95
NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA PILI Kikao cha Tisa – Tarehe 5 Februari, 2016 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Katibu. NDG. RAMADHAN I. ABDALLAH - KATIBU MEZANI: Hati za kuwasilisha Mezani. HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Nchini kwa kipindi cha Mwaka unaoishia tarehe 31 Disemba, 2014 (The Annual Insurance Market Performance Report for the Year ended 31st December 2014). WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI: Taarifa ya Mwaka ya Chuo Kikuu cha Dodoma kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 (The University of Dodoma Annual Report 2013/2014). MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Atupele Fredy Mwakibete Mbunge wa Busokelo sasa aulize swali lake.

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462467651...Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Nchini kwa kipindi cha Mwaka unaoishia tarehe 31

  • Upload
    others

  • View
    2

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    1

    BUNGE LA TANZANIA

    ____________

    MAJADILIANO YA BUNGE

    ______________

    MKUTANO WA PILI

    Kikao cha Tisa – Tarehe 5 Februari, 2016

    (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi)

    D U A

    Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua

    NAIBU SPIKA: Katibu.

    NDG. RAMADHAN I. ABDALLAH - KATIBU MEZANI: Hati za kuwasilisha

    Mezani.

    HATI ZA KUWASILISHA MEZANI

    Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:-

    NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO:

    Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Nchini kwa kipindi cha Mwaka

    unaoishia tarehe 31 Disemba, 2014 (The Annual Insurance Market Performance

    Report for the Year ended 31st December 2014).

    WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI:

    Taarifa ya Mwaka ya Chuo Kikuu cha Dodoma kwa Mwaka wa Fedha

    2013/2014 (The University of Dodoma Annual Report 2013/2014).

    MASWALI NA MAJIBU

    NAIBU SPIKA: Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Atupele Fredy

    Mwakibete Mbunge wa Busokelo sasa aulize swali lake.

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    2

    Na.102

    Tatizo la Maji – Jimbo la Busokelo

    MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:-

    Wananchi wa Jimbo la Busokelo hasa katika Kata za Kandete, Isange,

    Lutebe Lwangwa, Mpata, Kabula, Mpombo, Lufilyo Kambasegela, Ntaba,

    Lupata, Itete, na Kisegese wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji safi na salama;

    na kuna maeneo mengi ambayo mabomba uyamepita lakini maji hayatoki

    kutokana na kukosekana kwa matenki ya maj:-

    (a) Je, ni lini Serikali itatatua kero hiyo ya maji kwa kujenga matenki ya

    maji kwenye Kata hizo?

    (b) Mji wa Lwangwa ni Makao Makuu ya Halmashauri mpya ya Busokelo

    na kuna ongezeko kubwa la watu ukilinganisha na miundombinu ya maji

    iliyopo; je, Serikali ina mpango gani wa kujenga miundombinu mipya ya

    uzalilshaji wa maji kwenye eneo hilo jipya la mipango miji?

    NAIBU WAZIRI (TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA) alijibu:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-

    TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Fredy Atupele Mwakibete,

    Mbunge wa Busokelo lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

    (a) Mheshimiwa Naibu Spika, katika bajeti ya mwaka 2014/2015,

    Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ilipokea shilingi milioni 907 ambazo

    zimetumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji ya Mpanda katika Kata ya

    Lupata na miradi wa maji Kasyabone na Kisegese katika Kata ya Kisegese.

    Miradi hii inahusisha ujenzi wa matanki yenye ujazo wa mita za ukubwa 90 kwa

    Kata ya Lupata na matanki wawili ya mita za ukubwa 45 kila moja katika Kata

    ya Kisegese. Katika bajeti ya mwaka 1015/2016 Serikali imefanikiwa kupeleka

    shilingi milioni 171.94 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha

    Kanyelele Kata ya Kabula, Ilamba katika Kata ya Kambasegela na kijiji cha

    Mpata katika Kata ya Mpata.

    (b) Mheshimiwa Naibu Spika, ili kukabiliana na changamoto ya

    upatikanaji wa huduma ya maji katika Mji wa Lwangwa tayari Halmashauri

    imekamilisha upembuzi yakinifu wa ujenzi wa mradi wa maji kutoka chanzo cha

    maji Mano Sekondari. Katika bajeti ya mwaka 2015/2016 Serikali imetenga

    shilingi milioni 280 ili kuanza utekelezaji wa mradi huu.

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwakibete swali la nyongeza

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    3

    MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, asante kwa kunipa

    nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya

    Serikali, lakini kwa mujibu wa swali nilivyouliza pamoja na majibu ambayo

    yametolewa ni dhahiri kwamba kwa vijiji ama Kata ambazo amezisema mimi

    mwenyewe ni shahidi kwamba kuna hela ambazo hazijafika hadi sasa hivi na

    katika jibu lake la msingi amesema zimefika. Kwa mfano Kata ya Mpata,

    nimepeleka mabomba zaidi ya milioni 10 lakini Serikali mpaka sasa hivi haijatoa

    chochote. Mheshimiwa Waziri unaweza ukathibitishia wananchi wa Mpata

    kwamba hizo fedha zimefika kule? Hilo ni swali la kwanza.

    Swali la pili, kuna baadhi ya Kata ya Ntaba, kijiji cha Ilamba wananchi

    pamoja na wakazi wa eneo la pale wananyang’anyana maji, wananchi na

    mamba, na zaidi ya wananchi kumi na moja wameshauawa na mamba ama

    kuliwa na mamba kwa sababu ya kutafuta maji, je, Serikali inatoa tamko gani

    kwa ajili ya wananchi hawa na ikizingatiwa kwamba kuna mradi ambao

    umeshafanyiwa upembezi yakinifu tangu mwaka 2008 hadi leo hii kwa thamani

    ya shilingi milioni 100, haikufanya kitu chochote.

    NAIBU WAZIRI (TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA): Mheshimiwa

    Naibu Spika, asante.

    Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwa taarifa aliyosema kwamba fedha

    hazijafika ni kwamba ngoja nita-cross check vizuri katika Ofisi yangu nijue ni nini

    kilichotokea lakini kikubwa ni nini? Ni kwamba kuna changamoto ya upelekaji

    wa fedha, siyo mradi huo tu isipokuwa maeneo mengi sana, fedha zimeenda

    kwa kusuasua na hivi karibuni ndiyo maana Waziri wa Maji juzi juzi alikuwa

    anazungumza kwamba kutokana na kusuasua kwa kupeleka fedha katika

    miradi ya maji na miradi hii mingi sasa mingine ilikuwa imesimama, sasa Serikali

    iliamua kwamba ile outstanding payment ambazo zilikuwa zinakaribia karibuni

    bilioni 28, kwamba fedha hizi sasa zipelekwe katika maeneo mbalimbali ilimradi

    wale Wakandarasi walio-demise mitambo waweze kuendelea.

    Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge naomba nikuambia kwamba nitazifuatilia

    kwa karibu ilimradi kwamba huu mradi lengo letu liweze kufanikiwa na

    wananchi waweze kupata huduma ya maji.

    Lakini sehemu ya (b) ni kwamba kuna changamoto ya wananchi

    wanakamatwa na Mamba. Kwanza nitoe masikitiko yangu sana katika eneo

    hilo, kwa sababu kama watu wanaliwa na mamba ina maana kwamba ni

    changamoto kubwa, tunapoteza jamii ya Watanzania.

    Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge naomba nikiri kwamba nimesikia hili na

    nakumbuka tulifanya discussion juzi juzi kwamba katika ziara yangu

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    4

    nitakapokuwa nimeenda katika Mkoa wa Mbeya nimesema kipambele katika

    Jimbo lako la Busokelo litakuwa ni sehemu mojawapo ambayo nitaenda

    kutembelea ilimradi mambo haya yote kwa ujumla wake tuweze kuyatazama

    vizuri tukiwa site na kuweze kupanga mipango mizuri, mwisho wa siku wananchi

    wa Jimbo hili waweze kupata huduma ya maji, kila mtu aweze kujiona ana

    faraja na nchi yake.

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa pale nyuma, samahani naomba ujitambulishe

    MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Naibu Spika, Naitwa Willy

    Qambalo Mbunge wa Jimbo la Karatu.

    Kwa kuwa, matatizo ya maji yaliyoko Busekelo yanafanana kabisa na

    matatizo ya maji yanayoukumba Mji wa Karatu na vijiji vinavyouzunguka. Na

    kwa kuwa Mji wa Karatu unakua sana kutokana na shughuli za utalii

    zinazoendelea katika maeneo ya jirani. Je, ni lini Serikali itamaliza kabisa

    matatizo ya maji katika Mji wa Karatu na vijiji vinavyozunguka?

    NAIBU WAZIRI (TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA): Mheshimiwa

    Naibu Spika, ndugu yangu huyu tukiri kwanza Busokelo haifanani na Karatu kwa

    sababu kule Busokelo kuna mamba, na naamini Karatu hakuna mamba. Lakini

    kubwa zaidi ni jinsi gani kama Serikali itajielekeza kuhakikisha Mji wa Karatu

    unapata maji kwanza nikiri kwamba miongoni mwa Miji ambayo Tanzania

    tunaitegemea katika suala zima la uchumi ni Mji wa Karatu, kwa sababu ni

    center kubwa sana ya utalii katika nchi yetu.

    Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niseme kwamba Serikali kupitia Wizara

    ya maji katika programu ya pili tunayoenda nayo ambayo imeanza hii Januari,

    tumeweka kipaumbele katika Mji Mikakati yote ambayo kwanza ina vivutio vya

    Kitalii, lakini ni source kubwa sana ya uchumi wa nchi yetu kuipa kipaumbele

    katika suala zima la huduma ya maji.

    Mheshimiwa Naibu Spika, nikiri wazi kwamba katika suala zima la utalii

    kama nilivyosema awali, Karatu ni Mji tunaoutegemea sana. Kwa hiyo suala hili

    tunalilchukua kwa ujumla wake, Wizara ya Maji halikadhalika Wizara ya Nchi

    Ofisi ya Rais TAMISEMI, tutahakikisha jinsi gani tutaipa kipaumbele. Ile miradi

    ambayo imeanza Singida haijakamilika vizuri, au ni jinsi gani tutumie vyanzo

    vingine ili mradi tupate maji katika Mji wa Karatu, wananchi wa Karatu waweze

    kupata manufaa katika nchi yao.

    NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge niwakumbushe tu, maswali

    yanayoulizwa ya nyongeza yawe mafupi, ikiwa ni pamoja na ya muuliza swali.

    Lakini pia Mawaziri mjibu kwa kifupi kwa sababu kila swali limetengewa dakika

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    5

    sita tu. Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Momba sasa aombe swali

    lijibiwe.

    Na.103

    Kero ya Ushuru wa Mazao na Mifugo

    MHE. DAVID E. SILINDE aliuliza:-

    Wakati wa Kampeni za Urais mwaka 2015 wananchi wa Momba

    walipewa ahadi ya kutatuliwa kero ya ushuru wa mazao na mifugo kwenye

    vizuizi na minada:-

    (a) Je, mpaka sasa Serikali imefikia hatua gani katika kushughulikia kero

    hii?

    (b) Je, Serikali inatoa kauli gani juu ya mwenendo mbovu wa ukusanyaji

    wa ushuru huo?

    NAIBU WAZIRI (TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA) alijibu:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais

    (TAMISEMI), naomba kujibu swali la Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge

    wa Momba lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

    (a) Mheshimiwa Naibu Spika, ushuru wa mazao hutozwa kwa mujibu wa

    sheria ya fedha za Serikali za Mitaa Sura Na. 290 kwenye eneo ambalo zao hilo

    huzalishwa na kuuzwa. Kwa mujibu wa sheria hii ushuru unatozwa kwa mnunuzi

    wa mazao kutoka kwa mkulima asilimia tatu hadi asilimia tano ya bei ya

    gharama (farm gate price). Aidha, kwa upande wa ushuru wa Mifugo, ushuru

    huu hutozwa mnadani au sokoni baada ya mifugo kununuliwa.

    (b) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inasisitiza na kuwataka Wakurugenzi

    wote wa Halmashauri kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria, kanuni na taratibu

    zinazosimamia utaratibu wa utozaji na ulipaji wa kodi katika ushuru husikia.

    MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Naibu Spika, asante sana. Pamoja na

    majibu ya Mheshimiwa Waziri, ningependa kuuliza maswali mado mawili.

    Moja ya kero inayowakuta wafugaji wanapokuwa minadani, inatokea

    mahali mtu amekwenda kuuza bahati mbaya akiwa pale mnadani hajauza

    mfugo wake, na anapotoka pale anadaiwa ushuru wakati hajapata hiyo

    fedha. Sasa nilitaka nifahamu kauli ya Serikali juu ya wale wote ambao

    wanashindwa kuuza mazao ama mifugo yao katika maeneo hayo?

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    6

    Swali la pili, je, ni kiwango gani ambacho mtu anapaswa kulipa, kwa

    sababu kuna watu wanatoka mashambani labda ana mahindi wanakwenda

    nyumbani kwao kuyatunza. Sasa wakikutana na kizuizi, mtu ana gunia mbili,

    gunia tatu anaambiwa lazima alipe ushuru hata kwenye yale mahindi ya

    kutumia.

    Je, ipi ni kauli ya Serikali juu ya hili jambo? Ahsante.

    NAIBU WAZIRI (TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA): Mheshimiwa

    Naibu Spika, ni kweli katika mazoea ya kawaida watu wengine wanapeleka

    mazao yao sokoni, lakini kwa bahati mbaya wakifika pale wanakosa kuyauza.

    Ina maana na concept ya ushuru wa mazao, maana inataka mtu akishauza,

    yule mnunuzi sasa maana yake anatakiwa alipia ule ushuru. Lakini kama

    hajauza ukimwambia kwamba yule mkulima sasa aweze kutoa ushuru maana

    yake unambana mkulima. Na kauli ya Mheshimiwa Rais alipokuwa katika

    kampeni alizungumza wazi kwanza lengo lake ni kutoa huu usumbufu wa ushuru

    mdogo mdogo ambao unamkabili mwananchi wa kawaida.

    Mheshimiwa Naibu Spika, kikubwa zaidi nawahimiza Watendaji wetu hasa

    katika Halmashauri, jinsi gani wabainishe kwamba katika maeneo yao kuna

    watu hawa wa kawaida ambao wanaenda kuuza. Kuna mfanya biashara

    mkubwa ambaye anakuja kuchukuwa mazao pale site, akishachukua lazima

    alipie ushuru. Lakini yule mtu anayefanya kazi ya kuchuuza kwa ajili ya maisha

    yake tu hili ni jambo ambalo ni suala zima kuwaelekeza watendaji wetu katika

    Halmashauri zetu watafanya vipi kuondoa kero hii kwa wananchi.

    Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ni kwa kiwango gani, nadhani suala la pili

    sikulipata vizuri lakini kikubwa zaidi ni nini. Ni kwamba mifugo yote inayopelekwa

    pale eneo la mnada, ndiyo maana nimesema sijalipata vizuri swali la pili,

    tuangalie kwamba kwa sababu sheria ndiyo inaelekeza kati asilimia tatu mpaka

    asilimia tano, sasa mtu anapoenda kuuza mfano ana ng’ombe wake mmoja,

    ng’ombe wake wawili, ndiyo nimesema hapa utaratibu mkubwa unaotakiwa ni

    katika Halmashauri husika. Kwa sababu tunajua Halmashauri nyingine

    zinategemea asilimia karibuni 70 ya mapato yake katika ushuru wa mazao.

    Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jinsi gani kama Baraza la Madiwani

    pamoja na Watendaji wao watafanya kuangalia mazingira ya kijiografia katika

    eneo husika ili kuwasaidia wananchi hali kadhalika kuongeza uchumi katika

    Halmashauri zao.

    MHE. SULEIMAN A. SADDIQ: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa

    kunipa nafasi, naomba kumuuliza Mheshimiwa Waziri swali dogo la nyongeza.

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    7

    Kwa kuwa katika Halmashauri zetu, hususani Halmashauri ya Wilaya ya

    Mvomero kumekuwepo na tatizo kubwa sana la ushuru huu na unaleta

    matatizo makubwa na kwa kuwa kuna ahadi ya Rais kwamba hizi shughuli

    ndogondogo zitaangaliwa upya, je, Serikali sasa iko tayari kuziagiaza

    Halmashauri zote ziangalie upya maeneo ambayo kuna usumbufu mkubwa na

    ushuru huu, ili marekebisho yafanywe haraka na wananchi wasipate bugudha

    ikiwemo Wilaya ya Mvomore?

    WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza

    nimpongeze Naibu Waziri kwa majibu yake ya ufasaha, na mimpongeze

    Mheshimiwa Murad kwa ufuatiliaji wake kwa masuala yanayohusu Jimbo lake.

    Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba kama ambavyo nilisema

    wakati nachangia, tunakaa na wenzetu wa TAMISEMI pamoja na Wizara zingine

    ambazo zinahusiana na sekta ambazo zinahusu mambo ya makato makato na

    tulishasema tunayafanyia kazi mambo ya makato yote ambayo yanamgusa

    Mkulima na wafanyabiashara wadogowadogo. Lakini kwa leo nitamke tu

    kwamba kwa yale makato ambayo hayako kisheria, kwa makato ambayo

    yanawagusa wakulima ambayo hayako kisheria kuanzia leo hii wale

    wanaohusika waondoke na tamko hili kwamba wayaache, yale ambayo yako

    kisheria tunaenda kufuata utaratibu na kuangalia kama yote yabaki ama

    yabaki kiasi ili kuweza kuhakikisha kwamba tunawapa unafuu wakulima.

    Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini yale hayako kisheria na yale ambayo

    hayahusiani moja kwa moja na uendelezaji wa zao husika hayo yakome moja

    kwa moja kufuatana na kwamba yamekuwa yakiwapa mzigo wakulima bila

    kuleta tija katika kuongeza uzalishaji wa zao husika. Na tutachambua moja

    baada ya lingine na yale ambayo yanaafikiwa kwa kupitia makubaliano ya

    wadau wahusika, wasikubaliane wao na kuanza kuyatumia mpaka wapate

    ridhaa ya Wizara kwamba kuna mambo haya wamekubaliana na sisi tuweze

    kupima umuhimu wa kuwepo makato hayo katika uendelezaji wa zao husika.

    (Makofi)

    NAIBU SPIKA: Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Mheshimiwa

    Masoud Abdalla Salim, Mbunge wa Mtambile sasa aulize swali lake.

    Na.104

    Ajira Inayatokana na Sekta ya Viwanda

    MHE. MASOUD ABDALLA SALIM aliuliza:-

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    8

    Ajira iliyotarajiwa kuongezeka kutokana na ukuaji wa sekta ya viwanda

    haijafikiwa hasa baada ya viwanda vingi kubinafsishwa na kuachwa bila

    kuendelezwa:-

    Je, Serikali inasema nini kuhusu hili?

    WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI alijibu:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Masoud

    Abdalla Salim, Mbunge wa Mtambile, kama ifuatavyo:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nia njema kabisa Serikali ilibinafsisha

    viwanda na mashirika ya umma ikiwa na matumaini kuwa sekta binafsi

    ingeliweza kuendesha taasisi hizo kwa faida na kulipa kodi kwa Serikali, kuzalisha

    bidhaa au huduma na kutoa ajira kwa wananchi. Pamoja na malengo hayo

    Serikali ililenga kuachana na shughuli za biashara ikielekeza nguvu zake katika

    shughuli zake za msingi za Serikali.

    Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama anavyosema Mheshimiwa

    Masoud, makampuni mengi yaliyobinafsishwa hayakufanya vizuri, ikiacha

    mfano wa makampuni machache yakiwemo Tanzania Breweries, Morogoro

    Polister ambayo inaitwa Twenty First Century na Tanzania Cigarette Company.

    Mheshimiwa Naibu Spika, tathimini inayoendeshwa na Wizara yangu kwa

    kushirikiana na Msajili wa Hazina juu ya viwanda, mashamba na mashirika ya

    Serikalil yaliyobinafsishwa kuanzia mwaka 1992 inadhihirisha ukweli tunaoujua

    kuwa wengi kati ya waliyopewa taasisi hizo hawakutekeleza mikataba ya

    mauziano kikamilifu. Hivyo tunawafuatilia kwa karibu wale wote waliopewa

    mashirika ya umma kwa utaratibu wa ubinafsishaji.

    Mheshimiwa Naibu Spika, lengo letu ni kuhakikisha makampuni yote haya

    yanazalisha kwa tija ili tupate bidhaa, kodi ya Serikali na ajira kwa wananchi wa

    Tanzania. Wale wote watakaobainika kukiuka makubaliano yaliyomo katika

    mikataba ya awali, hatua stahiki zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuvitwaa

    viwanda au mashirika hayo na kutafuta Wawekezaji mahiri wa kuviendeleza.

    Mheshimiwa Naibu Spika, ili kutimiza adhma ya kutoa ajira kwa

    Watanzania, Wizara inafanya yafuatayo chini ya viwanda vidogo na vya kati

    unaoshirikisha SIDO na Halmashauri za Wilaya na Mikoa tunahamasisha shughuli

    za ujasiriamali ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani

    mazao na kilimo, uvuvi na ufugaji huku Mikoani.

    Pia kupitia mamlaka zetu za EPZA, TIC na NDC tunakaribisha na

    kuwaongoza wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika shughuli za kutoa

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    9

    ajira zaidi. Serikali kupitia Wizara yetu inaboresha mazingira ya uwekezaji hali

    itakayowajenga imani wawekezaji na kupelekea kupanua shughuli zao zaidi za

    kibiashara kupitia njia hii ajira zaidi itaongezeka.

    MHE. MASOUD ABDALLA SALIM: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru

    nina maswali mawili ya nyongeza kwa Mheshimiwa Naibu Waziri.

    Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na malalamiko mengi ya muda

    mrefu kwa wafanyakazi viwandani kupewa mishahara midogo lakini zaidi

    maneno ya kuudhi kwa wamiliki wa viwanda jambo ambalo halikubaliki.

    Mheshimiwa Naibu Spika, nimuulize Mheshimiwa Waziri, je, Serikali haioni

    sasa ni wakati muafaka wa kuunda Tume Teule ya kufuatilia malalamiko ya

    wafanyakazi hawa?

    Swali la pili, katika jibu la Mheshimiwa Waziri amesema kwamba wale

    wote watakaobainika kukiuka makubaliano yaliyomo katika mikataba ya awali

    hatua stahiki zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuvitwaa na kutafuta wawekezaji

    mahiri wa kuviendeleza hivyo viwanda.

    Kwa kuwa viwanda vya korosho vilivyobinafsishwa miaka 1970 na 1980

    ambapo Serikali ilikopa kutoka Italia na Japan dola milioni 20 na viwanda hivyo

    hadi leo haviendelezwi wamiliki wake wanajulikana. Sasa tatizo nini kwa Serikali

    mnaelewa kila kitu tumekuwa tukisema muda mrefu.

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa uliza swali.

    MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Je, nini mkakati wa ziada wa kuhakikisha

    kwamba viwanda vya korosho vimebinafsishwa kule Mtwara na Serikali mkatoa

    kwa vigogo wengine mnaowajua kwa bei chee! Je, viwanda hivyo ni lini

    vitarudi kwa wananchi?

    WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,

    ni kweli katika viwanda kuna malalamiko na kama mnavyojua tunao ndugu

    zetu wanafanya kazi viwandani, sioni haja ya kuunda Tume, Wizara yetu

    ikishirikiana na Wizara ya Ajira tumeanza kazi ya kufuatilia masuala haya na

    Kamishna wa Kazi yuko ana kazi maalum ambapo tutahakikisha kwamba

    wafanyakazi wetu wanatendewa haki.

    Mheshimiwa Naibu Spika, niwaeleze wawekezaji, sisi tunatengeneza

    viwanda kutengeneza ajira, kuzalisha bidhaa na kuwafanya mlipe kodi

    hatutengenezi viwanda kusudi waje kuteseka watu katika nchi yao, huo ndiyo

    msimamo wa Serikali na tunawahakikishia tushirikiane Waheshimiwa Wabunge,

    ninyi ndiyo macho yetu mtushauri na mtuelekeze.

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    10

    Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kutoa viwanda, viwanda vile viliuzwa

    kisheria, nimeshasema mara tatu bei waliyolipa ni pamoja na masharti ya

    kuzalisha bidhaa kwa tija, kutoa ajira na kulipa kodi.

    Kwa hiyo, kama ulimuuzia kisheria utamnyang’anya kisheria na

    niwahakikishie watu wanaotoka kwenye ukanda wa kulima korosho hakuna

    tatizo viwanda vitafanya kazi. Pamoja na hivyo wako wawekezaji wako tayari

    kuwekeza kwenye kutengeneza korosho, yaani korosho inatoka pale kiwandani

    inaingia mikononi mwa mteja tuna-add value, na tutatoka hapa tunakwenda

    kuuza Ulaya siyo tunatoka hapa tunauza India, India ipeleke Ulaya.

    Tunakwenda moja kwa moja sokoni na kazi hiyo naiweza tushirikiane. (Makofi)

    MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi nikushukuru

    sana kwa kunipa fursa na kwa sababu ni mara yangu ya kwanza nazungumza

    tangu nichaguliwe tena kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki na mimi

    niwashukuru Wanameru.

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Nassari tafadhali uliza swali la nyongeza.

    MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Naibu Spika, unapoongelea suala

    la ukuaji wa viwanda huwezi ukaacha kuongelea habari ya viwanda ambayo

    vilikuwemo lakini leo hii havifanyi kazi. General Tyre Arusha kilikuwa ni kiwanda

    pekee cha kuzalisha matairi Afrika Mashariki. Mwaka juzi ndani ya Bunge hili

    nimejibiwa na Mama Nagu hapa kwamba in less than a year kiwanda kingerudi

    kifanye kazi, mwaka jana nimejibiwa ndani ya Bunge hili na Mheshimiwa Janeth

    Mbene kwamba kufikia mwezi wa 11 mwaka jana kiwanda cha General Tyre

    kingerudi kufanya kazi.

    Sasa na mimi niiulize Serikali ya hapa kazi tu, kwamba ni lini kiwanda cha

    General Tyre kitarudi kufanya kazi kwa sababu tumechoshwa na ahadi za

    muda mrefu ndani ya Bunge hili na wananchi wa Mkoa wa Arusha ambao

    walikuwa wanapata ajira ndani ya viwanda vile leo wako nyumbani na matairi

    tunanunua Korea, India na Japan, lini General Tyre litaanza kufanya kazi?

    WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,

    General Tyre kinachoendelea General Tyre ni nini?

    Mheshimiwa Naibu Spika, General Tyre imeshatwaliwa aliyekuwa mbia

    mwenzetu mwenye asilimia 26 tumemlipa chake kiwanda ni chetu,

    kinachoendelea ni kurekebisha mitambo yote ya umeme. Lakini mitambo

    iliyokuwepo kwa ushindani wa sasa ni absolute zimepitwa na wakati. Tulikuwa

    tunatengeneza tyres zenye tube, sasa hivi soko linakula tubeless kwa hiyo,

    tunapaswa kuleta mitambo mingine. Lakini tunatafakari tuende vipi tutafute

    mbia mwingine au tutafute mtu wa kumwajiri afanye kazi. Kwa hiyo, sasa hivi

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    11

    kinachofanyika ikitoka Government Notice NDC itakwenda kupewa pesa bilioni

    60 na itafanya kazi hiyo.

    Mheshimiwa Catherine Magige amelifuatilia suala hili tumelizungumza

    sana, siyo suala la dakika moja naomba Mheshimiwa Mbunge uje au umuone

    Mheshimiwa Catherine Magige akueleze shule niliyompa masaa matatu kuhusu

    General Tyre. General Tyre is coming na iko kwenye score board yangu,

    nitapimwa kwa General Tyre. (Makofi)

    Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi/Kicheko)

    Na. 105

    Matatizo Yanayowakabili Wakulima wa Tumbaku Urambo

    MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:-

    Mfumo wa sasa wa kuwahudumia wakulima wa zao la tumbaku wa

    Wilaya ya Urambo na Mkoa wa Tabora kwa ujumla una mapungufu mengi

    yanayowaletea wakulima usumbufu kama vile bei za pembejeo kuwa kubwa

    kutokana na kuagizwa nje na riba kubwa za benki, masoko ya tumbaku

    kutokuwa na uhakika na hatimaye kusababisha kushuka thamani ya tumbaku,

    bei inayobadilika pamoja na uchache wa wanunuzi:-

    (a) Je, ni kwa nini hasara inayotokana na matatizo hayo ibebwe na

    mkulima peke yake?

    (b) Je, Serikali imejipanga vipi kuondoa matatizo hayo ili mkulima wa

    tumbaku anufaike na kilimo na hatimaye ajikwamue kiuchumi?

    NAIBU WAZIRI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa kwa niaba ya Waziri wa Kilimo,

    Mifugo na Uvuvi kujibu swali la Mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta, Mbunge

    wa Urambo, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

    (a) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inakubaliana na Mheshimiwa

    Mbunge kuwa yapo maeneo mbalimbali yanayomkosesha mkulima mapato.

    Maeneo haya ni pamoja na mfumo wa usambazaji pembejeo uliokuwa na

    mianya mingi inayosababisha madeni hewa, baadhi ya viongozi wa vyama

    kukopa fedha nyingi kupita uwezo wa vyama wa kuzalisha tumbaku na

    kadhalika. Kwa sasa Serikali imebadili mfumo huo na kuelekeza wagavi wa

    pembejeo hizo kuzifikisha moja kwa moja kwenye vyama vya msingi tofauti na

    utaratibu wa awali wa kupitisha pembejeo kwenye vyama vikuu.

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    12

    Aidha, ili kuwa na uhakika wa soko kilimo cha tumbaku nchini

    huendeshwa kwa mkataba kati ya wanunuzi na wakulima. Hivi sasa bei

    hupangwa kabla ya msimu wa kilimo kuanza ili mkulima ajue bei na kiasi

    anachotakiwa kuzalisha. Tatizo la soko na bei mara nyingi huwakumba wale

    wakulima wanaozalisha tumbaku bila kuwa na mikataba ambapo hujikuta

    tumbaku yao ikikosa soko au wakipewa bei ya chini.

    (b) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuchukua hatua za

    kukabiliana na changamoto zinazomkabili mkulima wa tumbaku. Hatua hizo ni

    pamoja na kuboresha mfumo wa upangaji wa bei ya tumbaku ambapo

    wakulima upendekeza bei yenye tija kwao na kuiwasilisha kwa wanunuzi kupitia

    vikao vya Halmashauri ya Tumbaku yaani Tobacco Council. Bei hiyo hujadiliwa

    na hatimae kufikia muafaka. Mfumo huu wa upangaji wa bei umeanza

    kutumika rasmi msimu wa mwaka 2015/2016. Sanjari na maboresho ya mfumo

    huu Serikali inaendelea na jitihada za kuongeza wanunuzi wa tumbaku kutoka

    China ili kuongeza ushindani kumwezesha mkulima kupata bei nzuri. Aidha,

    Serikali itapitia tozo za pembejeo zinazoingia nchini na kuangalia uwezekano

    wa kuziondoa ili kumpunguzia mkulimba gharama ya uzalishaji.

    MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na

    majibu mazuri ya Naibu Waziri ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza

    kama ifuatavyo:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri amekiri kwamba mfumo uliopo una

    matatizo katika kumhudumia mkulima. Lakini Serikali inashiriki kikamilifu katika

    kupanga bei katika mfumo mzima. Sasa kwa kuwa Serikali inashiriki kwa kupitia

    wakala wake bodi au council, je, Serikali haioni kwamba inawajibika kubeba

    sehemu ya hasara anayopata mkulima?

    Kwa kiasi gani mmefaulu kupata wanunuzi zaidi kutoka China ili soko liwe

    la haraka na wakulima wanufaike?

    NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika,

    Tobacco Council au Halmashauri ya Tumbaku inawakutanisha wadau

    mbalimbali wa sekta ya tumbaku. Serikali yenyewe haihusiki moja kwa moja

    katika kupanga bei lakini imeweka tu utaratibu ambao wadau wenyewe

    wanaweza kukaa kukutana kwa uhuru wao na kupanga bei. Hata hivyo, Serikali

    imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha kwamba bei ya tumbaku

    inaendelea kuwa nzuri.

    Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu kwamba tokea mwaka 2013

    Bunge hili lilipitisha Sheria mpya ya Vyama vya Ushirika, utaratibu mpya wa

    Vyama vya Ushirika ni utaratibu ambao pamoja na mambo mengine

    unawaruhusu wakulima wa mazao mbalimbali kuendesha shughuli zao kwa

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    13

    kuwa na uhuru zaidi. Lakini vilevile mpango ule umeunda Tume ya Ushirika

    ambayo inakuwa karibu na Vyama vya Ushirika ili kuwezesha kuondoa kero

    zilizopo. Tunafikiri kwamba utaratibu huu utaleta ufanisi zaidi katika kilimo cha

    tumbaku pamoja na mazao mengine ikiwa ni pamoja na kusaidia katika suala

    la bei.

    Lakini nitumie tu fursa hii kuwawelezea vilevile Waheshimiwa Wabunge

    kwamba pamoja na changamoto nyingi zilizopo kwenye sekta ndogo ya

    tumbaku, tunafikiri sekta ndogo ya tumbaku ni eneo ambalo limeanza

    kuonesha mifano ya kufanikiwa. Hii ni kwa sababu ndiyo sekta ndogo ya pekee

    ambayo mkulima anakuwa na uhakika wa kuuza zao lake tokea siku ya kwanza

    anapoanza kuweka mbegu shambani kwa sababu ni kilimo cha mkataba. Kwa

    hiyo, tukiondoa changamoto zilizopo tunafikiri ni eneo ambalo bado

    inawezekana kupata mafanikio makubwa. Lakini vilevile tungependa kutumia

    fursa hii kuwaeleza wakulima…

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri naomba ufupishe jibu lako

    tafadhali.

    NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika,

    namalizia. Kuwafahamisha kwamba kufanikiwa kutumia mfumo wa mkataba

    utasaidia tu kama kila mtu akiheshimu mkataba. Kwa mfano, mwaka huu tayari

    wakulima wanafahamu inatakiwa wazalishe tumbaku kiasi gani, tunaomba

    wale ambao hawako kwenye mkataba usizalishe tumbaku kwa sababu

    ukizalisha hautaweza kupata mnunuzi.

    Mheshimiwa Naibu Spika, kipengele cha pili cha swali ni kwamba ni kiasi

    gani na kwamba tumefikia wapi na kuwapata wanunuzi kutoka China.

    Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inajitahidi kuongea na wafanyabiashara

    kutoka China, tumefika hatua nzuri sana kilichobakia sasa ni wao kumaliza

    taratibu za nchi mwao ili nao waweze kuingia kwenye mfumo rasmi wa

    kununua tumbuku ili kuondoa ukiritimba ambao mpaka sasa hivi nchi nzima

    kampuni zinazonunua tumbaku ni nne tu.

    Kwa hiyo, tunafikiri kampuni zikiwa nyingi maana yake tunaondoa

    monopoly na hivyo bei itakuwa nzuri nashukuru sana.

    NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tuendelee na Wizara ya Mambo

    ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mgeni Jadi Kadika, Mbunge wa Viti Maalum,

    sasa aulize swali lake.

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    14

    Na. 106

    Usalama wa Maisha na Walemavu wa Ngozi

    MHE. MGENI JADI KADIKA aliuliza:-

    Kwa muda mrefu walemavu wa ngozi (albino) wamekuwa wakiishi kwa

    hofu katika nchi yao kutokana na kuuawa na kukatwa viungo vyao kwa imani

    za kishirikina ikiwemo kwa ajili ya kushinda uchaguzi au kujipatia mali:-

    Je, Serikali ina mpango wa kuwalinda na kuwahakikishia usalama wa

    maisha yao watu hao wenye ulemavu wa ngozi?

    NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya

    Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mgeni Jadi Kadika, Mbunge wa Viti

    Maalum kama ifuatavyo:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, kama ilivyowahi kujibiwa katika swali la msingi

    namba 99 na swali namba 60 katika mikutano tofauti ya Bunge la Kumi la

    Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu usalama wa ndugu zetu wenye

    ulemavu wa ngozi, Serikali kupitia Jeshi la Polisi na wadau wengine imekuwa

    ikichukua hatua za maksudi kukomesha mauaji hayo ikiwa ni pamoja na

    kuwasaka na kuwakamata watuhumiwa pamoja na kuwafikisha mahakamani.

    Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imefanya pia juhudi za kuanzisha vituo

    vya kuwahudumia watu wenye ulemavu wa ngozi ambavyo vimesaidia

    kuimarisha ulinzi. Pia Jeshi la Polisi kwa kutumia falsafa ya Polisi Jamii inatoa

    elimu kwa umma juu ya madhara ya vitendo vya ukatili na mauaji na kujerui

    yanayofanywa na baadhi ya watu kwa msukumo wa imani potofu ya ushirikina.

    Aidha, Jeshi la Polisi limekuwa likifanya operesheni maalum za mara kwa mara

    zikiwamo za kukamata waganga wa jadi wanaopiga ramli chonganishi

    ambazo ni kichocheo kikubwa cha ukatili dhidi ya walemavu wa ngozi.

    Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yangu kupitia Jeshi la Polisi ikishirikiana

    na Kamati ya Ulinzi na Usalama za Vijiji, Kata, Wilaya na Mikoa imeanzisha vikosi

    kazi hususan kwenye Mikoa na Wilaya zilizojitokeza kukithiri kwa matukio haya ili

    kuratibu na kusimamia kwa karibu ulinzi wa ndugu zetu wenye ulemavu wa

    ngozi. Vikosikazi hivyo hufanya kazi kwa kukusanya taarifa za kiintelejensia na

    kuzifanyia kazi.

    MHE. MGENI JADI KADIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu

    mazuri aliyonijibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    15

    Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni kesi ngapi zilizolipotiwa kwa kipindi hiki cha

    mwaka wa uchaguzi?

    Mheshimiwa Naibu Spika, pia ni kwa nini kesi zinacheleweshwa wale

    walemavu hawapi haki zao kwa haraka?

    Na je, ni mikoa mingapi inayoongoza kwa mauaji ya maalbino? (Makofi)

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kadika umeuliza maswali matatu, Naibu Waziri

    tafadhali jibu maswali mawili.

    NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika,

    kwanza kuhusu Mikoa ambayo inaongoza ni Mkoa wa Mwanza, Mkoa wa

    Shinyanga na Kigoma.

    Swali lake la pili anauliza kwamba ni kesi ngapi, takwimu halisi zilizotokea

    baada ya kumalizika uchaguzi naomba nimpatie baadaye lakini ninachoweza

    kusema ni kwamba toka mauaji haya yameanza mwaka 2006 mpaka mwaka

    jana takribani watu wanakadiriwa kwenye 40 mpaka 43 wameweza kufariki,

    lakini watuhumiwa karibu 133 na kati ya hao watuhumiwa ambao

    wamehukumiwa kwa adhabu ya kifo ni 19 tayari ambao wameonekana wana

    hatia. Kwa hiyo, hizi takwimu za baada ya uchaguzi mpaka saa hivi, hizi

    naomba nikupatie baadaye. (Makofi)

    MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa

    kuwa matatizo yaliyoulizwa na Mheshimiwa Mgeni kwenye swali namba 106

    yanafanana kabisa na matatizo yaliyoko Jimbo la Geita Vijijini. Takribani

    wanawake wazee wanne kwa mwezi wanauwawa kwa kukatwa mapanga

    kwa imani ya kishirikina na Jeshi la Polisi halijawahi kufanikiwa kuwakamata

    wakataji mapanga hao kwa kuwa jiografia ya kutoka Geita kwenda eneo

    husika ni mbali.

    Je, Serikali inajipangaje kupeleka gari maalum na kuunda Kanda Maalum

    kwa ajili ya kuokoa akina mama wanaokatwa mapanga kwenye Jimbo hilo?

    NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika,

    Jeshi la Polisi linajitahidi sana kuweza kukabiliana na mauaji haya, lakini kama

    ambavyo nimezungumza wakati nikijibu maswali wiki iliyopita kuhusiana na

    changamoto ambazo zinakabili Jeshi la Polisi. Naomba nichukue fursa hii

    kuweka sawa kidogo takwimu wakati nilikuwa najibu swali la Mheshimiwa

    Selasini juzi, nilieleza kwamba moja katika changamoto inakabili Jeshi letu la

    Polisi ni kwamba idadi ya polisi tulionao ni kidogo na kiukweli kihalisia takwimu

    zinaonyesha kwamba ukiangalia takwimu za kidunia polisi mmoja anatakiwa

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    16

    ahudumie kati ya watu 400 mpaka 450 takriban na siyo 300 mpaka 350. Sisi

    hapa nchi yetu polisi mmoja kwa upande wa Tanzania Bara anahudumia watu

    kwenye 1000 mpaka 1200. Kwa hiyo utaona ni tofauti kubwa.

    Mheshimiwa Naibu Spika, sasa changamoto hizi na changamoto nyingine

    ambazo tumekuwa tukikabiliana nazo hatua kwa hatua kama hii ya usafiri,

    nataka nimhakikishie tu Mheshimiwa Musukuma kwamba tumekuwa na

    changamoto ya usafiri kwa muda mrefu lakini tumepata magari takribani

    magari 387 ambayo yameweza kugawiwa katika maeneo mbalimbali.

    Tutaangalia eneo hilo kama halijafika gari tuone ni jinsi gani na uzito wa hali

    yenyewe ilivyo tushauriane tuone ni nini tutakachofanya ili tuweze kukabiliana

    na tatizo hilo. Lakini mengine ni changamoto ambazo tunaenda nazo kadri ya

    uwezo wa bajeti unavyoruhusu.

    Na. 107

    Uhaba wa Magari na Mafuta katika Vituo vya Polisi

    Wilaya ya Magharibi

    MHE. HAFIDH ALI TAHIR aliulliza:-

    Bunge la Jamhuri ya Muungano hupitisha Bajeti ya Serikali kwa kila Wizara

    kwa mwaka ikiwemo Wizara ya Mambo ya Ndani:-

    (a) Je, inakuwaje Wilaya yenye vituo saba vya polisi ina gari moja tu na

    inapatiwa lita tano hadi saba tu za mafuta kwa siku?

    (b) Je, Serikali iko tayari kuziongezea mafuta na magari Wilaya za

    Magharibi A na B zenye vituo vya polisi vya Fumba, Mbweni, Mazizini,

    Mwanakwerekwe, Kijitoupele, Fuoni, Airport na Mfenesini ambazo ni gari moja tu

    kila Wilaya ili kukongeza ufanisi na kuendana na kasi ya hapa kazi tu hasa

    ukizingatia kuwa Zanzibar inajiandaa na marudio ya Uchaguzi Mkuu?

    NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya

    Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir, Mbunge wa Dimani

    lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

    (a) Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kuwa

    Wilaya ya Magharibi A na B hazina magari na mafuta ya kutosha kwa shughuli

    za polisi. Hali hii ni changamoto kwa vituo vingi vya polisi hapa nchini, hata

    hivyo, mgawo wa vitendea kazi yakiwemo magari huzingatia jiografia ya

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    17

    Wilaya. Hali ya uhalifu na idadi ya watu wanaohudumiwa na kituo husika na

    siyo idadi ya vituo vidogo vya Polisi vilivyopo katika Wilaya husika.

    (b) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani

    ya Nchi, inakusudia kuwasilisha bajeti mbele ya Bunge lako Tukufu ili kuboresha

    hali ya vyombo vya usafiri, mafuta na vilainishi ili kukidhi mahitaji halisi ya Jeshi la

    Polisi hapa nchini, vikiwemo Vituo vya Polisi alivyovitaja Mheshimiwa Mbunge.

    MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru

    Mheshimiwa Naibu Waziri kwa jawabu zake, lakini swali langu lilikuwa na msisitizo

    ukizingatia kuwa Zanzibar inajiandaa na marudio ya Uchaguzi Mkuu, ndiyo

    sababu swali langu kubwa lilikwenda huko. Kurudiwa kwa Uchaguzi Zanzibar

    siyo jambo geni, mwaka 1961 Uchaguzi ulifutwa na ukarudiwa mwaka1963.

    (Makofi)

    Sasa kwa tokeo hili Mheshimiwa Waziri swali langu la kwanza, huoni

    kwamba kuna haja ya kuweka umaksudi wa kupatia usafiri Wilaya nilizozitaja

    wakati huu tukielekea katika uchaguzi ili yale mazombi yanayozungumzwa

    yapunguke kufanya kazi?

    Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali la pili, namwomba Waziri aniambie

    kwamba kwenye Bajeti ijayo ameahidi kwamba atatupatia magari Wilaya

    alizozitaja, Mheshimiwa Naibu Waziri naomba ukubali hii ni ahadi na nikungoje

    kwenye bajeti? Ahsante.

    NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika,

    naomba nimhakikishie kwamba nilizungumza vilevile kuhusiana na hili suala la

    magari ambalo kwa bahati mbaya kuna baadhi ya Waheshimiwa Wabunge

    wamelipotosha kwa makusudi ama hawajalielewa. Lakini naomba nichukue

    fursa hii kwa kueleza tu kwa ufupi ni kwamba Jeshi la Polisi na ninyi Wabunge ni

    mashahidi mara nyingi mmekuwa mkihoji, vituo vyangu havina magari, Jimbo

    langu kwenye kituo fulani hakuna magari, na ndiyo kwa kuzingatia hilo Serikali

    kupitia Jeshi la Polisi, likaandaa mkakati kabambe wa kupunguza hiyo hali.

    Mheshimiwa Naibu Spika, kulimaliza kwa wakati mmoja, siyo rahisi kwa

    sababu katika nchi tuna zaidi ya vituo 4,500, kwa hiyo, kupata gari 4,500 kwa

    mpigo ili kila kituo kiweze kupata gari ni jambo ambalo ni gumu. Kwa hiyo

    kulikuwa kuna mpango wa kwanza wa kuweza kupata gari 777 kupitia mkopo

    wa Exim Bank ya India, ambapo kati ya hizo tuliweza kupata gari 104, lakini pia

    Serikali iliweza kutoa gari takribani 203 kwa hiyo kufanya jumla ya idadi ya gari

    ambazo zilipatikana kuwa ni 387. Kati ya gari hizo, gari 37 zilipelekwa Zanzibar

    na nimhakikishie Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir kwamba gari hizi bado

    hazijagawiwa katika Wilaya, nina hakika kwamba wakati mgao utakapokuwa

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    18

    umefanyika, basi Wilaya hizo ambazo zimezungumzwa vituo vya Wilaya yake ya

    Magharibi A na Magharibi B vitapata gari.

    Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali lake la pili, alizungumzia kuhusiana

    na hali ya usalama kwa ujumla. Mimi nataka nimhakikishie tu kwamba pamoja

    niichukue fursa hii, kuwaeleza Wananchi wa Zanzibar kwamba Jeshi la Polisi

    ama Serikali itahakikisha inalinda usalama wa raia kama ambavyo majukumu

    yake ya msingi yanavyotaka. Kwa hiyo, wasiwe na wasiwasi wajitokeze kwa

    wingi kushiriki uchaguzi utakaporudiwa na hakuna wasiwasi wowote kila mtu

    ambaye atakuwa na haki ya kupiga kura, apige kura kwa usalama na amani.

    (Makofi)

    MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana,

    ninaomba niulize swali dogo la nyongeza.

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa shida ya ulinzi iliyopo Dimani

    inafanana sana na Jimbo la Ukonga, nina Kata 13, sina kituo kikubwa cha Polisi,

    na ni eneo la pembezoni ikiwepo Msitu wa Kazimzumbwi, lakini hata kituo cha

    Sitakishari ambacho kinahudumia Jimbo la Segerea na Ukonga hakuna gari,

    sasa nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri, atatujengea Kituo cha Polisi Ukonga

    au apeleke gari Segerea Sitakishari ili ihudumie wakati mipango mingine

    inaendelea?

    Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niwasilishe, ahsanteni.

    NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika,

    nadhani ule umuhimu wa magari ambayo nimekuwa nikiuzungumza

    umeongezeka uzito wake, sasa niweke tu wazi kwamba katika yale magari

    ambayo tumeyapata, magari mengi ni kwa ajili ya doria, operation na matumizi

    ya kawaida ya polisi. Hayo magari yanayoitwa ya washawasha sidhani hata 24

    sujui kama yanafika.

    Kwa hiyo, Mheshimiwa Waitara nadhani utakubaliana na mimi na

    Wabunge wengine kwamba, Jeshi la polisi linahitaji magari zaidi, ikiwemo katika

    Kituo chako ulichozungumza, mimi naomba hili nilichukue tuone tutalifanyia kazi

    vipi.

    MHE. SULEIMAN M. NCHAMBI: Mheshimiwa Naibu Spika, wabheja sana.

    Kwa kuwa Jimbo la Kishapu halikupata mgao wa magari mapya ya polisi katika

    awamu hii na Jimbo hili lenye watu sharp na askari wanaofanya kazi zao kwa u-

    sharp, lina magari mawili mabovu yenye umri wa zaidi ya miaka mitano.

    Je, Mheshimiwa Naibu Waziri, nilipata ahadi kuwa mwezi wa pili tutapata

    magari mapya ya polisi, uko tayari kunihakikishia Jimbo sharp litapata magari

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    19

    mapya ili Wananchi waweze kupata huduma hasa za kiusalama wanapohitaji

    kuliko hivi sasa polisi wangu wa Kishapu wanavyohangaika? Wabheja.

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Nchambi wakati Naibu Waziri akija, hayo

    maneno wabheja siyo lugha ya Kibunge, kwa hiyo nayafuta kwenye record

    karibu Mheshimiwa Naibu Waziri. (Makofi)

    NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika,

    nataka nimhakikishie Mheshimiwa Nchambi kwamba Serikali hii ya Awamu ya

    Tano ya hapa kazi tu huwa haina desturi za kutoa ahadi ambazo hazitekelezeki.

    Kwa hiyo, kama ni ahadi ambayo imetolewa, basi nitaifuatilia hiyo ahadi

    yenyewe halafu tuone hatua zilizofikiwa zimefikiwaje na kama imekwama

    imekwama vipi, halafu tutaonana mimi na yeye tuone ni jinsi gani ya kufanya.

    NAIBU SPIKA: Tuendelee Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia

    Wazee na Watoto, Mheshimiwa Halima Ali Mohamed, Mbunge wa Viti Maalum,

    sasa aulize swali lake.

    Na. 108

    Tatizo la Ugonjwa wa Moyo, Kisukari na Vidonda vya Tumbo

    MHE. HALIMA ALI MOHAMMED aliuliza:-

    Takwimu zinaonyesha kuwa kuna kasi kubwa ya ongezeko la wagonjwa

    wa maradhi ya moyo, kisukari na vidonda vya tumbo (ulcers):-

    Je, Serikali ina mkakati gani kukabiliana na tatizo hili?

    NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

    alijibu:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya

    Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Halima Ali

    Mohammed, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania imeshuhudia kasi kubwa ya ongezeko

    la magonjwa ya moyo, magonjwa ya kisukari na magonjwa ya vidonga vya

    tumbo, ambayo ni magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Hii imechangiwa na

    mabadiliko ya mfumo wa maisha kama ulaji usiyo sahihi, kutokufanya mazoezi,

    kutokula matunda na mboga mboga kwa wingi, uvutaji wa sigara na tumbaku

    na unywaji wa pombe uliyokithiri.

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    20

    Mheshimiwa Naibu Spika, matokeo ya utafiti wa STEPS uliyofanyika

    mwaka 2012 yalionesha kuongezeka kwa viashiria yaani indicators

    vinavyosababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Aidha, utafiti pia ulionesha

    karibu asilimia 9 ya Watanzania, wanaugua ugonjwa wa kisukari na wengi wao

    kwa bahati mbaya hawajijui. Kwa kutambua ongezeko hili Wizara yetu

    imeanzisha sehemu ya kushughulikia huduma ya magonjwa haya yaani kitengo

    cha Non Communicable Diseases, Mental Health and Substance Abuse chini ya

    Kurugenzi ya Tiba pale Wizarani. Miongozo na mikakati mbalimbali imekwisha

    kutengezezwa ikiwa ni pamoja na mkakati wa Kitaifa wa kukabiliana na

    magonjwa yasiyo ya kuambukiza yaani magonjwa ya kisukari, moyo na

    mengineyo.

    Mheshimiwa Naibu Spika, wito wangu kwa jamii ni kubadili mtindo wa

    maisha yaani life style kwa kula vyakula vinavyofaa, kupunguza unywaji wa

    pombe na uvutaji wa sigara na tumbaku na kuwa na tabia ya kufanya mazoezi

    ili kuepuka uwezekano wa kupata maradhi haya.

    MHE. HALIMA ALI MOHAMMED: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

    Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa ya Naibu Waziri nina maswali mawili

    madogo ya nyongeza.

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tafiti zinaonyesha kwamba

    wanawake wanaathirika zaidi na maradhi ya moyo kuliko wanaume.

    Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia wanawake hawa ambao

    ndiyo walezi wa familia hasa wale waliopo kule vijijini?

    Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, Serikali ina mkakati gani wa

    kudhibiti uingizwaji wa vyakula vibovu ambavyo havina kiwango katika nchi

    yetu? Ahsante (Makofi)

    NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA

    WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu maswali ya

    nyongeza kama ifuatavyo:-

    Swali la kwanza Serikali ina mkakati gani wa kupunguza kiasi cha

    magonjwa haya kwa wanawake ambao wanaathirika zaidi kuliko wanaume.

    Mheshimiwa Naibu Spika, tofauti ya upatikanaji wa magonjwa haya, kwa

    jinsia kwa maana ya baina ya wanawake na wanaume ni ndogo sana na kwa

    maana hiyo, mkakati wa kupambana na kuenea kwa magonjwa haya hauwezi

    kutofautishwa kwa jinsia. Hivyo mkakati wetu utakuwa ni wa pamoja na tayari

    Wizara ya Afya imeanza kutekeleza mkakati huo, kwanza kwa kutia umuhimu

    wa kipekee kwenye kuimarisha Kitengo cha NCD yaani Kitengo cha Magonjwa

    Yasiyo ya Kuambukiza pale Wizarani chini ya Kurugenzi ya Tiba.

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    21

    Mheshimiwa Naibu Spika, kitengo hiki tayari kimeishaaza mkakati wa

    kuandika mkakati wa kupambana na magonjwa haya na mkakati huu

    utawafikia hao akinamama wa vijijini na watu wote kwa ujumla wake kuanzia

    ngazi ya huduma za afya kule vijijini, kwa maana ya ngazi ya zahanati, ngazi ya

    vituo vya afya na ngazi ya hospitali za Wilaya, Mikoa na hata ngazi ya Kanda.

    Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni kweli kumekuwa na hisia kwamba

    kuna vyakula visivyo na viwango vinaingia nchini mwetu kutoka nchi za mbali.

    Serikali kwa kushirikiana kwa maana ya Wizara yetu Wizara ya Afya, ambayo ina

    kitengo cha TFDA (Tanzania Food and Drugs Authority) ambacho kipo chini ya

    Wizara yetu ya Afya, pamoja na Kitengo cha Viwango (TBS), wanaendelea

    kushirikiana kwa pamoja, kukagua mizigo yote ambayo inaingia nchini kwa njia

    za halali.

    Lakini pia vyombo vingine vya kusimamia Sheria kama Majeshi ya Polisi na

    Uhamiaji, wataendelea kuwa makini kwenye mipaka yetu yote, katika njia zilizo

    halali na hata zile ambazo siyo halali kudhibiti uingizwaji wa vifaa hivi ikiwemo

    vyakula na dawa ambavyo havijapitishwa kwa viwango vinavyostahili, kwa

    mujibu wa Sheria za nchi yetu. (Makofi)

    NAIBU SPIKA: Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mheshimiwa Risala Saidi

    Kabongo Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake.

    Na. 109

    Kuongezeka na Kuboresha Vyanzo vya Maji Arusha

    MHE. RISALA S. KABONGO aliuliza:-

    Vijiji vya Ngiresi, Sokoni II na Oldadai Kata ya Sokoni II Jimbo la Arumeru

    Magharibi vinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa maji ya bomba, kwa muda

    mrefu licha ya kwamba vijiji hivyo kuna vyanzo vingi vya maji na mabomba

    yanayopeleka maji Arusha Mjini:-

    (a) Je, Mamlaka ya Maji Jiji la Arusha inashindwa kutekeleza maombi ya

    wananchi wa vijiji hivyo ya kupatiwa maji kutoka kwenye mabomba kwa

    utaratibu wa kulipia?

    (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza na kuboresha vyanzo vya

    maji katika Jiji la Arusha na Halmashauri zake kutokana na ongezeko kubwa la

    wakazi wake?

    NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    22

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji,

    naomba kujibu swali la Mheshimiwa Risala Saidi Kabomgo, Mbunge wa Viti

    Maalum, lenye vipengele (a) na (b) kama ifuatavyo:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali katika kuondoa tatizo la maji Jiji la

    Arusha, imepata mkopo wa dola za Kimarekani milioni 210.96 kutoka Benki ya

    Maendeo ya Afrika (AfDB) ili kutekeleza mradi wa upanuzi wa mtandao maji

    safi na maji taka sambamba na kuboresha vyanzo vya maji.

    Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu mkubwa utawezesha Jiji la Arusha

    pamoja na viunga vyake, ikiwa ni pamoja na vijiji vyote vilivyopo umbali wa

    kilometa 12 kando kando ya bomba kuu, vikiwemo vijiji vya Ngilesi, Sokoni II na

    Oldadai ili kupata huduma ya majisafi na majitaka. Jumla ya gharama za ujenzi

    ni dola za Marekani milioni 233.92 sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 476.44.

    Mheshimiwa Naibu Spika, mkataba wa mkopo huu nafuu umesainiwa na

    Mamlaka ya Maji Arusha, kwa sasa inaendelea na taratibu za kupata Mhandisi

    Mshauri wa kusimamia mradi pamoja na Wakandarasi wa Ujenzi. Ujenzi wa

    mradi huu unatarajiwa kuanza mwaka wa fedha 2016/2017 na kukamilika

    mwaka 2019/2020. Mradi huu ukikamilika utaboresha vyanzo vya maji na

    utaongeza upatikanaji wa huduma ya maji katika Jiji la Arusha na Halmashauri

    zake ambazo zimekumbwa na ongezeko kubwa la wakazi.

    MHE RISALA S. KABONGO: Mheshimiwa, Naibu Spika nakushukuru.

    Nakushukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yako.

    Kwa kuwa, mradi huu ni Mkubwa na ni wa miaka mitano; je, Serikali

    inavipa vipaumbele gani vijiji hivi vya Oldadai na Sokoni II na Ngilesi, kwa kuwa

    wamekuwa na kero kubwa na ya muda mrefu ya kupata maji?

    Eneo la pili, nitaomba Mheshimiwa Waziri, atakapopata nafasi baada ya

    Bunge hili, aweze kutembelea maeneo haya na kujionea hali halisi katika

    vyanzo hivi ambavyo vinatunza maji yanayosaidia katika Mkoa wa Arusha.

    Ahsante. (Makofi)

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, la pili nadhani lilikuwa ni ombi, swali ni

    moja tu lililoulizwa.

    WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza

    kabisa ni kweli tumepata ufadhili wa mradi mkubwa ambao utekelezaji wake

    utachukua miaka mitatu. Jana tulikuwa na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,

    amekuja ofisini kwangu pamoja na Meya, pamoja na Mbunge na

    tumekubaliana kwamba, tutatengeneza mpango wa muda mfupi ili hivyo vijiji

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    23

    unavyovisema tuweze kuvitafutia angalau wapate maji wakati tunatekeleza

    huu mradi mkubwa.

    Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa kulikuwa na Mradi wa Vijiji Kumi,

    tumekubaliana kwamba Jiji la Arusha litakabidhi kwenye mamlaka yetu ya

    Arusha ili kusudi waweze kuunganisha kwenye mtandao baadhi ya maeneo

    ambayo Arusha hayapati maji.

    Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana pia kwamba na mimi nitakuja

    kuangalia utekelezaji wa mpago huu. (Makofi)

    MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi

    hii. Suala la Arumeru Magharibi linafanana sana na tatizo ambalo lipo Mikumi,

    je, Serikali ina mpango gani wa kuondoa kero ya maji katika Kata ya Mikumi,

    Ruaha, Uleling’ombe na maeneo ya Tindiga?

    NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika na

    Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Waziri katika majibu yake ametoa taarifa

    kwamba tunaingia katika progamu ya pili kupitia sera ya mwaka 2002 ya

    kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2020 asilimia 85 ya Watanzania wote

    watakuwa wanapata maji katika vijiji na asilimia 95 katika miji.

    Mheshimiwa Mbunge, kwa upande wa Jimbo lako la Mikumi na Kata

    zake, tutahakikisha kwamba tunazipa kipaumbele kuhakikisha zinapata maji

    katika hii progamu ya pili. Na ninakuomba sana baada ya Bunge hili tuwasiliane

    ili tuweze kupata taarifa iliyo nzuri zaidi tuanze utekelezaji.

    MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa

    kuniona. Kwa kuwa tatizo la Arumeru Mashariki linafanana kabisa na tatizo la

    maji la Lushoto.

    Je, ni lini Serikali itaondoa adha hii kwa wananchi wa Lushoto?

    NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,

    kwanza Wilaya ya Lushoto mlalo wake wa ardhi ni mzuri kuruhusu ujenzi wa

    mabwawa. Tumeweka mpango wa kujenga mabwawa katika awamu hii ya

    programu ya pili ambayo yatasaidia kwenye irrigation pamoja na kuhakikisha

    kwamba tunapata maji ya kunywa kwa wananchi wa Jimbo lake.

    Na. 110

    Kuanza kwa Mradi wa Bomba la Maji Ziwa Victoria

    MHE. RICHARD M. NDASSA aliuliza:-

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    24

    Je, ni lini mradi wa ujenzi wa bomba la maji ya Ziwa Victoria kutoka Magu

    - Sumve - Malya utaanza?

    NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji

    naomba kujibu swali la Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa, Mbunge wa

    Sumve kama ifuatavyo:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Uwekezaji

    ya Ulaya (EIB) na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza

    (MWAUWASA) inatekeleza miradi ya maji safi na maji taka kwa Jiji la Mwanza

    pamoja miradi ya maji safi katika miji mitatu ya Magu, Misungwi na Lamadi.

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mji wa Magu mradi huu unakadiriwa

    kugharimu kiasi cha Euro milioni 5.3 na Mkandarasi anatarajiwa kuanza ujenzi

    wa mradi ifikapo mwezi Julai, 2016. Idadi ya wananchi watakaonufaika na

    mradi huu inakadiriwa kuwa wananchi 73,363 ifikapo mwaka 2040.

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa miji ya Sumve na Malya, Serikali

    inaendelea kufanya uchunguzi wa awali ili kubaini gharama za eneo la

    kupitisha mradi. Kazi ya upimaji pamoja na usanifu itakamalika mwezi Aprili, 2016

    na ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza mwaka wa fedha 2016/2017.

    MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

    Kwanza naomba nisahishe jina langu hapa inasomeka Ngassa, siyo Ngassa ni

    Ndassa.

    Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na maelezo mazuri sana ya

    Mheshimiwa Naibu Waziri lakini naomba Serikali itambue kwamba suala la maji

    ni suala kila Mtanzania, kila mwananchi anahitaji maji na ndiyo maana unaona

    Wabunge wote wanasema kuhusu maji.

    (a) Swali langu, kwa sababu Serikali katika mwaka 2000 na 2004 iliamua,

    maamuzi magumu yenye tija, kuyatoa maji ya Ziwa Victoria kuyapeleka

    Kahama, Shinyanga. Je, Serikali ina mpango gani mrefu wa kupeleka maji ya

    Ziwa Victoria katika Mikoa tisa ili maji hayo yawanufaishe Watanzania na mikoa

    hiyo ni Mwanza, Mara, Kagera, Simiyu, Singida na Dodoma. Serikali ina mpango

    gani kwa sababu mahitaji ya maji ni makubwa na maji ya Ziwa Victoria yapo

    hayana kazi nyingine. Je, Serikali ina mpango mkakati gani wa kuhakikisha

    kwamba maji yanafika katika maeneo hayo?

    (b) Mheshimiwa Waziri wa Maji, wananchi wa Jimbo la Sumve katika Kata

    ya Nkalalo na Mabomba wanashida kubwa ya maji, naomba nikuombe

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    25

    pamoja na maelezo haya utembelee tuende ukajionee mwenyewe jinsi

    wananchi wa Tanzania wa Jimbo la Sumve wanavyopata taabu ya maji katika

    Jimbo langu.

    WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,

    nimezungumza jana kwamba tumeleta mapendekezo ya mwongozo kwa

    kutengeneza mpango wa miaka 2016/2017 na nilisema katika sekta ya maji

    tumetoa ahadi kwamba katika miji yote ya Mikoa inayozungukiwa na Ziwa

    Victoria tutahakikisha tunachukua maji ya kutosha kuyafikisha kwenye maeneo

    husika kwa kiwango ambacho tumeshasema kwenye Ilani, kwamba Miji Mikuu

    ya Mikoa ipate asilimia 95 ikifika 2020 na ipate asilimia 100 ikifika 2025.

    Kwa hiyo, naomba nilihakikishie Bunge hili kwamba azma hiyo ambayo

    pia Mheshimiwa Rais wetu ameahidi tutakwenda kufanya, tutaomba

    Waheshimiwa Wabunge muweze kutuunga mkono katika kupanua vyanzo vya

    upatikanaji wa fedha hasa kuongeza Mfuko wa Maji ili tuweze kutekeleza miradi

    yote hii ambayo kila Mbunge ameomba Serikali iweze kufanya, ahsante.

    (Makofi)

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbarouk

    MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Naibu Spika, jina langu naitwa

    Mussa Mbarouk, Mbunge wa Tanga Mjini.

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Serikali ilianzisha mpango wa maji safi

    na salama vijijini katika mradi uliofadhiliwa na World Bank na mradi ule

    umekwama. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha katika Halmashauri ya Jiji la Tanga

    ili kuondoa kero ya maji katika Kata za Mabokweni, Chongoleani, Kilale na

    Marungu?

    NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni

    kweli Serikali ilianzisha mradi wa vijiji 10 kupitia progamu ya Benki ya Dunia na

    mradi huo ungali unaendelea. Katika mradi huo tulikuwa na miradi 1,855 kama

    nilivyotoa taarifa ya awali kwamba katika miradi hiyo miradi 1,143 imekamilika

    na miradi 454 inaendelea.

    Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na tatizo la fedha ndiyo lililofanya hii

    miradi isikamilike kwa wakati lakini nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba

    katika eneo lako la Tanga kufuatia juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya

    Muungano wa Tanzania kukusanya fedha, fedha zimeanza kutoka na nikupe tu

    taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba wiki iliyopita tumeletewa shilingi bilioni 10

    kwa ajili ya kuendelea kulipa miradi hiyo mingi ambayo ilikuwa imesimama na

    siyo Tanga tu, ni karibu Mikoa yote miradi ilikuwa imesimama.

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    26

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nikuhakikishie kwamba Serikali inatoa

    fedha kuhakikisha miradi hiyo inakamilika ili katika progamu ya pili tuanze

    kuweka tena miradi mingine. (Makofi)

    NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Wizara ya Ujenzi,

    Uchukuzi na Mawasiliano, Mheshimiwa Victor Kilasile Mwambalaswa, Mbunge

    wa Lupa sasa aulize swali lake.

    Na. 111

    Kuweka Mizani katika Barabara ya Mbeya – Chunya – Makongorosi

    ili Kuilinda Iweze Kudumu kwa Muda Mrefu

    MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA aliuliza:-

    Barabara ya Mbeya – Chunya - Makongorosi imejengwa kwa kiwango

    cha lami kwa asilimia 80. Je, ni lini Serikali itaweka mizani katika barabara hiyo

    ya lami ili kuilinda iweze kudumu muda mrefu?

    NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO alijibu:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na

    Mawasiliano, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Victor Kilasile Mwambalaswa,

    Mbunge wa Jimbo la Lupa kama ifuatavyo:-

    Barabara ya Mbeya – Chunya – hadi Makongorosi yenye urefu wa

    kilometa 117 ni barabara kuu inayohudumiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na

    Mawasiliano kupitia Wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya. Barabara hii

    imejengwa kwa kiwango cha lami, sehemu ya barabara kati ya Mbeya hadi

    Chunya ambayo ni kilometa 72 na imekamilika hivi karibuni. Aidha, Serikali

    inafanya maandalizi ili kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya Chunya

    hadi Makongorosi ambayo ni kilometa 45.

    Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yangu inatambua kuwa katika Wilaya

    ya Chunya kuna shughuli nyingi za kiuchumi kama vile uchimbaji wa madini,

    kilimo na mazao ya misitu ambayo huchangia kwa kiwango kikubwa upitishaji

    wa magari yenye mizigo mizito na hivyo kuna umuhimu wa kuweka mizani

    kwenye barabara hii.

    Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itajenga mizani katika barabara ya

    Mbeya - Chunya hadi Makongorosi wakati wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa

    sehemu ya Chunya - Makongorosi. Aidha, katika kipindi hiki ambacho ujenzi wa

    mizani ya kudumu haujafanyika, Serikali kupitia TANROADS itaendelea kudhibiti

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    27

    uzito wa magari katika barabara hiyo kwa kutumia mizani ya kuhamishika

    (mobile weighbridge).

    MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA: Mheshimiwa Naibu Spika,

    ninakushukuru. Napenda kumshukuru sana Naibu Waziri amejibu vizuri sana na

    amejibu kitaalamu.

    Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imesema Chunya ina mazao mengi

    ambayo yakibebwa ndiyo yanaharibu barabara, sasa napenda nimwambie

    Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba wanaosomba tumbaku, magari

    yanayobeba tumbaku au mbao au mkaa yanabeba lumbesa, yanakuwa mara

    mbili, yakifika Mbeya yanagawa kwa sababu kuna mizani kule ndiyo yawe

    magari mawili na Serikali hapa imesema kwamba itadhibiti hiyo kwa kuweka

    mobile weighbridges.

    Je, ni lini itaweka kwa sababu Chunya sasa hivi sijaiona mobile

    weighbridge hata moja? Hilo ni swali la kwanza

    Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili nashukuru Serikali imesema kwamba

    ujenzi wa barabara hiyo kuanzia Chunya kwenda Makongorosi karibu utaanza,

    napenda nimwambie Naibu Waziri kwamba Mheshimiwa Rais akiwa

    Makongorosi aliwaahidi wananchi wa Makongorosi kwamba atawapa kilomita

    nne za lami pale Makongorosi na kwamba barabara hiyo ya Chunya

    Makongorosi itaanza kujengwa Makongorosi kuja Chunya.

    Je, hiyo barabara itanza lini kujengwa? (Makofi)

    NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa

    Naibu Spika, kama tulivyosema kwenye jibu la msingi la swali la msingi kwamba

    weighbridge itaanza hivi karibuni. Naomba kuchukua nafasi hii kumhakikishia

    Mheshimiwa Mwambalaswa kama yeye alivyo-concerned na uharibifu wa

    barabara hiyo na sisi ambao ndiyo wenye dhamana hiyo tuko concerned kwa

    kiwango kikubwa, ninamhakikishia hiyo weighbridge inatafutwa hivi karibuni

    itaanza kufanya kazi.

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali la pili naomba kumjulisha Mheshimiwa

    Mwambalaswa kwamba mara fedha zitakapopatikana barabara hii itaanza

    kujengwa na suala la ianzie wapi whether ianzie Makongorosi au ianzie Chunya

    nadhani ni muhimu tuwaachie wataalamu na ahadi ya kilomita Nne nayo

    katika eneo la Makongorosi itaangaliwa kwa umakini wake. (Makofi)

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    28

    Na. 112

    Uhakika wa Fidia kwa Wananchi Waliopisha Barabara

    MHE. DUA W. NKURUA aliuliza:-

    Katika ujenzi wa barabara ya Mangaka - Mtambaswala na Mangaka -

    Nakapanya, wapo wananchi ambao walishafanyiwa tathmini ya fidia ya

    kupisha ujenzi huo hawajalipwa na wengine wamepunjwa.

    Je, Serikali italeta lini wataalamu wa kuhakiki fidia hizo ili kila mwananchi

    apate haki yake?

    NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO alijibu:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na

    Mawasiliano, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Dua William Nkurua,

    Mbunge wa Nanyumbu, kama ifuatavyo:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, katika ujenzi wa barabara ya Mangaka –

    Mtambaswala na Mangaka - Nakapanya, Serikali ilitenga fedha shilingi milioni

    3,023.528 kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi waliokwisha fanyiwa tathmini ya

    mazao yao kati ya mwaka 2009 na 2012. Aidha, baada ya uthamini

    kuidhinishwa na Mthamini Mkuu wa Serikali mwaka 2013, fidia ililipwa mwaka

    2014 kwa kufuata taratibu na sheria.

    Mheshimiwa Naibu Spika, baadhi ya wananchi ambao mali zao

    hazikufanyiwa tathmini katika kipindi hicho hawakulipwa fidia. Tathmini ya fidia

    kwa mali za wananchi hao imefanyika mwezi Oktoba 2015 na taarifa ya

    uthamini imekamilika na imewasilishwa kwa Mthamini Mkuu wa Serikali kwa

    hatua ya kuidhinishwa ili malipo yaweze kufanyika.

    MHE. DUA W. NKURUA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu

    mazuri ya Mheshimiwa Waziri.

    Mheshimiwa Naibu Spika, katika wale ambao walifanyiwa tathmini ya

    awamu ya kwanza, wapo ambao mpaka sasa hawakulipwa, Majina yao

    yalirukwa katika Kijiji cha Misawaji, lakini pia wapo ambao walifanyiwa tathmini

    kwamba nyumba zao zitabomolewa nusu lakini zimebomolewa zote na hivi

    ninavyokwambia wamechanganyikiwa kabisa.

    Je, Mheshimiwa Waziri anaweza kutuma watu tumuoneshe watu ambao

    wameathirika ili wapate haki yao?

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    29

    Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa barabara kutoka Masasi

    mpaka Mangaka imekamilika, hadi sasa magari yenye uzito mkubwa kutoka

    Songea kuelekea Masasi yanatumia hiyo barabara.

    Je, Mheshimiwa Waziri haoni umuhimu wa kuleta mizani katika Mji wa

    Mangaka ili kuokoa barabara ambayo Serikali imetumia gharama kubwa?

    NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa

    Naibu Spika, nakubaliana nae kwamba tutatuma watu waende

    wakalichunguze hilo suala na hatimaye tuweze kulipatia ufumbuzi stahiki.

    Ninachoomba kumhakikishia tu ni kwamba Serikali hii inafuata sheria na yeyote

    mwenye haki ya kulipwa fidia atalipwa. (Makofi)

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali lake la pili nadhani anafahamu

    kwamba hizo barabara anazoziongelea bado hazijakamilika na hivi karibuni

    nimepiata katika eneo lake ingawa kwa bahati sikumjulisha kwa sababu ilikuwa

    ni dharura wakati natokea Jimbo la Namtumbo. Ninamhakikishia mara

    barabara hizi zitakapokamilika na umuhimu utakapoonekana kwamba kuna

    umuhimu mkubwa wa kuweka mizani, Serikali itafanya maamuzi stahiki. (Makofi)

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Keissy.

    MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa

    kuwa barabara ya kutoka Sumbawanga kwenda Mpanda takriban kilometa 50

    zimeshatengenezwa na magari makubwa ya mahindi zaidi ya tani 60, 70

    yanapita kuelekea Mpanda. Nimeshamwomba Waziri wa Ujenzi kupeleka gari

    ya mizani ili kudhibiti uharibifu wa barabara kabla wakandarasi hawajakabidhi

    kwa sababu barabara inaanza kuharibika kabla haijakabidhiwa. Je, ni lini

    Serikali itapeleka gari ya mizani ili kudhibiti barabara hiyo isiendelee kuharibika?

    NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa

    Naibu Spika, naomba kuchukua nafasi hii kumhakikishia Mheshimiwa Keissy na

    wananchi wa Sumbawanga hadi Mpanda kwamba barabara ile kwanza

    tutaikamilisha kuijenga. Tutakapoona umuhimu wa kuweka mizani kutokana na

    tathmini ya wataalam tutakaowapeleka kufanya shughuli hiyo tutaweka mizani

    hiyo.

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge kule nyuma ujitambulishe tafadhali.

    MHE. ALEX R. GASHAZA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa

    nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Naitwa Alex Raphael Gashaza,

    Mbunge wa Jimbo la Ngara.

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    30

    Kwa kuwa barabara ya Murugarama – Rulenge – Nyakahura yenye

    kilometa 85 ni barabara ambayo iliahidiwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya

    Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2008

    kwamba itaweza kujengwa kwa kiwango cha lami na miaka miwili iliyopita

    wananchi wa Jimbo la Ngara walikuwa wakielezwa kwamba tayari upembuzi

    yakinifu wa barabara hii umeanza.

    Naomba kumuuliza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ni lini

    mkandarasi atakuwepo site kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hii? (Makofi)

    NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa

    Naibu Spika, tumepata taarifa kutoka kwa Waziri mwenyewe wa Ujenzi,

    Uchukuzi na Mawasiliano juu ya upatikanaji wa fedha za kulipa madeni ya

    wakandarasi, kama jana mlimsikia alisema ni karibu shilingi bilioni 419

    zimeshatolewa. Kwa hiyo, katika lile deni la shilingi trilioni 1.268 sasa tumeshuka

    tuko kwenye shilingi bilioni 800 na zaidi. Naomba kuchukua nafasi hii

    kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba mara fedha zitakapopatikana

    kwa mradi huo, barabara yake itashughulikiwa kama ilivyoahidiwa na

    Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Na. 113

    Mkoa wa Shinyanga na Simiyu Kuunganishwa kwa Barabara za Lami

    MHE. GIMBI D. MASABA aliuliza:-

    Mkoa wa Shinyanga na Simiyu inaunganishwa kwa barabara ya vumbi,

    tofauti na mikoa mingine ambayo imeunganishwa kwa barabara za lami.

    (a) Je, Serikali itaunganisha lini mikoa hiyo kwa barabara ya kiwango cha

    lami kwa kumalizia kilometa 102 zilizobaki katika barabara ya Lamadi -

    Mwigumbi kupitia Bariadi?

    (b) Je, Serikali itaona umuhimu wa kuunganisha makao makuu ya Wilaya

    za Mkoa wa Simiyu kuunganishwa kwa barabara za kiwango cha lami?

    NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO alijibu:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na

    Mawasiliano, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Gimbo Dotto Masaba,

    Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama

    ifuatavyo:-

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    31

    Mweshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na ujenzi kwa kiwango cha

    lami wa barabara ya Mwigumbi - Maswa - Bariadi - Lamadi yenye urefu wa

    kilometa 171.8 kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha ikiwa na lengo

    la kuunganisha Mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mara na Mwanza na kwa

    barabara ya lami. Sehemu ya barabara hii kuanzia Bariadi - Lamadi yenye urefu

    wa kliometa 71.8 tayari imejengwa kwa kiwango cha lami na imekamilika.

    Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2015/2016, TANROADS

    ilitia saini mkataba wa ujenzi na mkandarasi CHICO kutoka China kwa ajili ya

    ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya pili ya barabara hiyo kuanzia

    Mwigumbi - Maswa ambazo ni kilometa 50.3 kwa gharama ya shilingi bilioni

    61.462. Hadi sasa mkandarasi yuko katika eneo la mradi na anaendelea na kazi

    za kujenga kambi, kuleta mitambo na wataalam kwa ajili ya kutelekeza mradi

    huo. Aidha, kwa sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa

    kiwango cha lami wa sehemu ya Maswa - Bariadi ambazo ni kilometa 50.

    Mheshimiwa Naibu Spika, ni wazi kuwa kukamilika kwa barabara hii

    inayoendelea kujengwa kutawezesha Makao Makuu ya Wilaya za Busega,

    Bariadi na Maswa zilizoko katika Mkoa wa Simiyu kuunganishwa kwa barabara

    za lami. Wilaya nyingine zilizobaki zitaungwanishwa kwa barabara za lami kwa

    awamu kutegemeana na upatikanaji wa fedha.

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Masaba swali la nyongeza.

    MHE. GIMBI D. MASABA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa

    nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza pamoja na majibu ya Mheshimiwa

    Waziri.

    Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa vile nchi yetu ina uhaba

    wa majengo ya shule, zahanati na vituo vya afya, je, Serikali iko tayari

    kumuagiza mkandarasi ambaye sasa hivi yuko site kujenga majengo ya

    kudumu ili baada ya mradi kukamilika majengo hayo yaweze kutumika kwa ajili

    ya matumizi ya shule, zahanati na vituo vya afya? (Makofi)

    Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa barabara za Mkoa wa

    Simiyu zinaunganishwa na barabara za vumbi na kwa sasa hazipitiki kutokana

    na mvua zinazoendelea.

    Je, Serikali iko tayari kutenga fedha kutoka kwenye Mfuko wa Barabara ili

    kuweza kutengeneza barabara hizo na ziweze kupitika kwa urahisi tofauti na

    ilivyo sasa? Ahsante.

    NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa

    Naibu Spika, mkandarasi aliyeko site mkataba wake ulishasainiwa. Hata hivyo,

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    32

    nawaagiza TANROADS Mkoa wa Simiyu waangalie uwezekano katika mkataba

    huo kama inaweza ikafanyika variation au kama kifungu hicho kipo wahakikishe

    majengo yanayojengwa na mkandarasi huyo yaweze kuangalia matumizi ya

    baadaye ambayo Mheshimiwa Mbunge ameomba. Kama itashindikana,

    Serikali itatafuta njia nyingine kupitia Wizara husika ya Afya. (Makofi)

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa swali la pili, naomba

    nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Mfuko huo anaoungelea ndiyo

    tunaoutumia kujenga na kukarabati barabara zote nchi nzima. Naomba

    akubali mfumo tulio nao ndiyo huo, hatuna mfuko maalum kwa ajili ya

    barabara hii peke yake.

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Gekul.

    MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa

    kuniona niulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa katika Mpango wa

    Maendeleo wa mwaka mmoja ulio mbele yetu, miundombinu si kipaumbele.

    Kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa

    Magufuli wakati akiomba kura aliahidi ujenzi wa barabara za lami nchini kote

    ikiwemo Jimbo langu la Babati Mjini ambako aliahidi ujenzi wa kilometa 20 za

    lami. Naomba nifahamu, ni lini ahadi hii itatekelezwa kwa wananchi wa Babati?

    NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa

    Naibu Spika, ahadi zote ambazo zimetolewa kwanza na Chama Tawala kupitia

    Ilani yake ya mwaka 2015 - 2020 Serikali hii ina wajibu wa kuzitekeleza. na

    tutaitekeleza

    Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hiyo anayoiongelea namuomba

    awasiliane na TANROADS mkoa ili kuangalia vipaumbele vya sasa vilivyopo

    katika mkoa ule. Kama barabara hiyo ni moja kati ya vipaumbele vya mkoa,

    namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaitekeleza katika kipindi hiki

    kama ambavyo iliahidiwa katika kipindi cha kampeni.

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Martha Mlata.

    MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa

    kunipa nafasi. Na mimi kama swali la msingi lilivyoongea kuhusu Mkoa wa Simiyu

    kuunganishwa na mikoa mingine, ni wazi kwamba Mkoa wa Simiyu bado

    haujaunganishwa na Mkoa wa Singida ambao unapitia katika Daraja la Sibiti –

    Mkalama - Nduguti - Iguguno. Nataka nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri, je,

    anafahamu kwamba Daraja la Mto Sibiti ndilo kiunganishi kikubwa katika Mkoa

    wa Simiyu na Singida na mpaka sasa mkandarasi hayupo site? Ahsante.

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    33

    NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa

    Naibu Spika, tunafahamu kwamba Daraja la Sibiti ni muhimu katika mawasiliano

    kati ya Mkoa wa Simiyu na Singida na ndiyo maana kazi kubwa inafanywa sasa

    kutokana na matatizo yaliyotokea ili kuhakikisha mawasiliano yanakuwepo.

    Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu mkandarasi, kwa kuwa fedha za kulipa

    madeni ya wakandarasi tumeanza kupata ambapo huyu naye ni mmoja kati

    ya wakandarasi wanaotakiwa kulipwa ili waendelee na kazi. Mara fedha

    zitakapopatikana, mkandarasi atarudi site ili aweze kukamilisha kazi ambayo

    alisaini kuifanya.

    Na. 114

    Serikali Kuanzisha na Kumiliki Bureau de Change

    MHE. FAIDA MOHAMED BAKAR aliuliza:-

    Je, Serikali ina mkakati gani wa kuanzisha na kumiliki Bureau de Change

    zake yenyewe badala ya kuacha huduma hiyo kuendelea kutolewa na watu

    au taasisi binafsi?

    NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO alijibu:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango,

    napenda kujibu swali la Mheshimiwa Faida Mohamed Bakar, Mbuge wa Viti

    Maalum, kama ifuatavyo:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali haina mkakati wa kufungua au

    kuanzisha Bureau de Change zake kwa sababu imejitoa kuhusika moja kwa

    moja na biashara ya fedha kama vile benki na Bureau de Change kutokana

    na mabadiliko ya mfumo katika sekta ya fedha nchini unaotekelezwa kuanzia

    mwaka 1991. Sekta binafsi imeachiwa jukumu la kuanzisha na kuendesha

    biashara ya fedha nchini chini ya usimamizi wa Benki Kuu.

    Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imebaki na jukumu la kuweka mazingira

    mazuri na salama ya uwekezaji katika sekta zote, ikiwemo sekta ya fedha ili

    kuiwezesha sekta binafsi kuanzisha, kuendesha na kutoa huduma bora za

    kifedha.

    Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeweka sheria na taratibu za kusaidia

    nguvu na juhudi za wananchi katika kuanzisha benki au taasisi za fedha katika

    maeneo yao ikiwa ni pamoja na maduka ya kubadilisha fedha za kigeni.

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    34

    Kwa hiyo, Serikali inategemea kuwa wananchi watatumia fursa hii ya

    mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo nchini na kuanzisha huduma za

    kubadilisha fedha za kigeni katika maeneo yenye uhitaji.

    Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania itaendelea

    kusimamia kwa ukaribu zaidi maduka ya kubadilisha fedha za kigeni nchini ili

    yaweze kutoa huduma bora na inayokidhi matakwa ya sheria na kanuni za

    biashara ya fedha. Hivi karibuni Benki Kuu imetoa kanuni mpya kwa lengo la

    kuimarisha usimamiaji wa maduka hayo. Maduka yote ya kubadilisha fedha za

    kigeni yanatakiwa kufunga mashine za EFDs ili kuiwezesha TRA na BoT kupata

    taarifa za moja kwa moja juu ya miamala inayofanywa kwenye maduka hayo.

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bakar swali la nyongeza.

    MHE. FAIDA MOHAMED BAKAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana

    kwa kunipatia nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza pamoja na majibu

    mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri.

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amesema

    kwamba Serikali imebaki katika kuweka mazingira mazuri, lakini naona kwamba

    mazingira mazuri hayo si kweli sana kwa sababu hayaonekani maana

    wananchi wanalalamika sana. Kwa sababu ukienda Bureau de Change hii ina

    rate hii, ukienda Bureau de Change nyingine ina rate tofauti na zimetapakaa

    sehemu zote kama sisimizi. Je, Serikali inachukua hatua gani kuhakikisha rates

    hizo zinalingana? (Makofi)

    Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, kwa kuwa Mheshimiwa Naibu

    Waziri amekiri kuwa Serikali imejitoa katika biashara hii ya kumiliki Bureau de

    Change lakini huo ulikuwa ni uamuzi wa zamani na tujue kwamba sasa hivi

    dunia imebadilika, ni dunia ya sasa. Je, atakubaliana nami kwamba sasa

    umefika wakati wa Serikali kumiliki huduma hii ili kuwaondolea wananchi wake

    matatizo ambayo wanakabaliana nayo? Ahsante.

    NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza

    nianze kwa kumshukuru kwa kuuliza maswali mazuri ya nyongeza ambayo

    yanakidhi haja na yanaakisi kinachoendelea katika maduka yetu ya kubadilisha

    fedha.

    Mheshimiwa Naibu Spika, jibu la swali lake la kwanza kwamba rates ni

    tofauti sana kutoka duka moja kwenda duka lingine, nakubaliana naye na hii

    yote ni kuonesha kwamba tuko ndani ya soko huria na kila mtu anatakiwa ku-

    charge anavyoona inafaa. Pia kiuchumi, sisi wachumi tunafahamu kwamba bei

    ya bidhaa yoyote ile hutegemea na demand na supply. Kwa hiyo, kama

    demand ya bidhaa hiyo ni kubwa bei zitakuwa tofauti kutoka kwa muuzaji

    mmoja kwenda kwa muuzaji mwingine. (Makofi)

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    35

    Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, Serikali iweze kurudi kwenye

    kuendesha biashara kama hizi na kwamba huo ulikuwa ni uamuzi wa zamani,

    naamini uamuzi ule ulikuwa ni sahihi na bora. Kama nilivyosema katika jibu

    langu la msingi kwamba tangu mwaka 1991 Serikali ilishajitoa kuendesha

    mabenki haya. Tunaendelea kusisitiza, sisi kama Serikali tutaendelea kutunga

    sera na sheria mbalimbali za kusimamia maduka haya ili yaweze kutoa huduma

    zilizo bora kwa wananchi wetu.

    Na.115

    Fursa Zitokanazo wa Mgodi wa Stamigold - Biharamulo

    MHE. OSCAR R. MUKASA aliuliza:-

    Mgodi wa Stamigold, Biharamulo uko kijijini Mavota katika Wilaya ya

    Biharamulo na wananchi wa Kijiji cha Mavota kwa sasa hawana fursa hata

    kidogo ya kufanya uchimbaji mdogo mdogo licha ya kwamba mgodi huo upo

    kijijini kwao, hali ambayo imekuwa chanzo kikubwa cha migogoro

    inayosababisha uvunjifu wa amani:-

    (a) Je, Serikali iko tayari kuwa na mazungumzo ya kimkakati na

    wananchi wa Kijiji cha Mavota kupitia Mbuge wao kwa

    manufaa ya uwekezaji na wanakijiji wa Mavota?

    (b) Kama Serikali haiko tayari kufanya mazungumzo hayo, je, ni kwa

    sababu zipi?

    NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI alijibu:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini,

    napenda kujibu swali la Mheshimwa Oscar Rwegasira Mukasa, Mbunge wa

    Biharamulo Magharibi, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

    Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ipo tayari kuwa na mazungumzo na

    wananchi wa Kijiji cha Mavota kwa lengo la kuwawezesha wananchi hao

    kutumia fursa zilizopo katika Mgodi wa Stamigold karibu na Mavota. Mgodi huo

    kwa sasa unamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 kupitia STAMICO ambapo

    Stamigold kampuni tanzu ya STAMICO ndiyo inayofanya shughuli za uchimbaji.

    Mheshimiwa Naibu Spika, mambo muhimu yatakayozingatiwa ni pamoja

    na kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji hao wadogo, kuwaelimisha

    namna ya kupata mitaji ya uchimbaji ikiwa ni pamoja na kutumia fursa za

    kuomba ruzuku Serikalini. Kadhalika, pamoja na kuwapa elimu na

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    36

    kuwahamasisha kuunda vikundi vya uchimbaji ili waweze kusaidiwa kwa

    pamoja. Aidha, Mgodi wa Biharamulo utawapatia mafunzo ya utaalamu wa

    kuchimba madini pamoja na kuwafundisha kanuni za usalama, afya na utunzaji

    wa mazingira katika migodi yao. Lakini pia watapewa mafunzo kwa vitendo

    katika mgodi wa Stamigold pale itakapohitajika kufanya hivyo.

    Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, mgodi huo uko tayari na ulishaanza

    kuwasaidia wananchi wa Kijiji cha Mavota. Kati ya tarehe 26 na 30 Juni, 2015,

    Mavota Gold Mine Group kilipewa ushauri wa namna bora ya kuendesha

    shughuli za uchimbaji na utafiti wa dhahabu katika eneo walilomilikishwa leseni.

    Kikundi hicho kilimilikishwa leseni ya uchimbaji mdogo yenye Namba PL

    001493WLZ iliyotolewa tarehe 23 Februari, 2015. Eneo hilo lina ukubwa wa hekta

    9.43.

    Mheshimiwa Naibu Spika, mgodi umetoa fursa za ajira kwa vijiji vya jirani.

    Vijana wenye ajira za muda mrefu kutoka vijiji vya jirani ni 15 na wafanyakazi

    wenye mikataba ya muda mfupi ni 54.

    Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, mgodi umetoa fursa za kibiashara kwa

    vikundi vitatu kutoka vijiji vya Mavota pamoja na Mkukwa ambapo wanavikundi

    hushirikiana kutafuta mazao ya kuuza mgodini kwa kuwasilisha mazao hayo kila

    wiki. Mazao hayo ni pamoja na viazi vitamu, mihogo, mboga za majani pamoja

    na matunda. Kutokana na kufanya biashara na Stamigold kati ya kipindi cha

    Julai 2014 na Disemba 2015, vikundi vyote vitatu vimeweza kujipatia zaidi ya

    shilingi milioni 200.

    NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mukasa swali la nyongeza.

    MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu

    mazuri yenye kuakisi nia ya Wizara na Serikali kushirikiana nasi, nina swali moja la

    nyongeza.

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye swali la msingi, imeelezwa vizuri kabisa

    kwamba uvunjifu wa amani ni moja ya matokeo hasi ya kukosekana kwa fursa

    hizi za wananchi wa Mavota kushiriki kwenye uchumi uliowazunguka. Kwa

    sababu suala la uvunjifu wa amani si suala la kusuburi, ni la haraka, je, Serikali na

    Wizara iko tayari kutoa kauli inayothibitisha uharaka wao katika kuja

    kuzungumza na wananchi wa Mavota?

    NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza

    kabisa nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hatua ambazo Serikali

    imechukua kupitia Wizara yetu ni pamoja na kuhakikisha kwamba uchimbaji

    salama na makini unafanyika kwenye eneo hilo.

  • NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT)

    37

    Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuzingatia umuhimu huo, ofisi yetu iko

    tayari kwenda kuzumgumza na wananchi kuwahakikishia amani zaidi kwenye

    shughuli za uchimbaji eneo la Mavota.

    NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tumefikia mwisho wa maswali yetu

    lakini nina matangazo kadhaa hapa, nitayasoma kabla hatujaendelea.

    Tangazo la kwanza linahusu wageni waliopo Bungeni asubuhi hii,

    tunaanza na wageni wa Waheshimiwa Wabunge.

    Kundi la kwanza ni wageni watano wa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani

    Bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe, ambao ni viongozi wa Baraza la Vijana

    la CHADEMA wakiongozwa na Ndugu Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa

    BAVICHA, karibuni sana. (Makofi)

    Kundi lingine ni wageni 18 wa Mheshimiwa Engineer Stella Manyanya,

    Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, ambao ni wanafunzi wa

    Chuo Kikuu cha Dodoma, karibuni sana. (Makofi)

    Wageni wawili wa Mheshimiwa Godbless Lema ambao ni Meya wa Jiji la

    Arusha, Ndugu Kalisti Lazaro na Diwani wa Kata ya Baraza, Ndugu George

    Mbitika, karibuni sana. (Makofi)

    Wageni wawili wa Mheshimiwa January Makamba, Waziri wa Nchi, Ofisi

    ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira ambao ni wapiga kura wake,

    karibuni sana. (Makofi)

    Wageni wawili wa Mheshimiwa Oscar Rwegasira Mukasa kutoka Jimbo la

    Biharamulo Magharibi ambao ni wat