Upload
robert-okanda
View
59
Download
0
Embed Size (px)
DESCRIPTION
Hotuba DC Makonda- Anzisha
Citation preview
HOTUBA YA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI BW.PAUL MAKONDA YA KUWAAGA WASHINDI WA TUZO YA ANZISHA (ANZISHA PRIZE) KUTOKA TANZANIA TAREHE 09 NOVEMBA 2015.
Mkurugenzi TPSF,
Ndugu Waandishi wa Habari,
Wageni Waalikwa,
Nimeelezwa kuwa leo tunakutana hapa kuwaaga na kuwatakia kheri vijana wa
kitanzania SirJeff Dennis (21) na George Mtemahaji (22) ambao watasafiri kesho
kuelekea Afrika ya kusini baada ya kushinda mchakato wa awali wa Tuzo za
Anzisha.
Hii ni fahari kubwa sio kwa hawa vijana tu bali na kwa Taifa kwa jumla na
tunawatakia kila la kheri katika fainali za kumpata mshindi mkuu (Grand Winner)
wa Tuzo ya Anzisha ambapo nimeambiwa fainali itafanyika baada ya kuhitimisha
mafunzo ya wiki mbili ya ujasiriamali.
Nawapongeza pia Chuo cha Uongozi Afrika (African Leadership Academy) cha
Afrika kusini kwa maandalizi ya Tuzo za Anzisha kwani pamoja na kuwawezesha
wajasiriamali vijana lakini pia Tuzo hii inasaidia kuunganisha vijana wa Afrika
kwani inahusisha vijana toka Afrika nzima.
Niseme tu kwamba nimekua na imani kubwa na vijana wetu SirJeff na George na
hii ni baada ya kupata taarifa kwamba kati ya maombi zaidi ya 500
yaliyoshindanishwa katika Tuzo ya Anzisha kwa mwaka 2015 mmefanikiwa
kuingia katika 12 bora, hii ni hatua ya juu sana...Nawapongeza mno katika hili na
inawezekana kabisa katika fainali mkashinda nafasi ya kwanza na ya pili.
Tunaamini kuwa safari yenu ya ujasiriamali imeongezwa nguvu katika mashindano
haya na itapanuka zaidi ili kuleta manufaa na mabadiliko chanya hapa Tanzania na
katika bara hili la Afrika.
Tunatambua kuwa vigezo vya kushiriki tuzo hii vinahitaji wajasiriamali vijana
sana kuanzia miaka 15-22 ambao tayari wanamiliki biashara zao, kwa umri huu
vijana wengi hapa Tanzania wanakua bado wapo mashuleni na hivyo kujikuta
wakishindwa kumiliki biashara lakini vijana hawa wameonyesha kuwa
inawezekana kujiajiri na kuendesha biashara yenye mafanikio hata unapokuwa
shuleni ama chuoni na bila kuathiri masomo yako.
Napenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwa TaasisiTaasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania (TPSF) kutokana na jitihada zao za kuinua wajasiriamali hapa nchini,
naamini kwamba jitihada hizi za TPSF zinahitaji kuungwa mkono kwani zinasaidia
ukuaji wa uchumi hapa nchini na uchumi unapokua hata mapato ya nchi yanakua
na hivyo kuiwezesha serikali kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi wake.
Nawatakia kila la kheri SirJeff Dennis na George Mtemahanji.