Upload
others
View
1
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
MODULI NAMBA 2
Uandaaji sahihi wa kitalu cha miche
MKULI
MA WA MITI
ShukuraniKIJITABU HIKI KIMEANDALIWA KWA AJILI YA KUFIKISHA MAUDHUI YA TAALUMA YA NAMNA YA KUANZISHA NA KUENDELEZA BUSTANI YA MITI KWA MKULIMA MDOGO NA MKUBWA PIA.
KIMEANDALIWA KWA MICHORO ZAIDI ILI KUMRAHISISHIA MSOMAJI KUJARIBU KILA KITU KWA USAHIHI ZAIDI. MARA BAADA YA KUKAMILIKA, KIMEPITISHWA KWA WADAU MBALIMBALI NA WATAALAMU WA MISITU ILI KUTOA UZOEFU NA UTAALAMU WAO ILI KUBORESHA UTOAJI WA MAFUNZO SAHIHI YA UANZISHWAJI NA UENDELEZAJI WA BUSTANI YA MITI HAPA TANZANIA.
NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA TAASISI YA UENDELEZAJI WA MISITU TANZANIA HUSUSANI KITENGO CHA huduma kwa wakulima wa miti KWA KUWEZESHA KAZI HII KUKAMILIKA.
PIA NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA WAFADHILI WA TAASISI HII AMBAO NI GATSBY NA dfid KWA KUWEZESHA KUFADHILI UANDAAJI WA KIJITABU HIKI.
MWISHO, NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA BWANA JOSEPH MAKANZA KWA KUCHORA MICHORO na kusanifu KIJARIDA HIKI NA PIA SHUKURANI ZA PEKEE KWA BWANA HAMISI MALINGA NA GEORG STRUNDEN KWA USHAURI WA KITAALAMU KUHUSIANA NA MICHORO NA MAUDHUI yA KITABU HIKI.
1
Utangulizi
Watafiti na wataalam wa misitu wanaamini kuwa watanzania wengi wamehamasika na wanapenda kilimo cha miti ya mbao.
Moduli hii inatoa maelekezo ya namna ya kuzalisha miche bora itokanayo na kupanda mbegu bora, inatoa mafunzo ya namna ya upandaji mzuri wa mbegu na uanzishaji mzuri wa mashamba ya miti.
Inatoa mwongozo kwa wenye bustani za miti ili nao watoe mafunzo ya namna ya upandaji mzuri kwa wanunuzi wa miche. Hatua zilizoelezewa humu zinahusisha uandaaji kwa mbegu za Milingoti na Paina pia.
Moduli hii itatueleza kisa cha MACHOKODO aliyenufaika kwa Kilimo cha Miti baada ya kujifunza na kutumia utaalam alioupata kutokana na mafunzo kujitengenezea faida na kubadili Maisha yake.
1. MAANDALIZI YA KUWATIKA MBEGU
2
HAKIKISHA UNATUMIA MBEGU BORA KWA KUWA ZITAKUPA UKUAJI WA HARAKA NA KUKUPA KIPATO KWA MUDA MFUPI. BUSTANI NZURI BILA MBEGU BORA HAINA FAIDA KABISA.
Unapotaka kuwatika MBEGU Chagua eneo ambalo linafaa kwa kutengeneza tuta la kusia mbegu ambalo lina mteremko, jua kidogo NA ULINZI KUHAKIKISHA MICHE AIHARIBIWI
Pima eneo ambalo ni msitatili KWa futikamba.
Pima kama futi 4 kwa futi 10 au zaidi kulingana na miche unayotaka kuzalisha.
JUU YAKE WEKA KAMA INCHI 2”-3” ZA MCHANGA WA KAWAIDA...MCHANGA JUU YA TUTA LA KUOTESHEA HUSAIDIA KATIKA UOTAJI WA MBEGU NA HURAHISISHA UNG’OAJI WA MICHE WAKATI WA KUHAMISHA MICHE KWENDA KWENYE VIRIBA
Weka sawa udongo kwa kutumia rake na kupigapiga udongo ili ulainike. Pia toa mawe, magugu na vijiti kwenye hilo tuta lenye sura ya kitanda
3
Lima kwa kuinua tuta lenye urefu tajwa AU PIGILIA MABANZI NA JAZA UDONGO. Sawazisha kwa kutumia jEMBE AU mpini wa jembe au ubao ili kupata tuta lililo na sura ya kitanda.
EPUKA MAKOSA/ZINGATIA
UsiwekE Mbolea ya samadi kwenye tuta la kuoteshea mbegu....Samadi huwa na vimelea wengi ambao huweza kuathiri uotaji wa mbegu. Samadi husababisha kuwepo na wadudu kama minyoo, funza na wadudu wengi ambao hukata mizizi ya miche na wadudu wengine hula mbegu kabla ya kuota na kusababisha hasara kubwa sana
Weka mchanga juu ya tuta ili kurahisisha Uotaji wa miche...
MCHANGA HUSAIDIA MBEGU KUOTA HARAKA, PIA HUSAIDIA UNAPOHAMISHIA KWENYE VIRIBA MCHANGA HUACHIA MICHE BILA KUNG’ANG’ANIA
4
INCHI 2-3 zA mchanga
udongo
2. KUSIA MBEGU KWENYE TUTA
Mbegu za milingoti (Eucalyptus) ni ndogo ndogo sana, changanya mbegu na mchanga Kipimo 1 cha MLINGOTI na vipimo 3 vya mchanga kisha sambaza juu ya tuta
Kwa mbegu za Paina chora vistari kwenye tuta na kuzimwaga bila kuchanganya na mchanga funika na mchanga kidogo.
Mwagilia maji taratibu bila kusababisha udongo kutepeta kwa maji.
Funika kwa nyasi KAVU kwa muda wa wiki moja (2) hadi tatu (3).... NYASI HUONGEZA JOTO KWA UDONGO NA KUSISIMUA UOTAJI WA HARAKA NA NYASI ZIONDOLEWE BAADA YA KUONA MAJANI MAWILI YAKIWA YAMEANZA KUTOKA KWA MBEGU ( KUOTA)
mbegu mchanga
5
Mwagilia mara mbili kwa siku vizuri, asubuhi na jioni.
kumwagilia maji mpaka udongo unatepeta KUNAWEZA kusababisha ugonjwa wa ukungu (Fangasi), wadudu waharibifu kama minyoo, funza na panzi....
Ukiona dalili zozote za magonjwa ya miche bustanini pata ushauri wa Mtaalamu wa Misitu ili akueleze ni dawa gani waweza kutumia
ASUBUHI JIONI
6
baada ya wiki 3 Funika kwa nyasi kwa paa la mwinamo...
KAMA ENEO LA BUSTANI LINA JUA KALI SANA FUNIKA MICHE KWA NYASI
EPUKA MAKOSA/ZINGATIA
usifanye hivi namna hivi
udongo wa msitunivipimo 3
udongo wa mfinyanzi.vipimo 3
mchanga.kipimo 1
Udongo wa kujaza
kwenye viriba.
3. KUCHANGANYA UDONGO WA KUJAZA KWENYE VIRIBA
Kwa Milingoti Weka:-
7
Kipimo: lori, tOLORI, beseni, DEBE
Kwa Paina Weka :-
udongo wa msituniVIPIMO 3
udongo wa mfinyanzi.VIPIMO 3
mchanga.KIPIMO 1
Udongo wa kujaza
kwenye viriba.UDONGO TOKA MSITU WA PAINA (MYCORRHIZA)
KIPIMO 1
Kipimo: lori, tOLORI, beseni, DEBE
Sasa unaweza kujaza Udongo kujaza kwenye viriba...
KABLA YA KUANZA KUJAZA UDONGO KWENYE VIRIBA, NYUNYIZA MAJI UDONGO, UCHANGANYE UDONGO VIZURI, INGIZA VIDOLE VIWILI NDANI YA KIRIBA, JAZA UDONGO, SHINDILIA VIZURI KISHA PANGA KWENYE MISTARI. UKUBWA WA VIRIBA NI INCHI 3-4 KIPENYO NA UREFU NI INCHI 3
8
EPUKA MAKOSA/ZINGATIA
Chekecha udongo ili kuondoa mizizi na takataka nyingine halafu changanya vizuri kabla ya kujaza kwenye viriba
DOKEZO KUHUSU VIRIBA
KILO MOJA YA PLASTIC NI SAWA NA VIRIBA TUPU 600 VYA INCHI 3 KWA 4. MCHANGANYO WA UDONGO TOLOLI MOJA NI SAWA NA VIRIBA 470
Ili kuhamisha miche Anzia kwenye kona YA TUTA KWA KUnyanyua udongo kwa kijiti, kisha ingiza mkono chini na inua mche au miche kadhaa mkononi.
4. KUHAMISHIA MICHE KWENYE VIRIBA
IWEKE MICHE HIYO KWENYE CHOMBO KAMA BAKULI IKIWA NA MAJI NA ANZA KUPANDIKIZA MICHE MMOJA KWA KILA KIRIBA
9
...hamisha mche kutoka katika tuta la kusia mbegu kwenda kwenye viriba...
Panga viriba vilivyo na miche kwenye mstari eneo ambalo ni safi kama uwanja.
MWAGILIA MICHE HIYO MARA MBILI KWA SIKU. MWAGILIA KILA SIKU ASUBUHI NA MAPEMA NA JIONI...TUMIA CHOMBO CHENYE MATUNDU MADOGO KUEPUSHA KUDHURU MICHE
10
Wakati wa Kuhamisha miche shika kwenye vijani viwili (coteledons) na usishike kwenye SHINA AU mizizi. Kwa kushika kwenye mizizi kunaweza kusababisha kufa kwa mche kwani... vidole huwa na chumvichumvi na mafuta ambavyo huDHURU mche.
IKIWA UMECHELEWA KUOTESHA MICHE UNAWEZA KUONGEZA UKUAJI HARAKA BUSTANINI KWA KUPIGA MBOLEA YA NPK YA MAJIMAJI INAYOITWA BUSTA PAMOJA NA KUPIGA DAWA YA KUUA WADUDU WAHARIBIFU WA MICHE
EPUKA MAKOSA/ZINGATIA
Epuka MIZIZI ILIYOJIKUNJA KAMA HERUFI (J)...TOBOA SHIMO LA KUTOSHA KWA KIJITI NA SI KWA KIDOLE, chomeka mchE halafu vuta juu kidogo ili mzizi usipinde
11
...EPUKA KUMWAGILIWA MAJI MENGI SANA MPAKA MICHE INAZAMISHWA KWENYE MAJI
5.KUPUNGUZA/KUKATA MIZIZIKata mizizi kila unapoona inaanza kuingia ardhini KWA KUtumia kisu kikali au waya....Au hamisha miche kila baada ya wiki mbili
Hiki ni kitendo cha kuikomaza miche kwa kupunguza kiwango cha umwagiliaji maji ili ianze kuzoea hali ya shambani itakakopandwa
6. KUIKOMAZA MICHE
12
mizizi haijakatwa
mizizi imekatwa
ng’oa magugu kwenye viriba
BAADA YA MIEZI SITA MICHE YAKO ITAKUWA TAYARI KWA KUPANDWA SHAMBANI AU KUUZA KWA MTEJA
...urefu unaofaa kwa kupandwa milingoti ni Sentimeta 20-25 na Mipaina ni sentimeta 10-15
SABABU YA KUIKOMAZA MICHE NI KWA AJILI YA KUIANDAA MICHE KWA MAZINGIRA MAGUMU YA SHAMBANI NA PIA HII HUFANYIKA KWA MICHE ILIYOBAKI MPANDO WA MWAKA HUO NA KUSUBIRI HADI MPANDO WA MWAKA MWINGINE...
KAMA NINATAKA KUANZISHA KITALU CHA KIBIASHARA MAMBO GANI YA KUZINGATIA?
ZINGATIA ENEO LA BUSTANI LIWE NA CHOO, STOO, OFISI, MAJI YA KUNYWA. PIA TUNZA KUMBUKUMBU ZOTE ZA UZALISHAJI NA MAUZO.
13
14
7. GHARAMA ZA KUKUZA NA KUUZA MICHE
dr ULALO WA FAIDA NA HASARA CR
MTAJI/ MAPATO MATUMIZI/ GHARAMA
Mtaji wa fedha (Saccos) 5,000 Kununua reki 700
Nyongeza ya mtaji 100,000 Kulipa vibarua 40,000
Kununua viriba 14,000
Kununua mbegu 50,000
Mauzo ya miche 200,000 Kununua jembe 2,000
Mauzo ya miche 50,000 Vibao vya kwenye matuta 500
Mauzo ya miche 20,000 Kutengeneza bango 1,000
Kununua makeni 3,000
Kununua madawa 3,000
Tofauti ( faida) 254,500
JUMLA 375,000 JUMLA 375,000
*angalizo: tarakimu zilizoandikwa hapa ni mfano tu.
Ukiona matumizi ni makubwa kuliko MAPATO Ujue umefanya biashara kwa HASARA
Ukiona Mtaji au mapato ni Makubwa kuliko matumizi ujue kuwa umefanya biashara kwa FAIDA. Jumlishia pembeni kwanza kisha jumla iliyo kubwa kati ya kulia na kushoto ndiyo iandikwe kwenye jumla kuu. Kisha kama kushoto ndio kudogo andika TOFAUTI HASARA au kama kulia ndio kudogo Zaidi hivyo juu ya jumla kuu andika TOFAUTI FAIDA
kisha andika hiyo tofauti ili UWEKE UWIANO/ BALANSI.
15
Vigezo vya mahali sahihi pa kuweka bustani
1. Mahali panapofikika vizuri kwa gari2. Mahali ambapo nguvukazi inaweza patikana
kiurahisi3. Mahali ambapo pana maji ya uhakika4. Mahali ambapo hapana mteremko mkali5. Mahali ambapo rasilimali muhimu kama udongo
vinapatikana mapema.6. maji kwa ajili ya umwagiliaji
Mbegu bora maana yake nini?
Ni mbegu zilizotokea kutoka kwenye miti iliyopandwa maalumu kwa ajili ya kuzalisha mbegu na kwamba Chavusha ( Poleni) hutoka katika uzao ambao ni bora na hufanywa kwa mikono ya wataalamu au wadudu toka katika miti ( Baba) yenye uzao mzuri.
Vitu vya muhimu kuwepo katika bustani ya kibiashara
1. Pawepo choo kwa ajili ya wafanyakazi na wageni2. Pawepo ofisi na stoo kwa ajili ya nyaraka na
vifaa vya bustani3. Weka wigo kwa ajili ya kulinda miche yako4. Maji safi kwa ajili ya kunywa wafanyakazi na
wageni bustanini5. Bango kwa ajili ya kutangaza biashara yako
(Biashara matangazo)
Jedwali la Kalenda ya shughuli za bustani za miti
SHUGHULI MUDA WA MWAKA
1. Kuchagua eneo la kuweka bustani Mei
2. Kuagiza/ kununua mbegu za Mipaina Mei na Juni
3. Kuandaa bustani ya mipaina Juni
4. Kukusanya udongo kwa ajili ya bustani Juni
5. Kutengeneza tuta la kusia mbegu Juni
6. Kuchanganya udongo kwa ajili ya
kuweka kwenye viriba Juni/ Julai
7. Kujaza udongo kwenye viriba Julai
8. Kuhamisha miche kwenye viriba Julai
9. Umwagiliaji wa miche iliyoko
kwenye viriba Julai- Desemba
10. Kuandaa bustani ya Milingoti Septemba
11. Kutengeneza tuta la kusia
mbegu za Milingoti Septemba
12. Kuchanganya udongo kwa Septemba/
ajili ya Milingoti Oktoba
13. Kuhamisha miche kwenye viriba Oktoba
14. Umwagiliaji wa miche iliyoko Oktoba/
kwenye viriba Novemba
15. Kung’oa magugu kwenye miche
ya Milingoti na Mipaina Novemba
16. Kukata Mizizi kwenye Mipaina
na Milingoti Novemba
17. Kukomaza miche Mipaina na Novemba/
Milingoti Desemba
18. Kupanda mashambani/ kuuza Desemba-
Mipaina na Milingoti Februari
16
FORESTRY DEVELOPMENT TRUSTUENDELEZAJ I M IS ITU TANZANIA
2 0 B A L O Z I R O A D , G A N G I L O N G A , I R I N G A , P O B O X 2
t : + 2 5 5 2 6 2 7 0 0 5 5 0 | I N F O @ F O R E S T RY- T R U S T. O R G