Upload
others
View
2
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 1 kati ya 21
Soma kwa makini maelekezo ya kujiunga na shule kisha mzazi athibitishe kukubali nafasi hii kwa
kulipa ada awamu ya kwanza kabla ya tarehe 30/06/2020.
Kufuatia kufungwa shule kutokana na ugonjwa wa CORVID -19, na kwa kuwa
serikali hivi karibuni itatangaza tarehe ya kufungua shule, Mzazi na mwanafunzi
mnashauriwa kujiandaa na kuwa tayari ili serikali itakapotangaza tarehe ya
kufungua shule zote tutakuarifu tarehe ya kuripoti shule kupitia mawasiliano ya
simu.
1. UTANGULIZI
MKUZO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL ni Shule ya Kiislamu ya bweni inayotazama Elimu
kuwa ni jambo la kwanza muhimu kwa Mwanadamu.Tunajifunza katika Qur`an kuwa Nabii
Adamu (a.s) kabla hajaletwa hapa ulimwenguni alifundishwa majina ya vitu vyote na kuahidiwa
kuletewa mwongozo (Rejea Qur`an, sura ya (2:31, 38).Vilevile tunajifunza kuwa mtume wa
mwisho Muhammad (s.a.w) kabla hajaanza kazi yake kubwa ya kuhuisha Uislamu alipewa
kwanza amri ya kusoma (Rejea Qur`an 96:1-5)
Mtume (s.a.w) amesisitiza kuwa ni faradhi (lazima) kwa kila Muislamu mwanaume na kila
Muislamu mwanamke kutafuta Elimu.Pia Mtume (s.a.w) amesistiza Elimu itafutwe hata ikibidi
ifungwe safari ya mbali (Uchina).
Kwa muhutasari tunalojifunza kutoka katika Qur`an na hadithi sahihi za Mtume (s.a.w) ni kuwa;
Kwanza, Elimu ni zana ya kwanza ya msingi ambayo Muislamu hana budi kuwa nayo ili aweze
kuishi maisha ya kiislamu na awe Khalifa (Kiongozi) wa Allah (s.w) hapa Duniani
Pili, tunajifunza kuwa katika Uislamu hapana ubaguzi wa Elimu ya dunia na Elimu ya akhera. Kila
fani ya Elimu inayomwezesha Mwanadamu kufikia lengo la kuwa Khalifa wa Allah (s.w) hapa
Duniani ni faradhi au wajibu kwa Waislamu wote.
2. LENGO LA SHULE
Lengo kuu la MKUZO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL ni kuwalea na kuwaelimisha
vijana wa Kiislamu ili kuwaandaa kuwa viongozi wa kutegemewa na jamii ya Kiislamu na
Taifa kwa ujumla.
Tahasusi (combination) zilizopo shuleni Kidato cha tano hadi cha sita ni zifuatazo:-
PCB, PCM, CBG, EGM, HGE, HGL, HGK, KLA*, HKL na ECA.
TANBIHI: A* = ARABIC
Masomo yanayofundishwa mbali na masomo ya tahasusi ni yafuatayo:-
i. Islamic Knowledge ii. Basic Aplied Mathematics
iii. General Studies iv. Introduction to Arabic
3. NAMNA YA KUFIKA SHULENI
MKUZO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL ipo katika Manispaa ya Songea mkoani
Ruvuma.
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 2 kati ya 21
Kama unatoka nje ya wilaya ya Songea, shuka kituo kikuu cha mabasi Msamala. Unaweza
kuchukua pikipiki (sh2000 – (3000 usiku)) au taxi (10,000) hapohapo wakulete shuleni au
kama ni mchana hauna mizigo unaweza kutoka nje ya stendi na kuomba uelekezwe
sehemu ya kupandia daladala za kwenda Mkuzo (Nauli Tsh 400) utashukia Mkuzo centre
kisha ulizia njia ya kuja shule utaelekezwa.
4. USAFIRI
Wanafunzi watajitegemea nauli kwa usafiri wa kuja shuleni na kurudi nyumbani wakati
wa likizo ya Mwezi Juni/Novemba. Nusu muhula, huwa hawarudi nyumbani.
Uongozi wa shule unao utaratibu mzuri sana wa kuwasafirisha wanafunzi wanaotoka
mikoani hasa wanaokwenda/kutokea Dar es Salaam, Morogoro, Iringa na Njombe
ambapo hukodi basi na wanafunzi husafiri kwa pamoja na husindikizwa na walezi wao.
Pia mikoa ya Mbeya na Mtwara siku ya kurudi nyumbani husafiri pamoja kwa utaratibu
maalumu ulioratibiwa na shule.
Siku ya safari kila mzazi atamleta /atakuja kumchukua mwanae stendi kuu ya mabasi
Ubungo (DAR)/vituo vyao vya mabasi (mikoa mingine) na kukabidhiwa kwa
mzazi/mlezi wake anayetambulika shuleni. Ni muhimu kuhakikisha kuwa mzazi amelipa
nauli kabla ya siku ya safari ili mtoto aweze kusafiri na wenzake.
ZINGATIA
Kwa wale watakaopandia njiani mfano Kibaha, Mlandizi, Morogoro n.k watafanya mawasiliano
na mwalimu mlezi anayesindikiza wanafunzi ili kujua basi litapita saa ngapi katika vituo
vyao.Namba ya mawasiliano kwa ajili ya mipango ya safari ni 0654876317/0658711844.
5. ADA YA SHULE
Mzazi anaruhusiwa kulipa ada yote kwa mkupuo mmoja au miwili au mitatu ndani ya
muda na kiwango kilichoainishwa. Viwango vya ada kwa awamu ni kama ifuatavyo: 6.
a.) Mkupuo wa kwanza Shilingi laki nane (800,000/=) kabla ya tarehe 30/06/2020.
b.) Mkupuo wa pili shilingi laki nne (600,000/=) kabla ya tarehe 25/09/2020.
c.) Mkupuo wa tatu shilingi laki nne (400,000/=) kabla ya tarehe 25/12/2020.
d.) Mkupuo wa nne shilingi laki nne (200,000/=) kabla ya tarehe 25/03/2021.
Mambo ya kuzingatia:
(i) Ada ikishalipwa hairudishwi kwa sababu yoyote ile.
(ii) Ada italipwa kupitia Amana bank kwa namba ya akaunti. 0011 2007 6370 001 au CRDB
namba ya akaunti 0150366789200. Kwa jina la Mkuzo Islamic High School.
(iii) Stakabadhi ya malipo ya benki (“Pay -in-slip”) iandikwe/ziandikwe jina la mwanafunzi
anayelipiwa ada na kidato anachosoma. (Mfano: ADA YA HAWA JUMA KIDATO CHA 5- 2020
) Mtoto au mzazi awasilishe nakala halisi ya Pay-in-slip kwa Mhasibu wa Shule siku ya kuripoti
shule ili kupatiwa Stakabadhi (risiti) ya malipo ya shule . Kama mzazi/mlezi atakuwa mbali na
shule, ni vema baada ya kulipa (kwa awamu nyingine) atume nakala ya stakabadhi kwa
“whastsApp” kwa mkuu wa shule (0764-749020) kumjulisha kuwa amelipa.
(iv) Tahadhari: Hairuhusiwi kulipa ada kwa pesa taslimu shuleni au kwa njia ya simu ya mtu
yeyote au kupitia mawakala wa mitandao ya simu au kupitia akaunti namba isiyokuwa ya shule.
7. FEDHA ZA MATUMIZI
Mwanafunzi anatakiwa kufungua akaunti ya CRDB na aje na kadi yake (ATM CARD) na
kama hajafungua aje na nakala ya cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya kufungua akaunti akiwa
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 3 kati ya 21
shule. Akaunti hii ndio atakayoitumia mzazi kutuma pesa za matumizi na atapewa
utaratibu wa namna kutoa fedha ya matumizi. Aidha akaunti hii ataitumia pia baada ya
kumaliza kidato cha sita yaani chou kikuu kwa ajili ya kupata mkopo kutoka bodi ya
mikopo.
8. MAWASILIANO
Kutokana na kuibuka matapeli wa mitandao ya simu ambao wakati mwingine wanatoa taarifa
zisizo sahihi kwa wazazi au walezi kwa lengo la kuwatapeli, uongozi wa shule unakusisitiza
mzazi kufanya mawasiliano na shule kupitia nambari zifuatazo kwa jambo lolote
1. Mkuu wa shule - 0654876317
2. Makamu mkuu wa shule - 0653392442
3. Patron (mlezi –wavulana) - 0658711844
4. Matron (mlezi –wasichana) – 0673843319
9. SARE ZA SHULE
a.) Sare ya Darasani
Wavulana
i. Suruali mbili.
ii. Nusu kanzu mbili.
iii. Kofia mbili.
iv. Soksi nyeupe.
v. Viatu vyeusi vya ngozi vya kufunga kwa kamba (visiwe na visigino virefu au muundo
wa buti).
vi. Saa ya mkononi.
vii. Sweta 1 la kijivu (lisilo na zipu vishikizo au kofia).
viii. Mkanda mweusi (wa ngozi).
Wasichana
i. Suruali (pajama)2.
ii. Shungi 2.
iii. Baibui 2.
iv. Viatu vyeusi vya ngozi vya kufungwa kwa kamba, na vifunike miguu visiwe na kisigino
kirefu.
v. Saa ya mkononi.
vi. Skafu nyeupe.
vii. Sweta 1 la kijivu (lisilo na zipu, vishikizo au kofia).
b.) Sare za nje ya Darasani.
Wavulana.
i. Suruali mbili.
ii. T-shirt (fauna) 2.
iii. Kanzu nyeupe ya mikono mirefu.
iv. Track-suit rangi ya kijivu yenye mistari mitatu pembeni kuanzia juu mpaka chini Kwa ajili
ya michezo/mazoezi (itakayovaliwa wakati wa mazoezi tu).
v. Raba kwa ajili ya mazoezi.
vi. Jacket 1 nyeusi (siyo sweta au plova) kwa ajili ya kuzuia baridi, visiwe na picha wala
maandishi yoyote wala rangi zilizopishana na lisiwe limeunganishwa na kofia.
vii. Nguo za kulalia, Bukta 2 ndefu zinazovuka magoti.
viii. Soksi nyeusi kwa ajili ya baridi.
ix. Mkanda mweusu (wa ngozi).
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 4 kati ya 21
NB: Track-suit zinazobana miguu kwa chini (baloteli) haziruhusiwi hapa shuleni.
Wasichana.
i. Baibui refu (2).
ii. Pajama 2.
iii. Kitenge jozi moja na sio kanga.
iv. Track-suit rangi nyekundu (yenye mistari mitatu pembeni kuanzia juu mpaka chini). Iwe
pana isiyobana wala siyo balotelli; kwa ajili ya michezo /mazoezi (itakayovaliwa wakati
wa mazoezi tu).
v. Raba kwa ajili ya mazoezi.
vi. Nguo za kulalia (Night dress) –Shumizi ndefu 2.
vii. Skafu nyeusi na soksi nyeusi za kuzuia baridi.
C. NGUO ZA MICHEZO
(i) Kwa wavulana wanatakiwa wawe na truck suit za kiume na wasichana wanatakiwa wawe na truck suit za kike
na ushungi maalum pamoja gauni lnalovuka chini ya magoti-aje nazo
(ii) kwa wavulana na wasichana wanatakiwa kuwa na Raba Pamoja na soksi za michezo- aje nazo
Upatikanaji wa sare.
Ili kuondoa tatizo la kutofautiana kwa rangi za vitambaa na muundo wa sare za shule; sare zote
za shule zitashonwa hapa shuleni kwa gharama zifuatazo:-
A.) Sare za wasichana
DARASANI NJE YA DARASA
Na BIDHAA IDADI KIASI Na BIDHAA IDADI KIASI
1 Gauni 2 41,000/= 1 Gauni 2 41,000/=
2 Suruali(pajama) 2 19,000/= 2 Suruali(pajama) 2 19,000/=
3 Shungi 2 39,000/= 3 Shungi 2 39,000/=
4 Sweta 1 10,000/= 4 Jaketi 1 25,000/=
JUMLA 109,000/= JUMLA 124,000/=
JUMLA KUU 233,000/=
B.) Sare za wavulana
DARASANI NJE YA DARASA
Na BIDHAA IDADI KIASI Na BIDHAA IDADI KIASI
1 Suruali 2 30,000/= 1 Suruali 2 30,000/=
2 Nusu kanzu 2 34,000/= 2 T -shirt (fulana) 2 20, 000
3 Kofia 2 4,000/= 3 Jaketi 1 25,000/=
4 Sweta 1 10,000/= 4
JUMLA 78,000/= JUMLA 75,000/=
JUMLA KUU 153,000/=
Vipimo vya sare vitafanyika hapa shuleni
Tanbihi:
i. Baada ya kupatiwa sare mwanafunzi hataruhusiwa kuvaa nguo nyingine yoyote
kwa hiyo wakati wa likizo atatakiwa kuzirejesha nyumbani nguo alizokuja nazo.
ii. Ni marufuku mwanafunzi kuvaa mapambo ya aina yoyote wakiwa shuleni au nje
ya shule
iii. Manukato ya aina yoyote hayaruhusiwi.
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 5 kati ya 21
iv. JEZI au nguo yenye nembo ya timu ya mpira au chama cha siasa au taasisi fulani
hairuhusiwi (isipokuwa nembo ya shule au nembo ya kiwanda mfano ADIDAS,
NIKE, N.K).
10. VIFAA VYA DARASANI
Mwanafunzi anaporipoti shuleni atatakiwa kuja na vifaa vifuatavyo:-
i. Madaftari /counter books QUIRE 2-3 kulingana na masomo yake.
ii. Mfuko wa kutunzia madaftari (School bag).
iii. Scientific calculator na mkebe wa vifaa vya hisabati (Mathematical set) kwa
wanafunzi wa PCM, EGM, PCB, HGE, na CBG.
iv. Koti la Maabara (Lab coat) linaweza kupatikana shuleni kwa sh 25,000/-
v. Gloves kwa wanafunzi wa PCM, PCB na CBG na Dissection kit kwa wanafunzi
wanaosoma biology tu.
vi. Graph Paper kwa wanafunzi wanaosoma BASIC APPLIED MATHEMATICS
(BAM), ADVANCED MATHEMATICS, GEOGRAPHY na ECONOMICS yaani
combinations za PCM, PCB, EGM, CBG, HGE, ECA na HGK.
11. VIFAA VYA BWENI:
i. Godoro la upana wa futi mbili na nusu (FT2½ X4 Inch).
ii. Shuka 2, 1 ya rangi ya Pink na 1 ya rangi ya kijani pia zinapatikana shuleni kwa Tsh
11,000/= zote mbili.
iii. Mto 1 na foronya 2 rangi ya pink 1 na kijani 1.
iv. Sendo za kushindia.
v. Ndala za kwendea maliwato.
vi. Kanzu nyeupe (kwa wavulana).
vii. Taulo na ndoo ndogo ya plastic.
viii. Blanketi zito.
ix. Chandarua cha pembe nne 4x6.
x. Sabuni za kufulia za unga na za kuogea pamoja na mafuta mazito ya kujipakaa (siyo
cream)
xi. Vyombo, vya chakula; Sahani, bakuli na kikombe. Kijiko siyo lazima.
Sahani kikombe na bakuli visiwe udongo au plastiki (Nunua Stainless steel au mfupa)
xii. Begi gumu la kufunga na kufuli (mbao, chuma, plastiki au kawaida) kwa ajili ya
kuhifadhia vitabu na vifaa vingine bwenini.
Angalizo: Taulo za kike (PEDI) ziwe za kufua. Mwanafunzi yeyote akija na taulo tofauti
na hizo, zitachukuliwa na kuteketezwa maramoja na hatarudishiwa.
Muhutasari wa Gharama zinazotakiwa kulipwa shuleni wakati wa kuwasili: -
Na Mahitaji Wavulana Wasichana Malipo 1. Ada (awamu ya kwanza) 800,000/= 800,000/= BANK
2. Sare za darasani jozi (pea) 2 78,000/= 109,000/= CASH 3. Sare za nje jozi (pea) 2 75,000/= 124,000/= CASH 4. Kitambulisho 5,000/= 5,000/= CASH 5. Shuka 2 11,000/= 11,000/= CASH 6. Vitabu 3 vya Islamic knowledge 20,000/= 20,000/= CASH
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 6 kati ya 21
Pesa ya TEHAMA ilipwe shuleni kwa mhasibu
Angalizo: Vitabu au vifaa ambavyo bei zake hazijaorodheshwa, mzazi amnunulie mtoto
aje navyo.
12 UANDIKISHWAJI
Siku ya kuripoti Shuleni, Mwanafunzi aje na vitu vifuatavyo: -
(i) Nakala Cheti cha kuzaliwa.
(ii) Nakala ya matokeo ya kidato cha nne (result sleep).
(ii) Fomu za utambulisho wa mwanafunzi na wazazi/Mlezi wa mwanafunzi zikiwa
zimejazwa na kubandikiwa picha.
(iii) Fomu ya daktari (Medical Examination form) iliyojazwa na Daktari wa Hospitali ya
Serikali ya wilaya au ya rufaa (imeambatanishwa).
(iv) Fomu ya wajibu wa mzazi/mlezi iliyojazwa na mzazi husika
(v) Nakala halisi za Pay-in-slip ya malipo ya ada.
(vi) Vitabu vya kiada (textbooks) vya kidato cha tano na sita vinapatikana (bei ziko
ukurasa wa mwisho). Mwanafunzi aje na pesa atalipia shuleni.
(vii) Kitabu cha dua (HISNUL MUSLIM). Kinaweza kupatikana shuleni kwa shilingi
2,000/=
(viii) fedha za Tehama (compyuta) sh.30,000/-
13. MAENDELEO YA DARASANI.
Shule inaweka mkazo wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuweza kufanya vizuri katika
mitihani yao. Kwa hiyo shule imeweka utaratibu mzuri wa kuwashindanisha wanafunzi na
kuwapa zawadi pamoja na walimu wao.
14.KAZI ZA NJE YA DARASA.
Kujibidisha katika kazi ni miongoni mwa nidhamu ya Kiislamu. Hivyo, kila mwanafunzi
atawajibika kushiriki kikamilifu katika kazi za usafi wa mazingira, huduma za kijamii na kazi
nyinginezo kama atakavyoelekezwa na walimu, walezi au viongozi wa wanafunzi. Kutega
kazi, iwe ya darasani au nje ya darasa ni kukiuka maadili anayotarajiwa awe nayo
mwanfunzi wa shule hii.
8. TEHAMA 30,000/= 30,000/= CASH
9. Qur’an ya tafsiri 15,000/= 15,000/= CASH
Jumla 1,039,000/= 1,158,000/=
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 7 kati ya 21
15.MALEZI
Shule hii ni ya Kiislamu. Kwa hiyo mwenendo wa wanafunzi na walezi unatarajiwa
uzingatie mafundisho ya Qur`an tukufu na Sunnah. Malezi ya shule yanalenga
kumwezesha mwanafunzi kuishi kwa kumuiga Mtume Muhammad (s.a.w).Upo mfumo
mzuri wa malezi ambapo wanafunzi wanapangwa kifamilia na kila familia inakuwa na
kaka au dada na baba au mama mlezi ambaye ni mwalimu. Wanafunzi wanaishi kama
familia kwa kupendana na kuhurumiana.
16.USTAWI WA WANAFUNZI
(i) Huduma za afya
Shule ina wahudumu wa afya na chumba maalum chenye vifaa na dawa kwa ajili ya
kuwahudumia wanafunzi muda wote. Kwa wanafunzi wenye maradhi yanayohitaji
matibabu ya juu na vipimo zaidi, mhudumu wa afya wa shule huwasindikiza kwenda
hospitali ya Mkoa iliyopo Songea Mjini kilometa chache kutoka Mkuzo. Kwa hiyo, watoto
wenye kadi za bima ya Afya wanatakiwa waje nazo ili kurahisisha matibabu nje ya shule
kwani gharama zake hutolewa na mzazi/mlezi na sio shule. Kwa wanafunzi wasio na kadi
ya bima ya Afya (chini ya miaka 18) waje na sh.54,000 ili wafunguliwe Bima ya Afya
(NHIF).
(ii) Chakula na malazi
Chakula cha shule ni kizuri (na cha kutosha-kushiba) kwa kuwa kinapikwa vizuri na bora yaani
mlo kamili ( hasa vitamini,wanga na protini) : matunda,maharage/mboga za majani,nyama
wali,ugali, mkate (skonzi).Kwa mwanafunzi mwenye matatizo ya kutokula vyakula vilivyotajwa
hapo juu, mzazi anashauriwa kutoa taarifa mapema kwa mkuu wa shule kabla mtoto hajaripoti
shule ili kujadiliana naye namna ya kumsaidia.
(iii) Mawasiliano ya wazazi na wanafunzi wakiwa shuleni
Uongozi wa shule unao utaratibu mzuri sana wa wazazi kuwapigia simu watoto wao pale
wanapokuwa na haja hiyo. Ofisi ya malezi ina jukumu la kuratibu mawasiliano ya
wanafunzi na wazazi wao ambapo wanao utaratibu wa wanafunzi kupiga simu kwa
kutumia simu maalumu zilizonunuliwa kwa shughuli hiyo.
Pia wazazi wanapokuwa na shida wanaweza kuwasiliana na uongozi wa shule kwa njia ya
simu muda wowote.
(iv) Siku ya wazazi na walezi kuwatembelea watoto (visiting day) ni Jumapili ya kila
mwisho wa mwezi tu (kwa miezi ya Februari,Machi,Aprili, Agosti,Septemba na Oktoba
tu) kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi kamili jioni).Ikitokea dharura mzazi au mlezi
kutaka kumuona mtoto katika siku tofauti anaweza kufanya hivyo kwa kupata kibali cha
mkuu wa shule au makamo wake.
Kwa miezi ya MACHI na AGOSTI, tutakuwa na kikao cha wazazi na uongozi wa shule
JUMAMOSI ya mwisho ya miezi hiyo. Hivyo, wazazi watatumia siku hizo kusalimiana na
watoto wao baada ya kikao
Tabihi: Kwa wazazi watakaoshindwa kuwatembelea watoto wao, wanaweza kusalimiana nao
kwa njia ya simu za ofisi ya malezi (matron na patron).
Endapo mzazi atapokea taarifa yoyote kutoka namba nyingine tofauti na hizo, au siyo namba ya
mkuu wa shule au makamu wake, asifanye jambo lolote la kimaamuzi bila kuwasiliana na mkuu
wa shule au makamo wake.
17.SAFARI ZA KIMASOMO NA KIMALEZI
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 8 kati ya 21
Tuna utaratibu wa safari za kimasomo na kimalezi kila mwaka/muhula. Mzazi/mlezi
atafahamishwa sehemu ya kwenda kwa muda husika na kiasi cha gharama za safari hiyo.
18.Vitu vifuatavyo haviruhisiwi mwanafunzi kuja navyo au kuvitumia
I. Marashi, Perfume, lotion, Cream na Sabuni za kuchubua ngozi
II. Mapambo ya aina yoyote kama vile pete, hereni, bangili, mikufu, vibanio vya
nywele n.k.
III. Nguo yeyote yenye maandishi au namba.
IV. Rangi za kucha, hina, piko n.k.
V. Redio, simu, CD’s, Camera, Memory Card, Flash, Laini ya simu, Pass na mashine
za kunyolea.
VI. Visu, panga au silaha ya aina yoyote
NB: Jezi wala (baloteli) au track-suit ambayo haijaelekezwa hairuhusiwi. Atakayekamatwa na
vitu hivi atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kunyang’anywa vitu hivyo na
hatarudishiwa.
19.KANUNI NA MWENENDO BORA WA SHULE
i. Kila mwanafunzi wa shule hii anapaswa kutambua kuwa yupo hapa kwa ajili ya Uislamu.
Kwa sababu hiyo mwenendo wake, matendo na maneno yake yanatakiwa yawe ya
Kiislamu.
ii. Kila mwanafunzi ajitahidi kukuza upendo wake kwa Allah(s.w), Mtume wake (s.aw) na
kwa waumini wenzake.
iii. Pamoja na haki za muumba zilizo juu ya kila Muislamu, yamwajibikia kila mwanafunzi
achunge haki za nafsi yake na atumie vipaji vyake katika uchamungu ndani na nje ya
shule.
iv. Kila mwanafunzi atumie muda wake vizuri katika kujielimisha kwa kutafuta radhi za
Allah.
v. Kila mwanafunzi atalazimika kuhudhuria vipindi vya masomo yote, kufanya mazoezi,
majaribio na mitihani yote itakayotolewa shuleni. Mwanafunzi atakayeshindwa
kuhudhuria darasani bila sababu yoyote ya msingi atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
vi. Wakati wote wa shule au wakati wa kwenda na kurudi likizo vazi rasmi ni sare ya shule
(ya darasani).
vii. Wanafunzi wote wanatakiwa wazingatie kanuni na sheria za mavazi ya Kiislamu wakiwa
ndani na nje ya shule. Wasichana wavae nguo za kuenea mwili mzima isipokuwa uso na
vitanga vya mikono rejea (24:31). Nikabu haziruhusiwi shuleni.
viii. Ni marufuku kwa mwanafunzi mvulana au msichana kuvaa mapambo aina yoyote.
ix. Ni marufuku kwa wavulana kuvaa suruali mlegezo au modo
x. Ni marufuku kwa mwanafunzi mvulana au msichana kuvaa nguo za kubana au
zinazoonesha rangi ya ngozi ya mwili (Transparent) akiwa shuleni au nje ya shule
xi. Ni marufuku kwa mwanafunzi yeyote kufuga kucha, kujipaka rangi za kucha, rangi za
midomo, kupaka hina, kunyoa nyusi, kuvaa viatu vya kuchuchumia au vinavyotoa mlio
(sauti), kukali nywele, kutia rangi, kusuka rasta au kubadilisha nywele, kucha au ngozi
kwa namna yeyote ile.
xii. Ni marufuku mwanafunzi kuchochea, kushawishi, kuhamasisha, au kushiriki mgomo kwa
namna moja au nyingine. Ni kosa kubwa kugomea amri au maelekezo ya viongozi wa
shule kwa ujumla
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 9 kati ya 21
xiii. Wanafunzi wasionekane katika vilabu vya pombe, nyumba za kupangisha wageni (guest
house), vibanda vya video au pahala pengine pasiporuhusiwa.
xiv. Kila mwanafunzi ni mlinzi wa mali ya shule, mali binafsi na mali za wenzake. Mwanafunzi
atakayeharibu, kusababisha mali ya shule kuharibika, kuibiwa au kupotea atachukuliwa
hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kulipa. Hivyo mwanafunzi atakapogundua
wizi wa mali ya shule au ya mwanafunzi mwingine atoe taarifa kwa walimu au viongozi
wanaohusika mara moja
xv. Kuiba ni kosa kubwa. Mwanafunzi atakayethibitika kuiba mali ya shule, na wenzake au
nje ya shule atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
xvi. Mwanafunzi anapokuwa na shida yeyote hapa shuleni, kwanza aanze kwa viongozi
wanafunzi na ndipo aende kumuona mwalimu wa zamu au wa darasa lake, au walimu
wengine wanaohusika. Kama wanafunzi baada ya kufuata ngazi hizo shida yake
haijatatuliwa aende kwa makamu Mkuu wa shule,kisha kwa mkuu wa shule, mwanafunzi
asishitakie shida zake nje ya shule kabla hajamuona mkuu wa shule .
xvii. Kila mwanafunzi awe msafi na ashiriki vyema katika usafi wa mwili wakebinafsi; kitanda,
nguo, nywele, kucha, na usafi wa madarasa, bweni bwalo la chakula na mazingira ya
shule kwa jumla.
xviii. Kelele za aina yoyote hazirusiwi, iwe darasani, kwenye baraza za madarasa, ndani ya
bweni, au popote iwe kwa mwanfunzi mmoja au wengi (kundi).Tunalazimika kuonesha
maadili ya Kiislamu katika mazungumzo yetu yote (Rejea Qur`an 31:19)
xix. Hairusiwi mwanafunzi kutoka na kulala nje ya shule bila ya kibali malum cha maandishi
kilichoidhinishwa na mkuu wa shule.
xx. Ni kosa KUBWA Mwanfunzi kulala au kwenda katika nyumba za watumishi isipokuwa
kwa kibali maalum.
xxi. Michanganyiko ya wavulana na wasichana hairusiwi. Pale itakapokuwa lazima wanfunzi
kusoma katika chumba kimoja lazima pawe na mwalimu. Kupigana ni kosa kubwa.
Mwanafunzi atakayepigana au kumpiga mwenzake atachukuliwa hatua kali za
kinidhamu.
xxii. Mwanafunzi anapaswa kuripoti shuleni kutoka likizo katika tarehe na muda uliopangwa.
Ikitokea kuchelewa kwa dharura, mzazi apige simu kwa mkuu wa shule au makamo wa
mkuu wa shule kueleza dharura hiyo.
xxiii. Wakati wa kuwatembelea wanafunzi, mzazi /mlezi haruhusiwi kuleta vyakula au vinywaji
vya kutengeneza nyumbani. Hii ni kwa sababu shule ni jumuiya ya watu wengi na
vyakula vinavyotengenezwa nyumbani vinatofautiana kwani kila mtu ana namna yake ya
upishi ndio maana tunachukua tahadhari hiyo. Aidha Mzazi anaweza kumletea mtoto
wake bidhaa za viwandani ziwe SILDI (HAZIJAFUNGULIWA) zenye TBS na matunda tu.
Vyakula au vifaa vitakavyoletwa ni lazima vithibitishwe na mwalimu mwenye jukumu
hilo kabla ya kukabidhiwa kwa mwanafunzi husika. Ni vyema kufahamu kwamba
tahadhari hii imetolewa na wataalamu wa afya wa serikali.
xxiv. Wanafunzi hawaruhusiwi kufanya biashara ya aina yoyote wakiwa shuleni. Kwa hiyo ni
marufuku mwanafunzi kuuza vifaa vyake au kununua vifaa vya mwenzake kwa muda
wote atakapo kuwa shuleni hata ikiwa amemaliza masomo yake. Mwanafunzi
anaruhusiwa kutoa sadaka kumpa mwenzake vifa kama anayo ziada.
xxv. Zaidi ya mashine ya kufanyia hesabu (calculator) na saa za mkononi, vifaa vya electronics
kama vile simu, camera, radio cassette, compyuta, Tv, hita, n.k havirusiwi mwanafunzi
kuwa navyo katika mazingira ya shule. Mwanafunzi atakaekutwa navyo vitu hivyo hapa
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 10 kati ya 21
shuleni, atachukuliwa hatua kali za kinidhamu, pamoja na kunyang’anywa vyote na
hatarudishiwa.Kwa mzazi mwenye compyuta anaruhusiwa kuitoa sadaka kwa shule ili
zitumike kwa wanafunzi wote, mtoto wake akiwepo.
xxvi. Mwanafunzi haruhusiwi kununua au kuagiza chakula kutoka nje ya shule.
xxvii. Kila mwanafunzi ana haki ya kumhoji mtu asiyemfahamu ambae yupo katika mazingira ya
bweni au mazingira ya shule.
20. MAKOSA YATAKAYOPELEKEA MWANAFUNZI KUFUKUZWA SHULE NI:-
Makosa makubwa ni yale yenye kukiuka maadili ya Uislamu, kufanya makosa ya jinai,
kusababisha kuvuruga amani na usalama wa jumuia ya shule, kuharibu mali ya Umma kwa
makusudi. Baadhi ya makosa hayo ni haya yafuatayo:
i. Kunywa pombe na kula au kunywa vitu haramu
ii. Kwenda nyumba za starehe kama vile kumbi za madansi disko n.k
iii. Uzinzi, kulawiti, usagaji au kukaribia zinaa kwa kuwa na rafiki wa jinsia tofauti (Boy
friend/ girlfriend)
iv. Kuvuta bangi, madawa ya kulevya, n.k
v. Kutosimamisha swala
vi. Kumiliki au kutunza vitu vya electronics kama simu au line ya simu, redio kamera,
compyuta, Cd, dvd, Tv, flash, n.k
vii. Utoro: Kukaa nje ya shule kwa muda wa siku 3 mfululizo bila kibali maalum
kilichoainishwa na mkuu wa shule
viii. Kueneza fitina, kuanzisha/kuchochea mgomo/vurugu kupigana au kuchochea watu wapigane.
ix. Kutoroka /kutofanya mitihani/jaribio bila ya sababu za msingi
x. Kutohudhuria vipindi darasani kwa zaidi ya siku tatu mfululizo bila sababu maalumu
za msingi.
xi. Migomo ya aina yoyote.
21. HITIMISHO
Ni matarajio yetu kuwa umesoma na kuelewa maelekezo yote ya shule. Uongozi wa shule
utaendelea kukumbusha kanuni za shule mara kwa mara.Hatutarajii mwanafunzi kukiuka
au kuvunja kanuni hizi kwani kuzikIuka kwa makusudi kutakupelekea kuchukuliwa hatua
za kinidhamu.
Nakutakia maisha ya furaha na amani kwa muda wote utakapokuwa hapa MKUZO ISLAMIC
SECONDARY SCHOOL KWA TAALUMA NA MALEZI BORA.
Kauli mbiu yetu ni``Soma Kwa Jina La Mola Wako Aliyeumba``
Wabillah Tawfiiq
Sombi JR
MKUU WA SHULE
“Best performance is our focuss”
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 11 kati ya 21
ORODHA YA VITABU VYA KIADA VILIVYOANDIKWA NA TAASISI YA ELIMU TANZANIA
(TET) VINAVYOPATIKANA MADUKANI MPAKA SASA NA BEI ZAKE
NO. JINA LA KITABU BEI YA KITABU
1. In organic chemistry Form five and six 15,500/=
2. Organic Cheistry form five and six 17,500/=
3. Physical chemistry form five and six 17,500/=
4. General chemistry form five and six 15,500/=
5. Biology form five 17,000/=
6. Biology form six 17,000/=
7. Basic Aplied Mathematics form five and six 20,000/=
8. Kiswahili kidato cha tano na sita (sarufi na lugha) 15,000/=
9. Kiswahili kidato cha tano na sita(fasihi) 15,000/=
10. Physics for Secondary school form five 17,000/=
11. Physics for Secondary school form six 17,000/=
TANBIHI: Vitabu hivi vinapatikana shuleni mtoto aje na pesa atalipa kwa mhasibu na kupatiwa vitabu
kwa mujibu wa tahasusi (combination yake) .
bei hizi zinaweza kubadilka.
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 12 kati ya 21
Kiambatanisho D
UTHIBITISHO WA KUKUBALI NAFASI
Shukrani zote anastahiki Allah (sw) na Rehema na Amani zimuendee Mtume Muhammad (s.a.w)
na wafuasi wake wote pamoja na wale wanaopigana katika njia ya Allah (sw).
Mimi Mzazi/Mlezi wa …………………………………………………………………………..…….
Kwanza nachukua fursa hii kushukuru kwa mtoto wangu kupata nafasi ya kujiunga na shule ya
sekondari ya mkuzo Islamic secondary school.
Nachukua fursa hii kwa niaba ya mwanafunzi mtarajiwa kuthibitisha kukubali nafasi hii baada ya
kupokea taarifa za kuchaguliwa mwanangu kujiunga na shule hii.
Ninaahidi kutekeleza wajibu wangu wa kulipa ada ya shule kabla ya tarehe ya mwisho ya kuthibitisha
kukubali nafasi hii.
Jina la Mzazi/Mlezi……………………………………….sahihi………………………Tarehe………………………….
Fomu hii ijazwe na irudishwe moja kwa moja shuleni .
Wabillah Tawfiiq
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 13 kati ya 21
Kiambatanisho C
WAJIBU WA MZAZI / MLEZI
Mzazi au mlezi ana wajibu wa kutimiza mambo yafuatayo:
1. Kulipa Ada ya shule kwa wakati
2. Kufuatilia maendeleo ya kila siku ya mtoto wake. Kwa hiyo mzazi au mlezi anatakiwa ashirikiane na
walimu kwa kuhudhuria siku ya wazazi kutembelea shule.
3. Mzazi / Mlezi ana wajibu wa kumnunulia mtoto wake vifaa / vitabu vyote na vitini anavyohitaji.
4. Mzazi / Mlezi anatakiwa atoe taarifa pindi mtoto wake anapokuwa na dharura
ya kumzuia kufika shule kwa wakati uliopangwa. Dharura zinazokubalika ni ugonjwa , kifo cha mtu
wa
karibu kama baba, mama n.k. Ada isiwe kigezo cha mtoto kuchelewa shule.
5. Mzazi / Mlezi ana wajibu wa kuhakikisha mwanae ana sare kamili za shule kama ilivyoelekezwa
katika
Maelekezo ya Kujiunga (Joining Instructions)
Nimesoma kwa makini na naahidi kutimiza wajibu wangu kwa kadiri ya uwezo wangu
Insha Allah.
Jina kamili la Mzazi/Mlezi……………………………………………..Sahihi……………………… Tarehe…………………
NB: Nakala moja Mzazi / Mlezi nakala nyingine irudishwe shuleni ikiwa imesainiwa.
Wabillah Tawfiiq
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 14 kati ya 21
WAJIBU WA MZAZI / MLEZI
Mzazi au Mlezi ana wajibu wa kutimiza mambo yafuatayo:
1. Kulipa Ada ya shule kwa wakati
2. Kufuatilia maendeleo ya kila siku ya mtoto wake. Kwa hiyo mzazi au mlezi anatakiwa ashirikiane na
walimu kwa kuhudhuria siku ya wazazi kutembelea shule.
3. Mzazi / Mlezi ana wajibu wa kumnunulia mtoto wake vifaa / vitabu vyote na vitini anavyohitaji.
4. Mzazi / Mlezi anatakiwa atoe taarifa pindi mtoto wake anapokuwa na dharura
ya kumzuia kufika shule kwa wakati uliopangwa. Dharura zinazokubalika ni ugonjwa , kifo cha mtu
wa
karibu kama Baba, Mama n.k. Ada isiwe kigezo cha mtoto kuchelewa shule.
5. Mzazi / Mlezi ana wajibu wa kuhakikisha mwanae ana sare kamili za shule kama ilivyoelekezwa katika
Maelekezo ya Kujiunga (Joining Instruction
Nimesoma kwa makini na naahidi kutimiza wajibu wangu kwa kadiri ya uwezo wangu
Insha Allah.
Jina kamili la Mzazi / Mlezi……………………………………………..Sahihi………………………
Tarehe……………………………
NB: Nakala moja Mzazi / Mlezi nakala nyingine irudishwe shuleni ikiwa imesainiwa.
Wabillah Tawfiiq
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 15 kati ya 21
Kiambatanisho A
UTAMBULISHO WA MWANAFUNZI
1. Jina kamili…………………………………………………………………
Tarehe ya kuzaliwa………………………umri……………………
Mkoa……………………………Kijiji/Mtaa……………………… Nyumba na:…………
2 Jina kamili la Baba………………………………………………
Kazi yake …………………………………………………………………
Anwani S.L.P………………………………………………
Simu ya nyumbani……………………………Simu ya Kazini………………………………
Kiwango chake cha Elimu…………………………………………………………………………
Mahali anapofanyia kazi……………………………………………………………………………
3. Jina kamili la Mama mzazi………………………………………………………………….……
Kazi yake ……………………………………………………………………….…………………………
Kiwango chake cha Elimu…………………………………………………………………………
Mahali anapofanyia kazi……………………………………………………………………………
4. Je, Wazazi wako wamezaliwa waislam au wamesilimu ukubwani ?
5. Je, umewahi kuhudhuria madrasa (chuo)? [Ndiyo/Hapana (kata
isiyohusika)]
Kama ndiyo kwa ujumla chuoni ulijifunza nini? ( Eleza kwa ufupi)
……………………………………………………………………………………………………………………
6. Je, kwa sasa unaishi na wazazi wako au unaishi na mlezi?
…………………………………………………………Kama unaishi na
Picha ya hivi
karibuni
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 16 kati ya 21
mlezi wazazi wako wapi?…………………………………………………………….……………Uhusiano na
mlezi…………………….(kaka,shangazi,n.k)
7. Jina kamili la Mlezi……………………………………………………………………………………
Anwani yake ni P.O. Box……………………………………………………………………….…
Simu yake ya nyumbani………………………….…Simu ya kazini……………………
UTHIBITISHO:
Nina/tunathibitisha kwa Jina la Allah (s.w) kuwa taarifa zilizotolewa hapa ni sahihi na za
kweli.
Sahihi ya Mwanafunzi……………………………………… Tarehe…………………………………
Sahihi ya Mzazi/ Mlezi……………………………………… Tarehe…………………………….……
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 17 kati ya 21
Kiambatanisho B
UTAMBULISHO WA WAZAZI / WALEZI WA MWANAFUNZI
Ili kuwa na uhakika ya wazazi (Baba na Mama) na walezi tutakaoshirikiana nao , tunaomba
wazazi / walezi wajitambulishe kama ifuatavyo:
WAZAZI WAWILI
Jina kamili………………………………………… Jina kamili……………………….………………
Anuani ……………………………………………… Anuani ……………………………………………
Simu namba …………………………………… Simu namba ……………………………………
Sahihi…………………………………………… Sahihi……………………………………………..
1 2
WALEZI
Jina kamili……………………………………….. Jina kamili………………………………………
Anuani…………………………………………….. Anuani……………………………………………
Simu namba …………………………………… Simu namba ………………………………….
Sahihi……………………………………………… Sahihi……………………………………………
MAMA BABA
Picha ya hivi
karibuni
Picha ya hivi
karibuni
Picha ya hivi
karibuni
Picha ya hivi
karibuni
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 18 kati ya 21
MUHIMU
1. Ni Wazazi / walezi hawa tu wenye picha na sahihi zao ndio
tutakaowasiliana nao kwa ajili ya maendeleo ya mwanafunzi.
2. Yeyote atakayetumwa kwa niaba ya wazazi / walezi wa mwanafunzi
waliotambulishwa kwa shule aje na barua yenye sahihi ya mmoja wao.
3. Jambo hili la wazazi / walezi kujitambulisha kwa shule ni muhimu sana kwani baadhi
ya wanafunzi watundu wakati mwingine huleta wazazi / walezi wa bandia.
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 19 kati ya 21
MEDICAL REPORT FORM
Admission to Mkuzo Islamic secondary School is condition upon receipt of a satisfactory
medical report. Report should be sent to:
HEAD MASTER
MKUZO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL
P.O.BOX 346
SONGEA
STUDENT’S SURNAME-----------------------------
OTHER NAMES ----------------------
SEX-------------
AGE------------
Has the examinee suffered from any of the following? If yes indicate date and Diagnosis. If NO
please write in appropriate space.
1. Tuberculosis------------
2. Pneumonia--------------
3. Pleurisy------------------
4. Asthma------------------
5. Rheumatic fever-------
6. Allergic disorder-------
7. Heart disease----------
8. Gastric or duodenal ulcer----
9. Recurrent indigestion----------
10. Jaundice-------------------------
11. Varicose Veins------------------
12. Kidney or Urinary disease-----
13. Rapture spleen-----------------
14. Diabetes------------------------
15. Epilepsy-------------------------
16. Poliomyelitis or other Neurological
disorder-----------
17. Nervous breakdown--------------
18. Psychiatric disorder---------------
19. Eye disorder-----------------------
20. Ear, Nose, or Throat disorder---
21. Skin disease------------------------
22. Anaemia-----------------------------
23. Gynacological disorder------------
24. Malaria or other Tropical disease-----
------------------------
25. Cholera-----------------------------
26. Operations-------------------------
27. Serious accident-------------------
28. Any other serious disorder------
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 20 kati ya 21
PHYSICAL EXAMINATION
1 Height-----------------------
2. weight-----------------------
3. Skin disease-----------------
4. Eye conjunctivae ----------
Sight without glasses-----
With glasses----------------
5. Please state condition of ears(if any
discharge)----------------
mouth and throat------- nose-------
Any clinical evidence of hyperacidity
or gastric-deodenal ulcer?
6. Respiratory System:
Any Abnormality ------------
7. Cardiovascular System;
Blood pressure--------------
Heart: Any murmer?----------
Arteries and Veins-----------
8. Abdomen:Hernia ------------Masses----
Kidneys---------- Hectal---------
Hydrocele-------- Masses--------
LABORATORY
1. Urine albumen---------------------
Sugar-------------------------------
(special emphasis on hookworms
and bilharzias)
Leucocytes----------------------
Bilharzia-------------------------
2.Stools------------------------------
3. Blood examination:
(a) Neutrophils--------------------------------
(b) Eosinophils-------------------------------
(c) Basophils------------------------------------
(d) Lymphocytes-----------------------------
(e) Monocytes--------------------------------
(f) X-Examination-----------------------------
(g) Blood group ---------------------------------
(h) HIV/AID’S------------------------------------
Maelekezo ya kujiunga kidato cha tano Julai 2020
Ukurasa wa 21 kati ya 21
CONCLUSION
I have examined Br/ Sr ------------------------------------- and consider that he /she is/ not physically and
mentally fit to be admitted to Mkuzo Islamic Secondary School.
Name---------------------------
Signature--------------------- Date ----------------------------
Title---------------------------
Qualification------------------
Address------------------------
Phone No.-------------------------
Official stamp
(GOVT HOSPITAL)