195
Ufafanuzi Wa Agano Jipya Matendo na Warumi www.africanpastors.org Na Dorothy Almond mwisho na Askofu Francis Ntiruka

Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

  • Upload
    others

  • View
    70

  • Download
    24

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

Ufafanuzi WaAgano Jipya

Matendona Warumi

www.africanpastors.org

Na Dorothy Almondmwisho na Askofu Francis Ntiruka

Page 2: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

Kimetolewa na:AFRICAN PASTORS FELLOWSHIP

Station House, Station Approach, AdishamCanterbury, Kent CT3 3JE

United Kingdom

www.africanpastors.org

Ufafanuzi WaAgano Jipya

Matendona WarumiDorothy Almond

© African Pastors Fellowship 2010

Page 3: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO665

MATENDO YA MITUMEYALIYOMO

UTANGULIZI(a) Mahali pake katika Agano Jipya na manufaa yake(b) Mpango wake(c) Mwandishi(d) Sababu za kuandika

UFAFANUZISEHEMU KUBWA YA KWANZAINJILI KUHUBIRIWA YERUSALEMU NA KANDOKANDO YAKESura 1-12

1: 1- 5 Yesu kuwatokea wanafunzi mara kwa mara1: 6-11 Yesu kuwaaga na Kupaa1:12-26 Wanafunzi kumngojea Roho Mtakatifu2: 1-13 Kushuka kwa Roho Mtakatifu2: 14-41 Mahubiri ya kwanza ya Kikristo2: 42-47 Jamii Mpya ya Kikristo3: 1-10 Kiwete kuponywa3: 11-26 Hotuba ya Petro4: 1-22 Petro na Yohana kukamatwa na kufungwa,

kushtakiwa barazani, na kufunguliwa.4:23-31 Kuwapasha wenzao habari hizo, kumwomba Mungu kwa

pamoja na kupewa nguvu mpya ya Roho4: 32-37 Jamii mpya ya Kikristo5: 1-11 Unafiki wa Anania na Safira5: 12-16 Wagonjwa wengi kuponywa5: 17-33 Mitume kufungwa, malaika kuwatoa, kuletwa barazani5: 34-42 Shauri la Gamalieli, Mitume kupigwa na kufunguliwa 6:1-7 Watumishi saba kuwekwa6: 8-15 Stefano kushtakiwa7: 1-53 Utetezi wa Stefano7: 54-60 Kifo cha Stefano8: 1- 3 Sauli kuwatesa Wakristo, nao wakatawanyika8: 4-13 Filipo kuwahubiri Wasamaria8: 14-25 Petro na Yohana kuja Samaria8: 26-40 Mkushi kumwamini Kristo na kubatizwa na Filipo9: 1- 9 Kuongoka kwa Sauli huko Dameski9: 10-25 Anania akambatiza, Sauli alimshuhudia Kristo9: 26-31 Sauli huko Yerusalemu halafu Tarso9: 32-43 Petro huko Lida - kiwete kuponywa - Dorkasi kufufuliwa

Page 4: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO666

10: 1-43 Petro na Kornelio10: 44-48 WaMataifa kushukiwa na Roho na kubatizwa11: 1-18 Petro kuwaelezea Wakristo wa Kiyahudi

sababu ya kumbatiza Kornelio11: 19-26 WaMataifa kuipokea Injili huko Antiokia11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa ajabu12: 20-25 Kifo kibaya cha Mfalme Herode

SEHEMU KUBWA YA PILIINJILI KUHUBIRIWA KATIKATI YA WAMATAIFA NA MAKANISAKUSIMAMISHWASura 13 – 28

UTANGULIZI13: 1-3 Kanisa la Antiokia kuwateua Barnaba na Sauli kwenda kuhubiri

Injili katika nchi zingine.

SAFARI KUBWA YA KWANZA 13:4-14:26; kama BK.46-48.13: 4-12 Barnaba na Sauli huko Kipro, Sauli ajiita Paulo.13:13-52 Kuhubiri huko Antiokia wa Pisidia, halafu kuwageukia

WaMataifa.14: 1- 7 Kuhubiri huko Ikonio.14: 8-20 Kuhubiri huko Listra na Derbe.14:21-28 Kurudia makanisa yaliyopandwa; kurejea Antiokia.

SURA YA 15: BARAZA KUU LA KANISA KUHUSU TOHARA.15: 1-21 Mwenendo wa Mkutano.15: 22-35 Barua ya kuuthibitisha uamuzi wao: Sila na Yuda kwenda

Antiokia.15: 36-39 Barnaba na Sauli kutengana: Barnaba na Yohana Marko

kwenda Kipro; Sila kujiunga na Paulo.

SAFARI KUBWA YA PILI: 15:40-18:221 5: 40-16:5 Paulo na Sila kuyarudia makanisa yaliyopandwa katika

Safari ya Kwanza: kumchukua Timotheo kijana.16: 6-10 Kupitia nchi za Galatia na Frigia; kufika Troa16: 11-40 Kuvuka mpaka Makedonia na Kufika Filipi 17:1- 9 Injili kuhubiriwa Thesalonike.17:10-15 Injili kuhubiriwa Beroya.17:16-34 Paulo katika Mji wa Athene.18: 1-18 Paulo huko Korintho.18: 19-23 Kupitia Efeso na kukutana na Prisila na Akila. 18:24-28 Apolo kufika Efeso, halafu kupelekwa Korintho.

Page 5: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO667

SAFARI KUBWA YA TATU YA INJILI: 18:23-21:1719: 1- 7 Paulo kufika Efeso na kukutana na wanafunzi walioujua ubatizo

wa Yohana tu.19: 8-12 Huduma sinagogini kwa Wayahudi.19: 13-20 Wana wa Skewa.19: 21-22 Mipango ya Paulo.19: 23-41 Ghasia iliyotokea Efeso.20: 1- 2 Kufika Makedonia na Uyunani.20: 3- 5. Paulo aliondoka Korintho na kurudi Troa kwa kupitia

Makedonia.20: 6-12. Hotuba ndefu ya Paulo pale Troa na Eutiko kuanguka kutoka

orofani na kufa na Paulo kumrudishia uhai wake.20: 13-16 Kutoka Troa mpaka Mileto.20: 17-38 Hotuba ya Paulo alipoagana na wazee wa Efeso21: 1-14 Safari kutoka Mileto hadi kufika Kaisaria na kukaa na Filipo21: 15-26 Kufika Yerusalemu: Nadhiri ya Wayahudi Wanne21: 27-40 Ghasia katika hekalu: Paulo kukamatwa.22: 1-21 Utetezi wa Paulo kwa Wayahudi.22: 22-30 Paulo kudai haki ya uraia wake wa Kirumi.23: 1-11 Utetezi wa Paulo mbele ya Baraza ya "Sanhedrin".23:12-22 Shauri la siri la kumwua Paulo.23:23-35 Paulo kupelekwa Kaisaria.24: 1-21 Paulo kuhukumiwa mbele ya Liwali Feliki.24: 22-27 Kesi kuahirishwa.25: 1-12 Paulo mbele ya Liwali Festo.25: 13-27 Paulo mbele ya Mfalme Agripa II na Bernike.26: 1-32 Utetezi wa Paulo mbele ya Mfalme Agripa II.

SAFARI YA KWENDA RUMI:27:1-4427: 1- 8 Kutoka Kaisaria na kupita Mira hadi Kisiwa cha Krete.27: 9-44 Dhoruba kali; meli kuvunjika; kufika Melita.28: 1-10 Paulo na wenzake katika kisiwa cha Melita; kumponya baba wa

Publio, mkuu wa Kisiwa.28: 11-16 Kufika Rumi, Paulo kukaa miaka miwili hali ya kulindwa na

askari28: 17-31 Paulo kuwaelezea Wayahudi na kuhubiri Injili kwa wote

waliomjia.

Page 6: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO668

UTANGULIZI(a) Mahali pake katika Agano Jipya na manufaa yake:Kitabu hiki cha Matendo kimewekwa mara baada ya Injili Nne. Mahali pazuri kwakuwa kina habari za matendo ya Mitume yaliyotendeka baada ya Yesu kuondokahali amewakabidhi kazi na kutoa maagizo ya kueneza Injili. Ni kitabu pekeechenye historia ya Kanisa katika maisha yake mapya ya kuwa Jamii Mpya yawatu wa Mungu, Israeli Mpya. Katika Injili tuliona wanafunzi wa Yesu walikuwana udhaifu mbalimbali, walimwacha wakati alipokamatwa, na kumrudiaalipofufuka.Pasipo habari hizo za Matendo tungekuwa na pengo kubwa la kufahamu jinsiwenzetu wa kwanza walivyoishi na kutenda.

(b) Mpango wake:Kitabu kina sehemu kubwa mbili: ya kwanza ni kutoka sura ya kwanza hadi suraya kumi na mbili. Katika sehemu hiyo Petro ametajwa sana akiwa kiongozi, naYohana ametajwa kidogo, na wengine hawatajwi isipokuwa kwa jumla. Katikasehemu hiyo ya kwanza wanafunzi walihubiri Injili Yerusalemu na kandokandoyake, makanisa yalipandwa kati ya Wayahudi na Wasamaria, mwishoni mwasehemu hiyo Injili ilihuburiwa kwa WaMataifa. Sehemu kubwa ya pili yaanza Suraya kumi na tatu mpaka sura ya ishirini na nane. Paulo ametajwa sana pamoja nawasaidizi wake, hasa Barnaba, Sila, Luka na Timotheo. Badala ya Yerusalemutumepewa habari za Antiokia na uenezi mkubwa wa Injili, makanisa yakipandwamahali pengi.

Iwapo Jina la Kitabu ni Matendo ya Mitume tusifikiri kwamba habari za kila Mtumena alivyofanya zimo humo pia tusifikiri Injili ilipelekwa kuelekea magharibi tu,tunafahamu kutoka maandishi mengine ya kwamba ilikwenda mpaka Misri naAfrika kaskazini, pamoja na nchi za mashariki.

Iwapo Kitabu chaitwa Matendo ya Mitume jina lingine ambalo lingefaa ni MatendoYa Roho Mtakatifu kwa kuwa asili ya mambo yaliyotendeka ilikuwa RohoMtakatifu kama tutakavyoona tunapoendelea na ufafanuzi wetu.

Mwanzoni Ukristo ulionekana kama tawi la dini ya Kiyahudi. Maana Wakristowalikuwa Wayahudi na Wayahudi waliotumia lugha ya Kiyunani walioitwa"Hellenists", nao waliendelea na desturi za Kiyahudi kama tohara na kuabuduhekaluni.

Ila nyongezo ilikuwa Ibada ya Ushirika na kuadhimisha Siku ya kwanza ya jumakwa kumkumbuka Yesu na Kufufuka Kwake. Mabadiliko makubwa yalitokeabaadaye, wakati wa WaMataifa wengi kumpokea Kristo na kubatizwa bilakutahiriwa. Neno hilo lilileta majadiliano makubwa (Sura 15) na kusababishafitina. Polepole hali ya kuonekana kama tawi la Kiyahudi ilipungua, Kanisa lilivuavazi la Kiyahudi na Ukristo ulitokea kama imani ifaayo walimwengu wote.

Page 7: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO669

(c) Mwandishi:Iwapo hakujitaja katika Kitabu yaonekana ni Luka. Katika 1:1 mwandishi alisemaanamwandikia Theofilo na ya kuwa hicho kitabu ni cha pili alichomwandikia;tukitazama Injili ya Luka 1:1-4 twakuta Theofilo ametajwa. Hali ya Kiyunani chakeni sawa na Injili hiyo, Kiyunani safi cha mtu aliyeelimika vizuri. Jambo linginelinalotusaidia kukubali ni Luka ni kwamba twajua alimfahamu Paulo na kwasababu alikuwa daktari alimsaidia kwa upande wa matibabu. Tena alisafiri nayemara kwa mara, na neno "tuli .. "ni dalili ya Luka kuwa pamoja na Paulo katikamsafara taz. Mdo. 16:10-17 20:6: KoI. 4:14; Filemoni 24: 2 Tim. 4:11.

Alikuwa na uwezo wa kutosha kuandika vitabu hivi; nafasi ya kupata habari kwaInjili ilipatikana alipokaa na Paulo huko Kaisaria wakati Paulo alipokuwamfungwa akingoja kwenda Rumi kuhukumiwa. Habari nyingi za Matendoalizipata kwa wajoli wa Paulo ambao aliwafahamu.

Twaweza kutegemea habari hizo zilizoandikwa na Luka maana alijishuhudiakwamba alitafuta usahihi wa mambo na kuyaweka kwa utaratibu mzuri Lu: I:I-4.Wataalamu wamehakikishia ukweli wa madai yake kwa kuona alitaja majina yawakuu kwa usahihi, maana kila mahali palikuwa na majina yake, pamoja namahali mbalimbali kuelezwa bila kosa.

(d) Sababu za kuandika:Ni kumpasha huyo Theofilo habari sahihi ya imani ya Kikristo na uenezi wa Injili.Yafikiriwa Theofilo alikuwa na cheo kikubwa katika serikali ya Kirumi. Watuwaliwaonea mashaka Wakristo kwa kuwa mara kwa mara ghasia ilitokea Injiliilipohubiriwa. Adui zao walieneza uvumi usio kweli juu yao. Luka alitaka Ukristouwazwe vema machoni pa serikali na uonekane kuwa imani ya kuwafaa watu waDola.

Ni dhahiri kwamba Luka alichagua yale mambo yaliyothibitisha Imani ya Kikristokuwa Imani pekee iwezayo kusimama peke yake mbali ya asili yake katika Imaniya Kiyahudi. Amekaza uenezi wa Injili kutoka Yerusalemu mpaka Rumi, Mji mkuuwa Dola, akafunga kitabu kwa kutaja waamini kuwapo Rumi penyewe. Tukitafutakiini cha kitabu hicho twaweza kujumlisha katika maneno machache: "Kristo nikwa ulimwengu mzima". Shabaha ya Kanisa ni kutekeleza Agizo Kuu la BwanaAgizo Kuu la Bwana Yesu (Math. 8:19-20) na kuleta watu kwa Kristo.

Page 8: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO670

UFAFANUZI

SEHEMU KUBWA YA KWANZAINJILI KUHUBIRIWA YERUSALEMU NA KANDOKANDO YAKE:Sura 1-12

1: 1-5: Yesu kuwatokea wanafunzi mara kwa marak.1: Kitabu kile cha kwanza ni Injili ya Luka 1:1-4. Kilitoa habari za matendo namafundisho ya Yesu alipokuwa duniani. "aliyoanza" katika mawazo ya Luka Yesuhakuacha kufanya hayo alipopaa na kurudi kwa Baba. Kwa njia ya Roho na kwakuwatumia wafuasi wake Yesu Mwenyewe aliendelea kufanya kazi k.2 Mitumewafanye kama alivyowaagiza, maana aliwachagua kwa kusudi hilo.

k.3 Yesu alikuwa amejifunua kwao, na baada ya Kufufuka na kabla ya Kupaaalijidhihirisha kwao mara kwa mara ili wajue hakika Yeye yu hai. Pia alitumiamuda huu wa siku arobaini ili awafundishe zaidi kuuhusu Ufalme wa Mungu. Bilashaka mafundisho hayo yaliwajenga sana hali wametiwa nuru zaidi kutokana naKifo na Kufufuka Kwake.

k.4. Alitaka wafanye kazi kwa pamoja na kwa umoja, kwa hiyo aliwaagiza wakaeYerusalemu na kusubiri Kushuka Kwa Roho Mtakatifu. Tukumbuke wengiwalikuwa Wagalilaya na nyumbani si Yerusalemu bali ni Galilaya. Twaonahekima ya Yesu kwa Agizo hilo kwa sababu hawataweza kutekeleza Agizo Kuula kuhubiri Injili katika ulimwengu wote wasipovunja uhusiano wao na nyumbani."waingoje ahadi ya Baba" watapewa Roho yuleyule aliyemwezesha Bwana Yesukutimiza huduma yake. Baba atamtuma Roho kama jibu lake kwa ushindi waBwana Yesu. Ishara ya kwamba Yesu ametawazwa huko juu. Kwa njia hiyowatakuwa wameingizwa katika mpango wa Mungu wa kuleta Ufalme wake wamsamaha wa dhambi na uzima wa milele. Vote yawategemea, ni kama Munguhana mpango mwingine, na wao wataweza kwa kumtegemea Roho Mtakatifu.

Roho atashuka kwa dalili ambazo watajua kwa uhakika Ameshuka

1: 6-11 Yesu kuwaaga na KupaaBaada ya siku zile arobaini Yesu aliagana nao rasmi, wazi, saa za mchana, haliamewakusanya pamoja na wao kumsindikiza mpaka Mlima wa Mzeituni. Kwanjia hii walikuwa na uhakika ameisha kurudi kwa Baba yake mbinguni. Hawanahaja ya kufikiri huenda leo atatutokea! na kwa kuwatokea na kutoweka mara kwamara alikuwa amewazoeza kutokuwa naye. Hivyo wataweza kujitia kabisa katikashughuli za Injili.

k.8: Yesu aliwapanua mawazo yao kuhusu upana wa kazi yao ya kuieneza Injili.Alikaza kazi yao ni kumshuhudia Yeye, wamekuwa naye na kuona yotealiyofanya na kusikia yote aliyofundisha, hivyo wastahili kumshuhudia kwa

Page 9: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO671

usahihi, nao watapata nguvu ya kufanya hivyo. Neno la Kiyunani kwa neno"nguvu" lina maana 'la "baruti inayopasua miamba" (dynamite).Kisha Yesu aliinuliwa juu, wingu likampokea wasimwone kwa kimwili tena.Huenda hao wawili waliovaa nguo nyeupe ni malaika, maneno "mbona…”ni kama kemeo kwa wanafunzi kuendelea kutazama juu baada ya Yesukupokelewa na wingu. Hata hivyo walipewa ahadi njema sana ya kwamba Yesuatarudi kwa wazi na kwa kuonekana wakati wa mbeleni.

Kupaa kwa Yesu ni thibitisho la Yesu kuwa Mwana wa Mungu, na ya kuwa Babaamempokea na kumtawaza huko juu. Hawatahitaji kumtafuta hapa na pale, Yeyeyuko kwa Baba, wayaelekeze mawazo yao kule Aliko, wasimwaze kwa kimwili.Kama alivyowaambia Yoh. 16:7 yafae aondoke ili Roho aje. Vote ni tayari kwaRoho kushuka.

1: 12-26: Wanafunzi kumngojea Roho MtakatifuWanafunzi walirejea Yerusalemu kama Yesu alivyowaagiza, wakawa pamoja haliwakimngojea Roho Mtakatifu kushuka. Kwa muda huo wa siku kumi walimsifuMungu hekaluni na kuomba pamoja katika nyumba walipoishi. Luka 24:52Mdo.1:14: na kutafakari Maandiko. Bila shaka walikariri habari za Yesu. Ni akinanani waliokuwepo? Idadi yao ilikuwa kama watu mia moja na ishirini k.15. Vikundivinne vimetajwa - kundi la Mitume kila mmoja akitajwa kwa jina; halafu walewanawake walioandamana na Yesu, akina Mariamu Magdalene, Yoana, n.k.ndipo Mariamu mama yake ametajwa peke yake, kisha ndugu zake wa kimwiliambao mwanzoni hawakumwamini Yoh. 7:5 Mk. 6:3. Mama yake hatajwi tenabaada ya hapo, kwa hiyo picha ya mwisho tuliyo nayo ni ya yeye kumsubiri Rohokama Mwana wake alivyoagiza. Luka 24:52 walihudhuria hekalu na ibada zake.Luka asema walijaa furaha badala ya huzuni. Yesu alikuwa amefaulu kuwashikawakati wa mambo magumu.

k.15 Petro kama kiongozi akawashauri wamchague mmoja badala ya YudaIskariote, akiongozwa na Maandiko kufanya hivyo.

Maandiko yasema sababu ni kwamba Yuda alikuwa amekosa. Baadaye Yakoboalipouawa hakuna aliyewekwa badala yake. Mitume walikuwa watu wa pekeewala hakuna watu kuingia urithi wao wa kuwa mashahidi wa kuona.

Luka ameandika kwamba Yuda alikufa kwa kuanguka kwa kasi na tumbokupasuka - Mathayo alisema alijinyonga. Yaonekana kuwa alipojinyonga, kambaau mti ulivunjika, ndipo akaanguka. Pia Luka amesema Yuda alinunua konde naMathayo amesema ni wakuu hapo tena hakuna haja ya kufikiri habariinagongana - Kweli wakuu ndio waliolinunua ila walitumia fedha ambayo kwahaki ilikuwa ya Yuda. "konde la damu" liliitwa hivyo kwa sababu fedhazilizotumiwa zilikuwa kima cha damu ya Kristo maana ni kiasi kilichotolewa kwakumpata Yesu, pia twaweza kuwaza ni kima cha damu ya Yuda.

Page 10: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO672

Ni mtu wa aina gani aliyehitajika? Masharti yaliwekwa: awe ameandamana naotangu Yohana Mbatizaji kufanya kazi mpaka mwisho wa huduma ya Yesualipopaa, hasa awe amemwona Yesu yu hai baada ya Kufufuka Kwake, maanani lazima awe na uhakika Yesu yu hai. Kama ambavyo tumekwisha kuona kazimuhimu ya Mitume ni kutoa ushuhuda wa kweli wa matendo na mafundisho yaYesu. Walipata wawili waliotimiza masharti hayo, mmoja aliitwa Yusufu BarsabaYusto, na wa pili Mathiya. Walichaguaje kati ya hao wawili? Waliomba pamoja,kisha walipiga kura na kura ilimwangukia Mathiya. Waliamini kabisa Mungualitawala hiyo kura, si kura ya bahati nasibu.

Kwanza waliongozwa na Maandiko, ndipo walitumia akili zao na kufikiri kwambahuyo atakayechaguliwa kuwa badala ya Yuda lazima awe ametimiza masharti yakuwa mmoja aliyeandamana na Yesu tangu mwanzo na kuwa amemwona yu haibaada ya Kufufuka Kwake. Ndipo walitafuta wa kutimiza masharti hayo,wakapata wawili. Wakamwomba Mungu awaonyeshe ni yupi kati ya hao wawiliwakikiri ni Mungu anayefahamu mioyo ya wanadamu wote; mwishoni wakapigakura wakiamini ya kuwa Yesu aliyewachagua zamani zile atamchagua yuleanayetaka kuziba pengo lililopo. Inaonekana watu wote walishirikiana katikakura, wale 120

Kwa nini wawe 12? Waonekane kuwa katika mfuatano wa Israeli ya zamaniyenye mababa kumi na wawili; wao ni Israeli Mpya. Hatusikii walitumia njia hiyoya kura tena, walitegemea Roho kwa kuwaongoza katika kuchagua watu nakatika kuchagua mahali pa kwenda n.k.

Picha tuliyo nayo ni ya watu kufanya mambo kwa pamoja, Petro kama kiongozisi juu yao bali ni kiongozi kati yao.

2:1-13 Kushuka kwa Roho Mtakatifu:Si mwanzo wa Roho - Mungu huwa Baba na Mwana na Roho katika umilelewake. Wala si mwanzo wa Roho kufanya kazi duniani. Alikuwapo katika UumbajiMw.1:2 Mdo.7:51. Stefano aliwaambia Wayahudi kwamba historia yao yoteimekuwa ya kumpinga Roho.

Roho alishuka katika Sikukuu ya Pentekoste. Maana ya Pentekoste ni hamsini,na Wayahudi waliiadhimisha siku ya hamsini baada ya Sikukuu ya Pasaka. Iliitwa"Idi ya Majuma" Kut. 34:22 Kum.16:10 na Siku ya Malimbuko Hes. 28:26. KatikaPasaka walitikisa mganda wa shayiri na Pentekoste walitikisa mikate miwili yaunga mwembamba Lawi 23:15 ku. Baadaye waliingiza kumbukumbu la Toratikutolewa Mlima Sinai.

Katika Sikukuu hiyo wageni wengi wa nchi nyingi walijaa Yerusalemu, wakatiufaao sana kwa uenezi wa Injili. Lile watakalosikia litasambazwa kwa mbali.Litasababisha maulizo mengi, kwa sababu Yesu alipouawa na kufufuka ilikuwa

Page 11: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO673

wakati wa Pasaka, na Roho aliposhuka na kuleta mabadiliko makubwa katikawafuasi wake ataendeleza hali ya watu kuwaza-waza maana ya hayo yote.

2:1-4: Hao watu wapata mia na ishirini walikuwa wameishi pamoja katika sikukumi za kumngojea Roho. Wamemtii Bwana Yesu na kukaa Yerusalemu. Kimwiliwalikuwa pamoja na kiroho pia walidumu katika kumsifu Mungu na kumwomba.Wameahidiwa Roho hata hivyo walidumu katika kuomba. Kama walikuwa katikanyumba 2:2: 1:13: 2:46b: au katika chumba kimoja cha hekalu Lu.24:53Mdo.2:46a; hatujui.

Luka ametaja wakati halisi Roho aliposhuka. "ilipotimia Siku ya Pentekoste".Alikujaje? kwa ghafula, iwapo walikuwa wakimtazamia tukio lenyewe lilitokea"ghafula". Pia "kutoka mbinguni" yaani nje yao pasipo ishara yo yote kutangulia.Kwa kawaida upepo hutoka upande fulani si kutoka juu. Pia kwa kelele. Kwanzakilikuwepo kitu cha kusikia: "kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi" siupepo ila kama uvumi wa upepo. Sauti yake iliijaza nyumba. Pili kilikuwepo kitucha kuona: "kama ndimi za moto" zilizogawanyika na kumkalia kila mmoja. Tenasi ndimi za moto ila kama ndimi za moto. Kila mmoja alimpata Roho binafsi katikahali ya kuwa pamoja. Tatu kilikuwepo hali ya kusema: ndimi zao ziliwezeshwakutamka lugha zingine zisizo za kwao .. ,

. ,Kwa hiyo walisikia, waliona, walitamka - masikio, macho, na ulimi - ila ilikuwazaidi ya hayo yote: walijazwa Roho ndani yao, mioyo yao iliguswa, na daharimpya ya Roho ilikuwa imeanza. Twaweza kufananisha upepo kuwa dalili yanguvu mpya waliyo nayo, moto ni utakaso mpya wa ndani, na kusema kwa lughanyingine ishara ya Injili kuwa kwa walimwengu wote Kila mmoja alikuwa na ujuziwa binafsi ya Roho, kila mmoja alijua hakika Roho ameshuka.

Tendo hilo ni la historia, sawa na Kuja kwa Kristo na Kuishi Kwake, Kufa Kwake,Kufufuka Kwake na Kupaa Kwake, Kutoa Roho ni tendo la mwisho katikamfuatano huo: halitarudiwa.

2:5-13: Katika sehemu hiyo Luka ameeleza habari za wanafunzi kusema kwalugha nyingine. Waliokuwepo Yerusalemu walikuwa akina nani? kwanza wotekwa asili walikuwa Wayahudi "watu wa kila taifa chini ya mbingu" maana yakewatu wa sehemu zile zote zilizofahamika, maana ramani yao ya ulimwenguhaikuwa sawa na ya kwetu, haikujulikana kuna nchi ya Amerika n.k. Halafualianzia mashariki na kuja mpaka magharibi akiwataja watu mbalimbali.Waongofu ni wale walioigeukia dini ya Kiyahudi na kutahiriwa. Walivutwawaliposikia wanafunzi wakitamka habari za Kristo katika lugha zao, hali wakijuawametoka Galilaya na hawana uwezo wa kufahamu lugha hizo. Mungualionyesha nia yake ya kutaka watu wote kumwamini Kristo alipowawezeshawafuasi wake kusema kwa lugha zingine.

Page 12: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO674

Neno hilo liliwashangaza watu na kuvuta usikivu wao. Wachache walidhihaki nakusema wamelewa, ila ilikuwa mapema.Katika habari hiyo twaona laana ya Babeli Mw.11 imeondolewa maana katikaKristo watu wataelewana na kupendana na kuwa na umoja.

2: 14-41: Mahubiri ya kwanza ya Kikristo:Petro alichukua nafasi ya wengi kuwa wamekutanika. Alijibu swali lao "maanayake nini mambo hayo?". AIianza kwa kukataa mashtaka ya kuwa wamelewa,akionyesha kwamba ni saa tatu tu si saa ya watu kulewa. Ndipo akaendelea nakuthibitisha kwamba matukio hayo ni matimizo ya unabii wa Yoeli 2:32. "jambohilo ni lile lililonenwa" kwa hiyo katika sehemu ya kwanza ya hotuba yake alitoamaelezo ya tukio la Roho kushuka.

k.17: "siku za mwisho" zimefika katika Roho kushuka, tangu wakati huo tumokatika "siku za mwisho" nazo zitaendelea hadi atakaporudi Bwana Yesu. Yoeli2:28. "nitamwagia" Roho ametolewa kwa ukarimu mno, Mungu amemwaga; tenakwa watu wote, maana yake si kwa kila mtu potelea mbali ana hali gani moyoni,ila kwa kila aina ya watu, haidhuru ni wa kike au kiume, vijana au wazee, au wacheo gani. "watatabiri" "wataona maono" "wataota ndoto" kwa jumlawatamfahamu Mungu, kama Yeremia alivyosema katika habari za Agano JipyaYer.31:31-34. Ndiyo sababu Roho atatuwezesha kumshuhudia Kristo kwa kuwaametuwezesha humfahamu Kristo.

k.19-20: Mambo hayo yaweza kuelezwa kwamba hayo yatatokea katika kipindihicho tangu Yesu kuondoka hadi atakaporudi, kama giza lilivyotokea alipokuwamsalabani, pia yaweza kuwa lugha ya ki-picha kueleza matukio na mabadilikomakubwa yanayotokea mara kwa mara katika jamii ya watu na kwa siasa.Tukumbuke Petro alisema neno la Yoeli limetimia.

k.20. Kwa wakati huu ni siku za wokovu, siku za nafasi kwa watu kumpokeaBwana na Petro kwa mahubiri yake aliwaita watu kutubu na kumwamini Kristo nakubatizwa kwa Jina Lake. Yesu atakapotokea mara ya pili nafasi itafungwa,imebaki hukumu.

2:22-36. Katika sehemu ya pili ya mahubiri Petro alionyesha uhusiano kati yamatukio ya siku ile ya Pentekoste na Yesu. Wakitaka kufahamu vizuriwanapaswa kuelewa si neno la Yoeli tu bali habari za Kristo. Aliwaita tenawamsikilize (Iing. k.14 na k.22) alipoendelea na habari za Yesu wa Nazareti.Tukumbuke kwamba ni muda mfupi tangu Yesu alipofanya huduma yake natangu walipomwua na Mungu kumfufua ni siku 50 tu. Kwanza alitaja hudumayake: alikuwa mwanadamu kweli ambaye alithibitishwa na Mungu kwa njia yakufanya maajabu; maajabu ya aina tatu: "miujiza" iliyoonyesha nguvu za Mungu;"ajabu" zilizoshangaza watu; na "ishara" zilizomdhihirisha kuwa Yule aliyetumwana Mungu. Ni Mungu aliyefanya kazi ndani ya hayo. Wao wenyewe walimwonana kuziona.

Page 13: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO675

2:23: Kifo Chake: Petro alitaja kifo chake kuwa aliuawa, kwa upande mmoja niMungu (si Yuda) aliyemtia mikononi mwao, kwa sababu ilikuwa mapenzi yaMungu afe kwa ajili ya dhambi, ni mpango wake kwa wokovu wa wanadamu,mpango uliopangwa tangu awali. Ila kwa upande wa pili ilifanyika na watuwabaya waliojaa wivu, waliomtia mikononi mwa Warumi ili asulubishwe Kwa hiyoyote mawili ni kweli, mapenzi ya Mungu na uovu wa wanadamu. Yote mawili nisehemu mbili katika jambo hilo moja. Kuta Kwake si ajali, wala bahati mbaya,wala wazo la baadaye la Mungu alipoona watu wamemkataa Mwana wake, lahata kidogo. Lilitokea sawa na unabii wa Isaya 53 na kwa kulingana na mfano waMwana Kondoo wa Pasaka.

Iwapo Mungu alifahamu kwa ukamilifu yote yatakayompata Yesu siyo kusemawaliofanya wamepunguziwa hatia. Wao hawakuelewa kwamba ni mapenzi yaMungu. Hatia itaondolewa watakapobadili uamuzi wao juu ya Yesu kwakumpokea badala ya kumkataa, na walipewa nafasi ya kufanya hivyo kwa hotubaya Petro waliposikia na kuchomwa mioyoni mwao k.37.

Twaona mabadiliko makubwa katika Petro, miezi miwili kabla aliogopa kukirikuwa mwanafunzi wa Yesu mbele ya mwanamke, sasa amesimama imara nakwa ujasiri kuwaambia wale waliomsulibisha Yesu kwamba walifanya vibaya.

2:24-32: Kufufuka Kwake: Mungu aliupindua uamuzi wao kwa Kumfufua Yesukutoka kwa wafu. Baraza la mbinguni halikuunga mkono uamuzi wao wakumhukumu afe. Haikuwezekana mauti imshike Mkuu wa Uzima Mdo.3:15 Yoh.1:4; 5:26; 10:18.Alikuja kuvunja kazi za Shetani, mtawala wa mauti Ebr. 2:14; IYoh.3:8 Petro aliendelea kwa kutumia Zab.16:8-11 na kuonyesha kwambamaneno hayo hayakumhusu Daudi ambaye kaburi lake lilikuwa pale baliyalimhusu Yesu. Daudi alikuwa akitaja habari za Masihi atakayekuja baadayek.30-31 Kaburi la Daudi lilikuwa pale Yerusalemu, na watu wote waliaminiamezikwa humo, wala hakuna aliyedai amefufuka. Lakini kaburi la Yesulilikuwepo, ni tupu, na maiti ya Yesu haikuonekana, na watu walidai kuwawamemwona yu Hai, na hata Petro alipata ujasiri wa kuhubiri kutokana nakumwona hai.

Kuadhimishwa Kwake: 33-36: Bila shaka walikumbuka maneno ya Yesualipoapizwa na Kuhani Mkuu akamjibu "mtamwona Mwana wa Adamu ameketiupande wa kuume wa nguvu ... " Kutoka huko juu amemwaga kipawa cha RohoMtakatifu na matokeo yake yaonekana wazi mbele za macho yao. "mnachokionana kukisikia" yaani kuona wafuasi wa Kristo wakitoa ushuhuda wazi mbele zao.Uhakika wa Yesu kuwa ametawazwa juu ni Kushuka kwa Roho k.33 na k.36.Daudi hakufufuka wala kupanda mpaka mbinguni. Bila shaka walisikia wasiwasiwingi walipotambua kwamba wamemwua Masihi wao wa kweli.

Page 14: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO676

2:37-41: Waliposikia maelezo hayo watu walichomwa mioyoni mwao na walitakakujua wafanye nini. Walitambua wanayo hatia ya damu ya Masihi wao ambaokwa siku nyingi walikuwa na hamu ya kumpata. Wamemwua aliyetumwa naMungu, Mwana wake mpendwa. Petro aliwaambia kwamba, kwanza - watubu,wabadili kabisa uamuzi wao kuwa Yesu hakufaa, wamkubali kimoyo-moyo kuwaMasihi wao. Pili wabatizwe katika jina la Yesu Kristo. Kwa Wayahudi ilikuwavigumu kukubali ubatizo maana waiibatiza WaMataifa waliotaka kufuata dini yao,wenyewe walitahiriwa.

Lazima wajinyenyekeze kabisa ndipo itakuwa dhihiri kwamba wamempokea yulewaliyemkataa hapo mwanzoni.

Watakapofanya hayo, yaani kutubu na kubatizwa ndipo Mungu atawapa vipawaviwili. Atawaondolea dhambi zao na hasa ile ya kumkataa Masihi wa kweli. Piaatawapa Roho, kipawa ambacho si kwa Mitume tu, wala kwa wale 120 tu, walakwa Wayahudi tu ila ni kipawa kwa yeyote atakayeuitika wito wa kutubu nakumpokea Yesu. Wito wake na vipawa vyake vimefungamana.Petro aliendelea kuwahoji na kuwaonya, aliwasihi wajitenge na wenzao nakujiunga katika jamii mpya ya watu wa Mungu, wawe Israeli Mpya. Wengiwaliitika, idadi yao yapata elfu tatu, katika siku hiyo moja tu idadi ya mia na ishiriniiliongezeka sana.

2: 42-47 Jamii Mpya ya KikristoHao ndio chanzo cha sharika za Kikristo, hatusemi Kanisa, maana watu waMungu wamekuwapo tangu siku za mababu. Luka ametaja alama zake kuwakujifunza, kupendana, na kuabudu. Walijifunza kwa Mitume habari sahihi yaKristo jinsi alivyoishi, na kufanya, na kufundisha. Walishirikiana wao kwa waokama familia kama Yesu alivyokusudia. Yohana alisema kwamba ushirika waopia ni pamoja na Baba na Mwana I Yo. 1:3. Walimega mkate, walishiriki Chakulacha Bwana, na kusali pamoja.

k.43 Mitume walikuwa na mamlaka ya kuongoza mambo kwa kuwa walikuwamashahidi waliyoyaona matendo ya Yesu na kuyasikia mafundisho yake. Mungualithibitisha ushuhuda wao kwa kuwajalia kufanya miujiza. Watu walishikwa nauchaji wa Mungu wakitambua Kuwepo Kwake kwa njia ya Roho Mtakatifu. Watuwalikuwa tayari kutoa vitu vyao ili wasaidie wenzao walio na shida. Hawakuachakuhudhuria hekalu na ibada zake. Itakuwa vigumu kufikiri waliendelea kutoadhabihu za wanyama kwa kuwa Kristo ni dhabihu yao, ila walikwenda kusali.

Walishirikishana chakula kwa furaha, hawakulazimika kufanya. Watuwalipowaona walivutwa kujiunga nao na Bwana alifanya kazi mioyoni mwa watu.Hivyo Kanisa lilizidi kukua.

Page 15: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO677

3: 1-10 Kiwete kuponywaKatika 2:43 tuliambiwa kwamba Mitume walifanya maajabu mengi. Hapo Lukaamechagua na kutuelezea ajabu moja hasa kwa sababu lilimpa Petro nafasi yakuhubiri, pia ilisababisha wakuu kukasirika na kuwakamata Petro na Yohana nakuwatia ndani usiku.

k.1: Mitume waliendelea kuhudhuria hekaluni hasa kwa saa za maombi. Huyukiwete alikuwa mtu mzima wa zaidi ya miaka arobaini ambaye kamwehajatembea hata siku moja. Kwa desturi aliwekwa mahali pazuri pa kuombasadaka kwa wale waliokwenda kusali, bila shaka wengi walimfahamu tangu sikunyingi, wakijua hakika amekuwa kiwete wakati wote wa maisha. Pengine hataalimwona Bwana Yesu na bila shaka alikuwa amewahi kujua habari zake, hatahabari za Kuuawa Kwake na Kufufuka Kwake.

k.3: Alipowaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliwaomba sadaka kamakawaida. k.4. Petro aliitika kwa kumkazia macho na kuvuta usikivu wake kwakumwambia "tutazame sisi" naye akawatazama akitarajia kupewa kitu. HalafuPetro akamwambia kuwa "hana fedha za kumpa" hata hivyo anao msaadamkubwa - katika Jina la Yesu asimame na kutembea!! Kwa mara ya kwanzaaliinuka na kutembea hata kuruka, sisi twahitaji kujifunza kutembea, yeye maraaliweza, Kwa kutaja Jina la Yesu Kristo alielewa ni Yesu aliyemponya, si Petrowala Yohana bali ni Yesu, maana Yeye yu hai, aliyefanya alipokuwapo dunianiilikuwa chanzo tu - 1:1; angali akifanya kazi kwa njia ya watumishi wake. Mitumehawakuponya watu kwa jina lao.

Petro alimwagiza wazi "si mama, uende" akamnyoshea mkono kwakumtumainisha ndivyo itakavyokuwa. Mara mwili wake ulipata nguvu, akasimamana kwenda, akaingia hekaluni hali akirukaruka na kumsifu Mungu. Bila shakawatu walikumbushwa juu ya Bwana Yesu. Alimpa Mungu sifa si Petro na Yohana,hivyo aliponywa kimwili na kiroho. Kamwe hatakuwa na haja ya kuombaombafedha, na wale watu waliozoea kumwona pale hawatamwona tena katika hali ileya zamani, ataingia pamoja nao na kusali pamoja nao. (twaona Luka kamadaktari ameeleza hali ya kuponywa kwake kwa lugha ya ki- daktari, "nyayo zakena vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu".

3: 11-26 Hotuba ya PetroHabari hiyo iliwavuta watu wengi na Petro alichukua nafasi na kuwahubiri habariza Yesu.

k.12: Petro na Yohana wangeweza kujipatia heshima na sifa kwa tendo hilo ilawakakataa, wakataka sifa zote ziende kwa Bwana Yesu. Wahubiri wa zamaniwalikaza sana uwezo wa Yesu. Aliwaambia wazi na kwa mkazo kwamba ni Yesualiyemponya kiwete kwa kuwa Mungu amemtukuza Yesu kinyume cha walewalioona hakustahili kuwa Masihi wao. Katika hotuba zote za kwanza twaonajinsi Petro alivyosema juu ya Mungu kufanya na kulinganisha na

Page 16: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO678

walivyofanya. Mungu amemtukuza Yesu na kumpa mamlaka na heshima zote;wao walimkataa na kumwua. Baraza lao la Sanhedrin waliamua na afe; Barazala mbinguni liliamua kuupindua uamuzi wao na kumtukuza.

k.14: Walikana na kumkataa Nani? Petro amemwita "Mtakatifu" "Mwenye haki""Mkuu wa Uzima"; Walimchagua Baraba, mwuaji, aliyeuondoa uzima wa mtu, nakukataa aliye "Mwenye Uzima". "Mwenye haki" hata alipohukumiwa kosahalikuonekana, Pilato mara tatu alisema "sioni hatia".

k.16: Ndipo Petro alitilia mkazo tena juu ya Jina la Yesu na nguvu yake, si jambola ushirikino au la siri; ni ishara kwao ya kuwa Yesu alikuwa Masihi wao wa kweli,naye angali akitenda kazi zake, hawawezi kumzuia, iwapo wamedhaniwamemwondoa sivyo ilivyo, wamemwondoa kimwili, ila kiroho kwa njia ya Rohoangaliko kati yao. Hawawezi kukana ajabu hilo maana yule mtu yu mbele yao,wanamwona kwa macho yao.

k.17: Baada ya kuwakemea aliwasihi sana kwa upendo wabadili uamuzi wao,watubu na kumpokea Kristo, maana ilikuwa mapenzi ya Mungu auawe iliulimwengu ukombolewe. Kwa Kifo Chake wataweza kusamehewa hata dhambiya kumwua Masihi, wao kwa sababu huyo Kristo atakuja tena kuchukua walioWake Kwake

k.20. Aliwakumbusha hata Musa alitabiri habari za Kristo na ya kuwa' watuwapaswa kumsikiliza Kristo hata kuliko mambo ya Torati na ya Musa.Watafarijika watakapotafakari jinsi manabii walivyotabiri mateso ya Kristo. Siudhuru kwa wale waliofanya kusudi, ila wengi hawakuelewa vema. Sasa wapewanafasi ya kutengeneza hayo yote, wachukue nafasi hiyo, maana wasipotubu nakumwamini wataadhibiwa vibaya k.23.

Hotuba hiyo ilijaa sifa za Bwana Yesu, Petro aliwavuta watu wamtafakari Yesu,si kiwete, wala si Mitume, ila Yesu tu. Hasa alitaka kuwaleta kwenye toba la kwelila kumwamini Kristo ili wapate baraka zake, msamaha wa dhambi zao hasa ileya kumkataa Masihi, halafu waonje baraka za maburudiko yatakayofuata tobalao, kisha wamsubiri Yesu kutoka mbinguni. Kweli hotuba ilijaa Kristo.

4: 1-22: Petro na Yohana kukamatwa, kufungwa, kushtakiwa barazani,na kufunguliwa:Watu walizidi kuwasikiliza Mitume na wakuu walifadhaishwa kwa jinsiwalivyowafundisha na kuwahubiri habari za Yesu na ufufuo wa wafu. Wakuu haowalihusika na hekalu, makuhani na maakida pamoja na Masadukayo. Penginewaliogopa ghasia, pia Masadukayo hawakuamini neno la ufufuo, kisiasawaliridhiana na Warumi waliotawala nchi. Pia walikwazwa kuona ya kwambaakina Petro na Yohana walithubutu kufundisha watu hali hawakusoma

Page 17: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO679

katika shule za marabi. Zaidi jinsi walivyofaulu kuvuta watu wengi kukata shaurina kuamini na kujiunga nao. Bila shaka walikumbushwa sana Bwana YesuMwenyewe, walidhani kwa kumwua wamekomesha mambo, kumbe, siyo.Twasoma idadi kama 5000 waliamini, hatuna hakika kama ndani ya idadi hiyo niwale 3000 waliokata shauri Sikukuu ya Pentekoste, au ni zaidi ya wale, kwa vyovyote Kanisa lilikuwa likikua haraka.

k.5. Baraza Kuu la Taifa lililoitwa Sanhedrin walikutanika asubuhi. Ni wale walewaliomhukumu Yesu afe miezi michache iliyopita. Mbele yao ni wavuvi wawili waGalilaya wasiodai lo lote ila kuwa wafuasi wa Yesu ambao walikuwawamemwona hali yu hai baada ya Kufa na Kufufuka Kwake. Bila shaka walijaribukuwatisha na kuwafanya wajisikie vibaya. Kwanza waliwauliza juu ya uponyaji wakiwete k.7 "kwa nguvu gani na kwa jina la nani ninyi mmefanya haya"?" walisemakwa dharau kwanza kwa kutumia ninyi, halafu kupunguza uzuri wa tendo lauponyaji kwa kusema "haya".

k.8: Petro alijaliwa ujasiri mkubwa, miezi kadha iliyopita aliogopa maneno yamjakazi akamkana Yesu, sasa amejifunza kutokujitegemea bali kumtegemeaRoho Mtakatifu, akawajibu bila wasiwasi wo wote. Mara alirekebisha lughawaliyotumia kuhusu uponyaji wa kiwete alibadili "haya" kuwa "tendo jema".

k.9-10: Aliwaambia wazi kwamba ni Yesu Kristo aliyemponya' kiwete - yulewaliyemwua - na Mungu akamfufua (tumeona Petro apenda sana kutaja jinsiwanadamu walivyofanya na itikio la Mungu kwa waliyotenda.) Inaonekana kiwetealiyeponywa alikuwa pale, kwa hiyo hawakuweza kukana tendo lenyewe lauponyaji, ila walijitahidi kulipuuzia.

k.11: Ndipo Petro aliwashambulia na Maandiko waliyoyafahamu sana, ni sehemualiyotumia Bwana Yesu juma la mwisho walipokuwa wakijadiliana nayeMath.21:42. Hao ni wajenzi katika Nyumba ya Israeli, walipaswa kukubali LileJiwe kuu la Pembeni, yaani Masihi wao, kumbe, walimtupa kando kama jiwelisilofaa, hata hivyo Mungu hakukubaliana na uamuzi wao, Yeye amemchukuana kumweka penye heshima kuu, mkono wake wa kuume. Wakristo walipendasana Maandiko hayo na waandishi wa Agano Jipya waliyatumia I Petro 2:6.(Zab:118:22)

k.12: Petro alisema kwa mamlaka juu ya wokovu kwamba hakuna wokovu katikamwingine awaye yote, mtu hawezi kumwepa Yesu akitaka kuokolewa, poteleambali ametoka wapi katika dunia. Kwa hiyo Petro hakuridhika kwakumzungumzia yule kiwete tu aliyeponywa kimwili bali aliwatazamisha kwauponyaji wa kiroho wa kuokolewa na dhambi, ambao hasa ni shabaha ya Yesu

4:13-22. "walipouona ujasiri wa Petro na Yohana" kumbe adui zao walitoaushuhuda juu ya uimara na uthabiti wa Mitume waliposimama kuhukumiwabarazani. Walifahamu kuwa hawakusoma katika shule za marabi, hata hivyo

Page 18: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO680

waliweza kuyatumia Maandiko, na zaidi walitambua "walikuwa pamoja na Yesu"hali yao yote ilifanana na Bwana Yesu Mwenyewe. Yesu alipokuwa naoaliwazoeza huduma na kuvumiliana nao walipokuwa wazito wa kujifunza hivyoakafaulu kuwaambukiza tabia zake na uthabiti wake. Ni kama uhakikishio waKufufuka Kwake, kwa kuwa hali yao ni tofauti na hapo nyuma, pili wasingaliwezakuwa,:imara kwa kiasi hicho kama walikuwa hawajamwona Yesu yu hai na yakuwa ni Yeye aliyewatuma.

Hata na sisi uhakika wetu utatokana na kushirikiana na Yesu ki-binafsi na kiroho.

k.14: Walishindwa kufanya lo lote juu ya Petro na Yohana, kwa sababu kiwetealikuwapo na Mitume licha ya kuwaogopa walithubutu kuwashambulia.

k.15 ku. Wafanyaje? Basi waliamua kuwatisha kwa kuwakataza wasiseme nawatu habari za Yesu. Neno lililowasumbua ni Jina la Yesu, si uponyaji wa kiwetepeke yake. Petro akajibu kwa kuwaambia wazi hawataweza kushika agizo lao lakunyamaza kwa sababu mambo wanayosema ni yale waliyoyaona na kuyasikiaHawakuwapiga kwa sababu waliogopa watu.

4:23-31: Kuwapasha wenzao habari hizo, kumwomba Mungu kwapamoja, na kupewa nguvu mpya ya Roho:

Walipoondoka barazani walikwenda kwa jamii ya waamini na kutoa ripoti yamambo waliyopata, ndipo wote kwa moyo mmoja walimwomba Mungu.Walitumia neno "Mola" kwa Mungu, neno la maana ya "Mtawala" kabisa, ndipowakataja uwezo wake katika uumbaji. Pia walitumia maneno ya Zaburi 2yanayoonyesha upuzi wa jitahada za wanadamu katika kumpinga Mungu, kwakuwa Mungu hakosi kuwa mshindi mwishowe. Kwa hiyo twaona msingi waoimara ni Maandiko. Wanadamu wakipenda wasipende, wakijua wasijue, hutimizasi kuzuia mapenzi ya Mungu, kama ilivyokuwa walipompinga na kumwua YesuKristo.

k.29: Hawakuwatakia adui zao mabaya - waliomba ujasiri wa kuendeleakutangaza habari za Kristo na Mungu kuthibitishia neno lao kwa kuwajaliakufanya maajabu kama uponyaji ili watu wasaidiwe kuamini katikati ya upinzaniuliopo.

k.31: Mungu hakukawia kuyajibu maombi yao, walijazwa Roho hata palewalipokusanyika palitikiswa, wakanena Neno la Mungu kwa ujasiri. Kusudi laMungu ni Injili ihubiriwe na watu waokolewe.

4:32-37: Jamii mpya ya Kikristo:Hii ni mara ya pili kupewa picha ya maisha ya waamini, jinsi walivyofanya katikamaisha ya kila siku. Alama moja dhahiri ni walikuwa na umoja mzuri sana wa

Page 19: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO681

kushirikishana vitu walivyo navyo ili asiwepo yeyote aliyekosa mahitaji yake yalazima. Walifanya kwa hiari na kwa furaha. Walitambua Mitume ni viongozi waona wahubiri wa Neno kwa sababu hao ndio waliokuwa pamoja na Yesu, wenyekumshuhudia kwa kweli. Neno kuu la ujumbe wao lilikuwa Kufufuka Kwa BwanaYesu. "neema nyingi ilikuwa juu ya wote" Mungu aliwajalia baraka nyingi isharaya kuwa alipendezwa nao. Hasa walitoa ushuhuda mkali kwa maana shida yawengi ni kujipenda na kupenda mali, hao kwa kupendana na kutoa maliwalionyesha maisha tofauti, ushuhuda wa neema ya Mungu maishani mwao.

k.36: Ndipo Luka alimtaja Barnaba mtu wa Kipro, Myahudi, na Mlawi. Yeye aliuzashamba na kuleta fedha yake kwa Mitume. Si kwamba yeye peke yake ndiyealiyefanya tendo la aina hiyo la, ila baadaye ataonekana zaidi katika Kanisa naatajiunga na Paulo katika Safari kubwa ya kwanza ya kueneza Injili.Tabia yake ilikuwa "kutia nguvu na faraja"; baada ya kutoa mali yake alitoamaisha yake kwa kumtumikia Kristo. Bila shaka hali njema ya waamini ilisaidiakuwavuta watu kumpokea Kristo.

5:1-11: Unafiki wa Anania na Safira:Iwapo picha tuliyo nayo ya wakristo wa kwanza ni picha nzuri sana tusifikirikwamba hawakuwa na matatizo wala ya kuwa shida hazikutokea kati yao. Nivema tuone ya kwamba Luka alikuwa mwaminifu na wa kweli akituelezea memana mabaya. Katika sura hiyo tunayo habari ya unafiki wa waamini wawili pamojana maelezo jinsi Kanisa na Petro kama kiongozi alivyokabili na kulitatua tatizohilo Wahusika ni Anania na Safira, mume na mke. Walikuwa na mali fulaniwaliyoamua kuiuza, kisha kuleta thamani yake kwa Kanisa, ila ubaya waowalikuwa wanafiki. Hawakuleta thamani yote, hii si vibaya, kama Petroalivyoonyesha alipowaambia kwamba ilikuwa juu yao kama kuiuza au siyo, nahata walipoiuza walikuwa na hiari ya kuamua walete kiasi gani, chote au sehemutu. Ubaya wao ulikuwa kuleta sehemu na kutosema wazi ni sehemu tu,walijifanya kama wameleta yote. Walitaka kuonekana kuwa watu wazuri hukumioyoni mwao hawawi wa kweli.

Tena wote wawili walikuwa wamepatana pamoja kufanya hivi. Si jambo laghafula, bali walipanga kwa mpango maalum. Kwa upande mmoja twawezakuwahurumia, kwa hali zilizokuwepo bila shaka haikuwa rahisi kuwa na mali nakuishikilia. lIa pia kwa jinsi Roho alivyokuwa akifanya kazi bila shaka walikuwawameinyamazisha sauti yake mioyoni mwao na kupatwa na mioyo migumu. Nivigumu kufikiri kwa nini mmoja hakuweza kumshauri mwenzake.

k.3: Petro alijuaje habari hiyo? yawezekana alifunuliwa na Roho au penginealikuwa amefanya utafiti kuhusu mali hiyo. lIa hakusita kumwuliza Anania usokwa uso juu ya unafiki wake, hakumwuliza maswali kuhusu mali na uuzaji waketu. Alimshtaki kuwa amemwambia Roho uongo! amemwambiaje Roho uongo?kwa sababu amesema uongo kwa Petro na waamini ambao Roho yu kati yao.

Page 20: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO682

k.4: Maswali ya Petro yaonyesha wazi kabisa kwamba waamini walikuwa na hiarikabisa kuhusu mali yao, ila hawakuwa na hiari ya kutumia uongo. Shetani ni babawa uongo Mwa.3:1-5 Yoh.8:44-45: wamemruhusu aingie mioyoni mwao nakupandikiza uongo, Petro alifahamu ni Shetani aliyewaongoza kusema uongo.Anania aliposikiliza Petro akitoboa wazi dhambi yao akaanguka, akafa, ni kamaalipatwa na mstuko wa moyo, hofu kuu ilimshika, akafa. Si Petro aliyemwua, walasi Petro aliyetoa uamuzi afe, la, yeye mwenyewe alikufa alipojisikia kushtakiwarohoni mwake.

Safira mkewe hakuwa na habari za tukio hilo, bila shaka alikuja katika hali yafuraha akijua bwana wake amemletea Petro sehemu ya ile mali waliyouza,asitambue lo lote.

Petro akamwuliza swali kuhusu mali ili ahakikishe kama yeye amejiunga nabwana wake katika udanganyifu huo. Alipomjibu Petro alijua hakika wamepatanawao kwa wao na yeye pia amestahili kupatwa na hukumu ya Mungu. Mama nayeakaanguka akafa, wakamzika pamoja na mumewe.

Kwa kuulizwa maswali wangaliweza kujihoji na kuungama dhambi yao nakusamehewa. Pengine twafikiri Petro aliyemkana Bwana wake asingalikuwamkali kiasi hicho, lakini Petro alitambua hatari kubwa kwa Kanisa kama watuwatawadanganya wenzao bila kutambulikana. Unafiki huo wafanana na mduduanayekula mmea kwa ndani, kwa siri, mwishowe huleta uharibifu mkubwa wammea kufa. Tukumbuke Kanisa wakati huo lilikuwa kama mmea mmoja tu katikaulimwengu. Ni changa, waamini ni wachache, Injili haijahubiriwa penginepo.Mmea huo ukiliwa na mdudu wa ndani wa unafiki, kweli ni hatari kabisa, kulikomateso ya Kanisa yaliyo dhahiri. Kwa hiyo Shetani amejaribu kutikisa Kanisa kwamateso ya nje na kwa dhambi ya siri ya ndani. Mungu alililinda Kanisa katikauchanga wake.

Pia ni vema tukumbuke kwamba kama wangalifaulu kumdanganya Petro naviongozi wengine, ingalikuwa rahisi kwa watu kuwadharau na kutokuwajali, nakazi zao zingalikosa nguvu.Iwapo hao watu walikufa kimwili Je! kiroho itakuwaje? Waliondoshwa kwa nguvuwasiwaambukize wengine, Je! watakuwa wamepotea kabisa? I Tim.1:20: IKor:5:5.

5: 12-16: Wagonjwa wengi kuponywa:Kufuatana na tukio hilo Kanisa lilifanikiwa: Mitume walijaliwa kufanya maajabu nakundi zima la waamini walikuwa na umoja na kusimama imara. Mambo mawiliyalitokea: wasiokuwa na nia njema waliogopa kabisa kujiunga na waamini; hatahivyo watu walizidi kuamini wanaume na wanawake. Hawakubagua kati yawanaume na wanawake Katika ulimwengu wa siku zile wanawake hawakuwa nasauti wala kuthaminiwa. Katika Kanisa walikaribishwa vizuri.

Page 21: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO683

Ilikuwa dhahiri Mungu yu kati yao. Habari zilianza kwenda nje ya Yerusalemukwa miji kandokando yake, na watu walileta wagonjwa na wenye pepo,wakaponywa wote. Ukumbusho wa huduma ya Bwana Yesu.

5:17-33: Mitume kufungwa, malaika kuwatoa, kuletwa barazani:Wakuu walijikuta wako mahali pagumu, watu walizidi kuongoka na idadi yawaamini ilikua zaidi na zaidi mpaka Yerusalemu wote umejaa habari za Kristo nahabari zao. Mitume walikuwa hodari, hawakujali hata kidogo agizo lao lakunyamaza. Pia matendo ya ajabu yasiyokanushwa yalifanyika. Ni vigumuwakuu kuwaacha waendelee maana watu watahesabu wameshindwa. Kwa hiyowafanyaje? Waliamua kufunga Mitume wote gerezani halafu kuwaleta barazanina kuwahukumu.

Mungu aliwatoa gerezani kwa ajabu kwa kutuma malaika wake. Huyo malaikaaliwaambia waende hekaluni kama kawaida na kutangaza habari za "Uzima huu"upatikanao katika Kristo. Mitume wakamtii, hata twasoma alfajiri wamekwishakufika na kuanza kufundisha. Hawakujihurumia, wala hawakutafuta kupumzikakidogo, ila, iwapo usiku wamefungwa ndani, alfajiri wamesimama hekaluni nakufundisha; wamejitoa kweli kweli.

Wakuu walidhani kwamba bado 'wangalimo gerezani, wakaitisha baraza lao,ndipo wakatuma watu kuwaleta Mitume. Walipofika gerezani, milango ingaliimefungwa, lakini walipoifungua wakakuta Mitume hawamo!! hata walinzihawana habari kwamba wafungwa wao hawamo; walihofu sana. Kisha mtu akajaakawaambia kwamba Mitume wamo hekaluni wakifundisha watu.

Wakaletwa kwa upole, hawakutaka ghasia, kwa kuwa watu walikuwa upande waMitume, kama wangalitumia nguvu watu wangaliwapiga.

Kuhani Mkuu ni yule aliyemhukumu Bwana Yesu. Aliwakumbusha agizowalilopewa juu ya kunyamaza, pia alishuhudia mafanikio yao "mmeijazaYerusalemu mafundisho yenu" halafu alitamka neno kuhusu "damu ya Yesu""mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu" (ling. Math.27:25 Je! walianzakuhofu kwamba walimwua Masihi wao?) Petro na Mitume wengine waliwajibukwa kusema wazi kwamba hawataweza kunyamaza kwa sababu ni Mungualiyewaamuru kutangaza habari njema kwa hiyo imewapasa kumtii Mungu kulikohao wakuu. Petro aliendelea kwa kupambanisha alivyofanya Mungu na waowalivyofanya - wao walimwua Yesu, na Mungu amemfufua kutoka kwa wafu; tenaMungu amemtukuza na kumweka kuwa Mkuu na Mwokozi, kusudi Israeli wapatetoba na msamaha. Hawana haja ya kumhofu ikiwa watabadili uamuzi wao nabadala ya kuendelea kumkataa, watubu na kumwamini. Mitume walitia sahihi yauhakika wao, maana walikuwa mashahidi waliomwona Kristo yu hai baada yaKufa na kutumwa naye.

Page 22: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO684

k.33: Kufungu cha ajabu, walichomwa mioyo yao, dhamiri zao ziliwashuhudiaukweli wa yale yaliyosemwa na Mitume, na tukumbuke Mitume wametokagerezani kwa ajabu, milango ilibaki imefungwa na walinzi wamo wakilinda, daliliya Mungu kuwa upande wa Mitume na kinyume chao, hata hivyo, hawawi tayarikutubu, walitaka kuwaua.

Mitume walikuwa wametoa ushuhuda mkali sana kwa kurudi hekaluni,hawakutafuta kujisalimisha kwa kunyamaza kwa muda. Kweli watu waliwezakutambua wametumwa na Mungu na nia yao yote imekazwa kumtii Mungu.Walionja nguvu za Mungu na upendo wake, baraka na mateso yakiandamanapamoja.

5: 34-42: Shauri la Gamalieli, Mitume kupigwa na kufunguliwaGamalieli alikuwa mmoja wa Baraza, Farisayo, na mwalimu wa torati,aliyeheshimiwa na watu. Paulo alifundishwa naye Mdo.22:3. Labda alikuwaamemsikia Yesu au amesikia habari zake; labda Nikodemo na Yusufu waArimathaya wamemwelezea mengine, hatujui. Alikuwa mtu wa busaraasiyechukuliwa moja kwa moja kwa wivu au chuki bila kuchunguza nenolenyewe. Alishauri wenzake katika baraza wajihadharini na jinsiwatakavyowatendea Mitume. Aliwakumbusha habari za wengine katika historiayao walioinuka na kudai kuwa Masihi" na jinsi baada ya muda hao walitowekapamoja na wafuasi wao.

k.38b: Ndipo alisema neno la maana sana, kama imani hiyo mpya ina asili katikawanadamu itatoweka kama zile za hapo nyuma, ila kama imetaka kwa Mungu,potelea mbali wafanye nini hawataweza kufaulu na kuikomesha.

k.40: Baraza lilikubali mashauri ya Gamalieli, ila kabla ya kuwaachilia Mitumewakawapiga na kuwaamuru tena wasinene katika Jina la Yesu.

Mitume walitoka kwa furaha kubwa, walihesabu ni heshima kubwa kuwawamepigwa kwa ajili ya Jina la Yesu. Hawakujali agizo la kunyamaza, wakazidikutangaza habari za Yesu, pale hekaluni, na manyumbani mwao. Math.5:11-12;10: 17-20; 24 ku. Hawakujihurumia, hawakuwachukia adui wala kuwalipizakisasi; walijua hakika wanakanyaga nyayo za Bwana Yesu na ni dhahiri niwafuasi wake wa kweli.

6: 1-7: Watumishi saba kuwekwa:Kutokana na sehemu hii twaona Kanisa lilikuwa na mpango wa kuwasaidiawajane, kwa kuwapatia mlo wa kila siku. lia shida ilitokea katika huduma hiyo,wengine walinung'unika kwamba waliachwa. Walikuwepo aina mbili za watu,Wayahudi halisi waliotumia lugha ya Kiebrania na Wayahudi waliotumia lugha yaKiyunani, huenda walizaliwa katika nchi zingine wakitoka katika Wayahudiwaliotawanyika. Kwa hiyo kuna namna ya ubaguzi, wote ni Wayahudi, ila si wotewaliozaliwa Palestina au waliotumia lugha ya asili.

Page 23: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO685

Hatuambiwi wazi kwamba mambo hayo yalikuwa kweli au siyo. Tujualo nikwamba Kanisa lilichukua hatua za kutengeneza kabla ya shida kuzidi. k.2:Mitume waliitisha jamii ya waamini na kuwashirikisha habari hiyo nakuwaangoza jinsi ya kufanya. Hawakujichukulia wenyewe kuamua kwa nguvuila waliwapa mwongozo. Wao wenyewe wataendelea na kazi maalum yakutangaza Neno la Mungu, maana hao ndio mashahidi.

Shauri lao lilikuwa nini? Kwanza wachague watu saba wenye sifazitakazowasaidia kufanya vizuri - watu wema, watu wa hekima; na waliojaa RohoMtakatifu. Kazi hiyo ni ya "mipango kuhusu huduma ya mezani na chakula" hatahivyo wapaswa kuwa watu waliojaa Roho. Waamini wote waliona shauri hilo nijema wakapatana kuchagua wale saba waliotakiwa.

Walichaguliwa na watu si Mitume. Walipokwisha kuwachagua wakawaleta mbeleya Mitume waliowaweka rasmi kwa kazi kwa kuwaombea na kuwawekea mikono.Tukitazama majina yaonekana waliochaguliwa walitoka kwa upande wa walewalionung'unika.

Sifa zilizotakiwa ziliwasaidia watu kuwapokea na kuwaamini. Katika habari hiyotunao mfano mzuri wa kufuatwa katika kuweka watumishi katika Kanisa, watuwenye sifa nzuri, na watu wenye kujaa Roho ambao wataongozwa na Rohohaidhuru kazi zao ni za kiroho hasa au za ki-utendaji.

Tumezoea kuwaita hao saba "mashemasi" ila twaona kwamba halikuwepo darajala "ushemasi" ndipo watu walichaguliwa kuliingia, bali hasa mkazo ni ile kaziiliyotakiwa kufanywa.

k.7. Luka ametuambia kwamba Kanisa lilizidi kukua pale Yerusalemu hatamakuhani wengi waliongoka kuwa Wakristo. Likipingwa lasimama imara, likipatashida litaitengeneza, ndiyo sababu lilizidi kukua. Ni vigumu kufikiri kwambaviongozi wake akina Petro na wenzake ni wale waliotembea na Bwana Yesuwakiwa na matatizo mbalimbali na wazito kutambua mambo ya kiroho na Yesukuwa Mtumishi Ateswaye, sasa wameelewa kabisa kabisa.

6: 8-15: Stefano kushtakiwa:Stefano alikuwa mmojawapo wa wale saba. k.8. Alifanya maajabu na ishara,alihubiri kwa ujasiri katika masinagogi kiasi cha watu kujadiliana naye kwa ukali;nao hawakuweza kumshinda kwa sababu ya hekima yake na kwa kuwa RohoMtakatifu alikuwa pamoja naye. Bila shaka msingi wa yote aliyosema ulikuwaMaandiko. Kisha wakaona hawana la kufanya ila kuwashawishi baadhi yaokuleta mashtaka juu yake na kumpeleka barazani. Kama walivyofanyawalipomhukumu Bwana Yesu walitafuta mashahidi waliotumia uongo wakigeuzaalivyokuwa akisema ili ionekane kama amemkufuru Musa na Torati na Hekalu.

Page 24: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO686

Alikuwa akihubiri nini hasa? Kweli hatujui kikamilifu, ila kwa mashtaka yaotwaelekezwa kufikiri kwamba alilenga kufafanua mambo matatu kutokana na kaziya Yesu.

Kwanza Yesu ametoa dhabihu kamili itoshayo kuondoa dhambi za walimwenguwote, hivyo hamna haja tena ya dhabihu za wanyama kutolewa hekaluni. VilevileYesu kama Kuhani Mkuu ameleta Mungu kwa watu na watu kwa Mungu kamampatanishi na mwombezi hivyo hamna haja ya Makuhani Wakuu na Makuhani.Mwili wake ni "jengo takatifu" hamna haja tena ya jengo la hekalu. Jengo ni watuwake, amewakusanya Kwake Ef.1:22 I Pe.2:5 Math.12:6.

Kuhusu Musa na Torati: Stefano alitambua Torati ilikuwa mpango wa mudakatika matayarisho ya kumleta Kristo duniani. Sasa Kristo ameishafika na kuletaMwongozo mpya na njia mpya ya kupata Haki kwa imani. Hivyo Torati imekwishakazi yake.

Hakuilaumu wala kumlaumu Musa aliyeileta wala hakusema haikutoka kwaMungu la! ila alijitahidi kuonyesha mahali pake na sasa mwisho wake katika kuwanjia ya kupata haki.

Kuhusu taifa teule: Wayahudi waliteuliwa kweli, na shabaha ya kuteuliwa kwaoilikuwa kutayarisha njia ya Kuja kwa Masihi. Kwa mipango na taratibu mbalimbali,kama Torati, na ibada, na kwa kushikilia kwa nguvu kuwa kuna Mungu Mmoja tu,Mwumbaji wa yote, na kwa kukaza Utakatifu na Haki yake walikuwa wamewekamsingi imara ili Kristo atakapodhihirika ataeleweka na kuelezwa kwa msingiuliokwisha kuwekwa tayari. Wao walibadili kusudi la kuteuliwa kwao, wakajionakarna wamependelewa na Mungu kwa hiyo Mungu hana haja ya wengine,kumbewamechaguliwa ili kwa njia yao mataifa yote yabarikiwe.

Mw. 12:3. Wakristo watarithi ahadi hizo nao watawekwa badala yao kupelekaInjili kati ya mataifa yote. Wakristo ni "taifa teule" "jamii mpya ya watu wa Mungu"I Pet.22:9. Yawezekana Stefano alikuwa wa kwanza-kwanza kutambua kiini chakazi za Kristo na kufahamu kwamba Wakristo wapaswa kuachana na desturi zaKiyahudi kusudi wafungue njia wazi kwa WaMataifa. Twajua waliomsikia Stefanowalichukizwa na mahubiri yake, waliyahesabu kuwa ya hatari kabisa, wakatafutakumkomesha.

7: 1-53: Utetezi wa Stefano:Alipoletwa mbele ya Kuhani Mkuu akapewa nafasi ya kujitetea. Kwa kupitia katikahistoria yao na kwa kuwataja watu mashuhuri aliwafafanulia Maandiko naTumaini lao la kupata Masihi na kuwaonyesha kuwa Yesu Kristo ni Masihiwaliyemtazamia na matimizo ya ahadi zote za Agano la Kale.

Page 25: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO687

Alianza na habari za Ibrahimu, baba wa taifa. Aliitwa alipokuwa angaliko katikanchi ya ki-pagani hali akiabudu miungu, dalili ya kuwa Mungu hafungwi katikamahali fulani. Iwapo aliahidiwa nchi ya kukaa humo, hakuwa na sehemu yo yotekama mali yake, tena aliishi katika mahema na kuhamahama humo. Na baadayake wazao wake waliishi Misri karibu miaka mia nne. Dalili tena ya Mungu kuwapamoja na watu wake potelea mbali wakiwa katika nchi ya ahadi au siyo. Mahalipatakatifu ni alipo Mungu si mahali fulani hasa, na watu wake ni wale wafanyaomapenzi ya Mungu haidhuru wanaishi wapi.

Baada ya kuzungumzia mambo ya Ibrahimu alisema juu ya Yusufu 7:9-10.Alionyesha kwamba waliopinga mapenzi ya Mungu walikuwa nduguze Yusufu,hata hivyo Mungu alitawala mambo hayo yote akawa pamoja na Yusufu hukoMisri, na katika nchi hiyo ya kigeni Yusufu alionja baraka za Mungu na ya kuwaMungu alikuwa pamoja naye. Hata WaMataifa walimtendea mema na kumwekakuwa wa pili wa Farao, ishara ya WaMataifa kumpokea Kristo baadaye. Mfanowa Kristo aliyekataliwa na taifa lake, hata hivyo Mungu amemweka mkono wakuume kwake.

Ndugu wa Yusufu walimtambua walipomjia kwa mara ya pili, Wayahudi naowatamtambua Kristo atakaporudi mara ya pili. Haifuati kwamba kukataliwa nandugu zake ni kukataliwa na Mungu pia, la. Yusufu aliyekataliwa na nduguzealikuwa njia na sababu ya wokovu wao wakati wa njaa. Yesu Kristo aliyekataliwandiye njia na sababu ya wokovu wa kiroho.

Ndipo alizungumza habari za Musa ambaye chini ya Mungu alitoa ndugu zakewatoke utumwani mwa Misri. Musa aliokolewa na hasira ya Farao alipozaliwa,vilevile Yesu aliokolewa na hasira ya Herode alipozaliwa. Alielimishwa naWamisri na kuwa hodari, matayarisho ya kuwa kiongozi wa watu wake.

Alipojaribu kuwasaidia watu wake waliokuwa watumwa wakamkataa, ilimbidiakimbilie jangwani na kuishi huko kwa miaka 40, matayarisho tena kwa wakatiatakapowaongoza watu wake kuishi humo wakiwa njiani kurudi Kanaani k.35,39.

Aliyekataliwa na wanadamu aliwekwa na Mungu; sawa na Kristo. Musa piaalisema kwamba Mungu atawainulia nabii kama yeye na itawapasa kumsikiayeye k.37 Kum.18:15,18.

Kwa kusema mambo kama hayo Stefano hakuwa na dharau yo yote kwamashuhuri hao ila alitaka kuwalazimisha wasikilizaji wake watambue kwambaMungu hafungwi katika nchi fulani au katika jengo fulani kama hekalu. Alikuwana Abramu na kumwita akiwa Uru wa Wakaldayo, alikuwa na Yusufu alipouzwakwa Wamidiani na kupelekwa Misri, alikuwa na Musa alipokuwa jangwani,alikuwa na Waisraeli jangwani akiwa na Hema yake kulingana na wao kuishikatika mahema yao. Kwa hiyo uzuri wa jengo si kitu.

Page 26: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO688

k.48-50. Mara nyingi wale wenye heshima katika historia yao hawakuheshimiwawakati walipoishi, wakakataliwa na kupingwa.

k.51-53 Kwa huzuni na kwa masikitiko makubwa Stefano alisema hayo, kishaakamaliza kwa kutoboa wazi hali yao, asifiche jinsi alivyowaza juu yao. Kwaujasiri mkubwa alisema "wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio,sikuzote mnampinga Roho Mtakatifu, kama baba zenu walivyofanya, na ninyivivyo hivyo" maneno makali sana, lakini ya kweli. Manabii waliteswa na baba zao,Kristo naye amesulibishwa nao, na wataendelea kuwatesa waliotumwa naMungu. Ni watu wasiofundishika, wasiojifunza neno lolote kutokana na historiayao. Wanaposhuhudiwa kwamba Kristo amefufuka katika wafu hawawi tayarikupokea ushuhuda huo na kutubu. Kweli wachache wameitika wito wa Petro nawenzake, lakini taifa kwa jumla haliwi tayari kubadili uamuzi wake juu ya Kristo.

7: 54-60: Kifo cha Stefano:Viongozi hawakuweza kuvumilia mashtaka hayo, wakamkasirikia mno Stefanowakamsagia meno tayari kumwua. Stefano mwenyewe alikuwa imara kabisa,akainua macho yake mbinguni hali akijua mwisho wake umefika. Aliona utukufuwa Mungu na Yesu hali amesimama tayari kumpokea. Yesu ameketi mkono wakuume wa Mungu, ishara ya kuwa kazi yake imekwisha, imekubalika na Mungu,hamna zaidi ya kufanyiwa kwa wokovu wa wanadamu. lIa Stefano alimwona haliamesimama ishara ya kuwa yu tayari kumpokea mtumishi wake mwaminifu. Walewaliosikia ushuhuda huo wakakasirika zaidi sana, wakaziba masikio,wakamburuta nje ya mji na kumpiga kwa mawe bila kusema kosa lake ni nini.Alipokuwa akipigwa mawe alimwomba Bwana Yesu apokee roho yake, bilashaka alikumbuka jinsi Yesu alivyomwomba Baba yake msalabani, piaaliwaombea wauaji wake msamaha kwa tendo hilo kama Yesu alivyofanyawalipompigilia misumari. Kisha akafa. Ni mtu aliyekolea kabisa tabia za BwanaYesu, ujasiri wa kutoa ushuhuda wa kweli, upendo wa kuomba msamaha kwaadui zake, na imani ya kujikabidhi kwa Baba yake. Njia ni wazi ya kumwendeaMungu kwa sababu Yesu yu mkono wake wa kuume, mwombezi wetu namdhamini wa Agano Jipya. Tena tunayo picha ya mapinduzi, baraza la dunianilimemhesabu Stefano hastahili kuishi, wa mbinguni wako tayari kumpokea kwashangwe'.

k.58: Luka ametaja habari za kijana mmoja aliyeitwa Sauli aliyekuwepo Stefanoalipouawa hata alikuwa mtunzaji wa nguo za wale waliovua mavazi ili wampigeStefano kwelikweli. Baadaye Luka atatuambia mengi kumhusu huyo Sauli.Luka anatuelezea yale mambo yaliyosababisha Injili kuenea na anatutayarishakwa wakati Injili itakapohubiriwa kwa Wamataifa. Stefano alikuwa mmojawapoaliyetambua kwa ndani jinsi Kanisa litakavyopaswa kuachana na dini yaKiyahudi, ni mtheologia aliyefunuliwa na Roho kutoboa mambo hayo.

Page 27: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO689

8: 1-3: Sauli kuwatesa Wakristo, nao wakatawanyika:Siku ile ile aliyouawa Stefano Sauli alianza kuwatesa wakristo kwa vikali.Hakuwahurumia, alikwenda nyumba kwa nyumba akiwakamata na kuwatiagerezani, haidhuru ni wanaume au wanawake. Ni kama dhoruba kali ya ghafulailiyopiga Kanisa, nia ya Sauli ilikuwa kulifutulia mbali akihesabu ni la hatari sanakuruhusu wakristo waendelee, maana watazidi kuvuta watu na dini ya Kiyahudiitafifia. Zaidi ya kuwafunga alitafuta wauawe 26:10. hatujui ni wangapiwaliouawa. Wakristo wengi waliondoka Yerusalemu na kwenda huko na hukokatika Yudea na Samaria, na kwa njia hiyo Injili ilipata kusambaa, wakiwaelezeajirani zao habari za Kristo. Kwa hiyo Shetani aliyemtumia Sauli alishindwakuizima Injili, kinyume chake, mateso yaliipulizia moto na kuieneza. Mitumewaliamua kubaki Yerusalemu, pengine kuwatunza waliobaki, pengine hawakuwakatika hatari kama hao Wayahudi wa Kiyunani, labda wakuu walifikiri si wa hatariwakiendelea kuabudu hekaluni n.k.

Mpaka wakati huo Mitume ndio walioihubiri Injili lakini watu wasio Mitume kamaFilipo walianza kuwahubiri Wasamaria na wengine. Ni hatua kubwa na ya maanakwa sababu Wasamaria hawakuwa Wayahudi halisi, ni watu mchanganyiko, haoni kama daraja la kuwaendea WaMataifa baadaye. Neno la Bwana Yesu kablaya kupaa latimizwa Mdo.1:8.

Wasamaria walikuwa watu gani hasa? Katika karne ya 10 kabla ya Kristomakabila kumi ya Israeli walijitenga na wenzao chini ya uongozi wa Yeroboamu,wakaweka makao yao makubwa pale Samaria. Samaria ulitekwa na WaashuruKK.722. wenyeji wengi walipelekwa utumwani na wageni waliletwa kuishi mahalipao. Walioana na wenyeji waliobaki. Wayahudi waliporudi kutoka utumwaniwalikataa msaada wa Wasamaria kujenga hekalu hivyo uadui ulizidi. Ndipobaadaye farakano lilitokea Wasamaria walipojenga hekalu lao Mlima Gerizimuna kukataa Maandiko isipokuwa vitabu vitano vya kwanza vya Musa. Wayahudiwalidharau Wasamaria wakiona kwamba hawawi Wayahudi halisi ki-dini walaki-taifa, ni wazushi na wa farakano.

Kwa hiyo ilikuwa hatua kubwa kwa Filipo kuwaendea na kuwahubiria Injili, ilimbidiaruke mpaka ki-mawazo na kiutendaji asifuate kawaida za siku zake. Lakinialisaidiwa na mfano wa Bwana Yesu, Yoh.4. na kwa kujazwa na Roho alielewakabisa kwa ndani Yesu yu tayari kuwapokea sawa na watu wake.

8: 4-13: Filipo kuwahubiri Wasamaria:Filipo hakuwa Mtume, ni mmoja wa wale saba waliochaguliwa kuongozaHuduma ya Mezani kwa wajane (sura ya 6). Mwenzake mmoja Stefano tayariameuawa, lakini Filipo hakusita kuwaendea Wasamaria. Wasamaria walifurahisana, Mungu alimjalia Filipo uwezo wa kufanya maajabu kati yao, thibitisho lakuwa ametumwa na Mungu na ya kuwa ni mapenzi ya Mungu kwa Wasamariakuokolewa.

Page 28: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO690

Halafu twapewa habari za mchawi mmoja Simoni aliyejulikana sana kwa uchawiwake hali amewashangaza wenyeji na kudai kuwa mtu mkubwa. AlipotokeaFilipo na kufanya maajabu ya kweli, bila kutoza fedha, na bila kujidai mwenyewekuwa mkubwa, basi walikuwa tayari kumwamini Filipo na ujumbe wake kulikoSimoni. Simoni alitambua itambidi na yeye mwenyewe kujiunga na waamini waFilipo, hivyo akabatizwa kama wao na kuandamana na Filipo. Huenda atagunduasiri ya uwezo wake na kuendelea na sifa zake kati yao. Alijua hakika maajabu yaFilipo ni ya kweli tena ni makubwa kuliko ya kwake.

8: 14-25: Petro na Yohana kuja Samaria:Habari iliwafikia Mitume pale Yerusalemu kwamba Wasamaria wamelipokeaNeno la Mungu, wakaamua kuwatuma Petro na Yohana kuangalia jinsi mamboyalivyo na kuwakaribisha Wasamaria kwa moyo kuwa pamoja nao katika Kanisamoja.

Iwapo Wasamaria wameamini na kubatizwa halikutokea tukio kama lilivyotokeaSiku ya Pentekoste. Kwa hiyo Petro na Yohana waliwaombea na kuwawekeamikono, nao wakampokea Roho Mtakatifu. Ni kama Pentekoste yao. Hatuambiwikama walisema kwa lugha au vipi ila ilijulikana Roho amewashukia hakika.

Neno hilo lina matatizo, maana katika 2:38 Petro alisema wabatizwe naowatapokea Roho, kama ni sehemu mbili katika jambo moja. Je! ndivyo ilivyo auvipi? Ni vema tutenge hayo mawili? Je! ni kweli ni Mitume tu wawezaokuwaombea watu na kuwawekea mikono ndipo wapate Roho? Siyo. Maanabaadaye Mkushi alishuhudiwa na Filipo, na kubatizwa, na bila shaka kupewaRoho. Je! huduma ya Filipo ilikuwa na upungufu ambao Mitume waliujaza? La!Kwa nini Mungu hakuwapa Roho mara? Huenda jibu si gumu. Mungu alitakaKanisa kuwa na umoja na kuwa moja.

Alichelewa kutoa Roho mpaka walipofika Petro na Yohana ili kujenga umoja katiyao. Mitume na Kanisa la Yerusalemu wapokee Wasamaria kwa mikono miwili(tukumbuke uadui uliokuwepo kati yao) na Wasamaria wajue wamepewa kipawakilekile walichopewa wakristo wa kwanza kabisa, wasisikie kupungukiwa chochote, pia watambue hawana haja ya kuanzisha Kanisa la Wasamaria,wajihesabu kuwa na umoja na wakristo wote potelea mbali ni wa kabila au taifagani.

k.18 Simoni mchawi alipoona jinsi Roho alivyotolewa na Petro na Yohanaalitamani sana kuupata uwezo huo, si kwamba alitaka Roho ila alitaka uwezo wakutoa Roho, na alikuwa tayari kuwapa fedha ili apate uwezo huo. Petroalimkemea vikali sana, alijua moyo wake si safi, nia yake haikulenga shabaha yaMungu, Alikuwa amezoea ushirikina na uchawi, na ilikuwa vigumu kwakeaachane na tabia hizo. Hakuonyesha toba la kweli, akashindwa kujiombea,akamwomba Petro amwombee.

Page 29: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO691

Petro alisimama imara tena kama alivyofanya wakati wa Anania na Safira.Twaona Shetani hujitahidi kuharibu Kanisa kwa njia mbalimbali, kwa wazi katikamateso, kwa ndani kwa hila na udanganyifu. Lakini Kanisa lina kipawa cha ajabucha kuliongoza, Roho Mtakatifu aliyewafunulia watu wake mambo ya kutenda, namambo ya kutahadhari nayo.

k.25: Petro na Yohana walirudi Yerusalemu wakipitia katika vijiji vya Wasamariana kuhubiri Injili, bila shaka walitiwa moyo na yote waliyoyaona kwa Wasamaria,na vilevile mbegu za kuwaza uenezi wa Injili zilioteshwa ndani yao.Ni vema tuone ya kuwa Maaskofu si badala ya Mitume, hao waliwekwa hasakuwa mashahidi wa kuyaona na kuyasikia yote aliyoyatenda Bwana Yesu, ilihabari kamili za Yesu zitunzwe. Ni wa pekee hakuna wa badala yao. Mfuatanowa Mitume ni katika kupokezana Mafundisho ya kweli, yaliyofundishwa naMitume, yaliyo sahihi, na ya kuaminiwa, yanayokabidhiwa kizazi kwa kizazi, nahasa yaliyomo katika Agano Jipya.

Kiambaza kati ya Wayahudi na Wasamaria kimevunjwa na Injili.

8: 26-40: Mkushi kumwamini Kristo na kubatizwa na Filipo:Filipo alikuwa Mkristo aliye tayari kuongozwa na kutumiwa na Mungu. Alikubalikuondoshwa pale Samaria, mahali ambapo kazi zake zilikuwa na mafanikio nakwenda mpaka jangwani bila kujua ni nini itakayompata huko. Alipofika hukojangwani, kumbe gari lilikuwa likitelemka kusini na kurudi Kushi, ndani yake niMkushi, mtu mkubwa chini ya malkia wa Kushi. Yeye alikuwa Yerusalemu kwaibada, huenda Sikukuu mojawapo. Kama alikuwa Myahudi kwa asili, aumwongofu wao, si wazi. Iliyo wazi ni kwamba pale Yerusalemu amejipatia nakalaya Kitabu cha Nabii Isaya, na alikuwa akikisoma njiani.

Roho wa Mungu alimwongoza Filipo ajiunge naye garini, labda yule mtu alishtukakumkuta mtu peke yake jangwani. Filipo alisikia anasoma unabii wa Isaya 53 juuya Mtumishi Ateswaye. Filipo aliona anayo nafasi ya kumwambia habari za Kristoila kwanza alimwuliza kama ameelewa yale anayosoma, na Mkushi akakirikwamba hakuelewa. Katika habari hiyo twaona uongozi mkamilifu wa Mungu.Kwanza kukutanisha watu wawili ambao kwa kawaida kamwe wasingaliwezakukutana. Mmoja aliyemfahamu Kristo na mmoja asiyemfahamu. Mmoja wahumo nchini na mmoja wa nchi nyingine ya mbali. Halafu mtu alikuwa akisomapalepale ambapo utabiri wa Kifo cha Yesu na maana yake umeonekana wazi.Pengine pale Yerusalemu Mkushi alipata habari za Wakristo, yawezekanaamekutana nao, huenda alikuwa amesikia habari za Kristo Mwenyewe - ilahatujui. Moyo wake ulikuwa na maelekeo makubwa, kwanza katika utayari wakewa kufunga safari ya mbali kwenda kuabudu, pili katika kujipatia Maandiko iliasome mwenyewe, na tatu katika kujinyenyekeza kwa Filipo na kuomba msaadawa kueleweshwa. Mungu alikuwa amemtayarisha Filipo, pia Munguamemtayarisha Mkushi.

Page 30: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO692

Mwisho Mkushi aliamini na walipofika kwenye maji, aliomba abatizwe na Filipoakambatiza. k.37: Maneno katika mraba hayaonekani katika nakala za zamani.Yafikiriwa ni ya liturgia ya ubatizo iliyotungwa wakati Kanisa lilianza kuwa namipango. Yawezekana yaliingizwa hapo na mwandishi mmoja aliyefikiri kwambabila shaka Filipo kabla ya kumbatiza alihakikisha kwamba anamwamini Kristomoyoni mwake.

Maneno "wakatelemka wote wawili majini" si lazima tufikiri kwamba aliyebatizwaalizamishwa majini, maana wote wawili walitelemka majini, yawezekana wotewawili waliingia majini mpaka kiunoni. Mara Roho akamnyakua Filipo na Mkushialiachwa kurudi nchini mwake peke yake, ila twasoma alikuwa na furaha sisikitiko. Alirudi bila mwinjilisti lakini pamoja na Injili, bila msaada wa kibinadamulakini pamoja na msaada wa Roho Mtakatifu. Filipo alirudi na njiani alihubirikatika miji. Kama alikwenda kuishi Kaisaria wakati huo si wazi ila baadaye aliishihuko; 21:8. Kushi ilikuwa kusini ya Misri, kwa hiyo Bara Afrika lililetewa Injili.

Yawezekana Luka aliingiza habari hiyo kuonyesha lengo lake la Kristo kuwa kwaulimwengu wote na jinsi Injili ilivyoanza kuhubiriwa nje ya Yerusalemu na kwawatu mbalimbali.

Kwa habari hiyo wainjilisti watiwe moyo wa kuona jinsi Mungu awezavyokuwakutanisha watu wasiomjua Kristo ambao amewatayarisha kusikia na kuitika,na wale wanaomjua Kristo ambao waweza kuwashirikisha wasiomjua.

9: 1-9: Kuongoka kwa Sauli huko Dameski:Sauli alikuwepo Stefano alipouawa akikubaliana na yote yaliyotendeka, na baadaya kifo cha Stefano aliamua kufanya juu chini kulifuta Kanisa. Alikuwa nautambuzi mkubwa rohoni mwake na kujua wasipokomeshwa Wakristo watazidikuwavuta Wayahudi wenzake na mengi katika dini ya Kiyahudi yataachwa nakupotea. Kama ni kweli Kristo ndiye dhabihu itoshayo kuondoa dhambi dhabihuzilizotolewa hekaluni hazihitajika tena wala kazi za kuzitoa za makuhani. Vivyohivyo kama Mwongozo wa Maadili ya Kristo utakubalika Torati itakosa nguvuhasa ikiwa haitakuwa njia ya kupata haki kwa sababu haki itapatikana kwa imani.

Vivyo hivyo Tohara kama ishara ya Agano la Kale haitatakiwa kama Agano Jipyalimesimamishwa. Sauli alishindwa kuona Yule aliyetundikwa msalabani ni Masihiwa kweli, maana Torati ilisema amelaaniwa kila aangikwaye mtini. Hakuwezakupokea habari ya Kufufuka kwa Yesu na ya kuwa yu hai, alihesabu ni uongo wawanafunzi wakitaka kuwadanganya watu. Kwa hiyo twaweza kusema alikuwa wakweli kwa kuwa alitenda kwa jinsi alivyoamini kwa dhati. lIa ni wazi kwa jinsialivyosema baadaye ushuhuda wa Stefano na wenzake uliendeleakugongagonga moyoni mwake na kumwondolea amani.

Page 31: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO693

Kibinafsi alijua kwamba iwapo amejitahidi mno kushika Torati kikamilifu hatahivyo hakusikia amani kama amefaulu kupata haki, mara kwa mara alijikutaamekosa. Kadiri dhamiri ilivyomshtaki ndivyo alivyojitahidi kuwatesa Wakristoakiamini kabisa kwamba hayo yampendeza Mungu. Kwa hiyo alipomalizakuwatafuta pale Yerusalemu akaamua kwenda Dameski hali amesikia Wakristowako huko nako. Akaomba barua ya Kuhani Mkuu ili aruhusiwe kuwatafutakatika masinagogi ya Dameski, mji kama maili 140 kaskazini ya Yerusalemu,safari ya kama juma moja.

Twaona Wakristo waliitwa "watu wa Njia hii" maneno yanayoonyesha kwambawaliishi kwa kanuni za ki-pekee, watu wa kufuata kielelezo cha Bwana wao.

Alipokaribia Dameski kwa ghafula yapata saa sita mchana 22:6 wakati jualinapong'aa sana mwanga kupita wa jua 26:13 ulimwangaza pande zote, ndipoakasikia sauti ikimwita kwa jina lake "Sauli, Sauli, mbona waniudhi?" ni YesuMwenyewe anayemwita, kumbe! yu Hai; tena kuwatesa Wakristo ni sawa nakumwudhi Kristo. Inaonekana Paulo alimwona Kristo: 9:17,27; 22:14; 26:16; IKor.9:1; 15:8. Yesu alifundisha kwamba lile Mkristo atendewalo limetendwa kwaKristo; Math.10:40: 25:40, 45; kama ni jema au kama ni baya. Sauli akatekewakwa jinsi mambo yalivyotokea ghafula kinyume cha mawazo yake vote ambayobila shaka yalijaa shughuli zilizomleta Dameski kwa kuwa ameukaribia tayarikuzianza. Akauliza "u nani Bwana?" Alijibiwa mara moja na Yesu kwa manenoya wazi "Mimi Ndimi Yesu unayeniudhi wewe". Mamlaka ya Yesu imedhihirikakatika maneno "Mimi Ndimi" Kutoka 3:14 na madai ya Yesu kama Yohanaalivyosema mara saba katika Injili yake, "Mimi ndimi Njia na Kweli na Uzima, -Mkate wa Uzima - Mlango - Mchungaji Mwema". n.k. Tena alimkumbushamaudhi. Kumbe Stefano alisema kweli, na Wakristo wasema kweli - si wakufurukama alivyodhani.

Yesu alimwagiza aingie mjini ndipo ataambiwa ya kufanya. Maisha yakeyamepinduliwa, mipango yake imepinduliwa, vote aliyokusudia yamepinduliwa,tena kwa dakika chache!!

Kristo Mwenyewe alijiingiza katika maisha ya Sauli wakati alipokuwa akimtesakwa nguvu, Kristo alimgeuza kabisa, wakati alipokuwa akitafuata kuwashikawafuasi wa Kristo alishikwa na Kristo FiI.3:12. Kama alivyosema katika Gal.1:15ilimpendeza Mungu kumdhihirishia Mwana Wake. Alikuwa mkali kama mnyamaakirarua wafuasi wa Kristo, kumbe aliingia Dameski kwa upole, kipofu, na mtualiyeishiwa nguvu. Kiburi kimekwisha, kujitegemea kumekwisha, wenginewalimwongoza njiani, hana budi kungoja mpaka Mungu amfunulie ya kutenda.Alibaki anaomba na kuzingatia sana kwa ndani maana ya hayo yote. Kwamasikitiko makubwa alikumbuka na kutubu maudhi yote aliyofanya kwa wakristo,wale waliouawa na kufungwa na kupigwa kutokana na juhudi zake za haponyuma. Pengine maono ya 2 Kor.12:1-4 yalimtokea wakati huo.

Page 32: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO694

26:14 "ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo" lugha hiyo yaonyeshakwamba iwapo alitokewa ghafula na Bwana Yesu kabla yake ametayarishwa,Yesu amesema naye rohoni mwake katika mashaka yake na katika ushuhuda waStefano na wenzake. Pia iwapo ni kama alilazimishwa kuitika hata hivyo ilikuwajuu yake kutii au siyo 22:10.

9: 10-25: Anania akambatiza, Sauli alimshuhudia Kristo:Pale Dameski Mungu alikuwa na mtu aliye tayari kumsaidia Sauli, ni Anania, mtualiyeshirikiana vema na Yesu kiroho, aliye tayari kumtii. Hatujui Wakristo waDameski ni wale walioondoka Yerusalemu adha kuu ilipotokea pale, au HabariNjema iliwafikia kwa njia gani, kwa wasafiri, wafanyi biashara au vipi. Hao niWayahudi, na inaonekana wangali wakisali katika masinagogi. Wakristowalikuwa wamepata habari ya Sauli kuja kwao ili awakamate na kuwafunga nakuwaleta Yerusalemu ili wahukumiwe k.2,13 Yawezekana waliposikia habari zaSauli kuwa Mkristo waliogopa ni hila yake na njia yake ya kuwafahamu ili afaulukuwakamata.

Anania alipewa habari ya mahali alipo Sauli, na ya kuwa atamkuta anaomba,tena anamtazamia Anania, na ya kuwa atamwekea mikono ili apate kuona tena.Anania alimwambia Bwana Yesu mashaka yake, ila Bwana Yesu alijua hakikaSauli amebadilika kabisa, na ya kuwa anayo makusudi juu ya maisha yake, kwahiyo Anania amwendee. Mungu amemwokoa kwa kusudi la kuipeleka Injili kwaWamataifa wengi, na katika kazi hiyo atateswa sana, mtesi atakuwa anateswa.(Twaona Wakristo waitwa kwa lugha mbalimbali - "watu wa Njia hii k.2; 19:9,23;22:4; 24:14,22 - "watu waitao Jina lako" 9:14 na "watakatifu" 9:13).

Mateso ni fungu la Mkristo 2 Kor.4:17; Math.5:11-12; I The. 3:3-4; Mdo.14:22.Anania akamwendea Sauli na kumpokea kwa mikono miwili akimwita "nduguSauli" ndugu kweli katika Yesu. Aliyekuwa adui mkubwa alikaribishwa kamandugu mpendwa akaingizwa katika familia yao, na Sauli alionyesha ukweli wakekwa kujiunga nao na kukaa nao 19b. akijihusianisha nao. Anania akamwekeamikono na Sauli alipata kuona tena, alipewa Roho Mtakatifu na kubatizwa, kishaakala. Hatuambiwi kama Anania alikuwa na cheo au siyo katika Kanisa, siMtume, ila twaona Bwana Yesu alimtumia kumsaidia Sauli, si Petro walaYohana!! Je! alisema kwa lugha wakati huo? I Kor.14:18.

Roho hutolewa kwa uenezi wa Injili na Mungu hutumia wale wanaomtii.Twajiuliza, Sauli alifaaje kuwa Mtume kwa WaMataifa, huku hawi Mmataifa.Alikuwa Myahudi halisi, na kufahamu dini yake sana sana, alikuwa ameishikiliakwa unyofu wa moyo, na kujua ni dini safi kuliko zote ulimwenguni, hata hivyokutokana na ujuzi wa maisha alijua haikuweza kumwokoa. Kwa upande wa elimualikuwa ameelimishwa ya kutosha, alikuwa na ubongo mkali, na Munguatamtumia katika maandishi ya nyaraka na katika kuzieleza kweli za Kikristokinaganaga. Kwa kuzaliwa Tarso alikuwa ameguswa na ustaarabu wa Kiyunanina wa Kirumi hivyo ataweza kujihusianisha na watu mbalimbali bila shida. Ni

Page 33: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO695

mtu aliyebadili historia ya sehemu ile yote kwa sababu ya juhudi zake katikakwenda mahali pengi na pa mbali katika kuieneza Injili na kuyapanda makanisa.Pia alisaidia Kanisa ili liondoe harufu ya Kiyahudi ili Imani ya Kristo ionekanekuwa Imani ifaayo walimwengu si Wayahudi tu. Katika sura ya kwanza ya Galatiatwaona jinsi Mungu alivyomchagua kabla ya kuzaliwa, hata hivyo alipokutana naBwana Yesu njiani ilimbidi auitike wito wake na kumtii.Mara Sauli alimshuhudia Kristo katika masinagogi ya Dameski na watuwalishangaa. Kwa sababu alikuwa mtaalamu wa Maandiko aliwaelezeaWayahudi kinaganaga habari za Masihi, akiwatia fadhaa wasiotaka kuaminindipo alikwenda Arabuni Gal.1:15-24 Hatujui kama alikwenda kuhubiri sehemuzile, au alikwenda kupata utulivu wa kuchunguza Maandiko asahihishe mawazoyake kutokana na badiliko la imani yake.

Hatujui alikaa muda gani, ila twajua kwamba alilazimika kuondoka Dameskialipopata habari ya hila ya Wayahudi kumwua Iwapo aliokolewa kwa ajabu Saulialitangaza habari za Kristo si habari zake, na kwa ujasiri k.27,28,29. Alipatamateso huko Dameski, halafu Yerusalemu, na popote alipokwenda.

9: 26-31: Sauli huko Yerusalemu halafu Tarso:Wakristo wa Yerusalemu walisikia wasiwasi juu ya kumpokea, hali wakikumbukahali yake zamani. Mmojawapo Barnaba alikuwa tayari kumsadiki na ni yeyealiyemleta kwa Mitume na kuwaelezea jinsi alivyokutana na Bwana Yesu njianina jinsi alivyomshuhudia Kristo huko Dameski. Alihubiri katika masinagogi yaYerusalemu hasa akiwashuhudia Wayahudi wa Kiyunani habari za Kristo. Bilashaka baadhi yao walikuwa wamemsikiliza Stefano. Tena hila ya kumwuailijulikana na ndugu waliamua ni afadhali arudi Tarso nyumbani mwake kwakupitia Kaisaria, alipokaa Filipo.Ndipo Kanisa lilipata kutulia na kujengwa sehemu za Uyahudi, Galilaya naSamaria.

Je! Sauli atafanya nini huko Tarso? Je! atapotea machoni pa Kanisa? Je!atapanda makanisa kati ya Wamataifa na Wayahudi wa Utawanyiko? Kwelihatujui alivyofanya. Iliyopo ni kwamba Luka amemleta mbele yetu, kamaalivyofanya na Barnaba na kututayarisha kupata habari nyingi juu yake baadaye.

9: 32-43: Petro huko Lida; kiwete kuponywa; Dorkasi kufufuliwaLuka amerudi kwa Petro na kutuambia habari kadhaa juu ya huduma yake kablaya kurudi kwa Sauli 11:25 Mateso yalipopungua Petro na wenzake walipatanafasi kwenda huko na huko. Pengine makanisa ya Lida na Yafa yalianzishwa naFilipo 8:42 au kwa ushuhuda wa wale waliookolewa wakati ule. Kwanza Petroalimponya Ainea aliyekuwa amelala kitandani miaka minane. Ni ukumbusho waYesu kumponya mtu aliyepooza aliyeletwa na rafiki zake wan ne, na bila shakaPetro alikumbuka jinsi Yesu alivyofanya. Uponyaji huo ulivuta wengi kumwaminiKristo.

Page 34: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO696

Wakati alipokuwa pale aliletewa habari za mwamini mmoja jina lakeTabitha/Dorkasi, mama mwenye sifa nzuri sana. Aliugua akafa, na walipojuaPetro yu karibu walimwomba aje. Hatujui kama walifikiri ataweza kumfufua katikawafu, au walimwita ili aje awafariji wajane waliosaidiwa sana na huyo mama.Petro hali akikumbuka jinsi Yesu alivyomfufua binti wa Yairo alitoa watu nje,akamwomba Mungu, halafu akanena "Tabitha ondoka" kumbe, huyo mamaakafumbua macho na kumwona Petro, akajiinua na kuketi. Kisha Petro akawaitandugu na wajane waje nao wakamwona Tabitha yu hai mbele yao. Wengiwalipata habari hizo na kumwamini Kristo. Petro alikaa siku kadha katika mji waYafa kwa mtu ambaye kazi yake ilikuwa kutengeneza ngozi. Wayahudiwalioshikilia sana dini yao wasingalipenda kuishi na mtu wa namna hiyo, ila Petroalizidi kulegeza uhusiano wake na mambo ya nyuma, maana Mungu alikuwaakimtayarisha kuvuka mpaka wa ukabila na kuhubiri kwa Mmataifa Kornelio;habari ambayo twapata katika sura ya 10.

10: 1-43: Petro na Kornelio:Kornelio alikuwa Mrumi, askari, mwenye mamlaka juu ya,kikosi cha askari mia,akitumika kwenye makao makuu ya Warumi huko Kaisaria. Alikuwa mcha Mungu,pengine alihudhuria sinagogi ya Kiyahudi. Ni mtu aliyevutwa na usafi wa dini yaKiyahudi, imani katika Mungu mmoja tofauti na Warumi walioabudu miungumingi. Pia katika dini ya Kiyahudi maadili yalifungamana na imani, tofauti na diniya miungu ya Kirumi ambayo haikujali maisha ya mtu mradi atimize mila nadesturi ya dini tu. Kornelio alikuwa akiomba daima, na kutoa sadaka, nakuonyesha huruma na fadhili, hata familia yake waliguswa na kielelezo chake k.2na katika kikosi chake baadhi ya maaskari waliguswa k.7. Alikuwa tayari kujifunzana kuongozwa katika maisha yake ya kumcha Mungu. Pengine alikuwa amesikiahabari za Yesu kwa sababu akida mmoja alikuwapo pale msalabani Yesualiposulubishwa Lu. 23:47, na mwingine alionyesha imani katika Yesu na Yesualimponya mtumishi wake Math.8:11 ku. Pia Filipo alikuwa mwinjilisti aliyeishiKaisaria, kwa hiyo huenda amekutana na wakristo walioishi huko. Tujualo hakikani kwamba alipata maono, alitokewa na malaika alipokuwa akiomba,aliyezungumza naye juu ya sala na sadaka zake kwamba zimekubalika naMungu kwa hiyo hatua iliyo mbele yake ni kupeleka watu huko Yafa na kumwitaSimoni Petro aje.

Mara alitii, akatuma watatu kwenda Yafa, wawili wa watumishi wa nyumbani naaskari mmoja mtauwa kama yeye. Neno la kuona ni kwamba ni juu ya Petro kujanyumbani kwake, si yeye kwenda kwa Petro, ishara kwamba ni Petro aliyehitajikuruka ukuta ulio kati ya Wayahudi na WaMataifa si yeye Kornelio.

Baada ya maono hayo yaliyomtayarisha Kornelio kumpokea Petro Petroalitayarishwa kumwendea Kornelio. Ilikuwa neno gumu kwa Myahudi kuingianyumbani mwa Mmataifa. Mungu alimsaidia Petro kwa njia ya maono. Katikamaono aliona chombo kikishuka kama nguo kubwa na ndani yake kuna aina zawanyama na ndege.

Page 35: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO697

Katika hao Wayahudi waliruhusiwa kula baadhi na wengine walikuwa mwiko.Sauti ilimwambia Petro achinje ale. Petro iwapo alikuwa akiumwa njaa akakataakwa nguvu. Aliambiwa kwa mara ya pili, sauti ikitoa onyo kwamba, asiviite najisivilivyotakaswa na Mungu. Halafu kwa mara ya tatu aliambiwa hivyo. Kishachombo kikapokewa mbinguni.

Wakati Petro alipopewa maono, wale watatu walikuwa njiani kuja kwake. NdipoPetro alipokuwa akiwaza-waza maana yake wale watatu wakafika na kuulizakama yuko mtu aitwaye Simoni Petro. Roho alimwambia Petro asione shidaaende pamoja na hao watu. Walipokutana wakamwelezea Petro maonoaliyoyapata Kornelio. Petro akawakaribisha wakae naye ndipo kesho yakewaliondoka wote pamoja na waamini sita wa Yafa (hao watakuwa mashahidi wakuona Roho akiwashukia Kornelio na wenzake).

Twaona uwezo wa Mungu wa kuwakutanisha wasiomfahamu Yesu na walewanaomfahamu, kusudi wasiomfahamu wapate kumjua. Pia twaona uwezo waMungu kuwasaidia watu kuruka viambaza vinavyowatenga watu wasikutane,ama kwa sababu ya mila zao au ukabila wao, au utaifa wao, au dini yao.

Pengine twashangaa kuona uzito wa Wakristo kuruka mipaka iwapo walikuwawamemwona Bwana Yesu na utayari wake wa kupokea watu mbalimbali. Piawaliagizwa kwenda ulimwenguni pote na kuwafanya watu kuwa wafuasi wake,na kabla ya Kupaa alikuwa akiwaambia watakuwa mashahidi wake katika Yudea,Samaria, hadi mwisho wa dunia. Ni onyo kwetu kujihadhari na mipakatunayoweka wakati wetu iwapo mingi imerukwa tayari.

24-33: Kornelio alikuwa akiwangojea kwa hamu sana, moyo wake u wazikuupokea ujumbe wa Petro. Alikusanya jamaa na rafiki zake ili washirikiane nayekatika hatua hiyo kubwa iliyo mbele yake. Kornelio akampa Petro heshima zoteakijua ametumwa na Mungu Petro akamkumbusha iwapo ametumwa na Munguyeye ni mwanadamu tu.

k.28: Mara moja Petro alikiri hali ilivyo kati ya Wayahudi na WaMataifa halafualitamka neno la maana kwamba Mungu amemwonya asifanye ubaguzi nakujiona bora.

k.33: Kornelio alimjibu Petro alipomwuliza sababu ya kumwita na kusema "sisisote tupo hapa mbele za Mungu, tupate kuyasikiliza maneno yote uliyoamriwa naBwana". Maneno mazuri mno, wako "mbele za Mungu" na mbele yao ni Petroambaye Mungu atamtumia kuwaeleza habari za Kristo.

k.34-43: Kwanza Petro alitamka kwamba Mungu hana upendeleo, wale wamchaona kutenda haki hukubaliwa naye potelea mbali ni wa taifa gani. Halafu Petroalisema habari za Kristo na huduma yake ya kutenda mema na kuponya watu,na jinsi yeye na wenzake walivyokuwa naye na kuona hayo

Page 36: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO698

yote. Alitaja Kifo cha Yesu na Kufufuka Kwake akisema jinsi walivyoona hayo naya kuwa walikula na kunywa naye baada ya Kufufuka Kwake uhakika wa ukweliwa kuwa Hai. Halafu Petro alisema Yesu alikuwa amewaagiza kutangaza habarizake na ya kuwa ni Yeye atakayewahukumu watu wote. Halafu alisema kwambakila atakayemwamini Kristo atapata ondoleo la dhambi.

10: 44-48: WaMataifa kushukiwa na Roho na kubatizwa:Kabla ya Petro kumaliza hotuba yake Roho aliwashukia wote waliokuwepowakimsikiliza. Wale sita waliokuja pamoja na Petro walishangaa walipoona Rohoamewashukia hao WaMataifa.

Walipewa Roho sawa na Wayahudi, Roho yule yule, dalili za kusema kwa lughana kumwadhimisha Mungu zilithibitisha Roho ameshuka. Petro alifanyaje?maana hawakutahiriwa, Je! watahiriwe kwanza au vipi? Petro aliamua wabatizwebila kutahiriwa kwanza. Walibatizwa na nani? inaonekana ni wale waliokuja nayekutoka Yafa, neno "akaamuru" linaonyesha si yeye aliyewabatiza. Walitaka akaenao zaidi, bila shaka kwa kusudi la kuwafundisha zaidi ili waelezwe mengi Yesualivyofanya na kufundisha.

Twaona ya kuwa Mungu alijiingiza katika maisha ya Petro na ya Kornelio ili Injiliipate kwenda katika WaMataifa. Mungu hupenda watu wote waokolewe, nayeametoa Roho kusaidia uenezi wa Injili.

11: 1-18: Petro kuwaelezea Wakristo wa Kiyahudi sababu ya kumbatizaKornelio:Mitume na waamini waliokuwa Yerusalemu walipata habari ya kuwa Petroaliingia nyumbani mwa Mmataifa na kula na watu wasiotahiriwa, walitaka kujuasababu.

Petro aliwaelezea mambo kwa utaratibu, jinsi alivyoona maono na walipofikawatu waliotumwa na Kornelio Roho Mtakatifu alimwambia aende pamoja naompaka Kaisaria na kwa nyumba ya Kornelio. Kisha aliwaambia jinsi Rohoalivyowashukia huku akiwa katika kuwahotubia wale watu, na jinsi alivyokubalikuwabatiza kwa kuwa hakuona vema kuwakataza ubatizo kwa kuwa Mungualikuwa amewapa Roho Mtakatifu, hata kabla hawajabatizwa. k.17: alifikiriakikataa atakuwa anampinga Mungu.

k.18: Uzuri wa wale waliomhoji ni katika utayari wao wa kupokea maelezo yaPetro na kuunga mkono kazi ya Mungu kwa hao Wamataifa, na kumtukuza.

Baadaye neno la tohara kwa watakaomwamini Kristo katika WaMataifa lilizukakwa nguvu wakati wa WaMataifa wengi kuwa Wakristo. Walipokuwa wachacheWayahudi hawakusikia shida ila baadaye walihofu watamezwa nao.

Page 37: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO699

11:19-26: WaMataifa kuipokea Injili huko AntiokiaKatika sehemu hiyo twaona jinsi ile adha kuu iliyotajwa katika sura ya 8 na tukiolililofuata la waamini kutawanyika huko na huko lilisababisha Injili kuhubiriwamahali mbalimbali na makanisa yalipandwa Foinike, Kipro, na Antiokia waShamu. Mwanzoni waliohubiriwa walikuwa Wayahudi ila baadaye hatuailichukuliwa hata kuwahuburia watu wa lugha ya Kiyunani. Tafsiri "Wayahudi waKiyunani" k.20 si nzuri, maana tangu mwanzo hao walikubalika, sura ya 6; hapojambo lililotajwa laonekana kama ni hatua mpya. Pengine ni WaMataifawalioshirikiana na Wayahudi kama wacha Mungu na waongofu. Kwa ninitwasema ni hatua mpya? kwa sababu Kanisa lilituma Barnaba aende nakuchunguza mambo.

Antiokia ulikuwa mji mkubwa, yasemekana ulikuwa wa tatu katika ulimwenguuliojulikana siku zile. Wakazi walikuwa Wayunani, Wayahudi, Warumi, na watuwa mashariki. Mji wa maana sana na mji uliofaa sana kwa wahubiri kuvuta watuwa kila aina wampokee Kristo.

Waliohubiri hawakuwa Mitume, majina yao hatujui, waonekana walikuwa walei,watu waliosambaa baada ya adha kuu, watu waliokimbia mateso ya Sauli.

Twaona hekima ya Kanisa katika kumtuma Barnaba kwa sababu kwa tabiaalikuwa mtu aliojaa neema ya Mungu, mwepesi wa kukubali wageni, kamatulivyoona Sauli alipofika Yerusalemu, alijaa Roho na imani. Alipoona kazi yaMungu huko Antiokia alijiunga na waamini wa pale na kuwatia moyo nakuwasaidia. Kisha alitambua hao watu walihitaji mtu atakayeweza kukaa nao nakuwafundisha na kuwaongoza katika maisha ya Kikristo. Huyo mtu atakayefaa ninani? Ni Sauli! Kwa hiyo Barnaba mwenyewe alikwenda kaskazini mpaka Tarsoakimtafuta Sauli na kumleta Antiokia. Sauli alikuwa mtu aliyeweza kujihusianishana watu mbalimbali, ni Myahudi halisi, pia amezaliwa Tarso kati ya Wayunani nakukolea ustaarabu wao, na pamoja na hayo alikuwa na "uraia" wa Kirumi.Alipataje uraia huo? labda aliurithi kwa baba yake, hatujui. lIiyopo ni kwambaSauli ni mtu mwenye uwezo wa kujihusisha na watu mbalimbali bila shida.Barnaba alikuwa mtu tayari kushirikisha kazi hakuwa na hali ya kutaka ukubwa,ni mtu aliyefurahishwa sana alipoona Injili inahubiriwa na watu wanaitika.

Twajifunza jinsi ilivyo neno muhimu kuchagua watu waliojaa Roho nakuongozwa na Roho ndipo Kanisa litapanuka na wengi watavutwa kwa Yesu.k.26: Neno "wakristo" lilitumika kwa mara ya kwanza hapo Antiokia. Penginelilitumika kwa dharau, au kama mzaha, ila kwa vyovyote lilifaa kuonyesha haowatu ni "wa Kristo" ni wafuasi wake. Laonekana mara mbili tena katika AganoJipya; Mdo.26:28 na I Petro 4:16.

Page 38: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO700

11: 27-30: Unabii wa Agabo kuhusu njaa:Manabii ni wakristo waliopewa kipawa cha kipekee na Roho, kipawa cha kutabirimatukio yatakayotokea ili Kanisa liwe tayari kuyakabili. I Kor.12:28; 14:29 ku.Ef.4:11; Mdo.13:1, 15, 32 na 21:9-10. Katika siku zile za kwanza kwanza zaKanisa lilipokuwa lingali changa, hao watu walipendwa sana na kuwa msaadamkubwa wakilinda Kanisa na hatari na shida. Agabo alikuwa mmojawapo wamanabii wa Kanisa la Yerusalemu naye akaja Antiokia. Dalili ya ushirikianomwema kati ya makanisa. Jitahada nyingi zilifanyika kuutunza umoja wamakanisa, kusudi lisitokee kanisa la Wayahudi, na la Wasamaria, na laWamataifa n.k. ndiyo sababu twaona watu wakijia kanisa fulani kutoa msaadahalafu kuondoka na kurudi makwao.

Agabo ametajwa tena 21:10. Agabo alifunua tukio gani ambalo litatokea karibunihivi? Ni njaa kali. Kwa nini wakristo wajue mapema habari hiyo? ili wauandaemsaada kwa wakristo wenzao wa huko Yerusalemu ambao watakumbwa na njaahiyo.

Yawezekana kwa jinsi walivyouza mali na kushirikishana vitu vyao wamekuwamaskini, hawakuwa na akiba, pia kwa mateso huenda wamenyang'anywa malizao. Kwa njia hiyo umoja na ushirikiano ulizidi na kama wengine walikuwa namashaka juu ya Wakristo walio WaMataifa, basi mashaka yao yatapungua.

Waliokwenda na msaada ni Barnaba na Sauli. Sauli alipata nafasi ya kujulikanazaidi na wakristo wa Yerusalemu, jambo la maana kwa kazi zake za mbeleatakaposafiri mbali sana na kuhubiri Injili katika nchi nyingi na kuanzishamakanisa katika majimbo ya Kirumi.

k.28 "na "tulipokusanyika" Je! "tu" ni dalili ya Luka kuwepo mapokeo mengineyasema Luka alikuwa mzaliwa wa Antiokia.

Alama moja kubwa ya Kanisa katika siku zake za mwanzoni ilikuwa mzigo wakekwa wenye shida za kimwili, walitunzana wao kwa wao, kama sehemu moja yamaisha ya Kikristo.

12: 1-4: Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro:Luka ametuambia hatua kwa hatua maendeleo ya Injili kuanzia na Siku yaPentekoste wakati elfu tatu walipookolewa, ndipo Wasamaria waliamini, ndipoMkushi, na Sauli, Kornelio, na mchanganyiko wa wakazi wa Antiokia. Neno laMungu lilikuwa likienea, ndipo katika sura ya 13 alitoa habari ya Injili kuhubiriwakatika majimbo ya Kirumi ya mbali na katika Wamataifa wenye miungu yaombalimbali. Lakini kabla ya kueleza safari kubwa za Paulo na wenzake alirudishamawazo yetu pale Yerusalemu na kwa mateso yaliyowapata Mitume, viongozi waKanisa tangu mwanzo.

Page 39: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO701

Aliyeongoza mateso hayo ni Mfalme Herode Agripa wa kwanza, mjukuu waHerode Mkuu. Yeye alitawala sehemu yote ya Palestina kama babu yake.Nia yake ilikuwa kujipendekeza kwa Wayahudi ambao hawakumpokea kwamikono miwili kwa kuwa alikuwa nusu Mwedomu mwenye kibali cha Warumiwaliotawala nchi. Alitaka kulinda cheo chake akijitahidi kutunza amani nchini,kwa hiyo, watu wa vikundi-vikundi walionewa mashaka. Basi alimwua MtumeYakobo, akasubiri kuona itikio la Wayahudi, na alipotambua wamefurahia kifocha Yakobo basi, akamkamata Petro, ila kwa sababu ni wakati wa Pasakahakumwua mara, akamtia ndani akiamua kumwua baada ya Pasaka kupita,Petro alilindwa kwa nguvu kiasi cha kukomesha tumaini lo lote kuwa atawezakutoka. (hapo nyuma alikuwa ameokolewa kwa ajabu 5:18-20).

12: 5-19: Petro kutolewa gerezani kwa ajabu:Kanisa lilibaki na silaha moja ya Kuitumia; maombi.Walidumu pamoja katika kumwombea "kwa juhudi" kwa muda wote, huenda jumalote la siku za mikate isiyotiwa chache. Ndipo Herode alikuwa tayari kumtoa,lakini si ye ye atakayemtoa ila Mungu. Picha ni ya amani ya Petro, alikuwaametulia na kushikwa na usingizi mzito iwapo alijua karibuni hivi ataletwabarazani.

Kwa jinsi walivyomshika bila shaka hakuona njia ambayo kwayo ataweza kutoka,minyororo mikononi, na askari wawili mahali alipolala, mmoja upande wa kuumena mmoja upande wa kulia, na walinzi mlangoni. Hata hivyo malaika wa Bwanaalimwamsha bila kuwaamsha walinzi, minyororo ikalegea, akajivika nguo, kishaakatoka na kumfuata malaika. Ilimbidi malaika amwambie kila kitu cha kufanyamaana Petro alidhani ni maono tu si jambo la kweli. Malaika alimwacha naalipobaki peke yake ndipo alipotambua yu nje ya gereza, alikuwa na hakikakwamba Bwana Yesu alikuwa ametuma malaika na kumtoa.

Sasa aende wapi maana asubuhi watakapotambua hayumo gerezani watafanyajuu chini kumtafuta na kumpata? Basi alikwenda kwa nyumba ya mama waYohana Marko mahali ambapo Wakristo wamekusanyika kwa maombi.

Kijakazi aliyeitwa Roda akaja asijue ni nani anayebisha mlangoni. Akatambuasauti ya Petro na kwa furaha alisahau kumfungulia, alimwacha bado amesimamamlangoni, akaingia ndani na kuwaambia, wakadhani amepotewa na akili.Alikazana kuwaambia ni Petro na Petro alikazana kubisha mlangoni, kishawakafungua mlango na kumkuta Petro, wakastaajabu. Kumbe walikuwawakimwomba Mungu kwa ajili yake bila kupokea kwa haraka jibu la Mungu.

Kweli Petro alikuwa katika hatari kubwa, na hata hao waamini walikuwa katikahatari hasa wakimficha na kutangaza habari zake. Baada ya kuwaelezea jinsialivyotolewa akawaacha, inaonekana hakuwaambia mahali atakapokwenda, ilaaliwaagiza kumjulisha Yakobo (ndugu wa Bwana Yesu) na ndugu wengine

Page 40: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO702

habari hizo. Mungu hakutaka Kanisa likose viongozi wote wakati huo, kwa hiyoMtume mmoja Yakobo aliuawa bila Mungu kujiingiza na kumwokoa, na Mtumemwingine Petro aliokolewa kwa njia ya Mungu kujiingiza kwa nguvu.

Twaweza kufikiri fedhehe ya Mfalme na wenzake asubuhi ile walipojua Petrohayumo, na wasiwasi nyingi za walinzi, kwa kuwa wengine watafikiri wamepewarushwa. Lakini ni vigumu wakubali rushwa maana walifahamu kwamba Mfalmeakikasirika atawaua, na ndivyo alivyofanya. Ni vigumu kufikiri kwambawalipatana kumwachilia. Basi Herode alirudi Kaisaria.

12: 20-25: Kifo kibaya cha Mfalme Herode:Ugomvi ulikuwa umetokea kati ya Mfalme na watu wa Tiro na Sidoni. Iliwabidiwautengeneze mapema kwa sababu walipata chakula kutoka sehemualiyoitawala Herode. Walimwomba Blasto awasaidie ili wakutane na Mfalme.Siku iliwekwa na Herode akaja amejivika umaridadi sana, akatoa hotuba yakuonyesha uzuri wake, akijitukuza sana. Watu walimshangilia na kumpa sifazilizomfaa Mungu si mwanadamu. Mara akashikwa na ugonjwa akafa palepale.Wakristo waliona alipatwa na hukumu ya Mungu. Neno la Mungu liliendeleakotekote.

SEHEMU KUBWA YA PILI

Sura 13 – 28

INJILI KUHUBIRIWA KATIKATI YA WAMATAIFA NA MAKANISAKUSIMAMISHWAUTANGULIZISehemu kubwa ya pili ya Kitabu cha Matendo inaanza na hatua kubwa kuhusuuenezi wa Injili. Bwana Yesu alisema "mtakuwa mashahidi wangu katikaYerusalemu, Yudea, Samaria, na hata mwisho wa nchi" 1:8. Katika sehemu yakwanza tumeona kwamba ushuhuda umekwisha kutolewa katika Yerusalemu,Yudea, na Samaria. pamoja na hayo mashuhuri wawili wameokolewa; mmoja niSauli aliyeteuliwa kuwa Mtume kwa WaMataifa, na Kornelio Mmataifa wa kwanzakuokolewa. lIa bado halijatokea tendo la kuvuka kwenda mpaka nchi zingine.

Katika sura ya 11:19-26 tuliona ya kuwa Kanisa la Antiokia lilianzishwa nawahubiri mbalimbali waliofika huko wakati wakristo walipotawanyika baada yaStefano kuuawa.

Waliwahubiria Wayahudi kwanza ndipo wakaanza kuwahubiria Wayunani nawengi waliamini. Kisha Kanisa la pale Yerusalemu lilimtuma Barnaba aendehuko achunguze yaliyokuwa yakitokea Baada ya kufika na kuona mamboalifurahi sana, akihesabu kwamba Injili inaenea kweli kati ya watu. Zaidi yakufurahi pamoja na waamini wapya wa Antiokia alitambua kwamba walikuwa na

Page 41: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO703

haja kubwa sana ya kufundishwa juu ya imani na maisha ya Kikristo. Ni naniatakayeweza kufanya kazi hiyo na ni nani atakayewaungamanisha washirikianevema wao kwa wao yaani waamini wa Kiyahudi na wa Kimataifa? Alipofikiriajambo hilo aliona huyo mtu ni Sauli. Hivyo alikwenda kumtafuta huko sehemu zaTarso, akampata, akamleta mpaka Antiokia. Kwa mwaka mzima Barnaba naSauli walifanya kazi ya kuwafundisha waamini na Kanisa la Antiokia lilipatanguvu ya kusimama.

Kwa hiyo mambo yote ni tayari. Tunapoanza sura ya 13 twakuta watu wameanzakuwaza kupeleka Injili mbele zaidi.

13: 1-3: Kanisa la Antiokia kuwateua Barnaba na Sauli kwenda kuhubiriInjili katika nchi zingineSi wazi kama wakristo wote walikuwa wakiomba na kufunga. Kanisa limetajwakatika k.1 pamoja na viongozi wao watano ambao tumepewa majina yao. Majinahayo yaonyesha mchanganyiko mkubwa wa wakristo wa pale. Wengine huwazakwamba Simeoni aitwaye Nigeri alikuwa Simoni wa Kirene aliyeubeba msalabawa Yesu. Alikuwa baba wa Iskanda na Rufo waliotajwa katika Marko 15:21. NaLukio alitoka Kirene Afrika ya Kaskazini. Antiokia ulikuwa mji mkuu wa pili waKikristo na Mama wa Ukristo wa KiMataifa. Pia ulikuwa mkubwa kwa upande wautawala wa Kirumi kwa majimbo ya Shamu na Kilikia. Wakazi walikuwaWayahudi, Wayunani, Warumi na Washamu, pamoja na watu wa mashariki, nikama walimwengu wa zamani walikutana humo.

Basi walisikia kuongozwa na Roho Mtakatifu kuwatuma Barnaba na Saulikwenda kuihubiri Injili katika nchi zingine.Waliongozwaje na Roho Mtakatifu? Pengine kwa njia ya unabii, mmoja waoakifunuliwa neno hilo; au kwa mmoja mmoja kusikia moyoni mwake. Hatujuikama Barnaba na Sauli walisikia kuitwa kabla ya hapo. lIa twajua waliaminiwametumwa na Kanisa na Roho Mtakatifu na watakaporudi watatoa ripoti kwaKanisa. Ndipo wakaomba na kufunga tena kisha wakawawekea mikono Barnabana Sauli na kuwaruhusu waende.

Neno jema ni kwamba Kanisa la Antiokia lilikuwa tayari kuwaruhusu hao wawiliambao wamekuwa msaada mkubwa kwao.

SAFARI KUBWA YA KWANZA 13:4 - 14:26: kama BK.46-48:

13: 4-12: Barnaba na Sauli huko Kipro, Sauli ajiita PauloKwanza walisafiri mpaka kisiwa cha Kipro alipotoka Barnaba 4:36 wakiwa nakijana mmoja Yohana Marko. Wakashuka SALAMI penye pwani ya mashariki.Kama desturi yao walianza kuwahubiria Wayahudi katika masinagogi maanawao wenyewe walikuwa Wayahudi wakifahamu kabisa desturi na imani yaKiyahudi kwa hiyo ilikuwa rahisi waanzie na hao. Pia walikuwa na Maandiko yaAgano la Kale, pia ni watu waliokuwa na matumaini ya kumpata Masihi.

Page 42: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO704

Taratibu za dini yao zilikuwa msingi wa kueleza kazi ya upatanisho alioufanyaKristo. Hatuambiwi kama walipata waamini au vipi, wala hatujui walipokelewaje.Walitoka SALAMI wakapita katikati ya kisiwa mpaka PAFO penye pwani yamagharibi na mahali pa makao makuu ya serikali ya Kirumi. Kwa hiyo walisafirimwendo wa kama maili 90 na inawezekana walihubiri njiani, ila hatuambiwi.PAFO walikutana na liwali jina lake Sergio Paulo, mpagani. Pia pamoja nayealikuwa Myahudi mmoja Bar Yesu, mchawi aliyeitwa Elami. Liwali alimwaminiKristo ila yule mchawi alijitahidi kumwondoa katika imani. Bila shaka alifikirikwamba kama hao wakifaulu kumvuta liwali heshima na nafasi alizo nazozitapungua. Ilimbidi Sauli amkabili mchawi na kusema naye kwa ukali k.10;halafu akamjulisha kwamba atakuwa kipofu kwa muda ili ajifunze kutokumpingaYesu. Hivyo liwali alizidi kuamini alipoona yaliyompata mchawi.

k.9. Sauli aliacha kujiita Sauli (jina la Kiyahudi) akaanza kutumia jina la Paulo;pengine aliwaza jina hilo litamsaidia anapozidi kwenda kwa WaMataifa.Twasoma "Paulo akijaa Roho Mtakatifu" k.9 maneno hayo yaonyesha kwambaujasiri na uwezo wa Paulo ulitoka kwa Mungu si kwake yeye mwenyewe. Kwanjia hiyo yule mwovu akashindwa.Kwa kujumlisha habari za Injili katika kisiwa cha Kipro iliyopo ni kwamba habarini chache, hatupewi picha ya Kanisa la pale, ila ni vema tukumbuke ya kuwabaadhi ya wale waliowahi kuleta Injili huko Antiokia walitoka Kipro 11:19.

13: 13-52: Kuhubiri huko Antiokia wa Pisidia, halafu kuwageukiaWaMataifa

Waliondoka Kipro na kuvuka bahari na kufika mji wa pwani ya Jimbo la Pamfiliaulioitwa PERGE. Hapo kijana Yohana aliwaacha. Hatuambiwi wazi sababu zake,pengine alisikia hamu ya nyumbani au alihofu safari ngumu ya kwenda ndani yanchi za kigeni, au pengine hakuelewa safari itakuwa ndefu kiasi hicho. Tujualo nikwamba Sauli hakupendezwa na kuondoka kwake wala hakuwa tayarikumchukua tena, ila Barnaba mjomba wake alikuwa tayari, akampa nafasi tena,taz. 15:36-40. (Liko wazo lingine la kufikiri kwamba Paulo ameanza kuwa mbeleya mjomba wake Barnaba, na hakupenda iwe hivyo, maana tangu hapo Pauloametajwa kwanza).

Hatupewi habari yo yote jinsi walivyofanya PERGE kama walihubiri au kamawalipita tu. Wazo liko la kufikiri Paulo aliugua vibaya alipokuwa sehemu za pwanikwa hiyo aliamua kupanda mpaka milima ya Pisidia ambapo alitarajia kupatanafuu. GaI.4:13.

Walisafiri mpaka ANTIOKIA wa PISIDIA, uliokuwa mji mkuu wa Jimbo la Kirumila Galatia Kusini. Hapo siku ya sabato waliingia sinagogini na kuwahubiriaWayahudi na wacha Mungu. Walipewa nafasi ya kutoa neno, ilikuwa desturi kwawageni kupewa nafasi hiyo.

Page 43: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO705

13:16 ku. Hotuba ya Paulo: Paulo alizungumza na Wayahudi juu ya historia yaoakionyesha jinsi Mungu alivyotayarisha njia ya Kuja kwa Masihi, yaani YesuKristo, kwa kulitumia taifa lao. Alianza kwa kutaja matendo makuu ya Mungutangu babu zao mpaka Mfalme Daudi. Ndipo kutoka kwa Daudi alisema moja kwamoja juu ya Kuja kwa Kristo, aliye timizo la ahadi kwa babu zao ahadi ya kupataMwokozi wa uzao wa Daudi k.23. Aliendelea kwa kueleza kwamba wakuu waYerusalemu hawakumjua Kristo wala Maandiko juu yake, hivyo walimwua. IlaMungu akamfufua kutoka kwa wafu, na Mitume walikuwa mashahidi wakumwona kwa macho yao baada ya Kufufuka Kwake.Paulo aliwakumbusha maneno ya Zaburi yaliyothibitisha hayo.

k.38-39: Wito wa kutubu na kupokea msamaha: Paulo aliufikia upeo wa hotubayake akiwaambia ya kuwa kwa Yesu watapata msamaha wa dhambi nakuhesabiwa haki. Kwa Torati yao haiwezekani wapate haki, maana hakunaawezaye kuzitimiza sheria zake na pasipo kuzitimiza hawatapata haki kwasheria. Aliwaita wakate shauri, pia aliwaonya juu ya kutokuamini.

k.42: Tukumbuke ilikuwa mara ya kwanza watu kusikia maelezo kama hayo naibada ilipokwisha watu walibaki katika hali ya kutaka kujua zaidi kwa hiyo Paulona Barnaba walipotoka sinagogini waliombwa warudi sabato ifuatayo. Baadhi yaWayahudi na waongofu wao waliotaka kuamini waliandamana na wahubiri.

k.44 Sabato ya pili ilipofika karibu mji wote ulikuwa umekusanyika. Ni wazikwamba tangu sabato ile ya kwanza watu wamechokozwa na mahubiriwaliyoyasikia na watu wameendelea kuzungumza wao kwa wao juu yake.Baadhi ya Wayahudi walisikia wivu kiasi cha kuchukulia hatua za kupinga nakuyakanusha maneno ya Paulo.

k.46: Itikio la Paulo na Barnaba lilikuwa kuamua kuwageukia Wamataifa nakuwaacha Wayahudi katika kutokuamini kwao.

k.48: WaMataifa walifurahi walipoona hayo na wengi waliamini Hata hivyoWayahudi waliokuwa bado wangali wakisikia wivu na chuki walizidikuwachochea watu kinyume cha wahubiri, nao walitumia watu fulani kuwatoakatika mji wao.Wale walioamini walijaa furaha ya Roho Mtakatifu.Neno la Mungu lilikuwa likizidi kuenea, na wahubiri walizidi kupingwa nakuteswa, k.50 chatuelekeza kufikiri walitolewa kwa nguvu na 2 Tim.3:10-11inathibitisha mateso waliyoyapata katika miji hiyo.

14: 1-7: Kuhubiri huko IkonioWalipoondoka ANTIOKIA WA PISIDIA wakaenda mpaka mji ulioitwa IKONIO. (NiKonya katika nchi ya Uturuki wa leo). Zamani zile wakazi walikuwa Wayahudi,Wayunani, Warumi na wenyeji wa asili. Ulikuwa kama maili 90 hivi kutoka Antiokia.

Page 44: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO706

Walianzia pale sinagogini kwa Wayahudi na kuwavuta Wayahudi wengi kuamini,pamoja na Wayunani. lIa baadhi ya Wayahudi wasiotaka kuamini waliwachocheabaadhi ya Wayunani ambao hao nao hawakuamini, wakawapinga wahubiri.Mungu alithibitisha neno la Barnaba na Paulo kwa kuwasaidia kufanya miujiza naishara GaI.3:5. Hivyo waliweza kuendelea kwa muda mrefu. Lakini kwa vile watuwalikuwa wamegawanyika wengine upande wa wahubiri na wengine upande waWayahudi; Wayahudi na WaMataifa walijiunga pamoja na wakuu waliokubaliananao, wakafanya ghasia na kufanya mpango wa kuwafukuza kwa kuwapiga kwamawe, ila walipata habari ya hila yao, wakaondoka kwa haraka wakaenda mpakaLISTRA NA DERBE, miji ya Likaonia

14: 8-20: Kuhubiri huko Listra na DerbePale Listra hatusikii juu ya mahubiri sinagogini, labda Wayahudi walikuwawachache. Twaona wenyeji walikuwa na miungu yao, pia walijaa ushirikino.

Kiwete mmoja aliponywa na Paulo na wenyeji walipoona jambo hilo walidhanikwamba miungu yao imewashukia kwa mfano wa wanadamu, wakamwitaBarnaba jina la Zeu na Paulo jina la Herme. Kuhani wa Zeu aliona vemawafanyiwe dhabihu ya ngombe na kuvikwa taji ya maua. Paulo na Barnabahawakutambua mapema mpango huu kwa sababu ya lugha ya kienyejiiliyotumika, lakini mara walipotambua wakatoka nje kwa haraka na kukataakabisa.

Katika kuwahutubia Paulo na Barnaba hawakugusa hata kidogo mambo yaKiyahudi bali walikaza juu ya Mungu kuwa mmoja, Mwumbaji Hai wa kila kitu,Mungu aliye Mwema awapaye mvua na mavuno na mema yote ya maisha.Waliwasihi waache desturi zao zisizo za maana, za ubatili, na kumgeukia huyoMungu Mwema, Mwumbaji. Kwa njia hiyo waliwazuia kwa shida wasiwatoleedhabihu n.k.

Paulo alisema kwamba kabla hajaja Kristo Mungu alikuwa amewaachia watuwafuate kile walichotaka wenyewe, ila tangu Kuja kwa Kristo Mungu anatakawatu wote wajirekebishe kwa kumpokea Kristo na wokovu wake. k.16. Katikakipindi kile kabla ya Kristo Mungu alikuwa amewaachia ushuhuda wa KuwepoKwake na Uhai wake, ila katika Kristo wokovu umepatikana na watu wawezakumfahamu Mungu na kushirikiana naye kibinafsi kwa njia ya Yesu Kristo.Twaona uvumilivu wa Mungu wa kusubiri mpaka Kristo alipokuja.

Shida iliwapata wahubiri wakati Wayahudi wasioamini walipofika kutoka Antiokiana Ikonio, nao waliwashawishi watu kumpiga kwa mawe Paulo kiasi cha waokufikiri wamemwua. Wenyeji waamini walikuja kumsaidia Paulo, wakamzunguka,kisha Paulo akasimama na kukaa usiku mjini na kesho yake aliondoka naBarnaba kwenda DERBE, safari ya kama maili 60.

Page 45: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO707

Twaona kigeugeu cha wenyeji hao ambao mwanzoni waliwapokea wahubirikama miungu, halafu baadaye waliwapiga kwa mawe. Bila shaka Pauloalikumbuka wakati ambapo yeye mwenyewe alikubaliana na wale waliompigaStefano kwa mawe na kumwua.

Twaona ni Wayahudi walioipinga Injili na kuwazuia watu wasiamini, naohawakuridhika kufanya hivyo mahali walipoishi tu bali wakawafuatia wahubirimpaka mahali po pote pale waliposikia watu wamekuwa tayari kuamini.

Jambo jingine ni kuona jinsi Paulo na Barnaba walivyoamua kuendelea mbelekatika kazi yao ya kuihubiri Injili, iwapo walikutana na vipingamizi mbalimbali,hawakukata tamaa, wakawa tayari kuvumilia magumu na mateso mengi kwa ajiliya Kristo. Kwa juhudi zao Injili iliwafikia wengi na makanisa yalipandwa.Hatuna habari nyingi za Injili kuhubiriwa DERBE ila tumeambiwa wengi waliamini.

14: 21-28: Kurudia makanisa yaliyopandwa; kurejea AntiokiaPaulo na Barnaba walirejea miji ile ya Listra, Ikonio, na Antiokia. Hasa kwakusudi la kuwaimarisha waamini waliopatikana. Waliwaonya wadumu katikaImani wakifahamu watapata dhiki na mateso maana hayo ndiyo fungu lao:Warumi 8:17; 2 The.1:4 ku. 2 Tim.2:12.

Pamoja na hayo walichagua na kuweka wazee katika kila kanisa watuwatakaowaongoza. Watu hao walitoka pale pale na iwapo hatujui ni wangapiwaliowekwa kila mahali ni wazi ni zaidi ya mmoja, si kama mpango wetu wa sikuhizi kuwa na pasta mmoja tu. Kisha wakaomba nao na kufunga na kuwakabidhikwa Bwana. Ilihitaji imani kubwa kuamini kwamba Mungu aweza kuwalinda haliwakiishi katika ulimwengu ulio kinyume chao.

14:24: Wamo katika safari ya kurudi. Walipitia PERGE, hapo walihubiri, ilahatuambiwi matokeo ya kuhubiri kwao.

14:26: Hawakupitia Kipro, wakarudi moja kwa moja mpaka ANTIOKIA waShamu, mahali walipoanza safari, na mahali ambapo waamini waliwaombea kwakazi iliyokuwa mbele yao, ambayo sasa wameitimiza.Kanisa lilikutana na Barnaba na Paulo waliwaelezea yote yaliyotokea katikasafari na hasa jambo kubwa la WaMataifa kumpokea Kristo.

k.28. Paulo na Barnaba walitulia pale Antiokia kwa muda wakishirikiana nawakristo wa pale.

Twaona umuhimu wa watu kushirikishwa habari za kazi ya Injili ili watu wajisikiewamo katika shughuli hizo kwa njia ya kuziombea na kuwaombea waamini wamahali mbalimbali.

Page 46: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO708

Tangu safari hiyo hali mpya imetokea, Kanisa limesimamishwa katikati yaWaMataifa na ni wazi kwamba baada ya muda idadi yao itazidi sana idadi yawaamini wa Kiyahudi.

SURA YA 15: BARAZA KUU LA KANISA KUHUSU TOHARA:

15: 1-21: Mwenendo wa Mkutano

k.1-2 Tumekwisha kuona kwamba Kanisa la Antiokia wa Shamu lilikuwa nanguvu hata kiasi cha kuwatuma Barnaba na Paulo kwenda kuhubiri Injili katikakisiwa cha Kipro na nchi za kaskazini.

Baadhi ya wakristo wa Kanisa la Yerusalemu ambao hapo nyuma walikuwaMafarisayo hawakupenda waamini waliotoka katika Wamataifa kubatizwa bilakutahiriwa kwanza. Walishikilia sana msimamo huo kiasi cha kwenda mpakaAntiokia kwa kusudi la kuwafundisha waamini ulazima wa kufuata desturi hiyo.Paulo na Barnaba hawakukubaliana nao hata kidogo, kwa kuwa wao walikuwawameona Mungu akifanya kazi kubwa kati ya watu na wengi walipata kuamini nakubatizwa bila tohara, na maisha yao ya Kikristo yalikuwa mazuri na yenye sifaya kumtukuza Mungu.

Basi walihojiana na kushindana nao sana bila mafanikio na waamini wa Antiokiawalikuwa katika hatari ya kuchanganyikiwa. Kanisa liliamua njia bora ni kwaBarnaba na Paulo na baadhi ya waamini kwenda Yerusalemu kusudi swala hilolizungumzwe na Mitume na wazee na uamuzi rasmi ufanyike ili watu wa toharawasizidi kusumbua hao walioamini wa Kimataifa. Tukumbuke hao walioleta shidani Wayahudi ambao wamemwamini Kristo, si Wayahudi wa kawaida.

k.3. Walipotelemka kwenda Yerusalemu Paulo na Barnaba walichukua nafasinjiani ya kuwaelezea watu jinsi WaMataifa wengi walivyomwamini Kristo, naowaliosikia walifurahi sana.

k.4. Pale Yerusalemu walipokelewa vizuri na Kanisa pamoja na Mitume naWazee. Walipewa nafasi ya kuwaeleza wote juu ya uenezi wa Injili kati yaWaMataifa katika nchi walizozipitia.

k.5. Hata hivyo baadhi ya waamini wa Kiyahudi walikazana kudai kwamba nilazima hao waamini wa KiMataifa watahiriwe na kuambiwa kushika Torati yaMusa. Bila shaka walizidi kuhofu walipoona umati wa watu wasio Wayahudiwamemkubali Kristo na kujiunga na Kanisa. Waliogopa kumezwa nao. Piawalifikiri kwamba wapagani wengi wakiingia Kanisa maadili yatapungua hasaikiwa hawatatakiwa kujiweka chini ya Torati.

Page 47: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO709

Kwa hiyo neno lililo mbele ya Baraza lilikuwa wazi - 15:1 "msipotahiriwa kamadesturi ya Musa hamwezi kuokoka" na k.5 "ni lazima kuwatahiri na kuwaagizakuishika Torati ya Musa"

k.6: Mkutano rasmi ulianza wakiwepo mitume na wazee, mkutano mzito na mbeleyake swala kubwa na uamuzi utakaotolewa utagusa kabisa mwenendo waKanisa mbeleni.

k.7. "baada ya hoja nyingi" Watu walipewa nafasi ya kuchanga mawazo. NdipoPetro alipewa nafasi ya kusema.

15: 7-11: Hotuba ya Petro: Aliwakumbusha jinsi Mungu alivyomtumia kwendakwa Kornelio Mmataifa na jinsi Roho alivyomshukia Kornelio na wote waliokuwawamekusanyika nyumbani mwake. Petro aliona ya kuwa hakuwa la kufanyaisipokuwa kuwabatiza bila tohara, sababu Mungu alikuwa amewapokea haliakijua mioyo yao na kuwapa Roho hata kabla hawajabatizwa. Katika k.8-9alisisitiza kwamba Mungu hakufanya tofauti kati ya Wayahudi na WaMataifa, niusafi wa ndani ulio sababu ya Mungu kuwapokea watu.

Ndipo Petro alionyesha msimamo wake akiwakabili wapinzani na kuwauliza"mbona mnamjaribu Mungu"? kwa sababu ni kweli kwamba hata Wayahudiwenyewe walishindwa kuitimiza torati, ambayo ni kama "kongwa" juu ya shingozao, wala haikufaulu kuwapatia haki. Kwa neema na imani watu huwa sawa.

k.12: Ushuhuda wa Barnaba na Paulo: Mkutano ulinyamaza. Petro alikuwaamewaelezea vizuri na kukataa kabisa tohara kwa waamini wa Kimataifa. HalafuBarnaba na Paulo waliwaelezea wajumbe wa Baraza juu ya matukioyaliyoonekana walipoihubiri Injili katika WaMataifa. Mungu aliuthibitisha ujumbewao kwa kuwajalia kufanya ishara na maajabu, na watu walimwamini Kristo, nakubatizwa bila tohara. Walishuhudia ukweli wa imani yao katika maisha yao yakila siku na zaidi katika kukubali dhiki na mateso kwa ajili ya Kristo, dalili za kuwaMungu amewakubali.

k.13-21: Hotuba ya Yakobo akijumlisha yaliyosemwa na kutoa uamuzi Upeoulifika aliposimama Yakobo na kutoa hoja yake. Huyo si Mtume Yakobo maanatumekwisha kuambiwa katika sura 12 juu ya Mtume kuuawa. Yakobo huyohufikiriwa kuwa ndugu wa kimwili wa Bwana Yesu I Kor.15:7, Bwana Yesualimtokea baada ya Kufufuka Kwake. Ameonekana kuwa kiongozi wa Kanisa lapale Yerusalemu. Yawezekana ni yeye aliyeuandika Waraka wa Yakobo.Aliheshimiwa sana, mtu mtaratibu.

Alijenga hotuba yake juu ya Maandiko yaliyosema juu ya WaMataifa kuingizwakatika mpango mzima wa "Mungu. k.14-15. Matokeo ya Wamataifa kuaminikatika miji ya Antiokia, Listra, na penginepo huthibitisha maneno ya manabiiwaliotabiri matokeo hayo. Ni dhahiri ni mapenzi ya Mungu.

Page 48: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO710

k.17. Alitoa uamuzi wake kwamba WaMataifa wasisumbuliwe, walawasilazimishwe kutahiriwa ila waombwe kuepukana na mambo fulani ambayohuwaletea shida Wayahudi wanapotaka kushirikiana na WaMataifa hasa kwakula pamoja Lawi 17 & 18.

Alitoa maneno ya kuwatuliza Wayahudi waliokuwa nguzo katika neno hilo kwakuwakumbusha kwamba kila sabato katika masinagogi mambo ya Musa naTorati yalihubiriwa wala haipo hatari ya desturi zao kutoweka. lIa WaMataifawawe huru nazo.

Kwa hiyo tangu mwanzo wa mkutano mkazo ulikuwa kwamba tangu zamaniMungu ameonyesha mapenzi yake kwa WaMataifa kuingizwa katika IsraeliMpya, jamii ya wote wamwaminio Yesu Kristo. Neno hilo lilionekana katikaMaandiko, lilithibitishwa wakati Mungu alipomtuma Petro kwa Kornelio, nalolilionekana wazi katika baraka za Mungu huko Antiokia na miji iliyofikiwa naBarnaba na Paulo. Watawezaje kumpinga Mungu?

lIa hakuna aliyeuliza juu ya ulazima wa tohara kwa Wayahudi Uzuri wa mkutanohuo ulikuwa katika watu kupewa nafasi ya kutoa mawazo yao, na wahusika kamaBarnaba na Paulo kupata nafasi ya kushuhudia kazi ya Mungu kati ya WaMataifa.

15: 22-35: Barua ya kuuthibitisha uamuzi wao; Sila na Yuda kwendaAntiokiaWalifanya mambo mawili kiutendaji ili kusimamisha uamuzi wao Kwanzawaliandika barua kwa wakristo wa makanisa ya Antiokia, Shamu, na Kilikia,iliyothibitisha uamuzi uliofanyika. Barua hiyo itawasaidia wakati wo wotewatakapopata shida na Wayahudi. Paulo na Barnaba walitajwa vizuri sanawakiwaita "wapendwa wetu" na kuelezwa kuwa watu "waliohatarisha maisha yaokwa ajili ya Kristo". Lugha ya kuzima mashaka juu yao.

Neno la pili kiutendaji lilikuwa kuwatuma wawili wao, wenye sifa nzuri, walio nakipawa cha unabii, kwenda Antiokia kushirikiana na wakristo wa huko. Nao niYuda Barsaba na Sila. Kwa njia hiyo ushirikiano utazidi kujengwa kati ya Kanisala Antiokia na la Yerusalemu.

Kutokana na barua hiyo twajifunza kwamba wale waliokwenda Antiokia nakuwasumbua wakristo hawakutumwa na Kanisa la Yerusalemu.

k.28: Iwapo ni watu waliouongoza mkutano, hasa aliyeushika usukani ni RohoMtakatifu, maana walikuwa tayari kuongozwa na Roho wakitaka mapenzi yaMungu yafanyike kwa swala hilo.

Page 49: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO711

15:30: Kisha Barnaba na Paulo pamoja na Yuda na Sila wakarudi Antiokia.Walipofika wakakusanya jamii ya waamini na kuwapa ile barua, nao walipoisomawalifurahi sana na kufarijika. Walijua itawasaidia kuendelea bila wasiwasi nawale ambao hapo nyuma wamewasumbua hawatakuwa na nguvu yakuwashambulia. Pamoja na hayo walifurahi kuwa na Yuda na Sila waliozidikuwajenga katika imani na maisha ya Kikristo.

15:33-34: Baada ya muda hao wawili waliruhusiwa kurudi Yerusalemu ila Silaakarudi Antiokia baada ya muda mfupi. Barnaba na Paulo pamoja na wenginewaliwafundisha wakristo.

15: 36-39: Barnaba na Sauli kutengana: Barnaba na Yohana Markokwenda Kipro; Sila kujiunga na Paulo.Paulo alipata wazo la kuyarudia makanisa yaliyopandwa katika safari ya kwanza.Barnaba alitaka kumchukua Yohana Marko tena, yule kijana aliyewaacha Pergekatika safari ya kwanza. Paulo alikataa kabisa, hata wakatengana. Kwa nini? Bilashaka kila mmoja alikuwa na sababu zake. Barnaba alikuwa mjomba wakeYohana na huenda Paulo aliona huo udugu ndio unaosababisha Barnabaamchukue. Barnaba kwa tabia alikuwa mwepesi wa kupokea watu nakuwatumaini, ni yeye aliyemleta Paulo kwa Mitume pale Yerusalemu wakati waowalipoogopa kwamba hakuokolewa kwa kweli. Ni yeye aliyetumwa na Kanisakuchunguza mambo pale Antiokia na kufurahia jinsi Injili ilivyokuwa ikienea katiya WaMataifa. Kwa hiyo si ajabu alifikiri kwamba Yohana apewe nafasi tena.

Yawezekana Paulo alifahamu safari hiyo ya pili itakuwa ndefu na ngumu kulikoile ya kwanza, hivyo haitakuwa vema waende na yule aliyeshindwa kumalizasafari ya kwanza.

Mwishowe Barnaba akamchukua Yohana Marko wakaelekea kisiwa cha Kipro,hatujui lo lote juu ya safari hiyo.

Paulo alimchukua Sila wakaelekea kaskazini kwa makanisa ya Shamu naKilikia, halafu Galatia na penginepo.

Iwapo twaweza kusema haikuwa vema wagombane kiasi cha kutengana, hatahivyo Mungu alileta baraka. Kwanza, safari mbili zilifanyika badala ya moja; pili,Yohana Marko alipata nafasi tena; tatu, Sila alipata nafasi kwa mara ya kwanza.

Uzuri wa kwenda na Sila ni kwa sababu alitoka Kanisa la Yerusalemu, na piliinaonekana alikuwa na uraia wa Kirumi kama Paulo alivyokuwa nao.KAO: Inaonekana Kanisa la Antiokia lilikuwa upande wa Paulo na Sila, ila siyokusema walikuwa kinyume cha Barnaba na Yohana

Page 50: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO712

SAFARI KUBWA YA PILI: 15:40-18:22:

15: 40-16:5: Paulo na Sila kuyarudia makanisa yaliyopandwa katikasafari ya kwanza na kumchukua Timotheo kijana:

Paulo na Sila waliondoka ANTIOKIA WA SHAMU. Tofauti na ile safari ya kwanzahawakuvuka mpaka kisiwa cha Kipro kwa sababu Barnaba na Yohanawalikwenda huko. Kwa hiyo walikwenda kwa nchi kavu kaskazini kupitia Shamuna Kilikia (mahali alipotoka Paulo) wakiyathibitisha makanisa ya sehemu zile.Baada ya hapo walikwenda kwa makanisa ya Derbe na Listra na hapowalikutana na kijana• Timotheo, ambaye mama yake alikuwa Mkristo na Myahudiila babaye alikuwa Myunani. Wakristo wa sehemu zile walimsifu sana Timotheokuwa Mkristo mzuri. Kwa sababu alikuwa na baba aliye Myunani Timotheoalikuwa bado hajatahiriwa. Paulo aliona kwamba kwa ajili ya matatizo mengiyaliyosababishwa na Wayahudi wasiotaka kuamini itakuwa vema amtahiri. Kwanini amtahiri? huku nyuma alishindana kabisa na watu wa tohara pale Antiokiana katika mkutano uliofanyika Yerusalemu. lIiyopo ni kwamba imekwishakuamriwa na Kanisa tohara si lazima kwa wokovu. Timotheo amekwishakuokolewa. lIa Paulo aliona vema atahiriwe ili kazi ya kuihubiri Injili isizuiliwe naWayahudi wa sehemu zile, asilete kwazo lo lote lisilo la lazima. Huenda Timotheoaliwekewa mikono na wazee wa Listra I Tim.1:18 4:14 2 Ti.16.

Tunaona kwamba waliwashirikisha waamini wa makanisa hayo ile baruailiyoandikwa na Baraza la Yerusalemu, makanisa hayo yakazidi kuimarika naidadi ya waamini ikakua. Bila shaka matembezi ya Paulo na Sila yalisaidiapamoja na ile barua. Paulo alifahamu kwamba hakuna maana yo yote yakupanda mbegu bila kuipalilia na kuimwagilia na kuitunza.

Tunaposoma Waraka kwa Wagalatia mabadiliko mabaya yalitokea katikamakanisa hayo ya Galatia mara baada ya Paulo kuondoka ilimbidi Pauloawaandikie barua kali sana.

16: 6-10: Kupitia nchi za Galatia na Frigia; kufika Troa.Baada ya kupitia nchi za Frigia na Galatia Paulo na Sila waliona vema waendekuhubiri mahali papya, ila swali ni "waende wapi?"

Inaonekana waliwaza kwenda Asia, ila walikatazwa na Roho Mtakatifu.Hatuambiwi ni kwa njia gani walikatazwa, ila tunaona watumishi hawa walikuwatayari kuongozwa na Mungu. Ndipo wakafikiri kwenda kaskazini mpaka Bithinia,lakini tena ilionekana siyo mapenzi ya Mungu. Hatujui ni kwa njia ganiwalitambua wasiende, twasoma "Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa". PengineRoho alisema nao kwa wazi, au pengine kwa unabii au labda walikosa amanimoyoni au pengine kwa shida za usafiri, hali ya hewa, mvua, vita, n.k.

Page 51: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO713

Si kwamba Injili haitahubiriwa katika sehemu zile ila si katika safari hiyo. Pauloalikuwa mtu aliye na mpango kwa safari zake ila pia alikuwa mwepesi wakuufuata uongozi wa Roho Mtakatifu.

Kwa hiyo waliamua kupitia Misia na kwenda mpaka Troa, mji kwenye pwani yaBahari ya Aegean. Hivyo walikuwa wametoka kusini mashariki mpaka kaskazinimagharibi, na bila shaka walikuwa na maswali mengi mioyoni mwao.

Hatuambiwi juu ya kazi walizofanya pale Troa, na kama waamini walipatikana.

16:9-10: Maono ya Paulo: Pale Troa Paulo alipata maono usiku yaliyomwelekezamahali pa kwenda. Alifunuliwa wavuke hiyo Bahari na kuingia Ulaya, wakielekeamagharibi zaidi. Pengine walikuwa wamezungumza wao kwa wao mahali pakwenda na walihitaji kuhakikishiwa kabla ya kuchukua hatua kubwa ya namnahiyo. Yawezekana jambo lingine liliingilia kati, maana katika

k.10 twakuta mabadiliko ya lugha - mpaka hapa tumeona ni wali. .. , waka ... ilasasa ni tuka .... kama mwandishi Luka yu pamoja nao, dalili ya yeye kukutananao Troa na kuamua kwenda nao walipovuka Bahari na kuingia Filipi. Wenginehuwaza kwamba Luka alikuwa mzaliwa wa Filipi ila wengine hufikiri ni mzaliwawa Antiokia wa Shamu. Kwa vyo vyote ule uhakika walioutafuta waliupata kwanjia ya maono hayo.

16: 11-40: Kuvuka mpaka Makedonia na Kufika Filipi.Twaona utii wao iwapo walizidi kwenda mbali zaidi na mahali walipoanzia.Wakafikia katika mji mmoja mkubwa wa jimbo la MAKEDONIA ulioitwa Filipi. Nimahali wakoloni yaani Warumi walipopenda kuishi. Huenda Wayahudi walikuwawachache maana hatusikii habari za Paulo kwenda sinagogini.

Waanzie wapi? wafanye nini? tukumbuke ni wageni katika mji mkubwa. Basiwakaenda siku ya sabato mahali nje kidogo na pale kando ya mto walikaa mahaliwalipofikiri ni mahali pa sala, na walianza kuzungumza na wanawake kadhawaliokutana pale. Twaona unyenyekevu wao, hawakutafuta makuu, wakaridhikana kusema na hao wanawake.

Mmoja wao alikuwa na biashara ya kuuza rangi ya zambarau, hakuwa mwenyeji,ilikuwa biashara hiyo iliyomleta Filipi. Ameitwa "mcha Mungu" yawezekanaameshirikiana na Wayahudi wakati fulani na kuguswa sana na imani yao.

Aliitwa Lidia. Mungu alifanya kazi moyoni mwake naye alikuwa tayari kabisakuyapokea maneno yaliyosemwa na Paulo. "Bwana aliufungua moyo wake"dalili ya Roho kuwa ulimwenguni akiwashauri watu mioyoni mwao tayari kwawakati ambapo watakapoisikia Injili. Baada ya Bwana kuufungua moyo wakeyeye alionyesha shukrani zake kwa kuifungua nyumba yake na kuwakaribisha

Page 52: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO714

wahubiri ili wawe na mahali pazuri pa kutunzwa wakiweza kutoka na kuingia bilashida.

16:16: Tayari mavuno yaonekana ila kijakazi mmoja aliwaletea shida kwa kupigakelele kila alipomwona Paulo na wenzake. Neno alilosema lilikuwa sawa, lakiniPaulo alisita kuchukua hatua ya kumtoa pepo wa uaguzi aliyekuwa naye kwasababu alitumikishwa vibaya na mabwana wake waliomtumia kwa faida yao. Bilashaka alimhurumia sana. Kisha baada ya muda mrefu akaamua kutoa pepo kwaJina la Yesu, na pepo akamtoka.

16:19 ku: Shida kubwa ilitokea kwa wahubiri, mara hao mabwana walipotambuawamepoteza faida yao. Pepo amemtoka mjakazi na faida imewatoka mabwanawake!! Hawakufikiri faida aliyoipata huyo mjakazi. Bila shaka hii ndiyo sababuPaulo hakutoa pepo mapema maana alitaka kuhubiri na kupata waamini kwanzakusudi asiondoke bila matunda.

Walifanyaje? waliwakamata Paulo na Sila kwa nguvu na kuwaleta mbele yawakuu wa mji na kutumia ukabila katika mashtaka, maana wengi hawakupendaWayahudi. Wakawapiga kwa bakora na kuwatupa ndani ya gereza, hatawakatiwa katika chumba cha ndani na kufungwa miguu kwa mikatale. Kwa vyovyote walifikiri hawataweza kutoroka wala kutoka humo.

Kwa nini Luka na Timotheo hawakukamatwa? Kwa sababu ni Sila na Pauloambao ni Wayahudi, pia hao ni viongozi. Luka alikuwa Mmataifa na Timotheonusu Mmtaifa.

Twaona ya kuwa Injili inapogusa mifuko ya watu watu huwa wakali.

16:25: Itikio la Paulo na Sila lilikuwa la ajabu sana. Tukumbuke walipigwa sanana bila shaka walisikia maumivu makali kwa jeraha zisizotibiwa lakini badala yakulaumu, na badala ya kujihurumia, walimwomba Mungu na kuimba nyimbo -nyimbo gani? za sifa!!! Kwa njia hiyo walikuwa wakitoa ushuhuda mkali kwawafungwa wote waliowasikia. Bila shaka wengi walijiuliza, "watu hawawamefanya kosa gani? kwa nini wamefungwa? wamepata wapi moyo huo mzuri?Na jibu ni, hao ni wafuasi wa Yesu.

k.26: Tetemeko la nchi liliitikisa misingi ya gereza na milango ikafunguka nanafasi ilikuwapo ya kutoroka. Mkuu wa gereza alihofu sana akitaka kujiuaakidhani kwamba wafungwa watakuwa wamekimbia. Kwa nini hawakutoroka?Kwa sababu huenda waliogopa kutoroka walipoona kielelezo cha Paulo na Silakuendelea kukaa; pia walizingatia tukio la tetemeko. Mkuu wa gereza alipoamuakujiua Paulo akamzuia na kumwagiza asijidhuru kwa sababu wafungwa wotewangalimo.

Page 53: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO715

k.28: Kuokoka kwa Mkuu wa Gereza: Baada ya kuhakikisha wafungwa wangalipona kutambua maisha yake yamesalimika mara aliwageukia Paulo na Sila nakuwauliza juu ya wokovu. Moyo wake uliyeyuka kabisa tayari kumwamini BwanaYesu. Dalili ya ukweli wa mabadiliko yake ni jinsi alivyowakaribisha nyumbanimwake saa ileile na kuwaosha jeraha. Ndipo akabatizwa pamoja na familia yake.Kisha wakala pamoja kwa furaha kubwa.Katika habari hiyo ajabu limejengwa juu ya ajabu.

Ajabu ya kwanza ni katika Paulo na Sila kuwa na neema ya kuimba na kumsifuMungu hali wamepigwa sana na kufungwa vibaya.

Ajabu ya pili ni tetemeko la nchi lililoletwa na Mungu kuwaokoa watumishi wake.

Ajabu ya tatu ni katika Paulo na wafungwa kutokutoroka.

Ajabu ya nne ni jinsi Paulo alivyomzuia mkuu wa gereza asijiue, alimpendabadala ya kutafuta kumlipiza kisasi.

Ajabu ya tano ni katika mkuu wa gereza na familia yake kumpokea Kristo nakumshuhudia wazi katika ubatizo.

16:35: Makadhi hawakutaka matatizo mengine basi walituma habari kwambaPaulo na Sila waruhusiwe kuondoka.

k.37: Paulo alikataa kuondoka hivi hivi, maana wamewapiga huku walikuwa nauraia wa Kirumi. Alisema ni juu yao kuja na kuwatoa. Basi wakuu hali wakiogopawatashtakiwa na Paulo wakaja kwa upole na kuomba watoke. Yawezekanaalifikiri jambo hilo litasaidia kanisa changa la pale baada ya wao kuondoka.

k.40: Walipotolewa wakaenda kwa Lidia na waamini na kuwafariji. Walijua haowaamini watabaki pale katika hatari ya vipingamizi mbalimbali, kisha wakawaagana kuondoka.

lIa waamini wa Filipi watakapokutana kwa ibada, mkuu wa gereza na familiayake watakuwa pamoja nao, ukumbusho wa daima wa uwezo wa Mungu.Twaona Luka mwandishi alichagua aina tatu za watu kati ya wote waliookolewapale Filipi kuonyesha uwezo mkuu wa Yesu wa kuwaokoa watu - mwanamkena mjakazi na mkuu wa gereza.

Inaonekana Luka alibaki pale Filipi Mdo.20:5.

Page 54: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO716

17: 1-9: Injili kuhubiriwa Thesalonike:Paulo na Sila na Timotheo waliendelea na safari, hawakukata tamaa walakujihurumia, wala hawakuamua kurudi I Thes.2:2. Walipitia miji ya Amfipoli naApolonia, pengine walilala usiku katika miji hiyo.

Wakaja THESALONIKE mji mkuu wa Jimbo la Makedonia, penye pwani, mji uliona bandari ya kusafirisha bidhaa nyingi, kwa hiyo Thesalonike ulikuwa mjimkubwa wenye mafanikio mengi. Walianza katika sinagogi, na kwa mfulizo wasabato tatu walihojiana na Wayahudi na waliomcha Mungu na Wayunani. Nenowalilozungumza na Wayahudi lilihusu Yesu kuwa Masihi wao na lazima ya Yesukuteswa na kusulubiwa na jinsi neno hilo lilivyotiwa muhuri wakati Mungualipomfufua katika wafu. Kama ambavyo tumeona neno la Msalaba lilikuwakikwazo kwa Wayahudi mahali pote na tangu mwanzo.

Basi wengine walipokea neno hilo na kuamini, hasa wacha Mungu wengi, maanahao walikuwa wamejiunga na Wayahudi na dini yao kwa sababu waliona ni dinibora kuliko dini zao za miungu mingi. Hao waliposikia habari za Kristo walifurahina kuamini. Hata wanawake wenye cheo wa sehemu zile walikata shauri lakumpokea Kristo.

Kwa hiyo ni mchanganyiko wa watu waliovutwa hata wapagani walioabudusanamu I Thes.1:9-I0. Aristarko na Sekundo walitoka kanisa hilo Mdo.20:4 na27:2. Mungu aliwajalia kufanya miujiza na ishara kuvuta usikivu wa watu:I. Thes.1:5.

Paulo na Sila waliendelea kwa muda wakivuta watu, ndipo Wayahudi waliokataakuamini walitunga hila juu yao kama mazoea yao kila mahali. Hasa hawakufurahikuona mafanikio ya Injili, walisikia wivu, kama wenzao wa zamani walivyosikiajuu ya Yesu Mwenyewe, wivu uliosababisha Kifo Chake. Waliwatumia wahuni wamji kufanya ghasia, ndipo wakaenda kuwakamata wahubiri ambao walidhaniwatawakuta kwa Yasoni. Kumbe hawakuwepo, hivyo wakamshika Yasoni nakumleta mbele ya wakubwa wakimshtaki amewapokea watu ambaowamesababisha fitina, watu wanaodai kuwa na mfalme wao, yaani Yesu.Mashtaka hayo yalikuwa mazito, hatari sana kwa wahubiri, maanawamehesabiwa wapinduzi na wasaliti, kwa sababu wamedai kuwa na Mfalmewao wenyewe. Bila shaka asili ya mashtaka ni katika wao kufundisha juu yaUfalme wa Mungu. Yasoni alitozwa dhamana ndipo yeye na wenzakewakaachiliwa.

Inaonekana walipatana na Yasoni kwamba ni lazima hao watu waondoke maramoja.

Adui wa Injili walisema kwamba "watu hawa walioupindua ulimwengu wamefikahuku nako" ni ushuhuda wa ajabu juu ya nguvu ya Injili, kila walipokwendawahubiri watu walipaswa kukata shauri juu ya imani hiyo, na karibu kila mahali

Page 55: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO717

walipingwa. Kwa njia hiyo wengi walipata kuisikia Injili na kufikirishwa kuzingatiamadai ya Bwana Yesu.

Kila mahali shirika la waamini liliachwa ili waendelee kumshuhudia Kristo nakuishi maisha safi ya Kikristo.Baada ya muda mfupi Paulo aliwaandikia Nyaraka mbili.

17: 10-15: Injili kuhubiriwa Beroya:Beroya ulikuwa maili kama 60 kutoka Thesalonike nao wahubiri walikuja usikukwa sababu ya ile shida iliyotokea. Wakaenda sinagogini nao waliwakutawayahudi waliotofautiana sana na Wayahudi ambao wamekutana nao katika mijiwaliyokwisha kupitia. Walitofautiana kwa vipi? Walimsikiliza Paulo kwa makinisana ndipo wakachunguza Maandiko ya Agano la Kale na kulinganisha nakuhakikisha ukweli wa ujumbe wa Paulo. Tena walifanya hivyo kila siku. Kwa hiyoWayahudi wengi waliamini, Wayunani pia waliamini pamoja na wanawake waKiyunani wenye cheo. Sopatro ni mwamini mmoja wa Beroya: 20:4.

lIa shida ilitoka kwa Wayahudi wa Thesalonike waliposikia kwamba wenzaowengi pale Beroya wameamini. Wakaja kuchafua kazi za Injili. Basi waaminiwaliamua kumsafirisha Paulo usiku aende Athene, ila Sila na Timotheowaliendelea kukaa kwa muda ili wawasaidie waamini kustahimili hizo fitina.Ni wazi watu waliona ni Paulo aliye kiongozi hodari. Hivyo ndugu wakamsindikizampaka Athene, maili kama mia tatu, huenda kwa bahari. Pale waliachana nayena kurudi hali wamepewa agizo kwa Sila na Timotheo kuja kwake bila kukawia.(Ling.18:5 I Thes.3:1-2 kuhusu Sila na Timotheo)

17: 16-34: Paulo katika Mji wa Athene:Paulo alisikia upweke alipofika mji huo mkuu wa elimu, mwenye sifa ya kuwa nawasomi wengi, na wafilosofia wengi, na dini nyingi. Mji uliojaa sanamu nyingi zadhahabu na fedha zilizochongwa kwa ustadi sana. Hata walikuwa wameijengasanamu moja kwa "mungu asiyejulikana" wasije wakakosa na kusahau munguawaye yote. Paulo alichukizwa sana alipopita-pita njiani na kuziona sanamu hizona kukuta watu ambao shughuli zao kubwa zilikuwa za kutoa habari na kusikilizahabari za mambo hayo.

Kama ilivyokuwa desturi yake alianzia kwa Wayahudi katika sinagogi.Hatuambiwi matokeo ya kuhojiana nao.

Alijihusisha na watu alipokutana nao siku kwa siku pale sokoni. Pia alizungumzana wafilosofia na wafuasi wao. Kwa njia hiyo habari zake zilienea na watuwalikuwa na hamu ya kumsikiliza na kujua habari mpya za Kristo, hasa kwasababu ya jambo jipya alilolileta la ufufuo wa wafu. k.18b, 31b-32.

Page 56: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO718

Pale Athene palikuwapo mahali maalum kwa watu kutoa hotuba, paliitwaAreopago, kumbe, wakamchukua Paulo mpaka pale ili atoe hotuba maalum.Pengine walitaka kupima mafundisho yake.

17:22-34: Hotuba ya Paulo katika Areopago:Paulo alianza kwa kuvuta usikivu wao kwa kuwasifu kuwa watu wa kutafakarisana mambo ya dini. Halafu alitumia jambo la ile sanamu kwa "munguasiyejulikana" akiwaambia kwamba atawaelezea habari za mungu huyo, kusudiwapate kumfahamu yule wasiyemjua ili wamwabudu kufuatana na alivyo kwakweli. Twaona busara yake hakupuuza ujinga wao wala ushirikino wao.

k.24-29: Aliwafunulia ukweli wa Mungu huyo:

(a) Mungu huyo ni Mwumbaji wa kila kitu mbinguni na duniani:

(b) Mungu huyo yu Hai, na ni Roho, wala hahitaji kitu cho chote kwa sababuYeye ndiye anayetoa kila kitu, uzima, pumzi n.k.

(c) Mungu huyo ndiye Mtawala peke yake, hakuna miungu mingine. Kila taifalimetoka Kwake, naye amewawekea wanadamu mipaka yao.

(d) Mungu huyo hawi mbali kama hahusiki na mambo yetu. La! Yeye yu karibunasi, na sisi tumo ndani yake. Hapo Paulo kwa busara alidondoa maneno yamtunga mashairi wao.

(e) Kwa upole alikemea sanamu zao.

k.30-31: Kisha Paulo alisema kwamba hapo nyuma Mungu alikuwa ameruhusumambo yawe hivyo, akijifanya kama hazioni sanamu zao n.k. 14:16. Hasa kwasababu halikuwepo jibu la kutatua shida kubwa ya wanadamu yaani dhambi,wala haukuwepo mwanga wa kutosha ili watu wautambue ujinga wao, nakumfahamu Mungu kwa jinsi ilivyowapasa. lIa tangu Kuja kwa Kristo badilikokubwa limetokea. Yesu, nuru ya ulimwengu, amekuwa mwanga kwa mataifayote, naye amewapatanisha wanadamu wote kwa Mungu kwa njia ya KufaKwake. Paulo aliwaambia kinaganaga kwamba ni Kristo atakayewahukumuwanadamu wote, na siku imewekwa tayari. Yampasa kila mtu atubu na kuandaakwa siku ile.

Neno hilo ni hakika maana Mungu alilithibitisha kwa kumfufua Yesu.

k.32-34: Itikio la watu: Baadhi walidhihaki neno la ufufuo, wengi wao waliaminikwamba roho ya mtu haifi, hawakuamini ufufuo wa mwili. Mwenyeji mmoja wapale pale aliamini, na mama mmoja Damari ametajwa kuwa aliamini pamoja nawengine. Huenda ni wachache walioamini.

Page 57: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO719

Inaonekana Sila na Timotheo wakaja Athene halafu akawatuma tena kwendaMakedonia. I Thes.3:1-2 .

18: 1-18: Paulo huko Korintho:Paulo aliondoka Athene kwenda mpaka mji mkubwa wa Jimbo la Akaya ulioitwaKORINTHO.

Korintho ulijengwa kwenye shingo ya nchi, mahali pembamba, pakiwa na bandarimbili, Kenkrea na Lekeumu, moja upande wa magharibi na moja upande wamashariki. Bidhaa nyingi zilisafirishwa kutoka bandari moja mpaka ya pili. Kwasababu ya mahali pake kijiografia mji ulisitawi sana nao ulikuwa mji mkubwa waJimbo la Akaya, jimbo ambalo lilisimama peke yake mbali na Jimbo la Makedoniakaskazini yake.

Katika I Kor.2:1-5 Paulo ametuambia jinsi alivyojisikia alipofika Korintho. Penginealisikitishwa na itikio la watu pale Athene. Pia aliona kazi iliyo mbele yake nikubwa sana maana Korintho ulijulikana kuwa mji wa ubaya mwingi, wenyejiwalijaa kiburi na kujiona, kweli itakuwa vigumu kwa Injili kupenya na kutia mizizimaishani mwao.

Alipoanza kazi ya kuhubiri Injili pale Korintho Timotheo na Sila walikuwa badohawajamfikia kutoka Makedonia. Alikwenda kuishi na Wayahudi wenzake Akilana Prisila, pengine aliwakuta pale sinagogini. Hao walikuwa na ufundi wakushona mahema kama yeye. Akila na Prisila walikuwa Wakristo, hatujuiwalipataje kusikia habari za Kristo, pengine huko Rumi, kwa kuwa walikuwawamefukuzwa Rumi kwa amri ya Kaisari. Seutonio mwandishi wa historiaaliandika kwamba Kaisari Klaudio aliwafukuza Wayahudi waondoke Rumi(BK.44) "kwa ajili ya Krestus". Yafikiriwa kwamba fitina ilitokea kati ya WayahudiInjili ilipohubiriwa Rumi kwa hiyo Klaudio alitoa amri ya kuwaondoa pale, haliasitambue tofauti kati ya wakristo na Wayahudi.

18:4: Kama ilivyokuwa desturi ya Paulo alihudhuria sinagogini kila sabato nakutoa hoja zake akiingiza habari za Kristo kati yao akijaribu kuwavuta kwa Kristo.

18:5-6: Kisha Sila na Timotheo walifika kutoka Makedonia nao walileta habarinjema ya makanisa ya Makedonia hasa Timotheo alileta ripoti nzuri juu ya kanisala Thesalonike I The.3:6-8 Paulo alifarajika sana na kutiwa nguvu ya kuendelea.Pia alipata kipawa kilichomsaidia asiwe na sababu ya kufanya kazi kupata riziki:2 Kor.11:8.

Hivyo alikazana kabisa katika kuwashuhudia Wayahudi. Neno ambalolimetumika lina nguvu, ni kama alisikia kusongwa au kubanwa kuwaambia juu yaKristo kuwa Masihi wao na Mtumishi wa kuteswa kama Isaya alivyotabiri.

Page 58: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO720

Wayahudi walimpinga na kumshutumu mpaka Paulo aliamua kuwaacha, yaanikutokuendelea sinagogini, kama alivyofanya pale Antiokia wa Pisidia 13:46,51.Alikung'uta mavazi yake ishara ya uamuzi wake akiwashuhudia wazi kwambahasikii kuwa na hatia juu ya wajibu wake wa kuhubiri Injili kwao. Kwa ishara hiyona kwa maneno yake mazito alitaka watambue uzito na hatari ya kukataa kwao.

Alikwenda kuishi na mtu aliyeitwa Tito Yusto ambaye nyumba yake ilipakana nasinagogi, mahali rahisi kwa watu kumpata. Wayahudi wataweza kuja pale pamojana wenyeji. Hivyo Paulo alibadili mahali pake na huduma yake itawalengaWaMataifa. Krispo mkuu wa sinagogi aliamini k.8.

Wakorintho walifurahi walipoona Paulo ameamua kuwahubiri na wengi waliamini.Mlango ulikuwa wazi. Pia Paulo alitiwa nguvu ya kuendelea kwa maono ya usikuYesu alipomwambia asiogope, tena aendelee kwa sababu Yeye atamlinda, tenaanao wengi ambao watamwamini. Alikaa muda mrefu kuliko mahali po potepenginepo katika safari hiyo.

18: 12-17: Fitina ya Wayahudi:lIa baada ya muda huo mrefu Wayahudi wasioamini hawakuweza kutulia zaidi,wakatunga mashtaka juu ya Paulo na kumleta barazani mbele ya Liwali Galio,mwaka kama BK.51. Alishtakiwa kwamba alikuwa akihubiri dini iliyo kinyume chasheria ya Kirumi.

Lakini Galio na maliwali wa Kirumi kwa kawaida hawakuwa na mzigo juu yaWayahudi na desturi zao za dini. Kila mahali Wayahudi walikuwa na sifa mbayaya kuwa watu wa fitina iwapo walikuwa wamependelewa kwa kupewa ruhusa yakufuata desturi za imani yao.

Galio alikataa kuingia kati na kumhukumu Paulo, akawafukuza waondokebarazani, ndipo waliokuwepo wakamshika Sosthene mkuu wa sinagogi nakumpiga pale pale barazani, na Galio hakujali, akawaachia wafanye walivyotaka.Kwa nini watu walimpiga Sosthene? huenda ni dalili ya chuki yao kwa Wayahudi.Kuna mtu wa jina hilo aliyetajwa na Paulo katika Waraka kwa Wakorintho IKor.1:1. Kama ni huyo kumbe alikata shauri kuwa Mkristo baadaye, ila jina hilolilikuwa la wengi wakati ule.

Tendo la Galio lililinda Wakristo wakati wa Ukristo kudhaniwa kuwa tawi katikadini ya Kiyahudi iliyoruhusiwa.

18:18: Paulo aliendelea kukaa Korintho kwa kuwa alisaidiwa na uamuzi wa Galioakisikia uhuru wa kuendelea kuhubiri Injili. Ni vigumu kujua kikamilifu muda wakemzima wa kuwa huko. Muda ulitosha kumsaidia kuwafundisha imani na maishaya Kikristo, ila kutokana na Waraka wa Kwanza wao walikuwa watu wenyematatizo mengi.

Page 59: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO721

k.18b. Paulo alikuwa ameweka nadhiri alipokuwa Korintho, pengine ni shukranizake kwa Mungu kwa kumlinda pale. Hes.6. Kabla ya kuondoka Kenkrea alinyoakichwa chake dalili ya kutimiza nadhiri.

18: 19-23: Kupitia Efeso na kukutana na Prisila na Akila.Baada ya kuwaaga waamini aliondoka pamoja na Prisila na Akila, wakajaEFESO. Hapo aliwaacha Prisila na Akila (hao walikwenda Rumi baadaye Rumi16:3) Kabla ya kuondoka Paulo alikwenda sinagogini na kuhojiana na Wayahudi.Angaliweza kuendelea ila aliona yampasa arudi mpaka Antiokia mahalialipoanzia safari hiyo ndefu. Kabla ya kuondoka aliwaahidi watu wa Efesokwamba akipata nafasi atarudi. Prisila na Akila walibaki na bila shaka hao walizidikuandaa nafasi kwa Paulo kurudi. Wakapanda meli na kusafiri mpaka Kaisaria,kutoka hapa wakaenda Yerusalemu kuwasalimia wakristo kisha wakarudi mpakaAntiokia .•

Kweli ilikuwa safari ndefu mno, yenye shida na magumu mengi, pamoja namafanikio mengi. Makanisa yalipandwa mahali pengi.

18: 24-28: Apolo kufika Efeso halafu kupelekwa Korintho:Paulo aliamua kwenda tena pamoja na Sila na kuyasalimia makanisayaliyopandwa zamani kwa kusudi la kuwaimarisha waamini katika makanisahayo. Pengine walikuwa na maulizo juu ya mwenendo wa kikristo, huendawalihitaji uongozi katika matatizo mbalimbali na kuelezwa zaidi juu ya imani.

Luka aliingiza habari hiyo hapa kabla ya Paulo na wenzake kufika Efeso kamaalivyowaahidi. Apolo alikuwa Myahudi aliyezaliwa Iskanderia, mji mkubwa wanchi ya Misri, mji uliokuwa na Wayahudi wengi sana. Alikuwa na ujuzi mwingikatika Agano la Kale. Alikuwa na mzigo wa kufundisha habari za Kristo ilaalionekana kuwa na upungufu maana alikuwa amebatizwa ubatizo wa Yohanatu. Alipofika Efeso na kutoa hotuba katika sinagogi Akila na Prisila walimsikia,wakamchukua nyumbani na kumwelimisha zaidi juu ya Kristo ..

Baadaye alisikia wito wa kwenda Korintho kusaidia Kanisa la pale na wakristo waEfeso waliunga mkono wazo hilo, wakamhimiza aende, nao wakawaandikiandugu wa Korintho wampokee. Mungu alimtumia sana, aliwajenga wengi katikaimani hasa Wayahudi, kutokana na ujuzi wake katika Agano la Kale. Paulo katikaI Kor.3 alisema juu yake "mimi nalipanda na Apolo akatia maji". Farakanolilipotokea katika Kanisa la Korintho baadhi ya waamini walidai kuwa "wa Apolo"ila hakuna dalili ya Apolo mwenyewe kuwa sababu yake.

Page 60: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO722

SAFARI KUBWA YA TATU YA INJILI: 18:23-21:17:

19: 1-7: Paulo kufika Efeso na kukutana na wanafunzi walioujua ubatizo waYohana tu:

Paulo na wenzake walikuwa wamesafiri kwa miguu kutoka Antiokia wa Shamukwa kupitia kaskazini kwa Galatia halafu wakaelekea magharibi na kufika Efeso.Kwa siku nyingi Paulo alitamani kuhubiri Injili katika mji huo mkubwa wa Asia, nakabla ya kumaliza safari ya pili alipitia pale na kutoa ahadi kwamba atarudi kwao.

Paulo akakutana na kundi la watu wapata 12 hivi. Wataalamu huwa na mawazotofauti katika kufikiri juu yao kama walikuwa wakristo wenye upungufu fulani auhawakuwa wakristo hasa.

Paulo alianzia kwa kuwauliza maswali. Swali la kwanza lilikuwa juu ya RohoMtakatifu, nao wakakiri kwamba walikuwa hawajasikia bado habari zake.Pengine maana yao ilikuwa hawakujua Roho amekwisha kutolewa, kwa sababuYohana alikuwa amemtaja Roho.

Ndipo Paulo aliwauliza juu ya ubatizo nao wakakiri kwamba wamebatizwaubatizo wa Yohana tu. Paulo akaitika kwa kutoa maelezo jinsi Yohanaalivyowaambia watu juu ya Kristo atakayekuja nyuma yake na ya kuwa watuwatapaswa kumwamini Kristo na kubatizwa katika Jina Lake.

Inaonekana maelezo hayo yaliwatosha, wakabatizwa katika Jina la Yesu, ndipoPaulo akawawekea mikono na Roho akaja juu yao, nao walisema kwa lugha nakutabiri, ishara za wazi zilizothibitisha wameingizwa katika Kristo.

Roho kushuka kwa ishara za namna hiyo kulitokea katika hatua kubwa za ueneziwa Injili; kama wakati wa Pentekoste kwa Wayahudi, na wakati Wasamariawalipompokea Roho, sura ya 8. na Kornelio, Mmataifa wa kwanza, sura ya 10.Ni dalili ya Mungu kutia muhuri yake kwa hatua hizo.

19: 8-12: Huduma sinagogini kwa Wayahudi:Paulo alikuwa amekwisha kujenga uhusiano na Wayahudi wa sinagogi alipopitapale mwisho wa Safari ya Pili 18:19. Alihojiana nao kwa ushujaa kwa muda wamiezi mitatu, ndipo kama ambavyo tumeona mara nyingi wale waliokataakumwamini Kristo walifanya matata na kuleta shida kiasi cha kumfanya Pauloaache huduma yake katika sinagogi na badala yake alitumia darasa la mtummoja jina lake Tirano. Bila shaka walipokezana zamu ili kila mmoja awe nanafasi yake. Yawezekana saa nyingine Paulo alifanya kazi za kujitegemea 20:34.

Page 61: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO723

Wale ambao walikwisha kumpokea Kristo wakaiacha sinagogi na kujiunga naPaulo pamoja na waamini Wayunani. Huduma hiyo iliendelea kwa miaka miwilimpaka neno lasema "wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana".Yawezekana makanisa saba yaliyotajwa na Yohana katika Kitabu cha Ufunuopamoja na makanisa ya Kolosai na Hierapoli yalipandwa wakati huo, huendawengine walifanya uinjilisti huo, siyo Paulo.

k.11-12: Mungu aliuthibitisha ujumbe wa Paulo kwa kumjalia kufanya miujizamikubwa iliyopita kawaida yake, wagonjwa waliponywa kwa kuletewa leso nanguo, na wenye pepo walitolewa mapepo yao.

19: 13-20: Wana wa Skewa:Tumekwisha kupata habari ya Wayahudi waliokuwa wachawi katika 8:9 Simonina 13:8 Elami. Efeso ulijaa mambo ya uchawi na Wayahudi walidhaniwa kuwawenye uwezo wa kupenya siri ya jina la Mungu.

Wana wa Skewa walifanya shughuli za uchawi, nao walipoona mapepoyalitolewa na Paulo kwa kutumia Jina la Yesu walijaribu kufanya vivyo hivyo.Iwapo Jina la Yesu lina uwezo wa kuokoa na kupona na kutoa pepo haliwezikutumiwa ovyo na watu wasiomjua Yesu kibinafsi. Wana wawili wa Skewawalijeruhiwa vibaya pepo alipowarukia. Pepo alikiri kwamba alimfahamu Yesu,pia alimfahamu mtumishi wake Paulo, ila hakuwafahamu hao.

17-20: Neno hilo lilisababisha tukio jema. Watu wa Efeso walipopata kujuayaliyowapata wana wa Skewa waliogopa sana Waliliadhimisha Jina la Yesu.Waamini wengi walitengeneza mienendo yao wakileta vitabu na vifaa vyauganga na kuvichoma moto. Kweli nguvu ya giza na uovu zilishindwa na Neno laMungu lilizidi kuenea na kupenya maisha ya watu.

19: 21-22: Mipango ya Paulo:Muda wa huduma yake pale Efeso ulifikia mwisho. Ilikuwa huduma iliyozaamatunda na kumtia moyo, ila Luka alinyamaza juu ya hatari zilizompata 20:19 IKor.15:32 2 Kor.1:8-10. Alianza kuinua macho yake kwenda Spania kwa kupitaRumi: Ru.15:24,28. Hakutaka kujenga juu ya kazi za wengine, aliona wito wakeni kwenda mahali ambapo Injili haijahubiriwa bado.

Paulo alifikiri kwamba makanisa ya Asia, Makedonia, Akaya na penginepoyamefikia hatua ya kuendelea bila yeye. lIa kwanza imempasa afike Yerusalemuna kukabidhi viongozi lile changizo ambalo makanisa ya Wamataifa yamefanyakwa ajili ya Wakristo maskini wa Yerusalemu I Kor. 16:1.ku. 2 Kor.8 na 9.Ru.15:25.ku. Paulo alikuwa na mzigo sana juu ya hilo changizo akiona lilifaa kwamawili, kwanza kuwasaidia wakristo maskini na pili kuujenga uhusiano mwemakati ya Kanisa la Kiyahudi lililoko Yerusalemu na makanisa ya Kimataifa.

Page 62: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO724

lIa kwanza alikaa Efeso kwa muda mfupi kwa sababu nafasi kubwa kwa Injiliilipatikana, pia wapinzani walikuwa wengi. Akawatuma Timotheo na Erastompaka Makedonia ili waiandae mipango ya kukusanya changizo na viongozi wakwenda nalo ndipo ye ye mwenyewe atawafuata mpaka Makedonia kishawataondoka na kuelekea Yerusalemu. 1 Kor.16:8-9.

Luka hakutaja Timotheo tangu 18:5 alipotoka Makedonia na Sila na kufika kwaPaulo pale Korintho. Twajua alikuwa pale Efeso pamoja na Paulo kwa kuwatwajua Paulo alimtuma kwenda Korintho na Filipi ila hatuna uhakika wa wakati IKor 4:17; 16:10; Fil.2:24. Hatujui kama Erasto huyo ni yule aliyetajwa Rumi16:23; huenda siye.

19: 23-41: Ghasia iliyotokea Efeso:Pale Efeso hekalu kubwa zuri kwa mungu mke Artemi lilikuwepo. Makuhanitowashi na makuhani wa kike walitumika humo na Artemi alihesabiwa kuwamungu mke wa sehemu ile yote na hasa wa Efeso. Jengo hilo lilihesabiwa kuwamojawapo katika maajabu saba ya ulimwengu ule wa zamani.

Kiwanja cha michezo cha Kirumi

Page 63: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO725

Zamani zile mafundi mbalimbali walijiunga katika vyama, na hapo twakuta chamacha wafua fedha. Lengo lao hasa lilikuwa kushirikiana pamoja tofauti na vyamavya wafanya kazi vya siku zetu vinavyolenga kuzipigania haki za wafanya kazi.

Ushuhuda wa nguvu ya Injili umeonekana katika maneno ya Demetrio, kiongoziau msemaji wa wafua fedha. Alisema kwamba kutokana na kazi ya Paulo yakuwafundisha watu kwamba visanamu n.k. havina ukweli wala maana watuwalikuwa wameacha kuvinunua visanamu vilivyotengenezwa na mafundi hao,visanamu vya hekalu na vya Artemi. Biashara yao ilipungua sana kwa sababuwatu wameacha kuvinunua. Yeye na wenzake waliumizwa kwa kukosa mapatokama walivyopata zamani. Lakini Demetrio alikuwa mjanja akataja habari za aibukwa Artemi mungu mke wao, kwa vile watu waliacha kuhudhuria hekalu lake nahivyo mungu mke wao yu katika hatari kubwa ya kudharauliwa. Ikitokea hivyohata heshima ya mji wao na jimbo lao itapungua.

Kwa kuchochewa na maneno kama hayo watu walighadhibika, wakawakamatabaadhi ya wakristo na kuwaleta kiwanjani ili wafanyiwe vibaya. Hao wawiliwalikuwa Aristarko wa Thesalonike na Gayo wa Derbe. Umati wa watuulikusanyika kiwanjani na wengi wao hawakujua sababu za ghasia hiyo. Pauloalizuiliwa na ndugu, pia na wakuu kadha wa mji, asifike kiwanjani. IskandaMyahudi mmoja alijaribu kujitetea ili Wayahudi wasifikiriwe kuwa na sehemukatika habari hiyo, maana wengi hawakutambua tofauti kati yao na Wakristo, naWayahudi kwa jumla hawakupendwa na watu. Watu hawakumjali na walipigakelele "Artemi wa Waefeso ni mkuu" kwa masaa mawili.

Karani wa mji mwenye madaraka katika uongozi wake alisimama na kuwatulizawatu. Aliwaambia wasiwe na wasiwasi, hakuna hatari kwa Artemi wala kwaWaefeso kwa hiyo hawana haja ya kufanya jambo lo lote kwa haraka. Ndipoakawatetea wahubiri akisema kwamba hao hawakusema lolote baya lakumtukana Artemi wala hawakuiba cho chote cha hekalu lake. Halafu alisemakwamba kama Demetrio na mafundi wanataka kuwashtaki Paulo na wenzakebasi wapaswa kutumia njia halali ya baraza na maliwali waliopo. Kishaaliwakumbusha watu wote kwamba wasipoangalia kuna hatari ya kushtakiwa naWarumi kwa ghasia hiyo maana haikuwa na sababu.

Kwa maneno hayo ya busara mkutano ulivunjwa na watu walirudi makwao. Niwazi kwamba mpaka wakati huo Dola ya Kirumi haikuwa na neno juu ya Ukristo,na watumishi wa Injili waliweza kuendelea na shughuli zao.

20: 1-2: Kufika Makedonia na Uyunani:Tumekwisha kuona kwamba Paulo alifikiri muda wa kukaa Efeso umekwisha.Basi baada ya ile ghasia aliwaita ndugu na kuagana nao halafu akaendaMakedonia kwa kupitia Troa - ling. na 2 Kor.2:12-13. Alikuwa na hamu sana yakukutana na Tito na kupata habari za Kanisa la Korintho maana shida kubwa

Page 64: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO726

ilitokea pale na Paulo alikuwa amekwenda kuwaona haraka alipokuwa Efeso, piaalikuwa amewaandikia barua kali, pia alikuwa amemtuma Tito na alitaka kujuahali halisi ya pale. Alipokosa kumkuta Tito pale Troa hakukaa na kuhubiri iwaponafasi njema ilikuwapo, bali aliondoka mara akaenda Makedonia, na alikutananaye huko.

Akayatembelea makanisa yaliyopandwa katika Safari ya Pili, Filipi, Thesalonike,Beroya. Yafikiriwa kwamba wakati huo alivuka mpaka Iliriko Rumi 15:19. Kusudilake lilikuwa kuwaimarisha waamini na kuwatia moyo hali akijua huendahawatamwona tena maana baada ya safari hiyo alikuwa na mpango wa kwendaRumi hadi Spania.

Paulo aliwaandikia Wakorintho Waraka wake wa Pili alipokuwa Makedonia nabaada ya Tito kumpasha habari ya nafuu iliyopo Korintho, Tito alikwenda nawaraka huo. Halafu Paulo mwenyewe akashuka mpaka Korintho na kukaa miezimitatu, bila shaka alikuwa na matatizo mengi ya kuyatatua katika Kanisa hilo.Alipokuwa pale aliuandika Waraka kwa Warumi.

20: 3-5: Paulo aliondoka Korintho na kurudi Troa kwa kupitia Makedonia.Badala ya kurudi Shamu na Yerusalemu kwa njia ya bahari alibadili mpangokwa kuwa alisikia habari za hila ya Wayahudi, wakitaka kumwua huenda kwakumtupa baharini. Basi akapanda mpaka Makedonia na kuvuka mpaka Troa.Alikutana na wale ambao walichaguliwa na makanisa kupeleka changizoYerusalemu, Luka ametuambia majina yao na mahali walipotoka. Twaonawaliwakilisha majimbo mbalimbali, ishara ya jinsi Kanisa lilivyoenea na kukuana dalili ya umoja wa makanisa hayo. Pale Filipi walikutana na Luka tena, taz.lugha ya "sisi" na "tuka .. " "tulipo .. " k.6 na 7.

Hao ndugu waliotajwa wakavuka mpaka Troa na Paulo na Luka wakabaki Filipina kuwafuata baada ya siku kadha.

20: 6-12: Hotuba ndefu ya Paulo pale Troa na Eutiko kuangukakutoka orofani na kufa na Paulo kumrudishia uhai wake.Twaona wakristo walizoea kukutana siku ya kwanza ya juma si kama Wayahudiambao walikutana siku ya saba. I Kor.16:2. Wakristo waliadhimisha Kufufuka kwaBwana wao siku ya kwanza ya juma na kufanya ibada ya Ushirika kama Yesualivyowaagiza.

Paulo alitoa hotuba ndefu sana, bila shaka ilikuwa hotuba ya kuagana nao kwasababu hakukusudia kurudi sehemu zile. Luka ametuambia juu ya kijana Eutikoaliyelemewa na usingizi na kuanguka vibaya hata akafa. Paulo akamkumbatiaakawa mzima tena. Bila shaka ndugu walifarijika sana. Paulo aliendelea kuongeanao hata alfajiri!!!

Page 65: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO727

20: 13-16: Kutoka Troa mpaka Mileto:Troa walikaa juma moja ndipo wote isipokuwa Paulo wakapanda merikebu nakuabiri kwenda Aso. Paulo alikuja Aso kwa miguu, hatujui kwa nini alifanya hivyo,huenda alitaka kuhakikisha kwamba Eutiko yu salama, pia yawezekana alihitajimuda wa kuwa peke yake kwa kuwaza na kuyaombea yote yaliyo mbele yake,maana huko Yerusalemu alifahamu wako Wayahudi wasiomtaka hata kidogo.

Kutoka Aso walipitia pwani-pwani mpaka walipofika Mileto kama maili 30 hivikutoka Efeso. Hapo merikebu ilikaa siku tatu nne hivi kabla ya kuondoka tena.Paulo hakutaka kucheleweshwa kwa kwenda Efeso kwa hiyo aliwaita wazee wamakanisa ya pale waje kwake. Walipofika alitoa hotuba maalumu kwao katikahali ya kuagana nao, ilijaa mausia yake.

20: 17-38: Hotuba ya Paulo alipoagana na wazee wa Efeso:Tukumbuke ya kuwa Luka alikuwepo katika safari hiyo na hotuba hiyo alisikiamwenyewe. Hotuba ilikuwa kwa viongozi wa wakristo katika makanisa yao.Hotuba zingine tulizo nazo ama zilikuwa za uinjilisti, au za utetezi.

Wasikilizaji waitwa "wazee" k 17 na "waangalizi / wachungaji" k.28, watuwalioitwa kutunza, kulisha, na kuangalia kundi la waamini. Siku zile waliwekatimu ya wazee katika kila kanisa.

20: 18b-21 : Paulo alianza kwa kusema juu ya huduma yake pale Efeso. Waowenyewe walifahamu jinsi alivyoishi kati yao. Labda alipoondoka baada ya ileghasia wengine walijaribu kuchafua jina lake na kutia mashaka juu ya nia zake.Aliwakumbusha juu ya unyenyekevu wake na jinsi alivyokubali kunyenyekezwawatu walipomshutumu. Pia machozi yake kutokana na mzigo wa kutaka watukuamini. Tena alipata majaribu na kuwekwa hatarini na hila za Wayahudi.Huduma yake daima ilikuwa ya kuhubiri na kufundisha usiku na mchanahadharani kwa watu, na kwa mmoja mmoja nyumbani. Ujumbe wake ulikazaumuhimu wa watu kutubu na kumwamini Yesu Kristo.

k:22-27: Halafu aliendelea kusema juu ya matazamio ya mbele. Mambo ambayoaliyajua kutokana na ushuhuda wa Roho Mtakatifu kila mahali alipokwenda.Pengine ni manabii katika makanisa waliomjulisha hayo 21:4,11, pamoja na yeye mwenyewe kusikia hayo rohoni mwake. Ni nini iliyo mbele yake? ni dhiki namateso, hasa yatakayompata atakapofika Yerusalemu. Ru.15:31.

Alikubali hayo yote, hakutaka kujisalimisha, kitu kikubwa kwake ni kuitimizahuduma aliyopewa na Bwana Yesu ya kuihubiri Injili na kumaliza mwendo wake.Huenda alikuwa akiwaza nia yake ya kwenda Rumi na Spania:, Kwa hiyoaliwafahamisha wazee hawatamwona tena. Aliwaambia kwamba dhamiri yakeilikuwa safi, kwa kuwa hakujiepusha na kuwaambia kusudi lote la Mungu, yaani

Page 66: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO728

alikuwa amewafundisha kikamilifu ukweli juu ya kumfuata Yesu na magumuyaliyomo.

k.28-35: Baada ya kuwatazamisha nyuma kwa huduma yake Efeso nakuwatazamisha mbele kwa kuachana nao na kwa mateso yanayomngojea hukoYerusalemu alitoa mausia yake.

Kwanza aliwaagiza "jitunzeni nafsi zenu" lazima wajihadhari wenyewe, wawewaaminifu na wa kweli, wajitoe kwa kundi lao.

Pili watunze wakristo waliokabidhiwa, kwa kuwalisha Neno la Mungu, kuwashaurina kuwachunga. Hao waamini ni wa thamani, ni mali ya Kristo wamenunuliwakuwa mali yake pale msalabani Pamoja na hayo ni Roho aliyewawekakuwachunga, maana yake ni kwamba walionekana kuwa watu ambao Rohoamewaandaa kwa kazi hiyo. Kanisa ni mali ya Mungu si mali ya wanadamu, tunahaja ya kukumbuka jambo hilo.

Watahadhari na "mbwa mwitu" yaani waalimu wa uongo watakaojaribu kupenyaKanisa na kusumbua waamini. Paulo aliwaza kwamba hata kati yao wenginewatajiinua na kuvuta watu kuwafuata badala ya kumfuata Kristo. Kutokana naNyaraka za Paulo kwa Timotheo na Tito twajifunza jambo hilo lilitokea baadaye.Si mara ya kwanza wamesikia habari hiyo, Paulo alishuhudia kwamba usiku namchana amewaambia hivyo kwa miaka yote ya kukaa Efeso, tena kwa machozi.

Mwishowe aliwakabidhi kwa"Mungu na kwa Neno la neema yake.Aliwakumbusha tena juu ya kielelezo chake. Hakutamani fedha wala vitu vyao.Yeye na wale waliokuwa pamoja naye walijitegemea kwa riziki na kufanya kazikwa mikono yao wenyewe. Alifunga na maneno ya Bwana Yesu "ni bora kutoakuliko kupokea" maneno yasiyoonekana katika Injili 4 ila ni manenoyanayopatana na mafundisho ya Yesu.

k.36-38: Kuachana na wazee na kuondoka Mileto: Kisha Paulo akapiga magotina kuomba pamoja nao. Wazee walihuzunika sana walipowaza kwambahawatamwona tena, wakamkumbatia na kumbusu halafu wakamsindikiza mpakamerikebuni.

21: 1-14: Safari kutoka Mileto hadi kufika Kaisaria na kukaa na Filipo.k.1: "kujitenga" neno ambalo limetumika hapa lina nguvu ni kama "walijitengakwa shida". Pia katika kifungu hicho twaona Luka mwandishi yu pamoja nao naataendelea kuwa nao "tulipokwisha" "tukafika" ..

Walipanda merikebu na kusafiri kwa kupitia Kosi, kisiwa kidogo, na Rodo kisiwakikubwa, na kufika Patara penye pwani labda walisafiri mpaka Mira. Pale Pataraau Mira wakapata merikebu iliyokuwa ikivuka bahari moja kwa moja

Page 67: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO729

mpaka Foinike, safari ya kama maili mia nane. Wakafika Tiro na katika muda wakungojea merikebu ishushe shehena wakashuka na kwenda mjini kutafutawakristo na kukaa nao juma moja 11:19; 15:3. Hao walimwambia Paulo kwambaRoho anaonyesha kwamba pale Yerusalemu atapata mateso, kwa hiyo asiende.Lakini merikebu ilipokuwa tayari kuondoka Paulo naye alikuwa tayari kuondokana kuelekea Yerusalemu. Wakristo, wazima kwa wadogo, wakawasindikizampaka pwani, hapo wakapiga magoti na kuomba pamoja, kisha wakaachana.

k.7: Kutoka Tiro wakafika Tolemai ("Acre"/"Akko" siku hizi) hapo wakawasalimiandugu ila hawakuweza kukaa nao maana siku ya pili merikebu ikaondoka nakwenda Kaisaria. Hapo ndugu wakashuka wakaenda kukaa kwa muda mrefu naFilipo, mmoja wa wale saba, aliyefanya uinjilisti katika Samaria. Filipo alikuwaamekaa Kaisaria kama miaka 20: 8:40. Alikuwa na mabinti mabikira wanne,waliokuwa na kipawa cha kutabiri.

10-11: Kufika kwa Agabo, nabii: Wakati wa kuwa pale Kaisaria Agabo alikuja(11:27-28). Hali ya kuongozwa na Roho Mtakatifu alitoa unabii kiutendaji kwakujifunga miguu na mikono na mshipi wa Paulo, halafu akasema kwamba aliyenao huo mshipi atafungwa huko Yerusalemu.

12:14: Wenzake Paulo, na Luka mwandishi alikuwa mmojawapo, walimsihiasiende Yerusalemu. Ni mara ya tatu Paulo amepewa maonyo hayo. PengineLuka anataka kutukumbusha jinsi Bwana Yesu alivyowaonya wanafunzi maratatu juu ya mateso yake alipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, safari yake yamwisho.

Lakini Paulo hakukubali kuacha mpango wake. Aliona wenzake wanazidikumletea shida na majaribu "mnafanya nini kulia na kunivunja moyo?". Alikuwaamekaza nia yake, yu tayari kuuawa kwa ajili ya Kristo ikiwa itatokea hivyo.Mwishowe ndugu wakanyamaza na kukubali mapenzi ya Mungu yatendeke.Je! Roho alikuwa na mawili, aende, na asiende, au vipi. Kwa jumla twawezakusema hasa Roho alionyesha yatakayotokea huko Yerusalemu, si kumzuiaasiende.

21: 15-26: Kufika Yerusalemu: Nadhiri ya Wayahudi Wanne:Baada ya muda wa kukaa Kaisaria Paulo na wenzake walitelemka mpakaYerusalemu, mwenendo wa kama siku mbili, maili kama 65. Wakristo wenginewa Kaisaria walisafiri pamoja nao, pia Mnasoni Mkristo wa siku nyingi, ambayealiishi Yerusalemu, ambaye watakaa naye.

Paulo na Luka na wawakilishaji wa makanisa ya KiMataifa walikaribishwa vizurina Kanisa, bila shaka changizo walilolileta lilikuwa dalili ya upendo wa wakristowa makanisa hayo. Kesho yake Paulo na wenzake walikutana na Yakobo, yulealiyeuongoza mkutano mkubwa kuhusu Torati kwa Wamataifa Mdo.15. Huenda

Page 68: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO730

Petro na Yohana walikuwa wameondoka Yerusalemu kwa kuwa kanisa lilikuwalimeenea mahali pengi. Wazee wa makanisa ya Yerusalemu walikuwepo, hatujuiwalikuwa wangapi.

Paulo aliwaelezea jinsi Mungu alivyofanya mengi katika WaMataifa kwa njia yahuduma yake. Waliposikia hayo walimtukuza Mungu sana.

Ndipo Yakobo aliitika kwa kutaja maelfu-elfu ya Wayahudi walioamini, kumbeMungu alikuwa akifanya kazi kwa Wayahudi na kwa WaMataifa. lIa hao waaminiwa Kiyahudi walikuwa na wivu juu ya Torati, nao walikuwa wamesikia uvumiuliosema kwamba Paulo licha ya kutokujali matakwa ya Torati kwa WaMataifahata kwa Wayahudi alikuwa amewafundisha hawana haja ya kutimiza matakwayake.

Kweli Yakobo na wenzake hawakuuamini uvumi huo ila walimtaka Paulo afanyejambo fulani ambalo litapoza huo uvumi. Ni nini walilotaka afanye. Walikuwepowanne waliofanya nadhiri na walitakiwa kupitia katika utaratibu wa kutakaswahalafu kutoa sadaka ya kufunguliwa nadhiri ndipo wataruhusiwa kunyoa vichwavyao. Taz. Hes. 6:14ku. Mdo.18:18. Paulo alishauriwa ajiunge nao katika utakasopia awagharimie sadaka za kufunguliwa nadhiri kusudi iwe dhahiri kwa wote yeyeni Myahudi na yu tayari kufuata desturi hiyo. Akakubali maana neno halikuhusuwokovu bali ushirikiano.

Paulo aliingia hekaluni kwa shughuli hiyo. Ling. I Kor.9:20.

21: 27-40: Ghasia katika hekalu na Paulo kukamatwa:Shida kubwa ilitokea kwa sababu Wayahudi kadha wa Asia walikuwawamemwona Paulo na Mkristo aliyetoka Efeso pale mjini. Hao walipomwonandani ya hekalu walidhani ameingia humo na huyo Trofimo. Basi wakamshikaPaulo huko wakiwataharakisha watu na kuwaita waje kuwasaidia. Walionyeshachuki yao na mashaka yao kwa kusema ni yeye anayefundisha watu wote kilamahali kinyume cha taifa letu na torati na mahali hapa.

Basi habari hiyo ilienea haraka watu wakaja kutoka sehemu zote za mji.Walimkokota Paulo nje wakatafuta njia ya kumwua. Lakini kelele hizo zilimfikiaJemadari wa ulinzi naye akaja na kikosi cha askari, na wale watu walipowaonawakaacha kumpiga Paulo. Paulo akafungwa na minyororo miwili kisha Jemadariakauliza "huyu ni nani?" na "amefanya nini?"

Watu walijibu tofauti tofauti kwa hiyo Jemadari akaamua aletwe ndani ya ngome.Pale darajani walipaswa kumbeba Paulo kwa sababu ya msukumo wa watuwaliopiga kelele na kusema "mwondoe huyo".

Paulo akamwomba Jemadari ruhusu ya kusema na watu. Yule Jemadariakashtuka alipoona Paulo amesema kwa Kiyunani. Alikuwa amemdhania kuwa

Page 69: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO731

mtu fulani aliyesababisha fitina hapo nyuma. Paulo akamjulisha ya kuwa yeye niMyahudi na mzaliwa wa Tarso wa Kilikia. Basi pale darajani Paulo alianzakusema na ndugu zake Wayahudi kwa lugha yao ya Kiebrania ili auvute usikivuwao.

22: 1-21: Utetezi wa Paulo kwa Wayahudi:Aliomba wamsikilize anapojitetea mbele yao katika lugha yao wenyewe.

1-3: Kwanza alisemea juu ya malezi yake ya kuwa Myahudi halisi aliyeelimishwavizuri sana katika dini ya baba zake. Hata alijifunza pale Yerusalemu miguuni paGamalieli mashuhuri wao. Zaidi ya kujifunza tu aliishikilia kikamilifu na kwa bidiisana. Alifanya juu chini kuzuia imani ya Kikristo akiwafunga wakristo wa kiumena wa kike po pote alipowakuta, hata akawafuatia mpaka Dameski alipopewabarua na Kuhani Mkuu kwenda kwa masinagogi yao. Wao walijua habari hizozote.

6-16: Ndipo aliendelea kwa kutoa habari ya kuokolewa kwake wakati wakuukaribia mji wa Dameski Adhuhuri alimulikiwa na nuru kuu iliyozidi nuru yamchana, akasikia sauti ikimwita kwa jina lake "Sauli, Sauli, mbona unaniudhi?"Akapewa jibu la ajabu "Mimi ni Yesu wa Nazareti ambaye wewe unaniudhi".Tukio hilo lilimbadilisha kabisa, lilimwia maisha yake yote. Tangu hapo alimpaYesu utiifu wake wote.

Aliingia Dameski, kipofu, akishikwa na kuongozwa na wale waliokuja pamojanaye. Halafu Anania, aliyekuwa Myahudi safi, mwaminifu, alitumwa kwake.Alipofika alipata kuona tena, kisha Anania akamfunulia wito wake na huduma iliyombele yake ya kwenda kwa Wamataifa kuwahubiri Injili. Anania akambatiza.Paulo alisisitiza sana jinsi ambavyo huyo Anania alikuwa Myahudi halisi.

17-21: Huo utume ulithibitishwa aliporudi Yerusalemu baada ya miaka mitatu.Alikuwa akisali hekaluni, akazimia roho, akamwona Yesu aliyemwagiza aondokeYerusalemu haraka kwa sababu watu hawawi tayari kuupokea ushuhuda wake.Akajaribu kumwambia Bwana kwamba yeye ndiye anayefaa kuwashuhudiaWayahudi maana anafahamu dini yao na hali yao yote na yeye ni mmoja wao.Alidhani watampokea na kusaidiwa na Myahudi mwenzao. Kumbe haitakuwahivyo, kinyume chake watampinga zaidi. Bwana alimhimiza aondoke na aendekwa nchi za Wamataifa. 9:29ku.

22: 22-30: Paulo kudai haki ya uraia wake wa Kirumi:Wakamsikiliza mpaka neno hilo la kutaja WaMataifa. Wakapiga kelele kubwa nakusema "mwondoe, haifai aishi" wakatupa mavazi yao na kurusha-rushamavumbi juu. Jemadari alipoona ghasia hiyo mara akamwingiza ndani ya ngome.lIa bado hajaelewa ni kwa kosa gani na kwa sababu gani Wayahudi walimchukiakiasi hicho.

Page 70: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO732

Jemadari aliamua apigwe kwa mijeledi ili aseme wazi makosa yake.Wakamfunga na kamba tayari kumpiga, ndipo Paulo akawaulizia kama ni halalikumpiga hali ana uraia wa Kirumi na bado hajahukumiwa kuwa na hatia. Akidaaliposikia hayo akaenda na kumpasha Jemadari habari hiyo. Basi Jemadari naaskari wakaogopa, wakamwacha asipigwe.

k.30: Shida ni kwamba mpaka hapo Jemadari hajapata kuelewa kosa lake kwahiyo aliona vema ahukumiwe kwanza na Baraza la Kiyahudi na kuona amehalifusheria zao kwa njia gani. Hivyo aliwaambia Wayahudi wakutanishe Baraza laondipo walipokuwa tayari akamleta Paulo na kumweka mbele yao ili ajitetee.

23: 1-11: Utetezi wa Paulo mbele ya Sanhedrin:Paulo alianza kwa kudai kuwa ameishi kwa dhamiri safi mbele za Mungu katikamaisha yake yote, hata kabla ya kuwa Mkristo na baada ya kuwa Mkristo, kwasababu hata alipoupinga Ukristo alifanya katika hali ya kutokujua na kwa kufikirialikuwa akimpendeza Mungu. 2 Tim. 1:3; Mdo.24:16; 26:9.

Madai hayo yalimkasirisha Kuhani Mkuu kiasi cha yeye kuamuru mtu ampigePaulo usoni, jambo lisilo halali wala zuri. Paulo aliitika kwa ukali "Munguatakupiga wewe, ukuta uliopakwa chokaa" halafu waliokuwa karibu na Paulowakamkemea "Je! unamtukana Kuhani Mkuu wa Mungu?" ndipo Paulo akajibuya kwamba hakujua alikuwa Kuhani Mkuu.

Je! ni kweli hakujua? Yawezekana hakumtambua ikiwa alikuwa hakuvaa vazi laKuhani Mkuu au hakukaa kama mwenye kiti. Tukumbuke mkutano ulikutanishwachini ya Warumi na pengine hawakukaa na kuvaa kama kawaida hasa ikiwawalikutanishwa kwa haraka. Wazo lingine ni kwamba alikuwa na maana yakusema kwamba hakufikiri mtu wa kuagiza apigwe atakuwa Kuhani Mkuu. Labdakatika kelele hakutambua ni yupi aliyekuwa amesema maneno hayo. Auyawezekana kwa shida za macho alikosa kumtambua sawasawa, kama ni hivyokumwambia ni "ukuta uliopakwa chokaa" ni kusema alikuwa na shida ya kuonavizuri, alidhani ni ukuta, kumbe, ni mtu aliyevaa kanzu jeupe, kwa hiyohakumshtaki unafiki. Paulo hakuomba radhi sawasawa bali kama nusunusu.

Yawezekana Paulo alitambua itakuwa vigumu ahukumiwe kwa haki kwa hiyoaliona njia ni kugawa Mafarisayo waliokuwa na tumaini la ufufuo tofauti naMasadukayo ambao hawakuamini ufufuo wala malaika n.k. Alipaza sauti katikaBaraza na kudai kwamba anahukumiwa kwa tumaini lake la ufufuo wa wafu. Nakwake ufufuo wa wafu ulitegemea Ufufuo wa Yesu I Kor.15: 12 ku. kwa hiyoalikuwa akisema kweli. Kwa kusema hivi Mafarisayo na Masadukayowaligombana wao kwa wao na hao Mafarisayo walijiweka upande wa Paulo nakusema kwamba hawakuona uovu wo wote ndani yake. Fujo kubwa ilizidi naJemadari aliogopa kwamba Paulo yu katika hatari ya kupigwa basi

Page 71: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO733

akawaamuru maaskari wamlete ndani ya ngome. Kwa hiyo Jemadari amebakibado hajapata neno kamili juu yake.

Wengine hufikiri Paulo hakufanya vizuri alipogawa hao watu juu ya ufufuo, nikama aliutumia ujanja. lIa kwa upande wa pili wengine wanaona kwamba ilikuwasawa kwa sababu kwa Paulo Ufufuo ulikuwa neno la msingi kabisa. Pia wenginewameona jinsi alivyodai kuwa Farisayo si jambo jema hali amegeuka kuwaMkristo.

k.11: Bila shaka Paulo alianza kufikiri atawezaje kufika Rumi, bado ziko hukumutatu zingine juu yake, bado iko miaka miwili ya kufungwa Kaisaria, pia bado kunasafari ndefu ya hatari nyingi baharini wakati wa kwenda Rumi, Je! kweli atafikasalama. Kweli hakufahamu habari hizo zote, lakini dalili zilikuwapo za shida nahatari kila mahali na kila wakati. Basi Bwana akamjia usiku ule na kumwambiaawe na moyo mkuu kwa maana atajaliwa kufika Rumi na kumshuhudia hukonako. Kwa hiyo wakati wote atakapoanza kuona hofu maono alioupata usiku uleutamfariji na kumtumainisha.

23: 12-22: Shauri la siri la kumwua Paulo:Wayahudi hawakufaulu kumnasa Paulo wakati alipohukumiwa. Basi zaidi yaWayahudi 40 walipatana kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywampaka wamemwua. Walifanya mpango wa siri jinsi ya kufanya. Waliomba wakuuwa Makuhani waombe Baraza likutane tena kana kwamba wanataka kuchunguzamambo zaidi, ndipo Paulo anapoletwa wao watakuwa tayari kumwua njiani. Kwelichuki yao ilikuwa imezidi. Hata hivyo Mungu ajua namna ya kuwaokoa watumishiwake. Mpwa wa Paulo alikuwepo Yerusalemu. Hatujui kama mama yake (dadawa Paulo) alikuwepo pia. Ni mara ya kwanza kupata habari za jamaa wa Paulo.Huyo kijana alisikia habari za hila yao, hatujui alifahamiana na wahusika kiasigani, wala hatujui kama walifahamu Paulo ndiye mjomba wake, kweli Lukahakutoboa wazi habari hizo. lIa alipopata habari hiyo akamwendea Paulo palengomeni na kumwambia vote aliyoyasikia. Ndipo Paulo akamwita akida nakumwomba ampeleke kijana kwa Jemadari, na Jemadari akamsikiliza faraghani.Kijana aliahidi kutunza siri hiyo. Mara moja Jemadari akachukua hatua zakumsalimisha Paulo kwa kumpeleka Kaisaria. Atalindwa kwelikweli njiani - watu470 watamlinda mtu mmoja!!!

23: 23-35: Paulo kupelekwa Kaisaria:

Jemadari aliwatuma na barua kwa Liwali Feliki iliyoeleza jinsi alivyojitahidikumlinda Paulo. Alisema kwamba hakuona kosa lo lote katika Paulo ila mashtakayalikuwa ya dini tu.

Safari ilikuwa kama maili sitini hivi, safari ya siku mbili. Usiku walilala Antipatrina kesho yake wakafika Kaisaria. Hapo liwali Feliki aliahidi kusikia kesi yakewatakapofika washtaki wake kutoka Yerusalemu. Akalindwa katika nyumba ya

Page 72: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO734

uliwali. Bila shaka hayo yote yalitokana na kudai uraia wake wa Kirumi,wakiogopa asije akapata madhara.

24: 1-21: Paulo alihukumiwa mbele ya Liwali Feliki:Bila shaka Wayahudi walishangaa waliposikia kwamba Paulo ameisha kufikaKaisaria, huku wao walikuwa wakitazamia mkutano utakutanishwa Yerusalemuna yeye ataletwa mbele yao. Wale waliopatana na kuapa ya kuwa watamwuanjiani walishindwa kabisa kuitekeleza mipango yao.

Kuhani Mkuu na baadhi ya wazee wakaenda Kaisaria ili kesi isikiwe tena chini yaLiwali Feliki. Wayahudi walimchukua msemi mmoja Tertulo, wakidhani kwambayeye atakuwa na ufundi wa kufanikisha mashtaka yao.Tertulo alianza kwa kumpaka mafuta Feliki, alizidi mno maana Wayahudihawakumpenda Feliki kwa sababu ya ukatili wake. Bila shaka alilengakumlainisha na kumwelekeza upande wao.

Alileta mashtaka matatu juu ya Paulo: kwanza alisema Paulo alikuwa mkorofialiyesababisha fitina kila mahali. Shtaka la hatari kama ni kweli maana ilikuwa juuya Warumi kukomesha fitina kila mahali hasa kama ilihusu upinduzi wa utawala.

Pili, alimshtaki Paulo kuwa mwanzilizi wa dhehebu la Wanazarayo, alitaka Felikiafikiri hao ni kinyume cha imani ya Kiyahudi.

Tatu, alimshtaki kwamba alijaribu kulinajisi hekalu akiwa sababu ya fujozilizotokea na Jemadari alijiingiza na kumwokoa mikononi mwao. Ndani ya nenohilo liko neno juu ya Lisia Jemadari kwa kuwa Wayahudi wenyewe wangaliwezakumhukumu. Kweli wangalihukumu kwa kumwua!!!

k.10-21:Ndipo Liwali akampa Paulo nafasi ya kuyajibu hayo mashtaka. Pauloalianza kwa kusema alifurahi kujitetea mbele ya liwali Feliki, akimsifu, ila si kwakiasi cha kumpaka mafuta kama Tertulo alivyofanya.

Paulo alikanusha kabisa shtaka la kuwa mkorofi. Aliwakumbusha ya kuwaimepita siku 12 tu tangu alipoingia Yerusalemu na ile fitina kutokea. Yeye alikuwaametulia, hakufanya mkutano na watu hekaluni, wala sinagogini, wala mjini. Kwanguvu alisema kwamba hawawezi kulithibitisha neno hilo.

Alijibu shtaka la pili kwa kukubali kwamba ye ye ndiye mfuasi wa "Njia hii". yaaniyeye ni Mkristo, ila Njia hiyo si ya uzushi, si kinyume chao, ye ye anamwabuduMungu wa baba zao na kuamini Maandiko yao na kutumaini ufufuo wa wafukama wao na kujitahidi kuwa na dhamiri safi mbele za Mungu kama wao.

Page 73: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO735

Kimsingi Paulo ni kama wao, yeye si kiongozi wa dhehebu la uzushi Kisha Pauloalikaza tumaini lake la ufufuo wa wafu, yu radhi kushtakiwa kwa tumaini hilo tu,si kwa mashtaka yasiyo kweli. Msimamo wake ni ufufuo wa wafu.

Ilikuwa vigumu kwa Feliki kutoa hukumu kwa kuwa Jemadari Lisia hakuona hatia,wala Sanhedrin 23:29; na Tertulo hakuweza kuyathibitisha mashtaka yake. WaleWayahudi wa Asia waliosema amemwingiza Mmataifa hekaluni hawakuwepo iliwalisimamishe shtaka lao, kwa hiyo Feliki alishindwa kuendelea ila kwa sababualitumaini kupata rushwa k.26 na kwa kufanya upendeleo kwa Wayahudi k.27aliahirisha kesi.

24: 22: Kesi kuahirishwa:Liwali Feliki alisema anafahamu kwa usahihi habari za Ukristo. Mke wake Drusilaalikuwa Myahudi, pengine alipata habari kutoka kwake. Yeye alikuwa binti waHerode Agripa I Md.112:1-23. Feliki alisema atahukumu kesi hiyo Jemadari Lisiaatakapofika, ila Luka amenyamaza hasemi lo lote juu ya kufika kwake. Pauloalilindwa kwa usalama wake, lazima wajihadhari kwa vile alivyokuwa na uraia waKirumi.

Aliweza kutembelewa na rafiki zake, twajua Luka alikuwa naye, na Filipo na bintizake walikaa Kaisaria na waamini walikuwepo 21:8-9: Bila shaka Luka alipatanafasi ya kusafiri Palestina na kukusanya habari za Yesu ili baadaye aiandikeInjili yake.

Feliki na mke wake wakamwita Paulo ili wapate habari za Kristo. Pauloaliwaelezea juu ya Yesu Kristo na kusema nao juu ya haki, kiasi, na hukumuijayo. Kufuatana na maisha yao yasiyo mazuri mambo hayo yalikuwa mazito, naFeliki aliogopa kusikia mambo hayo, hivyo waliachana bila Feliki kuitika vema.Hata hivyo aliendelea kumwita mara kwa mara ila Luka amesema kwambaalitarajia kupata fedha za rushwa akidhani Paulo atakuwa tayari kutoa fedha iliaachiliwe. Feliki alikuwa mkatili na mtu wa tamaa. Baadaye aliondoka na Festoalimpokea. Akamwacha Paulo kifungoni iwapo alishindwa kupata kosa lake,huenda alifanya hivyo kwa kuwapendelea Wayahudi. Bila shaka Paulo alionashida kukaa hivyo kwa miaka miwili alihitaji uvumilivu wa hali ya juu.

25: 1-12: Paulo mbele ya Liwali Festo:

Ilikuwa vema kwa liwali mpya kufahamiana mapema na wakuu waliokoYerusalemu, kwa hiyo baada ya kukaa Kaisaria siku 3 tu akaenda mpakaYerusalemu na kukutana na Kuhani Mkuu na wakuu. Hao hawakuchelewakumwambia habari za Paulo, nao wakamwomba Festo akubali aletwe kwao iliwampeleleze zaidi chini ya uongozi wa Festo mwenyewe. lIa Festo hakutakakukaa huko Yerusalemu kwa muda mrefu kwa hiyo aliwaomba wakuu kadhawarudi pamoja naye wakati atakaporudi. Baada ya kukaa siku chache akarudinao mpaka Kaisaria. Ni vigumu kufahamu Feliki amemwambia nini juu ya

Page 74: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO736

Paulo. Huenda pale Yerusalemu Festo alitafuta nafasi ya kuzungumza naJemadari juu yake.

k.6-12: Mara walipofika Kaisaria Liwali aliketi katika kiti cha hukumu na Pauloaliletwa. Wayahudi walimshtaki mengi sana ila hawakuyathibitisha, maanamashahidi hawakuwepo. Paulo alijibu kwa kuyakanusha mashtaka yao,akionyesha usafi wake, hakusikia amekosa katika maeneo yote waliyotaja, juuya Torati, wala juu ya hekalu, wala juu ya Kaisari. Wayahudi waliingiza mamboya Kaisari kwa sababu walifahamu kwamba Liwali hatajali mambo ya dini.

Liwali apite wapi? Mashtaka hayakuthibitishwa, njia nyofu ilikuwa kumwachiliaPaulo. Lakini ni vigumu kufanya hivyo kwa sababu akifanya hivyo atavuta chukiza Wayahudi ambao wakati wote walikuwa kama mwiba ubavuni mwa watawala,wakiwatisha watatoa ripoti kwa Kaisari, au watafanya ghasia, n.k. Walipotakakufanya kwa haki walibanwa vibaya kama ambavyo ilivyotokea wakati wa Pilatokumhukumu Yesu.

Festo aliona njia ni kumpa Paulo nafasi ya kurudi mpaka Yerusalemu nakuhukumiwa na Sanhedrin, na yeye atakuwapo. Huenda kwa njia hiyo Wayahudiwatatulia.

Paulo alikataa kabisa, aliona kwamba huko Yerusalemu hawezi kupata haki, kwavyo vyote Wayahudi watambana Festo. Pia haoni kosa lake, yu tayarikuhukumiwa hata kuuawa kama kosa likionekana kwake. Hakuridhiana na wazola Festo, kwa hiyo aliomba kesi yake iende mbele kwa Kaisari maana kwa uraiawa Kirumi alikuwa na haki ya kuomba hivyo. Kwa njia hiyo atatoka kabisa chiniya Wayahudi, na Festo atapumua vizuri.

25: 13-27: Paulo mbele ya Mfalme Agripa II na Bernike waliofika Kaisaria:Huyo Mfalme alikuwa mwana wa Herode aliyetajwa katika 12:20 na mjukuu waHerode aliyeishi wakati wa Bwana Yesu. Bernike alikuwa dada yake ilailidhaniwa aliishi na Mfalme kama mke wake. Bila shaka walikuja kumsalimialiwali mpya Festo nao wakakaa muda mrefu.

Liwali alitafuta msaada wa Mfalme katika habari za Paulo aliyekuwa akilindwapale akingoja kwenda Rumi kwa kesi yake kusikiwa. Festo alikuwa ameshindwakumpeleka kwa vile hakujua aandike nini juu ya Paulo, maana mashtakayalikuwa mengi lakini yalikosa uthibitisho, na mengine yalihusu dini ya Kiyahudina habari za Kristo na ufufuo. Kosa hasa juu ya serikali halikuonekana. Paulomwenyewe alikuwa amekataa kurudi Yerusalemu na kuhukumiwa na Wayahudi.Kwa hiyo kwenye ripoti yake aandike nini? aliona ni vigumu maana kama hananeno kamili mbona Paulo hakufunguliwa?

Agripa aliposikia habari hiyo alionyesha nia ya kutaka kumsikiliza Paulo na kuonaanasema nini maana habari zake zimeenea sana. Siku ilifika na Mfalme

Page 75: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO737

na Bernike wakaja kwa fahari nyingi hali wamevaa mavazi ya Kifalme, pia wakuuwa askari na wa mji wakaja. Ndipo Paulo akaletwa.

26: 1-32: Utetezi wa Paulo mbele ya Mfalme Agripa II:

Paulo alishukuru kwa nafasi hiyo ya kujitetea mbele ya Mfalme Agripa maanaalijua anafahamu vizuri desturi na mambo ya Kiyahudi. Aliomba amsikilize kwauvumilivu kwa sababu alijua maelezo yake yatachukua muda.

k 4-8: Maisha yake kama Farisayo: Alianza utetezi wake kwa kuwakumbusha juuya maisha yake alipokuwa Farisayo, jinsi alivyoishikilia kwa bidii Torati na tumainilao la kumpata Masihi na tumaini la ufufuo. Sifa yake ilijulikana sana. Ni ajabukufikiri sasa anahukumiwa na wale waliokuwa na tumaini hilo, kwa kuwamsimamo wake ni katika Mungu kulithibitisha neno la ufufuo kwa kumfufua YesuKristo. Kwa nini ifikiriwa kuwa jambo gumu huku limetokea!!

k 9-11: Maisha yake kama mpinzani wa Wakristo: Aliendelea kwakuwakumbusha juu ya bidii zake katika kuwapinga Wakristo. Alitoa picha yakutisha jinsi alivyowafanyia Wakristo katika masinagogi, akiwashurutishakukufuru, alisema aliwaonea hasira kama mwenye wazimu. Wala hakuridhikakufanya pale pale Yerusalemu tu bali aliwafuatia nje ya Yerusalemu. Aliwafungana walipohukumiwa kuuawa alitoa idhini yake.

Katika juhudi zake aliomba ruksa ya wakuu kwenda mpaka Dameski, akafungasafari kwenda huko.

26:12-18: Kuokolewa Kwake: Aliendelea kwa kutoa ushuhuda wake jinsialivyokutana na Bwana Yesu njiani na jinsi Yesu alivyomtuma kazi kati yaWayahudi na WaMataifa. Alimweka kuwa shahidi wake. Kazi yake ilikuwakuwafumbua macho ili watu waache mambo ya giza na kuenenda katika nuru, nawawekwe uhuru na mambo ya Shetani ili wamtumikie Mungu aliye hai, kusudiwasamehewe dhambi na kupata urithi pamoja na wote waliotakaswa.

k 19-20: Uaminifu wake kwa maono aliyoyapata: Alisema wazi kwa Mfalme"sikuyaasi yale maono ya mbinguni". Amesema neno moja kwa Wayahudi naWaMataifa, neno la kutubu na kumwamini Kristo na kuishi maisha yapatanayona toba.

k.21: Aligusa neno la kukamatwa katika hekalu na jaribio la kumwua. Kwa niniWayahudi walifanya hivyo? Ni kwa sababu ya utume wake wa kuwashirikishaWamataifa baraka za Injili sawa na Wayahudi ili wote wawe sawa.

k.22: Alifundisha nini hasa juu ya Kristo? Alifundisha ulazima wa Kufa Kwake,kama Mtumishi Ateswaye aliyetajwa na Isaya Is. 53. Pia jinsi ilivyopasa afufukekatika wafu, ishara ya kuwa Mungu alikuwa amemkubali na kupokea yote

Page 76: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO738

aliyoyafanya kuwa mapenzi yake. Yesu ndiye nuru kama Isaya alivyotabiri katika42:6; 49:6; 60:3.

k.24: Alipofika hapo Festo alijiingiza kwa sauti kuu. Bila shaka mengi yalipitaufahamu wake, aliona ni msomi wa hali ya juu ila kusoma kwingi kumemgeuzaakili, yu mwenda wazimu. Paulo akakataa: "sina wazimu" k.25, aliyosema ni yakweli na ya akili timamu. Mfalme Agripa alifahamu mambo hayo yote kwa hiyoalikuwa na ujasiri kusema hayo.

k.27: Ndipo Paulo alisema moja kwa moja na Agripa, iwapo ni Mfalmehakuogopa, akamwuliza: "Je! unaamini manabii?"

k.28: Paulo hakumpa nafasi kujibu akajibu badala yake "Najua unaamini". Bilashaka mbele ya umati wa watu ilikuwa vigumu Mfalme akiri lo lote wazi. Kwa hiyoakamwuliza Paulo swali "kwa maneno machache wadhani kunifanya kuwaMkristo?". Bila shaka kwa upande wa Paulo utetezi wake ulilenga kumsaidia nakumleta kwenye kukata shauri.

k.29: Paulo aliitika kwa kusema kwamba haidhuru ni kwa maneno machache aumengi, wala si yeye tu, hata na wote waliomsikia alitamani sana wawe Wakristokama yeye ila wasiwe wamefungwa kama yeye. Hapo mambo yaliishia. Mfalmena Liwali na wengine walitoka wakisema wao kwa wao kwamba hawakuona kosalo lote lililostahili auawe au kufungwa. Mfalme aliona angaliweza kufunguliwakama asingalitaka rufani kwa Kaisari.

SAFARI YA KWENDA RUMI: 27:1-44:

27: 1-8: Kutoka Kaisaria na kupita Mira hadi Kisiwa cha Krete:Hatuambiwi waliondoka wapi ila hufikiriwa kuwa Kaisaria mahali alipolindwaPaulo kwa miaka miwili. Paulo na wafungwa wengine walipanda merikebuwakilindwa na askari na akida wao aliyeitwa Yulio. Luka alikuwemo wakati wotewa safari, kila wakati ni "tu ... tu ... tu ... " na Aristarko wa kanisa la Thesalonikepia alikuwa pamoja nao.

Ilionekana merikebu ilipita pwani-pwani na walipofika Sidoni akida akampa Paulonafasi ya kushuka na kwenda kwa rafiki zake wakati walipopandisha aukushusha shehena. Wakatweka na kusafiri kwa kupitia kisiwa cha Kipro iliwakinge upepo mkali kisha wakafika Mira. Hapo walibadilisha chombo wakapatamerikebu ya kwenda Italia. Warumi walitegemea kupata ngano kutoka nchi yaMisri, na merikebu nyingi zilivuka Bahari ya Kati na kupeleka ngano mpaka Italia.Walianza kupata shida kubwa kwa sababu ya pepo za mbisho, zilizopunguzasana mwendo wao, hata mpaka iliwabidi watafute kupitia chini ya Krete pwanikwa pwani na kupata bandari ya kukaa mpaka hali ya hewa iwaruhusukuendelea. Wakati wa baridi ulikuwa mbaya kwa safari za kuvuka Bahari ya Kati.Wakafika bandari moja, lakini waliona afadhali

Page 77: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO739

waendelee mbele na kukaa bandari nyingine, bandari iliyo nzuri zaidi kwa kukaawakati wa baridi.

27: 9-44: Dhoruba kali; meli kuvunjika; kufika Melita:Paulo aliwaonya wasisafiri mpaka ile bandari nyingine wasije wakapotezashehena, merikebu na watu, ila nahodha na wenzake walimshauri akida kinyumecha Paulo, naye akawasikiliza. Walipoondoka upepo wa kusi uliwasaidia naowakadhani kwamba watafanikiwa kufika mahali walipoazimu.

k.14. Upepo wa Eurakilo: Bahari ya Kati ilijulikana kuwa ya hatari sana wakati wakuvuma kwa upepo wa Eurakilo. Mara nyingi merikebu nyingi zilipotea.Hawakuwa na la kufanya ila kuiachia merikebu ichukuliwe tu. Kitu walichoogopani kupelekwa magharibi na kukwamishwa kwenye mchanga mbaya wa pwani yaAfrika Kaskazini. Hivyo walifanya juu chini isitokee hivyo. Wakipelekwa kwenyebahari wazi watakosa kupata bandari na nchi kavu. Walifanya kazi tano:

Kwanza walipandisha mashua kwa shida ikae juu ya merikebu isiwe inavutwanyuma. Pili wakafunga merikebu kwa kamba na kukaza mbao zake. Tatuwakatua matanga ili yawe kama breki ili wasichukuliwe moja kwa moja. Nnewakatupa sehemu ya shehena. Tano wakatupa vyombo kadha.

Walisafiri bila kuona jua wala ,nyota kwa hiyo walikosa njia ya kutambua wakowapi wakaanza kukata tamaa ya kuwa salama.

k.21-26: Shauri la Paulo baada ya malaika kuzungumza naye Watu walishindwakula, huenda haikuwa rahisi kupika chakula na pengine sehemu ya chakulakiliharibiwa na maji, na labda wengine walikuwa wakitapika-tapika kwa jinsichombo kilivyorushwa na kupigwa na mawimbi na upepo.

Ndipo Paulo alisimama kati yao na kuzungumza nao akiwashauri "iweni na moyomkuu" neno la ajabu wakati ule. Akawaeleza jinsi malaika wa Mungu alivyomjiausiku na kumwambia kwamba merikebu itapotea ila wao wote wataokolewa. Kwavyo vyote yeye apaswa kufika Rumi na kuhukumiwa huko, na kwa sababu hiyoMungu amemwahidi wote wanaosafiri pamoja naye wataokolewa vilevile k.24;ling. na Mwanzo 18:26. Alisema aliuamini kabisa ule ujumbe wa malaika. Alikuwaamepata maono hapo nyuma kabla ya safari hiyo wakati Wayahudi walipokuwawakimwinda-mwinda ya kuwa atafika Rumi 23:11. Tukumbuke kwamba Paulohakuwa mgeni kwa usafiri wa bahari, alikuwa amevuka-vuka bahari katika safariza Injili na mara tatu alikuwa amevunjikiwa meli 2 Kor.11:25

27:27-44: Merikebu kuvunjika: Baada ya majuma mawili hivi walidhaniwamekaribia nchi kavu, kwa hiyo wakatupa bildi ili wapime-pime urefu wakwenda chini. Wakatambua ni kweli wameikaribia pwani fulani, ila wakaogopa

Page 78: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO740

wasije wakapwelea kwenye miamba. Wakashusha nanga nne zilizofanya kazikama breki ndipo wakaingojea asubuhi ili waone wako wapi na pwani ikoje.Paulo alisimama tena na kuwashauri wale chakula ili wawe na nguvu yakujisalimisha, maana walikuwa wamefunga kwa muda mrefu. Yeye alitoakielelezo kwa kuchukua mkate na kumshukuru Mungu na kula. Ndipo wakafuatakielelezo chake, wakala, na kuchangamka. Walihesabu wasafiri kuwa 276. Ndipowakatupa ngano.

Asubuhi mabaharia walijifanya kama wanatupa nanga lakini sivyo, walikuwawakishusha mashua ili wavuke maji na kufika katika pwani na kujisalimisha.Paulo alikuwa macho na kujua mpango wao, basi akawafahamisha askari naYulio akida kwamba mabaharia hao wasipokaa humo watu wote hawataokolewa.Basi Yulio na wenzake wakajali shauri la Paulo na askari wakakata kamba zamashua.

k.39: Asubuhi waliona nchi kavu ila hawakujua ni wapi. Wakajaribu kuegeshamerikebu kwenye pwani ila ikakwama na sehemu moja ilishikwa sana katikamchanga wa chini, na sehemu ya nje ikaanza kuvunjika kwa kupigwa na mawimbi.

Askari waliogopa kwamba wafungwa wataogelea na kukimbia ndipo waowataulizwa juu yao, kwa hiyo wakashauri wauawe. Akida hali akitaka kumhifadhiPaulo akawakataza wasiwaue wafungwa. Alishauri kwamba wenye uwezo wakuogelea waogelee mpaka pwani, wasioweza basi wakamate mbao au kitu chochote na kujitahidi kuifikia pwani. Hivyo wote walisalimika kama Pauloalivyosema, na kama Mungu alivyoahidi.

28: 1-10: Paulo na wenzake katika kisiwa cha Melita; kumponyababa wa Publio, mkuu wa Kisiwa:Walitambua wamefika kisiwa cha Melita. Hali ya hewa ilikuwa mbaya, mvua nabaridi, na wenyeji waliwahurumia na kuwakaribisha vizuri sana. Waliwasha motona Paulo alileta kuni za kuongezea ule moto. Kumbe, katika mzigo wa kuni nyokaalikuwa amejificha, akatoka na kumsonga Paulo mkononi. Wenyeji walipoonahayo wakadhani Paulo ni mtu mbaya ambaye iwapo hakupotea katika tufani sasaamepatikana. Walimwangalia wakifikiri atavimba na kufa, lakini wapi,hakudhuriwa, akawa mzima. Basi wakabadilisha mawazo yao na kumdhania nimungu.

k.7: Mkuu wa kisiwa Publio na babaye: Publio mkuu wa kisiwa aliwafadhili haowatu na kuwaita wakae kwake siku tatu. Baba yake alikuwa ameugua na Pauloalipofahamu neno hilo alimwombea na kumwekea mikono, naye akapona. Ndipowengine walileta wagonjwa wao, nao wakapona. Hatujui kama Luka aliye daktarialisaidia katika matibabu yao.

Page 79: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO741

Wenyeji waliwaheshimu sana na wakati wa kuondoka waliwapa vitu walivyohitaji,maana walipotewa na vitu vyao vyote merikebu ilipovunjika.

28: 11-16: Kufika Rumi, Paulo kukaa miaka miwili hali yakulindwa na askari Rumi:Pale Melita walikaa miezi mitatu kisha wakasafiri na merikebu ambayo vilevileilikuwa imekaa bandarini wakati wote wa baridi. Ilitoka Iskanderia ikiwa na ngano,kama ile nyingine iliyovunjika. Wakafika Sirakusa, mji mkuu wa kisiwa cha Sisilia,wakakaa siku tatu, ndipo wakafika Regio kusini kabisa ya nchi ya Italia, kishawakafika pale Puteoli. Hapa walikuta Wakristo na kukaa nao siku saba.Wakaenda kwa nchi kavu na njiani wakristo wakatoka Rumi na kuwalaki njiani,wengine wakaja maili zaidi ya arobaini mpaka Soko la Apio na wengine zaidi yamaili thelathini mpaka Mikahawa Mitatu. Kumbe safari ngumu inaelekea kwisha,Paulo alimshukuru Mungu alipokutana na wakristo wenzake, akachangamka.Miaka mitatu iliyopita alikuwa amewaandikia Waraka.

28: 17-31: Paulo kuwaelezea Wayahudi na kuhubiri Injili kwa wote waliomjia:Alipofika Rumi Paulo alipewa ruksa ya kukaa katika nyumba yake mwenyewe,alilindwa na askari, huenda alifungwa naye kwa minyororo laini. Yawezekanaakida Yulio alimtetea na kumpatia nafasi hiyo. Kesi yake itangoja mpaka serikaliimeiandaa vema na mpaka mashahidi na washtaki wamefika. Huenda barua yaFesto ilipotea wakati merikebu ilipovunjika.

Luka alikuwa pamoja naye wakati huo wote, bila shaka aliandika mihtasariiliyomsaidia alipoandika kitabu hicho cha Matendo kwa sababu ameandika kilakitu kilichotokea katika safari hiyo.

Huenda hakukaa na Paulo moja kwa moja pale Rumi ila alikuwepo mara kwamara: Filemoni 24: KoI.4:14.

17-31: Paulo akakaa siku tatu ili apumzike baada ya magumu na uchovu wasafari hiyo ngumu, ndipo akawaita wakuu wa Wayahudi waje kwake ili awaelezeevizuri juu ya sababu ya kuwa Rumi hali ni mfungwa.

Katika maelezo alisema mambo matatu hasa: Kwanza hakuwa na neno juu yaWayahudi. Pili yale waliyomshtaki hayakuwa kweli Tatu alipowekwa mikononimwa Warumi hao wangalimruhusu kwa kuwa walishindwa kuona kosa ilaalilazimika kuomba rufani kwa Kaisari Wayahudi walipopinga kufunguliwa kwake.Kwa hiyo hakuwa na neno juu ya Warumi.

Wayahudi walisema hawakuwa na habari ya mambo hayo wala hawakusikianeno lo lote baya juu yake. lIa walisema kwamba madhehebu hiyo ya Kikristoinanenwa vibaya mahali pote. Kwa hiyo itakuwa msaada kama atawaelezea juuyake. Akakubali.

Page 80: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO742

Tukumbuke kwamba Kanisa lilikuwa pale Rumi, lilikuwa na nguvu na sifa Rumi1:8. Hatujui hao Wayahudi walikuwa na uhusiano gani na hao wakristo.

k.23: Katika siku iliyowekwa wengi wakaja kumsikiliza Paulo na kwa siku nzimaalizungumza nao kutoka Maandiko akisema juu ya Ufalme wa Mungu na habariza Yesu Kristo.

k.24: Basi waligawanyika, wengine waliamini na wengine hawakuamini. Kabla yakuondoka Paulo aliwaonya juu ya maneno ya Is.6:9-10 yaliyosema juu ya mioyomigumu na macho yasiyoona n.k. Bwana Yesu alikuwa ameyatumia manenohayo Math.13:14-15 Mk.4:11-12 Yoh,12:37 ku. Itikio lao lilifanana na lile laWayahudi mahali pengi alipohubiri Paulo.

k.28: Kwa sababu wamekusudia kutokuamini neno la wokovu litahubiriwa kwaWaMataifa nao watalipokea 13:46; 18:6; 19:8-9

k.30-31: Kwa miaka miwili mizima Paulo aliwakaribisha wote (Wayahudi kwaWaMataifa) nyumbani mwake. Yawezekana alishona mahema kwa kujipatia rizikipamoja na kukaribisha watu waliomjia.

"kwa ujasiri mwingi" iwapo hakuwa na uhuru wa kwenda hapa na pale hata hivyoalimshukuru Mungu kwa nafasi alizojaliwa na alizitumia kwa kumtangaza Kristo.Bila shaka aliweza kuwashauri wakristo wa Rumi na kuwafundisha. Kwelialifungwa na minyororo na kulindwa na askari lakini hakuzuiliwa nafasi yakuwakaribisha watu na kuwashuhudia. Katika kubadilishana maaskariwaliomlinda wengi wao walipata habari za Kristo.

Kitabu kiliishia hapo, hatujui yaliyompata Paulo baada ya miaka miwili kamaalifunguliwa au vipi. Huenda kesi yake ilianguka kwa kupita muda uliowekwa.Katika nyaraka viko vifungu vinavyotuelekeza kufikiri aliruhusiwa halafuakakamatwa tena baadaye, kisha kuna maandishi yanayosema aliuawa pamojana Petro huko Rumi kama BK.64.

Kwa hiyo Luka alianza Kitabu chake pale Yerusalemu, mwanzo wa Kanisa,akakifunga na habari za Injili kuhubiriwa huko Rumi Jiji Kuu la Dola na mtumemashuhuri kwa Wamataifa.

Ni vema kusoma nyaraka zilizoandikwa na Paulo kwa makanisa yaliyopandwakatika safari zake ili tupate picha ya maendeleo yao.

Page 81: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

MATENDO743

MASWALI YAHUSU KITABU KIZIMA1. Kwa kupitia kila sura fikiri juu ya njia mbalimbali za Roho Mtakatifu

kusaidia Mitume na waamini.2. Orodhesha njia hizo na kuweka mifano mbalimbali kutoka kitabu cha

Matendo.3. Vipingamizi vikubwa vilikuwepo vilivyojaribu kuzuia maendeleo ya Injili.

Vilishindwaje? Toa mifano.4. Ni watu wa namna gani waliochaguliwa kuwa viongozi na wafanya kazi5. mbalimbali katika Kanisa? Toa mifano.6. Umoja wa Kanisa ulikuwa jambo muhimu. Kanisa lilichukua hatua gani

kuuhifadhi umoja? Toa mifano.7. Ni tabia na hali zipi zilizohitajika katika wale waliopanda makanisa

mapya? Je! wahubiri walikuwa na ujumbe mmoja tu? na ujumbe waoulikuwa nini? Wahubiri walijihusishaje na watu wa imani na dini zingine?Waliridhiana na dini zingine? waliona zote ni sawa? Toa mifano?

8. Kulingana na Kanisa la mwanzoni unapotazama Kanisa la siku hiziunafikiri Kanisa laweza kujifunza nini, pia Kanisa linahitaji kurekebishamambo gani?

Page 82: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI744

W A R A K A K W A W A R U M I

Y A L I Y O M O

U T A N G U L I Z I

a. Mwandishi wa Waraka

b. Walioandikiwa

c. Mahali ulipoandikwa Waraka

d. Tarehe ya kuandikwa kwa Waraka

e. Sababu za kuandikwa kwa Waraka

f. Mpango wa Waraka

g. Waraka katika historia na maisha ya Kanisa

UFAFANUZI

SURA 1 - 8: MAELEZO YA INJILI YENYEWE

1: 1- 7 Salaam8-15 Shukrani na Tumaini la Paulo kufika Rumi

16-17 Neno Kuu la Waraka - Haki ya Mungu imedhirishwa katika Injili18-32 Dhambi na Hatia ya WaMataifa

2: 1-29 Dhambi na Hatia ya Wayahudi

3: 1- 8 Makinzano ya Wayahudi9-20 Wanadamu wote ni wenye dhambi na hatia

21-31 Haki ipatikanayo kwa kumwamini Kristo

4: 1-25 Mfano wa Ibrahimu1-8 Kuhesabiwa haki kwa imani si matendo

9-12 Kuhesabiwa haki kulitokea kabla ya Tohara13-25 Ahadi ilitimizwa kwa njia ya imani siyo kwa sheria

5: 1-11 Baraka za kuhesabiwa haki kwa Imani12-21 Kuwa „katika Adamu‟ - kuwa „katika Kristo‟

6: 1-23 Kuunganika na Kristo - Uhuru na dhambi1-14 Kuunganishwa na Kristo hakupatani na dhambi

15-23 Kuwa watumwa wa Mungu-Utumwa unaoleta uhuru

Page 83: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 745

7: 1-25 Kuunganika na Kristo - Uhuru na sheria1- 6 Mfano wa Ndoa

7-13 Sheria na dhambi14-25 Mashindano ya ndani

8: 1-39 Kuunganika na Kristo - Uhuru na mauti1- 4 Roho ni „sheria‟ mpya

5-13 Roho anautiisha mwili14-17 Roho huushuhudia „uana‟ wetu18-25 Roho huudhamini urithi wetu26-27 Roho husaidia udhaifu wetu katika kuomba28-30 Mambo matano makubwa yasiyokataliwa31-39 Upendo wa Mungu na ushindi wa Imani

SURA 9 - 11: TATIZO LA KUTOKUAMINI KWA WAYAHUDI

9: 1- 5 Huzuni ya Paulo juu ya kutokuamini kwa Waisraeli6-13 Ahadi za Mungu hazikutanguka

14-18 Mungu si dhalimu19-29 Mungu ni mtawala30-33 Hasara ya Israeli ni kosa lake yenyewe

10: 1- 4 Mzigo wa Paulo juu ya Wayahudi wenzake5-13 Njia mpya ya haki ni kwa ajili ya watu wote

14-21 Wayahudi hawana udhuru kwa kutokuamini kwao

11: 1-12 Je! Mungu amewatupilia mbali watu wake?13-16 Uhusiano wa Waamini wa Kiyahudi na wa KiMataifa17-24 Mfano wa kupandikizwa katika Mzeituni Mwema25-32 Shabaha ya Mungu ni kuwahurumia wote33-36 Sifa kuu kwa Mungu

12 - 15:13 MWENENDO WA KIKRISTO - KUISHI KWAMUNGU

12: 1-21 Itikio kwa Rehema za Mungu ni kujitoa maisha yote1- 2 Kuwa dhabihu hai3-8 Karama za kiroho ni jinsi ya kuziwaza na kuzitumia

9-21 Upendo ni msingi wa maisha ya Kikristo

13: 1- 7 Mkristo na wajibu kwa serikali na wenye mamlaka8-10 Deni la kupenda

11-14 Umuhimu wa Wakati

Page 84: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI746

14 -15:13 Wenye nguvu na walio dhaifu wa imani‟14: 1-6 Ushauri wa Paulo

7-12 Kuishi kwa Bwana13-23 Uhuru na Wajibu

15: 1-13 Kielelezo cha Kristo

15: 14-21 Mambo ya binafsi22-33 Mipango ya Paulo

16: 1-16 Salaam za Paulo kwa Wakristo kadha wa kadha17-20 Onyo juu ya watu kadhaa21-24 Salaam za watu waliokuwa pamoja na Paulo25-27 Sifa Kuu kwa Mungu

U T A N G U L I Z I

a. Mwandishi wa Waraka:Ni Paulo kama alivyojijulisha katika 1:1. Wataalamu wote hukubali kwamba niPaulo. Ndani ya Waraka umo ushuhuda wa kutosha wa kumthibitisha kuwamwandishi. Ametaja mambo ya binafsi kama mipango yake, kazi zakezilizotangulia n.k. Sehemu kubwa ya Waraka ni kama Hati ya Theologia ambayoinadhaniwa kwamba hati ya jinsi hiyo isingaliweza kuandikwa na mwingine.Mafundisho yaliyomo yaonekana na kupatana na mafundisho katika Nyarakazake, hasa Waraka kwa WaGalatia. Ndani yake ni mafafanuzi ya Ujumbewaliohubiri yeye na Mitume.

b. Walioandikiwa:Katika 1:7 amesema „kwa wote walioko Rumi, walioitwa kuwa watakatifu‟. Kwahiyo, ni wazi alikuwa akiwaandikia Wakristo walioko Rumi. Yeye hakulianzishaKanisa la pale kwa kuwa alikuwa bado hajafika Rumi iwapo mara nyingialikusudia kufika akazuiliwa (1:10,13).Kama si yeye swali ni „kwa njia gani Injili iliwafikia watu wa Jiji hili? Hatujui kwauhakika. Sikukuu ya Pentekoste, Roho Mtakatifu aliposhuka juu ya Mitume nawengine huko Yerusalemu, walikuwapo watu waliotoka Rumi „wageni watokaoRumi, Wayahudi na waongofu‟ (Mdo.1:10). Huenda baadhi yao walirudi wakiwawamemwamini Kristo. Rumi lilikuwa Jiji kuu la Dola ya Kirumi na kama watuwalivyozoea kusema „barabara zote zaenda Rumi‟ watu walienda na kutoka Jijihilo kwa sababu mbalimbali. Wengine kwa ajili ya kazi za binafsi, na shughuli zabiashara na uchumi. Wengine walikuwa na vyeo na kutumika serikalini hivyokwa ajili ya shughuli zao iliwabidi wafike Rumi. Wengine walihamishiwa Rumi.Askari wa kijeshi walizoea kwenda na kutoka Rumi. Pia watalii walizuru Jiji iliwalione maana lilijengwa vizuri sana. Yawezekana kwa njia hizo Habari Njemaya Kristo ilipata kujulikana pale mapema sana.

Page 85: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 747

Japokuwa wengine wamewaza kwamba ni Mtume Petro aliyeanzisha Kanisahilo, wazo hilo ni vigumu kukubalika. Kwanza kwa sababu hamna ushuhuda waPetro akiwa Rumi kabla ya wakati wa Waraka kuandikwa ila upo ushuhuda wakusema Petro na Paulo waliuawa pale kama B.K.64. Ni vigumu kuelewa sababuya Paulo kutokumsalimia wala kumtaja. Katika sura ya 16 alitoa salaam kwawengi ila jina la Petro halipo. Tena Paulo alisema kwamba haikuwa desturi yakekujenga juu ya kazi za mwingine (15:20).

Kutokana na jinsi Paulo alivyowaandikia, inaonekana Kanisa limesimama vizuri,likiwa na mchanganyiko wa waumini wa Kiyahudi na KiMataifa. Huendamwanzoni lilianza kati ya Wayahudi katika masinagogi yao na kufikiriwa kuwamadhehebu ya dini ya Kiyahudi. Wayahudi wengi waliishi Rumi, bila shakabaadhi yao walishikilia sana desturi zao, na baadhi walilegea na kuwa tayarikupokea mawazo mapya.

Sababu za kufikiri hivyo ni kwamba Paulo alipofika Korintho kwa mara yakwanza kuhubiri Injili alikutana na Akila na Prisila, Wakristo ambao walikuwawameishi Rumi, halafu wakafukuzwa pamoja na Wayahudi wengine wakati waKaisari Klaudio kama B.K.49. Mwandishi mmoja wa historia ameandika kwambawalifukuzwa kwa ajili ya fujo iliyotokea kati ya Wayahudi hasa kwa ajili ya mmojaaliyeitwa „Krestus‟, jina hilo limesababisha wengine kufikiri ni „Kristo‟ na ya kuwafitina hiyo ilikuwa kati ya Wayahudi na Wakristo wa Kiyahudi (Mdo.18:2ku).

c. Mahali ulipoandikwa Waraka:Paulo alipokuwa Korintho alikaa na Gayo, na Tertio alikuwa mkalimani wake.Timotheo alikuwa pamoja naye na aliwataja wengine kama Erasto wakili wa mjina baadhi ya Wakristo, akina Lukio, Yasoni, Sosipatro, na Kwarto. Alikaa kamamiezi mitatu, muda wa kutosha kuandika waraka mzito kama huu (Mdo.20:2-3).

d. Tarehe ya Kuandikwa kwa Waraka:Kutokana na jinsi alivyoandika kuhusu mipango yake Paulo alikuwa amekaribiakumaliza safari kubwa ya tatu ya Uinjilisti. Kutoka Korintho alikusudia kuelekeaYerusalemu akichukua mchango uliofanywa na makanisa ya Asia kwa ajili waWakristo maskini wa Yerusalemu. Kwa hiyo, tarehe ni kati ya B.K.55 hadiB.K.57/58 (Mdo.19:21; Rum.15:23-26). Inafikiriwa Fibi aliichukua barua hiyompaka Rumi (Rum.16:1-2).

e. Sababu za Kuandikwa kwa Waraka:Paulo ameonyesha wazi shabaha ya kuandika waraka huo. Shabaha yakeilikuwa kuwatayarisha Wakristo wa Rumi pindi arejeapo akiwa amemalizashughuli zake huko Yerusalemu. Paulo alikuwa ametumia wakati wote tangukama B.K.47 hadi B.K.57 katika kufanya uinjilisti katika majimbo ya masharikiya Kirumi; Galatia, Makedonia, Akaya, Asia n.k. Makanisa yalipandwa katikamaeneo hayo na kuwekwa katika uangalizi wa viongozi wazuri. Matatizo

Page 86: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI748

yalipotokea Paulo alikwenda kuwaona au kumtuma mmoja wa wajoli wake aukuwaandikia barua na wakati wote aliwabeba katika maombi yake. Aliwekwa naMungu kuwa Mtume kwa WaMataifa na kwa kweli katika sehemu zile alikuwaametimiza utume aliopewa. Hivyo alifikiri wakati umefika wa kuwaachia wengineusimamizi wa makanisa hayo na kuelekea maeneo mapya.

Ilikuwa kanuni ya huduma yake asihubiri Injili mahali ambapo watumishiwengine walikuwa wamekwisha kufika. Yeye aliamua asijenge juu ya kazi zamwingine (Rum.15:20) kwa hiyo, alipoona amemaliza kuhubiri katika sehemu zamashariki ya Dola alitafuta maeneo mapya. Hivyo aliona itakuwa vizuri afikeRumi na kushirikiana na Wakristo wa pale, halafu aelekee nchi ya Spania,magharibi ya Italia. Bado alikuwa akitaka kuwa mtangulizi wa kuhubiri Injilimahali papya. Spania ya kusini ilikuwa imetawaliwa na Warumi kwa miakamingi, na ilienea ustaarabu wa Kirumi (Mdo.20:22; Rum.1:10-12; 15:24,28,29).

Bila shaka Paulo aliwaza umuhimu wa Jiji la Rumi katika utawala wa Dola hiyokubwa. Alipenda Kanisa liwe na nguvu ya kutosha ya kugusa maisha ya Dola,likiwa na Wakristo walio tayari kuisimamia Injili na wenye mzigo wa kuieneza.Hivyo aliona kwamba wao waweza kuwa msaada mkubwa kwake wakatiatakapoelekea Spania, na Kanisa la pale Rumi litakuwa kituo kizuri sana.Mwanzoni Kanisa la Yerusalemu lilikuwa kituo cha maana, ndipo Injiliilipopokelewa na WaMataifa wengi, Antiokia wa Shamu ilikuwa kituo chamaana, halafu miji kama Efeso. Kwa upande wa magharibi Kanisa la Rumililifaa sana kuwa kituo. Kama ambavyo tumeishasema Waraka ni kama Hati yaTheologia na ni vema tuulize, kwa nini Paulo aliandika Waraka wa namna hiyouliotaja hasa machache ya kwao? Pengine alitaka Mafundisho Makubwa yaUkristo yahifadhiwe kwa ajili ya Wakristo wote, kwa hiyo, alipeleka „Hati yaTheologia‟ kwa Kanisa la Jiji Kuu kwa niaba ya Kanisa Zima.

Katika 1:11 Paulo alisema kwamba alitaka kuwaimarisha. Tukitazama 14:10 na16:17-18 alitaja kuwepo kwa wengine waliofanya fitina na kuleta vikwazo. Bilashaka Paulo alitaka kuwakumbusha umoja walio nao, wao kwa wao, na kwaKanisa zima. Tunapotazama mambo yaliyomo twaona mkazo juu ya wote kuwawenye dhambi, wote kuokolewa kwa njia ya imani katika Kristo na wote kuwianakatika mpango wa Mungu, wote kuitwa wasaidiane kwa sababu wote wahitajimsaada wa wenzao. Kanisa hili mwanzoni lilikuwa na waumini wengi waKiyahudi na bila shaka hao walikuwa na sauti kubwa, ila baada ya haokufukuzwa na Kaisari Klaudio (B.K.49) Wakristo wa KiMataifa walikuwa wengina hao walipata sauti, hivyo „hali ya hewa‟ ilibadilika. Huenda Wakristo waKiyahudi walipoanza kurudi uvutano ulitokea baina yao na Wakristo waKiMataifa. Yadhaniwa sura ya 14 inatoa mwanga juu ya hali hiyo.

Sababu nyingine ya kuwaandikia alitaka wajiunge naye katika kumwombea.Alitambua kwamba pale Yerusalemu maisha yake yatakuwa hatarini maanaWayahudi kadha walikusudia kumwua (15:31)

Page 87: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 749

f. Mpango wa Waraka:Waraka una sehemu kubwa tatu:1. Sura 1- 8: Maelezo ya Injili yenyewe.2. Sura 9-11: Tatizo la Kutokuamini kwa Wayahudi.3. Sura 12-16: Maadili ya Kikristo.Waraka umejaa matunda ya huduma yake ya Injili kwa upande wa kuiwazakwa kina, na kwa kuihubiri kwa ujasiri kwa watu wa aina zote, na kwakuishindania katika mazingira mbalimbali. Pia una matunda ya ujuzi aliopatakatika huduma ya kuwaimarisha Wakristo wapya na kuziangalia shirika zaKikristo na kuyatatua matatizo yao. Pamoja na hayo ni kupevuka kwa maishayake mwenyewe ya kiroho. Katika Waraka tunayo hazina kuu kutoka kwamtumishi hodari na mwinjilisti wa bidii mno, mpigania Injili mshupavu, mtumwenye ubongo mkali aliyechunguza kwa ndani viini vya Injili na kuviwekawazi.

g. Waraka katika Historia na Maisha ya Kanisa:Waraka huu umegusa sana maisha ya Kanisa. Ni kama kitabu cha kwanza chatheologia. Augustino wa Afrika ya Kaskazini katika karne ya 4 aliguswa sana naWaraka huu. Wakati wa Matengenezo ya Kanisa, karne ya 16, maisha nahuduma ya Luther wa Ujerumani vilibadilishwa sana kutokana na Lutherkupokea fundisho la Kuhesabiwa haki kwa Imani. Hali na mwenendo wa Kanisakatika Ulaya vilibadilika sana kwa sababu ya kuzaliwa kwa Makanisa ya Kiinjilina Kiprotestanti. Katika Uingereza karne ya 18, mchungaji mmoja, jina lakeJohn Wesley aliguswa sana na huduma yake ilibadilika hata akawa mwinjilistihodari, ambaye chini ya Mungu, alisababisha Uamsho kutokea, na madhehebuya KiMethodisti yakazaliwa. Waraka umekuwa sababu ya uamsho mahalimbalimbali, na licha ya hayo yote Wakristo wengi wamebadilishwa kimaishakwa mafundisho yake.

U F A F A N U Z I

SURA YA 1 - 8: MAELEZO YA INJILI YENYEWE

1: 1-7 SalaamKama ilivyokuwa desturi ya wakati ule Paulo alijitambulisha ndipo mbele kidogoalitaja wale walioandikiwa. Alianza kwa kusema kwa kirefu juu yake mwenyewe.Alikuwa bado hajafika Rumi na wengi walioandikiwa hawakumjua isipokuwa kwakuambiwa habari zake. Yeye hakulianzisha Kanisa la pale. Kwa njia ya Warakaalitaka kujihusisha nao vizuri kwa kuwa alikusudia kupeleka Injili sehemu zamagharibi mbele ya Italia na alitaka wajiunge naye na kumsaidia.

Hivyo aliweka mbele yao sifa zake. Kwanza alisema alikuwa „mtumwa wa YesuKristo‟ maana yake alijihesabu kuwa mali ya Kristo aliyekuwa tayari wakati

Page 88: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI750

wote kuyafanya mapenzi ya Bwana wake. Alipenda sana cheo hicho cha„mtumwa‟ hakuona kwamba ni cheo cha dharau bali cheo cha heshima kubwa(Gal.1:1). Mtumwa hakuwa na haki zo zote, alikuwa „mali‟ ya bwana wake nakutumiwa kama alivyotaka bwana wake. Ila tusimfananishe Mungu kama bwanaaliyewatumikisha watumishi wake vibaya, la, ila Paulo alitaka kuonyeshakwamba Mungu alikuwa na haki ya kuongoza na kutawala maisha yake, na yeyePaulo, kwa upande wake, alikuwa tayari kumpa utiifu wake wote. Katika 2Kor.5:14 alisema „upendo wa Kristo watubidishe‟, alimpenda Kristo sana sana nakatika upendo huo alisukumwa ajitoe kufanya mapenzi yake kwa furaha. AlimtajaYesu Kristo mara tano katika sehemu hiyo akielekeza wasomaji wamwaze hasakama „mtumishi wa Kristo‟ potelea mbali wawe wamesikia nini juu yake.Hakuwaandikia kwa sababu alitaka kufanya hivyo ila kwa kuwa alihesabu nisehemu ya wito wake.

Halafu aliendelea kwa kusema „aliyeitwa kuwa Mtume‟ kwa sababu alipokwendaDameski kwa shabaha ya kuwatesa Wakristo alikutana na Bwana Yesu njiani, nawakati ule ule Yesu alimwita na kumpa utume wa kuhubiri Injili, hasa kwaWaMataifa (Mdo.9:6,15,16). Wito wake haukuanzia kwake katika matakwa yake,wala haukutoka kwa Kanisa. Mitume walikuwa wa pekee. Masharti ya kuwaMtume yalikuwa:(a) awe amemwona Yesu hai baada ya Kufufuka Kwake (Mdo.1:21; 1 Kor.9:1;

15:8)(b) awe ameitwa na Yesu Mwenyewe (Mt.10:1-2; Lk.6:12-13)(c) awe amepewa mamlaka na utume wa kuhubiri na kuanzisha makanisa na

kufanya maajabu na miujiza (Mdo.9:15; 26:16; Rum.15:18-20; Gal.1:12; 2Kor.12:12)

(d) awe mtu wa kuzifundisha na kuziweka kuwa kanuni kweli za Imani (2Kor.13:10; 1 Kor.14:37; 2 Pet.3:15-16).

Paulo aliyatimiza masharti hayo yote iwapo hakuwa miongoni mwa wale Mitume12.

Ndipo alitilia mkazo kuitwa kwake akisema „na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu‟maana yake Mungu alimweka kando kwa ajili ya kuhubiri Injili. Tukilinganisha naGal.1:15-16 alisema kwamba alitengwa kwa kazi hiyo hata kabla hajazaliwa,kama Nabii Yeremia zamani. Neno „kutengwa‟ laonyesha jinsi alivyojitoa kabisakatika kuutimiza wito na utume wake akiweka kando mambo mengine yote yamaisha. Hivyo kwa maneno matatu „mtumwa‟ „aliyeitwa kuwa mtume‟ na„kutengwa aihubiri Injili‟ aliweka wazi sifa zake ili waitambue mamlaka yakekatika andiko hilo. Paulo alikuwa na uhakika juu ya wito wake na alijua kabisakwamba kazi yake ni kuihubiri Injili.

k.1b-4 Ndipo katikati ya salaam zake Paulo alitaja ni jambo gani ambaloatalizungumzia katika Waraka na mara moja aliweka msingi wa mamboyatakayofuata. Jambo atakalozungumzia ni Injili aliyoihubiri, ule ujumbe ambaoaliuhesabu kuwa wa maana sana hata kumpita yeye mjumbe wake. Katika k.1b

Page 89: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 751

aliiita „Injili ya Mungu‟ akikaza asili yake ni Mungu si wanadamu. Halafu katikak.3 alisema ni „habari za Mwanawe‟ na katika k.9 alisema ni „Injili ya Mwana wake‟.

„Injili ya Mungu ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabiikatika Mandiko Matakatifu‟. Injili haikuundwa na wanadamu, ni ufunuo uliotokakwa Mungu. Injili yamhusu Mungu Mwenyewe na mambo makuu ambayoameyafanya kihistoria. Kiini chake ni Yesu Kristo, Mwana wake, ambaye Mungualiahidi kwamba atamtuma. Manabii walitabiri habari zake wakitayarisha njia yaKristo kwa kuwatazamisha Waisraeli juu ya Kuja Kwake. Manabii walichaguliwana Mungu kwa kazi hiyo, wakapewa ufunuo na uvuvio wake ili watanguliekusema habari za Kristo. Kwa hiyo, Injili si jambo jipya, ila upya wake ni katikamatendo makuu kuwa yamefanyika hivi karibuni. Si mpya kama wazo jipya aumpango mpya. Ina mizizi katika kazi ya Mungu kwa njia ya Taifa teule la Israeli.Hivyo Injili si jambo jipya ila ni matimizo ya mwenendo wa matendo ya Munguyaliyotangulia.

Injili ni Kristo na kuihubiri Injili ni kumhubiri Kristo na kutangaza habari zake, yalematendo makuu aliyoyatenda katika Kuishi Kwake, Kufa Kwake, KufufukaKwake, Kupaa Kwake na Kuadhimishwa Kwake. Kristo ni kiini cha Injili.Ametajwa mara nne katika vifungu hivi saba. Kutubu na kuamini si Injili ila ni njiaza kushirikishwa baraka zake.

(Tukiuliza kwa nini muda mrefu ulipita kati ya ahadi kutolewa na Kuja kwa Kristoyawezekana mawazo hayo yatatusaidia, ila ni mawazo tu. Muda ulikuwa mrefuili wanadamu wajifunze jinsi ambavyo dhambi hasa ni tatizo lao kubwa piawatambue jinsi jitahadi zao zote hazifaulu kuwaokoa. Pia wajifunze jinsi Mungualivyo na madaraka juu ya mambo yote, Yeye huongoza matukio ya historia nakutimiza mapenzi yake ndani ya matukio hayo. Pia ni kumfumba kinywa Shetaniapendaye kumlaumu Mungu na kutushawishi kufikiri kwamba Mungu si wa haki.Mungu amewapa wanadamu nafasi nyingi na muda mwingi wa kuishi kwajitahada zao wenyewe).

k.3 „habari za Mwanawe‟ Injili yamhusu Kristo ambaye kwa asili ni Mwana wamilele wa Mungu, sawa na Mungu. Huyo Mwana aliyekuwa sawa na MunguBaba alizaliwa mwanadamu katika ukoo wa Daudi (Mt.1:1; Lk.3:31). Alidumukuwa Mwana, ila alipokuwa hapa duniani alikuwa Mwana katika hali ya unyongena unyenyekevu. Ndipo alipofufuka alikuwa Mwana kwa uwezo na nguvu. Nikama hali mbili za kuwa Mwana, alikuwa Mwana katika unyonge wa kuzaliwamwanadamu, kisha alikuwa Mwana katika nguvu kwa kufufuliwa na RohoMtakatifu. (Rum.9:5; Flp.2:6ku. Kol.1:19;2:9; Rum.8:3,32; Gal.4:4; Mdo.2:36).Kwa maneno „aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi‟ tumeambiwa chanzo chakekihistoria, na kwa maneno „alidhihirishwa kwa uweza‟ tumeambiwa hatuanyingine katika historia yake. Kwa kuzaliwa alifanyika kuwa mwanadamuambapo hapo nyuma hakuwa mwanadamu.

Page 90: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI752

Kudhihirishwa ni neno la kuonyesha kwamba uwezo wake uliofichwausionekane alipokuwa katika mwili, kwa Kufufuka Kwake umeonekana.Alitangazwa rasmi na kwa wazi kuwa yule ambaye wakati wote ni „Mwana waMungu‟ (Mdo.2:36; Efe.1:20ku. Flp.2:ku. 1 Pet.3:21-22; 1 Kor.15:45; 2Kor.3:17-18). Tusiwaze kwamba alipandishwa cheo, ni vema tukumbuke yakuwa wakati wote alikuwa Mwana wa Mungu, katika Kudhiliwa Kwake, na katikaKuadhimishwa Kwake, katika kuwa Mtumishi na katika kuwa Bwana; katikahuduma ya hapa duniani, na katika utawala wake mbinguni.

„kwa jinsi ya mwili‟ Alikuwa mwanadamu kwelikweli, kwa mwili na roho, kwaufahamu na hekima (Yn.1:14; Gal.4:4; Lk.2:52; Ebr.2:14ku). Akawa mwanadamuhalisi kama sisi.„katika ukoo wa Daudi‟ Kwa nini Paulo aliingiza maneno hayo? Mungu alitoaahadi ya pekee kwa Mfalme Daudi. Kwa Hawa alitoa ahadi kwa wanadamu wote(Mwa.3:15) ndipo alitoa ahadi kwa Abramu kuonyesha kwamba Kristo atazaliwaMwebrania, ndipo alitoa ahadi atazaliwa katika kabila la Yuda (Mwa.49:10)halafu alitoa ahadi atazaliwa katika familia na nyumba moja ya Mfalme Daudi (2Sam.7:11ku. Is.9:7: 11:1). Katika Injili yake Mathayo aliweka ukoo wa Masihikutoka Ibrahimu na kupitia kwa Daudi na Luka aliweka ukoo wa Kristo kuanziakwa Adamu, wote wawili wakimthibitisha Kristo kuwa Masihi aliyeahidiwa.

k.4 Ni ufufuo uliomdhihirisha Yesu kuwa alivyo kweli, Yesu Kristo Bwana wetu.Yesu ni Jina la kumwonyesha kuwa Yesu wa kihistoria aliyezaliwa mwanadamu,lina maana ya Mwokozi (Mt.1:21). Kristo maana yake ni Masihi, yule aliyetiwamafuta ya Roho Mtakatifu kwa kazi ya Kuokoa na Kukomboa. Zamani za Aganola Kale Mfalme, Kuhani, na Nabii ni watu waliotiwa mafuta. Ni Mungu aliyemtiamafuta kwa kazi yake. Bwana ni Jina la Kifalme. Jina linaonyesha kwamba Yesuamepewa mamlaka yote mbinguni na duniani (Mt.28:18-20). Ni Bwana wetu kwakuwa tumeunganika naye ili tuwe waaminifu na watiifu wake. Bwanalinatukumbusha „Yehova‟ Jina la Mungu katika Agano la Kale.

k.5 Halafu Paulo alisema kwamba katika Kristo yeye alipewa neema na utumeili kwa kazi yake WaMataifa waletwe kwa Kristo kusudi wajitie chini ya Ubwanawake. „wapate kujitiisha kwa imani‟ Ilikuwa kazi yake kuihubiri Injili nakuwafahamisha watu kwamba Mungu anawaamuru kutubu na kuamini, wajuewamepaswa kutii kwa kumwamini Kristo katika utayari wa kufanya mapenzi yake(6:17; Mdo.17:30; 1 Yoh.3:23). Tunapokataa kuamini tunamwasi Mungu poteleambali maisha yetu yakoje. Hasa dhambi kubwa ni kutokumwamini nakutokumpokea Kristo. Kuamini ni tendo la utii.

Twaona kwamba katika kifungu hicho Paulo ametaja tena utume wake, kwakuwa alitaka Wakristo walioko Rumi wajue kwamba yeye ni Mtume sawa naakina Petro na Yohana na wengine. Wakati wote alishangaa kuona jinsi Mungu

Page 91: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 753

alivyomwokoa na kumweka awe Mtume. Aliona alitendewa kwa ajabu kinyumecha ustahili wake. Wakati ule ule alipookolewa aliitwa kuwa Mtume(Mdo.9:5,15-16; 26:12-18; Gal.1:15-16; 1 Tim. 1:12-16). Ni kwa neema yaMungu tu aliwekwa kuwa Mtume (Rum. 12:6; 15:15). Kwa neema Mungualimchukua „wa kwanza wa wenye dhambi‟ (1 Tim.1:12-17) na kumteua kuwaMtume (Mdo.9:15-16). Neema si hali fulani ya kusikia, wala kitu cha hewani, balini tendo la fadhili ambalo limeimarishwa katika Kristo na kupitia Kwake. Karamaaliyopewa kuwa mtumishi wa Injili hasa kwa ajili ya WaMataifa ilimwezesha nakumtosheleza aitimize huduma yake. Mungu kwa neema yake huwajalia watuwake karama za kufanya huduma mbalimbali. Katika kuhubiri Injili shabaha hasailikuwa kuleta watu, si kumwamini Kristo tu, bali zaidi, baada ya kumwaminiwafanye mapenzi yake, yaani wamtii, kusudi kuamini kwao kusiwe jambo jepesila kuwafurahisha tu, bali liwe jambo zito la kuwagharimia maisha yao. Hayo yotesi kwa baraka zao tu, bali zaidi kwa sifa na heshima ya Kristo Mwenyewe.

k.6 Ndipo Paulo aliwageukia Wakristo wa Rumi, na kama alivyojieleza habarizake katika mwanga wa imani ndivyo alivyoendelea kwa kueleza haowalioandikiwa jinsi walivyo katika mwanga huo huo. Kwanza alisemawalikuwemo miongoni mwa wateule wa Kristo. Watu waliopendwa na Mungu,walioitwa kuwa watakatifu. Sababu ya wao kuwa Wakristo ni Mungu aliwapenda,Mungu aliwahurumia na kuwaokoa. Kwa njia ya Injili waliitwa kumwamini Kristona wito huo ulikuwa na nguvu na matokeo na kwa uwezo wa Roho Mtakatifuwakaitika vema. Mungu aliwaita kuwa watakatifu, walitengwa na ulimwengu iliwamwishie Mungu. Tukilinganisha na kifungu cha kwanza wao wamekuwa sawana Paulo katika kuteuliwa na Mungu na kuitwa na kutengwa. Katika pendo laMungu wamefungamana. Maneno „teule‟ „kuitwa‟ „watakatifu‟ ni manenoyaliyotumika katika Agano la Kale kuhusu Israeli, sasa yahusu Israeli Mpya yaMungu, yaani Kanisa. Neno „watakatifu‟ ni neno lihusulo Wakristo wote, katikaAgano Jipya halitumiki kwa mtu mmoja mmoja wala Mtume mmoja mmoja.

Kama ilivyokuwa desturi yake, Paulo aliwatakia zile baraka kubwa za Injili,neema na amani. Neema ya Mungu ni upendo wake bure kwa wasiostahili, nikupokelewa na Mungu na kuletwa kwenye uhusiano mwema naye, kwa njia yaYesu Kristo. Amani ni tunda la neema hiyo, kwa sababu mwenye dhambialiyesamehewa dhambi zake na Kristo, ule uadui uliokuwapo kati yake na Munguumeondoka, na hana hofu ya kumkaribia Mungu wake kwa njia ya Yesu Kristo.Kwa hiyo, katika baraka hizo Paulo aliwatakia kila baraka iliyopo kwa Mkristo.Baraka hizo zatoka kwa Mungu Baba yetu. Mungu ni „Baba‟ kwa Mkristo, ni„yetu‟ kwa sababu tumeletwa katika uhusiano mpya kwa njia ya Yesu Kristo.Halafu Paulo alitumia maneno „na Bwana Yesu Kristo‟. Neno „na‟ lina maanakubwa sana, linamweka Yesu sawa na Mungu Baba na kuonyesha kwambaYeye ni Mwana wa Milele wa Baba. Tangu mwanzo Wakristo

Page 92: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI754

walimwadhimisha Kristo mno na kumweka sawa na Mungu Baba kuwa asili namtoaji wa baraka za Injili.

1:8-15 Shukrani, na Tumaini la Paulo kufika RumiKama ambavyo tumekwisha kuona Paulo alitaka kufika Rumi na kushirikiana naWakristo ambao wengi wao walikuwa bado hawajapata kumwona. Hivyoaliandika Waraka huo kwa lengo la kuwatayarisha kwa kufika kwake. AlipoanzaWaraka alitaja Injili na mbele aliendelea kuvifunua viini vyake ili wawe naufahamu kamili juu yake na juu ya ujumbe aliohubiri na msimamo wake.Walikuwapo watu waliomwonea shaka kwa sababu walisikia kwamba kilaalipokwenda shida na fitina zilitokea.

Katika vifungu hivi alisema kwa kibinafsi ili ajenge uhusiano mwema nao.Kwanza alimshukuru Mungu sana kwa ajili yao wote na kwa sababu imani yaoilisifiwa sana mahali pengi hata mahali pa mbali. Yeye pamoja na Wakristo wakila mahali walitiwa moyo waliposikia habari ya waumini wenzao walioishi katikaJiji kuu la Dola na kujua bendera ya Injili ilipepea katikati yake.

k.9 Iwapo yeye hakulianzisha Kanisa la pale Rumi, wala hakuwajua wengi wao,hata hivyo daima aliwaombea. Tazama vifungu hivi kuona tabia ya Paulo katikakuwaombea Wakristo wa makanisa mbalimbali - Efe.1:3; Flp.1:3ku; Kol.1:3, 1The.1:2; 2 Tim.1:3; Flm.4. Ni jambo jema sana kuwaombea Wakristotunaowafahamu, na ni jema zaidi kuwaombea wengine wa nchi nyingine ambaohatujapata kuwaona. Ni vema tukumbuke ya kwamba Paulo alikuwa mtu washughuli nyingi mno, wa safari nyingi, wa taabu nyingi, mtu wa kwenda hapa napale katika kuhubiri Injili na kama alivyosema katika 2 Kor.11:27-28 „baghairi yayote maangalizi ya makanisa‟ yalimgharamia wakati wake mwingi, hata hivyo,alikuwa mtu wa maombi, alijitoa kuwakumbuka waumini katika shirika zao.Twakumbuka mfano wa Yesu Mwenyewe ambaye aliamka mapema sanaasubuhi ili aombe.

Yote aliyofanya Paulo alifanya kwa kumtumikia Mungu kwa moyo wake wote,kwa dhati, na kwa kweli. Hakuhesabu ni kazi tu, au mambo ya kufanywa kwambinu za kibinadamu, bali kwake ilikuwa wito wa kufanya „kwa roho‟ kamautumishi wa kiroho. Tena alijibana katika shughuli za Injili, maana ndani ya „Injiliya Mwana wake‟ umekaa utajiri wote (Efe.3:8).

„Mungu ni shahidi wangu‟ kwa maneno hayo Paulo alitaka kuondoa wasiwasiwao kuhusu kutokufika kwake hapo nyuma na alitaka kuwahakikishia ukweli wania yake ya kufika na wa upendo wake. Maneno hayo yanaonyesha kwambaPaulo alikuwa tayari wakati wote kuongozwa na Mungu. Hii ni dalili yakushirikiana kwa ukaribu sana na Mungu wake.k.10-13 Alikuwa na hamu sana ya kuwaona na aliomba hasa ajaliwe nafasi yakufika Rumi. Alifikiri ni mapenzi ya Mungu apate kushirikiana nao, ndipo baadaya kushirikiana nao aende magharibi ya Italia mpaka Spania ili aihubiri Injili

Page 93: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 755

mahali ambapo uinjilisti bado haujafanyika (ling. na Sura 15). Ilikuwa desturiyake asijenge juu ya kazi za wengine (Rum.15:20). Ilimbidi awe mwangalifukatika kuwaandikia ili wasiwe na maswali kama „kwa nini anataka kuja kwetu?‟

Alisema wazi kwamba alitaka kuwaletea baraka ya kuwaimarisha ila hakutoboawazi ni baraka ipi, huenda ni kuwapa mafundisho zaidi. Kwa hiyo,, yeye atawapakitu na tunapoangalia k.12. yeye pia atapata kitu kwao, akisema „tufarijiane(maana yake tutieni moyo, tujengane) mimi na ninyi, kila mtu kwa imani yamwenzake‟. Aliamini kwamba Wakris to wanapokutana kila mmoja hujengwa nakutiwa moyo anapoona kazi ya Mungu katika maisha ya mwenzake. Ndivyo ilivyokila wakati na kila mahali. Hakuna „wa kupata‟ tu wala hakuna „wa kutoa‟ tu. Sikuhizi Wakristo katika makanisa ya magharibi, makanisa ya zamani yenye urithi wamiaka mingi wamebarikiwa sana kwa kuona imani ya Wakristo „wapya‟ katikamakanisa yaliyopandwa hivi karibuni na kufaidi kipawa chao cha uinjilisti.Yawezekana Paulo aliwaza kwamba atajaliwa kuzidisha hali ya kuaminiana katiya Wakristo wa Kiyahudi na wa KiMataifa, ila hakutaka kusema neno hilo wazi.

k.13 „sipendi msiwe na habari...‟ ni usemi ambao Paulo alipenda kuutumia(Rum.11:25; 1 Kor.10:1; 12:1; 2 Kor.1:8; 1 The.4:13). Alitaka wafahamu kwambaalikuwa amejaribu kuja kwao mara nyingi ila nafasi haikupatikana. Hatujui ni ninihasa iliyomzuia ila bila shaka sababu mojawapo kubwa ilikuwa shughuli zakenyingi. Ndipo alirudia kutaja kuwa „na matunda kwenu‟, yaani kuvuna matunda.Matunda gani? Matunda ya kupata waumini wapya? matunda ya kuwajengawaumini katika maisha yao ya kiroho? Huenda aliwaza atapata nafasi yakuwafundisha zaidi juu ya Injili hata kufafanua mafundisho mazito yaliyomokatika Waraka huo. Alitaja WaMataifa, kama hao ndio walio wengi pale.

k.14-15 Kisha akataja jinsi alivyojisikia mwenyewe kuhusu Utume wake. Si maliyake, bali ni mali ya watu wote. Alihesabu analo deni la kumwambia kilamwanadamu Habari Njema za Kristo, wa kila kabila na rika na ustaarabu. Alisikiakudaiwa na aina zote za watu kuwaambia Habari Njema za Kristo. Aliona niwajibu wake, si kwa Mungu tu, bali kwa wanadamu pia, maana wotewameumbwa na Mungu na wote wamekombolewa na Kristo. Injili ilikuwa „hewa‟yake aliyoipumua daima, tazama jinsi alivyosema katika Flp.1:12-21. Ni vemasisi nasi tuwe na mzigo huo. Je! tuna mzigo gani juu ya watu wa makabilamengine, au wa Mataifa mengine? Ni vema tukumbuke ya kuwa ni kwa sababuwengine walikuwa na mzigo juu yetu sisi wenyewe tumepata habari za Kristo,kwa hiyo,, ni juu yetu kuona ya kuwa na wengine pia wanapata habari Zake.

1:16-17Neno Kuu la Waraka - Haki ya Mungu imedhihirishwa katika InjiliPaulo alipoanza Waraka mawazo yake yalitawaliwa na Injili na Injili iliendeleakuongoza yote aliyoyasema. Aliieleza kinaganaga na kuvifunua viini vyake na

Page 94: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI756

sababu zake na umuhimu wake katika kukabili na kutengeneza haja kubwa yawanadamu. Yeye hakujua neno lo lote lingine lenye maana kuliko Injili.

k.16 Alianza hoja yake juu ya Injili kwa kusema kwamba hakusikia aibu juu yakena zaidi aliionea fahari kubwa (Gal.6:14). Iwezekanaje mtu aone aibu?Inawezekana mtu aone aibu kwa sababu ni habari ya mtu aliyezaliwa Palestina,nchi isiyokuwa na sifa, na katika nyumba ya watu maskini. Alifanya kazi yauseremala, halafu akauawa kwa kutundikwa msalabani kwa aibu kubwa kamamhalifu wa hali ya juu na zaidi kama mtu aliyelaaniwa na Mungu (Gal.3:13).Wengi hawakukubali kwamba alifufuka katika wafu. Watu walishindwa kukubalikwamba „mtu wa namna hii‟ aweza kuwaokoa! tena kwa kifo chake!! Ujumbe huoulivuta dhihaka za Wayunani na kuwa kikwazo kwa Wayahudi (1 Kor.1:18,23).Pia Injili inawanyenyekeza wanadamu wote kwa sababu inawaonyesha kwambakwa uwezo wao na matendo na jitahada zao hakuna hata mmoja atakayeokoka.

Kwa Paulo, huyo Yesu alikuwa Mwana wa Mungu, na Mwokozi wa ulimwenguambaye kwa Kufa Kwake aliukomboa ulimwengu. Ndiyo sababu Paulo, licha yakuionea Injili haya, hata akasikia fahari kubwa juu yake na juu ya wito wa kuwamhubiri wake. Hakuionea haya hiyo Injili kwa sababu ni uweza wa Mungu wakuwaokoa wanadamu. Injili si itikadi bali ni tendo la nguvu. Warumi walijua mengijuu ya uwezo wa kibinadamu. Walitawala Dola kubwa, eneo kubwa sana lenyenchi nyingi ndani yake kutoka magharibi hadi mashariki. Majeshi yalilinda amanindani yake na mipakani mwake, meli zilitawala Bahari ya Kati, barabara nzuriziliunganisha nchi za Dola na kurahisisha usafiri na kusababisha usitawi wauchumi. Kwa sheria nzuri na mipango mizuri utawala wao ulikuwa mzuriuliowaridhisha wengi.

Ila Paulo alikuwa akiusema „uweza‟ wa tofauti sana „uweza wa Mungu uletaowokovu‟ tena wokovu wa tofauti sana, si wa kuokoa nchi na vita au balaa, aumisiba, au maafa, ila uwezp wa kuwaokoa wanadamu na dhambi zao. Injili nihabari ya nguvu katika udhaifu (2 Kor.12:9) utajiri katika umaskini (2 Kor.8:9)uzima katika mauti (Gal.2:19-20). Mwana wa Mungu alisulibiwa kama mhalifu(Flp.2:6ku). Aliyekataliwa na ulimwengu ndiye aliyeteuliwa na Mungu (1Kor.1:18-31). Ili wokovu uwe wa Mungu peke yake bila kutegemea hali au tendolo lote la wanadamu. Tendo la wokovu Mungu amelifanya kwa njia ya Yesu Kristo.

Wanadamu hutamani sana „uwezo‟ wa kuwaokoa na hofu zao za uchawi,mashetani, na mamlaka ya giza; uwezo wa kisiasa wa kuwashinda mabeberu namaonevu yao; uwezo wa kiuchumi wa kushinda njaa, umaskini, ukosefu wamaendeleo ya kisasa; uwezo wa teknolojia (elimu ya ufundi) wa kuwainua nakuwapatia nafasi kati ya nchi za maendeleo. Ila uwezo wa aina hiyo si „uwezo‟au „wokovu‟ aliozungumzia Paulo.

Page 95: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 757

Uweza wa Mungu unalenga wokovu. Ni wokovu wa kuokoa na ghadhabu nahukumu yake (Rum.5:9). Pia ni wokovu wa kuleta uumbaji mpya wa jamii mpyaya wanadamu utakaokuwepo baadaye. Ni wokovu wa kurudisha hali njemazilizopotezwa katika Anguko la wanadamu; dhambi kushindwa na utu wemakushinda na wanadamu kuishi tena katika ushirikiano mwema na Mungu. Niwokovu wa kuleta tumaini la uzima wa milele na kuokoka na ghadhabu yaMungu. Ni wokovu unaotazamiwa na uumbaji wote (Rum.8:18ku).

Injili ni kwa akina nani, Mungu anawaokoa watu gani? Jibu ni „kwa kila aaminiye‟.Uwezo una Mungu, kwa kuwa ni Yeye aliye na uwezo na mamlaka juu ya nguvuza uovu zinazofunga wanadamu. Ila kila mtu ameitwa kuitika Habari Njema kwakuiamini na kwa kujikabidhi Kwake Kristo aliye Mwenyewe Habari Hiyo. Mfano niumeme, umeme una nguvu ndani yake ila kabla ya ile nguvu haiwezi kufanyakazi ya kuleta mwanga au kuleta moto, mtu anatakiwa kubonyeza kidude fulanindipo nguvu ya umeme inapita mpaka kwenye taa au chombo. Mambo yatabaka, kabila, cheo, elimu, mali, n.k. hayahusiki, ni imani tu inayotakiwa. Hainamaana kwamba watu wote wataokoka, ila wokovu ni kwa ajili ya wote, hakunamtu awezaye kusema „Mungu hawezi au hataki kuniokoa‟.

k.16b Paulo amekwisha kusema ni kwa kila aaminiye, ndipo aliongeza „kwaMyahudi kwanza na kwa Myunani (ye yote asiye Myahudi) pia‟. Maana yake sikwa Wayahudi tu, wala si kwa Wayahudi kwa sababu ni Wayahudi, balikihistoria wokovu ulianzia kwao. Bila shaka walikuwapo watu waliofikiriWayahudi hawakuhitaji wokovu wakidhani kwamba ni kwa WaMataifa hasa.Wayahudi waliteuliwa ili wafanye maandalio ya Kuja Kwake Kristo (Yn.4:22). Ilawokovu si kwa hao tu, bali ni kwa kila mtu asiye Myahudi pia. Hao ni sawa naWayahudi, ila Wayahudi walitangulia kwa sababu waliteuliwa kwa ajili ya hayomaandalio. Neno hilo Paulo atalifafanua katika sura za 9-11. Mkazo wake nikwamba wote ni wenye dhambi na wote wanahitaji wokovu.

Imani ni itikio la mtu kwa Injili, katika maana ya kujikabidhi kwa Kristo halafukuishi maisha yanayopatana na matumaini ya kuishi pamoja na Kristo katikauzima wa milele.

k.17 Ndipo Paulo alitaja kiini cha Injili „haki ya Mungu inadhihirishwa ndaniyake‟. Neno „kudhihirishwa‟ linaonyesha asili ya Injili ni nje ya wanadamu,haikubuniwa na wanadamu wala kuletwa na wanadamu. Ni nini hasa ambayoimeonyeshwa? Jibu ni Haki ya Mungu. Kwa sababu neno hilo ni neno kuu laWaraka ni vema tuchunguze maana yake.

Kwanza, twajua haki ni tabia mojawapo ya Mungu Mwenyewe, Yeye ni Mwenyehaki, mkamilifu, na mnyofu katika tabia zake zote, hamna kosa au hitilafu ndaniyake (Mwa.18:25). Yeye afanya kila neno kwa usawa na uadilifu wake ni wa juusana, hakuna awezaye kumfikia „hamna mwenye haki hata mmoja‟ (Rum.3:10).

Page 96: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI758

Tukiunganisha neno „wokovu‟ (k.16) na „haki‟ (k.17) twaona kwamba Munguadhihirisha haki yake katika kuwaokoa watu wake kama Nabii Isaya alivyoona.Kwa hiyo, katika Waraka huo hasa maana ya haki yahusu utendaji wa Mungu.Bila haki mtu hawezi kuokoka, na sisi wanadamu hatuna haki hiyo. Basi imekuwakazi ya Mungu atupatie haki hiyo. Yeye huwapa wenye dhambi haki yake. Kwatendo la ajabu la upatanisho kwa njia ya Kristo sisi wenye dhambitumekaribishwa na Mungu, tumepata kibali chake, tunao uhusiano mwema naye,na kikwazo cha dhambi zetu kimeondolewa. Bila tendo la ajabu kwa upandewake sisi tulikosa matumaini.

Paulo amekaza kwamba haki hiyo imeonyeshwa kuwa haki ya Mungu mwenyerehema ya kutoa haki kwa wanadamu (5:9) kuliko kuwa haki ya Mungu mwenyeghadhabu ya kudai haki. Kwa kawaida si haki hakimu amwachilie mkosaji nakumtendea kama hana kosa. Lazima iwepo sababu kuu ya kufanya hivi. Mfanomzuri ni wa mtu mwingine kukubali adhabu ya mwingine, kumlipia faini yake aukufungwa badala yake, ila ni juu ya hakimu kukubali iwe hivyo.

Hali nyingine ya haki ni sifa ya maisha mema ambayo aliyehesabiwa haki kwakumwamini Kristo aweza kuishi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ndani yake. Hivyohaki ki-hakimu na haki ki-adilifu zimeletwa pamoja. Bila kuhesabiwa haki (ki-hakimu) haiwezekani mtu kuishi maisha ya haki (ki-adilifu).

„toka imani hata imani‟ yaani hatua zote zahitaji imani. Kwa imani mtuhuhesabiwa haki, na kwa imani mtu huishi maisha ya haki katika uhusianomwema wa kumpendeza Mungu. Ni imani toka mwanzo hadi mwisho. Imani nikinyume cha hali zote za kujistahilisha, inaweka nje madai yote ya kufaa. Imanini chombo cha kuipokea Haki ya Mungu, mfano wa mkono kunyoshwa kwakupokea kitu, hatuwezi kujisifu eti! tumeamini kwa sababu tukifanya hivyotumegeuza imani yetu kuwa tendo jema la ustahili, imani ni kipawa (Efe.2:8- 10).

„mwenye haki ataishi kwa imani‟ maneno hayo yametoka Kitabu cha Habakuki(Hab.2:4) na Paulo ameyaweka kuwa hoja yake ya sura 1-8. Sehemu ya 1:(1:18-4:25) ni kuhusu „mwenye haki‟ na jinsi mtu apatavyo haki kwa imani. Ndiposehemu ya 2: (5-8) ni juu ya „kuishi‟ na jinsi mtu mwenye haki atakavyoishi.Aliyadondoa maneno ya Habakuki kuonyesha kwamba hata tangu zamani njiahiyo ya imani ilikuwepo. Wokovu ulitokea katika maisha ya Israeliwalipomtumaini Mungu na kujihusisha naye vema.

1:18-32 Dhambi na Hatia ya WaMataifaSehemu hiyo inatuonyesha haja kuu ya Injili. Katika k.17 Paulo alitaja „haki yaMungu inadhihirishwa, toka imani hata imani‟. Neno la „haki‟ ni kiini cha Waraka,kama ilivyo kiini cha Injili. Kwa kifupi ni „kuhesabiwa haki kwa imani‟. Hoja hiyoilitokana na ujuzi wake wa maisha. Paulo mwenyewe alitatizwa sana na jambohilo, alikuwa ameitafuta haki. „niwezaje kuwa „sawa‟ machoni pa

Page 97: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 759

Mungu? niwezaje kuwa na kibali chake? niwezaje kuwa na uhusiano mwemanaye?‟. Kabla ya kwenda Dameski alijaribu kupata jibu la swala hilo kwakushikilia sana desturi zote za dini ya Kiyahudi, hasa alijitahidi kwa nguvu zakezote kutimiza maagizo ya Torati, ili awe na „haki‟ aliyodaiwa na Mungu. Alijikutakwamba hata akifanya nini hakuweza kutimiza maagizo yote ya Torati, mara kwamara alikosea sheria fulani, pia alishindwa kufikia hali ya „utakatifu‟ uliotakiwa.Kutokana na ujuzi wa binafsi alijua hakika kwamba mwanadamu hawezi kuishibila kufanya dhambi na bila kuwa na upungufu kwa upande wa maadili.

Ndipo alipokutana na Kristo na kumwamini Yeye na upatanisho aliofanyaMsalabani, alisamahewa dhambi zake na kupata kibali cha Mungu akakutakwamba amehesabiwa kuwa „mwenye haki‟ na Mungu Mwenyewe. Dhambizake ziliwekwa juu ya Kristo na haki ya Mungu iliwekwa upande wake, kwa njiaya kumwamini Kristo na kazi yake Msalabani. Ndiyo sababu Paulo hakuioneahaya Injili. Ilifanya kazi maishani mwake naye alijua hakika kwamba Injili niuweza wa Mungu uletao wokovu.

Kwa hiyo, kuanzia 1:18 mpaka 3:20 shabaha yake ilikuwa kusimamisha hoja yakuwa wanadamu wote ni wenye dhambi na hatia mbele za Mungu, Wayahudikwa wasio Wayahudi, wazuri kwa wabaya, wote ni wenye dhambi. Wote huhitajihaki ya Mungu. Ni historia ya jamii nzima ya wanadamu, historia inayoonyeshaupungufu na upuuzi wa maisha, ustaarabu, na maendeleo ya binadamu bilakutatuliwa kwa tatizo kuu la dhambi.

Alianza na WaMataifa akichora picha ya uasi wao na maovu yao makubwa. Uasiuliodhihirika katika dini zao na ibada za sanamu na katika maisha mabaya. Pichahiyo inapatana na picha iliyochorwa na waandishi wa wakati ule ila wao walitajamabaya yaliyozidi hayo yaliyotajwa na Paulo. Alikuwa Korintho alipoandikaWaraka na mji huo ulijulikana sana kwa mabaya mengi yaliyofanyika humo, hatasifa yake mbaya ilienea kote kote. Kwa hiyo, pale alipo Paulo aliona thibitisho lamambo aliyoandika hapo.

k.18 Paulo alisema „kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa juu ya uasiwote na uovu wa wanadamu‟ (k.18). Maneno „kwa maana‟ yanaonyeshauhusiano wa sehemu hiyo na sehemu iliyotangulia, hasa k.16, k.17. Katika k.17alisema „haki ya Mungu inadhihirishwa‟ na k.18 alisema „ghadhabu ya Munguimedhihirishwa‟. Hivyo ghadhabu ya Mungu ni ufunuo wa Mungu na kwa sababuhiyo ni neno moja la kuzingatiwa sana tunapotafakari Injili. Paulo aliwekaghadhabu na haki ya Mungu pamoja, kama ni mambo mawili ya kushikwapamoja. Hakimu apaswa kuhukumu ili apate kuokoa. Ila tusiwaze ghadhabu yaMungu kwa kulinganisha na ghadhabu ya wanadamu iliyo na udhaifu wakibinadamu ndani yake ikichanganywa na chuki na wivu wa kupita kiasi nakutaka kulipiza kisasi. Sivyo ilivyo ghadhabu ya Mungu, haiongozwi na hisia aumaono ya ndani. Yeye hageukigeuki katika wema, yu mwema hata

Page 98: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI760

anapoonyesha ghadhabu yake, shabaha yake ni njema, sawa na babaanapomkanya mtoto wake. Anamkanya kwa sababu anampenda, bila kumpendaasingemkanya (Ebr. 12:5-11). Hata kwa upande wetu ni twakubali kwamba nisawa kwa watu wabaya kuadhibiwa wanapowafanyia wenzao vibaya. Wakristowanaingojea siku ambayo Mungu atayatengeneza mambo yote.

Ghadhabu ya Mungu ni itikio lake kwa uharibifu wa uumbaji wake mwema. Ni jibulake kwa dhambi na uasi, jibu limpasalo Mungu aliye Mtakatifu na Mwenye haki,hasa kwa sababu Mungu anajua zaidi yetu jinsi ambavyo dhambi imeharibu sanamaisha ya wanadamu. Kama Mungu asingekuwa na ghadhabu kwa uasi na uovuwa wanadamu asingekuwa na haki kamili. Ghadhabu ni tokeo la upendo wakemtakatifu ni upande wa pili wa pendo hilo. Upendo huo mtakatifu ulidhihirika paleGethsemane na Golgotha, Kristo alipoteswa na kuuawa, Mungu „alimwacha‟alipobeba dhambi zetu na kuchukua adhabu na laana ya Mungu mwilini narohoni mwake.

Katika sehemu hiyo tunaona mwungano wa dhambi na adhabu, ni mwunganouliowekwa na Mungu, ni utaratibu wake na kanuni yake. Uasi na udhalimuhuenda pamoja na utauwa na haki/uadilifu vile vile.

Kwa nini ghadhabu yake imedhihirishwa? Paulo alitaja uasi na uovu wawanadamu ambao ni kinyume kabisa cha haki ya Mungu. Alisisitiza kwambaWaMataifa waliweza kumfahamu Mungu, Mwumba wao. k.18b „waipingao kwelikwa uovu‟, maana yake maovu waliyofanya yalianzia katika wao kuikataa kweli,hawakumkubali Mungu ambaye walimfahamu Yuko. Neno „pinga‟ linaonyeshakwamba walifanya kwa kusudi wakikataa ile nuru waliyokuwa nayo kwa kuishikinyume chake. Katika Uumbaji Mungu amejidhihirisha kiasi cha kutosha kwamwanadamu ye yote kutambua kwamba Yeye yu Hai, ni Mwumba mwenyeuwezo, ni wa milele, ni Mungu halisi, aliye tofauti na wanadamu (Zab.19:1-4).Hakujificha bali alijidhihirisha ili wasifanye kosa la kumfananisha na kitu chochote alichokiumba. Kwa kifupi, Mungu ni Mungu si mwanadamu. Ufunuo huoumewaacha wanadamu wote wasiwe na udhuru kuhusu jinsi wanavyoishi(k.18b-20). Neno hilo lahusu wanadamu wote tangu kuumbwa kwa ulimwenguhata wale walioishi kabla ya Kuja kwa Kristo.

Katika k.21 Paulo ameweka wazi wajibu wa wanadamu kuishi kwa kupatana naujuzi walio nao, wapaswa kumtukuza Mungu, yaani wamkubali awe Mungu wamaisha yao mwenye madaraka ya kuwaongoza. Pia wamewajibika kumshukuru,kwa sababu ya uzuri wake ambao umeonekana katika uumbaji na hasa katikakuwaumba katika sura na mfano wake. Kwa kweli Mungu anazo sifa nyingine ilaPaulo aliona hizo alizotaja zilitosha kwa wanadamu kumtambua. Hasa hao watuhawakukana Kuwepo Kwa Mungu, ila hawakumpa Heshima na Sifa na Shukranizilizo haki yake.

Page 99: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 761

21b-23 Paulo ameonyesha kwamba maisha mabovu yamesababishwa na watukumkataa Mungu. „walipumbazika‟ Ni upeo wa ujinga kutokumkubali Mungu nakutokumruhusu awe Mungu. Si kwamba walikuwa na upungufu katika akili zao,la, ila walikuwa na upungufu wa moyo (k.21b). Matokeo ya kujiondoa kwa Mungualiye nuru ni „giza‟ na katika giza hilo wanadamu, badala ya kumwabudu Mungualiye Hai, asiye na uharibifu, wajifanyie „miungu‟ kutoka vitu visivyo hai,viharibikavyo, visivyoweza kuwaza, wala kusema, wala kuona. Pengine sanamuni mfano wa binadamu, au wa wanyama, n.k. kisha wazifanyie ibada. Asili ya„ujinga‟ huo ni „kuipinga kweli‟. Kwa kiburi wanadamu hujiinua juu ya Mungu nakujiamulia mambo yao wenyewe, kama wanajua zaidi ya Mwumba wao.Yawezekana Paulo alikumbuka habari za Anguko la Adamu kwa sababu alitaja„ndege, wanyama, na vitambaavyo‟ pamoja na kutumia maneno ya „utukufu,mfano, na sura‟ (Mwa.l). Mkazo wa Paulo ni juu ya wanadamu „kujua‟ k.19,21,32na kwa sababu wanajua hawana udhuru. Katika sehemu hiyo Paulo amesemajuu ya kosa la wapagani kwa upande wa dini katika kuabudu sanamu. Kiini chashida ni uasi wa kumkataa na kutokumheshimu Mungu.

k.24-26 Itikio la Mungu kwa hayo yote ni nini? Mungu aliwaruhusu wazifuatetamaa zao, na wakazidi kuchafuka. Walimdhalilisha Mungu, Mwumba wao, nakutukuza viumbe vyake. Kisha walifikia hatua ya kutokufuata kanuni za kuishipamoja, walitumia miili yao isivyo halali, wakapoteza heshima ya kuumbwa kwaokatika mfano na sura ya Mungu. Kwa hiyo,, mioyo na akili zao za gizaziliwaongoza kuiabudu miungu pamoja na kutenda maovu. Hayo yote kuwamatokeo ya mwenendo wao, pia ni adhabu ya Mungu, kwa sababu Munguametia muhuri mambo yale ambayo waliyachagua wenyewe walipoiasi ile nuruwaliyokuwa nayo. Ni kama wamesema „tunataka kuishi tupendavyo sisi‟ halafuMungu amejibu „nakubali, mwishi kama mpendavyo na kuvuna matokeo yake‟.Mungu amewakabidhi kwa dhambi!! dhambi ambazo wao wenyewewalizichagua!! Mwisho wa kutokumheshimu Mungu ni wanadamukutokuiheshimu miili yao. Hapo nyuma tuliona Paulo alisisitiza kujua kwao, nakatika k.23 k.25 k.26 amesisitiza neno la kubadili. Walibadili kweli kwa uongo,Mwumba kwa kiumbe, matumizi ya halali kwa matumizi yasiyo halali, nuru kwagiza.

k.26-27 Paulo alirudia kutaja itikio la Mungu la kuwaacha kufuata tamaa zao, ilapicha aliyochora ni ya vitendo vyao kuzidi kuwa vibaya. Walizidi kuishi kinyumecha mpango wa Mungu kuhusu uhusiano kati ya wanaume na wanawake,wakibadili matumizi ya miili yao. Waandishi wamethibitisha picha hiyo wakitajamaovu makubwa yaliyotendeka nyakati zile, watu walifanya walivyopenda bilakujizuia.

k.28-32 Kwa mara ya tatu Paulo amesema kwamba itikio la Mungu nikuwaacha wafuate akili zao zisizofaa na kufanya yasiyowapasa. Daimawalijidanganya wenyewe, walishindwa kuwaza kwa unyofu. Si kana kwamba

Page 100: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI762

Mungu aliwaruhusu kumwacha kwa kuondoa neema yake kwa siri, la. Ni zaidi yahilo, Mungu aliamua kuwaacha, ilikuwa adhabu yake kwao kwa kuwa waliamuakutokumfahamu na kufanya dhambi. Mwandishi mmoja C.S.Lewis ameandika„wale wanaopotea huonja daima uhuru wa kutisha waliodai, nao wajikutawamejitumikisha wenyewe‟

Katika sehemu hiyo Paulo ametaja aina 21 za maovu: udhalimu, tamaa, husuda,uuaji, fitina, hadaa, kunia mabaya, kusingizia, kumchukia Mungu, jeuri, kiburi,majivuno, kutunga mabaya, kutokutii wazazi, kuvunja maagano, wasiopendajamaa zao, wasio na rehema n.k. Ni orodha ya ajabu, na mwishowe Pauloalijumlisha kwa kusema kwamba hao watu wanajua sana kwamba ipo hukumuya haki ya Mungu, ambayo ni mauti. Tena alisema ni ustahili wao, kwa sababuwanafanya katika hali ya kuisukumia mbali nuru ya ufahamu wa Munguupatikanao kwa njia ya Uumbaji. Halafu aliongeza neno zito kwamba wakowengine wanaounga mkono wale watendao mambo hayo mabaya. Kwa hiyo,kuunga mkono dhambi ni vibaya hata pengine ni vibaya kuliko kuitenda. Orodhahiyo ni matokeo ya kubadili kweli ya Mungu kwa uongo. Tusifikiri anaelezamaisha ya mtu fulani au watu kadha bali anaonyesha aina nyingi za ubaya. Nikama daktari anayewaonyesha wagonjwa aina mbalimbali za ugonjwa ziwezazokumdhuru mtu. Ila ni faraja kujua kwamba wale ambao walio chini ya ghadhabuya Mungu waweza kuonyeshwa rehema zake (Efe.2:1-4; Rum.11:32). Ni jambola kutisha kusoma kwamba Mungu awaachie watu waendelee kufanya dhambi,hata hivyo, shabaha yake ni wapate kuutambua ubaya wao na kuuacha.

Kwa hiyo, inayohukumiwa si dhambi ya mtu anapojaribiwa ghafula na kuanguka,ila ni dhambi za wanadamu ambao kwa kusudi wamejiondoa kwa Mungu iliwasiwe naye katika maisha yao na mahali pake wamejiketisha wenyewe kwenyeutawala wa maisha, ili waamue na kufanya watakavyo wenyewe.

Ghadhabu ya Mungu imedhihirika katika kuwaacha wapatikane na matokeo yauchaguzi wao wa kunia wasimfahamu kwa kusudi, iwapo wanawezakumfahamu. Ghadhabu yake ni itikio la Utakatifu Wake kwa dhambi na uovu nauasi. Kweli Mungu hupenda sana kuonyesha rehema, ndiyo tabia yake, nambele, katika Waraka, ataonyesha kazi za rehema zake, ila kwanza imempasaPaulo aionyeshe kazi yake ya „ajabu‟ kama Isaya alivyoitaja kazi ya „ghadhabu‟(Isa.28:21) kazi asiyopenda kuifanya wala hana haraka ya kuifanya, tofauti nakazi zake za rehema anazofurahia kuzifanya, anapopokea kwa furaha wotewatubuo kwa kweli. Matokeo yaliyotajwa ni malimbuko ya ghadhabu ya Munguitakayodhihirishwa katika hukumu ya mwisho (1 The. 4:10).

Paulo ni kama daktari ambaye haogopi kumwambia mgonjwa matatizo na hatariya ugonjwa wake kwa sababu anao uhakika wa tiba, hivyo anampa mgonjwamatumaini ili akubali matibabu yake.

Page 101: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 763

Ni vema tujue kwamba „sanamu‟ ni kitu cho chote kinachowekwa mahali paMungu katika maisha yetu na kunasa usikivu na utiifu wetu. Yaweza kuwa gari,nyumba, shamba, mashine fulani, ama cheo, hata kazi, cho chote kilekinachotuzuia tusimtii Mungu kikamilifu. Chaweza kuwa kitu kibaya, vile vilechaweza kuwa kitu kizuri, cho chote kile ambacho tumeruhusu kitutawale.

Kama ni picha ya kukatisha tamaa, matumaini yapo, kwa sababu katika„maumivu‟ watakayopata kutokana na dhambi zao, watafanana na mgonjwaanayeumwa, watatafuta matibabu!!!.

MASWALI1. Paulo alijitambulishaje kwa wasomaji wake?2. Kwa nini alijitambulisha kwa aina hiyo?3. Eleza uhusiano wake na Kanisa la Rumi?4. Eleza Neno kuu la Waraka na maana ya „haki ya Mungu kudhihirishwa

kwa njia yake‟.5. Ni hoja gani Paulo aliyosimamisha katika sehemu hiyo?6. Alisemaje juu ya wanadamu wote kumjua Mungu: Je! waliweza kumjua?

Na waliweza kujua nini juu ya Mungu?7. Walikuwa na wajibu gani kwa ujuzi huo?8. Hasa, walikuwa na itikio gani?9. Itikio la Mungu kwa uasi wao lilikuwa nini?10. Uasi wa wanadamu umeonekanaje kwa upande wa dini na kwa upande wa

maisha?

INSHA:Andika maelezo machache juu ya wenyeji wa nchi yako na hali yao kabla ya kuja kwaUkristo hasa kuhusu ujuzi wao wa Mungu.

2:1-29 Dhambi na Hatia ya Wayahudik.1-16 Paulo aliendelea kuisimamia hoja ya wanadamu wote kuwa wenyedhambi na hatia mbele za Mungu. Alijua kwamba wengine hawatakubaliananaye hasa Wayahudi na waadilifu katika WaMataifa. Baadhi ya wapagani waliishimaisha mazuri nao wangalijiunga na hukumu ya Paulo juu ya wapagani wenzaowaliozama katika maisha mabaya jinsi Paulo alivyotoa habari zake katika1:18-32. Pia Paulo alijua ya kuwa Wayahudi daima waliwahukumu wapaganikwa maisha yao mabaya, wakijiona kuwa bora, hata hivyo, Paulo alitakakuwathibitishia hao wote kwamba wamo hatiani na chini ya hukumu ya Mungu.Tazama jinsi alivyouliza maswali kwa kuwa alifahamu Wayahudi na waadilifuhawakukubaliana naye (k.3-4).

k.1 Paulo alisema kwamba iwapo waliwahukumu watu wengine walifanyamakosa na dhambi zile zile. Je! kweli walifanya sawa na mabaya yaliyoandikwakatika sura ya kwanza? Inaonekana ndivyo walivyofanya, taz. k.21-22.

Page 102: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI764

Kuhukumu ni ishara ya mtu kuwa na dhamiri inayofanya kazi, na kama ni hivyo,apaswa kuongozwa nayo. Katika kuhukumu wengine walikuwa wamethubutukujichukulia kazi ambayo hasa ni kazi ya Mungu. Wamejiinua na kujifanya kuwamabwana wenye haki ya kuamua mambo, na kufanya hivyo ni sawa na kuabudusanamu. Maana wajifanya wenyewe kuwa „Mungu‟. Hali ya „kifarisayo‟ imomioyoni mwetu, twajiona kuwa bora (Lk.18:11) na kwa unafiki twatoa hukumu zatofauti tukihukumu wengine kwa yale ambayo wenyewe tunafanya na kuwiaradhi. Sisi wanadamu tu wepesi wa kutambua na kuhukumu makosa ya wenginehuku twakawia kuona makosa yetu wenyewe au tukiyaona twaelekea kuyatafutiaudhuru.

k.2-3 Watu hao walifahamu kabisa kwamba Mungu ni Mwenye Haki, na ya kuwaYeye atahukumu mambo jinsi yalivyo. Kama ni hivyo ni dhahiri kwamba ye yoteatendaye mabaya atapatikana na hukumu ya Mungu, awe ni Myahudi mwenyeTorati au ni mpagani mwenye nuru itokayo kwa Uumbaji na dhamiri, iwapo kiasicha ufahamu kinazidi kwa mwenye Torati. Ikiwa wapagani walio na nuru kutokaUumbaji hawana udhuru, kwa kuwa hata kwa nuru waliyo nayo waliweza kujuailiwapasa kumcha na kumheshimu Mwumba wao. Je! Myahudi mwenye nurukubwa zaidi kwa njia ya Torati Mungu atawezaje kumwachilia eti! ni mteule?(Mt.3:9; Yn.8:33-45). Twaweza kukubali Mungu ni Mwenye Haki huku tukitumainitutahukumiwa tofauti. Jambo la maana si kujua na kufahamu kwetu bali kutendakwetu.

k.4 Kama bado hawajapatikana na adhabu ni kwa sababu ya uvumulivu nawema wa Mungu katika kuwasubiri waje kwenye toba Kutokutubu ni kumdharauMungu na kutokuuthamini uteule wao. Hawakutia maanani jinsi Mungualivyowatendea, waelewe kwamba hata wao watahukumiwa na kipimo kile kilecha wengine wote, yaani kwa kadiri ya matendo yao. Mungu badohajawahukumu kwa sababu anataka sana waje kwenye toba, ila waelewekwamba subira yake haina maana kwamba hatawahukumu, hakikaatawahukumu. Wao walikosa katika kumaanisha rehema Zake, wakazitafsirikinyume cha shabaha Yake. Mungu hutoa baraka zake kwa wanadamu wote ilaWayahudi walizijua kipekee.

k.5 Pamoja na hayo kwa kutokutubu mioyo yao ilizidi kuwa migumu. HalafuPaulo alisema neno zito, la kutisha, la kuwaonya juu ya kukawia kutubu. Alisemakwamba walikuwa wakijiwekea akiba ya hasira kwa siku ya mwisho ya hukumuya Mungu (Sef.1:14-16; Amo.5:18-24). Kila siku ya kukawia kwao walikuwawakizidisha akiba hiyo. Ni ajabu kuona iliwezekana Wayahudi walio wateulewake wapatwe na mioyo migumu. Ni onyo kali kwa watu wa dini na maadili. Walewalio na sababu nyingi za kumheshimu Mungu mara nyingi hawamtii.

k.6-11 Katika sehemu hiyo Paulo ametoboa wazi msingi wa hukumu yaMungu, kila mtu atahukumiwa kwa kadiri ya matendo yake (Mt.16:27; 1

Page 103: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 765

Kor.3:8; 2 Kor.5:10; Ufu.2:23; 20:12; Rum.14:12) katika Biblia nzima msingi huoumewekwa (Ayu.34:11; Zab.62:12; Mit.24:12; Yer.17:10; 32:19) Kila mtuatahukumiwa kwa haki kamili ya Mungu akitumia kipimo kimoja cha matendo.Paulo aliendelea na mawazo kuhusu matendo. Katika k.7 alisema matendomazuri yamwongoza mtu kwenye uzima wa milele na katika k.8 alisema matendomabaya yamwongoza mtu apatwe na ghadhabu ya Mungu. Ndipo katika k.9alionyesha hukumu ya Mungu kwa matendo mabaya ya Wayahudi na yaWaMataifa na katika k.10 hukumu ya Mungu kwa matendo mema ya Wayahudina ya WaMataifa. Matendo mema ni matendo gani? Ni matendo ya kuwafikiriawengine na kumcha Mungu. Tazama neno „wanatafuta‟ nia yao imekazwawasiishi kwa kujipenda bali kwa kufanya mapenzi ya Mungu. Tena wana subira.Matendo mabaya ni ya wale ambao wamekataa kweli (1:25) watu wa kujipendana kujitafutia mambo yao tu na kwa sababu hiyo waishi katika dhuluma. Myahudihutangulia katika wokovu (1:16) na katika hukumu (2:2,9: Amo.3:2). Iwapo katikak.7 na k.10 Paulo amesema kwamba Mungu atawapa watendao mema tuzo lauzima wa milele, mbeleni katika 3:10,20 alionyesha kwamba hakuna mtuatakayehitimu, kwa sababu watu wote washindwa kutimiza mapenzi ya Mungu.

k.11 Mungu hana upendeleo, kila mtu atahukumiwa kufuatana na matendo yake.Ni kosa kubwa kwa mtu kutegemea ujuzi wa Torati bila kuifuata. Pia ni hatari kwamtu kuwa mshiriki wa Agano la Mungu na kuzaliwa katika taifa teule, ikiwabadala ya kutimiza wajibu wake ana hali ya kutokujali akifikiri kwamba kuteuliwakwatosha na kuhesabu kuteuliwa ni sawa na wokovu, ila uteule sio wokovu.

k.12-16 Katika sehemu hiyo Paulo alionyesha kwamba hukumu ya Munguitafuata kiasi cha nuru alicho nacho mtu. Alikuwa na shabaha ya kuonyesha yakuwa Wayahudi kwa WaMataifa, wote wanao wajibu wa kuishi maisha ya haki,kufanya yaliyo sawa kulingana na ufahamu walio nao. Mungu anatambuakwamba wako watu walio na sheria, yaani Torati ya Mungu, na wako watu wasiona sheria hiyo. WaMataifa wanayo sheria ya ndani, yaani wanatambua menginekuwa makosa iwapo hayalingani na Torati. Torati hudai utii na hairidhishwi nakitu kingine ila utii.

Kila mwanadamu anayo dhamiri ifanyayo kazi ndani yake ama kwa kumshtaki aukumtetea juu ya matendo yake. Dhamiri inahitaji kutiwa nuru ya Torati na nuruizidiyo ya Injili, hata hivyo, haikosi kamwe kushtaki au kutetea. Pasipo dhamirindani ya mtu Torati ingeshindwa kumgusa mtu kwa ndani. Hakuna mtu atendayemabaya matupu, wala hakuna mtu atendaye mema matupu, wanadamu wotehufanya mema na mabaya. Matendo yetu yanadhihirisha tulivyo kwa ndani, nikama matunda ya kanuni zinazotuongoza katika maisha ya kila siku. Kila mtuanasikia kuwajibika na anaelewa hali ya kukosa na kufaulu.

Page 104: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI766

Kwa hiyo, haki ni moja kwa Wayahudi na kwa WaMataifa, ila jinsiwalivyofunuliwa ni tofauti, Wayahudi kwa njia ya Torati, na WaMataifa kwautambuzi wa ndani na kwa ushuhuda wa dhamiri zao (Rum.9:1; 13:5). Kila mtuahitaji kuonywa juu ya hukumu ya Mungu.

Tusifikiri Paulo anafundisha kuokolewa kwa matendo, la, sivyo, ila anatilia mkazokwamba Mungu hana upendeleo. Sura hiyo ni sehemu katika kuendeleza hojayake ya wanadamu wote kuwa wenye dhambi, ndipo baada ya kuthibitisha nenohilo atatoa fundisho la kuhesabiwa haki kwa imani. WaMataifa wasio na dinikamili kama Wayahudi wamewajibika kuishi maisha maadilifu. Wanadamu wotewanao ushuhuda wa mema na mabaya ndani yao.

k.16 Paulo alirudia kutaja „siku ile ya hukumu ya Mungu‟ (k.5). Wanadamu wotewatahukumiwa kufuatana na walivyo hasa si kwa jinsi wanavyojiona, auwanavyodai kujua, au kuteuliwa n.k.k.17-29 Hapo Paulo anazidi kusema na Wayahudi akikaza hatia yao mbele zaMungu. Hao walikuwa karibu na Mungu zaidi ya wengine katika maandalio yawokovu wa wanadamu, hata hivyo walikuwa wenye dhambi.

k.17-18 Alianza kwa kutaja sifa zao. Jambo la kwanza ni jina, waliitwa Wayahudi,jina la heshima sana, jina la watu walioteuliwa na Mungu na kuwa na aganonaye. Hao waliamini kwamba Mungu ni mmoja tu kinyume cha umati wa watuwalioamini kwamba iko miungu mingi. Jambo la pili ni Torati, ni hao tu,waliopewa hiyo Torati na kwa sababu hiyo walitambulikana kuwa watu wa pekeewenye tumaini katika Mungu. Walikuwa na haki ya kujisifu kwa Mungu. Kwa njiaya Torati walielimishwa kujua yapi ni bora na katika nuru hiyo iliwapasakuyachagua na kuyafanya hayo.

k.19-20 Ndipo Paulo anataja mambo manne yaliyowaweka mbele ya wengine.Walikuwa viongozi wa vipofu, mwanga kwa walio gizani, wakufunzi wa wajinga,na waalimu wa watoto wachanga. Mungu alikusudia wawe „mwanga waWaMataifa‟ (Isa.49:6). Kwa hiyo, madai yao yalikuwa sawa, hawakukosawalipodai mambo hayo. Kosa lao lilikuwa katika kutokujenga juu ya kujua kwaona ukosefu wa kutimiza masharti yake. Hawataepuka hukumu ya Mungu eti!wanayo Torati. Hawana udhuru, kinyume chake hatia yao imezidi.k.21-24 Paulo aliweka wazi kosa lao kubwa. Walifundisha wengine bila kujifunzawenyewe, waliwaambia watu wasiibe, wasizini wasiabudu sanamu, na waowenyewe walifanya hayo hayo. Ni jambo zito kwa sababu wamekuwa wanafiki.Walisababisha Jina la Mungu kutukanwa na WaMataifa, na badala ya kuwamwanga wamekuwa giza kwao. Ni dhihaka kusema bila kutenda. Ni vematujiulize, ni kweli ndivyo walivyofanya? Bila shaka baadhi ya Wayahudi waliishivizuri wakijitahidi kushika Torati ila baadhi yao walivunja sheria mbalimbali, kiasicha kutosha kwa mashtaka hayo kusimama. Twajua kwamba Bwana Yesualiwashtaki Mafarisayo (maana ya jina hilo ni „wa safi‟ na hao walikuwa watuwaliokaza sana umuhimu wa Torati (Mt.23; Lk.11:39-52).

Page 105: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 767

Ulikuwepo ushuhuda wa kutosha juu ya Wayahudi kutikisa ule ujasiri wao wakujiona kuwa bora kuliko WaMataifa. Kiburi cha kiroho ni hatari sana. Ni onyokwa sisi Wakristo. Tunalo neno moja la kuona fahari juu yake, nalo ni Msalabawa Kristo (Gal.6:14).

k.25-29 Katika sehemu hiyo hoja ya Paulo ni juu ya hali ya ndani na hali ya nje.Katika habari hiyo alizungumzia jambo la Tohara, iliyowekwa kuwa ishara ya njeya kibali cha mtu kuishi kwa kushika maagizo ya Torati. Paulo hakuweza kuungamkono jinsi wengine walivyotenga ishara na kitu chenyewe, yaani kuthaminitohara bila kushika torati. Tohara ilikuwa ishara ya maana, ishara ya agano, ilawengine waliitumia kama „pasipoti‟ ya wokovu wakiihesabu kuwa sawa naagano. Paulo alikubali kwamba ilifaa (2:25; 3:1) ila faida yake ilitegemea utendajiwa sheria. Twaweza kufananisha tohara na pete ya ndoa ambayo ni ishara yanje ya ndoa, ina maana kwamba watu wanaishi kwa uaminifu wa ahadiwalizoahidiana wakati wa kufunga ndoa. Kutokuwa waaminifu kwafanya ndoaisiwe ndoa halisi na pete kuwa haina maana. Paulo hakuidharau tohara, kamaishara, ni nzuri, ila haikuweza kuwa badala ya sheria.

Halafu Paulo alisema juu ya mtu kufanya torati yaani kutenda matendo mazurina kutokufanya mabaya iwapo hakutahiriwa, jambo lililowahusu baadhi yaWaMataifa. Paulo alikubali kwamba inawezekana mtu awe na hali njema yandani, moyoni mwake, na nje awe na hali njema ya kutenda matendo mazuri,kwa kadiri ya ufahamu wake. Mtu wa namna hiyo atahesabiwa kuwa sawa namtu aliyetahariwa ni kama ametahiriwa „moyoni‟ iwapo nje, katika mwili,hakutahiriwa (2:14). Kwa hiyo, kutahiriwa kwaweza kugeuzwa kuwakutokutahiriwa na kutokutahiriwa kwaweza kugeuzwa kuwa kutahiriwa.

k.27 Hapo Paulo amesema neno la ajabu. MMataifa ambaye hakutahiriwaatamhukumu Myahudi aliyetahiriwa, maadam anafanya yaliyo sawa (Mt.12:41).(tukumbuke kwamba Wayahudi walihesabu WaMataifa kuwa wavunja sheria).

k.28 „kwa ndani‟ Paulo alikuwa na maana ya unyofu na ukweli na „kwa nje‟alikuwa na maana ya unafiki. Kutahiriwa hakumfanyi mtu kuwa Myahudi, ilakutahiriwa „kwa ndani‟ kulimfunua aliye Myahudi halisi.Ni onyo kwa Wakristo juu ya kugeuza baraka kubwa ya kumwamini Kristo kuwasababu ya kuona kiburi. Ndani ya kila mmoja yamo maelekeo ya kukuza ya njebadala ya ndani, ya taratibu na andiko badala ya roho, na ishara badala ya kituchenyewe. Mambo ya nje kama sakramenti n.k. ni mambo matakatifu tuliyopewana Mungu ila hata hayo yasikuzwe zaidi ya kazi ya Mungu mioyoni mwetu.Tutafsiri aliyosema Paulo kwa mambo ya Kikristo “Yeye si Mkristo aliye Mkristowa nje, wala Ubatizo/Ushirika si ule wa nje tu, bali yeye ni Mkristo aliye Mkristokwa ndani na Ubatizo/Ushirika ni ule wa moyo katika roho si ule wa Kitabu chaSala au utaratibu fulani tu”.

Page 106: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI768

Dhambi ndiyo sababu ya mauti, mambo kama „uteule‟ au „kutokusikia‟ habari zaKristo hayawi sababu ya mauti.

MASWALI1. Katika sehemu hiyo Paulo anazungumzia hoja gani?2. Wayahudi waliweza kumjua Mungu vizuri zaidi ya WaMataifa kwa sababu

gani?3. Walikuwa na wajibu gani kufuatana na mapendeleo waliyopewa?4. Waliitikaje? Walijifariji kwa kudai nini?5. Paulo alifundisha nini kuhusu hukumu ya Mungu?6. Paulo alipambanua Myahudi wa kweli na asiye Myahudi wa kweli kwa

mambo gani?

3:1-8 Makinzano ya WayahudiKatika safari za uinjilisti Paulo alijadiliana sana na Wayahudi kwa sababuhawakuweza kukubaliana naye kwamba „haki‟ yao ya Kiyahudi si hakiinayokubalika na Mungu. Bila shaka makinzano tunayokuta hapa yalitumiwa naWayahudi katika majadiliano. Yawezekana hata Paulo mwenyewe kabla yakuongoka alikuwa na mawazo kama hayo. Hapo Paulo ametumia mtindo wakuuliza na kujibu maswali.

k.1-2 Kinzano la kwanza lahusu faida ya kuwa Myahudi. k.1 „basi Myahudi anaziada gani?‟ na „kutahiriwa kwafaa nini?‟ Kufuatana na yale yaliyosemwa naPaulo katika 2:25-29 ilikuwa rahisi kuwaza kwamba Myahudi hakuwa na faidazaidi ya wengine. Kama kutahiriwa kuliwafaa wale tu waliotenda maagizo yaTorati (2:25; 1 Kor.7:19) na ikiwa Myahudi wa kweli ni yule „wa ndani‟ si yule „wanje‟ (2:28,29) inaonekana Wayahudi hawawi tofauti na wengine.

Paulo alijibu kwa kukaza kwamba Wayahudi walikuwa na faida, na faida yaoilitokana na Utume waliopewa na Mungu kuwa viongozi, waalimu, mwanga, nawakufunzi (2:17-20) ili wawe mwanga kwa WaMataifa. Walikabidhiwa „mausia yaMungu‟ maneno ya Mungu Mwenyewe, mausia yaliyojaa hekima na ufahamu wamapenzi ya Mungu, na kuwa amana ya pendo lake. Aliwapa ahadi ya Masihi.Kwao Mungu alijifunua kipekee. funuo wa Mungu hautokei hivi hivi tu, hapa napale, kama wapendavyo watu. Mungu Mwenyewe huchagua ni kwa njia gani nakwa akina nani atajifunua kwao. Kuhusu wokovu wa wanadamu aliwateuaWayahudi na kuwatayarisha ili wawe mfereji wa baraka zake kwa ulimwengu(Mwa.12:1ku) sawa na Yesu alivyosema kwa mama Msamaria „wokovu watokakwa Wayahudi (Yn.4:22). Paulo hakusema Mungu aliwapa mausia ila alisemaaliwakabidhi, neno „kabidhi‟ linaonyesha kwamba waliwekwa kuwa mawakili wamausia si wenye mali hiyo nao waliwajibika kuwa „mwanga wa WaMataifa(Isa.49:6). Walipewa heshima kubwa sana na wajibu mkubwa sana.

Page 107: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 769

k.3-4 Paulo aliendelea na maswali na kuyajibu. Itikio la Wayahudi kwa heshimawaliyopewa na kwa wajibu wao haukuwa mwema. Walikosa kuutimiza wajibuwao, hawakuwa waaminifu kwa Mungu na Agano lake, walivunja upande wao,mara kwa mara walimwasi Mungu, na hata Kristo alipokuja kwao, Masihialiyeahidiwa, licha ya kumpokea, wakamwua. Hivyo hatia yao ilizidi hatia yaWaMataifa. Ila Mungu alidumu kuwa Mwaaminifu kwao, wala kuasi kwaohakubadili uaminifu wake wala hakuweza kumzuia asitimize makusudi yake.Kutokuwa waaminifu kuliudhihirisha ukweli wa uaminifu wa Mungu. Haki yaMungu ilithibitika juu ya uasi wao. Katika Agano, kama wa upande mmojaamelivunja, uaminifu wa yule wa upande wa pili hauguswi, kwa hiyo, uaminifu waMungu ni thabiti. Mungu adumu alivyo, mwenye haki na wa kweli, haidhuruwanadamu waweje. Haiwezekani Mungu abadili hali yake, ni upuuzi kuwazahivyo. Mungu huwa „sawa‟ wakati wote au asingekuwa Mungu.

Paulo alitumia neno la nguvu alipokanusha ile dhana kwamba uaminifu waMungu unaweza kubadilishwa kwa sababu ya kutokuamini kwa wanadamu.Haidhuru wanadamu wote ni waongo au sio, kweli inayosimama ni ya Mungukuwa amini na kweli, mwenye tabia ya kuwasaidia, kuwarudisha, na kuwaokoawanadamu. Kwa kuwa Mungu hafanani na sisi Yeye aweza kutusaidia. Daudialitambua neno hilo alipofanya dhambi ya uzinifu, akatubu na kumgeukia Mungu.Dhambi yake ilimsaidia kufahamu haki ya Mungu. Aliona hata ikiwa haki yaMungu inaletwa mahakamani itadhihirika kuwa sawa. (Zab.51:4; 2 Tim.2:13).

k.5-8 Paulo aliendelea na maswali na majibu. Swali la kwanza katika k.5 lilikuwa„Je! Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu?‟ Paulo alijibu kwa kusema kwambaikiwa Mungu amedumu kuwa mwenye haki anapokabili udhalimu wa wanadamu,haiwezekani kusema Mungu ni dhalimu, ameacha kuwa mwenye haki.Anapohukumu udhalimu wa wanadamu Mungu hawezi kugeuka kuwa tofauti naAlivyo hasa, hata ikiwa udhalimu wetu umedhihirisha haki yake na kuithibitisha.Udhalimu ni wetu na haki ina Mungu. Si vema tuseme tuzidishe udhalimu ili hakiya Mungu izidi kuonekana. Wema na haki ya Mungu ni kamili, hakunakuvizidisha wala kuvipunguza. Vivyo hivyo udhalimu wa wanadamu unadumukuwa udhalimu iwapo uzuri wa wema wa Mungu unadhihirika. Neno hilolimekuwa wazi katika Msalaba wa Kristo. Tendo la kumwua Yesu lilikuwa tendobaya mno, ila matokeo yake yalikuwa ukombozi wa ulimwengu. Waliotendatendo hilo walikuwa na hatia taz. hotuba ya Petro siku ya Pentekoste „kwa mikonoya watu wabaya mlimwua‟ (Mdo.2:23-24).

Mwenye dhambi anastahili kuhukumiwa kwa dhambi zake, na Mungu amestahilikumhukumu kwa sababu Yeye ni mwenye haki, mwaminifu, na wa kweli. Munguhawezi kuachilia kuwahukumu wengine eti! kwa kufanya hivyo kutaudhihirishautukufu wake, lazima ahukumu kila dhambi. Bila kanuni hiyo hamna hukumu yakweli.

Page 108: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI770

Paulo alitumia neno „hasha‟ mara mbili akihesabu mawazo hayo ya upinzani niupuuzi na kinyume kabisa. Katika ulimwengu huu watu hupenda kumhukumuMungu kwa kuuliza maswali kama „Je! Mungu yuko?‟ „Je! Mungu ni Mwema? naowamekuwa na „mbona‟ nyingi..‟ mbona ameruhusu hili kutokea? „mbonaimekuwa hivi?‟ Wengine huthubutu kumlaani na wengine hukana KuwakoKwake. Ila mwishowe Yeye aliye tofauti kabisa na sisi atawahukumu watu wotekwa haki na kweli.

Mara nyingi watu walimshtaki Paulo kuwa mwongo na mara nyingi ilimbidiajitetee (Gal.1:20). Wengine walipotosha maana yake hasa alipojitahidikujihusisha na watu wa aina aina (1 Kor.9:22). Fundisho la kuhesabiwa haki kwaimani iliachia nafasi kwa wengine kusema kwamba alifundisha „tufanye mabaya,ili yaje mema‟. Neno hilo tutalikuta katika sura ya sita.

3:9-20 Wanadamu wote ni wenye dhambi na hatiaSasa Paulo amefikia upeo wa hoja yake ya wanadamu wote kuwa wenyedhambi. Alianza katika 1:18 na habari za WaMataifa, alichora picha ya ubayawao. Alionyesha ya kuwa waliweza kufahamu kwamba Mungu Yupo nakutambua uwezo wake na kuwako kwake kwa njia ya Uumbaji. Pia waliwezakutambua kwa kiasi matakwa yake kwa upande wa maadili kwa njia ya dhamirizao. Halafu katika sura ya pili alisema juu ya waadilifu na hasa Wayahudi nakuonyesha kwamba, iwapo waliteuliwa na Mungu, na kupewa mwongozo waTorati, walishindwa kuitii, wakawa wenye dhambi na wenye hatia kamaWaMataifa. Halafu mwanzo wa sura ya tatu alijibu makinzano ya Wayahudi kwanjia ya kuuliza na kujibu maswali kadha. Ndipo kuanzia k.9 alitilia mkazo hoja yawote kuwa wenye dhambi kwa kutumia dondoo za Maandiko.

k.9 Kwanza aliuliza swali na kulijibu kwa nguvu akisema kwamba amekwishakuwashitaki Wayahudi na Wayunani kwamba wote ni wenye dhambi, ndipoalitilia mkazo neno hilo kwa dondoo zilizotoka katika Maandiko ya Kiyahudiakitoa picha iliyochorwa na waandishi mbalimbali ya ubaya na upotevu wao.Kama Yeremia alivyosema „moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, unaugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?‟ (Yer:17:9). Alitaka kuonyeshakwamba iwapo Wayahudi walikuwa na fadhili za kipekee kutoka kwa Mungu,hizo hazikuwaepusha na hukumu ya Mungu, kwa sababu hawakuishi jinsiilivyowapasa kulingana na fadhili hizo (3:1-2). Neno kubwa si kuwa au kutokuwana fadhili, kuwa Myahudi au si Myahudi, neno kubwa ni wote kuwa wenye dhambina kwa sababu hiyo wote wahitaji rehema za Mungu na kutendewa kwa neema.Kwa upande wa maadili na haki wote walifilisika. Torati haikufaidi Wayahudi kwawokovu, lengo lake tangu mwanzo halikuwa hilo, bali ilifaa kwa muda tu. Kwanjia yake watu walipata kujua haki ni nini, na katika mwanga wake wote waliwezakutambua „dhambi‟ ili wajifunze kwamba Torati ama ya Kiyahudi au ya KiMataifa(sheria ya ndani) kamwe haina uwezo ndani yake ya kuokoa.

Page 109: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 771

k.9b „chini ya dhambi‟ Paulo alipenda kutumia usemi huo na kutoka 5:12 mpaka7:25 alifafanua maana yake. Alikubali kwamba kila mtu huwa na majukumu kwadhambi zake. Katika mawazo yake dhambi za watu ni dalili ya wanadamu wotekushikwa na pingu za „dhambi‟ hivyo mara nyingi alisema „dhambi‟ akijumlisha„madhambi‟. Aliona „dhambi‟ ni nguvu inayoshika watu wote (6:16) hata nauumbaji mzima (8:21).

Watu hufanya dhambi kwa hiari yao wenyewe, lakini ni kama wamelazimikakuifanya. Huchagua kufanya au isingehesabiwa ni dhambi, ila upo uvutano mkaliunaowavuta, ni kama utawala wasioweza kuushinda, wametumikishwa, hawawihuru. Kwa hiyo, wanadamu hawawi huru wa kutokufanya dhambi, iwapo hiariwanayo. Dhambi si kosa dogo dogo la mara kwa mara ila ni kuungana na „nguvu‟ya uovu yenye nafsi, kutoka nje, unaoshambulia ulimwengu (Efe. 2:2). Ni hali ya„anguko‟ nje na ndani yetu, wala hakuna asiyeguswa nayo.

k.10-18 Ndipo Paulo alitumia Maandiko ya Agano la Kale akitilia mkazo hojahiyo. Alidondoa maneno kutoka Vitabu vya Mhubiri, Zaburi, Isaya, na Mithali.Kwake Maandiko yalikuwa na nguvu na uhai, yenye uwezo wa kusema nakugusa hali ya wanadamu wote. Ni mara ya kwanza alitumia neno „dhambi‟ingawa alikuwa ametaja mabaya mengi (1:18ku).k.10-12: Dhambi juu ya Mungu, na hali halisi ya wanadamu:k.13-14: Dhambi za usemi:k.15-17: Dhambi juu ya jirani:k.18: Kiini cha Dhambi ni kutokumjali Mungu:

Kuna dhambi za kutenda na dhambi za kutokutenda:

k.10-12 „hakuna mwenye haki hata moja‟ (Mhu.7:20; Zab.14:1) Ni ushuhuda waMaandiko, kutoka mausia ya Mungu (3:2) maneno ya Mungu Mwenyewe. Niushuhuda usiokanika, na historia yote ya ulimwengu inaunga mkono ushuhudahuo. Ikiwa watu wote wamekosa haki ina maana kwamba wote ni wenye dhambi.Haki ndiyo kipimo anachotumia Mungu.Halafu katika k.11 wanadamu wamekosa ufahamu wa kweli wa Mungu na wawajibu wao kwake. Pia hawana nia ya kumtafuta. Hawataki kujihusisha nakushirikiana naye. Kutokumtaka Mungu ni dhambi nzito ya kuusukumia mbaliupendo wake.

k.12 Watu wameondoka katika njia zilizowapasa, na kama tunda lisilolika kwasababu limeoza, watu hawafai kwa jambo lo lote lifaalo. „La, hata mmoja‟.Hakuna mwanadamu aliye nje ya mashtaka hayo, na hasa Wayahudi kwasababu ni Maandiko yao yenye maneno hayo. (Zab.14:1-3; 53:1-3).

k.13-14 Dhambi za usemi: (Zab.14:2,3). 13a.b. (Zab.5:9) 13c. (Zab.140:3; Ling.na Yak.3). Upotevu wa wanadamu huonekana katika usemi. Paulo alitaja „koo‟„ndimi‟ „midomo‟ „vinywa‟ kuonyesha kwamba katika kila hali ya usemi

Page 110: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI772

wanadamu wamepotoka, kwa kutumia maneno laini ya kupaka mafuta, kwamaneno ya uongo na udanganyifu, kwa maneno ya matusi, kwa maneno makaliya kutisha na ya kuwaogofya watu n.k.

k.15-17 Baada ya kutaja dhambi za usemi Paulo ametaja dhambi za matendojuu ya jirani (Isa.59:7-8). Paulo alitaja „miguu‟ dalili ya watu kuwa wepesi wakuwafanyia jirani ubaya, hata kuwaua. Hutumia mabavu na kutisha watu,huanzisha ugomvi na mashindano, maana hawataki kuishi kwa amani na utulivu.

k.18 (Zab.36:1) Kisha Paulo alitaja dhambi ambayo ni kiini cha dhambi zote.Wanadamu hawamchi Mungu, hawamweki Mungu mbele yao, Mungu hawi katiya maisha yao. Wanaishi kama Mungu Hayupo. Wameamua kuwa kama „vipofu‟ili wasimwone.

k.19-20 Paulo alifuata ushuhuda huo mkali wa Maandiko kwa kujumlisha halihalisi ilivyo „Basi twajua..‟ kwa sababu Torati yenyewe imeshuhudia. Ni vemakuona „Torati‟ ni Maandiko yote kwa sababu dondoo alizotumia zilitoka katikavitabu vitano vya kwanza vya Agano la Kale vilivyoitwa „Torati‟ pamoja na vitabuvingine vya Agano la Kale. Kwa sababu ni ushuhuda wa Maandiko ya Kiyahudihawakuweza kudai kwamba hawakujua, tena ushuhuda huo ulilenga wale „waliochini ya Torati‟. Shabaha ni vinywa vyao wote vifumbwe. Kama haowameshtakiwa ina maana kwamba wengine wote wameshtakiwa pia, maanailikubalika kwamba Wayahudi walikuwa na ufunuo wa haki uliozidi wa wengine,na ikiwa vinywa vyao vimefumbwa, basi inafuata kwamba vinywa vya WaMataifapia vimefumbwa. Tunapowaza sheria ambazo hasa ni Amri kumi za Wayahudihata hivyo zaweza kuwa kanuni za maadili mema ya watu wengine. Haidhuru nikanuni zipi zilizopo, zote zinadhihirisha makosa ya watu mbele za Mungu.

Kwa hiyo, imempasa kila mwanadamu anyamaze mbele za Mungu na kujua kwauhakika kwamba njia ya kupata kibali cha Mungu kwa matendo ya sheriaimefungwa. Njia ile imefungwa. Kwa sheria twajitambua kuwa wenye dhambi, nakufahamu dhambi ni nini ila sheria haiwezi kutunusuru. Kazi nyingine ya sheriaimekuwa ya kutukatisha tamaa ili tumgeukie Mungu na kumtumaini Yeye tu narehema zake. Kwa hiyo, Torati ile ambayo Myahudi aliionea fahari ndiyo ileiliyomshtaki yeye pamoja na walimwengu wote. Tatizo kubwa la wanadamu nidhambi, pia ni tatizo kubwa zaidi kwa Mungu kwa sababu ya haki yake naghadhabu yake juu ya dhambi. Inawezekanaje ghadhabu yake itulizwe?

Mungu alipata njia nyingine ya kuidhihirisha haki yake mbali na Sheria na kwanjia hiyo alifaulu kuwapatia wanadamu ile haki wanayoihitaji, haki ya kuwaletakwenye uhusiano mwema na Mungu. Kwa hiyo, Paulo baada ya kuweka msingiimara kwamba haja kuu ya wanadamu wote ni kupata haki, yu tayari kufunua njiaya kuhesabiwa haki kwa imani.

Page 111: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 773

Tujumlishe mpaka hapa:Katika 1:16-17 Paulo alitaja neno kuu la Waraka, Injili ambayo ndani yake hakiya Mungu imedhihirishwa na kupatikana kwa imani. Katika 1:18 alisemaghadhabu ya Mungu imedhihirishwa juu ya uasi wote wa wanadamu. Ndipokutoka 1:18-3:20 alitoa ushuhuda mwingi uliowashtaki Wayahudi na WaMataifawote kuwa wenye dhambi. Alifunga kwa kuonyesha kwamba Torati ilishindwakutoa msaada kwa hiyo, wanadamu walibaki katika kuhitaji haki ambayowenyewe hawakuwa na uwezo wa kuipata. Kwa hiyo, swala kubwa ni „kwa njiagani mwenye dhambi aweza kusamehewa dhambi zake, kuachiliwa adhabuyake, na zaidi kuvikwa haki na kuhesabiwa mwenye haki?

3:21-31 Haki ipatikanayo kwa kumwamini Kristok.21 Alianza kwa maneno „Lakini sasa‟ baada ya habari mbaya ya wote kuwawenye dhambi na bila matumaini, sasa mambo yamebadilika na tumaini lipo.Kwa Kuja Kwake Kristo njia mpya imepatikana, maana Yeye amebadili kabisahali ya binadamu wote kuhusu uhusiano wao na Mungu. Njia hii ni tofauti sanana njia ya sheria, kwa sababu haitegemei utii wa masharti ya Torati wala Taratibuza Maadili. Mtu hana tumaini lo lote asipopewa haki itokayo nje yake nakuwekwa upande wake, yaani kuhesabiwa kwake. Njia hiyo ilipangwa katikaumilele, ilipangwa kabla ya Torati ila katika mwenendo wa historia kiutendajiikafuata Torati. Twajua neno hilo kwa sababu Ahadi ya Mwokozi ilitolewa kwaAdamu na Hawa mara baada ya uasi wao. Halafu njia hii ilionekana kwa Abramu(Mwa.17) na katika taratibu za Sadaka za Dhambi n.k. Manabii kama Isaya nawengine walitabiri habari za Kuja kwa Masihi, aliyeelezwa kuwa MtumishiAtakayeteswa na Mwana Kondoo wa Pasaka (Isa.53). Shabaha ya Torati ilikuwakuwahakikishia wanadamu kwamba ni wakosaji walioshindwa kutenda kwa haki.Tangu mwanzo Torati haikuwa na lengo la kupata haki wala kuwa njia yakuwaokoa wanadamu, hata hivyo, kwa Torati na Manabii, yaani kwa Agano laKale haki na maadili yalidhihirika, haki ile ile ambayo sasa yapatikana kwa imani.Tofauti si katika haki yenyewe, ila katika njia ya kuipata. Kwa hiyo, lengo la Toratihalikusahauliwa wala kubadilishwa. Kristo kwa maisha yake makalimifu aliitimizahaki ya Torati na kuridhisha madai yake na kwa kumwamini Kristo matunda yamaisha yake makamilifu yahesabiwa kwetu. Kwa hiyo, „haki‟ ya Torati imetimizwakatika njia hiyo mpya, na kwa sababu hiyo Paulo alisema katika k.31 „Toratiimethibitishwa‟.

k.22-23 Haki ya Mungu ni zaidi ya tabia yake, hasa ni utendaji wake wa kutupatiahaki. Kwa Haki yake ametengeneza ule uhusiano mbaya baina yetu na Munguuliosababishwa na dhambi zetu, uhusiano unaoelezwa na maneno „chini yaghadhabu yake‟ na kuleta uhusiano mwema ili tuwe „chini ya neema yake‟. Njiaya kuipata ni kwa kumwamini Kristo. Ni njia moja kwa Wayahudi na kwaWaMataifa, kwa sababu wote wamekosa kufikia kipimo cha ukamilifu unaodaiwana Mungu. Kwanza wote wamefanya dhambi. Iwapo wengine huzidi wenginekatika kiasi chake au katika ubaya wake, hata hivyo, wote wanafanya dhambi.Tena hakuna mwanadamu anayetimiza yote anayotazamiwa katika

Page 112: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI774

kuumbwa kwake katika mfano wa Mungu. Paulo alisema „na kupungukiwa nautukufu wa Mungu‟ hivyo kila mtu anao upungufu, hana ule uzuri wa Mungu.Wote ni watu wa „anguko‟ (Mwa.3). Imani inayompasa kila mtu ni imani katikaYesu Kristo aliye Mkombozi, Mpatanishi, na Bwana.

k.24a Kuhesabiwa haki ni wokovu. Neno „kuhesabiwa‟ ni tofauti na „kufanywa‟.Kuhesabiwa hakuleti tofauti ndani yetu ila katika uhusiano wetu na Munguambao utasababisha mabadiliko kimaisha. Mungu anatutangazia kuwa mwenyehaki, ni neno la sheria, tunao msimamo mpya mbele zake maana yakeanatutendea kama tu wenye haki si wenye dhambi. Jambo hilo latokea maratunapomwamini Kristo. Mfano wake ni wa Hakimu kumtangazia mshtakiwa „hunahatia‟.

Ni tendo la bure, la neema yake. Ni kipawa, wala haisababishwi na hali yo yotenzuri ndani yetu. Ni kwa fadhili yake, kwa sababu ya upendo wake mkuu alio naokwetu. Iwapo ni kipawa cha bure, haikutokea kwa Mungu kutangaza tu. Ni tofautina uumbaji, katika uumbaji Mungu alisema „iwe nuru, ikawa nuru‟. Munguhakuweza kusema kwa mwenye dhambi „nakupenda sana, dhambi zakezisamehewe‟. Kwa sababu ya Haki na Utakatifu wake ilimpasa afanye tendo lakutengeneza uhusiano baina yake na sisi, (siyo kusema tu) tendolitakaloridhisha Upendo wake pamoja na Haki na Utakatifu wake. Iwapo wokovuni bure, ni kwa neema, ni wokovu ulio wa ghali sana, ulimgharamia Mungu atoeMwana Wake Mpendwa, na huyo Mwana atoe maisha yake mpaka Kufa.

k.24b Hapo Paulo ameeleza tendo lenyewe, ambalo ni tendo la ukombozi, natendo hilo ni msingi wa kuhesabiwa haki bure kwa neema. Ukombozi, maana yaneno hilo ni kulegeza vifungo vya mtumwa au mfungwa au mnyama kwa njia yakulipa fidia. Kwa upande wa wanadamu utumwa ni utumwa wa dhambi (Yn.8:34;Rum.6:17). Wanadamu hawana cha kulipa, kila mmoja amefilisika, ila Mmojaamepatikana, aliyekuwa na uwezo wa kulipa fidia itakayokubalika, na Huyo niYesu Kristo. Yesu Mwenyewe alisema kabla ya Kifo chake „atatoa nafsi yake iwefidia ya wengi‟ (Mt.20:28; Mk.10:45; 1 Pet.1:18-19; Ebr.9:11-12).

k.25 „ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imanikatika damu yake‟ „kumweka‟ ni kukaza jinsi tendo hilo ni la Mungu Mwenyewenalo lilifanyika hadharani pale Kalvari. „awe upatanisho‟. Mungu alimtoa Kristo(1 Yoh.2:2; 4:10). Neno „upatanisho‟ lina maana gani hasa? Maana yake nikuridhisha, kutuliza, kuepusha kwazo. Dhambi ya wanadamu ni kwazo kwaMungu na imesababisha ghadhabu yake. Ghadhabu yake itaondolewaje?Itaondolewa kwa Kifo cha Upatanisho wa Kristo. Tusiwaze kwamba Munguanawaka hasira na kulipuka mara kwa mara kama „volkeno‟ La. ghadhabu yaMungu ni upinzani uliokazwa daima juu ya maovu yote, maana yake Yeye nikinyume kabisa cha dhambi. Mungu ni Nuru naye anaichukia giza. Kwa sababuhaiwezekani kutenga dhambi na yule anayetenda, Mungu huwa kinyume chetu

Page 113: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 775

kwa sababu Yeye hasa ni kinyume cha dhambi zetu. (Mt.18:8-10; 25:30:41,46:Yn.3:18-21; 36: Ufu.6:16-17; 19:15).

Fidia, upatanisho ni Kristo Mwenyewe na Nafsi yake, Yeye alituliza ghadhabuya Mungu juu ya dhambi. Aliepusha ghadhabu ya Mungu isitupate sisi, na badalayake Yeye aliipata. Yesu alistahili kufanya upatanisho kwa sababu mbili(1) Yeye Mwenyewe aliishi maisha ya Haki kamili, hakujua dhambi, hakuwa nadhambi, wala hakufanya dhambi. Yeye aliridhisha Torati na madai yake yote sikwa andiko la nje tu bali kwa maana yake ya ndani, na kwa kimoyomoyo.Twakumbuka Hotuba ya Mlimani na jinsi alivyofafanua maana ya ndani ya sheriazilizoandikwa (Mt.5-6). (2) Pale Msalabani Kristo alizichukua dhambi zetu, nahatia yake, na Mungu alizihukumu katika Yeye. Alikuwa badala yetu akichukuamahali petu ili sisi tuachiliwe dhambi zetu, tusihesabiwe kuwa na hatia walatusihukumiwe kwa ajili yake. (1 Pet.2:14; 3:18, 2 Kor.5:21, Yoh.3:14; ling. naHes.21:8-9: Rum.8:32). Si kwamba Mungu alimruhusu afe tu la! zaidihakumwachilia ghadhabu yake. Zaburi 22 inaonyesha taabu zake.

Kwa nini Paulo alitaja „damu yake‟ kwa nini hakusema „kwa kifo chake‟. Nikuuhakikishia ukweli wa kufa kwake na kumlinganisha na sadaka za Agano laKale. Uhai ni katika damu. Yohana Mbatizaji alimtangaza Yesu kwa maneno„Mwana Kondoo wa Mungu‟ (Yn.1:36). Vifungu vingi vinataja damu yake(Mdo.20:28; Efe.1:7;2:13; Ebr.9:12,10:19; 1 Pet.1:19; 1 Yoh.1:7, Ufu.1:5). KatikaEbr.9:22 imesema „pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo‟.

k.25b „ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili waMungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa‟. Wakati wote wa nyuma, kabla yaKuja kwa Kristo watu walifanya dhambi, ila dhambi zao hazikuhukumiwakikamilifu. Kweli watu walikufa, ila si mara walipofanya dhambi. Sadaka zaKiyahudi hazikuweza kuleta msamaha kamili kwa sababu dhamiri za watuziliendelea kuwashtaki. Zilikuwa tibu za muda. Kama asprin inavyoondoamaumivu ya kichwa bila kuondoa ugonjwa unaosababisha kichwa kuuma.Walitakaswa kwa nje ili waendelee na ibada na maombi. Mungu alivumilia kwasababu haikuwepo njia halisi ya kuondoa dhambi. Alijifanya kama hakuziona(Mdo.14:15-17; 17:30). Ilionekana kama Mungu si wa haki. Lakini hata wakati uleMungu alikuwa mwenye haki, kwa sababu alikuwa ameamuru kumtuma Kristona kumpangia afanye kazi ya upatanisho na ukombozi. Ameonyesha Haki yakekwa sababu Kristo alihukumiwa kwa dhambi zote za wakati wote, za nyuma, zasasa, na za baadaye, maana Yeye ni Mwana wa Milele wa Baba.

k.26 Twaona mkazo wa Paulo ni juu ya Mungu kuwa haki katika kuwaachiliawanadamu dhambi zao na kuwavika haki yake akisisitiza kwamba tendo lenyewelilikuwa la haki. Hakimu ye yote anayemwachilia mkosaji si hakimu wa kweliisipokuwa mwingine akubali kuaadhibiwa badala yake. Kristo alikuwa mjumbewa Mungu kwa wanadamu, na mjumbe wa wanadamu kwa Mungu. Kamamjumbe wa Mungu ametuletea neema iokoayo, ya msamaha wa

Page 114: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI776

dhambi, ya kutotuhesabia makosa, pamoja na neema ya kutuhesabia haki(Isa.45:21; Zek.9:9). Kama mjumbe wa wanadamu alibeba dhambi zetu na hatiana hukumu yake.

Kwa upande wa wanadamu inayotakiwa ni imani katika Yesu Kristo. Si imani yakichwa, bali imani ya kujikabidhi Kwake, kumtegemea kwa yote na kuamini kwadhati kwamba Alikufa kwa ajili ya dhambi zetu.

k.27-31 Kwa kuwa ndivyo ilivyo, Je! ipo nafasi yo yote ya kujisifu? Hamna nafasiyo yote. Sababu zote za kujisifu zimeondolewa. Hata ikiwa mtu anajisifu „eti miminimeamini‟ anakosa, maana anaweka imani kuwa stahili yake, la sivyo, imani nichombo tu cha kupokea kipawa cha haki. Hakuna awezaye kusema „nimepatahaki kwa kazi au matendo au jitahada zangu‟. Tena njia ni ile moja kwa Wayahudina kwa WaMataifa maana wote walikuwa chini ya ghadhabu ya Mungu. SasaMungu huwapokea kwa imani. Kwa hiyo, kwa njia ya Injili sheria iliyodhihirishadhambi imethibitishwa, dhambi imehukumiwa, haki imepatikana na Maandikoyametimizwa.

Uzuri wa kuhesabiwa haki kwa imani ni katika mtu kupewa haki ya Mungu hatakabla hajafanya lo lote la kuistahili kwa sababu anategemea Kustahili KwakeKristo. Ni tofauti sana na njia ya kupata haki kwa sheria, kwa sababu kwa njia yasheria mtu hawezi kuwa na uhakika wa kuhitimu, hana budi kusubiri mpakamwisho, na wakati wo wote wa kati aweza kuteleza na kuingia kosa, na akiingiakosa, basi ameharibu.

Mtu anahesabiwa haki mara moja tu anapomwamini Kristo. Haina maanakwamba amekuwa mkamilifu na mtu asiyeweza kufanya dhambi tena. La!.Ataendelea kuhitaji msamaha kila wakati, ila uzuri ni kwamba amekwishakukubalika na Mungu na kuwa na uhusiano mwema naye. Yu ndani ya Kristo,hawezi kuletwa mahakamani, maana hamna shtaki litakalosimama juu yake kwasababu Kristo ameisha kuhukumiwa mahali pake na badala yake (Rum.8:1,33-34; Mt.20:28; 2 Kor.5:21).

Katika sehemu hiyo yote neno ambalo limetumika mara nyingi ni imani. Katikakufafanua jambo la kuhesabiwa haki kwa imani Paulo alitumia lugha ya uhakimu(haki, sheria, kuhesabu) na lugha ya utumwa (ukombozi) na lugha ya sadaka (kiticha rehema, upatanisho, dhambi).

MASWALI1. Paulo alisemaje alipojumlisha hali ya wanadamu mbele za Mungu?2. Ni nini shida kubwa ya wanadamu?3. Watu wote wamekuwa chini ya nini?4. Mungu ni mwenye haki. Kwa sababu hiyo hawezi kufanya nini?5. Eleza kwa maneno yako mwenyewe fundisho la Kuhesabiwa Haki kwa

Imani kwa kuonyesha msingi wake na uwezekano wake na haki yake.

Page 115: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 777

4:1-25 Mfano wa IbrahimuNi vizuri kusoma Mwanzo 12:1-3; 15:1-6; 16:1-16; 17:15-22; 21:1-21 kwa kupatahabari za mambo makuu katika maisha ya Ibrahimu.

4:1-8 Kuhesabiwa haki kwa imani si matendoKatika sura ya 3:21 Paulo alisema „haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria;inashuhudiwa na torati na manabii‟ yaani katika Maandiko ya Agano la Kale.Katika sura ya 4 anafuata wazo hilo kwa kutumia mfano wa Ibrahimu, Baba waTaifa la Kiyahudi. Paulo angali akiwawaza Wayahudi na makinzano yao. Katikahistoria yao hakuna aliyempita Ibrahimu kwa uzuri (Mt.3:9; Yn.8:33,39). Aliitwa„rafiki wa Mungu‟ (Isa.41:8) nao walimwona kuwa mfano bora wa kupata hakikwa matendo yake mazuri nao walihesabu imani yake kuwa sehemu katikamatendo hayo (Mwa.26:5). Ikiwa Ibrahimu hakupata kibali cha Mungu kwa njiaya matendo yake ni nani atakayekipata?

k.2 Ila Paulo alikaza imani yake si matendo yake. Iwapo alikuwa na mambo yakujisifia, hayo hayakuwa msingi wa Mungu kumkubali wala wa yeye kujiona kuwaamestahili fadhili za Mungu. Kwa nini Paulo alikaza imani yake? Kwa sababuIbrahimu alimwaumini Mungu na ahadi ya kupata uzao, mrithi, nchi, na kuwamfereji wa baraka kwa ulimwengu mzima. Hasa aliamini ahadi ya Kuja kwa Kristona iwapo pengine hakuelewa yote yaliyomo katika ahadi aliyopewa, hata hivyoalielewa ya kutosha kuiamini (Mwa.15:6; Rum.4:21-22; Gal.3:6). Yesu alisema„Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; nayeakaiona, akafurahi..‟ (Yn.8:56-58). Alipoitwa kumtolea Isaka kuwa sadakaakakubali hata akawa tayari kumchinja. Katika tendo hilo Ibrahimu alifunuliwanjia ya ukombozi ambayo Kristo ataifuata (Mwa.22). Kwa hiyo, imani ya Ibrahimuhaikuwa imani ya hewani, ilikuwa imani katika Mungu na ahadi ya Masihi.

k.3 „Maana Maandiko yasemaje?‟ Paulo aliona Maandiko ni mwamuzi katikamambo hayo, aliamini kabisa kwamba njia ya wokovu imekuwa moja tu tangumwanzo na kwa wakati wote. Mungu alitumia njia moja tu hata kwa watuwalioishi nyakati za Agano la Kale. Aliendelea kusisitiza kwamba Ibrahimualihesabiwa haki kwa imani, alipata kibali cha Mungu na kuwa na uhusianomwema naye kwa kumwamini.

k.4-5 Katika vifungu hivi viwili Paulo amesema mambo mawili ya ajabu akitoboawazi ni nani anayehesabiwa haki. (i) Ni mtu asiyefanya kazi (k5b) yaani ni mtuasiye na matendo mema ya kumstahilisha na (ii) ni mtu „asiye mtauwa‟. Alitanguliakwa kuonyesha kwamba mtu anapolipwa kwa kazi amestahili malipo yake,malipo hayawezi kuhesabiwa „thawabu‟ wala kwamba „amefanyiwa kwa neema‟,ni haki yake alipwe. Kumbe! Ibrahimu „hakufanya matendo mema‟ na „hakuwamtauwa‟. Hii ni maneno ya ajabu. Lakini ndivyo ilivyokuwa. Hoja yake imekuwawote „wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu‟ kwa hiyo,Ibrahimu ni miongoni mwao; yeye pamoja na

Page 116: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI778

watu wote ni „watoto wa hasira‟ (Efe.2:3) Tazama maneno ya Yesu juu yaWayahudi (Yn.8:33-47). Mbeleni Paulo alisema „Kristo alikufa kwa ajili yetutulipokuwa „tungali wenye dhambi‟ pia „adui‟ na tulipokuwa „hatuna nguvu‟(Rum.5:6,8,10). Ibrahimu alipoitwa kwa mara ya kwanza alikuwa akiiabudumiungu pamoja na jamaa zake (Yos.24:2).

(Fikiri itakuwaje ikiwa Mungu atatulipa „mshahara‟ kwa matendo yetu. Je!tutapata nini? Kwa mema tutalipwa, na kwa mabaya tutapunguzwa, Je! tutabakina nini? Si afadhali kupokea zawadi ya bure!)

Daima Ibrahimu alisimama imara katika kuziamini ahadi za Mungu iwapomwenyewe hakuweza kufanya lo lote la kusaidia jambo hilo la kupata mrithi. Halizote zilikuwa kinyume chake. Alikuwa mzee sana, Sarai mkewe alikuwa tasa,tena mzee; Eliezeri mtumishi wake hakuwa na haki ya urithi, na Ishmaelialiyemzaa kwa Hajiri alikataliwa. Pamoja na magumu hayo yote ilimbidi asubirimuda mrefu sana. Kwa hiyo, hakuwa na la kufanya, ila katika udhaifu huo wotewa kushindwa kwake aliendelea kumwamini Yule Aliyemwahidi.

Habari jinsi Ibrahimu alivyohesabiwa haki inapatikana katika Mwa.15:1-6ku. Niimani yake hai katika Mungu iliyozaa matendo mazuri ya kumpendeza Mungu.

k.6-8 Kwa habari za Daudi ni vema kusoma 2 Sam.11; Zab.51; na Zab.32. Pauloaliendelea kusisitiza habari za Kuhesabiwa haki kwa Imani akitumia mfano waDaudi, Mfalme mashuhuri wa Wayahudi aliyeishi muda mrefu baada yaIbrahimu. Katika Zaburi 32 Daudi alinena juu ya mtu aliye heri, (bila shakaalikuwa akijinena habari zake) akisema huyo mtu ni yule ambaye Munguamhesabia kuwa na haki pasipo matendo. Jambo kubwa ni huyo mtukusamehewa dhambi zake na kupewa haki ya Mungu. Daudi alifanya dhambikubwa, alizini na mke wa Uria, halafu akapanga Uria auawe vitani. Daudialisamehewa dhambi hiyo ya uzinifu na uuaji na alisikia nafsini mwake baraka yakusamehewa dhambi zake na kuondolewa hatia yake machoni mwa Mungu.Mungu aliendelea kushirikiana naye. Kwa hiyo, kuna ulinganifu kati ya mtukuhesabiwa haki na mtu kutokuhesabiwa dhambi.

Katika Agano la Kale twasoma jinsi ilivyo chukizo kumwachilia mtu aliyekosa nani chukizo zaidi kumhesabia haki (Kut.23:7; Mit.17:15; Isa.5:23). Pauloaliwaweka Ibrahimu na Daudi kuwa sawa, kwa sababu kila mmoja alitendadhambi iwapo Ibrahimu alionekana kuwa mcha Mungu na mtiifu hata hivyoalikosa mara kwa mara. Ilikuwa dhahiri kwamba Daudi alitenda dhambi kubwa,hata hivyo alifanya matendo mazuri pia ila matendo mazuri aliyofanyahayakutosha kufunika dhambi zake.

Hata sisi wenyewe hatuwezi kukubali mkosaji asihukumiwe. Tuone jinsi watuwanavyoinuka na kupiga kelele wanapofikiri mtu hakuadhibiwa ya kutoshakulingana na makosa yake. Wanaodhulumiwa waona ni haki kabisa kesi zao

Page 117: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 779

zipelekwe mahakamani wakitazamia kwamba Hakimu atatoa hukumu za haki.Inahesabiwa ni vibaya sana hakimu kupokea rushwa ili kumwachilia mtu, tenawatu hukasirika wanapokuta jalada la kesi limepotea bila sababu. Ikiwa sisiwakosaji twajua neno la haki Je! si zaidi sana Mungu? Kwa hiyo, tuna haja yakufurahi sana kuona kwamba Mungu amepata njia ya kutuachilia sisi zile adhabutunazostahili, huku Mwana wake mpendwa ameadhibiwa mahali petu, huu ndioupendo wa ajabu, hii ndiyo neema ya ajabu!.

4:9-12 Kuhesabiwa haki kwa imani kulitokea kabla ya ToharaSwali kubwa ni „uheri huo wa kuhesabiwa haki kwa imani ni kwa waliotahiriwa aukwa wasiotahiriwa pia?‟. Ibrahimu alikuwa wa kwanza kutahiriwa, lakini ni linialipohesabiwa haki, kabla au baada ya kutahiriwa? Ni dhahiri kwamba alitahiriwabaada ya kuhesabiwa haki kiasi cha miaka 14 hivi. Kama ni hivyo tohara ilikuwana faida na kazi gani? Paulo alisema kwamba tohara ilikuwa muhuri wa ile hakialiyopata kwa imani mbali na torati na kabla ya tohara. Tohara ilikuwa alama yanje, thibitisho la imani ya ndani, kama uhakikisho wa ahadi iliyotolewa na ya hakiiliyopokelewa kwa imani miaka iliyotangulia (Yn.6:27; Efe.1:l3-14) Toharahaikuongeza kitu, kuhesabiwa haki ni kwa njia ya imani peke yake bila nyongezoya aina yo yote.

Kwa hiyo, Ibrahimu ni baba wa wote wanaomwamini Kristo, waliotahiriwa kamaWayahudi, na wasiotahiriwa kama WaMataifa, mradi Wayahudi pamoja naWaMataifa wanayo imani inayolingana na ile ya Ibrahimu. Maana yeyemwenyewe kabla ya kumzaa mwana hakuwa baba wa taifa, na kabla yakutahiriwa hakuwa Myahudi (Yn.8:34-44; Gal.3:6-24). Kwa hiyo, tohara ni isharayake si sababu yake. Ibrahimu ni baba wa waumini wa KiMataifa na baba wawaumini wa Kiyahudi. Kutahiriwa na kutokutahiriwa si kitu (Gal.5:6). Neno hilolahusu Wakristo na sakramenti zetuambazo ni muhuri si kitu chenyewe kwasababu zenyewe hazina uwezo wa kufanya lo lote bila imani ya mtu na zaidi bilaneema ya Mungu.

Walikuwapo Wakristo wa Kiyahudi waliowaza kwamba iwapo imani ni lazima nijambo muhimu kutahiriwa pia. Nao walisababisha shida na fitina nyingi katikamakanisa, hasa kwa sababu walitaka kuwalazimisha Wakristo wa KiMataifawatahiriwe, jambo la kigeni kwao. Walimfuatia Paulo sana wakijaribu kutikisaimani ya waumini wapya (Mdo.11:2-3; 15:1-5; Gal.2:12-15).

4:13-25 Ahadi ilitimizwa kwa njia ya imani siyo kwa sheriak.13 Baada ya kuzungumza neno la tohara ilimbidi Paulo azungumze habari zaTorati. Ahadi ya Mungu ilitangulia Torati. Ni jambo la historia, maana Ibrahimualiishi miaka mia nne na thelathini kabla ya Torati kutolewa (Gal.3:17). Ibrahimualipewa ahadi ya kuwa mrithi wa ulimwengu (si wa Palestina tu) mapema sana,na ahadi hii ya uzao (ambao hasa ni Kristo Gal.3:16). Ahadi ziliendelea kuwepohata baada ya Torati kuingia. Alikuwa mrithi si kwa sababu

Page 118: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI780

ya ukoo wake wala matendo yake, bali kwa neema. Ahadi haikuguswa na Toratikwa kuwa msingi wake ulikuwa wa kuhesabiwa haki kwa imani.

k.14a Hakuna haja kwa imani ikiwa Torati inaingia kwa sababu hali ya sheria nikufanya jambo, sheria na imani vinapishana. k.14b „ahadi imebatilika‟ kwasababu kwa sheria kamwe ahadi isingalipata kutimizwa.

k.15 Paulo aliweka pamoja maneno sheria, kosa, hasira na katika k.16 manenoimani, neema, ahadi. Kwa ahadi itikio ni kuipokea (Gal.3:18) Ni kuipokea bilakuwaza au kutegemea sababu za ustahili, ni ahadi, basi ipokelewe tu. Ibrahimualikuwa bado hajafanya lo lote la kuistahili ile ahadi aliyopewa, alikuwahajatahiriwa bado, na hakuweza kutimiza maagizo ya Torati kwa kuwa ilikuwahaijatolewa bado. Ni kwa neema ya Mungu tu alipewa. Kwa sababu aliipokeakwa imani Mungu alimhesabia haki, maana Ibrahimu aliweka tumaini lake lotekwa Mungu. Ahadi ilikuwa imara kwa sababu ilitoka kwa Mungu mwenye uwezowa kuitimiza (4:21), Ibrahimu aliamini kwamba Mungu anao uwezo wa kuhuishawafu na kuumba kitu kutoka pasipo na kitu (4:17). Kwake ahadi haikuwa manenomatupu tu, bali maneno yenye nguvu ya Mungu. Kwa sababu ahadi ilitoka kwaMungu ilikuwa na uhakika wa kutimizwa.

Torati haikutolewa kuwa njia ya kupata haki, kwa sababu hakuna mtu awaye yoteawezaye kuyatimiza maagizo yake kwa ukamilifu. Ilitolewa kwa shabaha yakuwahakikishia watu kushindwa kwao na kuwaonyesha hali yao halisi ya kuwawenye dhambi. Ilifunua dhambi, na zaidi ya kuifunua, hata ilichokoza dhambi.Ndani yetu umo uvutano wa dhambi, mara nyingi dhambi imetulia bila kujitokezampaka uchokozi fulani kama sheria au katazo fulani limetolewa, ndipo dhambiinaamka na kosa latendeka. Torati ni baraka kwa wote wazishikao amri zake ilani laana kwa wote wasiozishika, na kwa sababu ya udhaifu wetu laana imezidibaraka. Torati haifanyi watu kuwa wenye haki ila kinyume chake inadhihirishauasi wao wa kutokushika sheria za Mungu, na uasi huo unasababisha ghadhabuya Mungu.

k.17-22 Imani ya Ibrahimu ilikuwa sawa na kuamini ufufuo wa wafu: Mungualimwahidi Ibrahimu kwamba atakuwa „baba wa mataifa mengi‟ (Mwa.12:3;17:4). Ni Mungu aliyemweka kuwa „baba‟ tena wa „mataifa mengi‟ si wa taifamoja tu. Ibrahimu alimwamini Mungu kuwa Mungu halisi. Alimwamini Mungumwenye uwezo wa kuhuisha wafu. Imani yake haikuwa ya kichwa tu, yeyemwenyewe aliamini neno hilo kuhusu mwili wake na mwili wa mkewe. Miili yaoilikuwa katika hali ya kufa kwa upande wa kumzaa mtoto na kumpata mrithi.Mungu alitoa ahadi kwa huyo mtoto mrithi ambaye bado hajazaliwa kana kwambatayari amezaliwa, na Isaka aliirithi hiyo ahadi. Baadaye Ibrahimu aliitwa kumtoaIsaka awe sadaka, na Ibrahimu alimtii Mungu, akawa tayari kumchinja na dakikaile ile ya kunyoosha kisu juu yake Mungu akamwambia aache kumchinja(Mwa.22; Ebr.11:17-19). Mungu kwa Ibrahimu hakuwa dhana ya kichwani walaMungu wa mbali asiyehusika na mambo ya binafsi, la, kwake

Page 119: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 781

Mungu alikuwa yule aliyempa yeye, mkewe, na mwanawe, uzima. Ila tusisahaukwamba mara kwa mara Ibrahimu alikuwa na dosari katika imani yake(Mwa.16:1-3; 17:17-21).

Kwa mawazo na kwa hali za kibinadamu Ibrahimu hakuwa na tumaini lo lote lakupata mrithi. Hata hivyo alitazama hali hizo kwa imani katika Mungu mwenyeuwezo wa kuzibadili na kuzishinda, kutokana na ahadi aliyopewa na Mungu.Hakufumba macho kwa hali zake, aliweza kuziona, na mara kwa mara zilimpashida maana alijua hakika kwamba kwa hali za kibinadamu haitawezekana azaemtoto, hata hivyo aliendelea kuamini. Kadiri alivyoendelea kuishi na kuzeekandivyo alivyozidi kumtazama Mungu na kuitegemea ile ahadi aliyopewa, akizidikuacha kutazama mwili wa uzee wake. Hasa tegemeo lake lilikuwa katika ahadiya Mungu na katika Mungu aliyemwahidi.

Kuamini si jambo jepesi, kunaleta mashindano makali, na kwa vyo vyote lazimamtu akaze nia yake, amtazame Mungu, asiangalie hali na mazingara yake ili asijeakashindwa kuamini.

k.23-25 Imani ya Ibrahimu ilikuwa limbuko la Ufufuo wa Yesu. Ndipo Pauloalionyesha jinsi habari za Ibrahimu zinavyotuhusu sisi, maana sisi nasitunamwamini Mungu aliyemfufua Yesu kutoka wafu. Sisi sawa na Ibrahimutwamshuhudia Mungu kuwa „mwenye kuhuisha wafu‟. Yote aliyosema Pauloyametimizwa katika Ufufuo wa Yesu. Waumini wanahesabiwa haki kwa imanikatika Mungu aliyemfufua Yesu kutoka wafu. Ni imani ile ile katika Mungu yuleyule wa kuhuisha wafu. Mungu alimtoa Isaka kutoka mwili „mfu‟ wa Ibrahimu nawa Sarai. Mungu alimtoa Yesu kutoka kaburi la mauti. Mungu anawaita wauminiwatoke mauti ya dhambi na kuishi maisha mapya. Ni Uumbaji Mpya. Katika k.25Paulo amefupisha hayo yote, „kufa kwa ajili ya makosa, na kufufuliwa kwa haki‟.Katika hayo yote twaona upendo wa ajabu wa Mungu. Dhambi zetu zimemwudhisana, hata hivyo, kwa neema yake amethubutu kutupatia haki kamili, haki yakeMwenyewe. Kwa gharama ya Mwana wake kuuawa Msalabani na kuchukuadhambi zetu, hatia zetu, na adhabu zetu, mwilini mwake. Hii ni neema ya ajabu,na hayo yote bila sisi kuwa na nukta moja ya ustahili.

MASWALI1. Kwa nini Paulo alitaja habari ya Ibrahimu na Daudi? Alikuwa na shabaha

gani?2. Alionyesha kwamba Ibrahimu alihesabiwa haki kwa imani kabla ya .......

na kabla ya kutolewa kwa ...........3. Ibrahimu ni „baba‟ wa akina nani?4. Taja sifa za imani ya Ibrahimu.

Page 120: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI782

5:1-11 Baraka za Kuhesabiwa Haki kwa Imanik.1a „Basi tukiisha kuhesabiwa haki...‟ Sura zilizotangulia zimetutayarisha kwatangazo hilo. Tendo la kutuhesabia haki limekwisha kutendeka. Sasa Pauloaliendelea kwa kueleza baraka zake. Paulo hakutenga tendo lenyewe, ambaloni la mara moja, na matokeo katika kuishi maisha yawapasayo wale waliokwishakuhesabiwa haki kwa imani. Habakuki alisema „mwenye haki ataishi kwa imani‟(1:17). Ataishije? sura za 5-8 zatoa jibu la swali hilo. Kwa kuwa „urafiki‟umechukua nafasi ya „uadui‟ mlango umefunguliwa kwa waumini kupitia ndaniya kivuli cha neema na kukanyaga njia iendayo uzimani.

Baraka kubwa ya kwanza ni kuwa na amani na Mungu. Uadui uliokuwapo kwasababu ya dhambi umekwisha kwa sababu tatizo la dhambi limetatuliwa na Kifocha Yesu Msalabani. Amani hiyo ni „hali halisi‟ iliyopo kweli, si hali ya kusikia tu.Ni kipawa cha Mungu, na kama tulivyoamini ili tuhesabiwe haki vivyo hivyotwaendelea kuamini na kutegemea neema ya Mungu tunapoishi maisha mapya.Amani si raha tupu, wala utulivu kama ule wa makaburi. Hasa ni haliinayomruhusu mtu kutimiza shabaha ya kuumbwa kwake, shabaha ambayohapa nyuma ilizuiliwa na dhambi, ili awe „mzima‟ „Kwa njia ya Bwana wetu YesuKristo‟. Kama Yesu Kristo ni kiini cha upatanisho vivyo hivyo Yeye ndiye kiini chamaisha yetu mapya.

k.2a Baraka nyingine ni kupata nafasi na njia ya kumkaribia Mungu na kuishikatika „kibali‟ chake. Tumeletwa „karibu‟ ili tusimame katika „Kuwapo kwa Mfalmewetu‟ tumeletwa mbele zake, mahali pa heshima, tumesimama katika pendoLake, kibali chetu kimeitwa „neema hii‟ (Gal.5:4; Efe.3:12; 1 Pet.5:12). Katikakibali hicho mtu husikia usalama na uthabiti. Ana nafasi ya kumkaribia Munguwakati wo wote bila kizuizi cho chote. Hali hiyo inaanza mara mtu anapomwaminiKristo na inaendeleaendelea.

Baraka nyingine ya kuhesabiwa haki ni kufurahi katika tumaini la utukufu waMungu‟. Mtu aliyehesabiwa haki amemweka Mungu kuwa tumaini lake.Anatarajia kwamba mbeleni atashirikiana na Mungu kwa ukaribu sana katikauzima wa milele kwenye Utukufu wake. Katika siku ya mwisho Utukufu waMungu utadhihirika wazi kabisa na wote walio Wake wataushiriki (Mt.16:27;24:30; 25:31; Tit.2:13; 1 Pet.4:13; Yud.24; 1 Yoh.3:2). Pia waumini wenyewewatarudishiwa hali ya „utukufu‟ ambao dhambi iliwanyima (3:23). Kila mtuhufurahi anapotazama mbele kwa kutokea kwa jambo zuri, vivyo hivyo, Mkristohuyafurahia matazamio ya kufika mbinguni na kushirikiana na Mungu ana kwaana.

k.3-5 Furaha ya Mkristo haihusu mambo ya mbele tu, ila pia yahusu maisha yasasa, hata maisha ya dhiki. Agano Jipya lafundisha kwamba ni fungu la wauminikupatwa na dhiki na mateso kwa ajili ya Kristo na Paulo aliandaa mawazo yawaumini wapya juu ya jambo hilo ili wajue ni kawaida ya maisha ya

Page 121: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 783

Mkristo si jambo geni (Mdo.14:22; 1 The.3:3). Paulo hakusema tuivumilie dhikibali tuifurahie kwa sababu ya matunda inayoyazaa maishani mwetu.

k.3b Paulo alitaja kazi na faida ya dhiki. Inaleta saburi, mtu kwa magumuanayopata ajifunza kumtegemea Mungu na kusubiri msaada wake, hivyo mtumwenyewe huthibitika na kufanana na mtu anayeifaulu mitihani ya imani yake.Anahitimu kwa sababu anapokea dhiki na shida kwa furaha bila kumnung‟unikiaMungu. Hivyo anatiwa nguvu na kuimarika zaidi na zaidi hali akihakikishiwaukweli wa imani yake (2 Pet.1:5-7). Pia katika shida muumini hujifunzakumtumaini Mungu kwa msaada wa kumpitishia salaam katika shida.

k.5a Mwishowe hatatahayarika, atadhihirika kuwa mtu wa kweli mwenye imaniya kweli. Ana uhakika wa mwisho wa safari yake.k.5b. Zaidi ya yote atakuwa amejaa upendo wa Mungu moyoni mwake, atakuwana upendo ule ule aliokuwa nao Kristo alipotoa maisha yake Msalabani (1Yoh.4:10,19). Mungu ni pendo na mtu anayeshirikiana na Mungu hushirikishwatabia zake. Neno „kumiminwa‟ linaonyesha ukarimu wa Mungu. Upendo huo niwa binafsi tena tunapewa kwa njia ya Roho Mtakatifu. Hivyo waumini wazidikufanana na Kristo (1 Yoh.3:2; Yn.17;22,24; Rum.8:29; 2 Kor.3:18; Flp.3:21;Kol.3:4; 2 The.2:14).

k.6-11 Upendo mkuu wa Mungu: Paulo aliendelea kusema juu ya kuhesabiwahaki kwa imani akionyesha chanzo chake katika upendo wa ajabu wa Munguuliodhihirika alipomtoa Mwana Wake Mpendwa kwa kufanya upatanishouliohitajika.

Upendo wa Mungu umeonekana katika mambo mawili. Kwanza kwa kutazamaupande wa wanadamu na hali yetu. Mungu alimtuma Kristo tulipokuwa mbalinaye bila hali yo yote ya uvutifu au ustahili mbele zake. Tulikuwa waovu (k.6)tulikuwa tungali wenye dhambi (k.8) tulikuwa adui (k.10). Kwa kusema hivyoPaulo alitaka kuonyesha jinsi ambavyo hatukuwa na hali yo yote ya uvutifu auustahili. Kinyume chake tulikuwa na hali zilizostahili hukumu yake. Picha ni yawatu dhaifu, wasio na uwezo wala nia ya kutimiza torati au maadili. Ni wakatihuo huo wa sisi kuwa na hali hizo ambapo Mungu alitangulia kutenda tendo laupendo wa ajabu. Kwa hiyo, alitenda kwa wasiostahili. Mungu huwasaidiawale wasioweza kujisaidia.

Pili kwa kutazama upande wa Mungu, upendo wa Mungu umeonekana katikautendaji wake. Alimtuma Mwana Wake Mpendwa wa Pekee ili awe fidia yadhambi zetu na Kufa Msalabani kwa kumpatanisha Mungu na sisi. Hakutumakadi zenye salaam, bali alikuja kwetu katika Yesu Kristo. Kristo alipokuja akatoamaisha yake mpaka Kufa kwa ajili yetu. Kwa njia hiyo ya gharama kubwa Mungualifaulu kupata njia ya kutusamehe dhambi na kutuvika haki Yake.

Page 122: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI784

k.6 „wakati ulipotimia‟ ni ukumbusho wa wakati ulipofanyika huo upatanisho,ulikuwa wakati wa kufaa, wakati ambao nyakati zote zilizotangulia zililenga, nakatika wakati huo na kwa tendo lililotendeka wakati huo, makusudi makuu yaukombozi wa ulimwengu yalitimia (Gal.4:4; Ebr.9:26; 1 Kor.10:12).

k.7 Ni vigumu kujua maana yake hasa ya kifungu hicho ila inaonekana Pauloalitaka kuonyesha jinsi upendo wa Mungu ulivyo tofauti sana na upendo wetu. Nivigumu sisi kufa kwa ajili ya mtu, labda mara chache kwa mtu mzuri ila ni vigumumno mtu akubali kufa kwa ajili ya mtu mbaya au aliye adui. Sisi twashindwakuwaza licha ya kupenda na kutenda kama Mungu.

k.8 Maneno „Kristo alikufa kwa ajili yetu‟ ni Injili yenyewe. Kila aliposema Paulokuhusu upendo wa Mungu, au haki yake alisikia msukumo wa kutaja Kifo chaKristo Msalabani.

k.9 Kuhesabiwa haki kunatokea mara moja mtu anapomwamini Kristo na kaziYake ya ukombozi iliyofanyika Msalabani. Tokeo moja la baadaye ni kuokolewana ghadhabu ya Mungu katika siku ya mwisho. Katika siku hiyo Munguatahukumu dhambi na uasi wote wa wanadamu (Rum.2:5,8; 1 The. 1:9,10; 5:9;Ufu.6:16,17; Mt.3:7). Wamwaaminio Kristo hawatapatwa na ghadhabu ya Mungukwa sababu dhambi zao zimekwisha kuhukumiwa katika Kristo alipokufaMsalabani (Rum.8:1).

k.10 Ndipo Paulo alionyesha ya kuwa ikiwa tulipatanishwa wakati tulipokuwatungali wenye dhambi na bila nguvu, basi baada ya kupatanishwa nakupokelewa na Mungu kama rafiki na kuletwa kwenye uhusiano mwema naye,haikosi tutashirikishwa uzima wa Kristo. Kama Yeye Alikufa ndipo Akafufuka hatasisi tutafufuka katika siku ya mwisho, lakini si siku ile tu, hata sasa twashirikishwanguvu zake za Ufufuo kwa kuwa Yeye yu Hai sisi nasi tutakuwa hai kwa haki nawafu kwa dhambi (Efe.1:19)k.11 Kwa hiyo, badala ya kumhofu Mungu twamfurahia sana kwa njia ya Kristo.Upatanisho ni kipawa tunachopokea kwa imani, ni sawa na kuhesabiwa haki.Katika sehemu hiyo yote twaona mkazo wa Paulo kuhusu kila jambo kuwa „katikaKristo‟ na „kwa njia ya Kristo‟, Yeye Kristo ndiye KIINI cha mambo yote.

5:12-21 Kuwa ‘katika Adamu’ - kuwa ‘katika Kristo’Alianza na maneno „kwa hiyo,‟ kwa kuonyesha uhusiano na aliyosema katika5:1-11. Aliyosema hapo nyuma yalimhusu Ibrahimu na Kristo. Katika sehemuhiyo Paulo amepanua mawazo yake kwa kumwingiza Adamu, wa kwanza katikawanadamu wote. Paulo aliweka wanadamu wote chini ya „vichwa viwili‟ chaAdamu na cha Kristo. Adamu ishara ya „mauti‟ Kristo ishara ya „uzima‟. Kristo nimuhimu kwa ukombozi wa walimwengu wote. Kristo ni „Adamu wa mwisho‟ (1Kor.15:45) aliyekuja kutukomboa na hasara zote zilizoletwa na Adamu wakwanza.

Page 123: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 785

k.12 „mtu mmoja‟ Alianza na Adamu (japokuwa hakutumia jina la Adamu) nakusema kwamba kwa njia ya „mtu mmoja‟ dhambi iliingia ulimwenguni nahukumu ya mauti iliwafikia watu wote „kwa sababu wote wamefanya dhambi‟.Maneno hayo maana yake ni kwamba wanadamu wote walikuwa „katika Adamu‟alipofanya dhambi, kwa hiyo walikuwa pamoja naye katika dhambi yake. Kwahiyo, wamehukumiwa pamoja naye, na wote wanakufa kwa sababu hiyo. Kwahiyo, Paulo alifundisha kwamba watu wote walifanya dhambi Adamu alipofanyadhambi, kama alivyosema kwa wazi katika k.17-18. Kwa hiyo, watu wote niwenye dhambi kwa sababu ya kuwa katika Adamu si kwa kufuata mfano waketu, iwapo hii pia ni kweli (3:21).

k.13-14 Hapo Paulo aliachia hoja hiyo mpaka vifungu vya mbele Alijua wenginewatasema „Je! imekuwaje kwa upande wa Musa na Torati?‟ kwa sababu mtuhawezi kuasi sheria kama sheria haijatolewa bado. Katika k.13 alionyeshakwamba hata kabla ya kuja kwa Torati dhambi ilikuwamo na watu walikufa. Tenaalisema katika k.14 wengine hawakukosa kama Adamu, yaani hawakuasi amrifulani hasa kama ile iliyotoka kwa Mungu kama Adamu alivyofanya alipoambiwa„msile‟, hata hivyo walifanya dhambi na kufa. Dhambi ilikuwamo ulimwengunibila kuwapo kwa sheria. Ni sheria inayochokoza dhambi iliyofichwa ndani nakuitokeza nje ipate kuonekana katika kosa. Kwa hiyo, Torati haikuleta jambojipya hasa. Kazi yake ilikuwa kazi ya muda, ya kuidhihirisha dhambi na kuitokezanje ili ionekane wazi kusudi wanadamu wajue kwa uhakika kwamba ni wenyedhambi.

k.14 „Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja‟ yaani Kristo. Iwapo wotewawili wamefanana katika kuwa „vichwa‟ hata hivyo Kristo ametofautiana sanana Adamu kwa sababu amezipindua hali mbaya zote zilizosababishwa na uasiwa Adamu.k.15-18 Paulo amesema wazi dhambi iliingia kwa njia ya kosa moja la mtummoja Adamu, kosa lile la kutokumtii Mungu alipoambiwa asile matunda ya mtiwa ujuzi wa mema na mabaya (Mwa.2:17). Kwa kosa hilo wengi waliingizwakatika hali ya kuwa wenye dhambi na kuhukumiwa adhabu ya kufa. Katikaneema ya Mungu na kipawa chake cha kuwahesabia haki kwa kumwamini Kristodhambi nyingi za watu wengi zimesamehewa. Kwa tendo moja la utii la Kristohaki imepatikana na kwa haki uzima. Kwa hiyo, Kristo amepata baraka kubwasana ya kushinda hasara yote iliyosababishwa na Anguko la Adamu. Kristoalimtii Baba wakati wote katika yote na alifikia upeo wa utii alipotoa maisha yakempaka kufa pale Msalabani (Flp.2:5-8). Kwa hiyo, hata dhambi ilipozidihaikuwezekana ishinde neema tele ya Mungu. Kristo anao uwezo wa kuokoakuliko Adamu kuharibu.

k.17 Paulo amesema „mauti ilitawala‟ maneno hayo yaonyesha jinsi wanadamuhawakuwa na la kufanya, lakini wale wanaohesabiwa haki „watatawala katikauzima‟ si uzima utawatawala ila watu wenyewe watajaliwa nguvu za Kristokushinda dhambi. k.19 Kifungu hiki chakaza fundisho la Paulo

Page 124: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI786

juu ya Adamu na Kristo na juu ya kuasi kwa Adamu na tokeo la wengi kuingizwakatika hali ya wenye dhambi, na juu ya kutii kwa Kristo na tokeo la wengikuingizwa katika hali ya wenye haki. Kwa hiyo, katika Adamu mfuatano nidhambi, hukumu/adhabu, mauti; na katika Kristo mfuatano ni utii, haki, uzima.Wote wamo katika Adamu. wamo katika Kristo kwa njia ya kumwamini Yeye naKifo Chake cha Upatanisho. Kristo ni kichwa cha jamii mpya ya wanadamu.Wanadamu wote wamefungamana katika Adamu, wote wamwaminio Kristowamefungamana katika Kristo. Paulo alizidi kukaza „umoja‟ wa wanadamu katikadhambi na katika wokovu.

k.20-21 Paulo alirudia kuonyesha kazi ya sheria. Kama ambavyo tumeishasemaTorati ililetwa ili kosa liwe kubwa sana, badala ya kuwa kizuizi kwa dhambi (kamabreki ya baisekeli) ilikuwa kama kipachuzi (akselerata ya gari) cha dhambi. Uzuriwa ajabu ni kwamba neema ilizidi na kuja juu ya dhambi ikatupatia haki, hakikamili ya Mungu, tena ilipatikana kwa njia ya haki, ili neema itawale na tujaliweuzima kwa sasa hata milele.

MASWALI1. Taja baraka za kuhesabiwa haki kwa Imani:2. Paulo alisema Kristo alikufa kwa ajili yetu tulipokuwa:

a. ....................................................b. ....................................................c. ....................................................

3. Ni kitu gani kilichomsukuma Mungu atafute njia ya kuwapatia wanadamu haki?4. Katika „Adamu‟ wanadamu wote wamerithi nini?5. Katika „Kristo‟ kwa imani watu warithi nini?6. Eleza ni kwa jinsi gani Kristo na tendo lake kuu la utii ni muhimu sana kuliko

Adamu na uasi wake.

6:1-23 Kuunganika na Kristo - Uhuru na DhambiKuhesabiwa haki kwa imani si mwisho, bali ni mwanzo, mwanzo wa maishamapya ya haki na utakatifu. Watu huokolewa kwa imani peke yake, ila ile imaniinayookoa haiwi peke yake, inafuatwa na maisha ya matendo mema, uhakikishowa uhai wa ile imani na wa ule uhusiano unaoletwa na imani hiyo, ambao nithibitisho la ukweli wake. Imani si jambo la kichwa, ni jambo la kujikabidhi kwaKristo, kwa kumwamini na kumpenda na kumtii.

(a) 6:1-14 Kuunganishwa na Kristo hakupatani na dhambiPaulo alikuwa na shabaha ya kuonyesha kwamba Kufa na Kufufuka kwa Kristo

si matukio ya kihistoria tu, wala mafundisho maalumu ya Kikristo tu, bali pamojana hayo yote ni matukio yanayogusa maisha ya waumini. Kila muuminiameingizwa na kushirikishwa Kufa na Kufufuka Kwake Kristo kwa sababu Kifocha Kristo ni njia ya wokovu wetu pia ni mfano wa kuishi kwetu baada ya

Page 125: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 787

kuokolewa. Katika sura ya 5 Kristo alikufa kwa wenye dhambi, katika sura ya 6waumini waliifia dhambi. Paulo alitaja kufa mara nyingi katika sura ya 6.

Wakristo wote wameunganishwa na Kristo katika Kifo Chake, Kuzikwa Kwake,na Kufufuka Kwake. Hivyo hoja ya Paulo ni kwamba haiwezekani waendeleekatika dhambi. Kuanzia k.1 hadi k.14 Paulo amezungumzia jambo la kuunganikana Kristo na k.15 mpaka k.23 ametumia mfano wa utumwa kuonyesha ya kuwawaumini hawawi tena „watumwa‟ wa dhambi bali „watumwa‟ wa haki/Mungu.

k.1-14 Tukirudi kwenye 5:20b twakuta maneno „dhambi ilipozidi neema ilikuwanyingi zaidi‟. Maneno hayo na fundisho la kuhesabiwa haki bure kwa imani pekeyake yalisababisha wengine kumshtaki Paulo kwamba alifundisha „tuendeleekatika dhambi kwa sababu neema itazidi, Mungu atatusamehe tu?‟. Au „Kwa nininijitahidi kuishi maisha mema, kwa sababu Mungu anajua mimi ni mwenyedhambi ambaye sina nguvu ya kushinda dhambi?‟. Wengine waliona ya kuwamafundisho ya namna hiyo yalilegeza wajibu wa mtu kuishi maisha mazuri nakuelekeza watu kufikiri kwamba dhambi si jambo zito. Kama Mungu ametukubalikwa neema bila matendo kwa nini tusiishi jinsi tupendavyo? (Yud.4). Maneno ya5:20b ni maneno ya kutukuza neema ya Mungu siyo maneno ya kuiruhusu aukutoa udhuru kwa dhambi. Watu walikuwa wamekosa kuelewa maana yamaneno ya 5:21 ya kuwa ni haki inayotawala tunapokuwa „chini ya neema‟,tumeletwa kwenye eneo la haki tofauti sana na lile eneo la dhambi la hapo nyuma.

Ndiyo sababu Paulo alianza sura hiyo na maswali „tuseme nini basi?‟ „tudumukatika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?‟. Mara moja Paulo alikanusha mawazohayo kwa kutumia neno la nguvu „Hasha‟ ndipo alitoa mafundisho juu yakuunganika na Kristo. Twaona hakubadili au kupunguza fundisho la kuhesabiwahaki kwa imani, alikaza kabisa kwamba wokovu ni kipawa cha bure asichostahilimtu kupewa. Kwa Paulo fundisho hilo lilikuwa kiini cha Injili ya kweli potelea mbaliwatu watalilaumu au kulipuuza au kulimaanisha tofauti na maana yake ya kweli.Katika k.2 aliendelea kwa kuuliza swali lingine „sisi tuliofia dhambi tutaishije tenakatika dhambi?‟ Paulo aliona kwamba shida kubwa ya hao watu waliopingafundisho hilo ilikuwa katika kutokuelewa Mkristo ni mtu gani hasa. Mkristohuanzia maisha yake kwa „kuifia dhambi‟. Kifo cha Kristo kimekomesha uhusianowa mtu na dhambi; k.2b „tutaishije tena katika dhambi?‟. Kama ni hivyo niupumbavu kuuliza kama mtu anayo ruhusa ya kufanya dhambi, au aweza kutoaudhuru kwa dhambi zake. Atawezaje kuendelea kuishi katika kile kitu ambachoalikifia. Yawezekana, ila ni kinyume cha shabaha ya kumwamini Kristo. Tena nivigumu sana kuwaza hivi kwa sababu Kristo alikufa kwa ajili ya kutuokoa nadhambi.

Ni vema tuulize „ni wakati gani na kwa njia gani Mkristo alifia dhambi?‟ Inamaana gani? Jambo hilo lilitokea lini na kwa jinsi gani?

Page 126: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI788

k.3-5 Katika vifungu hivi Paulo alionyesha kwamba mtu aliyehesabiwa haki kwaimani ameunganika na Kristo. Kwanza Mungu alimhesabia haki „katika Kristo‟ nakumtangaza kuwa hana hatia. Jambo hilo liligusa maisha yake. Hakunakuhesabiwa haki na Mungu bila kuunganika na Kristo. Tuliifia dhambi wakatiKristo alipokufa kwa dhambi zetu, tulikuwa tukifa pamoja naye. Aliyofanya Yeyendiyo tuliyofanya kwa kuhesabiwa kuwa pamoja naye. Si kwamba tulisikiamaumivu na mambo yote yaliyompata, la, Yeye alikuwa wa kipekee, tazamaalivyosema Paulo katika k.5 „katika mfano wa mauti yake‟.

Paulo alikuwa akiwaza ubatizo wa aina gani?. Wengine wanafikiri alitumiaubatizo kuwa ishara ya mwungano wa muumini na Kristo. Katika ubatizo„tunatiwa ndani ya Kristo‟. Si kwamba ubatizo wenyewe unatuunganisha kwakuwa katika sura zilizotangulia ni wazi tunahesabiwa haki kwa imani peke yake.Ila Paulo ametaja ubatizo kuwa ishara ya nje ya ile imani ya ndani isiyoonekana,na imani ile inatiwa muhuri kwa njia ya ubatizo.

Ubatizo ni ishara nzuri sana kwa sababu kwenda ndani ya maji ni mfano wa KufaKwake Kristo, kwenda chini ya maji ni mfano wa Kuzikwa Kwake (thibitisho laKufa Kwake) na kutoka majini ni mfano wa Kufufuka Kwake. Zamani zile maranyingi watu walibatizwa hadharini kwenye mto au kijito cha maji. Lakini tusiwazekwamba maana ya ubatizo inategemea kiasi cha maji kinachotumiwa au njiainayotumiwa kama kunyunyiziwa au kuzamishwa majini. Kwa imani ya ndani nakwa ushuhuda wa nje wa ubatizo Mkristo ameunganishwa na Kristo na kuwekwa„katika Kristo Aliyekufa na Kuzikwa na Kufufuka‟. Ila liko wazo ya kwamba ubatizounaotajwa ni ule wa 1 Kor. 12:13: „Kwa maana katika Roho mmoja sisi sotetulibatizwa kuwa mwili mmoja....nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja‟. Kristo nikichwa na sisi tu viungo vya mwili wake (Efe.1:22,23).

k.6-11 „utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye‟ utu wa kale ni sisi jinsitulivyokuwa tulipokuwa „katika Adamu‟, chini ya ghadhabu ya Mungu, wenyeuhusiano mbaya na Mungu, maadui, wenye dhambi na wenye hatia, chini yautawala wa mauti na hukumu ya Mungu. Hali hii imekwisha, ilisulubishwa pamojana Kristo na sasa kwa kuunganika na Kristo na kuwa „katika Kristo‟ uhusianowetu na Mungu ni mwema, hatuwi chini ya ghadhabu ya Mungu bali tu katikaneema na kibali chake. Kristo hakuendelea kusulubiwa, wala hakuendelea kufa,mambo hayo yalitokea mara moja tu, vivyo hivyo, hali tuliyokuwa nayo katikaAdamu imekwisha, na tokeo lake ni „mwili wa dhambi ubatilike‟ maana yakeusihesabiwe kuwa na kazi tena, usiwe na nguvu tena kusudi tusiitumikie dhambitena. Katika k.12,13,19; 8:10,13 mwili ni chombo kinachotumiwa na dhambi iliipate nafasi ya kutenda mabaya. Si kwamba mwili wenyewe ni dhambi ila nivyepesi kwa dhambi kuvitumia viungo vyake, na kwa sababu hiyo mtu hushindwakuishi maisha ya kiroho. Mwili utafufuliwa na kutukuzwa baadaye (Flp.3:21).Hivyo Mkristo ahesabu kwamba dhambi haina haki yo yote ya kuwemo maishanimwake. Dhambi haina nguvu ya kumdai

Page 127: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 789

tena, maana Kristo amemlipia deni la madai yote ya dhambi, kwa hiyo,ametuweka uhuru mbali nayo.

Ila ni vema tuelewe vizuri maana ya kuwa „wafu kwa dhambi‟. Tusifikiri ni sawana „kuwa wafu kimwili‟. Wafu kimwili hawawezi kuitikia jambo lo lote, wakipigwawatakaa tu bila kufanya lo lote, wakiondolewa mahali fulani watabaki pale palewalipowekwa. Hata moto ukiwashwa hawatainuka na kuukimbia. Ni wafukwelikweli. Ila „wafu kwa dhambi‟ ni tofauti, bado waweza kusikia uvutiko wadhambi, bado waweza kujaribiwa kufanya dhambi. Hata inawezekana wafanyedhambi. Ni hatari sana kufundisha kwamba watu waweza kufikia hatua yakutokufanya dhambi. Neno la Mungu halifundishi hivyo. Ila Neno la Mungulafundisha kwamba dhambi haitatutawala, kwa nguvu ya Roho Mtakatifu tunaouwezo wa kuikataa na kuishinda. Katika Kristo maisha ya kale yalisulubishwa,twaishi kama hatuwi „katika Adamu‟ bali tu katika Kristo, na tulipohesabiwa hakitulianza maisha mapya. Tunapokuwa hapa duniani tumo katika dahari mbili,tungali katika dahari inayopita, dahari ya dhambi, mwili, na mauti; pia tumo katikadahari mpya iliyoletwa na Kristo, dahari ya neema, haki, roho, na uzima.Twawajibika kuishi kama watu wa dahari mpya.

k.10 Kifo cha Kristo kilihusu dhambi, alijitoa Mwenyewe kuwa dhabihu ya maramoja ili aiondoe dhambi, na Alifufuka ili asihusike tena na dhambi. Mkristoajihesabu vivyo hivyo, Kristo alipokufa Msalabani kwa ajili ya dhambi, yeye nayealikuwa pamoja naye akifa kwa dhambi, akisema „la‟ kwa dhambi, na KristoAlipofufuka yeye naye alifufuka pamoja naye ili aseme „ndiyo‟ kwa kumwishiaMungu na kufanya mapenzi yake (1 Pet.3:18; Ebr.7:27; 9:12,26-28; 10:10)Katika Efe.1:19 Paulo alitaja kwamba waumini wameshirikishwa nguvu ile ileiliyomfufua Kristo, ni uweza ulio „ndani yetu‟ na katika Efe.2:5-6 alisema„tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu, alituhuisha pamoja na Kristo‟ nakatika 2 Kor.5:17 „Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbekipya; ya kale yamepita; tazama yamekuwa mapya‟.

k.12-14 Katika vifungu hivi Paulo ametuonyesha wajibu wetu. Ametuita kuamkana kuvaa silaha na kupigana vita, kwa sababu kwa mara ya kwanza tunao uwezowa kuchagua kutokufanya dhambi. Njia ni kuacha kuvitumia viungo vyetu vyamwili kwa dhambi na kuvitoa kufanya mema. Uzuri ni kwamba ipo ahadi yaushindi wa dhambi, haitatutawala, kwa sababu tumepata matibabu ya kuishindana daktari wa uponyaji ni Kristo.

Katika sehemu hiyo yote twaona umuhimu wa akili na ufahamu kuhusu jinsitunavyowaza na kufikiri na kuhesabu. „hamfahamu ya kuwa...‟(k.3) „tukijua nenohili...‟(k.6) „tukijua ya kuwa...‟ (k.9) „jihesabuni kuwa...‟ (k.11).

(b) 6:15-23 Kuwa watumwa wa Mungu - Utumwa unaoleta uhuruPaulo alianza sehemu hiyo ya pili kama alivyoanza sehemu ya kwanza kwa

kuuliza maswali. „ni nini basi?‟ „tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya

Page 128: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI790

sheria bali chini ya neema?‟. Hoja ni ile ile isipokuwa hapo Paulo ameweka nenola sheria, kwa sababu baadhi ya watu waliwaza kwamba ikiwa hatuwi chini yasheria, na sheria ndiyo inayokataza dhambi, basi twaweza kufanya tupendavyona kufanya dhambi bila wasiwasi. Kama tu huru na „bwana sheria‟ basi tu hurukufanya tupendavyo.

Lakini Paulo alijibuje? Alijibu kama alivyojibu hapa nyuma, akitumia neno languvu „Hasha‟. Ni jambo lisilowazika hata kidogo. Kwa sababu kuwa chini yaneema si chini ya sheria haina maana kwamba tunaweza kuishi bila kujali.Neema ni kinyume cha dhambi. Tu huru kufanya yanayotupasa si tunayotaka. Niwajibu wetu kuishi kwa ajili ya Mungu si kwa ajili yetu wenyewe. Kamwewanadamu hawawezi kuwa „huru‟ bila „bwana‟ fulani, kwa sababu tu viumbe.Tangu tulipoumbwa tulipewa amri ya „kutii‟ ni sehemu ya ubinadamu wetu.Wanadamu hawana budi kuchagua kati ya mabwana wawili. Lazima kilamwanadamu achague ni yupi wa kumtumikia, na baada ya kuchagua hana budikumtii yule aliyemchagua. Aweza kuwa mtumwa wa dhambi, au mtumwa wahaki na Mungu. Paulo alitumia mfano wa utumwa kwa sababu zamani zilewalikuwapo watumwa wengi na kila mtu alifahamu mtumwa ni mtu asiye na hakiyo yote, usiku na mchana yu mali ya bwana wake. Ilikuwa rahisi kugundua yupini bwana wa mtumwa kwa kuona alimtii nani.

Ndivyo ilivyo kwa Mkristo, amewekwa huru mbali na dhambi na sheria ili awemali ya Mungu. Bwana Yesu amemkomboa na kwa sababu hiyo Yesu ni Bwanawa maisha yake. Mkristo si mtu asiye na „bwana‟ wala „wajibu‟. Utumwa wetu wadhambi ulianza tulipozaliwa, tulizaliwa wenye dhambi kama ambavyo tumeonakatika sura zilizotangulia. Utumwa wa haki ulianza tulipomwamini Kristo nakujitoa Kwake (k.17).„lakini mlitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake‟.Wakristo walipewa mwongozo jinsi ilivyowapasa kuishi. (1 Tim.1:10; 2 Tim.1:13;4:3; Tit.1:9, 2:1,8). Paulo alisema walikubali kwa moyo kuishi kwa kanuni zaKikristo, pia alisema „mliwekwa chini yake‟ lugha ya kuonyesha kwambawalitazamiwa kuyafuata katika maisha yao.

k.19 Paulo alifahamu kwamba mfano alioutumia ulikuwa na upungufu na yakuwa „utumwa wa Mungu‟ si sawa na utumwa wa siku zile, maana Mungu nitofauti na mabwana wa dunia hiyo, hata hivyo, mfano ulifaa kufundisha kwambaWakristo walipaswa kujitoa kabisa kwa Mungu na kumtumikia si kwa uzito balikwa moyo na kwa furaha. Hasa ni neema ya Mungu na upendo wake wa ajabuunaotudai tumtumikie kwa sababu Yeye ndiye, peke yake, aliyestahili kupatautiifu wetu wote, maana Yeye ndiye Bwana mzuri sana na „afya‟ ya maisha yetuimo mikononi mwake.

Matokeo ya kuwa watumwa wa dhambi ni mabaya; uchafu, na uasi mpaka uasi,yaani ni kutelezateleza katika ubaya. Matokeo ya utumwa wa haki na wa Munguni mazuri, ni haki mpaka utakaso. Kila aina ya utumwa ina mwenendo

Page 129: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 791

wake na unaendelea mpaka mwisho wake, ama wa mauti ama wa uzima.Watumwa wa dhambi wazidi kuwa wachafu na wabaya na watumwa wa hakiwazidi kuwa safi na wema. Twakumbushwa mfano wa Bwana Yesu juu ya njiambili (Mt.7:13). Pia twakumbushwa habari za mtu aliyetolewa pepo mchafu bilakumwingiza mwingine akae mahali pake, ndipo hali ya mwisho ilikuwa mbayakuliko ya kwanza (Mt.7:43ku). Hatuwezi kuwa „katikati‟ tunatolewa chini yanguvu ya dhambi ili tuonje nguvu ya Mungu. Twatoka utumishi wa „bwana‟dhambi ili tupate kumtumikia „Bwana‟ Yesu. Tulipompokea Kristo na haki yaketulikubali kuwa mali yake, na kuwa watiifu Kwake.k.21 Paulo aliuliza swali juu ya faida waliyopata walipokuwa watumwa wadhambi kabla ya kumpokea Kristo? Hakutoa jibu ila bila shaka lilikuwa „hamnafaida‟. Walisikia aibu nyingi walipowaza hali yao ya kwanza, waliona hawakuwana matunda, waliaibika, na mwisho wao ungalikuwa mauti. Ila sasa katika kuwawatumwa wa haki na wa Mungu wanayo faida kubwa ya kutakaswa, kuzidi kuwasafi na mwishowe ni uzima wa milele.Maisha tunayoishi ni thibitisho la ukweli wa imani yetu katika Kristo. Bwana Yesualisema „si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wambinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni‟(Mt.7:21ku).

k.22-23 Paulo alijumlisha sehemu hiyo kwa kusema mshahara wa dhambi nimauti, neno „mshahara‟ linaonyesha ni malipo ya haki. Dhambi ni kama „mwajiri‟inalipa watumishi wake mshahara, na mshahara huo ni mauti. Ila „karama yaMungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu‟. Paulo hakusema„mshahara wa haki‟ maana haki tuliyo nayo si yetu, tumeipewa kwa neema,kipawa cha bure, ni haki isiyopatikana nje ya Yesu Kristo. Mtu amestahili mautiya milele, lakini kamwe mtu hawezi kustahili uzima wa milele. Mshahara nakipawa ni mambo mawili tofauti sana.

Kwa hiyo, ujumbe wa sura nzima ni kwamba tumeunganika na Kristo katika Kufa,Kuzikwa, na Kufufuka Kwake na kwa sababu hiyo tumewekwa mbali na dhambina sheria ili tuwe watumwa (walio huru) wa haki na wa Mungu. Kama Kristoalivyojitoa kwa ajili yetu, sisi nasi twapaswa kujitoa Kwake.

MASWALI1. Baadhi ya watu walimaanisha vibaya fundisho la Kuhesabiwa

Haki kwa imani. Eleza walielewaje?2. Paulo aliwajibuje hao watu? Alifundisha nini?3. Eleza maana ya „tuliifia dhambi‟ ni kwa wakati gani?

na kwa njia gani? kama ilivyoelezwa katika sura hii.4. Maneno „kuwa wafu kwa dhambi‟ yana maana gani? Je! Mkristo

aweza kufikia hali ya kutokufanya dhambi? Eleza.5. Eleza uhusiano kati ya ubatizo na imani? Ipi inaleta mtu katika uhusiano

mwema na Mungu?

Page 130: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI792

6. Mtu awezaje kuwa „mtumwa wa Mungu‟ na kuwa huru? uhuru wake ni wanamna gani?

7. Paulo alisema „mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu niuzima wa milele‟. Kwa kutumia neno „mshahara‟ alitaka kufundisha nini? nakwa kutumia neno „karama‟ alitaka kufundisha nini? Kwa nini hakutumianeno mshahara kwa sehemu ya pili?

7:1-25 Kuunganika na Kristo - Uhuru na SheriaKatika sura hii Paulo ameonyesha uhusiano wa Mkristo na Sheria. Kwa nini nijambo muhimu kwa Mkristo kuwekwa uhuru na sheria? ni vigumu kuelewa nenohilo kwa sababu sheria inakataza dhambi na inaunga mkono haki. Kwa njia ganiMkristo amewekwa huru asiwe chini ya sheria? Torati ilikuwa muhimu sana kwaWayahudi na jambo la kupewa Torati liliorodheshwa katika baraka zao kubwa(Rum.9:4). Kwa hiyo, machoni pao ilikuwa kufuru kuweka imani badala ya sheria.

(a) 7:1-6 Mfano wa NdoaBaada ya mfano wa utumwa katika sura ya 6 Paulo alitumia mfano wa ndoa kwakufundisha uhusiano wa Mkristo na sheria. Ni kwa njia gani Mkristo amewekwahuru asiwe chini ya Sheria? Je! ina maana wasijali sheria tena? Mpaka leoWakristo watatizwa na swala la Amri 10 na mahali pake katika Imani yao.Shabaha ya Paulo ilikuwa kuonyesha jinsi isivyowezekana mtu kuhesabiwa hakikwa sheria, vile vile jinsi isivyowezekana mtu kutakaswa kwa sheria.

Alisema „torati humtawala mtu wakati anapokuwa hai‟ neno „humtawala‟linaonyesha sheria ni „bwana‟ inatoa maagizo kwa watu kuhusu la kufanya na lakutokufanya. Katika ndoa wawili wamepatana kisheria kuishi pamoja maadamuwote wawili wako hai. Ila kifo cha mmoja kitakapotokea, basi, uhusiano kati yaoumekwisha na patano lao limevunjika. Ndipo yule aliyeachwa amekuwa hurukuoa/kuolewa tena. Mwanamke akimwacha bwana wake kwenda kuishi namwingine ameitwa mzinzi, ila akifa bwana wake halafu aenda kuishi na mwinginehaitwi mzinzi. Kinacholeta tofauti asiitwe mzinzi ni kufa kwa mume wa kwanza.

k.4 Tusitafute maana ya kila neno la mfano, ila jambo kubwa ni kuhusu „kifo‟.Wakati wa kifo kutokea wajibu uliokuwapo kwa mume/mke wa kwanzaunakwisha. Muumini ni sawa na mjane aliyefiwa na „bwana‟ wake, yeye „ameifiatorati‟ ili aolewe na „bwana‟ mwingine, yaani Kristo. Lakini kifo kilichovunja uleuhusiano wa kwanza ulitokea lini, na wapi, na kwa nani? Kristo AlipokufaMsalabani alitimiza madai yote ya sheria (Efe.2:15). Alizaliwa chini ya sheria(Gal.4:4) alijiweka chini ya sheria kusudi atimize madai yote ya sheria kwa ajiliyetu. Kwa moyo wote alimtii Mungu kwa ukamilifu, aliheshimu sheria kwa sababuilitoka kwa Mungu. Kisha alibeba adhabu ya sheria juu ya dhambi

Page 131: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 793

mwilini mwake Msalabani, ili asidaiwe tena na sheria, wala sisi nasi tusidaiwetena. Tunahesabiwa tulikuwa pamoja naye alipotii sheria kwa ukamilifu piatulikuwa pamoja naye alipobeba adhabu ya sheria juu ya dhambi zetu. Kwakuunganika na Kristo katika Kifo Chake wamwaminio wamehesabiwa kuwa watuwalioifia sheria, hivyo sheria haina haki ya kuwadai tena, hawawi chini yake tena.Hivyo walitolewa katika eneo la utawala wa sheria na kuwekwa huru.Walifufuliwa pamoja na Kristo na kuingia eneo la Roho wakimtumikia Mungu kwamsaada wa Roho Mtakatifu.

Ni vema tuone ni kwa kusudi gani mambo yamekuwa hivyo na kuona ni kwashabaha gani tumewekwa huru. k.4b: „kusudi tumzalie Mungu matunda‟ na 6b:„ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho‟. Mambo ni mapya: tunayomaisha mapya, Paulo ametumia lugha ya kuwa wafu na kuwa hai kuonyeshautofauti wake. Tunao uhusiano mpya, tumefunga ndoa na Kristo. Tunalo kusudijipya la kumzalia Mungu matunda; pia tunao uwezo mpya ndani yetu, Roho waMungu. Kamwe sheria haiwezi kumpata mtu mfu, madai yake yote yamekwisha,hawezi kupelekwa mahakamani, vivyo hivyo sheria haitudai tena, tuliifia Kristoalipokufa Msalabani (8:1). Tumetoka chini yake, tu chini ya neema. Sheriaingaliko, haikufa, ila haina kazi katika kuwa njia ya kutupatia haki (10:4).

Mfano wa ndoa unatukumbusha uhusiano wetu na Mungu ni wa upendo, Munguanayo mapenzi tele juu yetu, mapenzi yaliyoonyeshwa katika Kumtoa Kristo nakusudi la Kuja Kwake ni „uzima tele‟ (Yn.10:10) sheria ni „baridi‟ haina nafsi.

k.5 Katika kifungu hicho maneno kadha yamewekwa pamoja, mwili, tamaa zadhambi, torati, mauti. Kabla ya kuwa Wakristo watu huishi kwa kufuata mamboya mwili, na sheria huamsha tamaa za dhambi zilizomo ndani yao, na mwishowa kufanya dhambi ni mauti. Mara nyingi sheria huchochea dhambi, kwa mfano,mtu akiona tangazo, „usipite katika majani‟ mara asikia ndani yake kwambaanataka kupita kwenye majani, bila kuona tangazo huenda asingalitaka kupitiapale. Fanya jaribio ili uone kama ni kweli au sivyo. Mwambie mtoto asiguse kitufulani, na uone itikio lake. Dhambi imejificha ndani hali imetulia, lakini maraikitokea amri au katazo fulani, au jambo la kutubana, basi inainuka. Maranyingine hata mtu mpole afoka akipatikana na hasara au ugumu ambaohakutazamia.

k.6 Ila tunapowekwa uhuru kutoka kwenye sheria twasikia uhuru wa kumtumikiaMungu kwa furaha na kwa moyo, sawa na jinsi mtu anavyomfurahia rafiki nakuandamana naye ili ampendeze. Maisha hayo yamzalia Mungu matundayakaayo. Mwisho wa k.6 Paulo alitumia neno „andiko‟ (ling. na 2 Kor.3:6).Yawezekana aliwaza „mapokeo ya wazee‟ (Mko.7:3). Ikitokea utengano wa Nenola Mungu na Roho wa Mungu ni hatari. Kwa mfano, tukichukua maneno yaYesu juu ya kusamehe mara saba kwa

Page 132: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI794

sabini. Mtu akiwaza maneno yenyewe tu ataanza kuhesabu kutoka 1 mpaka 490na kufikiri huo ndio wajibu wake. Lakini mtu mwingine atachukua maneno nakutafuta maana yake hasa ni nini, naye ataona ya kuwa maana yake nikusamehe bila kuhesabu na bila kuweka mipaka kama ya mara 490 (2Kor.3:18ku).

(b) 7-13 Sheria na DhambiKatika sehemu hiyo Paulo anakaza sana kwamba ni dhambi si sheria iliyo shidakubwa. Sheria yenyewe haina dosari, haiwezi kulaumiwa kwa kushindwa kwetu.Sheria na dhambi ni mambo mawili tofauti. Kama alivyofanya katika sehemuzilizotangulia aliuliza maswali. k.7 „Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? na k.13„Basi Je! ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? akajibu maswali yote mawilikwa neno la nguvu „Hasha‟ sawa na hapo nyuma. Katika sura ya 6 alisema„tuliifia dhambi‟ neno lisilo gumu la kukubali kwa sababu wote wajua kwambadhambi ni mbaya. Ila katika 7:4 alisema „tumeifia sheria‟, na sheria tofauti nadhambi si mbaya. Ikiwa ni hivyo Je! dhambi na sheria ni sawa? Mara Pauloalikanusha wazo hilo maana iko tofauti kubwa kati ya sheria na dhambi, ila upouhusiano pia kwa sababu alisema „sheria hufunua dhambi‟, halafu „sheriahuamsha dhambi‟ kisha „sheria huhukumu dhambi‟.

k.7 „sheria hufunua dhambi‟. Sheria ilimwonyesha Paulo makosa yake kimawazona kimatendo. Picha ni ya dhambi hali imetulia ndani ya mtu, ndipo kwa kusikiasheria fulani dhambi huamka na kumchokoza na kumshawishi afanye lile ambalosheria imemkataza. Maana yake, bila sheria tusingejua kuwepo kwa dhambindani yetu, wala tusingejua uhai na nguvu yake. Mtu fulani amesema „hakunakitu kifananacho na nyoka aliyekufa ila nyoka aliye hai hali ametulia kabisa‟.Mfano mwingine ni wa mtu ambaye hajisikii vizuri kiafya. Lakini mpaka aendekwa daktari na kuambiwa anao ugonjwa fulani hajui ni nini inayomsumbua.Ku‟funuliwa‟ na daktari ugonjwa wake si sawa na ugonjwa wenyewe, wala sisababu yake, wala matibabu yake. Ni ufunuo tu wa hali aliyo nayo. Kama sheriainachokoza dhambi ni wazi kwamba sheria si dhambi.

Paulo alisema „nisingalitambua dhambi‟ maana yake asingalitambua hali halisiya dhambi. Ndipo alitaja amri „usitamani‟, amri inayohusu tamaa za ndani, sitendo la nje tu. Bila amri hiyo asingalitambua kwamba kutamani ni dhambi, yaaniile tamaa tu ni dhambi, mbali na tendo. Twakumbuka jinsi Bwana Yesualivyofunua maana ya ndani ya amri mbalimbali katika Hotuba ya Mlimani (Mt.5).Kusema „asingalitambua‟ alikiri asingalitambua nguvu ya dhambi. Hivyo sheriailimsaidia sana kutambua kuwepo kwa dhambi na nguvu yake.

k.8 na k.11 Paulo aliona dhambi ilipata nafasi ya kufanya kazi, kwa sababusheria ilikuwa kama kituo kwa dhambi kuanza mashambulio, mfano wa askarikuweka kituo chake mahali fulani ili apate nafasi ya kumshambulia adui. Lakinisi vema tuilaumu sheria, afadhali tuisifu maana imefunua adui mkubwa ambayeametulia ndani akiingojea nafasi. Ubaya wa dhambi umekuwa ubaya mkubwa

Page 133: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 795

kwa sababu inatumia kitu chema, yaani sheria, ili ipate nafasi ya kufanya kaziyake, pengine hata kufaulu.

k.9 Ni vigumu kujua kama Paulo amesimulia habari zake au amejiunga nawanadamu wote katika Anguko la Adamu na Hawa katika Bustani ya Adeni.Waliishi bila kufanya dhambi na bila amri wakishirikiana vema na Mungu. Ilanyoka alipata nafasi kwa njia ya agizo walilopewa na Mungu, akawadanganya,nao wakamwasi Mungu na dhambi iliingia. Sheria ilikuwa na shabaha ya waokuendelea katika uhusiano mwema na Mungu, iwe sababu ya uzima wao, haliwakichagua kwa hiari kumpenda na kumtii Mungu, ila nyoka aliamsha tamaa yakuwa „kama Mungu‟ wakaanguka. Tukumbuke ya kuwa walipewa nafasi tele yakufanya mengi ila walikatazwa kitu kimoja tu, ambacho kiliwekwa kuwa kipimocha utii wao. Kama ni habari zake mwenyewe huenda maana yake ni kwambamwanzoni alikuwa „hai‟ hakusikia shida katika uhusiano wake na Mungu, ilamara alipotambua Torati imefunua dhambi zake basi papo hapo alikuwa„amekufa‟ akajua yu chini ya hukumu ya Mungu.

k.10 Paulo anarudia kusisitiza alivyosema hapo nyuma. Sheria iliyokusudiwakuleta „uzima‟ ilimletea „mauti‟ (10:5; Law.18:5). „amri iletayo uzima‟ ni manenoyanayofundisha kwamba sheria inaonyesha njia ya kuishi. Tazama jinsi BwanaYesu alivyomfundisha Bwana Sheria (Lk.10:25-28) „fanya hivi nawe utaishi‟sharti ni „fanya hivi‟ (Gal.3:21). Sheria ni maelezo mazuri ya mambo ya kufanyaili tuupate uzima. Shida imekuwa hatuna uwezo wa kuyatenda.

k.11-12 Paulo alitaja „kudanganywa‟ sawa na jinsi Hawa alivyokiri mbele zaMungu alipoulizwa juu ya kuchukua matunda ya mti wa mema na mabaya(Mwa.3:13). Paulo amesisitiza kwamba shida si sheria bali ni dhambi. Sheria nitakatifu, na ya haki, ni njema na k.10 „ni amri iletayo uzima‟. Imetoka kwa Mungu.

k.13 Kwa njia ya sheria dhambi imedhihirishwa kuwa „mbaya mno‟ kwa sababudhambi imetumia kitu chema, yaani, sheria, kwa lengo baya la kumwangushamwanadamu. Ni rahisi kuilaumu sheria kwa mfano, mfungwa ametiwa gerezanikwa kosa la wizi, mle ndani anawaza, kumbe, mimi nimo humo kwa sababu yasheria ya nchi isemayo „mtu akiiba sharti apewe adhabu ya miaka miwili ndani‟kumbe haoni ya kuwa shida si ile sheria, ila shida ni yeye na kosa lake la wizi.

Kwa kujumlisha sehemu hiyo twaona Paulo amefundisha mambo matatumakubwa kuhusu sheria - sheria hufunua dhambi, sheria huchokoza dhambi,sheria huhukumu dhambi. Sheria ni takatifu kwa sababu imetoka kwa Mungu nani ufunuo wa mapenzi yake.

Page 134: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI796

(c) 7:14-25 Mashindano ya ndaniPaulo bado angali akiendelea na hoja yake kuhusu sheria. Ameonyeshaugumu wa sheria ambayo haina huruma wala haihojiwi, maagizo yake yakaa,hakuna kuridhiana nayo wala kuyalegeza. Tumeona kwamba Kristo ametuwekauhuru mbali na sheria, hatuwi tena chini yake, hatudaiwi na sheria, kwa sababuKristo kwa Kufa Kwake amelipa deni letu lote kwa upande wake. Ndipotumefikiria udhaifu wa sheria, wala si udhaifu wa sheria tu, hata na udhaifuwetu pia. Tumeshindwa kuitimiza na yenyewe haina uwezo wa kutusaidiatutimize maagizo yake. Paulo hakutaka watu wawaze kwamba anaihukumu nakuishtaki sheria kuwa sababu kuu ya kushindwa kwetu.

Alionyesha kwamba Mkristo kwa moyo wake anaifurahia sheria. Kwa njia yakeameelimishwa juu ya haki ya Mungu. Anatafuta kuitimiza kwa uwezo wa RohoMtakatifu.

Kuanzia k.14 twaona Paulo ameandika kama ni hali ya wakati wa sasa, tofautina sehemu iliyotangulia. Kwa hiyo, vita anayoitaja ni vita ya Mkristo wakati huosi vita aliyokuwa nayo kabla ya kuwa Mkristo.

k.14-17 vina mawazo sawa na k.18-20 juu ya hali ya sasa ya Wakristo - ling.k.14 na k.18; ndipo alitaja mashindano ya wakati huo k.15 ling. na k.18-19;halafu alitaja tatizo kubwa ambalo ni dhambi - k.16-17 ling. na k.20.

Paulo alionyesha kwamba Mungu ni asili ya sheria. Ni „ya rohoni‟ (k.14) „naikiriile sheria ya kuwa ni njema‟ (k.16) „lile jema nilipendalo‟ (k.19) „naifurahia sheriaya Mungu kwa utu wa ndani‟ (k.22).Ndipo alitaja hali ya mtu aliye Mkristo: „bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwachini ya dhambi‟ (k.14b) „lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndiloninalolitenda‟ (k.16). „ndani ya mwili wangu, halikai neno jema‟ (k.18).

Shabaha ya Paulo ilikuwa kuwahakikishia wasomaji wake kwamba ndani yao„hamna neno jema‟ ni „wenye dhambi‟ na alifanya hivi kwa kusudi lakuwatayarisha kwa msaada wa ajabu wa Roho Mtakatifu ambaye atawaelezeahabari zake katika sura ya nane.

Paulo ameandika kwamba licha ya kupambana nayo ameshindwa katika hayomapambano. Bila shaka alitaka kuwaonya kwamba hata Mkristo akiachwapeke yake hawezi kushika sheria, aweza kuitambua kuwa ni njema, na awezakuifurahia, na aweza kutamani kuifanya, hali ambayo hakuwa nayo kabla yakuwa Mkristo. Kwa hiyo, bila msaada wa Roho Mtakatifu hawezi kuishikasheria. Dhambi ingalimo ndani yake. Bila kukiri hali hiyo hatutamlilia Munguatuokoe. Wakristo wamo „katika Adamu‟ pia wamo „katika Kristo‟. Kwa hiyo,Wakristo wanaishi chini ya dahari mbili kwa wakati huo wa sasa, kwa hiyo,uvutano upo. Tu watu wa mwili na damu, tu watoto wa Adamu, ila kirohotumehamishwa kutoka mauti mpaka uzima, kutoka giza mpaka nuru, kwa kufa

Page 135: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 797

pamoja na Kristo na kufufuka pamoja naye tumefufuliwa kwa maisha mapya,tumefanywa kuwa raia wa Ufalme wa Mungu, tu washiriki wa „uumbajimpya/jamii mpya‟ katika Kristo. Siku ya mwisho dahari hii ya sasa itakwisha nadahari mpya (iliyoanza Kristo alipokuja mara ya kwanza) itaingizwa kwaukamilifu (Kristo atakapokuja tena) ndipo uvutano kati ya dahari hizo mbilizitakwisha (Gal.5:17).

k.21-25 Katika sehemu hiyo Paulo ameeleza mashindano yake na ya kilaMkristo kwa kutaja sheria mbili zinazovutana ndani yake. Katika k.21 amesemakwamba anapotaka kufanya mema lipo baya. k.22 amesema „naifurahia sheriaya Mungu kwa „utu wa ndani‟ na k.23 alitaja „sheria ya akili zangu‟ halafuakataja „sheria nyingine katika viungo vyangu‟ sheria inayopiga vita na sheria yaMungu, ni „sheria ya dhambi‟ na kukiri ya kuwa sheria ya dhambi imemfanya„mateka‟. Ni kutambua jambo la kutisha kwamba ndani yetu ipo hali ya „anguko‟hata tunapokuwa waumini. Tena ni waumini wanaoitambua kwa sababu ni haowanaokwenda kinyume cha ulimwengu na kusikia zaidi nguvu ya uvutiko wake.Wale wanaokubaliana na ulimwengu na tabia zake hawasikii nguvu hiyo jinsiwaumini waisikiavyo. Tumehesabiwa haki ila bado tungali wenye dhambi.Hatuwezi kupata haki kwa sheria wala kwa sheria hatuwezi kutakaswa.

k.24-25 Katika vifungu hivi twakuta „vilio viwili vilivyo tofauti‟. Kilio cha kwanza„ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?‟ na kilio cha pili „namshukuruMungu kwa Yesu Kristo Bwana wetu‟ - kilio cha kukata tamaa na kilio chaushindi. Vilio hivi viwili ni vya Mkristo maadamu anaishi hapa duniani.Tunapopambana na dhambi na udhaifu wetu twalia tukitaka kuokolewa na halihiyo ya unyonge wetu. Vile vile twajua hakika kwamba mwenye nguvu yakutushindia ni Kristo kwa njia ya Roho akaaye ndani yetu. Ndipo katika siku yamwisho atatufufua na kutupa mwili mpya usio wa dhambi wala unyonge wowote.

k.25 Katika kifungu hicho Paulo amejumlisha vizuri pande zote mbili za maishaya Mkristo „kwa akili zangu, na kwa moyo wangu naitumikia sheria ya Mungu ilakwa mwili wangu naitumikia sheria ya dhambi‟. Dhambi ni „nguvu‟ ndani ya mtuinayomshinikiza kufanya lile asilotaka kulifanya. Dhambi ni kama nahodha wamwili. Maana yake ni kwamba hatuwi wabaya tupu wala wema tupu, hakunahata mmoja anayefanya mema yote anayokusudia kuyafanya. Hivyo Mkristo nimtu anayekiri kuwa mwenye dhambi pamoja na kuipiga marufuku maishanimwake. Kwa hiyo, shida kubwa ya wanadamu si hali na mazingira ya nje, si haliza ujamii, wala matatizo makubwa ya ulimwengu, ila shida hasa ni ndani yamoyo wake, ni dhambi.

Huenda ni vigumu kufikiri kwamba hayo aliyosema Paulo yahusu Mkristo. Ilahasa ni Mkristo anayetambua sheria ni njema na takatifu, na hasa ni Mkristoanayetambua ubaya wa dhambi zake. Kwa kawaida mtu asiyeaminihasumbuliwi na hali yake kwamba ni mwenye dhambi, mara nyingi hushindania

Page 136: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI798

haki yake, hasikii shida anapojilinganisha na wengine wengi, anafikiri yeye nisawa au bora. Sivyo alivyo Mkristo wa kweli, anapiga kifua chake na kusema„ole wangu mimi‟.

Japokuwa wataalamu wengi hukubaliana sehemu hii yote haihusu mtu asiyeMkristo si wote wanaokubali kwamba inahusu mtu anayemjua Kristo na RohoMtakatifu. Wengine hufikiri aliyezungumzwa ni mtu aliyetambua dhambi nakushtakiwa na sheria ya Mungu ila bado hajampokea Kristo maishani mwake.

Mpaka hapo Paulo amesema machache juu ya Roho Mtakatifu ila katika sura yanane amefundisha mengi juu yake na juu ya huduma yake katika maisha yaMkristo.

MASWALI1. Eleza maana ya kuwa „chini ya sheria‟2. Katika mfano wa ndoa Paulo alitaka kufundisha nini juu ya maneno

„mmeifia torati‟?3. Taja mambo matatu yanayohusu sheria na dhambi?4. Ubaya wa dhambi umeonekanaje?5. Kuhusu „mashindano ya ndani‟ Paulo alikuwa akiongelea mtu wa aina gani?

asiye Mkristo? Mkristo ambaye hajakata shauri sawasawa? au Mkristo?Toa maoni yako.

8:1-39 Kuunganika na Kristo - Uhuru na mautiKatika sura hii Paulo ameandika kwa kirefu juu ya Roho Mtakatifu na kazi yakekatika maisha ya Mkristo. Katika sura zilizotangulia ameeleza juu ya kuunganikana Kristo katika Kufa na Kuzikwa na Kufufuka Kwake. Kwa njia ya kuunganikana Kristo muumini aliifia dhambi na sheria na kuwekwa uhuru nazo.

Sura ya nane inahusika na sura zilizotangulia. Paulo alianza na maneno ‘Sasa, basi,hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu’. Ni tangazo lakuhesabiwa haki kwa imani, na kuonyesha kwamba waliohesabiwa haki wameunganikana Kristo katika Kufa na Kufufuka Kwake, wamo ‘katika Kristo’. Ila alikuwa badohajasema yote yaliyotakiwa kusemwa, hasa kumhusu Roho Mtakatifu kuwa ndani yetu,msaada wetu katika mashindano na mwili na dhambi, iwapo ushindi katika vita hiyoumekwisha kupatikana na Kristo.

Kwa sababu sura hii ni ndefu hayo ni mambo makuu ambayo itabidi tutazamevipengele vifuatavyo.

Jambo la kwanza lahusu kazi ya Roho kuhusu mwili, maisha yetu jinsi yalivyokutokana na kuzaliwa „katika Adamu‟.

Page 137: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 799

Jambo la pili lahusu kazi ya Roho na „uana wetu‟ katika kufanywa kuwa watotowa Mungu.

Jambo la tatu lahusu kazi ya Roho na urithi wetu wa baadaye, ambalo jambomojawapo ni mwili wetu kukombolewa siku ya mwisho.

8:1-4 Roho ni ‘sheria mpya’Maneno ya kwanza japokuwa ni maneno rahisi yana uzito mkubwa - „basi,sasa‟. Nini? „hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu‟ yaanikwa wale waliounganika na Kristo kwa njia ya kuamini Yeye na Kufa naKufufuka Kwake. Hamna hukumu ya adhabu sasa, wala haitakuwepo kamwe.Hali halisi ni „hakuna hukumu...‟ Hata dhambi ikitokea haitakuwa juu ya sheriabali juu ya upendo. Kwa mfano, mtu akiikosea sheria ya nchi hukumu ipo, balimtu akimkosea ndugu fulani katika familia yake haliwi kosa la kuletwamahakamani kama ile ya nchi. Walio katika Kristo wametolewa wasiwe chini yasheria kwa hiyo, hawatahesabiwa kuwa na hatia. Hii ni baraka kubwa yawokovu. Ina maana kwamba kwa upande wa waumini siku ya hukumuimeishapita, ila kwa wasioamini siku hiyo ingali mbele yao.

Jambo la pili ni kwamba kwa Roho Mtakatifu muumini amewekwa uhuruasitawaliwe na nguvu ya dhambi na mauti. Hii ni baraka kubwa ya pili ya wokovu.Haina maana kwamba dhambi itatoweka katika maisha yake, la, hata kidogo, ilahaitamtawala, anaye Bwana mwingine mzuri sana wa kumwongoza. Kwa hiyo,mambo hayo mawili yaenda kwa pamoja. Kuokolewa na hatia na adhabu yadhambi, na kuokolewa na nguvu na utawala wa dhambi.

k.2 Roho ametajwa mara ishirini katika sura hii. „sheria ya Roho wa uzima...‟neno sheria ina maana ya uwezo na utendaji na ushawishi wa Roho. „imeniachahuru‟ ni jambo ambalo limekwisha kutendeka, Roho ameunga mkono kazi yaukombozi wa Bwana Yesu na Yeye Roho huleta baraka zake ndani ya maishayetu ili tuwe na ujuzi wa kibinafsi wa kazi ya Kristo. Ni sawa na tulivyoona haponyuma kuhusu kuunganika na Kristo. Katika Kufa na Kufufuka Kwake, tuliifiadhambi na sheria, maana tulihesabiwa kuwa pamoja na Kristo alipokufaMsalabani.

Hizo baraka zimetokeaje? Jibu ni katika k.3. Ni Mungu aliyefanya mambo hayo.Amefanya yale yasiyowezekana kwa sheria. Iwapo sheria ilidhihirisha dhambi nasheria ni kinyume cha dhambi, haikufaulu kushinda dhambi. Kwa nini sheriahaikufaulu? ilishindwa kutokana na udhaifu wetu wa mwili. Mwili ni dhaifukutokana na shinikizo la uwezo wa dhambi, nao unashindwa. Mungu alimtumaMwana Wake Mwenyewe na kwa ukombozi alioufanya tumehesabiwa haki,ndipo kwa kumtuma Roho Wake tunatakaswa.

k.3 Paulo ameandika kwa uangalifu sana kuhusu Yesu Kristo na jinsialivyohusika na sisi na jinsi alivyohusika na dhambi. Alitaka kuonyesha

Page 138: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI800

uhusiano wake wa ukaribu sana na wanadamu walio wenye dhambi, bila YeyeMwenyewe kuishiriki dhambi. Kwa hiyo, aliandika „katika mfano wa mwili ulio wadhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili‟. Yesuhakuwa na mwili wa dhambi kwa sababu alikuwa bila dhambi. Hata hivyo mwiliwake ulikuwa mwili kweli, alikuwa mwanadamu kweli. Hata Adamu kabla yakuanguka alikuwa mwanadamu kweli, akiwa na mwili kweli, mwili usio na dhambi.Iliwezekana afanye dhambi maana alijaribiwa kweli, ila hakuwa „chini ya dhambi‟tofauti na sisi ambao tangu Anguko la Adamu ndiyo hali yetu.

Paulo alionyesha kwamba Kristo alikuja hapa duniani „kwa sababu ya dhambi‟maana yake alikuja ili apambane na dhambi, halafu awe „dhabihu ya dhambi‟ nakatika Yeye Mungu aliihukumu dhambi katika mwili. Dhambi zetu ziliadhibiwakatika mwili usio wa dhambi wa Kristo alipozibeba pale Msalabani (2 Kor.5:21)hivyo dhambi ilipigwa marufuku katika maisha ya wanadamu isiwe na haki yoyote ya kuwemo. Kristo hakuja ili awe Kiongozi wa Maadili bali awe Mwokozi waulimwengu.

k.4 Ingefikiriwa tungesoma „ili atuhesabie haki‟ lakini shabaha ya hayo yote ni„maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo yamwili, bali mambo ya roho‟. Kumbe haki iliyokuwa lengo la Torati sasalimewekwa kuwa lengo liwezekanalo katika maisha yetu. Katika Yer.31:31ku. naEze.37:26ku. tumeambiwa juu ya Agano Jipya litakaloandikwa mioyoni mwetu ilituzitimize sheria zake. Pia tumeambiwa habari za Roho kuhuisha mifupa mikavuna kuondoa moyo wa jiwe na kuweka moyo wa nyama ili tufanye maagizo yaMungu. Katika kuhesabiwa haki twahesabiwa kuwa tumetimiza sheria, hatahivyo bado twaitwa kufanya haki si kuhesabiwa tu.

Kwa hiyo, utakatifu ndio makusudi ya Kuja kwa Kristo na Kufa Kwake. Dhambiimehukumiwa ili utakatifu hutokea. Utakatifu ni nini, ni kutimiza maagizo (siandiko la nje bali maana yake ya ndani) ya torati, ni kufanya haki. Hapotwakumbushwa „Hotuba ya Mlimani‟ Bwana Yesu aliyofundisha wafuasi wake(Mt.5-7). Hivyo twafuata maagizo ya sheria si kwa shabaha ya kupata kibali chaMungu, maana tumehesabiwa haki kwa neema kwa kuamini tu; bali kwa sababundiyo mapenzi ya Mungu katika kutupokea. Twapewa Roho Mtakatifu ili tuzaematunda mema (Gal.5:22) huu ndio wajibu wa mtu aliyehesabiwa haki. Mti wamatunda hauzai matunda kwa sheria bali kwa uzima uliomo ndani yake, vile vileMkristo hazai matunda ya haki kwa sheria, bali kwa uzima wa Roho Mtakatifualiye ndani yake.

8:5-13 Roho anautiisha mwiliPaulo alipozungumzia Roho na mwili hakusemea hali mbili za ndani ya mtu,bali juu ya mamlaka au nguvu mbili zinazotafuta kutuongoza, ama Roho, amamwili. Kuenenda kwetu kunategemea sana kuwaza na kunia kwetu. (Mit.23:7„maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo‟). Kwa hiyo, nia yetu inatawalamatendo yetu. Ndipo Paulo alipambanua kati ya wale „waufuatao mwili‟

Page 139: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 801

(wasioamini) na wale „waifuatao roho‟ (waumini). Wa kwanza huwekamatumaini yao katika mambo ya dunia hii na kuyashughulikia. Wale „waifuataoroho‟ humwekea Mungu tumaini lao na kuyashughulikia mambo yanayomhusuMungu.

k.6 „Nia ya mwili ni mauti‟ wenye nia ya mwili ni wale wanaoshughulikia mamboya mwili. Nia ya roho ni uzima na amani, wenye nia hiyo ni walewanaoshughulikia mambo ya Roho. Kwa hiyo, jambo muhimu lahusu ni mamboyapi yanayovuta usikivu wetu na kuongoza mawazo na matendo yetu.Tunatumia wakati wetu, fedha zetu, na nguvu zetu katika mambo gani? Tunamalengo gani, na matakwa gani? Kwa kifupi, nia yetu imeelekezwa wapi. Je!tunaishi maisha yasiyomjali Mungu wala kumwekea nafasi; maisha yakujipendekeza, au tunaishi kwa kumjali Mungu na kumpa nafasi hali tukitafutakumpendeza?

Matokeo ya kunia mambo ya mwili ni mauti kwa sababu ni njia inayotupeleka kwadhambi, na dhambi hututenga na Mungu na kutengwa kwa Mungu ni „mauti‟ kwakuwa tumetengwa na „uzima‟. Kunia mambo ya roho ni uzima na amani ni njiaya kutakaswa na kwa njia hiyo tunauendeleza ushirikiano wetu na Mungu ambaondio huo uzima. Tena ni njia ya amani, amani na Mungu na amani ya Mungundani yetu.

k.7-8 Paulo aliongeza kusema juu ya wale waufuatao mwili kwamba „nia ya mwilini uadui kwa Mungu, hautii sheria ya Mungu wala hauwezi kuitii sheria yaMungu‟. Watu wa nia hiyo hawawezi kumpendeza Mungu. Kiini cha dhambi nikuwa kinyume na Mungu na amri zake, iwapo inawezekana watu wanafanyamatendo mazuri wafanya kwa sababu zao tu, si kwa kumpendeza Mungu.Tukiwa tungali „katika Adamu‟ basi tungali adui wa Mungu, na tunaendelea kuwahivyo mpaka tutakapomkubali Kristo aliyeuondoa ule uadui kwa Kifo Chake.

k.9-11 Hapa Paulo amesema juu ya Roho wa Mungu, ambaye pia ni Roho waKristo na mkazo wake ni juu ya Roho kukaa ndani ya waumini. Hii ndiyo tofautikubwa kati ya waumini na wasioamini. Ni baraka kubwa ya watu wa Mungu kuwana Roho ndani yao, na ni sawa na kuwa na Kristo ndani yao. Yu ndani yao iliawasaidie katika mashindano yao na dhambi na kuwapatia ushindi. Roho ndiyeanayetia ndani yetu yale matokeo ya kazi ya Kristo. Kristo alikufa kwa ajili yetu,na Roho anakaa ndani yetu. Ni Roho anayetuvuta kumpenda Mungu nakuichukia dhambi. Paulo alisema wazi kwamba asiye na Roho huyo si Mkristo,kwa hiyo, twampokea Roho wakati tunapomwamini Kristo. Kumpokea Roho sihatua ya pili baada ya kumpokea Kristo. Roho ameitwa Roho wa Kristo.

k.10-11 „mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi, bali roho yenu i hai kwasababu ya haki‟ Maneno hayo yana maana gani? Mwili wetu huelekea dhambi

Page 140: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI802

na mauti, kwa sababu bado tungali katika Adamu na katika Adamu sotetunakufa. Ila kwa sababu ya kuamini na kuhesabiwa haki roho zetu zimehuishwana Roho. Ndipo, iwapo miili yetu itakufa, katika siku ya mwisho Roho ataifufuandipo mwili na roho vitakuwa hai milele (2 Kor.5:5). Uhakika wa kufufuka kwetuni katika Kristo Kufufuka (1 Kor.6:14; 2 Kor.4:14; 1 The.4:14). Kwa hiyo, kwasasa, Roho anahuisha roho zetu halafu siku ya mwisho atahuisha miili yetu.k.12-13 Kwa sababu waumini wanaye Roho Mtakatifu ndani yao hawana deni,maana yake, hawadaiwi kuishi tena kwa kufuata mambo ya mwili. Iwapo Paulohakuendelea kusema wanalo deni la kuishi kwa kufuata mambo ya Roho ni wazikwamba ndiyo maana yake. Neno „deni‟ laleta wazo la „wajibu/jukumu‟. KwaRoho wamehuishwa, kwa Roho miili yao itahuishwa baadaye, na kwa Rohowamejaliwa nguvu na baraka walizo nazo. Hivyo wamewajibika kuishi maishamatakatifu, wasifanye lo lote lililo kinyume cha wito na wajibu wao. Ila Pauloalionyesha kwamba watayafisha matendo ya mwili kwa Roho, kwa sababu kwanguvu zao wenyewe hawataweza, ila Roho aliye ndani yao atawawezesha.Uhuru wa Kikristo ni uhuru wa kukata shauri la kutenda kama Roho atakavyo.Tazama neno „mkiyafisha‟ ni tendo la wakati huo, kwa sababu vita yetu nadhambi haijaisha bado. Ahadi ya Roho si ahadi kwa washindi ila ni ahadi yaMungu kuwa pamoja nasi maadamu tunapoishi katika mwili huo wa dhambi.Kama Roho Mtakatifu ametuhuisha haitegemewi kwamba tutafuata mambo yamwili ambayo ni njia ya mauti. Ni juu yetu kuyafisha matendo ya mwili, walatusiruhusu „mwili‟ na madai yake kuinuka na kusitawi au tutakufa kiroho. Hoja yaPaulo ni kwamba „twapaswa‟ „tu wadeni‟ twadaiwa kufanya hivyo.

8:14-17 Roho huushuhudia ‘uana’ wetuPaulo ameendelea kusema juu ya kazi ya Roho akiingiza wazo la Wakristokuwa „wana wa Mungu‟. Alisema juu ya walioongozwa na Roho kuwa „wana waMungu‟. Neno „wana‟ huleta mawazo ya „ukaribu‟ na „uzuri‟ wa uhusiano naushirikiano kati ya muumini na Mungu wake. Kwa neno hilo watu wa Munguhumkaribia bila wasiwasi na bila hofu, mfano wa mtoto na babake. Katikamaana hiyo si watu wote walio „watoto wa Mungu‟ Paulo alibagua kwa kusema„wale wanaoongozwa na Roho ni wana wa Mungu‟.

Tumefanywa kuwa „wana‟ na Roho Mtakatifu, hali ya „utumwa‟ na „kuhofu‟imeondoka. (Gal.4:5; Efe.1:5). Dalili ya kuwa „wana‟ imeonekana katika kumwitaMungu „Baba‟ na kumkaribia katika maombi kwa kumwita „Baba‟ sawa na BwanaYesu alivyofanya (Mko. 14:36; Gal.4:6). Yesu aliwafundisha wafuasi wakekuomba kwa kusema „Baba yetu uliye mbinguni...‟(Lk.11:2).

k.16 Wapo mashahidi wawili wa „uana‟ wetu (i) Roho anashuhudia (ii) rohozetu zinashuhudia. Ni Roho anayetupa ujasiri wa kumwita Mungu „Baba‟ natunapofanya hivyo roho zetu zinaunga mkono ushuhuda wa Roho, na kwa njiahiyo twathibitika katika imani yetu na kujua hakika kwamba tumefanywa kuwa

Page 141: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 803

„wana‟. Ni wazi kwamba kabla ya Roho kufanya kazi mioyoni mwetu hatukuwa„wana‟ wa Mungu. Kabla ya hapo tulikuwa „wana wa uasi‟ sawa na wanadamuwote walio „katika Adamu‟. Twapata „uana wetu‟ kwa kuunganika na Kristo nakuwa „katika Kristo‟ kwa neema na kwa kuamini.

k.17 Zaidi ya kuwa watoto tumekuwa warithi wa Mungu na warithi pamoja naKristo. Kwa sababu tu wana wa Mungu tutaushiriki utukufu wa Kristo aliyeMwana halisi. Sisi tume‟fanywa‟ (adopted) kuwa wana, kwa neema tumeingizwakatika familia ya Mungu kwa njia ya Yesu Kristo na kwa kazi ya Roho. Ila jambomoja limo katika fungu hilo, ni mateso. Tunapomfuata Kristo twamfuata Yulealiyeteswa, haikosi sisi nasi tutateswa tukimfuata kwa kweli. Kwa hiyo,, kwa sasatwaushiriki uana wake na mateso yake. Baadaye tutaushiriki utukufu wake.

8:18-25 Roho huudhamini urithi wetuWakristo ni kama wasafiri wanaorudi nyumbani kwa Baba ila njiani watakutanana vizuizi na shida. Watiwa moyo kwa kujua kwamba siku moja watafika kwaBaba na kupokelewa naye kwa shangwe kuu. Ndiyo sababu katika sehemu hiyoPaulo alipambanisha kati ya mateso na dhiki za wakati huu na utukufu wabaadaye uliotajwa katika k.17. Mateso ya sasa ni tofauti sana na utukufu wabaadaye kiasi cha Paulo kutumia maneno „si kitu‟ kwa mateso ya sasaalipoyalinganisha na utukufu wa baadaye, ambao utazidi kwa uzuri mawazo yetuyote. Aliendelea kuonyesha jinsi uumbaji mzima na uumbaji mpya, ambao niKanisa, unashiriki mateso ya sasa na utukufu wa baadaye. Wakati huu wa sasaviumbe vyote vinaugua, vile vile watu wa Mungu wanaugua. Ndipo baadayeviumbe vyote pamoja na watu wa Mungu watatukuzwa.

Adamu alipoanguka uumbaji wote uliingizwa katika anguko lake na kuwekwachini ya laana (Mwa.3:17-19). Adamu alichagua kumwasi Mungu, na uumbajiuliingizwa, haukuwa na uchaguzi. Mpaka leo wanadamu pamoja na uumbajiwanaendelea kushiriki „laana‟ na kuishi kwa taabu na shida. Ila mbeleni, watu waMungu watakapoingia katika urithi wao uumbaji pia utashirikiana pamoja naokatika utukufu na baraka.

k.19-22 Uumbaji unauguaKatika kila kifungu Paulo ametaja „viumbe vyote‟k.19: „viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi.....k.20: „viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili.k.21: „viumbe vyenyewe..na kutolewa katika utumwa wa uharibifuk.22: „viumbe vyote vinaugua pamoja, vina utungu .......

Picha ni ya ubatili, uharibifu, na maumivu vya uumbaji mzima ulioshikwa katikamzunguko wa kuzaliwa, kukua, kufa, na kuoza. Kwa sasa uumbaji hauonekanikuwa na maana yo yote kwa sababu mwisho wa kila kitu ni mauti. Ipo hali yabure, ya unyonge, na ya kutokutimiza lengo.

Page 142: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI804

Ila hali hiyo ni ya muda tu. Katika k.20 twasoma „viumbe vilitiishwa chini ya ubatilina Mungu katika tumaini‟. Kwa hiyo, mbeleni hali itabadilika. Katika k.21twasoma „viumbe vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu nakushiriki uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu‟. Kwa hiyo, utumwa, yaanikushikwa katika mzunguko wa bure utageuzwa kuwa uhuru, na uharibifuutageuzwa kuwa kutokuharibika. Sisi tutaushiriki utukufu wa Kristo (k.17)uumbaji nao utaushiriki utukufu wetu.

k.22 Maumivu ya uumbaji yameitwa „kuugua‟ na „utungu‟ maneno yahusuyouzazi, ina maana kwamba maumivu ya sasa hayawi bure, si ubatili, ni hatua tukatika mpango wa kurekebisha hasara zote zilizoletwa na Anguko la Adamu nahukumu ya Mungu juu ya uasi wake, kwa kuwa „dahari mpya‟ inazaliwa (Mt.24:18).

k.23-25 Wakristo wanaugua - Kanisa ni uumbaji mpya wa Mungu. Mwisho wak.22 twasoma „vina utungu pamoja hata sasa‟ na k.23 „Wala si hivyo tu; ila nasisi wenyewe .... tunaugua ..‟ Tunaugua kwa njia gani? Twaugua kwa sababuiwapo kwa wakati huu tumeokolewa, ni kwa sehemu tu. Mwili wetu ni dhaifu,unachoka, unapatwa na maradhi na maumivu, na mwishowe unakufa. Pia katikamwili wetu utu wa dhambi umekaa k.7,17,20,24. Kwa hiyo, ziko sababu mbili zakuugua kwetu, udhaifu wa mwili, na utu wa dhambi. Ndiyo sababu twasikiakulemewa, tunaugua, tukitamani sana kuondolewa hali hizo na kupata „ukomboziwa mwili wetu‟. Katika siku ya mwisho tutapewa mwili mpya, mwili wa ufufuo, uliona nguvu mpya, ambao dhambi haimo ndani yake.

Pia jambo jingine ni „kufanywa wana‟. Iwapo kwa upande mmoja tumekwishakufanywa wana, kwa upande mwingine bado hatujawa „wana‟ kamili. Iwapo„uana‟ wetu wa sasa ni mzuri utakamilika na kuwa mzuri zaidi baadaye. Badohatujafanana kabisa na Mwana wa Mungu (k.29) wala hatujafunuliwa wazi kwaulimwengu (k.19) na ulimwengu bado haujajua ya kuwa sisi ni wana wa Mungu(1 Yoh.3:1-2). Siku ya mwisho ndiyo siku ya sisi kufunuliwa kwa ulimwengu, piani siku ya sisi kuingia „uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu‟ na ni siku yaviumbe vyote kuwekwa uhuru na kutimiza lengo la kuumbwa kwake (k.21).Katika siku hiyo laana itaondolewa (Ufunuo 22).

Katika sehemu hiyo tumeona uhusiano mkubwa kati ya wanadamu na uumbaji.Wanadamu ni sehemu na upeo wa uumbaji. Wanadamu walipewa uangalizi namadaraka juu yake chini ya Mungu. Adamu alipoanguka, aliingiza uumbaji katikaanguko lake na Mungu aliilaani ardhi n.k. kwa sababu ya kosa lake. Hivyowanadamu pamoja na uumbaji hawatimizi lengo la kuumbwa kwake. Lakinibadiliko litatokea. Wakati ujao, wana wa Mungu watakapopata ukombozi wa miiliyao, ndipo na uumbaji utawekwa uhuru na kushirikishwa baraka pamoja nao (2Pet.3:13; Ufu.21).

Page 143: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 805

Uhakika wa mambo hayo ni katika kuwa na „malimbuko ya Roho‟. Ni faida kubwakuwa na Roho Mtakatifu, Yeye ndiye dhamana ya urithi wetu wa baadaye. Tenani „malimbuko‟ yake kwa sababu hata katika wakati huu twaonja nguvu za daharimpya maishani mwetu, tukishinda dhambi na kuishi kwa neema si kwa sheria.

k.24 Tuliokolewa kwa taraja, yaani tuliokolewa kwa sehemu hali tukiutazamiawokovu kamili siku ya mwisho, tutakapopewa mwili mpya na kuwekwa huru nadhambi ndani yetu na dhambi nje yetu katika mazingira yetu. Wakati huo dhambiitaondolewa kabisa. Ndipo tutafanana na Yesu Mwenyewe na haitakuwepohitilafu yo yote kati ya imani na nia yetu na matendo yetu.

8:26-27 Roho husaidia udhaifu wetu katika kuombaRoho anaugua: Kila Mkristo anao msaada mkubwa kwa upande wa kuomba kwasababu Roho anausaidia udhaifu wetu. Ni furaha na wajibu wa kila Mkristokumwomba Mungu Baba. Twamkaribia Mungu kwa njia ya Kristo na kwa njia yaRoho Mtakatifu (Efe.2:18). Pamoja na sisi kuomba Kristo aliye mbingunianatuombea (8:34 Ebr 7:25; 1 Yoh.2:1) pia Roho aliye ndani yetu anatuombea(Yn.14:16,17).

Kuhusu maombi, sisi tu dhaifu, hasa kwa sababu hatujui tuombe nini, maanahatutambui haja zetu za kweli kuwa nini, wala hatujui mapenzi ya Mungu ni nini,kwa hiyo, ni vigumu kuomba jinsi itupasavyo. Twahitaji mwongozo namasahihisho ya Roho. Twashindwa kuweka katika maneno hisia zetu za ndani,shauku tuliyo nayo, na hamu zetu za kuishi kama watoto wa Mungu (1Kor.2:9-16). Kuomba ni kazi ya Roho Mtakatifu na Baba anafahamu mioyo yetuna kujua yale ambayo tumeshindwa kuyatamka, pia anafahamu nia ya Roho nadaima Roho huomba yale yapatanayo na mapenzi ya Baba. Kwa hiyo, kuuguakwetu na kuugua kwa Roho ndani yetu kunaeleweka kwa Mungu. Mungu huwatayari kufanya zaidi ya kuwaza kwetu na kuomba kwetu (Efe.3:20). Tunapoombatukishindwa kutamka maneno si kitu, kwa sababu kulemewa kwetu na uzito wetuni ishara ya ukweli wa maombi yetu na Roho yu tayari kutusaidia.

8:28-30 Mambo matano makubwa yasiyokataliwaKatika sehemu hii Paulo ametazama mpango mzima wa Mungu ulioanza katikaumilele wa nyuma hadi umilele ujao. Shabaha yake ilikuwa kuwathibitishiawaumini kwamba wokovu wao umekazwa na umekuwa salama katika mwambausioweza kutikiswa wa mapenzi ya Mungu. Wokovu wao umetiwa mizizi ndaniya upendo mkuu wa Mungu. Hivyo wokovu wao tangu mwanzo mpaka mwishosi jambo la bahati nasibu, bali hatua zote zimekazwa na kutekelezwa na MunguMwenyewe. Chanzo ni upendo wake wa kutufanyia kwa neema bila kuangaliaustahili wetu au tendo lo lote jema la upande wetu.

Page 144: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI806

k.28 Paulo alianza kifungu hicho na neno „twajua‟ kwa kuwa hayo aliyosemayalitokana n ujuzi wa kibinafsi katika kuishi maisha ya imani katika Kristo. Nikifungu ambacho kimependwa na Wakristo wa vizazi vyote, kinatuhakikishia jinsiMungu au Roho Mtakatifu (aliyetajwa katika vifungu vilivyotangulia) awezavyokuchukua kila jambo linalompata Mkristo, haidhuru ni jambo zuri au baya, nakufanya mema yatokee mwishowe. Ni mfano wa mwanamke anayefuma swetaakitumia rangi mbalimbali, hata rangi ya weusi na kijivu. Sweti ikitazamwa kwaupande wa ndani haionekani kuwa nzuri, ila ikigeuzwa kwa upande wa nje,kumbe picha nzuri inaonekana na imepatikana kwa kila rangi kuingizwa nakufumwa pamoja. Ndivyo afanyavyo Mungu na mambo yote yanayowapata walewampendao. Anachukua shida, mateso, ugonjwa, pamoja na mambo mazuri nikufanya wokovu utokee. Hao ni kawa „wale wampendao‟ (upande wakibinadamu) na kwa „walioitwa kwa kusudi lake‟ (upande wa Mungu) kusudi watuwasifikiri kwamba wamestahili hayo kwa kuwa wamempenda, ila chanzo nikatika Mungu kutangulia kuwaita, na upendo wao ni itikio kwa kuitwa kwao.

Paulo aliendelea kwa kuyataja mathitibisho matano makubwayanayotuhakikishia wokovu wetu. Mambo hayo ni kama viungo vya mkufu, kilakiungo kinapokezana mwenzake.

Viungo viwili vya kwanza ni mambo yaliyotokea katika umilele uliotangulia.„Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili…‟ Paulo alianziakatika umilele wa nyuma na katika mawazo na nia ya Mungu alipoamua„kuwajua‟ ndipo „kuwachagua‟. Inaonekana ina maana kwamba Mungu alifanyahayo hata kabla ya kufahamu habari zao (Amo.3:2; Efe.1:4,5,11). Mungu alikatashauri kabla hawajazaliwa, hata kabla ya Kristo kuja duniani (1 Pet.1:2,20;Mdo.2:23) hata kabla ya Mungu kuumba ulimwengu (Efe.1:4). Kwa hiyo, wokovuwao umejengwa juu ya upendo na neema yake. Yeye aliweka upendo wake juuyao na kuwachagua. Ni fumbo kubwa lisilo na hoja, na pengine ni vigumukulipokea, ila vema tukumbuke kwamba Neno la Mungu lafundisha kwamba kilamtu anao wajibu kuhusu itikio lake kwa Mungu.

Ni kwa shabaha gani Mungu aliwajua na kuwachagua? Hapo ni vema kuangaliasana shabaha iliyotajwa; „wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awemzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi‟. Jamii ya kwanza yawanadamu (wale walio katika Adamu) hawakutimiza lengo la kuumbwa kwao,wakamwasi Mungu, wala hawakutaka kufanya mapenzi yake. Hivyo Mungualikusudia kuumba jamii mpya ya wanadamu, ili apate watu watakaofanyamapenzi yake na kuudhihirisha utukufu wake. Shabaha ni waishi maishamatakatifu ili wazidi kufanana na Kristo. Kwa hiyo, „uchaguzi wa Mungu‟unahusika na watu kuunganika na Kristo (Efe.1:4) na kuwa „katika Kristo‟. Jambohilo lilizungumzwa katika sura ya sita.

Page 145: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 807

Viungo viwili vinavyofuata ni mambo yanayotokea wakati huu wa sasa maadamuwatu wanaishi. „Mungu akawaita, na wale aliowaita, hao akawahesabia haki‟.Tumeona Mungu aliwajua na kuwachagua, halafu akawaita. Kwa njia ya Injilikuhubiriwa Mungu huwaita watu kumpokea Kristo na wokovu wake. Haowanaouitikia wito wake Mungu anawahesabia haki, anawapokea na kujihusishavema nao.

Mpaka hapa mkufu unavyo viungo vinne „Mungu kuwajua, Mungu kuwachagua,Mungu kuwaita, na Mungu kuwahesabia haki. Kimebaki kiungo kingine, nacho ni„na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza‟. Thibitisho hilo la tano ni labaadaye, mwishowe kabisa katika umilele ujao, ndipo na hao watu watatukuzwa.Twaona kwamba Paulo aliandika kama jambo hilo limekwisha kutokea. Kwanini? kwa sababu ya uhakika wake. Anajua kwa hakika kwamba hao watuwatafika katika uzima wa milele, na kuitimiza shabaha ya kuchaguliwa na kuitwakwao. Uhakika ni kwa sababu kila hatua imepangwa katika umilele uliopita. Niutendaji wa Mungu; ni Mungu aliowajua; ni Mungu aliowachagua; ni Mungualiowaita; ni Mungu aliowahesabia haki; kwa hiyo, mwisho wa mwenendo huo niMungu akawatukuza. Yote ni matendo makuu ya Mungu.

Japopo inaonekana jambo la mwisho ni watu kutukuzwa ila tukichunguza kwandani, zaidi ya yote, ni Kristo kutukuzwa, tukirudi kwenye k.29 „wafananishwe namfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa nduguwengi‟. Ili Kristo awe wa Kwanza kabisa, awe Juu kabisa ya wale wotewamwaminio. (Kol.1:15,18; Efe.1:6; Ufu.1:5; Ebr.2:11,12).

Twaona hayo aliyoandika Paulo yalihusu upande wa Mungu. Hakusema lo lotejuu ya upande wa wanadamu kama hiari ya mapenzi, kuishi maisha matakatifu,wala juu ya uinjilisti ambao utasababisha watu kuusikia wito wa Mungu nakuamini. Hasa shabaha yake ilikuwa kuwatia moyo waumini ili wajue hakikakwamba, potelea mbali wakutane na vipingamizi gani na mashambulio aina aina,hata hivyo, wokovu wao una uhakika, umekazwa katika mapenzi ya Mungu,mwishowe watatukuzwa.

8:31-39 Upendo wa Mungu na ushindi wa ImaniPaulo alifuata mambo makubwa matano na maswali matano. Alianza kwakuuliza „Basi, tuseme nini juu ya hayo?‟ maana yake, katika nuru ya yoteyaliyotangulia na zaidi katika nuru ya yale mathibitisho matano, twasema nini?Maswali yalijengwa juu ya kweli iliyo imara. Yalikuwa changamoto kwa kiumbecho chote cha mbinguni na cha duniani kujibu au kukana ukweli uliomo ndaniyake.

Swali la kwanza ni katika k.31: „Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juuyetu?‟ „akiwapo‟ ni neno la uhakika si la shaka. Maana yake Je! kuna nguvu auenzi yo yote ya aina yo yote yenye uwezo wa kutuzuia tusifike kwenye

Page 146: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI808

„kutukuzwa kwetu‟? Kama Paulo angeuliza „ni nani aliye juu yetu?‟ bila shakaangalipata majibu mengi. Alijua hakika kwamba wako adui wengi wanaowapingawaumini, wako wasioamini, iko dhambi ya ndani inayoinuka na kujaribukutuangusha, ziko hofu mbalimbali, yupo Shetani. Hayo yote huwa na nguvu yakutushinda. Ila „Mungu akiwapo upande wetu‟ yule aliyetujua, na kutuchagua,na kutuita, na kutuhesabia haki, na kututukuza, kama Huyo yu upande wetu,hakuna awezaye kumshinda Huyo wala sisi kwa sababu Mungu amejitoa kabisakuwa upande wetu. Ametufanyia mambo makuu haikosi ataendeleakutushughulikia na kutushindia.

Swali la pili ni katika k.32: „Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, balialimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamojanaye?‟. Ni swali la maana sana kwa sababu hali yetu yote humtegemea Munguna pendo lake. Je! iko hatari yo yote ya pendo lake kwetu kupungua aukubadilika? Mwana alikuwa kifuani mwa Baba na alipofanyika mwili aliendeleakuwa Mwana wake mpendwa, hata hivyo, Baba hakumwachilia bali alimtoa kwaajili yetu. Tena alimtoa awe dhabihu ya dhambi, „alifanywa kuwa dhambi‟ (2Kor.5:21) na laana (Gal.3:13). Mungu alimtoa ili apatwe na yote ambayo Shetanina mamlaka za giza na wanadamu wabaya wamfanyie, naye akawashinda(Kol.2:15) „lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza‟ (Lk.22:53). Iwapoilionekana Yuda Iskariote alimtoa kwa fedha, na Pilato kwa woga, na Wayahudikwa husuda, lakini hasa ni Baba aliyemtoa kwa upendo. Kwa sababu Munguamekwisha kumtoa Mwana wake, kipawa chake kikuu, cha ajabu, kwa ajili yawenye dhambi, haiwezekani kwamba atatunyima cho chote tunachohitaji katikakumfuata Kristo kwa uaminifu. Msalaba wa Kristo ni thibitisho la ukarimu waMungu.

Swali la 3 na 4 ni katika k.33 na k.34: „Ni nani atakayewashtaki wateule waMungu?‟ „Ni nani atakayewahukumia adhabu?‟. Ni kama tumefikishwamahakamani. Je! yupo ye yote awezaye kuwashtaki juu ya dhambi na kufaulukesi yake hata mtu ahukumiwe adhabu? Jibu ni la! hakuna shtaki liwezalokusimama wala hakuna hukumu ya adhabu itakayotolewa (8:1). Kwa nini? kwasababu Yesu ni mtetezi wetu na Mungu Hakimu amekwisha kuwahesabia hakiwateule wake, yaani wale aliowajua na kuwachagua na kuwaita... Mara nyinginemioyo yetu inatushtaki (1 Yoh.3:19-21) ndipo wako watu wanaotuhukumu, nawako adui wanaotushtaki. Lakini hayo yote si kitu, kwa sababu Kristo amekufakwa ajili ya dhambi zile zile ambazo wengine wanatushtaki. Pia Kristo alifufukakutoka wafu, dalili ya kwamba Kifo Chake kimefaa na kutosha kwa ondoleo ladhambi zetu, tena sasa Yeye yuko mkono wa kuume wa Mungu, mahali pautukufu na utawala na enzi. Wala si hivyo tu, hajaacha kujitoa kwa ajili yetu, kwakuwa anaendelea kutuombea (Ebr.7:24). Yeye anao mzigo mkubwa juu yausalama wetu, ishara ya upendo wake unaoendelea.

Page 147: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 809

Swali la 5 ni katika k.35: „Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo?‟ Kwaujasiri mkubwa Paulo aliuliza swali kuhusu uwezekano wa kutengwa na upendowa Kristo. Je! itakuwaje ikiwa tutashindwa kuwa wauminifu kwa Mungu, hasatunapokutana na majaribu makali, mateso, dhiki, n.k. Paulo alijua hakikakwamba hamna kitu cho chote kiwezacho kumzuia Kristo na upendo wakekwetu. Ndipo akaangaza macho yake ili aone kama ipo shida fulani au kitu fulanivitakavyoweza kututenga na upendo wa Kristo. Aliwaza mishurutisho ya njekutoka katika ulimwengu ulio kinyume cha Mungu, kama dhiki na adha na shida.Paulo alikuwa ameonja sana vitu vya namna hiyo (2 Kor.11:22-33). Ndipoaliwaza mambo kama njaa na uchi vinavyoweza kuwafikirisha watu wafikirikwamba Mungu hana mzigo juu yao, au pengine hatari fulani kama vita au uuajiau ujambazi n.k. Mara nyingi Paulo aliwaonya waumini kwamba watapatwa nadhiki, ni kama fungu lao ili wasitazamie kuishi bila shida (1 The.3:3; Mdo.14:22).

Kweli ni vigumu sana kuyavumilia mambo kama hayo, hata hivyo, Paulo alionaya kuwa hayawezi kuwatenga na upendo wa Kristo. Licha ya kuwatenga, baliyatawapatia ushindi mkubwa. Kristo alituhakikishia upendo wake kwetu kwamateso aliyoyapata, Alipata ushindi kwa njia ya „kushindwa‟ pale Msalabani, kwakuwa ilionekana ameshindwa. Yeye aweza kuzigeuza shida zetu zitupatieushindi, yaani sisi twaweza kuushiriki ushindi wake „kwa Yeye aliyetupenda‟.

k.38-39 Paulo alimalizia sehemu hiyo kwa wimbo wa sifa kuu ya ushindi mkuu.Alikuwa na uhakika kabisa kwamba hamna kitu cho chote katika maisha yetumazima kiwezacho kututenga na upendo wa Mungu uliodhihirishwa katika KristoYesu Bwana wetu.

Alitaja mauti na uzima, mambo mawili yaliyo mbele yetu, na aliona kwambahamna kitu kwa upande wa mauti, kama hofu au kutokujua tutakufa kwa njia ganin.k. au kwa upande wa kuishi, kama mabadiliko yanayotokea mara kwa mara,yawezayo kuwatenga na upendo wa Mungu. Halafu alitaja malaika na wenyemamlaka. Haieleweki alikuwa akiwaza nini alipotaja hayo. Huenda enzi nanguvu katika ulimwengu wa roho, Shetani, n.k. (Efe.6:12) ni vigumu kufikiri nimalaika wema. Hata hivyo aliona hata mambo hayo hayawezi kuwatenga naupendo wa Mungu. Ndipo alitaja yaliyopo, na yatakayokuwapo, potelea mbaliitokee nini kwa sasa au baadaye, aliona ya kuwa hamna jambo lo lotelitakalowatenga na upendo wa Mungu. Halafu alitaja wenye uwezo, hapo tena siwazi alikuwa akiwaza akina nani, pengine ni wenye mamlaka katika ulimwenguwa roho walio kinyume cha Mungu (Kol.2:15). Kisha alitaja yaliyo juu, na yaliyochini, yaani katika upana wa ulimwengu mzima, kutoka pande za juu mpakachini, hamna cho chote kiwezacho kuwatenga na upendo wa Mungu. Zamanizile, hata mpaka leo watu wafikiri maisha yao yatawaliwa na mwezi na nyotawakitegemea „watabiri‟. Kisha alijumlisha kwa kusema „wala kiumbe kingine chochote hakitaweza kuwatenga na upendo wa Mungu‟.

Page 148: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI810

Katika uhakika huo twaweza kuishi maisha yetu tukijua kwamba hatutakutana nashida au dhiki au mashaka au jambo lo lote lenye uwezo wa kututenga naupendo wa Mungu. Haiwezekani utokee ufa kati yetu na Mungu, kwa sababuMungu amekwisha kututhibitishia upendo wake alipotoa Mwana wake, Mpenziwake wa pekee. Hakusema anatupenda tu, bali alifanya tendo la kutuhakikishiaupendo wake. Vile vile Mwana alituthibitishia upendo wake alipotoa maisha yakekwa ajili yetu.Kwa kweli tunazo hofu na mashaka mbalimbali, kufuatana namalezi yetu na imani zetu za jadi, au kwa hali za maisha ya sasa. Kwa hiyo,wimbo huo wa ushindi ni msaada kwetu kwa kutufahamisha kwamba hamnajambo lo lote wala kitu cho chote kiwezacho kututenga na upendo wa Mungu,Mungu amejiweka upande wetu na kutuahidi kwa uaminifu upendo Wake wadaima

MASWALI1. Eleza ni kwa sababu gani „hakuna hukumu ya adhabu kwa wale walio

katika Kristo Yesu‟.2. Kwa nguvu ya Roho Mtakatifu Mkristo anaokolewa na ......... ya dhambi?3. Je! Yesu alikuwa ni mwili kweli na mwanadamu kweli?

Je! Yesu alikuwa na dhambi? Je! alijaribiwa kufanya dhambi?4. Yesu alifanana na Adamu kabla ya ........................5. Je! dhambi ina haki yo yote ya kuwemo maishani mwetu? Eleza.6. Lengo la maisha mapya katika Kristo ni ....................7. Roho anatusaidiaje katika maisha ya kila siku?8. Tunapataje kuwa „wana wa Mungu‟?9. Tunajuaje tu „wana wa Mungu‟?10. Kwa sababu tu „wana‟ tumekuwa nini zaidi?11. Uumbaji unaugua‟ Kwa nini unaugua?12. Kuugua Kwake kunaonekanaje? na hali hiyo itaendelea mpaka lini?13. „Wakristo wanaugua‟ Tunaugua kwa njia gani?14. Baadaye itatokea nini kuhusu miili yetu?15. Roho anahusikaje na kuomba kwetu? yaani anatoa msaada gani?16. Mungu ameahidi nini kwa wale wapendwao walioitwa kwa kusudi lake?17. Taja mambo matano makubwa yasiyokataliwa.18. Kwa mambo hayo twajifunza nini kuhusu wokovu wetu?19. Mungu anayo shabaha gani katika „kuwajua‟ na „kuwachagua‟ watu?

„..................................‟20. Taja maswali matano ya maana sana Paulo aliyouliza alipothibitisha

upendo mkuu wa Mungu na ushindi wa imani?

9-11 TATIZO LA KUTOKUAMINI KWA WAYAHUDIKatika sura hizi Paulo amezungumzia tatizo kuu la kutokuamini kwa Wayahudi.Kwa nini lilikuwa tatizo? Ni kwa sababu waliteuliwa na Mungu na kupewaupendeleo mkubwa mengi kwa shabaha ya kumpokea Masihi ambaye

Page 149: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 811

atazaliwa miongoni mwao. Huyo Masihi, Kristo, alipofika kwao hawakumpokeaisipokuwa baadhi yao tu, taifa kwa jumla lilimkataa.

Wokovu aliouleta Kristo haukuwa kwa njia waliyotazamia. Injili ni Habari Njemaya kuhesabiwa haki kwa imani, kwa hiyo, ye yote amwaminiye Kristo aokolewa,hivyo WaMataifa walifunguliwa mlango na wengi wao walimpokea Kristo. Lakininjia hii ya imani ilifunga njia kwa haki kupatikana kwa Torati, hivyo Wayahudiwengi waliomkataa Kristo hawakupata wokovu, iwapo waliteuliwa kufanyamaandalio yake. Imekuwaje?

Maswali yalizuka: Je! historia yao na kuteuliwa kwao vilikuwa na maana gani?Tena, Itakuwaje mbeleni? Wametupwa kabisa? Lilikuwa jambo la kweli kwambaMungu alijihusisha nao kipekee katika miaka ya nyuma, hata taifa lao lilitokanana wito wa Abrahamu, baba wa taifa. Sasa Je! Mungu anakusudia nini?

Paulo alisikitika sana sana alipoona watu wake wenyewe wamewekwa kandohuku WaMataifa wamechukua nafasi yao. Iliwezekanaje wawe wamechaguliwandipo wakakataliwa? Neno hilo lilimhuzunisha Paulo sana kwa sababu alijuahakika walipewa upendeleo mwingi na Mungu. Tena yeye mwenyewe alijitahidimno kuwahubiria Injili, maana alisema wazi Injili ni kwa Wayahudi kwanza (1:16)kwa nini wameshindwa kumkubali Kristo?

Katika sura hizo Paulo amethibitisha mambo matatu hasa:a) 9:1-19 Mungu ana mamlaka yote, yu huru kufanya Atakavyo kulingana na

tabia zake za upendo, haki, rehema:b) 9:30-10:21 Wayahudi walikuwa na wajibu kuhusu itikio lao:c) 11:1-36 Makusudi ya Mungu ni kurehemu, Wayahudi wengi wataokolewa

baadaye:

Ni rahisi kufikiri sura hizo tatu ni kama kipengele. Paulo alipomaliza sura ya nanealikuwa amejaa furaha kubwa na tunapotazama mwanzo wa sura ya 12 ni waziangaliweza kuendelea moja kwa moja baada ya sura ya 8. Alianza sura ya 9 kwauzito na kwa huzuni. Ila tunapotazama mambo ya sura 9-11 iwapo sauti yakeimebadilika, hoja yake ni ile ile ya kuwapo kwa Israeli wa kweli, wale wa imani,na ya kuwa si wote waliozaliwa Wayahudi ambao ni Wayahudi. Watoto wa kweliwa Abrahamu ni wale wanaohesabiwa haki kwa imani (4:11- 13) na katikamaana hii Paulo alisema kwamba „Neno la Mungu halikutanguka‟ (9:6).

9:1-5 Huzuni ya Paulo juu ya kutokuamini kwa WaisraeliSura hizo zakubaliana na hoja ya sura 1-8 ya kuwa wote wamefanya dhambina wote wahitaji rehema na neema za Mungu.

Page 150: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI812

Tunapofika sura ya tisa tunamwona Paulo hali sauti yake ikiwa imebadilika,amejaa huzuni na hali ya uzito. Kwa nini? Kwa sababu alipotupa macho yakekwa Wayahudi wenzake aliona kwamba isipokuwa kwa wachache taifa zimawalimpa kisogo Masihi wao wa kweli iwapo walichaguliwa ili wafanye maandalioyote yaliyotakiwa kwa Kuja Kwake na kwa Kumpokea. Paulo hakuacha kuwaMyahudi alipomkubali Kristo. Alikuwa amejaa upendo kwa ajili yao, kiasi chakuwa tayari kulaaniwa na kutengwa na Kristo kama ingaliwezekana ili waowampokee. Hata kuongoka kwa WaMataifa wengi kutokana na juhudi zakehakumfariji alipowaza juu ya Wayahudi wenzake. Yawezekana adui zake katikaWayahudi walimshtaki kuwa mnafiki na msaliti. Pengine ndiyo sababu alijiteteakwa nguvu, akiwaita „ndugu zake na jamaa zake kwa jinsi ya mwili‟. Kusema „kwajinsi ya mwili‟ kunaonyesha ukweli wa kuokolewa kwake na kutokuokolewakwao, kwa sababu katika imani ya Kikristo alikuwa amepata ndugu wengi wasioWayahudi.

Inaonekana pale Rumi mabadiliko yalikuwa yametokea katika shiriki za Kikristo.Mwanzoni wengi zaidi walikuwa Wayahudi lakini baadaye WaMataifa walizidikuokolewa na idadi yao ilizidi idadi ya Wayahudi. Huenda hao Wakristo waKiMataifa walifikiri kuwa Wakristo wa Kiyahudi ni watu wa kuhurumiwa sana,kama watu wachache waliookolewa mikononi mwa wenzao waasi. HuendaWakristo wa Kiyahudi hawakupenda taifa lao lilaumiwe.

k.1-3 Paulo alidai kwa nguvu kwamba hayo aliyosema juu ya huzuni na upendowake kwa Wayahudi wenzake yalikuwa kweli. Alitumia maneno „katika Kristo‟„katika Roho Mtakatifu‟ kama mkazo, na dhamiri yake kuwa shahidi. Kiasi chaupendo wake kimedhihirika katika utayari wake kuharimishwa na Kristo kamaingaliwezekana ili watu wake wamkubali Kristo. Ni kama hakuweza kuvumiliawazo la wao kupotea. Yote aliyosema hayakusemwa kwa chuki au uadui balikwa upendo na kwa majonzi.

k.4-5 Halafu aliendelea kwa kutaja mapendeleo waliyojaliwa katika heshima yakufanya maandalio ya Kuja kwa Kristo. Kila pendeleo au baraka ilidhihirishaukweli wa Mungu kuwateua.

Kwanza kabisa alitaja jina lao „Waisraeli‟ jinsi walivyoitwa kuwa „Israeli‟(Mwa.32:28; 48:16; Isa.48:1). Waliitwa kubeba jina hili takatifu lililofungamanana ahadi za Mungu kwa Yakobo, wa kwanza kuitwa hivyo. „wenye kule kufanywawana‟ Kutoka miongoni mwa Mataifa yote Mungu aliliteua Taifa la Israeli kuwa„mwana wake‟. Inaonekana kwa maneno hayo Paulo aliwaza habari zilizotajwakatika Kutoka 4:22ku. wakati Mungu alipoliita Taifa zima kuwa „mwanangu‟(Hos.11:1). Katika Kumbukumbu 14:1 wameitwa „wana wa Bwana‟. Hata hivyowalikuwa „wana katika utoto wao‟ iliwapasa kusubiri kule kufanywa wana kwajinsi kulivyoelezwa katika WaGalatia (3:23-24; 4:1-3; Yer.31:9; Mt.8:11-12).

Page 151: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 813

„ule utukufu‟ ni ule ulioonekana mara kwa mara, ishara ya Kuwako kwa Mungukati ya watu wake. Pale Sinai; wakati wa kusafiri jangwani wingu liliwaongozausiku na mchana; pale penye Kiti cha Rehema; wakati wa Kuwekwa wakfuhekalu. (Kut. 15:6,11; 24:16-17; 40:34; 1 Waf.8:10ku. 2 Nya.7:2; Law.16:2). „namaagano‟ Mungu alifanya maagano na watu wake, Ibrahimu, Musa, Daudi, n.k.Agano lilifanyika pale Mlima wa Sinai (Kut.24:8). Mungu alifanya agano naAbramu (Mwa.15:8,18; 17:4), na Israeli wakati wa Musa (Kut.24:8; 34:10;Kum.29:1ku) na Yoshua (Kum.27:2ku. Yos.8:3Oku; 24:25) na Daudi (2Sam.23:5; Zab.89:28). Iwapo Mungu alifanya maagano na watu mbalimbali hasaagano lilikuwa moja lililorudiwarudiwa kuanzia kwa Hawa (Mwa.3:15) mpaka kwaZekaria mpaka kwa Mariamu (Lk.1:13ku.30). Ndipo Nabii Yeremia alitaja ahadiya Agano Jipya ambalo Kristo atalifanya (Yer.31:31; Mt.26:26-28).

„na kupewa torati‟ Kwa kuweka neno „kupewa‟ Paulo alitaka wafikiri juu ya jinsiTorati ilivyotolewa. Mungu aliwakaribia watu na kusema nao kwa sauti iliyosikika(Kum.4:32-36; Ebr.12:18-21). Ilipotolewa Mungu aliudhihirisha utukufu wakekatika matukio makubwa. (Kut.19:9; 20:1ku).

„na ibada ya Mungu‟ Mungu aliwapa mwongozo halisi juu ya taratibu za ibadazao, kuanzia kwa hema ya kukutania ndipo kwa hekalu. Ibada zilikuwa „vivuli‟ na„mifano‟ ya Kristo na ukombozi wake (Ebr.9 na 10) nazo ziliwafahamishaWaisraeli njia halisi ya kumkaribia Mungu (Ebr.8:1-5). WaMataifa wenginehawakujua njia halisi ya kumkaribia Mungu (Mdo.17:23,27).

„na ahadi zake‟ ni ahadi zote za Mungu hasa ile ya Kuja kwa Masihi na kupatahaki kwa imani (4:13-21; Isa.55:1-3).

„ambao mababu ni wao‟ ingawa Paulo hakusema hao ni akina nani, bila shakani Ibrahimu, Isaka, Yakobo, na wanawe 12. Huenda watu kama Musa, Yoshua,na Daudi walikuwa miongoni mwao. Hao walimjua Mungu kibinafsi, Mungualiwaongoza, na kwa njia yao Mungu alisema na watu wake. Mungu aliitwa„Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo‟.

„katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili‟ (1:3;12:8) Hapo Paulo amefikia upeowa upendeleo wao. Yote yaliyotangulia katika historia yao yalipata maana hasakatika Kuja kwa Kristo. Walijaliwa heshima ya hali ya juu sana katika Kristokuzaliwa Myahudi kwa upande wa ubinadamu wake.

Ajabu ni kwamba Paulo alifunga sehemu hiyo kwa sifa kuu kwa Kristo/Mungu,„aliye juu ya mambo yote‟. Haiko wazi sana iwapo alimwaza Mungu au Kristo,yaweza kuwa Kristo, maana alikuwa amesema „kwa jinsi ya mwili‟ na kuendeleakutaja Uungu na Umilele wake. Ila baadhi ya wataalamu wameona ya kuwa sidesturi ya Paulo kumwita Yesu „Mungu‟ moja kwa moja, ila mara nyingi alimwekasawa na Mungu. Kwa hiyo, ni vema tuache ilivyo, ama ni Kristo, ama ni Mungu,ila neno kuu ni kwamba aliona ya kuwa Kristo/Mungu

Page 152: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI814

amestahili kuhimidiwa kwa yote yaliyofanyika hapo nyuma katika historia yaWaisraeli.

9:6-13 Ahadi za Mungu hazikutangukaKwa sababu Taifa la Israeli hawakumpokea Kristo iwapo walipewa ahadi za KujaKwake na Kuteuliwa kwa shabaha ya Kumpokea, basi, Je! Mungu amekosakuwa mwaminifu kwa ahadi zake? Je! mipango yake imekwenda kando yaalivyokusudia? Jibu la Paulo ni La! hata kidogo! kwa sababu hata katika historiayao ya nyuma mfano wa jinsi hiyo ulikuwa umetokea.

Paulo aliendelea kwa kuonyesha kwamba ahadi (k.4) zimetimizwa katika „Israeliya kweli‟. Hata katika sura ya pili alitofautisha kati ya Wayahudi waliozaliwaWayahudi kwa kimwili na wale Wayahudi waliokuwa Wayahudi „wa kweli‟waliotimiza kwa moyo na kwa kiroho shabaha ya kuteuliwa kwao. (2:28ku).Kwanza alipambanua kati ya wana wawili wa Ibrahimu, Ishmaeli na Isaka.Ishmaeli alizaliwa kwa uwezo wa kimwili na Isaka alizaliwa kwa ahadi ya Mungu.Ibrahimu aliamini kwamba uwezo wa Mungu utashinda unyonge na uzee wayeye na Sarai mkewe. Kwa hiyo, Mungu aliweka msingi wa „uana‟ kuwa katika„ahadi‟ na „imani katika ahadi‟ si katika uwezo wa kimwili.

Iliwezekana wengine waseme kwamba mama za hao wana walikuwa tofauti,mmoja alikuwa Hajiri na mmoja alikuwa Sarai. Paulo alibomoa mawazo kamahayo akionyesha kwamba Mungu aliendelea kufanya uchaguzi alipomchaguaYakobo badala ya Esau ili „uzao uteule‟ uendelee. Maana hamna tofauti katikababa yao na mama yao. Walizaliwa mapacha kwa wakati mmoja. Kwa kawaida,wa kwanza kuzaliwa angalimtangulia wa pili katika mambo ya urithi ila Mungualiamua mkubwa atamtumikia mdogo tena neno hilo halikuwahusu waowenyewe binafsi tu bali hata na Mataifa mawili yaliyotoka kwao; Yakobo na Taifala Israeli, Esau na Taifa la Edomu (Mwa.21-1:12; 25:21,23; Mal.1:1-2; Ling. naGal.4:22-31). Tukitazama 2 Sam.8:14; 1 Fal.22:47; 2 Fal.14:7 twapata habari zaTaifa la Edomu kutumikishwa na Taifa la Israeli/Yuda. Pia twaona jinsi Edomulilivyopatwa na hukumu ya Mungu (Zab.137:7; Isa.34:5ku; Yer.49:7ku.Eze.25:12ku.35:1ku).

k.13 „Nimempenda Yakobo bali Esau nimemchukia‟. Maneno hayo ni magumusana. Kwanza ni vema kuona ya kuwa Wayahudi walizoea kuwa na aina yausemi wa namna hiyo wakiweka matokeo kama ni sababu. Neno kuchukialaweza kumaanishwa kwamba Mungu alimpendelea Yakobo zaidi ya Esaualipomtanguliza Yakobo na kujifunua kwake, hivyo twaweza kusoma „Yakobonimempenda kuliko Esau‟ Yesu aliwaambia wafuasi wake „wachukie wazazi n.k.‟akiwa na maana kwamba wapaswa kufanya mapenzi yake kabla ya mapenzi yaoikiwa yanagongana (Mwa.29:30-33; Mt.10:37; Lk.14:26; Yn.12:25).

Page 153: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 815

Kwa hiyo, katika sehemu hiyo tumeona ya kuwa Mungu hakuwa na shabaha yakuwaokoa Waisraeli wote, maana Mungu hawezi kudaiwa na wanadamu. Munguanayo makusudi yake, na makusudi hayo yamejengwa juu ya uhuru wake wakufanya uchaguzi, na kwa sababu hiyo makusudi yake hakika yatafanikiwa(k.11b). Jambo la maana kwa wanadamu ni wito wa Mungu kwao, ambaowapaswa wauitikie kwa imani. Tena makusudi yake yote yamhusu Kristo.„mzao‟ wa Abramu hasa ni Kristo, na uzao huo umepanuka kuingiza wote walio„katika Kristo‟ (6:11). Wateule ni wale walio „katika Kristo‟ - wale walio „katikaKristo‟ ni wateule.

9:14-18 Mungu si dhalimuPaulo aliendelea kwa kuuliza na kujibu maswali kama desturi yake. Alijua watuwatasikia shida ya kukubali hoja yake na alifahamu watakuwa na mawazo namaswali mengi. Kufuatana na aliyotangulia kusema kwamba si Waisraeli wotewalio Waisraeli wa kweli, basi bila shaka baadhi ya watu walifikiri kwambaMungu ni dhalimu. Ndiyo sababu alianza kwa maneno „Tuseme nini basi? Kunaudhalimu kwa Mungu?‟. Mara moja Paulo akakanusha kwa nguvu wazo hiloakisema „Hasha‟ ni jambo lisilowazika.

k.15 Kwa mara ya kwanza aliingiza neno la „rehema‟ katika hoja yake, naalirudia kulisemea tena katika sura hizo tatu. Rehema haikuwa jambo jipya,ilitajwa katika habari za Mungu kumwambia Musa „nitamfadhili yeyenitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu‟ (Kut.33:19). Manenohayo yalisemwa wakati wa uasi mkubwa wa Israeli walipotengeneza ng‟ombe yadhahabu na kuiabudu. Musa aliwakasirikia sana halafu akamwendea Mungu nakumwomba awahurumie na kuwafunulia utufuku wake. Wote walistahilikuangamizwa kama Mungu angaliwafanyia kwa haki. Ila Mungu akamjibu Musana kumwambia „nitamrehemu yeye nitakayemrehemu‟ akionyesha kwamba nijuu yake kuamua kurehemu na kuamua ni akina nani watakaorehemiwa. Munguhalazimiki kurehemu ila ni tabia yake kurehemu. Yu huru kufanya apendavyoMwenyewe. Asipoonyesha rehema ni nani atakayepona? akifuata haki tupuhakuna atakayesalimika. Hakuna awezaye kuzuia mapenzi yake ya kurehemuna kuokoa, wala Farao zamani wala Waisraeli wakati wa Paulo.

Mungu katika rehema zake anakusudia kupata jamii mpya ya wanadamu kwakufanya watu kuwa „watoto wake‟. Katika mpango huo Yeye huchagua mtummoja mmoja kwa kusudi la kutekeleza mipango hiyo, ambayo mwishoweyahusu wanadamu wote (8:19).

k.17 Ila si Musa tu aliyehusika na Ukombozi wa Waisraeli ambao ni mfano waUkombozi wa baadaye uliofanyika na Kristo. Mwingine aliyehusika na habarihizo ni Farao aliyekuwa Mfalme wa Misri wakati ule. Katika kifungu hicho Pauloamesema kwamba ni Mungu aliyemsimamisha Farao na kumfanya awe na moyomgumu, asikubali kuwapa Waisraeli uhuru wa kurudi makwao. Paulo hakusemaFarao aliumbwa kwa kusudi hilo bali alisimamishwa na Mungu.

Page 154: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI816

Alikuwa Mfalme wakati huo muhimu katika historia ya Israeli Mungu alipokusudiakutekeleza mipango ya kuwatoa watu wake watoke utumwani na kurudi makwao.Kwa hiyo, Mungu anayerehemu ni Mungu yule yule anayemfanya mtu awemgumu. Kwa nini? ili hata Farao apate kufahamu ya kuwa iwapo yeye ni Mfalmemwenye madaraka, hana madaraka juu ya Mungu. Mungu alimwinua ili mapenziya Mungu yatendeke si mapenzi yake. Yeye Farao alifanya moyo wake kuwamgumu alipozidi kumkataa Musa na ombi lake, ila kwa sababu Mungu alikazanakuwatoa Waisraeli waondoke nchi ya Misri ilionekana Mungu ndiye sababu yaFarao kuwa mgumu. Kwa njia yake watu wa mataifa mengine walipata kujuakwamba uwezo na nguvu za Mungu zilimshinda Farao. Ni vema katika habarihiyo tuone ya kuwa kusudi la Mungu lilikuwa jema sana, alitaka kuwaokoa watu.Kama Farao angalikubali yeye na watu wake wasingalipatwa na hasara yo yote(Kut.4:21; Yn.12:37-40; Mdo.2:22-23; 4:27-28; 2 The.11-12; 1 Pet.1:8).

Matendo ya Mungu katika kurehemu na katika kuleta ugumu yasielezwe kuwamambo mawili tofauti. Hakuna anayelilaumu jambo la Mungu kurehemu, kwahiyo, Mungu asilaumiwe anapofanya wengine kuwa na mioyo migumu. Hayohutokea watu wanapozuia mapenzi yake mema yasitendeke. Ni Mungu Baba waBwana wetu Yesu Kristo afanyayo hayo yote. Ugumu uliotokea ulikuwa hatua yanjiani tu. Mungu alimfanya Farao awe na moyo mgumu ili wote wauone Uwezona Utukufu Wake katika kuwapatia Israeli uhuru wao. Baadaye Waisraeliwalifanya ukaidi (11:7,25) na ugumu wao ulikuwa hatua katika WaMataifakuokolewa, kwa sababu Wayahudi wengi walipokataa kuiamini Injili basi Injiliilipelekwa kwa WaMataifa, kisha Wayahudi kwa WaMataifa wataokolewa (9:24;11:25,26). Mwisho wa mambo yote ni rehema.

9:19-29 Mungu ni MtawalaPaulo aliendelea na mtindo wake kwa kuuliza swali ambalo lilisababishwa naalivyosema katika k.18. Iliwezaje wale waliofanywa ugumu wahukumiwe. Kamawamekuwa walivyo kwa sababu ya mapenzi ya Mungu na kama hakunakuyazuia mapenzi Yake, mbona walaumiwe kwa kuwa walikuwapo wakati wamatukio hayo.

Twaona ya kuwa Paulo alipojibu hakuonyesha wasiwasi juu ya jambo lililotajwakatika k.18, kwa hiyo, ina maana kwamba aliyosema ni kweli. Ila alionyeshakwamba si kazi ya mwanadamu, kiumbe cha Mungu, kumhoji au kumjibu Mungu,Mwumba wake. Alitumia mfano wa mfinyanzi wa chombo cha udongo, na uhuruwa mfinyanzi kufinyanga chombo cha aina yo yote kutokana na udongoanaoutumia. Lakini mwanadamu si udongo tu, mwanadamu ameumbwa katikamfano na sura ya Mungu, kwa hiyo, aweza kumjibu na kumhoji Mungu, ila kwahali impasayo kiumbe kwa Mwumba wake. Zamani akina Ayubu na Yeremiawalihojiana na Mungu, hali wakiendelea kuamini na kutaka kuwa waaminifuKwake. Mara kwa mara katika Agano la Kale mfano wa mfinyanzi umetumiwa(Isa.29:15,16; 45:9, 64:8; Yer.18:1-6).

Page 155: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 817

Paulo aliutumia mfano wa mfinyanzi kuuonyesha uhusiano kati ya Mungu nawanadamu kuhusu wokovu. Mfinyanzi hakuumba ule udongo anaoutumia ilaanaufanyia kazi. Mungu pia huchukua „fungu la udongo‟ yaani wanadamuwalioanguka, wenye dhambi, na kuwafanyia kazi. Mungu hakumwumbamwanadamu ye yote awe „chombo kisicho cha heshima‟ kwa sababu wanadamuwote wameumbwa katika sura na mfano wake. Paulo alisemea juu ya MunguMtawala si Mungu Mwumbaji. Tangu anguko la Adamu Mungu ametengeneza„vyombo vya heshima‟ kutoka udongo‟ yaani umati wa watu walio „katika Adamu‟na „chini ya dhambi‟. Hakuna astahiliye kufanyiwa kuwa chombo cha heshima.

k.22 Ni vema kukumbuka kwamba Paulo hakusema Mungu anafanya hivyo ila„ikiwa Mungu kwa kutaka....‟. Mungu ana madaraka juu ya yale anayofanyakatika historia. Pia ni vema kukumbuka ya kuwa wanadamu ni wenye dhambi,kwa hiyo, Mungu anatawala na kuongoza mambo ya ulimwengu hali yawanadamu wote kuwa wenye dhambi. Mungu hawawazi wanadamu kuwa„udongo‟ ila ina maana kwamba anapoongoza mambo anao uwezo juu yawanadamu mfano wa mfinyanzi aliye na uwezo juu ya udongo.

k.22b-23 Hapo Paulo ametaja „vyombo vya ghadhabu‟ na „vyombo vya rehema‟.Paulo alisema vyombo vya ghadhabu vilifanywa tayari kwa uharibifu bila kusemawazi kwamba ni Mungu aliyevifanya tayari, ila aliposema juu ya vyombo vyarehema alisema wazi „alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu‟. Ni vemakukumbuka kwamba hakuna astahiliye rehema za Mungu, wote wamestahilihukumu, kama ilivyosemwa katika sura tatu za kwanza. Kuhusu vyombo vyaghadhabu Mungu alichukuliana nao kwa uvumilivu mwingi, akicheleweshakutekeleza hukumu juu yao. Katika 2:4 wazo lilikuwepo la nafasi ya kutubu.Iliyopo ni kwamba kama Mungu aliwafanya, au wao walijifanya, mwisho waoutalingana na jinsi walivyokuwa katika maisha yao. Mungu hapendi mwenyedhambi apotee (1 Pet.3:8-9).

Kwa vyombo vya ghadhabu Mungu alidhihirisha ghadhabu yake na uwezo wakena uvumilivu wake. Kwa vyombo vya rehema Mungu alionyesha wingi wa utukufuwake. Rehema yake ni jumla ya tabia zake zote njema (Zab.85:9-11; Rum.11:33;Efe.1:7,12,14; 2:4,7; 3:8,16; Kol.1:27; 1 Tim.1:11). Mtu kuokolewa ni mwujizaupitao miujiza yote, hata malaika na enzi za juu hustaajabia na katika umileleujao habari hii itazidi kustaajibiwa na waliookolewa watazidi kushangaa. NiMungu tu peke yake anayewatayarisha watu wapate utukufu, ni mwenendo waneema na kazi ya neema maishani mwao mpaka waufikie utukufu na kutukuzwa(2 Tim.2:20,21). Kwa hiyo, wakati wote, ama kwa rehema au kwa ghadhabu,Mungu anaidhihirisha haki yake ila hasa apenda kurehemu. Mungu huwapatiawote nafasi ya kutubu, watakaotubu na wasiotubu (1 Pet.3:8-9).

Page 156: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI818

k.24 Ila katika hayo yote Paulo hasemi kama ni hoja iliyopoa, bali yahusuutendaji wa Mungu katika maisha ya wanadamu, Wayahudi kwa WaMataifa.Wayahudi waliteuliwa, na WaMataifa waliachwa nje ya mpango wake, hukuWayahudi wakiwafikiria WaMataifa kuwa „vyombo vya ghadhabu‟. Ila sasaMungu amewaita WaMataifa kumwamini Kristo, amewaingiza katika mpangowake nao wamepokelewa katika Kanisa huku Wayahudi kwa jumla wako nje kwakuwa wamekataa kumwamini Kristo. Ila baadhi yao, wachache, kama Paulo nawenzake wamemwamini. Lakini Paulo amekwisha kuonyesha kwamba hata kwaWayahudi si wote walioteuliwa ila baadhi tu. Uteule huo wa Mungu si jambolililotokea baada ya Wayahudi kumkosea Mungu ila ni mpango Wake wa asili.Mungu aliyakusudia mambo hayo katika umilele, naye anawaita watu kufuatanana makusudi hayo (Rum.8:28-30). Maana Mungu alimwambia Abramu „katikawewe jamii zote za dunia zitabarikiwa‟. Hivyo katika mchanganyiko wa Wakristowa Kiyahudi na wa KiMataifa katika shirika za pale Rumi si vema mtu athubutikujiinua juu ya mwenzake kwa kuwa hayo yote Mungu alipanga kulingana namakusudi yake ya milele.

k.25-29 Hapo Paulo amethibitisha hoja yake kwa kutumia Maandiko nakuonyesha kwamba mapenzi ya Mungu tangu awali yalikuwa kuwaletaWaMataifa (Hos.1:10;2:23). Katika mapenzi yake si Waisraeli wotewatakaookolewa ila „mabaki‟ tu (Isa.10: 22, 23; 1:9). Katika k.29 alitaja manenoya ajabu ya Isaya „Kama Bwana wa majeshi asingalituachia uzao, tungalikuwakama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora‟. Kwa hiyo, hata kubaki kwawaaminifu wachache ilisababishwa na rehema za Mungu. Katika mambo mengisisi wanadamu hatuna jibu, na hata kama watu waseme nini, Mungu hawezikulaumiwa. Yatupasa kungojea mwisho wa mambo yote ndipo tutaweza kuonauzuri wa ajabu katika mipango yote ya Mungu.

9:30-33 Hasara ya Israel ni kosa lake yenyewePaulo aliendelea kwa kuuliza na kujibu maswali. Katika majibu alieleza wazisababu za kosa la Israeli na mafanikio ya WaMataifa.

Israeli walikosa si kwa sababu hawakuteuliwa ila kwa sababu hawakujitia chiniya njia ya wokovu iliyowekwa na Mungu. Wao walikazana kupata haki kwamatendo ya sheria, njia iliyokataliwa na Mungu. Kweli walipewa torati, lakinishabaha ilikuwa kuwasaidia wajitambue kuwa wenye dhambi, ili wawe tayarikupokea haki kama kipawa, yaani wahesabiwe haki kama Ibrahimu baba wataifa alivyohesabiwa haki. Kama wangalitambua kwamba hawatafaulu kuipatahaki kwa matendo yao wangalikuwa tayari kumwamini Kristo, lakini waliendeleakatika njia zao. Nabii Isaya alitabiri neno hilo (Isa.8:13-17 na 28:16). Mwambauliowaangusha ni Kristo, na Kifo Chake msalabani (1 Kor.1:23; Kum.21:23;Gal.3:13). Kwa hiyo, ni wao waliotangulia kumkataa Mungu na njia yake yawokovu, si Mungu aliyewakataa.

Page 157: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 819

Ajabu ni kwamba WaMataifa ambao hawakumtafuta Mungu, haki yakewakaipata kutokana na mahubiri ya Injili, nao walipata nafasi baada ya Wayahudikuhubiriwa. Walikuwa tayari kukubali njia iliyowekwa na Mungu, njia yakumwamini Kristo. WaMataifa ambao hapo nyuma walikuwa nje ya ufunuo waMungu isipokuwa ule walioupata katika Uumbaji na dhamiri (Rum.1:18ku). Hakiinayozungumzwa ni kibali cha Mungu si haki ya maadili, kwa mtu ye yote aliyena uhusiano mwema na Mungu atazamiwa kuishi kwa kumpendeza Mungu.Kristo ni Mwamba anayeamsha imani katika wengine na kuwakwaza wengine (1Kor.1:18; 2 Kor.2:15), kwa hiyo, katika Yeye kuna kuteuliwa na kukataliwa. Kunauhusiano kati ya anayokusudia Mungu na jinsi mambo yanavyotokea katikamaisha ya watu.

Hoja ya Paulo ni kwamba wanadamu wanao wajibu kuhusu itikio lao kwa Munguna huo ndio mkazo wake katika sura ya 10.

10:1-4 Mzigo wa Paulo juu ya Wayahudi wenzakePaulo aliendelea na hoja yake. Kwanza alianza kama alivyoanza katika sura yatisa kwa kutaja jinsi yeye mwenyewe alivyojisikia kuhusu watu wake. Pauloaliweza kuwaelewa kwa sababu alikuwa sawa na wao kabla ya kukutana naKristo Aliye Hai wakati wa kwenda kuwakamata Wakristo huko Dameski.Alifanana nao katika juhudi, hata aliwazidi wengi wao, juhudi ambayo ilikosaufahamu wa haki ya Mungu (Mdo.26:5,8; Gal.1:14) Paulo alisema juu ya uteulewa mabaki tu uliosababishwa na neema ya Mungu, hata hivyo alitaka sana watuwake waokolewe, na katika maombi yake alidumu kuwaombea ili waokolewe.

Paulo alijua kwamba Mungu ameamua kuwaokoa baadhi tu ya Wayahudi hatahivyo wale wengine wameamua kwa hiari yao yenyewe kwambahawatamwamini Kristo.

k.2-3 Kiini cha shida yao si ukosefu wa juhudi, ila juhudi yao haikuwa njema,ilikosa maarifa, maana katika juhudi yao walimkataa Kristo, na kwa kumkataaKristo walikosa kuelewa haki ya Mungu, na badala yake waliinua haki yaowenyewe. Walipaswa kujua na kutambua kwamba haki ya Mungu inazidi hakiyao. Walifahamu kwamba neno kuu la dini ni haki, na ni ajabu walithubutu kufikirikwamba haki yao yatosha kuwapatia kibali cha Mungu. „hawakujiweka chini yahaki ya Mungu‟ Hivyo, potelea mbali wawe wema wa kiasi gani wamekuwa siowatii kwa Mungu, watu wasio tayari kukubali kwamba ni wenye dhambi na niMungu tu aliye na haki ya kuamua ni kwa msingi gani atawakubali. Kwa hiyo,juhudi si njia ya kuvuta kibali cha Mungu, lazima juhudi iandame na ujuzi wakweli wa Mungu.

k.4 Kristo ni „mwisho wa sheria‟, maneno hayo yana maana gani? kwa sababuneno „mwisho‟ lina maana mbili ya „hatima‟ na „lengo‟. Kristo ni mwisho wa

Page 158: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI820

utaratibu wa zamani kwa sababu ameleta utaratibu mpya wa „kuishi katika Roho‟.Kristo alitimiza sheria na amemletea kila mtu haki ipatikanayo kwa imani. Toratikama mwongozo wa haki ilikuwa kiongozi wa kutuleta kwa Kristo. Kristo alitimizamadai yote ya Torati na haki ya Kristo inahesabiwa kwetu tunapomwamini. Nikatika Kristo tu watu wanaletwa katika uhusiano mwema na Mungu.

10:5-13 Njia mpya ya haki ni kwa ajili ya watu wotek.5-7 Njia ya haki kwa sheria ni njia ngumu, ni kama kupanda ngazi mpakambinguni au kushuka kwenda kuzimu. Kristo alifanyika mwili na kuja duniani,halafu akafa akaenda kuzimu ndipo akafufuka kutoka wafu, yu hai. Kwa hiyo, njiaya imani si ngumu wala Kristo si mbali nasi, bali ni njia rahisi, na Kristo yu karibu.Po pote alipo, mtu aweza kumpata Kristo. Kwa kuamini, mtu hukubali Kristoalifanyika mwili na kuja duniani, kisha akafa akafufuka kutoka kwa wafu, akarudijuu. Kristo si Masihi wa maono wala wa dhana, wala si nabii mfu, bali ni Bwanaaliye hai. Yote yaliyotakiwa ili mtu aletwe kwenye uhusiano mwema na Munguyamefanyika na Kristo, iliyobaki ni mtu kujikabidhi kwa Kristo. Jambo hilo ni rahisi.

k.8-11 Paulo ametaja mambo mawili kwa upande wa mtu, moja kuhusu moyowake na jingine kuhusu kinywa chake, na yote mawili yanakwenda kwa pamoja.Pasipo kuamini kwa moyo kukiri kwa midomo hakuna msingi, kukiri kwa midomobila imani ya moyoni ni kama hewa tupu. Yawezekana kukiri alikotaja Paulo niukiri aliofanya mwongofu alipobatizwa hadharani. Wokovu ni jambo la kibinafsi,unashuhudiwa kwa wazi. Zamani za Agano Jipya ilikuwa desturi kwa watu kukirikwamba „Kristo ni Bwana‟ (1 Kor.12:3; Flp.2:11) na wakati wa mateso walewalioletwa mahakamani walilazimishwa kukiri „Kaisari ni Bwana‟ manenoambayo Wakristo walikataa kuyasema. Tena Paulo alisema watu wapaswa kukirikwamba waliamini Kristo alifufuka. Kwa kuamini kwa moyo mtu hupata haki namsamaha wa dhambi zake, na kwa kukiri kwa midomo hupata wokovu, na kwanjia hiyo imani yake huthibitika.

k.11 Paulo alirudia kutumia kifungu cha Isaya 28:6 ambacho alitaja katikaRum.9:33. Hakuna mtu amwaminiye Kristo ambaye ataona haya. Hata BwanaYesu alisema „kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele yaBaba yangu aliye mbinguni. Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, naminitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni‟ (Mt.10:32-33). Litakuwa jambola heshima kuu kumsikia Yesu akitaja mtu mmoja mmoja kwa jina katika siku ilekuu. Yeye hataona haya juu yetu, kwa hiyo, haitupasi sisi kusikia haya juu yakewakati huu wa sasa.

k.12-13 Njia hiyo ya wokovu ni kwa Wayahudi na WaMataifa, hamna tofautikati yao. Hapo nyuma Paulo aliwafungamanisha wote pamoja kuwa wenyedhambi (3:22-23) vivyo hivyo wote wamefungamana katika wokovu. Wotewamenyenyekezwa. Kama kuna tofauti katika „kiasi au uzito wa dhambi‟

Page 159: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 821

wengine wakizidi wengine katika kiasi au ubaya wa dhambi zao, wote huwawenye dhambi na wote hufanya dhambi. Mungu huwakirimia wote wingi waneema na msaada wake, mradi wamwitikie anapowaita. Wakristo waliitwa watu„wanaoliitia Jina la Bwana‟ (Mdo.9: 14,21; 22:16; 1 Kor.1:2; 2 Tim.2:22). Hivyo nirahisi kumpata Kristo, ni kwa kumwita tu! Maneno katika Yoeli 2:32yaliwahukumu Wayahudi wengi kwa kuwa hawakuliitia Jina la Bwana.

10:14-21 Wayahudi hawana udhuru kwa kutokuamini kwaoKatika kifungu cha 13 Paulo alisema juu ya ahadi ya Mungu iliyotolewa na Yoelikwa Waisraeli. Neno hilo lahusu Injili kuhubiriwa ulimwenguni. Kwa sababu watuwameambiwa wazi waliitie Jina la Bwana, basi ni lazima Injili ihubiriwe kote kote.Lakini kabla ya kumwita Bwana mtu anahitaji kuamini, na kabla ya kuaminianahitaji kuwa amesikia habari zake, na kabla ya kusikia habari zake inahitajikamtu atumwe kutangaza habari zake.Imekuwaje kwa Israeli? Je! Mungu ametuma kwao wahubiri wa Injili? Ndiyoametuma. Paulo mwenyewe ni mmojawapo aliyetumwa kutangaza habari zaKristo, tena alianza kwa Wayahudi ndipo kwa WaMataifa. Katika Agano la Kalewaliotumwa walihesabiwa kuwa wamepewa kazi nzuri sana (k.15).

Kwa hiyo, Paulo alionyesha kwamba Wayahudi walikuwa wamepewa nafasi yakutosha kumwamini Kristo. Shida ilikuwa upande wao kwa kuwa walikataakumwamini. Kusikia walisikia (k.18). Huenda hawakuelewa ujumbe walioletwa.La! waliufahamu. Wayahudi walijua kwamba WaMataifa wataingizwa katikaJamii ya Watu wa Mungu, na ya kuwa wao wataupoteza urithi wao, na yakwamba wataona wivu kwa kumwona Mungu akitumia mataifa mbalimbali katikakuwaadhibu watu wake, mataifa ambayo hapo nyuma hawakumfahamu Munguwa kweli. Musa, yule waliyemtegemea sana kwa kuwa aliwapa Torati alikuwaametoa habari hiyo. Tena Isaya alikuwa mjasiri alipothubutu kusema mambomawili ya ajabu kwamba WaMataifa watajaliwa kuhubiriwa Injili na kuipokeahuku Wayahudi watahubiriwa Injili wasiipokee. Tena wataikataa japokuwaMungu alikuwa akiwasihi sana sana kwa upendo mwingi na kwa muda mrefu.Walikuwa wakaidi watu wasio tayari kujinyenyekeza.

Kwa hiyo, hoja ya Paulo ni kwamba Israeli wamekataliwa, si kwa sababu Munguhakuwapa nafasi ya wokovu, alikuwa amewapa nafasi nyingi, ila wao walizikataa.

Dondoo za kutoka Isaya zilihusu wakati wa Utumwa wa Babeli. Isaya alionawaliwajibika kuvuta WaMataifa hasa baada ya kutoka Utumwani. Badala yakewalizidi kuyaangalia mambo yao, kukuza hali ya Utaifa, na kujiona kuwa bora.Walizidi kufafanua mambo ya Torati kwa ubaridi wa kisheria, wakishughulikia„andiko‟ tu bila kuchunguza maana yake ya ndani. Mwishowe hali ya Ufarisayoilitokea na hali hiyo ilitawala mambo ya dini ya Kiyahudi. Kisha Yesu alipokujawakashindwa kumpokea, na tunaposoma Injili twakuta kwamba Yesualiwahukumu vikali Mafarisayo na hali zao.

Page 160: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI822

11:1-12 Je! Mungu amewatupilia mbali watu Wake?Paulo alimaliza hoja ya sura ya 10 kwa kuonyesha kwamba Waisraeli walikuwawakaidi, watu waliokazana kumkataa Mungu na wito wake. Kwa hiyo,, alianzasura 11 na swali kama ilivyokuwa desturi yake katika sura hizo tatu. Je! Munguameacha kuwashugulikia Wayahudi? Je! anao mpango wo wote juu yao? Mara,baada ya kuuliza swali, akalijibu kwa nguvu sana. Paulo alitaka kuonyesha yakuwa si lazima Mungu aendelee kuwakataa wale wanaomkataa. Kwa kuteuliwawaliheshimiwa sana pia waliwajibika sana.

k.1 Mungu hakuwasukumia mbali watu Wake. Ushuhuda wa jambo hilo ni Paulomwenyewe, yeye alikuwa Myahudi kwelikweli ambaye aliongoka akawa Mkristohodari sana. Mwanzoni aliwapinga sana Wakristo, hata kuwatesa, hata hivyo,Mungu alimhurumia. Kwa nini Mungu alimchagua kuwa mhubiri wa Injili ikiwaamesukumia mbali watu wake?

k.2 Upo ushuhuda mwingine wa Mungu kutokuwatupa watu Wake. Wakati waEliya Waisraeli walimwasi Mungu sana wakiigeukia miungu ya jirani zao nakuabudu mabaali. Eliya aliwaza kwamba ni yeye peke yake aliyebaki mwaminifukwa Bwana. Alimlalamikia Mungu, lakini Mungu alimwonyesha kwambaamekosa katika kufikiri ni yeye tu aliyebaki. Walikuwako watu elfu sabawasiompigia magoti Baali na hao walihifadhiwa katika uuaji mkuu uliofuata.Katika hao waliobaki yalikaa matumaini ya Israeli (1 Waf.19:10-18).

k.4-6 „Nimejisazia‟ Mabaki hawakubaki kwa sababu walistahili kubaki ila kwasababu ya neema na mapenzi ya Mungu. Hata wakati wa Paulo walikuwapoWayahudi waliomwamini Kristo japokuwa taifa kwa jumla hawakumkubali Kristo.Hao ni dhamana ya Mungu kuwekea Israeli nafasi katika mipango yake yabaadaye.

k.7-10 Paulo alirudia kutaja tena kosa la Israeli. Walitafuta „haki‟ (9:30-31) lakinisi kwa njia ya imani, kwa hiyo, hawakuipata, wakakosa kuletwa katika uhusianomwema na Mungu, ila baadhi yao walijaliwa kumwamini Kristo, wakaingizwakatika Kanisa, na wengine „walitiwa uzito‟ (Isa.29:10; Kum.29:4; Zab.69:22-23;Isa.6:9). Hata Bwana Yesu alisema neno hilo (Mt.13:14ku. Mk.4:12; Lk.8:10;Yn.13:40; Mdo.28:26). Walikosa kumtambua Masihi wao, na kwa sababuhawakujali Neno la Mungu, Mungu aliwaadhibu kwa kutia muhuri uchaguzi waowa kukataa kuona hata watashindwa kuona. Katika Rum.1:24;26;28 tulionamaneno „Mungu aliwaacha‟ katika hali ile waliyochagua wenyewe. Pauloalikuwa akifuata mtindo wa kuwaza wa Kiyahudi akisema ni „Mungu aliwapa rohoya usingizi‟ maana haikuwezekana Wayahudi walioamini Kuwako kwa Mungu nautawala wake juu ya mambo yote kumaanisha hali hii kuwa bahati mbaya aukuwa na asili katika Shetani kama Shetani ni „mungu‟ wa uovu mwenye uwezojuu ya „Mungu wa utu wema‟. Kamwe wasingekubali kwamba upo „uwezo‟ ulionje ya Mungu. Upofu na uzito wao ulikuwemo katika utawala wa Mungu namakusudi yake.

Page 161: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 823

k.11 Ndipo Paulo aliuliza swali lingine na kulijibu kwa nguvu kama hapo nyuma.Kweli wameanguka, ila Je! wameanguka kabisa, wasiinuke tena? Kwa kuangukakwao baraka moja kubwa imepatikana, Injili imehuburiwa kwa WaMataifa naowameitika vema. Tena jambo hilo la WaMataifa wengi kuamini litawatiaWayahudi wivu (Kum.10:19) na baadaye wao wenyewe watatamani kumwaminiKristo (Mdo.13:46; 18:6; 28:28; Mt.8:12; 21:41,43; 22:7)

k.12 Halafu Paulo alitaja baraka kubwa zaidi itakayotokea mbeleni. Kwa kosa laWayahudi la kutokumwamini Kristo WaMataifa wamepata wokovu, kwa hiyo,baadaye itakuwaje wakati wa Wayahudi kubadilika hali yao na wengi waokumpokea Kristo? Kweli ulimwengu utajaa baraka tele. Kwa hiyo, Mungu anazidikutekeleza mapenzi yake ya walimwengu wote kuokolewa. Hivyo nenolililoonekana kuwa kosa kubwa ni „siri‟ juu ya njia atakayoitumia Mungu kutimizawokovu wa wote.

Tukijumlisha sehemu hiyo twaweza kusema, si Israeli wote waliokataliwa,mabaki walikuwepo; na kukataliwa kwao si kwa muda wote; na mwisho wa hayoyote ni mema kuzidi. Hakika mwishowe Israeli wote wataokolewa.

11: 13-16 Uhusiano wa Waumini wa Kiyahudi na wa KiMataifak.13 Katika Kanisa la pale Rumi mwanzoni Wakristo wa Kiyahudi walizidiWakristo wa KiMataifa, halafu baadaye Wakristo wa KiMataifa walizidi Wakristowa Kiyahudi. Kwa jinsi Paulo alivyosema nao katika sehemu hiyo inaonekanahao wa KiMataifa walikuwa katika hatari ya kujivuna na kuwadharau Wayahudi.

Paulo alisema na waumini wa KiMataifa moja kwa moja. Yeye mwenyewealikuwa sababu ya wengi wao kuamini kwa uinjilisti aliofanya kati yao kufuatanana Utume aliopewa na Mungu (9:15; Gal.2:7,9) na aliifurahia hiyo kazi. Hakuonahali hiyo kuwa kinyume cha manufaa ya Wayahudi maana alisema katika11:11-12 kwamba Wayahudi watatiwa wivu kwa kuwaona WaMataifa wakijaliwabaraka za Mungu hasa wakiwaona wanashirikiana vizuri na Mungu „wao‟. HivyoPaulo aliona ya kuwa WaMataifa wanapozidi kumkubali Kristo ni msaada kwaupande wa Wayahudi na hatua katika kuwatia wivu, aliona baadhi yaowamekwisha kuokolewa ila si wengi, Mungu hajaacha watu wake.

k.15 Alirudia wazo la hapo nyuma juu ya Kukataa kuamini kwa Wayahudikusababisha mlango kufunguliwa kwa WaMataifa, na jambo hilo limeletaupatanisho wa Mungu na ulimwengu. Halafu baada ya Injili kuhubiriwa kote naWaMataifa kupewa nafasi tele na kuitika vema, ndipo utakuja wakati waWayahudi kupewa tena nafasi ya kumpokea Kristo. Hoja ya Paulo ni kwambakama kuokolewa kwa WaMataifa wengi kumeleta baraka tele kwa ulimwengu,kwa vyo vyote baraka zitazidi baada ya wingi wa Wayahudi kuokolewa, hataalitumia lugha ya kusema itakuwa kama „uhai baada ya kufa‟. Baadhi yawataalamu huwaza kwamba maana ya maneno „uhai baada ya kufa‟ ni Ufufuowa mwisho, kwa hiyo, jambo hilo litakapotokea, Kristo atarudi kwa mara ya pili.

Page 162: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI824

Ila wengine huwaza kwamba yahusu Wayahudi wanaoongoka na kumpokeaKristo, kiroho, wanatoka mautini mpaka uzimani (Yn.5:24).

k.16 „donge na shina‟ Paulo hakusema wazi donge na shina ni nini hasa?vinafikiriwa kuwa Abramu na maandalio ya wokovu yaliyofanyika wakati wote waAgano la Kale, na Wayahudi waliookolewa wakati wa Paulo ni malimbuko yawale wengi ambao wataokolewa baadaye (11:28; 2:28-29).

11:17-24 Mfano wa kupandikizwa katika Mzeituni MwemaKwa mfano huu Paulo alionyesha hatua zilizoko katika utekelezaji wa mpangowa Mungu kuhusu wokovu wa watu wote. Hatua ya kwanza ilikuwa kuteuliwakwa Israeli, ili iwe chombo cha kutayarisha njia ya Kuja kwa Kristo. AlifanyaAgano na Abramu, Abramu alimwamini Mungu, naye akamhesabia haki kwa ajilihiyo. Israeli haikutimiza shabaha ya kuitwa kwake, na Kristo alipokuja taifa teulehalikumpokea ila baadhi tu. Kristo aliwakabidhi wale waliomwamini huduma yakuwahubiri wenzao Injili. Hata hivyo, hawakumwamini Kristo japokuwa ushuhudamkali ulitolewa wa Kufufuka Kwake, ila wachache tu waliamini.

Ndipo njia ilifunguliwa kwa WaMataifa kuhubiriwa na kuamini, nao wakaitikavema na wengi wao waliokolewa. Paulo ameeleza hatua hizo kwa kuutumiamfano wa matawi ya Mzeituni Mwema kukatwa, na matawi ya Mzeituni Mwitu(WaMataifa) kupandikizwa katika Mzeituni Mwema. Ni vema kuona ya kuwaMungu hakun‟goa Mzeituni na kupanda mwingine, na Wayahudi wameitwa„matawi‟ na WaMataifa wameitwa „matawi‟. Kazi hii ya kuwapandikiza WaMataifailikuwa kazi ya neema na uwezo wa Mungu, haikufuata kanuni ya kawaida yaupandaji. Ye yote aliyepandikizwa alilishwa na unono wa Mzeituni yaani urithi wamambo mema ambayo Mungu aliyafanya hapo nyuma alipojihusisha kipekee nataifa teule.

Paulo alikuwa akisemea hayo kwa ajili ya ushirika wa pale Rumi maana hatariilikuwepo kwa WaKristo wa KiMataifa kujivuna na kuwadharau waumini waKiyahudi. Kwanza iliwabidi wafahamu kwamba wao ni matawi yanayobebwa nashina ambalo ni Watu wa Mungu walioteuliwa zamani. WaMataifa asili yaoilikuwa katika upagani. Ila waliweza kujibu kwamba matawi ya asili yalikatwa iliwao waingizwe, kana kwamba wao ni bora.

k.20 Paulo aliwaunga mkono ila aliwakumbusha sababu ya Wayahudikukataliwa ambayo ilikuwa „kutokuamini kwao‟ na sababu ya wao kupandikizwailikuwa „kuamini kwao‟, kwa hiyo, hali yo yote ya kujiona na kujivuna ni kinyumekabisa, kwa sababu kiini cha „imani‟ ni kumtegemea Mungu kabisa nakutokujitegemea hata kidogo. Mara mtu aanzapo kujivuna ameachakumtegemea Mungu na Paulo aliwaonya kwamba hali inayokubalika ni „kuogopa‟.

Page 163: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 825

k.21-22 Wakristo wa KiMataifa wasifikiri kwamba hawataweza kufanyiwa kamaWayahudi walivyofanyiwa na kukataliwa ikiwa wataacha kuamini. Mungu awezakubadili mambo. Neno linalotawala uhusiano wa mtu na Mungu ni imani, kwahiyo, kuna usawa katika utendaji wa Mungu, potelea mbali mtu awe Myahudi auMMtaifa. Itikio la Mungu kwa imani ni mtu kuonja „wema‟ wake na itikio la Mungukwa kutokuamini ni mtu kuonja „ukali‟ wake. Neno hilo linalingana na neema naghadhabu kuwa hali mbili ziwianazo katika tabia zake. Vema wakae katika wemawa Mungu wakiendelea kumwamini Kristo na wasijione.

k.23-24 Tena kuna matumaini hata kwa Wayahudi wakiacha kutokuamini kwao.Ipo nafasi kwao ikiwa wataamua kuuacha ukaidi wao na kumgeukia Kristo nakumpokea. Ni rahisi zaidi kwa matawi ya asili kupandikizwa tena kuliko matawiya mzeituni mwitu kupandikizwa. Yote hutegemea uwezo wa Mungu. Munguaweza kuuondoa utaji uliowazuia Wayahudi wasiamini na kuwapa uwezo wakuiitikia Injili. Kwa hiyo, Paulo hajakata tamaa kabisa juu ya Wayahudi wenzake.Watu wa Mungu wa Agano la Kale na wa Agano Jipya ni wamoja, asili yao nimoja, wamepandikizwa katika Agano alilolifanya Mungu na Abramu na mababa,na wote wana mahali pao kwa neema na kwa imani.

11:25-32 Shabaha ya Mungu ni kuwahurumia woteHapo Paulo alitia muhuri hoja yake ya hapo nyuma akianza na usemi alioutumiamara kwa mara wakati alipotaka kuvuta usikivu wa wasomaji wake kwa nenomuhimu (1:13; 1 Kor.10:1; 12:1; 2 Kor.1:8; 1 The.4: 13). Angali akisema naWakristo wa KiMataifa wa pale Rumi akielewa kwamba walikuwa katika hatari yakudhani kwamba wao ni bora kuliko Wayahudi wenzao, wakijiona kuwa na akilizaidi kwa sababu wameuitika wito wa kumwamini Kristo.

Alitaja „siri hii‟ (16:25). Maana ya neno „siri‟ yahusu jambo ambalo lilifichwa ndaniya nia na makusudi ya Mungu, ambalo halikuweza kujulikana kwa wanadamukwa akili zao mpaka Mungu atakapowafunulia kwa sababu Mungu hutimizamapenzi yake kwa njia zisizo kawaida. Siri aliyosemea Paulo Mungu amekwishakuifunua, na Paulo alitaka wasomaji wake waifahamu kwa faida yao. Neno „siri‟laonyesha ni ukweli wa thamani sana.

Siri hiyo ni nini hasa? „ni kwamba kwa kiasi ugumu umewapata Israeli, mpakautimilifu wa Mataifa uwasili‟. Kwa hiyo, ni yale mambo mawili ambayo Pauloamekwisha kuyadokeza. Ule „ugumu‟ (maana yake wengi wamekataakumwamini Kristo) uliowapata Israeli si wa wakati wote, ni „mpaka‟ utimilifu waMataifa. (utimilifu, maana yake ni, wengi kumwamini Kristo). Tumekwisha kuonakwamba walikuwapo „mabaki‟ wasiokuwa wagumu, walimwamini Mungu katikanyakati za Agano la Kale, na hata Injili ilipohubiriwa baadhi ya Wayahudiwalimwamini Kristo. Lakini „kwa sehemu/kiasi‟ imekuwa „mpaka‟ kwa hiyo,yahusu muda. Kwa hiyo, ule ugumu uliowapata Israeli utakwisha, utaondolewa.

Page 164: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI826

Katika mpango wa Mungu umati mkubwa wa Israeli hawatamwamini Kristompaka umati mkubwa wa WaMataifa wamemwamini. „utimilifu wa Mataifa‟maneno hayo yahusu umati mkubwa wa WaMataifa kumwamini Kristo. Ni naniambaye angedhani kwamba WaMataifa wataingizwa katika mpango wa Munguna kupewa nafasi ya kuokolewa, na ya kwamba wokovu wao utatangulia wokovuwa watu wengi wa Mungu walioteuliwa!! WaMataifa walikuwa chini ya ghadhabuya Mungu (1:18) sasa wako chini ya rehema zake. Wayahudi walikuwa chini yarehema zake kwa sababu ya uteule wao, ila sasa wako chini ya ghadhabu yaMungu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Watu huwa chini ya „ghadhabu‟ au„rehema‟ za Mungu. Tusipozipokea rehema za Mungu katika Kristo tutapatwa naghadhabu yake. Faraja ni kwamba tunapokuwa chini ya ghadhabu yake shidatunazopata zatusukumu kutafuta rehema zake.

k.26-27 „Hivyo Israeli wote wataokoka‟. „Israeli wote‟ ni akina nani? Manenohayo yameelezwa kwa tofauti na wataalamu. Je! Israeli ni wale mabaki pamojana wale waliokuwa wagumu hapo nyuma? Je! ni Israeli ya kiroho (Gal. 6:16)wateule wote wa KiMataifa na Kiyahudi? „mpaka utimilifu wa WaMataifa‟ Je!mpaka ina maana mpaka ugumu umekwisha? kwa sababu neno „mpaka‟inaweza kuelezwa kwa maana mbalimbali.

Kihistoria, wakati huo wa sasa ni wakati wa WaMataifa kujaliwa kumwaminiKristo, na baadaye Israeli watajaliwa kumwamini na wengi wao watatubu nakuacha kutokuamini kwao, watashirikishwa baraka za Agano Jipya, za msamahawa dhambi na uzima wa milele. Baraka watakazopata ni zile za Injili sawa nawanazopata waumini wa KiMataifa, hamna baraka bora kuliko hizo. Munguatawafanyia hayo (Isa.59:20ku; 27:9; Yer.31:34).

Ni kwa mpango huo Israeli wataokolewa. Ni mpango wa Mungu na Paulohakutoa sababu za Mungu kutumia njia hiyo, ila alitoa matokeo ya mpango Wakekuwa Israeli wote kama WaMataifa wataokolewa kwa neema tu. Ila tusifikiri kilaMyahudi ataokolewa na kila MMataifa ataokolewa, la. Ila anasemea kila kundikwa jumla. Twaona Paulo hakusema mambo ya siasa juu ya Taifa la Kiyahudikurudishiwa hali ya Utaifa.

k.28 Hapo Paulo ametazama jambo hilo kwa pande mbili, upande wa Injili naupande wa Uteule. Kuhusu Injili Wayahudi wamekuwa adui, wako nje ya kibalina baraka za Mungu. Kwa wakati huo wanampinga Kristo, na kama Pauloalivyokwisha kueleza, jambo hilo limegeuka kuwa faida kwa WaMataifa, kwasababu Injili imehubiriwa kwao. Hata hivyo, kuhusu Uteule, iwapo Wayahudi niadui, kwa upande wa uteule ni wapenzi, kwa sababu ya baraka zote walizojaliwamababa zao. Mababa ni malimbuko na mashina yaliyotajwa katika k.16. Kwahiyo, Wayahudi ni maadui pamoja na kuwa wapenzi.

k.29 Paulo aliweka hayo yote katika msingi wa uaminifu wa Mungu asiye nakigeugeu, Yeye ni Mungu asiyebadilika, kamwe hajuti wala hasitisiti kuhusu

Page 165: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 827

ahadi zake na mipango yake. Aweza kutegemewa kabisa kuyatimiza Aliyoazimukuyafanya.

k.30-32 Hakuna awezaye kujidai kuwa bora kwa sababu wote wamekuwa waasi.Hali ya WaMataifa ilielezwa kinaganaga katika 1:18-32, nao walihitaji rehema zaMungu. Halafu na Wayahudi kwa ukaidi wao walimwasi Mungu aliyewateua, naowahitaji rehema za Mungu. Hivyo wote, Wayahudi kwa WaMataifa wamehitajirehema za Mungu. „Wote‟ maana yake ni wote bila kubagua kati ya Wayahudina WaMataifa.

Mwisho wa njia ni rehema, na kwa kila kundi ni njia ipitiayo kwanza katika uasi.Ni wenye dhambi tu wanaohurumiwa na Mungu. Mungu amewafunga wote katikakuasi ili awarehemu wote. (Gal.3:22-23). Katika rehema zake Mungu limekaatumaini kwa ulimwengu. Kwa hiyo, twaweza kujumlisha kwamba uasi hutanguliautii; kutokuamini hutangulia kuamini; ghadhabu hutangulia rehema; ndipomwishowe neema inashinda. Mtu ye yote hana jambo lo lote la kujisifia mbele zaMungu. Paulo anakaza kwamba Mungu apenda kurehemu.

11:33-36 Sifa Kuu kwa MunguBaada ya kutazama makusudi na mipango ya Mungu jinsi inavyotekelezwakatika historia ya ulimwengu Paulo alivutwa kumsifu na kumwabudu Mungu.Baada ya theologia ikafuata ibada. Aliona kuwa haki na rehema za Munguzimethibitishwa katika mwenendo wa historia kuanzia kwa Wayahudi kuteuliwandipo baada ya kuasi kwao WaMataifa kupandikizwa katika Mzeituni, kisha hatuaambayo bado haijatokea, Wayahudi kupandikizwa katika Mzeituni ule ule.Alikuwa ameonyesha kwamba dhambi na kutokuamini kwa Wayahudi na kwaWaMataifa kwageuzwa kuwa na matokeo mema.

Mungu amedhihirisha Uwezo mkuu na wingi wa hekima zake katika utekelezajiwa hatua zote za kuwapatia wanadamu wokovu halisi. Alikabili tatizo kuu ladhambi akafaulu kulitatua, ila kwa gharama kubwa ya kumtoa Mwana wake awedhabihu ya dhambi.

k.33 Paulo alimaliza sura ya nane na wimbo wa sifa kuu kwa upendo wa Mungu.Hapa mkazo ni juu ya hekima na maarifa ya Mungu. Tukumbuke Paulo alikuwaamesema juu ya „siri‟ aliyotaka Wakristo waifahamu, kwa hiyo, anaposema„hukumu zake hazichunguzuki, wala njia zake hazitafutikani‟ hakuwa na maanakwamba haiwezekani kufahamu makusudi ya Mungu ya kuokoa ulimwengu, ilahatutafikia kina wala mwisho wa hekima na maarifa yake. Kwa akili zetutwashindwa kuelewa kabisa njia zake, ila kwa moyo twamwamini na kujuakwamba Yeye ni wa kutegemewa kabisa kutimiza mapenzi yake. Hekimainaongoza kazi zake zote, hekima na maarifa yake ni kama „watumishi‟ warehemu zake za milele.

Page 166: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI828

k.34-35 Kwa maswali ya vifungu hivi twakiri kwamba Mungu amejaa uwezowote, hana haja ya kitu cho chote kutoka kwetu (Isa.40:13; Ayu.41:11). Yeye nitajiri mno, hamna cha kumpa, amejaa kila kitu chema.

k.36 Yeye ni asili ya vitu vyote, vyote vyaanzia Kwake, na kuendelea kwa uwezawake, na vitarejea Kwake ili Yeye apate kutukuzwa milele na milele (1 Kor.8:6).Wakati wote Paulo alikuwa na mzigo na wivu juu ya „utukufu wa Mungu‟ naalipotazama mpango mzima wa Mungu juu ya wokovu wa ulimwenguakashangaa akiona ya kwamba kwa kweli Mungu yuna Utukufu wote.

MASWALI1. Katika sura hizi tatu Paulo alizungumzia tatizo gani?2. Kwa nini neno hilo lilikuwa tatizo kwa Paulo?3. Katika sura hizo tatu Paulo alitoa mafundisho gani makubwa kumhusu

Mungu na madaraka yake? kuhusu taifa la Israeli na wajibu wake?kuhusu shabaha ya Mungu?

4. Kwa mfano wa kupandikizwa kwa matawi ya mzeituni Paulo alikuwaakifundisha nini juu ya mpango wa Mungu kihistoria kuhusu wokovu waWayahudi na WaMataifa?

5. Je! mtu aweza kudai kwamba Mungu hakumteua aokolewe?6. Mtu awezaje kuhakikisha wokovu wake?7. Ni sababu zipi zitakazomfanya mtu akataliwe?

12 - 15:13 MWENENDO WA KIKRISTO - KUISHI KWA MUNGU

Katika sura zilizotangulia Paulo alieleza kwa kina matendo makuu ya Mungu kwanjia ya Kristo. Hasa alifafanua jambo kuu la kuhesabiwa haki kwa imani namatokeo yake katika Mkristo kuwekwa huru na dhambi na sheria na mauti ili aishimaisha matakatifu. Baada ya kumaliza mafundisho hayo yote aliendelea kwakuonyesha jinsi mafundisho hayo yanavyomhusu Mkristo binafsi na maisha yakila siku, na maisha pamoja na Wakristo wenzake katika shirika zao, na maishaya kijamii na maisha kama raia wa nchi (13:1ku). Ndipo katika sura 14 aligusamambo ya kuhukumu na uhusiano kati ya Wakristo „dhaifu‟ na Wakristo „wenyenguvu‟.

Hapo nyuma alionyesha njia ya mtu kuletwa katika uhusiano mwema na Munguna kuendelea vema katika ushirikiano huo. Aliwapinga wale walioikejeri njia hiyoya kupata haki bure kwa imani na kusema kwamba itawafanya watu wasithaminijinsi waishivyo (Rum.6:lku). Katika sura hizo amekaza wajibu wa Mkristo kuishimaisha ya Kikristo ambayo msingi wake ni imani katika Kristo. Katika sura ya 6alionyesha kwamba mtu ambaye amemwamini Kristo ameunganika naye katikaKufa na Kufufuka Kwake, ameifia dhambi na kufufuka kwa shabaha yakumwishia Mungu. Kwa hiyo, iwapo sura hizo ni kama sehemu iliyo tofauti nasehemu zilizotangulia, sura zote za Waraka

Page 167: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 829

zinawiana na kutegemeana. Haki ya Mungu ipokelewayo kwa imani ya ndanibudi itokee nje katika maisha ya haki na maadili, ndiyo sababu Paulo alianzasura ya 12 na neno „basi‟ neno la kuunganisha yaliyotangulia na yanayokuja,kama daraja. Maadili ya Kikristo yana msingi katika mafundisho ya Kikristo.Mafundisho katika Biblia si ujuzi wa kichwa tu, bali ni ujuzi wa kutekelezwa katikamaisha (Yn.13:17; Efe.4:1; Kol.3:5). Imani inayookoa ni ile iwezayo na ipaswayokutendwa, na imani inayotendwa ndiyo ile inayookoa.

12:1-21 Itikio kwa rehema za Mungu ni kujitoa maisha yote12:1-2 Kuwa dhabihu haiPaulo alianza sehemu hiyo kwa kuwasihi Wakristo waliopo Rumi kwa upendo,akiwaita „ndugu zangu‟. (Efe.4:1; 1 Tim.2:1; 1 Kor.4:16). Msingi wa ombi lake nirehema za Mungu jinsi Mungu alivyomtuma Kristo awaokoe wenye dhambi wote,Wayahudi kwa WaMataifa, na kuwapa „haki yake‟ ipokelewayo kwa imani.

Ombi lake lilihusu miili yao na nia zao. Waitoe miili yao iwe dhabihu hai, yaaniwaitoe miili ambayo hapo nyuma waliitoa kwa dhambi sasa waitumie kwa haki.Paulo aligusa neno hilo alipozungumza nao habari ya kuunganika na Kristokatika Kufa na Kufufuka Kwake (6:11,13,19). Zamani katika dini zote watuwalizoea kutoa dhabihu mbalimbali na Wayahudi walifundishwa kutoa dhabihuza wanyama au ndege na kuwachinja. Sasa, tofauti ni kwamba wao wenyewewatakuwa „dhabihu‟ ila si za kuchinjwa, watakuwa „dhabihu hai‟ kwa kuwawamehesabiwa kuwa walikufa na kufufuka pamoja na Kristo, hivyo wako „hai‟.Dhabihu ni wao wenyewe. Katika imani na filosofia nyingi za siku zile „mwili‟ulidharauliwa na kuwazwa kuwa gereza la roho, lakini sivyo ilivyo katika Imani yaKikristo.

„dhabihu hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu‟ „dhabihu hai‟ yahusu kuishi kwaokila siku, maadam wapo hai. „takatifu‟ ina maana ya kujiweka wakfu kwa Mungu,yaani kuishi kwa ajili ya Mungu. „ya kumpendeza Mungu‟ yaani mtu apaswakuishi kwa jinsi Mungu amtakavyo si kwa jinsi anavyoamua mwenyewe, kwasababu mtu aweza kufanya mazuri ambayo hayalingani na mapenzi ya Munguwala hayafanywi kwa shabaha ya kumpendeza.

„ndiyo ibada yenu yenye maana‟ Tumezoea kuwaza „ibada‟ ni sala na ibada n.k.tunazofanya tunapokutana pamoja Kanisani, ila „ibada‟ ni zaidi ya hayo.Tunamwabudu Mungu kwa njia ya maisha ya kila siku tunapomstahi kwa uzurina ubora wa maisha yetu na kazi zetu. „yenye maana‟ ni haki tudaiwe kuishi kwakujitoa kama dhabihu hai, kwa kuwa Mungu alimtoa Kristo, Mwana wakempendwa, na Kristo alitoa maisha yake yote mpaka kufa kwa ajili yetu, hivyo nasisi nasi twapaswa kutoa maisha yetu. Tena, maisha yetu ya sasa yatakuwa namaana na kupata shabaha njema pamoja na matumaini mazuri kwa maisha yabaadaye.

Page 168: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI830

k.2 Pamoja na miili yao, nia zao pia zahusika katika jambo la kujitoa kamadhabihu hai. Kwanza waumini wapaswa kubadili kawaida zao za kuishi hapoduniani, ziwe tofauti na kawaida za watu wasioamini. Yabidi wasifuate kawaidaya kuthamini sana mali na fedha, na kufuata kwa nguvu mitindo mbalimbali k.m.mavazi, vyombo vya kisasa n.k. na kuishi kwa raha na anasa. Pia waangaliesana tabia zao, wajihadhari na majivuno, kiburi, kujipenda, kutumia mabavu,kujisukuma n.k. tabia ambazo wengi huona kuwa halali. Mambo kama hayohayana maana katika ulimwengu ujao, katika dahari mpya ambayo Mkristoamekwisha kuingizwa iwapo dahari ya zamani bado ingalipo. Dahari ya sasainapita pamoja na mambo yake (1 Yoh.2:17). Wageuzwe kwa kufanywa upya niazao, yaani wawaze tofauti, waishi kwa kupima mambo na kuamua yapi ni yamaana kwa kulinganisha na maisha ya Yesu na maisha ya baadaye. Watafutekwanza ufalme wa Mungu kwa sababu wamefanywa kuwa „raia wa Ufalme waMungu‟ (Flp.3:20). Ndipo watapata kuhakikishiwa mapenzi ya Mungu nakuwezeshwa kuyafanya kwa uwezo wa Roho waliyepewa, maana wamewajibikakuishi kwa Roho si kwa mwili (Rum.8:12:22). Kwa hiyo, wayawaze ndipowayafanye mapenzi ya Mungu, maana maadili ya Kikristo si fungu la amri namaagizo, bali ni kujitoa mwili, nafsi, nia, roho, yaani mtu mzima kwa kufanyamapenzi ya Yule aliyemwokoa kwa mapenzi makuu.

12:3-8 Karama za kiroho na jinsi ya kuziwaza na kuzitumiaKwanza Paulo alitaja neema aliyopewa, kwa hiyo, hayo aliyosema si maoni yakebali alisema kwa madaraka ya KiMitume.

Katika k.2 alisema Wakristo wageuzwe kwa kufanywa upya nia zao na katika k.3jambo la „nia‟ limetumiwa kuhusu matumizi ya karama za kiroho. Iwapo Pauloalikuwa akisema kwa waumini wote, neno lake lilimhusu kila mmoja wao.Kwanza, kila mtu aliambiwa asitamani makuu kupita ilivyompasa kutamani,kusudi asijione na kupatwa na dhambi ya kiburi. Ila pia, kila mtu alishauriwa „awena nia ya kiasi‟ maana yake asijidhili kupita kiasi na kujiona hafai. Kila mtuakumbuke kwamba ni mwenye dhambi aliyekombolewa kwa neema, kwa hiyo,kila mtu hana sababu ya kujithamini zaidi (1 Kor.4:7) hata hivyo kila mtuasiyedhili zaidi kwa sababu Kristo amekufa kwa ajili yake. Kujidhili nikutokuheshimu neema ya Mungu na kukosa kutumia karama aliyopewa naMungu. Kosa la kujiona ni katika kutaka kutawala mambo na kutokuwapawengine nafasi ya kuzitumia karama zao. Pia kwa kujidhili na kutokutumiakarama zao na wengine kunyimwa baraka za karama hizo. Maneno „kamaMungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani‟ yana maana gani?. Neno „kiasi‟linaleta wazo la wengine kuwa na imani nyingi na wengine kuwa na imani haba.Huenda si maana yake hasa, maana lengo la Paulo ni kuonyesha uwiano nakutegemeana katika jumuiya ya Kikristo. Pengine imani inayosemwa ni imani ilesafi mtu aliyo nayo anapomwamini Kristo kwa mara ya kwanza.

k.4 Tunapogeuzwa kwa kufanywa upya nia zetu twapata kujifahamu vizuri nakwa kushirikiana na waumini wenzetu ufahamu huo unapanuka. Wote

Page 169: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 831

waishiriki Imani moja ila kila moja huwa tofauti na wenzake kwa sababu yakarama za Mungu. Hivyo inatubidi kuwaza vizuri karama na tofauti zetu halitukikumbuka karama zote zimetolewa na Mungu, kwa shabaha ya kutumiwakatika jumuiya ya Kikristo kwa kutegemeana na kushirikiana. Hivyo twawekwahuru na mashindano ya kuona ni nani aliye bora au anamzidi mwenzake. Kwasababu tumewekwa huru na mashindano tumekuwa huru kwa kusaidiana. Mwiliwa kibinadamu ni mmoja wenye viungo mbalimbali na kila kiungo kina kazi yake.Vivyo hivyo, na Wakristo, hawawi mfano wa mwili tu bali ni Mwili, ni Kristoanayewafanya kuwa Mwili, ila Kanisa si sawa na Kristo Mwenyewe wala badalaya Kristo, ila Kanisa li ndani yake (1 Kor.12:12ku. Efe.4:16; Kol. 1:18).

k.6-8 Hapo Paulo ametoa orodha ya karama mbalimbali, si orodha kamili yakarama zote, ila ametaja baadhi (1 Kor.12:27-31; Efe.4:11ku). Baadhi ni uwezowa binafsi wa mtu aliyetiwa nguvu na Roho, nyingine ni uwezo wa kipekeealiopewa mtu baada ya kuamini, lakini zote zilitolewa kwa kusudi la kujenganasi kwa shabaha ya mtu kujifaidi binafsi. Vipawa vyatofautiana katika shabaha nakazi zake ila si katika thamani yao.

Karama ya kwanza iliyotajwa ni „unabii‟ „ikiwa unabii tutoe unabii kwa kadiri yaimani‟. Unabii ni nini hasa?ni kutoa ukweli wa Imani katika hali ya uvuvio wa Roho na kwa kuelewekavizuri. Ni chombo cha „ufunuo‟ wa mapenzi ya Mungu kuhusu hali zilizopo auzitakazokuwapo. Ni kutoa neno „hai‟ na kuleta „nuru‟ isiyo ya kawaida katikajambo fulani. Ni msaada kwa Kanisa kupewa uongozi wa namna hiyo (Mdo.13:1-2;20:27). kwa kadiri ya imani‟ ni vigumu kujua maana ya maneno hayo. Huendaina maana kwamba „unabii‟ unaotolewa inabidi upatane na kanuni za Imani nakupatana na Neno la Mungu. Au pengine maana yake nikwamba mwenye kutoa unabii atoe mpaka upeo wa imani yake. Siku zamwanzoni Kanisa liliwathamani sana manabii kwa kuwa walitoa uongozi pamojana kulinda Kanisa lisidanganyike.

Karama ya pili iliyotajwa ni „huduma‟ „ikiwa huduma, tuwemo katika hudumayetu‟. Yafikiriwa „huduma‟ ni kazi za matendo mema zilizofanywa na mashemasina watu waliowahudumia wengine kwa mahitaji yao ya kimwili, kazi za huruma.Iwapo hizo si „za kiroho‟ kama kuhubiri n.k. hata hivyo budi zithamaniwe najumuiya ya Kikristo, ni za maana sana. Wengine watakuwa wamepewa naMungu kipawa cha kufanya huduma hizo na kwa njia hiyo watapata nafasi yakumtumikia Mungu pamoja na wenzao. Linganisha na Matendo 6:1ku. mashartiyaliyohusu uchaguzi wa mashemasi wa kuwahudumia wajane yalikuwa „wawewatu wema, wenye kujawa na Roho na hekima‟.

Karama ya tatu iliyotajwa ni „kufundisha‟. „mwenye kufundisha, awemo katikakufundisha kwake‟. Tena twaona hao wanayo sehemu yao ya kutumia kipawachao. Hao wanafundisha kweli za Mungu kutokana na ujuzi walio nao kwa

Page 170: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI832

kuyachunguza Neno la Mungu. Wao hulinda kweli za Imani na kuzikabidhi kwawaumini wenzao, ili Wakristo wote wawe na ufahamu mzuri wa Imani yao. Kwanjia hiyo mafundisho ya Kanisa yahifadhiwa kizazi kwa kizazi.

Karama ya nne iliyotajwa ni „kuonya‟. „mwenye kuonya awemo katika kuonyakwake‟. Twaona „kuonya‟ ni wajibu wa wale waliopewa karama kwa kazi hiyo.Neno „kuonya‟ lina maana ya kufariji na kutia moyo, ambayo ni tabia ya RohoMtakatifu. Ni kusogea karibu na mtu na kuwa msaada kwake. (Yn.14:16).Kufundisha ni kuhusu ufahamu wa mtu, kuonya na kutia moyo ni kazi ya kugusadhamiri, moyo, na kujisikia kwa mtu.

Karama ya tano iliyotajwa ni „kukirimu‟ „mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe‟.Yahusu wale waliojaliwa karama ya kutoa „vitu‟ kwa wengine. Bila shaka haowaliwahudumia maskini, walioonewa na waliowekwa kando na jamii. Wafanyehuduma yao bila huzuni, wala masikitiko, wawe na moyo mweupe, wasiwe na niambili, wawe watu wanaopenda na kufurahia kutoa vitu vyao. Twajua katika sikuza kwanza za Kanisa Wakristo walijitahidi kushirikishana vitu wakiwahudumiawajane n.k. na kila muumini alitazamiwa awe na mzigo juu ya mwenzake.

Karama ya sita iliyotajwa ni „kusimamia‟ „mwenye kusimamia, kwa bidii‟. Wenginewaliwekwa kusimamia kazi na huduma mbalimbali. Wafanye kwa bidii, yaaniwawe tayari kujitoa kwa kutumia karama waliyojaliwa katika kusimamia vizurihuduma au kazi fulani, kama sivyo, wengine watalegea.

Karama ya saba iliyotajwa ni kurehemu „mwenye kurehemu, kwa furaha‟. Baadhiwalikuwa na kipawa cha kuwahudumia wengine, kama kuwatembeleawagonjwa, na kuonyesha fadhili za Kikristo kwa watu wenye shida n.k. Iliwapasawafanye kwa furaha.

Basi Wakristo wote waitwa kuonyesha fadhili na kuwa tayari kutoa mali zao nanafasi zao kwa wengine. Miongoni mwao walipewa kipawa cha kufanya hivyokama kumtumikia Kristo. Kwa hiyo, iwapo wote walikuwa na majukumu, baadhiyao walikuwa na jukumu la huduma hiyo.

12:9-21 Upendo ni msingi wa maisha ya KikristoPaulo alianza kwa kusema juu ya maisha yao ya pamoja katika shirika zao, nawao kwa wao. Aliweka pendo kuwa msingi wa maisha yote ya Kikristo, halafualiendelea kuonyesha jinsi upendo ufanyavyo kazi katika hali na uhusianombalimbali wa maisha. Maelezo hayo yafanana sana na mafundisho ya Yesukatika Hotuba ya Mlimani na ya Paul (1 Kor.13; Gal.5:22).

k.9 Alianza na tamko juu ya pendo „pendo na lisiwe na unafiki‟ (2 Kor.6:6; 1Pet.1:22). Maana yake liwe la kweli, na safi. Pendo ni zaidi ya kuona/kujisikia,akili na nia pamoja na maono yatakiwa ili pendo lifanane na pendo la Mungu

Page 171: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 833

lililoonyeshwa katika Yeye kuukomboa ulimwengu. Lipo „pendo‟ la ainambalimbali, lakini pendo la Mungu ni la kipekee na Wakristo waitwa kupendakama Yeye, maana wamepewa Roho Mtakatifu kwa kuwawezesha kuishi kwapendo (Rum.5:5,8).„lichukieni lililo ovu, mkaambatana na lililo jema‟. Mkristo wa kweli atachukia(neno la nguvu katika Kigriki) lililo ovu, hataridhiana nalo, atalikemea na kuliepa.Kinyume chake ataambatana (kama gundi, ndiyo maana ya neno katika Kigriki)na lililo jema, atalipenda sana. Ye yote asiyeuchukia uovu amepungua katikakuupenda utu wema. Kwa hiyo, mtu aliye na pendo la kweli ni mtu mwenyemsimamo juu ya uovu na utu wema.

k.10 Halafu Paulo alitaja „pendo la udugu‟ yaani pendo la Wakristowaliopokelewa katika familia ya Mungu. Kwa kawaida watu katika familia mojawaishi kwa kupendana na kushirikiana, iwapo sivyo ilivyo kwa kila familia. Ila nijambo muhimu kwa „familia ya Kikristo‟. Paulo alisema „mpendane ninyi kwaninyi‟ yaani wawe na moyo na juhudi wakijihesabu ni ndugu katika familia moja.Katika hali hiyo aliwaambia „kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu‟ maana yakemtu asijifikirie ni bora, kila mtu amwone Mkristo mwenzake kuwa kama ni KristoMwenyewe (Mt.25:31-46; Flp.2:3ku).

k.11 Ndipo walishauriwa wawe na bidii, wenye juhudi katika roho zao,wakimtumikia Bwana. Wakiwa na pendo la kweli bidii yao haitapungua,wataendelea kububujika katika roho zao kwa msaada wa Roho Mtakatifu, naowatafurahi kumtumikia Bwana. Bubujiko la kweli la Roho ni moyo wa kumtumikiaBwana, halibaki katika hali ya msimuko wa maneno tu (Mdo.18:25).

k.12 Hapo Paulo ameweka pamoja mambo matatu; tumaini, dhiki, na subira.Daima Mkristo huishi katika matazamio ya uzima wa milele na tumaini lakufanywa mwana na kuupata ukombozi wa mwili wake (8:23). Mkristo si mtuanayeishi kwa mipaka ya ulimwengu huu na katika yale yanayoonekana na yamuda tu. Matumaini yake yanamfanya afurahi wakati huo hata akipatwa na shidana mateso. Ndiyo sababu baada ya kutaja tumaini Paulo alitaja dhiki na haja yakusubiri, yaani kuvumilia. Ikiwa ulimwengu ulimchukia Kristo haikosi utamchukiamfuasi wake, hivyo Mkristo asiwaze ataishi bila shida (Mt.10:22; Yn.15:18;16:33; 2 Kor.4:17). Msaada wa kuvumilia utapatikana kwa maombi. Ni njia yakujaliwa neema na msaada wa Mungu ili mtu azidi kuwa mwaminifu wakati washida.

k.13 Katika shirika zao walikuwako waliopungukiwa na mahitaji ya lazima.Wengine walikosa kazi, pengine kwa sababu ya imani yao, wengine walitokakatika tabaka za chini n.k. Hivyo kila Mkristo aliwajibika kuwa na mzigo juu yawenzake walio na shida na kuwasaidia alivyoweza. Mkristo alipaswa kuzifurahianafasi hizo za kutoa msaada, asinung‟unike na kusikia kulemewa, afanye kwamoyo na kwa ukarimu. Bila shaka pale Rumi Wakristo walifikiwa na wageni wengina iliwabidi wawapokee vizuri. Kanisa halikuwa na majengo,

Page 172: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI834

walikutana katika nyumba zao kwa ibada n.k. kwa hiyo, waliitwa kuwakaribishawatu majumbani na kuwapokea na kuwahudumia kwa furaha. Kama zilikuwaponyumba/hoteli za wageni, mara nyingi zilikuwa mahali pa mabaya mengi, kamaukahaba na wizi n.k. (Mdo.2:43ku. 4:32ku. Yak.2:14ku. Ebr.13:1). Ndiyo sababukatika Nyaraka twaona neno la „ukaribishaji‟ limekazwa.

k.14-21 Katika sehemu hiyo Paulo aliwaza Wakristo na jinsi ya kuishi katikaulimwengu na kwa watu walio nje ya Kanisa wasiomwamini Kristo. Aliwaambia„wabarikini wanaowaudhi, barikini, wala msilaani‟ shauri ambalo Bwana YesuMwenyewe alilitoa katika Hotuba ya Mlimani (Mt.5:44). Wawe na itikio tofauti nalile ambalo wangalikuwa nalo kabla ya kuamini bila msaada wa Roho.Wamegeuzwa na kufanywa upya nia zao hivyo waweza kuitika kwa njia hiyo.Haina maana kwamba wakubaliane na matendo mabaya, lazima waichukiedhambi na kuyakemea matendo mabaya bila kuwalaani na kuwachukiawatendao mabaya. Wawe kama Stefano aliyemwomba Mungu asiwawekeedhambi hiyo (Mdo.7:60).

k.15 Aliwaambia Wakristo „wafurahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja naowaliao‟ yaani washirikiane na jirani zao katika furaha na huzuni zao. Yaonekanakuwa maneno mepesi ila si rahisi kuyatimiza kwa kuwa yampasa mtu asiwazeya kwake tu bali ajiweke mahali pa mwingine (1 Kor.12:26-27).

k.16 Hapo tena Paulo amerudia jambo la „nia‟ kwa sababu aliamini kabisakwamba matendo ya mtu huongozwa na mawazo yake. „Mpatane nia zenu ninyikwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambomanyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili‟. Mambo kama hayo Paulo alirudiakuyasema mara kwa mara kwa kuwa aliona ni hali muhimu katika jumuiya yaKikristo. Yawapasa waumini wawe na nia ya kudumisha umoja walio nao katikaKristo. Ilikuwa wajibu wa kila mmoja wao pamoja na kuwa wajibu wa shirika zimakuwa tayari kuyafanya mapenzi ya Mungu. Wajihadhari na kiburi na kujivuna nakujiona, hali zilizo hatari sana katika shirika zao. Dawa yake ni kuwa tayarikujishughulisha na mambo manyonge, kufanya kazi ndogondogo zisizo na sifana zisizoonekana wala kujulikana. Kwa kweli katika Kanisa ziko kazi nyingindogondogo za kufanywa, kazi hizo ni kama mafuta katika mashine, zikisaidiauenezi wa Injili na ushuhuda wa Kanisa. Mkristo asiwaze kwamba haimfai afanyekazi fulani ndogo kwa manufaa ya Wakristo wenzake. Zaidi Mkristo ajihusishe namaskini na wanyonge katika maonevu na shida wanazopata (Mt.25:40; Gal.2:10).

k.17 „Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote‟.Mara kwa mara Mkristo atatendewa vibaya na kwa kawaida mtu hutakakumrudishia mtu ubaya. Katika Agano la Kale fundisho lilikuwa „jino kwa jino najicho kwa jicho‟ na ilihesabiwa kuwa sheria njema kwa sababu ilimzuia mtuasizidi mpaka katika kumrudishia mwingine ubaya. Ilionekana ni haki kufanyahivyo na shabaha yake ilikuwa kuleta uwiano. Ila kwa Mkristo si vema afuate

Page 173: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 835

kanuni hiyo. Yeye asitafute kumrudishia mtu kulingana na alivyotendewa.Mkristo humkumbuka Kristo na kielelezo chake (1 Pet.2:20-24). „angalieni yaliyomema machoni pa watu wote‟ hatujui Paulo alikuwa na maana gani. KatikaKanisa si vema uwepo ubaguzi wa aina yo yote wa kugawa watu katika vikundi,na kujali watu fulani kuliko wengine. Mkristo apaswa kumpenda kila mtu bilaupendeleo (Mit.3:7; Mt.11:29; Yak.3:17). Mambo yake yawe dhahiri machoni pawote.

k.18 „Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote‟.Mkristo afanye juu chini kuishi kwa amani na watu wote. Yeye asiwe sababu auchanzo ya mashindano na ugomvi. Paulo alijua kwamba wako wenginewasiotaka amani, wachokozi na waleta fitina, kwa hiyo, itakuwa vigumu Mkristoaishi kwa amani na watu kama hao. Hii ndiyo sababu alitumia maneno „kamayamkini‟. Ila haina maana kwamba Mkristo aridhiane na maovu, si amani yanamna hii. Wala Mkristo asiache kufanya mapenzi ya Mungu kwa sababu italetafitina.

k.19-21 Katika sehemu hiyo yote Paulo anasema juu ya wajibu wa Mkristobinafsi, si juu ya mahakimu walio na wajibu wa kuhukumu. Kwa hiyo, Pauloanafundisha kwamba si juu ya mtu binafsi kujichukulia kazi ya kulipiza kisasi.Kazi hiyo ina Mungu peke yake, ni vema kumwachia Mungu aifanye. Katikautaratibu wa maisha ya wanadamu ziko kanuni za maadili na hizo zinafanya kazi(1:18). Haina maana kwamba twataka adui zetu wapatwa na kisasi cha Munguila twafahamu kwamba Mungu hawezi kuridhiana na maovu. Hasira na kisasichake ni tofauti na vyetu, ni rahisi sisi kuzidi mpaka, pia mara nyingi ipo hali yakujipenda (Yak.1:20).

k.20 Lakini ni jambo moja kutokumfanyia mtu ubaya kulingana na ubaya wakeila ni jambo jingine kumfanyia mema badala ya mabaya. Paulo ameeleza njia yakumtendea adui mema ni kumlisha akiwa na njaa, kumnywesha akiwa na kiu.„maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake‟ Maneno hayoyana maana gani? Ziko maana mbili. Moja ni kwamba mtu anapotendewa memana yule ambaye alimfanyia ubaya, huyo mtu atachomwa moyoni mwake nakutubu, mwishowe adui atageuzwa kuwa rafiki. Maana nyingine yatokana nadesturi iliyofuatwa katika nchi ya Misri wakati ule. Mkosaji alilazimishwakutembea wazi hadharani hali amebeba kichwani sahani yenye makaayawakayo moto. Huenda liko wazo la yule mtu kuaibika sasa ili asiadhibiwebaadaye. Mtu mmoja amesema „adui anatushinda anapotufanya kuwa kamayeye‟.

k.21 Paulo aliona ya kuwa kugeuzwa na kufanywa upya nia zetu kunasababishamabadiliko ya tabia na matendo ya mtu, ndipo, upendo unatawala maisha nauhusiano na wengine, rafiki kwa adui. Twafuata kielelezo cha Mungu Mwenyewekwa kuwa Yeye alituokoa tulipokuwa tungali adui (5:8)

Page 174: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI836

na Yeye huushinda uasi wote wa wanadamu kwa rehema zake, hivyo yatupasasisi nasi kuonyesha rehema kwa wapinzani na adui zetu (11:32).

MASWALI1. Wakristo wapaswa kufanya nini? na kwa sababu gani?2. Eleza maana ya „ibada‟ katika mawazo ya Paulo katika sehemu hiyo?3. Twamwabudu Mungu kwa njia gani?4. Wakristo huwa wamoja kwa njia gani na tofauti kila mmoja kwa njia gani?5. Ni tabia gani zilizokazwa na Paulo ili wategemeane?6. Ni nini msingi wa maisha ya Mkristo?7. Paulo alisema „pendo lisiwe na ..........‟ maana yake nini?8. Jadili katika vikundi: Ni kwa njia gani Wakristo waweza kuwasaidia jirani

zao kulingana na maisha ya kisasa

13:1-7 Mkristo na wajibu wake kwa serikali na wenye mamlakaNeno hilo lilikuwa muhimu sana kwa Wakristo walioishi Rumi na kwa Wakristowote, maana waliishi chini ya tawala dhalimu zilizotumia mabavu bila kujali hakiza kibinadamu. Wayahudi walichukia sana utawala wa kigeni, wakiamini kwambani Mungu tu aliye Mtawala wao na bila shaka Wakristo wa Kiyahudi walikuwa namawazo kama hayo na kujisikia vibaya walipojaribu kuwianisha wajibu wao kwaKristo na wajibu wao kwa serikali. Wayahudi walifukuzwa Rumi kama B.K.49wakati wa Kaisari Klaudio na inadhaniwa sababu ni fujo iliyotokea baina yaWakristo wa Kiyahudi na Wayahudi wasio Wakristo (Mdo.18:2).

Pamoja na hayo baadhi ya Wakristo walifuliza „uhuru‟ wao katika Kristo nakufikiri kwamba hawana haja ya kujiweka chini ya uongozi wo wote hasa ule waserikali. Waliuliza „kwa nini tuitii mamlaka ya dunia hii ikiwa sisi sio wa ulimwenguhuu?‟ (Yn.13:16) sisi „tu wageni na wapitaji tu‟ (Ebr.11:13) „uraia wetu ni ukombinguni‟ (Flp.3:20) „Kristo ameushinda ulimwengu‟ (Yn.16:33) hivyo hatunasababu ya kuwajali wenye mamlaka.

Ni vema kukumbuka kwamba Paulo aliandika mambo hayo kabla ya Kanisakupatwa na mateso makuu wakati wa Kaisari Nero (B.K.64) na Kaisari Domitiani(B.K.95). Katika Kitabu cha Ufunuo serikali imeonekana kuwa adui mkuu naYohana alitumia mifano ya wanyama wakali wenye vichwa vingi na pembe nyingikutoa picha ya serikali mbaya zinazowatesa Wakristo. Lakini hapo Pauloameandika kwa lugha tofauti sana.

Pengine alitaka kuwafahamisha Wakristo wa Rumi kwamba haji kwao kwashabaha ya kuamsha fitina na shida. Bila shaka walikuwa wamesikia kwambakila alipokwenda fujo ilitokea na huenda walitiwa wasiwasi walipofikiri juu yakufika kwake. Paulo mwenyewe aliufurahia uraia wake wa Kirumi ambaoulimsaidia mara kwa mara alipogongana na wakuu. Pia alijua kwamba Bwana

Page 175: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 837

Yesu Mwenyewe alihukumiwa kifo chini ya utawala mbaya. Hakufundishawafuasi wake kuipindua serikali, kinyume chake aliwafundisha kutoa kodi nakuwa watiifu kwa kiasi kile kilichowezekana bila kumwasi Mungu (Mt.22:15-22).Paulo alijua Wakristo ni kundi dogo wasio na nguvu ya kukabili uwezo mkuu waserikali. Ila hakutoa ushauri huo ili waepe shida, zaidi alitaka kuwafundishamahali pa serikali katika utawala mzima wa Mungu juu ya ulimwengu wote.

Sura ya 13 inasema juu ya mapenzi ya Mungu kuhusu uhusiano wa Mkristo nawenye mamlaka katika serikali na jamii za watu. Paulo alieleza hali bora kwawenye mamlaka na jinsi iwapasavyo kuhusu wajibu wao, ila alijuahaitawezekana wawe wakamilifu kabisa.

Mambo matatu katika mafundisho ya Paulo:k.1-2 Jambo la kwanza ni: Mamlaka yote yametoka kwa Mungu: Neno lake nikwa „kila mtu‟ kwa hiyo, ni wajibu wa kila mwamini kuitii mamlaka iliyo kuu naasiyeitii amemwasi, si mwenye mamlaka tu, hata na Mungu pia!! Kwa hiyo, kuitiimamlaka ni sehemu ya uaminifu wa Mkristo kwa Kristo. Ila si utii kwa lo lote lililokinyume cha mapenzi ya Mungu (Mdo.4:19,20; 5:29). Kwa hiyo, kuitii mamlakana kutokuitii mamlaka, yote mawili yamo katika kuwa mwaminifu kwa Kristo kwakupima kila jambo lilivyo. Ni wazi kwamba tuna deni la kuitii mamlaka piatunawajibika kuwaombea wakuu na wenye mamlaka (1 Tim.2:1ku).

Haki na uwezo wa mamlaka ya serikali na tawala mbalimbali zimetoka kwaMungu, ni vyombo vyake vya kutimiza mapenzi yake. Mungu ni mtawala mkuujuu ya mataifa yote, naye huinua na kuwakabidhi viongozi na watawala mamlakaya kushiriki sehemu ya utawala wake. Ni sehemu ya maana sana, naowamewekewa mipaka ili hawana haki ya kujiingize katika mambo yasiyowahusu.Hawakuwekwa wahusike na aina zote za dhambi, hasa waliwekwa kuzuia nakuhukumu matendo yote yaletayo fujo na kuvunja taratibu za kuishi kwa amanikatika jamii ya watu (2 Sam.12:7-8; Yer.27:5ku. Dan.2:21; 37ku. 4:17,25,32; 5:21). Katika k.2 Paulo alifundisha kwamba kuasi mamlaka kwaleta hukumu, sihukumu ya wenye mamlaka tu, hata hukumu ya Mungu, maana amri yao yakutoa hukumu wamepewa na Mungu.

k.3-4 Jambo la pili: Utawala umewekwa kwa kuuchochea na kuuendeleza utuwema na kuyazuia na kuyahukumu maovu.Wenye mamlaka wanapofanya kazi walizopewa ni „watumishi‟ wa haki ya Mungu(neno la haki ni neno kuu la Waraka). Mara mbili Paulo alitumia maneno„mtumishi wa Mungu‟ kusisitiza kwamba serikali zi ndani ya mpango wa Mungukatika kuuhifadhi usalama wa jamii. Ni juu ya serikali kuona kwamba watu wemawana nafasi nzuri ya kuishi maisha yao katika utulivu na amani, na kuchukuahatua juu ya wale wote watendao mabaya na kuleta fujo kati ya wenzao. Kwahiyo, watendao mabaya waogope kwa sababu wenye mamlaka huuchukuaupanga, maana yake, ni kazi yao kuadhibu makosa, hata kiasi cha

Page 176: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI838

kutoa adhabu ya kifo kwa dhambi kubwa kama uuaji. Upanga si dalili yamamlaka tu ila pia ni ishara ya haki ya kuutumia. Tuliona katika 12:19 Wakristowaliambiwa si kazi yao kulipiza kisasi. Hapo Paulo ameonyesha ni kazi ya walewaliopewa mamlaka nchini. Zipo hofu mbili, hofu ya kuogopa kufanya mabayakwa sababu ya adhabu itakayotolewa na hofu ya adhabu yenyewe.

k.4 „ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema‟. Mema hayo yameelezwakuwa „utulivu na amani katika utauwa wote na ustahivu‟ (1 Tim.2:2). Kwa hiyo,serikali ni kwa manufaa ya waumini pamoja na wengine ili waishi kwa utulivu haliwakiwa na nafasi za kufanya matendo mema kati ya jamii.

k.5-7 Jambo la tatu ni: Mamlaka ya serikali imekubalika na dhamiri ya Kikristo.Ni wajibu wa Mkristo kuitii mamlaka kwa ajili ya dhamiri kusudi dhamiriisimshtaki. Muumini anao utu mpya unaounga mkono utu mwema naunaokataa uovu basi inafuata kwamba Mkristo hatasikia shida kuhusu mamlakayaliyowekwa kwa shabaha hiyo ya kutoa nafasi kwa utu wema na kuuzuiauovu. Hivyo Mkristo atapenda kulipa kodi na ushuru, atawahesabia walewanaoshughulikia hayo kuwa wanamtumikia Mungu kwa kazi hiyo. Pauloaliendelea kwa kuonyesha kwamba Wakristo wapaswa kujali haki za watumbalimbali, kuwastahi na kuwaheshimu walio na vyeo na uongozi mbalimbali,si kwa ajili yao wenyewe tu ila zaidi kwa sababu wamewekwa na Munguwafanye mapenzi yake.

13:8-10 Deni la KupendaKatika k.7 Paulo alitaja jambo la „deni‟, Wakristo wawape wakuu mbalimbalihaki zao na katika k.8 wazo hilo linaendelea. Wakristo waishi bila madeni,yaani watimize wajibu wao kwa watu, wasiache kufanya yanayowapasawanapoishi kati ya watu na kati wa Wakristo wenzao. Hata hivyo, liko denimoja, ambalo hawawezi kuliepa, maana ni deni ambalo ni kiini cha imani yao,deni la kupenda. Deni hilo halitakwisha, na kwa kiasi wanacholilipa badohalijaisha. Kama mmoja alivyosema „twalipa kila siku, hata hivyo, badolingalipo‟.

Deni hilo ni kwa akina nani? tuwapende Wakristo wenzetu tu? au vipi? Katika k.8Paulo alitaja „ampendaye mwenzake‟ maneno hayo yaweza kuwahusu Wakristowenzetu. Halafu katika k.9,k.10 ametaja „jirani‟. Jirani atakuwa ye yotewanayekutana naye katika maisha, kazi na shughuli za kila siku. Hivyo Wakristowanalo deni la kuwapenda Wakristo wenzao katika Kanisa, na hasa kwa sababuwameunganika nao katika Kristo na kuwa Mwili Mmoja na kushirikiana kamafamilia ya Mungu. Pendo ni „gundi‟ ya kuwaunganisha (Yn.13:34-35).

Katika sura ya 12 Paulo alisema juu ya kujihusisha vema na adui zao. Kwa hiyo,pendo linalozungumzwa si lile la kawaida la watu kuwapenda jamaa.

Page 177: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 839

Pendo ni upande wa imani yetu unaoonekana katika uhusiano wetu na wenginena ni itikio letu kwao. Pendo lapenya ndani ya maneno ya Sheria na kuvifunuaviini vyake, na kuonyesha nia na shabaha ya Sheria ambayo inazidi yaliyotajwakatika maneno yake. Bwana Yesu alionyesha jambo hilo katika Hotuba yaMlimani (Mt.5: 17ku). Paulo alitaja amri kadha zenye makatazo. Katika kupendajirani nafasi haipo ya kumdhuru mwingine. Amri zinatufahamisha yaliyomo katika„pendo‟ ili pendo lisiwe wazo la hewani tu. Pendo ni utendaji wa sheria. „Utimilifuwa Sheria‟ maneno hayo yaonyesha sheria ni ya kutimizwa, na pendo ndilotimizo lake, pendo linaijaza, kwa hiyo, kufanya amri kwa ubaridi bila pendo niupungufu (Mk.12:28-34).

Hatuokolewi kwa sheria (ndiyo hoja ya Paulo tangu mwanzo wa Waraka) ilasheria ni mfereji wa kupitia wa maadili ya maisha mapya katika Kristo. Kwa hiyo,Paulo amejumlisha Sheria katika neno moja „pendo‟.

13:11-14 Umuhimu wa WakatiKatika sehemu hiyo Paulo ameukaza umuhimu wa Wakati, Ni muhimu kwasababu wakati wa sasa unapita, yaani dahari ya sasa inapita, inaelekea kwenyemwisho wake, ndipo dahari mpya ambayo imeishaingia itakamilika. Dahari mpyailianza Kristo alipokuja mara ya kwanza, nayo itakamilika atakaporudi. Pauloamekwisha kuwaelezea namna ya kuishi wakati huo, akisema wazi juu ya wajibuwao mbalimbali. Alianza Sura 12 na maneno „msiifuatishe namna ya dunia hii,bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu...‟ maana yake waishi maishakulingana na maisha yajayo, ya dahari mpya, wala wasiendelee kuishi maishayalinganayo na dunia ya sasa.

Ni vema wajue kwamba iwapo Kristo hajarudi, hakika atarudi. Limebaki jambomoja kubwa tu katika Kalendari ya Mungu, nalo ni Kurudi kwa Kristo, na jambohilo litatimizwa kwa wakati wake. Kwa hiyo, Wakristo wasiwaze „wakati‟ kamamaendeleo ya siku, mwezi, na mwaka tu, bali wauwaze kwa kutambua kwambadahari ya sasa imekwisha kuingiliwa na dahari mpya ya Kristo, na hiyo daharimpya itazidi kuwepo hadi Kristo atakaporudi na kuikamilisha. Katika sura ya 6waliambiwa walikufa pamoja na Kristo, na kuzikwa pamoja naye, na kufufukapamoja naye, basi waishi maisha kulingana na Kristo. Kwa sababu hiyo, ni hatarikulegea, inabidi wawe macho, wajiandae kwa Kuja kwa Kristo kwa kuvuamatendo yasiyofaa na kuvaa matendo yafaayo. Paulo alitumia mfano wa usikuna mchana kueleza dahari ya sasa na dahari ya baadaye. Inaonekana Wakristowalipenda kutumia maneno ya „giza na nuru‟, „usiku na mchana‟, huendayalitumika katika maandalio ya watakao kubatizwa. Kumvaa Kristo ni kuishikufuatana na tabia zake (Flp.2:5; 1 The.5:8; Kol.3:9,10; Efe.6:10) Wasiiachiedhambi nafasi yo yote.

Twaona umuhimu wa matendo yetu katika mwanga wa uzima wa milele. „Wakati‟ni wa maana sana kuhusu utendaji wetu wa kila siku. Mtu anapojenga nyumbampya haishughulikii nyumba yake ya zamani kwa kuipaka rangi n.k.

Page 178: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI840

kwa sababu anajua anakaa kwa muda mfupi ndani yake na ni hekima atumienguvu na nafasi zake katika kuandaa nyumba mpya. Ndivyo ilivyo kwa Mkristo.Hakika limebaki jambo moja kubwa, Kuja kwa Kristo, wakati wa sasahautaendelea bila kukoma (Ebr.9:28).

MASWALI1. Eleza uhusiano wa Mkristo na wajibu wake kwa serikali na wenye

mamlaka.2. Mkristo atafanyaje ikiwa watawala wake ni wabaya, apaswa kuwatii kwa

mambo gani na kutokuwatii kwa mambo gani?3. Kila Mkristo analo „deni‟ gani na „deni‟ maana yake nini?4. Kwa sababu wakati wa sasa unapita, Je!, Paulo alitoa ushauri gani kwa

Wakristo?

14:1-15:13 ‘Wenye nguvu na walio dhaifu wa imani’Katika sehemu hiyo Paulo anawashauri Wakristo jinsi ya kuishi pamoja wenyenguvu wa imani na walio dhaifu wa imani katika shirika zao pale Rumi.

14:1-12 Alionyesha kwamba hali ya dharau waliyokuwa nayo wenye nguvu nahali ya kuhukumu waliyokuwa nayo walio dhaifu zilihatarisha umoja wao. 14:13-23 Alionyesha kwamba wajibu wa kumtunza Mkristo mwenzake ni jambomuhimu linalotangulia haki za mtu mwenyewe.15:1-13 Alitumia kielelezo cha Kristo cha kutumika na kutokujipenda kuwamfano wa mwenendo bora kwa Wakristo.

Inaonekana matatizo kadha yalikuwepo katika Kanisa la pale Rumi, na Pauloalipata habari zake kwa sababu alifahamu Wakristo wengi wa pale (Rum.16) ilahakutoboa wazi matatizo yenyewe yalikuwa nini lakini alidokezea mambo yavyakula (14:2-3) kunywa divai (14:21) na kuadhimisha siku kadha, huendasabato na sikukuu na kufunga n.k.(14:5-6).

Huenda „udhaifu‟ wa „walio dhaifu‟ ulikuwa wa aina mbalimbali, maana Wakristowalitoka katika mataifa, mazingira, na mapokeo mbalimbali. Ila baadhi yawataalamu wafikiri walio dhaifu hasa walikuwa Wakristo wa Kiyahudiwalioendelea kushika maagizo ya Torati kuhusu vyakula na sabato. Wakristo waKiMataifa hawakuona shida kuhusu mambo hayo kwa sababu hawakuyazoeakatika maisha yao.

Katika 1 Kor.8: na 10:23-33 Paulo alisemea jambo la kula vitu vilivyotolewasadaka kwa sanamu, jambo lililowagawa Wakristo maana wengine walikula kwauhuru wakisema sanamu si kitu na wengine waliacha kula kwa sababuwalikumbuka uhusiano kati ya vitu vile na sanamu na miungu yake. Wayahudiwalipata shida sana kwa sababu tangu awali walifuata Amri ya Mungu iliyosema„usiwe na miungu mingine ila Mimi, usijifanyie sanamu ya kuchonga‟

Page 179: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 841

(Kum.5:7,8). Tena, kuhusu wanyama Wayahudi walikuwa na desturi yao yauchinjaji. Hayo yote yaliwaletea shida.Katika Waraka kwa Warumi na kwa Wakorintho mashauri ya Paulo yalifanana,hakuwa mkali, aliruhusu pande zote mbili kuendelea jinsi walivyoamuawenyewe. Ila katika Waraka kwa Wagalatia na kwa Wakolosai alitoa mashaurimakali sana, taz. Gal.4:10, Kol.2:16-24. Kwa nini alitoa mashauri tofauti? Ni kwasababu jambo lililozungumziwa lilikuwa tofauti. Katika makanisa hayowalikuwepo watu waliotaka kulazimisha waumini wa KiMataifa kutahariwa nakushika maagizo ya Torati ili "wakamilishe" wokovu wao, mafundisho yaliyokinyume kabisa cha kuhesabiwa haki kwa imani. Paulo akawapinga sana maanaaliona hii ni „Injili nyingine‟ (Gal.1:6).

Watu wengi wamefikiri Paulo alikuwa akisemea walio dhaifu wa imani ni baadhiya Wayahudi kwa sababu alipomaliza alitaja Wakristo wa Kiyahudi na Wakristowa KiMataifa (15:8). Pengine shida ilitokea hasa baada ya Wayahudi kurudiRumi. Walifukuzwa B.K.49 na kwa kuondoka kwao Wakristo wa KiMataifawalipata nafasi ya kuendeleza uhuru wao kwa kutokujali mambo ya Kiyahudi,ndipo Wakristo wenzao wa Kiyahudi waliporudi walikuta „hewa‟ ya Kanisaimebadilika na harufu ya Kiyahudi imepungua. Huenda baadhi yaohawakupenda hiyo hali. Ni mawazo tu, hatujui ndivyo ilivyokuwa.

14:1-6 Ushauri wa PauloPaulo alianza na neno kwa „wenye nguvu wa imani‟. Aliwaambia wawakaribishewalio dhaifu wa imani (huenda walikuwa wachache). Hao hawakukosa imani aukuwa na imani ndogo ila walikuwa bado hawajachunguza yaliyomo katika imaniyao kuhusu miiko fulani. Katika mambo ya lazima ya Imani hawakuwa na shida,mambo yanayozungumzwa si ya msingi wala „dhambi‟ bali ni miiko na mapokeoya hapo nyuma. Bado hawajawa na ujasiri wa kuacha mambo kadhaa ambayohayakuwa na maana yakilinganishwa na mambo makuu ya Imani. Hasa udhaifuulionekana katika kukosa nguvu ya kukata shauri juu ya mambo fulani.

Halafu Paulo aliendelea kuonyesha ni kwa hali gani wamkaribishe yule wa imanidhaifu. Kwanza wamkaribishe kama ndugu wa kweli katika Kristo (1 Kor.8:11)kwa mikono miwili, bila wasiwasi, kwa upendo wa Kikristo. Ila wasimkaribishekwa kusudi la kujadiliana naye juu ya maoni yake. Kumpokea aliye dhaifu nikumpokea Kristo maana ni Kristo anayetukaribia katika hao walio dhaifu nawaliodharauliwa. Msingi wa ushauri wa Paulo ni „ujuzi huleta majivuno baliupendo hujenga‟ (1 Kor.8:1). Ni vema tukumbuke neno hilo.

k.2-4 Chakula anachokula mtu si neno kubwa likilinganishwa na makosa yawatu wa kila upande. Hatari kwa mwenye nguvu ni kiburi na kumdharau yuleambaye hasikii uhuru wa kula vitu fulani. Hatari kwa aliye dhaifu wa imani nikumhukumu yule ambaye athubutu kula cho chote bila wasiwasi. Paulo alikuwa„mwenye nguvu‟ (15:1) alikuwa na uhuru wa ajabu sana katika Kristo, uhuru wa

Page 180: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI842

kufanya au kutokufanya mambo fulani kufuatana na jinsi alivyosikia amewiwaupendo wa kuwajenga watu katika imani zao. Kauli ya wale wenye nguvu ilikuwasahihi, na waliokuwa na imani dhaifu walikuwa wamepungua, ila kukata shaurikwa upande mmoja si dawa ya kutatua tatizo; tatizo hasa ni ukosefu wa upendopande zote mbili. Aliye dhaifu ameambiwa asimhukumu „alaye‟ kwa sababuMungu amemkubali, halafu katika k.4 alirudia kusema naye kwa kuuliza swali„wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? kwa bwana wakemwenyewe yeye husimama au kuanguka‟. Mtumwa hutoa hesabu kwa bwanawake si kwa mtumwa mwenzake. Kitu kikubwa ni aonavyo Mungu, kila Mkristoutiifu wake ni kwa Kristo. Ni wenye nguvu ambao wamesemwa kuwa na „kibali‟,kibali cha kufuata uhuru wa kutokujali desturi na miiko kadhaa (Gal.5:1). Waliodhaifu wamekubalika na Mungu na kuhesabiwa haki kwa imani yao katika Kristobila kujali udhaifu wao kuhusu miiko. Ni vema kuona kwamba nguvu ya „wenyenguvu‟ haitoki kwao wenyewe bali kwa Bwana anayewawezesha kuwa imara nahodari.

k.5-6 Tofauti zipo katika mambo madogomadogo, hata hivyo, siyo kusemakwamba hizo tofauti hazina maana yo yote. Kila hali na kila jambo ni nafasi kwaimani. Kwanza kila mtu ajihakikishie mwenyewe kilicho sawa kwake ili asijeakasikia kushtakiwa na dhamiri yake. Afanye kwa kumkabidhi Bwana mamboyake na kumshukuru, ila hawezi kufanya hivyo akiwa na mashaka (1 Tim.4:4- 5).Watu wa pande zote wadaiwa kuwa watiifu kwa Kristo. Hakuna kulazimisha wotewafanane, kila mmoja atoe jibu la dhamiri safi mbele za Mungu. Kwa hiyo, jambokubwa linalotawala mambo hayo ni shabaha yetu ya kumwishia Bwana iwapowengine wataendelea na desturi kadha ambazo Kristo hakuziamuru. Wote niwatumishi wa Bwana nao wanamtegemea Yeye. Twajumlisha kwa kusema:Umoja katika mambo ya lazima ya Imani yetu; Kuchukuana na tofauti katikamambo yasiyo lazima, na kuwa na hekima ya kutambua yapi ni lazima na yapiyasiyo lazima. Kisha shukrani kwa Mungu katika yote.

14:7-12 Kuishi kwa BwanaKatika sehemu hiyo Paulo ametaja jambo muhimu sana litakalowaongozaWakristo katika maisha yao. Kila Mkristo anaishi maisha yake „kwa Bwana‟. Tumali yake kwa sababu Yeye alitukomboa pale Msalabani, tu watumishi wakekatika maisha tunayoishi sasa katika nguvu za Kufufuka Kwake. Kifo chetuhakitabadili au kuuvunja uhusiano wetu naye. Kwa hiyo, ni juu ya kila Mkristokupata kibali cha Bwana kwa yale anayofanya.

k.9 Kristo alikufa na kufufuka kusudi awe Bwana juu ya watu wake. Tu mali yakekwa sababu alitukomboa (1 Kor.6:20). Katika hali ya kuwa Mungu Mwana anao„ubwana‟ juu ya wanadamu wote, ila kwa kuwa ni Mkombozi ana „ubwana‟ hasajuu ya wote ambao Baba amemkabidhi.

k.10-12 Hapo Paulo amerudia kusema moja kwa moja na wenye imani dhaifuna walio na nguvu ya imani ila hakusema kwa upole kama alivyosema katika

Page 181: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 843

k.3. Ni kama aliwakemea pande zote mbili kwa sababu wote waliwakoseaWakristo wenzao. Kwa makusudi alimwuliza aliye dhaifu wa imani „wewe je!mbona wamhukumu ndugu yako?‟ ndipo alimwuliza aliye na nguvu ya imani„wewe je! mbona wamdharau ndugu yako?‟. Hivyo alikaza wajibu wa kila mmojakwa kutumia neno „wewe‟ pia alikaza uhusiano wao kwa kutumia neno „ndugu‟na kwa neno hilo aliwakumbusha wajibu wao wa kupendana. Neno kubwa sikama wana hekima au siyo, wala jambo la dhamiri zao (1 Kor.4:4) bali ni Munguatakayemhukumu kila mmoja wao na kila mmoja atatoa habari za jinsialivyotenda, kwa hiyo, ni kazi bure pia ni ujinga kumhukumu au kumdharaumwingine.(2 Kor.5:10; Isa.45:23; Flp.2:10). Vema kila Mkristo ajipime mwenyewena kutia maanani matendo yake.

Hatuna mamlaka ya kuwalazimisha wengine, kila mmoja amewajibika kumfuataBwana kadiri anavyofahamu mapenzi yake. Ni juu ya kila Mkristo kuamuamwenyewe atakavyofanya hali amepata kibali cha Bwana kwa yale anayotenda.

14: 13-23 Uhuru na WajibuKatika sehemu hiyo yote Paulo bado angali akisema kwa wenye nguvu nawalio dhaifu wa imani. Wenye nguvu wanayo haki ya kuwa huru, ila pia wanaowajibu, na Paulo alitaka kuwaonyesha uwiano uliopo kati ya uhuru, upendo, naimani. Wenye nguvu ya imani wanao uhuru wa kutokuadhimisha siku fulani nakutokula chakula fulani, ila hawana uhuru wa kuwakwaza wengine, kwa sababuwakiwakwaza wameenenda kinyume cha upendo.

Wale walio dhaifu wa imani waliona ni sawa waiadhimishe siku fulani na kulachakula fulani ili dhamiri zao zisiwashtaki. Wakishawishiwa kuacha kufanyahivyo kwa kuwaiga wenzao, basi hao watakuwa wanafanya kinyume cha imaniyao na dhamiri zao.

Iliyopo ni kwamba wa kila upande wanapohukumiana wanavunja utaratibu wauumbaji, pengine bila kutambua, wakijaribu kuwafanya wengine wawe „katikamfano wao‟ si „mfano wa Mungu‟.

Paulo aliona kwamba kiini cha mambo hayo ni kutumia uhuru kwa njia halali,uhuru hupaswa kuwa mtumishi wa upendo, ili uhuru usiwe neno la mwisho walanjia ya kumletea mwingine hasara.

Uhuru wa Kikristo ni jambo kubwa, ila liko jambo jingine lililo kubwa zaidi, nalo niupendo, na Paulo alijenga maadili ya Kikristo katika msingi wa upendo (1Kor.8:1). Kwa hiyo, swali lililo mbele ya Mkristo SI „Je! Nina uhuru wa kufanyahivi?‟ bali NI „Je! Katika mwanga wa upendo ninawajibika nini?

k.13ku. Katika vifungu hivi inaonekana Paulo alikuwa akisema kwa wenyenguvu wa imani, ila maneno „tusizidi kuhukumiana‟ ni kwa pande zote mbili.

Page 182: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI844

k.13b ni kwa wenye nguvu. Wao wapaswa kukata shauri la kutokufanya lo lotelitakalowakwaza hata pengine kuwaangusha wenzao walio dhaifu wa imani(Mt.7:1-5; 17:27). Wa imani dhaifu watawezaje kukwazwa na kuangushwa?(a) kwa kumwona Mkristo mwingine akifanya jambo fulani ambalo katika mawazoyake (iwapo si mawazo sawa) yeye anahesabu ni kosa, na kufanya dhamiri yakelaini iumizwe (b) kwa kufuata mfano wa yule mwingine na kutenda vile vile, iwapoanasikia mashaka na dhamiri inamshtaki.

k.14 Paulo mwenyewe alijua kwa hakika kwamba hamna kitu cho chote kilichonajisi kwa asili yake, ila chahesabiwa kuwa safi au najisi kutokana na mawazo yamtu (Mt.7:15-23; Mdo.10:9ku. 1 Tim.4:4; 1 Kor.8:4,7; Tit.1:15). Bwana Yesualifundisha hivyo, na yeye mwenyewe alijua jambo hilo kutokana na ushirikianowake kiroho na Bwana Yesu. Maisha yote ni neema ya Mungu kwa hiyo, ni burekugawa maeneo fulani kuwa matakatifu na mengine kuwa ya kawaida tu. Ilaalifahamu kwamba si wote waliotambua hivyo. Kila kitu si safi kwa kila mtu.

k.15 Alimwambia mmoja mmoja kuanzia kwa mwenye nguvu „umeachakwenda.. kwa chakula chako usimharibu mtu yule..‟ Kumhuzunisha mwingine nikuacha upendo na kuthamini uhuru tu. Kumvuta mwingine afanye kinyume chadhamiri yake ni kumharibu, lugha ya nguvu sana ya kuonyesha uzito wa jambohilo. Halafu Paulo aliingiza jambo jingine, Kifo cha Kristo, katika habari hii ya„kula‟ ili atilie mkazo umuhimu wa mambo hayo. Mwenye nguvu alikumbushwakwamba aliye dhaifu wa imani ni mtu ambaye Kristo amempenda upeo, kiasi chakumfia Msalabani, ishara ya wingi wa upendo wa Kristo kwa hao walio dhaifu waimani. Mwenye nguvu wa imani amempenda dhaifu wa imani kidogo mnojapokuwa ameshindwa kuacha kula chakula fulani au kuadhimisha siku fulani?Tena ni Kristo aliyewaunganisha kuwa ndugu alipokufa kwa ajili ya wenye nguvuna walio dhaifu wa imani. Tena Kristo aliwafia wote wawili walipokuwa „hawananguvu‟ (5:6,8).

k.16 Iliwabidi wale wenye nguvu wasikubali „wema wao‟ yaani uhuru wao,kunenwa vibaya, kwa sababu ni jambo zuri kuwa huru. Kwa hiyo, wasiutumiekwa kuwaumiza baadhi ya Wakristo wenzao na kuwa sababu ya wenginekuilaumu Injili.

k.17-19 Paulo alitaja „ufalme wa Mungu‟ kwa kuwa Wakristo ni washiriki waufalme huo, wako chini ya utawala wa Mungu wakiwa na wajibu wa kufanyamapenzi ya Mungu. Katika ufalme huo mambo ya kula na kunywa nakuadhimisha siku kadha ni mambo madogo. Yaliyo makuu katika Ufalme waMungu ni haki, amani, na furaha katika Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, Wakristohuwa na wajibu wa kutenda yaliyo sawa na yale yanayoleta amani na furaha katiyao, ambayo ni matunda ya Roho. Twamtumikia Kristo katika mambo hayo nakupata kibali cha watu, na kumpendeza Mungu. Shabaha ni kujengana na kuishikwa amani. Ufalme wa Mungu usifanywe kuwa mambo ya kula na kunywa (1Tim.3:7; 6:1).

Page 183: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 845

k.20 Mungu anafanya kazi hata kwa walio dhaifu wa imani. Bila shaka wenyenguvu walijaribiwa kuwaza kwamba Mungu hakufanya kazi kwa bidii katika waledhaifu.

k.21 Ni juu ya wenye nguvu kuwapenda walio dhaifu hata kiasi cha kuacha kulachakula fulani na kuacha kunywa divai n.k. Sababu ni kwamba wenye nguvuwaweza kutoa nafasi katika imani yao kwa kupenda walio dhaifu kwa njia hiyobila kuidhuru imani yao. Lakini sivyo ilivyo kwa walio dhaifu. Hao hawawezi kutoanafasi katika imani yao kwa kuyaiga mambo yanayofanyiwa na wenye nguvu,kufanya hivyo kutaidhuru imani yao. Imani inayozungumzwa ni ule ushirikianousioonekana kati ya mtu na Mungu, yaani hali ya kuamini na kumtegemea.

k.22 Wenye nguvu wasijionyeshe kwa imani yao kwa kujivunia uhuru wao nanguvu yao ya kutokubanwa na mapokeo fulani. Wanayo heri ya kuwa huru, hatahivyo uheri huo hauondoi wajibu wao wa kujitawala na kutulia mbele za Munguna kuwa radhi kuacha kutumia uhuru wao.

k.23 Walio dhaifu wa imani wana hatari ya kula chakula fulani hali ya kuwa ndaniyao hawasikii uhakika kwamba ni sawa wafanye hivyo, ndipo kwa kufanya hivyodhamiri zao zawashtaki kuwa na hatia na kwa sababu hiyo wametenda dhambi.Kubadili utendaji wa jambo fulani bila kuwa na hakika juu yake ni kufanyadhambi. Tukumbuke ya kuwa mambo yaliyozungumzwa katika sehemu hiyo simambo yaliyo muhimu kwa wokovu.

MASWALI1. Je! Mkristo anao uhuru wa kufanya aonavyo vema mwenyewe bila

kuwajali Wakristo wenzake? Eleza.2. Twapaswa kumkaribisha kila Mkristo, hata kama ana matatizo, kwa

namna gani?3. Ni wajibu wetu kuishi na kuamua mambo mbele za............ hali tukiwa na

tahadhari juu ya wenzetu.4. Tumewekwa huru ila si uhuru wa?...........................5. Kristo alitoa kielelezo gani?.............................6. Ufalme wa Mungu unahusu mambo gani?.......................7. Hivyo usishushwe kuhusu mambo yapi?.......................

15:1-13 Kielelezo cha KristoPaulo bado angali akisema neno kwa wenye nguvu na walio dhaifu wa imanihasa akilenga Wakristo katika sharika za pale Rumi k.2,5,7,13. Paulo alijihesabukuwa miongoni mwa wenye nguvu (k.1) na kuona uhuru katika Kristo ni baraka.Ila kama alivyosema hapo nyuma katika sura 14 aliendelea kusisitiza kwambawalipaswa „kuuchukua udhaifu wa wasio na nguvu‟ maana yake wasiutumieuhuru wao kwa kuwakwaza‟. Alitumia neno „haitupasi‟

Page 184: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI846

kuonyesha kwamba wamewajibika wasijipende wenyewe, pia „kila mmojaampende jirani yake‟ kwa kufuata kielelezo cha Bwana Yesu k.2,3. Kristo alitoamaisha yake kwa ajili ya walio dhaifu na wanyonge, hata akakubali kulaumiwana kudharauliwa kwa jinsi alivyoshirikiana nao. Kama Kristo alifanya hivyo nijambo dogo kwa wenye nguvu kujinyima uhuru wao kwa kusudi la kushirikianavema na wenzao.

k.4-6 Ndipo Paulo alitaja habari za Maandiko Matakatifu, Agano la Kale. Yeyealiona kwamba shabaha ya Maandiko ni kuwafundisha watu hata waumini waleo. Si habari za kale tu. Maandiko yatawaelekeza kuwa na saburi na faraja iliwawe watu wa matumaini, wakitazamia matimizo ya imani yao katika uzima wamilele. Katika k.5 Paulo alimtaja Mungu kuwa „Mungu mwenye saburi na faraja‟ndiyo sababu watajifunza mambo hayo kutoka katika Maandiko kwa sababu niNeno lililotoka kwa Mungu.Hasa lengo ni umoja, wapate kunia mamoja katika msingi wa imani yao katikaKristo. Umoja wao usiwe hafifu, wala si umoja wa kupakana mafuta nakuridhiana tu. Kwa sababu ya tabia zake, Mungu huamsha tumaini ndani yetu,na umoja wetu ni kipawa cha kutoka Kwake.

k.7-12 Kama alivyoanza katika 14:1 Paulo alirudia kusema juu ya kukaribishana,kila mmoja wa kila upande ampokee mwenzake kama Yesu alivyomkaribisha kilammoja Kwake (14:3). Kwa njia hiyo watamtukuza Mungu. Tena Munguamewakaribisha Wayahudi na WaMataifa na kuwapokea katika Yesu Kristo. Wakwanza kupokelewa walikuwa Wayahudi, Kristo alikuwa mhudumu wa agano lakutahiriwa kwao, kwa sababu Mungu alitoa ahadi kwa mababa zao. Piaaliwakumbusha kwamba WaMataifa pia walishiriki ahadi hizo tangu mwanzo, sikama waliingizwa baadaye. Kihistoria waliingia baadaye, ila katika makusudi yaMungu walikuwemo tangu mwanzo. Inaonekana shida ilikuwepo pale Rumi katiya Wakristo wa Kiyahudi na wa KiMataifa. Ilibidi wazishinde hali zote za ubaguzi,maana katika ukombozi wote ni sawa.

Alitilia mkazo juu ya WaMataifa kuwemo katika mpango wa Mungu kwa kuingizadondoo kutoka Agano la Kale, pia alionyesha ni jambo la sifa na furaha. k.9b„nitakushukuru kati ya Mataifa‟ „nitaliimbia jina lako‟ k.10 „furahini Mataifa pamojana watu wake‟ k.11 „msifuni, mhimidini‟.

k.13 Paulo alifunga hoja ya sehemu hiyo akiomba baraka kwa „Mungu watumaini‟. Alitaka Mungu awajaze furaha na amani ili wazidi kuwa na tumaini kwanjia ya Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yao, wakifuata mashauri ya Paulo yakila mmoja kuwa na mzigo juu ya wenzake.

15:14-21 Mambo ya binafsiKama alivyofanya alipoanza Waraka aliwasifu tena (1:8ku). Pengine alfikiriwengine watauliza, kwa nini anatuandikia na yeye hakulipanda Kanisa letu?

Page 185: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 847

Tena kwa sababu yeye mwenyewe alisema kwamba si desturi yake kujenga juuya msingi wa mtu mwingine (k.20). Huenda aliwaza kwamba wenginehawatapendezwa na yeye kusema nao juu ya mambo mengine kama lile jambola wenye nguvu na walio dhaifu wa imani. Je! alifikiri wamepungukiwa kiroho auvipi? Kwa hiyo, Paulo alijieleza kwa adabu na kwa upole.

k.14 Alitumia lugha laini akiwaita „ndugu zangu‟ na aliwasifu kuwa watu waliojaawema, na kujazwa elimu, wenye uwezo wa kuonyana. Walikuwa wema nakuonyesha fadhili, wanyofu, watu wazima wa imani waliofahamu imani yao namaisha waliyodaiwa, vile vile waliweza kusaidiana. Kwa hiyo, kama Pauloameongea na wenye nguvu na walio dhaifu, (bila shaka walikuwapo au Pauloasingaliwataja) inaonekana hawakuwa na tatizo kubwa.

k.15 Paulo alionyesha ujasiri katika kuwaandikia, ujasiri uliotokana na kuitwa nakutumwa na Mungu kuwahubiri WaMataifa Injili. Kwanza alisema aliandika kwashabaha ya kuwakumbusha, pia kwa sababu aliona kwamba neema aliyopewana Mungu ilimruhusu aseme nao ili aitimize sehemu hiyo ya utume wake (1:5;11:13; 12:3) bila neema hiyo asingalithubutu kusema nao.

k.16 Alifunua mawazo yake kuhusu utume wake. Aliona amewekwa kuwamhudumu wa Yesu Kristo ili WaMataifa wapate kumwamini na kumtii, kwa hiyo,alijifananisha na Kuhani aliyetoa sadaka, ila sadaka yake kwa Mungu siwanyama bali ni watu, ni WaMataifa, ambao wametakaswa kwa kupewa RohoMtakatifu (Mdo.15:8ku). Ni sadaka iliyokubalika maana hata sadaka za kalezilitakiwa kuwa kamili na safi. Adui zake katika Wayahudi wasingaliwezakupokea mawazo kama hayo kwa sababu waliona WaMataifa wasiotahiriwa ni„wanajisi‟ (Mdo.10:14,15,28; Ling. na Isa. 66:18,20). Lugha ni ya ibada(taz.12:1-2).

k.17-20 Ilikuwa dhahiri kwamba utume wake ulikuwa umefanikiwa, ishara yayeye kuwa Mtume wa kweli aliyetumwa na Kristo. Yeye mwenyewe hakujiingizakatika huduma wala mwenyewe hakuwa asili ya uwezo uliosababisha WaMataifakuipokea Injili. Alikuwa na sababu za kuona fahari kwa kazi alizozitenda ila alijuahakika ni Yesu hasa aliyezifanya, hivyo sifa zina Yesu si yeye. Roho Mtakatifualimjalia kufanya ishara na maajabu zilizouthibitisha ujumbe aliohuburi. Yeyealikuwa mtumishi, si Bwana, katika hayo yote. Aliona fahari juu ya yale Kristoaliyoyafanya kwa njia yake. Mkazo ni utendaji wa Kristo kwa njia ya yeye kufanyauinjilisti.

Aliona aliitwa kuihubiri Injili mahali ambapo watu walikuwa bado hawajaisikia.Alitaja „tangu Yerusalemu....mpaka Iliriko..‟ (Iliriko ni Serbia, Croatia, Albania sikuhizi). Hatuna habari kamili juu ya uinjilisti katika Iliriko, lakini inawezekanaalikwenda pale alipokuwa Akaya na Makedonia, au ni „mpaka kwenye mipakayake‟. Ila tusifikiri Paulo alidai kwamba amewahubiri wote wa sehemu alizotaja,maana haikuwezekana kwa mtu mmoja kufanya hayo yote, ila kwa kusema

Page 186: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI848

„tangu Yerusalemu mpaka Iliriko‟ alionyesha eneo kubwa ambalo ndani yake Injiliimekwisha kuhubiriwa. Kwa desturi alifikia miji na kuyapanda makanisa humohalafu aliwaachia waumini waliopatikana kueneza Injili katika vijiji vyakandokando (1 Kor.3:10; 2 Kor.10:15,16; Efe.2:20). Kwa mpango huu eneokubwa liliguswa na wengine waliachiwa nafasi mahali penginepo ili usitokeeuvutano kati yao. Hata Injili ilipohubiriwa katika sehemu nyingine za Afrikaviongozi wa madhehebu walikubaliana waende sehemu tofauti, isije maeneofulani yakawa na watumishi wengi na maeneo mengine yalikosa watumishi.

k.21 Katika habari hiyo Paulo aliona neno la nabii Isaya limetimia (Isa.52:15).

15:22-33 Mipango ya Paulok.22 Kwa sababu hapo nyuma ameshikwa kabisa na shughuli za kuhubiri Injilialikuwa ameshindwa kuwafikia pale Rumi, iwapo alitamani sana kuwaona.

k.23 „sina wasaa tena pande hizi‟ maneno hayo hayana maana kwamba kazizote za Injili zimekwisha kufanywa sehemu ya mashariki ya Dola ila ina maanakwamba makanisa yamepandwa na kusimama imara na wengine wapo wakuendeleza shughuli za Injili katika maeneo hayo. Pengine Paulo aliwazakwamba Kristo hatakawia kurudi (ndivyo walivyowaza Wakristo wengi wakatihuo) kwa hiyo, alisikia wajibu wa kwenda mbali zaidi kabla ya Kuja Kwake.

k.24 Basi, aelekee wapi? mashariki zaidi? au magharibi zaidi? hata mbele yaRumi mpaka Gaul na Spania? ambayo pia ni majimbo ya Kirumi. Alifikiriatakwenda Spania, mahali pa barabara nzuri za kuunganisha wilaya zake nakurahisisha usafiri. Pia lugha ya KiLatini ilitumika. Spania iliingizwa katika Dolamiaka mia mbili na nusu iliyopita, na MaKaisari kama Trajan, Hadrian,Theodosius walitoka Spania pamoja na wanafalsafa mashuhuri Senaca nawengine.

Pia aliona Wakristo wa Rumi wataweza kuubeba mzigo na kumsaidia katikauinjistili huo kama watu wa Antiokia wa Shamu na Efeso walivyofanya haponyuma maana haitawezekana hao wamsaidie atakapokwenda mbali nao. Kwahiyo, akifika kwao, na kukaa nao kwa muda, na kuburudika kwa kushirikiana nao,na wote kufaidiwa kiroho (1:11-12) watapata kumfahamu.

k.25-28 Ila kabla ya hayo yote kufanyika Paulo alikuwa na mzigo wa kurudiYerusalemu, pamoja na wajumbe wa makanisa ya Makedonia, Akaya, AsiaNdogo, (Mdo.20:4) wakichukua mchango uliofanyika na makanisa kwa ajili yandugu zao, Wakristo wa Kiyahudi, waliokuwa katika hali ya umaskini. Mchangohuo ulitawala mawazo ya Paulo (1 Kor.16:1ku. 2 Kor.1ku. 9:1,12). Aliona kwanjia ya mchango huo Wakristo wa KiMataifa watakuwa kama wanalipa deni laokwa wenzao (hakutaka wajione kuwa wazuri) maana Ukristo ulizaliwa katika diniya Kiyahudi, ukatoka katika shina hilo, hivyo wakirudisha kitu cha kimwiliwataonyesha shukrani zao kwa kitu cha kiroho, yaani Injili, walichopata kwao.

Page 187: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 849

Pia shabaha ya Paulo ilikuwa kujenga ushirikiano mzuri kati ya waumini wote nakuondoa mashaka, hasa ya waumini wa Kiyahudi. Hata alitumia lugha ya ibada;„ila sasa ninakwenda Yerusalemu, nikiwahudumu watakatifu‟ mchango ulikuwasehemu ya hudumu yake na tendo la neema. Kwa nini walikuwa maskini? Hatujuisababu yake ila twajua Paulo na Barnaba walipeleka msaada kwao maranyingine kabla ya wakati huo (Mdo.11:27-30) Twajua Wakristo wa Yerusalemumwanzoni waliuza mali zao, mali ambazo zingalikuwa akiba na kinga wakati washida (Mdo.2:44-45; 4:32-5:11). Waliongozwa na upendo na kufanya kwa hiarina furaha.

k.29 Paulo hakujua kwa hakika kwamba atafika kwao, ila akijaliwa kufika atakujana baraka za Mungu, yaani mipango yake yote ilitegemea mapenzi ya Mungu.

k.30-33 Aliwasihi wajiunge naye katika kumwomba Mungu kwa ajili yake, kwasababu bila neema na uwezo wa Mungu yeye mwenyewe hakuwa na nguvu.Alitaja mambo matatu hasa ambayo alihitaji msaada wa Mungu.(i) Aokolewe na wasioamini katika Uyahudi, maana walikuwapo watu ambaowalimkataa Yesu na walimchukia Paulo kwa sababu ya juhudi zake katikakumtangaza Kristo, walimwona kuwa nguzo katika uenezi wa Injili.(ii) Alitaka waombe kwamba ule mchango upate kibali cha waumini waYerusalemu, maana kama ukikataliwa litakuwa pigo kubwa, na kinyume chaushirikiano wapaswao Wakristo wote. Paulo alijua wako watu pale Yerusalemuwalio na mashaka juu yake nao wangelitafsiri vibaya tendo hilo jema. Ripoti zauongo zilienezwa juu yake (Mdo.21:17-20).(iii) Alitaka waombe kwamba awafikie katika hali ya furaha, pia apatekupumzika kwao kwa muda. Atakapofika atafurahi kwa sababu atakuwaameokolewa na adui zake pale Yerusalemu, na ya kuwa matumaini ya kuwaonayamefanikiwa.

Twajua mambo hayakutokea kama alivyokusudia. Kweli alifika Rumi, ila katikahali ya kuwa mfungwa akakaa pale katika hali hiyo kwa miaka miwili akingojeauamuzi wa Kaisari juu ya kesi yake. Hatujui kwa uhakika ilitokea nini baada yamiaka miwili kama alifunguliwa au siyo. Katika Nyaraka nyingine ziko habarizinazotuelekeza kufikiri kwamba alifunguliwa na kurudi sehemu za mashariki.Katika Andiko lake, Klementi wa Rumi (B.K.95) aliandika kwamba „Paulo alikuwamtangazaji katika pande za mwisho za magharibi, .... alifundisha haki katikaulimwengu wote na alipofika kwenye mwisho wa mipaka ya magharibi alitoaushuhuda mbele ya watawala‟. Je! mwisho wa magharibi ni wapi? yawezekanani Spania? Ni vigumu kufikiri ni Rumi, maana Klementi alikuwa Rumi alipoandikaandiko hilo.Katika andiko liitwalo „Muratorian Canon‟ lililoandikwa Rumi, kuna maneno hayo„Paulo aliendelea kutoka Jiji la Rumi mpaka Spania‟.

Page 188: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI850

Iliyopo ni kwamba ombi lake la kufika Rumi lilijibiwa, ila si kwa njia aliyotazamia(Mdo.22:17 mpaka 28:31 ina habari za mambo yaliyompata pale Yerusalemu nanjiani kwenda Rumi).

k.33 Alifunga sehemu hiyo juu ya mipango yake kwa baraka ya kuwatakia woteamani kutoka Mungu wa amani.

MASWALI:1. Paulo alikuwa wapi alipouandika Waraka huu?.............. Mpango

wake ulikuwa kwenda wapi?.................ili afanyenini…………….na baada ya hapo aende .............. halafuBaadaye aende wapi? ………….. na kufanya nini?…………….

2. Alifikiri Wakristo wa pale Rumi watamsaidiaje?

16:1-16 Salaam za Paulo kwa Wakristo kadha wa kadhaSehemu hiyo ina salaam za Paul kwa watu mbalimbali katika shirika za Kikristopale Rumi, ambao alikuwa amewahi kukutana nao mahali mahali, na wengineamepata habari zao kutoka kwa watu waliowafahamu. Rumi, Jiji kuu la Dola yaKirumi, lilifikiwa na watu wengi, watu wa kabila nyingi walikwenda na kutoka pale,ama kwa shughuli za binafsi, za kazi, au za biashara. Wengine walikuwa watalii.Barabara nzuri ziliunganisha Jiji na majimbo ya Dola na kurahisisha usafiri, piajeshi lililinda mipaka ya Dola na kuihifadhi amani, na lugha ya Kiyunani ilitumikasana mfano wa lugha ya Kiswahili katika Afrika ya Mashariki siku hizi.

Karibu theluthi ya majina yaliyotajwa ni ya wanawake, dalili ya kuonyesha jinsiwanawake walivyothaminiwa na kupewa nafasi katika Kanisa. Paulo aliwasifukwa msaada wao katika shughuli za Injili.

k.1-2 Wa kwanza kutajwa ni Fibi, mwanamke mmoja aliyekuwa akienda Rumi,ila hatujui sababu za kwenda. Imefikiriwa ni yeye aliyeubeba Waraka huo mpakaRumi (siku zile hakuna posta kama leo). Hivyo Paulo alimtambulisha kwao.Kwanza, alimwita „ndugu yetu‟ yaani Mkristo mwenzetu, pili alisema „aliyemhudumu wa Kanisa lililoko Kenkrea‟. Kenkrea ilikuwa bandari ya kaskazini yaKorintho, na yeye alikuwa mmoja wa shirika hiyo. Paulo alikuwa na maana ganialipomwita „mhudumu‟? Je! alikuwa na cheo au uongozi pale? au ni lugha yakuonyesha kwamba alikuwa na juhudi katika kufanya shughuli za Kanisa. Nenohilo si wazi kwa sababu siku za mwanzoni jambo la „vyeo‟ halikuwekwa wazikama jinsi ilivyo siku hizi. Alikuwa MMtaifa kufuatana na jina lake la Kiyunani(jina la mungu mke wa mwezi). Paulo aliwaomba wampokee „katika Bwana‟maana yake wampokee kama Mkristo mwenzao, „kama iwapasavyo watakatifu‟yaani wampokee vizuri kama ilivyo wajibu wao wa Kikristo. Tena wawe tayarikumsaidia kwa jambo lo lote atakalohitaji. Ndipo Paulo alitoa sifa yake kwambahapo nyuma amewasaidia watu wengi pamoja

Page 189: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 851

na kumsaidia yeye pia. Hatujui ni msaada gani aliotoa kwa watu, penginealikuwa mkarimu wa kupokea watu nyumbani mwake (kama Lidia alivyofanyapale Filipi Mdo.16:15). Huenda Paulo alikuwa ametunzwa naye. Pengine katikakuhudumia watu aliwatembelea wajane na wagonjwa na kuwafadhili maskinipengine kutoka mfuko wa ndugu. Labda alikuwa tajiri au mtu aliyejulikana katikajamii, ila hatujui kwa uhakika.

k.3-5 Ndipo Paulo alitaja mume na mke (Akila na Priska) ambao alikuwaamewahi kukutana nao hapo nyuma. Alipofika Korintho kwa mara ya kwanza,hao nao walikuwa wamefika pale kutoka Rumi, hali wamefukuzwa wakati waKaisaria Klaudio (Mdo.18:18,19,26). Halafu baadaye alikutana nao tena Korintho(1 Kor.16:19) halafu wakarudi Rumi na baadaye aliwakuta Efeso (2 Tim.4:19).Kwa hiyo, ni watu waliofika sehemu mbalimbali na kujulikana na Wakristo wengi.

Akila alikuwa Myahudi kutoka jimbo la Ponto. Wengine hufikiri Priska ambayeameitwa Prisila (Mdo.18:3) pia alikuwa Myahudi ila wengine wanafikiri alikuwaMrumi kufuatana na jina lake. Walifanya kazi ya kushona mahema, kama Paulo,ndiyo sababu mojawapo ya Paulo kukutana nao na kuishi nao pale Korintho(Mdo.18:3ku). Mara nyingi Priska ametangulia kutajwa, labda alikuwa mama wanguvu nyingi. Wote wawili walimtumikia Kristo kwa moyo na bidii, hata Apoloalipofika Efeso walimkaribisha na kumwelimisha katika habari za Kristo kwausahihi zaidi, na alipokwenda katika Kanisa la Korintho, Wakristo waliandikiwawampokee vizuri (Mdo.18:26ku). Walitoa nafasi katika nyumba yao kwaWakristo kukutana kwa ibada na mikutano maana Kanisa bado halikuwa namajengo (1 Kor.16:19; Kol. 4:15; Flm.2).

Paulo alitaja kwamba walikuwa tayari kuhatarisha maisha yao kwa ajili yake,neno ambalo hatuna habari zake, ila waumini katika makanisa walifahamu habarihiyo, na wao pamoja na Paulo walijiunga katika kuwashukuru. Pengine ni wakatiwa fujo zilizotokea mjini Efeso. Paulo alizoea kupata shida na mateso.

k.5b Epaineto: Huyu mtu ametajwa hapo tu katika Agano Jipya, kwa jina nimwanaume MMtaifa. Paulo alimwita „mpenzi wangu‟ „aliye malimbuko ya Asiakwa Kristo‟ maana yake alikuwa miongoni mwa waumini wa kwanza kabisakatika Jimbo la Asia. Bila shaka ndiyo sababu Paulo alifurahi kumwita „mpenzi‟akimkumbuka sana kwa jinsi alivyoitika wito wa kumwamini Kristo, bila kukawia,alipohubiri Injili katika Jimbo la Asia.

k.6 Halafu alimtaja mwanamke jina lake Mariamu, (wako wengi walioitwa jinahilo). Inaonekana ametumika vizuri sana katika Kanisa la pale Rumi, kwa sababuPaulo alitumia maneno „alijitaabisha sana kwa ajili yenu‟, huenda alikuwammojawapo wa kwanza katika shirika hiyo. Yawezekana Paulo alipata habarizake kutoka kwa Priska na Akila waliokuwa washiriki wa Kanisa la pale kabla yakufukuzwa B.K.49.

Page 190: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI852

k.7 Androniko na Yunia wameitwa „jamaa zangu‟ maana yake walikuwa Wakristowa Kiyahudi, huenda walikuwa wa jamaa ya Paulo, ila hatujui kwa uhakika. Je!Yunia alikuwa mwanamke, na ikiwa ni hivyo, Je! alikuwa mke wake au dadayake? Wengine wafikiri ni mwanamke kwa sababu jina hilo limeonekana katikamaandishi ya Kiyunani mara 25O na mara zote ni mwanamke. Yafikiriwawalikuwa Wayahudi wa Kiyunani, kama wale waliotajwa katika Matendo 6, kamaakina Stefano na Filipo, na tunajua watu kama hao walianzisha Kanisa paleAntiokia ya Shamu (Mdo. 11:20). Paulo alisema walimwamini Kristo kabla yakekwa hiyo, walikuwa miongoni mwa Wakristo wa kwanza kabisa. Liko wazokwamba walikuwa baadhi ya watu waliokuwapo siku ya Pentekoste (Mdo.2:10)ambao waliporudi Rumi walianzisha Kanisa pengine pamoja na wengine. Pauloamesema „ambao ni maarufu miongoni mwa mitume‟. Paulo alitumia neno„mtume‟ mara chache. Kwanza neno lahusu wale kumi na wawili waliochaguliwana Bwana Yesu. Halafu wachache wengine wameitwa hivyo: Paulo na Barnaba(Mdo:14:14). Katika 1 Kor.15:5-7 alitaja „wale Thenashara‟ ndipo mbele „Mitumewote‟ kama ni wengine tofauti na wale Thenashara. Katika 2 Kor.8:23 wajumbewa makanisa wameitwa „mitume‟ na Epafradito ameitwa hivyo (Flp.2:25).Twafikiri kwamba hao walipewa „utume‟ wa kufanya uinjilisti na Kanisa. Je!Androniko na Yunia walimwona Kristo baada ya Kufufuka Kwake, maana hiiilikuwa sharti moja kuhusu Mtume?. Halafu neno jingine lililotajwa na Paulo„waliofungwa pamoja nami‟. Twajua Paulo alitiwa ndani mara nyingi (2 Kor.6:5;11:23). Walifungwa pamoja naye lini na wapi? hatujui. Labda kufungwa kwaokuna maana ya kushikwa sana na shughuli za Injili.

k.8 Ampliato, ambaye Paulo amemwita „mpenzi wangu katika Bwana‟. Jina hilolimeonekana katika pango la kuzikia watu, Pango la Domitilla, chini ya barabaraza Jiji, ambalo lilitumiwa katika karne ya kwanza. Jina hilo lilipendwa nawatumwa wa Kirumi.

k.9 Urbano tena ni jina la KiLatin lililopendwa na watumwa. Kwa jina hilo huyoamedhaniwa kuwa alizaliwa na kulelewa katika Jiji la Rumi. „mtenda kazi pamojanami katika Kristo‟ maana yake alikuwa amemtumikia Kristo katika maisha yake,huenda haina maana kwamba alikuwa amefanya kazi pamoja na Paulmwenyewe. Stakiski, mpenzi wangu, ni jina la Kiyunani, jina lililotumika nawatumwa. Paulo alimpenda sana, bila shaka kwa sababu Stakisti alimpendaYesu na kumtumikia vizuri.

k.10 Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo: si wazi kama alikuwa Myahudiau Myunani, ila kwa jinsi alivyomtaja Paulo alimhesabu kuwa Mkristo wa kweli,aliyeonyesha ukweli wa imani kwa maisha yake. Nisalimieni na watu wanyumbani mwa Aristobulo. Huenda Aristobulo mwenyewe alikuwa amefarikidunia au hakuwa Mkristo, ila katika nyumba yake walikuwako WaKristo.Wataalamu kadha wafikiri huyo Aristobulo ni mjukuu wa Herode wa kwanza na

Page 191: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 853

ndugu wa Herode Agripa wa kwanza aliyeishi Rumi akawa rafiki wa KaisariKlaudia.

k.11 Herodioni, jamaa yangu, maana yake ni Myahudi mwenzake, na penginealikuwa na uhusiano na Aristobulo, maana jina lake laelekeza mtu kuwazakwamba alitoka katika jamii ya MaHerode, pia kwa sababu ametajwa marabaada ya kumtaja Aristobulo. „Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Narkiso, waliokatika Bwana‟ pengine Narkiso alikuwa amefariki dunia. Adhaniwa kuwa waziritajiri aliyeuawa wakati wa Kaisari Nero. Huenda watumwa wake walichukuliwana jamii ya Kaisari na kuingizwa katika nyumba yake, na baadhi yaowalimwamini Kristo.

k.12 Trifiana na Trifosa, ni wanawake ambao pengine walikuwa mapacha, kwasababu kawaida ya siku zile ilikuwa kwa sehemu ya kwanza ya majina yamapacha kufanana. Sifa yao ni walikuwa „wenye bidii katika Bwana‟. HuendaPaulo ameambiwa habari zao.

k.12b Persisi, tena ni mwanamke, ama ni jina la Kiyunani au Kiajemi, huendaalikuwa mtumwa au mtumwa aliyewekwa huru. Paulo alimwita, „mpenzialiyejitahidi sana katika Bwana‟ kwa hiyo, sifa yake ni kuhusu jinsi alivyomtumikiaYesu kwa bidii.

k.13 „Nisalimieni Rufo, mteule katika Bwana, na mamaye, aliye mama yangupia‟. Rufo amejulikana kama mtu aliyefanya jambo fulani kipekee, kiasi chakuitwa „mteule‟. Wengi humfikiri kuwa mwana wa Simoni, Mkirene, aliyeubebamsalaba wa Kristo (Mko.15:21). Paulo amemwita mkewe Simoni mama yake, sikwamba alikuwa mama hasa, ila wakati fulani alimtunza Paulo kama mama. Niwakati gani? kweli hatujui wala hatuambiwi. Ila twajua Kanisa la pale Antiokia yaShamu lilianzishwa na watu wa Kipro na Kirene (Mdo.11:20). Wakati waBarnaba kumleta Paulo mpaka Antiokia (Mdo.11:25) Je! alimtunza Paulo? KatikaMdo.13:1 Simoni ametajwa, Je! huyo ni yule aliyeubeba msalaba wa Kristo?Kweli hatujui, ni mawazo tu.

k.14 Hapo Paulo ameweka watu watano, pamoja na ndugu walio pamoja nao.Ni kundi la waumini, ambao hatupewi habari nyingine juu yao, pengine walikuwawatumwa au watumwa waliowekwa huru.

k.15 Hapo tena Paulo amejumlisha watu kadha kwa pamoja. Huenda Yulia nimkewe Filologo. Hapo yawezekana walikuwa watumwa au watumwawaliowekwa huru. Tena walitajwa pamoja na „watakatifu wote walio pamoja nao‟.

k.16 Busu takatifu limetajwa katika 1 Kor.16:20; 2 Kor.13:12; 1 The.5:26 naPetro ametaja busu la upendo (1 Pet. 5:14). Mara nyingi ilitumika katika ibada.

Page 192: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI854

Busu ilikuwa kawaida ya kuamkiana katika nchi za mashariki, limeitwa „busutakatifu‟ si busu la kuamsha tamaa za kimwili.

Ndipo Paulo alitoa salaam za makanisa yote ya Kristo, yaani kuwasalimia kwaniaba ya Kanisa zima la upande wa mashariki. Amefikia kikomo cha hudumayake katika maeneo ya mashariki na mawazo yake ni kuendelea na hudumakatika maeneo ya magharibi, hivyo aliona vema ayaunganishe makanisa yasehemu zile za huduma yake katika salaam zake kwa Kanisa la Jiji kuu la Dola.

Tunapochunguza hiyo orodha ya majina ya watu waliosalimiwa na Paulo, nenokubwa ni kuona utofauti wa watu waliotajwa, theluthi moja ilikuwa wanawake,dalili ya Kanisa kuwa limewakaribisha kabisa na kuwathamini sana. Pia wako watabaka mbalimbali, wale wa vyeo pamoja na watumwa, pamoja na „akina yahe‟.Tena kwa kabila walikuwa Wayahudi, WaMataifa, Wayunani, WaRoma, n.k.Walithaminiwa kama watu, si kwa ajili ya cheo, au kabila, au jinsia yao (Gal.3:28).Hawakuwa nyuso au majina tu bali walikuwa watu, kila mtu na nafsi yake na sifayake, tazama lugha ya Paulo „wapenzi, na jamaa, waliofungwa pamoja nami,waliokubaliwa katika Bwana, waliofanya kazi kwa bidii, wateule‟. Kila mmojaalipata umuhimu wake kutokana na uhusiano wake na Kristo na bidii zakekuhusu Injili na maisha yake ya Kikristo.

Mtume Petro hakutajwa, kwa hiyo, inaonekana hakuwepo Rumi wakati ule waWaraka kuandikwa.

Waraka haukuwa „baridi‟ kama hati ya theologia, bali uliandikwa kwa watumbalimbali, mchanganyiko wa waumini katika makanisa. Uliandikwa kwashabaha ya kuwaelimisha katika Imani na Maisha ya Kikristo.

16:17-20 Onyo juu ya watu kadhaaMara baada ya salaam hizo zilizojaa upendo alibadili sauti yake ghafula. Mpakahapa katika Waraka hajathubutu kusema kwa nguvu, maana alifahamu yeyehakulianzisha Kanisa pale, kwa hiyo, si vema ajichukulie mamlaka. Hata hivyo,kama Mtume wa Yesu Kristo, aliona amewajibika kama mchungaji wa kutunzakondoo wa Bwana kusema nao juu ya hatari fulani iliyowakabili.

Ni vigumu kujua watu waliosemwa walikuwa akina nani maana hakusemawametoka nje au vipi. Alisema hao ni watu wa fitina na watu waletao vikwazombele za watu wanyofu. Kwa tabia walikuwa wadanganyifu, wakitumia manenolaini ili wanase usikivu wa waumini wasio werevu. Pengine walikuwa waumini waKiyahudi, wale waliorudi Rumi baada ya kufukuzwa wakati wa Kaisari Klaudio,waliojaribu kuwalazimisha waumini wa KiMataifa kuzishika desturi za Kiyahudikuhusu miiko ya chakula n.k. Labda ni waumini wa KiMataifa waliojivunia uhuruwao na kufundisha kwamba wanao uhuru wa kufanya lo lote, maana Kristoamewaweka huru, mwili si kitu, roho ndiyo kitu cha maana (Flp. 3:19). Nikwamba hao watu walijaribu kutikisa imani na kuyapotosha

Page 193: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 855

mafundisho waliyopewa Wakristo na wale waliowaletea Injili. Paulo alieleza haliyao kwa ukali, alisema kwamba hawakuwa watumishi wa kweli wa Kristo, baliwalijitumikia na kutafuta faida yao wakijipendekeza tu.

k.19 Paulo alishuhudia kwamba Wakristo wa Rumi wamejulikana sana kwa utiiwao na sifa yao imeenea sana. Aliwashauri wajiepushe na hao watu, waendeleekutenda mema na kuacha mabaya (Mt.10:16).

k.20 Aliwapa faraja na kuwatia moyo kwamba, Mungu ambaye ni Mungu waamani (15:33) tofauti na wale waletao fitina, atawapa ushindi, na Shetani aliyeasili ya udanganyifu na fitina atasetwa chini yao, bila kukawia (2 Kor.11:13-15).Ndipo akamaliza kwa baraka ya neema kama alivyofanya mara nyingi katikanyaraka zake.

16:21-24 Salaam za watu waliokuwa pamoja na PauloKisha Paulo aliingiza salaam za watu waliokuwa pamoja naye pale Korinthowakati wa kuandika. Wa kwanza kutajwa ni Timotheo, mtu aliyejulikana sanakuwa mfanya kazi pamoja na Paulo. Halafu alitaja watatu, Lukio, Yasoni, naSosipatro aliyewaita „jamaa zangu‟ kwa hiyo, wafikiriwa kuwa waumini waKiyahudi. Hatuna uhakika wa hao kuwa nani hasa. Katika Mdo.13:1 Lukio fulaniametajwa, Mkirene aliyekuwa Antiokia wakati wa Paulo. Halafu Paulo alikaa namtu aliyeitwa Yasoni pale Thesalonike alipofika kwa mara ya kwanza(Mdo.17:5-9) halafu Sosipatro fulani ametajwa katika Mdo.20:4, alikuwa mtu waBeroya. Hayo yote ni mawazo tu, maana katika siku zile hadi siku zetu watuwana majina yanayofanana.

k.22 Tertio alichukua kalamu tena ila atoe salaam zake. Yeye alikuwa mkalimanialiyemsaidia Paulo katika kuuandika Waraka. Bila shaka alifurahi kujiunga nayekatika Waraka huo mstadi.

k.23 Paulo aliendelea kwa kumtaja yule aliyemkaribisha nyumbani mwake iliakae naye, jina lake Gayo. Aliongeza maneno „na wa Kanisa lote pia awasalimu‟.Huenda Wakristo walizoea kukutana katika nyumba yake, au ni maneno yakuonyesha kwamba watu wengi walizoea kufika pale na kukaribishwa naye.Erasto alikuwa wakili wa mji, mtu wa cheo, ambaye pia alikuwa Mkristo NdipoKwarto ametajwa, Paulo alimwita „ndugu yetu‟ hatujui maana yake katikakumtaja hivyo, yeye pia ni Mkristo wa pale.k.24 Baraka hii Paulo amekwisha kuitumia katika k.20b. Katika nakala zazamani maneno hayo hayapo.

16:25-27 Sifa Kuu kwa MunguMwishowe kabisa Paulo aliufunga Waraka na Wimbo wa Sifa kuu kwa Mungu.Alistaajabishwa na mambo makuu aliyoongozwa kuandika kuhusu mipangomizima ya Mungu kuwaletea watu wote wokovu, Wayahudi kwa WaMataifa,

Page 194: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI856

wokovu kwa njia ya Yesu Kristo. Mipango hiyo ilianza kwenye umileleuliotangulia, katika nia na makusudi ya Mungu ya kuwaokoa walimwengu wote.Jambo hilo lilifichwa zamani za kale ila sasa limefunuliwa kwa Kuja Kwake Kristo,na sasa wote waitwa kumwamini na kumtii Kristo.

k.25 Paulo alimsifu Mungu kwa uwezo wake wa kuwategemeza waumini iliwapate kusimama imara, wasidanganywe na mafundisho yaliyo kinyume chaInjili ya kweli, wala wasiishi wala kuridhiana na hali na maisha ya mazingira yao(1:11; Efe.3:10). Wao wenyewe hawakuwa na uwezo wa kutosha ila Munguanao uwezo wa kuwasaidia. Hivyo Mungu amestahili kutukuzwa kwa uwezowake utendao kazi katika maisha yao.

„sawasawa na Injili yangu‟ Wafanywe imara katika nini? Jibu ni „katika Injiliyangu‟ yaani katika Injili aliyokabidhiwa na kuihubiri (2:26; 1 The.1:5; 2 Tim.2:8;1 Kor.15: 1; Gal.1:11; 2:27; Efe.3:6; 1 The.2:4; 1 Tim.1:11). Wengine walitokeawenye kuhubiri injili nyingine isiyolingana na Injili ya kweli. Mara nyingi Pauloalipambana na waalimu wa uongo. „na kwa kuhubiri kwake Yesu Kristo‟ Nimatangazo ya kweli kumhusu Kristo, ule kweli uliotangazwa na Mitumewalioandama na Kristo alipokuwa duniani, ambao walikabidhiwa kazi hiyo. Kwahiyo, Mungu aweza kuwafanya imara katika Injili ya Kristo, kusudi waamini nakuishi katika kweli za Yesu Kristo.

k.25b Halafu Paulo alitaja „ile siri iliyositirika tangu zamani ya milele‟ (1:3; 3:21).Ni Injili iliyo‟undwa‟ katika mapenzi ya Mungu. Siri hiyo ilikuwamo katikaMaandiko ya Kale ila watu hawakuitambua. Ndipo Kristo alipokuja ilifunuliwawazi na Mitume na wenzao nao wakapata kuifahamu (1 Pet.10-12; 1Kor.2:6,7,10; 15:51; Efe.3:3-6,9; Kol.1:26-27; 2:2-3). Ndani ya siri hiyo ilifichwahabari ya WaMataifa kuingizwa katika mpango huo wa Mungu wakuwashirikisha wokovu wa Kristo. Akina Paulo na wenzake waliongozwa naMungu, wakawa watangazaji wa Injili kwa WaMataifa na kwa njia yao WaMataifawengi walimwamini Kristo na kumtii. Wahubiri wa kwanza walitumia sanaMaandiko kwa kuyathibitisha mahubiri na mafundisho yao.

Walihubiri kwa maagizo ya Mungu (15:15,16; Tim.1:1; Tit.1:3) hivyo makusudi yaMungu ya kuwaokoa wanadamu yaliendelea kutimizwa hata Warumi naowamepata kumwamini na kumtii Kristo.

Alipotafakari hayo yote Paulo alibaki na mshangao mkubwa akamsifu Mungukwa hekima yake na uwezo wake. Aliona ni Yeye peke yake aliyestahilikutukuzwa milele na milele.

Page 195: Matendo na Warumi - African Pastors Fellowship · 11: 27-30 Unabii wa Agabo kuhusu njaa 12: 1- 4 Mfalme Herode kumwua Yakobo na kumfunga Petro 12: 5-19 Petro kutolewa gerezani kwa

WARUMI 857

MASWALI:1. Twajifunza nini kutoka katika salaam hizo mbalimbali?2. Paulo alifunga Waraka na nini?

INSHA:Umejifunza mambo gani makubwa na umesaidiwa nini kwa Waraka huu kwaWarumi?