196
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA TISA Kikao cha Nne – Tarehe 10 Novemba, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae, Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, leo tunaanza kama kawaida Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Josephine Genzabuke, Mbunge wa Viti Maalum. Na. 39 Hospitali ya Wilaya MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:- Wilaya za Kakonko, Buhigwe na Uvinza ni Wilaya mpya ambazo hazina Hospitali za Wilaya. Je, ni lini Serikali itajenga Hospitali za Wilaya katika Wilaya hizo?

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

  • Upload
    others

  • View
    0

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE___________

MKUTANO WA TISA

Kikao cha Nne – Tarehe 10 Novemba, 2017

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua

MWENYEKITI: Tukae, Katibu.

NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, leo tunaanzakama kawaida Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa JosephineGenzabuke, Mbunge wa Viti Maalum.

Na. 39

Hospitali ya Wilaya

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:-

Wilaya za Kakonko, Buhigwe na Uvinza ni Wilaya mpyaambazo hazina Hospitali za Wilaya.

Je, ni lini Serikali itajenga Hospitali za Wilaya katikaWilaya hizo?

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Josephine Johnson Genzabuke, Mbunge wa VitiMaalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti ya mwaka wafedha 2017/2018 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonkoimeidhinishiwa jumla ya shilingi milioni 500 kuanza ujenzi waHospitali ya Wilaya. Ujenzi wa hospitali hiyo unatarajiwakugharimu shilingi bilioni 1.5 hadi kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya yaUvinza imetenga eneo la ekari 80 na imekamilisha michoroya jengo la Hospitali ya Wilaya. Halmashauri imeshauriwakuweka kipaumbele na kutenga bajeti katika mwaka wafedha 2018/2019 ili kuanza ujenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya yaBuhigwe inaendelea na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya kwakuanza na jengo la wagonjwa wa nje, utawala na maabaraunaogharibu shilingi milioni 450. Katika mwaka wa fedha2017/2018 Halmashauri imetengewa shilingi milioni 500kuendelea na ujenzi. Kazi hii inatekelezwa na SUMA JKT nakazi inaendelea. Ujenzi wa hospitali unafanyika kwa awamukulingana na upatikanaji wa fedha na unakadiriwakugharimu shilingi bilioni 6.4 hadi kukamilika.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Genzabuke.

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Namshukuru Mheshimiwa Naibu Wazirikwa majibu yake mazuri lakini nina maswali mawili yanyongeza.

Kwa kuwa wananchi wa Wilaya ya Kakonko kwa sasawanapata huduma katika Kituo cha Afya cha Kakonko nakituo hicho kimezidiwa kwa sababu msongamano wa watu

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

ni mkubwa. Kituo hicho kinahudumia wananchi kutoka hadiMkoa jirani wa Kagera kwa maana ya wananchi waNyakanazi, Kalenge pia na wakimbizi kwa sababu katikaWilaya ile kuna kambi za wakimbizi, Waziri amesemakwamba mwaka 2017/2018 zimetengwa shilingi milioni 500.

Je, Waziri yupo tayari sasa kutokana na jinsi wananchiwanavyopata shida pamoja na waganga na wauguzi kwasababu watu wakiwa wengi waganga naowanachanganyikiwa, yupo tayari kufuatilia hizo shilingi milioni500 ziweze kwenda mara moja Kakonko kwenda kuwasaidiawananchi? (Makofi)

Swali la pili; kwa wakati huu ambapo Wilaya ya Uvinzahaina Hospitali ya Wilaya, wananchi wanapata hudumakatika vituo vya afya na zahanati, lakini vituo hivyo vya afyapamoja na zahanati havina watumishi wa kutosha.

Je, katika mgao huu wa wafanyakazi ambaowataajiriwa kwa sasa, Serikali iko tayari kabisa kupelekawatumishi wengi wa kutosha kwenda kusaidia katika Wilayaya Uvinza ambayo haina Hospitali ya Wilaya? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): MheshimiwaMwenyekiti, napenda kumshukuru sana MheshimiwaGenzabuke kwa jinsi ambavyo anafuatilia huduma hasa kwawanawake katika Mkoa wa Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza,napenda kumthibitishia kwamba fedha hizo ambazozimetengwa kwenye bajeti ya 2017/2018 nitazifuatilia nakuzisimimamia mimi mwenyewe binafsi kuhakikisha kwambazimekwenda haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali la pili, wiki hiiiliyopita tumekamilisha upatikanaji wa watumishi 2,008ambao sasa hivi wanaendelea kugawanywa katika

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

Halmashauri mbalimbali. Leo hii nitahakikisha kwambaHalmashauri ya Wilaya ya Uvinza imepata watumishi wakutosha angalau kwa mahitaji ya asilimia 50. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Hongoli.

MHE. JORAM I. HONGOLI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kupewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Jimbo la Lupembe, Halmashauri ya Wilaya ya Njombeni moja ya Halmashauri ambayo haina Hospitali ya Wilayana tuna vituo vya afya vinne, kituo cha afya kimoja chaLupembe ni cha zamani, hivi karibuni tumefungua chumbacha upasuaji tayari operation zinaendelea pale. Tuna Kituocha Kichiwa ambacho tunatarajia pia tuwe na theater ilikuwahudumia akina mama wasitembee umbali mrefukwenda Kibena.

Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya kujenga aukuanzisha chumba cha upasuaji ili akina Mama katika Kituocha Afya cha Kichiwa ili akina Mama wasisafiri umbali mrefukwenda hospitali ya Kibena ambayo ipo mbali sana nawanapoishi ambapo Jimbo la Lupembe lipo. Ahsante.

MWENYEKITI: Majibu Mheshimiwa Waziri wa kifupi,ajiandae Mheshimiwa Ungando.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja namajibu mazuri ya Naibu Waziri, napenda kujibu swali laMheshimiwa Mbunge wa Lupembe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kituo cha afya chaKichiwa kumbukumbu zangu katika programu yetu ya vilevituo vya afya vya kwanza 172, katika vituo vile kuna fedhaambazo tulipata kutoka Canada, fedha zile zimeshaendeleakatika maeneo mbalimbali na baadhi ya vituo sasa hiviwameshafika level ya renta, lakini kuna zile fedha kutokaWorld Bank ni kwamba upelekaji wake wa fedha utakamilikandani ya wiki hii.

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikuhakikishieMheshimiwa Mbunge ni kwamba wananchi wako watarajiekwamba jinsi gani waweze kushiriki kazi lakini fedha ziletutatumia force account. Niwasihi hasa viongozi wetu hukokatika Mamlaka ya Serikali za Mitaa, zile fedha zinapokujalazima wazisimamie vizuri tupate value or money nawananchi waweze kupata huduma. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ungando.

MHE. ALLY S. UNGANDO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante.

Halmashauri ya Kibiti ni Halmashauri moja ambayoimetoka Wilaya ya Kibiti na kituo chake kikubwa cha afyaKibiti lakini hivi sasa kimezidiwa kutoa huduma.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha Hospitaliya Wilaya ya Kibiti? (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli hojaanayoizungumza Mheshimiwa Ungando ni hoja ya kweli nakwa sababu nilikuwa naye katika vile visiwa 40 vya Deltakwa kutwa nzima na changamoto ya afya kule ni kubwasana, ndiyo maana katika kipindi cha sasa tumepeleka fedhakatika kituo cha afya kimoja ambacho mimi na MheshimiwaMbunge tulizunguka mpaka usiku pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala zima la progamu yauanzishaji wa Hospitali ya Wilaya ya Kibiti, naomba nikusihiMheshimiwa Mbunge kwamba tutashirikiana kwa pamojakwa sababu lengo letu kubwa zile Wilaya zote zilizokosahospitali sasa tuweze kuwa na progamu maalum kwa ajiliya kujenga hospitali. Kwa hiyo, Mheshimiwa Ungandonaomba nikupe faraja kwamba tutashirikiana kwa pamojatuangalie way forward tunafanyaje tupate Hospitali ya Wilayaya Kibiti kwa sababu population ya watu pale ni kubwa hasaukiangalia barabara ya Kilwa lazima tuhakikishe kwambatunafanya jambo hilo kwa haraka. (Makofi)

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

MWENYEKITI:Ahsante, Mheshimiwa Almas.

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kuniruhusu niulize swali la nyongeza.

Kwa vile matatizo haya ya afya katika Wilaya yaKakonko yanafanana sana na ukosefu wa Hospitali ya Wilayaya Uyui na Wilaya ya Uyui tumejitahidi kupitia Halmashaurikujenga hospitali lakini tumeishia kwenye OPD na tungeombaSerikali ituambie; je, inaweza kutuongezea hela ili tuwezekumalizia OPD yetu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli palehawana Hospitali ya Wilaya na wameanza programu yaujenzi wa OPD, lakini sasa hivi tunafanya needs assessmentkatika maeneo yote ambayo majengo yalianza badohayajakamilika. Ndiyo maana katika harakati zetu sasa hivitunakamilisha Kilolo, Mvomero lakini tunaenda kule Sihaninaamini kwamba Uyui. Naomba nikuhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba katika mchakato tunaofanya hivi sasa nawataalam wangu pale ofisini tutaangalia nini tufanye, lengokubwa tuikamilishe hospitali yetu ya Uyui na waleWanyamwezi wa Tabora pale waweze kupata hudumakama Wanyamwezi wengine hapa Tanzania. (Makofi)

Na. 40

Mpango wa Elimu Bure

MHE. JOSEPH R. SELASINI (K.n.y MHE. YOSEPHER F.KOMBA) aliuliza:-

Ni dhamira ya Serikali kutekeleza mpango wa elimubure kuanzia chekechea hadi kidato cha nne, lakini mpangohuu una changamoto ambazo zisipotatuliwa zitasababishakushuka kwa ubora wa elimu.

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

(a) Je, ni nini tamko la Serikali juu ya wanafunziwanaoanza kidato cha kwanza kwa kigezo cha kutofaulukwa kiwango cha kianzia alama 100 na kuendelea?

(b) Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha ujenziwa maabara unakamilika kwa wakati?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Yosepher Ferdinand Komba, Mbunge wa VitiMaalum lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, tamko la Serikali ni kwambamwanafunzi anahesabiwa kufaulu mtihani wa Taifa wadarasa la saba endapo atapata alama kuanzia 100 hadi250 katika masomo yote aliyoyafanya. Hata hivyo, wanafunziwalio na alama chini ya 100 huhesabika kuwa ni miongonimwa waliokosa sifa za kujiunga na kidato cha kwanza katikashule za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, wanafunziwalioshindwa kufikia alama 100 na kuendelea, hushauriwakujiunga na mfumo usio rasmi wa Elimu Masafa (OpenDistance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu ya WatuWazima, vyuo vya ufundi au shule za sekondari za binafsi.Wanafunzi wanaojiunga na mfumo huo wa elimu hawamokatika utaratibu wa utekelezaji wa mpango wa elimu msingibila malipo, lakini wanafunzi wanaosoma katika utaratibuhuo watakaofaulu mtihani wa Taifa wa kidato cha nnehuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule zaSerikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la (b); ujenzi wamaabara katika Halmashauri zote unaendelea ili kuboreshamazingira ya kujifunzia na kufundishia masomo ya sayansi.Kati ya maabara 10,387 zinazohitajika nchini, ujenzi wamaabara 6,287 sawa na asilimia 60.5 ya mahitaji umekamilika.

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

Nazikumbusha Halmashauri zote kukamilisha mapema ujenziunaoendelea kwa kushirikisha wadau na nguvu za wananchi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Selasini.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Sera ya Elimu Bure imewasaidia baadhi ya wazaziwasio na uwezo kuandikisha watoto shuleni, lakini wakatihuo huo bado kuna michango kadhaa inayoendelea kwabaadhi ya shule na michango hii imerudisha nyuma moraliya wazazi kuchangia kwa juhudi katika maendeleombalimbali ya shule.

Je, Serikali ipo tayari sasa kutoa elimu kwa wananchikwamba sera ni elimu bila ada na siyo elimu bure ilikuwafanya wananchi waweze kuchangia kwa nguvu kamailivyokuwa zamani? (Makofi)

Swali la pili, shule za Sekondari za Keni, Shimbi naBustani katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ni shuleambazo zimejengwa kwa mtindo wa ghorofa kwa sababuya uhaba wa ardhi katika Wilaya ya Rombo na sasa zinamuda karibu wa zaidi ya miaka 10 wananchi wameshindwakuzikamilisha.

Je, Serikali ipo tayari katika bajeti ijayo katika bajetiijayo kuzipokea hizi shule na kuzikamilisha ili kuweza kuungamkono nguvu za wananchi katika jitihada zao za kufanyamaendeleo mengine kama kumalizia maabara?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.Jiandae Mheshimiwa Waitara na Mheshimiwa Upendo.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS – TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): MheshimiwaMwenyekiti, nakubalina na Mheshimiwa Selasini kwambakuna michango ambayo inaruhusiwa. Lakini michango ileina utaratibu kwamba ili kusudi mchango uweze kukubalikakisheria ni lazima Kamati ya Shule au bodi ya shule iweimeujadili na kupeleka kwa wadau ambao ni wazazi,

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

wakipitisha wanaomba kibali kwa Mkuu wa Mkoa, wakipatakibali basi hapo wanaweza wakaendelea nakuchangishana. Huo ni utaratibu ambao ni mzuri, namshauriMheshimiwa Mbunge autumie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa swali lakela pili, sisi Ofisi ya Rais, TAMISEMI pamoja na Wizara ya Elimutupo tayari kukaa na Mheshimiwa Mbunge ili tuweze kujadilinamna ambavyo tunaweza tukaboresha utaratibu wakuzikamilisha hizi shule ambazo anazizungumzia. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Upendo, halafuMheshimiwa Waitara.

MHE. UPENDO F. PENEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kuniona.

Katika suala la elimu bure, moja ya changamoto nipamoja na utoro unaowakabili hasa watoto wa kike. Sasaningependa kujua Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba Serikalisasa ina mpango gani kuhakikisha ya kwamba watoto wakike wanaoingia shuleni wanabaki shuleni kwa kumaliza, kwaSerikali kuweka pesa za ruzuku kwa ajili ya sanitary pads (vifaavya hedhi) kuziongeza katika capitation fund ili kuwezakupunguza suala la utoro mashuleni. Sasa Serikali ina mkakatigani katika bajeti ijayo kuongeza pesa hizo ili watoto wetuwaweze kupata pedi hizo bure mashuleni? Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, katikamakubaliano ya Jumuiya ya East Africa nadhani ni miongonimwa jambo ambalo lilikuwa likijadiliwa sana hasa tatizokubwa la watoto wasichana wanapokosa hivi vifaa kwaajili ya kujikimu wakiwa shuleni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tulichukue hili kwasababu ni jambo la msingi basi tukifika kwenye mchakatowa bajeti sisi sote tushirikiane kwa pamoja tuangalie nini

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

tufanye ili mradi kuhakikisha kwamba tuweze kusaidia vijanawetu watulie masomoni na wapate elimu vizuri. Kwa hiyo,tunalichukua kama mchango mzuri katika mchakatotutakuja tutaijadili. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Waitara, ajiandaeMheshimiwa Dkt. Mponda.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru, naomba niulize swali dogo la nyongeza.

Hivi karibuni Naibu Waziri wa Elimu ametoa kauliakisema watoto wakitaka kuolewa wawe na cheti chakumaliza form four, wakati huo huo Serikali ilisema walewanafunzi ambao wanapata ujauzito wakiwa shuleniwasiendelee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ningependa nipatekauli ya Serikali katika mkanganyiko huu, nini hasa ni kauli yaSerikali sahihi. Vipi wanafunzi ambao wanapata mimbawakiwa shuleni na hawaendelei kwa mfumo wa shule, lakinina kauli ya Waziri ya kusema anayetaka kuolewa awe nacheti cha form four? Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS – TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) -MHE. JOSEPH G. KAKUNDA:Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa majibu sahihi kwaMheshimiwa Waitara pamoja na Watanzania wotewaliopata mkanganyiko kuhusu kauli hiyo ni kwamba,nil isema Sera Mpya ya Elimu ya mwaka 2014 hukotunakoelekea inabadilisha mfumo wa sasa wa elimu kwendakwenye mfumo mpya ambao utahitaji mtoto aanzechekechea mwaka mmoja, asome shule ya msingi miakasita, shule ya sekondari miaka minne na hii itakuwa ni lazimakwa yeyote atakayeanza darasa la kwanza hadi amalize formfour. Kwa hiyo, nikasema kwamba tutakapofika wakati huo,kithibitisho muhimu kwamba huyu mtoto sasa amemalizaform four ni school leaving certificate, wakati huo siyo leo.

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ndugu yanguMheshimiwa Waitara huo ni ufafanuzi sahihi kabisa wa serampya. Sasa hivi tunaandaa utaratibu na maandalizi ikiwepopamoja na miundombinu ili tuweze hatimae kuitekeleza hiyosera muda utakapofika. Kwa hiyo, usiwe na mkanganyikondugu yangu Waitara. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Dkt. Mponda.

MHE. DKT. HADJI H. MPONDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja lanyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jibu la msingi Waziriamezungumzia kwamba baadhi ya Halmashauri tayariwameshamaliza ujenzi wa maabara katika shule za sekondarina mojawapo ya Halmashauri hii ni Halmashauri ya Malinyitumeshamaliza karibu asilimia 90 ya maabara ya masomoya sayansi katika shule za sekondari na baadhi ya majengohaya sasa hivi yanaanza kuharibiwa na wadudu wau ndegeaina ya popo.

Je, ni lini Serikali watakamilisha utaratibu wa kupelekavifaa ili maabara hizo zianze kutumika rasmi.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukurukwamba tuliweza kununua vifaa kwa ajili ya maabara zaidiya 1,000, tumeweza kuvisambaza. Ninafahamu MheshimiwaDkt. Mponda hata tulivyofika kule kwako Malinyi tuliona kweliulitoa concern hiyo.

Kwa hiyo, tutafanya kila liwezekanalo kuona jinsi yaupelekaji wa vifaa. Hata hivyo, katika ile shule ambayoulisema ina changamoto kubwa, kabla ya mwezi wa pilinadhani tutafanya kazi kubwa kuhakikisha kwamba shuleile tunaiboresha, wananchi wa Malinyi ambao wanachangamoto kubwa sana waweze kupata elimu vizuri.(Makofi)

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana swali la Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora,Mheshimiwa Chikota.

Na. 41

Hitaji la Maafisa Ugani

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:-

Ili kuleta mapinduzi ya kweli ya kilimo, ujuzi na maarifaya wataalam wa kilimo unatakiwa uwafikie wakulima marakwa mara.

Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa kibali cha kuajiriMaafisa Ugani wa kutosha na kuwapeleka kwenye Mamlakaza Serikali za Mitaa?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ni mara yanguya kwanza kusimama hapa baada ya uteuzi, naombanichukue nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. JohnPombe Magufuli kwa imani kubwa aliyoonesha juu yangu,wananchi wa Wilaya ya Newala na kwa hakika wananchiwote wa Mkoa wa Mtwara, wamepokea uteuzi wake kwashangwe kubwa. Na mimi nataka nichukue nafasi hiikumuahidi Rais nitatekeleza majukumu yangu ya kumsaidiabila upendeleo wala woga na siku zote nitamuombaMwenyezi Mungu anisaidie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nijibu swali laMheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, Mbunge wa Nanyamba,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuleta mapinduzi ya kweliya kilimo, ujuzi na maarifa ya watalaam wa kilimo unatakiwauwafikie wakulima mara kwa mara. Serikali imekuwa ikitoavibali vya ajira za Maafisa Ugani katika Mamlaka za Serikali

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

za Mitaa kila mwaka wa fedha kutegemea uwezo wake wabajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zilizopo zinaoneshakuwa kati ya mwaka 2013/2014 hadi 2016/2017 jumla yaMaafisa Ugani 5,710 waliajiriwa katika Mamlaka za Serikaliza Mitaa.

Mheshimwa Mwenyekiti, naomba kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikaliimetoa kibali cha kuajiri Maafisa Ugani 1,487. Aidha, Serikaliitaendelea kutoa nafasi za ajira kwa Maafisa Ugani kadri yamahitaji na uwezo wa bajeti.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chikota.

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu mazuriya Mheshimiwa Waziri, naomba sasa niulize maswali mawiliya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa upungufu huo waMaafisa Ugani ni mkubwa sana kwenye Halmashauri ambazozimeanzishwa hivi karibuni, kama Halmashauri ya Mji waNanyamba; je, Serikali ina mpango gani wa upendeleo kwamamlaka hizi mpya za Serikali za Mitaa ambazozimeanzishwa hivi karibuni?

Swali langu la pili, ukiangalia takwimu za ajirazilizotolewa hivi karibuni kwa Maafisa Ugani, na kwa kuwanchi yetu ina takribani vijiji zaidi ya 12,000 utaona kwambakuna vijiji vingi sana vinakosa Maafisa Ugani.

Je, Serikali ina mpango gani au mkakati gani waharaka wa kuhakikisha kwamba kila kijiji katika nchi yetukinakuwa na Afisa Ugani ili kuleta mapinduzi ya kweli katikakilimo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: MheshimiwaMwenyekiti, Wizara ya Utumishi inatambua kwambaMamlaka mpya za Serikali za Mitaa zilizoanzishwa zinahitajiupendeleo mpya, hasa katika kupanga watumishi. Natakanimuahidi kwamba siyo Nanyamba tu, Nanyamba niMamlaka mpya ya Serikali za Serikali za Mitaa, Halmashauriya Mji wa Newala ni mpya, Halmashauri ya Mji wa Tarime nimpya, Halmashauri ya Mafinga ni mpya, maeneo yale yoteambayo tumeanzisha Halmashauri mpya najua wakati wakugawana watumishi zile mamlaka mpya hazikupatawatumishi wengi. Kwa hiyo, nitakachofanya ni kuhakikishazile mamlaka mpya zote zinapata watumishi wa kutosha ilizilingane, kama ni upungufu ulingane na zile mamlakazilizokuwepo kabla.

Swali lake la pili, ni kweli kwamba vijiji vingi havinahawa Maafisa Ugani, hili limetokea kwa sababu muda mrefukatika nchi yetu, vile vyuo vinavyofundisha vyeti vya kilimovilikuwa vimesimama, lakini baadae vimefufuliwa, sasa hivikazi kubwa inaendelea. Nataka nimhakikishie kwambatutaanzisha programu maalum kwa kushirikiana na Wizaraya Kilimo kuhakikisha kwamba vyuo vile wanachukuawanafunzi wengi zaidi ili wanapomaliza waweze kuajiriwana Serikali katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Qambaloajiandae Mheshimiwa Ritta.

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na umuhimuwa watumishi katika kada hii ya Maafisa Ugani kama kwelitunataka kuleta mapinduzi ya kilimo kwenye nchi yetu. Jamboambalo tunaliona sasa hivi ni kwamba kutokana nakutokuajiriwa kwa Watendaji wa Vijiji na Watendaji wa Katawa kutosha, baadhi ya watumishi katika kada hii ya kilimosasa ndiyo wamekaimishwa zile ofisi za Kata kwa maana yakuwa Watendaji wa Vijiji na Watendaji wa Kata.

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

Je, ni lini Serikali itaajiri watumishi katika kada hiyo yautendaji ili watumishi hawa muhimu wa eneo la kilimowarudi kufanya kazi ya kilimo na wananchi? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli pale mahali ambapo Maafisa Watendajiwa Kata hawapo, Maafisa Ugani wamekaimishwa nafasihizo, hii imetokana na upungufu wa kutotosheleza Watendajiwa Kata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilieleze Bunge lako Tukufu,kazi moja wapo ya Afisa Mtendaji wa Kata ni kusukumamaendeleo ndani ya kata, watu waliofanya vizuri sana katikashughuli hii ni Walimu, Maafisa Kilimo, Mabibi Maendeleo,kwa hiyo pale ambapo Afisa Kilimo anakaimishwa Kata siyomakosa, ni nafasi nzuri ya kumuangalia keshokutwa huendaakawekwa moja kwa moja. Jambo la msingi hapa nikwamba Wizara yangu inakubali kwamba kuna haja yakulifanyia kazi suala hili kuhakikisha kwamba Kata zetu zotena vijiji vyetu vinakuwa na Maafisa Watendaji wa kudumu.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Ritta, ajiandaeMheshimiwa Ghasia.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niulize swali dogo tula nyongeza.

Kwa kuwa uhaba wa Maafisa Ugani uko sawasawakabisa na uhaba wa wataalam wa mifugo. Je, Serikali inampango gani wa kuajiri Maafisa Mifugo wa kutosha iliwananchi wasaidiwe haki katika Halmashauri zetu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.Ajiandae Mheshimiwa Ghasia, atafuatiwa na Innocent.

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: MheshimiwaMwenyekiti, Serikali itashughulikia tatizo la uhaba wa MaafisaUgani sambamba na tatizo la Maafisa wa Mifugo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ghasia, ajiandaeMheshimiwa Innocent, atafuatiwa na Mheshimiwa Zacharia.

MHE. HAWA A. GHASIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Nami napenda kuuliza swali la nyongeza kwa kakayangu, Mheshimiwa Kapteni Mkuchika kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo la watumishi katikasekta ya kilimo ni sawasawa sana au zaidi ya katika sekta yaafya. Sasa hivi maeneo mengi, hasa vijijini, kuna upungufumkubwa sana wa watumishi katika sekta ya afya.

Je, ni lini Serikali itaona umuhimu wa kuajiri watumishiwa sekta ya afya ili kunusuru maisha ya Watanzania, hasaakina mama na watoto? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi,anataka kujua ni lini tu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli kwamba maeneo muhimu ambayowananchi wanategemea kupata huduma ni upande waafya, maji, hayo ni mambo yanayogusa maisha ya kila sikupamoja na elimu na barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka yote Serikali inapoajiriimekuwa ikiweka umuhimu mkubwa sana upande wawatumishi wa afya, kwa sababu Waziri wa Utumishi anaajirihawa Maafisa Afya baada ya kuwa tayari wameshafunzwana kuhitimimu, nataka niliahidi Bunge lako Tukufu kwambanitazungumza na Waziri mwenzangu wa Elimu na Wizara yaAfya wapate mafunzo watumishi wengi zaidi katika fani yaafya ili wakazibe mapengo haya yaliyopo katika Mamlakaya Serikali za Mitaa.

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

MWENYEKITI: Mheshimiwa Innocent, ajiandaeMheshimiwa Zacharia.

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swalila nyongeza.

Pamoja na kwamba wananchi wana haki ya kupatahuduma ya watumishi, hasa walimu, wauguzi na watendajiwa vijiji na kata, pia jitihada nzuri ya Serikali inayoifanya yakupeleka fedha za maendeleo vijijini inahitaji watumishihawa waweze kusimamia miradi hii. Kwa upande waKaragwe kuna shortage kubwa ya Walimu wasiopungua 850,kuna shortage kubwa ya wauguzi.

Je, nini tamko la Serikali, maana kila mwaka wa fedhaSerikali inasema itapanga bajeti ya kutosha kwa ajili yakuhakikisha tunakuwa na watumishi wa kutosha. Nini tamkola Serikali kuhusu hii shortage ya watumishi ya sasa hususanWilaya ya Karagwe? Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi,wote wanataka kujua ni lini tu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: MheshimiwaMwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa walimu namatabibu na wataalam wa idara ya afya na imekuwaikichukua hatua kuona kwamba tunaziba mapengo haya.Kama mtakumbuka Waheshimiwa Wabunge, wakatitunaanza sekondari zetu za kata uhaba wa walimu ulikuwamkubwa sana, lakini Serikali kwa kutambua umuhimu wakuwepo walimu wa kutosha imefanya jitihada ya kuajiriwalimu wengi na hivi sasa katika shule zetu za sekondari,hali ya walimu imekuwa nafuu ukiondoa labda mapungufumakubwa yaliyopo katika upande wa walimu wa masomoya sayansi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni kazi ya kudumuninamuahidi tu kwamba Serikali itaendelea na kasi ileile ya

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

kuajiri watumishi wa afya na elimu ili wananchi wetu wapatehuduma ya afya bora, ili watoto wetu wapate elimuinayojitosheleza. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, tunaendelea na MheshimiwaZacharia Issaay.

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Nimpongeze Waziri kwa kuteuliwa kwakepamoja na Mawaziri wengine wote.

Katika mwaka wa fedha wa 2016/2017, Serikali ilikuwana nia njema ya kuajiri watumishi 52,000; je, Serikali sasaitatekeleza mpango ule wakati gani ili vijana wetu waliopomitaani waweze kupata nafasi ya ajira?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli kwamba baada ya mchujo wawatumishi hewa, Mheshimiwa Rais ametoa idhini, Serikaliimeidhinisha waajiriwe watumishi wapya 15,000, hilo zoezilinafanyika. Pia katika mwaka huu wa fedha kuna kibali chakuajiri watumishi 52,000, zoezi hilo litaendelea, natakanihakikishe kwamba nafasi na fedha za kuwalipa zipo, kazihiyo itatekelezwa. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante.

Na. 42

Kushindwa kwa Mpango wa MKURABITA

MHE. GEORGE M. LUBELEJE aliuliza:-

Mpango wa MKURABITA ni muhimu katika kuwaleteawananchi maendeleo lakini unakabiliwa na tatizo kubwa laukosefu wa fedha na hivyo kushindwa kuendesha shughuliza urasimishaji kwa ufanisi.

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha mfuko waurasimishaji utakaokuwa maalum katika Serikali za Mitaa ilikutatua tatizo la ukosefu wa fedha za kuendeleza shughuliza urasimishaji?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali landugu yangu, mdogo wangu, somo yangu, MheshimiwaGeorge Malima Lubeleje, Mbunge wa Mpwapwa, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa MKURABITA nimuhimu katika kuwaletea wananchi maendeleo, lakinimpango huu unakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wafedha na hivyo kushindwa kuendesha shughuli za urasimishajikwa ufanisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango wa KurasimishaRasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ulianzishwa naSerikali kwa lengo la kuwapa nguvu ya kiuchumi wananchikwa kuwawezesha kumiliki ardhi na kuendesha biasharakatika mfumo rasmi na wa kisasa unaoendeshwa kwa mujibuwa sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua uwepowa tatizo la upungufu wa rasilimali fedha kwa ajili yakutekeleza shughuli za urasimishaji na ndiyo maana Serikaliimedhamiria kuanzisha Mfuko Maalum wa Urasimishajiutakaowezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekelezamajukumu yake ya urasimishaji bila vikwazo. Mfumoutakaotumika ni kwa Serikali kupitia MKURABITA kuweka fedhaza dhamana katika taasisi za fedha zil izokubalika il ikuwezesha Halmashauri kukopa na hivyo kuendesha shughulizake za urasimishaji. Kwa kutumia mfumo huu urasimishajiutakuwa nafuu, haraka na endelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, MKURABITA kwa kushirikianana Benki ya NMB imekamilisha utaratibu wa utekelezaji wa

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

miradi ya majaribio katika Manispaa ya Iringa na Halmashauriza Wilaya za Mbozi na Momba Mkoani Songwe. Baada yamajaribio haya ambayo yamepangwa kufanyika kwa miakamiwili, utekelezaji utaanza nchi nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imetenga kiasi chashilingi milioni 243, fedha ambayo itatumika kama dhamanakwa ajili ya mikopo ambayo itakopwa na Halmashauriambazo zitatekeleza miradi ya maendeleo. Aidha,urejeshwaji wa mikopo hii utatokana na michango yawananchi wenyewe.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lubeleje.

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, nina maswalimawili.

Swali la kwanza, kwa kuwa MKURABITA katika Wilayaya Mpwapwa walichagua vijiji viwili; Kijiji cha Inzomvu naKijiji cha Pwaga, lakini kwa upande wa Kijiji cha Pwagamambo ni mazuri, mradi ulitekelezwa, masijala ilijengwa nawananchi walipewa Hati za Kimila. Lakini katika Kijiji chaInzomvu hakuna kil ichofanyika, baada ya kupimamashamba wananchi walipewa mafaili tu wakaenda nayomajumbani, hakuna chochote na ofisi ya masijala haipo.

Swali la pili, Mheshimiwa Waziri utakubaliana na mimikwamba ipo haja sasa ya Serikali kuleta muswada hapa ilitubadilishe chombo hiki MKURABITA ambao unategemea zaidifedha za mfadhili na fedha za Serikali ni kidogo sana ilitubadilishe uwe mfuko wa urasimishaji ili wadau wengiwaweze kuchangia na chombo hiki kiwe na fedha za kutoshaili wananchi wengi waweze kunufaika?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

Mwenyekiti, nimefurahi kusikia kwamba Mpwapwa iliingiakatika majaribio, walipata vijiji viwili, kijiji kimoja kinafanyavizuri kingine hakijafanya vizuri. Nimuombe tu ndugu yangu,Mheshimiwa George Malima Lubeleje apange mudaanaoona yeye inafaa ili mimi na yeye twende katika kijiji hichoambacho kimesahauliwa na mimi nikajifunze nikajuekimetokea nini, nichukue hatua ili vijiji hivyo pacha viwezekufanana katika utekelezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja kwamba kuletwemuswada utakaobadilisha chombo hiki, Serikali inapokea raihii, lakini nataka nieleze kwamba kama nilivyosema tangumwanzo tunakusudia kuanzisha Mfuko Maalum waUrasimishaji, wakati wa kuanzisha mfuko maalum waurasimishaji ikionekana haja iko ya kubadili sheria, suala hilolitazingatiwa na taratibu za kubadilisha sheria zinafuata ngazikwa ngazi, itatekelezwa kadri Serikali itakapoona inafaa.

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa tunaendelea naWizara ya Maji na Umwagiliaji Mheshimiwa Kiza HusseinMayeye.

Na. 43

Upatikanaji wa Maji ya Kudumu- Mkoa wa Kigoma.

MHE. KIZA H. MAYEYE aliuliza:-

Mkoa wa Kigoma umebarikiwa kuwa na ZiwaTanganyika, Mto Malagarasi na vyanzo vingine vya maji lakiniMkoa huu unakabiliwa na changamoto kubwa ya maji.

Je, Serikali inawaambia nini wananchi wa Kigomahususan katika Jimbo la Kigoma Kaskazini katika kuhakikishawanapata maji ya kudumu ya kwenye mabomba?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Maji na Umwagiliaji, naomba kujibu swali la

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

Mheshimiwa Kiza Hussein Mayeye, Mbunge wa Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Programu yaMaendeleo ya Sekta ya Maji inaendelea kutekeleza miradiwa maji vijijini katika Halmashauri ya Wilaya Kigoma iliyopoKaskazini mwa Mkoa wa Kigoma. Hadi kufikia mweziSeptemba, 2017 jumla ya miradi mitatu ya maji yaNyarubanda, Kagongo na Nkungwe imekamilika nawananchi wanapata huduma ya maji. Mradi mmoja waKalinzi upo katika hatua za mwisho na utekelezaji wakeumefika asilimia 90. Katika mwaka wa fedha 2017/2018Halmashauri hiyo imetengewa shilingi milioni 649.8 kwa ajiliya utekelezaji wa mradi ya maji vijijini.

Vilevile Serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Ubeligijiimeanza utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji vyaHalmashauri za Mkoa wa Kigoma utakaogharimu shilingibilioni 20.6 na itatekelezwa katika kipindi cha miaka minnekuanzia mwaka 2017 hadi 2021. Mradi huo utanufaisha wakazi207,785 katika vijiji 26 vya kipaumbele katika Halmashauri zaMkoa huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa mijini,Serikali inatekeleza mradi wa maji Mjini Kigoma kwa gharamaya Euro milioni 16.32. Mradi huo unahusisha ujenzi wa chanzocha maji ukingoni mwa Ziwa Tanganyika eneo la AmaniBeach chenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 42 kwasiku, ikilinganishwa na lita milioni 12 zinazozalishwa sasa. Kazinyingine zitakazofanyika ni pamoja na ujenzi wa matankimatano yenye ujazo wa lita milioni mbili kila moja na tankimoja lenye ujazo wa lita 500,000; ulazaji wa bomba kuu lenyeurefu wa kilometa 22 na mabomba ya kusambaza maji urefuwa kilometa 132, ujenzi wa vioski 70 vya kuchotea maji katikamaeneo mbalimbali.

Aidha, katika kuboresha huduma ya usafi wamazingira, mabwawa ya kutibu majitaka yenye uwezo wakutibu mita za ujazo 150 kwa siku yatajengwa pamoja naununuzi wa gari la kunyonya na kusafirisha majitaka.

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi kufikia mwezi Oktoba2017, kwa ujumla utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia76 na unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba 2017.Kukamilika kwa mradi huo kutaongeza upatikanaji wamajisafi na salama kutoka asilimia 69 za sasa hadi kufikiaasilimia 100.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kiza.

MHE. KIZA H. MAYEYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Naomba kumuuliza Mheshimiwa Waziri maswali yanyongeza kama ifuatavyo:-

(a) Je, ni lini sasa Serikali mtatimiza ahadi yenu nakutekeleza mradi huu wa Maji katika Mji ya Manispaa yaKigoma Mjini kufika katika Mji Mdogo wa Mwandiga?

(b) Serikali haioni sasa ni muda muafaka maji hayaya Ziwa Tanganyika kwenda katika Wilaya ya Kasulu?Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi nahongereni Wabunge Viti Maalum wapya, mnauliza maswalimazuri. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda nimshukuru sanaMheshimiwa Mbunge kwa maswali yake mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upatikanaji wa maji kwa Mjiwa Mwandiga unategemeana kabisa na utekelezaji wamradi huu mkubwa ambao utakamilika mwezi huu Disemba.Mradi huu utazalisha lita milioni 42 na mahitaji ya Mji waKigoma ni lita milioni 20. Kwa hiyo, kutakuwa na maji yakiasi kikubwa ambayo tutaweza kuyapeleka katika Mji waMwandiga. Kikubwa nataka niwahakikishie wananchi waMwandiga subira yavuta kheri na kheri itapatikana katikaupatikanaji wa maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali la pili kuhusu

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

suala la upatikanaji wa maji katika Mji wa Kasulu natakanimhakikishie ndugu yangu Mheshimiwa Mbunge wali wakushiba unaonekana kwenye sahani. Serikali imefanya kazikubwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu mkubwa wamaji, sasa hivi Mji wa Kasulu upo miongoni mwa miji 17ambayo kupitia fedha za India utapata maji. Kikubwatumsubiri Mhandisi Mshauri atatushauri vipi ili tupate maji ilikuhakikisha kwamba wananchi wa Kasulu wanapata majikwa wakati. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Munde,Mheshimiwa Nape halafu Mheshimiwa Mbatia.

MHE. MUNDE A. TAMBWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa fursa hii na mimi niweze kuuliza swalidogo la nyongeza.

Kwa kuwa swali la msingi linafanana kabisa namatatizo yaliyopo katika Wilaya ya Urambo na Kaliua naSerikali imekuwa ikituambia kwamba imekamilishamchakato wote wa kutoa maji Mto Malagarasi kupelekaKaliua na Urambo, fedha tu ndiyo bado hazijapatikana tokamwaka jana walituambia fedha hizo zitapatikana.

Je, status ya kupata pesa kupeleka maji katika Wilayaya Urambo na Kaliua ikoje mpaka sasa kwa sababu hali nimbaya sana kwa wananchi hao? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli tunao mradi wa usanifu unakamilika wakutoa maji Malagarasi kupitia Kaliua kuja Urambo hadiTabora, pia Mheshimiwa Rais ametuagiza kwamba huumradi unaotoa maji Solwa kutoka Ziwa Victoria kupelekaTabora wakati unaendelea tayari tumeshaagiza Mamlakayetu ya Maji ya Tabora iangalie uwezekano wa kuwekamabomba mengine kutoka matanki ya Tabora kupelekaUrambo na ikiwezekana yafike mpaka Kaliua.

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuhakikishie MheshimiwaMunde kwamba Serikali inafanya kazi kuhakikisha Kaliua naUrambo wanapata maji safi na salama. (Makofi).

MWENYEKITI: Mheshimiwa, Nape Nnauye, ajiandaeMheshimiwa Mbatia na ajiandae Mheshimiwa Kuchauka.

MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya upatikanaji wa majikatika Mikoa ya Lindi na Mtwara bado ni mbaya sana naaliyekuwa Naibu Waziri wa Maji ambaye sasa ni Waziri waMaji alipotembelea Mikoa ya Lindi na Mtwara alikaguabaadhi ya miradi ambayo inaendelea katika Jimbo laMtama, Mradi wa Maji wa Nyangamara na pengine hakufikalakini Mradi wa Maji wa Namangale na alituhaidi kwambacertificates za miradi hiyo zikifika Wizarani mara moja pesazitalipwa, mpaka sasa huu ni mwezi wa pili au wa tatucertificates hizo zimefika Wizarani na hazijalipwa.

Je, ni lini Serikali italipa pesa hizi za hawa wakandarasiili miradi hii ipate kukamilika wananchi wangu wapate maji?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, Waziri wa Fedha na Mipango jana ametupatiashilingi bilioni 12. Kwa hiyo, nikuhakikishie kwamba hizocertificates kama zimeshaletwa wiki ijao tutahakikishatumezilipa ili mkandarasi aendelee kutekeleza ilani ya Chamacha Mapinduzi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa James Mbatia, ajiandaeMheshimiwa Kuchauka na Mheshimiwa Shekilindi ajiandae.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya maji nchini kwa

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

ujumla siyo nzuri na lengo Namba 6 la ajenda ya 2020/2030ni maji, upatikanaji wa maji safi, salama kwa wote dunianina Tanzania ni mwanachama. Katika Jimbo la Vunjo sehemuza kata….

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbatia muda wetu nimdogo tuende moja kwa moja kwenye shida ya Jimbo lako.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,sawa. Katika Kata ya Mwamba Kusini na Mwika Kusini haliya maji ni mbaya sana na wananchi wananunua maji ndoomoja kwa shilingi 500.

Je, Serikali inachukuliaje jambo hili kwa dharura iliupatikanaji wa maji uweze kupatikana kwa haraka?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, hali ya upatikanaji wa maji nchi ni nzuri kupitiaprogramu ya maendeleo ya sekta ya maji awamu ya kwanza.Tulilenga kutekeleza miradi 1,810, tayari tumeshatekelezamiradi 1,433, tumejenga vituo vya kuchotea maji 117,000 navituo vyote vingetoa maji vijijini sasa hivi tungekuwa naasilimia 79 ya upatikanaji wa maji safi na salama. Kutokanana mabadiliko kidogo ya tabianchi vyanzo vingi vya majikukauka sasa hivi hiyo asilimia kidogo imeshuka, lakini tayaritumejipanga kuhakikisha maeneo yote ambayo hayatoi majitumetenga fedha kwenye bajeti ya mwaka huu tulionao ilihayo maeneo yaweze kupatiwa vyanzo vingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la VunjoMheshimiwa Mbunge naomba tukutane, tujadili ili tuone ninamna gani tutatoa kitu cha dharura kuhakikisha walewananchi wanapata maji.

MWENYEKITI: Ahsante ameshakuelewa. MheshimiwaKuchauka, ajiandae Mheshimiwa Shekilindi na MheshimiwaChumi.

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Kutokamilika kwa miradi ya maji katika Halmashaurizetu kumekuwa ni tatizo sugu, niliwahi kumuuliza MheshimiwaNaibu Waziri wakati huo ambaye sasa ndiyo Waziri alisemapesa Wizarani zipo ila watu wapeleke certificate. Ninasikitikakumwambia kwamba hapa ninayo makabrashi ambayo nicopy ya hizo certificate ambazo zimeshafika kwenye Wizarayake sasa ni zaidi ya mwaka mzima hizo pesa hazijawahikutolewa, na kuna miradi kadhaa katika vijiji vya Kipule,Ngongowele pamoja na Mikunya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kauli ya Serikali nilini miradi hii itakamilika ili wananchi wa vijiji hivi wawezekupata maji. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, kwa sababu certificate, ni masula ya kiutendajiMheshimiwa Mbunge, ninaomba baada ya Bunge hili leotukutane, twende kwa watendaji tukaangalie certificatekama zipo, kama nilivyosema kwamba tayari nina fedha iliwiki ijayo tuweze kulipa.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Shekil indi,ajiandae Mheshimiwa Chumi.

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa niweze kuuliza swali dogola nyongeza Wilaya ya Lushoto ina vyanzo vingi sana vyamaji lakini wananchi wa Lushoto hawana maji safi na salama.

Je, Serikali ina mpango gani wa kumtua mama ndookichwani hasa akina mama wa Makanya, Kilole, Kwekanga,Kwemakame, Ngulwi, Ubiri, Handeni na Miegeo? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu. Mheshimiwanajua Naibu wako ni midadi ungemwachia achia naye

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

kidogo, maana majibu anayo mazuri. Mheshimiwa Waziribasi endelea.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, nilitembelea Lushoto nikakuta hilo tatizo nanikamuelekeza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Tanga awezekutekeleza miradi ya maji katika Halmashauri yake, hadi jananimepiga simu tayari wamekamilisha taratibu za manunuzi,Baada ya siku 14 mikataba itasainiwa, utekelezaji uanze.

Mheshimiwa Mbunge nikuhakikishie kwambamaeneo yote ya Halmashauri yako yatapata maji.

MWENYEKITI: Waheshimiwa muda wetu ni mdogonajua kuna kero kubwa ya maji, muda tuliobakiwa nao ninusu saa tu. Mheshimiwa Chumi.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi na kuniona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mji wa Mafinga ni kati ya mijiinayokuwa kwa kasi sana hapa nchi na hivyo uhitaji wa majiumekuwa ukiongezeka kwa kasi. Kutokana na jitihadambalimbali ambazo wananchi wa Mafinga wanajituma nauwekezaji katika mazo ya misitu.

Je, Serikali, iko tayari lini kutupa kibali kwa ajili yakuanza utekelezaji wa miradi ya mwaka huu wa fedha wa2017/2018?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, Waziri mpyalakini data kibao.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana, lakini nimpongezeMheshimiwa Mbunge, kaka yangu Mheshimiwa Cosato Chumikwa kazi kubwa anazozifanya na namna anavyofuatatilia iliwananchi wake wapate maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka sasa Wizara

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

imeshatoa kibali kwa mradi wa Mji wa Bumilianga ilikuhakikisha kwamba wananchi wanapata maji. Ahsantesana. (Makofi)

MWENYEKTI: Ahsante. Waheshimiwa Wabungetunaendelea na Wizara ya Ardhi Mheshimiwa Lucia MichaeliMlowe.

Na. 44

Serikali Kuendesha Zoezi la Mipango Mijina Matumizi Bora ya Ardhi

MHE. LUCIA M. MLOWE aliuliza:-

Msongamano wa magari, ujenzi holela, miundombinuduni ya maji taka na kadhalika katika miji mikubwa hapanchini vinatokana na udhaifu wa upangaji wa matumizi boraya ardhi (poor land use planning).

Je, Serikali imejiandaa vipi kuendesha zoezi laMipango Miji na matumizi bora ya ardhi katika miji mipyaikiwemo Halmashauri ya Mji wa Njombe?

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEOYA MAKAZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waArdhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, naomba nijibu swalila Mheshimiwa Lucia Michael Mlowe, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu Namba 7(1) chaSheria ya Mipango Miji Na. 8 ya mwaka 2007 kinaelekezakuwa jukumu la upangaji na uendelezaji miji lipo chini yamamlaka za upangaji ambazo ni Halmashauri za Majiji,Manispaa Miji, Wilaya na Mamlaka za Miji Midogo. Kutokanana umuhimu wa kuwa na Miji iliyopangwa kiuchumi nakijamii, Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemouandaaji wa mipango kabambe itakayotumika kuongoza,

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

kusimamia na kudhibiti uendelezaji wa Miji pamoja naurasimishaji wa makazi yasiyopangwa katika maeneombalimbali nchini.

Hadi kufikia Oktoba 20, 2017 maandalizi ya mipangokapambe ya miji 29 nchini ilikuwa imefikia katika hatuambalimbali. Maeneo hayo ambayo tayari mipango yake ipokatika hatua mbalimbali ni Majiji ya Mwanza, Da es Salaam,Arusha na Tanga na kwa upande wa Manispaa tunayoMtwara - Mikindani, Iringa, Musoma, Tabora, Singida,Sumbawanga, Songea, Shinyanga, Morogoro, Lindi, Bukoba,Moshi, Mpanda na Kigoma Ujiji. Kwa upande wa miji midogoni Kibaha, Korogwe, Njombe, Bariadi, Geita, Babati, Ifakara,Mahenge, Malinyi, Tunduma na Mafinga. Kati ya maeneohayo, mipango kabambe kwa Manispaa ya Mtwara -Mikindani, Musoma, Iringa na Singida imeshaidhinishwa nakuzinduliwa na hivyo imeanza kutumika rasmi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uandaaji wa mipangokabambe hufanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadaumbalimbali yakiwemo makampuni ya upangaji na upimajiardhi yaliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria, wamiliki wa ardhi,taasisi za Serikali, watu binafsi na asasi za kiraia pamoja nataasisi, zinatoa huduma mbalimbali za miundombinu kamavile TANESCO, TANROADS na Mamlaka za Maji Safi na MajiTaka. Utekelezaji wa mipango hiyo husaidia kutatuachangamoto zilizopo na hatimae kuwa na miji iliyopangwana yenye mtandao mzuri wa miundombinu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango kabambe wa Mjiwa Njombe unaandaliwa na Kampuni ya CRM Land Consultya Dar es Salaam kupitia programu ya Urban LocalGovernment Strengthening Program iliyofadhiliwa na Benkiya Dunia chini ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Hadi sasa rasimu yakwanza ya mpango kabambe ya mji huo imeandaliwa nahatua inayofuata ni kuwasilisha rasimu hiyo kwenye mikutanoya wadau kwa ajili ya kupokea maoni na mapendekezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa wito kwa mamlakaza upangaji ambazo hazina mipango kabambe, kuanza

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

maandalizi ya mipango hiyo pamoja na kongeza kasi yakupanga maeneo mapya, kurasimisha makazi yasiyopangwana kudhibiti uendelezaji holela kwa kushirikiana namakampuni yaliyosajiliwa kufanya kazi hiyo kwa mujibu washeria.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mlowe.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili yanyongeza.

Swali la kwanza, wananchi wapatao 200 waMakambako Kata ya Kivavi, Mtaa wa Mashujaawaliondolewa katika maeneo yao mwaka1997 bila kupewafidia, kwa ajili ya kupisha ujenzi wa soko la kimataifa,wamefuatilia wananchi hawa lakini hadi leo hakuna majibu.Pia kuna wananchi wa Idofi waliondolewa maeneo yao kwaajili ya kupisha ujenzi wa mizani hadi leo hawajapata fidia.

Je, Serikali inampanga gani wa kuwalipa wananchihawa fidia zao?

Swali la pili, kwa kuwa kila Halmashauri kuna MaafisaMipango Miji. Je, ni kwa nini wananchi wanajenga sehemuzisizo sahihi na Serikali inawaangalia tu mwisho wa sikuwanaanza bomoa bomoa? Naomba kupata majibu(Makofi).

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEOYA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na sehemu yakeya kwanza wananchi 200 wa Makambako na wale wa Kidozikwamba walipisha miradi ya Serikali na mpaka leohawajalipwa fidia. Naomba nimhakikishie tu MheshimiwaMlowe kwamba mara pesa zitapopatikana watalipwa, kwasababu Serikali inatambua kwamba ililitwaa lile eneo kwaajili ya matumizi ya Serikali, kwa hiyo, asiwe na wasiwasi pesaikipatikana watalipwa.

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili anaongeleahabari ya maafisa kwamba watu wanajenga ovyo nawanaangalia na hakuna hatua zinazochukuliwa baadaewanakuja kuwabomolea. Naomba nitoe rai tu kwa sababupia ni sehemu ya Halmashauri na tunakaa katika vikao vyetuvya Halmashauri kwa maana ya Baraza la Madiwani, hayayanapotokea ni wajibu wetu pia kutoa maonyo kwa waleambao wamepewa wajibu huo wa kufanya kazi lakinihawasimamii sawasawa. Kwa hiyo, namuomba MheshimiwaMbunge atakapokuwa amekaa katika Baraza lake laMadiwani wajaribu kuwakumbusha hasa wale watendajiambao hawatimizi wajibu wao vizuri.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mabula.

MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi kuuliza swali dogo la nyongeza.

Pamoja na kazi nzuri na jitihada za Serikali katikakuhakikisha miji inapangwa na zoezi zima la urasimishaji wamakazi ikiwemo upimaji shirikishi, naomba tu kujua Serikaliinayo mkakati gani kuhakikisha kwamba pamoja na upimajihuu unaofanyika sasa ile gharama ya premium inaonekanakuwa mzigo mkubwa kwa wananchi na matokeo yakewanashindwa kufikia hatua ya kupewa hati miliki, hivyoinawapelekea kubaki katika maeneo ambayo yamepimwabila hati hizo.

Je, ni nini mkakati wa Serikali kuondoa kabisa hiziasilimia 2.5 zilizopunguzwa japo ilikuwa Saba ikapunguzwa,nini mkakati wa Serikali kuondoa hizi lakini kuongeza mudawa upimaji shirikishi ili wananchi wengi zaidi wawezekupimiwa kuhakikisha maeneo yao yote yamekamilika?Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu, ni lini tu.

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEOYA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Bunge hili Tukufukwanza naomba nimshukuru Mheshimiwa Mabula kwa

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

sababu jana pia wakati anachangia Mpango wa Maendeleoamezungumzia suala la kuwajali sana wananchi na hasakatika suala zima la urasimishaji na mpango unaoendelea.Ametupa changamoto kama Wizara na sisi tunamshukuruna tumeona iko haja kweli ya kuangalia hawa wananchiambao walitumia nguvu zao kujenga katika maeneoambayo pengine hatukuwa makini katika kuwahi kupangana wao wakavamia, basi tumesema kwa sababu hoja nikupunguziwa mzigo, tumelichukua suala lake kuondoapremium na kabla ya mwisho wa mwezi huu tutakuwatumempa jibu.

Je, ni lini zoezi hili litaendelea, naomba nimfahamisheMheshimiwa Mbunge kwamba kwa maeneo yale ambayoyanarasimishwa na yamekwishaanza kwa mwaka huututavumilia mpaka mwisho wa mwaka huu wa fedha.Baada ya mwaka wa fedha tuna imani na mipango mijikatika maeneo hayo, mipango kabambe katika maeneohayo itakuwa tayari kwahiyo ukomo wao itakuwa ni mwishowa mwaka wa fedha mwaka huu 2017/2018.

MWENYEKITI: Ahsante ameshakuelewa. WaheshimiwaWabunge tunaendelea na swali la Mheshimiwa AngelinaMalembeka.

Na. 45

Upimaji wa Ardhi katika Taasisi za Umma

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA aliuliza:-

Kutokana na uvamizi wa ardhi katika maeneo yamashule, masoko na zahanati.

(a) Je, ni lini Serikali itakamilisha upimaji wa maeneohayo?

(b) Je, kutokana na ukubwa wa gharama za upimaji,kwa nini zoezi la upimaji lisitolewe bure kwa taasisi za ummakupitia Halmashauri hizo?

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEOYA MAKAZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waArdhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, naomba nijibu swalila Mheshimiwa Angelina Adam Malembeka, Mbunge wa VitiMaalum kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo ya shule, soko,zahanati, vituo vya afya, hospitali, vyuo, ofisi za Serikali, vituovya polisi, mahakama, maeneo ya majeshi, hifadhi za misituna wanyama na maeneo ya makumbusho hutengwamaalum kwa ajil i ya matumizi ya umma na shughulimbalimbali za Serikali. Maeneo yote haya yapo chini yausimamizi na uangalizi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa auSerikali Kuu. Hata hivyo, maeneo mengi kati ya hayoyamekuwa yakisimamiwa na taasisi za Serikali bila kupimwawala kuwa na hatimiliki badala yake yamekuwayakimilikishwa kwa utaratibu wa kupewa governmentallocation.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu huu pamoja nakwamba umekuwa ukifanywa kwa nia njema, umetoamwanya kwa wananchi wenye nia ovu kuyavamia,kuyamega na kuyaendeleza maeneo ya Serikali kinyume nautaratibu. Ili kuhakikisha kuwa changamoto ya uvamizi wamaeneo ya umma unakomeshwa, Serikali kupitia Wizarayangu iliagiza kuwa maeneo yote ya umma, yapimwe nayamilikishwe kwa taasisi husika kupitia barua yenye Kumb.Na. AB225/30/305/01 ya tarehe 7 Septemba, 2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuitikia wito huubaadhi ya taasisi za Serikali ikiwemo TBA, Hazina na TANROADSzinaendelea kuyatambua maeneo yake na kuyamilikishamaeneo wanayoyasimamia. Nitoe rai kwa Wakuu wote wataasisi za umma kuhakikisha wanakamilisha zoezi hilimapema na kwa maeneo ambayo yamevamiwa ni vemawavamizi wakaondoka kwa hiari yao na wasisubiri mkondowa sheria uwakumbe. Aidha, nampongeza sana Mkuu waMkoa wa Tabora na timu yake kwa kutekeleza agizo la Waziri

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

kwa vitendo na ni vema Wakuu wote wa Mikoa wenginewakachukua hatua ili kuondoa wavamizi kwenye maeneoyote ya umma.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, gharama elekezi zahuduma za upimaji ambazo kwa mara ya mwisho zilifanyiwamapitio mwaka 2016 siyo kubwa kama inavyodhaniwa kwakuwa upimaji wa ardhi hufanywa kwa misingi ya kurejeshagharama pakee. Gharama hizo hujumuisha vifaa vyaupimaji, shajara, usafiri, matengenezo ya vifaa namawasiliano ya kitaalam. Aidha, kukamilika kwa mtandaowa upimaji (Taref 11) tutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguzagharama za upimaji nchini.

Mheshimia Mwenyekiti, natoa rai kwa taasisi zote zaSerikali nchini kuhakikisha zinapima na kumilikishwa maeneoyao ili kuwa na miliki salama kwa kuwa ulinzi wa ardhiwanayomilikishwa ni jukumu la taasisi husika. Aidha, taasisizote za umma nchini zinahimizwa kutenga fedha katikabajeti zao kwa ajili ya kuharakisha upimaji wa maeneo yotewanayoyasimamia.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Malembeka.

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibumazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, Angelina mwenzangu,nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Swali la kwanza, kwa kuwa Mheshimiwa naibu Waziriamekiri kuwa wananchi wanavamia na kuyamega maeneoya Serikali kinyume na utaratibu; na kwa kuwa ametoa raiwananchi waondoke maeneo hayo kabla sheria haijachukuamkondo wake, sasa isije ikawa kwa wananchi kilio, kwawatendaji vigelegele.

Je, Serikali ina kauli gani juu ya watendaji ambaowanalipwa mshahara kwa kazi ya upimaji na katika maeneoyao hawajafanya lolote hadi sasa?

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

Swali la pili, kwa kuwa katika majibu ya msingi,Mheshimiwa Naibu Waziri amesema gharama elekezi zahuduma ya upimaji siyo kubwa kama inavyoonekana auinavyodhaniwa.

Je, kwa nini gharama hizo zisiwekwe wazi ili wananchina taasisi nyingine wafahamu na kuzitambua na wawezekujipanga kwa ajili ya kulipia? Ahsante.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupitafadhali.

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEOYA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Swali lakwanza ameulizia habari ya adhabu kwa watendaji ambaowanafanya makosa na tunaadhibu pengine wananchi. Kamanilivyomjibu muulizaji wa swali namba 44 majukumu nauwajibishaji yako chini ya mamlaka husika hasa katikamaeneo yetu kwenye Halmashauri za Wilaya. Kwa hiyo, hayayanapobainika basi tuyachukulie hatua papo hapo ilitusiweze kuwafanya wananchi waumie zaidi kwa makosaya watendaji wetu.

Swali la pili, ametaka kuewekewa gharama zaupimaji wazi. Naomba niseme tu tutazitoa na tutawagawiaWaheshimiwa Wabunge wote, lakini kwa kifupi tu nikianzakuzungumzia habari ya miji kwenye Mamlaka za Miji naManispaa katika gharama za upimaji kuanzia square metermoja mpaka square meter 400 gharama yake kwa maeneoya residential ni shilingi 65 lakini maeneo ya commercial nishilingi 350 kwa square meter, kwenye industrial ni shilingi 450na kwenye maeneo ya social services ni shilingi 150. Kwa mijiyetu ya kwaida kwenye township ni shilingi 200 kwa makazi,maeneo ya biashara ni shilingi 300, maeneo ya viwanda 350na maeneo ya services ni shilingi 100. Vivyo hivyo kwenyetrading center ni shilingi 100 kwa makazi, shilingi 200 kwacommercial, shilingi 200 tena kwa industrial na shilingi 100kwa services. Kwa sababu mlolongo pia unategemeana naukubwa wa kiwanja vina-range kuanzia shilingi 300,000mpaka milioni 14 kutegemeana na ukubwa kuanzia hekari

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

moja mpaka 10 ni shil ingi milioni tatu, zinakwendazinaongezeka kadri ya ukubwa, tutaziandaa natutawasambazia Waheshimiwa Wabunge wote.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Shanagzi, MheshimiwaKomu halafu Mheshimiwa Mbarouk na Mheshimiwa Umbulla.

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kuniona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shamba la Mnazi Estate kuleLushoto - Mlalo limevamiwa kwa sababu Mmiliki ambaealikuwa anendelea kulimiliki ameshindwa kuliendesha. Je,pamoja na mchakato ambao tulikuwa tumeuanza wakufuta, Serikali imefika hatua gani ya kumuondoa mmilikikatika ardhi hiyo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwakifupi, Mheshimiwa Waziri mhusika.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwenye kijiji chaMnazi kuna Kampuni inatiwa Lemash Enterprise ambayoilikuwa inamiliki shamba la Mkonge lenye hekta 1,275 lakininataka nimhakikishie Mheshimiwa Shangazi kutokana najitihada zake za kuondoa kero ya wananchi na katikakutekeleza spirit ya Mheshimiwa Rais Dkt. John PombeMagufuli walitimiza wajibu wao na nataka kumhakikishiakwamba na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli nayeametimiza wajibu wake. Tarehe 4 Septemba, 2017 shambahilo l imefutwa rasmi na mmiliki ameshaambiwa,nimeshachukua hatua ya kulitangaza kwenye Gazeti laSerikali kwa order ya Rais na hivi sasa nimeshamwandikiaMkuu wa Mkoa wa Tanga ili atupe mapendekezo mazuri zaidiya namna ya kulitumia shamba hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo nakuombaMheshimiwa Shangazi kwa kuwa umelianza, basi naombaushirikiane na Mkuu wa Mkoa wa Tanga kulimalizia mletemapendekezo mazuri yatakayowezesha kutumika shamba

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

hilo kuinua uchumi wa wananchi wa Mnazi. Tungependashamba hili liendele kuwa shamba la Mkonge lakini ninyi watuwa Tanga muamue nani aendesha kilimo hicho kwa ajili yakuongeza tija ya ajira na uchumi wa Taifa. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Komu atafuatiwana Mheshimiwa Mbarouk.

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Moshi vij i j ini kunamashamba ambayo toka mwaka 1968 yalitaifishwa nakimsingi ni mashamba ya umma, lakini baada ya kutaifishwana kupewa Vyama vya Ushirika yamekuwa yakigawanywakwa taasisi mbalimbali kwa ajili ya shughuli za wananchi.Sasa hizo taasisi zikitaka kupima hayo mashamba sasakulingana na shughuli ambazo zinafanyika inakuwa vigumukwa sababu tayari kuna hati ambazo zilikuwepo toka wakatihuo, ikiwa ni pamoja na eneo kama la Uru Seminari ambalonilishalifikisha kwa Mheshimiwa Waziri.

Naomba kujua kutoka kwenye Serikalini ni lini Serikaliitakwenda kufanya upimaji upya ili kutoa hati kulingana namatumizi ambayo yapo sasa hivi katika yale mashambakatika Kata zote hizo?

MWENYEKITI: Mheshimwia Waziri ni lini muda wetuumekwisha jaribuni kuwa na majibu mafupi.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Mkoa waKilimanjaro na mashamba ya ushirika ni tatizo kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamna mashambahaya yalikuwa ni ya settlers, uamuzi wa Baba wa Taifayalichukuliwa yakapewa Vyama vya Ushirika na mashambahaya ni mengi sana Mkoa wa Kil imanjaro ambayoyalimilikishwa Vyama vya Ushirika. Wizara yangu kwakushirikiana na Wizara ya Kilimo nimeshamwandikia lakini

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

tunazungumza nia njema zaidi ya kuhakiki upya mashambayanayomilikiwa na Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro hivi sasa. Nikweli Vyama vya Ushirika zamani vilipewa, lakini leo matumiziyake ya vyama vya ushirika na ushirika wenyewe ni tofautina madhumuni ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka MheshimiwaMbunge na Wabunge wote wa Mkoa wa Kilimanjaro maanahoja hii siyo ya Mheshimiwa Mbunge peke yake, Wabungewote wa Kil imanjaro mashamba haya yanawahusu.Watuachie bado tuko kwenye mazungumzo na Wizara yaKilimo ambaye ndiyo Msajili wa Vyama vya Ushirika ili tuonenamna gani njema ya kuyahuisha mashamba yote ya ushirikaya Mkoa wa Kilimanjaro ili yawe na tija kwa wananchi wotekulingana na mazingira ya sasa. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbarouk.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kuniona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jiji letu la Tanga kunaupimaji unaoendelea katika eneo la Amboni kwa ajili yakuongeza Kiwanda cha Saruji cha Sinoma cha Wachina.Katika maeneo yale kuna tatizo kubwa la kwamba,wananchi wenye mashamba yao wanaambiwa watalipwafidia ya mazao ya muda mrefu tu na mazao ya muda mfupikama mahindi, mihogo na mengineyo hayatalipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali inalifahamu hilona utaratibu huu ni utaratibu wa sheria gani inayotumikakulipa mazao ya muda mrefu, na pia pana maji koto ausulphur water pale katika eneo la Amboni ambayo ni kamatunu kwa mambo ya utalii.

Je, Serikali inafanya juhudi gani kuhakikisha ile sulphurbath itaendelea kuwepo ambayo iliendelezwa na Galanoslakini pia na wananchi wenye mzao mafupi nao watalipwafidia yao?

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri mhusika kwa kifupisana please.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili ni la Tanga.Walioamua kufanya haya ni Halmashauri ya Jiji la Tangakwenye shamba hili. ningemuomba Mheshimiwa Mbungekwa sababu kazi hii hata tathmini ya pale imesimamiwa nakufanywa na Wathamini waliopo kwenye Jiji la Tanga naupitishaji wa viwango huu ulikuwa shirikishi na maelekezohaya yametolewa pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba, unajua ni rahisikufikiri kwamba Waziri akiwa hapa Dodoma anaweza akajuana akalitolea ufafanuzi kila jambo lakini jambo hili ni shirikishilimefanywa na Watendaji wenye Mamlaka ya Kisheria yakutenda wa Jiji la Tanga kwahiyo kama halikufanyika vizuri,wale wananchi wanajua Bungeni hapa mwaka huummetunga Sheria ya Bodi ya Mfuko wa Fidia. Ninawaombawaisome, Waheshimiwa Wabunge muwasidie wananchihawa wakate rufaa kwenye Bodi ya Mfuko wa Fidia ili iwezekufikiaria vinginevyo, lakini mimi kama aziri hapa siwezikusimama nikatengua uamuzi halali uliofanywa naHalmashauri ya Jiji la Tanga. Hivyo, naomba wafuate hiyosheria. (Makofi)

Na. 46

Huduma ya Matibabu ya Saratani - Hospitali ya Bugando

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:-

Kutokana na msongamano mkubwa wa wagonjwawa saratani katika Hospitali ya Ocean Road pamoja nagharama kwa ndugu wa wagonjwa ya kuwaleta nakuwauguza ndugu zao.

Je, Serikali haioni haja ya kuanza kutoa huduma hiyokatika Hospitali ya Rufaa ya Bugando?

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII (K.n.y WAZIRI WAAFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO)alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa ni mara yanguya kwanza leo nasimama hapa toka niteuliwe naMheshimiwa Rais, naomba na mimi nimshukuru MheshimiwaRais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuniamini na kunipamajukumu zaidi kwenye Serikali yake, pia niwashukuruwananchi wa Jimbo la Nzega Vijijini, Wilaya ya Nzega naMkoa wetu wa Tabora kwa ujumla kwa ushirikiano ambaowameendelea kunipa. Napenda kusema tu kwa wotekwamba kwa hakika sitowaangusha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watotonaomba kujibu swali la Mheshimiwa Leah Jeremiah Komanyakama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimuwa kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za matibabukwa wagonjwa wenye Saratani ili kusogeza huduma hizikaribu zaidi na wananchi na kupunguza msongamano katikaHospitali ya Ocean Road, pia kupunguza gharama kwawagonjwa na ndugu. Kwa sasa Serikali inakamilishamaandalizi ya kuanzisha matibabu ya saratani kwa mionzikatika Hospitali ya Bugando ambapo baadhi ya majengokwa ajili ya huduma husika yamekamilika, yakiwemo jengomaalum ambalo ni kwa ajili ya kudhibiti mionzi, ambapoukuta wake umejengwa kwa zege nene la mita moja(bunkers), jengo la kutolea huduma za mionzi, baadhi yawataalam wapo na baadhi ya mashine za matibabu kwamionzi zimeshanunuliwa zikiwemo Cobalt 60 na CT Simulator.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha brachytherapy naimmobilization devices zinatarajiwa kuwasili mwezi Disemba,2017. Kwa sasa huduma za tiba ya saratani zinazopatikanaBungando ni zile za matibabu yasiyo ya mionzi (chemotherapy)na zilianza mwezi Januari mwaka 2009, kufuatia sera yaSerikali ya kutoa huduma hizo kikanda. Takwimu zinaonyesha

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

kuwa, kwa kipindi cha mwaka 2009 - 2017 hospitali imetoamatibabu kwa wagonjwa 39,300 kati yao 12,200 wakiwa niwapya, sawa na wastani wa waginjwa 1,500 kwa mwaka.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Komanya.

MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na juhudi nzuri za Serikali, takwimu zinaonyeshakuwa, asilimia 60 ya wagonjwa wanaohudumiwa Hospitaliya Ocean Road wanatoka Kanda ya Ziwa, lakini katikahuduma zinazotolewa kwa sasa katika Hospitali ya Rufaa yaBugando zipo changamoto kubwa ikiwemo uhaba wafedha wakati wa ku-service ile mashine. Hospitali yenyewehaijitoshelezi na kusababisha huduma hiyo kusitishwawakisubiri fedha na kuendelea kuleta usumbufu kwawagonjwa katika Hospitali ya Ocean Road. Je, Serikali haionihaja ya kupeleka ruzuku ya kutosha katika kitengo chasaratani kilichopo Bugando?

Swali langu la pili, tafiti zinaonesha kuwa majiyaliyoachwa kwenye gari lililopo kwenye jua na yakakaa kwamuda mrefu katika vyombo vya plastiki inaonyeshainapopata joto kuna chemical zinatoka kwenye plastiki ainaya dioxin ambazo zinaonyesha kuna uwezekano wa kupatasaratani hususani saratani ya matiti. Je, Wizara ina mikakatigani ya kutoa elimu kwa wananchi?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu, na wewe nimtaalamu wa afya vilevile.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII (K.n.y. WAZIRI WAAFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO):Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwanza kuhusu ruzukukuongezwa kwa ajili ya kituo cha tiba ya saratani kilichopoKanda ya Ziwa kwa maana ya Hospitali ya Rufaa ya Bugandondiyo kwanza kimeanza kufanya kazi, kwa hiyo, tunatarajiauwepo wa changamoto mbalimbali ambazo zitajitokezampaka pale ambapo kita-stabilize. Kwa hivyo, ninaombaniichukue hii kama changamoto na tutatazamachangamoto hii inasababishwa na nini il i wakati wa

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

mchakato wa bajeti inayokuja, tuone ni kwa kiasi ganitunahitaji kuongeza ruzuku kwenye kituo hiki ili kiweze kutoahuduma bora zaidi katika mwaka wa fedha unaokuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali lake lapili ambalo linahusu plastics ambazo zinatumika kuwekeamaji ambayo yakikaa kwenye jua kwa muda mrefuinasemekana yanaweza yakasababisha saratani, hili ni jamboambalo limekuwa likisemwa kwenye mitandao mara nyingilakini halina ukweli wowote ule na naomba niwatoewasiwasi Waheshimiwa Wabunge pamoja na wananchiwote kwamba Serikali iko makini na haiwezi kuruhusu kituchochote kile ambacho kinauzwa kwa ajili ya matumizi yabinadamu na kikawa na madhara kikaingia kwenye soko,kwa sababu tunafanya uchunguzi pia tunafanya udhibiti wabidhaa zote ambazo zinaenda kutumika kwa wananchikupitia taasisi yetu ya Tanzania Foods and Drugs Authority(TFDA) - (Mamlaka ya Chakula na Dawa) ambapo mamboyote haya yakisemwa ama yakizungumzwa kwenye jamiihuwa tunayafanyia utafiti wa kimaabara na hatimayekuthibitisha kama yana ukweli ama hayana ukweli ndaniyake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili analolisema MheshimiwaKomanya tulikwishalifanyia kazi na tukabaini ni uzushi nahalina ukweli wowote ule na kwa hivyo hakuna sababu yakuendelea kuwatia wasiwasi wananchi.

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Waziri, MheshimiwaMtolea.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja lanyongeza.

Hospitali ya Ocean Road ambayo ndiyo maarufu nainafanya kazi kubwa ya kuhudumia wagonjwa hawa wasaratani ndiyo hospitali ya siku nyingi na miundombinu yakepia ni ya kizamani lakini idadi ya wanaopata huduma hapoimeongezeka maradufu. Mbali na hayo hospitali ile haifikiki

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

kirahisi kwa sababu iko pembeni na vituo au barabara zausafiri wa umma kwa maana ya daladala. Hivyo, wananchiwanatakiwa kutembea umbali mrefu kwa zaidi ya kilometamoja kufika hospitalini pale umbali huu si rafiki kwa mgonjwaau watu wanopeleka wagonjwa hospitali. Je, Serikali inampango gani wa kujenga hospitali nyingine kubwa ya kisasajijini Dar es Salaam ili kuzihamisha huduma hizi za magonjwaya saratani ziweze kufanyika katika kituo kimoja kikubwa nacha kisasa?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu anatakakujua ni lini tu.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII (K.n.y. WAZIRI WAAFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO):Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa hatuna mpango kwakweli wa kujenga kituo kingine cha kutoa tiba ya saratanikatika Jiji la Dar es Salaam, kwa sababu kituo cha OceanRoad kinajitosheleza na kinajitosheleza kwa maana ya kutoahuduma kwa Kanda nzima ya Mashariki na hata wagonjwawanaotokea Kanda ya Kati wanaweza wakapata hudumazao pale Ocean Road.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu ni moja kituo kilehakipaswi kuwa kama hospitali ya kwenda kila siku, kile kituoni kituo cha rufaa. Kwa sasa kilikuwa ni kituo pekee cha rufaacha Kitaifa lakini kwakuwa toka tumeingia Awamu ya Tanotumeanzisha utaratibu wa kufungua vituo vingine kwenyesatelites/kwenye Kanda zote kwa maana ya Kanda ya Kusinipale Mbeya, Kanda ya Ziwa pale Bugando na Kanda yaKaskazini pale KCMC ndio maana sasa tunakichukulia kituohiki cha Ocean Road kama cha Kanda hii ya Mashariki naKanda zozote zilizo karibu na Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huduma ile ya sarataniinayotolewa pale ni ya rufaa ni huduma ya ngazi ya juukabisa, kwa hivyo kwa vyovyote vile hatuwezi kusambazahuduma hizi kila sehemu kwamba tuweke na upandemwingine, hapana. Hospitali kubwa zipo nyingi Dar esSalaam ikiwemo ile mpya ya Mloganzila ambayo itatoa

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

huduma nyingine zozote pembeni lakini siyo huduma zasaratani kwa sababu gharama za kuanzisha kituo chasaratani ni kubwa sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante tumekuelewa. WaheshimiwaWabunge, tunaendelea Wizara ya Maliasili MheshimiwaRichard Philip Mbogo.

Na. 47

Kubadili Mipaka ya Hifadhi za Misitu kwa Mujibu wa Sheria ya Misitu

MHE. RICHARD P. MBOGO aliuliza:-

Katika mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa Mkoawa Katavi uliofanywa na Halmashauri ya Mpanda mwaka2004 kwa kushirikisha ngazi ya Mkoa na ngazi ya Wizara,zililipwa sehemu za Hifadhi za Misitu North East Mpanda (JB94)na Msanginia (JB215) na ramani mbalimbali kuidhinishwaikiwemo 48870, 48893 na 40250.

Je, ni lini Serikali itabadili mipaka hiyo kwa mujibu waSheria ya Misitu ya 2002 (Namba 14) Kifungu cha 28?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa ni mara yanguya kwanza kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu naombanichukue nafasi hii kwanza kumshukuru sana Mwenyezi Mungukwa kunipa uhai na kuniwezesha kufika siku hii ya leo. Pili,nimshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwa kuniaminina kuniteua katika nafasi hii. Tatu, nimshukuru MheshimiwaSpika pamoja na uongozi mzima wa Bunge la Jamhuri yaMuungano wa Tanzania pamoja na Wenyeviti wa Kamatinilizokuwa Mjumbe kwa malezi yao ambayo wameyatoakwangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

Maliasili na Utalii naomba kujibu swali la Mheshimiwa RichardPhilip Mbogo, Mbunge wa Nsimbo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Misitu wa hifadhi waMpanda North East na Msangimya ni misitu ya Serikaliinayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.Msitu wa North East Mpanda umehifadhiwa kwa tangazo laSerikali Na. 296 la mwaka 1949. Aidha, Msitu wa Msangimyaumehifadhiwa kwa Tangazo la Serikali Na. 447 la mwaka 1954na inasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya Misitu Na. 14 yamwaka 2002 Sura ya 323.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya yaMpanda ilipima maeneo ya Hifadhi ya Msitu wa MpandaNorth East na Msangimya kupitia ufadhili wa Shirika la Africarechini ya mradi wa Ugalla Ecosystem ili kuanzisha maeneo yausimamizi wa Wanyamapori (Wildlife Management Area-WMA) na makazi pamoja na kuandaa mpango wa matumizibora ya ardhi ya vijiji. Baada ya upimaji huo ramani 48870,48893 na 40250 zilichorwa na Halmashauri husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, l icha ya nia njemailiyokuwepo ya kuwapatia wananchi makazi yaliyopimwakwa mujibu wa sheria na uanzishwaji wa maeneo ya usimamiziwa wanyamapori (WMA) na kuandaa mpango wa matumizibora ya ardhi ya kijiji, utaratibu huu haukuzingatia Sheria yaMisitu Na. 14 ya mwaka 2002 pamoja na Sheria yaWanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009. Kwa mujibu wa kifungucha 31(1) cha Sheria ya Wanyamapori, WMA zote zinaanzishwakwenye misitu iliyoko kwenye ardhi ya kijiji au ardhi ya ujumlana siyo kwenye misitu ya Hifadhi ya Serikali Kuu. Aidha,mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji inafanyika kwenyeardhi ya kijiji husika na siyo kwenye misitu iliyohifadhiwakisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili ardhi ya msitu wa hifadhiuweze kutumika kwa matumizi mengine, Sheria ya Misitu Na.14 ya mwaka 2002 katika kifungu cha 29 inatoa utaratibuwa kisheria wa kufuta hadhi ya msitu wa hifadhi ambapoWaziri wa Maliasili na Utalii anaweza kufuta sehemu ya msitu

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

au msitu wote wa hifadhi baada ya kujiridhisha kunaumuhimu ya kufanya hivyo. Mara baada ya mchakato huukukamilika ndipo ardhi ya msitu itatumika kwa matumizi nashughuli zingine za kibinadamu mbali na uhifadhi. Aidha,Waziri wa Maliasili na Utalii atatoa maamuzi hayo baada yakushauriana na Kamati ya Taifa ya Ushauri wa Misitu (NationalForestry Advisory Committee) ambayo inatajwa katika Sheriaya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 katika Kifungu cha 10.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mchakato wakupima sehemu ya misitu ya hifadhi niliyoeleza hapo juuumefanyika kinyume cha sheria na taratibu zilizopo, hadhiya misitu hiyo ya hifadhi inaendelea kubaki kisheria kamailivyoainishwa kwa mujibu wa matangazo ya Serikaliniliyoyataja hapo juu. Aidha, Serikali itaangalia kamakunaweza kuwa na uwezekano wa maeneo hayo kutolewakwa ajili ya matumizi mengine kwa mujibu wa sheria, lakiniikiweka kipaumbele kwanza kitatolewa kwa maslahimapana ya Taifa na kwa kufuata ushauri utakaotolewa naKamati ya Taifa ya Ushauri ya Misitu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbogo.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante.

Pamoja na majibu ya Serikali, ningependaniikumbushe Serikali kwamba wakati Halmashauri ya WilayaMpanda inafanya mpango wa matumizi bora ya ardhiilizingatia mahitaji ya wananchi pamoja na maendeleo yaokwa wakati huo, kwa sasa hivi tunavyozungumza Wilaya yaMpanda, Mkoa wa Katavi idadi yake ya wananchiimeongezeka. Haya matangazo ya Serikali, Tangazo Na. 447ya mwaka 1954 Na. 296 ya mwaka 1949 hayaendani nauhalisia na hali i l ivyo chini kutokana na ramani hizikuidhinishwa na Wizara ya Ardhi mwaka 2008 na zilianzakuidhinishwa na ngazi ya Mkoa mpaka na Wizara ya Ardhikwa Kamishna wa Upimaji na Ramani. Kwa sasa hivitunaenda kwenye nchi ya viwanda na maeneo mengiyanahitaji wakulima kwa ajili ya kulima mazao mbalimbali

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

na Mkoa wa Katavi tuna mkakati wa kuanzisha zao lakorosho. Kulingana na matangazo ya Serikali yanatofautianana ramani zilivyo, uhalisia na mahitaji ya wananchi. Je,Mheshimiwa Waziri yuko tayari hii Kamati ya Ushauri ya Taifajuu ya Misitu iambatane na Mbunge wa Jimbo la Nsimbobaada ya Mkutano huu wa Tisa kwenda kuangalia hali halisiili waweze kumshauri Waziri na waweze kubadilisha mipakakwa mujibu wa kifungu cha 29 cha Sheria ya Misitu ya mwaka2002?

Swali la pili, kutokana na uhitaji mkubwa wananchikwa maeneo haya na masika tayari imekwishaanza natunajua Waziri wa Maliasili na Utalii kwa mujibu wa Sheria yaMisitu ya mwaka 2002 yeye ndiye mwenye dhamana ya kutoakauli. Je, yuko tayari kuwaruhusu wananchi katika Kijiji chaMatandarani na Igongwe Kata ya Isalike waweze kupatamaeneo ya kujihifadhi kwa kulima, wakati Kamati ya ushauriikiendelea kupitia maeneo na kuweza kumshauri Waziri?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi,mko tayari kwenda naye? Ni hilo tu ndiyo jambo kubwa.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza tuko tayari baada ya Mkutano huu waTisa kumalizika Kamati ya Ushauri itapita maeneo yoteambayo yana migogoro nchi nzima ili iweze kumshauriMheshimiwa Waziri na aweze kutoa maamuzi sahihi.

Swali la pili, kuhusu kulima ni kweli wananchi walenimefika katika lile eneo wana matatizo mengi, lakinininaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tulipokaa naMheshimiwa DC pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauriwalikubali kwamba wametenga eneo la ekari zaidi ya 700ambalo sasa linatolewa kwa wananchi wale ili wawezekuendelea na hizo shughuli. Kwa hiyo, hatutaweza kuruhusukwa sasa hivi waendelee na shughuli hizo kwa sababu tayariwameshaondolewa na ukiwaruhusu kupanda zao la koroshoambalo ni la muda mrefu mpaka lije lianze kuvunwa itakuwani muda mrefu sana, kwa hiyo tutakachokifanya nikuwapeleka katika hayo maeneo ambayo tayari

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

yameshatengwa na Serikali ili waendelee na shughuli zaozile ambazo zipo.

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabungetunaendelea na Mheshimiwa Augustino Manyanda Masele,Mbunge wa Mbogwe.

Na. 48

25% ya Ada ya Uwindaji - Kitalu cha Kigosi North

MHE. AUGUSTINO M. MASELE aliuliza:-

Katika Wilaya ya Mbogwe kuna Kitalu cha Kigosi Northkilichopo katika Pori la Akiba la Kigosi.

(a) Je, ni lini Serikali itaanza kulipa Halmashauri yaWilaya ya Mbogwe asilimia 25 ya ada ya uwindaji?

(b) Je, ni lini Serikali italitengeneza greda lililoko KifuraKibondo Makao Makuu ya Mapori ya Kigosi Moyowosi ililisaidie matengenezo ya barabara ndani ya mapori haya?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waMaliasili na Utalii, ninaomba kujibu swali la MheshimiwaAugustino Manyanda Masele, Mbunge wa Mbogwe, lenyesehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu imekuwa nautaratibu wa kutoa fedha kiasi cha asilimia 25 kwenyeHalmashauri za Wilaya zinatokana na malipo ya ada yawanyamapori (game fees) wanazowinda kwenye maeneoyanayopakana na Wilaya husika kwa ajili ya kusaidia shughuliza maendeleo na uhifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitalu cha Kigosi Northkimekuwa kikitumika kwa ajili ya utafiti wa madini uliokuwaunafanywa na Kampuni ya TANZAM na siyo kwa shughuli za

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

uwindaji wa kitalii. Hali hiyo inafanya Halmashauri ya Wilayaya Mbogwe isipate fedha za asilimia 25 kwa ajili ya uwindajiwa kitalii katika kitalu hicho. Kitalu cha Kigosi East ndiyo kitalukilichotengwa kwa shughuli za uwindaji wa kitalii kwa kipindicha mwaka 2013 hadi 2018. Hata hivyo, mwekezaji katikakitalu hicho amejaribu kuleta wageni mara mbili mwaka 2013na 2014 kwa ajili ya kuwinda lakini hakuweza kuwindakutokana na kuwepo kwa ng’ombe wengi badala yawanyamapori katika kitalu hicho. Kwa sababu hiyo, hakunawanyamapori waliowindwa kwa kipindi cha mwaka 2013hadi 2016 kutokana na kuwepo kwa ng’ombe na hivyo kitaluhusika kurudishwa Serikalini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na jitahada zaSerikali za kuondoa mifugo katika maeneo yote ya hifadhi,ni wazi kuwa mazingira ya asili pamoja na wanyamaporiwatarejea na hivyo kuwezesha kitalu hicho kutumika kwauwindaji wa kitalii kuanza kufanyika. Kufanyika kwa uwindajiwa kitalii katika kitalu hicho kutawezesha upatikanaji wafedha ambazo zitaweza kuanza kuwasilishwa katikaHalmashauri ya Wilaya ya Mbogwe. Wizara yangu inatoawito kwa Wilaya zote zenye uvamizi wa mifugo kwenyemaeneo yaliyohifadhiwa kuhakikisha mifugo inaondolewaili kurejesha hadhi ya vitalu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kutengeneza greda,Wizara yangu tayari imeshatengeneza greda lililopo Kifurakatika Pori la Akiba Moyowosi Kigosi na sasa linafanya kazi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Augustino Manyanda.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Wazirinina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Swali la kwanza, Mheshimiwa Naibu Waziri amesemakwamba hiki kitalu kimetolewa kwa ajili mambo ya utafitiwa madini lakini kwa mujibu wa Sheria Na. 5 ya mwaka 2009ya Wanyamapori inazuia kufanyika kwa utafiti katikamaeneo ya hifadhi. Je, ni taratibu zipi ambazo Serikali

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

imetumia kukigawa hiki kitalu ili kifanyiwe mambo ya utafitiwakati sheria hairuhusu?

Swali la pil i, kwa kuwa mapori haya yanachangamoto mbalimbali, je, Naibu Waziri atakuwa tayarikuambatana na mimi pindi Bunge litakapomaliza shughulizake ili aweze kuja kuziona hizo changamoto zinazoyakabilihaya mapori na kuweza kuzitatua?

MWENYEKITI: Majibu kwa kifupi sana muda wetuumekwisha Waheshimiwa.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza naomba nichukue nafasi hii kumpongezaMbunge kwa kazi kubwa amekuwa akifanya katikakuwatetea wananchi wake wa Jimbo la Mbogwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu TANZAM ambayealipewa kitalu hicho, kwa mujibu wa Sheria Na. 5 ya mwaka2009 kifungu cha 20(2)kinazuia kabisa shughuli zote za utafitiwa madini ya aina zote kufanyika katika maeneo ya hifadhi.Hata hivyo, kifungu hicho cha 20(3)kinatoa mamlakakwamba ni aina tatu tu za madini zinaruhusiwa kufanyiwautafiti, madini hayo ni uranium, gesi na mafuta. Kufuatanana mwekezaji aliyekuwa amepewa hiki kitalu yeye alikuwaanafanya utafiti wa madini ya dhahabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba pamoja na leseniya huyu mwekezaji ilimalizika tereha 31 Desember 2014,baada ya kumalizika, tarehe 1 Juni, 2016 Serikali ilimuandikiabarua ya kumuomba aondoke katika eneo na aondoe vituvyote lakini hadi leo bado mwekezaji yule yupo opale naameweka vifaa vyake wakati hana leseni na ilishapita. Tarehe28 Aprili, 2017 alikumbushwa juu ya suala hili na mpaka sasahivi bado hajasema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie nafasi hiikutoa siku saba, yule mwekezaji aondoe hivyo vitu vyote,kwa sababu viko pale kinyume na taratibu na sheria iliyopo.(Makofi)

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

Baada ya kumalizika, tarehe 1 Juni, 2016 Serikaliilimuandikia barua ya kumuomba aondoke katika eneo naaondoe vitu vyote lakini hadi leo bado mwekezaji yule yupoopale na ameweka vifaa vyake wakati hana leseni nailishapita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 28 Aprili, 2017alikumbushwa juu ya hili suala na mpaka sasa hivi badohajasema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie nafasi hiikutoa siku saba, yule mwekezaji aondoe hivyo vitu vyote kwasababu viko pale kinyume na taratibu na Sheria iliyopo.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge,tunaendelea. Mheshimiwa Balozi Adadi Rajab Mbunge waMuheza.

Na. 49

Uuzaji wa Vitalu vya Miti kwa Njia ya Mnada Muheza

MHE.BALOZI ADADI M. RAJAB aliuliza:-

Vitalu vya miti ya tiki – Lunguza Muheza huuzwa kwanjia ya mnada hali inayosababisha viwanda vidogo vidogovya Muheza kukosa miti.

(a) Je, ni lini Serikali itahakikisha wenye viwanda katikamaeneo hayo wanapata vitalu ili kulinda ajira za wanavijiji?

(b) Je, kwa nini wanaopata vitalu wasichane magogohayo hapo Wilayani ili kulinda viwanda vidogo vidogo vyaMuheza?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waMaliasili na Utalii naomba kujibu swali la Mheshimiwa Balozi

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Adadi Mohamed Rajab, Mbunge wa Muheza lenye sehemu(a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye biashara ya miti yamisaji, njia mbili ambao ni mnada na makubaliano binafsihutumika. Mbinu mbalimbali zimekuwa zikitumika katika kuuzamiti ya misaji ili kuongeza bei ya miti kwa kutumia ushindaniwa bei iliyopo sokoni. Hivyo, ili kupata bei ya soko, mbinuinayotumiwa ni pamoja na kuuza kiasi kidogo cha ujazo wamiti ya kuvuna kwa njia ya mnada. Hivyo, asilimia 30 yamalighafi inayotarajiwa kuvunwa katika shamba husikahuuzwa kwa utaratibu huu. Njia hii inasaidia kubaini nguvuya soko na kuongeza mapato ya Serikali. Njia ya makubalianobinafsi hutumika pia katika uuzaji wa miti mara baada ya beiya soko kupatikana katika mnada. Hivyo asilimia 70 huuzwakwa makubaliano binafsi ili kutoa fursa kwa wadau wengizaidi kushiriki kwenye biashara hiyo. Utaratibu huu kwa kiasikikubwa umewawezesha wenye viwanda wanaoshindwakununua kupitia njia ya mnada kupata malighafi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuongeza wigo wa sokola ndani, Wizara imeanzisha utaratibu utakaowawezeshawanunuzi wengi wa miti ya misaji walioko nchini kunufaika.Utaratibu huu unawalenga wale wote wenye viwandavinavyotengeneza samani vilivyopo nchini. Hivyo, katikamwaka wa fedha 2017/2018 asilimia 10 kati ya asilimia 70 yaujazo wa miti uliotengwa kwa ajili ya kuuzwa kwa njia yamakubaliano binafsi utauzwa kwa watengenezaji wa samanindani ya nchi ili kuongeza thamani ya mazao yao nakuongeza ajira. Matangazo ya mauzo ya miti hufanyika kwakubandika katika mbao za matangazo na kutolewa katikamagazeti kwa muda wa siku 14 kabla ya mauzo. Wenye niaya kuvuna na wenye kumiliki mashine za kupasua magogoikiwemo wana vijiji wanaozunguka shamba letu la miti laMtibwa na Longuza hupewa matangazo hayo kuhusu mnadahuo ili nao waweze kujitokeza katika kununua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kulinda viwanda vya ndanina kuongeza ajira kwa Watanzania, uchakataji wa magogoyanayovunwa katika mashamba ya miti hufanyika ndani ya

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

nchi. Baada ya kuuziwa malighafi kutoka katika mashambaya miti, uchakataji hufanywa na mteja mwenyewe kulinganana mahali alipoweka kiwanda chake. Sheria na mwongozowa uvunaji wa mazao ya misitu haimlazimishi mwenyekiwanda kujenga kiwanda mahali malighafi inapopatikana.

Nashauri Waheshimiwa Wabunge, tuendeleekuhimiza Halmashauri zetu ziweke mazingira wezeshi kwawawekezaji wa viwanda vidogo na vikubwa katika maeneoyaliyo karibu na mashamba ya miti ili kuongeza ajira kwawananchi wanaoishi karibu na mashamba hayo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Adadi.

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: MheshimiwaMwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa NaibuWaziri, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza utaratibu huoambao wa kuwauzia watu binafsi kwa makubaliano kwaasilimia 70 na huu wa asilimia 30 kwa kupeleka kwenyemnada hautumiki kabisa. Labda wanatumia asilimia 100wanapeleka kwenye mnada. Kitendo hiki kimefanya vileviwanda vidogo vidogo Muheza pale, karibu viwanda kumivyote vimekufa na ajira ambayo kila kiwanda kilikuwakinachukua labda watu kutoka 100 – 150 wote kukosa kazi.

Sasa nataka kumuuuliza Mheshimiwa Waziri, kwa niniwasirudishe ule utaratibu ambao ulikuwepo wa hiyo asilimia70 kwa makubaliano ili wale wenye viwanda vidogo vidogoambao wanatunza ile misitu(tiki) pale waweze kupata ajirana kuendelea kupata morali ya kuanza kutunza?

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ni kwa nini hata waleambao wananunua kwa mnada ambao utakuta anakujatajiri mmoja ananunua mitiki yote pale. Sasa ni kwa nini nayeye asilazimishwe kutengeneza kiwanda cha kukata ile mitikipale pale Muheza kwa sababu hayo ni madaraka ambayoanayo Waziri kufuatana na regulations ambazoanazitengeneza? Nakushukuru Mheshimiwa Waziri.

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi,muda wetu umekwisha.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALI: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli kabisa kwamba ukiuza kwa njia yamnada wananchi wengi wanakuwa hawana uwezo wakushinda ndiyo maana tumeweka utaratibu kwamba niasilimia 30 ndiyo itakayouzwa kwenye mnada. Asilimia 30itategemeana na makubaliano binafsi, maana yaketunafuata bei ile iliyokuwa na mnada, tunaangalia viwandavyote vilivyoko katika eneo husika. Wale wote wanaohitajiwanapeleka maombi na wanapatiwa ili waweze kujijengeauwezo na kuweza kuzalisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala la pili ambaloamesema kwamba tumshauri huyu atakayekuwa ameshindaaweze kuwekeza katika eneo husika mimi nafikiri ni ushaurimzuri. Tutalifanyia kazi mara tutakapopata mudahusika.Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante, Wizara ya Madini MheshimiwaNjalu Daudi Silanga kwa niaba, Mheshimiwa Kiswaga.

Na. 50

Kuzifutua Leseni Kampuni za Wachimbaji WasiofunguaMigodi

MHE. KISWAGA B. DESTERY (K.n.y. MHE. NJALU D.SILANGA) aliuliza:-

Maeneo mengi yamefanyiwa utafiti na kampuni zakigeni kwa muda mrefu bila kufikia hatua ya kufungua migodi.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuzifutia lesenikampuni hizo na kuwapatia wachimbaji wadogo wadogo?

NAIBU WAZIRI WA MADINI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

Kwanza kabisa na mimi kwa sababu nimesimamahapa kwa mara yangu ya kwanza nimshukuru MwenyeziMungu kwa kunipa nafasi hii kufika hapa leo. Vilevilenimshukuru pia Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwakuniamini na kuniweka katika Wizara hii mpya. Vilevilenimshukuru Mheshimiwa Spika, Wabunge wote na Wajumbewa Kamati ya Viwanda na Biashara kwa malezi yao mazurina kunifikisha hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo napendasasa kujibu swali la Mheshimiwa Njalu Daudi Silanga lililoulizwana Mheshimiwa Kiswaga ambaye ni Mbunge wa Magu kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Madini ya mwaka2010 na kanuni zake inatambua umiliki wa leseni za utafutajimkubwa wa madini na uchimbaji mdogo wa madiniinayotolewa kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulingana na Sheria yaMadini ya mwaka 2010 kama ilivyorekebishwa mwaka 2017,leseni za utafutaji wa madini aina ya metali, viwandani nanishati (makaa ya mawe na urani) hutolewa kwa muda wamiaka minne ya awali na kuhuishwa kwa mara ya kwanzakwa miaka mitatu na mara ya pili kwa miaka miwili. Hivyoleseni ya utafutaji mkubwa wa madini ya aina hizo hubakihai kwa kipindi cha miaka tisa. Aidha, leseni za utafutaji wamadini na vito na ujenzi hutolewa kwa mwaka mmoja nahaziwezi kuhuishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, iwapo mmiliki wa leseniatashindwa kuendesha shughuli za utafutaji wa madini, leseniyake hufutwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka2010 na Marekebisho yake ya mwaka 2017. Aidha, katikakipindi cha mwaka 2014/2015 hadi 2016/2017 jumla ya leseni423 za utafutaji wa madini zilifutwa ambapo mwaka 2014/2015 zilifutwa leseni 2013, mwaka 2015/2016 zilifutwa leseni155 na mwaka 2016/2017 zilifutwa leseni 65.

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la leseni lililofutwahutathminiwa na Wakala wa Jiolojia yaani Geological Surveyof Tanzania (GST) kwa ajili ya kutengwa kwa wachimbajiwadogo endapo litaonekana kuwa na mashapo yenye tija.Katika kipindi cha mwaka 2014/2015 hadi 2016/2017 jumlaya maeneo 19 yenye ukubwa wa jumla takriban hekta69,652.88 yalitengwa kwa wachimbaji wadogo katikamaeneo mbalimbali nchini.

Aidha, Serikali itaendelea kufuatilia na kujadiliana nakampuni zilizomiliki leseni za utafutaji wa madini ili kuonauwezekano wa kuachia baadhi ya maeneo yanayofaa kwauchimbaji mdogo.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Kiswaga.

MHE. KISWAGA B. DESTERY: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali.

Kwa kuwa Serikali imekiri kufuta leseni 423 yenye eneola hekta 69,652.88; je, Serikali iko tayari kuwapatia wachimbajiwadogo wadogo eneo hili ambalo limefanyiwa utafiti iliwaweze kujiajiri na kujipatia ajira na waweze kulipa kodistahiki?

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, je, Serikali iko tayarikuwanunulia vifaa vinavyohusiana na wachimbaji wadogowadogo ili waweze kukodisha kuliko ilivyo sasa wanachimbabila utaalam na vifaa vinavyostahili?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.Waheshimiwa tutakuwa hatuna tena maswali ya nyongezakutokana na muda.

NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,swali la kwanza ni kwamba Serikali iko tayari kuwasaidiawachimbaji wadogo. Imekwisha kutenga maeneo 11ambayo yana jumla ya hekari 38.9 kwa ajili ya wachimbajiwadogo wadogo. Kwa hiyo, kwa maeneo haya ambayoyamesharudishwa Serikalini, Serikali itaendelea kufanya

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

mpango wa kuweza kuwapatia wachimbaji wadogowadogo ili waweze kuchimba na wao waweze kupata faidana waweze kunufaika na madini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wachimbajiwadogo kupitia ruzuku iliyokuwa inapitia SMMRP ambayoilikuwa inatoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo na wadauwengine wa uchimbaji iliweza kutoa fedha ili kuwezakuwasaidia wadau waweze kununua vifaa kwa ajili yauchorongaji, kufanya utafiti na kuweza kusaidia walewachimbaji wengine wadogo wadogo kwa kukodisha. Lakinivilevile STAMICO ambayo iko chini ya Wizara ya Madinipamoja na GST na yenyewe ina juhudi za dhati kabisakununua vifaa ambavyo wachimbaji wadogo watakuwawanakodisha ili waweze kujua mashapu yaliyopo ni mashapuambayo yana faida ambayo wanaweza wakachimba nawakapata uchimbaji wa tija ili kujiondoa katika ule uchimbajiambao wanachimba kwa kubahatisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo Serikali iko pamoja nawachimbaji wadogo. Ahsante sana.

MWENYEKITI: Ahsante, ameshakuelewa. Ahsante.Wizara ya Nishati, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, kwa niabayake, Mheshimiwa Mchengerwa.

Na. 51

Hitaji la Transfoma Maeneo ya Munguatosha na Hondogo

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA (K.n.y. MHE.RIDHIWANI J. KIKWETE) aliuliza:-

Maeneo ya Munguatosha na Hondogo ni baadhi yamaeneo ambayo yanahitaji transfoma ili umeme uwake.

Je, Serikali ina mpango gani juu ya kupelekatransfoma katika maeneo hayo?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali laMheshimiwa Ridhiwani Jakaya Kikwete, Mbunge wa Chalinzekama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kij i j i cha Hondogokimewekwa katika mradi wa REA Awamu ya III kupitia Mradiwa Densification Awamu ya Kwanza ulioanza mwezi Machi,2017 unaotekelezwa na kampuni ya STEG. Mkandarasi tayariamesimamisha nguzo 111 na kuvuta waya wenye urefu wakilometa 4.5. Hatua inayofuata ni ufungaji wa transfomayenye uwezo wa kVA 50 itakayofanyika mwishoni mwakamwezi Novemba, 2017. Wateja wapatao 65 wanatarajiwakuunganishiwa umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kitongoji cha Munguatoshakilichopo katika Kiji j i cha Makore kimejumuishwa nakitapatiwa umeme kupitia REA awamu ya III chini ya Gridextension utakaotekelezwa na kampuni ya SengeremaEngineering Group Limited.

Kazi ya kupeleka umeme katika Kitongoji chaMunguatosa inajumuisha ujenzi wa njia ya umeme wamsongo wa kilovoti 0.4 yenye urefu wa kilometa mbili, ufungajiwa transfoma yenye uwezo wa kVA 50 pamoja nakuunganisha wateja wapatao 46. Utekelezaji wa mradi huuulianza mwezi Julai, 2017 na utakamilika mwezi Juni, 2019.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mchengerwa.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaMwenyekiti, kumekuwepo na kilio kikubwa sana cha mahitajiya umeme Kata ya Mkange pale Chalinze ukizingatia kuwasehemu hii inachangia kwenye uchumi wetu wa Taifa hususankatika Wilaya ya Bagamoyo, pia na Halmashauri ya Chalinzena Tanzania kwa ujumla hususan katika viwanda pamoja nautalii.

Je, Serikali inajipangaje kusaidia wananchi pamojana wawekezaji wa viwanda umeme ili kupunguza ukali wamaisha wa eneo hili la Kata ya Mkange? (Makofi)

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi mkubwa wa StiglersGorge unadhamiria kuikomboa nchi yetu katika umemehususan katika viwanda vinavyojengwa pamoja na treni hiiya umeme.

Je, Serikali inawaachaje wananchi wa Jimbo la Rufijiambao wametunza bwawa hili pamoja na Mto Rufiji kwamiaka mingi sana hususan wakazi wa Kata ya Mwaseni,Kipugira, Ngorongo na Mkongwa? (Makofi)

MWENYEKITI: Hilo swali umechomekea lakini Wazirilijibu.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nashukuru kwa maswali mawili ya nyongeza yaMheshimiwa Mbunge Mchengerwa na naomba nimpongezekwa jitihada zake za kufuatilia changamoto mbalimbali zanishati katika jimbo lake pamoja na muuliza swali la msingi.Ameuliza swali juu ya mahitaji ya umeme kwenye Kata yaMkange iliyoko Jimbo la Chalinze na ni kweli Kata hii yaMkange imepakana na Mbuga ya Saadani.

Naomba nimtaarifu kwamba katika mradi ambaounaendelea waUrban Peri Urban Edification Project of CoastRegion na Kigamboni – Kata ya Mkange itapata umemekupitia Miono. Kwa hiyo, naomba nimtaarifu kwamba Serikaliimezingatia na kwa kuwa ina dhamira kwamba kila kijiji ifikapo2020/2021 kipate umeme kwa hiyo Kata ya Mkange itapataumeme kupitia Miono.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ameuliziasuala la Stiglers Gorge. Naomba nilitaarifu Bunge lako Tukufuni kweli Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi waMheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kwadhati kuongeza upatikanaji wa nishati nchini kwetu naimedhamiria kwa dhati kutekeleza mradi huu ambaoutaongeza megawati 2100, tender imeshatangazwa na zaidiya makampuni…

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

Mheshimiwa Mwenyekiti, na nimtaarifu tu MheshimiwaMbunge kwa kuwa mradi huu unatekelezwa katika maeneoya Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Pwani eneo la Rufiji Kataalizotaja Mwaseni na Ngorongo ni Kata ambazo ni kwelizimetunza bwawa hil i na zitafaidika kwanza kupitiaupatikanaji wa nishati hii ya umeme lakini pia kupitia ajiraambazo zitapatikana kipindi cha ujenzi wa bwawa hili, lakinitatu, Wilaya hii ya Rufiji imekuwa ikikumbwa na mafuriko yamara kwa mara. Kupitia ujenzi wa bwawa hili ni dhahirikwamba ule uhifadhi wa maji utasaidia kuzuia masuala yamafuriko katika maeneo haya.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, ahsante!

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: …lakini langu lingine piaujenzi wa bwawa hili litasaidia shughuli za kilimo chaumwagiliaji kwa maeneo yale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. NaombaWatanzania muamini mradi huu unatekelezwa kwa pesa zandani za nchi yetu. (Makofi/Vigelegele)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea.Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa PascalHaonga.

Na. 52

Vigezo Vinavyotumika Kupata Mikopo Elimu ya Juu

MHE. PASCAL Y. HAONGA aliuliza:-

Kigezo kimojawapo cha kuwanyima mkopowaombaji wa mkopo ya elimu ya juu ni kama muombajialisoma shule za binafsi.

(a) Je, Serikali haioni kuwa baadhi ya wanafunzihulipiwa ada ya shule za binafsi na ndugu, jamaa, marafikina NGO’s hivyo wanafunzi hao wanapofikia elimu ya juuhushindwa kumudu gharama za elimu hiyo?

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

(b) Je, Serikali ipo tayari kufuta kigezo hicho ilikuwapatia waombaji wa mikopo haki yao ya kupata elimuya juu?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia naomba kujibu swali laMheshimiwa Pascal Yohana Haonga Mbunge wa Mbozilenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, sifa za msingi za kupatamkopo wa elimu ya juu zinaainishwa katika kifungu cha 17(1)cha Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juuya 2004 (Sura ya 178) ya Sheria za Tanzania kama ifuatavyo;awe Mtanzania, awe amedahiliwa kwenye chuokinachotambulika, awe ameomba mkopo kwa njia yamtandao, awe hana chanzo kingine cha kugharamia elimuyake. Mbali na sheria, vigezo vingine ni uyatima, ulemavu,uhitaji na mahitaji ya rasilimalwatu kwa ajili ya vipaumbelevya maendeleo vya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa kuwasilishamaombi ya mkopo wa elimu ya juu muombaji hutakiwakuwasilisha taarifa muhimu zikiwepo shule au vyuo alivyosomakabla ya kujiunga na elimu ya juu. Bodi ya Mikopo hutumiataarifa hizi ili pamoja na mambo mengine kubaini historia yauchangiaji wa gharama za elimu katika ngazi ya sekondariau chuo ili kumpangia mkopo stahiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale inapothbitika kwamaandishi kwamba mwanafunzi husika alisaidiwa aukufadhiliwa na ufadhili huo umekoma Bodi ya Mikopohuwakopesha kwa kuzingatia hali zao za kiuchumi kwa wakatihuo. Kwa mfano, katika mwaka wa masomo wa 2016/2017jumla ya wanafunzi 719 waliothibitika kufadhiliwa aukusaidiwa katika masomo yao ya sekondari walipata mkopo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Haonga.

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

MHE. PASCHAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, siku za hivikaribuni tumeisikia Bodi ya Mikopo imeongeza masharti auvigezo vipya kwa wakopaji, kwa mfano wale viongoziwanaojaza fomu za maadili ya viongozi wa umma wakiwepoMadiwani nao pia ni miongoni mwa watu ambao watotowao wananyimwa mikopo. Kwa kuwa tunajua kabisakwamba Madiwani hawana mishahara na wanategemeaposho ambayo ni kidogo sana je, Serikali haioni kwamba,huu ni unyanyasaji ambao kwa namna yoyote hauvumilikina hitakiwi kuufumbia macho unaofanywa na Bodi yaMikopo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, siku za hivikaribuni wote tunajua kabisa kwamba Bodi ya Mikopoimeongeza makato kwa wanufaika wa mikopo. Kwa mfanoawali ilionekana kwamba, wanufaika wa mkopo walikuwawanalipa wanarejesha asilimia nane ya mkopo waliokuwawamekopa kwa maana ya makato ya asilimia nane, lakinikwa sasa wanakatwa asilimia 15. Hali hii imesababisha walewanufaika wa mkopo kama walimu na watumishi mbalimbaliambao walikuwa wamebakisha fedha kidogo ambazowalikuwa wanapata mwisho wa mwezi, leo hawanamshahara hata kidogo na kuna watumishi wanaacha kazi.Je, Serikali haioni ni wakati muafaka sasa kurudi kwenyeasilimia nane ya makato, ili angalao watumishi hawawaliocha kazi waweze kurudi makazini na maisha yawezekwenda vizuri? Ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupisana.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NAUFUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli alivyosemakwamba katika mwaka huu wa masomo kuna vigezovimeongezwa kwa ajili ya watu ambao hawastahili kupatamikopo, ikiwa ni pamoja na viongozi wa umma wanaojazafomu za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma. Lengo

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

la kufanya hivyo ni kwamba, tunajaribu kuhakikisha kwambamkopo ule unatumika kwa wale ambao hawana uwezokabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kuhusu Madiwanikama wana uwezo au hawana uwezo tunajaribu kuangaliakipato chao wanachoweza kupata kwa mwaka nakulinganisha na Watanzania wengine wengi ambao hawanakipato kabisa. Kwa hiyo, lengo ifahamike tu ni kwamba nikujaribu kutoa fursa kwa wale ambao hali yao ni mbaya zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hitaji la sasa lakwamba waombaji wa mikopo ambao wanatakiwakurudisha wanakatwa asilimia 10 inatoka kwenye mshahara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nilifahamisheBunge lako Tukufu kwamba mkopo ule ukishachukua kigezocha pekee cha kwamba unatakiwa kurudisha fedha nikwamba wewe umekopa, maana yake ilitakiwa paleunapomaliza shule uanze kurudisha.

Sasa kwa muda mrefu sana ule mkopo umekuwaunashindwa kuwanufaisha watu wengi kwa sababu watuwengi hawarudishi na ndio maana sasa tumelazimishakwamba, ni lazima kwamba, mtu ambaye atakuwaamepata ajira aweze kulipa kwa asilimia 15 ya mshaharawake, lakini vilevile kuna kigezo kingine ambacho tumewekakwamba, tunatoa kipindi cha mpito au grace period ya miezi24 toka mwanafunzi amalize shule, lakini baada ya hapokama hajaanza kulipa tunaanza vilevile kutoza riba ya asilimia10. Lengo ni kwamba tunahitaji kuufanya mfuko ule uweendelevu ili wananchi wengi waweze.

Waheshimiwa Wabunge nafahamu kuna baadhiambao nao wanadaiwa mikopo, katika siku hizi za karibunitunakuja na orodha ya wale ambao ni wadaiwa sugu. Kwahiyo, nawaombeni ushirikiano…

MWENYEKITI: Mheshimiwa waandikie barua, inatosha.

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

Tunaendelea Wizara ya Kilimo. Mheshimiwa MartinMtonda Msuha, Mbunge wa Mbinga Vijijini.

Na. 53

Kushuka kwa Uzalishaji wa Zao la Kahawa

MHE. MARTIN M. MSUHA aliuliza:-

Kwa takwimu za miaka ya hivi karibuni uzalishaji wakahawa Wilayani Mbinga umeonekana kushuka kwamkulima mmoja mmoja (out growers). Na sababu mojawapoya kushuka kwa uzalishaji huo ni kuzeeka kwa miti ya kahawa.

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapelekeawakulima wa Mbinga mbegu mpya ili kuinua uzalishaji?

(b) Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka mnadawa kahawa Wilayani Mbinga, badala ya minada hiyokuendelea kufanyika Moshi?

(c) Je, Serikali ina mkakati gani wa kupiga marufukukabisa uuzaji wa kahawa mbichi ikiwa shambani, maarufukama “magoma” Wilayani Mbinga?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waKilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Martin Msuha,Mbunge wa Mbinga, swali lenye sehemu (a), (b) na (c), kamaifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa Serikali wakuwapelekea wakulima wa Mbinga mbegu mpya ili kuinuauzalishaji ni kwa kutekeleza mpango mkakati wa kuendelezazao la kahawa kwa miaka kumi (2011 – 2021). Katika mpangohuo utafiti na usambazaji wa miche bora, ili kuondokana namiche yenye tija duni na iliyo zeeka ni mojawapo yakipaumbele. Utekelezaji wake unafanyika kwa kushirikianana wadau, hususan Tanzania Coffee Research Institute

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

(TaCRI). Kituo cha utafiti na uzalishaji miche cha Uganokilichoko Wilayani Mbinga katika mwaka 2016/2017 kilizalishana kusambaza miche bora ya kahawa 270,869 na kaziinaendelea. Aidha, Mfuko wa Maendeleo ya Kahawa(Tanzania Coffee Development Fund) umefadhili nakupunguza bei kutoka shilingi 300 kwa mche mmoja hadishilingi 150 kwa vituo vyote nchini vilivyoko chini ya TaCRI ilimiche hiyo isambae kwa kasi.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, mnada wa kahawahuendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Kahawa Namba 23ya mwaka 2001. Serikali haina mpango wa kuanzisha Soko laMnada wa Kahawa - Mbinga au mahali pengine nchini kwasababu, uwepo wa miundombinu ya mashine ya kielektronikiya kuendesha mnada iliyopo Moshi, maabara ya kuonjeakahawa, wataalam wa kuendesha mnada hu, gharama zamnunuzi ambapo atalazimika kwenda katika kila mnada,kama utawekwa kila mahali ambapo kahawa inazalishwauzoefu unaonesha kuwa nchi nyingi duniani huweka mnadasehemu moja tu, ili kurahisisha uendeshaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, tangu kuanzishwakwake kabla ya uhuru mnada uliwekwa Moshi kwa kuwandiko kulikua na wanunuzi na biashara ukilinganisha namaeneo kama Kagera, ingawa uzalishaji unafikia hadi asilimia40 ya nchi nzima. Mnada unauza kahawa ikiwa kwenyemaeneo ya uzalishaji kwa mfano kule Mbinga na Mbeya, n.k.KInachopelekwa Moshi ni sampuli tu kwa ajili ya uonjaji.

Aidha, Serikali imeanzisha soko la bidhaa (CommodityExchange) ili kupunguza gharama za uendeshaji wa masokoya mazao ikiwemo kahawa.

(c) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa KifunguNamba 29(ii) cha Kanuni za Kahawa 2013, ni kosa kwa mtuyeyote kununua matunda ya kahawa (ripe cherry) kwa hiyo,Serikali inakataza biashara ya kahawa mbichi. Naomba nitoeagizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga na Mkoa wa Ruvumakwa ujumla, wote kwa pamoja na wahusika wengine wotekwamba, hairuhusiwi kabisa uuzaji wa kahawa mbichi.

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

MWENYEKITI: Mheshimiwa Martin.

MHE. MARTIN M. MSUHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali,ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, jambomojawapo linaloyumbisha uzalishaji wa kahawa hususanMbinga, ni kutokuwa na bei ya uhakika mwaka hadi mwaka.Je, Serikali haioni umuhimu wa kuanzisha mfuko wa kuimarishabei ya mazao hususan kahawa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. MheshimiwaNaibu Waziri yuko tayari kuambatana na mimi baada yamkutano huu, ili akajionee mwenyewe ni jinsi gani utekelezajina uzambazaji wa miche mipya ya kahawa unavyofanyikana Kituo cha TaCRI - Ugano, kama ilivyojibiwa kwenye swalila msingi? Ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupisana.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti,awali ya yote naomba nimpongeze sana MheshimiwaMbunge wa jimbo hilo kwa ajinsi ambavyo anafuatilia kwaukaribu sana katika zao zima hili la kahawa katika Jimbo lake.Lakini nikija katika swali lake la (a) ni kwamba, sisi kama Wizarakupitia Bodi ya Kahawa tunatoa bei elekezi kwa wakulimawale wadogowadogo wote kwa maana ya kwamba, farmgate market kwamba wawe wanapata bei elekezi kupitianjia ya mtandao wa simu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini vilevile tumegunduakwamba, njia hii ya mtandao wa simu iko more effectiveukilinganisha na ile minada mingine, lakini hii tunaifanya kilawiki. Lingine naomba nitoe rai hata kwa wakulima walewadogowadogo wote katika mashamba kwamba,wanapaswa wazingatie sana ubora wa zao hili la kahawa.

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine vilevile kuleMoshi ambako tunafanya mnada, huu mnada kule Moshihatuwezi tukafanya kwa bei elekezi kwa sababu, mnada wakule unategemea sana soko la dunia na kwa maana hiyo,soko la dunia inategemea na wakati wa ile market priceiliyoko wakati huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho naombanimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba niko tayarikuongozananae kwenda kujithibitishia zao la kahawa.Ahsante.

MWENYEKITI: Hilo la mwisho ndio muhimu, muendewote hilo.

Waheshimiwa Wabunge, maswali yamekwisha. Swalila maji limetuchukulia muda mwingi sana. Sasa ni muda wamatangazo, wageni waliopo Bungeni asubuhi hii wageni waWaheshimiwa Wabunge.

Wageni 30 wa Mheshimiwa Jenista Mhagama,Mbunge na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, ambao ni vijanawawakilishi kutoka Wilaya za Kibaha, Temeke, Mtwara, Ilala,Lindi na Kilombero wanaojishughulisha na Mradi waUwezeshaji Vijana Kiuchumi unaofadhiliwa na Jumuiya yaUlaya na kusimamiwa na Shirika la Plan International. Karibunisana. (Makofi)

Pia kuna wageni 108 wa Mheshimiwa AntonyMavunde Mbunge na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuuambao ni wanafunzi 103 wa kidato cha sita na walimuwatano kutoka Dodoma Secondary School Mkoa waDodoma. Karibuni Dodoma. (Makofi)

Kuna wageni kumi wa Waheshimiwa WabungeEdward Mwalongo na Joram Hongoli, ambao ni walimu nanena wanafunzi wawili kutoka Mkoa wa Njombe. KaribuniBungeni. (Makofi)

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

Wageni 11 wa Mheshimiwa Jitu Soni (Mbunge),ambao ni watendaji walioko masomoni, wanatokea Babati,Mkoa wa Manyara. Karibuni.(Makofi)

Wageni 36 wa Mheshimiwa Vedastus Manyinyi,ambao ni viongozi na wachezaji wa timu kutoka Mkoa waMara, wakiongozwa na Ndugu Issa Salote. Karibuni Dodoma.(Makofi)

Mheshimiwa Joyce Sokombi anaombakumtambulisha mgeni wake anaitwa Lucy Miliga kutokaIringa, karibu. (Makofi)

Kuna tangazo Waheshimiwa Wabunge, MheshimiwaMussa Hassan Mussa Mbunge, Jimbo la Amani anaombakuwatangazia Waheshimiwa Wabunge wote kuwa uongoziwa Fantasy Village unawaalika Waheshimiwa Wabunge wotekwenye sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la Hoteli yaFantasy Village iliyopo Msalato Senje, kwa Mwinyi, kesho sikuya Jumamosi, tarehe 11 Novemba, saa 04:00 asubuhi katikaviwanja vya hoteli hiyo. Aidha, mgeni rasmi katika sherehehiyo ni Mheshimiwa Job Yustino Ngugai Mbunge, Spika,waBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mnaombwawote kuhudhuria bila kukosa. Karibuni sana, ahsanteni.(Makofi)

Tangazo la semina; Waheshimiwa kesho Jumamosi,tarehe 11 Novemba, kutakuwa na semina kwa Wabungewote kuhusu Muswada wa Sheria ya Wakala wa Meli kwamwaka 2017 (The National Shipping Agency Bill, 2017). Seminahiyo, itafanyika katika Ukumbi wa Msekwa kuanzia saa 04:30asubuhi. Na Jumapili, terehe 12 Novemba, 2017 kutakuwana semina kwa Wabunge wote kuhusu Kampuni ya MaxcomAfrica Plc, Max Malipo. Semina hiyo pia itafanyika katikaUkumbi wa Msekwa na itaanza saa 05:00 asubuhi, Wabungewote mnakaribishwa.

Katibu.

MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH - KATIBU MEZANI:Hoja za Serikali.

MWENYEKITI: Ngoja, ngoja.

MHE. MBUNGE FULANI: Mwongozo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chumi pamoja na Msigwa,wawili tu leo.

Mheshimiwa Amina, kaa please.

Waheshimiwa saa 5:15 asubuhi hii, saa nyinginemaswali yanakuwa mengi ya nyongeza yanatuchukuliamuda mwingi sana kwa hiyo, tuvumiliane.

Mheshimiwa Chumi.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Nilikuwa naomba Muongozo kutokana na jambolililotokea leo kutoka swali namba 52.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna taasisi moja imetoamatangazo ya kwamba wanafunzi waliokosa mikopowatapata mikopo wa-apply kwenye hiyo taasisi naapplication fee ni shilingi 30,000.

Sasa nilipenda kufahamu u-genuine wa hii taasisi,what suppose watoto wakalipa hiyo shilingi 30,000, let saywamelipa watoto 10,000, wamepata karibu milioni 300, halafumwisho wa siku taasisi ikaja kutoa mikopo kwa watu kumi.Kwa hiyo, nilitaka nifahamu Muongozo wa Serikali howgenuine is that taasisi inayotaka kutoa mikopo? Ahsante.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Msigwa.

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikushukuru kwa kunipa nafasi. Nimesimama hapa kwaKanuni ya 47.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni Serikali yaTanzania imechoma vifaranga 6,000 vya mfanyabiashara waKitanzania alivyovinunua kutika Kenya kinyume kabisa naWildlife Act ya 2008 ya Haki za Wanyama. Na kama vilehaitoshi ng’ombe wa Kenya 1,300 waliokuja Tanzaniawalitaifishwa na Serikali wakanadiwa kwa wastani wang’ombe mmoja kunadiwa kwa shilingi 71,000. Na hivi karibunitumemsikia Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, AminaMohamed, akilalamika juu ya mahusiano mabaya yakidiplomasia ambayo tunayafanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikimnukuu Rais Kikwetewakati anaondoka madarakani, ilikuwa tarehe 6…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa, nenda kwenyehoja moja kwa moja.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ndio naenda, naomba univumilie kidogo, samahani. Ilikuwatarehe 06/10/2015 alisema; “Naondoka nikiwa naachauhusiano wa Kenya na Tanzania ukiwa mzuri kuliko wakatimwingine wowote, nina uhakika hautabadilika labda tupatempumbavu kwelikweli na wa ajabu sana, ambapo kwaTanzania watu wapo wachache sana wa aina hiyo.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala ya mahusiano nanchi j irani ni ya muhimu kwa aji l i ya biashara namatengamano ya kimahusiano. Jambo hili limekera sana nalinaharibu mahusiano yetu na Kenya. Na Wakenyawamekamata ng’ombe 4,000 lakini kwa sababu yamahusiano wanaona wasiwanadi kama ambavyotumefanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naomba hili jambotulijadili kama jambo la dharura, ili tujenge mahusiano na nchi

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

nyingine kwa ajili ya ustawi wa jamii yetu. Naomba kutoahoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, kaeni kwanza.Bunge hili linaendeshwa kwa Kanuni Mheshimiwa Msigwa,Waheshimiwa Wabunge. Mambo ambayo Kanuni uliyotumiani jambo lililotokea mapema Bungeni, ambalo umekiukaKanuni hiyo. Umeleta jambo nje ya Kanuni hiyo, saa nyinginehuwa tunavumilia sababu tunataka Wabungetunapowakubalia linapohusu majimboni mwenu, ili na ninyimpumue, i l i wapiga kura wenu wawasikie namnamnavyowatetea.

Sasa Mwongozo huu, hoja yako wewe…

MBUNGE FULANI: (Hapa hakutumia kipaza sauti).

MWENYEKITI: Aah, sasa si ndio nakuja na nini.

MBUNGE FULANI: (Hapa hakutumia kipaza sauti).

MWENYEKITI: Sawa. Sasa mimi sijaliona kama linaudharura kwa kipindi hiki. Nitakuomba ulichukue ulipelekekwenye Kamati inayohusika, ili wakalijadili wao na waowatakupa majibu.

Waeshimiwa Wabunge, hili suala la elimu Serikali hebulijibuni.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI:Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa yakutoa ufafanuzi kuhusiana na taasisi ambayo inajiita Mfukowa Elimu ya Juu (Tanzania Social Support Foundation)ambayo ni kweli imekuwa ikitoa matangazo kwamba inatoamikopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba Wizarayangu haiitambui hiyo taasisi na nieleze kwa masikitikokwamba nimepewa gazeti sasa hivi ambalo linaoneshatangazo kwamba hii taasisi inawatangazia wanafunzi na

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

inawachaji shilingi 30,000 na wanasema watakuwa namkutano ambao mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Elimu,Profesa Joyce Ndalichako. Siitambui hii taasisi,hawajanikaribisha na tarehe ya huo mkutano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nitumie fursa hiikutoa tahadhari kwa Watanzania kwamba wawe makini kwasababu unapoona mtu anatumia jina lako kabla hatahajafika kwako, ni jambo ambalo kama Serikali nisemetumelipokea tutalifanyia kazi, ili kujua uhalali wake. Na kwakipindi hiki nitoe tahadhari kwa watu ambao wataamuakulipa hizo shilingi 30,000, wafanye lakini wajue kwambaSerikali haihusiki na jambo hili. Nashukuru.

MWENYEKITI: Ahsante. Katibu.

NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH - KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifaunaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na

Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwaMwaka wa Fedha 2018/2019

MWENYEKITI: Katibu.

NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH - KATIBU MEZANI:Kamati ya Mipango.

KAMATI YA MIPANGO

(Majadiliano Yanaendelea)

MWENYEKITI: Tukae.

Waheshimiwa tunaanza na ratibab yetu ya Mipangona tunaanza na Mheshimiwa Nape, ajiandae MheshimiwaTurky.

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangiakwenye Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa 2018/2019. Pamoja na kazi nzuri na jitihada kubwa ambayoinafanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuletamaendeleo katika nchi yetu. nimepongeze MheshimiwaWaziri, Naibu Waziri na watendaji kwa wizara kwa kazimnayofanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango huu umeletwahapa ili tuuboreshe, tutoe mawazo yetu ambayo yanawezakutumika kuboresha ili tufikie lengo la kuleta maendeleokatika nchi yetu. Na mimi nina amini Waziri na wenzakewatatusikiliza na watachukua mawazo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma hayamapendekezo ya Mpango, utagundua humu ndaniimeorodheshwa miradi mikubwa ya aina mbili; unaweza uka-group unavyoweza lakini iko ya aina mbili. Iko miradi ambayoni ya kihuduma, miradi ambayo inahusiana na maji, afya,elimu, utawala na maeneo mengine. Miradi ambayo kwaasili yake haiendeshwi kibiashara, lakini upande wa pili kunamiradi ambayo kwa asili yake inaweza kuwekezwa nakuendeshwa kibiashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa huu mgawanyo waaina hizi mbili za miradi, niliposoma nilishtuka kidogo kuonaSerikali inapendekeza kuwekeza pesa za Serikali kwenyemiradi ambayo inaweza kuendeshwa kibiashara. Nilitegemeamiradi hii tungeruhusu sekta binafsi, tukatengeneza mazingiramazuri ya sekta binafsi kuwekeza kwenye miradi hii badalaya kuchukua pesa za Serikali na kuipeleka kule kwa sababumadhara yake ni makubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Mpango huuutatekelezwa kama ulivyo, miradi hii inakwenda kuua uchumiwa nchi yetu. Nitatoa mfano, miradi hii mikubwa ambayoninaizungumzia ni miradi kama ya uzalishaji wa umeme nahapa imekuwa ikizungumzwa Stiegler’s Gorge kwa mfano,miradi ya ujenzi wa reli, uboreshaji wa Shirika la Ndege, mradi

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

wa bandari na baadhi ya barabara ni miradi ambayo kwaasili yake inaweza kuwekezwa kibiashara, kuendeshwakibiashara na ikajilipa kibiashara. Sababu ya kuchukua helaza Serikali kupeleka kwenye miradi hii kwa kweli sijaiona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sifa ya miradi hii kwanza nimiradi mikubwa sana, lakini ya pili kwa ukubwa wake ni miradiambayo ina gharama kubwa; ukiingalia ni mabilioni kadhaaya dola kwa asili yake, lakini sifa ya tatu miradi hii niliyoitoleamfano hapa ni miradi ambayo uwekezaji wake utachukuamuda mrefu na hivyo payback period yake ni ya muda mrefusana. Sio miradi ya kulipa kesho, ni miradi ambayo itachukuamuda mrefu kwa vyovyote vile. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi siipingi miradi hiinaomba niweke rekodi vizuri isipokuwa ninapingana namapendekezo ya Serikali ya namna ya kuiwekeza nakuiendesha miradi hii kwa kutumia pesa za Serikali. Tafsiri yauamuzi wa kutumia pesa za Serikali kwenye miradi hii ni hiiifuatayo:-

Moja, itailazimisha Serikali kukopa hela nyingi kwavyovyote vile kwa sababu ni miradi mikubwa, gharama yakeni kubwa, kwa hiyo ni lazima Serikali iende ikakope. Serikaliikienda kukopa na kwa sababu miradi hii inachukua mudamrefu, maana yake ni moja tutaanza kulipa deni hilolililokopwa kabla ya miradi hii haijaanza kulipa faida kwa nchiyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na tafsiri yake ni kwambatutachukua hela kwenye maeneo mengine tuilipie denimiradi hii. Hapo maana yake ni kwamba tutaendeleakufunga mikanda muda mrefu, sasa tunafunga mkanda kwanini? Ndio maana nahoji kwa nini Serikali inafikiri kwambakuwekeza pesa za Serikali kwenye miradi ambayo ingewezakuwekezwa kibiashara na sekta binafsi ni jambo la tija kwauchumi wa nchi yetu, mimi nadhani hapana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa vyovyote vile ukichukuapesa za maeneo mengine maana yake utaathiri maeneo

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

hayo, maana yake utaathiri miradi ile ya huduma kama maji,afya, elimu na utawala na mtafika mahali hata malimbikizoya wafanyakazi itashindikana kulipa kwa sababu tunachukuapesa za Serikali kuzipeleka kwenye miradi ambayo ingewezakujiendesha kibiashara. Kwa hiyo, mimi nadhani hili la kwanzasio sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna madharamakubwa kwa Deni la Taifa kuchukua hela za Serikali ambazonyingi kama nilivyosema itabidi tuzikope kuziwekeza kwenyemiradi hii. Na hapa Waheshimiwa Wabunge nataka twendekwa takwimu vizuri kwa mahesabu na ndipo hapa ninapohojiuzalendo wa wachumi wetu kuishauri Serikali na MheshimiwaRais kuwekeza hela za Serikali kwenye miradi hii, hapa miminapata taabu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa ripotiuliyotupa hapa Mheshimiwa Waziri, deni letu la taifa limefikiadola bilioni 26 ambayo ni sawa na asilimia 32 ya ustahimilivuwa deni la taifa. Ukomo ni asilimia 56, sasa kama 26imetupeleka kwenye 32 unahitaji dola bilioni 45 kufikia ukomowa asilimia 56 ambayo ni mwisho wa kukopesheka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa twende tuchukuemfano wa miradi mitatu, acha miradi mingine yote kwambahatukukopa, hatukukopa maji ambayo tunachukua hela zawahindi, hatukukopa kwenye barabara, elimu na walakwenye umeme na maeneo mengine yote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu chukua miradi mitatu;mradi wa kwanza ni mradi wa ujenzi wa reli ya kati ambaokwa tathmini yake unaweza ukagharimu approximately dolabilioni 15, ziweke dola bilioni 15, chukua mradi wa Stiegler’sGorge wa uzalishaji wa umeme ambao kama ninavyosemaleo ukikohoa wawekezaji wanakuja, tunataka kuweka helaza Serikali, dola bilioni tano, jumla 15 na tano unapata dolabilioni 20. Halafu chukua uboreshaji wa Shirika la Ndege, kwaujumla wake mpaka umalize karibu dola bilioni moja kwa hiyounazungumzia dola bilioni 21.

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama una dola bilioni26 deni la taifa ukijumlisha dola bilioni 21 maana yakeunazungumzia dola bilioni 47 na ukomo wetu ni dola bilioni45, kwa vyovyote vile hii ime-burst. (Makofi)

Sasa kama inakwenda ku-burst maana yaketunakwenda kutokopesheka, kama tusipokopesheka inamaana gani kwa uchumi wetu? Kwa nini tunatakakung’ang’aniza kuchukua hela ya Serikali na tumeanzakwenye reli na ndege tumeweka na kwenye Stiegler’s nakwenyewe tunakwenda, mwisho wake uitakuwa nini?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nadhani hebu tufikirieupya, hii thinking ya kwamba sekta binafsi tunaiandikakwenye makaratasi kwamba ndio itakayotekeleza mpangohuu, lakini kimsingi kwa matendo yetu tumeiweka pambeni,kwa nini tusiitumie? Awamu ya Pili ya Mzee Mwinyi walianzakuiruhusu sekta binafsi na akatengeneza mazingira,inawezekana kuna mapungufu yake lakini sekta binafsi ilianzakupata mwanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Awamu ya Nne MheshimiwaWaziri Mheshimiwa Rais wa sasa Magufuli alikuwa Waziri waUjenzi. Wakati wake waliruhusu wakandarasi kutoka sektabinafsi wakachukua mikopo ya benki, wakaanzishamakampuni, leo hii tunavyoongea hawa watu mortgage zaozinauzwa. Na zinauzwa kwa kuwa wana madeni wanaidaiSerikali, lakini Serikali imeamua kuanza kuchukua mkondo washughuli zake za ujenzi kutekelezwa na Serikali yenyewe. Kwahiyo, hawa tuliowatengeneza kwa miaka yotetunawakosesha hela sasa, they are starving and they aredying.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu mpango wako mzurindio lakini hebu rudini kwenye thinking ya kuruhusu sektabinafsi kufanya kote, duniani kote mambo yanakwendahivyo. Jana mmesikia mifano hapa na Mheshimiwa Spikaalitoa mfano, Warusi ambao walikuwa waumini wakubwawa ujamaa wameruhusu sekta binafsi mpaka viwanja vya

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

ndege; sisi leo kiwanja chetu cha ndege pale karibu dolabilioni 560 hivi, hela nyingi kweli. Hivi tungeruhusu watu binafsiwakawekeza nani asingekuja pale, kwa vyovyote inalipa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini mradi kama Stiegler’sgorge pamoja na kwamba nauunga mkono, sina hakikakama tumefanya tathmini ya madhara yake ambayoyanatokana na shughuli za kibinadamu zinazoendeleakuuzunguka mradi wenyewe. Tuna miradi mingine ya majihapa nchini ambayoo yote ina-prove failure; tumechukuatahadhari gani katika mradi huu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu huu wa kuaminikwamba Serikali itafanya kazi ya kuzalisha umeme yenyewe,ndio utaratibu unaotesa Mikoa ya Lindi na Mtwara.Tumevunja Mkataba wa Symbion tunasema tutawekezamitambo wenyewe pale, leo Lindi na Mtwara tunakaampaka siku tatu au nne umeme hakuna, maishayanasimama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi kama hali hiyo ingekuwainatokea Dar es Salaam kwamba mnakaa siku tatu/nneumeme hakuna Serikali mngevumilia? Hawa watuwanavumilia hali mbaya lakini kwa sababu gani, tunatakakuwekeza wenyewe kwa kutumia pesa za Serikali kwenyesuala la kuzalisha umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya Serikali ibakikutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji badala ya sisiwenyewe kwenda, tunatumia hela hii kidogo kwa uchumihuu mchanga tunataka tuwekeze kwenye miradi mikubwa.Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mahesabu ya kawaida kabisaMheshimiwa Waziri, mipango hii inakwenda kuua uchumi wanchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi nilitegemeahebu tufikirie upya pesa kidogo tuliyonayo twendenitukaboreshe maslahi ya wafanyakazi, twendeni tukawekezekwenye maji, afya na maeneo mengine ya huduma badala

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

ya kuichukua na kupeleka kwenda kuwekeza kwenye miradiambayo inaweza ikajiendesha kibiashara. Kila siku sisitunapeleka sura mbaya, tunaanza kuonekana kama vilehatutaki sekta binafsi ifanye kazi katika nchi yetu. Utaratibuhuu mbaya utaua uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Nape. MheshimiwaTurky ajiandae Mheshimiwa Mgimwa.

MHE. SALIM HASSAN TURKY: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante na mimi nashukuru kupata fursa leo ya kuwezakuchangia. Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwakutujalia afya, sote tu wazima na tupo katika Bunge hilitukijenga Taifa letu. Pia nachukua fursa hii kumpongeza Raiswetu kwa kufanya maamuzi magumu ya kuongoza Taifa hilina kwa kweli anastahili kila sifa kwa nia yake njema ya kutakakuifanyia Tanzania ya leo iwe ya viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hayo sasa natakaniingie kwenye Mpango. Huu Mpango ni mzuri sana lakini kwakweli heading yake ina matatizo tena ina matatizo makubwasana. na matatizo yake Mpango unasema ni maendeleo yaTaifa lakini nikitazama tafsiri ya taifa siikuti Taifa bila yaZanzibar. Katika mpango huu hakuna sehemu hata mojailiyotaja Wazanzibar na kwa kweli Mpango huu kwa njia mojaau nyingine umetudhalilisha Wazanzibar kama vile hatustahilikupangiwa chochote katika Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, kama ni kosa basinafikiri lirekebishwe kwa kuandikwa kwamba Mpango waMaendeleo wa Tanzania Bara au uandikwe Mpango wa Taifabasi na Taifa la Zanzibar liwekwe katika Mpango huu lakinizero hakuna chochote. Hakuna mahali ilipoandikwa Pemba,Unguja wala Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hil i si jui kamalimefanywa kwa makusudi na kama limefanywa kwa

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

makusudi basi naomba Mheshimiwa Waziri wa Fedhaawatazame sana watendaji wake kwa sababu yeye nimsimamizi wa sera pengine hakuwa na time nzuri ya kusoma,lakini kwa kweli hili limetuangusha sana Wazanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme kwambakuna watendaji wa Serikali ambao kwa kweli hawaitendeihaki Zanzibar na hasa katika mambo ya kufanya biasharabaina ya Zanzibar na Bara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati zilizopita tulipatabahati ya kutembelea mipaka yetu, tulikwenda mpaka waSirari tukaona wafanyabiashara wadogo sana kilamfanyabiashara ana baiskeli ya rally nzuri madhubuti, lakinikazi yake yeye akiamka asubuhi anasukuma baiskeli kupitaboarder anakwenda zake Kenya anachukua dumu la mafutaanaleta, akimaliza kinachotakiwa Kenya anakichukua kwabaiskeli anaenda zake anapeleka na hakuna anayemuulizakwa sababu ni mwananchi anayeishi maeneo yale, kwahivyo, biashara hiyo inafanyika kwa baiskeli lakini unawezakukuta ikifika jioni basi canter zima mtu kapenyeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi upande wa Zanzibar, leomiaka saba mimi nipo katika Bunge hili, kuna jambo mojadogo sana ambalo linatudumaza sisi Wazanzibar nalo ni lilela longroom pale Dar es Salaam. Wafanyabiasharawanaokuja sasa hivi kama mnavyojua Zanzibar inasifiwa kitalii,tuna utalii wa nje na wa ndani. Hawa watalii wa nje wakijakutembea Zanzibar mtu akinunua chochote Zanzibar akifikalongroom pale akionesha risiti anaambiwa hapana tuoneshena document ya importation ya kitu hiki, hivi kwelitunatendewa haki jamani Wazanzibari na Waziri wa Fedhaupo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hil i ninaomba sanalishughulikiwe kama wewe kweli ni muumini wa haki basi hilinaomba ulisimamie Wazanzibar wasinyanyaswe pale. Mtuakija na tv moja ni biashara ni sawa sawa na mtu ambayeamenunua Morogoro akaja Dar es Salaam. Sasa leoninashangaa leo watu wakienda wakinunua kitu kidogo

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

Zanzibar akipita pale inakuwa kesi kubwa sana. Kwa hivyo,hilo ninaomba safari hii angalau tuhakikishe adha hii hii ndogobasi iishe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiacha hilo,tunazungumzia uhusiano wa mapato baina ya wananchikulipa mapato na Serikali kupokea mapato. Lakini TRAilipoanzishwa kulikuwa na kauli mbiu inatumika kwamba sisini partners katika maendeleo ya nchi yetu, sasa hivi tafsirihiyo inaondoka. TRA sasa hivi wamekuwa ni watu wa bunduki,watu wa kutumia nguvu, wanaingia kila mfanyabiasharaanatafirika. Wewe mwenyewe ulitoa tafsiri katika mwakauliopita ulisema maduka 4,000 yamefungwa, hiyo ni kwasababu ya ukali wa TRA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yako mamboyanazungumzika, Serikali hii ilipoingia madarakani, Serikaliiliyopita ililegeza mambo mengi sana, ninyi mmeingiammekaza, mna haki ya kufanya hivyo, hakuna tatizo. Lakinikwa nini mnawaadhibu hawa kwa awamu iliyopita naawamu hiyo wewe Waziri, Rais wetu, sote tulishiriki, tulikuwemokatika Serikali iliyopita. Na sote kama kuna makosa yalitokeabasi sisi pia ni wakosa wa Serikali iliyopita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Serikali hii ilishaamuakwamba twende vingine, basi tukubaliane kwamba twendekwa mwendo tunaotakiwa. Sasa tusiambiwe kwa makosaya Serikali iliyopita, Serikali hii naiheshimu sana na tunatakatufanye kazi kwa pamoja na tuitekelezee kila wanachokitaka,tutakaza miguu tutafuata. Sisi private sector tunaamini kabisampango wa Rais wetu Dkt. Magufuli wa kutaka kuendelezaviwanda ni mzuri sana na utafuzu kwa nguvu zote, na yeyeana nia njema kabisa, lakini watendaji wetu wanatuangusha.Naomba Mheshimiwa Waziri hili ulisimamie kwa nguvu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo nalo nimuhimu, wakati wa awamu zote zilizopita, biashara bainaya Bara na Visiwani, sisi Visiwani tunaitegemea Bara kwaasilimia 90 kwa maisha yetu ya kila siku Zanzibar. Unachosemawewe sisi tunanunua Bara ndiyo tunapeleka Zanzibar. Lakini

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

awamu zote zilizopita kulikuwa na ulegevu fulani palebandarini Wazanzibari waweze kuleta bidhaa zao ziuzike,sasa hivi awamu hii imetu-tag sisi Wazanzibari ni wezi, hatutakikufanyiwa biashara, biashara yetu ni kuiba tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kutokana na fursaambazo tulikuwa tukipewa na awamu zilizopita, naiombaawamu hii kwa sababu wamekaza kamba sasa wakubalianena hii hoja ambayo naiomba kwako wewe Waziri kwa kupitiaMwenyekiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba mazingira yakufanya biashara Zanzibar na Bara ni mawili tofauti kabisakatika East Africa nzima. Sisi leo kama tutaagiza mzigo kutokanje, tukauleta Zanzibar, basi tutalipa kodi pale, tutaushushamzigo Zanzibar, utaenda zake godown, atakuja mtejaataununua mzigo ule utapakiwa tena kutoka godownutakuja bandarini utapakiwa katika vyombo utakuja Bara,utapakuliwa, utakaguliwa, halafu upakuliwe tena ndiyo ufikesokoni, angalia safari zako hizi zote zilizopita, ni gharama mnokwa kufanya biashara Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Zanzibar kama tunavyojua,miaka yote nenda rudi ndicho kituo cha kufanya biasharana sisi sote nguvu zetu tuko katika kuendeleza Zanzibar iwekituo cha biashara. Na hili nataka niombe sana Serikali yetu,tusione kwamba Wazanzibari ni wakorofi, tuone ni ndugu zetuambao tunataka tushikamane nao, leo uchumi wa Zanzibarukikua ndiyo uchumi wa Bara unakua. Haiwezekani uchumiwa Zanzibar ukawa mzuri wa Bara ukawa chini. Bado BOTndiyo regulator wetu, haiwezekani uchumi ukawa wa upandemmoja na wa upande mwingine usiwe, uchumi wetuutakuwa chini tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kutokana na hilo,naomba sana hizi tozo za TRA kwa maana ya duty, sales taxna nini zilizoko katika Muungano wetu, kwa Zanzibar tufikiriweangalau tushushiwe. Kwa Zanzibar, kama Dar es Salaam ni25 percent, basi Zanzibar iwe 25 percent lakini database ileile ikubalike. Mtu akishalipa kodi pale basi sawa iwe mzigo

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

ule kutoka Zanzibar kuja Bara iwe ni rahisi wala hakunamatatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hivi tunavyofanyianani sawasawa na mfanyabiashara mkubwa kumuua mdogo.Uchumi wa Zanzibar huwezi ukaulinganisha na uchumi waBara. Kwa maana hiyo, mtazame kwamba katika kutekelezani kwamba lazima kila mtu alipe kodi kwa uhakika wake nauhalali wake. Basi sasa tuangalie kodi zetu nazo ziwe rafikikwa pande zote mbili. Hiyo inakuwa ni double taxation.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo naombasana Wizara ya Fedha ilitazame ni kwamba awamu iliyopitaukienda TRA kodi watu walikuwa wakilipa basi mara nyingisana ni ile kodi ya chini kabisa mtu ndiyo bei anayotiliwaanalipa, ukiingia sokoni bidhaa zinauzika, au analipa kodi beiambayo hata katika database haipo, lakini inapitishwa watuwanalipa.

Awamu hii Ma Sha Allah imekuja vizuri sana mna-collect kodi vizuri sana, lakini kilichotokea, watu badala yakutazama database bei za chini au za kati, wamekwendakuzivamia za juu kabisa. Kilichotokea ni mfumuko wa bei kwaTanzania nzima, vitu vyetu sisi vimekuwa ghali. Na kamaunajua soko la Kariakoo ndiyo centre ya kulisha; Burundi,Rwanda na Kongo wote wananunua Kariakoo, bidhaa nyingisana pale. Na ninaamini karibu asilimia 30 mpaka 40 ya kodiinatokana na Kariakoo. Lakini leo maduka yale yoteyamekufa kwa sababu ya kodi kutozwa namna hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu kwa Seriikaliyangu ni kwamba hizi tozo tusitafute hiyo njia ya panyaisiwepo, lakini hizi kodi angalau zitazame pale database beiya chini. Kitakachofanya sasa hivi biashara hizi zinakuwa tenakwa nguvu sana, lakini sio Tanzania, watu wanakwendakununua Kenya, soko hili la Rwanda, Burundi, Kongo, sasahivi mambo yote watu wanakwenda kununua Mombasa,Nairobi, ndipo inapofanyika biashara hii. Tulioumia ni sisiWatanzania, biashara imeanguka kwetu, kwa hiyo hili nalolitazamwe. (Makofi)

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana, Mheshimiwa Mgimwaajiandae Mheshimiwa Anthony Komu kwa dakika saba nanusu.

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Naomba nichukue fursa hiikumshukuru sana Mwenyezi Mungu aliyenipa afya nipatenafasi ya kuchangia kwenye ajenda hii muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nichukuefursa hii kumshukuru sana na kumpongeza Mheshimiwa Dkt.Mpango pamoja na Naibu Waziri na wasaidizi wao kwaujumla kwa kazi kubwa wanayoifanya katika Wizara yao.Lakini namshukuru tena Mheshimiwa Dkt. Mpango, amesemakwenye maandiko yake kwamba atatuzingatia na kuufanyiakazi ushauri wetu. Nakuomba Mheshimiwa Dkt. Mpango,haya tunayozungumza kama Wabunge wenzako uyachukuena kuyafanyia kazi kama ulivyoahidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu unaanzakujielekeza kwenye hali ya kiuchumi. Mheshimiwa Dkt.Mpango amesema uchumi wa Tanzania unakua, ni kweli kwamaelezo yake uchumi wa Tanzania unakua. Lakini unapotakakuangalia vigezo vya kukua kwa uchumi, lazima tuangaliena hali halisi ya Mtanzania, je, iko sawa, inaenda sambambana ukuaji wa uchumi anaouzungumza Mheshimiwa Dkt.Mpango? Ukiangalia utaona mambo yako tofauti,tunazungumza uchumi unakua, lakini hali za Watanzaniazinaendelea kuwa mbaya siku baada ya siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Dkt.Mpango, kwa hiyo inawezekana vigezo ulivyovitumia kusemauchumi wa Tanzania unakuwa ni tofauti na vile ambavyotunavifikiria sisi. Kwa mfano, kupata hela ni tatizo, lakini leo hiiukipata pesa unaweza ukashindwa hata kujua umetumiakununua nini, purchasing power inazidi kushuka siku baadaya siku.

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka MheshimiwaDkt. Mpango atuambie, tuko kwenye inflation period audeflation period. Kwenye deflation period kama upatikanajiwa pesa unakuwa mgumu, automatically unawasaidia walewaliokuwa na pesa kidogo kuweza kununua vitu vingi katikacirculation, lakini mtu anakuwa na hela ndogo aliyoipata,uki-change shilingi 10,000 hata hujui imefanya nini. Kwa hiyo,Mheshimiwa Dkt. Mipango mimi nakuomba uliangalie jambohili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tujiangalie, tupokwenye depression au tuko kwenye recession period. Hayomambo yote mawili tunatakiwa tuyaangalie kwa wakatimmoja...

MWENYEKITI: Anaitwa Dkt. Mpango, siyo Dkt. Mipango.

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Dkt. Mpango, tupokwenye depression au tuko kwenye recession period, miminaona kama tunakwenda kwenye depression, tunatokakwenye recession kwenda kwenye depression. Kwa hiyoninamuomba sana Mheshimiwa Dkt. Mpango aliangaliejambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejitahidi kwenyesuala la bureau de change, lakini bado tuna tatizo kwenyedollarization, bado matumizi ya dollarization yanaendeleakutawala katika nchi hii na shilingi ya Tanzania inaendeleakushuka siku baada ya siku. Sasa unatuambia uchumiunapanda, shilingi inashuka, uki-compare unaona hapa kunatatizo. Kwa hiyo, vigezo ambavyo Mheshimiwa Dkt. Mpangoamevizungumza tunaona haviendani na hali halisi ambayoiko mtaani. Kwa hiyo namuomba sana Mheshimiwa Dkt.Mpango aangalie na haya mambo ambayo yanawahusuWatanzania wa kawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika document yakehii ya Mpango mzima hawajazungumzia hali halisi yawakulima ambao nchi hii asilimia 67 mpaka 72 ni ya wakulima.Kwa hiyo, unakuta mpango mzima wa maendeleo wa nchi

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

hii umewaweka kando wakulima na hawa wakulima ndiyowanaotuweka hapa madarakani. Kwa hiyo, ninaona hapakwenye eneo la kilimo kwa ujumla kuna tatizo. Kwa hiyonamuomba sana Mheshimiwa Dkt. Mpango aliangalie na hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tuliahidikwamba tutatengeneza Kiwanda cha Mbolea hapa nchinikule Mtwara lakini mpaka leo kiwanda hichohakijatengenezwa. Kingeweza kutengenezwa kiwanda kilecha mbolea kule Mtwara nina uhakika mbolea ingekuwachini kuliko ilivyo sasa hivi. Tulikuwa tumekwenda kwenyempango wa bulk procurement, bei imeshuka kidogo, lakinitungekuwa tumetengeneza kiwanda chetu hapa nchini beiingekuwa chini zaidi na nina uhakika kwamba haya ambayowakulima na Wabunge wengi tunalalamikia yasingekuwakama ilivyo sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano tunajiuliza, kwanini wenzetu wa Zambia wanauza gunia la mahindi shilingi20,000 kwa nini sisi tunauza shilingi 35,000? Kwa hiyo tunamaana kwamba mbolea kule iko cheap zaidi kuliko kwetu,lakini sisi tuna access ya kutengeneza mbolea hapa ndaniya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hata ule uchumiwa viwanda ambao ndugu yangu, Mheshimiwa Jafo,anauzungumzia sana, tunaomba uliangalie eneo hili sensitivela wakulima kwamba kile kiwanda cha mboleatulichokizungumzia ambayo raw material tunayo ya kutoshakule Mtwara kingeanza as soon as possible tuwasaidiewakulima walio wengi katika eneo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi namuombasana Waziri wa Fedha atakapokuja atuambie kile kiwandaambacho tumekivumilia miaka mingi kwa nini mpaka leohakijaanzishwa na sababu zipi zinazopelekea kutokuanzishwakwake. Sasa matokeo yake ni kwamba kila siku tunakuja namiradi mipya ambayo haina tija. Unaanza mradi wa zamanito a level fulani unafika unauacha unakuja kwenye mradimpya. Kwa hiyo hapa ni tatizo.

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabungewengi wamezungumzia suala la mahindi, na mimi nataka ni-declare interest, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Kilimo. Kwenyekilimo tumelizungumzia na bahati nzuri leo Mheshimiwa Waziriamelizungumza na baadhi ya Wabunge wanaotoka kwenyemaeneo hayo. Kamati yetu tulikaa na Mheshimiwa Waziri sikutatu kuzungumzia tatizo la mahindi, tumbaku na mbaazi natukatoa directive kwamba Mheshimiwa Waziri aje hapakwenye Bunge lako Tukufu aeleze mkakati wa Serikali kuhusumahindi yatauzwaje, mbaazi itauzwaje na tumbakuitauzwaje, lakini amekaa kimya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na sisi Wajumbe wa Kamatitulikuwa tunategemea yale ambayo yanaulizwa naWaheshimiwa Wabunge yangekuwa yameshazungumzwahapa Bungeni kabla na Wabunge wakatoa maazimio yapamoja. Kwa hiyo, wakulima wetu wanakwenda mwezi wa11 wanaanza kupanda mahindi, hawajui nini wafanye hatakama tumekubaliana leo kwamba tunataka kufunguamasoko, bado ni tatizo. Aje hapa kwenye Bunge lako Tukufuatoe tamko la Serikali kwamba kuanzia leo watu wauzemahindi yao popote wanapotaka ili waweze kupata hakizao za msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, umeme, kama nilivyosemahapo awali, kila siku Serikali ina mawazo mapya. Tulikuwatunategemea tutatengeneza umeme kwa kutumia makaaya mawe, wenzetu wa Mchuchuma, Ngaka, Kiwira. Lakinimpango huu upo zaidi ya miaka 30, sasa tukijiuliza kwa ninitunaenda kwenye mipango mingine wakati mpango huuambao ulikuwa umeshaanza tumeuacha. Kwa hiyo unakutahata baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wakisema kunabaadhi ya miradi imekuwa biased, watu wanaamua kwendakwenye miradi mingine wanaacha miradi mingine, hililitatuletea matatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Waziriatuambie kwa nini wameamua kuacha mradi wa umeme.Sweden kuputia Kampuni yao SIDA Grand walikubali kutoahela, dola milioni 60, kwa ajili ya kusaidia kutengeneza

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

transmission line ya kutoka Makambako mpaka Ngaka, lakiniSerikali imekaa kimya. Na tatizo la pale ni transmission line tuna umeme ule ni cheaper kuliko umeme mwingine wowote.Kwa hiyo, tunataka kwenda kwenye vyanzo vingine vyaumeme wakati tulikuwa tunaweza kupata umeme wa rahisiambao Serikali ilikuwa haiingizi hela yoyote kama alivyosemaMheshimiwa Nape pale, kwa nini twende kuingiza helakwenye miradi ambayo haina tija katika nchi hii?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi naombatuangalie na mje na majibu kwa nini mradi wa umeme waNgaka mpaka sasa hivi haujaanza kazi. Kwa nini mradi wauchimbaji wa chuma mpaka sasa hivi haujaanza kazi kuleLiganga. Hii inakatisha tamaa sana, tunaona kwamba kunabaadhi ya maeneo wanapewa priority ya hali ya juu na kunabaadhi ya maeneo hawapewi kitu chochote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukija kwenye maeneo yabarabara, tunatakiwa tuendelee kufungua barabara. Kunabarabara ya kutoka Kinyanambo A kwenda Isalavanu,Madibira mpaka Rujewa, ni barabara imezungumzwa karibukatika awamu tano. Toka mwaka 2000 ile barabarainazungumzwa, na ni barabara muhimu sana kiuchumi. Kwawatu wanaotoka Mbeya wakiamua kukatisha kwenyebarabara ile wanapunguza zaidi ya kilometa 75 kulikowakipita barabara ile ya kupitia Makambako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwenye uchumi hili nijambo zuri sana. Lakini kila siku wanasema tutaanza keshoau kesho kutwa, lakini ukianglia katika mpango wake na ilebarabara is very sensitive, inapitia kwenye mbuga zawanyama, inapitia kwenye maeneo ya kilimo kikubwa champunga, inapitia kwenye kilimo kikubwa cha mahindi,inapitia kwenye maeneo ya madini, wameiacha haijaanzakushughulikiwa. Kwa hiyo kuna walakini hapa.

La pili, unakuta barabara ya kutoka Mafinga kwendaMtiri mpaka Mgololo. Barabara ile ina zaidi ya viwandavikubwa kumi ambavyo vinatoa kodi zaidi ya shilingi bilioni50 lakini Serikali haitaki kuijenga kwa kiwango cha lami. Kwa

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

hiyo, hili ni tatizo; watu ambao wanachangia hela nyingikwenye nchi hii wanasahaulika. Kwa hiyo, mimi namuombasana Mheshimiwa Waziri mipango yake awe anaangalia nawatu wana-contribute nini katika Taifa hili, sio ajielekezekwenye maeneo tu ambayo anayaona yeye. Watuwanachangia hela nyingi kwenye Mpango wa Taifa lakinimatokeo yake ni kwamba hatupeleki kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumefanikiwa kwenye eneola umeme lakini bado kwenye eneo la maji. MheshimiwaWaziri amezungumzia eneo la maji Dar es Salaam tu, inamaana watu wa Tanzania wengi wanakaa Dar es Salaam.Katika Mpango wake mzima ameonesha kwamba majiyanatakiwa yaende kwa wingi katika Mkoa wa Dar esSalaam, kwa nini kwenye Mikoa, Wilaya, Vijiji na Majimbomengine yasiende? Kwa hiyo kama tulivyofanya kwenyemaazimio ya Bunge lililopita kwamba tuli-ringfence kwa ajiliya kupata umeme wa uhakika, sasa hivi nguvu zetuzielekezwa kwenye eneo la maji ili maji yapatikane katikamaeneo mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kwenye Kamati yetutumependekeza hata Bunge lililopita tuongeze shilingi 50kwenye kila lita ya mafuta ili maji yaende kwenye maeneoyaliyokuwa mengi, lakini tukikwambia utasema kwambatutaongeza inflation rate, hatuwezi kuongeza inflation ratekwa utaratibu huo. Kwa sababu sisi kama Wabungetumekubali na tutakuwa tayari kwenda kutetea hoja zetu,kwamba tuna sababu za msingi za kuongeza shilingi 50kwenye maji ili maji yaende kwenye maeneo mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwakunipa nafasi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Antony Komu kwadakika saba na nusu.

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru na mimi kupata nafasi ya kuchangia huuMpango ambalo ni jambo muhimu sana.

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa sehemu ilekwenye hotuba ya Waziri, Mheshimiwa Dkt. Mpango,ambapo anazungumza kwenye ukurasa wa tano juu yakuweka nguvu kwenye maeneo ambayo yanawahusu watuwalio wengi. Anasema tuweke nguvu kwenye maeneo hayoambayo ni kilimo, uvuvi, pembejeo na mitaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninachojiuliza naambacho mimi naona kwamba ni shida kubwa sana katikahuu Mpango ni uhalisia wa hilo tamko ambalo ameliwekahapa na mambo ambayo yanafanyika. Kwa sababutunapaswa tujiulize tukienda kwenye kilimo tuna mikakati ganiambayo inashikika ya kufanya mapinduzi ya kilimo, uhalisiahauko hivyo. Na kama hatutarekebisha hali hii kwa kwelitutaendelea kubaki watu wa kusema maneno tu na hakunakitu ambacho kitakuwa kinafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mabonde makubwa,tuna mabonde tisa ambayo ni Rufiji, Kihansi, Pwani nakadhalika. Lakini ukijiuliza kuna mipango gani ya makusudiya Serikali ambayo inafanya haya mabonde yaweze kuletamapinduzi ya kilimo, ukweli ni hakuna. Na nimeangaliakwenye ukurasa wa 19 wa hotuba ya Mheshimiwa Dkt.Mpango anasema katika utekelezaji wa bajeti iliyopitawameweza kutenga vyanzo vya maji 78 na kutangazakwamba haya ni maeneo tengefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ni utani, kwa sababukwa taarifa ambayo sisi tulipata kwenye Kamati yetu yaMazingira, Bonde la Kihansi peke yake lina vyanzo 901, katikavyanzo hivyo ni asilimia 27 tu ambayo imeshatambuliwa,kuwekewa mipaka na kutangazwa kama ni maeneoambayo ni tengefu. Maana yake kuna maeneo zaidi ya 600hayajafanyiwa chochote na maana yake ni kwambahayawezi kutumika vizuri kwa ajili ya kuleta mapinduzi yakilimo. Kwa hiyo, katika hali kama hii unaweza ukasemakwamba hatuko serious na hatumaanishi haya ambayotunayasema.

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Kamati yetu vilevileya mazingira tulianzisha hapa Mfuko wa Mazingira naukazinduliwa na Mheshimiwa Rais na wako watu wa muhimunawenye uwezo mkubwa sana kwenye ule Mfuko waMazingira. Lakini mfuko huu ulitengewa shilimhi bilioni mbilimpaka leo tunavyozungumza, Serikali imetoa shilingi milioni34 tu kwa ajili ya huo Mfuko wa Mazingira, sasa katika halikama hiyo tunapigaje hatua. Ukienda kuangalia kwenyeeneo hilo la kilimo tuna Benki inaitwa ya Kilimo hapa, hiyoBanki ya Kilimo inafanya nini, Serikali imeipa nguvu kiasi ganiili iweze kufanya mapinduzi ya kilimo katika nchi hii,nimeangalia wametoa mikopo ya kama shilingi bilioni 6.5 kwawatu 2000 na kitu maana yake ni wastani wa kama shilingimilioni 2.6 kwa mtu mmoja. Tunaweza tukafanya mapinduziya kilimo katika nchi hii kwa stahili ya namna hiyo!

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kule Moshi kulikuwepo namradi unaitwa Moshi Lower Irrigation Scheme ambao huuuligharamiwa na Wajapani, baada ya Wajapani kuondokaekari ambazo zilikuwa zimekwishatayarishwa na kujengewamiundombinu zilikuwa 1,100 na zilikuwa na uwezo wakuhudumia watu zaidi ya 4,500 leo hii tunapozungumzakutokana na uchakavu, kutokana na mabadiliko yatabianchi leo ni ekari 417 tu ambazo zinatumika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni wazi kwambatunarudi nyuma hatupigi hatua na kama Serikali haitachukuahatua za makusudi za kuwekeza kwenye maeneo kama hayana kuangalia maeneo ya miradi ya namna hiyo katika nchinzima tutaendelea kuwa maskini na hatuwezi kufanya hatuayoyote. Tukienda kwenye uchumi wa viwanda, ni lazimatukubaliane na watu wengi hapa wamezungumza kwambatunataka kujenga uchumi wa aina gani, uchumi wa kijamaaau wa kibepari au wa kati, kwa sababu ukiangaliatunazungumza kuwa tunataka kujenga uchumi wa viwandalakini unaona kwamba Serikali bado inarudi kule ambapotulishatoka miaka mingi. Leo hii Serikali inamiliki TTCL kwa 100%,leo hii Serikali inamiliki kiwanda cha General Tyre kwa 100%,leo hii TBA inafanya kazi za ujenzi.

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi wajibu ule wa Serikaliambao tunauzungumza wa kujenga mazingira wenzeshi,unaendanaje na hali kama hii? Lakini tunazungumza uchumiwa viwanda tumetenga maaneo kwa miaka mingi EPZ naZSS, na baada ya kuyatenga hakuna hatua za makusudi nauwekezaji wa makusudi katika hayo maeneo kwa ajili yakujenga miundombinu, kwa ajili ya kuyafanya yale mazingirayaweze kuwa wezeshi, kwa ajili ya kulipa fidia hakuna hatuaambazo za kulizisha. Matokeo yake ni kwamba tunatarajiawawekezaji waje, wajenge barabara, waweke umeme nawaweze kujenga viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri atuambie ni mtuexposed sana na sina matatizo naye, ni wapi hapa dunianihata kule China ambapo ardhi ilitengwa halafu...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante dakika saba na nusu,Mheshimiwa Pascal Haonga kwa dakika saba na nusu.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana na mimi naomba niweze kuchangiamapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wamwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote...

MWENYEKITI: Ajiandae Mheshimiwa Mbarouk.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,awali ya yote na mimi naomba niungane na Watanzaniawenzangu kutoa pole kwa Ndugu yangu Tundu Lissu kwa yaleambayo yalimkuta na nitoe pole na niseme tu kwamba hataniliposikia jana kuna baadhi ya Wabunge wenzetu wachahewanaanza kuleta vijembe kwenye suala kama hili kwa kwelililiniumiza sana. Lakini niseme tu kwamba siku zote matatizohayana itikadi na matatizo yanaweza kumkuta mtu yeyoteyule.

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa niingiekwenye Mapendekezo ya Mpango, tunafahamu wotekwamba kwenye hili kablasha tuliopewa na ndugu hapa Dkt.Mpango ukweli ni kwamba amezungumza vitu vingi sanakuhusu viwanda, kilimo na mambo mengine, lakini hatuwezikupata viwanda bila kujali kilimo. Wenzangu wamezungumzamengi sana na jana niwapongeze waliotangulia kuzungumzakuhusu kilimo, lakini ukweli unapozungumza habari yaviwanda huwezi kuacha kilimo na ukakiweka pembeni,historia inaonesha nchi zote ambazo leo zina viwanda, nchikama China na nchi nyingine nyingi ambazo leo zimeendeleani kwa sababu walifanya mapinduzi katika kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Tanzania tunafahamukwamba tunapotaka kufika mwaka 2020/2025 tunasemakwamba nataka Serikali hii iwe angalau wananchi wake walena uchumi wa kati, uchumi ambao utaendeshwa kwakutegemea viwanda. Lakini ukweli je, ni kwa sasa? Kwasababu kwa muda huu ukiangalia kama lengo ni kupatamalighafi kwa mfano kwenye viwanda vyetu ni kweli lazimatuangalie kilimo, lakini kwa sasa hali ilivyo wananchi wetuwamezalisha sana na wanalia kila kona hawana masoko yamazao yao na viwanda vya kuweza kuwa-accomodatehayo mazao, kuweza kusindika mazao hayo hazipo. Kwenyehili tumebugi sana na hili niweze kusema kwamba tumerudinyuma na wanachi wetu wanateseka sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo wakulima wotewaliolima tumbaku wanalia, wanalia wote waliolima mahindina hivi ninavyozungumza Kanda za Nyanda za Juu Kusinikatika Mkoa wa Songwe, Mkoa Mbeya, Mkoa wa Rukwa,Mkoa wa Ruvuma na mikoa mingine wanalia sana, mahindiyamekaa ndani, hakuna ayenunua yale mahindi, hivyoviwanda mlivyosemakwamba tupate malighafi kwa ajili yakusindika mazao yetu tuonyesheni basi viwanda hivyowakulima wetu wakauze mazao hayo kwenye hivyo viwandabasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ni mbaya kwelikweliamezungumza vizuri ndugu yangu jana mmoja, leo mkulima

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

anayelima ananunua mbolea bei kubwa, anakodi shambabei kubwa, ananunua mbegu bei kubwa, lakini mwisho wasiku tunakuja kumfungia mipaka eti asiuze mahindi nje ya nchilakini pa kuuza wakati huo Serikali haitoonyeshi tukauze wapi.Dhambi hii ambayo inatendwa na Serikali yetu na viongoziwa Chama cha Mapinduzi lazima niwe muwazi hapa jambohili kama hamuwezi mkajadili kwenye caucus zenu mnajadilimambo mengine wananchi wetu msimu wa kulima ndio huuhapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili ni baya sana namwaka 2019/2020 hili jambo litawaghalimu na mjiandaekuondoka, kwaheri Chama cha Mapinduzi kwa sababu sualahili wameshindwa kujadili mambo ya msingi, wanajadilimambo mengine wanaacha suala hili la wakulima wetu. Miminiseme kwamba leo tunazungumza 60% ya chakulakinachozalishwa nchini kinatoka Kanda ya Nyanda za JuuKusini, mkulima huyo hawezi kununua mbolea bila kuuzamahindi, hawezi kusomesha watoto bila kuuza mahindi,hawezi kufanya jambo lolote lile bila kuuza mahindi, leowakulima hawa wanalalamika mimi naamini hasira hizi namachozi haya mwaka 2019/2020 wajiandae haowaliosababisha na Serikali hii na Chama cha Mapinduzi walasio Serikali ya CHADEMA, wala sio ya CUF. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninajua wako wakulima piawa tumbaku wanalalamika, wako wakulima wa mbaaziwanalalamika, wakulima wa korosho wenyewe wanasemabei imekuwa nzuri, lakini kiukweli bado hata wa korosho haopia wamekopwa, bado hawajalipwa. Kiukweli kabisatusipokuwa makini kwenye suala la kilimo mimi naamni kabisaWatanzania wengi watarudi nyuma kwasababu kilimo ndokinaajiri 70% na kuendelea ya Watanzania walio wengi.

Naomba nizungumzie jambo lingine linalohusuutawala bora. Leo tumezungumza kuhusu utawala bora lakiniukweli ni kwamba viongozi wengi wanaotuhumiwa na rushwakama ma-DC leo wanapandishwa vyeo wanakuwa Wakuuwa Mikoa. Hivi unawezaje kumpandisha cheo mtu ambayealikuwa DC unampa Ukuu wa Mkoa anathumiwa kwa rushwa

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

na ushahidi upo, TAKUKURU wameenda wamnachunguza kilakitu, kila mtu ameona kabla TAKUKURU hawatoa majibu leoRais anaenda kumpa DC kuwa Mkuu wa Mkoaanayetuhumiwa kwa rushwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa hakuna utawala borana hapa hali ni mbaya kweli kweli kama tutakuwa tuna-promote wanaoharibu nchi yetu, kwa kweli najua kabisakwamba utawala bora, dhana ya utawala bora tuiondoekabisa kwenye awamu hii ya tano. Lakini leo tunafahamuwote wanapozungumzia utawala bora tunafahamu misingiya utawala bora ni pamoja na uwazi, leo Ndugu yanguMpango hapo tumeambiwa Serkali imeokota vichwa vyatreni pale Dar es Salaam bandarini, hivi ni kweli Serikali haijuini kwamba vile vichwa vya treni vimetoka wapi. Uwazi ukowapi kwenye utawala bora lazima kuna uwazi, uwazi ukowapi, halafu vile vichwa vya treni vinajulikana vimeandikwakabisa na majina. Sasa haya mambo leo Serikali inatakakununua vile vichwa vya treni, inanunua kutoka kwa naniinafanya biashara na nani, ni suala ambalo lazima tujuekabisa kwamba utawala bora ni tatizo ni janga kubwa nanana Dkt. Mpango ulichokizungumza kwenye ile kablashakuhusu utawala bora, umezungumza tu kidogo tu mahakamasijui kujenga kufanya nini vitu vingi sana vya msingi ilitakiwatuwaeleze Watanzania vinakaa vipi. Kwa hiyo kiukwelikwenye hili ni tatizo kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante dakika saba na nusuzimekwisha. Mheshimiwa Mbarouk jiandae, ukimaliza weweataingia Mheshimiwa Jaku.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante na mimi nichukue fursa hii kwanza kumshukuruMwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana katika Bungeletu hili tukajadili mambo ya nchi yetu na hususani Mpango

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

huu wa Maenedeleo wa 2018/2019. Baada ya hapo vilevilepia bado niendelee kushukuru chama changu kwa nafasiniliyoipata. Lakini mimi nianze kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli usiopingikakwamba Serikali yetu imekuwa na mipango sana. Lakinikatika mipango hii mingi imekuwa haina tija, na nianze kwakutoa mfano, tulikuwa na mpango wa MKUKUTA One, Twoand Three lakini mpaka leo hatujui mpango ule umeashiliawapi. Umetajwa hapa asubuhi MKURABITA bado unamatatizo, lakini pia palikuwa na Big Result Now hatuelewiimeishia wapi, lakini palikuwa na Kilimo Kwanza, watuwakakopeshwa matreka leo hii taarifa tulizozipata kwenyeKamati yetu imebidi baadhi ya matrekta yakamatwekwamba watu wameshindwa kulipa.

Lakini pia palikuwa na mpango wa shilingi milioni 50za vijana kila Wilaya hatujui umeashilia wapi, lakini vilevilepalikuwa na mabilioni ya JK nayo haya tukiulizana sijui nanialiyepata. Lakini kama hilo halitoshi bado palikuwa naMpango wa MMEM wa ujenzi wa shule za msingi na sekondariMMES, lakini bado palikuwa na mpango wa kujenga vituovya afya kila kijiji nao hatujui umeashia wapi. Sasa napatataabu nkuona hii mipango tunayoipanga yote kwanini hainatija Watanzania wanatuelewa vipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi nilikuwanashauri tu Serikali ni bora iwe na mpango mmoja ambaoutakuwa unafuatiliwa na kufanyiwa tathimini kila baada yamwaka mmoja na nusu kuona kwamba faida iliyopatikanakutokana na mpango huo ni ipi na kama hakuna faida basimipango tuiache, lakini jambo lingine tumekuwa kukisemakilimo ni uti wa mgongo wa Taifa letu na 75% ya Watanzaniawanaishi vijijini wamejiajiri wenyewe kupitia kilimo, lakinitujiangalie kama Taifa ni kweli tunathamini kwamba kilimo niuti wa mgongo wa Taifa letu? Haiingii akilini kwamba kilimoni uti wa mgongo wa Tifa letu lakini ni theoretically siopractically. Kwa hiyo, mimi niseme tu lazima kama kwelitumeamua kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa tujuevilevile kwamba kilimo ndio kitakachotoa material ya kwenda

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

katika Tanzania ya viwanda. Sasa kama kilimo chenyewetumekipuuza leo tunajadili hapa masuala ya mahindi kukosabei. Wananchi wameweza kufanya kazi kubwa sana bila yakuwezeshwa na Serikali kwa mfano katika Mkoa ninaotokamimi hatutumii pembejeo sisi tunalima kutokana na ardhiambayo ipo na ina rutuba by nature. Lakini leo mahindiyamerundikana hayana bei wananchi wameshindwakusomesha watoto wao, wananchi wanashindwakuendeleza nyumba zao za kisasa. Serikali ndio inayozuiamahindi hasiuzwe nje ya nchi, sasa tujitazame tunafananana nchi za wenzetu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mahindi yana soko kwambayanahitajika Southern Sudan, mahindi yanahitajika Kenya,mahindi yanahitajika maeneo ya Ethiopia huko, lakini sisibado tunazuia mahindi yasiuzwe. Mimi niishauri Serikalituondoe kikwazo kwa uuzaji wa mahindi, kama Serikaliwakala wake wa chakula ameshindwa kununua mahindihaya tuwaache wafanyabiashara wenye uwezo, wanunuemahindi wauze katika nchi za nje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kama hilo halitoshi piavilevile mazao kukosa bei mi naweza nikasema ni Serikalihaikutaka kutafuta bei ya soko la mahindi. Kwa hiyo, lazimawananchi waache watafute soko wenyewe, haiingii akilinikwa sababu kwa mfano yupo mfanyabiashara mmoja wamabasi anaitwa Sumry ameamua kuachana na biashara yamabasi imeingia kwenye kilimo. Sasa hivi kweli anawezaakaamua kulima mahindi ya kula yeye mwenyewe binafsi,kwa ekari ya zaidi 10,000 au 15,000 alizokuwa nazo! Ni wazianaamua kuingia kwenye kilimo afanye kilimo cha biashara,amevuna mahindi wanamwambia asiyauze, hapahukumsaidia bali unamrudisha nyuma katika umaskini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kama hilo halitoshi,ushauri wangu niseme pamoja na kuwaachia wananchikutafuta masoko ya mahindi lakini basi tuwawezeshe kamatunaweka vikwazo hivi angalau tuwape mashine za kusagaunga sasa badala ya kupeleka mahindi ghafi, makapi yamahindi yapaki kuwa vyakula vya mifugo kama ng’ombe

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

wa maziwa lakini wauze unga angalau tumekuwatumewasidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, laini lingine nije katika sualaloa uvuvi bahari kuu. Mimi ninatoka Tanga, Tanga tuna baharikuanzia Jasini karibu na Kenya mpakani huko mpakaKipumbwi karibu na Mkoa wa Pwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania tumejaaliwabahari kutoka Jasini mpaka Msimbati lakini ukiwatazamawavuvi wa ukanda wa Pwani ni maskini wa kutupwahohehahe. Badala ya Serikali kuwasaidia imewarundikia kodilukuki na ushuru mbalimbali, mimi niseme tu wavuvi tuwasaidiekwanza kwa kuwaondolea hizi ushuru na kodi mbalimbali,kwa mfano, mashua moja inachukua wavuvi 25 mpaka 30lakini wavuvi hawa 30 kila mmoja anatakiwa awe na leseniya uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini kwenye basianayekuwa na leseni dereva peke yake turn boy hana leseniwala kondakta hana leseni, kwa nini kwenye vyombo vyauvuvi isiwe mwenye leseni nahodha peke yake?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi tuulizane WaheshimiwaWabunge katika meli kubwa zinazokukuja kutoka nje kwamfano ile meli iliyokamata na samaki waliyoitwa samaki waMagufuli hivi wale watu wa mazingira waliwakamatawakawauliza mpaka mabaharia kwamba walikuwa na leseniya uvuvi, kwa nini tunawaacha watu wa nje wanufaiketunawakandamiza Watanzania wazalendo wenzetuwadhalilike na waendelee kuwa maskini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naishauri Serikaliiondoe...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

MWENYEKTI: Ahsante chama chako kina maelekezowewe nusu na mwenzio nusu, namwita sasa MheshimiwaKhatib Said.

MHE. KHATIB S. HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia namekusimama hapa mchana wa leo siku tukufu ya Ijumaa ili nameniweze kusema machache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nianze kuwapongzakwanza Waheshimiwa Wabunge wenzetu wote walionekanana Mheshimiwa Rais wanafaa kuwa Mawaziri na wamepatauteuzi ule, nawapongeza sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee napendanimpongeze kwa dhati kabisa Mheshimiwa Mbungemwenzetu Lazaro Nyalandu kwa uamuzi wake mtukufu kabisawa kuamua kuhama Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza kwa dhati naniwaombe wenzetu pale wenzetu wanapofanya maamuziwa huku kuja huko au wa huko kuja huku isichukuliwe ni uaduitunabadilishana tu kila jambo na wakati wake, msianzekuwapa majina mabaya mukasema wanarembua macho,ni mafisadi hakuna.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna orodha ya wotemnaowadhania huku hawafai kuweko huko hawahawatafaa kuweko huku, kwa hivyo mnabidi muwaelezemapema kama ninyi hana sifa kuwepo. Msingoje akitokahuko akija huku ndio mnaanza kufichua mabayayake kichokuwa shinda kukila msikitie hila. Ahsanteni sana.(Makofi)

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye Mpango, kwamara ya kwanza baada ya Mheshimiwa Spika juzi kuwatakaWabunge wafunguke kuishauri Serikali kuhusiana na Mpangohuu nimefurahi kuona kwamba hakukuwa na utofauti baliwalikuwa ni Wabunge wote wa Bunge hili kutoa mawazoya kuionesha Serikali pale inapokosea na inapotakiwakujirekebisha. Kwa dhati kabisa niwapongeze MheshimiwaBashe, Mheshimiwa Serukamba, Mheshimiwa Msigwa,Mheshimiwa Sugu na wenzao wote ambao haionekanitofauti ya kiitikadi ya kivyama bali wote tunalenga katikakuilekeza Serikali maana na uhalisia wapi tunataka kwenda.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika yote kwa dhati,nimwambie Mheshimiwa Mpango, katika mamboyaliyotusikitisha hapa wengine ni pale Wajumbe wa Kamatiya Bajeti wanaposimama hapa na wakasema kwambaunakaidi kupokea mashauri na maelekezo yao. Sasa kamaKamati ndiyo wawakilishi wa Bunge zima katika sektawanayoisimamia kwa hivyo unapoanza kuidharau Kamatikatika mashauri wanayokupa maana yake ni kwamba hatasisi humu utatupuuza lakini na sisi tunatimiza wajibu wakusema yale tunayoona yanafaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo dhamira ya Rais wetuna mpango mkuu wa kufufua viwanda hatuoni mafanikioyanayopatikana kama wenzetu walivyosema kwambakuiachia Serikali kila kitu itekeleze kwa pesa yake hilo jambohaliwezekani. Hayo ni mashauri ya kutaka private sector iingiekatika kuendesha biashara ili tukwamuke. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikupe mfano mdogo, leoni mwaka wa 10 Mheshimiwa Mpango tumekuwa tukiimbanyimbo ya kukifufua Kiwanda cha General Tyre cha Arushalakini hebu niambie leo tumefikia wapi?

Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara,tumefanya ziara mara kadhaa, tumependekeza marakadhaa, kama kuna umuhimu wa viwanda vya sukari piakatika kiwanda muhimu katika nchi ni kiwanda cha matairi.

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

Leo hebu niambieni ni Mbunge gani anayefika hapa bilakutumia gari? Gari linakwendaje bila tairi? Mahitaji ya tairi nimakubwa sana. Kama tunashindwa kufufua kiwandamuhimu kama kile ambacho ukiangalia kwa umakini sokola matairi yatakayozalishwa pale ukienda kwenye Taasisi zaSerikali na Mashirika ya Umma pekee hawawezi kulibeba sokola matairi yatakayozalishwa pale General Tyre, tunataka nini?

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwavile muda wangu ni mfupi sana, nataka nijielekeze…

MWENYEKITI: Muda wako umekwisha,mmeshagawana.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Dakika tano?

MWENYEKITI: Wakati mmetoa maamuzi alishatumiadakika zako kwa sababu maamuzi yaliletwa yamechelewa,alishatumia dakika zako wewe mbili na nusu.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Basi nipe nimalizie.

MWENYEKITI: Nakuomba tafadhali Mheshimiwa Khatibkaa, kama unakwenda kusali nenda kasali ni jambo muhimuhilo. (Kicheko)

Mheshimiwa Saada Mkuya, ajiandae MheshimiwaJaku.

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana na mimi namshukuru Mwenyezi Mungu katikaIjumaa hii ya leo kupata nafasi hii adhimu ya kuchangiaMpango huu wa Maendeleo ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nachukua fursa hiikumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

pamoja na wasaidizi wake wote kutokana na kasi ya utendajina utekelezaji wa mipango yetu ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza kuchangiaMpango, Mheshimiwa Turky aligusia kidogo tittle ya kitabuhiki ni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifamwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani Taifa hili la Jamhuriya Muungano wa Tanzania linaundwa na pande mbili. Chakusikitisha na cha fadhaa kabisa ni kuona hakuna hata eneomoja lililopangiwa mpango angalau tu ikaelekezwa katikaupande mwingine wa Jamhuri ya Muungano na hili natakaniliseme wazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia kwako, MheshimiwaWaziri wa Fedha wakati tunajadili bajeti mwezi Juni, 2017baadhi ya wenzangu tunaotoka katika upande wa pili waJamhuri tulichangia maeneo fulani fulani, lakini kwamasikitiko makubwa hakuna hata eneo moja lililoguswalikajibiwa hoja angalau kule upande wa pili wakasikia. Miminilichukua hatua ya kwenda kumuuliza Mheshimiwa Waziriwa Fedha mbona hujajibu angalau basi hoja mbili iliwananchi wa upande mwingine wa Muungano waonekwamba na wao they are part and parcel ya Jamhuri yaMuungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Fedhaaliniambia muda mchache na majibu yalikuwa mengi.Nilijisikia vibaya kwa sababu kama una responsibility ya pandembili za Jamhuri maana yake angalau ungechukua hoja mbiliukazijibu. Sasa aliniambia kabisa kwamba muda mchache,hoja zilikuwa nyingi kwa hivyo mimi nitakupa documentusome, this is exactly jambo ambalo ameniambianimesikitika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunachangia hapa nanimeona tendency ya Wabunge ambao wanatoka upandemwingine wanachangia. Tuombeni Mungu angalau hojambili, tatu zijibiwe muda uwepo. (Makofi)

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukienda katika Mpangokuna jambo lingine kabisa la kusikitisha, kwenye eneo la utalii,biashara na masoko, hivi kwa namna gani au kwa namnayoyote unapotaka ku-promote utalii unaiachaje Zanzibar?Yaani hakuna na haielezeki! Utakuwaje na mpango wa ku-promote utalii Tanzania bila kuiingiza Zanzibar, haiwezekani!(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, majibu yanaweza yakawavery simple ukisema habari ya Zanzibar majibu yanakuwa verysimple kwamba hilo siyo jambo la Muungano. Hivi jamanikama kutakuwa kuna Wizara tatu za Muungano kwa nini sisiWabunge tusiwe watatu tu humu ndani kutoka Zanzibar?Kwa nini tuko 53? Kuna masuala mengine hayahitaji lazimaiwe ni Wizara inayoshughulika na Muungano. Kuna issuesnyingine zinahitaji coordination za pande mbili. Kama hii issueya utalii, hivi kweli kutakuwa na programu au project yoyotebila kui-include Zanzibar? Is not possible, haipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kwenye elimuya juu, hii imo kwenye jambo la Muungano, there is nothing,Waheshimiwa hakuna jambo lolote ambalo limeguswa. Sasasijui huu Mpango wa Taifa lipi hatujui.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna eneo lingine kwenyemasuala ya habari, utamaduni, sanaa, ustaarabu, burudanina michezo. Sasa hivi tumeona Tanzania inaingia katikaramani ya michezo, lakini hakuna specific plan ambayoitaweza ku-accommodate angalau kujenga uwezo wawachezaji wa michezo mbalimbali katika kuitangazaTanzania, hakuna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hii sanaa ya uigizaji,hawa waigizaji wameachwa kabisa. Toka juzi tunasikia waowenyewe wamekwenda Kariakoo, sijui wanapambana nawale piracy na kadhalika, lakini sisi kama Serikali hakunampango wowote wa kuwasaidia wasanii wa Tanzania. LeoGDP ya Nigeria imekuwa rebased kutokana na contributionya sanaa katika uchumi wao. Sisi tumefanya rebase kwa ajiliya kuingiza sectors mpya ikiwemo hii ya sanaa lakini hakuna

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

mpango wa kuendeleza sanaa hii. Kwa hiyo, katika Mpangowetu wa Maendeleo naona hilo limeachwa kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna masuala ya ushirikianowa kimataifa, inasikitisha na inashangaza kuona katika eneomuhimu la diaspora l imeachwa. Diaspora Ethiopiawameungana pamoja wanajenga hospitali kubwa kabisaambayo ownership ni karibu asilimia 90 ya Waethiopiawanaoishi nchi za nje, sisi kwetu hakuna jambo lolote ambaloangalau tumeweka consideration ya kuangalia mobilizationya resources kutokana na diaspora, hakuna! Vile vyanzo vyetuvya mapato ni vilevile tokea Taifa hili lilipozaliwa.

Mheshimiwa Dkt. Mpango wewe ni mweleditumeshakuwepo sana katika semina na vikao vya resourcemobilization lazima tuangalie njia mpya ya kuweza ku-tapresources zilizopo ili kuelekeza katika Mpango wetu waMaendeleo. Kuna role ya diaspora iko wapi, wenzetu wanai-issue diaspora bond na katika article moja ya World Bank,Tanzania imo kabisa katika nchi ambazo zina potentialkubwa ya kuweza ku-mobilize diaspora bond. Hebu liangaliehili tutapata pesa nyingi. Watanzania wenzetu wapo kulelakini hawaoni kama Serikali ina nia ya kuweza kuwasogezakaribu ili na wao wakasaidia kuchangia maendeleo pamojana uchumi wa nchi yao kama ambavyo wanafanya wenzetuwa Nigeria, Ethiopia na Uganda. Naomba eneo hili tuliangaliekwa mapana yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika ujenzi waTanzania ya Viwanda, sera ambazo zinakuwa employed naSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zina effect hatakule Zanzibar. Tumeona na tunasifu kazi nzuri sana ya Serikalikwenye list ya viwanda ambavyo vinaendelea kujengwa naambavyo vimeshajengwa. Waheshimiwa, the list is long lakinihakuna hata sehemu moja tukasema angalau tutashirikianana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ku-tap investors ambaowataweza kujenga kiwanda kitakachotumia malighafi yakarafuu, hiyo consideration hakuna, inasikitisha! SasaMpango huu wa Taifa, Taifa lipi bila ya Zanzibar, inasikitisha!(Makofi)

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini juu ya hivyo, nimesahaujambo moja, nimepata kuulizia hivi jamani MheshimiwaWaziri wa Fedha anashughulika na pande mbili zaMuungano, at any point of time tokea ameteuliwa kuwepopale ofisini alipata kwenda Zanzibar katika kikao cha kazi,siyo kikao cha kero za Muungano, kikao cha kazi?Nikaambiwa hajafika. Nadhani ni jambo ambalo linasikitisha.Nimeambiwa umekwenda katika vikao vya kero zaMuungano, tunashukuru sana kwa sababu ku-participate nikatika hatua ya kutatua kero za Muungano, lakini kikao tucha kuona kwamba kuna mashirikiano baina hizi Wizarambili, ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibarnimeambiwa hatujamuona Mheshimiwa Waziri. TunakuombaMheshimiwa Waziri katika sehemu zako za kazi ni pamojana Zanzibar uwe unafika angalau usikie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna eneo moja ambalotulipata faraja kusikia around two weeks ago kwambaMakamu wa Rais amezindua Sera ya Microfinance, lakinikwenye Mpango na katika maeneo ya vipaumbele kwamwaka 2018/2019 hakuna sehemu ambapo kuna mkakatimaalum wa kuweza kusaidia hizi microfinance institutionszikiwemo SACCOs pamoja na VICOBA. Hizi institutionszinasaidia sana hususani akina mama ambao wako vijijinilakini lazima wawe katika aidha policy framework au legalframework ili na wao waweze ku-access mikopo kutokakatika banks. Sasa haijawekewa kitu chochote katikaMpango huu wa maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu Mheshimiwa Wazirikama nafasi itakuruhusu utakapokuwa unajibu hoja, naombaujibu pamoja na hili i l i wananchi wakusikie hususaniwanawake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine kwenyepromotion za utalii kule Zanzibar kuna vivutio, tunajaribukuweka mambo mbalimbali pamoja na wakati wa lowseason watalii hawaendi lakini sisi tunajaribu kuweka matukioili tupate ku-tap. Tuna Zanzibar International Film Festival (ZIFF)pamoja na Sauti za Busara, ni vitu ambavyo angalau basi

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

vingekuwa taped katika haya masuala ya mipango ili kuonakwamba utalii umo katika Mpango wa Taifa kusaidia Zanzibarpamoja na Tanzania lakini imekuwa ni competition. Sasa hivinimesikia kumeanzishwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa kwa mchangowako. Mheshimiwa Jaku, ajiandae Mheshimwa Papian.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Kwanza nichukue fursa hii kukupongeza kwadhati kwa kuniruhusu kuchangia hoja hii. Bila kuniruhusunisingeweza kuchangia hoja hii kwa hiyo nakushukuru sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hiikumpongeza tena Mheshimiwa Rais wa Tanzania, Dkt. JohnPombe Magufuli kwa jitihada anazochukua kwa wananchiwake na kwa jinsi anavyowatumikia. Nichukue fursa hii tenakuwapongeza wale Mawaziri na Naibu Mawaziri waliopandahivi juzi kwa kupata vyeo hivi na niwape pole waliokuwawakitegemea, lakini hawajapata nafasi hizi mpaka mudahuu. Niwaombe wasikate tamaa, Mwenyezi Mungu siyoAthumani lakini niwaambie tu uteuzi wao huu wanaujua ninimaana yake? Uteuzi huu Mheshimiwa Rais aliotoa Mawazirina Naibu Mawaziri ili wamsaidie kutumikia wananchi kinyumechake Mawaziri na Naibu Mawaziri simu mnazifunga,hamuwatumikii wananchi, siyo kitu kizuri. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kaziteua Wizara kamaWizara ya Afya wenye matatizo ya afya waende afya, Wizaraya Elimu waende wenye matatizo na elimu, Wizara ya Ardhiwaende wenye matatizo ya ardhi lakini kwa masikitiko simuukimpigia Waziri hapokei, ukimpigia Naibu Waziri hapokei,humu ndani tumo sawasawa haya mambo yanageuka.Aliyeko mbele mngoje nyuma, aliyeko juu msubiri chiniatateremka tu. Hivi vyeo ni dhamana na tutakwendakuulizwa siku ikifika tumewatumikia vipi wananchi. Kuna

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

milango mitatu ya kuingilia humu ndani ya Bunge hili, kunaJimbo kutoka Ikulu, kuna Viti Maalum na uchaguzi wawananchi, hiki chombo kina uzito kutokana na wananchi.Wananchi ndiyo waliopotupa dhamana ya kuja kusemamatatizo yao humu ndani. Kuna siku tutakwenda kuulizwahizi dhamana zetu tumezitumia vipi, haya mambo ya kupitatu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije katika mchango wangusasa kuhusu TRA. Mheshimiwa Waziri kwa masikitiko naunyonge mkubwa sana kitendo ulichokifanya cha kutatuakero ya Kenya na Tanzania kuhusu maziwa na cigaretteumechukua muda mfupi sana, lakini kero ya Zanzibar badokila Waziri kinamshinda. Leo Muungano wetu huu tunasemakwa mdomo tu tunataka uendelee kudumu kwa vitendo.Mali inayotoka Uganda, Kenya, Burundi, Zaire, Zambia ikiingiaTanzania wala huulizwi kitu, leo mali inayotoka Zanzibarukiingia nayo Dar es Salaam utafikiri umeleta unga, huuuonevu wa aina gani? Dkt. Mpango Wazanzibari hamtufanyiihaki. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Mzanzibar kachukuagauni zake tatu anakuja hapo bandarini anaambiwa wekachini, tv tu moja, mbili anaonewa, hii haki ikoje? Nimpongezesana dada yangu Mheshimiwa Saada Mkuya, kazungumzavizuri sana lakini huu Muungano tunaosema ni wa upandemmoja tu jamani? Tunasema huu Muungano uendeleekudumu na mimi nasema uendelee kudumu, Zanzibarukiacha zao la karafuu tegemeo kubwa ni biashara. WenzetuTanzania Bara Alhamdulillah, endeleeni kushukuru tunamadini, mbuga na neema nyingi tunazo lakini leo biasharaile nguo tatu au nne, miche mitatu ya sabuni unasumbuliwapale mwisho mchele unaonunua pale bandarini unalipishwapana kimizani kidogo kimewekwa pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala siyo la upandemmoja Mheshimiwa Saada kazungumza bado hujafikaZanzibar, mimi nikuombe ufike. Pindipo utakapokusanyamapato Mheshimiwa Rais atakusifu, tuangalie biashara, hukukidogo, huku kidogo, kuku anataga yai moja ukamlazimisha

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

mayai matatu utamuua, utakosa kuku. Chukua huku kidogo,huku kidogo pishi inajaa lakini kuku yule anataga yai moja,unamlazimisha leo leo atage matatu atakwenda wapi,tutaua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu twende Kariakooukaangalie milango ya maduka nani anaitaka saa hizi?Samora mlango ulikuwa unakodishwa bei kubwa sasa hivimilango imefungwa. Fikiri Mheshimiwa Waziri huu ni ushauriwangu wa bure wala sitaki kulipwa mimi. Kaa nawafanyabiashara utazame nini tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu Muungano Zanzibartunauhitaji kwa kila hali miongoni mwao ni mimi kutokanana udogo wetu, lakini mzigo utoke Kenya, Rwanda, Burundihauulizwi kitu, mzigo ukitoka Zanzibar ukifika hapa aibu. TRAni moja, formula yake ni moja, vigezo vyake ni vimoja, Wazirinikuombe kwa masikitiko makubwa, Wanzanzibar ukiachakarafuu wanategemea biashara. Juzi umetatua tatizo laKenya kwa muda mfupi tu, leo unatuaacha sisi ndugu zakowa damu. Umetatua juzi tu tumekupongeza lakini litatue nahili pia. Taa huwashi nje, unawasha kwanza ndani ya nyumbayako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utawashaje nje kabla yakuwasha ndani huwezi kuona na sadaka sisi tunasemainaanzia nyumbani ndipo utoe nje. Kwa hii kero dada yangukazungumza sana hapa, fanya uwaite wafanyabiashara,wanafunga milango wanaanza kuondoka. Tembea na kamauko tayari tufuatane nikakuoneshe mlango huu umefungwa,huu umefungwa utahesabu milango mingapi. Tufike wakatitupunguze, tujihurumie jamani mapato tunahitaji wewekusanya mapato mazuri uone Mheshimiwa Raisatakavyokusifu. Nchi inataka kwenda kwa mapato lakinitukianza kubana kwa marungu, leo watu wananyang’anywakomputa zao wanavamiwa na TRA, polisi imekuwa TRA sasahivi watu wanasumbuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuombe MheshimiwaWaziri sisi sote humu ndani vyeo vyetu vimoja tunaitwa

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

Waheshimiwa tofauti tu ni Waziri na Waheshimiwa na hayamambo yanageuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo,naomba kukaa. (Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Papian.

MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza napongeza kwa Mpangomzuri ambao umeletwa na Mheshimiwa Dkt. Mpango kwaajili ya kutengeneza dira ya uchumi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza nalotakakuzungumza ni kuhusu mazao ya kilimo ambayo ni yabiashara, haya mazao ya tumbuku, chai na kahawa, nimazao ambayo kwa muda mrefu yameshapoteza masokohayana bei na wakulima wetu wanateseka. Nilitaka kuishauriSerikali kwamba sasa iangalie namna gani haya mazao yakibiashara yanaweza yakapata masoko ili Serikali iwezekupata kodi, lakini na wakulima wetu waweze kupata faida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo lingine nilitakakushawishi, hili zao la mahindi nilitaka sasa na lenyewe liingiekwenye Mpango kwamba ni zao la biashara. Mkulimaanapolima aweze kupata mazao yake, auze anapotakaaendelee na maisha yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais ameshasema Serikalihaina chakula cha kumgawia mtu, wakulima wameshawekareserve chakula chao, chakula kilichopo hii bumper harvestiliyopo watu waruhusiwe waweze kupeleka mazao yaowanapotaka. Mtu asije na hoja kwamba tuna mikoaambayo ina upungufu wa chakula, mwaka huu katikatimwezi wa saba na wa nane watu walikuwa wanachukuamahindi Kilindi na Kiteto kupeleka Shinyanga, leo hayomahindi hayaendi kama kuna deficit Shinyanga kwa ninibiashara hii haifanyiki leo? Ruhusuni watu wapeleke mahindiwanapotaka ili waweze kupata faida na waondoke kwenyeumaskini.

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaelekea kweye kupandawatu wanahitaji mbolea na pembejeo, wapeni nafasiwakauze mazao yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Zambia wamezalishamahindi mengi sana na kwa Wilaya za kina MheshimiwaKandege mazao yana trespass kwa njia za kawaida za panyayanaingia hapa. Mazao mengine yanapakiwa pale borderyanapita yanakwenda upande wa Kenya. Ukiyaangalia yalemahindi ni meupe ni masafi wanapeleka Kenya hatupatikodi. Hivi leo sisi Watanzania wangepakia wakapeleka Kenyanchi yetu ingekusanya kodi. Mheshimwa Mpango unahitajikukusanya kodi kutoka kwenye haya mahindi yanayokwendaKenya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, gunia la kilo mia Kenya ni7,500 mpaka 8,000, it means unazungumzia karibia shilingishilingi 140,000. Mheshimiwa Dkt. Mpango ukikusanya pesaya kodi pale mpakani Holili na Himo, wewe unahitaji pesa,mkulima amepata faida na barabara zetu hazijachimbwana magari ya wengine badala ya magari yetu na mkulimawetu ameshapata faida. Turuhusu mazao yaende mkulimaata-debate mwenyewe wapi atapata chakula Raisameshawaaga kwamba hakuna chakula cha msaada.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la lingine tumekuwana Kakono Project ambayo mwaka jana tuliiwekea mpangohapa fedha zake zipo, mkopo upo wa African DevelopmentBank, Malagarasi ipo, pelekeni pesa hii miradi ianze ili iwezekuongeza umeme kwenye Gridi ya Taifa tuweze kupata faida.Nilihudhuria kikao kimoja pale Kakono, Mtukula nikakaa paleMisenyi, nikazungumza nikaona wale watu wa AfricanDevelopment Bank baadhi yao ni wa Kenya wanaendeleana project. Nilipokaa nikawaza kama this guy’s wapo kwenyehii project wana uwezo wa kuikwamisha mpaka TANESCOyetu hii miradi isiweze ku-take over ili kupata umeme.

Mheshimiwa Mpango naomba hili uende nalouliangalie ili tuweze kuona ni wapi imekwamia hii Kakono

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

Project na Malagarasi ili tuweze kuzalisha huu umeme wamaji. Leo ukienda Mtera inazalisha megawati 80 lakini Mteramaji hamna, yamekauka, yatashuka kesho kutwa huwezikuzalisha hizo megawati lakini ule umeme wa Kakono ni majiya Nile hayatakatika, hayatashuka megawati zetu 87zitaingia kwenye Gridi ya Taifa na bado tutaendelea kupatafaida, naomba hili liangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine uvuvi baharikuu. Kuna Mheshimiwa mmoja amezungumza hapa, uvuviwa bahari kuu sasa hivi Tanzania wanachofuata ni suala laleseni shilingi milioni 30, sijui shilingi milioni 40, ukivua saa mbilindani ya bahari kuu una meli yako unatengeneza shilingi trilionimoja. Hicho ni chanzo Mheshimiwa Mpango nenda nacho,uje na mpango wa kutuambia tunanunua meli, tunavuabahari kuu, samaki za kwetu tu-export samaki tupate faida.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Benki ya Kilimo, asilimia 70%,80% ya Watanzania wanaenda kwenye kilimo, uje na mpangowa kuniambia benki hii inapataje pesa, wewe ndiyo unazo.Hii Benki ya Kilimo leo ndiyo inayokwenda kuokoa watu, benkinyingine sasa hivi zimesha-stuck, haziwezi ku-invest kwenyekilimo kwa sababu ya hali ilivyo na mikopo mingi chechefusasa hivi ni ile ambayo wali-inject kwenye kilimo hawawezikwenda zaidi kwa maana hiyo sasa kilimo kitaenda kushuka.Nikuombe Mheshimiwa Mpango, Benki ya China (ChinaAgricultural Bank) ina uwezo wa kutukopesha, itafutie hii benkimtaji iweze kukopesha wakulima wetu ambao ndiyo pesahiyo itakayozunguka mwisho wa siku utakutana nao kwenyeTIN, vioski na mama ntilie, upate watu wa kutoza kodi ambaowameshapata huku kwenye kilimo. Mheshimiwa Mpango hiibenki naomba ukija utuambie unaenda kutengeneza shilingingapi huko ndani unaichomekea hapo ili iweze kusogeambele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, liko suala la afya. Miaka ya85 kurudi nyuma tulikuwa na vyuo vyetu vya RMAs (RuralMedical Aids), tulikuwa tuna-produce wale watu ambaowalikuwa wanakwenda kufanya kazi kwenye zahanati zetu

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

kule vijijini leo zahanati tunazozijenga kwenye mpango waWizara ya Afya kwa maana ya afya hazina wataalamu.Tufanye mpango tuwarudishe hawa Rural Medical Aidswakafanye kazi kwenye zile zahanati zetu kwa sababu kunanurse mmoja atagawa dawa, atazalisha wanawake auatafunga vidonda. Watu hawa wakipatikana kwenyezahanati zinazojengwa nchi nzima afya za watu wetuzinaweza kubaki salama. Nikuombe muangalie ni namnagani mtapanga kurudisha wataalam hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mpangonikushukuru kwanza jambo moja ambalo umeonyeshakwenye Mpango hapa, suala la kujenga barabara ya kutokaHandeni - Kibirashi - Kiteto – Chemba - Kondoa – Singida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuombe hii barabara sasakwa sababu imeingia kwenye Mpango ipate pesa iwezekutengenezwa. Wakati hii barabara inatengenezwatunaomba mtutafutie wafadhili kwenye ukanda huo huo wakutengeneza viwanda vya kuchambua mchele, kutengenezaunga, kusindika mafuta ya alizeti, kuzalisha juisi ya matundahuko Tanga ili along that road na bomba la mafuta wakatilinapita, magari yanapita kupeleka mizigo bandari ya Tangaili ile mizigo inapopita kuelekea Kanda ya Ziwa, Rwanda,Burundi, Uganda na Kongo basi kuwepo na hivyo viwandaviweze kuzalisha na hayo mazao ya mbegu yaende kwenyehizo nchi ili na sisi wakulima wetu na wananchi kwenye hizokanda waweze kuwa wamepata faida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayonikushukuru lakini nikuombe msiwafunge Watanzaniawaweze kutembea East Africa. Mmeona speech ya Musevenikule kwenye bomba la mafuta Tanga ametukana watuweupe hataki kusikia hii biashara, anasema East Africa tunapopulation ya one seventy thousand people ambapotunaweza kuwa ni soko la mazao na kitu chochotetunachozalisha hapa nchini. Watanzania msiwafunge acheniwatoke mkiwabana sana they will burst. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mwakibete.

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa fursa hii na mimi niweze kushirikikuchangia maoni yangu juu ya Mpango. Kabla kuanzakuchangia kwanza, nimshukuru Mwenyezi Mungu lakini pianiwapongeze Mawaziri wote walioteuliwa na zaidinimpongeze Mheshimiwa Mpango na Naibu wako pamojana watendaji wote katika Wizara hii ya Mipango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Mpango wetuukianza na ule ukurasa wa 34 hasahasa katika suala la afyaimeonesha kwamba utajikita zaidi katika kuboresha Hospitaliza Kanda na Mikoa mbalimbali. Mimi nataka niongezeejambo moja kwamba katika Sera ya Afya kama ambavyotunajua wote inatakiwa kila kijiji kiwe na zahanati, kila kataiwe na kituo cha afya na kila Wilaya iwe na hospitali. Kwamantiki hiyo katika huu ukurasa wa 34 sijaona kama hayammeyazingatia kufuatana na Sera ya Afya ambavyo inataka.Kwa hiyo, ningependa hili jambo mlizingatie mtakapokuwamnaleta ile final draft.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo la pili katikajambo hilo hilo ni katika suala la matibabu (telemedicine).Nimeona mmekazia sana kupeleka ama kutibu watu ambaotayari wameshaathirika na magojwa mbalimbali, aidha, iwenyemelezi ama yawe magojwa yale ya kuambukiza. Kwahiyo, nilitaka nitoe maoni yangu kwamba ni muhimu sasakutoa elimu kwa jamii kuhusu magonjwa mbalimbali kablaya kuanza kuyatibu kwa sababu tunasema prevention isbetter than cure kwa maana nyingine ni kheri kinga kulikotiba na ndiyo maana Serikali inatumia pesa nyingi sana kutibuwakati pengine tungetumia fedha nyingi zaidi kutoa elimukwa hayo magojwa nafikiri kizazi chetu cha Tanzaniatungekuwa tuko salama zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ningependekezakwamba muongeze neno ama teknolojia ya kutibu kwa njiaya mtandao (telemedicine). Hii teknolojia nimekuwanikizungumza humu Bungeni tangu mwaka jana kwa maanaitarahisisha kupunguza kwanza muda wa mgonjwa kwendakwa daktari lakini pili elimu hii ama teknolojia hii itatibu

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

wagonjwa wengi zaidi kwa sababu daktari anaweza akawayuko Dar es Salaam anatibu wagonjwa ambao wakomikoani. Kama ambavyo mnafahamu madaktari tulionaoni wachache inabidi daktari mmoja huyohuyo awe fullyutilized kutibu wagonjwa wengi zaidi kwa njia ya mtandaokwa maana kwamba mgonjwa anaenda sehemu ambapokuna mawasiliano na anawasiliana na daktari wake throughtelemedicine. Kwa hiyo, ningefurahi zaidi kuona hiitelemedicine inakuwa implemented hapa nchini Tanzania.Najua mmeshaanza pilot study lakini ni vizuri zaidi kuwezakufanya haraka zaidi kwa mikoa mingine kwa sababuwagonjwa wengi wanarundikana mahospitalini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine nikijakatika suala la nishati kwa maana ya umeme, ukisoma katikaMpango wetu tumetilia mkazo zaidi kwenye umeme wa maji.Umeme huu wa maji kama mnavyofahamu kwambaunatokana zaidi na maji lakini wakati mwingine mazingirayanakuwa si rafiki sana kwa kuwa vyanzo vya maji huwavinakauka kufuatana na mabadiliko ya tabia ya nchi yadunia.

Kwa hiyo, ningependekeza kwamba ni vizuri sasa piatukajikita katika umeme unaotokana na joto ardhi(geothermal), sijaona katika Mpango wetu hapa. Geothermalni muhimu kwa sababu ule ni umeme ambao tunaita nirenewable tofauti na maji yakishatumika wakati mwinginekama vyanzo vimekauka na huku umeme hatutawezakupata.

Umeme upo wa aina nyingi kuna ule wa upepo, wagesi ambao tuko nao lakini nao bado haujawa effectivelyfully utilized pia ni vizuri tukaendelea kuu-utilize, kuna umemewa solar energy, biomass energy lakini nikazie zaidi katikageothermal kwa sababu kuna maeneo mengi katika nchiyetu ya Tanzania geothermal ama jotoardhi umeme huuunapatikana. Zaidi katika umeme kuna hili jambo la bombala gesi ningefurahi ama Watanzania wengi wangefurahikuona bomba hili linaanza sasa kusambazwa mikoani kotena lisiishie tu Dar es Salaam. (Makofi)

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nikija katikasuala la maji, maji ni uzima, maji ni uhai, maji ni utu na majini roho. Waheshimiwa Wabunge wengi mmelalamikia hapamara nyingi ukisoma ule ukurasa wa 32 tunaona kuna baadhiya miradi ambayo itaendelea katika mpango ujao, ni vizurikatika Mpango wetu kama tutaunda chombo maalum kamaambavyo imeundwa TARURA kwamba chenyewe kijikitezaidi katika kuleta maji kwa maana ya vijijini na mijini. Sasahivi kwa tafiti niliyoifanya nimeona Halmashauri nyingi sanahazina wataalamu na ndiyo maana miradi mingine mingiinashindwa kuendelea kwa sababu hamna ile M&E (Monitoryand Evolution) katika ufuatiliaji wa miradi. Kwa hiyo, ombilangu ni kwamba kiundwe hicho chombo maalum kwa ajiliya suala hili la maji vijijini na mijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nikija katika suala lakilimo, ukisoma ule ukurasa wa 28 utaona kwamba kilimokimetiliwa mkazo lakini wewe Mheshimiwa Waziri unafahamukwamba sasa tuna shida kubwa sana na masoko ya mazaoambayo tumezalisha, kila zao bei yake imeshuka. Kwamfano, ukichukulia mahindi yameshuka, viazi nichukuliemfano kwa mfano kule tulikokuwa tunalima nyumbani debemoja lilikuwa linauzwa shilingi 10,000 hadi shilingi 15,000 lakinisasa hivi debe moja ni shilingi 2,000 kwa maana ya guniazima ni shilingi 10,000 badala ya shilingi 65,000.

Kwa hiyo, kupitia Wizara ya Viwanda na Biasharakatika Mpango wetu kama wataanzisha section ambayoitakuwa inatoa taarifa kupitia njia ya teknolojia kama simuwhatever kwa wakulima wote, tuwe na database yawakulima ambao wanalima mahindi, choroko na kila ainaya zao wanapewa taarifa kupitia hizo simu walizonazo amahiyo database ili wawataarifu sehemu gani masoko hayokwa sasa bei ipo juu. Kwa hiyo, kama Mpango huuungezingatia hilo ingekuwa ni jambo zuri na lenye tija.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika kuwekeza kwenyekilimo tumeona mazao kama chai, mahindi na baadhi yamaeneo bei ya chai ipo chini sana, lakini wenzetu jirani Kenya

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

iko bei za juu, kwa sababu wametafuta masoko nje yanchiyao hasa hasa Uingereza. Kwa hiyo na sisi kamatungeweza kutafuta hayo masoko ingekuwa rahisi zaidi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nikija katika suala lateknolojia, tumeona katika ukurasa ule wa kwanza wamwongozo wa maandalizi wa mpango wa bajetiumezungumzia mifumo mingi ambayo itatengenezwa, miminitoe angalizo hapa. Tumeona teknolojia hii imekuja kwakasi katika nchi yetu ya Tanzania pia nitoe angalizo kwamaana ya mifumo hiihiii ndiyo inatumika katika masuala yaudukuzi.

Kwa hiyo, lazima tuwe very sensitive sana tunapo-implement mifumo hii kwa kuwa hata wale wanaofanyaprogramming, coding na vitu vingine vyote wanajua namnagani ya kuiba kupitia mifumo hii kwa kuwa mimi na weweambao ni end user hatuwezi kujua lakini kwa kuwa miminimeyaishi haya nafahamu. Kwa hiyo, ni vizuri sana hayamambo yazingatiwe katika Mpango wetu. Tusilete tu mifumokama kuleta lakini tujue pia na consequences baada yakutumia mifumo hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tumeona katika hiimifumo kwa mfano hii ya EFD, EFD ni mifumo ambayoinatumika kukadiria mapato lakini risiti zake zile baada yamuda, ukinunua leo bidhaa ukapewa risiti baada ya wikimoja ama wiki mbili au mwezi zinafutika maana yakeunakuwa hakuna tena ushahidi wa kusema wewe ulitumiaile EFD. Kwa hiyo, ni vizuri zaidi kama hizo integrated systemszitakuwa na mifumo ambayo inatoa risiti ambayo nipermanent. Kwa nini mfano ukitoa photocopy karatasi idumuzaidi wakati EFD ambayo ni ya fedha isidumu, kwa hiyo, nafikirihilo pia mliweke vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kwa kuwa hiziteknolojia ni nyingi wakati mwingine wanatumia commercialsoftware ambazo ni gharama zaidi, tunaweza tukafikiritunapunguza gharama lakini kumbe tunaongeza gharama.

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ningeshauri watumieopen software ambazo zinatumika nchi nyingi za Scandinaviana ambazo ndizo ziko applicable duniani kwa sasa, kwasababu hizi commercial software ni gharama na tunakuwahatujapunguza chochote kile zaidi ya kuongeza gharama.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho katika suala laTEHAMA, ingependeza na ingefaa zaidi kuundwe Bodi yawana-TEHAMA kama ambavyo kuna Bodi za Uhasibu, Bodiza Ukandarasi, kwa sababu teknolojia ndani ya nchi yetuinakuja kwa speed zaidi. Kama tutakuwa na hawa watukwa pamoja maana yake itaturahisishia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi zingine kama Finlandwameendelea zaidi kwa sababu waligundua ile Kampuniya Nokia, ukienda Korea Kusini kuna Samsung, ukiendaMarekani hivyo hivyo lakini tukiwa na Bodi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, jioni tutakuwana Mheshimiwa Kiza Mayeye, Mheshimiwa Devotha Minja naMheshimiwa Matiko, kama kawaida makubaliano yenu nitwo in one. Bunge linarejea.

(Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nasitishashughuli za Bunge mpaka saa 11.00 jioni.

(Saa 7.00 Mchana Bunge Lilisitishwa Mpaka Saa 11.00 Jioni)

(Saa 11.00 Jioni Bunge Lilirudia)

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

MWENYEKITI: Tukae. Katibu!

NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifaunaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na

Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwaMwaka wa Fedha 2018/2019

KAMATI YA MIPANGO

MWENYEKITI: Tukae.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea. Wachangiajiwetu wa jioni leo anaanza Mheshimiwa Kiza Mayeye,ajiandae Mheshimiwa Devotha Minja na Mheshimiwa Matiko.

MHE. KIZA H. MAYEYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Awali ya yote napenda kumshukuru MwenyeziMungu, muumba wa mbingu na ardhi kwa kunipa uzima naafya tele na kunifikisha mahali hapa siku hii ya leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nikishukuru chamachange, Chama cha Wananchi (CUF) chini ya Mwenyekitimahiri Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na Naibu KatibuMkuu Mheshimiwa Magdalena Sakaya kwa kusimamia vizuriKatiba ya Chama cha Wananchi (CUF). (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe shukrani zangu za dhatikwa Wabunge wote wa Bunge hili la Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kwa ushirikiano, kutupokea vizuri, kuwa pamojana sisi, kutuelekeza na kutufundisha mambo mbalimbali tokatulivyoingia Bungeni mpaka siku hii ya leo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napendanimpongeze Mheshimiwa Waziri Dkt. Phillip Mpango kwaMpango huu wa Maendeleo, Mpango huu ni mzuri lakinihaimaanishi kila kitu kizuri hakina kasoro. Kwa hiyo, mimi

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

nimpongeze lakini pia naomba nichangie kama ifuatavyokatika Mpango huu wa Maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu wakwanza nataka nianzie katika suala zima la hawawawekezaji. Serikali yetu inasisitiza na inasema kwambatunahitaji wawekezaji. Kwa hiyo, ningeomba Serikali yetuiwape wawekezaji uwezo wa kuja kuwekeza katika maeneombalimbali katika nchi yetu ya Tanzania. Kuna maeneoambayo kwa mfano ninakotoka Mkoa wa Kigoma, huu nimkoa ambao uko katika plan hii ya Regional Economic Zone.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Kigoma mpakasasa kuna zaidi ya heka 690 katika eneo la Kisezi ambalolimetengwa kwa shughuli hizi za uchumi. NingemuombaMheshimiwa Waziri, mhakikishe kwamba mnavutiawawekezaji katika eneo hili kwa sababu eneo hili ni potential,ni eneo ambalo tukilitumia vizuri kwa uchumi tutainua Patola Taifa na hata mkoa kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nimwambieMheshimiwa Waziri katika eneo hili la Kisezi tayari kunamwekezaji ambaye anatengeneza umeme wa jua na mpakasasa ameshatengeneza megawati tano, lakini kunaukwamishaji. Nimwombe Mheshimiwa Waziri, kama Serikaliyetu inasema kwamba inatoa kipaumbele katika sektabinafsi ihakikishe umeme huu wa jua ambao mwekezaji huyuameuweka katika eneo lile uweze kuunganishwa naTANESCO Kigoma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, umeme huu TANESCOwanakataa kuunganisha, lakini mpaka leo Kigomahatujaingia katika Gridi ya Taifa. Ningeomba tuingie katikampango wa Gridi ya Taifa na sio Kigoma tu bali ni Mikoayote ya Magharibi ikiwepo Sumbawanga, Katavi na Kigoma.Kwa hiyo, naomba katika Mpango huu mhakikishe kwambamikoa hii tunaingia katika Gridi ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia TANESCO Kigomawanasema kwamba hawawezi kuunganisha umeme huu

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

lakini katika akili ya kawaida unajiuliza ni kwa nini hawataki?Kwa sababu kama mwekezaji huyu anatumia shilingi 490 kwaunit moja TANESCO Kigoma inatumia shilingi 700 ka unit mojakwa akili ya kawaida unaona kabisa kwamba mwekezajihuyu umeme wake uko chini. Ni kwa nini Serikali haitakimwekezaji huyu umeme wake uunganishwe TANESCO Mkoawa Kigoma? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie katikamaeneo yale ambayo Serikali imeyatenga kama maeneo yamaendeleo, nirudi Kigoma. Kigoma mpaka dakika hiibandari kavu imeanzishwa, hii Central Corridor, Umoja waNchi za Maziwa haya Makuu wamefikia uamuzi kwambaKigoma iwe ni bandari ya mwisho kwa mantiki kwamba watukutoka Burundi, Kongo badala ya kufuata mizigo Dar esSalaam wataweza kuifuata Kigoma na tayari eneolimetengwa la Katosho – Kahagwa, tunatengeneza kitutunasema CIF Kigoma. Kwa hiyo, tutakuwa na bandari kavupale na tayari watu wamepisha ujenzi. Kwa hiyo, naombaMheshimiwa Waziri katika Mpango huu tuhakikishe kwambabandari hii inaanza mara moja kwa sababu kupitia bandarihii vijana wa Kigoma watapata ajira lakini sio Kigoma tuTanzania nzima kwa sababu huu mpango ni wa Taifawatapata ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyeiti, pia nimwambie Wazirikwamba mbali na ajira mzunguko wa pesa utakuwa nimkubwa katika Mji wa Kigoma na mzunguko wa pesa ukiwamkubwa katika Mji wa Kigoma hilo ni Taifa, Taifa tutapatapato. Kwa hiyo, niombe Mheshimiwa Waziri ufanyeunavyoweza bandari hii ianze mara moja. Labda ningejua,Wizara ya Fedha mpaka sasa mmejipangaje katika suala hilina Mamlaka ya Bandari imefikia wapi katika utekelezaji wamaamuzi haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimepitia Mpango waMheshimiwa Waziri. Hakuna mahali ambapo nimeona kunauwezeshaji wa kijana na mwanamke. Hakuna mtu asiyejuakwamba kijana ni mtu muhimu katika Taifa hili lakini hakunamtu asiyejua kwamba mwanamke ni mtu muhimu katika

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

familia na Taifa. Naomba sasa Serikali ije na Mpangomadhubuti wa kumwezesha kijana huyu ambaye leoanamaliza shule lakini hana ajira na mama huyu ambayeamekaa nyumbani hana kazi. Tuandae mikakati ambayoitamwezesha mama, wote tunajua mama ni nani katikafamilia, ukimwezesha mama atasomesha watoto. Kwa hiyo,tuwe na vyanzo vya kuwasaidia akina mama, mabenki yatoemikopo kwa akina mama. Kwa hiyo, ningeombaMheshimiwa Waziri katika Mpango unaokuja umfikirie sanakijana na mama wa Kitanzania, SACCOS za akina mamaSerikali iweze kuzisaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie tena suala lauwekezaji. Kumekuwa na maeneo mengi ambayowawekezaji wanataka kwenda kuwekeza lakini hakunaushirikiano mzuri. Kwa taarifa nilizozipata katika eneo hili hilila Kisezi, Mkoani Kigoma Serikali ya Japan inataka kujakuwekeza, watengeneze bidhaa wao wenyewe na watafutemasoko wao wenyewe masoko wao wenyewe na watumieuwanja wa ndege wa Kigoma. Hata hivyo, Serikali haioneshiushirikiano na wawekezaji hawa. Kwa hiyo, MheshimiwaWaziri ningeomba kama kweli tunataka kusonga mbelekatika maendeleo ya Taifa tutoe kipaumbele katika sualazima la uwekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie katikasuala zima la kilimo. Hakuna mtu asiyejua kwamba kilimo niuti wa mgongo. Wote hapa leo ni Mawaziri, Wabunge wengitumesomeshwa na wazazi wetu kwa sababu ya kilimo.Naomba Mpango huu utakaokuja sasa muwasaidiewakulima, muwape pembejeo, mbolea, muwasaidie kupatamasoko kwa sababu tunaposema leo tuna nchi ya viwanda,huwezi kuwa na viwanda kama wewe mwenyewe hunaproduct za kupeleka kwenye kiwanda chako. Huwezi kusubirimahindi kutoka Kenya, huwezi kusubiri korosho kutoka nchijirani, tuhakikishe sisi wenyewe tunakuwa na product zetuambazo tutazipeleka katika viwanda vyetu. Kwa hiyo,nimuombe sana Waziri, Wabunge wengi wameongeleakuhusu suala la kilimo, naomba kilimo kipewe kipaumbele,kilimo ni uti wa mgongo. Kama Serikali tunataka kusonga

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

mbele tuhakikishe kilimo kinathaminiwa kwa asilimia 100.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa niongeleesuala la elimu. Miundombinu ya elimu katika nchi yetu nimibovu. Walimu wengi nyumba zao ni mbovu. Walimu hawandiyo wametufikisha mahali hapa leo. Walimu hawa ndiyowamekutoa wewe Waziri, mimi Mbunge.

Kwa hiyo, naomba tuwathamini walimu kuanziakwenye makazi, nyumba wanazokaa ni chache. Mikoa mingiina changamoto walimu hawana nyumba na hata nyumbaambazo zipo unakuta haziko katika mazingira mazuri. Kwahiyo, nimuombe Mheshimiwa Waziri atakapokuja na Mpangohuu ahakikishe miundombinu kwa walimu,waongezewe mishahara lakini nyumba na makazi yawemazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika elimu nizungumziesuala la madarasa. Maeneo mengi hasa ya vijijini wanafunziwanasomea nje, hakuna madarasa. Serikali ijitahidi kuwekamadarasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa nizungumziemiundombinu ya wanafunzi. Shule nyingi vijijini watotohawana vyoo. Sasa jiulize kama tunashindwa kuwekamatundu ya vyoo katika shule, binti huyu ambayeamekwenda shule, kwa sababu tayari kuna watoto wadarasa la saba wameshaanza kuona hali ya usichana wao,ameingia katika hali ya usichana hakuna maji, hakuna choomnamweka katika mazingira gani binti huyu wa kike? Kwahiyo, mnamfanya sasa huyu binti akishaingiwa na ile hali nawenzie wamemuona, kesho hawezi kurudi shule. Kwa hiyo,tunaomba Mheshimiwa Waziri mhakikishe mnawajaliwanafunzi katika huduma za maji mashuleni, vyoo na hasamtoto wa kike mumsaidie apate huduma hizi ili awezekwenda shule kama watoto wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya,naomba kuunga mkono hoja, ahsante. (Makofi)

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Minja dakika sabana nusu na Mheshimiwa Matiko dakika saba na nusu.

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimepitia sana kitabu chaWaziri Mpango, nisikitike tu kusema mambo mengitunayoyaona ni yale yale, hakuna mambo mapya.Mheshimiwa Mpango nilitegemea ungekuja na mikakatimipya kuhusu suala la bandari. Tukizungumzia bandari,tumeambiwa bandari ikisimamiwa vizuri inaweza ikasaidiakuongeza Pato la Taifa hili tukaachana na kukimbizana nawatu wanyonge, wafanyabiashara wadogo ambao hawananguvu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bandari ilivyo hivi sasaukiwauliza wafanyakazi wa bandari wanakwambia hawaijuisiku yao wala saa. Bandari imegeuka kuwa siasa, viongozimbalimbali wanakwenda na camera kwenda kutumbuaviongozi wa bandari, wakurugenzi wa bandari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mpangoatuambie asione aibu, kama unahitaji kusaidiwa kwenyebandari usione aibu sema. Nchi zingine zenye bandarizinafanya nini zinafanikiwa, kwa nini Tanzania hatufanikiwi?Tafuta experts wa kusaidie tufanyaje bandari yetu iwezekusonga mbele ichangie Pato la Taifa. Kila siku MheshimiwaMpango wewe unazungumzia, ooh, kodi zitaongezwakwenye sigara na kadhalika, kumbe tuna bandari ambayoingeweza kusaidia hata hizi sigara ambazo tunasema zinamadhara tukaachana nazo kwa sababu kuna sikuWatanzania wataamka watalielewa neno “no smoking” nasijui mapato tutapata wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano Bandari ya Mtwara,yenye kina kirefu, lakini tumeifanyia kazi kwa kiasi gani? Leotulikuwa tukisikia TRA wanatangaza mapato yao wamepatakiasi gani, lakini ukienda bandarini hakuna meli, meliutakayoikuta imebeba kokoto inapeleka Qatar kwenye

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

kuandaa Kombe la Dunia. Kwa nini meli zisiwepo paleambazo tunajua zime-import tunahakikisha tunapatamapato? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mpango usioneaibu, tafuta namna ambayo utashauriwa na wataalamwaweze kusaidia tufanyaje bandari ya Tanzania iwezekusaidia kuongeza pato na kuwapunguzia mzigoWatanzania ambao wanakimbizana huko, mtu unamkutaana kamtaji kake ka laki mbili anaambiwa anunue EFDmachine ya shilingi laki nane, hii ni ajabu sana. Kamtaji kalaki mbili, laki tano unaambiwa nunua EFD machine ya lakinane, are we serious? Bandari isimamiwe na ifanye kazi yakevizuri iokoe jasho na vilio vya Watanzania. (Makofi)

T A A R I F A

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimpe taarifa msemaji anayezungumza sasa hivi,bandari yetu sasa hivi kwa takwimu inachangia asilimia 44ya mapato na hilo siyo pato dogo, asilimia 44. Bandari yaMtwara sasa hivi iko katika matengenezo inafanyiwaukarabati wa kuongeza kina chake tayari kazi imeanza, sasasijui anazungumza kitu gani? Naomba nimpe hiyo taarifa.(Makofi)

MWENTEKITI: Taarifa hiyo Devotha.

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa siipokei, nilifikiri ananiambia kwamba bandariinafanya kazi kwa zaidi ya asilimia 100, ananiambia 40?Bandari tunayo miaka mingapi toka uhuru mpaka sasa hivitunazungumzia bandari hiyo hiyo? (Makofi)

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze kuhusu fine zabarabarani. Traffic wametoka kwenye lengo la kusaidiakupunguza ajali za barabarani, sasa hivi wamegeuka kamamaofisa wa makusanyo wa TRA. Nikizungumza hayowanaotoka Dar es Salaam wanaelewa, shida wanazokutananazo watu wenye magari, traffic hivi sasa wanafunguampaka bonnet kuhakikisha wanakusanya mapato na kilamwisho wa mwezi wanatoa tathmini, tumekusanya milionikadhaa kwa sababu ya matatizo na makosa mbalimbali yabarabarani, hivi hii ni faida ni hasara? Hivi hili ni tatizo au?Kwa sababu huwezi ukasema umekusanya mapato kwa fineza barabarani maana yake hujafanya kazi yako ipasavyo.Tulitegemea wangekuja na taarifa kwamba ni namna ganiwamepunguza ajali kutoka asilimia fulani kwenda asilimiafulani na siyo kutuletea mapato, hii sio kazi yao, ni kazi yaTRA hii. Kama tuna nia ya kukuza uchumi ni lazima tuangalievitu hivi na sijui kama Mheshimiwa Mpango kwenye hiliamewawekea traffic wapi maana wanaonekana naowanafanya kazi ya kukusanya sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze kuhusu habariya viwanda. Nimesikia kwamba hivi sasa mikoa inatakiwakuwa na viwanda 100. Hivi ni viwanda vipi? Tunasema mtuakiwa na cherehani tano tayari ni kiwanda, are we serious?Tuna viwanda vingapi ambavyo vimekufa hivi sasahavieleweki? Mkoa wa Morogoro wenyewe una viwandazaidi ya 20 vime-collapse, hakuna ajira, wengi wanafugiambuzi hivi sasa. Viwanda vya Morogoro watu walichukuawakafanya kama collateral kwenda kuchukulia mikopokufanya shughuli zao zingine lakini viwanda vimekufa. Kwanini tusivitazame viwanda hivi ambavyo tayari vipo ambavyovilianzishwa kwa nguvu ya Mwalimu Nyerere? (Makofi)

T A A R I F A

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, tungependa sana Wabunge wanapochangiawawe na uhakika na data wanazozitumia. MheshimiwaMbunge ameendelea kulalamika kwamba Serikali haifanyikazi yoyote, anategemea viwanda vilivyoanzishwa naMwalimu Nyerere na anatoa mfano wa Morogoro vingewezakuwa vimefufuliwa na vinaanza kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumpa taarifakwamba Serikali yetu, Serikali sikivu imeshaanza kutekelezajambo hilo na yeye kama Mbunge wa Mkoa wa Morogorohawatendei haki wananchi wa Morogoro kama ha-supportnguvu za Serikali ambazo tumezifanya katika mamboyafuatayo:-

(i) Kiwanda kilichokuwa kinatengeneza maturubai,Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeshamaliza utaratibu wakimfumo na kimkakati wa kukifufua kiwanda kile nakuhakikisha wananchi wa Morogoro wanapata ajira. (Makofi)

(ii) Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika Mkoa waMorogoro imeshaanzisha mradi mkubwa wa kufufua Kiwandacha Sukari kwenye Gereza la Mbigili na inaanzisha kiwandakingine kikubwa cha sukari eneo la Mkulazi na huo ni Mkoawa Morogoro. (Makofi)

(iii) Kwa kushirikiana na wawekezaji katika Mkoa waMorogoro Mheshimiwa Waziri Mkuu ameenda kukaguakiwanda kipya kikubwa sana ambacho kitakuwakinatengeneza sigara za kuuzwa nje ya nchi ya Tanzania.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba tuWaheshimiwa Wabunge wakati mwingine wanapochangiawawe wanajua pia na juhudi za Serikali zilizofanywa.Hatukatazi watusaidie kutushauri lakini wa-appreciate piajuhudi za Serikali zilizofanyika. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa taarifa?

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa siikubali. Mimi nilifikiri angenieleza kwamba tayariviwanda vimeanza kufanya kazi. Hizi hadithi anazosematumeanza kuzisikia siku nyingi tu. Kusema leo tutafufua, keshotutafufua, watu wa Morogoro tulishazoea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niangalie kwenye sekta yautalii. World Bank wanatuambia sekta ya utalii ikisimamiwaipasavyo ina uwezo kabisa wa ku-cover budget yetu kwamwaka. Hivi sasa tunajiuliza pamoja na vivutio tulivyonavyo,hifadhi tulizonazo lakini bado hakuna kitu ambacho tunaonakama vile tunafanya kwa malengo ya kuhakikisha sekta hiiinanyanyuka na inachukua nafasi kusaidia Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia hojazinazoendelea hivi sasa tunataka kuona Waziri anasimamiapale kwenye sekta ya utalii kutoa ushauri na kuangaliatufanyaje tuende mbele badala yake sasa Waziri anayepatanafasi yeye ana kazi ya kuangalia aliyetoka alifanya nini navijembe. Aje na mkakati kwamba yeye atafanya ninikutupeleka wapi ili sekta hii itusaidie, si kufufua makaburiMawaziri wengine wamefanya kitu gani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri kuna mahali ambapotumekosea, ni lazima tuwe na mipango mikakati ambayoitatusaidia ili sekta hii ya maliasili na utalii iende kuwasaidiaWatanzania kama vile…

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

TAARIFA

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nilitaka kumpa Taarifa mzungumzaji kwa maneno aliyoongeakuhusiana na Waziri anapiga vijembe. Mimi niko kwenyeKamati ya Maliasili na ni Mjumbe mwenzangu, mamboyanayofanywa na Waziri huyu aliyeteuliwa sasa yanaungwa

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

mkono na Watanzania wengi, kwa hiyo, tusikatishane tamaabadala ya kupongezana tunaanza kupigana vijembe humu.Tunampongeza sana Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla aendeleekufukua makaburi ili tuwakamate hawa waliotutesa mudamrefu. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Devotha, taarifa?

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,huyu naye ni Mjumbe mwenzangu kwenye Kamati mimininashangaa sana kwenye Kamati anasema vile huku leoanasema hivi. Yeye juzi hapa amesema MheshimiwaKigawangalla akae vizuri vinginevyo atatumbuliwa kamaMheshimiwa Maghembe au siyo, sasa sasa hivi anatupataarifa ipi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi kuzungumza kukuzauchumi bila kuangalia jinsi ya kukuza uchumi wa mtu mmojammoja. Ukiangalia hali ilivyo hivi sasa huwezi kuwatoa watuambao ni matajiri wanaoishi kama malaika useme waishikama mashetani, haiwezekani, hivi vitu vyotevinategemeana. Sasa ifike mahali watu waangalie sektabinafsi zinafanya nini na Serikali ione ni jinsi gani ya kusaidiasekta hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa tunaona hasaraambazo zinapatikana kwa hivi sasa kwenye sekta nyingi. Kwamfano, Club Bilicanas iliyokuwa inamilikiwa na MheshimiwaMwenyekiti Mbowe ilivunjwa kwa jazba na kadhalika lakinihivi sasa club ile magari yana-park; kulikuwa kuna migahawa,kuna Gazeti la Tanzania Daima, watu wangapi wamepotezaajira? Wafanyakazi wangapi walikuwa wanategemea palekuishi maisha yao? Leo hii kweli, taxi ndiyo zina-park pale?Hatuwezi kujenga uchumi kwa kuumiza watu. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEOYA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

TAARIFA

NAIBU WAZIRI ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpa Taarifamzungumzaji anayezungumzia habari ya Bilicanas kuvunjwa.Bilicanas ile ilivunjwa na Serikali baada ya Mwenyekiti waokushindwa kulipa deni kubwa alilokuwa akidaiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ilichukuliwa naalishindwa kesi ambayo mwenyewe alikuwa ameifungua.Kwa hiyo, ilivunjwa ili kumuondoa na mpango wa Serikali nikupaendeleza pale kulingana na Master Plan ya Jiji la Dar esSalaam. (Makofi)

MWENYEKITI: Haya, Mheshimiwa Devotha, taarifa?

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimuulize Waziri, sasa baada ya kuvunja ndio Serikali imelipwahilo deni? (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchumi hauwezi kujengwakwa uonezi. Tunafahamu aliyekuwa DC wa Hai ambayealienda kwa jazba kuvunja mashamba ya MwenyekitiMheshimiwa Mbowe na baadaye akawa promoted kwendakuwa RC. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbowe alikuwaanafanya kilimo cha green house lakini sasa…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,hivi niulize kilimo cha green house kina conserve mazingiralakini watu wa Kagera wanaolima kwa jembewameambiwa walime mpaka mtoni hawaharibu mazingira.(Makofi)

Kilimo cha green house ambacho kinatumia waterdrip, ni maji kidogo sana, lakini matokeo yake ni…

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

WABUNGE FULANI: Ahaaaa, bado Mheshimiwa,hajamaliza dakika zake.

MWENYEKITI: Waheshimiwa, ngojeni. MheshimiwaDevotha hebu kaa. Ulianza exactly na dakika 10, sasa hiviumetumia dakika…

WABUNGE FULANI: Kulikuwa na taarifa.

MWENYEKITI: Sasa si dakika saba na nusu za kwakoza halali na dakika saba na nusu za taarifa.

WABUNGE FULANI: Hapana.

MWENYEKITI: Hapana nini sasa? (Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea naMheshimiwa Matiko, ajiandae Mheshimiwa Kapufi.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Kwa sababu muda ni mchache menginitawakilisha kwa maandishi lakini kwa uchache huu niendekuzungumzia baadhi ya mambo kwenye Mpango huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukirejea ukurasa wa 40kipengele cha kwanza kabisa kimeainisha misingi namatarajio ya ukuaji wa uchumi. Kwenye kipengele chakwanza kinasema kuendelea kuwepo kwa amani, usalama,utulivu na utengamano wa jamii ndani na pia nchi za jirani.Nafikiri hapa ingetakiwa ibadilishwe iandikwe kuimarishwakwa amani, usalama, utulivu na mambo mengine kwasababu sasa hivi ilivyo huwezi kusema kwamba Tanzania tunausalama ilhali tukishuhudia wananchi wanatekwa,wanauawa, wengine viongozi wakubwa kabisa wanapigwarisasi nyumbani sehemu ambayo ni secured. Hatuwezi kusema

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

kwamba tuna amani ilhali maisha ya Watanzania ni magumusana. Wale wote ambao mfano wametolewa kwa vyeti fakena wale wengine wameambiwa ni darasa la sabahawajapewa pension, gratuity ya kuondoka leo usemekwamba kuna amani Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tumeshuhudia naMheshimiwa Msigwa ameomba Mwongozo hapa nchi jiraniKenya kwa yale ambayo yamejiri kwenye kuchomwa kwavifaranga, ng’ombe kukamatwa na mambo mengine. Kwahiyo, kipengele namba moja ukibadilishe kiseme,kutakuwepo na matarajio ya ukuaji wa uchumi iwapokutaimarishwa amani, utulivu, usalama na mambo menginelakini sio kwamba kuendelea kuwepo ilhali hivyo vitu hatuna.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine siku zote nasemahatuna uhalisia kwenye mipango yetu na bajeti ambazotunazileta hapa. Tusipokuwa na uhalisia ni dhahiri hatutafikapale ambapo tunataka kufika kama nchi. Leo ukiangaliakwenye kitabu chako mwenyewe umeainisha bajeti yamaendeleo ya mwaka 2016/2017 ambayo ilikuwa ni shilingitrilioni 11.8 ilitekelezwa kwa asilimia 55 tu. Hii ya sasa hivi kwaquarter moja ya mwaka 2017/2018 imetekelezwa kwa asilimia11, on average mpaka tunamaliza itakuwa asilimia 44 mpaka50 au ikienda au ikienda zaidi tuseme 60. Sasa ikienda natrend hii ina maana tunapanga vitu bila kuangalia uhalisia,time frame, vipaumbele ni vipi, mwisho wa siku tunakuwatunapoteza rasilimali za wananchi kukaa hapa tunajadili.Siku zote nashauri kwamba ni bora tuweke vitu ambavyotunajua tutavifikia ndani ya muda kwa resources tulizonazowalau tunapokuwa tumekuja ku-discuss Mpangomnatuambia kwa mwaka uliopita tumeweza kufanyamambo ya maendeleo kwa asilimia 80 au hata 85, 90 siokwa asilimia 44 au 50. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine na hiki naombakabisa tuwe sober kwa nachoenda kukiongelea sasa hivi.Kwenye allocation ya kodi za wananchi, maana imechukuadiscussion nyingi hapa na watu wamekuwa na hisia tofauti.

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

Mimi natokea Kanda ya Ziwa lakini hili nalipinga na nalipingawith facts na sisi kama wawakilishi wa wananchi ambaotumetumwa hapa Bungeni tukalitafakari ili tuweze kuishauriSerikali vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunaambiwa ujenzi wajengo la TRA Chato, ghorofa kubwa sana limejengwa kule.Leo tujiulize Chato kuna mzunguko gani mkubwa wa fedha,kuna biashara gani kubwa kule Chato mpaka twendetuwekeze ghorofa? Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)inakusanya mapato gani kule Chato tukawekeze lile ghorofala mamilioni ya kodi za Watanzania? Tutafakari kamaWabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni Uwanja wa Ndegewa Chato, kabisa. Mimi sipingi uwanja wa ndege kujengwaChato lakini Uwanja wa Ndege wa Chato ulitakiwa kuwa nichini ya kilometa moja ya run way.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo pamoja na kwambakuna kukiukwa kwa Sheria ya Fedha za Umma ambayotulipitisha hapa shilingi bilioni mbili, lakini naambiwazimetumika zaidi ya shilingi bilioni 39, hiyo ni hoja lakini siohoja kubwa sana kwangu, tujiulize sisi Watanzania na hawaambao wanamshauri Rais…

T A A R I F A

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, Taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, Mheshimiwa Esther Matiko ni Mchumi mzuri….

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Kanuni?

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: Sina mudawa kupoteza Mheshimiwa Msigwa, Kanuni najua…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: Sina mudawa kupoteza kuisoma hiyo Kanuni, tunawapotezea mudawachangiaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimkiwa Matiko niMchumi mzuri na nataka tu kumpeleka kwenye hichokipengele anachosema kwamba hataki kuzungumzia sanalakini anam-acuse Waziri wa Fedha kwamba Sheria ya Fedhaimevunjwa. Nataka nimkumbushe Mheshimiwa Esther MatikoSheria ya Bajeti (Budget Act) Na.11 ya mwaka 2015, akiendakusoma kifungu cha 41 pamoja na Kanuni ya 28(1) na (2),Waziri amepewa mamlaka ya kufanya uhamisho usiozidiasilimia tano ya bajeti yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kulisema hili kwasababu naona Wabunge wanalichukulia jambo hili kama nikosa kubwa lililofanywa kwa nia fulani lakini Budget Act,kifungu cha 41, narudia kusema, Sheria ya Bajeti kifungu cha41 kimempa mamlaka Waziri wa Fedha kufanya mabadilikohayo. Sasa nataka kujiuliza hiyo shilingi bilioni 39 inayosemwa,je, inazidi kweli hiyo asilimia tano?

Naomba kumpa Taarifa Mheshimiwa Esther kwambaanataka kupotosha maana ya sheria na mamlaka aliyopewaWaziri wa Fedha. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Esther kwanza kaa.

Waheshimiwa Wabunge, mipango ya Serikali kunastrategies nyingi sana. Kuna strategy za usalama, majeshi,rapid deployment ya forces. Maeneo yale yakivamiwa lazimakuwe na uwanja wa kuweza kubeba ndege kubwa za jeshiambazo tunazo za kupeleka majeshi. Tuna uwanja mkubwa

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

Mtwara, tuliujenga kwa madhumuni mawili, ulinzi wa Kusinina kupeleka mafuta Zambia, hizi ni strategy za Serikali.(Makofi)

Mheshimiwa Matiko endelea.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,inabidi nicheke kidogo. Wakati tunapitisha na kwenye kitabuchake cha Mpango wakati ule tunapitisha kwa ajili yaupembuzi yakinifu zile shilingi bilioni mbili walisema ule uwanjawa Chato unajengwa kwa ajili ya usafiri ndani ya Geita namikoa jirani hawakusema otherwise.

TAARIFA

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Taarifa.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nilinde, kingine nasema kuhusiana na…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Taarifa.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Muda wangu muulindemaana bado.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kumpa taarifa mzungumzaji, dada yangu,anayetoka Kanda ya Ziwa, amezungumza kuhusiana naghorofa iliyojengwa kwa ajili ya TRA pale Chato. Sasa nilitakakumuuliza ni kanuni ipi au ni sheria gani kwenye nchi hiiinayosema ofisi mpya za TRA zinazojengwa huko mkoanitujenge slope? Ni sheria gani anayotaka kuitumia kwambakujengwa ghorofa Chato la TRA ni makosa Chatotuwajengee slope?

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Matiko, Taarifa.

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,huyu hajatoa taarifa ameuliza swali, nitamjibu kesho wakatiwa kipindi cha maswali na majibu kama Waziri Kivuli waeneo husika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, point hapa ipo nimejibukwamba wakati inakuwa allocated hapa ilikuwa ni uwanjakwa aji l i ya usafiri ndani ya Geita na mikoa jirani.Hawakusema kwamba kwa ulinzi, usalama na mambomengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwa MheshimiwaJenista, ilikuwa ni shilingi bilioni mbili, ukiongeza shilingi bilioni39 inakuwa ni shilingi bilioni 41, sijui ni sheria ipi hiyo? Piareallocation yake tunataka tujue imekuwa reallocatedkutoka kwenye kifungu kipi kuja kwenye hizo shilingi bilioni39? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine nimesema kwanguissue siyo sheria zaidi, lakini unaenda kuwekeza huo uwanjamkubwa pale Chato wa runway zaidi ya kilometa tatu nindege gani inaenda kutua pale kubwa hivyo? Hiyo ni misuseya hela za walipa kodi wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikajiuliza mara mbili, leotunasema kwamba Serikali inahamia Dodoma, of which Isupport 100%; Makamu wa Rais anahamia Disemba,Mheshimiwa Rais tunaambiwa anahamia mwakani. Bungela Kumi tulipitisha uwanja wa Msalato ujengwe mpaka leohaujajengwa, Rais akija hapa tunatarajia wakija wale Marais,like Trump akija hapa ana ndege ambayo ni Boeing 737 itatuahapa Dodoma au itaenda kutua Chato? Why don’t werethink tukaja tukajenga kwenye uwanja wa Msalato maanaitakuwa ni double cost kwa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo wanakuja Marais ambaowanatumia ndege kubwa, Rais Magufuli anaondokaDodoma kwenda kuwapokea Dar es Salaam maana hakaka-uwanja ka-Dodoma hakawezi kuwapokea. Kwa nini hizohela tusingeweza kujenga hapa Msalato, kule Chato

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

tumjengee uwanja wa kuweza kutua ndege ya kawaida likePrecision, Bombadier na ndege ya Serikali kuliko kujengauwanja mkubwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo ndiyo hoja yangukubwa au basi kama tunataka tuijenge Chato tungewezakujenga hospitali kubwa kabisa ku-save maisha yaWatanzania kuliko ku-sink shilingi bilioni 39 kwenye uwanjaambao hautatumika au tungeweza kujenga Chuo Kikuu palekama tunataka tuijenge ile Chato ikue vizuri, unliketulivyofanya sasa hivi. (Makofi)

TAARIFA

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: MheshimiwaMwenyekiti, Taarifa.

MWENYEKITI: Waheshimiwa, muda wetu ni mchachesana.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,waambie watulie watajibu baadaye.

MWENYEKITI: Bado tuna wachangiaji wengi, kwamaana hiyo, kuna watu watakosa kuchangia hapa sasa.Haya Mheshimiwa Innocent.

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nimpe taarifa Mheshimiwa Esther Matikokwamba ukiangalia geopolitics za East Africa na nchi zaGreat Lakes, kujenga uwanja Chato uko strategically located.Ukiangalia upande wa Ngara kuna deposit kubwa za nikelambapo katika Bara la Afrika hamna deposit kubwa kamailiyopo pale Ngara. Isaka kuna dry port, Serikali inajenga relikwenda Kigoma na Mwanza lakini pia kwenda Rwanda. Kwahiyo, kwa upande wa miundombinu kujenga uwanja Chatoni kuweka miundombinu ambayo inashabihiana katikakukuza uchumi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, ameshakuelewa. (Makofi)

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

Mheshimiwa Matiko hebu kaa kidogo. MheshimiwaMwinyi, wewe ni rubani mzoefu sana na mimi ni ex-engineerwa ndege. Uwanja wa Dodoma, hebu tueleze kwa uzoefuwako 3,000 metres Boeing 757 inatua au haitui?

MHE. CAPT. ABBAS ALI MWINYI: MheshimiwaMwenyekiti, kwa kweli haiwezi kutua, haitui. (Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Sawa, lakini Trump akija haji na ndegeanakuja na Helicopter One. Haya, Mheshimiwa Matiko.(Makofi)

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ndugu yangu Mheshimiwa Innocent pale, mtani wangu,kwanza taarifa yake siipokei lakini pili, ngoja nimsamehenilikuwa nampa dongo moja ila nimsamehe, niendeleekuchangia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Innocentnilimuona juzi wakati Rais amezuru kule, anapiga magotikumuomba shilingi bilioni 30 za maji. Wajibu wako kamaMbunge ni kuisimamia Serikali hela za walipa kodi zije zifanyekazi kule, not to kneel down before the President ili uwezekuletewa mradi wa maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea, Chato bado,tumeona ujenzi wa traffic lights pale Chato, nikajiuliza hawawatu wanamuogopa Magufuli kwa nini wasimshaurivilivyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nini dhima kubwa ya hili,ukiangalia kuna miji mingi na ina high congestion ya magarileo mmeenda kujenga Chato na kuna picha niliona sitakikuamini kama kweli ni ya kule lakini nilivyopita mimi Chatosikuona kama kuna congestion kubwa ya magari mnawekatraffic lights Chato, wanapita punda. Misuse of funds zawalipa kodi wa Tanzania wakati tuna majengo ya shulehajajengwa, hospitali nyingi zinakosekana wamamawajawazito wanafariki hakuna huduma proper, mnaendakujenga traffic lights za Chato. (Makofi)

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo ndiyo the only waykwa kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda kama ingeendavizuri, tungewekeza kwenye kilimo tungeweza kufikia hiindoto ya Tanzania ya viwanda. Ukiangalia bajeti ya ruzukuya mbolea na mbegu ya mwaka 2015/2016 tuliweza ku-allocate kwa kaya zaidi ya 900,000 lakini ukija 2016/2017 tume-allocate ruzuku ya mbolea na mbegu kwa kaya 370,000 tu.Leo tunasema tunaleta ukombozi kwa hawa Watanzaniahalafu wakilima wanataka kuuza mazao yao, mnawazuiabadala ya kuwatafuta masoko. Mwaka 2015 kahawa Tarimeilikuwa inauzwa shilingi 2,000 kwa kilo leo ni shilingi 600 halafutunasema nini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mpango nawatu wako wanaokushauri naomba ukae uangalie vizuri nijinsi gani tunaweza ku-move na haya ambayo tunakupa hapakama Wabunge myafanyie kazi ili Tanzania tunayoitakaiweze kufikiwa. Nina imani kabisa kwa vivutio ambavyoTanzania tumepewa, tungewekeza kwenye utalii kwa nchihii tusingekuwa wategemezi tungeweza kujitosheleza kabisa.Tuna vivutio vingi vya kitalii ambavyo vingi havipatikani hatakwenye mataifa mengine lakini tume-underutilize, kwa nini?Ni kwa sababu priority zetu zinaenda kwa kinyume, we arethinking backward. Leo TTB ingepewa fedha za kutoshaingeweza kutangaza utalii wetu.

MWENYEKITI: Nimekuongezea dakika mbili zile zamisukosuko. (Kicheko)

MHE. ESTHER N. MATIKO: Ooh! Nakushukuru sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungeweza kuiwezesha TTBkupitia Tourist Development Levy tukapeleka fedha nyingi ilisasa waweze kuvitangaza vivutio vyetu na kufanya wajibuwao kama inavyotakiwa. Leo unakuta TTB wakiomba fedhaili waweze kujiendesha wanapata chini ya asilimia 30,tunashindwa kuvitangaza vivutio vyetu. Ukiangalia tunabeaches nyingi sana, kuna nchi zingine zinajiendesha kwavivutio vya utalii walivyonavyo ambavyo ni vichache

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

ukilinganisha na Tanzania. Sisi Tanzania aliyeturoga nadhanialishafariki, tulishapewa laana ambayo haifutiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukae tujitafakari sisi kamaWabunge wa Bunge la Kumi na Moja tukiondoka tutakuwatumeisaidia vipi nchi yetu. Ni wengi humu wanasafiri nchimbalimbali ikiwemo Mawaziri, mnaposafiri huko mnajifunzanini ambacho mnakileta Tanzania ili tuweze kukitumiakuhakikisha kwamba nchi yetu ina-move? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Deni la Taifa. Nazungumziadeni la ndani, kuna wakandarasi ambao wanaidai Serikali…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Kapufi naajiandae Mheshimiwa Mwalongo.

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Na mimi nianze kuchangia Mpango huu kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la kwanza ni eneo lakilimo. Mimi eneo la kilimo naomba niliweke katika surazaifuatazo. Namwomba Mheshimiwa Waziri mipango yetuna kama ambavyo mmeeleza hapo iendelee kujikita katikakuzingatia tafiti mbalimbali. Nalisema hilo kwa sababugani?

Leo hii isitokezee kwamba kwa sababu korosho inabei kubwa basi kila mtu akatamani kulima korosho, twendekwa tafiti. Kwa misingi hiyo kama ambavyo nimeendeleakusema hapo kwa kupitia tafiti tunaweza tukafahamu nikanda zipi zinafaa kitu gani na isitokezee tu kwamba kwasababu leo pamba ina bei nzuri basi kila mmoja akatakakulima pamba, naomba mipango ituelekeze huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, eneohilo hilo la kilimo upande wa mahindi ambao kila mmojaamezungumzia hapa, mimi nitatoa mfano na wanasema

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

kama huna vielelezo, haujafanya utafiti usiongee, naombaniongee kwa vielelezo na kwa utafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nililima maharagelakini baada ya kulima maharage nikafanya maoteokwamba mahindi yatanipatia pesa nzuri, kwa hiyo, nikabilishamaharage kununua mahindi. Ni mkulima mimi niliyelimamaharage, lakini nikanunua mahindi, nikayahifadhi kwamaana nipate fedha nzuri kwa maana ya maoteo. Leo hiinisipopewa nafasi ya kuuza mahindi yangu, sitokuwa nanafasi ya kulima tena hata maharage, nitakuwa nimekatwamiguu.

Kwa hiyo, naomba sana katika maeneo hayo, walewote ambao wamelima mahindi wapewe nafasi vinginevyotutakwenda kutengeneza mazingira ya watu hao kutowezakusimama kwa miguu yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua kwamba nusu ya2017 kilimo kilichangia kutoka asilimia 2.7 mpaka 3.1,umuhimu wa kilimo uko pale pale. Nafahamu kwamba kwakupitia kilimo ni sehemu kubwa ambayo inaajiri Watanzaniawalio wengi, lakini mipango iendelee kutusaidia. Kilimo hikiambacho ni cha kijungujiko (hand to mouth) sort of economy,tunatakiwa tutoke huko. Haiwezekani ikawa Watanzaniawengi wako kwenye kilimo lakini mwisho wa siku kilimo hikikisifanye watu tujitegemee. Ni bora hata wachachewakalima lakini wakalima kilimo chenye tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa niongeleesuala la afya. Nilishauri mara ya mwisho, ni kweli nimeonahospitali kama ya Muhimbili na Bugando tunaendelea kuzipavifaa tiba na kuongeza vifaa mbalimbali. Ushauri wanguunabaki pale pale, tuna mipango ya kuboresha Hospitali zaMikoa, mimi binafsi natoka Mkoa wa Katavi, tukiboreshaHospitali za Mikoa tunapunguza msongamano wa watukwenye Hospitali hizo za Bugando, Muhimbili na kwingineko.Kwa hiyo, niliombe sana hilo tuendelee kufanyia kazi kwamaana ya kuboresha maeneo haya ya chini. Ukiniboresheamimi Katavi, ukimboreshea wa Kigoma na wa Tabora

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

tutapunguza watu kutegemea maeneo hayo. Eneo la afyanaomba nitoke kwa sura hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la maji. Itakuwa nikichekesho, mara ya mwisho nilizungumza hapa pianikasema nchi hii tuna uwezo wa kufanya muunganiko wamaji kuwa kama design ya buibui. Mtu wa Nyasaakiunganishwa kupitia Ziwa Nyasa na Viktoriawakiunganishwa kupitia Ziwa Viktoria, Tanganyikatukiunganishwa kwa kupitia Ziwa Tanganyika, nchi hii itakuwana mtandao wa mabomba ya maji. Hatuna sababu yakwenda kwenye vyanzo ambavyo siyo vya uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi leo hii katika Mkoa waKatavi tunazungumzia habari ya Bwawa la Milala na chanzokingine cha Ikorongo wakati Ziwa Tanganyika lipo kilometa120 kufika Manispaa ya Mpanda. Miradi mingine tunayoionaya kutoa maji VI-ictoria iwe ni dira kwenye maeneo mengine.Hatuna sababu, nimesema kwingineko duniani watuwanabadilisha mpaka maji ya bahari kuwa maji safi yakunywa, sisi hatutakiwi kufika huko kwa sababu vyanzovingine vya maji safi, baridi ya kutumia tunavyo, ni mipangotu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la misitu, naombaeneo hili nilizungumze kwa kina. Leo tunazungumzia miradimbalimbali, tukizungumzia hata suala la Stiegler’s Gorge nakwingineko. Nilifarijika sana mtaalam mmoja majuzi katikasemina ile tulipokuwa tunazungumzia suala la Sera ya Taifaya Misitu alipotuambia pasipo misitu hata suala la umemetunaouhitaji hautokuwepo, habari ya Stiegler’s Gorge nakwingineko kwa sababu maji hayatapatikana. Hatatukizungumzia suala la utalii, lina uhusiano wa moja kwamoja na misitu kwa sababu kwa kupitia misitu kunabiodiversity ambayo hiyo moja kwa moja inakwenda namasuala ya ecosystem, tukikosea hapo iko shida kubwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nikuombeMheshimiwa Waziri kwenye mipango yetu tuendelee

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

kuboresha suala hilo la misitu. Leo mkizungumzia mipangoyote, yawe ni mabwawa ama vitu vingine bila kujikita kwenyekuhifadhi misitu, tatizo ni kubwa, umeme hatutokuwa naona wakati mwingine hata kilimo pia itakuwa shida na eneohili naomba tuendelee kupewa elimu pana. Wakatimwingine ukiona miti imetunzwa sehemu, sio kwa sababuanatakiwa mnyama awe pale, ni kwa ajili ya kutengenezabiodiversity pamoja na ecosystem ambayo ina nafasi kubwakwenye kumsaidia binadamu. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa muda wako umekwisha,chama kimeleta maelekezo na ninyi mtapunguziwa mudakwa kuongeza wachangiaji. Kwa hiyo, muda wakoumekwisha lakini nikupongeze kwa mchango mzuri naumewatendea haki wana Jimbo kwa mchango mzuri,ahsante. Mheshimiwa Mwalongo, ajiandae MheshimiwaMwambalaswa. (Makofi)

MHE. EDWARD F. MWALONGO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Awali ya yote,nimpongeze Mheshimiwa Waziri kwa kutuletea Mpango huuwa maandalizi ya maendeleo wa mwaka 2018/2019.

Pia nitakuwa ni mchache wa fadhila kamasitampongeza Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwakazi nzuri ya kuiendesha na kuisimamia nchi yetu. Sisi Wana-Njombe kwa maana ya Jimbo la Njombe tunamshukuru sanaMheshimiwa Rais kwamba tumepata mafanikio makubwakatika kipindi chake, tunajengewa kituo cha kisasa kabisacha afya katika Kijiji cha Ihalula chenye thamani ya shilingimilioni 500, tunajengewa soko la kisasa katika Mji wa Njombelenye zaidi ya shilingi bilioni nne lakini pia tunajengewa stendiya kisasa kabisa katika Mji wetu wa Njombe. (Makofi)

Kwa hiyo, hayo ni mafanikio mazuri na nampongezasana Mheshimiwa Rais na tunamshukuru sana kwa kutupatiahizo fedha za maendeleo. (Makofi)

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na kuchangiaMpango wa Maendeleo ambao upo mbele yetu, sisi Njombetunaitwa Njombe Mjini, lakini ni wakulima, kwanza kabisanianze na suala la wakulima. Watu wengi wameongeleasuala la mahindi, ni kweli kabisa suala la mahindi kiuchumi,mfumuko wa bei katika nchi yetu unashikiliwa na mahindi.Kama Serikali inaliona hilo na inataka kweli wananchi hawawanaolima mahindi waweze kunufaika na kilimo, lakinivilevile waisaidie Serikali kuweza kushikilia mfumuko wa beibasi ihakikishe kwamba Serikali inawekeza vizuri kwawakulima kwa maana ya kuwapa pembejeo, wataalam waugani na mbegu zilizo bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale Njombe kuna Kituo chaUsimamizi wa Mbegu Bora, kituo kile kina wataalamwachache, kina gari moja linatumika Kanda nzima kwa ajiliya udhibiti wa mbegu. Sasa hawa wakulima wanaolimamahindi na kile kituo ndio kinadhibiti mbegu za aina zote zampunga, mahindi na kahawa, kwa kweli inaonekanakwamba tunafanya tu kwa sababu sheria imesema, lakininia ya dhati ya kusaidia wakulima inaonekana haipo,wakulima wanauziwa mbegu fake, wanaletewa mboleazisizofaa na kadhalika. Niombe sana tuimarishe huduma kwawakulima wakati tunatambua kabisa kwamba mahindi ndiyoyanayoshikilia shilingi ya Tanzania iweze kuwa imara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiendelea kwa suala lawakulima, lipo zao la viazi Njombe ambapo vinadhurikasana. Viazi tunalima Mkoa wa Njombe lakini vilevile Mkoawa Mbeya, Tanga na Kilimanjaro. Viazi vya Tanzaniavinaathiriwa sana na viazi kutoka nje hasa katika ujazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu niombe sasa Serikalikupitia Idara ya Vipimo tutengeneze mifuko maalum kwaajili ya zao la viazi. Mazao mengine kama kahawa na koroshoyana magunia na viazi tuwekwe mifuko maalum ya viaziambapo unajua kabisa piga ua mfuko huu hauzidi kilo 90na huo ndio mfuko wa viazi, yeyote atayekutwa sokoni namfuko tofauti na ile maana yake huyo awe ni mhalifu,itakuwa imeasaidia sana wakulima.

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

Mheshimiwa Mwenyekiti, lipo zao la parachichi katikaJimbo langu la Njombe Mjini, parachichi za Njombe ni zaexport. Mwaka huu tume-export tani 700 lakini kwa bahatimbaya sana tuna-export kwenda nchi jirani na wale wa nchijirani ndio wanapeleka Ulaya. Niiombe sasa Serikali itusaidie,wakulima hawa wa parachichi kwanza kabisa wapatiwembegu bora, lakini pia tupate wataalam kutoka Serikalinikwa sababu parachichi hizi ni za export maana yake tayarizitatusaidia kupata fedha za kigeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kwambatatizo kubwa la parachichi ni kwamba hatuna pack house.Katika Halmashauri yetu tuna pack house moja tu na hawawanaokuja kutoka nchi za nje kuchukua parachichiwanakuja na magari yao maalum yenye ubaridi. Kwa hiyo,Serikali ione kwamba kuna nafasi ya kuwekeza kwenyemiundombinu ya ubaridi ili kusudi wananchi wanaolimaparachichi waweze kupata mahali maalum pa kutunzia hiziparachichi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kutokana namfumuko wa kilimo hiki, wananchi wengi wameitikia sanana parachichi zinaendelea kuongezeka. Itusaidie kwambasasa parachichi ziwe exported kutoka Njombe kwendamasoko ya nje Ulaya na kadhalika lakini tukipeleka Kenyamaana yake wanatulipa Tanzanian shillings halafu wao ndiyowanapata dola na sisi hapa tuna shida kubwa sana ya dola.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambaonapenda kuliongelea ni umeme. Upo umeme wa REAAwamu ya Tatu lakini vilevile lipo suala la TANESCO. TANESCOndiyo wanaweka umeme katika maeneo ya mijini paleNjombe tuna vijiji vilivyo karibu na mji kilometa tano kamaItulike havina umeme na havina umeme kwa sababu havimokwenye REA, lakini vilevile vinatakiwa viwe TANESCO nauwezo wa TANESCO wa kupeleka umeme uko chini sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe kwenye bajetiitakayoandaliwa tuone TANESCO wanavyopewa miradi yamjini angalau wapewe miradi unayokwenda mpaka

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

kilometa tano, wanapewa mita 700, 600 au 300. Sasa utaonavijiji vilivyo karibu na mji havipati umeme, kwa hiyo, niombesana hilo liangaliwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, i l i tuweze kufanikiwakiuchumi tunahitaji barabara nzuri. Katika Jimbo langu laNjombe Mjini iko barabara inayoenda Ludewa inaitwabarabara ya Itoni – Manda. Awamu zote za uongozizimekuwa zikiisemea barabara hii iwekwe lami, lakini mpakaleo katika Jimbo langu kazi hii ya kuweka lami haijaanza.Niombe sana katika Mpango ujao basi litekelezwe hili kwasababu barabara hii inasaidia wananchi kusafirisha mazaoya kilimo lakini inasaidia vilevile huduma mbalimbali kwaWilaya ya Ludewa na kuendelea mpaka Ziwa Nyasa huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la elimu,tunahamasisha viwanda lakini tusipowapa elimu watu wetuhapa tunarudisha umanamba. Vijana hawa wataingiakwenye viwanda hivi watafanya kazi ya kupanga vitukwenye maboksi na hatutajivunia kwamba vijana wetuwamepata ajira, itakuwa wamepata ajira lakini watakuwawamepata ajira ya kijungujiko na yenye manung’uniko.Watakuwa watu wa kuhangaika tu kukunja mashati kuwekakwenye mifuko, tuwape elimu vizuri ya ufundi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika elimu ya ufundiambayo tunapaswa kuwapa vijana hawa iko elimu inaitwaindustrial maintenance. Katika industrial maintenance vijanawatajifunza mambo yanayohusiana na marekebisho yamitambo mbalimbali ndani ya viwanda. Leo hii VETA mtaalawanaotumia kufundisha, wanafundisha watu kutengenezavigae vya moto wa mkaa, ndiyo ataenda kufanya kazikiwandani huyo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango mzuri, Jimboniwamekusikia unavyowatetea. Tunaendelea na MheshimiwaMwambalaswa kwa dakika saba.

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Napenda nichukue nafasi hiinimpongeze Waziri wa Fedha na Mipango, Naibu Waziri nawataalam wote kwa kazi nzuri. Nia ya kuuleta Mpango hapaBungeni ni kuujadili na kuuboresha ikiwezekana, kwa hiyo,sidhani kama kuna Mbunge yeyote ambaye anaudhihaki nakuukejeli, kazi yetu ni kuuboresha na kuujadili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna Mbungemwenzangu ambaye hajui tunu za Tanzania nataka nirudiemimi. Tunu za Tanzania ya kwanza ni lugha yetu ya Kiswahili,ya pili Muungano wetu, ya tatu ni utu na udugu wetu na yanne ni amani na utulivu. Hizi tunu hazikuja Tanzania kwabahati mbaya, viongozi/waasisi wetu walitumia nguvu naresources nyingi sana kuzi-inculcate kwa Watanzania na ndiyomaana Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa duniani kwasababu ya hizo tunu nne. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa zinapoanza kutokeakauli za kutugawa kwa majimbo na ukanda humu ndanizinasikitisha sana. Unajua sisi Wabunge ni viongozi na kiongozikwenye jamii yoyote watu unaowaongoza wanapendakuiga lile unalosema na unalotenda. Kwa hiyo, tunayoyasemahumu watu wetu kule wataiga. Naomba Bunge lako hizi tununne tuzilinde kwa nguvu zetu zote, ahsante sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niongelee kidogoMpango aliouleta Mheshimiwa Mpango. Ameanza namiundombinu kwamba inasaidia kuchochea maendeleokwenye nchi kama Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye umeme.Nimeona miradi mingi ya kuongeza uzalishaji wa umemekwa sababu umeme ni driver kubwa ya kuchocheamaendeleo ya uchumi. Stiegler’s Gorge itazalisha megawati2,100 ikikamilika, na source kubwa ya maji ya mtounaokwenda kulisha Stiegler’s Gauge ni Mto Ruaha. UkiuonaMto Ruaha ulivyokuwa mwaka 2008 na ukiuona leo,inasikitisha.

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

Kwa hiyo, naiomba Serikali inapopanga kwendakuweka mtambo wa kuzalisha umeme pale Stiegler’s Gorgeiweke mpango kabambe sana wa kufanya conservation yaThe Great Ruaha, vinginevyo tutakuwa hatuna maji yakuzalisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania tumejaliwa kuwana vyanzo vingi vya umeme, wengine wamesema asubuhijotoardhi, jua, upepo, naomba Serikali iangalie kote huko ilituweze kuwa na umeme mwingi wa kutosheleza viwandavyetu na umeme mwingi wa ku-export.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu wa Chinawameendelea mpaka kufika hapo walipo walikoanzia nimbali sana. Kwanza walikuwa na revolution ya kilimo, lakinibaadaye wakaona waanze viwanda vidogo vidogo,wakawapeleka vijana wao kwenda kusoma kokote kule njekwa gharama yoyote na waliporudi kwa fani ile aliyosomea,walikopeshwa fedha na vifaa waende kufanya hiyo shughuliambayo walisomea; hao ndio wameanzisha viwandaambavyo sasa hivi China ina mabilionea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani hata sisi, juziMheshimiwa Rais alikuwa Kagera, Kiwanda cha Kagera Sugarkinafanya vizuri sana; kimeajiri vijana wa Kitanzaniawanafanya kazi pale. Serikali inaweza ikafanya vivyo hivyo,ikawachukua vijana wa Kitanzania waliosoma, kama nikilimo, iwawezeshe, iwakopeshe, iwape ardhi waanzie kuletuwe na mapinduzi ya kilimo kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye maji, wenzanguwengi wamesema, miaka mitano, sita ijayo maji yatakuwani crisis sana duniani. Naomba Serikali ianzishe Wakala waMaji Vijijini na Mijini kama ilivyo kwa Wakala wa Barabara,kama il ivyo kwa Wakala wa Umeme na kama il ivyoTANROADS. Ni muhimu sana Serikali ianzishe Wakala wa MajiVijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika miundombinuambayo nilikuwa nimesema, nije kwenye reli ya kati ya SGR,

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

reli ya Tanga kwenda mpaka Musoma, reli ya kutoka Mtwarakwenda mpaka Liganga, lakini reli ya TAZARA ni reli ambayotayari ni standard gauge, inahitaji kuboreshwa tu nakuwekewa umeme. Naomba Serikali iangalie sana reli hii kwasababu nayo itaifungua nchi yetu kwa nchi ambazo zipokusini mwa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile reli hii itakuwa inapitakwenye dry port ambayo itaanza kujengwa pale Mbeya, kwahiyo tunakuwa na block trains za kutoka Dar es Salaamkwenda Kigali na Bujumbura. Kutakuwa na block trainskutoka Dar es Salaam kwa reli ya TAZARA kwenda Mbeya,kwenda kuwasaidia wenzetu wa Zambia, wa Malawi na waZimbabwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nirudie, tunu zaTanzania ni hizo nne nilizozisema, nimesema Muungano, Lughaya Kiswahili, utu na udugu na amani na utulivu. Bunge lakolizienzi na kuzilinda tunu hizi kama mboni za macho yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Ahsantesana. (Makofi)

MWENYEKTI: Ahsante, Mheshimiwa Paresso unandakika tano, Mheshimiwa Susan kwa dakika kumi.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia katikampango huu uliowasilishwa na Serikali hapa Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza, napendakushauri Serikali inapoleta mipango hasa kwenye miradimikubwa, isiwe na miradi mikubwa mingi ambayoitagharimu fedha nyingi tena za mkopo, lakini matokeo yakeinachukua muda mrefu. Ni vizuri mkawa na miradi michache,hata kama mtakopa lakini angalau iwe michache mwishowa siku iweze kuwa na ufanisi. Kama ambavyo mmefanyahapa, kuna miradi mingi lakini ukiangalia hata mipango yamiaka miwili nyuma iliyopiata hivyo vivyo, mmekuwa na

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

miradi mingi sana ambayo hata leo ukifanyia tathmini nafikirihakuna hata mmoja ambao tayari umeshaanza kuoneshamatokeo, lakini tena mmekopa maana yake mnaendeleakuendeleza Deni la Taifa.

Kwa hiyo, ushauri wangu ni bora muwe na miradimichache yenye matokeo ya haraka lakini itakayotumiafedha kidogo au hata kama ni nyingi lakini kwa ukopajiambao utakuwa si wa kiwango kikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, nichangiekatika Sekta ya Utalii. Pato la Taifa asilimia 17.2 inachangiwana Sekta ya Utalii. Maana yake ni kwamba asilimia 25 ya fedhaza kigeni inatokana na utalii. Lakini ukiangalia hapo kwenyempango ambao umewasilishwa na Serikali hamjatilia mkazowa kutosha wa namna gani sekta hii ya utalii ambayoinaingiza kiwango kikubwa cha Pato la Taifa inawezeshwaili kuhakikisha utalii huu ambao unaingizia fedha za kigeninchi hii uweze kuendelea kwa kiwango kikubwa. Mfano,umesema hapa Mheshimiwa Waziri, kuimarisha mifumo yaukusanyaji wa mapato yanayotokana na utalii. Maana yakeni kwamba mmekuwa mkizoea kuendeleza kuongeza kodikwenye sekta ya utalii au kwa watu ambao wanafanyabiashara ya utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana tuliwashaurihapa wakati tunapitisha bajeti kwamba mfute baadhi yakodi zilizopo kwenye utalii, hamkufuta, wenzetu wa Kenyawakafuta, sisi hapa tukaongeza. Maana yake ni kwambaunaendelea kufanya sekta ya utalii ni ghali sana hapa nchini,mwisho wa siku mzungu au mtalii yeyote atachagua kwendakwenye eneo ambalo ni rahisi na ataona vile vitu ambavyoanavitaka, kwa hiyo mkiwa mnashauriwa, Waziri mpokeeushauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mtu anayewekezakwenye hoteli za kitalii analipa kodi 46. Mheshimiwa Waziri nivizuri sana muwe na kodi chache ili watu wengi waingiekwenye kuwekeza kwenye utalii ili tuendelee kupata wageni

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

maana yake utalii utakuwa ni rahisi. Tulimshauri sanaMheshimiwa Profesa Maghembe kipindi hicho lakini hakusikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kodi nyingine ni ya TALAlicense, unalipa dola 2,000 kwa magari matatu. Uwe namagari 100 unalipa dola 2,000. Ni kwa nini msifanye kodi hiiikalipwa kwa gari? Ukilipa kwa gari maana yake utawa-encourage watu wengi wawe na magari, utalii utakua,ushindani utakuwa mkubwa, biashara itakua. Unalipa dola2,000, magari 100; wale Leopard Tours Arusha, makampunimakubwa wana magari 100 mpaka 200 lakini analipa dola2,000. Kijana wa Kitanzania aliyepambana amepata hela anamagari matatu analipa dola 2,000, hii ni nini MheshimiwaWaziri?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeishauri Serikali,tulimshauri sana Mheshimiwa Maghembe hapa hakusikiaakaendelea kushukilia msimamo huo, nafikiri ni vizurimuangalie hilo. Lakini sekta hii ya utalii pia imeajiri vijanawengi ambao walikosa ajira lakini wameji-engage huku. Kwahiyo, tunategemea kwamba jinsi ambavyo utalii utaongezaPato la Taifa ndivyo ambavyo wawekezaji wataingia kwenyesekta hii, ndivyo ambavyo pia vijana wetu wengi watapataajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viwanda, Serikali yaAwamu ya Tano mliingia kwa nguvu kubwa sana mkasemanchi hii ni nchi ya viwanda, Tanzania ya viwanda. Lakini sikuhizi wimbo huu umeanza kupotea, sijui mnaendeleaje,hausemwi kwa nguvu ile ambayo mlianza nayo mwanzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na matamko yakutafuta kiki za kisiasa. Mheshimiwa Waziri jana wamezindua,wanasema kila mkoa utajenga viwanda 100, maana yakemikoa 26 tunategemea kuwa na viwanda 2,600. Sasa hiviviwanda mnavyotamka, kwanza mtupe tafsiri yake, kwasababu akija Waziri wa Viwanda anasema vyerehani vitatukiwanda, akija mwingine anasema viwanda ni viwanda,mtupe tafsiri sahihi ya viwanda ni nini ili siku tunapowafanyiatathmini ya hivyo viwanda ambavyo mmekuwa

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

mkiwaambia Watanzania tujue ni viwanda kweli au siviwanda. Kwa hiyo msitafute kutafuta cheap kiki za kisiasakuwanufaisha Watanzania wakati sio sawasawa...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Susan, dakikakumi.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kukubali ombi la Mheshimiwa Paresso ilianiachie dakika kumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza na maswali, yaanini hivi, tunajadili hapa maswali yaulizwa Bungeni naMheshimiwa Dkt. Mpango yupo na anajua swali ganilikiulizwa karibu Bunge zima linasimama. Lakini unapokujakuweka mipango ili Watanzania wengi wanufaike unatuleteamipango ya kujenga reli kutoka Dar es Salaam mpakaDodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi ndiyo reflection yaWaheshimiwa Wabunge kwamba wao wanataka reli yaDodoma? Ni reflection ya Watanzania kwamba waowanataka kiwanja cha ndege cha Chato? Ni kweli nimatakwa ya Waheshimiwa Wabunge, wao wanatakabombardier? Kwa nini mnatufanyia namna hii? Kwa niniwakati Bunge watu wanauliza maswali katika mipango yanchi hii huangalii ni nini watu wanataka ndani ya Tanzania,sisi ndio wawakilishi wao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wanasimama wengikwenye maji, lakini leo unatuletea mipango ya maji ya vijijitotototo, wakati Tanzania tuna mito, tuna maziwa, tuna kilakitu. Kwa nini usituletee maji ya bomba, mpango ambaoutaonekana mnakwenda kutega sasa maji katika milima,katika mito ambayo tutakuwa na kilimo cha umwagiliaji namaji yatatiririka kila kijiji? Kwa nini mnakwenda kutuchokozeaardhi chini ili ituletee matetemeko ndani ya nchi ya Tanzania?

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

Kwani Mungu aliweka Mito hapa Tanzania alikosea nini?Naomba mipango inapokuja ndani ya maji usituleteemipango mingi ya visima. Tumia mito, maziwa ili tupate majiya umwagiliaji na maji ya bomba salama na kunywa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata umeme huo. Umemewa maji nasikia ni rahisi. Huko nyuma katika vitabu nilisikiasana wana mipango, kwa mfano kule Mlimba kuna mtomkubwa kabisa ambako unakwenda kumwaga maji mpakahuko Kilombero, mpaka Rufiji, huko kwenye Stiegler’s, lakinikule mmekusahau kabisa. Mlisema mtazalisha umemekwenye Mto Mpanga, leo katika mipango yenu hakuna kitu,mmedandia Stiegler’s Gorge. Nini? Tatizo liko wapi, kwa ninimnapanga mipango halafu mnaiachia njiani, kwa ninihammalizi? Kwa hiyo, mimi nilitegemea mipango iweendelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja kwenye gesi,Watanzania wote walijua sasa gesi imepatikana, tukasifiwahapa kwamba gesi sasa ndiyo mkombozi wa Watanzania,kila mmoja alijua baada ya miaka fulani gesi…, sasa hivimimi niko kwenye Kamati ya Nishati na Madini; gesi sasa hivini kitendawili, na wakati ule Mheshimiwa Mnyika alikuwaWaziri Kivuli wa Nishati na Madini alisema leteni mikatabaya gesi hapa Bungeni, mikataba mnayosema tofauti namliyoingia kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini leo utakuta eti Serikaliimedhamini Songas imekwenda kuchukua hela huko halafuSongas hawana chochote. Mitambo ya TPDC, mitambo yaTANESCO, lakini Songas kamuajiri tena huyo mbia Pan AfricanEnergy, halafu huyo huyo anaunasibu tena wa TPDC. Helatumekopa Tanzania; kuna gesi hapa?; halafu Serikali ndiyoinakwenda kulipa ule mkopo. Ule mkopo hailipi Serikali,inalipa kwa Watanzania, wapigakura wetu. Nini ninyi? Hayamambo gani mnatuletea hapa? Hizi figisufigisu hapa za nini?(Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kuna matatizomakubwa ndani ya nchi yetu. Labda kama unashinikizwa,

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

maana tumuonee huruma na huyu jamaa. Hapa unaambiwahii nchi hakijachakuliwa Chama cha Mapinduzi,amechaguliwa mtu mmoja, alichukua fomu peke yake, kwahiyo hata ukiwa Waziri ukibisha tu imekula kwako. (Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Susan, nenda kwenye hoja,usitumie maneno ya dhihaka Kanuni zikakubana, nakuombanenda kwenye hoja changia mchango wako ukimaliza kaachini, tulia uende nyumbani.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,sawa bwana, lakini Mheshimiwa Spika jana alisema tusemetu tusiwe na wasiwasi, sasa wasi wasi wa nini Wabunge waCCM, lakini na mimi mwenyewe si Mwenyekiti wangukaniambia niseme?

Mheshimiwa Mwenyekiti, shida za Watanzania kwamfano kule Mlimba na maeneo mengine ni kuunganishwabarabara za mikoa na wilaya kwa sababu Watanzaniawengi ni wakulima. Lakini leo Mheshimiwa Dkt. Mpangoatuambie, katika mpango huu unaokuja, je, ni barabarangapi nchini Tanzania zitakwenda kuanzishwa na kujengwakwenye viwango vya lami?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inasaidia nini? Inasaidiakwa sababu Watanzania wengi ni wakulima. Kwa hiyo,watapitisha mazao yao lakini itasaidia sana wanawakeambao wanajifungua katika mazingira magumu na Hospitaliza Wilaya ziko mbali. Haki ya Mungu wanaokufa nchi hii nivijijini. Kwa hiyo, barabara zitaokoa uchumi kwa wakulima,zitaokoa vifo vya akina mama na watoto. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukipata barabarainawezekana kabisa tutapunguza vifo vya akina mama kwasababu sera ya Taifa kila kata kuwe kituo cha afya, kila kijijizahanati. Hebu tuambie mpango madhubuti wa kutimizasera ya Taifa kwamba kuna vijiji vingapi nchini Tanzania vinazahanati, kuna kata ngapi zina vituo vya afya na mpangowa Serikali ni nini katika kutatua haya matatizo. Hatuwezikukubali wananchi wanakufa huko, hasa akina mama na

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

watoto. Tunaomba uje na huo mpango ili utuambietupunguze vifo, tuokoe akina mama na watoto na tuokoewakulima wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye elimu miminilitegemea uje na mpango, kwa kuwa tayari tuna vituo vyaJKT na hii tunasema kwenye nchi ya viwanda, ungekuja nampango hapa kwamba JKT itachukua vijana iwe darasa lasaba, iwe vyuo vikuu, watakwenda kufanya huko stadimbalimbali na kufundishwa uzalendo halafu wakitoka hukowanakuwa na package ya kuwakopesha kwendakutengeneza viwanda. Mngechukua hata wataalam kutokaChina, na hiyo ilikuwa Ilani ya CHADEMA, tulisema JKT itakuwasi tena mabunduki tu, kutakuwa na mpango maalum vijanakwenda huko kujifunza mafunzo mbalimbali ili kwendakuokoa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkopo wa reli, mmechukuamkopo mnajenga reli mpaka Dodoma, lakini TAZARAmmeisahau. Tatizo ni nini? Hii TAZARA inapita hata Selous,watalii walikuwa wanatoka Dar es Salaam wanakwendakwa treni mpaka Mlimba, au wengine wanapita kwabarabara mpaka Mlimba wanaingia Selous; lakini leobarabara hakuna, reli yenyewe haina uhakika. Tatizo likowapi? Uje na mpango katika kukuza utalii kule Selous ili hawawatalii waje kwa barabara au waje kwa TAZARA ili tuonekwamba tunakuza uchumi wetu.

Mheshimwa Mwenyekiti, afya nimeshazungumza. Kwaujumla naomba angalia hoja za Waheshimiwa Wabunge,angalia maswali ya Waheshimiwa Wabunge. Unapokuja namipango yako zikusanye ujue tatizo ni nini halafu ukija nampango elekeza kule ambako Wabunge wengi wanaletamaswali Bungeni ili tutatue haya matatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo mengine yabombardier na nini yatakuja tu, hivyo viwanja vya Chato, hiitumeshakula bogi umetuingizia huku mabilioni ya helawakati wengine hata maji hatuna, umetuingizia hukumabilioni ya hela, unakopa wakati sisi hapa ulitakiwa ukope

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

turudi vijijini kwetu tuwaambie tumekopa kwa sababutunajenga barabara, tumekopa kwa sababu tunajenga vituovya afya, tumekopa ili tujenge zahanati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tungekuwa radhi kabisakuiunga mkono Serikali kwa kukusanya kodi, tungefungamikanda kwa sababu tunajua mpaka kufikia mwaka fulanimatatizo ya maji litaisha, barabara pamoja na zahanatiyataisha, lakini sasa hivi hatujui hiyo mikopo itamaliza tatizogani. Sisi watu wa Mlimba hatuna shida ya ndegebombardier, hatuna shida ya kiwanja cha Chato lakinimadeni hayo yanatupata wote, hiyo si tabia nzuri, acheni.(Makofi)

MWENYEKITI: Haya umemaliza? Mheshimiwa SalumRehani, ajiandae Mheshimiwa Janeth Massaburi.

MHE. SALUM MWINYI REHANI: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Na mimi nashukuru kuweza kupatanafasi hii adhimu ya kuchangia kwenye Mpango huu wamwelekeo wa mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiangalia mpango katikanchi hii lazima uwe na vyanzo ambavyo vitawezeshautekelezaji, lakini vile vile utawezesha upatikanaji wa maptoya nchi hii; lakini vile vile utaonesha taswira ya mabadilikoya maendeleo. Mimi sina tatizo na mipango iliyokuwemokwenye masuala ya miundombinu, iko vizuri na tunakwendavizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini mpango mkubwaambao unatazamiwa uweze kuleta mabadiliko chanyakatika nchi yetu ni wa uanzishwaji wa viwanda mbalimbali,na hasa hivi ambavyo vimetangazwa na WaheshimiwaMawaziri katika kila mkoa. Navyo vimejikita kwenye uzalishajiwa kilimo na mazao mbalimbali ambayo tunategemeatuweze kuyachakata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimepitia hivi vitabu vyoteviwili, mwelekeo na mpango wenyewe uliopo bado kama

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

nchi hatujaonesha mwelekeo thabiti kwenye uzalishaji wetuukoje. Hakuna projections sahihi ambazo tunalenga kwambamwaka huu tutaweza kuzalisha mazao kiasi fulani. Kwabaadhi ya mambo tayari tumeshatoa maelekezo na ushauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tulikujatukaishauri hapa Wizara ya Kilimo na Serikali ijikite kwenyeuanzishaji wa mbegu mpya za pamba. Leo mikoa ya Kusinitumetoa maelekezo na tunatarajia kama kweli watawezakufanikisha ule mpango tuliokuwa tumewapa wa uzalishajiwa hekta zile zilizokuwa zimeshatengwa, tutaweza kupatampaka marobota kwenye 600,000; kitu ambacho kwauzalishaji uliokuwepo nyuma kilikuwa ni ndoto. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tukija kwenye upandewa mazao ya mahindi, bado Serikali haijaweza kusaidiakatika eneo hili. Mahindi kwetu ndicho chanzo kikuu cha kilakitu; chakula na viwanda ambavyo vimo ndani ya maeneoyetu. Lakini leo bado nchi haijaweza, kuanzia kwenye mbegutu ambazo tungeweza kuwapa wakulima wetu wakazalishakatika kiwango ambacho kinastahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, takiwimu za kitafizinaonesha kuwa asil imia 75 ya wakulima Tanzaniawaliozalisha mazao mbalimbali wanazalisha chini ya asilimia30 ya mazao ambayo wangetarajia kuyapata ya asilimia 100.Nina maana gani? Maana yangu ni kwamba kwamba kilawakulima 100 kama ingeweza kuzalisha gunia 40; kwa ekamoja mkulima huyu uwezo wake anazalisha gunia 12. Sasahapa bado hatujajipanga, wakulima wanatumia nguvu zaidimbegu bora haipatikani, mbolea bora haipatikani lakini vilevile na pembejeo za viuatilifu hazipatikani kwa wakati.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatakiwa ijipangeitie msukumu zaidi kwenye uzalishaji wa mbegu bora, kwenyeuzalishaji wa kuhakikisha kwamba tunazalisha mbolea katikanchi yetu. Lakini vilevile Serikali iweze kuhakikisha kwambaviwanda vile vya viuatilifu vilivyokuwa vimeanzishwa hapanchini vizalishe viuatilifu.

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kubwa zaidi nchiinatakiwa iweze kuwa na maono, kuwe na teknoloji ambayondiyo itaweza kututoa katika uzalishaji mdogo kwendakwenye uzalishaji mkubwa hatimaye kupata bidhaa au rawmaterials kwa ajili ya viwanda tunavyotaria kuvianzisha. Tunauzalishaji mkubwa wa chai katika maeneo yetu lakini ndaniya masoko ya nje Tanzania ni nchi ambayo inazalisha kidogosana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii chai sisi tunazalishakati ya tani 35,000 lakini wenzetu Kenya wao wako kwenyetani zaidi ya 400,000, lakini hizo 400,000 Tanzania sisitunachangia kuwapa Kenya bidhaa. Mimi niipongeze Wizaraya Kilimo kwa uwamuzi thabiti wa kuanzisha mnada wa chaindani ya nchi, na hii itawasidia sana Watanzania kile kidogocha pesa za nje zinazopatikana ziweze kutumika ndani yanchi. Ile chai iliyopo maeneo ya Iringa, Mbeya, Njombe namaeneo mengine kule Arusha na sehemu nyingine itawezakusaidia sasa kuanzisha soko la minada ya chai kamatunavyofanya kwenye minada ya kahawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vivyo hivyo kama nchitutaweza kuwashawishi wenzetu wa Malawi, WaburundiWarwanda kuunga katika huu mnada ambao tuliokuwa naohapa hivyo kuhakikisha kwamba tunapandisha bei ya chaikutoka shilingi 600 kwenda kwenye 1000 na zaidi. Wito wanguni kwamba Serikali ijikite kwenye vile vyanzo ambavyotutaweza kuongeza mapato zaidi kuliko kuangali kwenyemambo ya miundombinu tu peke yake. (Makofi)

Kuhusu mifugo, Tanzania tunazaidi ya ng’ombe milioni28 lakini kwa kweli katika uzalishaji wa maziwa hatumokwenye ramani ya uzalishaji wa maziwa; tunazalisha wataniwa lita milioni mbili tu ambazo vile vile hazina takwimu sahihi.Lakini Tanzania nchi moja ambayo inaagiza maziwa mpakakutoka Zimbabwe, hii kwa kweli ni aibu. Kitu ganitunachoweza kushindwa kukifanya ndani ya nchi hii kuwezakukauka maziwa na kutengeneza maziwa ya unga?Tukichukua hao indigenous breed tuliokuwa nao hatoi litamoja moja tu kwa ng’ombe milioni nane , lita milioni…

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Janeth Massaburi,ajiandae, Mheshimiwa Leah Komanya na ajiandaeMheshimiwa Chikota Abdallah. Mheshimiwa JanethMassaburi bado?

MHE. JANETH M. MASSABURI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wahuruma, si mwepesi wa hasira mwingi wa rehema ambayeyeye ndiye amenipa kibali kuwa katika Bunge hili leo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kipekee naombanimshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli,Rais wetu mpendwa wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzaniakwa kuniamini na kuniteua kuwa Mbunge katika Bunge lakoTukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru MheshimiwaSpika pamoja na ninyi Wenyeviti wote. Kwa kipekee vilevileniwashukuru Wabunge wote kwa mapokezi mazuri naupendo waliouonesha kwangu. Naomba Mwenyezi Munguazidi kuwabariki Wabunge wote wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania tuzidi kuwatetea wananchi wengi wa Tanzaniawalio wanyonge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikishukuru chamachangu, Chama cha Mapinduzi, chama chenye kuletamatumaini kwa Watanzania hasa wanyonge kwa kunileavyema na kunishauri, na hapa nilipo ni Chama changu chaMapinduzi ndiye mlezi thabiti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kuishukurufamilia yangu, wazazi wangu, watoto wangu, shemeji zangu,majirani ndugu na marafiki kwa kunilea na kunipa moyo nahasa wakati mgumu nilipoondokewa na rafiki yangu mpenziwangu Didas Massaburi. Mwenyezi Mungu azidi kumpokeakatika makao yake ya milele.

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mpango huu miminimeona kuna mambo mazuri mengi, lakini si maanakwamba yote ni mazuri tu na ndiyo maana kuna miakamitano ya kujisahisha na ndiyo maana kuna bajeti za kilamwaka, penye mapungufu unajaza, unatoa wazo la kuletamanufaa.

Katika mpango wa miaka mitano (2016/2017 - 2020/2021) wametenga kanda tano maalum za kiuchumi. Kunaeneo maalum la uwekezaji la Bagamoyo hilo liko Mkoa waPwani, lengo kuu ni kujenga bandari ya kisasa ambayoitaruhusu meli kubwa na eneo hili litakuwa lango kuu labiashara za kikanda na kimataifa, lakini kutakuwa pia naviwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kituo cha viwanda chaKurasini Dar es Salaam. Mradi huu pia utaimarisha ushirikianowa kibiashara kati ya Tanzania na mataifa mengine kupitiauwekezaji katika miundombinu ya kubiashara na ujenzi waviwanda; huo kumbuka ni Mkoa wa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu kuna maeneomaalumu ya uwekezaji ya Mkoa wa Kigoma. Lengo kuu lamradi ni kuwa na eneo maalumu wa uwekezaji llitakalokuwana bandari huru (free port). Kutakuwa na mitaa ya viwanda,kongani za kitalii na kituo cha biashara. Hili limetengwakutumia vizuri fursa za kijiografia ambayo itaweza kuhudumianchi za Kongo, Burundi, Rwanda na Zambia. Kumbuka niMkoa gani huo? Ni Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna eneo la uwekezajiMkoa wa Mtwara eneo hili pia kutakuwa na uwekezaji jumlaya hekta 110 ambazo zimetengwa maalum kwa lengo lakujenga bandari huru ambapo kuna kampuni ambazozinaendelea kufanya utafiti katika eneo lile na vilevilewatajenga viwanda, Mkoa wa Mtwara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tano ni Mkoa waRuvuma, kuna uwekezaji wa jumla ya hekta 2030 kwa ajili yaujenzi wa viwanda vikubwa (heavy industries)

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

vitakavyotumia malighafi ya gesi na chuma. Viwanda vyakuongeza thamani na mazao ya kilimo kama korosho naviwanda vya vito vinatoka Mtwara hii ni Mikoa mitanoPwani, Dar es Salaam, Kigoma Mtwara na Ruvuma hii Mikoayote inatoka Kanda ya Ziwa? Mikoa inatoka Chato?Tusipotoshe wananchi wetu, Watanzania wana akili sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna vipaumbele kwamwaka wa fedha 2018/2019. Miradi mikubwa ambayo naonainasemwana sana, mradi wa Stiegler’s Gorge naonaumekuwa ni mjadala mkubwa. Hata hivyo hiki ni chanzocha nishati ya umeme. Tumesema Tanzania ya viwanda bilaumeme hatuwezi kuwa na viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini vilevile kuna reli.Nakumbuka mimi katika Bunge la mwaka 2005 mpaka 2010kulikuwa na mjadala wa Bunge kuhusu reli, barabarazinaharibika magari makubwa yanatumia barabara kilamwaka kuna fedha za kutengeneza barabara. Sasa sisitunashauri Serikali inatekeleza, imekuwa kazi! Shirika landege… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango mzuri, ahsantesana, Mheshimiwa Leah ajiandae Mheshimiwa Chikota.

MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipatia nafasi hii jioni ya leo na mimi niwezekutoa mchango wangu katika mpango wa mwaka mmoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuanza naomba kwakuongelea utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Kwanzanianze kwa kuishukuru Serikali kwa kulipa madeni yawakandarasi wa miradi ya maji katika Halmashauri ya Wilayaya Meatu. Wakandarasi wamelipwa shilingi milioni 672 kwaajil i ya kutekeleza miradi ya maji. Nina aminiwatakapokamilisha wataenda kumtua ndoo mwanamke na

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

vijiji vya Lubiga, Itinje, Mwandoya, Igobe, Mwanuzi, Mkoma,Mwamalole na Bukundi vitanufaika na miradi hii ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni nipende pia kuongeleafedha za miradi ya maendeleo. Kumekuwa na upungufu wakutokuletwa au kuchelewa kwa fedha za utekelezaji wamiradi ya maendeleo. Hil i ni tatizo katika takribaniHalmashauri zote za nchi nzima. Miradi imekuwa ikitekelezwanusu nusu au kwa kusuasua au kutekelezwa kwa kipindi kirefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wamekuwawakitekeleza hatua yao ya utekelezaji wa miradi yamaendeleo. Hata hivyo Serikali imekuwa ama inaleta fedhakidogo za CDG ama kutokuleta kabisa fedha za CDG amakutokuleta kabisa fedha za CDG na kusababisa miradi mingikuwa viporo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano Halmashauri yaWilaya ya Meatu mpaka sasa ipo miradi viporo ya miaka 10,tisa na nane. Halmashauri ya Wilaya peke yake kwa kipindicha kuishia Juni, 2017 walikuwa na miradi ya viporo ya shilingibilioni tano na walitenga shilingi milioni mia tano zikiwa nifedha za CDG na mapato ya ndani kwa ajili ya kutekeleza.Kwa hiyo, nimshauri Mheshimiwa Waziri aweze kutenga fedhakwa ajili ya kukamilisha miradi iliyo viporo. Kama Halmashauriya Wilaya ya Meatu peke yake tu inadai shilingi bilioni tano,na kwa mwaka mmoja tu imepanga milioni 500; kwa hiyoitachua miaka 10 kukamilisha miradi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Meatu ilikuwa natatizo la uvamizi wa wanyama pori katika makazi yawananchi pamoja na mashamba ya wananchi nakusababisha vifo ama mavuno yao kuliwa na wanyamapori.Hata hivyo sioni jitihada yoyote inayofanywa na Serikali yakuwafidia wananchi ambao mazao yao yalikuwa tayarikuvunwa lakini yakaliwa na wanyama poli. Naiomba Wizarapia iweke mpango wa kulipa fidia hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais alisemaMkuu wa Wilaya ambaye ataleta tatizo la njaa latika Wilaya

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

yake ataonekana kwamba hatoshi; lakini sisi Wilaya ya Meatuwananchi wamejitahadi lakini wanyamapori wamekulamazao yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie kuhusuukamilishaji wa Daraja la Mto Sibiti. Ni muda mrefu sasawananchi wamekuwa na kiu ya kuona daraja hilo sasalimekamilika. Hata hivyo tangu Septemba, 2016 katika kikaocha ushauri wa Mkoa tulihaidiwa kwamba vyuma vyakufunga daraja hilo vinatengenezwa China, lakini mpakaleo ni mwaka wa zaidi vifaa hivyo havijafungwa natulihaidiwa kwamba masika hii tutapita. Mimi binafsinimekuwa mpitaji wa hiyo sioni dalili yoyote ya kukamilikakwa daraja hilo. Binafsi ninaona mradi unaenda pole pole.Kukamilika kwa daraja hilo kutainua uchumi wa Mkoa waSimiyu hususani katika Wilaya ya Meatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hata vifaa vyaujenzi vimekuwa vikipanda bei kutokana na mzungukokwamba vipite Shinyanga ndipo vije Mkoani Simiyu, lakinikukamilika kwa daraja hili kutakuwa ni mkombozi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie kuhusu elimu yabila malipo. Tunaishukuru Serikali kwa kuleta mpango waelimu ya bila malipo. Hata hivyo mpango huu umesababishaongezeko la udahili kwa wanafunzi na kusababisha upungufuwa miundombinu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Meatu kunachangamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu mpakakwenda kusoma na kusababisha mahudhurio kuwa hafifu.Kwa mfano shule ya sekondari Mwamaloe form one walianzawanafunzi 78, lakini waliohitimu ni wanafunzi ni 23. Moja yasababu iliyosababisha ni umbali mrefu. Kwa hiyo, wanafunziwaliacha shule kwa ajili ya umbali mrefu. Kwa maana hiyoninaomba shule ya bweni ya Wasichana ya Nyalanja ijengeweuwezo ikiwa ni kuongezewa mabweni pamoja...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango wako,Mheshimiwa Chikota, ajiande Mheshimwa Julius Kalanga,ajiandae Mheshimiwa Mwita Waitara.

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kutoamchango wangu kuhusu Mapendekezo ya Mpango waMaendeleo wa mwaka wa fedha 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nitaanza namchango wangu kipengele cha mazingira wezeshi kwauendeshaji wa biashara na uwekezaji na hasa sehemu yamiundombinu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hiikuipongeza Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi kwa kazikubwa inayoifanya katika ujenzi wa barabara katika nchiyetu. Pia kipekee nichukue nafasi hii kuishukuru Serikali kwakuanza barabara ambayo Wabunge wa Mtwara tulikuwatunaipigia kelele, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lamikutoka Mtwara – Nanyamba – Tandahimba – Newala hadiMasasi; barabara yenye urefu wa kilometa 210. Sasa hivimkandarasi yuko site anaanza ujenzi wa kilometa 50 kwakiwango cha lami kutoka Mtwara hadi Nnivata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni matarajio yetuWanamtwara kwamba mpango ujao sasa utaoneshamaendelezo ya ujenzi wa barabara hii. Tunatarajia sasa tuonekipande kingine cha kilometa 50 kutoka Nnivata kuendeleahadi Newala na hatimaye tukamilishe kilometa 210.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii ni muhimu sanakwa uchumi wa korosho. Tunapozungumzia korosho Tanzaniatunazungumzia Wilaya ya Nanyamba, Tandahimba, Newalana Masasi. Takribani asilimia 60 za korosho ya nchi hiiinazalishwa katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hiikuipongeza Serikali kwa wazo la kuanzisha Wakala waBarabara za Vijijini na Mijini (TARURA). Wazo hili ni jema, na

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

wazo hil i l itaharakisha ujenzi wa barabara ambazozinamgusa mkulima, zile feeder roads. Hapa ninaombaniishauri Serikali yangu, kwanza niwapongeze TARURAkwamba wameanza vizuri sana. Kuna Mtendaji Mkuu yupona Wakurugenzi wake wanaanza kuchakarika kwa kasikubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtandao wa barabara zaTARURA ni takriban kilometa 108,000. Mtandao huo nimkubwa na tukiendelea na formula ile ya zamani wa kwenyeRoad Fund yaani TANROADS wanachukua share kubwa kulikohii TARURA, sabini kwa thelathini, TARURA watashindwa maramoja.

Kwa hiyo ninaomba Mheshimiwa Waziri wa Fedhautakapokuja na mpango wa maendeleo wa mwaka 2018/2019 utueleze TARURA sasa itapata asilimia ngapi ya fedhaza Road Fund na TANROADS watapa asilimia ngapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na ningependekeza, kwasababu mtandao wa barabara wa TARURA ni mkubwa,kama nilivyosema ni takriban kilometa 108,000 tufanye nusukwa nusu; yaani 50 iende TANROADS na 50 iende TARURA iliikajenge barabara ambazo mkulima wan chi hii anatumiakila siku akiwa na baiskeli, bodaboda akibeba mazao yakena kupeleka shambani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu wa piliunahusu matumizi ya gesi. Wasemaji wengi sanawamechangia kuhusu gesi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado nchi yetu imejaaliwakuwa na reserve kubwa ya gesi, lakini kama walivyosemawachangiaji wengi hatujatumia hii fursa vizuri. Matumizi yakebado ni ya kusuasua. Mwekezaji aliyopo Mnazi bay (MNP)ana uwezo wa kuzalisha au kutupa cubic feet milioni 136kwa siku ili zitumike pale Madimba na Mtwara lakini kwasiku tunatumia cubic feet milioni 40 tu, kwa hiyo utaona nikiasi gani yule mwekezajia anazalisha lakini hakitumiki.(Makofi)

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaiomba sana Serikaliyangu kuongeza kasi ya matumizi ya gesi; mtumiajimmojawapo ni kiwanda cha Dangote. Hadi leo pamoja namaamuzi ambayo alitoa Mheshimwia Rais akiwa paleMtwara, kwenye ziara kwamba Dangote apewe gesi hadileo kiwanda cha Dangote hakujapewa gesi. Kuna urasimuusio wa lazima, hebu tupunguze urasimu tumpe Dangotehiyo gesi na kiwanda cha Dangote kikipata gesi hata bei yasaruji anasema itashuka mpaka shilingi 8,000 kwa mfuko, nahii itawasaidia Watanzania wetu. Kwa hiyo, naomba Serikaliyangu iongeze kasi ya kutataua changamoto ambazozinakwanza Dangote kupewa gesi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ukisoma Mpango waMaendeleo wa mwaka jana ulisema kuna mradi wa kujengamiundombinu ya kusambaza gesi majumbani kwa mikoa yaMtwara na Lindi, mradi huu hadi leo haujaanza. NaiombaSerikali yangu itoe pesa kwa TPDC ili mradi huu uanze. Mradihuu ukianza basi matumizi ya gesi yataongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti. kuna mradi mkubwa wakuchakata gesi na kuwa kimiminika ule wa Lindi, Mradi waLNG. Mradi huu kila siku tunaambiwa kwamba tupo kwenyemaandalizi ya eneo la mradi. Maelezo haya sasatumeyachoka ni ya muda mrefu tunaomba sasa tuwe nalugha nyingine. Ni mradi mkubwa na naomba Serikali iongezekasi ya kukubaliana na hawa wafadhili ili mradi huu uanze.Mradi huu ukianza utatoa fursa nyingi za ajira kwa vijanawetu wa Mtwara na Lindi na vile vile tutaongeza matumiziya gesi ambapo sasa bado gezi ipo ya kutosha lakinimatumizi yake bado ni ya kususua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusu maji;hakuna Tanzania ya viwanda bila maji ya kutosha. Tangumwaka juzi tukiwa Bungeni hapa tumeambiwa kuhusu miradi17 ya maji ambayo itapata ufadhili kutoka Benki ya India.Miradi hii itanufaisha miradi ya Makonde, Muheza, Njombena Zanzibar. Hadi leo hii tunaambiwa bado kusainiwafinancial agreement… (Makofi)

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango mzuri,Mheshimiwa Julius Kalanga hayupo, nafasi yake itachukuliwana Mheshimiwa Joseph Mkundi dakika tano na MheshimiwaWaitara dakika kumi.

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Kwa dakika zangu tano nitachangia mambomachache katika Mpango huu wa mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la kwanza, sotetunajua tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda kama kaulimbiu ya Serikali ilivyo, lakini hakuna namna yoyote kamawalivyosema wachangiaji waliotangulia kwamba tuelekeekwenye uchumi wa viwanda bila kufanya mapinduzi yakilimo. Kwa hiyo, ni muhimu sana kwanza tukaboresha kilimochetu na hasa aina ya kilimo tunachokifanya. Tuna vyanzovingi, tuna rasilimali nyingi lakini sasa ni namna ganitunatumia rasimali zile. Wamesema wachangiaji wengi,malalamiko ni mengi, wakulima wamelima mazao mengilakini hayawezi kuendelezwa na kuweza kusafirishwa iliwaweze kuimarisha uchumi wao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hoja yangu kwenyeeneo hili ni kwamba tuangalie ni namna gani tunavyowezakutumia rasilimali tulizonazo kuimarisha kilimo chetu nahasakujenga mfumo wa kilimo cha umwagiliaji. Kanda ya Ziwakuna Ziwa kwa mfano na maeneo mengine, lakini namnagani tunatumia rasilimali hii ya maji kuweza kutengenezakilimo cha umwagiliaji tuweze kuzalisha mazao ambayoyanaweza kutumika kama rasilimali kwenye viwanda vyetulakini hasa kuimarisha uchumi wa wanachi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni eneo la afya.Tunapoelekea kwenye uchumi wa viwanda, tunapojengamfumo wa kuimarisha uchumi wetu ni vizuri na ni muhumisana tukaimarisha afya za watu wetu vilevile ili wawezekushiriki kwenye uchumi huu. Lakini namna gani sasa maeneo

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

yetu na watui wetu tumewajengea mazingira ya kuimarishaafya zetu? Nimepitia mpango huu lakini sioni eneno lolotelinaloongelea kuendelea kutoa elimu kwa watu wetu katikakujikinga na maradhi lakini na kuimarisha mazingira ya afyakwenye ngazi za msingi. Tumeongelea kuimarisha Hospitaliza Rufaa na Hospitali nyingine za Mkoa lakini tunawezatukapunguza msongamano kwenye hospitali hizi kamatutaimarisha vituo vya afya na zahanati kwenye maeneoyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tutawekeza nguvukubwa sana kweye hospitali za level ya juu tukasahaumaeneo ya chini, bado watu wetu wanapoteza sana maishakule chini kwa sababau katika ngazi za msingi huku zahanatina vituo vya afya hazina uwezo, wataalam wa kutosha,vifaa vya kutosha kuweza kuimarisha afya zao. Vilevilehawana elimu ya kutosha kujikinga na maradhi. Kwa hiyo,kwenye mpango huu tuweke kipengele kinachojumuishakutoa elimu na kuongeza package kwa ajili ya kujengazahanati, kumalizia maboma yaliyojengwa huko nyumaambayo hayajakamilika ili tuweze kuimarisha afya kwenyemaeneo ya msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini eneno lingine ni enenola mawasiliano, kwa sababu hatuwezi kuimarisha uchumiwetu kama mawasiliano kwenye maeneo yetu hayako vizuri.Wamesema wachangiaji waliotangulia, haiwezekanikwamba tujenge uchumi ulio imara kama mazaoyanayolimwa hayawezi kusafirishwa kutoka point mojakwenda point nyingine. Maeneo yetu mengine bado hayakovizuri sana kimawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Mpango huuinaonesha kwamba kuna kuimarisha usafiri kwenye maziwayetu, lakini bado hatujaimarisha sana Shirika la Meli (MSL).Tungeweza kuimarisha Shirika hili tukaweza kuwapa uwezowa kutosha, watajenga mfumo mzuri sana wa mawasilianokwenye maziwa yetu na kwa maana hiyo sasa watu waliokovisiwani na maeneo mengine yaliyoko pembezoni wanawezasasa kusafirisha mazao yao kwenda kwenye masoko na hivyo

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

kuimarisha uchumi wa watu wao kimsingi kwenye maeneoyake yaliyo pembezoni. Vile vile kuweka mfuatano wa usafiriwa mazao na watu kwenye mazingira yetu. Bila kufanya hivyobado huu wimbo wa ujenzi wa uchumi ulioimara utakuwana kasoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ningeshauri,pamoja na mambo mengine yote yaliyoongelewa kwenyempango tuimarishe vilevile Shirika hili la Wakala wa Meli ilikuiweza kuwa na nguvu ya kutosha kuimarisha usafiri kwenyemaeneo ya maziwa. Kwa mfano sehemu kama kutoaUkerewe kuunganisha na sehemu ya nchi kavu, kunamatatizo makubwa sana ya usafiri wa meli, hali ambayoinafanya mazao mengi ya watu kutoka kwenye visiwa hivyokupotea na kwa maana hiyo kuathiri uchumi wao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nilifikiriniliongelee, wamesema…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waitara, ajiandaeMheshimiwa Bukwimba

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru, na mimi niungane na wenzangu wote ambaowanamshukuru Mungu kwa kuponywa kwa MheshimiwaTundu Lissu na anaendelea vizuri na afya yake inazidikuimarika. Lakini nianze na mambo machache ya jumla.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza kwenyevipaumbele hivi vilivyopangwa, nimeona vipaumbele vipokumi, ile kaulimbiu ya Serikali ya Tanznaia ya viwanda hai-reflect kwenye vipaumbele. Kwenye mpangilio huu viwandani kipaumbele cha kumi, maana yake kwenye mpangilio nicha mwisho kwa hiyo maana yake ni kwamba inawezekanatunaendelea kuibadilisha hiyo kaulimbiu ya Serikali ya Awamuya Tano. (Makofi)

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo jinginela jumlaambalo nadhani ningemshauri Mheshimiwa Waziri Mpangoalipokee ni kwamba mwaka wa jana mpango ulikuja wamwaka mmoja, na vipaumbele vilikuwepo na mwaka huuvimekuja tena. Tulishauri na mimi ningeomba nirudie tena,kwamba Mheshimiwa Waziri ni muhimu tukubaliane kwambahivi sisi kama Watanzania, kama Taifa tunaweza kupata kiasigani kwa ajili ya miradi yetu ya maendeleo? Ukishapatakiwango ambacho unaweza kupata kutoka whatever thesources kama ni nje, ndani, vyovyote vile tukubaliane nimambo gani machache ambayo yanaweza kutekelezwayakakamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na utakumbuka kwenyebajeti ile ilikuwa shilingi trilioni 29.5 lakini haikufika hata asilimia70 katika utekelezaji wake. Mwaka wa jana tena imekujashilingi trilioni 31.4 hatutafika asilimia 70 mpaka 80 kwamwenendo ulivyo mpaka sasa. Sasa maana yake ni kwambamipango mingi tuliyopitisha itakwama na hiyo kimsingi ndiyoinazua malalamiko mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu la jumlaambao nashauri hapa, inawezekana watu wanapotoamaoni kuna tafsiri tofauti, watu wanaleta hisia za ukandana nini, lakini ukweli ni kwamba kama kuna mipango, miradimbalimbali inatekelezwa ambayo miradi hiyo haikujadiliwakinagaubaga kwa uwazi Bungeni hapa watu watalalmikahakuna namna, yaani hiyo msikwepe. MwambieniMheshimiwa Rais wazi kama analazimisha mipangotunayotaka itekelezwe ni hii mliyoleta hapa tukapitisha,mkitekeleza hii hakuna atakayelalamika. Kwa hiyo, watuwasikwepe wasikimbie kivuli chao. Ni kwamba mipangoiliyopangwa itekelezwe, kama kuna mapungufu sheriainaruhusu na Katiba inaruhusu tuje tubadilishe mlete maombiinaruhusuiwa. Fedha kama ikipungua usitumie kinyemela,rudini Bungeni hapa, lete mapendekezo tutaridhia hichondicho ambacho Wabunge wanasema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kumekuwa nakauli mkanganyiko sana na hizo kauli ni jambo la jumla sana.

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

Kwenye miradi mbalimbali, Mheshimiwa Rais akisema kaulimaeneo mbalimbali watu wanashituka kwa sababuWatanzania wanajua kwa mujibu wa Katiba hii Raisanapatikana kwa kura nchi nzima na kanda zotezimemchangua. Kwa hiyo, unapoona kiongozi mkuu wa nchianakwenda mahali anatamka kauli ya kiupendeleo hiyowatu hawawezi kuishangilia, wataipinga, watalalamika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ninyi cha muhimuni kupokea mambo, mwambieni Mheshimiwa Rais kwambahuyu ni kiongozi wa nchi akizungumza tunataka atoe suluhuna tiba kwa kero za Watanzania hayo mahitaji yaWatanzania, kwa hiyo msikimbie kivuli chenu na walamsilalamike hapa kuna mjadala wa ukanda hakuna ukanda.Maneno yanayozungumzwa aidha na Mawaziri na viongozimbalimbali na Mheshimiwa Rais yanawagawa Watanzania.Kwa hiyo, mkifuta hiyo kauli, mshaurini kimya kimya ni muhimuabadilishe kauli za namna hiyo, azungumze kama Rais wanchi. Hayo ni mambo ambayo kimsingi hayana upendeleowowote myapokee na kuyafanyia kazi ni ushauri tu…

MWENYEKITI: Nenda kwenye hoja MheshimiwaWaitara.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,sasa…

MWENYEKITI: Rais hana upendeleo wowote.

MHE. MWITA M. WAITARA: …nilisema natoa ushauriwa mambo ya jumla sasa nakwenda kwenye Mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, habari ya umemekipaumbele cha kwanza, mimi Mheshimiwa Mpangonakushauri, kwa sababu kumekuwa na mpango wa umemewa REA na Watanzania wote na Wabunge wote wanasubiriumeme utekelezwe; umeona kuna malalamiko hapawanasema wakandarasi walitangazwa lakini baadhi yamaeneo hawaonekani tena, walizindua miradihaijatekelezwa.

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili ni muhimulitekelezwe likamilike kila mahali, kwa maana ya nchi nzima.Hauwezi kuzungumza habari ya viwanda; yaani umeme kwamatumizi ya kawaida haujakamilika, haupo maeneo mengini giza, kwenye shule ni giza. Kuna visima vya majivimechimbwa maeneo mbalimbali hauwezi kutumia majikwa sabbau hakuna umeme na hakuna uwezo wa kununuajenereta. Pelekeni umeme wa kawaida kwanza halafu hiyoziada iende kwenye viwanda, watu watakuelewaMheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni ujenzi wamiundombinu. Hawa Wabunge wanasema kuna maeneoambayo mpaka leo Mkoa kwa Mkoa haujaunganishwa,Wilaya kwa Wilaya haijaunganishwa, hilo jambolimezungumzwa mara nyingi. Kama unazungumza habari yaujenzi wa miundombinu nendeni mkamilishe uhakikishekwamba Mkoa kwa Mkoa kuna mawasiliano ya kutosha,Wilaya kwa Wilaya halafu uhamie kwenye ajenda nyinginemsiguse guse hapa na pale mnahama mnaacha viporo vingizaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala lamifugo. Kumekuwa na malalamiko, kwa kweli hii ni lanakubwa katika Taifa hili. Watu wote hapa mnategemea kulanyama na mifugo kwa kweli ni mali kubwa sana. Viatu nihumo humo, ni kila kitu lakini inawezekanaje sasa hivi mtuakiwa na mifugo inaonekana kama ni uadui? Yaani kunaugomvi mkubwa kati ya wakulima na wafugaji. Hakunamalisho ya wanyama, hakuna mahitaji muhimu katikamaeneo yale, mifugo inakufa, mifugo inachomwa na hilijambo mnalifahamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa mfano pale Dares Salaam kuna mnada mkubwa sana wa Pugu ambaounaitwa mnada wa kimataifa, lakini ukienda katika eneohili ukimwambia mtu wa kawaida kwamba ni mnada wakimataifa hawezi kukuelewa. Hata kama lile ndilo eneopekee ambalo Dar es Salaam wanalitumia kwa nyama lakinini eneo la hovyo. Hakuna josho, hakuna mabwawa, hakuna

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

vyoo, hakuna uzio, ratiba haijulikani, rushwa nje nje! Sasamambo haya ukiyazungumza watu wanasema kwambalabda ni kuituhumu Serikali, si kuituhumu Serikali tunasema ilimkayafanyie kazi, mkarekebishe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kuna ugomvimkubwa kati ya wafugaji na wakulima, ugomvi kati yawafugaji na hifadhi za wanyama. Wale watu wa hifadhiwanachukua mifugo ya wananchi, wanaitoa nchi kavuwanapeleka kwenye mapori, wanawatoza fedha nyingikweli kweli. Kwa hiyo, mpaka wale wananchi wanaofugawanaona kwamba kufuga ni laana wanaamua kuachanana ile biashara lakini watu wa vijijini ng’ombe ndiyo benkiyao. Ukitaka kuzungumza hapa elimu mtoto asomeshwehawa ambao wamekosa mikopo ya Bodi ya Mikopo maanayake mtu kama ana ng’ombe wake atauza ili asomeshemtoto. Sasa ng’ombe mmechukua, mmewatelekeza,wamekufa, wanachomwa na wananyang’anywa. Kwa hiyonadhani jambo hili lazima pia lifanyiwe kazi vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonimeliona hapa ni miradi ya maji. Mheshimiwa Kiwangaamesema hapa kwamba Mheshimiwa Waziri unatakiwauwe na akili ya kawaida, yakiulizwa maswali hapa na weweMwenyekiti asubuhi umesaidia maswali mengi kwenyeupande wa maji ni kwamba kama watu wanahoji sanamaana yake maji ni shida karibu kila kona. Ukisema hiviMbunge wa Dar es Salaam Ukonga utafikiri kuna maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kule kuna watu mpaka leowanachota maji kwa kutumia zile kata, mvua ikinyesha ndiyomaji wanayokunywa. Sasa jambo hili limekuwa wimbo wakila siku. Mheshimiwa Mpango wewe kama Waziri legacy yakoitakuwa ni nini? Tuambie basi angalau katika mpango huuumeweka miradi ile yote ya maji ambayo imeanzishwaikamilike, uibue miradi mingine mipya, Wabunge wakija hapatuache kupiga story ya maji kila siku kama watu ambaohatuna uelewa, tuzungumze jambo lingine. Ile miradimliyoanzisha kamilisheni, ile miradi mikubwa angalau basimwaka ukiisha utuambie mimi kama Waziri wa Mipango na

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

timu yangu nimetekeleza mpango huu umekamilika tukosemaswali. Hilo nafikiri ukilifanya utakuwa umetenda haki sanakwa Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani kila mwaka,kila Mbunge hapa, hakuna Mbunge ambaye halilii maji katikaeneo lake, umekuwani wimbo wa Taifa. Kwa hiyo,Mheshimiwa Mpango utusaidie, pangeni vipaumbele, kiliocha Wabunge kipokee, tekeleza ili maneno humu ndaniyaweze kupungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, susla la utawala bora. Miminilikuwa nataka nishauri, maendeleo haya hayawezi kujakama kuna hofu katika Taifa, kama watu hawana amanikatika shughuli zao, kama mtu anafunga duka. Hivi nimfanyabiashara gani mjinga ambae atakwenda kukopamkopo wa Benki, afungue biashara halafu mwanaumemmoja anasema kuanzia leo funga maana yake ukifungaduka lake akafungwa na yeye hawatawekeza MheshimiwaMpango, na wewe unajua ni mtaalam, hawatawekeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna watu ambao ni verysensitive kama matajiri ambao wana fedha zao. Anatakamahali ambapo kuna amani, utulivu na kuaminiana,anakuwa confortable na anawekeza katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa katika Taifa hili utawalabora na demokrasia imekuwa ni shida. Sisi hata haya mambotunayozungumza hapa tukitaka kukosoa tu kwamba datahizi si za kweli, Pato la Taifa figure hizi si za kweli unaambiwaukamatwe uwekwe ndani. Sasa lazima tujadili, maendeleoni pamoja na demokrasia, maendeleo maana yake ni uhuruwa kuzungumza, kupokea maoni. Kama mnafanya kazi nzurikwa nini mnakamata watu? Kwa nini watu watishiwe maisha?Kwa nini watu wapigwe risasi? Kama kunafanywamaendeleo, sisi tuacheni tuseme tunavyosema bila kuvunjasheria, bila ku-personalize mambo halafu ninyi mtende kazi.Muwaambie ninyi CHADEMA, CUF mlikuwa mnapiga kelelesisi tulitekeleza hiki na hiki, tushindane kwa namna hiyo.Fanyeni kazi tukose hoja.

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa hoja zipo nyingikweli kweli tunazoweza kuzijibu. Hoja zipo na hazina majibu,ni kwa sababu ninyi mna-concentrate kutushughulikia hapa,ni muhimu huu utaratibu uishe. Wekeni uhuru wa kutoamaoni, tuikosoe Serikali, tukosoe mipango ya MheshimiwaMpango halafu mkatekeleze mtuambie ninyi mlipiga kelelesasa sisi tumefanya moja, mbili, tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ya bure, bahati nzurimimi ni mwalimu kitaaluma. Hili jambo ni jema, wanafunziwameandikishwa darasa la kwanza wengi sana. Sasa shidailiyopo umezuka ugomvi sasa kati ya wazazi na walimu.Serikali ilisema elimu ni ya bure sasa…

(Hapa kkengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante!

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekitihaya lakini ilikuwa bado.

MWENYEKITI: Ahsante dakika kumi zimekwisha.Waheshimiwa Wabunge zimebaki dakika 45 ni za Wabungewatatu wa CCM, wamekubaliana kugawana muda. Kwahiyo Wabunge ninaowataja sasa wajiandae tutaanza naMheshimiwa Bukwimba, ajiandae Mheshimiwa Musa Ntimizi,Mheshimiwa Mipata, Mheshimiwa Jitu, Mheshimiwa Kanyasu,Mhesimiwa Dau, Mheshimiwa Kigua, Mheshimiwa Shekilindina Mheshimiwa Maige. Tunaanza na Mheshimiwa Bukwimbakwa dakika tano.

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangiakatika Mpango wa Taifa mwaka 2018/2019. Kabla ya hapokwanza nianze kwa habari ya uwanja wa ndege wa Chato.Mimi binafsi napenda kusema kwamba Chato iko Geita naGeita kuna watu lakini na kanda yote ile kuna watu, kwahiyo tunahitaji huduma ya kiwanja cha ndege. Kwa hiyo,Serikali haijafanya makosa kujenga kiwanja Chato kutokana

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

na shughuli za kiuchumi zilizopo kule. Sisi Wabunge nawananchi kwa ujumla tunahitaji kuwa na kiwanja tenakikubwa zaidi ya hicho. Kwa hiyo, niombe Serikali iendeleekuwekeza fedha zaidi ili kuwezesha ujenzi wa hicho kiwanjacha Chato kwa sababu kitawezesha wananchi wote waGeita, Kahama pamoja na sehemu mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku za nyuma tulikuwatunatumia uwanja wa Mwanza. Uwanja wa Mwanza ni mbalina wakati mwingine kuvuka feri pale unaweza ukakuta ferihaipo kwa hiyo unaweza ukachelewa hata ndege. Sasa hivikwa kuwa na kiwanja Chato kinaturahisishia maisha. Na sisini Watanzania vilevile kama Watanzania wengine ambaowana viwanja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la ujenzi wajengo la TRA kule Chato. Mimi nadhani tunatakiwa kujengavitu vya viwango. Kwa hiyo, mimi niipongeze TRA kwakujenga jengo zuri katika eneo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayoniende sasa katika Mpango. Nampongeza Mheshimiwa Waziripamoja na Naibu wake kwa kutuletea Mpango mzuri. Kwaupande wa barabara nilikuwa naangalia jinsi ambavyowamejikita kuangalia miundominu muhimu kwa ajili yakuwezesha uchumi wa kati, kulingana na Sera ya Taifa,kwamba tumejipanga kuwa na uchumi wa kati mpakakufikia mwaka 2025. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hiyo nilikuwanapenda kupongeza kwa upande wa barabara. Niombesasa kwamba kwa upande wa barabara ile Sera ya Taifa yakusema kwamba tutaunganisha kwa barabara za lami mikoakwa mikoa, lakini vilevile wilaya kwa mkoa. Kwa hiyo, miminilikuwa nashauri tuwekeze fedha nyingi kwenye upande huoili kuweza kuwezesha kuiunganisha mikoa. Kwa mfano kunahii barabara ya kutoka Geita ambayo inaunganisha Mkoawa Shinyanga pamoja na Mkoa wa Geita. Barabara kutokaGeita kupitia Bukoli kwenda mpaka Kahama ni barabaramuhimu sana kiuchumi. Kwanza ndio barabara inayotumika

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

na magari mengi yanayobeba mizigo mbalimbali kwa ajiliya kupeleka shughuli bidhaa kwenye shughuli za madinikatika mgodi wa GGM pamoja na wachimbaji wadogowadogo. Kwa hiyo, ninaomba barabara hii isisahaulikekwenye mpango ujao ili ianze kujengwa kwa sababu nibarabara ya muda mrefu imekuwa siku nyingiinazungumziwa lakini hatuoni utekelezaji wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ili tuweze kufikiauchumi wa kati lazima Serikali iwekeze kwenye kilimo. Kwamfano sehemu ambazo kuna maziwa pamoja na mitotuangalie kil imo cha umwagiliaji. Nikiangalia Getiatumezungukwa na Ziwa Victoria, tuanzishe miradi yaumwagiliaji ili kuwawezesha wananchi kuweza kuwa navyakula pia kuwa na uwezo wa kupata bidhaa ili ziwezekutumika katika viwanda vyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu upande wa elimu. Ilituweze kuwa na Tanzania ya viwanda lazima tuwekezekwenye elimu. Kikubwa zaidi, kuwianisha na Sera ya Taifa yakuwa na VETA kila wilaya mkoa. Niombe suala hili Serikaliiwekeze kwenye mpango, kwamba kila mkoa tuwe na chuocha VETA. Kuna wilaya na mikoa mingi ambako hatuna VETA.Kwa kuwa vijana wengi wanahitaji elimu ya VETA kwa hiyoniombe sasa kwenye mipango yetu na bajeti zijazo tuhakikishefedha zinatengwa kwa ajili ya kujenga VETA katika wilayana mikoa yote ili kuwawezesha vijana wetu kupata ujuzimbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa hivi tunatarajiakupeleka umeme kwenye kila kijiji…(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango wako…

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana.

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

MWENYEKITI: Mheshimiwa Musa Ntimizi ajiandae,Mheshimiwa Mipata, ajiandae Mheshimiwa Jitu.

MHE. MUSSA R. NTIMIZI: Nashukuru kwa kupata nafasina mimi pamoja kwamba ni dakika tano at least nichangiekatika Mpango huu ulio mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza nampongezaMheshimiwa Waziri kwa kuleta Mpango huu mzuri ambaona sisi kama Waheshimiwa Wabunge tunatimiza wajibu wetukatika kuongeza yale ambayo tunadhani yanaweza kusaidiakatika kuleta maendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango huu wa Taifaunajumuisha mipango midogo midogo tuliyokuwa nayokatika maeneo yetu, katika wilaya zetu, katika majimbo yetundio wanatengeneza mpango mkubwa wa Taifa letu. Mengiyameshazungumzwa lakini na mimi nilitaka niseme mambomachache kwa haraka haraka kwa sababu ya muda.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzangu wamezungumziaeneo la kilimo. Eneo la kilimo likitengenezewa mkakatimkubwa linaweza kusidia mapato ya nchi yetu, linawezakusaidia wakulima wetu, linaweza kusaidia wakulima wetu,wakapata mapato yaliyo bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi najikita katika zao latumbaku. Serikali lazima, lazima, lazima iangalie Mpangoulio bora wa kuliimarisha zao la tumbaku. Zipo changamotonyingi; lakini nataka niseme pamoja na juhudi zinazofanywana Serikali yetu bado zao la tumbaku halijamkomboamkulima na halijachangia vizuri Pato la Taifa. Kama zao latumbaku likisimamiwa vizuri linaweza likachinga katika Patola Taifa kwa kiasi kukubwa sana. Niombe sana MheshimiwaWaziri katika Mpango wako tuangalie namna ya kupata sokozuri la tumbaku nina hakika kabisa wakulima wetu kule tunawahamasisha wafanye kilimo ili waondokane na umaskini,wanaweza kuondokana na umaskini kwa kiasi kikubwakama zao hili la tumbaku litasimamiwa viilivyo vizuri zaidi.

Page 178: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

Halmashauri zetu zinategemea sana sana mapatoyanayotokana na kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu miundominu.Nipongeze kwa kuanzisha TARURA, lakini kama walivyosemawatu wengine TARURA inahitaji iwezeshwe kifedha ili kusaidiaujenzi wa barabara katika maeneo yetu. Unapohamasishaviwanda, viwanda hivi vinatakiwa vipate pembejeokutokana na mazao ya wakulima wetu. Wakulima wanalimavijijini barabara ni mbovu, kutoa mazao toka vijijini kuletakatika soko ni tatizo kubwa sana. Tukiimarisha TARURA,malengo yake yakatimizwa sawa sawa, mipango yake ikawamizuri nina hakika kabisa itatusaidia sana katika maeneoyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la afya, hilitunalizungumza kila siku. Tuweke mpango uliothabiti wakujenga vituo vya afya katika kila kata katika nchi yetu yaTanzania. Tunapoimarisha Hospitali za Wilaya na za Mikoahazitosaidia sana kama hatutoimarisha vituo vya afya katikakila kata, vituo vya afya vitasaidia kupunguza msongamanokatika Hospitali za Wilaya na katika Hospitali zetu za Mikoa,hili ni jambo la msingi sana. Katika mpango nimeonatunaimarisha sana Hospitali za Rufaa na za Mikoa. Lakinihazitosaidia sana kama wananchi wengi watakuwawanatoka katika zahanati zetu wanaenda moja kwa mojakutibiwa kwenye Hospitali za Rufaa. Wanatakiwa wakitokakwenye zahanati waende kwenye vituo vya afya il ikupunguza msongamano katika Hospitali zetu za Wilaya naza Mikoa; hili ni jambo la msingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni kuhusuwafugaji wetu. Wafugaji wakitengenezewa mpango uliobora wataleta pato kwa taifa, viwanda vyetu vitapatabidhaa za maziwa, ngozi na tutapata viwanda vyakutengeneza viatu. Hata hivyo leo wafugaji wanaonekanani adui katika nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wafugaji hawa ndio wapigakura wetu, lakini kama nilivyosema tukiangalia vizuri na

Page 179: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

tukawatengenezea mazingira yaliyo bora wafugaji hawawataleta pato kubwa sana katika nchi yetu na kuchangiakatika kuboresha uchumi wetu. Tuwatengenezee mazingirabora ya kufugia badala ya kuendelea kuangaika nao. Kamahawajatengewa mazingira yaliyo bora tutaendeleakusumbuana naona haitotusaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani nimetumia mudawangu vizuri nashukuru kwa kupata muda huo, ahsante sana.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Mipata ajiandaeMheshimiwa Jitu.

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kupata nafasi na mimi nitoe mchangowangu katika hotuba yetu ya mpango. Mimi nina maeneomatatu/manne na la kwanza ni kilimo. Tunapoingia kwenyeuchumi wa viwanda hatuna namna ya kukwepa kuendelezakilimo na wachangiaji wengi wameeleza. Manufaa ya kilimoyanaonekana na yako wazi, kwanza ina mchango mkubwasana kwenye uchumi wa Taifa, lakini pia imewaajiriWatanzania wengi. Kilimo kinaweza pia kikatusaidia kwenyesoko la ndani la bidhaa zinazotokana na viwanda. Kwa hiyo,kwa vyovyote vile hatuwezi kukwepa. Sasa ninavyoona mimikwenye Mpango huu na Mipango yote iliyopita hatujatiamkazo wa kutosha kwenye kuimarisha kil imo chetu,ninaomba hili jambo lizingatiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano sisi Mkoa waRukwa katika msimu uliopita tumezalisha zaidi ya tani 710,602;mahitaji yetu sisi ni tani 257,553. Kiasi cha mahindi ambayosisi tumetoa nje ya mkoa na kwa sababu tuna utaratibu wetukwenye njia zinazotka nje ya mkoa; tumetoa tani 50,189.Ziada tuliyonayo leo ni zaidi ya tani 402,859.

Kwa hiyo nina wasiwasi hata takwimu za MheshimiwaWaziri; tulikuwa tunaongea nae leo kwamba anasema Taifalina ziada ya tani 700,000 za chakula kwa sasa ikiwa sisi Mkoawa Rukwa tu tuna tani 402,859.62.

Page 180: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa wananchi wetumahindi ndiyo kila kitu. Ndiyo kwenda shule, mahindi ndiyoafya zao na ndio uchumi wao. Kwa hiyo, usipoweka mfumomzuri wa masoko katika mahindi sisi umetuumiza. Nilikuwanafikiri kama Taifa tuangalie, kwa sababu uzalishaji wamahindi utaendelea kuwepo, haiwezekani kila mwakatunakuja hapa kuzungumza kwa kutoa mishipa mingi, kukazamaneno ya hovyo, Wabunge kuweka vikundi vikundi. Lazimakama Taifa mjue kwamba kuna wakulima wa mahindi namahindi yataendelea kulimwa. Sasa ni lazima tuwe na mfumounaoeleweka, mkaanzisha hata kitaasisi au NFRAikaimarishwa, ikapewa hata mtaji ili iwe inanunua katikamaeneo ambayo kilimo kinafanya vizuri halafu baadayeinaweza ikafanya biashara ama nje ya nchi au sehemuambazo kuna upungufu wa chakula katika mataifa menginekuliko kuwa na jambo lisilo na majibu ya uhakika kila mwaka.Hii nafikisi si nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuimarisha kilimo ninakata yangu ya Nkandasi. Kuna shamba la Milundikwa StateFarm limenyang’anywa na Jeshi na wananchi sasa zaidi ya2000 hawana shughuli ya kufanya. Sasa watachangiaje katikaMpango huu? Ninaiomba Serikali itume wataalam wakewakaone jinsi wananchi hawa ambao wamekaa miaka 18katika eneo hili lakini leo wanakuja kufukuzwa na Jeshi bilasababu za kutosheleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, waagizeni viongoziwakafanye utafiti waone haki iko wapi kwa sababu eneohili walipewa kihalali na maandishi yapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la maji.Nimeona Mipango mizuri sana katika ukurasa wa 53 katikakitabu chetu cha Mpango na nimeona pia Wizarainavyojitahidi katika kushughulikia suala hili kwa kipindi hiki,hasa baada ya Bunge kuamua kushughulikia suala hilikikamilifu.

Mheshimiwa Mwneyekiti, dosari niliyoiona ni utoaji wapesa. Zile pesa ambazo zinapatikana moja kwa moja kutoka

Page 181: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

Wizarani, zinazokwenda kwenye Wizara kwa maamuzi yaBunge zinakwenda vizuri kwenye kusukuma miradi. Lakini zileambazo zinapatikana kutoka Wizara ya Fedha zinachelewana hazitusaidii sana kusukuma miradi, hii iangaliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niweke vizuri, Wilayaya Nkasi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante! Mheshimiwa Jitu, ajiandae,Mheshimiwa Kanyasu.

MHE. JITU V. SONI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.Kwanza naomba nimshukuru Mwenyekiti Mungu kwa kunipafursa ya kuchangia leo, lakini pia niipongeze Wizara kwakuleta Mpango, ni Mpango huu wa miaka mitano ambaotunanyofoa vipande vipande kila mwaka ili kuutekelezampango huu. Hakuna cha ajabu na hakuna kitu kipya, nimambo tuliyoyapitisha mwaka wa kwanza tulipoingiaBungeni. Muhimu ni vipaumbele, mimi naona tumepishana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye vipaumbele kunamambo ambayo tungebadilisha, yale ya kusogea hukombele na yale ambayo tungeanza nayo. Muhimu kabisakatika mpangio huu, na kitu ambacho sijaona kamakimewekwa katika mpango wa mwaka huu ambaotunataka kuutekeleza, (2018/2019) ni suala la utafiti. Hakunanchi inayoweza kuendelea bila ya kuwekeza katika utafitikatika Nyanja zote, iwe kilimo, mifugo, uvuvi, elimu, sayansi,afya na masuala mengine yote kwa kweli hata bajeti ambayohuwa tunatenga kwenye utafiti huwa inakuwa ni ndogosana, haitoshi hata kwa kitengo kimoja. Katika vituo 16 vyautafiti vile vifaa vyote sasa hivi vimekaribia kuwa vimepitwana wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia sehemu nyingineambayo ingeweza kutusaidia sana ni katika masuala ya hali

Page 182: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

ya hewa, tungewekeza zaidi huko. Kama tunataka wakulimawetu wanufaike tukiwekeza kwenye masuala ya hali ya hewa,kama ilivyo kwenye nchi za wenzetu unaambiwa kesho mvuaitanyesha muda wa saa fulani, hata wakulima wetu, mimininaweza kwenda kupanda mbegu leo kwenye udongowakati mkavu lakini nina uhakika wa mazao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba Serikali ikaepamoja na kuangalia suala zima la uratibu. Hapa kila Wizarainajitegemea kama vile ni Serikali yenyewe; mfanye kazi kamatimu. Niwapongeze juzi Mawaziri wannne walipozindua ulempango wa viwanda kila mkoa na viwanda, huo ndiouratibu inatakiwa mkae mfanye kazi kwa pamoja. Tunamifano mingi, tumechimba visima leo mwaka wa tatuumeme haujafikishwa, lakini ingekuwa mnafanya kazi kwakuratibu Wizara zote, idara zote zinafanya kazi kwa pamojamiradi ile ingekuwa inatekelezwa na mafanikio yangekuwayanaonekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala lakuwa na sera na mfumo wa kodi ambao ni stable, ambaohaubadiliki kila wakati. Mwaka huu tunaweza tukapitishajambo fulani watu wakaona sera imekaa vizuri na masualaya kodi, tax regime imekaa vizuri mwakani tumebadilishatunarudisha, hiyo ndiyo inafanya watu warudi nyuma na kwamfumo huu hatutoweza kuendelea kwenye masuala yaviwanda tunayotarajia kwamba itashika kasi. Ni muhimuviwanda vile vidogo na vidogo kabisa mngevi-regulate;haya mambo ya Osha, fire, nani mngewaondoa mtuakishalipa leseni yake na muanzishe one stop center kilamkoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwenye sheria mtuasipojua sheria haikupi kinga mahakamani lakini tungekuwana center moja; mimi nikienda uniambie ni kiasi fulani nikilipamasuala mengine yote wao ndio watanielekeza. Kila mkoakuwe na one stop center watu wafanye kazi na viwandavidogo na nini kama mlivyo-regulate kwenye uzalishajimdogo vivyo hivyo fanyeni kwenye viwanda, pasiwe naurasimu mkubwa utakuwa na mafanikio makubwa.

Page 183: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

Mheshimiwa Mwenyekiti, muhimu kuliko yote pia nikuwekeza kwenye Benki ya TADB. Wakulima hawahitajikupewa sadaka wala ruzuku, wekeni pesa kwenye benkitukakope na si wajanja wajanja. Wakulima wanawezakukopa, wakafanya shughuli zao wakalipa hizo hela.Hiyobenki leo haina hela. Mkulima wa kati na wa juu kamaanashindwa kukopa pale mdogo atapataje? Kwa hiyo,ninaomba tuwekeze pale na tuhakikishe kwamba benki hiyoinakuwa na mtaji wa kutosha.

Mheshimiwa Mawenyekiti, lingine tukirudi kwenyesuala la utafiti ni cost of production. Utakuwa na viwanda,lakini kutokana na utitiri wa hizi regulatolly bodies yaani taasisiza udhibiti unakuta tozo zao zinakuwa ni nyingi kiasiambacho hata tukizalisha gharama ya ile bidhaa yetu sikuzote itakuwa juu kuliko bidhaa ambayo unaagiza kutokanje ya nchi. Leo hii hata mfumo wetu ukiagiza bidhaa kutokanje nyingi hazina kodi, hasa zinazotoka kwenye nchi za AfrikaMashariki na Kati. Hayo usipoyafanyia kazi hata tukiwa naviwanda hapa bidhaa zetu hazitauzika. Kwa hiyo, ni vizurindani ya Wizara ya Fedha na Mipango mfanyie kazi suala lautafiti ili tuweze kupata…(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango mzuri.Mheshimiwa Kanyasu, ajiandae, Mheshimiwa Dau,atafuatiwa na Mheshimiwa Kigua.

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana na mimi naomba nimshukuruMwenyezi Mungu kwa kupata nafasi ya kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwanza kwakuzungumzia uwanja wa ndege wa Chato. Mimi ni Mbungewa Jimbo la Geita Mjini na ninashangaa sana watuwanaoona uwanja wa ndege unaojengwa Geita/unaojengwa Chato kwamba ni matumizi mabaya ya fedha.Watu wana-define uwanja mkubwa kwa urefu wa runway,

Page 184: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

lakini nadhani wanapungukiwa exposure. Uwanja mkubwani facilities na uwanja ule ili uwe mkubwa ungekutalinajengwa jengo la abiria kubwa, kwa hivyo ndipoungesema uwanja mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwakumbushe tu,wamesema uwanja wa ndege uko pale strategically,wanasahau kwamba kutoka Chato kwenda Rubondo nikilometa 30 na tunahamasisha utalii. Pia wanasahau kutokaChato kwenda Biharamulo ambapo kuna mbuga zawanyama za Buligi pamoja na Biharamulo pale ni kilometa50. Wanasahau kwamba tuko karibu kilometa 100 kwendampakani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunaposema nistrategic airport watu wengi hawaelewi tunazungumza nini,wanawaza tu kwamba ni uwanja wa Rais kwenda nyumbani.Mimi nasema ule uwanja umejengwa sehemu sahihi nauwanja ule sisi tunauhitaji ungejengwa katika eneo lolotelile. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo jingine ambalowatu ni lazima walifahamu Rais alikuwa akitua Mwanzakwenye uwanja wa ndege wa Mwanza kwenda Chatoanatembea kilometa 270 anakwenda kupumzika. AkituaBukoba anatembea kilometa 250 kwenda kupumzika. Sasaamejenga uwanja karibu anapokwenda kupumzikawanapiga kelele. Mimi nataka niwashauri, issue ya ukubwasi urefu wa uwanja, nenda kasome, issue ya ukubwa ni facilitiesza uwanja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, habari ya TRA, jengo la TRAwatu wanafikiri kurudi nyuma unakwenda mbele unaendawapi? Badala ya kusema tunajenga jengo likae miaka 50mbele wewe unawaza kujenga slope.

Mimi nasema hata ofisi za Serikali tuache sasa, tuanzekujenga majengo ya ghorofa. Habari ya taa ni habari yaHalmashauri yenyewe hata kama wangepita pundatunaangalia usalama wa raia. (Makofi)

Page 185: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la madini.Serikali ilipoanza kusimamia vizuri madini sisi watu wa GeitaMjini tumeona manufaa yake na nataka nitoe takwimu hapa.Kabla ya Serikali kuweka mikono yake kwenye madini,mapato ya Halmashauri yangu Januari-Machi ilikuwa shilingimilioni 514; Aprili-Juni shilingi milioni 750; yakaongezekakidogo hapo. Ilipofika Julai-Septemba tumepata bilioni mojakasoro, maana yake ni nini? Kulikuwa kuna wizi mkubwa sanaunafanyika hapa kwenye madini. Wito wangu hapa kwaMheshimiwa Waziri ninashauri ufanyike uchunguzi kurudinyuma kuona kwa nini baada ya Serikali kutuma wawakilishikwenye hizi kampuni za madini mapato ya Halmashauriyangu yameongezeka kutoka shilingi milioni 500 mpakashilingi bilioni moja wakati kazi ni ile ile? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri,tulipitisha Sheria hapa ya Local Content, bado watu wamgodi wanapiga. Bado wana walinzi kutoka nje, bado wanakampuni nyingi kutoka nje ambazo zinaweza kufanya kazina Watanzania. Wakati wa Mpango wa mwaka uliopitanilishauri hapa kwamba tuna kampuni nyingi sana ambazozinafanya kazi kwa remote, kampuni iko South Africa, ikoAustralia, inafanya services katika Mgodi wa Geita, hawalipikodi! Bado halijafanyiwa kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapokwenda kuwaombahawa watu watulipe service levy wanakwambia hii kampunihaipo Tanzania. Naomba kushauri, sheria hii tuliyoipitishahapa Bungeni, yaelekezwe haya makampuni ya madiniyaweze kuisimamia vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu tunajenga relikuja Dodoma, mimi nasema fine, tunakopa, tunafanya nini,mimi nasema fine, lakini wasiwasi wangu ni mmoja tu, hii reliitakapofika Dodoma kabla haijafika Mwanza itakuwa hainamsaada mkubwa kwenye uchumi wa Tanzania. Natakakushauri, badala ya kufanya vipande vipande kwa mudamrefu ufanyike uamuzi wa mara moja wa kuwekeza reli hiimoja kwa moja kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza iliitakapokamilika manufaa yake yaanze kuonekana. (Makofi)

Page 186: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi mimi na WaheshimiwaWabunge wenzangu tulipata bahati ya kwenda China natukaenda katika jimbo moja la Guangdong. Tulipotembeleapale, Meya wa mji ule anatuambia jimbo lile limejengwa naprivate sector, anasema Serikali haijajenga miundombinukatika jimbo lile. Airport, barabara, madaraja wamejengaprivate sector. Tuache kukopa kujenga miundombinu,tukaribishe… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango mzuri.Mheshimiwa Dau, ajiandae Kigua. (Makofi)

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa fursa hii na mimi nianze kwakumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetujalia uzima na uhai kwasiku ya leo. Nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwawasilisho lake zuri. Mimi kwa haraka haraka nitaanza na hiliambalo Senator Ndassa jana alilizungumza kwa undani sanahapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muda wa siku nne hapatumekuwa tukijadili huu Mpango wetu, lakini wengi waliojikitakatika kujadili hili wamezungumza suala la ubia kati ya sektabinafsi na sekta ya umma. Sasa mimi sitaki kurudia kwenyemjadala huo kwa sababu mengi yameshasemwa. HuuMpango na Waziri mwenyewe anakiri kwamba katika hilihatukufanikiwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi nimuombe tuMheshimiwa Waziri atakapokuja ku-wind up hoja yakepengine Bunge hili linasubiri sana kusikia kauli yake moja tuakisema kwamba anakivunja kile Kitengo cha Sekta Binafsipale Wizarani. Aweke timu mpya pale, tuanze upya na hatakama ikiwezekana tumtafute mtaalam wa nje aongoze kilekitengo na hili wala sio jambo geni. Tulipoanzisha TANROADSlilikuwa ni jambo jipya, lilikuwa jambo gumu, tukamuweka

Page 187: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

raia wa Ghana pale akaanzisha kile kitengo na sasa wenyewetumeweza kukiendesha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilikuwa namuombasana Mheshimiwa Waziri, vunja Kitengo cha Sekta Binafsi palekwenye Wizara yako, tafuta wataalam hata kama ikibidikutoka nje, tuanze upya, haiwezekani huu mwaka wa tanotunaimba tu sekta binafsi, sekta binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri katikahali ya kawaida hata wewe mwenyewe unatakiwa uweembarrassed katika situation inavyokwenda sasa hivi. Kilasiku tukisoma makabrasha hapa UDART! Hivi UDART ile kweliunaweza sema kwamba ni mfano mzuri wa ushirikiano bainaya sekta ya umma na sekta binafsi? Mheshimiwa Waziri kamaninakuuliza pale, hiyo sekta binafsi mle kwenye UDARTimeingiza kiasi gani unaweza ukanijibu? Katika hali yakawaida zile pesa ni za World Bank na yule aliyeingia palesijui Simon nani sijui ndiyo sekta binafsi pale ni ubabaishajimtupu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kila siku mimi toka nikoChuo Kikuu nasikia habari ya Chalinze - Dar es Salaam RoadToll mpaka leo iko kwenye makaratasi. Sasa anzisha kitengokile upya, wape malengo walau kwa mwaka basi hatatukipata mradi mmoja mkubwa mimi naamini tutasongambele sana. Haiwezekani Chalinze - Dar es Salaam miakasijui sita, hiyo UDART mimi kwangu wala siihesabu kama nimfano mzuri wa ushirikiano baina ya sekta binafsi na sektaya umma. Lakini katika hali ya kawaida hata hiyo habariinayoitwa kiwanda sijui ya madawa katika hali ya kawaidahicho nacho pia hakiwezi kuwa ndiyo mfano mzuri.Mheshimiwa Waziri tunakuomba sana utakapokuja hapauanze na kuvunja kile kitengo tuanze upya, wape malengowakishindwa toa weka wengine mpaka tutafanikiwa, hilolilikuwa la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nimeangalia huuMpango, kuna eneo umesema eneo la kuimarisha utalii,biashara na masoko, ujenzi na ukarabati wa kutengeneza

Page 188: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

miundombinu na kutangaza vivutio vya utalii hususan kilekinachoitwa Southern Circuit, kwa maana ya kwamba utaliiwa maeneo ya Kusini. Mimi nitagusia sehemu ndogo tu.Najua eneo la Kusini ni pana sana, nitagusia Kisiwa cha Mafia.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kisiwa cha Mafia ni maarufusana kwa utalii, tuna samaki pale anaitwa potwe (whaleshark), ni samaki ambaye ni wa ajabu na ni mkubwa kulikosamaki wote ukiondoa nyangumi ambaye si samaki nasamaki huyu hajatangazwa. Lakini hata kama mkitangazabado kuna suala la miundombinu. Kwa masikitiko makubwasana Bandari ya Nyamisati huu sasa ni mwaka wa pili bajetiya mwaka 2015/2016 zimetengwa shilingi bilioni 2.5 mpakamwaka umekwisha bandari haijajengwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante! Mengine mwandikieMheshimiwa Waziri. Mheshimiwa Kigua, MheshimiwaShekilindi, tutamaliza na Mheshimiwa Maige. Kama Maigehayupo nafasi yake itachukuliwa na Mheshimiwa InnocentBashungwa.

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Mwenyekiti, namimi nikushukuru jioni ya leo kwa kunipa nafasi niwezekuzungumzia juu ya Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yamezungumzwa mengi.Waliozungumza wamezungumza lakini nataka tu niwaambieWaheshimiwa Wabunge wenzangu kwamba ukipitia kitabuhiki mengi ya msingi Mheshimiwa Waziri ameyazungumzaukianzia ukurasa wa 42 mpaka 53 yote ambayo yanayohusumaendeleo ya Tanzania yamezungumzwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitajikita kwenye vituvitatu au vinne tu, ni Public Private Partnership. MheshimiwaWaziri mimi naomba ujikite hapa, tutapunguza matatizo kwa

Page 189: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

sababu nchi hii ni kubwa, ina changamoto mbalimbalihatuwezi ku-invest kwa kutumia our own funds, lazima tujikitekwenye Public Private Partnership. Mfano mzuri tu ni Darajala Kigamboni. Tumeona jinsi ambavyo return kubwainapatikana pale. Kuna usafiri DART, yote hiyo ni mifanomizuri. Mimi naomba usipate kigugumizi Mheshimiwa Waziri,hebu tuone namna gani tunaweza kujikita huko zaidi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni suala la VETA,naomba mfumo wa VETA ubadilike. Elimu inayotolewakwenye VETA ni nzuri sana na tunakwenda kwenye nchi yaviwanda, lakini elimu inayotolewa si ya kisasa. Tuone namnaya kuwaandaa vijana wetu tuweze kutoa elimu ambayoitasaidia kupata vijana tuweze kuwaajiri katika viwandavyetu hivi. Ukizingatia viwanda ni vya kisasa, kwa hiyovitahitaji vijana ambao wanasoma au wanapata elimuyenye IT base.

Meshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la viwanda,tunazungumza kufufua viwanda, mimi naamini vile viwandavya enzi ya Mwalimu Nyerere havifai tena. Viwanda sasa hivini teknolojia ya kisasa ni eneo dogo kwa hiyo tujikite kuwana viwanda vichache lakini ambavyo vitakuwa na tija nanchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambaloningependa kulizungumzia ni suala la bomba la mafutaambalo linatokea Uganda hadi Tanga. Nimeona katikaMpango huu mmezungumzia namna ya kuwekamiundombinu na moja wapo ya eneo ambalo mmeligusiani eneo la barabara ambalo linatokea Handeni hadi Singida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kabisa kwambampango huu ni lazima utekelezeke kwa sababu njia hiiukiacha bomba la mafuta linapita, lakini pia litasaidia kuinuauchumi wa mikoa minne ya Tanga, Singida, Dodoma.Nimeona niyazungumzie hapa nikiamini kabisa ni maeneomuhimu ambayo yatasaidia kuinua uchumi wa nchi yetu.(Makofi)

Page 190: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambaloningependa kwenda haraka haraka ni eneo la research anddevelopment. Watu tunazungumza hapa, yamezungumzwamengi sana lakini naomba sasa Mheshimiwa Waziri wa Fedhahebu tuwekeze kiasi kikubwa sana kwenye research. Researchna development ndiyo ambayo inaweza kututoa hapa kuonakwamba tubebe yapi tuache yapi na tuwe pia na mpangowa muda mfupi na mpango wa muda mrefu. Kwa sabbumipango ni mingi na yote inatakiwa kutekelezeka lakinitukitumia research and development maana yake tunawezatukajua kwamba tuwe na priority ipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe mfano mmoja tu; hatanchi za China na Malaysia, wenzetu viongozi waliotoka hukombali walitumia wataalam. Hebu nikuombe Dkt. Mpangona Naibu Waziri hebu kaa na timu, kaa na panel ya wachumiuje na mpango mdogo ambao unaweza kututoa hapaTanzania tulipo na kwenda mbele zaidi. Hayawanayolamimika Waheshimiwa Wabunge ni maeneo yamsingi kabisa na ninaamini mawazo ambayo yanatokakatika maeneo yetu ya uwakilishi yana maana kubwa.

Mimi sipendi kukulaumu lakini naamini kabisa hayaambayo waheshimiwa Wabunge wameyasema yana tija nayana faida kubwa na mimi naomba kupitia wataalam wako,hebu yachukue yafanyie kazi. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Shekil indi,ajiandae Mheshimiwa Maige, nafikiri hayupo, kwa hiyojiandae Mheshimiwa Bashungwa.

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii na miminiweze kuchangia Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nimshukuruMwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kunijaalia afyanjema na mimi niweze kuongea katika Bunge lako hili Tukufu.(Makofi)

Page 191: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya yote nianzekumpongeza kipenzi cha Watanzania, mtetezi wawanyonge, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwaanayoifanya. Hii ni tunu tuliyopewa na Mwenyezi Mungu nakama huamini hilo au kama kuna wale ambao hawaamnihilo basi wangeangalia leo jinsi anavyotoa somo paleUganda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nimpongeze WaziriMpango kwa kuja na mapendekezo ya Mpango waMaendeleo 2018/2019. Na mimi nijikite katika kuchangiahususan katika kilimo. Hatuwezi kuzungumzia mapinduzi yaviwanda bila kuzungumzia mapinduzi ya kilimo. Kilimo ni utiwa mgongo katika taifa hili, lakini mimi ninachoamini aunilichoona uti wa mgongo unaelezewa tu kwenye vitabulakini sio kwa vitendo. Kama kweli tunataka twende kwenyemapinduzi ya viwanda ni lazima tuhakikishe kwambatunaboresha kilimo chetu hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakulima walio wengi hapanchini wanategemea jembe la mkono. Kwa hiyo, nimuombesasa Mheshimiwa Mpango, hebu panga mipango yako mizurisasa kuhakikisha kwamba unaweka mipango mizuri katikawakulima wetu hawa kuwawezesha ili waweze kulima kilimocha kisasa na kuweza kuzalisha malighafi ambayoitasababisha kujenga katika viwanda vyetu. Ahsante sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo kuna sualala maji. Maji ni uhai na Tanzania yetu hii bahati nzuriimezungukwa na miito na maziwa makubwa sana. Lakinikuna changamoto sana ya upatikanaji wa maji. MheshimiwaWaziri Mpango sasa aje na mpango kabambe, naaminikabisa kwenye vitabu hivi kwa kweli mpango wake ni mzurikuhusu maji lakini apeleke pesa za kutosha katika suala zimala maji kwa sababu maji ndiyo kila kitu. Ukizungumzia kilimolazima uzungumzie na maji, kwa hiyo naomba sasa katikampango wake Mheshimiwa Mpango ahakikishe anaandaapesa za kutosha kupeleka kule kwa wakulima hususan katikasuala zima la kujenga mabwawa.

Page 192: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuingie kwenye suala labarabara. Barabara ndio uti wa mgongo, ndiyo uchumikatika taifa hili. Ili uchumi wa nchi hii ukue unahitaji barabara.Kwa mfano kule kwetu Lushoto, kuna barabara ambazozinatakiwa kupandishwa hadhi lakini mpaka sasa ni miakamitano barabara zile hazijapandishwa hadhi, kwa hiyonimuombe Mheshimiwa Waziri huyu katika mpango wakehuu basi zipandishe barabara zile hadhi. Kuna barabara yakutoka Mlalo – Ngwelo – Mlola – Makanya – Mlingano hadiMashewa ambapo barabara hii kwa kweli ni barabara yakiuchumi endapo itafunguliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala tena la barabarakutoka Mombo – Soni – Lushoto – Mlalo – Mlola, barabara hiini nyembamba mno kiasi kwamba hata juzi mwezi wa nnetulipopata mafuriko kwa kweli wananchi wa Lushotowalipata taabu sana, walikaa zaidi ya wiki mbili bila kupatahuduma za msingi. Kwa hiyo, nimuombe sasa MheshimiwaMpango katika mipango yake hii basi apange pesa zakutosha ili barabara ile iweze kupanuliwa. Pamoja na hayokuna barabara za kupandisha hadhi ziweze nazokupandishwa hadhi. Pia nimshukuru Dkt. Mpango auniishukuru Serikali yangu kwa kuja na TARURA, MheshimiwaDkt. Mpango nakuomba sana TARURA ni jambo zuri…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Haya, ahsante na TARURA. Sasatunakwenda kwa Mheshimiwa Maige, kama hayupoMheshimiwa Inno.

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niwezekutoa mchango wangu katika Mpango wa Bajeti yaMaendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Nianzekwa kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwawasilisho zuri la Mapendekezo ya Mpango huu na nimtie moyokwa sababu ameleta Mpango huu ili tuweze kumpa ushaurina naamini kabisa mna muda wa kutosha kuweza kufanya

Page 193: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

review kwa ku-take into account ushauri ambao tunawapasisi Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze pia kwa kuishukuruSerikali ya Awamu ya Tano kwa namna ya kipekeewalivyoweza kusaidia kutoa commitment ambayo iko seriouskwa Mradi wa Maji wa Rwakajunju kwa Wanakaragwe,nawashukuru sana Serikali. Pia nawashukuru kwacommitment ya kuweka lami barabara ya Bugene kwendaBenako ambayo itafungua fursa kubwa sana katika Wilayayetu na Ngara pamoja na nchi za jirani za Rwanda.Nawashukuru pia kwa commitment ya kuweka lamibarabara ya Mgakorongo kwenda Morongwa itatufunguliafursa na ndugu zetu wa Uganda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya shukurani hizo pianitumie nafasi hii kuzungumzia suala la uwanja wa Chato.Mimi nadhani wenzetu upande ule wamekosa, hoja kwasababu huwezi ukatumia muda mahsusi wa kuchangiaMpango wa Maendeleo wa Taifa unazungumzia taakufungwa kwenye uwanja wa Chato. Taa za shilingi milionitano unasimama Bungeni unasema Serikali imetumia shilingimilioni tano, yaani ni kukosa hoja kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia jiografia ya nchiyetu na nchi za jirani East African Communities na nchi zaGreat Lakes ni sahihi kabisa kuweka uwanja pale Chato kwasababu lazima tuangalie future, tusiangalie leo. Chato inaaccess ya Ziwa Victoria pale, kwa hiyo, ukiweka uwekezajiwa reli ambao utaenda mpaka Rwanda, ukaweka dry portya Isaka (bandari kavu), ukaweka potential ya kutumiausafirishaji wa maboti ya mizigo kwenda Kenya na Uganda,Chato iko strategically located kwa ajili ya kuhudumia mikoaya kule upande wa Kagera, Geita hata Kigoma, DRC, Burundina Rwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye siasa tufanye lakinisi kwenye mambo ya maendeleo ambayo yako serious.(Makofi)

Page 194: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi katika mpango wamaendeleo ulioko mbele yetu nipende kushauri Wizara yaFedha, kwamba mfanye re adjustment approach. Serikali nanchi yetu, vision ya kuwa na uchumi wa viwanda by 2025uko clear kwa wananchi wetu, kwa wadau wa maendeleona kwa private sector na dunia nzima. Kwa hiyo jambo hiloni muhimu sana kwa sababu tuna vision ambayo tunatakatuhakikishe mpango mkakati unatupeleka kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo ninachokionaambacho ni changamoto na muda wa kubadilisha mkakatiupo Serikali ime front load sana uwekezaji kwenye sekta yaviwanda na biashara moja kwa moja badala ya kuwekaeffort kubwa ya ku-facilitate sekta binafsi iwekeze katikaviwanda halafu nguvu ya Serikali m-front load bajeti kubwaiende kwenye sekta ambazo zinawahusu Watanzania waliowengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mpangowewe ni mchumi, ukiichukua ile Douglas Production Functionkwa uchumi wa Tanzania ambao hauko complicatedmambo ya financial market, financial derivatives sisi Tanzaniawe have to do the best with what we have. Tuna ardhiambayo ni arable tunaweza tukafanya kilimo, tuna laborforce ya kutosha, asilimia 67 ya Watanzania wako kwenyesekta ya kilimo.

Kwa hiyo, tunachohitaji pale ni kuwa karibu na hawawakulima, wafugaji, wavuvi na kuangalia katika maisha yaoya kila siku zile shughuli ambazo wanazojishughulisha nazo,tTukiwasaidia wakapiga hatua mbili, ile asilimia 67 yaWatanzania ambao wana…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: ... itasaidia kukuzauchumi na kupunguza umaskini.

Page 195: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa na mambo kadhaaya kuchangia lakini kwa sababu ya muda nina…

MWENYEKITI: Unayo fursa ya kumwandikia Waziri iliakujibu. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, orodha yote ya leoimekwisha na kila mtu aliyeandikwa kwenye orodha navyama vyake wote wamechangia. Niwashukuru naniwatakie kila la kheri. Bunge linarejea.

(Bunge Lilirudia)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Kunamatangazo ndiyo maana nimewaambia mkae. Kawaidainakuwa juu kwa juu tu.

Waheshimiwa Wabunge, Kamati ya Miundombinuinatakiwa ikutane kesho Jumamosi saa nne asubuhi kwenyeukumbi wao wa Kamati. Kamati ya Bunge ya Miundombinukesho asubuhi ikutane saa nne asubuhi na mtawasiliana naMakatibu wenu wawaambie ni ukumbi gani mtakutana.Semina ambayo ilikuwa ifanyike kesho haitakuwepo.

Tangazo lingine, Waheshimiwa Wabungemnatangaziwa kwamba mnaalikwa kushiriki katika mbio zamarathon zinazojulikana kama Dodoma Marathon 2017zitakazofanyika siku ya Jumapili tarehe 12 Novemba, 2017.Mbio hizi zitaanza katika uwanja wa Jamhuri kuanzia saa 12asubuhi na kuzunguka maeneo mbalimbali ya Manispaa yaDodoma.

Waheshimiwa Wabunge, mbio hizi zinalenga kuiungamkono Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa naMheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli katika uamuziwake wa kuhamishia Serikali hapa Dodoma. Hivyo basi,Wabunge wote wenye nia ya kushiriki kwenye mbio hizowanaombwa kujiorodhesha kesho Jumamosi saa tatuasubuhi katika eneo la mapokezi lango kuu la kuingiliakwenye ukumbi wa Msekwa.

Page 196: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920615-10 NOVEMBA 2017.pdf · Distance Learning) unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

Basi, tangazo hili tulishasoma toka asubuhi. Kwa hiyosemina ambayo imefutwa ni ya kesho. Semina ya Jumapiliiko kama kawaida. Jumapili semina itakuwa saa tanoasubuhi, Ukumbi wa Msekwa.

Baada ya maneno haya, katika mjadala hapa jionililiibuka suala la uwanja wa Dodoma na nikamuuliza rubanina bado nikatofautiana naye nikampa mahesabu akanijibu,mita 3,000 ni kilometa tatu. Boeing zinatua lakini kwaDodoma kwa sasa haitui kwa sababu effective runwayinayotumika kwa ndege kutua, kwa sasa kwa uwanja waDodoma ni chini ya mita 3,000 kwa maana uwanjahaujakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwanja ukikamilika kwamita 3,000 ndege hizi zinatua na ni strategic area, kwa hiyonilitaka kuipongeza Serikali kwa hatua hii ya kujenga nakuongeza length ya uwanja huu ili utumike kibiashara kwenyestrategy zingine muhimu za kiulinzi na usalama wa Taifa hili.(Makofi)

Baada ya maneno haya naahirisha shughuli za Bungempaka siku ya Jumatatu saa tatu asubuhi.

(Saa 1.40 Jioni Bunge liliahirishwa mpaka Siku ya Jumatatu,Tarehe 13 Novemba, 2017, Saa Tatu Asubuhi)