18
Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikisha viwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji Jarida la Baraza la Habari Tanzania Toleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 20 Uk 9 Mmetoa mchango mkubwa - Warioba

Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

  • Upload
    others

  • View
    2

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikishaviwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji

Jarida la Baraza la Habari TanzaniaToleo la 159, Novemba, 2020ISSN 0856-874X

EJAT 2020 yaanza

Wahariri wazungumzia changamoto

MCT yapata hadhi ya uangalizi

Uk 5 Uk 20Uk 9

Mmetoa mchango mkubwa - Warioba

Page 2: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

BODI YA UHARIRI:Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji – MCTDavid Mbulumi Meneja ProgramuHamis Mzee Mhariri

MAWASILIANOKwa Maoni na Malalamiko:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzani (MCT)S.L.P. 10160, Dar es SalaamSimu: +255 22 27775728, 22 2771947Simu ya Kiganjani: +255 784 314880Fax: + +255 22 2700370Baruapepe: [email protected]: www.mct.or.tzFacebook:- www.facebook.com/mediacounciltanzania Twiter:- www.twitter.com/mctanzania

2

TAHARIRIJarida la Baraza la Habari Tanzania

Habari za wananchi zipewe umuhimuVyombo vya habari vinaogopa, dhaifu ama havizingatii

hali halisi na kupuuza kuripoti kuhusu wananchi na kuweka mkazo kuripoti kinachosemwa na uongozi?

Mtazamo huu unaochokoza mawazo ulitolewa katika uzinduzi wa Bodi ya tisa ya Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Ni kweli ni bahati mbaya, vyombo vya habari – vya utangazaji na magazeti vimekuwa vikipuuza habari za wananchi na badala yake vinapaza sauti za viongozi.

Lakini nini kimesababisha hali hii katika vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vimechangamka na makini - wakati wa chama kimoja ambavyo vilikuwa vinamilikiwa ama na serikali au chama tawala na baada ya kuingia mfumo wa siasa za vyama vingi na kuanzisha sera za uliberali vyombo vya habari vimeongezeka kwa wingi na aina pia?

Kashfa zilifichuliwa kutokana na uandishi habari za uchunguzi na makala za utafiti zilizoibua mawazo na maoni zilichapishwa lakini sasa mambo hayo hayapo tena.

Hata hivyo kwa kuuliza maswali haya hatuna maana kuwa ya kujifanya hatufahamu mazingira magumu kutokana na sheria mbaya zilizopitishwa na ambazo zinakwaza vyombo vya habari.

Baadhi ya sheria hizo kama sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016 iliyoanzishwa kwa ahadi ya kuboresha maslahi ya waandishi wa habari wakati ni sheria inayobinya.Kwa mfano, magazeti yanatakiwa kuwa na leseni kila mwaka ambazo zinaweza kusimamishwa au kufutwa kabisa wakati wowote wasimamizi wanatakapojisikia.

Utoaji wa matangazo ya serikali sasa unasimamiwa na chombo kimoja na vyombo vinavyochambua habari vina nafasi finyu ya kuyapata.

Licha ya MSA kuna sheria kadhaa na kanuni zinazokwaza vyombo vya habari vyote – magazeti, redio, runinga na vya mtandaoni. Hata hivyo licha sheria hizi zisizo rafiki vyombo vya habari haviwezi kuacha kuwatumikia wananchi.

Kuna masuala mengi ya kijamii, kiuchumu na hata ya mazingira yanayoathiri wananchi ambayo vyombo vya habari vinaweza kuyatangaza bila kuudhi wenye mamlaka.

Kwa kutangaza masuala ya wananchi kuna matokeo yenye faida mara tatu – walio kwenye madaraka watafahamu matatizo ya wananchi kwa maana ya kupata mrejesho, wananchi watakuwa wameeleza matatizo yao na vyombo vya habari vitanufaika kwa kusikilizwa, kusomwa na kuangaliwa na watu wengi na pia kwa namna nyingine kujiongezea mapato. Uzoefu unaonyesha kuwa habari za wananchi zinawavutia wengi.

Kwa hiyo vyombo vya habari vijitahidi kurekebisha hali iliyopo na kutoa mkazo zaidi kwa habari za wananchi na kutoa nafasi za kuwezesha kuchapishwa kwa maoni ya wananchi kupitia safu za barua za wasomaji au hata mashairi.

Vyombo vya habari viweke mazingira ya kuboresha utoaji wa maoni ya wananchi pamoja na viongozi kwani pande hizo zote zinahitajiana.

MCT, MSHINDI WA TUZO YA IPI 2003

FREE MEDIA PIONEER

Waziri Mkuu mstaafuna mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Baraza la Habari Tanzania (MCT), Joseph Warioba , akiwa pamoja na baadhi wajumbe wa Bodi mpya .Kushoto walioketi ni Makamu wa Rais aliymliza muda kutumika Baraza, Hassan Mitawi, Rais wa MCT, Jaji mstaafu Juxon Mlay , wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga na kulia ni Balozi wa Norway nchini Elisabeth Jacobsen. Waliosimama kutoka kushoto ni Happiness Nkya, Edda Sanga, Bakari Machumu, Dr. Joyce Bazira na Makamu wa Rais wa Baraza Yussuf Khamis.

Page 3: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limetoa mchango mkubwa katika kukuza maendeleo ya tasnia ya

habari nchini. “Baraza limefanya kazi kubwa

… ninachohimiza mimi ni maboresho zaidi”, Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MCT , Joseph Warioba amesema.

Warioba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Kamati ya Maadili ya Baraza lilipoanza shughuli 1997 alikumbusha kuwa awali kulikuwa na magazeti machache na redio chache na hakukuwa na kituo cha runinga, alisema na kuongeza kuwa siku hizi vipo vingi.

Pia alisema hakukuwa na kanuni za maadili wakati huo lakini sasa zipo zinazohusu vyombo aina mbalimbali vya habari.

Alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya MCT uliofanyika katika hoteli ya Courtyard Jijini Dar es Salaam Novemba 20, 2020.

Bodi hiyo yenye wajumbe tisa ilichaguliwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza (NGC) uliofanyika Septemba 28, 2020 Jijini Tanga.

Bodi hiyo mpya inaongozwa na Jaji mstaafu Juxon Mlay ambaye ni Rais na Makamu wake ni Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Zanzibar, Yusuf Khamis.

Wajumbe wengine wa Bodi hiyo ni Tido Mhando – Mtendaji Mkuu wa Azam Media ambaye anakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Happiness Nkya mtaalamu wa fedha na ukaguzi anayekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ambapo wajumbe wengine wa Bodi ni Teddy Mapunda, Edda Sanga, Bakari Machumu, Dk. Joyce Bazira na Anna Henga.

Makamu wa Rais Khamis, Mhando, Nkya, Dk. Bazira na

Teddy Mapunda wanajiunga na Bodi hiyo kama wajumbe wapya wakati Rais mpya Mlay, Machumu, Sanga na Henga

walitumikia Bodi hiyo kuanzia 2017. Jaji Mlay alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya

3

Habari

Toleo la 159, Novemba, 2020

MCT imetoa mchango mkubwa – Warioba

Endelea Ukurasa wa 4

Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Bodhi ya Wadhamini wa Baraza la Habari Tanzania, Joseph Warioba akizindua Bodi mpya ya Baraza Novemba 20,2020 Jijini Dar es Salaam.

Page 4: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

4

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Maadili.Warioba aliwakabidhi wajumbe

hao wa Bodi vitendea kazi ikiwamo katiba ya Baraza.

Akizungumzia hali ya vyombo vya habari nchini, Warioba alivitaka kuandika masuala yanayowahusu wananchi.

Alieleza wasiwasi kwamba inaelekea watu wengi sasa wanavutiwa na habari zinazotangazwa na vyombo vya habari vya nje kulinganisha na vya hapa nchini.

“Mimi napenda habari na madereva wangu wanajua … wakati wowote nikiwa kwenye gari… wanafungulia TBC ama

Radio One”, alisema.Lakini mambo yamebadilika.

Badala ya kufungulia vituo vya redio vya hapa nchini sasa wanafungulia DW, VOA ama kituo kingine chochote cha nje, alisema.

Alisema pia kuwa rafiki yake mmoja alipendekeza kwake katika mazungumzo ya simu kwamba kituo cha runinga cha Star kina kipindi cha Dira ya Dunia (kipindi cha BBC ) saa 3.00 usiku.

Hii inamaaninisha nini? Warioba alihoji na kueleza kuwa inaelekea vyombo vya habari vya ndani haviwatoshelezi wananchi.

Waziri Mkuu mstaafu alisema

kuwa hali ya sasa kwenye vyombo vya habari ni kuandika habari za viongozi na kutaka wananchi waelimishwe.

Alitofautiana na mtazamo huo kwa kueleza kuwa viongozi nao wanahitaji kujifunza kutoka kwa wananchi.

Alisema pia kuwa inaelekea vyombo vya habari vinahofu kuripoti masuala na kukumbusha utaratibu wa taaluma ya habari kwamba mbwa akimuuma mtu siyo habari bali mtu akimuuma mbwa ni habari. Alisema pia kuwa habari za uchunguzi zimedorora na hata habari za uchambuzi zinazochokoza masuala hazipo kabisa.

MCT imetoa mchango mkubwa – WariobaInatoka Ukurasa wa 3

Mjumbe wa Bodi Happiness Nkya akipongezwa na Rais wa Baraza la Habari la Tanzania, Jaji mstaafu Juxon Mlay baada ya kupewa vitendea kazi na Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Baraza, Joseph Warioba( wapili kulia) na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza, Kajubi Mukajanga na kushoto ni Makamu wa Rais aliyemaliza muda kulitumikia Baraza, Hassan Mitawi.

Page 5: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wetu

Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushirikiana na washirika wake linawahimiza waandishi wa habari kuende-

lea kushiriki katika Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2020 kwa kuandika habari zenye kukidhi vigezo vya mashindano hayo.

EJAT 2020 ilizinduliwa Septemba 28, 2020 mkoani Tanga katika kilele cha Tuzo za mwaka 2019, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela alikuwa mgeni rasmi na ndiye aliyezindua Tuzo za EJAT

2020. Hii itakuwa ni kwa mara ya 12 kwa

Kamati ya Maandalizi ya EJAT kuandaa mashindano haya ambayo kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka 2009. Tuzo hizi zinalenga kuwatambua na kuwatuza waandishi wa habari waliofanya kazi zao vizuri katika makundi mbalimbali ya kushindaniwa.

Washirika wa EJAT 2019 ni pamoja na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika- Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Chama Cha Waandishi wa Habari

Wanawake Tanzania (TAMWA).Washirika wengine ni Umoja wa

Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), HakiElimu, Sikika na Agriculture Non-State Actors Forum (ANSAF).

Kwa uzinduzi huu waandishi wa habari wa magazeti, radio, habari za mtandao na runinga wanahimizwa kuwasilisha kazi zao kwenye Baraza katika makundi yafuatayo ya Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchumi na Biashara na Fedha na Tuzo ya Uandishi wa Habari za Michezo na Utamaduni.

Mengine ni Tuzo ya Uandishi wa Habari za Biashara ya Kilimo, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Elimu, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utalii na Uhifadhi, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi, Tuzo za Uandishi Data na Tuzo za Uandishi wa Habari za Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Makundi mengine ni Mpiga Picha Bora – Magazeti, Mpiga Picha Bora – Runinga, Mchora Katuni Bora, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Jinsia na Watoto, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini na Tuzo ya Uandishi wa Habari za Walemavu

Pia Tuzo hizo zitakuwa na makundi ya Tuzo ya Uandishi wa Habari za Afya, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Ubunifu na Maendeleo, Tuzo ya

5

Toleo la 159, Novemba, 2020

Endelea Ukurasa wa 6

Waandishi wahimizwa kuwasilisha kazi kuwania EJAT 2020

Washindi wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2019 wakiwa na tuzo na vyeti walivyopewa baada ya kuibuka washindi katika makundi mbalimbali ya mashindano hayo wakiwa pia pamoja na mgeni rasmi wa Tuzo hizo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Habari

Page 6: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

6

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Uandishi wa Habari za Usalama Barabarani, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Hedhi Salama na Kundi la Wazi.

Fomu za ushiriki wa EJAT 2020 zinapatika katika tovuti ya Baraza la Habari Tanzania www.mct.or.tz, ambapo mwisho wa kuwasilisha kazi zinazowasilishwa kwa ajili ya mashindano ni Januari 31, 2020.

Baadhi ya vigezo vinavyotumika katika Tuzo hizo ni pamoja na mwandishi anatakiwa kuwasilisha kazi ambayo imesaidia kutoa maarifa mapya kuhusu masuala muhimu katika jamii.

Habari iwe na upekee, umahiri katika matumizi ya lugha, habari ionyeshe ujasiri katika kuitafuta na umahiri katika kuiandika, habari hiyo iwe imezingatia maadili na weledi wa taaluma ikiwa ni pamoja na kuandika ukweli, usahihi wa taarifa na urari wa vianzo vya habari.

Vigezo vingine ambavyo vinatazamwa katika mashindano hayo ni jitihada za kutafiti habari husika ikiwa ni pamoja na matumizi za vyanzo vya habari vya watu na taarifa za maandishi au picha. Uwezo wa mwandishi wa kufanya uchambuzi wa kina wa suala ambalo analiandikia na ubunifu wa kazi ya kiuandishi inayowezesha kutoa mtizamo mpya wa masuala na jinsi gani yanaathiri jamii.

Katika kupitia kazi zilizowasilishwa jopo la majaji pia hufanya tathmini ya ugumu au changamoto alizopata mwandishi katika kutafuta habari husika na ukamilifu wa habari inayoshindanishwa.

Kwa upande wa picha bora majaji wanaangalia picha yenye viwango stahiki vya kiufundi, yenye kuvuta hisia za mtazamaji, na inayoonyesha umahiri wa mpigapicha katika kunasa kitu au tukio lenye umuhimu au lenye mvuto wa aina ya kipekee, picha iwe na maelezo mafupi yenye kutoa ujumbe unaoeleweka kwa msomaji na

unaotimiza vigezo vya uandishi wa habari.

Halikadhalika majaji wanafuatilia picha yenye ubunifu wa hali ya juu kwa jinsi mpigaji picha alivyochagua upangaji wake kiufundi na kimaudhui, yenye kujitosheleza bila ya maelezo ya ziada. Picha iwe na maudhui muhimu yenye manufaa kwa jamii, izungumzie tukio ambalo halijapitwa na wakati na lenye maslahi kwa jamii.

Kwa mujibu wa vigezo hivyo picha izungumzie ajenda muhimu za kijamii au kitaifa. na izingatie maadili ya upigaji picha/uandishi – isiwe ya kughushi uhalisia, na isiwe imepigwa katika maeneo ambayo yamekatazwa kisheria. Isiwe inaonyesha utupu, kushabikia tabu za mtu/umauti na isiwe imebadilishwa kidigitali.

Mwandishi wa habari anayewasilisha kazi katika mashindano anatakiwa kujaza fomu ambazo zinatakiwa kuambatanishwa na kazi zinazoshindanishwa kuzingatia yafuatayo;

Kwa upande wa magazeti, mwandishi anatakiwa kuwasilisha nakala moja halisi ya kazi iliyochapishwa kwenye gazeti au kivuli kilichothibitishwa kwa kugongwa muhuri wa ofisi.

Kwa upande wa runinga na ya mtandaoni , mwandishi atatakiwa kuwasilisha DVD iliyohaririwa na isiyozidi dakika 5 kwa habari na dakika 20 kwa vipindi vya makala maalum.

Waandishi wa habari wanaoandikia radio, wanajukumu la kuwasilisha CD moja ya kazi iliyohaririwa isizidi dakika 5 kwa habari na dakika 15 kwa vipindi maalumu.

Kwa upande wa picha, mwandishi wa habari ana jukumu la kuwasilisha nakala moja ya picha iliyopigwa kwenye CD na nakala moja ya picha iliyotoka kwenye gazeti.

Kwa upande wa picha za picha ya runinga mwandishi wa habari anajukumu la kuwasilisha nakala moja ya DVD iliyohaririwa na isiyozidi dakika tano kwa habari na dakika 20 kwa makala au vipindi maalum ambapo kwa katuni, mwandishi anatakiwa kuwasilisha nakala za katuni zisizozidi tatu na zilizochapishwa kwenye gazeti au runinga.

Makala au habari zilizowasilishwa zionyeshe zilichapwa au kutangazwa kwenye chombo kipi cha habari na tarehe ya kuchapishwa au kutangazwa. Kama ni makala mfululizo ni lazima ielezwe hivyo. Kama ni safu ya kudumu basi pia inaweza kushindanishwa kama mfululizo. Kazi za kubuni hazitakubaliwa.

Waandishi wahimizwa kuwasilisha kazi kuwania EJAT 2020Inatoka Ukurasa wa 5

Majaji wa Tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2019 wakipitia kazi zilizowalishwa kuwania tuzo hizo.

Page 7: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Kauli ya Rais John Pombe Ma-gufuli kwamba hakuna uhuru bila wajibu ni onyo la wazi sio la kificho kwa vyombo vya

habari na wanasiasa.Ingawa katika hotuba yake awali

alitoa matuamini kwa vyombo vya habari na wanasiasa alipotangaza dhamira ya kuzingatia uhuru wa habari na demokrasi, onyo lake kuhusu uhuru na demokrasi limeweka bayana msimamo wake kwa vyombo vya habari.

“Nafikiri nimeeleweka”, Rais alisema bila kufafanua zaidi.

Alikuwa anafungua mkutano wa kwanza wa Bunge lenye wabunge wapya wengi wa chama chake na wapinzani wachache mjini Dodoma Novemba 13, 2020.

Mtamshi haya ya mtu ambaye yumo kwenye rekodi akieleza vyombo vya habari kuwa “ angalieni…hamko huru kwa kiwango hicho” yanaonyesha wazi kuwa kuna hali ngumu zaidi kwa vyombo vya habari.

Rais pamoja na wabunge wengi wa chama tawala CCM walichaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 28, 2020.

Vyombo vya habari vilikuwa na wakati mgumu kuandika habari za kampeni za uchaguzi mkuu huku baadhi ya vyombo vikifungiwa ama kuonywa mara kwa mara na mamlaka za usimamizi.

Katika siku ya pili ya kampeni za uchaguzi mkuu Agosti 27, 2020 Clouds Media Group walikuwa majeruhi wa kwanza ilipoamuliwa kufunga kituo chake cha runinga na redio kwa wiki moja kwa madai ya kukiuka kanuni za utangazaji.

Amri hiyo ilikuwa ni utekelezaji onyo lililotolewa na Tume ya Uchaguzi baada ya baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kuwa baadhi ya wagombea wamepita bila kupingwa baaa wapinzani wao kuenguliwa.

Gazti la Tanzania Daima lilifutiwa leseni yake na ingawa limeomba tena halijafanikiwa kupata leseni nyingine hatua iliyofifisha matumaini ya kupwa leseni kabla ya uchaguzi

mkuu.Ingawa msajili wa magazeti

alisema kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya gazeti hilo kupewa maonyo mengi lakini habari

inayofikiriwa iliyomsumbua msajili ni wito ulichapishwa wa kutaka kuwepo maandamano ya amani kudai Tume Huru ya Uchaguzi.

7

Habari

Toleo la 159, Novemba, 2020

Magufuli ‘aweka msimamo kwa vyombo vya habari’

Endelea Ukurasa wa 9

Rais John Magufuli akihutubia Bunge kufungua kika chake cha kwanza baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28,2020.

Page 8: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Na Mwandishi wa Barazani

Changamoto kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba,

imepokewa kwa hisia na mitazamo tofauti na wahariri.

Kauli ya Warioba katika hotuba yake fupi na muhimu wakati wa uzinduzi wa Bodi ya tisa ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) Novemba 20, 2020 Jijini Dar es Salaam imeibua majadiliano ya kina mtandaoni miongoni mwa wahariri.

Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya

Udhamini ya Baraza, alitoa mwito kwa vyombo vya habari kuandika habari za wananchi .

Alisema kwamba inaonekana kuwa vyombo vya habari nchini havikidhi matakwa ya habari ya wananchi na wafuatilie zaidi vyombo vya habari vya nje.

Alisema mwenendo wa kwenye vyombo vya habari ni wa kuripoti zaidi kuhusu viongozi na mkazo zaidi ya kuhimiza wananchi waelimishwe lakini yeye alikuwa na mtazamo kuwa viongozi nao lazima wajifunze kutoka kwa wananchi.

Alikumbusha kuwa huko nyuma iliyokuwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo sasa ni

TBC ilikuwa na vipindi vya habari kuhusu wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini lakini sasa havipo.

Aidha alisema wakati wa vita vya 1979 dhidi ya nduli Idi Amin wa Uganda, serikali wakati huo ilibaini kuwa watanzania wengi walikuwa wanasikiliza zaidi matangazo ya vituo vya radio vya nje. Alisema ilijadili suala hilo na hali ilibailika.

Amesema kuwa siku hizi kuna mdororo wa habari za uchunguzi na za utafiti wenye kuamsha uchokozi wa mawazo.

Baadhi ya wahariri katika kuzungumzia changamoto hiyo ya

Wahariri wazungumzia changamoto ya Warioba

Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Baraza la Habari Tanzania Joseph Warioba akifurahia jambo na Makamu wa Rais aliyemaliza muda kulitumikia Baraza, Hassan Mitawi baada ya kumkabidhi kumbukumbu ya utumishi wake. Kushoto ni Rais wa MCT, jaji mstaafu Juxon Mlay.

8

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Endelea Ukurasa wa 9

Page 9: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Baadhi ya wahariri walisema katika vipindi tofauti kuwa “ ni magumu” na kuomba uchaguzi umalizike haraka.

“Tunakabiliana na mwenendo mgumu” mhariri mmoja alisema na mwingine alisema ili kuweka mambo sawa wamiliki wa vyombo vya habari wanaamua aina ya vichwa vya habari vya kutumia kwa kuwaogopa wenye mamlaka.

Kwa kuwa uchaguzi sasa umemalizika, vyombo vya habari vinaweza kupumua lakini kutokana na onyo lililotolewa na ofisi kuu nchini, ni lazima watakuwa waangalifu.

Katika kipindi cha miaka mitano serikali ya Magufuli ilipitisha sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari mwaka 2016 ambayo imeshutumiwa na wadau wa habari.

Sheria hiyo ilipingwa katika Mahakama ya Afrika Mashariki na

wadau ambao walishinda ambapo serikali ilitakiwa kuvifanyia marekebisho vifungu 16 vya sheria hiyo vinavyokinzana na mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Hatua ya kupinga sheria hiyo mbaya ilichukuliwa na Baraza la Habari Tanzania, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Umoja wa Kutetea Haki za Binadamu Tanzania(THRDC).

Jitihada za serikali kukata rufani dhidi ya hukumu hiyo ya Machi 18, 2019 hazikufanikiwa kwa kuwa Juni 2020 Kitengo cha Rufaa cha Mahakama ya Afrika Mashariki kilitupilia mbali notisi ya kutaka kukata rufani.

MCT, LHRC na THRDC, ndiyo waliomba Mahakam hiyo ya Rufaa kuitupilia mbali taaarifa hiyo ya kukata rufani.

Serikali hadi sasa haijatekeleza hukumu ya EACJ.

Licha ya msimamo wa serikali

kuhusu MSA, wadau wa habari wameamua kuzungumza na serikali jinsi ya kuiboresha sheria hiyo.

Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga amesema kuwa watazungumza na kuwaelimisha wahariri, waandishi waandamizi na umma kuhusu sheria jinsi inavyowahusu kwa lengo la kuiboresha na maamuzi ya mahakama yanamaanisha nini kwao na kuhakikisha kuwa watu wasikwazwe tena na vifungu vya sheria ambavyo havipo.

MCT kwa upande wake imefanya juhudi kupitia mikutano na mafunzo kuwaelimisha wanahabari, mameneja , wahariri na wahadhiri wa uandishi wa habari kuhusu umuhimu wa maamuzi ya mahakama na kwa nini ni muhimu kufungua mashitaka kufuatilia haki za wanahabari na kuzuia vikwazo visivyostahiki kwa uhuru wa habari ambavyo ni visababishi ya ukiukaji wa wa uhuru wa habari.

Licha ya MSA sheria zingine zinazokwaza vyombo vya habari ni Sheria ya mawasiliano ya posta nay a kieletroniki na kanuni zake za mtandaoni na raido na runinga, uhalifu wa mtandaoni.

Inatoka Ukurasa wa 7

Magufuli ‘aweka msimamo kwa vyombo vya habari’

9

Toleo la 159, Novemba, 2020

Habari

Wahariri wazungumzia changamoto ya WariobaWarioba walishangaa kama Waziri Mkuu huyo mstaafu hafahamu mazingira ya sasa yenye sharia ambazo si rafiki kwa vyombo vya habari.

Ufungaji, usimamishaji na vyombo vya habari kutozwa faini kubwa na mamlaka za usimamizi vimesababisha kuwepo hali kubwa ya hofu, walisema.

Pia ilielezwa na wahariri kuwa vyombo mbalimbali vina hali ngumu kiuchumi kwa kukosa matangazo na pia hata yanapopatikana malipo hucheleweshwa.

Chini ya sheria mpya ya habari, matangazo ya serikali yanasimamiwa na kutolewa na mamlaka moja ambapo vyombo vya habari vyenye tabia ya kupinga

pinga ama kufuatilia habari kwa kina havina matumaini ya kunufaika na utaratibu huo wa matangazo.

Kwa jumla maoni ya wahariri mbalimbali mtandaoni ni kuwa mtazamo unaochukuliwa ni kuepuka matatizo na wenye mamlaka.

Matukio ya karibuni yameonyesha kuwa hata vituo vya redio vya nje kama katika matangazo kuna habari inayoonekana kuwa kuwa siyo nzuri, habari hiyo hurukwa na badala yake kuwekwa matangazo na kuendelea na taarifa zingine.

Hali hii inajitokeza katika vituo vyote vya nchini vnavyounganisha matangazo kutoka radio za nje.

Taarifa ya Chama cha ACT Wazalendo ikielezea madhila

yaliyokisibu wakati wa uchaguzi Visiwani iliyowasilishwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi haikuripotiwa na wala kutangazwa na vyombo vya habari kumfanya mhariri mmoja kuuliza katika mtandao wa Whatsapp wa Jukwaa la Wahariri kama wahariri waliiona ripoti ile ya ACT.

Licha ya matatizo yanayovikabili vyombo vya habari, maoni ya Warioba yamepokelewa vizuri na baadhi ya wananchi wanaona kuna umuhimu vyombo vya habari vikawa mstari wa mbele kufichua matatizo ya kijamii na kijamii yanayowakabili.

Uchunguzi mdogo wa jarida hili umeonyesha kuwa watu wanakabiliwa na matatizo mbalimbali hasa kuhusu afya na utoaji huduma.

Inatoka Ukurasa wa 8

Page 10: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

10

Tanzia

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Na Saidi Nguba

Mwanahabari mwingine nguli amatutoka. Ni Patrick Segeja Chokala. Alikuwa mwanahabari

aliyeiva na mwanadiplomasia aliyebobea. Alikuwa mcheshi, mwenye bashasha, mtu wa masihara, anayefurahisha na mchekeshaji lakini pia ni muungwana sana na mtu wa Mungu katika siku zake za mwisho za maisha yake hapa duniani.

Tumekumbwa na upungufu mkubwa wanahabari

nguli. Balozi Chokala, 72, ametutoka Novemba 6, 2020 baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa kwenye makazi yake ya kudumu makaburi ya Kondo jinini Dar es Salaam, Novemba 9. Ameacha mke na watoto watatu – mwanamke na wanaume wawili. Kabla ya hapo, siyo muda mrefu uliopita, Mei 11, tuliagana na nguli mwingine wa habari Fili Karashani, 82, ambaye aliugua kwa muda mrefu. Naye alilazwa kwa heshima kwenye makaburi ya Kinondoni, pia Jijini Dar es Salaam.

Mapema mwaka 2005, Balozi Chokala alijitosa katika kinyang’anyiro cha kugombea Urais,

kupitia tiketi ya CCM. Hakufanikiwa lakini aliongeza

kitu katika wasifu wake mrefu uliojaa mengi.

Wakati huo nilikuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi na alikuja mpaka ofisini kwangu Tabata

Relini na kuniambia: Saidi, wewe ni mwanahabari wa kwanza kukudokezea nia yangu hii ya

kugombea Urais. Nilimwambia lakini mashindano

ni makali mno ila alinijibu ana matumaini. Akanisimulia hata hadithi ya kale ya chura mdogo kiziwi: “Katika mashindano ya vyura kumpata atakayemudu kupanda mlingoti mrefu na kufika kileleni, vyura wengi walishindwa na kuporomoka kwa kuzomewa kwa kukatishwa tamaa. Lakini akatokea chura mmoja mdogo ambaye, licha ya makelele mengi ya kumkatisha tamaa, akafanikiwa kufika kileleni. Ilibainika baadaye kuwa huyo chura

Endelea Ukurasa wa 13

Patrick Segeja Chokala: Mwandishi mahiri , Mwanadiplomasia makini

Hayati Patrick Chokala

Page 11: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Simon Mkina

Maisha ya mmoja wa mwanahabari bora wa habari za uchun-guzi na mshirika wa

vita dhidi ufisadi nchini

Ghana, Manasseh Awuni yako hatarini. Amekuwa akipokea vitisho kwa sababu tu yeye ni mwandishi wa habari. Awuni ambaye hivi karibuni , ali-pokea zawadi ya cheti, ngao na fedha baada ya kuibuka mwandishi bora wa Afrika

Magharibi. Aliibuka baada ya kushinda waandishi wengine 200 kutoka nchi 11 za eneo hilo la Afrika.

Kutokana na kazi yake ya kuwa mwandishi, hasa wa habari za uchunguzi, maisha yake yamekuwa kama digidigi. Anawindwa kuuawa na majahili.

Kutokana na vitisho, serikali ya Ghana imempa ulinzi wa askari kila anapokwenda. Pamoja kwamba wanaompa ulinzi, huenda ndiyo haohao wanaopanga kumuua.

Awuni anasema, pamoja na vitisho vingi, na jaribio la kuondoa uhai wake, bado hataacha kuandika. Hatakoma na kuwa baada ya vitisho vingi, hivi sasa ndiyo ameamua kuandika zaidi na kuibua maovu.

Tukio moja la kupokonya maisha yake lilitokea wakati akifuatilia habari ya chama

11

Makala

Toleo la 159, Novemba, 2020

Mshindi mara tatu wa uandishi wa habari za uchunguzi wa Ghana Manasseh Awuni (kushoto) akiwa Simon Mkina.

Endelea Ukurasa wa 12

Vyombo vya habari Ghana vyaendelea kufichua ufisadi licha vitisho

Page 12: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Makala

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

12

Vyombo vya habari Ghana vyaendelea kufichua ufisadi licha vitishotawala cha NDC kilipounda jeshi na kufungwa na wanajeshi wastaafu. Kabla ya kuchapisha habari hiyo, Awuni alitonywa juu ya mpango wa kumuua na namna majahili watalavyotekeleza ujahili wao.

Alitoa taarifa serikalini na ndipo Waziri wa Usalama wa Taifa, Albert Kan Dapaah akampa ulinzi. Awuni aligundua kwamba kiongozi wa mafunzo hayo alikuwa mlinzi wa zamani wa Rais Nana Addo-Akufo.

Mwandishi mwingine, Emmanuel Dogbevi, mwandishi wa habari za uchunguzi na mwanzilishi wa habari Ghana Business News alisema "Sijisikii salama sana, haswa tangu Serikali hii iingie madarakani.

Vitisho vya waandishi hao wawili, vitisho vikali na unyanyasaji wa mwili ni tone tu la maji katika bahari ya sekta ya habari ambayo inaiweka Ghana kama moja ya nchi za Kiafrika ambazo sio salama kufanya shughuli za uandishi wa habari.

Mnamo Januari, 2019, mwandishi wa habari wa uchunguzi, Ahmed Hussein-Suale alipigwa risasi na kuuawa na genge lililoajiriwa maalum kwa kazi hiyo.

Vyombo vya habari nchini Ghana vilikuwa na nguvu sana kabla ya utawala wa sasa na inasemekana kuwa vilipimwa kama muhimili wa nne wa Serikali.

Vyombo vya habari viliibua idadi kubwa ya matukio ya ufisadi, matumizi mabaya ya ofisi za umma na visa vingine vingi vibaya.

Waundaji wa katiba ya 1992, labda, walijua hii itatokea, kwa hiyo waliwapa nguvu vyombo vya habari kuwajibisha Serikali kwa watu.

Vyombo vya habari nchini Ghana vimekuwa katika kipindi kirefu cha ukandamizaji hadi mwaka 1992, wakati katiba ilipowapa uhuru.

Ghana sasa ina karibu vituo 400 vya redio na makumi ya vituo vya televisheni. Mtandao umewezesha mamia ya milango ya habari kushindana na magazeti kwa umakini.

Magazeti kama vile The Chronicle, The Enquirer, The Crusading Guide, na kwa kiwango fulani, The Palaver ni mifano ya vyombo vya habari ambavyo vilifanya uandishi wa habari bila woga. Magazeti ya wakati huo yalionekana kushindana katika harakati za kuzidiana kwa kufichua kashfa na kuwafanya watu na taasisi kuwajibika.

Katika miaka kumi iliyopita; Walakini, idadi ya vyombo vya habari vilivyojitolea kupigana dhidi ya ufisadi nchini Ghana imepungua. Shirika moja la habari ambalo linaongoza kufichua ufisadi kupitia uandishi wa habari za uchunguzi ni Joy FM na Joy News TV.

Kwa ushahidi wa wazi, uandishi wa habari muhimu nchini Ghana sasa unakufa. Sababu ambazo vyombo vya habari vinashindwa katika vita vyao dhidi ya ufisadi ni nyingi lakini moja wapo ni kwamba, waandishi wengi wameamua kuacha kazi hiyo, huku wakibaki wachache ambao nao wanajiunga na

shetani wa rushwa.Awuni katika mahojiano na

mwandisshi wa Makala haya alisema wakati mwingine, shida ni wamiliki wa vyombo vya habari wamekuwa wakikataa kuchapisha habari za dhidi ya ufisadi.

"Mwaka 2013, tulimpoteza mmoja wa wanahabari bora nchini Ghana, Samuel Agyemang wa Metro TV. Samuel alifanya kazi nzuri ya uchunguzi kwenye kampuni fulani lakini akazuiwa kuirusha kwenye Metro TV, ambako alikuwa akifanyia kazi.

Ilibidi aichapishe kwenye YouTube na akajiuzulu baadaye.

Mwandishi wa habari yeyote anayetaka kupambana na ufisadi nchini Ghana atatambua kuwa wapinzani wake ni waandishi mwenzake, kwa sababu moja au nyingine, anaitetea na kulinda ufisadi kwa kuwa naye ni miongoni mwa wanaofaidi," anasema Awuni.

Hata hivyo, pamoja na usaliti wa waandishi, wamiliki na uonevu wa serikali dhidi ya waandishi, wananchi wa Ghana kama ilivyo kwa nchi nyingi, ikiwamo Tanzania, bado umuhimu wa vyombo vya habari unabaki kuwa tumaini na kimbilio la wanyonge.

Kinachotakiwa ni waandishi kuungana na kukataa kuonewa na kuhakikisha wanakuwa wamoja zaidi kuliko kuacha tatizo la mmoja au chombo kuonekana ni lake. Kupiga kelele kwa pamoja ni suala pana na ngumu, lakini inawezekana kabisa kuwatisha wenye nguvu kubwa ya fedha na madaraka.

Inatoka Ukurasa wa 11

Page 13: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Patrick Segeja Chokala: Mwandishi mahiri, Mwanadiplomasia makinialikuwa kiziwi na hivyo hakubugudhiwa na makelele yale, wala hakuwa akiyasikia,” Balozi Chokala alisema na kumalizia: “Mimi ndiyo huyo chura mdogo kiziwi.” Ni kweli, pamoja na kuwa hakushinda kuteuliwa kuwa Rais, lakini alikuwa ni “chura mdogo kiziwi” kwa vile amefanikiwa kuwa na sifa ya mwandishi makini na mwanadiplomasia mahiri.

Balozi Chokala, ambaye alifahamika zaidi na ni maarufu kwa jina la “Chocks” , ambalo yeye mwenyewe binafri alikuwa analipenda, alijiriwa kufanyakazi Chumba cha Habari cha Radio Tanzania, RTD (sasa TBC), mwaka 1973, akitokea moja kwa moja Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Aliajiriwa pamoja na hivi sasa naye mwanahabari mkongwe, Dk. Samwilu Mwaffisi. Ajira yao ilitokana na mpango wa aliyekuwa Mhariri Chumba cha Habari RTD, Sammy Mdee, kuingiza damu mpya katika Chumba cha Habari. Nami nilikuwa sehemu ya mpango huo. Chocks na Mwaffisi walinikuta pale nikiwa nimeajiriwa miaka miwili nyuma yao, pia moja kwa moja kutoka shuleni. Chocks alisoma Fasihi UDSM kwa vile wakati huo hapakuwepo na Shule ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano na Umma. Lakini mara moja akajifunza na kuumudu Uandishi wa Habari. Kwa vile Mhariri Mdee alikuwa na dhana kuwa Mwanahabari mzuri wa Radio ni vema akapata msingi wa Uandishi wa Habari wa Magazeti, Chocks akapelekwa Accra, Ghana, kwenye Gazeti la Daily Graphic mwaka 1974 kwa utaratibu wa mafunzo kwa vitendo kazini. Baada ya kurejea Tanzania, mwaka mmoja baadaye, 1975, Chocks akajiunga na Wizara ya Mambo ya Nje na kupanda hadi kufikia cheo cha Mshauri-balozi (Counsellor) kati ya mwaka 1980 hadi 1985. Baadaye, mwaka 1986, alipelekwa Ikulu katika Serikali ya Awamu ya Pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi, kwanza akiwa Mwandishi wa Habari Msaidizi chini ya Habib Halahala aliyekuwanaye Chumba cha Habari RTD na baadaye

Mwandishi wa Habari wa Rais, baada ya kifo cha ghafla cha Habib kutokana na ajali ya Helikopta, Ndanda, Mtwara mwishoni mwa mwaka 1990. Baadaye alirudi tena Wizara ya Mambo ya Nje na kuwa Mkurugenzi wa Habari na Utafiti, kati ya mwaka 1996 na 2002 na baadaye kuwa Balozi kamili aliyeiwakilisha nchi, Moscow, Urusi kati ya mwaka 2002 hadi alipostaafu mwaka 2008.

Katika masihara yake, nilipomuuliza kwa nini ameacha tena kuvuta mtemba aliokuwa ameuzoea, Chocks alicheka, kama kawaida yake, na kunijibu kwamba ameacha kabisa kuvuta tumbaku. “Niliacha baada ya suti zangu kadhaa kuungua…unatembea kwenye ushoroba wa Ikulu halafu unakutana na Rais anakuja mbele yako. Kwa tabia nzuri, heshima na adabu huwezi kuwa unaendelea kuvuta mtemba huku moshi unafuka, hivyo itabidi uufiche katika mfuko wa suruali au koti huku ukiwa unawaka,” Chocks alisema na kuongeza: “Baada ya matukio kadhaa ya namna hiyo, nimeamua sasa kuacha kabisa kuvuta…”.

Mara ya mwisho nilipokutana na Chocks katikati ya jiji, eneo la Posta, nilimjulisha kuwa nimekwishastaafu katika utumishi wa umma na kwa vile nimezaliwa Kariakoo ingawa baba yangu alitokea Ujiji, Kigoma, bado nipo hapa hapa jijini. Nilimuuliza kutaka kujua yeye atarudi lini kwao kijijini mkoani Shinyanga kwa vile naye amekwishastaafu kitambo. “Saidi, siwezi kurudi huko. Nani ananijua katika vijiji vya Shinyanga? Nimeishi karibu maisha yangu yote Jijini Dar es Salaam na nitaendelea kuishi hapa. Sitaki niende huko kijijini na kuingia katika unywaji wa pombe za kienyeji na wazee ambao watakuwa wanakutilia shaka kwa vile hawakujui vizuri. Nitaonekana ni mgeni tu…”. Kwa hiyo, aliishi, amefariki na kuzikwa hapa hapa jijini. Wanahabari kadhaa watamkumbuka Chocks kwa makaribisho yake Ikulu kwa mikutano ya habari ya kila wiki huku akijibu na kufafanua masuala kadhaa ya waandishi. Wakati

mwingine, kwa masuala ya kiuchumi, alikuwa anamshirikisha Profesa Juma Ngasongwa, ambaye naye alikuwa mmoja wa washauri wa Rais wa Masuala ya Uchumi. Chocks alikuwa muwazi na mtu wa msaada mkubwa katika kuhakikisha kazi ya kila mmoja inakwenda vizuri.

Haitokuwa sahihi kwa mimi peke yangu kutoa ushuhuda kuhusu maisha ya kitaaluma na kijamii ya mtu huyo mashuhuri. Hapa yupo Dk. Samwilu Mwaffissi ambaye walianza kazi pamoja na Balozi Chokala Chumba cha Habari RTD mwaka wa 1970. “Tumekuwa tukifuatana tangu mwaka wa 1970. Kwanza nilikutana na Chocks kwenye kambi ya JKT tulipokuwa tukitumikia kwa mujibu wa Sheria na kuanza kufahamiana. Urafiki wetu ulikua tulipojiunga wote na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Julai mwaka 1970. Baadaye tukaajiriwa pamoja Chumba cha Habari RTD. Baada ya Chocks kumaliza muda wake kwenye Gazeti la Daily Graphics Accra mwaka 1974 nilipelekwa mimi huko mwaka 1975 na nikakaribishwa vizuri kwa vile aliacha sifa nzuri na msingi mzuri wa mahusiano. Alipewa jina “Balozi wa Tanzania kwenye Gazeti la Daily Graphics…”.

Ushuhuda mwingine ni kutoka kwa Balozi Ombeni Sefue. Anasema alipoteuliwa kwenda Ikulu kuwa mmoja wa Wasaidizi wa Rais katika miaka ya mwishoni ya 1980 alifadhaika kwa kuwa hakujua utaratibu wa kufanya kazi huko kwa Rais. “Ni Chokala aliyenijulisha masuala ya msingi katika kazi hiyo ya usaidizi Ikulu na hivyo akafanya maisha yangu yawe rahisi,” Balozi Sefue alisema wakati wa mazishi. Mwanadiplomasia mwingine, kati ya Mabalozi kadhaa wastaafu waliohudhuria maziko, Balozi Christoher Liundi, alimtaja Balozi Chokala kuwa “Mwanadiplomasia wa kiwango cha juu”.

Mwandishi ni Mwanahabari na Mhariri mkongwe nchini

Tanzania. Simu ya Mkononi/WhatsApp: 0754-388418.

Barua-pepe: [email protected]

Inatoka Ukurasa wa 10

13

Toleo la 159, Novemba, 2020

Tanzia

Page 14: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

UZINDUZI WA BODI MPYA YA BARAZA

Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Baraza la Habari Joseph Warioba, akipeana mkono na Makamu Rais wa MCT Yusuph Khamis wakati akimkabidhi vitendea kazi.

Rais mpya wa Baraza la Habari Tanzania Jaji mstaafu Juxon Mlay akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya tisa ya Baraza.

Mtangazaji mkongwe , Edda Sanga akikabidhiwa vitendea kazi na Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Bodiya Wadhamini ya MCT, Joseph Warioba wakati wa uzinduzi wa Bodi ya tisa ya Baraza.

Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Habari Tanzania, Bakari Machumu,akipeana mkono na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MCT, Joseph Warioba baada ya kukabidhiwa vitendea kazi.

Rais wa Baraza la Habari Tanzania Jaji mstaafu, Juxon Mlay, akikabidhiwa vitendea kazi na Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MCT Joseph Warioba. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza, Kajubi Mukajanga.

Dk.Joyce Bazira, mjumbe mpya wa Bodi ya Baraza la Habari Tanzania akipongezwa na Rais wa MCT Jaji Juxon Mlay baada ya kukabidhiwa vitendea kazi na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Baraza, Joseph Warioba (wapili kulia) na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza, Kajubi Mukajanga.

14

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

15

Toleo la 159, Novemba, 2020

HabariHabari

Page 15: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

16

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Uchambuzi

Na Gervas Moshiro

Katika miaka mitatu au zaidi iliyopita zimekuweko juhudi za mamlaka za utawala

kutaka kufanya vyombo vya habari nchini viwe vinaunga mkono kauli zote zinazotolewa na serikali, jambo ambalo sio baya ikiwa kuunga mkono huko kunafanywa kwa uburu na imani kuwa jambo hilo ni jema kwa maslahi ya jamii.

Baadhi yetu ambao tulikuwa waandishi wa habari miaka ya sabini na themanini, hatukuwaza kuhusu mwelekeo au lengo la habari tulizokuwa tunaandika kwa sababu kulikuweko na malengo rasmi yaliyoainishwa ya utendaji wa taaluma ya habari. Huduma ya habari, ikiwa kama sehemu ya sekta ya utawala, ilikuwa na maadili yake na malengo yake kwa jamii. Maudhui ya vyombo vya habari vyote nchini yalikuwa ya kiuanaharakati kuunga mkono serikali na wakati mwingine vyombo hivyo vilianzisha juhudi za kipekee za kiuanaharakati kwa masuala ya maendeleo ya jamii.

Nakumbuka, kwa mfano vyombo vya habari kushadidia kampeni ya Mtu ni Afya iliyolenga usafi wa mazingira, Chakula ni Uhai iliyolenga kufanya wananchi kuzalisha zaidi chakula, ripoti na makala kutoka vijijini na mikoani kuangaza maendeleo ya ujenzi wa siasa ya ujamaa, maoni na makala za mhariri zilizolenga kubadili fikra na falsafa za watu ili wawe wajamaa, kwa kifupi kila maudhui yalikuwa na lengo la kuchangia katika ujenzi wa jamii ya kijamaa. Hatukuwa na aina nyingine ya uandishi wa habari tuliojua. Hata kusoma nje ya nchi tulipelekwa nchi za kijamaa – Cuba, Misri, Yugoslavia, Chekoslovakia,

Hungary, Urusi, na Ujerumani Mashariki. Nchini kulikuweko na chuo cha Chama (TANU/CCM) cha Kivukoni kilichofunza viongozi wote wa vyombo vya habari kuhusu ujamaa, nikiwa mmojawapo niliyehitimu mafunzo ya miezi tisa. Hatukuwa na mbadala wa fikra na mwelekeo wa taaluma yetu.

Ujamaa ulipoanza kupungua nguvu duniani miaka ya tisini, vyombo vya habari navyo vikachukua aina ya uandishi wa habari utumikao katika nchi zenye demokrasia ya kijamii isiyokuwa ya kijamaa. Katika demokrasia vyombo vya habari ni taasisi huru zenye kufuata maadili zilizojitungia zenyewe yenye kulinda maslahi mapana ya jamii. Chimbuko lake linatokana na kwamba katika demokrasia kuna vyama vingi vya mirengo tofauti na kila kimoja kinatumia vyombo vya habari kueneza itikadi na falsafa yake kuhusu maisha. Ili kulinda wananchi na matumizi hasi ya nguvu za vyombo vya habari, ilibidi vyombo hivyo vijiwekee utaratibu ambao unalinda maslahi mapana zaidi ya jamii kwa kuhakikisha taarifa zinazotolewa ni ukweli mtupu na zisizopendelea upande fulani. Kama kuna maoni, yanabainishwa hivyo ili mwananchi aelewe kuwa hayo ni maoni ya mtu binafsi na si hali halisi ilivyo kwa wote.

Tofauti kati ya uandishi wa habari asilia na uanaharakati upo kwenye kanuni hiyo ya kutopendelea – kutoa ukweli wote kama ulivyo. Mwandishi wa habari atatoa ukweli wa hali halisi ilivyo bila kujali matokeo yake kwa jamii, ambapo kama ni mwanaharakati atachapisha vile vipengele vinavyoendana na fikra na lengo lake tu kwa kitu anachokipigania kwa wakati ule. Katika ngazi ya juu zaidi, sio maudhui tu yanayotumiwa,

bali hata kuwanyima watu vyombo fulani vya habari vinavyoweza kuonesha ukweli ulipo, kama vile kuvifungia.

Uanaharakati waweza kutekelezwa na watu katika umoja fulani au taasisi kama vile serikali. Kinachotumiwa ni maudhui yenye kushawishi umma ufanye au usifanye jambo fulani. Zana itumikayo ni vyombo vya habari. Kunyima umma huduma ya habari ili usiweze kufahamu au kuwa na mwamko wa kutenda jambo fulani, nao ni uanaharakati.

Uandishi wa habari nchini ulipata mtihani mkubwa wakati wa kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita, hasa kwa vile, kwa mara ya kwanza, vyombo vya habari mtandaoni vilidhibitiwa kwa kunyimwa matumizi ya mitandao ya kijamii, kama vile Facebook, You Tube, Instagram, Twitter, WhatsApp na nyingine kwa namna ambayo haikudhaniwa kuwa ingetokea nchini. Waliofanya hivyo waliona ndiyo njia ya kuzuia mitandao ya kijamii isisambaze habari za uzushi na pia kama njia ya kuzuia mawasiliano ili watu wasihamasishane kuandamana. Kuna haja ya kufuatilia kufahamu ufungiaji ule uliathiri vipi maisha ya wananchi na vyombo vya habari na ufanisi wake kwa jumla.

Ama hakika, kama wasemavyo wahenga, ‘wapiganapo fahali wawili, nyasi huumia’. Simu za mkononi zimekuwa chombo muhimu sana, sio tu kwa ajili ya mawasiliano, bali kwa kila aina ya maisha mengine – biashara, kilimo, kazi za ofisi na nyingine. Kunyimwa kutumia mitandao kuliathiri kwa kiasi kikubwa waendeshaji wa biashara mtandaoni, ambao ndio mtindo mpya wa kuuza na kununua vitu siku hizi. Maelfu

Endelea Ukurasa wa 17

Uandishi wa habari na uanaharakati …

Page 16: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

17

Uchambuzi

Toleo la 159, Novemba, 2020

ya watu walipata hasara na kupoteza wateja. Walihusika vipi kwenye mgongano huo wa serikali na vyombo vya habari au tuseme walikuwa wahanga wa uchaguzi huo? Labda.

Japo uchaguzi ulimalizika , ile falsafa ya Machiaveli kuwa matokeo huhalalisha njia iliyotumika kuyafikia, wakati huu haikukubalika na wengi, hasa mataifa yaliyo wabia wa maendeleo yetu ambao walitoa tahadhari kwa serikali kuwa kinachofanyika ni kinyume cha haki za binadamu. Vyama vya upinzani navyo vilipinga waziwazi suala hili kwani kufungia mitandao ni ishara ya ukandamizaji unaofifisha demokrasia. Kwa vyombo vya habari nchini ilikuwa kama kuweka chumvi kwenye kidonda kwani tayari vilikuwa vinalalamikia sheria za habari kuwa ni kandamizi.

Miezi michache tu kabla ya uchaguzi mkuu – Julai mwaka huu, serikali ilikuwa imetoa kanuni mpya za kudhibiti maudhui ya vyombo vya habari mtandaoni. Kanuni hizi zinahusu maudhui ya aina zote na kuweka adhabu kali za kifungo, faini au kufungiwa chombo ikiwa zitakiukwa.

Pamoja na makatazo hayo, huko nyuma vitisho na sheria kali vilitamalaki na kufanya wanahabari kukwepa utendaji itakiwavyo kitaaluma. Mifumo ya habari yenye uwezekano wa kuchukiza mamlaka imekuwa ikikwepwa, kama vile habari za uchunguzi, uchambuzi na maoni kinzani. Ili kuwa salama zaidi vingi ya vyombo vya habari hupendelea maudhui ya burudani kama michezo, muziki, katuni, tamthilia, umbea na hadithi na kukwepa tafakuri na majadiliano ya siasa za fani hizo.

Wakati mwingine waweza kujiuliza: Hivi vyombo vya habari ni kwa ajili ya nani – kuwafurahisha watawala au kuendeleza maslahi ya wananchi au vyote kwa pamoja? Wakati anafungua Bunge la 12 jijini Dodoma, Novemba 12, Rais Magufuli alionesha

kuridhika na utendaji wa vyombo vya habari katika kufanikisha uchaguzi mkuu uliopita na kuahidi kulinda uhuru na haki ya watu wote ikiwemo vyombo vya habari. Aliendelea kusema, pamoja na mengine kwa msisitizo kuwa uhuru na haki vinakwenda sambamba na huendana na wajibu na kumalizia kwa kusema, “Nadhani nimeeleweka vizuri” alisema.

Binafsi naona maneno hayo ya mwisho ya Rais huenda yanaashiria ukali wa hatua ambazo zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayedhaniwa kuwa ameenda kinyume na matakwa yake. Nadhani kutakuwa na hofu zaidi katika vyumba vya habari itakayofanya waandishi kujizuia zaidi wasibainishe ukweli wa mambo, jambo ambalo halitakuwa la manufaa kwa jamii. Hakutakuweko tena na kinga ya matumizi mabaya ya nguvu za kisiasa.

Katika mataifa yote, vyombo vya habari ni mhimili wa maendeleo. Katika nchi ya kidemokrasia kama ilivyotajwa kwenye katiba ya nchi yetu, umiliki na matumizi ya vyombo vya habari una jukumu la kuendeleza mifumo na taratibu za jamii hiyo. Vitaunga mkono miundo na mifumo ya utawala pamoja na ya uzalishaji ambayo ni ya asili kwa jamii bila kujali matakwa, mahali na aina ya watu wa sehemu fulani. Kama maelezo hayo ni sahihi, basi hatutarajii watawala walalamike kuwa vyombo vya habari vinapinga serikali au haviungi mkono jitihada za serikali. Kwa mantiki hiyo hiyo, haitarajiwi kuwa serikali itatengeneza mazingira ya kisheria au mengine yasiyo rafiki kwa utekelezaji wa vyombo vya habari inavyotarajiwa kuwa katika mfumo wa kidemokrasia.

Ni bahati mbaya sana kuwa kila upande unasuta mwingine kuwa kipingamizi cha juhudi zake. Hata yatolewe maelezo gani, ukweli unabaki kuwa kwa miaka yote umekuweko uhusiano wa kupendana na wakati huo huo kuchukiana. Na hili lipo katika mifumo yote ya

jamii zenye demokrasia. Kwa asili, serikali huwa na kawaida ya ‘kuficha’ mambo, wakati vyombo vya habari huwa na kawaida ya ‘kufichua’. Inakuwa vigumu kuwa na msimamo wa pamoja wa uhusiano wao.

Serikali inachukulia kuwa vyombo vya habari ni taasisi zenye kufanya kazi kwa ridhaa yake, japo haiwezi kuvifuta na kubaki bila chombo. Navyo vyombo vya habari vinaiona serikali kama mwezeshaji – mwekaji mazingira yafaayo ili viweze kutekeleza majukumu yake.

Matumizi ya vyombo vya habari ni kitu cha lazima katika jamii, kiasi kwamba wengine wanataka sekta ya habari itambulike kama mhimili wa nne wa dola, baada ya utawala, bunge na mahakama. Umuhimu wa vyombo vya habari umedhihirika vyema baada ya ujio wa njia-kuu ya habari, yaani intaneti, inayowezesha matumizi ya vyombo vya kijamii. Wakati utafika jamii itagundua kuwa bila vyombo vya habari mihimili yote ya dola haiwezi kutekeleza kwa ufanisi majukumu yake.

Ugonjwa wa COVID 19 umeashiria hali inayokuja. Katika nchi nyingi, mikutano ya baraza la mawaziri, bunge, mahakama na taasisi nyingine imekuwa ikifanywa kupitia mtandao. Utaratibu huu ukizoeleka utakuwa ndio utamaduni mpya kwani unaokoa gharama, muda, salama kwa maisha na manufaa mengine. Wananchi wa kawaida hupata mrejesho wa haraka na pia waweza kujumuisha mtu yeyote katika mijadala kwa urahisi kama njia mojawapo ya kukuza demokrasia. Hivyo Rais anapoahidi kuwa utawala wake utaendeleza vyombo vya habari, asisahau kuwa huko tuendako ni muhimu sana kwa sekta hiyo kuimarishwa kwani inaingiliana na maendeleo ya sekta nyingine zote.

Kizungumkuti kiko hapo: ni vyombo vya habari vya serikali na chama chake au vile binafsi vilivyo huru? Kwa miaka minne hivi nimegundua kuwa vyombo

Uandishi wa habari na uanaharakati … Inatoka Ukurasa wa 16

Endelea Ukurasa wa 18

Page 17: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Uchambuzi

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

18

vya habari vinathaminiwa tu ikiwa vinakubali kutumiwa kwa malengo ya utawala na si vinginevyo. Dhana ya vyombo huru vinavyofanya kazi kwa maslahi ya umma na kulinda misingi ya demokrasia haikubaliki. Hii inakinzana na uelewa wangu wa dhima ya mwandishi wa habari katika jamii, ambayo pamoja na mengine, inahusu kufurahisha na kuudhi kwa maslahi mapana ya jamii.

Vyombo vya habari vina watu wenye elimu na waliopata mafunzo mbalimbali ya nadharia na vitendo katika taaluma ya uandishi wa habari. Hawana upungufu wa elimu, na wanajua kabisa kuwa katika kutenda kazi zao kuna wakati watakwaruzana na mamlaka mbalimbali. Ndivyo wanavyofundishwa.

Uadilifu wa vyombo vya habari ni kuwafanya wasiotekeleza majukumu ipasavyo kuwajibishwa na wananchi kwa kuonesha wanavyokwenda kinyume cha tunu zetu.

Uaminifu wa umma kwa vyombo vya habari ulikuwa mkubwa kwa vile vyombo hivyo vilikuwa vinazingatia vyema maadili ya wakati huo. Kulikuwa hakuna kabisa kitu matusi au lugha za kuudhi kama ilivyo siku hizi kwenye baadhi ya mitandao. Mawazo mbadala yalivumiliwa na kukaribishwa. Hili ndilo lililofanya uandishi wa habari wakati ule usionekane kuwa ni uanaharakati mtupu.

Moja ya mienendo inayotia hofu ya viongozi wetu wa kisiasa ni kutaka kufanya uandishi wa habari uwe uanaharakati wa kutetea awamu nzima ya serikali bila kujali hali ya mwananchi mmoja mmoja katika jamii ambapo kunakuwa hakuna wa kumtetea. Chombo kinachojaribu kufanya hivyo kinachukuliwa kuwa adui na kwa kuhofia madhara yake inabidi kutosa uhuru wa taaluma. Hali inazidishwa na ukweli kuwa wengi wa wamiliki

wa vyombo binafsi, tunavyoamini kuwa ndivyo huru, ni makada wa chama kinachotawala, na wakati mwingine wanaweza kuwa kwenye safu ya uongozi wa chama. Wamiliki wa aina hii mara zote hujiamini sana kiasi cha kutoa maelekezo ya kiuhariri katika masuala mbalimbali.

Kadhalika kuna ukweli kuwa ajira ya waandishi siku hizi imepungua sana kutokana na uchumi wa vyombo hivyo kufifia kwa sababu mbalimbali, na hivyo wanahabari wanajikuta wakifuata malekezo yaliyo kinyume na taaluma yao ili wabaki kwenye ajira. Kinachotoka kwenye vyombo hivyo ni uanaharakati mtupu na sio uandishi wa habari.

Tunapojivunia uadilifu wa vyombo vya habari, kanuni kubwa ni kule kuhakikisha maudhui yanalenga maslahi ya jamii na kwamba hakuna hongo, rushwa wala vitisho vitakavyoweza kuzuia utekelezaji wa azma hiyo ya kulinda maslahi ya umma. Kwa bahati mbaya, kama ilivyoripotiwa katika makala za nyuma za jarida hili, vyombo vingi vimeacha kujishughulisha na maudhui yanayolinda maslahi ya umma kama vile uandishi wa uchunguzi, utafutaji maoni kuhusu masuala nyeti ya jamii na barua na maoni kwa mhariri - kwa kifupi uandishi wa ulinzi. Badala yake tunashuhudia uandishi wa kujihami unaokwepa masuala tata, kusifu serikali hata kama hakuna stahili, kujaza muda na nafasi kwa maudhui ya burudani kama muziki, michezo, mahojiano na wasanii, maudhui ya elimu ya shule na makala zenye kuonesha kuelezea utengenezaji wa vitu mbalimbali. Wanakwepa kabisa masuala yahusuyo siasa na utekelezaji wake katika kuleta maendeleo ya fani hizo za burudani.

Sisemi kuwa maudhui ya burudani hayatakiwi, ila iwepo tahadhari isije ikatawala na kuchukua nafasi ya maudhui ya ulinzi wa umma, hata kama ni

kwenye maudhui hayo hayo ya burudani kwani ni yetu na ni utamaduni wetu, hatuna budi kuulinda. Hakuna mwandishi anayeweza kudai kuwa hafahamu maslahi ya umma ni yapi. Katiba ya nchi yetu (1977) inaonesha vizuri ni nini kinahitaji kulindwa. Kifungu chochote cha katiba hiyo chahitaji ulinzi kisivunjwe na ikiwa imetokea, yabidi waandishi wawe wa kwanza kuutaarifu umma. Haijalishi heshima ya huyo mtu kwenye jamii, kwani hata Rais wa nchi anaapa kuilinda na kuitetea katiba.

Sera za nchi zinatokana na katiba na ambazo huongoza utungaji wa sheria mbalimbali. Matumizi na utekelezaji wa sheria hizo wahitaji uangalizi mkubwa wa vyombo vya habari. Kwa bahati mbaya tumekuwa tunasikia zaidi utetezi wa haki za mwananchi zilizowekwa kwenye Sura ya Kwanza Sehemu ya Tatu – Haki na Wajibu Muhimu na kupumbazwa kabisa tukasahau kuwa sehemu nyingine saba zilizosalia za katiba nazo zastahili jicho la mwandishi wa habari. Ingesaidia sana ikiwa uchambuzi na tahakiki zifanywazo zinatokana na uelewa wa katiba inasema nini kuhusu utawala wa masuala ya nchi. Uwepo wa ufahamu huo unampa mwandishi ujasiri wa kukabiliana na vitisho na kutenda kazi bila hofu na upendeleo. Ufahamu wa nini kinachofanya maslahi ya jamii au umma ndio ngao ya kwanza ya ulinzi dhidi ya yeyote.

Mwandishi wa habari tujuavyo anapaswa, kutokana na kanuni kuripoti ukweli wote bila kujali matokeo yake hata kama ikiwa kwa kufanya hivyo anaenda kinyume cha imani na manufaa ya jamii yake. Uandishi wa habari wa aina hiyo unatoweka haraka duniani na badala yake upo uandishi wa kuwajibika wenye kupima kwanza manufaa ya kinachochapishwa kwa jamii na kama kufanya hivyo haki imetendeka. Ni mchanganyiko wa uanaharakati na uandishi wa habari unaowajibika.

Inatoka Ukurasa wa 17

Uandishi wa habari na uanaharakati …

Page 18: Mmetoa mchango mkubwa - WariobaToleo la 159, Novemba, 2020 ISSN 0856-874X EJAT 2020 yaanza Wahariri wazungumzia changamoto MCT yapata hadhi ya uangalizi Uk 5 Uk 9 Uk 20 Mmetoa mchango

Na Mwandishi wa Barazani

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limepewa hadhi ya uangalizi katika Tume ya Haki za Binadamu ya

Afrika (ACHPR). “Haya ni mafanikio makubwa

kwa MCT”, amesema Katibu Mtendaji wa Baraza, Kajubi Mukajanga.

Akizungumzia hadhi mpya ya Baraza, Mukajanga alisema “tutaitumia kukuza ajenda za MCT na kufikisha masuala mbalimbali katika chombo hicho cha juu cha Bara la Afrika na mbele zaidi”.

Tangazo hilo la kuipa MCT hadhi ya uangalizi halikuwa limetegemewa kutokana na ukweli kwamba Baraza limekuwa likifuatilia ombi lake kwa miaka miwili bila dalili zozote za maana kutoka Tume hiyo, alieleza Mukajanga katika taarifa aliyoitumia Bodi ya Baraza.

Hii maana yake nini kwa Baraza? MCT sasa itakuwa na uwezo wa kushiriki katika vikao vya wazi vya Tume na kuweza kuwasilisha ripoti.

“Tunaweza pia kualikwa kushiriki katika vikao vya ndani vinavyoshughulikia masuala yanayotuhusu”, Mukajanga amesema na kwamba Mwenyekiti wa Tume anaweza kutoa nafasi kwa waangalizi kujibu maswali yanayowahusu yanapoulizwa na washiriki katika mikutano.

Aidha alisema Baraza linaweza pia kuomba kuwa na masuala yake kuingizwa kwenye ajenda za Tume kulingana na Taratibu na Kanuni za Tume.

MCT hivi karibuni ilishiriki katika mikutano ya mtandaoni kuanzia Novemba 9, 2020. Mkutano wa kwanza ulikuwa ni jukwaa kwa ushiriki wa taasisi zisizo na kiserikali na za kijamii katika Mkutano wa Kawaida wa 67 wa ACHPR na kufuatiwa na mkutano wa 67 wa ACHPR.

MCT ilipatiwa hadhi ya uangalizi katika kikao cha

kawaida cha 67 cha Tume kilichofanyika Novemba 17, 2020 na mojawapo ya agenda za kikao hicho ilikuwa kusikiliza maombi

ya hadhi ya ushiriki kutoka taasisi za haki za binadamu za kitaifa na hadhi ya uangalizi ya mashirika yasiyo ya kiserikali.

MCT yapewa hadhi ya uangalizi Tume ya Haki za Binadamu Afrika

Kamishna Jamesina Essie L. King aliyependekeza kufikiriwa kwa ombi la Baraza la Habari la Tanzania kupewa hadhi ya uangalizi katika Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika (ACHPR).

Habari

Toleo la 159, Novemba, 2020

19