245
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA WA KUMI NA TANO Kikao cha Ishirini na Tatu – Tarehe 8 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae, Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa 15 na Kikao cha leo ni cha 23. Katibu! NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2019/2020. SPIKA: Ahsante sana Engineer, tunakushukuru sana. Katibu! NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU MEZANI:

MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

  • Upload
    others

  • View
    2

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA_________

MAJADILIANO YA BUNGE_________

MKUTANO WA WA KUMI NA TANO

Kikao cha Ishirini na Tatu – Tarehe 8 Mei, 2019

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

DUA

Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae, WaheshimiwaWabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa 15 na Kikaocha leo ni cha 23.

Katibu!

NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU MEZANI:

HATI ZA KUWASILISHWA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO:

Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wafedha 2019/2020.

SPIKA: Ahsante sana Engineer, tunakushukuru sana.

Katibu!

NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU MEZANI:

Page 2: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

MASWALI NA MAJIBU

SPIKA: Swali la kwanza linaelekezwa Ofisi yaMheshimiwa Waziri Mkuu, litaulizwa na Mheshimiwa MuniraMustapha Khatib, Mbunge wa Viti Maalum, MheshimiwaMunira.

Na. 186

Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vyaWafanyakazi

MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB aliuliza:-

Vyama vya Wafanyakazi nchini licha kuwa na uwezowa kujitegemea bado vinaendelea kutoza ada kubwa yaUachama mathalan, Chama cha Walimu (CWT) kinatozaasilimia mbili.

Je, Serikali haioni kuwa kuna haja ya kulinda maslahiya Watumishi kwa kuleta Sheria ya kupunguza makato hayo?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa WaziriMkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Munira MustaphaKhatibu, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napeda kuelezakwamba, Serikali imeweka utaratibu chini ya Sheria ya Ajirana Mahusiano Kazini Namba sita (6) ya mwaka 2004 unatoauhuru na haki kwa Chama cha Wafanyakazi na Chama chaWaajiri, kuamua na kufanya mambo yao wanayotaka kwamaslahi yao ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu Katibazao. Kifungu cha 11 cha sheria hiyo, kimeeleza bayanakuhusiana na haki hizo.

Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha na kuboreshamaslahi ya Wanachama, Wanachama wa Chama cha

Page 3: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

Wafanyakazi wanao uhuru na haki ya kufanya mabadilikokatika Katiba zao ambazo zinasimamia uendeshaji washughuli za chama chao. Hivyo, suala la kupunguza makatoya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi lipo chini yamamlaka ya Chama cha Wafanyakazi husika na Wanchamawenyewe kupitia vikao vya kikatiba kwa kufanya mabadilikokatika Katiba ya chama chao.

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kusimamia viwangovya michango ya wanachama ni kukiuka Mikataba ya Shirikala Kazi Duniani (ILO) Na. 87 na 189 juu ya uhuru wa kujumuikana majadiliano ya pamoja ambayo Serikali yetu imeridhiana kuzingatia katika Katiba ya nchi na Sheria mbalimbali zaKazi nchini.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutoa elimu juuya haki na wajibu, uhuru wa kujumuika na mambo muhimuyahusuyo Wanachama na Katiba zao.

SPIKA: Mheshimiwa Munira nilikuona.

MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB: Mheshimiwa Spika,nashukuru, kwa kuwa watumishi wengi hasa wanaoanza kaziwamekuwa wakiunganishwa kwenye mikataba yawafanyakazi bila ya ridhaa yao.

Je, Serikali haioni haja sasa ya kutoa mwongozo kwamaafisa utumishi juu ya kulinda haki za watumishi hao?(Makofi)

Swali la pili, Serikali ina mkakati gani wa kujiondoakuwa mawakala wa makato ya wafanyakazi?

SPIKA: Swali la pili liweke vizuri.

MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB: Mheshimiwa Spika,Je, Serikali ina mkakati gani wa kujiondoa kuwa mawakalawa vyama vya wafanyakazi?

SPIKA: Kivipi yaani, ili ujibiwe swali lako.

Page 4: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB: Mheshimiwa Spika,kwenye majibu yake ya msingi, amesema vyama vyawafanyakazi, naomba ninukuu” watumishi wa vyama vyawafanyakazi licha ya kuwa na mamlaka nchini, wafanyakazihusika, vyama vya wafanyakazi hupitia vikao vyao , katibakwa kufanya mabadiliko katika…

SPIKA: Ahsante sana Munira, Mheshimiwa Waziri jibuhilo swali la kwanza.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika,utaratibu wa wafanyakazi kujiunga katika vyama vyawafanyakazi ni utaratibu ambao umewekwa kwa mujibu washeria na kuna uhuru wa wafanyakazi kujiunga ambapochama husika kwa kuzungumza na mwajiri, hufanya mikutanona kutoa elimu mbalimbali na baadaye ndiko wafanyakaziwanajiunga.

Mheshimiwa Spika, hivyo, niseme tu kwambawafanyakazi wengi wanajiunga kwa mujibu wa taratibu zakisheria ambazo zimewekwa na Katiba na katika mazingiraambayo wafanyakazi wanalazimishwa kujiunga pasipo waokufahamu na ridhaa yao, hiyo ni kinyume na utaratibu nanitoe tu maelekezo kwamba vyama vyote vya wafanyakazivihakikishe kwamba vinazingatia sheria za kazi ili wanachamawote wanaojiunga wawe wanajiunga katika uhuru na ridhaayao.

SPIKA: Ahsante tunaendelea na swali la MheshimiwaKiteto Zawadi Koshuma, Mheshimiwa Kiteto!

Na. 187

Kuwawezesha Vijana Kupata Ajira Nchini

MHE. KITETO Z. KOSHUMA aliuliza:-

Je, Serikali haioni umuhimu wa kuelekeza taasisi zotenchini kuwa sifa mojawapo ya kuajiriwa iwe ni umri wa miaka

Page 5: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

21- 35 ili kuwezesha Vijana wengi wanaotoka vyuoni kupataajira.

SPIKA: Majibu ya swali hilo, bado tuko Ofisi yaMheshimiwa Waziri Mkuu, litajibiwa na Naibu Waziri AnthonyMavunde, Mbunge wa Dodoma Mjini.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa WaziriMkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kiteto ZawadiKoshuma, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa mijibu wa Sheria ya Ajira naMahusiano Kazini Na. 6 ya Mwaka 2004, Kifungu cha 5kimekataza mtoto chini ya umri wa miaka 18 kuajiriwaisipokuwa katika mazingira maalum yaliyotajwa katika kifunguhiki. Kwa msingi huo, umri wa kuajiriwa ni miaka 18 nakuendelea pamoja na masharti yaliyotajwa katika kifungucha 5 cha Sheria Na. 6 ya mwaka 2004. Hivyo nakubalianana Mheshimiwa Mbunge kuendelea kuwahimiza waajiri wotekutii Sheria za kazi na kuhakikiahsa vijana wote wenye sifawanapomaliza mafunzo yao na kutimiza umri wa kuajiriwawanaajiriwa kwa kuzingatia fursa zilizopo kwa waajiri namasharti ya kazi husika.

SPIKA: Mheshimiwa Kiteto!

MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Spika, pamojana sheria kuelekeza umri wa kuajiriwa kazini, bado ajira nyingizinapotangazwa hapa nchini hutoa sharti la kuwa na uzoefuwa kazi, kuanzia umri wa miaka mitano na kuendelea, nahivyo hii huwaondolea fursa vijana wengi wanaotoka vyuonikutokupata ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivyo, naomba Serikali itoe majibuhapa kwamba ni lini itatoa tamko kwa waajiriwa kuondoasharti la vigezo ili kuwapa fursa vijana wanaotoka vyuoni,isipokuwa tu kwa zile ajira ambazo zinahusu nafasi za juu?

Page 6: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

SPIKA: Hivi wewe Kiteto ukiwa una ajira zakomwenyewe utampa mtu asiyekuwa na uzoefu! Mambomengine Waheshimiwa Wabunge, majibu Mheshimiwa NaibuWaziri.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika,kwa kutambua kwamba kumekuwepo na changamotokubwa sana kwa vijana wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vyaelimu ya juu kupata kazi kwa kikwazo cha uzoefu. Ofisi yaWaziri Mkuu katika utekelezaji wa programu ya ukuzaji ujuzinchini, imeanzisha program maalum kabisa ambayoMheshimiwa Waziri Mkuu alizindua miongozo yake yamafunzo ya Uanagenzi na mafunzo ya Vitendo Kazini(Internship). Ambayo hivi sasa kwa mujibu wa utaratibutuliouweka, tunawachukua vijana kutoka vyuo vikuu,kutokana na fani walizonazo na makubaliano ambao.

Mheshimiwa Spika, sisi Serikali tumeingia na chamacha waajiri na sekta binafsi, tunawapeleka katika kampunihusika kwenda kufanya kazi kivitendo, ambako wanakaamiezi sita mpaka miezi 12 na baadaye mwajiri katika eneohusika, anampatia cheti cha kumtambua kama nimwanachuo ambaye amekaa kwake katika fani husika kwamiezi 12 ili baadaye ikitangazwa nafasi ya ajira ya kaziambayo ameifanyia kwa vitendo, iwe pia ni sehemu ya yeyekumsaidia kupata ajira, kwa maana ya kutumia uleutambulisho wa kwamba tayari ameshafanya kazi katikamwajiri husika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kama Serikali na sisitumeliona jambo hilo, na ndiyo maana tumeweka nguvukubwa sasa hivi katika kuhakiksiha kuwa tunawajengea ujuzivijana wetu ili waweze kuwa na sifa za kuajirika na baadayekuwasaidia kupata ajira pasipo kikwazo cha uzoefu.

SPIKA: Safi kabisa Mheshimiwa Naibu Waziri, hiyo ndiyonjia ya kufanya, wafanye internship, wajue nini cha kufanya,waajiriwe, lakini hii ya kusema tu, twende twende. Mwakajokanimekuona.

Page 7: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.Mheshimiwa Naibu Waziri mwaka jana niliuliza swali kuhusianana vijana wanaosindikiza kopa zinazovuka mpaka waTunduma kuelekea Dar es Salaam zinazotoka Zambia naCongo, wamefanya kazi zaidi ya miaka mitatu na miakaminne pale, lakini mpaka leo hawajapata mikataba ya ajirana uliagiza ukasema kwamba Kazi Mkoa atahakikishakwamba anashughulikia jambo hil, mpaka leohalijashughulikiwa. Nini kauli ya Serikali Mheshimiwa NaibuWaziri?

SPIKA: Mheshimiwa Mwakajoka swali hilo halinauhusiano kabisa na swali la msingi, swali la msingi linahusianana vijanan wanaomaliza vyuo vikuu kupata ajira moja kwamoja bila kulazimika kuwa na uzoefu kazini. Kwa hiyo, hilonalikataa, tunaendelea na Ofisi ya Rais TAMISEMI, ProfesaJumanne Maghembe.

Na. 188

Uhaba Mkubwa wa Walimu wa Shule za MsingiWilayani Mwanga

MHE. PROF. JUMANNE A. MAGHEMBE aliuliza:-

Kuna uhaba mkubwa wa Walimu wa Shule za MsingiWilayani Mwanga:-

Je, ni lini Serikali itapeleka Walimu 384 wanaohitajika?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa MwitaMkwabe Waitara, tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziriwa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), naomba kujibu swali la

Page 8: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

Mheshimiwa Profesa Jumanne Abdallah Maghembe,Mbunge wa Mwanga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna changamoto yaupungufu wa walimu wa shule za msingi nchini, naHalmashauri ya Wilaya ya Mwanga ina jumla ya shule zamsingi 110, za Serikali zenye jumla ya walimu 590, hadi kufikiaNovemba, 2018 kulikuwa na upungufu wa walimu 384.

Mheshimiwa Spika, Mwezi Aprili, mwaka 2019, Serikaliimeajiri walimu 4,549 wa shule za msingi na sekondari ili kuzibanafasi zilizoachwa wazi katika maeneo mbalimbali nchiniikiwemo Halmashauri ya Mwanga, na kati ya walimu hao3,089 ni kwa shule za msingi na walimu1,460 ni shule zasekondari. Walimu hawa wameshapangwa katikahalmashauri mbalimbali nchini na walipaswa kulipoti kuanziajana mpaka tarehe 21 na wale ambao hawataripoti, nafasizao zitapewa watu wengine ambao wana uhitaji kama huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halmashauri ya Mwangaimepelekewa walimu 21 wa shule za msingi nawalimu watanowa shule za sekondari. Serikali itaendelea kuajiri walimu kwakadri ya upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Haya Profesa umeletewa walimu, swali lanyongeza Mheshimiwa Maghembe tafadhali.

MHE. PROF. JUMANNE A. MAGHEMBE: MheshimiwaSpika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi kuuliza maswalimawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwanza ningependa kuwapa polesana wananchi wa Machame na hasa familia ya MarehemuDkt. Reginald Mengi kwa msiba uliowapata. TunamuombaMwenyezi Mungu aiweke roho haye mahali pema peponi.

Mheshimiwa Spika, sasa niulize maswali mawili yanyongeza, kwanza, uhaba wa walimu 384 tumepewa walimu

Page 9: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

21! Katika shule zetu, shule 50 zina walimu wawili wawili nashule zingine 40 zina walimu watatu watatu, sasa ujue hizozingine ndiyo… na shule za msingi zina madarasa nane,darasa la awali na madarasa saba, kwa hiyo, hali iliyoko paleni ngumu sana.

Mheshimiwa Spika, na kwa sababu uhaba huuumetokana na walimu kustaafu, kuhama na kufariki. Suala lafedha halipo hapa, kwa sababu nafasi zipo, na mishaharaipo, ni kwa nini sasa Serikali haichukui hatua ikaajiri bilakutumia visingizio ambavyo havina msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, ni lini Serikali itabadilishaurasimu huu, kama mwalimu yupo na yuko kwenye ikama,na amestaafu. Kwa nini Serikali hairuhusu halmashauri ikaajirikutoka kwenye soko mara moja ili kutoathiri upatikanaji waelimu katika shule. Inaacha mpaka shule zinakuwa namwalimu mmoja?

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Mwikwabe MwitaWaitara, maswali hayo muhimu sana, Mwanga upungufu wawalimu 300, Kongwa upungufu walimu 1000. Majibu tafadhali.(Makofi)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaSpika, ni kweli, tuna upungufu wa walimu wa shule za msingi66,000 nchi nzima, na upungufu wa walimu wa sekondari14,000, kwa hiyo, ni kweli kwamba kuna upungufu, ni jamboambalo liko wazi.

Mheshimiwa Spika, lakini kama nilivyosema kwenyejibu langu la msingi, hizi ajira mpya ni ajira za kuziba nafasi.Sasa hivi inayofuata ni ajira zile za kawaida za kila mwaka zakuongeza na kupunguza upungufu uliopo. Kwa hiyo, naombaniwahakikishie kwamba Serikali imeshaliona hili, tulifanyauhakiki, pamoja na watumishi hewa, waliofariki, waliofukuzwakazi na wengine wamestafu na wengine wameacha kwa

Page 10: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

sababu mbalimbali. Kwa hiyo, hili ilikuwa ni kuziba nafasi hizi,sasa inakuja ya ajira za kila mwaka za kuweza kuziba kwautaratibu wa kawaida na hili linafanyiwa kazi na Serikali inajuakwa kweli kuwa kuna upungufu mkubwa nchini wa walimu.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, ni kwamba, nikuziba nafasi kwa maana ya kutoa kibali kwa halmashauri.Hizi ni ajira, cha muhimu hapa siyo kuruhusu utaratibuusioelekeweka utumike kuajiri walimu, kumekuwa na mambomengi sana katika halmashauri zetu ambayo yanafanyikakatika ajira hizi, kwa hiyo, tunajiridhisha kwanza. Lakini chamuhimu ni kwamba tumekubaliana kama Serikali kuchukuahatua mahususi kupunguza upungufu wa walimu shule zamsingi na sekondari.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Maswali ya nyongeza wanatakiwa wasimamewalimu tu. Mwalimu Susan Kiwanga!

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante,kama ilivyo kwa Mheshimiwa Maghembe Mwanga, Wilayaya Kilombero yenye majimbo mawili ilikuwa na upungufu wawalimu 1,118 na hivi juzi tu tumeletewa walimu 34, wanne wasayansi sekondari na 30 wa msingi na kufanya nakisi upungufuhuo ubaki 1,084.

Je, Serikali ni lini sasa itapeleka walimu ndani yaHalmashauri ya Wilaya ya Kilombero, ili watoto wale wapatechakula cha akili, ukizingatia na miundombinu yetu si rafiki?

SPIKA: Majibu ya swali hilo ambalo ndiyo la Wabungewalio wengi, najua ulijibu lakini hebu rudia tena MheshimiwaNaibu Waziri.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaSpika, ni kweli, kama nilivyosema, tumeajiri walimu 4,549, tunashule za msingi 16,000 za Serikali na tuna shule zaidi ya 4000za sekondari. Katika hali ya kawaida upungufu huo naupokea

Page 11: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

kama Serikali ni kweli, kuna upungufu mkubwa natusingeweza kupeleka kila mahali. Lakini tuliangalia kwamfano kuna shule ambazo pale kulikuwa na wakumu ambaowanapelekwa shule za msingi, wameenda mahitaji maalumu,wameenda na masomo ya sayansi na hisabati.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, angalau tukaangaliashule ambazo zina upungufu mkubwa zaidi tukapeleka pale,kwingine tumepeleka walimu mpaka watano, wenginewanne.

Mheshimiwa Spika, lakini, Mheshimiwa Susan Kiwangawiki iliyopita aliuliza swali hap ana walimu hao. Tumeshatoamaelekezo, kwanza kuna walimu wapo kwenye halmashauri,makao makuu ya wilaya au ya mji, lakini unakuita pembezonikule unakuta walimu ni wachache, lakini walimu wapo.Tumeshapeleka fedha katika halmashauri zote nchini zakuweza ku-balance ikama.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunatarajia kwamba kazihii itafanyika kwa kusimamiwa na Makatibu Tawala Mikoana Wakurugenzi, ndani ya wiki mbili mpaka tatu, tupatetaarifa rasmi.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ilikuwa kuhamishawalimu kupeleka pembezoni ilikuwa ni ngumu kwa sababufedha hazipo, sasa fedha wameshapelekewa Halmashaurizote, zinatakiwa kazi ifanyike, halafu ajira inayofuatatutazingatia maeneo yote ambayo yana upungufu mkubwa.Shule za msingi, hisabati na masomo ya sayansi.

Mheshimiwa Spika, ahsante, likiwemo na eneo laKongwa.

SPIKA: Ahsante sana nakushukuru sana.

Waheshimiwa Wabunge tunaedelea, bado tukoTAMISEMI, swali linaulizwa na Mheshimiwa Mbunge waMbogwe, Mheshimiwa Augustino Manyanda Masele.

Page 12: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

Na. 189

Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya-Mbogwe

MHE. AUGUSTINO M. MASELE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi waHospitali ya Wilaya ya Mbogwe.

SPIKA: Majibu ya swali hilo la Mtemi wa Wasukuma,Mheshimiwa Masele, Mbunge wa Mbogwe tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaSpika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI,naomba kujibu swali la Mheshimiwa Augustino ManyandaMasele, Mbunge wa Mbogwe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/2019Serikali ilitoa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali67 za Halmashauri. Aidha, katika mwaka wa fedha 2019/2020Serikali imetenga shilingi bilioni 23.9 kwa ajili ya ujenzi wa vituovya afya 52 na Hospitali 27 za Wilaya. Halmashauri ya Wilayaya Mbogwe ni miongoni mwa Hospitali hizo 27 naimetengewa shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuanza ujenzi waHospitali ya Wilaya.

SPIKA: Mheshimiwa Masele swali la nyongezatafadhali.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Spika,ahsante pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa NaibuWaziri, naomba niulize maswali madogo ya nyongeza. Swalila kwanza ni kwamba Wilaya ya Mbogwe ni Wilaya mpyana katika Mkoa wa Geita, ni Wilaya pekee ambayo kwa kweliina watumishi wachache sana wa Idara ya Afya: Je, Serikaliina mpango gani wa kutuongezea watumishi hao?

Swali la pili ni kwamba Serikali imejitahidi kutupatiavituo viwili vya afya na huduma mojawapo ni ya mortuary;

Page 13: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

lakini kuna shida ya mortuary cabinets, yale mafriji yakuhifadhia maiti hayajaletwa na watu MSD. Sasa Serikali inampango gani kupitia MSD kutuletea hiyo huduma maramoja? Ahsante.

SPIKA: Majibu ya maswali hayo mawili MheshimiwaJosephat Sinkamba Kandege, Naibu Waziri TAMISEMItafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaSpika, katika swali lake la kwanza Mheshimiwa Maseleanaongelea upungufu wa watumishi wa Kada ya Afya katikaWilaya yake ambayo ni miongoni mwa Wilaya mpya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli usiopingika nawewe umekuwa shuhuda kwamba wakati mwingizinapoanzishwa Halmashauri mpya kumekuwa nanakutopata watumishi wa kutosha. Kwa hiyo, naombakwanza niagize Ofisi ya RAS wahakikishe kwanza ndani yaMkoa watazame ikama ilivyo ili katika maeneo ambayo yanaupungufu mkubwa kama eneo la Mheshimiwa Mbungewaweze ku-balance.

Mheshimiwa Spika, nimwambie Mheshimiwa Mbungekwamba wakati nafasi nyingine zikitoka kwa ajili ya kuajiri,tutahakikisha kwamba tunazingatia maeneo yenye upungufuikiwa ni pamoja na eneo lake kuwapeleka watumishi wale.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pil i ni juu yakupatikana kwa friji kwa ajili ya kutunza maiti. Naombanimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ni azima yaSerikali kuhakikisha maeneo yote ambayo mortuaryzimejengwa, friji zinapelekwa. Naomba tuwasilaine naMheshimiwa Mbunge baada ya kipindi cha maswali namajibu ili tujue MSD lini watapeleka hayo masanduku.

SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Gashaza, swali lanyongeza.

Page 14: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

MHE. ALEX R. GASHAZA: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kunipa nafasi niliulize swali dogo la nyongeza. Hospitaliya Nyamiaga ni Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngaraambayo ilipatiwa hadhi kutoka kituo cha afya mwaka 2013,lakini mpaka sasa hivi hakuna maboresho ya miundombinukatika hospitali hiyo. Kwa hiyo kuna upungufu wa jengo lautawala, jengo la upasuaji, jengo la X-Ray, mortuary na laborWard:-

Ni lini Serikali itaweza kutenga fedha kwa ajilikuboresha hospitali hiyo ukizingatia kwamba hatuna hospitaliya Wilaya?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu WaziriTAMISEMI, Mheshimiwa Kandege tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaSpika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI,naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Gashazakama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kwambamaeneo mengi ambayo vilikuwa aidha vituo vya afya auilikuwa zahanati ikapandihswa hadhi; kwanza tumekuwa nachangamoto ya eneo, hata pale ambapo tumepandishahadhi kituo cha afya kuwa hospitali ya Wilaya inakuwa hainahadhi ya kulingana na hospitali ya Wilaya.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbungeatakubaliana nami kwamba Serikali katika utaratibu mziwawa kuboresha na kujenga Hospitali za Wilaya zile za mwanzozinaanza kuonekana kwamba zimeanza kuwa outdated.Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa kadriambavyo tumeanza na hosptali 67, zikaongezeka 27 kwakadri bajeti itakavyoruhusu hakika na wao hatutawasahau iliwale na Hosptali ya Wilaya yenye hadhi ya kulingana naHospitali za Wilaya za Halmashauri nyingine.

SPIKA: Mheshimiwa Lubeleje, swali fupi.

Page 15: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.Kwa kuwa ujenzi wa Kituo cha Afya Mbori ambacho hatawewe unakifahamu, Waziri wa TAMISEMI anakifahamu, sasani zaidi ya miaka kumi kinajengwa kwa nguvu za wananchina Halmashauri ambayo haina fedha; na kwa kuwanimeomba shilingi milioni 500 TAMISEMI wasaidie kukamilishajengo lile:-

Je, TAMISEMI au Serikali inasemaje kuhusu kukamilishaKituo cha Afya Mbori?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu WaziriTAMISEMI.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaSpika, kama kuna Waheshimiwa Wabunge ambaowamekuwa wakiongelea kituo cha afya kwa kurudia maranyingi ni pamoja na Mheshimiwa Lubeleje; na hivi karibunialipata fursa ya kuonana na Mheshimiwa Waziri mwenyedhamana na akamhakikishia.

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni tumepata fedha kiasi,tumepeleka kwenye hospitali na vituo vya afya ikiwa nipamoja na Kongwa shilingi milioni 400. Naomba nimhakikishieMheshimiwa Lubeleje, ahadi ya Mheshimiwa Waziri hakikaatatekeleza kama alivyomwahidi. Naomba avute subirafedha yoyote ikipatikana hatumsahau Mheshimiwa Lubeleje.

SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea na Wiazara yaKilimo, swali la Mheshimiwa Yussuf Salim Hussein, Mbunge waChambani, kwa niaba yake.

Na. 190

Kilimo Kisichotumia Mbolea za Viwandani

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM (K.n.y. MHE. YUSSUFSALIM HUSSEIN) aliuliza:-

Page 16: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

Tanzania ina ardhi kubwa yenye rutuba ya kutoshana inawezekana kabisa kulima mazao yasiyotumia mboleaza viwanda ambayo bei zake ni kubwa sana katika Soko laDunia:-

(a) Je, Serikali imeweka mikakati gani ya kutoa elimuhiyo kwa wakulima?

(b) Je, Serikali inachukua hatua gani kuona kuwaTanzania ni nchi inayoongoza kwa kuzalisha mazaoyasiyokuzwa kwa kutumia mbolea za viwandani?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Mgumba,Naibu Waziri Kilimo, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA)alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimonaomba kujibu swali la Mheshimiwa Yussuf Salim Hussein,Mbunge wa Chambani, lenye sehemu (a)na (b) kwa pamojakama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Taasisiza Sekta Binafsi imeendelea kutoa elimu ya kilimo borainayojumuisha matumizi sahihi ya mbolea za asili, viuatilifu vyaasili, mbegu bora na hifadhi ya mazingira ili kuzalisha mazaokwa tija na kuwa na kilimo endelevu.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza mpango wamuda mrefu wa matumizi sahihi ya virutubisho vya udongo,Serikali kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania yaani (TARI)inafanya utafiti wa afya ya udongo katika Kanda zote sabaza kiikolojia za kilimo nchini. Utafiti huo unalenga kubaini ainaza virutubisho na tabia za udongo katika maeneo mbalimbalinchini ili kuweza kutoa elimu kwa wakulima kuhusu kiasi, ainana matumizi sahihi ya mbolea za viwandani na asili. Utafitihuo umeanza kwa kuchukua sampuli za udongo katikaKanda za Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kati, Kanda ya

Page 17: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

Kaskazini na sehemu ya Kanda ya Mashariki na utaendeleakatika maeneo mengine nchini na utakamilika Juni 2020.

Mheshimiwa Spika, kwa kutambua ongezeko lamahitaji ya mazao na bidhaa za kilimo zinazozalishwa kwakutumia mbolea za asili na viuatilifu vya asili, Serikaliimeboresha mtaala wa mafunzo katika Vyuo vya Kilimoambapo mada za kilimo hai na hifadhi ya mazingirazimejumuishwa ili kuwawezesha Maafisa Ugani na wakulimakupata elimu hiyo.

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana naTanzania Organic Agriculture Movement, SustainableAgriculture Tanzania, Ecology Agriculture chini ya SWISSAID,Zanzibar Organic Producers, Tanzania Alliance for Biodiversityna TANCERT inatoa elimu ya kilimo hai kwa wakulima na kutoavyeti vya ubora wa mazao kwa ajili ya masoko maalum.Baadhi ya mazao ambayo yanazalishwa katika mfumo wakilimo hai hapa nchini ni pamoja na kakao, kahawa, pambana viungo.

SPIKA: Mheshimiwa Masoud, uliuliza swali.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Nina maswali mawili ya nyongeza yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kasi ya uzalishaji wa kilimo chaviungo kama vile hiliki, mdalasini, pilipili manga, binzarinyembamba kwa nyumbani Zanzibar tunaita uzile, imekuwabado ni ndogo sana na kuna maeneo mengi ambayoyanaweza yakastawi mazao haya.

Mheshimiwa Spika, Serikali ituambie katika kuhakikishakwamba kwa hali ya hewa na udongo, mahitaji ya mazaohaya bila mbolea, ina mkakati gani wa ziada kuona kwambamazao haya yanalimwa na wakulima wakapata faida naSerikali inapata tija kubwa?

Mheshimiwa Spika, la pili, kuna malalamiko makubwakwa baadhi ya wakulima kwamba Maafisa Ugani hawatoi

Page 18: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

elimu inayostahili katika maeneo ambayo wakulimawangeweza kulima kilimo cha aina yoyote bila kutumiambolea: Serikali ituambie ina mkakati gani katikakuwawezesha Maafisa Ugani ili waweze kuwafikia wakulimawalio wengi zaidi?

SPIKA: Majibu ya maswali hayo Mheshimiwa NaibuWaziri wa Kilimo, Mheshimiwa Omary Tebweta Mgumbatafadhali.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Spika, nashukuru. Swali la kwanza la MheshimiwaMasoud anataka kujua mkakati wa Serikali ambao tunawezakuwawesha wakulima ili waweze kuongeza uzalishaji na tija.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katika jibu langula msingi, yaani kilimo tulichokuwa tunalima, kilikuwa chakubahatisha; mkakati mkubwa wa Serikali uliopo sasa kwanzani kufanya utafiti wa afya ya udongo ili kubaini asili nakuangalia aina ya udongo iliyoko pale ili kuwashauri wakulimani zao gani ambalo linakubali kwa udogo wa ikolojia eneowalipo? Kwa hiyo, huo mkakati ambao utakamalizika mudamfupi ili kwamba tutoe elimu sahihi na kuwashauri wakulimaaina gani ya zao walime? Mbolea gani watumie? Namnagani ambayo wanaweza kufaidika kwa kuongeza uzalishajina tija?

Mheshimiwa Spika, katika swali la pili, anazungumziakuhusu Maafisa Ugani kwamba wapo lakini hawawafikiiwakulima kutoa elimu sahihi. Kwanza, nichukue nafasi hiikueleza kwamba Maafisa Ugani ni kweli anachosemaMheshimiwa Mbunge kwamba wako wachache. MahitajiMaafisa Ugani ni zaidi ya 20,000 nchini hii, tuliokuwa nao ni8,600. Kwa hiyo, tuna upungufu zaidi ya 11,400.

Mheshimiwa Spika, kama Serikali, kwa kujua hilo kwasasa hivi ni kwamba Serikali imeshaanza kutoa vibali kwa ajiliya kuajiri watumishi na mkazo mmoja utaelekezwa huko ilitupate Maafisa Ugani kwa ajili ya kwenda kutoa elimu.

Page 19: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, kama Serikalituna mkakati ambao ulikuwepo tangu katika ASDP I wakujenga vituo vya elimu kwa wakulima kila Kata, mkakati huoutaendelea, lengo ni kuwakusanya wakulima kutoka katikavijiji mbalimbali kukutana pale kunapokuwepo na mashambadarasa ya mazao yanayokubali katika maeneo yao iliwapate elimu ya pamoja kwa ajili ya kuwasaidia katikakuongeza tija na uzalishaji. (Makofi)

SPIKA: Tunaendelea na Mheshimiwa Ester MichaelMmasi, bado tuko Wizara ya Kilimo. Kwa niaba yake,nimekuona Mheshimiwa Shally Rymond.

Na. 191

Ushiriki wa Wanawake Kwenye Fursa ya Kilimo

MHE. SHALLY J. RAYMOND (K.n.y. MHE. ESTER M. MMASI)aliuliza:-

Changamoto kubwa inayowafanya wanawake waTanzania wasishiriki kwenye Sekta ya Kilimo na ufinyu wa Bajetina mitaji kutoka kwenye Taasisi za Kifedha:-

Je, ni nini kauli ya Serikali juu ya ushiriki wa wanawakekwenye Sekta ya Kilimo ukizingatia changamoto hizo?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA)alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waKilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ester MichaelMmasi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Kilimo inajumuisha sektandogo za kilimo mazao, mifugo, uvuvi na misitu. Bajeti yaWizara za Sekta ya Kilimo zinajumuisha bajeti ya Wizara zasekta husika, Bodi za mazao na Taasisi mbalimbali zilizo chiniya Wizara hizo za Kisekta. Utekelezaji wa bajeti hizohuwawezesha wanaume na wanawake katika shughuli za

Page 20: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

kilimo. Wanawake wanachangia asilimia 90.4 ya nguvukaziya wanawake inayotumika katika shughuli za kilimo nahuchangia wastani wa asilimia 70 ya mahitaji ya chakulanchini.

Mheshimiwa Spika, katika kutatua changamoto hizo,Serikali inaendelea kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifaya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 kupitiamifuko ya uwezeshaji ikiwemo Mfuko wa Maendeleo yaWanawake ambao huchangia 4% ya mapato ya Mamlakaza Serikali za Mitaa kwa kila mwaka. Kwa mfano, katikamwaka 2017/2018, jumla ya shilingi 15,633,312,764.91zimetolewa kwa vikundi 2,919 vya wanawake na vijanavyenye jumla ya wanawake wajasiriamali 29,190 katikaHalmashauri mbalimbali nchini.

Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu wawanawake katika kilimo Serikali, imeilekeza Benki yaMaendeleo ya Kilimo (TADB) katika mikopo inayotoa yoteisipungue asilimia 20, mikopo hiyo itolewe kwa vikundi vyawanawake na miradi inayoongozwa na akina mama. HadiJanuari, 2019, asilimia 33 ya mikopo iliyotolewa katika vikundivya wanawake na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ilienda kwawanawake.

Mheshimiwa Spika, vilevile, benki za NMB na Azaniazimeanzisha madirisha maalum ya kutoa mikopo kwa vikundivinavyojishughulisha na kilimo na miradi mbalimbali. PiaSerikali imehamisisha wanawake kujiunga kwenye vikundi vyaushirika wa akiba na mikopo kama SACCOS, VICOBA ilikupata huduma za kifedha na mikopo kwa urahisi ili kuongezamitaji yao katika kilimo.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeuelekeza Mfuko waPembejeo za kilimo kutoa kipaumbele kwa vikundi vyawanawake vinavyoomba mikopo ya kuendeleza kilimo.Vilevile, Serikali imeendelea kutoa hatimiliki za ardhi za kimilana hatimiliki za ardhi za muda mrefu kwa ajili ya kuwawezeshawanawake kumiliki ardhi na kuzitumia hati hizo kamadhamana, kukopa katika Taasisi mbalimbali za kifedha ili

Page 21: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

waweze kupata mitaji ya kununua pembejeo na zana boraza kilimo ili kuongeza uzalishaji, tija na kuanzisha viwandavidogo vidogo vya usindikaji wa mazao kwa kuongeza tijana vipato vyao.

SPIKA: Mheshimiwa Shally Rymond, nimekuona.

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, ahsantesana. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Awaliya yote, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali nanimeyapokea.

Swali la kwanza; kwa kuwa Benki ya Kilimo mpaka sasahaijaweza kuwa katika Mikoa yote na hizo benki nyinginealizozizungumzia kama NMB na alitaja benki mbili zote hizo niCommercial na zinahitaji wewe unayekwenda kukopa lazimauwe na dhamana na wanawake wengi hawana nyumbawala hawana dhamana ambazo zinatambulika kibenki: Je,Serikali iko tayari ku-guarantee mikopo hiyo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Tatizo katika kilimo nipamoja na mbegu bora na mara nyingi unakuta kwambambegu hizo ni ghari na pia siyo rahisi kumfikia mkulima. Ni linisasa mbegu hizo zitagaiwa kwa wanawake hao kupitia katikaKata zao? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa NaibuWaziri Kilimo, Mheshimiwa Omary Tebweta Mgumba,tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Spika, nashukuru. Swali la kwanza la MheshimiwaShally Rymond anataka kujua kwamba kwa sababu benkiya Maendeleo ya Kilimo haipo kila Mkoa na kwamba hizibenki nyingine ni za kibiashara, anataka kujua mikakati yaSerikali kama iko tayari kudhamini mikopo hii.

Mheshimiwa Spika, kwanza Serikali tupo tayari natulishaanza na ndiyo maana kama alivyosema Benki yaMaendeleo ya Kilimo haipo kila Mkoa, ni kwa sababu hii ni

Page 22: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

Benki ya Maendeleo, ni benki ya kimkakati na lengo lake nikuwasaidia wakulima kupitia madirisha mbalimbali ya Taasisiza Fedha.

Moja, tulichokifanya, Serikali kupitia Benki yaMaendeleo ya Kilimo tumedhamini mikopo yote ambayoinayotolewa na Benki ya NMB ili kwenda kwenye Sekta yaKilimo hususan pamoja na akina mama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili kwamba ni lini Serikaliitatengeneza mazingira ya mbegu hizi zikapatikana katikangazi za Kata ili wanawake wazipate kiurahisi?

Mheshimiwa Spika na Mheshimiwa Mbunge, nikwamba Serikali siku zote kwamba tuko tayari. Mbegu hizikupitia Shirika letu la Mbegu (ASA) na Taasisi nyingine binafsina mawakala mbalimbali, tumeweka mazingira mazurikwamba mbegu hizi zinapatikana Tanzania kote, siyo kwakwenye Kata tu, mpaka ngazi za vijiji kwa kuzingatia mahitaji.Kama kuna mahitaji maalum katika eneo unalotoka, baadaya Bunge hili tuone ili tuwaelekeze wenzetu wa ASA ili wawezekupeleka mbegu haraka iwezekanavyo ziwafikie wakulima.

SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Mlinga.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Ukiacha Taasisi nyingi kutoa mikopo kwavikundi vya wanawake lakini Benki ya Kilimo ndiyo yenyedhamana ya kutoa mikopo. Benki ya Kilimo imekuwa na tabiaya ubaguzi, inatoa mikopo kwa wale wanawake ambaowana uwezo au wake za vigogo, lakini wale wanawakeambao wana uwezo mdogo na wamejiunga kwenye vikundiwamekuwa wakipewa masharti magumu.

Je, Serikali inatoa kauli gani hususan kwa wanawakewa Ulanga, Kilimanjaro na juzi nilikuwa Mbeya kule, hamnahata mmoja aliyepata mkopo?

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu ya tuhumahiyo nzito, tafadhali.

Page 23: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Spika, nashukuru. Napenda kujibu swali moja lanyongeza la Mheshimiwa Mlinga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza siyo kweli kama Serikalikupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo tunatoa mikopo kwakibaguzi. Hii kama nilivyosema ni benki ya maendeleo, ni benkiya kimakakati na tumeianzisha maalum kwa ajil i yakuendeleza sekta ya kilimo hapa nchini. Kwa hiyo hizi ni pesaza umma, kama pesa za umma lazima zina taratibu zake nazina masharti. Labda hao wanaoona wanapata maana yakeni wanawake waliotimiza vigezo vinavyohitajika na benki iliwaweze kupata mikopo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo niendelee kumshaurikama nilivyosema kwenye jibu letu la msingi, tumewaelekezawanawake hao hususani wale wa vijijini wajiunge kwenyevikundi, vile vikundi vyao ndiyo vitatumika kama dhamanana benki hii itaendelea kutoa mikopo. Hivi ninavyozungumza,pamoja na maelekezo ya Serikali tuliwaambia kwambamikopo wanayotoa asilimia 20 watoe kwa akinamama, lakinibenki hii imeweza kutoa mpaka leo tunavyozungumzia zaidiya asilimia 33 ya mikopo yote waliyotoa imekwenda kwaakinamama.

SPIKA: Mheshimiwa Mwambe nilikuona tafadhali.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kwenyeWizara ya Kilimo. Serikali kupitia Wizara ya Kilimo mwaka juziwalianzisha utaratibu wa kwamba zao la korosho lilimwekatika kila mkoa hapa Tanzania kwenye mikoa 17. Wakatiwa uhamasishaji huo, wakawahamasisha pia akinamamawengi sana kwenye Wilaya ya Masasi, Wilaya ya Tandahimbaikiwemo pamoja na Newala, Lulindi pamoja na Ruangwawakope pesa kwenye mabenki lakini pia walikopeshwa pesapamoja na Halmashauri. Sasa bahati mbya sana mpaka sasahivi Serikali haijalipa pesa hizo za hao akinamama nawameanza kutaifishwa, kufilisiwa na wanashindwa kufanyashughuli zao na hapa tunasema tunataka tuwawezeshe

Page 24: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

akinamama. Sasa nataka tusikie kauli ya Serikali, je, ni liniwatawalipa akinamama hao waliozalisha miche iliyopelekwamikoa mingine 17 pesa zao?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu WaziriKilimo.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Spika, nashukuru. Napenda kujibu swali moja lanyongeza la Mheshimiwa Mwambe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza ni kweli Serikali miaka yotetuna mradi wa kuongeza uzalishaji wa korosho hapa nchinikutoka tani 300,000 za sasa kwenda tani milioni moja ndaniya miaka mitano ijayo.

Kwa hiyo miongoni mwa miradi hiyo lazima tulikuwatuongeze eneo la uzalishaji na moja ya mikakati ilikuwakwamba kuzalisha miche zaidi ya milioni 10 kwa kila mwakakwa muda wa miaka hiyo mitatu. Pia ni kweli kwamba michehii ilizalishwa kwa vikundi mbalimbali vya akinamama navijana, lakini baada ya kupitia yale madeni, tumegunduakwamba kuna kasoro nyingi katika yale madeni.

Mheshimiwa Spika, kama ninavyosema siku zotekwamba hizi ni pesa za umma, kama Serikali tuliona ni busarakwamba tufanye uhakiki wa kina ili tujue, tubainishe nakutambua yapi madai halali na yapi madai yaliyopikwa iliwale halali waweze kulipwa. Niendelee kumsihi tuMheshimiwa Mwambe na wengine wote waendelee kuvutasubira, jambo hili karibu linafika mwisho, timu ya uchunguziiko katika hatua za mwisho kumaliza, tukimaliza hela zipo natutawalipa wote waliozalisha miche hii.

SPIKA: Sijui utaratibu huo utaendelea auhautaendelea. Mheshimiwa Mama Sitta.

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, ahsantekwa kunipa nafasi na mimi niulize swali la nyongeza kamaifuatavyo:-

Page 25: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

Mheshimiwa Spika, moja ya changamotowanayoipata wakulima wakiwemo Wanawake hasawanaolima tumbaku ni upatikanaji wa pembejeo kwa wakatihususan mbolea aina ya NPK.

Je, Serikali inawahakikishiaje wakulima wa tumbakukwamba watapata mbolea ya NPK kabla ya mwezi wa Nanemwaka huu?

SPIKA: Majibu ya swali hilo muhimu sana la mboleaya NPK.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Spika, nashukuru. Napenda kujibu swali moja lanyongeza la Mheshimiwa Sitta kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli yaani mwaka jana mboleazilichelewa kufika kwa wakulima na sababu ndiyo mwakawa kwanza ambao tulikuwa tunatekeleza ule mfumo wa bulkprocurement (uagizaji wa mbolea kwa pamoja) na kituchochote kikiwa cha kwanza lazima kina changamoto zake.Tumeona hizo changamoto, lakini mwaka huu ambaomchakato wa kufahamu kiwango cha uzalishaji na mahitajiya mbolea tumeshakifanya mapema na tayari sasa hivi watutuko kwenye mchakato wa kupata Mawakala wa kuagizahizo mbolea na vyama vyenyewe tumevipa ruhusa yakuagiza. Kwa hiyo, hilo tatizo mwaka huu halitakuwepo nambolea zitafika kwa wakati kwa wakulima wa tumbaku nahasa akinamama wa Tabora.

SPIKA: Nashukuru. Sasa tuendelee na Wizara yaNishati. Swali la Mheshimiwa Daimu Idd Mpakate, Mbungewa Tunduru Kusini. Mheshimiwa Mpakate uliza swali lako.

Na. 192

Umeme wa REA Katika Vijiji 61- Tunduru Kusini

MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza:-

Page 26: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

Jimbo la Tunduru Kusini lina jumla ya vijiji 65, kati yahivyo ni vijiji vinne tu ndiyo vimefikiwa na umeme wa REAAwamu ya I na ya II:-

Je, ni lini Serikali itapeleka umeme wa REA katika vijiji61 vilivyobaki?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziriwa Nishati, Mheshimiwa Subira Mgalu tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati,napenda kujibu swali la Mheshimiwa Daimu Idd Mpakate,Mbunge wa Tunduru Kusini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa NishatiVijijini (REA) inatekeleza miradi ya kusambaza umeme katikavijiji vyote nchini. Jimbo la Tunduru Kusini lina vijiji 65, kati yavijiji hivyo Vijiji vinne vya Azimio, Chiwana, Mkandu na Mbesandivyo vimekwishapata umeme kupitia mradi wa REA II naVijiji vingine vinne vya Mchuluka, Umoja, Masalau na Msinjivinatarajiwa kupatiwa umeme kupitia mradi wa REA IIImzunguko wa kwanza unaoendelea na unaotegemeakukamilika mwezi Juni, 2020.

Mheshimiwa Spika, kazi ya kupeleka umeme katikaJimbo la Tunduru Kusini inahusisha ujenzi wa njia ya umemewa msongo wa kilovolt 33 yenye urefu wa kilometa 9.4, ujenziwa njia ya msongo wa umeme wa kilovolts 0.4 yenye urefuwa kilometa nane, ufungaji wa transfoma nne za KVA 50pamoja na kuwaunganishia umeme wateja wa awali 275.Gharama za kupeleka umeme katika vijiji hivyo ni shilingimilioni 644.

Mheshimiwa Spoika, vijiji 57 vya Kata za Chiwana,Mchuluka, Mtina, Nalasi, Mchoteka, Ligoma, Tuwemacho naLukumbulu vitapatiwa umeme kupitia Mradi wa REA Awamuya III, mzunguko wa pili unaotarajiwa kuanza mwezi Julai, 2019na kukamilika mwezi Juni, 2021. ahsante.

Page 27: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

SPIKA: Mheshimiwa Mpakate tafadhali, nimekuonaswali la nyongeza.

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Spika, ahsantekwa kunipa fursa ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.Katika Vijiji alivyovitaja kuwa vilipata umeme awamu yakwanza na ya pili vya Azimio, Chiwana, Mkandu na Mbesaumeme ulipita barabarani ndani ya mita 100 kutoka barabarakuu ilikopita nguzo kubwa. Je, ni lini mradi wa kujazilizia mitaailiyobaki katika Vijiji hivyo vya Azimio, Chwana, Mkandu naKijiji cha Airport itaanza?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, mwaka 2017 nilipelekamaombi maalum kuongeza vijiji katika Mradi wa REA katikaVijiji vya Tuwemacho, Chemchem, Ligoma, Makoteni, Nasia,Semeni, Mtina, Angalia, Nalasi, Mchoteka, Kitani, Mkololapamoja na Masakata. Nini kauli ya Serikali kuhusu uwekajiwa awamu ya tatu ya umeme katika Vijiji hivyo?

SPIKA: Majibu ya maswali hayo Mheshimiwa NaibuWaziri wa Nishati Mheshimiwa Subira Khamis Mgalu.Namwona Mheshimiwa Waziri amesimama, MheshimiwaWaziri, tafadhali.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kwanzanimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri yaswali la msingi la Mheshimiwa Mpakate, lakini vilevile nichukuenafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Mpakate jinsianavyofuatilia umeme katika Jimbo lake.

Mheshimiwa Spika, ni kweli vijiji vingi tuliviweka kwenyeround II ya awamu ya tatu inayoendelea, lakini baada yakuona changamoto kubwa sana katika Jimbo la TunduruKusini tulifanya mapitio mapya na vijiji 13 tuliviingiza kwenyeround inayoendelea. Kwa hiyo katika utaratibu tunaojengaline kwa sasa kutoka Tunduru Mjini mpaka Msingi umbali wakilometa 20 tumechukua vijiji vingine 13 vikiwemo vijijiambavyo anavisema vya Angalia, Semeni ambakoMheshimiwa Mbunge anatoka lakini mpaka Tuwemacho,Chemchem mpaka Chilundundu kwa vijiji vyote hivyo viko

Page 28: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

kwenye mpango. Pia Wakandarasi kupitia TANESCO sasawanavifanyia kazi, kwa hiyo nimpe tu taarifa MheshimiwaMbunge pamoja na kumpongeza, vijiji 13 vya nyongeza tayarivimeshaanza kufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu nyongezaya vijiji vya ujazilizi; mradi umeshaanza na utekelezaji wamaeneo ya kujaziliza, maeneo ya vitongoji unaanza mwezihuu utachukua miezi 12, lakini maeneo ya Azimio pamoja naMbesa ambako tayari umeme upo kwenye Vitongoji 17,tayari pia TANESCO wameanza kuvifanyia kazi.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri. Huu mradiwa kujazilizia ni muhimu mno maana yako maeneo yenyemakosa mengi mno yanahitaji kusahihishwa.

Nilikuona Mheshimiwa Monko, swali la nyongeza.

MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.Jimbo la Singida Kaskazini lina miradi ya REA II, REA III, phaseI pamoja na umeme wa backborne kwenye vijiji 54. Hadi sasani vijiji 13 tu ndiyo ambavyo vimekwishakufikiwa na umemena vingine mpaka sasa bado. Je, Mheshimiwa Waziri waNishati yuko tayari kuambatana nami kutembelea Jimbo laSingida Kaskazini kujionea changamoto zilizopo?

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Subira Mgalu ukotayari kwenda Singida Kaskazini?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika,napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Monkokama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Monko amerejea Mradi wa REA awamuya pili ambapo kwa kweli kama Serikali tuliwaomba radhiwakazi wa Mkoa wa Singida na Kilimanjaro baada ya makosaambayo yalitendeka katika Mradi wa REA awamu ya pili natukafanya kazi na kumweka Mkandarasi mpya ambayeanaendelea na kazi kwa kushirikiana na REA.

Page 29: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

Mheshimiwa Spika, swali lake ameulizia utayari wetuwa kuambatana naye; nataka nimthibitishie MheshimiwaMbunge nipo tayari mimi pamoja na Waziri kwa wakati tofuatikutembelea Jimbo lake kama ambavyo tulishafanya mweziwa Nane tulitemebelea Jimbo lake ikiwemo Kijiji cha IddiSimba na tuliwasha umeme pia aliwakilishwa na MheshimiwaMbunge Aisharose Matembe. Kwa hiyo Mheshimiwa Mbungeniko tayari muda wowote kutembelea eneo lake nakuendelea kuwasha umeme na kukagua kazi inavyoendelea.Ahsante sana.

SPIKA: Ahsante sana. Nawaona Waheshimiwamasuala ya umeme mnayo mengi, lakini niwaombe tutuvumiliane kidogo kwa sababu muda uliobakia ni mdogosana.

Tunaendelea na swali la Mheshimiwa Ester AmosBulaya, Mbunge wa Bunda Mjini, kwa niaba yakeMheshimiwa Esther Matiko, tafadhali muulizie.

Na. 193

Malipo ya Fidia Kwa Wananchi wa Kijiji cha Nyabeu,Wilaya ya Bunda

MHE. ESTHER N. MATIKO (K.n.y. MHE. ESTER A. BULAYA)aliuliza:-

TANESCO Mkoa wa Mara katika zoezi la kupelekaumeme vijijini walipitisha nguzo za umeme kwenye maeneoya watu katika Kijiji cha Nyabeu, Kata ya Guta na uthaminiulifanyika na iliahidi malipo kufanyika lakini hadi leohawajalipwa na badala yake wanaambiwa maeneo hayoni ya TANESCO:-

(a) Je, ni lini Serikali itawalipa wananchi hao fidiastahiki?

(b) Je, ni kwa nini TANESCO inamiliki maeneo kablaya kulipa fidia?

Page 30: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziriwa Nishati, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati,napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ester Amos Bulaya,Mbunge wa Bunda Mjini, lenye sehemu (a) na (b) kwapamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, miradi ya kupeleka umeme katikaWilaya za Serengeti, Bunda na Ukerewe ilitekelezwa kati yamwaka 2003 na 2006 chini ya ufadhili za Serikali za Swedenna Hispania kupitia Mashirika yake ya Kimataifa yaMaendeleo SIDA na Spanish Funding Agency pamoja naSerikali ya Tanzania. Kazi ya tathmini ya mali za wananchiwaliopisha mradi ilifanywa na Mtathmini Mkuu wa Serikali namalipo yalifanyika mwaka 2009. Ulipaji wa fidia hiyo ulifanyikakwa kuwashirikisha Watendaji wa Vijiji, Kata, Tarafa, Wilayana Mkoa kuridhia orodha ya wananchi waliostahili kulipwafidia hiyo. Jumla ya Sh.135,820,993 zililipwa kwa wananchiwaliopisha mradi huo ikiwa ni pamoja na wananchi wa Kijijicha Nyabeu.

Mheshimiwa Spika, TANESCO huchukua maeneobaada ya kufanya tathmini kupitia Mthamini Mkuu wa Serikalina kuwalipa wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi.

SPIKA: Mheshimiwa Esther Matiko, swali la nyongeza.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nashukuru.Kwa sasa tunajua kwamba tuna mradi wa REA ambao ndiyoumejielekeza kupeleka umeme vijijini. Katika Kijiji cha Sazirakatika Jimbo la Bunda Mjini ambalo lina Vitongoji vitatu chaNyamungu, Wisegere na Kinamo havijawahi kupitiwa namradi huu wa REA phase I, phase II na hata phase III. Sasaningependa kujua hawa wananchi wa Kijiji cha Sazira ni liniwatapatiwa umeme ili na wenyewe waweze kupata umemekatika shughuli zao za kimaendeleo?

Page 31: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

Mheshimiwa Spika, swali la pili; katika Mji wa Tarimepia tumepitiwa na umeme wa REA ambao unapita kwenyeaidha Kijiji sehemu ndogo tu au kata. Ningependa kujuamaeneo ambayo yana Taasisi kama sekondari, zahanati auvituo vya afya na shule ya msingi kama vile Kitale tuna Kijijicha Nkongole ambacho kina hizo Taasisi zote, KenyamanyoriSenta tuna Kibaga ambayo ina mgodi pale haijapitiwa naumeme wa REA. Ni lini sasa Serikali itahakikisha kwambainapeleka huu umeme wa REA kwenye yale maeneoambayo hayajaguswa kabisa na Mheshimiwa Naibu Wazirialiniahidi kwamba ungeweza kwenda Tarime kujihakikishiahayo maeneo ambayo kila siku nayauliza hapa? Ahsante.

SPIKA: Kwenda Tarime inabidi apate ruhusa yaMheshimiwa Waziri Mkuu maana kule Tarime ni Kandamaalum. Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaSpika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza yaMheshimiwa Esther Matiko, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza ameulizia Kijijicha Sazira ambacho kipo Bunda Mjini ambacho kina vitongojivitatu na hakina umeme. Kama ambavyo tumepata kujibumaswali hapa ya msingi kwamba mpango wa Serikali nikupeleka umeme vijiji vyote. Kwa sasa tuna mradi huuunaoendelea wa REA awamu ya tatu ambao unahusisha vijiji3,559 lakini ukichanganya na miradi mingine yote ya Ujazilizi,BTIP tunatarajia kufikisha umeme ifikapo Julai, 2020 kwa vijiji9,299.

Kwa hiyo kijiji ambacho amekitaja kwenye Wilaya yaBunda Mjini hapo vipo katika mpango wa REA awamu yatatu, mzunguko wa pili ambao utaanza Julai, 2019 nakukamilika 2021. Kwa hiyo niwatoe hofu tu wananchi wotenchi nzima, mpango wa Serikali ya Awamu ya Tano nikupeleka umeme katika vijiji vyote nchi nzima.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ameulizia suala laJimbo lake la Tarime; ni kweli niliahidi kutembelea Jimbo hilo

Page 32: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

kama utaratibu wetu ndani ya Wizara, lakini nitazingatiaangalizo lako kwamba kwa ruhusa ya Mheshimiwa WaziriMkuu, lakini nimtoe hofu tu Mheshimiwa Esther kwamba katikamaeneo ambayo ameyataja na hasa Taasisi za Umma,Wizara imetoa maelekezo mahususi na naendelea kurejeahayo maelekezo kwamba Taasisi za umma ni moja yakipaumbele katika kuzipelekea umeme iwe shule ya msingi,sekondari, kituo cha afya au miradi ya maji.

Kwa hiyo naomba niwaelekeze Wakandarasikuzingatia maelekezo hayo na Mameneja wote wa TANESCOna wasimamizi wa miradi hii ya REA kwamba umemeufikishwe kwenye Taasisi za Umma ili kuboresha utoaji wahuduma ambazo zinatokana na hizo Taasisi za umma.

Mheshimiwa Spika, katika haya maeneo aliyoyasemaMheshimiwa kwanza mojawapo lipo katika REA awamu yatatu, mradi unaoendelea na Mkandrasi Derm yupo,anaendelea vizuri na ni moja wa Wakandarasi ambao kwakweli wanafanya kazi vizuri na nimhakikishie tu mpaka Juni,2019 hii miradi itakuwa imekamilika. Ahsante.

SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea na Wizara ya Maji,swali la Mheshimiwa Peter Ambrose Lijualikali, tafadhali ulizaswali lako.

Na.194

Kufuta Kodi za Vifaa vya Kusambaza Maji

MHE. PETER A. LIJUALIKALI aliuliza:-

Je, kwa nini Serikali isifute kodi kwenye vifaa vyakusambazia maji kutokana na matatizo ya maji tuliyonayokatika Taifa letu?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu WaziriJumaa Hamidu Awesu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Page 33: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji,naomba kujibu swali la Mheshimiwa Peter Ambrose Lijualikali,Mbunge wa Jimbo la Kilombero, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tarehe 12 Septemba, 2017, Bungelako Tukufu lilipitisha marekebisho ya Sheria mbalimbaliikiwemo Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, Sura ya148. Marekebisho ya Sheria hiyo ya VAT yalihusisha vifunguvya 6 na 7 pamoja na aya ya 9 ya sehemu ya pili ya Jedwalila Sheria ya VAT ambayo vina lengo la kupunguza gharamaza utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuongeza tija yamatumizi ya fedha za umma na kuhakikisha miradiinayotekelezwa kwa fedha za Serikali na za washirika wamaendeleo inakamilika kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Maji tayariimeshasambaza Waraka wa Hazina namba sita uliotolewana Wizara ya Fedha na Mipango kuhusu utaratibu wa kutoamsamaha wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa miradiya maji itakayotekelezwa kote nchini. Ni wajibu kwa MaafisaMasuuli wote kuzingatia utaratibu ulioainishwa na Serikalikatika misamaha ya kodi kwa vifaa vya kusambazia maji ilimiradi yetu ya maji ikamilike kwa wakati.

SPIKA: Mheshimiwa Lijualikali.

MHE. PETER A. P. LIJUALIKALI: Mheshimiwa Spika,nafahamu Serikali imetoa msamaha wa kodi kwenye miradiyake lakini natamani nifahamu ni kwa nini sasa miradi ya watubinafsi wanaofanya kazi hii wenyewe hawapati misamaha?Maana yangu ni kwa nini kwenye vifaa vingine watuwanaofanya kazi hizi hawapati misamaha ya kodi ili kusaidiaSerikali kupeleka huduma hii? Msamaha huu ungekuwainclusive yaani usiwe tu kwa watu wanaofanya kazi Serikalipeke yake. Kwa hiyo, napenda kufahamu ni kwa nini watuwengine pia hawapati misamaha huo?

Mheshimiwa Spika, pia naomba nifahamu kamaMheshimiwa Waziri atakubali kwenda nami sambambakwenye Jimbo langu hasa kwenye Kata za Kipangalala na

Page 34: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

Kibaoni ambako kuna miradi mikubwa ya maji ya takribanishilingi milioni 600 lakini ni kama vile imesimama na fedha hizini kama zimelala. Kwa hiyo, naomba nifahamu commitmentya Mheshimiwa Naibu Waziri kwa sababu anafahamu hayamambo nilishakaa naye ofisini kwake na kuzungumza kwakirefu.

Kwa hiyo, naomba nijue kama yuko tayari twendeJimboni kwangu ili tukaone nini shida na tupate majibukwenye mambo haya. Nashukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa NaibuWaziri, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaSpika, kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza MheshimiwaMbunge kwa swali lake zuri lakini kubwa sisi kama Wizara yaMaji lengo letu na nia ya Mheshimiwa Rais ni kumtua mwanamama ndoo kichwani na kuhakikisha Watanzania waishiomijini na vijijini wanapata maji safi salama na yenyekuwatosheleza. Kwa mazingatio na ushauri wako niseme tukwamba tumepokea ushauri na tutaufanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la commitment yamimi kuongozana naye katika Jimbo lake, MheshimiwaLijualikali mimi sina kikwazo chochote, nipo tayari kuhakikishatunakagua miradi ya maji. Ahsante sana.

SPIKA: Mheshimiwa Asha Mshimba Jechauliza swalilako la mifugo na uvuvi.

Na. 195

Kufaidika na Ukanda wa Bahari na Maziwa

MHE. ASHA MSHIMBA JECHA aliuliza:-

Tanzania imebarikiwa kuwa na Ukanda wa Bahari naMaziwa.

Page 35: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

Je, wananchi wa maeneo hayo wameandaliwajekufaidika na rasilimali zinazopatikana katika Ukanda waBahari na Maziwa?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Naibu Waziri Mifugo naUvuvi, Mheshimiwa Ulega, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziriwa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa AshaMshimba Jecha, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, sekta ya uvuvi nchini inasimiwa nasera, sheria pamoja na miongozo mbalimbali iliyoandaliwakwa lengo la kuhakikishwa wananchi na Taifa linanufaika narasilimali za uvuvi. Pia Sera ya Uvuvi inaelekeza ushirikishwajiwa wananchi katika kusimamia rasilimali za uvuvi ambapovimeanzishwa vikundi vya usimamizi shirikishi wa rasilimali zauvuvi kwa maana ya BMU. Vikundi hivi vinalengakuwawezesha wananchi katika maeneo vilipoanzishwa kuwawanufaikaji wa kwanza wa rasilimali hizi kwa kuwapatiamafunzo mbalimbali ya uvuvi endelevu.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanzisha Wakala waMafunzo ya Uvuvi ili kuwapatia elimu vijana wa Kitanzaniakuhusu masuala ya uvuvi ili nchi inufaike na rasilimali za uvuvitulizojaliwa. Pia, Serikali imeanzisha Taasisi ya Utafiti yaaniTAFIRI ili kufanya tafiti na kuvumbua teknolojia zitakazosaidiakuleta tija kwenye tasnia ya uvuvi. Taasisi hizi husaidiakuwapatia elimu na maarifa wadau wa uvuvi.

Mheshimiwa Spika, vilevile Wizara ina mikakatimbalimbali inayolenga kuleta maendeleo katika sekta yauvuvi na kuwasaidia wavuvi ambayo ni pamoja na:-

(i) Kuendelea kutoa elimu kwa wavuvi na wadau wotekuhusu uvuvi endelevu, sera, sheria na kanuni za uvuvi ilikulinda, kusimamia, kuhifadhi na kuendeleza rasilimali za uvuvinchini kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo;

Page 36: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

(ii) Kuwekeza katika uvuvi wa bahari kuu kwa kufufuaShirika la Uvuvi (TAFICO), kujenga bandari ya uvuvi, kununuameli mbili kubwa za uvuvi ili kuchochea ukuaji wa viwandavya kuchakata samaki, kuongeza thamani ya mazao, ajirana kuongeza mapato ya Serikali; na

(iii) Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wavuvi kuhusuukuzaji wa viumbe katika maji yaani aquaculture na ufugajisamaki kwenye vizimba kwa lengo la kuongeza uzalishaji wasamaki kwenye maziwa na baharini.

Mheshimiwa Spika, Wizara imeanzisha Dawati la SektaBinafsi ili kuwasaidia wavuvi kutatua changamoto mbalimbalizinazowakabili ikiwemo kupata mikopo kutoka kwenye taasisiza fedha.

SPIKA: Mheshimiwa Asha nimekuona, uliza swali lako.

MHE. ASHA MSHIMBA JECHA: Mheshimiwa Spika,pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, nina sualamoja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mipango mizuri yaSerikali lakini bado wavuvi wana hali ngumu, uduni wa vifaa,utaalam na kadhalika. Je, ni lini Serikali itaanzisha vyuo vyauvuvi vingine kwa sababu navyofahamu chuo kilichopo nikimoja tu lakini hata wahitimu wake hawapati nafasi yakuajiriwa pamoja na kwamba tumezungukwa na ukandamkubwa wa bahari na maziwa. Je, Serikali ina mikakati ganiya kuwatumia wataalam wanaomaliza katika chuo hicholakini pia kuanzisha vyuo vingine kwa lengo la kuwanyanyuawavuvi ili waweze kuwa na tija na bahari na maziwa?Ahsante. (Makofi)

SPIKA: Majibu ya maswali hayo mazuri kabisa, NaibuWaziri Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Abdallah Ulega,tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaSpika, naomba kujibu maswali mawili mazuri sana ya

Page 37: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

nyongeza ya Mama yangu Mheshimiwa Asha MshimbaJecha, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali tunao mpango wakuhakikisha tunafungua vyuo vingine. Hapa karibunitumefungua chuo cha uvuvi katika Mikoa ya Kusini kwamaana ya Mtwara Mikindani, Chuo cha FETA ambachokinafanya kazi ya kutoa elimu. Mipango mingine ya Serikalini pamoja na kuboresha chuo chetu kilichopo pale Panganimaarufu kama KIM kwa kushirikiana na Taasisi ya Chuo Kikuucha Dar es Salaam na Halmashauri ya Pangani kwa lengo lakuhakikisha wananchi hasa vijana walio wengi wa maeneohaya ya ukanda wa bahari wanapata elimu. Kwa upandewa Ziwa Victoria chuo chetu kilichopo katika Wilaya ya Roryapale Gabimori na chenyewe tunakwenda kukiongezeanguvu ili kusudi kitoa elimu zaidi kwa wananchi wengi wamaeneo haya.

Mheshimiwa Spika, swali la pili ameuliza mipango yetutuliyonayo ya kuhakikisha wale wataalam wanaotoka katikavyuo hivi wanakwenda kupata kazi na kuisaidia jamii yetu.Katika majibu yangu ya msingi nimeeleza kuwa Serikali inaompango wa kufufua Shirika letu la Uvuvi la TAFICO na tayaritumeshalifufua, hivi sasa tunakwenda katika hatua yakununua meli. Tayari tumepata msaada kwa maana yagrants kutoka Serikali ya Japan wa takribani bilioni nneambazo tunakwenda kununua meli na kutengenezamiundombinu ya kuhifadhia samaki katika eneo la ukandawa pwani. Hii ni chachu kwa ajili ya kuhakikisha kwamba walewengi wenye utaalam wataajiriwa na mashirika haya.

Vilevile tunao mpango wa kuhakikisha wanajiajiri waowenyewe kwa kufanya kazi za uvuvi endelevu wa kisasa navilevile ufugaji wa samaki.

SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Dau, uliza swali lako.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Napenda kumuuliza Mheshimiwa Naibu Wazirini lini Serikali sasa itahakikisha kwamba bandari ya uvuvi

Page 38: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

inajengwa ili fursa ya uvuvi wa bahari kuu iweze kutumikavizuri sana? Ahsante.

SPIKA: Majibu ya swali hilo muhimu kutoka kwaMbunge wa Mafia, Mheshimiwa Dau, bandari ya uvuvi.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaSpika, naomba kujibu swali la nyongeza la ndugu yanguMbunge wa Mafia, jirani yangu, Mheshimiwa MbarakaKitwana Dau, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni lini bandari itajengwa. Hivi sasatuko katika kumalizia mchakato wa upembuzi yakinifu waeneo itakapokwenda kujengwa bandari ya uvuvi. Tayarimkandarasi huyu kupitia pesa zetu wenyewe, pesa za ndanitumeshamlipa na anamalizia kazi ya kutuelekeza mahali ganikatika ukanda wetu wa pwani tutakwenda kujenga bandariya uvuvi.

Mheshimiwa Spika, habari njema zaidi, nadhani wotetumemsikia Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa katikaMei Mosi pale Mbeya ameeleza juu ya nia njema ya nchirafiki ya Korea ambapo wameonesha nia ya kutakakushirikiana nasi katika kwenda kujenga bandari hii ya uvuvi.

Naomba niwahakikishie Waheshimiwa Wabungewote na Watanzania kwa ujumla kwamba nia yetu hiiitakwenda kutimia na hatimaye kuweza kupata faida yauvuvi katika eneo la bahari kuu.

SPIKA: Ahsante sana Waheshimiwa Wabunge,tuendelee na matangazo.

Naomba niwatambulishe wageni 20 wa MheshimiwaSpika ambao ni wanachana wa Chama cha Wanasayansiwa Maabara za Afya hapa nchini wakiongozwa na Rais waChama hicho Ndugu Yahya Mnung’a. Wanamaabarakaribuni sana wageni wetu hapa Bungeni. (Makofi)

Page 39: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

Wamekuwa na maonesho yao pale Nyerere Square,Waheshimiwa Wabunge tunakaribishwa kushiriki pale tujifunzemambo mbalimbali na advancement ya masuala yamaabara za afya hapa Tanzania. Tukipita mjini katikati paletupitie pale Nyerere Square tuone shughuli zao zinazoendeleapale. Ahsante sana ndugu zangu wa maabara. (Makofi)

Wageni wa Waheshimiwa Wabunge ni pamoja namgeni wa Mheshimiwa Japhet Ngailonga Hasunga, Waziriwa Kilimo ambaye ni mpiga kura wake kutoka VwawaMkoani Songwe, Ndugu Agripa Mwashambwa. Karibu sanaAgripa. (Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa Mwita Waitara, Naibu Waziriwa TAMISEMI ambaye ni Mbunge Mstaafu kutoka RoryaMkoani Mara, Ndugu Gregori Mogendi. Karibu sana MbungeMstaafu Mogendi. (Makofi)

Wageni wanne wa Waheshimiwa Jumaa Aweso,Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambao ni ndugu zakekutoka Dar es Salaam na Tanga wakiongozwa na msaniiNdugu Thadei Onesmo. Sina hakiki kama na Ndugu NurdinAlly naye yupo, kama yupo karibuni sana, msanii maarufuhuyo. Ahsante sana. (Makofi)

Wageni 61 wa Mheshimiwa Cosato Chumi ambao niwanafunzi 57 na walimu wanne wa Real Hope SecondarySchool kutoka Mafinga Mkoani Iringa wakiongozwa naMkurugenzi wa shule hiyo Ndugu Dickson Mwipopo. Aisee,hii shule ya Hope Mafinga inaelekea ni moja ya shule nzurisana. Naona vijana mko smart kabisa. Hongereni sana nakaribuni sana hapa Bungeni. (Makofi)

Kwa kweli haishangazi kuona Iringa kule kuna shulenzuri namna hii, kabisa. Maana nil ikuwa namuonaMheshimiwa Lukuvi leo, Mheshimiwa Cosato Chumi naWabunge wengine wa Mkoa wa Iringa tumekutana naoasubuhi wananisalimia wanasema Kamwene, Kamwene,nikasema nini tena? Nikaelewa tu ni yale mambo yale, Iringabwana hakuna mchezo. Kama hamuamini Iringa wako moto

Page 40: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

waulizeni Yanga. Yanga bwana, sijui baridi ya Iringainawafanyaje? (Makofi/Kicheko)

Wageni 30 wa Mheshimiwa Rose Tweve ambao niwanakwaya wa Tanzania Assemblies of God kutoka JijiniDodoma wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kwaya hiyo NduguHappy Mwajunga. Karibuni sana kutoka TAG Dodoma.(Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa John Kadutu ambaye ni mtotowake kutoka Jijini Dar es Salaam, Ndugu Peter Kadutu. Karibusana. (Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa Zuberi Kuchauka ambaye nimpwa wake kutoka Mang’ula Mkoani Morogoro, NduguMikidadi Kilwanda. Karibu Mikidadi. (Makofi)

Wageni watatu wa Mheshimiwa Profesa AnnaTibaijuka ambao ni Maafisa wa Umoja wa Mataifa kutokaGeneva Uswisi, Eng. Wilhelmina Malima, Dkt. Simon Msukwana Eng. Upendo Kimaro. Wale pale karibuni sana kutoka hukoGeneva. (Makofi)

Wageni wawili wa Mheshimiwa Esther Matiko ambaoni wapiga kura wake kutoka Tarime, Ndugu John Magangana Ndugu Saimon Chacha. Karibuni sana wageni kutokaIsiebania huko. (Makofi)

Wageni 10 wa Mheshimiwa Kassim Jamal ambao niwadau wa afya ya uzazi wa mpango na afya kwa ujumlakutoka Jijini Dar es Salaam wakiongozwa na Ndugu SalvatoryHokororo. Karibu sana Hokororo. (Makofi)

Wageni waliopo Bungeni kwa ajili ya mafunzo niwanafunzi 22 na walimu wanne kutoka Shule ya Awali naMsingi ya Aglam iliyopo Wilayani Mpwapwa, Mkoa waDodoma ambao wamelitembelea Bunge kujifunza jinsilinavyofanya kazi zake. Wale wa kutoka Mpwapwa, karibunisana na Mbunge wenu Mheshimiwa Lubeleje yuko hapa.(Makofi)

Page 41: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

Wale msiofahamu Mpwapwa ni Kiswahili lakini jinalenyewe kabisa panaitwa Mhanvwa. Kwa hiyo, karibuni sanawageni wetu kutoka Mhanvwa. (Makofi/Kicheko)

Wageni wanne kutoka Benki ya CRDB, tawi laDodoma ambao ni Mameneja Mahusiano kuhusiana nawateja maalum wakiongozwa na Meneja wetu maarufuAgusta Mfuru. CRDB pale mlipo karibuni sana, ahsante sana.(Makofi/Vigelegele)

CRDB makofi hayo ni kwa ajili ya Grace kwa hudumazako nzuri. Tunaomba timu iliyotoka Makao Makuu mpelekesalamu za Wabunge kwa uongozi wa CRDB kwa kazi nzurianayofanya Grace. Anastahili kupandishwa cheo, nimfanyakazi bora kwa makofi haya. (Makofi/Vigelegele)

Pia Grace anawataarifu kwamba credit cards mpyaza CRDB mpitie kule muweze kuzipata. Za hivi sasa ni matatakabisa. Kwa hiyo, mpitie huko muweze kuchukua kadi zenu.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, nina matangazo mawili,tangazo la kwanza, baadhi yetu hatuko makini kidogo namatumizi ya bendera za Wabunge, zile zinazopepea kwenyemagari. Yamepatikana baadhi ya magari yakipuyanga hukomikoani yana bendera ya Mbunge lakini hata Mbungemwenyewe hayupmo ndani ya gari. Sasa vitu hivyo vinawezakukuletea matatizo tu bure, matumizi ya bendera yanaendakisheria na yana taratibu zake. Hilo gari lako linawezakupatikana na magendo huko na lina bendera yakolikakuharibia kabisa mfumo na mpangilio wako wa maisha.Kwa hiyo, naomba tuwe makini sana na matumizi ya benderahizo.

Waheshimiwa Wabunge, lakini bendera zinginezinatundikwa kwenye magari ambayo hayana hata hadhi,kule Afrika Kusini wanaita Skorokoro. Wewe gari mkwecheina bendera ya Mbunge, kweli, si uache tu kwani kuna hsidagani? Wewe mwenyewe umekaa pale kigari kinakwendahakieleweki na hasa rafiki zangu fulani sitaki kuwataja. Kwa

Page 42: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

hiyo, tujitahidi bendera iende na hadhi yako mwenyewe nachombo chenyewe pia, tuangalie jambo hili ni muhimu sana.(Makofi/kicheko)

Pia nina tangazo la Mheshimiwa Shally JosephaRaymond, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu ThomasMoore hapa Bungeni, anasema leo Jumatano tarehe 8 Meikutakuwa na Ibada ya Misa ya Wakristo Wakatoliki marabaada ya kuahirisha shughuli za Bunge saa 7.00 mchana palePius Msekwa, ghorofa ya pili ambapo huwa mnakutana.Mnaopenda kwenda kwenye Ibada hiyo basi mfanye hivyo.Leo Jumatano Wakatoliki Msekwa, ghorofa ya pili muwezekukutana.

Baada ya matangazo haya, naomba sasa nimpisheMheshimiwa Naibu Spika ili aweze kuendelea na ratiba zilizokohapa mezani.

Hapa Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alikalia Kiti

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tutaendelea.

Katibu!

NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka

wa Fedha 2019/2020

(Majadiliano Yanaendelea)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaendeleana majadiliano. Tutaanza na Mheshimiwa George MalimaLubeleje, atafuatiwa na Mheshimiwa Profesa Anna Tibaijuka,Mheshimiwa Anna Gidarya ajiandae.

Page 43: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi, ili niweze kuchangia hoja yaWizara ya Afya. Kwanza nimpongeze sana MheshimiwaWaziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu pamoja na watendaji wotewa Wizara hii kwa kazi nzuri wanayoifanya katika nchi hii yakutoa huduma za afya kwa Wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili naiunga mkono hojahii asilimia 100. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza ni ujenzi wazahanati pamoja na Vituo vya Afya. wananchiwamehamasika wanajenga Vituo vya Afya, wanajengazahanati kila kijiji. Lakini changamoto kubwa ambayo tunayopamoja na ujenzi wa zahanati na Vituo vya Afyachangamoto ambayo inatukabili ni upungufu wa watumishiwa Idara ya Afya kada mbalimbali. Kwa hiyo, nilikuwanaishauri Serikali iongeze watumishi katika vituo vya afya,zahanati pamoja na hospitali za wilaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Afya ilikuwa nampango wa kujenga vyuo kwa ajili ya ku-train wahudumuwa afya, kwa mfano matabibu, hawa clinical officers pamojana tabibu wasaidizi (clinical assistants), sasa mpango huuuliishia wapi? Kwa sababu, ilikuwa ndio mikakati ya Wizarahii ili kuongeza watumishi katika vituo vya afya na zahanati.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ni kuhusu Bohariya Dawa – MSD. Bohari ya Dawa – MSD inafanya kazi nzurisana; Bohari ya Dawa ndiyo inayosambaza dawa nchi nzima,vituo vya afya, zahanati, hospitali za wilaya, hospitali zamikoa, hospitali za rufaa. Lakini pamoja na kuongeza fedhaza dawa katika bohari ya dawa bado changamoto hiyoinaikabili bohari ya dawa. Sasa Mheshimiwa Waziri je, mwakahuu mmeongeza fedha kiasi gani kwa ajili ya bohari ya dawakwa sababu, zahanati zinaongezeka, vituo vya afyavinaongezeka, lakini dawa ni zilezile? Sanduku moja la dawahalitoshi kwenye zahanati kwa sababu, sasa kuna ongezekokubwa sana la wananchi. kwa hiyo, je, mwaka huummeongeza fedha kiasi gani kwa ajili ya bohari ya dawa?

Page 44: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tatu, ni kuhusuvyuo vya maafisa afya. Mpwapwa kuna chuo cha maafisaafya, lakini chuo hiki hakijakarabatiwa, hakina vifaa vyakutosha, walimu ni wachache.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilikuwa naishauriSerikali kwamba, hivi vyuo vya afya vyote nchini naombaMheshimiwa Waziri hawa maafisa wa afya vilevile niwatumishi katika idara yako, lakini vyuo hivi sijui Wizara yaafya kama mnaviangalia kwa kweli, kwa sababu hii kada yamaafisa afya ni muhimu sana na hawa ndio wanashughulikiahasa zaidi afya, kinga na ndio wanaopambana namagonjwa ya kuambukiza.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sasa vyuo hivi naombasana Mheshimiwa, kwanza bajeti mnayovitengea ni kidogosana, halafu vifaa havitoshi, walimu hawatoshi, majengohayafanyiwi ukarabati, kwa hiyo, nil ikuwa nashauriMheshimiwa Waziri uviangalie kwa huruma vituo hivi vyamaafisa afya, na bahati nzuri mimi ni afisa afya mstaafu kwahiyo, kada hii naifahamu vizuri sana. Hawa ndiowanaopambana na magonjwa ya kuambukiza, kutoa elimuya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeona kwenye hotubayako umeelezea mambo ya elimu ya afya kwa umma (HealthEducation), elimu ya afya ni muhimu kweli. Katika Wizara yaAfya tuna kinga na tiba, sasa tunasema kinga ni bora kulikotiba kwa sababu, kinga ni gharama ndogo, lakini tiba nigharama kubwa. Kwa hiyo, nadhani kada hii ni muhimu sanaMheshimiwa Waziri ungeiangalia kwa huruma zaidi, ili wawezekupata maslahi ya kutosha, vyuo hivi mdahili wanafunzi wakutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo jingine ni upungufuwa watumishi katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa.Mheshimiwa Waziri, Wilaya ya Mpwapwa ni kubwa, inawananchi zaidi ya 400,000 na tuna vituo vingi kamanilivyosema, lakini tuna upungufu wa watumishi kama 450 wakada mbalimbali za afya. Kwa hiyo, nilikuwa naomba sana

Page 45: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

Idara ya Utumishi, Wizara ya Utumishi, tukiomba tukipelekamaombi yetu pale kutaka watumishi tunapata watumishi 6,tunapata watumishi 10, lakini tuna upungufu wa watumishizaidi ya 450 kwa hiyo, tulikuwa tunaomba watumishiwaongezewe katika Hospitali hii ya Wilaya ya Mpwapwa.

NAIBU SPIKA: Asante sana Mheshimiwa, kengele yapili imeshagonga. Waheshimiwa Wabunge, ili muwezekujipanga vizuri wachangiaji wote wa CCM wanachangiakwa dakika 7 kila mmoja anayeitwa. Na wachangiaji waChama cha Demokrasia na Maendeleo wanachangia kwadakika kumi, kumi wachangiaji wa Chama cha Wananchi –CUF wanachangia kwa dakika tano kila anayeitwa.

Mheshimiwa Profesa Anna Tibaijuka, atafuatiwa naMheshimiwa Anna Gidarya, Mheshimiwa Selemani Zediajiandae.

MHE. PROF. ANNA K. TIBAIJUKA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana kwa kunipa nfasi. Naomba nianze kabisakuungana na Taifa kwa ujumla katika simanzi kubwailiyotukuta kuondokewa na mojawapo ya Mtanzania maarufualiyefanya mambo mengi, Dkt. Reginald Abrahamu Mengi.Nachukua nafasi hii kutoa pole sana kwa wanafamilia napia kumshukuru sana kwa msaada wake alioutoa kwa watumbalimbali, hususan kwa sisi ambao tunashughulikia elimubora kwa wasichana ambao hawana uwezo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mengi alikuwani mtu mkarimu na waswahili wanasema kutoa ni moyo sioutajiri. Kwa hiyo, tunaomba sana familia yake iyachukuekama yalivyokuja na Mwenyezi Mungu ampe pumziko lamilele.

Mheshimiwa Naibu Spika, sina budi kusema kwamba,pigo kubwa kwa sababu, siku kadhaa zilizopita wakatiMarehemu Ruge Mutahaba amefariki, pia na EphraimKibonde wote tulikuwa katika chumba kimoja pale Karimjee,lakini hizo ndizo njia za Mwenyezi Mungu ni pigo kubwa kwaTaifa. Na ninasimama hapa kwa majonzi makubwa leo, jana

Page 46: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

tumempoteza Prof. Robert Mabele wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na yeye nichukue nafasi hii kumshukuru kwamchango wake katika kufundisha wachumi wengi ndani yachumba hiki, nadhani na Waziri wetu wa Fedha ni wanafunziwake kwa hiyo, ni pigo kubwa kwa Taifa, Mwenyezi Munguamrehemu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana sasa niendekwenye ajenda, nianze kuungana pia na wenginekumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Ummy na Makamuwake kwa kazi nzuri wanayoifanya. Mheshimiwa Dkt.Ndugulile alipata nafasi kunitembelea kule na kwa sababuyeye ni daktari mambo ya Muleba aliyaona kwa karibu naalifuata hata na Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu ulifikapale Rubya Hospital ukatembelea hospitali teule ya wilaya,kwa hiyo, naomba nianzie hapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu wa nchi hii katikakutoa huduma ya afya ambayo sina budi kupongeza juhudikubwa ambazo zimefanyika katika Awamu ya Tano. Juhudiambazo tumesikia wakati Waziri Jafo anaorodhesha hospitaliambazo tumejenga za wilaya ni jambo la kujivunia.Mwemyewe kwa upande wa Muleba Kusini tunashukurukwamba, vituo vya afya viwil i Kimea na Kaigaravimeimarishwa, upasuaji sasa hivi unaendelea. Jambo hili kwakweli, tunashukuru sana juhudi hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, na kwa Hospitali Teule yaWilaya ya Rubya naomba niseme kwamba, nikiiangaliaRubya kwa karibu, lakini na hospitali nyingine kwa ujumla hizizinaitwa designated hospitals. Utaratibu wa public privatepartnership naomba nichukue nafasi hii kusema kwamba, niutaratibu muhimu sana. Na tunapoboresha hospitali za Serikalitusisahau pia umuhimu wa kuhakikisha kwamba, zole ambazotulikuwanazo nazo tunalinda uwezo wake kwa sababu, isijeikawa ni wazungu wanesema, you rob Peter to pay Paul;tusimuibie Paulo kumlipa Petro, hapa inatkiwa balance.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaomba sanaMheshimiwa Waziri anapojumuisha tusikie mkakati alionao

Page 47: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

kuhakikisha kwamba, hizo hospitali tulizokuwanazozinaendelea pia, kufaidika na hii partnership iliyokuwepo lasivyo tunaweza tukajikuta kwamba, hospitali zinadidimia. Sinabudi kusema kwamba, hospitali sio majengo, hospitali nihuduma na katika hili niunganishe hapohapo kusemakwamba, Mheshimiwa Waziri pia, aangalie hali halisi yareferral hospital zake.

Mheshimiwa Naibu Spika, napongeza sana juhudi zaSerikali ya Awamu ya Nne iliyokamilisha Hospitali yaMloganzila, lakini Mloganzila hospitali majengo, hakunaHospital town pale kwa ajili ya madaktari kukaa karibu nahospitali. Na hata huyo Profesa Mabele ambaye namsemakafia Mloganzila nilikwenda kumuangalia tu juzi nikakutakwamba, kama kuna dharura daktari anafikaje Mloganzila?Kwa hiyo, nadhani kuna haja ya kufanya uwekezajikuhakikisha kwamba, kituo kinafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikija kwenye Hospitali yaRubya ninaomba sana Mheshimiwa Waziri Ummyunapafahamu, ulikuwa unataka kuleta mashine ya viral loadkwa ajili ya upimaji. Sasa hivi mashine hiyo tunasikia kwamba,imehamishwa imepelekwa Bukoba na vifaa vingine. Hata nawatumishi wa maabara tunapozungumza hospitali haina anydegree holder kwenye pharmacy.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni hospitali inayohudumiawilaya, wakazi laki saba. Kama una wananchi 700,000, hunamaabara ambayo ina a qualified technician unaonakwamba, hapo huwezi kwa kweli, kutoa huduma inayostahiki.Kitengo cha meno pale kiko katika hali mbaya kwa hiyo,nafikiria kwamba, Mheshimiwa Waziri kwa kazi nzurimnayoifanya na utaalamu mlionao ni muhimu sana kwamba,pia, kuweko na uboreshaji tuhakikishe kwamba, hospitali zetuza zamani hazitasambaratika.

Mheshimiwa Naibu Spika, na mwisho kabisa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

Page 48: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha Mheshimiwa,ahsante sana. Mheshimiwa Anna Gidarya, atafuatiwa naMheshimiwa selemani Zedi, Mheshimiwa Azza Hilal Hamadajiandae.

MHE. ANNA J. GIDARYA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Naomba kwanza kabisa niungane na hotuba yaKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichangiemaeneo machache katika Wizara hii ya Afya, nianze na eneola maboma wazi katika maeneo yetu ya vituo vya afya. Tunamaboma wazi katika maeneo mengi nchini na maboma wazihaya yamejengwa na wananchi, lakini Serikali haipeleki helakwa kile kiwango ambacho kimeridhiwa kwamba, wananchiwanajenga maboma na Serikali inamalizia. Mpaka sasa kunamaboma zaidi ya 3000 nchi nzima ambayo hayajaezekwana ni nguvu za wananchi zinapotea bure. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee namiradi isiyokidhi hadhi. Miradi hii ipo mingi, lakini unaendakwenye zahanati unaenda kukagua zahanati unakuta kunamapungufu mengi na zahanati nyingi zimejengwa chini yaviwango, huu ni ubadhirifu wa pesa za umma. TunaombaWizara iangalie ni jinsi gani wanaweza kwenda mbele zaidikwa kutafuta wakandarasi wenye elimu na wenye utaalammzuri katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niende kwenyeeneo la ukusanyaji wa damu salama. Katika maeneo mengiya mikoa kulianzishwa vituo vya ukusanyaji damu salama,lakini tangu mwaka 2015 mfadhili aliyekuwa wa mradi huualikabidhi magari ya Red Cross Serikalini, lakini magari hayompaka sasa hayajawahi kufanya kazi, jambo ambalolinasababisha vifo vingi kwa sababu vituo hivi vimeshindwakukusanya damu salama katika maeneo mengi. Mfano mzurini Mkoa wa Kagera na Mkoa wangu wa Manyara damusalama haiko kabisa. (Makofi)

Page 49: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niende kwenyeeneo la ustawi wa jamii. Kumekuwa na tabia ya ukatili wawatoto katika maeneo mengi, lakini tuna mabarazayanayohusika katika maeneo mengi, kwenye kata kwenyemikoa kwa ajili ya kusikiliza hizi kesi za watoto, lakini mabarazahayo hayafanyi kazi vizuri. Tuna kesi nyingi ambazo hazitatuliwikwa wakati, lakini nyingi zinazimwa na watoto tayariwameshapata madhara makubwa. Sasa Wizara ituambiewana mpango gani wa kuwawezesha maafisa maendeleoya jamii katika maeneo mengi nchini, ili waende sasawakafanye hii kazi kwa weledi?

Mheshimiwa Naibu Spika, watoto wengi wameathirikana wamefanyiwa vitendo vya kikatili. Mfano mzuri ni Hanangambapo ni Basutu, Balangalalu na Babati pia wapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niende kwenyeeneo la utatuzi wa migororo ya ndoa na matunzo ya watoto.Kila siku hapa Bungeni tunalia na hali ya kusema watoto wamitaani. Watoto wa mitaani tunawatengeneza sisi wenyewe,kwa nini tunawatengeneza sisi wenyewe? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara hii inayotakiwaisimamie unakuta kesi nyingi zinaendeshwa, lakini kwa sababuunakuta mama au mzazi mmojawapo hana uwezo mzuri kesitayari imepelekwa Mahakamani, kesi inaamuliwa mtotoaende kwa upande mmoja wa mzazi mmoja. Matokeo yakeule mgogoro kama haukutatuliwa vizuri ndio maana unaonaunasikia kesho mkoa fulani watoto wamechinjwa, mkoa fulanibaba ameuwa mtoto, haya ni mambo yanayoumiza Taifa,lazima yaangaliwe kwa wakati na lazima yasimamiwe nawizara husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumechoka kusikia vifo vyawatoto kila siku watoto wanachinjwa, Tanzania nzima hakunasiku mtoto hachinjwi ni kwa sababu ya ubadhirifu wakutokutumia sheria. Hongo zinatembea huko, mzazi anasemaana uwezo wa kumchukua mtoto wake, anamchukuaanampeleka kwa mama wa kambo, yule mtoto anaendeleakunyanyasika, mwisho wa siku kisaikolojia anaathirika halafu

Page 50: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

tunasema tuna watoto wa mtaani, hiyo haiwezekani.Nendeni mkakae mliangalie hili namna ya ku-solve watotowa nchi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna eneo la vyumba vyawagonjwa mahututi. Hospitali nyingi za wilaya hazina vyumbaambavyo vinakidhi mahitaji ya mgonjwa mahututi; mfanomzuri ni Hospitali ya Mrara chumba cha wagonjwa mahututini sawa na gereji ya magari. Nendeni mkaangalie paleBabati, mkashuhudie hili ninalozungumza, boresheni hizihuduma mtusaidie, tuwasaidie Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumzie eneomoja ambalo nafikiri litakuwa ni la mwisho. Maeneo mengiukienda kwenye hospitali za wilaya, kila unapomfikishamgonjwa, hasa wale wagonjwa wanaopata ajali wanasemadamu haipo. Sasa kwenye hotuba ya Waziri ameandikaamesema damu sijui lita elfu ngapi hizi, hizi damu kwa nchinzima hazitoshi na tunasema tunachangia damu salama kwahiyari, ile kampeni endelezeni, ili tusaidie Watanzania waliowengi. Hii idadi ya damu uliyoandika hapa Mheshimiwa Wazirihaitoshi kwa nchi nzima Tanzania kila siku watu wanahitajidamu salama na wanahitaji kuongezewa damu kupitiamagonjwa mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nikushukuru wewekwa haya machache niliyochangia. Kuna eneo hili lamaendeleo na uwezeshaji wa wanawake. Eneo hili sidhanikama Wizara inafuatilia vizuri katika maeneo yake. HawaMaafisa Maendeleo ya Jamii kwenye maeneo yaowamekuwa miungu watu. Hii mikopo mnayosema namna yakuwezesha wanawake VICOBA, hawa watu hawafanyi hiikazi kwa weledi. Afisa Maendeleo anataka rushwa ili mraditu wanawake wapate mkopo. Hii siyo sahihi! Hii ni haki yaoya msingi akina mama kupata huu mkopo na upo kwenyesera. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, angalieni hivi vituambavyo vinagusa jamii. Kila siku tunaimba hapa issue ya

Page 51: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

dawa lakini kuna mambo ambayo tukiyasimamia mambomengine yanaweza yakaenda sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa SelemaniZedi, atafuatiwa na Mheshimiwa Azza Hamad naMheshimiwa Bupe Mwakang’ata ajiandae.

MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kuchangiakatika Wizara ya Afya ambayo ni muhimu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwakumpongeza kwa dhati Waziri wa Afya, Naibu Waziri, KatibuMkuu kwa kazi kubwa anayofanya na hakuna mtu yeyoteambaye ana mashaka na uchapakazi wao. Hongereni sana.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, miaka miwili iliyopita,nilisimama hapa Bungeni nikalalamika sana kuhusu ubovuwa X-Ray katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega ambapo kunawakati fulani ilikuwa inachukua mpaka miezi sita X-Rayhaifanyi kazi. Leo hii nasimama hapa kutoa pongezi za dhatikwa niaba ya wananchi wote wa Wilaya ya Nzega kwambaSerikali sasa imesikia kilio hicho na imetupatia X-Ray mpyakabisa ya kidigitali ambayo inafanya kazi kwa ufanisi nainatoa picha za ubora. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya aananchi waNzega lazima niishukuru Serikali kwa kutupatia X-Ray hiyompya kabisa. Kwa hiyo, sasa hivi uchunguzi wa magonjwaunafanyika kwa usahihi na maana yake ni kwamba tibaitapatikana kwa usahihi. Ahsanteni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee kuipongezaSerikali. Nimeangalia ukurasa wa 54, kwa kweli kuna mambomakubwa ambayo sisi kama wawakilishi wa wananchi nilazima tuipongeze. Kabla ya mwaka 2017, kuna matibabumakubwa ya kibingwa yalikuwa hayawezi kufanyika hapa

Page 52: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

nchini, lakini sasa yanafanyika. Kwa mfano, kupandikiza figo,jambo hili limeokoa zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa kipindihiki tu ambapo wagonjwa 38 wameweza kupandikizwa figo.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kuna mambomakubwa yamefanyika. Kwa mfano, kabla ya mwaka 2017,hatukuwa na uwezo wa kupandikiza vifaa vya usikivu kwawatoto wadogo. Hili ni jambo kubwa ambalo sisi wawakilishiwa wananchi tunatakiwa kutoa pongezi za dhati. Fikiria mtotoanazaliwa hawezi kusikia, lakini anafanyiwa operesheni,anawekewa vifaa vya usikivu, anaweza kusikia. Kwa hiyo,anaweza kufanya mambo yote ya kupata elimu na hakinyingine zote.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hili ni jamboambalo siyo dogo, ni kubwa na ninachukua fursa hiikuipongeza Serikali kwa kufanikisha jambo kama hili. Piajambo kama hili linaokoa fedha nyingi ambazo zinatumikakatika mambo mengine muhimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaungana namapendekezo ya Kamati ya Huduma za Jamii. Ukiangaliaukurasa wa 20 mpaka 21, Kamati imeitaka Wizara ya Afyakuwaangalia kwa makini wahudumu wa afya katika ngaziya jamii kwa sababu hawa wanasaidia sana katikakuhakikisha kwamba tunapata kinga na kila mmoja anajuakwamba kinga ni bora kuliko tiba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mapendekezoyote ya Kamati ya Huduma za Jamii yaliyo katika ukurasawa 20 mpaka 21 ninakubaliana nayo kwamba Wizara ya Afyaiangalie namna ambavyo itaweza kuwa-accommodatehawa wahudumu wa afya ngazi ya jamii i l i tuwezekuhamasisha akina mama wakajifungulie kwenye zahanati,tuweze kuhamasisha matumizi bora ya vyoo, tuhamasisheunywaji wa majisafi na salama ili kuepuka magonjwa ambayoyanaweza yakasumbua. (Makofi)

Page 53: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalonapenda kuongelea ni uhaba wa watumishi hasa Wagangakatika zahanati zetu. Ningependa Wizara ingetoa mwongozowa kuhakikisha kwamba angalau katika kila zahanatikunakuwa na Mganga.

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ilivyo sasa hivi, kwamfano katika Halmashauri yangu ya Nzega Vijijini, katikazahanati 39 tulizonazo, zahanati 12 hazina kabisa Waganga,zinaendeshwa na Ma-nurse. Jambo hili siyo jema kwa sababutunapaswa tuwe na Waganga ambao mgonjwa akifikaanahudumiwa, anakuwa prescribed na Mganga halafundiyo wanahudumiwa na Nurse.

Mheshimiwa Naibu Spika. Zahanati 12; Zahanati yaMboga, Zahanati ya Semembela, Zahanati ya Nkindu,Ikindwa, Lakui, Mwangoye, Mwasala, Malilita, Uhemeli,Mirambo Itobo, Magengati na Shila; hizi zahanati hazinakabisa Waganga. Kwa hiyo, ombi na ushauri wangu kwaWizara ni kwamba tuhakikishe kwamba zahanati hiziambazo tayari zipo angalau zinakuwa na Waganga iliwagonjwa wakifika pale waweze kupata huduma za tiba zauhakika.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili litakwenda sambambana Ilani yetu ya uchaguzi ambayo tunahimiza kwamba kilaKijiji kiwe na zahanati. Kwa hiyo, maana yake ni kwambatunakwenda kujenga zahanati za kutosha nyingi. Sasazahanati ili ziweze kufanya kazi, ni lazima ziwe na Wagangana Ma-nurse. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwaasilimia mia moja. Nawapongeza Wizara kwa kazi kubwawanayofanya kuimarisha afya katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsanteni sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Azza HillaryHamad, atafuatiwa na Mheshimiwa Bupe Mwakang’ata naMheshimiwa Taska Mbogo ajiandae.

Page 54: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

MHE. AZZA H. HAMAD: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa fursa hii. Awali ya yote nianze kwakumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya na uzimana hatimaye nimeweza kusimama na kuweza kuchangiabajeti ya Wizara ya Afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa pongezi nyingikwa Wizara ya Afya, kwa Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri,Katibu Mkuu na Watendaji wao wote katika Wizara ya Afya.Kazi mnayoifanya ni kubwa na hakika mmeleta mabadilikomakubwa katika Sekta ya Afya. Hongereni sana. Mwenyemacho haambiwi tazama, yanaonekana yale yote ambayommeyafanya katika Sekta ya Afya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nawapongeza pia kwauboreshwaji wa huduma katika hospitali zetu maalum;Hospitali ya Ocean Road, Hospitali ya Jakaya Mrisho Kikweteya kitengo cha Moyo na hospitali zote za mikoa, Wilaya nauboreshwaji wa vituo vya afya. Hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu muda ni mfupi,niende moja kwa moja katika Mkoa wangu wa Shinyanga iliniwasemee wananchi walionileta ndani ya ukumbi huu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kuisemea Hospitaliya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Mwaka 2018 nilisimamahumu ndani nikasema kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Rufaaya Mkoa wa Shinyanga. Ujenzi huu umeanza bajeti ya mwaka2013/2014; kuna jengo moja kubwa ambalo limekamilika,jengo la utawala. Jengo hili wanaishi popo, halina kazi yoyote.Namshukuru Mheshimiwa Waziri, tarehe 24/01/2019alitembelea ujenzi wa hospitali hii katika Mkoa wa Shinyangana baada ya kutembelea alitoa ahadi kwamba atatoafedha, shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya maternity block ili hospitaliile ianze kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namkumbusha MheshimiwaWaziri wa Afya, ahadi yake Wana-Shinyanga tunaisubiri kwasababu ulisema jengo lile litakamilika na mwishoni mwa

Page 55: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

mwaka huu hospitali i le itaanza kufanya kazi, si juiumekwamishwa na kitu gani? Nakuomba sana, nakusihi sana,ahadi ni deni. Vitabu vya dini vinasema, ukiahidi halafu bahatimbaya Mwenyezi Mungu ikatokea lolote, umekufa deni.Naomba ahadi hii uitekeleze Wana-Shinyanga tunaisubiri kwahamu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati wa bajeti mwaka2018 nilisimama nikasema ubovu wa X-Ray machine katikaHospitali ya Mkoa wa Shinyanga. Namshukuru MheshimiwaWaziri pia alipokuja Shinyanga alituahidi wana Shinyangakwamba atatuletea X-Ray machine ya kisasa, lakini mpakasasa hivi hatujapata X-Ray machine ile.

Mheshimiwa Naibu Spika, bado namkumbushaMheshimiwa Waziri, aliahidi mwenyewe na Wana-Shinyangatunasubiri na watendaji wake wanamsikia. Ahadi ni deni,tunasubiri X-Ray machine ya kisasa kwa sababu tuliyonayoni mbovu na haifanyi kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,niendelee kukumbusha ahadi za Serikali. Wakati wa ziara yaMheshimiwa Waziri Mkuu katika Mkoa wa Shinyanga,nilisimama katika Jimbo la Ushetu nikaomba ambulance kwaajili ya Jimbo la Ushetu. Bahati nzuri Mheshimiwa Waziri Mkuualipokea ombi hilo na akatuahidi kwa Mkoa wa Shinyangakutuletea ambulance nne na Mheshimiwa Waziri mwenyeweakiwepo. Tunahitaji Ambulance kwa ajili ya Kituo cha Afyacha Tinde, kwa ajili ya Jimbo la Ushetu, Jimbo la Msalala naJimbo la Kishapu. Ahadi hizo hazijakamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee kusemea kuhusuwatumishi katika Mkoa wa Shinyanga. Watumishi wa Idaraya Afya katika Mkoa wa Shinyanga mahitaji ni 3,606, walioponi 1,446 na upungufu ni 2,160. Naomba Wizara, tutazameni,mmeboresha vituo vya afya lakini vituo hivi kama havinawatumishi bado vitakuwa haviwezi kufanya kazi vizuri.Upungufu tulionao ni mkubwa, watumishi waliopowanalazimika kufanya kazi kwa shida kwa sababuwanafanya kazi ambazo zinawazidi uwezo. Watumishi ni

Page 56: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

wachache katika vituo, kwa hiyo, tunawaomba sana fanyeniutaratibu muweze kutuongeza watumishi katika idara yaafya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naishukuru Serikali katikaujenzi wa vituo vya afya 11 ndani ya Mkoa wa Shinyanga.Vituo hivi vimekamilika, lakini kinachonisikitisha mpaka sasahivi hatujapata vifaa tiba. Kwa hiyo, niwakumbushe Wizaraya Afya, vituo hivi vinahitaji kufanya kazi ili viende vikatimizelengo ambalo mmelikusudia.

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo hil i ni zuri nalinapendeza hata ukiangalia hali ambayo inaonekana katikavituo vyetu vya afya, lakini haviwezi kufanya kazi kwa sababulengo lililokusudiwa halijaanza kufanya kazi. Hakuna vifaaambavyo vimeletwa katika vituo vyetu vyote 11 vilivyopondani ya Mkoa wa Shinyanga na hivyo lengo lile la kwendakufanya upasuaji bado halijaanza kufanya kazi. Kwa hiyo,niwaumbushe mtuletee vifaa tiba katika vituo 11 ambavyommetujengea katika Mkoa wetu wa Shinyanga. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nirudie kusema kwambanaipongeza sana Serikali, nilikuwa nikisema sana kuhusuHospitali ya Wilaya ya Shinyaga, hospitali sasa hivi inaendelea.Nawashukuru sana kwa kazi kubwa ambayo mmeifanya.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naona unanitazama,nakushukuru na ninaunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa BupeMwakang’ata, atafuatiwa na Mheshimiwa Taska Mbogo naMheshimiwa Sonia Magogo ajiandae.

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangiakatika Wizara hii muhimu. Kwanza kabisa, napendakumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uzima natunaweza kusimama katika Bunge lako Tukufu. (Makofi)

Page 57: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue nafasi hiikumpongeza Waziri wa Wizara hii, Mheshimiwa UmmyMwalimu na Naibu wake Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulilekwa kazi kubwa wanazozifanya. Hakika wanaitendea hakiWizara hii. Mheshimiwa Ummy, kwa kweli umetupa heshimawanawake wenzio, Mwenyezi Mungu aendelee kukupiganiana kukuinua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwapongeze pia KatibuWakuu, Naibu Katibu Mkuu na Madaktari wote Tanzanianzima kuanzia Taifa na wale wa wilayani na mikoani. Kwakweli madaktari wanafanya kazi nzuri na kubwa. MwenyeziMungu aendelee kuwatia nguvu na kuwabariki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee, nampongeza sanaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri anazozifanya.Ndani ya kipindi kifupi ameweza kufanya mambo makubwa;nikianza la kwanza, ameweza kuboresha upatikanaji wamadawa hospitalini; pia ameweza kukarabati vituo vya afyatakribani 325; na amefanikiwa kutoa shilingi bilioni 1.5 kwaajili ya ujenzi wa hospitali za mikoa mipya. Kazi nyingi sanaamezifanya Mheshimiwa Rais, nikianza kuziorodhesha hapanina dakika saba zitaisha. Kwa kweli anastahili pongezi.Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, siwezi nikaitendea haki rohoyangu bila kumwombea Mheshimiwa Rais, Dkt. John PombeMagufuli. Naanza kwa kusema Baba katika Jina la Yesu,mbariki sana Mheshimiwa Dkt. Magufuli, mbariki MheshimiwaWaziri Mkuu, mbariki Mheshimiwa Ummy Mwalimu, wabarikiMawaziri wote akiwemo Mheshimiwa Jenista Mhagama,wabariki Mawaziri wote na Wabunge wote wa Bunge laJamhuri ya Tanzania. Mwenyezi Mungu kibariki Chama chaMapinduzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayonasema wote tuseme Amen. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Amen! (Makofi/Kicheko)

Page 58: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa NaibuSpika, niingie sasa kwenye hoja za msingi. Nianze kwakuomba. Jimbo la Nkasi Kusini lipo umbali mrefu sana kutokaMakao Makuu ya Wilaya. Wanawake wanaotoka Kata zaKara, Ninde na Nkandase wanapata shida sanawanapopata ujauzito.

Mheshimiwa Naibu Spika, juzi juzi mwanamke mmojaamefia njiani wakati anakwenda hospitali kujifungua.Namwomba mdogo wangu Mheshimiwa Ummy Mwalimuatufikirie sana Jimbo la Nkasi Kusini kutuletea ambulance.Wanawake wale wakipata ambulance tutakuwa tumeokoamaisha ya akina mama wengi katika Tanzania hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa niipongezeSerikali kwa kutujengea Hospitali za Wilaya. Katika Mkoa waRukwa wilaya zote zimepata Hospitali za Wilaya, lakini badoWilaya moja ya Sumbawanga Mjini haijapatiwa Hospitali yaWilaya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia bajeti iliyopita ilipangakujenga Hospitali ya Rufaa katika Mkoa wa Rukwa ambapoilipanga kujenga katika Kijiji cha Milanzi, lakini mpaka sasahivi hatujaona ujenzi ukianza Hospitali ya Rufaa Mkoa waRukwa. Pia hospitali i l iyopo ya mkoa majengo yakeyamechakaa, jengo la mortuary limechakaa, halina hadhiya mkoa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tulikuwatunaomba Mheshimiwa Waziri aliangalie hili, ile hospitali yarufaa ianze kujengwa, itasaidia sana kuepusha msongamanokatika hospitali iliyopo ya mkoa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niongelee sasa Wilaya yaNkasi, kuna vituo vya afya vimeanza kujengwa, wananchiwanajenga kwa nguvu zao.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

Page 59: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bupe Mwakang’ata mudawako umeisha, lakini kwa maombi uliyopiga, nakuongezadakika mbili. (Makofi)

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante. Nakushukuru sana, Mungu akubariki sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Akasu, Kate, Nindena King’ombe wameanza kujenga maboma ya vituo vyaafya. Naomba Mheshimiwa Waziri atuongezee nguvu, awapemoyo wale wananchi wanaojenga wapate support yaSerikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimpongezeMkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Mjini, kaka yanguJacob Ntalitinginya ameweza kuwakopesha wanawakevikundi karibia 99 ambapo walikuwa wanasubiri kwambalabda Benki ya Wanawake ingejengwa Mkoa wa Rukwalakini haijajengwa. Yeye ameweza kuwakopesha wanawake,pia ameweza kukusanya mapato karibia asilimia 110. Kwahiyo, nampongeza sana Jacob Ntalitinginya, Mkurugenzi waManispaa ya Sumbawanga. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, dakika mbili zimeisha nanilikuwa na hoja nyingi lakini naomba kwa haya tu, niongeleesana suala la ambulance kwa wanawake katika Jimbo laNkasi Kusini kwa Mheshimiwa Mipata.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na naungamkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa BupeMwakang’ata, naona Mheshimiwa Waziri Mkuu hapa alikuwaanapokea hayo maombi kwa namna ya tofauti kidogo, kwahiyo naamini Mheshimiwa Ummy atasema neno.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea nawachangiaji wetu; Mheshimiwa Taska Mbogo, atafuatiwa naMheshimiwa Sonia Magogo, Mheshimiwa Hamida MohamedAbdallah ajiandae.

Page 60: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa muda huu ili kuchangia Wizara yaAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Kwanzakabisa napenda kumshukuru Mungu kwa kutupa uhai leo hiina uzima. Napenda niungane na Watanzania wote kutoapole kwa kifo cha Mheshimiwa Dkt. Mengi ambayeamesaidia sana makundi mbalimbali ya jamii, natoa polekwa wananchi wote wa Tanzania, familia yake na wotewalioguswa na msiba huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,napenda nitoe pongezi nyingi sana kwa Mheshimiwa WaziriUmmy na Makamu wake, Mheshimiwa Dkt. Ndugulile, kwakazi nzuri wanazozifanya za kuboresha afya za Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hapo, naombanitoe pongezi kwa Madaktari wote wa nchi hii ya Tanzaniakwa huduma wanazotupatia za kuboresha afya zaWatanzania wote, ndiyo maana tunaweza kuja humuBungeni na tunaweza kufanya kazi zetu kwa sababu yaMadaktari.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,kwa sababu muda ni mdogo, niende moja kwa moja kwenyechangamoto. Mkoa wetu wa Katavi baada ya ilechangamoto ya kuwatoa Madaktari na Manesi feki,tumekumbwa na tatizo la uhaba wa watumishi. NimwombeMheshimiwa Ummy aweze kutupatia Madaktari kule Mkoanikwetu Katavi, atupatie Madaktari Bingwa; hatunaGynecologist, hatuna Madaktari wa Macho, hatunaMadaktari wa Mifupa, kiasi kwamba mtu akivunjika mguu kuleKatavi inabidi asafiri kutoka Katavi mpaka Muhimbili kwendakufanyiwa matibabu ya mguu. Kwa hiyo niombe sanawatakapokuwa wanaajiri Madaktari auangalie Mkoa wetuwa Katavi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine ambachonapenda kukiomba Mkoani kwetu Katavi, naombakukiombea Kituo cha Afya cha Mamba, naomba akipatieambulance, kituo hiki kipo umbali wa kilometa 150 kutoka

Page 61: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

pale Mpanda Mjini na hakina ambulance. Pia nimwombeMheshimiwa Waziri, kuna kituo cha afya kilikuwa kinajengwacha Mwamapuli katika Jimbo la Kavuu, naomba akipatiepesa ili kiweze kwisha kwa sababu anafahamu jiografia yaMkoa wetu wa Katavi, Jimbo la Kavuu liko kiasi cha kilometa150 kutoka Mpanda kwenda Makao Makuu ya Wilaya, kwahiyo naomba akiangalie kituo hiki cha afya. Niombe piavitendeakazi kama x-ray na ultra sound kwa vituo vya afyavyote vya Mkoani kwetu Katavi kwa sababu viko mbali sanana Makao Makuu ya Wilaya, umbali wa kilometa 150. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ambacho napendakuzungumzia, nimwombe Mheshimiwa Ummy, iko Sera yaWazee ambayo Serikali ilipitisha toka mwaka 2003, niombesasa alete Sheria ya Wazee kwa sababu Sera ya Wazeeimekaa umri wa miaka 15, lakini hakuna Sheria ya Wazee,sasa sera ikikaa hivihivi kama sera inaweza siku nyingineSerikali ikaamua tu kwamba inafuta ile Sera ya Wazee lakiniikiwa ndani ya sheria wazee watakuwa protected zaidi.(Makofi

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine ambachoninakiomba ni kuhusu kuajiri hii Sekta ya Afya upande waCommunity Health Service. Hawa watu ni muhimu sana kwasababu wao wanakwenda deep kwenye kaya, ina maanawana uwezo wa kwenda nyumba kwa nyumba kwendakufundisha mambo ya afya. Ukiangalia kwamba mara nyinginchi yetu huwa tunapata matatizo ya kipindipindu, ni kwasababu tuna uhaba wa hawa Maafisa Afya Jamii. Hawa nimuhimu sana kwa sababu wao wanakwenda kwenye kijiji,wanaweza kufundisha umuhimu wa kutumia vyoo, umuhimuwa kunawa mikono kabla ya kula, hii yote itasaidia wananchiwa Tanzania wasiweze kupata magojwa ambukizi. Kwa hiyo,niombe waweze kuajiri hawa Maafisa Afya Jamii kwamanufaa ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ambaloningependa kulizungumzia, Mheshimiwa Ummy katika Sektaya Afya amefanya vizuri sana upande wa madawa, upandewa kujenga hospitali, upande wa kujenga vituo vya afya,

Page 62: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

lakini upande wa wanawake nimwombe kabla hajaondokaaweke legacy kwa wanawake, aangalie sheria ambazozinamkandamiza mwanamke, zije humu Bungeni zibadilishwe.Nafikiri hiki ndicho kitakachomfanya aweke historia kwawanawake, Sheria kama ya Ndoa ya Mwaka 1971, kipengelecha 13 ambacho kimekuwa kigugumizi katika nchi hiikubadilisha umri wa mtoto wa kike kuolewa na mtoto wakiume kuoa, aweke legacy kwa kubadilisha sheria hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, zipo sheria nyingine piaambazo ni kandamizi kwa wanawake. Kwa mfano, ipo GNya mwaka 1963 ambayo ina vipengele vingi sanavinamkandamiza mwanamke. GN hii bado inatumika nanashangaa sana hata kuna kesi ambayo ilishatolewakwamba GN hii ifutwe, lakini bado nimeona kwamba nikigugumizi sana kufuta GN hii. Haiwezekani utumie GN yamwaka 1963 kwa wanawake wa Tanzania ambayoinawabagua sana katika mambo ya mirathi, inawabaguasana katika kutumia ardhi mume wako akifa na pia inakipengele ambacho kinasema kwamba mwanamke akifiwana mume wake arithiwe na mdogo wake na akikataa atokekatika ukoo huo.

Nimuombe sana afuatilie hizi sheria zote azilete hapana atakuwa ameweka legacy. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, GN hiyohiyo piainamtambua mtoto wa kiume kwamba ndio mrithi halali,wanamwita principal heir, lakini haimtambui mtoto wa kikekwamba ni mrithi wa mali za baba yake. NimwombeMheshimiwa Waziri basi aweke legacy kwa kubadilisha sheriahizi ambazo ni mbovu, zinamnyanyasa mtoto wa kike ilitutakapoondoka katika Bunge hili, basi akinamama wasemetulikuwa na Waziri mwanamke ambaye pia alishughulikiamasuala ya wanawake. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Taska Mbogo kengele yapili imegonga muda mrefu sana, lakini kwa umuhimu wa hojaulizokuwa unasema ilibidi nikuache umalize. Ahsante sanakwa mchango mzuri.

Page 63: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea naMheshimiwa Sonia Magogo, atafuatiwa na MheshimiwaHamida Mohamed Abdallah, Mheshimiwa Balozi Dkt.Diodorus Kamala ajiandae.

MHE. SONIA J. MAGOGO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia katikaWizara hii. Kwanza kabisa nianze kwa kuwapongezawatendaji wote wa Wizara hii kutokana na ugumu wa kaziyao, lakini pamoja na vile wanavyojitahidi kuendana na hizochangamoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilikuja na mpangomzuri sana wa huduma ya afya kwa wannachi na hii imekuwaikiwasaidia sana wananchi wengi, hasa pale wanapopatamatatizo mbalimbali ya afya. Hata hivyo, tumekuwatukishuhudia mrundikano wa watu wengi kwenye madirishazinapotolewa huduma hizi kwenye hospitali zetu, hivyokusababisha wagonjwa kuchukua muda mrefu sana mpakakuja kuhudumiwa. Naiomba Serikali iangalie utatuzi wachangamoto hii kwa kuongeza waajiriwa, hasa katikamadirisha haya yanayotoa huduma hizi za afya kwenyehospitali zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuongelea kuhusuwatoto; tumekuwa tukizungumza sana kuhusu tatizo la lishekwa watoto wetu na tumeona changamoto zinazojitokeza,hasa maeneo ya vijijini. Kwa upande wangu sioni kamachangamoto hapa ni ukosefu wa chakula, kwa mfano, kamatunavyoongelea huko vijijini ambako ndiyo kuna vyakula vingivinapatikana na vingi ni natural kabisa, lakini bado watotowengi wa maeneo hayo wanapata utapiamlo na udumavu.Hivyo hapa naona tatizo ni elimu kwa hii jamii na hivyo Serikaliiangalie uwezekano wa kuwapa elimu hawa wananchi hasawa vijijini ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia watoto waowakapata lishe bora na kuondokana na haya matatizo yaudumavu na utapiamlo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile jamii ingefundishwakuhusu sheria mbalimbali ambazo zinasaidia kumlinda na

Page 64: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

kumtetea mtoto anapokutana na changamoto mbalimbalihuko katika jamii. Changamoto nyingi zimekuwa zikijitokeza,lakini unakuta mzazi hajui aanzie wapi, inasababisha mtotoanakosa haki yake na kuishia kuishi kwenye janga la umaskiniama kuishia kwenye matatizo ambayo baadaye yanakuwani changamoto kubwa sana kwake. Hivyo niiombe Serikaliiendelee kutoa elimu kwa jamii kuwasaidia hawa watoto nakuwalinda ili tuweze kujenga kizazi bora cha kesho. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo lingine nililoliona nikatika tafiti na elimu mbalimbali. Kwenye jamii yetu sasa hivikuna matatizo mbalimbali ya kiafya, mathalani, tunaonawatu wengi hata kushika mimba limekuwa ni tatizo; pia kunatatizo lingine la kutoka mimba kabla ya wakati; kuna tatizola mimba kutunga nje ya kizazi; kuna vifo vya watotowachanga; na kuna tatizo la nguvu za kiume. Haya matatizoyamekuwa ni mengi sana katika jamii na hivyo napendakuishauri Serikali ifanye tafiti mbalimbali na kuja na majibuambayo yataisaidia jamii yetu kuondokana na haya matatizoambayo yamekuwa ni changamoto kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niiombe pia Wizara iangaliehospitali zetu. Hospitali nyingi zinakuwa hazina vifaa vyakutosha, mathalani ni Kituo cha Afya cha Mombo. Kile kituocha afya kipo katika njiapanda na kinahudumia watu wengisana, lakini kituo kile hakina x ray, hakina ultra sound, hakinahata jenereta. Hivyo niwaombe watusaidie kwa sababu nisehemu kubwa sana ya wananchi wanaohudumiwa na kituokile, lakini kutokana na changamoto hizi wanashindwakutekeleza kazi zao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa HamidaMohammed Abdallah atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt.Diodorus Kamala na Mheshimiwa Deo Sanga ajiandae.

MHE. HAMIDA M. ABDALLAH: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi. Nami niendelee kuungana naWaheshimiwa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi katika

Page 65: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

kuhakikisha kwamba tunaendelea kumpongeza MheshimiwaWaziri Ummy na Naibu wake na timu nzima ya Wizara hii yaAfya katika kuhakikisha kwamba wanaendelea kuchapa kazina kazi zao zinaonekana. Mheshimiwa mmoja amesema aliyena macho haambiwi tazama, kwa sababu kazi hizizinaonekana, tunaendelea kuboresha afya za Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia niendelee kumpongezana kumshukuru Mheshimiwa Ummy Mwalimu kwa kufanyaziara katika Mkoa wetu wa Lindi. Imeleta tija sana na faidakubwa kwetu, lakini ameweza kujionea changamotombalimbali ambazo zipo katika Mkoa wetu wa Lindi katikaeneo hili la vituo vya afya ambavyo vinaendelea kujengwa.Vipo ambavyo vimekamilika na vipo ambavyo havijakamilikalakini vinaendelea viko katika hatua nzuri sana, tunaendeleakuvisimamia kuhakikisha kwamba vituo hivi vinakamilika navianze mara moja kutoa huduma. Vile vile vipo vituo vyaafya ambavyo vimekamilika; Kituo cha Mnazi Mmoja paleLindi Manispaa, lakini kituo kimoja pale Lindi Vijijini, kuleNyangamala, tunasubiri tu ufunguzi ufanyike vituo hivi vianzekufanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunamshukuru MheshimiwaUmmy Mwalimu, alifanya uzinduzi wa upimaji wa Saratani yaShingo ya Kizazi pale Sokoine, Lindi Manispaa, huduma hiiimeweza kusaidia kuwafikia wanawake wengi wamewezakujitokeza katika kuhakikisha kwamba wamekwenda kupimatatizo hili la Saratani ya Shingo ya Kizazi. Niendeleekuipongeza Serikali na niishauri Serikali kuendelea kutoahuduma hii ya mobile katika maeneo mbalimbali nchiniTanzania kuhakikisha kwamba wanawake wengiwanajitokeza kuendelea kupima tatizo hil i ambalolinaonekana sasa linakua kwa kasi kubwa katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kufanyakampeni ya utoaji wa chanjo ya saratani ya shingo ya kizazikwa watoto wetu wa kike kuanzia umri wa miaka 14 japokuwatunapata changamoto ya kwamba wazazi wa watoto hawahawawaruhusu kupata hii chanjo. Naomba tuendelee kutoaelimu kwa wazazi hawa na watoto wetu ili waweze kupata

Page 66: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

kinga hii ambayo inatolewa na Serikali kwa sababu tatizo hilimbele ya safari linasababisha wanawake kunyanyapaliwana waume zao kutokana na tatizo hili la kansa ya shingo yakizazi na wanawake wengi wanapoteza maisha kutokanana tatizo hili kubwa ambalo linaendelea kukua katika nchiyetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tulishirikiana na MheshimiwaUmmy Mwalimu katika kuhakikisha kwamba tunahamasishawananchi kujiunga na NHIF katika Mkoa wetu wa Lindi. Tatizolililopo ni kwamba wananchi wengi hawana elimu ya kutoshaya upatikanaji wa kadi hizi za bima ya afya. Nashuhudiapale Ruangwa alitoa elimu na wananchi palepale hospitaliwalidiriki kukata na kujiunga na NHIF. Kwa hiyo, suala kubwani tuendelee na kampeni kuwahamasisha wananchi wetukujiunga na NHIF ili waweze kupata huduma ya matibabupale wanapopatwa na matatizo na inasaidia palewanapokuwa hawana fedha, basi kupata matibabu bure.

Mheshimiwa Naibu Spika, la msingi ni kuendeleakuimarisha vituo vyetu vya afya vyote viwe na dawa zakutosha ili wananchi wale wenye bima za afya wasikatetamaa na itakuwa ni njia nzuri ya kuwafanya hao wenye bimaya afya kuendelea kuhamasisha watu wengine ili wawezekujiunga na wao katika mpango huu wa bima ya afya.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mafanikiomakubwa tuliyoyapata katika ujenzi wa vituo hivi vya afya,bado tunazo changamoto mbalimbali. Ukiangalia katikaMkoa wetu wa Lindi eneo hili la watumishi tuna changamotokubwa sana na Mheshimiwa Waziri Ummy alipokuja alipatataarifa ya mahitaji ya watumishi katika Mkoa wa Lindi.Mahitaji yalikuwa ni watumishi 4,898 lakini watumishi walioponi 1,784, sawa na asilimia 36 na pungufu ilikuwa ni 3,114 sawana asilimia 64. Kwa hiyo upungufu huu wa watumishi katikaeneo hili la afya katika Mkoa wa Lindi ni kubwa sana na nichangamoto kwa sababu wananchi wengi wanakosakupata huduma hii kwa kukosa Madaktari na watumishimbalimbali katika maeneo haya ya vituo vyetu vya afya,

Page 67: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

zahanati na hospitali ambazo zipo. Kwa hiyo, tunamwombaMheshimiwa Ummy Mwalimu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa, kengele yapili imegonga.

Mheshimiwa Balozi Dkt. Diodorus Kamala, atafuatiwana Mheshimiwa Deo Sanga na Mheshimiwa Edwin Sanndaajiandae.

MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA: MheshimiwaNaibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii. Naombanianze kwa kusema kwamba naunga mkono hoja kwaasilimia mia moja. Nina mambo machache ambayonapenda nichangie kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza, natoashukrani zangu za dhati kwa fedha iliyotolewa na Serikali kwaajili ya kukarabati Kituo cha Afya cha Bonazi, nashukuru sana.Mara nyingi huwa nasema mafanikio ni baba wa matatizokwa sababu unapokarabati kituo cha afya kikawa boramaana yake kitavutia wagonjwa wengi zaidi kukitumia namaana yake ni kwamba kituo kikishakuwa bora zaidikukitumia na ni kwamba kituo kikishakuwa bora zaidi kikavutiawagonjwa wengi zaidi maana yake unahitaji kuongeza bajetiya madawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana nasemamafanikio ni baba wa matatizo na huwezi ukaliepuka hilokwa sababu ukiliepuka hatutaendelea. Kwa hiyo, nimwombeMheshimiwa Waziri wa Afya na TAMISEMI wafanye kilakinachowezekana kuongeza bajeti ya Kituo cha Afya chaBunazi na hasa upande wa madawa ili tuweze kukabilianana ongezeko la wagonjwa ambao sasa watatumia kituohicho na wameanza kukitumia kwa sababu sasa opereshenipale zinaweza kufanyika na mambo mengine ambayo hapokabla yalikuwa hayafikiriwi kufanyika pale sasa yanafanyika.

Page 68: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nichukuenafasi hii kuishukuru Serikali kwa kazi nzuri iliyofanya kwakujenga Kituo cha Afya cha kisasa Kabyire. Mheshimiwa Waziriniliwasilisha maombi maalum kwa ajili ya kituo hicho chakisasa ambacho ni bora kuliko vituo vyote katika Mkoa waKagera, naweza nikasema, lakini changamoto kubwa nibajeti, inabidi tutoe bajeti maalumu kwa ajili kuhakikisha kituohicho kinafanya kazi kama ilivyokusudiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama unavyofahamuWilaya yetu ni mpya, hatuna Hospitali ya Wilaya, tunatumiaHospitali Teule. Tulishatenga eneo la kujenga Hospitali yaWilaya, tunaomba sana Serikali ituweke katika awamuitakayofuata ili na sisi tuweze kujenga hospitali hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kitabu cha hotubaMheshimiwa Waziri ameonyesha fursa mbalimbali za Tanzaniakatika ununuaji wa madawa na sasa tunawakilisha nchi 15.Pia nampongeza amefuta tozo mbalimbali na ameelezakwamba wameandaa mwongozo wa uwekezaji katikaviwanda vya dawa. Nimejaribu kutafuta mwongozo huosijauona lakini uzoefu wangu unanituma kwamba mwongozokama unaeleza tu fursa zilizopo bila kueleza incentive zakisheria zitakazotolewa kwa wale watakaowekeza, bila kutoaardhi, mimi niseme Halmashauri ya Misenyi tuko tayari kutoaheka 400 kwa ajili ya kujenga viwanda vya madawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi kama Mbunge waeneo hilo nikizungumza na Halmashauri ya Misenyiimezungumza, mje niwakabidhi eneo hilo ili muweke hiyocenter ya madawa. Ukijenga center ya madawa Misenyimaana yake umejenga Afrika Mashariki kwa sababu utaendaUganda, South Sudan, Rwanda, utaenda kokote kule. Kwahiyo, nachukua nafasi hii kuwakaribisha ili tufanye ujenzi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, naombaMheshimiwa Waziri katika bajeti yake atenge fedha zakutosha za madawa, tunaita noncommunicable disease kwasababu katika ngazi ya zahanati na vituo vya afya maranyingi bajeti zao ni ndogo, madawa ya presha na kadhalika

Page 69: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

wanakuwa hawana. Mara nyingi nimekutana na watu wengiwako Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wakifuatilia dawa hizonikawa najiuliza kama ikishajulikana fulani anaumwa na yukosehemu fulani na dawa anazotumia ni aina fulani na katikaHospitali ya Rufaa zipo, utaratibu ufanywe kuhakikisha dawahizi zinapelekwa mpaka ngazi ya vijij i na vitongoji il ikuwasaidia wagonjwa hawa kupata dawa ambazo vituovyetu au zahanati haviwezi kuwa nazo.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,naunga mkono hoja kwa asilima mia moja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Deo Sanga atafuatiwa na Mheshimiwa EdwinSannda na Mheshimiwa Vedasto Ngombale.

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kuishukuru Serikaliinayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Magufuli pamoja nawanaomsaidia kazi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu yuko hapaambaye kila wakati tunamweleza matatizo ya maeneo yetuna Mawaziri wote wanaotusaidia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee nimshukuru Waziri,Mheshimiwa Ummy pamoja na Naibu Waziri wake naMakatibu Wakuu na watendaji wote wa Wizara ya Afyapamoja na TAMISEMI kwa maboresho waliyofanya ndani yasekta ya afya. Wanafanya kazi nzuri nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza na Jimbo langu laMakambako, nilipewa shilingi milioni 400 kwa ajili ya kujengaKituo cha Afya cha Lyamkena, shughuli ya ujenziimeshakamilika tangu Desemba, 2018. Tunaomba sasatupatiwe vifaa tiba na waganga ili kituo kile kiweze kuanzakufanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo la pil i,tunaomba kituo mama ambacho kilikuwa kama ni hospitali

Page 70: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

ya mji wa Makambako ambacho ni Kituo cha Afya chaMakambako ambacho kinafanya kazi nzuri lakini tatizokubwa ni ukosefu wa X-ray na Utra Sound. Mheshimiwa Raisalivyokuja tulimueleza matatizo yetu na nashukuru aliwaagizawatendaji ikiwemo Wizara ya Afya na TAMISEMI na bahatinzuri nilipokutana na Waziri wa Afya ambaye ni MheshimiwaUmmy Mwalimu nilikueleza juu ya jambo hili na uliniahidikwamba utanipa X-ray. Nakushukuru kwa dhati kabisa kwaniaba ya wananchi wa Jimbo la Makambako. Vilevileniombe sasa atakapotupa X-ray usisahau muwasiliane nawenzako wa TAMISEMI angalau tupate Utra Sound ili vifaatiba hivi viweze kukamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tunaiomba Serikaliangalau tupate fedha za kujenga wodi ya akina baba.Mlitupa fedha za kujengea wodi ya akina mama na watotoimeshakamilika na inafanya kazi katika Kituo hiki cha AfyaMakambako bado wodi ya akina baba.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba tupate wodi yaakina baba kwa sababu jengo lililopo ambalo lilijengwa kwaajili ya kuweka vifaa tiba vya X-ray na Utra Sound ndiyovyumba kadhaa vimegawiwa vinafanya kazi kama wodi.Kwa hiyo, tunaomba tupate fedha kwa ajili ya kujenga wodiya akina baba.

Mheshimiwa Naibu Spika, niishukuru Serikali kwakutupa fedha za kujenga hospitali ya halmashauri yetu shilingibilioni moja na milioni mia tano. Kwa dhati nakushukuru sanakwamba sasa tunakwenda kupata ukombozi wa tiba kwawananchi wetu wa Makambako.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tuna zahanati nyingiambazo tumezijenga katika halmashauri yetu. Halmashauriyetu kwa kushirikiana na wananchi, mimi Mbunge,Waheshimiwa Madiwani na wadau wengine zimejengwazahanati zaidi ya 13. Tulitegemea katika bajeti hii ambayotunaendelea nayo angalau tungepata fedha kiasi ili zahanatikadha kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020 ziwezekukamilika. (Makofi)

Page 71: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

Mheshimiwa Naibu Spika, tumefikia mahali pazuri,zimeshapigwa lipu na kadhalika. Zimeshakamilika vimebakivitu vidogo tu. Tumeshaanza kujenga nyumba za wagangakatika zahanati hizo. Naomba Serikali ione umuhimu wakutupatia fedha mwaka huu wa 2019/2020 ili baadhi yazahanati hizi ziweze kukamilika. Hata hivyo, naishukuru Serikalikwa kuongeza fedha kwa ajili ya afya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, nimwombeWaziri mwenye dhamana, Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Kituocha Afya mama cha Makambako kipo katika center kubwaya Makambako, kwenda Njombe, Mbeya, Iringa na sehemunyingine, mtuongezee dawa kwa sababu tunapata kwakiwango kidogo sana wakati kituo hiki kilikuwa kama hospitalikabla ya kutupa fedha za kujenga hospitali. Nikuombe sanauone namna ya kutuongezea dawa ili kukidhi kuwahudumiawananchi wa Makambako.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Edwin Sannda atafuatiwa na MheshimiwaVedasto Ngombale, Mheshimiwa Aisharose Matembeajiandae.

MHE. EDWIN M. SANNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa fursa hii. Nianze kwa kupongeza sanaWizara hii kwa wasilisho wao, nikupongeze Waziri (shemejiyangu), nikupongeze Naibu Waziri (kaka yangu) lakini pia naMakatibu wote Wakuu na watendaji wa Wizara kwa kazi nzuriambayo tunathibitisha kwamba mnaendelea kuifanya. Pianaunga mkono hoja hii iliyopo mbele yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hospitali ya Mji wa Kondoaimeendelea kukua na kuongeza uhitaji wa huduma kwamaeneo mbalimbali. Hospitali ya Kondoa Mjini inahudumiazaidi ya halmashauri tano, tunazungumzia Vijijini, Chemba,Kiteto mpaka Babati na Katesh wengine wengiwanategemea huduma ya Kondoa Mjini. Mara baada ya

Page 72: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

barabara yetu kumalizika, uhitaji umekuwa mkubwakwelikweli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wale watu ambaotulikadiria wataudumiwa na hospitali ile takribani 60,000 sasaimekwenda zaidi ya wagonjwa, siku hizi wanawaita wateja,zaidi ya 400,000 au 500,000, sasa tumekuwa na upungufumkubwa sana kwanza ni suala la ambulance. Nimekuwanikipigia kelele sana kuhusiana na kupata ambulance.Tumejitahidi tukakarabati iliyokuwa mbovu lakini tunaombasana tupate ambulance. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya barabara ile yakutoka Dodoma kwenda Kondoa kumalizika ajalizimeongezeka, uhitaji wa wagonjwa kupatiwa rufaa kwendaDodoma umekuwa mkubwa lakini hatuna ambulance.Mwaka jana hata Mbunge mwenzetu mmoja alipata ajalipale tulilazimika kuungaunga, unaomba Chemba, KondoaVijijini na ile mbovu ya kwetu kuwaleta majeruhi hapaDodoma. Tunakuomba sana Mheshimiwa Waziri na timu yakoangalia Hospitali ya Mji wa Kondoa ipate ambulance.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwa uongezekaji wamahitaji ya huduma hivyo hivyo hatuna X-ray. X-ray yetuimekuwa ni ya muda mrefu ni ya toka 2000, inaharibika marakwa mara, ni ya zamani kweli kweli, inakaa hata miezi mitatumpaka sita, sasa inatokea ajali watu inabidi kupata X-ray tuwaje mpaka Dodoma. Nakuomba sana Mheshimiwa Wazirituangalie kwenye hili suala la X-ray kwenye Hospitali ya MjiKondoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaendelea kuipongezaSerikali yetu kwa ajili ya kutengeneza miundombinu yabarabara. Sasa barabara imekuwa nzuri lakini pia na ajali nawatu wanaopoteza maisha wanaongezeka, mochwari yetuni ndogo na ya zamani sana, kichumba kile ni kidogo hatamaeneo ya kuoshea, fridge ni mbovu na imezeeka.Nakuomba sana Mheshimiwa Waziri tuangalie kwenyeHospitali yetu ya Mji Kondoa tuweze kupatiwa mochwari

Page 73: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

itakayokidhi mahitaji na haja ya huduma za afya paleKondoa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mtanzamo huo huotena bajeti yetu kwenye basket fund inatuangalia sisi watuwa Kondoa peke yake ilhali tunahudumia watu zaidi ya400,000 au 500,000. Sasa hivi bajeti yetu kwa mwaka tupokwenye milioni 32 wakati tukiangalia mahitaji inakwendakwenye milioni 100 mpaka milioni 120. Hebu na hapo piamtufikirie tuweze kuwahudumia wagonjwa ambaowanaitegemea Hospitali hii ya Mji Kondoa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri yetu wa Mji waKondoa imegawanyika katika kanda kama tatu. Kanda yakwanza ya Kusini, Kanda ya Kati ndiyo Hospitali ya Mji ipopale na Kanda ya Kaskazini. Tunazo zahanati na tunashukuruSerikali tumepata kituo cha afya kimoja kwenye hii Kandaya Kusini kwenye Kata moja Kingale. Watu sasa kutokaUkanda wa Kusini wanakwenda kupunguza uhitaji wakwenda mjini kwa ajili ya kufuata huduma za afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunachoomba tupatiwewalau kituo kingine cha afya kwenye hii Kanda ya Kaskazinikatika Kata ya Kolo na jambo ambalo nimeliongea sanakwenye Bunge letu hili Tukufu ili kuwaondolea adha ya kusafiriumbali mrefu wananchi hawa wa kutoka Ukanda huu waKaskazini kutafuta huduma za afya kwenye Hospitali yaKondoa Mji. Tukipata Kituo cha Afya, Kata ya Kolo, matokeoyake tutakuwa tumewasaidia watu wote wa Ukanda huu waKaskazini pamoja na Kata za Bolisa na majirani wa Sowerana kadhalika. Tunaomba sana Mheshimiwa Waziri tuwezekupatiwa kituo hiki cha afya ili tusogeze huduma karibu kadiriya mpango na sera zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayonaunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Vedasto Ngombale atafuatiwa na Mheshimiwa

Page 74: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

Aisharose Matembe, Mheshimiwa Zaynab Matitu Vuluajiandae.

MHE. VEDASTO E. NGOMBALE: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuungana naWatanzania kwa msiba mzito uliotupata wa Dkt. Mengi. Sisiwatu wa Kilwa tunamkumbuka sana Dkt. Mengi. Mwaka 1993Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliitisha harambee yakuchangisha ujenzi wa sekondari ambapo Mheshimiwa Dkt.Mengi alitoa milioni 20, tutakukumbuka daima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niongelee suala zima lakuhitaji mtaalam wa mionzi katika Hospitali ya St. MarksKipatimu. Hospitali hii tayari tumepata X-ray mpya lakinihatuna huyo mtaalamu. Naomba Serikali itupatie huyomtaalamu ili wananchi waweze kupata uduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili naomba nizungumziegharama za utoaji maiti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,kuna changamoto kubwa. Kama ambavyo tunafahamuHospitali ya Muhimbili ndiyo hospitali kuu ya rufaa, kwa hivyo,wagonjwa wengi wakishindikana wanakwenda pale na upouwezekano wakatibiwa kwa muda mrefu sana. Sasa ikitokeamgonjwa amepata umauti kuna mtihani mkubwa wagharama na kinachofanyika pale ni kuzuia maiti isitoke.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na tatizo kubwasana hili na wauguzaji walio wengi wanashindwa kugharimiagharama hizo na matokeo yake ile maiti inazuiwa nahatimaye huenda kuzikwa na city. Naomba tuangalie upyautaratibu katika suala hili kwa sababu binadamu anastahiliheshima na azikwe kwa mujibu wa mila na desturi zake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kiti chako kilishawahi kutoaruling kikasema kwamba marehemu hadaiwi, sasa hii sijuiinakuwaje? Kusudio siyo kukopa ni kupata tiba na ni haki yake,sasa hana uwezo na yeye ameshafariki kwa nini wauguzaji

Page 75: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

wasiruhusiwe kuchukua maiti wakamzike ndugu yao kwaheshima kubwa? Naomba Serikali iangalie suala hili ni tatizokubwa, Wabunge tumekuwa tukipigiwa simu mara kwa marakusaidia katika hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo ningeonaniliseme leo ni kuhusiana na suala nzima matibabu ya wazeena hii Sera ya Matibabu Bure kwa Wazee. Ni sera ambayoimeanza kutekelezwa lakini kwa kusuasua. Niishauri Serikalibasi ilete Muswada wa sheria ili sasa iwe kwa mujibu wa sheriana siyo sera ili basi wazee wetu wa kuanzia miaka 60 wawezekupata matibabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la Kituocha Afya Njinjo pale kwangu, tungeomba Serikali itupatiefedha kama ambavyo vituo vingine vimepata. Kituo kilekimekuwa chakavu sana, tunaomba nacho kipatiwe fedhahizo ili kiweze kutoa huduma kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia wananchiwameanza kujenga Kituo cha Afya Chumo na Somanga.Tunaiomba Serikali nayo itusaidie ili vituo hivi vikamilike.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni suala zima laUKIMWI. Wafadhili wameendelea kujiondoa katika kufadhiliugonjwa huu. Kwa mfano, hawa wenzetu PEPFAR waowenyewe wamepunguza msaada wao katika suala nzimala UKIMWI kwa kiasi cha dola milioni 119. Hii ni kwa sababukasi ya kupima bure kufikia asilimia 90 ni kama inaenda kwakusuasua. Kwa hiyo, ni nini mkakati wa Serikali wa kuwaruhusuwananchi wajipime binafsi kwa kutumia kile kipimo cha mate.Naomba Serikali iharakishe ili wafadhili hawa waendeleekutusaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni suala zima la homaya ini. Sisi Wabunge tumepata chanjo ya homa ya ini ni vizurilakini Watanzania walio wengi bado hawajapata chanjo hii.Niiombe Serikali iangalie uwezekano wa kutoa chanjo hii kwaWatanzania wote kwa sababu ugonjwa huu ni hatari naunatishia amani. (Makofi)

Page 76: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la bimaya afya kwa wote. Mimi ni miongoni mwa Wabungetuliotembelea nchi ya Rwanda kuona namna gani wenzetuwanatoa hii bima ya afya kwa wote. Wenzetu wamefanikiwasana na wanachokifanya ni kuhusisha wahudumu wale wangazi za chini, wanawapa majukumu na wao ndiowanafanya ushawishi kwa wananchi lakini wanawa-train kiasikwamba wawe wanaweza kutoa huduma ya kuzalisha,kuchoma sindano na vitu vya namna hiyo. Niombe Serikaliije na huu Muswada wa Sheria ili basi huduma ya bima yaafya itolewe kwa watu wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Aisharose Matembe, atafuatiwa na MheshimiwaZaynabu Matitu Vulu, Mheshimiwa Susan Anselm Lyimoajiandae.

MHE. AISHAROSE N. MATEMBE: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotuba hiimuhimu ya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kumshukuruMwenyezi Mungu kwa kunijalia uzima na kutuwezesha kufikiamwezi huu Mtukufu wa Ramadhani. Niwatakie Waislam wotekheri ya Mfungo wa Ramadhani hususani wananchi wa Mkoawa Singida.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitumie nafasi hiikuipongeza sana Serikali ya chama changu chini ya uongoziwa Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli kwa kazi nzuriwanayoifanya ya kuwatumikia wananchi wa Tanzania.Uzalendo uchapakazi wake maono amejipambanua nikiongozi makini na ni mfano wa kuigwa Mheshimiwa Raisendelea kuchapa kazi sisi Watanzania tuko nyuma yako natunakuombea sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze sanaMheshimiwa Waziri wa Afya dada yangu Ummy Mwalimu,

Page 77: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

Naibu wake Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndungulile, KatibuMkuu bi. Zainab Chaula pamoja na watendaji wote waWizara ya Afya hakika wanafanyakazi nzuri sana. Nimekisomakitabu hiki cha hotuba ya afya kwa namna kilivyopangwana kilivyochapishwa, inaonyesha viongozi wa Wizara hii wakomakini sana nawapongeza sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli usiopingika afyandiyo utajiri na afya ndiyo mtaji wa kila mwanadamu.Niipongeze sana Serikali kwa juhudi kubwa inazochukua zakuboresha huduma za afya nchini kote. Kwa niaba yawanawake wa Mkoa wa Singida ninaomba kumshukuru sanaMheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutupa zaidiya shilingi bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya 11,katika wilaya zangu zote za Mkoa wa Singida tumepata Kituocha Afya Mkalama, Iramba, Singida Manispaa, Singida Vijijinipamoja na Wilaya ya Manyoni.

Mheshimiwa Naibu Spika, Namshukuru sanaMheshimiwa Rais hakika uwepo wa vituo hivi vya afyaumeokoa sana vifo vya akinamama na watoto. Lakini Seraya afya inasema kwamba kila kata iwe na Kituo cha Afya,basi niombe pamoja na uwepo wa vituo hivi vya afya jiografiaya Mkoa wangu wa Singida ni ngumu sana niombe vituo vyaafya viongezwe ili wananchi waweze kupata huduma boraza afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naishukuru sana Serikalikwa kutupa bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa hospitali zawilaya, hospitali ya Mkalama na hospitali ya Singida DC. Sasahivi ziko katika hatua ya ujenzi na mwaka huu pia katika bajetihii tumepata hospitali kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilayaya Ikungi naishukuru sana Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pamoja na pongezihizi na shukrani hizi mkoa wangu wa Singida una changamotolukuki katika sekta ya afya. Nikianza na hospitali ya Wilayaya Manyoni, hospitali hii ilijengwa kama kituo cha afyamwaka 1971 na ni ya muda mrefu. Kwa hiyo, majengo yaOPD limeshakuwa ni finyu na dogo, wodi ya akinababa, wodi

Page 78: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

ya watoto, wodi ya majeruhi haiendani kabisa na idadi yawatu katika wilaya hii ya Manyoni. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na ifahamike kwambawilaya ya Manyoni ipo katika barabara kuu ya Mkoa waSingida na Dodoma na ajali nyingi zimekuwa zikitokea kwahiyo inakuwa ni changamoto sana kuwahudumia wagonjwaau majeruhi inapokuwa majeruhi hawa ni wengi ninaiombasana Serikali itupatie fedha ili tuweze kujenga hospitali mpyaya Manyoni itakayoendana sambamba na idadi ya watukwa wilaya yangu ya Manyoni lakini pia vilevile iweze kutoahuduma bora zaidi za afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambaloningependa kuchangia ni kuhusu hospitali yangu ya Rufaaya Mkoa wa Singida, hospitali hii ina changamoto nyingi nahospitali hii ilianza kujengwa mwaka 2009 ni takriban sasamiaka tisa imepita hospitali hii haijakamilika lakini jambokubwa la kusikitisha hospitali hii ya rufaa kwa mwaka wafedha uliopita haijatengewa fedha zozote na inatoa hudumakatika maeneo mawili ipo hospitali ya rufaa ambayo ni yazamani, ipo katika Kata ya Ipembe, lakini pia hospitali ya rufaaambayo ni mpya iliyoko katika Kata ya Mandewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa jambo hili linapelekeakwa kweli ugumu katika uendeshaji wa hospitali hizi mbili kwawakati mmoja. Nimuombe Mheshimiwa Waziri najua nimsikivu na ananisikia ifike wakati sasa zitengwe fedha zakutosha ili kumalizia ujenzi wa hospitali hii.

Mheshimiwa dada yangu Ummy ninakuomba sanakwa kuwa sasa imepelekea bajeti ndogo ambayo tunaipatakulipia bili za maji, umeme, ulinzi na usafi…(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa kengele yapili ilishagonga. Asante sana.

Page 79: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

MHE. AISHAROSE N. MATEMBE: Mheshimiwa NaibuSpika, nauunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zaynabu Matitu Vuluatafuatiwa na Mheshimiwa Susan Anselm Lyimo, MheshimiwaMussa Mbarouk ajiandae.

MHE. ZAYNABU M. VULU: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kupata nafasi hii. Nianze kwanza kwakumshukuru mwenyezi mungu kwa kutujaalia leo kuwezakujadili bajeti hii ya Wizara ya Afya. Lakini pia nimpongezeMheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John PombeMagufuli, halikadhalika nimpongeze Waziri wa AfyaMheshimiwa Ummy Mwalimu na Naibu wake MheshimiwaFaustine Ndungulile, Katibu wa Wizara wajina wangu ZainabChaula pamoja na watendaji wote wa Wizara ya Afya kwakazi nzuri wanayoifanya na wala haina kificho kwa sababutunaona na tunashuhudia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza ambalotunaliona katika awamu hii ambayo limefanywa kwa juhudikubwa ni Taasisi ya Moyo ambayo wameweza kupeleka vifaavingi vya kisasa wameleta wataalam kutoka nje pamoja nawataalam wa ndani wakisimamiwa na Prof. Jannabitunawapa pongezi nyingi sana kinachobakia hapo nikuhakikisha wale wagonjwa ambao wako nje ya mji wa Dares Salaam, wako nje ya mikoa wako vijijini wengi wapowanaopata matatizo ya moyo elimu ipelekwe na utaratibuuelekezwe jinsi gani tunaweza tukawatoa kule wakaja kupatahuduma hapo kwenye Taasisi ya Moyo Dar es Salaam.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hilo limedhihirisha kwambaWizara yetu pamoja na Serikali imesimama kidete kuwekamadaktari wengi, kuweka vifaa tiba vingi matokeo yake idadiya wagonjwa ambao ilikuwa wanakwenda kutibiwa njeimepungua kutoka 683 2014/2015 hadi wagonjwa 62 kwamwaka huu tunaongea leo hii inabidi tuwapongeze naningekuwa kwenye mkutano wa nje ningesema watu wotewawapigie makofi Wizara hii. (Makofi)

Page 80: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

Mheshimiwa Naibu Spika, twende kwenye suala lamatibabu lakini kupitia bima ya afya, bima ya afya ni sualaambalo ni muhimu kwa Taifa letu bado Serikali ina jukumu lakuhakikisha Watanzania wote wanapata elimu na kujua faidana umuhimu wa bima ya afya. Baadhi ya Wabunge humundani wamezungumza jinsi mgonjwa anavyoenda kutibiwaanakutwa na deni kubwa anashindwa kulipa maitizinashindwa kutolewa kwa sababu ya deni lakini elimu yabima ya afya ikitolewa vya kutosha yule mtu hatodaiwa naniseme tu kwa maiti za kiislamu lazima itangazwe anadaiwaau hadaiwi?

Sasa kama anadaiwa tunamtwisha mzigo ambaohaustahili nishauri tu suala la bima ya afya liendelee kutolewaelimu na ikiwezekana uwekwe utaratibu wa kuwa na bimaya afya ambayo kila mtu ataimudu, kila mtanzania atamuduna kila mtanzania ataitumia hiyo bima ya afya kokote kuleisiwe tu kama mimi natoka Mkoa wa Pwani basi bima ile iishiePwani hapana siku nikipelekwa Muhimbili nitatibiwa na tibagani kwa hiyo naomba hilo nalo litizamwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la Sera ya tiba yawazee hili lifanyiwe bidii wakati ndiyo huu unakuta wazeewengi ukienda huko kwa watani zangu Shinyanga wengiwanapigwa wanauwawa hawana mahala pa kukimbiliampaka wapate hifadhi kwa hiyo kuna haja ya kutengenezasera si tu matibabu waangaliwe na mambo mengine muhimuwazee wote watarajiwa ndiyo sisi na wengine wanakuja wezekupata utaratibu mzuri wa sera ya wazee kwa ajili ya maishayao na tiba halikadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara kwa kuhakikishaelimu ya afya ya mama mzazi mtarajiwa ilivyoboreshwa lakinibado kuna haja na kuna kila sababu hawa akinamama hukochini zahanati zetu tumeziboresha, vituo vya afyatumeboresha tuhakikishe basi wanakwenda hospitali.Nimeona takwimu kwenye jedwali humu kwambawanatakiwa waende mara nne katika kipindi cha ujauzitolakini wengi wamekwenda mara moja wengine mara mbilibado kuna haja ya kuboresha zahanati zetu na vituo vya

Page 81: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

afya ili mama mjamzito ashawishike kwenda kwa sababukwingine huduma hazipo zipo mbali kwa hiyo inamuwiavigumu kuna haja ya kuongeza miundombinu ya vifaa tibana hata watumishi katika zahanati zetu katika vituo vya afyaili waweze kwenda sambamba na mahitaji ya jamiiwanayowazunguka.

Mheshimiwa Naibu Spika, nagusa kidogo kidogo kwasababu muda hautoshi.

NAIBU SPIKA: Kengele ya pil i imeshagongaMheshimiwa. Ahsante sana.

MHE. ZAYNABU M. VULU: Mheshimiwa Naibu Spika,naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Susan AnselmLyimo atafuatiwa na Mheshimiwa Mussa Mbarouk,Mheshimiwa Joseph Kasheku Musukuma ajiandae.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuchangiana kipekee nipongeze sana hotuba ya kamati pamoja nahotuba ya Kambi ya Upinzani ambapo ni mwanakamati.Ninaomba sana Wizara itekeleze yale yote hasa maoni hayoambayo kwa kweli ni ya msingi na ninaamini mkiyachukuatutaboresha sana sekta ya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianze kwa sualazima la bajeti. Wizara hii kama ambavyo wote tunajua niWizara muhimu sana kwa afya ya Taifa letu na hata hivyotunavyosema kwamba Tanzania ya viwanda haitawezekanakama rasilimali watu wetu watakuwa wagonjwa na hawapatihuduma bora.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni jambo la kusikitisha sanakuona kwamba Wizara hii pamoja na kutengewa bajetikubwa tulipitisha takriban shilingi trilioni moja lakini kwenyefedha za maendeleo tulipeleka bilioni 561 mpaka leotunapozungumza imeenda shilingi bilioni 91 tu sawa na

Page 82: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

asilimia 16, hivi kweli asilimia 84 ya fedha tulizozipitisha ndaniya Bunge hili bado hazijapatikana na tunafikia mwisho wamwaka tunaomba kujua ni kwa kiasi gani tunategemeaubora wa huduma za afya kama fedha ambazo tumekaahapa ndani kwa kipindi cha miezi mitatu haziendi tunaiulizaSerikali tuna sababu gani ya kukaa hapa Bungeni tunapitishafedha nyingi kiasi hicho ambacho tunaamini zinaendakufanyakazi lakini fedha hazitoki huku tukiambiwa kwambaSerikali inakusanya fedha fedha nyingi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilikuwa naombaMheshimiwa Waziri atapokuja ku-windup atuambie hivi hiyoasilimia 84 inategemewa kwenda lini na hizo huduma zoteambazo zimekwama kwa huu muda ni kwa kiasi ganiwananchi wame-suffer ni kwa kiasi gani watu wamefariki kwasababu ya kukosa hizi fedha? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hapo kutokanana uchache huu wa fedha naamini ndiyo sababu tunakuwana matatizo mengi kwenye Wizara hii. Kwa mfano kuna watuwengi sana wanaenda kwenye hospitali wanafanyiwavipimo lakini vipimo vinakuwa tofauti na ugonjwa alionao.nitatoa mifano hata Waziri akiita baadhi ya Wabunge ambaowamepata matatizo hayo ni wengi sana. Kwa mfano majuzihapa niliangalia kwenye TV kuna binti mmoja amepimwaMuhimbili, amekutwa na matatizo ameambiwa ana matatizoya ini, ini limeungua amekaa karibu anakufa amepelekwaIndia only to find ana matatizo ya moyo sasa watu wa namnahii wako wengi kiasi gani. Nilikuwa naomba Waziri atuambietatizo ni uelewa wa madaktari wetu au technician au tatizoni vifaa tulivyonavyo haifanyi kazi nilikuwa naomba hilo sana.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la magonjwayasiyoambukiza limekuwa kubwa sana na tatizo kubwa sasahivi pamoja na diabetes ni pamoja na tatizo kubwa la kansa.Leo tunavyozungumza ni hospitali mbili tu za Serikali zinamashine ya mionzi yaani radiograph sasa na hii iko hospitaliya Ocean Road na hospitali ya Bugando lakini tuna hospitalizaidi ya mbili za rufaa tuna hospitali ya Kanda ya Mbeya,

Page 83: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

tuna hospitali ya Kanda ya Kilimanjaro kwa maana ya KCMCKanda ya Kaskazini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nipo kwenye kamati yamaendeleo ya jamii kwa muda mrefu madaktari au wakuuwa hospitali hizi mbili kilio chao kikubwa kimekuwa ni fedhakwaajili ya kununua bunkers kwa ajili ya kuweka hizo bunkersili waweze kuweka hizo mashine hospitali ya KCMC nahospitali ya Mbeya.

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna sababu yakupandisha hadhi au kuwa na hospitali za Kanda kamahatuna vifaa. Kwa hiyo, tatizo la Ocean Road kuwa namrundikano litakuwa palepale kwa sababu wagonjwa katikaKanda kwa mfano Nyanda za juu kusini, wagonjwa katikaKanda ya Kusini, wagonjwa katika Kanda ya Kaskazini,wanapopata matatizo ya kansa wameshakuwawameshatambulika wana kansa wanatakiwa wapate mionzihawapati mionzi wanatakiwa tena waende Ocean Roadkwa hiyo tunarudisha tatizo palepale. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na ukiangalia hata kitabucha maendeleo cha mwaka huu hakuna fedha yeyote yamaendeleo iliyotolewa katika hospitali ya KCMC walahospitali ya Mbeya. Kwa hiyo, wagonjwa wetu katika maeneohusika wataendelea kufariki kwa kukosa huduma za msingikwa sababu tunaambiwa huduma kansa inaweza ikatibikakama imeweza kujulikana mapema lakini watu wamegundualakini bado hawana access kwenye hizo hospitali, kwa hiyo.nilikuwa naomba hilo pia Waziri atusaidie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nije kwenye suala zima lawatumishi ni wazi kwamba watumishi wa Wizara ya Afya,sekta ya afya kwa ujumla wake ni wachache sana na Waziriwanakiri ni karibu asilimia 50 lakini vijijini asilimia mpaka 74hakuna wauguzi, hakuna wataalam wa afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa na tunaendelea piakujenga vituo vya afya tunaendelea kujenga zahanati lakinisuala la watumishi halijaonyeshwa. Inasikitishwa kuambiwa

Page 84: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

kwamba ni kwasababu ya kuondolewa kwa wale waliokuwana vyeti feki, sijui waliokufa. Wewe unatambua kwambakama ikama ipo tayari na fedha zao za mishahara zipo sasakama hawa wameondolewa replacement ipo madaktariwapo kibao wana-graduate lakini vilevile wauguzi wanajaasasa hoja ni nini hapa watuambie labda Serikali haina fedhalakini kutuambia wanaendelea na uhakiki na uhakiki wakatihawa watu walikuwa kwenye ikama na fedha zao zipomaana yake ukimuondoa, lazima umrudishe ambaye yupona wapo mitaani ukipiga filimbi hapa madaktari ambaowako mitaani wapo kibao manesi wako kibao kwa sababukila siku kila mwaka wana-graduate. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kwa kwelitunaendelea kuweka afya za watu wetu rehani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nielezee kwamba nimakamu mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa chama changuna kwa maana hiyo sina budi kuongelea suala la wazee, tokanimeingia kwenye Bunge hili tumekuwa tukiambiwa tuna Seraya wazee toka 2001 lakini mpaka ninavyozungumza sheriahaijaja na ndiyo sababu wazee wanaendelea kudhalilikakatika nchi hii. Wazee wanaendeshwa kwa sera kwamiongozo kwa taratibu lakini hakuna sheria nilikuwa naombakila siku tunapigwa danadana tuwambia kwanini wanasemawanaendelea kuboresha, wanaendelea kufanya hivi lakinikwa nini msilete sheria? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi kweli hatuoni aibukwamba wazee hawa ndiyo wametulea wazee hawa ndiowameleta uhuru katika nchi hii lakini wazee hawa leommesema mara mtawapa vitambulisho, mara sijui mtawapanini lakini wazee hawa wananyanyasika kwelikweli na ninajuakwamba siyo wazee wote hawana uwezo lakini hata walewasio na uwezo ikija sheria itawatambua kwa sababu hataleo nikimuuliza Waziri mwenye dhamana tuna wazee kiasigani katika nchi hii sidhani kama wana-database. Kwa hiyo,nilikuwa naomba sana suala la wazee ni la muhimu lakinivilevile suala la pensheni ya wazee ni la muhimu siyo wazeetu waliokuwa wanafanyakazi, hata wasiokuwa na kazi

Page 85: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

walitakiwa walau wawe na posho ambayo itawasaidiakujikimu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nije kwenye suala landoa za utotoni limeelezwa kwa kina lakini niseme ni jambola aibu sana kuona kwamba sheria yetu ya mwaka 71 badondiyo tuliyonayo lakini kipekee niseme kwamba jambo hilililipelekwa mahakamani na tayari limeshakuwa ruled outkwamba sheria hiyo ibadilike vile vifungu vil itakiwavibadilishwe lakini kinachosikitisha Serikali kupitia AGwamekata rufaa.

Sasa nashindwa kuelewa hivi ni kweli tunataka watotowetu waolewe katika umri huo? Sheria ya mwaka 71 wakatitulikuwa hatuna shule leo tunasema kila mtoto aende shuleyeye eti sheria bado ni ileile kwahiyo kuna confusion na nilazima huo utata uweze kutatuliwa kwa sisi Wabunge kukaapamoja na kuona umuhimu wa kubadili sheria hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo ambalo nilitakakuzungumiza ni suala zima la huduma ya unasihi. Tunamatatizo makubwa sana Tanzania. Sasa hivi kuna suala stressna sonona (depression) na hii inatokana na changamoto zamaisha ikiwa ni pamoja na kutopandishwa mishahara ikiwani pamoja na vyuma kukazwa na mambo mengi. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwahiyo, jambo hili linahitaji ushauri nasaha. Tuna vyuo vyetu vyaMaendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii, hasa cha Ustawiwa Jamii…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Susan kengele ya piliilishagonga. Ahsante sana. Nilikuwa nasubiri umalizie hojayako muhimu.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, yakwanza.

Page 86: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

NAIBU SPIKA: Zimeshagonga mbili Mheshimiwa.Ahsante sana.

Mheshimiwa Mussa Mbarouk, dakika tano atafautiwana Mheshimiwa Joseph Kasheku Musukuma na MheshimiwaMargaret Sitta ajiandae.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Labda nami niungane na wenzangu katika kutoapole kwa Watanzania wote baada ya kuondokewa na mzeewetu, Reginald Mengi. Namkumbuka tu Tanga, baadakuanzishwa kwa ITV alituletea television kubwa sana palekatika uwanja wa Tangamano ikawa wananchi wa Tangawanapitia taarifa na burudani mbalimbali kupitia katikatelevision hiyo. Mwenyenzi Mungu amweke mahalipanapostahili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kusemakwamba katika taarifa ya Kamati iliyotolewa, kuna upungufuulielezwa kwamba Kamati ilivyotembelea miradi, miradi mingiilikuwa haijapelekewa fedha za kutosha. Vile vile hataukingalia katika bajeti, nayo inakuwa imetekelezwa kwa 16%badala ya 100% na 84% bado haikuweza kutimizwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile niwape pongeziMheshimwia Waziri na Naibu wake wa kufanya kazi katikamazingira magumu. Pamoja na hivyo, naitaka Serikali nayosasa iangalie kwamba Wizara ya Afya ndiyo kitengo auWizara muhimu katika maisha binadamu, kwa sababubinadamu bila kuwa na afya bora hapawezi kukawa nauzalishaji mali, hapawezi pakawa na Jeshi ambalo lina ngumukamili, lakini pia sekta mbalimbali zinaweza kufeli kamawatumishi watakuwa hawana afya bora. Kwa hiyo, pamojana mazingira magumu, lakini endeleeni kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni kwambawakati mwingine lazima Serikali yetu nayo inapopanga bajeti,basi ihakikishe kwamba bajeti inapelekwa. Kuna jambolingine gumu ambalo naliona katika bajeti zetu, mafungumakubwa ya fedha tunategemea katika fedha za wahisani.

Page 87: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

Wakati mwingine wahisani nao ama hawatuletei fedha kwawakati ama wanatoa visingizo na matokeo yake fedha hizozinakuwa haziji na matokeo yake mambo hayakamili.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,niende katika hotuba hii ya Kambi Rasmi ya Upinzani, kunaeneo limesema kwamba kwa mwaka wanakufa akina mamawajawazito 11,000,000, sawa na akina mama 30 kila sikukutokana na vifo vya uzazi. Kwa nchi kama Tanzania ambapokuna Madaktari wasomi wakubwa, ina rasilimali nyingi;kushindwa kulishughulikia suala hili kwa kweli naona ni tatizokubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika akili za kawaida, kilasiku kuna akina mama 30 wanapoteza maisha kutokana navifo vinavyotokana na uzazi. Naomba Mheshimiwa Waziriatakapokuja hapa atueleze, wana mkakati gani wakupunguza vifo hifo hivi? Kwa sababu Watanzania 30kupoteza maisha kutokana na vifo vya uzazi, hii idadi ya nikubwa sana. Kwa mwaka watu 11,000,000. Hili siyo jambodogo. Yakipangwa majeneza hapa 30 kwa siku au kwamwaka kwamba ni watu 11,000,000 ni idadi kubwa sana.Naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja atueleze wanampango gani kuhakikisha jambo hili linakwisha? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo linginelimezungumzwa hapa kwamba katika Mkoa wa Tabora kunaWakunga wanaozalisha kwa kutumia mifuko ya rambo aumifuko ya plastiki. Serikali imeshapiga marufuku mifuko yaRambo, sijui Wakunga huko Tabora watatumia vitu gani katikakuzalisha akina mama? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama hilo halitoshi, kwenyeziara ya Mheshimiwa Rais alipokwenda Malawi, amepatataarifa moja ilinifariji, kwamba Malawi wameweza kuanzakutoa chanjo ya Malaria. Malawi ndiyo nchi ya kwanza BaraniAfrika kuanza kutoa chanjo ya Malaria. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Mheshimiwa Waziriatakapokuja ku-wind-up naomba atueleze, nasi Tanzania

Page 88: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

tuna mpango gani wa kutoa chanjo ya Malaria ili nasi tuwenchi ya pili Barani Afrika kwa kutoa chanjo ya Malaria?Tukumbuke kwamba kila dakika tano, Tanzania Malaria inauaMtanzania mmoja. Sasa hili nalo naomba tuje tuelezwe, tunampango gani na sisi kuwa nchi ya pili kutoa chanjo yaMalaria?

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine nirudi kwenye…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Kengele imeshagonga Mheshimiwa.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa JosephKasheku Musukuma, atafuatiwa na Mheshimiwa MargaretSimwanza Sitta na Mheshimiwa Selemani Kakoso, ajiandae.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushuru sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia.Naomba niipongeze sana Wizara ya Afya. Kipekee kabisanampongeza sana Mheshimiwa Waziri pamoja na KatibuMkuu wake. Wao wanajua ni kwa nini nawapongeza. Bilajitihada zako Mheshimiwa Ummy ukishirikiana na mamawakati akiwa TAMISEMI, sisi watu wa vijijini huko Nzeratusingekuwe na Hospitali. Nataka nikuhakikishie kazimliyoifanya ni kubwa sana na tutawakumbuka milele.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, huwa nazungumza maranyingi, hii Wizara wakati tunaanza Ubunge ilikuwa ni Wizaraambayo kila mtu anailalamikia, lakini leo Wizara hii ukisikilizamichango ya Wabunge, nadhani mwaka ujao tutakuwatunaijadili siku moja tu mambo yanaisha tunapitisha bajeti.Hata kama kungekuwa na tuzo ya kutunzwa MheshimiwaWaziri anayefanya vizuri, kiukweli bila upendeleo Mheshimiwa

Page 89: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

Ummy unastahili kuwa Waziri bora kabisa katika Bunge la 2018.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba sanaMheshimiwa Waziri, alipopita kule kwetu aliahidi hospitali,umetupa. Jimbo zima watu laki 500,000 hatuna kituo cha afya.Kwa huruma yake alipandisha vituo viwili. Tusaidiwe pesa ilituweze kupata kituo cha afya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tunajenga Hospitali yaRufaa ya Mkoa wa Geita. Hii hospitali imesimama toka mweziwa Kwanza, certificate hawataki kulipa. Lipeni certificatetuweze kujenga hospitali yetu. Kuna tatizo gani?Tunategemea hiyo hospitali ndiyo iwe hospitali yakutukomboa sisi watu wa Geita. Tuko zaidi milioni tano nakitu. Tusaidieni kulipa hiyo certificate ili waweze kuendeleakujenga hospitali yetu ya mkoa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, kwanza nimpongezeMheshimiwa Waziri sana kiukweli, alipofanya ziara kwenyeHospitali ya Rufaa ya Bugando alitualika Wabunge wa Kandaya Ziwa, nami nilikuwepo. Bahati nzuri Gwajima alikuwa badoWizarani, naye alikuwepo. Niwapongeze sana. Katika miakayote inaoneka kweli Serikali mmekuwa serious kutukomboasisi watu wa Kanda ya Ziwa. Ninaona kabisa jitihada za Serikalikujiona ni sehemu ya ile Hospitali ya Kanda ya Ziwa ya Rufaaya Bungando. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pale tukiwa na MheshimiwaWaziri tulizungukia majengo, aliyaona majengo mazuri, lakinikule ndani hakuna MRI na wagonjwa wengi wanatoka Kandaya Ziwa. Tunamwomba Mheshimiwa Waziri aweke mpangomkakati tununuliwe MRI, watu wetu wanakufa kwa kukosagharama za kufuata MRI Dar es Salaam. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile tunaishukuru Serikali.Tunatibu wagonjwa wa saratani. Wagonjwa wa sarataniTanzania wanaongoza toka Kanda ya Ziwa. Tunaomba mletewataalam wakae Mwanza. Mtu wa kuanzia Singida hananauli ya kuja Dar es Salaam, atakuja Mwanza. (Makofi)

Page 90: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

Mheshimiwa Naibu Spika, pia watujengee wodi,pamoja na kwamba vifaa vipo, lakini mtu anapotakakufanyiwa operation, hakuna wodi ya kuwalaza wale watu.Kwa hiyo, tunamwomba sana Mheshimiwa Waziri kwa ukaribualionao, namkushukuru sana Mheshimiwa Waziri naninamwomba sasa awe karibu na hiyo hospitali awezekutusadia watu wa Kanda ya Ziwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tunashukuru, juzinilitembelea nikaona; mlituahidi kutujengea jengo la TB kamala Kibong’oto na lenyewe limejengwa kwa shilingi milioni 120.Ni suala ambalo kweli tunaona Serikali mpo karibu na watuwa Kanda ya Ziwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia waliahidi kutoamatibabu ya bure kwa wagonjwa wenye saratani. Tunaona,tunatuma watu wetu wanasaidiwa masikini bure. TunaiombaSerikali ingalie kwa jicho la huruma, ikamilishe vitendea kazikwenye hospitali yetu ya Bugando. Hiyo ndiyo hospitalikombozi kwenye kanda ya ziwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Ummyanakumbuka, wakati tulikuwa tunaenda, hospitali ilikuwainakusanya shilingi bilioni mbili. Leo inakusanya shilingi bilionitisa. Na mimi napenda huyu mtu mngempongeza Wabungewa Kanda ya Ziwa. Kutoka shilingi bilioni mbili hadi shilingibilioni tisa na siyo matibabu ya kugombana, ni matibaburafiki; leo watu hawaendi hospitali za mtaani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, zamani ilikuwa ukiambiwaunaenda Bugando unajihesabu unaenda kufa, lakini leoukifika pale unatibiwa vizuri, unakaribishwa vizuri na watuwanatoa pesa zao bila wasiwasi. Watu kama hawa,Wakurugenzi akina Makubi wangekuwa wanaalikwa kwenyeMabunge kama haya tunawapa pongezi na wao wanajisikiaili waweze kwenda kuongeza morali.

MBUNGE FULANI: Yuko hapo.

Page 91: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Yuko hapa, nashukurusana Mheshimiwa Waziri. Leo ukienda Bugando, ni kwelikabisa, hata operation za mitaani zimepungua. Watuwanapewa motisha kule ndani, Bugando imekuwa nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, yangu ni hayo.Nakupongeza sana Mheshimiwa Ummy; ya Jimboni kwanguunikumbuke lakini na hospitali yetu ya Bugando hatuhitajisana kuwafuata Madaktari Dar es Salaam, tunataka tutibiweMwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushuruku sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Niwakumbushe tuWaheshimiwa Wabunge, wakati mwingine mnawezamkakosa majibu kwa ku-address watu mahsusi. Humu Bungenikinakuwa addressed kiti. Kwa hiyo, inabidi uzungumze naanayezungumza hapa mbele na sio moja kwa moja na Waziri.

Mheshimiwa Ummy pongezi zote hizo zimekuja lakinizilitaka kuja moja kwa moja hivi. Kwa hiyo, tuzungumze nakiti kwa sababu wakati wa majibizano huwa tunapatachangamoto kidogo, lakini Bunge likiwa limetulia namna hiitunayaacha yanaenda. Tukumbuke tu kuzungumza na kitibadala ya kuzungumza na mwenye hoja moja kwa moja.

Waheshimiwa Wabunge, nilikuwa nimeshamtajaMheshimiwa Margaret Simwanza Sitta, atafuatiwa naMheshimiwa Selemani Kakoso na Mheshimiwa Oscar Mukasaajiandae.

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi name nichangie hoja iliyokomezani. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uhai, lakinibado naendelea kuwashukuru wananchi wa Urambo kwakunipa ushirikiano. Nami niungane na wenzangu kuipa polefamilia iliyoondokewa na Mzee wetu, Marehemu ReginaldMengi, naomba Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahalipema Peponi.

Page 92: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

Mheshimiwa Naibu Spika, nawajibika kuishukuru sanaWizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na kadhalikakwa jinsi ambavyo wanachapa kazi katika Awamu hii yaTano. Namwomba Mwenyezi Mungu awabariki sanaMheshimiwa Ummy mwenyewe ambaye anathibishawanawake wanaweza. Pia nampongeza Mheshimiwa Dkt.Ndungulile kwa namna anavyochapa kazi na Mwenzie.Nampongeza pia Katibu Mkuu, Dkt. Chaula, kwa kweli hawawatu wanafanya kazi wakisaidiwa na wafanyakazi. MwenyeziMungu awapeni nguvu, endeleeni kuchapa kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili ni shukrani kwa niabaya wananchi wa Urambo kwa kumaliziwa Kituo cha Afya chaUsoke. Naishukuru sana Serikali kwa kutupa shilingi milioni 400kwa kumalizia Kituo cha Afya cha Usoke na sasa hiviwametuongezea kimoja ambacho kinaendelea kujengwakatika Kata ya Uyumbu Usoke Mlimani.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya shukurani hiyo,naomba niielezee Serikali kwamba sisi kama Urambo tunakata 18. Maana yake ni kwamba kituo hiki cha pili kikimalizikatutakuwa na vituo viwili vya afya. Ni ombi kwa niaba yawananchi wa Urambo kwamba tuongezewe kituo cha afyaangalau katika Kata ya Songambele; na ikiwezekena hataviwili katika kata pia ya Vumilia.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni jambo la uwazi kwambasisi kama Urambo bado tunahudumia Wilaya ya Kaliuaambao bado; ukienda kwenye wodi ukitembelea wagonjwawaliolazwa utashangaa, wengi wanatoka Kaliua, wenginewanatoka kwa jirani zangu Uyui hasa maeneo ya Ndono nampaka Uvinza sisi tunapata. Kwa hiyo, tunapoomba hudumaya afya kuongezewa ni kwa sababu pia tunahudumiawananchi wanaotoka katika maeneo ya jirani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe shukrani za pekee kwaMheshimiwa Waziri Ummy. Alikuja kufanya ziara na ziara yakeilizaa matunda. Tulipoenda Usoke alifurahishwa sana na kaziiliyofanywa pale Usoke ya kumalizia kituo cha afya ambapoulikuwa ni mradi uliokuwa wa ADB tangu 2010. Mheshimiwa

Page 93: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

Ummy alifurahi kwa jinsi ambavyo kituo kilimalizwa vizuri naakaahidi kwamba majengo mengine ambayo yapoyanaharibu sura ya kituo kile kwamba atatoa shilingi milioni50. Mheshimiwa Waziri tunashukuru sana kwa ahadi yako,naamini itatimizwa tu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Kituo cha Afyacha Usoke kilikuwa ni mabaki ya mradi wa ADB, ADB iliachamradi mwingine ambao bado haujakamika. Inasikitishakwamba tangu mwaka 2010 theater ambayo ipo karibu nawodi ya akina mama ilianza kujengwa pale, sasa hivi ikokwenye ngazi ya lenta, kwa kujua kwamba wakitoka paletheater wanaingizwa kwenye wodi ya akina mama. Mpakaleo haijaisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali imalize ilietheater nasi tunaamini kwamba tukipewa shilingi milioni 200itamaliza hiyo theater ili akina mama ambao wapo karibu,ambao walikuwa walengwa, wakitoka theater palewanaingia wodini na vice versa, wakitoka wodiniwanapelekwa theater. Tunaomba theater ikamilishweambayo iko kwenye ngazi ya lenta. Inasikitisha, jengo zurilakini tangu 2010 halijaisha ambayo itausaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi theater kwa kuwatunahudumia na watu kutoka maeneo mengine, wengineinabidi wasubiri lakini theater ikiisha wagonjwa, wakiwepoakina mama na watoto watanufaika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, halikadhalika tuna mradimwingine ambao uliachwa, ni mradi wa LGDB ambapo niICU. Huwezi kuamini Urambo hatuna ICU na ni Hospitali yaWilaya. Tunaomba kwa heshima na taadhima kabisa Awamuya Tano itusaidie tuwe na ICU na sisi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hali kadhalika na X-Ray,nimeshukuru Wabunge wengine wamesimama hapawanafurahi kwamba tuna X-Ray ya kisasa ya kidijitali, sisi badotupo kwenye analogy.

Page 94: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

Mheshimiwa Naibu Spika, nisaidie nawe kuiombaSerikali itusaidie X-Ray ya kisasa. Kwa sababu hata hayamajibu tunayopata sasa hivi tuna wasiwasi nayo, kwa sababubado tupo kwenye enzi ya Ujima, tunatumia X-Ray yaanalogy. Tunaomba tusaidiwe hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hali kadhalika, suala lawafanyakazi ni la muhimu sana. Bado tuna uhaba wawafanyakazi kwa asilimia 48. Tunaomba nasi mtakapokuwamkipanga wafanyakazi mtukumbuke nasi Urambotuongezewe wafanyakazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilifurahi sana ziara yaMheshimiwa Waziri Ummy. Namwomba Mwenyenzi Munguampe afya ili arudi tena aone mabadiliko gani tumeyafanyatangu alipotoka. Kuna maneno mazuri uliyaacha Urambobado watu wanakukumbuka nayo na hasa paleulipokumbuka kile Kituo cha Afya cha Uyogo kinachojengwakwa kushirikiana na Waingereza. Nawe ulitaka kuonyeshakuunga mkono nguvu ya wananchi na marafiki zao kutokaUingireza ukaahidi shilingi milioni 20. Tushukuru sana kamautawapa shilingi milioni 20 Uyogo ili wamalizie kituo chao.

Mheshimiwa Naibu Spika, zaidi ya yote, badowanamkumbuka Mheshimiwa Waziri alipotamka neno lamaana sana kwamba atawapa ambulance. Kwa sababuwao wapo mbali na Hospitali ya Wilaya, akiwapa ambulanceitawasaidia sana kuwawahisha akina mama hasawanaokwenda kujifungua usiku, maana yake saa zakujifungua huwa hazijulikani; usiku na kadhalika, ambulanceitasaidia sana. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Naibu Spika, halikadhalika Mheshimiwa Waziri alipokwenda zahanati yaItebulanda, aliahidi nako shillingi milioni 20. Mheshimiwa Wazirituna imani kabisa utatimiza kwa sababu uliipenda sana ilezahanati, inafanya kazi vizuri na imeanzisha wodi ya akina

Page 95: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

mama na kwamba utawaunga mkono kwa shilingi milioni20.

NAIBU SPIKA: Muda wako umeisha Mheshimiwa.Ahsante sana.

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Naibu Spika,namshukuru Mheshimiwa Waziri, nashukuru Wizara nzima naninaunga mkono hoja. Endeleeni kuchapa kazi. Ahsantenisana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa SelemeniMoshi Kakoso atafutiwa na Mheshimiwa Oscar Mukasa,Mheshimiwa Khatib Haji ajiandae.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kupata nafasi hii kuweza kuchangia hotubaya Wizara ya Afya. Awali ya yote, niungane na wenzangukumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa kazi kubwa ambayoanayoifanya akisaidiana na wasidizi wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara hii ni muhimuimefanya kazi karibu maeneo yote ya nchi yetu. Mkoa waKatavi hatuna Hospitali ya Mkoa. Mheshimiwa Wazirianafahamu na fedha ambazo zimetengwa na Wizara nikidogo sana. Tulikuwa tunaomba Mheshimiwa Waziri aangaliemazingira ya Mkoa wa Katavi aongeze fedha ili tuwezekujenga Hospitali ya Mkoa ambayo itasaidia kutoa hudumaya afya kwenye maeneo ya mkoa na kutoa huduma za afyakwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunampongezaMheshimiwa Waziri kwa kutoa fedha za ujenzi wa Hospitaliya Wilaya ya Tanganyika, imepata shilingi bilioni moja na nusukwa aji l i ya ujenzi wa Hospitali Tanganyika. Hilotunawapongeza sana Wizara kwa kazi kubwa naMheshimiwa Waziri na timu ya wataalam ambao wametoahizo fedha kwa ajili ya kutoa huduma. Nimwombe sanaMheshimiwa Waziri aendelee kutusaidia kwenye Vituo vyaAfya ambavyo viko kwenye maeneo husika. Nilishamwomba

Page 96: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

Kituo cha Afya cha Nyagala, naamini anakikumbuka,naomba sana hiki Kituo akiwekee kipaumbele kwa ajili yakuwapa wananchi wa eneo hilo. Walishaanza hatua zaawali, wamejitolea, wamejenga baadhi ya majengo, kwahiyo tunategemea Mheshimiwa Waziri kwenye fedhaatakazozipata, atusaidie kituo hicho ili tuweze kuwasaidiawananchi wa eneo husika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambasamba na hilo,tunaipongeza Serikali kwa kujenga Vituo vya Afya vya Mwesena Mishamo. Kwenye hivyo vituo viwili ambavyo vilitolewafedha na Serikali upo upungufu ambao tunahitaji Wizaraisaidie. Tunaomba vifaa tiba, kwa ajili ya Kituo cha Afya chaMwese, tunaomba vifaa tiba kwa ajili ya Kituo cha Mishamo.Naamini tukipata hivyo vifaa tiba vitawasaidia kutoa hudumailiyo nzuri na wananchi wakanufaika na kile kilichoelekezwana Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwombe sanaMheshimiwa Waziri kwenye maeneo ambayo alifikaMheshimiwa Waziri, alifika eneo la Kituo cha Afya chaKarema, eneo li le tunahitaji watusaidie watupatieambulance, yeye aliahidi na alifika akaona mazingira yalivyo,kwa hiyo tunaomba kumkumbusha Mheshimiwa Waziri ahadiambayo aliwapa Wanatanganyika, eneo lile la Karemaaweze kukamilisha ili aweze kuwasaidia wananchi kwenyemaeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, tunaombaMadaktari na vituo vya afya, zahanati na hospitaliinayojengwa sasa inahitaji wahudumu wa afya, Wilaya yaTanganyika ina Daktari mmoja tu. Naomba kwenye bajetihii, aangalie uwezekano wa kupeleka wataalamwatakaotoa huduma kwenye vituo vya afya. Vituo vya afyahivyo vilivyojengwa ni vizuri, lakini vina tatizo la wahudumuambao wanaweza wakatoa huduma kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,naunga mkono hoja na naendelea kumpongeza kwa kazinzuri ambazo anazifanya. Ahsante. (Makofi)

Page 97: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa OscarMukasa, atafuatiwa na Mheshimiwa Khatib Haji naMheshimiwa Dkt. Rashid Chuachua ajiandae.

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana. Kwa kipaumbele cha juu kabisa,namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa hii nafasi yakufanya shughuli ya leo. Pia nawashukuru wananchi waBiharamulo kwa kuendelea kuniunga mkono, lakini kwanamna ya pekee napenda kuipongeza Serikali, MheshimiwaRais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Sekta hii ya Afyamambo yanaonekana, lakini Mheshimiwa Ummy Mwalimu,Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile na wasaidizi wenu KatibuMkuu na wengine wote tunawapongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushahidi uko wazi, miminitatoa ushahidi mmoja kwamba mkononi kwangu nina ripoti,utafiti uliofanywa na Taasisi ya Institute for Health Metrics andEvaluation, moja ya mambo ambayo wamepima ni habariya maternal mortality kwa watoto wa chini ya miaka mitanona infants wale chini ya mwaka mmoja, inaonesha kabisatakwimu ziko wazi hapo kwamba hatujafika tunapotakiwakufika, lakini tunakwenda vizuri kulingana na matarajio namnawanavyopima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nawapongezasana, lakini tumesikia hapa, Mheshimiwa Mbunge mmojaamesema namna ambavyo Wizara hii inapata pesa kidogoukilinganisha na mahitaji ambalo sio jambo zuri, lakini hataMheshimiwa Ummy na Mheshimiwa Ndugulile na timu yao,kwa kweli wamejitahidi sana kuratibu wadau wengine wanje ya Serikali. Ndiyo maana mambo mengine yanakwenda,ukipata fursa ya kuwa nao karibu utaona hilo na kweli huwalinanitia moyo sana, naona mwanga. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niseme mawili yaBiharamulo; moja tunashukuru tumejengewa Kituo cha AfyaNemba, lakini kinaleta mahitaji kwa sasa tutafanya upasuajipale wa akinamama wajawazito, wale wanaohitaji upasuaji,tunahitaji ambulance, jiografia ya Biharamulo ni ngumu sana

Page 98: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

kwa sasa tuna Kituo Nyakahura na Nyakanazi ambavyo nimbali sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambasamba na hilo,tunahitaji wataalam wengine wa dawa za usingizi, yakomatukio kadhaa ya upungufu yanayosababisha vifo vyaakinamama kutokana na upungufu wa wale wataalam wadawa za usingizi. Tuna Madaktari, ama MD mmoja amawawili, wako kwenye hivyo vituo, lakini kwa sababu watu wausingizi hawatoshi, mara nyingine ucheleweshwaji inakuwahaiwezekani kufanya upasuaji kwenye Kituo cha Afya nasafari ya kwenda Biharamulo Mjini kwa ajili ya upasuajiinakuwa ndefu inasababisha vifo. Hayo ndiyo mahitaji yetumawili makubwa kwa Biharamulo.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nije suala la Kitaifa,pamoja na pongezi na kazi nzuri inayofanyika yako maeneoya kuboresha. Ukitazama ripoti hii hii ya Institute of HealthMetrics and Evaluation, inasema kwa mwaka 2017wamelinganisha 2007 na 2017, hii ni taasisi maarufu sanaduniani na inaheshimika, wame-rank wameweka uwiano,wamepanga ule uzito wa sababu za vifo kwenye nchi yetuhii. Katika sababu hizo, ziko ambazo zinatokana na UKIMWI,TB, Malaria lakini hata na magonjwa ya kuhara ni miongonimwa sababu kumi za vifo ambavyo zinachukua uzito wa juu.Metrics

Mheshimiwa Naibu Spika, na sababu za vifo, kablaya wakati, yaani zile pre-mature death wame-rank mambohapo, kuna tuberculosis, lakini kuna protein energymalnutrition, mambo ya utapiamlo, mambo yanayozuilikakabisa na sababu za ulemavu, inayoongoza kabisa ni dietaryiron deficiency na ukiangalia zaidi kwenye ripoti yaowanasema, vifo pamoja na ulemavu kwa pamoja sababuinayoongoza ni malnutrition, utapiamlo, yaani nchi hii tunatatizo kubwa la utapiamlo, pamoja na kufanya kazi vizuri sanahuko kwenye tiba.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ningependa, nijikitezaidi kwenye utapiamlo huo, Sera ya lishe nchi hii, imepitwa

Page 99: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

na wakati, toka mwaka 1992. Kwa bahati mbaya, ilikuwainatazama zaidi mchango wa lishe kutoka kwenye Sekta yaAfya, haitazami mchango wa lishe kutoka kwenye sektanyingine, hili ni tatizo. Tunaomba tufanye mapitio ya Sera,kama asilimia, tatizo linaloongoza kwa habari ya vifo naulemavu kwa pamoja, namba moja ni utapiamlo wala siokipindupindu, sio jambo lingine wala sio malaria. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima twende kwenyeSera yetu, tuone namna gani sekta zote zitaingia.Nakumbuka mwaka jana, waliwaita Wakuu wa Mikoa hapa,nikaona wanaweka sahihi, lilikuwa ni jambo zuri, lakini nikawanajiuliza hivi hizi sahihi zitatusaidia, kama hatuna framework?Pia sijasikia ushahidi wowote kwamba hizo sahihi zimesaidia,wameleta improvement, ni kwa sababu lazima likae kimfumo,tuzialike Sera zote kisera na tunaomba katika hili, ikae Seraya Lishe sio kuchukua habari ya lishe kuiweka kwenye Seraya Afya, kwa sababu hili jambo ni mtambuka na kubwa.Naomba kusema kwamba hili tutalipigia kelele sana.Tunaomba Sera ya Lishe ije haraka iwezekanavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, usafi; moja ya sababuzinazosababisha vifo, ukichanganya vifo na ulemavu kwapamoja, ni habari ya wash, mtu anatoka kujisaidia hanawimikono, anakuja kumsalimia mwenzake na hapa ukiangaliakama mtu angekuwa anapima watu tunavyosalimiana, hapakwa mikono lakini asilimia zaidi ya sabini ngapi hawanawimikono baada ya kujisaidia. Hili linahitaji elimu tu nawamesema Wabunge wengi hapa, twende kule kwenyezahanati na vituo vya afya tuweke wahudumu wa afya wakwenda kuelimisha vijijini wa kutosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeona kwenye Ikama yaWatumishi wa Afya wanayo ya zahanati inasema ClinicalOfficer kwa siku aone wagonjwa 40. Mtu wa madawa kwasiku ahudumie prescription 40, lakini ikifika kwa yuleCommunity Health Worker inasema aunganishe tu kituo nakijijini, haimpi kwamba leo katazame vyoo saba ukatazamewangapi wameweka sehemu za kunawa, twende huko,tuondoke kwenye tiba sasa tumeshafanya vizuri, twende

Page 100: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

kwenye afya. Watanzania wanahitaji Afya, nimesikia watuwanawapongeza Madaktari na mimi nawapongeza, lakiniifikie hatua, tuanze kupongeza, tunawapongeza MabwanaAfya, wamehamasisha sasa huku hatuharishi, kwa sababuukiangalia hapa inasema asilimia 2.7 ya wananchi nchi hiihawana vyoo kabisa...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mukasa kwamchango huo. Nilikuwa nimemwita Mheshimiwa Khatib Hajidakika tano, atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt. RashidChuachua, halafu Mheshimiwa Fatma Toufiq ajiandae.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. Namshukuru Mwenyezi Mungu kunijaliakuweza kusimama hapa, na niwatakie heri na baraka katikamfungo wa mwezi wa Ramadhani wananchi wote waTanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwa kutoashukrani na pongezi za dhati kabisa kwa namna MheshimiwaWaziri, Naibu wake na Watendaji wake wanavyoisimamiaWizara hii, Wizara ambayo ni uhai wa Taifa la Tanzania, niuhai wetu sote. Mimi binafsi hata kama sitasema hadhara,lakini kwa kusema kweli naikubali sana Wizara hii naWatendaji wake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nianze kuhusu sualala wagonjwa wa figo, Mheshimiwa Waziri, binafsi anafahamu,mimi nimewahi kuugua ugonjwa huo, nimepitia mazitoambayo kwa kweli kati ya magonjwa mazito na magumusana ni ugonjwa wa figo. Kwa hivyo ninapozungumza hapanazungumza kitu ambacho nimekipitia, nakijua nanaendelea nacho.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, natakaMheshimiwa Waziri, kuna jambo moja linatatiza sanawagonjwa wa figo, jambo hili ni upatikanaji wa dawa za

Page 101: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

wagonjwa wa figo, wagonjwa wa figo ambao wako kwenyebima, Watanzania wengi hali zao za kiuchumi ni za chini sana,wale walioko kwenye bima, hizo bima hata ukikata lakini kunamasharti ya kufikia kupata dawa za figo, yako masharti, mtukawaida ukikata ile bima unaambiwa lazima ikae muda fulaniiwe ndiyo inakuwa matured ya kuweza kupatiwa dawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna binadamu yeyoteanayejiombea ugonjwa kumfika, kama imewezekana kwawagonjwa wa UKIMWI kupewa dawa hizi pasipo na mashartina wagonjwa wa figo waangaliwe urahisi wa kuzipata dawahizi. Kwa kweli, hili jambo ni la kuliangalia sana, pamoja nahilo Mheshimiwa Waziri anajua mgonjwa wa figo anapopatatu ugonjwa huu, akithibitika kuna hatua za kupitia wakatianasubiri upasuaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, huduma ya uchujaji wadamu, huduma za uchuchaji wa damu, kwa mtu asiye nabima ya afya sasa hivi ni 180,000. Watanzania wa hali ya chinikwenda kupatiwa huduma hii kwa 180,000 kila sikuanayokwenda kwenye huduma hii ni jambo zito na ambaloWatanzania wengi hawawezi kulimudu. Hili linapelekea vifovyao kabla hata hawajafikia kwenye kufanyiwa transplant.Kwa hiyo namwomba Mheshimiwa Waziri, aliangalie hili sana,kwa sababu Watanzania wengi wasio na uwezo wanafikia,hawafikii hatua ya kutafuta ndugu kuwasaidia upandikizajitayari wamekuwa wamekufa katika hatua ya kufanyiwauchujaji wa damu dialysis, kwa hivyo naomba suala hililiangaliwe nalo kwa umakini sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo mimi ni mmoja wawanachama wa Chama cha Wagonjwa wa Figo nawanachama wenzangu wamenituma hapa nilisemee hilo,kwa hivyo Mheshimiwa Waziri, naomba alichukue kwa uzitostahiki. Naongea kama Khatib na naongea kama mwakilishiwa wagonjwa wenzangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ninalotakakulizungumzia, Mheshimiwa Ummy katika Hospitali ya Rufaaya Bombo lipo tatizo, lipo tatizo ambalo sasa ni karibu miaka

Page 102: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

mitano, tatizo la lift katika wodi ya Galanosi ambayo wazaziwanakaa kwenye ghorofa ya tatu, theatre room iko chini.Kinachotokea sasa hivi anapofanyiwa operation, akipelekwakule juu lazima abebwe mzega mzega. Tanzania ya leomgonjwa kubebwa kwenye machela akapandishwa kwenyengazi hilo ni jambo ambalo halikubaliki. Akinamama hao,ambao wanajifungua kwa operation wako chini, akinamamahao Mheshimiwa Waziri ajue ndiyo wengine wanajifunguaMarais, wengine watajifungua Mawaziri Wakuu, wenginewatajifungua Waziri wa Afya kama yeye, wenginewatajifungua wachungaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ni vizuri sanaMheshimiwa Waziri jambo hili aliangalie na nataka nimpe rai,kwa sababu mimi ni mdau wa Tanga, mimi ni mpiga kuraambaye natokea Zanzibar lakini mimi ni mkazi wa Tanga nafamilia yangu yote. Namwomba sasa, kama hili jambolimekuwa zito na mwaka wa tano limeshindikana, tuna bahatisana Mkoa wa Tanga na Jimbo la Tanga Mheshimiwa Waziriwa Afya ni mtu wa Tanga; Katibu Mkuu wa Wizara hii ni mtuwa Tanga, Dkt. Chaula; yupo Mbunge wa Jimbo la TangaMheshimiwa Mussa Mbarouk na nipo Mbunge mimi kutokaZanzibar, lakini ni mdau mkubwa wa Tanga.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa Waziriahitishe harambee mimi na wenzangu nil iowatajatuwashirikishe matajiri wa Tanga wapo pale wa kina RATCO,yupo pale Raha Leo, yupo Simba Mtoto, tuitishe na harambeekubwa ambayo itasaidia kuitengeneza lift ile ili wagonjwawetu, akinamama wetu wa Tanga waepukane na adhabuile. Namwomba sana Mheshimiwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Khatib.

Sina hakika kama anapiga kura mara mbili ama vipi,naona kama amepata kigugumizi hivi, anaweza kuwa nimpiga kura wako Mheshimiwa Ummy. (Kicheko)

Page 103: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

Waheshimiwa Wabunge, tumalizie na Wabungewaliosalia, Mheshimiwa Dkt. Rashid Chuachua, atafuatiwana Mheshimiwa Fatma Toufiq, Mheshimiwa JosephineGenzabuke atamalizia.

MHE. RASHID M. CHUACHUA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa mimi kupata fursa ya kuzungumza kidogokwa ajili ya kuchangia hotuba ya bajeti hii ya Wizara ya Afya.Nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuisimamia Wizarahii, lakini kusimamia na kupigania afya za Watanzania. Tunaoushahidi, tunaona kwa macho, Hospitali zinajengwa, hospitaliza rufaa na vinajegwa vituo vya afya kila kona. Kwa kweli,kazi kubwa inafanyika, lakini nimpongeze sana mama yetumama Ummy, Watanzania wanamwona namnaanavyofanya kazi na hakika Mwenyezi Mungu atamlipa.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nikumbushemambo machache yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza,Mheshimiwa Ummy alikuja Mtwara wakati wa ziara yaMheshimiwa Rais katika Mkoa wa Mtwara, MheshimiwaUmmy alisikia kilio cha Wabunge wa Mtwara na Wabungewa Kusini kwa ujumla pamoja na wananchi kuhusiana nasuala zima la Hospitali ya Kanda ya Kusini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Ummy kwakweli moyo wake mwema, uendelee hivyo hivyo kwakuhakikisha kwamba hospitali hii inajengwa na inakamilikakwa sababu kwa muda mrefu ujenzi ule umesimama na sisitunaisubiri kwa hamu sana hospitali hiyo ili tuweze kupatahuduma za afya kubwa kubwa kama wanavyopata katikamaeneo mengine waliopata Hospitali za Kanda za Rufaa.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nitumie fursa hiikumkumbusha Mheshimiwa Ummy alipokuja Masasi katikaziara yake ya kikazi, alipata fursa ya kufanya mkutano wa

Page 104: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

hadhara. Katika mkutano ule tulimwomba ambulance mojana aliahidi kutupatia, tunaomba moyo wake mwema,uendelee hivyo hivyo atusaidie tuweze kupata ambulancehiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakumbusha tenaMheshimiwa Ummy kwamba alipata fursa ya kutembeleaHospitali ya Mkomaindo, aliona changamoto kubwatuliyonayo kwenye upande wa x-ray, x-ray ni chakavu nahaifanyi kazi. Tunamwomba moyo wake uendeleekuwaangalia kwa jicho la kipekee watu wa Masasi atuleteex-ray mpya ya ki-digital kama katika maeneo mengine iliwananchi waweze kupata huduma inayostahili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimkumbushe tena dadayetu Mheshimiwa Ummy, kwamba ameona hali halisi yaHospitali yetu ya Mkomaindo na namna ambavyo chumbacha upasuaji hakiwezi hata kuchukua zaidi ya mgonjwammoja katika kutoa huduma. Tunaomba mabadilikomakubwa ya chumba hiki ili wananchi wetu waweze kupatahuduma inayostahiki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimkumbushe tenaMheshimiwa Ummy, kwamba kama ilivyo katika maeneomengine, tuna uhaba mkubwa wa Madaktari na wahudumuwa afya katika Jimbo la Masasi, tunaomba pia atuangaliekwa mikono miwili.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema manenohayo, naunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa FatmaToufiq, tutamalizia na Mheshimiwa Josephine Genzabuke.

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa na mimi fursa ili niweze kuchangiahoja iliyopo mbele yetu. Nami niungane na wenzangu wotekumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wetu Bi. UmmyMwalimu, lakini pia nimpongeze Naibu Waziri, Dkt. FaustineNdugulile. Watendaji wote, Katibu Mkuu wa Afya, mdogo

Page 105: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

wangu Dkt. Zainabu Chaula, pongezi sana pamoja na KatibuMkuu wa Maendeleo ya Jamii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba niungane namaoni ya Kamati kwamba fedha zote ambazohazijakamilishwa kutolewa katika Wizara hii zitolewe kwawakati ili kusudi waweze kutekeleza majukumu yao kwaufanisi zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika ukurasa wa 121 wahotuba ya Mheshimiwa Waziri amezungumzia kuhusumpango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawakena watoto 2017/2018 hadi 2021/2022. Naipongeza sanaSerikali kwa kuratibu na kuanzisha hizi Kamati za Ulinzi waWatoto na Wanawake na inasemekana mpaka sasa hiviKamati hizi zimefikia 7,383. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo,napenda tu kufahamu kwamba Wizara imejiandaaje katikakuhakikisha kwamba mpango huu unafahamika zaidi katikajamii yetu hasa kule pembezoni. Kwa sababu mpango huudhima yake najua ni nzuri sana kuhakikisha kwambawanawake na watoto wanakuwa hawafanyiwi ukatili.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia napenda kufahamuSerikali ina mkakati gani wa kutunga sheria ya jinsia ili kusudisasa iweze kuangalia masuala yote kwa jicho la kijinsia. Kamatukiwa na sheria hii naamini kabisa masuala mengi ya kijinsiayanaweza yakafanyiwa utekelezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tafiti zimebainisha kwambaukatili unaanzia majumbani na wengi wanaofanyia watuukatili ni ndugu wa karibu. Wizara imejipangaje kuelimishajamii kuhusiana na suala hili ili kusudi watu wasione tabukulizungumzia na hatimaye wahusika wanaofanya ukatiliwaweze kuchukuliwa hatua zinazostahiki? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nizungumziekuhusu ustawi wa wazee, wenzangu wengi wamezungumzia.

Page 106: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

Suala la ile sheria na mimi pia naomba nisisitize kwamba sheriainabidi itungwe kwa sababu nchi yetu imeridhia matamkombalimbali lakini pia mwaka 2016 Umoja wa Afrika ulikuwaumekubaliana kupitisha mwongozo kuhusu haki za wazeelakini inaelekea kwamba nchi yetu bado haijaridhiamakubaliano hayo. Naomba basi ifanyike ili kusudi wazeewetu waweze kupata tija, kwa kweli wazee nao wanahitajifursa nyingi na mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nizungumzie kuhusumakao ya wazee. Kwa kweli kuna changamoto kubwa sana,haya makao ya wazee 17 ambayo ni ya Serikali bado yakokatika hali mbaya sana. Naomba Serikali ifanye matengenezoyanayohitajika ili kusudi hadhi ya wazee iweze kupatikanakwa sababu inaonekana kwamba wazee wameachwanyuma sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumziekuhusu masuala ya makuzi ya watoto, hii imezungumziwakatika ukurasa wa 123 hadi 132 katika hotuba hii. Sasa hiviwatoto wengi sana ambao tulikuwa tukiwategemea wawemayaya au walezi wanakwenda kusoma shule. Kwa sababuya elimu bure watoto wengi wa kike siku hizi tena hawaendikufanya kazi za majumbani.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilichokuwa naombanishauri ni kwamba Serikali ione utaratibu wa kufanya ili kusudiviwepo vituo vingi vya malezi ya watoto wakati wa mchanaili kusudi sasa wazazi na walezi waweze kuwapeleka watotowao katika vituo hivi. Watoto kwa kukaa katika vituo hivi ni iliustawi wa wale wao uwepo lakini pia waweze kuwa katikamazingira salama. Vituo hivi vitumike kama sehemu bora yaulinzi na usalama wa watoto. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba nizungumziekuhusu suala la afya ya kinywa na meno. Tatizo ni kwambasasa hivi watu wengi sana wamekuwa na tatizo hili la afyaya kinywa na meno Serikali ituambie ina mkakati gani wakwanza kuzuia ili kusudi watu wengi wasipate madhara napia wataalam wengi wa masuala ya kinywa nao pia

Page 107: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

wapatikane. Kwa sababu inaonekana kwamba maeneomengi wataalam hao hawapo, kwa hiyo, wananchiwanapata shida sana kwa ajili ya afya ya kinywa na meno.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,nashukuru sana kwa kunipa nafasi, naunga mkono hoja.Ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Josephine Genzabuke.

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuruMwenyezi Mungu kwa kunipa kibali cha kusimama ndani yaBunge lako na kuchangia hoja hii ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Kwanzanapenda nimpongeze Waziri wa Afya, Mheshimiwa UmmyMwalimu, Naibu Waziri Mheshimiwa Dkt. Ndugulile, KatibuMkuu - Dkt. Chaula kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Wizarahii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nipongeze kwamoyo wa dhati kabisa jinsi Serikali ya Awamu ya Tanoinavyofanya kazi ya kujenga hospitali pamoja na vituo vyaafya. Naomba nishukuru kwa moyo wa dhati kabisa kwaSerikali kuweza kusaidia Hospitali ya Maweni kwa kupelekashilingi milioni 500 ili kuendelea kuimarisha hospitali ile ambayoinatumiwa na wananchi wote wa Mkoa wa Kigoma. Ahsantesana, tunaamini pesa hizo zikifika zitaendelea kukarabatihospitali yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nishukuru Serikalikwa kuweza kukubali kujenga Hospitali ya Wilaya ya Kakonko.Waziri Mkuu alipokuja alikubali kupeleka shilingi bilioni 1.5 kwaajili ya ujenzi wa Hospitali ya Kakonko na tayari shilingi milioni500 zimepangwa kwa ajili ya kuanza ujenzi huo. Nashukurukwa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya Hospitali ya Kasulu DC, tayari

Page 108: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

fedha zimeshafika na tayari wameshaanza ujenzi. Nashukuruna ujenzi wa hospitali inayoendelea katika Wilaya yaBuhigwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeshuhudia wakati huuvituo vya afya vinakarabatiwa na vingine vinajengwa,tunaishukuru sana Serikali. Naomba vituo hivyovinavyojengwa ambavyo vipo tayari na vingine ambavyobado viweze kupelekewa madaktari, wauguzi pamoja navifaa tiba, sambamba na wataalamu wa dawa za usingizi.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi kwa Waziri wa Afyapamoja na Katibu Mkuu, kwa sababu wao ni akina mama,vipo vituo vingine karibu na hospitali ya wilaya lakini kunamaeneo mengine yapo mbali kabisa. Kwa mfano, kutokaKasulu Mjini kwenda eneo moja la Kitanga ni kilometa 123lakini hawana kituo cha afya. Lipo eneo lingine tena linaitwaKagera Nkanda, kutoka Kasulu Mjini ni kilometa 78. Naombakwa vile wao ni akina mama washirikiane na Waziri waTAMISEMI kuona ni namna gani wanaweza kuwasaidia akinamama ambao wanaishi umbali mrefu sana na hawana vituovya afya ili tuweze kupata vituo vya afya katika maeneo hayoambayo yako mbali kutoka Wilaya ya Kasulu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba vilevile katikaWilaya ya Kakonko, Gwanuku wameshapata kituo cha afyalakini Mgunzu pamoja na eneo moja linaitwa Muhangi nawao wako mpakani hawana vituo vya afya. Naomba na waowaangaliwe kwa sababu wako mpakani waweze kupewavituo vya afya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine nil ichotakakuzungumzia, mara nyingi sana wananchi wanapoendakutibiwa katika maeneo mbalimbali wakipangiwa kwendamaabara kupima hawezi kurudi bila kuambiwa kwambahajapatikana na tatizo la UTI. Kila vipimo vinapotoka mgonjwaakipimwa ni lazima ataambiwa kwamba ana tatizo la UTI.Namwomba Mheshimiwa Dkt. Ndugulile atueleze ni kwa niniwagonjwa walio wengi hasa vijijini na hata mijini hawawezi

Page 109: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

kutibiwa bila kuambiwa kwamba wana UTI? Ni kwa ninimaeneo mengi wanapatikana na matatizo hayo? Nilitakanijue ni vipimo gani vinavyotoa majibu mengi yanayofanana?Kwa sababu mimi napata wasiwasi isijekuwa kuna maeneomengine watu wanaambiwa kwamba wana UTI kumbe watuwanafanyabiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wazee maeneo mengiwanalalamika kwa kutokupata huduma ya kutibiwa bure.Hiki kimekuwa ni kilio kikubwa cha wazee, maeneo mengiukienda hata tunapoenda kwenye ziara wazee wengiwanatulalamikia kwamba Serikali ilisema itatoa huduma yamatibabu bure lakini bado huduma hiyo maeneo menginehawajaweza kutibiwa bure. Yapo maeneo ambayowanatibiwa bure lakini maeneo mengine bado wazeehawajapa huduma hiyo ya kutibiwa bure. Nafahamu Serikaliyangu ni sikivu, itafanya utaratibu ili wazee hawa wawezekupata huduma bure na hasa walete sheria Bungeni ili iwezekufanyiwa utaratibu kusudi itambulike kihalali kabisa kwambawazee wote sasa wanatakiwa kutibiwa bure.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayomachache, naomba niunge mkono hoja lakini nisisitizehospitali na vituo vya afya vile ambavyo havina wagangana wauguzi wapatiwe wataalam hao ili wananchi wetuwaweze kupata huduma bora.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naungamkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tumefikamwisho wa kipindi chetu cha uchangiaji. Nina mambo mawili,moja ni tangazo kutoka kwa Katibu wa Bunge.Mnatangaziwa kuwa kwaya ya SPA Church ya Yombo DovyaJijini Dar es Salaam ambayo ilitembelea Bunge siku yaJumatatu tarehe 6 Mei, 2019, kwa kushirikiana na Mbungewa Temeke Mheshimiwa Abdallah Ally Mtolea imetoa zawadiya vitabu kwa Wabunge wote kwa lengo la kusaidiakuongeza furaha ya kiroho na amani ya moyo. Vitabu hivyovitagawiwa bure kwa Wabunge wote na vitatolewa kupitia

Page 110: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

masanduku yetu ya nyaraka kwa maana ya pigeon holes.Kwa hiyo, mvichukue hivi vitabu ambavyo vitasaidia kwenyefuraha ya kiroho na amani ya moyo, naamini watu wotetunapenda kuwa na amani. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, jambo lingine ni lakukumbushana Kanuni yetu ya 154 kwa sababu tunapokaaBungeni hatuko peke yetu, wako wenzetu ambao huwahawaji siku zote lakini pia wapo wageni wanaokuja kujifunzanamna tunavyoendesha Bunge. Kanuni ya 154 inatuongozakwenye kutoa pongezi lakini pia kutoa pole zile ambazoBunge linapaswa kutoa. Bunge lilikwisha kutoa pole kwamsiba mkubwa uliolipata Taifa letu na kwa mujibu wa Kanunizetu watu wanapaswa kuendelea kwenye michango mojakwa moja.

Hata hivyo, wale ambao waliendelea kutoa pole hizohawakukumbushwa matumizi ya Kanuni hizi kwa sababumuda wao uliendelea kuhesabiwa. Niwakumbushe tumatumizi ya kanuni ambazo tumejitungia wenyewe ili wageniwetu wasione Wabunge ambao hawajatoa pole kwa namnafulani kwamba pengine wao hawatambui uzito. Kanuni zetuzinatuongoza, kwa hiyo, Bunge kama Bunge linatambua uzitowa jambo lil i lotupata kama Taifa. Wote mtakuwa nimashahidi kwa uzito huo huo Mheshimiwa Spika ameelekeahuko kwa ajili ya maziko. Kwa hiyo, Bunge kama Bungelinatambua jambo zito ambalo Taifa limetupata. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayo,nasitisha shughuli za Bunge mpaka saa kumi alasiri leo.

(Saa 7.00 Mchana Bunge Lilisitishwa hadi Saa 10.00 Jioni)

(Saa 10.00 Jioni Bunge lilirudia)

Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alikalia Kiti

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa, tukae. Katibu!

NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI:

Page 111: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka

wa Fedha 2019/2020

(Majadiliano Yanaendelea)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, majadilianoyanaendelea. Ilikuwa tuanze na Mheshimiwa Mwita Waitara,Mheshimiwa Kandege, atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt.Faustine Ndugulile.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaNaibu Spika, nakushukuru kwa kupata fursa ya kuwezakuchangia hoja iliyowasilishwa na Wizara ya Afya, Jinsia,Maendeleo ya Jamii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwa kuungamkono hoja na kipekee naomba uniruhusu nimpongezeMheshimiwa Waziri mwenye dhamana Mheshimiwa UmmyMwalimu na Naibu wake na Katibu Mkuu na Watumishi wotekwa ushirikiano ambao wamekuwa wakitoa kwetu sisi Wizaraya Ofisi ya Rais, TAMISEMI na kimsingi Watanzania wote nimashuhuda. Kazi kubwa ambayo inafanywa katikakuboresha afya za Watanzania haitiliwi mashaka hataMtanzania mmoja. Kwa hiyo, naamini kwa moto huu ambaoumeanza hakika Watanzania watarajie mambo makubwamazuri chini ya uongozi wa viongozi wetu hawa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wako Wabunge wengiambao wamechangia na karibu wote walikuwawakipongeza. Kama kuna mtu ambaye hakupongeza basilabda amepongeza kimoyo moyo lakini hata upande wa pilinao ni mashuhuda kwamba kazi nzuri inafanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna hoja ambazozimeibuliwa na ambazo sisi kama TAMISEMI ni vizuri tukajibukiasi. Katika hoja mojawapo ni pamoja na upungufu wa

Page 112: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

watumishi wa afya katika hospitali za Wilaya, vituo vya afyana zahanati. Tunakiri kabisa kwamba kuna upungufu, mpakasasa hivi tunao watumishi wapatao 56,881 sawa sawa naasilimia 48, kwa hiyo tuna upungufu wa asilimia 52, lakinimaelezo yapo ambayo yanajisheheni kwamba kwaninitunao upungufu kiasi hicho.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi sote Watanzania nimashuhuda kwamba kama kuna sehemu ambayo uwekezajiumefanyika ni katika Sekta ya afya, vituo vya afyavimeongezeka, zahanati zimeongezeka, kwa vyovyote vilelazima ionekane kwamba kuna gap, lakini pia kuna sababunyingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kwa mfano, katikawataalam ambao wanazalishwa tumekuwa na wataalamwachache sana hasa madaktari kuhusiana na masualamazima ya meno, lakini hata kuhusiana na suala zima lamionzi lakini ziko jitihada ambazo zimechukuliwa na Serikaliza makusudi kuhakikisha kwamba upungufu huu ambaounaonekana kwa sababu azma ya Serikali inayoongozwa naDkt. John Pombe Joseph Magufuli, afya ya Mtanzania ndiyokipaumbele. Kuna jitihada za makusudi ambazo zinafanywaili kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anapata huduma yaafya tena kwa umbali usiokuwa mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Ofisi ya Rais,TAMISEMI tumeomba na naamini kibali kitapatikana,tumeomba kuweza kuajiri watumishi 15,000. Lakini pianaomba nichukue fursa hii kupongeza Mfuko wa BenjaminiMkapa na wametusaidia wameajiri watumishi kama 300 kwamuda wa miaka miwili na sasa hivi wanafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi ambalo naombanitoe maelekezo katika Mikoa yote, tuhakikishe maeneo yalena hasa ya pembezoni na vijijini ambako ndiyo kunaupungufu mkubwa, tuhakikishe kwamba wataalam hawawanapelekwa kwa sababu kumekuwa na namna unakutamijini wako watumishi wa afya wengi lakini ukienda vijijiniunakuta wako wachache. Kwa hiyo, pale ambapo inatajwa

Page 113: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

upungufu, ukienda maeneo ya mjini hukuti upungufu kamaambavyo iko mijini. Nitoe maelekezo mahsusi tuhakikishekwamba inafanyika redistribution ili maeneo yenye upungufumkubwa yaweze kupelekwa hao wataalam.

Mheshimiwa Naibu Spika, wewe mwenyewe nishuhuda, tukiwa hapa wakati Mheshimiwa Waziri wa Utumishialiwasihi Wabunge kama kuna kituo chochote au zahanatiyoyote ambayo inalazimika kufungwa kwa sababu etihakuna mtumishi, aliwaomba Waheshimiwa Wabungewaandike barua ili tuweze kujaza pengo hilo na aminiWaheshimiwa Wabunge walitenda haki katika hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna hoja pia zimeibuliwakuhusiana na Community Health Workers, hoja ya msingitunaiunga mkono lakini ni vizuri tuka-balance hizi equation.Si rahisi pamoja na nia njema ya kuhakikisha kwambatunawaajiri hawa, lakini itakuwa si busara pale ambapo tunakituo cha afya au tuna zahanati ambayo tunashindwakuifungua kwa sababu hakuna mhudumu wa afya tukaendakuwaajiri hawa. Kwa hiyo, pamoja na nia njema ni vizuritukatumia structure iliyopo, tunao Maafisa Ustawi wa Jamii nirahisi kuweza kuwa-train na wakaweza kuwasaidia watu wetulakini azma kwa siku za usoni tutahakikisha kwamba nao watuwanaweza kuajiriwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabungewamelisema vizuri kuhusiana na suala zima la lishe. Hakunanamna pekee ambayo unaweza ukawekeza kuhakikishakwamba unawapata Watanzania wenye brain nzuri kamahatuwekezi katika siku 1,000 za mwanzo. Wataalamwanatuambia kwamba tunaanza kuhesabu tangu paleambapo mimba inatungwa mpaka mtoto anapokujakuzaliwa na miezi ile miwili ndiyo muhimu sana katika kuwezakuhakikisha tunawekeza katika hicho.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi Ofisi ya Rais, TAMISEMItumepokea, tunajua umuhimu wa jambo hili na ndiyo maananina kila sababu ya kumshukuru Makamu wa Rais pamojana Mheshimiwa Waziri Mkuu, tumewekeana mikataba na

Page 114: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

Wakuu wa Mikoa wote Tanzania, Mikoa 26 kuhakikishakwamba suala la udumavu linabaki historia na tumekuwana utaratibu wa kupimana kila baada ya miezi sita namuelekeo ni mzuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hiikuwaomba Waheshimiwa Wabunge na sisi kwa nafasi zetuza uongozi ni mabalozi, tunapofanya mikutano yetu ni vizuritukahakikisha kwamba elimu hii tunaifikisha kwa Watanzaniawenzetu. Maana hakuna namna pekee ambayo unawezauhakikisha kwamba watoto wetu wanakuja kushindana namataifa mengine kama hatujawekeza katika umri waowakiwa bado watoto wadogo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia niwasihi WaheshimiwaWabunge limesemwa juu ya kujihakikishia afya kwa kilaMtanzania. Namna pekee na Mheshimiwa Waziri mwenyedhamana atakuja aliseme kwa kirefu ni kuhakikisha kwambaWatanzania mwelekeo ni kujiunga na Bima ya Afya. Bima yaafya ndiyo mkombozi wa kuhakikisha kila Mtanzaniaanaenda kupata tiba pale ambapo anapatwa ugonjwatena tiba ambayo ya kisasa kabisa. Haipendezi pale ambapoinatokea Mtanzania anaenda wakati anaumwa,anashindwa kupata matibabu eti kwa sababu hana fedhaau hajajiunga na bima ya afya. Niwaombe WaheshimiwaWabunge sisi ni viongozi ni vizuri tukatoa hamasa kwaWatanzania, mataifa yote duniani utaratibu ndiyo huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia WaheshimiwaWabunge walichangia na alianza kusema MheshimiwaNachuma, akataja Mkoa wake wa Mtwara na hasa namaeneo yote ambayo ni mwambao mwa bahari. Kunamazalia mengi sana ya mbu, akaomba ifanyike jitihada zamakusudi. Sisi sote ni kwamba Tanzania tuna kiwanda chetucha viuadudu ambacho kipo pale Mkoa wa Pwani nakipekee Mheshimiwa Rais naomba tumshukuru aliwezakuwekeza shilingi bilioni 1.3 na fedha hizo zikatumika katikakununua viuatilifu hivyo kwa ajili ya kusambaza halmashaurizote Tanzania. (Makofi)

Page 115: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ni wajibu wetuWakurugenzi wote Tanzania tuhakikishe kwamba hichoambacho kilianzishwa na Mheshimiwa Rais kiwe endelevukwa kuhakikisha kwamba tunatenga kwenye bajeti zetufedha kwa ajili ya kuanza kununua viuatilifu kwa ajili yakuhakikisha kwamba tunapambana na mazalia ya mbu.Lakini pia ni vizuri hamasa ikatolewa kuhakikisha kwambamazalia ya mbu tunatokomeza. Wenzetu Zanzibarwameweza Tanzania Bara pia tunaweza, ni suala la kuamuana tukishirikishana sisi sote inawezekana.

Mheshimiwa Naibu Spika, itoshe katika hayo ambayosisi yamejitokeza tukaona tuyatolee ufafanuzi, naombaniendelee kuunga mkono hoja, ahsante sana kwa nafasi.(Makofi)

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba nichangie hoja hii kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kuhusuwahudumu wa afya katika ngazi ya jamii. Serikali imetoamafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii 10,000.Wahudumu hawa wamekuwa msaada mkubwa sanakwenye ngazi ya jamii kwa kuzuia vifo vya watoto na akinamama lakini Serikali haiajiri tena wahudumu hawa. NaombaSerikali ione namna ya kuwapatia motisha na siyo mishahara.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, bima ya afya. NaombaSerikali iharakishe Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote kwakuwa matibabu ni gharama na watu wengi wanapotezamaisha kwa kukosa pesa za matibabu. Pia watu wanaotumiabima wanakosa baadhi ya dawa za magonjwa makubwakama moyo na mengine. Hivyo, naomba bima hizo ziingizematibabu yote na siyo baadhi ya magonjwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, Maafisa Ustawi waJamii. Maafisa hawa ni muhimu sana lakini hawana bajeti yakutosha. Mara nyingi wanatumia fedha zao za mfukoni kwa

Page 116: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

ajili ya kazi za kutembelea na kufuatilia watoto wanaoishikatika mazingira hatarishi. Hivyo, naomba Maafisa Ustawi waJamii wapewe bajeti ya kutosha kwa ajili ya kutembelea nakufuatilia familia mbalimbali zenye matatizo pamoja nawatoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nne, ada ya usajili wa dentalclinics. Gharama za usajili wa clinic hizi ya Sh.1,000,000 nikubwa. Naomba gharama hizo zipunguzwe kwani ni hudumakwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. OMARI A. KIGODA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza kabisa, napenda kuwapongeza Waziri na Naibuwake kwa kazi kubwa wanayoifanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Handeni Mji niya zamani na kwa sasa inaelemewa sana na idadi yawagonjwa. Inahudumia majimbo almost manne na mpakasasa hakuna utaratibu wa kupata hospitali katika majimbohaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi langu, tuna zahanatieneo la Kwamagome ambalo Mheshimiwa Waziri Ummyalifika kwenye ufunguzi, tumefikia pazuri na ikiwezekanatunaweza kupafanya pale na kuwa kituo cha afya. NaombaWaziri aliangalie eneo hili ili kuondoa msongamano wawagonjwa kwenye hospitali yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, kule kwetuhatujapata mgao wowote kwenye kuongeza au kujengakituo cha afya. Tunaomba Wizara itufikirie na sisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba Hospitali ya Wilaya katika Manispaa ya Moshi.Manispaa ya Moshi ina mahitaji makubwa sana ya Hospitaliya Wilaya kwa vile Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi imezidiwa

Page 117: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

na wagonjwa na Hospitali ya KCMC pia imezidiwa nawagonjwa. Hospitali zote hizi mbili zinahudumia wagonjwakutoka maeneo mbalimbali nje ya Manispaa ya Moshi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Manispaa ya Moshi inaeneo ambalo imelitenga kwa ajili ya ujenzi huo wa Hospitaliya Wilaya. Hivyo, ni matumaini yangu kwamba Serikaliitalifanyia kazi ombi langu kwa niaba ya wananchi wa MoshiMjini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupandishwa hadhi vituovitatu vya zahanati kuwa vituo vya afya. Manispaa ya Moshiimeleta maombi ya muda mrefu Serikalini ya kupandishahadhi zahanati tatu za Shirimatunda, Msaranga na LonguoB. Maombi hayo ni muhimu sana kwa vile idadi ya watuinaongezeka kila siku katika Manispaa ya Moshi. Kutokanana ongezeko hilo, mahitaji ya huduma ya matibabuyanaongezeka kwa kasi. Naomba Serikali ipandishe hadhizahanati tajwa hapo juu kuwa vituo vya afya ili kuwasaidiawananchi kupata huduma kirahisi zaidi na kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwa niaba yawananchi wa Manispaa ya Moshi, Serikali itenge fedha kwaajili ya kuboresha kituo cha afya kimoja katika Manispaa yaMoshi ili kutoa huduma bora kwa wakazi wa Manispaa yaMoshi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Naibu Spika,nitangulie kwa kuunga mkono hoja hii ya Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumpongezaMheshimiwa Ummy Mwalimu na Naibu wake, MheshimiwaDkt. Ndugulile, bila kumsahau Katibu Mkuu wa Wizara hii,Mheshimiwa Dkt. Zainab Chaula kwa kazi nzuri wanayoifanyakatika nchi hii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na pongezi hizi,naomba kukukumbushia ahadi ya Mheshimiwa Waziri wa

Page 118: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alipokujaItigi katika Hospitali ya Rufaa ya St.Gaspar katika Siku yaWauguzi 2017 na kuahidi kutoa gari kwa Kituo cha AfyaMitundu ambacho kipo zaidi ya kilometa 100 toka Hospitaliyetu ya Wilaya ya Manyoni. Nia yangu ni kukukumbusha tuahadi hii aliyoitoa kwa wananchi wa Halmashauri ya Itigi,Jimbo la Manyoni Magharibi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nirudie kuunga mkono hojahii kwa asilimia mia moja, ahsante.

MHE. AISHAROSE N. MATEMBE: Mheshimiwa NaibuSpika, niipongeze sana Serikali kwa kazi nzuri inayofanya yakuboresha huduma za afya nchini kote.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuelezeachangamoto za Hospitali yangu ya Rufaa ya Mkoa waSingida. Hospitali hii inatoa huduma katika maeneo mawili.

Mheshimiwa Naibu Spika, ipo hospitali ya rufaa yazamani katika Kata ya Ipembe na hospitali mpya ya rufaailiyopo katika Kata ya Mandewa. Uendeshaji wa hospitali hizimbili kwa wakati mmoja imepelekea gharama za uendeshajikuwa kubwa kwa kuwa inatumika bajeti moja kulipia bili yamaji, umeme, ulinzi na usafi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa nini sasa Serikaliisimalizie Hospitali ya Rufaa ya Mandewa yale majengomuhimu kama maabara, pharmacy, wodi ya upasuaji kwamagonjwa ya kwaida na mifupa, wodi ya watoto, jengo lamacho na jengo la meno? Iwapo majengo hayayatakamilika yatasaidia sana hospitali ya rufaa ya zamaniiliyopo Kata ya Ipembe kuhamia hospitali ya rufaa mpya yaMandewa. Naiomba Serikali itenge fedha za kutosha ilikumaliza Hospitali hii ya Rufaa ya Mandewa kwa kuwamajengo ambayo yalishakamilika yameanza kuchakaa hatakabla ya kutumika.

Mheshimiwa Naibu Spika, hospitali yangu ya rufaa inachangamoto lukuki; haina madaktari bingwa wa kutosha,

Page 119: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

waliopo ni sita tu na kati ya hao sita hakuna daktari bingwawa magonjwa ya wanawake na watoto lakini pia ina wauguziwachache. Wauguzi waliopo katika hospitali hii ni 144 katiya 305 wanaotakiwa. Naomba Serikali itupatie watumishi wakutosha wakiwemo wauguzi kwani hospitali hii ndiyo tegemeola wananchi wa Mkoa wa Singida katika kupata huduma zaafya za kibingwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hospitali hii pia haina garila kubebea wagonjwa (ambulance), gari lililopo lilipataaccident takribani miaka mitano iliyopita. Jambo hilinimekuwa nikilileta kwenu mara kwa mara, naomba sanasana kwa niaba ya wanawake wa Mkoa wa Sindida ifikewakati sasa Hospitali hii ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ipatiwegari la kubebea wagonjwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hospitali zangu zoteza Wilaya ikiwemo ya Wilaya ya Iramba na Manyoni hazinamagari ya kubebea wagonjwa. Naomba sana hospitali hiziza Wilaya zipatiwe magari ya kubebea wagonjwa ili kuokoavifo vya akina mama na watoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja,naomba kuwasilisha.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Naibu Spika,maombi ya vifaa vya upasuaji. Naishukuru Wizara kwakuelewa hali halisi ya Hospitali ya Mafinga ambayoinahudumia Halmashauri ya Mafinga Mji, Mufindi DC naWilaya za jirani ikiwemo Mbarali (Madibira), Mlimba, IringaVijijini na Makambako na hivyo Serikali kutupatia fedha zakujenga na kuboresha Kituo cha Afya cha Ihongole angalauimeleta nafuu kwa Hospitali ya Mafinga ambayo pia ipokandokando ya barabara kuu ya Tanzania-Zambia (TANZAMI).

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na hudumakuendelea kuboreshwa, tumejikuta idadi ya watuwanaohudumiwa ikiongezeka hasa akina mama wajawazitoambao theluthi moja hufanyiwa upasuaji. Kutokana na hali

Page 120: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

hiyo, tulipata msaada kutoka Ubalozi wa Japan ambapotumejenga jengo la upasuaji. Hata hivyo, msaada huo ulihusujengo tu na siyo vifaa. Halmashauri tumejipanga natumenunua baadhi ya vifaa. Naomba Wizara ioneuwezekano wa kutusaidia baadhi ya vifaa ili tufungue natuanze kutoa huduma kwa baadhi ya vyumba kwa kuwajengo lina vyumba vitatu vya upasuaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mchango huuwa maandishi, naambatanisha barua ambayo niliwasilishakwako na maelezo ya ziada kuhusu mradi huu. Naaminichochote kitu, anything can make a difference. Nafahamumna jukumu kubwa kupitia MSD, tunaomba sehemu ya vifaatusaidiwe kwa kiwango chochote.

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa fursa ya kuchangia bajeti hii. NampongezaRais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa maono yakemakubwa ya kuwasogezea wananchi wa Tanzania hudumamuhimu za jamii, hususan katika sekta hii ya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sanaMheshimiwa Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo yaJamii, Jinsia, Wazee na Watoto; Naibu Waziri, MheshimiwaDkt. Faustine Ndugulile na Makatibu Wakuu wote kwa kazikubwa na ya kutukuka wanayoifanya kwa uadilifu, upendo,bidii na weledi mkubwa. Tunapongeza huduma kubwa zakisasa na utaalam mkubwa katika hospitali zetu za rufaa.Nipongeze utolewaji wa miundombinu ya vifaatiba namadawa. Tunapongeza sana juhudi za kukuza uwezo wawatumishi wa sekta hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na pongezi hizo,naomba nitoe rai kwa Wizara hii kuzingatia umuhimu na hajaya kuajiri watumishi wengi katika zahanati na vituo vya afya,hasa katika kada ya Medical Officers ambao wanahitajikakwa wingi sana. Naomba kutoa rai pia kwa Wizarakuhakikisha kuwa zahanati zilizojengwa katika vijiji vyetu kwanguvu za wananchi zinamalizika na zilizomaliziwa zipatiwevifaa na watumishi ili zifanye kazi.

Page 121: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Jimbo langu la Wilayaya Ileje, Kituo cha Afya Mbebe bado hakijamaliziwa na kwasasa kwa miundombinu ya Wilaya ya Ileje wananchiwanalazimika kupeleka wagonjwa Malawi ambako ni karibuzaidi kuliko kwenda Itumba kwenye Hospitali ya Wilaya.Zahanati ya Mapogoro hukohuko Mbebe haijamaliziwa nahivyo kuifanya Mbebe ikose huduma za afya kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi walijitoa kujengaKituo cha Afya Itale, tunaomba Serikali itusaidie fedha zakumalizia kituo hiki cha afya. Tunashukuru Serikali kwa kutoaambulance ndogo, tunaomba basi Kituo cha Afya cha Italekikamilishwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaiomba Serikali itusaidiekuwezesha Vituo viwili vya Ibaba na Lubanda vilivyomaliziwakwa fedha ya Serikali basi vizinduliwe ili vianze kazi.Mheshimiwa Ummy aliahidi ambulance Kata ya Lubanda,tunaomba sasa ipatikane.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Ikinga, Zahanati yaKikota imemaliziwa ujenzi bado kufunguliwa. Tunaombaifunguliwe ili wananchi wa Ikinga wapate huduma hii muhimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Isongole ni kubwana ipo kwenye Mji Mdogo wa Wilaya ya Ileje. Kata hii inawatu wengi sana lakini inakosa kituo cha afya na kuifanyaZahanati ya Isongole kuzidiwa na wagonjwa na kushindwakumudu mahitaji ya huduma za afya kwa wananchi. Sasahivi barabara kuu inajengwa na imepita Isongole kwa hiyokutakuwa na ongezeko kubwa zaidi la wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ileje ina miundombinumigumu sana na Mheshimiwa Waziri alishatembelea,anafahamu. Kata ya Ndola inahitaji kituo cha afyakupunguza adha kwa wananchi wa Ndola. Kata ina hosteliya wasichana na changamoto zikitokea wanakosa huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Itumba ndiyoMakao Makuu ya Wilaya na ndipo ilipo hospitali ya wilaya.

Page 122: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

Tunaendelea kuishukuru Serikali kwa kutupatia fedha zakujenga hospitali ya wilaya shilingi bilioni 1.5 pamoja nazilizotolewa siku za nyuma. Hospitali itakuwa na majengomuhimu saba na itajitosheleza lakini kwa sasa tunahitaji X-ray mashine ya kisasa ya radiologist na friji ya kuhifadhiadamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Isoko ni hospitaliya mission lakini imekuwa ikitoa huduma kubwa sana kwaWanaileje na kuunga mkono juhudi za Serikali. TunaombaWizara iwafanyie secondment Medical Officers kwenda Isokokuziba pengo. Hospitali ya Isoko haina uwezo wa kuajiriMedical Officers kuziba pengo lakini kwa kuwawanahudumia wananchi wa Ileje na Watanzania na kwakuwa wanashirikiana na Serikali, tunaomba sana Serikaliiridhie kutoa secondment kwa watumishi wawili au watatukwenye ngazi ya Medical Officer ili kukidhi ufanisi wa hudumazinazotolewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. JITU V. SONI: Mheshimiwa Naibu Spika, naombanichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa siku yaleo. Nimpongeze Rais wetu mpendwa, Mheshimiwa Dkt. JohnJoseph Pombe Magufuli, kwa kazi nzuri na kubwa anayofanyakatika sekta ya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwapongeze piaMheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Wakurugenziwote na wataalam mbalimbali waliopo Wizarani na katikataasisi zetu chini ya Wizara hii. Mheshimiwa Waziri ni msikivusana na anapokea ushauri kutoka kwa kila mdau. NaibuWaziri pia amekuwa mstari wa mbele kutoa ushauri wakitaalam na kuweka mfumo bora katika utekelezaji washughuli za Wizara. Wataalam wote hutupa ushirikiano wakaribu na pia elimu tunapohitajika.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe ushaurikatika maeneo machache ili kuboresha huduma. Kwanza,nishauri kuendelea kupunguza gharama zisizo za lazima ili

Page 123: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

kuongeza ufanisi kama mlivyopokea ushauri wangu wa ujenziwa vituo vya afya na hospitali kutoka shilingi bilioni 4.5 kituocha afya hadi milioni 500 au milioni 400 na Hospitali za Wilayakutoka shilingi bilioni 705 hadi shilingi bilioni 1.5, hali ambayoilifanya tujenge vituo vingi zaidi na pia hospitali nyingi zaWilaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri Kitengo chaManunuzi (procurement) cha MSD kiboreshwe na tuwe nateam ndogo nyingine ambayo itafanya kazi ya kuhakikimanunuzi. Naamini bado tunaweza kupunguza gharama zamanunuzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia niwapongeze kwakuendelea kutumia force account. Muhimu pia ni kutumiamfumo wa PPP katika kuboresha huduma za afya. Mfanoeneo la huduma za maabara, nchi nyingi huwa na wataalamna vifaa vya maabara ambazo wanashirikiana na hospitali,vituo vya afya na zahanati kutoa huduma. Siyo lazimatuwekeze sisi katika kila hospitali au kituo cha afya. Piahuduma za Radiology za X-Ray, Utrasound, CT-Scan, MRI,tushirikiane na watoa huduma private. Naamini kwa kufanyahivyo bei za huduma hizo zitateremka.

Mheshimiwa Naibu, nishauri pia suala la telemedicinelipewe kipaumbele. Hii itasaidia kusogeza huduma yamabingwa katika maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri kitengo chakutengeneza viungo bandia kiboreshwe. Watanzania wengiwenye uhitaji wa viungo bandia hushindwa kuvinunuakutokana na kuwa na gharama kubwa. Tuangalie namnaya kuboresha na kutoa huduma hii katika maeneo mbalimbalinchini badala ya maeneo machache kwa bei kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nishauri Serikali iangalienamna ya kuwa na mpango wa Bima ya Afya kwa Woteitakayokuwa ni lazima (universal health care insurance).Leteni sheria mapema Bungeni ili Watanzania wengi wapatebima ya afya.

Page 124: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nishauri tuendeleze serayetu ya kinga bora kuliko tiba. Katika magonjwa mengitunaweza kutoa elimu ya kinga badala ya kuingia gharamaya tiba.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika suala la usalama wachakula na lishe, nashauri Serikali tujikite katika kingakupunguza tatizo la lishe bora ili kuepuka tatizo la kudumaana utapiamlo. Nashauri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto ishirikiane na Wizara ya Kilimo, Mifugona Uvuvi, Maliasili na Utalii na Viwanda na Biashara ili kwapamoja tuweke mpango na mkakati wa kutokomezautapiamlo na suala la kudumaa (malnutrition stunting). Piaelimu zaidi juu ya namna ya kupata lishe na mazoezi kwa ajiliya magonjwa yasiyoambukiza (non-communicable diseases)itolewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, nishauri TFDA iweke vifaavya kupima mazao hasa ya mboga mboga na matundakatika masoko yetu yote makubwa. Leo hii tunakula vyakulahasa mbogamboga na matunda vilivyopigwa dawa (sumu)kabla ya kumaliza muda maalum wa tahadhari kumalizika(chemical residuals from insecticides). Pia katika mifugotunalishwa nyama na maziwa ya mifugo kutoka kwa mifugoiliyopigwa chanjo na dawa za matibabu kabla ya mudamaalum kuisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nishauri pia Serikaliiangalie uwezekano wa kuondoa kodi katika vifaa tiba navifaa wanaotumia wenye matatizo mbalimbali ya afya.Mfano baiskeli za walemavu na viti maalaum vya wagonjwa(wheel chairs) pamoja na magongo na vifaa mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, niombe pia Serikali isaidiekuboresha huduma katika Kituo cha Wazee Sarame-Magugu.Pia kutupatia X-Ray katika Kituo cha Afya Magugu.Niwashukuru kwa kupata vituo viwili Jimbo la Babati Vijijini,Magugu na Haiti. Naomba sana kupata vifaa vyote katikavituo hivyo ili kuboresha huduma za afya.

Page 125: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri Serikali iangalienamna ya kuboresha na kuweka utaratibu wa kuboreshasekta ya dawa za asili. Katika nchi mbalimbali hasa Bara laAsia na Mashariki ya Mbali (South East Asia), wamewezakuratibu, kuweka rekodi na kufanya utafiti wa mimea nadawa za asili kwa manufaa ya raia wao.

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa Tanzania katika kilaeneo kuna dawa za asili na zote hazina rekodi wala kufanyiwautafiti katika maabara ili kuwa na uhakika wa hizo dawa nanini kipo ndani yake (herbal medicine). Nashauri tungeanzishamafunzo ya dawa za asili katika vyuo vyetu. Tuna rasilimalinyingi sana ambazo zinaweza kutumika kuleta tiba mbadala(homeopathy na allopathy).

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, nashauri wataalam wajadi au wa asili wapatiwe mafunzo ya kitaalam. Mfano tunaowataalam wa asili wenye uwezo wa kufunga mifupa,kurudisha mifupa iliyosogea katika sehemu zake (dislocation),wakipatiwa mafunzo zaidi wanaweza kutoa huduma vizurizaidi. Hospitali ya Daseda Haydom wanawashirikisha nakuwasaidia kusoma X-ray ili wafunge mifupa vizuri. NashauriSerikali iweke maabara maalum kwa ajili ya kupima mimeambalimbali na dawa hapa nchini pamoja na kuweka rekodiza dawa hizo ili kupata dawa za uhakika na bora.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiboresha sekta hii na piakatika vipodozi (cosmetics) tunaweza kukuza ajira nakuongeza mapato na ikawa ni kivutio cha utalii. MfanoMorocco, Jordan, India, Indonesia, Thailand na nchi zinginezinapata mapato makubwa kutokana na dawa za asili navipodozi (cosmetics). Ni sekta kubwa sana, nashauri vyuovyetu vya tiba na maendeleo ya jamii viboreshwe sana.Mitaala yake iboreshwe na vifaa vya kufundishia na kujifunzaili wanaohitimu wawe na viwango vya juu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho nirudie, tuboreshevyuo vyetu vya uuguzi pamoja na vya afya (nursing andmedicine) nchini ili Watanzania wengi wasome na hata kamahakuna ajira nchini waweze kwenda nchi za nje. Tukiwa na

Page 126: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

wataalam wetu nje ya nchi, watatangaza nchi yetu na kuletamapato ya fedha za nje. Nchi nyingi za Asia hufanya hivyo.Huduma pia ya mazoezi ya viungo ni muhimu na wataalamni wachache (physiotherapists).

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: MheshimiwaNaibu Spika, kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungukwa kuniwezesha kusimama katika Bunge hili Tukufu nakuchangia machache kwa maandishi, hotuba ya bajeti yaWizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto. Pia, nachukua nafasi hii kumpa pongezi MheshimiwaWaziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na wataalam wa Wizaranzima.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inafanya mambomengi mazuri, hasa kuhusu mambo ya afya ikiwepo ujenziwa vituo vya afya na upatikanaji wa dawa. Natoa shukranikwa Hospitali yetu ya Mkoa/Rufaa Morogoro kwa kutupatiaX-ray ya kidigitali, tunashukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na umuhimu waHospitali ya Rufaa Morogoro, tunaleta ombi letu kuhusukupewa mashine ya CT-Scan ambayo ni muhimu sana. Hii nikukumbushia ahadi ambayo ilitolewa hapo awali na viongoziwetu wa taifa wakati wa ziara Morogoro. Nashukuru kwa yotemazuri yaliyotendeka kwa kutupatia gari la wagonjwa na X-ray, kwa imani hii naamini hata CT-Scan tutapewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri na naombaHospitali za Wilaya za Mkoa wetu za Gairo, Ifakara, MorogoroVijijini na Mjini ziendelee kupewa fedha na kujengwa nakukamilika. Mheshimiwa Waziri nasema haya kwa sababuHospitali ya Mkoa inazidiwa na wagonjwa (mrundikano wawagonjwa) kwani Wilaya za Mkoa hazina hospitali.

Mheshimiwa Naibu Spika, napongeza kwa ujenzi waKituo cha Afya Mikumi, majengo ni mazuri na hivi karibunikitaanza kutumika. Mpaka sasa ameletwa daktari mmoja,

Page 127: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

naomba na kushauri waletwe wataalam wengine zaidi kusudiwananchi wapate matibabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo nililoliona katika kituohiki ni ukosefu wa jengo la mortuary. Ujenzi mzima unaendeleakukamilika ila hakuna mpango wa mortuary. Naiomba Serikaliyangu ifikirie jambo hili kwani Mikumi, hususan Wilaya ya Kilosa,kuna watu wengi na hivyo hata jengo hili ni muhimu ingawajewatu hatutaki kusikia kifo.

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa pongezi kwa vituovya afya vinavyoendelea kujengwa. Nashauri mpango huuuendelee kuvifikia vituo vya afya ambavyo wananchiwamejenga na kuachia ngazi ya maboma.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukarabati wa Vituo vya AfyaDutumi na kumalizia majengo yaliyokaa muda mrefu, hilo niombi letu wananchi wa Morogoro Vijijini. Katika ziara zanguZahanati ya Hembeti ambayo inatumika pia kama Kituo chaAfya kwenye Kata ya Hembeti, Wilaya ya Mvomero, majengoyake yamechakaa sana tena sana. Naiomba Serikalizahanati/kituo cha afya hiki kikarabatiwe. Pia, hakunawataalam wa kutosha kuanzia madaktari hadi manesi. Kituohiki nashauri kiangaliwe vizuri ili kizidi kutoa huduma nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu ina tatizo lautapiamlo na hasa udumavu kwa watoto chini ya miakamitano. Tatizo kubwa ninaloliona ni elimu kwa wananchi.Nashauri elimu ya lishe ya mkakati na ya vitendo itolewe zaidi.Wananchi wakipata elimu ya kutosha kuhusu mambo ya lishehasa kwa akina mama wajawazito na akina mamawanaonyonyesha utapiamlo utapungua au utakwisha kabisahapa nchini Tanzania kwani kwa ujumla vyakula vya kutoshatunavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, vituo vya maendeleo yajamii. Naomba na kushauri ukarabati wa vituo hivi. Ni kweliwataalam wa maendeleo ya jamii wanatakiwa sana namuhimu kwa kusukuma maendeleo ya jamii yetu hapa nchini.Watumishi hawa ni muhimu sana kwa kusukuma maendeleo.

Page 128: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

Nashauri kila kijiji kiweze kupata Afisa Maendeleo ya Jamii ilikuharakisha maendeleo ya wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Ndoa. Na miminaungana na Wabunge wenzangu kusema kuwa kutokanana hali na maendeleo tuliyonayo sheria hii ni ya muda mrefuna imepitwa na wakati. Nashauri iletwe humu Bungeni iliibadilishwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ugonjwa wa malariaudhibiti wake uangaliwe kwa undani.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuchangia hayo,naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa NaibuSpika, kumekuwa na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawakena watoto wa kike, hasa majumbani na wapatapo shidahawana pa kuwatunzia wakati usuluhisho unaendelea hivyokupelekea kurudi katika majumba yao ambayo sio salamakwa wakati huo. Nashauri Serikali ijenge majengo salama kwausalama wa waathirika.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumekuwa na upungufu wawodi za wanawake, hasa katika Hospitali ya Makandana,Tukuyu. Tunaomba Wizara kwa kusaidiana na Halmashauriya Rungwe kutatua tatizo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimba za utotoni.Tunaomba Wizara itoe tamko kwa mabinti wapatao mimbakatika umri mdogo kurudi shule hasa walio chini ya miaka 15kwani kutorudi shuleni kunapoteza haki yao ya kupata elimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, dawa/chanjo ya mbwa.Kwa wagonjwa waliong’atwa na mbwa matibabu ni ghalisana. Tunaomba Wizara ipunguze kama sio kutoa burechanjo hizo kwa waathirika.

Mheshimiwa Naibu Spika, vipodozi hatarishi. Wizarana wadau wa afya kwa pamoja wafuatilie madawa/vipodozi

Page 129: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

hatarishi vinavyoathiri afya za wanawake na watoto.Kumekuwa na madawa yasiyo rasmi katika maduka mengina dawa kama za kuongeza makalio, matiti, uume na hatawanaojichubua, Wizara ya Afya, TFDA na TBS kwa umojawasaidie jamii yetu kutopata matatizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, uhaba wa watumishi.Wizara ipeleke wataalam hasa wa magonjwa ya wanawakena watoto katika Mkoa wa Mbeya, Wilaya za Chunya naMbarali, ndiyo zenye changamoto kubwa.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Naibu Spika,nianze kwa kuunga mkono hoja sambamba nakupompongeza Mheshimiwa Waziri kwa wasilisho lake zuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kuzuia miili yamarehemu (maiti) kama sababu ya deni la matibabuhususani katika Hospitali za Muhimbili na Mloganzila ni kerokubwa sana na ni jambo ambalo limekuwa likiigombanishaSerikali yetu na wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali iliangaliesuala hili na ilifanyie uamuzi wa kulifuta haraka iwezekanavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine nimapambano dhidi ya malaria. Tuna kiwanda chetu paleKibaha cha kutengeneza dawa ya kuulia vimelea vya viduduvya malaria. Kiwanda kile kinakabiliwa na changamoto yasoko. Lile agizo la Mheshimiwa Rais kuwa kila Halmashauriikanunue dawa pale halijatekelezwa sawasawa. NiiombeSerikali yangu sikivu kukiokoa kiwanda kile kwa kukipatia sokola uhakika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru na naungamkono hoja.

MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Naibu Spika,nampongeza Waziri na Naibu Waziri pamoja na timu nzimakwa kazi nzuri ya bajeti waliyotuletea.

Page 130: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeahidiwa gari lawagonjwa Kituo cha Afya Engusero. Tunaombayatakapopatikana basi tupatiwe gari.

Mheshimiwa Naibu Spika, upungufu wa watumishi.Tuna watumishi 296 na upungufu ni watumishi 210, tunaombatupatiwe watumishi hao kwa ajili ya zahanati, vituo vya afyana hospitali ya wilaya. Vilevile, tunaomba Waziri kutembeleaWilaya ya Kiteto kuzungumza na watumishi na kuangaliauchakavu wa Hospitali ya Wilaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho naunga mkonohoja, Mungu awabariki.

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Naibu Spika,nawapongeza sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, KatibuMkuu, Wakurugenzi na wafanyakazi wote wa Wizara hii kwakazi kubwa wanayoifanya. Hakika mnaitendea haki Wizarahii, nawatakia kila la kheri.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunashukuru sanakutembelewa na Mheshimiwa Waziri na Katibu Mkuu kwanyakati tofauti. Ziara zote zimezaa matunda ya msaada wakifedha na vifaa, ahsante sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Wilaya ya Uramboina vijiji 59, zahanati 22, tunaomba tusaidiwe kumaliziamaboma 8 ambayo yamejengwa ili tuongeze huduma kwawananchi. Tuna kata 18, vituo vya afya vipo viwili, kimojakimekamilika tunashukuru na kimoja kinaendelea kujengwa.Tunaomba tuongezewe vituo viwil i katika Kata zaSongambele na Vumilia ambapo wananchi wameanzamsingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Kituo cha Afya Uyogoambacho wananchi wanajenga kwa kushirikiana na marafikikutoka Uingereza. Tunaomba ahadi za Waziri zitimizwe zaambulance kwa kuwa ni mbali na Hospitali ya Wilaya natupewe shilingi milioni 20 alizoahidi ili kukamilisha kituokinachojengwa. Vilevile, tunaomba tupewe shilingi milioni 50

Page 131: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

alizoahidi Waziri alipotembelea Kituo cha Afya cha Usoke kwalengo la kukamilisha miundombinu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kupitia mradiwa ADB ulianza kujenga jengo la theater ambalo liko tangumwaka 2010. Tunaomba Serikali itusaidie kumalizia jengo hiloambalo linahitaji fedha zipatazo shilingi milioni 200.

Mheshimiwa Naibu Spika, Urambo haina chumba chawagonjwa mahututi (ICU). Kuna jengo lililoanza kujengwakwa mpango wa LGDG linaloweza kukamilika kwa gharamaya shilingi milioni 20. Tunaomba Waziri akumbuke ahadi hiina aitekeleze.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Mheshimiwa Wazirialiahidi kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha wodiya akina mama. Tunaomba tusaidiwe fedha hizo kwa ajili yaZahanati ya Itebulanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Urambo ina X-ray ya kizamani ya analogue. Tunaomba X-ray ya kisasa yadigital.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, tunaomba tuongezewewafanyakazi kwa kuwa tuna upungufu wa asilimia 48.

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Naibu Spika,nachukua nafasi hii kuwapongeza Viongozi wa Wizara hii,Waziri Mheshimiwa Ummy Mwalimu na Naibu wakeMheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile kwa kazi nzuriwanayofanya ya kusimamia Wizara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu utajikitakatika maeneo matatu. Kwanza, Hospitali ya Rufaa Kandaya Kusini inayojengwa Mtwara. Ujenzi wa Hospitali hiiumeanza muda mrefu na sasa umesimama. MheshimiwaWaziri alipotembelea ujenzi huu mwaka juzi aliahidi kuwa nibora jengo lililopo likakamilika na baadhi ya Idara zikaanzakufanya kazi. Nashauri ujenzi uendelezwe kwenye eneo hili

Page 132: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

na hospitali ifunguliwe kwa kuanza na idara ambazozinaweza kutumia jengo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, Hospitali ya Rufaa yaMkoa ya Mtwara (Ligula). Hospitali hii inahitaji ukarabatimkubwa wa majengo yake na ina idadi chache ya watumishikwa maana ya madaktari na wauguzi. Hatua zichukuliwe ilikukabiliana na changamoto hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, dawa za magonjwayasiyoambukiza (kisukari na shinikizo la juu la damu). Kunaongezeko kubwa la wagonjwa wa magonjwa hayo na kwakuwa wagonjwa hao hutumia dawa muda mrefu na bei zakeni za juu, nashauri Serikali iangalie kwa karibu tatizo hili kwakufanya yafuatayo:-

(i) Kuwa na programu za kutoa elimu kwa jamii ilikupunguza watu wanaoambukizwa;

(ii) Kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana kwa beinafuu hadi ngazi za chini; na

(iii) Kliniki za binafsi zidhibitiwe kwa kuwa zinatoahuduma kwa bei ya juu.

MHE. ENG. EDWIN A. NGONYANI: Mheshimiwa NaibuSpika, naunga mkono hoja kwa asilimia 100 kwa sababuMheshimiwa Waziri Ummy Ally Mwalimu na Naibu Waziri, Dkt.Faustine Ndugulile wametufanyia mambo makubwa ikiwa nipamoja na yafuatayo:-

(i) Wamehamasisha upatikanaji wa shilingi milioni 400kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Namtumbo na ujenziumekamilika.

(ii) Wamehamasisha upatikanaji wa shilingi milioni1,500 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Namtumbona ujenzi unaendelea.

Page 133: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

(iii) Wamenihamasisha mimi Mbunge wa Namtumbokutumia Mfuko wa Jimbo pamoja na mchango wangu binafsikukamilisha ujenzi wa zahanati saba za Njoomlole,Mwangaza, Namanguli, Mageuzi, Ruvuma, Kitanda naSongambele, pamoja na zahanati zinazoendelea kujengwakwa nguvu za wananchi na mchango kidogo wa mimiMbunge za Nahimbo, Ulamboni, Mwinuko, Ukiwayuyu, Msufini,Mhangazi na Luhangano. Hatua hii ikikamilika tutakuwatumeongeza vijiji 15 vitakavyokuwa na zahanati.

(iv) Wamehamasisha nguvu za wananchi zitumikekuunga mkono Mbunge wao katika kujenga Kituo cha Afyacha Mchomoro na kukamilisha ujenzi wa baadhi ya majengoya Kituo cha Afya cha Lusewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hiikumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namnaalivyotuchekecha sisi Wabunge na kugundua kipaji kikubwacha uongozi na unyenyekevu alionao Waziri na kumteuakuwa Waziri mwenye dhamana ya afya ya Watanzania.Nampongeza sana Mheshimiwa Rais na Waziri hongera kwakazi iliyotukuka unayoifanya. Naamini chini ya ushawishi waWaziri akiungwa mkono na Serikali ya Awamu ya Tanoinayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe JosephMagufuli, wana Namtumbo wanatarajia yafuatayo:-

(i) Vituo vya afya kwa umuhimu na au mpangilio huuwa Lusewa, Mchomoro, Mkongo Gulioni na Mtakaninivitaimarishwa kwa kujenga majengo mapya.

(ii) Vituo vya afya nane vilivyopo na vitakavyojengwakatika Wilaya ya Namtumbo viimarishwe kwa kupatiwawahudumu wa afya, vifaa tiba, vitendanishi na madawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Namtumbo inachangamoto kubwa za upatikanaji wa huduma za upasuaji.Kutokana na umbali uliopo kwenda Kituo cha Afya chaLusewa na Hospitali ya Mkoa kunakopatikana huduma hiyoya upasuaji, naomba tusaidie kwa uharaka utakaowezekana

Page 134: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

tupatiwe fedha za kujenga Kituo hicho cha Lusewa pamojana vituo vingine vitatu vya Mchomoro (ambako MheshimiwaRais ameahidi kuchangia shilingi milioni 100), Mkongo Gulioni(kinahudumia Kata sita za Mkongo Gulioni, Mkongo, Luchili,Limamu, Ligera na Lisimonji na mwisho Kituo cha Mtakaninikilichoahidiwa na Mheshimiwa Benjamini William Mkapa, Raiswa Awamu ya Tatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli huduma za afyabure kwa watoto wa chini ya miaka mitano, wajawazito nawazee wenye umri zaidi ya miaka 60 ni changamoto kubwalakini kabla ya miundombinu ya afya kukamilika kujengwa nikazi bure.

Mheshimiwa Naibu Spika, nirudie kukupongeza nakukushukuru kwa namna unavyoakisi dhamira ya MheshimiwaRais ya kuwagusa na kuwainua wanyonge katika sekta zakohususan sekta ya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha nanaunga mkono hoja.

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika,vifaa kwa ajili ya ICU. Pamoja na mazingira magumukijiografia kwenye visiwa vya Ukerewe bado Hospitali yaWilaya ya Ukerewe haikuwa na ICU. Hivi sasa tumepatamfadhili anayetujengea jengo la upasuaji (theatre). Hivyobasi, lililokuwa jengo la upasuaji linabadilishwa kuwa chumbacha wagonjwa mahututi (ICU) lakini patakuwa hakuna vifaakwa ajili ya chumba hicho. Naomba Wizara isaidie kutoa vifaakwa ajili ya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwenyeHospitali ya Wilaya ya Ukerewe (Nansio).

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la umeme. Shughuliza utoaji huduma za afya zinaathiriwa sana na tatizo laumeme. Mpango wa wilaya ilikuwa kutumia shilingi milioni70 kutoka mfumo wa RBF lakini pesa hizo zimezuiliwa mpakasasa kutokana na mgongano kati ya Wizara mbili, pesa hiziilikuwa zitumike kununua generator/solar system kamastandby power system. Naomba Wizara itusaidie kupata

Page 135: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

ruhusa ya kutumia pesa hizi kutatua tatizo la umeme kwenyeHospitali ya Wilaya ya Ukerewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, gari la wagonjwa. Baadaya ajali ya MV Nyerere tarehe 20/09/2018 katika Kisiwa chaUkara, Mheshimiwa Rais alielekeza ujenzi/ukarabati wa Kituocha Afya Bwisya ambacho kiko hatua za mwisho kukamilika.Tarehe 15/11/2018 Mheshimiwa Waziri wa Afya wakati akijibuswali langu Bungeni aliahidi kutupatia gari la wagonjwa kwaajili ya Kituo cha Afya Bwisya. Gari hili ni muhimu sana kuokoamaisha ya watu wetu katika visiwa hivi. Naomba gari hililitolewe na kupelekwa kwenye Kituo cha Afya Bwisya.

Mheshimiwa Naibu Spika, vituo vya afya. Ili kufikakatika Kisiwa cha Irugwa inakubidi utumie zaidi ya saa nnekwa usafiri wa majini. Hali hii ya kijiografia inaweka hatarinimaisha ya wananchi walio katika Visiwa hivi vya Irugwavyenye wakazi zaidi ya 20,000. Hivyo, Kituo cha Afyakinahitajika kwenye kisiwa hiki ili kuokoa maisha ya watu wetu.Kwa kuwa wananchi wameanza ujenzi wa Kituo cha AfyaIrugwa basi Wizara ituunge mkono ili tukamilishe kituo hiki kwakukiingiza kwenye mpango wa uboreshaji wa vituo vya afyanchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, watumishi na vifaa. Kwakuwa Kituo cha Afya Bwisya kinakamilika kama ilivyo Kituocha Afya cha Muriti, Wizara ifanye maandalizi ya kupelekavifaa na watumishi kwenye vituo hivi bila kusahau Hospitaliya wilaya ili wananchi wetu wapate huduma ili kukidhimalengo tarajiwa.

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Naibu Spika,Jimbo la Tabora Kaskazini lina kituo kimoja tu cha afya.Namwomba sana Waziri tuipandishe hadhi Zahanati yaIlolangulu iwe kituo cha afya ili kwa jumla tuwe na vituo viwilivya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Waziri naNaibu Waziri kwa kazi nzuri wanayofanya, hongereni sana.Pia nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuwajali

Page 136: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

wanyonge, Wilaya ya Uyui tumepewa Hospitali ya Wilayainayojengwa kwa shilingi bilioni 1.5 pia Kituo cha Afya chaUpuge kwa shilingi milioni 500. Namkaribisha MheshimiwaWaziri atembelee Jimbo langu na Kituo cha Afya cha Upugelakini pia Zahanati ya Ilolangulu ili ajionee mwenyewe ujenziuliofanyika hasa katika zahanati na akiridhia kiwe kituo chaafya.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, naomba gari lawagonjwa (ambulance) kwa ajili ya Kituo cha Afya chaUpuge.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Naibu Spika,naunga mkono hoja. Nampongeza Mheshimiwa Waziri UmmyMwalimu kwa hotuba nzuri ya Wizara ya Afya. NampongezaWaziri kwa utendaji mzuri na kuiongoza Wizara vizuri.Nampongeza Naibu Waziri, Mheshimiwa Dkt. Ndugulile kwauchapakazi wake na watendaji wakuu wa Wizara ya Afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Jimbo la NkasiKusini kupatiwa gari la wagonjwa liende Kata ya Kalaambayo iko kilomita 150 kufika Makao Makuu ya Wilaya.Umbali huu umesababisha vifo vingi vya akina mama nawatoto hasa wanapopata uzazi pingamizi kwa vile hudumazilizopo Kata ya Kala ni za kiwango cha zahanati ambapowataalam hawapo lakini pia hakuna gari la wagonjwa ilikunusuru wazazi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi Desderius John Mipatatuko Wilaya moja na Mheshimiwa Keissy ambaye alipewaambulance mbili. Nina wakati ngumu sana wakati kiuhalisiaJimbo langu kijiografia ni gumu zaidi. Kwa heshima nataadhima namwomba Mheshimiwa Waziri anipe gari mojatu la wagonjwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi la pili, watumishi waafya Wilayani Nkasi ni wachache sana. Pale Wilayaninamuona Dkt. Mwakapimba pekee ndiyo yuko active zaidi

Page 137: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

na mwenye uwezo mzuri wa kielimu na anafanya kazi sanasana. Yeye ni Medical Officer, wapo AMO’s wengine lakinikiutendaji utagundua kuwa MD’s ni muhimu waongezekeasiwe yeye pekee maana Mkuu wa Idara mara nyingi yukokwenye mambo ya utawala zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, manesi yaani wauguzi niwachache sana. Pia clinical officer ni wachache sana,zahanati nyingi zinaendeshwa na manesi na wahudumu.Watumishi wa usingizi ni wachache sana Nkasi au nisemehatuna. Naomba suala hili la kupatiwa watumishi lipewekipaumbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, vitambulisho vya wazeekutibiwa bado Halmashauri hawajatoa kipaumbele licha yakuagizwa na Madiwani mara kwa mara. Naomba uwaagizena kufuatilia hasa Nkasi District Council.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, nawaombeaWaziri, Naibu Waziri na watendaji wote wa Wizara Munguawajalie afya na nguvu ili muendelee kusaidia Watanzania.Kwa ujumla Watanzania wanaridhishwa na utendaji kazi waWizara hasa upatikanaji wa dawa, mmefanya vizuri sana.

MHE. ZAINAB M. AMIR: Mheshimiwa Naibu Spika, awaliya yote, niwapongeze Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimupamoja na Naibu Waziri, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulilekwa kazi nzuri wanazozifanya katika Wizara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Serikali fedhazinazopitishwa katika bajeti zifikishwe kwa wakati ili majukumuyaliyopangwa yaweze kutekelezwa kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kipimo cha Dengue ni ghalisana kwa wananchi wenye kipato cha chini. Mfano katikaHospitali ya Temeke ni Sh.40,000 na Regency Hospitali niSh.77,000 na hata kama una Bima ya NHIF ya Bunge unalipiacash hususan Regency Hospitali. Nashauri kutokana naugonjwa huu kuwa katika Mikoa ya Pwani, Tanga, Dar esSalaam na kadhalika na kipindi hiki cha mvua watu wengi

Page 138: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

huugua na kushindwa kupata fedha za kulipia kipimo chaDengue, Serikali ipunguze gharama za upimaji wa ugonjwahuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Rufaa TemekeDar es Salaam, eneo lake ni dogo na wodi nyingi ni chakavuna hazikidhi mahitaji ya wagonjwa. Nashauri zile wodi zazamani zibomolewe yajengwe maghorofa. Mfano mzuriRegency Hospitali Dar es Salaam eneo lilikuwa dogolikabomolewa wakajenga maghorofa ili kukidhi mahitajiwagonjwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Rufaa Muhimbilina Mloganzila Dar es Salaam. Naishauri Serikali ijenge jengola kusubiria wagonjwa kwa wale ndugu na jamaawanaowasindikiza wagonjwa wao watokao Mikoani iliwaweze kutoa msaada wa kijamii kwa wagonjwa waomaana siyo wagonjwa wote wana ndugu katika Mkoa waDar es Salaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Serikali itoe elimuya kutosha kwa wale wananchi wanaonunua miwani hovyobila kupimwa iwe kwa ajili ya urembo au la, wasivae bilakupewa ushauri kutoka kwa madaktari wa macho. Maanakuna baadhi ya wananchi wamepata matatizo ya machokwa kununua miwani bila kufuata ushauri wa daktari.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka jana nilitoa ushauriSerikali iondoe tozo katika maiti hususani katika hospitali zetuzote. Maana ni kero kwa wafiwa na wakati mwinginewalimuuguza ndugu yao kwa kipindi kirefu na walitumiagharama nyingi sana na marehemu wakati wa uhai wakealikuwa na mlipa kodi mzuri kwa kununua bidhaa mbalimbalikwa mahitaji ya kila siku. Hivyo, naishauri Serikali iondoe tozo/malipo kwa maiti katika hospitali zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na matangazomengi haswa Dar es Salaam ya Waganga wa Jadi navipeperushi vingi hugaiwa katika makutano ya barabara.Naishauri Serikali hawa Waganga wa Jadi watoe matangazo

Page 139: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

yao katika vyombo husika kama redio, televisheni namagazeti na siyo kubandika katika nguzo za umeme, miti nakutoa vipeperushi barabarani.

MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,nimpongeze Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Waziri wa Wizarahii, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri, KatibuMkuu na watendaji wote kwa hotuba nzuri yenye uelewa,pia kwa kazi nzuri wanayofanya kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nishukuru sana kwaongezeko la madawa na vifaa tiba. Ushauri; kwa kuwaHospitali ya Rufaa Kitete ina majengo ambayohayajakamilika, niombe Serikali ikamilishe ili yaweze kutumikahasa Chuo cha Uuguzi. Nishauri pia katika majengoyanayojengwa sasa ni vema yakazingatia ujenzi na jengo lamama Ngojea, ili wanawake wengi waweze kupumzikawanaposubiri kujifungua, ishirikiane na Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Wizara kutengasehemu maalum katika kila Kituo cha Afya kwa ajili yakutunzia watoto Njiti.

Mheshimiwa Naibu Spika, magonjwa; niombe elimuiendelee kutolewa kwa ajili ya ugonjwa wa dengue, Ini, iliwananchi wengi waweze kujua tiba yake, tahadhari pia. Kwanini ugonjwa huu wa dengue haupo kwenye Bima za Afya?Kwani wananchi wengi wanasumbuka.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile naomba Serikaliipeleke mashine za kupimia sukari katika Vituo vya Afya naZahanati ili kuokoa maisha ya wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Benki ya Wanawake; kwakuwa benki hii tangu ianze haijatoa gawio lolote mpaka sasana mimi nikiwa ni mhanga wa kutoa hisa (hisa Milioni mbili)nini hatima yangu? Kwa kuwa fedha yangu imekaa mudamrefu, je, naruhusiwa kuuza hisa zangu, ili niipate fedhayangu.

Page 140: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Benki ya Wanawake liniitafika Mkoa wa Tabora ili wanawake waweze kukopa.Niombe Serikali iweke Dirisha la ukopaji kwenye Benki ya TPB.

Mheshimiwa Naibu Spika, usafi wa mazingira, kwakuwa maeneo mengi hususan Hospitali ya Rufaa Kitete kunavifaa chakavu kama vile vitanda, meza na magari, je, hakunautaratibu wa kuuza au kuviondoa kwenye eneo la hospitalina kupeleka eneo lingine? Kwa kuwa vinawekwa eneo lanje na kusababisha mazalia ya mbu. Niombe Wizaraitembelee hospitali yangu na kuona hali halisi (Kitete Tabora).

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Ndoa ya mwaka1971; niishauri Serikali kuleta haraka Sheria ya Mabadiliko yaSheria Ndoa ili wanawake na watoto wapewe haki zao. Ukatiliwa kijinsia unaongezeka hapa nchini, kunyimwa haki wajanena kudhulumiwa mali zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono.

MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa NaibuSpika, pongezi kwa Serikali kwa ujumla na kwa Wizara kwanamna ya pekee kwa kazi nzuri. Changamoto za Wizara hii(Sekta ya Afya) ni nyingi na za muda mrefu na za ainambalimbali, hivyo, hata utatuzi wake unahitaji muda, rasilimalifedha na kadhalika, lakini taratibu zitapungua sana kutokanana kasi hii. Nawatakikakila la kheri.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto Kitaifa, zikonyingi bado, lakini hotuba ya Waziri Ukarasa 155 wa kitabucha hotuba umeainisha vipaumbele vya Wizara na Bajeti kwamwaka huu. Wakipata fedha kila mwaka, kamawanavyoomba watafanikiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika vipaumbele 11,nimechagua kipaumbele cha (iii) na cha (v) ambavyovinagusa pia moja kwa moja Jimbo la Tunduru Kaskazini naHalmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa ujumla.

Page 141: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Wataalam; uhabawa Wataalam Kitaifa ni 50% na Tunduru ni 35%. Serikaliiendelee kuzalisha Wataalam kupitia Vyuo vyetu vilivyopo,Mabaraza ya Wanataaluma na Bodi za Ushauri yafanye kazizao vema, ikiwa ni pamoja na kusimamia Professional Ethics,Kanuni za Kusimamia Taaluma ikiwemo mafunzo ya utarajalizikamilike na zitumike, pia (CPD - Continuing ProfessionalDevelopment) iwekewe msisitizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua za kushughulikianidhamu ya Wataalam zitokane na Vyombo vya Taaluma,isipokuwa kwa makosa yasiyokuwa na kitaalam, watumishiwaboreshewe maslahi yao, Vyuo viongoze udahili, uwiano(Ratio) kati ya Madaktari na Wataalamu wa Kada nyingineza juu na Wataalam wa Kada za Kati kwa mujibu wa ILOuzingatiwe. Hatua hii itatoa nafasi ya utoaji wa huduma bora,concentration na kupumzika vikiwa ni vichocheovinavyotegemeana.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto Halmashauriya Wilaya ya Tunduru na Jimbo la Tunduru Kaskazini; Hospitaliya Wilaya ni ya siku nyingi, imechakaa (miundombinu),tunaomba ifanyiwe ukarabati. Chumba cha upasuajimkubwa (major theatre), chumba cha upasuaji mdogo,(minor theatre) OPD, X –Ray, RCH, Maabara, Wardsmiundombinu yote hii ni chakavu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Vifaa tiba; Vituo vya Afyana Zahanati; Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Jimbo laTunduru Kaskazini lina Kata 24, lakini kuna Vituo vya Afya viwilina kimoja ambacho kinajengwa. Tunaomba Ambulanceziweze kusaidia kutoa huduma kwa Vituo vya Afya viwiliambavyo viko kilomita 64 pande tofauti (1800).

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba Kituo cha Afyacha Nakapanya kipatiwe fedha kwa ajili ya ukarabati kamatulivyobahatika kwa Kituo cha Matemanga. Hii inachagizwana ukweli huu wa idadi ndogo ya Vituo vya Afya, vitatu tukatika Kata 24. Zahanati pia ni chache, lakini kwa sasatukiboreshewa Vituo vya Afya tulivyonavyo kwa Wataalam,

Page 142: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

miundombinu na Vifaa tiba na kupatiwa Ambulancesitatusaidia sana.

MHE. MANSOOR S. HIRAN: Mheshimiwa Naibu Spika,nampongeza Mheshimiwa Waziri wa Afya, Maendeleo yaJamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kazi nzuri ambayoanafanya na wasaidizi wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue nafasihii kushukuru kwa kutuletea ambulance mpya kwa ajili yaKituo cha Mwamashimba.

Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Kwimbaambayo iko Ngudu ina changamoto nyingi; hatuna mashineya kufua nguo, x-ray ni ya zamani sana inaharibika mara kwamara, ni analogue, tunaomba digital, duka la dawa la MSD,tunaomba watufungulie pale kwenye hospitali yetu iliwananchi wapate dawa kwa bei nafuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Daktari wa Machowalituletea lakini sehemu ya kufanyia kazi hakuna, hatunachumba cha huduma ya macho, tuna jengo, lakinihalijakamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri watoto wetuwanaokwenda shule za msingi na sekondari wengi wanamagonjwa yafuatayo; pumu, sikosell, kisukari. Watoto wengiwanapata shida shuleni lakini Mwalimu hana uwezo wakuwasaidia kwa sababu hatujawawezesha. NashauriMheshimiwa Waziri awapatie emergency kit kwenye shulezote za msingi na sekondari na Walimu wafundishwe jinsi yakutoa first aid kwa mtoto ili wakati anapelekwa hospitali aweamepata huduma ya kwanza ili maisha yake yapone.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mji wa Hungumarwaunakua kwa kasi kubwa sana, tunaomba watujengee kituocha afya kwani zahanati zinaelemewa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

Page 143: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Naibu Spika,naunga mkono hoja. Nampongeza Mheshimiwa Waziri kwauwasilishaji mzuri sana na nimtakie mfungo mtukufu waRamadhani (Ramadhan Kareem).

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niishukuru sanaSerikali kwa kutuboreshea Kituo cha Afya cha Malya, kwaniaba ya wananchi wanaozunguka kituo hicho pamoja nawa Jimbo la Maswa, tunaomba kutupatia watalaam hasadaktari, aliyepo ni clinical officer, Wauguzi na wahudumupamoja na watalaam wa maabara, Wafamasia nakadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumkumbushaMheshimiwa Waziri ombi la gari kwa ajili ya hospitali ya Sumvekama barua yetu kwako tuliyowasilisha kutokana na jiografiaya eneo. Gari hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuokoamaisha ya wazazi na watoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitangulize ombila kukiboresha Kituo cha Afya cha Nyambiti. Nyambiti ni Mjiunaokuwa kwa kasi na kwa haraka sana kutokana na kuwana viwanda viwili vya kuchambua pamba. Kuna kituo chatreni (railway station), sekondari mbili, shule za msingi nne najamii inayoendelea kukua. Naomba katika mpango wauboreshaji wa vituo vya afya, Kituo cha Afya cha Nyambitikiwe kimojawapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimtakie Mheshimiwa WaziriUmmy kila la kheri katika njozi zake na Mungu atamsimamia.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono.

MHE. GRACE S. KIWELU: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kuchangia machache katika Wizara hii muhimu kwaafya ya Watanzania. Nianze kwa kuunga mkono hotuba yaKambi ya Upinzani ambayo imesheheni ushauri na mambomazuri kwa sekta yetu ya afya.

Page 144: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuipongezaTaasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete chini ya uongozi mzuri waProfesa Janabi na pongezi hizi ziende kwa madaktari wote,wauguzi na watumishi wote wa taasisi hiyo. Taasisi hii imekuwaikifanya kazi nzuri na imesaidia sana kupunguza gharama zamatibabu nje ya nchi, lakini bado kuna mtatizo ya vitendeakazi ambavyo vitarahisisha matibabu kwa wagonjwa na hatakwa watoa huduma. Mfano, kuwa na mashine zote kwa ajiliya vipimo hapo hapo hospitali kuzuia kwenda kufanya vipimonje.

Mheshimiwa Naibu Spika, Taasisi hii imekuwainakusanya fedha nyingi, lakini pale inapoomba tena fedhaambazo walikusanya wao hawapati. Mfano, mwaka janawaliomba bilioni nne, hawakupata wakati waliweza ku-savezaidi ya shilingi bilioni 12 za kwenda kutibu wagonjwa nje yanchi. Nashauri Serikali itenge 30% ya mapato hayo ilikuwawezesha kuboresha huduma kwa wagonjwa nakurahisisha kazi kwa madaktari wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, udhaifu wa vipimo vya tibakatika hospitali zetu, kumekuwa na tatizo hili kwa wagonjwakupewa majibu tofauti na maradhi waliyonayo na hiihusababisha wagonjwa kutopona maradhi waliyonayopamoja na kupewa dawa ambazo si sahihi kwa magonjwahayo na kufanya dawa hizo kuwa sumu mwilini, badala yakuwa tiba na hata kusababisha vifo kwa wagonjwa wetu.Wanaopona ni wale wenye uwezo wa kwenda hospitalinyingi kwa ajili ya kupima upya au kwenda nje ya nchi. Je, niwangapi ambao hawana uwezo huo wanapoteza maisha.Nashauri Serikali kuchukua hatua kwenye suala hili ili kunusurumaisha ya Watanzania na kuhakikisha umakini unakuwepo.

Mheshimiwa Naibu Spika, uwajibikaji wa watumishi waSekta ya Afya; zipo taratibu na sheria zilizowekwa kwa ajili yauwajibishaji wa watumishi wa afya, yapo Mabaraza yaMadaktari na Baraza la Wauguzi; haya ndiyo yenye jukumula kuwawajibisha na si vinginevyo. Toka Awamu hii ya Tanoimeanza tumeona viongozi wa kisiasa na wasiokuwa namamlaka wala taaluma hiyo kuingilia kuwawajibisha

Page 145: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

Madaktari na Wauguzi pasipo kufuata taratibu. Tunajua upoupungufu unaofanwa na watumishi hao, lakini ni muhimukufuata taratibu zilizopo. Tusipofanya hivyo tunapunguzamorali wa kufanya kazi kwa watumishi hao muhimu wa sektaya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilishamchango wangu huo mdogo wa sekta hii ya afya.

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika,nachukua nafasi hii kuipongeza Serikali yetu ya Awamu yaTano chini ya Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli kwa jitihada zake za kuboresha huduma ya afyakote nchini hususan ujenzi wa miundombinu ya majengonchini kote; kupunguza upungufu mkubwa wa dawa navifaatiba kote nchini; kupunguza upungufu mkubwa wawatumishi wa kada za afya kote nchini; kupambana namaambukizi ya VVU nchini na mpango mkakati wake wakuboresha sekta hii kila mwaka, hali inayowafanya wananchikuwa na imani kubwa kwa Serikali yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara itazame upyamtawanyiko wa Madaktari katika Hospitali za Wilaya naMikoa ili kuhakikisha angalau kila hospitali inapata mtaalammmoja kwa kila kitengo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Serikali iangalie sera yafamilia kutunza wazee na watoto kupitia familia zao badalaya kutelekeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, maombi ya Hospitali ya Mjiwa Mbulu kupatiwa gari la kusafirisha wagonjwa(ambulance) kwani gari l i l i loko limechakaa sana nawagonjwa wengi wanapata rufaa ya kupelekwa Hospitaliya Rufaa ya Haydom na KCMC Moshi nako ni mbali sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi la Tarafa ya Nambiskatika Halmashauri ya Mji wa Mbulu haina hata kituo kimojakatika kata zote tano na ni mbali kutoka Hospitali ya Wilaya

Page 146: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

hali inayosababisha akinamama wajawazito kukosa hudumana kutembea zaidi ya kilomita 30 mpaka 40 kufika Mbulu Mjini.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho naombaMheshimiwa Waziri wa Afya afanye ziara katika Jimbo laMbulu Mjini hususan Tarafa hiyo ya Nambis kwa kuwaalishaahidi kufanya ziara hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwaasilimia mia moja.

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Naibu Spika,nampongeza Mheshimiwa Waziri na Katibu Mkuu kwa kazinzuri wanazofanya. Nashukuru kwa kuimarisha huduma yaafya ya Mama na Mtoto hali ambayo imesababisha katikaHospitali ya Temeke mwezi Machi hakuna kifo cha uzazi. Yotehayo yametokana na kuimarika kwa huduma zote za afyaya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Temeke.

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo yafuatayoyazingatiwe (changamoto):-

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba mashine za CTScan kwa Hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam, Temeke,Mwananyamala na Amana. Hospitali hizo hazina mashineza kufulia nguo, mashuka mpaka yapelekwe Muhimbili jamboambalo linafanya kipindi fulani mashuka yanapunguahospitalini.

Mheshimiwa Naibu Spika, gharama kubwa zamatibabu kwa hospitali zinazopitia Wakala wa CRDB,unatakiwa ununue kadi kwa Sh.10,000 au utumie ya Wakalakwa Sh.2,000 kila unapokwenda hospitali. Mifumo ya Serikaliitumike, kwani inaweza kusaidia zaidi wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, malipo ya fedha kwa maitini changamoto kubwa. Mtu anapofariki na deni la dawaanatakiwa kulipiwa na ndugu, unafikia wakati nduguwanashindwa kulipia hapo viongozi tunashirikishwa na maiti

Page 147: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

kukaa muda mrefu. Naomba Serikali watoe ufafanuzikuhusiana na jambo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, unapoenda na mgonjwamara nyingine Emergeny Muhimbili unamlipia mgonjwa, tenaunapewa bill ya dawa usiku Sh.500,000 na zaidi, lakini baadaya sekunde unakuta mgonjwa amefariki. Kutokana na panicunaacha kila kitu, kwa nini tusiwe na kianzio cha dawa kwawagonjwa wanaokuja kuanza matibabu kabla ya kupewabill?

Mheshimiwa Naibu Spika, hospitali/zahanati yaMbagala Zakhem imezidiwa sana, eneo ni dogo nawananchi wanaohitaji huduma ni wengi sana kutokana nakukua kwa Mji wa Mbagala na ongezeko kubwa la watu.Pamoja na jitihada za halmashauri kujenga zahanati ya MajiMatitu na Charambe, lakini jiografia inakataa kwa kuwamgonjwa akitoka Zakhem anaenda Temeke na Zakhem nikatikati ya Mji wa Mbagala. Naomba Serikali isadie hatakujenga ghorofa la OPD kwa wagonjwa wa kawaida.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwaasilimia mia moja.

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa NaibuSpika, napenda kuunga hoja mkono na kuchangia kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sanaMheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Watendajiwote kwa kazi nzuri inayoonekana. Hata hivyo, badoningependa kushauri na kujua hatima ya uanzishaji wa Chuocha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) maeneo yaAmani -Muheza. Majengo ambayo Mheshimiwa Waziriameyaona yanazidi kuharibika bila kutumiwa, ningeshukurukama suala hili litapewa umuhimu wa kipekee. Aidha, badotunakumbushia suala la gari la wangonjwa, (Ambulance)ambapo katika Jimbo la Muheza hatuna kabisa.

Page 148: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la dawa ya nyokakupewa bure kwa wananchi naomba lizingatiwe kwani beiya dawa hizo ni ghali sana.

MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Naibu Spika,awali ya yote napenda kuipongeza sana Serikali ya Awamuya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John PombeJoseph Magufuli na Wizara ya Afya kwa juhudi kubwazinazoonekana za kuongeza na kuboresha huduma za afyana usafi wa mazingira nchini. Hivyo kwa dhati kabisa naungamkono hoja kwa asilimia mia moja na kuwatakia utendajiuliotukuka.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishukuru sana Serikali kwafedha za ujenzi wa hospitali shilingi bilioni 1.05 na ukarabatiwa kituo cha afya cha Mgori shilingi milioni 400 na Msangeshilingi milioni 700. Sambamba na mafanikio haya, tulipatapia usajili wa Hospitali ya St. Carolos Mtinko kuwa HospitaliTeule ya Wilaya. Sambamba na upatikanaji wa dawa kwakiwango cha kuridhisha, hongera sana kwa MheshimiwaUmmy na timu yake kwa mafanikio haya katika Jimbo laSingida Kaskazini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye mafanikio hakukosikuwa na changamoto, Jimbo la Singida Kaskazini linawananchi zaidi ya 250,000 ambapo kwa wastani wa watu5,000 kwa kituo cha afya tuna uhitaji wa zaidi ya vituo vitatuvya afya ili kuboresha utoaji wa huduma za afya. Hivyoniombe Wizara kwa moyo wa dhati kutusaidia fedha zaukarabati kwa kituo cha afya cha Ilongero na angalauukamilishaji wa majengo yaliyoanzishwa na wananchi kwaKata za Ngimu na Makuro ambayo yana zaidi ya miaka nanekusubiri kupauliwa. Ningeshauri kwa hatua ya sasa tuombeshilingi milioni 300 kukamilisha hatua ya awali tukisubiri upanuzikatika awamu zinazokuja.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunatambua pia juhudi zaSerikali katika kuongeza Watumishi wa Sekta ya Afya, hivyoniombe sana Serikali kutusaidia watumishi katika HospitaliTeule ya Wilaya (St. Carolos Mtinko) na zahanati na kituo cha

Page 149: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

afya. Vilevile uboreshaji na usimamizi wa Maendeleo ya Jamiiunahitajika maana kuna huduma zisizoridhisha kabisa kwawananchi hasa vijijini. Hii inatokana na usimamizi usioridhishana ukosefu wa vitendea kazi ambavyo vimekuwa ndiyovisingizio vya kutokutekeleza wajibu wao. Mheshimiwa Waziritumefanya kazi kubwa ila tusipoangalia watendaji hawawatatuangusha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa wananchitutaendelea kushiriki katika miradi ya maendeleo inayopatafedha kutoka Serikalini na kuendelea na ujenzi wa zahanatikatika vijiji vyetu ili kuunga mkono juhudi za Serikali kuboreshahali ya huduma nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Naibu Spika,naipongeza Wizara ya Afya kwa juhudi inazofanya zakuboresha Sekta ya Afya nchini. Katika Jimbo la Korogwelenye tarafa tatu na kila tarafa ikiwa na kituo cha afya, tunagari moja tu la kubebea wagonjwa. Gari ambalo na lenyewelimechakaa sana maana ni la muda mrefu, naiomba sanaWizara kwa unyenyekevu mkubwa watusaidie tupate gari lawagonjwa maana vituo vya afya viko mbali na hospitali.

Mheshimiwa Naibu Spika, tulipokea fedha za ujenziwa Kituo cha Afya kipya katika Kata za Mkumbara, kituokimekamilika. Tunaiomba Wizara kwa kushirikiana naTAMISEMI kutupatia vifaa ili kituo hiki kianze kufanya kazi yakutoa huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, upungufu wa watumishikatika Wilaya ya Korogwe kwa zaidi ya 46%; tunaiombaWizara kusaidia upatikanaji wa watumishi hawa ili kuboreshahuduma za afya wilayani.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuboresha na kuratibuvizuri huduma za wazee, ni vyema Serikali ikaandaa Sheriaya Wazee kama ilivyo kwa watoto.

Page 150: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

Mheshimiwa Naibu Spika, viko vituo vya afya vyamuda mrefu kama Kituo cha Afya cha Magoma na Bunguambavyo vinahitaji ukarabati na upanuzi. Pamoja na uhitajiwa ukarabati na upanuzi, pia vifaa kama vitandavimechakaa sana vinahitaji kubadilishwa kama siyokuongezwa. Naiomba Wizara ianzishe utaratibu wa kuongezavifaa kwenye vituo vya afya kwa awamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ustawi wa Jamii; viko vituovya kulelea watoto/makao ya watoto ambavyo havinahadhi ya kuwa makao ya watoto na vingine vinatuhumiwakwa kashfa mbalimbali kama unyanyasaji na ukatili wa kijinsiana Maafisa Ustawi walioko wilayani baadhi yao siyowaaminifu, ni vyema Wizara iimarishe utaratibu wa ukaguziwa makao ya watoto.

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Naibu Spika,pongezi kwa Serikali kwa kutujengea Kituo cha AfyaMalangali, Kata ya Malangali ambacho kitatoa hudumakatika Kata tatu za Ihwanza, Idunda na Malangali yenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, pongezi pia kwakutujengea Hospitali ya Halmashauri ya Mufindi ambayoitahudumia kata 27 katika Wilaya ya Mufindi pia itatoahuduma kwa watu wote ndani na nje ya Watanzania sababuni Halmashauri yenye wafanyakazi wengi sana na wawekezajiwengi wakubwa na wadogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali kumaliziaKituo cha Afya cha Kata ya Mtwango na Kituo cha Afya chaKata ya Mninga. Serikali imalizie ujenzi wa Zahanati katikaKijiji cha Nzivi, Kinegembasi, Iramba, Nyigo, Udumka naIkaning’ombe.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Serikali ituleteeWatumishi katika vituo vyetu tuna tatizo kubwa la watumishikatika Jimbo la Mufindi Kusini. Nitashukuru sana kama Serikaliitatekeleza kwa muda maombi hayo.

Ahsante na naunga mkono hoja.

Page 151: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA: Mheshimiwa NaibuSpika, awali ya yote, naunga mkono hoja, lakini pia naombakumpongeza Waziri, Naibu Waziri na Watendaji wote waWizara kwa kazi nzuri wanayofanya. Pamoja na kazi nzurizinazofanywa na Wizara, naomba kuchangia hoja kwakuangazia maeneo machache kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, uhamasishaji waakinamama kujifungulia zahanati, vituo vya afya na hospitali.Kuna changamoto kubwa ya wodi za kujifungulia, wataalamna vifaa katika facilities tulizonazo katika Wilaya ya Longido.Vijiji vingi havina zahanati na kwa vichache viliyonavyo nafasina huduma hazitoshelezi kulingana na uhitaji.

Naomba Serikali iongeze kasi katika kujenga zahanatina vituo vya afya katika vijiji na Kata za Ketumbeine,Kimokouwa/Namanga na Tarafa ya Enduiment.

Mheshimiwa Naibu Spika, Suala la Afya kwa Umma(Public Health); Wilaya ya Longido tuna changamoto kubwaya kutokuwa na gari la kuzoa taka kwenye miji yetu midogona pia gari la kunyonya maji machafu vyoo vinapojaa.Naomba kumuuliza Waziri kuwa Serikali ina mpango gani wakuhakikisha kuwa watu kila wilaya (Halmashauri) imepata garila taka na la kunyonya maji machafu kwenye vyoo hasa vyaTaasisi za Umma kama hospitali, shule na kwingineko?

Mheshimiwa Naibu Spika, upatikanaji dawa kwenyezahanati na vituo vya afya; katika Wilaya ya Longido, tunakata ambazo zinategemea zahanati moja tu kamaNamanga ni kuwa Idadi ya Wakazi ni kubwa sana (zaidi yawakazi 12,000) mgao wa dawa wanayopata kila baada yamiezi mitatu toka MSD hazimalizi hata mwezi mmoja kablaya kwisha na wananchi hulazimika kwenda kununuamadawa kwenye maduka ya binafsi. Hali hii imepelekeawananchi kutoona manufaa ya kujiunga na Mfuko wa Bimaya Jamii (CHF) kwa sababu hawapati dawa nyakati zote.Naomba kuishauri Serikali kugawa dawa kulingana na idadiya watu na wanaohudumiwa katika kituo husika badala yakuangalia kiwango kuwa ni zahanati au kituo cha afya.

Page 152: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

Mheshimiwa Naibu Spika, Mandatory Health Cover,ulazima wa kila mtu/Mtanzania kuwa na Bima ya Afya);naunga mkono hoja ya kutaka kila Mtanzania kuwa na Bimaya Afya, lakini nashauri kuwa kabla ya kupitisha Sheria yakusimamia zoezi hili, Serikali ihakikishe kuwa kila kituo chahuduma ya Afya (Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali)kinakuwa na dawa zate za msingi wakati wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, Uhaba wa nyumba zaWahudumu wa Afya hasa vijijini; katika Wilaya ya Longidotuna changamoto kubwa ya nyumba za Wauguzi hasakatika Zahanati zetu za vijijini. Kwa mfano katika Kijiji chaLosirwa, Kata ya Iloinenito, Tarafa ya Longido, Madaktari naNesi wanaishi ndani ya zahanati kutokana na ukosefu wanyumba za kuishi na kijiji kilichoko katika eneo lenye mazingiramagumu kwa barabara, mawasiliano na hata maji.Naomba Serikali itenge bajeti ya kusaidia maeneo kamahayo katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumalizia ujenzi wa vituovitatu vya afya, naomba kushukuru Serikali kwa kuwailitutengea fedha mwaka uliopita kwa ajili ya ujenzi wa vituoviwili vya Afya – Kata ya Engiromibor shilingi milioni 400 naKata ya Kimokouwa shilingi milioni 700. Kwa Vituo hivi vikokatika hatua za umaliziaji na fedha tulizopewa zimemalizika,naomba Serikali itenge tena fedha katika bajeti hii ili tuwezekumalizia Kituo cha Engareneibor kinahitaji shilingi milioni 269kumalizika ni Kimokouwa tunahitaji shilingi milioni 310kumalizia.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile tuna Kituo cha Afyakipya tulichoanza kujenga kwa nguvu za wananchi katikaTarafa ya Ketumbeine, Kata ya Ketumbaine. Tumewezakujenga hadi kupaua na sasa naomba Serikali ituunge mkonoili kumalizia kituo hicho mwaka huu wa fedha ili kianze kutoahuduma kwa wananchi wa vijiji 20 vya Tarafa ya Ketumbeineambao kwa miaka yote wamekuwa wakifuatilia huduma zaafya Longido ambavyo kwa vijiji vingine ni zaidi ya kilomita110 kwenye barabara mbovu za vumbi.

Page 153: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,naomba tena kusema naunga mkono hoja.

MHE. DKT. HADJI H. MPONDA: Mheshimiwa NaibuSpika, naunga mkono hoja ya Waziri, lakini pia naipongezaWizara yote kwa ujumla kwa kutekeleza majukumu yao kwaufanisi pamoja na changamoto ya ufinyu wa Bajeti (fedha)zinazowakabili.

Mheshimiwa Naibu Spika, huduma za kinga hususanchanjo ni muhimu sana katika suala la afya za watoto miakawalio na umri wa chini ya miaka mitano na wanawakewajawazito. Ili Wizara iweze kutekeleza kwa ukamilifuhuduma hii inahitaji uwepo wa dawa, chanjo na vifaa vyakutolea chanjo pamoja na usafiri.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Malinyiinatekeleza huduma za chanjo kwa ugumu sana kwakutokuwepo na gari la chanjo. Kubwa zaidi wilaya inakabiliwana uhaba mkubwa na magari, hivyo kusababisha Idara yoteya Afya katika Wilaya ya Malinyi haina kabisa gari lakuhudumia shughuli za afya ikiwemo huduma za utoajichanjo.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kutokuwepo na garila chanjo au gari maalum kwa huduma za afya katika Wilayaya Malinyi; nimemtaarifu Waziri wa Afya Mheshimiwa UmmyMwalimu naye aliahidi kutupatia gari moja zitakapowasili garimaalum za chanjo mwishoni kwa 2018. Gari hizo za chanjozimefika, lakini Wilaya ya Malinyi haijatengewa gari hatamoja, tunaomba gari moja toka Wizara ya Afya kwa hudumaza afya katika Wilaya ya Malinyi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

MHE. EDWARD F. MWALONGO: Mheshimiwa NaibuSpika, Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa mikoainayojengewa Hospitali za Rufaa. Hospitali ya Mkoa waNjombe imewekwa jiwe la msingi na Mhe. Dkt. John PombeJoseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Page 154: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

Mheshimiwa Waziri katika maelezo yake kabla kuwekewa jiwela msingi mbele ya Mheshimiwa Rais na mbele ya umati wawananchi wa Njombe Mjini, aliahidi hospitali yetu itaanza kazimwezi Julai na maelezo hayo yalirudiwa tena wakati wakumkaribisha Mheshimiwa Rais kuweka jiwe la msingi.Wananchi wa Njombe tungefurahi sana kuona Hospitali yetumpya inaanza kutoa huduma kama alivyoahidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jambo ambalo linanitiashaka wakati Mheshimiwa Waziri akiwasilisha bajeti yakehajaonesha bayana kama hospitali hii itafunguliwa kamaalivyoahidi. Nimepitia Kitabu cha Hotuba sijaona kabisa fungumahususi kwa vifaa vya hospitali vipya. Naomba wakati wakuhitimisha hotuba, Mheshimiwa Waziri atoe kauli ya Serikalindani ya Bunge kututhibitishia wananchi wa Mkoa waNjombe kuwa hospitali yetu itaanza kutoa huduma kamaalivyotuahidi. Vinginevyo namfahamisha mapemaMheshimiwa Waziri kwamba nitazuia shilingi ya mshaharawake.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. MUHAMMED AMOUR MUHAMMED: MheshimiwaNaibu Spika, awali ya yote ni vyema nikamshukuru MwenyeziMungu wa rehema kwa kunipatia afya njema na busara yakuweza kuchangia mada il iyopo hapa mezani. Pia,nikushukuru kwa kunipa fursa nami niweze kuchangia hojahii.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa homa yamatumbo ya kuendesha, imekuwa ni tabia ya kawaida kilabaada ya miongo ya mvua hutokea maradhi ya milipuko yamatumbo. Ni vyema Serikali ingefikiria zaidi namna yakuwalinda wananchi wetu ili kuzuia maafa haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu masuala yamaambukizi ya UKIMWI, ni hali yenye kutisha, mazingira yakupambana na UKIMWI hayajaridhisha kabisa, bado vijanawetu hawajakuwa na hadhari ya kutosha na maambukizibado yanaendelea kutisha.

Page 155: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

Mheshimiwa Naibu Spika, niende sasa kuhusiana namaradhi yasiyo ya kuambukizwa. Kumekuwa na hadharikubwa kuwaeleza wananchi kufanya mazoezi na timumbalimbali zimeanzishwa ili kukidhi haya mahitaji lakini je,Serikali ina mkakati gani mahususi wa kulisimamia hili nakulipigia debe kwa wananchi wote hasa vijijini?

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niende kwenyemedical instruments kama ct-scan, ultra sounds, x-rays tube.Hivi vyombo ni muhimu na ni bado havijaenea nchini, badovijijini hizi zana hazijafika. Niombe sana Serikali kwa namnaya pekee ieneze hizi zana kwa haraka sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. MGENI JADI KADIKA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza namshukuru Mungu kwa kunipa afya njema nakuniwezesha kuchangia hoja hii. Pia napenda kuwapongezakwa dhati Waziri na Naibu wake kwa kazi kubwaanazozifanya kwa kweli, wanajituma kwa nguvu zao zotekuhakikisha wananchi wanapata huduma ya matibabu yaafya kwa kutupatia dawa na kupatikana vifaatiba katikahospitali zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, NHIF; huduma ya matumiziya kadi ya bima ya afya NHIF tunahitaji watu wote wapatehuduma hii ili wapate matibabu kwa kutumia huduma hii kwaurahisi, lakini bado tuko nyuma, mpaka sasa wanaotumiahuduma hii ni asilimia 34 tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza Watanzaniawanataka elimu ya kutosha itolewe hasa vijijini, ili wapateuelewa juu ya matumizi ya bima ya afya na vievile wawezekutibiwa kwa daraja lake ili yule mwenye maisha duni awezekutibiwa kwa uwezo wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu viongoziwanaotumia huduma hii mfano Wabunge, wanatibiwa yeyepamoja na mwenza wake na watoto wanne, lakini mzazi

Page 156: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

wake hapati huduma hii. Swali langu ni hili je, hatuoni Serikalihaijawatendea haki wazee kuwakosesha huduma hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, sina budi kuipongeza Serikalikwa Taasisi ya Moyo kuweza kutupatia tiba na wataalammbalimbali kuhusu tatizo hilo. Tunaomba tiba hii ipatikanekatika hospitali nyingine za rufaa mbalimbali katika nchi yetu,ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Muhimbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, Madaktari na Wauguzipamoja na wafanyakazi mbalimbali wa sekta ya afya. Hawawote wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokanana kazi zao. Kwanza tunaomba waangaliwe, maslahi yaoyaboreshwe ili waweze kupata ari na upendo wa kazi yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Madaktari, Wauguzi na Nesiwana changamoto mbalimbali zikiwemo posho ya nyumba,motisha ya saa za ziada. Hili tatizo kubwa linaweza kuathiriutendaji kazi wao, kwa hiyo, naiomba Serikali iliangalie tatizohili kwani hawa ndio wanaotuokoa katika maisha yetu yakila siku.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu vifo vya wajawazitobado ni changamoto katika nchi yetu, baada ya kupunguabado vinaongezeka katika Taifa letu. Kwanza naipongezaSerikali kupitia Wizara ya Afya, juzi nilishuhudia kwenyevyombo vya habari kuwa inatoa michango mbali ya fedhakutaka kuwasajili Wakunga wa Jadi ili kuweza kusaidiakupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto.Ahsante sana Waziri Ummy, wanawake tunaweza.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya mchangowangu, naunga mkono hoja.

MHE. SILAFU J. MAUFI: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kuwashukuru na kuwapongeza Waziri, Naibu Waziri,Katibu Mkuu na wataalam wa afya kwa kazi nzuri zilizotukukana kumuunga mkono wa dhati Rais Dkt. J.P. Magufuli nakuwezesha kuwa na matumaini ya kutimiza azma yake kwaakinamama na watoto hapa nchini.

Page 157: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

Mheshimiwa Naibu Spika, tunashukuru sana Mkoa waRukwa wamepatiwa pesa kwa ujenzi wa vituo vya afya nahospitali za wilaya zote nne na kuanza maandalizi ya awaliya ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa. Ombi letu ni Wizaraya Afya kutoa msukumo kwa TAMISEMI kuhakikisha wanaungamkono jitihada na nguvu za wananchi katika kuyakamilishamaboma ya majengo ya zahanati yapatayo 50. Piatunaomba vifaa tiba kwa wakati, ili zahanati takribani 15zilizokamilika zipatiwe watumishi na zianze kazi kikamilifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunashukuru kujengewavituo vya afya vya kihistoria na bajeti ya 2019/2020tumeongezewa vituo viwili ndani ya mkoa, ingawa badomahitaji ni makubwa kwa Mkoa wa Rukwa kwani tupopembezoni mwa nchi yetu (Congo DRC na Zambia).Tunaomba vifaa tiba na watumishi wa kukidhi mahitaji kwanimajengo mazuri bila kuwa na hayo mahitaji hatutakuwatumewafikishia wananchi huduma njema kwao.

Naomba Wizara kuona umuhimu wa Vituo vya Afya –Sopa, Kitete, Kala, Kabwe na kadhalika. Tuzingatie jiografiaya Rukwa ni mtihani kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na juhudi kwa halihalisi ya Waziri, bado Mkoa wa Rukwa tunaomba kuangaliwakwa jicho la aina yake kwani, akinamama na vijanawameibuka katika kuinua uchumi wao kwa kujiunga kwenyevikundi vya ujasiriamali, tatizo lililopo ni elimu kwao, lakiniMaafisa wa Maendeleo ya Jamii hawakidhi mahitaji. Si rahisimmoja kushika vijiji viwili au mitaa sita au kata tatu, utendajiwao unakuwa hauna ufanisi na hata tija haipo. Tunaombaajira itendeke kwa sasa, watumishi hawa ni muhimu sanavijijini, mitaani kwa afya, uchumi, maendeleo na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, maafisa hawa hawanausafiri. Tunaomba usafiri kwao na pikipiki kwa vijiji, mitaa nakata, magari kwa ngazi ya wilaya na mkoa kwani sasainategemea huruma ya Mkurugenzi au RAS. Tunawarudishanyuma kiufanisi kwao.

Page 158: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba upande waMaafisa wa Maendeleo ya Jamii kuwa na ukaimu kwenyenafasi zao. Tunaomba eneo husika kuona kama vigezovinakubalika waweze kupata nafasi hizo kikamilifu, ili wafanyekazi kwa tija na ufanisi uliotukuka kwa maslahi ya nchi yetu,hususan Mkoa wa Rukwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri wakati wa shereheza Siku ya Wanawake Duniani, Mkoa wa Rukwa, alitoa ahadiya kutoa ambulance ya Manispaa na Hospitali ya Mkoa,hivyo tunasubiri bado hizo ambulance mbili. Tunaomba Waziriaone namna ya kutimiza ahadi hii, kwani akinamamawanayumba sana kwa huduma hii ya usafiri.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunashukuru kwa hatuailiyofikiwa hadi sasa. Tunaomba kasi kuongezwa ili tufananena mikoa iliyokamilishiwa kwa asilimia 50.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, tunaombautaratibu wa Bima ya NHIF ukamilishwe haraka kwa kutolewakwa wananchi wote kwa gharama nafuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kuchangia hoja hii muhimu kwa mustakabali waafya za wananchi wa Tarime. Kwanza niombe Wizara izingatiemaoni yaliyotolewa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,hasa maeneo ya Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 kufanyiwamarekebisho ili kuweza kumlinda mtoto wa kike, maana ilivyosasa inakinzana na sheria nyingine zinazomlinda mtoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili ni kuhusu hospitali yanguya Mji wa Tarime ambayo ina hadhi ya kuwa Hospitali yaMkoa wa Tarime/Rorya au kuifanya angalau hospitali yawilaya. Tunakuwa treated kama vile hospitali inahudumiawananchi wa Tarime Mjini tu ilhali tunahudumia na wananchiwote toka Tarime Vijijini, Serengeti, baadhi ya maeneo yaRorya na wengine wanatoka nchi jirani ya Kenya, lakini fedhatunazopokea za basket fund ni ndogo sana pamoja na stahiki

Page 159: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

nyingi za kuwezesha utolewaji wa huduma bora ya afyakama vile idadi ya Wauguzi/Wauguzi Wasaidizi inatolewa kwaidadi ya population ya Mji wa Tarime. Hii sio haki nainasababisha utolewaji wa huduma duni za afya na hatimayekusababisha umauti.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna upungufu mkubwa waMadaktari uliopelekea mosi na uchukuliwaji na ugawaji wabasket fund kwa kuzingatia idadi ndogo kuliko uhalisia; zoezila vyeti feki; kustaafu na vifo. Tuna upungufu mkubwa sana.Wahudumu hawa, Madaktari wanafanya kazi kwa mudamrefu sana bila mapumziko na stahiki zao haziridhishi. NiiombeSerikali na juzi nilisema Bungeni kuwa tuna shida na Daktariwa Meno baada ya aliyekuwepo kufariki kwa ajali mwakajana. Niombe sana suala hili lipewe kipaumbele maana sasawananchi wanapata shida sana. Serikali ilichukulie kamajambo la dharura ili kuokoa afya ya kinywa na meno kwawananchi wa Tarime.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia Wizara hiiiweze kujenga utamaduni wa kutembelea magereza ili kujuamanyanyaso wanayoyapata wanawake hawa wawapokwenye mikono ya Jeshi la Polisi (vituoni), wengi wanabakwana kudhalilishwa kijinsia.

Pia waweze kuona ni jinsi gani wanawake maskiniwanavyoonewa na kukosa misaada ya kisheria. Wengiwanakamatwa kwa makosa ya wanaume zao, wenginewana kesi za kudhaminika ila wapo, tena wengine wapo nawatoto wadogo/wachanga, wengine ni mabinti wadogosana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kitendo cha Jeshi la Polisikubaka/kuingilia kinyume wanawake tena mabinti ni kinyumekabisa na sheria na kanuni za kazi. Huu udhalilishaji ni lazimaWizara iufanyie kazi ili kulinda utu wa mwanamke.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni wakati sasa Serikali itengefedha kwa ajili ya kitengo cha lishe. Serikali ya Awamu yaTano haijawahi kutenga fedha.

Page 160: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho ni mahitaji yaambulance kwenye Kituo cha Afya cha Magena (Nkende)na kile cha Kenyamanyori. Upanuzi wa zahanati ile yaNkongore Kenyamanyori na Ganasara (Nyandoto) kuwaKituo cha Afya, ni muhimu sana na sisi tupate fedha zakukarabati na kupandisha hadhi ili ziweze kutoa hudumastahiki. Natambua huwa kuna fedha zinakuja tuwezekupatiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, cha kusikitisha mwaka huuwa fedha, yaani 2019/2020 hakuna bajeti ya uzazi na mpango(family planning). Ningependa kujua ni kwa nini hamna au nikufuatia kauli ya Rais.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara lazima itoe elimu juuya ugonjwa wa ini (hepatitis), magonjwa yasiyo yakuambukizwa, kuwekeza kwenye kutoa elimu juu ya UKIMWI(HIV). Muhimu kuwekeza kwenye lishe, chanjo, vitamini kwamama na watoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Naibu Spika,afya ni nguvu kazi ya Taifa lolote. Kamwe Tanzania yaViwanda haitawezekana kama wananchi wake hawanahuduma bora za afya. Pamoja na unyeti na umuhimu waafya bado Wizara hii imetengewa fedha kidogo sana.Pamoja na Bunge lako Tukufu kupitisha zaidi ya trilioni moja,lakini zilizoenda za maendeleo ni 16% tu. Hii haiendani kabisana ubora wa afya kwani, miradi mingi imekwama, lakinipamoja na upungufu huo bado fedha zinapungua hadi bilioni866.2. Hali hii haina ishara njema kwa afya zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na watumishiwachache na kufanya kazi kwenye mazingira magumu badoviongozi wa kisiasa na Kiserikali wasio na taaluma hiiwamekuwa wakiwadhalilisha kwa ama kuwasimamisha kaziau kutaka kujieleza mbele ya wananchi. Hivyo, ni muhimutabia hii mbaya ya kuwa-demorolise madaktari wetuwanaopatikana kwa gharama kubwa sana iachwe.

Page 161: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

Mheshimiwa Naibu Spika, UKIMWI una uhusianomkubwa sana na TB. Ni kama vile suala la TB halishughulikiwisana. Hii ni hatari kubwa kwa kuwa, mgonjwa wa TB mmojaasiyetibiwa anaweza kuambukiza watu 10 – 20 kwa mwaka,lakini mbaya zaidi 40% ya wagonjwa wa UKIMWI pia, wanaTB. Hivyo magonjwa haya yana mahusiano makubwa basiuzito unaopewa UKIMWI pia, uwekwe kwenye TB.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri nasaha ni muhimusana hasa ikizingatiwa binadamu lazima akumbane nachangamoto za maisha. Hivyo, ni muhimu kitengo hiki kupitiaIdara ya Ustawi wa Jamii kujipanga kimkakati kuona ni jinsigani watakavyotoa huduma hii hata ikibidi kwa gharamakwa kuwa, kuna wanasihi binafsi (wachache) wanaotoafedha. Pia, vijana (wanafunzi) wawe wanapewa mafunzokwa vitendo ili wamalizapo waende kusaidia wananchiwenye sonona na misongo ya akili.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndoa za utotoni ni tatizokubwa sana. Sheria hii ibadilishwe ili iendane na wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, afya kwa wote hainamjadala ni muhimu sana, lakini Mtanzania awe na bima.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuondolewa kwa tozo yaVAT katika pads bado ni kizungumkuti. Pamoja na Serikalikuondoa VAT bado fedha ni zilezile 2,000/= per pct na zaidisuala la je, kwa nini mpaka leo bado gharama ni ileile auzaidi?

Mheshimiwa Naibu Spika, Sera ya Wazee toka 2001hadi leo haina sheria. Ni lini Muswada wa Sheria utaletwa iliwazee hawa wapate ahueni?

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu imesaini mkataba(Abuja Declaration) ambapo kila nchi husika zilikubalikutenga asilimia 15 ya bajeti kuu ya Serikali kugharamia sektabinafsi. Ni jambo la ajabu kwamba, sasa inaonekana Serikalihaioni umuhimu huo kwa kuwa, hivi majuzi Waziri wa Fedha

Page 162: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

alikiri haiwezekani kila mkataba tuutekeleze kama tulivyosainikwa kuwa, sekta nyingine hazitapata kitu, nazo ni muhimu.

MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipatia nafasi ili nami niweze kuchangiakwenye Wizara hii muhimu ya Afya. Kama inavyojulikana ningumu sana nchi yoyote kupata maendeleo kama wananchiwake hawana afya bora.

Mheshimiwa Naibu Spika, Watumishi wa Afya; pamojana jitihada za kujenga mahospitali na vituo vya afya, lakinitumekuwa na upungufu mkubwa sana wa watumishi wa afyanchini. Mfano mpaka mwezi Machi, taarifa za Wizarazinaonesha zina upungufu wa watumishi kwa asilimia 48 nahii inaonesha kuwa kasi utoaji wa vibali vya kuajiri uko chinisana ukilinganisha na ongezeko la wagonjwa. Pia, ongezekohili la ujenzi wa hospitali na vituo vya afya ni vema sanaungekwenda sambamba na ajira mpya za watumishi waafya sambamba na kuwalipa watumishi wa afya waliopowanaodai stahiki zao ili kuweza kuongeza tija ya utendaji kaziwao.

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi la magari yawagonjwa Jimboni Mikumi; Jimbo la Mikumi lina jiografiambaya sana na katika kata 15 za Jimbo la Mikumi tuna vituovya afya vinne tu navyo ni kuwa viwili, yaani Kituo cha Afyacha Kidodi na Kituo cha Afya cha Ulaya na vituo vipya vyaafya vya Mikumi na Kituo cha Afya cha Malolo.

Kwa hali hiyo inasababisha wananchi wengi kufianjiani wakati wanasafirishwa umbali mrefu sana ambapo nikutokana na ukosefu wa magari ya wagonjwa. Jimbo zimahalina gari hata moja la wagonjwa kwenye zahanati zotepamoja na vituo vya afya vyote. Tunaiomba sana Serikaliitusaidie magari ya wagonjwa mawili au zaidi ili tuwezekuwaokoa wananchi hawa wa Jimbo la Mikumi, hasa mamana watoto. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri, DadaUmmy Mwalimu, atusaidie na kuokoa maisha ya wanawakena watoto wa Mikumi.

Page 163: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

Mheshimiwa Naibu Spika, NHIF; uandikishaji wa Bimaya Afya ya NHIF umekuwa mdogo sana. Mfano, mwaka 2016/2017, walisajili 27% tu; mwaka 2017/2018, walisajili 32% tu;mwaka 2018/2019, walisaji l i 33%; na kusuasua hukukunatokana na ufinyu wa bajeti. Tunaomba sana Serikaliizingatie sana bajeti ya afya kwa ujumla. Pia, Serikali iharakishekuleta Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote yaani UniversalHealth Coverage ili tuweze kuupitisha na kuleta tija zaidi yakuwasaidia na kuwaokoa Watanzania wengi zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuajiri Maafisa Maendeleoya Jamii; ni vema sasa tukajikita zaidi kwenye kinga kulikotiba na watu wanaoweza kutusaidia zaidi kwenye jambo hilila kinga ni Maafisa Maendeleo ya Jamii ili waweze kusaidiajamii zetu huko chini ili wapate elimu zaidi ya afya kwani nikweli tupu kwamba, kinga ni bora kuliko tiba.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza naunga mkono hotuba ya Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni. Ni ushauri wangu Serikali ione namna ya kuchukuaushauri wa hotuba hiyo ili kuboresha maendeleo ya Wizaranchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, afya ni kitu muhimu sanakwa binadamu yeyote. Bila kuwa na afya bora, hakuna kaziau maendeleo hapa duniani au Tanzania. Hivyo basi, pamojana mambo mengi yanayofanyika, bila afya bora ni mzigomkubwa kwa Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara hii inashughulika nawazee, watoto na wanawake ambaPo wanawake hao nikiwanda namba moja cha kuleta watoto duniani. Nianze nakuzungumzia afya ya mama na mtoto ndani ya Jimbo laMlimba.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kuwepo naKituo cha Afya Kata ya Mlimba ambacho kinahudumiatakribani wakazi wa kata 10 na watu wasiopungua laki moja

Page 164: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

na zaidi, inasababisha kituo hicho kuzidiwa na wagonjwa kwaupungufu wa madaktari ambapo wapo wanne tu na kufanyatatizo kubwa katika kutoa huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia dawa zinazopelekwamara kadhaa hazikidhi haja kutokana na hadhi ya kituokuhudumia watu wa kata 10. Hivyo tunaomba tufikiriwekuongeza vituo vya afya ili kupunguza mzigo mkubwa katikaKituo cha Afya Mlimba. Naomba angalau tupate vituo vyaafya vitatu ambapo kila kata tatu zitahudumiwa na kituokimoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Jimbo la Mlimbaliko kilometa 220 hadi kufika Hospitali ya Rufaa St. Francis namiundombinu ya barabara ni mbaya sana kwa barabarakutopitika kwa mwaka mzima, hivyo kuhatarisha maisha yamama wajawazito na wagonjwa wanaopata rufaa, naombatupate bajeti ya kutosha ili tujenge Hospitali ya Halmashauriambapo kwa bajeti hii. Tumetengewa shilingi milioni 500 tu,ambayo itachukua muda mrefu ujenzi kwisha. Naombatuongezewe hela ili tujenge haraka na kuokoa jamii yaMlimba. Pia tunaomba gari la wagonjwa kwani gari lililopo nichakavu na linaharibika mara kwa mara. Pia ahsante kwakupeleka hela ya kuboresha Kituo cha Afya cha Mchombe.

Mheshimiwa Naibu Spika, wazee waishio vijijiniwanashindwa kupata huduma kutokana na ukosefu wa vituovya afya na kushindwa kupata huduma kwa sababu yaumbali wa kufikia kituo cha afya Mlimba.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Wazirialipotembelea Wilaya ya Kilombero, pamoja na mambomengine, aliamuru watumishi/wauguzi na madaktari wotewaliokuwa wanalipwa na Serikali katika Hospitali ya Rufaaya St. Francis waondolewe na wapelekwe kwenye vituo auzahanati za Serikali. Uamuzi huo ingawa umefanywa kwa nianjema, lakini umesababisha upungufu mkubwa wa madaktarina wauguzi kwenye Hospitali hiyo ya Rufaa ambapo nitegemeo kubwa kwa wakazi wa Wilaya ya Kilombero, Malinyina Ulanga.

Page 165: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo nashauri uangaliweupya uamuzi huo kwani Mheshimiwa Waziri alipoagizawaangalie upya gharama ya matibabu, waliitekeleza kwakuwashirikisha wadau na kupunguza gharama za matibabu.Hivyo, tatizo lililopo ni upungufu mkubwa wa madaktari nawauguzi. Ni matumaini yangu kuwa atalichukulia hilo kwaumuhimu.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika,nashauri Bima ya Afya iangalie utaratibu wa kupatia BimaWatanzania wote na bei ipungue.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Hospitali ya Mrarainahitaji ujenzi wa wodi ya wazazi na watoto. Tunashukurukwa mkopo wa Bima ya Afya milioni 108 kwa hospitali hiyo.Tunaomba mtuongezee kwani bajeti yake ni zaidi ya shilingimilioni 800.

Mheshimiwa Naibu Spika, Vituo vya Afya na Zahanatikatika Kata zote za Babati Mjini vimejengwa na nguvu zawananchi, lakini hakuna fedha zozote za Serikali zimepelekwakukamilisha maboma hayo. Tunaomba fedha za ukamilishajimaboma hayo ambayo ni Zahanati ya Singe, Sigimo, Mutuka,Himiti na Chemchem.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tunaombaambulance katika Hospitali ya Mrara.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawawatakia kila la herikatika majukumu yenu.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika,health tourism ni eneo ambalo bado halijafanyiwa kazivyema wala halijastawishwa sana. Naamini kama tukiwekahili kimkakati, mfano Mbeya kwa Zambia na Malawi; auKagera kwa Burundi na DR Congo itakuwa vyema. Pia lazimakama nchi tuwe na specialized areas ambazo zitavutamajirani kufuata matibabu.

Page 166: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

Mheshimiwa Naibu Spika, tumearifiwa kuwa kunafedha za mkopo wa riba ndugu juu ya early childhooddevelopment kiasi cha shilingi milioni 200 kwa miaka mitanona kuweza kusaidia eneo hili. Tunaambiwa the money hasbeen waiting for us - we drag our feet and the 0-5 child is notdeveloped.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, Wizara imetenga partnerfund ili Serikali iweze ku- access fund kwenye taasisi, mashirikaya ufadhili ambayo yana masharti hayo? Je, ni kiasi ganihicho ambacho kimetengwa?

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza kabisa nichukue fursa hii kumshukuru MwenyeziMungu kwa kunifikisha kwenye kipindi hiki cha Ramadhaniya mwaka huu, kwani wapo tuliofunga nao mwaka jana, 2018leo wako mbele ya haki na wengine wameshindwa kushirikiRamadhani hii kwa hali na maradhi mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa leo naomba nianzemchango wangu kwanza kwa kumshukuru MheshimiwaWaziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Manaibu MakatibuWakuu na Watendaji wote kwenye wizara hii kwa kazi kubwawanayoifanya ya kuhudumia jamii yetu kwenye sekta hiimuhimu ya kulinda afya zetu. Namwomba Mungu awapeumri mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kumshukuruMheshimiwa Waziri kwa bajeti ya mwaka 2018 kwa kunipawatumishi 80 wa Sekta ya Afya, lakini kutokana na uhabamkubwa tulionao watumishi wale wamekuwa kama tone ladamu baharini. Bado Hospitali ya Wilaya ya Liwale yenyewodi nne zinahudumiwa na mhudumu mmoja tu kwa shift yausiku kutokana na uhaba wa watumishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nitoe shukrani kwenyebajeti hii kwani wilaya yetu imetengewa shilingi milioni 500kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, maana ile iliyopoilikuwa ni kituo cha afya, hivyo kushindwa kukidhi hadhi ya

Page 167: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

kuitwa Hospitali ya Wilaya. Ombi langu ni fedha kuja kwawakati ili ujenzi huu uanze.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na ujenzi waHospitali ya Wilaya na vituo viwili vya afya vya Mpengerewa,Kibutuka, bado Halmashauri ya Liwale inakabiliwa na uhabamkubwa sana wa gari la wagonjwa (ambulance). Jiografiaya Liwale yenye vijiji 76 ni ngumu sana. Hivyo, namna yakuwafikisha wamama hasa wajawazito ni ngumu sana,ukizingatia kuwa zahanati zetu hazina wataalamu na vifaavya kutosha. Kwa hiyo, uhitaji wa gari la wagonjwa ni mkubwasana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kupunguza mlundikanowa wagonjwa kwenye hospitali na zahanati zetu, wakati sasaumefika wa kuimarisha kada ya Mabwana na Mabibi Afyakwenye Kata na Vijiji vyetu. Watumishi hawa ni muhimu sanakwenye jamii zetu. Waswahili husema, “kinga ni bora kulikotiba.” Elimu ya afya ikiwafikia wanajamii juu ya kutunza afyazetu na mazingira yetu kwa ujumla tutaepuka magonjwa yamlipuko. Kada hii ya Mabwana/Mabibi Afya ni kamaimesahauliwa kwa sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ajira kwa watoto ni jambolinalotishia maisha ya watoto wetu kwani kila kukicha badoongezeo la ajira kwa watoto mitaani linaongezeka siku hadisiku hasa kwa mijini. Wako watoto wanaosukuma baiskelikuwatembeza watu wenye ulemavu wa viungo na wasioonakwenye shughuli zao za kuombaomba. Vilevile wako watotowanaotumwa na wazazi wao kwenda mitaani kupitakuombaomba. Hivyo, naiomba Wizara kuja na mkakatimaalum wa kukomesha ajira hizi za watoto na kuwaondoawatoto wanaoombaomba mitaani.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jeshi la Wananchi waTanzania kukosa kuwaingiza kwenye mpango wa Bima zaAfya (NHIF) ni kutokuwatendea haki, kwani familia za Maaskariwetu zimekuwa zikihangaika sana hasa zile familia zinazoishiuraiani. Pamoja na kazi ngumu wanazofanya za kulinda nchi

Page 168: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

yetu, lakini bado hawana uhakika wa afya zao na familiazao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sera ya Wazee nchini nichangamoto kubwa hapa nchini kwani hadi leo Serikalihaitaki kuleta Sheria ya Wazee ili kuweza kutambua haowazee. Pamoja na kuwa na matangazo sehemu mbalimbalikama vile “Pisha Mzee”, “Wazee Kwanza”, matangazoambayo yanashindwa kuwatambua wazee hao, kwanihakuna sheria inayowatambua; kwa nini Serikali inakuwa nakigugumizi cha kuleta Sheria ya Wazee hapa Bungeni iliwazee hawa waweze kutambuliwa? Tukumbuke kuwa sisisote ni wazee watarajiwa. Hivyo, hiki tunachokifanya nikujikaanga kwa mafuta yetu.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa NaibuSpika, kupitia njia ya maandishi nichangie bajeti ya Wizaraya Afya. Awali ya yote nichukue fursa hi kuunga mkono hojabajeti hii na niwapongeze viongozi na watendaji wote waWizara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii kuishauriWizara iweze kupitia upya upangaji wa watendaji maalumkatika wizara hii ili angalau kila mkoa upate hao wataalamuwa msingi. Mfano, mwezi wa tatu Mkoa wa Kagera kwahospitali zote Umma na binafsi hakukuwepo Mganga kwaajili ya magonjwa ya akina mama (gynocologist). Hoja hapani kuhakikisha kila mkoa unapata wataalamu hawa na hatawakati wa kutoa ajira muhimu, kutoa nafasi kwa utaratibuhuo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kupitia bajeti hii,nishauri juu ya upangaji na ujenzi wa zahanati, vituo vya afyana hospitali. Ushauri wangu ni kuwa suala hili lisimamiwe naWizara ya Afya ambayo katika busara ya kawaida watatumiaweledi kupanga maeneo ya taasisi hizo. Nikirejea ujenzi,uboreshaji wa zahanati na vituo vya afya katika Jimbo langu,inasikitisha kuona kuwa maeneo ambayo yalipashwakupewa nguvu baada ya wananchi kuonyesha juhudi kwakujenga maboma hayajafikiriwa. Hii inaonyesha ukosefu wa

Page 169: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

utaalamu katika kubaini wapi paendelezwe, kwani maeneomengine yanaachwa bila huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Wizara ipitie ujenziwa zahanati 12 zilizojengwa na wananchi kwa kipindi chamiaka mitatu ili tupate somo juu ya haja ya kuendelezazahanati na vituo vya afya kwa ulinganifu na kwa kuzingatiazaidi mahitaji, lakini zaidi Serikali itusaidie kwa kuendelezaangalau Zahanati za Rutoro, Bumbire na Crogllo kati yazahanati hizo 12 kwa kuanzia.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine la kuangaliani upangaji wa wataalamu wa sekta ya afya. Ili kuepuka tatizola sasa ambapo sasa kila wizara inataka watendajiwanaohusika na sekta zao walioko katika Halmashauri zaWilaya wawajibike Wizarani. Wizara ya Afya na TAMISEMIwapitie upya usimamiaji wa watendaji hawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa hii ni Serikali moja,unaweza kuwepo utaratibu ambapo wataalamu wa Wizaraya Afya wanaweza kupata miongozo tokea Wizara ya Afyaikiwa ni pamoja na kupata stahili zao wakiwa Halmashauriza Wilaya. Uwepo wa zahanati wa vituo vya afya ambavyohavina wataalamu ni kutokana na upungufu tu wa msimamizi(DED) kutokuwa na uelewa wa mguso wa sekta.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na umakini waSerikali katika kutoa vibali vya kuajiri, naomba na kushaurivibali vya kuajiri watendaji wa sekta hii ni muhimu vitolewe.Hii italeta umaana wa kujenga miundombinu ya zahanati,vituo vya afya na hospitali.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho lakini siyo kwaumuhimu, nichukue fursa hii kupongeza msimamo wa Serikalikatika kuwasimamia watendaji wa Sekta ya Afya. Siyo busarakwa kila atakayesimama amwelekeze na kumkemea Nurse,Daktari au Mtendaji wa Afya. Kazi nyingine unawezakuzifanya kwa sababu unajua kongea. Sekta ya Afyawatendaji wake wanatumia muda mwingi shuleni, wanahitajiutulivu na wanashughulika na afya na uhai wa binadamu.

Page 170: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Naibu Spika,Wilaya ya Tandahimba ina hospitali moja ya Wilaya na vituviwili vya afya ambavyo ni vya zamani. Hata hivyo,tunaishukuru Serikali kwa kutupatia fedha shilingi milioni 400za Tanzania kwa ajili ya ukarabati wa Kituo cha Afya Mahuta.Fedha hizi zimetumika vizuri. Kwa hiyo, ombi langu ni kupatafedha kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa kituo hikiambacho kinahudumia zaidi ya kata kumi zilizopo jirani. Hatahivyo, Wilaya ya Tandahimba jiografia yake ni ngumu kidogo,kwa hiyo, naomba Wizara itusaidie fedha kwa ajili ya kujengana kuendeleza vituo vya afya vipya vilivyojengwa nawananchi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Mnyawa wananchikwa kupenda maendeleo wamejenga vituo vya afyaambavyo vinahitaji msaada wa Serikali ili tuweze kumalizia.Kata ya Mndumbwe nayo wananchi wamejitolea kujengakituo cha afya. Tunaomba msaada kwa Serikali iwezekutusaidia tumalize ujenzi huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba Wizara itujengeeKituo cha Afya katika Tarafa ya Litehu ambayo inahudumiawakazi zaidi ya 30,000. Tunaomba tupate kituo cha afyakatika Kata ya Kitama I. Kituo ambacho kitasaidia kuboreshahuduma za afya katika maeneo jirani kama Kata ya Miute,Michenjele, Mihambwe na Mkoreha. Wananchi wako tayarikujitolea, nami kama mwakilishi wa Jimbo la Tandahimba namzaliwa wa Kitama, naahidi kuchangia mifuko 600 ya sarujikwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho. Kwa unyenyekevu mkubwanaunga mkono hoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naombakuwasilisha.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika,katika aya ya 185 ukurasa wa 136 Mheshimiwa Waziriameeleza kuwa ili kuhakikisha haki za wazee zinalindwa,Wizara imeendelea kuratibu uanzishwaji wa Mabaraza ya

Page 171: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

Wazee katika ngazi mbalimbali za Halmashauri ambapo hadikufikia Machi, 2019, jumla ya Mabaraza ya Wazee 9,083yameanzishwa katika Halmashauri mbalimbali nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, Mabaraza hayoyameanzishwa huku kukiwa hakuna Sheria ya Wazee nchiniwala sheria ya kuwezesha kuanzishwa kwa Mabaraza hayo.Hivyo katika majumuisho Mheshimiwa Waziri aeleze ni liniSheria ya Wazee italetwa Bungeni ambayo pamoja namambo mengine itaeleza kuweka muundo na majukumu yaMabaraza ya Wazee nchini. Aidha, sheria hiyo itawezeshakuundwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Wazee Nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande mwingine, ipohoja ya kutungwa kwa Sera ya Maendeleo ya WanawakeNchini. Sera hiyo ifuatiwe na kutungwa Sheria ya Baraza laWanawake la Taifa na kusimamiwa kwa Mfuko waMaendeleo ya Wanawake nchini na wanawake wenyewekupitia Baraza lao. Naomba kupata maelezo ya Serikalikuhusu hatua iliyofikia katika kuunda Mabaraza ya Watotokatika Jimbo la Kibamba. Haya yatawezesha watotokujijenga ikiwemo Stadi za Uongozi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara imewezeshakuandaliwa kwa kanuni za mashirika yasiyo ya kiserikali zamwaka 2018 na kutangazwa katika Gazeti la Serikali Na. 609la tarehe 19 Oktoba, 2018. Baadhi ya vifungu na vipengelevya kanuni hizo umekamilika na wadau yakiwemo mashirikayasiyo ya kiserikali. Hivyo, Wizara ikae tena na mashirika yasiyoya kiserikali kupitia vifungu na vipengele vilivyolalamikiwa nakufanya marekebisho. Aidha, Wizara iharakishe kuwekakanzidata ya mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kuwa sualahili limechukua muda mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Vituo vya Maendeleo yaJamii na Vituo vya Ustawi wa Jamii unaweza kuwa namalengo makubwa kwenye maendeleo na ustawi wa jamii.Vituo hivyo vilianzishwa wakati ambapo mazingira ya kisiasa,kiuchumi na kijamii ni tofauti na sasa. Hivyo Wizara ifanye

Page 172: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

tathmini ya Mitaa na mazingira ya vituo hivyo na kuja namapendekezo ya maboresho kwa kuzingatia hali halisi iliyopo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mitaala ya vituo hivyoilenge kujibu changamoto zinazokabili jamii yetu kwa sasana baadaye. Kadhalika Wizara itoe maelezo ya athari zafedha za maendeleo kutolewa kidogo katika Fungu la 53,Idara Kuu ya Maendeleo ambapo hadi kufikia mwezi Februari,2019 kiasi cha shilingi bilioni 1.13 tu sawa na asilimia 23.0 tu yafedha iliyotengwa kilikuwa kimepokelewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Afya, Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ina wajibu wa kuzisimamiakwa karibu mashirika na taasisi yaliyoko chini ya Wizara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali (CAG) alikagua Bohari Kuu ya DawaMSD na kubaini kuwa vifaa tiba ya shilingi bilioni 3.55vil ivyonunuliwa kwa mfumo wa manunuzi maalumvilivyorudishwa kutokana na kuzidi kiasi walichoagiza wateja.kutokuwa na sifa zilizotakiwa na wateja au kuzidi kiasiwalichoagiza wateja. Baadhi ya vifaa tiba vilivyorudishwavilikuwa vikikaribia kikomo cha muda. Hivyo, mfumounapaswa kuboreshwa kuhakikisha kuwa hali kama hiihaijirudii.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia CAG alibaini katikamwaka 2017/2018 malipo ya shilingi bilioni 480 yalifanywa naMfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kwa vituo vya tiba ya afyakwa wateja ambao hawakuchangia mfuko. Hali hii kama nikweli ni hatari kwa mustakabali wa mfuko.

Mheshimiwa Naibu Spika, kadhalika, yapo madaikwamba malipo ya shilingi bilioni 13.99 yalifanyika kwawanaodaiwa kuwa watoto wategemezi, lakini ukweli ni kuwawamevuka miaka 18, hali ambayo inahitaji NHIF kuharakishakuanzisha kanzidata ya umri wa wategemezi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri Wizara itumiemajumuisho kueleza sababu ya madeni yasiyolipika (bad

Page 173: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

debts) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoka shilingimilioni 941.32 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 mpaka shilingibilioni 1.44 kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2013 na 2016palifanyika uthamini (actual valuation) mara mbili kwa Mfukowa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Uthamini wa mwaka 2013ulionyesha kwamba uendelevu bora na mfuko kwa maanaya mfuko kuanza kupata hasara ulikuwa mwaka 2040. Hatahivyo, uthamini wa mwaka 2016 ambao ripoti yake ilitolewamwaka 2018 unaonyesha kwamba kiwango kimeshukampaka mwaka 2025. Hii ni kutokana na uwiano wa malipoya huduma za afya kukua kila mwaka ukilinganisha na malipoya Bima za Afya. Wizara inapaswa ieleze nini chanzo chahali hiyo na ni ufumbuzi upi wa kukabiliana na hali hiyo?

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua hizo zihusishe piakuboresha mfumo wa Bima ya Afya kwa wastaafu kwakuwekeza kiwango cha michango ya wanachama ili makatohayo yaje kusaidia malipo ya wanachama katika kipindi chakustaafu kwao.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuanzishwa kwaManispaa mpya katika Jiji la Dar es Salaam, Hospitali za Mikoaza Amana, Mwananyamala na Temeke zinapaswakuhudumia Manispaa za Ilala, Kinondoni na Temekemtawalia. Hivyo, kuna haja ya kuanzishwa kwa hospitali zamikoa kwa Manispaa mpya za Ubungo na Kibamba. Kwaupande wa Wilaya ya Ubungo Makao Makuu mapya yaWilaya yanajengwa katika Kanda ya Kwembe eneo laLuguruni.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia patakuwa na ujenzi wamji mpya wa pembeni (satellite town) eneo la Luguruni. Hivyo,mji unapanuka kuelekea eneo la Kibamba. Kwa mantiki hiyo,napendekeza badala ya kupandisha hadhi Hospitali yaWilaya ya Sinza, Palestina, mchakato uanze wa kujengaHospitali ya Mkoa Kibamba na Kwembe.

Page 174: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Afya, Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa upande wa Sekta yaAfya, ina jukumu la kuboresha utoaji wa huduma za afya kwakutekeleza afua mbalimbali. Kwa upande wa Hospitali yaMloganzila, nimetembelea hospitali hiyo hivi karibuni nakubaini kwamba vipo vipimo ambavyo wagonjwawanalazimika kwenda kuvipata kwenye Hospitali ya Taifa yaMuhimbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika majumuisho,Mheshimiwa Waziri wa Afya alieleze Bunge, ni vipimo nahuduma zipi ambazo wagonjwa wanalazimika kutokaMloganzila au vipimo vyao kuchukuliwa kupelekwa Hospitaliya Taifa ya Muhimbili na ni mpango gani umewekwa wakuhakikisha vipimo na huduma hizo zinapatikana katikaHospitali ya Mloganzila?

Mheshimiwa Naibu Spika, katika maeneo niliyopita nikwamba hata huduma ya CT-Scan wagonjwa kwa sasawanalazimika kwenda kupata kutoka Hospitali ya Taifa yaMuhimbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande mwingine,utaratibu wa rufaa kutoka Hospitali za Mikoa ya Dar es Salaamzinapaswa kuboreshwa. Kwa sasa hauangalii umbali tokawagonjwa wanapoishi au wanaowahudumia wanapotokakatika kupanga kama mgonjwa husika apelekwe Muhimbiliau Mloganzila. Hii inasababisha mathalan mgonjwa wa Ilalakupelekwa Mloganzila wakati ambapo ingekuwa ni rahisizaidi kwa mgonjwa kama huyo kupelekwa Muhimbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika majumuisho, Wizaraieleze ni utaratibu gani umewekwa wa rufaa kuhakikishakwamba wagonjwa na wanaowahudumia hawaendi umbalimrefu? Aidha, utaratibu wa rufaa uzingatie uwiano ili kuwena urari wa idadi ya wagonjwa kati ya Muhimbili naMloganzila kwa kuzingatia miundombinu, watumishi nahuduma zilizopo katika hospitali tajwa.

Page 175: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Dkt. JohnPombe Magufuli alitoa maelekezo mbalimbali tarehe 3Oktoba kuhusu uendeshaji wa Hospitali ya Mloganzila. Katiya maelekezo aliyoyatoa ni pamoja na kuagiza wagonjwakutoka Muhimbili kutohamishiwa katika Hospitali yaMloganzila. Wakati Mheshimiwa Rais anatoa maagizo hayo,natambua kwamba wapo wagonjwa ambao tayariwalikuwepo kwenye wodi za Mloganzila na pia Hospitalihaikuwa na watumishi na huduma kwa kiwango kilichoposasa. Matokeo ya maagizo hayo ni madai ya wagonjwawaliohamishiwa wengine kufariki kutokana na udhaifu wahuduma. Aidha, wapo wagonjwa ambao walihamishwawakiwa katika hali mbaya na kupoteza maisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika majumuisho,Mheshimiwa Waziri aeleze ni wagonjwa wangapi walifarikikatika kipindi hicho cha mpito na ni hatua gani zimewezakuchukuliwa kupunguza idadi ya vifo vilivyotokea?

Mheshimiwa Naibu Spika, panakuwepo pia mgogorowa mipaka baina ya Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa waPwani kuhusu wapi hasa ipo Hospitali ya Mloganzila? Naombakatika majumuisho au katika mjadala, Mheshimiwa Wazirimwenye dhamana na suala hili, atangaze kuwa Hospitali yaMloganzila ipo katika Jili la Dar es Salaam Manispaa yaUbungo.

MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Naibu Spika,naipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kupitia taasisimbalimbali zinazotoa matibabu ya kibingwa. Pianawapongeza Waheshimiwa Mawaziri wa Wizara ya Afyakwa ushirikiano wao kwa Waheshimiwa Wabunge katikakuhudumia wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu afya ya uzazi, mamana mtoto; Serikali imejitahidi sana kujenga zahanati na vituovya afya na hivyo kupunguza mwendo mrefu wa wananchipamoja na kinamama wajawazito ili kufikia huduma za afya,lakini bado vifo vya mama na mtoto idadi ipo juu hususanakina mama wajawazito ambapo takwimu zinaonesha kuwa

Page 176: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

akina mama 24 wanafariki ki la siku wanapokuwawanajifungua.

Mheshimiwa Naibu Spika, vifo vingi hutokana nasababu mbalimbali ikiwemo kutokwa na damu nyingi wakatiwa kujifungua, kutokufanya maamuzi ya njia za kujifunguamapema kama vile upasuaji, ukosefu wa dawa aina yamisoprostol and oxytocin hususan vijijini na pia ukosefu wavifaa tiba na wataalam wa kutosha katika vituo vya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, suluhisho ni kwamba Serikaliiweke mkakati wa kuajiri Community Health Workers nawasambazwe maeneo yote hususan katika zahanati na vituovya afya vya vijijini ili waweze kutoa huduma za afya na elimukwa akina mama wajawazito. Ni vyema Serikali itenge fedhakwa ajili ya kukabiliana na vifo vya mama na mtoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa, naombaSerikali iharakishe mchakato wa kuleta sheria ya UniversalHealth Coverage ili kuwezesha wananchi wote wapatehuduma bora za afya kwa usawa. Pia Serikali ijitahidi kutafutawafadhili ili kusambaza vifaa kwa ajili ya kuanzia kusajiliwananchi na huduma ya NHIF iliyoboreshwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kuchangia mambo machache katika Wizara yaAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Kwanzanianze na suala la uzazi wa mpango. Kuna msemo unasemaif you fail to plan you have planned to fail. Ongezeko la watukatika nchi yetu limekuwa likiongezeka kwa asilimia 27 katikanchi yetu. Tanzania inakadiriwa kuwa na watu milioni 150ifikapo mwaka 2050.

Je, kama nchi tumejiandaa kuhudumia ongezeko hilola watu ukizingatia ongezeko hilo la watu na limited resourcestulizonazo?

Page 177: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

Mheshimiwa Naibu Spika, nafahamu dhana ya Serikaliya kuongeza matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpangokutoka 32% - 45% ifikapo mwaka 2020, pia kupunguza vifovya akina mama wakati wa kujifungua kutoka vifo 556 - 292kwa vizazi hadi vifo 100,000, ifikapo mwaka 2020; kupunguzamimba za utotoni toka 27% - 22% ifikapo 2020. Naomba majibuya Serikali, sasa hivi tumefikia wapi katika malengo tajwahapo juu ikiwa tumebakiza mwaka mmoja tu kufika mwaka2020?

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda pia kuzungumziasuala la Community Health Workers (CHWs)au watoa hudumaza afya ngazi ya jamii wamekuwa na mchango mkubwa sanakatika kupunguza vifo vya akina mama wajawazito nawatoto chini ya miaka mitano. CHWs wamekuwa wakitoaelimu kuhusu lishe ya watoto, akina mama wajawazito nakuhamasisha akina mama wajawazito kwenda kujifunguliakatika vituo vua afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano hai ni Kijiji cha UturoMbarali hakijaripoti kifo cha akina mama kwa zaidi ya miakamitano kwa sababu wamekuwa wakiwatumia CHWs katikajamii. Nafahamu mpango mkakati wa IV wa Wizara ya Afyaumetambua kada hii na umeonesha kwamba mpakamwaka 2020 itakuwa imeajiri CHWs 5000, lakini mpaka sasaSerikali haijaajiri hata CHW mmoja licha ya service schemekukamilika mwaka 2018, Desemba.

Mheshimiwa Naibu Spika, Global Funds walitoa pesakwa ajili ya motisha kwa CHWs na mradi huu unakamilikamwaka 2020, lakini Serikali imegoma kuwatumia CHWs kwapesa za Global Funds.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa Waziriakija kuhitimisha anijibu maswali yafuatayo:-

(a) Ni lini Serikali itaajiri CHWs kama ilivyoahidi kwenyemkakati wa IV wa Wizara ya Afya?

(b) Pesa zilizotolewa na Global Funds ziko wapi?

Page 178: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

(c) Kwa nini Halmashauri zinazotaka kuajiri CHWs kwamakato yao ya ndani zinakatazwa kuajiri?

(d) Ni nini mkakati wa Serikali kupunguza vifo vya akinamama wajawazito hasa wanaojifungulia majumbani ikiwaSerikali haitaki kufanya kazi na kuwatambua CHWs?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa NaibuSpika, kwanza kabisa nampongeza Mheshimiwa Waziripamoja na team yake kwa ujumla kwa kazi kubwawanayoifanya. Mwenyezi Mungu awabariki sana ADDS -Head Radiology.

Mheshimiwa Naibu Spika, Lushoto ni Wilayaisiyopungua takribani watu 800,000 na wote hawawanategemea Hospitali ya Wilaya. Cha kusikitisha, hospitalihii haina huduma muhimu kama X-Ray mashine na hiiimesababisha wananchi wengi kukosa huduma hiyo naukizingatia wananchi wengi hawana uwezo wa kwendambali kupata matibabu. Kwa hiyo, naomba Serikali yanguTukufu ipeleke X-Ray mashine ili wananchi wa Lushotowaweze kupata huduma hiyo kuliko iliyo sasa, kwaniwananyanyasika mno.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni kuhusu maendeleoya jamii. Suala la huduma kwa wazee imekuwa ni mtihanisana, kwani wazee hasa wa Lushoto wanapata adha kubwakwa kukosa vitambulisho, hasa wale ambao wapo vijijiniambako hakuna hata zahanati.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hayo, kunawananchi wengi wanaoishi vijijini, hata wale ambaowanauhitaji maalum pamoja na walemavu hawapatimahitaji yao kabisa. Kwa hiyo, naiomba Serikali yangu ipelekedawa na vifaa tiba vyote vinavyohusika kwa watu hawa,ukizingatia vijijini hakuna zahanati wala kituo cha afya. Kwamtaji huo, sasa Serikali itumie magari ya afya ili kufikishahuduma hii kwa walengwa.

Page 179: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

Mheshimiwa Naibu Spika, Lushoto ni Wilaya yenyemilima, kwa hiyo, hata wananchi wakitaka kufuata hudumaza afya, ni lazima wafunge safari ya siku mbili au tatu hasaikitokea mgonjwa amezidiwa na anahitaji usafiri wa gari. Hiiimepelekea wagonjwa wengi kupoteza maisha hasa kwaakina mama wajawazito. Kwa hiyo, naiomba Serikali yanguTukufu tuangalie watu wa Jimbo la Lushoto hasa kwa Kituocha Afya Mlola tuweze kupata gari la wagonjwa, kwani kwasasa hali ni mbaya, wagonjwa wanapoteza maisha kila sikukwa ajili ya kukosa gari la wagonjwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, naishukuruSerikali yangu Tukufu kwa kutupatia shilingi milioni 700 kwaajili ya kujenga majengo matano na vifaa tiba. Kwa sasamajengo yemekamilika, kwa hiyo, tunahitaji sasa vifaa tibaili kituo chetu kianze kufanya kazi; na kwa kuwammeshatutengea fedha, shilingi milioni 300, naomba Serikaliyangu ipeleke vifaa hivyo ili kuwahisha huduma kwawananchi na kupunguza msongamano katika Hospitali yaWilaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna upungufu mkubwawa Watumishi wa Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Lushotopamoja na kwenye Vituo vya Afya na Zahanati zetu. Mfano,sasa hivi Jimbo la Lushoto nina zahanati zaidi ya sita, zotezimekamilika, zinahitaji vifaa tiba pamoja na watumishi. Hivyobasi, naiomba Serikali yangu ipeleke vifaa tiba pamoja nawatumishi katika zahanati zilizopo katika Jimbo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, Lushoto kulikuwa nahospitali kwa watu wanaopatwa na vichaa ambayo ilikuwainamilikiwa na Kanisa, lakini huduma ile kwa sasa haipo. Kwahiyo basi, naiomba Serikali yangu ione ni jinsi gani ya kufufuahuduma ile muhimu, maana sasa hivi watu wenye ugonjwahuo wana pata taabu kusafiri umbali mrefu; na kamainavyofahamika watu wenye kupatwa na ugonjwa wakichaa kumsafirisha inakuwa ni shida sana. Nisisitize tanaSerikali yangu irudishe ile huduma ya kituo cha watu wenyeugonjwa wa kichaa.

Page 180: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwaasilimia mia moja.

MHE. MARY D. MURO: Mheshimiwa Naibu Spika,ningependa kuchangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Serikali kuongezawatendaji katika Sekta ya Afya, kwani Madaktari niwachache, hivyo wanazidiwa na kazi, wanachoka na hivyokufanya kazi chini ya kiwango.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Wizara hiikuhakikisha inatoa elimu juu ya afya za Watanzania badalaya kusubiri waugue ndipo wawaelimishe. Pia Wizara ya Afyaitoe kinga nyingi ili kupunguza gharama za matibabu.Naishauri Serikali kutoa ufadhili kwenye magonjwayasiyoambukiza, kwa mfano, kisukari kinawapata watuambao uwezo wao wa kutafuta fedha za kujitibia hawana,hivyo, wazee hawa wanakufa kabla ya muda.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaendelea kuishauriserikali kuwa wagonjwa wa UKIMWI hawafi kwa kutotumiaARV bali wanakufa kwa magonjwa kama Kifua Kikuu,kuharisha na typhoid. Hivyo tunashauri kwenye ARV ziwepoceptrine ili pale mgonjwa anapopata magonjwa nyemeleziwaweze kupewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nyongeza yaMadaktari wa upasuaji katika Hospitali ya Tumbi kwanihospitali hii inapokea wagonjwa wa ajali za barabara yaMorogoro. Wawili waliopo hawatoshi, tuongezewe, kwanihospitali hii imepandishwa hadhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bima ya Afya imeoneshakasoro nyingi ikiwepo usumbufu wa kutopata huduma stahiki,mfano dawa mara nyingine uambiwe ukanunue au maranyingine uambiwe ni kwa magonjwa baadhi tu.

Page 181: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba wahudumu waafya msingi waajiriwe ili kusaidia huduma za vijijini. Wahudumuhawa walikuwa msaada sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, matibabu kwa wazee nishida. Bima walizoahidiwa hawajapewa na waliopewahawapati huduma hizo hospitalini.

MHE. PROF. ANNA K. TIBAIJUKA: Mheshimiwa NaibuSpika, naunga mkono hoja. Nianze kwa kuungana na Taifazima kuomboleza kifo cha Mheshimiwa Dkt. Reginald Mengikilichotikisa Taifa zima. Dkt. Mengi amefanya mengi katikaTaifa hili, hivyo tumuenzi kwa kuendeleza mema na wemawake. Aidha, kifo chake kimetokea kikifuatana na cha kijanamahiri Ruge Mutahaba na Ephraim Kibonde. Ni pigo kubwapia jana tu tumempoteza Mtanzania mwingine Prof. RobertMabele kilichotokea Hospitali ya Mloganzila. Profesa Mabeleamewafundisha wengi na hata Waziri wetu wa Fedha,Mheshimiwa Dkt. Mpango ni mwanafunzi wake. Tuwaombeewote pumziko la milele.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nijikite katika hoja yaleo ya afya. Nami naungana na wengi kupongeza kazi nzurianayofanya Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu na msaidiziwake Mheshimiwa Dkt. Ndugulile. Wote wametembeleaWilaya ya Muleba na kuona maendeleo na changamotoambazo naomba niziorodheshe.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri anajuatuna Hospitali Teule ya Wilaya ya Rubya, aliitembelea. Tatizoni kwamba utaratibu wa PPP katika kutoa huduma unawezakuleta mkanganyiko ikiwa utaratibu wa kulinda uwezouliojengwa hautawekwa bayana. Hospitali Teule ya Rubyaimepoteza wafanyakazi muhimu na vifaa, wamehamishwa.Kwa hiyo, hakuna degree holder tena katika ukurasa wa tatuutaona hakuna maabara wala generator.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, mashine ya viral loadimehamishwa na kwenda Bukoba. Hii inadhoofisha uwezowa hospitali teule kuhudumia wananchi takriban 700,000

Page 182: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

katika Wilaya. Upanuzi wa hospitali mpya usimaanishekudhoofisha zile za zamani. Naomba kujua mkakati wakuepusha jambo hili, tusipoteze uwezo uliopo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Rubya piakitengo chake cha meno hakitoshi kabisa, ni kama hakipo.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile uboreshaji wa vituovya afya viwili; Kaigara na Kimeya tumeshuhudia na sasaupasuaji unaendelea. Hata hivyo, bado kuna upungufu wamaboma. Ninaomba jambo hili liangaliwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ujenzi wa zahanatikadhaa kwa nguvu za wananchi unaendelea karibu katikakata zote. Tatizo ni fedha za kununua vifaa vya viwandani;saruji, nondo, vioo na kadhalika.

Naomba Wizara iangalie jinsi gani ya kupata fedhakukamilisha ujenzi wa zahanati hizo ikiwemo zifuatazo:Buhangaza, Buganguzi, Kishando – Muleba, Burunguna,Muzinga – Nshamba, Kashanda – Kubirizi, Kasindaga – KataKamombi – Kangazo – Nyakabango.

Mheshimiwa Naibu Spika, unaona kwamba mahitajini makubwa sana. Bila Wizara ya Afya na TAMISEMIkutuwekea nguvu itakuwa vigumu kumaliza zahanati hizi.Eneo linalohudumiwa ni kubwa. Sina budi kuwashukuruTANAPA kutusaidia katika ujenzi wa zahanati kisiwa cha Ikuza.Ni Ukombozi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunamshukuru sanaMheshimiwa Waziri Ummy kutusaida kupata ambulance yaHospitali ya Rubya. Pia, tunazo kwenye vituo vyetu vya afya,lakini wakati mwingine ambulance inasimama kwa sababuya kukosa dereva. Ni suala la TAMISEMI, lakini ninaamini Wizaraya Afya ni mdau mkubwa katika jambo hili. Jamani hospitalikusimama kwa sababu tu hakuna dereva! Kama haupoutaratibu, tunaomba mwongozo utolewe wa kumewezeshaMkurugenzi kuhakikisha kamwe ambulance haisimami kwakukosa dereva.

Page 183: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ajira kwa Madaktarina Wauguzi. Ni jambo la kushangaza kuwa baadhi yaMadaktari wanahitimu lakini wanahangaika kutafuta ajira nawengine kukata tamaa na kwenda nje ya nchi. Ninaombakujua, hivi sasa tuna Madaktari wangapi ambao badohawajaajiriwa, huku uhaba wa Madaktrai na Wauguzimbalimbali wakiwa hawatoshi katika hospitali zetu. Naombamkakati wa manpower planning kwa Sekta hii uwekwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Mloganzilaimekamilika na ninapongeza juhudi za Awamu ya Nnezilizoijenga, lakini naamini ni muhimu sasa kuwa na mpangowa kujenga hospitali town. Hivi sasa madaktari hawanamakazi na sijui kama dharura ikitokea itakuwaje.

Mheshimiwa Naibu Spika, MSD ya Kanda ya ZiwaMagharibi ipo Muleba. Mheshimiwa Waziri anajua kulikuwepona tetesi kwamba itahamishwa kwenda Bukoba. MheshimiwaWaziri Dkt. Ndugulile alitembelea MSD hiyo na kuona athariza kuihamisha. Aidha, mantiki ya kuiweka Muleba ni kwa kuwani katikati ya eneo la huduma; Kagera, Geita na KigomaKaskazini. Naomba hofu hii ya kuhamisha MSD ya Kandaiondolewe ili maendeleo yaliyopangwa yaendelee. Eneo lakutosha ekari tano zimetolewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bima ya Afya ni mkombozina tunapongeza maendeleo yake. Changamotozinazojitokeza ni ngazi ya referral system. Inaonekana hakunamanual ya recommended drugs kwa Hospitali za Rufaa.Hicho hicho cha hospitali za kawaida ndicho kinatumikaHospitali za Rufaa. Hii ina ukakasi, kwani Hospitali za Rufaazina utaalamu zaidi na wanaweza kukubadilishia dawa. Sasakuna Wakaguzi wa NHIF na uthibiti wa abuse, ni muhimu kwasababu wakaguzi hao wanaweza wasikubaliane na daktaribingwa, inaleta ukakasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, nil imwombaMheshimiwa Waziri Ummy atambue Hospitali ya Mkoa yaBukoba haikidhi viwango vya referral kutoka Hospitali Teuleya Rubya. Kwa hiyo, Bima ya Mkoa wa Kagera referral iwe

Page 184: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

Bugando, hata kwa Bima ya jamii, yaani zahanati - wilaya -Bugando hadi Rubya Hospitali ya Mkoa itakapoboreshwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri huduma zasaratani ziendelee kuboreshwa. Tunapongeza Ocean Roadna Bugando kwa huduma zao lakini hazitoshi. Pia tuwekezekatika kuzuia kuenea kwa saratani, tupime afya, tusingojeemionzi. Prevention is better than cure. Inahitaji Wizara kupigakampeni ya rollback cancer.

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: Mheshimiwa NaibuSpika, awali nawapongeza Mheshimiwa Waziri na NaibuWaziri kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya katika Sektahii muhimu sana kwa maisha ya mwanadamu.Nawapongeza pia Katibu Mkuu, viongozi na watumishi wotewa Wizara kwa bajeti nzuri na kwa kuchapa kazi. MwenyeziMungu aendelee kuwawezesha.

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Serikali kwamaboresho makubwa katika Sekta ya Afya nchi nzima. Hii nikazi kubwa sana na ni ukombozi kwa wananchi wa Tanzania.Kufungamananisha uchumi na maendeleo ya wananchikunaonekana katika sekta hii. Sasa naiomba Serikali yanguilete Muswada Bungeni wa Sheria ya Bima ya Afya kwa woteili wananchi wafaidike na huduma bora za afya nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishukuru Serikali kwakulipatia Jimbo langu zaidi ya shilingi bilioni moja kujenga vituovya afya viwili na kuvipatia vifaa tiba. Vituo hivyo ni Keregena Matimbwa. Vituo hivi vitachangia sana kuboreshahuduma ya afya Bagamoyo. Kituo cha Afya Kerege kimeanzakufanya kazi isipokuwa cha Matimbwa (Yombo) badohakijaanza kazi. Namwomba Mheshimiwa Waziri atusaidiekupata samani, vifaa tiba na watumishi wa ajili ya Kituo chaAfya cha Matimbwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vijiji zaidi ya 20 (kata tano)katika barabara ya Bagamoyo Msata (kilometa 64) havinahuduma ya kituo cha afya. Namwomba Mheshimiwa Waziri

Page 185: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

atupangie kituo cha afya katika eneo hilo kubwa tokaBagamoyo mpaka Msata.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. ZAINAB MUSSA BAKAR: Mheshimiwa Naibu Spika,Wizara hii ni muhimu sana ukitoka Wizara ya Elimu. Hii ni Wizarayenye kushikilia maisha ya Watanzania. Bila kuimarisha Wizarahii, hakuna Serikali ya Viwanda wala Tanzania ya Viwandakwani afya ni kila kitu. Watanzania wakiwa na afya bora ndiyoshughuli za kiuchumi zitakuwa na maendeleo, kwani mwenyekuleta maendeleo ni wananchi wenye afya bora na nguvukazi ya Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,naomba nitoe maoni yangu katika Wizara hii. Kwanza niupungufu wa rasilimali watu katika Wizara hii ya Afya. Sektahii ina upungufu mkubwa wa rasilimali watu. Sekta hii inaupungufu wa watumishi kwa asilimia 49 katika mwaka wafedha 2016/2017. Tunaomba Serikali itoe hitaji la watumishiwa sekta hii ya afya ili wananchi wapate matibabu kwawakati na kwa ubora wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba MheshimiwaWaziri aone kilio cha Watanzania juu ya hitaji hili muhimu.Imekuwa na usumbufu kwa wananchi wanapohitajimatibabu wanachukua muda mrefu hospitalini, mtuanakwenda saa 12.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni ndiyoanapata matibabu kutokana na uhaba wa wahudumu.Mhudumu ana daktari mmoja, huyo anahitajika zaidi yavitengo vitatu kwa wakati mmoja. Hii ni shida.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali ituambieni lini itatatua tatizo hili la upungufu wa watumishi katika sektahii?

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nitazungumzia hali yamaambukizi ya VVU na UKIMWI nchini Tanzania. Hali hiiinaendelea kukua kwa kasi zaidi kinyume na hali iliyotarajiwa.Dhana nzima ya 90 – 90 – 90 iliyoanzishwa na Umoja wa

Page 186: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

Mataifa kuhusu HIV/AIDS mwaka 2013 kwamba ili kufikiamwaka 2020 kusiwepo na maambukizi ya UKIMWI Duniani.Kwa maana, kutambulika, waliotambulika wako kwenyematibabu ya ARV na wenye matumizi ya ARV, virusi vitakuwavimefubaa na hakutakuwa na maambukizi mapya. Hii ndiyoazma ya 90 – 90 – 90.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Tanzania, hatujafikiahatua hii, ni hatari sana na ndiyo kwanza maambukiziyanazidi. Kwa mfano, vijana kati ya miaka 15 - 49 ndiyo rikahatari zaidi na wenye kuleta maambukizi zaidi. Hawa ni vijanaambao wako shuleni na vyuoni kwa asilimia 46. Je, Tanzaniatumefikia wapi katika kufikia lengo la 90 – 90 – 90 natukizingatia umebaki mwaka mmoja na nusu kufikia mudauliowekwa na Umoja wa Mataifa? Serikali itufahamishe.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Serikali na Sekta hii itoeelimu kuhusu HIV/UKIMWI na isione haya kueleza vituvinavyosababisha maambukizi, bila kificho. Kama Serikalihaitaacha kupiga marufuku condom UKIMWI utaendeleakuwepo, kwani hivi ni vichochezi vya zinaa. Vitabu vya dinivinasema tusikaribie zinaa, zikishamiri maradhi yatazidi amamajanga na hili ni janga na siyo maradhi kwani kila maradhihuwa yana tiba ila UKIMWI hauna tiba. Ili UKIMWI uondoke,tuache zinaa tutake tusitake.

Mheshimiwa Naibu Spika, hali hii inatisha sana hasatukizingatia maambukizi kwa vijana hawa wadogo. Hii inamaana nguvukazi ya Taifa hii inapungua na kufa pia kwakasi sana na tusipochukua tahadhari tatizo hili ni zito nakubwa sana, huenda miaka ya mbele tutakosa kabisa vijanawenye afya bora wa kujenga Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna haja ya kuwekamikakati madhubuti ya kuzuia maambukizi mapya na kuwekasheria, kama ni kosa la jinai kufanya zinaa au vitendo hivi bilaya kuwa na ndoa. Kinyume na hayo tutatenga pesa amafedha nyingi za kutibu na maambukizi yataongezeka namwisho tutakosa nguvukazi za Taifa na hivyo Tanzania yaViwanda itabaki kuwa ndoto.

Page 187: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. HASNA S. K. MWILIMA: Mheshimiwa Naibu Spika,nami nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri, NaibuWaziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Watendaji wotewa Wizara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya pongezi hizo,nianze sasa kuchangia Wizara hii. Kwanza nitoe shukrani zadhati kwa Mheshimiwa Waziri kwa kunipatia ambulance mbiliKata ya Buhingu, kwenye kituo cha afya na ya pili Kituo chaAfya Kata ya Uvinza. Sambamba na shukrani hizi bado tunachangamoto kubwa kwenye Kituo cha Afya Kalya, kinaumbali wa kilometa 250. Mheshimiwa Waziri alipofanya ziaraalituahidi ambulance ya Kituo cha Kalya, tunaomba tuletewehiyo ambulance.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunavyo vituo vya afyavinne vinavyojengwa ndani ya Jimbo langu. Vituo vitatuUkanda wa Ziwa Tanganyika na kituo kimoja ukanda wa reli.Vituo hivyo ni hivi vifuatavyo: Kituo cha Afya Kabeba, Kituocha Afya Kazuramimba na Kituo cha Afya Igalula (Rukoma).Tunazo pia zahanati mbalimbali zinazojengwa kwa jitihadaza wananchi na kupitia Mfuko wa Jimbo. Mheshimiwa Waziriakiona inampendeza atusaidie fedha kwa ajili ya kumaliziamaboma haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaishukuru Serikali kwakutupatia shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali yaWilaya. Ujenzi umeshaanza, tunaendelea. Tunaomba kwenyebajeti hii tutengewe fedha nyingine kwa ajili ya kuendelezahospitali hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, majengo hayawezi kwishabila vifaa na watumishi. Hivyo, tunaomba Mheshimiwa Wazirikwenye mgao wa watumishi, Uvinza iangaliwe kwa jicho lahuruma, kwani jimbo ni kubwa na watumishi ni wachachesana. Sambamba na watumishi, tunaomba pia vitendeakazi,kwa mfano Ukanda wa Ziwa Tanganyika na Kituo cha

Page 188: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

Nguruka wapate vifaatiba kama X-Ray, Ultrasound na vifaavingine, kwani wagonjwa ni wengi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunatambua fikaHalmashauri ya Uvinza ilianzishwa tarehe 18 Mei, 2012 lakinihakuna idara hata moja iliyo na gari. Hii inasababisha Wakuuwa Idara kupata taabu sana kwenye kufanya ufuatiliaji wautekelezaji wa fedha zinazopelekwa huko chini kwenye kata,vijiji na vitongoji.

Namuomba Mheshimiwa Ummy atupatie gari moja,Land Cruiser ya watumishi kufuatilia miradi na utendaji kaziwa watumishi kwani malalamiko ya wananchi ni mengi, nivyema gari ikapatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, nimkumbusheMheshimiwa Ummy Mwalimu ahadi yake ya kumpongezaNesi Zainabu, anayefanya kazi kwenye Zahanati yaMwakizega kwa kazi nzuri hadi wananchi wakaandamanakumlilia Nesi Zainabu. Maana tangu mwaka 2017 hakunamotisha yoyote aliyopewa kwenye Halmashauri ya Uvinza.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa, niendeleekumpongeza mdogo wangu, Mheshimiwa Ummy Mwalimu,kwani ataacha kumbukumbu muhimu sana kwenye hiiWizara. Sote ni mashahidi, anafanya kazi yenye tija nakuridhisha sana. Baada ya pongezi naomba kuunga mkonohoja hii asilimia mia moja.

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza naomba nitoe pongezi zangu kwa Serikali ya Awamuya Tano, pia kwake Mheshimiwa Waziri Ummy na Naibu wake,Mheshimiwa Dkt. F. Ndugulile, kwa kufanya kazi kwa weledimkubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na shukrani hizi,naomba nikumbushe jambo moja kwamba Dongobesh, Kituocha Afya na Jimbo la Mbulu Vijijini hatuna kabisa gari lawagonjwa (ambulance) la kuwahudumia wananchi. Pia

Page 189: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

Mheshimiwa Mheshimiwa Ummy akumbuke ilikuwa ahadiyake pale Dongobesh baada ya ziara yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kweli nakubali kaziwanayofanya Mheshimiwa Ummy na Naibu Waziri,Mheshimiwa Dkt. Faustine, wamefanya ziara ya kuonachangamoto za Mbulu Vijijini. Pia tumejengewa kituo kimojacha afya cha Dongobesh, ahsanteni sana. Hospitali yaHalimashauri ya Wilaya inajengwa, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawaombea Mungu waruditena katika nafasi zao baada ya mwaka 2020 katika UchaguziMkuu. Mungu atujalie, ahsanteni.

MHE. PETER A. LIJUALIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika,Wilaya ya Kilombero haina Hospitali ya Wilaya, Hospitaliinayotumika ni Mtakatifu Fransisco lakini gharama zake nikubwa kidogo kwa watu wengi kuweza kumudu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tuna Vituo vya Afya vyaKibaoni, Mang’ula na Kidatu. Vituo hivi havikidhi mahitaji yakihuduma na tiba.

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wa Kilombero ni zaidiya 500,000. Bila ya kupata Hospitali ya Wilaya, bado bituohivi vitakuwa na kazi kubwa hivyo kupunguza ufanisi.Tunaomba kupatiwa Hospitali ya Wilaya ya Kilombero.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA: Mheshimiwa NaibuSpika, naunga mkono hoja. Hivi karibuni Mheshimiwa Raisalifanya ziara Mkoani Mbeya, akiwa Wilayani Chunya,aliombwa na wananchi fedha za kukarabati Hospitali yaWilaya. Mheshimiwa Rais aliahidi shilingi 200,000,000/= kwaukarabati huo. Naiomba Wizara ifuatilie na kutekeleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

Page 190: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

NAIBU SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Dkt. FaustineNdugulile dakika ishirini.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naombanianze kwa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunijaliaafya njema na kuniwezesha kuwepo katika Bunge lako Tukufuna kuweza kuchangia hoja iliyowasilishwa hapa Bungenitarehe 07 Mei.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa njia ya pekee kabisanaomba nimshukuru sana Mheshimiwa Dkt. John JosephPombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakwa kuendelea kuniamini kutumikia nafasi hii ya Naibu Waziriwa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.Aidha, napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Samia SuluhuHassan, Makamu wa Rais pamoja na Waziri Mkuu KassimMajaliwa Majaliwa kwa maelekezo mbalimbali ambayoameendelea kutupatia katika utekelezaji wa majukumuyangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa njia ya kipee kabisanapenda kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, MheshimiwaUmmy Mwalimu, mimi namwita Daktari kwa ushirikiano wakewa hali ya juu sana na miongozo mbalimbali ambayoameendelea kunipatia katika utekelezaji wa majukumu.Amekuwa ni nguzo moja muhimu sana na mafanikio hayatunayapata ni kwa sababu ya uongozi wake mahiri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Kamati yaHuduma na Maendeleo ya Jamii kwa michango yao, maoniyao na ushauri wao kwa kiasi kikubwa sana wamekuwa nidira na miongozo wetu na tunaahidi kwamba tutazingatiamaoni na ushauri wao katika kutekeleza majukumu yetu yamsingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwashukuru timu yawataalam ambao na sisi tunawaongoza, Makatibu Wakuuwawili, Dkt. Zainabu Chaula, Katibu Mkuu wa Fungu 52 na

Page 191: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

Dkt. John Jingu wa Fungu 53 kwa kazi kubwa na nzuri ambayowameendelea kuifanya. Kazi nzuri inaonekana kwa sababuna kazi nzuri ambayo wao kama Makatibu Wakuu naWatendaji wote wameendelea kuifanya pamoja na Wakuuwa Taasisi, vyuo vya mafunzo na hospitali zetu zote ambazona sisi kama Wizara tunazisimamia.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini haya yoteyasingeweza kwenda vizuri kama nisingepata support yawale wananchi ambao wamenileta hapa, wananchi waKigamboni na naomba nitambulishe pale juu gallery leo ninaviongozi wa Chama cha Mapinduzi natumaini utapata fursaya kuwatambua kutoka Wilaya ya Kigamboni naWaheshimiwa Madiwani wote kutoka Wilaya ya Kigamboninao wapo hapa kuja kushuhudia wasilisho la hotuba hii.Niendelee kusema kwamba Kigamboni tunawakilisha vizurindani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayomachache sasa naomba nijielekeze katika baadhi ya hojaza msingi ambazo ziliweza kutolewa na WaheshimiwaWabugne na nianze na hoja za Fungu 53, Fungu laMaendeleo ya Jamii. Niseme tu kwamba moja ya hoja yamsingi ambayo ilijadiliwa sana na Wabunge wengi ni sualala wazee, na suala la wazee sisi kama Serikali tunapaswatujivunie sana. Katika moja ya mafanikio ambayo Serikali hiiimeweza kufanya ni kuhakikisha kwamba umri wa Mtanzaniakuishi umezidi kuongezeka, hivi tunavyoongea wastani waMtanzania kuishi ni miaka 64.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, maana yake ninini, ni kwamba ni mafanikio ya mikakati yetu ya lishe lakinimafanikio ya vilevile ya mkakati yetu ya kuhakikisha kwambaWatanzania hawa tunapata huduma nzuri za afya, na ndiyomaana tuna kundi kubwa la wazee ambalo lipo natunatarajia kwamba kwa hali tuliyokuwa nayo watu wengiwatafika zaidi ya miaka 60 ya umri wakiwa na afya njemana kuweza bado wakiwa na nguvu ya kuendelea kutumikianchi yetu.

Page 192: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna Sera ya Wazee yaMwaka 2003, tunayo na tunaamini baada na sisi kuingaliatumeiona kwamba tunahitaji tuifanyie maboresho na kujamkakati sasa ambao utakwenda kutibu baadhi yachangamoto hizi za wazee.

Lakini naomba niseme kitu kimoja, Serikali inatambuana kuthamini mchango wa wazee ndani ya Taifa letu, nandiyo maana sisi kama Serikali tuna makazi 17 ya wazee ndaniya nchi lakini tunawahudumia takribani wazee 510 ndani yamakazi haya 17. Utaratibu uliokuwepo ni mmoja; sisi kamaSerikali tunawachukua wale wazee ambao kwanza hawanawatoto wa kuweza kuwahudumia, na kama wale wazeehawana watoto basi tunajaribu kuangalia, je, wazee hawahawana ndugu wa kuwahudumia, na je, kama hawa wazeehawana ndugu wa kuhudumia, je, jamii haiwezi ikabebajukumu hilo. Kama katika vigezo vyote hivi vitatu havipo basisisi Serikali tunawachukua wale wazee na tunawagharamiakwa vitu vyote, malazi, makazi na mavazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema idadiambayo ya wazee ambayo tunayo ni takribani 510 na wazeehawa tunawapa huduma hizo zote za msingi na katika jamboambalo tunalihakikisha Wizara ni kuhakikisha kwamba, hawawazee wanapata chakula, malazi na mavazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sambamba na hilotumeendelea kuhamasisha halmashauri kuzingatia agizo laSerikali la kuwapatia wazee vitambulisho kwa ajili yamatibabu ili wazee wapate matibabu kwa mujibu wa Seraya Afya ya mwaka 2017 ambayo inasema wazee watapatamatibabu bure. Lakini tulienda mbali zaidi na kuhakikishakwamba hospitali zetu zote zinakuwa na dirisha la wazee, iliwazee wakifika pale waweze kupata matibabu bure.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Sera mpya ya afyaambayo tunayo sasa hivi, tunataka sasa tuende mbali kuonakwamba kuna suala zima la matibabu ya magonjwa yawazee, kwa sababu wazee hawa kadri kundi linavyozidikubwa wanakuwa na magonjwa yao ambayo ni mahsusi,

Page 193: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

geriatric Medicine kwa lugha ya kitaalam nayo tumeshalionatunaliwekea mkakati ili kuhakikisha kwamba hawa wazeenao tunaweza kuwahudumia vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja katika jambo ambaloMheshimiwa Waziri aliliongea katika hotuba yake, ni pamojana haya magonjwa sugu ya non communicable diseaseambayo tumeona kweli changamoto na mara nyingiwakienda katika hospitali, dawa nyingi wanazokosa ni ziledawa za pressure, za kisukari na nini, hilo tumeliona na ndiyomaana tumeazimia kama tulivyokuwa tuna mapambano namagonjwa mengine kama kifua kikuu, TB na malaria,tunataka tuanzishe Mpango wa Taifa wa MagonjwaYasiyoambukiza na ambayo sasa yatakwenda kushukampaka katika ngazi ya chini ili huduma hizi za msingi zahuduma za matibabu utambuzi, matibabu na tiba yamagonjwa yasiyoambukiza iweze kupatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala jingine ambalonilikuwa nataka kuligusia ni suala la NGO’S, asas zisizokuwaza Kiserikali. Hivi karibuni tulibadilisha Kanuni, mara nyingitunatambua mchango mkubwa sana wa Mashirika yasiyoya kiraia katika kuleta maendeleo na kutusimamia kama sisiSerikali, na tunathamini, tunatambua mchango wao. lakinihivyo hivyo kama walivyotaka kutusimamia sisi na kutakakupata uwazi na uwajibikaji na sisi tunataka tupate uwazi nauwajibikaji katika taasisi zisizo za kiserikali. Ndiyo maanatumebadilisha Kanuni ili sasa kuwepo na uwazi katika fedhaambazo wanazozipata, lakini uwazi katika uwajibikaji katikayale maeneo ambayo walisema wanaenda kuyafanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumekuwa na changamotokuna baadhi ya NGO’s zimepata fedha nyingi sana, lakinihaziendi katika malengo yale ambayo yalikuwayanakusudiwa. Na baadhi ya NGO’s zimetoka katikamalengo na makusudio ambayo yalikuwa yanayafanya,wameenda kujiingiza katika mambo mengine. Wenginewanapata dola milioni 100 lakini zinazofika kwa walengwa nichini ya dola milioni moja.

Page 194: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tumeweka utaratibukwamba fedha zote zinazoingia lazima tuzijue, zinaendakufanya kazi wapi, lakini tunataka tulete uwiano kwambakuna baadhi ya maeneo ndani ya nchi yetu huku, zimekuwana NGO’s nyingi sana lakini kuna maeneo ndani ya nchi yetuhazina NGO’s hata moja na kote huko kuna Watanzania. Sasatunataka tuweke utaratibu mzuri, tumeanzisha Kanzi data,tuna NGO’s karibuni 9,000 ndani ya nchi yetu, mpaka sasahivi tumeshaziingiza kwenye Database NGO’s takribani 6,000,tunaendelea na usajili na lengo ni kusudio ni kwamba kilammoja kule kule alipo hahitaji kuja Dodoma. Tunawezatukapata taarifa zake tukajua yuko wapi, anafanya nini nafedha alizokuwa nazo kiasi gani, anawajibika kwa utaratibugani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niendeleekuwatoa shaka ndugu zangu lengo siyo baya, lengo nikuweka uwajibikaji na uwazi ili kabisa kuhakikisha kwambahizi NGO’s ambazo na sisi kama Serikali tunatambuamchango wao ili waweze kufanya kazi zao vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ambaloliligusiwa na Waheshimiwa Wabunge ni masuala ya Mitaalaya Vyuo vyetu vya Maendeleo ya Jamii na Vyuo vya Ustawiwa Jamii, haya Waheshimiwa Wabunge tumeyapokea,tutaenda fanyia kazi ili sasa Mitaala hii iendane na mazingiraya sasa na uhitaji wa sasa wa Tanzania ambayo tunaelekeakatika Tanzania ya viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa nijielekezekatika maeneo mengine ya Sekta ya Afya hususan Vote 52.Namshukuru sana Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMIamegusia suala la watumishi, rasilimali watu. Na miminiendelee kuongezea kidogo tu katika hili, pamoja nachangamoto hii tuliyokuwanayo ya rasilimali watu, sisi kamaWizara ya Afya hatujakaa tukalala. Tumeangalia ubunifuambao tunaweza tukatumia kuangalia jinsi gani tunawezakutumia rasilimali chache, watu hawa tuliokuwa nao ilikuweza kuleta tija katika utoaji huduma za afya.

Page 195: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya jukumu ambayotumeweza kulifanya katika lugha ya kitaalam wanaita taskshifting…

MBUNGE FULANI: Yes.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: …kwa sababu unaweza ukaenda katikakituo cha afya, daktari yule, kwa mafunzo ambayo tunayo,mimi ninaweza nikachoma sindano, nikafunga kidonda naninaweza nikatoa dawa. Sasa inawezekana mtu akawa paleamemaliza majukumu yake, anaweza akaenda akafanyajukumu lingine ambapo ndani ya kituo. Tumeona tuweze ku-reorient haya majukumu ili basi huduma kwa mwananchiiweze kutolewa, kwa sababu wataalam wengi wa afyatumeweza kupata mafunzo katika nyanja mbalimbali.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile tumeanza kutumiawataalam wengine ambao sio wataalam wa afya,wamepata orientation, kwa mfano kwa masuala ya upimajina uchukuaji wa vipimo. Wameweza kupata orientation nawanaweza wakafanya hayo majukumu. Tunataka tufanyeorientation ya Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Ustawiwa Jamii, basi nao waweze kutusaidia kutoa huduma katikabaadhi ya maeneo ambayo tunaona yana tija. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tumeanza kutumia elimumtandano (telemedicine). Kwa sasa hivi tunafunga mashineza digitali, dunia nzima ilishatoka huko. Sasa hivi Marekani X-Ray zinasomwa Australia ama inasomwa India. Nasi kwa niniwataalam wetu hawa wachache; na tumeshaanza, paleMOI na Muhimbili tunafunga mashine za kisasa, kutakuwana screen ziko pale. Mashine zote hizi za X-Ray ambazotunazifunga Tanzania nzima, itakuwa picha zake zotezinapelekwa Muhimbili na MOI zinasomwa na ndani ya dakika15 au 20, mtu wa Tunduma, Ruvuma, Mbinga anawezaakapata majibu yake yamesomwa na wataalam. Hizi nibaadhi ya innovation ambazo tunaendelea kuzitumia.(Makofi)

Page 196: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Madaktari wetuBingwa hawa wachache tuliokuwa nao, tumesema pamojana kwamba wako katika maeneo ya mjini na katika hospitalizetu kubwa, nami nashukuru sana Hospitali zetu za JKCI,Bugando, MOI, Mloganzila na KCMC wamekuwa wanatoawataalam wao, wamekuwa wanaenda katika kambimbalimbali mikoani, wanaendesha kambi za muda mrefu iliwale wananchi wa kule nao waweze kupata huduma hizi zakibingwa na zimekuwa na mchango mkubwa sana natutaendelea na utaratibu huu kuhakikisha kwamba hudumaza kibingwa nazo zinapatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, innovation tunazonyingi na ndiyo maana unaona kwamba pamoja nachangamoto tulizokuwanazo, hali ya utoaji huduma za afyabado zinaendelea kwa ubora ule ule ambao upo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilitukabidhi Hospitaliza Rufaa za Mikoa, nasi tunaendelea kuzipanga. Mkakatiwetu wa kwanza ni kuhakikisha kwamba hizi Hospitali za Rufaakatika mikoa ambayo hatuna, ni Hospitali za Rufaa za Mikoandiyo tunataka kuanza nazo; Mkoa wa Songwe, Njombe,Geita, Katavi na Simiyu. Ndiyo maana tumeweka nguvukubwa sana katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua ya pili tunataka sasakatika maeneo ambayo tayari kulikuwa kuna majengo kwamaana ya Mikoa ya Singida, Tanga kule na Shinyanga,tunawekeza nguvu yale majengo yaanze kupata matumizilakini awamu ya tatu sasa tutajielekeza katika hizi RRHnyingine kuhakikisha kwamba zile huduma za msingi nazozinaweza kupatikana ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa vifaana rasilimali watu. Tumewekeza sana sasa hivi katika mafunzoya wataalam wa afya ili kuhakikisha sasa zile huduma zakibingwa na Madaktari Bingwa wanaweza kupatikana katikamaeneo haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naamini katikamwaka wa fedha peke yake tumepata kama shilingi bilioni1.5 kufundisha wataalam zaidi ya 300 na tunataka kwenda

Page 197: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

mbali. Katika moja ya jambo ambalo tunalitafakari sasa hivini kubadilisha mfumo wetu wa mafunzo kwenda kwautaratibu wa fellowship. Badala ya watu kukaa darasani,watu wanaweza wakaendelea kutoa huduma kule kuletukawapima zile competence zao ambazo tunazitaka nakuwatambua kwamba hawa ni Madaktari Bingwa. Wenzetuwameshapiga hatua kubwa sana katika utaratibu huu, nasitunaamini ndani ya muda mfupi sisi kama Wizara tutakuwatumepiga hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie na mambomakubwa mawili au matatu kabla sijarudishia Wizara hii, kunahoja ilikuja hapa kuhusiana na chanjo ya Malaria. Kwa niniwenzetu wa Malawi wamekuwa na chanjo ya Malaria nakwa nini sisi Tanzania tusianzishe chanjo ya Malaria?

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe maelezo yakitaalam kidogo kwamba mpaka sasa hivi hakuna chanjoya Malaria ambayo imethibitika asilimia 100 kutoa kinga dhidiya Malaria. Chanjo nyingi tulizokuwa nazo hapa zinachezakati ya asilimia 20 mpaka 40. Hamna chanjo ambayo imezidizaidi ya hapo. Kwa hiyo, chanjo nyingi bado zipo katika ngaziya hatua ya utafiti na naomba niseme kwamba Tanzaniatuko vizuri sana katika masuala ya utafiti wa Malaria. Taasisiyetu ya NIMR inafanya kazi nzuri sana ya utafiti na Taasisi zetuza Ifakara Institute nayo inafanya kazi nzuri sana. Paletutakapobaini kwamba kuna chanjo ambayo inaweza ikawaina tija, basi na sisi kama Tanzania tutakuwa ni wa kwanzaku-adopt hizo chanjo kwa ajili ya kuwakinga wananchi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie fursa hii kusemakwamba uwepo wa chanjo hauondi dhana ya sisi kuendeleana mikakati mingine yoyote ya kujikinga dhidi ya ugonjwawa Malaria. Kwa hiyo, tuendelee kwa sababu mazalia hayahaya ya mbu ndiyo hayo hayo mazalia ya ugonjwa waDengue, Zika, Kichungunya na magonjwa mengi sanaambayo yapo. Kwa hiyo, nami nataka niwaombeWatanzania tuendelee na mikakati yetu mingine, tunapigahatua katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria lakinitunahitaji tuongeze kasi.

Page 198: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

Mheshimiwa Naibu Spika, chanjo ya gonjwa la ini,tuna tatizo la ugonjwa wa ini ndani ya nchi. Chanjo yaugonjwa wa ini tunatoa kwa watoto wote chini ya miakamitano, ni sehemu ya chanjo ambayo tunaitoa na kwa watuwazima tumekuwa tunatoa kwa wale ambao wako kwenyerisk zaidi ikiwa ni pamoja na wataalam wa afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu ambaotutakwenda nao na tulishakubaliana na Mheshimiwa Wazirini kwamba kwa yule atakayekuwa anahitaji, tutawekautaratibu wa chanjo hizi kupatikana kwa gharama nafuu ilimtu mwingine atakayekuwa anajisikia, basi aweze kuchanjakama nasi Waheshimiwa Wabunge tulipata fursa ya kuwezakuchanjwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho kabisa naombaniongelee suala la upimaji. Ni kweli tumekuwa nachangamoto kubwa sana ya watu kubainishwa na ugonjwawa Typhoid na UTI. Nimesema sana na ninaomba nitumiefursa hii kuongea na Bunge lako. Ukienda hospitali na ndaniya dakika tano Daktari akwambia UTI ama una Typhoid,naomba umwulize maswali ya msingi sana huyo daktari.Amejuaje?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa utaalam wetu sisimadaktari inahitaji kati ya masaa 48 mpaka 72 na achukuekipimo cha mkojo na achukue na kipimo cha damu kujakukwambia wewe una ugonjwa wa Typhoid au una UTI.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nawaomba sanana Waheshimiwa Wabunge mtusaidie kutoa elimu kwa jamiikuwahoji wataalam wetu wa afya kwa sababu wengi sasawameamua kwa kutumia homa ya UTI na Typhoid kamachanzo cha kupata fedha, lakini kimsingi hatuna tatizo kubwasana la UTI na Malaria kama inavyosemwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,naomba kumaliza hizi hoja kama nyingi zi l ivyokuwazimejitokea na nitoe fursa sasa kwa Mheshimiwa Waziri awezekuendelea na hoja nyingine. (Makofi)

Page 199: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, namwitasasa Mheshimiwa Ummy Mwalimu, mwenye hoja ya Wizaraya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.(Makofi)

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEENA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwakunipa fursa hii. Namshukuru sana Mheshimiwa Naibu WaziriMheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile kwa kutoa ufafanuzi wabaadhi ya hoja. (Makofi)

Mhesimiwa Naibu Spika, naomba kuchukua fursa hiikuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote waliochangiakwa kuzungumza na kwa maandishi wakati wa hoja ambayoiko mbele ya Bunge lako Tukufu. Kipekee napendakumshukuru sana Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yaHuduma na Maendeleo ya Jamii, Mheshimiwa Peter JosephSerukamba ambaye aliwasilisha maoni na ushauri wa Kamatiya Kudumu ya Bunge kuhusu utekelezaji wa maagizo yaKamati pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara yangu kwa mwaka 2019/2020.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia napenda kuwashukuruKambi ya Upinzani ingawa mambo mengi yameandikwa kwakukosa taarifa na takwimu sahihi ya hali ya Sekta ya Afyainavyokwenda mbele toka Mheshimiwa Rais Dkt. John PombeMagufuli ameingia madarakani. Kwa hiyo, nitawajibu hojazao. Katika hatua hii tunawashukuru kwa kutoa hoja ambazohazina mashiko ya takwimu sahihi na hali halisi ya utoaji wahuduma za afya nchini Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee napendakuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote ambaowamechangia hotuba yangu kwa kuzungumza na kwamaandishi ambao ni Wabunge 112; kati yao Wabunge 44wamechangia kwa kuzungumza na Wabunge 59wamechangia kwa maandishi. Aidha, WaheshimiwaWabunge tisa walichangia wakati wa hotuba ya MheshimiwaWaziri Mkuu.

Page 200: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

200

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli hoja ambazozimetolewa na Waheshimiwa Wabunge ni nyingi, kwa hiyo,nitashindwa. Haya makaratasi yote ni majibu ya hoja ambazozimetolewa. Kwa hiyo, nitatoa tu ufafanuzi katika baadhi yamambo makuu. Naomba niwaambie WaheshimiwaWabunge kwamba tumepokea maoni na ushauri wenu natutaufanyia kazi katika kuhakikisha kwamba tunaboreshahuduma za afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunawashukuru katikahatua hii ya awali kwa pongezi kubwa nyingi ambazowametupatia mimi, Naibu Waziri pamoja na Watendaji waWizara na Katibu Mkuu. Naomba kupitia kwako niwaahidiWaheshimiwa Wabunge wote, pongezi hizi hazitatufanya sisitukalewa sifa, bali ni chachu ya kufanya kazi vizuri zaidi ilituweze kuhakikisha huduma bora za afya, maendeleo naustawi wa jamii zinapatikana kwa Watanzania, lakini hasawa kipato cha chini.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapozungumzia UniversalHealth Coverage hatuzungumzii tu Bima ya Afya, maanayake kila Mtanzania wa hali yoyote masikini, kipato cha kati,tajiri wa kijijini, wa mjini aweze kupata huduma za afya bilaya kikwazo chochote ikiwemo kikwazo cha fedha. Kwa hiyo,niseme tu kwamba tumepokea ushauri na pongezi lakinitutaendelea kufanya kazi kuhakikisha tunatatuachangamoto za Sekta ya Afya katika nchi yetu, kwanitunatambua bila afya hakuna elimu, bila afya hakunamaendeleo, bila afya bora hakuna uchumi na bila afya borahakuna ulinzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijatoa ufafanuzi,natambua kwamba Kanuni za Bunge zilishatoa pole, lakinikabla sijaendelea, naomba nami kuungana na WaheshimiwaWabunge na Bunge lako Tukufu kutoa pole kwa familia yaDkt. Reginald Mengi ambaye amekuwa mdau mkubwa waSekta ya Afya. Kwa hiyo, tunawapa pole familia natunawaombea Mwenyezi Mungu awape subira naustahimilivu katika kipindi hiki kigumu.

Page 201: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

201

Mheshimiwa Naibu Spika, wewe ni shahidi, Dkt. Mengiamekuwa akitupa nafasi katika vyombo vyake ITV, RadioOne, East Africa Radio kutoa Elimu ya Afya kwa Umma kuhusumasuala mbalimbali. Pia ameweza kusaidia watu wenyeulemavu. Kubwa, tutamkumbuka na kum-miss katika Sektaya Afya kwa sababu alianza kuwekeza kujenga Kiwanda chaDawa M-Pharmaceuticals Bagamoyo, lakini MwenyeziMungu hakupenda ndoto yake iweze kutimia.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,sasa niruhusu nijibu baadhi ya hoja. Nikianza na hoja ambazozimetolewa na Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleoya Jamii; tumepokea ushauri na maoni ya Kamati na kwakweli yote tutayafanyia kazi. Jambo kubwa ambalowalilitolea maoni ni kwamba Serikali ihakikishe fedhazilizotengwa kwa Mwaka 2018/2019 zinatolewa zote na kwawakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunakubaliana na ushaurihuu na niwaahidi Waheshimiwa Wabunge kwambatutaendelea kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango ilikuhakikisha kwamba fedha zote ambazo zimetengwa katikabajeti ambayo inaisha Juni zinatolewa kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninazo habari njema.Mheshimiwa Dkt. Mpango na timu yako ninakushukuru sana.Katika mwezi wa Pili ambapo tulishatoka kwenye Kamati,tumepata shilingi bilioni 62 kutoka Hazina, shillingi bilioni 20tumepata kwa ajili ya dawa; shilingi billioni 32 tumepewabaada ya kuwa tumeshawasilisha makadirio yetu kwenyeKamati ambazo zitatumika kwa ajili ya kuboresha hudumaza matibabu ya kibingwa ikiwemo upandikizaji wa kutumiachembe chembe za mwili tunaita bone marrow transplant.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tumepata kutokaHazina shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kuboresha huduma katikaHospitali za Rufaa za Mikoa. Nje ya bajeti ambayo ilipitishwana Bunge lako Tukufu Mheshimiwa Oscar Mukasa amesemahapa, sisi pia; mimi na Naibu Waziri na Katibu Mkuu,tunahangaika kutafuta vyanzo vingine vya fedha. Kwa hiyo,

Page 202: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

202

nje ya bajeti ambayo imetolewa, ndani ya mwezi wa Nnetumepata shilingi bilioni 58 kupitia Mfuko wa Pamoja wa Afyaambao tumepeleka katika zahanati, katika hospitali zawilaya, katika vituo vya afya kwa ajili ya fedha za uendeshaji.Kwa hiyo, tunapokea maoni na ushauri wa Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Mheshimiwa RaisDkt. John Pombe Magufuli ni Serikali ya kushughulikia nakutatua changamoto za watu hasa wanyonge na ndiyomaana fedha hizi zimeendelea kutoka kwa ajili ya kuboreshahuduma za afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili ambalolimeelezwa na Kamati ni kwamba Serikali ikamilishe mchakatowa kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya.Tunakubaliana na ushauri huu na tunaamini, kamatulivyoahidi katika hotuba yangu, mwezi wa Tisa tutakujaBungeni kwa ajili ya kuleta mapendekezo ya Sheria ya Bimaya Afya ambayo itamlazimu kila Mtanzania sasa kuwa naBima ya Afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na hoja zaWaheshimiwa Wabunge. Mtanzania masikini kama huna helani changamoto kupata matibabu. Tukiangalia takwimuambazo nimezionesha katika kila Watanzania 100 niWatanzania nane tu ndio wana Bima ya Afya ya NHIF. SasaMtanzania huyo awe na tatizo amezungumza kaka yanguMheshimiwa Khatib kutoka Pemba, unatakiwa kufanyadialysis session moja ni shilingi 180,000/= mpaka shilingi250,000/=.

Mheshimiwa Naibu Spika, Daktari anawezaakakwambia ufanye dialysis, yaani kuchuja damu sijuikusafisha damu au kutakasa damu (sijui dialysis kwa Kiswahili),Kutakasa damu nadhani kwa Kiswahili kizuri. Anawezaakakuandikia ufanye mara tatu; minimum anawezakukwambia ufanye mara mbili kwa wiki. Mara mbili Mtanzaniagani anaweza ku-afford shilingi 400,000/= kila wiki kwa ajili yahuduma za dialysis?

Page 203: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

203

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tumeoneshwa hudumaza kupandikiza figo, kupandikiza vifaa vya kuweza kuwasaidiawatoto kusikia, ni Bima ya Afya ndiyo zimefanya hii kazi yakutoa huduma hizo ambazo zilikuwa zinapatikana kwa shilingimilioni 30 mpaka shilingi milioni 80. Kwa hiyo, tunakubalianana Waheshimiwa Wabunge kwamba tutaleta Muswada waSheria, lakini pia kabla ya kuleta Muswada wa Sheria,tutaendelea pia kufanya uhamasishaji na kutoa elimu kwajamii kuhusu umuhimu wa kujiunga na Bima ya Afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, siyo kwamba Watanzaniahawana pesa, kuna suala la willingness to pay na affordabilityto pay. Kwa hiyo, Watanzania wengi bado hawako tayarikulipa Bima ya Afya. Nitumie Bunge lako Tukufu kutoa rai kwaWatanzania. Ule utamadumi tuaojenga kuchangiana harusi,kuchangiana Kitchen Party, tuujenge katika kuchangianakununua Bima za Afya kwa ajili ya Watanzania masikini.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalolimeongelewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge, jambo la tatu,ni suala la kufanya uboreshaji wa huduma za uzazi katikamaeneo mbalimbali. Tunakubaliana na ushauri wa Kamati.Waheshimiwa Wabunge wenyewe ni mashahidi, hata vituovya afya vinavyoboreshwa na vilivyoboreshwa 352, asili yakeya andiko la vituo hivi ni kuboresha huduma za uzazi, mamana mtoto. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hili tuliona, hivi sisi kamaMawaziri; nilikaa nikasema, hivi mimi Ummy Mwalimu, Wazirimwanamke, sina background ya Udaktari, lakini badoMheshimiwa Rais ameniamini niongoze Wizara ya Afya,naacha legacy gani kwa Watanzania? Kwa hiyo,nawashukuru sana wataalam wa Wizara, tuliweza tukakaatukaandika andiko na ndiyo maana sasa tunaboresha vituovya afya takriban 350. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sanaMheshimiwa Jafo na timu yake kwa sababu walijiongeza naDkt. Chaula. Sisi tungeweza tu tukatafuta fedha, lakini wao

Page 204: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

204

wakaja na wazo la Force Account ambalo limeleta mafanikiomakubwa katika uboreshaji wa miundombinu ya afya. Kwahiyo, tunakubaliana na maoni ya Kamati. Tutaendeleakuboresha huduma za afya ya mama na mtoto. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nami nataka kusema mbeleya Bunge lako Tukufu, tunataka Watanzania hasa wanawakeambao ndio wapigakura wa chama changu Chama chaMapinduzi kujionea kwamba huduma za afya ya mama namtoto zimeboreka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na vituo vyaafya, pia tumeanzisha kampeni mbalimbali za kuhamasishauwajibikaji na matokeo chanya katika kupunguza vifo vyaakina mama na mtoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sanaMheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwandio mlezi wa kampeni hii. Tumeweza pia kuhakikishatunaweka wataalam wakiwemo wataalam wa kutoa dawaya ganzi na usingizi ambapo tumeweza kugharamia mafunzotakriban ya watu 200.

Mheshimiwa Naibu Spika, wifi yangu, sijui kamanaruhusiwa kusema hivyo, Mheshimiwa Esther Matikonitamjibu baadaye, lakini anaweza akasema labdatunasema. Ukitaka kupima, je, tunakwenda mbele katikaeneo hili la afya ya mama na mtoto au hatuendi mbele?Tunaangalia viashiria vikuu ambavyo vimewekwa na Shirikala Afya Duniani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kiashiria cha kwanza: Je,huduma za uzazi wa mpango zinaendelea? Kwa mujibu watakwimu zetu, tumeongeza kiwango cha watumiaji wahuduma za uzazi wa mpango kutoka asilimia 32 hadi asilimia38. Hizi ni takwimu za NBS. Tukiangalia program data tutakuwatuko vizuri zaidi.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

Page 205: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

205

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEENA WATOTO: Huo ndiyo ukweli.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, wakati wenuwa kuchangia Mheshimiwa Waziri alikuwa kimya akiwasikilizana ninyi msikilizeni anapowajibu. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther Matiko naMheshimiwa Catherine Ruge mtulie, mpeni nafasiMheshimiwa Waziri. Tukianza kujibizana hapa, tutaanzakuzitafuta Kanuni zetu zinasemaje. Tafadhali, naombamsijibizane. Mheshimiwa Waziri endelea.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEENA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, huo ndiyo ukweli. Hatatukiangalia akina mama wanaojifungulia katika vituo vyakutoa huduma za afya, kabla Mheshimiwa Dkt. Magufulihajaingia madarakani ilikuwa ni asilimia 65 lakini kwa sababuhuduma za uzazi za mama na mtoto zimeboreka,tumeongeza idadi ya akina mama wanaojifungua katikavituo vya kutoa huduma za afya kufikia asilimia 32. Huu ndiyoukweli, hata katika ngazi ya mikoa, inaonekana kwamba haliya huduma za mama na mtoto zinaendelea vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la tatu ambalo ndiyoviashiria vikuu vya afya ya uzazi ya mama na mtoto, je, kunaongezeko la akina mama wajawazito ambao wanahudhuriakliniki angalau mara nne katika kipindi cha ujauzito wao.Tumeonyesha pia kwamba lipo ongezeko la zaidi ya asilimia30 la wanawake ambao wanahudhuria kiliniki angalau maranne. Kwa hiyo, hivi ndiyo viashiria vikuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunakuja kwenyetakwimu, je, vifo vimepungua au havijapungua. Utafitiuliofanywa na Taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), ulikuwa niutafiti wa mwaka 2015, kwa hiyo, sasa hivi hatuna takwimuzaidi ya hizo.

Page 206: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

206

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, nasimamambele ya Bunge lako Tukufu, NBS akifanya utafiti mwingine,sina shaka, vifo vya akina mama wajawazito vitakuwavimepungua kwa zaidi ya asilimia 50. Tukikusanya takwimuambazo tunazo katika mikoa, sipendi kuzitaja kwa sababusiyo takwimu rasmi, lakini hali inaonyesha kwambatumepunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya akina mamawajawazito. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya nne ambayoimeelezwa na Kamati na ambayo tumeipokea ni suala lamaambukizi ya UKIMWI na kwamba katika maambukizimapya ya UKIMWI asilimia 44.6 ni vijana wakati sheriainakataza mtu mwenye umri wa miaka 18 kupima UKIMWIbila ya ridhaa ya wazazi lakini pia inakataza mtu kujipimaUKIMWI mwenyewe isipokuwa apime katika vituo vya kutoleahuduma za afya. Tumepokea ushauri na tayari tumeandaamarekebisho ya Sheria ya VVU na UKIMWI, Sura ya 431ambayo tumependekeza turuhusu mtoto mwenye umri wachini ya miaka 18 kupima UKIMWI bila kuhitaji ridhaa ya mzaziau mlezi.

Pia tunapendekeza kwamba tutafanya marekebishoya sheria hiyo, kifungu 13(4) ili kuondoa ulazima wa watukupima VVU katika vituo vya kutolea huduma za afya tu. Kwahiyo, hayo tunategemea kuja katika Bunge lako Tukufu mweziSeptemba ili tuweze kufanya marekebisho haya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na Kamatikwamba hatuwezi kufikisha lengo la pili na la tatu lakuhakikisha tunatokomeza UKIMWI kama hatutatimiza lengola kwanza ambalo sasa hivi takwimu rasmi za NBS zinaonyeshakwamba ni asilimia 51. Takwimu rasmi za programu datatunaonyesha kwamba watu ambao wanaishi na Virusi vyaUKIMWI na wanajua hali yao ni asilimia 75. Kwa hiyo, sinashaka kwamba tukifanya haya marekebisho mawili yakuruhusu watu kujipima UKIMWI na watoto kuruhusiwakujipima bila ridhaa ya wazazi/walezi kwa sababuwanaolewa kwenye miaka 15 au 16 tutaweza kuongeza kasiya kupambana na UKIMWI.

Page 207: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

207

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la tano ambalolimeongelewa na Kamati ni suala la afya ya usafi na mazingirakwamba tushirikiane na Wizara ya Maji, Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia. Tumepokea yote haya na ni kwelinikiwa kama Waziri ambaye nasimamia sekta ya afya,tunaona mzigo mkubwa wa wagonjwa, takribani katika kilawagonjwa 100 wanaohudhuria OPD kwa maana yawagonjwa wasio wa kulazwa asilimia 60 ni magonjwa hayayanayotokana na suala zima la usafi. Pia tuna taarifa ya Benkiya Dunia ambayo imeonesha kwamba Tanzania tunapotezatakriban shilingi bilioni 400 kila mwaka kutokana na hali duniya usafi. Kwa hiyo, tumepokea ushauri kuhusiana na hali duniya usafi na tutayafanyia kazi masuala haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la sita ambalolimezungumzwa na Kamati kwa upande wa Fungu 52 nihuduma za lishe. Tunalipokea na sisi tutaendeleakuhamasisha wananchi kuhakikisha kwamba wanazingatialishe bora.

Mheshimiwa Naibu Spika, niende katika hojazilizoletwa na Kamati kwa upande wa Idara Kuu yaMaendeleo ya Jamii na kubwa lilikuwa Serikali ihakikishekwamba Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii inatengewafedha kwa ajili ya kufanya kazi za maendeleo na ustawi wajamii. Tumepokea ushauri huu na naamini Mheshimiwa Dkt.Mpango ananisikia kwamba Idara Kuu ya Maendeleo yaJamii na Ustawi wa Jamii nao wana mchango mkubwa katikakuhakikisha tunajenga Tanzania ya Uchumi wa Viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kuwathibitishiaWaheshimiwa Wabunge, hata juzi nimeongea na Watendajiwa Wizara, Wizara hii ni moja, kwa hiyo, lazima sasa tuoneshekwamba hakuna Vote ya Maendeleo ya Jamii ya Jamii auVote ya Afya, bali ni Wizara moja. Kwa hiyo, tunaona Sektaya Afya inapata rasilimali nyingi kutoka kwa wadau, kwa hiyo,tumeamua tutakuwa tunakata asimilia ya fedha za wadauambazo tunazipata kwenye Sekta ya Afya, tutazipelekakwenye Sekta ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii.

Page 208: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

208

Mheshimiwa Naibu Spika, suala kubwa ambalolilitolewa sasa na Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani. Kunajambo moja naomba niliseme, hii hotuba ukisoma, kunamaneno mengine unasema, hivi huyu ni Mtanzania ambayeyuko Tanzania au yuko nje ya nchi, anazungumza mamboambayo hajui nini kinaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mtu anasema,anasema majigambo ya Serikali kwamba imeboresha sektaya afya nchini ni kutafuta umaarufu wa kisiasa. Hivi unajiulizahivi huyu, anajua analolisema au basi tu anataka kusema iliaweze kusikika anaposema. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, binadamu mwema ni yulemwenye kushukuru, lakini pia kazi kubwa imefanyika chini yaUtawala wa Rais, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli...

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther Matiko, shida ikowapi Mheshimiwa Esther Matiko tafadhali, hajakutaja weweanaongea kwenye hotuba, kwa nini usimpe mudaazungumze amalize, kwa nini usimpe nafasi azungumze?Tafadhali Mhjeshimiwa Esther Matiko, hii ni mara ya mwishonakutaja jina humu ndani, tafadhali. Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEENA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, tunaposema hudumaza afya zimeboreka hatutafuti umaarufu wa kisiasa, bali ndiyoukweli.

Naomba nitoe mifano kama minne, wakatiMheshimiwa Dkt. Magufuli anaingia madarakani, watotowaliokuwa wanapata chanjo ni chini ya asilimia 85, leoasilimia 99 ya watoto wote wenye umri wa chini ya mwakammoja wanapata chanjo na nieleze ni halmashauri ganiimekosa chanjo za watoto. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati naingia, wazaziwamejifungua watoto hawana chanjo za kuwazuia nakifaduro, kifua kikuu, leo chanjo zinapatikana za watoto katikakila watoto 100, watoto 99 wanapata chanjo. (Makofi)

Page 209: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

209

Mheshimiwa Naibu Spika, katika huduma za matibabuya kibingwa, Wabunge wameona, kabla Mheshimiwa Dkt.Magufuli hajaingia madarakani, niambieni kama kulikuwa naupandikizaji wa figo, niambieni kama kulikuwa na upandikizajiwa vifaa vya kuweza kusikia, lakini leo hadi ninaposemakuanzia mwaka 2017, Watanzania 38 wamewezakupandikiziwa figo katika Hospitali yetu ya Taifa Muhimbili;Watanzania saba wameweza kupandikiziwa figo katikaHospitali yetu ya Benjamin Mkapa. Hawa Watanzania,hawawezi kusema ni umaarufu wa kisiasa, ila wanamshukuruMheshimiwa Rais kwa sababu amewezesha huduma hizikupatikana na zingekuwa zinapatikana nje ya nchi,wasingeweza kutoa milioni 100, milioni 120 kupata hudumahizi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, cochlear implant,upandikizaji watoto wa vifaa vya kuwasaidia kusikia,havijawahi kufanyika, vimefanyika wakati wa MheshimiwaDkt. Magufuli, watoto 21 wamefanyiwa. Sasa unajiuliza, hivihuyu anaposema ni umaarufu wa kisiasa, nadhanitumsamehe bure. Hivi anaposema ni umaarufu wa kisiasa,anaandika kwenye speech, umaarufu wa kisiasa, watoto 21wamepandikizwa vifaa vya kuwasaidia kusikia! cochlear

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalize kutoa mifano,health centers, vituo vya afya 352 vinaboreshwa navimekamilika, tuna Hospitali za Wilaya 67 zinaendeleakujengwa, lakini pamoja na msomaji wa Kambi Rasmi yaUpinzani, ana Kituo cha Afya kinaitwa Magena kimepatamilioni 400. Halafu atasema ni umaarufu wa kisiasa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kusema, yapomambo makubwa ambayo yamefanywa na Serikali yaAwamu ya Tano na kwa kiasi kikubwa huduma za afyazimeboreshwa. (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kukiri kwamba,changamoto za afya bado ni nyingi na tutaendeleakuzifanyia kazi, lakini lazima tushukuru mambo makubwa namazuri ambayo yamefanyika.

Page 210: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

210

Mheshimiwa Naibu Spika, tena nimalize, suala la pili,ambalo Kambi Rasmi ya Upinzani imehoji, kwamba bajeti yaafya imepungua kutoka shilingi trilioni moja hadi shilingi bilioni866, lakini pia tunategemea fedha za wazungu. Kwa hiyo,hawa hawa Wabunge ndiyo wamekuwa wakituambiatupunguze utegemezi wa wahisani! Kwa hiyo, kilichopungua,Mheshimiwa Dkt. Mpango ni shahidi, tumepunguza fedhazilizotoka kwa wahisani, lakini fedha za ndani ya nchi, fedhaza walipa kodi wa Tanzania, zimeendelea kuongezeka.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiangalia bajeti yamwaka 2017/18 ilikuwa bilioni 628, lakini mwaka 2018/2019bilioni 681; mwaka 2019/2020 bilioni 686.6, kwa hiyo, unazionafedha za ndani zinaendelea kukua, lakini ni kweli fedha zanje tumepunguza! Tulianza mwaka 2017/2018 ilikuwa ni bilioni449, tumepunguza mpaka bilioni 184 na mwaka huutunaomba fedha za nje bilioni 272. Kwa hiyo, inategemeaunaliangalia kwa perspective gani, lakini kama ni kuongezafedha za ndani, hakuna fedha ya afya ambayo imepungua.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna swali pialimezungumzwa na Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu suala laPPP, hilo sisi niseme tulishaanza kulifanyia kazi na kwa mfanokatika kufunga mashine za kupima maambukizi ya damu,tumeweza pia kuingia mikataba na mdau ambayeamefunga mashine hatutumii fedha za Serikali, lakini piatumetangaza tenda ya kuweza kuhakikisha tunafungavifaatiba bila kutumia fedha za Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalolimeelezwa na Kambi Rasmi ya Upinzani ni suala la hudumaya afya bila malipo kwa wanawake, lakini pia tumewasikia,suala la Wakunga wa Jadi kwamba wamezuiliwa.Tulichokitaka, siyo kuwazuia Wakunga wa Jadi, tunaendeleakutambua na kuthamini mchango wa Wakunga wa Jadikama wadau wakubwa wa huduma za afya ya uzazi, mamana mtoto. Sasa tunachokifanya, tunataka hawa watu wawekama ni daraja letu kati ya vituo vya kutoa huduma za afyapamoja na Watanzania.

Page 211: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

211

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunasemakwamba Wizara itaendelea kuwaelimisha Wakunga wa Jadikuhusu umuhimu wa kuwashauri wajawazito kwenda katikavituo vya kutolea huduma mapema ili kupata huduma borana salama za kujifungua.

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani hayo ndiyomakubwa ambayo ningetaka kuyajibu kutoka kwenye KambiRasmi ya Upinzani, lakini mengine yote tunakubaliana nawao, ikiwemo kuendelea, kuhakikisha tunatumia CommunityHealth Workers, amezungumza Mheshimiwa Kandegekwamba changamoto ambayo tunaipata na kuna baadhiya Wabunge wametoa mfano, kuna vituo vya afyavinaongozwa na Medical Attendant (Mhudumu wa Afya),lakini kuna vituo vya afya unakuta vinaongozwa na Wauguzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hapo sasa ndiyo tunajaribukuweka balance, uwiano. Je, tujaze watumishi wa kwenyefacilities au twende kwenye Community Health Worker, lakinias a matter of sera, ikiwa ni suala la kimsingi, tunakubaliananalo na especially mimi katika ajenda yetu ya kuhakikishatunaongeza hali ya lishe kwa akinamama wajawazito nawatoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, lakini piatunaongeza watu ambao wanajua maambukizi ya Virusi vyaUKIMWI na katika mapambano ya kifua kikuu tunaaminikwamba wahudumu wa afya ngazi ya jamii watatomchango mkubwa. Tunategemea kuajiri takriban 600 kupitiafedha ya Mfuko wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu naMalaria.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja zilizoelezwa ni nyingi,ikiwemo uboreshaji wa huduma katika ngazi zote tumepokeana lengo letu kwa kweli tunataka kutoka kwenye borahuduma twende huduma bora na ndiyo maana Wizara yaAfya tunayo idara ya kusimamia uhakiki wa ubora wahuduma za afya. Kwa hiyo, tutahakikisha kinafanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tunakusudia kutoa usajiliwa vituo vya kutoa huduma za afya vya Serikali na binafsi.Lengo letu tukiona, hata cha Serikali tukikiona hakina ubora,

Page 212: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212

tunataka kukifungia kama vile tunavyofungia vituo vya afyavya binafsi. Kwa hiyo, hili ni eneo ambalo tumekubalianakwamba tutalifanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la vifaa navifaatiba kwa ajil i ya vituo vya afya vil ivyoboresha,Mheshimiwa Naibu Waziri ameongea kwamba tumeanzakununua lakini tutahakikisha kwamba, kwa sababu hata zoezihili la kukarabati vituo vya afya, lilienda kwa awamu, kwahiyo niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwambatutahakikisha tunanunua vifaatiba na kuvifunga katika vituovya afya vilivyoboreshwa ili viweze kutoa huduma borazilizokusudiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lilikuwa wazo, hoja ambazopia zimetolewa na Waheshimiwa Wabunge ni suala la X-Raymachines; wengi wameeleza kwamba hazifanyi kazi au niza zamani. Naendelea kuwathibitishia WaheshimiwaWabunge kwamba tumeshaagiza x-rays takriban 70 za kisasa,kwa hiyo, tutazisambaza katika Hosptali za Rufaa za Mikoa,lakini pia katika Vituo vya Afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mzee wangu Deo Sanga,nimemsikia kuhusu Makambako, nakubaliana na yeye, hatakama ni kituo cha afya, kwa kweli tutahakikisha kwambaanapata x-ray ili kuweza kutoa huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kumezungumzwa sualala ambulance, Waheshimiwa Wabunge tumewasikia sanana tulikuwa tunaongea na Mheshimiwa Waziri Mkuu hapa,mahitaji ya ambulance ni mengi, lakini kama nilivyoelezakatika hotuba yangu, tayari tumeagiza ambulances 50, kwahiyo tutazigawa katika maeneo yenye uhitaji, lakinitutaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kugawa ambulance.

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijamaliza,nizungumzie suala ambalo pia limeongelewa naWaheshimiwa Wabunge, kwamba maiti anachajiwa,anadaiwa sijui. Kwa kweli, tunapata changamoto, lakininaomba Waheshimiwa Wabunge watuelewe, angalau

Page 213: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

213

katika Tanzania na hasa Hospitali yetu ya Taifa Muhimbili,kipaumbele wanakiweka kwa mgonjwa kupata huduma.Maana bora mtu angekufa kwamba kakosa huduma, lakinimtu kwanza anapata huduma, akishapata huduma ndiyolinakuja suala la deni. Nilikuwa naongea na Profesa Museru,Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali yetu ya Taifa, Muhimbili,amenieleza, Mheshimiwa Waziri ambao wanakuja kwako pia,saa nyingine hawafuati taratibu. Kwa hiyo, nitoe rai kwaWatanzania, kwanza kuhakikisha tunawekeza kwenye afyazetu kwa kukata bima ya afya, lakini pale ambapo hatunauwezo wa kulipia, basi tufuate utaratibu wa kupata matibabubila malipo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninazo takwimu hapa,tukiangalia Hospitali ya Taifa Muhimbili, kuanzia Julai mpakaDisemba, iliweza kutoa msamaha kwa wagonjwa wenyethamani ya shilingi bilioni 2.7, kwa hiyo, watu wanasamehewa.Vile vile tukiangalia Hospitali ya MOI, Julai hadi Desemba,ilitoa msamaha kwa wagonjwa wenye thamani ya shilingimilioni 347. Tukiangalia Mloganzila Julai hadi Desemba, 2018walitoa msamaha kwa wagonjwa wenye thamani ya shilingimilioni 178.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninazo takwimu mpaka zaHospitali zetu za Rufaa za Mikoa, kwa hiyo, WaheshimiwaWabunge tunaomba watuelewe, hapo hapo tunahitajikuboresha huduma, sasa tukisema tu jamani kila kitu burebure bure, jamani bure, bure ni gharama, bure ni gharama.

Mheshimiwa Naibu Spika, narudia tena bure nigharama, kwa hiyo muhimu tuendelee kuhakikisha kwamba,kwanza tunawekeza kwenye afya zetu, lakini pili piatunafuata taratibu katika kupata huduma za afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumze sualamoja ambalo limeongelewa na Mheshimiwa dada yanguTaska Mbogo, kuhusu Customary Declaration Order, ni yazamani na kandamizi na inabagua wanawake. Nakubalianasana na Mheshimiwa Mbogo, kwamba sheria hii ni ya zamani,lakini kuna maamuzi ya Mahakama Kuu kwenye Kesi Na. 82

Page 214: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

214

ya mwaka 2005 ambayo inatambulikana kama ElizabethStephen na mwenzake dhidi ya Mwanasheria Mkuu waSerikali, ambayo ilitolewa maamuzi tarehe 8 Mwezi wa Tisamwaka 2006, mbele ya Majaji watatu wa Mahakama Kuukuwa, Serikali imeweka kifungu cha 12 cha Sheria yaJudicature and Application of Laws Act, ambacho kinamtakamtu yeyote atakayeona kuna mila kandamizi inayomzuiakupata haki yake, kufuata utaratibu uliowekwa katika kifunguhicho kwa kuwasilisha maombi ya kubatilisha mila hiyo kupitiaWaziri wa TAMISEMI.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini naomba kusema hiini changamoto. Dada yangu Mheshimiwa Taska Mbogo,naomba nilichukue, tutakwenda kulifanyia kazi ili kuhakikishaikiwezekana tunafuta sheria hii. Kwa sababu hoja ambayoipo ni kwamba kuna baadhi ya mila zetu ambazo zimo ndaniya sheria hii siyo mbaya, za kutunza wazee na watoto wandugu. Kwa hiyo, tutaangalie yale ambayoyanamkandamiza mwanamke tutaweza kuyafanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mdogo wangu MheshimiwaAmina Mollel amezungumzia suala la unyanyasaji wawasichana hasa wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu.Sera ya Usawa wa Jinsia na Maendeleo ya Wanawakeinahimiza kuanzishwa kwa Madawati ya Jinsia katika Taasisi,Wizara na Idara za Serikali. Kwa hiyo, nitumie fursa hii kuvitakavyuo vya elimu ya juu nchini kuanzisha Madawati ya Jinsia ilikuweza kushughulikia changamoto mbalimbali za jinsiaikiwemo vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanafunzikatika vyuo vyetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nipongeze sanajitihada za Kamishna Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia naKupambana na Rushwa ambaye ameanzisha Dawati la Jinsiandani ya TAKUKURU ili kuweza kupambana na rushwa yangono. Kwa hiyo, nitoe pia wito kwa wanafunzi wa vyuo vyaelimu juu ambao wananyanyaswa au wanakumbana navitendo vya ukatili wa kijinsia kuhakikisha kwamba wanatoataarifa katika Dawati hili la Jinsia ambalo limeanzishwamwaka huu chini ya TAKUKURU.

Page 215: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

215

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema, hojaambazo zimeongelewa ni nyingi lakini kipekee niwathibitishieWaheshimiwa Wabunge wa kutoka Mikoa mipya ya Katavi,Songwe, Njombe, Simiyu na Geita kwamba kipaumbelechetu kama Wizara tumekubaliana mwaka huu ni kukamilishaHospitali za Rufaa za Mikoa ili ziweze kutoa huduma za rufaakatika mikoa hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia katika Mkoa waSingida na Shinyanga, mdogo wangu Mheshimiwa AisharoseMatembe na ndugu yangu Mheshimiwa Azza Hillal, kamaWizara tumejipanga kuhakikisha tunakamilisha ujenzi waHospitali za Rufaa za Mikoa. Lengo ni ili sasa tuweze kukabidhiHospitali ya Shinyanga kwa Manispaa ya Shinyanga, piatukabidhi Hospitali ya Singida kwa Manispaa ya Singida. Kwahiyo, mdogo wangu Mheshimiwa Aisharose na ndugu yanguMheshimiwa Azza Hillal tunataka kuwathibitishia kwambajambo hili pia tutalikamilisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini katika hospitalinyingine za Rufaa za Mikoa kama tulivyosema tumezipokeakuanzia tarehe 1 Julai 2018. Tunachokifanya, tumeamuakuwekeza katika maeneo makubwa manne. Eneo la kwanzani kuhakikisha tunakuwa na miundombinu ya kutoa hudumakwa wagonjwa wa dharura na ajali (emergence medicine)na tayari tumeanza kupata fedha kutoka Global Fundtutaanza kuweka vitengo vya dharura katika hospitali saba.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la pili ni kuwekahuduma za ICU, huduma kwa wagonjwa wanaotakauangalizi maalum. Huduma hii tutafanya pia katika hospitalizote za Rufaa za Mikoa. Eneo la tatu ni kuboresha hudumaza uzazi. Eneo la nne tunataka kuhakikisha tunawekaMadaktari Bingwa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa yote.Tumebainisha maeneo nane ya kipaumbele, tunatakakuhakikisha tuna Madaktari Bingwa wa magonjwa ya uzazina wanawake angalau wawili, magonjwa ya watotoangalau wawili, upasuaji angalau wawili, upasuaji wa mifupaangalau wawili, usingizi na radiolojia na magonjwa ya ndani(internal medicine).

Page 216: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

216

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hayo ni maeneoambayo tumeyabainisha na tutahakikisha kwamba kilaHospitali za Rufaa za Mikoa zinakuwa na wataalam hawa.Kama alivyosema Naibu Waziri tayari tumeanza kusomeshamadaktari na ili tuweze kukupa ufadhili wa kusoma mastersya udaktari tutawafungisha mkataba ili wakimaliza wawezekufanya kazi katika Hospitali zetu za Rufaa za Mikoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema mamboni mengi lakini kwa kweli kipee nimshukuru sana MheshimiwaRais, Dkt. John Pombe Magufuli, asiye na macho haambiwitazama, kazi kubwa na nzuri imefanyika katika utoajiwahuduma za afya. Mimi niseme tutaendelea kuhakikishatunatimiza ndoto yake ya kuifanya Tanzania ya viwanda kwakuboresha huduma za afya kwa kuhakikisha kwambaWatanzania wanakuwa na afya bora badala ya kusubirikwenye mambo ya tiba.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabungetumewasikia, Mzee wangu Mheshimiwa Lubeleje tumekusikia,tunataka na sisi tuondoke kwenye taifa la kulilia dawa, dawa,lakini liwe ni taifa la kulilia afya na lishe bora. Kwa hiyo, jambohili pia tutalifanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda pia kumshukuruMheshimiwa Makamu wa Rais, mama Samia Suluhu Hassanambaye kwa kweli amekuwa akinipa msaada mkubwakatika utekelezaji wa majukumu yangu. Namshukuru sanamama Samia katika kuimarisha afya ya uzazi ya mama namtoto. Mheshimiwa dada yangu Mariam Kisangi ameonesha,watu wanaosema hakuna mabadiliko, Hospitali ya Mkoa waRufaa ya Temeke hakuna kifo kimetokea mwezi Machi, mamaKisangi ni shahidi na watu wanaona. Halafu watu wanasemahakuna kazi imefanyika, kazi imeonekana ndiyo maanahakuna vifo vya akina mama wajawazito.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru sana WaziriMkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa uongozi wake mahirina nawashukuru sana Waheshimiwa Mawaziri wote. Kipekeenimshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu

Page 217: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

217

Waziri kwa mchango mkubwa sana ambao ananipatia.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mara nyingi niliambiwaunajua hawa madaktari wanaweza wakadharau lakini NaibuWaziri amekuwa akinipa mchango na heshima kubwa katikautendaji wa kazi zangu. Mheshimiwa Naibu Wazirinakushukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nimshukuru pia KatibuMkuu (Afya), Dkt. Zainabu Chaula. Kwa kweli tunafurahi sanakama Wizara ya Afya tumepata mama ambaye anajuakusukuma mambo na anajua kusimamia utendaji katikaWizara ya Afya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia namshukuru sana Dkt.John Jingu ambaye naye ni Katibu Mkuu, Maendeleo yaJamiii kwa kazi kubwa na nzuri ambayo amefanya katikakusimamia Sekta ya Maendeleo ya Jamii. Tunamshukuru sanapia Mganga Mkuu wa Serikali na madaktari wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hili tunawashukurumadaktari, wauguzi na watoa huduma za afya nchini. Hapanaongea kama Waziri wa Afya, nitoe maelekezo na maagizokwa viongozi wenzangu, tuache kuingilia fani za kitaaluma.(Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama kuna daktari aumuuguzi amekosea ashughulikiwe kwa mujibu wa taratibuza Utumishi wa Umma. Narudia tena, kama kuna daktariamekosea tuleteeni kwenye Baraza la Madaktari, tutafutausajili wake. Kama kuna muuguzi amekosa tuleteeni kwenyeBaraza la Wauuguzi na Wakunga tutafuta usajili wake. Kamakuna mfamasia amekosea tuleteeni kwenye Baraza laWafamasia ambalo ndiyo limeanzishwa kisheria kushughulikiachangamoto kama hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, miaka mitatu ambayonimekaa katika sekta ya afya, Naibu Waziri ameongea, kaziya wauguzi watano inafanywa na muuguzi mmoja halafu

Page 218: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

218

bado huwezi ku-appreciate (kuthamini)? Madaktari hawawanajituma sana, kwa kweli lazima tutambue mchango waona tuheshimu kazi kazi yao nzuri. (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi na Naibu Waziritutaendelea kuwatetea madaktari na wauguzi wetu kwasababu mwisho wa siku wanaopata matatizo ni Watanzaniawanyonge. Mwenye hela zake haendi kwenye hospitali yaSerikali au kituo cha afya cha Serikali. (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli inatia uchungu,sisi ambao tuko kwenye sekta hii tunaelewa changamotoambazo watoa huduma za afya wanapata. Kwa hiyo, sisemikwamba wote ni malaika au ni wazuri, hapana, wapowabaya lakini tufuate taratibu za kuwawajibisha watumishiwatoa huduma za afya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia niwashukuruWaheshimiwa Wabunge wote kwa ushirikiano mkubwa namzuri ambao wamekuwa wakinipatia katika kutekelezamajukumu yangu. Kipekee, nawashukuru wadau wetu wamaendeleo hususani wanaochangia Mfuko wa Afya waPamoja ambao ni Denmark, Canada, KOICA, UNICEF naWorld Bank, nadhani nimewamaliza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nawashukuru na wadauwengine ambao hawachangii kwenye Mfuko wa Afya lakinimchango wao ni mkubwa ikiwemo Global Fund, Mfuko waRais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI pamoja nawatu wa GAVI, Abbott Fund wote hao wanatusaidia, pamojamashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya dini.

Nawashukuru sana Wakuu wa Taasisi na Idara zaSerikali, Hospitali zetu za Taifa Muhimbili, Bugando, JakayaKikwete, Ocean Road, MOI, Benjamini Mkapa na hospitalinyingine zote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tu niwaambieWaheshimiwa Wabunge tutajibu hoja zenu zote kwamaandishi. (Makofi)

Page 219: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

219

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,sasa naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa NaibuSpika, naafiki.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, hojaimeungwa mkono, ahsanteni sana, Katibu.

NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH - KATIBU MEZANI:

KAMATI YA MATUMIZI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 52 - Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto

Kif.1001 - Administration Human Resources Management………......................Sh. 8,450,857,436/=

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, kwa mujibu waKanuni zetu hiki ndiyo kifungu chenye mshahara wa Waziri.Nimeletewa majina hapa kwa mujibu wa Kanuni zetu tenawatu ambao wanataka ufafanuzi kwenye kifungu hiki.Tutaanza na Mheshimiwa Oscar Mukasa.

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Mimi hoja yangu nataka commitment ya Serikalitena ya muda mfupi ya kufanya mapitio ya Sera ya Lishekwa sababu imepitwa na wakati lakini pia haijumuishi sektazote kwenye kupambana na utapiamlo na mambo mengineyanayoendana na lishe. Utakumbuka kwenye mchangowangu nilitoa takwimu hapa zinaonesha risk factors auvisababishi vya vifo na ulemavu malnutrition ndiyo inaongozapamoja na kwamba tunafanya vizuri sana kwingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakusudia kushika shilingiya Waziri endapo sitapata maelezo ya kuridhisha.

Page 220: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

220

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Afya.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEENA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sanaMheshimiwa Oscar Mukasa. Kwa kweli nakubaliana na hojayake lakini ningemwomba kwa kuwa sasa hivi Wizarainatengeneza Sera mpya ya Afya kwa sababu tumekuwana Sera nyingi mwisho wa siku utekelezaji umekuwa siyo mzuri.Kwa hiyo, tumekubaliana na single heath care policy yaTanzania ambapo tutaweka specific chapter kwa ajili yamasuala la lishe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza tayari kunaMultisectoral National Strategy ya kuboresha hali ya lishe, kwahiyo, mimi badala kutengeneza Sera tu ya Lishe, kwa sababulishe ni jambo mtambuka, linahusisha sekta nyingi, kwa hiyo,kwenye Sekta ya Afya tutengeneze hiyo policy statementkuhusu lishe lakini tutakuja sasa na mkakati wa kitaifa ambaoutakuwa ni multisectoral wa kuweza ku-address masuala yalishe. Nakubaliana naye kwamba kwa kweli kiwango cha lishenchini kwetu hasa kwa watoto wa umri wa chini ya miakamitano na akina mama wajawazito hakiko vizuri, kwa hiyo,tunahitaji kuongeza jitihada.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mukasa, naonaumesimama.

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nafurahi utayari wa Mheshimiwa Waziri lakini napata shidatunapishana tena pale anaposema tuwe na Sera moja yaAfya ambayo na lishe ni sehemu mojawapo hapo tunazuatatizo lingine…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mukasa, katika hatua hiikama umekubaliana na maelezo ya Mheshimiwa Waziriutakuwa umekubaliana nayo, kama hukukubaliana nayounatoa hoja ili uungwe mkono.

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Mwenyekiti,natoa hoja ya kushika shilingi, sikubaliani naye.

Page 221: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

221

MWENYEKITI: Hoja haijaungwa mkono. (Kicheko)

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Mwenyekiti,imeungwa.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, hojaimeungwa mkono, waendelee kusimama wale wanaotakakuchangia kwenye hoja hii. Mheshimiwa Vulu, MheshimiwaKemilembe Lwota, Mheshimiwa Jitu Soni, Mheshimiwa ShallyRaymond, Mheshimiwa Kitandula na Mheshimiwa Waziri waNchi, Ofisi ya Waziri Mkuu. Tuanze na Mheshimiwa ZaynabuMatitu Vulu.

MHE. ZAYNABu MATITU VULU: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Mimi sina haja ya kushika shil ingi yaMheshimiwa Waziri lakini hoja yangu ni kwamba hili suala lasera ni muhimu na umuhimu wake ni kwamba Wizara ya Afyapeke yake hawawezi wakalitekeleza peke yao kwa sababuni suala la mtambuka, kuna haja ya kuunganisha na Wizaranyingine, Wizara ya Maji, Wizara ya Afya yenyewe, TAMISEMI,Elimu, Kilimo, hata Wizara ya Kilimo na wenyewe wanapaswawawepo. Kwa hiyo, ningeomba suala hili kama itawezekanalijumuishe Wizara hizo zote na litengenezwe, Wizara ya Afyainaweza ikachukua asilimia 20…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Kengele imegonga Mheshimiwa, sasahatujajua unaunga mkono hoja ama huungi mkono hoja yaMheshimiwa Mukasa, neno moja tu.

MHE. ZAYNABU M. VULU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga hoja ya Mheshimiwa Mukasa lakini si kwa maana yakutoa shilingi ya Waziri. (Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Vulu, kote ni kuunga mkonotu, ukishasema unaunga mkono maana yake unaungamkono. (Kicheko)

Page 222: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

222

Tunaendelea na Mheshimiwa Kemilembe Lwota.

MHE. KEMILEMBE J. LWOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Mimi naunga mkono hoja ya MheshimiwaMukasa kwa sababu kiukweli kabisa suala lishe ni muhimusana katika nchi yetu na ni bomu ambalo tunatengenezalitakuja kuwa tatizo kubwa sana siku za usoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaoneshaNyanda za Juu Kusini ambako ndiyo kuna chakula kingi lakinibado tuna tatizo kubwa sana kwenye utapiamlo. Hili sualalinaanzia kuanzia kwa akina mama wajawazito mpaka umriwa miaka mitano ambao Mheshimiwa Waziriameuzungumzia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi namwombaMheshimiwa Waziri isiwe chapter moja kwa sababu ni sualakubwa na mtambuka. Nashauri itengenezwe sera ambayoitasimamia lishe kwa ujumla nchini kwetu. Nakushukuru.(Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, wakatitukiendelea na michango, tujikumbushe tu sisi wenyewemichango yetu tunazungumza kana kwamba hii sera haiwezikutengezwa na Wizara ya Afya peke yake, wakati tukijadilihapa navyosikiliza. Kwa hiyo, hata tunaposema tunaungamkono ile hoja ya kwamba kuwe na sera moja kwa ajili tu yalishe halafu Waziri wa Afya ndiyo aseme maana yakeMawaziri wote tunaowataja wote wakakae pamoja.

Tunaendelea na Mheshimiwa Jitu Soni.

MHE. JITU V. SONI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsantesana. Mimi naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Mukasa nanaomba Serikali iiangalie kwa upana wake. Yeye alichoombani commitment kwamba badala ya kufuata utaratibu wakawaida ambao utachukua muda mrefu atupe mudamaalum kwamba ndani ya muda fulani Serikali itaweza kukaana kuhakikisha Wizara zote ambazo zinahusika katika sualahili zima la lishe liweze kufanyiwa kazi.

Page 223: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

223

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata kama Wizara ya Afyaitakuwa inasimamia jambo hilo lakini Wizara zote ambazo nimtambuka ambazo zinashughulikia suala hilo wote wahusikepamoja kwa sababu ni tatizo kubwa kuliko mambo mengineyote. Kinga ni bora kuliko tiba. Ni vizuri tuwekeze kwenye kingana Wizara zote zihusike, gharama itakuwa ni ndogo kulikohuko tunakoelekea kwenye tiba. Kwa hiyo, naunga mkonohoja yake ifanyiwe kazi haraka. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Shally Raymond.

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru, hili suala la lishe ni mtambuka, liko Kilimo, likoElimu, liko TAMISEMI, liko kote na Taifa lijalo litakuwa na viwatuvimedumaa. Sisi hapa wote tulikuwa na lishe bora ndiyomaana tuko namna hii na mbaya zaidi sasa hiyo asilimia yawatoto wa umri wa miaka mitano inafika asilimia 34 yaTanzania katika data zile za mwaka 2015/2016 sijaona hizi zakaribuni za 2017/2018. Sasa kama halitafanyiwakazi mapematukisema tu ni sera ni sera na elimu kule hawana, watu haohao lishe ni duni hata walio darasani wanapelekewa Uji tuna Maharage bila chochote, hivi kweli tutakuwa na Taifalenye nguvu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo ni la haraka nadharura, naomba kuwasilisha. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dunstan Kitandula.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru, naungana na Mheshimiwa Mukasa kwambaiko haja ya kuwa na a standalone policy ya lishe na sababuni nini? Sababu ni kwamba jambo hili ni cross cutting lakinituna wasiwasi kwamba likiachwa hivi lilivyo kwamba lika-appear kama chapter moja tu kwenye Sera jumuishi linawezakusababisha matatizo makubwa na maeneo mengineyakasahaulika hasa tukizingatia kwamba interventionzinazotokana na sekta ya afya peke yake zina-solve tatizohili kwa asilimia 20 tu, asilimia 80 inatokana na maeneo

Page 224: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

224

mengine kwa hiyo ipo haja ya kulifikiria vizuri eneo hilo.(Makofi)

MWENYEKITI: Nadhani tunarudi pale pale asilimia 20ndiyo tunashikia mshahara leo siyo? Asilimia 80? MheshimiwaJenista Mhagama.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana. Kwanza naomba nimpongezeMheshimiwa Waziri wa Afya kwa kulisemea hili vizuri lakininiwapongeze Waheshimiwa Wabunge kwa kulizungumzajambo la lishe kama ni jambo la kipaumbele katika Taifa letu.Lakini niwapongeze pia Waheshimiwa Wabunge wameonakwamba jambo hili la lishe ni jambo mtambuka, siyo jamboambalo linaweza likachukuliwa na sekta moja tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba tu nikuhakikishiekwamba Ofisi ya Waziri Mkuu kama Ofisi ambayo imepewajukumu la kuratibu sera zote kaatika Taifa letu tayariimeshaliona jambo hili kama ni jambo la msingi kabisa. Ndiyomaana kwa kuanzia ili kuzikutanisha sekta zote kwa pamojatayari Ofisi ya Waziri Mkuu imeshatengeneza mkakati waKitaifa wa kupambana na tatizo la lishe nchini ambapomkakati huo unaunganisha sekta zote ikiwemo sekta ya afya,sekta ya kilimo na sekta nyinginezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namuelewa MheshimiwaOscar anaona katika Wizara hii ya Afya labda Waziri ndiyoangefanya commitment lakini akifanya commitment Waziriwa Afya peke yake kuwa na sera kwenye sekta ya afyahaitatutoa kwenye tatizo ambalo tukonalo. Naombaniwahakikishie Waheshimiwa Wabunge sisi kama Ofisi yaWaziri Mkuu, waratibu wa sekta na waratibu wa mambo yoteambayo yanatakiwa kuratibiwa na sekta zote tunalibebajambo hili kama ni jambo la msingi ili tulifanyiekazi na kupatamajibu ya pamoja kwa Taifa zima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hali hiyo nimuombesana Mheshimiwa Oscar Mukasa kwa sababu Serikali inaona

Page 225: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

225

umhimu wa lishe bora nchini na inatambua kufanyacoordination ya sekta zote ili kutatua tatizo la lishe amuachieMheshimiwa Waziri shilingi yake na siis kama Ofisi ya WaziriMkuu tuendelee kuliratibu jambo hili na mwisho wa siku tuwena Sera ambayo itasaidia ku-coordinate sekta zotekupambana na tatiz la lishe nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Oscar Mukasa.

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru, nawashukuru pia Mheshimiwa Ummy,Mheshimiwa Jenista na wachangiaji wengine wote,Mheshimiwa Kitandula na wengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, amesema vizuri sanamwishoni hapa Mheshimiwa Jenista ingawa hataMheshimiwa Ummy amasema vizuri yeye alikuwa anasemakwa upande wake wa sekta ya afya lakini nianze na mfano;UKIMWI ni jambo mtambuka, Sheria iko Wizara ya Afya, Seraiko Ofisi ya Waziri Mkuu na ndiyo maana tunafanya vizuri. Kwahiyo, nakubaliana na Mheshimiwa Jenista kwamba tupokeehiyo commitment tukazungumze tuone ili kuiweka kwenyeSheria moja ya afya ukilinganisha na kuiweka kama jambomtambuka kwa pamoja tukubaliane tunatoka vipi. Kwa hiyo,naiachia shilingi, naomba tuendelee lakini Serikali tuzungumzebasi.

MWENYEKITI: Ahsante sana. Nadhani MheshimiwaWaziri wa Afya hiyo haiondoi umuhimu wa kuweka vifungumahususi vinavyohusu Wizara yako. Mheshimiwa MwitaGetere.

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kupata ufafanuzi. Naombakupata ufafanuzi; center ya kugawa madawa katika nchiyetu iko kwenye Shirika letu la MSD lakini Shirika hili sasa linadaikulipwa hela nyingi sana kutoka Serikalini karibu bilioni 222.Hivi karibuni, Shirika hili la MSD limepata heshima ya kutoa

Page 226: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

226

huduma ya vifaa tiba katika Nchi 16 za SADC, ni heshimakubwa ambayo nchi yetu imepata kupitia Shirika hili lakinitusisahau Shirika hili limesifiwa na CAG na pia MheshimiwaRais amelisifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika hili hivi karibunilimepewa jukumu la kununua, kugawa na kutoa vifaatibakatika vituo vyote vya afya vinavyojengwa nchi nzima. Shirikahili pia ndilo linalo-determine madawa yetu katika Nchi nzimakwamba yanakwenda vizuri katika maeneo haya. Sasanaomba commitment ya Serikali, ni lini sasa litalipwa hizo helazinazodai karibu bilioni 22? Nisipopata maelezo ya kutoshanitaingia kwenye kutoa mshahara wa Mheshimiwa Waziri.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Getere hili jambo kwamujibu wa Kanuni zetu kwa sababu umetoa maelezo marefunitampa Mheshimiwa Waziri fursa ya kuzungumza lakini siyojambo linaloweza kuzungumzwa kwenye kifungu hiki kwasababu wewe umeuliza swali na umeuliza swali kuhusu malipokwa MSD ambayo umeyataja kabisa ni kiasi gani kwa hiyosiyo jambo ambalo Kikanuni unaweza kuuliza kwa namnahiyo. Pengine Mheshimiwa Naibu Waziri unataka kutoaufafanuzi? (Kicheko)

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali hiiimeendelea kuwekeza katika Bohari hii ya dawa na bajetiya dawa imeongezeka kutoka bilioni 31 Mwaka 2015/2016hadi kufikia bilioni 270 katika Mwaka huu wa fedha.

Tunatambua kweli kulikuwa na deni hili la MSD, na sisikama Serikali kupitia hazina wamefanya uhakiki wa hili denina Serikali kupitia hazina wameendelea kulilipa hili deni kadriuwezo wa Serikali uliopo na labda nimtoe shaka tu kwambauwepo wa hili hauathiri utendaji wa MSD kwa maana yaupatikanaji wa dawa hapa nchini lakini hautaathiri hali yaupatikanaji wa dawa katika Bara zima na nchi za SADC. Kwasababu utaratibu wa fedha na ununuzi wa dawa SADChauna muingiliano kabisa na utaratibu wa dawa katikamifumo yetu hapa ndani.

Page 227: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

227

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa EstherMatiko.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru, kabla sijakwenda kwenye shilingi yanguningependa tu kuweka sawa; kwanza nashukuru hotuba yetuumeisifia kwa asilimia 80 ukaponda tu vitu viwili lakini kwenyematernal mortality niweke tu data sawa; wewe mwenyeweumekiri kwamba kuanzia 2015 bado hakuna statisticstulizonazo lakini 2017/2018 ulituletea hapa taarifa kwambavizazi vifo vya 2016/2017 ilikuwa ni vifo 444 kwa vizazi hai lakimoja, Mwaka jana ukatuambia 556 kwa vizazi hai laki mojaina maana inapanda. Mwaka huu umekula chaka baadaya kuona inapanda so we judge with that trend.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kingine bajeti;utekelezaji wa maendeleo asilimia 16 halafu tusiseme kweli?We are not prayers and worship teams here tunaisimamiaSerikali ifanyekazi zake.

Mheshimiwa Mwenyeiti, hoja yangu ya msingi sasa;wazee wa Taifa hili wamelitumia sana Taifa na kwa kweliwanatakiwa kuenziwa…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Matiko hilo ni jambo tofautina hapa inabidi jambo liwe moja sasa umezungumzia habariza uzazi sasa hivi unakwenda Wazee. Ni jambo la uzazi, malizahoja yako huwezi kurukia wazee ndiyo Kanuni zetuzinavyosema, jambo mahususi moja.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimesema naanza kile alichokuwa amesema sija…

MWENYEKITI: Hapana, hapana utakuwa unakoseaKanuni na unafahamu utaratibu Mheshimiwa, hapana. Kamahoja yako ni ya wazee ulitakiwa uende kwenye wazee ndiyoutaratibu. Huwezi kuwa umeanza wewe kuchangia na Kanuniunazijua kwa hiyo nikikupa fursa zungumza habari ya uzazisiyo tena wazee kwa sababu Wazee ni hoja nyingine tofautina wewe Kanuni unazifahamu.

Page 228: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

228

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,naona mnakimbia majukumu, anyway I will go with that uzazi,nitazungumzia vizazi there is no problem.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vifo vya wakinamama wajawazito na watoto; nikianza tu kwa kuangaliatrend hata kwenye hiki kitabu cha maendeleo ambachokimekuja, bajeti iliyotengwa kwa Mwaka 2018/2019 ilikuwabilioni 12, Mwaka 2019/2020 bilioni tano kwa hiyo hapanitashika shilingi nisiporidhika. Kwa takwimu ambazonimezitoa awali na sasa hivi nataka kupata mkakati thabitiwa kupunguza vifo vya mama na watoto kujenga vituo vyaafya tu tena vichache kati ya vituo 4000 tulizonazo,mmejenga…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Esther ngoja tuongozanevizuri kwa sababu kengele imeshagonga, hoja yako ni nini?dakika moja, hoja yako ni nini?

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nipate mkakati thabiti ambao utakwenda kupunguza vifovya Mama na mtoto Tanzania na siyo story.

MWENYEKITI: Hawa Wabunge wa siku nyingiinavyoonekana hizi Kanuni tunahitaji semina. MheshimiwaWaziri ufafanuzi. (Kicheko)

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEENA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nisemeMheshimiwa Esther Matiko takwimu za 556 katika kila vizazihai laki moja ni takwimu rasmi ambazo zimefanywa na Taasisiya takwimu ya Taifa. Kwa mwaka tuna deliveries, tuna wazazitakribani milioni mbili kwa hiyo ukifanya calculation nitakribani ni hao hao watu 11,000 kwa Mwaka Wanawakewanafariki kutokana na uzazi na sawa sawa na Wanawake30 kwa siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo bado hakunamgongano wowote kwenye takwimu lakini nikasema hivi;kwa sababu ya uwekezaji mkubwa ambao Serikali ya Awamu

Page 229: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

229

ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli imefanya katikakuboresha huduma za uzazi, Mama na mtoto tunategemeaukifanyika utafiti rasmi, Mwaka 2019/2020 tutakuwa natakwimu ambazo ni chache sasa anasema kuna mkakatigani wa Serikali wa kupunguza vifo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumesema hakukuwepo navituo, kwanza niseme; asil imia 80 ya wakina Mamawajawazito wanajifungua bila complication ni normaldelivery, asilimia 20 ndiyo wanakuwa na complication ndiyomaana tukaboresha vituo vya afya kujenga kitu kinaitwaSIMOC ili kuviwezesha kutoa huduma za uzazi wa dharuraikiwemo upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni maana yakemwanamke mjamzito akiwa na tatizo la uzazi pingamizi sasahivi atapata huduma pale pale katika eneo lake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika bajeti hii zamaniwanawake kwanini wanafariki? Kumwaga damu nyingi.Dawa ya kuzuia mwanamke mjamzito kumwaga damubaada ya kujifungua (oxytocin) inapatikana mpaka zahanatiTarime Mjini, zinapatikana bure. Dawa kwa aji l i yawakinamama mjamzito kuzuia kifafa cha mimba (magnesiumsulfate) zinapatikana bure sasa anataka mikakati gani zaidiya kuboresha miundombinu, zaidi ya kuhakikisha upatikanajiwa dawa, zaidi ya kuhakikisha tuna wataalam. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepeleka wataalam wakusomea usingizi 200 hospitali zetu za Taifa za Muhimbili,Bugando na MOI kwa ajili ya kujifundisha. Kwa hiyo, mikakatiipo lakini tumeenda mbali tukasema mambo mazuri badoWanawake wajawazito wanafariki ndiyo maana tukaja nakampeni “jiongeze tuwavushe salama”. Kwanza Mamamjamzito mwenyewe ajiongeze, anatakiwa kwenda clinicmara tu akijiona mjamzito, aende ngalau mara nne lakinitunataka watoa huduma za afya wajiongeze. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakubali changamoto yavifo vya wakina Mama wajawazito na watoto bado ipo lakininakuhakikishia kwenye Bunge hili tukifanya utafiti vitapunguazaidi ya asilimia 50. Tunazo takwimu vifo havizidi 3000 sasa

Page 230: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

230

hivi kwa hiyo mikakati ipo tuendelee kutekeleza. NamuombaMheshimiwa Esther wifi yangu niachie shilingi yangutukatekeleze kazi ya kuboresha huduma za uzazi, Mama namtoto.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Esther Matiko.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,sijaridhika kabisa na majibu ya Mheshimiwa Waziri ambayoamesema ni wifi yangu kwa sababu ni Mwanamke naumetaja vizuri kabisa kwamba complication ambazozinatokana ni 20 percent sasa out of 20 percent wanafarikiwatu 30 kwa siku…

MWENYEKITI: Toa hoja Mheshimiwa ijadiliwe kwa kuwahujaridhika

MHE. ESTHER N. MATIKO: Natoa hoja tu-discuss hii kitu.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge hoja imeungwamkono wabaki wamesimama wanaotaka kuchangia kwenyehoja hii. Mheshimiwa Salome Makamba, Mheshimiwa FrankMwakajoka. Huwezi kupewa hujawahi, kupewa na mimi?Mbona mnakuwa namna hiyo!! Mheshimiwa Mch. Msigwayaani tuwe tunaheshimiana wewe ushapewa nafasi maranyingi mbona unakuwa hivyo? Mbona unakuwa na mambo!Wewe! Ulivyozungumza ulitaka usisikiwe? Nimekusikia naumeshapewa mara nyingi na ni kweli leo hupewi, ni kweli leohutapewa Mheshimiwa kwa hiyo, vumilia tu. MheshimiwaBashe

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mchungaji Msigwatumeshalimaliza hilo naomba unyamaze, naomba unyamazetafadhali, naomba unyamaze. Mheshimiwa Ally Keissy,Mheshimiwa Kigwangala, Mheshimiwa Waitara, MheshimiwaNaibu Waziri wa Afya. Mheshimiwa Salome Makamba.

Page 231: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

231

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru, naomba niunge mkono hoja ya MheshimiwaEsther Matiko kuhusu vifo vya Mama na mtoto. Ninachokionahapa Serikali kwanza inakiri kwamba NBS haijafanya utafitikuanzia Mwaka 2015 leo tunazo statistical data kutoka AMREFna SIKIKA zinazoonyesha na sasa hizo ndizo recent yastatistical data tulizonazo kwamba vifo vya Mama na mtotovimeongezeka na Waziri anakubali wala hajapinga. Ukiachahilo nadhani hili ndiyo chanzo cha Serikali kuja na ile idea yakwamba bila takwimu inayokuwa approved na Serikalihatupokei takwimu yoyote kwa sababu na ndiyoanatuambia hapa tusubiri 2019/2020 tupate data za Serikali.Haya ni Mashirika ya Kimataifa na yameshasema kwambakifo cha Mama na mtoto kimeongezeka Tanzania. Serikalimpaka…

MWENYEKITI: Mheshimiwa kengele imegonga,unaunga mkono hoja ama hapana? Kengele imeshagonga.

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimsema tangia mwanzo naunga mkono hoja yaMheshimiwa Esther Matiko.

MWENYEKITI: Basi ahsante sana. Mheshimiwa FrankMwakajoka.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi kwanzanimeshangaa sana Mheshimiwa Waziri alichokuwaanazungumza hapa maana yake amegoma kwambahawana takwimu hapa katikati wanatumia takwimu zamwaka 2015.

Lakini ukweli kwenye bajeti ya Mwaka 2016/2017 vifovya Mama na mtoto viliripotiwa kutokana na taarifa yaMheshimiwa Waziri, hotuba yake, kati ya vizazi laki moja, vizazi444 walikuwa wanapoteza maisha. Mwaka jana 2017/2018,kati ya vizazi lakini moja, 556 walikuwa wanapoteza maishalakini leo wanasema kwamba wana data za…kwa hiyo hizidata za katikati hapa zilikuwa zinatoka wapi?

Page 232: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

232

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia tunaona bajetiinaendelea kushuka. Mwaka 2017/2018 bajeti ilikuwa juu leoiko bilioni tano peke yake kati ya bilioni kumi na kitu sasatunasema hivi vifo vya wakinamama na mtoto naniatavipunguza kama Serikali haijaweka mkono kati yakuhakikisha kwamba jambo hilo linafanyika? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili…

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa. MheshimiwaHussein Bashe.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nataka nimwombe dada yangu Mheshimiwa Estheramwachie Mheshimiwa Ummy shilingi yake na kwa sababu,tukiwa fair kabisa swali la Mheshimiwa Esther ni very clear;nini mkakati? Mheshimiwa Ummy amejibu mkakati wakwanza as a country tumefanya expansion ya uwepo wavituo vya afya zaidi ya 300 ambapo mwanzo havikuwepo.Kwa hiyo, ni service delivery, imekwenda. Tukitazama bajetikutokana na Wizara ya Afya peke yake tutakuwa hatuko fair.Suala la health linahusu TAMISEMI vilevile how much i-spendkwenye health component kwenye suala la TAMISEMI.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nchi, kuna plan yakuwepo kwa universal health system. Kwa hiyo, ina maanahuu ni mkakati kwamba tunataka mkakati globally, Wizaraya Afya ime-play a great role, lakini tunapo-comparetakwimu mbona tunasahau component ya growth yapopulation ambayo ina-grow? Kwa hiyo, akina mama nawenyewe wataongezeka, hakuna anayeunga mkono mamakupoteza uhai, lakini kama Bunge tunaona clear planinayofanywa na Wizara ya Afya katika eneo hili. Let us supportWizara ya Afya na nadhani kama tutakuwa fair, Wizara hiiimefanya jitihada kubwa sana kuleta awareness ya haki ya…(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

Page 233: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

233

MWENYEKITI: Ahsante sana. Muda umekwisha.Mheshimiwa kengele imegonga. Mheshimiwa Ally Keissy.

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,mimi simuungi hoja Mheshimiwa Esther Matiko kwa sababuna sisi wenyewe tunachangia vifo wa akina mama nawatoto. Haiwezekani mwaka mmoja mimba mbili na ushahidikwa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge humu wamo.

Sasa na sisi tuwahamasishe nyota ya kijani kwanza.Serikali imejitolea kujenga vituo vya afya na hospitali nchinzima na Waganga wameajiriwa lakini nasi Wabungetuhamasishe nyota ya kijani. Haiwezekani! Kuna ushahidi kwabaadhi ya Wabunge humu, mwaka mmoja mimba. Hivyo,tutaongezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siungi mkono hoja. (Makofi/kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza hatuwezi…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kigwangalla unasikikawewe, endelea.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza hatuwezi kuzungumzia kupungua amakuongezeka kwa takwimu za vifo vya akinamama wajawazitona watoto katika kipindi hiki kwa sababu the Tanzaniademographic and health survey huwa inatoka kila baadaya miaka mitano na huu ndiyo utafiti pekee ambao utatupahali ya sasa ikoje katika Sekta ya Afya nchini. Kwa maanahiyo, utafiti wa mwisho ulifanyika mwaka 2014 na matokeoyakatoka 2015 na yatatoka tena mwaka 2020. Nina uhakikayatakapotoka matokeo ya Demographic and Health Surveyya mwaka 2020 lazima tutaona kuna upungufu wachangamoto ambazo zimeonekana kwa sasa. (Makofi)

Page 234: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

234

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu mikakati mingi yakupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watotowakati wa kujifungua na baada ya kujifungua imefanyikasana na kasi kubwa zaidi kuanzia mwaka 2016 mpaka leo namikakati yenyewe ni pamoja na aliyoitaja Mheshimiwa Waziri.Mmojawapo ni huo wa kutoa oxytocin wakati akinamamawanaenda kujifungua kuhakikisha kuna damu na akinamama wanaongezewa damu katika vituo vya afya na vilevile ujenzi wa vituo vya afya zaidi ya 350 ambavyo hata kuleTarime tumepeleka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mikakati hiyopamoja na kutoa antibiotics pamoja na kuhakikisha kunadawa za kutosha kwenye ngazi ya vituo vya afya, itatusaidiasana ifikapo mwaka 2020 kushusha idadi ya vifo ambavyovinatokana na uzazi. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge,tuvute subira mpaka mwaka 2021 kama tutajaliwa tunawezatukajadili mambo haya. Kwa sasa tunatumia takwimuambazo ni za nyuma sana, kabla ya Demographic andHealth Survey. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Mheshimiwa Esther Matiko ameuliza swali zurikwa Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Waziri amempamajibu mazuri sana kwa sababu alitaka kujua mkakati ni upi?Mheshimiwa Waziri amesema mkakati wa mwaka huukwenye bajeti hii ni kumalizia na kuimarisha hospitali za rufaaza mikoa yote, ambao ni mkakati mkubwa sana kila mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili labda niseme nikwamba, kule Tarime Mheshimiwa Esther Matiko amesemaHospitali ya Wilaya ina shida ina msongamano mkubwa sana,lakini tumeelekeza TAMISEMI kwamba fedha zipelekwe paleili wakaimarishe hospitali ile. Kwa hiyo, ina maana akinamamawatapata huduma muhimu. Pale Nkende wamepata shilingimilioni 400, Sirari wamepata shilingi milioni 500, Nanyakwatumepata shilingi milioni 800, Kerende pale Nyamongo

Page 235: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

235

tunajenga kituo cha afya na gari ya wagonjwa linapelekwa.Sasa hiyo ni mikakati ya akina mama kwamba wakipatacomplication kwenye uzazi wapate huduma haraka ya uzazisalama na Mheshimiwa Waziri ameji-commit. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unaweza ukaona michangoyetu, Mheshimiwa Ummy Mwalimu ni mwanamke mwenzaohawa akina Mheshimiwa Esther Matiko; amesifiwa hotubayake il ikuwa hot kweli huku ndani, kila mtu alikuwaanashangilia. Nilitarajia Mheshimiwa Esther Matiko asimamehapa ampongeze mwanamke mwenzake amtie moyo bajetiipite na tukafanye kazi kubwa sana. Akina mama lazimawaungane mkono. Sasa katika mazingira hayakukwamishana inakuwaje? (Makofi/kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi/kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Peter Serukamba.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimuombe Mheshimiwa Esther Matiko ondoa shilingi kwasababu zifuatazo: Waheshimiwa Wabunge tukubaliane,Wizara ya Afya kwa miaka hii mitatu wamefanya makubwasana kuokoa maisha ya akina mama na watoto. Kamamtakumbuka Wizara ya Afya iligawa ambulance 100; nimkakati. Tumejenga vituo vya afya; ni mkakati. Tunajengahospitali za Wilaya nchi nzima; ni mkakati; Tunajenga Hospitaliza Rufaa za Mikoa; ni mkakati. Yote haya ni kutaka kuhakikishaakina mama wa nchi hii wanajifungua salama. Effort nikubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi ya hayo, tuangalietrend ya bajeti ya Wizara ya Afya hasa katika eneo hilo lakuokoa maisha ya akina mama na watoto. Trend ni kubwa,fedha zinaongezeka kila mwaka, yote hii ni mikakati. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho ambaloMheshimiwa Waziri amelisema kwamba baada ya kuangaliahali nzima, wanakuja na sera pana ya afya nchini ili kuangaliatunavyotatua changamoto za afya Tanzania. Nadhani tunalo

Page 236: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

236

jukumu kama Waheshimiwa Wabunge, kuwaunga mkono iliwaendelee kutatua hizi changamoto zilizopo nchini. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Muda umekwishaMheshimiwa. Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naombaniwashukuru wachangiaji wote. Kama alivyosemaMheshimiwa Dkt. Kigwangalla kwamba hizi takwimu zinatokabaada ya miaka mitano, lakini sisi kama Wizara tunakusanyakitu kinaitwa routine data, ndiyo maana tunaweza kusimamakifua mbele kusema baada ya miaka mitano tutakapokuwatunatakiwa tukadirie kiasi kingine, vifo vya akina mamaTanzania vitakuwa vimepungua sana. Hii inatokana namikakati yote hii ambayo inakwenda na siyo tu ndani ya Sektaya Afya, lazima tuangalie hata hili suala la elimu bure nalolinachangia sana mabinti kuchelewa kupata ujauzito nakupunguza idadi ya akina mama wanaojifungua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala la barabaraambazo zinajengwa na Serikali, masuala ya umeme ambayowanafanya, yote haya yana mchango mkubwa sana.Niendelee kumwomba tu Mheshimiwa Esther Matiko,mtuamini tunachokisema hapa. Bahati nzuri katika Sekta yaAfya hatupigi porojo, takwimu tulizonazo zinaonesha kwambahatuna vifo vya akina mama 30 kwa siku wala hatuna vifowa akina mama 11,000 ndani ya mwaka mmoja. Hivyohavitakuwepo kutokana na mikakati hii ambayo ipo. Kwahiyo, tunaomba mturudishie shilingi ili tuweze kwendakutekeleza majukumu yetu. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Esther Matiko.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru, naomba tu kusema kwamba kwanza kabisaalichokisema Mheshimiwa Keissy na Wabunge wa CCM

Page 237: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

237

mkaki-support kwa asilimia kubwa inaonesha ni jinsi gani tunaWabunge ambao hampo kwa maslahi ya Watanzania. Nijuzi tu tumetoka kutaka kuongeza shilingi kwenye majimkakataa. Hivi nyie mnafurahia akina mama 30 kufariki kwasiku! No wonder, mnafurahi hata watu wakitekwa mnaonasiyo! Yaani ni Tanzania tu mnaweza kuangalia Mtanzaniahata mmoja akifariki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema tumejenga vituova afya sijui Nkende, Sirari, hamna watalaam wamamawakienda pale. Pia tuzingatie katika vituo vya afyawanavyojenga 300 tuna Kata 4000, kuna vijiji 19,800,miundombinu ya barabara dhoofu ilhali wamamawajawazito wa Tanzania watafika kwenye health centerambako kuna Kata moja iko imekuwa scattered sana. Watu11,000 ni sawa sawa na Jimbo moja la Zanzibar au mawili,wanakufa and then mna-clap makofi. Nataka mkakati Serikaliya Chama cha Mapinduzi, mtatimiza vipi sera yenu ya kuwana kituo cha afya kila Kata, zahanati katika kila kijiji tuwe nawatumishi wa kutosha na vifaa tiba kupunguza vifo vyamama na mtoto? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mnavyotoa prioritykwenye Wizara ya Ujenzi, narudia; kama nilivyosema juzi tutoefedha hapa tujenge miaka 58 ya uhuru, tunazungumzia vituo300 and we clap. Nakubali Nkende nimepata, but is notenough. Kituo kimoja cha afya out of nane! Siwezi… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Muda wako umeisha Mheshimiwa.Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea. Umesema...

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,umesema tupige kura maana yake sijaridhika ili sasa ijulikane.

MWENYEKITI: Umemaliza. Waheshimiwa Wabunge,kwanza tuelewane vizuri kunakuwa na upotoshaji huko njemtu akiwasha mic saa ya kuitika kura. Sisi wote humu ndani

Page 238: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

238

ni watu wazima na kuna watu hawajisikii vibaya kufanyaupotoshaji. Sasa humu mnafahamu kwa idadi wapi wakowengi. Kwa hiyo, tuangalie vizuri na kama kuna sababu,kanuni zetu zinaruhusu ili kura zihesabiwe. Tuwe wavumilivu.Kama kuna mtu ana taabu, kanuni zetu zinaruhusu utaratibu,lakini tusifanye upotoshaji ambao hauna sababu yoyote.

Waheshimiwa Wabunge nitawahoji.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kukataliwa)

MWENYEKITI: Kwa hiyo, tutaendelea na MheshimiwaAbdallah Mtolea.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Ukiangalia Sera ya Afya inasema kwambahuduma za matibabu katika nchi hii ni za uchangiaji.Imetumia neno “uchangiaji”, haijatumia neno “malipo”,maana yake ni kwa sababu kiasi ambacho mwananchianalipa kwa huduma ya afya ni kidogo sana kulingana nathamani halisi ya huduma anayopewa na Serikali inachangiakwa kiasi kikubwa. Tunaipongeza Serikali kwa kutembeakatika sera hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitendo cha hospitali kuzuiamaiti zisitoke hospitalini mpaka deni la matibabu lilipwe, hiihaijakaa vizuri. Nimemsikia Mheshimiwa Waziri wakati anajibuamesema kwa jitihada kubwa ambazo Serikali inazifanya siyorahisi isamehe kila deni la matibabu ya kila mgonjwaanayefariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja hapa siyo kusamehemadeni, lakini tunataka Serikali iweke utaratibu ambao mtuakifariki ndugu, jamaa, marafiki na majirani wawezekuchukua maiti wakazike na bado wawe na fursa ya kujakulil ipa li le deni baadaye, kwa sababu kitendo chakuendelea kubaki na maiti hakileti picha nzuri. Maana yakemaiti inakuwa bond ya gharama za matibabu, jambo

Page 239: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

239

ambalo siyo la kiungwana na siyo la kiutamaduni kwa milazetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naombacommitment ya Serikali katika hili na kama nisiporidhika, basinakusudia kutoa shilingi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa AbdallahMtolea. Waheshimiwa Wabunge, kwa mujibu wa kanuni zetu,muda uliobaki unanitaka nihoji mafungu kwa pamoja. Katibu.

NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH - KATIBU MEZANI:

KITABU CHA PILI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fung 52 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto

Kif. 1001 – Administration and Human Resources Management..........…………....…Sh. 8,450,857,436/=

Kif. 1002 – Finance and Accounts Unit……Sh. 1,486,211,596/=Kif. 1003 – Policy and Planning Unit………..Sh. 1,261,499,537/=Kif. 1004 – Internal Audit Unit………………… Sh. 391,551,336/=Kif. 1005 – Government Communication

Unit.....................................................Sh. 386,423,562/=Kif. 1006 – Procurement Management Unit...Sh. 302,732,000/=Kif. 1007 – Legal Service Unit…………………..Sh.162, 660,063/=Kif. 1008 – Information and Communication

Technology Unit..............................Sh. 280,096,480/=Kif. 2001 – Curative Service…….………... Sh. 219,991,668,419/=Kif. 2003 – Chief Medical Officer………… Sh. 37,502,929,116/=Kif. 2004 – Nursing and Midwifery Services

Division………….…….......................Sh. 552,896,936/=Kif. 2005 – Pharmaceutical Services Unit……Sh. 385,051,336/=Kif. 3001 – Preventive Services……….…… Sh.19,266,898,424/=Kif. 3002 – Health Quality Assurance

Division...............................................Sh. 516,151,382/=Kif. 4002 – Social Welfare……….…………….. Sh. 399,555,336/=

Page 240: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

240

Kif. 5001 – Human Resource Development….......................…. Sh.12,590,595,556/=

Kif. 6001 – Amana Regional Referral Hospital- Dar es Salaam..............Sh. 5,806,680,932/=

Kif. 6002 – Bombo Regional Referral Hospital- Tanga…………..............Sh. 5,098,106,324/=

Kif. 6003 – Dodoma Regional Referral Hospital…………….….... Sh. 6,847,156,802/=

Kif. 6004 – Geita Regional Referral Hospital……………….....Sh. 1,601,737,746/=

Kif. 6005 – Iringa Regional Referral Hospital………..………. Sh. 5,394,379,596/=

Kif. 6006 – Kagera Regional Referral Hospital………......……. Sh. 3,915,547,873/=

Kif. 6007 – Katavi Regional Referral Hospital………………… Sh. 2,368,264,624/=

Kif. 6008 – Ligula Regional Referral Hospital – Mtwara….............……. Sh. 3,285,599,596/=

Kif. 6009 – Manyara Regional Referral Hospital………......……. Sh. 2,814,757,772/=

Kif. 6010 – Mara Regional Referral Hospital………………… Sh. 3,701,590,622/=

Kif. 6011 – Maweni Regional Referral Hospital - Kigoma…............……. Sh. 3,056,223,596/=

Kif. 6012 – Mawenzi Regional Referral Hospital – Kilimanjaro...Sh. 5,843,907,828/=

Kif. 6013 – Mbeya Regional Referral Hospital…………………..Sh. 4,208,295,596/=

Kif. 6014 – Morogoro Regional Referral Hospital…………..…….. Sh. 6,840,236,932/=

Kif. 6015 – Mount Meru Regional Referral Hospital - Arusha…....… Sh. 5,660,399,596/=

Kif. 6016 – Mwananyamala Regional Referral Hospital- DSM…............. Sh. 4,974,388,436/=

Kif. 6017 – Njombe Regional Referral Hospital...……………… Sh. 1,537,033,448/=

Kif. 6018 – Sekou Toure Regional Referral Hospital – Mwanza …. Sh. 4,970,951,386/=

Kif. 6019 – Shinyanga Regional Referral Hospital………………….Sh. 3,637,721,596/=

Page 241: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

241

Kif. 6020 – Simiyu Regional Referral Hospital…………………Sh. 1,857,080,648/=

Kif. 6021 – Singida Regional Referral Hospital….………………Sh. 3,762,526,632/=

Kif. 6022 – Sokoine Regional Referral Hospital – Lindi….…….. Sh. 3,347,827,596/=

Kif. 6023 – Songea Regional Referral Hospital – Ruvuma.....…Sh. 5,733,932,596/=

Kif. 6024 – Songwe Regional Referral Hospital………....……….. Sh. 821,246,811/=

Kif. 6025 – Sumbawanga Regional Referral Hospital – Rukwa…...... Sh. 2,804,199,596/=

Kif. 6026 – Tabora Regional Referral Hospital…………....…… Sh. 3,402,726,055/=

Kif. 6027 – Temeke Regional Referral Hospital- Dar es Salaam.............Sh. 6,158,812,756/=

Kif. 6028 – Tumbi Kibaha Regional Referral Hospital – Pwani…...…. Sh. 1,635,150,495/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 53 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto

Kif 1001 – Administration and Human Resources Management...............................Sh. 2,323,579,813/=

Kif. 1002 – Finance and Accounts Unit………Sh. 415,150,000/=Kif. 1003 – Policy and Planning Unit………..…Sh. 877,588,800/=Kif. 1004 – Internal Audit Unit…………………..Sh. 323,676,301/=Kif. 1005 – Government Communication

Unit…………………….....................Sh. 2,575,929,598/=Kif. 1006 – Procurement Management Unit...Sh. 478,857,000/=Kif. 1007 – Information and Communication

Technology.......................................Sh. 479,459,943/=Kif. 1008 – Legal Service Unit………………….Sh. 236,464,500/=Kif. 2001 – Training and Folk Development…Sh. 211,044,000/=Kif. 2002 – Community Development…….Sh.11,650,733,357/=Kif. 3001 – Gender Development ……………Sh. 944,777,000/=Kif. 3002 – Children Development……………Sh. 867,140,000/=

Page 242: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

242

Kif. 4001 – Non-Government Organizations...............................…Sh. 784,298,120/=

Kif. 5001 – Social Welfare Division………….Sh. 6,426,671,568/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

KITABU CHA NNE

MIPANGO YA MAENDELEO

Fungu 52 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto

Kif. 3001 – Policy and Planning Unit………Sh. 45,188,873,128/=Kif. 2001 – Curative Services……………….Sh. 42,891,039,000/=Kif. 2005 – Pharmaceutical Services

Unit...............................................Sh. 200,000,000,000/=Kif. 3001 – Preventive Services…………...Sh. 256,057,990,469/=Kif. 3002 – Health Quality Assurance Division……....…….. Sh. 0Kif. 5001 – Human Resource Development………………. Sh. 0

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 53 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto

Kif. 2002 – Community Development……..Sh. 1,000,000,000/=Kif. 3001 – Gender Development…………..Sh. 1,124,040,000/=Kif. 3002 – Children Development……………Sh. 191,350,000/=Kif. 5001 – Social Welfare Division……………Sh. 444,671,013/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

(Bunge lilirudia)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae, Mtoa Hoja.

Page 243: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

243

T A A R I F A

WAZIRI WA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibuwa kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari 2016 kanuniya 104(3) (a) na (b) kwamba Bunge lako lilikaa kama Kamatiya Matumizi, limekamilisha kazi zake. Naomba taarifa yaKamati ya Matumizi ikubaliwe na Bunge lako.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge hoja imeungwamkono ahsanteni sana sasa kwa utaratibu wetu niwatahoji.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwakawa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Afya, Maendeleo yaJamii, Jinsia, Wazee na Watoto yalipitishwa na Bunge)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nianze kwanzakwa kutoa pongezi nyingi kwa Waziri, Mheshimiwa NaibuWaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji wote wanaofanya kazikatika Wizara hii. Pongezi hizi nadhani nyingi mmezipokeakutoka kwa Waheshimiwa wabunge. Sasa kwa sababu Bungelimeshafanya uamuzi kuhusu yale mliyokuwa mmeyaletakwetu pamoja na yale ambayo Kamati imewashauri na ninyimmeyachukua, kwa hiyo, niwapongeze kwa niaba yetu sisisote kwamba mnafanya kazi nzuri pamoja na changamotoza hapa na pale, lakini kwa ujumla wake mnafanya kazi nzurindiyo maana Waheshimiwa Wabunge wanatambua uwepowenu kwenye majimbo yao na uwepo wa kazi zenu kwenyeMajimbo yao. (Makofi)

Kwa hiyo, yale ambayo wamechangia humu ndanitunaamini kwamba yataboresha utendaji kazi wenu, lakini

Page 244: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

244

pengine hapa na pale panapohitaji marekebisho, basimtafanya hayo marekebisho kwa kadri mlivyoshauriwa naKamati na Waheshimiwa Wabunge wale ambaohawakupata fursa ya kushiriki kwenye Kamati. Nasi tuchukuefursa hii kuwatakia kila la kheri kwenye utekelezaji wa yaleyote ambayo umeyaahidi kwamba mnaenda kuyafanya napia yale ambayo mmesema mnaenda kuboresha kwa mujibuwa Waheshimiwa Wabunge walivyotoa mapendekezo yao.Tunawatakia kila la kheri. (Makofi)

Pia kwa yale ambayo yamezungumzwa hapa yajumla moja ni kuhusu Bima ya Afya kama Bunge na sisitungependa kutoa huo msisitizo na Waheshimiwa Wabunge;sisi kama Wawakilishi wa Wananchi ni vizuri kuendeleakuzungumza na wananchi wetu tunapopata fursa yakuonana nao kuona umuhimu wa kuwa na bima. Kwa hiyo,tuendelee kuwashauri, siyo jambo litakalobadilika kwa sikumoja lakini naamini kwa sababu wananchi waliokuamini kujahumu ndani wanawaamini pia mkiwapa ushauri. Tusichokekuendelea kuwashauri wananchi tunaowawakilisha humundani ili waone umuhimu wa kuwa na Bima ya Afya.

Jambo lingine Mheshimiwa Naibu Waziriamezungumza hapa baada ya michango ya WaheshimiwaWabunge kuhusu vipimo vya homa ya matumbo na piavipimo vya maambukizi kwenye mrija au mirija ya haja ndogo,nadhani tukisema tu sisi tukienda hospitali ndio tuwaulize siowote wenye ujasiri wa kumwuliza daktari anaposemaamepima kitu fulani na majibu yametoka.

Nadhani ni muhimu kwa upande wa Wizara ya Afyakutoa mwongozo mahususi ili wale watu wanapotupimawatupime kitaalam kwenye hayo huenda ndiyotunayoumwa, lakini watupime kitaalam, wasitupimewakatupa dakika mbili kwa majibu yanayochukua siku mbili.Nadhani hiyo sasa ni ya upande wenu kuliko sisi tukiwawagonjwa maana wakati mwingine mgonjwa anawezakuwa anaogopa, daktari akamwandikia sindano hata kamakuna vidonge kwa sababu anajua amemwuliza maswalimagumu. (Makofi)

Page 245: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA WA KUMI NA TANOparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1560254254-8 MAY 2019.… · Na. 186 Kupunguza Makato ya Watumishi kwa Vyama vya Wafanyakazi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

245

Kwa hiyo, tafadhali kwenye hili Wizara ya Afyamtusaidie kwa sababu maana yake watu wanaweza kuwawanakunywa dawa ambazo hawaumwi magonjwa hayo nabaadaye wanaweza kuja kupata changamoto za magonjwamakubwa kama aliyokuwa anataja Mheshimiwa Khatibhapa. Kwa hiyo, hilo nadhani ninyi mnaweza kulifanyia kazikwa haraka, siyo jambo gumu ili wenzetu wa vipimo wawewanatupima sawasawa.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kuzungumzahayo yaliyo ya jumla, wapo wageni ambao tuko nao Bungenijioni hii. Tunao wageni 18 wa Mheshimiwa Dkt. FaustineNdugulile ambaye ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo yaJamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambao ni viongozi wa Chamacha Mapinduzi, Madiwani na watumishi kutoka Wilaya yaKigamboni Jijini Dar es Salaam. Hawa wameongozwa naMwenyekiti wa CCM Wilaya ambaye ni ndugu Henry Chaula.Karibuni sana. (Makofi)

Tunao pia wageni 80 wa Mheshimiwa GodfreyMgimwa ambao ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma,wanaotokea Jimbo la Kalenga karibuni sana.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya matangazo hayo,naahirisha shughuli za Bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi.(Makofi)

(Saa 12.01 jioni Bunge liliahirishwa hadi siku ya Alhamisi,Tarehe 9 Mei, 2019 Saa Tatu Asubuhi)