20
www.biblecentre.org www.biblecentre.org -1- KANISA KATIKA AGANO JIPYA

Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

  • Upload
    others

  • View
    39

  • Download
    6

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 1 -

KANISA

KATIKA AGANO

JIPYA

Page 2: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 2 -

UTANGULIZI

Madhumuni ya kiji tabu hiki ni kueleza mambo kumi yanayoambatana nakanisa kwenye Agano Jipya. Ni ombi la waandishi kwamba maneno hayayangetumiwa na Mungu kutia moyo na nguvu imani ya waumini; na halikadhalika kuwaamsha kusoma zaidi kuhusu somo hili ambalo ni la thamanisana kwa moyo wa Kristo.Katika Biblia, neno "Kanisa" lina maana ya kusanyiko au kundi la watu. Haitajimahali ambapo wanakusanyika kama inavyoonyeshwa katika vifungu vifnatavyo:

"...Kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu."

(Matendo 8:1)

"...Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa..."

(Matendo 11:22).

"...Vivyo hivyo nasalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao".

(Warumi 16:5).

"... Kama Kristo naye alivyolipenda kanisa akajitoa kwa ajili yake"

(Waefeso 5:25)

Tafadhali soma Warumi 10:8-13 na 1 Wakorintho 15:1-4. Maandiko hayayanaeleza kinaganaga ujumbe wa Injili. Watu wote ambao wameiamini Injiliwameokolewa kwa kuwa na imani katika Bwana Yesu Kristo. Wao ni sehemuya "Kanisa" ambalo kwalo Kristo Mwenyewe alimwaga damu yake ya thamanimsalabani Kalvari. Wao ni watu wake Kristo viungo vya mwili Wake.

"Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila

mmoja kwa mwenzake." (Warumi 12:5).

=================

Ili kukua katika kuelewa ukweli wa Neno la Mungu, ni lazima kwanzatuache mapenzi yetu tuchukue mapenzi yake na tuache mawazo yetu tuchukuemawazo yake. Huu ndio UFUNGUO

"Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo.

Page 3: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 3 -

YALIYOMO

1. MSINGI

2. MWILI MMOJA

3. KRISTO, KICHWA

4. NENO LA MUNGU, KIPIMO

5. ROHO MTAKATIFU HUONGOZA KATIKA MKUSANYIKO

6. KILA MWAMINI NI KUHANI

7. UTENGANISHO

8. KRISTO 'SHINA' LA MKUSANYIKO

9. CHAKULA NA MEZA YA BWANA

10. JINSI AMBAVYO NINAWEZA KUPATA MAHALI AMBAPO KRISTO

YUPO KATIKATI YA KUSANYIKO LA WATU WAKE

Page 4: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 4 -

"Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye

hai.

Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili

na damu havikukufunulia h i l i , bali Baba yangu aliye mbinguni.

Nami nakuambia, Wevve ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga

kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda."

Mathayo 16:16-18

Uutu tukutu wa Bwana wetu Yesu Kristo ni msingi "MWAMBA" ambaokanisa limekaa juu yake. Ni Mungu, Mwana wa milele. Ni Kristo, Masiha.Katika maandiko ya hapo juu, kukiri kwa Petro juu ya Kristokumekubaliwa kuwa msingi huu imara. Hakuna mwingine!

“Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni

ule uliokwisha kuwekwa yaani, Yesu Kristo”

1 Wakorintho 3:11

Page 5: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 5 -

2. MWILI MMOJA

Katika Mathayo 16:18 kama ilivyonukuliwa hapo mbeleni tunaona kitu kimojamuhimu: Bwana Yesu alisema: “Nitalijenga kanisa langu”. Hiiinatuonyesha kwamba kanisa halikuwepo wakati ule, bali kilikuwa ni kituambacho kingelikuja baadaye. Tunajifunza katika maandiko yafuatayokwamba kanisa halikutokea kuwepo mpaka baada ya Bwana wetu Mbarikiwakufa na kufufuka tena na akawa amepaa kwenda mbinguni. Kwa hivyo hakunahata mmoja kati ya waumini wa Agano la Kale aliyekuwa katika Kanisa lake -hata Yohana Mbatizaji. Kristo tena alizungumzia juu ya kanisa katikaMathayo 18:17, lakini bado kilikuwa ni kitu cha baadaye. Neno "Kanisa"halitumiwi tena katika maandiko mpaka katika Matendo 2:47 ambapotunasoma maneno haya:

"Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa."

Kanisa lilianzia katika Matendo, sura mbili. Wakati huo wa siku ya Pentekoste,Roho Mtakatifu alishuka kutoka mbinguni kuishi ndani ya waumini nakuwaunganisha katika mwili mmoja.

"Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja

kwamba, tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa

tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho Mmoja" (1 Wakorintho 12:13).

Hapo basi, Bwana Yesu alianza kulijenga kanisa lake. Halikuwa ni marekebishoau ongezeko kwa dini ya Kiyahudi. Kanisa ni kitu ambacho ni kipya kabisa.

".. KANISA AMBALO NDILO MWILI WAKE, UKAMILIFU WAKE

ANAYEKAMILIKA KWA VYOTE KATIKA VYOTE."

WAEFESO 1: 22-23

“MWILI

MMOJA”Waefeso 4:4

Page 6: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 6 -

MWILI MMOJA (kuendelea)

Kanisa ambalo Bwana Yesualianza kujenga wakati wa siku ya

Pentekoste bado linajengwa. Watu wanao-iaminiInjili ya wokovu wanaongezwa kila siku na Roho Mtakatifu

kwa jengo hili la ajabu." (Waefeso 1:13).Kila mmoja ni "Jiwe lililo hai" likikaa kwenye msingi imara wa

Bwana Yesu Kristo Mwenyewe, na kila mmoja ni kiungo cha"Mwili Mmoja".

(Tazama 1 Petro 2:5, Waefeso 2: 20-22, na Waefeso 4:4).

Machoni pa Mungu, kanisa ni Moja daima. Haliwezi kugawanywa kwa sababu nisehemu muhimu sana ya Kristo Mwenyewe (Tazama 1Wakorintho 12:12).Ni kweli kwamba ushuhuda wa nje wa umoja huu umeharibiwa na uasi wa

mwanadamu na hivi sasa kuna madhehebu mengi, migawanyiko, na hata makanisayale yanayoitwa ya "kujitegemea".

Lakini ukweli unabaki kuna kanisa moja tu katika Biblia.

"Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake."(Waefeso 5:25).

Ni mapenzi ya Mungu kwamba umoja wa kanisauonyeshwe katika ulimwengu huu. Yeye sio mtungaji wa machafuko.

Hebu tuyageuze macho yetu kwa Neno Takatifu la Mungu tujifunzemawazo yake juu ya kanisa (Tazama 1 Wakorintho 1:10).

"Wala pasiwe kwenu faraka."

MADHEHEBU YANAKANA UKWELI JUU YA MWILI MMOJA.Korintho wengine walisema "mimi ni wa Paulo". Wengine walisema: "mimi ni waApolo". Wengine wakasema "mimi ni wa Kefa (Petro)". Hata wengine walijifikirikuwa mbali na ndugu zao kwa kudai kuwa na uaminifu maluum kwa kusema: "Mimini wa Kristo." Hakuna hata moja kati ya nia hizi tenganifu ni ya Mungu . Katika sikuzetu hizi Wakristo wengine huchagua mafundisho maalum. au desturi fulani maalumau kitu kingine cho chote ili wawe tofauti na wengine katika mwili wa Kristo. Hayayote hayaambatani na ukweli unaopatikana katika Neno la Mungu. Tafadhali soma1 Wakorintho 1:9-13

Page 7: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 7 -

MWILI MMOJA (kuendela)

KUNA UMOJA KATIKA UTARATIBU WAKANISA LINALOPATIKANA KATIKA MAANDIKO.

Ni kwa kuziyenyekea kanuni za ukweli zinazopatikana katika Neno laMungu t u ; ndipo tunaweza kuufurahia utendaji wa UMOJA huu sikuhizi.

K a t i k a Agano J i p y a waumini wote k a t i k a sehemu f u l a n iwalichukuliwa kuwa kanisa (kusanyiko) la Mungu mahali p a l e .Walikuwa ni mfano wa kudhihirisha mwili mmoja wa Kristo mahali pale.1 Wakorintho 1:2 ni mfano: ".... Kwa kanisa la Mungu lilioko Korintho." Hatahivyo palikuwepo na ushirika kamili kati ya mashirika yote. Ikiwa mtu alikuwakatika ushirika Rumi, angepokelewa Yerusalemu anapotembelea huko.

Ushirika katika mikusanyiko h i i u l i o n y e s h w a na kuunganishwaifaavyo na "Barua za kujulishana" - Barua hizihazikutoa s i fa tu kwa mtu kupokelewa kuumegamkate, bali zilibeba salamu za upendo kutokakwa kanisa moja, hadi nyingine. Makanisa yakujitegemea hayakuwepo, na wazo kama hilo ni

kinyume n a u k w e l i w a " M W I L I MMOJA".

"Namkabidhi kwenu F i b i , ndugu yetu." (Warumi 16:1)

" ... barua zenye s i fa . . . " ( 2 Wakorintho 3 : 1 )

Kusanyikola

Korintho

Kusanyikola

Antioki

Kusanyikola

Yerusalemu

Page 8: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 8 -

3. KRISTO, KICHWA

mbinguni

katika dunia

Yeye ni kichwa cha mwili wake, yaani kanisa; yeye ni chanzo cha uhai wa

huo mwil i . Yeye ndiye mwanzo, mzal iwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka

wafu i l i awe na nafasi ya kwanza katika v i t u vyote." (Wakolosai 1 :18 ) .(Agano Jipya: Kiswahili cha kisasa.)

Ni wazi ilioje jinsi ambavyo Maandiko Matakatifu yanadhihirisha wazikwamba Bwana Yesu Kristo ni kichwa cha kanisa! Yeye ni Mtu mtukufualiye mbinguni; na mwili wake umeshikanishwa kikamilifu kwake mwenyewekwa uwezo wa uunganishi wa Roho Mtakatifu. Kama kichwa, anauongoza mwilikatika mambo yote: “ .... hushika kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote

ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa

maongeo yatokayo kwa Mungu" (Wakolosai 2:19). Wakati ambapo sehemuzingine kwenye mwili huu zinapomwitikia yeye kama kichwa, kunaumoja wa kuonekana wazi . Kukua, furaha, na aina nyingine zab a r a k a z i n a f u a t a . U k w e l i w a u o n g o z i w a k e k a ma k i c h wa ,hudumishwa vile vile wakati kusanyiko katika pahali pamojal inapokubal i uamuzi wa kusanyiko kat ika pahal i peng ine kwa sababuuamuzi huu ulifikiwa katika Jina la Bwana Yesu Kristo.

Tunapata maelezo mengine ya utukufu huu wa Uongozi wa Kristo kamakichwa katika Waefeso 1:22, ambapo imeandikwa kwamba yeye n i

"Kichwa juu ya vitu vyote kwa aji li ya kanisa . " Yeye ni Mshauri wa Ajabuwa Mungu; Mwenye Mamlaka juu ya yote. Kanisa litakuwa mwenzakekukishiriki cheo chake kikuu. JE, NI NEEMA ILIOJE !

MWILI

WAKE

KRISTO

Page 9: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 9 -

HIVI

Bwana Yesu Kristo ana mamlakayote ya kuliongoza Kanisa lake. Yeyepekee huwapa ruhusa watumishi wakekumtumikia na "Mwili" (Kanisa)kulingana na uwezo anaompatia kilammoja. "Bali Mungu amevitia viungo

kila kimoja katika mwili kama alivyotaka,"

(1 Wakorintho 12:18)

"Naye (Kristo) alitoa wengine kuwa

mitume na wengine kuwa manabii, na

wengine kuwa wainjilisti na wengine

kuwa wachungaji na waalimu, kwa

kusudi la kuwakami l isha

w a t a k a t i f u , h a t a k a z i y a

huduma itendeke, hata mwili wa

Kristo ujengwe". (Waefeso 4:11-12)

Ijapokuwa wanaongozwa nay e y e p e k e e y a k e ( K r i s t o )katika kazi yao, watumishi waKristo hata sasa ni sehemu ya"Ule mkusanyiko". Kwa hivyoinawapasa kuishi maisha m a t a -k a t i f u k a t i k a unyenyekevu nakuheshimu dhamiri za ndugu zao.(Tazama 2 Wakorintho 4:1-2).

SIO HIVI

Kanisa Ia Agano Jipya haliko kamamfano huu.

Agano J ipya ha l i fund i sh i wazo lakukomboana kwa mamlaka ya mitumeau aina yo yote ya chama kikuu.

Ni kweli kwamba mitumewaliwachagua watu kushikilia v i k a ov y a u s i m a m i z i n a jukumupahal i fu lan i miaka y a m w a n z ow a k a n i s a .

Tazama Matendo 6:6 na Tito 1:5.

Hata hivyo kwa vile siku hizihakuna mitume, u t a r a t i b u h u uw a v y e o hauwezi kuendelea nakibali cha maandiko.

Mtume Paulo hakulikabidhi Kanisakwa wale waliomfuata, baliali l ikabidhi kwa Mungu na kwaneno la neema yake. Tazama Matendo

20:32.

KRISTO

Mitume,Manabii

WainjilistiWachungaji

Waalimu

KRISTO

Mipango yamwanadamuna utaratibu

wa vyeo vyao wenyewe

K A N I S A

Page 10: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 10 -

4. NENO LA MUNGU, KIPIMO

Biblia ni neno la Mungu aliye hai. Ni kipimio cha pekee cha ukweli woteambao Mungu amewafunulia watu. Mawazo yake juu ya kanisa namaagizo yake kwa matendo yake yote yako katika kitabu hiki cha thamani.

Maandiko yamet imia yakit i l ia maanani historia yote ya kanisaikianzia wakati wa siku ya Pentekoste na ikimalizia na "Unyakuzi wakanisa" wakati ambapo Yesu atawanyakua wale wake ambaoamewakomboa kabla ya lile teso kuu.Soma 1 Wathesalonike 4:14-17, na vile vile Ufunuo 3:10-11

Nyaraka zilizoandikwa na mtume Paulo ni za umuhimu maalum kwaufahamu wetu wa mawazo ya Mungu kuhusu kanisa. Zisome zote kwauangalifu . Tazama Waefeso 3 : 1 - 1 0 .

Mtumishi huyu huyu mpendwa wa Kristo aliyaandika maneno hayakatika 1 Wakorinto 14:37:

"Hayo ninayowaandikia ya kwamba ni maagizo ya Bwana".

"Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi

asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli ."

(2 Timotheo 2:15)

"Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa

kuwaonya watu makosa yao na kuwaongoza, na kwa kuwaadabisha

katika haki"

(2 Timotheo 3:16)

“Wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho

Mtakatifu” (2 Petro 1:21).

Page 11: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 11 -

MCHANGA

Kanisa la Mungu halikai kwa sehemu yoyote ile, juu ya nguzo dhaifu yafikira za watu, ziwe ni elimu ya dini, utamaduni, fikira au kitu chochotekingine kile. Waumini wa kwanza katika Bwana wetu Yesu Kristowalisikiliza maneno haya tu-: "SIKIZA ASEMAVYO BWANA”

"Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawa sawa na

neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi." (Isaya 8:20.)

"Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana" (1 Wathesalonike 4:15).

"Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema

yake, Ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote

waliotakaswa." (Matendo 20:32.)

Page 12: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 12 -

5. ROHO MTAKATIFU NDIYE HUONGOZA KATIKA KUSANYIKO

Tafadhali soma sura zote hizi yaani 1 Wakorintho sura 12, 3 na 14. Katikasura hizi tunapata mawazo ya Mungu kuhusu mpango wake katika mikutanoya Kanisa au kikundi mkusanyiko.

1 Wakorintho 12: -----------------------------------------------Muundo wa Kanisa

1 Wakorintho 13: -------------------------------------------------Upendo, Uwezo

I Wakorintho 14: -----------------------------------------------Kanisa katika utendaji

Tunaona katika Agano Jipya, kwamba, wakati waumini walikusanyikapamoja katika mkusanyiko (kanisa), walikusanywa na Roho Mtakatifukatika Jina la thamani la Bwana Yesu Kristo.

Walikuja mbele yake kwa imani kama vile Yesu alivyosema katika Mathayo18:20: "Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu nami nipo papo

hapo katikati yao”.

“Katika Jina Lake” inaongea kuhusu mamlaka yake juu ya mkutano ambapoataongoza na Roho wake. Hakuna mtu aliyetambuliwa kama kiongozi walamipango haikupangwa mbeleni. Roho Mtakatifu alipewa uhuru wakuongoza kulingana na Neno la Mungu, kwa sbabaha ya faida ya kirohokwa kila mmoja."Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana." (1 Wakorintho12:7)"Lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule ak imgawia

k i la mtu peke yake kama apendavyo yeye ." (1 Wakorintho 12:11)

ROHO

MTAKATIFU

WIMBO OMBI NENO LA

BUSARA

NENO LA

HEKIMA

KUONGOZA

AU

KUKARIPIA

NA

LENGINE

Page 13: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 13 -

TARATIBU YA MKUTANO UONGOZWAO NA

ROHO MTAKATIFU

1. Kutanikeni katika Jina la Bwana Yesu Kristo pekee. Tazama Mathayo 18:20.

2. "Mjazwe na Roho Mtakatifu" (Waefeso 5:18). Muwe na Kristo na Neno laMungu mbele ya mioyo na akili zenu.

3. Muwe na dhamiri njema. (Tazama Matendo 24:1-6). "Wala

msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu" (Waefeso 4:30)

4. Epukeni kumpinga Roho Mtakatifu anapokuwa akitafuta kuwatumiakumwinua Kristo na muwe wa kutiana moyo wenyewe kwa wenyewe.

"Msimzimshe Roho," 1 Wathesalonike 5:19 na 20.

5. Muwe macho kukitambua cho chote ambacho ni kinyume cha Neno la Mungu.".... Na wengine wapambanue". Tazama 1 Wakorintho 14:29."Jaribuni mambo yote" 1 Wathesalonike 5:21.

6. Wapeni nafasi wengine ambao Mungu angewatumia kupeleka ujumbewake. Tazama 1 Wakorintho 14:31 na 32.

7. Zungumzeni mmoja baada ya mwengine, na mjifunze kujizuiawenyewe. Tazama 1 Wakorintho 14:31 na 32.

8. Na wanawake wajiepushe, kufudisha, kuhubiri, na kusema kwenyemkusanyiko. Tazama 1 Wakorintho 14: 34 na 35. Vile vile 1 Timotheo 2:11.

Tukumbuke ya kuwa kazi ya Roho Mtakatifu ni kutuongoza katika ukweliwote. Maongozi yake daima ni kuambatana na maandiko na sio kinyumekamwe na ule ufunuo ulioandikwa. Hakuna mahali popo te ka t ikaBib l i a ambapo tunasoma kwamba mtu yeyote a limuomba RohoMtakatifu. Yeye ni Mungu R.oho na mmoja wa Utatu wa Mungu. Hufanyakazi ya kumwinua Baba na Mwana kupitia kwa waumini.

"Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenyekweli. yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenywe.....Yeyeatanitukuza mimi." (Yohana 16:13 na 14)

Page 14: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 14 -

6. KILA MWAMINI NI KUHANI

“Nyini nanyi, kama mawe yaliyo hai,mmejengwa muwe nyumba ya roho, ukuhanimtakatifu, mtoe dhabihu za Roho,zinazokubzaliwa na Mungu kwa njia ya YesuKristo” (1 Petro 2:5)

“Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wakifalme, taifa takatifu watu wa milki yaMungu mpate kuzitangaza fadhili zake yeyealiyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuruyake ya ajabu” (1 Petro 2:9)

Kila mwamini katika Bwana Yesu Kristo ni kuhani aliyezaliwa kiroho."Tumezaliwa tena" na sisi sasa ni sehemu ya jamii ya ukuhani wa kiroho(Tazama 1 Petro 1:23).

Hii hailingani kwa njia yoyote na sehemu tulio nayo katika jamii, mafunzo,ikiwa tu waume au wake wala kipawa chetu.

Kama makuhani tunao uhuru wa kuingia, katika Roho, kwa imani ,mahali pale pale ambap o Kristo yuko sasa mkononi wa kuume waMungu, Baba, kumwabudu. Ibada kama hii ni mfuliko wa mioyo yetutunapofikiria Mungu ni nani, na yale ambayo amekwishafanya.Yaweza paa wakati wowote na sio tu wakati ule ambapotumekusanyika na waumini wengine katika mkutano. (SomaWaebrania 10:19) Ukuhani huu hauhusiki na swala la dhambikamwe, maana jambo hili la dhambi lilimalizwa kabisa mara moja tuna damu ya thamani ya Bwana Yesu Kristo alipokufa msalabaniKalvari. "HAPANA TOLEO TENA KWA AJILI YA DHAMBI' (WAEBRANIA 10:18)

Kama makuhani, tuna ruhusa pia kuwa ushuhuda kwa utukufu wa Mungukatika dunia hii. Kwa kweli hii ni huduma ya "Kifalme"!

Yapasa iwe mapenzi ya kila mwamini atumie aina zote mbili za ukuhani wake,akiziweka katika mizani kamili .

MAKUHANIWATAKATIFU

KWAIBADA

MAKUHANIWAKIFALME

KWAHUDUMA

UKUHANI WA KILA MWAMINI

Page 15: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 15 -

7. UTENGANISHO

“MUNGU AKATENGA NURU NA GIZA” (Mwanzo 1:4)

Kanuni ya UTENGANISHO inapita kote katika Neno la Mungu. Munguhavichanganyi vitu. Anatenganisha nuru na giza; kikukuu na kipya; kizuru na kiovu;na watu wake kutoka kwa wengine. Vivyo hivyo na kanisa pia.

Kuziasi sheria(dhambi)

Neema Sheria

Kutokuwana tumaini

Wokovu Matendo (kazi)

Fujo (Ghasia) Kupumzika(raha)

Kurudiwa-rudiwaKwa sherehe

Giza Nuru Vivuli(mifano)

Kutojali(ubaridi)

Kazi ilyo kamilishwaya upatanisho

Dhabihuzisizokamilika

DUNIA KANISADINI ZA

KIYAHUDI

Page 16: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 16 -

UTENGANISHO(Kuendelea)

Shaka Imani Kanuni za kidini

Uchungu wa dunia Tumaini la mbinguni Tumaini la kidunia

Mungu hajulikani Kila mwaminini kuhani

Chama maalum chaMakuhani

Ibada za sanamu Kutaniko ya kirohoYa ibada (kwa Kristo)

Kutaniko ya ibada yaKiulimwengu(Yerusalemu)

Siasa (Mambo ya utawala) Maombi Majivuno la taifa

Kanisa sio sehemu ya ulimwengu huu. Bwana Yesu Kristo alisema"WAO SI WA ULIMWENGU, KAMA MlMl NISIVYO WAULIMWENGU” (Yohana 17:16). Tazama pia 1 Yohana 2: 15-17.

Kanisa si sehemu ya Uyahudi. Dini hii ihanzishwa na Mungu kwamwanadamu katika mwili, lakini sasa imewekwa kando na MunguMwenyewe. Ujumbe wa kisasa kwa Wakristo unapatikana katikaWaebrania 13:13: "BASI NA TUTOKE TUMWENDEE (KRISTO) NJE YAKAMBI TUKICHUKUA SHUTUMU LAKE”.

"KAMBI" sasa ndio dani ya Kiyahudi ya kale pamoja na kanuni zote zakidunia na sherehe zake. Ninasema kwa masikitiko, sehemu kubwa yadini hii ya zamani imeigwa na kuletwa katika wale wanaojidai kuwa niWakristo. Hapa dini hii haina nafasi kwa kuwa inaleta uharibifu katikaushuhuda wa kikristo na kuzuia uwezo wake.

Hamu ya Mungu kwa watu wake sasa ni watengane na uovu “KILAALITAJAYE JINA LA BWANA NA AUACHE UOVU". Tazama 2Timotheo 2 : 19-21.“WACHENI KUTENDA UOVU JIFUNZENI KUTENDA MEMA” (Isaya1:16- 17)

DUNIA KANISA DINI ZA

KIYAHUDI

Page 17: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 17 -

8. KRISTO, “SHINA” LA KUSANYIKO

K R I S T O

Bwana Yesu Kristo Mwenyewe alizitaja kanuni za kukusanyika katika Mathayo18:20.

"KWA KUWA WALIPO WAWILI WATATUWAMEKUSANYIKA KWA JINA LANGU,NAMI NIPO PAPO HAPO KATIKATI YAO."

WAPI..............................................................Mahali pa namna ya MunguWAWILI AU WATATU..............................Ushuhuda wa namna ya MunguWAMEKUSANYIKA...............Uwezo wa kukusanyika wa namna ya MunguPAMOJA................................................................Ushirika wa namna ya MunguKWA JINA LANGU..................................Mamlaka ya namna ya MunguNIPO PAPO HAPO ........................................Kuwapo kwa namna ya MunguKATIKATl YAO........................................... ..............Shina namna ya Mungu

Msitari mwingine wa maana ni:- 1Wakorintho 5:4"KATIKA JINA LA BWANA WETU YESUKRISTO NINYI MKIWA MMEKUSANYIKAPAMOJA NA ROHO YANGU, PAMOJANA UWEZO WA BWANA WETU YESU KRISTO".

Ukristo wa kweli unautofauti ulioje, na dini ya Kiyahudi ya zamani.(Kwa maelezo zaidi soma Kumbu-kumbu la Torati 12: 5-14). Katika diniya Kiyahudi palikuwepo mahali pakionekana. Katika Ukristo ni Mtu,Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye "ndiye Shina."Bwana Yesu Kristo al iahidi kuwapo kwake na wale ambaowamekusanyika katika jina lake kulingana na maandiko ya hapo juu. Nihapo, al ipo mwenyewe ndipo mamlaka na nguvu zake vinapatikana.

Hii haitumiki kwa kila mahali ambapo mwamini mmoja akutana namwingine kikawaida, kwa mfano, barabarani, kazini, shuleni, N.K.Katika mambo kama haya, panaweza kutokea wakati wa ushirika wafuraha wa kuonana kwa kawaida, bali sio kama vile kukusanyika katikaJina la Bwana Yesu Kristo kulingana na Mathayo 18:20 na 1 Wakorintho5:4. Vile vile ukweli huu wa thamani kuu hauwezi kutumiwa mahaliambapo jina jingine badala ya lile la Wakorintho Kristo pekee limewekwakuwa "shina" la kukusanyikiwa (Tazama 1Wakorintho 1: 10-13)

Page 18: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 18 -

9a. CHALUKA CHA BWANA

"AKATWAA MKATE, AKASHUKURU, AKAUMEGA, AKAWAPA,AKISEMA HUU NDIO MWILI WANGU UNAOTOLEWA KWA AJILI YENU,FANYENI HIVI KWA UKUMBUSHO WANGU. KIKOMBE NACHO VIVYOBAADA YA KULA, AKISEMA, KIKOMBE HIKI NI AGANO JIPYA KATIKADAMU YANGU INAYOMWAGIKA KWA AJILI YENU." Luka 22: 19 na 20.

"KWA MAANA MIMI NALIPOKEA KWA BWANA NILIYOWAPA NYINYI,YA KUWA BWANA YESU USIKU ULE ALIOTOLEWA ALITWAA MKATE,NAYE AKIISHA KUSHUKURU AKAUMEGAAKASEMA, HUU NDIO MWILI WANGU 'ULIO KWA AJILl YENU,FANYENl HIVI KWA UKUMBUSHO WANGU. NA VIVI HIVI BAADA YAKULA AKAKITWAA KIKOMBE AKISEMA. KIKOMBE HIKI NI AGANOJIPYA KATIKA DAMU YANGU FANYENl HIVI KILA MNYWAPO, KWAUKUMBUSHO WANGU. MAANA KILA MWULAPO MKATE HUU NAKUKINYWEA KIKOMBE HIKI MWAITANGAZA MAUTI YA BWANAHATA AJAPO." 1 Wakorintho 11: 23-26.

Maandiko hayo hapo juu yanaleta ujumbe wa ajabu mioyoni mwetu. KatikaMatendo 20:7, tunaona ya kuwa Wakristo wa kwanza walikusanyikakatika ushirika kumkumbuka Bwana Yesu Kristo katika kifo chake,wakati wa siku ya Bwana; siku ya kwanza ya juma. Ilikuwa desturi yao.Walishiriki katika chakula cha Bwana kwenye Meza ya Bwana . Huu piau l ikuwa ni udh ih i r i sho wa umoja (ushi r ika) wa mwi l i wa Kris tokama inavyofunzwa kat ika 1 Wakorintho 10:16-21. Kila mwamini wakweli ana nafasi Mezani pa Bwana, na anaalikwa na Bwana Yesu Kristomwenyewe "kuumega mkate" kila mara katika mkusanyiko pamoja nawaumini wengine. Wakris to wenye shukrani huikar ib isha nafas i h i ikumpendeza Bwana wao. Ni ruhusa ambayo pia inapendeza mioyo yetuwakati ambapo mateso yake Kristo yanapokumbukwa kuleta ibada ya upendo nasifa kwake.

Page 19: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 19 -

10. VILE AMBAVYO NINAWEZA KUPATA MAHALI AMBAPO KRISTO

YUPO KATIKATI YA KUSANYIKO LA WATU WAKE SIKU HlZI:

“WATAKA TUANDAE WAPI?"

(Luka 22:9)

Tafadhal i soma Luka 22 : 7-20

Wanafunzi wal ipewa maagizo dhahiri ,kwa kupapata mahali ambapo BwanaYesu angelikutana nao: Walikuwawamfuate "mwanamume ambayeamechukua mtungi wa maji ." Hadithi hii ina masomo ya kifananishokutufunza leo: Yule "mwanamume" aweza kufikiriwa kama Roho waMungu na vile vile kama mtumishi fulani wa Mungu ambaye ametumwakuleta Neno la Mungu mbele ye tu . Mara nying i ka t ika maandiko"Maj i " hutumiwa kwa kutoa mfano wa Neno la Mungu. Kulifuata Neno laMungu ni jambo lenye maana sana! Vile vile katika hadithi hiyo hapojuu, "nyumba" ni mfano wa kusanyiko (kanisa) ambapo wanafunziwengine wangepatikana wamekusanyika kwa Kristo.

WANAFUNZI WA KWANZA WALIUACHA UCHAGUZI KWA KRISTO. NASI PIA

TUNAWEZA: NA YATUPASA, PIA.

HIZI NDIZO ALAMA ZINAZOTOFAUTISHA MEZA YA BWANA NAUSHIRIKA WAKE NA MEZA NA MASHIRIKA YALIYOTENGENEZWANA MWANADAMU.1. BWANA YESU KRISTO NDIYE ANAYEANGALIWA - 'SHINA' LAKUSANYIKO - waumini huenda kukutana naye (Matheo 18:20)2. MAFUNDISHO NA USHIRIKA WA MITUME HUAMBATANA NAMEZA HII. Vitu vinavyofundiswa na vitu vinavyofanywa vinalinganana Neno la Mungu lililoandikwa badala ya desturi au mawazo yawanadamu.3. ILIANZA NA UNYENYEKEVU KWA BWANA YESU KRISTOKULINGANA NA KANUNI ZA UKWELI ZINAZOPATIKANA KATIKANENO LA MUNGU (Matendo 2:42)Muulize Bwana akuongoze kwa ushirika unaofaa na wauaminiweng ine ambao wa mekusanyika ka t i ka j i na l a Yesu Kr i s towakiufuata mwongozo huo hapo juu. "UKAFUATE HAKI, NA IMANI NAUPENDO NA AMANI, PAMOJA NA WALE WAMWITAO BWANA KWAMOYO SAFI." (2 Timotheo 2:22).

Page 20: Kanisa Katika Agano Jipya - Biblecentrebiblecentre.org/documents/Kanisa Katika Agano Jipya.pdf · 2019. 12. 28. · kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:16-18

www.biblecentre.org

www.biblecentre.org - 20 -

Unakaribishwa kuandika kupitia kwaAiiwani iliyopeanwa kupata habari zaidi:

1)“Tafuteni”P.O.Box 81040MOMBASAKENYA

2)

P.O.C.C. (Promotion des Œuvres

Chrétiennes du Congo)

s/c Mr. .MILAMBU ILA

9, Avenue Parc

Salongo sud/Lemba

KINSHASA