Upload
others
View
6
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
machokodo atunza
shamba la miti
MODULI NAMBA 4
Usimamizi washamba la miti
MKULIMA WA MITI
1
ShukuraniKIJITABU HIKI KIMEANDALIWA KWA AJILI YA KUFIKISHA MAUDHUI NA TAALUMA YA NAMNA YA KUSIMAMIA SHAMBA LA MITI KWA MKULIMA MDOGO NA MKUBWA PIA. KIMEANDALIWA KWA MICHORO ZAIDI ILI KUMRAHISISHIA MSOMAJI KUJARIBU KILA KITU KWA USAHIHI ZAIDI.
MARA BAADA YA KUKAMILIKA, KIMEPITISHWA KWA WADAU MBALIMBALI NA WATAALAMU WA MISITU ILI KUTOA UZOEFU NA UTAALAMU WAO ILI KUBORESHA UTOAJI WA MAFUNZO SAHIHI YA USIMAMIZI WA SHAMBA LA MITI HAPA TANZANIA.NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA TAASISI YA UENDELEZAJI WA MISITU TANZANIA HUSUSANI KITENGO CHA huduma kwa wakulima wa miti KWA KUWEZESHA KAZI HII KUKAMILIKA.
PIA NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA WAFADHILI WA TAASISI HII AMBAO NI GATSBY FOUNDATION NA DFID KWA KUWEZESHA KUFADHILI UANDAAJI WA KIJITABU HIKI.
MWISHO, NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA BWANA Joseph makanza kwa kuchora na kusanifu kitabu hiki pia bwana HAMISI MALINGA NA GEORG STRUNDEN KWA USHAURI WA KITAALAMU KUHUSIANA NA MICHORO NA MAUDHUI yA KITABU HIKI.
UtanguliziWatafiti na wataalam wa misitu wanaamini kuwa watanzania wengi wamehamasika na wanapenda kilimo cha miti ya mbao. Moduli hii inatoa maelekezo ya namna ya kusimamia na kulihudumia shamba la miti kutokana na miche bora itokanayo na kupanda mbegu bora.
Inatoa mafunzo ya namna ya Usimamizi wa shamba la miti. Moduli hii pia inatoa mwongozo kwa wawezeshaji vijijini ili nao watoe mafunzo ya namna ya kukitumia kijitabu hiki kufikisha mafunzo kwa wakulima.
Hatua zilizoelezewa humu zinahusisha namna ya usimamizi wa shamba la Milingoti na Paina pia.
Moduli hii itatueleza kisa cha MACHOKODO aliyenufaika kwa Kilimo cha Miti baada ya kujifunza na kutumia utaalam alioupata kutokana na mafunzo kujitengenezea faida na kubadili Maisha yake.
2
1. KUpalilia shamba la miti
Kupalilia ni kuondoa
magugu shambani ili kuuacha mti
kutumia mbolea kwa ajili ya mti
kukua vizuri
zipo Aina kadhaa za kupalilia...
unaweza Kupalilia kwa visahani vyenye Kipenyo
cha sentimeta 100...
au Kupalilia kwa msitari -
Upana sentimeta 100 mche katikati
2. KUfyekea na kuliweka katika hali ya usafi
4
...pia Kupalilia
shamba lote...kwa mwaka wa kwanza palilia
shamba la miti kama mazao mengine
ya kilimo
Miti ikiwa na umri
wa miaka mitatu, miti huwa mirefu
kidogo hivyo hutakiwa kufyekewa nyasi zote ili kuweka usafi wa
shamba
3. kupogolea shamba la miti
Kupogolea ni kuondoa
matawi hasa ya chini ili mkulima aweze
kupita vizuri shambani na mti uweze kutoa gogo lililonyoka
kwa ajili ya kupasua mbao zenye
ubora.
Vifaa vya kukatia ni Msumeno maalumu
wa kupogolea na panga ambalo lina makali sana ili kutosababisha kovu
kubwa
namna ya kujua urefu wa matawi ya kuondoa
1/3 ya urefu wa mti ukiwa
na miaka 3-4 ndio iondolewe matawi. Ikiwa na miaka 7-8 matawi tena
yaondolewe na pia miti ikiwa na miaka 12-13 matawi tena yaondolewe kwa urefu wa 1/3 iondolewe na kuacha
2/3 ya urefu wa mti ukiwa na matawi
miaka 3-4
miaka 7-8
5
6
unapo ondoa matawi, Anza kukata chini kisha
malizia juu ya tawi.
Sababu ya kuanzia
chini ili kutosababisha
tawi linapoanguka kuchuna gamba na kuweka kovu kubwa
ambao huathiri uzuri wa ubao
pia husababisha gogo/ mti kupata
ugonjwa wa ukungu
6
epuka makosa/zingatia
shamba la mipaina
iliyopogolewa huonekana hivi
unaweza kupogolea ni miti aina zote,
mipaina..
na milingoti
pia
usikate matawi mpaka juu kabisa
karibu na mwisho kanabaki kama mkia wa mbuzi
usipogolee mti kwa
kutumia panga butu,
8
4. kupunguzia miti shambani
Wakati wa kupandwa
miti huwa karibu karibu lakini ikikua
huwa matawi yanagusana na kusababisha
ukuaji kuwa hovyo.
Miti inayotakiwa kupunguzwa
huwekwa alama
Miti inayotakiwa
kuondolewa ni ile ambayo imepinda,
yenye matawi makubwa toka chini, iliyokatika
juu, iliyodumaa kukua
kwa mipaina Muda wa kupunguzia ni miaka 7-8 na miaka 12-13 ili kukusaidia
kupata magogo makubwa ambayo ni manyoofu yasiyo
na matawi ovyo ovyo.
...na kisha upande wa piliwa mti, malizia ili kule ulikoanzia kukata ndio uelekeo ambao mti utangukia
Ukisha angusha ondoa matawi na kisha pima kulingana na uhitaji wa soko wa hilo gogo au nguzo.
9
unapoangusha mti kata kipande
uelekeo wa kuangushia...
miti ambayo
huondolea shambani lazima iwe inauzika kwa ajili ya matumizi
mbalimbali
10
5. usimamizi wa machipukizi
Hutakiwa kupunguzwa mara tatu ndipo unafikia hatua ya kuvuna zao la mwisho.
Miti aina ya milingoti ndiyo
ambayo ina nguvu ya kutoa machipukizi.
Mipaina haina machipukizi.
Kwenye shina kwa
kawaida huwa kuna machipukizi
mengi sana lakini haya hutakiwa kupunguzwa
ili kupata tena mazao mengine
ya miti.
1 2 3
11
Mwaka wa 2-3 ondoa na kubakiza machipukizi 3
Mwaka wa 6-7 ondoa na kubakiza machipukizi 2
Mwaka wa 9-10 ondoa na kubakiza Chipukizi 1
Kutegemeana na mteja
inawezekana kabisa ukubwa wa nguzo za umri wa 9-10 zinafaa.
mkulima anaweza kuvuna zote na kumuuzia
mteja wake
Nguzo za miaka 6-7
pia kulingana na uhitaji wa mteja
zinaweza kuvunwa zote na kwenda
sokoni
Wadudu huleta magonjwa ambayo huathiri ukuaji wa mti na pia husababisha mbao au nguzo kuwa mbaya
12
6. kudhibiti wadudu wa magonjwa shambani
Mchwa husababisha kuua kabisa milingoti hasa maeneo ambayo ni makame.
Namna ya kudhibiti ni kuchimba vichuguu vyote karibu na shamba na kumuua malkia, pia fuatilia njia ambazo hupitia (Mashimo) na kumwagilia dawa ya Attacan au Dimipridi- hizi hupatikana kwenye maduka ya pembejeo
Magonjwa mengine ni ya ukungu kwa mipaina ambapo vidudu kama chawa vinaitwa Aphidi hufyonza majimaji kwenye mti na kuua. Ukiona mtu kama huo umeathirika ni kuukata na kuuchoma
13
zingatia
Viumbe waharibifu na magonjwa ni moja ya tishio kubwa kwa ukuaji na mafanikio ya kiuchumi ya shamba la miti.
Baadhi ya nchi zinazolima miti ya aina hii wameishakumbana/wameshakabiliana na mlipuko wa magonjwa na viumbe waharibifu na kusababisha hasara kubwa.
panda aina nyingine za miti inayostahimili hayo magonjwa na viumbe waharibifu. Unachotakiwa kujua ni kuwa hayo magonjwa na wadudu wanaweza kuingia na kuenea hapa nchini na kwenye shamba lako la miti.
Ni muhimu kukagua shamba lako la miti mara kwa mara ili kugundua na kutoa taarifa zake (kama zipo) kwa afisa Misitu kwenye eneo lako.
14
Uandaaji wa mashamba kwa kutumia moto kuwe na udhibiti
Wavuta sigara wahakikishe vichungi wanavizima kabisa kabla ya kutupa
7. udhibiti wa moto kichaa
Wawindaji wawe wanatembea na maji ili wakishachoma nyama porini wazime kabisa moto
Warina asali kwa kutumia moto...wabadilike na watumie uvunaji wa kisasa wa kutumia vifaa vya kurinia asali
Moto ni adui
mkubwa wa miti. Vyanzo vya moto ni warina asali, uandaaji
wa shamba, Wavuta sigara,
wachunga ng’ombe, radi,
wapiti njia, magari n.k
15
Moto ukitokea na ukiona piga yowe kuita watu waje kusaidia kuuzima
Vifaa vya kuzimia ni matawi, matairi ya magari yaliyochanwa na kuwekwa mipini, pia ni pampu za maji za kubeba mgongoni
Kwa makampuni makubwa pia hutumia helikopta na mashine za kuangusha miti kama moto ni wa angani
Tengeneza barabara za kuzuia moto
shambani
Mikakati mingine wananchi wajitungie sheria ndogo kupitia kwenye vikao vya viongozi wa kijiji na wananchi wote
zingatiaJitihada za makusudi zinatakiwa ili kuzuia moto na kutambua kwa wakati matukio ya moto ili kuandaa nguvukazi za kuukabili.
Ni lazima kwa kila shamba la miti lizungukwe na barabara ya kuzuia moto maarufu kama fire line. Fire line iwe angalau na upana wa mita 5 na isiwe na kitu chochote kinachoweza kuchochea moto kirahisi
Kinga ni bora kuliko tiba. Ili kupunguza matukio ya moto kwenye maeneo ya mashamba ya miti, jamii kupitia serikali za vijiji lazima zikubaliane kwenye hatua za namna ya kudhibiti moto wa msituni.
Iwapo moto utatokea umakini mkubwa unahitajika ili kupunguza uwezekano wa kutokea ajali wakati wa kuzima moto.
Taasisi mahususi kwa ajili ya kuzima moto ni muhimu kuwepo ili ielekeze matumizi sahihi ya mbinu za kupambana na moto na uwepo wa vifaa vya kuzimia moto.
pale ambapo wananchi wamekosa uwezo wa namna ya kupambana moto mkubwa uhitaji kupata msaada kutoka ofisi za serikali zilizopo jirani.
17
15
FORESTRY DEVELOPMENT TRUSTUENDELEZAJ I M IS ITU TANZANIA
2 0 B A L O Z I R O A D , G A N G I L O N G A , I R I N G A , P O B O X 2
t : + 2 5 5 2 6 2 7 0 0 5 5 0 | I N F O @ F O R E S T RY- T R U S T. O R G