5
Bismillhari Rahmanir Rahiim NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL P.O.BOX 11404, TEL: 0786-417685, OR 0785 -417680 MWANZA – TANZANIA Email:, [email protected] /[email protected] MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2018 “JOINING INSTRUCTIONS”. Soma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya shule kisha uthibitishe kukubali nafasi hii kwa kujaza fomu zilizoambatanishwa na kulipa ada kabla ya tarehe 25/12/ 2017, kisha toa taarifa kwa sms au email kupitia namba zilizotajwa hapo juu kwa muda uliopangwa ili nafasi isitolewe kwa muhitaji mwingine. Watakaothibitisha kujiunga, shule itafunguliwa tarehe 30/12/2017 1. UTANGULIZI:- Nyasaka Islamic High School ni Shule ya Kiislamu inayomilikiwa na taasisi ya Islamic Propaga- on Centre (IPC). Kwa kuwa jambo la kwanza muhimu kwa mwanadamu ni Elimu kama il- ivyoelezwa kaka Qur’an kuwa Nabii Adam (a.s) kabla hajaletwa duniani kwa kazi yake ya ukhalifa alielimishwa kwanza kuhusu mazingira yake (rejea Qur’an 2:31). Vilevile tunajifunza kuwa Mtume wa mwisho, Muhummad (S.A.W) kabla hajaanza kazi yake kubwa ya kuhuisha uislamu alipewa kwanza Amri ya kusoma. (Rejea Qur’an 96:1-5). Mtume (saw) mwenyewe akasisitiza kuwa ni faradhi kila Muislamu mwanaume na kila muislamu mwanamke kutafuta elimu. Tunalojifunza kutoka kwenye Qur’an na Hadithi sahihi za Mtume (s.a.w) ni kuwa; Kwanza, elimu ni zana ya kwanza ya msingi ambayo muislamu hana budi kuwa nayo ili aweze kuishi maisha ya kiislamu na awe Khalifa wa Allah (s.w) hapa duni- ani. Pili, tunajifunza kuwa katika Uislamu hapana ubaguzi wa Elimu ya dini na elimu ya dunia. Kila fani ya elimu inayomwezesha mwanadamu kufikia lengo la kuwa Khalifa wa Allah (sw) hapa duniani ni faradhi kwa Waislamu. 2. .LENGO LA SHULE: Nyasaka Islamic High School ina malengo ya jumla yafuatayo:- (i) Kuwaelimisha na kuwalea vijana wa Kiislamu kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. (ii) Kuwaandaa vijana kuwa viongozi waadilifu watakaoinusuru jamii ya Kiislamu na Taifa kwa ujumla na ufisadi. Ili kufikia malengo haya: - (a) Shule inasimamia kwa makini maadili ya kiislamu kivitendo kwa wanafunzi wote wakiwa shuleni na hata nje ya shule. (b) Shule inasimamia na kufuatilia kwa ukaribu ufundishaji wa masomo yote kwa mtazamo wa uislamu na si vinginevyo ili kuepusha upotoshaji unaoweza kujit- 1 15. MAKOSA YANAYOWEZA KUSABABISHA MWANAFUNZI KUFUKUZWA SHULE:- Pamoja na maelekezo yote hayo mwanafunzi anaweza kufukuzwa shule mara moja kama atachupa kwa makusudi mipaka ya Uisalamu kama vile:- i) Kutosimamisha swala za faradh na sunnah (qiyamulayl n.k). ii) Kuzini au kukaribia zinaa, kuwa na rafiki wa jinsia tofauti (Boy friend /Girl- friend) ndani ya shule na nje ya shule. iii) Wizi au kushiriki njama ya wizi wa aina yeyote .. iv) Kunywa pombe au kutumia ulevi wa aina yoyote. v) Kwenda kwenye madansi (Disko) vi) Kuharibu kwa makusudi mali ya shule / Umma. vii) Kugoma, kuchochea migomo, kuongoza mgomo au kuvuruga amani na usalama wa shule / jamii. viii) Utoro wa aina yeyote. ix.) Kukataa adhabu au amri halali ya viongozi wa wanafunzi na walimu kwa makusudi, n.k. x.) Kutoka nje ya shule bila kibali maalum ( kutoroka shule). xi) Kukiuka kwa makusudi kanuni na taratibu za shule. xii) Kupigana au kuchochea ugomvi. xiii). Kukwepa Mtihani wa Somo lolote linalofundishwa hapa shuleni. xiv.) Kupatikana na simu ya mkononi ,line, memory card au redio ya aina yeyote xv) kukamatwa na barua, vipeperushi, vijitabu, picha na CD zinazochochea uzinzi 16. HITIMISHO Shule inaendeshwa kwa ushirikiano wa karibu baina ya wafanyakazi wote wa shule, wazazi pamoja na wanafunzi. Hivyo kutakuwa na vikao vya wazazi na uongozi wa shule mwezi MACHI na SEPTEMBA ili kutoa ushauri kuhusu malezi na taaluma za watoto wetu. Hivyo wazazi/ walezi watakuwa wakiarifiwa tarehe za vikao na uongozi wa shule ambavyo ni mara 1 kila muhula. Tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya kutafuta Elimu na Allah akufanyie wepesi na akuongoze – Aamin!!! “Karibu Mwanza! Karibu Nyasaka Islamic secondary School” “ SUCCESS IS OUR ENDEVOURWabillaah Tawfiiq. 8

“JOINING INSTRUCTIONS”. - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-niss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya shule kisha ... Tunalojifunza kutoka kwenye Qur’an

  • Upload
    ngonhi

  • View
    332

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: “JOINING INSTRUCTIONS”. - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-niss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya shule kisha ... Tunalojifunza kutoka kwenye Qur’an

Bismillhari Rahmanir Rahiim

NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL P.O.BOX 11404, TEL: 0786-417685, OR 0785 -417680 MWANZA – TANZANIA

Email:, [email protected] /[email protected]

MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2018

“JOINING INSTRUCTIONS”.

Soma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya shule kisha uthibitishe kukubali nafasi hii kwa kujaza fomu zilizoambatanishwa na kulipa ada kabla ya tarehe 25/12/ 2017, kisha toa taarifa kwa sms au email kupitia namba zilizotajwa hapo juu kwa muda uliopangwa ili nafasi isitolewe kwa muhitaji mwingine. Watakaothibitisha kujiunga, shule itafunguliwa tarehe 30/12/2017

1. UTANGULIZI:-

Nyasaka Islamic High School ni Shule ya Kiislamu inayomilikiwa na taasisi ya Islamic Propaga-tion Centre (IPC). Kwa kuwa jambo la kwanza muhimu kwa mwanadamu ni Elimu kama il-ivyoelezwa katika Qur’an kuwa Nabii Adam (a.s) kabla hajaletwa duniani kwa kazi yake ya ukhalifa alielimishwa kwanza kuhusu mazingira yake (rejea Qur’an 2:31). Vilevile tunajifunza kuwa Mtume wa mwisho, Muhummad (S.A.W) kabla hajaanza kazi yake kubwa ya kuhuisha uislamu alipewa kwanza Amri ya kusoma. (Rejea Qur’an 96:1-5).

Mtume (saw) mwenyewe akasisitiza kuwa ni faradhi kila Muislamu mwanaume na kila muislamu mwanamke kutafuta elimu.

Tunalojifunza kutoka kwenye Qur’an na Hadithi sahihi za Mtume (s.a.w) ni kuwa;

Kwanza, elimu ni zana ya kwanza ya msingi ambayo muislamu hana budi kuwa nayo ili aweze kuishi maisha ya kiislamu na awe Khalifa wa Allah (s.w) hapa duni-ani.

Pili, tunajifunza kuwa katika Uislamu hapana ubaguzi wa Elimu ya dini na elimu ya dunia. Kila fani ya elimu inayomwezesha mwanadamu kufikia lengo la kuwa Khalifa wa Allah (sw) hapa duniani ni faradhi kwa Waislamu.

2. .LENGO LA SHULE:

Nyasaka Islamic High School ina malengo ya jumla yafuatayo:-

(i) Kuwaelimisha na kuwalea vijana wa Kiislamu kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.

(ii) Kuwaandaa vijana kuwa viongozi waadilifu watakaoinusuru jamii ya Kiislamu na Taifa kwa ujumla na ufisadi. Ili kufikia malengo haya: -

(a) Shule inasimamia kwa makini maadili ya kiislamu kivitendo kwa wanafunzi wote wakiwa shuleni na hata nje ya shule.

(b) Shule inasimamia na kufuatilia kwa ukaribu ufundishaji wa masomo yote kwa mtazamo wa uislamu na si vinginevyo ili kuepusha upotoshaji unaoweza kujit-

1

15. MAKOSA YANAYOWEZA KUSABABISHA MWANAFUNZI KUFUKUZWA SHULE:-

Pamoja na maelekezo yote hayo mwanafunzi anaweza kufukuzwa shule mara moja kama atachupa kwa makusudi mipaka ya Uisalamu kama vile:- i) Kutosimamisha swala za faradh na sunnah (qiyamulayl n.k).

ii) Kuzini au kukaribia zinaa, kuwa na rafiki wa jinsia tofauti (Boy friend /Girl- friend) ndani ya shule na nje ya shule.

iii) Wizi au kushiriki njama ya wizi wa aina yeyote ..

iv) Kunywa pombe au kutumia ulevi wa aina yoyote.

v) Kwenda kwenye madansi (Disko)

vi) Kuharibu kwa makusudi mali ya shule / Umma.

vii) Kugoma, kuchochea migomo, kuongoza mgomo au kuvuruga amani na usalama wa shule / jamii.

viii) Utoro wa aina yeyote.

ix.) Kukataa adhabu au amri halali ya viongozi wa wanafunzi na walimu kwa makusudi, n.k.

x.) Kutoka nje ya shule bila kibali maalum ( kutoroka shule).

xi) Kukiuka kwa makusudi kanuni na taratibu za shule.

xii) Kupigana au kuchochea ugomvi.

xiii). Kukwepa Mtihani wa Somo lolote linalofundishwa hapa shuleni.

xiv.) Kupatikana na simu ya mkononi ,line, memory card au redio ya aina yeyote

xv) kukamatwa na barua, vipeperushi, vijitabu, picha na CD zinazochochea uzinzi

16. HITIMISHO

Shule inaendeshwa kwa ushirikiano wa karibu baina ya wafanyakazi wote wa shule, wazazi pamoja na wanafunzi. Hivyo kutakuwa na vikao vya wazazi na uongozi wa shule mwezi MACHI na SEPTEMBA ili kutoa ushauri kuhusu malezi na taaluma za watoto wetu. Hivyo wazazi/ walezi watakuwa wakiarifiwa tarehe za vikao na uongozi wa shule ambavyo ni mara 1 kila muhula.

Tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya kutafuta Elimu na Allah akufanyie wepesi na akuongoze – Aamin!!! “Karibu Mwanza! Karibu Nyasaka Islamic secondary School”

“ SUCCESS IS OUR ENDEVOUR”

Wabillaah Tawfiiq.

8

Page 2: “JOINING INSTRUCTIONS”. - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-niss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya shule kisha ... Tunalojifunza kutoka kwenye Qur’an

Masomo yanayofundishwa kwa kidato cha I– IV ni:-

1. QUR’AN (kuisoma, tafsiri na mafunzo).

2. MAARIFA YA UISLAMU (Islamc Knowledge).

3. Lugha ya Kiarabu (A*).

4. ENGLISH (L)

5. KISWAHILI (K)

6. BASIC MATHEMATICS (M).

7. PHYSICS (P)

8. CHEMISTRY (C)

9. BIOLOGY(B)

10. GEOGRAPHY(G)

11. HISTORY(H)

12. CIVICS (C )

13. COMMERCE(C*)

14. BOOKKEEPING(BK)

ZINGATIA:- HATUPOKEI WAHAMIAJI ILA KWA KIDATO CHA KWANZA NA KIDATO CHA TANO KWA MUHULA WA KWANZA TU.

.3.MAHALI ILIPO SHULE: Nyasaka Islamic High School ipo eneo la Nyasaka, kata ya Nyasaka, wilaya ya Ilemela jijini Mwanza. Shule ipo umbali wa Kilometa nane (8Km) kutoka mjini kati na kilometa tatu (3km) kutoka stendi ya mabasi Buzuruga. Barabara ni nzuri kutoka buzuruga hadi shuleni.

.4 USAFIRI:

Wanafunzi watajitegemea kwa usafiri wa kuja shuleni na kurudi nyumbani wakati wa likizo. Uongozi wa shule utahusika kuwafanyia mpango wa usafiri wa pamoja wanafunzi wanaotoka nje ya Mwanza ili kutafuta nafuu ya gharama wakati wa kurudi nyumbani kwa ajili ya likizo. Pia wanaotoka mikoa ya Pwani, kupitia Dar, Mbeya, wanao fursa ya kupanda ndege (Fast Jet) kuja Mwanza kwa bei nafuu – wasiliana na uongozi ili kufanya booking mapema.

5.ADA YA SHULE: Ada ya shule ni Sh. 1,700,000/= kwa mwaka na italipwa kwa awamu moja au kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ni Tsh. 900,000/= itakayolipwa DESEMBA 2017 na awamu ya pili ni Tsh. 800,000/= itakayolipwa JUNI 2018.

Fedha zote za Ada zilipwe benki na liandikwe jina la mwanafunzi na kidato kwenye stakabadhi ya fedha, na mwanafunzi atatakiwa kuwasilisha shuleni uthibitisho wa malipo ( Pay-in slip) ikiwa ni original copy kabla au tarehe 31/12/2017.

MUHIMU:-

(i) Malipo yote yafanyike bank na stakabadhi zianishe juu ya malipo yaliyofanyika.

(ii) Ada ilipwe kabla ya tarehe 25 / 12 / 2017 kwa kuandika jina la mwanafunzi ili kujihakikishia nafasi.

(iii) Nakala kivuli (Photocopy) ya stakabadhi ya benki (Pay-in Slip) haita kubaliwa kuandikiwa risiti.

(iv) Haturuhusu malipo yeyote ya shule kwa njia ya simu kwa mtu yeyote. Ikitokea shule haitawajibika kwa ukosefu wa kumbukumbu.

(v) Ada isiyokamilika kwa mujibu wa taratibu zilizoelezwa hapo juu itasababisha mwanafunzi asipokelewe.

(vi) Akaunti ya Shule ni NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL (NBC, AKAUNTI NO. 015103007569). Au AMANA BANK AKAUNTI No. 006120202500001.

(vii) Ada ikishapokelewa haitarudishwa kwa sababu yoyote ile.

2

Wanafunzi wote wanatakiwa wavae nguo za Kiislamu wakiwa ndani na nje ya shule. Kwa wasichana wana-takiwa wavae nguo za kusitiri mwili mzima isipokuwa uso na vitanga vya mikono (Hijabu) rejea Qur’an(24:31).

viii) Ni marufuku kwa wanafunzi wa jinsia zote kuvaa mapambo wakati wakiwa shuleni na wakiwa nje ya shule.

ix) Wavulana watavaa nguo zinazoendana na maelekezo ya uislamu wakiwa ndani na nje ya shule(zisiwe na picha ,maandishi , mifuko mingi, kubana, kulegeza n.k.)

x) Ni marufuku kwa wasichana kuvaa nguo za kubana, fupi au zinazoonesha ndani (transparent) akiwa shuleni au nje ya shule.

xi) Ni marufuku mwanafunzi kufuga kucha, kujipaka rangi za kucha, rangi za Midomo, kupaka wanja, kupaka hina, kunyoa nyusi, kuvaa viatu vya kuchuchumia au vinavyotoa sauti, kukali nywele au kutia rangi au kusuka rasta au kufunga nundu la nywele kichwani.

xii) Ni marufuku mwanafunzi kuchochea, kushawishi, kuhamasisha au kushiriki mgomo kwa namna yoyote hata kama mwanafunzi anayo sababu ya msingi.

xiii) Mwanafunzi asionekane kwenye vilabu vya pombe, nyumba za kupangisha Wageni (Guest House) kumbi za dansi na sinema, Beach Fiesta, Mashindano ya urembo, Summer jam, Valentine, Picnic n.k

xiv) Ni marufuku kwa mwanafunzi kwenda nyumba ya mfanyakazi wa shule hata kama ni wazazi wake hadi ruhusa maalumu. Vinginevyo atachukuliwa hatua sawa na aliyetoroka shule.

xv. Kila mwanafunzi ni mlinzi wa mali ya shule, mali yake binafsi na mali ya wenzake, mwanafunzi atakaeharibu au kusababisha mali ya shule kuharibika ama kuibiwa au kupotea atachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kulipa. Hivyo, mwanafunzi atakapogundua wizi wa mali ya shule au ya mwanafunzi mwingine atoe taarifa kwa walimu au wanaohusika mara moja.

xvi. Kuiba ni kosa kubwa, mwanafunzi atakayethibitika kuiba mali ya shule au mwanafunzi mwenzake au nje ya shule atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufukuzwa shule.

xvii. Mwanafunzi anapokuwa na shida yoyote hapa shuleni aanze kuwaona viongozi wa wanafunzi na ndipo aende kumuona mwalimu wa bweni au mwalimu wa darasa au walimu wa zamu wanaohusika. Kama mwanafunzi baada ya kufuata ngazi hizo shida yake haijatatuliwa, aende kwa Makamu Mkuu wa shule kisha kwa Mkuu wa shule itakapobidi. Mwanafunzi asishitakie shida yake nje ya shule kabla hajamuona Mkuu wa Shule.

xviii. Kila mwanafunzi awe msafi na ahakikishe anashiriki vyema katika usafi wa mazingira ya shule. xix. Kelele za aina yoyote hazitaruhusiwa ziwe darasani, kwenye korido, ndani ya bweni au popote

iwe mwanafunzi mmoja au wengi (Kundi). Tunalazimika kuonesha maadili ya Kiislamu katika mazungumzo yetu yote. (Rejea Qur’an 31:19).

xx. Shule hairuhusu Mwanafunzi kutoka nje ya eneo la shule bila kibali maalum cha maandishi. Wa-kati wa likizo fupi (Midterm break) wanafunzi wote watabakia katika eneo la shule

xxi. Kila Mwanafunzi analazimika kushirikiana katika wema na Ucha Mungu na Wazazi, Waalimu na Wanafunzi wenzake kufikia lengo la shule.

xxii. Kupigana ni kosa kubwa, mwanafunzi atakayepigana atachukuliwa hatua kali za Kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufukuzwa shule.

xxiii. Kusema uongo na kueneza uzushi usiokuwa na ushahidi ni kosa. Mwanafunzi ataka-yebainika atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

xxiv. Wazazi wa Wanafunzi wanaruhusiwa kuanzia saa 3:00 asubuhi (saa tatu kamili asubuhi) mpaka saa 11:00 jioni ( saa kumi na moja kamili jioni) kuwatembelea wanafunzi shuleni siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi JANUARI, APRIL, JUNI, JULAI, SEPTEMBA, NA NO-VEMBA TU.

xxv. Hairuhusiwi kumletea mwanafunzi vyakula au vinywaji shuleni . xxvi. Ni marufuku mwanafunzi kuwa na simu, redio, CD player, walk man au sim Card.

Mwanafunzi atakayekutwa na chochote katika hivi atafukuzwa shule. xxvii. Ni kosa kubwa kutoroka shule au kutoka nje ya shule bila ruhusa maalum. Mwana-

funzi yeyote atakaye toroka au kutoka nje ya shule bila ruhusa atafukuzwa shule. xxviii. Ni marufuku mwanafunzi kuwasiliana nje ya shule kwa jambo lolote kwa njia

yeyote bila idhini ya mkuu wa shule

7

Page 3: “JOINING INSTRUCTIONS”. - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-niss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya shule kisha ... Tunalojifunza kutoka kwenye Qur’an

.6MAHITAJI YA MWANAFUNZI:

Kabla ya kuripoti shuleni mwanafunzi atapaswa kulipia sare na vifaa ambavyo atapewa shuleni kama ifuatavyo:-

MUHIMU:-

Fedha za vifaa vilivyoorodheshwa hapo juu zilipwe benki pamoja na ada kabla ya mwanafunzi hajaripoti shuleni. Mwanafunzi aje na uthibitisho ( pay-in slip), vinginevyo hatapokelewa.

Mwanafunzi anaweza kulipiwa sare zaidi ya jozi moja ili kudumisha usafi 7. VIFAA:-

i) Mwanafunzi anaporipoti shuleni atatakiwa kuja na vifaa vifuatavyo:-

ii) Madaftari /counter books (14) (2 OR 3 QUIRE)

iii) Mfuko wa kutunzia madaftari (School bag).

iv) Mkebe wa vifaa vya hisabati ( Mathematical set).

S/No MAHITAJI GHARAMA WASICHANA GHARAMA WAVULANA

1 ADA MUHULA WA I 900,000/- 900,000/-

2 SARE (YA KUSHINDIA JOZI 1, NA YA SHULE JOZI 1) 110,000/- 95,000/-

3 KITABU CHA MAARIFA YA UISLAMU (EDK) 10,000/- 10,000/-

4 TAHADHARI 10,000/- 10,000/-

5 MSAHAFU (TAFSIRI – YENYE UTANGULIZI) 15,000/- 15,000/-

6 MATIBABU & FOMU YA UCHUNGUZI 35,000/- 35,000/-

7 MCHANGO WA MAKTABA 25,000/- 25,000/-

8 VIFAA VYA USAFI 10,000/- 10,000/-

9 VITAMBULISHO(2) 10,000/- 10,000/-

10 RIM(DOUBLE A) 12,000/- 12,000/-

Jumla 1,137,000/- 1,122,000/-

3

Mwanafunzi mwenye nidhamu mbaya hataruhusiwa kurudi shule mwisho wa mwaka hata kama amaefaulu masomo ya darasani.

Mwanafunzi atalelewa na wenzake kuanzia chumbani kwake, darasani na msikitini chini ya usimamizi wa waalimu na ushauri wa uongozi wa shule pamoja na wazazi/walezi.

Mzazi atashirikishwa kikamilifu katika malezi ya mwanae.

13. AFYA NA USTAWI

Mwanafunzi atapimwa afya yake vizuri atakapofika shuleni. Mzazi anatakiwa kuwa mkweli kutoa taarifa sahihi. Historia ya mtoto kiafya na ziambatanishwe na uthibitisho wa daktari (kwa wenye matatizo ya kudumu) ili mtoto aangaliwe vizuri kiafya.

Shule itatoa huduma ya kwanza kwa Afya ya mwanafunzi na pale itakapothibitishwa na daktari wa shule kuwa mwanafunzi anatakiwa kupata matibabu/ vipimo zaidi nje ya shule, mzazi/ mlezi atapaswa kumchukua na kumshughulikia mtoto nje ya shule na kumrudisha shule akiwa na vyeti vya matibabu au kuwasiliana na uongozi wa shule juu ya gharama zinazohitajika ili shule imsaidie kumpeleka hospitali (kwa walio nje ya Mwanza tu).

Mwanafunzi mwenye maradhi ambayo yanahitaji chakula au mazingira maalumu katika mazing-ira ya shule itakuwa ni vigumu shule kumhudumia, hivyo ni vizuri akatafutiwa shule nyingine ( sharti hili haliwahusu wenye vidonda vya tumbo, kwa kuwa wanapewa mboga za majani bada-la ya maharage tu)

Mwanafunzi atakayepatwa na maradhi mara kwa mara na kumzuia kuingia darasani, mzazi/mlezi atashauriwa kumtibu hadi apone ndipo amrudishe shuleni. Akitumia muda wa wiki sita(6)

wakati wa masomo atalazimika kurudia darasa.

14. KANUNI NA MWENENDO BORA WA SHULE;-

i. Kila mwanafunzi wa shule hii anapaswa kutambua kuwa yupo hapa kwa ajili ya Uislamu. Kwa sababu hiyo chochote kilichopo nje ya Uislamu hakina nafasi katika shule hii, kiwe kwa mane-no au kwa vitendo.

ii. Lugha za mawasiliano zinazotumika shuleni ni KIINGEREZA na KIARABU, atakaye bainika ana-zungumza tofauti na lugha hizo mfano Kiswahili ataadhibiwa

iii. Kila mwanafunzi atafunzwa utii wa kweli kwa Allah (sw) na Mtume wake (s.a.w), kwa jili ya maisha ya dunia na akhera..

iv) Pamoja na haki za Muumba zilizo juu ya kila muislamu, yamwajibikia kila mwanafunzi achunge haki na nafsi yake na atumie vipaji vyake katika Ucha Mungu ndani na nje ya shule hii.

v) Kila mwanafunzi atatumia muda wake vizuri katika kujielimisha kwa ajili ya Allah (sw) ikizingati-wa kuwa kujielimisha kwa ajili ya Allah (sw) ni amri ya kwanza kwa kila Muislamu.

vi) Kila mwanafunzi analazimika kuhudhuria vipindi vya kila somo, kufanya mazoezi, majaribio na mitihani yote itakayotolewa shuleni.

NB: Mwanafunzi asiyefanya mtihani wowote ule bila sababu yoyote ya msingi amejifukuzisha shule.

vii) Wakati wote wa shule na wakati wa kuja au kurudi nyumbani, vazi rasmi ni sare ya shule na kutokua na sare wakati huo ni kosa.

6

Page 4: “JOINING INSTRUCTIONS”. - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-niss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya shule kisha ... Tunalojifunza kutoka kwenye Qur’an

i) Viatu vyeusi vya ngozi na kamba vinavyofunika miguu na soksi nyeupe. (viatu visiwe vya kisigino kirefu au muundo wa buti). Pamoja na kiwi na brash yake

ii) Godoro la upana wa futi 2 ½ .( linapatikana shuleni – 40,000/-)vita raha

iii) Shuka tatu (3) za pinki, light bluu na nyeupe zisiwe na maandishi wala maua.( zinapatikana shuleni @7,000/-)file mbili (2) 3000/-

iv) Blanket la kijivu futi 2 ½ .( linapatikana shuleni 10,000)

v) Chandarua cha pembe nne futi 2 ½ na Saa ya mkononi yenye alarm)

vi) Sanduku la bati lenye kufuli.( Trunk) linapatikana duka la shule ( Tsh. 22,000)

vii) Sahani, bakuli, kikombe na kijiko ( Vyombo visiwe vya udongo au plastic) vinaweza kuwa vya bati au mfupa.

viii) Ndoo mbili za lita 10 za plastic. (zinapatikana duka la shule @3500/-)

ix) Jozi moja ya vitenge, Shimizi mbili na Night dress mbili kwa wasichana tu.

x) Sabuni za kufulia, kuogea, mswaki, dawa ya meno na mafuta ya kupaka ya mgando (jelly), na taulo

xi) viatu na nguo za michezo (Track suit na fulana isiyo na maandishi au picha), Fulana za wasichana ni lazima ziwe za mikono mirefu.

xii) Jacket nyeusi au dark blue lisiwe na , picha. Na kofia

xiii)Kanzu nyeupe na kofia nyeupe atakayovaa (wavulana tu)

MUHIMU:- vitu vifuatavyo haviruhisiwi mwanafunzi kuja navyo Marashi, Perfume, lotion, Cream, Shampoo, Sabuni za kuchubua ngozi

Mapambo ya aina yoyote kama vile pete, hereni, bangili, kacha, mikufu, mabanio ya nywele n.k.

Nguo yeyote yenye maandishi au namba.

Rangi za kucha , hina, piko n.k .

Redio, simu, CD’s, Camera, Memory Card, Line ya simu, Pasi na mashine za kunyolea.

NB: Atakayekamatwa na vitu hivi atanyang’anywa hapo hapo na HATARUDISHIWA TENA na hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa SHERIA na KANUNI ZA SHULE.

8. UANDIKISHWAJI:-

Wakati wa kuripoti shuleni mwanafunzi atatakiwa kuwa na fomu zilizojazwa na kukamilika kama ifuatavyo:-

Fomu ya utambulisho wa wazazi / Walezi

Fomu ya wajibu wa mzazi / mlezi

Picha za baba, mama, walezi (me / ke) na mwanafunzi.

4

MUHIMU:- Fomu zikamilike kwa kubandika picha husika kwa gundi.

Uandikishwaji utafanyika katika ofisi ya Makamu Mkuu wa Shule au sehemu itakayo-pangwa na mkuu wa shule.

Mwanafunzi lazima aje na vitu vyote alivyoagizwa na shule vinginevyo hatoandikish-wa hadi vikamilishwe.

Mwanafunzi aje na cheti chake cha kuzaliwa, kama hana mzazi atapewa miezi miwili (2) tu ya kukileta shule.

9. KUFUNGUA SHULE

Shule itafunguliwa siku ya jumamosi tarehe 30/12/2017, na kwa hiyo wanafunzi wafike shuleni siku hiyo kabla ya saa 10. 00 alasiri. Muda huu ndio wa mwisho kufika shuleni hata wakati wa likizo au ruhusa. Mwanafunzi hatapokelewa kuripoti shuleni zaidi ya mu-da huo (saa 10:00 alasiri) ila kwa dharura yenye taarifa iliyokubaliwa na uongozi wa shule.

.10 MALENGO YA DARASANI

Mwanafunzi ataruhusiwa kuendelea Kidato kinachofuata kwa kupata wastani usiopungua alama 45 (na awe amepata daraja C na kuendelea masomo Saba (7), vinginevyo atakariri darasa.

Mwanafunzi atakayefeli somo la elimu ya dini ya kiislamu, Hisabati na kiarabu “F” atalazi-mika kufanya mtihani wa marudio wakati wenzake wanaondoka kwenda likizo ya juni.

Mwanafunzi atakayekosa vipindi bila taarifa atachukuliwa hatua kali, hii ni pamoja na wale wanaochelewa kuripoti shule tarehe iliyopangwa bila taarifa kwa mkuu wa shule.

Mwanafunzi atakayeshindwa kufikisha wastani wa alama 45 muhula wa kwanza hataenda likizo na mzazi atalipia program maalum ya kumsaidia.

Hakuna fursa ya kuendelea kidato kingine kama haujakidhi viwango vilivyotajwa hapo juu

Kujituma katika kazi ni katika nidhamu ya kiislamu. Hivyo, kila mwanafunzi atawajibika kushiriki kikamilifu katika kufanya kazi za usafi binafsi, mazingira, ujenzi, na kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na walimu au viongozi wa Wanafunzi. Kutega kazi iwe ya darasani au nje ya darasa ni kukiuka maadili anayotarajiwa awe nayo Mwanafunzi wa shule hii na hatavumiliwa kwa namna yeyote ile.

Shule hii ni ya kiislamu. Hivyo mwenendo wa wafanyakazi na wanafunzi wake unataraj-iwa uwe wa kiislamu. Kukiuka maadili ya Qur’an na Sunnah ni kukiuka maadili ya shule. Mwanafunzi atachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa kukiuka maadili ya Qur’an na Sunnah pamoja na miongozo mbalimbali ya shule.

5

11. KAZI ZA NJE YA DARASA:-

12. MALEZI:-

Page 5: “JOINING INSTRUCTIONS”. - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-niss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya shule kisha ... Tunalojifunza kutoka kwenye Qur’an

Bismillhari Rahmanir Rahiim

NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL P.O.BOX 11404, TEL: 0786-417685, OR 0785 -417680 MWANZA – TANZANIA

Web: www.nyasakaislamic.co.tz , Email: [email protected]

Bismillhari Rahmanir Rahiim

NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL P.O.BOX 11404, TEL: 0786-417685, OR 0785 -417680 MWANZA – TANZANIA

Email: [email protected], [email protected]

FORM 4 FORM 6