10
MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA RASILIMALI MIANZI AFRIKA YA MASHARIKI KWA KUSHIRIKIANA NA NCHI YA UHOLANZI NA CHINA- KENYA TAARIFA ZA KIUFUNDI UJENZI WA TANURU LA MATOFALI LA MKAA WA MIANZI UTANGULIZI Katika nchi nyingi zinazoendelea na ambazo hazijaendelea Asia na Afrika, kuni na mkaa ni chanzo cha nishati inayotumika katika kaya, hii imepelekea ukataji wa miti na uharibifu wa misitu ya asili. Hiki ni kiashiria cha uhitaji wa kupata haraka vyanzo mbadala vya nishati ili kutumika kama mbadala wa nishati ya kuni na mbao. Mianzi unaweza kutumika kama mbadala endelevu wa nishati ya kuni na mbao. Mianzi unakua haraka na ku- komaa kati ya miaka 4 mpaka 6. Mara shina la mianzi unapofika umri wake wa kukomaa, inatoa fursa ya uvunaji endelevu wa kila mwaka na kusaidia kutokata ovyo misitu na uharibifu wa mazingira. Muanzi unaweza ukatu- mika moja kwa moja kama kuni au unaweza ukabadilishwa kuwa nishati ya mkaa. Kiutamaduni, mkaa unazalishwa kwa njia ya kienyeji, huchimbwa shimo na kufunikwa na udongo au tanuru la asili. Uzalishaji na uvunaji wa mkaa kwa njia hii ni mdogo. Njia mbadala ya kuzalisha na kuvuna mkaa mwingi ni kutumia tanuru lililojengwa kwa tofari lenye umbo kama tufe, ufanisi wa uzalishaji wa mkaa kwa njia hii ni mkubwa na ni salama. Mkaa unatengenezwa kwa njia ya kudhibiti hewa inayoingia na kutoka kwenye tanuru, ambapo unazalishwa mkaa mzuri wa viwango bora na kiwango kikubwa cha moto na joto na majivu machache. NAMNA YA KUCHAGUA ENEO Tanuru la kuzalisha mkaa wa mianzi linatakiwa kujengwa karibu na eneo lililo na mianzi mingi (misitu ya mianzi, mashamba ya mianzi na sehemu za makazi zilizo na mianzi ya kutosha) ili kupunguza gharama za usafiri. Tanuru la kutengeneza mkaa pia linatakiwa kuwa karibu na miundombinu ya barabara, relii n.k ili kusafirisha mkaa na brikuiti sokoni kiurahisi.

MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA ......Kwa kujenga sehemu ya juu iliyo na umbo la tufe, wenye unene wa ukuta kwa sentimita 9, ujazo wa mita 0.7 za tofari zitahitajika. Tafadhari piga

  • Upload
    others

  • View
    4

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA ......Kwa kujenga sehemu ya juu iliyo na umbo la tufe, wenye unene wa ukuta kwa sentimita 9, ujazo wa mita 0.7 za tofari zitahitajika. Tafadhari piga

MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA RASILIMALI MIANZI AFRIKA YA MASHARIKI KWA KUSHIRIKIANA NA NCHI YA UHOLANZI NA CHINA- KENYA

TAARIFA ZA KIUFUNDI

UJENZI WA TANURU LA MATOFALI LA MKAA WA MIANZI

UTANGULIZI

Katika nchi nyingi zinazoendelea na ambazo hazijaendelea Asia na Afrika, kuni na mkaa ni chanzo cha nishati inayotumika katika kaya, hii imepelekea ukataji wa miti na uharibifu wa misitu ya asili. Hiki ni kiashiria cha uhitaji wa kupata haraka vyanzo mbadala vya nishati ili kutumika kama mbadala wa nishati ya kuni na mbao.Mianzi unaweza kutumika kama mbadala endelevu wa nishati ya kuni na mbao. Mianzi unakua haraka na ku-komaa kati ya miaka 4 mpaka 6. Mara shina la mianzi unapofika umri wake wa kukomaa, inatoa fursa ya uvunaji endelevu wa kila mwaka na kusaidia kutokata ovyo misitu na uharibifu wa mazingira. Muanzi unaweza ukatu-mika moja kwa moja kama kuni au unaweza ukabadilishwa kuwa nishati ya mkaa.Kiutamaduni, mkaa unazalishwa kwa njia ya kienyeji, huchimbwa shimo na kufunikwa na udongo au tanuru la asili. Uzalishaji na uvunaji wa mkaa kwa njia hii ni mdogo. Njia mbadala ya kuzalisha na kuvuna mkaa mwingi ni kutumia tanuru lililojengwa kwa tofari lenye umbo kama tufe, ufanisi wa uzalishaji wa mkaa kwa njia hii ni mkubwa na ni salama. Mkaa unatengenezwa kwa njia ya kudhibiti hewa inayoingia na kutoka kwenye tanuru, ambapo unazalishwa mkaa mzuri wa viwango bora na kiwango kikubwa cha moto na joto na majivu machache.

NAMNA YA KUCHAGUA ENEO

Tanuru la kuzalisha mkaa wa mianzi linatakiwa kujengwa karibu na eneo lililo na mianzi mingi (misitu ya mianzi, mashamba ya mianzi na sehemu za makazi zilizo na mianzi ya kutosha) ili kupunguza gharama za usafiri.Tanuru la kutengeneza mkaa pia linatakiwa kuwa karibu na miundombinu ya barabara, relii n.k ili kusafirisha mkaa na brikuiti sokoni kiurahisi.

Page 2: MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA ......Kwa kujenga sehemu ya juu iliyo na umbo la tufe, wenye unene wa ukuta kwa sentimita 9, ujazo wa mita 0.7 za tofari zitahitajika. Tafadhari piga

MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA RASILIMALI MIANZI AFRIKA YA MASHARIKI KWA KUSHIRIKIANA NA NCHI YA UHOLANZI NA CHINA- KENYA

TAARIFA ZA KIUFUNDI

UJENZI WA TANURU LA MATOFALI LA MKAA WA MIANZI

MCHAKATO WA HATUA KWA HATUA

Maandalizi ya ardhi

1) Sawazisha sehemu ya kujenga tanuru katika seh-emu ulilopanga kujenga (kiwango cha chini ni mita 5 X 5).

2) Tengeneza sehemu iliyoinuka (jukwaa) kama msingi: Ukubwa: 5 M X 5 M. Tumia vifaa vinavyopa-tikana eneo husika kama mawe au matofali kwa seh-emu ya nje ili kubeba udongo ndani.

3) Weka zege lenye ujazo (unene) wa inchi 2 mpaka 3 (faida ya kujenga jukwaa kwa simenti, itakuwa rahisi kutunza mkaa na brikuiti). Pia unaweza ukajenga juk-waa kwa udongo.

4) Jenga muundo rahisi au sehemu ya kivuli kwa ajili ya kazi ( Mita 5 X 5 ) kwa kutumia vifaa vinavyopati-kana kufunika tanuru la mkaa (mfano nguza za miti). Paa laweza kufunikwa kwa mabati au mabati ya CGI (kutegemeana na bajeti).

Page 3: MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA ......Kwa kujenga sehemu ya juu iliyo na umbo la tufe, wenye unene wa ukuta kwa sentimita 9, ujazo wa mita 0.7 za tofari zitahitajika. Tafadhari piga

MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA RASILIMALI MIANZI AFRIKA YA MASHARIKI KWA KUSHIRIKIANA NA NCHI YA UHOLANZI NA CHINA- KENYA

TAARIFA ZA KIUFUNDI

UJENZI WA TANURU LA MATOFALI LA MKAA WA MIANZI

MICHORO

Ujengaji wa tofari katika msingi

Muonekano wa Tanuru la Tofari

Angalia: sehemu ya kuwashia moto ipo juu ya tanuru na sio sehemu ya chini.

Ujengaji wa tanuru la mkaa ndani ya eneo la kazi lililofunikwa

Pembe tofauti/kutegemea na vipimo

Eneo la kufanyia kazi za kutengeneza brikuiti na

kutunzia mkaa

Tanuru la mkaa lenye sura ya tufe

Nusu kipenyo sm 120

Kipenyo sm 140

Jinsi duara linaloanza kujengwa na linavyoonekana

Page 4: MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA ......Kwa kujenga sehemu ya juu iliyo na umbo la tufe, wenye unene wa ukuta kwa sentimita 9, ujazo wa mita 0.7 za tofari zitahitajika. Tafadhari piga

MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA RASILIMALI MIANZI AFRIKA YA MASHARIKI KWA KUSHIRIKIANA NA NCHI YA UHOLANZI NA CHINA- KENYA

TAARIFA ZA KIUFUNDI

UJENZI WA TANURU LA MATOFALI LA MKAA WA MIANZI

1) MatofariUkubwa wa tofari unatofautiana nchi kwa nchi au mkoa kwa mkoa.Mfano 1: Kama ukubwa wa tofari ni sentimita 22 X 9 X 5; wastani wa tofari zitakazohitajika itakuwa ni 1700.Mfano 2: Tofari kubwa, sentimita (19 X 9 X 9) kwa ukuta wa chini mrefu, wastani wa tofari 1150: tofari ndogo, ukubwa wa sentimita (19 X 9 X 4) sehemu ya juu yenye umbo ya tufe: tofari zinahitajika wastani wa 1000.Makadilio: Ikiwa sehemu ya chini yenye ukuta wenye unene wa sentimita 19, ujazo wa mita 1.80 ya tofari zitahi-tajika. Kwa kujenga sehemu ya juu iliyo na umbo la tufe, wenye unene wa ukuta kwa sentimita 9, ujazo wa mita 0.7 za tofari zitahitajika. Tafadhari piga hesabu ya tofari zinazohitajika kwa mujibu wa ukubwa wa tofari zilizopo.

Vifaa vinavyotakiwa

Mpangilio wa tofari kwa tanuru lote lenye umbo la tufe

Tafadhari kumbuka:Unapojenga sehemu ya ukuta wa chini, to-fari kubwa zinaweza kutumika; unapojenga sehemu iliyo na umbo la tufe, sehemu ya juu ya ukuta, matofari yenye unene mdogo ni mazuri kutumika (tofari zenye unene chini ya sentimita 4) ni rahisi kujengea.

Page 5: MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA ......Kwa kujenga sehemu ya juu iliyo na umbo la tufe, wenye unene wa ukuta kwa sentimita 9, ujazo wa mita 0.7 za tofari zitahitajika. Tafadhari piga

MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA RASILIMALI MIANZI AFRIKA YA MASHARIKI KWA KUSHIRIKIANA NA NCHI YA UHOLANZI NA CHINA- KENYA

TAARIFA ZA KIUFUNDI

UJENZI WA TANURU LA MATOFALI LA MKAA WA MIANZI

Vifaa vinavyotakiwa

2) UDONGO WA MFINYANZITafuta udongo wa mfinyanzi un-aotumika kufinyanga vyungu au udongo mfinyanzi unaonata.

3) SAMADI YA NG’OMBETumia samadi ya ng’ombe mbi-chi.

4) MAJANITumia majani ya mpunga/ngano kama kifaa cha kunatisha udon-go. Majani marefu unakatakata katika urefu mdogo (sentimita 2 mpaka 5) ili iwe rahisi kuchang-anya na udongo.

5) MFUNIKO WA CHUMAMfuniko wa chuma wenye kipe-nyo cha sentimita 60 na mshikio juu kwa ajili ya kufunika sehemu ya juu baada ya kuwasha moto.

Tafadhari kumbuka: Kwa ku-jenga muundo wa umbo la tufe, kwanza siliba na udongo ulio na mchanganyiko wa udongo wa mfinyanzi, samadi ya ng’ombe mbichi na majani (10:1:1; na mara ya pili na mara ya tatu, siliba na mchanyanyiko wa udongo wa mfi-nyanzi na samadi ya ng’ombe mbichi kwa uwiano wa 1:1

Madhumuni ya kuongeza samadi ya ng’ombe mbichi na majani ni kuimarisha plasta, kwani inasaidia kushikamanisha plasta pamoja. Hii ni kwa sababu udongo wa mfinyanzi unapokauka unasinyaa na kusababisha nyufa, lakini hizi nyufa zi-naweza kupunguzwa kwa kuchanganya udongo na majani.

Lowanisha udongo wa mfinyanzi, samadi mbichi ya ng’ombe na majani kwa kiwango kilichokuba-lika kwa maji kwa usiku mzima ili kulainisha mabonge ya udongo, ili yawe rahisi kuchanganya na kuongeza uwezo kunata zaidi.Tope la udongo ulioandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa tanuru, linapaswa liwe imara, ili kushikamanisha vizuri.

Page 6: MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA ......Kwa kujenga sehemu ya juu iliyo na umbo la tufe, wenye unene wa ukuta kwa sentimita 9, ujazo wa mita 0.7 za tofari zitahitajika. Tafadhari piga

MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA RASILIMALI MIANZI AFRIKA YA MASHARIKI KWA KUSHIRIKIANA NA NCHI YA UHOLANZI NA CHINA- KENYA

TAARIFA ZA KIUFUNDI

UJENZI WA TANURU LA MATOFALI LA MKAA WA MIANZI

MCHAKATO WA HATUA KWA HATUA

Ujenzi

1) Weka alama sehemu ya katikati ya tanuru. Weka ufi-to wa muanzi ulionyooka au ubao wa futi 10 au mita 3 kwa urefu, funga kamba iliyo wima ili kujua iwapo tanuru limenyooka au halijanyooka.

2) Kutoka katikati, weka alama ya duara (sentimita 120 nusu kipenyo).

3) Katika sehemu ya chini au weka alama 6 ya tofari moja kila alama/shimo kwa urefu ulio sawa.

4) Weka alama sehemu ya mlango wa mbele (sm 75).

5) Anza kujenga kwa ndani kwa kufuata alama na kukazia na tope la udongo (changanya udongo was mfinyanzi, samadi mbichi na pumba za mpunga kwa chini).

Uwekaji wa Matofari

Tofari mbili katika kuta (~ sm 20). Weka tofari kwa kupishana (isiwe sawa tofari juu ya tofari lingine): na tope la udongo liwekwe kati ya nafasi ya tofari moja na lingine (urefu na wima) kwani inaongeza nguvu na kufunga njia za kuin-giza na kutoa hewa.

Page 7: MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA ......Kwa kujenga sehemu ya juu iliyo na umbo la tufe, wenye unene wa ukuta kwa sentimita 9, ujazo wa mita 0.7 za tofari zitahitajika. Tafadhari piga

MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA RASILIMALI MIANZI AFRIKA YA MASHARIKI KWA KUSHIRIKIANA NA NCHI YA UHOLANZI NA CHINA- KENYA

TAARIFA ZA KIUFUNDI

UJENZI WA TANURU LA MATOFALI LA MKAA WA MIANZI

Ujenzi

6) Endelea kujenga mpaka urefu wa sm 70 na weka alama ya mashimo ya hewa yenye idadi ya sita (6) kwa kuweka tofari diagonal katika shimo la kwanza (anga-lau nyuzi 45 kwa wastani).

7) Unapojenga sehemu ya juu ya mlango wa mbele, tumia bati la chuma lililopindwa juu kama umbo la duara au muanzi uliokunjwa sehemu ya juu kama umbo la duara au umbo la duara lilitengenezwa na mbao. Urefu wa umbo la duara juu ni sms 30.

Endelea kujenga mpaka urefu wa sm 135 na weka alama ya mashimo ya hewa yenye idadi ya sita (6) kwa kuweka tofari diagonal katika shimo la kwanza (anga-lau nyuzi 45 kwa wastani).

8) Maliza kujenga mpaka urefu wa sms 140. Sasa iki-wa sehemu ya kujenga tofari mbili mbili imemalizika kutoka chini kwenda juu (sehemu ya wima). Kutoka hapo, jenga ukuta kwa tofari moja moja na anza kuli-jenga umbo la dome tufe lililowazi juu)

Namna gani ya kujenga umbo la tufe (dome)?Kwa kutumia mbao, weka alama sehemu ya katikati na acha duara la (sms 60) na funga kamba kuzunguka mduara wa juu mpaka kwenye ukuta ulio wima ulio-jengwa. Ning’iniza kamba kwa kufunga mwishoni mwa matofari.

Page 8: MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA ......Kwa kujenga sehemu ya juu iliyo na umbo la tufe, wenye unene wa ukuta kwa sentimita 9, ujazo wa mita 0.7 za tofari zitahitajika. Tafadhari piga

MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA RASILIMALI MIANZI AFRIKA YA MASHARIKI KWA KUSHIRIKIANA NA NCHI YA UHOLANZI NA CHINA- KENYA

TAARIFA ZA KIUFUNDI

UJENZI WA TANURU LA MATOFALI LA MKAA WA MIANZI

Ujenzi

Njia mbadala wa kujenga tanuru

Chagua 1:Ongeza tope la udongo zaidi sehemu ya nje na kidogo sehemu ya nda-ni (kama inavyooneka-na katika picha).

Chagua 2:Upangaji wa tofari, laza mlalo katika upande wa kwaza kwa ndani kidogo kwa wastani wa sms 1 (kama inavyoonekana katika picha).

Tafadhari kumbuka: Wakati wa kujenga, tumia tepu ya kupimia ili kuhakikisha kwamba umbali kutoka katikati ni sawa.

1) Ukiwa ndani ya tanuru kutoka chini wima, anza kujenga umbo la tufe (dome).

3) Endelea kujenga mpaka tanu-ru lifikie urefu wa sms 200 kuto-ka chini na kisha weka alama ya mashimo (madirisha) sita (6) kwa kuweka tofari (diagonal kama mashimo (madirisha) yaliyopita, wastani wa nyuzi 45).

2) Wakati wa kujenga tofari, sehemu unapounganisha tofari moja na lingine, juu yake usi-weke tofari sehemu moja ye-nye kuungana kama ilivyokuwa tofari la chini bali zipange kwa kuzitofautisha tofautisha (ziwe zinapishana)

Endelea na ujenzi mpaka urefu wa sms 240.Kumbuka: Wakati unajenga tanuru lenye umbo la tufe (dome), baada ya kufika nusu ya ujenzi- ruhusu likauke usiku kucha ili kuboresha dhamana ya matofali na tope la udongo lenye mchanganyiko wa udongo mfinyanzi, samadi mbichi na pumba za mpunga.

4) Kuongeza uimara, weka tope la udongo ndani na nje ya tofari za uku-ta zinazojengwa.

Hakikisha tope la udongo lenye mchanganyiko wa udongo mfin-yanzi, samadi mbichi na pumba za mpunga limeshikamana vizuri. Seh-emu ya juu yenye shimo iwe sms 60, sawa na ukubwa wa mfuniko wa bati la chuma.

Page 9: MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA ......Kwa kujenga sehemu ya juu iliyo na umbo la tufe, wenye unene wa ukuta kwa sentimita 9, ujazo wa mita 0.7 za tofari zitahitajika. Tafadhari piga

MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA RASILIMALI MIANZI AFRIKA YA MASHARIKI KWA KUSHIRIKIANA NA NCHI YA UHOLANZI NA CHINA- KENYA

TAARIFA ZA KIUFUNDI

UJENZI WA TANURU LA MATOFALI LA MKAA WA MIANZI

MCHAKATO WA HATUA KWA HATUA

Kupiga Plasta

Kupiga plasta kwa kutumia mchanganyiko wa udongo wa mfinyanzi, samadi mbichi na pumba za mpunga ni muhimu sana. Ukishaelewa umuhimu wa plasta, muundo wa udongo wa plasta (udongo wa mfinyanzi, samadi mbichi na pumba za mpunga), changanya vizuri kwa uwiano, hii inasaidia kuimarisha ukuta. Kupiga plasta kuta, angalau kufanyike mara 4 kwa unene uliokubalika.Siliba (plasta) mara ya kwanza na tena siliba (plasta) mara ya pili: udongo mchanganyiko wa mfinyanzi, samadi mbichi ya ng’ombe na majani au pumba za mpunga ziwe kwa muunganiko wa 10:1:1. Tope la udongo huo liimarike na kuwa nene.Siliba (plasta) mara ya tatu na tena siliba (plasta) mara ya nne: mfinyanzi, samadi mbichi ya ng’ombe na majani au pumba za mpunga ziwe kwa muunganiko wa 1:1:1. Tope la udongo kidogo liwe laini au lenye maji mengi ili tope hilo liweze kuziba nyufa zilizojitokeza.

Kwanza siliba (plasta)Tumia tope kupiga plasta eneo lote la tanuru la mkaa (eneo la ndani na nje). Unene wa plasta ya kwanza uliyo-siliba iwe kati ya sms 1-2.

Page 10: MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA ......Kwa kujenga sehemu ya juu iliyo na umbo la tufe, wenye unene wa ukuta kwa sentimita 9, ujazo wa mita 0.7 za tofari zitahitajika. Tafadhari piga

MPANGO WA MAENDELEO WA KUENDELEZA RASILIMALI MIANZI AFRIKA YA MASHARIKI KWA KUSHIRIKIANA NA NCHI YA UHOLANZI NA CHINA- KENYA

TAARIFA ZA KIUFUNDI

UJENZI WA TANURU LA MATOFALI LA MKAA WA MIANZI

Kwa taarifa zaidi, tafadhari wasiliana na Meneja wa mradi, ukanda wa Afrika Mashariki- Mr. Jayaraman Durai, barua pepe: [email protected]

Mratibu wa Mradi Kitaifa, kwa nchi ya Kenya- Ms. Nellie Oduor, +254.722.241.036, barua pepe: [email protected]

Siliba mara ya piliBaada ya plasta ya kwanza kusiliba, ruhusu kukauka kwa siku 2 mpaka nyufa kubwa zimetokea. Plasta ya pili, tumia tope nene (mchanganyiko wa mfinyanzi, samadi mbichi na pumba za mpunga) kwa mkono kwa kulivin-girisha kujaza nyufa. Acha plasta ya pili ikauke kwa siku 2 mpaka nyufa ndogo ndogo zimetokea.

Kupiga Plasta

MUONEKANO WA MATANURU TOFAUTI YA MKAA YALIYOKWISHA KUJENGWA

Plasta ya tatu na ya nne Tumia tope jembamba au lililo na maji maji kufunika nyufa zilizojitokeza na uku-ta uwe sawa bila nyufa.

Kumbuka: Kwa uzalishaji wa mkaa wa mianzi kwa kutumia tanuru lenye umbo la tufe (dome), tafadhari rejea TB: Uzalishaji wa mkaa katika tanuru