12
1 MWONGOZO WA JATROPHA KWA WAKULIMA WANAOSHIRIKI KATIKA MAJARIBIO YA JATROPHA Jinsi ya kukuza Jatropha pamoja na mimea ya chakula. Imetolewa na Ab van Peer kwa Max Havelaar. www.jatropha.pro

Mwomgozo wa Jatropha corr...huku akikuza mimea ya ziada ya biashara ili kuzalisha mapato ya ziada. Ukuzaji wa Jatropha haustahili kwa njia yoyote kuvuruga mchakato huu. Kwa hivyo maelekezo

  • Upload
    others

  • View
    8

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mwomgozo wa Jatropha corr...huku akikuza mimea ya ziada ya biashara ili kuzalisha mapato ya ziada. Ukuzaji wa Jatropha haustahili kwa njia yoyote kuvuruga mchakato huu. Kwa hivyo maelekezo

1

MWONGOZO WA JATROPHA KWA WAKULIMA WANAOSHIRIKI KATIKA MAJARIBIO YA JATROPHA

Jinsi ya kukuza Jatropha pamoja na mimea ya chakula.

Imetolewa na Ab van Peer kwa Max Havelaar. www.jatropha.pro

Page 2: Mwomgozo wa Jatropha corr...huku akikuza mimea ya ziada ya biashara ili kuzalisha mapato ya ziada. Ukuzaji wa Jatropha haustahili kwa njia yoyote kuvuruga mchakato huu. Kwa hivyo maelekezo

2

Maudhui: Ukurasa

Maudhui 2

Dibaji 3

Utangulizi 4

Maelezo ya mimea 5

Hali ya makuzi 6 • Udongo

• Virutubisho • Maji

• Hali joto Modeli ya upandaji tangamanifu 7 – 8

Kupanda 9

• Maandalizi ya shimo la kupanda • Kupanda

o Mbegu o Vipandikizi

o Mikoba ya sandarusi

Matunzo 10-11

• Kupalilia • Kupogoa

• Matunda • Magonjwa

Bidhaa ya Jatropha 12

______

Marejeo:

1. Kukuza Jatropha, kukijumuisha mbinu za uenezaji wa Jatropha curcas. Max Havelaar/AvP

2. Kijitabu cha mwongozo cha Jatropha. Hoja ya Msingi 3. Njugudawa-Jatropha curcas L. Inaendeleza uhifadhi na matumizi ya mazao

yanayotumika kwa kiwango cha chini na yaliyosahaulika. Joachim Heller.

4. Kijitabu cha Jatropha. Reinhard Henning

Page 3: Mwomgozo wa Jatropha corr...huku akikuza mimea ya ziada ya biashara ili kuzalisha mapato ya ziada. Ukuzaji wa Jatropha haustahili kwa njia yoyote kuvuruga mchakato huu. Kwa hivyo maelekezo

3

Dibaji

Chini ya uratibu wa Msingi wa Max Havelaar wa Uholonzi, Shirika la Fairtrade Labelling (FLO) hutekeleza uchunguzi wa uwezekanokuhusu uthibitisho wa

biashara ya haki ya Jatropha curcas L. Kuwa sehemu ya utafiti huu ni majaribio ya kilimo, yaliyotekelezwa kwa kiwango kidogo katika maeneo matatu tofauti huko

Tanzania. Huu ni “MWONGOZO WA JATROPHA KWA WAKULIMA WANAOSHIRIKI

KATIKA JARIBIO LA JATROPHA” umetolewa ili kuwazoeza wakulima

wanaohusika na maswala ya kilimo yanayohusiana na kukuza Jatropha kama zao.

Jatropha curcas L.ni mmea wa kawaida nchini Tanzania, unaotumika kuonyesha mipaka ya mashamba na makaburi. Kiasi kikubwa cha mimea kinaweza

kupatikana katika maeneo karibu na Arusha, Singida na Shinyanga, ambako mimea inatumika kuweka mipaka ili kuepuka migogoro inayohusiana na umilikaji

wa ardhi. Hata hivyo, mmea wenyewe haujawahi kupandwa kama zao.

Lengo la mwongozo huu ni mkulima anayehusika katika jaribio. Kwa ufafanuzi mkulima huyu anakuza mazao kwa matumizi yake binafsi (kilimo cha chakula),

huku akikuza mimea ya ziada ya biashara ili kuzalisha mapato ya ziada. Ukuzaji wa Jatropha haustahili kwa njia yoyote kuvuruga mchakato huu. Kwa hivyo

maelekezo ya mwongozo huu yanalenga mchanganyiko wa Jatropha na mazao ya chakula katika mbinu inayotomia vitendo sahihi vya kilimo, vikitoa mazao bora

kabisa bila ya ushindani na kupungua kwa udongo.

Maeneo hayo matatu ya majaribio yanatarajiwa, kutekelezwa, kuungwa mkono

na kufuatiliwa na wanaagronomia watatu, waliofunzwa hasa katika ujuzi wa kukuza Jatropha na kuteuliwa na mashirika husika ya wakulima wa kahawa.

Kwa KCU iliiyoko Bukoba mwanaagronomia ni Dunstan Ndamugoba na jaribio

liko katika eneo la Ruhanga (Luhanga) Kwa KNCU iliyokoMoshi mwanaagronomia ni Gerald Msilanga na jaribio liko katika

eneo la Mbosho. Kwa Kilicafe iliyoko Mbinga mwanaagronomia ni Eliud Doto na jaribio liko katika

eneo la Muhekela

Wanaagronomia hawa wanapatikana ili kuwasaidia wakulima wanaohusika na watatoa maelekezoari yoyote ya ziada ikiwa

itahitajika.

AvP. www.jatropha.pro Januari 2012

Page 4: Mwomgozo wa Jatropha corr...huku akikuza mimea ya ziada ya biashara ili kuzalisha mapato ya ziada. Ukuzaji wa Jatropha haustahili kwa njia yoyote kuvuruga mchakato huu. Kwa hivyo maelekezo

4

UTANGULIZI

Jatropha CURCAS L ni sehemu ya familia ya Euphorbiaceae. Jina hili limetokana na (Kigiriki iatros = daktari na trophe = lishe), hivyo, jina la kawaida

njugudawa (physic nut). Jina la kawaida nchini Tanzania ni Mbono, Mbono Kaburi or Mchimba Kaburi.

Jatropha ina asili ya Amerika ya Kati na Meksiko na imenawiri katika maeneo mengi ya tropiki na tropiki ndogo, yakiwemo tropiki ya Asia, Afrika, na Amerika

ya Kaskazini. Mbegu ya Jatropha curcas L. ilienezwa na wafanyabiashara wa Kireno ambao walileta mbegu katika Visiwa vya Cape Verde na. Kutokana na

athari za sumu yake na ugumu wake, ulikuwa mmea muhimu wa ua sehemu nyingi.

Miti midogo iliyokomaa huzaa maua tofauti ya kike na kiume kwa mashada, na

haiwi mirefu sana. Kama ilivyo na idadi ya nyingi ya familia ya Euphorbia, Jatropha ina misombo yenye sumu kali. Nchini Tanzania angalau spishi 12 tofauti

za Jatropha zinajulikana, miongoni mwao pia ni spishi kadhaa za mapambo. Jatropha curcas L. inatumika a.o kuzalisha mafuta ya Jatropha yasiyoliwa, kwa

kutengeneza sabuni, na kama keki ya kisibiti kwa kuzalisha mafuta na bayodizeli

(Picha:Jatropha iliyokomaa nchini Tanzania (Babati)

Kasoro Jatropha curcas L. kuna spishi nyingine nyingi:

Jatropha podagrica Mmea ulioumbwa

kama tumbo la Buddha au mmea wa

chupa, unaotumika kutia rangi ya hudhurungi kwenye ngozi na kuzalisha

rangi nyekundu nchini Meksiko na sehemu za kusini mwa Marekani.

Jatropha multifida L. au mmea wa matumbawe: maua yenye rangi ng’avu nyekundu, kama

matumbawe mekundu, yaliyoainishwa kwa matawi yenye chanjo kali.

1

2

Page 5: Mwomgozo wa Jatropha corr...huku akikuza mimea ya ziada ya biashara ili kuzalisha mapato ya ziada. Ukuzaji wa Jatropha haustahili kwa njia yoyote kuvuruga mchakato huu. Kwa hivyo maelekezo

5

Maelezo ya muundo wa mmea (imetoholewa kutoka kwa Hella-Njugudawa. (3)

Katika mazingira ya asili yake Jatropha curcas L. ni spishi inayostahimili ukame

nakukuzwa kwa wingi katika maeneo ya tropiki kama ua hai na mti wa mipaka. Sehemu nyingi za mmea zinatumika kwa madawa ya kienyeji. Mbegu nyingi,

hata hivyo, ni sumu kwa wabinadamu na wanyama wengi. Njugudawa, kwa ufafanuzi, ni mti mdogo au kichaka kubwa ambacho kinaweza

kufika urefu wa hadi mita 5-7. Ubwete na utoaji wa maua unachochewa na kubadilikabadilika kwa mvua na hali joto.

Matawi yana ulimbo wa mpira. Kwa kawaida, mizizi tano hutengenezwa kutoka kwa miche, mmoja mkuu na nne ya pembeni. Kwa kawaida mzizi mkuu

hauundwi kutoka kwa mimea inayoota kwa kuzalishwa (2). Jatropha ina matawi

yanayofanana na umbo la ndewe na urefu na upana wa sentimita 6 hadi 15, ambayo yamepangwa kwa miingiliano. Shaziua huota kwenye ncha za matawi na

kwa kawaida huwa na maua ya kike na kiume.

Jani la Jatropha Jatrophacurcas huchavuliwa na wadudu, nyenyere, nondo nk.

Bidhaa zitokanazo ya Jatropha:

Matunda

Mbegu

Maganda

Kiini

Mafuta

Matunda na mbegu 3 nyeusi (wakati mwingine 2-4), na kadiri ya mafuta ya kati

ya asilimia 32-40.

Page 6: Mwomgozo wa Jatropha corr...huku akikuza mimea ya ziada ya biashara ili kuzalisha mapato ya ziada. Ukuzaji wa Jatropha haustahili kwa njia yoyote kuvuruga mchakato huu. Kwa hivyo maelekezo

6

HALI YA KUKUZA.

UDONGO.

Kama mimea mingi, Jatropha curcas L.inahitaji maji ili kukua, ingawa mmea

hustahimili misimu mirefu ya ukame au mvua nyingi. Hata hivyo, Jatropha haistahimili maji yaliyojaa. Ni lazima aidha udongo uwe unapitisha maji au uwe

kwenye mteremko. Udongo ulio mchanga wenye maji na virutubisho ya kutosha ndio mzuri wa kukuza Jatropha lakini kwenye udongo mzito kilimo cha Jatropha

pia kinawezekana, mradi hakuna kujaa kwa maji.

Jatropha kwenye udongo wa mfinyanzi

Jatropha kwenye udongo ulio na mchanga

Virutubisho.

Jatropha itastahimili udongo mbaya na mkavu. Hata hivyo, itakuwa ni vigumu

sana kwayo kuzalisha matunda yoyote. Maji na virutubisho ni muhimu ili

kuhakikisha mavuno ya kutosha. Kwa hivyo ni lazima mbolea imwagiliwe kila mara. Mara baada ya miti kuza matunda, keki ya kisibiti inayopatikana baada ya

kusaga ni mbolea nzuri sana. (Angalia kupanda na kutunza)

Maji

Mvua ya kutosha au umwagiliaji unahitajika. Jatropha inahitaji kiwango cha chini

cha mvua cha mililita 900-1200 kwa mwaka ili kuzalisha matunda. Katika maeneo ya mvua nyingi zaidi (1200 na zaidi) ni muhimu kuwa na msimu tofauti

mkavu kwa uzalishaji wa maua. Kwa mwaka wa kwanza wa kupanda na katika maeneo yenye mvua chache umwagiliaji wa ziada (udondoshaji) unaweza

kuhitajika.

Hali joto

Jatropha ni mmea wa kitropiki. Ukuaji na uzalishaji unapungua na matukio ya

magonjwa yanaongezeka kwa haraka kwa hali joto ya chini inayosababishwa na hali ya hewa ya eneo au mwinuko.

Page 7: Mwomgozo wa Jatropha corr...huku akikuza mimea ya ziada ya biashara ili kuzalisha mapato ya ziada. Ukuzaji wa Jatropha haustahili kwa njia yoyote kuvuruga mchakato huu. Kwa hivyo maelekezo

7

MODELI YA UPANDAJI TANGAMANIFU.

Upandaji tangamanifu wa Jatropha na mazao ya chakula (au mazao ya chakula na Jatropha) si tatizo kulingana na mtazamo wa kiagronomia. Uzalishaji wa

Jatropha unaweza kuingizwa ndani ya mazao mengine kama katika mfumo wa kawaida wa kilimo cha mseto, na mahitaji na huduma yake yote. Kwahiyo,

ukuzaji wa Jatropha unastahili kwenda sambamba na vitendo bora vya kilimo kwa mazao ya chakula, kama kutumia mbegu bora,

zilizothibitishwa, kupanda kwa wakati na kwa safu, misongamano sahihi

wa kupanda, kupalilia, mbolea, nk.nk. Kwa njia hii, uzalishaji wa Jatropha utaongeza uzalishaji wa chakula pia.

Mchanganyiko wa Jatropha na mazoa mengine utaunda mfumo ambamo mimea

inafaidika mmoja kwa mwingine. Jatropha itatoa uthibiti wa mmomonyoko, hali ya hewa bora kwa eneo dogo na keki ya kibiti baada ya uzalishaji wa mafuta.

Mazao ya chakula yatafaidika kutoka kwa keki ya kisibiti na kuunda mazingira mazuri kwa wadudu ambao kwa upande wao watachavusha Jatropha itakayotoa

mazao bora.

Jinsi ya kupanga shamba la Upandaji wa Mseto.

Mkulima wa Tanzania amezoea kuchanganya mazao tofauti ya chakula. Mahindi, maharagwe na mbaazi ni mchanganyiko wa kawaida wa mazao katika shamba

moja. Hata hivyo, yote ni mazao ya mara moja kwa mwaka hivyo inamaanisha kuwa zao tangamamifu linaweza likabadilishwa kila msimu au kila mwaka. Hivi

sio ndivyo ilivyo na Jatropha, kwa sababu Jatropha ni zao la kudumu.

Page 8: Mwomgozo wa Jatropha corr...huku akikuza mimea ya ziada ya biashara ili kuzalisha mapato ya ziada. Ukuzaji wa Jatropha haustahili kwa njia yoyote kuvuruga mchakato huu. Kwa hivyo maelekezo

8

Modeli ya upandaji tangamanifu wa Jatropha ni modeli ya kudumu kwa miaka mingi. Kwa hivyo modeli hii inapaswa kutekelezwa vizuri tangu mwanzo.

• Hakikisha kuwa unamiliki haki ya shamba kwa miaka mingi ili ufaidike

kutokana na mavuno ya Jatropha • Hakikisha kuwa eneo halina makuku kabla ya kuansa kupanda.

• Mwanzo panda safu ya Jatropha. Umbali wa 2x2 kupanda katika mistari miwili. Ili kupanda kiwango cha mimea cha kuridhisha katika eneo fulani, mistari

miwili ya Jatropha inapaswa kupandwa, kama ilivyoonyeshwa kwenye mchoro

wa chini na kwenye ukurasa wa juu. Matokeo ya modeli ni umbo la vichochoro vya Jatropha (upana wa mita 4) na zao la chakula (upana wa mita 6)

• Tumia kamba kupanda Jatropha (na pia mazao ya chakula) kwa safu nyoofu,

hii inawezesha utunzaji na upandaji tangamanifu. Katika maeneo ya milimamilima Jatropha inapaswa kupandwa kwenye mitaro.

Modeli hii inahakikisha kuwa asilimia 40 ya shamba pekee inatumika kwa

Jatropha na asilimia 60 inapatikana kwa mazao ya chakula. Majaribio nchini Tanzania yalidhitisha kuwa wanaweza kufidia kwa urahisi hasara ya shamba la

uzalishaji wa chakula kwa mavuno zaidi kupitia kwa vitendo halisi vya kilimo.

Page 9: Mwomgozo wa Jatropha corr...huku akikuza mimea ya ziada ya biashara ili kuzalisha mapato ya ziada. Ukuzaji wa Jatropha haustahili kwa njia yoyote kuvuruga mchakato huu. Kwa hivyo maelekezo

9

KUPANDA

Maandalizi ya shimo la kupanda

Jatropha inaweza kupandwa kutokana na mbegu, miche na vipandikizi. Katika

hali yote mashimo ya kupanda yanapaswa kuandaliwa mapema. Mashimo ya kupanda yanapaswa kuwa na ukubwa wa ujazo wa takribani lita 20-30 (sentimita

30x30x30) na kujazwa na udongo wa eneo hilo, uliochanganywa na angalau kilo 1 ya mbolea mahuluku au keki ya kisibiti ya Jatropha iliyochachushwa.

Tengeneza vyema mashimo ya kupanda mapema kabla ya wakati wa kupanda, ili kuunyausha mchanganyiko wa udongo shimoni. Umbali kati ya mashimo ya

kupanda unategemea modeli ya kupanda. Kwa ua panapaswa kuwa na sentimita 30 kati ya mimea. Kwa upandaji tangamanifu hii inapaswa kuwa mita 2x2 na

safu mbili. (Angalia modeli ya upandaji tangamanifu)

Mbegu. Kilo moja ya mbegu za Jatropha ina mbegu 1200-1400. Mbegu hazistahili

kuhifadhiwa na kutumiwa baada ya miezi 6. Iwapao unakusanya mbegu kimaeneo, chukua tu mbegu kutoka kwa mimea iliyo na matunda mengi.

Alamisha mimea hiyo ukiiona shambani kwa ajili ya matumizi ya baadaye.

Upandaji mbegu wa moja kwa moja Mbinu ya upandaji mbegu wa moja kwa moja ni rahisi sana na ya gharama nafuu

ya kuanzisha mashamba ya Jatropha. Pia hutoa mmea bora sana kwa siku za baadaye, kwa sababu miche inakua na mzizi kuu na kwa hivyo ni lazima iweze

kustahimili misimu ya ukame.

Upandaji wa mbegu wa moja kwa moja Upandaji wa mikoba ya sandarusi

Juu ya upandaji wa moja kwa moja wa mbegu ni mbinu inayojulikana sana na wakulima wengi, kwa sababu mahindi na mazao mengine yanapandwa kwa njia

hiyo. Tumia mbegu 2 kwa kila shimo la kupanda na uondoe miche hafifu sana

baada ya kuota. Upandaji wa mbegu moja kwa moja unawezekana tu kwa muda fulani kukiwa na mvua (zaidi ya miezi 2)

Upandikizi wa moja kwa moja

Chukua vipandakizi vya urefu wa takriban sentimita 40 na mduara wa hadi sentimita 3 kutoka kwa misitu inayojulikana kuzalisha sana ya Jatropha. Panda

vipandikizi hivi kwa urefu wa sentimita 20 katika mashimo ya upandaji yaliyotayarishwa awali wakati mvua ni nyingi. Tengeneza vipandikizi kutoka

Page 10: Mwomgozo wa Jatropha corr...huku akikuza mimea ya ziada ya biashara ili kuzalisha mapato ya ziada. Ukuzaji wa Jatropha haustahili kwa njia yoyote kuvuruga mchakato huu. Kwa hivyo maelekezo

10

kwenye matawi ya Jatropha iliyo na gome la rangi ya kijivu, kwa sababu

matawi yakiwa mabichi yataoza au kukauka.

Upandaji wa moja kwa moja

Wakati maji sio hoja, miche ya Jatropha inaweza kupandwa kwa matuta na baada

ya miezi miwili kungo’olewa ili kupandwa moja kwa moja shambani.

Hii ni njia rahisi sana ya kukuza miche nyingi ya Jatropha katika eneo ndogo.

Miche iliyopandwa kwenye mikoba ya sandarusi au vipandikizi.

Tumia mchanganyiko wa udongo, mchanga na mbolea kujaza mikoba ya sandarusi (2-2-1). Panda kindakizi kimoja au mbegu moja na umwage maji kwa

kiasi. Itachukua takriban miezi miwili kukuza mmea wa Jatropha ambao uko tayari kupandikizwa. Upandaji wa kutumia mikoba ya sandarusi ni ghali zaidi

kuliko upandaji wa moja kwa moja, lakini mimea huishi vyema katika misimu mikavu.

Katika hali yote, mwagilia vipandikizi moja kwa moja baada ya kupanda ikiwa

hakuna mvua.

UTUNZAJI

Kupalilia

Baada ya kupanda, kupalilia wakati wa miezi ya awali ya ukuaji ndiyo shughuli

muhimu sana ya udumishaji, kwa sababu mimea midogo ya Jatropha haiwezi kushindana na magugu.

Kupogoa

Wakati mimea ya Jatropha imefikia urefu wa magoti, sehemu ya juu inastahili kukatwa ili kuendeleza uzalishaji wa matawi. Upogoaji wa pili unastahili kufanywa

kwa urefu wa kiuno wa tatu katika urefu wa mabega. Upogoaji unahitajika ili kupata matawi mengi iwezekanavyo, kwa sababu maua yanakua tu juu ya tawi.

Upogoaji unastahili kufanywa kabla tu ya kuanza kwa msimu wa mvua. Tumia

makasi au kisu kikali.

Umepogolewa tu siku 14baada ta kupogoa. Hakuna kupogoa

Page 11: Mwomgozo wa Jatropha corr...huku akikuza mimea ya ziada ya biashara ili kuzalisha mapato ya ziada. Ukuzaji wa Jatropha haustahili kwa njia yoyote kuvuruga mchakato huu. Kwa hivyo maelekezo

11

Wakati mimea imekomaa, upokogoaji unastahili kufanywa mara kwa mara, ili kuizuia hiyo misitu dhidi ya kuwa mirefu sana au kuzeeka sana. Ili kuepuka

matatizo ya kuchuma weka mpaka wa urefu wa mti wako kwa mita mbili kwa kupogoa mara kwa mara.

Matunda

Kulingana na hali ya hewa, Jatropha itaanza kuzaa matunda kwa mwaka wa kwanza au wa pili baada ya kupanda. Hata hivyo itachukua miaka 4-5 kupata

mazao mazuri. Mlimbuko na wingi wa mavuno unaweza ukaboreshwa ikiwa mimea ya Jatropha inapokea mbolea kila mwaka. Wakati uzalishaji uko kwenye

mpangilio, mboloea nyingi inaweza kubadilishwa na keki ya kisibiti. Keki ya kisibiti inaweza pia kutumika kwa mmea tangamanifu.

Kuchuma Matunda.

Inachukua karibu siku 80 hadi 100 kutoka kwa kuchanua maua hadi kwa matunda yaliyokomaa.

Matunda yaliyokomaa huwa yenye rangi ya njano na nyeusi na yanaweza kuchumwa kwa urahisi kwa

kutumia mkono.

Kukausha matunda

Baada ya kukusanya, matunda yanapaswa kukaushwa

kwa siku 3-4 ili kupunguza unyevu na kuwezesha uondoaji wa maganda. Ukaushaji wa matunda kwa ajili

ya uzalishaji wa mafuta unaweza kufanywa kwenye jua kali. Kukausha matunda kwa ajili ya uzalishaji

kunapaswa kufanywa katika eneo kavu na lenye kivuli; kamwe sio kwenye jua kali.

Magonjwa.

Kuna baadhi ya wadudu na magonjwa yanayoshambulia mimea ya Jatropha na matunda, hasa ikiwa changa. Katika mfumo wa upandaji wa mseto hili kwa

kawaida haliwi tatizo, isipokuwa kama hali ya kukuza sio nzuri. Ikiwa magonjwa yanaenea kwa haraka sana, hatua mwafaka inastahili kuchukuliwa.

Magonjwa au wadudu wa kawaida nchini Tanzania ni Mende mwenye rangi ya Dhahabu, Ukungu na mdudu wa rangi mbalimbali.

Nyenyere

Ukungu

Page 12: Mwomgozo wa Jatropha corr...huku akikuza mimea ya ziada ya biashara ili kuzalisha mapato ya ziada. Ukuzaji wa Jatropha haustahili kwa njia yoyote kuvuruga mchakato huu. Kwa hivyo maelekezo

12

Uharibifu wa mende Mende Mdudu wa rangi mbalimbali

BIDHAA YA JATROPHA

Lengo kuu la kupanda Jatropha ni kuzalisha mafuta kutoka kwenye mbegu.

Mafuta yanaweza kutumika kwa injini ya kawaida, mwangaza na uzalishaji wa sabuni na kwa uzalishaji wa biodizeli.

Utafiti wa kijeografia unachunguza ikiwa uzalishaji na uuzaji wa mbegu na uzalishaji na uuzaji wa mafuta na mapato ya ziada unaweza ukatekelezwa kwa

kiwango cha muungano mkuu.

TAHADHARI: MAFUTA YA JATROPHA NI SUMU NA HAYAWEZI KUTUMIKA KAMA MAFUTA YA KUPIKIA.!!

Keki ya kisibiti ya Jatropha Mafuta ya Jatropha Sabuni ya Jatropha

Ili kuzalisha kiwango kikubwa cha mafuta, vitoaji mafuta vinahitajika.

Keki inayobaki baada ya mchakato wa utoaji mafuta ni mbolea kaboni nzuri sana

(baada ya kuchachusha), uzuri wake ni sawa sawa na inawezekana ikawa ni bora kuliko mbolea mahuluku. Keki vilevile inaweza kutumika kama nishati wakati

inaminywa kuwa kama tofali.

____________