16
Makati Wa Utafiti Kwa Ikweta Suluhisho La Maendeleo Endelevu Kwa Watu/ Wanajamii, Asili/Mazingira Na Jamii Imara Tanzania MTANDAO WA JAMII WA USIMAMIZI WA MISITU TANZANIA (MJUMITA) Empowered lives. Resilient nations.

MTANDAO WA JAMII WA USIMAMIZI WA MISITU TANZANIA … · katika utunzaji wa misitu. Usimamizi wa misitu wa jamii ni moja wapo ya aina za “PFM” ambazo zitatumika kwa misitu ambayo

  • Upload
    others

  • View
    55

  • Download
    2

Embed Size (px)

Citation preview

Makati Wa Utafiti Kwa IkwetaSuluhisho La Maendeleo Endelevu Kwa Watu/ Wanajamii, Asili/Mazingira Na Jamii Imara

Tanzania

MTANDAO WA JAMII WA USIMAMIZI WA MISITU TANZANIA (MJUMITA)

Empowered lives. Resilient nations.

MFULULIZO WA MKAKATI WA UTAFITI WA SHIRIKA LA MAENDELEO DUNIANI KWA IKWETABaadhi ya machapisho au tafiti zimeweza kuelezea vizuri jinsi ambavyo jitihada kama hizi zilivyoweza kubadilika kulingana na wakati, ukubwa wa athari, au jinsi gani zilivyoweza kubadilika baada ya muda. Baadhi bado wanaendelea kufanya jitihada za kuelezea hadithi/ visa na wataalamu katika jamii wanawaongoza katika masimulizi. Mkakati wa ikweta una lengo la kujaza pengo hilo.

Tuzo ya usawa ya ikweta ya mwaka 2014 ilitolewa kwa wenyeji wa jamii za watu 35 wanaofanya kazi katiaka kukabiliana na changamoto za hali ya hewa na za kimaendeleo kwakupitia uhifadhi na matumizi endelevu ya asili/mazingira. Waliochaguliwa kati ya washiriki 1,234 kutoka nchi 121, washindi walitambuliwa kwa mafanikio yao katika sherehe za Tuzo iliyofanyika kwa muunganiko na kuzingatia na

mkutano wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa katika masuala ya hali ya hewa na watu na mazingira/asili katika mji wa New York. Msisitizo wa kipekee uliwekwa katika misitu na urejeshwaji wa mazingira ya awali, utunzaji wa mazingira, usalama wa chakula na kilimo, maji na usimamizi wa bahari. Marejeo yafuatayo ni mwendelezo wa utafiti unaochambua matendo yaliyo chujwa na yaliyopitiwa kwauangalifu yenye lengo la kushawishi midahalo ya sera inayohitajika, kutoa mafanikio katika kuimarisha misingi ya ujuzi wa dunia uliojikita katiak mazingira ya asili na utatuzi wa kimaendeleo, na kutumika kama mifano bora ya marejeo. Tafiti bora huonwa na hueleweka kwa marejeo ya yaani matendo ya nguvu ya asili: somo la miaka 10 ya Tuzo ya ikweta, muhtasari wa masomo yaliyofundishwa na mwongozo wa sera unaotokana na rejeo za masomo.

MUHUTASARI WA MRADI Hifadhi za misitu ya vijiji vya Angai. Ipo katika eneo la milima kusini mwa Tanzania, inajumuisha eneo lenye ukubwa wa hecta karibu 1400,000 za miombo.Misitu hii ni chanzo cha vyakula, madawa yatokanayo na mitishamba, kuni, pamoja na mazao meingine yatokanayo na misitu, inakadiriwa jumla ya watu 30,000 wanaishi kwenye vijiji 24 vinavyosimamia hifadhi hizo.Pamoja na hayo zaidi ya miaka 20, umasikini umesababisha baadhi ya wanajamii kufanya shughuli haramu za kukata miti/magogo na kubadilisha ardhi hiyo kwa matumizi ya kilimo. Mwaka 2011 Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) ukishirikiana na wadau wengine kama halmashauri ya Wilaya ya Liwale na Shirika la Kuhifadhi Mpingo na Maendeleo, waliendeleza mradi wa Usimamizi shirikishi wa Misitu ya vijiji vya Angai. Mradi huu ulifanisha ugatuzi wa madaraja ya Usimamizi wa msitu huu kwenda kwa wanajamii, na matokeo yamekuwa mazuri kwani wanakijiji sasa wanafaidika kutokana na matumizi endelevu ya bidhaa za misitu kama vile, kurina asali, uvunaji endelevu wa miti ya mbao,. Kwa mchakato huu jamii ya Angai imebadilisha mtazamo wake wa namna ambavyo wameuchukulia msitu huo na sasa wanautambua kama mali yenye thamani na faida kwa muda mrefu

MAMBO MUHIMU Mshindiwa Tuzo ya usawa

2015

imeanzishwa

2007

Mahali

Halmashauri ya Wilaya ya Liwale katika Mkoa wa Lindi, Tanzania

Wanufaika

Inakadiriwa takribani watu 30,000 wanaishi katika vijiji 24 wakisimamia hifadhi ya misitu na ardhi ya kijiji cha Angai

Maeneo Muhimu

Utunzajiwamisitu, upandajiwamiti, ushirikishaji wa jamii katika usimamizi wamisitu, jamii kuzingatia na kuongeza uelewa mabadiliko ya tabia ya nchi, shughuli endekevu za kiuchumi, na kujenga uwezo

Maendeleo Endelevu Malengo yaliyo ainishwa

MSHINDI WA FILAMU WA TUZO ZA USAWA 2015

4

HISTORIA NA MUKTADHA

Tanzania ni miongoni mwa nchi 12 za kibaolojia kwa Africa na Duniani kote kwa idadi kubwa ya wanyama, ya pili kwa ukubwa wa mimea, ya tatu kwa idadi kubwa ya ndege, na ya nne kwa idadi kubwa ya amphibians na reptile, vyote hivyo vinatunzwa na misitu ya taifa. Kuna Zaidi ya hekari 46 milioni za misitu Tanzania, sawa na inavyokadiriwa asilimia 50 ya eneo lote la ardhi ya nchi. Zaidi ya asilimia 30 ya misitu inalindwa. Japokuwa ufaharibifu wa misitu kwa Tanzania ni changamoto isiyo zuilika au kuepukika kwa Zaidi ya makadirio ya 500,000 hekari za misitu hupotea kila mwaka kutokana na kutokuwa na matumizi endelevu ya ardhi, uvunaji wa mazao yatokanayo na misitu, na shughuli za kibinadamu.

Kwa muitikio wa mafanikio ya mpango wa majaribio mbalimabail pamoja na mabadiliko ya sera mwanzoni mwa miaka ya 1990. Tanzania ilianzisha mpango wa kitaifa wa usimamizi wa misitu kwa kushirikisha watu katika kuhifadhi na kutunza misitu. Usimamizi wa misitu wa jamii

ni moja wapo ya aina za mpango ya kitaifa ya usimamizi wa misitu kwa kushirikisha watu “PFM” kwa kushirikisha watu katika utunzaji wa misitu. Usimamizi wa misitu wa jamii ni moja wapo ya aina za “PFM” ambazo zitatumika kwa misitu ambayo inamilikiwa au kusimamiwa na Halimashauri za Vijiji na zitapelekea kuanzishwa kwa hifadhi za misitu na ardhi. Tananzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza barani Africa kwa kutekeleza hizi sera, kukiwa na Zaidi ya hifadhi za ardhi na misitu, 500 zilizo anzishwa kuanzia mwaka 1995. Mazingira ya misitu ya Angai ni makubwa miongoni mwa maeneo ya hifadhi ya ardhi na misitu yaliyotangazwa na mengine 11 yapo katika hatua tofauti za “CBFM”. Japokuwa kuanzishwa kwa Angai “VLFR” ilikuwa taratibu kutokana na uhaba wa uwezo wa kuanzishwa umilikishwaji na usimamizi wa mazoa ya misitu.

Ikiwa katika eneo la kusini mwa milima katika mkoa wa Lindi-Tanzania, Angai ni eneo kubwa lililobakia la vitalu vya taifa. Ina jumuisha eneo lenye hekari 140,000 miti ya

5

miombo, ambayo hifadhi, ya Nyati, Ngiri (warthogs), Tembo, Mbwa Mwitu, na Simba. Eneo hili pia ni mojawapo ya mabaki makubwa ya hifadhi ya misitu ya Savannah kwa dunia na inatofautiana kutoka eneo la wazi hadi kwenye vichaka. Kwa sababu ya utajiri wake wa viumbe hai, miti ya miombo imetambulika na Mfuko wa Dunia kwa Asili, (World Wide Fund for Nature) (wwf) kama sehemu mojawapo ya Dunia inayohitajika kulindwa mpaka kufikia 2020.

Msitu unatoa chakula, mitishamba/madawa, kuni, na mazai mengine kwa Zaidi ya watu 30,000 wanaoishi kwenye vijiji 24 vinavyozunguka eneo hilo. Lakini ukataji hovyo wa misitu unatishia uhai wa misitu kwa zaidi ya miaka 20, kama jamii inaishi kwenye umasikini ndiyo maana wanafanya shighuli haramu kama ukataji wa magogo, na kuibadilisha ardhi kwa matumizi ya kilimo, kwa matumaini ya kuongeza kipato chao. Mabadiliko ya tabia nchi, yamesababisha kupotea kwa wanyama pori, kutokana na makazi yao kupotea, ni uthibitisho tosha wa kuelezea madhara ya matendo haya yasiyoepukika. Vitisho vingine kwa misiti hii ya miombo inajumuisha barabara,

uzio, shughuli za uchimbaji na kilimo ambazo huzuia au kusitisha kuhama kwa wanyama, wakati wa kiangazi, kukata na kukushanya kuni, kuchoma mkaa, uwindaji haramu wa Tembo na nyingine nyigi.

Kuanzia mwaka 2011, Asasi mbili za kiraia, Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa MIsistu Tanzania (MJUMITA) na Mpingo Conservation and Development Initiatives, (MCDI), wameshirikiana kwa pamoja kufanya kazi kwenye msitu wa Angai kwa kuishirikisha Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Mpango huo umefadhiliwa na Lindi na Mtwara Agribusiness Support bilateral development project, ambayo kwa pamoja imedhaminiwa na Serekali ya Tanzania na Finland. Dhumuni lake ni: kuwapa wanakijiji haki ya kumiliki ardhi, kuandaa mpango kazi wa kijiji wa matumizi ya ardhi na Mpango wa Usimamizi wa Misitu katika kijiji cha Angai (VLFRs), kuimarisha uwajibikaji wa wa Jamii katiaka taasisi za kijiji na Wanajamii, na kukuza uelewa wa umuhimu juu ya usimamizi mzuri wa misitu na Serekali.

MJUMITA Asili na Muundo

MJUMITA ilianzishwa mwaka 2000 na Kikundi cha Uhifadhi wa Misitu Tanzania kwa dhumuni la kuhamasisha, na kushirikiana na Jamii katika Usimamizi wa Misitu, (PFM). Kuanzia kuanzishwa kwake kama Asasi ya Kiraia mwaka 2007, shirika hili limejumuisha Zaidi ya wanajamii, 15,000 kutoka mikoa 12 na wilaya 23 na vijiji 450.

Dhumuni kuu la Shirika Ni:

■ Kutambua na kusaidia Jamii inayoishi karibu na misitu katika kuimarisha maisha yao kwa kupitia programu mbalimbali;

■ Kukuza uelewa kwenye maendeleo endelevu na usimamizi wa misitu ya asili Tanzania Bara kupitia tafiti, mafunzo, semina, uhamasishaji wa kimtandao, na kuwajengea uwezo wa kimaendeleo taasisi zinazo simamia misitu, kama washiriki wa MJUMIT, pamoja na Washikadau wengine.

■ Kutoa nafasi kwa Taasisi zinazo simamia Misitu na washiriki wa MJUMITA kubadilishana ujuzi, maarifa, mawazo, na uzoefu kwenye mambo mbalimbali katika usimamizi endelevu wa misitu Tanzania Bara;

■ Kusaidia taasisi za vijiji na washiriki wa MJUMITA kufanya kazi na kutoa maamuzi sahihi katika kazi zao kwenye PFM na kuongeza uwezo wa watanzania kuishi karibu na misitu;

■ Kutafuta fedha na rasilimali kwa ajili ya kutekeleza dhumuni kuu la MJUMITA na kusaidia MJUMITA kusonga mbele katika kutambua Dira yake.

■ Kuijengea uwezo Jamii katika kushiriki kikamilifu kwenye kufanya maamuzi kwa utunzaji endelevu wa misitu kitaifa na misitu isiyo tunzwa.

MJUMITA inafanya kazi katika kanda 6 ya kijiografia: Ukanda wa Mashariki na Ukanda wa Pwani, Ukanda wa Kusini, Ukanda wa Kaskazini, na Ukanda wa Magharibi. Zaidi ya wafanyakazi 30 wameajiriwa na taasisi inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mwanamke.

Bodi ina jumuisha wawakilishi wa jamii kutoka kanda zote 6 ambapo, Asasi za Kiraia zinasimamia mtandao. Bodi inachaguliwa na wanachama kila baada ya miaka mitatu katika MJUMITA kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka, MJUMITA ina saidiwa na Wataalamu wawili wa Kiufundi, Mtaalamu mmoja anatoka kwenye Kikundi cha Uhifadhi wa Misitu Tanzania, na mwingine anaaajiriwa na Taasisi yenyewe. MJUMITA pia inashirikiana na kupokea ushauri wa kiufundi kutoka kwa washirika wake, ikujumuisha, Vyuo Vikuu vya Ndani, na Wizara ya Mali Asili na Utali kwenye kitengo cha uhifadhi wa Nyuki na Misitu.

6

CHANGAMOTO ZA NDANI

Ukataji miti na Uharibifu wa Ardhi

Ukataji miti, uharibifu wa misitu, na mabadiliko ya matumizi ya ardhi ni sababu kuu mbili zinazo sababisha uzalishaji/kusambaa kwa hewa ya ukaa ambayo inachangia asilimia 17 ya uzalishwaji wote duniani. Kiwango cha ukataji wa misitu Tanzania kwa mwaka ina kadiriwa kuwa Zaidi hekari 500,000 kwa mwaka na inakadiriwa kuwa ni asilimia moja ya misitu ya Taifa.

Ukataji miti huu unapelekea uharibifu wa mazingira na kupotea kwa makazi ya asili ya wanyama pori. kwa mfano kwenye milima ya misitu ya miombo pale ambapo misitu huaribiwa kwa moto na kama ikichomwa kukua upya kwa mimea katika hutawaliwa na aina ya mmea kama madole

matano (pteridium spp.) ambayo huathiri/ kukandamiza ukuaji wa miti na kuchangia ukuaji wa jangwa/ ardhi isiyokubali mazao/ isiyofaa.

Kisababishi kikubwa cha ukataji wa miti ni usafishaji wa maeneo na matumizi yasiyo endelevu ya ardhi kwaajili ya kilimo, ufugaji wa mifugo inayozidi malisho, uchomaji moto, ukusanyaji na ukataji wa kuni kwaajili ya kupikia na shughuli zinazoendana na hizo, ukataji wa magogo kinyume cha sheria kwaajili ya kujengea na kupata mbao kwaajili ya kuuza, kuchoma mikaa na uchimbwaji wa madini katika hifadhi za misitu.

7

Uzalishaji wa mkaa ndiyo chanzoo kikuu cha mapato kwenye misitu ya miombo. Kuzalisha mkaa, watu wanatumia njia za asili kwa kuchimba matanuru kama njia rahisi, haiitaji ujuzi wowote, na inatumia mtaji kidogo kuwekeza. Njia hii ya asili ya kubadili kuni/mbao kuwa mkaa hupoteza zaidi ya kama asilimia 70 ya thamani halisi ya miti kwa sababu kufukia matanuru/mashimo ni vigumu na ni hatari kwa opereta kukarabati. Matokeo

yake ni kuvuja kwa hewa hakuwezi kudhibitiwa na mkaa unakuwa majivu na baadhi ya sehemu ya rundo la mkaa kabla haujakamilika vizuri. Njia hii isiyo na ufanisi katika uzalishaji wa mkaa inaongeza shinikizo katika misitu ya miombo kwani katika hali nyingi wazalishaji wa mkaa hawapandi miti kama mbadala/ kuchukua nafasi ya miti iliyokatwa hivyo kupelekea uharibifu wa misitu.

Mabadiliko ya hali ya hewa na uhaba wa maji

Kunyesha mvua katika eneo la miombo hakutabiriki, hivyo kupelekea hupelekea uhaba/ukosefu wa vyakula kwa vipindi kutokana na kupungua kwa uwezekano vyanzo vya asili vya vyakula na bidhaa nyingine za asili ambazo zingeweza kuvunwa na kuuzwa au kubadilishwa kwa chakula. Jamii inayotegemea mazingira ya misitu ya angai tayari wameshajionea mabadiliko ya vipindi vya mvua ambayo yameathiri kilimo cha mvua.

kupotea kwa misitu, na kuharibika kwa misitu, pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na kumesababisha madhara

ambayo huathiri maisha ya binadamu na mazingira yao. Athari moja wapo muhimu ni tofauti/ kutotabirika katika ubora na wingi wa maji yanayosambazwa kutoka kwenye makingio ya maji, ambayo hupelekea uhaba wa maji kwa jamii.

Kukinga na kuchota maji ni njia ya asili na kazi ya wanawake kwenye vijiji. Kutokana na bidhaa hii kuwa adimu vifaa vya maji vimeongezeka kama vipau mbele muhimu kwa wanavijiji wengi.

Ukosefu wa uwezo wa usimamizi wa misitu ya Angai

Kwa Zaidi ya miaka 20 jitihada za kutambulisha usimamizi endelevu wa misitu kwenye misitu ya Angai haijafanikiwa kutokana na ukataji haramu wa magogo na usimamizi hafifu ndani ya jamii. Haki za jamii kwenye ardhi na

usimamizi wa misitu zimeanzishwa Tanzania, shEria ya ardhi na misitu, lakini inahitaji wanajamii kuchukua majukumu mapya na kutekeleza katika usimamizi wa misitu.

8

MWITIKIO WA JAMII

Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Asili

Serekali za vijiji zinazozunguka Misitu ya Angai ikiju-muishwa na Wilaya ya Liwale Mkoa wa Lindi; Wizara ya Mali Asili na Utali, na Washirika wenginE wanaofanya kazi katika kuandaa utaratibu wa kisheria na taasisi kwa usi-mamizi shirikishi wa misitu, (PFM), kuanzia mwaka 1994. Na mwaka 2001, mfuko wa hifadhi wa ardhi na misitu wa Angai, (VLFR) ulipendekezwa rasmi na kuanzishwa chini kifungu cha sharia ya misitu ya (2002) na shEria ya vijiji ya Ardhi ya mwaka (1999) na kupitishwa umilikishwaji na usimamizi kwa vijiji 13, ambavyo vilikuwa vimegawanywa kwenye vijiji 24 mwaka 2009. Muundo huu wa vijiji vipya umefanya umuhimu wa kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi (LUPs) kwa sehemu ya misitu inayomilikiwa na vijiji.

Kila mwakijiji, (VLFR) sasa anasimamiwa na taasisi za ndani kwakupitia utekelezaji wa mpango wa kijiji wa matumizi ya ardhi (FMP) na shEria ndogo ndogo, zilizotengenezwa na wanajamii wenyewe na kupitishwa na Halimashauri.

Mabadiliko ya sasa ya umiliki wa misitu ya Angai kwa jamii kwakupitia mtu mmoja mmoja, VLFRs inategemea kuwa-saidia kufuata mpango wa matumizi ya ardhi, (LUPs), na kusitisha kukata misitu kwa ajili ya kilimo ndani ya hifadhi za misitu. Kufanikisha hili ni muhimu kwa kipato kitokana-cho na misitu kitumike vyema kutokana na matakwa ya jamii na isimamiwe vyema. Kama jamii haitaona na haita-faidika na misitu wataendelea kudabili maeneo ya misitu kwa kilimo.

Kwakushirikiana na MJUMITA na Halimashauri ya Wiliya ya Liwale, (MCDI) imeongoza taasisi za vijiji kuchukua utaalamu wa kiufundi kwenye hesabu KUCHUKUA UTAALAM WA KUTAMBUA UKUBWA NA IDADI YA MISITU na maandalizi ya mpango wa usimamizi na kutambulisha njia mpya za kujipatia kipato, kama vile urinaji mdogo wa asali, na uvunaji endelevu wa mbao.

MAMBO MUHIMU

Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Asili

■ Baadhi ya viumbe hai kama Tembo, hawaJAonekani kwa miaka mingi kwenye misitu ya Angai, lakini idadi yake imeongezeka kwa kiasi cha kusababisha uharibifu wa mashamba yanayomilikiwa na wanajamii. MJUMITA, kwakupitia AFISA WANYAMA PORI WA Halimiashauri ya Wiliya ya Liwale, wametoa mafunzo kwa wanavijiji juu ya njia za kuwafukuza wanyama bila ya kuwaua.

■ Jamii mbalimbali zinachukua njia stahiki katika kukabiliana ukataji haramu wa magogo, ambayo imepunguzwa kwenye sehemu nyingi kwa kufanya DORIA ambazo hupelekea kukamatwa kwa wakataji magogo haramu na kuzitaifisha mbao haramu. Kama matokeo ya usimamizi madhubuti, mwaka 2015 DORIA ZimeongezEKA kwenye misitu na kuzuia matukio 17 na kufanikiwa kuwakamata watu 25, na KUtaifisha magogo 2,478 yenye thamani ya dola za kimarekani 16,000 ($16,000).

9

Kujenga uwezo shirikishi wa usimamizi wa misitu

Kwakupitia sheria mpya walizizipata za uhifadhi wa misitu ya vijiji, (VLFRs), jamii ya Angai sasa wanaweza wakauza mbao zilizo katwa kiuendelevu. Kutokana na kuuza mbao kama chanzo kipya cha mapato kuna mambo muhimu yakufanya ili kuhakikisha uwazi wa maamuzi yanayohusiana na suala la misitu na mapato yatokanayo na misitu.

Kwa muktdha huu, MJUMITA imeanzisha njia kwa kuzisaidia mamlaka Za serekali za mitaa kwenye kushiriki na kuandaa Mpango wa Matumizi wa Ardhi, (LUPs), hatua ya kwanza kwa usimamizi wa misitu kwa jamii. Wakati wa hatua za mpango wa matumizi ya Ardhi, jamii inatathimini mahitaji ya ardhi ya kilimo na kwenye vijiji vingi wametambua kwamba Zaidi ardhi ya misitu inaweza kuelekezwa katika hifadhi za misitu tofauti na na walivyokuwa wakifikiria hapo awali.

Jamii inaelewa kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yatasababisha vipindi vya mvua kubalika na kuwa vya kutoeleweka na kusababisha kilimo cha mvua kuwa kigumu kutegemeWa. Wanatambua pia wanaitaji misitu kama chanzo cha mali ghafi, na usimamizi wa kinga maji. Kwakuwa jamii sasa inafahamu kwamba ardhi ni mali yao, na LUPs zimetengenezwa, kulinda rasilimali zao na maisha yao, umiliki wa misitu kwa wanajamii unategemewa kutoa

motisha na kuipa jamii hamasa ya kufuata mpango bora wa matumizi ya ardhi, na kuacha kufyeka misitu kwa matumizi ya kilimo ndani ya hifadhi za misitu.

Kwakuongezea kuendelezwa kwa LUPs, MJUMITA vimetoa mchango muhimu katika kuwabadilisha watu kifikra kutoka kutumia misitu, mpaka kuwa wamiliki wa misitu kwa kuisaidia jamii kuamua jinsi ya kutumia mapato yatokanayo na misitu kwa uwazi na kwa uwajibikaji. Kwa mfano kwenye baadhi ya vijiji mapato yatokanayo na misitu hutumika kwa ajili ya miundombinu, ikiwa ni pamoja na kuanzisha vitalu kwa ajili ya upandaji miti, kujenga kwa madaraSA kwenye shule za msingi, na sekondari, kujenga zahanati na vituo vya afya, kuchimba visima vya maji, na kujenga ofisi za kijiji na usajili wa ardhi ambao ni sharti la kwanza la kupata haki za msingi za kuishi kwa wanajamii wote. Kama sehemu ya mchakato huu, MJUMITA imetoa mafunzo kwa wanajamii, na taasisi za kijiji kwa matendo, juu ya utawala na usimamizi wa fedha na kusaidia kuwajengea ujuzi, na uwezo wa kiutawala ndani ya rasilimali za asili za vijiji kwenye kamati na Halimashauri za vijiji. Kuimarika kwa usimamizi wa fedha na mchakato wa kiutawala kumeongeza utoaji wa taarifa na ushirikishwaji wa jamii na kuruhusu jamii kuwa na ushawishi katika utoaji wa maamuzi unaofanywa na Serekali ya kijiji.

MAMBO MUHIMU

Kuwajengea uwezo wa kushiriki katika usimamizi wa Misitu

■ Chombo cha Usimamizi wa misitu cha kijiji kimetekelezwa kwenye vijiji vyote 24 vya Angai. Matokeo makubwa ya utekelezaji wake ni kuongeza usimamizi wa msitu wa kijiji na kuimarisha uwezo wa jamii katika kuwawajibisha viongozi wao. Nyenzo hii imewezesha jamii katika ushawishi wa kutoa maamuzi dhidi ya rasilimali za misitu na matumizi ya mapato yatokanayo na misitu. Serekali za vijiji pia zimeanzisha utoaji na ushirikishwaji wa taarifa kwenye mchakato wa biashara ya mbao na mapato yatokanayo na misitu kwakutumia nyenzo hiyo. Vijiji pia vimetumia nyenzo hiyo kuanzisha vipindi vya atawala madhubuti katika kuendesha vikao na kufanya msako/ DORIA kwenye misitu.

■ Mpaka sasa vijiji 13 vimekamilisha mpango wa LUPs, na mpango wa usimamizi wa misitu (FMPs,). Vilivyobakia 11 vipo katika hatua tofauti tofauti za kuandaa mpango wao wa LUPs na FMPs.

10

MATOKEO YA SERA

Matokeo ya Sera ya Taifa

MJUMITA, inafanya kazi na mamlaka mbalimbali za serekali kuanzia ngazi ya kijiji, wilaya, na inashirikisha kitengo cha misitu na uhifadhi wa nyuki katika Wizara ya Mali Asili na Utalii. Sera ya misitu ya mwaka 1998 na Sheria yamisitu namba 14 ya mwaka 2002 inatawala usimamizi wa misitu kwa Tanzania. MJUMITA, kwakushirikiana na Asasi nyingine za Kiraia walishiriki kwenye kutoa mapendekezo ya kupitiwa upya kwa sera ya Taifa ya misitu, zote za mwaka 1998 na 2016.Zaidi kwa sasa mwaka 2017, MJUMITA wamechagua kikosi kazi kuhamasisha kupitiwa upya kwa mchakato ambao unatafuta kupata maoni ya wadau Zaidi.

Kabla ya hapo mwaka 2015, MJUMITA, kupitia mradi wa haki ya misitu Tanzania uliopelekea kuanzishwa kwa jamii kutumika kwenye mkutano mkuu kudai wagombea wao kuwahakikishia utendaji mzuri ndani ya hifadhi za misitu na

usimamizi wa misitu Zaidi sana kuhusu kufuatia mipango ya usimamizi wa misitu, wanajamii wakajenga Imani, nakuimarisha haki za jamii ndani ya agenda kwa kutaja maHitaji ya jamii kwakupitia midahalo, na wanasiasa na taasisi za serekali.

Taasisi imeendelea kufanya kazi na serekali za mitaa katika kuhimarisha utambuzi wa jamii juu ya umiliki wa misitu, haki na haki za usimamizi wa misitu. Ugatuzi kamili wa usimamizi wa kijiji cha Angai umebakia kuwa ni kazi inayoendelea kama jamii inavyoendelea kuitaji umuhimu wa ushirikiano kutoka njee, Zaidi kuwajengea uwezo katika kusimamia misitu yao kikamilifu na kuendeleza biashara endelevu kwamujibu wa sharia ndogo ndogo za mpango wa usimamizi wa misitu, na taratibu nyingine za utawala.

11

Mchango wa ajenda Kimataifa

MJUMITA’s inafanya kazi Tanzania na inalenga usimamizi wa misitu shirikishi na ushirikiano wa uhifadhi na uendelevu wa maisha, hivyo basi inatoa mjumuiko wa malengo MBALIMBALI ya maendeleo endelevu, (SDGs). Mradi wa, MJUMITA unaainisha muunganiko baina usimamizi endelevu wa misitu, na mambo mengine ya SDGs ikijumuisha, kupunguza umasikini, usalama wa chakula, na uendelevu wa lishe, ukuaji wa uchumi endelevu, na ajira kwa wote, uendelevu wa kuzalisha na kununua, usawa wa kijinsia, na mabadiliko ya tabia nchi.

Usawa wa kijinsia ni jambo muhimu kwa, MJUMITA (SDG 5). Shirika limehakikisha usawa wa kijinsia unazingatiwa katika shughuli zake zote. Hii imeanza wakati wa maandalizi ya kuomba fedha ambapo maombi yote yanazingatia usawa wa kijinsia, kuhakikisha wanaume kwa wanawake, na pia walioko pembezoni wanashirikishwa kikamilifu. MJUMITA inatumia njia ya kufanya kazi kutokea ngazi ya vitongoji, mpaka kwenye ngazi za vijiji kwasababu vitongoji ni mojawapo inayojumuisha washiriki wote wajamii, sana sana wananchi maskini, wanaume, wanawake, vijana na wale wa pembezoni. Usimamizi wa misitu wa kijiji umeendeleza MJUMITA na kuwawezesha wanakijiji wenyewe to kusimamia ukamilifu wa ushiriki wao wanaume, wanawake kwenye taasisi za vijiji za usimamizi wa misitu.

MJUMITA, pia ina angazia katika masuala ya afya (SDG 2), kuhakikisha inatoa uelewa ndani ya jamii kuhusu maambukizi ya UKIMWI na VIRUSI vya UKIMWI, (HIV/AIDS) na kuwakumbusha kuchukua tahadhari na kinga katika kusambaza kwa ugonjwa. Vikundi vya kijamii wanashirikiana na MJUMITA kutoa elimu juu ya misitu na masuala ya afya pia juu ya UKIMWI na MAAMBUKIZI YA UKIMWI (HIV/AIDS) kama njia ya uvumbuzi yakutoa uelewa kwa jamii. MJUMITA, imeendeleza mpango wa elimu ya UKIMWI makazini kuwafanya wafanyakazi kuwa na uelewa jinsi ya kuwaelimisha wanajamii juu ya UKIMWI. MJUMITA, imehamasisha wanajamii na serekali za vijiji kutumia fedha zinazopatikana kutokana na misitu kujenga vituo vya afya, kwenye vijiji vyao, na kulipia bima za afya kwa wanavijiji wote ambao ni masikini.

Shirika pia limeshawishi ajenda za kisiasa za ndani na kimataifa kwa kufanya kazi na wanahabari kwa mafanikio, katika kuchapisha magazeti, vipindi vya redio, na runinga katika maada zinazohusiana na usimamizi wa misitu na kuhamasisha watu kwenye siasa na wafanyakazi wa serekali. Lakini pia shirika limeshirikiana na jamii za kimataifa kwenye masuala ya REDD+ na usimamizi wa misitu kupitia mikutano ya kimataifa na Umoja wa Mtaifa kwenye ajenda ya mabadiliko ya tabia nchi.

12

UHABA NA UENDELEVU

Marudio

MJUMITA, imekuza shirikisho la usimamizi wa misitu katika ngazi ya usimamizi wa jamii kwenye shughuli za misitu na imehusisha jamii Zaidi ya 100 na vijiji 450 vimehusiSHWA kwenye usimamizi wa misitu, (PFM) unaoendelea Tanzania ambayo imejirudia ujuzi wa taasisi kwenye maeneo mengine ya nchi.

Kwakuongezea MJUMITA, inafanya kazi ndani ya Tanzania, muundo wa MJUMITA, umerudiwa Kenya na Uganda kuanzia mwaka 2005 mpaka 2009. Kikundi cha Uhifadhi wa Misitu Tanzania kimetekeleza mpango wa kibara kwakushirikiana na Kenya na Uganda unaoitwa

‘kuiwezesha jamii kushiriki kwenye usimamizi wa misitu Afrika Mashariki’ (Empowering Communities on Participatory Forest Management in East Africa”). Chini yampango huu, lengo moja lilikuwa kuanzisha mtandao wa misitu ndani ya muundu wa MJUMITA. Kama matokeo mtandao wa misitu wa Uganda,na muunganiko wa jamii wa Taifa wa misitu Kenya umeanzishwa na unafanya kazi mpaka sasa. (The Uganda Network for Collaborative Forestry Association and the National Alliance of Community Forestry Associations of Kenya were established and remain operational to date).

Marudio

MJUMITA inasaidiwa na washiriki mbalimbali katika nchi kama, kikundi cha uhifadhi wa misitu Tanzania, ofisi ya WWF Tanzania, jukwaa la maliasili Tanzania, na mpango wa uhifadhi na maendeleo wa mpingo wa marudio ya kazi zao kwenye jamii Zaidi ya 100 kwakushirikiana na mitandao ya kijamii.

MJUMITA’s inafanya kazi Angai inanufaika kutokana na uzoefu wa mtandao huu ambao pia unachangia kwenye kusanyiko kuu la mwaka la MJUMUTA linaloileta jamii pamoja kuwakilisha mitandao ya ngazi za chini na kutoa jukwaa kwa wajengea uwezo, ushirikiano na hamasa.

Ni nafasi ya kuhamasisha na kusaidia marekebisho ya kitaifa na kimataifa ya sera ambazo zinaweza kupanua mitandao kwa ngazi ya kitaifa.

Kwakuongezea, MJUMITA, imetekeleza miradi mingi ya ushiriki wa usimamizi wa misitu,(PFM) kitaifa. Jamii nyingi za Angai zimeshiriki kwenye mipangom ya kitaifa iliyo pangwa kupitia miradi hii, ambayo inajumuisha kusaidia vijiji kwenye ufanisi wa hesabu na ukaguzi, pia kuimarisha utawala na uwazi kwakupitia mapato yatokanayo na misitu, kubadilishana maarifa, na kushirikishana matokeo

13

katika mtandao. Hilo ndilo somo walilojifunza kutokana na ujuzi wa taasisi kwenye maeneo katika kutoa matokeo

kukuza na kuimarisha kazi zake sehamu nyingine za nchi.

Uendelevu wa MJUMITA

MJUMITA, imepiga hatua kubwa kuelekea Uendelevu Kama Shirika la msingi. Wanachama wanatoa michango inayotakiwa kila mwaka. Japokuwa shirika linatafuta njia nyingine za kujipatia kipato kupitia Kwa wafadhili na vyanzo vingine, kama kuuza fulana, wakati wa vikao.

Chanzo kingine muhimu cha mapato kwa asasi hizi za kiraia ni mikopo na michango kutoka kwa washiriki walioendelea, watu binafsi, taasisi binafsi, na taasisi mbalimbali katika kuendelea kuwajengea uwezo washiriki wake kushiriki kikamilifu kwenye usimamizi

shirikishi wa misitu na kuimarisha hali ya maisha yao.

MJUMITA, pia imejenga uwezo kwa mitandao ya kitaifa kujitegemea. Shirika linatoa mafunzo kwa mitandao ya kitaifa jinsi ya kukusanya mapato na kupanga miradi na usimamizi. Hivyo ndivyo mitandao ya kitaifa inavyotekeleza shughuli za ukusanyaji wa mapato yatokanayo na mazingira. MJUMITA, inaunganisha mitandao ya ndani na taasisi za fedha kama Mfuko wa Fedha wa Misitu Tanzania, na wafadhili watakaotoa misaada kusaidia mipango hii.

MIPANGO YA MBELENI ■ Kupanua utekelezaji wa uzalishaji wa mkaa endelevu ili kukidhi maitaji ya wateja na kutoa kipaumbele

uhifadhi wa misitu. Jamii za Tanzania zimeanzisha Zaidi ya vijiji 800 vya hifadhi ya misitu vinavyo chukua hekari 2.3 milioni za misitu na miti ya mbao; uzalishaji endelevu wa mkaa utatoa mapato Zaidi kutoka kwenye hifadhi hizi na kutoa ajira kwa watu wa vijijini.

■ Inatafuta ushirikiano na wafadhili katika kukuza miradi ya MJUMITA kwenye jamii mpya kuzunguka Tanzania.

■ Inaanzisha miradi ya kukopa na kuhifadhi fedha kwa wanajamii ili kuwawezesha kupata mikopo kwa masharti nafuu na pia kuanzisha vyanzo vidogovidogo vya mapato. Pendekezo limewekwa pamoja kusaidia mradi huu.

WASHIRIKA ■ WWF Tanzania: WWF Tanzania is a networking and

project partner with MJUMITA focused on activities in the southern part of Tanzania.

■ Tanzania Forest Conservation Group (TFCG): TFCG helped to establish MJUMITA as a network and is a key partner for the organization.

■ Tanzania Natural Resources Forum (TNRF): MJUMITA is a member of Tanzania working group hosted by TNRF and TNRF is a partner in networking and information sharing.

■ Mpingo Conservation and Development Initiative (MCDI): Project and information-sharing partner that provides support to some of the communities in which MJUMITA works.

■ The Ministry of Natural Resources and Tourism: MJUMITA engages as a service provider to the National Forest and Beekeeping Program under the Ministry of Natural Resources and Tourism, provides the program with technical support on governance and land use planning.

■ Sokoine University of Agriculture: The University is a project partner.

■ Institute of Resource Assessment of the University of Dar es Salaam (IRA): The Institute is a project partner.

■ Forest Training Institute: The Institute is a project partner.

■ Care International: Care International is a networking partner.

14

Mradi na Wafadhili Washirika Mafanikio Makubwa/makuu

REDD+ (Norway) TFCG Fedha kwa mradi wa REDD+ kwa jamii za Lindi na Wilaya ya Kilosa Tanzania. Kama matokeo 26 ya mpango wa matumizi ya ardhi, (LUPs) ilikamilika, 26 VLFRs ilitangazwa, kama wanufaika washiriki wa misitu, na chombo hicho kilianzishwa na kujaribiwa na jamii iliyo wezeshwa katika usimamizi wa misitu, uhifadhi wa kilimo, na ufugaji wa nyuki.

Sustainable Charcoal (SIDA)

TFCG Kuhamasisha mchakato wa LUPs na kuanzishwa kwa VLFRs, maendeleo na uvumbuzi endelevu wa mkaa, mafunzo kwa jamii, juu haki katiaka ardhi kwa kupitia hati za kimila (CROs), na kuwajengea uwezo juu ya utawala wa misitu na usimamizi wa fedha, kwa Wilaya za Kilosa, Mvomero, na Morogoro kwa Mashariki ya Tanzania, (Eastern Arc Mountain Ecosystem).

National awareness on REDD+ (Norway)

IRA Kuhamasisha Taifa juu ya REDD+ issues.

Scaling up PFM in Ruvuma Landscape

WWF TCO, MCDI, District Councils

Kuanzisha VLFRs 9 na kukuza uwezo wa jamii kwe kuelewa, kuchambua, na kuhamasisha uhimarishaji wa ardhi na haki za misitu, na kuhamasisha utendaji mzuri wa jamii juu ya taasisi zinazo simamia misitu, na wanachama wa MJUMITA juu ya umiliki wa ardhi yao, misitu yao, na rasilimali fedha zao, kwenye vijiji 20 katika ukanda wa Ruvuma Kusini mwa Tanzania.

Mama Misitu Compaign (Finland na Norway)

TNRF Kuongeza utawala na uwajibikaji wa kijamii miongoni wa taasisi za ndani na kitaifa zinazo simamia misitu, kwa Rufiji, Kilwa, Lindi naWilaya ya Nachingwea Kusini Mwa Tanzania, kwa kutangazaPFM na biashara nzuri ya Misitu

Sustainable Agriculture and Climate Change (DFID)

TFCG Kukagua na kutangaza uhifadhi wa dhana za kilimo miongoni mwa Jamii, kwenye milima ya Kusini.(Eastern Arc Mountains).

Forest Justice in Tanzania (DFID)

TFCG Kuhamasisha uongozi mzuri kwa PFM na mipango kwenye vijiji 300, na Wilaya 13, kwa Tanzania Bara kwa njia ya Mtando na kusimamia utekelezaji wa sharia, kimataifa REDD+ na viwango vya Misitu (kwa mfano FSC), kwakutumia chombo cha dashboard (dashboard tool)

CBFM in Angai (LIMAS)

MCDI, and Liwale DC

Kuhamasisha LUPs, uanzishwaji wa VLFRs, uwezeshwaji wa jamii kwenye kutekeleza LUPs na PFM , kuwajengea uwezo wa usimamizi wa rasilimali fedha, mtandao, na kutangaza kwenye vijiji 24 vya Angai

Improving Values of Eastern arc Montain Forests (EU)

TFCG & (TFS)

Uhamasishwaji wa LUPs, uanzishwaji wa VLFRs, kutangaza ushirika wa usimamizi wa misituna kuijengea jamii uwezo mzuri wa usimamizi wa misitu, mtandao, na uhamasishaji.

ECOPRC (Norway) FTI and SUA

Kuijengea uwezo jamii inayoishi pembezoni mwa misitu ya asili kote Tanzania juu ya kupunguza na kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa.

15

NUKUU ZAIDI ■ Clinton Climate Initiative, Angai Village Forest Reserve. Available online here. ■ Doggart Nike, Tanzania’s Community Forestry Network wins the prestigious Equator Prize 2015, 2015. Available online

here. ■ Government of Tanzania / Government of Finland, Lindi & Mtwara Agribusiness Support PROJECT DOCUMENT, 2011.

Available online here. ■ Jew, Eleanor et al., ‘Miombo woodland under threat: Consequences for tree diversity and carbon storage’, Forest

Ecology and Management, 2016. Available online here. ■ Katani, Josiah et al., ‘Participatory forest carbon assessment in south-eastern Tanzania: experiences, costs and

implications for REDD+ initiatives’, Fauna & Flora International, 2015. Available online here. ■ Lerise, Fred et al., The case of Lindi and its region, Southern Tanzania. Briefing Paper Series on Rural-Urban Interactions

and Livelihood Strategies, International Institute for Environment and Development (IIED), 2001. Available online here.

■ Ministry of Natural Resources and Tourism of Tanzania, Community Based Forest Management Guidelines for the Establishment of Village and Forest Reserves and Community Forest Reserves, 2007. Available online here.

■ MJUMITA, About Us. Available online here. ■ Monela, G.C. and Abdallah, J.M., Overview of Miombo Woodland in Tanzania, 2007. Available online here. ■ Mpingo Conservation and Development Initiative (MCDI), Angai Forest, 2013c. Available online here. ■ Southern Voices, Report on Organisational Capacity Assessment of Community Forestry Conservation Network of

Tanzania – MJUMITA 2011, 2011. Available online here. ■ Tanzania Forest Conservation Group (TFCG), Monitoring village forest governance with the MJUMITA dashboard tool.

Available online here. ■ The REDD Desk, REDD in Tanzania, 2017b. Available online here. ■ UN-REDD Programme, About REDD+, 2017. Available online here. ■ United States Agency for international Development (USAID), Tanzania Environmental Threats and Opportunities

Assessment, 2012. Available online here. ■ WWF, Earth’s most special places, 2017. Available online here.

SHUKRANIMkakati huu wa ikweta unatoa shukrani za pekee kwa Bwana, Rahima Njaidi, na Bwana, Aklei Albert hasa katika mwongozo na mchango wa kuhariri Makala hii. Photos courtesy of MJUMITA. Maps courtesy of CIA World Factbook and Wikipedia.

Toleo la lugha ya uingizaji wa hati hii ilitafsiriwa kwa kushirikiana Bwana Peter Laurent Kamhama na Bwana, Shadrack Mziray, waliojitolea katika mtandao wa Umoja wa Mataifa kufanikisha kazi hii na kuhamasishwa kupitia www.onlinevolunteering.org.

WahaririMhariri mkuu: Anne VirnigMhariri msaidizi: Maria Caram

Waandishi WaliochangiaMarcela Torres, Nicole DeSantis and Anne Virnig

KubuniKimberly Koserowski

Dondoo LililopendekezwaShirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa 2018. (United Nations Development Programme) 2016. Mtandao Wa Jamii Wa Usimamizi Wa Misitu Tanzania (Mjumita), Tanzania.. Mkakati wa mfululizo wa Utafiti wa Ikweta (Equator Initiative Case Study Series. New York, NY).

Equator InitiativeSustainable Development ClusterUnited Nations Development Programme (UNDP)304 East 45th Street, 15th Floor New York, NY 10017www.equatorinitiative.org

Shirika la Maendeleo Duniani (UNDP), kwa kushirikiana na watu katika ngazi zote katika jamii linasaidia kujenga nchi ambazo zinaweza kuhimili migogoro na kujiendesha na ukuaji endelevu ambao unalenga kuboresha maisha ya kila mtu.

Mkakati wa ikweta unaleta pamoja muunganiko wa mataifa, serikali, asasi za kiraia, biashara na taasisi zilizopo ngazi za chini kutambua na kuendeleza suluhisho la maendeleo endelevu kwa jamii na watu, mazingira na jamii imara.

Mkakati wa ikweta ©2018 Haki zote zimehifadhiwa

Empowered lives. Resilient nations.