35
Mussa Shekinyashi

Mussa Shekinyashi · Ni sharti mtenda kazi yoyote ajue misingi ya kazi ietendayo kabla hajaifanya. Kadharika, mfasiri ni sharti ajue misingi ya kinadharia ya kazi ya utafsiri. Hii

  • Upload
    others

  • View
    17

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

Mussa Shekinyashi

Dhana ya Tafsiri

Tafsiri ni mchakato wa uhawilishajiwa mawazokatika maandishi kutoka lugha moja hadinyingine.

Kufasiri ni kuchukua mawazo yaliyo katikamaandishi kutoka lugha moja (lugha chanzi) nakuweka badala yake mawazo yaliyolinganakutoka lugha nyingine (lugha lengwa).

Mfasiri ni mtu anayefanya kazi ya kufasiri matini.

Tafsiri huzingatia mawazo kati ya lugha chanzina lugha lengwa kuwiana.

Tazama michoro hii…

LughaChanzi

Wazohusika

Wazohusika

LughaLengwa

Mfasiri lazima azifahamu lugha zote mbili kwakina.

Mfasiri hana budi kufahamu kwa kina lugha zote mbilianazozifanyia kazi.

Yaani lugha chanzi na lugha lengwa.

Umahiri huu anaotakiwa kuwa nao mfasiriunajumuisha kuufahamu msamiati kwa kina nakuzifahamu sheria za lugha zote mbili kwa kina.

Pia, mfasiri hana budi kuzifahamu mbinu mbalimbaliza matumizi ya lugha kulingana na mazingira au muktadha.

Mfasiri ajue misingi ya kazi ya tafsiri

Ni sharti mtenda kazi yoyote ajue misingi ya kaziietendayo kabla hajaifanya.

Kadharika, mfasiri ni sharti ajue misingi ya kinadhariaya kazi ya utafsiri.

Hii humpa nafasi mfasiri kujua ni aina gani ya fasirianaitumia kulingana na mahitaji ya hadhira yake.

Kukosekana kwa ufahamu juu ya misingi ya tafsirihupunguza mantiki ya matini iliyotafsiriwa.

Mfasiri awe mweledi Mfasiri ili awe mahiri katika shughuli za utafsiri hana

budi kuwa na upeo mpana katika nyanja zote zamaisha: kiuchumi, kisiasa, tiba, sayansi na kijamii.

Ni vyema basi, akawa na tabia ya kuyafuatilia masualahaya kwa jinsi yanavyotokea duniani.

Ujuzi huu utamwezesha mfasiri kuwa na msamiati wakutosha katika shughuli zake za kutafsiri.

Mfasiri afahamu kiwango cha uelewa cha wasomaji anaowatafsiria

Kufahamu lugha zote mbili vizuri haitoshi kumfanyamfasiri kuwa mahiri.

Pamoja na yote hayo ni sharti mfasiri awe na uwezo wakufahamu kiwango cha uelewa cha wasikilizaji nawasomaji wake.

Hii itamwezesha kufasiri matini kutoka lugha chanzikuja lugha lengwa kwa kutumia msamiati wenyeuwiano na uelewa wa wasikilizaji.

Kuisoma Matini Nzima Jambo la msingi analopaswa kulizingatia mfasiri ni

kuisoma matini nzima kwa kina.

Kuisoma matini kutamuwezesha mfasiri, kwanza; kuelewa maudhui ya matini chanzi.

Pia, humsaidia mfasiri kuandaa marejeleoyatakayomwezesha mfasiri kuandaa kamusimahususi, orodha ya misamiati mipya na orodha yaistilahi ghafi.

Hurahisisha pia, maafikiano baina ya wafasiri wawiliwanaofanyia kazi maini moja.

Kubaini Lengo la Matini Kabla ya kuanza mchakato wa kufasiri matini ni

vyema mfasiri akafahamu lengo la matini chanzi.

Mara nyingine ufinyu wa uelewa wa lengo la matinichanzi hupelekea kupotoshwa kwa lengo hilo katikamatini lengwa.

Kwa namna nyingine, mfasiri anapobaini lengo la matini chanzi huweza kufasiri kwa namna aionayo nisahihi na kwa lengo analolipendekeza.

Kubaini Lengo la Mfasiri Ni sharti mfasiri ajue lengo lake la msingi la katika

matini anayoifanyia kazi.

Je, lengo lake ni kuwapa wasomaji wake athariinayolingana na ile ya matini chanzi?

Mara nyingine mfasiri hubali lengo la matini kwakunuia athari tofauti kwa wasomaji wake wa matinilengwa.

Lengo la mfasiri huzingatia pia kiwango cha uelewacha wasomaji wa matini lengwa.

Kubaini Wasomaji wa MatiniLengwa Mfasiri anapaswa ajiulize maswali haya:

Hadhira ya matini chanzi ni ipi?

Je, msomaji wa matini yake lengwa ni yupi?

Ana elimu, umri na jinsia gani?

Haya ni baadhi ya maswali yambayo yatamsaidiamfasiri kutafsiri matini huku akifahamu ni kwa kiasigani matini yake itapokelewa na kueleweka namsomaji wa lugha lengwa.

Kubaini Mtindo wa Matini Chanzi Kufahamu mtindo uliotumika kuiandika matini

chanzi ni muhimu kwa mfasiri.

Ni vyema afahamu kama matini chanzi imeandikwakifasihi, kirasmi au kitaaluma.

Kwa kufahamu hilo kutamsaidia kufahamu ni kwamtindo gani anatakiwa kuifasiri matini yake kwendalugha lengwa.

Kadharika, nadharia ya tafsiri inasisitiza kuwa mtindowa matini katika lugha chanzi uendane na ule walugha lengwa.

Kubaini ubora na mamlaka yaMatini Ubora hubainika kwa kuzingatia lengo na na matarajio

ya mwandishi katika matini aliyoiandika.

Mmlaka ni hubainika kupitia umahiri na hadhi yamwandishi.

Mfasiri anajukumu la kujua haya ili kama matinichanzi imeandikwa kwa ustadi wa hali ya juu namwandishi mwenye hadhi kubwa basi naye hana budikuhamisha hadhi na ubora huo katika matini yakelengwa.

Kusoma Matini kwa mara yaMwisho Ni vyema, baada ya kuyafahamu masuala hayo

yaliyojadiliwa hapo juu mfasiri akaisoma tena upyamatini chanzi ili aanze mchakato wa kutafsiri matinihiyo.

Lakini pia si lazima vipengele hivyo apo juu vifuatwena mfasiri kama vilivyopangwa hapo, vinaweza kuwavinginevyo lakini jambo la msingi ni kwamba vyotevizingatiwe kwa kina.

Maandalizi Hatua hii hujumuisha mambo ya msingi

yanayozingatiwa na mfasiri kabla ya kuanza kutafsiri.

Mambo hayo ni kama:

Kuisoma matini nzima, kubaini lengo la matinichanzi, kubainisha lengo la mfasiri na kubaini mtindowa matini hiyo.

Mbali na hayo pia katika hatua hii mfasiri inampasakuchunguza taarifa kama; historia yamwandishi,mazingira yaliyomkuza na hadhi yakekatika jamii aliyoiandikia matini hiyo.

Uchambuzi Katika hatua hii mfasiri anapaswa kuvitambua na

kuweka wazi visawe na maelezo yanayohitajiufafanuzi wa kina katika matini chanzi.

Hapa ndipo mfasiri hupitia marejeo mbalimbali ,kamaensaiklopidia na kamusi ili kubaini visawe vya tafsiriyake.

Hatua ya uchambuzi humpa nafasi mfasiri kurahisishakazi yake ya Tafsiri.

Uhawilishaji Hapa mfasiri huamisha mawazo kutoka lugha chanzi

hadi lugha lengwa akitumia visawe alivyovibainishakatika hatua ya uchambuzi.

Kimsingi katika hatua hii ndipo hasa zoezi la msingi la tafsiri hufanyika

Mbali na hayo bado mfasiri ana nafasi ya kuongeza au kupunguza visawe kwa mujibu wa mahitaji ya matinilengwa na lengo la mfasiri.

Usawidi wa Rasimu ya Kwanza yaTafsiri Usawidi wa rasimu ni kuiandika rasimu ya kwanza kwa

kadri ya ufasiri.

Mfasiri huzingatia umbo na mtindo wa matini chanzikuyapangilia mawazo katika matini lengwa .

Hatua hii hufuatwa baada ya hatua ya uhawilishaji,

Hapa ndio mfasiri huanza kuiona picha ya matinilengwa katika mchakato mzima wa ufasiri.

Udurusu wa Rasimu ya Kwanza yaTafsiri

Baada mchakato wa usawidi ni wazi kwamba mfasirianapaswa kuisoma tafsiri aliyoifanya.

Wataalamu wanashauri mfasiri asome matinialiyoitafsiri baada ya kuimaliza kuiandika.

Na ni vyema akaisoma kwa sauti ili kuweza kubainimakosa mbalimbali kama vile; makosa ya kisarufi, makosa ya kimatumizi ya lugha na pia kubaini uwianoulioo baina ya matini hiyo na matini chanzi.

Kusomwa kwa Rasimu na Mtu waPili Baada ya durusu ya mfasiri rasimu ya tafsiri inapaswa

isomwe na mtu mwingine.

Dhima kuu ni kubaini usahihi wa mtiririko wamawazo na ujumbe katika tafsiri hiyo.

Kwa kuisoma kwa makini msomaji wa pili atawezakubaini makosa na kuyawekea alama ili yasahihishwe.

Kama rasimu itasomwa vyema na msomaji wa pili nakufanyiwa marekebisho basi rasimu hiyo itaondokeakuwa nzuri.

Usawidi wa Rasimu ya Mwisho yaTafsiri

Hatua hii hujumuisha mchakato mzima wa kuyafanyiakazi mawazo yaliyopendekezwa na msomaji wa pili warasimu.

Usawidi huu ukipita basi matini lengwa hukamilika.

Tayari kutumiwa na hadhira lengwa.

Nyenzo ya mawasiliano

Kueneza utamaduni wa jamii

Nyenzo ya kufundisha lugha za kigeni

Hupanua mawazo na fikra za wasomaji

Husaidia kuziba mapengo ya kimsamiati na kimaanabaina ya lugha.

M. Shekinyashi

Ukalimani ni nini? Mshindo (2010) anasema ukalimani ni shughuli ya

kiakili inayowezesha kuwasiliana kwa manenoyaliyosemwa au ishara zinazooonyeshwa baina ya watuambao hawasemi lugha moja au ambao hawatumiiishara za aina moja.

Wanjara (2011) anasema ukalimani ni kuhawilishaujumbe ulioko katika mazungumzo, pamoja nauamilifu wake, kutoka lugha chanzi kwenda lugha kwalengwa kwa kuzingatia isimu, utamaduni namuktadha wa jamii husika.

Aina za Ukalimani

Kuna aina kuu mbili za ukalimani:

Ukalimani wa Papo kwa Papo

Ukalimani wa Ufuatizi

Ukalimani wa papo kwa papo Aina hii ya ukalimani hutokea ambapo msemaji wa matini

chanzi na msemaji wa matini lenga hupishana kwa mudakidogo sana .

Hapa si rahisi msikilizaji kuhisi kuwa mkalimani husikilizakabla hajakalimani kwa sabau sauti ya msemaji katikalugha chanzi haipishani kabisa na sauti msemaji katikalugha lengwa.

Kukalimani katika aina hii ya ukalimani inampasamkalimani awe na uwezo na ujuzi wa hali ya juu.

Aina hii ya ukalimani hutumika sana katika mikutano yakimataifa, mihadhara ya kidini na pia katika mahakama zakimataifa.

Ukalimani wa Ufuatizi ( maandalizi) Hii ni aina ya ukalimani ambayo msemaji wa matini chanzi

na msemaji wa matini lenga hupishana kwa kipindi kirefukatika kusema.

Hapa, hadhira hutambua wazi kwamba kuna watuwanaozungumza kwa kupokezana.

Msemaji wa matini chanzi husema kwa kituo ili kumpanafasi msemaji wa lugha lengwa kuyafafanua kwa lugha yamatini lengwa .

Kupokezana huko kunaweza kuwa kila baada ya sentensi, aya au hata matini nzima alimuradi mkarimani anapewanafasi kujiandaa .

Aina hii hutumika katika mihadhara ya kidini na maranyingine katika mikutano ya kisiasa.

Sifa za Mkalimani Uelewa wa kina juu ya lugha anazozitumia: hii

inajumuisha utajiri wa msamiati, kujua sheria nataratibu za lugha na pia kuelewa matumizi ya lughakatika miktadha mbalimbali.

Kuielewa kwa kina hadhira inayohusika: kufahamu kiwango cha elimu, umri, mtazamo namatarajio ya hadhira.

Kuelewa mbinu za kimawasiliano: hii inajumuishamatumizi ya ishara na lugha za alama kusindikizaufafanuzi wa kikalimani. Sauti pia ni nyenzo nzuri yakimawasiliano inayovuta usikivu.

Umuhimu wa Mkalimani Nyenzo ya mawasiliano

Nyenzo muhimu ya kujifunzia lugha

Nyenzo mahususi kudumisha amali za jamii

Nyenzo muhimu ya umoja baina ya jamii lugha tofauti

Nyenzo ya maendeleo

Kuenea kwa dini mbalimbali na tamaduni mbalimbaliduniani.

Swali…1. Kwa mifano, fafanua sifa za mkalimani kwa

mujibu wa Wanjala (2011)2. Jadili mambo ya msingi yanayozingatiwa na

mzungumzaji na mkalimani katika ukalimani.

Asanteni kwa Kunisikiliza