13
Maelekezo ya kujiunga na shule 2018 1 ن الرحيم لرحم بسمAMBASHA ISLAMIC HIGH SCHOOL Maelekezo ya kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2018. Soma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya shule kisha uthibitishe kukubali nafasi hii kwa kulipa mkupuo wa kwanza wa ada kabla ya tarehe22/12/2017. Ada isipolipwa katika muda uliotajwa, nafasi itatolewa kwa mwanafunzi mwingine. Shule itafunguliwa tarehe 30/12/2017. 1. Utangulizi AMBASHA ISLAMIC HIGH SCHOOLniShule ya Kiislamu inayotazama elimu kuwa ni jambo la kwanza muhimu kwa mwanadamu. Tunajifunza katika Qur’an kuwa Nabii Adam (a.s) kabla hajaletwa hapa ulimwenguni kwa kazi yake ya ukhalifa (uongozi), alielimishwa kwanza kuhusu mazingira yake (Rejea Qur’an, sura ya 2:31). Vile vile tunajifunza kuwa Mtume wa mwisho Muhammad (s.a.w) kabla hajaanza kazi yake kubwa ya kuhuisha Uislamu alipewa kwanza amri ya kusoma (rejea Qur’an 96:1-5). Mtume (s.a.w) akasisitiza kuwa ni faradhi (lazima) kwa kila Muislamu mwanamume na kila Muislamu mwanamke kutafuta elimu. Pia Mtume (s.a.w) amesisitiza kuwa elimu itafutwe hata ikibidi ifungiwe safari ya mbali (Uchina). Tunalojifunza kutoka katika Qur’an na hadithi sahihi za Mtume (s.a.w) ni kuwa: Kwanza, elimu ni zana ya kwanza ya msingi ambayo Muislamu hana budi kuwa nayo ili aweze kuishi maisha ya Kiislamu na awe Khalifa (kiongozi) wa Allah (s.w) hapa duniani. Pili, tunajifunza kuwa katika uislamu hapana ubaguzi wa elimu ya dunia na elimu ya akhera.Kila fani ya elimu inayomwezesha mwanadamu kufikia lengo la kuwa Khalifa wa Allah (s.w) hapa duniani ni faradhi (wajibu/lazima) kwa Waislamu wote. 2. LENGO LA SHULE: AMBASHA ISLAMIC HIGH SCHOOL ina malengo ya jumla yafuatayo: (i) Kuwaelimisha na kuwalea vijana wa Kiislamu kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha sita. (ii) Kuwaandaa vijana kuwa viongozi (Makhalifa)wa kutegemewa na jamii ya Kiislamu na Taifa kwa ujumla. Ili kufikia malengo haya shule hii inatoa mafunzo katika kiwango cha kawaida (O’Level)na kiwango cha juu (A’Level).

AMBASHA ISLAMIC HIGH SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-aihs-F1-2018.pdf · Maelekezo ya kujiunga na shule 2018 1 ميحرلا نمحرل الله مسب AMBASHA

  • Upload
    buibao

  • View
    271

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

Maelekezo ya kujiunga na shule 2018

1

بسم هللا لرحمن الرحيم

AMBASHA ISLAMIC HIGH SCHOOL

Maelekezo ya kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2018.

Soma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya shule kisha uthibitishe kukubali nafasi hii kwa kulipa mkupuo wa kwanza wa ada kabla ya tarehe22/12/2017. Ada isipolipwa

katika muda uliotajwa, nafasi itatolewa kwa mwanafunzi mwingine.Shule itafunguliwa tarehe 30/12/2017.

1. Utangulizi AMBASHA ISLAMIC HIGH SCHOOLniShule ya Kiislamu inayotazama elimu kuwa ni jambo la kwanza muhimu kwa mwanadamu. Tunajifunza katika Qur’an kuwa Nabii

Adam (a.s) kabla hajaletwa hapa ulimwenguni kwa kazi yake ya ukhalifa (uongozi), alielimishwa kwanza kuhusu mazingira yake (Rejea Qur’an, sura ya 2:31). Vile vile tunajifunza kuwa Mtume wa mwisho Muhammad (s.a.w) kabla hajaanza kazi yake

kubwa ya kuhuisha Uislamu alipewa kwanza amri ya kusoma (rejea Qur’an 96:1-5).

Mtume (s.a.w) akasisitiza kuwa ni faradhi (lazima) kwa kila Muislamu mwanamume na

kila Muislamu mwanamke kutafuta elimu. Pia Mtume (s.a.w) amesisitiza kuwa elimu itafutwe hata ikibidi ifungiwe safari ya mbali (Uchina).

Tunalojifunza kutoka katika Qur’an na hadithi sahihi za Mtume (s.a.w) ni kuwa: Kwanza, elimu ni zana ya kwanza ya msingi ambayo Muislamu hana budi kuwa nayo ili aweze kuishi maisha ya Kiislamu na awe Khalifa (kiongozi) wa Allah (s.w) hapa duniani.

Pili, tunajifunza kuwa katika uislamu hapana ubaguzi wa elimu ya dunia na elimu ya akhera.Kila fani ya elimu inayomwezesha mwanadamu kufikia lengo la kuwa Khalifa wa Allah (s.w) hapa duniani ni faradhi (wajibu/lazima) kwa Waislamu wote.

2. LENGO LA SHULE:

AMBASHA ISLAMIC HIGH SCHOOL ina malengo ya jumla yafuatayo:

(i) Kuwaelimisha na kuwalea vijana wa Kiislamu kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha sita.

(ii) Kuwaandaa vijana kuwa viongozi (Makhalifa)wa kutegemewa na jamii ya

Kiislamu na Taifa kwa ujumla. Ili kufikia malengo haya shule hii inatoa mafunzo katika kiwango cha kawaida (O’Level)na kiwango cha juu (A’Level).

Maelekezo ya kujiunga na shule 2018

2

Masomo yanayofundishwa kwa kidato cha I - IV ni: (1) Qur-an

(2) Elimu ya Dini ya Kiislamu (3) Arabic Language (4) English Language

(5) Kiswahili (6) History (7) Geography

(8) Basic mathematics

(9) Pysics (10) Chemistry (11) Biology

(12) Commerce (13) Book Keeping (14) Civics

3.MAHALI SHULE ILIPO: AMBASHA ISLAMIC HIGH SCHOOL ipo katika kijiji cha Shengejuuwilaya ya Wete,

Mkoa wa Kaskazini Pemba. Kilipo kibao cha shule hadi shuleni ni umbali wa kilometa 1.4

4. USAFIRI:

Usafiri wa kufika shuleni unategemea na eneo atokalo mwanafunzi. Kwa wazazi/walezi nawanafunzi wanaotoka Tanzaniabara wanaweza kufika shuleni Ambasha Islamic High School kwa namna zifuatazo:

(i) Kusafiri kwa basi hadi Tanga kisha kusafiri kwa Meli ya Azam Sea Link -2hadi bandari ya mkoani kisha utapanda gari zinzoelekea Konde na kushuka kijiji cha Shengejuu hapo utaona kibao kinachokuelekeza shule ilipo.

(ii) Usafiri wa basi hadi Tanga kisha utasafiri kwa ndege hadi mji wa Chakechake

Pemba ambapo utachukua taksi hadi kituo cha daladala na kupanda gari

zinazoelekea Konde na kushuka kijiji cha Shengejuu hapo utaona kibao kinachokuelekeza shule lipo.

(iii) Usafiri wa Meli ya Azam Sea Link - 1 kutoka Dar es Salaam hadi Pemba kupitia

Unguja kisha utapanda gari za kuelekea Konde na utashuka Shengejuu hapo pana kibao kinachokuelekeza shule ilipo.

Wanafunzi watajitegemea kwa usafiri wa kuja shuleni na kurudi nyumbani wakati wa likizo.Uongozi wa shule utahusika kuwafanyia mpango wa usafiri wa pamoja ili kutafuta nafuu ya gharama na usalama. Wazazi na walezi wenye wanafunzi wanaotokea

Tanazania bara watafahamishwa utaratibu wa safari ya pamoja kupitia namba zao za simu zilizopo kwenye fomu za maombi ya kujiunga na shule.

5. ADA YA SHULE : Ada ya shule kwa mwaka 2018 ni Tshs 1,600,000/=(milioni moja na laki sita.) Ada italipwa kwa awamu mbili;

a) Awamu ya kwanza Tshs 1,000,000ilipwe kabla ya tarehe22/12/2017. b) Awamu ya pili Tshs 600,000/= ilipwe kabla ya tarehe 30 /6/ 2018.

El

imu

ya Dini ya Uislamu

Maelekezo ya kujiunga na shule 2018

3

Ada, pesa za matumizi ya Mwanafunzi (pocket money) na pesa za vifaa vinavyopatikana shulenizote zilipwe benki katika tawi lolote la benki zifuatazo:

(i) NMB A/C NO. 20210005308 (ii) PBZ ISLAMIC DIVISION A/C NO 53120100007372 kwa

jina la AMBASHA ISLAMIC HIGH SCHOOL.

Mambo muhimu ya kuzingatia juu ya malipo:

(a) Baada ya kulipa, tuma stakabadhi ya benki (pay in slip) kwa njia ya whats

App kwa namba0786 573938. (b) Siku ya kuripoti shule mtoto awasilishe nakala halisi ya stakabadhi ya benki

(pay in slip) shuleni ili aandikiwe stakabadhi(receipt) ya shule. Nakala kivuli (Photocopy) ya Pay-in-slip haitapokelewa kwa sababu zozote zile.

(c) Malipo yakishafanyika hayatarudishwa kwa sababu yoyote ile.

(d) Mwisho wa kulipa mkupuo wa kwanza wa ada ni tarehe 22/12/2017. Kulipa

mkupuo wa kwanza wa ada ndio kuthibitisha kukubali nafasi. Kwa hiyo baada ya tarehe hii, kwa mzazi ambaye atakuwa hajafanya malipo nafasi ya mtoto wake inaweza kutolewa kwa mhitaji mwingine.

(e) Pay-in-slipziwe tofautitofauti. PiaPay-in-slip iandikwe/ziandikwe jina la mwanafunzi anayelipiwa na kidato anachosoma ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza (Mfano: 1. Ada ya Ahmed Ally- Form one.

(f) 2.Pocket money ya Ahmed Ally- -Form one 3. Gharama za Vifaa na vitabu vya Ahmed Ally- Form one n.k.

(g) Baada ya kulipa, Tafadhali wasilisha nakala halisi (original) Pay-in-slips

kwaMhasibu wa shule ili kupatiwa stakabadhi ya malipo (receipt). Hakikisha unatunza stkabadhi ya shule kipindi chote mpaka mtoto kuhitimu masomo katika ngazi husika.

(h) Shule haitahusika na upotevu wa aina yoyote wa fedha za mwanafunzi. (i) Mwanafunzi asielipa ada kamili hatopokelewa

6. SARE ZA SHULE

(A) Sare ya Darasani

i)Wavulana 1) Suruali 2 rangi ya “Khaki”

2) Nusu kanzu 2 nyeupe; urefu wa kufika magotini, mikono mirefu,zisizopasuliwa na zisizo na kola.

3) Kofia mbili nyeupe zisizokuwa na urembo wa aina yoyote na ziwe za kitambaa sio za kufuma kwa nyuzi.

Maelekezo ya kujiunga na shule 2018

4

4) Viatu vyeusi vya ngozi vya kufunga kambajozi moja, unene wa soli ya viatu usizidi nchi mmoja (1 inch) soksi nyeusi au dark blue.

ii)Wasichana 1) Nusu kanzu 2 (nyeupe), ndefu zenye mikono mirefu isiyona mifuko.

2) Suruali (pajama) 2za rangi ya Khaki.

3) Shungi (juba) 2 nyeupe kubwa ya duara yenye urefu waKufika magotini. 4) Baibui 2 (pana na ndefu) za rangi ya khaki. 5) Viatu vyeusi vya ngozi vya kufungwa kwa kamba jozi (1), unene wa soli

ya viatu usizidi nchi moja (1 inch) vifunike miguu, na soksi za dark blue au nyeusi. Zingatia:Mwanafunzi hataruhusiwa kuingia darasani na ikibidi anaweza kurudishwa

nyumbani iwapo atakiuka utaratibu wa sare ya shule hata kwa kipengele kimoja

(B) Sare za Nje ya Darasa (a) Wavulana

(i) Suruali 2 nyeusi (siyo Jeans, Lee, wala Corduroy) zilizoshonwa kwamshono wa suruali za kawaida.

(ii) Fulana 2 za rangi ya (Dark blue), zisizo namaandishi wala picha ya

ainayoyote, zisizo na kola na ziwe za mikono mifupi. (iii) Kanzi nyeupe (iv) Track-suitya rangi ya darkblue au nyeusi (sio jezi za mpira)na raba kwa

ajili ya michezo/mazoezi.

(v) Jacket la rangi dark blue au nyeusi lisilo na kofia na maandishi. (vi) Gun boot kwa matumizi ya kazi za nje ya darasa kipindi cha mvua

(b)Wasichana

(i) Gauni refu, panana mikono mirefu la rangi yaugoro lisilopasuliwa, lisiloungwa

na lisilokuwa na mikunjo kiunoni. (ii) Pajama ya rangi ya ugoro. (iii) Ushungi mkubwa wa mviringo (juba),urefu wa kufika magotini wa rangi ya

ugoro. (iv) Kitenge jozi mojana wala sio kanga. (v) Nguo za michezo: Track suit (dark blue au nyeusi napana kiasi),

(vi) fulana isiyobana (dark blue au nyeusi) ya mikono mirefu na raba. (vii) Nguo za kulalia (night dress) –shumizi ndefu 2 za rangi nyeupe. (viii) Gun boot.

Zingatia:

i) Zaidi ya sare, mwanafunzi hataruhusiwa kuwa na nguo nyingine yoyote.

Maelekezo ya kujiunga na shule 2018

5

ii) Nguo yoyote inayobana au inayoonesha ndani (transparent) au iliyoshonwa kinyume na maagizo haitakubaliwa kama sare ya shule.

iii) Ni marufuku kwa wanafunzi kuvaa mapambo ya aina yoyote wakiwa shuleni au nje ya shule (likizo) wakati bado ni mwanafunzi wa shule hii.

iv) Mwanafunzi atakayekiuka utaratibu huu na kuthibitishwa na uongozi wa Shule,

atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na Kunyang’anywa mapambo hayo na hatarudishiwa.

Muhimu:

Ili kuondoa tatizo la kutofautiana kwa rangi za vitambaa na muundo waSare za shule; sare zote za shule zitashonwa hapa shuleni kwa gharama zilizotajwa kwenye kifungu namba saba (7) (Gharama za mashono)

7. GHARAMA ZA MASHONO YA SARE ZA SHULE (A)Sare za Darasani (i) Wavulana

1. Suruali 2 2. Nusu kanzu 2 Jumla = 65,000/= 3. Kofia 2

(ii)Wasichana 1. Baibui 2

2. Pajama 2 Jumla = 76,000/= 3. Nusu kanzu 2 4. Ushungi (Juba) 2

Sare za Nje (i)Wavulana 1. Suruali nyeusi 2 Jumla = 40,000/=

2. Fulana (dark blue) 2 (ii)Wasichana

1. Gauni 2 2. Pajama 2 Jumla = 60,000/= 3. Ushungi 2

Muhimu: Vipimo vya sare vitafanyika hapa shuleni.

8. VIFAA VYA MASOMO Mwanafunzi atalazimika kununua vifaa vyote vya masomo vinavyohitajika

kama vile : i. Madaftari makubwa (counter books 3Quires) ya kila somo. ii. Kalamu na mkebe wa vifaa vya hisabati (Mathematical set).

Maelekezo ya kujiunga na shule 2018

6

iii. Kutokana na uchache wa vitabu vya kiada na ziada kila mwanafunzi anashauriwa kujinunulia vitabuili aweze kujisomea kikamilifu akiwa ndani na nje ya

shule.Angaliajedwalila orodha ya vitabu vinavyohitajika. iv. Jalada (file) la kutunzia mitihani na majaribio. v. Graph paper pad.

vi. Mfuko wa kuhifadhia madaftar usio na maandishi wala picha ya aina yoyote

9. VIFAA VYA BWENI:

(i) Godoro la upana wa futi mbili na nusu (2

12 ft x3 lnch). Ili kuondoa

(ii) tatizo la kusafiri na magodoro,magodoro yanapatikána hapa shuleni kwa Tshs 40,000/= kwa magodoro ya DODOMÁ.

(iii) Shuka mbili za rangi ya pink pia zinapatikana shuleni kwaTsh (iv) 13,000/= Kila moja niThs 6,500/=.

(v) Mto na foronya mbili. (vi) Taulo. (vii) Chandarua cha pembe nne.

(viii) Sabuni za kutosha za kufulia (za unga) na za kuogea. (ix) Vyombo, vya chakula; sahani, bakuli, na kikombe. Sahani na (x) bakuli visiwe vya udongo (nunua stainless steel au pembe).

(xi) Begi kwa ajili ya kuhifadhia vitabu na vitu vingine. (xii) Ndoo ya kuhifadhia maji.

Zingatia: Sanduku la chuma(tranker)HALIRUHUSIWIshuleni. Mzazi anatakiwa aje na vifaa vyote ambavyo havikuonyeshwa kuwa vinapatikana

shuleni. Muhimu: Mwanafunzi atakapoacha, kufukuzwa au kuhama shule vifaa vyake kama vile godoro,

begi n.k hana budi kuondoka navyo. Pindi atakapoviacha shule haitakuwa na dhamana ya vifaa hivyo.

10. UANDIKISHWAJI Siku ya kuripoti shuleni, mwanafunzi awe na vifaa vifuatavyo:

(i) Fomu za Utambulisho wa mwanafunzi na wazazi/walezi(Kiambatisho A) wa

mwananafunzi zikiwa zimejazwa na kubandikwa picha.

(ii) Fomu ya daktari (Medical Examination form) iliyojazwa na Daktari wa hospitali ya serikali na kugongwa muhuri.(Kiambatisho B).

(iii) Fomu ya wajibu wa mzazi/mlezi (Kiambatisho C).

(iv) Kopi ya cheti cha kuzaliwa. (v) Fedha za kitambulisho Tsh. 2,500/= (vi) Pay-in-slip ya malipo ya adana malipo mengine.

Maelekezo ya kujiunga na shule 2018

7

(vii) Swadaqah ya kuchangia ujenzi Tsh 100,000/= (viii) Vitabu vya kiada (angalia orodha ya vitabu)

(ix) Rim moja (1) ya karatasi nyeupe (x) Fyekeo (slasher) moja.

MUHIMU;

Mwanafunzi atakayeshindwa kukamilisha mahitaji haya hatapokelewa. 11. MAENDELEO YA DARASANI.

Kila mwanafunzi anatakiwa kufanya bidii katika masomo yake kwa kuhudhuria vipindi vyote, kufanya kazi za darasani katika kila kipindi,kufanya majaribio na mitihani yote inayotolewa shuleni,kutumia maktaba ya shule kujisomea vitabu na majarida mbalimbali

ya kielimu ili kujiongezea maarifa zaidi. Ili kufaulu kuingia kidato kingine, mwanafunzi anatakiwa afikishe wastani waangalau alama 45 (daraja C) au zaidi na crediti7 au zaidikatika masomo yake yote

anayosoma. Crediti ni madaraja C, B, na A. 12. KAZI ZA NJE YA DARASA

Kujibidiisha katika kazi ni katika nidhamu ya Kiislamu. Hivyo, kila mwanafunzi atawajibika kushiriki kikamilifu katika kutenda kazi za usafi wa mazingira, ujenzi na kazi

nyinginezo kama atakavyoelekezwa na walimu au viongozi wa wanafunzi.Kutegea kazi, iwe ya darasani au nje ya darasa ni kukiuka maadili anayotarajiwa awe nayo mwanafunzi wa shule hii na haitavumilika.

13. NIDHAMU

Shule hii ni ya Kiislamu. Hivyo mwenendo wa wanafunzi na wafanyakazi wake

unatarajiwa uwe wa kiislamu. Kukiuka maadili ya kiislamu kwa mujibu wa Qur’ani tukufu na Sunnah sahihi za Mtume (S.A.W)ni sawa na kukiuka maadili ya shule. Mwanafunzi yeyote atakaekiuka kwa makusudi kanuni na mwenendo bora wa shule,

atachukuliwa hatua kali za kinidhamu. 14. KANUNI NA MWENENDO BORA WA SHULE

i. Kila mwanafunzi wa shule hii anapaswa kutambua kuwa yupo hapa kwa

a. ajili ya Uislamu. Kwa sababu hiyo chochote kilichopo nje ya Uislamu

b. hakina nafasi katika shule hii, kiwe kwa maneno au kwa vitendo.

ii. Kila mwanafunzi atakuza pendo lake kwa Allah (s.w) na mtume wake

a. (s.a.w), dini yake na waumini wenzake. iii. Pamoja na haki za muumba zilizo juu ya kila Muislam, yamwajibikiakila

mwanafunzi achunge haki na nafasi yake na atumie vipaji vyake katikauchamungu ndani na nje ya shule.

Maelekezo ya kujiunga na shule 2018

8

iv. Kila mwanafunzi atatumia muda wake vizuri katika kujielimisha kwa ajili ya Allah(s.w) ikizingatiwa kuwa kujielimisha kwa ajili ya Alla(s.w) ni amri ya

kwanza kwa kila muislamu. v. Kila mwanafunzi atalazimika kuhudhuria kila kipindi cha somo, kufanyamazoezi,

majaribio ya kila somo na mitihani yote itakayotolewa shuleni.Mwanafunzi

atakayeshindwa kuhudhuria darasanikwa sikutatu mfululizo au zaidi bila sababu yoyote ya msingi, atakuwa amejifukuzisha shule.

vi. Kila mwanafunzi anapaswa kuzingatia na kufuata ratiba na utaratibu wa shule

kikamilifu.Ni kosa kubwa kutoonekana katika eneo husika kwa mujibu wa ratiba kama vile; kuonekana bwenini wakati wa masomo. Wanafunzi wagonjwa wanapaswa kuripoti kwa mwalimu wa zamu na darasa ili wapewe kibali cha kwenda zahanati.

vii. Wakati wote wa kuja shule au wakati wa kurudi nyumbani, vazi rasmini sare ya shule. Kutokuwa na sare katika wakati huo ni kosa lisilovumilika.

viii.Wanafunzi wote wanatakiwa wavae nguo za Kiislamu wakiwa ndani na nje ya

shule. Wasichana wavae nguo za kuenea mwili mzima isipokuwa uso na vitanga vya mikono rejea Qur-an {24:31}.

ix. Ni marufuku kwa mwanafunzi wa jinsia yoyote kuvaa mapambo wakatiakiwa

shuleni na nje ya shule. a. Wavulana wavae nguo za heshima na zisizo na maandishi au picha ya aina

yoyote. Ni Maarufuku kuvaa kaptura, jeans, msuli au carwash katika

maeneo ya shule. b. Ni maarufuku kwa wasichana kuvaa, nguo za kubanaa, fupi au

zinazoonesha ndani (Transparent) akiwa shuleni au nje ya shule.

x. Ni marufuku kwa mwanafunzi yeyote kufuga kucha, kujipaka rangi zakucha,rangi za midomo, kupaka hina, kunyoa nyusi,kupaka wanja,kutumia manukato kwa wasichana, kuvaa viatu vya kuchuchumia au vinavyotoa sauti, kukali nywele, kutia rangi, kusuka rasta au kubadilisha nywele, kucha, au ngozi kwa namna

yoyote ile na kufuga nywele kwa wavulana.

Angalizo:Kwa wasichana itakapobidi kutumia manukato watatumia Nivea ya kupaka

kwapani tu (Rolling)ambayo harufu yake ataihisi mpakaji mwenyewe.Ama body spray na manukato ya aina zote ni makosa kukutwa nayo.

xi. Ni marufuku mwanafunzi kuchochea, kushawishi, kuhamasisha,au kushiriki mgomo kwa namna moja au nyingine hata kama kuna sababu za msingi. Ni kosa kubwa kugomea amri au maelekezo ya viongozi waserikali ya wanafunzi, walimu

na uongozi wa shule kwa ujumla. xii. Mwanafunzi asionekane katika vilabu vya pombe, nyumba za Kupangisha wageni

(guest house), kumbi za dansi na sinema.

xiii.Kila mwanafunzi ni mlinzi wa mali ya shule, mali yake binafsi na yawenzake. Mwanafunzi atakayeharibu, kusababisha mali ya shule kuharibika, kuibiwa au kupotea atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kulipa. Hivyo mwanafunzi atakapogundua wizi au uharibifu wowote dhidi ya mali ya shule au

Maelekezo ya kujiunga na shule 2018

9

ya mwanafunzi mwingine atoe taarifa kwa walimu au viongozi wanaohusika mara moja.

xiv. Kuiba ni kosa kubwa, mwanafunzi atayethibitika kuiba mali ya shule au mwanafunzi mwenzake au nje ya shule atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufukuzwa shule.

xv. Mwanafunzi anapokuwa na shida yoyote hapa shuleni, kwanza aanze kwa viongozi wanafunzi na ndipo aende kumuona mwalimu wa zamu au wa Darasa lake, au walimu wengine wanaohusika. Kama mwanafunzi baada ya kufuata

ngazi hizo shida yake haijatatuliwa, aende kwa makamu Mkuu wa shule, kisha kwa mkuu wa shule itakapobidi kufanya hivyo. Mwanafunzi asishitakie shida zake nje ya shule kabla hajamuona mkuu wa shule.

xvi. Kila mwanafunzi anatakiwa awe msafi wakati wote, ashiriki vyemakatika usafi

wa mwili wake binafsi; kitanda, nguo, nywele, kucha, na usafi wa madarasa, bweni,bwalo la chakula na mazingira ya shule kwa jumla.

xvii. Kelele za aina yoyote hazitaruhusiwa, ziwe darasani, kwenye barazaza

madarasa, ndani ya bweni, au popote iwe kwa mwanafunzi mmoja auwengi (kundi). Tunalazimika kuonesha maadili ya Kiislalmu katika mazungumzo yetu yote.(Rejea Qur’ani 31:19).

xviii. Shule haimruhusu mwanafunzi kutoka na kulala nje ya eneo la shulebila ya kibali maalum cha maandishi kilichoidhinishwa na Mkuu wa shule. Wakati wa mapumziko mafupi (mid-term break) wanafunziwatabakia katika eneo la

shule. xix. Mwanafunzi hatakiwi kulala au kwenda katika nyumba za watumishi isipokuwa

kwa dharura maalum itakayoidhinishwa na mkuu wa shule.

xx. Wanafunzi wa jinsia tofauti hawaruhusiwi kuchanganyika katika jambo lolote bila ya uangalizi wa mwalimu iwe faragha au bayana, kufanya hivyo ni kosa la kukaribia zinaa ambalo adhabu yake ni kufukuzwa shule.

xxi. Kupigana ni kosa kubwa. Mwanafunzi atakayepigana au kumpiga Mwenzake

atachukuliwa hatua kaliza kinidhamu. xxii. Mwanafunzi anapaswa kuripoti shuleni katika tarehe na muda uliopangwa

baada ya Likizo, atakapochelewa kwa dharura, taarifa itolewe kwa mkuu wa

Shule kabla ya kufunguliwa shule, na baada ya hapo aje na mzazi/mlezi wake anaetambulika kiofisi ndani ya siku saba (7) baada ya shule kufunguliwa, atakayechelewa zaidi ya hapo atakuwa amejifukuza shule mwenyewe.

xxiii. Wazazi wa wanafunzi wanaruhusiwa kuwatembelea wanafunzi (watotowao) shuleni siku za Jumamosi na Jumapili za kila mwisho wa mwezi.Hata hivyo kutokana na uhaba wa makazi shuleni, shule haitahusika kumpatia mzazi/mlezi

malazi atakapomtembelea mwanae. xxiv. Wakati wa kuwatembelea wanafunzi, mzazi/mlezi haruhusiwi kuleta vyakula au

vinywaji vya aina yoyote kwa mwanafunzi. Vifaa vitakavyoletwa kwa wanafunzi

vikabidhiwe kwanza kwa mwalimu wa zamu/darasa ili vikaguliwe. xxv. Zaidi ya mashine ya kufanyia hesabu (calculator), vifaa vyote vya Electronics

kama vile simu, camera, radio, radio cassette n.k haviruhusiwi mwanafunzi kuwa navyo katika mazingira ya shule. Mwanafunzi atakayekutwa navyo vitu

Maelekezo ya kujiunga na shule 2018

10

hivyo hapa shuleni, atapewa adhabu kali ikiwa ni pamoja na kufukuzwa shule na havitarudishwa.

xxvi. Ni kosa kwa mwanafunzi kukaa na pesa taslimu bwenini zinazozidi Tsh 5,000/=. Pesa zote zihifadhiwe kwa Mhasibu wa shule. Kutakuwa na utaratibu wa kuchukua pesa kiasi kidogo kwa ajili ya matumizi.

xxvii.Shule imetenga maeneo maalum kwa ajili ya michezo.Hivyo ni marufuku

mwanafunzi kukutwa anacheza mpira na michezo mingine ya kutimua vumbi na

kushawishi kelele za kishabiki na mfano wake katika maeneo yanayozunguka bweni,darasa na maeneo mengine mfano wa hayo nje ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michezo.

xxviii. Swala ni nguzo kuu ya kumtambulisha mtu kuwa ni muislamu na ufunguo wa milango ya mafanikio.Hivyo shule haitamvumilia mwanafunzi yeyote atakayeonekana kupuuza swala kwa makusudi hata kama ni kwa tabia ya

kuchelewachelewa na kukosa jamaa msikitini.

xxix. Mbali na mzazi kuruhusiwa kumtembelea mtoto wake na kujua maendeleo yake

kitaaluma na kitabia kila Jumamosi na Jumapili ya mwisho wa mwezi,pia anakaribishwa shuleni au kuwasiliana na uongozi wa shule wakati wowote kwa lengo la kuleta ufanisi kwa mwanae na jamii ya waislamu kwa ujumla.

15. MAKOSA YANAYOWEZA KUSABABISHA KUFUKUZWA SHULE.

Pamoja na maelezo yote hayo, mwanafunzi atakayechupa kwa makusudi mipaka ya Uislamu na kuvunja maadili na kanuni za shule kwa kutenda makosa makubwa kama yalivyoainishwa atafukuzwa shule;

(i) Kunywa pombe.

(ii) Kwenda nyumba za starehe kama vile kwenye kumbi za madansi, disko n.k (iii) Uzinzi au kukaribia zinaa kwa kuwa na rafiki wa jinsia tofauti (boy Friend/girl

friend).

(iv) Kuvuta bangi,sigara, madawa ya kulevya, n.k (v) Kutosimamisha swala (vi) Kumiliki vitu vya electronics kama simu au line, redio, kamera n.k

(vii) Kukaa nje ya shule kwamuda wa siku 3 bila kibali maalum kilichoidhinishwa na Mkuu wa shule.

(viii) Kuanzisha, kuchochea, kushiriki au kuongoza mgomo.

(ix) Kuhatarisha amani ya shule kwa kupigana au kuchochea watu wapigane. (x) Wizi, uporaji na uharibifu wa mali ya shule na ya wanafunzi au wakazi wa

kituo.

(xi) Kukosa mitihani/jaribio bila ya sababu za msingi. (xii) Kutohudhuria masomo/darasani bila sababu maalumu za msingi. (xiii) Kujirudiarudia katika makosa ya uvunjifu wa kanuni na mwenendo bora wa

shule.

Maelekezo ya kujiunga na shule 2018

11

16. HITIMISHO

Ni matumaini yetu kuwa Mzazi/ Mlezi na mwanafunzi mtarajiwa mmeyasoma maelekezo haya vizuri na kwa makini na kuyaelewa ipasavyo. Mwanafunzi unatakiwa kuzingatia na kutekeleza maelekezo yote ili kuepusha usumbufu. Mzazi/Mlezi unashauriwa kujitahidi kushirikiana nashule kwakutekelezawajibu wako

kikamilifu ikiwa ni pamoja na kulipa ada kwa wakati na kumlea mtoto wako katika maadili ya Kiislamu hasa wakati wa likizo. Ambasaha Islamic High Schoolni shuleyenye mazingira mazuri sana ya kusoma na

malezi ya maadili mema ya kiislamu.

Maelekezo ya kujiunga na shule 2018

12

ORODHA YA VITABU VYA KIADA VYA KIDATO CHA KWANZA.

VITABU HIVI VINAPATIKA NA KATIKA MADUKA YA VITABU (BEI ZINAWEZA KUBADILIKA)

NA TITILE/ JINA LA KITABU PUBLISHER/A UTHOR BEI @

1 TAFSIRI YA QUR-AN ABDALLAH SALEH ALFARSY 15000/=

2 MAARIFA YA UISLAMU DARASA LA WATUWAZIMA JUZUU

YA 3

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE 8500/=

3 ELIMU YA DINI YAKIISLAMU SHULE ZA SEKONDARI

KITABU CHA KWANZA

ISLAMIC EDUCATION PANEL 8500/=

4 TAFSIR YA KISWAHILI YA RIYADH-SWALIHIIN OTHMAN M. ALI 25000/=

5 LUGHA YA KIARABU KITABU CHA KWANZA ISLAMIC EDUCATION PANEL 5000/=

6 GEOGRAPHY FOR SECONDARY SCHOOL BOOK ONE OXFORD 8,500/=

7 CIVICS FOR SECONDARY SCHOOL BOOK ONE OXFORD 8,000/=

8 BASIC MATHEMATICS BOOK ONE OXFORD 8,500/=

9 CHEMISTRY STUDENTS BOOK FORM 1 OXFORD 10,000/=

10 PHYSICS STUDENTS BOOK FORM 2 OXFORD 10,000/=

11 BIOLOGY STUDENT BOOK FORM 1&2 OXFORD 10,000/=

12 COMMERCE FOR SECONDARY SCHOOL. TIE 10,000/=

13 BOOK KEEPING FOR SECONDARY SCHOOL. TIE 10,000/=

14 OXFORD STUDENT DICTIONARY OXFORD 20,000/=

15 ENGLISH (Class Reader) -MABALA THE FARMER BEN AND COMPANY 5,000/=

16 ENGLISH (Class Reader) READ-HAWA THE BUS DRIVER BEN AND COMPANY 5,000/=

17 ENGLISH (Class Reader) -KALULU THE HARE 5,000/=`

18 ENGLISH (Class Reader) -MAGIC GARDEN 4,000/=

19 HISTORY FOR SECONDARY SCHOOL FORM ONE OXFORD 8,000/=

20 KISWAHILI SHULE ZA SECONDARY KIDATO CHA

KWANZA

OXFORD 9,000/=

21 ENGLISH FOR SECONDARY SCHOOL BOOK ONE OXFORD 10,000/=

TUNAKUTAKIA MAANDALIZI MEMA NA KARIBU

AMBASHA ISLAMIC HIGH SCHOOL

Kauli mbiu: “Soma kwa jina la Mola wako Aliyeumba”(96:1)

Wabillah Tawfiiq

© MKUU WA SHULE

Maelekezo ya kujiunga na shule 2018

13

2017