12
Tafiti za Equator Initiative Mbinu endelevu za kienyeji zenye ufumbuzi wa maendeleo kwa watu, mazingira asili na jamii zinazohimili matatizo Kenya NORTHERN RANGELANDS TRUST Empowered lives. Resilient nations.

NORTHERN RANGELANDS TRUST - Youth Space Network · 2016. 7. 30. · New York, N.Y. MUHTASARI WA MRADI Northern Rangelands Trust ni mtandao wa uhifadhi wa jamii 27 - ambazo kwa pamoja

  • Upload
    others

  • View
    0

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: NORTHERN RANGELANDS TRUST - Youth Space Network · 2016. 7. 30. · New York, N.Y. MUHTASARI WA MRADI Northern Rangelands Trust ni mtandao wa uhifadhi wa jamii 27 - ambazo kwa pamoja

Tafiti za Equator InitiativeMbinu endelevu za kienyeji zenye ufumbuzi wa maendeleo kwa watu, mazingira asili na jamii zinazohimili matatizo

Kenya

NORTHERN RANGELANDS TRUST

Empowered lives. Resilient nations.

Page 2: NORTHERN RANGELANDS TRUST - Youth Space Network · 2016. 7. 30. · New York, N.Y. MUHTASARI WA MRADI Northern Rangelands Trust ni mtandao wa uhifadhi wa jamii 27 - ambazo kwa pamoja

MSURURU WA TAFITI ZA UNDP EQUATOR INITIATIVEJamii asili za kienyeji kote duniani zinaendeleza ubunifu na ufumbuzi wa maendeleo endelevu yenye manufaa kwa watu na mazingara asili. Machapisho machache au tafiti za masomo huhadithia kwa ukamilifu jinsi mipango hufuka, upana wa athari zao, au jinsi zinazobadilika kwa mda. Wachache pia ndio wanasimulia hizi hadithi zikiongozwa na wafanyikazi maarufu katika jamii. Equator Initiative inalenga kuziba pengo hili.

Ushirikiano baina ya UNDP’s Equator Initiative na ENDA Tiers Monde (ENDA), Open Society Initiative for Southern Africa (OSISA), United Nations Convention to Combat Desertification (UNCCD) na kufadhiliwa na Global Environment Facility (GEF), mifano inayotambulika ya kinyumbani , uvumbuzi, na uongozi katika Sustainable Land Management (SLM) katika maeneo kame ya jangwa la Sahara. Utafiti huu ni moja wapo ya msururu unazoelezea vitendo bora zaidi katika usimamizi wa SLM ambao umechunguzwa na kupitiwa na wataalamu wa kimasomo wa rika moja, kwa lengo la kuhamazisha mjadala wa sera zinazohitajika kuchukua mafanikio ya kienyeji kwa kiwango cha juu, kuboresha msingi wa maarifa duniani juu ya mazingira ya kienyeji na ufumbuzi wa maendeleo ya jamii, na kutumika kama mfano mzuri wa kuigwa.

Bonyeza katika ramani ya miradi ya Equator ili upate kupata habari zaidi.

WahaririMhariri Mkuu Joseph CorcoranMhariri Msimamizi: Alan PierceMhariri Aliyechangia: Eva Gurria

Waandishi waliochangiaAlan Pierce, Eva Gurria, Annie Virnig, Elizabeth Shaw, Anthony von Arx, Joshua Voges, Qiang Li, Kathryn McCann

UbunifuKimberly Koserowski

ShukraniEquator Initiative inatambua na kuthamini Northern Rangelands Trust. Picha zote ni kwa hisani ya Northern Rangelands Trust, Ian Craig, Sophie Harrison, Juan Pablo Moreiras, Joanna O’Brien, na Charlie Pye Smith. Ramani kwa hisani ya CIA World Factbook na Wikipedia. Tafsiri kwa hisani ya Donald Odhiambo na marekebisho ya tafsiri kwa hisani ya Alex Omari.

Mtajo uliopendekezwaUnited Nations Development Programme. 2015. Northern Rangelands Trust, Kenya. Msururu wa tafiti za Equator Initiative. New York, N.Y

Page 3: NORTHERN RANGELANDS TRUST - Youth Space Network · 2016. 7. 30. · New York, N.Y. MUHTASARI WA MRADI Northern Rangelands Trust ni mtandao wa uhifadhi wa jamii 27 - ambazo kwa pamoja

MUHTASARI WA MRADI Northern Rangelands Trust ni mtandao wa uhifadhi wa jamii 27 - ambazo kwa pamoja zimekwea kilomita 31,000 za mraba ya ardhi kaskazini mwa Kenya - zinazoendesha harakati za uhifadhi wa jamii asilia katika mstari wa mbele wa udhibiti wa shamba, uhifadhi wa wanyamapori na mbinu endelevu ya mifugo. Ikisaidia zaidi ya wanachama 315,000 wa hifadhi, ‘Trust’, pia imesaidia kukabiliana na matatizo sugu ikianza na ukame, mgogoro wa kikabila, ukosefu wa huduma za serikali kama vile afya na elimu na uwindaji haramu wa wanyamapori.Mapato mapya yanayopatikana kwa njia ya maisha mseto na kuboresha usimamizi wa ardhi yameelekezwa katika elimu ya kikwetu na miundo mbinu ya afya. Maelfu ya hekta za malisho zilizoharibiwa zimerejeshwa, na shahada ya amani na utulivu wa kiuchumi imeanzishwa katika mkoa huu wenye historia tete.

MAMBO MUHIMUMshindi wa Tuzo la Equator: 2014

Ilianzishwa: 2004

Eneo: Kaskazini mwa Kenya

Walengwa: Wahifadhi wa jamii 27, watu 315,000

Bioanuwai: Nyanda za marejesho; na hatari ya wanyama-pori maarufu wa Afrika.

3

YALIYOMO

Usuli na mukhtadha 4

Shughuli muhimu na Uvumbuzi 5

Athari 7

Athari za viumbe hai 7

Athari za kiuchumi na jamii 7

Jinsia 9

Athari za Sera 9

Udumishaji endelevu 10

Uigizaji 10

Washirika 11

NORTHERN RANGELANDS TRUSTKenya

Page 4: NORTHERN RANGELANDS TRUST - Youth Space Network · 2016. 7. 30. · New York, N.Y. MUHTASARI WA MRADI Northern Rangelands Trust ni mtandao wa uhifadhi wa jamii 27 - ambazo kwa pamoja

44

Hifadhi za Northern Rangeland Trust (NRT) zimekwea - 31,000 kilomita za mraba - na miziki ya kiikolojia katika eneo la kaskazini mwa Kenya, ambayo ni kati ya mazingira ya pwani – ikiwa pamoja na fukwe, miamba ya matumbawe, milango ya mito, mikoko iliyosimama na misitu kando ya mito - bara na nyasi kwa mabonde, kiwara, misitu asili na milima. Spishi zinazopatikana katika hifadhi ya pwani ya NRT ni mbega nyekundu wa mto Tana na Mangabey aliyehatarishwa huko mto Tana. Eneo hilo pia ni nyumbani kwa nguva waliokuwa katika mazingira ngumu na spishi kadhaa wa aina ya kasa baharini. Wanyamapori maarufu wa Afrika wanaopatikana kwa hifadhi ya malisho ya NRT ni pamoja na; tembo, simba, duma, chui, twiga, kiboko, swala twiga, choroa na swala pala. Aina fulani za spishi zilizo na shaka katika uhifadhi ni; mbwa mwitu wa Afrika aliye hatarini na pundamilia wa Grevy, hirola aliyehatarishwa zaidi na vifaru weusi; aina ya mwisho ya spishi wamefugwa tena katika hifadhi ya Sera.

Hifadhi ya jamii za Northern Rangeland Trust zimejumuisha makundi 16 tofauti ya kikabila Wengi wa wanachama hao ni wafugaji au wanaofanya kilimo na ufugaji, ingawa uvuvi ni maisha bora katika hifadhi ya pwani. Licha ya utofauti wa makazi, makabila na maishilio, wanajamii katika hii Hifadhi wanashirikiana katika uzoefu kadhaa wa kawaida kwamba maisha ya kijijini, maeneo ya ukame na nusu ukame - yaani ukame unaokuja mara kwa mara, huduma duni za afya na upeo mdogo wa huduma za serikali.Maisha chaguzi yamekuwa na upeo mdogo sana na viwango vya umaskini kati ya baadhi hifadhi nchini iko katika kiwango cha juu zaidi. Utapiamlo umeenea, na usajili katika shule za msingi kaskazini mwa Kenya ni asilimia 25 tu, na kati ya hao, wasichana waliohudhuria ni wachache sana. Kuongezea matatizo haya, ghasia za kikabila, wizi wa mifugo, jambazi wenye silaha, na windaji haramu wa pembe za ndovu yamekithiri katika eneo hili kwa miongo kadhaa.

Usuli na mukhtadha

Page 5: NORTHERN RANGELANDS TRUST - Youth Space Network · 2016. 7. 30. · New York, N.Y. MUHTASARI WA MRADI Northern Rangelands Trust ni mtandao wa uhifadhi wa jamii 27 - ambazo kwa pamoja

5

Shughuli muhimu na uvumbuzi

Ujumbe wa kauli ya Northern Rangeland Trust ni “kuendeleza uhifadhi wa jamii aspringi yenye kubadilisha maisha, amani thabiti na kuhifadhi rasilimali.” Kuelekea tamati, shirika hili linastawisha maendeleo vijijini, ajira za ndani, ushirikiano azimio, marejesho ya makazi na mipango ya kupambana na ujangili. NRT inasaidia maisha ya wafugaji wa mifugo kwa njia ya ununuzi wa moja kwa moja wa mifugo kutoka kwa mwanachama wa hifadhi. Mkakati huu huwapa wanachama mathubuti, faida katika soko ya mifugo tegemezi na wakati huo huo kuzungumzia ubora na upatikanaji wa nyanda za malisho kwa mifugo na wanyamapori.

Mfano wa Hifadhi ya Jamii

Northern Rangelands Trust ni shirika ambalo limejumuisha mashirika mengi na hutoa msaada, uongozi, mafunzo na utaalamu wa kiufundi kwa uhifadhi wa jamii.Hifadhi za jamii kwa jumla zinamilikiwa na kusimamia ardhi ambazo utekeleza uhifadhi na mbinu endelevu ya usimamizi wa ardhi. Hifadhi ya jamii ni huru, taasisi iliyosajiliwa kisheria na bodi ya wakurugenzi iliyochaguliwa kidemokrasia. Bodi ya wakurugenzi kwa kawaida na memba kumi na mbili na huchaguliwa kutoka mikoa ndani ya kila mipaka ya Hifadhi. Bodi hii ya hifadhi pia inajumuisha wanachama wadhifa wa NRT, Shirika la Kenya la Wanyamapori na maafisa wa serikali.Katika kila hifadhi, bodi huajiri meneja, wanamgambo na watawala, na imeteua kamati ya kusimamia malisho, utalii na shughuli za fedha.Wajumbe wa bodi hufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu na jukumu lao ni kusimamia bajeti ya hifadhi. Bajeti ukaguliwa kwa ukinaifu kila mwaka ili kuhakikisha uwazi.Kila hifadhi inaweka sahii mkataba wa makubaliano na Northern Rangelands Trust uelezea usimamizi wa vitendo kama inavyotarajiwa.

Utawala wa jamii ya Northern Rangelands Trust unaitwa Baraza la Wazee. Wengi wa almashauri ujumuisha wenyekitiwa hifadhi waliochaguliwa, kisha wakilishi kutoka shirika la Kenya la wanyamapori, almashauri za mitaa kata, shirika lisilo la serikali, na sekta ya kibinafsi hujiunga nayo. Baraza la Wazee hufanya mapitio ya utendakazi wa wanachama wa hifadhi na kuhakikisha kuwa wao huambatana na viwango na kanuni za NRT. Baraza la wazee pia huteua wanachama wanane kati ya wanachama 15 wa Bodi ya wakurugenzi ya NRT.

Usimamizi za nyanda ya malisho kwa kiujumla

Ufugaji umekuwa njia ya maisha kwa vizazi vingi katika eneo la kaskazini mwa Kenya, lakini kuongezeka kwa idadi ya watu sehemu hii, mifugo wengi, mvua bovu, ukame na kuchubuliwa kwa malisho umechangia maeneo makubwa ya malisho kuharibika, na kuyafanya yasiwe maeneo stahiki kwa mifugo na wanyamapori. Utafiti uliofanywa mnamo 2014 na World Agroforestry Centre uligundua kwamba asilimia 70 ya maeneo ya malisho katika hifadhi ya NRT yameharibiwa sana, na zaidi ya asilimia 50 ya eneo lina momonyoko wa udongo. Kupunguka kwa ubora wa maeneo ya nyanda za malisho umeleta athari kubwa katika maishilio na umesababisha migogoro kati ya makundi ya wafugaji kuhusu maeneo bora ya malisho yaliyobaki.Katika mwaka wa 2008, NRT ilitekeleza majaribio ya mpango wa usimamizi wa malisho ya mifugo kwa lengo la kupunguza migogoro na kurejesha maeneo ya nyanda za malisho ya mifugo na wanyamapori. Kilichowatia motisha wafanyakazi wa NRT na wanachama wenyeji wa hifadhi hilo ni ziara ya mafunzo kule

Page 6: NORTHERN RANGELANDS TRUST - Youth Space Network · 2016. 7. 30. · New York, N.Y. MUHTASARI WA MRADI Northern Rangelands Trust ni mtandao wa uhifadhi wa jamii 27 - ambazo kwa pamoja

6

ranchi ya Dimbangombe eneo la kaskazini mwa Zimbabwe, walianza kazi wakishirikiana na wafugaji 20 na ng’ombe 200 kwa kipande cha shamba cha hekta 1,200 katika hifadhi ya West Gate.

Badala ya kuruhusu malisho ya mifugo kila mahali, mifugo wanaweza kuvinjari daima, maeneo makubwa bila kuruhusu muda uliyoshamiri malishoni (kama ilivyofanywa kale), mifugo walisanywa kwenye sehemu chache za malisho.Hapa ng’ombe walifugwa, wakakanyaga na kufinyilia udongo kwa kwato zao na wakaweka mbolea kwa kiwango ambacho kilifanya udongo uwe na rutuba. Baada ya muda, ng’ombe walihamishwa hadi sehemu nyingine mpya huku maeneo yaliyotumiwa hapo awali kulishia ng’ombe yakiachwa bila kulimwa ili kuruhusu nyasi kumea tena. Kurejeshwa kwa maeneo yenye nyasi ya kudumu iliwezesha mbinu ya kulisha ng’ombe kwa mzunguko kati ya sehemu za malisho, na katika nyanda za malisho ziliboreshwa zaidi na mimea vamizi aina ya mikambala kuondolewa.Halikadhalika, nyanda zilizotengwa zilitengenezwa hili kuweka hakiba ya nyasi” ya mifugo na wanyamapori katika kipindi cha ukame.Nyanda za malisho ziliboreshwa kwa kiasi kwamba ng’ombe zaidi ya 300 waliletwa katika eneo lilo hilo mwaka uliofuata. Ubora wa malisho katika kipande cha shamba cha majaribio kulileta matokeo ya kukuzwa kwa ng’ombe wanene, wenye afya nzuri ambao bei yao sokoni ilizidi ya ng’ombe waliolishwa kwa mfumo wa kale na kiasi kinachoweza kutoshana na dola themanini za marekani kwa kila ng’ombe. Mbinu hii ya ujumla kwa ukarabati wa nyanda za malisho hatimaye imekumbatiwa na hifadhi kadhaa za NRT.

Kuboresha usalama

Kaskazini mwa Kenya mna historia ya vurugu, hivi majuzi ikianzishwa na hali ya heka heka baina ya makabila na kuwepo wa silaha za AK-47 ambazo zinapatikana kwa urahisi, na zinaingizwa humu nchini kutoka nchi ya Somalia kinyume cha sheria. Matukio ya wizi wa mifugo wa kila mara, uwindaji haramu na ujambazi katika barabara kuu umechangia kujenga sifa ya uhalifu katika eneo hili basi kufanya usalama kuwa kipao mbele kwa wahifadhi wa NRT. Akisafiri hivi karibuni kwa safari ya kuelekea kwa hifadhi ya NRT ya kaskazini mwa Kenya, Titus Letaapo, mratibu wa ardhi za malisho za Northern Rangelands Trust, alisisitiza ukali wa ghasia katika eneo hilo.

“Kama tungekuja hapa miaka michache iliyopita, tungekuwa katika hatari kubwa ya kuuwawa na majambazi au wezi wa ng’ombe. Hata tembo alijua hili eneo sio salama. Kama wao wangepitia hapo usiku, wangekuwa wakikimbia.Twiga, swala twiga na pundamilia wote waliuawa kuwa kitoweo.Siku hizo zilikuwa nyakati nzuri kwa tai. “

Kuyatatua matatizo ya usalama, NRT iliweka mpango wa wanamgambo katika Hifadhi. Tangu mwaka 2010, zaidi ya wanamgambo 330 wa Hifadhi wameelimishwa na huduma kwa wanayamapori wa Kenya katika huo mkongamano wa ekevu, ufuatiliaji wa wanyamapori, kusimamia hali ya kupambana na usanifu wa vichaka. Baadhi ya wanamgambo wamepewa cheo cha polisi wa kawaida na kuruhusiwa kubeba silaha amabazo serikali iliwapa.Wanagambo wahifadhi wana jukumu la kulinda wanyamapori na kudhibiti migogoro.Wakati ambapo hifadhi ina makundi mawili au zaidi ya kikabila, hifadhi kuhakikisha usawa baina ya makabila na timu ya mgambo.

Timu 9-1, ni jina lililopewa baada ya ishara ya radio yao; ni timu ya wasomi wa usalama iliyoundwa kwa kuajiri wakurutu kutoka NRT Sera, Biliqo-Bulesa, Namunyak na hifadhi ya Melako. Ilianzishwa kwa ajili ya ombi la wakilishi wa wanajamii na makabila mbalimbali ya jeshi la usalama ili kushughulikia unyanyasaji wa muda mrefu katika eneo hilo.Timu 9-1 ilielimishwa katika uga wa; matumizi ya silaha, shughuli za wanachama wa polisi wa kawaida wa Kenya, huduma ya Kenya kwa wanyamapori na Afisa wa zamani wa Jeshi la Uingereza kupeana huduma ya kwanza.

Utofauti wao wa makabila mbalimbali umewezesha timu kupata imani na akili kutoka kwa wanakijiji wanaoishi katika hifadhi ambazo wanapiga doria.Tangu kuajiriwa katika sehemu hiyo, matukio ya ujangili, ujambazi wa barabara na wizi wa mifugo umepungua.Kwa sababu ya mahusiano yao ya karibu na polisi wa kawaida, wanachama wa timu 9-1 wameonekana kama polisi wa jamii zote mbili na walezi wa wanyamapori.Mafanikio ya timu 9-1 imesababishwa kuundwa kwa timu 9-2 aambayo inafanya kazi na hifadhi huko kusini mwa mto Ewaso Nyiro .

NRT pia imeunda timu ya Utatuzi wa Migogoro ambayo kazi yake ni kujenga mazingira ya amani kati ya makundi ya kikabila na jamii.Timu hii inaongozwa na mkuu wa mstaafu mwandamizi na wazee tisa wanaojulikana kwa ujuzi wao katika utatuzi wa migogoro.Timu hii hupatanisha migogoro ya masuala kama vile; haki ya kulisha mifugo, haki ya kutumia maji au mzozo wa uchaguzi , na husaidia kwa hila ufumbuzi wa pande nzuri na migogoro, mara nyingi kusababisha kuundwa kwa sheria mpya au memoranda ya uelewano. Zaidi ya suluhisho la Migogoro ya timu hii, NRT iliapisha mashindano ya mbio ya Kom Peace mwaka wa 2011. Malengo ya mbio hizo yalikuwa kujenga tukio la kuruhusu makabila mbalimbali kutoka hifadhi tano kuja pamoja, kuwasiliana na kutangamana.Kwa baadhi ya washindani, ilikuwa ni uzoefu wao wa kwanza wa mazungumzo na wanachama wa makabila mengine. Mbio ya kwanza ilikuwa yenye mafanikio na iliitishwa tena mwaka uliofuata.Usiku kabla ya mbio, wanariadha wadogo walikula chakula kwa pamoja, waliiambiana hadithi, walicheza na kuimba pamoja.Mikutano kama hiyo yenye usawa wa makabila mbalimbali ingekuwa haina dhamira katika miaka michache iliyopita. Hakika, watu 15 waliuawa wakati wa ghasia za kikabila katika Kom mwaka wa 2009. Akizungumza kuhusu mbio, Mohammed Jirma, mgambo kutoka hifadhi ya Biliqo-Bulesa, alisema: “Hili ni jambo nzuri sana, kuona vijana hawa kutoka makabila mbalimbali kujumuika pamoja. Jambo moja la hakika - kama tuna amani, ni kwa sababu vijana wanataka amani. “

Page 7: NORTHERN RANGELANDS TRUST - Youth Space Network · 2016. 7. 30. · New York, N.Y. MUHTASARI WA MRADI Northern Rangelands Trust ni mtandao wa uhifadhi wa jamii 27 - ambazo kwa pamoja

7

Athari

ATHARI YA VIUMBE HAIWengi wa wanyamapori nchini Kenya huishi nje ya maeneo rasmi ya ulinzi, na takribani robo ya idadi ya wanyamapori nchini huishi ndani ya misitu na maeneo ya malisho ya kaskazini mwa Kenya.Kwa hiyo, uhifadhi wa jamii ya Northern Rangelands Trust ina jukumu kuu la kuhifadhi wanyamapori nchini.Mradi wa usimamizi wa malisho ya NRT unakarabati makazi ya wanyamapori. Kwa sasa, zaidi ya hekta milioni 1.8 za ardhi katika hifadhi 14 nchini zimeboreshwa na huo mradi wa usimamizi wa malisho ya NRT.Marejesho ya nyasi kunawiri umewaleta wanyama kama vile choroa na pundamilia wa Grevy aliye hatarini kwa maeneo waliohofia kuwa na ukosefu wa lishe hapo awali. Utafiti wa hivi majuzi unaonyesha ya kwamba idadi ya spishi muhimu za wanyamapori zinaongezeka na kuwa imara katika hifadhi nyingi za NRT, minghairi ya simba, ambao mara nyingi uuwawa na wafugaji.Wanamgambo wa hifadhi wa timu 9-1 na 9-2 wamechangia katika uboreshaji wa usalama wa wanyamapori.Kwa mfano, tangu mwaka 2012, asilimia 43 ya ujangili umepungua dhidi ya windaji haramu wa ndovu katika mashamba ya hifadhi.

Pia, NRT imeunga mkono utekelezaji wa miradi inayolenga aina ya spishi waliomo hatarini. Mpango wa ukarabati wa malisho ya hifadhi ya NRT, ikihusisha mradi wa tamasha la chanjo ya kimeta, yamefanya idadi ya pundamilia wa Grevy kuongezeka. Leo, karibu asilimia 60 ya pundamilia wote wa Grevy waliobaki wanapatikana katika shamba la Hifadhi ya jamii ya NRT. Katika mwaka wa 2012, hifadhi ya Ishaqbini ilitenga 3,000 hekta iliyojengwa ua kuzuia kongoni kuliwa na mnyama mla nyama.Kuanzia na idadi ya wanyama 48, idadi ya watu imesitawi, ikiongezeka kwa asilimia 22 kila mwaka.Katika 2014, Sera ilianzisha jumuiya ya kwanza iliyomiliki vifaru weusi katika Afrika Mashariki.Vifaru 15 weusi wamekuwa wakiletwa na hifadhi ya Sera, eneo ambapo walizurura mara moja.Vifaru hao hufanyiwa sikio-kipembe kwa ajili ya kuwatambua na pembe zao zimewekwa transmita.Maskauti 24 watakaofuatilia vifaru watapewa mafunzo maalum ya kuangalia hilo eneo na kushirikiana na polisi wa kawaida wa kulinda mbuga hiyo, kwa kuongezea msaada unaopeanwa na huduma ya Wanyamapori ya Kenya na timu ya usalama ya NRT.

ATHARI ZA KIUCHUMI YA JAMII Wanachama wa hifadhi ya Northern Rangelands Trust wanatekeleza shughuli ambazo zinaleta ajira za kawaida, kuboresha usalama, kuzalisha kwa misaada ya kifedha kwa shirika la vijana, kuwapa wanawake mamlaka na kujenga miundombinu muhimu kama vile shule, vituo vya afya na visima.Marejesho ya makazi, maisha bora na miundombinu bora inatia jamii ujasiri na mabadiliko ya tabia na huongeza ustawi wa jamii.

Kukuza utawala bora

Utawala bora hutoa msingi kwa ajili ya hifadhi na ufanisi wa jamii. Ni muhimu kwa kuleta usaidizi wa jamii, kuhakikisha usalama na kukuza maendeleo ya jamii na uhifadhi.Kila mwaka NRT hupata alama ya juu ya utendaji hifadhi dhidi ya seti ya vigezo ambayo hupima: 1) uwajibikaji, uwakilishaji, uwazi na usawa; 2) usimamizi wa fedha, mahusiano ya wafadhili na mchango; na 3) shughuli za hifadhi. Utaratibu wa kupata

Page 8: NORTHERN RANGELANDS TRUST - Youth Space Network · 2016. 7. 30. · New York, N.Y. MUHTASARI WA MRADI Northern Rangelands Trust ni mtandao wa uhifadhi wa jamii 27 - ambazo kwa pamoja

8

alama nzuri hutoa uchambuzi wa haraka kwa jimbo la utawala bora katika hifadhi na pia husaidia NRT kuweka msaada kipaumbele katika hifadhi.Hifadhi yenye nafasi ya juu hutambuliwa na tuzo la hifadhi ya Northern Rangelands Trust. Ingawa alama ya utawala imeboresha idadi ya hifadhi, changamoto kubwa hubaki, ikizingatia ukosefu wa uwezo wa ndani na ukabila unaoendelea na mabishano ya jamii.Tisho la milele linaoleta changamoto kwa utawala ni vurugu.Mnamo 2014 , kuongezeka kwa wizi wa mifugo ulishuhudiwa kwa kasi na idadi ya watu waliouawa katika matukio ya kukosekana kwa usalama, ikiwa pamoja na hasara ya milele ya kwanza ya NRT Rangers (wawili waliuawa wakati walikuwa wakifuatilia matukio mawili tofauti ya wizi wa mifugo).

Kutengeza fursa za ajira

Moja ya malengo muhimu zaidi ya NRT ni kuonyesha jinsi uhifadhi unaweza kutoa faida kwa wanachama.Bila kuona moja kwa moja faida ya maisha kutokana na uhifadhi, jumuiya ina motisha ndogo ya kuboresha maeneo ya malisho au kulinda wanyamapori. Kwa sababu hiyo, imejenga ajira za ndani, uchumi wa mseto na husaidia maisha ya mashambani ambayo ni muhimu kwa uhifadhi wa wanyamapori kaskazini mwa Kenya.Katika 2014, hifadhi na biashara zinazowiana ziliajiri watu 765 wanaofanya kazi kila siku,na 641 wafanyakazi wa muda mchache. Utalii umezalisha zaidi ya ajira 186 kwa wanachama wa hifadhi.Kazi hizi ni uthibitisho kwamba uhifadhi unaweza kutewa mtambo wa kiuchumi. Hizi ajira pia hujenga uwezo muhimu ndani ya hifadhi.

Utalii

Utalii ni muhimu na ni chanzo cha kuongezeka kwa mapato kwa hifadhi ya NRT. Hivi sasa, hifadhi kumi za NRT angalau huwa na nafasi ya kituo moja cha utalii, wakati mwingine hifadhi kadhaa hupokea msaada wa fedha kutoka kwa vyumba vya kulala vya watalii katika hifadhi jirani.Baadhi ya vyumba hivo vya kulala vimeshiriki katika soko kuu ya mwisho ya utalii, lakini pia imejumuisha baadhi ya utalii wa kitamaduni ambayo unahusisha mitaa.Katika 2014, utalii ulichangia milioni 47.6 shilingi za Kenya (461,000 dola za marekani) kwa hazina ya hifadhi.Faida kutokana na utalii inatumika kusaidia shule kwa kuwapa misaada ya kifedha (zaidi ya 1,000 ya misaada ya kifedha zilitolewa mwaka 2011), mishahara ya mgambo, utengezaji wa barabara na gharama msingi ya hifadhi.

Mradi wa soko la hisa la Mifugo la NRT

NRT imetengeneza mradi wa soko l mifugo ili kutuza hifadhi ambazo zimetekeleza mazoea ya nyanda za malisho kwa jumla na shughuli nyingine muhimu ya uhifadhi. NRT hulipa bei nzuri na ya haki sokoni ili kupata ng’ombe, na moja kwa moja hununua wanyama kutoka kwa wafugaji katika hifadhi iliyo na bidii.Ununuzi wa moja kwa moja wa ng’ombe huokoa wafugaji kutoka mchakato mgumu wa ng’ombe sokoni, ambayoni gharama kubwa, hatari na mara nyingi husababisha upungufu wa uzito kwa mifugo.Baada ya kununuliwa na NRT, ng’ombe hutengwa katika hifadhi ya wanyamapori ya Lewa, na baadaye kunoneshwa na kuchinjwa katika hifadhi ya Ol Pejeta.Mpango huu hutuza usimamizi endelevu wa maliasili na huwapa wafugaji faida ambayo hawangeweza kupokea katika soko hilo la nje.Wafugaji wameukaribisha mpango huo lakini wanajua vyema kwamba ushiriki wao utatokana na utendaji wao wa Hifadhi. Nura Ali, mchungaji kutoka kijiji cha Dima-Ado, anahitimisha hali hiyo kwa njia hii: “Sisi tuna

uwezo wa kuwa kwa huu mradi kama usimamizi wa hifadhi utafanyika vizuri na kuwachunga wanyamapori. Kama hatutaweza haya, basi NRT haitanunua ngombe wetu.”Faida kutokana na uuzaji wa mifugo unajumuisha gharama ya biashara ya NRT na kuweka tayari chanzo cha mapato kwa hifadhi.Katika 2014, kaya ya wafugaji 1063 ilichuma milioni 68.3 shilingi za Kenya (660,000 USD) kutokana na mauzo ya ng’ombe.Takwimu hii inawakilisha ongezeko la asilimia 300 kutoka mwaka uliopita na kutabiri vizuri upanuzi wa kuendeleza huo mradi.

Biashara ya NRT

Mnamo mwaka wa 2006, Northern Rangelands Trust ilianzisha biashara; mfumo wa maendeleo ya biashara ambao unasaidia wanajamii wa hifadhi hiyo katika uzalishaji na uuzaji wa bidhaa zilizotengenezwa kienyeji kama vile shanga na ufundi (katika mwaka wa 2014, biashara ya NRT ilipata hadhi isiyoisha). Hadi sasa, biashara ya NRT imetoa mafunzo kwa wanawake zaidi ya 900 katika nyanja za ufundi, uhasibu, uuzaji na uongozi. Mnamo mwaka 2013, mauzo ya shanga na bidhaa za ufundi yalileta karibu milioni moja dola za marekani, yakitoa mapato madhubuti kwa wanawake hao.Wanawake ambao walifanikiwa kumaliza mafunzo ya uhasibu na biashara ya NRT wanahitimu kupata mikopo kupitia mipango ya mikopo midogo midogo. Utaratibu huu wa kutoa fedha huwapa wanawake fursa ya kuanzisha biashara ndogo ndogo na vyanzo mbalimbali vya mapato. Baada ya kipindi cha miezi miwili, wanawake hao lazima walipe mkopo huo katika kipindi cha mwaka mmoja kwa riba ya asilimia 5.Kufikia sasa, hakuna hata kikundi kimoja cha wanawake ambacho kimekosa kulipa mkopo.Wanawake wengi wametumia mikopo yao kuanzisha biashara za ufundi, huku wengine wakianzisha maduka ya rejareja, ushonaji na buchari.Mwanamke mmoja alitumia mkopo wake kununua chombo cha nishati ya Jua na kuanzisha biashara ya kuchaji simu katika kijiji chake.Maisha ya wanawake yanabadilika kutokana na uwezo wao wa kupata fedha kwa njia tofauti tofauti.Hafaro Galimogle, mwenyekiti wa kikundi cha wanawake katika Laisamis, kwa hifadhi ya Melako , alisema: “Katika siku za awali, ilikua lazima tuwaulize waume wetu fedha ili kununua bidhaa zetu au za watoto wetu.Lakini sasa tuna fedha zetu, tunaweza kulipa karo ya watoto wetu na kununua vyakula bora.”

Page 9: NORTHERN RANGELANDS TRUST - Youth Space Network · 2016. 7. 30. · New York, N.Y. MUHTASARI WA MRADI Northern Rangelands Trust ni mtandao wa uhifadhi wa jamii 27 - ambazo kwa pamoja

9

JINSIANRT inahimiza uundaji wa makundi ya wanawake katika hifadhi hizo.Leo, kuna wanawake 2,235 katika makundi 135 ya hifadhi 12.Mengi ya makundi ya wanawake hupata elimu kupitia kwa miradi ya mafunzo ya biashara za NRT.NRT inahimiza hifadhi za wanachama kujumuisha wanawake katika timu za ukurugenzi na usimamizi, lakini hadi sasa, wanawake wachache tu wametwaa majukumu ya uongozi.Hivi majuzi, Mikakati ya NRT iliyochapishwa ilionyesha kiwango cha chini cha uwakilishaji wa wanawake katika majukumu ya kufanya maamuzi katika hifadhi kama udhaifu wa shirika. Akizungumza kuhusu umuhimu wa kujumuisha wanawake katika uhifadhi ya mazingira na utatuzi wa migogoro, Beatrice Lempaira, ambaye ni meneja wa hifadhi ya jamii ya Naibunga, alisema:

“Uwakilishaji wa wanawake katika hifadhi za NRT umekuwa chini sana na mtindo huu unafaa kubadilika. Wanawake wana jukumu muhimu katika mustakabali wa hifadhi ya jamii.Mwanzo, wanaunda uwiano unaofaa wa idadi ya watu katika hifadhi ya jamii ya NRT, na wao hutangamana na rasilimali yao ya asili kila siku. Wao huelewa mazingira, na huwa na maarifa ya kipekee ya jadi.Pia, ingawa wanaume hawawezi kubali kamwe, wanawake wana jukumu la kuunganisha jamaa zao. Wanawake wanaweza kuwa vyombo dhabiti vya utatuzi wa migogoro. “

Ili kufanikisha uwezo mkubwa wa wanawake, mitazamo ya muda mrefu ya utamaduni na desturi katika mkoa, ikiwa pamoja na ndoa

za kulazimishwa za wasichana wadogo, kazi ya kutengeza shanga na ukeketaji, ni lazima kushughulikiwa. Kuhusu suala hili, NRT inashirikiana na Samburu Girls Foundation kufanya warsha za mitaa ili kuwawezesha wanawake, kuhamasisha jamii kuhusu tamaduni mbaya, kupeana mafunzo ya uongozi na utawala, na kuhamasisha wanajamii kuwa mabingwa kwa uwakilishi sawa na elimu ya wasichana wadogo.

ATHARI YA SERANorthern Rangelands Trust na Jumuiya ya hifadhi ya jamii ya Kenya inang’ang’ania kutambuliwa kwa hifadhi ya jamii kwa miaka na serikali. Mnamo Desemba 2013, juhudi za NRT za kushawishi uhifadhi wa wanyama pori zilifanikishwa baada ya bunge kupitisha muswada huo. Wiki mbili baadaye muswada mpya wa Wanyamapori ulitiwa saini na rais, kuwa sheria.Muswada huo unawezesha uhifadhi wa jamii kutambuliwa kisheria na umetenga viti viwili katikia bodi ya Shirika la Wanyamapori la Kenya, na hivyo kutoa fursa kwa jamii kushiriki katika usimamizi na maamuzi kuhusu wanyama pori. Sheria hiyo inatoa mwito wa ugatuzi wa usimamizi wa wanyamapori kupitia kuundwa kwa kamati za uhifadhi za wanyamapori na fidia. Masharti zaidi ya sheria ni pamoja na: kuanzishwa kwa majaliwa ya kusaidia uhifadhi nje ya hifadhi za taifa; kuanzishwa kwa fedha za fidia katika jamii kutokana na vifo, majeruhi au uharibifu wa mali uliosababishwa na wanyamapori; na uwekaji wa adhabu kwa uwindaji haramu.

“Usimamizi bora wa maeneo ya malisho - ambayo inajumuisha mipango madhubuti ya malisho iliyoanzishwa na bodi hifadhi - maana yake ni kwamba wanyamapori na mifugo watafaidika.

Wingi wa wanyamapori unahimiza utalii, ambao kwa upande mwingine unaimarisha miseto ya riziki mbalimbali miongoni mwa wanajamii wengine.”

Northern Rangelands Trust

Page 10: NORTHERN RANGELANDS TRUST - Youth Space Network · 2016. 7. 30. · New York, N.Y. MUHTASARI WA MRADI Northern Rangelands Trust ni mtandao wa uhifadhi wa jamii 27 - ambazo kwa pamoja

10

UDUMISHAJI ENDELEVUWanachama wote wa hifadhi 27 ya jamii ya Northern Rangeland Trust wanategemea sana fedha za wafadhili, ambazo zinapatikana kupitia NRT.Maendeleo ya utalii na soko ya mifugo imeweka hifadhi kwa mapato ya maduhuli, sehemu ambayo hutumiwa kufadhili shule za mitaa, vituo vya afya, na gharama za kuendeshaji Hifadhi, ikiwa ni pamoja na mishahara ya wanamgambo na urekebishaji wa magari.Maboresho katika hali ya malishoni inaruhusu wafugaji kupanua makundi ya ng’ombe na idadi ya mifugo wanaouzwa kwa NRT, kuongeza zaidi kwa mapato ya jamii ya mwaka.Kurejeshwa kwa hali nzuri ya maeneo ya malisho umevutia zaidi ya wanyamapori, kupanua chaguzi za maendeleo ya utalii kwa jamii. Malipo ya Huduma ya mazingira ina uwezo wa kuongeza mapato kwa hifadhi katika siku zijazo.Kwa mfano, Hifadhi ya Ngare Ndare imepata mapato ya shilingi milioni 6.1 za Kenya (59,000 dola za Marekani) katika mwaka wa 2014 kwa minajili ya kulinda huduma ya maji.Hifadhi inayoboresha maeneo ya malisho yao inaweza kupata mapato ya ziada kutoka soko la kaboni. Hadi sasa, mapato ya kibiashara yanayotokana na utalii, mifugo na shirika la malipo ya mazingira limerudisha kati ya asilimia 12 na 18 ya gharama za uendeshaji wa hifadhi ya jamii kila mwaka.Mbali na kutekeleza mipango iliyoundwa na kufikia kiwango fulani cha uchumi ili kujitosheleza miongoni mwa wanachama wa hifadhi, NRT inanuia kukuza jamaa endelevu kwa muda mrefu kwa njia ya kukuza utawala bora na utatuzi wa migogoro.

UIGIZAJINorthern Rangelands Trust ni kiongozi katika usimamizi wa maliasili ya kijamii. Kanuni zake za utahirisho, ikiwa pamoja na utawala bora, maisha nyumbufu, usalama, uhifadhi na maendeleo vijijini, umekuwa ukipitishwa na kutumika kwa juhudi za hifadhi ya jamii barani Afrika.Nchini Kenya, jamii huendelea kujongea katika shirika kwa ajili ya mwongozo na ufadhili.Mnamo mwaka 2013, hifadhi saba mpya za jamii zilianzishwa kwa ufadhili wa NRT,ikisababisha uanzishaji wa makao makuu ya kimwezi kwa hifadhi sita kwenye ukanda wa pwani ya kaskazini ya Kenya, sasa inafanya kazi ikitumia jina NRT-Coast.

Munira Bashir, ambaye ni mkuu wa viwanda vya jamii katika shirika la wanyama pori la kenya anaunga mkono kazi ya NRT na angependa kuiona ikiongezeka zaidi:”Sisi tunaangalia NRT kama mfano wa kusaidia hifadhi, na tunatarajia kuona kitu kinachofaa kuigwa katika maeneo mengine ya nchi. “

Hivi majuzi, Northern Rangelands Trust imetengeneza mfumo wa kufuatilia usimamizi wa hifadhi, mfumo huu hauna gharama ya kufuatilia mabadiliko mengi ya wanyamapori katika hifadhi.Mfumo wa ufuatiliaji unatekelezwa na wanamgambo wa hifadhi ambao huweka maeneo pembejeo halisi ya mandhari ya wanyamapori katika kihisio.Basi wanamgambo wanapokea mafunzo ya kompyuta na kufundishwa jinsi ya kuandaa histogram na ramani.Leo, zaidi ya wanamgambo 200 wanakusanya takwimu kila siku katika hekta

Udumishaji endelevu na Uigizaji

Page 11: NORTHERN RANGELANDS TRUST - Youth Space Network · 2016. 7. 30. · New York, N.Y. MUHTASARI WA MRADI Northern Rangelands Trust ni mtandao wa uhifadhi wa jamii 27 - ambazo kwa pamoja

1111

milioni moja.Mpango huu umeonyesha kwamba gharama ya ufuatiliaji jamii wa wanyamapori ni wa kiwango cha chini na unaweza kuleta habari za kuaminika.Takwimu kutoka mfumo wa ufuatiliaji sasa unatumika kama sehemu ya mradi wa ufuatiliaji wa mauaji haramu ya tembo ya CITES .Mfumo wa ufuatiliaji unaonyesha uwezekano mkubwa wa kuigwa humu nchini na dunia kwa kuwa na juhudi za hifadhi ya kijamii ikishirikiana katika usimamizi wa wanyamapori.

WASHIRIKAKatika muongo uliopita, Northern Rangelands Trust imeunda ushirikiano muhimu kwa zaidi ya mataifa 35 na mashirika ya serikali, misingi, mbuga za wanyama, na mashirika yasiyo ya kiserikali. Kusaidia shughuli za msingi na mipango mikubwa imetolewa na Shirika la Kimataifa la msaada ya Marekani (USAID), shirika la kimataifa ya maendeleo ya Kifaransa (AFD), Idara ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID), na maendeleo ya kimataifa ya Uholanzi na ubalozi wa Denmark.Asili ya hifadhi na chama ya kimataifa ya wanyama na mimea imeweka ufadhili katika shirika na utaalamu wa kiufundi na pia hutumika kama taasisi ya wanachama

kwenye bodi ya NRT. Msingi wa kimataifa wa tembo unauunga mkono NRT kwa juhudi za kupambana na ujangili, hasa vitengo 9-1 na 9-2 inayopambana na ujangili. Usalama wa Tusk Trust fund na shughuli za mgambo kama vile gharama msingi za matumizi ya mwanachama wa hifadhi ya NRT ya jamii.Wale waliochangia katika uanzishaji wa hifadhi ya vifaru ya Sera imejumuisha shirika la Marekani la Wanyamapori na Samaki na, Hawksford Foundation na Lundin Foundation. Ushirikiano na mbuga ya wanyama ya Victoria inayopatikana Australia imepata mkondo muhimu kwa shanga na ufundi zinazozalishwa na biashara za NRT. Kufanya kazi kwa ushirikiano baina ya wahifadhi wa Wanyamapori wa Lewa na hifadhi ya Ol Pejeta imeimarisha shughuli za usalama na mpango mifugo ya NRT. Chuo Kikuu cha Purdue, USA, na Chuo Kikuu cha Egerton Kenya, vimetoa utaalamu wa kiufundi na kisayansi kwa mradi wa usimamizi wa malisho, hasa kwa heshima na mahusiano kati ya mifugo na wanyamapori. Mashirika ya kiserikali ni pamoja na shirika la msitu na shirika la wanyama pori nchini Kenya, na shirika la pili limeshikilia kiti katika bodi ya NRT. Orodha kamili na maelezo kuhusu washirika wanaotoa misaada kwa NRT inapatikana katika mtandao: hapa.

“Haiwezekani kutia chumvi umuhimu kwamba NRT unahusisha na kuhamasisha mahusiano mazuri kati ya makabila. Huanza na kuhamasisha mazungumzo kupitia mikutano ya amani na

wazee wa makabila jirani, ambao wengi wao wamekubali kamwe kuwa hawangesalimiana kwa mikono miaka michache iliyopita. Basi ni kwajili ya utawala bora wa hifadhi ambayo jamii

inahisi hali ya umiliki wa.” Northern Rangelands Trust

Page 12: NORTHERN RANGELANDS TRUST - Youth Space Network · 2016. 7. 30. · New York, N.Y. MUHTASARI WA MRADI Northern Rangelands Trust ni mtandao wa uhifadhi wa jamii 27 - ambazo kwa pamoja

Equator InitiativeSustainable Development ClusterUnited Nations Development Programme (UNDP)304 East 45th Street, 6th Floor New York, NY 10017Tel: +1 646 781-4023 www.equatorinitiative.org

UNDP wanashirikiana na watu katika matabaka yote ya jamii ili kusaidia kujenga mataifa ambayo yanaweza kuhimili matatizo, na kuendeleza na kudumisha usitawishaji ambao unaboresha thamani ya maisha kwa kila mtu. Katika nchi na maeneo zaidi ya 170, tunatoa mtazamo wa kimataifa duniani na umaizi wa kienyeji ili kusaidia kuwezesha maisha na kujenga mataifa yanahimili matatizo.

Equator Initiative inaleta pamoja Umoja wa Kimataifa, serikali, vyama vya kiraia, biashara na mashirika ya ngazi ya chini ili kut-ambua na kuendeleza ufumbuzi wa kienyeji na maendeleo endelevu kwa watu, mazingira asili na jamii zinazohimili matatizo.

©2016 Equator Initiative Haki zote zimehifadhiwa

KUMBUKUMBU ZAIDI ■ Tovuti ya Northern Rangelands Trust. Inapatikana katika mtandao hapa

■ Kanda ya Northern Rangelands Trust. Inapatikana katika mtandao hapa

■ Uhifadhi wa Wanyamapori Kenya na muswada wa usimamizi wa mwaka wa 2013. Inapatikana katika mtandao hapa

WASHIRIKA WA MRADI

WASHIRIKA WA EQUATOR INITIATIVE

Empowered lives. Resilient nations.

Empowered lives. Resilient nations.