24
LIJUE SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM Soko La Hisa La Dar es Salaam Machi, 2015

Handbook Dse - March-2015- Kiswahili

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Dar es Salaam Securities Exchange, Kiswahili

Citation preview

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM 1

    LIJUE SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

    Soko La Hisa LaDar es Salaam

    Machi, 2015

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM 3

    KURASA

    1. DIRA 4

    2. AZMA 4

    3. UTANGULIZI 4

    4. NAFASI YA MASOKO YA MITAJI KWENYE MFUKO WA FEDHA

    KATIKA UCHUMI 4

    5. MFUMO WA USIMAMIZI WA KISHERIA 5

    6. MAJUKUMU YA SOKO LA HISA 5

    7. WANACHAMA 6

    8. MUUNDO WA UONGOZI WA SOKO 7

    9. KANUNI ZA KUORODHESHA HISA NA DHAMANA 7

    10. ADA ZINAZOTOZWA NA SOKO 11

    11. MAKAMPUNI YALIYO ORODHESHWA 14

    12. MFUMO WA MNADA 17

    13. KUHAMISHA MILIKI YA HISA 17

    14. USIMAMIZI WA SOKO 17

    15. ULINZI KWA WAWEKEZAJI 17

    16. ELIMU KWA UMMA 17

    17. VIVUTIO VYA USHIRIKI KWENYE MASOKO YA HISA 17

    18. WASHIRIKI WA SOKO LA HISA 19

    18. ANUANI YA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM 22

    YALIYOMO

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM4

    1.0 DIRAKuwa soko endelevu la mitaji ambalo ni injini ya kukuza uchumi wa Tanzania.

    2.0 AZMAKutoa huduma bora ya soko la mtaji lenye kuwezesha maendeleleo ya uchumi wa nchi na kuwezesha wananchi kiuchumi.

    3.0 UTANGULIZIIli kuyaelewa masoko ya mitaji na majukumu yake kwenye uchumi, ni muhimu kuelewa nafasi ya masoko haya kwenye mfumo mzima wa fedha katika uchumi; muundo wa masoko ya mitaji, mfumo wa kisheria na namna masoko haya yanavyofanya kazi. Inakubalika kuwa hakuna uchumi wa kisasa ambao ukajengeka bila ya kuwa na mfumo imara wa fedha. Mfumo imara wa fedha kwenye uchumi unaweza kufananishwa na mafuta ya kulainisha injini katika gari. Kama ambavyo injini ya gari huweza kulainishwa na mafuta ili ifanye kazi vizuri, vivyo hivyo mfumo wa fedha huwezesha uchumi kufanya kazi kwa kukutanisha pande mbili, zile zenye mitaji ya ziada inayotafuta sehemu za kuwekeza na zenye kuhitaji mitaji hiyo. Pande hizi mbili hukutana kupitia masoko ya fedha, mitaji huwekezwa na kutoa faida kwa pande husika na hivyo kuwezesha ufanisi wa matumizi ya mitaji.

    4.0 NAFASI YA MASOKO YA MITAJI KWENYE MFUMO WA FEDHA KATIKA UCHUMI

    (i) Maana ya Mfumo wa fedha katika UchumiMfumo wa fedha katika uchumi unajumuisha masoko ya fedha, taasisi zinazohusika na usimamizi wa mfumo wa fedha, sheria, kanuni na taratibu ambazo zinasimamia uuzaji na ununuzi wa hatifungani, hisa na dhamana nyinginezo zinazohusika, na hatimaye faida (yield) hubainika.

    (ii) Masoko ya fedhaMasoko ya fedha yanajumuisha masoko yote yenye kuhusika na mitaji ya muda mfupi, kwa kawaida pungufu ya mwaka mmoja, (money markets) na yale yenye kuhusika na dhamana za muda mrefu, zaidi ya mwaka mmoja ambayo ni masoko ya mitaji (capital markets). Kwa hiyo, masoko ya fedha ni masoko ya dhamana za muda mfupi na mrefu.

    (iii) Masoko ya mitajiMasoko ya mitaji ni mfumo na taasisi zinazowezesha wenye mitaji kuiwekeza kwenye vitega uchumi vyenye kuzalisha na kupata faida. Masoko ya mitaji huwezesha wenye fedha za ziada kuzitoa kwa wenye kuzihitaji kwa kuilipia kwa bei iliyo sahihi. Masoko ya mitaji yamegawanyika kwenye mafungu mawili: Sokolaawali;na Sokolapili.

    (iv) Soko la awaliHaya ni masoko ya mitaji yanayoshughulika na mauzo ya dhamana kwa mara ya kwanza. Mfano ni kama kampuni inapouza hisa au hatifungani zake kwa umma kwa mara ya kwanza. Hisa na hatifungani hizi baadaye huuzwa kwenye soko la pili.

    (v) Soko la piliHaya ni masoko yanayoshughulika na hisa na hatifungani zilizoko mikononi mwa wawekezaji waliozinunua kwenye soko la awali. Soko la Hisa la Dar es Salaam

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM 5

    nimojawapo ya taasisi za soko la pili la mitaji. Wawekezaji kwenye soko la pili hukutanishwa na madalali kwa ajili ya kuuza na kununua dhamana zilizoorodheshwa. Soko la Hisa la Dar es Salaam ni mojawapo ya taasisi muhimu kwenye mfumo wa fedha wa Tanzania.

    5.0 MFUMO WA USIMAMIZI WA KISHERIAUsimamizi wa kisheria wa masoko ya mitaji umejengwa kwenye nguzo kuu tatu za kisheria.

    (i) Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya Mwaka 1994 (Cap 79) kama ilivyorekebishwa

    Hii ndiyo sheria mama inayoratibu na kusimamia masoko ya mitaji hapa Tanzania. Mamlaka ya masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ndiyo taasisi inayosimamia utekelezaji wa sheria hii.

    (ii) Sheria ya Makampuni ya 2002 (Cap. 212) Sheria hii inasimamia mambo kadhaa yanayohusu makampuni ikiwa ni pamoja

    na uanzishwaji wa kampuni binafsi na za umma, uuzaji wa hisa, haki za wanahisa, yanayotakiwa kuwepo kwenye nyaraka za matarajio,majukumu ya wakurugenzi na uongozi wa kampuni. Mtekelezaji wa sheria hii ni Msajili wa Makampuni.

    (iii) Kanuni na taratibu zilizotungwa na Mamlaka na pia Soko la Hisa Masoko ya mitaji ni dhana inayohitaji uelewa maalum na ambayo usimamizi wake

    hubadilika mara kwa mara. Ili kuweza kwenda sanjari na maendeleo na mabadiliko hayo ya mara kwa mara bunge kupitia sheria ya Masoko ya Mitaji limetoa fursa kwa Mamlaka na Soko kutunga kanuni za kusimamia masoko haya. Soko la Hisa nalo limeandaa taratibu maalum za usimamizi wa soko ambayo ziko katika Kitabu cha Kanuni cha Soko. Maelezo zaidi yatapatikana kwenye Kitabu cha kanuni.

    6.0 MAJUKUMU YA SOKO LA HISA

    Soko la dhamana zilizoorodheshwa(i) Huwezesha wauzaji na wanunuzi kushiriki kwa kuuza na kununua dhamana

    zilizoorodheshwa. Soko la Hisa linatoa fursa ya kutoka na kuingia kwenye vitega uchumi kwa urahisi.

    (ii) Utambuzi wa bei Soko la Hisa huwezesha kupatikana kwa bei ya hisa na dhamana zilizoorodheshwa

    kwenye Soko la Hisa. Bei hupangwa na nguvu ya soko, na sio Soko wala dalali anayepanga bei ya hisa na dhamana.

    (iii) Huwezesha uwazi Kanuni za soko kuhusu utoaji taarifa muhimu hulazimisha kampuni zilizoorodheshwa

    sokoni kutoa taarifa zao mapema iwezekanavyo. Taarifa hizi huwezesha wawekezaji kuweza kufikia uamuzi wa kuuza ama kununua wakiwa na taarifa zote muhimu kuhusu kampuni.

    Taarifa hutolewa kwa ngazi mbili, wakati hisa zinatolewa kwa mara ya kwanza ambapo kampuni inatakiwa kutimiza masharti maalum na wakati ikishaorodheshwa hutakiwa kufuata masharti ya kudumu ya kutoa taarifa zote muhimu wakati wote

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM6

    inapokuwa bado imeorodheshwa. Soko la Hisa linakuwa kama kituo cha taarifa kwa makampuni na wawekezaji.

    (iv) Kuwezesha ubinafsishaji na umiliki mpana wa hisa za makampuni

    yanayobinafishwa Soko la Hisa limewezesha ushirikishwaji wa wananchi wengi zaidi katika umiliki

    wa yaliyokuwa mashirika ya umma ambayo hisa zake zimeuzwa na Serikali kwa wananchi kupitia Soko la Hisa.

    (v) Huwezesha upatikanaji wa mitaji Soko la Hisa huwezesha makampuni kuuza hisa na hivyo kuyawezesha kupata mitaji

    kwa gharama nafuu. Uzoefu umeonyesha kuwa wawekezaji walio wengi wako tayari kulipia hisa bei kubwa na kukubali riba ndogo kwa hatifungani pindi makampuni husika yanapokuwa yamekidhi masharti ya kuingia Soko la Hisa, kuliko hisa na hatifungani za makampuni mengine ambayo hayafahamiki ama kuorodheshwa kwenye Soko, ambayo wawekezaji hulipia bei ndogo na wakopeshaji hudai riba kubwa kutokana na hatari au hasara ya uwekezaji kuwa kubwa kwenye makampuni hayo.

    (vi) Huwezesha kujenga utajiri Masoko ya mitaji yanatoa faida halisi kubwa kwa wawekezaji kwa sababu hisa kwa

    ujumla hufunika mfumuko wa bei na zimeweza kufanya hivyo kwa muda mrefu. Faida itokanayo na uwekezaji kwenye hisa imekuwa kubwa kuliko mfumuko wa bei na kumpatia mwekezaji faida inayoweza kufidia kupungua thamani ya fedha, ikilingwanishwa na amana za mabenki ambazo riba yake ni ndogo kuliko mfumuko wa bei. Na pia kwa kuwekeza kwenye hisa mitaji hukua baada ya muda tofauti na kuweka fedha kwenye amana za mabenki.

    (vii) Kuchangia kukuza utamaduni wa uwekaji akiba Soko la Hisa lilipoanzishwa miaka tisa iliyopita, sio Watanzania wengi waliokuwa

    wanajua kuhusu masoko ya hisa. Kwa sasa, wengi wameshaelewa na wana shiriki kwenye masoko hayo. Ushiriki wao umewezeshwa na Soko la Hisa kutoa maelezo na elimu kwa umma kuhusu masoko ya mitaji. Lengo la Soko la Hisa ni kuendelea kutoa elimu kwa umma ili Watanzania wengi zaidi washiriki kwenye masoko ya hisa na umiliki wa hisa kama njia mojawapo ya kujiwekea akiba.

    7.0 WANACHAMA WA SOKO LA HISA

    Wanachama wa Soko la Hisa la Dar es Salaam wamegawanyika kwenye mafungu makuu mawili: Madalali;na Wanachamawashiriki.

    Madalali:Hawa ni wanachama walioruhusiwa kushiriki kwenye minada ya Soko la Hisa inayofanyika kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa. Madalali wanashiriki kwenye Soko la Hisa kwa kuuza na kununua hisa kwa niaba ya wateja wao au kwa ajili yao wenyewe.

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM 7

    Wanachama washiriki: Hawa siyo madalali, lakini wana maslahi na kukua kwa masoko ya mitaji hapa Tanzania. Wanachama hawa ni pamoja na kampuni zilizoorodheshwa katika Soko, zenye wasifu wa kuorodheshwa, wawekezaji wakubwa, Taasisi za kitaaluma na pia mtu mmoja mmoja. (Maelezo zaidi yanapatikana kwenye Kitabu cha Kanuni cha Soko la Hisa).

    8.0 MUUNDO WA UONGOZI WA SOKO Soko la Hisa ni kampuni iliyoandikishwa mwaka 1996 chini ya Sheria ya Makampuni 2002 (Cap 212) kama kampuni iliyo na dhima ya udhamini bila ya kuwa na mtaji. Uongozi wa Soko umejengwa kwenye nguzo kuu tatu.

    Nguzo ya kwanza ni Mkutano Mkuu wa wanachama ambao hukutanisha wanachama wote.Nguzo ya pili ni Baraza la Soko (the Council) ambalo huteuliwa kwa mujibu wa Katiba ya Kampuni. Majukumu yote ya uongozi yamekabidhiwa kwa Baraza la Soko. (Maelezo zaidi yapo kwenye Kitabu cha kanuni).

    Nguzo ya tatu ni Uongozi wa Soko (Management), chini ya Mtendaji Mkuu. Uongozi wa Soko umeundwa na Mtendaji Mkuu na Mameneja ama Wakuu wa Vitengo. Uongozi unawajibika kwa Baraza la Soko.

    9.0 KANUNI KORODHESHA HISA NA DHAMANA Katika kuorodhesha hisa na dhamana, Soko la Hisa limegawanyika katika sehemu kuu mbili: SokoKuu SokolakukuzaUjasiriamali

    NAMBA KIGEZO SOKO KUU SOKO LA KUKUZA UJASIRIAMALI

    1. Historia ya Angalau miaka mitatu. Hakuna. Iwapo kamuni hainza bishara historia ya kufanya biashara, inatakiwa kuonyesha kuwa ina mtaji wa kutosha kuanzisha mradi uliofanyiwa utafiti na gharama zake kujulikana.

    2. Historia ya Kuwa na faida baada ya kodi Hakuna. kupata faida kwa ngalau miaka miwili kati ya mitatu ya historia ya biashara ya kampuni.

    3. Mtaji wa Angalau 1 bilioni TZS Angalau TZS 200 milion kampuni uliokwisha kulipiwa

    4. Kusajiliwa Kampuni imesajiliwa Tanzania Kampuni imesajiliwa Tanzania kama kampuni ya umma, au kama kampuni ya umma, au kama ni kampuni inayojisajili kama ni kampuni inayojisajili kutoka nje ya Tanzania, sheria kutoka nje ya Tanzania, sheria ya

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM8

    ya makampuni iwe inafanana na makampuni iwe inafanana na ya ya Tanzania. Tanzania.

    5. Mali halisi ya Kampuni iwe na angalau 50% Kampuni iwe na angalau 50% ya kudumu ya mali ya kudumu ndani ya mali ya kudumu ndani ya Tanzania. Tanzania.

    6. Aina ya Makamuni yote kutoka sekta Makamuni yote kutoka sekta kampuni yoyote yanaruhusiwa yoyote yanaruhusiwa yanayoruhusiwa kuorodheshwa. kuorodheshwa. kuorodheshwa 7. Njia ya kutoa Toleo kwa umma, kudhamini au Toleo kwa umma, toleo kwa hisa kwa umma njia zote mbili. wawekezaji wachache, kudhamini au njia zote tatu. 8. Shughuli za Kampuni inatakiwa kuwa na Maelezo ya kina yanayohusu biashara mradi maalum biashara husika ikiwa ni pamoja inayoushughulikia na kumilikiwa na: Mpango wa biashara wa na kampuni inayouza hisa kwa miaka mitano, riporti ya umma. uchambuzi yakinifu kwa makampuni yaliyokuwa na uzoefu kwenye biashara wa chini ya mwaka mmoja.

    9. Umiliki wa Angalau 25% ya hisa zote Angalau 10% ya hisa kumilikiwa umma zilizoorodheshwa. Wawekezaji na umma. binafsi hawaruhusiwi kuwa na zaidi ya 1% ya hisa zote na taasisi 5% ya hisa zote. 10. Idadi ya Isipungue 1000 ukiondoa Angalau wanahisa 100. wanahisa baada wafanyakazi wa kampuni. ya kutoa hisa kwa umma na kuorodheshwa. 11. Kipindi cha Sio lazima. Ikiwa kampuni haina historia ya kizuizi. miaka mitatu, waanzilishi hawarhusiwi kuuza hisa zao kabla ya mwaka mmoja.

    12. Matumizi ya Kutoa maelezo ya kiasi Kutoa maelezo ya kiasi mtaji kitakachopokelewa (baada ya kitakachopokelewa (baada ya uliopokelewa. kutoa gharama) ikibainishwa kutoa gharama) ikibainishwa matumizi ya kila sehemu mtaji matumizi ya kila sehemu mtaji huo utakakotumika. huo utakakotumika.

    Endapo makusanyo hayatatosha Endapo makusanyo

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM 9

    kuanzisha mradi uliokusudiwa, hayatatosha kuanzisha mradi kampuni itatakiwa kuonyesha ni uliokusudiwa, kampuni itatakiwa wapi itapata mtaji wa ziada na kuonyesha ni wapi itapata kiasi kilichopungua. mtaji wa ziada na kiasi kinachopungua. Endapo matumizi halisi hayafahamiki kwa kiwango Endapo matumizi halisi chochote cha makusanyo, hayafahamiki kwa kiwango kampuni itatakiwa kutoa chochote cha makusanyo, maelezo ya ujumla ya matumizi kampuni itatakiwa kutoa ya mtaji utakaopatikana maelezo ya ujumla ya matumizi utakapowekezwa. Kampuni pia ya mtaji utakaopatikana itatakiwa kutoa maelezo ni kiasi utakapowekezwa. Kampuni pia gani cha chini kitakachokubaliwa itatakiwa kutoa maelezo ni kiasi kama mtaji wa kuwekeza kwenye gani cha chini kitakachokubaliwa kampuni endapo toleo halitaleta kama mtaji wa kuwekeza kwenye mtaji uliotarajiwa. kampuni endapo toleo halitaleta mtaji uliotarajiwa.

    13. Washauri Sio lazima. Ni lazima kampuni iwe na maalum. Mshauri Maalum kwa kipindi chote wakati imeorodheshwa.

    14. Wakurugenzi na Maelezo kuhusu umri, sifa na Kuwepo na viongozi wenye viongozi uzoefu wa miaka mitano. uzoefu maalum wa mwaka waandamizi mmoja kabla ya kuorodheshwa.

    15. Mahesabu ya Lazima yatayarishwe kwa Lazima yatayarishwe kwa kampuni kuzingatia viwango vya kuzingatia viwango vya mahesabu vya kimataifa na mahesabu vya kimataifa na kukaguliwa na mkaguzi kukaguliwa na mkaguzi aliyeidhinishwa na bodi ya Taifa aliyeidhinishwa na bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi wa ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu. hesabu.

    16. Wakaguzi wa Wawe wameandikishwa na bodi Wawe wameandikishwa na hesabu ya Taifa ya wakaguzi wa hesabu bodi ya Taifa ya wakaguzi wa na kuidhinishwa na Mamlaka ya hesabu na kuidhinishwa na Masoko ya Mitaji na Dhamana. Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana.

    17. Uongozi Angalau miaka miwili kabla ya Hakuna haja. Mkazo umewekwa usiobadilika kuorodheshwa. kwenye uzoefu wa viongozi hawa.

    18. Kamati za Ni lazima kuwa na kamati ya Ni lazima kuwa na kamati ya ukaguzi ukaguzi kama inavyopendekewa ukaguzi kama inavyopendekewa na miongozo ya Mamlaka ya na miongozo ya Mamlaka ya masoko ya mitaji kuhusu utawala masoko ya mitaji kuhusu utawala bora. bora.

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM10

    19. Mtaji wa Wakurugenzi kutoa maoni yao Wakurugenzi kutoa maoni yao kutosha wa kuhusu kuwepo kwa mtaji wa kuhusu kuwepo kwa mtaji wa kufanyia kutosha wa kuendesha biashara kutosha wa kuendesha biashara biashara kwa angalau kipindi cha miezi 12. kwa angalau kipindi cha miezi 12.

    20. Barua ya Kampuni kuleta barua ya Kampuni kuleta barua ya uthibitisho uthibitisho kutoka kwa uthibitisho kutoka kwa kutoka kwa wasimamizi yake wa kisheria. wasimamizi yake wa kisheria. wasimamizi wa kisheria

    21. Katiba ya Katiba kuwa na kipengele chenye Katiba kuwa na kipengele chenye kampuni kuonyesha kuwa kampuni kuonyesha kuwa kampuni inaruhusiwa kutoa hisa kwa inaruhusiwa kutoa hisa kwa umma, kulinda maslahi ya umma, kulinda maslahi ya wawekezaji wadogo, kuhamisha wawekezaji wadogo, kuhamisha umiliki wa hisa, majukumu ya umiliki wa hisa, majukumu ya wakurugenzi kwenye kukopa, na wakurugenzi kwenye kukopa, na kanuni za utawala bora wa kanuni za utawala bora wa kampuni kampuni

    22. Wajumbe wa Kampuni kuwa na angalau 1/3 ya Kampuni kuwa na angalau 1/3 ya bodi ya wakurugenzi wasio watendaji wakurugenzi wasio watendaji wakurugenzi 23. Waraka wa Waraka wa matarajio ni lazima Waraka wa matarajio ni lazima matarajio upitishwe na mamlaka. upitishwe na mamlaka. kupitishwa na Mamlaka 24. Kutimiza Kampuni kuweka nadhiri ya Kampuni kuweka nadhiri ya masharti ya kutekeleza masharti ya utawala kutekeleza masharti ya utawala utawala bora bora kama yanavyotakiwa na bora kama yanavyotakiwa na kanuni za utawala bora za kanuni za utawala bora za Mamlaka ya masoko ya mitaji Mamlaka ya masoko ya mitaji (CMSA) kama zitakavyotolewa (CMSA) kama zitakavyotolewa mara kwa mara. mara kwa mara.

    25. Sera ya gawio Kampuni kutoa sera bayana ya Kampuni kutoa sera bayana ya gawio. gawio.

    26. Kutoa taarifa Kampuni inatakiwa kutoa Kampuni inatakiwa kutoa kwenye muhtasari wa waraka wa muhtasari wa waraka wa magazeti matarajio kwenye magazeti. matarajio kwenye magazeti.

    * (Kanuni zote hizi zinapatikana kwenyue kitabu cha kanuni cha soko la hisa).

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM 11

    10.0 ADA ZINAZOTOZWA NA SOKO

    (a) ADA YA KUORODHESHA

    (i) Hisa

    SOKO KUU SOKO LA KUKUZA UJASIRIAMALI

    Kuorodhesha hisa kwa mara Asilimia 0.2% ya Asilimia 0.1% ya thamaniya kwanza (kampuni thamani ya soko ya ya soko ya hisainapoorodheshwa kwenye hisa zilizoorodheshwa, zilizoorodheshwa,soko la hisa kwa mara ya kiwangi cha chini kiwangi cha chini kikiwakwanza) kikiwa ni TZS 2 milioni ni TZS 1 milioni na cha juu na cha juu kikiwa ni kikiwa ni TZS 10 milioni. TZS 20 milioni. Ada ya kuorodhesha hisa za Asilimia 0.1% ya Asilimia 0.05% ya thamaniziada (hulipwa na kampuni thamani ya soko ya ya soko ya hisa yenye hisa zilizoorodheshwa hisa zilizoorodheshwa, zilizoorodheshwa, yenye kuongeza hisa zaidi kiwangi cha chini kiwangi cha chini kikiwakwenye soko la hisa) kikiwa ni TZS 2 milioni ni TZS 1 milioni na cha juu na cha juu kikiwa ni kikiwa ni TZS 10 milioni. TZS 20 milioni. Ada ya mwaka ya Asilimia 0.05% ya Asilimia 0.025% yakuorodheshwa (hulipwa na thamani ya soko ya thamani ya soko ya hisakila kampuni iliyoorodheshwa hisa zilizoorodheshwa, zilizoorodheshwa, kwenye soko la hisa) kiwangi cha chini kiwangi cha chini kikiwa kikiwa ni TZS 2 milioni ni TZS 2 milioni na cha juu na cha juu kikiwa ni kikiwa ni TZS 20 milioni. TZS 20 milioni.

    (ii) Hatifungani

    Kuorodhesha hatifungani kwa mara ya Asilimia 0.05% ya thamani ya soko yakwanza (kampuni inapoorodheshwa hatifungani zilizoorodheshwa, kiwangokwenye soko la hisa kwa mara ya kwanza) cha chini kikiwa ni TZS 500,000/= na cha juu kikiwa ni TZS 5 milioni.

    Ada ya kuorodhesha hatifungani za ziada Asilimia 0.025% ya thamani ya soko ya (hulipwa na kampuni yenye hatifungani hatifungani zilizoorodheshwa, kiwango zilizoorodheshwa yenye kuongeza cha chini kikiwa ni TZS 250,000/= nahatifungani zaidi kwenye soko la hisa) cha juu kikiwa ni TZS 2.5milioni.

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM12

    Ada ya mwaka ya kuorodheshwa Asilimia 0.0125% ya thamani ya soko (hulipwa na kila kampuni ya hatifungani zilizoorodheshwa, iliyoorodheshwa kwenye soko la hisa) kiwangi cha chini kikiwa ni TZS 500,000/= na kiwango cha juu kikiwa ni TZS 2.5 milioni.

    (b) USHURU KWENYE SOKO LA PILI

    (i) Manunuzi ya Hisa

    Kiwango cha Ada ya Ada ya soko Mfuko wa Jumla yamauzo madalali na Mamlaka fidia ghamara kwa mwekezaji

    Mauzo hadi 1.70 0.28 0.02 2.00TZS 10 milioni

    Mauzo hadi 1.50 0.28 0.02 1.80TZS 40 milioni

    Mauzo yoyote zaidi 0.80 0.28 0.02 1.10%ya TZS 50 milioni

    (ii) Manunuzi ya Hatifungani

    Thamani ya mauzo Ushuru unaotozwa

    Hadi TZS 40 milioni 1/16%

    Kiasi chochote zaidi ya TZS 40 milioni 1/32%

    Kiwango cha chini cha ushuru TZS 5,000

    (c) Ada za hifadhi ya hisa

    (i) Kwa mwekezaji

    Namba Aina ya ada Soko kuu Soko la kukuza ujasiriamali

    (i) Ada kwa kila manunuzi TZS 1,000 TZS 1,000

    (ii) Kuunganisha umuliki wa hisa TZS 1,000 TZS 1,000

    (iii) Kudurufu hati ya hifadhi (kila hati) TZS 2,000 TZS 2,000

    (iv) Kuhamisha miliki bila kuuza TZS 1,000 TZS 1,000

    (v) Taarifa kuhusu umiliki TZS 5,000 TZS 5,000

    (vi) Kutoa hisa kwenye hifadhi TZS 25,000 TZS 25,000

    (vii) Kuweka na kutoa hisa rehani TZS 1,000 TZS 1,000

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM 13

    (ii) Kwa makampuni

    Namba Aina ya ada Soko kuu Soko la kukuza ujasiriamali

    (i) Hifadhi ya Hisa TZS 1,000 TZS 1,000

    (ii) Kutayarisha hati za hifadhi Asilimia 0.5% ya thamani Asilimia 0.25% ya thamani wakati wa mauzo ya hisa ya soko ya hisa ya soko ya hisa ya awali zilizoorodheshwa, kiwango zilizoorodheshwa, cha chini kikiwa ni TZS 2 kiwango cha chini kikiwa milioni na cha juu kikiwa ni ni TZS 1 milioni na cha TZS 10 milioni juu kikiwa ni TZS 5 milioni

    (ii) Ada za ISIN

    Namba Ada Kiasi

    (i) Ada kwa hisa na hatifungani zilizo orodheshwa TZS 300,000 kwenye soko (ada ya mara moja tu)

    (ii) Ada ya matoleo ya ziada ya hisa na hatifungani TZS 150,000

    (iii) Ada kwa kwa hisa na hatifungani ambazo hazija TZS 150,000 orodheshwa kwenye soko (ada ya mara moja tu)

    (iii) Ada ya Uanachama wa Soko La Hisa

    Namba Aina ya ada Kiasi

    (i) Ada ya kiingilio TZS 2,000,000

    (ii) Ada ya mwaka TZS 1,000,000

    (iv) Ada ya Uanachama wa Hifadhi ya Hisa (CDS)

    Namba Aina ya ada Kiasi

    (i) Ada ya kiingilio TZS 1,000,000

    (ii) Ada ya mwaka TZS 2,000,000

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM14

    11.0 MAKAMPUNI YALIYOORODHESHWA

    (a) Hisa

    (i) Kampuni za kitanzania Jina lakampuni Tarehe ya Idadi ya Hisa Aina ya biashara kuorodheshwa zilizo tolewa

    TOL Gases Ltd. 15 Aprili, 1998 55,835,490 Uzalishaji na usambazaji wa(zamani ikiitwa TOL Ltd.) gesi, vifaa vya kuchomelea(TOL) na hospitali.

    Tanzania Breweries Ltd. 9 Septemba, 294,928,463 Uzalishaji na uuzaji wa bia(TBL) 1998

    Tanzania Tea Packers Ltd. 17 Disemba, 18,657,254 Kilimo cha chai, usindikaji, (TATEPA) 1999 uuzaji na usambazaji wa chai

    Tanzania Cigarette Co. Ltd. 16 Novemba, 100,000,000 Uzalishaji na usambazaji wa(TCC) 2000 tumbaku

    Tanga Cement Co. Ltd. 26 Septemba, 63,671,045 Uzalishaji na usambazaji wa(SIMBA) 2002 saruji

    Swissport Tanzania Ltd. 26 Septemba, 36,000,000 Kutoa huduma kwenye(zamani ikiitwa DAHACO) 2003 viwanja vya ndege

    Tanzania Portland Cement 29 Septemba, 179,923,100 Uzalishaji na usambazaji waCo. Ltd. (TWIGA) 2006 saruji

    Dar es Salaam Community 16 Septemba, 67,827,897 Benki ya BiasharaBank Ltd (DCB) 2008

    National Microfinance 6 Novemba, 500,000,000 Benki ya BiasharaBank Ltd (NMB) 2008

    CRDB Bank Plc (CRDB) 17 Juni, 2009 2,176,532,160 Benki ya Biashara

    Precision Air Services Plc 21 Disemba 2011 160,469,800 Usafiri wa anga

    Maendeleo Bank (MBP) 1 Novemba 2013 9,066,701 Benki ya Biashara

    Swala Gas and Oil 11 Agosti 2014 99,954,467 Madini Gesi na Mafuta

    Mkombozi Bank 29 Desemba 2014 20,615,272 Benki ya Biashara

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM 15

    (ii) Makampuni ya nje

    Jina lakampuni Tarehe ya Idadi ya Hisa Aina ya biashara kuorodheshwa zilizo tolewa

    Kenya Airways Ltd 1 Oktoba, 2004 1,496,469,034 Usafirishaji wa abiria na(KA) mizigo kwa njia ya anga sehemu mbalimbali duniani

    East African Breweries 29 Juni, 2005 790,774,356 Kampuni mama yaLtd. (EABL) makampuni kadhaa zenye kuhusika na Uzalishaji na uuzaji wa bia nchini Kenya, Uganda na Mauritius.

    Jubilee Holdings Ltd 20 Disemba, 2006 59,895,000 Kampuni mama ya(JHL) makampuni kadhaa zenye kuhusika na huduma za bima nchini Kenya, Uganda na Tanzania

    Kenya Commercial 17 Disemba, 2008 2,970,340,000 Benki ya BiasharaBank Ltd (KCB) National Media Group 21 Februari 2011 188,542,286 Kampuni ya utangazaji naPlc habari

    Acacia Mining Plc 7th Disemba, 2011 410,085,499 Kuchimba na kuzalisha dhahabu

    Uchumi Super Market 15 Agosti 2014 364,965,594 Maduka ya bidhaa (USL) mbalimbali (supamaketi)

    (iii) Historia ya Manunuzi ya hisa

    Jina la Bei ya Idadi ya Hisa Thamani ya Mtaji Kiasi Idadi yakampuni Hisa zilizo Mauzo ya uliopatikana cha walionunua kipindi tolewa hisa mtaji Hisa cha uliopat- kuorod- ikana heshwa TOL1 500 7,500,000 3,750,000,000 3,598,086,000 96 10,500TBL2 550 23,594,277 12,976,852,350 9,630,874,000 74 23,000TATEPA 330 1,584,912 523,020,960 571,461,000 109 2,000TCC 410 19,500,000 7,995,000,000 9,394,125,000 118 7,508SIMBA 300 20,693,090 6,207,927,000 24,210,915,300 390 14,228SWISSPORT 225 17,640,000 3,969,000,000 31,196,340,000 786 41,025TWIGA 435 53,975,900 23,479,516,500 86,419,680,855 368 18,300NICOL 300 50,000,000 15,000,000,000 5,601,735,000 37 2,987

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM16

    DCB 275 5,454,546 1,500,000,150 3,704,094,900 247 5,446NMB 600 105,000,000 63,000,000,000 224,999,340,000 357 27,303CRDB 150 125,429,692 18,814,453,800 50,719,410,000 270 21,282PRECISION 475 58,841,750 27,949,831,250 12,091,030,000 43 7,057TBL3 2,060 58,985,693 121,510,527,580 297,593,326,800 245 2,081MAENDELEO BANK 500 9,066,701 4,000,000, 000 4,533,350,500 113 2528SWALA 500 9,600,000 4,800,000,000 6,643,900,000 138 1867MKCB 1000 5,000,000 5,000,000,000 3,776,820,000 76 2618

    (b) HATIFUNGANI ZA MAKAMPUNI

    KAMPUNI AINA YA TAREHE YA RIBA KUIVA HATIFUNGANI TOLEO

    ALAF LTD. Hatifungani zenye 24 Februari, Wastani wa Faida Kurejeshwa kikamilifu thamani ya TZS 2008 wa dhamana za mwisho wa 15.07 bilioni zisizo siku 182 za serikali hatifungani tarehe na dhamana, za karibuni na 17 Disemba 2015 toleo la kwanza Malipo zitakazoiva zikiongezewa mwaka 2015 riba

    BANK M Hatifungani zenye 4 Februari, Riba isiyobadilika Kurejeshwa kwa LIMITED thamani ya TZS 2011 ya 15% kwa pamoja tarehe 14.5 bilioni zisizo mwaka inayolipwa 4 Februari, 2016 na dhamana na kuanzia 4 kuiva mwaka 2016 Februari 2012 hadi tarehe ya kupevuka pamoja STANDARD Hatifungani zenye 22 Octoba, Riba isiyobadilika Kurejeshwa kwa CHARTERED thamani ya TZS 2010 ya 11%, Faida awamu 10 tofautiBANK LTD. 10 bilioni zisizo na hadi kuiva za kiwango cha dhamana, toleo la inayolipwa mara 1,000,000,000 kila kwanza zitakazoiva mbili kwa mwaka moja pamoja na mwaka 2015 riba hadi tarehe 21 Octoba 2015

    PROMOTION Hatifungani zenye 8 Novemba, 1. Wastani wa Faida Kurejeshwa kwa OF RURAL thamani ya TZS 2015 wa dhamana za awamu 6 tofauti zaINITIATIVES 14.5 bilioni zisizo siku 364 za serikali kiwango sawa kilaAND na dhamana na za karibuni na moja kila baada yaDEVELOPMENT kuiva mwaka 2015 malipo miezi 6 kuanziaENTERPRISES zikiongezewa riba Novemba 2012LTD (PRIDE) kwa 2% juu ya kiwango kilichopo 2. Riba isiyobadilika ya 11.75% kwa mwaka

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM 17

    12.0 MFUMO WA MNADA Mnada unafanyika kwenye mtandao wa kompyuta (ATS). Kupitia mtandao huu madalali

    wa Soko wanauziana hisa na hatifungani wakiwa kwenye ofisi zao.

    Mfumo huu unategemewa kuwezesha kusaidia huduma kuwafikia Watanzania walio nje ya Dar es Salaam siku za karibuni.

    13.0 KUHAMISHA MILIKI YA HISA Uhamishaji miliki ya hisa na hatifungani hufanyika kupitia mfumo wa kompyuta wa

    kusimamia uhamisho wa miliki ulioanza tangu mwaka 1999. Mfumo huu husimamia uhamishaji wa miliki unaotokana na mauzo na manunuzi, hisa kutolewa kama zawadi na kurithisha hisa kutoka kwa marehemu. Mfumo huu huwezesha kuhamisha miliki kwa muda mfupi (ndani ya siku 3 kwa hisa na siku moja kwa hatifungani baada ya mauzo).

    14.0 USIMAMIZI WA SOKO Mamlaka na Soko la Hisa kwa pamoja husimamia mnada ili kubaini kama kuna

    udanganyifu, upotoshaji na ushiriki wenye mgongano wa maslahi. Soko la Hisa linawajibika na usimamizi wa moja kwa moja ambapo wataalam wa Mamlaka husimamia kwa kuangalia jinsi mnada unavyoendelea wakiwa ofisini kwao.

    15.0 ULINZI KWA WAWEKEZAJI Kwa mujibu wa Sheria ya masoko ya Mitaji na Dhamana, Soko la Hisa limeanzisha Mfuko

    wa Fidia utakaotumika kufidia wawekezaji watakaopata hasara kutokana na udanganyifu au matumizi mabaya ya fedha zao na madalali wa Soko. Mfuko huu hutunzwa na Soko la Hisa. Mfuko pia hutumika kufidia hasara itokanayo na uzembe wa madalali. Fidia inayolipwa kwa sasa haizidi Shilingi 100,000/= kwa hasara apatayo mwekezaji.

    16.0 ELIMU KWA UMMA Elimu kwa wawekezaji hutolewa na Soko la Hisa kupitia semina zinazoandaliwa na Soko la

    Hisa, kupitia taasisi nyinginezo na pia kupitia mafunzo kwa wawekezaji wanaotembelea Soko la Hisa ili kuona mnada unavyoendeshwa.

    Soko la Hisa linaendesha elimu ya uwekezaji na utunzaji fedha kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini ambapo wanafunzi hupewa nafasi ya kushiriki kwenye shughuli za mafunzo wa vitendo kwa kuuza na kunua hisa kwa kipindi cha miezi mitatu.

    Majarida yanayotoa maelezo kuhusu Soko la Hisa huchapishwa mara kwa mara na Soko la Hisa yakilenga kutoa maelezo kuhusu uwekezaji na wakati wa kampuni mpya inapokuwa imeorodheshwa Sokoni.

    17.0 VIVUTIO VYA USHIRIKI KWENYE MASOKO YA HISA Serikali imetoa vivutio muhimu vya kuwezesha ushiriki mpana kwenye masoko ya mitaji.

    (a) VIVUTIO KWA MAKAMPUNI(i) Kodi ya makampuni imepunguzwa kutoka 30% hadi 25% kwa kipindi cha miaka

    3 iwapo kampuni itamilikiwa kwa 35% na umma. Punguzo hili litaendelea kwa miaka 5 baada ya kuorodheshwa kwa kampuni hiyo katika Soko la Hisa.

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM18

    (ii) Punguzo la kodi ya makampuni kutoka 30% hadi 25% kwa makampuni yote yaliyoorodheshwa katika soko la hisa na ambayo yametoa angalau 30% ya hisa zao kwa umma.

    (iii) Gharama za kuuza hisa kwa umma zinazokubaliwa na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kama gharama za uendeshaji kwenye ukokotoaji wa faida na hasara ya kampuni kwa ajili ya kutafuta kodi ya mapato.

    (iv) Kodi ya zuio kwenye mapato yatokanayo na vyombo vya uwekezaji wa pamoja ni kodi ya mwisho. Wawekezaji wa mifuko hii hawalipi kodi tena.

    (b) VIVUTIO VYA WAWEKEZAJI(i) Hakuna kodi ya ongezeko la mtaji, ikilinganishwa na 10% kwa kampuni ambazo

    hazijaorodheshwa.

    (ii) Hakuna ushuru wa stempu kwenye mauzo ya hisa zilizoorodheshwa, ikilinganishwa na 6% kwa kampuni zisizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa.

    (iii) Kodi ya zuio kwenye gawio ni 5% ikilinganishwa na 10% kwa kampuni zilizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa.

    (iv) Hakuna kodi za zuio kwa mapato ya riba yatokanayo na jhatifungani zilizoorodheshwa zenye kuiva baada ya miaka mitatu na zaidi.

    (v) Kodi ya zuio kwenye mapato ya mfuko wa uwekezaji imeondolewa.

    (vi) Mapato ya wawekezaji kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja yamesamehewa kodi.

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM 19

    18.0 WASHIRIKI KATIKA SOKO LA HISA

    (a) MADALALI

    CORE securities Ltd Orbit Securities Co. Ltd Rasilimali LtdGhorofa ya Nne Jengo la Elite City, Ghorofa ya Nne, Ghorofa ya Saba,Kwenye kona ya barabara za Jengo la PSPF Golden Jubilee Jengo la Samora TowersSamora na Morogoro Towers, Barabara ya Ohio, Barabara ya Samora, Dar es Salaam Dar es SalaamSimu: +255 (22) 2123103,Nukushi:+255 (22 2122562 Simu: +255 (22) 211 1758 Simu: +255 (22) 211 1711Barua Pepe: [email protected]; Nukushi: +255 (22) 211 3067 Nukushi: +255 (22) 212 2883Tovuti: www.coresecurities.co.tz Barua Pepe: [email protected] Barua Pepe: [email protected]

    Tanzania Securities Ltd Vertex International Solomon Stockbrokers Co. LtdGhorofa ya Saba, Jengo la IPS, Securities Ltd Sakafu ya ardhini,Kona ya barabara za Jengo la Annex- Ubalozi Jengo la PPF House, kona yaSamora na Azikiwe, Dar es Salaam Zambia, Kona ya barabara za Samora na Morogoro, barabara za Sokoine Dar es SalaamSimu: +255 (22) 211 2807 na Ohio, Dar es SalaamNukushi: +255 (22) 211 2809 Simu: +255 (22) 211 2874Barua Pepe: Simu: +255 (22) 211 6382 Nukushi: +255 (22) 213 [email protected] Nukushi: +255 (22) 210387 Barua Pepe: Barua Pepe: [email protected] [email protected]

    ZAN Securities Ltd Ghorofa ya Pili, Jengo la VIVA Towers, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi Dar es salaam S.L.P 2138 Ghorofa ya kwanza, Muzammil Centre, barabara ya Malawi, Zanzibar

    Simu: +255 (22) 2126415, Nukushi: 255 (22) 2126414 Simu ya rununu: +255 (786) 344767 / (755) 898425

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM20

    (B) WASHAURI WATEULE

    Enterprise Growth Marker Advisors Ltd TSL Investment Management LtdGhorofa ya kwanza Ghorofa ya sita, Jengo la IPSJengo la Alfa House ploti ya 25 Mtaa wa Samora na AzikiweBarabara Mpya ya Bagamoyo S.L.P. 9821S.L.P. 79807 Dar es SalaamDar es Salaam Simu: +255 22 2760145, +255 759 191 093 Simu: 255 (22) 21 12807 Simu ya mkononi: +255 754 222 450 Nukushi: 255 (22) 21 12809 Barua pepe: [email protected] Barua Pepel: [email protected]

    ARCH Financial & Investment Exim Advisory Services Ltd. Advisory Limited (Fund Manager)Ghorofa ya Pili, Wingi ya C, Jengo la NIC Life Ghorofa ya 8, Jengo la Ofisi ya AcademyMtaa wa Sokoine na Ohio Plot ya 2385/12, Mtaa wa AzikiweS.L.P 38028 S.L.P. 3219,Dar es Salaam Dar es Salaam.

    Simu. +255 22 732922396Nukushi +255 22 732928489

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM 21

    (c) WASHAURI WA UWEKEZAJI

    FTC Consultants Limited Orbit Securities Co. Ltd LJK Konsulting LimitedGhorofa ya pili, Ghorofa ya Nne, Jengo la Plot No. 294, Regent EstateJengo la Osman Towers, PSPF Golden Jubilee Towers, S.L.P. 20651mtaa wa Zanaki Mtaa wa Ohio, Simu/Nukushi +255 (22) 2124383Dar Es Salaam, Tanzania S.L.P. 31831, Dar es Salaam Barua Pepe: Simu: +255 (22) 211 1758 [email protected]: +255 (77) 467 6676 Nukushi: +255 (22) 211 3067Nukushi: +255 (22) 213 0519 Barua Pepe: [email protected] Tovuti: www.ftc-tz.com Tovuti: www.orbit.co.tz Gem Consulting Limited Trident East Africa Limited Sifa Advisory LimitedGhorofa ya Nane, Ghorofa ya Tatu, S.L.P 412338028Jengo la Office Maktaba Complex Dar es SalaamAcademy Scheme, (Jengo la Tanzania Simu. +255 (22) 2137570Plot 2385/12, mtaa wa Azikiwe, Library Services) Nukushi: +255 (22) 2136570Dar es Salaam Barabara ya Bibi Titi, Tovuti: www.sifacapital.com Dar es Salaam Barua Pepe: [email protected]

    River Capital Partners ARCH Financial & Skylink Financial ServicesGhorofa ya 10, Investment LimitedJengo la Amani Place Advisory Limited Ghorofa ya 4, Amani Place,mtaa ya Ohio Ghrofa ya Pili, Wing C, Opposite Serena Hotel,Simu: +255 22 2126050 Jengo la NIC Life House Mtaa wa OhioNukushi: +255 (22) 21216049 Kona ya barabara ya Sokoine Dar es Salaam. Drive na mtaa Ohio Dar es Salaam Simu: +255 (22) 2115381 Simu: +255 (22) 732922396 Nukushi: +255 (22) 2112786/ Nukushi: +255 (22) 732928489 2114562 Barua Pepe: info@ skylinkfinancialservices.com

    Exim Advisory Services Ltd Solomon Stockbrokers Co. Tanzania Securities Ltd(Fund Manager) Ltd (Fund Manager)Ghorofa ya nane, Ghorofa la Chini, Ghorofa ya Sita,Jengo la Office Academy Jengo la PPF House, Jengo la IPS,Scheme Building kona ya barabara za Samora Kona ya barabara zaPlot 2385/12, Mtaa wa Azikiwe na Morogoro, Samora na Azikiwe, Dar es Salaam Dar es Salaam Dar es Salaam Simu: +255 (22) 211 2874 Simu: +255 (22) 211 2807 Nukushi: +255 (22) 213 1969 Nukushi: +255 (22) 211 2809 Barua Pepe: Barua Pepe: [email protected] [email protected] Tovuti: www.solomon.co.tz Tovuti: www.tanzaniasecurities.co.tz

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM22

    Standard Chartered Bank Rasilimali Ltd Consultants for ResourcesTanzania Limited Ghorofa ya Saba, Evaluation Limited (CORE)Jengo la International House Jengo la Samora Towers Ghorofa ya Nne Barabara ya Garden Avenue Barabara ya Samora Jengo la Elite City,Dar es Salaam Dar es Salaam Kwenye kona ya barabaraSimu: 255 (22) 2122160 / za Samora na Morogoro2122162 Simu: +255 (22) 211 1711 Tovuti: 255 (22) 2122089 Nukushi: +255 (22) 212 2883 Simu: +255 (22) 2123103, Barua Pepe: Nukushi:+255 (22) 2122562 [email protected] Barua Pepe: [email protected]; Tovuti: www.coresecurities.co.tz

    Unit Trust of Tanzania Ernst &Young Advisory Enterprise Growth Market(Fund Manager) Services Advisors Limited (EGMA)Ghorofa ya 3, Jengo la Sukari, Jengo la Utalii House Ghorofa la kwanza, Kona ya Mtaa wa 36 Barabara ya Laibon, Jengo la Alfa House, ploti ya 25Sokoine na Ohio, Oysterbay, Barabara Mpya ya Bagamoyo,Dar es Salaam Dar es Salaam S.L.P 79807Simu: + 255 (22) 212 8460 Dar es Salaam.Nukushi: + 255 (22) 213 7593 Simu: +255 (22) 266 6853 / Simu: +255 22 2760145,Barua Pepe: 266 7659 +255 (759) [email protected] Nukushi: +255 (22) 266 6869 Nukushi: +255 (22) 2126414Tovuti: www.utt-tz.org Barua pepe: [email protected] Barua pepe: [email protected]

    Bank M Tanzania Limited Equity for Tanzania Ltd. NBC Bank Limited Money Centre Namba 8, (EFTA) Kona ya barabara ya Sokoine nabarabara ya Ocean Road, S.L.P 1747 Moshi. mtaa wa Azikiwe,Dar es Salaam. Simu: +255 (27) 2750657 S.L.P 1863, Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 (22) 2127824Nukushi: +255 (22) 2127825 Simu: +255 (22) 2199793/Tovuti: www.bankm.co.tz +255 768 980 191 Nukushi: +255 (22) 2112887/ 2113749 Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.nbctz.com

    19.0 ANUANI YA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

    Afisa Mkuu Mtendaji, Soko la hisa la Dar es Salaam,Ghorofa ya 14, Jengo la PSPF - Golden Jubilee Tower,

    Mtaa wa Ohio, S.L.P 70081, DAR ES SALAAM.Simu: 255 (22) 2128522/2135779/2123983

    Nukushi : 255 (22) 2133849Barua pepe: [email protected]

    Tovuti: www.dse.co.tz

  • SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM24

    Soko la Hisa la Dar es Salaam,Ghorofa ya 14, Jengo la PSPF Golden Jubilee

    Towers, Mtaa wa Ohio,S.L.P 70081, DAR ES SALAAM

    Simu: 255 22 212 8522 / 213 5779 / 2123983 Nukushi: 255 22 213 3849Barua pepe: [email protected]

    Tovuti: www.dse.co.tz