17
1 TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. BENJAMINI WILLIAM MKAPA KATIKA ZIARA YA TAREHE 08.07/2017 1.0 UTANGULIZI. Mkoa wa Simiyu unazo Wilaya tano (5) za Kiutawala, ambazo ni Bariadi, Busega, Itilima Maswa na Meatu. Aidha, Mkoa unazo Halmashauri za Wilaya tano (5) na Halmashauri ya Mji moja (1) ambazo ni Halmashauri za Wilaya za Bariadi, Busega, Itilima, Maswa, Meatu na Halmashauri ya Mji Bariadi. Mkoa ulianza mwaka 2012 ukiundwa na Wilaya za Bariadi, Maswa na Meatu zilizokuwa sehemu ya Shinyanga na Busega iliyokuwa sehemu ya Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza. Kwa ufupi, Mkoa huu uliundwa na Wilaya zilizokuwa nyuma wakati huo. Hivyo umeanza ukiwa na changamoto kubwa za miundo mbinu na upungufu wa watumishi ambapo kwa sasa tunaupungufu wa watumishi wa sekta ya Afya 2,145 kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri za Serikali za Mitaa. 2.0 HALI YA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA KATIKA MKOA WA SIMIYU Mkoa una jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya 212 ambavyo ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Hospitali za wilaya 3 za Maswa na Meatu na Hospitali ya shirika la Dini 1 (AICT Mkula) iliyopo wilaya ya Busega , vituo vya afya 17 na zahanati 191, Jedwali hapo chini linaonesha mchanganuo wa vituo hivyo kwa kuzingatia uhitaji, vituo vilivyopo na upungufu kwa kila Halmashauri. Jedwali Na.1: Idadi ya Hospitali,Vituo vya afya,Zahanati na upungufuwake kwa Mkoa Na. SEKRETARIETI YA MKOA/HALMASHAURI HOSPITALI VITUO VYA AFYA ZAHANATI Hitaji zilizopo upungufu Hitaji Vilivyopo Upungufu Hitaji Vilivyopo Upungufu 1 Sekretarieti ya Mkoa 1 1 0 0 0 0 0 0 0 2 Bariadi DC 1 0 1 21 2 19 84 28 56 3 Bariadi TC 1 0 1 10 2 8 92 18 74 4 Busega 1 1 0 15 4 11 59 22 37 5 Itilima 1 0 0 22 3 19 102 44 58 6 Maswa 1 1 0 36 3 33 120 50 70 7 Meatu 1 1 0 26 3 23 106 29 77 Jumla 7 4 2 130 17 113 563 191 372

TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

  • Upload
    others

  • View
    7

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

1

TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. BENJAMINI WILLIAM MKAPA KATIKA

ZIARA YA TAREHE 08.07/2017

1.0 UTANGULIZI.

Mkoa wa Simiyu unazo Wilaya tano (5) za Kiutawala, ambazo ni Bariadi,

Busega, Itilima Maswa na Meatu. Aidha, Mkoa unazo Halmashauri za

Wilaya tano (5) na Halmashauri ya Mji moja (1) ambazo ni Halmashauri za

Wilaya za Bariadi, Busega, Itilima, Maswa, Meatu na Halmashauri ya Mji

Bariadi.

Mkoa ulianza mwaka 2012 ukiundwa na Wilaya za Bariadi, Maswa na

Meatu zilizokuwa sehemu ya Shinyanga na Busega iliyokuwa sehemu ya

Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza. Kwa ufupi, Mkoa huu uliundwa na Wilaya

zilizokuwa nyuma wakati huo. Hivyo umeanza ukiwa na changamoto

kubwa za miundo mbinu na upungufu wa watumishi ambapo kwa sasa

tunaupungufu wa watumishi wa sekta ya Afya 2,145 kwa ofisi ya Mkuu wa

Mkoa na Halmashauri za Serikali za Mitaa.

2.0 HALI YA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA KATIKA MKOA WA SIMIYU

Mkoa una jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya 212 ambavyo ni

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Hospitali za wilaya 3 za Maswa na

Meatu na Hospitali ya shirika la Dini 1 (AICT Mkula) iliyopo wilaya ya

Busega , vituo vya afya 17 na zahanati 191, Jedwali hapo chini linaonesha

mchanganuo wa vituo hivyo kwa kuzingatia uhitaji, vituo vilivyopo na

upungufu kwa kila Halmashauri.

Jedwali Na.1: Idadi ya Hospitali,Vituo vya afya,Zahanati na upungufuwake kwa Mkoa

Na. SEKRETARIETI YA

MKOA/HALMASHAURI

HOSPITALI VITUO VYA AFYA ZAHANATI

Hitaji zilizopo upungufu Hitaji Vilivyopo Upungufu Hitaji Vilivyopo Upungufu

1 Sekretarieti ya Mkoa 1 1 0 0 0 0 0 0 0

2 Bariadi DC 1 0 1 21 2 19 84 28 56

3 Bariadi TC 1 0 1 10 2 8 92 18 74

4 Busega 1 1 0 15 4 11 59 22 37

5 Itilima 1 0 0 22 3 19 102 44 58

6 Maswa 1 1 0 36 3 33 120 50 70

7 Meatu 1 1 0 26 3 23 106 29 77

Jumla 7 4 2 130 17 113 563 191 372

Page 2: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

2

Aidha, Mkoa umefanikiwa kuongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma za

afya kutoka vituo 167 (2013) mpaka 212 (2017) Sawa na ongezeko la 27%

ikiwa bado kuna upungufu wa vituo 488 (70%) kwa kuzingatia sera ya

serikali ya kila Kijiji kuwa na zahanati , kila Kata kuwa na kituo cha Afya na

kila Wilaya kuwa na Hospitali.

2:1. Taarifa za vitengo katika idara ya afya

2:1:1 Huduma za afya ya Mama na Mtoto

Huduma za Mama na Mtoto katika Mkoa wa Simiyu zimeendelea kutolewa kwa kujumuisha makundi kama:- Wanawake walio katika umri wa kuzaa, Watoto umri chini ya miaka 5 na Watoto umri mwaka 1. 2:1:2 Huduma ya uzazi wa mpango

Mkoa wa Simiyu umeendelea kutoa huduma za uzazi wa mpango kwa wakina

mama walio katika umri wa kuzaa tangu mwaka 2013,hata hivyo huduma za

uzazi wa mpango zimekuwa zikiongezeka kwa kiasi kidogo mwaka hadi

mwaka tukiwa chini ya wastani wa kiafa wa kufikia 60%.jedwali hapo chini

linaonesha mwenendo wa huduma za uzazi wa mpango kwa wakina mama .

Jedwali Na:2. Idadi ya wazazi waliopata huduma za uzazi wa mpango

MWAKA 2013 2014 2015 2016 JAN-MAY

2017

Waliotegemewa kupata huduma za uzazi wa mapango

303,399 303,399 272,277 314,774 320,622

Waliopata njia za uzazi wa mpango

46,885 68,225 81,007 92,564 36,733

Asilimia ya waliohudumiwa (%) 16 22 25 26 11

Kwa hivyo Uhamasishaji na mafunzo yanaendelea kutolewa kwa watoa

huduma vituoni na huduma za mkoba ili kuongeza kiwango cha utumiaji wa

njia za uzazi wa mpango.

Page 3: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

3

2:1:3 Huduma za wajawazito

Mahudhurio ya akinamama wajawazito kliniki sio ya kuridhisha hususani

hudhurio la kwanza ujauzito chini ya wiki 12 na akina mama wanaokamilisha

mahudhurio manne, kama inavyoonekana katika jedwali lifuatalo:-

Jedwali Na:3. kuonesha wajawazito walio hudhuria kliniki

MWAKA 2013 2014 2015 2016 Jan-may

2017

WAJAWAZITO WALIOTARAJIWA

94,653 93,745 70,247 75,321 30,275

WALIOHUDHURIA <WIKI 12

10225 11% 9460 10% 9471 13% 11759 16% 3779 12%

HUDHURIO LA NNE 19,757 21% 25,308 27% 25,879 37% 31,429 41% 13,058 43%

2:1:4 Huduma kwa akina mama (wazazi) wakati wa kujifungua

Idadi ya akina mama wajawazito kujifungua katika vituo vya kutolea huduma

za Afya na kusaidiwa na watoa huduma wenye ujuzi bado iko chini

ukilinganisha na lengo la Taifa la 80% ya kina mama watarajiwa kujifungulia

katika vituo vya kutolea huduma za Afya,jedwali hapo chini linaonesha

mwenendo wa akina mama kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za

Afya:-

Jedwali Na:4. kuonesha idadi ya wajawazito waliojifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya

MWAKA 2013 2014 2015 2016 JAN-MAY 2017

Waliotegemewa 88,773 89,576 65,124 73,249 29,214

Waliojifungulia kituoni

23,543 26% 31,226 35% 36,390 56% 38,652 53% 17,484 60%

Waliosaidiwa na watoa huduma wenye ujuzi

19,429 22% 27,762 31% 34,586 53% 36,618 50% 16,004 54%

2:1:5 Huduma baada ya kujifungua

Mahudhurio ya akinamama waliojifungua imeendelea kuongezeka mwaka

hadi mwaka kutoka 24% mwaka 2013 hadi kufikia 65% mwaka 2016,

ingawa bado haijafikia lengo la Taifa la 80%.Jedwali hapo chini linaonesha

mahudhurio ya akina mama baada ya kujifungua;

Page 4: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

4

Jedwali Na:5. Kuonesha idadi ya mahudhurio ya akinamama baada ya

kujifungua

MWAKA 2013 2014 2015 2016 JAN-MAY

2017

WALIOTEGEMEWA 88,773 89,576 65,124 73,249 29,214

WALIOHUDHURIA 21,247 32,816 20,085 48,278 8,613

ASILIMIA 24% 37% 31% 65% 29%

2:1:6 Vifo vya akinamama wajawazito.

Vifo vya akinamama wajawazito vinazidi kuongezeka, Aidha juhudi

zinafanyika kupunguza vifo vya akina mama wajawazitoikiwa ni pamoja na

kuongeza vituo vya upasuaji wa dharura, ununuzi wa madawa na vifaa tiba

pamoja na mafunzo kwa watoa huduma.

Jedwali Na:6. Kuonesha idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi

MWAKA 2013 2014 2015 2016 JAN-MAY

2017

IDADI YA

VIFO

44 29 43 45 22

Idadi ya vifo vitakanavyo na uzazi imeendelea kuwa juu na hivyo uboreshaji

wa huduma za mama wajawazito unaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na

kuhamasisha wajifungue katika vituo vya kutolea huduma za Afya,kuengeza

vituo vinavyotoa huduma za upasuaji.

2.2 Hali ya maambukizi vvu na ukimwi

Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa Tanzania ambayo imeathirika na

ugonjwa wa UKIMWI.Kutokana na tafiti zilizofanyika mwaka 2011-2012 Mkoa

wetu ulibainika kuwa na ushamiri wa maambukizi ya VVU kwa 3.6%. Mkoa

wa Simiyu umeendelea kupambana na maambukizi ya VVU na UKIMWI kwa

kutekeleza afua mbalimbali kama ifuatavyo:-

Page 5: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

5

2:2:1 Huduma ya utoji nasaha na upimaji (HTC)

Mkoa una vituo76 vya kutolea huduma za unasihi na upimaji wa

Hiari(VCT).Jumla ya wateja 339,181walipewa huduma ya ushauri nasaha na

upimaji ,na kati ya hao wateja 8576 walibainika kuwa na VVU sawa na

ushamiri wa VVU 2.5%.Ufuatao ni mtiririko wa hudumaza upimaji na

kiwango cha ushamiri wa VVU kuanzia mwaka 2012 hadi 2016

Jedwali Na:7. Idadi ya wateja wa upimaji wa hiari

Mwaka Wateja

waliopimwa

Waliogundulika

kuwana VVU

Ushamiri

2012 47656 2949 6.1%

2013 158,695 5520 3.4%

2014 234,208 7995 3.4%

2015 262862 8631 3.4%

2016 339181 8576 2.5%

2:2:2: Huduma za tiba na matunzo (CTC)

Hadi kufikia mwezi Disemba Mwaka 2016 mkoa una vituo 48 vyenye usajili

ambavyo vimeendelea kutoa huduma ya Tiba na Matunzo kwa WAVIU.

Mkoa unaendelea kufanya upembuzi yakinifu ili kutambua vituo ambavyo

vinasifa ya kutoa huduma hizi. Kwa mpango wa mwaka 2017-2018

tunatarajia kuongeza vituo 15 ilikufikia vituo 63 (30%) lengo likiwa ni

kusogeza huduma hizi za tiba na matunzo karibu na wanchi (care and

treatment services) .Huduma hizi katika mkoa wetu zimekuwa zikitolewa

kama inavyoonesha katika jedwali hapa chini.

Jedwali Na.8: huduma Tiba na matunzo ya WAVIU

Mwaka Waliosajiliwa Walioanzishiwa dawa za ART

Wanaoendelea na dawa ART

2013 28,913 16931(58.5%)

2014 30,291 19,827(64.5%) 11,926(60%)

2015 40048 28724(71.7%) 15150(53%)

2016 41,782 36,239(86.7%) 22027(61%)

Page 6: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

6

2:2:3 Huduma za kuzuia maambukizi ya vvu kutoka kwa mama kwenda

kwa mtoto.

Huduma za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto

katika mkoa wetu zilizinduliwa mwaka 2013 kufuatia uzinduzi wa kitaifa

uliofanyika mwaka 2012 na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Huduma hizi zimeendelea kutolewa katika vituo

168 kati ya vituo 212 vya kutolea huduma mkoani kwetu (79%).

Jedwali Na: 9. Huduma za kuzuia maambukizi ya vvu kutoka kwa mama

kwenda kwa mtoto

Mwaka Vituo OPTION B+ sites

Wajawazito waliopimwa VVU

Walioathirika na VVU

2012 133 30(main ctc) 20143 547(2.7%)

2013 154 148 35497 732 (2%)

2014 160 160 65,213 1160(1.7%)

2015 168 168 92,964 1515(1.6%)

2016 168 168 84408 1355(1.6%)

Aidha huduma hizi huenda sambamba na utambuzi na ufuatiliaji wa watoto

waliozaliwa na mama mwenye maambukizi ya VVU(exposed infant)ili mtoto

huyo aweze kupata fursa ya kukingwa na maambukizi hayo kwa kupewa

dawa kufubaza VVU(nevirapine),lakini pia huchukuliwa vipimo maalum vy

damu kavu(DBS) ili kutambua kama mtoto ameathrika au la.

Jedwali Na :10. Idadi ya watoto waliozaliwa na mama wenye VVU

waliofatiliwa na kutambuliwa kuwa na VVU

Mwaka Watoto waliopimwa positive Waliosajiliwa

CTC

2012 843 79 (9.3%) 79

2013 431 20(4.6%) 19

2014 822 37(4.5%) 37

2015 953 83 58

2016 1139 45 55

Page 7: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

7

2:2:4 Huduma za tohara kwa wanaume

Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa 12 Tanzania bara ambayo ushamiri

watohara kwa wanaume ulikuwa chini ya 30% na hivyo kufanya wepesi wa

kuambukizwa VVU.

Kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyiak nchini Uganda, Afrika ya kusini na

Kenya Imebainika kuwa tohara kwa wanaume huweza kupungunza

maambukizi ya VVU kwa 60%.

Hivyo tohara ya Kitabibu ya hiari kwa wanaume ni moja ya njia kuu za

kupambana na maabukizi ya VVU. Huduma hizi zilianza mkoani kwetu mwaka

2010,mpaka Disemba 2016 idadi ya wanaume-walikuwa tayari wamepata

huduma hii ya tohara ni kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini.

Jedwali Na:11.Idadi ya wanaume waliofanyiwa tohara

Mwaka Wanaume

waliosajiliwa

waliotahiriwa Wenye

maambukizi

2012 44542 44542 335 (0.7%)

2013 45,364 45,364 36 (0.7%)

2014 30447 30447 79 (0.2%)

2015 74184 74184 157 (0.2%)

2016 15443 15443 46 (0.2%)

2:2:5 Huduma zingine zitolewazo katika mapambano ya vvu na ukimwi

ni pamoja na:-

Kutibu magonjwa yangono na via vya uzazi (STI/RTI)

Uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi kwa akina mama pamoja na wamama waviu.

Utoaji wa elimu kuhusu UKIMWI na jinsi ya kujikinga na hasa suala zima la watu kubadili tabia.(behavioral change).

Uhamasishaji wa matumizi sahihi ya kondom kama njia mojawapo ya kujikinga na maambukizi ya VVU(condom programming).

Page 8: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

8

Mradi wa damu salama (safe blood transfusion)kwa hospitali zote zinazotoa huduma hii kuhakikisha damu inafanyiwa uchunguzi dhidi ya `maambukizi.

Huduma za wagonjwa wenye maambukizi ya VVU & UKIMWI ngazi ya jamii(community based HIV and AIDS SERVICES)

Upimaji wa magonjwa ya kaswende kwa akina mama wajawazito

(ANC-Siphylis).

2:3 Juhudi za kupunguza ugonjwa wa malaria

Katika kuhakikisha juhudi za kupambana na ugonjwa wa Malaria katika Mkoa

wa Simiyu na kwakushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,

Wazee, na Watoto, Mkoa umehakikisha kuna ongezeko la upatikanaji wa

vipimo vya ugonjwa wa Malaria (MRDT) na dawa za Mseto kwa kila kituo cha

kutolea Huduma za Afya. Aidha Mkoa umeweza kugawa vyandarua 1,133,637

katika kaya zote za Mkoa wa Simiyu

2:4 Huduma za chanjo

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto kupitia Mpango wa

Taifa wa Chanjo, imekuwa ikitoa huduma za chanjo ili kutoa kinga dhidi ya

magonjwa mbalimbali. Magonjwa hayo ni Kifua kikuu, Kupooza, Kifaduru,

Dondakoo, Pepopunda, Kuhararisha, Kichomi, Homa ya ini , Surua, Rubella, Uti

wa mgongo. Chanjo hizi zimekuwa zikitolewa kwa watoto chini ya miaka

mitano na akina mama wenye uwezo wa kuzaa.

Huduma za chanjo zinaendelea kutolewa kwenye vituo vyote vinavyotoa

huduma za chanjo mkoani.Pamoja na huduma za mkoba na huduma

tembezi(Outreach na Mobile services). Hapa chini ni majedwali

yanayoonyesha mafanikio ya utoaji wa chanjo. Mkoaumeendelea kufanya

vizurikama inavyooneshwa kwenye jedwali hapo chini:-

Page 9: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

9

Jedwali Na; 12. Idadi ya vituo vinavyotoa huduma za chanjo

Na Wilaya Jumla ya vituo vya kutolea huduma

Vituo vinavyotoa huduma za chanjo

Asilimia ya vituo vinavyotoa chanjo

Mwaka 2013 2014 2015 2016 2013 2014 2015 2016 2013 2014 2015 2016

1 Bariadi DC 25 25 27 28 23 23 27 27 92 92 96 96

2 Bariadi TC 16 16 18 21 14 14 15 15 87.5 88 85 71

3 Busega DC 25 25 26 28 21 21 25 25 84 84 96 89

4 Itilima DC 27 30 30 30 27 28 30 30 90 93 100 100

5 Maswa DC 46 46 46 46 38 38 42 42 83 83 91 91

6 Meatu DC 46 46 47 54 38 38 42 48 83 83 89 88

Total 185 185 194 207 161 162 181 187 87 88 93 90

Halmashauri zimeendelea kuongeza vituo vya kutolea chanjo kama

ilivyojionyesha kwenye jedwali hapo juu.

Kiwango cha chanjo ya BCG,OPV3,PENTA 3,PCV-13 3,Rota -2, Measles na

TT2+ kilichofikiwa-2013

Jedwali Na;13. Mwenendo wa upatikanaji wa chanjo 2013.

13 Wilaya Idadi ya Walengwa

BCG OPV3 Penta 3 PCV 13-3 Rota 2 Measles

TT2+

1 Bariadi DC 14260 119

84 81%

38

65

101 80

2 Bariadi TC 8584 142 102 85% 43.4 59 103 92

3 Busega DC 8942

107

69

65%

46 49 83

57

4

Itilima Dc

18837 107

94 78%

38

55

105 61

5 Maswa DC 19807 108

90 80%

62 70 99 79

6 Meatu DC 17439 109

90 85%

66 76 91 68

Jumla 87869 113 93 89

50 64 104 72

Kwa mwaka 2013 chanjo ya surua rubella haikuwepo hivyo dozi ya pili ya surua rubella haikuwa ikitolewa pia Chanjo mpya ya Kuzuia kichomi na kuharisha zilianzishwa.

Page 10: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

10

Kiwango cha chanjo ya BCG,OPV3,PENTA 3,PCV-13 3,Rota -2, MR -2 na TT2+

kilichofikiwa-2014

Jedwali Na;14. Mwenendo wa upatikanaji wa chanjo 2014.

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto kupitia mpango wa

taifa wa chanjo, ulianzisha chanjo mpya ya surua rubella ambayo ilitolewa

dozi mbili kwa mtoto dozi ya kwanza alipata akiwa na umri wa miezi tisa na

dozi ya pili alipata akiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi sita. Kiwango

cha chanjo kiliendelea kupanda kama jedwali linavyoonyesha hapo juu.

Kiwango cha chanjo ya BCG,OPV3,PENTA 3,PCV-13 3,Rota -2, MR -2 na TT2+

kilichofikiwa-2015

Jedwali Na;15. Mwenendo wa upatikanaji wa chanjo 2015

Na Wilaya Idadi ya Walengwa

BCG OPV3 Penta 3 PCV3 Rota 2 MR 1 MR2 TT2+

1 BARIADI DC 10514 236 144 135 115 129 137 105 149

2 BARIADI TC 8904 205 109 109 107 112 120 58 111

3 BUSEGA DC 9247 136 96 89 98 96 88 62 252

4 ITILIMA DC 12996 202 151 144 141 153 168 158 144

5 MASWA DC 13796 131 119 119 116 119 108 85 127

6 MEATU DC 11700 165 129 128 128 128 126 58 125

7 TOTAL 67157 178 126 122 119 125 126 91 149

Na Wilaya Idadi ya Walengwa

BCG OPV3 Penta 3

PCV3 Rota 2

MR 1

MR2 TT2+

1 BARIADI DC 13934 128 111 103 69 79 110 18 96

2 BARIADI TC 8468 190 107 103 93 100 124 20 121

3 BUSEGA DC 8398 121 101 99 97 107 104 27 128

4 ITILIMA DC 15109 156 144 135 122 127 128 27 120

5 MASWA DC 23509 110 96 96 94 96 97 34 91

6 MEATU DC 18450 102 88 88 88 89 89 18 74

TOTAL 87868 129 107 103 94 99 106 25 99.5

Page 11: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

11

• Huduma za chanjo ziliendelea kutolewa kwenye vituo vyote vinavyotoa huduma za chanjo mkoani.Pamoja na huduma za mkoba.

• Idadi ya watoto waliopatiwa chanjo iliongezeka kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo juu.

Kiwango cha chanjo ya BCG,OPV3,PENTA 3,PCV-13 3,Rota -2, MR -2 na TT2+ kilichofikiwa-2016

Jedwali Na; 16. Mwenendo wa upatikanaji wa chanjo 2016.

Na Wilaya Idadi ya Walengwa

BCG OPV3 Penta 3 PCV3 Rota 2

MR 1

MR2 TT2+

1 BARIADI DC 12393 165% 107% 117% 107% 121% 86% 60% 83%

2 BARIADI TC 10494 143% 79% 86% 84% 89% 71% 46% 101%

3 BUSEGA DC 10900 164% 107% 94% 92% 89% 73% 46% 100%

4 ITILIMA DC 15319 156% 98% 101% 103% 114% 81% 58% 96%

5 MASWA DC 16261 148% 80% 94% 90% 97% 68% 53% 99%

6 MEATU DC 14158 142% 77% 90% 91% 97% 94% 46% 114%

7 TOTAL 79525 143% 91% 97% 95% 102% 79% 52% 98%

Huduma za chanjo zimeendelea kutolewa katika vituo vyote vinavyotoa

huduma za chanjo sambamba na huduma za mkoba Kiwango cha chanjo

kimeendelea kuongezeka kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo juu .

Kiwango cha chanjo ya BCG,OPV3,PENTA 3,PCV-13 3,Rota -2, MR -2 na TT2+

kilichofikiwa-jan-may 2017

2:5 Utekelezaji wa shughuli za ustawi wa jamii

Kitendo cha Ustawi wa jamii ni mojawapo vitengo vya Idara ya Afya

kinachotoa huduma kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na familia

zenye migogoro, watu wenye dhiki, watu wenye ulemavu, watoto wazee,

akina baba, akina mama, vijana wenye shida na matatizo mbalimbali

wakihitaji ushauri nasaha/nasihi, msaada wa kisaikolojia, nyenzo au vifaa vya

kujimudu ili waweze kuishi maisha yaliyo bora

2:5:1 Watoto Walio Katika Mazingira Hatarishi (WWKMH)

Mkoa kupitia Halmashauri zake sita 6 umeweza kutekeleza kuwatambua

watoto wanaoishi katika mazingira hatalishi zaidi (WWKMH)ili kujua idadi na

mahitaji yao ya kipaumbele zaidi kama huduma za elimu, afya, mavazi,

malazi, ulinzi na usalamakwa kushirikisha jamii kupitia mpango maalum

Page 12: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

12

wa Taifa unaosimamiautoaji wa huduma kwa WWKMH.

Mpaka sasa jumla ya WWKMH 43,757 (Me22, 601naKe 21,156) wanapata

huduma mbali mbali kupitia serikali za vijiji, kata na Halmashauriwanazotoka

kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali.

Jedwali: Na. 17. Idadi ya watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi wanaohudumiwa kwa kila Halmashauri.

Na. Halmashauri Idadi ya WWKMHkwa miaka 5

2013 2014 2015 2016

1 Bariadi DC 4,036 4,142 12,783 2,952

2 Bariadi TC 2,837 2,837 2,837 2837

3 Busega DC 1,934 5,617 19,979 15187

4 Itilima Dc 0 700 6,718 3821

5 Maswa DC 4,882 14,667 14,667 14,667

6 Meatu DC 2,854 2,854 4,293 4,293

Jumla 16,543 30,817 61,277 43,757

2:5:2 Huduma za Afya Kwa Wazee na Watu wenye Ulemavu

Katika kuleta ustawi kwa makundi maalum hususan wazee, Mkoa

umeendelea kutoa kipaumbele cha huduma za afya kwa wazee (“free health

services to the elders”) ikiwa ni kwa kutenga madirisha na kuwapatia

vitambulisho vya matibabu,pia katika vituo vya kutoa huduma za afya

tumeweza kuweka bango linalosomeka ‘MZEE KWANZA:MPISHA MZEE

APATE HUDUMA’ Aidha kwa hospitali za Wilaya Maswa na Wilaya ya Meatu

pamoja na hospitali ya rufaa ya Mkoa tumeweza kutenga madirisha mahususi

kwa ajili ya wazee huku Wilaya ya Busega wakitenga madirisha katika vituo

viwili vya afya ili kuwawezesha wazee kupata huduma bila usumbufu.

Page 13: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

13

Jedwali:Na.18. Idadi ya wazee waliotambuliwa na kupatiwa fomu maalum/vitambulisho kwa ajili ya matibau

Na. Halmashauri Wazee waliotambuliwa(60) Vitambulisho

vilivyotolewa Me KE Jumla

1 Bariadi vijijini 4536 5265 9801 3801

2 Bariadi Mji 2861 4858 7719 860

3 Busega 4931 7519 12,450 3750

4 Itilima 7165 9010 16175 1100

5 Maswa 4725 5727 10452 1361

6 Meatu 5660 7178 12,838 0

Jumla 29878 39557 69435 10872

Bado kuna idadi ndogo ya wazee waliopatiwa vitambulisho vya matibabu

ikiwa ni 16% na hivyo juhudi zinaendelea kufanyika na kuhakikisha wazee

wote wenye umri wa miaka 60 na kuendelea wanapatiwa vitambulisho hivyo.

2:5:3 Huduma kwa watu wenye Ualbino

Huduma mbalimbali ziliendelea kutolewa kwa watu wenye Ualbino zikiwemo

Afya, Elimu, Malezi bora, kisaikilojia/ushauri nasihi, Ulinzi na Usalama,

misaada mbalimbali kulingana na mahitaji.

Aidha, Mkoa umeweka utaratibu maalumu wa kuwahudumia watu wenye

Ualbino kwa kuwapatia losheni na mafuta kwa ajili ya kinga ya ngozi dhidi ya

magonjwa kama saratani ya ngozi pia Mkoa kwa kushirikiana na shirika lisilo

la kiserikali liitwalo hisani “Standing Voice” pamoja na Hospitali ya KCMC

kitengo cha magonjwa ya ngozi, watu wenye ulemavu wa ngozi wanafanyiwa

uchunguzi wa saratani ya ngozi Sambamba na kupatiwa elimu ya kinga kwa

mionzi ya jua ambapo hushauriwa kuvaa kofia pana, nguo ndefu na kuvaa

miwani.

Page 14: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

14

Jedwali Na;19 Idadi ya watu wenye Ualbino wanaohudumiwa kwa kila

Halmashauri

H /Shauri

Idadi ya Watu wenye Ualbino kwa makundi Huduma

wanazopata

Na.

Watoto chini ya miaka 5

Watoto Umri 6

– 17

miaka 18-40

Zaidi ya

miaka 40

Ke Me JML

1 Bariadi DC 8 108 14 5 72 62 134 Lotion,elimu

2 Bariadi TC 0 - - - 15 18 33 Lotion,elimu

3 Busega DC 0 0 65 0 22 38 60 Lotion,Elimu

4 Itilima DC 0 13 41 0 21 33 54 Lotion,elimu

5 Maswa DC 0 24 49 0 36 37 73 Lotion,elimu

6 Meatu DC 0 13 17 0 21 22 43 Lotion,Elimu

Jumla 8 158 186 5 187 210 397 Lotion,Elimu

2:6 Hali ya lishe mkoa wa simiyu

Mkoa wa Simiyu umekuwa ukikabiliwa na hali duni ya lishe kila mwaka mbali

na juhudi zinazofanywa na Mkoa katika kukabiliana na hali hii hasa ya

utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano. Makundi yanayoathirika zaidi

na matatizo ya hali duni ya lishe ni watoto wenye umri chini ya miaka 2,

watoto wenye umri chini ya miaka 5, Wanawake wajawazito na

wanaonyonyesha, Wazee pamoja na wale wenye magonjwa yasiyokuwa ya

kuambukiza; mfano, Kisukari, Shinikizo kubwa la damu na watu wanaoishi na

VVU/UKIMWI. Matatizo yanayojitokeza ni pamoja upungufu wa wekundu wa

damu, upungufu wa vitamin A, upungufu madini joto na upungu wa utomwili

na wanga.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na AMREF-Uzazi uzima (2014) na Taasisi

ya Chakula na Lishe Tanzania (2014). Kuna upungufu wa wekundu wa damu

kwa watoto umri chini ya miaka mitano wapatao asilimia 79 na kwa

wanawake wenye umri kati miaka 15 na 49 wapatao asilimia 50; udumavu

kwa watoto asilimia 26.1, utapiamlo mkali na kadri asilimia 3, uzito pungufu

asilimia 10.9; kaya zinazotumia madini joto zinakadiriwa kuwa asilimia 35.3,

watoto wanaoanzishiwa maziwa ya mama mara tu baada ya kuzaliwa wakiwa

chini ya asilimia 31.2 na watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama hadi

Page 15: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

15

miezi sita bila kupewa chakula kingine wapatao asilimia 46.2. watoto

waliopatiwa matone ya vitamin A ni wastani wa asilimia 94.5na dawa za

minyoo ni wastani wa asilimia 90.3. Vituo vipatavyo vinne (4) vinatoa

huduma ya utapiamlo mkali na kadiri (in-patient and out-patient); na vituo

ishirini na nane (28) vinatoa huduma kwa watoto wenye utapiamlo wa kadiri

(out-patient), hii ni sawa na asilimia 13.3 ya vituo vyote vya kutolea huduma

241.

2:7 Wagonjwa wa kifua kikuu, ukimwi na ukoma Toka mwaka 2013 hadi 2016, jumla ya wagonjwa wa Kifua Kikuu 5,843 waligunduliwa kuwa na Kifua Kikuu na kupatiwa matibabu. Jumla ya wagonjwa 137 wameripotiwa kuwa na ugonjwa wa Ukoma katika kipindi cha mwaka 2013 hadi 2016. Jedwali Na. 20. Kuonesha wagonjwa wa Kifua kikuu na Ukoma UGONJWA 2013 2014 2015 2016 JUMLA KIFUA KIKUU 1,311 1,231 1,556 1,745 5,843 UKOMA 64 36 19 18 137

3:0 MAFANIKO:

Huduma za chanjo zinatolewa katika vituo vyote vinavyotakiwa kutoa huduma hizo.

Jumla ya wagonjwa 5,843 wamegundulika kuwa na Kifua kikuu na kuanzishiwa matibabu mwaka tangu mwaka 2013 hadi 2016.

Jumla ya wagonjwa 137 wamegundulika kuwa na ugonjwa wa Ukoma

na kuanzishiwa matibabu mwaka tangu mwaka 2013 hadi 2016 Hospitali ya rufaa mkoa,Halimashauri ya Wilaya Meatu na Maswa

walipatiwa mashine za Genexpert kwa ajili ya kupima Kifua Kikuu,(ambayo ni technologia mpya ya kupima Kifua Kikuu)

Page 16: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

16

4:0 CHANGAMOTO

• Kiwango kidogo cha matumizi ya njia za Uzazi wa Mpango.

• Kiwango kidogo cha wajawazito wanahudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vya huduma za Afya

• Kiwango kidogo cha akinamama wanaohudhuria kiliniki baada ya

kujifungua.

• Kuongezeka kwa vifo vya akina mama wajawazito.

• Upungufu wa watumishi wenye ujuzi kwenye vituo vya kutolea huduma

• Upungufu wa vituo vya kutolea huduma za afya kwa kuzingatia sera ya selikari ya kila kijiji kuwa na zahanati , kila kata kuwa kituo cha Afya na kila wilaya kuwa na Hospitali

• Jamii haina ufahamu juu ya masuala ya lishe na hivyo kutotambua

umuhimu wake kwa ujumla

• Uelewa finyu wa Jamii juu ya taratibu na sheria za mirathi, malezi, makuzi na maendeleo ya watoto na hasa watoto wanaoishi katika mazingira magumu/hatarishi.

• Ongezeko kubwa la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi zaidi.

5:0 MIKAKATI ILIYOPO

• Kuongeza wigo mpana wa matumizi ya njia za uzazi wapango vituoni na

huduma za masafa.

• Mkoa unaendelea kuweka nafasi za kuajili watumishi wapya kwenye

bajeti za kila mwaka

• Kuendelea kutoa elimu ngazi ya jamii kuhusu sheria na haki za watoto,

wazee, watu wenye ulemavu ili hatua sahihi ziweze kuchukuliwa katika

kushughulikia masuala yanayohusu ustawi na stahiki zao

Page 17: TAARIFA YA MKOA WA SIMIYU KWA RAIS MSTAAFU WA …

17

6:0 SHUKRANI

Uongozi wa Mkoa wa Simiyu unatoa shukrani zake za dhati kwako binafsi kwa namna na jinsi ulivyotoa msaada wa hali na mali ili kuleta maendeleo kwa jamii ya Simiyu hasakwa kuweza kujenga jumla ya Nyumba za watumishi 19 pamoja na ujenzi wa nyumba ya upasuaji (Theathre) moja (1) kama ifuatavyo:- Halmashauri ya Wilaya ya Busega nyumba 5 na zote zinatumika,Halmshauri ya Wilaya ya Maswa nyumba 5 na zote zinatumika,Halmashauri ya Wilaya Meatu nyumba 5 na zote zinatumika,Halmashauri ya Wilaya Bariadi nyumba 4 na zote zinatumika na Halmahsuri ya Mji wa Bariadi nyumba moja ya Upasuaji(Theatre) nayo pia inatumika.

Aidha, Mkoa wa Simiyu uliamua kujenga Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa

kuanza kujenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na jumla ya Tsh:

1,940,530,000 Zimeshaletwa na Serikali,pia jengo hilo liko katika hali ya

kumalizika na tena katika ziara ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoifanya Mkoani Simiyu tarehe11

Januari 2017 alitoa ahadi ya kutoa shilingi bilioni kumi (10) kwa ajili ya

kujenga majengo yaliyobaki ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Uongozi wa Mkoa

wa Simiyu unakuomba utufikishie shukrani zetu za dhati kwa Mh. Rais wa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwisho tunakutakia Afya njema na maisha mema na karibu tena Mkoani kwetu Simiyu

J . A. Sagini

KATIBU TAWALA WA MKOA SIMIYU