16
Sau za Wananchi Julai, 2018 Kuwapasha viongozi? 1. Utangulizi Serikali ya awamu ya tano, chini ya uongozi wa Rais Dr. John J.P Magufuli, ilianza kwa kishindo. Punde tu baada ya Rais mpya kuapishwa Novemba 2015, hatua madhubu zilizochukuliwa kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma ziliungwa mkono na kupongezwa ndani na nje ya nchi. Utafi wa Sau za Wananchi mwaka 2016 ulionesha kiwango cha juu sana cha kukubalika kwa utendaji wa Rais (96%). 1 Mapema Januari 2016, hofu ilianza kujitokeza kutokana na uamuzi wa serikali wa kusisha matangazo ya moja kwa moja (mubashara) ya vipindi vya bunge. 2 Japokuwa utendaji wa Rais umeendelea kupongezwa na kuungwa mkono na watendaji mbalimbali, umekuwa ukikosolewa mara kwa mara, hususani kwenye maeneo makuu mawili. Kwanza, wakosoaji wameonesha kukiukwa kwa misingi ya kidemokrasia na kutoheshimiwa kwa haki za raia. Vikwazo vipya vimewekwa kwenye sheria, utendaji na uhuru wa kisiasa wa vyama vya upinzani, vyombo vya habari, vyama vya kiraia na hata wananchi. Hii ikihusisha katazo la mikutano na mikusanyiko ya kisiasa kwa wanachama na viongozi nje ya majimbo yao; kukamatwa kwa wanasiasa kadhaa wa vyama vya upinzani kwa kosa la uchochezi na makosa mengine; kuzuiwa na kufungiwa magaze binafsi kadhaa; na udhibi wa masuala ya kisiasa ikiwemo uhuru wa maoni. Wadau mbalimbali wanaonekana kutokuafiki msimamo wa serikali kuwa uhuru wa maoni na mikutano ya kisiasa inachelewesha maendeleo. Maoni ya wananchi kuhusu siasa nchini 1 Rais wa Watu? hp://twaweza.org/go/sau-government-performance-2016 2 hp://www.thecizen.co.tz/News/Chaos-rocks-Bunge-as-govt-cuts-live-coverage/1840340- 3052474-kdep4a/index.html Muhtasari huu umeandikwa na umeandaliwa na Twaweza East Africa. S.L.P 38342, Dar es Salaam, Tanzania. +255 22 266 4301 | [email protected] | www.twaweza. org/sau Muhtasari Na. 48

Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

  • Upload
    others

  • View
    2

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

Sauti za Wananchi Julai, 2018

Kuwapasha viongozi?

1. UtanguliziSerikali ya awamu ya tano, chini ya uongozi wa Rais Dr. John J.P Magufuli, ilianza kwa kishindo. Punde tu baada ya Rais mpya kuapishwa Novemba 2015, hatua madhubuti zilizochukuliwa kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma ziliungwa mkono na kupongezwa ndani na nje ya nchi. Utafiti wa Sauti za Wananchi mwaka 2016 ulionesha kiwango cha juu sana cha kukubalika kwa utendaji wa Rais (96%).1

Mapema Januari 2016, hofu ilianza kujitokeza kutokana na uamuzi wa serikali wa kusitisha matangazo ya moja kwa moja (mubashara) ya vipindi vya bunge.2 Japokuwa utendaji wa Rais umeendelea kupongezwa na kuungwa mkono na watendaji mbalimbali, umekuwa ukikosolewa mara kwa mara, hususani kwenye maeneo makuu mawili.

Kwanza, wakosoaji wameonesha kukiukwa kwa misingi ya kidemokrasia na kutoheshimiwa kwa haki za raia. Vikwazo vipya vimewekwa kwenye sheria, utendaji na uhuru wa kisiasa wa vyama vya upinzani, vyombo vya habari, vyama vya kiraia na hata wananchi. Hii ikihusisha katazo la mikutano na mikusanyiko ya kisiasa kwa wanachama na viongozi nje ya majimbo yao; kukamatwa kwa wanasiasa kadhaa wa vyama vya upinzani kwa kosa la uchochezi na makosa mengine; kuzuiwa na kufungiwa magazeti binafsi kadhaa; na udhibiti wa masuala ya kisiasa ikiwemo uhuru wa maoni. Wadau mbalimbali wanaonekana kutokuafiki msimamo wa serikali kuwa uhuru wa maoni na mikutano ya kisiasa inachelewesha maendeleo.

Maoni ya wananchi kuhusu siasa nchini

1 Rais wa Watu? http://twaweza.org/go/sauti-government-performance-2016 2 http://www.thecitizen.co.tz/News/Chaos-rocks-Bunge-as-govt-cuts-live-coverage/1840340-

3052474-kdep4a/index.html

Muhtasari huu umeandikwa na umeandaliwa na Twaweza East Africa.

S.L.P 38342, Dar es Salaam, Tanzania. +255 22 266 4301 | [email protected] | www.twaweza.org/sauti

Muhtasari Na. 48

Page 2: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

2

Pili, maoni ya baadhi ya Watanzania yanaonesha dalili za kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi nchini. Ingawa wasiwasi kuhusu upatikanaji wa chakula mwishoni mwa 2016 na mwanzoni mwa 2017 umepungua, wasiwasi kuhusu uchumi kwa ujumla umeongezeka. Kwa kiasi fulani, hali hii inasemekana imesababishwa na kushuka kwa uagizaji na uuzaji wa bidhaa ndani na nje ya nchi na kuminywa mikopo kwa sekta binafsi.3 Vilevile kutokana na kusemekana kwamba masharti ya kufanya biashara yamekuwa magumu: idadi ya wananchi waliotaja umasikini au masuala ya kiuchumi kama changamoto kuu nchini imeongozeka kutoka 34% 2015 hadi 72% mwaka 2018.4

Muhtasari huu umebeba takwimu kuhusu maoni ya wananchi katika masuala ya kisiasa nchini. Wananchi wanaelewa nini kuhusu demokrasia, katiba na uchochezi? Je, wanaona mabadiliko yoyote kwenye uhuru wa kujumuika na uhuru wa maoni katika miaka michache iliyopita? Wananchi wanasema nini ni kazi ya vyama vya upinzani, na ni kwa kiasi gani wanaunga mkono udhibiti wa mamlaka ya Rais? Ni vyama gani vya siasa wananchi wanasema wapo karibu navyo? Na je, wanapima vipi utendaji wa wawakilishi wao waliowachaguwa, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Takwimu za muhtasari huu zinatoka Sauti za Wananchi. Sauti za Wananchi ni utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi. Una uwakilishi wa Tanzania Bara pekee (Zanzibar haihusiki kwenye utafiti huu). Taarifa kuhusu mbinu za utafiti huu zinapatikana kupitia www.twaweza.org/sauti. Takwimu za muhtasari huu zilikusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,241 kutoka awamu ya 27 ya kundi la pili la Sauti za Wananchi, zilizokusanywa kati ya tarehe 15 na 24 Aprili 2018.

Matokeo muhimu ni: • Walipokuwa wakieleza maana ya demokrasia wananchi walisema uhuru wao ni

muhimu zaidi kuliko chaguzi • Wananchi wanasema uhuru umepungua nchini mwaka 2018 kuliko ilivyokuwa miaka

mitatu iliyopita. • Uungaji mkono wa haki za vyama vya upinzani umeongezeka tangu 2016. • Wananchi wengi wanasema Rais anapaswa kuwajibishwa na Bunge na kuheshimu

sheria na mahakama. • Wananchi wengi wanavifahamu vyama vikuu vitatu nchini yaani Chama cha Mapinduzi

(CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF)

• Wananchi wengi wangewachagua wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kama uchaguzi ungefanyika wakati wa mahojiano.

• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka• Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea kushuka. • Asilimia 55 ya wananchi wanaunga mkono utendaji wa Rais Magufuli. • Uungaji mkono wa CCM na utendaji wa Rais umeshuka sana maeneo ya vijijini.

3 https://www.ippmedia.com/en/news/mps-arms-over-steep-decline-exports-figures 4 Sauti za Wananchi, kundi la 2: Awamu ya 1 (Aug-Sept 2015), Awamu ya 18 (Aprili 2017) na Awamu

ya 26 (Jan 2018), chapisho kuzinduliwa hivi karibuni, linapatikana kwa anayehitaji

Page 3: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

3

2. Mambo tisa muhimu kuhusu maoni ya wananchi katika siasa nchini Jambo la 1: Wananchi wengi wanaeleza maana ya demokrasia kuwa ni uhuru na si chaguzi Karibu nusu ya watanzania (47%) wanaeleza maana ya demokrasia kwa kuihusisha na uhuru wao kama vile uhuru wa maoni na kujumuika, mara mbili zaidi ya wale wanaosema demokrasia ni chaguzi (21%). Wananchi wanne kati ya kumi (37%) wamesikia dhana hiyo lakini hawaelewi inamaanisha nini.

Asilimia 45 ya wananchi wanalielewa neno katiba kumaanisha kanuni zinazotumika kuongoza nchi au tamko la kisheria linalotumika kuongoza nchi (30%). Wananchi watatu kati ya kumi (30%) hawana uhakika na uelewa wao wa dhana hiyo.

Kielelezo cha 1: Unaelewa nini kuhusu maneno “demokrasia”, “katiba” na “uchochezi”?5

47%21%

5%4%

45%30%

3%

28%15%

11%11%

5%3%2%

38%

30%

4%

Uhuru (mf. wa kuzungumza, kukusanyika, n.k.)Chaguzi huru kuchagua viongozi

Haki za kiraia kuwalinda watu na unyanyasaji wa serikali Serikali ina�i sheria

Sijawahi kusikia neno hilo / sijui

Kanuni zinazotumika kuongoza nchiAndiko la kisheria linalotumika kuongoza nchi

Andiko la haki za binadamu

Sijawahi kusikia neno hilo / sijui

Umbea/kusengenya kwa lengo bayaKusababisha vurugu/mtafaruku/ugomvi

KudanganyaKusababisha watu wagombane

Kitendo chochote kinachovuruga amaniWatu kudanganya ili kuleta migogoro

Kuunda vikundi na kuzungumza mabaya ili kusababisha vuruguSijawahi kusikia neno hilo / sijui

"Dem

okra

sia"

"Ka�

ba"

"Uch

oche

zi"

Chanzo cha Takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi, Awamu ya 27 (Aprili 2018) Msingi: wahojiwa wote (1,241) (jibu zaidi ya moja linaruhusiwa)

5 Jumla ya asilimia zote zinaweza zisifike 100% kutokana na makadirio

Page 4: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

4

Linapokuja suala la neno uchochezi wananchi wametoa majibu mbalimbali, japokuwa yote yakizunguka kwenye wazo la jitihada za makusudi za kusababisha uvunjifu wa amani au vurugu. Majibu haya yanaendana kwa karibu na maana ya uchochezi kutoka kwenye kamusi: maneno au vitendo vyenye lengo la kuhamasisha vurugu ama kutoelewana.6

Jambo la 2: Wananchi wanasema uhuru wao umepungua ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita Kutoka kwenye aina mbalimbali za uhuru, wananchi wanasema uhuru wao binafsi umepungua ndani ya miaka mitatu iliyopita. Kupungua huko kunaonekana kwenye taasisi binafsi: wananchi sita kati ya kumi wanasema uhuru wa vyama vya upinzani (64%), vyombo vya habari (62%) na asasi za kiraia (58%) umepungua. Wananchi wanasema pia uhuru wao binafsi umepungua, ikiwemo uhuru wa maoni kuhusu masuala ya kisiasa (54%), kuunda vikundi au mashirika (47%) na kujiunga kwenye mashirika ya kisiasa (37%).

Kielelezo cha 2: Ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita, unadhani uhuru umeongezeka au umepungua kwenye maeneo yafuatayo?

12%

13%

12%

18%

16%

18%

24%

25%

30%

28%

38%

45%

64%

62%

58%

54%

47%

37%

Uhuru wa vyama vya upinzani/wagombeakufanya mikutano/kutoa maoni yao

Uhuru wa vyombo vya habari kuripo� makosa yaserikali au kuikosoa serikali

Uhuru wa makundi huru kuzungumza, kufanyamikutano au kutoa maoni yao

Uhuru wako wa kuzungumza utakacho kuhusumasuala ya siasa

Uhuru wa watanzania kuunda vikundi vyao aumashirika kwa sababu yoyote ile

Uhuru wako wa kujiunga na shirika lolote la

Umeongezeka Umebaki pale pale/sijui Umepungua

kisiasa unalotaka

Chanzo cha Takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi, Awamu ya 27 (Aprili 2018) Msingi: wahojiwa wote (1,241)

Jambo la 3: Uungaji mkono wa haki za vyama vya upinzani umeongezeka tangu 2016 Wananchi wanne kati ya kumi (37%) wanasema vyama vya upinzani vinapaswa kuikosoa na kuifuatilia serikali baada ya chaguzi ili kuiwajibisha, ongezeko la kutoka wananchi wawili kati ya kumi (20%) waliosema hivyo mwaka 2016. Idadi kubwa ya wananchi (63%) bado wanaunga mkono kauli ya kuwa vyama vya upinzani vikubali kushindwa na kuunga mkono jitihada za serikali za kuieletea nchi maendeleo baada ya chaguzi. 6 https://sw.oxforddictionaries.com/ufafanuzi/uchochezi

Page 5: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

5

Vilevile, uungaji mkono wa haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano imeongezeka, kutoka wananchi watano kati ya kumi (51%) mwaka 2016, mpaka wananchi sita kati ya kumi (64%) mwaka 2018. Mtazamo mbadala wa kwamba mikutano ya vyama vya upinzani baada ya kipindi cha kampeni inaondoa umakini wa serikali – umeshuka katika kipindi hicho hicho.

Uungaji mkono wa demokrasia ya vyama vingi umeendelea kuwa imara, kwa kiasi kikubwa haujabadilika tangu 2016. Wananchi watano kati ya sita (84%) wanaunga mkono kauli ya kwamba vyama vingi vya siasa vinahitajika, wakati mwananchi mmoja kati ya sita (16%) ambaye anasema kuwa vyama vya siasa vinaleta mgawanyiko na mkanganyiko.

Kielelezo cha 3: Miongoni mwa kila kundi la kauli, ipi unayokubaliana nayo zaidi?

20%

51%

86%

80%

49%

14%

37%

64%

84%

63%

36%

16%

2016

2018

2016

2018

2016

2018

Baada ya kushindwa uchaguzi, vyama vya upinzani viifua�lie na kukosoa serikali ili kuiwajibisha

Vyama vingi vya siasa vinahitajika kuhakikisha watanzania wanachagua nani wa kuwaongoza

Mara baada ya chaguzi kwisha, upinzani ukubali kushindwa na kuisaidia

serikali kujenga nchi

Vyama vya siasa huleta makundi na mkanganyiko hivyo siyo lazima kuwa na

vyama vingi vya siasa nchini Tanzania

Pale vyama vya upinzani vinapofanya mikutano baada ya chaguzi, huiweka serikali kwenye mstari, husaidia kuleta maendeleo

Mikutano ya vyama vya upinzani baada ya kipindi cha uchaguzi huondoa

umakini wa serikali kwa wananchi, hurudisha nyuma maendeleo

Chanzo cha Takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi, Awamu ya 27 (Aprili 2018) na Awamu ya 11 (Agosti 2016)

Msingi: wahojiwa wote (1,241 Awamu ya 27; 1,602 Awamu ya 11)

Jambo la 4: Wananchi wengi wanataka serikali ya Rais Magufuli iwajibike Wananchi sita kati ya kumi (59%) wanasema Bunge limwajibishe Rais kwa matumizi ya fedha za umma, wananchi waliobakia (41%) walisema Rais anapaswa kuwa na uwezo wa kufanya shughuli za maendeleo bila kulazimika kuyaeleza matendo yake.

Idadi kubwa ya wananchi (78%) wanasema ni lazima wakati wote Rais aheshimu sheria na mahakama. Wananchi wawili kati ya kumi (22%) waunga mkono mtazamo mbadala wa kuwa Rais alichaguliwa kuongoza nchi na hivyo anapaswa asibanwe na sheria au maamuzi ya mahakama asiyokubaliana nayo.

Page 6: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

6

Kielelezo cha 4: Miongoni mwa kila kundi la kauli, ipi unayokubaliana nayo zaidi?

59%

78%

41%

22%

Bunge lihakikishe kuwa Rais anatoa taarifa mara kwa mara ya namna serikali yake inavyotumia fedha za umma

Rais anapaswa kuheshimu sheria na mahakama, hata kama anadhani hazipo sahihi

Kwa kuwa Rais alichaguliwa kuongoza nchi, asibanwe na sheria au maamuzi ya mahakamaa ambayo anaona siyo sahihi

Rais awe na uwezo wa kujikita kujenga nchi badala ya kupoteza muda

kuelezea kazi anazozifanya

Chanzo cha Takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi, Awamu ya 27 (Aprili 2018) Msingi: wahojiwa wote (1,241)

Tafiti za Afrobarometer (2014 na 2017) 7

Jambo la 5: Wananchi wengi hawavijui vyama vidogo vya siasa Karibu wananchi wote wanafahamu vyama vikuu vitatu vya siasa nchini ambavyo ni CCM (100%), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) (97%) na Chama cha Wananchi (CUF) (83%). Umaarufu wa vyama vingine miongoni mwa wananchi ni mdogo sana. Miongoni mwa vyama vingine, National Convention for Construction and Reform (NCCR Mageuzi) (54%) kinajulikana zaidi, kikifuatiwa na Tanzania Labour Party (TLP) (41%) na ACT-Wazalendo (32%).

Jamii kwa ujumla inavifahamu vyama vikubwa vya siasa. Kwa upande wa vyama vidogo vinafahamika zaidi miongoni mwa wanaume, vijana, wananchi wenye uwezo wa kifedha na wakazi wa maeneo ya mijini.

7 Angalia Afrobarometer.org

Page 7: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

7

Kielelezo cha 5: Vyama gani vya siasa unavifahamu?

100%

99%100%

99%100%

100%99%

100%99%

100%100%100%99%99%

97%

95%99%

97%97%

97%98%95%96%

99%96%96%98%95%

83%

81%85%

81%86%

85%81%79%84%

86%83%81%84%

80%

54%

47%60%

53%55%

51%55%52%58%

62%53%

47%58%

49%

41%

31%51%

40%43%

42%41%39%42%

48%46%

39%34%35%

32%

24%40%

29%37%

36%34%29%23%

40%39%

30%25%24%

wote

umri 18-2930-3940-49

50+

matajiri sanamatajiri

maisha ya ka�masikini

masikini sana

CCM CHADEMA CUF NCCR TLP ACT

wanawakewanaume

vijijinimijini

Chanzo cha Takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi, Awamu ya 27 (Aprili 2018) Msingi: wahojiwa wote (1,241)

Jambo la 6: Kama uchaguzi ungefanyika wakati wa mahojiano wananchi wengi wangewachagua wagombea wa CCM Kama uchaguzi ungefanyika wakati wa mahojiano wananchi wengi wangewachagua wagombea wa CCM katika nafasi za udiwani (51%), ubunge (51%) na urais (55%). Wagombea wanaowakilisha CHADEMA wangeungwa mkono na mwananchi mmoja kati ya sita (15-18%), na vyama vidogo vingeungwa mkono na idadi ndogo ya wananchi.

Hata hivyo inaonekana kuwa wananchi watatu kati ya kumi (29%-30%) hawana uhakika wa nani wangempigia kura.

Page 8: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

8

Kielelezo cha 6: Kama uchaguzi ungefanyika wakati wa mahojiano, mgombea wa chama gani ungempigia kura, kwenye kila nafasi zifuatazo?

51% 51%55%

16% 18% 15%

1% 1% 0%1% 1% 1%1% 1% 1%

30% 30% 29%

CCM CHADEMA CUF ACT Kingine Hakuna/sijui/kukataa kujibuDiwani Mbunge Rais

Chanzo cha Takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi, Awamu ya 27 (Aprili 2018) Msingi: wahojiwa wote (1,241)

Jambo la 7: Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa inaongezeka Mwananchi mmoja kati ya wanne (24%) hayuko karibu na chama chochote cha siasa. Idadi hii imeongezeka mara mbili ya ilivyokuwa 2014 (12%) Idadi ya wananchi wanaosema wapo karibu na CCM au CHADEMA imeshuka tangu 2015. CCM imeshuka kwa 4% (62% - 58%), wakati CHADEMA imeshuka kwa 11% (27% -16%).

Page 9: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

9

Kielelezo cha 7: Ni chama gani cha siasa unaona uko karibu nacho, kama kipo?

65%

54%

54%

62%

63%

58%

4%

8%

12%

5%

17%

24%

26%

32%

27%

27%

17%

16%

3%

4%

4%

2%

1%

1%

0.7%

0.9%

0.9%

1%

1%

0.3%

0.5%

0.3%

2%

1%

2%

2%

2012

2013

2014

2015

2017

2018

CCM Hamna chama Chadema CUF ACT NCCR Kingine

Chanzo cha Takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi, Kundi la kwanza (Okt-Des 2012), Awamu ya 10 (Okt 2013) na Awamu ya 24 (Sept 2014); kundi la 1 Msingi (Okt-Des 2012),

Kundi la 2 Awamu ya 1 (Agosti- Sept 2015), Awamu ya 18 (Aprili 2017) na Awamu ya 27 (Apr 2018)

Msingi: wahojiwa wote (1,241 kwenye awamu ya 27) * 27% kwa Chadema mwaka 2015 ikiwemo 2% ambao walisema wapo karibu na “UKAWA”

Wazee (76%) wana uwezekano mkubwa wa kusema wapo karibu na CCM kuliko vijana (49%); wanawake (63%) wapo karibu zaidi na CCM kuliko wanaume (53%); na wasio na elimu (66%) wapo karibu zaida na chama tawala kuliko wenye elimu ya juu (46%). Hakuna tofauti kubwa ya uungaji mkono CCM kati ya maeneo ya mijini na vijijini. Hata hivyo ifahamike kuwa, uungaji mkono wa CCM hapo nyuma ulikuwa mkubwa maeneo ya vijijini ukilinganisha na maeneo ya mjini (66%-57% mwaka 2017), lakini uungaji mkono wa maeneo ya vijijini umeshuka mpaka kulingana na ule wa maeneo ya mijini.

Page 10: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

10

Kielelezo cha 8: Ni chama gani cha siasa unaona uko karibu nacho, kama kipo?

58%63%

53%59%

56%49%

55%63%

76%

66%61%

46%

24%24%

23%21%28%

29%23%

23%14%

22%21%

31%

2%1%

3%2%

2%2%4%

2%2%

2%2%

2%

16%12%

20%17%

14%20%19%

13%9%

11%16%

21%

wote

umri 18-2930-3940-49

50+

CCM Hamna chama Chama kingine cha upinzani Chadema

wanawakewanaume

vijijinimijini

hawana elimuelimu ya msingi

elimu ya sekondari na kuendelea

Chanzo cha Takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi, Awamu ya 27 (Aprili 2018) Msingi: wahojiwa wote (1,241)

Jambo la 8: Uungaji mkono wa wananchi kwa wawakilishi waliochaguliwa umeendelea kushuka Asimilia sawa ya wananchi wanaukubali utendaji wa wabunge (44%) na madiwani wao (45%) tangu walipoingia madarakani. Kukubalika kwa wenyeviti wa mitaa/vijiji ni mkubwa zaidi (56%). Kwenye masuala yote haya, viwango vya kukubalika vimeshuka katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

Page 11: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

11

Kielelezo cha 9: Asilimia ya wanaokubali namna watu wafuatao wanavyotekeleza majukumu yao tangu walipoingia madarakani:

88%80%

82%88%

78%66%

56%

85%71%

86%63%

74%59%

45%

79%71%

70%63%

68%58%

44%

2012201320142015201620172018

2012201320142015201620172018

2012201320142015201620172018

Mw

enye

ki�

wak

ow

a ki

jiji/m

taa

Diw

ani w

ako

/ b

araz

aM

bung

e w

ako

Chanzo cha Takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi, Kundi la 1 (Okt-Des 2012), Awamu ya 10 (Okt 2013) na Awamu ya 24 (Sept 2014); Kundi la 2 Awamu ya 1 (Agosti-Sept 2015), Awamu ya

11 (Sept 2016), Awamu ya 18 (Apr 2017) na Awamu ya 27 (Apr 2018)Msingi: wahojiwa wote (1,241 kwenye Awamu ya 27)

Jambo la 9: Asilimia 55 ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais MagufuliAsilimia 55 ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli tangu alipoingia madarakani mwaka 2015. Kukubalika huku kumepungua kutoka 96% mwaka 2016, na 71% mwaka 2017. Kiwango cha kukubalika kwa Rais kimeshuka kutoka kwenye rekodi ya juu kuwahi kuwekwa na Rais wa Tanzania mpaka rekodi ya chini tangu takwimu hizi zianze kukusanywa mwaka 2001.

Page 12: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

12

Kielelezo cha 10: Asilimia ya wanaokubali namna Rais anavyotekeleza majukumu yake tangu alipoingia madarakani:

90%85%

93% 89%84% 82%

87%81%

96%

71%

55%

2001 2003 2005 2008 2012 2013 2014 2015 2016 2017 2018

Afrobarometer Sau� za Wananchi

Rais Mkapa Rais Kikwete Rais Magufuli

Chanzo cha Takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi, kundi la 1 Msingi (Okt-Des 2012), Awamu ya 10 (Okt 2013) na Awamu ya 24 (Sept 2014); Kundi la 2 Awamu ya 1 (Agosti-Sept 2015),

Awamu ya 11 (Sept 2016), Awamu ya 18 (Apr 2017) na Awamu ya 27 (Apr 2018);Tafiti za Afrobarometer (2001, 2003, 2005, 2008)8

Msingi: wahojiwa wote (1,241 kwenye awamu ya 27)

Wazee (71%) wana uwezekano mkubwa zaidi kuliko wengine kukubali utendaji wa Rais, huku chini ya nusu ya wananchi wenye umri wa miaka 18-29 (46%) wakiukubali.

Wanawake wengi zaidi (57%) wanaukubali utendaji wa Rasi kuliko wanaume (53%), na wananchi wasio na elimu (58%) wanaukubali zaidi kuliko wananchi wenye elimu ya juu (47%).

Kwa mara nyingine tena, suala la vijijini na mijini linafaa kuzingatiwa. Mwaka mmoja uliopita, 2017, wananchi wa maeneo ya vijijini (72%) waliukubali zaidi utendaji wa Rais kuliko wale wa maeneo ya mijini (70%). Lakini, takwimu hizi zinaonesha kwamba kukubalika kwa utendaji wa Rais kumeshuka zaidi vijijini kutoka 72% (2017) hadi 52% (2018) ukilinganisha na mijini 70% hadi 59%.

8 Angalia Afrobarometer.org

Page 13: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

13

Kielelezo cha 11: Asilimia ya wanaokubali namna Rais anavyotekeleza majukumu yake tangu alipoingia madarakani:

55%

57%53%

52%59%

46%54%

57%71%

58%57%

47%

wote

wanawakewanaume

vijijinimijini

umri 18-2930-3940-49

50+

hawana elimuelimu ya msingi

elimu ya sekondari na kuendelea

Chanzo cha Takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi, Awamu ya 27 (Aprili 2018) Msingi: wahojiwa wote (1,241)

Page 14: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea

14

3. Hitimisho Bila shaka, hitimisho kuu kutoka kwenye muhtasari huu ni kushuka kwa viwango vya kukubalika kwa wawakilishi waliochaguliwa.

Haitakuwa vizuri kama tutajikita tu kwenye hili. Kwa sababu kuna taarifa nyingi hapa (na kwenye tafiti nyingine za hivi karibuni za Sauti za Wananchi), ambazo zinaweza kutoa mwanga wa kwa nini wananchi wana mashaka, na nini ambacho viongozi wanapaswa kufanya kurudisha imani kwa wananchi.

Kwanza, wananchi wa kawaida, wanaharakati na wachambuzi wa maswala ya demokrasia na haki za raia wanalalamikia vitendo vya kuminywa kwa uhuru wa maoni na haki za kisiasa – kwa wananchi na kwa taasisi kama vile vyombo vya habari, asasi za kiraia na vyama vya siasa vya upinzani. Wananchi wengi wanataja uhuru wao kama kipengele muhimu cha uelewa wao wa neno “demokrasia” kuliko wanaotaja chaguzi. Wako wazi kuwa haki nyingi na uhuru umepungua katika miaka ya hivi karibuni. Wanaendelea kutetea haki za vyama vya upinzani na wanaunga kuwajibishwa kwa serikali ya Rais Magufuli. Msimamo wa serikali hii kuwa baadhi ya haki za raia kama vile kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa kunachelewesha maendeleo unaanza kufifia.

Pili, kushuka kuungwa mkono kwa CCM na kushuka kwa viwango vya kukubalika vya Rais kumejitokeza sana vijijini. Hili ni jambo jipya. Kwa kawaida, vyama vya upinzani kwa ujumla na hususani CHADEMA vimekuwa vikiungwa mkono zaidi kwenye maeneo ya mijini, huku CCM na serikali ikiungwa mkono zaidi kwenye maeneo ya vijijini. Nini kimebadilika zaidi vijijini kuleta matokeo haya?

Je, wafanye nini viongozi wa kisiasa kutokana na ujumbe huu wa wananchi? Kama wasiwasi wa wananchi uko kwenye uhuru wa kisiasa na hali ngumu ya uchumi, ili kuifanya serikali iendelee kukubalika ingesema wazi kuwa inaunga mkono uhuru wa kisiasa, na kuonesha kwa vitendo kama vile kwa kurudisha matangazo ya moja kwa moja ya vipindi vya bunge na kuondoa vikwazo kwa shughuli za vyama vya upinzani. Pili, serikali itafute njia za kujenga upya imani ya kufanya biashara na kuelekeza msaada wa kifedha kwa wakazi wa maeneo ya vijijini.

Mwisho, kuna dondoo muhimu kwa vyama vya upinzani. Japokuwa Chadema, CUF, ACT na NCCR Mageuzi vinafanya kazi kwenye mazingira magumu, vinapaswa kujiuliza kwa nini viwango vya kukubalika kwa viongozi waliochaguliwa vimeshuka. Zaidi, kwa nini vyama hivi vinahangaika kutafuta kuungwa mkono kwenye maeneo ya mijini, ambayo tayari wanaungwa mkono? Ikiwa vyama hivi vimejikita zaidi kwenye masuala ya kisiasa, labda ni wakati mwafaka sasa wa kuangalia uwezekano wa kushughulikia wasiwasi wa wananchi kuhusu hali zao za kiuchumi.

Page 15: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea
Page 16: Kuwapasha viongozi? - Twaweza...• Idadi ya wananchi ambao hawako karibu na chama chochote cha siasa umeongezeka • Kukubalika na wananchi kwa wawakilishi waliowachagua kumeendelea