiyo list ambayo imekuja kwakoambayo nimesema haikuwa na consensus liliandikwa nashamba la Karamu, shamba la Karamu tumefanyamazungumzo na Halmashauri pamoja na mmilikitumembana na amekubali kuingia kwenye terms ambazoHalmashauri kwa maana wananchi wa Meru wanafaidika,viji j i vinavyozunguka kwa maana viji j i vya Ndato naMkwaranga wanapata share yao na Halmashauri inapangaule Mji na ule ni Mji ambao ukiangalia master plan ambayounakuja kuizundua mwezi wa Agosti Arusha, imependekezalile eneo liwe ni eneo la residential, low density na hilo ndilolengo letu tunakoelekea.

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukisema tulete kwako ufuteatakwenda Mahakamani atakufunga mikono tena tutafanyanini, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri ninaomba tu kwamba hiloliweke kwenye kumbukumbu zako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikia kengele niseme tumengine nitayaleta kwenye maandishi ikiwemo mgogorowetu ikiwemo na wa Hifadhi ya Arusha na vij i j ivinavyozunguka na Momela na mingine pia na issue ambayoameiongea Mheshimiwa Mbowe lile shamba la Valeskatuende kwa staili aliyoifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwakunisikiliza. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Nassari.Tunaendelea na Mheshimiwa Daniel Mtuka baadayeMheshimiwa Joram Hongoli na Mheshimiwa Moshi Kakosoajiandae.

MHE. DANIEL E. MTUKA: Ahsante MheshimiwaMwenyekiti, kwa nafasi hii fupi nitazungumzia mambo mawilitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niipongeze Wizara,nimpongeze Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri,niseme tu kwamba Wizara hii mmeibadilisha mmeitoa mbalimmeibadilisha, wataalam wa ardhi tunajivunia sana kwakweli kazi mnayoifanya mko aggressive, lakini pia mna-confidence na lakini la mwisho ni wachapakazi,tunawapongeza kwa hilo sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo maombi mawilimafupi, ombi la kwanza niunge mkono pia Wabungewenzangu, retantion scheme ile asilimia 30 ya makusanyo yakodi ya ardhi, naomba ibaki kwenye Halmashauri isiendehuko Hazina, kwa sababu ikienda kule hairudi harakamnatuchelewesha sisi tunataka tupime viwanja, squatterzinatusumbua, ninaomba sana hilo Mheshimiwa Waziriwakati una wind up hebu liweke vizuri.

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

Mheshimiwa Mwenyekiti, unalia hapa kwambamalengo hayakutimia kwenye kupima viwanja na wataalamumeshawasambaza kwenye Kanda, acheni tupime ardhiWilayani huku kwenye Halmashauri mnazipeleka hizo pesaza nini huko, nilikuwa nataka kulisisitiza hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, tuna ombi Manyoni,tunao upungufu wa watumishi. Wataalam wa ardhi tulionaopale Halmashauri wanatakiwa wawe 21 lakini wapo wawanne tu, watafanya kazi gani? Squatter hizi zitaendeleapamoja na hayo tunajitahidi kweli tangu mwaka juzi mpakasasa ninavyozungumza tumepima viwanja karibu 991ambavyo tayari tunavigawa kule, kwa shida kwa kujibanabana lakini viwanja 1,400 tumevipima viko kwenye hatua zamwisho tunakamilisha cadastral survey kwa ajili ya kupataapprove.

Mkeshimiwa Mwenyekiti, 220 tumefanya regulazationtunaanda hati tupo kwenye hatua za mwisho, watumishiwanne hawa tunajitahidi. Kama haitoshi tumejibana fedhakwa shida, tume-order GPS RTK sisi watu wa Manyoni inakujana tumeshailipia, tunaomba basi mtusaidie mtuunge mkono,hatuna gari kwa hawa watalaam wa ardhi, MheshimiwaLukuvi tusaidie gari kama juhudi zote hizi tumejitahidi simtuunge mkono jamani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, tunayo SheriaNamba 8 ya Mipango Miji ya mwaka 2007, tangu mwakahuo imetungwa lakini haina regulations hazijatungwa,inatekelezwaje hii sheria bila regulations? Naomba mjitahidihii sheria itungiwe regulation zake. Tunasema kwambaplanning ndiyo inayoanza, sasa mnafanyaje kazi bilaregulations tangu muda wote ule?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni hili la ujumla, hebutuitumie ardhi vizuri, ujezi wa horizontal ambao wamtawanyiko siyo mzuri tunamaliza ardhi hii, ardhi itaisha Dares Salaam kama tunge-opt vertical development tungekuwatumeishia Magomeni tu pale. Ile population ya Dar es Salaamsiyo watu wengi, lakini kila mmoja anataka amiliki kiwanja

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

na eneo afuge mpaka kuku, siyo rahisi ardhi itaisha hii, tuendejuu tusitawanyike tubakishe na maeneo ya kulima, tutalimawapi? Sasa kila mahali ni kujenga tu, haiwezekani lazima tu-plan.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimefurahi National Housingwanavyojenga, kwa mfano nimeona ghorofa za Wanajeshihapa Dodoma hapa, ziko vizuri, na scheme zingine zakujenga hebu waende ghorofa mbili tu juu watoe mfano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo machachenaunga mkono hoja, lakini retention scheme, ile fedha ibakikwenye Halmashauri ili iwasaidie kupima viwanja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja,ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Hongoli.

MHE. JORAM I. HONGOLI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kupata nafasi nami kuchangia kwenye Wizarahii, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri na NaibuWaziri kwa kazi kubwa wanayofanya kuhahakisha kwambawananchi wanapata makazi bora lakini pia kutatuamigogoro ya ardhi nawapongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya mudaniseme mambo machache hasa kuhusu watumishi wa Idaraya Ardhi. Halmashauri nyingi hasa hizi Halmashauri za Wilaya,Halmashauri za vijijini hizi hazina watumishi wa kutosha waidara hii ya ardhi, hasa Maafisa Ardhi wateule. Wilaya yaNjombe mpaka sasa hatuna Afisa Ardhi Mteule, tukitakakusaini hati tunamtumia Afisa Ardhi Mteule wa Halmashauriya Mji, kwa hiyo, mara nyingi tunapotaka kusaini hizi hatizimekuwa zikichelewa kwa sababu na yeye ana majukumuya Halmashauri yake. Kwa hiyo, niombe Mheshimiwa Waziriukishirikiana na TAMISEMI tuweze kupata Afisa Ardhi awezekutusaidia kuweza kupata hati.

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

Mheshimiwa Mwenyekiti, hati za viwanja zimekuwazikichelewa na kwenye Halmashauri yangu tuna wananchiwengi ambao wana mashamba ya chai na wangependawapate hati ambazo zingeweza kutumika kwa ajili ya kupatadhamana kwenye mikopo na sehemu mbalimbali, lakinizimekuwa zikichelewa kwa sababu tu hatuna Afisa Ardhi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uzoefu unaonyeshakwamba maeneo yote ambayo yana Maafisa Ardhi Wateulendio maeneo ambayo migogoro inapungua sana, kwa hiyo,wanafanya kazi kubwa sana za kupunguza migogoro, lakinimaeneo ambayo yanakuwa hayana Maafisa Ardhi Wateulemigogoro inakuwa mingi. Kwa hiyo, tukiajiri Maafisa ArdhiWateule wa kutosha katika Halmashauri zetu naaminimigogoro mingi itapungua. Mfano ni pale Halmashauri yaMji wa Njombe, tulikuwa na migogoro sana ya ardhi miakaya nyuma, lakini sasa hivi imepungua na inaendeleakupungua kwa sababu tuna Afisa Ardhi ambaye anafanyakazi vizuri sana. Tunaomba Halmashauri zetu zote ziwe naMaafisa Ardhi Wateule na maafisa wengine wawepo ili kasiya upimaji wa ardhi na kasi ya utoaji wa hati iwezekuongezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni kuhusumikopo ya nyumba. Nampongeza Waziri kwamba kunampango wa kuanza kukopesha nyumba kwa wenye vipatovidogovidogo, mpango huu umejikita sana kwenye maeneoya mijini, tuende vijijini ambako kuna wakulima wadogowadogo na vijana ambao wanafanya kazi za bodabodana shughuli ndogondogo waweze nao kumiliki nyumba.Tufuate utaratibu ule wa VIGUTA ambao wanajenga nyumbaza bei rahisi sana. Wanajenga nyumba mpaka za shilingimilioni 15, shilingi milioni 25 lakini wanajenga nyumba zaghorofa moja mpaka za milioni 60 na wamejenga maeneoya Kibaha pia sasa hivi wanajenga maeneo ya Dodoma.

Kwa hiyo, twende vijijini hawa wakulima wetuwadogo wanahitaji nyumba, naamini kwamba kupitiashughuli zao za kilimo, kupitia shughuli zao za bodaboda na

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

ujasiriamali mdogomdogo wakiwekewa utaratibu mzuriwanaweza wakamiliki hizi nyumba, wanaweza wakajenganyumba na wakarudisha hizo fedha kupitia hizo shughuli zaoza kila siku kwa maana ya bodaboda au ujasiriamali nakilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme pia juu ya beiviwanja. Bei ya viwanja bado iko juu kwenye baadhi yamaeneo. Kuna maeneo hasa viwanja vile ambavyovinapimwa na makampuni au mashirika mbalimbali kwakushirikiana na Halmashauri, viwanja hivi vinauzwa bei yaaghali sana. Kwa mfano, utakuta kiwanja kinauzwa shilingimilioni 10, shilingi milioni 20 eti kwa sababu tu barabaraimetengenezwa au maji yamepelekwa. Ukiangalia utakutakwamba wananchi wa kipato cha chini ambao wana uwezomdogo wa kupata hizi fedha hawawezi kumiliki hivi viwanjakwa sababu ni vya bei ya juu sana. Tuweke utaratibu mzuriwa kuhakikisha kwamba tunathibiti bei za hivi viwanja,tukiacha hivi makampuni haya kama hali iliyopo utakutakwamba wananchi wa chini watashindwa kumiliki viwanja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia wanaowezakununua hivi viwanja shilingi milioni 10, shilingi milioni 20 niwale watu wenye uwezo tu, ni wale watu wenye kipato chajuu. Utakuta hawa wananchi wenye kipato cha chiniwanazidi kwenda pembezoni, wanaondoka katika maeneoyale kwa sababu hawana uwezo wa kumiliki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayonaunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Hongoli,Mheshimiwa Kakoso, Mheshimiwa Ruth Mollel na MheshimiwaSusanne Maselle wajiandae.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia Wizarahii. Awali niipongeze sana Wizara hii kwa jitihada za kaziwanazozifanya ndani ya Wizara hii. Mheshimiwa Waziri, NaibuWaziri wake pamoja na wasaidizi wake wamefanya kazi nzuri

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

sana. Tunawapongeza hasa kwa kutatua migogoro mingiambayo kimsingi il ikuwa inawagusa sana wananchi.Tunawapongeza na kuomba tuwaombee heri sanawaendelee kutenda haki na misingi iliyowekwa ya kisheriajuu ya kuwasaidia wananchi hasa walalahoi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kuzungumzia tatizola migogoro ya ardhi ya vijiji vya Kabage, Sibwesa, Mkungwi,Kagunga na Kapanga vilivyoko kwenye Wilaya ya Mpanda.Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ina mgogoro wa mudamrefu sana wa vijiji hivi, tunaomba sana Mheshimiwa Waziriapange ziara aje amalize tatizo hili, akishirkiana na Wizaraya Maliasili. Wananchi wengi wanataabika hawana ardhiya kufanyia kazi wakati ni vijiji halali ambavyo kimsingi kamavitasimamiwa tatizo hil i tutakuwa tumelipunguza nakuwafanya wananchi waendelee kufanya shughuli zao.Naomba sana Waziri husika aje atatue matatizo ya Mkoawa Katavi hasa Wilaya hii ya Tanganyika iliyoko kwenyeHalmashauri ya Wilaya ya Mpanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambaloningependa kuzungumzia ni tatizo la kupata hati za kimilakwenye Wilaya ya Tanganyika. Karibu maeneo yote ya vijijinituna tatizo kubwa sana la kukosa huduma ya kupata hatiza kimila. Kuwasaidia wananchi hawa wanapopata hati zakimila tunawajengea uwezo wa kiuchumi, kwani watapimamashamba yao na watakuwa na nafasi ya kutumiadhamana ya hati miliki ili waweze kwenda kwenye taasisi zafedha, huduma hiyo kwetu sisi hatuna. Naomba Waziri aonekwamba ni wakati muafaka sasa kupeleka huduma hiikwenye maeneo yote ya nchi yetu hasa maeneo yapembezoni kwenye Wilaya hasa zile ambazo ni changa.Tunahitaji huduma hii ili iweze kutatua matatizo yanayoikabiliWilaya kwa kukosa huduma ya hati miliki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambaloningependa kuzungumzia ni uhaba wa wafanyakazi.Wataalam wa ardhi hasa Wilaya mpya, naamini na nchinzima bado kuna tatizo kubwa sana. Tunaomba MheshimiwaWaziri anapokuja aje na majibu sahihi yatakayosaidia kutoa

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

suluhisho hasa wataalam hawa ambao kimsingi wanahitajikaili waweze kufanya kazi ambazo zitawasaidia wananchi nakutatua migogoro mingi ambayo iko kwenye Halmashauriza Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo tunahitajikupata vitendea kazi, wataalam ambao wapo hata hukokwenye Wilaya hawana vitendea kazi vya shughuli ya upimajiambavyo ni pamoja na magari. Unakuta Halmashauri hainagari, haina vifaa ambavyo vinahitaji kwa shughuli za kupimahivyo viwanja, matokeo yake wanaenda kwa miguu kituambacho hawawezi kutekeleza na kwenda na kasi ambayoipo. Tunaomba sana hasa kwenye Wilaya yangu tupate waleambao wana uwezo wa kufanya hiyo kazi ili tuwasaidieWatanzania. Kimsingi tukitekeleza hili tutakuwa tumetoa kerokubwa ambayo inawakabili wananchi kwa kukosa huduma.Tukipata hao watalaam nina imani kwamba eneo zima lasuala la ardhi na migogoro ambayo tunaizungumziaitapungua kwa kiwango kikubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana na naungamkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lucia Mlowe.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Wizarahii ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niungane na wenzangukuwapongeza Waziri na Naibu wake pamoja na Watendajiwote wa Wizara hii kwa kazi nzuri mnayoifanya.

Pamoja na kazi hii nzuri mnayoifanya naomba nielezeematatizo yaliyoko hasa katika Mkoa wangu wa Njombenikianza na migogoro ya wananchi na watu wa TANAPA.Kwa mfano, nikiangalia maeneo ya Wanging’ombe, Kijiji chaRuduga kuna tatizo la wananchi na watu wa TANAPA, marakadhaa wamekuwa wakiwasumbua sana na kuna kipindiwaliwakatia mazao yao.

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

Kwa hiyo, nimuombe Waziri kufika maeneo yalekutusaidia kutatua tatizo hili kwa sababu limekuwa ni tatizola muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi hawa sasawametishiwa kwamba watatakiwa kuhama kwenye kile Kijijicha Mpanga. Sasa wanakaa kwa wasiwasi wana hofukubwa kwamba watahama na wana shida kwa sababu yahofu hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee suala la migogorokatika Wilaya ya Makete. Katika Wilaya ya Makete kumekuwana migogoro kati ya Hifadhi ya Kitulo na wananchi wa kijijicha Misiwa. Watu wa hifadhi wameweka beacons kwenyemashamba ya wananchi wa maeneo yale ya Kitulo,wanasema kwamba wanapanua hifadhi. Hivyo, nimuombeWaziri kutusaidia suala hili angalau hawa wananchikuwaondoa hofu maana yake nao sasa hivi wanashindwakufanya uzalishaji kwa sababu wanaona wanaendeleakuingil iwa, mwisho wa siku hata mashamba yoteyatachukuliwa, ninawaomba sana mtusaidie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile naomba niongeleesuala la migogoro Makete na Wanging’ombe. Kuna tatizola mipaka kati ya Wanging’ombe na Makete, vilevile kunatatizo kati ya shamba la Ludodolelo, kuna mwekezaji ambayeyuko katika shamba la Ludodolelo ambaye anawasumbuasana wananchi, sasa wanavutana kati ya wananchi na yulemwekezaji. Kwa hiyo, niwaombe Serikali mtusaidie mfikemaeneo yale kusudi tuweze kutatua tatizo hili. Ahsante.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa. Tunaendeleana Mheshimiwa Susanne Maselle na baadaye MheshimiwaMchengerwa ajiandae.

MHE. SUSANNE P. MASELLE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia katikaWizara hii. Kabla sijaanza kuchangia napenda kutoa polekwa wananchi wa Mwanza kwa tetemeko ambalo

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

limetokea jana na pia nitoe pole nyingi kwa askari wetuJoyce ambaye alifariki kwa kupata mshituko na majeruhiwengine ambao wamepelekwa hospitali, natoa pole sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ulikujaMwanza najua ulifanya mambo mazuri sana kamaalivyoongea Mbunge wa Nyamagana, lakini kuna migogoroambayo hukuipitia, kuna migogoro ambayo iko Ilemela.mwaka 2009 Jeshi la Wananchi lilifanya utambuzi wa maeneoyake na iligundulika eneo la Mlima wa Nyagungulu Kata yaIlemela ilikuwa inafaa kwa makazi ya Jeshi. Sasa utambuzihuu baada ya kufanyika ilionekana kuna kaya 448 ambazozilikuwa na makazi ya kudumu na tarehe 04 Novemba, 2014ilifanyika tathmini ambapo Serikali ya Mkoa pamoja na Jeshila Wananchi waliona kwamba wananchi hao wanapaswakulipwa, na waliamua kwamba baada ya tathmini hiyowalisema kwamba ndani ya miezi sita wananchi haowangekuwa wameshalipwa, lakini mpaka sasa badohawajalipwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna nyumba zingineambazo ni za udogo mpaka zimeanza kuanguka hawawezikufanya marekebisho yoyote au kuzikarabati kwa sababuwanaogopa eneo hilo l inachukuliwa na Jeshi. SasaMheshimiwa Waziri ninaomba umalize huu mgogoro kwasababu hawa wananchi wanateseka na wananchi wengiwamekuwa wakilalamika, wameandika barua nyingi sana.Wameandika barua kwa Mkuu wa Mkoa, barua hizi hapanitakuletea, wameandika kwa Mbunge…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Susanne,tunaendelea na Mheshimiwa Mchengerwa.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi nami nianze kwakumshukuru sana Mwenyezi Mungu. Pia nimshukuru sana

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

mzalendo namba moja nchini ambaye ni Rais wetu Dkt. JohnPombe Magufuli kwa kufanya kazi nzuri sana siku tatuzilizopita za kusimamia rasilimali za nchi yetu hii Tanzania.Niliwahi kusema hapa kwamba, Dkt. John Pombe Magufulini mzalendo namba moja, na uzalendo wake tunauonahapa kwa namna ambavyo anawatetea watanzania.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatoa pongezi kwaWaheshimiwa Mawaziri wote wa Wizara hii, kwanza kwaMheshimiwa Lukuvi, Naibu wake pamoja na Wasaidizi waowote, kwa kweli Wizara hii ni ngumu lakini Mheshimiwa Lukuviamefanya kazi nzuri sana kwa kipindi kifupi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kuzungumziaumaskini uliopo katika Jimbo langu la Rufiji. Jimbo la Rufijilina square kilometer 13,600 na eneo la Bonde la Mto Rufijiambalo linafaa kwa ajili ya kilimo ni zaidi ya hekta 500,000.Kutokana na utapeli wa madalali na kutokana nawawekezaji matapeli ambao wameingia Rufiji, leo hii ukifikaTIC hauwezi kupata eneo la uwekezaji Rufiji. NimuombeMheshimiwa Waziri kuliangalia hili na kuangalia uwezekanowa kunyanganya maeneo yote ambayo wawekezajimatapeli wamechukua ardhi yetu ya Rufiji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, umaskini tulionao ni kwasababu matapeli hawa wamehodhi maeneo haya nahawayafanyii shughuli yooyote. Leo hii Rufiji tusingekuwamaskini kwa sababu ardhi ndio utajiri wa hali ya juu.Nikuombe Mheshimiwa Waziri sasa Serikali yetu ya Chamacha Mapinduzi, Serikali yetu ya Awamu ya Tano iwezekupambana na matapeli hawa. Yako maeneoyaliyochukuliwa na watu wa RUBADA, pia yako maeneoyaliyochukuliwa na watu wanaojifanya ni wawekezaji lakinisiyo wawekezaji wa kweli. Ninakuomba Mheshimiwa Wazirimaeneo hayo uyarudishe il i sasa wale wawekezajiwanavyopita TIC waweze kuelekezwa na kufika Rufijiwapatiwe maeneo ya uwekezaji. Kwa sababu, maeneotuliyonayo ni ya kutosha, ardhi ipo tupu, wananchiwanashindwa kushiriki kwenye shughuli za kilimo.

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia namwombaMheshimiwa Waziri, kama sio yeye au Waziri anayehusika,atakapofika hapa atupe taarifa ni kwa nini mwaka 2006Serikali iliamua kuhamisha mifugo kutoka Bonde la Ihefu nakuleta mifugo katika Bonde la Mto Rufiji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunataka tufahamu sababuya kuhamisha mifugo Bonde la Ihefu. Tunafahamu kabisakwamba uhamishwaji wa mifugo kutoka Bonde la Ihefukupelekwa maeneo mbalimbali ya nchi ulitokana na uharibifumkubwa wa Bonde la Ihefu. Sasa nataka nifahamu, je, Serikaliilidhamiria kuleta mifugo katika Bonde la Rufiji ili sasa nabonde hili liweze kuharibika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba majibu hayoMheshimiwa Waziri; kama sio yeye au Waziri yeyoteanayehusika atakapofika hapa atupatie majibu haya, iliWarufiji waweze kufahamu kiini cha matatizo haya, kwasababu wakulima leo hii wanashindwa kushiriki katikashughuli za kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kwambaWarufiji walikuwa na ndoto za kupatiwa kiwanda katika eneola Muhoro pamoja na Chumbi. Mheshimiwa Waziriatakapofika hapa, naomba atuambie, je, ardhi ile ambayoilitengwa kwa ajili ya mwekezaji, bado ipo? Je, mwekezajihuyu anaifanyia utaratibu gani ili sasa tuweze kupata majibuya jambo hili? (Makofi)

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,Kuhusu Utaratibu.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, jambo lingine ambalo naomba…

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,Kuhusu Utaratibu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mchengerwa naombaukae. Kuhusu Utaratibu.

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

KUHUSU UTARATIBU

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Naomba nipate Mwongozo Kuhusu Utaratibu, hasakuhusu Kanuni ya 149(3)(b) ya Uvaaji Ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mbunge anayechangiahajavaa mavazi ya Kibunge. Mavazi ya Kibunge kamaunavaa hiyo baraghashia ya Kiislam, lazima uvae na kanzu.Yeye amevaa hiyo na suti. Ni kinyume kabisa na kanuni.(Kicheko/Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimepokeahuo utaratibu. Ni kwamba kofia hiyo, inaweza kuvaliwa nanguo yoyote kwa mujibu wa sheria. Kwa hiyo, naombaumalizie dakika zako. (Makofi)

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, msemaji alini-miss tu. (Kicheko)

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti,Kuhusu Utaratibu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mchengerwa, naombaumalizie ukavae kanzu. (Kicheko/Makofi)

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, tarehe 3 Machi, 2017, Mheshimiwa Rais Dkt. JohnPombe Magufuli alifika Rufiji na katika maeneo aliyofika,alifika Ikwiriri na katika kauli alizowahi kuzitoa MheshimiwaRais aliwaambia Watanzania wa Rufiji, hususan Wenyevitiwa Vijiji kutouza maeneo yao. Aliwaambia wawe makinisana na madalali na matapeli wanaotaka kuchukua ardhiyetu pale Rufiji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 9 Septemba, 2016Waziri Mkuu pia alifika Rufiji, lakini pia katika maeneo ambayoyana mgogoro mkubwa wa ardhi ni eneo letu la Kata yaChumbi. Tarehe 4 Mei, 2017 Waziri wa Ardhi aliniandikia baruaya kutatua mgogoro wa ardhi pale Chumbi. Kwa bahati

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

mbaya, Mheshimiwa Waziri hakuweza kufika Chumbi, lakiniwananchi wa Kata ya Chumbi wanaamini labda mimi ndionimemzuia Mheshimiwa Waziri kufika Kata ya Chumbi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziriatakaposimama hapa, atoe majibu, ni kwa nini hakufikakatika Kata ya Chumbi ambako kuna mgogoro mkubwawa ardhi? Miongoni mwa malalamiko ya wananchi nikwamba, Mwenyekiti wa Kijiji ameuza ardhi ambayo inaukubwa wa takriban zaidi ya ekari 2,400 kwa Sh. 9,700/= kwaekari moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, Mheshimiwa Raisalishatoa tamko la Wenyeviti wa Vijiji kutouza maeneo yao,naomba Mheshimiwa Waziri akifanya majumuisho, basi atupemajibu ya jambo hili. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mchengerwa.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana na naunga mkono hoja.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunamalizia uchangiajiwetu kwa Mheshimiwa Waitara na Mheshimiwa MagdalenaSakaya.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Naomba nimpongeze Mheshimiwa Wazirina Mheshimiwa Naibu Waziri kwa sababu nilikuwa namgogoro wa Kazimzumbwi kwa kweli yeye na MheshimiwaWaziri Mkuu waliingilia kati. Nawashukuru sana Waheshimiwahawa, kwani walifunga safari kutoka hapa mpaka Ukongana wakahakikisha kwamba jambo hilo linajadiliwa kwamanufaa ya watu wa Ukonga. Kwa hiyo, nawashukuru sana,nawatakia kazi njema.

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani WaheshimiwaMawaziri wapo humu. Hizi pongezi ambazo MheshimiwaLukuvi anapewa na wengine, nadhani Mawaziri wangefanyakazi kama hiyo tungekuwa hatuna mgogoro mkubwa. Kwahiyo, ni muhimu wakajifunza mambo mazuri kama haya.Anapokea simu na Naibu wake, wanakusikiliza, wanakupamajibu, wanatembelea Majimbo; na kama jambohaliwezekani, anakwambia hili kwa mujibu wa sheriahaliwezekani. Mheshimiwa Lukuvi nafikiri kwa sababu yauzoefu wake, anaweza akatoa tuition kwa wenzake ilitukaenda vizuri. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, Mheshimiwa Lukuvinaomba anisaidie kumaliza migogoro maeneo yafuatayoUkonga. Moja, kuna mgogoro wa UVIKIUTA, nyumbazimevunjwa zaidi ya mara tatu, anaufahamu vizuri. Tunahitajiwatu wale wapate amani, wapate maelekezo ya kisheriawaishi kwa amani katika eneo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mgogoro upo palePugu Kajiungeni. Ni eneo la wazi, hakuna eneo lingine, vijanawalikuwa wanacheza mpira, akinamama wanafanya kazizao; nyumba zilivunjwa usiku wa saa 9.00. Ofisi ya Mkoatumeenda mara nyingi sana, lakini hatuna majibu mpakaleo. Kwa hiyo, tunaomba atusaidie tupate majibu katika eneohilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Kipunguni hainaShule ya Sekondari, haina huduma za kijamii, ni kata mpya.Eneo pekee ambalo lilikuwa limebaki, limevamiwa na watu,hawana documents zozote zile, lakini majibu hayapatikanimpaka sasa. Kwa hiyo, tunaomba atusaidie pia, kupatamajibu katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro mwinginemkubwa wa ardhi ni wananchi ambao walihamishwa kutokaeneo la Uwanja wa Ndege wakapelekwa maeneo ya Buyuni,Zavala na maeneo mengine kule. Wale watu

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

wameondolewa kutoka hapa Uwanja wa Ndege Kipawa,kule hawakupewa ardhi, lakini bahati mbaya pia wakapewamaeneo ya watu. Kwa hiyo, kuna ugomvi kati ya watuambao wametoka Kipawa na wale ambao ni wenyejiwaliokutwa katika eneo lile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Lukuvi kwasababu yupo tayari, akutane na watu hao awasikilize, kwanini kilio cha muda mrefu na kweli wana shida kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni bomoabomoa. Eneo la Kata ya Pugu Station, Kata ya Ukonga naKata ya Gongo la Mboto, maeneo yaliyobomolewa kupishaujenzi wa reli kwa kiwango cha standard gauge; hatupingi,lakini wale watu wengine walikuwa na hati,wamechanganywa kule kule na hakuna fidia yoyote ile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mambo kama hayawakiyafanya ni muhimu watu wafahamu sheria zinasemanini? Haki zao ni zipi? Wakati mwingine kutoa taarifa inadvance ili kama kuna mtu ana-vacate, aweze ku-vacate iliasipoteze mali zake zote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, neno la mwisho ni upimajiwa maeneo ya umma. Migogoro mingi iliyopo katikamaeneo yetu hayapimwi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Lukuvi,achukue hatua mahususi kupima maeneo haya ili kuondoamigogoro kati ya wananchi na maeneo ya umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa umeshafahamika. Ahsantesana. Tunamalizia na Mheshimiwa Magdalena Sakaya.

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi hii adimu sana.Naungana na Waheshimiwa Wabunge kumpongezaMheshimiwa Waziri, Naibu wake na Watendaji wote waWizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siri kubwa ya mafanikio yaWizara hii, wanasikil iza tatizo, wanakwenda site,wanalishughulikia na wanaweka mifumo ya kuhakikishakwamba tatizo halijirudii. Hongera sana Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba MheshimiwaWaziri spirit aliyotumia ya kuweza kutatua migogoro maeneombalimbali, aje Kaliua akishirikiana na Wizara ya Maliasili naUtalii atatue migogoro ambayo inawasumbua wananchi waKaliua kwa muda mrefu na kuondokana na mateso namaumivu wanayopata wananchi wa Kaliua kwa sababu yamigogoro ya ardhi ya kati ya wananchi na hifadhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni la upimaji waardhi. Speed ya kupima ardhi bado ni ndogo, asilimia 25 nindogo sana. Tunatamani kwamba mwananchi anapohitajiardhi aweze kupewa kiwanja ambacho tayari kimepimwa.Kwa hiyo, naomba sana kwenye Mfuko wa Kupima Ardhilazima kuhakikisha kwamba kuna fedha ya kutosha. Iwepofedha ya kutosha na vifaa vya kupima ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Ardhi imewekakipengele kwamba Waziri atatenga eneo la mifugo; eneolitapimwa, litakuwa gazetted na pia litalindwa. Kwa hiyo,naomba wakati wa kupima ardhi kwenye maeneombalimbali, Mheshimiwa Waziri ahakikishe anatengamaeneo ya mifugo na pia maeneo yawe gazetted na yawezekulindwa. Ndiyo inayosababisha migogoro mikubwa sanandani ya nchi yetu kutokana na migogoro ya ardhi kwawakulima na wafugaji na hifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine naomba ahadi yaNational Housing; pamoja na kazi nzuri wanayoifanya, wafikeKaliua. Ni Wilaya ambayo ni mpya, lakini inakwenda speed

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

sana kwa maendeleo, waje wawekeze ndani ya Wilaya yaKaliua, kujenga nyumba nzuri nasi tuweze kuwa wa kisasakama ambavyo Wilaya nyingine wameweza kujengewanyumba na National Housing.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, hawa watu wa Mfukowa Kujenga Nyumba za Watumishi (Utumishi Housing),usambae uende maeneo mengi, ufike mpaka Kaliua.Watumishi wetu hawana nyumba, wamepanga nyumbandogo ndogo za vijijini huko. Tunaomba na wenyewe wajeKaliua wapanuke katika maeneo mengi; sasa hivi wame-concentrate kwenye maeneo machache sana. Mfukouongezwe ili watumishi wetu wa maeneo mengi wawezekupata nyumba za watumishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine. Migogoromikubwa ya ardhi inasababishwa na uelewa mdogo pia waWenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa. Naomba umaliziesentensi yako ya mwisho.

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba sana Mheshimiwa Waziri atoe elimu kwaViongozi wa Vijiji. Viongozi wa Vijiji wanatoa maeneomakubwa sana. Sheria inaruhusu ukomo wa kutoa eneo lakijij i, lakini wanatoa mpaka hekta 1,000 au 2,000 nawanapokea rushwa, wanaleta watu bila hata wananchikujua. Kwa hiyo, naomba itumike busara viongozi wapewesemina na mafunzo waweze kutumia Sheria ya Ardhi kugawamaeneo ndani ya vijiji vyao ili kuondokana na migogoroinayosababishwa na kugawa ardhi bila kufuata Sheria yaArdhi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa MagdalenaSakaya.

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kutoa shukrani za dhati kwa Waziri mwenyedhamana, Mheshimiwa William Lukuvi pamoja na Naibuwake Mheshimiwa Angeline Mabula, sambamba na timunzima ya Wizara chini ya Jemadari Kayandabila.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe malalamikoyangu kuhusu hatua ambazo zinachukuliwa na Idara ya ArdhiKanda ya Kaskazini; tunalo shamba letu la Mnazi Sisal Estateambalo kwa sasa linamilikiwa na mwekezaji wa Kenya kupitiakampuni ya Le-Marsh Enterprises ambayo inamilikimashamba matatu yenye hati zifuatazo; tittle No.44144, ekari562; tittle No. 17146, ekari 1188, pamoja na tittle No. 11247,ekari 2442.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Lushotoilitoa barua ya Notice of Revocation yenye Kumb. Na. LDC/L.10/VOL.111/245-09/12/2016 kwenda kwa Kamishna wa ArdhiKanda ya Kaskazini. Naomba nitoe masikitiko yangu kuwabarua hii inakaribia kumaliza mwaka lakini hadi sasa hakunakinachoendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekuwa nikichukua hatuaza ufuatiliaji mara kwa mara kwenye Ofisi ya Kanda, lakinimara zote nilikuwa napata ushirikiano hafifu, ikiwemo maraya mwisho, Mheshimiwa Waziri tulivyofanya mazungumzo,walitujibu kuwa kuna matatizo ya kiufundi kwenye taarifaya notisi. Hili kwetu tunaliona kama ni hujuma kwa kuwabarua za Kiserikali hujibiwa kwa taratibu zake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama walivyo wawekezajiwote wababaishaji huyu Le Marsh Enterprises ni miongonimwao na amekuwa akiwahadaa wananchi, Halmashaurina sasa anaonekana na baadhi ya Maafisa wa Ardhi Kanda,wanamlinda hivyo kusababisha chuki kubwa kwa wananchihusika wa Kata za Mbaramo, Mnazi, Lunguza ambaowanazungukwa na mashamba hayo.

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuna nia ya kumuoneamtu lakini tunahitaji kuona wananchi wanafaidika narasil imali zao na pia kuona mapato ya Halmashauriyanapatikana bila kikwazo chochote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hitimisho; mwekezaji katikaMashamba ya Katani ya Mnazi ameshindwa kwa kiasikikubwa kuyaendeleza mashamba anayoyamiliki. Kati yaekari 4192 ni ekari 500 tu ndizo ambazo ameziendeleza kwakupanda mkonge na kuvuna, ekari 1942 mkonge upo porini,kwenye vichaka hautunzwi kabisa. Ekari 1023 ni msitu mtupuambao unatumiwa na wafugaji wa jamii ya kimasai kamamalisho ya mifugo yao. Pia mmiliki huyo hajalipia kodi yaardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa fursa hii nimpongeze MheshimiwaWaziri kwa hotuba nzuri ya bajeti. Nianze na mgogoro washamba la Tumaini lenye ukubwa wa ekari 4,000 ambaloMheshimiwa Waziri, kwa uzalendo wa hali ya juu wakuthubutu alifuta hati miliki ya shamba lile. Hicho ni kitendocha kijasiri kabisa na chenye kuendana na utekelezaji waIlani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua kuwa suala hililipo mahakamani, lakini wananchi wa Mafia wanaungamkono uamuzi wa Mheshimiwa Waziri wa kuifuta hati nakulirejesha shamba miliki kwa wananchi. Ombi letu ni marabaada ya shauri lililopo Mahakamani kumalizika tunaombamgao wa shamba hili ufanywe na Halmashauri yetu ya Mafiakulingana na vipaumbele vyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii piakumwomba Mheshimiwa Waziri alifute shamba la ng’ombeambalo limebaki pori kubwa na ongezeko la watulimepelekea ongezeko kubwa la mahitaji ya ardhi kisiwaniMafia.

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Nyumba la Taifa(NHC); Halmashauri ya Mafia tumetenga eneo kubwa lakutosha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kupitia Shirika hili.Nimwombe sasa Mheshimiwa Waziri, aagize uongozi waShirika hili kuanza mradi huu haraka sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naungamkono hoja.

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,aidha, ni kitu muhimu sana katika nchi yetu na dunia nzimakwani kila kiumbe kinachoishi duniani kiko chini ya ardhiambapo kumekuwa na changamoto nyingi ambazozinaikabili Wizara hii ambayo ni lazima kuwepo na mikakatiya makusudi kumaliza changamoto hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, migogoro ya wakulima nawafugaji; suala hili limekuwa ni changamoto kubwa kwanchi yetu ambayo imesababisha madhara makubwa sanaikiwemo vifo kwa wakulima na wafugaji na pia kwawawekezaji hasa kama hakukuwa na ushirikishwaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mipaka, ni vyemaWizara ikawa na utaratibu madhubuti wa kupitia upyamipaka ya maeneo mbalimbali ikiwemo vijiji na vitongojilakini maeneo yaliyotengwa kwa uwekezaji pamoja namaliasili zote ili kuondoa migogoro mbalimbali inayowezakujitokeza katika maeneo yetu. Upatikanaji wa hati miliki,suala hili limekuwa na changamoto kubwa hasa kwawananchi wa vijiji ambao makazi yao hayajapimwa, nakumekuwa na urasimu mkubwa kwa maafisa wa ardhi katikaHalmashauri mbalimbali nchini ikiwemo Mkuu wa Mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upungufu wa Maafisa Ardhikwenye Halmashauri ikiwemo Halmashauri ya Manispaa yaSumbawanga; nashauri Serikali kuongeza Maafisa Ardhikwenye Halmashauri mbalimbali nchini ili kuondoa migogoroisiyo ya lazima. Kutolewa mafunzo kwa Maafisa Ardhi naMaafisa Mipango Miji ili kuweka ufanisi katika maeneo nakazi zao ambao hazitaleta usumbufu kwa wananchi.

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la upimaji wa ardhi,suala hili limekuwa na changamoto kubwa, lakini linatokanapia na maafisa ambao sio waaminifu kwa kujipatia viwanjaambavyo Halmashauri na Serikali kwa ujumla hazinufaikikabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upatikanaji wa hatikuchukua muda mrefu na kupelekea mianya ya rushwa sualahili limekuwa likiwakatisha tamaa wananchi ambao hawanahati miliki. Nashauri Serikali kufuatilia suala hili kwa ukaribu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Nyumba; kunachangamoto kubwa hasa kwa suala la gharama kwanigharama za nyumba zinazojengwa ni kubwa ambazowananchi wakiwemo wa Mkoa wa Rukwa hawawezikumudu kabisa nyumba zijengwe kulingana na jiografiahusika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wenyeviti wa Serikali zaMitaa, Vijiji na Vitongoji wapewe ramani ili wayajue maeneoyao. Hii kwa kiasi kikubwa itachangia kuondoa migogoroisiyo na sababu.

MHE. JULIUS K. LAIZER: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza napenda kuipongeza Wizara na Mheshimiwa Wazirikwa juhudi wanazofanya katika kuyapatia ufumbuzi masualaya migogoro ya ardhi nchini ikiwemo Monduli. MheshimiwaWaziri anakumbuka mwaka jana 2016 Machi alipokujaMonduli alikabidhiwa mashamba 13 yaliyofutwa na Rais kwaajili ya wananchi lakini mpaka sasa wananchi wamezuiwakutumia ardhi pamoja na kwamba wao wameshapangamatumizi na kubainisha maeneo ya malisho na eneo la kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko wamiliki waawali waliyapeleka malalamiko kwa DC na DC kuzuiawananchi kutumia ardhi hiyo, mpaka itakapoenda tume yakuchunguza kama mchakato wa kufutwa ulifuatwa.Masikitiko yetu ni kwamba Rais ameshafuta mashamba je,kuna mtu mwingine mwenye mamlaka zaidi ya Rais?Naomba kauli ya Mheshimiwa Waziri kuhusu mashamba

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

ambayo Rais ameshayafuta lakini bado wananchiwananyimwa kuyatumia. Naomba Ofisi yake itoe warakawa kuelekeza namna bora ambayo wananchi wanaruhusiwakutumia ardhi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo MheshimiwaWaziri alitoa agizo kuhusu Ndugu Olemilya Mollelaliyejichukulia ardhi kinyume na taratibu ambapo pia aliagizayeye kuondoa walinzi wa jeshi wenye silaha wanaolinda ardhiyake ambayo ni pori tu, miti na majani, (agizo lakehalikutekelezwa) badala yake wananchi sasa wanakamatwana kutozwa hadi milioni moja kama faini na mwenye shamba(naomba kauli yake ili kunusuru wananchi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, uanzishaji wa Baraza la ArdhiWilaya ambapo sisi tumetoa jengo tayari. Tunaombakupatiwa Afisa Ardhi Mteule. Tunaomba wananchi wapeweangalau miaka mitano ya kulipia nyumba za NHC.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hotuba ya Mheshimiwa Waziri. Ardhi katikamaisha ya mwanadamu ndiyo rasilimali msingi katikamaendeleo ya mwanadamu kwa vile miundomisingi yotehufanyika juu ya uso wa nchi. Uso wa asili, maji, barabara,Maziwa, reli, makazi na shughuli za kilimo, wanyama wakufugwa pamoja na pori la akiba na hifadhi zote ziko juu yauso wa nchi na kwa ajili hiyo basi ni vema Serikali kupitiaWizara hii ikajipanga kikamilifu kupata mipango mijiiliyosanifiwa kikamilifu na kuendelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo changamotombalimbali zinazoikabili Sekta ya Ardhi nchini ikiwemo kubwakabisa uhaba wa wataalam pamoja na vitendea kazi haliinayopelekea kutokuwepo kwa matumizi bora na endelevuya ardhi mjini na vijijini. Ongezeko la watu pamoja na mifugoni changamoto nyingine kubwa inayopelekea mwingilianowa shughuli za kibinadamu kwa maana ya wakulima nawafugaji pamoja na changamoto ya ucheleweshwaji wamalipo ya fidia kwa wananchi ambao ardhi yao inatwaliwakwa ajili ya shughuli za uwekezaji. Katika sekta mbalimbali

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

ikiwemo kilimo, viwanda maeneo ya kimkakati kama vile,special economic zone na kadhalika. Uharibifu wa mazingiravile vile hufanyika juu ya uso wa nchi. Hivyo basi, ipo hajakwa Wizara hii kuwezeshwa kiutendaji kwa kuongezewabajeti yake ili iweze kuajiri wataalam wengi zaidi pamoja navitendea kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya yetu ya Mbogwetunayo nafasi nzuri sana ya kuweza kujipanga vizuri katikaSekta hii ya Ardhi kwa vile wilaya yetu ni mpya kabisa hataujenzi holela haujawa wa kiwango cha juu. TunachohitajiWilaya na Halmashauri ya Mbogwe ni kuunga mkono katikajitihada za kuipima ardhi yetu. Hivyo basi, tunaiomba Wizaraituangalie wananchi wa Mbogwe kutupatia Afisa MipangoMiji ili asaidie katika kupanga kitaalam wilaya yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa jitihada za kupatamaendeleo katika shughuli za upimaji Wilayani MbogweMfuko wa Jimbo umechangia ununuzi wa kifaa cha upimajikiitwacho Total Station, kinachotakiwa kingine kiitwachodifferential ili tuweze kukamilisha uchapishaji wa upimaji waardhi hasa viwanja na mashamba ya wananchi na hatimayewaweze kumilikishwa kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunalipongeza kwa dhatiShirika la Nyumba NHC kwa kazi nzuri sana linazozifanya.Naishauri Serikali kuliwezesha Shirika hili ili liweze kujenganyumba nyingi zaidi nchini ikiwepo Wilayani Mbogwe. Naungamkono juhudi na jitihada zinazoendelea kufanywa na Wizarahii. Ombi, letu Mbogwe ni kupewa Afisa Mipango Miji katikaHalmashauri ya Wilaya Mbogwe pale Wizara itakapoanzakuajiri watumishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naipongeza sana Wizara, kwa kazi nzuri mnayoifanya kutatuamigogoro ya ardhi katika nchi yetu. Naiomba Serikali,kuendelea na juhudi ya kutatua migogoro ya ardhi katikaMikoa, Wilaya, Kata na Vijiji. Kuna migogoro ya kugombania

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

mipaka kati ya wilaya na wilaya nyingine, mipaka ya katana kata, kuna migogoro ya kijiji na kijiji. Ili kumaliza kabisamigogoro hii naishauri Serikali kupima ardhi yote ili kupatamatumizi bora ya ardhi nchini. Kuna tatizo la ujenzi holelakatika miji yetu naishauri Serikali, kusimamia upangaji wa mijiyetu, kuwa na master plan ya miji na kuwaelimisha watukufuata sheria ya mipango miji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iwapimie mashambawakulima il i ki la mkulima kuwa na shamba ambalolimepimwa na analipia. Katika upimaji naiomba Serikaliiwapimie wananchi kwa bei nafuu ili hata watu wenye vipatovidogo, waweze kusajili mashamba yao na kupimiwa. Serikaliipunguze bei ya upimaji wa viwanja, wananchi wanashindwakununua viwanja vya Serikali sababu bei ipo juu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri, NaibuWaziri na Uongozi mzima wa Wizara. Ni jambo lisilo na shakahata kidogo Wizara hii ni miongoni mwa Wizara chache sanazinazochapa kazi hasa chini ya uongozi wa MheshimiwaWilliam Lukuvi, pamoja na Naibu Waziri, hongereni sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie hotuba hii katikamaeneo yafuatayo:-

Migogoro ya Ardhi, kila kona ya nchi utasikia migogorohii. Nipongeze tena jitihada zinazofanywa na Wizara katikakutatua migogoro mfano ni upimaji wa maeneo ya wafugajina wakulima katika Mkoa wa Morogoro. Bila shaka mfanohuu utakwenda maeneo yote nchini mfano katika Jimbolangu la Kilindi lenye nusu wakulima na nusu wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mfumo huu piauelekezwe huku kwa sababu migogoro inaongezeka kila siku.Suluhu ni kupima tu. Wizara imeelekeza Halmashauri zitengefedha kwa ajili ya kupima, lakini ni ukweli usiofichika badoHalmashauri zetu hazina uwezo wa kupima kwani baadhi

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

ya Wilaya zina maeneo makubwa sana mfano wilaya yanguina vijiji 102, vitongoji 650, hivi itachukua miaka mingapikupima?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Migogoro ya Ardhi, (mpakakati ya Kilindi na Kiteto). Mimi binafsi nichukue fursa hiinimpongeze Mheshimiwa Waziri Mkuu; Waziri wa Ardhi; naWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, ambao walifikampakani na kujionea mgogoro uliodumu zaidi ya miaka 30ambapo Mheshimiwa Waziri Mkuu aliagiza Wizara kupitiawapimaji kupitia GN 65 ya mwaka 1961 inayotenganishaMkoa wa Tanga na Arusha kwa sasa Manyara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze MheshimiwaWaziri kwa jitihada zake wapimaji walifika na kufanya kazikubwa ya kubainisha mpaka huu, gharama za fedha zaumma zimetumika kwa watumishi hawa lakini cha kusikitishani kuona zoezi hili limesimama alama (Beacons) hazijawekwa,wananchi wanataka wapate majibu ya Wizara hii, tatizo likowapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchiwamekwishatambua wapi mpaka wao upo kwa mujibu wataarifa ya wapimaji ambapo, mimi, Mkuu wa Wilaya na Mkoawa Tanga tunazo, nadhani zoezi hili ni vema lingekamilishwaili wananchi wa wilaya hizi mbili, (Kiteto na Kilindi) ambaowanaishi kwa hali ya wasiwasi na kutofanya shughuli zakilimo na mifugo wanachoomba kupata suluhu ya kudumuambayo ni kuweka alama za kudumu (Beacons).

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kauli ya Wizara juuya jambo hili ambalo linabeba mustakabali wa maisha yawananchi wa Kilindi na Kiteto, kutowaona wapimajikumalizia zoezi hili kunatoa picha isiyoleta matumaini.Wananchi wana imani kubwa na Mheshimiwa Waziri kwaniutendaji wake bila shaka umemletea sifa kila kona ya nchihii, ni imani yangu hatapata kigugumizi katika hili ili kuletahaki kwa wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

MHE. AMINA N. MAKILAGI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru, naomba nianze kwa kukushukuru wewe naMwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi ya kusimama na kutoamchango wangu katika sekta ambayo, ili kuendelea katikamambo manane, ardhi ndiyo ya kwanza; bila kuwa na ardhihatuwezi kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja kwaasilimia mia moja kwa sababu nne (4) zifuatazo:-

Kwanza, kitabu cha hotuba kimeandaliwa vizuri sana,maneno machache, takwimu kwa wingi.

Pili, Mheshimiwa Waziri William Lukuvi, Naibu WaziriMheshimiwa Angelina Mabula, Katibu Mkuu, Naibu KatibuMkuu na timu yake, wanafanya kazi nzuri sana ya (kupigiwamfano). Ni ukweli usiopingika kuwa, watendaji walio wengiwa Wizara ya Ardhi wamebadilika, hongereni sana, ongezenibidii zaidi ili muwakomboe Watanzania hasa wanawake.

Tatu, mipango ya kusikiliza kero za wananchi; naungamkono kwa sasa, Wizara imeweka mipango mizuri ya kutatuakero za wananchi kupitia Mabaraza ya Ardhi, Mahakama zaArdhi, Ofisi za Wakuu wa Wilaya na Mikoa na Halmashauri zaWilaya.

Nne, Hati zilizofutwa/kurudishwa kwa wananchi;naunga mkono kwa sababu Serikali imefuta baadhi ya hatiambazo zilimilikiwa na watu wachache kwa muda mrefubila kuendelezwa na kurudishwa kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na ushauri ninayomambo ya kuishauri Serikali katika, sehemu chachenilizochagua kuzitilia mkazo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, mpangilio waMatumizi ya Ardhi, Wanawake na kumiliki Ardhi, pamoja nakuishukuru Serikali kwa kuhakikisha wanawake na wanaumewanapata fursa, katika umiliki wa ardhi kwa mujibu wa Sheriaya Ardhi ya Kijiji ya 1979 kifungu cha (4-5). Katika kutoa nafasi

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

ya umiliki wa ardhi kwa akinamama bado taratibu za kimilahazitoi fursa kwa wanawake hasa wa vijijini kumiliki ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri, Serikali itazameupya taratibu za kimila kwa kuzifanyia marekebisho ili kutoafursa kwa akinamama kumiliki ardhi. Ningependa Waziriatakapokuja hapa kuhitimisha Hotuba yake atuambie nawanawake wasikie kwamba, Serikali ina mpango gani wakuhakikisha taratibu za kimila ambazo ni kandamizizinazowanyima wanawake fursa ya kumiliki ardhi sambambana wanaume zinaondolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, migogoro ya wakulimana wafugaji, hifadhi na wananchi; pamoja na kazi nzuriinayofanywa na Serikali ya kutatua migogoro ya ardhi, badotatizo ni kubwa. Ushauri wangu, Serikali itafute fedha yakupima ardhi yote ya Tanzania. Ni muhimu sasa Serikali Kuuitafute fedha hata kwa njia ya mkopo kwa ajili ya kupimaardhi yote ya Tanzania na kupanga matumizi bora ya ardhi.Kila eneo lipangiwe matumizi yake ili kuondoa migogoro yawakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikigharimu maishaya Watanzania wengi. (Suala la kupima ardhi lisiachwe kwaHalmashauri iwe ni ajenda ya Kitaifa).

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, utoaji wa Hati zaViwanja; pamoja na kazi nzuri ya utoaji wa hati kwa wakati,bado wananchi wanaotumia ardhi karibu asilima 80 hawanahati miliki. Mfano; katika mwaka wa fedha 2016/2017, Serikaliiliahidi kutoa hati miliki za ardhi 400,000 lakini hadi kufikiatarehe15 Mei, 2017, Serikali ilikuwa imetoa hatimiliki 33,979tu, sawa na asilimia 8.5 ya lengo zima (ukurasa 18). Kiwangohiki ni kidogo sana ukilinganisha na uhitaji wa hatimiliki hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri, Serikali iwekemipango itakayohakikisha wananchi wote wanaotumiaardhi wanapata hati miliki. Matokeo ya mipango hii nikwamba, viwanja vya wananchi vitawaletea tija kwakutumia hati zao kufikia fursa za kiuchumi. Pia Serikali itapatamapato ya uhakika; sasa wananchi watakuwa wanalipiakwa mujibu wa sheria (kodi ya kila mwaka). Swali langu, je,

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

Serikali imejipangaje kwa mwaka 2017/2018, kuhakikishalengo la utoaji wa hati miliki ili kuendana na kasi ya ongezekola idadi ya watu na mifugo inafanikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nne, Mipango Miji; pamojana kuipongeza Serikali kwa kuhakikisha Miji na Majijiyanapangwa. Naomba niishauri Serikali, kuhakikisha Miji yoteinakuwa na master plan ili kuondoa tatizo la kuwa miji holelaambayo haikupangwa halafu baadaye tunapotaka kujengamiundo mbinu tunalazimika kuhamisha wananchiwaliojenga kabla ya miji kupimwa na kusababisha hasarakwa Serikali, kulipa fidia pia ujenzi wa miundombinu ya maji,umeme na zinapotokea ajali za moto tunashindwa kuwafikiawananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tano, Ujenzi wa Nyumbaunaofanywa na National Housing na Kampuni ya WatumishiHousing: Pamoja na kulipongeza Shirika la Nyumba naKampuni ya Watumishi Housing kwa kujenga nyumba nakuwakopesha wananchi. Swali langu ni kwamba, je Mashirikahaya yana mkakati gani wa kujenga nyumba za bei nafuuzaidi ambazo wananchi wengi hasa watumishi wa ummawa kipato cha chini wataweza kumudu kununua? Ujenziwa nyumba za milioni 40 bado hii ni gharama kubwa sanakwa Watanzania ambao bado ni maskini hasa walewanaoishi vijijini na wafanyakazi wenye kipato cha chini hasawanawake ambao ndio walezi wa familia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sita, Mabaraza ya Ardhi naNyumba ya Wilaya, Mabaraza ya ardhi na Nyumba ya Wilayabado hayapo kwenye wilaya nyingi. Kwa hiyo, wananchiwengi wanakosa haki zao kutokana na mabaraza hayakutokuwepo. Pia utengenezwe utaratibu wa kuendesha kesiambao ni rahisi kwa wananchi kuweza kuandika maandikojuu ya matatizo hayo. Nauliza, Serikali ina mpango ganikuhakikisha mabaraza haya yanakuwepo katika kilaHalmashauri/Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, saba, Kodi ya majengo kwasasa inakusanywa na TRA, Serikali iweke utaratibu mzuri wa

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

TRA kuwafikia wananchi au kushuka kwa wananchi ilikukusanya kodi hizi na aidha, Serikali ifanye tathmini kwa kiasigani imeweza kukusanya mapato yanayotokana na kodi yamajengo ili kuona kama kuna mafanikio mara baada yakazi hii kukabidhiwa TRA badala ya Halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nane ni kuhusu mashine zakufyatua matofali. Pamoja na shukrani nyingi kwa Shirika laNyumba la Taifa chini ya Mkurugenzi Ndugu Mchechu, kutoamikopo ya mashine za kufyatua matofali kwa vikundi vyavijana katika Halmashauri. Je, Shirika la Nyumba la Taifalimejipangaje kwa mwaka 2017/2018 kuhakikisha kuwamikopo ya mashine za kufyatua matofali inatolewa kwavikundi vya akinamama ili kuweza kujipatia kipato nakujenga nyumba?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru na naungamkono hoja.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,niongelee Mabaraza ya Ardhi; mojawapo ya malengo yakuanzisha mabaraza haya ni kupunguza migogoro ya ardhikatika maeneo mbalimbali hapa nchini na pia kuharakishausuluhishi wa kesi za ardhi. Pamoja na malengo haya mazurimabaraza haya haiwezekani kutekeleza majukumu yake,ufanisi umekuwa mdogo kwa kukosa vitendea kazi,watumishi wachache wenye maslahi duni na kutopelekewafedha za kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto kubwa zaidiipo katika Mabaraza ya Kata ambapo ndipo kuna kesi nyingina hawapatiwi fedha za kuendesha shughuli zao. Serikalikuwaachia Halmashauri wawezeshe mabaraza haya ni kuzidikuyadumaza mabaraza haya kwani Halmashauri zenyewevyanzo vyake ni vya kusuasua na wakati mwingine hazinafedha kabisa kwani mahitaji ni mengi zaidi ya fedha hizo zaown source katika Halmashauri zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Serikali ifanyeyafuatayo:-

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

Kwanza, kuyawezesha mabaraza ya Ardhi ya Wilayaikiwa ni pamoja na kuongeza watumishi ili mabaraza hayayatimize majukumu yao kwa mujibu wa sheria; na

Pili, Wizara ichukue jukumu la kuyawezesha Mabarazaya Kata kuliko kuziachia Halmashauri, kwani mapato yaHalmashauri hayatoshelezi. Sehemu ya fedha za kodi ya ardhikatika Wilaya husika kiasi fulani zibaki ili kuyawezeshaMabaraza ya Kata katika Wilaya husika.

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kukushukuru wewe kwa kunipa fursa hii yakuchangia katika hotuba hii ya Waziri wa Ardhi. Pili,nampongeza Waziri pamoja na watendaji wake wote kwamashirikiano yao yaliyopelekea kutayarisha hotuba hii nakuiwasilisha kwa utaalam mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia hotuba hiinapenda kuchangia maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Usimamizi wa Ardhi, hivi sasanchi yetu inakabiliwa na ongezeko kubwa la watu. Watukutoka nje ya nchi yetu wanafika nchini kuomba umiliki waardhi kwa matumizi mbalimbali. Hivyo, Serikali yetu ni lazimaiendelee kuweka utaratibu mzuri wa ugawaji wa ardhi ilikuepuka kutoa fursa kwa wageni na kuwanyima wazawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, migogoro ya ardhiinaendelea kuongezeka siku hadi siku hasa kati ya wafugajina wakulima. Hii inatokana na ongezeko kubwa la wafugajina upungufu wa maeneo. Nashauri Serikali kuweka mpangomaalum wa kutofautisha maeneo ya wafugaji na yale yawakulima ili kuondosha migogoro hii ambayo inaendeleakupelekea watu wa makundi hayo kuuawa. Aidha, Serikaliiweke kima maalum cha ufugaji kuwa na kima maalum chawanyama ili kuepuka matatizo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwaulinzi wake kwetu sisi sote. Pili, naomba kumpongeza sanaMheshimiwa Waziri na Naibu wake wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kazi kubwawanayoifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli usiopingikakwamba Mawaziri hawa wanafanya kazi kubwa na nzurisana ya kuhakikisha wanaondoa kero zote zisizo za lazima,hasa migogoro baina ya wakulima na wafugaji. Miakamichache iliyopita tulishuhudia mapigano na uvunjifu waamani baina ya wananchi mbalimbali kwa sababu ya amakuingil iana kimipaka ama wasio na uwezo wengikunyang’anywa ardhi zao na matajiri wachache. Hata hivyo,tangu Mheshimiwa Lukuvi pamoja na Naibu wakeMheshimiwa Angelina Mabula waingie kwenye Wizara hii, kerohiyo imepungua kwa asilimia kubwa sana. Hivyo, naombatena kutumia fursa hii kuwapongeza sana kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku zote penye mafanikiohapakosi changamoto. Niendelee kuiomba Wizara hiikuendelea kupanga miji yetu na kutoa elimu juu ya matumizimazuri ya ardhi. Kwani ardhi haiongezeki bali watu ndiyowanaongezeka sasa ni wakati muafaka wa Serikali yetukuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha kunakuwa namatumizi sahihi ya ardhi ili kuliondosha Taifa letu lisiingiekwenye migogoro isiyo ya lazima huko tuendako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa tunayo Tume yaTaifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi na kwa mujibu washeria No.6 ya mwaka 2007 inayoipa Tume hii mamlaka yakupanga Ardhi kwa matumizi endelevu ili kuondoa umaskiniwa wananchi wetu. Basi niliombe Bunge lako Tukufu litengebajeti ya kutosha ili kuwezesha Tume hii kuweza kutekelezamajukumu yake kama ilivyokusudiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi sote tunafahamu kuwawanaochangia uchumi wa nchi hii kupitia kil imo ni

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

wanawake, lakini kwa bahati mbaya sana sheria za kimilazinamnyima mwanamke haki ya kumiliki. Katiba ya nchipamoja na Sheria ya Ardhi zote zinatambua mwanamkekumiliki ardhi lakini sheria za kimila zinamfanya mwanamkeku-access ardhi na siyo ku-own ardhi. Hii inafanyika kupitiamumewe au wazazi wake. Pale owner ambaye ni mume aumzazi anapofariki mwanamke huyu hunyang’anywa ardhihiyo kwa kuonekana ardhi ni mali ya mwanaume.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu katika hili nikwamba, tunaomba sheria hizi za kimila ziletwe Bungeni,zitazamwe upya ili ziweze kumpa haki mwanamke kumilikiardhi. Naomba pia nizungumzie kwa ufupi migogoro bainaya wakulima na wafugaji. Tatizo hili bado ni kubwa sanakatika maeneo mengi ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, ningeshauriSerikali iweke mpango mkakati ili kuweza kutenganishamaeneo ya kilimo na ufugaji. Pia, wafugaji wetu wapatiweelimu ya kutosha ili waweze kuacha kufuga kizamani baliwaweze kufuga kisasa na kibiashara zaidi. Hii itasaidia sanakupunguza migogoro isiyo ya lazima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, niipongeze Ofisi yaRais kupitia MKURABITA. MKURABITA wamesaidia sanakushirikiana na Halmashauri mbalimbali nchini kurahisishaardhi na kuwapatia wananchi hati za kimila. Hati hizizimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza migogoro yakimipaka baina ya wananchi. Vile vile, wananchi wamewezakutumia hati hizo kukopa fedha katika benki mbalimbali nakuwasaidia kufufua wajasiriamali. Hali hii imepunguza sanakwa kiasi kikubwa umaskini kwa wananchi wetu. Hivyo basi,naomba sana Wizara hii ya Ardhi iweze kushirikiana naMKURABITA ili wananchi wengi hasa wasio na uwezo wawezekumiliki ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nianze mchango wangu kwa maandishi kwanzakwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kufanyakazi hii ya kuwawakilisha wapiga kura wangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upimaji ardhi, ili kuionaTanzania ya viwanda ni lazima upimaji wa ardhi upeweumuhimu wa kutosha. Kwani hivi sasa uwekezaji wamashamba makubwa ni mgumu sana kwani vijiji vingi hivisasa bado havijaingia kwenye mpango wa matumizi boraya ardhi. Jambo linalofanya Halmashauri kukosa wawekezajikwenye mashamba makubwa ya mazao ya kilimo na ufugajiwa kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano katika Halmashauriya Liwale yuko Mwekezaji mmoja toka Japan. Huyu nimzaliwa wa Liwale, mwaka 2015 aliamua kurudi nyumbanina mradi wa kilimo cha alizeti lakini hadi leo anahangaikakupata shamba japo Halmashauri ilishafanya maamuzi yakumpatia ardhi mwekezaji huyu mzawa. Hatua ya uhaulishajiardhi ndio kikwazo kikuu kilichobakia katika kukamilishamradi huu. Namwomba Mheshimiwa Waziri, mwenyedhamana kuhakikisha Mwekezaji huyu anapata ardhi kwaustawi wa Wanaliwale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Serikali isiziachieHalmashauri shughuli za upimaji wa Vijiji ili kuviingiza katikamatumizi bora ya ardhi. Kwani Halmashauri nyingi hazinamapato ya kutosha kumudu kazi hii. Hivyo kuvifanya vijiji vingikukosa wawekezaji, kwani kigezo cha kwanza cha uwekezajivijijini ni kijiji kuwa na matumizi bora ya ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uhaba wa watumishi,Wizara hii ina tatizo kubwa sana la upungufu wa watumishihasa kwenye Halmashauri zetu. Jambo hili linaongeza makaziholela katika Halmashauri nyingi kutokana na uhaba waviwanja na Halmashauri kushindwa kupima viwanja kwawakati na jambo linaloongeza rushwa kwa ugawaji waviwanja na makazi yasiyopimwa. Mfano, katika Halmashauriya Liwale hatuna Afisa Ardhi mwenye taaluma ya kutosha

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

na hatuna wapimaji wa ardhi tunategemea toka katikaHalmashauri ya Nachingwea. Jambo hili linafanya gharamakubwa za upimaji wa viwanja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Gereza la Liwale limechukuaardhi ya wananchi tangu mwaka 1982 lakini hadi leowananchi wenye mashamba yaliyotwaliwa badohawajalipwa fidia ya mashamba yao. Naomba Wizara yaArdhi wakishirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani wamalizemgogoro huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile mgogoro wampaka kati ya wanakijiji cha Kikulyungu na Wizara ya Maliasilina Utalii. Ni bora sasa Wizara zote mbili wakashirikiana katikakutatua mgogoro huu. Mgogoro wa Kikulyungu na hifadhiya Selous ni wa muda mrefu sana.

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kodiya Ardhi, maelekezo yalitoka kwenye hotuba ya ardhikwamba wananchi wote wanaomiliki ardhi iwe imepimwaau haijapimwa lazima walipe kodi, sasa ardhi hiyo ambayohaijasajiliwa kisheria italipiwaje kodi? Je akilipia kodi atawezakutumia receipt hiyo kwa ajili ya dhamana yoyote? Serikaliifuate sheria ndiyo maana tulizitunga ambapo wananchihulipa kodi kwenye ardhi iliyopimwa tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Nyumba (NHC),Shirika hili limekuwa likifanya kazi nzuri kujenga nyumba zabiashara na makazi lakini madhumuni ya kuanzisha NHCyalikuwa ni pamoja na kujenga nyumba za bei nafuu ili kilaMtanzania aweze kuishi kwenye nyumba kwa haki. NHCimeshindwa kujenga nyumba kwa bei nafuu kutokana navifaa vya ujenzi kuwa na bei ya juu sana na kupelekea ujenzikugharimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nia ya Serikali ya Awamu yaTano ni kuwasaidia wanyonge, lakini kwa mtindo huu wabei za nyumba wanazoziita ni za bei nafuu za milioni 60 nimfanyakazi/Mmachinga yupi wa kawaida atakayewezakulipia bei hiyo? Ushauri, Serikali ishushe kodi kwenye vifaa

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

vya ujenzi kwa nyumba zinazojengwa na NHC ili wawezekuendeleza kazi nzuri wanayojitahidi kuifanya kwa ajili yaWatanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uhaba wa vitendea kazi nawataalam, pamekuwepo na uhaba mkubwa wa vitendeakazi na wataalam kwenye kitengo cha kupima ardhi ambakokunapelekea wananchi kwenda kutumia wapima ardhibinafsi na wanatoza pesa nyingi ambapo inapelekeawananchi wengi kutopima ardhi zao. Serikali inapoteza fedhanyingi kwa kutopokea kodi ya ardhi. Je, Serikali imetengafedha kiasi gani kwa ajili ya vifaa kwa nchi nzima ikiwa nipamoja na kuajiri wataalam wa kutosha kwa nchi nzima?Mfano pale Moshi Vijijini (Wilaya ya Moshi) hawana vitendeakazi kabisa hata usafiri haupo. Ni kwa nini hata kwa kuanziawasiwe hata na pikipiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, napendanimpongeze Waziri, Naibu Waziri na Watumishi wote waWizara kwa kazi nzuri wanayofanya kwa kujaribu kupunguzamigogoro ya ardhi. Nawashauri mjaribu kutatua matatizoyaliyobaki kuna uhaba wa wataalam na vifaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mategemeo yanguwatachukua maoni ya Upinzani na wayafanyie kazi kwafaida na maendeleo ya nchi yetu na wananchi wetu.

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kuhusu Mabaraza ya Ardhi; migogoro mingi ya ardhiinachangiwa sana na muundo wa Mabaraza haya ya Katahasa kutokana na kutawaliwa sana na rushwa. Hiiinasababishwa na kukosekana kwa mafunzo ya mara kwamara na hivyo wajumbe kukosa weledi katika kutafsiri sheriahata kufikia maamuzi jambo ambalo linaishia kugombanishajamii. Pia wajumbe wa mabaraza haya hata Makatibu waMabaraza kutokuwa na pato lolote kunapelekea vitendovya rushwa. Hivyo nashauri yafuatayo:-

(a) Kutolewe mafunzo ya mara kwa mara kwamabaraza haya (semina) ili kuwaongozea uelewa na uzoefu

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

Wajumbe wa Mabaraza ya Kata. Jambo hili litawawezeshakukabili kesi zinazojitokeza kwenye maeneo yao.

(b) Kutolewe ruzuku kwa ajili ya kuendeshamabaraza ya ardhi ya Kata, kukosekana kwa ruzukukunasababisha mazingira magumu sana ya uendeshaji nahivyo kujenga mazingira ya rushwa.

(c) Halmashauri zipewe nguvu/mamlaka yakuyavunja mabaraza haya pale inapothibitika kuwayamekiuka maadili. Kwa hali ilivyo hivi sasa, kuna urasimumkubwa katika kuchukua hatua kwa Mabaraza ya Ardhi.Jambo hili limepelekea matatizo yetu na bado wajumbehawa wanakuwa na jeuri kwa kuamini kuwa si rahisikuchukuliwa hatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Baraza la ardhi Wilaya,katika ngazi ya Wilaya Mabaraza yetu yanakosa wataalam.Mfano, katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, kunamrundikano mkubwa wa kesi kutokana na kukosaMwenyekiti wa Baraza. Mara kwa mara Wilaya imekuwainapata huduma ya Mwenyekiti ambaye haishi pale namatokeo yake anahudumia mara moja kwa mwezi na kwamuda usiozidi masaa sita. Hili limepelekea kuwepo kwa kesiza mipaka miaka miwili zisizofanyiwa maamuzi. Ombi,Baraza la Ardhi la Wilaya ya Ukerewe lipangiwe Mwenyekitiwa Baraza ambaye atakuwepo muda wote ili kupunguzamigogoro ya ardhi hasa ikizingatiwa kuwa eneo katikaWilaya hii ni dogo na hivyo kuwa na migogoro mingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vifaa vya upimaji;kuwe na utaratibu mzuri wa kupatikana kwa vifaa vyakupima ardhi ili mipango mizuri ya matumizi ya ardhiiwezekane.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mabaraza ya Ardhi, nilichangia katika hotuba ya Utumishina Utawala Bora, kwamba mabaraza haya tuyajengeeuwezo japo hata kutembelewa na Mwanasheria as anobserver ili tu kujionea proceedings kusudi upungufu

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

utakaobainika, itafutwe namna ya kuupunguza kwa kutumiaama semina au mafunzo ya muda mfupi kadri ya mazingirayao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Diaspora vs Umiliki wa Ardhi;lililoko tamko ambalo limeleta mkanganyiko hasa kwaWatanzania ambao wanaishi nje ya nchi lakini wamebakina utaifa/uraia wao kama Watanzania. Tafsiri ya watu wengiwalioko nje ni kwamba kwa Mtanzania anayeishi nje hastahilikumiliki ardhi kumbe iwekwe wazi kwamba ni haki kwaMtanzania kumiliki ardhi hata kama anaishi nje ilimradi tu niraia wa Tanzania kwa wale waliobadilisha uraia diasporaper se, utaratibu mbele ya safari uje utazamwe ilimradikufungua fursa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mafinga Mjini vs upimaji waardhi na uwepo wa Master Plan. Mji wa Mafinga unakuakwa kasi sana kutokana na biashara ya mazao ya misitu(mbao, nguzo, milunda na kadhalika.) Ukuaji huu umeletamahitaji ya ardhi iliyopimwa kwa kasi, hata hivyo uwezo(capacity) wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga kuendana naspeed hiyo umekuwa mdogo kutokana na uhaba wawatumishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi/ushauri, Wizara ifikiriekuwezesha upimaji/uandaaji wa Master Plan kwa Mji waMafinga na maeneo mengine ambayo ni miji ili kuepukanana ujenzi holela/squatters. Kwa jitihada zangu nilionana naProfesa Lupala ambaye kwa ushirikiano na ushauri wake,wanafunzi wa field wa Ardhi University watatusaidiakukusanya data ili baadaye Wizara kwa kushirikiana naHalmashauri yetu tutakamilisha Master Plan. Nimewasilishaombi la kupewa baadhi ya watumishi wa ilivyokuwa CDAhasa Maafisa Ardhi, Mipango Miji na Wapimaji kama jitihadaza kukabiliana na uhaba wa watumishi wa kada ya ardhi ilikufanikisha azma ya kupanga Mji wa Mafinga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango wa Matumizi Boraya Ardhi; naamini ni jambo la gharama kubwa lakini kamasehemu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

kukabiliana na migogoro ya wakulima na wafugaji, hatunanamna zaidi ya Wizara hii ku-take lead kwenye suala hiliambalo linagusa kilimo, maliasili na hata usalama wa nchi.Tukifanikisha jambo hili tutaondokana na malalamiko mengiya kila mmoja katika Taifa kuanzia kilimo, kufuga, hifadhi nahata uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutengwa maeneo yaIndustrial Clusters; wakati tunapoelekea uchumi wa viwandani muhimu kila Halmashauri kutenga maeneo kwa ajili yaviwanda na kwa kuwa uwezo wa kupima maeneo yote nimdogo, basi angalau tuanze na jambo hili kwa kushirikianana Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambayoimekuwa ikil isema jambo hili mara kwa mara katikakulitekeleza. Nashauri utolewe Waraka kwa kushirikiana naTAMISEMI kuziagiza Halmashauri kutenga hizo Industrial clusters.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza kabisa nimpongeze Rais wangu kwa kazi kubwaanayoifanya kwa kuwatumikia wananchi hasa walewanyonge. Pia nimpongeze Waziri wa Ardhi, Nyumba naMaendeleo ya Makazi pamoja na timu yake kwa hotuba yakenzuri iliyojaa matumaini makubwa yenye nia ya dhati nayenye kugusa na kuondoa kero zote za Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nishauri Serikaliiwape fedha Wakala wauzaji wa vifaa vya ujenzi vya beinafuu. Kama kweli Serikali inataka Watanzania wenye kipatocha chini wawe na uwezo wa kununua nyumba za bei nafuu.Basi tuwawezeshe Wakala wa vifaa vya Ujenzi. Pamoja nahayo, wakala wawe wanatoa elimu ya ufundi. Kwa hiyo,wakala wale wapewe uwezo ili wafike mkoani hadi wilayanikutoa elimu kwa vijana wetu wa Kitanzania ili vijana wetuwakishapata elimu waweze kujiajiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia niishauri Serikaliyangu, iharakishe na kutoa mafungu katika Wilaya ilimafungu haya yaendane na kasi ya upimaji na upatikanaji

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

wa hati kwa haraka. Kwa mfano, Wilaya ya Lushotowananchi wapo tayari kupimiwa na kupewa hati lakini kunaukiritimba katika idara ya ardhi. Kwa hiyo, tunaombaMheshimiwa Waziri afuatilie hili suala katika Ofisi ya ArdhiLushoto ili wananchi wangu wasinyanyasike pindi tuwanapotaka kupimiwa shamba na hao wananchiwameshajua umuhimu wa kupima ardhi na ukizingatia watuwanahitaji kupata mikopo kwenye mabenki. Pamoja nahayo kuna rushwa sana katika Idara ya Ardhi, maanawananchi wengi wametoa fedha zao ili wapate hati lakinifedha zinaliwa na hati hawapati. Naomba MheshimiwaWaziri aondoe tatizo hili katika Wilaya ya Lushoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niishauri Serikaliyangu Tukufu ili migogoro katika nchi hii iishe ni kupima ardhiyote ya nchi hii. Naamini maeneo yote yakipimwa na kilamtu akamiliki ardhi kihalali migogoro hii itakwisha. Pianiiombe Serikali yangu itenge mafungu ya kutosha yaendekatika kupima ardhi kuliko kutegemea wafadhili. MheshimiwaWaziri nimependa sana zoezi lile linaloendelea katika Mkoawa Morogoro, Wilaya ya Kilombero. Kwani ni mpango mzurina wenye tija. Kikubwa wapewe mafungu ya kutosha ilikuharakisha zoezi lile. Pamoja na kuwaongeza wataalam ilikumaliza zoezi kwa haraka na ikiwezekana ifikapo 2020 Ardhiyote ya Tanzania iwe imeshapimwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga hoja kwa asilimiamia moja.

MHE. RISALA S. KABONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kutoamchango wangu kwenye Wizara hii muhimu kwa utoajihuduma katika sekta ya Ardhi. Migogoro ya ardhi nchini nimikubwa mno hivyo naomba kuendelea kuishauri Serikali,kupitia Wizara hii ya Ardhi kuweka mpango madhubuti,kutenga maeneo ya wakulima na wafugaji ili kuepukamigongano hii ambayo haina tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Nyumba la Taifa(NHC). Kumekuwa na changamoto kubwa ya kodi nyingi

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

kwenye ujenzi wa nyumba za NHC, hivyo kupelekea nyumbahizi kuendelea kuuzwa bei ya juu. Kama Mjumbe wa Kamatiya Ardhi, Maliasili na Utalii nimekuwa nikitoa maoni yangukuhusu Wizara ya Miundombinu, Nishati na Madini,Maji naUmwagiliaji ili kuona ni namna gani ya kupunguza mzigokwa NHC ambao imekuwa ikiubeba na kugharamia kila kituna kufanya gharama hizi kwenda kwa mnunuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, gharama kubwa za upimajiwa ardhi; kumekuwa na malalamiko makubwa kwenyesuala la upimaji wa ardhi na hivyo kupelekea wananchi wengikutokupima ardhi zao. Ushauri, Wizara ya Ardhi ishirikishe sektabinafsi katika suala la upimaji. Maeneo mengi kwenyeHalmashauri zetu hayajapimwa hivyo kufanya ugumu wauwekezaji katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishauri Wizara ya Ardhikujikita kwenye mikoa mipya na inayokuwa ili kuendeleakupanga mipango miji ambayo ni tatizo kubwa sana katikanchi yetu, sambamba na kujenga maeneo ya uwekezajikuvutia wawekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Songwe ni mkoampya, nashauri Wizara itoe upendeleo wa kipekeekuendeleza Mkoa wa Songwe kwa kupima viwanja, kutengamaeneo ya uwekezaji i l i kuvutia wadau mbalimbalikuendeleza mkoa, sambamba na ujenzi bora wa nyumbaza kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: MheshimiwaMwenyekiti, pongezi kwa Waziri kwa hotuba nzuri pamojana watendaji wote wa Wizara kwa kazi inayoleta faraja kwawananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kazi nzuriinayoendelea kufanywa yapo mambo yanayohitajikakufanyiwa kazi kuwa nguvu:-

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

- Wizara kuongeza speed ya kupima ardhi yoteya Taifa hili. Kiasi cha asilimia 15% ni kidogo sana, eneo kubwabado halijapimwa.

- Kupima maeneo kwa ajili mifugo na malisho.Sheria ya Ardhi imeelekeza Waziri kutenga ardhi kwa ajili yamifugo na malisho, kuyagazeti na kuyalinda.

- Serikali itueleze ni maeneo kiasi gani na wapimaeneo ya malisho yametengwa na kupimwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuongeza speed yakuanzisha Mabaraza ya Ardhi katika Wilaya zote hapa nchini,ili kurahisisha usuluhishi wa migogoro ya ardhi. Mabarazatuliyonayo ni 53 tu, yanayofanya kazi ni machache sana.Mabaraza haya yawezeshwe kifedha ili yaweze kutekelezamajukumu yao vizuri. Pia Serikali iwezeshe Wajumbe waMabaraza kwa kuwapa posho wanapokaa wafanye kazi yaovizuri. Serikali/Wizara kufanya follow-up kwa Maafisa Ardhipopote walipo watekeleze majukumu yao kwa kuwajibikana kuuza ardhi mara mbili (double allocation).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Viongozi wa Vijiji wapeweelimu wafuate Sheria ya Ardhi katika kugawa ardhi yawananchi. Viongozi wanakula rushwa wanauza maeneomakubwa bila kuitisha mikutano ya wananchi. Waziri atoetamko hapa Bungeni lakini pia semina kwa viongozi wa Vijijini kiasi gani cha ardhi kinaweza kuuzwa na viongozi wa vijijina kiasi gani hawaruhusiwi. Wafugaji wanapokelewa vijijiniwanatoa fedha nyingi, wanapewa maeneo ya kufugiawakati wananchi wengine hawana habari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima kama Taifa tuwazemiaka 100 ijayo mbele. Leo tunajivunia Tanzania tuna ardhikubwa, tusipopanga matumizi bora na hii ardhi tutakosaardhi kwa matumizi muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mashirika na Taasisizinazojenga majengo na nyumba za makazi wajengenyumba kwenda juu (flats) na sio kwenda chini.

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

Mheshimiwa Mwenyekiti, wawekezaji wa miradimbalimbali wapewe ardhi kuendana na mradi wao au eneolinalofaa kwa mradi huo. Maeneo ya kilimo yabaki kwa kilimo,maeneo ya malisho yabaki kwa malisho na maeneo ya ujenziyasiwe ya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo la uanzishwaji wa mijikiholela bila utaratibu; maeneo mengi kila leo miji mipyaimeanzishwa kando kando ya barabara, hakuna maelekezoyoyote, hakuna udhibiti, hayo yanakuwa makazi holela.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Watumishi Housewaongeze speed ya kujenga nyumba za watumishi, speedyao ni ndogo sana. Wafike kwenye wilaya mpya ikiwepoKaliua wajenge nyumba za watumishi kusaidia makazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Nyumba (NationalHousing) waliahidi kuja Halmashauri ya Kaliua kujenganyumba tangu mwaka 2016. Napenda kujua ni lini watafikana maeneo tulishayatayarisha ya kutosha na yapo mjini.

MHE. DEVOTA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nichangie hotuba ya Waziri kwa maandishi kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nimpongezeWaziri na Naibu Waziri wa Ardhi kwa kazi nzuri wanayoifanyakatika kuhakikisha ardhi inawanufaisha Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo baadhi ya mamboambayo lazima tuseme ili kusaidia kusukuma Wizara hiimuhimu kwa Watanzania. Ofisi za Ardhi za Kanda, mpangohuu ulipoanzishwa ulikuwa na nia ya kusogeza hudumakaribu na wananchi. Kanda ya Kati, Mkoa wa Morogorondipo yalipokuwa Makao Makuu na Wizara/Serikali ilijengaOfisi za Ardhi za Kanda kwa gharama kubwa. Ofisi hiizimesaidia sana chini ya Kamishna imepunguza kwa kiasifulani migogoro na malalamiko ya ardhi hususan Mkoa waMorogoro.

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri amesema katikahotuba yake, Serikali imebadilisha/kuhamisha Ofisi ya KandaMorogoro na kuhamishia Dodoma, hii si sawa. Kwa kipekeeMkoa wa Morogoro utazamwe kwa namna nyinginekutokana na kukithiri kwa migogoro ya ardhi ya mara kwamara ambayo imegharimu maisha ya watu kwa kusababishavifo na majeruhi hasa katika Wilaya za Kilosa, Kilombero,Mvomero na Morogoro Vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukosefu wa vifaa vyakupimia ardhi; Maafisa Ardhi wanafanya kazi katika mazingiramagumu ambapo unakuta mfano, Mvomero ina kifaa kimojatu cha kupima, hali inayosababisha ucheleweshaji wa upimajiwa ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kero ya bomoabomoa; katika vitu vinavyolalamikiwa na wananchi niuvunjaji wa nyumba za wananchi wanaojenga kwa jashokwa vibali vyote kwa kuzingatia masharti mbalimbali hasawaliopo kando ya barabara ambapo hivi sasa Serikali kupitiaTANROAD wanakusudia kuvunja nyumba za wananchi nabarabara ya Dar es Salaam, Morogoro kwa zaidi ya mita 20kila upande.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hizi zinafanyaje kaziArdhi na Miundombinu? Kwa nini kusiwe na mpango wakuzuia wananchi kujenga badala ya kusubiri wananchiwajenge kisha waje kubomoa. Yapo maeneo ambayowananchi nao wamepelekewa huduma muhimu kama maji,umeme na kadhalika

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mgogoro wa ardhi ya vijiji-Kakonko; Vijiji vya Nyakayenzi naKiga vina mgogoro wa mpaka wa muda mrefu kwenyebonde la Mto Ruhwiti. Mgogoro huo ulipelekea Kijiji cha Kigakuhodhi ardhi ya Nyakayenzi kwenye mpaka wa vijiji hivyo.Mheshimiwa Waziri alipokuja Kigoma, akiwa Kibondoviongozi wa Nyakayenzi walifanikiwa kuonana na kuongeana Waziri aliagiza DC ashughulikie kutatua mgogoro huoambao maamuzi aliyotoa hayakuwaridhisha wananchi wa

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

Kijiji cha Nyakayenzi maana wananchi wa Kiga walipewahaki ya mashamba kwenye eneo la Nyakayenzi. Wananchiwa Nyakayenzi walitaka mashamba hayo yaendeleekutambuliwa kama ya Nyakayenzi huku yakilimwa nawananchi wa Kiga kwa mujibu wa ramani na mipaka yavijiji hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, walikata rufaa kwa WaziriBunge lililopita na kuwasilisha kwa Naibu Waziri wa Ardhi.Ushauri, naomba Serikali/Wizara isimamie na kumalizamgogoro huo kwa kujibu au kushughulikia rufaa hiyo. Badowananchi wa Nyakayenzi wana imani na Wizara kuwa hakiitatendeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro wa ardhi kambiya JKT Kanembwa na Vijiji; kumekuwepo na mgogoro katiya eneo la Kambi ya JKT Kanembwa na Kij i j i chaKazilemihunda kwani mipaka imekuwa ikibadilika mara kwamara kwa Kambi kuongezea eneo na kuingia katika ardhiya Kijiji cha Kazilamihunda. Ushauri, maeneo hayo yapimwekwa kushirikisha Serikali ya Kijiji cha Kazilamihunda na uongoziwa Kambi ya Kanembwa JKT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ardhi ya wananchiiliyochukuliwa Kambi ya Wakimbizi-Mtendeli. Kuna wananchiwa Kasanda walionyang’anywa ardhi ili kupisha wakimbizikwenye Kambi ya wakazi Mtendeli. Baada ya ardhi hiyokuchukuliwa wananchi hawakupewa ardhi nyingine kwamatumizi ya kilimo na mifugo. Ushauri, wananchi haowapewe ardhi nyingine pamoja na fidia kwa mazaoyaliyoharibika hasa eneo la juu ya Kambi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri juu ya bomoabomoa, kumekuwepo na bomoa bomoa ya nyumbazilizokwishajengwa hasa zile ambazo zimekamilika ama kwakigezo cha nyumba, kujengwa eneo lisilostahili kama vilehifadhi ya barabara, open space, hifadhi ya Mto, Ziwa, Bahari,na kadhalika. Mjenzi anakuwa na documents zote za ardhi,kama vile ramani, kiwanja na amelipia na kadhalika. Ushauri,kwa nini ardhi wasisimamie kuhakikisha hawatoi kibali cha

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

ujenzi bila kuwasiliana na Wizara ya Miundombinu naMazingira kujiridhisha kuwa eneo hilo linaruhusiwa kujengwanyumba kuliko kuacha ijengwe kisha inabomolewa.

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na mikakati mingi mizuri ya Wizara ya Ardhi, badokuna changamoto nyingi katika Halmashauri zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti hii ungewekwamkakati wa dharura wa kuhakikisha inawapimia mapemakabla hawajajenga wawe na hati ili kuondoa migogoro yafidia kupunjwa na kunyanyasa wanaopisha ujenzi wa miradiya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, migogoro ya ardhi Manispaaya Mpanda; Kata nyingi za Manispaa ya Mpandahawajapimiwa je, ni lini sasa Wizara kupitia Ofisi za Kandaitaharakisha kupima maeneo haya ili wananchi wapate hatiambazo zinaweza kuwasaidia kukopa fedha katika benki.Kata ya Ilembo, Misunkumilo, Kata ya Kakese, Kata yaMwamkulu na Kata ya Kashamili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara isisubiri watuwajenge nyumba zao nzuri halafu inakuja kubomoa nakuwalipa fidia ndogo na za kucheleweshwa. Katika Bajetihii Mheshimiwa Waziri ameonesha wazi kuwa na dhamiraya kutatua kero ya fidia kwa kuanzisha Bodi ya Fidia hiiikasimamiwa vizuri itasaidia vizuri na kuondoa kero zamalalamiko nchini, hii nadhani ipangiwe mkakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro wa ardhi kati yaJeshi na wananchi wa Kata za Mpanda hotel na Misunkumilo;naomba bajeti hii ione namna ya kutatua mgogoro huu niwa muda mrefu sana .

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupunguza gharama zauuzaji nyumba za NHC Manispaa ya Mpanda; mpaka sasahakuna faida iliyopatikana kutokana na uuzaji wa nyumbahizi, je hamwoni kuendelea kuziacha nyumba, kama

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

gharama haziwezi kupungua basi zipangishwe kwawatumishi wa Serikali kwa sababu kuna uhaba wa nyumba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miundombinu katikanyumba hizo bado haitoshi, barabara, hospitali, shule,masoko. Hivyo kwa kuzingatia ukosefu wa miundombinu hiindio inasababisha watu kushindwa kuhamia kule.

MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kuzungumza juu ya mgogoro wa muda mrefu washamba la Malonje. Serikali inatakiwa kumaliza mgogoro huuambao Serikali imekuwa ikipiga danadana kila siku. Hakunajambo linaloweza kushinda Serikali kwani tunashuhudia jinsiMheshimiwa Waziri Lukuvi anavyojitahidi kutatua migogorombalimbali katika nchi hii na mara ya mwisho aliwaahidiwananchi wa Vijiji vinavyozunguka shamba hilo kuwaatakuwa Waziri wa mwisho kuzungumzia mgogoro huo.Hivyo wananchi walishajenga imani kubwa sana kwake kwakauli aliyoitoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamwomba aumalizemgogoro huu. Kama kuna makosa yaliyofanywa na viongoziwa Wilaya, Mkoa ndiyo maana yote hayo yamefikishwakwake hakuna sababu tena ya kukwepa jambo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro wa ardhi kati yawananchi wa Tarafa ya Kipeta na hifadhi ya akiba ya UwandaGame Reserve. Tunaomba mipaka ichunguzwe upya kwaniuwekaji wa mipaka ya hifadhi hiyo imeingilia maeneo ya Vijijijambo linalofanya wananchi wa maeneo hayo kukosa ardhiya kilimo na mifugo, tunaomba Serikali ifuatilie jambo hiliharaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa vijiji hivyowapo hapa Dodoma kutaka kuonana na Mheshimiwa WaziriLukuvi, pia ikishindikana kumwona Mheshimiwa Waziri,wamwone Mheshimiwa Rais. Tunaomba wasikilizwe (ni juuya shamba la Malonje).

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kuna tatizo kubwa kwenye Mabaraza ya Ardhi, Vijiji na Kata,ni vurugu na mambo ya ajabu. Mfano, hukumu inampaushindi mtu kwa kuwa alileta mashahidi wengi kuliko upandewa pili. Wananchi wanazungushwa sana katika rufaahawapewi hukumu mpaka anakata tamaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeruhusumakampuni binafsi ya upimaji waweze kushirikiana naHalmashauri zetu kibiashara/Huduma. Watendaji waHalmashauri bado hawataki kushirikiana na Makampuni hayomfano ni Halmashauri ya Biharamulo. Tunaombauharakishwaji wa utatuzi wa migogoro mikubwa ambayonimeorodhesha tayari. Mfano Mgogoro wa Jeshi na Kijiji chaRwebya unasumbua sana.

MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,niruhusu nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwamageuzi makubwa aliyoyafanya na anayoendelea kuyafanyakatika Wizara hii. Namtakia kila la kheri na ni matarajio yangukuwa tutafika mahali pazuri pa kuwa na Wizara na Taasisizinazowajibika ipasavyo. Katika sekta hii muhimu sana kwamaendeleo ya kijamii katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi na dirahizi naomba nimshauri Mheshimiwa Waziri, kupitia kwa kinabila hiyana hotuba ya Kambi ya Upinzani na kuyafanyia kazimengi ya mapendekezo yake. Sote katika Bunge lako hiliTukufu tupo kwa maslahi ya wananchi wetu na si vinginevyona hivyo tukishirikiana itapatikana tija zaidi nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nimshauriMheshimiwa Waziri, kushughulikia kwa kina suala lakuwapatia na kuwahakikishia watumishi wa umma nchinimakazi bora na ya uhakika katika maeneo mbalimbali. Hivisasa NHC inaonekana kuweka mkazo zaidi katika kujengana kuuza badala ya kupangisha hata kwa watumishi waumma.

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

Mheshimiwa Mwenyekiti, watumishi wa umma kwaasili yao si watu wa kudumu katika maeneo yao ya kazi balikatika maeneo yao ya kuzaliwa. Hivyo msisitizo unapowekwakatika kuwauzia nyumba watumishi panatengenezamazingira ya kuwafanya watumishi wa umma, kutaka kubakimaeneo waliyopangiwa na wakati mwingine kutumia hatanjia chafu kuhakikisha kuwa hawa hawahamishwi. Hali hii sizuri kwa kujenga kada ya watumishi wa umma waadilifu nawalio tayari kutumikia popote nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata Wabunge wako wenginikiwemo mimi mwenyewe, tumehangaika kwa zaidi yamwaka na nusu sasa kutafuta makazi ya kukaa hapa hapaDodoma, Makao Makuu ya Serikali. Hii ni dalili wazi kuwaWizara hii na Serikali kwa ujumla haijatoa kipaumbele auhaijajipanga ipasavyo katika eneo la makazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianzena kuwapongeza, Waziri Mheshimiwa Lukuvi, Naibu WaziriMheshimiwa Angelina Mabula, Katibu Mkuu na Watendajiwote wa Wizara kwa kuleta bajeti hapa Bungeni ili tuijadili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Migogoro ya Ardhi,niipongeze Wizara na Waziri mwenye dhamana ya Wizarahii kwa kuendelea kutatua migogoro mingi nchini ikiwemoya wakulima na wafugaji. Ni kwa nini Serikali isingetengemaeneo ya wafugaji peke yake na yakaainishwa nayakawekewa miundombinu kwa ajili ya kuwezesha wafugajikutohama hama?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo ipomigogoro inayowahusu Maafisa Ardhi katika Halmashaurizetu. Tunashukuru hata hivi Mheshimiwa Waziri na NaibuWaziri wanafanya juhudi kubwa sana kuwasaidia wanyongewaliokuwa wakipokonywa ardhi zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wanagawiwaardhi ya eneo moja zaidi ya watu wawili na kusababisha

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

usumbufu mkubwa sana, lakini huwa tunapata tabu sana,Afisa anayeharibu Halmashauri moja badala ya kubadilishaanahamishiwa eneo lingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upungufu wa Wataalam waArdhi; Halmashauri zetu nyingi nchini bado zina upungufumkubwa na kunasababisha wananchi wengi kupatausumbufu mkubwa wanapotaka kupimiwa ardhi au kupatahati na sasa hivi na hili la vyeti feki nalo limechangia kwakiasi kikubwa sana kuendelea kuwa na idadi ndogo yawafanyakazi. Ni vizuri Serikali ikaweka utaratibu wa kujuanafasi hizi mapema ili kusaidia utendaji katika Halmashaurizetu na kupunguza kero kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mipango Miji, ni kwa nini mijiyetu mingi haijapangwa, je kazi ya Maafisa Mipango Miji ninini? Kumekuwa na mwingiliano mkubwa sana wa shughulikatika miji yetu kama vile hakuna wataalam. Ushauri wanguni vizuri Maafisa Mipango Miji wangekuwa wanasimamia ilemichoro iliyopangwa au kama miji haujapangwa basiwasigawe viwanja kabla ya kupitishwa michoro. Hata hivyo,kuna maeneo ambayo hayajapimwa ungekuwepo utaratibumaalum ili kuweza kusaidia jamii, kwa sababu kuna baadhiya maeneo hayafikiwi kihuduma, wananchi wamekuwawakipata mateso makubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu NHC, niipongezeSerikali kwa ajili ya kazi nzuri inayofanywa na Shirika hili, lakinituombe majengo haya yajengwe hata katika miji midogosababu hata wafanyakazi wanapata shida sanawanapohamishiwa mikoani. Ni kwa nini Halmashauri zetuzisitenge maeneo na kuingia ubia nao ili iweze kusaidiaupungufu uliopo katika Halmashauri zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, hayamashirika yanayojenga nyumba kwa ajili ya Walimu kamaWatumishi Housing nao wangefika katika Halmashaurizilizopo pembezoni ambako kuna matatizo makubwa sanaya nyumba za watumishi wakiwemo Walimu hata kama ya

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

kawaida sana ya vyumba vitatu au viwili ili kuyafanyamaeneo hayo pia wafanyakazi waweze kuishi kama mijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, malalamiko ya ukarabati wanyumba za mjini, naomba kujua je kuna sheria yoyoteiliyotolewa na Serikali nyumba za kati kati ya mji zisikarabatiwezijengwe maghorofa. Sababu kunakuwa na malalamiko kwawananchi wa Manispaa ya Iringa kutopatiwa vibali vyakukarabati nyumba zao hata kama ni magofu nakusababisha majengo mengi kuwa na hali mbaya sana.Sababu hawana uwezo wa kujenga maghorofa sasatunaomba Serikali itupatie ushauri. Sasa hivi hakunawawekezaji kabisa kutokana na hali ya uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. DKT. CHRISTINA G. ISHENGOMA: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungualiyeniwezesha leo kupata nafasi na kuweza kuchangiaangalau kwa maandishi. Pili, nichukue nafasi hii kukupongezakwa kazi nzuri, pamoja na Mheshimiwa Spika, na Naibu Spikana Wenyeviti wenzako. Nizidi kuwapongeza MheshimiwaWaziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Wataalam na watendajiwote kwa kazi nzuri wanayoifanya, nawaombea Munguwasonge mbele kwa kazi yao nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sote tunajua kuwaMorogoro ni mkoa ulioweka historia, kwa migogoro yawafugaji na wakulima. Nichukue nafasi hii kuipongeza Serikalikwa kazi nzuri inayoendelea nayo, ya kupima, kurasimishana kutoa hati miliki kwa wananchi. Upimaji wa ardhi nakuwamilikisha wananchi kwa kupewa hati ya kumilikisha ardhihii ni mkombozi wa kutatua migogoro. Naomba nimwambieMheshimiwa Waziri na Naibu Waziri, upimaji wa vijiji namashamba pia ni utatuzi tosha wa migogoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ilifikia wakulima kushindwakwenda mashambani na hasa Mbigili, Kilangali na sehemuza wakulima wa Mpunga Wilayani Kilosa kama

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

Mabwerebwere. Kundi kubwa la wanawake, ambao ndiowakulima wakubwa, kweli, hali ilikuwa mbaya mpakamapigano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mifugo pia ilifikia wakatiikakatwakatwa mpaka wengine kufa. Mifugo ilihamia katikaWilaya zote za Mkoa wa Morogoro, Kilosa, Gairo, Mvomero,Morogoro Vijijini, Morogoro Manispaa, Kilombero, Malinyi naUlanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru na kuipongezaSerikali kwani baadhi ya Mawaziri walifika na hasa Mvomerona Kilosa ili kuona na kutatua migogoro hii kwa kusaidianana Uongozi wa Mkoa na Wilaya, nawapongeza. Tatizokubwa lilikuwa ni kutafuta malisho na maji katika ardhi iliyowazi ambayo haijapimwa kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru na kupongezaSerikali ya Uingereza Sweeden na Dernmark kwa kupitiakwenye Mashirika yao ya Maendeleo DANIDA,SIDA,na DFID,kwa ufadhili wao wa upimaji ardhi mpaka kutoa Hatimilikina kujenga Masjala ya Ardhi katika Wilaya ya Kilombero,Ulanga na Malinyi. Naamini, upimaji kiasi chini ya Serikaliumefanyika Mvomero na kidogo Kilosa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upimaji ardhi ni gharama,Nashauri na kuiomba Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi,fedha ziendelee kutafutwa, kama tulivyosaidiwa na nchi rafikizetu kwenye mradi huu wa Kilombero, Ulanga na Malinyi,kusudi wananchi wote katika Wilaya hizi, kila mmoja apimiweardhi yake na kupewa hati miliki. Wakati mwingine tunashauri,taasisi Mheshimiwa Waziri, hata maeneo ya taasisi zetuzikapimwa na kupewa Hati miliki za maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali yetu ionekuwa upimaji ardhi na matumizi bora ya ardhi ni muhimukwa utatuzi wa migogoro ya ardhi. Nishauri maeneo yote yawilaya zote za Morogoro yapimwe na wananchi wapewehati miliki zao. Matumizi bora ya ardhi kwa kuchanganua niwapi kilimo, mifugo, ifanyike na kadhalika. Hii itasaidia

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

wananchi na kwa kuambatanisha na miundombinu kamamabwawa na majosho. Sasa hivi tumetulia kwa sababumalisho yapo baada ya mvua kunyesha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ikiwezekana Mikoa/Wilaya zote zenye migogoro, ardhi yao ipimwe. Pia Hati milikiinaweza kutumika katika kuomba mikopo. Naomba benki(CRDB, NMB, NBC) wazipokee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Nyumba (NHC)pamoja na Watumishi Housing, natoa pongezi kwa Serikalikwa kazi hii, liko tatizo nyumba hizi ni ghali. Nashauri, Serikaliitathmini tena ili gharama zipungue, wananchi na hasa vijanawapate pa kuishi na kumudu maisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wataalam wa ardhi niwachache, kwa hiyo, nashauri kwa kupitia Chuo Kikuu chaArdhi, Chuo cha Tabora na Morogoro udahili uongezeke.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkonohoja.

MHE. DESPERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. Pia nampongeza Waziri, Naibu Waziri,kwa kuchapa kazi, wamejitahidi kufanya kizalendo nawametatua migogoro mingi sana. Wananchi wamekuwasasa na imani na Serikali yao kuhusu namna migogoro yaardhi inavyoshughulikiwa. Wito wangu waendelee kufanyakazi na kusimamia haki za wananchi katika masuala yaardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Nkasi Kusini linamashamba na hifadhi nyingi za kufanya wananchi kukosaardhi ya kilimo. Nashauri Wizara kuona kama mashambayaliyopo Jimboni yanaendeshwa kwa ufanisi au la ili kuwezakutoa uamuzi wa kuongeza ardhi kwa wananchi.

- Shamba la Nkundi l inalotumiwa naMheshimiwa Mzindakaya. Wananchi jirani hawana ardhi ya

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

kutosha na sehemu kubwa halitumiki ipasavyo lipunguzwewapewe wananchi wangu.

- Shamba la Kalambo Ranchi lina ukubwa wahekta 23,000, lakini lina ng’ombe 710 tu. linatumika chini yakiwango eneo kubwa halitumiki. Lipunguzwe wapewewananchi wangu.

- Shamba la Milundikwa kwa eneo walilopewaJKT mwaka jana ni kubwa lote halitumiki na wananchi wengiwanalima ndani bila kuruhusiwa kwa sababu ya ukosefu waardhi ya kilimo, lipunguzwe wapewe wananchi.

- Shamba la China linatumika lakini tuone kamalazima lote liwe kwa mtu mmoja wakati watu wengihawana ardhi ya Kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mamlaka ya Misitu ya TFSimepora ardhi ya Kijiji cha Kasapa na kufanya kijiji kukosakabisa eneo la kulima. Naiomba Wizara ione namna yakuwasaidia wananchi wa kijiji hiki. Maeneo yao ambayowamekuwa wakilima miaka yote, tangu miaka ya 1956yametwaliwa na kufyeka mazao yao. Wizara inisaidie kutatuamgogoro huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Vij i j i vya King’ombe,Mlambo, Ng’undwe, Mlalambo, Nkata na Kasapa vinadaiwakuwa Ndani ya Mbuga ya Lwanfi Game Reserve, kwa hiyo,wananchi hawana ardhi na wanapata usumbufu mkubwa.Kamati ya Migogoro ya Ardhi itembelee kuona shida iliyopo.

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga hoja mkono kwa asilimia mia moja. Baada ya hayo,natoa pongezi kwa Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, KatibuMkuu na watendaji wote wa Wizara na taasisi husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ardhi ni rasilimali muhimukwa kilimo, ufugaji, viwanda, misitu, hifadhi na kadhalika,hatimaye kwa kutuhifadhi sote tutakapokufa. Bahati mbayasana, Mungu alishamaliza kuumba ardhi. Kwa namna hii

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

lazima usimamizi wa ardhi ufanyike kwa uangalifu mkubwasana. Mpango wa matumizi bora ya ardhi unahitajika sanana Serikali ina wajibu wa kuziwezesha na kusimamiaHalmashauri zote nchini, vijiji vyote na mpango wa matumizibora ya Ardhi ya Vijiji chini ya Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka1999.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto, yakomashamba makubwa katika maeneo mbalimbali ambayohayaendelezwi vizuri na baadhi kuwa mashamba pori. Kwakuwa baadhi ya mashamba haya; umiliki umebatilishwa naHati kufutiwa, ni lini sasa mipango ya matumizi ya mashambahayo itafanyika? Ushauri wangu ni kwamba, hayo mashambayagawiwe vyama vya ushirika na vijiji, badala ya kugawakwa watu binafsi. Kwani ni wengi na itasababisha migogorozaidi, mbaya zaidi wananchi wengine huuza maeneowaliyogawiwa. Katika mashamba hayo yatengwe piamaeneo ya uwekezaji wa viwanda, ujasirimali wa vijana,shule, vituo vya afya na mahitaji mengine ya shughuli za Jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maamuzi yaliyofanywamwaka 1973 kumilikisha mashamba makubwa ya kahawakwa Vyama vya Msingi vya Ushirika huko Kilimanjaro, tunaonafaida zake hadi sasa. Baadhi ya wawekezaji wanalipa kodiya pango kwa Vyama vya Ushirika, lakini pia wanatoamaeneo kwa shughuli za jamii. Muhimu zaidi ni kwambabado wanaendeleza zao la kahawa. Ombi, wawekezajihawa washauriwe kuelimisha jamii inayowazunguka jinsi yakuendeleza zao la kahawa kupitia CSR –Corporate SocialResponsibility.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. ENG. STELA M. MANYANYA: MheshimiwaMwenyekiti, awali ya yote nampongeza kaka yanguMheshimiwa William Vangimembe Lukuvi, Waziri; na Naibuwake Mheshimiwa Angelina Mabula kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu ni moja tu kwaMheshimiwa Waziri. Nyasa ni Wilaya changa, lakini ina

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

potential nyingi hasa beach. Tunaomba msaada wa ruzukuya upimaji wa ardhi ili kuipanga Wilaya yetu vizuri. Gharamaza kodi za ardhi ni kubwa hasa kwa taasisi za Serikali ambazozimehitaji maeneo makubwa na ulipaji wa ardhi hizo niSerikali yenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini maeneo ya Serikalikama Vyuo mfano (UDOM), Sokoine na Vyuo vingine kamaFDCs ambavyo maeneo hayo ni muhimu kwa ajili ya shughuliza vitendo kwa nini yasimilikishwe na kupewa hati kwagharama za upimaji tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Wazirialifikirie hilo kwa niaba ya ombi la Wizara ya Elimu, Sayansina Teknolojia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na nawasilisha.

MHE. SILAFU J. MAUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kutoa pongezi za dhati kwa Waziri, Naibu Waziri,Katibu Mkuu na Watumishi wote. Kwa umakini wao ndaniya Wizara hii, kwa matokeo mazuri hadi sasa kwa wananchina kuwapa matumaini ndani ya changamoto zao za ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na changamotonyingi za ardhi kwa wananchi wetu na kupelekea miji yetukuwa na majengo ndani ya ujenzi holela na maeneoyasiyopimwa yanaleta magomvi kwa wananchi wetu,mandhari ya mji itakuwa siyo nzuri kiusalama na malalamikoya wananchi hayapati ufumbuzi kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamwomba Waziri kwaumahiri wake aone uwezakano wa kuteua Kamati zaKugawa Ardhi ngazi ya Wilaya haraka iwezekanavyo, kwaniMkoa wa Rukwa unachipukia kukua na wananchi kuwa nakasi ya maendeleo yao na Wilaya moja (Nkasi) tu ndio yenyeKamati ya Kugawa Ardhi. Wilaya ya Kalambo naSumbawanga tushughulikiwe, hali mbaya hivi sasa, miji yetuitashindikana kupangiwa hapo baadaye.

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Rukwa upopembezoni, lakini kwa mujibu wa taarifa ya Halmashaurizilivyotekeleza katika kutoa Hati miliki, Vyeti vya Ardhi ya Kijji,Hati Miliki za kimila. Ukurasa Na. 109 umedhihirisha kwenyejedwali Na.4 kwa Mkoa wa Rukwa haujafanya vizuri nikutokana na rasilimali watu na rasilimali fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Mkoa wa Rukwakuangaliwa kwa ukaribu zaidi, tukifahamu wazi kuwa tupompakani mwa nchi mbili (Zambia na DRC) ni vematukavihakikisha vijiji vyetu na wenye maeneo kuwa nahatimiliki. Ni vema ukawekwa kipaumbele kwa mikoa yapembezoni inayopakana na nchi mbalimbali, kupimiwa ardhiyao na kuipanga, kuepukana na migogoro ya ndani na nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuona umuhimuwa kupatiwa kibali cha kuajiri Maafisa Ardhi wa kutoshakwenye Halmashauri na vitendea kazi kulingana na mahitajiya nchi kwa hii bidhaa adimu ya ardhi, kwa kila sekta. Nivema Wizara ikaweka malengo ya utekelezaji kwenyeHalmashauri na kufuatiliwa na kutathminiwa ili kila mmojaaweze kuwajibika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkonohoja.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Wizara hii, badonapenda kuikumbusha Serikali kupitia Wizara hii kumalizakulipa fidia Kurasini. Tathmini imefanywa muda mrefu lakinihadi leo wananchi wale hawajalipwa fidia hiyo pamoja namapunjo yao. Fidia inapokaa muda mrefu huleta matatizokwa raia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziriawahimize NHC kuharakisha makubaliano yetu ya kujengajengo la biashara ya fenicha pale Keko.

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kumekuwa na wimbi kubwa sana la migogoro ya ardhi hapanchini; migogoro ya wakulima na wafugaji na migogoro hiiinasababishwa na wawekezaji hasa maeneo ya hifadhi

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mzuri ni Kata yaKyanyari, wananchi wanateseka sana wamefukuzwa kwenyemakazi yao kwa lengo la Serikali eti kupisha hifadhi.Wananchi hawa toka wamefukuzwa wanahangaika sanahadi sasa hawana makazi maalum ya kuishi na hawanamatumaini ya maisha yao, je, Serikali ina mpango ganikuhakikisha inawapa makazi ya kuishi wananchi hawapamoja na mashamba (maeneo) kwa sababu maeneowaliyofukuzwa ndiyo yaliyokuwa yanawasaidia kwa makazipamoja na mashamba lakini kwa sasa hawana sehemu yakulima na wananchi hawa walitegemea sana kilimo ili kuinuakipato cha maisha yao ya kila siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwaondoa kwenyemaeneo yao kumewaathiri sana wananchi wa Kata yaKyanyari wanateseka na kutia huruma. Napende kuishauriSerikali iwe inawatengea maeneo mbadala kabla yakuwahamisha wananchi kwa lengo la kupisha hifadhi tofautina sasa kuwahamisha wananchi bila kuwatengea maeneokwani wanapowaondoa bila kuwatengea maeneowanategemea wananchi hao watakwenda wapi? PiaHalmashauri husika ihakikishe inasimamia na kutetea hakiya wananchi wake katika maeneo husika.

MHE. RUTH H. M0LLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru Mungu kwa kunipa nafasi ya kuchangia hoja iliyopomezani. Pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Waziri pamojana Makamu wake, ninayo machache ya kushauri upimaji waardhi yote ya Tanzania ambayo ni 950,000 square kilometres,matumizi yake yajulikane na vile vile wamiliki halali wajulikanena kudhibiti wageni kumiliki ardhi nchini mwetu. Maeneo yamlimani Usa Arusha kuna mashamba makubwa, mengineyana farasi kwa ajili ya burudani. Je, wenyewe hawa niwamiliki halali? Je, matumizi yake ndiyo yaliyokubaliwa naWizara au Kituo cha Uwekezaji?

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itumie sekta binafsikatika upimaji na kupanga matumizi ya ardhi, kwa sababuwataalam Serikalini hawatoshi, vinginevyo itachukua miakamingi sana zoezi hilo kukamilika. Serikali isitumie udhaifu wakekuumiza wananchi kwa mujibu wa sheria na kanuni. Kodihulipwa kufuatana na eneo na matumizi ya ardhi,haiyumkiniki kusikia Tamko la Waziri kwamba, kodi italipwakwa maeneo yote ambayo hayajapimwa. Je ni kosa la nanikwamba ardhi hiyo haijapimwa? Je, kodi hiyo italipwa kwakigezo gani? Hakuna mtu wala taasisi iliyo juu ya sheria.Serikali yenyewe ndio imetunga Sheria ya Ardhi na lazimaizingatie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwamba kunaimprovement kwenye mchakato wa kupata hati miliki yaardhi, bado juhudi zaidi inahitajika, bado kuna watumishiwanaojivuta. Napendekeza utoaji hati miliki zisizo namigogoro kwa wakati kiwe kigezo cha kupima utendaji wawatumishi wanaohusika na utoaji wa hati miliki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali sasa ifanye maamuzimagumu ya kutatua kero ya migogoro ya ardhi iliyodumukwa miaka mingi Serikali sasa iepuke kukwepa kufanyamaamuzi ya kero hii kwa kuunda Tume na Kamati za kutoamapendekezo miaka nenda, miaka rudi. Pamekuwepo naKamati/Tume zaidi ya tatu na bado migogoro hii haijapatiwaufumbuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

MHE. JITU V. SONI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naombanichukue fursa hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu kwaafya na fursa ya kuchangia leo. Nimpongeze Waziri, NaibuWaziri na Katibu Mkuu na timu yake ya wataalam kwa kazinzuri sana waliyofanya. Naomba masuala machacheyafanyike il i kuboresha huduma ya Wizara ya Ardhiinayoendana na maendeleo ya makazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza jimboni kwangu,Serikali iharakishe kupitia mgogoro wa ardhi ya miaka mingi

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

iliyotutesa na kusababisha migogoro hii kutumika kisiasawakati wote. Migogoro ya Vijiji vya Ayamango, Gedamarna Gidejabong na TANAPA Tarangire, Serikali ndio iliwekavijiji hivyo hapo katika eneo la hifadhi. Wapatiwe eneombadala na pia shamba la Galapo Estate pia lisitoleweviwanja na badala yake iwe eneo la kuwapa haowanaondolewa katika hifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba suala lamashamba ya Bonde la Kisu, migogoro ya ekari 25. Tunaombapale mapendekezo ya Wilaya na Mkoa zifanyiwe kazi piaSerikali itoe tamko la kuvamia mashamba na kuharibu maliya wawekezaji ambayo wana haki na wanatimiza wajibukisheria. Pia tunaomba ardhi ya kilimo ilindwe kisheria ilimatumizi ya ardhi ya kilimo isiweze kubadilishwa bila Bungekupitisha mabadiliko hayo kuwa ya makazi, viwanda aumatumizi mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunaomba Wizaraiandae program ya kila Halmashauri kupata vifaa vya kupimakwa mkopo pamoja na vifaa vya kuweka kumbukumbu yahati na vifaa vya kuchapa hati. Kwanza tutaweza kulipandani ya muda mfupi. Leo Halmashauri nyingi hawana bajetiya kununua kwa fedha taslim.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunaomba Wizara yaArdhi iangalie namna ya kulipia gharama ya matumizi yasatellite. Hii itafanya upimaji kwa ramani iliyopo inakuwa borana wa uhakika. Leo hii ramani nyingi zina tatizo sababuhawana fursa ya kutumia hiyo huduma ya satellite.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri pia tuwena sheria ya kuzuia kuuza kiholela kwa ardhi hasa yenye hatiya kimila ili wenye uwezo wasinunue ardhi nyingi nawasiokuwa na uwezo kukubali kuwa vibarua na mbele yasafari tutakuwa na hatari sawa na Afrika Kusini na nchi zinginekama Kenya ya wachache kuwa na ardhi. Leo kila Mtanzaniaana uwezo wa kuwa na ardhi.

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho naomba Serikaliitumie fursa hii kutoa tamko kwa umma na sisi wanasiasakutumia ardhi kisiasa na kuhamasisha vurugu kwa maslahiya kisiasa na hasara kwa umma na wamiliki wa ardhi, hifadhimbalimbali na vyanzo vya maji.

MHE. HASNA S. K. MWILIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba niungane na wachangiaji wenzangu kwakuwapongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, kwakuchapa kazi ya kusimamia Wizara hii na kupunguzamigogoro ya ardhi nchini na migogoro ya wakulima nawafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kuzungumziamigogoro ya mipaka ya vij i j i na hifadhi, natambuaMheshimiwa Waziri ni mzoefu wa kupunguza migogoro yaardhi na kwa kuwa migogoro ya hifadhi na vijiji vilivyosajiliwavinamgusa kwenye Wizara yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe sana tena sanaMheshimiwa Waziri Lukuvi tushirikiane kwa ukamilifu sana naWizara ya Maliasili na Utalii na TAMISEMI ili basi mgogoro wahifadhi na Vijiji vya Sibwesa na Kalilani, unaweza kutatuliwana kwisha ili basi wananchi na hifadhi wenyewe wawezekufanya shughuli za kimaendeleo na kufanya mahusiano yakijamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upungufu wa watumishi waardhi; niombe kwa Mheshimiwa Waziri akipata watumishi waardhi, basi atukumbuke Halmashauri ya Uvinza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nizungumzie suala laNHC, kwanza nimpongeze Mtendaji Mkuu wa Shirika laNyumba la Taifa Tanzania (NHC). Kwa kuchapa kazi na kwakasi kubwa anayofanya ya kuwajengea Watanzania nyumbaza bei ya kati ambayo Watanzania wengine wamemudukununua. Rai yangu katika hili tuombe NHC nao wawezekutoa fursa kwa Watanzania kulipa asilimia 10 na baadayewalipe kila mwezi hadi hapo mkataba utapokwisha ndiowapewe Hatimiliki.

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ya kulipa asilimia 10 halafuzilizobaki mtu alipe ndani ya miezi mitatu kwa kweliinatunyima fursa Watanzania wengi kuweza kununuanyumba hizi na wadau ni wengi, mtu anaweza kuwa nanyumba Dar es Salaam akapenda kuwa na nyumba piaArusha, lakini kwa utaratibu wa kulipa 10% halafu miezi mitatuawe amemaliza kwa kuchukua mkopo Benki, hili ni gumu.Sababu ni kwamba, wapo Watanzania tayari wana mikopomingine benki ya biashara, sasa akichukua mkopo benki kwaajili ya kununulia nyumba mikopo inakuwa mingi inamzidia.Hivyo, nimwombe Mheshimiwa Waziri, aone namna yakuchukua mfumo wa NSSF mtu analipa downpayment yamiezi mitatu kisha kila mwezi analipa pango hadi amalize.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe pia MheshimiwaWaziri, NHC waje Uvinza kutujengea nyumba za bei za katina bei za nafuu katika ukanda wa Ziwa Tanganyika. Ziwahili lina mandhari nzuri sana na viwanja tunavyo. Sambambana hili tunaomba pia waje kujenga Uvinza, viwanja vikubwakwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizi tunavyo na huku kwa vileni Wilaya mpya watumishi wengi wa Serikali na Taasisimbalimbali hawana nyumba za kuishi, hivyotunawakaribisha NHC kuja kujenga nyumba za bei nafuu nakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya,niendelee kumpongeza Mheshimiwa Waziri na MheshimiwaNaibu Waziri kwa kazi nzuri wanayoifanya kwenye Wizara.Naomba kuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

MHE. ZAINABU N. MWAMWINDI: MheshimiwaMwenyekiti, awali ya yote nianze kwa kumshukuru sanaMwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kuwana afya njema na kushiriki katika Mkutano huu wa Saba waBunge la Bajeti. Nampongeza Mheshimiwa Job Ndugai, Spikawa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Naibu Spika,Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson; Wenyeviti wa Bunge, Katibuwa Bunge Dkt. Kashililah , pamoja na watendaji wote waBunge kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yao.

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hiikumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. John Pombe JosephMagufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwautekelezaji mzuri wa majukumu yake; Makamu wa Rais,Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan; Waziri Mkuu, MheshimiwaKasim Majaliwa pamoja na Baraza lote la Mawaziri, kwa kazikubwa wanayofanya katika Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana tenasana Mheshimiwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi,Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi; Naibu Waziri,Mheshimiwa Angelina Mabula pamoja na watendaji wotewa Wizara kwa kazi kubwa na nzuri sana ya kuendeleakutatua migogoro ya ardhi katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na ziara aliyoifanyaNaibu Waziri Mheshimiwa Angelina Mabula katika Mkoa waIringa na kutatua mgogoro uliokuwepo kati ya Manispaa nawananchi waliopo kwa maeneo waliyonunua kwenye Serikaliya Kijiji cha Igumbilo, Kata ya Igumbilo. Nashukuru sanamgogoro uliokuwepo unaelekea kumalizika kwa maelekezosahihi aliyoyatoa au kuagiza Manispaa itekeleze, wananchiwamepatiwa viwanja katika maeneo yao, nampongezasana Mheshimiwa Waziri Mheshimiwa Angelina Mabula.Ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mji wetu wa Iringaunaendelea kupanuka kwa majengo pamoja na idadi yawatu kuongeza bado ujenzi holela nao unaongezeka,nimwombe Mheshimiwa Waziri, Ndugu yangu Lukuviatusaidie kupunguza eneo la mipaka ya Manispaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nampongeza sanaMheshimiwa Waziri kwa kuzirudisha nyumba za NationalHousing Serikali Kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na naunga mkonohoja.

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Mwenyekiti,tatizo la maeneo ya mipaka lipo katika maeneo mengi hasamipaka ya Mbulu na Iramba; Manyara na Karatu; na Mbuluna Hanang. Tunaomba wapimaji waje kutatua na kusoma(GN) i l i wananchi wajue wanapotakiwa kuwajibikakimaendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la mgogorowa ardhi Yayeda Chini na mwekezaji aliyepora eneo lawananchi bila kupewa na Serikali ekari 3903. Mara nyingiSerikali hukubali kutoa eneo kwa wingi wa wananchi kusemaapewe, lakini Wahadzabe, Wabarbaig mara nyingi jamii hizihazijapewa elimu kuhusu ardhi, hivyo panapotokea mtummoja kuwadanganya wanaweza kutoa eneo hilo nabaadaye mgogoro hautakwisha. Sasa kwa kuwaWahadzabe ambao mara nyingi wana hamahama kutafutamatunda na asali pia wanahitaji ardhi hiyo na kwa bahatimbaya wapo wachache katika jamii. Ushauri wangu nikwamba, wakati mwingine haki ya wachache izingatiwe ilijamii isipate tabu.

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Mwenyekiti,migogoro ya ardhi nchini ni moja ya kero kubwainayokwamisha maendeleo ya kiuchumi na ya watu wetu.Migogoro hii imedumu muda mrefu na kama nchi lazimatunatakiwa kuchukua hatua sasa. Ili kumaliza migogoro hiiSerikali ni lazima ihakikishe ardhi yote imepangwa, imepimwana kumilikishwa kisheria. Kuhusu migogoro ya mipaka katiya Mkoa na Mkoa, Wilaya na Wilaya na Kijiji na Kijiji, nishauriSerikali kufanya utaratibu wa kutafsiri GN zilizounda manenohayo ili haki itendeke.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Karatu inayomashamba 40 ya wawekezaji (Mikataba). Mengi yamashamba hayo hayajaendelezwa kwa kiwango chakuridhisha na yamekuwa chanzo cha migogoro. Shamba laTembo na Tembe lenye ekari 562 na 545 ambayo yoteyametekelezwa kwa chini ya 50% yamekuwa kero kubwakatika Wilaya ya Karatu. Naomba Serikali ichukue hatua yakuyachukua mashamba hayo au hata sehemu yake.

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

Mheshimiwa Mwenyekiti, shamba la Acacia Hill, lenyeekari 1556, nalo tunaomba sehemu yake irudishwe kwawananchi maana nalo limeendelezwa kwa chini ya asilimia50%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shamba la Bendhu Limitedlenye ekari 472 limetelekezwa baada ya mmiliki wake kufariki.Tayari Halmashauri ya Wilaya imeshaomba shamba hilokufutiwa umiliki na lipewe wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho niiombe Wizaraiongeze wataalam wa ardhi na vifaa katika Wilaya ya Karatu.

MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia katika sualahili. Kwa sababu ya muda naomba nianze kumpongezaWaziri wa Ardhi, Mheshimiwa Lukuvi na Naibu wakeMheshimiwa Angelina Mabula, pamoja na wataalam waWizara hii kwa kazi nzuri wanayofanya kukabiliana nachangamoto mbalimbali za ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wangu wa Kijijicha Lukonde wana matatizo makubwa, wanapata kipigokutoka kwa mwekezaji wa Shamba la Kidago alilopata kwanjia ambazo sio halali toka Uluguru Toiler aliyewanyang’anyawananchi bila ya kufuata taratibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro huu ni mkubwasana kwa Kijiji na Kitongoji cha Kidago, Lukonde, nyumbazao zaidi ya sitini (60) zimechomwa moto zaidi ya mara tatutofauti na kwa miaka tofauti na kuchoma mazao yao namfugaji huyo aliyepewa ardhi hiyo. Ombi langu, MheshimiwaWaziri baada ya Bunge hili kumalizika naomba afike kidogona kujionea hali halisi na kuwasaidia wananchi hawa iliwaweze kuishi katika nchi yao kwa amani na usalama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nataka kushauri Serikalikutenga Bajeti na kupima ardhi yote ya Halmashauri yaMorogoro Vijijini. Kwa kuzingatia mpango wa matumizi bora

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

ya ardhi, kupanga matumizi ya ardhi kwa ajili ya wakulimana wafugaji na hifadhi na kujenga miundombinu ya kiufugajikama majosho, mabwawa katika maeneo ya wafugaji nakutoa elimu kwa wafugaji kufuga kisasa na umuhimu wakuwa na mifugo kutokana na ukubwa wa ardhi waliyonayona miundombinu ya mifugo iliyopo sehemu husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuwaondoa wafugajiwavamizi waliokuja Morogoro vijijini na Morogoro kwa ujumlabila kufuata sheria Kanuni na taratibu za kuhamisha mifugotoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine na kuharibumazingira, mashamba ya wakulima, vyanzo vya maji nabarabara zetu tulizojenga kwa gharama kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.Ahsante.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,naanza kwa kumshukuru Mungu kwa kunijalia afya njemana kuweza kunijaalia kuchangia. Naunga mkono Hotubaya Kambi Rasmi ya Upinzani na pia nawapongeze Mawazirikwa kazi .

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu nikwamba, hapo zamani za kale Tanzania hapakuwepo namigogoro ya ardhi hususan ya wakulima na wafugaji, lakinisiku za karibuni migogoro ipo kila kona ya Tanzania. Sababukubwa watu wamejua thamani ya ardhi kuwa ni mali. Ardhini rasilimali muhimu ambayo pia ni urithi na utajiri wa asilitoka kwa Mwenyezi Mungu. Naishauri Serikali, ardhi yetuipimwe, ipangiliwe isiwe nchi nzima ni viwanda, barabara,makazi na maeneo ya vijijini tu ndio mashamba. Ardhi ipimwena imilikiwe na wananchi kama ilivyo kwa South Africa, Kenyana kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mashamba ya Mkonge(Amboni Company Limited). Halmashauri ya Jijiji la Tangalina mashamba makubwa ya Mkonge ya Amboni CompanyLimited sasa (COTAIL) ambayo imechukua nafasi ya Amboni

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

Limited. Naipongeza Kampuni ya Cotail Limited kwa kuipaHalmashauri ya Jiji la Tanga ardhi kwa ajili ya shughuli zamaendeleo yenye ukubwa wa takriban heka 400.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yamejitokeza matatizobaada ya Halmashauri kupata mwekezaji wa Chinaanayetaka kujenga Kiwanda cha Cement. Kuna wakulimaambao wanalalamika kuwa wamepunjwa fidia, hivyonaomba, Mheshimiwa Waziri tukatembelee eneo husika ilikutatua kero ndogo ndogo na kuweza kufanya mradimkubwa wa Kiwanda cha Cement uanze bila malalamikoya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mashamba ya Marungu naKwamkembe. Sheria inaelekeza kuwa majij i hayanamashamba yenye zaidi ya 50 hectors, lakini Jijji la Tanga katikaKata ya Marungu kuna mashamba tajwa hapo juu ambalosiku za karibuni wameuziwa na wamiliki wenye Hatimiliki,wameondoa wananchi waliokuwa wakilima mazao yachakula na biashara, yaliyowezesha kupata kipato cha kilasiku na kulipia ada za watoto. Waliahidi kuwakatia wakulimabaadhi ya maeneo kwa ajili ya kilimo (mashamba yana zaidiya ekari 2000 – 4000). Namwomba Mheshimiwa Waziri hili piaalishughulikie na kupata ufumbuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kijiji cha miaka 21-Tanga. Hilini eneo lil i lotwaliwa kinyume na taratibu. Nashauri,Mheshimiwa Waziri, Ofisi yake ilirudishe Halmashauri yaManispaa ya watu wa Tanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la Ngamiani Kusini Katina Kaskazini. Eneo hili ni katikati ya mji kuanzia Barabara 1-21, kuna nyumba zaidi 10,000 na ni eneo la kihistoria lakiniwamiliki wake hawana hatimiliki wana Hati ndogo (offers)tu. Ushauri, naomba Wizara ya Ardhi isaidie katika kupimaau kutoa Hatimiliki (99 years) ili wananchi waweze kutumiakatika shughuli za maendeleo kama kukopa mabenki kwaajili ya biashara na kilimo. Tukumbuke wananchi hawawanalipa property tax.

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu 30% ya makusanyo,naiomba Wizara irudishe 30% ya mapato ya ardhi katikaHalmashauri ili zitumike kwa shughuli za Maendeleo.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nampongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri kwajitihada kubwa walizofanya kuleta mabadiliko makubwa yakiutendaji katika Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, rasilimali ardhi ina umuhimuwa kipekee kwa uhai wa maendeleo ya binadamu,wanyama, mimea na viumbe vyote. Kwa uchumi wa Taifaletu ambalo wananchi walio wengi wanategemea sanakilimo kama sekta muhimu katika kukidhi mahitaji yao yakila siku; rasilimali ardhi inakuwa na umuhimu wa kipekee,kiasi kwamba ni haki ya kila mwananchi kupata, kuimiliki,kuitumia na kuitunza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wimbi la kuwepo kwamigogoro ya mipaka na uvamizi wa ardhi katika maeneoya vijiji limeendelea kuwa tatizo kubwa katika nchi yetu.Tatizo hili ni kikwazo kwa maendeleo ya wananchi na Taifakwa ujumla. Tumeendelea kushuhudia migogoro hiiikisababisha upotevu wa mali za wananchi, vifo nakuendeleza uhasama kati ya jamii na jamii na hivyokuwafanya wananchi kubaki maskini na kuishi maisha duni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kasi ndogo ya upimaji ardhiimeendelea kuwa donda ndugu, wataalam wa ardhikutowashirikisha wananchi wakati wa uwekaji wa mipaka;na kutowaelimisha wananchi juu ya mipaka iliyowekwa,kama Taifa hatuwezi kuiacha hali hii iendelee. Wizara ichukuehatua za makusudi kuhakikisha kuwa wataalam wa ardhiwanawashirikisha na kuwaelimisha wananchi wakati wauwekaji wa mipaka. Wizara iongeze kasi ya upimaji wakatiwa uwekaji wa mipaka. Wizara iongeze kasi ya upimaji ardhiili kuzuia wajanja wachache kuvamia maeneo pasipoviongozi wa vijiji kujua na hatua kali zichukuliwe kwa viongoziwa vijiji wanaogawa ardhi kinyume na taratibu.

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

Mheshimiwa Mwenyekiti, migogoro ya wakulima nawafugaji imeendelea kuwa chanzo cha machafuko naumwagaji damu nchini. Lazima kasi yetu ya kutenga maeneomaalum ya wafugaji na wakulima iandamane na utunzajiwa sheria kali utakaozuia uvamizi wa maeneo unaofanywana pande hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, bado mashambamakubwa yasiyoendelezwa yameendelea kuwa chanzokikubwa cha migogoro ya ardhi nchini. Bado mfumo wetuwa kufuta miliki ya ardhi isiyotumika ipasavyo kwa mujibuwa makusudio ya umiliki wa ardhi husika umeendelea kutoamwanya wa watu wachache kuhodhi ardhi bila kuitumiana kuwaacha wananchi wengi wakitaabika kwa kukosaardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali kufanyamapitio ya Sheria ya Umiliki Ardhi na kanuni zake ili tupunguzeurasimu katika mfumo wetu ili mashamba yaliyotelekezwayaweze kufutiwa hati za umiliki mara tu yanapothibitika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mara nyingine niletekilio cha muda mrefu cha wananchi wa Wilaya ya Mkinga,ambayo ni miongoni mwa wilaya zinazokabiliwa namigogoro ya umiliki wa ardhi na mashamba yaliyotelekezwakwa muda mrefu. Licha ya jitihada kadhaa ambazo kwanyakati tofauti Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkingana mimi binafsi tumewasilisha Wizara ya Ardhi mapendekezoya Wilaya kuhusu utatuzi wa migogoro hiyo; bado utatuziwa migogoro hii umekwama kupata majawabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati mapendekezo yaOfisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga yaliwasilishwaWizara ya Ardhi tangu mapema mwaka 2007 wakati huoMkinga ikiwa bado ni sehemu ya Wilaya ya Muheza; ofisiyangu iliwasilisha tena maombi hayo kupitia mchango wanguwa maandishi wakati wa Bunge la Bajeti mwaka jana nakufuatiwa na barua kwa Waziri wa Ardhi yenye Kumb. Na.MB/MKN/Ardh 01/2016 ya tarehe 30 Mei, 2016. Napenda

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

kuikumbusha Wizara juu ya maombi haya ambayo kimsingiyamechukua muda mrefu kupatiwa ufumbuzi.

(i) Shamba la Kilulu; shamba hil i ndipopalipojengwa Makao Makuu ya Wilaya ya Mkinga. Shambahili kwa mara ya kwanza lilimilikishwa kwa Bwana Van Brandisna Bibi Mary Van Brandis hadi tarehe 31 Oktoba,1959 ambapoumiliki ulihamia kwenda ama Bwana Akberali Walli Jiwa.Mmiliki huyu hakuendeleza shamba hili lenye ukubwa waekari 5,699.9 hadi umiliki wake ukafutwa mwaka 1972. Baadaya kufuta umiliki, Serikali ililipa fidia na shamba likawa chiniya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadaye Wilaya ya Muhezailipokea maombi ya kumilikishwa shamba hilo toka Kampuniya M/S Arusha Farms Limited (CHAVDA). Taratibu zotezilizofanyika na alimilikishwa ekari 2,699.9 na ekari 3,000walipewa wananchi wa vijiji jirani vya Vuo, Mwachala naParungu Kasera waliokuwa na shida ya ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, M/S Arusha Farms Limitedwalipewa barua ya toleo (Letter of Right of Occupancy) yatarehe 10 Mei, 1991 ambayo ilisajiliwa na Msajili wa hati tarehe10 Mei, 1991 ambayo ilisajiliwa na Msajili wa hati tarehe 13Mei, 1990 kwa Land Office Number 125127.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mmiliki huyu aliomba mkopokutoka CRDB Bank kwa kuweka rehani barua ya toleo. Aidha,alishindwa kurejesha mkopo huo na CRDB waliuza shambakwa M/S Mbegu Technologies Limited tarehe 27 Juni, 2004ambao walilipa mkopo huo. Hata hivyo, pia hakuwezakuliendeleza shamba hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bwana Akberali Jiwa lichaya kunyang’anywa shamba hilo na kulipwa fidia aliwasilishaombi lake la kurejeshewa umiliki wa shamba hilo. Ombi lakeliliwasilishwa katika Kikao cha Kamati ya Kugawa Ardhi tarehe10 Oktoba, 1996 na iliazimiwa liwasilishwe katika Kamati yaUshauri wa Ardhi Mkoa. Kamati hiyo chini ya Uenyeviti wa

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

Mkuu wa Mkoa iliridhia Bwana Akberali Jiwa apewe shambahilo kwa vile M/S Arusha Farms Limited ameshindwakuliendeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Muhezailitoa barua ya toleo kwa miliki ya miaka 99 kuanzia tarehe 1Oktoba, 1998 kwa Akberali Jiwa kwa jina la Kampuni ya Kilulu(2000) Limited. Baada ya tatizo hilo la double allocationkujitokeza, Halmashauri ya Muheza iliandika barua Kumb. Na.MUDF/3844/63 ya tarehe 2 Aprili, 2007 kwenda kwa Kamishnawa Ardhi kwa ajili ya kuomba kufuta miliki hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, licha ya ufuatiliajiuliofanywa wa mara kwa mara, kwa mujibu wa taarifa yaHalmashauri hadi leo Halmashauri haijapata hati yoyoteinayoonesha kufutwa milki ya shamba tajwa. Kikao cha RCCkilichofanyika mwaka jana kiliridhia hati ya shamba tajwaifutwe; hivyo kuagiza taratibu za kutoa notice zifanyike. Hatahivyo, tangu wakati huo kumekuwa na urasimu mkubwa wautoaji notice tajwa. Naiomba Wizara ifuatilie jambo hili.

(ii) Shamba la Moa; shamba hili lina ukubwa waekari 15,739.60 na linamilikiwa na Mkomazi Plantations Limitedwa S.L.P. 2520 Dar es Salaam kwa hati Na. 4268,9780 &9781.Halmashauri ya Wilaya ilituma notisi ya kuwafutia hati milikiyao kwa kutoendeleza na kutolipia kodi. Baada ya hapoHalmashauri ya Wilaya iliwasilisha barua ya Mapendekezokwa Kamishna wa Ardhi yenye Kumb. Na MKG/LD/F/2/54 yatarehe 28 Julai, 2009.

Mheshimiwa Mwenyekiti, taratibu za ufutaji hati milikiziliendelea Wizarani, lakini Halmashauri ilipokea barua yammiliki akieleza kuwa jina la umiliki lilibadilika na kuwa MoaPlantation & Aquaculture wa S.L.P. 364 Dar es Salaam nakwamba wanataka kuendeleza shamba hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Halmashauri yaWilaya ilishawasilisha Wizarani barua ya mapendekezo yakufuta hati miliki, ililazimika kumwandikia Kamishna wa Ardhi

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

barua yenye Kumb. Na. MKG/LD/F/2/56 ya tarehe 9 Juni, 2011kumweleza kupokea barua hiyo na kwamba shamba hilolina vijiji vinne ambavyo vimeanzishwa na kusajiliwa (Moa,Ndumbani, Mayomboni na Mhandakini).

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, vijiji hivyo tayari vinahuduma za jamii kama shule, zahanati, barabara nakadhalika katika maeneo hayo; hivyo aendelee na taratibuza ufutaji hati miliki au kama atasitisha ufutaji basi wamilikiwakubali kumega maeneo yanayokaliwa na viji j i nakuendelezwa na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati hali ikiwa hivyo,mwaka 2013 mmiliki wa shamba atengeneze PP na kuombakubadilisha matumizi ya sehemu ya shamba ili kupimaviwanja 450 vya makazi. Hata hivyo, viwanja hivyohavikuwahi kupimwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatilia ucheleweshajiusioeleweka wa kufuta hati ya shamba hili, mnamo mweziOktoba, 2016 mmiliki wa shamba alitumia mwanya huokutengeneza PP nyingine ya eneo lote la shamba ili kupimaviwanja. Aidha, amekabidhi hati ya shamba tajwa iliipelekwe kwa Afisa Ardhi Mteule-Moshi i l i taratibuzinazokusudiwa ziweze kufanywa. Naiomba Wizara iingiliekati mchakato huu ili ardhi tajwa irejeshwe mikononi mwaHalmashauri ya Wilaya.

(iii) Mwele Seed Farm; shamba hili lina ikubwa wahekta 954. Mmliki ni Wizara ya Kilimo. Wakati ambaposhamba hili lilikusudiwa kuwa shamba la kuzalisha mbegu,hali halisi ni kwamba kwa kipindi cha takribani miaka 15 sasashamba hili limeshindwa kutumika kama ilivyokusudiwa nasehemu kubwa kubaki kuwa pori.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa vij i j ivinavyozunguka shamba hili Mbambakofi, Maramba A,Maramba B na Lugongo ndio wamekuwa nguvukazi ya

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

kulifanyia usafi shamba hili pale wanaporuhusiwa kufunguamashamba mapya na kulima mazao ya muda mfupi kilamsimu mpya wa kilimo unapowadia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnamo tarehe 21 Septemba,2007, Halmashauri ya Wilaya iliandika barua kwa Kamishnawa Ardhi Kumb. Na. MUD/ASF/VOL.VI/35 ikipendekezakumegwa kwa shamba hili na kugawiwa kwa wananchi wavijiji jirani kutokana na uendelezaji wake kuwa mdogo sanana kodi kutolipwa. Hata hivyo, maombi haya hayakuwahikupatiwa majibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shamba hili lilipakana na Kijijicha Mbambakofi chenye takriban kaya 500 zenye jumla yawananchi wapatao 3173. Mbambakofi ni kijiji pekee katikaWilaya ya Mkinga ambacho kimekosa hata eneo la kujengahuduma muhimu za kijamii kama shule ya msingi na zahanati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, shamba hil ilimepakana na Mji Mdogo wa Maramba ambao unakua kwakasi kubwa, ukiwa na takriban watu 30,000 na kuzungukwana mashamba makubwa ya Maramba JKT, hekta 2,445;Lugongo Estate, hekta 6,040; Kauzeni Estate, hekta 189.66; naMtapwa Estate, hekta 476.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya kutekelezwa kwashamba hili imezidi kuwa mbaya sana sasa kuliko ilivyokuwamwaka 2007, wakati Halmashauri ya Wilaya ilipoomba kwamara ya kwanza kumegwa kwa shamba hili. Kwa sasa haliimekuwa mbaya kiasi kwamba hata majengo mengiyaliyokuwepo yameanguka na machache yaliyosaliayamekuwa magofu, mashine na mitambo yote ya kilimoiliyokuwepo shambani hapo imeharibika na michacheiliyosalia imehamishiwa Morogoro. Kwa sasa shamba limebakina wafanyakazi wasiozidi watatu kutoka ishirini na vibaruathelathini waliokuwepo miaka ya 1988 – 1995.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya Halmashauri yaWilaya kusubiri kwa muda mrefu jibu la Kamishna wa Ardhi

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

bila mafanikio, kikao cha RCC kiliiagiza Halmashauri kuandaamaelezo kuhusiana na shamba hili ili Mkuu wa Mkoa awezekuandikia Wizara husika kuomba rasmi Halmashaurikukabidhiwa eneo tajwa. Tayari Halmashauri imetekelezamaagizo haya. Naiomba Wizara ya Ardhi isaidie katika utatuziwa kero hii ambayo inawasumbua sana wananchi.

(iv) Kwamtili Estate; shamba hili lina ukubwa wahekta 1,150 na linamilikiwa na Kwamtili Estate Limited yenyeCertificate of Incorporation Na. 2649 iliyosajiliwa tarehe 9Januari, 1961 ikiwa na wanahisa wafuatao:-

S/N JINA LA MWENYE HISA

ANAPOISHI MAELEZO

1 DENNIS Martin Fielder 4 Market Square Tenbery,Wells Worcestershinre –UK

Amerudi Uingereza

2 National Aggriculture & Food Corporation (NAFCO

Box 903 Dar es Salaam Shirika limefutwa

3 Handrick Tjails Scheen

CI/30 Algamines Bank, Amsterdam, Netherland

Amefariki

4 Louis Van Wagenburg

Laycsan Ag Vaghel, Holland Amefariki

5 Schoonmarkers Bart Vandrbug

De Congqabsen,163 Schikher, Holland

Amefariki

6 Tracey Elan Allison The Willos Terrigton, Herefordenshire, UK

Amefariki

7 Juvent Magoggo 42 Block S. Mikanjuni Box 5855 Tanga

Anaishi Tanga

8 W.J. Tame Ltd Box 118 Tanga Amefariki 9 Jacobus Cornelius

Josephus Moris

Logtamburg Vaghel Holland Amefariki

 

Mheshimiwa Mwenyekiti, shamba hili lililopo katikaeneo la Kwamtili, Kata ya Bosha Wilaya ya Mkinga, lilitumikakwa kilimo cha kibiashara cha zao la kakau. Hata hivyo,kwa muda wa miaka takriban 26 sasa shughuli za kilimo chazao la kakau zimesimama baada ya iliyokuwa Menejimentiya Kampuni chini ya Ndugu Dennis Fielder kutelekeza shamba.

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, baada ya shambakutelekezwa, mmoja wa wanahisa Ndugu Juvent Magoggoamekuwa akifanya shughuli ndogo ndogo ikiwemo kuvunamiti ndani ya shamba hili kwa lengo la kupata fedha zakufanyia uzalishaji mdogo mdogo; na hali kadhalika kuruhusuwananchi wanaozunguka shamba hilo kulima mazaoambayo si ya kudumu. Hata hivyo, kwa sasa nduguMagoggo ameshindwa kuendelea kufanya shughuli hizobaada ya kunyimwa vibali vya kuvuna miti kusafirishamagogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na kuwepo kwaombi la umiliki wa shamba hili, yamezuka makundi ya watuyanayodai kuwa na haki ya kumiliki shamba hili na hivyokuwakodisha wananchi wanaozunguka shamba hili maeneoya kulima kwa kuwalipisha sehemu ya mavuno yatokanayona matumizi ya ardhi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kumekuwa na wimbila kujitokeza raia wa kigeni kwa kutumia kivuli cha aliyekuwaMkurugenzi Mtendaji wa shamba na kulitekelezaNdugu.Dennis Fielder kufanya uharibifu wa mali za kampuni,ikiwemo upasuaji wa mbao na kuanzishwa michakato yakujimilikisha ardhi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili, wananchiwanainyooshea kidole Ofisi ya Wakala wa Hifadhi ya Misitu,Wilaya ya Mkinga kutaka kujiingiza katika kufanya udalaliwa ardhi hii. Wananchi bado wanakumbukumbu nzuri yajinsi watumishi hawa wa TFC Wilayani Mkinga walivyotumikakuwezesha mwekezaji wa Kiitaliano aliyejaribu kupatiwaardhi ya Mkinga takriban hekta 25,000 kinyume na taratibu ilikulima Jatropher.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Serikali haijawezakulipatia ufumbuzi tatizo l ingine ambalo kimsingilimeanzishwa na TFC kutaka kupora ardhi ya wananchi katikashamba la Segoma, TFC hiyo hiyo inataka kuzalisha mgogoromwingine wa kupora ardhi nyingine katika Wilaya ya Mkinga.

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

Hatupo tayari kuona hili likitokea hasa ikizingatiwa kuwaKwamtili inakabiliwa na tatizo kubwa la ardhi. TunaiombaSerikali kutumia busara kuacha jambo hili na kuirejesha ardhihii kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Kwamtili naKata ya Bosha kwa ujumla wamebaki katika umaskini wakutupa baada ya shughuli za kilimo cha kakau katika shambala Kwamtili ambacho ndicho kilitoa ajira kwao kusitishwa.Nusura pekee kwa wananchi hawa ni kupatiwa maeneokatika shamba hili ili kwa kutumia utaratibu wa wakulimawadogo waweze kufanya shughuli ya kilimo na hivyo kujikimukimaisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali ifanyeuamuzi wa kufuta hati ya shamba la Kwamtili na kishakuligawa kwa wananchi kwa ajili ya kilimo na sehemunyingine kwa wananchi kuwa hifadhi ya msitu wa kijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambuachangamoto kubwa inayowakabili wananchi wa Kwamtili,RCC iliagiza mmiliki wa shamba hili kupewa notice ili taratibuza kufutiwa hati ziweze kufanyika. Kwa masikitiko makubwakumekuwa na urasimu mkubwa wa taratibu wa kutolewanotice tajwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, licha ya Afisa Ardhi Mteuletoka Ofisi ya Kanda-Moshi kuja Mkinga kufanya zoezi la uhakikimwanzoni mwa mwezi April i hadi leo hakunakinachoendelea licha ya kukumbushwa mara kadhaa kwasimu na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mkinga. NaiombaWizara iingilie kati jambo hili ili ujanja ujanja usitumikekuvuruga mchakato wa kuwapatia haki wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo haya,naunga mkono hoja. Aidha, naomba Wizara ya Ardhi kwakushirikiana na TAMISEMI itusaidie Halmashauri ya Wilaya yaMkinga tuweze kuajiri Afisa Ardhi Mteule ili atusaidie kuondoamigogoro.

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

MWENYEKITI: Tumemaliza wachangiaji upande waWaheshimiwa Wabunge, tunaanza na Mheshimiwa NaibuWaziri wa Ardhi kwa dakika 40 na baadaye Mtoa Hojaatakuja kumalizia kwa dakika 10.

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEOYA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote, napendakumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa fursa hii ambayoamenipa na kunipa afya njema na hatimaye kuwezakusimama katika Bunge lako Tukufu na kuweza kujibu baadhiya hoja ambazo zimetolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaendelea, naombanichukue fursa hii kutoa pole kwa wananchi wa Mkoa waMwanza na mikoa ya jirani ambao jana wamepatwa natetemeko na hususan Jimbo langu ambalo karibu Kata sabazote zimepitiwa na tetemeko hilo. Tunamshukuru Mungukwamba madhara hayakuwa makubwa sana natunamwomba Mungu amrehemu yule Askari ambayeamepoteza maisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze sanaMheshimiwa Spika, Naibu Spika, pamoja na Wenyeviti wotewa Bunge hili kwa kazi nzuri ambayo mnaifanya nammekuwa mkituongoza vizuri katika shughuli nzima yakuendesha Bunge letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, nampongeza sanaMwenyekiti wa Kamati yetu pamoja na Makamu wakeambao wamekuwa wakitupa ushauri kupitia Kamati yaBunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii ambayotumekuwa tukifanyanao kazi vizuri. Namshukuru sana piaWaziri Kivuli ambaye naye amefanya kazi nzuri katikakuwasilisha hotuba yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nachukua fursa hiikuwashukuru sana wananchi wa Jimbo langu la Ilemela kwakuniamini. Nashukuru Chama cha Mapinduzi kwa kuniamini,lakini Serikali pamoja na Viongozi wa Dini ambaowamekuwa pamoja nasi.

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naungana nawachangiaji wote waliotangulia kumpongeza sanaMheshimiwa Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli kwa kazi nzuri sana ambayo anaifanya. Kwa kweli,amekuwa ni kiongozi wa mfano, kiongozi wa vitendo,kiongozi ambaye anasimamia kauli zake. Nasi wasaidizi waketunasema tutakuwa tayari kumsaidia pale ambapo tunahitajikusaidia kwa kadiri alivyotuamini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Waziri wetuMkuu pamoja na Makamu wa Rais. Kwa kweli wamekuwawakitupa ushirikiano mzuri na kutupa maelekezo mazuri yakuweza kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapokea pongezizilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge. Naomba nichukuefursa hii kuwashukuru sana, lakini niseme pongezi hizohazikutustahili sisi peke yetu, ni sisi pamoja na ninyiWaheshimiwa Wabunge kwa sababu, ushirikiano mliotupaumefanya pia kazi yetu iwe rahisi. Kwa hiyo, nasitunawashukuru sana. Maandiko yanasema, “moyo usio nashukrani hukausha mema yote.” Hivyo hatuna budikuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa ushirikianowenu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shukrani na pongezimlizozitoa, kwetu sisi ndani ya Wizara ni chachu ya kuzidikuongeza kasi ya kutenda kazi vizuri na kuweza kusaidia jamiiambayo muda wote inategemea utendaji wetu.Nawashukuru sana pia Watendaji wetu ndani ya Wizaraambao wamekuwa wakifanya kazi nzuri sana katika kuonakwamba, shughuli hizi zinafanyika vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya kipekeekabisa, nimshukuru sana Waziri wangu, Mheshimiwa Lukuvi.Ni Waziri ambaye amekuwa ni mentor wangu mzuri, nikiongozi ambaye anaweza kuelekeza vizuri, ni kiongoziambaye anasimamia maamuzi, ni kiongozi ambaye kamani mwanafunzi mzuri, kwa kweli utafuata nyayo. Mheshimiwa

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

Waziri nakushukuru sana kwa sababu umenifanya niwe kamanilivyo katika Wizara hii ambayo ina changamoto nyingisana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda sasa nisemekwamba Sekta ya Ardhi inakabiliwa na changamoto nyingi.Wote ni mashuhuda, tumeona namna ambavyoWaheshimiwa mmechangia katika kutoa hoja zenu. Katikamichango yenu jumla ya Waheshimiwa Wabunge 77wamechangia; 40 wamechangia kwa njia ya kuzungumzana 37 wametoa kwa maandishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu kubwa ya michangoya Waheshimiwa Wabunge waliyoitoa, imejikita katika sualazima la utawala wa ardhi ambapo sehemu hii inahusumigogoro ya matumizi ya ardhi baina ya watumiajimbalimbali wakiwemo wakulima, wafugaji, wawekezaji nahifadhi zetu ambazo zipo nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, kuna suala la kutolipwakwa fidia kwa wakati kama ambavyo mmesema, lakini kunaucheleweshwaji wa utoaji wa Hakimiliki za Ardhi. Yote hayayako katika utawala wa ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya pili ambayo piaimezungumziwa na Waheshimiwa Wabunge wengi sana nisuala zima la upimaji na ramani. Katika maeneo hayalimezungumziwa suala la uhaba wa wataalam wa upimajina vitendea kazi, gharama kubwa za upimaji, umuhimu wakuimarisha mipaka ya nchi, migogoro ya mipaka ya Vijiji, yaKata, Wilaya kwa Wilaya, lakini pia migogoro kati yawananchi kwenye vijiji pamoja na hifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa MipangoMiji, nako Waheshimiwa wengi wamezungumzia. Maeneomengi waliyozungumzia upande huu walikuwa wakitoakama ushauri; suala la kuharakisha zoezi la urasimishaji wamakazi katika miji mbalimbali ambalo tayari limekwishaanza;Waheshimiwa Wabunge wameishauri Wizara kuongeza kasiya uaandaaji wa mipango kabambe, ushauri tumeupokea,

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

lakini pia limezungumziwa suala la uhaba wa watumishi navitendea kazi katika Halmashauri mbalimbali. Tunakiri uhabahuo upo na ni kikwazo kikubwa katika kupanga miji yetu ilikuwa na miji salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine lililozungumziwana Waheshimiwa Wabunge, ni la maendeleo ya nyumba.Hili limezungumziwa na Waheshimiwa Wabunge wengi sana.Kubwa hapa lilizungumziwa kuhusu gharama kubwa zaujenzi wa nyumba kwa wananchi, imekuwa gharama nikubwa kwa hiyo, vipato vyao ni vidogo na hawawezikumudu kulingana na bei ambayo imewekwa na NationalHousing. Pia, mmezungumzia uhaba wa nyumba kwawatumishi katika maeneo hasa ya vij i j i . Haya yotetumeyapokea kwa sababu ni michango; ni hali halisi ambayoipo, lakini bado tutazungumzia majibu yake kwa baadaye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, l ingine ambalolimezungumziwa ni suala la Mabaraza ya Ardhi na Nyumbakatika Wilaya zetu. Upande huu umezungumziwa uhaba wawatumishi wa mabaraza katika Mabaraza yetu kwenyeWilaya, lakini pia mkazungumzia suala zima la azma yaSerikali ya kuwa na mabaraza haya katika kila wilaya. Nikweli, hatujaweza kutimiza azma hiyo, lakini nia ya Serikali ninjema na tutaendelea kuifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kutoa utanguliziwa maeneo ambayo Waheshimiwa Wabungewameyachangia, naomba sasa nianze kujibu hojambalimbali ambazo zimetolewa, nikianza na hoja kutokakwenye Kamati yetu ya Bunge ya Kudumu ya Wizara ya Ardhi,Maliasili na Utalii ambayo imetoa hoja mbalimbali. La kwanzaamezungumzia ufinyu wa bajeti katika Tume yetu ya Mipangoya Matumizi Bora ya Ardhi ambayo imekuwa ikipatiwarasilimali kidogo kulingana na kazi wanazozifanya na ndivyojinsi ambavyo mmeliona suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niwahakikishiekwamba Serikali imekuwa inatoa fedha kulingana na bajetiinavyopata katika Tume ile. Kwa sasa Tume ile inalo Fungu

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

lake, inayo Vote yake Na. 3 ambayo sasa imeanzakutengewa bajeti kuanzia mwaka 2016. Mwanzoni ilikuwaiko ndani ya bajeti ya Wizara kwenye Fungu Na. 48, lakinikwa kasi ambayo yao na kazi wanayofanya, wamewezakufanya majukumu yao kulingana na pesa waliyopata nawanafanya kazi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa mafungukadiri yatakavyozidi kuongezeka, tutawaongezea kwasababu Tume hii ni muhimu sana katika kufanya shughuli zaupangaji miji yetu katika maeneo yetu hasa katika mipangoya matumizi bora ya ardhi. Kwa hiyo, niseme tu kwambatumepokea maoni hayo na tutazidi kuyafanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha huuwa 2017/2018 Serikali imeipatia Tume vibali vya ajira kwawatu saba. Kwa sababu wakati mwingine pia utekelezajiwake haukuwa mzuri sana kwa sababu hawakuwa napersonnel ya kutosha. Kwa hiyo, wataongeza wataalamwengine saba ambao ni kutoka katika kada mbalimbalikwenye eneo lao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali kupitiaWizara yangu itaendelea kuipatia Tume ushirikiano mzuri,hasa wa rasilimali fedha na watumishi pamoja na vitendeakazi ili waweze kufanya ile kazi ambayo wote tumeitambuakwamba ni muhimu, Tume hii ifanye kazi yake vizuri katikakusaidia katika mpango wa matumizi bora ya ardhi katikamaeneo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala pia la kuongezakasi ya elimu kwa umma kwa matumizi ya ardhi ambayoyameonekana kwamba kwa watumiaji mbalimbali imekuwani shida. Katika kutekeleza jambo hili, majukumu ya kuandaamipango ya matumizi bora ya ardhi, ngazi ya Kata na Vijiji,Tume hutoa elimu kwa timu za usimamizi wa ardhi kwenyevijiji na hususan katika Halmashauri. Hili limekuwa likifanyikana kumekuwa na ushirikiano mzuri sana.

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, timu ya kusimamiamipango ya matumizi bora ya ardhi katika Wilaya hujengewauwezo wa kuratibu na kupanga utekelezaji na usimamizi huuwa mipango ya matumizi bora ya ardhi nchini. Hivyo, katikamwaka wa fedha 2016/2017 Tume ilitoa elimu katikaHalmashauri 24 nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Tume imekuwaikifanya kazi yake vizuri, pamoja na ufinyu wa bajeti ambaoumekuwa ukitokea. Pia Tume hii huandaa vipindi maalumvya elimu kwa umma. Hii yote ni katika kupanua uelewakatika maeneo yetu ili kusaidia kujenga uelewa wa pamoja.Imekuwa ikitumia njia mbalimbali ikiwemo kutumia vyombovya habari, maonesho ya Saba Saba, Nane Nane, Wiki yaUtumishi na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya yote yanafanyika ilikuweza kupanua wigo wa kutoa elimu. Vipindi hivi piavimekuwa vikihusisha sheria, taratibu na miongozo yakupanga na kusimamia matumizi bora ya ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango wa Elimu kwaUmma umeandaliwa kwa kushirikisha wadau wa matumiziya ardhi kama Taasisi za Umma na Asasi Zisizo za Kiserikali.Care International Tanzania, Haki Elimu, Ardhi Oxfarm naUjamaa Community Resource Team. Hawa wote wamekuwawakishiriki katika zoezi hilo. Kwa hiyo, kazi inayofanyika ninzuri kiasi kwamba ni kiasi cha kufuatilia tu zile programuzinapokuwepo ili watu waweze kujengewa uelewa mzurizaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala linginewamezungumzia kuwa Serikali itenge fedha za kutosha ilikuyafikia maeneo mengi zaidi nchini yenye migogoro yamipaka ya ardhi. Katika suala hili Serikali itaendelea kutengafedha kadri zinavyopatikana. Aidha, Wizara pia itaendeleakushirikiana na wadau wa Sekta binafsi ili kufikia maeneomengi katika kutoa elimu na masuala ya ardhi ili kuepushamigogoro hii. Kwa hiyo, Serikali peke yake haiwezi, ndiyo

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

maana tunashirikisha sekta binafsi ambazo zipo katikataaluma hii ili kuweza kufikia wananchi wengi kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukosefu wa fedha pengineunakuwa nao ni kikwazo sana, lakini Serikali itaendeleakuishughulikia changamoto hii katika kuweza kupatarasilimali hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati imetoa ushaurikatika mambo mengi na sisi tunayachukua na tumeyapokeakama yalivyo, wamezungumzia suala la Serikali ihamasisheHalmashauri kukopa ili kutekeleza miradi ya kupima viwanja.Hilo tumelipokea. Kuwezesha Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhiiweze kutekeleza majukumu yake tumelipokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile kuhusu Wizarakuendelea kufanya kazi kwa pamoja na wadau wengine,tumelipokea na tunaendelea kulifanyia kazi; kuhusu Sheriaya Ardhi kwamba iboreshwe na kusimamiwa kikamilifu ilikuondoa migogoro baina ya watumiaji ardhi, huo ushauritumeupokea, tunaendelea kuufanyia kazi; kuongeza kasi yakutoa elimu nimesema tunaendelea, kwa hiyo, ushauri huotumeupokea na tunaufanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwamba Serikali itengefedha za kutosha kwa ajili ya kuanzisha Mabaraza ya Ardhi.Kama nilivyosema kwenye utangulizi, nia ya Serikali ni kuwana mabaraza haya katika nchi nzima. Tuseme tu kwambakwa mujibu wa Sheria ya Mabaraza ya Ardhi ya Na.2 yamwaka 2002, kila Wilaya inatakiwa kuwa na Baraza. Lengola Serikali ni kuwa na Mabaraza haya katika kila Wilaya. Hadikufikia 15 Mei, 2017 Serikali tayari ilikuwa imeshaundaMabaraza 97 kati ya yale Mabaraza 100 tuliyokuwatumekusudia kuweka, ambapo kati ya hayo Mabaraza 53tayari yanatoa huduma; na Mabaraza 44 hayajaanza. Kwahiyo, nia ya Serikali ni njema na tunaendelea kuifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2017/2018, Serikali inatarajia kuajiri watumishi 291 na kati yahao, watumishi 98 ni ajira mpya katika Mabaraza. Kwa hiyo,

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

tuna imani tukishawapata hao, basi yale maeneo yoteambayo yana upungufu wa watumishi hao katika Sekta hiyo,watakuwa wamepata. Kwa hiyo, nawaomba sanaWaheshimiwa Wabunge tuwe na uvumilivu, Serikali ina nianjema na itaweza kufanya haya yote kadri ya mudaunavyoruhusu na bajeti inavyoruhusu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine ilitolewakwamba, Serikali iangalie namna ya kupunguza gharamaza ujenzi wa nyumba za National Housing. Hil izimezungumzwa na wachangiaji wengi, lakini Kamati piaimelizungumza. Naomba niseme kwamba Serikali imepokeaushauri huu, lakini pamoja na hayo Mheshimiwa Raisalishatolea maelekezo, kwa sababu wengi walilalamikiagharama kwamba zimekuwa kubwa. Tumekuwa tukilielezasiku zote kwamba pengine gharama kubwa inachangiwana National Housing kufanya kila kitu wao wenyewe; kwakuweka miundombinu ya barabara, maji na umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, hili tayariMheshimiwa Rais ameshalitolea maelekezo kwamba Taasisizinazohusika na huduma, kabla National Housinghawajaweza kufanya uwekezaji wao, basi kama ni barabaraiwe imeenda, miundombinu ya umeme iwe imesogea namaji yawe yamekwenda. Wakiweza kusongeza huduma hizo,ni wazi gharama ya nyumba itapungua. Kwa hiyo, hililinafanyiwa kazi na Mheshimiwa Rais ameshalichukulia hatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili limefanyika hata kwenyehizi nyumba za Iyumbu zinazojengwa sasa hivi hapa, tayarimaelekezo yalishatolewa. Kwa hiyo, nina imani kwamba kwasababu maelekezo yamekwenda katika Halmashauri zotekatika kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais, WaheshimiwaWabunge ambao mnataka kuwekeza katika maeneo yenukwa kuwashirikisha National Housing, basi nadhanitukitekeleza hayo pia kwao itakuwa ni rahisi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, National Housing wakotayari kwenda maeneo yote na siyo National Housing pekeyake, hata Watumishi Housing ambao wanajenga nyumba

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

za watumishi nao wanahitaji kuwa na miundombinu hiyohiyo ambayo inatakiwa kuwekezwa. Hii itapunguza sanagharama za nyumba ambazo tunazungumzia. Kwa hiyo, hilitumelichukua na Rais amelitolea agizo na litatekelezwa kadriambavyo miradi itakavyozidi kuwekezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine ilitaka Wizaraihakikishe Manispaa ya Dodoma inatekeleza dhima iliyokuwaikifanywa na CDA na kupeleka huduma ya jamii yamiundombinu. Hii ilikuwa ni hoja ya Kamati na walizungumziaIyumbu na nimeshaizungumzia. Kwa hiyo, suala lamiundombinu limewekwa sawa.

Mheshimiwa Mwenyeiti, kuna suala lingine ambalolimezungumziwa, kuhusu kusimamia utekelezaji wa Sheria yaMipango Miji kwani kuna changamoto nyingi. Niseme tukwamba Sheria Na. 8 ya 2007 inazipa Halmashauri zetu zaWilaya na Miji pamoja na Manispaa mamlaka ya kupangana kudhibiti uendelezaji wa miji. Wizara kama msimamizimkuu, kwa Waraka wake Na.1 wa mwaka 2006 unaoelekezataratibu za kufuata katika kubadili matumizi ya ardhi namgawanyo wa viwanja na mashamba, hili linasimamiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile Wizara ilitoa WarakaNa. 4 mwaka 2006 ambao unatoa maelekezo ya miongozoya udhibiti ya undelezaji miji. Kwa hiyo, jukumu hili bado likokatika Halmashauri zetu kwa sababu sheria zipo. Tukiangaliatu Wizara peke yake tunaweza pengine tukachelewa kudhibitihili suala.

Mheshimiwa Mwenyeiti, naomba sana katika hiliHalmashauri zetu Sheria Na. 8 ya mwaka 2007 hii ya MipangoMiji lazima isimamiwe katika maeneo hayo. Haya yoteyataepusha hizo changamoto ambazo tunazisema. Kwahiyo, Wizara kama msimamizi, tuko karibu sana naHalmashauri kushirikiana nazo, lakini Waheshimiwa Wabungeni jukumu letu pia kuhakikisha kwamba tunapoona haliinakuwa siyo nzuri, kwa sababu tunahitaji miji iliyopangikana miji ambayo ni salama, ni jukumu letu pia kuwakumbushawataalam wetu kuweza kusimamia mambo hayo.

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la mipangokabambe ya miji ambayo inatakiwa isiishie kupanga tu mijimikubwa, bali ipanue wigo wake. Hili linafanyika na sasahivi kuna kujumla ya mipango kabambe 26 ambayo ikokatika hatua mbalimbali. Mpaka sasa mji wa Mtwarapamoja na Musoma mipango yake kabambe imekamilikatoka mwezi Mei na Mheshimiwa Waziri alikwenda kuzindua.Kwa hiyo, mipango mingine bado iko kwenye mchakato natutaendelea kufanya hivyo. Wizara imeandaa programu yautayarishaji wa mipango kabambe kwa nchi mzima ikiwemomiji midogo ambayo inakua kwa kasi. Kwa hiyo, hilitunalichukulia kwa uzito wake na tutaendelea kulisimamia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa hoja za hotubaya Waziri Kivuli, ametoa hoja nyingi sana. Niseme tu kwaujumla wake pamoja na zile ambazo nimemaliza kuzijibukwamba tunaandaa pia kitabu ambacho kitajibu hoja zote,maana kwa muda uliopo siwezi kuzijibu zote, nitajibu chachetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la kupima ardhiya Mkoa wa Morogoro kama mpango wa dharura ilikupunguza migogoro; wameongelea kwenye hotuba hiyo.Niseme tu Tume inaendelea na mipango ya matumizi boraya ardhi. Kama nilivyosema awali na hata katika kujibumaswali tunapojibu, Morogoro ilichukuliwa kama eneoambalo Serikali ilikuwa inaliangalia kwa jicho pana zaidikutokana na migogoro yake iliyokuwepo. Ndiyo maana zileWilaya tatu ambazo sasa tunapima ardhi yote, imeanziaMorogoro, ni kwa sababu ya tatizo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hil i nalotunalichukua, hivyo vipande vya ardhi vyote vitapimwa nakuwekewa alama za kudumu ili kuweza kuepusha hiimigogoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ambalo limeongelewakwenye maeneo ya Hembeti, Ndimboho, Buguma, Mkindo,Kigugo, Kambara vilivyopo katika bonde la Mto Mgongola

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

Wilaya ya Mvomero, nadhani Serikali itachukua taratibu zakevizuri kuweza kuona kwamba tunafanyaje, kwa sababu halihalisi kila mmoja anaifahamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume inashirikiana naprogramu ya kurasimisha ardhi katika Wilaya tatunil izowaambia. Kwa hiyo, hatua zinachukuliwa natunaendelea. Vile vile Tume inashirikiana na Halmashauri zaWilaya Mvomero na asasi za kiraia kama ile ya PELUMTanzania TFCG na IWASHI katika kutoa elimu. Lazima elimuiwafikie ili waweze kutambua ni nini kinatakiwa kufanyika.Kwa hiyo, haya yanafanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine, Kambi Rasmiimeongelea kuhusu changamoto kubwa ya kibajeti katikaWizara na wakashauri pengine Serikali iongeze nguvu katikakushirikiana na Sekta binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa Urasimishaji katikaeneo la Kimara ni mojawapo ya mfano ambao tunawezakuusemea. Mradi huu lengo lake pia ulikuwa umekusudiakurasimisha viwanja 6,000, lakini mpaka tunavyoongeleasasa, viwanja 4,333 tayari vilikuwa vimeshapimwa naHatimiliki zimetolewa 82 na kuna barabara ya urefu yakilomita tisa imetengenezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ile speed ndogo ya kutoahati inachangiwa na wananchi wenyewe. Kama Wizaraimeweza kupima viwanja 4,333 kati ya 6,000, ilikuwaimekusudiwa watu wote 4,333 wawe wamechukua hati. Sasahiyo huwezi kusema kwamba ni tatizo la Wizara. Ni tatizo lawananchi ambalo tunasema tunawapa elimu ili wawezekuona manufaa ya kurasimishiwa maeneo yao ili pia wawezekutumia zile hati katika shughuli za maendeleo. Viwanjavimepimwa lakini watu hawachangii. Ni jukumu letuWaheshimiwa Wabunge kuendelea kuhamasisha wananchiwetu kuchukua hati zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie fursa hii kwa walewote ambao zoezi hili linaendelea ikiwemo na Mkoa wa

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

Mwanza katika zile Wilaya za Nyamagana na Ilemela, lakinitunao wenzetu wa Musoma, Lindi, Kigoma, Uji j i naSumbawanga; nawaomba sana, zoezi hili ni kwa nia njemaya kutaka kuwasaidia wananchi. Kwa hiyo, pale ambapourasimishaji unafanyika, nawaomba sana wananchi, kwanzamchango siyo mkubwa ukilinganisha na gharama halisi yaupimaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kwambania ya Serikali ni nzuri. Kwa hiyo, watumie fursa hii ya sasaambayo ipo. Mkishaweka mipango kabambe katika maeneoyenu, unaweza kukuta urasimishaji tena hauna nafasi natusingependa tufikie hapo. Kwa hiyo, hatua tuliyonayo sasani vizuri wananchi wanakaifanyia kazi iliwaweze kufaidikana zoezi hili linaloendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabungewameongelea suala la migogoro kati ya mpaka wa KisopaKing’azi na Mloganzila; fidia ilishalipwa kama ambavyoilikuwa imetajwa katika masuala mazima ya uendelezaji nahii iko katika Wilaya ya Kisarawe ambayo ilikuwa imeanzishwakwa GN hiyo 117 ya tarehe 28 Novemba, 1980. Katika ulemgogoro uliokuwepo pale, wale ambao walikuwawameendeleza walikuwa tayari Serikali imelifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa GN 69 ya29/1/2016, eneo hilo la Ubungo ilimega sehemu ya Kinondoniambayo ilijumuisha maeneo ya Kisopa na King’azi, Mloganzilahiyo ilikuwa ni chanzo cha migogoro. Napenda kulitaarifuBunge lako Tukufu kuwa Wizara itashirikiana na TAMISEMI ilikupata suluhu ya mgogoro huu. Kwa sababu kamakunakuwa na mgongano wa GN au kunakuwa namgongano wa kijiji na kijiji, bila kuwa na elimu kwa walehasa walioko katika maeneo yale inaweza ikaleta shida;suala la mipaka wakati mwingine linakuwa lina shida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara nyingi Wilaya mpyainapoanzishwa siku zote inakuwa na changamoto zake, hasaupande mmoja unaposhindwa kuridhia ama kuachia baadhiya maeneo. Kwa hiyo, migogoro kama hii inakuwepo tu,

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

lakini Serikali itaendelea kushirikiana na TAMISEMI kuhakikishamgogoro huu unakwisha katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja nyingineinayosema Serikali imalize ufafanuzi kuhusu mgogoro wampaka kati ya vijiji na hifadhi ya wanyama Serengeti, ambayoimezungumziwa hasa katika maeneo ya Vijiji vya Marenga,Nyamakendo, Mbalimbali na vijiji vingine kama vilivyo, hivivyote katika Wilaya ya Serengeti vina mgogoro na hifadhikama ambavyo ilivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshauri tu MheshimiwaMbunge kuwa ni vema tukasubiri maamuzi ya Mahakama,sababu hili suala liko Mahakamani na hatuwezi kulitoleamaamuzi hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala lingine ambalolilikuwa limezungumziwa na Kambi Rasmi ya Upinzanikwamba Serikali ieleze Bunge sababu za kuipa TRA mamlakaya kukusanya kodi ya majengo ambayo ilikuwa ni chanzomuhimu kwa Halmashauri zetu. Tumesema TRA ilipewa jukumula kukusanya kodi ya majengo ili kuimarisha mfumo waukusanyaji kodi. Hii yote ilipangwa kwa nia njema katikakurahisisha ukusanyaji maduhuli ya Serikali na zoezi limeanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile limezungumziwasuala zima la kupanga rates ambazo pengine wakatimwingine zinaweza kuwa ziko juu au zipangwe kulinganana viwango. Hii tumechukua kama ushauri ambao tunawezakwenda kuufanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamezungumzia suala lakutatua migogoro ya eneo la mnada wa Pugu Kajiungenina UKIVIUTA, Kipawa. Eneo la Mnada wa Pugu Kajiungenilipo chini ya Wizara ya Kilimo na Mifugo na eneo hililimevamiwa na wananchi na kuendelezwa. Utatuzi wamgogoro huu utahusisha wadau mbalimbali ikiwemo Wizarayenyewe ya Kilimo.

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba wavutesubira kwa sababu itafanyiwa kazi. Vile vile kuhusu UVIKIUTA,suala hili lilifikishwa Mahakamani na Mahakama ilitoa ushindikwa UKIVIUTA. Kwa hiyo, nalo tayari lilishatolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna lingine limeongelewakwamba Wizara iandae takwimu za hati ambazo zipo.Ushauri umezingatiwa, tutalifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wameongelea pia suala laWakuu wa Wilaya kuingilia majukumu ya Mabaraza ya Ardhi.Suala hili, kwa mujibu wa Sheria ya Mabaraza ya Ardhi, SuraNa. 216 kama ambavyo imerejewa mwaka 2002, Mabarazaya Ardhi na Nyumba Wilaya ni chombo huru cha kuamuamigogoro ya ardhi. Hivyo haipaswi kuingiliwa na chombochochote katika kutekeleza majukumu yake. Kwa hiyo,masuala haya yako kisheria na tunasema yataendeleakusimamiwa chini ya sheria husika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la kuhamishaajira ya Watumishi wa Sekta ya Ardhi kutoka Halmashaurikwenda Serikali Kuu. Serikali itaendelea kutekeleza ile dhanaya D by D, hatuwezi kusema leo tunaibadilisha hapa kwasababu tayari utekelezaji wake unakwenda vizuri na wotetunaona, lakini hayo yote yatafanyika kwa utaratibu ambaoSerikali imepanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa kuhamishaajira za watumishi katika Sekta ya Ardhi kutoka Halmashauri,unakinzana na dhana hii ambayo Wabungewanaipendekeza. Ili kuongeza huduma kwa wananchi,Wizara imefungua ofisi za Kanda, kwa hiyo, tutashirikiana naWatumishi wa Ardhi kwenye Halmashauri kuona kwamba kazihizi zinafanyika katika utaratibu mzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabungewamezungumzia suala la Serikali kuwa na vipaumbele vyakutekeleza kulingana na mapato yake kuliko kuwa navipaumbele vingi ambavyo wakati mwingine havitekelezeki.

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kwambaSerikali imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kuwekavipaumbele muhimu ikiwa ni pamoja na kutekeleza bajetikulingana maoteo yanayopangwa katika projections zetutunazozifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, suala la kuwa navipaumbele vingi sidhani kama ni sahihi sana kwa sababuwakati mwingine unapanga ukitarajia kwamba maoteoyanakwenda kufanya kazi katika utaratibu uliopangwa.Isipokuwa wakati mwingine ufinyu wa bajeti unafanyausitekeleze jukumu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi kusema kwambausipange, maana hizi ni projection ambazo ni lazimauziandae. Kwa hiyo, unapoandaa unategemea pia utapatapesa na tunafanya kazi kwa cash budget, kwa hiyo, lazimapia haya nayo tuyazingatie. Pia fedha ya Serikali inatolewakutegemeana na makusanyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nawaomba tuWaheshimiwa Wabunge, tusisitize katika kukusanya pato laSerikali i l i tuweze kuhudumia bajeti zetu ambazotumezipitisha. Ni vema wananchi walipe kodi zao kwawakati ili kuwezesha Serikali kutekeleza majukumu yake.Usipolipa kodi kwa wakati, matokeo yake shida inakuwa nihiyo. Sasa hivi watu mpaka wafuatwe na Polisi, Summons zaMahakama ndiyo walipe kodi. Kwa nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tukiwa wazalendokweli, kila mmoja akatimiza wajibu wake; unajua unatakiwakulipa kodi ya ardhi kila mwaka, wewe lipa. Kwa niniunangoja mpaka uletewe Summons? WakipelekewaSummons za Mahakamani, kesho yake unaona foleni kubwaiko kwenye Ofisi za Wizara. Sasa hivi ukienda TRA hapaingilikikatika zile kodi za majengo. Watu wamejaa pale,wanashinda pale. Kwa nini unangoja mpaka ufikie hatuahiyo? Lipa kodi kwa wakati ili uondoe usumbufu. Tukiweza

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

kuwajibika, haya yote hayatakuwa tena na usumbufu katikautekelezaji. Kwa hiyo, ni jukumu letu kuona ni jinsi ganitunasaidiana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kupitia hojambalimbali za Kambi Rasmi ya Upinzani, naomba sasa nianzekujibu hoja za Waheshimiwa Wabunge mmoja mmoja nanitaziunganisha zile zinazofanana ili kwenda na wakati nakwa zile ambazo nitakuwa nimezijibu wakati najibu hoja zaKamati pamoja na Kambi Rasmi ya Upinzani, nitaziruka nasitazirudia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa InnocentBilakwate, Mheshimiwa Abdallah Ulega na Mheshimiwa ZuberiKuchauka, walikuwa wanazungumzia suala la kupunguzaurasimu katika upimaji ardhi kwa wananchi wa vijiji ilikuwaondolea usumbufu. Wizara yangu imepunguza sanagharama. Walikuwa wanazungumzia gharama nakupunguza urasimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu imepunguzasana gharama na hata kama kwenye bajeti mmesikia,tumezidi kupunguza gharama. Lengo letu ni kuhakikishausumbufu kwa wananchi haupo. Kwa hiyo, ni jukumu letukuwahamasisha wananchi wetu waweze kuona umuhimuwa kupima maeneo yao ili waweze kuwa na umiliki halaliambao utawasaidia pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la Wizara ni kuendeleakuhakikisha tunawawezesha wananchi. Unamwezesha kwakutumia ile ardhi yake; ukiweza kumpa Hakimiliki kisheriatayari utakuwa umemsaidia. Kwa hiyo, niseme kwambaWizara itaendelea na utaratibu wa kupata vifaa vya upimajiili waweze kupimiwa kwa urahisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa habari njema tu, kamammesoma magazeti ya jana, tayari kuna tenderimetangazwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa hivyo na ile Noobjection tuliyokuwa tunaisubiria kutoka World Bank, nayotayari imetoka. Kwa hiyo, tuna uhakika vifaa hivi mtakwenda

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

kuvipata na kazi itafanyika na watu watapimiwa,tuwahamasishe tu wajitokeze kwa wingi i l i wawezekupimiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala lingine ambalolimeongelewa na Wabunge kama wanane; ameongeaMheshimiwa Mama Makilagi, Mheshimiwa Paresso,Mheshimiwa Shekilindi, Mheshimiwa Mwassa, MheshimiwaBashungwa, Mheshimiwa Bilakatwe, Mheshimiwa Chumi naMheshimiwa Allan. Wamezungumzia kwamba Serikali itengefedha kwa ajili ya kuanzisha mabaraza. Nilishalizungumzialakini bado limejirudia. Lengo letu bado lipo pale pale,tumechukua hoja zetu na tutafanya kama ambavyoimekusudiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ule utaratibu wamaeneo ambayo pengine hayana Wenyeviti, nachukua fursahii kumwomba sana Mkuu wa Mkoa wa Singida pamoja naMkuu wa Mkoa wa Tabora; tunajua huko kuna matatizo naWenyeviti ambao muda wao tayari ni kama ulikwisha lakiniWizara il ishawaandikia barua kwa aji l i ya kuletamapendekezo katika hatua ile. Mpaka leo hawajatoa nalimejitokeza hapa kama ni tatizo. Kwa hiyo, nawaombasana Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa katika maeneo hayowatusaidie ili tuweze kutatua tatizo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia suala la uwezeshajiMabaraza nalo limezungumzwa na Mheshimiwa Paressotena, likazungumzwa na Mheshimiwa Makilagi, yamejirudiakatika maeneo hayo. Mabaraza yana changamoto nyingina ndiyo maana yamezungumzwa sana. Wenginewamezungumzia suala la kutoa elimu kwenye Mabaraza yaKata. Napenda niwakumbushe tu Waheshimiwa Wabungekwamba suala la Mabaraza ya Kata yapo chini ya TAMISEMI.Kila tunapokwenda katika ziara tumekuwa tukishirikiana naokuweza kutoa elimu katika yale mabaraza kwa kutumia waleWasajili wetu wa Mabaraza kwenye yale maeneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulishasema kwambaHalmashauri yoyote iliyopo tayari, Wizara ipo tayari kutoa

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

wawezeshaji wakisaidiana na Mwanasheria wa Halmashaurikuweza kuwapa elimu wale Wajumbe wa Mabarazawaweze kufanya kazi yao vizuri. Hii ni kwa sababu haya yapochini ya TAMISEMI, lakini kwa sababu yote yanasimamia Sektaya Ardhi, basi tunashirikiana kuhakikisha tunawapa elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la elimu lilizungumzwana Waheshimiwa Wabunge hapa ni kwamba wapewemafunzo ambayo imezungumzwa pia na MheshimiwaChumi, Mheshimiwa Bilakwate na Mheshimiwa Allan iliwaweze kufanya kazi yao vizuri. Tutaendelea kusaidiana naHalmashauri zetu. Lengo letu ni kuhakikisha kwamba hawawatu wanapata elimu na wanawasimamia masuala yoteya ardhi katika maeneo yao kwa sababu wao ndio hasawaliopo kwenye zile changamoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Bunge lako hili,nawashukuru sana viongozi wa Mkoa wa Katavi naSumbawanga, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya pamojana Wakurugenzi, wamechukua hatua mahususi ya kuwezakuanza utaratibu wa kutoa mafunzo ya mabaraza hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Wilaya yaKalambo walitoa mafunzo ya siku ya zaidi ya 20 kutakakuwezesha yale Mabaraza. Jambo hili linawezekana paleambapo dhamira ya dhati katika maeneo na viongozi husikawakiliona kwamba ni changamoto, inawezekana kuyapatiaufumbuzi. Nitumie fursa hii kuwapongeza na nitoe rai kwamikoa mingine kuweza kuiga mikoa hii miwili ambayoimeweza kufanya kazi nzuri katika kuelimisha Wajumbe waMabaraza waweze kufanya kazi zao vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa MbarakaKitwana alikuwa anazungumzia mgogoro wa Shamba laUtumani lenye ukubwa wa hekari 4,000 na shauri hili lipoMahakamani, kwa hiyo akataka sasa watu wa Mafiawafanyiwe ugawaji. Sasa nasema, hili suala bado halijafikiahatima yake. Kwa hiyo, haliwezi kufanyika jambo lolotekatika utaratibu huo, lazima hatua za Kimahakama ziishe ilituweze kwenda kwenye hatua nyingine.

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mheshimiwa Shangaziamezungumzia suala la Mnazi Sisal Estate la Lushoto ambalonalo amelizungumzia. Taratibu za kufuta zimekwamakutokana na miliki za shamba hili kuwekwa dhamana benki.Hii ni kwa sababu kuna wamiliki wengi wa mashambawengine walichukulia mikopo na hasa kwa Korogwe, Mkoawa Tanga, mashamba mengi sana yamechukuliwa mikopobenki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo linapokuwalimewekwa dhamana ya benki, huwezi kuanza kufanyataratibu nyingine. Kasoro hizi ambazo zinatokana na hiyo,Halmashauri inaagizwa pia itume tena ilani katika shambahilo ili benki waweze kupewa nakala ya ilani hiyo na ufutajiutaendelea baada ya taratibu zote kukamilika. Kwa sababukuwa na dhamana isiwe ni kikwazo. Tumeni tena ilani nabenki wapewe nakala ili wajue pamoja na kwamba wanadhamana hiyo, lakini shamba hili lina changamoto zake.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mwakasakaalizungumzia suala la nyumba za NHC, watu kununua kwawingi na kupangisha. Sina uhakika na malalamiko yake labdaangetupa mfano mzuri ni wapi, kwa sababu Tabora, Uyui naIgunga kuna nyumba zimejengwa pale, hazijapatawapangaji na hazijanunuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa aliyenunua na kuhodhinyingi ni zipi? Kwa sababu hiyo ni case study ambayo ikowazi kwamba nyumba zipo, lakini hazijanunuliwa. Ni vyemaakatufahamisha ni wapi ambapo nyumba zimenunuliwa namtu mmoja halafu anaanza kupangisha ili tuweze kuchukuahatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Lupembe vilevile amezungumzia nyumba ambazo zimejengwa lakinizinakaa idle. Niseme kwamba nyumba kukaa idle wakatimwingine Halmashauri pia zinakuwa zinahusika. Mnaombakujengewa, zinajengwa. Zikishajengwa zimekamilika, hamkotayari kuchukua. Sasa hii kidogo inakuwa ni shida. Ndiyo

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

maana tukasema, Mheshimiwa Kalanga alikuja na wazo lakwamba watu wapewe miaka mitano kulipa lakini Shirikala Nyumba linatoa miaka 10 kwa mpangaji mnunuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe maelekezokatika nyumba zilizojengwa ambazo Halmashauri hazijawatayari kuzichukua, utaratibu wa shirika utabadilika kulikokuacha ziharibike, zitakwenda kwenye ile sera ya mpangajimnunuzi na zitauzwa kwa mtu yeyote aliyeko tayari kununuaili zile nyumba ziweze kupata wapangaji. Ikienda kwampangaji mnunuzi, maana yake una miaka kumi ya kuwezakulipa. Mheshimiwa Kalanga aliomba miaka mitano, lakiniNational Housing wameweka miaka 10. Kwa hiyo, badonafasi tunayo ya kuweza kutumia nyumba hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana, kwa sababutusipofanya hivyo, haya mambo wakati mwingine tunawezatukawa tunawalaumu wawekezaji, tunalaumu NationalHousing lakini sisi wenyewe tunaohitaji pia tunakwamisha.Niwape mfano mzuri wa Jimbo la Busokelo, waliombawakajengewa nyumba nzuri za mfano na tayariwamechukua; na Jimbo la Momba pia nao wamejengewanyumba nzuri na zinafanya kazi na wanakwenda hatuanyingine ya pili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Halmashauri zetu,mnapohitaji muwe tayari pia kuhakikisha kwambamnakwenda kuzichukua nyumba zile ili kuepusha uwekezajiunaokwenda kudumaa. National Housing hawawezikusonga mbele kama wanawekeza halafu haziendi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Sakayaameongelea wawekezaji wa miradi mbalimbali kwambawapewe ardhi kuenenda na maeneo yanayofaa katikamiradi husika. Viongozi wa Vij i j i wapewe elimu. Hil itumelichukua kwa sababu Sheria ya Ardhi iko wazi na inatoautaratibu mzima wa ugawaji ardhi. Sasa katika hili nadhanini elimu tu izidi kutolewa kwa watu wetu waweze kujua nijinsi gani ya kuweza kusimamia haya.

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tatizo la ujenzi holelaambalo limeongelewa na Mheshimiwa Kigola. Nadhaninimeliongelea kwa upana wakati nazungumzia masuala yauandaaji wa mipango kabambe na kuhamasisha wananchikutojenga ili kuepuka hili. Wizara inashirikiana na mamlakaza upangaji katika maeneo hayo ili kuandaa mipangokabambe na hili suala litakuwa limepungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Cosato Chumiameongelea kupewa baadhi ya Watumishi nyumba za CDA.Wizara haihusiki moja kwa moja na utoaji wa nyumba hizikatika kupangia watumishi, lakini haya yamepokelewa nayanaweza kufanyiwa kazi kulingana na maombi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Watumishi wa CDAkutawanywa katika maeneo mengine, hili pia lipo chini yaWizara husika kwa sababu CDA sasa hivi ipo chini yaManispaa ya Dodoma, maana yake ipo chini ya Ofisi yaTAMISEMI. Hivyo, Wizara inayohusika kwa kushirikiana naWizara yetu, kwa sababu wako pia Watumishi wengi tu waSekta ya Ardhi, basi tutaona ni jinsi gani bora ya kuwezakutatua hilo tatizo na hasa katika kuwapanga watu katikamaeneo yanayotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani muda umekuwafinyu na mambo ni mengi. Naomba uniruhusu tu nizungumziesuala moja la asilimia 30 ambayo imezungumziwa. Nduguzangu suala la asilimia 30 limezungumziwa na WaheshimiwaWabunge nane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nirudie tena;baada ya ile Sheria ya Bajeti mwaka 2016 tulivyoipitisha yakuondoa mambo ya retention, asilimia 30 haipo tena. Ndiyomaana tulisema na nikipita katika ziara nawaambiakwamba Halmashauri zinazopanga bajeti ya asilimia 30kutegemea Wizara, tunapotosha bajeti zetu, kwa sababuhiyo iliondolewa katika bajeti iliyopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pesa zinazokuja kwenyeHalmashauri, zinatokana na OC ambayo Wizara inakuwa

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

imepangiwa shilingi bilioni kumi kwa mwaka 2016/2017 kwanchi nzima na zinatolewa kutegemeana na zinavyoingia.Kwa hiyo, haiji kama asilimia 30 ambayo wewe unaiweka.Kwa hiyo, unapoweka kwenye bajeti yako asilimia 30kwamba unadai Wizara, kibajeti kidogo inakuwa haiko sahihisana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nisisitize katikahili maana limekuwa likijirudia, hakuna asilimia 30 kama 30inavyorudi kule. Kinachokuja ni OC kwa ajili ya kuziwezeshaHalmashauri zetu kwa shughuli za sekta na pesa hizo lazimazifanye kazi ya Sekta ya Ardhi na siyo Mkurugenzi kupangamatumizi yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sana,zitakuja kwa kadri zinavyoingia kutegemeana na bajeti yaWizara iliyowekwa kuliko hiyo ambayo ninyi mnaitegemeasasa kwamba ni asilimia 30, inapotosha kila kitu katikamaelezo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naunga mkono hoja na nawashukuru kwa kunisikiliza.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziriwa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa majumuishomazuri. Sasa namkaribisha mtoa hoja, Mheshimiwa Waziri waArdhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili aweze kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana wewe naWaheshimiwa Wabunge, kwa heshima mliyotupa Serikalikupitia Wizara yangu kwa michango mizuri sana. Kila mmojaalikuwa anatamani kusikiliza michango kuanzia mtu wakwanza mpaka wa mwisho, yaani tumefanya kazi ya kibungevizuri. Hakuna jambo ambalo mimi sikuandika; kila jambo

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

nimeandika. Ingawa sikuandika maneno yote, lakini angalaukila hoja ya mtu naijua. Naweza kusema tulikuwa very seriouskatika kujadili mjadala huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nawapongezasana nasi kama Wizara tutaendelea kutekeleza mwongozowa Rais, Mheshimiwa Dkt. Magufuli; yeye kila siku anasemakwamba yeye ni Rais wa CCM, ametokana na CCM ndiyo,lakini amechaguliwa na Watanzania wote na kila maraamekuwa anasisitiza tutoe huduma bila ubaguzi wowote.Kwa hiyo, ndiyo maana spirit ya Wizara yangu ni kutoahuduma kwa wananchi wote na wananchi wotetutaendelea kuwahudumia bila ubaguzi wa aina yoyote.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ndugu zangunawashukuru sana kwa niaba ya Wizara yangu na wenzanguwote, tuendelee kushirikiana, maana yake hii kama ninyimsingekuwa mnashirikiana nasi pengine tusingejua matatizoyenu. Kwa hiyo, tuendelee kushirikiana na moto ni huo huo.Tuna Ofisi hapa Dodoma, tuna Ofisi sasa kwenye Kanda nahapa nyuma yangu nimeleta viongozi wote wa Kanda nane.Kwa hiyo, kila jambo mlilolisema kama linahusu Mabarazaya Ardhi, Msajili wa Mabaraza yupo hapa, Amina. Kamalinahusu ardhi Kanda ya Magharibi, Kamishna na Msajili wapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge li jalo Munguakipenda, mtazungumza mkiwa na Mthamini wa Kanda,Mpima wa Kanda, Kamishna wa Kanda, Msajili wa Kandana wote hawa watakuwa wamekamilika na watumishi waona vitendea kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili alilosema MheshimiwaNaibu Waziri, tumesema moja ya jambo ambalommelizungumza watu wengi humu ndani, kwambatunakwama kupanga na kupima mashamba na wananchikupata viwanja vyao kwa sababu hamna vifaa;tumeshaagiza vifaa.

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumetangaza kwenyegazeti, tutavisambaza hivi vifaa tena kwa teknolojia mpya,kwa sababu sasa tunatumia satellite na vifaa vya mapokeziya satellite tumewaonesha jana, tumevinunua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tutakuwa na vifaaambavyo vinapima kwa upana mkubwa kwa teknolojiampya na tutawafundisha Maafisa wenu wote. Tutawaita hivikaribuni, Maafisa wenu wote Wapima, hawavijui hivi vitu,tutawafundisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkipata nafasi, kule nyumatumeweka Maonesho ya Wapima Binafsi, baadhi ya vifaavya kisasa vya upimaji viko nyuma kule tunakofanyia sherehe.Atakayepata nafasi aende. Tunaposema RTK mtaziona kule,kwa nini kifaa hiki kinaweza kikapima mpaka kilometa 30kwa wakati mmoja na kikatumia watu wawili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Wilaya yako yoteinaweza ikapimwa kwa siku tano au sita tukapimamashamba yote. Kwa hiyo, teknolojia hii tumeagiza natutasambaza kwenye Kanda na awamu ya pili tunakwendakuandika tunataka tupeleke vifaa hivi kila Wilaya ili hatakama unamwita mpima binafsi, basi uwe una kifaa chakoinapunguza gharama. Kwa hiyo, tutatatua kero za ana kwaana, lakini tunafikiri vilevile twende kwenye mifumo nabaadaye tutakuja kwenu kuomba sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachowashukuru nikwamba mmetusaidia sana kuainisha mambo mbalimbalina haya sasa siyo kujibu tu kwa maandishi lakinitutayapangia na ratiba, tutakuja Mikoani kote huko. TutakujaKilimanjaro kufanya audit, tutakwenda Chumbi kwa rafikiyangu Mchegerwa, tutakwenda Mikoa ya Kagera kuleKaragwe, tutaenda kila mahali. Tutakuja mikoani. Sasa hatujimikoani tukisubiri ratiba za mikoa, tutakuja kuthibitisha haya.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshajua mambo yakuanza nayo. Tutakuja kila mkoa. Mkoa wa Manyara, Iringa,

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

Ruvuma mpaka Mbinga tutakuja na kila mahali tutakuja,angalau tuna mambo ya kuanzia. Nataka kuwahakikishienikwamba haya yote tutayaandika, lakini tutawapa majibu ilimjue lakini yatatusaidia sana tukija mkoani kufuatilia hayana kuhakikisha tunayatatua on the spot. Kwa hiyo, tutakujandugu zangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepanga Kanda vizuri,sasa tunateua Watendaji wetu wapya kwenye Kandawafanye hii kazi, mambo yote tutayafanya. Dar es Salaamtutakuja wenyewe nami bado nipo pale, yale yote ya Dar esSalaam tutayamaliza; ya Dodoma hapa tutayamaliza namikoa yote tutafika na kuyafanyia kazi. Kwa hiyo, nafikiriWaheshimiwa Wabunge hebu msubiri tuje. Tuna ratiba yamiezi 12 kabla hatujakutana hapa, tushirikiane huko hukomikoani kutatua haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo mengi yatatatuliwa,tutaulizana tena huko mikoani na wenzangu wanaotokahapa wanaanza kuyafanyia kazi. Inawezekana baadhi yamambo mkirudi huko mtakuta yamekwisha kwa sababuviongozi wangu wa kanda wote wapo hapa wamesikiliza.Sasa tumewawezesha na magari mapya, wanakimbia kilamahali, kwa hiyo, hawana shida sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ndugu zangunawashukuru sana kwa haya yote mliyoyasema natakakuwaahidi kwamba tutawajibu kwa maandishi, lakinitutakuja huko mikoani, tutajadiliana sana, tutafanyamakongamano, tutaitisha na viongozi wengine wa mikoatuzungumze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi inayoendeleakubatilisha mashamba ya watu ambao hawayatumii,tutaendelea kuifanya kila mahali; kazi ya kukagua mashambayasiyotumika, tutafanya; kazi ya kupima kwa kasi ili kila mtuamilikishwe kiwanja, tutafanya. Leo ingawa badomnazungumza gharama, lakini hizo gharama mnazozijuatumepunguza tozo kwa asilimia 67. Kwa hiyo, Mheshimiwawa Mbinga hebu angalia taarifa yako. (Makofi)

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

Mheshimiwa Mwenyekiti, gharama kubwa ambazohata ninyi Waheshimiwa Wabunge mna offer nilizowapa,angalieni ile kitu inaitwa premium mlicholipa; 67 ya ilemliyolipa imepungua. Kwa hiyo, umilikishaji sasa utakuwanafuu sana na tungependa kutoka sasa Halmashauri zotezisiruhusu hata kidogo watu kujenga katika maeneo auviwanja ambavyo havijapimwa na kupangwa. Kwa sababukilio chao cha kupunguza tozo tumefanya, gharama zaupimaji zitapungua sana na hivyo hakuna sababu mtukuendelea kuvamia na kujenga katika maeneo ambayohayajapimwa. (Makofi)

(Hapa kengele ya kwanza ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Nafikiri ni kengele ya kwanza!

MWENYEKITI: Ndiyo.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Eeeh!

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimwambie nduguyangu Mheshimiwa Malocha, alizungumza juzi hapa kwauchungu sana juu ya shamba lake la Malonjo. Watu wakommelitoa nje ya Mahakama mzungumze. Malizenimazungumzo, mimi nasubiri. Wakati ule niliwashauri mpelekenotice na mtu wangu alisaidia kuandika notice tuka-servenotice kwa Efatha, lakini akawapeleka Mahakamani. Ninyimmetoa kesi Mahakamani mzungumze. Zungumzeni, miminawasubiri. Kwa hiyo, kabla mambo hayajaja kwangu,msinilaumu. Nilisema miezi sita mkileta kwangu nitakuwanimeamua, lakini haijaja kwangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nafikiritutashirikiana na nimemwomba Mkuu wa Mkoa wa Rukwaasimamie hayo mazungumzo yenu, Mheshimiwa Malocha naWabunge mshiriki haya mazungumzo ili yaishe vizuri. Kwasababu hata yule mwekezaji ajue, lolote atakalofanya,

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

hataweza kulima lile shamba kwa ustaarabu kwa sababuwale wananchi wamechukia. Kwa hiyo, kwa mwekezajilazima ajue kwamba lile shamba ni moto na wananchimtekeleze haya mazungumzo yenu vizuri, win-win situation,mwendelee na hilo shamba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na shukrani zanguzote nimalizie kwa kusema changamoto zilizoainishwakwenye mapendekezo yenu na hoja zenu ni nyingi sana, yaaninashindwa hata nianzie wapi; lakini ya Watumishiimezungumzwa sana hapa, Watumishi hatunao.Tutakachokifanya cha dharura kwanza, tutashirikiana naTAMISEMI kuangalia watumishi waliopo tuwapange vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika zunguka yangunimegundua kuna Wilaya zimependelewa, kuna Watumishiwengi sana. Ilemela na Nyamagana wana Watumishiwasiopungua 100 Wilaya mbili wa Sekta ya Ardhi,tutawaondoa huko. Hii ni kwa sababu kuna Wilaya nyinginehaina Mtumishi hata mmoja wa Sekta ya Ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutapita, kabla yakuajiri wapya, tutaangalia uwiano wa jinsi walivyopangwaili tuwa-switch angalau kazi za dharura ziweze kufanywa kwawatumishi waliopo tugawanye vizuri ili watumishi hawawasambae maeneo mengine. Watu watapangwa upyahalafu baada ya hapo ndiyo tutasimamia vibali kwaMheshimiwa Angellah Kairuki ili wapya wakipatikana,tuwapange vizuri. Upangaji haukuwa mzuri tutaurekebisha.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wengi mmezungumzahabari ya asilimia 30; masuala haya ya upangaji na kodi yaasilimia 30, kinachosisitizwa hapa ni kwamba tungependamiji yetu ipangwe, watu wajenge kwenye viwanjavil ivyopangwa, lakini watu wamilikishwe mashambaangalau wapimiwe ili wapate hati. Sasa imekuja tu asilimia30 lakini faida kubwa zaidi ya watu kujenga kwenye viwanjavilivyopangwa ni kuendeleza miji yetu vizuri.

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, msiangalie tuasilimia 30, mwangalie vilevile kwamba hawa watu koditunazokusanya tunazikusanya kwenye viwanja ambavyovimepangwa na kupimwa, kwa hiyo, Miji yetu imepangika.Kwa hiyo, tuendeleze kasi ya kushirikiana ya kupanga Miji yetuili iweze kupangika vizuri na kuwawezesha wananchi kupatahati. Kila mwananchi akipata hati, tutaelewana.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Waziri. Naombauhitimishe hoja.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, MheshimiwaKiongozi wa Upinzani, lile suala la kutoza kodi kwa viwanjavya mijini na mashamba madogo madogo ya mijini ambayohayajapimwa, nina maelezo ya ziada. Nitakutafuta wewena Mheshimiwa Mwassa wenye hoja hii, tuzungumze,tujadiliane. Kinachokufanya wewe useme ni shamba lakomjini ni nini? Hicho hicho tuta-register.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu haiwezekaniwewe unapata faida kubwa pale mjini, una ekari 40 Dar esSalaam, una ekari 4,000 Dar es Salaam hutaki kupima, lakiniunauza vipande vipande unapata hela; hulipi capital gain.Hivyo hivyo, unavyojifanya wewe vinavyokutambulishakwamba ni shamba lako, tutavisajili hivyo hivyo na utatulipapesa, lakini nitawatafuta ninyi wawili, msishike shilingi iliniwafahamishe vizuri. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, MwenyeziMungu awajalie wale wanaoendelea kufunga na sisi walafutari, makobe, tupo, tutawasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri waArdhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuhitimishahoja. Katibu.

WABUNGE FULANI: Hajatoa hoja.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, naafiki.

(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

MWENYEKITI: Ahsante, hoja imeungwa mkono. Katibu,tuendelee.

NDG. LAWRENCE MAKIGI – KATIBU MEZANI:

KAMATI YA MATUMIZI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 48 – Wizara ya Ardhi, Nyumba naMaendeleo ya Makazi

Kif. 1001 Administration and HR Mgnt.. … Sh. 6,736,586,549/=

MWENYEKITI: Tumeshapokea majina ambayotutaanza nayo. Tunaye Mheshimiwa Lwakatare na hukutunaye Mheshimiwa Jitu Soni na Mheshimiwa Ester Mmasi.Tuanze na Mheshimiwa Lwakatare.

MHE. WILFRED M. LWAKATARE: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Katika mchango wetu kama Kambiya Upinzani, tulilizungumza kwa kina na kulihoji suala labomoa bomoa pale Dar es Salaam. Sitaingia kwenye angleambayo wakati wa kujibu Serikali ilizungumzia masuala yaMahakamani kwamba haiwezi kutoa maelezo. Ni suala laprinciple tu, ambayo nikiacha historia niliyoieleza ya barabara

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

ile ya Morogoro, lakini ningetaka Serikali itufafanulie na kwafaida ya wananchi hasa upana wa barabara na huu utataunaozungumzwa sana na kuleta sintofahamu, unaanziawapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu nikiendakwenye sheria ya mwaka 2007 ambayo il ikujakutengenezewa kanuni mwaka 2009, upana unaotamkwaunakuwa na maana ya pande zote mbili. Kama upanaukitamkwa wa mita 60, maana yake inakuwa 30 kwa 30;ukitajwa upana wa mita 90, maana yake ni 45 kwa 45; naikitajwa 121 maana yake ni half ya hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hii ya 121 upandemmoja na 121 upande mwingine, barabara yenye upanawa 240 na kitu, yaani ni viwanja vya mpira viwili na kitu,inatoka wapi? Ni barabara ya wapi hii? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatukatai Serikali inawezaikawa na shughuli za kimaendeleo katika eneo fulani;tunafahamu kabisa watu waliolipwa fidia ni mita 28.85, sasawatu wanaokuwa nje ya mita hizo mbona hawazungumziwikwenye fidia?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba majibu nayasipotoka kisawasawa, nakamata shilingi yako, sijui utakulawapi?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kupatafursa hii ili niweze kufafanua hoja ya bomoa bomoa ambayoWaziri Kivuli, Mheshimiwa Lwakatare, ameiongelea. Naombatu nimweleze kwamba eneo hilo lina historia ndefu nakulishawahi kuwa na kesi na hatimaye Mahakama ikaamuakatika eneo hilo. Wanaokaa pale wanalifahamu sana,mwanzo kwa kupitia Mawakili wao na hatimaye kesiikaamuliwa.

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

Mheshimiwa Mwenyekiti, lile eneo liko maalum, linafuti, maana wakati huo masuala ya mita hayakuwepo katikasheria, lina futi 400 kila upande na ndiyo msingi wa kesiambayo iliendeshwa na hatimaye Serikali ikashinda. Kesiiliamuliwa mwaka 1997, kwamba eneo hilo ndiyo hifadhi yabarabara na ilipangwa muda mrefu tu tungeshawezakuliendeleza hilo muda mrefu lakini hiyo kesi ndiyo ilikuwaimesimamishwa kwa muda mrefu na bahati nzuri tunashukurukesi iliisha na hivi sasa tunatekeleza tu hukumu ya Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upana ni futi 400 ambayoukija kuibadilisha kwa mita unapata mita 121.5. Huo ndiyomsingi wa maamuzi hayo, ni ya siku nyingi; ni eneo ambaloSerikali ilishali-claim, ilishalilipia fidia kwa wale ambaowalistahili kulipwa fidia mwaka 1977 na hatimaye ugomviwa pale uliisha. Kwa kweli nashukuru sana wananchi wengikatika maeneo yale wanalifahamu hilo na wako tayarikubomoa maeneo yale. Walikuwa wanadhani tu kwambamipango ya Serikali labda imesimama kwa muda mrefu, kwahiyo, wakayaendeleza yale maeneo huku wakijua kwambawako ndani ya hifadhi ya barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami naomba sana nduguzangu, mtupe fursa ya kujenga miundombinu na katika eneohilo, lipo kwa mujibu wa sheria na uamuzi ulishapita mwakahuo niliosema, 1997. Hukumu ilitoka.

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri,umeeleweka. Mheshimiwa Lwakatare.

MHE. WILFRED M. LWAKATARE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Mheshimiwa Naibu Waziri sijuikama anakwenda na reality ambayo ipo. Kwa kweli katikasuala hili naomba nitoe shilingi ili Waheshimiwa Wabungewapate nafasi ya kujadili hoja hii, kwa sababu eneo lililolipiwafidia ni la mita 28.8 na ushahidi upo. Sasa Mheshimiwa Wazirianapozungumza kwamba hilo eneo lote limelipiwa, ni uongona nina uwezo wa kuthibitisha nikipewa muda, kwambaeneo lingine halijalipiwa na watu wanadai. (Makofi)

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nieleze, hizi futi 400ambazo ame-convert kwenye mita 121, ni kutoka wapi?Katikati ya barabara kwenda pande zote au ni katikati,tunazigawanya mara mbili? Ndiyo hilo nataka nipate majibuhapo. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa hujatoa hoja.

MHE. WILFRED M. LWAKATARE: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kuondoa shilingi.

MBUNGE FULANI: Toa hoja.

MHE. WILFRED M. LWAKATARE: MheshimiwaMwenyekiti, natoa hoja ya kujadiliwa.

MHE. JAMES K. MILLYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naafiki.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tizeba, Mheshimiwa Jafona huku Mheshimiwa Millya na mwanamke, MheshimiwaMwassa. Wanatosha. Basi Wanatosha hao jamani,tunaendelea.

MBUNGE FULANI: Mwenye Jimbo.

MBUNGE FULANI: Tunawahi kwenda kuswali!

MWENYEKITI: Mwenye Jimbo! Basi tumtoe mmoja,tunamweka mwenye Jimbo. Haya, tunaanza na MheshimiwaJafo.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikia hojaya kaka yangu hapa, Mheshimiwa Lwakatare, ni hoja yamsingi, lakini nadhani Mheshimiwa Waziri hapa, nina wasiwasiinawezekana tukam-slaughter bure, tutamwonea kwa eneolake kwa sababu mshahara wake huo wa Waziri ambapotukienda nayo inawezekana tukamwonea.

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana tulikuwa na jambokubwa la consensus kwamba leo mjadala huu uende vizuritumalize salama; na kwa sababu najua jambo hili ilibidil i lelewe vizuri katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano, ndiyo kama tungekamata mshahara waMheshimiwa Waziri ingekuwa kidogo na utamu wake.(Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niombe tuMheshimiwa Lwakatare, nadhani hoja yako ni ya msingiimesikika. Kama Serikali, tumesikia hizi concern kuona ninitutafanya kuboresha mambo mengine ya msingi ili mradiwananchi wapate huduma yao vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hilo tu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa mwenye Jimbo halafukatika ninyi wawili, mmoja. Tumekubaliana.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi nami nichangie hoja yaMheshimiwa Lwakatare.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziriameliambia Bunge kwamba wananchi wa eneo hili wapotayari kubomoa na wapo tayari kuhama. Habari hii siyo yakweli. Wananchi wa Kimara na Mbezi hawako tayarikubomoa. Ndiyo maana wanajiandaa sasa hivi kwendaMahakamani kuomba zuio ili eneo hilo lisibomolewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Wazirianasema katika maelezo yake, kwamba eneo hili ni eneo labarabara na kwamba barabara hiyo imekuwepo kwa miakayote hiyo, lakini wananchi wa Kimara wanaishi pale kwa hatiya kijiji iliyotolewa mwaka 1974.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Wazirianazungumzia mambo ya 1977. Kama barabara walijuamwaka 1977 kwamba itapita Kimara, kwa nini mwaka 1974

Page 178: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

walitoa hati ya kuishi? Hati ya wananchi wa Kimara,wananchi wa Mbezi ni ya mwaka 1974 ya Vijiji vya Ujamaa.Mheshimiwa Waziri anazungumzia mambo ya mwaka 1977.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wako tayarikuhama, lakini ni lazima walipwe fidia. Haiwezekani watuwamefanya kazi miaka 30, 40, wamejinyima, wamejenganyumba zao halafu Serikali ikabomoe hizo nyumba bila kulipafidia. Mbona maeneo mengine wamelipa fidia? Mbonakatika maeneo ya Majimbo mengine wamelipa fidia? Kwanini wananchi wa Kimara, Ubungo, Mbezi na wananchi waJimbo la Kibamba wasilipwe fidia?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatupingi ujenzi wabarabara, tunachotaka wananchi ni wananchi walipwefidia.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Tunaendelea na Mheshimiwa Mwassa.

MBUNGE FULANI: Iko Mahakamani tayari.

MHE. SALMA M. MWASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Nami niendelee kuunga mkono hoja ya MheshimiwaLwakatare hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, NaibuWaziri, mimi naona bado hujaelewa vizuri Sheria za Ardhi.Kwa sababu unavyotuambia kwamba toka mwaka 1970,kama umeweka 1970 mark ya eneo ina maana hilo eneoulitakiwa ulilinde. Kama watu wamejenga wewe ukiwepo,kuna maghorofa makubwa, watu wamekaa, ulikuwa wapi?Sasa kwa nini uweke alama? Kwa sababu umiliki wa ardhi

Page 179: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

unasema kwamba mmiliki lazima alinde eneo lake. Sasakama ni road reserve, ulikuwa wapi mpaka mwananchianajenga? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi mtu ambayealizaliwa mwaka 1970 ni mzee na Sheria ya Ardhi ya Mwaka1999 inasema kwamba mtu akikaa kwenye eneo husikamiaka mitano anapata umiliki wa asili. Basi wale wana umilikiwa asili, kwa sababu tayari wana miaka zaidi ya 40 pale.Kwa hiyo, wana haki ya kulipwa fidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Ardhi,Wizara hii ni mtambuka, ashirikiane na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano waende kwenye hilo eneo, Mbezina Kimara, wawapatie fidia zao. Hawawezi kuwawekea ‘X’miaka!

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza hizo ‘X’ zilizowekwazimewekwa miaka isiyozidi hata mitano na ile markingimewekwa hivi karibuni, siyo miaka ya 1970. Kwa hiyo, wanahaki ya kulipwa fidia. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Eng. Kamwelwe, NaibuWaziri wa Maji, halafu Mheshimiwa Tizeba.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kupata nafasihii ili nitoe historia kidogo. Barabara ya Morogoro ina hifadhiya futi 400 kila upande. Hifadhi hiyo iliwekwa na Mwingerezabaada ya Vita Kuu ya Pili. Eneo hilo lililipwa na Mwingerezaikiwa ni pamoja na mashamba ya katani na cheque zamashamba ya katani zilikuwa zimeandikwa ‘X’ Enemy.(Makofi)

(Hapa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliongea bila mpangilio)

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Subirininiwaambie. Kwa hiyo, hiyo ni hifadhi ya barabara naMwingereza aliweka na maandishi yapo. Ni kwa nini aliweka

Page 180: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

hifadhi hiyo? Ni kwa sababu alikuwa amelenga kwambaMiji ya Dar es Salaam na Morogoro itaungana na akaonakwamba maendeleo yatakuwa makubwa kiasi kwambacontainer terminals hazitakaa kule Bandari ya Dar es Salaam,ila zitakuwa ziko pembeni ya barabara ya Morogoro nakwamba zitajengwa trams kutoka Dar es Salaam kwendaMorogoro, ndiyo maana aliweka hifadhi hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbungeanasema kwamba walilipa mita 28.8. Kipindi Mwingerezaanalipa fidia, concentration ya binadamu ilikuwa kaeneokadogo kwa sababu ni miaka hiyo ya nyuma. Maeneomengine yalikuwa ni mapori ndiyo maana ukienda kupatarecord utakuta kaeneo kalikolipiwa fidia ni kadogo kwasababu watu waliokuwa wanaishi hilo eneo walikuwa niwachache. Kwa hiyo, eneo hilo tayari lilishalipiwa fidia naushahidi upo na cheques zipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kulikuwa na kesi.Kwenye hiyo kesi, mimi nilikuwa shahidi wa Serikali natulishinda. Wananchi wa Kimara walishtaki na aliyekuwaanawasaidia ni Mwalimu mmoja wa Chuo Kikuu anaitwaProfesa Mgongofimbo. Mimi nilikuwa shahidi wa Serikali nakesi hiyo tulishinda na ushahidi wa kushinda upo. Kwa hiyo,huwezi ukalipa fidia mara mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba tuMheshimiwa Mbunge arudishe shilingi ya Mheshimiwa Wazirikwa sababu ushahidi wote upo. Eneo hilo limelipiwa, ni halali,ni mali ya Serikali. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa kwa historia fupi,tunaendelea na Mheshimiwa Tizeba.

WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba niendelee hapo alipokomeaMheshimiwa Eng. Kamwelwe kwamba, suala likishaamuliwaMahakamani, mtu yeyote ambaye hakuridhika na uamuziwa Mahakama, haji Bungeni isipokuwa anakwenda tenaMahakamani. (Makofi)

Page 181: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa sababuuamuzi ulishatolewa na Mahakama katika kesi mbalimbali,mimi niwashauri sana Mheshimiwa Lwakatare na MheshimiwaKubenea, yule ambaye anadhani kwamba kilichotendekasiyo haki anayo nafasi bado ya kuendelea kutafuta haki yakeMahakamani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, sheria mbilizinazotawala mambo ya ardhi katika miji, Sheria Na. 378 yaMipango Miji na Sheria Na. 167 ya Barabara zinataja wazisize za mabarabara katika maeneo ya miji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maeneo ya mijibarabara ni kiwanja kama kingine; ina urefu na upana nakila kitu na vyote vinafahamika. Kwa maana hiyo, nirejeekwa hoja aliyoisema Mheshimiwa Mwassa kwamba kunawatu kwa sheria fulani wamekaa miaka mitano, hilo jambohaliendi automatically. Unaweza ukapata haki hiyo kamamwenye hilo shamba au hicho kiwanja amekuwahakulalamikii kwamba uwepo wako pale unavunja haki yakeya umiliki wa hicho kiwanja au shamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mamlaka za Serikalizimekuwa mara zote zikiwaambia wananchi wa Kimarakwamba hapo mnapojenga ni eneo la hifadhi ya barabaraau ni right off way ya barabara ya Morogoro - Dar es Salaam.Kwa hiyo, haya mambo kwa yeyote ambaye anadhanikwamba bado mambo yake hayajafanyiwa haki, arejeeMahakamani, akate rufaa, haki yake itapatikana huko.

Mheshimiwa Lwakatare, mwachie Mheshimiwa Wazirishilingi yake na wale wote wanaofikiri wako bado aggrieved,wanayo haki ya kurudi Mahakamani kutafuta haki yao.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lwakatare umeridhika amatulihoji Bunge?

MHE. WILFRED M. LWAKATARE: Mheshimiwa ni hivi,kaka yangu Mheshimiwa Lukuvi ananielewa. Sualalinalotakiwa hapa ni jepesi tu, la kuangalia tuendeje mbele.

Page 182: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

Sitaki kuingia kwenye mtazamo wa mmoja wa WaheshimiwaWabunge ambaye amesema majibu ya Mheshimiwa Wazirianayashangaa huenda alikuwa hajafika hata Dar es Salaam,pamoja na kwamba yeye ni shahidi. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nilichotaka kujua,Kanuni za mwaka 2009, urefu unapotajwa wa barabara,tafsiri yake inakua ni kuanzia katikati ya barabara,unaigawanya mara mbili; kwenda huku na kwenda huku.Nataka kujua, hiyo 121 kwenda hivi na 121 kwenda hukummetoa kwenye Kanuni zipi? Hilo ndilo swali nililotakakujibiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, Serikali inapaswaitambue, kuna watu wana hati na wanazilipia mpaka hatajana kwenye eneo hili. Serikali wako wapi tangu hiyo miakatunayotajiwa hapa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, ningefurahi sanatungekwenda na mkondo aliouzungumza Naibu Waziri waTAMISEMI, Mheshimiwa Jafo kwamba hii issue inacomplications zake. Ni vizuri Serikali, TAMISEMI, Ardhi nawananchi, pamoja na TANROADS wakakaa, hili jambolikazungumzika kutokana na facts zilizopo badala ya kilammoja kuleta hadithi za mwaka 1947 za Queen Elizaberth,sijui lilitokea wapi, ambalo litatuingiza kwenye hoja nyinginempya…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lwakatare kwa hiyo,umeridhika baada ya maelezo hayo? Umeridhika eeh? Hayaahsante sana, tunaendelea.

MHE. WILFRED M. LWAKATARE: Naomba commitmentya Mheshimiwa Jafo aliyoshauri hapa, naomba tuendeleembele.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bulaya.

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kamaWaziri wa Sera wa huku, hatuna shida na kurudisha shilingi

Page 183: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

ya Mheshimiwa Lukuvi, tunachosema, commitment aliyotoaMheshimiwa Jafo ni jambo la msingi sana; na tumeanza vizurihapa, umeona; kuliko haya mambo mengine yote ambayoyanaendelea.

MBUNGE FULANI: Ya Queen Elizabeth!

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Serikali pamoja na watu wa kule wakae waone ni namnagani tutalimaliza hili kwa commitment ya Mheshimiwa Jafo,hatuna tatizo kabisa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa mtoa hoja.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kwetu huku upande waSerikali, Serikali ni moja; whether limefanywa na Ujenzi,limefanywa na Mheshimiwa Jafo au Mheshimiwa Lukuvi,Serikali ni moja. Serikali hii inatekeleza wajibu wake kwakutumia Sheria. Kwa hiyo, mimi ni mlipa fidia kwa waathirika.Kama hamstahili fidia, Serikali haiwezi kupitisha hela kwaWizara kulipa fidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Ujenzi hawa(TANROADS) ndio walipa fidia, ninyi wenyewe hamtapitishafedha hapa ya kulipa fidia kwa jambo ambalo halistahili fidia.Kwa hiyo, jambo hili ingekuwa kuna fidia imekwama kwanguimeletwa, lakini haijafikishwa kwa mwenyewe, ndiyomngeshika shilingi. Fidia haijaja kwangu kwa sababu sistahilikupata hizi fedha kuwalipa huku.

Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wabunge,kwa hiyo, ushauri wangu ni mambo mawili. Kama kuna kesi,mmepata faida hapa, Mheshimiwa Halima dada yangu niMwanasheria na ame-practice sheria ndani ya Serikali, anajua;amekuwa Mwanasheria wa Serikali yeye. Kama kweli kunahukumu ambayo mlishindwa, mmepata faida,hamjachelewa. Hata namna ya kurudisha kesi iliyoisha muda,kukata rufaa mnajua. Vile vile juzi mmetunga Sheria nyinginena kuanzisha Bodi ya Fidia.

Page 184: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninachosema nikwamba Wizara ya Ardhi haiwajibiki na kulipa fidia kwajambo hili kwa sababu hatujapata fedha za kulipa fidia kwasababu jambo lenyewe halilipiki fidia, halina sifa ya kupatafidia. Tutakapowezesha kupata sifa ya kulipa fidia, fedhazitakuja kwangu, nitalipa fidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa sasa naombatu kwa sababu Serikali ni moja, mimi kwa kweli naungamkono maelezo ya Manaibu Waziri kwa sababu hawa niWahandisi waliofanya kazi ya TANROADS na yule ndioanawakilisha TANROADS. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli hil i mimihalinihusu sana. (Kicheko)

MWENYEKITI: Ahsante. Kama hujaridhika nalihojiBunge. Ameshatoa hoja, mimi nalihoji Bunge.

MHE. WILFRED M. LWAKATARE: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kwa mujibu wa taratibu za Bunge,Bunge lihojiwe kwa suala hili.

MWENYEKITI: Sawa, ulishatoa hoja ndiyo maananasema sasa nitalihoji Bunge kuhusu hoja yako, kama Bungelinakubali au kukataa.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kukataliwa)

MWENYEKITI: Hoja imekataliwa. Tunaendelea naMheshimiwa Jitu Soni. (Makofi)

MHE. JITU V. SONI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsantesana. Katika mchango wangu wa maandishi pia namchango wa kuongea hapo mapema, nilikuwa nimeombaSerikali kwa kupitia Wizara ya Ardhi iangalie namna; kwanzaniwapongeze kwamba tayari wana mpango wa kuleta vifaa

Page 185: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

kwenye Kanda. Nipongeze kwa jambo hilo kubwa, lakinianasema awamu ya pili ndiyo wataleta hivyo vifaa katikangazi ya Halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara iangalienamna, pawe na program, Halmashauri tupatiwe vifaa hivyosasa hivi kwa sababu program ya mwaka mmoja baadayekwenye bajeti inayokuja, hatutapata hivyo vifaa; na ndaniya mwaka kazi ya kupima inaweza kufanyika kubwa kabisana inaweza kukaribia kwisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara ituwekeedhamana kwamba kampuni inayotengeneza hivi vifaa auinayouza vifaa au itupatie namna ituwekee guarantee ilitukope kwa sababu Halmashauri nyingi hazina uwezo washilingi milioni kama 200 au 300, lakini Wizara ilipie gharamaza satellite imaging ili hivi vifaa vinapotumika, tuweze kuonazile satellite images. Ukiwa na zile satellite images utawezakupima ardhi vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, viwanjavilivyopimwa Babati, leo vina mgogoro mkubwa kwasababu tulipima bila kutumia vifaa hivyo na satelite imagingunakuta kiwanja chako kipo korongoni, kipo juu ya mlimakwa sababu wanatumia ramani hizi za topography zazamani, lakini tukienda na huu mfumo wa kisasa, Wizaraikalipia satellite imaging na tukakopeshwa hivi vifaa pamojana vifaa vya kutolea hati, kwa mfano computers, printer naza kuwekea data, utakuta sehemu kubwa ya matatizo hayaya kupatiwa hatimiliki…

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa umeeleweka.

MHE. JITU V. SONI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naombaWizara itupe uhakika: Je, inaweza kufanya hivyo il iHalmashauri zote mwaka huu kuanzia sasa badala ya kusubiriawamu ijayo ya bajeti?

MWENYEKITI: Mtoa hoja.

Page 186: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeagiza vifaa hivi RTKtukijua tulikuwa tunakwama zamani kupima kwa sababuvifaa vyote vya zamani tulikuwa tunahitaji hizo satelliteimage, hivi havihitaji. Ndiyo maana tumeweka link kila mahaliza satellite straight. Kwa hiyo, technology hii inayokuja nitofauti, ndiyo maana nimewaalika Waheshimiwa Wabunge,kule nyuma vifaa hivi vipo. Ungeenda kuviona vile, swali hilipengine usingeuliza.

Mheshimiwa mwenyekiti, habari ya satellite image nivery expensive, hata sisi imetukwamisha, hatuwezi. Upimajiwa mashamba umekwama sana kwa sababu lazimasatellite; tumejitahidi hata ku-download kwenye Google nanini, ni very expensive! Hivi vifaa vina uwezo vyenyewe huhitajitena satellite image na ndiyo maana vinapima mpaka ekarielfu 30 kwa wakati mmoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tumetafutatechnology mpya na yeyote ambaye anataka kuthibitishaangalau kidogo kuona jinsi vinavyofanya kazi, tunamwalikapale nyuma, Makampuni haya yako pale. Tunanunua sasavya kutosha kwenye Kanda ili kila Halmashauri ikodishe palebure, ikapimie, lakini baadaye tunaandika sasa mradi wapili ambao pesa tunazo, tunataka tununulie kila Halmashaurivifaa hivi na tutawapa bure wakati tunawa-train. (Makofi)

MWENYEKITI: Tunaendelea na Mheshimiwa Mmasi.Hukutoa hoja Mheshimiwa Jitu? Haya tunaendelea naMheshimiwa Mmasi.

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Nimepata ukakasi kidogo kwenye fungu lamaendeleo Vote number 48 kwa bajeti hii ya Wizara ya Ardhikwa mwaka huu unaoishia 30 Juni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia fungu hili lamaendeleo tunaona kabisa Wizara il itengewaSh.25,300,000,000/=, ni sawa na 4% ya bajeti nzima ya Wizarahii. Pia katika tengeo hili tumeona kulikuwa na tengeo la

Page 187: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

shilingi bilioni 13 ambapo katika hizi ulikuwa umetengewamradi ule wa Land Tenure Support System ambapo katikahizi shilingi bilioni 13, shilingi bilioni 10 zilikuwa ni fedha kutokanje ya nchi, yaani fedha za wahisani lakini katika hiyo shilingibilioni 10 zilitoka Sh.3,400,000,000/=. Siyo hivyo tu, katikatengeo hili tuliona fedha za ndani zilitengwa shilingi bilionitatu lakini zilizoenda kwenye matumizi mpaka Mei, 2017 nishilingi milioni 400 tu, katika shilingi bilioni tatu ambayo nisawa na asilimia 13.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tukiangalia, ukakasi huuumepelekea miradi mingi ya Wizara kukwama. Mathalani,katika bajeti hii ya Wizara ya Ardhi, walikuwa wamejitengeakwa mwaka huu waweze kutoa hatimiliki za makazi 400,000lakini wameishia kutoa hatimiliki za makazi 39,779.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hivyo tu, walikuwawamejipanga kutoa Hati za Kimila 57,000, lakini mpaka sasahakuna hata hati ya kimila iliyotoka, tunaambiwa kupitiareport ya Kamati Wizara imeweza kuratibu hati 33,000…

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Mmasi.

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba maelekezo ya Serikali ni kwa nini Serikali isioneumuhimu wa kutenga fedha za ndani ili akinamama wawezekukopesheka katika mabenki kupitia miradi hii ya urasimishajiwa ardhi, lakini pia suala la ardhi ni suala nyeti sana…

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa. Mtoa hoja.

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba maelezo ya kina. Kwa kweli nitakuwa mchawikama nitashika mshahara wa Mheshimiwa Waziri.

MWENYEKITI: Mheshimiwa umemaliza muda wako.

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba majibu ya kina kutoka kwa Mheshimiwa Waziri.Ahsante. (Makofi/Kicheko)

Page 188: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

MWENYEKITI: Mtoa hoja.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilishatoa hoja wakatinawasilisha hapa nilisema msiangalie bajeti yangu kwatakwimu hizi za shilingi bilioni 68, mimi nina hela nyinginehapa na ndiyo maana kazi inaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimechukua na magazetihapa, ukiangalia kurasa zilizomo humu, matangazo yoteWizara ya Ardhi kuna mabilioni hapa, kazi inaendelea. Kwahiyo, niliwaambia kuna miradi inayoendelea ya kuboreshaSekta ya Ardhi ikiwa ni pamoja na upangaji na upimaji huounaosema wa Land Tenure. Hatuwezi kuchukua pesa zoteHazina tukakaa nazo, tunafanya kazi halafu tunaomba pesa.Hata yule Balozi amekuja jana, fedha zote zipo Tanzania,lakini hatuwezi kuzipeleka kwenye account hii mpaka tufanyekazi. Kwa hiyo, pesa tunayo, usiwe na wasiwasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwamba fedha nyingi sanaza maboresho ya sekta hii ziko kwenye mradi wa World Bankambapo fedha zile ziko Tanzania hivi sasa. Tunafanya kwaawamu kila tunapotangaza tenda ya kazi fulani fedhazinatoka na ushahidi wa Magazeti ni huu. Hata hivyo,yaliyosababisha kutokufikia malengo ya kupima na kupangahati hizi, siyo haya peke yake, mengine ni matatizo ya ndani.Wananchi wale hata viwanja vilivyopangwa na kupimwahavinunuliki, bei ni kubwa na gharama za kupima ni kubwa.Kwa hiyo, sisi tumeenda kwenye source.

Mheshimiwa Mwenyekiti, gharama ya kupima kwasababu wapimaji binafsi hawana vifaa, wapimaji wa Serikalihawana vifaa, tuwanunulie vifaa. Tunamwaga vifaa.Ukipima na kupanga kiwanja pamoja na orodha yote hiyoya kodi, lakini tozo il ikuwa inachukua asil imia 67,tumepunguza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafikiri kwambamfanyabiashara yeyote anayepata faida ni yule anayeuzabidhaa nyingi sana kwa faida ndogo ndogo lakini anapata

Page 189: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

faida. Kwa hiyo, nasi tumekwenda kibiashara zaidi, kwambahebu tupange, tumilikishe kwa gharama ndogo lakiniwamiliki watu wengi zaidi, tutapata fedha ya Serikali lakinikwa sababu watakaomiliki hata ingekuwa bure, kila mwakawataendelea kulipa kodi ya Serikali. Tumeongeza wigo wawalipa kodi wa Serikali.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge usiwe na wasiwasi,kuna fedha hujaziona humu, nakualika Ofisini kwangu nanitakuelekeza vizuri.

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri. Kwakutumia Kanuni ya tano (5) na kwa kuzingatia muda waibada, tayari tunaingia kwenye guillotine.

Fungu 48 - Wizara ya Ardhi, Nyumbana Maendeleo ya Makazi

Kif. 1001 - Administration and HR Mg’nt.....Sh. 6,736,586,549/=Kif. 1002 - Finance and Accounts…………...Sh. 848,465,000/=Kif. 1003 - Policy and Planning…...………….Sh. 696,730,000/=Kif. 1004 - Management Information Syst......Sh. 718,244,000/=Kif. 1005 - Internal Audit Unit......…………….Sh. 350,066,000/=Kif. 1006 - Procurement Mg’nt Unit...............Sh. 283,944,000/=Kif. 1007 - Gov’nt Communication Unit...….Sh. 395,910,000/=Kif. 1008 - Legal Service Unit…..…………….Sh. 319,870,000/=Kif. 2001 - Land Administration Division.....Sh. 13,790,040,000/=Kif. 2002 - Survey and Mapping Division…..Sh. 3,995,954,000/=Kif. 2003 - Registration of Titles Unit..………...Sh. 960,226,000/=Kif. 2004 - Valuation Unit…..…………...……Sh. 884,859,000/=Kif. 2005 - Dar es Salaam Zone..……………...Sh.446,760,000/=Kif. 2006 - Eastern Zone...…………………………………Sh.0/=Kif. 2007 - Central Zone…..…………………..Sh. 449,010,000/=Kif. 2008 - Western Zone…..………………….Sh. 282,040,000/=Kif. 2009 - Lake Zone…..……………………...Sh. 492,590,000/=Kif. 2010 - Northern Zone…..…………………Sh. 485,080,000/=Kif. 2011 - Southern Zone...…………………...Sh. 314,800,000/=Kif. 2012 - Southern Highlands Zone…….......Sh. 326,600,000/=Kif. 2013 - Simiyu Zone…..……………………Sh. 369,120,000/=Kif. 3001 - Rural and Town Planning Div......Sh. 3,964,556,609/=

Page 190: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

Kif. 3002 - Housing Division...……………….Sh. 1,929,513,768/=Kif. 3003 - District Land &Housing Trib.Unit...Sh. 4,214,118,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 03 - Tume ya Taifa ya Mipangoya Matumizi ya Ardhi

Kif. 1001 - Finance and Admin. Division......Sh. 1,751,692,000/=Kif. 1002 - Planning Unit…..…………………...Sh. 37,640,000/=Kif. 1003 - Procurement and Mg’nt Unit……..Sh. 18,240,000/=Kif. 1004 - Internal Audit Unit…..……………...Sh. 22,740,000/=Kif. 1005 - Legal Service…………...…………...Sh. 19,440,000/=Kif. 2001 - Physical Planning Division…….......Sh. 134,140,000/=Kif. 2002 - Landuse Coord, Communication and Policy Division…...................Sh. 66,290,000/=Kif. 2003 - Research and Documentation…....Sh. 65,190,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

MIPANGO YA MAENDELEO

Fungu 48 - Wizara ya Ardhi, Nyumbana Maendeleo ya Makazi

Kif. 1001 - Administration and HR Mgnt......Sh. 1,100,000,000/=Kif. 2001 - Land Administration Division.....Sh. 20,000,000,000/=Kif. 2002 - Survey and Mapping Division…..Sh. 4,000,000,000/=Kif. 3001 - Rulal and Town Planning Division……………Sh. 0/=Kif. 3002 - Housing Division………...…………Sh. 300,000,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

NDG. LAWRENCE MAKIGI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kutoa taarifa kwamba Kamati ya Matumiziimekamilisha kazi yake.

Page 191: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

MWENYEKITI: Bunge linarejea.

(Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae. Mtoa hoja taarifa.(Makofi)

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge lako lilikaa kamaKamati ya Matumizi na limekamilisha kazi zake. Naombataarifa ya Kamati ya Matumizi ikubaliwe na Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka2017/2018 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo

ya Makazi yalipitishwa na Bunge)

MWENYEKITI: Hoja imeungwa mkono naimekubaliwa. Kwa hiyo, natangaza rasmi kwamba bajeti yaWizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2017/2018imepita na imepitishwa na Bunge hili. Kwa hiyo, nachukuafursa hii kuipongeza sana Wizara ya Ardhi, Mheshimiwa Waziripamoja na Naibu Waziri na timu yao nzima ya Wizara hiikwa kazi nzuri waliyoifanya. Naamini kwamba Wizaranyingine zitafanya hivyo na zipongezwe.

Waheshimiwa Wabunge, hapa nina matangazomawili, kwanza moja linatoka kwa Mheshimiwa Balozi Adadi,anawatangazia Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bungeya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuwa kile kikaokilichokuwa kifanyike leo saa 8.30 kimeahirishwa.

Tangazo la pili, ni kutoka kwa Meneja wa BungeSports Club, Mheshimiwa John Kadutu anasema keshoasubuhi anawatangazia Waheshimiwa Wabunge kuwakutakuwa na mchezo kati ya timu ya Bunge na Azam Staff

Page 192: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510753374-26 MEI, 2017.pdf · kiangazi na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

kabla ya mchezo wa Simba na Mbao; na pia anasema tiketiza mchezo wa Simba na Mbao zinapatikana Canteen kwaNyange. Wote mnaarifiwa hilo tangazo.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayo…

MBUNGE FULANI: Hawalipii hizo tiketi?

MWENYEKITI: Hawalipii? Ni tangazo kwambazinauzwa hizo tiketi.

Jamani Waheshimiwa Wabunge, nawashukuru sanakwa kumaliza vizuri Wizara ya Ardhi, nami niwatakieWatanzania wote kila la heri na baraka zote kwa mweziMtukufu wa Ramadhani na pia Mwenyezi Mungu atujaaliesisi ambao tutafunga tupokelewe funga zetu na tuwezekupata malipo mema. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayo,nawashukuru sana. Naahirisha Bunge hadi tarehe 29 Mei, 2017siku ya Jumatatu saa 3.00 asubuhi.

(Saa 7.30 mchana Bunge liliahirishwa Mpaka Siku yaJumatatu Tarehe 29 Mei, 2017, Saa Tatu Asubuhi)