91
LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI Kitabu cha Mafunzo na Rejea

LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

  • Upload
    others

  • View
    22

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

LISHE KWA WATUWANAOISHI NA VIRUSI

VYA UKIMWI

Kitabu cha Mafunzo na Rejea

Page 2: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

LISHE KWA WATUWANAOISHI NA VIRUSI

VYA UKIMWI

Kitabu cha Mafunzo na Rejea

Page 3: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Lishe kwa Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWIKitabu cha Mafunzo na Rejea

Kitabu hiki kimetayarishwa na:Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH)United Nations Rd./Kilombero Str.Plot No. 432, Flat No. 3S. L. P 8218, Dar es Salaam, TanzaniaSimu/Faksi: +255 22 2152705 au +255 744 279 145Barua pepe: [email protected]

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:MkurugenziKituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH)

Kimefadhiliwa na:Rapid Funding Envelope for HIV/AIDS (RFE)P. O. Box 1559Dar es Salaam, Tanzania

© COUNSENUTH, 2004

ISBN 9987 - 8936 - 9 - 4

Sehemu yoyote ya kitabu hiki inaweza kunakiliwa kwa ajili ya matumizi yasiyo yakibiashara ili mradi ionyeshwe kwamba taarifa hizo zimetoka kwenye kitabu hikikilichoandikwa na COUNSENUTH.

ii

WahaririMary G. MateruTuzie EdwinRestituta ShirimaVictor MsindeBelinda Liana

Waliosimamia uboraDr. Calista SimbakaliaMs. Grace Muro

Page 4: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

iii

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

YALIYOMO

VIFUPISHO . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . vi

SHUKRANI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . vii

DIBAJI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . viii

UTANGULIZI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11. MAMBO MUHIMU KUHUSU VIRUSI VYA UKIMWI

• Hali ya UKIMWI nchini Tanzania . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 3

• Jinsi uambukizo wa virusi vya UKIMWI unavyotokea . . . . . . . . . . . . 3

• Njia zinazoambukiza na zisizoambukiza virusi vya UKIMWI . . . . . . 3

• Athari za UKIMWI kijamii na kifamilia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 4

• Virusi vya UKIMWI na kinga ya mwili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 5

• Tofauti kati ya kuwa na VVU na kuwa na UKIMWI . . . . . . . . . . . . . . 6

• Mnyanyapao na Ubaguzi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 7

2. ELIMU YA MSINGI YA CHAKULA NA LISHE• Umuhimu wa chakula kwa binadamu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11

• Virutubishi, umuhimu na vyanzo vyake . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11

• Makundi ya vyakula na mlo kamili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 14

3. MATATIZO MAKUU YA LISHE TANZANIA• Upungufu wa nishati na protini . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 18

• Upungufu wa wekundu wa damu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 19

• Upungufu wa vitamini A . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 21

• Upungufu wa madini joto . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 22

4. LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI• Uhusiano wa lishe na virusi vya UKIMWI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23

• Ulaji bora . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 24

• Mbinu za utayarishaji na uboreshaji wa chakula . . . . . . . . . . . . . . . . . . 25

• Vidokezo muhimu vya kuboresha lishe . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 28

5. USAFI NA USALAMA WA CHAKULA NA MAJI• Usafi wa mtayarishaji wa chakula . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 31

• Usafi wa vyombo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 31

• Usafi wa sehemu ya kutayarishia chakula . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 31

• Usafi na usalama wa chakula . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 32

• Usafi na usalama wa maji ya kunywa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 32

Page 5: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

6. LISHE NA ULAJI WAKATI WA BAADHI YA MATATIZO YAKIAFYA YANAYOAMBATANA NA KUISHI NA VIRUSI VYAUKIMWI• Kukosa hamu ya kula . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 33

• Vidonda kinywani au kooni na utandu mweupe kinywani . . . . . . . . . . 34

• Kichefuchefu au kutapika . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 34

• Kuharisha . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 35

• Kupungua uzito . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 36

• Kukosa choo au kupata choo kigumu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 36

• Mafua na kikohozi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 37

• Homa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 37

• Upungufu wa wekundu wa damu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 38

• Kifua kikuu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 38

• Matatizo ya ngozi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 39

7. UHAKIKA WA CHAKULA KATIKA KAYA• Uhusiano kati ya uhakika wa chakula katika kaya na kuwepo kwa

virusi vya UKIMWI au UKIMWI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 41

• Jinsi ya kuzitambua kaya zisizokuwa na uhakika wa chakula . . . . . . . 41

• Jinsi ya kuboresha uhakika wa chakula katika kaya . . . . . . . . . . . . . . . 42

8. TATHMINI YA HALI YA LISHE• Historia ya ulaji wa chakula . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 45

• Vipimo vya umbile la mwili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 45

• Vipimo vya kibailojia na kikemia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 47

• Historia ya maradhi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 47

9. UHUSIANO KATI YA MATUMIZI YA DAWA NA CHAKULA• Jinsi chakula kinavyoingilia matumizi ya dawa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 49

• Jinsi dawa zinavyoingilia matumizi ya chakula mwilini . . . . . . . . . . . . 49

10. ULISHAJI WA MTOTO• Ulishaji wa mtoto wakati mama hana virusi vya UKIMWI au hafahamu

hali yake ya uambukizo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 53

• Ulishaji wa mtoto aliyezaliwa na mama mwenye virusi

vya UKIMWI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 57

• Uambukizo wa virusi vya UKIMWI kutoka kwa

mama kwenda kwa mtoto . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 58

• Vipengele muhimu vya kuzingatia wakati wa kutoa unasihi . . . . . . . . . 58

iv

Page 6: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

• Njia zinazoweza kutumika kumlisha mtoto mchanga aliyezaliwa na

mama mwenye virusi vya UKIMWI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 59

• Njia zinazoweza kutumika kumlisha mtoto mchanga tangu

anapozaliwa mpaka miezi 6 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 59

• Kutumia maziwa ya mama . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 60

• Kutumia maziwa mbadala . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 63

• Vyakula na maziwa yasiyofaa kumlisha mtoto mwenye umri

chini ya miezi sita . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 66

• Kumlisha mtoto wa miezi 6 hadi miaka 2 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 66

11. UNASIHI• Sifa za mnasihi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 69

• Aina za unasihi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 69

• Mahali pa kutolea unasihi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 70

• Mbinu za unasihi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 71

• Maadili katika unasihi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 72

• Unasihi unaohusu virusi vya UKIMWI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 72

• Unasihi kuhusu lishe . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 75

12. TANGAMANO NA UTANDAISHAJI• Umuhimu wa tangamano na utandaishaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 77

• Tangamano na utandaishaji katika huduma kwa watu wanaoishi na

virusi vya UKIMWI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 77

• Vidokezo muhimu vya kujenga tangamano na utandaishaji . . . . . . . . . 78

BIBLIOGRAFIA . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 79

FARAHASA . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 81

v

Page 7: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

VIFUPISHO

ARV – Antiretroviral

BMI – Body Mass Index

COUNSENUTH – The Centre for Counselling, Nutrition and Health Care

GDP – Gross Domestic Product

Ml – Mililita

NACP – National AIDS Control Programme

SHDEPHA+ – Service, Health and Development for People LivingPositively with HIV/AIDS

TACAIDS – Tanzania Commission for AIDS

TB – Turbeculosis

UKIMWI – Upungufu wa Kinga Mwilini

UNAIDS – Joint United Nations for AIDS

UNICEF – United Nations Children’s Fund

VCT – Voluntary Counselling and Testing

VVU – Virusi Vya UKIMWI

WAMATA – Walio katika Mapambano na UKIMWI Tanzania

WHO – World Health Organization

vi

Page 8: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

SHUKRANICOUNSENUTH inatoa shukrani za dhati kwa Rapid Funding Envelope for HIV/AIDS (RFE)kwa ufadhli ambao umewezesha kitabu hiki kutayarishwa na kutolewa.

Mashirika mbalimbali na watu binafsi wameshiriki kwa njia mbalimbali, katika hatua zakutayarisha kitabu hiki. Shukrani za pekee kwa Idara ya Sayansi na Teknolojia ya Vyakula yaChuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine na kwa Dr. John Msuya binafsi kwa kushiriki katikautayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki.

Shukrani zetu pia kwa Chuo cha Kilimo (MATI) – Uyole kwa kushirikiana nasi katika hatuambalimbali za utayarishaji wa kitabu hiki, vilevile kwa Pathfinder International, ofisi ya Tanzaniaambao walifadhili baadhi ya mafunzo ambayo yalitumika kwa majaribio ya awali ya kitabu hiki.

Tunatoa shukrani nyingi kwa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, Wizara ya Afya, ambaoawali walifadhili baadhi ya vijitabu kuhusu lishe kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWIambavyo ndio chimbuko kubwa la kitabu hiki. Vilevile tunapenda kumshukuru Dr. Roland Swaiwa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI kwa ushauri wa mara kwa mara, ambao pia ulitutiamoyo wa kuendelea na kazi hii.

Shukrani kwa washiriki wa mafunzo ya wakufunzi (TOT) ya lishe kwa watu wanaoishi na virusivya UKIMWI wa mikoa ya Arusha, Dar Es salaam, Kilimanjaro, Mbeya na Pwani na wale waChuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ambao walitumia kitabu hiki kwa majaribio na kutoa maonimengi ambayo yamesaidia kukiboresha.

COUNSENUTH inapenda pia kutambua wafuatao ambao walishiriki katika hatua mbalimbali:1. Abdallah Memba (SHDEPHA+)2. Belinda Liana (COUNSENUTH)3. Dr. Daniel Nyagawa (TFNC)4. Dr. John Msuya (SUA)5. Dr. Lunna Kyungu 6. Dr. Margareth Nyambo (Ilala Municipal Council)7. Eligy C. Mosille (RACC – Kilimanjaro)8. Hyacintha Musaroche (TAHEA)9. Mary G. Materu (COUNSENUTH)10. Mwanaisha Kikari (MATI – Uyole)11. Restituta Shirima (COUNSENUTH)12. Tuzie Edwin (COUNSENUTH)13. Victor Msinde 14. Virginia Kainamula

Wengi walichangia kwa njia mbalimbali, kwa kuwa hatujaweza kuwataja wote; tunatoa shukraninyingi kwa wote na tunawahakikishia kwamba COUNSENUTH inathamini sana michangoyenu yote.

Tunamalizia kwa kushukuru tena RFE ambao ndio waliowezesha kazi hii kukamilika.

vii

Page 9: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

DIBAJIWakati juhudi za kutafuta tiba ya UKIMWI zinaendelea, ni muhimu kutumia mbinu mbalimbalikatika kuboresha lishe, afya na maisha ya mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI au UKIMWI.Pamoja na kuwepo kwa dawa za kurefusha maisha kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWIau UKIMWI lishe bora na ulaji unaofaa huweza kuchangia katika kuboresha maisha nakupunguza ukali wa maradhi yanayoambatana na kuishi na virusi vya UKIMWI.Hali mbaya ya lishe kwa mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI ina madhara makubwa, hata katikahatua za mwanzo tu za uambukizo wa virusi vya UKIMWI. Matatizo mengi yanayoambatana nakuishi na virusi vya UKIMWI yanaingiliana na ulaji wa chakula na hali ya lishe, na mengi yamatatizo hayo yanaweza kupunguzwa kwa kuzingatia ulaji unaofaa wakati wa matatizo hayo.Shirika la Chakula Duniani lilipozindua kitabu kuhusu lishe na virusi vya UKIMWI (2003)ilitamkwa kwamba, “Lishe kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI imesahaulika kwa mudamrefu. Msisitizo umekuwa kwenye dawa zaidi; mara nyingi ujumbe umekuwa “tumia vidongeviwili baada ya kula chakula” lakini chakula chenyewe kimesahaulika”. Hii inatukumbushaumuhimu wa kuhakikisha kwamba lishe inapaswa kupewa kipaumbele.Lishe bora ni muhimu kwa binadamu yeyote hususan kwa mtu anayeishi na virusi vya UKIMWIau UKIMWI katika kipindi chote. Chakula sio dawa ya UKIMWI bali huboresha na kudumishalishe na afya ya mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI au UKIMWI. Chakula hufanya maishayawe bora zaidi na hivyo huweza kuchangia katika kurefusha maisha ya mtu anayeishi na virusivya UKIMWI.Katika nchi yetu uzoefu umeonyesha kwamba, watu wengi wamekuwa wakipata taarifa ambazosi sahihi na mara nyingine za kupotosha au kutatanisha kuhusu ulaji bora kwa mtu anayeishi navirusi vya UKIMWI au UKIMWI. Hii imewaacha watu wengi wenye virusi vya UKIMWI auUKIMWI katika hali ya mashaka na hata kuwafanya waache kabisa kutumia baadhi ya vyakulamuhimu bila sababu za msingi.Imeonekana pia kwamba, watu wengi hawana taarifa za kutosha kuhusu lishe kwa ujumla hatabila ya virusi vya UKIMWI. Hii imefanya waandishi wa kitabu hiki kuona umuhimu wa kutoakwanza taarifa kuhusu lishe kwa ujumla na kisha kuzungumzia lishe na UKIMWI. Mtuanapokuwa na taarifa sahihi na za kutosha kuhusu lishe katika hali ya kutokuwa na virusi vyaUKIMWI inakuwa rahisi kujifunza namna ya kuboresha lishe wakati mtu anaishi na virusi vyaUKIMWI au UKIMWI.Kitabu hiki pia kimetolewa wakati muafaka ambapo Taifa linaingia katika taratibu za kutoa dawaza kurefusha maisha. Taarifa za kuboresha lishe ni muhimu kwani lishe bora huchangia dawazinazotumika kufanya kazi vizuri mwilini.Tungependa kuwashauri wadau wanaohusika na utoaji wa huduma mbalimbali pamoja na unasihikwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI au UKIMWI kukisoma kitabu hiki. Kitabu hikikimeweka pamoja taarifa zilizopo kuhusu lishe kwa mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI kwanamna na lugha ambayo inaeleweka na wengi. Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWIwatanufaika moja kwa moja na taarifa zilizopo ndani ya kitabu hiki.Tukisome kitabu hiki, tujitahidi kufuata yaliyoshauriwa na tuishi kwa matumaini...!!!!!!!!!

viii

Meja Jenerali (Mstaafu) Herman C. LupogoMwenyekiti MtendajiTume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS)

Page 10: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

UTANGULIZIKwa kiasi kikubwa juhudi za kuwahudumia watu wanaoishi na virusi vya UKIMWIzimekuwa zikielekezwa katika kutibu maambukizo mbalimbali yanayohusiana nakuwepo kwa virusi hivyo. Hata hivyo taarifa zinaonyesha kwamba utapiamlo au lisheduni imechangia kwa kiasi kikubwa katika kudhoofisha afya ya watu wanaoishi na virusivya UKIMWI na kusababisha vifo.

Ni kweli kwamba chakula hakiwezi kuponyesha UKIMWI, lakini chakula kinawezakuboresha afya na ubora wa hali ya maisha kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI.Kula chakula cha kutosha na chenye mchanganyiko wa vyakula vya aina mbalimbalihusaidia kudumisha uzito wa mwili na kujenga misuli. Ulaji bora husaidia kudumisha nakuboresha ufanisi wa mfumo wa kinga ya mwili, ambao husaidia mwili kujikinga navimelea mbalimbali vya maradhi.

Mengi ya matatizo au maradhi yanayoambatana na hali ya kuishi na virusi vya UKIMWIau UKIMWI yanaathiri mfumo wa chakula mwilini, ambao hujumuisha ulaji wachakula, uyeyushwaji na usharabu wa virutubishi mwilini. Baadhi ya maradhi hayo piahuathiri hali ya umetaboli wa mwili. Lishe bora huweza kusaidia kukabiliana namatatizo yanayoambatana na kuishi na virusi vya UKIMWI. Hivyo ni muhimu kutumiambinu mbalimbali kuboresha chakula na ulaji kwa watu wanaoishi na virusi vyaUKIMWI ili kuboresha hali ya afya na lishe ya watu hao, na hivyo ubora wa maisha.

Kwa sasa katika Tanzania masuala ya jinsi ya kuwahudumia watu wanaoishi na virusivya UKIMWI upande wa lishe hayafahamiki kiasi cha kutosha na wakati mwinginetaarifa zilizopo ni za kiingereza na hivyo kuwa vigumu kwa watu wengi kuzitumia. Kwakuzingatia ukweli huo, Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH)kimeamua kukusanya pamoja katika kitabu hiki mada muhimu zinazopatikana kwa sasakuhusiana na suala hili. Mada hizi zimejadiliwa na kuchambuliwa kwa kina nawataalamu na wadau mbalimbali kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbalizinazohusika na afya, lishe; na pia watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI hapaTanzania.

Kitabu hiki kina sura kumi na mbili, kikianza kwa kuelezea kwa ujumla mambo muhimukuhusu virusi vya UKIMWI na UKIMWI (Sura ya Kwanza) ikiwa ni pamoja na jinsiuambukizo unavyoweza kutokea, tofauti kati ya kuwa na virusi vya UKIMWI na kuwana UKIMWI, na athari za UKIMWI kijamii na kifamilia. Ili kuwa na uelewa mzuri wajinsi ambavyo lishe inahusiana na UKIMWI, ni muhimu kufahamu elimu ya msingi yachakula na lishe. Sura ya Pili imelenga katika kumpatia msomaji elimu hiyo, wakati suraya tatu imeainisha matatizo makuu ya lishe hapa kwetu Tanzania. Msomaji ambaye anamsingi mzuri wa elimu ya chakula na lishe anaweza akaanza sura ya nne moja kwa mojaambayo inaeleza mada mbalimbali za lishe kwa mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI auUKIMWI. Sura hii inaonyesha uhusiano wa lishe na virusi vya UKIMWI, ulaji bora na

1

Page 11: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

mbinu zinazoweza kutumika kuboresha chakula, pamoja na mambo muhimu yakuzingatia ikiwa ni pamoja na mambo ya kuepuka.

Suala la lishe na ulaji unaofaa wakati wa matatizo mbalimbali yanayoambatana nakuwa na virusi vya UKIMWI au UKIMWI yameelezwa kwa kina katika Sura ya Sita.Matatizo hayo ni pamoja na kukosa hamu ya kula, kichefuchefu au kutapika,kuharisha, kupungua uzito, vidonda vya kinywani au kooni na utandu mweupekinywani. Mengine ni kukosa choo au kupata choo kigumu, mafua na kikohozi,homa, upungufu wa wekundu wa damu, kifua kikuu na matatizo ya ngozi.

Kitabu pia kimegusia masuala mengine muhimu kwa mtu anayeishi na virusi vyaUKIMWI. Masuala hayo ni pamoja na usafi na usalama wa chakula na maji (Sura yaTano), uhakika wa chakula katika kaya (Sura ya Saba), na jinsi ya kutathmini hali yalishe ya mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI (Sura ya Nane). Mengine ni unasihi(Sura ya Kumi na Moja) na tangamano na utandaishaji (Sura ya Kumi na Mbili). Kwakuwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI au wale ambao wana UKIMWIwanatumia dawa za aina nyingi katika kukabiliana na maradhi yanayoambatana nakuishi na virusi vya UKIMWI, Sura ya Tisa inaelezea uhusiano uliopo kati yamatumizi ya dawa na chakula, hasa kudokeza jinsi ambavyo dawa na vyakulavinavyoweza kuingiliana. Kwa watu wengi, bado kuna utata kuhusu jinsi yakumlisha mtoto aliyezaliwa na mama mwenye virusi vya UKIMWI. Kwa kutumiataarifa zinazotolewa na mashirika ya kimataifa yanayoshughulikia afya na watotoDuniani na taasisi za kitaifa, kitabu hiki kimelielezea kwa kifupi suala hili katika Suraya Kumi.

COUNSENUTH inaamini kwamba huduma ya lishe bora ni muhimu sana kwa mtuanayeishi na virusi vya UKIMWI, hivyo ingependa kuona, kupitia kitabu hiki, madazilizopo zinawafikia wale wote wanaowahudumia watu wanaoishi na virusi vyaUKIMWI. Kipekee kitabu hiki ni rejea nzuri kwa wale wanaotoa mafunzo kwawanasihi, waelimishaji, wahudumu wa afya pamoja na watoa huduma nyingine kwawatu wanaoishi na virusi vya UKIMWI.

2

Page 12: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

MAMBO MUHIMU KUHUSU VIRUSI VYAUKIMWI

Mtoa huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI akiwepo mnasihi inabidiaelewe mambo ya msingi kuhusu virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwani atalazimikamara kwa mara kujibu maswali ya wateja kuhusu ugonjwa huo. Vilevile moja yamajukumu ya mtoa huduma na mnasihi ni kusahihisha taarifa potofu kuhusu virusi vyaUKIMWI au UKIMWI na kutoa taarifa sahihi. Sura hii inaelezea mambo muhimukuhusu virusi vya UKIMWI au UKIMWI.

Hali ya UKIMWI nchini TanzaniaMnamo mwaka 1983, watu watatu wenye UKIMWI waligundulika katika mkoa mmojana ilipofika mwaka 1986 mikoa yote Tanzania bara ilishatoa ripoti za kuwepo kwawagonjwa wa UKIMWI. Hali inaendelea kuwa mbaya kwani idadi ya watu wanaoishina virusi vya UKIMWI na wenye UKIMWI inaongezeka kila mwaka.

Vilevile maambukizo ya maradhi ya ngono yameendelea kuripotiwa. Hii inaashiria kuwawatu hawafanyi ngono salama na hivyo kuongeza hatari ya uambukizo wa virusi vyaUKIMWI.

Hapo awali mkazo mkubwa wa kupambana na virusi vya UKIMWI uliwekwa kwenyeelimu ya kuzuia uambukizo na unasihi kabla na baada ya kupima. Hivi sasa mkazoumewekwa pia kwenye unasihi endelevu, lishe bora, kumpa mtu matumaini, utunzaji wawagonjwa majumbani, usafi na matibabu ya magonjwa nyemelezi.

Jinsi Uambukizo wa Virusi vya UKIMWI Unavyotokea

Virusi vya UKIMWI huhitaji aina fulani ya majimaji ili kuweza kuishi. Majimajiyanayoweza kueneza virusi vya UKIMWI ni kama; damu, uteute wa ukeni, maziwa yamama, shahawa, majimaji mengine ya mwili kama maji ya vidonda, usaha, n.k.

Majimaji haya huhitaji mlango wa kupitia ili uambukizo utokee. Mlango waweza kuwa:

- Sehemu iliyokatwa au kuchubuka kama kidonda

- Tishu laini inayoitwa utando telezi (mucus membrane) iliyoko kwenye uke, kichwacha uume, mkundu, macho au pua.

Njia zinazoambukiza na zisizoambukiza virusi vya UKIMWI

Njia zinazoambukiza virusi vya UKIMWI

Zipo njia kuu nne zinazoweza kufanya mtu aambukizwe virusi vya UKIMWI, nazo ni:

• Kufanya ngono na mtu mwenye virusi vya UKIMWI bila kutumia kinga. Ngonohiyo inaweza kuwa ya ukeni, mkunduni au mdomoni.

• Mama kumwambukiza mtoto wakati wa mimba, uchungu na kujifungua aukunyonyesha.

1

1. M

AM

BO

MU

HIM

U K

UH

US

U V

IR

US

I V

YA

UK

IM

WI

3

Page 13: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

4

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

• Kupewa damu au vitu vitokanavyo na damu yenye virusi vya UKIMWI au majimaji mengine ya mwili.

• Kuchangia sindano, mabomba ya sindano, nyembe na vifaa vyenye ncha kaliambavyo vimetumika kwa mtu mwenye virusi vya UKIMWI.

Njia kuu za kuambukizwa virusi vya UKIMWI nchini TanzaniaHapa Tanzania takwimu zilizotolewa na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI(Machi 2003) zimeonyesha kwamba uambukizo unatokea kama ifuatavyo: • Kwa kujamiiana na mtu wa jinsi tofauti aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI –

82.1%• Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua

au wakati wa kunyonyesha – 5.9%• Kuongezewa damu yenye virusi vya UKIMWI – 0.3%• Njia nyingine – 1.7%• Chanzo hakikujulikana – 10%

Chanzo: NACP Surveillance Report, 2003

Njia zisizoambukiza virusi vya UKIMWI

Mtu hawezi kuambukizwa virusi vya UKIMWI kwa:

• Kuumwa na mbu au wadudu wengine

• Kukohoa au kupiga chafya kunakofanywa na mtu aliyeambukizwa virusi vyaUKIMWI

• Kula pamoja na mtu mwenye virusi vya UKIMWI

• Kuchangia vyoo au bafu na mtu mwenye virusi vya UKIMWI

• Kusafiri pamoja na mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI

• Kuchangia mabwawa ya kuogelea

• Kuchangia vikombe na vifaa vya kulia chakula

• Kupeana busu kavu

Athari za UKIMWI Kijamii na Kifamilia• UKIMWI ni tatizo linaloathiri maendeleo na linagusa sekta zote muhimu katika

maisha ya jamii. Juhudi zote za maendeleo zilizofanyika katika miaka ya hivi karibunizinadhoofishwa na mzigo wa kuwahudumia waathirika na kupungua kwa nguvu kazikutokana na vifo vinavyotokana na UKIMWI.

• Sekta muhimu kama Afya, Kilimo, Biashara na Elimu zimeathirika. Kwa mfanokatika sekta ya Afya, UKIMWI unazidi kudhoofisha huduma za hospitali na vituovya afya kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wa UKIMWI wanaohitaji huduma

Page 14: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

hizo. Hivi sasa zaidi ya nusu ya nafasi za kulaza wagonjwa katika hospitali za serikalizinatumiwa na wenye maradhi yanayohusiana na UKIMWI. Huduma za msingi kwawagonjwa hao zimekuwa hazitoshi kutokana na wagonjwa wa aina hiyo kuongezekasiku hadi siku.

• Kwa familia, UKIMWI umeongeza umasikini kwa kupunguza uwezo wa familiakujihudumia.

• Wagonjwa wenye kifua kikuu wameongezeka mara tano tangu 1983 hadi 2001.Nusu ya wagonjwa wa kifua kikuu wameambukizwa virusi vya UKIMWI.

• Idadi ya watu wanaokosekana sehemu zao za kazi kwa ajili ya kuumwa aukuwatunza wanafamilia wenye virusi vya UKIMWI na vifo vya waajiriwavinavyotokana na UKIMWI vinaongezeka.

• Matarajio ya muda wa kuishi umepungua. Umri wa kuishi kwa wastani ulikuwamiaka 53 (mwaka 1988) na mwaka 1998 ulikuwa miaka 48.

• Uambukizo zaidi uko kwa watu wenye umri kati ya miaka 20 hadi 49. Watu hawandiyo nguvu kazi ya taifa. Kwa hiyo UKIMWI unaangamiza sehemu kubwa yawazalishaji.

Virusi vya UKIMWI na Kinga ya Mwili Virusi vya UKIMWI hushambulia kinga ya mwili ya mwanadamu. Mfumo wa kinga yamwili wa mwanadamu umegawanyika katika makundi ya chembechembe maalumzenye kazi mbalimbali kama:-

- Macrofeji – Chembechembe hizi hutuma taswira ya ugonjwa kwa nahodha

- B Cell – Kiwanda cha kinga ya mwili; hutengeneza kinga ya mwili (antibodies)

- CD4 T Cell – Nahodha au amiri jeshi mkuu, hutoa maagizo au maelekezo

- T8 Cell – Hutoa sumu ya kuua

Virusi vya UKIMWI hushambulia aina ya chembechembe zijulikanazo kama CD4 TCell. Chembechembe hizi ni muhimu sana kwani ndizo zinazotoa maagizo aumaelekezo kwa makundi mengine kujibu mashambulio ya maradhi mwilini. Kwamantiki hiyo virusi vya UKIMWI vikiua CD4 T Cell, mfumo wa kinga mwilinihauwezi kufanya kazi kwani chembechembe nyingine hazipati maagizo au maelekezoyoyote. Mfumo wa kinga ya mwili unapokosa maagizo au maelekezo ya kushambuliaviini vya maradhi, mwanadamu hushambuliwa na maradhi mengi kwa wakati mmoja.Maradhi hayo ambayo yasingemshambulia mwanadamu kama angekuwa na mfumothabiti wa kinga yanajulikana kama “magonjwa nyemelezi”.

5

Page 15: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

6

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Tofauti kati ya kuwa na virusi vya UKIMWI na kuwa na UKIMWIMtu anapoambukizwa virusi vya UKIMWI haanzi kuugua mara moja, mtu huwezakuishi na virusi hivyo kwa muda mrefu bila kuonyesha dalili zozote. Aliyeambukizwahuweza kuishi katika hali hiyo hata kwa muda wa miaka 15 na zaidi.

Mtu mwenye UKIMWI ni yule ambaye amekwishaanza kuonyesha dalili za magonjwanyemelezi yanayotokana na kinga yake ya mwili kuharibiwa na virusi vya UKIMWI.Magonjwa hayo ni kama kuharisha, kukohoa, kuvimba matezi, ugonjwa wamalengelenge ya neva ngozini (mkanda wa jeshi) na utando mweupe kinywani. Lakiniikumbukwe kwamba, siyo kila mtu anayeugua magonjwa hayo ana virusi vyaUKIMWI. Kwa hiyo njia ya kuthibitisha uambukizo ni kupima.

Kwa kifupi kuna hatua kuu tatu ambazo mtu anapitia kuanzia kuambukizwa hadikuugua UKIMWI. Hatua hizo ni:

Kipindi ficho

Hiki ni kipindi baada tu ya mtu kuambukizwa. Katika kipindi hicho mtu anaishi navirusi vya UKIMWI katika damu yake bila ya kuonyesha dalili zozote na hata vipimovya maabara haviwezi kutambua. Hata hivyo mtu huyo ana uwezo wa kumwambukizavirusi vya UKIMWI mtu mwingine. Kipindi hicho huweza kudumu kwa muda wamiezi mitatu hadi sita baada ya kuambukizwa.

Kipindi tuli

Hiki ni kipindi ambacho aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI haonyeshi dalili zozoteingawa vipimo vya maabara vitaonyesha dalili za kuwepo kwa virusi hivyo. Kipindihicho kinaweza kudumu kati ya miezi mitatu hadi miaka 15 au zaidi.

Utata mwambata wa UKIMWI

Hiki ni kipindi cha kujitokeza kwa ugonjwa na dalili zisizo mahususi kama vilekuvimba tezi, kichefuchefu, kuharisha kwa muda mrefu, upungufu wa uzito, homa nauchovu.

Ugonjwa kamili wa UKIMWI

Hiki ni kipindi ambapo mtu huonyesha dalili za wazi za UKIMWI ambazo ni zamaambukizo ya magonjwa nyemelezi. UKIMWI kamili ni ile hatua ya mwisho yauambukizo wa virusi vya UKIMWI. Katika hatua hii bila matibabu, mgonjwa anawezaakafariki baada ya muda mfupi.

Page 16: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Sababu zinazochangia kuongezeka kwa uambukizo wa virusi vya UKIMWI

• Utamaduni wa ukimya katika masuala ya ngono

• Mahusiano ya jinsia, ambapo mara nyingi mwanamke hana uwezo wa kufanyamaamuzi kuhusu ngono

• Umaskini

• Kutengana kwa wanandoa kwa sababu mbalimbali

• Ukosefu wa maandalizi thabiti ya vijana kuhusu masuala ya ujinsia na uzazi

• Mnyanyapao na Ubaguzi

Mnyanyapao na UbaguziMnyanyapao ni mtazamo au fikra zinazolenga kudhalilisha na kuondoa hadhi ya mtuna utu, zikilenga wale wanaodhaniwa kuwa ni tofauti katika jamii na ni aibu mbele zawatu wengine. Ni hisia zinazompunguzia au kumuondolea mhusika thamani, heshima,umaarufu na stahili ya kupata haki mbalimbali. Hatimaye mhusika kutengwa kutokakundi la jamii linalohisi kuwa bora, takatifu au maarufu zaidi kuliko mtu au jamiinyingine. Kumekuwa na tabia ya kuwanyanyapaa na kuwabugua watu wanaoishi navirusi vya UKIMWI na wenye UKIMWI. Zipo sababu kuu mbili kwa nini watuhufanya hivyo.

Kielelezo Na. 1: Mchoro wa mabadiliko ya hali ya UKIMWI mwilini

Chanzo: Peace Corps, Mwongozo wa stadi za maisha, 2001

7

Page 17: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Sababu hizo hutokana na mawazo potofu:

• Kwanza, watu hupenda kuhusisha kuambukizwa virusi vya UKIMWI na ngono,ukosefu wa maadili, dhambi, n.k. Kwa hiyo mtu mwenye UKIMWI huchukuliwakama amejitafutia mwenyewe ugonjwa kutokana na tabia yake.

• Pili, watu huwanyanyapaa watu hao kwa kuhofu kwamba wakiwa karibu nao auwakiwahudumia wataambukizwa.

Fikra hizo potofu huwafanya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI au UKIMWIkubaguliwa na wanafamilia (ambao ndiyo wanaopaswa kuwahudumia), wanajamiiwengine au waajiri wao.

Mnyanyapao wa UKIMWI ni mchanganyiko wa aibu na woga. Mnyanyapaohuchochewa na:

- Kutokuwa na taarifa sahihi kuhusu ugonjwa

- Mila na imani potofu kuhusu uenezwaji wa ugonjwa

- Majivuno

- Ukosefu wa tiba

- Mila zinazohusiana na ngono

- Kuhusisha ugonjwa na kufa

- Watu wasiojali

Athari za mnyanyapao na ubaguzi

- Huzuia watu kutafuta tiba na huduma

- Huzuia uwazi kuhusu UKIMWI

- Hurudisha nyuma majadiliano ya wazi

- Huwafanya watu wenye virusi vya UKIMWI au UKIMWI kujitenga na hudumambalimbali

- Ni kikwazo katika kuzuia kuenea kwa virusi vya UKIMWI

- Huwanyima watu wenye virusi vya UKIMWI au UKIMWI nafasi za kazi, mahalipa kuishi, bima, n.k.

- Watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI hukata tamaa na wengine kujiua

- Huwafanya watu wengine kueneza virusi vya UKIMWI kwa makusudi

- Husababisha watu kuchanganyikiwa

- Jamii huathirika kiutendaji

8

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Page 18: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Ni muhimu kuacha mnyanyapao na ubaguzi

• Jamii ipate elimu ya kutosha kuhusu uambukizo wa virusi vya UKIMWI

• Mtu hawezi kuambukizwa virusi vya UKIMWI kutokana na mahusiano ya kawaidamfano kula pamoja, kushikana mikono, kuchangia vyoo au bafu, n.k

• Jamii na familia zipate mafunzo kuhusu utunzaji wa mtu anayeishi na virusi vyaUKIMWI au UKIMWI

• Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI apate mahitaji muhimu yakiwemo ya kirohona lishe

• Jamii ifundishwe kuachana na imani potofu zinazochangia kuwepo kwamnyanyapao zikiwemo imani kwamba mtu huyo ni mdhambi au amekosa maadili

• Jamii ijenge tabia ya kuwapenda na kuwatunza wagonjwa

9

Page 19: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

10

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Page 20: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

ELIMU YA MSINGI YA CHAKULA NALISHE

Umuhimu wa Chakula kwa Binadamu Chakula na lishe bora ni muhimu kwa binadamu wote. Chakula ni kitu chochotekinacholiwa na kuupatia mwili virutubishi; ambapo lishe ni sayansi ya jinsi mwiliunavyokitumia chakula. Lishe inahusisha jinsi mwili unavyosaga na unavyoyeyushachakula na hatimaye virutubishi kusharabiwa (kufyonzwa) na kutumika mwilini.

Faida za chakula kwa binadamu:- Kutengeneza seli za mwili na kurudishia seli zilizokufa au kuharibika

- Ukuaji wa akili na mwili

- Kuupa mwili nguvu, joto na uwezo wa kufanya kazi

- Kuupa mwili kinga dhidi ya maradhi mbalimbali

Ulaji bora ambao unazingatia chakula mchanganyiko na cha kutosha ni muhimu kwabinadamu wote, na ni muhimu zaidi kwa wagonjwa wakiwemo wale wanaoishi na virusivya UKIMWI au UKIMWI.

Inasisitizwa kula chakula mchanganyiko na cha kutosha mara zote kwani hakunachakula kimoja pekee ambacho kinaweza kumpatia binadamu mahitaji yake yote yakilishe isipokuwa maziwa ya mama tu kwa mtoto katika kipindi cha miezi sita yamwanzo.

Virutubishi, umuhimu na vyanzo vyakeVirutubishi ni viini vya kikemia vilivyoko kwenye vyakula ambavyo mwili hutumia ilikufanya kazi mbalimbali. Karibu vyakula vyote vina virutubishi zaidi ya kimoja ila kwakiasi tofauti. Vyakula vingine huwa na virutubishi vya aina fulani kwa wingi zaidi. Kilakirutubishi kina kazi yake katika mwili wa binadamu, na vingi hutegemeana ili kufanyakazi vizuri mwilini. Zifuatazo ni aina za virutubishi:

- Kabohaidreti

- Protini

- Mafuta

- Vitamini

- Madini

2

11

2

EL

IM

U Y

A M

SIN

GI Y

A

CH

AK

UL

A

NA

LIS

HE

Page 21: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

• KabohaidretiHiki ni kirutubishi muhimu kwa kuupa mwili nishati (nguvu) kwa ajili ya kufanya kazimbalimbali pamoja na joto. Kabohaidreti ndio inayochukua sehemu kubwa ya mlo.Kabohaidreti inajumuisha wanga, sukari na nyuzinyuzi. Vyakula vyenye kabohaidretikwa wingi ni pamoja na mahindi, mchele, uwele, ngano, viazi vya aina zote, mihogo,ndizi, sukari na baadhi ya matunda. Nyuzinyuzi ni muhimu sana katika uyeyushwajiwa chakula.

• Protini

Protini ni muhimu sana kwa ukuaji wa mwili na akili. Protini husaidia mwilikutengeneza seli mpya, kutengeneza vimeng’enyo mbalimbali na wakati mwingineprotini huupa mwili nishati kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Baadhi ya vyanzo vizurivya protini ni aina zote za nyama, samaki, aina za mikunde kama choroko, kunde,maharagwe, soya, karanga, pia maziwa, mayai, dagaa na wadudu wa aina mbalimbaliwanaoliwa kama kumbikumbi, senene, n.k.

• Mafuta

Mafuta huhitajika mwilini kwa ajili ya kuupa mwili nguvu na joto pamoja na kusaidiausharabu wa baadhi ya vitamini. Mafuta pia hulainisha chakula na kukifanya kiwe naladha nzuri, na hivyo kumfanya mlaji ale chakula cha kutosha. Mafuta hupatikana kwawingi kwenye samli, siagi, baadhi ya nyama, baadhi ya samaki, mbegu zitoazo mafutakama ufuta, korosho, mbegu za maboga, karanga, alizeti, mbegu za pamba, kweme,mawese pamoja na nazi.

• Vitamini

Vitamini zinahitajika mwilini kwa ajili ya kulinda mwili pamoja na kuufanya mwiliufanye kazi zake za umetaboli vizuri. Vitamini ziko za aina nyingi na zinapatikana kwawingi kwenye mboga-mboga, matunda na kwenye vyakula vinavyotokana na wanyamakama maziwa, aina zote za nyama, mayai, dagaa, samaki, n.k.

• Madini

Madini kama ilivyo vitamini hulinda mwili na kuufanya ufanye kazi zake za umetabolivizuri. Kuna aina nyingi za madini, na baadhi ya vyakula vyenye madini kwa wingi nipamoja na vyakula vinavyotokana na wanyama, dagaa, samaki, mboga-mboga namatunda.

12

KUMBUKAVyakula huwa na kirutubishi zaidi ya kimoja, hivyo vyakula vinavyotajwa

kwenye kirutubishi fulani humaanisha vyakula hivyo vina kirutubishi hicho kwa wingi.

Page 22: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

13

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Jedwali Na. 1: Baadhi ya virutubishi, umuhimu na vyanzo vyake

Chanzo: FANTA, 2003

Page 23: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Makundi ya vyakula na mlo kamiliPamoja na kuzungumzia virutubishi mbalimbali, ni muhimu kukumbuka kwamba mtuanapokula hafikirii virutubishi bali chakula. Hivyo ni muhimu katika kujifunza ulajibora, kutumia makundi ya vyakula badala ya aina za virutubishi. Pia ni muhimukukumbuka kwamba vyakula vingi vina virutubishi zaidi ya kimoja, na pia kiasihutofautiana.Kwa afya na lishe bora, inashauriwa kula mlo kamili (chakula mchanganyiko). Mlokamili hutokana na vyakula ambavyo vimewekwa pamoja kwa namna ambayo vikiliwapamoja huupatia mwili virutubishi vyote muhimu kwa afya bora. Hutayarishwakutokana na mchanganyiko wa angalau chakula kimoja kutoka katika kila kundi, katikamakundi yafuatayo:

• Vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi:Vyakula hivi ndivyo vinavyochukua sehemu kubwa ya mlo na kwa kawaida ndiyovyakula vikuu. Vyakula katika kundi hili ni pamoja na mahindi, mchele, mtama, ulezi,ngano, uwele, viazi vikuu, viazi vitamu, mihogo, magimbi, viazi mviringo na ndizi.

• Vyakula vya mikunde na vyenye asili ya wanyama:Vyakula vilivyoko katika kundi hili ni pamoja na maharagwe, njegere, kunde, karanga,soya, njugu mawe, dengu, choroko na fiwi. Vile vyenye asili ya wanyama ni pamoja nanyama, samaki, dagaa, maziwa, mayai, jibini, maini, figo, senene, nzige, kumbikumbi nawadudu wengine wanaoliwa.

• Mboga-mboga:Kundi hili linajumuisha aina zote za mboga za majani zinazoliwa, zile zinazolimwa nazinazoota zenyewe. Mboga-mboga ni pamoja na mchicha, majani ya maboga, kisamvu,majani ya kunde, matembele, spinachi, mnafu, mchunga, pia aina nyingine za mbogakama karoti, pilipili hoho, biringanya, matango, maboga, nyanya chungu na bamia,bitiruti, kabichi na figiri.

• Matunda:Kundi hili linajumuisha matunda ya aina zote kama mapapai, maembe, mapera,malimau, mapesheni, mananasi, peasi, machungwa, machenza, zambarau, mafenesi,mastafeli, mabungo, pichesi, topetope. Aidha “matunda pori” yana ubora sawa namatunda mengine. Matunda hayo ni kama ubuyu, ukwaju, embe ng’ong’o, mikoche,n.k.

• Mafuta na sukari:Mafuta na sukari ni muhimu ingawa vinahitajika kwa kiasi kidogo mwilini. Mafutayanaweza kupatikana kutoka kwenye mimea kama mbegu za alizeti, ufuta, karanga,mawese, mbegu za pamba n.k na kutoka kwa wanyama kama siagi, samli na nyama yamafuta. Sukari inapatikana kwenye sukari, miwa, asali na vyakula ambavyovinatengenezwa kwa sukari nyingi kama jamu.

14

Page 24: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

� Maji

Maji kwa kawaida hayahesabiwi kama kundi la chakula, lakini yana umuhimumkubwa katika afya na lishe ya binadamu. Inapaswa kunywa maji ya kutosha,angalau lita moja na nusu (glasi nane) kwa siku au hata zaidi. Inashauriwa kunywamaji zaidi wakati wa joto kali ili kuzuia upungufu wa maji mwilini. Vilevile unawezakuongeza maji mwilini kwa kunywa vinywaji kama supu, madafu, juisi za matundambalimbali.

Mtu anatakiwa kula mchanganyiko wa vyakula kwenye mlo mmoja kwa sababuhakuna chakula kimoja chenye virutubishi vyote muhimu kwa ajili ya lishe na afyabora. Vilevile baadhi ya virutubishi hutegemeana ili kuweza kufanikisha kazi zakemwilini. Kwa mfano madini ya chuma yanayopatikana kwenye vyakula vya mimeakama mboga-mboga za kijani husharabiwa vizuri mwilini kama kuna vitamini Cambayo hupatikana kwa wingi kwenye matunda. Mfano mwingine ni zile vitaminikama A, D, E, K ambazo usharabu na utumikaji wake mwilini hutegemea kuwepokwa mafuta. Vilevile nishati huweza kutumika vizuri mwilini iwapo kuna aina zavitamini B kwenye vyakula.

Kwa mtu yeyote ni muhimu kula mlo ulio kamili angalau mara mbili au tatu kwa sikuna asusa (vitafunwa) kati ya mlo mmoja na mwingine.

KUMBUKA

Katika jamii zetu, matumizi ya mboga-mboga na matunda yamesahaulikasana. Inabidi kusisitiza umuhimu wa kuhakikisha kwamba mboga-mboga

na matunda vinakuwa sehemu ya mlo

15

Page 25: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

16

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Page 26: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

MATATIZO MAKUU YA LISHE TANZANIAKuna matatizo mengi ya utapiamlo hapa nchini Tanzania yanayotokana na

upungufu wa virutubishi mwilini. Matatizo makuu ni upungufu wa nishati na protini,upungufu wa wekundu wa damu, upungufu wa vitamini A na upungufu wa madini yajoto. Hali hizo zinaweza kusababishwa na ukosefu wa chakula cha kutosha na chenyevirutubishi muhimu na magonjwa. Pia zipo sababu zilizofichika na za msingi kamazilivyoonyeshwa katika kielezo Na. 2 cha “Dhana ya Utapiamlo”.

Dhana ya Utapiamlo inaweza kutumika kuelezea sababu za matatizo ya lishe. Dhana hiiina sehemu kuu tatu nazo ni : sababu za karibu, sababu zilizofichika na za msingi.

Kielelezo Na. 2: Dhana ya Utapiamlo

3

Chanzo: Imetafsiriwa kutoka WHO/UNICEF/BASICS, Nutrition Essentials,1999

3. M

AT

AT

IZ

O M

AK

UU

YA

LIS

HE

TA

NZ

AN

IA

17

Page 27: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

18

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Upungufu wa nishati na protiniUpungufu wa nishati na protini husababishwa na:

• Ulaji duni hasa ule wa vyakula vya nishati na protini

• Maradhi hasa yale ya mara kwa mara kama homa na malaria

• Maradhi ya muda mrefu kama vile saratani na UKIMWIKatika Tanzania tatizo hili la upungufu wa nishati na protini huwapata hasa watotowalio chini ya umri wa miaka mitano, wanawake wajawazito, wanawakewanaonyonyesha na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI. Lakini tatizo hili huwezapia kuwapata watu wengine.

Athari za upungufu wa nishati na protini

• Tatizo la upungufu wa nishati na protini linapowapata wanawake wajawazitohuweza kusababisha ukuaji duni wa mtoto akiwa tumboni na hivyo mtotokuzaliwa na uzito pungufu (chini ya kilo 2.5).

• Kwa watoto, upungufu wa nishati na protini husababisha ukuaji duni, maradhi yamara kwa mara, na hata vifo.

• Kwa watu wazima, upungufu huu husababisha mtu kupungua uzito, kukonda sanana hivyo kuwa dhaifu.

Kudhibiti upungufu wa nishati na protini� Mwanamke mjamzito na anayenyonyesha anaweza kudhibiti upungufu huo kwa:

• Kula chakula cha kutosha na cha mchanganyiko

• Kuongeza idadi ya milo au kiasi cha chakula kwa siku

• Kupunguza kazi nyingi na nzito

• Kupata huduma muhimu za afya kama vile za kutibu maradhi , chanjo, kupatavidonge vya kuongeza wekundu wa damu na huduma za uzazi wa mpango

� Kwa watoto, upungufu huo unaweza kudhibitiwa kwa:

• Kumnyonyesha mtoto mara baada ya kujifungua katika saa moja ya mwanzona kuhakikisha mtoto anapata maziwa ya mwanzo yenye rangi ya njano

• Kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee mpaka afikishapo umri wamiezi sita

• Kumnyonyesha mtoto kila anapohitaji kunyonya, usiku na mchana

• Kumwanzishia mtoto chakula cha nyongeza mara afikishapo umri wa miezi 6,huku akiendelea kunyonyeshwa maziwa ya mama mpaka afikishe umri wamiaka miwili au zaidi

• Kumpa mtoto chakula cha kutosha na cha mchanganyiko si chini ya mara 5kwa siku

• Kutibu maradhi yote mapema

Page 28: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

• Kupata huduma zote zinazotolewa kliniki

� Kwa wagonjwa:

• Kula chakula cha mchanganyiko na cha kutosha

• Kula milo midogo midogo mara kwa mara

• Kutibu maradhi yote mapema

� Kwa jamii nzima:

• Kula chakula mchanganyiko na cha kutosha

• Kuzuia maradhi na kutibiwa mapema

• Kutumia huduma ya uzazi wa mpango (kwa wale walioko kwenye umri wakuzaa)

Upungufu wa wekundu wa damuUpungufu wa wekundu wa damu ni moja ya matatizo ya utapiamlo yanayoathiri watuwengi ikiwemo wanaoishi na virusi vya UKIMWI na huweza kusababisha vifo.Upungufu wa wekundu wa damu pia huwapata zaidi wanawake wajawazito na watotowalio chini ya miaka mitano.

Upungufu wa wekundu wa damu hutokana na sababu nyingi zikiwemo:

• Kutokula chakula cha kutosha na chenye virutubishi muhimu kwa ajili yautengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu kama vile madini ya chuma,protini na vitamini.

• Utayarishaji wa chakula usio bora. Kwa mfano kuosha mboga za majani baada yakukatakata, kupika kwa muda mrefu na kumwaga maji yaliyopikiwa mboga-mbogahasa za kijani.

• Kunywa vinywaji vyenye kafeini kwa wingi wakati wa mlo. Vinywaji vyenyekafeini kwa wingi kama chai na kahawa vinapotumika wakati wa mlo huingiliausharabu wa madini ya chuma yanayopatikana kwenye vyakula vya mimea.

• Maradhi mbalimbali hasa malaria, UKIMWI, saratani, vidonda vya tumbo naminyoo kama safura na kichocho.

• Uzazi wa karibu karibu. Ujauzito huongeza mahitaji ya virutubishi mwilini ikiwani pamoja na madini ya chuma ambayo hutumika kutengeneza chembechembenyekundu za damu ya mama na mtoto. Mimba nyingi na za karibu karibuhusababisha mwili kushindwa kurudisha akiba ya madini ya chuma yaliyotumikakatika mimba zilizotangulia hivyo kuleta upungufu mkubwa wa wekundu wa damumwilini hasa kama ulaji wa chakula wa mama ni duni.

• Matatizo ya hedhi hasa za muda mrefu na kutoka damu nyingi yameonekana piakusababisha upungufu wa wekundu wa damu.

19

Page 29: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

20

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Dalili za upungufu wa wekundu wa damuUpungufu wa wekundu wa damu hujitokeza kwa namna nyingi. Baadhi ya dalili zaupungufu huo ni:

• Uchovu na ulegevu wa mwili

• Mapigo ya moyo kuongezeka

• Kizunguzungu

• Kupumua kwa shida

• Kutokupata usingizi wa kutosha

• Vidole kufa ganzi

• Weupe usio wa kawaida kwenye macho, midomo, kucha, viganja, ufizi, ulimi nahata ngozi

• Hamu ya kula udongo kwa wanawake wajawazito

• Kuvimba uso na miguu iwapo upungufu wa wekundu wa damu ni mkubwa sana

• Masikio kuvuma

Athari za upungufu wa wekundu wa damuAthari za upungufu wa wekundu wa damu ziko nyingi. Baadhi ya athari zaupungufu wa wekundu wa damu ni:

• Kupungua kwa uwezo wa mtu kufanya kazi;

• Kupungua kwa uwezo wa akili kufikiri na kutafakari;

• Kupungua kwa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi mbalimbali;

• Kwa wanawake wajawazito, kuzaa mtoto kabla ya siku (mtoto njiti), mtotomwenye uzito pungufu au mtoto mfu, mimba kuharibika, wakati mwingineuwezekano wa kifo wakati mama anapojifungua. Vilevile kuugua mara kwa marakwa sababu ya kinga hafifu;

• Kwa watoto chini ya miaka mitano, upungufu wa wekundu wa damuhusababisha ukuaji na maendeleo ya mtoto kuwa hafifu, kuugua mara kwa marana wakati mwingine vifo hutokea.

Mbinu za kuzuia tatizo la upungufu wa wekundu wa damu

Upungufu wa wekundu wa damu ni tatizo linaloweza kuzuilika na kudhibitiwaiwapo mbinu sahihi zitachukuliwa. Baadhi ya mbinu hizo ni:

• Kuzingatia utayarishaji bora wa vyakula na hasa mboga-mboga za kijani.

• Kuwa na mgawanyo mzuri wa chakula katika kaya unaozingatia makundiyanayoathirika zaidi kama watoto wadogo, wanawake wajawazito, wanawakewanaonyonyesha na wagonjwa.

• Kuimarisha elimu ya afya na lishe kwa jamii.

Page 30: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

• Kuimarisha huduma za msingi katika jamii.

• Wanawake wajawazito na watu wengine walio katika hatari ya kupatwa naupungufu wa wekundu wa damu, kutumia vidonge vyenye madini ya chuma nafoliki asidi kama watakavyoshauriwa na wataalamu wa afya.

• Kutibu mapema maradhi kama malaria na minyoo.

• Kuwa na uhakika wa chakula katika kaya au jamii.

• Kuimarisha mila na desturi zinazodumisha afya bora ya jamii na kuepuka zilezinazochangia kuleta hali mbaya ya lishe.

Upungufu wa vitamini AUpungufu wa vitamini A hutokea pale kunapokuwa na upungufu wa akiba ya vitaminiA mwilini. Upungufu huo huweza kusababishwa na ulaji duni usiotosheleza mahitaji yavitamini A mwilini, pia kutokula vyakula vyenye vitamini A pamoja na mafuta kwaniusharabu wa vitamini hiyo hutegemea mafuta. Magonjwa hasa ya njia ya hewa piahuweza kusababisha upungufu huo.

Katika jamii, watu wanaoathirika zaidi na tatizo hili ni watoto wadogo walio kati yaumri wa miezi 6 na miaka 6 ingawa watoto walio zaidi ya umri huo pia huwezakuathirika. Wagonjwa, wakiwemo watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, wanawakewajawazito na wanaonyonyesha pia huathirika.

Upungufu wa vitamini A usipodhibitiwa huweza kusababisha mtu kupata maradhi yamara kwa mara na hata vifo hasa kwa watoto wadogo; ukuaji hafifu kwa watoto, upofuna matatizo ya uzazi.

Ili kudhibiti upungufu wa vitamini A inashauriwa:• Kula vyakula vyenye vitamini A kwa wingi, kama vile vitokanavyo na wanyama,

mboga za kijani na zile za njano, matunda hasa ya rangi ya njano, nafaka, mawese,n.k;

• Kutumia mafuta kiasi katika kupika au kutumia vyakula vyenye asili ya mafutakama vile karanga, kweme, ufuta, alizeti, nyama, n.k;

• Kulima bustani za mboga-mboga na matunda kwa matumizi ya nyumbani;

• Kulisha watoto ipasavyo, ikiwa ni pamoja na kuwanyonyesha maziwa ya mama napia yale ya mwanzo na kuongeza mafuta katika vyakula vyao vya nyongezawanavyokula wafikapo umri wa miezi sita na kuendelea;

• Watoto wapate chanjo zote zinazotakiwa surua, kifua kikuu, polio na pia maradhikama kuharisha na yale ya njia ya hewa yatibiwe mapema;

• Kutoa vidonge vya vitamini A kwa watoto wote kwa kufuata mwongozouliowekwa kitaifa kwa walio na umri chini ya miaka mitano, wenye surua, wenyekuharisha, na wale walio na tatizo la upungufu wa nishati na protini; na

• Kutoa vidonge vya vitamini A kwa wanawake waliojifungua, mara baada yakujifungua au katika wiki sita tangu kujifungua.

21

Page 31: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

22

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Upungufu wa madini joto Madini joto kwa kawaida hupatikana ardhini. Mimea na maji hupata madini jotokutoka ardhini. Vyakula vingi hutokana na mimea inayopandwa ardhini.

Upungufu wa madini joto husababishwa na kula vyakula ambavyo havina madini hayoya kutosheleza mahitaji ya mwili au kuwepo kwa “goitrogens” ambazo zinaingilia nakuzuia matumizi ya madini hayo mwilini.

Upungufu wa madini hayo hutokea zaidi sehemu za milima na zenye miinuko kwasababu madini joto yaliyoko ardhini husombwa na maji ya mvua na hivyo kusababishamimea inayopandwa kwenye ardhi hiyo kuwa na upungufu wa madini hayo. Hatahivyo watu wanaoishi katika sehemu nyingine huweza kuathirika pia na upungufu huokwa sababu ya kutumia vyakula vinavyotoka maeneo yenye miinuko.

Athari za upungufu wa madini jotoUpungufu wa madini joto hapa nchini huathiri makundi yote ya jamii. Kwa wanawakewajawazito upungufu huu huweza kusababisha mimba kuharibika, maendeleo hafifu yaukuaji wa viungo mbalimbali vya mtoto tumboni, hasa ubongo, kuzaa mtoto kabla yasiku, kuzaa mtoto mfu. Upungufu mkubwa wa madini joto huweza kusababisha kuzaamtoto aliyedumaa (dwarf), taahira au kiziwi. Kwa watoto, upungufu wa madini hayohusababisha maradhi ya mara kwa mara na ukuaji duni, na kwa watu wazimahusababisha upungufu wa uwezo wa kufanya kazi.

Kudhibiti upungufu wa madini jotoUpungufu wa madini joto mwilini unaweza kudhibitiwa kwa jamii kutumia chumviiliyoongezwa madini joto na kula vyakula vya baharini kwani vyakula hivi huwa namadini joto kwa wingi. Vilevile vidonge vya madini joto hutolewa sehemu zilizo naupungufu mkubwa wa madini hayo.

Kielelezo Na. 3: Nembo ya chumvi yenye madini joto

Nembo hii huwekwa kwenye pakiti au mfuko wachumvi iliyotengenezwa Tanzania ili kuonyeshachumvi yenye madini joto

Page 32: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

23

LISHE KWA WATU WANAOISHI NAVIRUSI VYA UKIMWI

Uhusiano wa lishe na virusi vya UKIMWIKuna uhusiano mkubwa kati ya lishe na virusi vya UKIMWI. Ni dhahiri kwambavirusi vya UKIMWI husababisha kupungua kwa kinga ya mwili. Virusi vya UKIMWIpia husababisha ongezeko la mahitaji ya baadhi ya virutubishi mwilini. Ongezeko hilolinaposhindwa kukidhiwa huweza kusababisha utapiamlo. Utapiamlo nao husababishakupungua kwa kinga ya mwili na wakati huo huo virusi vya UKIMWI navyohupunguza kinga ya mwili. Hii husababisha hali ya afya na lishe ya mtu anayeishi navirusi vya UKIMWI kuwa mbaya na pengine kufupisha kipindi cha tangu mtukuambukizwa virusi vya UKIMWI mpaka kuugua UKIMWI.

Kielelezo Na. 4: Uhusiano kati ya Lishe na virusi vya UKIMWI

4

Chanzo: Imechukuliwa kutoka RCQHC na FANTA, 2003

4. L

IS

HE

K

WA

W

AT

U W

AN

AO

IS

HI N

A V

IR

US

I V

YA

U

KIM

WI

Page 33: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Athari za virusi vya UKIMWI kwenye lisheKuna athari mbalimbali za virusi vya UKIMWI kwenye lishe. Athari hizo huwezakuleta utapimalo. Athari hizo ni:

❒ Ulaji duni:

Kukosa hamu ya kula, kichefuchefu, utando mweupe kinywani, vidonda kinywanina kooni, mawazo na sononeko humfanya mtu ashindwe kula chakula cha kutoshahata kama chakula kipo.

❒ Uyeyushwaji na usharabu duni wa virutubishi

Kutapika na kuharisha hufanya mwili upoteze virutubishi kwani chakula hakikaitumboni muda wa kutosha kuyeyushwa na virutubishi kusharabiwa, hivyo mtuanakuwa na hatari ya kupata utapiamlo. Pamoja na kuharisha na kutapika,mabadiliko au uharibifu wa seli za utumbo pia husababisha uyeyushwaji wa chakulana usharabu wa virutubishi kuwa duni.

❒ Mabadiliko katika umetaboli (ujenzi na uvunjaji wa kemikali mwilini)

Hali ya kuwa na virusi vya UKIMWI huweza kusababisha mabadiliko katikaumetaboli. Pamoja na uyeyushwaji duni wa chakula tumboni na usharabu duni wavirutubishi mwilini, mwili pia hushindwa kutumia kikamilifu baadhi ya virutubishihasa mafuta, protini na kabohaidreti.

Ulaji bora Ulaji bora hutokana na kula chakula mchanganyiko na cha kutosha, na ni muhimu kwabinadamu wote. Hii ni pamoja na kutumia sukari, mafuta na chumvi kwa kiasi,kuzingatia usafi usalama wa chakula na maji, usafi binafsi, usafi wa mazingira nakujikinga na maradhi mbalimbali. Ni muhimu sana kwa mtu anayeishi na virusi vyaUKIMWI kuzingatia ulaji ulio bora kwa ajili ya:

• Kuboresha kinga dhidi ya magonjwa nyemelezi;

• Kutengeneza seli mpya na kurudishia seli zilizochakaa;

• Kurudisha vitamini, madini na virutubishi vingine vinavyopotea kutokana namaradhi kama kuharisha na kutapika;

• Kusaidia dawa zinazotumika kufanya kazi vizuri mwilini;

• Ukuaji wa mwili na akili;

• Kumpa mtu nguvu ya kufanya kazi mbalimbali; na

• Kuboresha afya, hivyo kuweza kurefusha muda wa kuishi kutoka kupatauambukizo wa virusi vya UKIMWI hadi kuugua UKIMWI.

Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI kama binadamu mwingine yeyote anahitaji kulamlo kamili kama ilivyoelezwa katika Sura ya Pili. Ni muhimu kuhakikisha kwamba mlohuo unatayarishwa katika hali ambayo unakuwa ni rahisi kula na kutumika kutegemeahali ya mtu wakati huo. Kutokana na ongezeko la mahitaji ya nishati mwilini, ni

24

Page 34: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

25

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

muhimu kuongeza idadi ya milo na ikiwezekana kula milo midogo midogo mara kwamara, hasa wakati ambapo mtu hawezi kula chakula cha kutosha kwa mara moja.

Mbinu za utayarishaji na uboreshaji wa chakula Baadhi ya mbinu zinazoweza kutumika ili kukifanya chakula kiwe bora zaidi, rahisikula na kutumika mwilini. Mbinu hizo ni pamoja na:

• Kuponda au kusaga chakula: Kitendo cha kuponda au kusaga chakula hukifanya chakula kiwe rahisi kula na piahusaidia uyeyushwaji wake tumboni.

• Kuongeza vyakula vyenye virutubishi vingi:Ni muhimu kuongeza vyakula vyenye virutubishi kwa wingi kwenye vyakula hasavile vya wanga. Vyakula vinavyoweza kuongezwa ni pamoja na karanga, maziwa,mbegu mbalimbali zitoazo mafuta zilizopondwa, mafuta au tui la nazi. Hiihuongeza ubora wa chakula.

Imethibitishwa kwamba, mahitaji ya nishati kwa mtu anayeishi na virusi vyaUKIMWI huongezeka kwa asilimia 15 wakati wa kipindi tuli na asilimia 20 hadi30 wakati wa ugonjwa kamili wa UKIMWI

Chanzo : Imetafsiriwa kutoka FAO, 2002

KULA CHAKULA MCHANGANYIKO

Maz

iwa

Mafuta na Sukari

Unga

Asali

Mafuta yamimea

Sukari

Parachichi

mafuta yawanyama

Siagi

Mchele

Mtama

Matunda

Maji

Mboga-mboga

Nyama,Samaki,Mayai,

Nafaka, Mizizi na Ndizi

Mikunde

Page 35: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

26

• Kutumia viungo vya vyakula:

Matumizi ya baadhi ya viungo kama mdalasini, kitunguu saumu, iliki, tangawizi,n.k. yameonekana kusaidia kuongeza hamu ya kula, kusaidia uyeyushwaji wachakula na usharabu wa virutubishi mwilini.

• Kuchachusha vyakula (fermentation):

Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI mara kwa mara huwa na matatizo yauyeyushwaji wa chakula na usharabu wa virutubishi. Vyakula vilivyochachushwahuyeyushwa kwa urahisi na hatimaye virutubishi kusharabiwa. Aidha vimeonekanakusaidia uyeyushwaji wa vyakula vingine na ufyozwaji wa virutubishi. Baadhi yavyakula hivyo ni kama maziwa ya mtindi, togwa na vinywaji vinginevilivyochachushwa ambavyo havina kilevi.

• Kuotesha vyakula (germination/sprouting):

Kama ilivyo kwa vyakula vilivyochachushwa, vyakula vilivyooteshwa huyeyushwakwa urahisi na husaidia uyeyushwaji wa vyakula vingine. Mbegu mbalimbali zanafaka na mikunde huweza kuoteshwa na kutumika kama vyakula au pamoja navyakula mbalimbali. Mbegu hizo ni kama; mbegu za mahindi, mtama, ulezi, uwele,choroko, kunde, maharagwe, n.k. Mbegu zilizooteshwa sio lazima zikaushwe nakutengenezwa unga, zipo ambazo zinaweza kupikwa mara tu baada ya kuota nakutumiwa kama mboga. Kwa mfano maharagwe, njegere, choroko, kunde, n.k.

• Kupika kwa mvuke

Kupika chakula kwa mvuke (kutokosa) hufanya chakula kuwa rahisi kuyeyushwana kusharabiwa mwilini. Vilevile kupika kwa mvuke husaidia kuhifadhi virutubishivilivyoko kwenye chakula. Hii ni njia nzuri ya kupika mboga za aina mbalimbalikama mboga za majani, karoti na vyakula vingine. Kwa mfano baadhi ya makabilahupika kwa mvuke kwa kufunga vyakula ndani ya jani la mgomba, na kuweka ndaniya chombo cha kupikia chenye maji kidogo kisha kufunika na kupika mpakachakula kiive bila ya chakula hicho kugusa maji.

Aina ya mbegu Kiasi cha mbegu Muda wa Muda wa kuotesha Kimea Urefu wa mbegu iliyoota

kwenye chombo kuloweka mbegu ikiwa tayari kuliwa

Alfalfa/lucerne Vijiko vya kula 3-4 Saa 4 Sentimeta 3

Maharage Kikombe 1 Saa 12 Siku 4-7 Sentimeta 1

Choroko Kikombe 1 Saa 12 Siku 2-5 Sentimeta 1/2 - 1

Kunde/Njegere Kikombe 1 Saa 12 Siku 2-5 Sentimeta 1

Mtama/uwele/ulezi Kikombe 1 Saa 8 Siku 2-3 1/2 Sentimeta

Mahindi Kikombe 1 Saa 12 Siku 3-4 Sentimeta 1

Alizeti (Bila maganda) Kikombe 1 Saa 12 Siku 1-3 Sentimeta 1/2 - 1

Karanga (nzima) Kikombe 1 Saa 12 Siku 1-2 Haioti bali inavimba

Jedwali Na 2: Chati ya kutengeneza kimea kwa kutumia mbegu mbalimbali

Siku 4-6 mpakazimetoamajani ya kijani

Chanzo: Imetayarishwa kutoka NAP+, Food for people living with HIV/AIDS.

Page 36: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

KUMBUKA

Kufanya chakula kuwa rahisi kuyeyushwa tumboni na virutubishikusharabiwa mwilini yafuatayo yanaweza kufanyika:• Kukamulia limau, ndimu au kuweka maganda yaliyokatwakatwa

vipande vidogo sana ya limau au chungwa kwenye vyakula hasa vilevyenye mafuta mengi kama nyama, korosho, karanga, n.k.

• Kupika nyama na papai bichi lililokatwakatwa au kula nyama pamoja napapai bivu kwani papai husaidia uyeyushwaji wa protini iliyoko kwenyenyama.

• Kuongeza viungo katika vyakula mbalimbali kwani hivi husaidiakuongeza bakteria wazuri ambao husaidia katika uyeyushwaji wachakula. Vilevile kutengeneza na kutumia vinywaji vinavyotokana naviungo.

• Kula milo midogo midogo mara nyingi. Milo midogo midogohuyeyushwa haraka na hatimaye virutubishi kusharabiwa vizuri.

• Maji ya moto yenye limau au ndimu husaidia katika uyeyushwaji wachakula. Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI anaweza kutumiakinywaji hiki kwa kiasi kwani limau lina tindikali nyingi ambayo huwezakudhuru tumbo kama ikizidi.

• Kupika chakula kwa mvuke. Chakula kilichopikwa kwa mvuke huwa nirahisi kuyeyushwa na kusharabiwa mwilini. Vilevile kupika kwa mvukehusaidia kuhifadhi virutubishi vilivyoko kwenye chakula.

• Kuponda chakula na kutafuna vizuri pia kunasaidia katika uyeyushwajiwa chakula na usharabu wa virutubishi mwilini.

• Kufanya mazoezi kama kutembea haraka haraka au kufanya kazizitumiazo viungo vya mwili kunasaidia chakula kuyeyushwa tumbonivizuri na hatimaye virutubishi vyake kusharabiwa na mwili.

27

Page 37: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

28

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Vidokezo muhimu vya kuboresha lisheVifuatavyo ni baadhi ya vidokezo muhimu vya kuboresha lishe ya mtu anayeishi navirusi vya UKIMWI:

• Kula vyakula vya aina mbalimbali:Vyakula vina virutubishi vya aina mbalimbali na kwa kiasi tofauti. Ulaji wa vyakulambalimbali husaidia mwili kupata virutubishi vyote muhimu kwa ajili ya lishe naafya bora kwani hakuna chakula kimoja pekee kinachotosheleza mahitaji ya mtu.

• Kula milo midogo midogo, mara kwa mara:Kutokana na matatizo ya uyeyushwaji wa chakula na usharabu wa virutubishi, watuwanaoishi na virusi vya UKIMWI au UKIMWI wanashauriwa kula milo midogomidogo, mara nyingi kwa siku ili kukidhi mahitaji ya mwili kilishe.

• Matumizi ya virutubishi vya nyongeza (nutrient supplements):Virutubishi vya nyongeza huweza kuwa katika mfumo wa kidonge, unga, aukimiminika. Mfano wa virutubishi hivyo ni vitamini A, vidonge vya madini yachuma, madini ya joto, vitamin B na “Folic Acid”. Kinga ya mwili inapopungua,mahitaji ya virutubishi mwilini huongezeka. Wakati mwingine si rahisi kupatamahitaji yote ya virutubishi kutoka katika chakula. Inapohitajika, mtu anayeishi navirusi vya UKIMWI anaweza kutumia virutubishi vya nyongeza. Ni vizuri kupataushauri wa daktari au mtaalamu wa afya ili kufahamu ni aina gani inahitajika na kwakiasi gani. Hata hivyo ikumbukwe kwamba:

- Vipo virutubishi vya nyongeza ambavyo ni bora na vinavyoweza kupatikanakwa bei nafuu.

- Virutubishi vya nyongeza visitumike badala ya chakula bali vitumike baada yakupata mlo kamili.

- Virutubishi vya nyongeza visichukuliwe kama dawa ya kutibu UKIMWI.

- Ni vyema kujaribu kupata virutubishi vingi iwezekanavyo kutoka katikachakula.

• Mazoezi ya mwili:Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI au UKIMWI wanashauriwa kufanyamazoezi ya viungo. Mazoezi husaidia kujenga misuli ya mwili, na vilevile chakulakuyeyushwa na kutumika mwilini. Mazoezi ni pamoja na kutembea na kukimbiataratibu. Shughuli mbalimbali zinazotumia viungo vya mwili kama kazi za bustani,kufyeka, kazi za nyumbani pia zinaweza kuwa sehemu ya mazoezi ya mwili.

• Kuepuka matumizi ya pombe:Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI au UKIMWI wanashauriwa kuepukaunywaji wa pombe. Pombe huingilia ulaji wa chakula, uyeyushwaji wa chakula,

Page 38: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

usharabu, uwekaji akiba na utumikaji wa virutubishi mbalimbali mwilini.

• Kuepuka matumizi ya sigara na tumbaku:Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI au UKIMWI wanashauriwa kuacha uvutajisigara au tumbaku kwa sababu matumizi ya vitu hivi hupunguza hamu ya kula napia huongeza hatari ya mtu kupata magonjwa ya saratani na kifua ikiwa ni pamojana ugonjwa wa kifua kikuu.

• Kujikinga na kutibu maradhi yote mapema:

Ili kuboresha lishe, inashauriwa pia kujikinga na kutibu maradhi yote mapema. Hii nipamoja na kuzingatia usafi na usalama wa chakula na maji, usafi binafsi, usafi wamazingira na kujikinga na maradhi mbalimbali.

• Kuendelea kujielimisha kuhusu afya:

Ni muhimu kwa mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI au UKIMWI kuendeleakujifunza na kutafuta habari zaidi kuhusu afya na jinsi ya kuishi na virusi vyaUKIMWI.

29

Page 39: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

30

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Page 40: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

USAFI NA USALAMA WA CHAKULA NAMAJI

Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI wapo katika hatari ya kupata uambukizo wamaradhi mbalimbali kwa urahisi zaidi kutokana na kupungua kwa kinga mwilini.Chakula na maji vinaweza kuwa miongoni mwa vyanzo vya maambukizo mbalimbaliikiwa usafi na usalama wake hauzingatiwi. Ili chakula na maji viwe safi na salama nimuhimu kuzingatia usafi wa mtayarishaji wa chakula, vyombo, sehemu ya kutayarishiachakula, chakula chenyewe na maji ya kunywa.

Usafi wa mtayarishaji wa chakula:Mtayarishaji wa chakula ni muhimu:

• Kuosha mikono kwa sabuni na maji ya kutosha kabla na baada ya kutayarishachakula. Majivu yanaweza kutumika pale ambapo hakuna sabuni.

• Kunawa mikono mara baada ya kutoka chooni au kujisaidia.

• Kuzingatia usafi wa mwili na nguo ikiwa ni pamoja na kuoga na kuvaa nguo safi.

• Kufunga vidonda vya mkononi ili kuzuia sibiko (contamination) wakati wakutayarisha chakula.

Usafi wa vyombo:Ni muhimu:

• Kutumia vyombo visafi kwa kutayarishia na kupakulia chakula.

• Kuosha vizuri vyombo na vifaa vinavyotumika kutayarisha vyakula na hasavilivyotayarishia nyama mbichi, samaki wabichi, au mayai mabichi kwa maji yakutosha na sabuni kabla ya kuvitumia kwa matayarisho ya vyakula vingine. Majivuyanaweza kutumika pale ambapo hakuna sabuni.

• Kuwa na kichanja cha kuanikia vyombo. Vyombo viondolewe punde vinapokauka.

• Iwapo kitambaa cha kukaushia vyombo kitatumika, ni muhimu kifuliwe mara baadaya kutumika, kianikwe juani na ikiwezekana kupigwa pasi.

Usafi wa sehemu ya kutayarishia chakula:• Kuweka safi sehemu zote za kutayarishia chakula, ikiwa ni pamoja na kufagia jiko au

kudeki kila wakati ili kuzuia wadudu watambaao na panya.

• Kukusanya uchafu na mabaki ya vyakula katika ndoo au chombo chenye mfuniko nabaadaye kutupwa ipasavyo kwenye shimo la takataka.

31

5

5. U

SA

FI N

A U

SA

LA

MA

WA

CH

AK

UL

A N

A M

AJ

I

Page 41: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

32

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Usafi na usalama wa chakula:• Kuhakikisha vyakula vya aina ya nyama, samaki na mayai vimepikwa na kuiva vyema

ili kuepuka uambukizo wowote kwenye mfumo wa chakula ikiwa ni pamoja naunaosababishwa na vimelea vya “salmonella”. Vyakula hivi visiliwe vikiwa vibichi,kwani vikiwa vibichi vina hatari kubwa ya kusababisha uambukizo (food poisoning).

• Kupika chakula mpaka kiive vizuri na kuhakikisha vitu vya maji maji vimechemkasawasawa. Chakula kilichopikwa kiliwe kingali moto.

• Kuosha matunda na mboga-mboga hasa zile zinazoliwa bila kupikwa kwa maji yakutosha (ikiwezekana yaliyochemshwa). Matunda pia yanaweza kumenywa.

• Kufunika chakula kuzuia wadudu, hasa inzi na mende.

• Kuepuka vyakula vilivyosindikwa pale inapowezekana, kwani mara nyingi vyakulahusindikwa kwa kemikali ambazo wakati mwingine sio nzuri hasa kwa mgonjwa.

• Kuepuka nafaka au vyakula vingine vilivyoota ukungu.

• Kiporo au chakula kilichokaa zaidi ya saa mbili baada ya kupikwa kipashwe motompaka kichemke kabla ya kula hata kama bado kina uvuguvugu.

• Kuhakikisha hakuna mwingiliano wa vyakula vilivyopikwa na vyakula vibichivinavyoweza kuleta uambukizo kama nyama mbichi, samaki wabichi na mayaimabichi.

• Kuhakikisha muda wa kutumia vyakula haujapita (expiry date) hasa kwa vyakula vyamadukani.

Usafi na usalama wa maji ya kunywa:• Kuhakikisha maji ni safi, na yachemshwe na kuacha yaendelee kuchemka kwa muda

wa dakika 5 – 10 ili kuua vimelea vya maradhi.

• Kutunza maji katika chombo safi chenye mfuniko na kuweka mahali pa baridi.

• Maji ya kutengeneza barafu au juisi pia yachemshwe.

Page 42: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

LISHE NA ULAJI WAKATI WA BAADHI YAMATATIZO YA KIAFYA YANAYOAMBATANANA VIRUSI VYA UKIMWI AU UKIMWI

Vyakula mbalimbali vinaweza kutumika kupunguza ukali wa baadhi ya maradhiyanayompata mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI au mwenye UKIMWI. Hata hivyoni muhimu kumuona daktari mapema tatizo linapotokea. Yafuatayo ni baadhi yamatatizo au maradhi na ushauri kuhusu chakula na lishe.

Kukosa hamu ya kulaKukosa hamu ya kula ni tatizo linaloweza kujitokeza mara kwa mara kwa mtuanayeishi na virusi vya UKIMWI au mwenye UKIMWI. Hii huweza kusababishwa nauambukizo wowote, msongo-mawazo, uchovu, maumivu ya kinywa au koo, kutokulakwa muda mrefu au matumizi ya baadhi ya dawa.

Mgonjwa ajaribu:

- Kuongeza viungo kama tangawizi, limau, mdalasini, kotimiri au iliki kwenyevinywaji au vyakula mbalimbali kwani viungo vimeonekana kuongeza hamu yakula.

- Kula milo midogo midogo mara nyingi kwa siku.

- Kutotayarisha vyakula mwenyewe pale inapowezekana au kukaa jikoni ama karibuna jiko kwani harufu za vyakula vinavyopikwa huweza kupunguza hamu ya kula.

- Kunywa vinywaji na kula vyakula anavyovipenda zaidi.

- Kula pamoja na familia au marafiki pale inapowezekana.

- Kutokunywa na kula wakati mmoja kwani hii itasababisha tumbo kujaa haraka.Mgonjwa anywe kati ya mlo mmoja na mwingine.

- Kuongeza aidha karanga, maziwa au mafuta kwenye vyakula mbalimbali ilikuviongezea ubora na kuvifanya viwe rahisi kula na kumeza.

- Kubadili ladha na aina ya vyakula anavyokula mgonjwa kwani hii huongeza hamuya kula.

- Kufanya mazoezi mbalimbali kama kutembea haraka haraka na mengine ilikusaidia kuongeza hamu ya kula.

- Kula chakula kwa kujilazimisha kwani chakula ni muhimu sana.

33

6

6. L

IS

HE

NA

UL

AJ

I W

AK

AT

I W

A B

AA

DH

I Y

A M

AT

AT

IZ

O

YA

KIA

FY

A Y

AN

AY

OA

MB

AT

AN

A

NA

VV

U

Page 43: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

34

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Vidonda kinywani au kooni, na utandu mweupe kinywaniVidonda vya kinywani au kooni na utandu mweupe kinywani (fangasi) huwezakufanya ulaji wa vyakula kuwa mgumu na hivyo kupunguza kiasi cha chakulaanachoweza kula mgonjwa.

Yafuatayo huweza kusaidia:

- Kula vyakula laini au vilivyopondwa kama mtindi, mtori, uji au matunda kamaparachichi, papai, ndizi, n.k.

- Kuepuka vyakula vyenye viungo au ladha kali.

- Kuepuka vyakula vya moto au vyenye pilipili kali.

- Kuepuka vyakula vyenye sukari nyingi kwani sukari huchochea kuongezeka kwafangasi.

- Kusukutua kinywa kwa kutumia maji yaliyochemshwa yenye kitunguu saumu aumdalasini. Rudia kila baada ya saa 3 hadi 4.

Kutumia mrija wakati wa kunywa au kula pale inapowezekana

- Kujaribu kumung’unya barafu (iliyotengenezwa kwa maji yaliyochemshwa) kamainapatikana kwani huweza kupunguza maumivu kinywani.

- Kujaribu kutumia maziwa ya mgando (mtindi) mara kwa mara, kwani mtindihutuliza maumivu na pia huzuia ukuaji wa fangasi.

.

Kichefuchefu au kutapikaKichefuchefu huweza kusababishwa na vyakula mbalimbali, njaa, maradhi mbalimbali,ukosefu wa maji ya kutosha mwilini na pia baadhi ya dawa. Kichefuchefu hupunguzahamu ya kula.

Mgonjwa ajaribu yafuatayo anapokuwa na kichefuchefu au kutapika:

- Kuepuka vyakula vyenye viungo vingi, mafuta mengi au sukari nyingi kwanivyakula hivyo huweza kusababisha kichefuchefu kuongezeka.

- Kula vyakula vichachu kidogo, au vikavu na vyenye chumvi kidogo kama mkate,kwani hivi hupunguza kichefuchefu.

- Kunywa maji, supu na vinywaji vya viungo kidogo kidogo na kuendelea navyakula laini.

- Kula vyakula visivyo vya moto sana.

- Kunywa juisi ya limau au ndimu iliyochanganywa kwenye kikombe cha maji yamoto kwani huweza kusaidia kupunguza kichefuchefu.

- Kula milo midogo midogo mara kwa mara (si chini ya mara 5 hadi 6 kwa siku).

- Kula wakati amekaa wima au ajiegemeze kidogo kwenye mto. Asijilaze mara tubaada ya kula (asubiri dakika 30 hadi saa 1 baada ya kula).

Page 44: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWILishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

- Kula taratibu ili kupunguza kichefuchefu au kutapika.

- Kutokaa muda mrefu bila kula au kunywa chochote kwani kufanya hivyo huwezakusababisha kichefuchefu.

- Kuepuka pombe au vyakula vyenye kafeini kama chai na kahawa.

- Kumuona daktari kwa ushauri zaidi.

KuharishaKuharisha mara nyingi husababishwa na kula vyakula au vinywaji vilivyosibikwa auvyenye vimelea vya maradhi, uambukizo mbalimbali katika mfumo wa chakula,minyoo na baadhi ya dawa kama kiua-vijasumu (antibayotiki).

Kuharisha huweza kusababisha upotevu wa maji na virutubishi mwilini kwaniuyeyushwaji wa chakula na usharabu wa virutubishi huwa duni. Wakati mwinginekuharisha husababisha kutokuwa na hamu ya kula.

Mgonjwa anapoharisha ajaribu kufanya yafuatayo:

- Kunywa maji safi na salama kwa wingi ili kuzuia upungufu wa maji mwilini (zaidiya lita moja na nusu (glasi 8) kwa siku).

- Kunywa vinywaji vya maji-maji kwa wingi zaidi. Vinywaji kama maji ya mchele,madafu, togwa, supu, juisi ya matunda na maji yenye mchanganyiko wa sukari nachumvi (ORS) vinaweza kutumika.

- Kula matunda kama ndizi mbivu, tikiti maji na mboga-mboga zilizopikwa kamakaroti, maboga, n.k ili kurudisha mwilini madini na vitamini zinazopotea kutokanana kuharisha.

- Kutafuna kwa muda mrefu au kula vyakula laini kwani ni rahisi kumeza navirutubishi vyake kuyeyushwa na kusharabiwa.

- Kula vyakula vyenye uvuguvugu na sio vya moto sana au baridi sana.

- Kuepuka vyakula vyenye mafuta mengi, viungo vingi au pilipili nyingi kwanivyakula hivi huweza kuzidisha kuharisha.

- Kujihadhari kutumia matunda yasiyoiva vizuri au yenye uchachu mkali kamanyanya, machungwa, machenza, limau kwani wakati mwingine huweza kuongezatatizo.

- Kuepuka vyakula na vinywaji vinavyosababisha gesi kwa wingi tumboni kamamaharagwe, kabichi au soda.

- Kuepuka vinywaji vyenye kafeini kwa wingi kama chai na kahawa, kwani hivihusababisha upotevu zaidi wa maji.

35

Ni muhimu kurudia ulaji wa vyakula vya kawaida mara tu tatizo linapokwisha

Page 45: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

36

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

- Kuepuka matumizi ya pombe kwani huzuia baadhi ya virutubishi kusharabiwa nahuongeza upotevu wa maji.

- Kuepuka maziwa mabichi kama yanasababisha kuharisha na ajaribu kutumiamtindi.

- Kuepuka vyakula vyenye nyuzinyuzi (dietary fibre) nyingi kama nafakazisizokobolewa au vyakula vya mikunde vyenye maganda, kwani haviyeyushwikwa urahisi na hivyo huongeza kuharisha.

- Kuponda vitunguu saumu na kuchanganya kwenye vinywaji kama supu navinginevyo vilivyochemshwa.

- Kula milo midogo midogo mara nyingi ili kurudisha virutubishi vinavyopotea nakukidhi mahitaji ya mwili kilishe.

- Kumuona daktari mapema kwa ushauri zaidi.

Kupungua uzitoKupungua uzito kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI huweza kusababishwa naongezeko la mahitaji ya baadhi ya virutubishi, ulaji duni, uyeyushwaji na usharabuduni wa virutubishi mwilini na pia baadhi ya maradhi.

Kupungua uzito kunaweza kudhibitiwa kwa:

- Kuongeza aina, kiasi cha chakula na idadi ya milo kwa siku.

- Kuongeza vyakula kama karanga, mafuta, siagi, maziwa, sukari, asali, ainambalimbali za mbegu za mafuta, n.k. kwenye vyakula mbalimbali.

- Kutumia asusa (snacks) kama karanga, matunda, mtindi, n.k. mara kwa mara katiya mlo na mlo, kwani hii itasaidia kukidhi mahitaji ya mwili.

- Kuweka viungo katika chakula ili kuongeza hamu ya kula na kusaidia uyeyushwajiwake.

- Kutumia vyakula vilivyochachushwa au kuoteshwa kama mtindi, togwa na kimeaili kusaidia uyeyushwaji na usharabu wa virutubishi.

- Kufanya mazoezi kwani mazoezi huongeza hamu ya kula na pia hujenga misuli.

Kukosa choo au kupata choo kigumuKukosa choo au kupata choo kigumu ni tatizo mojawapo linalojitokeza kwa watuwanaoishi na virusi vya UKIMWI. Hii huweza kusababishwa na homa ambazohupunguza maji mwilini au kutokula chakula cha kutosheleza mahitaji ya mwili nahasa chenye nyuzi nyuzi.

KUMBUKANi muhimu kurudia vyakula na ulaji wa kawaida mara

tu hali ya kuharisha inapokwisha

Page 46: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Mgonjwa anashauriwa kufanya yafuatayo:

- Kunywa maji mengi yaliyochemshwa angalau lita moja na nusu kwa siku (glasi 8)au zaidi.

- Kutumia vyakula vinavyotokana na nafaka ambazo hazijakobolewa kama dona,unga wa ngano usiokobolewa sana, n.k.

- Kula matunda na mboga-mboga kwa wingi, pia vyakula vya aina ya mikunde kamakunde, choroko, maharagwe, n.k. kwani huwa na nyuzinyuzi nyingi.

- Kutumia matunda kama papai, parachichi au embe kwani vimeonekana kusaidiakulainisha choo.

- Kutumia matunda yaliyokaushwa kama yanapatikana.

- Kujaribu kufanya mazoezi kwani husaidia chakula kuyeyushwa.

- Kujipa muda wa kutosha chooni wakati wa kujisaidia.

Mafua na kikohoziMafua na kikohozi ni maambukizo yanayowapata watu wanaoishi na virusi vyaUKIMWI na wenye UKIMWI mara kwa mara. Wakati mwingine mafua na kikohozihusababisha homa.

Mgonjwa ajaribu yafuatayo:

- Kunywa maji ya kutosha au vinywaji vingine na kupumzika.

- Kutumia vinywaji vya limau, tangawizi, kitunguu maji, nanaa, n.k. katika kipindichote mtu anapokuwa na mafua na/au kikohozi.

- Kujifukiza kwa kutumia mvuke wa maji ya moto.

- Kuchanganya limau na asali na kutumia mara kwa mara katika kipindi chote chaugonjwa.

- Kumuona daktari kikohozi kikizidi ili kupata matibabu na ushauri zaidi.

HomaHoma husababishwa na uambukizo mbalimbali unaompata mtu yeyote ikiwa nipamoja na mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI au mwenye UKIMWI.

Mgonjwa ajaribu yafuatayo:

- Kunywa maji na vinywaji vingine kwa wingi mara kwa mara kupunguza joto lamwili na kuepuka upotevu wa maji mwilini.

- Kula milo midogo midogo mara nyingi ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya mwiliwakati wa homa.

- Kupunguza nguo nzito mwilini.

- Kuoga kwa maji ya uvuguvugu.

- Kumwona daktari kwa ushauri.

37

Page 47: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Upungufu wa wekundu wa damuUpungufu wa wekundu wa damu huweza kusababishwa na ulaji duni hasa kula vyakulavyenye upungufu wa madini ya chuma na pia maradhi kama: malaria na minyoo. Mtuanayeishi na virusi vya UKIMWI huathirika kiafya haraka zaidi iwapo ana tatizo laupungufu wa wekundu wa damu.

Upungufu wa wekundu wa damu huweza kukabiliwa kwa:

- Kula vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi kama vile maini, nyama, samaki,dagaa, mboga za kijani (kama mchicha, spinachi, kisamvu, matembele, majani yamaboga), maharagwe, njegere, choroko, dengu, mbaazi, karanga na mbegu za ainanyingine.

- Kula matunda kwa wingi pamoja na mlo, hasa matunda yenye vitamini C kwawingi ili kusaidia usharabu wa madini ya chuma yanayopatikana kwenye vyakulavya mimea. Matunda kama mapera, machungwa, machenza, pesheni, nanasi,mabungo, ubuyu, ukwaju na nyanya yana vitamini C kwa wingi.

- Kuepuka vinywaji vyenye kafeini kwa wingi kama chai na kahawa wakati wa mlo,kwani huzuia usharabu wa madini chuma yanayopatikana kwenye vyakula vyamimea.

- Kutafuta ushauri wa daktari kuhusu matumizi ya vidonge vya madini ya chuma,foliki asidi na kutibiwa maradhi kama vile malaria na minyoo.

Kifua kikuuKifua kikuu ni mojawapo ya magonjwa nyemelezi kwa watu wanaoishi na virusi vyaUKIMWI au wenye UKIMWI. Kifua kikuu huathiri mapafu na sehemu nyingine zamwili kama figo, uti wa mgongo na mfumo mzima wa njia ya chakula. Mtu mwenyekifua kikuu anashauriwa yafuatayo:

- Kula chakula mchanganyiko na cha kutosha.

- Kula vyakula vyenye protini kwa wingi kama vile aina zote za nyama, samaki,wadudu wanaoliwa kama senene na kumbikumbi. Pia maziwa mabichi, mtindi,jibini, mayai na jamii ya mikunde kama soya, maharagwe, kunde, n.k.

- Kula kwa wingi vyakula vyenye wingi wa vitamini B6 kama vile viazi vitamu,maharagwe, mahindi, parachichi, nyama na samaki kwa vile baadhi ya dawa zakutibu kifua kikuu zinaweza kuingilia matumizi ya vitamini hii mwilini.

- Kula matunda kwa wingi

- Kukabili dalili za kifua kikuu zinazofanana na matatizo yanayoambatana na kuishina virusi vya UKIMWI au UKIMWI kwa kufuata ushauri uliotolewa kwenye Suraya Sita.

- Kupata muda wa kupumzika

- Kukumbuka kuendelea na matibabu kama ilivyoshauriwa.

38

Page 48: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

39

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Matatizo ya ngoziMatatizo ya ngozi huweza kumpata mtu yeyote, ingawa yameonekana zaidi kwa watuwanaoishi na virusi vya UKIMWI au wenye UKIMWI. Baadhi ya matatizo ya ngozihusababishwa na upungufu wa baadhi ya vitamini kama vitamini A na B6. Ingawajemagonjwa ya ngozi yanaweza kuhitaji matibabu, ulaji wa vyakula vyenye vitamini Ana/au vitamini B6 kwa wingi huweza kupunguza au kuzuia maradhi hayo. Vyakulavyenye vitamini A kwa wingi ni mboga zenye rangi ya kijani, mawese, maini, mayai,maziwa, jibini, pia matunda na mboga zenye rangi ya njano au “orange” kama embe,papai, karoti na maboga. Vyakula vyenye vitamini B6 kwa wingi ni kama maharagwe,viazi vitamu, mboga za kijani, karanga, mahindi, nyama na parachichi.

Page 49: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

40

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Page 50: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

41

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

UHAKIKA WA CHAKULA KATIKA KAYAUhakika wa chakula katika kaya ni upatikanaji wa chakula cha kutosha na

chenye virutubishi kwa watu wote waliopo katika kaya na wakati wote kwa ajili ya afyabora. Ukosefu wa uhakika wa chakula katika kaya hufanya watu kuwa na hali mbayaya lishe. Pamoja na sababu nyingine nyingi, maradhi na hasa ya muda mrefu kamaUKIMWI huweza kusababisha ukosefu wa chakula cha kutosha katika kaya, kwakupunguza nguvu kazi ya watu.

Uhusiano kati ya uhakika wa chakula katika kaya na kuwepo kwavirusi vya UKIMWI au UKIMWIKuwepo kwa virusi vya UKIMWI katika jamii kumeathiri uhakika wa chakula katikakaya. Hii ni kwa sababu:

- Watu wengi wanaoishi na virusi vya UKIMWI au wenye UKIMWI wako katikaumri wa kuzalisha mali na chakula. Uwezo wa kufanya kazi na kuzalisha mali nachakula wa watu hao hupungua na hivyo kuathiri uhakika wa chakula katika kayakwa kiasi kikubwa.

- Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI au wenye UKIMWI huwa dhaifu na hivyokutoweza kufanya kazi ngumu na kwa muda mrefu. Hali hiyo inapunguza mapatona uzalishaji wa chakula.

- Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI au wenye UKIMWI huwa wanaugua marakwa mara na hivyo huhitaji kutunzwa na wanafamilia pamoja na ndugu. Hali hiihupunguza muda wa kuzalisha chakula au kufanya kazi zinazoleta kipato.

- Wakati mwingine mali mbalimbali, akiba na mapato ya kaya huweza kutumikakwa ajili ya matibabu badala ya kutumika kwa kuzalishia mali au kununua chakula.

- Kutokana na vifo vya mapema vya wazazi na walezi, urithishaji wa maarifa yakilimo, ufugaji na shughuli nyingine za mikono hukosekana.

- Kadri upatikanaji wa chakula unavyopungua, ndivyo hatari ya utapiamlo namaradhi mengine kwa wanakaya inavyoongezeka.

Jinsi ya kuzitambua kaya zisizokuwa na uhakika wa chakulaVigezo mbalimbali huweza kutumika katika kutambua kaya zisizokuwa na uhakika wachakula. Ili kutambua kaya zisizo na uhakika wa chakula, vigezo vifuatavyo vinawezakutumika:

- Hali ya lishe ya watu na hasa watoto katika kaya. Lishe ya watoto wenye umrichini ya miaka mitano huathirika zaidi.

- Maradhi ya mara kwa mara kwa wanakaya. Watu wasiopata chakula cha kutoshana chenye virutubishi muhimu huugua mara kwa mara.

- Kupungua kwa chakula kilichohifadhiwa. Mara nyingi kabla ya kuuza mali za

7

7. U

HA

KIK

A W

A C

HA

KU

LA

KA

TIK

A K

AY

A

Page 51: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

kaya, watu hujaribu kutumia chakula kilichohifadhiwa.

- Kuuza vitu kama wanyama wanaofugwa, samani (fenicha) na vitu vingine vyathamani ili kupata fedha za kununua chakula. Uuzaji wa namna hiyo unapofanyikakuliko ilivyo kawaida inaashiria kupungua kwa uhakika wa chakula katika kaya.

- Kupungua kwa kiasi na aina ya vyakula vinavyoliwa katika kaya. Mara nyingiwanakaya hupunguza kiasi, aina ya vyakula na idadi ya milo kama hatua yakukabiliana na upungufu wa uhakika wa chakula katika kaya.

- Kubadili kazi toka kwenye kilimo kwenda kwenye kazi zenye ujira wa haraka hatakama kipato ni kidogo. Mara nyingi wanakaya wengi huacha mashamba na kayazao na kwenda sehemu nyingine kutafuta kazi kwa ajili ya kipato.

- Kupungua kwa aina za mazao yanayolimwa. Watu hujaribu kubadili na kulimamazao ya muda mfupi na ambayo huhitaji pembejeo kidogo (mara nyingi hutoamazao kidogo).

- Kupungua kwa shughuli za kuongeza kipato na badala yake muda mwingihutumika kutafuta chakula na kuhudumia wagonjwa kuliko shughuli za uzalishaji.

- Kuuza ardhi na hivyo kupungua kwa ardhi kwa ajili ya kilimo. Baada ya kuuza malizote, kaya huishia kuuza mashamba na pengine hata nyumba.

Jinsi ya kuboresha uhakika wa chakula katika kaya

• Majukumu ya kaya- Kujikinga na uambukizo wa virusi vya UKIMWI

- Kuanzisha miradi midogo midogo ili kuongeza kipato kwa ajili ya matumizi yakaya ikiwa ni pamoja na chakula.

- Kuboresha njia za uhifadhi wa chakula ikiwemo kusindika kwa njia za asili.

- Kutumia njia bora za utayarishaji wa chakula hasa zile zinazohifadhi nakuboresha upatikanaji wa virutubishi.

- Kulima bustani za matunda, mboga-mboga na vyakula vingine na kuvitumiakwa chakula.

- Kufuga wanyama wadogo kama kuku na sungura na kuvitumia kwa chakula.

- Kutumia vyakula vya asili na vilivyosahaulika, hasa vinavyopatikana kwaurahisi kwenye mazingira husika.

- Kupata elimu kuhusu umuhimu wa uhakika wa chakula na maji.

- Kuzingatia usafi na usalama wa chakula, mazingira, na kuzuia maradhi.

- Kujua kiasi cha chakula kinachotosheleza kaya kwa mwaka mzima

42

Page 52: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

43

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

• Majukumu ya Serikali ya Kijiji/Mtaa- Kuhamasisha jamii kuhusu kujikinga na virusi vya UKIMWI

- Kuhakikisha watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI au wenye UKIMWIhawanyanyapaliwi.

- Kufuatilia uhakika wa chakula katika kaya za watu wanaoishi na virusi vyaUKIMWI.

- Kuhamasisha wanajamii kusaidia watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ilikuhakikisha uhakika wa chakula katika kaya zao.

- Kuzisaidia kaya kutambua kiasi cha chakula kinachotosheleza kaya kwa mwakamzima

• Majukumu ya Serikali Kuu- Kusimamia sera mbalimbali zinazolenga kuongeza kipato na chakula kwa

wananchi.

- Kusimamia programu za jamii zinazohusu chakula.

- Kusaidia kaya wakati wa majanga kama ukame, mafuriko, n.k.

- Kusimamia sera na kuandaa mikakati ya kukabiliana na matatizo yatokanayo naUKIMWI

• Majukumu ya Taasisi zisizo za Kiserikali- Kuhamasisha jamii kuhusu kujikinga na virusi vya UKIMWI na kuwahudumia

watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI au wenye UKIMWI.

- Kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa uhakika wa chakulakatika kaya.

- Kusaidia kaya zilizoathirika ili ziweze kupata kipato cha kutosha na hivyochakula.

- Kushinikiza upangaji wa sera za serikali zinazoboresha uhakika wa chakulakatika kaya.

Wanajamii wanaweza kubuni mbinu mbalimbali za kuhakikisha kaya zina uhakika wachakula. Ni muhimu kwa jamii kusaidia kaya ambazo zina upungufu wa chakula. Jamiizinaweza kuwa na utaratibu wa kuchangia chakula kwa ajili ya kaya zisizo na chakulacha kutosha hasa zenye watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI au UKIMWI.

Page 53: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

44

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Page 54: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

45

TATHMINI YA HALI YA LISHEUfuatiliaji na tathmini ya hali ya lishe ya mtu anayeishi na virusi vya

UKIMWI ni muhimu katika kugundua mapema dalili zozote za matatizo ya kiafya nautapiamlo. Lishe duni ni moja ya matatizo makuu kwa mtu anayeishi na virusi vyaUKIMWI. Lishe duni huweza kusababisha matatizo mengi ya kiafya na hata kifo chamapema, hivyo ni muhimu kufuatilia na kutathmini hali ya lishe mara kwa mara, ilikuboresha lishe na afya ya mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI.

Tathmini nzuri inajumuisha taarifa zinazohusu ulaji na hali ya chakula, vipimo vyaumbile la mwili (anthropometry), vipimo vya kibaiolojia na kikemia (bio-chemicalassessment) na historia ya maradhi.

Lengo hasa la kutathmini hali ya lishe ya mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI nikuangalia au kufuatilia maendeleo ya kilishe ya mtu huyo ili kuweza kumshauriipasavyo. Zifuatazo ni baadhi ya mbinu zinazoweza kutumika katika kutathmini haliya lishe.

Historia ya ulaji wa chakulaHii huangalia kiasi, aina ya chakula mteja anachokula, idadi ya milo, vyakulaanavyopendelea na asivyopendelea, miiko katika vyakula, matatizo katika ulaji wavyakula kama kukosa hamu ya kula, usafi katika uandaaji wa vyakula, jinsi mtejaanavyohifadhi vyakula, wapi anakula chakula, nani anapika, anatumia nishati ganikupikia, anapataje chakula chake, matumizi ya virutubishi vya nyongeza na dawa, n.k.

Vipimo vya umbile la mwiliTathmini ya hali ya lishe huweza pia kufanyika kwa kuangalia vipimo vya umbile lamwili. Vipimo hivyo vipo vingi na vifuatavyo ni baadhi ya viashirio:

Uwiano wa uzito na urefuKiashirio hiki hutumia uwiano wa uzito na urefu ili kutathmini hali ya lishe ya mtu.Uzito wa mwili ni jumuisho la uzito wa mifupa, maji, misuli na mafuta yaliyokomwilini. Urefu ni kimo cha mwili wa mtu. Kipimo hiki kinapotumika kwa vijana waliokatika umri kati ya miaka 9 na 24, chati maalumu ambayo inahusisha umri na jinsihutumika kutambua hali ya lishe.

Kutumia Body Mass Index (BMI)BMI ni kielezo cha umbile la mwili ambacho hutumika kutathmini hali ya lishe ya mtu.Kielezo hicho cha uwiano wa urefu na uzito hakitumiki kwa wanawake wajawazito.Ni muhimu kupima uzito na urefu wakati huohuo ili kupata uwiano sahihi. Uwianohuo wa uzito katika kilo na urefu katika mita hupatikana kwa kutumia kanuni ifuatayo:

Uzito (kg)

Urefu2 (m2) = BMI

8

8. T

AT

HM

IN

I Y

A H

AL

I Y

A L

IS

HE

Page 55: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

(Adapted from: Semper, Stockholm)

Njia hii hutumika kutathmini hali ya lishe ya mtu kwa haraka. Huweza kutumikakupima watu wengi, ni rahisi kutumia mahali popote na haina gharama kubwa.Mahitaji yake ni mizani ya kupimia uzito na kifaa cha kupimia urefu (height measure). BMI huwa na viwango vinavyoashiria hali ya lishe ya mtu. Vifuatayo ni viwango hivyokama vilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Viwango vilivyotajwa hapochini hutumika watu wazima tu.

BMI chini ya 18.5 = Hali duni ya lisheBMI kati ya 18.5 mpaka 24.9 = Hali nzuri ya lisheBMI kati ya 25.0 na 29.9 = Unene uliozidiBMI ya 30.0 au zaidi = Unene uliokithiri au kiribatumbo

Ikumbukwe kuwa viwango hivi vya BMI vilivyoonyeshwa kwenye KielelezoNa. 5 hutumika kwa watu wote wazima na si maalumu kwa watu wanaoishina virusi vya UKIMWI au wenye UKIMWI. Viwango hivyo vinapotumikakutathmini hali ya lishe ya vijana kati ya miaka 9 hadi 24, umri na jinsihuhusishwa. BMI haiwezi kutumika kwa wanawake wajawazito.

Kielelezo Na. 5: Chati ya BMI kwa watu wazima

46

UFUNGUO:

Hali duni ya lishe

Hali nzuri ya lishe

Unene uliozidi

Unene uliokithiri au kiribatumbo

Kilo

Sen

tim

ita

Page 56: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Historia ya maradhiTathmini ya lishe ya mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI au mwenye UKIMWIinaweza pia kufanyika kwa kuchukua historia ya maradhi yanayompata mara kwamara. Dadisi juu ya:- Maradhi katika mfumo mzima wa chakula, mfano kuharisha, kichefuchefu,

kutapika, n.k.- Upataji choo.- Magonjwa nyemelezi.- Magonjwa kama kisukari, malaria, n.k.

Uzito wa mwiliKiashirio hiki hutumika kuangalia mabadiliko ya umbile la mwili. Uzito wa mwilihupimwa kwa kutumia mizani. Kipimo hiki cha uzito kinashauriwa kufanyika marakwa mara, angalau mara moja kwa wiki. Kupungua kwa kilo 6 – 7 kwa mwezi bilakukusudia huashiria hali mbaya ya lishe na afya.

Vipimo vya kibaiolojia na kikemia

Hii inajumuisha tathmini ya virutubishi mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitamini namadini. Hata hivyo kiashirio cha kibailojia na kikemia kinachotumika zaidi ni kipimocha wekundu wa damu (Haemoglobin (Hb).

Kupima wekundu wa damu (Hb)Upungufu wa wekundu wa damu unaweza kuonekana kwa macho au kupimwamaabara. Tathmini ya maabara inahusisha kupima kiasi cha wekundu wa damu(haemoglobin) na kuona kama wekundu unafikia kiwango rasmi kilichowekwa nashirika la Afya Duniani (WHO) kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali lifuatalo:

Jedwali Na. 3: Kiwango cha Haemoglobin (HB) kinachoashiria Upungufuwa Wekundu wa Damu

47

Chanzo: Imetafsiriwa kutoka The Population, Health and Nutrition Information, 2003

Uwiano wa uzito na umriKiashirio hiki mara nyingi hutumika kutathmini hali ya lishe kwa watoto walio chini yaumri wa miaka mitano. Kipimo hiki kinahitaji kumpima mtoto mara kwa mara angalaumara moja kwa mwezi ili kuweza kupata picha kamili ya kasi ya ukuaji wa mtoto nahali yake ya lishe. Kipimo hiki hutumika kwenye kliniki za watoto hapa nchini.

Page 57: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

48

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Page 58: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Ni muhimu kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na mtengenezaji wa dawa audaktari kuhusu matumizi ya dawa na chakula kwani kutokufanya hivyo

kunaweza kusababisha madhara

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

UHUSIANO KATI YA MATUMIZI YADAWA NA CHAKULA

Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI au wenye UKIMWI mara nyingi huwawanatumia dawa za aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na dawa za kurefusha maisha(ARVs), na dawa za kutibu au kupunguza kasi ya magonjwa nyemelezi pamoja namatatizo mengine ya kiafya yanayotokana na uambukizo wa virusi vya UKIMWI.Pamoja na umuhimu wa chakula kwa mgonjwa yeyote, hususan mtu anayeishi na virusivya UKIMWI au UKIMWI, chakula na dawa huweza kuwa na mwingiliano ambaohuwa na faida au athari. Katika mwingiliano huo, chakula huweza kusaidia dawakufanya kazi vizuri mwilini au kuathiri namna dawa inavyofanya kazi. Vilevile dawahuweza kuathiri usharabu, usafirishwaji na utumikaji wa virutubishi vilivyoko kwenyechakula.

Jinsi chakula kinavyoingilia matumizi ya dawaChakula huweza kuingilia usharabu wa dawa, usambazwaji wake mwilini na pia utoajiwa mabaki ya dawa mwilini. Baadhi ya vyakula huweza kuboresha usharabu na namnadawa inavyofanya kazi, na vyakula vingine huweza kudhoofisha.

Jinsi dawa zinavyoingilia matumizi ya chakula mwilini• Baadhi ya dawa huweza kuingilia usharabu wa virutubishi, matumizi ya virutubishi

na utoaji mabaki mwilini. Baadhi ya athari zitokanazo na dawa huweza kumfanyamgonjwa ashindwe kula chakula cha kutosha, pia kudhoofisha usharabu wavirutubishi mwilini. Kwa mfano, baadhi ya dawa husababisha kichefuchefu,mabadiliko ya ladha, kukosa hamu ya kula, kutapika, n.k. Baadhi ya athari hizi nikama zile za matatizo yanayoambatana na kuishi na virusi vya UKIMWI, hivyozinaweza kukabiliwa kama ilivyoelekezwa hapo awali katika Sura ya Sita.Kubadilika kwa ladha kinywani huweza kukabiliwa kwa kutumia viongeza ladha(flavour enhancers) kama vile chumvi kiasi, sukari, viungo, siki (vinegar), ndimu aulimau ambavyo huweza kusaidia kuongeza ladha ya chakula na kuficha ladha mbayainayoletwa na dawa.

• Baadhi ya dawa zinapotumika pamoja na baadhi ya vyakula zinaweza kuleta athariambazo sio nzuri kwa afya na lishe. Kwa mfano baadhi ya dawa zikitumiwa pamojana pombe huleta matatizo katika kongosho.

49

9

9. U

HU

SIA

NO

K

AT

I Y

A M

AT

UM

IZ

I Y

A D

AW

A N

A C

HA

KU

LA

Page 59: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Uchunguzi wa kina wa athari za dawa, hasa zile za kurefusha maisha kwa watu wenyevirusi vya UKIMWI au UKIMWI umefanyika zaidi katika nchi zilizoendelea ambazowatu wake wana hali nzuri ya lishe. Hata hivyo athari za dawa hizo kwa watu wenyehali duni ya lishe bado hazijajulikana vizuri. Ni muhimu kuwasaidia wagonjwakutambua athari zinazojitokeza wakati wanapotumia dawa fulani na kutoa taarifa ilizichunguzwe zaidi. Vilevile ni muhimu kupata na kufuata maelekezo yanayotolewa namtengenezaji wa dawa au daktari kuhusu matumizi ya dawa na chakula ili kuepukakuathiri matibabu na hali ya lishe ya mgonjwa.

Jedwali Na. 4: Baadhi ya dawa, ushauri wa chakula na athari zinazowezakujitokeza

50

Page 60: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Mtumiaji wa dawa ashauriwe kuchunguza na kuripoti hali mbalimbali autatizo linapojitokeza ili apate ushauri zaidi.

Kumbuka kuzingatia muda wa kumeza dawa. Kwa mfano dawailiyoelekezwa kumezwa mara tatu kwa siku, inatakiwa imezwe kila baada yasaa 8. Vilevile dawa iliyoelekezwa kumezwa mara moja kwa siku, inatakiwa

imezwe muda huo huo kila siku. Hivyo ni muhimu kwa mtoa hudumakumsaidia mgonjwa kupanga utaratibu mzuri ambao utahakikisha dawa

inatumiwa ipasavyo.

51

Chanzo: Imetafsiriwa kutoka FANTA, 2003

Page 61: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

52

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Page 62: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

ULISHAJI WA MTOTOSura hii inatoa maelekezo kuhusu ulishaji wa mtoto wakati mama hana

virusi vya UKIMWI, hajui hali yake ya uambukizo na pia wakati mama anaishi navirusi vya UKIMWI. Elimu kuhusu ulishaji watoto katika hali ya kawaida ni msingimuhimu kwa mama kuelewa jinsi ya kumlisha mtoto wakati ana virusi vya UKIMWI.

Sura hii haitoshi kumfanya mtoa huduma au mnasihi kuwa na stadi na utaalamu wakutosha kwenye eneo hilo. Ili kuweza kutoa huduma kamilifu kwa mama anayeishi navirusi vya UKIMWI kuhusu kumlisha mtoto, mtoa huduma anahitaji mafunzo zaidikama itakavyokuwa imeelekezwa na sekta ya Afya. Aidha mtoa huduma ambayehajapata mafunzo ya kutosha, atahitaji kuwafahamu watoa huduma ambao wamepatamafunzo hayo ili waweze kushirikiana kwa kutoa rufaa kwa mama ili apate hudumakamilifu. Taarifa ambazo zimewekwa kwenye sura hii ni za kumwezesha mtoa hudumakupata mwanga au kuelewa kwa kiasi jinsi ya ulishaji wa mtoto aliyezaliwa na mamaanayeishi na virusi vya UKIMWI.

Kwa wanawake ambao hawana virusi vya UKIMWI, wale ambao hawajui hali zao zauambukizo na wale waliopima lakini hawakuchukua majibu; wote wanakuwa katikakundi moja; ambapo hushauriwa kumlisha mtoto kama kawaida na kufuata taratibu zakawaida za kunyonyesha.

Maziwa ya mama ndiyo chakula pekee na bora zaidi kwa mtoto mchanga kulikomaziwa mengine yoyote. Kugundulika uwezekano wa maziwa ya mamakumwambukiza mtoto virusi vya UKIMWI kumesababisha wataalamu kushauriutumiaji wa maziwa mbadala au kurekebisha namna ya kunyonyesha ili kupunguzauwezekano wa uambukizo wa virusi vya UKIMWI kwa mtoto. Ni muhimuikumbukwe kuwa chakula cha mtoto chini ya umri wa miezi sita ni maziwa pekee.

Ulishaji wa mtoto wakati mama hana virusi vya UKIMWI auhafahamu hali yake ya uambukizo

Kunyonyesha maziwa ya mamaNi dhahiri kuwa maziwa ya mama ndiyo lishe bora kwa mtoto mchanga kuliko maziwamengine yoyote. Kunyonyesha maziwa ya mama kunampa mama pamoja na mtotofaida nyingi.

• Faida kwa mtoto:

- Humpatia virutubishi vyote anavyohitaji kwa uwiano ulio sahihi kwa ukuaji waakili na mwili kwa miezi sita ya mwanzo;

- Humpatia kinga dhidi ya maradhi mbalimbali kama kuharisha, maradhi ya njiaya hewa na masikio;

- Huleta uhusiano mzuri na wa karibu kati ya mtoto na mama;

- Watoto walionyonya maziwa ya mama huwa na mwenendo mzuri pamoja na

10

53

10

. U

LIS

HA

JI W

A M

TO

TO

Page 63: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

akili zaidi ukilinganisha na wale wasionyonya maziwa ya mama.

- Maziwa ya mama huyeyushwa kwa urahisi tumboni mwa mtoto na hivyokusharabiwa na kutumiwa na mwili kwa ufanisi.

• Faida kwa mama:

- Mama anaponyonyesha mara baada ya kujifungua husaidia tumbo la uzazikurudi katika hali ya kawaida mapema. Pia husaidia kupunguza damu kutokabaada ya kujifungua hivyo huchangia kuzuia upungufu wa wekundu wa damu;

- Hupunguza uwezekano wa kupata ujauzito katika miezi sita ya mwanzo kamamama atamnyonyesha mtoto maziwa yake pekee mara nyingi (zaidi ya mara 10)kwa siku na pia kama hajapata hedhi katika miezi sita ya mwanzo;

- Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya mfuko wa uzazi na matiti;

- Hujenga uhusiano wa karibu kati ya mama na mtoto; na

- Iwapo mama aliongezeka uzito mkubwa wakati wa mimba, kunyonyeshahusaidia kumrudishia mama umbile lake la kawaida.

• Faida nyingine za maziwa ya mama:- Ni safi, salama na hupatikana muda wote katika joto sahihi kwa mtoto na

hayahitaji matayarisho;

- Hayaharibiki ndani ya titi na hata yakikamuliwa huweza kukaa kwa muda wasaa 8 katika joto la kawaida bila kuharibika, na saa 72 kwenye jokofu;

- Gharama yake ni ndogo ukilinganisha na maziwa mbadala;

- Nchi huokoa fedha za kigeni ambazo zingenunulia maziwa mbadala na dawa;

- Huokoa muda wa mama na fedha za familia ambazo zingenunua maziwambadala au kulipia matibabu;

- Hayaleti matatizo ya mzio (allergies) kama pumu na magonjwa ya ngozi;

- Kunyonyesha maziwa ya mama huchangia kutunza mazingira, kwani hayaachimabaki kama makopo na chupa ambavyo hutumika kwa maziwa mbadala;

- Maziwa ya mama yana maji ya kutosha hivyo mtoto chini ya miezi sita hahitajimaji;

• Mapendekezo ya kumsaidia mama ili anyonyeshe kwa ufanisi

- Mtoto aanze kunyonya maziwa ya mama mara tu baada ya kuzaliwa (katika saamoja ya mwanzo);

- Mama aliyejifungua kwa operesheni, asaidiwe ili aanze kunyonyesha maraanapopata fahamu. Inaweza kuchukua hadi saa sita kupata fahamu, mtotoasipewe maji ya sukari au ya kawaida. Mama ambaye hakupewa dawa yausingizi anaweza kuanza kunyonyesha mapema zaidi;

- Mtoto anyonyeshwe kila anapohitaji usiku na mchana ili kuendeleza utokajimzuri wa maziwa ya mama;

54

Page 64: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

- Mtoto asipewe kitu kingine chochote hata maji, isipokuwa maziwa ya mamampaka afikie umri wa miezi sita;

- Mtoto apakatwe kwa namna ambayo anafikia titi vizuri (Angalia picha 1 (a));

- Wakati wa kunyonyesha, chuchu yote na sehemu kubwa ya eneo jeusilinalozunguka chuchu liingie kinywani kwa mtoto (Angalia picha 2(a));

- Mtoto afikishapo umri wa miezi sita inashauriwa kuanza kumpa chakula chanyongeza huku akiendelea kunyonya maziwa ya mama. Mtoto apewechakula cha nyongeza kwa kutumia kikombe au kibakuli na kijiko;

- Mtoto anyonyeshwe kwanza, ndipo apewe chakula cha nyongeza (baada yamiezi 6);

- Vyakula vya nyongeza viwe ni vya mchanganyiko wa makundi yafuatayo yavyakula:

- Vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi- Vyakula vinavyotokana na wanyama na jamii ya mikunde- Mboga-mboga- Matunda- Mafuta na sukari (kwa kiasi)

- Mtoto aendelee kunyonya mpaka afikie umri wa miaka miwili au zaidi,huku akipewa chakula mara tano au zaidi kwa siku;

55

Picha 1 (a)

inaonyesha njia sahihi yakumshika mtoto ili afikie titivizuri. Tumbo la mtotolimemwelekea mama na usoumeangalia na umesogelea titi.

Kielelezo Na. 6: Jinsi ya kumpakata na kumweka mtoto kwenye titi

Page 65: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

MUHIMUMtoto anayepewa chakula cha nyongeza, ni vyema

anyonyeshwe kabla ya kulishwa

Picha 1 (b) inaonyesha njiaambayo si sahihi ya kumshikamtoto. Hapo mtoto hatawezakuingiza titi kinywani vizuri.

Picha 2 (a) inaonyesha mtotoambaye titi limeingia vizurikinywani yaani chuchu pamoja nasehemu nyeusi inayozungukachuchu imeingia kinywani.Midomo iko wazi na kidevukimegusa titi. Mtoto atanyonyavizuri.

Picha 2. (b) inaonyesha mtotoambaye hakuingiza titi vizurikinywani. Mtoto huyu ananyonyachuchu tu, midomo haikufungukavizuri na kidevu kiko mbali na titi.Mtoto hataweza kunyonya vizuri.

56

Page 66: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWILishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Ulishaji wa mtoto aliyezaliwa na mama mwenye virusi vyaUKIMWI

Uambukizo wa virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtotoKwa kawaida sio wanawake wote wenye virusi vya UKIMWI huwaambukiza watotowao. Inakadiriwa kuwa kiasi cha asilimia 60 hadi 70 ya watoto wanaozaliwa nawanawake wenye virusi vya UKIMWI hawaambukizwi kabisa hata kama hakuna hatuazozote zilizochukuliwa kupunguza uwezekano wa uambukizo. Inakadiriwa asilimia 30hadi 40 ya watoto huambukizwa virusi vya UKIMWI ambapo:

- Asilimia 5 – 10 ya watoto wanaambukizwa wakati wa ujauzito

- Asilimia 10 – 20 wanaambukizwa wakati wa uchungu na kujifungua

- Asilimia 5 – 20 wanaambukizwa wakati wa kunyonyeshwa

Mambo yanayochangia kuongeza hatari ya uambukizo wa virusi vya UKIMWIkutoka kwa mama kwenda kwa mtoto:� Mama kuambukizwa virusi vya UKIMWI wakati wa ujauzito au wakati wa

kunyonyesha. Wakati mama anapoambukizwa, huwa na virusi vingi mwilini kwahiyo uwezekano wa kumwambukiza mtoto ni mkubwa zaidi.

� Mama kuwa na UKIMWI. Uwezekano wa kumwambukiza mtoto ni mkubwakwani mama atakuwa na virusi vya UKIMWI vingi mwilini mwake.

� Mama kuwa na maambukizo ya magonjwa ya ngono wakati wa ujauzito.Magonjwa ya ngono husababisha michubuko ukeni ambayo huongeza hatari yauambukizo wa virusi vya UKIMWI iwapo mama hafanyi ngono salama.

� Taratibu zinazotumika wakati mama anapojifungua. Kwa mfano kuongeza njia yauzazi, uchanaji mapema wa utandu, mtoto kunyonywa uchafu baada ya kuzaliwa.

� Hali ya lishe ya mama. Mama mwenye hali nzuri ya lishe huwa na mfumo thabitiwa kinga ambao huchelewesha mama huyo kupata UKIMWI.

� Hali ya matiti ya mama. Matiti yenye vidonda au michubuko, chuchu zinazotoadamu na majipu ya titi huongeza hatari ya mama kumwambukiza mtoto wakeiwapo mtoto ananyonyeshwa.

� Ulishaji wa kuchanganya maziwa ya mama na vinywaji au vyakula vingine.Vyakula na vinywaji kama maziwa mbadala, maji, chai, uji, maji ya matunda, n.k.huweza kusababisha michubuko kwenye utumbo wa mtoto na hivyo kutoamwanya kwa uambukizo wa virusi vya UKIMWI.

� Muda wa kunyonyesha. Kadiri kipindi cha kunyonyesha kinavyokuwa kirefu,ndivyo uwezekano wa kumwambukiza mtoto unavyoongezeka. Hatarihuongezeka zaidi iwapo mama mwenye virusi vya UKIMWI atamnyonyeshamtoto wake kwa zaidi ya miezi sita kwani wakati huo mtoto hupewa vyakulavingine.

57

Page 67: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

� Hali ya kinywa cha mtoto. Vidonda vya kinywani au kooni na utandu mweupekinywani kwa mtoto huweza kuongeza hatari ya uambukizo wa virusi vyaUKIMWI kupitia sehemu hizo zenye vidonda.

Ikumbukwe kuwa njia kuu ya kuzuia mtoto kupata virusi vya UKIMWI niwazazi kuzuia wasiambukizwe virusi hivyo. Jukumu hilo ni la baba na mama.

Kumlisha mtoto mchanga aliyezaliwa na mama mwenye virusi vyaUKIMWI (miezi 6 ya mwanzo)

Tamko rasmi lililotolewa na mashirika ya kimataifa (WHO/UNAIDS/UNICEF)linasisitiza mambo muhimu yafuatayo:

• Mama mwenye virusi vya UKIMWI aelekezwe kikamilifu kuhusu hatari yakuambukizwa mtoto kupitia maziwa ya mama na njia nyingine;

• Wanawake wahimizwe na wapewe huduma za ushauri nasaha na kupima virusi vyaUKIMWI kwa hiari (VCT);

• Mwanamke mwenye virusi vya UKIMWI apewe taarifa muhimu na zilizo sahihi,kumwezesha kufanya uamuzi sahihi wa njia ya kumlisha mtoto wake, iwe nikunyonyesha kwa maziwa yake au kutumia maziwa mbadala.

Vipengele muhimu vya kuzingatia wakati wa kutoa unasihiIkumbukwe kuwa kwa kusoma sura hii tu, mnasihi hawezi kuwa na stadi za kutoshakumsaidia mama mwenye virusi vya UKIMWI kuhusu ulishaji wa mtoto wake.Mnasihi azingatie vipengele vifuatavyo katika kumshauri mama mwenye virusi vyaUKIMWI kabla ya kupata mimba, wakati wa ujauzito au akishajifungua:

• Ni vizuri mnasihi awafahamu wanasihi waliopewa mafunzo ya kutosha kuhusuulishaji wa mtoto aliyezaliwa na mama mwenye virusi vya UKIMWI ili wawezekushirikiana;

• Kila mama apewe unasihi peke yake;

• Mama aelezwe njia zote zinazoweza kumwambukiza mtoto virusi vya UKIMWIikiwemo unyonyeshaji maziwa ya mama;

• Mama afahamishwe kiwango cha hatari iliyopo ya uambukizo wa virusi vyaUKIMWI kupitia maziwa ya mama na njia nyingine;

• Mama ana haki ya kuelezwa kwa ufasaha njia zote ambazo zinaweza kutumikakumlisha mtoto mchanga katika hali kama hii; pia faida na athari za kila njia yaulishaji;

• Mama afahamishwe kwamba watoto wasionyonya maziwa ya mama wana hatari

58

Page 68: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

kubwa zaidi ya kupata maradhi kama vile ya kifua, masikio, kuharisha, mzio(allergies) na kupungukiwa kinga ambayo watoto wanaonyonya huipata kwenyemaziwa ya mama;

• Mama asaidiwe ili aweze kujipima uwezo wake kifedha, kuona kama anawezakumudu njia aliyoichagua (kama kununua maziwa na vifaa), kimazingira(upatikanaji wa maji safi na salama na hali ya usafi) na huduma za afya;

• Mama asaidiwe aweze kupima iwapo kutakuwa na athari zozote kwa familia yakekutokana na njia atakayoichagua;

• Mama ahimizwe kuendelea kumpeleka mtoto kliniki kama kawaida ili apate chanjona kufuatilia ukuaji wake na hali yake ya afya;

• Mama aelezwe umuhimu wa kuishirikisha familia yake hasa mume au baba wamtoto kuhusu uamuzi wake, na ikiwezekana washirikishwe kwenye hatua zote zakufanya uamuzi huo;

• Mama aelekezwe mahali anapoweza kupata ushauri au msaada zaidi wa njiaaliyoichagua, hasa kama kuna wanawake wengine wenye uzoefu zaidi;

• Mama asiyejua hali yake ya uambukizo wa virusi vya UKIMWI, ashauriwekunyonyesha maziwa yake kama kawaida. Pia ashauriwe kwenda kupima ili ajuehali yake.

Njia zinazoweza kutumika kumlisha mtoto mchanga tangu anapozaliwampaka miezi sita kwa mama anayeishi na virusi vya UKIMWIKumbuka kuwa katika miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto yeyote, maziwa ndiyochakula pekee na muhimu sana. Maziwa hayo yanaweza kuwa ya mama au maziwamengine. Ikiwa mtoto hanyonyeshwi maziwa ya mama basi apate maziwa menginekiasi cha mililita (ml.) 150 za maziwa kwa kila kilo moja ya uzito wake kwa siku. Kwamfano mtoto mchanga mwenye kilo tano anahitaji mililita (ml.) 750 za ujazo za maziwa(yaani ml. 150 x kilo 5) kwa siku, kiasi hiki kinaweza kugawanywa katika milo mitanoau zaidi kwa siku. Ni muhimu kutumia kikombe kumlisha mtoto badala ya chupa yakunyonya. Hii hupunguza hatari ya maradhi ya kuhara kwani ni rahisi kusafishakikombe kuliko chupa.

59

KUMBUKANi muhimu kuhakikisha kwamba wanawake ambao hawajaambukizwa virusi vya

UKIMWI na wale wasiojua hali zao za uambukizo wanaendelea kushauriwakunyonyesha maziwa yao, na wasishawishike kutumia maziwa mbadala kwa

kuwaona wengine walioshauriwa na kuamua kutumia maziwa hayo.

Page 69: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

60

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Kuna njia kuu mbili zinazoweza kutumika kumlisha mtoto aliyezaliwa na mamamwenye virusi vya UKIMWI. Njia hizi ni kutumia maziwa ya mama na kutumiamaziwa mbadala.

� Kutumia maziwa ya mamaMama aliyeamua kuchagua kutumia maziwa yake ana njia kuu tatu ambazo anawezakuamua ni ipi itakayomfaa yeye na mtoto wake. Njia hizi ni:

� Kunyonyesha maziwa ya mama pekee tangu mtoto anapozaliwa hadi miezi sita;

� Kunyonyesha maziwa ya mama kwa muda mfupi (chini ya miezi sita);

� Kutumia maziwa ya mama yaliyokamuliwa na kuchemshwa.

• Kunyonyesha maziwa ya mama pekee tangu mtoto anapozaliwa hadi miezi 6Tafiti zimeonyesha kuwa kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee kunapunguzauwezekano wa mtoto kupata uambukizo wa virusi vya UKIMWI kutoka kwa mamayake ukilinganisha na kumnyonyesha mtoto na wakati huo huo kumpa maziwamengine, vinywaji au vyakula vingine. Iwapo mama atachagua njia hii anashauriwa:

� Kumnyonyesha mtoto wake maziwa yake pekee kwa miezi sita ya mwanzo bila yakumpa mtoto kitu kingine chochote hata maji. Kumpa mtoto maziwa mbadala,vinywaji au vyakula vingine huweza kuongeza hatari ya uambukizo wa virusi vyaUKIMWI kwa mtoto. Vinywaji au vyakula hivyo huweza kusababisha michubukokwenye utumbo wa mtoto na hivyo kuruhusu virusi vya UKIMWI kupenya kwaurahisi;

� Kuhakikisha mtoto ananyonyeshwa kila anapohitaji, usiku na mchana;

� Kumpakata na kumweka mtoto vizuri kwenye titi ili kuzuia matatizo ya matitiyanayoweza kujitokeza, kama chuchu kupata mipasuko au michubuko. Matatizohayo huongeza hatari ya uambukizo wa virusi vya UKIMWI kutoka kwa mamakwenda kwa mtoto (Angalia Picha 1(a) na 2 (a) ukurasa wa 55 - 56) ;

� Kuhakikisha matatizo kinywani kwa mtoto yanatibiwa mapema, kwa mfanoutandu mweupe kwani huongeza hatari ya uambukizo wa virusi vya UKIMWIkwa mtoto;

� Kuacha kabisa kumnyonyesha mtoto baada ya miezi sita. Wakati huo mamaanaweza kukamua na kuchemsha maziwa yake akampa mtoto, huku akimpatiavinywaji na vyakula vingine.

• Kunyonyesha maziwa ya mama kwa muda mfupiKumwachisha mtoto kunyonya maziwa ya mama yake mapema husaidia kupunguzauwezekano wa mtoto kuambukizwa virusi vya UKIMWI kupitia maziwa. Kwakufanya hivyo muda wa mtoto kuwa kwenye hatari ya uambukizo wa virusi vyaUKIMWI hupungua.

� Iwapo mama mwenye virusi vya UKIMWI atachagua njia hii anashauriwa kuachakumnyonyesha mtoto wake mapema iwezekanavyo kabla ya miezi sita. Mudahalisi wa kuacha kumnyonyesha mtoto utaamuliwa na mama mwenyewe kwa

Page 70: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

kuzingatia uwezekano wa kupata maziwa mbadala na uwezo wa kuyatumiaipasavyo.

� Mama akumbuke kumnyonyesha mtoto maziwa yake pekee bila kumpa maziwambadala, vinywaji au vyakula vingine vyovyote. Uchanganyaji wa maziwa yamama na maziwa mbadala, vinywaji au vyakula vingine huongeza hatari yauambukizo wa virusi vya UKIMWI kwa mtoto. Mama anashauriwa kumpakata nakumweka mtoto vizuri kwenye titi ili kuzuia matatizo ya matiti yanayowezakujitokeza.

� Mama anapoamua kuacha kumnyonyesha mtoto wake ashauriwe kufanya hivyokatika muda mfupi. Ili kuweza kuzuia hatari ambazo zinaweza kujitokeza katikakipindi hicho cha mpito au kutokana na mabadiliko ya ghafla, mama ashauriwekuanza kukamua maziwa yake katika wiki mbili kabla ya kumwachisha mtoto nakumnywesha mtoto maziwa hayo kwa kutumia kikombe. Hii itamwezesha mtotokuweza kuzoea kutumia kikombe.

� Mtoto aliyeachishwa kunyonya maziwa ya mama yake kabla ya miezi sita apewemaziwa mbadala au mama akamue maziwa yake na kuyachemsha kabla ya kumpamtoto. Mtoto anyweshwe maziwa hayo mara tano au zaidi kwa siku, akizingatiakipimo cha mililita 150 kwa kila kilo ya uzito wake kwa siku.

� Mama anayeamua kuacha kumnyonyesha mtoto wake mapema anapaswakusaidiwa kufanya hivyo kwa ufanisi na usalama ili kuepusha madhara yoyoteyanayoweza kutokea kwa mtoto.

� Mama akiwa na hali mbaya, hasa anapopata magonjwa nyemelezi na akawamgonjwa sana ni vyema aache kunyonyesha.

• Kutumia maziwa ya mama yaliyokamuliwa na kuchemshwaVirusi vya UKIMWI vilivyoko kwenye maziwa ya mama vinaweza kuharibiwa kwakuchemsha maziwa hayo yaliyokamuliwa. Tafiti zimeonyesha kuwa virusi hivyo hufabila kuharibu kingamwili zilizopo kwenye maziwa iwapo yatapashwa moto kati yanyuzi joto 56°C – 63°C kwa muda wa dakika 20. Lakini katika mazingira ya kawaidasio rahisi kupima nyuzi joto hizo hivyo inashauriwa kuacha maziwa hayo mpakayachemke. Mara tu yakichemka yaipuliwe. Kwa kuchemsha maziwa hayo baadhi yakingamwili na virutubishi vilivyomo hupungua. Ni muhimu mama apate ushauri wadaktari au mtaalamu wa afya kuhusu virutubishi vya nyongeza vya kumpa mtoto.

Iwapo mama ataamua kutumia maziwa yake aliyoyakamua na kuyachemsha yafuatayoni muhimu:

- Mama aelekezwe njia sahihi ya kukamua maziwa yake bila ya kusababisha maumivuya titi lake;

- Maziwa hayo yachemshwe na yaipuliwe pindi tu yanapoanza kuchemka;

- Maziwa hayo yapoozwe kwa haraka aidha kwa kutumbukiza chombo chenyemaziwa ndani ya maji baridi au kuweka ndani ya jokofu;

- Mtoto anyweshwe maziwa hayo kwa kutumia kikombe;

61

Page 71: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

- Maziwa yachemshwe kiasi cha kutosha mlo mmoja tu. Maziwa yaliyochemshwayasihifadhiwe kwa matumizi ya mlo unaofuata.

- Mama anapochagua njia hii kama ilivyo kwa njia nyingine anapaswa kupata unasihina kusaidiwa.

Kielelezo Na. 7: Jinsi ya kukamua maziwa ya mamaMaelezo muhimu:Maziwa yaliyokamuliwa yanaweza kukaa kwenye joto la kawaida bila ya kuharibikakwa saa 8 na kwenye jokofu kwa saa 72. Maziwa yaliyokamuliwa yahifadhiwe kwenyevyombo safi na yafunikwe

Shika sehemu nyeusiinayozunguka chuchu kwakuweka vidole vinne upandewa chini na kidole gumbaupande wa juu, kishabonyeza kwa kugandamizakuelekea kifuani.

Bonyeza sehemu nyeusi yatiti kati ya vidole vinne nakidole gumba.

Bonyeza pia sehemu zapembeni kuhakikishamaziwa yote yanatoka

62

Page 72: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

� Kutumia maziwa mbadalaMaziwa mbadala yanaweza kutumika kumlisha mtoto aliyezaliwa na mama mwenyevirusi vya UKIMWI. Maziwa mbadala ni pamoja na maziwa yaliyotengenezwamaalumu kwa watoto wachanga, maziwa yanayotayarishwa nyumbani kutokana namaziwa ya wanyama kama ng’ombe au mbuzi, maziwa ya unga yenye mafuta (dried fullcream milk) au maziwa yaliyochevushwa (evaporated milk).

• Maziwa yaliyotengenezwa maalumu kwa watoto wachanga (maziwa yawatoto ya kopo)

Maziwa hayo hutengenezwa kutokana na maziwa ya ng’ombe, mbuzi au soya na yanavirutubishi vinavyokaribiana sana na vile vilivyoko kwenye maziwa ya mama. Kwakawaida huwa yameongezwa vitamini na madini.

Iwapo mama ataamua kutumia maziwa hayo kumlisha mtoto wake, ni muhimukufahamu vipengele vifuatavyo:

- Mama anahitaji wastani wa makopo 40 yenye uzito wa nusu kilo (gramu 500) ilikuweza kumlisha mtoto wake kwa miezi sita ya mwanzo;

- Maziwa kwa ajili ya mtoto yanapaswa yachaguliwe kulingana na umri wake;

- Maelekezo yaliyoandikwa kwenye kopo yanapaswa kuzingatiwa na kufuatwa;

- Ni muhimu kutumia kikombe wakati wa matayarisho kwa vile uoshaji wake nirahisi;

- Mama anapaswa kumlisha mtoto kwa kutumia kikombe huku akiwa amempakatakaribu naye ili kujenga uhusiano wa karibu;

- Usafi wa mtayarishaji, mazingira na vifaa vya kutayarishia maziwa uzingatiwe;

- Mama ahakikishe kuwa muda wa kutumika maziwa hayo haujapita (expiry date);

- Mama anapaswa kuwa mwangalifu sana na kupata msaada unaotakiwa ili mtotoasipate magonjwa ya kuambukizwa hasa ya kuharisha;

- Maziwa yatengenezwe ya kutosha mlo mmoja tu na iwapo yatabaki yasiwekwe kwamatumizi ya baadaye. Wapewe watoto wakubwa au yachanganywe kwenye chakulachao;

- Ni muhimu mtoto apelekwe kliniki ili apate chanjo zote na kufuatilia ukuaji wakekwa karibu. Ni muhimu aonwe na daktari mapema tatizo linapotokea.

Maziwa ya mama yaliyokamuliwa na kuchemshwa bado ni borakuliko maziwa mbadala

Wakati wa kumpa mama ushauri wa njia ya kumlisha mtoto wake, mnasihiakumbuke, ili kutumia maziwa mbadala ni muhimu kuhakikisha kuwa hatari yamtoto kufa kwa kutumia maziwa mbadala ni ndogo kuliko hatari ya mtoto kufa

kwa UKIMWI kupitia maziwa ya mama. Mama asaidiwe kuelewa hilo.

63

Page 73: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

• Maziwa ya ng’ombe au mbuzi

Vifuatavyo ni vipengele muhimu, iwapo mama ataamua kumlisha mtoto wake kwakutumia maziwa ya ng’ombe au mbuzi:

- Maziwa lazima yachanganywe na maji yaliyochemshwa na kuongeza sukari kidogo(vipimo viwili vya maziwa na kipimo kimoja cha maji). Kwa mfano kila ujazo wamililita 100 za maziwa ya ng’ombe au mbuzi ziongezwe mililita 50 za ujazo za majiyaliyochemshwa na sukari vijiko vidogo viwili visivyojazwa sana (kijiko mfuto);

- Mchanganyiko huo uchemshwe vizuri;

- Mtoto apewe maziwa hayo yaliyopoozwa kwa kutumia kikombe;

- Kwa siku mtoto apewe kiasi cha mililita 150 kwa kila kilo ya uzito wake;

- Mtoto huyo lazima aonwe na daktari au mtaalamu wa afya atakayetoa ushaurikuhusu aina ya madini na vitamini atakazohitaji mtoto kama nyongeza kwanimaziwa hayo yanaweza kuwa na upungufu wa madini ya chuma, zinki, folic acid navitamini A;

- Usafi wa vifaa vya kutengenezea maziwa, maji safi na salama pamoja na mazingirasafi ni muhimu sana.

Jedwali Na. 5: Mfano wa mahitaji ya siku kwa mtoto kwa kutumia maziwambadala ya ng’ombe au mbuzi

• Maziwa ya unga yenye mafuta (dried full cream milk) au yale yaliyochevushwa(full cream evaporated milk)

Maziwa haya yanaweza kutumika kama maziwa ya aina nyingine hayapatikani. Iwapomaziwa haya yanatumika, yafuatayo ni muhimu:

- Maziwa yatengenezwe kwa kutumia maji yaliyochemshwa na kufuata maelekezokwenye paketi au kopo lake. Unapochanganya hivyo unapata maziwa kama yang’ombe. Baada ya hapo fuata maelekezo yaliyotolewa hapo juu ya jinsi yakutengeneza maziwa ya ng’ombe ili kumfaa mtoto mchanga;

- Mtoto huyo lazima aonwe na daktari au mtaalamu wa afya atakayetoa ushauri wamadini na vitamini za nyongeza atakazohitaji mtoto kwani maziwa hayo yanawezakuwa na upungufu wa madini na vitamini;

64

Page 74: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

65

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

- Usafi wa vifaa vya kutengenezea maziwa, maji safi na salama pamoja na mazingirasafi ni muhimu sana;

- Mtoto apewe maziwa hayo kwa kutumia kikombe.

Namna ya kumlisha mtoto mchanga kwa kutumia kikombe

Kumlisha mtoto kwa kikombe kunapunguza hatari ya uambukizo ambao unawezakutokea kwa kutumia chupa. Kikombe ni rahisi kuosha, na anayemlisha mtotoinalazimu ampakate vizuri, na hivyo kujenga upendo na ukaribu zaidi kati ya mtotona mlezi. Zingatia yafuatayo:

• Mpakate mtoto na muweke nusu wima (kama ameketi);

• Shikilia kikombe cha maziwa kwenye midomo ya mtoto mchanga;

• Kikombe kikae kwenye mdomo wa chini wa mtoto mchanga na kingo zakikombe ziguse mdomo wa juu. Kikombe kiinamishwe ili maziwa yatiririkepolepole kwenye kinywa cha mtoto mchanga;

• Mtoto mchanga huonyesha kuwa tayari kwa kufungua mdomo nakuchangamka. Mtoto mchanga aliyezaliwa na uzito pungufu atachukua maziwakwenye kinywa na ulimi, lakini yule aliyezaliwa na uzito wa kutosha atafyonzamaziwa;

• Usimimine maziwa kwenye kinywa cha mtotomchanga bali shikilia kikombe tu kwenyemdomo naye atafyonza;

• Kama mtoto mchanga amekunywa maziwa yakutosha atafunga mdomo na hatakunywa zaidi.Ikibainika kuwa mtoto mchanga hakunywamaziwa kiasi cha kutosha, aidha atakunywa zaidiwakati mwingine au inashauriwa kumnyweshamara kwa mara. Unashauriwa kupima kiasi chamaziwa aliyokunywa mtoto baada ya saa 24 nasiyo baada ya mlo mmoja.

Page 75: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

• Vinywaji na maziwa yasiyofaa kumlisha mtoto mwenye umrichini ya miezi sita• Maziwa yaliyotolewa mafuta (skimmed milk) na yale yaliyopunguzwa maji na

kuongezwa sukari (sweetened, condensed milk);• Maji ya matunda au maji ya sukari;• Maziwa yaliyoganda (mtindi);• Chai, uji au vyakula vingine.

Kumlisha mtoto wa miezi sita hadi miaka miwiliMtoto anapofikisha umri wa miezi sita anahitaji vyakula vingine vya nyongeza ikiwa nipamoja na maziwa. Kwa mama mwenye virusi vya UKIMWI, yafaa mtoto huyoasiendelee kunyonyeshwa kwani wakati huu hatari ya uambukizo huongezeka.Yafuatayo ni muhimu:

• Mtoto apewe maziwa ya aina nyingine yoyote angalau mara tano kwa siku. Wakatihuu maziwa ya ng’ombe au mbuzi yasichanganywe na maji.

• Maziwa ya mama yaliyokamuliwa na kuchemshwa yanaweza pia kutumika.

• Pamoja na maziwa, mtoto pia apewe chakula cha familia kilicholainishwa au chakulakilichotayarishwa kwa ajili ya mtoto mara tano au zaidi kwa siku.

• Chakula cha mtoto kiwe na mchanganyiko wa angalau chakula kimoja kutokakatika makundi yafuatayo:

� Nafaka na vyakula vitokanavyo na mizizi au ndizi (mahindi, ulezi, mchele,mtama, viazi vya aina zote, mihogo au ndizi).

� Vyakula vitokanavyo na wanyama na mikunde kama mayai, maziwa, samaki,maini, nyama, dagaa, maharagwe, kunde, karanga, njegere, choroko, dengu,mbaazi, n.k.

� Mboga-mboga kama mboga za kijani, karoti, maboga, n.k.

� Matunda kama mapapai, machungwa, maembe ndizi, nanasi, n.k.

� Mafuta na sukari. Mafuta ni pamoja na mbegu zitoazo mafuta kama alizeti,ufuta na karanga, pia siagi au samli. Sukari ni pamoja na asali na sukari.

KUMBUKAMnasihi atumie mbinu za msingi za unasihi kutafuta taarifa zilizo sahihi kutokakwa mama na pia kumpa mama taarifa zilizo sahihi. Njia yoyote ambayo mama

atachagua kutumia kumlisha mtoto, apewe msaada unaowezekana ili awezekufanikisha njia hiyo kwa usahihi na usalama iwezekanavyo

66

Page 76: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

� Vyakula vya mtoto viwe laini ila visiwe vyepesi sana. Ongeza vyakula kamamafuta, sukari, siagi, asali, mbegu zitoazo mafuta kama karanga au korosho,kweme, tui la nazi au maziwa ili kuongeza ubora wa chakula na kufanya kiwe laini.Kimea pia chaweza kutumika kulainisha uji ulio mzito.

� Mtoto aanze kwa kupewa chakula cha aina moja katika mlo. Vyakula vingivisichanganywe kwa mara moja. Hii itasaidia kuzoea kwa urahisi na kujua vyakulavinavyoweza kumletea mtoto matatizo ya mzio (allergies).

� Mtoto aongezewe kiasi cha chakula taratibu kadiri anavyoendelea kukua.

� Mtoto mwenye umri zaidi ya miezi 6 anaweza kutumia maziwa mengine yoyoteyakiwemo maziwa ya mgando (mtindi). Maziwa yaliyotolewa mafuta (skimmedmilk) sio bora kwa mtoto.

67

Page 77: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

68

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Page 78: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

UNASIHIUnasihi ni mazungumzo ya ana kwa ana baina ya mtu mwenye matatizo

(mteja) au kikundi cha watu (wateja) wenye matatizo na mtaalamu mwenye uwezo wakutoa huduma hiyo. Unasihi ni tofauti na ushauri ambao hutolewa na mtuanayemfahamu mwenye tatizo kwa kutumia uzoefu wake. Unasihi hutolewa na mtuasiyemjua mteja na katika kuzungumzia tatizo humwezesha mteja kuelewa tatizo lakekwa kina, kujielewa mapungufu yake, uwezo wake na mipaka yake na kuunda mkakatiwa kulitatua, unaolingana na uwezo wake. Mnasihi lazima awe na uwezo na nia yakumsaidia mteja kufanya maamuzi ya busara kuhusu tatizo lake na mteja lazima awetayari kuzungumzia tatizo lake kwa uwazi na ukweli.

Sifa za mnasihi- Awe na ujuzi wa taaluma ya unasihi- Aielewe vizuri jamii anayoihudumia; utamaduni wake, mila, desturi na matatizo na

utatuzi wake- Aielewe saikolojia ya watu anaowahudumia kama saikolojia ya vijana, watu

wanaoishi na virusi vya UKIMWI, yatima, n.k.- Awe mtunza siri- Awe mkweli- Aweze kukubali utofauti wa watu- Aendane na mazingira- Awe mchangamfu- Awe mwaminifu- Apende kusikiliza zaidi kuliko kuongea- Afahamu mipaka yake- Awe anayejali na kuthamini utu

• Aina za unasihiKuna aina kuu mbili za unasihi:- Unasihi wa mtu mmoja- Unasihi wa kikundi

Unasihi wa mtu mmoja Aina hii ya unasihi ni nzuri ingawaje ni huduma iliyo ghali, kwani hutumia mudamwingi wa kiutaalamu kwa mteja mmoja tu ukilinganisha na ule unaotumika kwakikundi. Katika unasihi huu ni rahisi kushughulikia matatizo binafsi tena kwa kina.

Unasihi wa vikundiAina hii ya unasihi inahusisha watu wenye tatizo linalofanana na wakati mwingine halizinazofanana kiuchumi na kijamii. Unasihi wa kikundi unaweza kufanyika kwa familia,

69

11

11

. U

NA

SIH

I

Page 79: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

mtu na mwenzi wake (couple), yatima, watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI auUKIMWI, n.k.

Unasihi wa familia ni lazima uzingatie:

- Umuhimu wa familia kwa kila mtu

- Tofauti ya wanafamilia na majukumu ya kila mtu

- Sheria zinazotawala maisha ya kifamilia

- Uwezo wa familia katika kukabiliana na mabadiliko

Familia nzuri yenye mafanikio ni ile ambayo wanafamilia wanathaminiana, wanamawasiliano mazuri na wanatumia muda wao wa kupumzika pamoja na wanamuduhali ya wasiwasi au hatari kwa ushirikiano.

Faida za unasihi wa kikundi- Mteja huona kuwa matatizo siyo ya kwake tu- Mteja anapata fursa ya kujifunza mbinu mpya za kukabiliana na matatizo kutoka

kwa wenzake- Wateja katika kikundi hukosoana na kuimarishana

Hasara za unasihi wa kikundi- Siyo rahisi kushughulikia matatizo ya kibinafsi

- Matatizo ya wateja hayashughulikiwi kwa kina

- Kikundi kisipoongozwa vizuri kinaweza kupoteza malengo na kufanya mamboyasiyokusudiwa

Mahali pa kutolea unasihiHuduma ya unasihi itolewe mahali:- Penye faragha- Penye utulivu- Pasafi- Penye hewa ya kutosha na mwanga wa kutosha - Penye samani (furniture) za muhimu mfano; viti, kabati ya kufungia taarifa za

mteja, meza pembeni kwa ajili ya kuandikia, n.k- Penye kujulikana katika jamiiNi vyema muda wa kutoa huduma uwekwe wazi na usiwe unabadilishwabadilishwa.

Unasihi wa mtu na mwenzi wake

Matatizo mengi katika unasihi hasa unaohusu virusi vya UKIMWI yanawezakushughulikiwa kwa mafanikio zaidi kama utahusisha mteja na mwenzi wake.

70

Page 80: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Mbinu za unasihiHatua kuu tatu na za msingi za kufuata wakati wa unasihi

1. Kujenga uhusianoMnasihi ajenge uhusiano na mteja kwa kumkaribisha, kumchangamkia, kumtaja kwajina lake kumjali na kumheshimu. Hii ni hatua ya mwanzo na ya msingi ambayoinarahisisha huduma ya unasihi. Hata hivyo lazima unasihi uwe na mipaka.

2. Kuchunguza au kutafiti tatizo

Katika hatua hii mnasihi hutumia mbinu mbalimbali za mawasiliano ili kulielewa tatizola mteja kwa kina. Hatua hii ikifanyika vizuri humwezesha hata mteja kulielewa vizuritatizo lake.

3. Kutengeneza mkakati au programu ya utatuzi

Hii ni hatua ya mwisho inayomwezesha mteja kujitengenezea mkakati wa kutatuatatizo lake.

Mbinu nyingine za kusaidia katika hatua za msingi zilizotajwa hapo juu

Usikivu: Ni muhimu kusikia maneno na ujumbe usioelezwa kwa maneno kwakumtazama vizuri mteja ili kusoma lugha ya vitendo (Non-verbal communication) aukusikiliza vizuri sauti yake n.k.

Fasili (paraphrasing): Urudie ujumbe aliosema mteja kwa maneno mengine ilikufafanua na kuhakikisha ujumbe aliosema mteja umeeleweka.

Kumueleza kwa maneno hisia unazotambua kwake-(reflection of feelings): Hii nikuhakikisha kuwa unaelewa vizuri hisia zilizoleta tatizo lake.

Kutoa muhtasari wa ujumbe (summarizing): Mnasihi atoe muhtasari wa taarifa yamteja. Hii husaidia kuelewa tatizo kwa kina. Vilevile husaidia kujenga uhusiano.

Ushirikeli (empathy): Mnasihi aonyeshe ushirikeli kwa mteja. Hii ni mbinu yakuonyesha kwa maneno au vitendo kuwa unalielewa tatizo la mteja bila ya kukumbwana hisia. Kwa mfano kama tatizo ni la huzuni mueleze mteja kuwa unaona tatizo ni lakuleta huzuni lakini usilie.

Dodosa mteja (probing): Msaidie mteja kueleza kwa kina tatizo lake kwa kumuulizamaswali zaidi.

Uliza maswali yaliyowazi (open-ended questions): Uliza maswali ambayoyatamfanya mteja aeleze zaidi juu ya tatizo lake na siyo yanayojibiwa ndiyo au hapana.

Kulenga tatizo (focussing): Msaidie kila mara maelezo yake yawe kwenye tatizoanalolielezea.

71

Page 81: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Maadili katika unasihi

Ustadi: Wanasihi watoe huduma katika maeneo ya ustadi wao kufuatana na:

- Elimu yao na uzoefu wao

- Mipaka ya uwezo wao na ustadi wao

- Uwezo wao wa juu katika kazi au taaluma yao

Kutunza siri: Wanasihi wasitoe taarifa za wateja; wawe wasiri na hata wanapotakiwana vyombo vya dola kutoa maelezo fulani, basi watoe yale tu wanayoulizwa kwa ajiliya kazi.

Ukamilifu: Wanasihi lazima wawe wakamilifu katika kazi yao ya kutoa huduma yaunasihi. Ukamilifu utaonyeshwa kwa kuheshimu wateja, kuwa wakweli na kuwatendeahaki wateja.

Kujielewa: Wanasihi lazima wajielewe vizuri; imani zao, vitu wanavyovithamini,mahitaji yao, mipaka yao na athari za yote hayo kwa kazi yao. Wanasihi wasikubalizawadi mbalimbali kutoka kwa wateja

Majukumu ya kiutaalamu: Wanasihi lazima wawe waadilifu katika kazi yao,wawajibike na kukubali jukumu. Wanasihi wawe wakweli na wasitoe ahadi kwa mtejakatika mambo ambayo hawawezi kuyatimiza.

Kuheshimu utu na kazi za watu: Wanasihi lazima waoneshe heshima, utu nakutambua haki za binadamu. Wanasihi watambue na wathamini tofauti za mila kati yawatu mbalimbali, wasibague wateja kwa sababu yoyote ya jinsi, utamaduni, dini auutaifa.

Unasihi unaohusu virusi vya UKIMWILengo la unasihi unaohusu virusi vya UKIMWI ni:

- Kutoa taarifa au maelezo sahihi juu ya virusi vya UKIMWI na kusahihisha taarifazisizo sahihi

- Kuzuia vishawishi vya kujiua

- Kuisaidia familia katika kumsaidia mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI ili awezekukabiliana na hali aliyonayo kifikra na jamii inayomzunguka

- Kumsaidia mteja kuweza kuishi kwa matumaini

- Kuweka mikakati ya kupunguza uwezekano wa kupata uambukizo

Unasihi unaohusu virusi vya UKIMWI au UKIMWI una hatua kuu tatu, nazo ni:

• Unasihi kabla ya kupima

• Unasihi baada ya kupima

• Unasihi wa ufuatiliaji. Huu ni ule unaotolewa ili kumsaidia mtu anayeishi na virusi

72

Page 82: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

vya UKIMWI au yule mwenye UKIMWI kwa muda mrefu. Unasihi wa aina hiihujumuisha unasihi unaohusu lishe.

Hatua za kuzingatia katika kutoa unasihi kabla na baada ya kupima • Unasihi kabla ya kupima

- Anzisha maelewano/uelewano

- Kujua sababu ya kupima

- Uliza juu ya historia au mahusiano ya kimapenzi/ngono

- Eleza juu ya virusi vya UKIMWI

- Rudia kukumbusha juu ya uwezekano wa majibu baada ya kupima, kwambayanaweza kuonyesha kuwepo (chanya) au kutokuwepo (hasi) kwa virusi vyaUKIMWI

- Tafuta au panga malengo baada ya majibu

- Tafuta jambo lolote lenye umuhimu ili lizungumziwe

• Unasihi baada ya kupimaIwapo majibu yameonesha kutokuwepo kwa virusi vya UKIMWI

- Muonyeshe mteja furaha

- Rudia kueleza yale yote muhimu ambayo ulikwisha yazungumzia ikiwa ni pamojana kurudia kupima baada ya miezi mitatu

- Mshawishi mteja aje na mwenzi au mpenzi wake

- Zungumzia jinsi ya kuendelea kuzuia uambukizo

Iwapo majibu yameonesha kuwepo kwa virusi vya UKIMWI

- Mpe mteja majibu yake

- Angalia jinsi gani mteja ameyapokea majibu ili kujua hisia alizonazo

- Muulize mteja kujua kama ana lolote lililo muhimu ili kulizungumzia

- Mueleze mteja jinsi ya kuishi kwa matumaini

- Mpe mteja rufaa kwa unasihi endelevu

- Kabla ya kuagana na mteja ni vyema kufahamu ni jinsi gani atakwemda nyumbani

- Muanzishie mteja au muonyeshe mteja mbinu za mkakati binafsi wa kuzuiauambukizo

73

Page 83: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Mnasihi anatakiwa kuchunguza:

� Tabia bayana zinazoweza kumuweka mteja katika hatari ya uambukizo wavirusi vya UKIMWI au UKIMWI na utayari wa mteja katika kubadilika.

� Namna jamii, utamaduni, uchumi na masuala ya jinsia yanayoweza kuathirihali yake.

� Vizuizi binafsi (internal barriers).

� Na kKumweleza mteja msaada wowote wa kijamii anaoweza kuupata pamojana namna anayoweza kufanikiwa kubadili mwenendo.

Mambo mengine ya kuelezea:

� Hisia binafsi

� Jinsi ya kujali hali ya afya na lishe

� Kuhusisha familia na jamii

� Misaada ya kiroho

� Hali na misaada ya kiuchumi

� Misaada ya kisheria

� Magonjwa nyemelezi

� Umuhimu wa mwenzi au familia kupewa taarifa sahihi zinazohusu virusi vyaUKIMWI na UKIMWI

� Taratibu zinazotumika kumrufaa mteja kwa wanaowatunza watu wanaoishi navirusi vya UKIMWI au UKIMWI katika jamii anayotoka

� Rufaa na uhusiano wa mashirika yanayotoa huduma mbalimbali

Ni muhimu kutambua wadau katika jamii wanaoshughulika na masuala yaUKIMWI, kama kupima, unasihi na misaada mbalimbali kwa watu wanaoishi na

virusi vya UKIMWI/UKIMWI

74

Page 84: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

75

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Unasihi kuhusu lisheKati ya matatizo makuu yanayomkabili mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI auUKIMWI ni yale yanayohusu lishe, ambayo huathiri kwa kiasi kikubwa afya yake.Mtu anayeishi na VVU/UKIMWI huhitaji elimu na unasihi kuhusu lishe. Ni vizurimnasihi afanye tathmini ya lishe ya mteja hasa kupima uzito na urefu.

Katika kutoa unasihi wa lishe taratibu za kawaida za unasihi hufuatwa. Ina maanamnasihi anatumia stadi zake za unasihi kumfanya mteja wake aweze kufanya maamuzisahihi kuhusu chakula na lishe kulingana na hali iliyopo kiafya, kiuchumi, n.k. ili awezekuboresha hali yake ya afya na lishe.

Ili kufanikisha unasihi wa lishe, ni muhimu kuchukua historia ya mteja inayohusuchakula na ulaji wake. Hii ni pamoja na vyakula anavyopenda, vyakula asivyopenda,miiko, mtu anayepika chakula chake, hula mara ngapi kwa siku, namna anavyopatachakula, nani ananunua (kama kinanunuliwa), njia anazotumia kuhifadhi chakula,nishati anayotumia kupikia, n.k. Chunguza kama ana vyakula maalumu alivyoshauriwakula au kutokula na kwa nini, dawa anazotumia, n.k. Huu ni msingi mzuri kwa ajili yakutoa unasihi.

Maelezo hayo yanaweza kupatikana vizuri katika unasihi wa mtu mmoja, familia auwatu wanaokula pamoja.

Kwa makundi makubwa zaidi (watu ambao hawali pamoja), ni vizuri zaidi kutoa elimuya lishe. Hii itawawezesha kupata taarifa sahihi zinazohusu chakula na lishe lakini siounasihi kwani historia ya kila mmoja inaweza kutofautiana na mwingine.

• Ikumbukwe kwamba nia sio kubadili sana namna mtu anavyokula balini kuboresha vyakula ambavyo anakula na kuhimiza utaratibu mzuriwa kula

• Pale inapowezekana mteja ajizoeshe kubadili vyakula ambavyo havinavirutubishi vingi au visivyo muhimu na kutumia vile ambavyo ni bora aumuhimu zaidi. Kwa mfano:- Mteja anayetumia soda kwa wingi au pombe, anaweza kujizoesha

polepole kupunguza soda au pombe, na badala yake kutumia vinywajivingine kama juisi ya matunda halisi au maziwa.

- Mteja anayetumia chai au kahawa kwa wingi, ajizoeshe kupunguzataratibu. Atumie zaidi vinywaji vinavyotokana na viungo kamatangawizi, vitunguu saumu, nanaa, mdalasini, mchaichai, n.k.

• Kumbuka katika jamii zetu, matumizi ya mboga-mboga na matundayamesahaulika sana. Inabidi kusisitiza sana umuhimu wa kuwa namboga-mboga na matunda katika mlo.

Page 85: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Tofauti kati ya elimu ya lishe na unasihi wa lishe

Elimu ya lishe:

• Huweza kuwafikia watu wengi kwa mara moja mfano kutoa elimu katika kikundi,kutumia radio, televisheni, vitabu, vipeperushi, magazeti, n.k.

• Gharama ya elimu ya lishe ni ndogo kwani huchukua muda mfupi, wahudumuwachache , n.k.

• Sio rahisi kukidhi kikamilifu mahitaji ya mtu binafsi.• Huweza kutoa taarifa nyingi katika muda mfupi.

Unasihi wa lishe:

• Unaweza kumuelewa zaidi mteja na kumpa ushauri unaofaa kufuatana na haliiliyopo.

• Huhitaji muda mwingi.• Huhitaji sehemu ya faragha.• Huweza kufanyika kwa watu wachache na gharama ni kubwa zaidi kwani huhitaji

muda, wahudumu na sehemu ya kutolea huduma.• Huduma hii ni bora zaidi kwani hulenga hali halisi ya mteja mmoja mmoja.

76

Page 86: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

TANGAMANO NA UTANDAISHAJIKumekuwa na mawazo kwamba, kwa kuwa virusi vya UKIMWI au

UKIMWI vinahusu ugonjwa, tatizo hilo ni la kiafya na kwa hiyo linahusu sekta ya afya.

Mawazo hayo yameendelea kubadilika kwa kuwa UKIMWI umeonekana kuathirisekta zote. Hivyo watu wote wanatakiwa kushirikiana na kuchangia katika juhudi zakuzuia madhara yanayotokana na virusi vya UKIMWI au UKIMWI. Hii itawezekanaiwapo kuna tangamano (collaboration) na utandaishaji (networking).

Tangamano na utandaishaji ni utaratibu unaokuza ubadilishanaji wa taarifa, uzoefu,kujenga umoja na kuwezesha kuwepo kwa programu zinazosaidiana na kuimarishana.Tangamano inaweza kuundwa na kikundi cha watu au asasi ambazo kwa hiari yaohubadilishana taarifa au hufanya shughuli zao pamoja kwa njia ambayo humwongezeauwezo kila mmoja wao.

Umuhimu wa tangamano na utandaishajiTangamano na utandaishaji ni muhimu sana kwa watoa huduma hususanwanaowahudumia watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI au UKIMWI. Hakuna mtuyeyote binafsi, taasisi au programu ambayo inajitosheleza katika huduma inazotoa.Ubia, tangamano na utandaishaji vitaimarisha taasisi na programu kwa kubadilishanataarifa, uzoefu, rufaa, ukusanyaji taarifa na shughuli nyingine. Nyenzo na rasilimalihuweza kuchangiwa, hivyo kusaidia taasisi au programu kutumia rasilimali kidogoiliyopo kwa ufanisi zaidi.

Watoa huduma wanatakiwa kufahamu sekta nyingine, makundi mengine, taasisi nawatu binafsi wanaotoa huduma zinazohusiana au kuendeleza zile ambazo hutolewa nataasisi moja.

Mifano ya matumizi ya tangamano, ubia na utandaishaji:

• Kuwafahamu watu wanaotoa huduma zinazofanana na zako, na kuwasaidia watejawako kutumia huduma zilizo karibu nao zaidi.

• Kutoa rufaa kwa huduma mbaimbali. Huduma hizo ni kama vile huduma zakisheria, msaada kwa yatima, huduma za kiroho, shughuli za uzalishaji mali, unasihikatika jamii, huduma za chakula na lishe, n.k.

• Kuchangia nyenzo; kwa mfano kutumia vitabu na vifaa vingine vya kujifunzia nakufundishia vilivyoandaliwa na mashirika au taasisi nyingine.

Tangamano na utandaishaji katika huduma kwa watu wanaoishi navirusi vya UKIMWI au wenye UKIMWITangamano na utandaishaji kati ya watu na asasi zinazowahudumia watu wanaoishi navirusi vya UKIMWI ni muhimu sana. Huduma kamili kwa watu hao zinatakiwakupatikana katika sehemu nyingi zilizo kwenye ngazi za hospitali hadi majumbani.

77

12

12

.

TA

NG

AM

AN

O N

A U

TA

ND

AIS

HA

JI

Page 87: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Katika hali hiyo ya mwendelezo wa matunzo, tangamano na utandaishaji wakuaminika na rufaa ni muhimu. Rufaa inaweza kutoka au kwenda kwenye vituo vyaunasihi na upimaji, hospitali au kliniki, huduma zilizo kwenye jamii na programu zautunzaji wa wagonjwa majumbani.

Ni vyema kuwafahamu wadau muhimu katika jamii ili kuunda tangamano nautandaishaji. Watendaji na watoa huduma mbalimbali katika jamii ambao wanawezakuunda tangamano na utandaishaji ni pamoja na:

• Wanafamilia na wanakaya

• Wanajamii

• Zahanati ya kijiji

• Kituo cha afya

• Uongozi wa wilaya

• Mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali

• Mashirika ya kijamii

• Waganga na wakunga wa jadi

• Viongozi wa kidini na kijadi

• Watu wengine ambao jamii inawaheshimu au imewachagua

Vidokezo muhimu vya kujenga tangamano na utandaishajiWatoa huduma na wadau wengine wanatakiwa:

• Kuwasiliana, ikiwa ni pamoja na kukutana mara kwa mara ili kujadili mafanikio namatatizo wanayoyapata katika utekelezaji wa shughuli zao.

• Kubadilishana mawazo kuhusu uzoefu na mikakati wanayotumia kutatua matatizowanayokumbana nayo ili kuboresha huduma.

• Kuelewa vizuri nani anafanya nini na yuko wapi.

KumbukaMawasiliano hudumisha uhusiano

78

Page 88: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

BIBLIOGRAFIA1. Bijlsma, M., Nutritional Care and Support for People with HIV: Review of

literature, initiatives and educational materials in Sub-sahara Africa, andrecommendations for developing national programmes. Report to FAO, July2000.

2. Bijlsma, M., Living Positively: Nutrition Guide for People with HIV/AIDS,Muntare City Health Department, Zimbabwe, Second Edition, 1997.

3. Burgess, A. and others, Community Nutrition for Eastern Africa, AfricanMedical and Research Foundation, Nairobi, Kenya; 1994.

4. COUNSENUTH, Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vyaUKIMWI: “Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara”: COUNSENUTHinformation series No. 3, Toleo la Pili, January, 2004.

5. COUNSENUTH, “Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI”:COUNSENUTH information series No. 2, Toleo la Pili, January, 2004.

6. COUNSENUTH, Ulishaji wa Mtoto Aliyezaliwa na Mama Mwenye Virusivya UKIMWI: Vidokezo Muhimu kwa Washauri Nasaha, COUNSENUTHinformation series No. 1, Toleo la Pili, January, 2004.

7. COUNSENUTH, Matumizi ya Viungo vya Vyakula katika Kuboresha Lishena Afya, COUNSENUTH information series No. 6, Toleo la Kwanza,March, 2004.

8. COUNSENUTH, Unyonyeshaji Bora wa Maziwa ya Mama: VidokezoMuhimu kwa Jamii, COUNSENUTH Information Series No. 5, June, 2003.

9. Davidson S., Passmore R., Brock J.F., Truswell A. S,. Human Nutrition andDietetics; Seventh Edition. Wilture Enterprises, (International) Ltd. 1979.

10. FAO/WHO, Living well with HIV/AIDS: A manual on Nutritional Care andSupport for People Living with HIV/AIDS, Rome, 2002.

11. Food and Nutrition Technical Assistance (FANTA), Food and NutritionImplications of Antiretroviral Therapy in Resource Limited Settings. Academyfor Educational Development, Washington DC, June 2003.

12. Food and Nutrition Technical Assistance (FANTA), HIV/AIDS: A Guide forNutrition, Care and Support. Academy for Educational Development,Washington DC, 2001.

13. Friis, H., “The Possible Effect of Micronutrients in HIV Infection. SCN News,United Nations Systems Forum on Nutrition, Number 17, December 1998.

14. IBFAN Africa, Infant Feeding Options in HIV/AIDS: Information for HealthWorkers. Mbabane, Swaziland, may 2002.

15. Ministry of Health, The United Republic of Tanzania; A National Guide onNutritional Care and Support for People Living With HIV/AIDS, TFNC

79

Page 89: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

(DRAFT), May, 2003.

16. NFTRC, Healthy Eating, Shopping for Food and Food Safety Guidelines.

17. Ndungi, H.K., Food and Nutrition for Schools and Colleges, Nairobi, 1992.

18. RCQHC/FANTA/LINKAGES, Nutrition and HIV/AIDS: A Training Manual,October 2003.

19. UNICEF/UNAIDS/WHO/UNFPA, HIV and Infant Feeding: A Guide forHealth Care Mangers and Supervisors, September 2003.

20. UNICEF/UNAIDS/WHO/UNFPA, HIV and Infant Feeding: Guidelines forDecision Makers, September 2003.

21. The Network of African People Living in HIV/AIDS (NAP+). Food for PeopleLiving with HIV/AIDS, July 1996.

22. Tull, A., Food and Nutrition, GCSE Edition, Oxford University Press, 1991.

23. The Population, Health and Nutrition Information, Anaemia Prevention andControl: What works, 2003.

24. WHO/UNICEF/BASICS, Nutrition Essentials: A Guide for Health Managers,1999.

80

Page 90: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

81

FARAHASAUsharabu - Absorption

Sibiko - Contamination

Kuchachusha vyakula - Fermentation

Kutokosa - Steaming

Tangamano - Collaboration

Utandaishaji - Networking

Unasihi (Ushauri nasaha) - Counselling

Mnasihi - Counsellor

Maziwa yaliyochevushwa - Evaporated milk

Mzio - Allergy

Lehemu - Cholestrol

Mnyanyapao - Stigma

Kipindi ficho - Window Period

Kipindi tuli - Honey moon Period

Kipindi pevushi - Incubation Period

Page 91: LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA …counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe Kwa Watu...utayarishaji, kutoa ushauri na kupitia kitabu hiki. Shukrani zetu pia kwa Chuo cha

Kuhusu COUNSENUTH:Kituo cha ushauri nasaha, lishe na afya

(COUNSENUTH) ni asasi isiyo ya kiserikali yenyemakao yake Dar es Salaam.

Dhumuni la COUNSENUTH ni kuboresha Afya naLishe ya Watanzania kwa kutoa huduma mbalimbali

za lishe na unasihi kwa kushirikiana na asasi navikundi mbalimbali vilivyoko katika jamii.

ISBN 9987 - 8936 - 9 - 4

Designed & printed by: Desktop Productions LimitedP.O. Box 20936, Dar es Salaam, Tanzania

Contact: 0748 387899, Email: [email protected], 2004