Nafasi za masomo Charles de Foucauld High Schoo6

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Nafasi za masomo kwa mhula wa 2013/14

Citation preview

  • Charles de Foucauld High School

    P.O.Box 15873 Arusha.

    Phone: 0764 722 365/0754 499 113

    Email: [email protected]

    TANGAZO

    NAFASI ZA MASOMO KWA KIDATO CHA TANO MWAKA 2013: KLF, HKL.

    Shule ya sekondari CHARLES DE FOUCAULD HIGH SCHOOL yenye namba za usajili S. 4523, inatangaza

    nafasi za masomo ya kidato cha 5 kwa wanafunzi wenye sifa za kujiunga na kidato cha 5, michepuo ya KLF

    na HKL. Masomo yataanza mwezi wa saba 2013.

    CHARLES DE FOUCAULD HIGH SCHOOL ni shule ya bweni kwa wavulana na wasichana. Ina mazingira

    mazuri na tulivu ya kusoma, ina viwanja vya michezo, pia ina vitabu vya kutosha vya kiada kwenye maktaba

    ya shule.

    Shule inafundisha lugha tatu: Kiswahili, Kingereza na Kifaransa ambazo zitawezesha wanafunzi kuingia

    katika soko la ajira ndani ya nchi, katika ukanda wa Afrika Mashariki na duniani.

    Wanafunzi wote (pamoja na wa mchepuo wa HKL) watasoma Kifaransa na wataweza kupata Diploma ya

    Kifaransa ambayo inatambulika kimataifa.

    Wanafunzi watakaohitimu kidato cha sita wataweza kujiunga na Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi.

    Fomu za maombi ya kujiunga zinapatikana kwa Tsh 15,000/= sehemu zifuatazo:

    . ARUSHA: Gaimo construction company- Moshono 0754 499 113.

    . DAR ES SALAAM:Chuo Kikuu (Tanzania Fisheries Research Institute-Kunduchi)-0784 515 893/0715 262

    142.

    . MOSHI: Roman catholic bookshop 0756 751 748.

    . MWANZA: Kanisa Katoliki Nyakato 0756 090 464.

    . TANGA: - 0753 993 716.

    . SHULENI: Charles de Foucauld High SchooL - 0764 722 365/0754 499 113.

    Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 30 Juni 2013.

    MAHALI ILIPO: CHARLES DE FOUCAULD HIGH SCHOOL ipo katika Manispaa ya Arusha, kijiji cha Olkereyan

    karibu na eneo jipya la Shule ya Arusha Modern School. Unapitia Njiro karibu na kituo kikuu cha umeme

    Tanesco cha Njiro. Ni 3.5 km tu kutoka hapo Tanesco Njiro mpaka shuleni.

    Kwa maelezo zaidi fika shuleni au piga simu: 0764 722 365/0754 499 113 saa za kazi au kwa email ya

    shule: [email protected]