44
:LW[LTILY6J[VILY ,KP[PVU :LW[LTILY6J[VILY ,KP[PVU /V[ ;:/ $ 2:/: $ <:+ ZWVY[HNL TVKLSSPUN YLJYLH[PVU THSL THNHaPUL Mastaa Wanne Mastaa Wanne Katika Soko la Filamu na Mitindo Katika Soko la Filamu na Mitindo Steve Tabasamu ya Blue Imeniweka Juu. News IFM College Ndani ya Hotspot. Usajili wa Yanga Wizi Mtupu Kaseja Dully Sykes Niko kibiashara zaidi. KRWVSRWVLQGG 30

Hotspot Magazine Issue 2

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Hotspot Magazine is a Tanzania Entertainment Magazine and also is the first online magazine in Tanzania.

Citation preview

Page 1: Hotspot Magazine Issue 2

Mastaa WanneMastaa WanneKatika Soko la Filamu na MitindoKatika Soko la Filamu na Mitindo

SteveTabasamu ya Blue Imeniweka Juu.

News

IFM CollegeNdani ya Hotspot. Usajili wa Yanga Wizi Mtupu

Kaseja

Dully Sykes

Niko kibiashara

zaidi.

Page 2: Hotspot Magazine Issue 2
Page 3: Hotspot Magazine Issue 2

FOREWORD

Page 4: Hotspot Magazine Issue 2

Michael Jackson

Richa,Henry,Ally & Om

Nira Children Orphans Foundation

Tribute

Cover Stories

Beauty Tips & Food Recipe

Health

Page 5: Hotspot Magazine Issue 2
Page 6: Hotspot Magazine Issue 2

London

BIOGRAPHY

Page 7: Hotspot Magazine Issue 2

A former music-video girl who appeared in clips by Pharrell and Ludacris before making her big-screen debut in ATL, Los Angeles native Lauren London possesses a small-town beauty with a distinctive smile and a slight city-girl edge. It was during London’s stint in the Las Angeles public school system that the aspiring actress first began dabbling in theater and drama, and though she would later be home-schooled for her last three years of high school, the desire to perform never went away. Appearances in a handful of music videos helped to get London comfortable in front of the cameras, and when buzz began to build around the production of

an upcoming film called ATL, she hired an acting coach and convinced director Chris Robinson’s assistant to get her an audition. Despite being two hours late for the audition, London performed well enough under pressure to land the role of roller-skating rich girl New New — who changes her identity and soon begins dating former high-school hotshot Rashad (played by hip-hop recording artist T.I.). With buzz around the rising starlet subsequently beginning to gain momentum, London next appeared in episodes of Everybody Hates Chris and Entourage while preparing for a role in the holiday-themed family drama This Christmas.

A former music-video girl

Page 8: Hotspot Magazine Issue 2

Introduction

Page 9: Hotspot Magazine Issue 2
Page 10: Hotspot Magazine Issue 2

Richashujaa anastaili tuzo ya sifa

Alipendezesha kurasa za magazeti

mengi ikiwa ni sambamba na kutajwa

na kila mtu ambaye aliona au kusikia

yaliyokuwa yanazungumzwa katika

redio na kusomwa kwenye magazeti,

kwa mhindi kutwaa taji la Miss Tanzania

mwaka 2007. Alipotangazwa kuwa

ndio mshindi wa taji la urembo la wilaya

ya Kinondoni 2007 (Miss Kinondoni

2007)watu wengi walifurahia. Kitimtimu

kilianza pale alipotangazwa kwamba ndio

mshindi wa taji la urembo wa Tanzania

(Miss Tanzania 2007) Lakini punde suala

la Utanzania likaibuka.

Suala la rangi ya ngozi, asili ya wazazi wake na yeye mwenyewe kuwa au kuonekana mhindi lilitawala na sio

Utanzania wake hapa namzungumzia Rricha Addhia. Naweza kusema kitendo kilichoonyeshwa wazi wazi cha

kumbagua mwanadada Rricha ndicho kilichomfanya hata asifanye vizuri katika kinyang’anyiro cha Miss World

mwaka 2007. Rricha ni binti aliyezaliwa miaka 21 iliyopita jijini Dar- es-salaam, na kukulia jijini Mwanza na

kufanikiwa kupata elimu yake ya msingi huko huko mwanza, baada ya miaka kadha alirudi Dar, na kujiunga

na elimu ya sekondari ya Shabaan Robert mwaka 2005 na baadae kufanikiwa kupata kazi katika kampuni ya

Berger Paints Ltd (Robbialac) akiwa kama mkurugenzi mtendaji. Ni mtanzania halisi............?

COVER Story

Page 11: Hotspot Magazine Issue 2

i a

Kwa mara ya kwanza ukikutanaye katika mazingira

fulani ambayo hayuko katika fani yake unaweza

ukasema ni mtangazaji au mwanamuziki, hii ni kutokana

na umbo lake, mavazi yake pamoja na muonekano

wake kwa ujumla.

Hapa namaanisha Ally Hassan maarufu kama Ally

Model ambaye amekuwa akitikisa katika masuala ya

uwanamitindo kwa zaidi ya miaka 6.

Mtu aliyemvutia katika masuala ya umwanamitindo ni

msanii wa muziki kutoka marekani ambaye anajulikana

kama Tyrees, lakini mbali ya husuda kwa gwiji hilo

ilimchukuwa muda sana kuzoea kupanda katika jukwaa

kutokana na macho ya watu na uwoga.

Anasema kabla ya hapo alikuwa anafanya

uwanamitindo alipokuwa chuo katika mashindano

mbalimbali. “Nilipenda kuwa mwanajeshi, na wakati

huo huo kuwa huru, jambo lilishindikana na hivyo

kunilazimu kukodolea fani zingine kama utangazaji na

uwanamitindo, fani ambazo nilikuwa nazipenda ndizo

hizi nazifanyia kazi hadi hivi sasa, anaeleza

. Anasema katika dunia ya uwanamitindo aliingia rasmi

mwaka 2003, ikiwa ni sambamba na shoo yake ya

kwanza ambayo ilikuwa inajulikana kama ‘Beat Galla

Night’ ambayo ilifanyika katika ukumbi wa Golden Tulip.

Tangu mwaka 2003 hadi sasa nimefanya shoo nyingi

sana kiasi kwamba hadi nasahau. Ally kwa sasa yuko

katika ‘website’ ya Mwanamitindo bora wa Afrika

inayojulikana kama Black Butterfly (Black Model) ya

Afrika Kusini.

“Kwa hapa Tanzania najiona mimi ndio bora kuliko

wote, kwa sababu watu ambao nashindana nao katika

Black Butterfly ni wanamitindo ambao wanajulikana

duniani kote”.alisema Aliwataja madizaina ambao

amefanya nao kazi kama Mustafa Hassanally, Hindu,

Rose Vallentine, Irida Same, Asia Idarusi, Manji,

Ally Remtulla, na Farha. Anasema Uwanamitindo

umemletea faida nyingi ikiwemo kufanya matangazo ya

VodaCom,kampuni ya sigara ya SM, kampuni ya maji

ya Kilimanjaro na kampuni ya simu ilikuwa ikijulikana

kama Celtel.

Anasema mbali na uwanamitindo, Ally ni mtangazaji na

mwandaaji wa kipindi cha ‘ulimwengu nadhifu’ ambacho

kinarushwa katika kituo cha channel ten kila ijumaa.

Alibaainisha kwa kusema kwa kuwa uandishi wa habari

aliupenda basi akamua kwenda kusomea katika chuo

kilichokuwa kinajulikana kama TIMES kwa sasa ni

Dar-es-salaam School of Journalism (DSJ). “Kama

kijana jitahidi utimize malengo yako uliyo jiwekea katika

maisha yako.”

Ally Hassan

Page 12: Hotspot Magazine Issue 2

Ni mmoja kati ya waigizaji maarufu nchini Tanzania. Lakini kutokana na rangi yake, watu

wengi wamekuwa wakihoji kwamba imekuwaje mhindi kaingia katika sanaa ya bongo,

kila mtu amekuwa akisema yake bila kujua wanaongea nini.

Namzungumzia mcheza filamu ambaye anajulikana kwa jina la OM, ambaye

ameonekana katika filamu mbalimbali ,ambazo zinafanya vizuri katika ulimwengu wa

filamu za bongo ambazo amecheza kama muigizaji mkuu (Starring).

Akiwa mwenyeji wa mkoa wa kilimanjaro, Om amekuwa akifanya vizuri katika fani yake

ya uigizaji pamoja na uwanamitindo.

Alipokuwa akiongea na Hotspot, Om aliweka wazi maisha yake na jinsi alivyoweza

kufikia hapo. Anasema, maisha yake katika sanaa ya uigizaji alianza mwanzoni mwa

mwaka 2008.Hapo alishiriki kwenye filamu iitwayo ‘Ama zako Ama zangu’.

Filamu hiyo iliweza kumtambulisha vizuri katika anga za waigizaji wa Tanzania.

“filamu hiyo niliyoshiriki ilifanya nijizolee sifa na umaarufu mkubwa kwa washabiki

pamoja na wasanii wakongwe, hapo ndipo nikaanza kushirikishwa katika filamu

mbalimbali.

Anasema , alishirikishwa tena katika filamu iliyokuwa inakwenda kwa jina la ‘Kipenzi

Changu’, (My Love) ambayo nayo alicheza kama muigizaji mkuu.

Om ameshiriki katika filamu iitwayo Full Moon ilitoka hivi karibuni .Filamu hiyo ambayo

ina ‘part 1’ na ‘part 2’ akiwa na aliyekuwa Miss Tanzania 2007 anaejulikana kama

RRicha Adhhiaa.

Anaelezea kwa ufupi filamu ya Full moon. RRicha kama mke wangu ambaye naishi

naye kwa furaha ila mfanyakazi wa nyumbani (House Girl) anaingilia mapenzi yetu kwa

kunitaka mimi huku mimi simtaki, basi anafanya visa hadi mke wangu anafariki na

sehemu ya kwanza inaishia hapo, sehemu ya pili (part 2) mke wangu anafufuka kama

mzimu na kulipiza kisasi kwa ‘house girl’.anaeleza

Anasema mambo hayo yapo katika nyumba nyingi, house girl ukimwachia mwanya

lazima ampiku mama mwenye nyumba na sio ‘mahouse girl’ peke yao hata ‘mahouse

boy’ nao wana tabia hizo ila kwa vile imesha zoeleka kwamba wafanyakazi wa kike

ndio wanachukwa wanaume za watu. Anasema anatarajia kuwa mwaandaaji na

muongozaji wa filamu kwa miaka ya usoni mungu akimjalia uzima.

Mpaka sasa OM ameshiriki katika filamu kama Ama Zangu Ama Zako, Kipenzi Changu

na ‘Full Moon’.

Mbali na uigizaji Om pia ni mwanamitindo ambaye ameanza tangu mwaka 2005.

“Uwanamitindo naupenda sana, vilevile nilikuwa na vigezo vyote vya kuwa

mwanamitindo lakini kutokana na rangi yangu niliogopa, na nikapiga moyo konde

nikafanikiwa hadi leo, watu wananikubali katika fani hii”alieleza. Hadi sasa nimeshiriki

shoo nyingi na madizaina wa ndani na nje ya nchi.

Anawataja baadhi ya madizaina ambao anafanya nao kazi, kama Ally Remtulla, Mustafa

Hassanally, Aloisi Martin, Farha Farouq, Latif wa Uganda pamoja na John Kaveke wa

Kenya.

Mbali na uwanamitindo, Om ni msomi mwenye stahashada ya ufamasia ambayo

ameipata katika Chuo Kikuu cha Muhimbili. “Wengi wamekuwa wakizadharau kazi

ambayo tunafanya ya uigizaji na uwanamitindo ni vitu ambavyo tunavipenda siyo

kwamba tunakimbilia huku hatuna elimu” anaelezea. Om ni kijana aliyezaliwa mjini

moshi katika hospitali ya (KCMC) na kufanikiwa kupata elimu yake ya awali katika shule

ya msingi ya moshi, elimu yake ya sekondari amepatia Mount Kilimanjaro.

Page 13: Hotspot Magazine Issue 2

Natarajia kuwa msanii na mwanamitindo wa kimataifa

Ukimwangalia kwa haraka haraka unaweza kusema ni Mmarekani ambaye amekuja Tanzania kutalii, hayo yote yanatokana na jinsi alivyo, mavazi anavyopangilia, kifupi jinsi anavyoendesha maisha yake. Huyu ni Henry Mwiki ambaye amekuwa aking'ara katika luninga pamoja na mabango ya matangazo mbalimbali, kama ‘home shopping centre’ yanayoonekana maeneo mbalimbali jijini. Katika mazungumzo na Hotspot , Henry alieleza kwa undani juu ya maisha yake, hadi hapo alipofikia kwa sasa. Baada ya kumaliza kidato cha sita mwaka 2008 alijitosa rasmi katika masuala ya uwanamitindo kwa kupata sapoti kutoka kwa rafiki yake ambaye anajulikana kwa jina la Edie, ambaye aliwahi kushiriki mashindano ya ‘Mr Dar handsome’ miaka ya nyuma.

Akizungumza na Hotspot Henry anasema, kwa vile nilikuwa na vigezo vyote, nilipomwambia nahitaji kuwa mwanamitindo, alikubali kunisaidia na kunipeleka kushiriki shoo ya ‘Nivana’ ambayo ilifanyika mwaka jana. "Uwanamitindo ni fani ambayo nilikuwa naipenda tangu niko mdogo, lakini kutokana na kubwanwa na shule niliaamua kusubiri nimalize kidato cha sita ndio niingie rasmi katika fani hii, kwa hiyo naona kama ndoto yangu niliyokuwa nawaza imetimia" anasema Henry. Mwaka 2008 alifanikiwa kufanya shoo ya ‘Nivana’ ambayo ilikuwa ni mara ya kwanza tangu aingie katika fani hiyo ya ulimwengu wa uwanamitindo. Shoo ya ‘Nivana’ ilimpatia umaarufu mkubwa kwa jinsi alivyoweza kumiliki jukwaa kama mtu ambaye amekuwa katika fani hiyo kwa muda mrefu. Mwaka huu alishiriki katika ‘Most Handsome Tanzania’ iliyofanyika katika ukumbi wa New Africa Hotel na kufanikwa kuwa mshindi wa pili. Kutokana na uwezo wangu ambao ninaonyesha katika ulimwengu wa uwanamitindo” anasema.

‘Utanashati ndio unaonisaidia katika fani ya uwanamitindo, wengi wamekuwa wakisema kwamba uwanamitindo ni uhuni, si uhuni , ni sanaa kama sanaa nyingine’. Aliwataja wanamitindo Om na Ally kuwa ndio waliomfanya avutiwe na fani hiyo. Anaendelea kusema kuwa alianza kujihusisha katika filamu mwishoni mwa mwaka 2008. Henry si mwanamitindo tu, bali pia ni msanii chipukizi wa filamu ambaye anatarajia kuliteka soko la filamu nchini kutokana na uwezo wake ambao ameuonyesha katika filamu inayojulikana kwa jina la ‘Siku Yangu’. Ameshiriki katika filamu iitwayo ‘Siku Yangu’ ambayo amecheza kama muigizaji mkuu (Starring) ambaye ameoa mfanyabiashara huku yeye akiwa anasoma chuo, huku akilipiwa ada na mke wake, kumbe naye mke wake alikuwa akipewa fedha hizo za kumsomesha na mwanaume mwingine, kitu ambacho alikuja kikigundu baada ya muda mrefu sana. "Siku Yangu ni filamu yangu ya kwanza kucheza na ninatarajia kufanya makubwa zaidi ya hata hayo niliyoyafanya katika filamu ya Siku yangu "anasema Henry amezaliwa Julai 2 mwaka 1988 jijini Dar es Saalam, alifanikiwa kupata elimu yake ya msingi katika shule ya Hananasif iliyopo kinondoni, alihitimu elimu yake ya sekondari katika shule ya kibaha mwaka 2005, mwaka 2006 alijiunga kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya mzumbe, na kufanikwa kujiunga na elimu ya juu katika chuo cha IFM.

aammmekuja Tana zazaninia a kukuttalilii,i, h hayayo o yoyotete y yanannatatatokokokkananana a a nana j jinsi alivvyyooo, nrrn y Mwiki amambabayeye a amemekukuwawa a akikingng'a'arara k katttikikka a aa luluulunininingngn a a papamomojajaa yyoonekakanana m maeaeneneo o mbmbalalimimbabalil jjijijinni.i. K Katatikka a mamamaazuzuzungnggumumzozo nnaaa kkwa sassa.a. BaBaadada a yaya kkumumala izzaa kikidadatoto c chaha s siti a a a mmwmwmwwakakaa aa a 2002 088

wawaa r afiki yaakeke aambmbayaye e ananajajululikikanana a kwkwa a jij nan lla a EdEddieieieiee, , ,, amamambaab yee

ninn lipopoppppppppp mwmwmwwamamama bibia a nanahihitatajiji k kuwuwa a mwmwananamamittinindoodo, alalalalikikikikkubububu allijajaannana. . "" UwUwwanananannaamama ititi inndodo nnii fafanini a ambmbayayo o ninililikukuwawaaa n n naiaiaiaiipepeppppendnddnda a aa taat ngnggn u uzzeee k kididdatato chchchha a aa a sisiss tataa nndid o o nin iningigie e rarasmsmi kakatitikaka fffananna i i i hhihihih i,i,ii, kkkk wawwawaa hh h hiyiyiyyo o

iii m mararara a a yaya kkwwawawaanznzn a a tangu aiaingngieie k katatikikaa fafanini hiyo o yyayaaa uliliiimmmmwwwenene gguuuu vyoweza kukuummimililikki jukkwawaa a kakamam mtu ambmbayaye ammeekekkuwuwwwaa kakatikkaaaa nnzazaninia’a i ilililiyoyyoyoyofafafanyika kakatitikka ukumbi wa Neww A frica a HHHooteteeel l nan eseseshahaha k k kkatatatikika ulimmwwengu wa uwanamitindo” a anaseemmmaam .

wakisemaa k kwamba uwanamitindo ni uhuni,i, si uhuunni i , , nini waliomffananya avutiwe na fani hiyo. Anaenndedelea kuusees maama kkuwuwa awanamamitindo tu, bali pia ni msanii chchipipuukizi wa filammuu aammbabaye euonynyesha katika filamu inanayoyojujulilikakana kwa jina la ‘Siku ma mumuigigizizajajii mkmkuuuu ( (StStararriringng) ) amambaye ameoaoa m mfanyabbiaashhaaraa aye mke wakake alalikikuwuwa a akkipi ewa fedha hizoo zza a kukumsommeseshah refu sana. "Siku u Yaangu u ninn filamu yangu yayaa k kkwawannza kuchhezeza a uu yayaya S SSikikikuu u yayay ngngu u "aananaseemaa Henry amezezzaalaliwiwwaa a Julai 2 mwmwaakkkkaaaaa aa aa a a a a aaaa aaa aaulule e yayaa H HHananananannasasasa ififif ilililiyiyiyyopopopoo o kik nondoni, alihihiittititimmumuuuuuuuuuu eeee limumu y yakakee yaya o ccchahaa t tanano o nanana s ssititita a kakakatitikkaa shulee y yaa sesekokkko dddndndarariiiii yaya m mzuzumbmbe,e,e,e,,, n n n n aaa a a aa a a a a aa a

Henry

Page 14: Hotspot Magazine Issue 2

2009 Dodge

What’s New for

2009For 2009, the Dodge Charger’s available V8 gains more power and better fuel economy, while the optional all-wheel-drive system has been similarly upgraded to enhance fuel economy. The Charger SRT8 also sports improved fuel economy as well as a new Super Bee package with orange paint. All Chargers feature minor exterior and interior detail revisions.

Charger Vehicle Overview

AUTO Mobile

Page 15: Hotspot Magazine Issue 2

Dodge Charger Vehicle Overview

Page 16: Hotspot Magazine Issue 2

Beauty Tip of the MonthBeauty Tip of the MonthImportant DIET for maintaining your health.

HEALTH Habits

FASHION

Page 17: Hotspot Magazine Issue 2

Animals CrueltyANIMAL Article

Page 18: Hotspot Magazine Issue 2

Miss h

FASHION

Page 19: Hotspot Magazine Issue 2

s higher learning 2009

Page 20: Hotspot Magazine Issue 2

vodacom d

Picha No2 Picha No4 Picha No3 Picha No1

CORPORATE Event

Page 21: Hotspot Magazine Issue 2

dar marathon

Picha No6 Picha No4 Picha No1 Picha No5

Page 22: Hotspot Magazine Issue 2

Models on the Beach aRivals on the runway but relax on the beach as f

Shoma

Lizzie

HANG Out

Page 23: Hotspot Magazine Issue 2

h at Kipepeo. as friendly competitors

Wambui

Wambui

Hidaya (Lady Dread)

Gloria

Page 24: Hotspot Magazine Issue 2

S

J

S

"Wengi wamekubali kipaji changu kwa kupitia wimbo ambao nilishirikishwa na Mr Blue unaojulikana kama Tabasamu."

Hiyo ni kauli ya msanii Steve William ambaye ni maarufu kama Steve.

Steve alitoka na ngoma zake mbili ambazo zilikuwa zinajulikana kama 'Nisamehe' na 'Nimeshindwa' kwa bahati mbaya hazikuweza kufanya vizuri katika anga la muziki wa kizazi kipya.

Mafanikio yalianza kuja baada ya kushirikishwa katika wimbo wa Mr Blue unaojulikana kama 'Tabasamu' ambao aliimba kiitikio na kuonyesha uwezo mkubwa zaidi na kuonekana ni mmoja wa wasanii vinara wa bongo fleva.

"Sikutarajia kama ningeweza kupata mafanikio ya haraka kama ku-perform katika shoo za fiesta, ikiwa sambamba na kupata meneja anayesimamia kazi zangu ambaye ni Tippo maarufu kama ZIZZOU, ukweli ni kwamba tabasamu ndio wimbo ulioniweka katika ramani ya muziki Afrika mashariki," alisema.

Kwa sasa msanii huyu anatamba na wimbo unaojulikana kama 'Sogea Karibu' akiwa amemshirikisha Dataz, uliorekodiwa studio za combination sound na video ikiwa imefanywa na John Kallage, wimbo huo umeendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni.

"Watu watarajie kusikia wimbo wangu mpya ambao nimefanya na Albert Mangwea maarufu kama Ngwear utakaokuwa unajulikana kama 'Najisikia furaha' ambao ninatarajia kuuachia muda wowote kuanzia sasa."

CELEBRITY News

Page 25: Hotspot Magazine Issue 2

Sijafulia

nakuja na zaidi ya

Halua na Tende

J.I:

Spark "Baba ndio aliyenilipia studio nyimbo yangu ya kwanza"

Page 26: Hotspot Magazine Issue 2

w

s

k

t

g

k

z

a

y

u

i

a

i

i

w

k

w

z

Endru G.

Jinsi alivyo ni wimbo uliotokana na historia ya kweli

ambayo imemtokea msanii kutoka nyumba ya vipaji (THT)

anayejulikana kama Endru G.

Akizungumza na Hot Spot alisema: “Ni kitu ambacho

kilinitokea siku ambayo nilikuawa Club na rafiki zangu ndipo

hapo nikamuona huyo demu ambaye alinivutia kwa muda

mfupi nilipotaka kumfuata rafiki zangu walisema niachane

naye huyu binti ni malaya kutokana na uzuri wake.

“Kutokana na roho yangu ilikuwa imeshapenda nikaamua

kujitosa kumbe na yeye alikuwa amenizimia basi bila

kuchelewa tukaenda kucheki afya tukakuta tuko safi pia

alikuwa anasimamia kampuni ya baba yake ya kuuza

magari bila kujua baadhi ya marafiki zangu walivyoona

nakula good time wakaanza kupaka kwamba fedha na

magari aliyokuwanayo anahongwa na mafataki.”

Alimalizia kwa kusema hata matonya aliimba usilolijua ni

usiku wa giza”

Historiaya kweli

Ukimya wangu wa kibiashara zaidi-Dully SykesWengi walimfahamu kwa kupitia nyimbo

zake kama Salome, Hi, Julieta na nyinginezo

nyingi, anajulikana kama Mr.Misifa au Dully

Sykes.

Msanii huyo amekuwa kimya kwa muda mrefu kitu ambacho

wengi wamekuwa wakijiuliza kashindwa ‘game’ au yuko

likizo, hivi karibuni kavunja ukimya kwa kutoka na nyimbo

mbili tofauti, moja tayari amesha itambulisha inayojulikana

kama ‘Loud Speaker’, na nyingine anatarajia kuitambulisha

siku za usoni itakayokuwa inajulikana kama ‘Pull up’ ambayo

ame ifanyia katika studio yake ya Dhahabu Record ikiwa

imeandaliwa na yeye mwenyewe, wimbo huo unatarajiwa

kufanyiwa video hivi karibuni, alisema.

Akiongea na Hotspot alisema, “Ukimya wangu ni wakibiashara

zaidi, siwezi kutoa nyimbo mfululizo bila maslahi yoyote,

lazima nilenge na muda wa kuachia nyimbo zangu, muda

mzuri wa kuachia nyimbo ni kipindi cha likizo pamoja na fiesta

na matamasha mengine ya katikati ya mwaka.”

Alimalizia kwa kusema kingine kinachochangia ukimya

wangu ni studio yangu ambayo kwa sasa nakaa mwenyewe

katika kutengeneza ngoma za wasanii mbalimbali, alitaja

wasanii ambao amewatengenezea nyimbo ni Mh Temba,

Mwana FA, Madee na wengine wengi, kwa hiyo washabiki

wangu wategemee ngoma kibao kutoka kwa mkali wao,”

alisema Dully.

Page 27: Hotspot Magazine Issue 2

Wengi humuita Barnaba Boy, lakini kwa wazazi wake

wanamfahamu kama Elias Barnabas ambaye anatingi-

sha Afrika Mashariki na wimbo wake wa ‘Njia Panda’

Msanii huyo hivi karibuni anatarajia kupanda ndege

kwa safari ya Ufaransa baada ya kupata mwaliko ku-

toka kwa mwanamuziki wa nchi ya Kidemokrasia Con-

go mwenye makazi yake nchini Ufaransa anayejulikana

kwa jina la Fally Ipupa ambaye aliwahi kuja nchini Tan-

zania miezi kadhaa iliyopita kwa ajili ya kufanya shoo.

Akizungumza na Hotspot alisema. “Nakumbuka siku

ambayo Fally Ipupa alipotutembelea (THT) nyumba

ya vipaji, alinikuta nikiimba nyimbo zake alivutiwa na

uwezo mkubwa wa kuimba nilionao akahitaji asikie ny-

imbo zangu, basi nami sikusita kumwimbia hapo ndipo

alipo kubali kipaji na kuniomba nifanye naye shoo siku

iliyofuata, sambamba na shavu la kufanya naye ny-

imbo ndipo hapo tukapeana mawasiliano, hivyo muda

wowote kwanzia sasa naondoka na kuelekea Ufaransa

kufanya naye kazi.”

Alimalizia kwa kusema. “Kutokana na ubunifu nilionao

washabiki wangu mtegemee vitu vipya toka kwangu

zaidi ya Njia Panda pindi nitakaporudi toka Ufaransa”

“Haya basi yameisha tutapanga upya saa na dakika ili usin-

iache nikalialia,” ni moja kati ya mistari ambayo ameimba ka-

tika wimbo alioshirikishwa , wimbo ambao unajulikana kama

‘Njia Panda,’ si mwimbaji mwingine bali ni Doreen maarufu

kama Pipi Pipi ni msanii kutoka Nyumba ya Vipaji Tanzania

(THT) hivi karibuni anatarajia kutoa wimbo wake wa kwanza

ambao utakaokuwa unajulikana kwa jina la ‘Usinune.’ Wim-

bo huo ameurekodia katika studio za Bongo Record chini ya

muaandaji, (producer) P-Funk. Kwenye Usinune, Pipi amejibu

mapigo kwa kumshirikisha rafiki yake wakaribu maarufu kama

Barnaba Boy. Pipi alielezea sababu za kumshirikisha Barn-

aba, anasema “Barnaba ni mwimbaji ambaye namkubali ku-

tokana na kipaji alichonacho, ndio maana nikamuona anafaa

katika wimbo wangu.” Aliongeza, “Vile vile nimelipa shukrani

kwa kunitoa katika giza nene liliotanda katika anga la muziki

wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’, ninaamini bila yeye mimi nis-

ingefika hapa nilipo, ingenichukua muda sana kujulikana na

wadau pamoja na wapenzi wa muziki huu”.

“Mashabiki wangu watarajia vitu vizuri zaidi ya vile nilivyo vi-

imba kwenye wimbo wa ‘Njia panda’.”

Page 28: Hotspot Magazine Issue 2
Page 29: Hotspot Magazine Issue 2

Hussein Machozi umetupotosha na Kafia Ghetto. Dhumuni la page hii ni kupunguza makosa yanafanywa na wasanii pamoja na Wandaaji wa video na nyimbo. Leo tunaanza na wimbo wa Hussein Machozi ‘KAFIA GHETTO’ sambamba na video yake.

Mashairi ya Kafia Ghetto Siku nyingi binti namfukuzia alishanitosa nilishakata tamaa sikujua kama kwangu angekuja nilitoa matumaini ya kumpata, leo hii kaja mwenyewe mchumba ghetto kwangu mpaka ndani kaingia nilimuuliza naweza kumsaidia, akacheka kisha kaniambia ombi langu lile amenikubalia siku zote alikuwa akinifikiria, niliruka kwa furaha kubwa sana sikuamini kama mchumba ningempata, ‘usilolijua ni usiku wa giza’ ningetambua bora ningemtimua .

Nani ataniona mi mkweli, Nani nikimuelezea ataniamini, Nani ataniona sio katili, Nani atanisaidia mimi.

Baada ya story binti nilimuuliza kinywaji gani angeweza kutumia, alinieleza kisha mimi nikainuka

nikaelekea dukani kununua, huwezi amini nyuma nilipomuacha baada ya kurudi ndio kizaazaa, binti alikuwa kitandani kajilaza nilimuamsha lakini hakuamka pumzi zake zilikuwa zimekata nilizani labda kazimia maji ya baridi kichwani nilimwagia lakini hata hakushtuka ‘kumbe tayari ameshakufa’ nimekwisha Hussein bila kujua.

Hee mola nimekosa nini, Hee mola niokoe mimi, basi nipe akili mimi nifanye nini furaha yangu imekuwa kilio changu, ndoto zangu leo machozi kwangu nitawaeleza nini walimwengu,

Rudia korasi x2 kisha namalizia kwa kusema

HIVI UNGEKUWA WEWE UNGEFANYA NINI?

Ushauri kwa Hussein Machozi Msanii kazi yake ni kuelimisha na kufundisha, je, Husseni ametufundisha nini kama sio kutupoteza kwa kutuuliza ingekuwa sisi tungefanya nini bila kutupa jibu kwanza kisha ndio atuulize swali.

HitimishoWasanii wengi wamekuwa wakiimba

kitu kama alicho kiimba hussein

machozi, lakini kutokana na kufatilia

radha sana kuliko ujumbe imetufanya

tuizoee hali hiyo,lakini kikweli hapo

wasanii wamekuwa wakitudanganya

siku hadi siku.

Kwa asilimia kubwa maadhira ndio

wanatakiwa kubeba lawama hizi,

kutokana na kukubali kitu ambacho

hakijakamilika na kukipokea kwakifupi

hakina ujumbe matokeoyake inakuwa

ni maswali kwao je hizi lawama ziende

kwa nani ukiangalia kila mtu anahusika.

Mimi naona lawama hizi anatakiwa

abebe producer wa video natimu yake

nzima, ikifatiwa na msanii mwenyewe

kila mtu hapo ana lawama zake,

kwa upande wa msanii kuwa makini

katika utunzi wa mashahiri wake, kwa

upande wa producer wa video kujitaidi

kuonyesha maana nzima ya wimbo

unavyo hitaji, kikubwa ni ubunifu wa

producer kwa sababu yeye ndiye

sehemu ya mwisho inamaana chochote

ambacho kitakuwa kimepungua au

kuongezeka ni lawama kwake.

Kama msanii na producer wa video

wataelewana nina amini hakuto weza

kutokea kitu kama alicho kifanya

brother Hussein machozi na wasanii

wengi.

Audio

video. Basi kama ilishindikana ange onyesha hata kwenye video yake lakini cha ajabu video inaishilia kwa kuonyesha huseni anapigwa je ataendelea kupigwa maisha yako yote au. Audio. Pia akatoa remix yake ambayo nilitegemea angetoa muendelezo wa huo wimbo

kwa kuwafahamisha washabiki wake kwamba alifanikiwa kupata suluhu kwa kutumia njia gani lakini cha ajabu alibadilisha ala tu mashairi yale yale,ushauri wangu kwako toa remix ya tatu nadhani hapo utatuweka sawa washabiki wako ok.

KAFIA

GHETTO

Wasanii wengi

wamekuwa

wakiimba kitu

kama alicho kiimba

hussein machozi,

lakini kutokana

na kufatilia radha

sana kuliko ujumbe

imetufanya tuizoee

hali hiyo,lakini.......

Page 30: Hotspot Magazine Issue 2

ANTIPA HERBALS

For more details,please contact us:

Dr. Samson Kibona, Antipa Natural Therapies Centre P.O.Box 20669 Dar es Salaam, Tanzania

Cell:+255 754 464 525/784 220181 E-mail: [email protected]/[email protected]

Page 31: Hotspot Magazine Issue 2

AVProdu

ction

ADVERTISING & SUBSCRIBE IN HOTSPOT MAGAZINE

Page 32: Hotspot Magazine Issue 2

Biography 0n Michael Jackson

Tribute

Page 33: Hotspot Magazine Issue 2

Biography 0n Michael Jackson

Page 34: Hotspot Magazine Issue 2
Page 35: Hotspot Magazine Issue 2
Page 36: Hotspot Magazine Issue 2

IFM College ndani ya HotSpot Magazine

COLLEGE Views

Page 37: Hotspot Magazine Issue 2
Page 38: Hotspot Magazine Issue 2

NIRA CHILDREN AND YOUTH ORPHANS FOUNDATION

Page 39: Hotspot Magazine Issue 2

UnderTenisi

kushiriki Junior Tornament TIMU ya tenisi ya Gymkhana chini ya miaka

14 inatarajia kwenda Rwanda na Burundi

kushiriki mechi za Junior Tornament

zinazotarajia kufanyika mwezi ujao huku

zikiwa zinajumuiisha timu za Afrika

Mashariki.

Akizungumza na Hotspot, kocha wa timu

hiyo Salum Mvita alisema “timu inatarajia

kwenda Rwanda na Burundi kushiriki

michuano ya junior tornament ambayo

inatarajiwa kufanyika mwezi huu, michuano

hiyo ikiwa inajumuiisha timu kutoka nchi za

jumuiya ya Afrika Mashariki”.

Hivi sasa timu hiyo iko katika mashindano

ya Tango Open ambayo yanafanyika katika

viwanja vya Club Gymkhana, yakiwa

yanashirikisha timu za ndani kwa ajili ya

kufanya mchujo wa wachezaji ambao

watakwenda kushiriki mechi za kimataifa.

“Nina uhakika na timu yangu kwenda

kufanya vizuri katika mashindano hayo

yaliyokuwa mbele yao kutokana na mazoezi

na mbinu ninazo wafundisha”alisema

Salum.

Aliongezea kwa kusema katika mchezo

huu wasichana ni wachache sana kwa hiyo

anaomba wasichana wajiunge kwa wingi

ilikuwe na mchanganyiko, huu sio mchezo

wa wavulana tu, ni wa watu wote.alisema

Page 40: Hotspot Magazine Issue 2

TIMU ya taifa ya gofu ya Gymkhana chini ya

miaka 18 inatarajia kwenda kushiriki mich-

uano ya Junior Coast Open Championship

itakayofanyika nchini Kenya Agosti mwaka

huu.

Akizungumza na Hotspot, nahodha wa

timu hiyo Salim Shariff alisema “Tunatarajia

kwenda Kenya kushiriki michuano ya ‘junior

coast open championship’ mwaka huu,

michuano hiyo huwa inafanyika kila mwaka

ikiwa inajumuiisha wacheza gofu wa Afrika

Mashariki.”

Timu hiyo imefanikiwa kutwaa makombe

mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, hivi kari-

buni imefanikiwa kushika nafasi ya tisa kati

ya timu 15 katika michuano ya All Africa Golf

iliyofanyika Aprili mwaka huu.

“Hivi sasa tunafanya mazoezi kujiandaa na

michuano hiyo tukiwa chini ya mdhamini

wetu Malinzi ambaye amekuwa nasi kwa

muda mrefu, kwa niaba timu ya vijana chini

ya miaka 18 napenda kusema tunamshukuru

sana kwa msaada wake”.

Alimalizia kwa kusema “vijana wenzangu

msiogope kujifunza mchezo wa gofu, kwa

kuhofia kwamba ni mchezo wa kitajiri, huu ni

michezo wa watu wote haubagui ila watu we-

nyewe ndio wanajibagua, vilevile tunaomba

wadau pamoja na wadhamini wawekeze ka-

tika mchezo huu ili uweze kupata wachezaji

wengi zaidi chipukizi” alisema Salim.

Page 41: Hotspot Magazine Issue 2

VINARA wa kili RBA 2002 sinza

warriors wenye makazi yao

sinza wamejigamba kurudi upya

katika ulimwengu wa kikapu hivi

karibuni.

Akizungumza na Hotspot, na-

hodha wa timu hiyo Dian Chake

anasema “tunatarajia kurudi upya

kwa nguvu zote ili kurudisha

heshima tuliyokuwanayo zamani,

kutokana na mazoezi tunayofanya

tunatarajia mwaka kesho kushiriki

mashindano ya mtoano, mungu

akitujalia uzima”

Sinza warriors club ilifanikwa

kushika nafasi ya pili mwaka

2002 Kili RBA, mwaka 2007 club

hiyo ilishuka daraja katika ligi

ya mtoano kutokana na sababu

mbalimbali.

Alimaliza kwa kusema tunaomba

wizara ya michezo, habari na

utamaduni itilie mkazo na mchezo

wa kikapu siyo kuangalia mchezo

mmoja tu, hata Raisi wa Marekani

Barrack Obama alimwomba Raisi

Kikwete akuze mpira wa kikapu

Tanzania alipokutana nae katika

moja ziara yake.

Sinza Warriors

imerudi tena

USAJILI WA KASEJA YANGA WIZI MTUPU Hivi karibuni Mlinda mlango Juma

Kaseja amesaini mkataba wa kuiche-

zea simba baada ya ule wa awali na

yanga kumalizika rasmi juni 5 mwa-

ka huu, huku yanga ikiwa imetumia

mamilioni ya fedha bila mafanikio.

Mwaka jana Kaseja aling’oka Simba

kwa kitita cha Tsh milioni 36 na kue-

lekea yanga ikiwa kama fungu la usa-

jili wake wa kuelekea yanga.

Vilevile kaseja alikuwa analipiwa

pango (nyumba) kwa Tsh.milioni 3,

na timu ya yanga ikiwa ni moja kati

ya masharti ya mkataba ulivyokuwa

unasema.

Yanga imnunua kinara huyo kwa ku-

tumia Tsh. milioni 25 kwa klabu ya

simba kwa ajiri ya kumchukuwa kwa

muda wa mwaka mmoja.

Kaseja alikuwa anapokea mshahara

kwa mwezi Tsh. milioni 1 kwa mwa-

ka Tsh. milioni 12 kutoka kwenye

Timu yake ya zamani nina maanisha

Yanga, gharama hizo ni nje ya posho

ambayo alipokea Tsh. 2.5

Usajiri Tsh. 36,000,000.

Pango (nyumba) sh. 3,000,000.

Malipo kwa simba

Tsh. 25,000,000.

Mshahara kwa mwaka

Tsh. 12,000,000.

Jumla ni Tsh. 76,000,000+2.5

ambayo ni posho.

Tukijumlisha gharama walizotumia

Yanga kwa Kaseja kwa mwaka inafi-

ka Tsh. milioni 76 gharama hizi zote

hazihusiani na matibabu, chakula na

maradhi wakati akiwa kambini.

Yanga walifanikiwa kutwaa ushindi

wa Ligi kuu ya Tanzania Bara msimu

uliopita ikiwa na mlinda mlango

Juma Kaseja.

Ukiangalia gharama mbazo wame-

tumia Yanga kwa mlinda mlango

huyo je zina fanana na kitu ambacho

amekifanya kwa mwaka mzima? au

ni Wizi Mtupu kama alivyo sema Ma-

sanja Mkandamizaji.

Page 42: Hotspot Magazine Issue 2
Page 43: Hotspot Magazine Issue 2
Page 44: Hotspot Magazine Issue 2