43
i HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA RASIMU YA MPANGO WA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA MSITU WA HIFADHI YA KASEMBE. KIJIJI CHA IKOLA HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA S. L. P. 1 MPANDA

HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

  • Upload
    others

  • View
    17

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

i

HALMASHAURI YA KIJIJI CHA

IKOLA

RASIMU YA MPANGO WA

USIMAMIZI SHIRIKISHI WA

MSITU WA HIFADHI YA

KASEMBE.

KIJIJI CHA IKOLA

HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA

S. L. P. 1

MPANDA

Page 2: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

ii

MAELEZO YA JUMLA YA MPANGO........................................................................................................... 1

MAELEZO.................................................................................................................................................. 2

Msitu wa Hifadhi ya Kijiji cha Ikola .......................................................................................................... 2

MATUMIZI YA MSITU WA HIFADHI YA KIJIJI CHA IKOLA ......................................................................... 3

KIJIJI CHA IKOLA ....................................................................................................................................... 4

Sehemu ya tatu: ....................................................................................................................................... 5

Madhumuni ya mpango wa usimamizi wa msitu wa kijiji cha Ikola ........................................................ 5

ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MANDA. ................................................................................................. 6

ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA KALOFWESI ............................................................................................ 6

ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA KASEMBE ............................................................................................... 7

SEHEMU YA PILI ....................................................................................................................................... 7

MPANGO WA UTEKELEZAJI...................................................................................................................... 7

Meneja Mteule ........................................................................................................................................ 7

Uwezo na Majukumu ya Kamati ya Mazingira ........................................................................................ 8

Majukumu ya Mwenyekiti wa kamati ya Maliasili ya Kjiji ....................................................................... 9

Majukumu ya Katibu wa kamati ya mazingira: ......................................................................................10

Majukumu ya Mtunza hazina: ...............................................................................................................11

Msimamizi wa Doria: .............................................................................................................................11

Majukumu ya Wahusika Wengine .........................................................................................................11

Halmashauri ya Kijiji:..............................................................................................................................11

Wanakijiji ...............................................................................................................................................12

Wataalamu wa Misitu katika ngazi mbalimbali .....................................................................................12

Viongozi wa Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa, na Taifa (Mtendaji kata, Diwani, Katibu Tarafa, Mkuu wa

Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji (W), Mbunge, Mkuu wa Mkoa na Waziri).............................................13

UTENDAJI KAZI WA KAMATI YA MALIASILI YA KIJIJI. .............................................................................13

MAELEZO MENGINEYO ..........................................................................................................................13

UTOAJI TAARIFA .....................................................................................................................................13

UWEKAJI WA KUMBUKUMBU ...............................................................................................................14

MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA KAMATI YA MALIASILI ..............................................................14

MATARAJIO YA UFANISI WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA USIMAMIZI WA MSITU.........................14

UTUNZAJI KUMBUKUMBU .....................................................................................................................15

Page 3: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

iii

VITABU VYA KUMBUKUMBU .................................................................................................................15

KITABU CHA MAKOSA NA FAINI ............................................................................................................15

KITABU CHA STAKABADHI......................................................................................................................15

VITABU VYA VIBALI ................................................................................................................................16

KITABU CHA DORIA ................................................................................................................................16

KITABU CHA AKAUNTI ............................................................................................................................16

KITABU CHA MAPATO NA MATUMIZI....................................................................................................17

USIMAMIZI WA FEDHA ..........................................................................................................................17

WAHUSIKA WAKUU; ..............................................................................................................................17

AFISA MUWAJIBIKAJI WA MASUALA YA FEDHA ....................................................................................17

MATUMIZI YANAYOIDHINISHWA; .........................................................................................................18

Mipaka ya Msitu wa hifadhi wa kijiji cha Ikola ......................................................................................19

MAELEKEZO MAALUM ...........................................................................................................................19

ULINZI NA UKAGUZI WA ENEO LA MSITU WA KIJIJI CHA IKOLA ............................................................19

Sifa za Walinzi wa Msitu. .......................................................................................................................20

Wajibu, Majukumu na Mafao ya Walinzi wa Msitu wa Hifadhi ya Kijiji ................................................20

OPERESHENI ...........................................................................................................................................21

ZAWADI YA PONGEZI KWA MWANA DORIA ........................................................................................21

Kanuni za Kutumia Msitu wa Hifadhi ya kijiji .........................................................................................21

Kanuni za matumizi ya msitu: ................................................................................................................22

Matumizi ya Msitu yanayohusu Ukataji wa Miti ...................................................................................22

TARATIBU NA SHERIA NYINGINEZO .......................................................................................................22

Adhabu ...................................................................................................................................................22

MCHAKATO WA KUMSHUGHULIKIA MKOSAJI NA KOSA .......................................................................22

FAINI NA ADHABU KWA KILA KOSA .......................................................................................................23

FAINI ZA KUTOWAJIBIKA ........................................................................................................................24

KUUENDELEZA MSITU ............................................................................................................................24

UTANGULIZI: ..........................................................................................................................................25

UVUNAJI WA MITI ..................................................................................................................................25

HATUA ZA HARAKA ................................................................................................................................26

UFUATILIAJI ............................................................................................................................................26

Vigezo vya Mafanikio: ............................................................................................................................26

Wafuatiliaji .............................................................................................................................................27

Taarifa ya Ufuatiliaji Itatolewa kwa: ......................................................................................................27

Muda wa Kufanya Ufuatiliaji..................................................................................................................27

Page 4: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

iv

RATIBA YA UTEKELEZAJI .........................................................................................................................28

Hatua za Awali za Utekelezaji: ...............................................................................................................28

Hatua Zitakazofuata ...............................................................................................................................28

MUDA WA MPANGO, MAREKEBISHO NA MAPITIO YAKE: ....................................................................28

VIAMBATA ..............................................................................................................................................30

MPANGO WA UVUNAJI KWA AINA MBALIMBALI ZA MITI KATIKA EDU ZA KASEMBE ..........................30

JEDWALI Na 1: ORODHA YA MITI YA INAYORUHUSIWA KUVUNWA - EDU YA KASEMBE. ....................30

JEDWALI Na. 2: MAJUMUISHO YA TAKWIMU KUTOKA KATIKA PLOTI ZA SAMPULI .............................31

JEDWALI Na 3 FOMU ‘C’ YA TATHIMINI.................................................................................................33

JEDWALI NA. 5: MIHIMILI YA MSINGI KUONYESHA WINGI WA MITI MSITU WA MIOMBO

USIOHARIBIWA ......................................................................................................................................35

...............................................................................................................................................................35

JEDWALI Na 6. UFUPISHO WA MPANGO WA UVUNAJI KATIKA EDU YA KASEMBE KWA MWAKA

2017/2018 HADI 2021/2022 ..................................................................................................................36

JEDWALI Na 7: ORODHA YA MITI YA INAYORUHUSIWA KUVUNWA - EDU YA KASEMBE .....................37

JEDWALI Na. 8: MPANGO KAZI WA UTEKELEZAJI WA USIMAMIZI WA MSITU WA HIFADHI WA

KASEMBE KIJIJI CHA IKOLA .....................................................................................................................38

Page 5: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

1

MPANGO WA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA MSITU WA HIFADHI YA KIJIJI CHA

IKOLA

SEHEMU YA KWANZA - UTANGULIZI

MAELEZO YA JUMLA YA MPANGO Mpango huu wa usimamizi umeandaliwa na timu ya Tathimini Shirikishi ya Rasilimali

za Msitu kwa kushirikiana na wataalamu wa misitu wa Halmashauri ya wilaya ya

Mpanda.

Maandalizi ya mpango huu wa usimamizi wa msitu wa kijiji cha Ikola umefanyika

kwa niaba ya wananchi wa Kijiji cha Ikola ambao ndio wamiliki wa msitu huu.

Mpango huu umepitishwa na Halmashauri ya kijiji na kusomwa kwenye mkutano

mkuu wa kijiji cha Ikola na kuidhinishwa na Halmashauri ya Wilaya Mpanda.

Uamuzi wa kutenga na kuuhifadhi msitu huu wa kijiji cha Ikola kuwa msitu wa

hifadhi wa kijiji umetokana na wanakijiji wenyewe kuona umuhimu wa kuuhifadhi kwa

manufaa yao na Tanzania kwa ujumla na kuweka taratibu za kisheria ili kuwezesha

kijiji kupata manufaa yatokanayo na mazao na huduma za msitu na kuepusha vizazi

vijavyo kukosa kabisa rasilimali za msitu huu.

Malengo makuu ya mpango huu wa usimamizi wa msitu wa kijiji cha Ikola ni

kuhifadhi, Kuuendeleza na Kutumia kwa namna endelevu kwa manufaa ya kizazi

cha sasa na kijacho

Page 6: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

2

MAELEZO Msitu wa Hifadhi ya Kijiji cha Ikola Msitu wa Hifadhi ya kijiji cha Ikola unamilikiwa kuhifadhiwa na Halmashauri ya Kijiji

cha Ikola kwa niaba ya wananchi wote wa Ikola. Madhumuni ya msingi ya kuhifadhi

msitu huu ni kutunza na kuhifadhi uoto wa asili uliopo kwa wingi kwenye msitu huu,

kutoa mazao ya msitu na huduma ya/za misitu kwa kuzingatia misingi ya matumizi

endelevu na kuhifadhi bioanuai muhimu zinazopatikana ndani yake kwa manufaa ya

vizazi vya sasa na vijavyo vya Tanzania na ulimwengu kwa jumla.

Msitu huu wa hifadhi ya kijiji ni matokeo ya zoezi la Mpango wa Matumizi Bora ya

Ardhi ya kijiji cha Ikola lililofanyika mwezi Mei mwaka 2016 na kuridhiwa na wananchi

wote wa Ikola.

Msitu huu umeenea kwenye safu ya Milima Wansisi, mlima Kamba, eneo la

matambiko la Lyamizimu hadi mlima Mbamba.

Msitu huu una uoto wa miti mchanganyiko na sehemu nyingi vilevile ambazo zina uoto

mchanga. Kwa juu msitu umefunga kwa viwango tofauti tofauti toka sehemu moja hadi

nyingine. Ndani ya msitu huu kuna sehemu zilizofunga wastani hasa kando kando

mwa vyanzo vya maji na mito kama mto Manda, Sambimalala, mto kasenga na

Msamvula ambayo humwaga maji kwenye mto Msengusi na kuelekea ziwa

Tanganyika Pia ndani ya msitu huu kuna sehemu zilizo wazi hasa kutokana na uvamizi

kwa ajili ya kilimo na zile sehemu za mabonde na mbuga ambazo ni vyanzo vya maji.

Ndani ya msitu huu kuna njia za miguu zinazounganisha kijiji cha Ikola na baadhi ya

vitongoji Kalumbi na vijiji jirani vya kafisha na Bujombe. Pia kuna njia nyingi zisizo

halali za miguu ambazo hutumiwa na wavamizi wa msitu kwa ajili ya kilimo, wapasua

mbao na wategaji wa wanyamapori.

MSITU WA HIFADHI WA KIJIJI CHA IKOLA;

Msitu huu umeenea kaskazini mwa Kijiji cha Ikola. Msitu huu una ukubwa wa hekta

5465 wenye bioanuai nyingi muhimu kwa kijiji na taifa kwa ujumla. Msitu huu

umeathiriwa na shughuli za kibinadamu kama vile uchungiaji wa mifugo, uchomaji

moto, uvunaji holela, Kilimo na makazi holela msituni.

Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na

uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje ya kijiji cha Ikola.

Page 7: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

3

Moto ni tishio la msitu wote wa hifadhi ya kijiji cha Ikola. Madhara ya moto ndani ya

msitu wa hifadhi ya kijiji cha Ikola ni kuwa umeathiri ustawi wa uoto wa msitu huu.

Vyanzo vya moto ndani msitu wa hifadhi ya kijiji cha Ikola ni wawindaji wa

wanyamapori, wakulima na warinaji wa asali kwa kutumia moto.

Msitu huu pia una vivutio vingine vya utalii kama vile safu za Milima na maeneo mengi

yanayopendelewa na Sokwe kwa ajili ya malazi na chakula hasa milima ya wansisi

inayotenganisha Kijiji cha Ikola na Kijiji cha Bujombe.

Mmiliki mkuu wa msitu huu ni Halmashauri ya Kijiji Cha Ikola, kutokana na muundo

wa serikali za mitaa, itaiteua kamati ya Maliasili ya Kijiji kusimamia msitu huu kwa

niaba ya wananchi wote wa kijiji cha Ikola kwa kuwa hii ndiyo kamati inayohusika na

usimamizi wa masuala ya mazingira ya kijiji kwa ujumla.

MATUMIZI YA MSITU WA HIFADHI YA KIJIJI CHA IKOLA

Kabla ya kuanza kwa utaratibu huu wa usimamizi shirikishi hapa kijijini, msitu huu

haukuwa na utaratibu wowote wa jinsi ya kutumia au kuvuna rasilimali zake, na kila

mtu aliingia kwa wakati wake na kuvuna chochote alichohitaji kwa manufaa yake na

kutoka bila ya kuhojiwa na mtu. Hali kadhalika, ndani ya msitu huu kuna wafugaji na

wakulima ambao huchangia miti midogo kupotea kabisa kama itakavyo onyeshwa

kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu.

Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji kulingana na uwezo wa msitu hupelekea

kutoweka kwa miti muhimmu kama Mninga, Mpilipili, Mkora na Msawala katika msitu

huu. Hali kadhalika uchomaji moto unaofanywa na wafugaji ili kupata nyasi mpya na

wawindaji ili kurahisisha kazi yao ya kuwinda. Vitendo hivi huua kabisa makuzi ya

machipukizi na hivyo msitu hubaki na kizazi cha miti mikubwa tu ambayo ndiyo ilikuwa

ikivunwa.

Kwa upande wa matumizi ya rasilimali za msitu huu zipo rasilimali zipatikanazo katika

msitu huu ambazo zina manufaa kwa uchumi wa kila mwananchi na kijiji kwa ujumla,

hizi ni pamoja na; -

▪ Msitu huu ni makazi ya wanyamapori ambao ni faida kwa kijiji na taifa kwa

ujumla.

Page 8: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

4

▪ Ipo miti yenye manufaa kiuchumi kwa wananchi mfano miti ya mbao kama

Milembela, Mitundu, Mininga, Mibanga, Mikurungu, Mpilipili, ambayo ina

umuhimu kiuchumi na kwamba itakinufaisha kijiji endapo utaratibu wa uvunaji

utasimamiwa ipasavyo na kwa uaminifu,

▪ Ndani ya msitu huu kuna makorongo ambayo ni mito ya misimu na mengine

hutiririsha maji mwaka mzima, hivyo kama yakitumiwa vizurini fursa ya utalii

asilia utakao ingizia kijiji kipato.

▪ Kuni ni moja wapo ya matumizi muhimu kiuchumi toka katika msitu huu.

▪ Aidha, watumiaji wakuu wa rasilimali za msitu huu wa kijiji cha Ikola, ni wanakijiji

wenyewe wa Ikola, pili ni wananchi toka vijiji jirani kama Kafisha. Watumiaji

wengine ni wale wakutoka nje ya kijiji na kata hii ya Ikola. Pamoja na taratibu

za kulipia zatakazowekwa lakini yapo mahitaji mengine ambayo wanakijiji wa

Ikola pekee wataruhusiwa kuingia na kuvuna bila malipo bali kwa utaratibu

maalum.

KIJIJI CHA IKOLA

Kijiji cha Ikola ni miongoni mwa vijiji hamsini na tano (55) vya wilaya ya Mpanda. Kipo

katika Kata ya Ikola, Tarafa ya Karema, Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi. Vijiji

vingine vilivyomo kwenye kata hii ni pamoja na Kafisha na mchangani. Kijiji hiki

kilianzishwa mwaka 1974 wakati wa operesheni vijiji, Jina la kijiji limetokana na neno

kukolola likiwa na maana kukata. Kwa hiyo jina la kijiji Ikola wametohoa kutoka kwenye

kitendo hicho cha kukolola baada ya machifu wawili kupigana na mmojawao kumkata

mwenzake sehemu za siri (Kumkolola).

Kijiji hiki kina vitongoji vinane (8) ambavyo ni Bujombe, Ikola Stoo, Isigo, Kalumbi,

Mpalamawe A, Mpalamawe B, Utinta A na Utinta B. Katika upande wa Kaskazini, kijiji

kinapakana na kijiji cha Bujombe, upande Kusini kinapakana na Ziwa Tanganyika

upande Mashariki kinapakana na kijiji cha Kafisha na Mchangani, Magharibi

kinapakana na kijiji cha Isengule. Kijiji kina ukubwa wa hekta 29,098.00. na Katika

upande wa Kaskazini, kijiji kinapakana na kijiji cha Bujombe. Kijiji hiki kina

mchanganyiko wa makabila kadhaa.

Page 9: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

5

Kijiji kina makabila ya aina mbalimbali kama Watongwe, Wafipa, Wasukuma, Waha,

Watabwa, Wabende, Wahutu, Wanyamwezi, Wapimbwe, Wanyakyusa n.k.

Shughuli za kiuchumi za wakazi wa kijiji cha Ikola zinategemea sana kilimo Mazao

yanayolimwa katika kijiji cha Ikola ni kwa ajili ya chakula na biashara. Mazao yote

yanayolimwa katika kijiji hiki ni kwa ajili ya chakula na biashara ambayo ni mahindi,

mbaazi, karanga, mihogo, viazi vitamu, maharage, kunde, mtama, ulezi, miwa,

vitunguu, choroko, mpunga, na mbogamboga za majani.

Aidha, shughuli ya ufugaji hufanywa na kabila la wasukuma, wanyamwezi na wafipa

kwa kiasi kikubwa pia mifugo midogo midogo kama mbuzi, kondoo bata na kuku.

SEHEMU YA PILI

MADHUMUNI YA MPANGO WA USIMAMIZI WA MSITU WA KIJIJI CHA IKOLA

Msitu wa hifadhi ya kijiji cha Ikola ni msitu wa kijiji unaohifadhiwa kwa lengo la

kuhifadhi na kutunza vyanzo vya maji pamoja na kuwezesha upatikanaji wa mazao na

huduma za msitu kwa njia endelevu. Kutokana na uharibifu wa msitu unaoendelea

kufanyika madhumuni hayo ya msingi yanaendelea kuathiriwa. Hivyo dhumuni kuu la

mpango huu ni kuimarisha ulinzi, uendelezaji na utumiaji wa eneo hilo la msitu kwa

kushirikisha wananchi ili kurejesha hali nzuri ya msitu iliyokuwepo. Hii itafanikiwa kwa

kufanya yafuatayo:

▪ Kuweka taratibu / kanuni za kutumia, kulinda, na kuendeleza msitu kwa njia

endelevu.

▪ Kuboresha ushiriki wa wadau wote katika usimamizi wa msitu.

▪ Kuongeza ushirikiano kati ya wananchi, Halmashauri ya Kijiji, Halmashauri ya

Wilaya na wakala wa huduma za misitu Tanzania.

▪ Kuwaelimisha wanakijiji wa Ikola juu ya umuhimu wa msitu kwao, Taifa na

Ulimwengu na jukumu lao la kufuata taratibu za utunzaji na matumizi

zilizowekwa na kukubalika.

▪ Kuuweka msitu wetu katika udhibiti madhubuti unaokubalika na wanakijiji wote

ili kwamba kusiwe na uvunaji holela, uvamizi wa mifugo, na ujenzi wa makazi

holela au kupanua mashamba kuingia katika msitu huu. Kwa kufanya hivi,

tutasaidia msitu huu kuwa chini ya umiliki wa kijiji chote kwa manufaa yetu na

Page 10: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

6

kwamba rasilimali zilizopo zitumike katika misingi endelevu kwa faida ya kizazi

hiki na kijacho.

Msitu huu umegawanyika katika maeneo makuu Matatu ya usimamizi (3) yaitwayo

“maeneo madogo ya usimamizi” (EDU) kama ifuatavyo; -

▪ ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MANDA

▪ ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA KASEMBE

▪ ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA KALOFWESI

ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MANDA. Eneo hili dogo la usimamizi (EDU) la Manda (milima ya Wansisi) ambalo linaanzia

kaskazini mwa msitu wa kijiji cha Ikola kwenye milima ya Wansisi, Kwa upande wa

kusini inapakana na EDU ya Kasembe. Eneo hili lina mapito, malisho na makaazi ya

Wanyamapori kama sokwe. Pia kuna maporomoko, mawe na makorongo marefu

ambayo hayafai kwa shughuli zozote za kibinadamu. Lengo kuu la EDU hii ni

“UHIFADHI”. Ndani ya msitu huu kuna milima na maporomoko marefu na vyanzo vya

maji. kutokana na hali ya eneo hili lilivyo, matumizi yatakayoruhusiwa katika EDU hii

ni pamoja na

▪ Ufugaji nyuki

▪ Uchimbaji wa dawa za asili (miti shamba)

▪ Matambiko

▪ Utalii asilia

▪ Utafiti

ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA KALOFWESI Linaanzia Kaskazini mwa eneo la malisho la kijiji cha Ikola, mlima Kamba na eneo la

matambiko la Lyamuzimu. Kwa upande wa kaskazini linapaka na EDU ya Kasembe.

Ndani ya eneo hili kuna mapito ya wanyamapori, vyanzo vya maji kama mto Msengusi,

Kalofwesi na mto kamba ambayo hutiririsha maji hadi ziwa Tanganyika. Vyanzo hivi

vya maji hutumika kulisha maji eneo la ufugaji ambalo linapakana naloHivyo basi kwa

kuwa na hali hii lengo la EDU hii litakua ni UHIFADHI wa wanyamapori wanaoishi

humo ndani ya msitu, na matumizi yasiyo haribifu ambayo yataruhusiwa katika eneo

hili ni kama yalivyo orodheshwa hapa chini;

▪ Ufugaji nyuki na Urinaji wa asali

Page 11: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

7

▪ Uchimbaji wa dawa za asili [miti shamba]

▪ Kusenya kuni zilizokauka.

▪ Ukataji wa nyasi za kuezekea nyumba

▪ Shughuli za Utalii.

▪ Matambiko

▪ Vyanzo vya maji

▪ Utafiti

ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA KASEMBE Eneo hili lipo katikati ya EDU za Kalofwesi na Manda, kuzunguka maeneo ya. Lengo

la kutenga eneo hili ni MATUMIZI” wa Shughuli zingine zitakazoruhusiwa katika EDU

hii ni pamoja na

▪ Ufugaji nyuki

▪ Utalii wa asilia

▪ Kuchuma uyoga, mboga pori na matunda

SEHEMU YA TATU MPANGO WA UTEKELEZAJI

meneja mteule Katika mpango huu wa usimamizi wa msitu wa hifadhi wa Kijiji cha Ikola, meneja

atakuwa ni Halmashauri ya kijiji cha Ikola. Halmashauri ya kijiji cha Ikola itaiteua

kamati ya maliasili ya kijiji ili kusimamia msitu huu kwa niaba yake na wanakijiji wote

kwa ujumla. Kamati hii ni ile inayoelekezwa katika muundo wa uongozi wa vijiji.

Kamati hii itakuwa na wajumbe 14 kwa mchanganuo ufuatao;

▪ Wawakilisha toka kila kitongoji cha kijiji.

▪ Skauti wa kijiji wasiopungua wawili kama hawapo basi hata askari mgambo

wanaweza kutumika badala ya Skauti wa kijiji.

▪ Mtu / watu maarufu katika kijiji wanaoweza kuchangia katika suala zima la

uhifadhi. mfano wazee maarufu na wakongwe wa kijiji n.k.

Page 12: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

8

▪ Wanawake (Theluthi moja au 30% ya wajumbe wote) maalumu kwa nafasi ya

upendeleo kwa wanawake

KAMATI HII ITAPATIKANA KWA KUFUATA UTARATIBU UFUATAO; -

▪ Wajumbe hawa watapendekezwa na halmashauri ya kijiji

▪ Baada ya majina hayo kupatikana mkutano mkuu wa Kijiji huketi na

kuyathibitisha majina ya wajumbe wa kamati hii.

▪ Kamati hii itakuwa madarakani kwa muda wa miaka mitatu (3) baada ya hapo

uchaguzi unafanyika tena. mjumbe anaweza kuchaguliwa tena kulingana na

imani ya wananchi kwake.

▪ Mwenyekiti, katibu na mweka hazina watachaguliwa miongoni mwa wajumbe

waliochaguliwa na mkutano mkuu na kuthibitishwa na Halmashauri ya kijiji.

▪ Kamati hii itapewa nguvu ya kisheria ya kusimamia sheria ya kijiji na

itawajibika kwa Halmashauri kuu ya Kijiji.

▪ Itaandika taarifa ya utekelezaji kwa Halmashauri ya kijiji mara moja kila mwezi,

yenye nakala kwa Afisa Misitu (W).

▪ Itafanya vikao vyake mara moja kila mwezi na vya dharura pale inapobidi.

▪ Itapokea, kujadili na kufuatilia taarifa za walinzi wa msitu (Kamati ya doria) na

vikundi vingine vitakavyo undwa kuisaidia Kamati ya Mazingira katika

kutekeleza majukumu yake.

UWEZO NA MAJUKUMU YA KAMATI YA MAZINGIRA ▪ Kuhakikisha kuwa mipaka yote ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Ikola inaeleweka

waziwazi kwa wanakijiji wote wa Ikola.

▪ Kusimamia utekelezaji wa mipango yote inayohusu utumiaji, ulinzi na uendelezaji

wa msitu wa hifadhi ya kijiji cha Ikola.

▪ Kutunza kumbukumbu zote zinazohusu shughuli za utumiaji, ulinzi, na uendelezaji

wa msitu wa hifadhi ya kijiji. Kumbukumbu hizo ni: -

• Mihtasari ya mikutano

• Doria

• Uhalifu na faini

Page 13: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

9

• Vibali vilivyotolewa

• Mapato na matumizi ya fedha za msitu

▪ Uoteshaji na upandaji miti, pia shughuli zote za uhifadhi mazingira ndani ya

maeneo ya kijiji

▪ Kuhakikisha kuwa walinzi wa msitu (timu ya doria) wanatekeleza kazi yao

kikamilifu na kuchukua hatua zinazopasa kuondoa dosari zinazojitokeza katika

kazi ya ulinzi.

▪ Kufanya ukaguzi wa msitu wa hifadhi ya kijiji angalau mara mbili kwa mwezi.

▪ Kuhakikisha matumizi endelevu ya msitu yanazingatiwa kulingana na kanuni za

matumizi zilizowekwa na kukubaliwa.

▪ Kuwashughulikia wahalifu wa msitu kwa mujibu wa kanuni za adhabu

zilizowekwa na kukubalika kwa ushirikiano na Halmasahauri ya kijiji.

▪ Kwa ushirikiano na Halmashauri ya kijiji, kuwahamasisha wanakiiji kushiriki

katika suala zima la uhifadhi wa msitu na mazingira ya kijiji kwa ujumla.

▪ Kutumia na kutunza vitabu vya stakabadhi vilivyoidhinishwa na Halmashauri ya

Wilaya ya Mpanda.

▪ Kufungua Akaunti Benki ya Kamati ya Mazingira ya kijiji kwa ajili ya kuweka fedha

za mapato ya msitu (ushuru na faini).

▪ Kuhakikisha kuwa fedha za Akaunti ya Kamati ya Mazingira zinatumika kama

zilivyokusudiwa na kuidhinishwa na Halmashauri ya kijiji cha Ikola.

▪ Kuweka utaratibu wa utoaji wa vibali ili kuhakikisha kuwa vibali vinavyotolewa ni

vile vilivyoko katika mamlaka ya Kamati ya Mazingira na kwamba utoaji wa vibali

unakwenda sambamba na mahitaji yaliyopo na sio vinginevyo.

Majukumu ya Mwenyekiti wa kamati ya Maliasili ya Kijiji ▪ Kuhakikisha kuwa mikutano ya Kamati ya Mazingira inafanyika ipasavyo kwa

kufuata ratiba iliyopangwa. (angalau mara moja kila mwezi)

▪ Kuhakikisha kuwa Mhasibu na Katibu wa Kamati ya Mazingira wanafanya kazi

zao ipasavyo kwa kuweka kumbukumbu zote za vibali, doria, faini, idadi ya

wahalifu, fedha zilizopo, matumizi n.k.

▪ Kuhakikisha kuwa Kamati ya doria ya msitu wa hifadhi ya kijiji wanafanya kazi

yao ipasavyo na wanapewa haki zao kama zilizoainishwa kwenye Mpango huu.

Page 14: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

10

▪ Atakuwa mmoja wa watia sahihi wa Akaunti ya Kamati ya Mazingira wakati wa

kutoa fedha Benki kwa matumizi yaliyoidhinishwa na Halmashauri ya kijiji kwa

ajili ya uendelezaji wa msitu na shughuli zingine za maendeleo kijijini.

▪ Atawajibika kuhudhuria vikao vyote vya Halmashauri kuu ya kijiji na kutoa taarifa

ya utendaji kazi wa kamati.

Majukumu ya Katibu wa kamati ya mazingira: Atawajibika Kuweka na kutunza kumbukumbu zifuatazo: -

▪ Kumbukumbu za mikutano yote (Kitabu cha kumbukumbu za mikutano)

▪ Doria zilizofanyika, uhalifu/uharibifu ulioonekana kwenye kitabu cha

Doria.

▪ Uhalifu ulioonekana, wahalifu waliohusika, faini zilizotozwa, tarehe ya

uhalifu na faini zilizolipwa kwenye kitabu cha “Uhalifu na faini”

▪ Vibali ilivyotolewa, kwa nani, kwa ajili gani, fedha zilizolipwa, tarehe,

namba ya risiti, n.k kwenye kitabu cha Vibali

▪ Fedha zilizotolewa, tarehe, kwa ajili gani, namba ya risiti kwenye kitabu

cha Risiti na fedha.

▪ Atahakikisha kuwa Akaunti ya Mazingira inafunguliwa na mara kwa mara baada

ya kupokea fedha na kuziingiza kwenye vitabu vinavyohusika zinapelekwa

Benki na Mweka Hazina.

▪ Atakuwa mmoja wa watia sahihi wa Akaunti ya Kamati ya Mazingira wakati wa

kutoa fedha Benki kwa matumizi yaliyoidhinishwa na Halmashauri ya kijiji kwa

ajili ya uendelezaji wa msitu na shughuli zingine za maendeleo kijijini.

▪ Atawajibika kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Serikali ya Kijiji na

Halmashauri kuu ya kijiji

▪ Atawajibika kuandaa taarifa ya utendaji kazi wa kamati na maendeleo ya msitu

kila mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka na kuwasilisha katika

mkutano mkuu wa kijiji wa robo mwaka baada ya kupitiwa na Halmashauri kuu

ya kijiji.

▪ Ataidhinisha doria kufanyika kwa maandishi maalumu ambayo mwenyekiti wa

kijiji pia atapaswa kujulishwa kwa wakati utakaoonekana unafaa kulingana na

mazingira.

▪ Atapokea taarifa ya doria mara baada ya kumalizika na kukagua daftari la doria.

Page 15: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

11

▪ Atatunza kumbukumbu za kesi zote za wavunaji haramu wa mazao ya msitu

wa hifadhi ya kijiji cha Ikola.

▪ Atawajibika kutunza orodha ya wavunaji wote wa rasilimali za msitu wa hifadhi

ya kijiji cha Ikola pamoja na kiasi walichovuna na kuwasilisha kwa DFO/DED

kila mwezi.

▪ Atawajibika kusimamia mapato na matumizi kwa umakini na kutoa taarifa kwa

Halmashauri ya kijiji kila inapoonekana inafaa.

Majukumu ya Mtunza hazina: ▪ Atawajibika kutunza kumbukumbu zote za mapato yatokanayo na leseni za

uvunaji wa mazao ya misitu na vibali mbalimbali.

▪ Atawajibika kutunza kumbukumbu za matumizi yote ya fedha zitokanazo na

maduhuli ya mazao ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Ikola kama ilivyoidhinishwa

na vikao husika vya kijiji cha Ikola na siyo vinginevyo.

▪ Ataandaa taarifa ya Mapato na Matumizi ya fedha ya Kamati ya Mazingira na

kuiwasilisha kwenye vikao vya Kamati ya Mazingira.

▪ Atakuwa mmoja wa watia sahihi wa Akaunti ya Kamati ya Mazingira wakati wa

kutoa fedha Benki kwa matumizi yaliyoidhinishwa na Halmashauri ya kijiji kwa

ajili ya uendelezaji wa msitu na shughuli zingine za maendeleo kijijini.

Msimamizi wa Doria: ▪ Atatakiwa kusimamia doria zote na kuziongoza

▪ Atatunza daftari la kila mtu atakayekamatwa katika msitu wa kijiji akivuna

mazao ya misitu bila idhini (kibali) cha kijiji.

▪ Atawajibika kumuweka chini ya ulinzi mtu yeyote pamoja na maliasili

aliyokamatwa nayo (kama ipo) na kumkabidhisha kwa mtendaji wa Kijiji kwa

hatua zaidi za kisheria.

▪ Atawajibika kuhakikisha ulinzi wa mipaka ya msitu unadumu na kuwa imara ili

msitu usivamiwe kwa kilimo, makazi au kuchungia.

MAJUKUMU YA WAHUSIKA WENGINE Halmashauri ya Kijiji: Itakuwa mhusika mkuu katika utekelezaji wa mpango huu kwa upande wa kijiji na

itakuwa na wajibu na majukumu yafuatayo: -

▪ Kusimamia utekelezaji wa mpango

▪ Kutunga na kusimamia Sheria ndogo

Page 16: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

12

▪ Kuhakikisha kuwa Kamati ya Mazingira inafanya kazi yake ipasavyo.

▪ Kushirikiana na wataalamu wa Misitu wa ngazi zote katika kuandaa mikakati

mipya ya uhifadhi misitu na mazingira kwa jumla.

▪ Kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa mpango huu, kwa kuwa na

agenda ya kudumu katika vikao vyake vya kila mwezi pia kutembelea msitu wa

hifadhi angalau mara moja kila mwezi.

Wanakijiji Watashiriki katika shughuli za utumiaji, ulinzi na uendelezaji wa msitu wa hifadhi

kama ifuatavyo: -

▪ Kuzuia na kuzima moto katika maeneo yao ya makazi, mashamba na misitu

inayowazunguka.

▪ Kusafisha mipaka ya nje ya msitu wa hifadhi ya kijiji na kuhakikisha kuwa iko

wazi wakati wote wa mwaka.

▪ Kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

▪ Kuotesha na kupanda miti kwa lengo la kupunguza utegemezi wa misitu ya asili

kwa kila zao au huduma ya msitu.

▪ Kushiriki katika mikutano na kuchangia katika kuandaa mikakati mipya ya

kutumia, kulinda na kuendeleza msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga.

▪ Kubuni na kutekeleza shughuli mbadala za kuongeza kipato ili kupunguza

umaskini kwa kutumia rasilimali zilizo ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji, zilizo

katika maeneo ya makazi. Baadhi ya mbinu hizo ni ufugaji wa nyuki kwa njia

za kisasa, usukaji wa mikeka kwa kutumia ukindu kwa ajili ya soko, Kuzingatia

matumizi ya majiko banifu, nishati mbadala na matumizi sahihi ya mazao ya

misitu.

Wataalamu wa Misitu katika ngazi mbalimbali ▪ Kutoa msaada wa kitaalam katika kubuni mikakati mipya ya kuhifadhi msitu wa

hifadhi ya kijiji cha Ikola

▪ Kusaidia shughuli za uoteshaji na upandaji miti.

▪ Kusimamia Sera ya Misitu na Sheria ya Misitu 14, 2002.

▪ Kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa mpango huu wa usimamizi.

▪ Kusaidia utekelezaji wa mpango.

Page 17: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

13

Viongozi wa Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa, na Taifa (Mtendaji kata, Diwani, Katibu Tarafa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji (W), Mbunge, Mkuu wa Mkoa na Waziri).

▪ Kutoa msukumo katika utekelezaji wa mpango

▪ Kuhakikisha kuwa Polisi na Mahakama zinatekeleza wajibu wao ipasavyo

katika utekelezaji wa Sheria ya Misitu No. 14, 2002 na Sheria zinazosimamia

rasilimali za misitu.

▪ Kushirikiana na Idara ya Misitu na Nyuki.

▪ Kutoa msukumo katika utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za kutunza na

kulinda misitu.

▪ Kusaidia utatuzi wa migogoro inapotokea.

UTENDAJI KAZI WA KAMATI YA MALIASILI YA KIJIJI. ▪ Itafanya kazi zile zile zilizoainishwa katika majukumu ya kamati ya kudumu ya

maliasili ya kijiji

▪ Itakutana mara moja kila mwezi

▪ Itatunza mihutasari ya mikutano yake

▪ Mkutano utafanyika iwapo tu idadi ya wajumbe imefika nusu.

▪ Katika kila mkutano watapaswa kupokea taarifa ya doria na mwenendo wa

uvunaji wa mazao ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Ikola kutoka kwa kiongozi wa

doria.

▪ Watatakiwa kujua idadi ya leseni zilizotolewa katika mwezi husika, kiasi cha

maliasili kilichovunwa na mapato yaliyopatikana.

▪ Watapokea na kujadili maombi ya leseni za kuvuna mbao na kuwasilisha kwa

Serikali ya Kijiji.

MAELEZO MENGINEYO utoaji taarifa

▪ Kamati ya Maliasili ya kijiji itatoa taarifa ya utekelezaji kwa Halmashauri ya kijiji

mara moja kwa mwezi yenye nakala kwa Afisa Misitu wa Wilaya Mpanda.

▪ Afisa Mtendaji wa Kijiji (VEO) atatoa taarifa ya maendeleo ya shughuli za msitu

wa hifadhi ya kijiji na kwa Mkutano Mkuu mara nne (4) kwa mwaka yenye

nakala kwa Afisa Mtendaji Kata (WEO) na Afisa Misitu (W).

Page 18: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

14

uwekaji wa kumbukumbu Kumbukumbu zifuatazo zitawekwa na kuhifadhiwa na Kamati ya Mazingira ya Kijiji:

▪ Mihutasari ya vikao vya kamati

▪ Uhalifu na faini zilizotozwa

▪ Doria zilizofanyika

▪ Stakabadhi ya fedha na Hati ya malipo.

▪ Vibali vilivyotolewa

▪ Akaunti ya Kamati ya Mazingira

▪ Mapato na matumizi ya fedha za msitu.

MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA KAMATI YA MALIASILI Mapato ya Kamati ya Mazingira yatatokana na:

▪ Faini zitakazotozwa wahalifu wa msitu wa hifadhi ya kijiji.

▪ Malipo ya mazao na huduma ya msitu yaliyoruhusiwa kwa kulipia katika

Mpango huu.

▪ Mauzo ya mazao ya msitu yaliyokamatwa na zana zilizokamatwa katika ulinzi.

▪ Wafadhili na wasamaria wema watakaotoa fedha/ msaada kwa ajili ya

Usimamizi wa msitu wa hifadhi ya kijiji.

Mapato yatokanayo na mazao na huduma za msitu wa kijiji cha Ikola yatakua ni mali

ya kijiji cha Ikola kwa asilimia 100% na hayatagawanywa kati yake na Halmashauri

ya Wilaya ya Mpanda.

MATARAJIO YA UFANISI WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA USIMAMIZI WA MSITU

Katika matembezi ya kukatiza msitu vikwazo Matatizo yafuatavyo vilibainika msituni;

▪ Moto kichaa

▪ Uvunaji haramu wa mbao

▪ Uchungiaji wa mifugo

▪ Kilimo msituni

▪ Ukataji wa miti

Mpango wa usimamizi ukitekelezwa vilivyo kwa msitu huu hifadhi wa kijiji cha Ikola

kwa kuzingatia vikwazo vilivyobainika katika matembezi ya kukatiza msitu kama

yalivyofupishwa hapo juu yafuatayo yanatarajiwa kuonekana;

Page 19: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

15

▪ Kupungua au kutoweka kabisa kwa matukio ya moto

▪ Kushughulikiwa kwa watuhumiwa wa kesi za uchomaji moto hovyo msituni kwa

utaratibu wa kukubalika/kwa kufuata taratibu za nchi.

UTUNZAJI KUMBUKUMBU Mpango huu wa usimamizi unaainisha bayana ni kumbukumbu zipi zitatunzwa,

zitatunzwa katika vitabu gani na vitabu hivyo vitatunzwa na nani kwa utaratibu gani.

Ufuatao ni ufafanuzi; -

VITABU VYA KUMBUKUMBU Hiki ni kitabu kitakachohusika na kutunza kumbukumbu zifuatazo,

▪ Kumbukumbu za mihutasari ya vikao vya kamati

▪ Kumbukumbu za maamuzi mbalimbali ya kamati

▪ Tukio lolote linalofanywa na kamati au watu wachache waliotumwa na kamati.

▪ Matokeo ya shughuli yoyote iliyofanywa na kamati au watu wachache

walioteuliwa na kamati

▪ Kumbukumbu za ukaguzi wowote uliofanywa na kamati au baadhi ya

wanakamati waliotumwa na kamati

KITABU CHA MAKOSA NA FAINI Kumbukumbu za makosa yoyote yaliyofanywa na mhalifu dhidi ya sheria ndogo za

Kijiji cha Ikola ya Kuhifadhi Msitu wa Kijiji.

▪ Jina la mkosaji na kosa alilokosa, Kiasi alichotozwa, tarehe aliyotozwa na

namba ya stakabadhi aliyopewa kwa faini aliyotozwa.

▪ Ionyeshwe ni katika akaunti gani pesa hiyo imeingizwa.

▪ kama idhini ya kutumika nimetolewa na mamlaka husika, onyesha hapa

imetumika kufanyia nini?

KITABU CHA STAKABADHI Hivi ni vitabu ambavyo Mtunza hazina wa Halmashauri ya Wilaya atatoa kwa kijiji,

lakini ionyeshwe nani kapewa vitabu vingapi kuvitumia ndani ya kamati.

Page 20: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

16

VITABU VYA VIBALI Kazi ya kitabu hiki ni kutunza kumbukumbu za vibali vyote vilivyoidhinishwa na kamati

ya Maliasili ya Kijiji, Kitabu hiki kionyeshe mambo yafuatayo; -

▪ Kuainisha lengo la kibali, jina la aliyepewa kibali hicho,

▪ kiasi cha malipo aliyolipa,

▪ Namba ya stakabadhi iliyotolewa kwa mteja

▪ tarehe ya kutolewa kibali na ya kuisha kutumika kibali hicho.

▪ Pia kitabu kionyeshe jina la mjumbe atakayekagua kibali hicho na la mjumbe

atakayesimamia matumizi ya kibali hicho.

Kimsingi, leseni na vibali vitasainiwa na katibu/ Mhasibu wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji

kugongwa muhuri wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji.

KITABU CHA DORIA Hiki ni kitabu kitakachokuwa kinatunzwa na msimamizi wa doria. kinapaswa

kuandikwa mambo yafuatayo;

▪ Tarehe ya doria,

▪ Majiina ya wanaofanya doria siku hiyo,

▪ eneo ambalo watu hao watafanya doria,

▪ ni uharibifu gani umefanyika katika eneo hilo la msitu ambalo watu hao

wamepangiwa kufanya doria.

▪ Pia katika taarifa ya hao waliopangiwa kufanya doria katika eneo husika

wakiona kitu mfano, wanyamapori. wanapaswa kutoa taarifa kwa kamati ya

maliasili ya Kijiji.

KITABU CHA AKAUNTI Baada ya muda kijiji kitakuwa na fedha nyingi kutokana na mapato ya msitu, hivyo

kutakuwa na kitabu cha benki kwa ajili ya kumbukumbu za kibenki. Katika kitabu hiki

kutakuwa na majina ya watia saini. watia saini watakuwa kama ifuatavyo;

▪ mtia saini kundi ‘A’ – toka Serikali ya Kijiji,

Page 21: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

17

▪ Mtia saini kundi ‘A’ – toka Kamati ya Maliasili ya Kijiji,

▪ Mtia saini kundi ‘B’ – toka Serikali ya Kijiji

▪ Mtia saini kundi ‘B’ – toka Kamati ya Maliasili ya Kijiji.

Izingatiwe kuwa hakuna fedha itakayo chukuliwa benki bila ya kuwa na saini za watia

saini wawili toka makundi mawili tofauti pamoja na muhtasari wa kikao cha mkutano

mkuu wa kijiji ulioidhinisha matumizi ya fedha hizo.

KITABU CHA MAPATO NA MATUMIZI Hiki ni kitabu kitakachukuwa kinatunza kumbukumbu za fedha zote zinazoingia kutoka

katika faini na ada za vibali au leseni mbalimbali. Pia kitakuwa na kumbukumbu za

matumizi yote ya fedha zinazotumika ikionyesha saini ya aliyechukuwa na

viambatanisho vya uthibitisho kuwa malipo hayo yameidhinishwa na mamlaka husika.

Mfano wa malipo ni pamoja na zawadi ya pongezi kwa wafanya doria kwa kazi nzuri

itakayokuwa imethibitishwa na kuidhinishwa kuwa wapewe kiasi kadhaa kwa

maandishi. Hapa ni lazima mpokeaji athibitishe kuwa amepokea pesa hiyo.

USIMAMIZI WA FEDHA Katika kifungu hiki sisi wanakijiji cha Ikola tunaainisha mfumo utakaotumika

kusimamia fedha hususani katika matumizi yake.

WAHUSIKA WAKUU; Mtu atakaye husika kushika vitabu vya risiti na kupokea fedha toka kwa mlipaji

atakuwa ni mtunza fedha. Fedha hizo zitahifadhiwa kwa muda na kisha kupelekwa

benki kwenye akaunti ambayo imefunguliwa kwaajili ya fedha zitokanazo na msitu wa

hifadhi ya kijiji cha Kagunga.

AFISA MUWAJIBIKAJI WA MASUALA YA FEDHA Afisa muwajibikaji wa fedha za Msitu wa Kijiji atakuwa AFISA MTENDAJI WA KIJIJI

kwakuwa huyu ndiye anayewajibika kwa masuala yote yahusuyo fedha hapa kijijini.

Anaweza kumhoji mtunza fedha na kukagua vitabu vya fedha wakati wowote

atakapoona inafaa. Hata hivyo mtunza hazina anapaswa kutoa taarifa ya mwenendo

wa makusanyo ya fedha kila wiki.

Hata hivyo, kwa kuzingatia misingi ya uhuru wa habari na taratibu za utawala bora

mwananchi yeyote anaweza kuomba kukagua kitabu cha makusanyo. pamoja na

taratibu hizi za pekee, Mamlaka inayowajibika ya juu kabisa katika kijiji ni Mkutano

Page 22: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

18

mkuu, hivyo, taarifa ya mapato na matumizi yatasomwa kila baada ya miezi mitatu

katika mikutano mkuu wa kijiji kama ilivyo desturi ya mikutano hiyo hapa kijijini.

Kwa upande wa ukiukwaji wa taratibu au tuhuma dhidi ya mtunza hazina taratibu

zifuatazo zitatumika;

Endapo mtunza hazina /fedha atahisiwa kuwa katumia fedha tofauti na utaratibu au

ridhaa ya wananchi hatua zifuatazo zitumike; -

▪ Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji ataitisha kikao cha kamati yake

na kumhoji juu ya tuhuma husika

▪ Ikiwa ameshindwa kutoa maelezo ya kujitosheleza na kushindwa kuondoa

mashaka hayo, Taarifa hiyo itapelekwa kwa mwenyekiti wa kijiji ambaye

anapaswa kuitisha kikao cha Serikali ya Kijiji kumhoji juu ya tuhuma husika,

kama maelezo yake hayajajitosheleza kiasi cha kuuongezea uongozi wa

kijiji mashaka, Atapewa barua ya kujieleza ikiwa ni nafasi ya kujieleza

kufuatia tuhuma au mashaka dhidi ya matumizi mbaya ya fedha ya kijiji.

▪ Endapo maelezo yake katika barua hayataondoa utata, mwenyekiti

ataitisha Halmashauri ya kijiji iliyomchagua na kuwasilisha hoja ya

kumsimamisha kazi ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake. Hoja

ikipitishwa VEO ataandika barua ya kumsimamisha kazi hadi hapo

mahakama/baraza la kata itakapo amua kuwa ana hatia ama la,

▪ Baada ya kusimamishwa kazi VEO atamfikisha mtuhumiwa

polisi/mahakamani/baraza la kata. moja ya vyombo hivyo ndicho

kitakachotoa tamko la mwisho.

▪ Akipatikana na hatia atafukuzwa kazi hiyo na kutekeleza adhabu

zilizoamriwa, na mara moja Mwenyekiti wa kijiji kufanya taratibu za kuziba

pengo la mtunza hazina aliyepita.

MATUMIZI YANAYOIDHINISHWA;

Kwanza ifahamike kuwa matumizi makuu ya fedha itokanayo na uhifadhi wa msitu

wetu yatagawanyika katika makundi makuu matatu kama ifuatavyo; -

▪ 50% itatumika katika shughuli za maendeleo ya kijiji kwaajili ya wananchi wote

▪ 25% pesa hii itatumika kwaajili ya kuboresha kamati ya maliasili ya Kijiji.

Page 23: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

19

▪ 25% itatumika kwaajili ya kufanya shughuli za uhifadhi wa msitu wa kijiji cha

Ikola kuwa endelevu kama vile:

• Ununuzi wa vitabu vya kumbukumbu kama vilivyoainishwa katika

“Kugharamia marekebisho ya mipaka".

• Kugharamia tathimini ya Rasilimali na kuboresha Mpango huu wa

Usimamizi

• Kugharamia uendeshaji wa kesi.

• Kutoa motisha kwa kikosi cha doria na Kamati ya Maliasili ya Kijiji katika

kutekeleza majukumu yao.

• Kununua zana za doria mfano sare, mahema, tochi, makoti ya mvua n.k.

• Kugharamia mahitaji wakati wa doria kama chakula n.k.

MIPAKA YA MSITU WA HIFADHI WA KIJIJI CHA IKOLA Msitu huu wa hifadhi ya kijiji cha Ikola haujawekewa bikoni zinazozunguka mipaka ya

nje ya msitu huu Zaidi ya zile zinazotenganisha Kijiji cha Ikola na vijiji jirani vya Kafisha,

Bujombena Isengule.

MAELEKEZO MAALUM Katika maelekezo haya inasisitizwa kwamba maamuzi yote kuhusu usimamizi wa

msitu wetu turejee vipengele vilivyoelekezwa na kukubaliwa na sisi wenyewe katika

mpango huu. Hatutegemei tena wataalamu toka wilayani kuja kufanya maamuzi kwa

ajili yetu bali kuwaomba ushauri katika kupambanua mkwamo fulani ili baadaye sisi

tufanye maamuzi.

ULINZI NA UKAGUZI WA ENEO LA MSITU WA KIJIJI CHA IKOLA Kila mwanakijiji wa Ikola ana jukumu la kulinda na kutunza hifadhi ya msitu wa kijiji.

Hili jukumu litafanyika kwa kutekeleza yafuatayo:

▪ Kutoa taarifa za uhalifu

▪ Kutambua na kutoa taarifa za wahalifu wa msitu wa hifadhi ya kijiji na zana za

uvunaji haramu ndani na hifadhi ya msitu wa kijiji.

▪ Kuzuia moto usitokee na kuzima unapotokea.

Page 24: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

20

▪ Kushiriki katika shughuli za uoteshaji miche ya miti na upandaji wa miti katika

maeneo ya makazi na mashambani.

▪ Ni wajibu wa wakazi wote wa kijiji cha Ikola kushirikiana katika ulinzi wa msitu

wa hifadhi ya kijiji.

▪ Doria za ukaguzi katika msitu wa hifadhi ya kijiji zitafanywa na kamati ya doria

angalau mara mbili kwa mwezi.

▪ Walinzi wa msitu na hifadhi watachaguliwa na Halmashauri ya kijiji na

kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa kijiji kutoka katika vitongoji vyote vya kijiji

kwa uwakilishi wa Vitongoji.

SIFA ZA WALINZI WA MSITU. Zifuatazo ni miongni mwa sifa ambazo inabidi mlinzi wa msitu sharti awe nazo:

▪ Awe na tabia na mwenendo mzuri.

▪ Wenye kujituma na mwaminifu.

▪ Mkakamavu na mwenye afya nzuri.

▪ Asiwe mlevi

▪ Awe mkazi wa kijiji cha Ikola na raia wa Tanzania.

▪ Awe na umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.

▪ Ajue kusoma na kuandika.

WAJIBU, MAJUKUMU NA MAFAO YA WALINZI WA MSITU WA HIFADHI YA KIJIJI

▪ Walinzi watachagua kiongizi wao (Kamanda) kutoka miongoni mwao ambaye

atawajibika kupanga utaratibu kwa kushirikiana na walinzi wenzake wa doria

na utoaji taarifa kwa Kamati ya Mazingira.

▪ Walinzi wa msitu hawatalipwa mishahara lakini watapata motisha kama

itakavyoamuliwa na Serikali ya kijiji. Aidha walinzi husika wanaweza kupewa

25% ya faini anayotozwa mhalifu.

▪ Walinzi wa msitu wanaweza kusamehewa kazi nyingine za maendeleo kijijini.

▪ Walinzi watakaokwenda kinyume na maadili yao ya kazi wataadhibiwa kwa

kuonywa, kutozwa faini na kufukuzwa au kushitakiwa Mahakamani kutokana

na ukubwa wa kosa lililotendeka.

▪ Walinzi watatoa taarifa yao ya doria kila wanapofanya doria kwa Kamanda wao

ambaye atapaswa kutoa taarifa kwa Kamati ya Mazingira haraka iwezekanavyo

(isizidi siku moja).

Page 25: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

21

▪ Walinzi waliofanya kazi nzuri watazawadiwa kila mwisho wa mwaka na

Halmashaurii ya Kijiji. Walinzi hao watapendekezwa na Kamati ya Mazingira na

kuthibitishwa na Halmashauri ya kijiji. Zawadi/ motisha kwa walinzi waliofanya

vizuri itakuwa kama ilivyopendekezwa hapo juu.

OPERESHENI Yapo mazingira ya pekee ambapo kikosi pekee hakitoweza kukabiliana na uhalifu

fulani wa mpito, hivyo operesheni maalumu itaandaliwa kwa idhini ya mwenyekiti wa

kijiji kupitia kamati yake ya serikali ya kijiji kwa ushauri wa kamati kuu mbili; -

▪ Kamati ya Ulinzi ya Kijiji na

▪ Kamati ya Maliasili ya Kijiji.

N.B: Maandalizi haya lazima yawe ya siri sana.

ZAWADI YA PONGEZI KWA MWANA DORIA Kutakuwa na utaratibu wa kutoa zawadi ya pongezi au motisha kwa mwana kikosi cha

doria ambaye atafanya kazi kwa ujasiri, ushujaa na uadilifu mkubwa utakao thibitishwa

na wajumbe wa mkutano wa Halmashauri kuu ya Kijiji na Kuungwa mkono na Mkutano

Mkuu wa Kijiji. Kiasi cha pongezi au motisha kitapangwa na Halmashauri kuu ya kijiji.

zawadi hii itatolewa hadharani na kuwekwa katika kumbukumbu za vitabu husika.

Kifungu Cha Kumi Taratibu

KANUNI ZA KUTUMIA MSITU WA HIFADHI YA KIJIJI ▪ Mkazi yeyote wa kijiji cha Ikola, Afisa Misitu au mtu yeyote aliyeruhusiwa

wanaweza kuingia ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji kwa idhini ya Kamati ya

Mazingira.

▪ Afisa Misitu yeyote wa Idara ya Misitu na Nyuki wakati wowote anaweza kuingia

ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji aidha akiwa peke yake au kwa kushirikiana

na Kamati ya Mazingira ya kijiji kwa lengo la kufanya ukaguzi na kutoa ushauri

kwa Kamati ya Mazingira ambao unapaswa kupokelewa na kufanyiwa kazi kwa

lengo la kuboresha uendelezaji wa eneo hilo la msitu.

▪ Sio ruksa kwa mtu yeyote kuingia msitu wa hifadhi ya kijiji bila kibali kutoka kwa

Kamati ya Mazingira isipokuwa Walinzi wa msitu, Halmashauri ya kijiji, Kamati

ya Mazingira na Afisa Misitu wanaweza kufanya hivyo bila kibali.

Page 26: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

22

▪ Wageni wote wenye vibali toka Wizarani, Wilayani au wafadhili ni sharti wapite

kijijini na kuonyesha vibali vyao kwa Kamati ya Mazingira ya kijiji kabla ya

kuanza kufanya kazi yoyote ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji.

KANUNI ZA MATUMIZI YA MSITU Mahitaji yaliyoruhusiwa yatapaswa kupatikana kutoka maeneo ya matumizi ndani ya

msitu wa hifadhi ya kijiji cha Ikola. Maeneo yaliyohifadhiwa hayataruhusiwa kupata

mahitaji ya mbao, miti ya nguzo/miamba ya nyumba na mengineyo yasiyoruhusiwa.

MATUMIZI YA MSITU YANAYOHUSU UKATAJI WA MITI Mahitaji yote yanayohusu ukataji miti aina fulani kwa ajili ya mbao, nguzo na miamba

ya nyumba ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Ikola yanaruhusiwa katika EDU ya

Kasembe kwa kibali kitakachotolewa na Kamati ya Maliasili na kuwekwa alama kwa

kutumia nyundo maalum ya Idara ya Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda. Miti

husika itavunwa kwa kiwango ambacho hakitaathiri lengo la msingi la kuhifadhi msitu

ambalo ni kuhifadhi vyanzo vya maji na upatikanaji endelevu wa rasilimali na huduma

ya msitu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

TARATIBU NA SHERIA NYINGINEZO Adhabu Uwezo wa Kamati ya Mazingira ya kijiji cha Ikola kutoza faini umetolewa kwake na

Halmashauri ya kijiji cha Ikola kulingana na Sheria za Serikali za Mitaa (Serikali za

Vijiji) 1982 No. 7 zilizoundwa chini ya kifungu cha 120 (i) na 167.

Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya matumizi ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Ikola

yaliyowekwa na kukubaliwa atatozwa faini kwa mujibu wa Sheria Ndogo ya kijiji cha

Ikola ya kulinda na kutunza msitu wa hifadhi ya kijiji.

Kifungu Cha Kumi na Moja Adhabu

MCHAKATO WA KUMSHUGHULIKIA MKOSAJI NA KOSA ▪ Hairuhusiwi kwa mwanakijiji, mwanakamati, mlinzi au kiongozi yeyote kumtoza

faini mhalifu akiwa peke yake.

▪ Mazao ya misitu yaliyovunwa kinyume cha utaratibu pamoja na zana

zilizotumika katika uhalifu huo yakikamatwa ni lazima yafikishwe kwenye ofisi

ya kijiji ambapo hatua zaidi itachuliwa na Kamati ya Mazingira ya kijiji.

▪ Iwapo itabainika kuwa mtu au watu wamekiuka taratibu za matumizi ya msitu

wa hifadhi ya kijiji, mtu huyo au watu hao watafikishwa mbele ya Kamati ya

Page 27: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

23

Mazingira ya kijiji na suala lao litashughulikiwa kwa utaratuibu ufuatao hapa

chini:

• Mhalifu/wahalifu watafikishwa katika ofisi ya kijiji ambapo Afisa Mtendaji

wa Kijiji atamuweka/atawaweka chini ya ulinzi. Afisa Mtendaji wa Kijiji

atawaarifu viongozi wa kamati/wajumbe wa Kamati ya Mazingira

angalau wawili ili kuwatoza faini wahalifu iwapo watakiri/atakiri kosa kwa

kuweka sahihi katika daftari la “makosa na faini”

• Iwapo mhalifu/mtuhumiwa atakataa kukiri kutenda kosa kwa kukataa

kuweka sahihi katika daftari, mtu huyo atatakiwa kupelekwa

mahakamani.

• Endapo mhalifu/wahalifu watakiri kutenda kosa, faini yote lazima iwe

imelipwa katika muda wa siku tatu (3) toka siku ya kukiri kutenda kosa

hilo. Hata hivyo mhalifu atalazimika kuwekewa dhamana na mtu

anayekubalika katika kijiji cha Ikola.

▪ Katibu atapokea malipo ya faini iliyolipwa kwa kuandika stakabadhi ambayo

atampatia mhalifu. Namba ya stakabadhi iliyotolewa itaandikwa kwenye daftari

la “Makosa na Faini” na kumkabidhi Mweka Hazina azipeleke kwenye akaunti

ya Kamati ya Mazingira ya kijiji.

▪ Iwapo mtu anayetuhumiwa kutenda kosa atakataa kukiri kosa mbele ya Kamati

ya Mazingira na mbele ya Mwenyekiti wa Kijiji au Afisa Mtendji wa Kijiji basi

itabidi vyombo hivyo vya utendaji vifikishe shauri hili mahakamani kwa uamuzi

zaidi.

▪ Iwapo mhalifu atashindwa kulipa faini katika kipindi kilichokubaliwa basi Kamati

ya Mazingira au Afisa Mtendaji wa Kijiji atafikisha suala hilo mahakamani.

FAINI NA ADHABU KWA KILA KOSA

Mtu yoyote atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa lolote lililoidhinishwa katika kifungu

cha 10 cha sheria ndogo hizi ataadhibiwa kama ifuatavyo:

▪ Kosa la kuingiza na kuchunga mifugo atatozwa Tshs 1,000/= kwa

kila mbwa, ng’ombe na Punda na Tsh 5000/= kwa mbuzi na

kondoo. Atakayeshindwa kulipa mifugo yake itaifishwe kulingana na

gharama ya faini.

Page 28: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

24

▪ Kosa la kuingia msituni bila kibali adhabu yake itakuwa ni faini

isiyopungua Tsh 10,000/= na isiyozidi Tsh 50,000/=

▪ Kosa la Kuchoma mkaa faini shilingi Tsh 50,000/= na kutaifisha mkaa

huo.

▪ Kosa la Kukata miti bila kibali adhabu itatolewa kulingana na thamani

ya mti uliokatwa na faini isiyopungua Tsh 10,000/= na isizidi Tsh

50,000/= pamoja na kutaifisha miti hiyo.

▪ Kosa la Kufanya shughuli za kilimo faini shilingi elfu hamsini

(50,000/=) kwa hekari moja, kutaifisha mazao na kupelekwa

mahakamani.

▪ Kosa la Kuchoma moto faini ya isiyopungua Tsh 20,000/= na isiyozidi

Tsh 50,000/= na atashitakiwa kwa mujibu wa sheria ya kosa husika.

▪ Kosa la Kufanya shughuli nyingine yoyote isiyohusika katika msitu

huo atatozwa faini Tsh 30,000/=

FAINI ZA KUTOWAJIBIKA Iwapo mjumbe yeyote katika Halmashauri ya Kijiji, Kamati ya Mazingira au walinzi wa

msitu atakiuka taratibu za kiutendaji kuhusiana na uhifadhi wa msitu wa hifadhi ya kijiji

cha Kagunga, atakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria hii na atatozwa faini

itakayojulikana kama faini ya wenye dhamana/madaraka. Faini hiyo itakuwa mara

mbili ya faini zitakazotozwa kwa watu wasiokuwa na madaraka kijijini/ zilizoainishwa

hapo juu.

• Pamoja na faini hizo, makosa ya viongozi hao lazima yajadiliwe kwenye vikao

vya juu katika kijiji na kuwachukulia hatua kali kama vile barua za onyo la

maandishi, kusimamishwa na kuwaondoa kwenye nafasi zao baada ya

kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji.

• Kwa wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji, Afisa Mtendaji Kata ataitisha Kikao

kujadili hatima ya kiongozi aliyefanya uhalifu huo.

Kifungu Cha Kumi na Mbili Kuboresha msitu na Ukarabati wake

KUUENDELEZA MSITU Kwa bahati nzuri utengaji wa msitu ulizingatia maeneo ya kulima kuchungia mifugo,

makazi n.k. hivyo hakuna mvutano wa mgogoro wa hitaji la shughuli hizi katika eneo

la msitu huu. Shughuli kama hizi zitafanyika nje ya msitu kwa kujitosheleza. Hapa

Mpango huu wa Usimamizi wa Msitu unapiga marufuku kufanyika shughuli za aina hii

ndani ya msitu.

Page 29: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

25

Aidha, ni marufuku mtu au kikundi cha watu kupanda mti wowote wa kigeni ndani ya

msitu huu.

Aina pekee za miti zinazoruhusiwa kuvunwa na kiasi chake zimeorodheshwa katika

majedwali yaliyoambatanishwa na mpango huu. Hairuhusiwi kutumia msumeno wa

mnyororo katika msitu huu.

Kifungu Cha Kumi na Tatu Matumizi

UTANGULIZI: Msitu huu ni msitu wa matumizi na Uhifadhi hivyo uvunaji wa miti ya mbao

unaruhusiwa kwa kiwango kilicho ainishwa katika mpango huu, uvunaji wa rasilimali

za msitu unaruhusiwa katika EDU ya kasembe. Lakini jambo la kuzingatia ni kiasi,

wakati na utaratibu wa uvunaji kama ilivyo ainishwa katika mpango huu. EDU ya

Uhifadhi ya Kalufwesi na Manda haitaruhusiwa kufanyika shughuli zozote za uvunaji

kwani ni kwa ajili ya Uhifadhi na matumizi mengine yasiyokuwa ya uvunaji wa miti na

kutokana na kuwa maeneo yanayopendelewa na wanyamapori aina ya sokwe pia

makorongo marefu, vyanzo vya maji na bioanuai mbalimbali muhimu. Hivyo basi,

Mahitaji yaliyoruhusiwa yatapaswa kupatikana kutoka maeneo ya matumizi ndani ya

msitu wa hifadhi ya kijiji cha Ikola. Maeneo yaliyozuiliwa/hifadhiwa hayataruhusiwa

kupata mahitaji ya mbao, miti ya nguzo/miamba ya nyumba na mengineyo

yasiyoruhusiwa.

UVUNAJI WA MITI Uvunaji wa miti unaoruhusiwa ni kwa miti ya aina zilizoorodheshwa katika Jedwali Na

1. EDU hii ina jumla ya miti kama inavyoonyeshwa katika Jedwali (tazama katika

viambata) ikiwa ni pamoja na matumizi mengineyo ya EDU hii.

Kiasi kamili cha miti ya kuvunwa kwa kila aina ya mti vimeonyeshwa katika jedwali

namba 5 na 7. Katika majedwali haya imeonyeshwa bayana kiasi gani cha kuvunwa

kwa kila mwaka na ni aina gani ya miti. Inapaswa kuzingatiwa bila kuongeza hata

kidogo.

Page 30: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

26

Kifungu Cha Kumi na Nne Ratiba

HATUA ZA HARAKA ▪ kamati ya maliasili kijiji na Timu ya Doria zinapaswa kuchaguliwa katika

mkutano mkuu wa kijiji

▪ Kamati ya Maliasili ya Kijiji inapaswa kufanya mkutano wake wa kwanza

▪ Taratibu za ununuzi wa vitabu vya kumbukumbu zinatakiwa zifanyike ili Kamati

ikutane na Mtunza Hazina wa Wilaya. zoezi hili litakamilishwa na Hafla au

mkutano utakaohudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya kwa uzinduzi

rasmi.

▪ Mwezi June 2017 ni mwezi wa kuanza kazi rasmi kwa utekelezaji wa Mpango

wa Usimamizi wa Msitu huu wa hifadhi ya kijiji cha Ikola.

UFUATILIAJI Vigezo vya Mafanikio: Vifuatavyo ni Vigezo vya mafanikio vitatumika katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa

Mpango huu wa Usimamizi wa msitu wa hifadhi ya kijiji:

▪ Wanakijiji kuunga mkono juhudi za uhifadhi kwa:

• Kutoa ushirikiano kwa Kamati ya Mazingira na walinzi wa msitu na

hifadhi.

• Kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

• Kuotesha na kupanda miti katika maeneo ya kaya na mashamba.

• Kuheshimu na kutekeleza taratibu za ulinzi na utunzaji Misitu.

▪ Kupungua kwa matukio ya upasuaji mbao, moto, uwindaji wa wanyama pori,

uvamizi wa msitu kwa ajili ya kilimo na ufugaji.

▪ Kupungua na kufunga kwa njia zisizoruhusiwa msituni.

▪ Kuongezeka kwa uoto wa asili na hivyo msitu kufunga hasa katika maeneo

yaliyoharibiwa.

▪ Kurejea au kuongezeka kwa wanyama pori, ndege na viumbe vingine hai katika

msitu wa kijiji.

▪ Kuongezeka kwa kiwango cha maji kwenye mito, chemchem au kufufuka kwa

chemechem zilizokufa kutokana na uharibifu.

▪ Kuongezeka kwa makundi ya nyuki ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji.

Page 31: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

27

▪ Mipaka ya nje ya msitu wa hifadhi kuwa wazi, safi na kuonekana bila ugumu

wowote.

Wafuatiliaji Wafuatao watahusika kufanya ufuatiliaji kwa kukusanya taarifa kuhusu vigezo vya

mafanikio:

▪ Wataalamu wa Misitu wa ngazi zote.

▪ Halmashauri ya kijiji

▪ Kamati ya Mazingira ya kijiji.

Taarifa ya Ufuatiliaji Itatolewa kwa: ▪ Afisa Misitu (W)/ Afisa Misitu (M)

▪ Mkutano Mkuu wa kijiji.

▪ Mkuu wa Wilaya/Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya.

▪ Halmashauri ya kijiji.

Muda wa Kufanya Ufuatiliaji Kamati ya Mazingira: Itafanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mpango huu mara mbili

(2) kila mwezi na kuandaa taarifa kwa Halmashauri ya kijiji mara moja kwa mwezi

yenye nakala kwa Afisa Misitu (W).

Halmasahauri ya kijiji: Itafuatilia mpango huu mara moja (1) kila mwezi

▪ kwa kutembelea msitu wa hifadhi ya kijiji angalau mara moja kila mwezi

▪ kuwa na agenda ya kudumu katika vikao vyake

▪ Kwa kutumia taarifa ya Kamati ya Mazingira.

Wataalam wa Misitu & ngazi za Eneo, (W)/ (M):

▪ Wataalam wa ngazi ya Eneo (Kata/Tarafa) watafanya ufuatiliaji wa mpango huu

mara moja kila mwezi.

▪ Wataalam wa ngazi ya Wilaya & Mkoa watafuatilia utekelezaji wa mpango huu

mara moja kila baada ya miezi mitatu (3) yaani robo mwaka.

IKUMBUKWE: Taarifa ya matokeo ya ufuatailiaji itajadiliwa mara baada ya kazi ya

ufuatiliaji kukamilika.

Page 32: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

28

Mpango huu unaweza kufanyiwa marekekebisho baada ya miaka mitano (5) ya

utekelezaji kwa kuzingatia taarifa za ufuatiliaji na uamuzi uliofikiwa wakati wa kujadili

taarifa hiyo.

RATIBA YA UTEKELEZAJI Hatua za Awali za Utekelezaji:

▪ Kuchagua Kamati ya Mazingira na walinzi wa msitu (Kamati ya doria) itafanyika

mara baada ya mpango wa utekelezaji kupitishwa na Mkutano Mkuu wa kijiji.

▪ Kikao cha kwanza cha Kamati ya Mazingira na walinzi kitafanyika siku moja

baada ya uchaguzi wao kufanyika.

▪ Kununua vitabu vya kumbukumbu itafanyika baada ya Kamati ya Mazingira

kufanya kikao chake cha kwanza.

Hatua Zitakazofuata ▪ Kuweka mabango ya matangazo.

MUDA WA MPANGO, MAREKEBISHO NA MAPITIO YAKE:

Mpango huu wa utekelezaji utatumika kwa miaka mitano (5) kuanzia mwaka 2017 –

2021. Marekebisho ya mpango yatafanyika kwa kuzingatia mahitaji yatakayojitokeza

kwa lengo la kuuboresha na Kamati ya Mazingira ya kijiji itahusika kwa ushirikiano na

Afisa Misitu (W) Mpanda.

Page 33: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

29

Page 34: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

30

VIAMBATA

MPANGO WA UVUNAJI KWA AINA MBALIMBALI ZA MITI KATIKA EDU ZA

KASEMBE

JEDWALI Na 1: ORODHA YA MITI YA INAYORUHUSIWA KUVUNWA - EDU YA KASEMBE.

MITI MUHIMU MITI MINGINEYO MATUMIZI MENGINEYO

Mbanga Mkalya Urinaji wa asali

Mlembela Mhongolo Uvunaji wa miti ya mbao

Mkurungu Mbombo Kukata nyasi

Mtundu Mitonga Kukusanya kuni

Msongati Ukatajiwa boriti, nguzo na fito

Matambiko

Page 35: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

31

JEDWALI Na. 2: MAJUMUISHO YA TAKWIMU KUTOKA KATIKA PLOTI ZA SAMPULI Kijiji IKOLA Jina la Msitu

Idadi ya ploti sampuli (N) 88

Jina la EDU

Eneo la EDU (ha) (A) 3750 eneo la ploti sampuli(ha) (P) 0.04

DBH <4 4 - 7 8 - 14 15 - 29 30 - 49 50+

Mea

sure

d to

tal (

T)

Fm

u to

tal

(F)

Mea

sure

d to

tal (

T)

Fm

u to

tal

(F)

Mea

sure

d to

tal (

T)

Fm

u to

tal

(F)

Mea

sure

d to

tal (

T)

Fm

u to

tal

(F)

Mea

sure

d to

tal (

T)

Fm

u to

tal

(F)

Mea

sure

d to

tal (

T)

Fm

u to

tal

(F)

Miti muhimu

Mninga 0 2 2,131 6 6,392 5 5,327 1 1,065 0

Mkurungu 6 6,392 27 28,764 33 35,156 11 11,719 2 2,131 0

Ikongwa 0 1 1,065 1 1,065 0 0 0

Mfila 1 1,065 11 11,719 4 4,261 0 0 0

Mkola 0 1 1,065 0 0 0

Mnembela 0 3 3,196 12 12,784 20 21,307 13 13,849 3 3,196

Mpilipili 0 1 1,065 2 2,131 1 1,065 1 1,065 0

Kibula 38 40,483 55 58,594 5 5,327 4 4,261 0 0

Kabamba 48 51,136 153 162,997 69 73,509 36 38,352 5 5,327 1 1,065

Mbanga 2 2,131 10 10,653 13 13,849 4 4,261 1 1,065 3 3,196

Mgando 0 0 1 1,065 4 4,261 3 3,196 1 1,065

Masaka 0 0 2 2,131 0 0 0

Mtungulu 2 2,131 17 18,111 30 31,960 8 8,523 0 0

Msubhu 1 1,065 3 3,196 3 3,196

Mbarebare 1 1,065

Jumla 104,403 298,295 193,892 102,273 27,699 8,523

Idadi kwa kila hekta 28 80 52 27 7 2

Page 36: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

32

Miti mingineyo

Msongati 26 27,699 106 112,926 79 84,162 7 7,457 0 0

Mlama 1 1,065 1 1,065 5 5,327 5 5,327 2 2,131 0

kabumbu 0 0 1 1,065 3 3,196 3 3,196 0

Kapara 4 4,261 17 18,111 16 17,045 12 12,784 0 0

Mfuru 0 0 0 2 2,131 0 0

Kapepe 0 2 2,131 0 0 0 0

Kapangalala 1 1,065 0 0 0 0 0

Msebeje 0 1 1,065 1 1,065 1 1,065 0 0

Msigisigi 0 6 6,392 5 5,327 1 1,065 0 0

Lukali 0 1 1,065 2 2,131 0 0 0 0

Mkalakala 0 0 0 0 0 1 1,065 0 0

Mkalya 0 0 1 1,065 0 0 0

Mpapa 1 1,065 42 44,744 29 30,895 16 17,045 3 3,196 0

Kalya wa fyula 2 2,131 1 1,065 7 7,457 1 1,065 0 0 0 0

Msakanka 0 3 3,196 1 1,065 0 0 0 2 2,131

Mgunga 1 1,065 0 0 0 0 0 0

Kagobore 0 1 1,065 0 0 0 0 0

Busenga 2 2,131 4 4,261 2 2,131 3 3,196 0 0 0

Mhongolo 1 1,065 2 2,131 8 8,523 2 2,131 0 0 0

Msantu 0 2 2,131 2 2,131 0 0 0 0

Mnyenye 0 0 1 1,065 1 1,065 0 0 0

Mbula 0 0 3 3,196 1 1,065 0 0 3 3,196

Buketya 0 0 5 5,327 3 3,196 0 0 0

Mlugala 0 0 1 1,065 0 0 0

Mdawa 0 0 1 1,065 0 0 0

Kankundu 0 1 1,065 0 0 0 0

Page 37: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

33

Kifunfwe 0 2 2,131 0 0 0 0

Nsunga 2 2,131 1 1,065

Jumla miti mingineyo 43,679 204,545 182,173 62,855 8,523 5,327

wastani kwa hekta 12 55 49 17 2 1

JEDWALI Na 3 FOMU ‘C’ YA TATHIMINI

Kijiji Jina la Msitu Idadi ya ploti za sampuli (N)

Jina la EDU Eneo la EDU (ha) (A) Plot area (ha) (P)

Madaraja ya vipenyo

<4 4 - 7 8 – 14 15 – 29 30 - 49 50+

Ju

mla

ili

yo

pim

wa

(T

)

Ju

mla

kw

en

ye

E

DU

(F

)

Ju

mla

ili

yo

pim

wa

(T

)

Ju

mla

kw

en

ye

E

DU

(F

)

Ju

mla

ili

yo

pim

wa

(T

)

Ju

mla

kw

en

ye

E

DU

(F

)

Ju

mla

ili

yo

pim

wa

(T

)

Ju

mla

kw

en

ye

E

DU

(F

)

Ju

mla

ili

yo

pim

wa

(T

)

Ju

mla

kw

en

ye

E

DU

(F

)

Ju

mla

ili

yo

pim

wa

(T

)

Ju

mla

kw

en

ye

E

DU

(F

)

Miti muhimu

Miti Mingineyo

Page 38: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

34

Jumla (F) = A/P * T/N: A = eneo la EDU (ha), P = ukubwa wa ploti ya sampuli (ha), T = idadi ya miti iliyopimwa (kwenye ploti zote za sampuli), N = idadi ya ploti za sampuli

JEDWALI Na 4: MIHIMILI YA MSINGI KUONYESHA WINGI WA MITI KATIKA EDU YA KASEMBE.

28

80

52

27

7

3

0

10

20

30

40

50

60

70

80

90

<4 4 -7

8 - 14 15 -29

30 -49

50+

Idad

i ya

mit

i/h

a

DBH (cm)

MITI MUHIMU

12

55

49

17

2 1

0

10

20

30

40

50

60

<4 4 -7

8 - 14 15 -29

30 -49

50+iD

AD

I YA

MIT

I KW

A H

EKTA

dbh (cm)

MITI MINGINEYO

Page 39: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

35

JEDWALI NA. 5: MIHIMILI YA MSINGI KUONYESHA WINGI WA MITI MSITU WA MIOMBO USIOHARIBIWA

0

50

100

150

200

250

300

350

400

450

500

< 4 cm 4 – 7 cm 8 – 14 cm 15 – 29 cm 30 – 49 cm 50+

Nu

mb

er o

f tr

ees

per

hec

tor

Diameter classes (cm)

Ideal (target) size, DBH distribution

Actual (Target)

Page 40: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

36

JEDWALI Na 6. UFUPISHO WA MPANGO WA UVUNAJI KATIKA EDU YA KASEMBE KWA MWAKA 2017/2018 HADI 2021/2022

Ziada na pungufu kwa miti muhimu

Dbh madaraja Idadi ktk EDU Idadi halisi Iliyotarajiwa Ziada/pungufu Iliyopo kuvunwa (50% ya

ziada) Uvunaji kwa mwaka (5yrs)

Maoni

< 4 104,403 1,706,250 -1,601,847 (800,924) (160,185) 4 -7 298,295 1320000 -1,021,705 (510,853) (102,171) 8-14 193892 592500 -398,608 (199,304) -39861

15- 29 102273 37500 64,773 32,387 6477 30- 49 27699 18750 8,949 4,475 895

50+ 8523 7500 1,023 512 102

Ziada na pungufu kwa miti mingineyo

Dbh madaraja Idadi ktk EDU Iliyotarajiwa Ziada/pungufu Iliyopo kuvunwa (50% ya

ziada) Uvunaji kwa mwaka (5yrs)

Maoni

<4

4 -7 4364 1,706,250.00 (1,701,886.00)

8-14 204545 1,320,000 (1,115,455.00)

Page 41: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

37

15- 29 182173 592500 -410327

30- 49 8523 37500 -28977 -14488.5 (2,898)

50+ 5327 7500 -2173 -1087 (217)

JEDWALI Na 7: ORODHA YA MITI YA INAYORUHUSIWA KUVUNWA - EDU YA KASEMBE MITI MUHIMU MITI MINGINEYO MATUMIZI MENGINEYO

Kabamba Mbarebare Urinaji wa asali

Mlembela Msongati Uyoga na matunda pori

Mkurungu Mkalya Uvunaji wa miti ya mbao

Mbanga Mhongolo Uchimbaji wa dawa za kienyeji

Mbombo Kukata nyasi

Mpapa Kukusanya kuni

Kabumbu Kamba za miti

Mgando Ukataji wa boriti, nguzo na fito

Page 42: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

38

Maji

Matambiko

JEDWALI Na. 8: MPANGO KAZI WA UTEKELEZAJI WA USIMAMIZI WA MSITU WA HIFADHI WA KASEMBE KIJIJI CHA IKOLA

S/Na LENGO MKAKATI SHUGHULI MAHITAJI WAHUSIKA MUDA WA UTEKELEZAJI

1

Kuzuia uvunaji haramu, ufyekaji miti na ujangili ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji

1. Kutoa elimu kwa jamii 1. Usafiri 1. Kamati ya Maliasili ya kijiji

December 2017 - December 2022

2. Kufanya doria msituni 2. Shajala 2. Halamashauri ya kijiji

3. Kutunga sheria ndogo za usimamizi wa msitu 3. wataalam 3. VGS

4. Kuhamasisha jamii juu ya kuunda vikundi vya ufugaji nyuki

4. Rasilimali fedha 4. Jamii

5. Vifaa vya doria 6. Halmashauri (W)

7. Serikali kuu

2 Kuzuia shughuli zisizo rasmi ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji

1. Kutoa elimu kwa jamii 1. Usafiri 1. Kamati ya Maliasili ya kijiji

December 2017 - December 2023

2. Kufanya doria msituni 2. Shajala 2. Halamashauri ya kijiji

3. Kutunga sheria ndogo za usimamizi wa msitu

3. wataalam 3. VGS

4. Rasilimali fedha 4. Jamii

Page 43: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA IKOLA - BirdLife International · 2018-08-02 · kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu. Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji

39

4. Kuhamasisha jamii juu ya kuunda vikundi vya ufugaji nyuki

5. Vifaa vya doria 5. Wafadhili

6. Halmashauri (W)

7. Serikali kuu

3

Kuzuia uharibifu wa vyanzo vya maji vilivyomo ndani ya msitu wa hifadhi

ya kijiji

1. Kutoa elimu kwa jamii 1. Usafiri 1. Kamati ya Maliasili ya kijiji

December 2017 -

2. Kufanya doria msituni 2. Shajala 2. Halamashauri ya kijiji

3. Kutunga sheria ndogo za usimamizi wa msitu 3. wataalam 3. VGS

4. Kuhamasisha jamii juu ya kuunda vikundi vya ufugaji nyuki

4. Rasilimali fedha

4. Jamii

5. Kukarabati maeneo ya vyanzo vya maji yaliyo haribiwa kwa kupanda miti 5. Wafadhili

6. Kuhamasisha jamii kufuata kanuni za kilimo bora

6. Halmashauri (W)

7. Serikali kuu