C O U N S E N U T H I n f o r mation series No. 3 Toleo la ...counsenuth-tz.org/sites/default/files/Lishe na Ulaji Bora kwa Watu... · kienyeji na la kuku wa kisasa? ... za ufugaji

Embed Size (px)

Citation preview

  • C O U N S E N U T H

    I n f o rmation series No. 3Toleo la Pili, January, 2004

  • 2

    UTANGULIZIWatu wanaoishi na virusi vya UKIMWIwamekuwa wakitafuta taarifa zaidi kuhusuulaji wa vyakula mbalimbali siku hadi siku.Baadhi ya taarifa wanazozipata, zimeonyeshakuwa na utata, hivyo kuwafanya watu haokuwa na maswali mengi yanayohusu ulaji wavyakula mbalimbali.

    Ni dhahiri kwamba, lishe bora ni moja yavipengele muhimu katika kuboresha afya yamtu anayeishi na virusi vya U K I M W I. Kituocha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya(COUNSENUTH) kiliandaa kijitabu cha Lishena Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Vi r u s ivya UKIMWI: Maswali yanayoulizwa marakwa mara, Information series No. 3, ili kujibubaadhi ya maswali yaulizwayo mara kwam a r a .

    Kutokana na kuongezeka kwa maswali na ariya watu hao ya kutaka kujua zaidi juu ya lishena ulaji unaofaa, COUNSENUTH imetayarishatoleo la pili la kijitabu kilichopita. Toleo hilil i m e b o resha baadhi ya majibu ya maswali yatoleo lililopita na kuongeza maswaliyaliyojitokeza baada ya toleo hilo na majibuy a k e .

    Ni matarajio yetu kwamba kijitabu hikikitasaidia kuondoa utata kwa wengi na hasawatu wanaoishi na virusi vya UKIMWI.

    MASWALI NA MAJIBU

    SWALI:Je, nyama nyekundu ina madhara gani kwamtu anayeishi na virusi vya UKIMWI?

    JIBU:Kuna nyama za aina mbili, nazo ni nyama

  • 3

    nyeupe na nyama nyekundu. Nyama nyeupeni pamoja na samaki, kuku, ndege wa ainazote, bata, wadudu; na nyama nyekundu nipamoja na ngombe, mbuzi, kondoo,nguruwe na wanyama wa porini. Nyama inavirutubishi vingi muhimu kwa afya yabinadamu kama protini, vitamini na madini.Madini ya chuma yanayopatikana kwenyenyama ni rahisi sana kusharabiwa(kufyonzwa) mwilini na ni muhimu kwakuongeza wekundu wa damu.

    Uwezo wa miili ya watu wanaoishi na virusivya UKIMWI kuyeyusha chakula nakusharabu (kufyonza) virutubishi hupungua.Utumiaji wa nyama nyekundu kwa wingiunaweza kuwaletea matatizo hasa katikauyeyushwaji tumboni kwani nyama nyekundusi rahisi kuyeyushwa ukilinganisha na nyamanyeupe.

    Hata hivyo katika nchi yetu watu walio wengiwanatumia nyama kwa kiasi kidogo sana namara chache. Si vyema watu hawa waachekabisa nyama nyekundu. Jambo la muhimu nikutumia njia mbalimbali ili kuifanya nyama hiiiyeyushwe kwa urahisi tumboni. Namna ya kusaidia uyeyushwaji ni pamojan a : - Kutafuna vizuri au kutumia nyama ya

    kusaga (kwa wanaoipata). Kupika nyama na viungo vinavyosaidia

    kulainisha kama vile papai bichi, limao,vitunguu saumu n.k.

    Kula nyama pamoja na papai

    Inashauriwa kwa anayepata nyama nyekundukwa wingi, kupunguza kiasi cha nyama hiyona kuongeza kiasi cha nyama nyeupe. Na kwayule asiyepata nyama nyeupe, apatapo nyamanyekundu asiache kutumia kwani inaumuhimu mwilini mwake.

  • 4

    SWALI:Je, ni nini tofauti kati ya yai la kuku wakienyeji na la kuku wa kisasa?

    JIBU:Kilishe mayai yote ni sawa. Vi r u t u b i s h ivinavyopatikana kwenye yai la kuku wakienyeji kama protini, vitamini A, madini yachuma na virutubishi vya aina nyingine,ndivyo hivyo vinavyopatikana pia kwenye yai

    la kuku wa kisasa. Tatizo linawezakutokea pale ambapo wafugaji wakuku wa kisasa hawafuati taratibuza ufugaji na pengine hawawapikuku vyakula muhimuwanavyohitaji, hivyo wakati

    mwingine kiini cha yai la kuku wakisasa huonekana kupungua rangi ya

    njano kuliko kiini cha yai la kuku wa kienyeji.Mtu anashauriwa kula yai bila kujali ni lakuku gani, kwa kutegemea ni yai lipilinapatikana kwa urahisi.

    SWALI:Je, ulaji wa yai bichi una madhara gani?

    JIBU:Yai bichi linaweza kuwa na vijidudu viitwavyokwa kitaalamu SALMONELLA vinavyowezakusababisha tumbo kuuma, kichefuchefu napia kuharisha. Vijidudu ya Salmonellavinaweza kusababisha madhara makubwakwa watoto, wazee na wale wenye hali dhaifuya kimwili kama wagonjwa wa UKIMWI. Pia

    Un a weza pia kulainisha vipande vya nyamambichi kwa kuigonga-gonga, mpaka ilainike

    kabla ya kupikwa.

  • 5

    yai bichi lililowazi linaweza kuwa zalio zuri lavimelea vya maradhi mbalimbali. Inashauriwakupika yai mpaka liive kabisa, na kuhakikishakwamba hakuna ute unaoteleza. Kama ni yaila kuchemsha, lichemshwe kwa dakika kumizaidi baada ya maji kuchemka. Pia ni muhimukuhakikisha kwamba vyombo vilivyotumikak u k o rogea yai bichi vinaoshwa kwa maji nasabuni kabla ya kuvitumia tena kwa matumizimengine ili kuepuka maradhi.

    SWALI:Je, unywaji wa soda una madhara gani?

    JIBU:Soda ni kiburudisho ambacho si muhimu sanakwa afya. Aina nyingi za soda zina kafeiniambayo huzuia usharabu (ufyonzwaji) wamadini ya chuma mwilini hasa yatokanayo navyakula vya mimea

    Hata hivyo soda zinaweza kutumika kwa kiasikidogo kama kiburudisho, ila tunapotakaubora zaidi wa afya zetu inafaa kupunguzamatumizi ya soda na badala yake kutumiavinywaji vyenye virutubishi muhimu kamavile maji ya matunda, maziwa, madafu auasusa kama vile matunda, karanga na ainambalimbali za mboga mfano karoti. Hiiinasaidia pia kutumia fedha kidogo tuliyonayo kwa vyakula muhimu, hasa ukizingatiabadala ya soda moja unaweza kupata mayaimatatu au nusu lita hadi lita moja ya maziwa.

    Ikumbukwe kuwa, mtu anayeishi na virusivya UKIMWI amepungukiwa na kinga yamwili, kwa hiyo ni muhimu kujiepusha na

    chochote kinachoweza kuleta hatari yakuambukizwa magonjwa

  • 6

    SWALI:Je, matumizi ya chai na kahawa yana madharag a n i ?

    JIBU: Kwa kawaida chai na kahawa ni viburidishoambavyo huchangamsha mwili, kutokana nakuwepo kafeini ndani ya vinywaji hivyo,lakini sio muhimu mwilini. Si vizuri kutumiavinywaji hivi pamoja na chakula, kwanikafeini huzuia usharabu (ufyonzwaji) wamadini ya chuma mwilini, yatokanayo navyakula vya mimea. Kwa kuwa mtu anayeishi

    na virusi vya UKIMWI anahitaji madinihayo, ni bora kupunguza sana

    matumizi ya chai na kahawahasa wakati wa chakula.Inapobidi kutumia vinywajihivi, vitumike kwa kiasikidogo, na kiasi cha majani

    au kahawa inayowekwa ndaniya kinywaji iwe kidogo; na

    vitumike angalau saa moja kabla yachakula au saa moja baada ya kula.

    Ni vizuri kujaribu vinywaji vya aina nyinginebadala ya chai, kwa mfano vilevinavyotengenezwa kutokana na viungo,majani ya mchaichai, majani ya mlimao, choya( rozela), nanaa, tangawizi na vinginevyo.

    SWALI:Je, utumiaji wa virutubishi vya nyongeza(Dietary/Nutrient Supplements)una umuhimu gani kwa mtuanayeishi na virusi vyaU K I M W I ?

    JIBU:Kinga ya mwili inapopungua,mahitaji ya vitamini, madini na virutubishi

  • 7

    vingine huongezeka. Pia matumizi ya baadhiya dawa huongeza mahitaji ya virutubishi.Kwa kiasi kikubwa mahitaji hayo yanawezakukidhiwa kwa ulaji bora ambao unazingatiamatunda, mboga-mboga na chakulamchanganyiko na cha nyongeza. Badoupungufu mwilini waweza kutokea kwasababu ya ongezo la mahitaji ya kilishe nakuathirika kwa uyeyushwaji wa chakula naufyonzwaji wa virutubishi. Inashauriwakwanza kutumia mbinu za kubore s h auyeyushwaji wa chakula na ufyonzwaji wavirutubishi, kama vile kupika mboga kwamuda mfupi, kupika kwa mvuke, kutumiambegu zilizooteshwa na vyakulavilivyochachushwa kwa mfano mtindi natogwa; ndipo ufikirie kutumia virutubishi vyan y o n g e z a .

    Nyongeza ya vitamini, madini au virutubishivingine ni jambo zuri kwani huwezakuusaidia mwili iwapo vitatumika ipasavyo.Ni muhimu ikumbukwe kwamba virutubishihivi sio badala ya chakula bali ni nyongeza,baada ya mlo uliokamilika; ndio maanavikaitwa supplements yaani nyongeza.Vinapohitajika, ni vyema kupata ushauri wamtaalamu wa Afya kuhusu aina za virutubishivya nyongeza ambavyo ni muhimu, na wapivinapatikana kwa bei nafuu. Virutubishi vyanyongeza visichukuliwe kama dawa yaU K I M W I .

    Hebu tujiulize; je, ni busara kununuavidonge vya vitunguu saumu kwa bei kubwa

    TUTUMIE VIZURI FEDHAKIDOGO TULIZO NAZO KWA AJILI

    YA CHAKULA MCHANGANYIKONA CHA KUTOSHA KWANZA,

    NDIPO TUONGEZE VIRUTUBISHIVYA NYONGEZA

  • 8

    ambapo tunapata vitunguu saumu halisi kwabei ndogo sana? Ni bora kununua kwanzachakula cha kutosha na vitunguu saumuhalisi, ndipo tukiwa na ziada tununue vituvya nyongeza.

    Je, ni busara kununua supplementszilizotengenezwa kutokana na asali kwa beikubwa sana iwapo tunaweza kupata asalihalisi kwa bei nafuu?. Ni bora kununuakwanza chakula cha kutosha, ndipo tukiwana ziada tununue virutubishi vya nyongeza.

    SWALI:Mara nyingi tumeshauriwa kutumia juisi. Je,juisi bora zaidi ni ipi?

    JIBU:Juisi ni maji ya matunda halisi au aina fulaniza mboga. Hiki ni kinywaji kizuri kwa mtuanayeishi na virusi vya UKIMWI. Juisi bora ni

    ile iliyotengenezwa kwa kutumia matundahalisi au mboga kama karo t i ,

    matango na mengineyo kwanihuwa na virutubishi muhimu,hasa vitamini na madini. Juisi

    ambazo ni rahisi sanakutengeneza ni pamoja na juisi ya

    machungwa, papai, ukwaju, ubuyu,karakara (pesheni), nanasi, embe, limao,nyanya na mengineyo. Baadhi ya matundayanaweza kuhitaji nyenzo zaidi kutengenezajuisi. Juisi itengenezwe kwa hali ya usafi na nimuhimu kutumia maji safi yaliyochemshwa,katika kutengeneza juisi.

    Sio vizuri kudhani kwamba aina moja ya juisindio bora zaidi, ni muhimu kubadilibadili paleinapowezekana au hata kuchanganya, kwanihii huongeza ubora wa virutubishi.Tatizo lililojitokeza sana ni watu wengikutoelewa tofauti kati ya maji ya matundahalisi (juisi) na vinywaji vinavyotengenezwa

  • 9

    kwa kutumia maji, rangi, sukari na ladhabandia ya matunda. Vinywaji hivi ambavyo nivingi, sio maji ya matunda halisi. Ikibidikununua juisi halisi dukani, soma maelezo(lebo) vizuri kabla ya kununua ili kuepukakununua juisi bandia. Zingatia tarehe yamwisho ya matumizi (expiry date).

    Tunaweza kupata maji ya matunda halisi kwagharama ndogo iwapo tutanunua matundayenyewe, kuliko kununua vinywaji hivyovyenye maji, rangi, sukari na ladha.

    SWALI:Je, kunywa maji mengi kunapunguza uzito?

    JIBU:Asilimia sabini ya mwili wa binadamu ni maji.Maji ni muhimu kwa uhai. Ni muhimukunywa maji ya kutosha yaliyo safi na salama,angalau lita moja na nusu (glasi nane) kwas i k u .Si kweli kwamba kunywa maji mengihupunguza uzito. Ila kunywa maji mengikabla tu au wakati wa kula hujaza tumbo nahivyo kufanya mtu ale chakula kidogoambacho hakitakidhi mahitaji ya mwili. Hiihuweza kusababisha kupungua uzito.Kunywa maji mengi kupita kiasi piahuahirisha njaa na hivyo huweza kupunguzahamu ya kula, hivyo mwili kutumia akiba yavirutubishi na pengine husababisha kupunguauzito. Kwa mgonjwa asiyeweza kula chakulakingi kwa mara moja, inashauriwa kunywamaji baada ya kula au kati ya mlo mmoja nam w i n g i n e .

    Inashauriwa kutengeneza juisi kutokanana matunda halisi

  • 10

    Ikumbukwe kuwa kunywa maji angalau litamoja na nusu (glasi nane) kwa siku ndiyo kiasicha kawaida kinachohitajika na hayo sio maji

    mengi

    SWALI:Mara nyingi tumeshauriwa kutumia vitunguusaumu. Je, tutumie vitunguu saumu kwa kiasig a n i ?

    JIBU:Vitunguu saumu husaidiak u b o resha kinga ya mwili na piahusaidia kupigana na vijidudu vyamagonjwa hasa yale ya tumbo(njia ya chakula) na yale yamapafu, na fangasi za kinywani.Vitunguu saumu pia kama ilivyoviungo vingi, hubore s h auyeyushwaji wa chakula tumboni.Vitunguu hivi vyaweza kutumika kwakuongeza kwenye chakula wakati wa kupika,kwenye vinywaji, saladi au kutafunwa kwak i a s i .

    Tatizo huweza kutokea iwapo vitatumika kwawingi mno na hivyo kusababishakichefuchefu au kutapika. Ikumbukwekwamba vitunguu hivi inabidi vitumike kwakiasi. Inashauriwa kutumia vitembevisivyozidi sita kwa siku.

    SWALI:Je, ni maziwa yapi bora zaidi, mtindi (maziwaya mgando) au maziwa mabichi (fre s h i ) ?

    JIBU:Maziwa aina zote yana virutubishi muhimuhasa protini, madini na vitamini. Mtu anawezakutumia aina yoyote, kutegemea matumizi

  • 11

    yake. Hata hivyo, mtindi huyeyushwa kwaurahisi zaidi tumboni. Pia husaidiauyeyushwaji na usharabu wa vyakula vingine.Kwa watu ambao wakinywa maziwa mabichiyanawapa matatizo kama kujaa tumbo,kuharisha au kuumwa tumbo, wanawezakujaribu mtindi. Vile vile kwa wale wenyefangasi za kinywani wanashauriwa kujaribukutumia mtindi mara kwa mara, kwani huzuiafangasi kuendelea kukua.

    SWALI:Je, maji ya mchele hutengenezwa namna gani?

    JIBU:Watu wengi wamekuwa wakishauriwakutumia maji ya mchele pale wanapoharisha.Imeonekana kuwa utengenezaji wa maji hayani tatizo kwa wengi. Na linapotumika jinamaji ya mchele, wengi hudhani ni yale majiyanayooshea mchele. Hii sio sahihi, majiyanayoshauriwa ni yale yanayochemshiamchele, pengine tungeweza kuyaita supu yamchele.

    JINSI YA KUTENGENEZA MAJI YAMCHELE Mahitaji:- mchele, maji na chumvi

    k i d o g o .- Weka kikombe kimoja cha mchele

    kwenye vikombe vinne hadi sita vyamaji yanayochemka;

    - Funika vizuri sufuria au chungu napika kwa moto mdogo kwa saa moja;

    - Ongeza chumvi kidogo na hapo majiau supu ya mchele ni tayari;

    - Unaweza kuongeza vitu vinginekama; karoti iliyokatwakatwa,mdalasini, vitunguu saumu kidogon.k. kama unapenda.

    Chanzo: Tafsiri kutoka: Bijlsma, M., 1997

  • 12

    Pia unaweza kutengeneza maji ya mchelekwa kupika uji mwepesi kwa kutumia ungawa mchele.

    SWALI:Je, maji yaliyochachushwa (sour water)h u t e n g e n e z w a j e ?

    JIBU:Maji yaliyochachushwa hayana tofauti sana natogwa, ila togwa huwa na virutubishi vingizaidi kwani hutengenezwa kwa kutumiaunga. Maji yaliyochachushwa yanasaidiakatika uyeyushwaji wa chakula tumboni.Hapa chini kuna mifano ya kutengeneza majiyaliyochachushwa .

    MAJI YA UCHACHU YA NAFAKA Tumia nafaka yoyote uliyonayo kama,

    mtama, ulezi, au mahindi n.k.- Osha nafaka na iloweke kwenye maji;

    kikombe 1 cha nafaka na vikombe 3vya maji yaliyochemshwa na kupoa;

    - Funika vizuri chombo chako chaplastiki na acha kwa siku 2 hadi 3;

    - Maji ya uchachu ni tayari paleyanapoanza kuonyesha povu;

    - Chuja maji na yaweke mahali pab a r i d i ;

    - Unaweza kutengeneza maji zaidi kwakutumia nafaka hiyo hiyo; kwakuongeza maji yaliyochemshwa nakupoa na baada ya siku mojayatakuwa tayari.

    Chanzo: Modified from: Bijlsma, M., 1997.

  • 13

    Chanzo: Tafsiri kutoka: Bijlsma, M., 1997.

    SWALI:Je, mboga-mboga na matunda yenye ranginyekundu au zambarau huongeza damuz a i d i ?

    JIBU:Baadhi ya mboga-mboga na matunda yenyerangi nyekundu, zambarau na hata kijanikibichi na njano huwa na virutubishi kwawingi zaidi hasa madini na vitamini. Baadhi yavirutubishi hivi huchangia sana kuongezadamu. Mfano mmea wa choya (rosela) ambaouna rangi nyekundu, umeonekana kuwa namadini chuma kwa wingi ambayo huchangiakuongeza damu. Lakini haimaanishi kuwa,kila chakula au kinywaji chenye rangi hizohuongeza damu.Hata hivyo kuchanganya mboga na matundaya rangi mbalimbali huongeza ubora wa

    MAJI YA UCHACHU YA KABICHI Tumia kabichi mbichi iliyokatwakatwa

    vipande vidogovidogo.- Loweka kikombe kimoja cha kabichi

    iliyokatwakatwa kwenye vikombe 3 vyamaji yaliyochemshwa na kupoa kwenyechombo cha plastiki chenye mfuniko;

    - Funika vizuri chombo chako na achakwa siku mbili;

    - Chuja maji na yaweke mahali penyeu b a r i d i ;

    - Unaweza kutengeneza maji zaidi kwakutumia kabichi hiyo hiyo kwakuongeza maji yaliyochemshwa nakupoa kwenye kabichi uliyoitoa maji;ila si zaidi ya mara 2;

    - Acha kwa siku moja;- Maji ni tayari na weka mahali penye

    u b a r i d i ;- Unaweza kuichemsha kabichi

    iliyotumika na chumvi na kula nachakula chochote unachopenda.

  • 14

    chakula unachokula. Hivyo ni vizuri kujaribukuchanganya rangi kadiri inavyowezekana.Baadhi ya mboga-mboga au matundavinaweza kutumika kutengeneza supu auv i n y w a j i .

    Watu wengi hudhani kwamba vinywaji vyarangi ya zambarau au nyekundu vyenye ladhabandia ya matunda mfano black curre n t huongeza damu. Hii si kweli; vinywaji hivimara nyingi hutengenezwa na maji, sukari,rangi na ladha bandia.

    SWALI:Je, pombe ina madhara kwa mtu anayeishi navirusi vya UKIMWI?

    JIBU:Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWIanashauriwa kupunguza sana matumizi yapombe na ikiwezekana kuacha kabisa.

    Pombe (kilevi) haina virutubishi vingimuhimu, japokuwa ina nishati. Hata hivyomatumizi ya nishati hii mwilini hayajaelewekavizuri. Hivyo ni bora zaidi kupata nishatikutoka katika vyakula vingine.

    Matumizi ya pombe yameonyesha madharambalimbali katika mwili kwa kuingilia ulajiwa chakula, uyeyushwaji wa chakula naufyonzwaji wa virutubishi mwilini pamoja nauwekaji akiba wa virutubishi. Pombehusemekana kuzuia upatikanaji wavimengenyo hai (enzymes), vinavyosaidiauyeyushaji wa chakula na ufyonzwaji wavirutubushi mwilini. Pia imeonekana kuharibuseli za tumbo na utumbo, ambazo ni muhimukwa usharabu (ufyonzwaji) wa virutubishi.Hata kama chakula kikiyeyushwa navirutubishi kufyonzwa; pombe huweza

  • 15

    kufanya virutubishi hivyo visitumike vizurimwilini, kwa kuingilia usafirishwaji wake nauwekaji akiba. Kwa mfano; matumizi yapombe hupunguza akiba ya vitamini Akwenye ini. Pia, pombe hupunguza akiba yavitamini nyingine kama C, D, E, K na B, nazaidi ya hayo pombe hupunguza maji mwilini.

    Vile vile pombe huchangia kuwa naupungufu wa wekundu wa damu, kwanihuingilia ufyonzwaji na matumizi ya vitaminina madini muhimu katika utengenezaji wazindiko (antibodies) kwa kiasi kikubwa.Pia imethibishwa kwamba pombe inaongezahatari ya kupata magonjwa sugu kamasaratani hasa za kinywa, koromeo, zoro t o(larynx) na ini. Huongeza pia hatari ya kupatavidonda vya tumbo na magonjwa ya moyo.

    Pombe (kilevi) huathiri uwezo wa kufikiri nakufanya maamuzi, jinsi ya kuonyesha hisia,utulivu na mawasiliano ya viungo vya mwilina hivyo huwa na athari kwa afya na maishakwa jumla. Pombe pia huweza kuathirinamna ya kufanya maamuzi kuhusu ngono nakufanya ngono salama na hivyo huwezakuchangia katika kueneza maambukizi yaU K I M W I .

    SWALI:Je, uyoga una faida gani?

    JIBU:Uyoga una protini kwa wingi pia madini navitamini ambazo husaidia kuboresha afya.Ubora wake umekaribia ule wa vyakula vyamikunde na maziwa. Uyoga piauna vitamini na madini muhimukatika kuboresha kinga ya mwili.Uyoga unaweza kutumika kamasehemu ya chakula kwa mtu

  • 16

    anayeishi na virusi vya UKIMWI. Lakiniikumbukwe kwamba, hakuna chakula kimojapekee kinachotosheleza mahitaji yote yamwili kilishe, kwa hiyo bado ni muhimu kulachakula cha mchanganyiko na cha kutosha.

    Ikumbukwe kwamba sio kila aina ya uyoga inaliwa

    SWALI:Je, asali ina faida gani?

    JIBU:Asali imeonekana kuwa na aina ya kemikalizinazoitwa Antioxidants ambazo husaidiamwili usiharibiwe na kemikali nyinginembaya. Vilevile imeonekana kuua baadhi yabakteria mwilini hivyo imeonyesha kuwa nauwezo wa kutibu vidonda. Aidha asali inanishati kwa wingi na baadhi ya vitamini namadini. Nishati iliyopo kwenye asali, husaidiapia katika kuongeza uzito.

    SWALI:Je, ni sahihi kwa mama mwenye virusi vyaUKIMWI kunyonyesha?

    JIBU:Kunyonyesha maziwa ya mama ni njiamojawapo ambayo inaweza kutumikakumlisha mtoto aliyezaliwa na mama mwenyevirusi vya UKIMWI.

    Mama mwenye virusi vya UKIMWI anawezakumnyonyesha mtoto wake, ila ni muhimukupata ushauri wa kutosha ili kufikia uamuzihuo. Ushauri atakaopata ni pamoja na namnaya kunyonyesha na kipindi ambacho anawezakumnyonyesha mtoto bila kuongeza hatari yauambukizo wa virusi vya UKIMWI kutoka

  • 17

    kwa mama kwenda kwa mtoto. Kwa hiyo nimuhimu mama mwenye virusi vya UKIMWIanapopanga kupata ujauzito, akiwa mjamzitoau akijifungua amuone mshauri nasahamwenye taarifa za kutosha kuhusu ulishaji wamtoto. Hii itamsaidia kupata maelezo sahihiyatakayomwezesha kufanya uamuzi kuhusunjia bora ya kumlisha mtoto wake.

    HITIMISHOLishe bora ni muhimu kwa binadamu wote,na umuhimu unazidi kwa watu wanaoishi navirusi vya UKIMWI. Tunaamini kwambakijitabu hiki kitawasaidia watu wanaoishi navirusi vya UKIMWI, washauri nasaha na watuwanaowatunza wagonjwa wa UKIMWIwanapokabiliwa na maswali kama haya. Wa t uwanaoishi na virusi vya UKIMWI wakumbukekula vyakula vya aina mbalimbali kila wakatikwani hakuna chakula kimoja ambacho kinavirutubishi vyote muhimu kwa lishe na afyabora. Chakula mchanganyiko na cha kutoshakitasaidia kuboresha hali ya lishe na afya yamtu anayeishi na virusi vya UKIMWI.

    VYANZO:Baadhi ya majibu yamepatikana kutokavyanzo vifuatavyo:

    1 . Bijlsma, M., Nutritional care and supportfor people with HIV: Review of literature ,initiatives and educational materials in sub-sahara Africa, and recommendations fordeveloping national programmes. Reportto FAO, July, 2000.

    2 . Bijlsma, M., Living Positively: Nutritionguide for People with HIV/AIDS, MuntareCity Health Department, Zimbabwe,Second Edition, 1997.

  • 18

    3 . COUNSENUTH, Ulaji bora kwa watuwanaoishi na virusi vya UKIMWI:COUNSENUTH information series No. 2,January, 2000.

    4 . FAO/WHO, Living well with HIV/AIDS: Amanual on nutritional care and support forpeople living with HIV/AIDS, Rome, 2002.

    5 . The Network of African people living inHIV/AIDS (NAP+). Food for people livingwith HIV/AIDS, July, 1996.

    6 . Food and Nutrition Technical Assistance( FA N TA), HIV/AIDS: A Guide for Nutrition,C a re and Support. Academy forEducational Development, Wa s h i n g t o nDC, 2001.

    7 . Friis, H. The possible effect ofm i c ronutrients in HIV infection. SCNNews, United Nations Systems Forum onNutrition, Number 17, December, 1998.

    8 . W C R F, Alcoholics drinks: Inform a t i o nseries 1, Fact sheet 06, 2001.

    9. h t t p : / / w w w . n i a a a . n i h g o v

    1 0 . http://www. alcoholisim.about.com

    SHUKRANI

    COUNSENUTH inatoa shukrani kwaWA M ATA, SHDEPHA+, MATI-Uyole, SUA nawatu binafsi ambao wameshiriki katikak u b o resha kijitabu hiki.

    Shukrani za pekee kwa RFE kwa ufadhili.

  • 19

    VIJITABU VINGINE KUHUSU LISHENA VIRUSI VYA UKIMWI

    VILIVYOTOLEWA NA COUNSENUTH:

    1 . Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Vi r u s ivya UKIMWI: Vidokezo MuhimuCOUNSENUTH information series No. 2,Toleo la Pili, January, 2004.

    2 . Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wa n a o i s h ina Virusi vya UKIMWI: Vy a k u l av i n a v y o b o resha uyeyushwaji wa chakulana ufyonzwaji wa virutubishi mwilini:COUNSENUTH information series No. 4,M a rch, 2003.

    3 . Ulishaji wa mtoto aliyezaliwa na mamamwenye virusi vya UKIMWI: Vi d o k e z omuhimu kwa washauri nasaha.COUNSENUTH information series No. 1,Toleo la Pili, January, 2004.

  • ISBN 9987 - 8936 - 6 - x

    Kwa maelezo zaidi wasiliana na:M k u r u g e n z i

    Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya

    ( C O U N S E N U T H )S . L . P. 8218, Dar es Salaam,

    Ta n z a n i aSimu: (22) 2152705 au 0744 279145

    Fax: (22) 2152705

    Kijarida hiki kimetolewa na:The Centre for Counselling, Nutrition and Health Care

    ( C O U N S E N U T H )United Nations Rd./ Kilombero Str.

    Plot No. 432, Flat No.3P.O. Box 8218, Dar es Salaam Ta n z a n i a .

    Kimefadhiliwa na:

    Rapid Funding Envelope for

    HIV/AIDS (RFE)

    Designed & printed by:

    Desktop Productions Limited

    P.O. Box 20936, Dar es Salaam, Tanzaniawww.dtptz.com [email protected]