13
KANUNI ZA JAMII Toleo la 2.0 2016 2016 KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm [Ushirikiano Group Dsm-(UG)]tu. Marekebisho ya kanuni hizi yalifanywa3Aprili 2016

KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm ... ZA JAMII.pdf · 1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano. ... 2.1 Kwa mujibu wa sehemu

  • Upload
    others

  • View
    14

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm ... ZA JAMII.pdf · 1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano. ... 2.1 Kwa mujibu wa sehemu

KANUNI ZA JAMII

Toleo la 2.0 2016

2016

KwaMatumizi ya Wanachama wa

Kikundi cha Ushirikiano-Dsm

[Ushirikiano Group Dsm-(UG)]tu.

Marekebisho ya kanuni hizi

yalifanywa3Aprili 2016

Page 2: KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm ... ZA JAMII.pdf · 1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano. ... 2.1 Kwa mujibu wa sehemu

Ushirikiano Group - Kamati ya Jamii. 1

YALIYOMOUkurasa

1. Tafasiri ya maneno. ............................................................................................................... 2

2. Taratibu za Jamii za Kikundi ............................................................................................. 3

3. Utaratibu wa kutoa taarifa ................................................................................................. 4

5. Utaratibu wa kushiriki kwenye misiba. ......................................................................... 5

6. Utaratibu wa kushiriki harusi/sendoff na shughuli zingine za Jamii. ................ 7

7. Ushiriki wa wanachama walio njeya Dar es salaam/Tanzania (nje ya nchi) ... 8

8. Siku ya USHIRIKIANO ya Mwaka. ..................................................................................... 8

9. Miiko na faini katika shughuli za Kijamii. ..... ERROR! BOOKMARK NOT DEFINED.

10. Udhuru…………………………………………………………………………………………………………..8 11. Idara ya akina mama………………………………………………………………………………………9 12. Viongozi wa idara ya akina mama……………………………………………………………......10 13. Mabadiliko ya kanuni………………………………………………………………………………...…11

Page 3: KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm ... ZA JAMII.pdf · 1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano. ... 2.1 Kwa mujibu wa sehemu

Ushirikiano Group - Kamati ya Jamii. 2

1. TAFASIRI YA MANENO.

1.1 Kushirikiana - kujitoa kwa Hali na Mali ikiwemo kutoa Michango ya mawazo na mali pamoja na kushiriki katika matukio mbali mbali ya kikundi.

1.2 Mwanachama - Ni familia kwa mujibu wa katiba na katika Shughuli za kijamii ni ushiriki wa baba na mama Katika shughuli za kijamii.

1.3 Mtoto - Mtoto wa kuzaliwa na mwanachama kwa mujibu wa sharia za nchi.

1.4 Baba/Mama Mkwe - Ni wazazi wa kike na kiume wa wanandoa wawili wa wanachama.

1.5 Ndoa - Muunganiko wa Mke na mme (mmoja) unaofanya familia, wenye ndoa inayotambulika kisheria (Kimila , kidini au kiserikali).

1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano.

Page 4: KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm ... ZA JAMII.pdf · 1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano. ... 2.1 Kwa mujibu wa sehemu

Ushirikiano Group - Kamati ya Jamii. 3

2. TARATIBU ZA JAMII ZA KIKUNDI

2.1 Kwa mujibu wa sehemu ya 3(b) ya katiba ya ushirikiano Group, Kila mwanachama atatakiwa kushiriki kwa hali na mali katika shughuli zote za jamii za kikundi.

2.2 Ili kuleta ufanisi wa kuendesha shughuli za kijamii mwanachama atatoa taarifa ya tukio/shughuli kwa mujibu wa utaratibu za taarifa ulioonyesha hapo chini.(kwa mujibu wa kifungu 2.7).

2.3 Kila mwanaushirikiano atahakikisha anatekekeleza wajibu wake wa kujitoa na kujitolea kwa hali na mali bila kubagua katika shughuli zote za jamii za kikundi.

2.4 Kikundi hakitakubali majungu,umbea na uchonganishi katika shughuli zote za jamii,taratibu za kueleza dukuduku/mawazo/changamoto ni pamoja na kueleza waziwazi kwenye vikao husika. Kamati ya maadili itachukua hatua kwa mujibu wa kanuni kwa mtu atakayeenda tofauti/kinyume na kanuni hizi za jamii.

2.5 Wakati wa shughuli au tukio Mwanachama (mume na mke) watapimwa ushiriki kila mmoja ili kuleta nidhamu na uwajibikaji katika kikundi.

2.6 Ili kuleta ukaribu wa wanachama na familia zao, kamati itaandaa utaratibu wa kutembeleana kwa mujibu wa vikao maalum vitakavyopangwa.Vilevile kamati ya jamii itaandaa siku ya USHIRIKIANO ya mwaka itakayowahusu familia zote za wanachama.

2.7 Taarifa za kutokushiriki katika shughuli zitatolewa kwa mwenyekiti wa kikundi au mwenyekiti wa kamati ya kijamii,madaftari ya mahudhurio yatatayarishwa kwa kila mwanachama kusaini katika ushiriki wa shughuli yeyote ya jamii.

2.8 Atakayeshindwa kushiriki bila taarifa atatozwa faini kadri ya utaratibu wa faini ulioonyeshwakatika kifungu cha 9.0 cha

Page 5: KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm ... ZA JAMII.pdf · 1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano. ... 2.1 Kwa mujibu wa sehemu

Ushirikiano Group - Kamati ya Jamii. 4

kanuni hizi. Mwanachama atakayefikisha faini ya matukio Matatu (3) mfululizo atafikishwa kwenye kamati ya maadili.

3. UTARATIBU WA KUTOA TAARIFA

3.1 Kama ilivyoelezwa katika katiba, shughuli za jamii zitakazowashirikisha wanakikundi/ wanachama ni pamoja na:

3.1.1 Msiba

3.1.2 Ugonjwa

3.1.3 Ndoa/send off.

3.1.4 Matukio mengine kama kuunguliwa moto,siku ya ushirikiano n.k.

3.2 Taarifa za shughuli/matukio zitatolewa aidha kwa simu , mtandao (e-mail), maandishi, ana kwa ana kwa Mwenyekiti wa Ushirikiano /Mwenyekiti wa Jamii.Taarifa iwe kamili kwa kueleza ni wapi , lini , uhusiano na utaratibu upi uliopo Shughuli/tukio husika.

3.3 Mwenyekiti wa kikundi/Mwenyekiti wa Jamii atatoa taarifa kwa wanakikundi na kuwafahamisha wajumbe wa kamati ya jamii kama kuna utaratibu utakaofaa kuendeshwa kulingana na tukio/shughuli husika.Taarifa hizi zitatolewa kwa wanaushirikiano wote.Taarifa zisichukue muda mrefu ili kufanya utekelezaji uwe wa haraka.

3.4 Taarifa zingine zisizo kwenye utaratibu lakini zinajenga mahusiano na upendo ndani ya wanakikundi kama kuhitimu/kufaulu kiwango Fulani cha elimu kwa mwanachama ,mtoto wa mwanachama , kufaulu kibiashara , kujenga/kununua nyumba , gari , kusherehekea siku ya kuzaliwa , kipaimara , Ubatizo , kupata mtoto n.k . zitatolewa kwenye kamati ya kijamii ili kuwashirikisha wanakikundi.

Page 6: KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm ... ZA JAMII.pdf · 1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano. ... 2.1 Kwa mujibu wa sehemu

Ushirikiano Group - Kamati ya Jamii. 5

4. UTARATIBU WA KUSHIRIKI KWA MGONJWA

4.1. Taarifa zote za ugonjwa wa mwanachama au mwanafamilia wa mwanachama zitatolewa kadri ya utaratibu wa kutoa taarifa kifungu(3.0) hapo juu.

4.2. Wanachama watashiriki kwa kwenda kumuona mgonjwa na kushiriki kumsaidia kwa hali na mali ili kumwezesha apone. Upendo wa kumfariji kila wakati utakuwa ndio utamaduni wa wanakikundi.

5. UTARATIBU WA KUSHIRIKI KWENYE MISIBA.

5.1 Kama ilivyoanishwa katika katiba (kifungu namba 7 - ( a), misiba itakayo wahusu wana kikundi moja kwa moja ni pamoja na:-

5.1.1 Msiba wowote utakaotokea nyumbani kwa mwanachama isipokuwa wa kuhamishiwa.

5.1.2 Msiba wa mwanachama mwenyewe(mke au mme)

5.1.3 Mtoto wa mwanachama.

5.1.4 Baba / Mama mzazi wa mwanachama ( wa mme /mke wa familia).

Taarifa zitatolewa kwa mujibu wa kanuni za taarifa (kifungu 3.0).

5.2 MSIBA WA DAR ES SALAAM - Wanachama watahudhuria wote kadri ya taarifa zitakavyotolewa, michango ya kuendesha shughuli za msiba itatolewa kwa njia ya daftari kwa kushirikiana na makundi mengine ya kijamii. Wanakikundi watakuwa mstari wa mbele wakati wote kufanikisha shughuli ya msiba.

5.2.1 Daftari la mahudhurio litakuwepo wakati wote wa msiba ili wanachama kuonyesha ushiriki wao.

Page 7: KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm ... ZA JAMII.pdf · 1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano. ... 2.1 Kwa mujibu wa sehemu

Ushirikiano Group - Kamati ya Jamii. 6

5.2.2 Kila mwanachama atatakiwa kutoa mchango wa Tshs. 50,000.00 kwa ajili ya kufanikisha shughuli za msiba . Kiwango hiki kitabadilika kadri wanachama watakavyoona katika mkutano wa mwezi au wa Dharura.

Rambirambi ya kikundi itakuwa

a) Mwanachama - shs 700,000/=

b) Mtoto wa mwanachama - shs 700,000/=

c) Baba/baba mkwe - shs 600,000/=

d) Mama/mama mkwe - shs 600,000/=

e) Mtu mwingine aliyefia nyumbani - shs 500,000/=

5.2.3 Kiwango hiki kitabadilika kadri wanachama watakavyoona inafaa , mabadiliko yatapitishwa na mkutano wa kila mwezi au wa dharura.

5.3 MSIBA NJE YA DAR ES SALAAM - Mwanachama aliye nje ya

Dar es salaam akipata msiba nyumbani

5.3.1 Taarifa zitatolewa kama kawaida , wanachama watashirikikishwa michango ya kufanikisha msiba (Kama ilivyoanishwa kifungu 5.2.2 ; 5.2.3), taarifa za maendeleo ya musiba zitakuwa zinatolewa .

5.3.2 Kamati ya jamii itapendekeza wawakilishi wa wanaushirikiano ili kushiriki vyema kwenye musiba wa mwanakikundi aliye nje ya Dar es salaam.

5.4 MSIBA UTAKAOTOKEA NJE YA FAMILIA(MAKAZI) YA MWANACHAMA:

5.4.1 Msiba wa mwana kikundi unaotokea nje ya familia (makazi) (mikoani) kwa walengwa (kwa mujibu wa kifungu 5.1.2, 5.1.3 na 5.1.4), taarifa zitatolewa, kikundi kitashirikishwa kutoa kiwango cha rambirambi .Rambirambi ya kikundi itakuwa

a) Mwanachama - shs 700,000/=

b) Mtoto wa Mwanachama - shs 700,000/=

c) Baba/baba Mkwe - shs 600,000/=

Page 8: KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm ... ZA JAMII.pdf · 1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano. ... 2.1 Kwa mujibu wa sehemu

Ushirikiano Group - Kamati ya Jamii. 7

d) Mama/Mama Mkwe - shs 600,000/=

Ili kusaidia kufanikisha ushiriki wa mwanachama kwenye msiba. Kiwango hiki kitabadilika kadri wanachama watakavyoona, mabadiliko yatapitishwa na mkutano wa kila mwezi au wa dharura.

5.4.2 Wanafamilia wafiwa watakaporudi kamati ya jamii itapanga siku ya kwenda kuhani kwa mwanachama. Wanachama wote watatakiwa kuhudhuria.

5.5 MSIBA NJE YA UTARATIBU WA USHIRIKIANO Msiba ulio nje ya utaratibu itatolewa taarifa na kamati ya jamii kupitia kwa Mwenyekiti wa Ushirikiano/Jamii ili kuwashirikisha wanachama kuendeeleza upendo kwa kushirikishana.

6. UTARATIBU WA KUSHIRIKI HARUSI/SENDOFF NA SHUGHULI ZINGINE ZA JAMII.

6.1 Wanachama watashirikishwa katika harusi kuaga binti (Sendoff) katika makundi yafuatayo:

6.1.1 Mwanachama Mwenyewe.

6.1.2 Mtoto wa kuzaliwa na Mwanachama au kwa mujibu wa sheria za nchi.

6.2 Taarifa zitatolewa kwa mujibu wa taratibu za kutoa taarifa , wanachama watatakiwa kushiriki bila kukosa kwa makundi yaliyo kadri ya katiba. Ushiriki utaratibiwa na kamati ya jamii.

6.3 Kwa mwanachama asiyeshiriki bila taarifa atatozwa faini na akifikisha matukio 3 mfululizo atafikishwa kwenye kamati ya maadili ili kuchukua hatua kwa kadri ya kanuni za maadili.

6.4 Siku ya Harusi/Send off wanachama watashiriki kutoa zawadi itakayoondaliwa kwa mujibu wa kanuni. Zitakuwa kama ifuatavyo:

a) Mwanachama - Tshs. 500,000/=.

b) Mtoto wa kuzaliwa wa mwanachama - Tshs. 400,000/=.

Uwakirishi utatumika kwa shughuli yoyote itakayofanyika nje ya Dar es salaam.

Page 9: KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm ... ZA JAMII.pdf · 1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano. ... 2.1 Kwa mujibu wa sehemu

Ushirikiano Group - Kamati ya Jamii. 8

6.5 Michango ya wanachama katika kufanikisha mandalzi ya harusi

/send off kadri ya makundi yaliyoainishwa katika katiba kitakuwa kuanzia shilingi laki moja (100,000/=) na kuendelea. Kiwango kitabadilika kadri itakavyoamuliwa naMkutano Mkuu.

7. USHIRIKI WA WANACHAMA WALIO NJEYA DAR ES SALAAM/TANZANIA (NJE YA NCHI)

Wanachama watapata hudumu kama kawaida kwa mujibu wa katiba na kanuni mbalimbali.

8. SIKU YA USHIRIKIANO YA MWAKA.

8.1 Kama ilivyoanishwa hapo juu siku hii itaweza kuwakutanisha wanakikundi na familia zao ili kuweza kufahamiana kwa kushiriki chakula , vinywaji , kucheza kwa pamoja.

8.2 Utaratibu utaandaliwa na kamati ya jamii wakishirikiana na kamati yake ndogo iliyo chini ya mwenyekiti wa jamii, na kuwashirikisha wanachama katika maandalizi kila mwaka, siku hii itakuwa mara moja kwa mwaka. Kila familia itatakiwa kushiriki katika michango, maandalizi na kuwepo kwenye shughuli hii.

8.3 Siku ya ushirikiano itapendekezwa na kamati ya jamii kila mwaka mpya ukianza na kuwasilishwa kwenye mkutano mkuu wa wanaushirikiano unaofanyika kila mwezi au mkutano wa dharura, siku (tarehe) hiyo ikipitishwa na mkutano mkuu, kamati ya jamii ikishirikiana na kamati yake ndogo itaanza maandalizi ya kufanikisha siku hii.

9. MIIKO NA FAINI KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII.

Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za jamii za ushirikiano , ifuatayo ni miiko na faini zitakazo-tuongoza(neno moja) na zitakazo-tumika(neno moja) katika utelelezaji wa kanuni na katiba ya ushirikiano;

Page 10: KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm ... ZA JAMII.pdf · 1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano. ... 2.1 Kwa mujibu wa sehemu

Ushirikiano Group - Kamati ya Jamii. 9

9.1 Uchelewaji Vikao mbalimbali - Ili kuleta nidhamu katika kikundi mwanachama ni mwiko kuchelewa vikao husika vilivyotolewa taarifa na viongozi.

FAINI: Tshs. 2,000/= kwa kila mwanachama (mume au mke) atakayechelewa kwenye vikao.

Mwanachama atakaye kosa vikao 3 mfululizo bila taarifa atatakiwa kutoa taarifa kwa maandishi kamati ya Jamii kama haitaridhika nayo itapelekwa kamati ya maadili.

9.2 Kutohudhuria shughuli/Tukio - Ili kuleta ufanisi na nidhamu

katika ushiriki kwemye shughuli zote za jamii ni mwiko kutokuhudhuria bila taarifa maalumu.

FAINI: Tshs. 5,000/= kwa kila mwanachama (mume au mke) asiyehudhuria kwenye shughuli/tukio bila taarifa. Mwanachama atakaye kosa vikao 3 mfululizo bila taarifa atatakiwa kutoa taarifa kwa maandishi kamati ya Jamii kama haitaridhika nayo itapelekwa kamati ya maadili.

9.3 Kutoa maneno ya uchochezi/uchonganishi/umbeya katika

shughuli za jamii . Ni mwiko kama ilivoonyeshwa kwenye taratibu za jamii.

FAINI: Kamati ya jamii itahitaji maelezo kwa maandishi juu ya tukio/kitendo na baadaye itapeleka tukio la mwanachama husika kwenye kamati ya Nidhamu kwa hatua husika kadri ya kanuni za maadili.

10. 0 UDHURU Kutakuwa na udhuru unaokubalika kutohudhuria shughuli za vikao ni

kama ifuatavyo:-

10.1. Udhuru wa kutohudhuria kikao/ vikao vya ushirikiano:-

Page 11: KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm ... ZA JAMII.pdf · 1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano. ... 2.1 Kwa mujibu wa sehemu

Ushirikiano Group - Kamati ya Jamii. 10

i). Ugonjwa. ii). Kuwa safarini.

Iii). Kuuguza/ kuuguliwa. iv). Kupata msiba. v). Uzazi, baada ya kujifungua ndani ya miezi mitatu.

Udhuru unatakiwa utolewe taarifa kwa mwenyekiti wa jamii, au kikundi siku moja au mbili kabla ya kikao, na wala sio siku ya kikao.

Mwanachama aliyetoa udhuru unaokubalika hatalipa faini yoyote, isipokuwa tu kama taarifa imeletwa kuomba udhuru usiokubalika ambao haukutajwa kwenye kifungu hiki. Utalipa faini kama inavyosomeka kwenye kanuni hizi (kifungu cha 9.2).

10.2. Udhuru wa kuchelewa kufika kwenye kikao kutokana na dharura

isiyotarajiwa.

Udhuru huu utakubalika tu kama utawasilihwa kwa mwenyekiti wa jamii kwa njia ya simu, meseji, barua pepe au njia yoyote inayokubalika nakueleza dharura iliyokupata ukiwa unakuja kwenye kikao. Vinginevyo utalipa faini iliyoainishwa kwenye kanuni hizi (kifungu 9.1).

11. IDARA YA AKINA MAMA Kutakuwa na idara ya akina mama itakayoitwa “UG Women”. Kila

mwanamama aliyeko kwenye kikundi cha ushirikiano ni mwana “UG Women”. 11.1 MALENGO YA UG WOMEN 11.1.1 Kusaidiana kwa kutoa huduma mbalimbali za kijamii

zinazowahusu akina mama na familia zao. 11.1.2 Kupeana pole na kupongezana wakati wa kujifungua, harusi,

kuhitimu masomo na kumuaga binti (sendoff). 11.1.3 Kununua vifaa vya kutumika kwenye shughuli za kijamii kama

vyombo vya kupikia kwa ajili ya kurahisisha kutoa huduma lengwa.

11.1.4 Kuwa na mfuko wa jiko ambao unaweza kutoa mahitaji muhimu ya kuanzia kwa familia ya mwanachama katika hali ya dharura kama misiba.

11.1.5 Na huduma zingine zinazokubalika kwa idara ya akina mama.

Page 12: KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm ... ZA JAMII.pdf · 1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano. ... 2.1 Kwa mujibu wa sehemu

Ushirikiano Group - Kamati ya Jamii. 11

11.2 WAJIBU WA KILA MWANAMAMA NDANI YA IDARA HII. 11.2.1 Kuhudhuria vikao vyote vinavyoitishwa na uongozi wake. 11.2.2 Kulipa michango kila mwezi wa shilingi 5000 (Kiwango hiki

kinaweza kurekebishwa kulingana na thamani na mahitaji ya fedha).

11.2.3 Utunzaji wa fedha za idara hii zitawekwa kwenye akaunti ya ushirikiano na zitafuata kanuni za fedha za ushirikiano.

11.2.4 Kushiriki katika shughuli za matukio ya kifamilia kwa mwanachama, kama vile kwenda kutoa pole na hongera kwa mwanamama aliyejifungua, anayeuguliwa na mtoto, mume au ndugu anayeishi naye na ugonjwa na zingine zilizoorodheshwa kwenye kifungu cha 11.1.2 hapo juu.

11.2.5 Mwanamama asiyelipa michango yake mfululizo kwa miezi mitatu atakuwa amekosa haki ya kupata huduma zilizoainishwa kwenye kifungu 11.1.

11.2.6 Mwanamama huyo atatolewa taarifa na Mwenyekiti au katibu wa UG Women kwa mwenyekiti wa Kamati ya Jamii ili aandikiwe barua kumkumbusha alipe michango yake anayodaiwa kwa lengo la kwenda sambamba na wenzake katika kufanikisha malengo yaliyowekwa.

11.2.7 Asipolipa madeni ya michango yake kanuni za maadili za Ushirikiano zitafanya kazi. 11.2.8 Matatizo yote ya idara ya akina mama yatatatuliwa na

uongozi wa ‘’UG Women’’ na kama bado hayajapata ufumbuzi yatapelekwa kwa mwenyekiti wa kamati ya jamii.

11.3 VIONGOZI WA IDARA YA AKINA MAMA Idara hii itakuwa na viongozi wafuatao:- 11.3.1 Mwenyekiti. 11.3.2 Katibu 11.3.3 Mweka hazina Viongozi hawa watahudumu kwa kipindi cha miaka mitatu, na uchaguzi

utafanyika kuchagua viongozi wapya. Uongozi wa idara ya akina mama utakwenda sambamba na mabadiliko ya uongozi wa kikundi cha ushirikiano.

11.4 MNUFAIKA WA IDARA YA UMOJA WA AKINA MAMA Ni familia ya mwana mama wa UG ikijumuisha watu anaoishi nao kama:- 11.4.1 Mume. 11.4.2 Watoto. 11.4.3 Ndugu anaokaa nao.

Page 13: KwaMatumizi ya Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano-Dsm ... ZA JAMII.pdf · 1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano. ... 2.1 Kwa mujibu wa sehemu

Ushirikiano Group - Kamati ya Jamii. 12

11.4.4 Wakwe (wazazi) wa wanandoa kwenye familia. 11.5 MAWASILIANO KWA AKINA MAMA Taarifa zote zitatolewa kupitia mtandao wa kundi la whatsup la akina Mama lijulikanalo kama “UG Women”, kupiga simu ama kuandika ujumbe

mfupi wa maandishi (sms) au kwa kutumia njia yoyote watakayoona inafaa kwa mwenyekiti au katibu.

12. MABADILIKO YA KANUNI Kanuni za jamii zinaweza kubadilika kadiri ya mahitaji ya wanachama Itavyoelekezwa.

13. MUDA WA KUANZA KUTUMIKA KANUNI HIZI

Kanuni hizina mabadiliko yake zimeanza kutumika mara baada ya kupitishwa na Mkutano wawanachama wote kwa mujibu wa Katiba tarehe 3/04/2016.

Mrs. Hellen Kiheka Mr. Samson Manda Jeremiah Nkiya

Katibu Kamati ya Jamii Mwenyekiti Kamati ya Jamii

Mr. John AtanasMlyabope

Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushirikiano TAREHE:

3/04/2016