9
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inaweza Kuepuka Laana Hiyo Kihalisia? Na: Prof Handley Mpoki Mafwenga Simba Ph.D (Finance), MSc (Finance), MBA (Mg.Eco), LLM (Taxation), PGDTM, LLB, ADTM, ICSA (UK) [Mchambuzi wa Sera za Uchumi, Bajeti na Kodi] Laana ya rasilimali au Kitendawili cha Utajiri wa rasilimali ni pale ambapo Tanzania ina uwingi wa maliasili, hasa mali ghafi yenye thamani kubwa kama vile mafuta na gesi ambayo huendana na ukuaji mdogo wa Uchumi na matokeo mabovu ya Maendeleo kama vile kuongezeka kwa Umaskini, kutokuwepo kwa hali ya Usawa katika jamii na huduma dhaifu za Umma. Nchi inayotegemea sana kuuza mafuta na gesi nje ya nchi, huzalisha mapato makubwa yanayopelekea bila kufahamu uwepo wa Uchumi uliodumaa na hali ya kisiasa isiyo imara. Nchi zenye maliasili nyingi za mafuta na gersi na ukuaji mdogo wa Uchumi ni Gabon, na Nigeria ambazo zilikuwa kati ya nchi Hamsini tajiri Duniani kwenye miaka ya sabini na kwa sasa zimetokea kuwa ndiyo nchi Maskini za kwanza Duniani zinazozalisha mafuta na gesi ikiwemo Nchi ya Zambia. Aidha, zaidi ya nusu ya Wananchi wa Msumbiji nchi ambayo pia ina utajiri wa mafuta na gesi wanaishi ndani ya wimbi la Umaskini pamoja na maliasili nyingi walizonazo. Hii inaonesha kuwa mafuta na gesi hunufaisha Kampuni za kigeni za Kimataifa na Wanasiasa. Swali la kujiuliza ni kuwa; Kwanini Nchi kama Tanzania inapaswa kutegemea mafuta, gesi na madini katika Uchumi wake? Ukweli ni kuwa wakati chanzo chake kikubwa cha mapato ni uuzaji wa malighafi Kwenye Soko la Kimataifa, Uwekezaji kutoka nje na Teknolojia vinahitajika kutumika katika maliasili hizo na Uwekezaji hufanywa na Kampuni za Kimataifa zenye Uwezo mkubwa. Tarakibu ya Ugonjwa wa Kidachi unalenga Kwenye uhamaji wa mahitaji kutoka kwa Wawekezaji. Nchi kama Gabon inazalisha Zaidi ya mapipa 300,000 ya mafuta kwa siku. Ni nchi inayopata mvua za kitropiki lakini ni vigumu kupata hata zao la ndizi ambalo huzalishwa sana Nchini Cameroon. Gabon ni nchi ambayo ina sekta ya kilimo yenye nguvu, lakini kitendo cha kutegemea mafuta kuuza nje ya nchi kumedhoofisha matumaini ya Maendeleo endelevu. Nchi ya Zambia katika hali ya kawaida, kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni kilipanda kwa asilimia 15%

LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inaweza Kuepuka Laana Hiyo Kihalisia

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inaweza Kuepuka Laana Hiyo Kihalisia

LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je

Tanzania Inaweza Kuepuka Laana Hiyo Kihalisia?

Na: Prof Handley Mpoki Mafwenga Simba Ph.D (Finance), MSc (Finance), MBA (Mg.Eco), LLM (Taxation), PGDTM, LLB, ADTM, ICSA (UK)

[Mchambuzi wa Sera za Uchumi, Bajeti na Kodi]

Laana ya rasilimali au Kitendawili cha Utajiri wa rasilimali ni pale ambapo Tanzania ina uwingi wa maliasili, hasa mali ghafi yenye thamani kubwa kama vile mafuta na gesi ambayo huendana na ukuaji mdogo wa Uchumi na matokeo mabovu ya Maendeleo kama vile kuongezeka kwa Umaskini, kutokuwepo kwa hali ya Usawa katika jamii na huduma dhaifu za Umma. Nchi inayotegemea sana kuuza mafuta na gesi nje ya nchi, huzalisha mapato makubwa yanayopelekea bila kufahamu uwepo wa Uchumi uliodumaa na hali ya kisiasa isiyo imara. Nchi zenye maliasili nyingi za mafuta na gersi na ukuaji mdogo wa Uchumi ni Gabon, na Nigeria ambazo zilikuwa kati ya nchi Hamsini tajiri Duniani kwenye miaka ya sabini na kwa sasa zimetokea kuwa ndiyo nchi Maskini za kwanza Duniani zinazozalisha mafuta na gesi ikiwemo Nchi ya Zambia. Aidha, zaidi ya nusu ya Wananchi wa Msumbiji nchi ambayo pia ina utajiri wa mafuta na gesi wanaishi ndani ya wimbi la Umaskini pamoja na maliasili nyingi walizonazo. Hii inaonesha kuwa mafuta na gesi hunufaisha Kampuni za kigeni za Kimataifa na Wanasiasa.

Swali la kujiuliza ni kuwa; Kwanini Nchi kama Tanzania inapaswa kutegemea mafuta, gesi na madini katika Uchumi wake? Ukweli ni kuwa wakati chanzo chake kikubwa cha mapato ni uuzaji wa malighafi Kwenye Soko la Kimataifa, Uwekezaji kutoka nje na Teknolojia vinahitajika kutumika katika maliasili hizo na Uwekezaji hufanywa na Kampuni za Kimataifa zenye Uwezo mkubwa. Tarakibu ya Ugonjwa wa Kidachi unalenga Kwenye uhamaji wa mahitaji kutoka kwa Wawekezaji. Nchi kama Gabon inazalisha Zaidi ya mapipa 300,000 ya mafuta kwa siku. Ni nchi inayopata mvua za kitropiki lakini ni vigumu kupata hata zao la ndizi ambalo huzalishwa sana Nchini Cameroon. Gabon ni nchi ambayo ina sekta ya kilimo yenye nguvu, lakini kitendo cha kutegemea mafuta kuuza nje ya nchi kumedhoofisha matumaini ya Maendeleo endelevu. Nchi ya Zambia katika hali ya kawaida, kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni kilipanda kwa asilimia 15%

Page 2: LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inaweza Kuepuka Laana Hiyo Kihalisia

katika robo ya kwanza ya Mwaka, 2008 ukilinganisha na hali ya robo ya kwanza ya Mwaka, 2005 kwa ajili ya kukua kwa zao la Mafuta. Ukuaji wa bei ulisababishwa na kupanda kwa thamani ya fedha yao ya Kwacha ambayo pamoja na kuwepo kwa Biashara huria kulisababisha kilimo cha uzalishaji kupungua. Zambia haina udhibiti wa Mitaji, ilipunguza Ushuru wa forodha na ilijiingiza katika Utaratibu wa kubadilisha fedha za kigeni kwa kuzingatia soko la fedha na hali ya Uchumi uliopo.

Picha Na 1: Utaratibu na Muundo wa Laana ya Rasilimali

Tarakibu ya Uchumi Jumuishi wa Kisiasa inachambua Motisha na Vikwazo vya Serikali. Mifumo yake ina dhana isemayo “Kodi ni chanzo cha Laana ya rasilimali” . Kodi kwenye rasilimali kunasababisha ukosefu wa tija na ukengeufu wa tabia katika nchi yenye Taasisi dhaifu, isiyoweza kutafuta vyanzo vingine vya mapato na kuwa na Usimamizi imara wa Mapato. Nadharia ya Uhai wa Mzunguko wa Kodi ni kitu kikubwa kukiangalia katika Sekta ya Mafuta na Gesi. Nadharia hii inahitaji Kodi iwe kwenye mzunguko kupitia kwenye masoko kuliko kuwekwa na Serikali. Katika nchi zenye Kodi kubwa maliasili huhamasisha dhana ya Kisiasa kuwa na miliki, wakati ambapo nchi zenye Kodi ndogo Serikali lazima iwape motisha watu wake kuwa na utajiri. Hii husababisha kupata manufaa ya Uoanishaji wa kiuchumu na Kukuza Usawa ndani ya Jamii ikiwa ni pamoja na Kukuza Taasisi za Kiraia kwa ujumla. Mfano; Nchi ya Gabon imekuwa ikishuhudia kushuka kwa hifadhi ya Kodi kubwa iliyokuwa imewekwa.

Page 3: LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inaweza Kuepuka Laana Hiyo Kihalisia

Mazingira magumu yaani Vulnerability ni aina ya Laana ya Rasilimali ambayo inasababishwa na myumbo mkubwa wa bei za bidhaa za mafuta. Nchi zenye utajiri wa maliasili mara nyingi zinakabiliwa na Matumizi makubwa ya fedha zitokanazo na Mafuta yaani “Mzunguko wa Ukuaji na Mpasuko wa Mapato”. Hii ni kwasababu, Maliasili zinahama kwa kuzingatia shinikizo la Mahitaji; hata hivyo, kama kutakuwa na Uchumi ambao una Muundo wa kuuza mafuta nje kutasababisha na Mazingira magumu kutokana na myumbo wa bei kwenye mafuta na gesi. Kukua kwa Sekta ya mafuta na gesi kulikosababishwa na kupanda kwa bei ya maliasili hizo katika soko la Dunia au kwa kuwa na kupata mafuta mapya kwenye uchimbaji kunasababisha ukuaji wa mapato kwa nchi, ambapo pia husababisha kuongezeka kwa Uingizaji wa bidhaa kutoka nje na Matumizi ya ndani kwa bidhaa zote za Kibiashara na zisizo za Kibiashara.

Katika Laana ya rasilimali, Utajiri wa maliasili ya mafuta na gesi unahamasisha nchi kujiingiza kwenye Mikopo iliyokithiri ambapo maliasili hizo huwa ni dhamana ya Mkopo. Aidha, Hali ya kutokuwa na uhakika wa mapato ya maliasili hizo husababisha Usimamizi mbovu wa Mapato kwa kufanya matumizi ya mapato hayo hata pale ambapo kuna miradi isiyo ya kudumu; na hii hutokea wakati wa ufinyu wa Bajeti au kama kuna ukosefu wa Uwezo wa kufanya matumizi au kuna Mzunguko wa Ukuaji na Mpasuko wa Mapato ambapo Matumizi hupanda na kushuka bila mpangilio wowote wa maana. Kwavile Mafuta na Gesi na uzalishaji wake una myumbo mkubwa katika Uchumi, Serikali nyingi zinazotegemea rasilimali hizo husababisha Mzunguko wa Sera ya Bajeti kuwa na tabia ya kuongeza Matumizi wakati Mapato ya Mafuta na Gesi yako juu na pia Sera hiyo huwa na tabia ya Kupunguza Matumizi wakati Mapato yameshuka.

Athari za Ukuaji wa rasilimali katika Uchumi ni Jambo kubwa la kufanyiwa tathmini. Ukuaji wa maliasili unaathiri Uchumi katika njia mbili (1) Athari za Uhamaji wa maliasili ambapo uongezekaji wa bei kwenye Sekta ya Nishati unaongeza thamani ya ongezeko la uzalishaji wa ajira katika Sekta ya Nishati na unaondoa Msawazo wa malipo ya ajira kwa kuongeza malipo ya ajira kuwa juu, hii inasababisha ajira kuhama kutoka kwenye Sekta za uzalishaji na Sekta zisizo za kibiashara kwenda kwenye Sekta ya Mafuta na gesi. Hii ni kwavile watu hupenda kulipwa Mishahara mikubwa muda wote.

Uhamaji wa Soko la ajira hutokea kwavile Sekta mbalimbali katika Uchumi hushindana kwa kuajiri Wafanyakazi wenye Ujuzi na kwavile kuna uhaba wa Ujuzi katika soko la ajira ndipo huwa rahisi Waajiriwa kuhamia kwenye Sekta ya Nishati na Mafuta ambako kuna Mshahara mkubwa. Athari zake kubwa ni bei za ndani

Page 4: LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inaweza Kuepuka Laana Hiyo Kihalisia

kuwa juu na hii husababisha kupungua kwa Ushindani kwenye bidhaa zitokanazo na Sekta za Kibiashara za kuuza bidhaa nje na kununua bidhaa mbadala kuzileta nchini.

Picha Na 2: Myumbo wa Sera Za Bajeti Kati ya Ukuaji wa Mapato na Matumizi ya Serikali

Tanzania inaweza isiepuke na laana ya rasilimali kwa sababu ya Myumbo wa Uchumi hasa Ugumu wa kukadiria Kiwango cha Mapato. Kuna ugumu wa kukadiria na kupanga Kiwango cha Mapato, Kupanga Bajeti na Kufanya Matumizi kwa sababu ya Myumbo wa mapato ya rasilimali unaosababishwa na bei za bidhaa na Ukosefu wa Ujuzi maalum na Elimu ya Tasnia ya Uziduaji ambayo inaweza isiwe ya kutosha Tanzania. Mfano, Nigeria Mnamo Mwaka, 2006 ilikadiriwa kupata kiasi cha Dola za Marekani Bilioni 36 kila Mwaka kutoka kwenye Tasnia ya Petroli; makadirio mengine ni kiwango cha Mapato yanayokadiriwa kuwa Zaidi ya Bilioni 45. Hata hivyo, ndani ya Miaka Hamsini ya ongezeko la uzalishaji wa mafuta na gesi, Nigeria imebaki kuwa ni nchi maskini kati ya nchi maskini Duniani zenye Miundombinu ya Jamii mibovu.

Je Tanzania Inaweza Kuondokana na Laana ya Rasilimali?

Tanzania inaweza kuepukana na Laana ya rasilimali kwa Kuzingatia Mambo yafuatayo;

Page 5: LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inaweza Kuepuka Laana Hiyo Kihalisia

kupunguza Rushwa na Utawala Mbovu; Nigeria kwa Mfano hali ya rushwa na utawala mbovu bado uko juu na ni nchi ambayo inakadiriwa kupoteza dola bilioni 380 kwa ajili ya rushwa na huu ni upotevu kati ya Mwaka 1960 hadi 1999. Tangia hapo, hali imekuwa mbaya Zaidi hata kwenye Sheria za Uraia, pamoja na juhudi kubwa zilizofanywa na Asasi ya kupambana na rushwa iitwayo Economic and Financial Crime Commission (EFCC), ikiwemo pia Asasi ya Independent Corrupt Pratices Commission (ICPC) na Taasisi ya Kimataifa ya Uwazi iitwayo Transparency International iliyo chini ya Benki ya Dunia. Nchi ya Guinea imeingia katika Mikataba mingi kwa njia ya rushwa ambayo imesababisha kuwepo na Mikataba mibovu. Katika Mwaka, 2012 nchi ya Guinea ilifanya marejeo ya Mikataba ya Utafiti wa Madini ya Chuma na yatoayo zao la Alumini (Bauxite). Katika Mwaka, 2011 Guinea ilitunga Sheria mpya ya madini inayokidhi Viwango vya Kimataifa na Kukuza Uwazi na Utawala Bora.

Ili Tanzania ifanikiwe kuondokana na laana ya rasilimali, inabidi iongeze jitihada ya kupambana na rushwa. Izibe mianya ya ushawishi wa rushwa kutumia Sheria na Kanuni ikiwa ni pamoja na kuboresha Utawala wa Sheria; kuboresha Usimamizi wa Haki za Binadamu; Kuimarisha Taratibu za Kidemokrasia na Asasi zake; kuongeza Usimamizi wa ngazi zote za Serikali; Huduma za raia ikiwa ni pamoja na Polisi na Jeshi; na Mahakama; Kufafanua vizuri Zaidi Haki za Umiliki wa Mali katika maeneo yote ya rasilimali za kwenye maeneo ya Uchimbaji yaliyopo kwa Wazawa. Ili kupata Maana ya rushwa na kuziba mianya kwenye Sheria na Kanuni ni vyema kurejea Kanuni ya Hesabu ifuatayo;

Rushwa=[Mamlaka+ Uwezo wa Hiari+Wajibu]-Uwajibikaji

Kupitia kwenye Uchumi na Mipango Mseto; Tanzania yafaa ihusike na Uchumi mchanganyiko kwa kuachana na kuhangaika na Sekta za Mafuta pekee na Kufungamanisha Sekta hiyo na Sekta zingine kama Uwekezaji kwenye Kilimo na Kuboresha Uzalishaji. Kujenga Viwanda ikiwa ni pamoja na Huduma kama vile Teknolojia ya Habari, Usafirishaji na Huduma za kutoka nje ya Nchi zinazopitia Tanzania ili kuzinusuru kuwa katika mrundikano wa Uchumi na Sekta ya Mafuta. Kuboresha Myororo wa Usambazaji wa Bidhaa na Huduma ndani ya Sekta ya rasilimali; iwe kupitia kwenye eneo la Bahari Kuu kufungamanisha na Tasnia zingine za rasilimali, au kupitia kwenye Uimarishaji wa Ufungamanishaji na rasilimali msingi na Viwanda vya Uchakataji nje ya Bahari Kuu. Mfano, Wazalishaji wa Mafuta kama nchi ya Angola na ya Chad hazina Uchumi Mseto na ni moja ya Nchi Maskini kutokana na Uwiano wa Kipato wa asilimia 64% na Idadi kubwa ya watu iko chini ya Mstari unaopima kiwango cha Umaskini. Lakini, Nchi nyingine

Page 6: LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inaweza Kuepuka Laana Hiyo Kihalisia

zinazozalisha mafuta zilizofanikiwa katika Kuwa na Uchumi Mseto ziko katika kiwango kizuri katika kipimo cha Umaskini; nchi hizo ni kama Indonesia na Malaysia. Nchi ya Nauru imefaidika sana na kiwango cha juu cha Ukuaji Uchumi baada ya kupata Uhuru kutokana na uchimbaji mkubwa wa madini ya phosphate. Kwa matarajio ya kumalizika kwa uchimbaji wa madini hayo, uwekezaji mkubwa ulifanywa kwenye Mifuko ya Dhamana kusaidia kusukuma hali ya Mpito na kufanya Uchumi wa baadaye wa Nauru uwe imara. Hata hivyo, kwa sababu ya Matumizi makubwa kutoka kwenye Mifuko ya Dhamana, ikiwa ni pamoja na shughuli za uwekezaji zisizo na tija, Serikali iliishia kuwa na hali ya Kufirisika.

kuchanganya Sera imara za Bajeti na za Uchumi Jumla ili kuzuia laana ya rasilimali; Iwapo Tanzania itachanganya Sera husaidia kuzuia Uchumi wa ndani kwenye Myumbo wa Mapato ya bidhaa na hivyo husaidia kuwa na Bajeti Imara na Endelevu. Mfano, Nchi ya Botswana ilipitisha Sera imara ya Uchumi Jumla dhidi ya Ugonjwa wa Kidachi. Ikiwa na Usimamizi mzuri wa Matumizi, Botswana iliweza kuondokana na Matumizi mabaya wakati wa kipidi chake cha neema ya Mapato na ilijizuia katika Kukopa kipindi ambacho Mapato yalishuka. Hii iliwezesha Botswana iweze kupandisha kiwango cha ukuaji Uchumi kutoka Nchi ya 25 kati ya nchi Maskini Mwaka 1966 hadi kufikia nchi ya Juu yenye Kipato cha Kati ndani ya Miaka 30. Myumbo wa Uchumi una athari katika ukuaji wa Uchumi. Kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni hupanda wakati wa Mzunguko wa Neema ya Mapato na wakati wa bei kuwa juu kwenye soko la Kimataifa la bidhaa, na hupungua wakati wa Mzunguko wa Mpasuko wa Mapato kwa ajili ya Matumizi. Hii huathiri nidhamu ya Kibajeti, udhibiti wa fedha za Umma na Mipango ya muda mrefu.

kupitisha Nadharia ya Urithi wa rasilimali kwa kizazi kijacho na Ugawanyaji wa Maliasili; Hii ina maana Tanzania inapaswa kuwekeza katika Kilichowekezwa, na kuanzisha Mfuko wa Mapato nje ya Nchi yaani “Sovereign Wealth Fund”. Kuunda Mifuko ya mafuta na gesi ambayo ni ya aina mbili; (1) Mfuko wa Kuimarisha Mapato ambao unapunguza athari za myunbo wa bei za rasilimali katika Uchumi na unaboresha Uhakika wa Bajeti kwa Kuimarisha aina ya Matumizi; (2) Mfuko wa Kuhifadhi Mapato ambao unahakikisha kuwa Uwiano wa Utajiri wa rasilimali utakuwepo muda wote kwa ajili ya Kizazi kijacho hata baada ya rasilimali zitakapokwisha. Mfano, Mfuko wa kudumu wa Alaska yaani Alaska Permanent Fund unahifadhi Mapato ya Sekta ya Mafuta na unagawa nusu ya mapato yaliyowekezwa kwa uwiano sawa, raia wanajua kwa kiwango gani watumie fedha zao kwa ubora Zaidi kuliko hata Serikali inavyoweza kufanya; Mifuko mingine ni kama ule Mfuko wa Nchi ya Norway uitwao State Petroleum Fund, Mfuko wa Nchi ya Venezuela uitwao Venezuela Stabilization Fund na Mfuko wa Nchi ya Kuwait

Page 7: LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inaweza Kuepuka Laana Hiyo Kihalisia

uitwao Kuwait Reserve Fund. Nchi ya Botswana pia ina Mfuko uitwao Pula Fund ambao unahifadhi Mapato kutoka kwenye madini ya Almasi. Mfuko huu umewekezwa kwenye dhamana zilizothamika katika fedha za kigeni kama Mfuko wa Hifadhi ili kukabili ushukaji wa thamani wa Almasi na kama lindo la kifedha dhidi ya Myumbo wa Uchumi.

Picha Na 3: Muundo wa Mambo Muhimu ya Mfuko wa Kuhifadhi Mapato ya Mafuta na Gesi Kutegemea na Malengo ya Sera Ambayo Malengo ya Mfuko Yatafikiwa

LENGO MUHIMU LA SERA

MAELEZO

Uimarishaji Kuhakikisha Uzuiaji wa Myumbo wa Sera ya Bajeti ambayo inaweza kuzuia athari za myumbo mkubwa wa bei za bidhaa kwenye Mapato ya Mafuta

Tahadhari Kulinda dhidi ya mabadiliko yasiyo ya kawaida katika hali ya Matumizi ya nchi kwenye Bajeti (Mfano: Maafa ya asili, Vita n.k)

Hifadhi kwa ajili ya Kizazi Kijacho

Kuweka Mapato kwa ajili ya Kizazi kijacho au mahitaji ya kizazi kilichopo (Mfano: Mahitaji ya Mafao ya Uzeeni ya baadaye yaani Pensioni)

Kuhakikisha Kizazi Kijacho kinafaidi rasilimali zetu sawa na Kizazi kilichopo

Uwekezaji Kuweka Matumizi endelevu ya muda mrefu (kubuni vynazo vipya vya mapato nje ya rasilimali za mafuta na gesi)

Kusaidia Wananchi au Maendeleo ya Uchumi ya Taifa

Kwa Kukosekana kwa fursa zilizopo kwa ajili ya Uwekezaji wa ndani au Matumizi ambayo hutoa manufaa sawa na yaliyopo kama vile Uwekezaji wa Kifedha.

Dhana ya Ushirikishwaji wa Umma, Uwekezaji wa ndani wa Sekta binasfi, Uwazi na Uwajibikaji; Uwazi na Uwajibikaji unapatikana kama Tanzania itashirikisha Umma katika Usimamizi wa Mapato kwa ajili ya kudhibiti utegemezi kutoka nje ya nchi. Taasisi kama Asasi zisizo za Serikali za Kimataifa, Benki ya Dunia, na Asasi ya Uwazi katika Tasnia ya Uziduaji yaani (EITI) ndizo zenye kuhusiana nazo sana. Asasi ya Uwazi katika Tasnia ya Uziduaji inashauri kufuata Viwango vya Kimataifa vya Uadilifu kuhusiana na Viwango vya ajira, kuepuka vitendo vya rushwa na kulipa kodi stahiki kwa Serikali inayotokana na rasilimali zetu.

Uimarishaji wa Wajibu kwa Jamii (CSR) na Uwezeshaji na Ushirikishwaji wa Wananchi; Wajibu wa Kampuni za Kimataifa ni kuhakikisha zinawajibika kwa jamii. Mfano, Nchi ya Angola ina historia ndefu katika Sekta ya Mafuta na Gesi Zaidi ya miaka 30 sasa ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika. Hata hivyo, ajira za ndani na Uwezeshaji na Ushirikishwaji wa Wananchi bado upo chini sana. Nchi kama Norway toka ilipoanza kuchimba mafuta mika ya 1960, imeishia kwenye kiwango kidogo cha Uwezeshaji na Ushirikishwaji wa Wananchi kwa kuwa na Wageni tu kwenye maeneo ya Bahari kuu na nje ya Bahari Kuu ikiwa ni pamoja na

Page 8: LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inaweza Kuepuka Laana Hiyo Kihalisia

Myororo wa Usambazaji bidhaa na huduma uliopo. Ajabu ni kuwa kwa Miuongo mitatu iliyopita Uwezeshaji na Ushirikishwaji kwa Norway ilikuwa asilimia 70% na sasa umeshuka hadi asilimia 50%.

kuimarisha Uwezo na kuepukana na Ufanisi mbovu wa Serikali; Tanzania inakabiriwa na Changamoto hizi za Kusimamia utajiri wa rasilimali kwa dhana ya kuendeleza shughuli za Uchumi. Uwezo na Ufanisi wa Serikali unaweza kuathiriwa na Miundo mibovu ya nchi ikiwa ni pamoja na Mifumo ya Usimamizi, Matumizi mabovu ya Mapato kwa muda mfupi, na Kukosekana kwa Uwezo. Mifumo mibovu kama vile Utawala wa Sheria na Udhibiti wa rushwa unaruhusu Matumizi mabaya ya Mapato na hivyo kuishia kuwa na Serikali ya Ukandamizaji. Mfano, Nchi ya Equatorial Guinea kutokana na Mifumo mibovu ya Serikali na Uhaba wa Programu za Jamii unaifanya Serikali kupata shida kuhudumia Wananchi wake.

Katika nchi ya Msumbiji, rushwa na matatizo ya Wanasiasa katika shughuli za Biashara na zabuni za Serikali ni tatizo kubwa. Mnamo Mwaka, 2011 Kipimo cha Mitizamo ya Uwazi na Rushwa yaani “Transparency International Corruption Perceptions Index” kiliiweka Msumbiji kuwa na kiwango cha Uwiano wa 2.7 kwa kipimo cha kuanzia sifuri hadi namba kumi wakati sifuri ina maanisha nchi yenye kiwango kikubwa cha rushwa na kumi ina maana ya nchi kuwa safi bila rushwa. Msumbiji ina Uwezo mdogo na itakuwa muhimu kwa Serikali kujenga Uwezo katika kuzuia rushwa, na kuweka jukwaa la Mazungumzo kati ya Serikali na raia na kati ya Serikali na Vyama vya Upinzani.

Kuweka Mfumo Imara wa Kanuni za Bajeti; Kanuni za Bajeti ni za miaka mbalimbali yenye dhana ya kuhusika na Vikwazo dhidi ya fedha za Serikali ambapo hubainishwa kwa malengo yanayowekwa kwa nambari. Tanzania inapaswa kuwa na Kanuni za Bajeti ambayo ni hatua ya kuweka dhamira, inayolazimisha Serikali kuwa na malengo ya muda mrefu ya Bajeti na hivyo, huwa ni Dira ya muda mrefu kwa ajili ya Usimamizi wa Fedha za Umma. Kanuni hizi zinazuia Matumizi mabaya na huzuia Serikali kuzidisha Matumizi haraka. Kanuni hizi huihamasisha Serikali kuweka Sera ya Bajeti ya Kuzuia Myumbo wa Fedha na huzuia athari mbaya zitokanazo na Myumbo wa Mapato. Aidha, zinakuza Uaminifu kwa Serikali dhidi ya dhamira yake ya kuweka Sera za Bajeti Imara zinazoweza kuchochea Uwekezaji kwa Sekta binafsi. Kwa Mfano, nchi kama Chile ina Kanuni za Bajeti ambazo zinaweza kutoa mfano mzuri wa Sera imara ya Bajeti. Nchini Chile Muundo wa Kanuni Sawia wa Bajeti hufanya Serikali ione rahisi kutekeleza Sera za kupambana na Myumbo wa Uchumi kwa kuwa na uwezo wa kukabili ufinyu wa Bajeti wakati wa hali mbaya ya Uchumi na kujenga Uchumi

Page 9: LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inaweza Kuepuka Laana Hiyo Kihalisia

bora wakati wa hali nzuri ya Uchumi. Kanuni inayojumuisha hisa au hifadhi na mtiririko wa mambo mengine imeundwa kwa kulenga Kiwango cha Muundo wa Bajeti yenye ziada yaani ‘structural’ fiscal surplus rate (SFSR) kwa asilimia 1% ya mwenendo wa kiwango cha ukuaji Uchumi.

Kuimarisha Ukadiriaji wa Mapato ya rasilimali za Taifa; Huu ni Mfumo wa Sera ya Uchumi Jumla na wa Bajeti. Tanzania inapaswa Kuimarisha uwezo wa kubuni na kuhakiki mifumo ya Bajeti ya muda wa kati na ya muda mrefu na hata kuunda Bajeti za Mwaka. Hii inapaswa kwenda pamoja na kupitisha Tarakibu ya Kukuza maeneo ya kiuchumi kwenye kila miradi ya rasilimali. Kuwa na Mazingira imara ya Uwekezaji na yenye kutabirika kwenye Sekta ya gesi kukua; ambayo itahusisha kuheshimu Mikataba na Haki za Kumiliki mali kama vile Mikataba ya Uzalishaji na Ugawanaji Faida; Kuwapa Wawekezaji Mazingira ya Kujiamini kuwa watabaki katika milki ya miradi yao.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA”