40
M W O N G O Z O W A M A F U N Z O Y A U Z A L I S H A J I W A M A Z A O Y A M B O G A M B O G A November, 2019 KITINI NAMBA 2:

November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

  • Upload
    others

  • View
    6

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

MWONGOZO WA MAFUNZO YA UZALISHAJI WA MAZAO YA MBOGAMBOGA

November, 2019

KITINI NAMBA 2:

Page 2: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa
Page 3: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

ii

YALIYOMO

1. KILIMO BORA CHA NYANYA ............................................................................................... 1

1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA ......................................................................................... 1

1.2 AINA ZA NYANYA ................................................................................................................ 1

1.3 UKUZAJI WA MICHE YA NYANYA ..................................................................................... 1

1.4. UTUNZAJI WA ZAO LA NYANYA ...................................................................................... 1

1.5. WADUDU WAHARIBIFU.................................................................................................... 3

1.6 MAGONJWA YA NYANYA .................................................................................................. 5

2. KILIMO BORA CHA NYANYA CHUNGU ............................................................................ 9

2.1. UTANGULIZI ........................................................................................................................ 9

2.2. AINA ZA NYANYA CHUNGU ............................................................................................ 9

2.3. HALI YA HEWA .................................................................................................................. 9

2.4. UTAYALISHAJI WA SHAMBA .......................................................................................... 9

2.5. UTAYALISHAJI WA MBEGU NA KUPANDA ................................................................... 9

2.6. MATUNZO YA SHAMBA ................................................................................................. 10

2.7 MAGONJWA NA WADUDU .............................................................................................. 10

2.8. UVUNAJI ............................................................................................................................ 10

3. KILIMO BORA CHA BILINGANYA ..................................................................................... 11

3.1. UTANGULIZI ....................................................................................................................... 11

3.2. MAHITAJI YA ZAO KATIKA UZALISHAJI ...................................................................... 11

3.3. KUTUNZA SHAMBA......................................................................................................... 12

3.4. WADUDU WAHARIBIFU NA MAGONJWA. .................................................................. 13

4. KILIMO BORA CHA PILIPILI HOHO ................................................................................. 15

4.1. UTANGULIZI ......................................................................................................................... 15

4.2. UCHAGUZI WA ENEO ................................................................................................. 16

4.3. UANDAJI WA SHAMBA NA UPANDAJI ......................................................................... 16

4.4. KUTUNZA SHAMBA .................................................................................................... 18

Page 4: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

iii

4.5. MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU ............................................................... 18

5. KILIMO BORA CHA MATANGO ....................................................................................... 22

5.1. UTANGULIZI ..................................................................................................................... 22

5.2. AINA ZA MATANGO ....................................................................................................... 22

5.3. MATUMIZI ....................................................................................................................... 22

5.4. UDONGO NA HALI YA HEWA ....................................................................................... 22

5.5. UPANDAJI ......................................................................................................................... 22

5.6. MATUNZO YA MATANGO ............................................................................................. 23

5.7. MAGONJWA ..................................................................................................................... 23

5.8. WADUDU ......................................................................................................................... 24

5.9. KUVUNA ........................................................................................................................... 25

6.1 UTANGULIZI ..................................................................................................................... 26

6.2 UANDAAJI WA SHAMBA ................................................................................................ 26

6.3 UOTESHAJI ....................................................................................................................... 26

6.4 KUTUNZA SHAMBA ........................................................................................................ 27

6.5. MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU: ................................................................. 27

6.6. KUVUNA........................................................................................................................... 29

7. KILIMO BORA CHA VITUNGUU ........................................................................................... 30

7.1 UTANGULIZI ...................................................................................................................... 30

7.2 KUCHAGUA ENEO ........................................................................................................... 30

7.3 KUOTESHA MBEGU KATIKA KITALU ........................................................................... 30

7.4 KUTAYARISHA SHAMBA ................................................................................................. 31

7.5 KUPANDIKIZA ................................................................................................................... 31

7.6 KUTUNZA SHAMBA ........................................................................................................ 32

7.7 MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU ................................................................... 32

Page 5: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

1

1. KILIMO BORA CHA NYANYA

1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa maua na matunda. Zao hili hupenda kipindi kirefu cha jua na joto ili kuongeza ukuaji wa matunda na kupunguza magonjwa ya aina ya ukungu/kuvu. Zao hili halipendi mvua nyingi ingawa linahitaji maji kwa wingi. Katika kipindi chenye mvua nyingi na jua kidogo nyanya hushindwa kutoa maua na matunda ya kutosha bali huweka majani mengi. Katika kipindi hiki pia, nyanya hushambuliwa sana na magonjwa ya ukungu. Nyanya hupendelea udongo unaopitisha maji kwa urahisi na wenye rutuba ya kutosha na hivyo hupenda samadi /Mboji. Udongo uwe umetifuliwa vya kutosha kuruhusu mizizi kushika vema.

1.2 AINA ZA NYANYA Kuna aina kuu mbili za nyanya kulingana na ukuaji wa mmea: yaani nyanya inayo refuka zenye kuhitaji egemezi (mfano Money maker) na aina ya pili ni nyanya fupi zenye kutoa matawi mengi mfano Roma na Cal J.

1.3 UKUZAJI WA MICHE YA NYANYA Miche ya nyanya huzalishwa kwenye kitalu kwa kupanda mbegu. Mbegu za nyanya huota baada ya siku 5 hadi 10. Baada ya kukua kitaluni kwa muda wa wiki 4 hadi 5 toka kuota kwa mbegu, miche hupandwa shambani. Kabla ya kupandikiza shambani miche huandaliwa kwa kupunguza umwagiliaji maji kwa siku moja au mbili ili miche izoee hali ngumu kabla ya kuhamishiwa shambani.

Hapo shambani miche hupandikizwa kwa kuzamishwa katika kina kirefu zaidi ya ilivyo kuwa kitaluni. Hii inasaidia miche kutoa mizizi ya pembeni mingi zaidi kwa ajili ya kufyonza maji pamoja na virutubisho aridhini. Baada ya kupandikiza mwagilia maji ya kutosha. Usimwagilie maji juu ya mche wa nyanya. Katika kipindi cha jua kali, tandaza nyasi kwenye tuta ili kupunguza upotevu wa maji na unaweza kuweka kivuli kwa kutumia majani ya miti au migomba.

Kulingana na aina ya nyanya na rutuba ya udongo, nafasi ya kupandia ni sm 60 kati ya mstari hadi mstari na 45 hadi 60 nafasi ya mche hadi mche. Kama udongo hauna rutuba ya kutosha inapendekezwa kutumia nafasi kubwa ya kupanda 60 kati ya mstari hadi mstari na 60 kati ya mche hadi mche.

1.4. UTUNZAJI WA ZAO LA NYANYA Nyanya fupi zisizo refuka kwenda juu, ni rahisi sana kutunza na hazihitaji huduma nyingi. Tatizo kubwa ni kukua kwa kutambaa chini, katika kipindi cha mvua huwa karibu na magonjwa yatokanayo na udongo. Katika kipindi cha jua kali, matunda huungua kwani mmea huwa na majani machache tu yanayo kinga matunda yasipigwe na mionzi ya jua.

Page 6: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

2

1.4.1 Mbolea Licha ya mbolea ya kupandia kama mboji au samadi, unashauriwa kuongeza mbolea kipindi cha wiki mbili au tatu baada ya kupandikiza miche bustanini. Mbolea hii ya kukuzia (hususani chai ya mimea/samadi iwekwe kuzunguka shina la mmea. Mbolea hii inaweza kuwekwa mara mbili kabla ya mvuno wa kwanza.

Ili kurefusha kipindi cha uzaaji wa zao la nyanya (na hata mazao mengine yatoayo matunda kama vile nyanya chungu, biringanya, pilipili hoho, nk) inapaswa kuongezea chai ya mimea/samadi katika kipindi cha uvunaji mfano baada ya kuvuna mara mbili unashauriwa kuongeza mbolea ya samadi au chai ya mboji. Hii inasaidia mmea kuendelea kutoa maua bila kuchoka. Kwa kawaida nyanya fupi jamii ya “Roma” huweza kuzaa na kuvunwa kwa kipindi cha wiki 6 hadi 8 tu. Lakini kama utakuwa unaongezea mbolea na kukazania matunzo ya bustani (hasa usafi wa bustani na kumwagilia maji ya kutosha), nyanya zinaweza kuendelea kuzaa kwa muda mrefu zaidi. Hii ni tofauti na mazoea ya wakulima wengi kuwa mara nyanya zianzapo kuzaa huduma za palizi na usafi wa shamba huachwa na kutilia maanani kazi ya kuvuna pekee. Hii inajitokeza zaidi kwenye aina ya nyanya fupi.

Kwa nyanya fupi ni vizuri kuhakikisha kuna matawi mengi iwezekanavyo ili kuweza kupata matunda mengi zaidi. Hivyo usipunguze matawi katika aina hii ya nyanya. Kwa nyanya ndefu zenye kuhitaji egemezi, tunashauriwa kukuza nyanya kwa tawi moja lisilo na vichipukizi pembeni au matawi mawili na kuacha mnyanya urefuke.

Kupunguza majani ni muhimu pia katika kupunguza maambukizo ya ukungu katika shina na pia kutoa nafasi ili mwanga kupenya na kuruhusu mzunguko wa hewa. Majani yapunguzwe kipindi cha asubuhi kwa kutumia mkono na siyo kisu kwani kinaweza kueneza magonjwa kutoka mche hadi mche.

Kwa nyanya ndefu, majani ya chini ya matunda huondolewa kadiri unavyo endelea kuvuna. Unashauriwa usitoe zaidi ya majani matatu katika mmea kwa mara moja.

1.4.2 Umwagiliaji wa nyanya Nyanya ni zao linalohitaji maji mengi sana kwa ajili ya ukuaji wa mmea na matunda yake. Umwagiliaji uwe wa kulingana kwa kila siku iliyo pangwa. Usibadilishe ovyo kiasi cha maji na ratiba ya kumwagilia. Hii inasababisha kuoza kwa kitako cha nyanya. Pia ili kutunza maji katika udongo, inashauriwa kuweka matandazo katika mzunguko wa shina la nyanya au bustani yote. Nyanya inayokua vizuri hutumia maji lita mbili kwa siku katika kipindi cha jua kali.

Katika umwagiliaji ni busara kuzingatia kiasi hiki cha maji katika kipindi kama hiki. Pia kama unatumia keni, mpira au bomba usimwagilie maji juu ya matawi ya nyanya kwani umwagiliaji wa namna hii utasababisha kuenea kwa magonjwa ya ukungu.

Page 7: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

3

1.5. WADUDU WAHARIBIFU

1.5.1. Kantangaze (tuta absoluta) Funza huyu ni mdudu kama kipepeo ambae hutaga mayai juu ya majani. Mayai yakianguliwa hutokeza funza ambao huanza kula shina kutokea juu ya majani hadi ndani ya shina kufwata uelekeo wa mizizi. Vilevile mdudu huyu huharibu matunda na kadri anavyoendelea kula shina anaendelea kukua na kubadilika kuwa buu. Baada ya muda mfupi huwa mdudu kamili (kantangaze) ambae ataruka kwenda kutaga mayai sehemu nyingine. Ili kumdhibiti kantangaze pulizia dawa yenye mchanganyiko wa Mwarobaini na pilipili au mwarobaini pekee kabla ya mashambulizi ili kukinga mimea.

1.5.2. Funza wa vitumba (American bollworm) Huyu funza hushambulia mazao mengine kama vile pamba, mahindi, mtama, maharage n.k. Mdudu huyu hushambulia matunda ya nyanya kwa kutoboa na hivyo kuyafanya yapoteze soko kwasababu hayafai kuuzwa katika soko na pia yanaweza kuoza wakati wa usafirishaji.

Ili kuthibiti piga dawa ya kudhibiti wadudu kama Muarobaini au mchanganyiko wa mwarobaini na pilipili katika kupunguza uharibifu wa mdudu huyu.

Page 8: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

4

1.5.3. Inzi weupe Wadudu hawa huruka ruka kwenye shamba la nyanya na kukaa chini ya majani. Mdudu huyu hueneza magonjwa ya virusi kama vile “ukoma wa nyanya”. Usafi wa shamba na mazingira yake ni muhimu katika kupunguza kuzaana kwa wadudu hawa.

Ili kudhibiti wadudu hawa kwenye bustani ya mboga na pia katika maficho yao, piga dawa za wadudu kama vile mwarobaini na pilipili mara kwa mara. Panda mimea mingine inayo vutia wadudu hawa kwenye maeneo ya bustani ili kuwadhibiti kwa wingi kwenye eneo dogo.

1.5.4. Minyoo fundo (Nematodes) Mdudu huyu hukaa kwenye udongo wenye unyevu wa kutosha. Huvamia mizizi ya nyanya na kuharibu mfumo wa usafirishaji maji na chakula kwenye nyanya iliyo athirika. Uking'oa mche wa nyanya utaona vifundo kwenye mizizi.

Kuzuia Mbinu za kuthibiti ongezeko la wadudu hawa ni kuharibu hali ya udongo inayo mfanya aishi na kuzaana. Mbinu hizi ni:

Kulima shamba kwa kutifua baada ya kuvuna nyanya ili udongo wa chini ukae juani na kukauka. Hii inasaidia kuangamiza wadudu hawa kwa joto na ukosefu wa maji. Chimba shimo refu na kufukia mabaki ya nyanya baada ya kuvuna. kuzungusha aina ya zao la nyanya au jamii ya nyanya na mazao mengine yasiyovamiwa na adui huyu. Hii huwafanya minyoo wasipate hifadhi na chakula kutoka kwenye mimea wanayo tumia kuishi na kuzaliana. Hivyo idadi yao kupungua katika udongo. kabla ya kupanda zao weka samadi nyingi katika udongo kwenye eneo lililoathiriwa na wadudu hawa kwani hawapendi udongo wenye samadi nyingi. Panda mibangi pori (Tagetes spp) au marejea katika eneo lililoathirika na minyoo hawa, mimea hii hutoa sumu ya aina fulani ambayo huathiri ukuaji na kuzaliana kwa minyoo hawa.

1.5.5. Sota (cutworm) Hawa ni funza wakubwa wenye rangi ya kijivu. Hupendelea kujichimbia katika udongo wakati wa mchana na kujitokeza wakati wa usiku au asubuhi sana kukata miche michanga karibu na usawa wa ardhi. Zuia wadudu hawa kwa kutumia majivu au dawa yenye mchanganyiko wa mwarobaini na pilipili kali mara baada ya kupanda. Kama mche utakatwa mtoe mdudu kwa kumfukua na kumuua kisha pandikiza mche mwingine. Njia nyingine ya kumzuia mdudu huyu ni kuweka shamba na mazingira yake katika hali ya usafi ili wasiweze kuzaliana kwa wingi. Ikiwezekana tifua udongo bila ya kupanda zao lolote kwa muda wa mwezi mmoja

1.5.6. Utitiri (Red spider mites) Hawa ni wadudu wadogo vyenye rangi ya machugwa yalioiva, nyekundu au kahawia. wadudu hawa hushambulia kwa kufyonza utomvu chini ya majani Majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya njano na hukunjamana, hukauka na hatimaye kufa. Dhibiti kwa kutumia dawa zilizotengenezwa na utupa au mwarobaini na pilipili.

Page 9: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

5

Utitiri na utando wao (kushoto) na nyanya iliyoharibiwa na utitiri (Kulia)

1.5.7. Vidukari /wadudu mafuta (aphids) Ni wadudu wadogo wenye rangi kijani, nyeusi au kahawia. Baadhi yao wana mabawa na wengine hawana. Hufyonza utomvu wa majani na kusababisha mmea kudhoofu, kudumaa, majani, kunyauka na hukauka. Zuia kwa kutumia dawa za kilimo hai kama vile mwarobaini na utupa mchanganganyiko wa mwarobaini na pilipili zinazowasha.

1.6 MAGONJWA YA NYANYA Uchunguzi umeonyesha kuwa katika maeneo mengi, nyanya na mazao mengine jamii ya nyanya ndiyo hushambuliwa sana na magonjwa kuliko mazao mengine ya mboga.

1.6.1 Ukungu Huu ni ugonjwa unaopenda hali ya unyevu mwingi hewani. Hivyo hujitokeza zaidi wakati wa masika. Pia sehemu zenye umande mwingi wakati wa usiku, ugonjwa huu hujitokeza hata wakati wa kiangazi.

Dalili zake Ugonjwa huu hushambulia shina, maua na matunda. Kuungua kwa majani kama vile yamechomwa na maji moto. Chini ya jani utaona unga unga mweupe. Matunda pia hushambuliwa na ugonjwa huu na hugeuka kuwa meusi na magumu.

Bakajani tangulia/wahi (Early blight) Bakajani chelewa

(late blight

Page 10: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

6

Kuzuia Inabidi kuchanganya mbinu mbali mbali za kupambana na ugonjwa huu. Kwanza ni usafi wa shamba kwa ujumla yaani hakikisha unaondoa magugu katika bustani. Tandaza nyasi juu ya matuta yaliyopandwa nyanya. Ondoa majani yaliyozeeka na yanayoonyesha dalili za ugonjwa huu. Katika kupunguza majani, hakikisha sehemu za chini ya mmea ni wazi na kuna mzunguko mzuri wa hewa. Punguza majani katika mmea ili kupunguza umande na ukungu kwenye mmea. Baada ya kupunguza majani na machipukizi hakikisha unatupa mbali majani hayo na siyo kuyaacha kwenye tuta la bustani. Ondoa kabisa mmea ulio na dalili za ugonjwa huu Kupiga dawa iliyotengenezwa kwa majani ya mpapai au mchanganyiko wa maziwa na maji katika kipindi cha mvua mara baada ya mvua kubwa. Fanya hivyo mara moja au mara mbili kwa wiki kutegemea na wingi au mfululizo wa mvua. Unapoona jua limetoka piga dawa ili ugonjwa usijitokeze tena.

Muarobaini pia unaweza kutumika kupunguza ugonjwa huu. Changanya unga unaotokana na mbegu za muarobaini kiasi cha nusu kilo ya unga katika lita 20 za maji. Blue Copper imekuwa ikitumiwa kudhibiti ugonjwa huu pia.

1.6.2. Mnyauko au kausha Ugonjwa wa mmea wa nyanya kuoza sehemu ya shina inayogusa udongo na mmea kunyauka kama vile umekosa maji Wadudu wanaosabisha ugonjwa huu hupatikana ardhini (minyoo fundo). Hakuna dawa ya kutibu ugonjwa huu baada ya dalili kujitokeza. Epuka kupanda nyanya au mazao jamii ya nyanya katika eneo moja kwa muda mrefu mfulilizo. Baadhi ya mazao yanayohusiana na nyanya ni bilinganya, pilipili, ngogwe, mnavu, n.k.

1.6.3. Kata kiuno Ugonjwa wa miche michanga ya nyanya kuoza sehemu ya shina inayogusa udongo na kufa ghafla. Ugonjwa huu hushambulia miche kitaluni na husabishwa na wadudu waishio ardhini. Mara baada ya dalili, ugonjwa huu hauna dawa ila unaweza kukingwa kwa kutumia njia zifuatazo:

Choma moto udongo wa kutengezea kitalu kabla ya kupanda mbegu zako. Kutumia mboji husaidia kukinga miche dhidi ya ugonjwa huu. Epuka kumwagilia maji kupita kiasi na kutumia kuvuli kizito.

1.6.4. Matunda ya nyanya kuoza kitako. Huu ni ugonjwa unaosababishwa na:

Umwagiliaji wa nyanya bustanini usio na mpangilio maalumu. Mfano, kumwagilia mimea maji mengi kisha kuiacha bila maji kwa siku kadhaa. Upungufu wa virutubisho aina ya chokaa.

Dalili Matunda ya nyanya kuoza sehemu ya kitako na kuonyesha rangi nyeusi.

Page 11: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

7

Kuzuia ugonjwa huu, zingatia kuwa na utaratibu mzuri wa kumwagilia maji ambao haubadiliki ovyo kiratiba na kiasi cha maji yanayowekwa. Rutubisha mimea kwa madini ya chokaa kwa kutumia mifupa iliyosagwa.

1.6.5. Mnyauko bakteria (Bacterial wilt) Ugonjwa huu husababishwa na bacteria. Mmea ulioshambuliwa hunyauka ghafla hasa wakati wa jua kali. Mnyauko bakteria unaweza kuzuiwa kwa kubadilisha mazao shambani. Endapo ardhi itashambuliwa na ugonjwa huu zao la bilinganya lisipandwe katika eneo hilo kwa muda wa miaka mitatu hadi mitano

1.6.6. Ugonjwa wa ukoma wa nyanya Huu ni ugonjwa wa virus unao enezwa na inzi mweupe. Inzi hawa hushambulia zaidi nyanya wakati wa kiangazi, hasa kipindi cha joto kali.

Dalili Majani machanga hujikunja na baadaye majani yote. Kupungua kwa utoaji maua na matunda na hata yakitokea matunda huwa ni madogo. Mmea kudumaa na kutozaa kabisa.

Kuzuia Mbinu madhubuti ni kupunguza kuenea kwa ugonjwa huu kwenye shamba kwa kudhibiti kuzaana na kuenea kwa mdudu (inzi mweupe) kama tulivyo ona katika kupambana na mdudu huyo, yaani:

Kuondoa mimea michache iliyo shikwa na ugonjwa maana wadudu hawa wanachukua ugonjwa huu kutoka mimea hii. Kutumia mbegu zilizo hakikishwa kuwa zinaweza kuvumilia ugonjwa huu na kutoa mavuno mazuri. Usilime nyanya karibu na eneo lililo na mazao kama bamia, mipapai maana mimea hii huhifadhi inzi mweupe. Epuka kuchanganya zao la nyanya na mazao mengine yanayohifadhi hawa nzi kama vile mipapai na bamia. Ng'oa na kufukia chini sana mimea yote iliyougua ugonjwa huu.

Page 12: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

8

Batobato (Tobacco Mosaic Virus) tomato yellow leaf curl

Uenezwao na nzi weupe

Page 13: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

9

2. KILIMO BORA CHA NYANYA CHUNGU

2.1. UTANGULIZI Nyanya Chungu au Ngogwe ni zao linalostawi katika maeneo yenye joto linalotoa mazao yake kama matunda na kutumika kama mboga, kuna aina mbalimbali za nyanya chungu ambazo ni nyanya chungu ambazo ni za asili na zingine ni chotara sio chungu kama za asili. Rangi ya matunda huwa kijani kibichi au kijani-njano, au njano-nyeupe, na yakipevuka kabisa hugeuka mekundu. Matunda yafikia hatua ya kupevuka huwa hayafai tena kuliwa, ila kwa kutoa mbegu za kupanda. Matunda hupikwa au kukaangwa na kufanywa mchuzi, au huchanganywa na mboga zingine.

2.2. AINA ZA NYANYA CHUNGU

2.3. HALI YA HEWA Nyanya chungu za aina zote hustawi sana sehemu yenye jua na udongo wenye kupitisha maji vizuri na udongo wenye uchachu yaani pH kati ya 5.5 na 6.8. Gilo ni aina ambayo hustawi sana kwenye joto la mchana la kati ya 25°C na 35°C (77°F na 95°F). Kumba hustawi maeneo yenye joto sana kufikia 45°C na unyevu kidogo, Shum inahitaji joto na unyevu ili kustawi. Hakuna aina ya Nyanya chungu inayovumilia kwenye baridi kali na hali ya majimaji.

2.4. UTAYALISHAJI WA SHAMBA Lima shamba lako vizuri kwa kutumia trekta, jembe la ng’ombe, jembe la mkono au pawatila, hakikisha shamba linakuwa halina nyasi, changanya samadi au mboji na udongo ili kuongeza rutuba.

2.5. UTAYALISHAJI WA MBEGU NA KUPANDA Mbegu za nyanya chungu zinauzwa kutoka baadhi ya makampuni ila kuna njia ya kupata mbegu kutoka kwenye tunda. Chukua nyanya chungu iliyokomaa menya vizuri baada ya hapo kusanya mbegu zilizopo ndani ya tunda, baada ya hapo ziweke kwenye kipande cha karatasi ili zikauke katika sehemu isiyopitisha mionzi ya jua ya moja kwa moja. Mbegu zikisha kauka zinaweza kutunzwa kwa miaka mingi na kuendelea kutumika. Mbegu lazima zioteshwe kwenye kitalu cha sentimita 15 (6 inch) au zaidi hadi kufikia sentimita 20 (8 inch) ya safu.

Page 14: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

10

Kupanda Kutoka kwenye kitalu miche hupandikizwa bustanini ifikiapo kimo cha sentimeta 15 hadi 20 au majani 5, kwa umbali wa sentimita 50 kwa 75 au sentimeta 90 kwa 90, hadi 120 kwa 120; hii hutegemeana na ukubwa wa kichaka chake. Mimea ya “Ngogwe” hutunzwa kama bilinganya, huhitaji ardhi yenye rutuba na unyevu wa kutosha. Mazao huanza kuvunwa miezi miwili baada ya kupandikizwa na uvunaji huendelea kwa muda mrefu kidogo.

2.6. MATUNZO YA SHAMBA Mbolea Zao hili unashauriwa kutumia mbolea za asili (samadi au mboji) kuongeza uzalishaji wa mazao, mmea wa nyanya chungu unahitaji sana madini. Shamba la nyanya chungu linatakiwa lipaliliwe kwa kuondoa nyasi na liwe safi ili kudhibiti magonjwa na wadudu, unyevu unahitajika ili kuongeza mavuno.

2.7 MAGONJWA NA WADUDU Nyanya chungu ni mmea mgumu, kwani unaweza kustahimili upungufu wa maji kuliko aina nyingine za Mboga. Vile vile haushambuliwi sana na baadhi ya Magonjwa yasababishwayo na mvua au uchepechepe mkubwa. Ingawa yako magonjwa na wadudu ambao hushambulia zao hili, madhara yake si makubwa sana kiasi cha kutisha au kumkatisha tamaa mkulima. Usafi wa bustani na kubadilisha mpando wa mazao, vinaweza kuondoa tishio hilo.

2.8. UVUNAJI Nyanya chungu huvunwa wakati zikiwa bado mbichi, hukomaa baada ya siku 100 mpaka 120 kutoka kupandwa, unashauriwa uvune kabla hazija badilika rangi Ili ziweze kukaa kwa muda mrefu (hata majuma mawili) bila kuharibika. Inapendekezwa kuzichuma pamoja na sehemu ya vikonyo vyake. Vikonyo hivyo hukobolewa wakati wa kuzitayarisha kwa ajili ya kupikwa. Kwa hiyo, zao hili linaweza kusafirishwa hadi masoko ya mbali bila kuharibika.

Page 15: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

11

3. KILIMO BORA CHA BILINGANYA

3.1. UTANGULIZI Ni zao linalotumika kama mboga au kiungo cha Mboga peke yake au kuchanganywa na mboga zingine

3.2. MAHITAJI YA ZAO KATIKA UZALISHAJI

3.2.1. Hali ya Hewa Zao hili huhitaji hali ya hewa ya joto huweza pia kulimwa si chini ya nyuzi 10 0C lakini hustawi vizuri katika nyuzi 26 0C hadi 29 0C

3.2.2. Udongo Japo zao hili linaweza kukua kwenye kila aina ya udongo hukuwa na kustawi vema katika udongo tifutifu usio twamisha maji. Udongo ulio katuliwa vizuri huwezesha mizizi kukua vizuri kufikia urefu wa milimita 600.

Hivyo ni mhimu kuliandaa shamba lako vizur kabla ya kupanda. Miezi mizuri inayoshauriwa katika kilimo hiki ni miezi isiyokuwa na Mvua nyingi kwa kuwa kukiwa na unyenyevu mwingi zao hili huwa halitoi mazao ya kutosha na pia kwenye ukame kusipokuwa na maji ya kutosha huwa halitoi mazao mengi ya kutosha na Inasemekana kutokana na sifa hizi huwenda ndiyo husababisha kutokuwa na Mafuriko mengi ya zao hili.

Page 16: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

12

3.2.3. Kuotesha mbegu. Mbegu huoteshwa kwanza kwenye vitalu na baadaye miche kuhamishiwa shambani. Kabla ya kusia mbegu tengeneza tuta lenye upana wa mita moja na urefu wowote. Weka mbolea ya asili kama vile samadi au mboji iliyoiva vizuri, kiasi cha ndoo moja au mbili katika eneo la mita moja. Sia mbegu kiasi cha gramu mbili mpaka tatu katika eneo hilo. Kumbuka gramu 200 za mbegu zinatosha kusia katika eneo la ekari moja.

Lakini pia ikumbukwe nafasi kati ya mstari na mstari lazima iwe sentimeta 10 hadi 15 na kina kiwe sentimeta 1.5. Gramu 200 za mbegu zinatosha eneo la ekari 1.

3.2.4. Kuhamisha miche ya bilinganya. Miche huwa tayari kupandikizwa shambani mara baada ya wiki sita hadi nane. Wakati ikiwa na urefu wa sentimmita 15 hadi 20 ambayo ni sawa na kalamu moja ya risasi. Lakini unakumbushwa ya kwamba kabla ya kupeleka miche shambani ni muhimu kurutubisha shamba vizuri kwa mbolea za asili. Weka kiasi cha viganja viwili kwa kila shimo vya mbolea ya asili kama mboji au samadi.

KUMBUKA Pia Mbegu huweza kupandwa moja kwa moja kwenye mashimo na baadae kupunguzia umbali wa mita 1.8 hadi 2.5 mche hadi mche kulingana na rutuba ya udongo. Miche 10000 huweza kupandwa kwenye ekari moja.

3.3. KUTUNZA SHAMBA.

3.3.1. Kuweka matandazo. Mara baada ya kupandikiza miche, tandaza nyasi kavu. Matandazo husaidia kuhifadhi unyevu, huzuia magugu yasiote lakini pia huongeza rutuba katika udongo.

3.3.2. Palizi. Hakikisha shamba lako ni safi muda wote ili kuzuia ushindani wa chakula, maji na mwanga kati ya mmea na magugu. Lakini pia palizi husaidia kubomoa maficho ya wadudu na kuzuia kuenea kwa wadudu.

3.3.3. Mbolea. Weka mbolea za maji za kukuzia kama chai ya mimea /samadi wiki tatu mara baada ya kupandikiza mimea. Mbolea hiyo huwekwa kwa kiwango cha mililita 250 kuzunguka kila mche.

3.3.4. Kukata kilele. Wiki mbili baada ya kupandikisha miche, kata sehemu ya juu ya mmea kama umepanda aina ya mbegu ndefu. Kufanya hivi kusaidia kutengeneza umbile la kichaka.

3.3.5. Kumwagilia. Zao la bilinganya hustawi vizuri endapo litamwagiliwa vizuri, lakini ikumbukwe kwamba umwagiliaji unaweza kufanyika mara mbili yaani asubuhi na jioni kutegemeana na hali ya hewa.

Page 17: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

13

3.4. WADUDU WAHARIBIFU NA MAGONJWA.

3.4.1. Wadudu Waharibifu

3.4.1.1. Vinyantomvu wa Bilinganya (Eggplant Lacebugs) Wadudu hawa hushambulia zaidi sehemu ya chini ya jani. Hufyonza utomvu wa majani na kusababisha majani kuwa na mabaka meupe au njano. Mashambulizi yakizidi majani huanguka chini. Vinyatomvu wanaweza kuzuiwa kwa kunyunyiza dawa za wadudu zenye viua sumu vifuatavyo; pilipili, utupa na mwarobaini.

3.4.1.2. Vidukari au Wadudu mafuta (Cotton Aphids) Hawa ni wadudu wadogo wenye rangi nyeusi. Hushambulia majani machanga na kuyasababisha kudumaa na kukunjamana. Zuia wadudu hawa kwa kutumia dawa za kilimo hai kama pilipili na mwarobaini.

3.4.1.3. Utitiri wa Mimea (Red Spider mites) Ni vidudu vidogo venye rangi nyekundu iliyoiva. Hushambulia majani kwa kufyonza utomvu. Majani yaliyoshambuliwa huonyesha utando kama wa buibui. Mashambulizi yakizidi mmea hudumaa, majani hukauka na hatimae hufa. Utitili unazuiwa kwa kutumia dawa za kilimo hai kama vile mwarobaini na pilipili za kuwasha

3.4.1.4. Minyoo Fundo (Root Knot nemtodes) Wadudu hawa hushambulia mizizi hutoa kinyesi ambacho ni sumu kwa mmea. Sumu hii husababisha mizizi kuwa na nundu kama ya mizizi ya maharagwe. Mashabulizi yakizidi mmea hudumaa, hunyauka na hatimaye hufa. Njia ya kuzuia wadudu hawa ni kubadilisha mazao. Kwa mfano; baada ya kuvuna zao hili, zao linalofuata lisiwe la jamii moja na bilinganya, kama vile nyanya, pilipili na viazi mviringo.

Page 18: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

14

3.4.2. Magonjwa 3.4.2.1. Mnyauko Bacteria (Bacteria Wilt) Ugonjwa huu husababishwa na bacteria. Mmea ulioshambuliwa hunyauka ghafla hasa wakati wa jua kali. Mnyauko bakteria unaweza kuzuiwa kwa kubadilisha mazao shambani. Endapo ardhi itashambuliwa na ugonjwa huu zao la bilinganya lisipandwe katika eneo hilo kwa muda wa miaka mitatu hadi mitano. Njia nyingine ni kupanda aina za bilinganya kama vile Matale, Kopek na Rosita ambazo huvumilia mashambulizi ya ugonjwa huu.

3.4.2.2. Mnyauko vaticilium (Verticillium Wilt) Huenezwa na maji na husababisha mmea kudumaa, majani kukunjamana na kuanguka. Magonjwa ya Phomopsis Vexans na Verticillium Wilt yanaweza kuzuiwa kwa kung'oa na kuchoma moto mimea iliyoshambuliwa, kubadilisha mazao na kuweka shamba katika hali ya usafi wakati wote.

3.5. KUVUNA Bilinganya huanza kutoa matunda yaliyokomaa baada ya miezi miwili hadi mitatu tangu kupandikiza. Uvunaji huendelea kwa muda wa zaidi ya miezi minne na hauna budi hufanyike mapema mara matunda yanapokomaa. Matunda yaliyokomaa sana hayafai kuliwa kwa sababu huwa na kambakamba na mbegu zilizokomaa. Vuna mara mbili au tatu kwa wiki, kwa kutumia kisu kikali ili usiumize matunda.

Mavuno kwa kila ekari kwa wiki ni takribani viroba 50 ambapo kama bei ya kiroba ni shilingi 10000/-kwa viroba 50 ni sawa na 500’000/- kwa wiki kwa miezi mitatu hadi sita mfululizo inategemea na utunzaji hasa umwagiliaji.

Page 19: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

15

4. KILIMO BORA CHA PILIPILI HOHO

4.1. UTANGULIZI Pilipili hoho hutumika kwa matumizi ya nyumbani kama kiungo kuongeza ladha na harufu katika vyakula. Vilevile pilipili hoho hutumika kwa matumizi ya usindikaji viwandani katika kutengeneza rangi za asili za vyakula na vipodozi ambazo kwa sasa hupendwa zaidi kuliko zile zinazotokana na kemikali.

Aina za Pilipili hoho Kulingana na umbo la tunda kuna aina mbili za pilipili hoho ambazo ni pilipili zilizochongoka na pilipili za duara. Pilipili zilizo chongoka zinanukia sana ukilinganisha na pilipili za duara. Kwa Tanzania pilipili zinazolimwa kwa wingi ni zile zenye umbo la duara kwa sababu ni nene na hivyo zina soko zuri.

Aina za mbegu Kuna aina tofauti za mbegu za pilipili hoho zinazopatikana Tanzania kama vile Calfornia wonder, Emerald Giant, Sweet Neapotitan, Yolo Wonder, Pimiento na Keystone Resistant Giant. Mbegu zinazopendelewa na wengi ni;

Calfornia wonder: huzaa matunda makubwa, matamu yenye umbo la duara na kuta nene.

Page 20: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

16

Yolo wonder: hustahimili magojwa ya batobato na kuzaa sana matunda ya kijanimakubwa ya duara yenye kuta nene.

4.2. UCHAGUZI WA ENEO Ni vyema eneo litakalotumika katika kilimo cha pilipili hoho liwe na urahisi wa upatikanaji maji kurahisisha umwagiliaji kwa kilimo cha umwagiliaji. Shamba la pilipili hoho liwe mbali iwezekanavyo kutoka mahali lilipo shamba la tumbaku ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa batobato ya tumbaku unaoenezwa na wadudu kama vidukari na nzi weupe. Vile vile shamba ambalo limetumika kwa kilimo cha mazao ya nyanya, viazi na bilinganya lisitumike katika kilimo cha pilipili hoho mpaka baada ya muda wa misimu minne kwa kuwa mazao haya ni jamii moja (solanaceous) na pilipili hoho hivyo magonjwa na wadudu wanaoshambulia mazao haya huweza pia kushambulia zao la pilipili hoho.

Hali ya Hewa na Mwinuko Pilipili hoho hustawi vizuri katika maeneo ya mwinuko tofauti tofauti hadi mita 2000 kutoka usawa wa bahari yenye mgawanyo mzuri wa mvua kuanzia kiasi cha mm 600 mpaka mm 700 cha mvua kwa mwaka. Mvua inapokuwa nyingi huweza kuathiri utokaji wa maua na kusababisha kuoza kwa matunda. Pilipili hoho hustawi katika maeneo yenye hali joto tofauti kuanzia nyuzi joto za sentigredi 16 mpaka 28 lakini hustawi vizuri zaidi katika maeneo yenye joto la nyuzi za sentigredi 20 mpaka 25. Hali joto chini ya nyuzi za sentigredi 16 kwa masaa 120 (siku tano) mfululizo husababisha kuwa na utengenezaji mdogo wa matunda na matunda yasiyo na mbegu wakati joto zaidi ya nyuzi joto za sentigredi 30 husababisha upotevu wa maji kwa wingi katika mmea.

Udongo Kwa ujumla pilipili hoho hustawi karibu kwenye udongo wa aina zote wenye rutuba, kina na husiotuamisha maji wenye uwezo wa kuifadhi maji vizuri. Udongo wa kichanga uliorutubishwa vizuri hufaa sana katika maeneo yenye hali ya baridi kwa sababu ya kuwa na tabia ya kupata joto kwa urahisi na hivyo kufanya mizizi kukua vizuri katika joto linalostahili. Udongo wenye tindikali nyingi huzorotesha ukuaji wa pilipili hoho hivyo udongo mzuri kwa pilipili hoho ni ule wenye uchachu (pH) kati ya 6.0 – 6.8.

4.3. UANDAJI WA SHAMBA NA UPANDAJI

Kupima shamba (field layout) Ni muhimu kuanza kupima shamba kabla ya kuanza kuandaa matuta ili kupata matuta yaliyo katika mpangilio mzuri na mistari ya mimea shambani iliyonyooka vizuri. Kabla ya kupima matuta ni muhimu pia kujua nafasi ya kupandia utakayo tumia ili kupata ukubwa sahihi wa kila tuta. Kwa mfano kwa nafasi ya kupandia ya sm 60 × sm 40 kwa matuta makubwa unaweza kutengeneza kila tuta katika upana wa sm 1.2 na urefu wowote. Acha nafasi ya m 1 kuzunguka shamba na njia kila baada ya tuta upana wa sm 50. Tumia futi kamba (Tape measure) au kamba yenye vipimo kupima shamba huku ukiweka alama za matuta na njia kwa kuchomeka mambo (pegs) katika kila kona ya tuta na kuzungushia kamba.

Kuweka matuta Inashauliwa kupanda pilipili hoho katika matuta ili kusaidia mizizi kukua vizuri na udongo kuhifadhi maji. Wakati wa kiangazi, tengeneza matuta yaliyodidimia kidogo ili kufanya maji yaweze kukaa kwenye udongo na wakati wa masika matuta yainuliwe kidogo toka kwenye usawa

Page 21: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

17

wa ardhi ili kuzuia maji yasituame. Matuta yanaweza kuwa makubwa au madogo kulingana na matakwa ya mkulima. Matuta makubwa hupandwa mistari miwili na matuta madogo hupandwa mstari mmoja. Tengeneza matuta kwa kufuata alama zilizowekwa wakati wa kupima shamba.

Upandaji

Kiasi cha Mbegu Kiasi cha gramu 1 ya mbegu za pilipili hoho inakadiliwa kuwa na idadi ya mbegu 160 hivyo kiasi cha gramu 100 za mbegu za pilipili hoho kinatosha kupanda eneo la ekari moja ambalo huchukua miche karibu 10,000 hadi 15,000.

Kupandikiza Tabia za miche ya kupandikizwa Miche ya pilipili hoho inayofaa kupandikizwa shambani ni ile yenye afya ambayo haikuathiriwa na magonjwa wala wadudu yenye kimo cha sm 10 hadi 15 ikiwa na majani halisi matano mpaka sita.

Muda wa Kupandikiza Katika mazingira mazuri miche huwa tayari kwa kupandikizwa baada ya wiki nne tangu kusia. Inapendekezwa kupandikiza miche wakati wa jioni ili iweze kupona kwa urahisi na kuzoea hali ya shambani bila ya kupata mshtuko (transplanting shock).

Nafasi ya kupandia Miche ipandikizwe kwa kuzingatia nafasi pendekezwa katika mistari iliyonyooka. Pilipili hoho kutegemeana na aina huweza kupandwa katika nafasi tofauti tofauti sm 60 mpaka sm 75 mstari hadi mstari na sm 30 mpaka sm 45 shimo hadi shimo. Ni muhimu kusoma pakiti ya mbegu husika kujua nafasi pendekezwa kabla ya kuchagua nafasi ya kutumia.

Hatua za kupandikiza Unaweza kupandikiza miche shambani kwa kufuata hatua zifuatazo;

1. Mwagia maji ya kutosha shambani na kitaluni masaa kumi na mbili kabla ya kupandikizaili kulainisha udongo kurahisisha uong’oaji na upandikizaji.

2. Chimba mashimo ya kupandia yenye kimo cha sm 10 katika nafasi iliyopendekezwa kwambegu itakayotumika mistari miwili miwili kila tuta kwa kutumia kamba iliyowekwavipimo.

3. Weka viganja viwili vya mkono vya samadi iliyoiva katika shimo la kupandia kishachanganya na udongo kupata mchanganyiko mzuri.

4. Tifua udongo wa kitalu kwa kunyanyulia kwa kutumia koleo au umma wa shambani bilakuathiri mizizi ya miche ili kung’oa miche yenye udongo kidogo kuzunguka mizizi yake.

5. Pandikiza miche ikiwa na udongo wake katika mashimo ya kupandia kisha fukia kwaudongo ulio pembeni. Miche ambayo mizizi yake imezungukwa na udongo inaponaharaka shambani ukilinganisha na miche ambayo mizizi yake haina udongo. Pandikizamiche ya pilipili hoho katika kina kilekile kama ilivyokuwa kitaluni.

6. Shindilia udongo kuzunguka mche uliopandikizwa kwa kutumia vidole vya mikonomiwili kisha mwagilia maji ya kutosha.

Page 22: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

18

4.4. KUTUNZA SHAMBA a) Kuweka matandazo

Tandaza nyasi kavu ili kuhifadhi unyevu ardhini, kuzuia utoaji wa magugu na mmomonyoko wa udongo.

b) PaliziPalilia shamba kila magugu yanapoota. wakati wakupalilia pandishia udongo kuzunguka shina ili kuifunika mizizi na kuzuia mmea usianguke.

c) Kumwagilia majiPilipili hoho hustawi vizuri iwapo zimepata maji ya kutosha. Hivyo umwagiliaji wa mara kwa mara hasa wakati wa kiangazi ni muhimu sana.

d) Kuweka mboleaNi muhimu kuweka mbolea za kukuzia kwa zao hili, hususani chai ya mimea au samadi.

e) Kusimikia miti (staking)Mmea wa pilipili hoho kama ilivyo kwa zao la nyanya huitaji kusimikwa miti ili zisianguke kutokana na mzigo wa matunda na upepo. Simika miti katika bustani ya pilipili hoho wiki tatu tangu kupandikiza hasa baada ya kutoka kwa ua la kwanza. Simika miti yenye urefu wa m 1.5 hadi mita pembeni ya kila mmea umbali wa sm 5 kutoka kwenye usawa wa majani na kufunga kwa kamba shina la mmea na mti kwa kifundo chenye umbo la namba nane. Hakikisha unatumia miti imara isiyooza kwa haraka yenye unene usiopungua sentimita 2.

f) KupogoleaKatika mmea wa pilipili hoho upogoleaji hufanyika kwa kundoa majani yaliyo zidi na yaliyo athirika na magonjwa ili kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa katika mmea. Kwa mbegu chotara zinazozaa kwa muda mrefu pogolea matawi na majani baada ya kuvuna katika kila ngazi ili kuruhusu utengenezwaji mzuri wa matunda kwa ngazi ya juu yake. Vilevile inashauriwa kukata ncha ya shina baada ya kutokea kwa ngazi tano au sita katika mmea ili kuzuia ukuaji wa mmea kwenda juu na kuchochea ukuwaji mzuri wa matunda. Ondoa ua la kwanza la pilipili hoho kuchochea utokaji wa maua na matunda mengi. Epuka upogoleaji uliokithiri kwani huweza kusababisha hitilafu ya kuungua kwa matunda ya pilipili hoho kutokana na mwanga wa jua.

4.5. MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU

4.5.1. Wadudu

i) Vidukari Au Wadudu Mafuta (Aphids)Hivi ni vijidudu vidogo vyenye rangi nyeusi, kijani aukahawi. Hushambulia majani kwa kufyonza utomvuwake na husababisha mmea kudumaa. Dawailiyotengenezwa kwa mwarobaini au mchanganyiko napilipili inaonyesha matokeo katika kudhibiti waduduhawa

ii) Fukusi wa Pilipili (pepper weevil)Mdudu huyu ni hatari sana kwa zao hili na mashambulizi hufanywa na funza wake wenye ranginyeupe. Funza hawa hula sehemu ya ndani ya vichomozo na matunda machanga na husababisha

Page 23: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

19

kuanguka. Tumia pilipili za kuwasha na mwarobaini na kufuata mbinu bora za uzalishaji wa kilimo hai.

iii) Vithiripi (Thrips)Hivi ni vidudu vidogo vyenye rangi ya njano. Hushambulia majani na husababisha mmea kuwana rangi nyeupe inayong’aa. Mmea pia hunyauka kuanzia kwenye ncha ya jani. Ili kuwadhibititumia dawa iliyotengenezwa kwa pilipili za kuwasha na majani ya mwarobaini.

iv) Sota (cutwoms)Hawa hukata mmea kutokea ardhini (kwa maelezo Zaidi rejea ukurusa 13)

V) Inzi weupe (White flies)Ni wadudu wadogo Vyenye rangi nyeupe nahuonekana kama vumbi la unga vikiwa kwenyemajani. Mmea ukitikiswa huruka. Hushambuliammea kwa kufyonza utomvu wake ,na huenezavirusi wanaosababishwa kujikunja kwa majani.Kupulizia dawa zilizotengenezwa kutokana namwarobaini na pilipili au mchanganyiko wa utupana pilipili mara kwa mara kunasaidia kufukuzawadudu hawa na kupunguza athari.

vii) Utitiri Mwekundu (Red spidermites)Hawa ni wadudu wadogo wenye rangi nyekundu au rangi ya machungwa yaliyoiva. Huonekanaupande wa chini wa majani na hushambulia mmea kwa kufyonza utomvu wake. Zuia utitiri kwakutumia dawa kama vile pilipili za kuwasha, mwarobaini na majani ya nyanya.

Page 24: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

20

viii) Mbawakau (Leaf eating beetles)Ni wadudu wenye rangi nyeusi waliochanganyika na kahawia. Mbawakau kwa kawaida mabawayao ya nje ni magumu. Wadudu hawa hufanya mashambulizi kwenye shina karibu na usawa waardhi na kulifanya kuweka nundu.

4.5.2 Magonjwa

(i) Magonjwa ya virusiMagonjwa haya hutokana na virusi. Husababisha majani kudumaa, kukunjamana, na kuwa narangi ya njano.

Ili kuzuia magonjwa haya, zingatia yafuatayo; Panda aina ya pilipili zinazostahimili mashambulizi ya magonjwa haya. Ng'oa miche inayoonyesha dalili za magonjwa haya. Zuia wadudu wanaoeneza magonjwa ya virusi kwa kutumia dawa Badilisha mazao kwa kupanda mazao tofauti na mazao yaliyo kwenye familia ya nyanya (bilinganya, mnafu, pilipili n.k).

(ii) Chule (Anthracnose)Ugonjwa huu husababishwa na ukungu. Hushambulia matunda na kuyasababisha kuwa namakovu ya mviringo yenye rangi nyeusi iliyochanganyika na kahawia. Zuia ugonjwa huu kwakunyunyiza mojawapo ya dawa zifuatazo:

Majani ya mapapai au Copper i.e Blue copper

Page 25: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

21

(iii) Madoa Bakteria (Bacterial Leaf Spot)Ugonjwa huu husababishwa na viini vya bacteria. Hushambulia majani machanga na baadayematunda. Dalili zake ni kuonekana kwa madoa ya njano kwenye majani na matunda. Zuiaugonjwa huu kwa kupanda mbegu bora zisizoathiriwa na ugonjwa.

(iv) Kuoza Mizizi (Root Rot)Huu ni ugonjwa wa ukungu unaoshambulia mizizi na kusababisha kuoza. Mimea hunyauka nahatimaye hufa. Ugonjwa huu hupendelea sana hali ya unyevuunyevu na joto jingi, hivyo zuia halihii kwa kuepuka kupanda pilipili kwenye sehemu inayotuamisha maji.

(v) Mnyauko Verticilium (Verticilium Wilt)Huu pia ni ugonjwa unaoletwa na ukungu ambao hupatikana kwenye udongo. Hushambuliashina na kulisababisha libadilike rangi na kuwa ya kahawia. Baadaye mmea hunyauka na kufa.Unaweza kuzuia ugonjwa huu kwa kubadilisha mazao. Dawa zilizotengenezwa kwa majani yampapai zinasaidia kuzuia magonjwa ya ukungu pamoja na mnyauko.

3.6. Kuvuna Pilipili hoho huwa tayari Kwa kuvunwa baada ya wiki 10 hadi 14 tangu kupandikiza miche. Uvunaji huendelea kwa muda wa wiki nane hadi 10. Muda wa kuvuna hutegemea aina na matumizi. Pilipili kwa ajili ya matumizi ya nyumbani huvunwa zingali na rangi yake ya kijani kibichi inayong'aa. Zile za kusindika kiwandani huvunwa zikiwa zimekomaa na zenye rangi nyekundu. Matunda yakivunwa yangali machanga hunyauka kwa urahisi, husinyaa na kupunguza wingi wa mazao. Wastani wa mavuno kwa hekta ni tani 30 hadi 45

Page 26: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

22

5. KILIMO BORA CHA MATANGO

5.1. UTANGULIZI Tanzania matango hulimwa katika mikoa ifuatayo: Tanga, Morogoro, Mbeya, Lindi, Mtwara na Pwani ambako kuna jua la kutosha. Pia mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kilimo cha matango hukubali.

5.2. AINA ZA MATANGO Zipo aina nyingi za matango ya kisasa na kienyeji lakini hutofautiana kwa umbo na rangi. Aina zinazojulika na kulimwa zaidi hapa kwetu ni: Colorad, Telegraph, Palmetto, Chicago, Pickling, Straight 8 na Marketer.

Straight 8 pickling marketer

5.3. MATUMIZI Matango hutumiwa kama matunda na pia ni aina ya mboga ambayo huongeza vitamin A, C na maji mwilini. Matunda haya yanaweza kutumika pia kama kachumbari wakati wa mlo. Mbegu za matango ya kienyeji hukaushwa na kukamuliwa mafuta, pia hutumika kama kiungo cha mboga.( kutengeneza tui).

5.4. UDONGO NA HALI YA HEWA Eneo linatakiwa liwe na maji ya kutosha na udongo wenye chachu (pH) ya 6.0 hadi 7.5 na hali ya joto wastani wa nyuzi 20 hadi 25 zinahitajika kwa ukuaji bora. Matango hukua na kukomaa kwa haraka zaidi katika udongo mwepesi, lakini hutoa mavuno makubwa zaidi katika ardhi nzito kiasi. Hata hivyo ardhi inayotuamisha maji haifai kwa kilimo cha matango, na ikibidi mimea ipandwe kwenye matuta.

Kabla ya kupanda udongo unatakiwa utifuliwe vizuri na majani yaondolewe kabisa. usafi bustanini unashauriwa ili kuondoa mimea mingine ambayo inaweza kuwa chanzo

cha magonjwa.

5.5. UPANDAJI Panda mbegu moja Kwa moja shambani, sia mbegu moja kiasi cha sentimita moja chini ya udongo, na umbali kati ya mbegu na mbegu ni sm 60 na kati ya mstari na mstari ni sm 90.

Page 27: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

23

Sehemu ya kupandia iwe na jua la kutosha kwani matango huhitaji kiasi cha jua kisichopungua masaa 6 - 8 kwa siku, mwagilia maji ya kutosha angalau mara moja kwa siku hasa nyakati za jioni. Hii itasaidia ukuaji bora wa mazao yako hivyo kukuhakikishia mavuno mazuri.

5.6. MATUNZO YA MATANGO

5.6.1. Mbolea: Kabla ya kupanda weka viganja 2 vya mbolea ya samadi au mboji katika kila shimo na changanya na udongo.

5.6.2. Palizi Palilia kila wakati magugu yanapojitokeza, ni muhimu sana, hii husaidia kuepuka magonjwa na kushindania chakula kati ya zao na magugu. Palizi hutakiwa kufanywa kwa kutumia jembe la mkono ili kuepuka kuharibu mizizi.

5.6.3. Chomeka miti (staking) ya kupandia: Chomeka miti ya kupandia matango yanayotambaa. Hii husaidia matango yanayotambaa kupanda kufuata miti uliyoikita/chomeka.

5.7. MAGONJWA Ni magonjwa machache tu yanayoathiri kilimo cha matango ambayo husababishwa na virusi, fungus na bakteria. Ni vizuri kufuata kanuni bora za kilimo ili kuweza kujikinga/kuzuia uwezekano wa mimea kushambuliwa. Magonjwa hayo ni:

(a) Mnyauko bacteria (Bacteria Wilt)Hushambulia majani, majani yaliyoshambuliwa hudhoofu na hatimaye hufa. Mmea ukikatwa huchuruzika ute mzito. Kudhibiti ugonjwa Pulizia dawa ya ukungu kama vile blue copper kila baada ya siku 10 na tumia aina ya mbegu zenye uvumilivu mkubwa kama vile Palmetto.

(b) Ubwiri unga au ukungu (Powdery Mildew)Ukungu wake hushambulia majani na mashina. Maeneo yaliyoshambuliwa na ugonjwa huu, hufunikwa na unga unga mweupe au wakijivujivu ambao huonekana kama vumbi vumbi. Vimelea au chembe chembe zinazoshambulia ni ndogo ndogo sana na hazionekani dhahiri kwa macho, ila kwa darubini. Chembe chembe hizi zinapozaliana kwa wingi katika maeneo ya mshambulizi, ndipo huonekana kamaunga unga mweupe/kijivu.

Kudhibiti Fanya usafi unaohitajika bustanini na tumia dawa za kuzuia ukungu za kilimo hai kama majani ya mpapai na maziwa. Mmea ulioshambuliwa na ukungu.

Page 28: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

24

(c) Magonjwa ya virusi (Cucumber Mosaic Virus) – Ugonjwa huu husababishwa na virusi, ikiwa mmea hautatibiwa mapema, mmea hugeuka na kuwa wa njano, hudumaa na hushindwa kutoa matunda. Virusi wa Ugonjwa huu huenezwa na magugu au wadudu kama vidukari na inzi weupe. Kudhibiti Weka shamba katika hali ya usafi, na upande mbegu zinazovumilia ugonjwa. Pulizia dawa za kufukuza wadudu kama vile mwarobaini na pilipili kali.

Ugonjwa wa virusi

5.8. WADUDU a. Dudu kobe wa matango

Huyu hutafuna miche ya matango mara ichipuapo, pia hushambulia majani ya mimea michanga na kuathiri ukuaji.

Mbinu husishi za udhibiti wa wadudu zinaleta matokeo mazuri katika kudhibiti wadudu hawa. Husisha matumizi ya dawa asilia kama majani ya mwarobaini na pilipili kali katika mpango wa matumizi ya mbinuhusishi za kudhibiti wadudu.

b. Vidukari au wadudu mafuta (Aphids) Wadudu hawa hufyonza utomvu kwenye majani machanga na kudumaza mmea kuufanya ushindwe kuzaa matunda. Kuzuia wadudu hawa inabidi kutumia Mwarobaini na pilipili za kuwasha. Hakisha dawa inafikia upande wa chini wa majani ili kuhakikisha wadudu wote wamekufa.

c. Buu au funza (Pickle Worm) Buu au funza hujipenyeza ndani ya ua, kisha kwenye tunda. Kudhibiti Tumia pilpili za kuwasha na mwarobaini.

d. Konokono Hawa ni wadudu ambao wanakata na kula miche ya matango Ili kuwadhibiti fanya yafuatayo:-

Zingatia usafi wa shamba, pia hakikisha unafanya usafi kuzunguka shamba.(Tengeneza njia zenye upana wa mita 3 kuzunguka shamba).

Page 29: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

25

Tumia njia za asili kuwadhibiti kama vile kuwaua au kuwamwagia chumvi paleunapowaona.

Fanya ukaguzi wa shamba mara kwa mara.

5.9. KUVUNA Matango huwa tayari kuvunwa kuanzia siku 50 hadi 60, yaani mwezi mmoja na nusu hadi miwili baada ya kupanda, na pia matunda yanatakiwa kuwa na urefu wa sentimita 15 mpaka 20, urefu pia unaweza kutofautiana kulingana na aina ya matango yaliyopandwa. Baada ya mvuno wa kwanza mkulima anaweza subiri wiki tatu kabla ya kuvuna mvuno wa pili.

Page 30: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

26

6.0. KILIMO BORA CHA KAROTI

6.1 UTANGULIZI Karoti ni aina ya mboga yenye vyanzo vingi vya calcium, iron na wingi wa vitamin B. Kwa jina la kisayansi inajulikana kama Daucus carota , na hustawi sana kwenye udongo wa tifutifu wenye pH ya 6-6.5 na joto (temperature) la 18-24

Karoti inalimwa maeneo mengi sana nchini ikiwa pamoja na mbeya, morogoro( maeneo ya uluguru na mgeta), iringa pamoja na kilimanjaro.

Aina za caroti Nantes: Hii inapatikana maeneo mengi na inalimwa sana hapa Tanzania. inakuwa kwa haraka na nitamu sana. Chantenay: Hii pia ina ladha nzuri nainataka kufanana na Nantes lakini mizizi yake ni dhaifu ukilinganisha na Nantes.

6.2 UANDAAJI WA SHAMBA Shamba linatakiwa liandaliwe vizuri kuondoa magugu yote na udongo unatakiwa kutifuliwa vizuri kurahisisha mizizi kupenya vizuri kwenye udongo na maji kupenya vizuri. Na pia matuta yake yawe yameinuka kuzuia maji kutuama kwenye tuta, kwani maji kutuama husababisha mizizi kuoza na mmea kutokukua vizuri.

6.3 UOTESHAJI Karoti hupandwa kwa kutumia mbegu moja kwa moja shambani (direct sown), kiasi cha mbegu kinachotumika kupanda (seed rate) ni3.5-4 kg per ha, na mara nyingi hairuhusiwi kuhamisha miche (no transplanting) kwa sababu mizizi yake ni dhaifu ambayo haitastahimili kukua baada ya kuhamishwa.

Baada ya wiki ya nne kutoka kupandwa hufuatia kungolea miche iliyorundikana (thinning) kuipa nafasi kwa ajili ya kufanya miche iwe na afya nzuri.

Page 31: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

27

Mbegu za karoti ni ndogo sana ambazo zinatakiwa kupandwa kwenye urefu wa (1.9 -2.5) cm.

6.4 KUTUNZA SHAMBA Kumwagilia maji

Hakikisha udongo una unyevu wa kutosha hasa siku za mwanzo. Karoti zilizokosa maji kwa muda mrefu huzaa mizizi midogo midogo. Pia udongo mkavu ukipata maji mengi ghafla husababisha karoti kupasuka. Hivyo mwagilia shamba mara kwa mara kuhakikisha udongo una unyevu wa kutosha wakati wote, kama hali ya hewa ni ya jua kali.

Kupunguza micheMimea ya karoti inahitaji kupunguzwa mara mbili. Mara ya kwanza hupunguzwa ikiwa na majani matatu mpaka manne au wiki mbili tangu kupandwa na kuachwa katika nafasi ya sentimita tano mpaka saba. Mara ya pili hupunguzwa ikiwa na urefu wa sentimita 10 mpaka 13, na kuachwa katika nafasi ya sentimita 10 mpaka 15. Karoti zinazopunguzwa zinaweza kutumika kwa chakula.

PaliziZao la karoti linahitaji kupaliliwa mara kwa mara. Palilia kwa kupandishia udongo na kuwa mwangalifu ili usikate mizizi.

6.5. MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU:

5.5.1 Magonjwa a. Madoajani (Leaf Spot):

Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hutokea wakati karoti zina urefu wa sentimita 13 mpaka 15. Hushambulia majani na kuyafanya yawe na madoa yenye rangi nyeusi iliyochanganyika na kijivu au kahawia. Sehemu zinazozunguka madoa haya hubadilika rangi na kuwa njano. Ugonjwa ukizidi majani hukauka.

Zuia uonjwa huu kwa kunyunyizia dawa zozote za ukungu

b. Kuoza mizizi (Sclerotinia Rot)Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hushambulia mizizi na majani. Dalili zake ni kuoza kwa mizizi na majani. Baadaye sehemu hizi hufunikwa na uyoga mweupe. Kwenye uyoga huu huota siklerotia kubwa zenye rangi nyeusi.

Zuia ugonjwa huu kwa kuzingatia yafuatayo; (i) Epuka kustawisha karoti kwenye maeneo yaliyoshambuliwa na ugonjwa huu.

Page 32: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

28

(ii) Pulizia dawa ya ukungu majani ya mipapai au blue Copper

c. Karoti kuwa na mizizi Mingi (Folking)

Hii hutokea kama karoti zimepandwa kwenye udongo wenye takataka nyingi na usiolainishwa vizuri. Kuweka kiasi kikubwa cha mbolea na mizizi. Hali hii inaweza kuzuiwa kwa kulainisha udongo vizuri na kutumia mbolea za asili zilizooza vizuri.

d. Madoa Meusi (Black Leaf Spot)Huu pia ni ugonjwa na ukungu unaoshambulia majani na mizizi. Majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya majani ambayo baadaye hubadilika na kuwa kahawia. Mizizi huwa na madoa meusi yaliyodidimia.

Ugonjwa huu unaweza kuzuiwa kwa kutumia mbegu zilizothibitishwa kitaalamu, kubadilisha mazao na kuepuka kujeruhi karoti wakati wa kupalilia, kuvuna au kusafirisha.

Majani ya karoti yaliyoshambuliwa na madoa meusi

6.5.2.2 Wadudu i. Minyoo Fundo

Minyoo hii hushambulia mizizi na kuifanya iwe na vinundu. Hali hii husababisha mmea kudumaa na kupunguza mavuno. Minyoo fundo huweza kuzuiwa kwa kubadilisha mazao. Baada ya kuvuna usipande mazao ya jamii ya karoti kama vitunguu au mazao yanayoshambuliwa na wadudu hawa. Unaweza kupanda mazao ambayo hayashambuliwi na minyoo fundo kama vile mahindi. Pia hakikisha shamba ni safi wakati wote.

Page 33: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

29

ii. Inzi wa KarotiMashambulizi hufanywa na funza ambaye hutoboa mizizi. Ili kuzuia wadudu hawa tumia dawa za wadudu zilizopo kwenye maduka ya pembejeo za kilimo. Pia badilisha mazao na wakati wa kupalilia pandishia udongo kufunika mizizi.

6.6. KUVUNA Karoti huwa tayari kwa kuvuna baada ya wiki 10 hadi 12 tangu kupandwa kutegemea hali ya hewa. Wastani wa mavuno kwa hekta moja ni tanu 25 au zaidi.

Page 34: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

30

7. KILIMO BORA CHA VITUNGUU

7.1 UTANGULIZI

Zao la vitunguu hulimwa karibu kila mahali hapa nchini Tanzania. Vitunguu na majani yake ni viungo maarufu kwa kuongeza harufu nzuri na ladha katika vyakula. Vile vile hutumika katika kutengeneza supu, siki na kachumbari. Kiafya vitunguu ni muhimu kwani hutupatia madini na vitamini.

7.2 KUCHAGUA ENEO Vitunguu huhitaji udongo tifutifu wenye rutuba nyingi na usiotuamisha maji. Hustawi vizuri zaidi kwenye sehemu zenye mwinuko wa kuanzia mita 800 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari. Hupendelea hali, ya ubaridi kiasi wakati wa kuotesha mbegu mpaka vinapoanza kuweka tunguu na joto la wastani (nyuzi joto 20 hadi 27 za Sentigredi "20 - 27 °C") hadi kuvuna. Hivyo ni vizuri vioteshwe wakati wa baridi ili viweze kuvunwa kipindi cha jua.

7.3 KUOTESHA MBEGU KATIKA KITALU Mbegu za vitunguu huoteshwa kwanza kwenye kitalu na baadaye huhamishiwa shambani. Matayarisho ya kitalu hufanyika wiki moja au mbili kabla ya kupanda mbegu. Tengeneza tuta lenye upana wa mita moja na urefu wowote kutegemea mahitaji yako. Weka mbolea ya asili kiasi cha ndoo moja hadi mbili katika kila mita mraba mmoja. Changanya mbolea hii na udongo vizuri. Sawazisha kwa kutumia reki au kifaa chochote.

Page 35: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

31

Mwagilia kitalu siku moja kabla ya kupanda. Sia mbegu katika mistari yenye nafasi ya sentimita 10 hadi 15 kutoka mstari hadi mstari. Kiasi cha mbegu konachotakiwa kuotesha katika eneo la mita mraba moja ni gramu tano ambacho ni sawa na kijiko kidogo cha chai. Kiasi hiki pia hutoa miche inayotosha kupandikiza eneo la mita mraba 100. Kilo mbili hadi 2.5 za mbegu hutoa miche ambayo inatosha kupandikiza katika eneo la hekta moja.

Baada ya hapo weka matandazo kama vile nyasi, kisha mwagilia mara mbili kila siku (asubuhi na jioni) hadi mbegu zitakapoota. Mbegu bora huota baada ya siku 10 mpaka 12.

Aina za vitunguu Aina za vitunguu zinazoshauriwa kustawishwa katika ukanda wa joto ni:- Singida Local, Red Creole, Red Bombay na Pretoria Grano.

7.4 KUTAYARISHA SHAMBA Tayarisha shamba vizuri mwezi mmoja kabla ya kupandikiza. Kisha lainisha udongo katika kina cha kutosha (sentimita 30). Kisha lainisha udongo wiki mbili kabla ya kupandikiza. Weka mbolea za asili zilizooza vizuri ili kuufanya udongo ushikamane vizuri na uweze kuhifadhi unyevu kwa muda mrefu. Kiasi kinachotosha hekta moja ni tani 20 au zaidi. Kwa hali halisi kupata kiasi kikubwa cha mbolea hizi ni nadra sana. Kwa hiyo njia rahisi ya kubana matumizi ya mbolea hizi pindi utakapopata kiasi kisichoweza kutosha shamba lako ni kuweka kiasi kidogo kwenye kila shimo. Kiasi cha kiganja kimoja au viwili kwa kila shimo hutosha kwa kila mche.

Kutokana na kwamba nafasi utakayopandikiza itakuwa ya kubanana kiasi (sentimita 8 hadi 12) na kuweka kiganja cha mbolea za asili kwa kila shimo itakua changamoto yani utaweka mashimo mengi sana kwa sehemu ndogo na itakupa kazi sana, basi unaweza kumwaga mbolea hizo kidogo kidogo kwa upana wa kiasi cha kiganja kimoja au viwili kwa kufwata mstari kisha changanya mbolea hii kwa kutumia ncha ya reki au jembe dogo.

Lakini unavyomwaga mbolea hii kwa kufuata mstari hakikisha unapandikiza wakati huo huo ili kuhakikisha unapanda sehemu husika yenye mbolea hiyo. Ukishachanganya mbolea hiyo vizuri na udongo unaweza kupandikiza. Kama una eneo dogo la kupandikiza unaweza kumwaga mbolea hizo za asili kwenye shamba hilo alafu changanya vizuri ndipo upandikize.

Matuta yanafaa pia kwenye kilimo cha vitunguu kwa kutumia nafasi nitakazo kupa kwenye maelezo yanayofuata kwenye makala hii. Kama hutotumia matuta hakikisha kina cha udongo ni kikubwa sana (sentimita 30 kwenda chini) ili upate vitunguu vikubwa na vyenye afya.

7.5 KUPANDIKIZA Miche inakuwa tayari kwa kupandikizwa shambani baada ya wiki sita tangu kusia mbegu. Wakati huo miche inakuwa na urefu wa sentimita 12 hadi 15 na unene uliosawa na kalamu ya risasi.

Loanisha kitalu siku moja kabla ya kung'oa miche ili kuepuka kukata mizizi. Tumia kijiti au chombo chochote kinachofaa kwa kung'oa. Baada ya kung'oa punguza majani na mizizi ili kuzuia upotevu wa maji.

Page 36: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

32

Pandikiza miche katika nafasi ya sentimita 30 kutoka mstari hadi mstari na sentimita 8 hadi 12 mche hadi mche. Vitunguu vilivyopandwa kwa nafasi hii hukomaa mapema na idadi ya mimea kwa eneo ni kubwa.

Chagua miche yenye afya na ambayo haikushambuliwa na wadudu wala magonjwa. Miche michanga sana au iliyokomaa sana haifai kwa kupandikiza. Miche ipandikizwe katika kina kama vile ilivyokuwa kwenye kitalu. Pandikiza wakati wa asubuhi au jioni ili kuepuka jua kali na joto linaloweza kuunguza miche. Mara baada ya kupandikiza mwagilia maji.

Endelea kumwagilia asubuhi na jioni mpaka miche itakaposhika vizuri.Top of Form

7.6 KUTUNZA SHAMBA (i) Kuweka MboleaMbolea ya kukuzia kama vile chai ya samadi huwekwa shambani katika wiki ya tatu na ya sitabaada ya kupandikiza.

(ii) KumwagiliaKila wakati hakikisha shamba lina maji ya kutosha. Punguza kumwagilia wakati vitunguuvinakomaa. Vitunguu vinavyokomaa majani hubadilika rangi kuwa njano. Maji mengihusababisha vitunguu kuoza baada ya kukomaa.

(iii) PaliziPalilia na tifulia mara kwa mara uonapo magugu yanaota, na hasa miche inapokuwa badomichanga. Palizi ifanyike kwa uangalifu bila kuikata mizizi. Wakati unapopalilia katikati yamatari ni vema kung'oa magugu kwa mikono na kufunika shina kwa kupandisha udongo kuzuiamizizi isipigwe na jua.

7.7 MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU

7.7.1 Magonjwa a. Ubwiri Vinyonya (Downy Mildew)Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hupendelea hali ya unyevu unyevu. Dalili zake nimajani kuwa na ukungu au uyoga wa rangi ya njano iliyochanganyika na nyeupe. Kwa kawaidamajani yaliyoshambuliwa hukauka kabla ya vitunguu kukomaa.

Ubwiri vinyoya huzuiwa kwa kuzingatia yafutayo; Kubadilisha mazao. Baada ya kuvuna vitunguu, zao linalofuata lisiwe la jamii moja kama

vile vitunguu saumu na vitunguu majani.

Page 37: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

33

Nyunyuzia mojawapo ya dawa za kuzuia ukungu kama vile majani ya mpapai maziwana"blue Copper"

b. Purple BlotchHuu pia ni ugonjwa uletwao na ukungu na hushambulia majani, shingo na vitunguuvilivyokomaa. Dalili zake ni, majani huonyesha vidonda vyenye na vilivyodidimia. Baadaye bakala zambarau huonekana katikati ya jani. Baka hili baadaye huwa jeusi na hufunikwa na uyoga auukungu. Shina lililoshambuliwa hulegea na huanguka katika wiki ya tatu au ya nne baada ya daliliza ugonjwa huu kuonekana. Vitunguu vilivyokomaa huoza kuanzia shingoni, hugeuka rangi nakuwa njano iliyochanganyika na nyekundu.

Mmea ulioshambuliwa na purple blotch Zuia ugonjwa huu kwa kuzingatia yafuatayo;

Panda vitunguu vilivyothibishwa na wataalamu Badilisha mazao Vuna vitunguu kwa wakati unaotakiwa Epuka kukwaruza au kuchubua vitunguu wakati wa kuvuna. Ondoa masalia ya mazao shambani baada ya kuvuna na kuyachoma. Panda vitunguu vinavyovumilia mashambulizi ya ugonjwa huu kama vile vitunguu

vyekundu.

c. Kuoza Shingo (Neckrot)

Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hupendelea sana hali ya unyevu. Hushambulia vitunguu vilivyokwisha vunwa na kuhifadhiwa. Vitunguu vilivyoshambuliwa na ugonjwa huu huwa laini, kubonyea na huonekana kama vilivyopikwa. Ugonjwa huanzia kwenye shingo na baadae huenea kwenye kitunguu chote na kufunikwa na ukungu wa kijivu. Mwisho machipukizi madogo hujitokeza.

Ugonjwa huu unazuiwa kwa kuzingatia yafuatayo; Vuna vitunguu vilivyokomaa kwa wakati

Page 38: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

34

Ondoa na yachome moto masalia ya mazao baada ya kuvuna. Epuka kuchubua au kukwaruza vitunguu wakati wa kuvuna. Kausha vitunguu vizuri baada ya kuvuna. Hifadhi vitunguu kwenye sehemu zisizo na unyevu mwingi

Page 39: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa
Page 40: November, 2019 · 2020-06-02 · 1 1. KILIMO BORA CHA NYANYA 1.1 MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa

SHUK RANI

Kitini hiki cha “Mwongozo wa mafunzo ya uzalishaji wa mazao ya mbogamboga” kime andaliwa

na shirika la SWISSAID Tanzania kwa ushirikiano na Kilimo Endelevu Tanzania (SAT –

Sustainable Agriculture Tanzania). Kitini hiki kimepitiwa na kuidhinishwa na wawakilishi wa

Ofisi ya Kilimo ya Mkoa wa Mtwara, Ministry of Agriculture Training Institute (MATI)

Naliendele, Sustainable Agriculture Tanzania (SAT), Tanzania Organic Agriculture

Movement (TOAM), Tanzania Alliance for Biodiversity (TABIO), Tanzania Official Seed

Certification Institute (TOSCI-Mtwara), Shirika la Uhifadhi Misitu Asilia Tanzania (TFCG),

wawakilishi wa wakulima na SWISSAID Tanzania katika warsha iliyofanyika tarehe 25 – 27

September 2019 katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara. Pia, msaada wa kifedha kutoka

Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Liechtenstein Development Service (LED) na Swiss

Agency for Development and Cooperation (SDC) umefanikisha kwa kiwango kikubwa katika

kugharamia uandaaji, kupitia na kukamilisha uchapishaji wa kitini hiki.

“Kitini hiki cha mafunzo kipo chini ya hati miliki ya kimataifa nambari 4.0 (CC BY-NC-DC 4.0), hairuhusiwi kuuzwa ama kunakiriwa pasipo idhini ya mmiliki.”

"This training manual is licensed under a Creative Commons Attribution-Non Commercial-NoDerivatives 4.0 International (CC BY-NC-ND 4.0) license"