28
Elimu Tanzania Majibu ya Maswali yanayoulizwa mara kwa mara na Marafiki wa Elimu

Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

  • Upload
    others

  • View
    78

  • Download
    7

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

Elimu TanzaniaMajibu ya Maswaliyanayoulizwa mara kwa mara

na Marafiki wa Elimu

Page 2: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

Waandishi: Mary Nsemwa, Betty Malaki, Finike GogomokaWachangiaji: Marafiki wa Elimu, Lilian R. KallagheWachoraji: Nathan Mpangala,Victor Simon na Goodluck MashallaMhariri: Rakesh Rajani

HakiElimu, 2004SLP 79401, Dar es Salaam,TanzaniaAnwani pepe: [email protected]: www.hakielimu.org

ISBN 9987-423-03-5

Nukuu: Unaruhusiwa kunakili sehemu yeyote ya kijitabu hiki kwa minajili isiyo yakibiashara.Unachotakiwa kufanya ni kunukuu chanzo cha sehemu iliyonakiliwana kutuma nakala kwa HakiElimu.

c

Page 3: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

Yaliyomo

Utangulizi

Maswali kuhusu Sera za Serikali1. Maswali yanayohusu MMEM......................................................................... 3

1.1 MMEM ni nini? 1.2 MMEM ni mpango wa miaka mingapi? Utaendelea mpaka lini?1.3 MMEM inasaidiaje shule za watu binafsi?1.4 MMEM inafika pia Zanzibar?

2. Fedha za MMEM na michango.................................................................... 32.1 Serikali imefuta ada/karo na michango ya lazima, lakini kama

mwananchi anadaiwa afanyeje?2.2 Ruzuku ya Maendeleo (Development Grant) ni nini?2.3 Nini kifanyike kunapokuwa na matumizi mabaya ya fedha katika shule? 2.4 Ruzuku kwa kila mwanafunzi (Capitation Grant) ni nini?

3. Maswali yanayohusu MMES......................................................................... 63.1 MMES ni nini?3.2 Ikiwa mwanafunzi amefaulu darasa la saba na akakosa shule ya

kujiunga, afanyeje?

4. Kushiriki na Kushirikishwa katika elimu.................................................... 74.1 Kuna umuhimu gani wanafunzi kuwa katika kamati ya shule?4.2 Watoto wenye umri wa kwenda shule lakini hawako shuleni wanasaidiwaje?4.3 Mtoto asiye na sare ya shule hana haki ya kupata elimu?4.4 Kwa watoto wanaotoka katika familia zisizo na uwezo kiuchumi wanawezaje

kupata masomo ya ziada?4.5 Wasichana wanaopata mimba shuleni hufukuzwa: Sheria/Sera ya

Serikali inasemaje?4.6 Inaruhusiwa wanafunzi kufanya kazi nyumbani kwa walimu? Sera ya

Serikali inasema nini kuhusu ajira ya watoto? 4.7 Kwa nini mitaala inabadilika mara kwa mara na walimu hawatayarishwi?

5. Utawala bora na ushiriki wa jamii.............................................................. 105.1 Wazazi wanaweza kuchukua hatua gani ili kukomesha ukosefu wa

nidhamu kwa walimu? 5.2 Wanafunzi wanatembea umbali mrefu kutokana na ukosefu wa shule

katika baadhi ya vijiji. Je, tatizo hili litatatuliwaje?5.3 Serikali ina mpango gani kuhusu chakula cha mchana shuleni?

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu i

Page 4: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

5.4 Ni mashirika gani yanayotoa misaada ya kujenga madarasa, kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia, kulipa mishahara ya walimu, ada na sare za shule hasa kwa watoto yatima na wasiojiweza kiuchumi?

5.5. Hatua muhimu za kufuata kama una tatizo linalohusu maswala ya elimu

Maswali kuhusu HakiElimu6. Maswali yanayohusu HakiElimu ............................................................... 13

6.1 HakiElimu inafanya shughuli gani?6.2 Harakati za Marafiki wa Elimu ni nini?6.3 Uhusiano kati ya Rafiki wa Elimu na HakiElimu ukoje?6.4 Ninawezaje kujiunga na Marafiki wa Elimu?6.5 Ninaweza kushirikiana vipi na HakiElimu?

7. Msimamo wa HakiElimu kuhusu elimu na sera mbalimbali.................... 147.1 Nini msimamo wa HakiElimu kuhusu adhabu ya viboko? Adhabu

mbadala ni zipi?7.2 Kwa nini HakiElimu haitoi misaada ya kulipia gharama za masomo kama vile ada,

vitabu, sare, n.k.7.3 HakiElimu inamsimamo gani juu ya wazazi wanaolazimisha watoto wao kuoa au

kuolewa wakiwa shuleni? 7.4 Wasichana wanaopata mimba shuleni hufukuzwa: Nini msimamo wa HakiElimu?7.5 HakiElimu inafanya nini kuhusu watoto yatima, walemavu, masikini na

walioathirika na UKIMWI?7.6 Nini msimamo wa HakiElimu kuhusu matumizi ya kondomu kama kinga ya

UKIMWI?7.7 HakiElimu inafanya nini kuhusu walimu?

8. HakiElimu inavyofanya kazi........................................................................ 178.1 Ninaweza kuwa wakala wa HakiElimu? 8.2 Kwa nini HakiElimu haiendi vijijini na haifungui matawi mikoani?8.3 HakiElimu ina mpango gani kuchora picha za ukutani (murals) zaidi vijijini?8.4 HakiElimu ina uhusiano wa namna gani na redio za kijamii?8.5 HakiElimu ina mpango wa kuendesha semina vijijini?8.6 HakiElimu ni kwa ajili ya wanafunzi pekee?8.7 HakiElimu inatoa elimu kwa njia ya posta?8.8 HakiElimu inatoa misaada ya fedha kwa miradi ya kijamii au

mashirika mengine? Ninaweza kupata wapi fedha kwa ajili ya miradi?8.9 Nini msimamo wa HakiElimu kuhusu kujibu maswali ya kitaaluma k.m.

hesabu, sayansi, nk.

9. Viambatanisho............................................................................................ 209.1 Vyanzo vya Taarifa9.2 Anwani za baadhi ya vyombo vya habari

ii

Page 5: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

UtanguliziKwanza kabisa tunataka kutoa shukrani zetu za dhati kwa Marafiki wote ambaowamekuwa wakiwasiliana nasi. Tunawapongeza kwa ripoti za kazi nzuri wanazozifanyakatika maeneo yao.

Tumepokea barua nyingi zenye maswali mbalimbali kuhusu Harakati za Marafiki wa Elimu,kazi za HakiElimu, Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na mambo menginemengi. Pia tumepokea barua zenye maoni yanayohusu namna ya kuboresha elimu nchini.Tunawashukuru kwa maoni yenu ambayo mara nyingi yanatoa changamoto kwa jamii nahata kwetu HakiElimu na kutusaidia kuboresha shughuli zetu na elimu hapa nchini.Tunathamini michango yenu na tunafurahi mnapo tuandikia.

Kwa sababu baadhi ya maswali yamekuwa yakiulizwa na watu wengi, tumeamuakutengeneza kijitabu hiki ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi kwa mara moja.

Hata hivyo HakiElimu tunaamini kuwa majibu mazuri ya maswali yanayoulizwa na Marafikiyanaweza kupatikana katika jamii, viongozi wenu, mashirika na taasisi nyinginezinazoizunguka jumuiya yenu na si HakiElimu pekee. Pia tunathamini na tunazingatiakufanya kazi kwa pamoja na kujifunza kutoka kwa wengine.

Katika kijitabu hiki tumeandaa majibu ya maswali yanayoulizwa na Marafiki mara kwamara. Endapo maswali yako hayatajibiwa kwenye kijitabu hiki tunakushauri kwanzauyajadili na wengine wanaopenda maendeleo ya elimu katika eneo lako, wasiliana nakamati ya shule na viongozi wa ngazi mbali mbali kuanzia katika ngazi ya kijiji/mtaa, kata,wilaya hadi taifa. Hatua za kufuata zimeonyeshwa katika kiambatisho cha 5 katika kijitabucha Uimarishaji wa Taratibu za Kitaasisi (uk. wa 35) kinachoonyesha muundo wa jumla wakitaasisi kwa ajili ya utekelezaji. Kijitabu hiki kinapatikana HakiElimu.

Unaweza pia kutuma maswali au maoni yako moja kwa moja kwa mashirika na taasisinyingine ambazo zinaweza kukupa majibu ya maswali yako. Orodha hii inapatikana katikavyanzo vya taarifa nyuma ya kijitabu hiki.

Pia unao uhuru wa kutuma maoni na kero zako moja kwa moja kwa vyombo vya habariili jamii ichangie na kutoa maoni yao. Kwa njia hii sauti yako itasikika ambapo maoni nakero zako zitawafikia wahusika.Tunaambatanisha anwani za vyombo vya habari nyuma yakijitabu hiki.

Kama Rais Mkapa alivyosema kwenye hotuba yake iliyohusu Mpango wa Maendeleo yaElimu ya Sekondari (MMES) kwa Taifa mwisho wa mwezi wa Oktoba mwaka 2004:

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu 1

Page 6: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

“...Tanzania lazima ijengwe na Watanzania wote, wa kike na wa kiume, kutokamikoa na maeneo yote ya nchi yetu. Kama elimu bora ya sekondari ndio njia yakuwaandaa watakaoongoza na kuijenga nchi yetu, lazima elimu hiyo wapewevijana wetu, wa kike na wa kiume, kutoka mikoa na maeneo yote. Na kazi hiilazima tuifanye sote, serikali na wananchi.”

Ikiwa kuna shughuli yoyote inayofanywa na Marafiki wa Elimu katika eneo lako inayohusuuboreshaji elimu usisite kutuandikia.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu2

Page 7: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

Maswali kuhusu Sera za Serikali

1. Maswali yanayohusu MMEM

1.1 MMEM ni nini? Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) ni programu ya Serikali ya kuboreshaelimu ya msingi kwa watoto wote nchini. Hii inajumuisha wasichana na wavulana, matajirina maskini pamoja na watoto wenye ulemavu, hakuna hata mmoja atakayeachwa. Kwakuwa hii ni programu ya kitaifa, shule zote za msingi nchini za serikali zitafaidika.

MMEM ni mpango wenye mwelekeo mpana kwa maendeleo ya elimu ya msingi.Vipengelevyake vinne muhimu ni:-

• Ongezeko la uandikishaji• Kuinua kiwango cha ubora• Kujenga uwezo na• Matumizi ya fedha na miundo ya kitaasisi

Mpango huu pia unalenga katika masuala muhimu ya jinsia na UKIMWI

1.2 MMEM ni mpango wa miaka mingapi? Utaendelea mpaka lini? MMEM ni mpango wa miaka mitano kuanzia Januari 2002 hadi Desemba 2006. Bila shakaSerikali itaendelea kutoa elimu ya msingi na kuhakikisha juhudi za kuboresha elimuTanzania zinaendelea hata baada ya 2006.

1.3 MMEM inasaidiaje shule za watu binafsi? MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali. Shuleza watu binafsi zina taratibu zake, ila taratibu hizo zinafuata sera na miongozo ya Serikali.Fedha zinazotolewa na MMEM ni kwa ajili ya shule za serikali tu na siyo za watu binafsi.

1.4 MMEM inafika pia Zanzibar? MMEM ni kwa ajili ya elimu ya msingi Tanzania Bara. Mfumo wa elimu wa Tanzania bara nitofauti na ule wa Zanzibar. Zanzibar ina wizara yake ya elimu ambayo ina jukumu lakuongoza na kuendesha shughuli za elimu.

2. Fedha za MMEM na michango

2.1 Serikali imefuta ada na michango ya lazima, lakini kama mzazianaombwa fedha ndipo mtoto wake aandikishwe afanyeje? Kwa mujibu wa MMEM viongozi hawaruhusiwi kudai michango ya lazima kutoka kwawazazi. Michango yote inayotolewa na wazazi iwe ya hiari. Serikali kupitia MMEM imefuta

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu 3

Page 8: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

michango yote ya lazima ili kuwawezesha watoto wote kupata elimu.Ikiwa mwananchi analazimishwa kutoa michango anaweza kufuata hatua zifuatazo:-

a) Kujadili na watu wengine walioko katika jamii yake b) Baada ya kujadili wanaweza kuwasilisha malalamiko hayo kwa kamati ya shulec) Ikiwa ufumbuzi hautapatikana wanaweza kuwasilisha malalamiko hayo katika ngazi

ya kata, Afisa Elimu wa wilaya husika na kwa Katibu Mkuu, Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa (TAMISEMI), SLP 1923, Dodoma, nakala kwa Katibu Mkuu,Wizaraya Elimu na Utamaduni, SLP 9121, Dar es Salaam. Pia mhusika anaweza kupelekataarifa kwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB) SLP 4865, Dar es Salaam au katikawilaya husika.

d) Wanaweza kutumia pia vyombo vya habari ili jamii ichangie na kutoa maoni yao(anuani za vyombo vya Habari zinapatikana katika kiambatisho mwishoni mwakijitabu hiki).

2.2 Ruzuku ya Maendeleo (Development Grant) ni nini?Hizi ni fedha kwa ajili ya ujenzi mkubwa kama vile kuongeza madarasa, nyumba za walimu,nyenzo za maji na vyoo. (Rejea kipeperushi 4k Shule za Msingi na Fedha). Zinaweza piakutumika kufanya ukarabati mkubwa. Fedha zinazotumwa zinategemea mahitaji halisi yawilaya na shule.Wilaya zenye upungufu mkubwa zinapokea fedha nyingi zaidi.Wilaya nazozinaamua kutuma fedha kwenda katika shule kwa kuzipa kipaumbele shule zenye mahitajimakubwa zaidi.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu4

Page 9: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

2.3 Nini kifanyike kunapokuwa na matumizi mabaya ya fedha katika shule? Serikali inasisitiza uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za shule ikiwa nipamoja na fedha za shule. Jukumu la kusimamia mapato na matumizi ya shule ni la kamatiya shule. Kama una taarifa ya matumizi mabaya ya fedha unaweza kuchukua hatuazilizotajwa chini ya swali 5.5

2.4 Ruzuku kwa kila mwanafunzi (Capitation Grant) ni nini?Kwa mujibu wa MMEM (kijitabu cha MMEM, ukurasa wa 41, kiambatisho cha 6, rejea piakipeperushi 4k Shule za Msingi na Fedha) gharama za mwanafunzi mmoja ni dola 10(takribani shilingi 10,000). Hizi ni fedha kwa ajili ya kununulia vitabu kwa ajili ya mitihani,vifaa vya kufundishia na maswala ya kawaida ya utawala, pia ukarabati na matengenezomadogo madogo. Kati ya hizi dola 10, dola 6 (takribani shilingi 6,000) kwa kila mwanafunzizinapaswa kwenda moja kwa moja shuleni, na dola 4 (takribani shilingi 4,000) kwenyeHalmashauri ya Wilaya kununulia vitabu kwa ajili ya shule.Taarifa mbalimbali zinaonyeshatangu kuanzishwa kwa MMEM shule zinapokea kiasi kikubwa cha fedha kuliko ilivyokuwaawali.

Mtu yeyote anayependa kujua zaidi juu ya matumizi ya hizi fedha anaweza kuwasiliana nakamati ya shule au mkuu wa shule ili kujua ni kiasi gani cha hizi fedha kimeifikia shule

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu 5

Page 10: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

3. Maswali yanayohusu MMES

3.1 MMES ni nini?MMES ni Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari, 2004 - 2009 uliondaliwa nakutangazwa na Serikali. Lengo la kwanza la mpango huu ni kuongeza nafasi za elimu yasekondari, ya kawaida na ya juu. Ifikapo mwisho wa mpango huu, nusu ya vijana waliokatika rika linalolengwa la miaka 14-17, wawe wanasoma katika shule za kawaida zasekondari (K1-K4); na kuhakikisha kuwa nusu ya wanaohitimu kidato cha nne wanapatanafasi kidato cha tano.

Mwaka 2004 walikuwepo karibu wanafunzi 433,000 katika shule za sekondari. Ni lengo laMMES kuwa ifikapo mwaka 2010 wawe wamefikia 2,000,000 yaani zaidi ya mara nne yawaliopo sasa (rejea hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MheshimiwaBenjamin William Mkapa, kwa wananchi, 31 Oktoba 2004).

Mpango huu unalenga kujenga shule 1,500 katika miaka 5 ijayo, nyumba za walimu, namabweni, hasa kwa watoto wa kike.

3.2 Ikiwa mwanafunzi amefaulu darasa la saba na akakosa shule yakujiunga, afanyeje?Ikiwa mwanafunzi amefaulu na akakosa shule atoe taarifa kwa Afisa Elimu wa Wilaya yake.Hata hivyo katika Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) Serikali imepangakuongeza shule mpya za sekondari katika maeneo yaliyokuwa na shule chache. Kwa

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu6

Page 11: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

misingi hiyo watoto wote waliofaulu katika shule za msingi watapata nafasi ya kuendeleana elimu ya sekondari. Pia katika bajeti ya mwaka 2004/2005 Serikali imetangazakupunguza ada kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Serikali kutoka Sh. 40,000 hadiSh. 20,000 kwa mwaka kuanzia Januari 2005. Serikali pia itaongeza maradufu ruzuku yaelimu ya sekondari kwa watoto maskini kutoka wanafunzi 6,000 hadi 12,000 kwa mwaka.Serikali itatoa ruzuku ya uendeshaji shule ya Sh. 15,000 kwa mwanafunzi kwa shule zasekondari zisizo za serikali ambazo si za kibiashara na si za kiseminari. (Rejea Hotuba yaWaziri wa Elimu Mhe. Mungai, 2004/2005 k.23-24) Maelezo zaidi ya hatua za kufuatakupata ada kwa wasiojiweza kifedha na kuhusu mfumo wa elimu kupitia halmashauri zawilaya yanapatikana chini ya kifungo na. 7.2

4. Kushiriki na Kushirikishwa katika elimu

4.1 Kuna umuhimu gani wanafunzi kuwa katika kamati ya shule?Serikali kupitia MMEM inahimiza kuwepo wanafunzi katika kamati ya shule kwa ajili yakuongeza demokrasia, ushiriki na uwajibikaji katika kuendesha elimu ya msingi (kwamaelezo zaidi rejea kiambatisho na 6 uk. 36 -37 kwenye Uimarishaji wa Taratibu zaKitaasisi ambacho pia kinapatikana HakiElimu na kipeperushi 2K Majukumu ya WanafunziKatika Utawala wa Shule). Kwa kushiriki katika kamati ya shule wanafunzi wana nafasi yakuwasilisha maoni na mahitaji ya wanafunzi wote wakiwemo wale walioachwa pembezonina wenye mahitaji maalum.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu 7

Page 12: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

4.2 Watoto wenye umri wa kwenda shule lakini hawako shuleniwanasaidiwaje?Kwa mujibu wa MMEM kufikia 2005, watoto wote wenye umri wa kwenda shulewatakuwa shuleni. Wazazi ambao hawatawapeleka watoto shule wanawajibika kisheria.Watoto ambao watakuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 10 na ambao hawajaanzadarasa la kwanza wanatakiwa kuandikishwa chini ya Mpango wa Elimu ya Msingi KwaWaliokosa (MEMKWA).

4.3 Mtoto asiye na sare ya shule hana haki ya kupata elimu?Kupata elimu ni haki ya kila mtoto. Sera inasema wazazi wana wajibu wa kuwapa watotomahitaji muhimu ya shule. Pia inasisitiza watoto wote wavae sare za shule lakini kamamtoto hana sare ya shule asifukuzwe.

4.4 Kwa watoto wanaotoka katika familia zisizo na uwezokiuchumi wanawezaje kupata masomo ya ziada?Serikali haina mpango wa kutoa msaada kwa ajili ya masomo ya ziada (tuisheni). Ikiwamasomo ya ziada yatatolewa bure yatawasaidia watoto wote hata wale wasio na uwezokifedha. Baadhi ya shule zina utaratibu wa kutoa masomo ya ziada bila malipo ambapowalimu hujitolea kufundisha kwa lengo la kuongeza ufanisi katika shule husika. Ikiwa jamiiina uwezo, inaweza kujitolea na kuchangia katika kutoa tuisheni. Hata hivyo sera inasemamasomo yote yafundishwe kwa ufasaha wakati wa vipindi. Si sahihi kwa mwalimukutokufundisha vizuri katika vipindi vya kawaida ili kuwalazimisha watoto kuhudhuriavipindi vya ziada.

4.5 Wasichana wanaopata mimba shuleni hufukuzwa:Sheria/Sera ya Serikali inasemaje?Kanuni ya Wizara ya Elimu na Utamaduni inasema kuwa wanafunzi hao wafukuzwe kwakuwa kitendo hicho kinadhalilisha shule, ni ukosefu wa maadili/nidhamu. Kwa mujibu washeria ya elimu ya mwaka 1978, mwanafunzi ataweza kufukuzwa au kusimamishwa iwapo

a) atakuwa na tabia ambayo inaweza kuchafua jina la shule na kuvuruga kabisaviwango vya nidhamu vilivyowekwa hapo shuleni,

b) atatenda kosa la jinai au,c) ataoa au kuolewa

Hata hivyo, Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto (UNCRC) ambao Tanzania imeridhiaunasema watoto wote wana haki ya kupata elimu. Hii ina maana kwamba Sera ya Serikaliinawezekana haiendi sambamba na wajibu wa kimataifa. Kwa maelezo zaidi wasiliana naKatibu Mkuu,Wizara ya Elimu na Utamaduni (MOEC) SLP 9121, Dar es Salaam.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu8

Page 13: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

4.6 Inaruhusiwa wanafunzi kufanya kazi nyumbani kwa walimu?Sera ya Serikali inasema nini kuhusu ajira ya watoto? Watoto wanatakiwa kupata muda mrefu zaidi katika masomo na sio kugeuzwa kuwawafanyakazi. Pia hii inaweza kuwaweka watoto katika hatari ya kunyanyaswa kijinsia. Ikiwawalimu wanafanya hivyo ni vizuri kutoa taarifa kwa kamati ya shule ili suala hili lijadiliwe.Kila mtoto ana haki ya kukua na kupata maendeleo katika mazingira ya kutolazimishwakufanya kazi itakayoathiri maendeleo yake. Ni jambo la kawaida kwa watoto kusaidia kazindogondogo katika jamii na hata shuleni ila kazi hizo zilingane na umri wao. Mkataba waKimataifa wa Haki za Mtoto (Kifungu cha 32 na 36) ambao Tanzania imeridhia unakatazawatoto kufanya kazi ambazo ni hatari, zinazoweza kuathiri maendeleo ya watoto kamavile kuwazuia kupata elimu.

4.7 Kwa nini mitaala inabadilika mara kwa mara na walimuhawatayarishwi?Sera ya elimu inahimiza mabadiliko ya mitaala ili iendane na nadharia na stadi za maisha.Mabadiliko ni muhimu ili kuweza kuendana na maendeleo na kufanya elimu iwe nauhusiano na maisha ya watanzania. Hata hivyo mabadiliko ya mara kwa mara yanawezayakaathiri utendaji wa walimu. Ni muhimu mabadiliko hayo yaendane na mafunzo kwawalimu na utoaji vifaa vya kufundishia. Kwa maelezo zaidi wasiliana na Katibu Mkuu,Wizara ya Elimu na Utamaduni, SLP 9121, Dar es Salaam au na Taasisi ya Elimu Tanzania,SLP 35094, Dar es Salaam.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu 9

Page 14: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

5. Utawala bora na ushiriki wa jamii

5.1 Wazazi wanaweza kuchukua hatua gani ili kukomesha ukosefuwa nidhamu kwa walimu?Kamati ya shule ina mamlaka ya kushughulikia masuala ya shule ya kila siku kwa kutumiamiongozo ya Serikali. Hivyo wazazi baada ya kuthibitisha ukweli wa taarifa za utovu wanidhamu wanaweza kuwasilisha malalamiko kwa kamati za shule. Malalamiko hayoyanaweza pia kuwasilishwa kwa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika wilaya husikaau CWT taifa kupitia SLP 2196, Dar es Salaam. Kauli mbiu ya CWT ni haki na uwajibikaji.Hivyo chama kina wajibu wa kuhakikisha kuwa walimu wanazingatia kauli mbiu hiyo. Ikiwaufumbuzi hautapatikana malalamiko hayo yanaweza kuwasilishwa katika ngazi ya kata,wilaya, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) au Wizara ya Elimuna Utamaduni.

5.2 Wanafunzi wanatembea umbali mrefu kutokana na ukosefu washule katika baadhi ya vijiji. Je, tatizo hili litatatuliwaje?Kulingana na sera ya elimu Serikali inakusudia kujenga shule karibu na wananchi. Ikiwashule iko mbali na wananchi, wananchi wanaweza kutoa mapendekezo yao kwa Serikali ilishule ijengwe karibu. Fedha za MMEM zimetengwa kwa ajili hiyo na wananchiwanahimizwa kujitolea kwa kuchangia nguvukazi kujenga shule. Wananchi wanawezakujadili na kupeleka mapendekezo yao kwa serikali ya kijiji ili yaingizwe katika mipango yamaendeleo ya kijiji na kata.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu10

Page 15: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

5.3 Serikali ina mpango gani kuhusu chakula cha mchana shuleni? Serikali haina mpango wa kuwapa watoto wote wa shule chakula. Wazazi na wanajamiiwanaweza kushiriki katika kuchangia chakula kwa watoto wao. Katika sehemu nyingine zaTanzania wanafunzi wanapata chakula shuleni. Chakula hicho kinatokana na michango yawazazi ya nafaka au fedha kulingana na uwezo na makubaliano kati yao, wanafunzi nawalimu. Serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu isipokuwa kwa kushirikiana nawananchi. Pia kuna sehemu chache ambapo miradi kadhaa inatoa chakula kwa wanafunzikwa mfano kupitia Mpango wa Chakula Duniani (WFP).

5.4 Ni mashirika gani yanayotoa misaada ya kujenga madarasa,kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia, kulipa mishahara yawalimu, ada na sare za shule hasa kwa watoto yatima nawasiojiweza kiuchumi? Jukumu la kujenga madarasa, kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na kulipamishahara ni la Serikali. (Rejea MMEM na kipeperushi 4K Shule za Msingi na Fedha).Yapobaadhi ya mashirika (rejea Kiambatisho 9.1) yanayosaidiana na Serikali katika juhudi hizina yanatoa misaada ya kujenga madarasa, kununua vifaa vya kufundishia kama CareInternational SLP 10242, Dar es Salaam, kutoa mafunzo kwa walimu na misaada kwawatoto maskini Plan International SLP 3517, kuboresha elimu ya msingi Aide et ActionSLP 21496, Dar es Salaam. Mashirika ya kijamii yanaweza kupata fedha kutoka Foundationfor Civil Society ambayo inafadhili mashirika yanayojihusisha na kupunguza umaskini nakukuza ujuzi, pia Mfuko wa Jamii wa Jumuiya ya Madola (CEF) ambao wanawezeshamashirika ya kijamii kutekeleza mipango katika kuboresha elimu. Serikali ina utaratibu wakulipa mishahara ya walimu pia katika MMEM na MMES na inaboresha miundombinukatika shule za msingi na sekondari.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu 11

Page 16: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

5.5 Hatua muhimu za kufuata kama una tatizo linalohusu maswalaya elimuIkiwa kuna tatizo linalohusu masuala ya elimu katika eneo lako ni vizuri kulifikisha katikavyombo au ngazi husika ili litafutiwe ufumbuzi. Kwa mfano chombo cha kwanza katikakushughulikia matatizo yanayowagusa wanafunzi ni Baraza la Wanafunzi kupitiawawakilishi wa kila darasa. Kamati ya shule imepewa mamlaka ya kusimamia uendeshajiwa shule. Hivyo ina jukumu la kushughulikia matatizo yanayohusu shule husika na kutoataarifa katika baraza la kijiji au kamati ya mtaa.

Serikali ya mtaa/kijiji itajadili tatizo lako kisha mapendekezo yataandikwa na serikali hizo nakuwasilishwa katika ngazi ya kata, ambayo nayo itajadili maombi hayo kwenye kikao chakecha Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC). Iwapo ombi lake litapitishwa,WDC italiwasilishakatika Halmashauri ya Wilaya ambayo itachukua hatua kulingana na uwezo wake.

Hatua hizi zikichukuliwa zitasaidia kuleta ufumbuzi wa matatizo yanayohusu elimu:1. Jadili na watu wengine walioko katika jamii yako 2. Wasilisha malalamiko kwa kamati ya shule3. Ikiwa ufumbuzi hautapatikana, wasilisha malalamiko katika ngazi ya Kata4. Ikiwa ufumbuzi haupatikani, wasilisha malalamiko kwa Afisa Elimu (DED) wa wilaya

husika 5. Ikiwa ufumbuzi haupatikani, wasilisha malalamiko kwa Katibu Mkuu TAMISEMI,

nakala kwa Katibu Mkuu,Wizara ya Elimu na Utamaduni.6. Unaweza kutumia pia vyombo vya habari ili jamii ichangie na kutoa maoni yao

Rejea Uimarishaji wa Taratibu za Kitaasisi, Agosti 2001. uk. 35 kiambatisho 5

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu12

KAMATI YA UONGOZIMMEM

TAMISEMI MOEC

SEKRETARIATI YAMKOA

MAMLAKA YASERIKALI YA MKOA

UKAGUZI WAWILAYA

KAMATI YAMAENDELEO

YA KATA

BARAZA LAKIJIJI/KAMATI YA

MTAA

BARAZA LASHULE

WANAFUNZI

KAMATI YA SHULE

UKAGUZI WAKANDA

KAMATI YA MAENDELEO YAELIMU YA MSINGI

(BEDC)

UFUNGUO

Uongozi

Ufundi

Ushauri

Page 17: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

6 . Maswali kuhusu HakiElimu

6.1 HakiElimu inafanya shughuli gani? HakiElimu ni shirika la hiari linalolenga kufikia usawa, ubora, haki na demokrasia katikaelimu na jamii. Tunafanya hivyo kwa kuwezesha jamii kupata habari, kubadili shule namfumo wa uundaji wa sera; kuchochea ubunifu wa mijadala ya umma; kufanya utafitiyakinifu, uchambuzi wa sera na utetezi na kushirikiana na wadau ili kuendeleza manufaaya pamoja na kuzingatia haki za jamii. HakiElimu sio mfadhili na haitoi misaada kwa ajili yakujenga madarasa, kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia, kulipia ada na sare za shule,warsha na mafunzo na mahitaji kama hayo.Kwa kufanya hivyo, lengo la HakiElimu linakuwani kutoa taarifa kwa wananchi na kuwezesha sauti za wananchi kusikika.

6.2 Harakati za Marafiki wa Elimu ni nini? Ni harakati za wananchi, mashirika na taasisi zinazojali kuboresha elimu na demokrasianchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu nazinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika maswala yanayohusu elimu.Kama rafiki unaweza kushiriki kikamilifu katika kamati ya shule yako kama vile kwakuchangia mawazo. Unaweza kuanzisha mijadala na majirani zako. Unaweza kupelekamaoni yako ya jinsi ya kuboresha elimu kwa mamlaka za elimu. Kila mtu anaweza kuwaRafiki wa Elimu bila kujali umri, jinsi wala mahali anapotoka kwa kuandika kwa:

Marafiki wa Elimu, c/o HakiElimu, SLP 79401, Dar es Salaam,Tanzania au Barua pepe: [email protected]

Hakuna gharama yoyote kwa anayetaka kujiunga. Mafanikio ya Harakati za Marafiki waElimu yanategemea ushiriki wa Rafiki.

6.3 Uhusiano kati ya Rafiki wa Elimu na HakiElimu ukoje?HakiElimu ni mraghabishi wa Harakati za Marafiki wa Elimu anayewajibika kukupa taarifaza Marafiki wa Elimu na kuzisambaza kwa Marafiki wengine.

Ukiwa katika harakati za Marafiki wa Elimu ni muhimu kukumbuka kwamba wewe simwakilishi wa HakiElimu. Hii ina maana kwamba madai au matamshi utakayotoayanawakilisha maoni yako binafsi na si ya HakiElimu. Hii haimaanishi kwambahatutakubaliana nawe, pengine mara nyingi tutakubaliana!

Watu binafsi, vikundi na wengine watakaojiunga na Harakati za Marafiki wa Elimuwatawajibika kwa shughuli zao. Matendo yao yatafanyika kwa niaba yao wenyewe na siyokwa namna yoyote au wakati wowote kwa niaba ya HakiElimu. HakiElimu haitawajibikakisheria kwa namna yoyote kutokana na vitendo vya Marafiki wa Elimu watakaodai kufanyakazi kwa niaba ya HakiElimu.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu 13

Page 18: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

Harakati za Marafiki wa Elimu zisiwe kwa namna yoyote ile na uhusiano wa moja kwa mojana maswala ya kisiasa, rangi ya mtu au dini. Zinapaswa kuwa wazi na siyo za unyanyasajiwa kidini, ubaguzi wa rangi, kijinsia au imani.

6.4 Ninawezaje kujiunga na Marafiki wa Elimu? Unaweza kujiunga kwa kujaza fomu inayopatikana katika kipeperushi cha Marafiki wa Elimuna kuituma HakiElimu SLP 79401, Dar es Salaam. Pia unaweza kujaza fomu iliyoko katikatovuti www.hakielimu.org kwa kubonyeza Marafiki wa Elimu kisha bonyeza ‘fomu maalumya kujiunga’.

6.5 Ninaweza kushirikiana vipi na HakiElimu? Unaweza kushirikiana na HakiElimu kwa kujiunga na Harakati za Marafiki wa Elimu.HakiElimu kama mraghabishi wa harakati hizi itakutumia taarifa mbalimbali zinazohusuelimu. Taarifa hizo unaweza kuzitumia katika kujadiliana na watu wengine ili kuboreshaelimu katika jamii. Kama una uwezo wa kuwasiliana kwa mtandao wa kompyuta, unawezapia kutuandikia au kutoa maoni yako kupitia kwenye tovuti www.hakielimu.org Vilevileunaweza kushirikiana na HakiElimu kwa kuonyesha wajibu wako katika jamii yako.

7. Msimamo wa HakiElimu kuhusu elimu nasera mbalimbali

7.1. Nini msimamo wa HakiElimu kuhusu adhabu ya viboko?Adhabu mbadala ni zipi?HakiElimu inaamini kuwa adhabu ya viboko haifai kwa sababu haimsaidii mtoto kujifunzabali inaweza kujenga chuki na humfanya mtoto ajisikie ameonewa.Adhabu ya viboko piainahatarisha afya ya mtoto. Utafiti unaonyesha kuwa wanaopigwa wakiwa watotowanapokua huwa na hasira na matatizo mengine. Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto(kifungu cha 2 na 37) unakataza unyanyasaji na adhabu kali kwa wototo.Tunaamini kuwamtoto anaweza kuwa na nidhamu bila kuumizwa. Kwa maelezo zaidi kuhusu sheriainayohusu viboko unaweza kuwasiliana na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Utamaduni.Unaweza pia kupata taarifa kuhusu adhabu hiyo kutoka katika Kituo cha Kutetea Haki zaWatoto cha Kuleana.Anwani yao ni Kuleana, SLP 27, Mwanza.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu14

Page 19: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

7.2 Kwa nini HakiElimu haitoi misaada ya kulipia gharama zamasomo kama vile ada, vitabu, sare, n.k.HakiElimu haitoi misaada ya kugharamia masomo kwa kuwa utaratibu huo haupo ndaniya mikakati yake. Shughuli zake ni kuboresha ushiriki wa umma katika elimu. HakiElimuinawasaidia wananchi kujua haki na wajibu kwa kuwapa taarifa mbalimbali ili wawezekuchangia kuboresha elimu. Inatambua kuwa yapo matatizo yanayoweza kukwamishawatoto kwenda shule ila haiwezi kufanya kila kitu. Inasisitiza kuwa wajibu wa kumpatiamtoto elimu uanzie kwa mzazi, jamii inayomzunguka na Serikali.

Serikali kupitia Halmashauri za Wilaya hapa nchini ina utaratibu maalum wa kuwasaidiawatu wasio na uwezo wa kujiendeleza kielimu kutokana na sababu mbalimbali zikiwemohali ngumu ya kiuchumi. Utaratibu unaofuatwa ni kwamba mhusika (au familia yake)ataandika barua kwa serikali ya mtaa/kijiji. Serikali ya mtaa/kijiji itajadili ombi lake nakuthibitisha kama kweli anahitaji kusaidiwa. Kisha mapendekezo yataandikwa na serikalihizo na kuwasilishwa katika ngazi ya kata, ambayo nayo itajadili maombi hayo kwenyekikao chake cha Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC). Iwapo ombi lake litapitishwa,WDC italiwasilisha katika Halmashauri ya Wilaya ambayo itachukua hatua kulingana nauwezo wake kifedha. Kwa mujibu wa utaratibu huo, kipaumbele hutolewa zaidi kwawanafunzi ambao wamefaulu kujiunga na shule za sekondari na vyuo lakini wakashindwakujiunga kutokana na uwezo mdogo wa kifedha. Kwa maelezo zaidi wasiliana na mamlakahusika kuanzia uongozi wa mtaa wako.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu 15

Page 20: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

7.3 HakiElimu ina msimamo gani juu ya wazazi wanaowalazimishawatoto wao kuoa au kuolewa wakiwa shuleni?Kwa mujibu wa Sheria ya Elimu ya mwaka 1978, mwanafunzi ataweza kufukuzwa aukusimamishwa iwapo ataoa au kuolewa. HakiElimu inaamini kuwa elimu ni haki ya kilamtoto. Inahimiza wazazi kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto na madhara yakuwakosesha watoto elimu. Wazazi wanaowalazimisha watoto wao kuoa au kuolewawakiwa shuleni wachukuliwe hatua kisheria na waelimishwe zaidi.

7.4 Wasichana wanaopata mimba shuleni hufukuzwa: Ninimsimamo wa HakiElimu? HakiElimu inaamini kuwa elimu ni haki ya kila mtoto wakiwemo waliopata mimba. Mimbahaiondoi haki ya kupata elimu kwa kuwa licha ya kuwa na mimba bado ni mtoto.Wasichana wajawazito wanahitaji elimu zaidi kuliko wengine. Ndio maana HakiElimuinatetea wasichana hao wapate fursa ya kupata elimu na watiwe moyo ili wawezekuendelea na masomo baada ya kujifungua. Kuwafukuza watoto hao shuleni nikuwanyanyasa wao na watoto watakaozaliwa ambao hawana makosa. Baadhi ya watotowamepata mimba kwa kulazimishwa kufanya ngono au kubakwa. Elimu ndio njia nzuri yakuwakomboa wanawake na wasichana katika jamii, hasa wale walioathirika na mimba.Kama alivyosema Mwalimu Nyerere,“Kwa watu masikini kama sisi elimu inatakiwa kuwachombo cha ukombozi”. Katiba ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto (UNCRC)pia inasisitiza watoto wote - wakiwemo na waliopata mimba - wana haki ya kupata elimubila kubaguliwa.

7.5 HakiElimu inafanya nini kuhusu watoto yatima, walemavu,maskini na walioathirika na UKIMWI?HakiElimu inasisitiza kuwa watoto hao wasitengwe na wapewe fursa sawa.Watoto wotebila ubaguzi wa aina yoyote wana haki ya kupata elimu ya msingi. HakiElimu haishughulikimoja kwa moja na watoto yatima, walemavu, masikini na walioathirika kwa UKIMWI. Hatahivyo katika ngazi ya taifa HakiElimu inashirikiana na mashirika mbalimbali kutetea haki zawatoto wanaoishi katika mazingira magumu. Sera yetu ya utetezi na machapisho yetuvinasisitiza ushirikishwaji wa wote. Katika kufanya hivi tunajitahidi kuwapa nafasiwawakilishi wa walioadhirika kutoa maoni na kusikika.

7.6 Nini msimamo wa HakiElimu kuhusu matumizi ya kondomukama kinga ya UKIMWI?HakiElimu inasisitiza elimu ya wazi kuhusu matumizi ya kondomu ianzie shuleni na ianzemapema kabla watoto hawajaanza kujihusisha na ngono. Elimu hiyo izingatie stadi zamaisha, iwe ya wazi na mbinu za ufundishaji ziwe shirikishi na za majadiliano. Utafitiuliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya (WHO) na UNAIDS unaonyeshakwamba aina hii ya elimu inawasaidia vijana kupunguza hatari ya maambukizo ya UKIMWI.Utafiti huu pia unaonyesha kwamba elimu wazi haiwasisimui vijana kujihusisha zaidi nangono. Utafiti umeonyesha kuwa 50% ya watoto hufanya ngono kabla ya kumaliza darasa

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu16

Page 21: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

la saba. Kutoshiriki ngono ni njia nzuri ya kujikinga. Kwa wale wanaofanya mapenzi,kondomu ni njia moja ya kujikinga na maambukizi ya UKIMWI na magonjwa mengine yazinaa. Ikitumika ipasavyo inaweza kukinga kwa kiasi kikubwa ingawaje siyo 100%.

7.7 HakiElimu inafanya nini kuhusu walimu?HakiElimu inashirikiana na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kutetea na kuendelezamaslahi ya walimu na pia kuboresha kazi na uwajibikaji wao. Kwa mfano imeshirikiana naCWT kufanya utafiti kuhusu maisha na mazingira ya kazi kwa walimu. Matokeo ya utafitihuo yatatoka mapema 2005. Pia HakiElimu imeshirikiana na CWT kuhakikisha kilamwalimu anaweza kupata nakala ya katiba ya CWT. HakiElimu inaamini kuwa walimu ndiokitovu cha elimu na elimu haiwezi kuwa bora bila walimu. HakiElimu inasisitiza ushiriki wawalimu katika utungaji na usimamizi wa sera.

8. HakiElimu inavyofanya kazi

8.1 Ninaweza kuwa wakala wa HakiElimu? HakiElimu haina utaratibu wa kutumia mawakala katika shughuli zake ila inafanya kazi namashirika yanayojihusisha na maswala ya elimu na demokrasia kwa ubia na kupitiamitandao. Mashirika hayo yanaweza kusaidia katika kusambaza machapisho ya HakiElimu.Vilevile HakiElimu inasaidia mashirika mengine kusambaza machapisho yanayoelimishajamii. Inafanya kazi na Marafiki wa Elimu ambao wapo katika nchi nzima mijini na vijijini.Marafiki ni watu wanaojali na ambao wamedhamiria kuchangia katika kuleta mabadilikokatika elimu.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu 17

Page 22: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

8.2 Kwa nini HakiElimu haiendi vijijini na haifungui matawimikoani?HakiElimu haiendi vijijini wala haifungui matawi mikoani kwa sababu ni shirika dogo nahaliwezi kuifikia nchi nzima kwa njia hiyo. HakiElimu siyo watekelezaji wa mabadiliko baliwananchi wenyewe ndio watakaoleta mabadiliko. Shirika linachofanya ni kuwawezeshawatu kuleta mabadiliko pale walipo kwa kuwatumia machapisho yenye habari mbalimbaliza elimu na kuwaunganisha Marafiki wa Elimu na mashirika mbalimbali hapa nchini ilikupata habari zaidi. Machapisho ya HakiElimu yanasambazwa katika wilaya zote nchini. PiaHakiElimu inatumia redio na televisheni kupeleka ujumbe ambao unawafikia wananchikaribu nchi nzima kwa muda mfupi.

8.3 HakiElimu ina mpango gani kuchora picha za ukutani (murals)zaidi vijijini?HakiElimu ilishirikiana na mashirika mbalimbali kuchora picha ukutani katika baadhi yamikoa nchini Tanzania. Kwa sasa haiendelei na kazi hiyo. HakiElimu inashauri shughuli hiyoifanywe na wasanii walioko vijijini kwa ushirikiano na tawala za mitaa pamoja na jamii ilihabari za jamii zipewe kipaumbele. Ipo tayari wakati wowote kuwapatia picha na michoroinayoweza kuchorwa.

8.4 HakiElimu ina uhusiano wa namna gani na redio za kijamii?HakiElimu inaamini kuwa vyombo vya habari zikiwemo redio za kijamii ni muhimu kwaajili ya kupasha habari na kuibua mijadala katika jamii. Wakati wote ipo tayari kupeleketaarifa na machapisho yake katika redio hizo. HakiElimu inatoa taarifa kuhusu sera za taifakwa redio za kijamii ili nao watoe taarifa kwa jamii. HakiElimu inashauri redio za kijamiizitoe nafasi kwa wananchi wa kawaida ili sauti zao zisikike.

8.5 HakiElimu ina mpango wa kuendesha semina vijijini?Kwa kawaida HakiElimu haiendeshi warsha wala semina kwani inaamini kuwa zipo njianyingine bora za kuleta maendeleo. Inazingatia zaidi upashanaji wa habari na midahalo yaumma iliyo wazi na ambayo huweza kufanyika mahali popote ikishirikisha watu wengi zaidikutoa maoni. HakiElimu inatumia vyombo vya habari ili kuwafikia watu wengi zaidi badalaya semina ambazo zinahusisha watu wachache tu. Mara nyingi gharama za kuendeshasemina ni kubwa ukilinganisha na matokeo ya semina hizo!

8.6 HakiElimu ni kwa ajili ya wanafunzi pekee?HakiElimu ni kwa ajili ya watu wote wanaotaka kuboresha elimu na demokrasia bilaubaguzi wa aina yoyote. HakiElimu inafanya kazi na makundi yote ya jamii yenye nia yakuleta mabadiliko katika elimu kama vile wanafunzi, walimu, wazazi, mashirika, taasisi zaserikali na viongozi. Kila mmoja anaweza kutoa maoni na mapendekezo, kufuatilia sera,utekelezaji na kuchangia uwajibikaji.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu18

Page 23: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

8.7 HakiElimu inatoa elimu kwa njia ya posta?HakiElimu inatambua kuwa zipo njia mbalimbali za kutoa elimu mojawapo ikiwa ni kwanjia ya posta. Inatumia posta kusambaza machapisho yenye ujumbe kuhusu elimu. Jamiiinaweza kuyachambua machapisho hayo na kujadili na wengine ili iweze kuleta mabadilikokatika elimu. HakiElimu haitoi elimu rasmi. Serikali kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazimainatoa elimu kwa njia ya posta. Kwa maelezo zaidi wasiliana nao kupitia SLP 20679, Dares Salaam.

8.8 HakiElimu inatoa misaada ya fedha kwa miradi ya kijamii aumashirika mengine? Ninaweza kupata wapi fedha kwa ajili yamiradi?HakiElimu haitoi misaada ya fedha kwa miradi ya jamii, mashirika wala kwa mtu mmojammoja kwani sio mfadhili. Inawezesha watu wenyewe kuleta mabadiliko ya elimu katikamaeneo yao kwa kuwasaidia wananchi kujua haki na wajibu wao katika kuleta mabadilikokatika elimu na demokrasia. Mashirika kama ya Foundation for Civil Society (FCS), SLP7192, Dar es Salaam na Mfuko wa Elimu wa Jumuia ya Madola (CEF), SLP 10414, Dar esSalaam yanatoa misaada ya fedha kwa ajili ya miradi. Kwa habari zaidi wasiliana nao.

8.9 Nini msimamo wa HakiElimu kuhusu kujibu maswali yakitaaluma kama hesabu, sayansi, nk.HakiElimu haina utaratibu wa kujibu maswali ya kitaaluma ila ina wajibu wa kutoa taarifazinazohusu sera ya elimu na jinsi wananchi wanavyoweza kubadili elimu. Ikiwa una maswaliya kitaaluma unaweza kuwasiliana na walimu katika eneo lako. Unaweza pia kusomamakala katika magazeti ambayo yanajibu maswali mbalimbali ya kitaaluma kwa mfanomajira

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu 19

Page 24: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

9.Viambatanisho

9.1 Vyanzo vya taarifa Tumeorodhesha maelezo ya vyanzo vya taarifa vinavyoweza kukusaidia kama mshiriki waHarakati za Marafiki wa Elimu. Orodha hii haijakamilika. Ikiwa una vyanzo vingine vyataarifa ambavyo unadhani vinaweza kuwanufaisha wengine tafadhali tujulishe.

ActionAid, www.actionaidtz.orgSLP 21496, Dar es Salaam.Action Aid imekuwepo nchini Tanzania tangu 1997. Makao yakemakuu yapo mjini Dar es Salaam. Inashirikiana na zaidi ya watu 65,000 katika miradimitatu, Mtwara, Kigoma na Lindi. Mtazamo wake ni kuhakikisha kwamba watu wanaoishivijijini na wale waliokosa nafasi awali wanapata elimu bora.

Aide et Action, www.aide-et-action.orgSLP 2065, Mwanza: Ni shirika lisilo la kiserikali linaloinua na kuboresha elimu ya msingikatika baadhi ya wilaya Tanzania. Shughuli zake ni ujenzi wa madarasa, kuzipa uwezo kamatiza shule na kutoa vifaa vya ujenzi.

Benki ya Dunia Tanzania, www.worldbank.org/tz Tovuti ya Benki ya Dunia Tanzania, inalenga kutoa kwa undani chanzo cha taarifazinazohusu kupunguza umaskini na ongezeko la uchumi Tanzania. Inatoa ufafanuzi waprogramu ya msaada wa Benki ya Dunia na maktaba yenye taarifa za sekta mbalimbali,machapisho na nyaraka mbalimbali zinazohusika zinazotolewa na Benki hiyo na wafadhiliwengine.

Bunge la Tanzania, www.bunge.go.tzBunge la Tanzania ni taasisi inayowakilisha watu wote wa Tanzania. Bunge lipo kwa mujibuwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika tovuti hii utapata taarifazinazohusu shughuli za bunge.

Education for All - Mtandao wa Elimu, www.elimu.orgHuu ni mtandao unaofanya kazi kuhakikisha kwamba kila mtu anapata elimu ya msingibure na bora. Mtandao unasaidia mashirika ya kiraia kuunda umoja wa kitaifa ambaounajenga mtazamo wao wa mageuzi pamoja na agenda yao ya utetezi.

Foundation for Civil SocietySLP 7192, Dar es Salaam: The Foundation for Civil Society inafadhili shughuli ambazozinaleta ushirikiano na kukuza ujuzi na zitakazoendeleza stadi na ufahamu wa masuala yasera na utawala. Inafadhili jumuia za kijamii zinazojishughulisha na kupunguza umaskini kwakujenga uwezo wa vyama na mitandao ya kiraia. Inafadhili jumuia ambazo hazilengi katikakupata faida binafsi.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu20

Page 25: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

Forum for African Women Educationalists (FAWE Tz)SLP 63319, Dar es Salaam: FAWE inajaribu kuhakikisha kwamba watoto wa kike wotewanakwenda shule, wanamaliza masomo yao na wanafanya vizuri katika ngazi zote zaelimu. Hapa Tanzania FAWE inaendesha programu ya utetezi ili kuongeza ushiriki wawanawake katika elimu na kukusanya taarifa na maelezo yatakayobadili mfumo wa sera.

Hakikazi Catalyst, www.hakikazi.orgSLP 781,Arusha: Hakikazi inatetea shughuli zinazowapa uwezo watu wasio na sauti katikajamii kusikika na kuweza kuchochea mabadiliko ya maamuzi yanayogusa maisha yao ya kilasiku na kuwa na haki ya kisiasa na kufurahia haki sawa na wengine katika jamii yao, kitaifana kimataifa.

Kuleana - Kituo cha kutetea haki za watoto SLP 27, Mwanza na SLP 14335, Dar es Salaam: Kuleana ni shirika la kutetea haki za watotonchini Tanzania. Kuleana inashughulika na uhamasishaji na utetezi wa haki za watoto nchiniTanzania kupitia mipango ya utafiti, uchapishaji na uraghabishi. Ni moja ya mashirika yaliyomstari wa mbele katika kampeni dhidi ya adhabu ya viboko shuleni.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),www.humanrightstz.orgSLP 75254, Dar es Salaam: Kituo hiki kinafanya kazi ya kuelimisha juu ya sheria na haki zabinadamu hasa kwa watu wasio na uwezo kifedha katika jamii. Kituo kinatoa mafunzo yakisheria, msaada wa kisheria na machapisho mbalimbali.

Mfuko wa Elimu wa Jumuia ya Madola (CEF)c/o Save the Children UK, SLP 10414, Dar es Salaam: CEF inasimamiwa na ActionAid,Save the Children na Oxfam. Lengo la mfuko huu ni kuwezesha mashirika ya kijamiikutekeleza mipango inayolenga katika kuboresha elimu Tanzania. Inafadhili zaidi mashirikana jumuia za kijamii hasa zilizofanya kazi pamoja.

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)www.poralg.go.tzSLP 1923, Dodoma: TAMISEMI ni Wizara inayoshughulikia Serikali za Mitaa. Ni moja yaWizara zilizoandaa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM). Pamoja nashughuli zingine inawajibu wa kusimamia uendeshaji wa shule za msingi Tanzania.

Plan International, www.plan.international.org/tanzaniaSLP 3517, Dar es Salaam: Plan International ni shirika la kimataifa lenye kuhimiza haki zawatoto. Shirika hili linafanya kazi kwa kushirikiana na familia na jamii kusaidia watotokufahamu uwezo wao katika maisha. Hapa nchini shirika linafanya kazi katika miradimbalimbali pamoja na miradi ya elimu katika baadhi ya mikoa.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu 21

Page 26: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

Research on Poverty Alleviation (REPOA), www.repoa.or.tzSLP 33223, Dar es Salaam: REPOA ni shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na utafiti.Linaiwezesha jamii kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu kuondoa umaskini.REPOA inachangiakatika uandaaji na ufuatiliaji wa Mkakati wa Kupunguza Umaskini (PRS).

Save the Children (UK), www.savethechildren.org.ukSLP 10414, Dar es Salaam: Save the Children UK inaamini kwamba watoto wana haki yakuwa na furaha, afya na usalama wa maisha yao. Shirika hili linafanya kazi ili kujenga mazingiramazuri kwa watoto duniani. Kwa hapa nchini shirika hili lina makao yake makuu jijini Dar esSalaam. Miradi yake ipo Lindi, Unguja na Pemba.

Serikali ya Tanzania, www.tanzania.go.tzTovuti hii ya Serikali ya Tanzania ina taarifa mbalimbali kama vile hotuba na matamko ya Rais,tafiti zinazohusu uchumi wa nchi, idadi ya watu nk.

Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA) SLP 42984, Dar es Salaam: Hili ni shirika linalotetea haki za walemavu wakiwemo wenyemtindio wa ubongo, viziwi, zeruzeru, wenye ulemavu wa viungo na wasioona. Shirika hililinashughulikia masuala yanayohusu elimu,afya,masuala ya kijamii na kiuchumi kwa walemavu.

Tanzania Online, www.tzonline.orgHii ni Tovuti ya marejeo ya nyaraka mbalimbali zinazohusiana na maendeleo Tanzania. Kwamfano bajeti ya Serikali, sera za Serikali,Mkakati wa Kuondoa Umaskini Tanzania na Utaratibuwa Kufuatilia Umaskini.

Tanzania Education Network /Mtandao wa Elimu Tanzania(TEN/MET) SLP 13547, Dar es Salaam: TEN/MET ni mtandao wa kitaifa unaounganisha vikundi namashirika yenye nia ya kuendeleza na kuboresha elimu Tanzania. TEN/MET ni mtandaomuhimu ambao unaweza kukuunganisha na mashirika mengine yanayofanya kazi katika eneolako.

Tanzania Education website, www.tanedu.orgTovuti ya elimu inatoa taarifa zinazohusu masuala mbalimbali ya elimu kama vile sera ya elimu,MMEM, majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha I na V; pia matangazo yanafasi za kazi.Vilevile katika tovuti hii zipo nukuu mbalimbali zinazohusu elimu.

Tanzania Gender Networking Program (TGNP), www.tgnp.orgSLP 4361,Dar es Salaam:TGNP ni mtandao wa jinsia wa Tanzania unaotetea usawa wa kijinsiana kijamii kwa kuwapa nguvu wanawake na watu wasio na sauti katika jamii. Ina idara yauchapaji pamoja na maktaba muhimu iliyoko katika ofisi zake mabibo, jijini Dar es Salaam.

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu22

Page 27: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

Tanzania Movement for and with Children (TMC),www.tmc.kabissa.orgSLP 21159, Dar es Salaam:TMC ni muungano wa kitaifa unaochochea na kuwezesha watukushirikiana katika kuchambua, kujadili na kuboresha upatikanaji wa haki za watoto.Unawawezesha watoto na vijana kuungana pamoja na kufanya sauti zao zisikike kikamilifukatika ngazi zote; na unatoa fursa kwa watoto na vijana kushiriki katika mchakato wamaendeleo.TMC inatekeleza Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watoto.

The Tanzania Development Gateway, www.tanzaniagateway.orgHii ni tovuti yenye taarifa mbalimbali zinazohusu maendeleo kama vile kilimo, biashara,elimu na utawala bora. Unaweza kupata taarifa yoyote inayohusu Tanzania kama vilembuga za wanyama, biashara, kilimo, miradi mbalimbali inayoendeshwa nchini nk.

Tovuti ya Tanzania ya Kufuatilia Umaskini,www.povertymonitoring.org.tzTovuti hii ina habari kuhusu maendeleo na matokeo ya Mkakati wa Kuondoa UmaskiniTanzania na Utaratibu wa Kufuatilia hali ya Umaskini. Imeandaliwa na Ofisi ya Makamu waRais.

United Nations Children’s Fund Tanzania (UNICEF),www.unicef.orgSLP 4076, Dar es Salaam: UNICEF ni Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watotona vijana. Shirika lina ofisi zake jijini Dar es Salaam. Pia lina kituo cha habari zinazohusuwatoto na vijana ambacho kipo wazi kwa watu wote. UNICEF inafanya kazi katika wilayanyingi nchini kote juu ya maswala ya elimu, afya, UKIMWI na masuala mengine.

Umoja wa Asasi Zisizo za Kiserikali juu ya Sera/NGO Policy Forum(NPF) SLP 38486, Dar es Salaam: NPF inazileta pamoja takribani asasi 90 za kitaifa na kimataifazinazojihusisha kwa undani na michakato ya sera Tanzania. NPF inalenga katika Mkakati waKuondoa Umaskini (PRS), Uhakiki wa Matumizi ya Umma (PER) na Serikali za Mitaa.Lengo kuu ni kuzifanya sera ziwe wazi zaidi, za kidemokrasia na zenye kuwajibika kwawatu.

Wizara ya Elimu na Utamaduni (MOEC) SLP 9121, Dar es Salaam: Hii ni Wizara inayowajibika katika kuendeleza, kusimamia nakuandaa sera na miongozo mbalimbali ya elimu nchini.Wizara hiyo ni moja ya wizara kuuzilizoandaa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Mpango wa Maendeleoya Elimu ya Sekondari (MMES).

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu 23

Page 28: Elimu Tanzania Majibu ya Maswali...MMEM ni mpango wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania unaoratibiwa na Serikali.Shule za watu binafsi zina taratibu zake,ila taratibu hizo zinafuata

9.2 Anwani za baadhi ya vyombo vya habari

VYOMBO VYA HABARI FAKSI SIMU SLPAlasiri 2773582 2700735/7 31042, Dar es SalaamBusiness Times 2130033 2118378/9 71439, Dar es SalaamDaily News 2112881 2110595 9033, Dar es SalaamDTV/CTN/Channel 10 2113112 2116342 14678, Dar es SalaamEast African Radio 2775915 2775916 21122, Dar es SalaamFinancial Times 2773583 2700735/7 31042, Dar es SalaamIkulu 2113425 2116913 31042, Dar es SalaamMaelezo Hall 2113814 2122771Majira 2118382 2118377 71439, Dar es SalaamMsanii Afrika 2500713 2503262 1732, MwanzaMtanzania 2461459 2461459 4793, Dar es SalaamMwananchi 2180183 2180647 19754, Dar es SalaamNipashe 2700146 2700735/7 31042, Dar es SalaamRadio Uhuru 2182369 2181700 9221, Dar es SalaamRadio Free Africa 2500713 2503262 1732, MwanzaRTD 2865569 2865563 4793, Dar es SalaamRTD 2865569 2865563 9191, Dar es SalaamStar TV 2773583 2700735/7 1732, MwanzaTaifa Letu 2773583 2700735/7 31042, Dar es SalaamTaifa Letu 2461459 2461459 31042, Dar es SalaamThe African 2773582 2461459 4793, Dar es SalaamTvT 2772603 2700464 31042, Dar es SalaamTvT 2182659 2182665 31519, Dar es SalaamThe Citizen 2120791 2120897 20588, Dar es SalaamThe Citizen 2461459 2461459 19754, Dar es SalaamUhuru/Mzalendo 2183780 2461459 4793, ArushaUhuru/Mzalendo 2183780 744-691490

744-308529 9221, Dar es SalaamVictoria FM 2622944 2622091 1102, MusomaVoice of Tabora 744-261761 84, Tabora

Majibu ya Maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu24