Upload
others
View
3
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
machokodo na shamba
la miti
MODULI NAMBA 3
Uanzishaji waShamba la Miti
MKULIMA WA MITI
ShukuraniKIJITABU HIKI KIMEANDALIWA KWA AJILI YA KUFIKISHA MAUDHUI NA TAALUMA YA NAMNA YA KUANZISHA SHAMBA LA MITI KWA MKULIMA MDOGO NA MKUBWA PIA. KIMEANDALIWA KWA MICHORO ZAIDI ILI KUMRAHISISHIA MSOMAJI KUJARIBU KILA KITU KWA USAHIHI ZAIDI.
MARA BAADA YA KUKAMILIKA, KIMEPITISHWA KWA WADAU MBALIMBALI NA WATAALAMU WA MISITU ILI KUTOA UZOEFU NA UTAALAMU WAO ILI KUBORESHA UTOAJI WA MAFUNZO SAHIHI YA UANZISHWAJI WA SHAMBA LA MITI HAPA TANZANIA.
NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA TAASISI YA UENDELEZAJI WA MISITU TANZANIA HUSUSANI KITENGO CHA huduma kwa wakulima wa miti KWA KUWEZESHA KAZI HII KUKAMILIKA.
NATOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA joseph makanza kwa michoro na kusanifu kijitabu hiki. pia NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA WAFADHILI WA TAASISI HII AMBAO NI GATSBY FOUNDATION NA dfid KWA KUWEZESHA KUFADHILI UANDAAJI WA KIJITABU HIKI.
MWISHO, NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA BWANA HAMISI MALINGA NA GEORG STRUNDEN KWA USHAURI WA KITAALAMU KUHUSIANA NA MICHORO NA MAUDHUI yA KITABU HIKI.
Utangulizi
Watafiti na wataalam wa misitu wanaamini kuwa watanzania wengi wamehamasika na wanapenda kilimo cha miti ya mbao.
Moduli hii inatoa maelekezo ya namna ya kuanzisha shamba la miti kutokana na miche bora itokanayo na kupanda mbegu bora.
Inatoa mafunzo ya namna ya Uandaaji wa shamba, upandaji mzuri wa miche na inatoa mwongozo kwa wawezeshaji vijijini ili nao watoe mafunzo ya namna ya kukitumia kijitabu hiki kufikisha mafunzo kwa wakulima. Hatua zilizoelezewa humu zinahusisha namna ya uanzishaji wa shamba la Milingoti na Paina pia.
Moduli hii itatueleza kisa cha MACHOKODO aliyenufaika kwa Kilimo cha Miti baada ya kujifunza na kutumia utaalam alioupata kutokana na mafunzo kujitengenezea faida na kubadili Maisha yake.
1. KUANDAA SHAMBA LA kupanda MITI
2
KILIMO CHA MITI NI SAWA NA KILIMO CHA MAZAO
MENGINE, ANDAA SHAMBA KWA KUSAFISHA KABISA...
Ondoa magugu, vichaka na miti
Kusanya takataka na
vichaka vyote mahali pamoja au kwenye misitari na
ikibidi unaweza kutumia moto kwa uangalifu
mkubwa sana
KUSANYA TAKATAKA KATIKATI NA SEMBUA KWENYE MSITARI UTAKAOPANDA MITI, NAFASI
KATI YA MSTARI UWE NI KAMA MITA TATU NA KATI YA MSTARI
NA MSTARI NYASI ZIKATWE ZIWE FUPI
3
UNAWEZA KUANDAA SHAMBA KWA kumwaga dawa ya kuulia magugu inayoitwa Glaifoseti
SAFISHA KWENYE VISAHANI
VYA UPANA WA KIPENYO CHA MITA MOJA KWA AJILI YA MASHIMO YA KUPANDA
MITI, KATIKATI YA VISAHANI NYASI ZIKATWE ZIWE
FUPI
UKITAKA MITI IKUE
VIZURI NA HARAKA SANA HASA MILINGOTI
LIMA SHAMBA NAMNA HII KAMA MAZAO MENGINE
YA KILIMO
4
EPUKA MAKOSA/ZINGATIA
USIPANDE MITI ikabanana
hivi
ILI KUPANDA MITI, KATUA SHAMBA,
LIMA SHAMBA KAMA UNAVYOLIMA MAZAO
MENGINE
USIPANDE MITI KWENYE
VICHAKA NA NYASI NDEFU HIVI, MITI
MINGI ITAKUFA NA PIA IKIPONA ITAKUWA
DHAIFU SANA
2. KUANDAA MASHIMO YA kupanda miti
5
ANZA KUNYOOSHA
MSTARI MMOJA UPANDE HUU WENYE ALAMA YA MITA TATU TATU KAMA MHIMILI WA
MISTARI MINGINE YA KUPANDIA
CHIMBA MASHIMO YENYE KINA CHA SENTIMETA 30 KWA 30 ILI KUPANDA MCHE
TENGANISHA udongo wa juu ukae upande mmoja na udongo wa ndani ya shimo uweke upande wa pili
KWA KUTUMIA MSTARI WA KWANZA ANZA
KUPIMA SHAMBA ZIMA NA KUWEKA ALAMA ZA MAMBO
KILA MITA TATU TATU
MITI HII INA MIAKA 20 HII NI MITI YA MIAKA 20
USIPANDE MITI HOVYO HOVYO HIVI
EPUKA MAKOSA/ZINGATIA
6
usiibane miti wakati wa kupanda. matokeo
yake ni kupata miti myembamba kama hivi
KABLA YA KUSAFIRISHA MICHE IMWAGILIE VIZURI, IWEKE KWENYE VIBOX/ TREI NA WALA USIIPANDANISHE ILI ISIVUNJIKE AU KUHARIBIKA
7
3. kupanda miti
ONDOA KARATASI YA PLASTIKI ULICHOOTESHEA MCHE KWENYE KITARU
weka mche ndani ya shimo ANZA KUFUKIA KWA KUTANGULIZA UDONGO WA juu
Usipakie kwenye pikapu au lori kwa kuimwaga na kupandanisha miche bila trei/ vibox
Fukia mche vIzuri kwa miguu na siyo kwa mikono kama ilivyozoeleka
8
....KIPIMO CHA GRAMU 30 NI
SAWA NA GANDA LA KIBERITI
weka mbolea ya npk
gramu 30 pia mbolea ya
kukuzia baada ya miezi 3 hadi 4
miti
hupandwa na kuwekewa
mbolea ya kupandia pia
mbolea ya kukuzia kama ilivyo kwa
mazao mengine
4. kuweka mbolea
...BAADA YA
KUFUKIA MCHE, CHORA
MSTARI MITHIRI YA MFEREJI
9
5. kukagua uotaji wa miche
zunguka shamba lote
kukagua maendeleo ya uotaji wa miche uliyopanda uweze
kubaini miche inayokufa, iliyodhoofu, na iliyo
na magonjwa
rejeshea au panda tena miche
ambayo imekufa ndani ya muda usiozidi wiki mbili
...HAKIKISHA KUWA MICHE INAYOPANDWA NI YA AINA NA UBORA UNAOFANANA KUTOKA KWENYE KITALU
HUSIKA
10
6. kupalilia shamba WEKA SHAMBA LA MILINGOTI NA MIPAINA SAFI
DHIDI YA MAGUGU ZAIDI, KAMA MAZAO YA KILIMO. PALILIA
KILA MAGUGU YANAPOJITOKEZA SHAMBANI.
...KUNA NJIA KUU NNE ZA KUPALILIA
...NJIA YA PILI, PALILIA KWA MSTARI NA KATIKATI
YA MSITARI NA MSTARI FYEKA NYASI
ZIWE FUPI KAMA HIVI
...NJIA YA tatu, PALILIA
SHAMBA LOTE KAMA MAZAO MENGINE YA KILIMO, NJIA HII
NDIYO NZURI YENYE KULETA MAFANIKIO
MAKUBWA YA KILIMO CHA MITI
1 m
...NJIA YA NNE,
KUPULIZIA DAWA YA MAGUGU IITWAYO
GLAIFOSETI...Onyo dawa hii
inauwa miti, weka kwa uangalifu
isiguse miti iliyokusudiwa
kalenda ya msimu wa upandaji miti
11
SHUGHULI MUDA / MWEZI
kUANDAA SHAMBA LA MITI
NOVEMBA-DESEMBA
KUNYOOSHA MISTARI, KUWEKA ALAMA NA KUCHIMBA MASHIMO
DESEMBA - JANUARI
kupanda desemba - januari
kupalilia januari-machi
Kuweka mbolea decemba - machi
kukagua uotaji na kurudishia
desemba - januari
KULIMA KUKATUA SHAMba
NOVEMBA-DESEMBA
barabara za moto juni - julai
FORESTRY DEVELOPMENT TRUSTUENDELEZAJ I M IS ITU TANZANIA
2 0 B A L O Z I R O A D , G A N G I L O N G A , I R I N G A , P O B O X 2
t : + 2 5 5 2 6 2 7 0 0 5 5 0 | I N F O @ F O R E S T RY- T R U S T. O R G